Search This Blog

Tuesday, 1 November 2022

KILIO CHA NAFSI - 4

 






Simulizi : Kilio Cha Nafsi

Sehemu Ya Nne (4)





****

Siku iliyofuata aliamka mapema sana kitu kilichomshangaza kila mtu nyumbani hapo,kumbumbuku ya ndoto ya jana jioni aliyoiota ilikuwa bado ikikisumbua kichwa chake hakuwa na uhakika kama kweli msichana huyo mdogo alikuwa akiitwa Naomi na kwanini alimuote! Nini kilikuwa katikati yake.

“Dada chai iko tayari?”

“Ndiyo. Shikamooo.”

“Marhaba niandalie nakuja.”

“Aya,” alijibu na kuelekea mezani huku akimuacha Dk. Samweli alielekea chumbani kwake kiunoni akiwa amefunga taulo.

“Naomi …Naomi.. kwanini nakuwaza hivi kwanini unaichanganya akili yangu wewe ni nani hasa?” aliwaza akiwa bado anaoga dakika kadha alikuwa ameshamaliza kuoga na kuvaa hivyo alitoka na kupitiliza moja kwa moja mezani, alitumia dakika tano kukamilisha zaoezi hilo kisha alitoka nje kwa lengo la kuondoka.

“Dokta leo mbona mapema kiasi chicho?” mama yake aliyekuwa mtu wa matani sana kwa Samweli alimuuliza mara baada ya kumuona akimpita bila kuaga maana haikuwa kawaida yake kuondoka nyumbani hapo bila kuagana na wanafamilia wake.

“Nisamehe mama nadhani nimepitiwa.”

“Au Naomi anakuchanganya?” alimuuliza huku akimtazama machoni tazama hiyo ilipelekea Samweli kuyakwepesha macho yake kana kwamba alikuwa binti akitazamwa na mvulana aliyekuwa akimpenda.

“Ha..hapaana ila …nimepitiwa acha niwahi utamuaga baba.”

Aliyauma uma meneno kisha aliondoka eneo hilo na kuliendea gari lake alifungua na kuingia safari ya kuelekea Muhimbili ilianza njia nzima alikuwa akimuwaza Naomi.





Kitu cha kwanza kukifanya mara baada ya yeye kufika hospitali hapo alianza kumtafuta msichana aliyeletwa jana yake, haikuwa kazi ngumu sana kumpata kwani alipowaulizia manensi walimuelekeza wapi alipo. Alitembea kwa wasiwasi huku moyo wake ukidunda kana kwamba alikuwa amefumaniwa, kila hatua aliyopiga kuelekea chumbani humo ndipo mapigo ya moyo wake nayo yalizidi kudunda.

“Nakipenda kisichana hiki haki ya nani?” aliwaza peke yake huku akiufungua mlango wa chumba alichokuwa amelazwa Naomi.

“Hujamba mtoto mzuri?” Akamsalimia mara baada ya kufika kitandani hapo na kusimama pembeni yake macho yake yakiwa juu ya paji la uso wa masichana huyo aliyeonekana akiugulia kwa maumivu makali sana ndani ya mwili wake.

“Sijamabo shikamooo.”

“Mara-haba unaendelea?”

“Vizuri kiasi,” Naomi alijibu kwa sauti ya chini huku akiwa amelala chali ile ongea yake ya kigonjwa kigonjwa ilipelekea Dk. Samweli kuumia sana. Tayari alishangudua kitu kilichokuwa kikiumiza moyo wake ni mapenzi tena mapenzi ya dhati kwa msichana huyo wa miaka kumi na tano! Alionekana ni msichana mzuri sana tena aliyekuwa na sifa za kuitwa mrembo ila hali yake ya ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu na maisha magumu ya mtaani vyote vilipelekea yeye kuipoteza sifa hiyo amabayo alitunukiwa siku ya kuzaliwa.

“ Uliumia nini?”

“Mguu ulivunjika hapa,” alisema huku akimuonesha sehemu ya paja iliyokuwa imefungwa bandeji mara baada ya kufanyiwa upasuaji, tayari mguu wake ulikuwa umeshushwa chini mara baada ya yeye kuzinduka masaa kadhaa yaliyokuwa yamepita.

“Pole sana utapona sawa,”

“Ndiyo,” aliitikia huku akijilazimisha kuachia tabasamu lakini alishindwa mara baada ya kifua chake kupokea maumivu makali yaliyosababisha kushindwa hata kuongea.Alibaki akimtazama Dk. Samweli bila kuongea kwani maumivu aliyokuwa akiyasikia yalikuwa makali mno.

“Unatatizo gani?”

Naomi hakuweza kuongea zaidi ya kukishika kifua chake ishara ya kumueleza kile alichokuwa kikimsumbua.

“Ni tatizo la muda?” Dk. Samweli alimuuliza tena akiwa amechanganyikiwa hakutaka kuona mtu aliyempenda kuwa katika hali hiyo, alitoka ndani ya chumba hicho mbio hadi ofisini kwake huko nako alikosa cha kufanya zaidi ya kuzunguka huku na huko.

“Anatakiwa afanyiwe kipimo cha x-ray haraka iwezekanavyo,” aliwaza peke yake akiwa amesimama dirishani hapo hapo alichukua simu yake na kupiga chumba cha x-ray.

“ Habari za asubuhi Dk. Samweli?” Upande wa pili ulijibu mara baada ya simu kupokelewa.

“Nzuri kiasi upo ofisini?”

“Hapana bado sijafika je kuna shida ya haraka?”

“Ndiyo kuna mgonjwa anatakiwa afanyiwe kipimo haraka iwezekanavyo,” alisema kwa wasiwasi huku akizunguka zunguka jasho jepesi lilianza kuusumbua mwili wake.

“Daaah! Na leo kuna foleni sana ila nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu kwani anahali mbaya sana?”

“Ndiyo Dokta fanya haraka.”

“Basi acha niliache gari sehemu salama kisha nichukue pikipiki.”

“Ahsante sana.”

Alishukuru na kukata simu kisha alitoka mbio hadi chumbani kwa Naomi, alishangaa kukuta idadi ya manesi wakiwa wamekizunguka kitanda cha msichana huyo aliyekuwa akihangaika kwa maumivu makali ya kifua.Huku akiwa ameshapoteza fahamu. Manesi hao walionekana wakikikandamiza kifua cha Naomi kama moja ya huduma ya haraka kwa mgonjwa huyo.

“Mmegundua tatizo?”

“Ndiyo ni mshtuko wa moyo na tumefanyia huduma ya kwanza kiasi imemsaidia.Ila anaonekana na tatizo jingine tunamuadaa kwa ajili ya kuchukua kipimo cha x-ray haraka iwezekanavyo.”

“Hawezi akapigwa miozi kwa sasa tusubiri kwanza ashtuke.”alijibu kwa unyonge zaidi akiwa anamtazama Naomi kwa macho ya huruma sana.

“Haya dokta!!”Wote walimuitikia wakiwa wanamshanga sana kwani hata siku moja hawakuwahi kumuona akiwa katika wakati kama huo. Daima alikuwa mtu mpole na mtaratibu sana, hakuwa muongeaji zaidi ya kutekeleza majukumu yake.



Dakika saba Naomi alitundikiwa dripu ya dawa aina ya asprin ili kuutibu ugonjwa uliokuwa umeonekana kwa wakati huo.Walifanya hivyo ili kumrejesha katika hali yake ya kawaida kabla ya kwenda kumfanyia kipimo cha x-ray kubaini ugonjwa uliokuwa ukimsumbua.



“Dk. Tinti hebu niambie majibu ya yule mgonjwa?” Dk.Samweli alimuliza Daktari mwanzake mwanamke aliyekuwa akihusika na upigaji wa mionzi hiyo akiwa chumbani kwake.

“Anaonekana ana Arijina(Argina) hii imesababishwa na mgando wa mafuta kwenye moyo wake kwa muda mrefu sana,mgando huu umepoteza nafasi ya moyo wake kupokea damu yenye oksijeni hivyo anatakiwa afanyiwe huduma haraka iwezekanavyo ili kuyaokoa maisha yake.” Aliongea huku akimkabidhi Dk. Samweli majibu ya vipimo hivyo. Siku moja baada ya yeye kuwa katika hali ya kawaida kidogo.

“Nipo tayari kumshugulikia haraka iwezekanavyo na hata kulipia gharama zote.”

“Nami nitakuwa nawe bega kwa bega.”

Walitoka ndani ya chumba hicho mara baada ya kutoa maagizo kwa manesi kumuanda kwa ajili ya upasuaji ili kuyaondoa mafuta yaliyokuwa yamegandamiana katika moyo wa Naomi msichana mdogo sana.



****http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Ulikuwa ni upasuaji uliochukua masaa sita upasuaji uliofanyika kwa usahihi zaidi kati ya madaktari hao, walihakikisha wanaitumia vyema elimu yao waliyoichukua ili kuwaokoa watanzania waliokuwa wakiteseka na magonjwa ya moyo.Mara baada ya upasuaji huo Naomi alitolewa ndani ya chumba hicho akiwa hajitambui kabisa dripu za maji na damu nazo hazikuwa nyuma kuingia ndani ya mwili wake kupitia kwenye mishipa yake.



“Mungu akusaidie mpenzi,” alisema peke yake huku akikaa juu ya kiti chake na kuwaruhusu wagonjwa wengine kuonana naye. Kila siku hakusita kumtembelea Naomi kumjulia hali yake maendeleo ya Naomi yalikuwa faraja sana kwake pia hakuwa nyuma kumkumbuka katika sala zake kila alipopata muda wa kufanya hivyo. Siku tano mbele Naomi alitolewa ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi mara baada ya afya yake kutengemaa kiasi, kutolewa kwa Naomi chumbani humo kulizidi kumfurahisha sana Dk. Samweli aliyekuwa akitumia muda mwingi kumtembelea.



“Siku njema kwako mrembo.”

“Haha,” alicheka kwa furaha mara baada ya kusikia neno hilo ambalo lilikuwa kawaida yake kutoka mdomoni mwa Dk. Samweli mara baada ya kuonana na Naomi. Ile cheka yake ilipelekea vishimo vidogo vya kwenye mashavu yake kuonekana japo alikuwa amekondea lakini havikuwa nyuma kutokeza, havikuwa vishimo pekee bali hata meno yake meupe yaliyokuwa na mpangilio mzuri mdomoni mwake nayo alipata nafasi kuyaona.

“Sasa unajisikiaje?”

“Sijambo kabisa nahisi kupona ahsante kwa moyo wako wa upendo.”

“Ni haki yangu kufanya haya maana nimesoma kwa ajili ya kuwaokoa watanzania na wewe ukiwa mmoja wapo” aliongea huku akiendelea kumtazama Naomi kwa macho ya upendo zaidi, alitamani hata kumtoa juu ya kitanda hicho ili apate nafasi ya kumtazama vizuri uzuri wa sura yake uliashilia hata umbo lake lilikuwa zuri pia.



Mwezi mmoja na wiki mbili Naomi alipewa ruhusa ya kuondoka hospitali hapo kwani afya yake ilikuwa nzuri kabisa, moyoni alifurahi sana kupona ugonjwa uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu ila upande mwingine hakuwa na furaha kabisa tayari alikuwa ameshayazoea maisha ya hospitali. Maisha yaliyokuwa mazuri kwake, kila alipozifikilia adha za maisha ya mtaani alichoka kabisa alitamani hata augue tena ili aendele kubaki eneo hilo.

“Naomi mbona huoneshi furaha.” Dk. Samweli alimuuliza mara baada ya kumuona amenyong’onyea sana.

“Sina pa kuishi Dokta,”aliongea huku akitazama chini kope za macho yake zikianza kulowana kwa machozi.

“ Usilie nifuate.”

Walitembea hadi eneo alilokuwa amepaki gari lake alifika na kumfungulia mlango kisha naye alizunguka upande wa pili alifungua na kuingia kisha aliwasha gari na kuondoka hospitali hapo. Njia nzima Dk.Samweli aliitumia kumtazama Naomi kupita kioo chake cha gari, alimuona ni mwanamke mzuri sana katika mboni zake za macho akili yake ilimtuma kuwa hakukuwa na mwanamke mzuri kiasi kile duniani kote kila alipomtazama mapigo yake yalizidi kuongezeka na kuufanya moyo wake kusukuma damu tofauti na kawaida yake.



Safari yao iliishia ndani ya hoteli.

“Agiza unachotaka.”

“Sina njaa usijali.”

“Hutakiwi kuniogopa uko sehemu salama kuwa uhuru.”

“Okay sawa.”

Naomi aliiagiza soda aina ya Fan’ta huku Dk. Samweli alihitaji maji.

“Unaweza ukanieleza sababu ya wewe kukosa eneo la kuishi?” Dk. Samweli alimuogelesha huku akiulamba mdomo wake wa chini na kumtazama Naomi ambaye alikuwa kimya kabisa uso wake ukiwa chini kwa aibu iliyokuwa imechanganyikana na woga hali iliyopelekea kushindwa kuzungumza na kujikuta akianza kulia kitendo kilichomshtua sana Dk.Samweli.







Dk.Samwel alipata wakati mgumu sana kumtuliza Naomi aliyekuwa akilia sana na kumfanya kuumia sana, hakupenda kumuona akiwa katika hali hiyo.

“Naomi kwanini unalia?”

“Na….aaaanaaaa….umi…aaaa…sitaki….kuyazumgumza hayaaaa…naumia sana ninapomkumbuka mama yanguuuuuuu,” akazungumza huku akizidi kulia na safari hii kilikuwa kilio cha sauti kabisa hali iliyopelekea baadhi ya watu waliokuwa wamekaa ndani ya Hoteli hiyo kuanza kuwatazama wao tu kitendo kilichomkwaza sana na kubaki akiumia sana.

“Naomi usilie kwanini unafanya hivyo?”

“Naumia…..naumia sana sijui pa kuuushii…maisha yangu ni mateso kila siku laiti mama angekuwepo angenisaidia dunia inanicheka.”

“Nakuomba nyamaza,” akamtuliza na kutoa kitambaa chake cha mkononi rangi nyeupe akaanza kumpaguasa machozi yaliyokuwa yakiendelea kutiririka na kuyalowanisha mashavu yake mazuri, mara baada ya kukamilisha zoezi hilo akamshika mkono na kumnyanyua kisha wakatoka nje na kunyosha moja kwa moja ndani ya gari lao.

“Naomi!”

“Abeee!”

“Kwanini unapenda kuniumiza kiasi hicho?”

“Sikuumizi kaka sina nia mbaya ya kukukwaza ila sina jinsi yanipasa kulia kila inapotokea kufanya vile nisamehe sana,” akazungumza huku akitaka kupiga magoti lakini Dk.Samweli akamzuia na kumvutia kifuani kwake akamkumbatia kwa nguvu sana macho yake akiwa ameyafumba kwa hisia za hali ya juu.

“Nakupenda sana Naomi nisubuli nije,” akazungumza huku akifunguo mlango wa gari hilo na kutoka nje akimuacha Naomi akiwa na mawazo chungu nzima.Dakika tano akarejea akiwa na dada aliyekuwa amebeba vinywaji.

“Sasa nieleze kinachokuliza mamy sawa?”

Alianza kwa kuongea mara baada ya wote kupata huduma hiyo mwanzo Naomi alikuwa mgumu sana kuelezea maisha yake lakini ushawishi wa Dk. Samweli ulipelekea yeye kuongea kila kitu alichokuwa akikifahamu kwa wakati huo.

“Pole sana ila hutakiwi kukata tama maisha hayana mwisho na kesho yako huifahamu”

“Ni kweli lakini nitaanzaje?”

“Kwani ulifahamu siku moja utakuja upone ugonjwa wako wa miaka mingi?”

“Hapana!”

“Basi na maisha yako vivyo hivyo wakati wa wewe kukata tamaa ndipo mkono wa Mungu huinuka kwako na je mtu akijitokeza kukusomesha utakuwa tayari?”

“Ndiyo tena nitafanya kwa bidii kabisa napenda kusoma nataka kuwa msoni wa hali ya juu kabisa.”

“Utapenda kusomea nini?”

“Nataka niwe kama wewe.”

“Hahaha! Safi sana sasa nitakusaidia kwa asilimia mia moja ili uhakikishe ndoto yako inatimia.”

“Kweli! Dokta?”

“Ndiyo.”

Naomi alifurahi kupita maelezo alimsogelea Dk. Samweli na kumkumbatia kwa nguvu furaha aliyokuwa nayo ilikuwa haielezeki alitamani hata kumbeba juu juu amtembeze mjini kote akimtangaza kuwa alikuwa Mungu wake wa duniani.

“Sijui nitakulipa nini Dokta sijuiiiii,” alisema huku akilia kilio cha furaha.

“Usijali nipo kwa ajili yako nafanya hivi kwa sababu nakupenda sana nataka siku moja uje uwe mke wangu na mama watoto wangu ila kwa sasa sitakugusa kwa chochote na ukijitahidi nitakupeleka chuo nchi za mbali sawa chaurembo.”

“Ahsante sana…. Ahsante…”



Hakika ilikuwa furaha sana kwa Dk. Samwel kumpata mtu aliyeoneka ni sahihi kwake, mara baada ya maongezi alimchukua Naomi hadi nyumbani kwao alikofika na kumtambulisha kisha aliwaeleza nia ya yeye kwa binti huyo hakuna aliyepinga wazo la Dk. S amwel na siku hiyo hiyo Naomi aliaza kufundishwa kusoma na kuandika kabla ya kutafutiwa mwalimu aliyekuwa akimfuata nyumbani hapo. Kama Dk. Samwel alivyomweleza Naomi hakutaka kumsogelea hata kidogo zaidi ya kumsaidia katika masomo yake na akimheshimu kama dada yake wa damu.



Uelewa wa Naomi uliwashagaza sana wote kwani ndani ya wiki tatu aliweza kusoma na kuandika vizuri kabisa hali iliyokuwa ikimfurahisha Dk. Samweli.

“Kesho nitakupeleka shule nataka ukaanze kusoma darasa la kwanza.”

“Hapana Dokta naomba ukaniombee nisome darasa la tatu.”

“Utaweza?”

“Ndiyo,” alijibu kwa kujiami sana kweli siku iliyofuata Naomi alipelekwa shule alikopokelewa kwa furaha na ili kuhakikisha kuwa alikuwa na uwezo wa kusoma darasa la tatu uongozi wa shule ulimpatia jaribio alilolifanya vizuri kabisa na hata kuwashangaza walimu wote. Darasa la tutu alilisoma kwa muda wa miezi minne kisha aliomba kufanya jaribio la darasa la nne. Kwa kuwa walimu hawakuwa na hiyana naye pia walikuwa wakimpenda kwa dhati hawakuwa nyuma kumpatia jaribio hilo alilolifanya kwa usahihi na kufaulu vizuri kabisa hata wanafunzi waliokuwa wakimtania mama wa darasa walianza kumpa heshima.

“Naomi Mlema kuanzia leo utahamia darasa la nne.”

“Ahsante sana mwalimu.”

Siku hiyo alifurahi sana na hata alipozifikisha taarifa hizo nyumbani nao waliungana naye kwa furaha mtu aliyekuwa na furaha iliyopitiliza ni Dk. Samweli.

“Sijui nikufanyie nini uamini kama nina furaha na kitendo hicho Naomi.”

“Naomba uninulie vitabu vya darasa la tano, sita na saba sitaki kuendelea kuwa darsaa la nne nikifaulu tu mtihani wa kuingia darasa la tano nitasomo kwa mwezi mmoja kisha namuomba mwalimu kujiunga la saba.”

“Kweli mpenzi?”

“Ndiyo niamini,”alisema huku akimbusu shavuni busu lililomfurahisha sana Dk.Samweli siku iliyofuta alimletea Naomi vitabu hivyo alivyokuwa akivisoma kila siku, hakuwa na muda wa kucheza ama kuangalia runinga yeye alikuwa na madaftari kila dakika. Matokea ya kuingia darasa la tano yalipotoka Naomi alikuwa miongoni mwa wanafunzi kumi wa mbele waliofanya vizuri hivyo Naomi akawa ametumia mwaka mmoja kusoma madarsa manne! Kitu kilichokuwa cha ajabu kabisa.



“Mwalimu naomba unisajili darasa la saba.”

“Naomi utaweza?”

“Ndiyo nimetumia meizi mitano kujifunza masomo ya darsa la sita na hata ya la saba nina uhakika wa mimi kufanya mtihanai wa taifa vizuri.”

“Nani alikuwa akikufundisha.”

“Nina mwalimu nyumbani naomba unisanidie.”

“Usijali nitazungumza na mkuu wa shule na kesho nitakupa jibu sawa.”

“Nitashukuru sana.”

Aliondoka ofisini humo kwa furaha sana kila alipowatazama wanafunzi wa darsa la saba alitamani kuwa mmoja wao siku hiyo aliitumia kumuomba Mungu akafanye wepesi wa yeye kupata ruhusa ya kujiunga na darasa la saba.Kama alivyodhamiria kweli siku ya pili Naomi alipewa nafasi ya kujiunga na darasa la saba kitu kilichozidi kuwashangaza watu wote. Alisoma kwa bidii sana, ili kuukabili mtihani uliokuwa mbele yake miezi minne tu.



“Dk. Samweli nimefauluuuu kujiunga nakidato cha kwanza,” aliongea Naomi huku akikimbia kwanda chumbani kwa Dk. Samweli aliyekuwa amejipumzisha kidogo mara badaa ya kutoka kazini.

“Usinitanie Naomi.”

“Kweli matokea haya hapa,” alitoa kipande cha karatasi kilichokuwa na orodha ya wanafunzi waliofanya vizuri na kumpatia.

“Naomi….Naomiiiii ooooh!” Alishindwa kuzungumza vizuri zaidi ya kumnyanyua juu huku akiwa anatoa machozi ya furaha, hakuishia kumnyanyua peke yake bali alimshushia mvua ya mabusu mwili mzima.

“Naomi nakupenda sana nakupenda mpenzi.”

“Nami nakupenda sana nafanya hivi kwa ajili yako,” alisema huku akimtazama machoni Dk. Samweli aliyeshindwa kujizuia alimvuta karibu yake na kuyashika mashavu yake kwa mikono yake miwili kisha aliusogeza mdomo wake kinywani mwa Naomi.

“Mwaaaah! Nakup…”

Hakuweza kumalizia sentesi yake mara baada ya kuuingiza ulimi wake kinywani mwa Naomi aliyekuwa akitetemeka mwili mzima toka azaliwa hakuwahi kuwa karibu na mwanaume kama siku hiyo, kila kitu kilikuwa kipya kwake.Utundu wa ulimi wa Dk. Samwli kinywani mwa Naomi ulimfanya Naomi kujihisi tofauti kabisa.

“Naaaom”

Dk. Samweli alizidi kuchanganyikiwa alimbeba hadi kitandani na kumtupia kisha alimlalia juu yake huku mikono yake ilichezea kifua cha Naomi aliyekuwa akijigeuza geuza na kugugumia kwa mahaba. Macho ya Dk. Samweli yalibadilika na kuwa mekundu kupita maelezo utadhani siku hiyo alibwia unga.

“Nakupenda sana Mpenzi akazidi kuzungumza huku akiuchezea mwili wa Naomi aliyekuwa akizidi kujigeuza geuza na asijue cha kufanya.

“Noooo….niacheee D”

“Nimesh….,” hakuweza kuimalizia sentensi yake akaanza kuzitoa nguo za Naomi aliyekuwa akikitetemeka mwili mzima.







Maneno ya Naomi hayakuweza kumuingia Dk. Samwel kama Naomi alivyokuwa akifikiria alimshangaa jinsi alivyokuwa amebadilika mwili mzima, mishipa yake ya kichwa ilisimama wima na mwili wote ulituna mithili ya simba aliyekuwa akimkimbiza mnyama porini.

“Doktaaa,”Naomi akamuita kwa taabu mno huku akizidi kujigeuza geuza kitandani macho akiwa ameyafumba macho asitake kuuona uso wa Dk.Samwel aliyekuwa akihangaika kuitoa siketi yake mara baada ya kuitoa blauzi ya juu.

“Kwanini unataaaaka kunitenda hiviiiiiiiiii”

“Siyo ila naombaa kidogo tuuuuuu,”akazungumza huku akizimg’unya chuchu za Naomi hali iliyopelekea Naomi kupiga ukulele wa hali juu sana kitendo kilichomshtua Dk. Samwel akamziba mdomo wake kwa kiganja chake cha mkono wa kulia akiwa amemlalia kwa juu.

“Mbona hivyo mamy?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Unavunja ahadi yako kwanini unataka kunifanyia hivi Dokta…..nitawezaaaa kweli kusoma naiogapa mimba Doktaaa,”akazungumza huku akilia kitendo kilichomuumiza sana Dk.Samwel akatoka kifuani kwa Naomi na kukaa kisha akamyanyua na kumpakata kifuani kwake akiwa amemkumbatia kwa nguvu zake zote akiendelea kumnyamazisha.

“Nani alikwambia utapata mimba?”

“Ma…mamaaa alinieleza nisifanye hivi hata siku moja naweza pata mimba,”akazungumza taratibu bila kumtazama machoni uso wake ulilitazama shuka la kitandani akiwa anazitafuna kucha zake ambozo hata hazikuwepo kabisa.

“Nisamehe”

“Uliniahidi kutonifanyia hivi hadi nitakapomaliza masomo yangu kwanini unataka.”

“Nisamehe Naomi nimeshindwa kuvumilia.”

“Hapana nakuomba uvumilie tafadhali.”

“Okay,” alijibu kwa unyonge na kumkumbatia kwa dakika kadhaa macho yake yakitoa machozi ambayo hakuyafahamu yalitokana na nin kumbatia hiyo ikawapelekea kutabasamu kwa pamoja kisha wakachekana kama vile walikuwa wajinga huku wakipigana makofi ya kimapenzi.



“Nahisi usingizi Dokta.”

“Njoo ulale mimi mwenyewe nataka kulala si uliniamsha.”

“Hahahaha mimi sikufahamu nisamehe acha nilala hapa,”akazungumza huku akiuruhusu ubavu wake kulala juu ya godoro hilo dakika moja Dokta naye akalala karibu kabisa na Naomi na kumpitishia mkono wake kiunoni huku kichwa cha Naomi akikilaza kifuani kwake.

Majira ya saa mbili usiku ndipo waliposhtuka tena mara baada ya kugongewa kwa ajili ya chakula cha usiku, walitoka na kujumuika mezani na familia nzima wakiwa na furaha sana kila mtu alimpongeza Naomi na siku iliyofuata familia hiyo ilimfanyia Naomi sherehe ndogo ya kumpogeza kwa kile alichokifanya huku kila mtu akimuahidi kumsaidia kwa chochote.



Mwaka uliofuata Naomi alijiunga na kidato cha kwanza na cha pili kwa elimu ya watu wazima iliyokuwa ikifahamika kama QT, aliendelea na juhudi zake kama kawaida na kufanikiwa kufaulu vizuri sana japo elimu hiyo ilikuwa kifahamika kama ngumu sana lakini kwa Naomi ilikuwa nyepesi sana juhudi zake binafsi ndizo zilizomsaidia kupata maksi za juu.

Mwaka uliofuata aliingia kidato cha tatu na nne, alizingatia kile walimu walichokuwa wakimfundisha hatimae alifanya vizuri kidato cha nne hali iliyozidi kuchochea mapenzi kwa Dk. Samwel. Siku ya yeye kupokea ushindi huo Dk. Samwel hakuwaza kuamani alilia kama mtoto mdogo kila alipomtazama Naomi aliyekuwa msichana wa miaka kumi na tisa sasa hakuweza kuamini na siku hiyo hiyo walilala pamoja kitu kilichozidi kumfurahisha sana.



Maisha ya kitado cha tano na sita kwa Naomi yalikuwa ya furaha sana alihakikisha anaitumia vizuri miaka yake hiyo miwili ili kuipata nafasi aliyokuwa ameahidiwa na Dk. Samwel siku walipozungumza kwa mara ya kwanza, alisoma kwa bidii sana na kujituma kila alipopatwa na tatizo lolote hakusita kumshrikisha Dk. Samwel aliyekuwa kama mwalimu wake, alimsaidia kwa asilimia kubwa japo walikuwa wapenzi lakini hawakuyaruhusu mapenzi yao kumteka sana Naomi.Miezi mitatu ya mwisho Dk. Samwel hakutaka kumsumbua kabisa Naomi zaidi ya kumsaidia kimasomo hadi alipofanikisha kumaliza mitihani yake ya kidato cha sita.

“Natamani sana matokeo yatoke haraka nina uhakika wa kufanya vizuri.”

“Nami vivyo hivyo na ujiandae kwa kwenda Marekani nataka ukasomee chuo nilichosomea mimi.”

“Kweli mpenzi?”

“Kwanini isiwe hivyo ahadi ni deni hivyo lazima nilipe sitaweza kukukatisha kiu yako ya kuwa daktari nataka uwasaidie watanzania wenzako.”

“Sijui nitakulipa nini? Sioni zawadi ya kukutosha kwa wema ulionitendea, mwili wangu naona kama hautoshi.”

“Naomi upendo wa dhati ni zawadi tosha kwangu wewe ni mwanamke sahihi wa maisha yangu nakuomba ujitunze na ujithamini usidanganyike kwa chochote tambua wanaokutamani ni wengi ila anayekupenda ni mmoja tanzama nimejitoa maisha yangu yote kukupenda wewe hivyo naomba unithamini kama ninavyofanya mimi.”

“Nakuahidi mpenzi nitakuwa mwaminifu kwako,” alisema huku akijiegemeza kifuani kwa Dk. Samwel wiki moja mara baada ya yeye kuhitimu kidato cha sita.



*****

Ilikuwa ni siku yenye furaha sana kwa wapenzi hao siku iliyokuwa ikisubiliwa kwa muda wa miezi kadhaa, siku iliyozidi kudumisha upendo wao.Hakuna aliyeamini kama kweli Naomi alikuwa amepata ufaulu wa daraja la kwanza kulia walishindwa kucheka walishindwa zaidi ya kutazamana kama majongo waliokuwa wakitaka kupigana.

“Ndoto yako imewadia unaenda kuitwa Dk. Naomi muda si mrefu.’

“Sina neno la kumshukru Mungu sina neno la kukushukru ila wema wako utalipwa.”

“Amina.

Dk. Samwel alihakikisha Naomi anapata nafasi ya kujiunga na chuo nchini Marekani hivyo siku hiyo hiyo alianza kufatilia taratibu za kutuma maombi chuoni hapo, kwa kuwa alikuwa na marafiki wengi nchini humo hakupata ugumu kuipata nafasi hiyo ya Naomi kwenda kusoma chuoni hapo.Kwanza kabla ya kuondoka Tanzania alisafiri kwa mara ya kwanza toka watoroke na mama yake mkoani Kilimajoro kwa lengo la kumtafuta baba yake japo alitoka akiwa mtoto mdogo lakini aliyakumbuka vyema mazingira ya kijijini kwao.

“Shikamo bibi,”akamsalimia mwanamke aliyeonekana mzee kiasi akiwa anachuma kawaha shambani kwake mita kadhaa mahali ilipokuwa nyumba yao, mara baada ya yeye kufika kijijini hapo majira ya saa kumi na moja jioni.

“Mar-haba bibi karibu,”akamjibu huku akiahirisha zoezi lake la uchumaji wa kahawa na kumtazama Naomi msichana aliyeonekana mgeni kabisa machoni mwake kila alipojitahidi kurejesha kumbukumbu ni wapi alikowahi kumuona lakini hakupata chochote katika kumbukumbu hiyo.

“Bibi namulizia mzee Mlema Swai alikuwa akiishi eneo hili kwa muda mrefu.”

“Aaaah! Yule alishafariki miaka mingi sana alifia kirabuni na hata eneo lake kwa sasa linamilikiwa na mtu mwingine kwani wewe nani yake?”

“Mwanae.”

“Mwanae!Mwanae yupi sisi tunafahamu alikuwa na mtoto mmoja tu na aliondoka na mama yake miaka mingi iliyopita.”



Ikabidi Naomi amsimlie kila kitu kilichowahi kutokea katika maisha yake taarifa iliyomuumiza sana bibi huyo asiamini kile alichokisikia kutoka kwa Naomi.

“Ndiyo hivyo bibi yangu baba yako alikufa.”

Naomi alishtushwa sana na habari hiyo alilia sana na kujiona mtu mwenye mikosi dunia nzima, japo baba yake alikuwa amewafukuza nyumbani miaka mingi iliyopita yeye na mama yake lakini alikuwa ameshamsamehe na alikuwa na mapenzi ya dhati kwa baba yake.Alijifuta machozi na kumshukru bibi huyo kisha aligeuza na kurudi jiji Dar esa salaam akiwa mtu mwenye huzuni moyoni mwake.



“Hutakiwa kuhuzunika sana wewe mshukru Mungu kwa kila kitu cha muhimu ni kuzingatia masomo yako basi huyo ndiye ndugu yako aliyebaki.”

“Nitafanya hivyo mpenzi,” alisema na kukilaza kichwa chake kifuani kwa Dk. Samweli wakiwa ndani ya ndege walieleka nchini Marekani.



****



Naomi aliyaanza rasimi maisha ya chuoni yaliyokuwa mageni kwa asilimia mia moja, haikuwa maisha tu bali hata mazingira ya nchi hiyo yalikuwa mageni kwake, alikuwa miongoni mwa wanafunzi waliokuwa watiifu na waliozingatia masomo lakini mwishoni mwa mwaka wa kwanza Naomi alibadirika akawa mpenda starehe alitumia muda mwingi katika shughuli hiyo ya starehe kuliko masomo, japo ilikuwa kawaida yake kuwasiliana na Dk. Samwel kila siku usiku akimuahidi kusoma vizuri lakini ilikuwa tofauti kabisa. Hakuwa Naomi aliyekuwa akimfahamu kwa miaka mingi alibadirika sana!

Mwanzoni mwa mwaka wa pili wa yeye kuwa chuoni alijiunga na kundi la wasichana waliokuwa wakijiunza ndani ya makasino makubwa huko ndiko alikokutana na Naija mwanamke kutoka nchini Napel, yeye ndiye aliyekuwa akiwatafutia wateja huku akichukua nusu ya malipo waliyokuwa wamekubaliana, Naija alikuwa mpenda pesa sana hivyo alilazimu kuwapangishia chumba ili aweze kupata vizuri pesa kutoka kwa wanaume waliokuwa wakizuru eneo hilo kwa lengo la kujipatia huduma ya kingono!

“Naomi unaendeleaje na masomo mpenzi.”

“Nashukru Mungu mambo yanenda kama tulivyopanga kila kitu kipo sawa ila nimepungukiwa na pesa ya matumizi lazizi.”

“Hakuna tatizo kesho nitakutumia.”

“Ahasnte sana.”

Hivyo ndiyo ilivyokuwa, Naomi akawa mtu wa kuomba pesa kila alipoona zimepungua hakuhudhulia darasani kwa muda mrefu sana. Miezi saba ya yeye kufanyishwa kazi ya ngono Naija alikamatwa na kurejeshwa nchini kwao lakini hakuwa nyuma kuwaita wasichana hao ambao walikuwa kama mtaji kwake.

***

Taarifa za kuondoka kwa Naomi chuoni hapo zilimfikia Dk. Samwel ambaye hakuamini kile alichokisikia kutoka kwa rafiki yake, siku hiyo ilikuwa mbaya sana kwake alitumia muda mrefu kuwaza na kuwazua kama kweli msichana huyo aliyekuwa akimpenda na mkuthamini kwa zaidi ya asilimia mia moja alikuwa amefanya kitendo hicho.

“Nitaondoka mara moja lazima nikahakikishe mwenyewe,” aliwaza huku akidriki kutoa chozi la maumivu kiapo alichokuwa amekula kwa Naomi kilianza kumtesa alitamani ingekuwa ndoto tena ya mchana.

“Hivi kweli anaweza kunifanyia hivi mimi?”

“Nani baba?” Mama yake alimuuliza mara baada ya kusikia mtoto wake akizungumza peke yake jioni mara baada ya kutoka kazini.

“Naomi mama…Naomi… katoroka chuoni na mbaya zaidi amekuwa mtu wa kujiuza nini hakukipata toka kwangu nitauficha wapi uso wangu mimi kama kweli amenifanyia hivyo,”akazungumza huku akilia sana mkononi akiwa na picha ya Naomi siku moja wote wakiwa bichi nchini Marekani.

“Mwanangu nyamaza huna haja ya kulia sawa baba?’

“Mama hapana bora nife lakini si kuendelea kuyaona haya na kuyasikia kwanini lakini acha nikafanye loloteeee,”akazungumza huku akinyanyuka na kuelekea chumbani kwake akilia sana.

“Wewe usiende kufanya mabaya baba.”

“Mama niache sina thamani kwa sasa nahitaji kufaaaa.”

Akaingia na kuubamiza mlango kisha akaufunga kabisa hali iliyomtisha sana mama yake.







Mara baada ya kuingia chumbani kwake alifika na kujitupia kitandani akiendelea kulia kila kitu alichowahi kufanya na Naomi kilianza kurejea akilini mwake akaliona tabasamu lake zuri na lenye kuivutia akili yake, akayasikia maneno na ahadi walizowahi kupeana alipofika hapo alichoka kabisa akazidi kulia huku akikipiga piga kifua chake kilichokuwa kimejaa hasira na maumivu makali sana moyoni mwake.

Akanyanyuka kitandani na kutembea polepole hadi mbele ya kabati lake kabla hajafanya chochote akasimama mbele ya kioo na kuuona mwili wake kupitia uso wa kioo hicho akiwa amesimama eneo hilo akili yake ikaanza tena kumuwaza Naomi.

“Nakupendaaaaaaa mwaaaaaaah!”

“Mimi pia ona unavyoonekana kwenye kioo.”

“Hahahahah naonekana kama mzee eti?”Akazungumza huku akiwa amesimama mgongoni kwa Naomi mikono yake yote akiwa ameipitisha mabegani kwa Naomi na kumkubatia kimahaba wote wakiwa wamesimama mbele ya kioo hicho muda mfupi mara baada ya wao kutoka bafuni wiki kadhaa kabla ya Naomi kwenda Marekani.

“Akuuuu nani kwakwambia mzee mwanaume hazeki uzee utoke wapi nakupenda na uzee wake hivyo hivyo ulivyo.”

“Kweli?”

“Huamini mpenzi naku….,”

“Mfyaaaaaa,”akajifonza peke yake mara baada ya kuyakumbuka maneno hayo na vitendo walivyovifanya siku hiyo, kwa hasira akainama na kuifungua droo yake na kuitoa bastola yake akaikagua ili kuhakikisha kama ilikuwa na risasi za kutosha.

“Acha nife tu lakini si kuendele kuumia kila sekunde nitauficha wapi uso wangu mimi kipi nilikukosea Naomi yako wapi maneno yako uliyonieleza,kiko wapi kihapo chako mbele ya ndugu zangu na wazazi wangu nitaishi vipi mimi, kwanini umenifanyia hivi wewe?”Alizungumza kana kwamba alikuwa akiongea na mtu akiwa ameuelekezea mdomo wa bastola hiyo kichwani mwake tayari kwa kuyakatisha maisha yake kisa mwanamke!

Sumu ya mapenzi ilianza kuisumbua akili yake akayaona maumivu makali yaliyokuwa ndani ya moyo wake ambao aliupatia kazi nyingine ya kupenda wakati kazi yake kubwa ilikuwa ni kusukuma damu tu!

“Kweli Rose alikuwa na haki ya kulia sikufahamu kama alikuwa akiyasikia maumivu makali kama haya niyapoatayo kwanini lakini…kwanini nini kosa langu chanzo cha yote ni upendo wangu kwako? Kosa langu ni kukupenda!Nijibu Naomi nijibu,”akaiuliza ile picha ambayo Naomi alionekana akicheka sana ukimya wa picha hiyo ukazidisha maumivu ndani ya mtima wake na kujikuta akidondoka chini bila kutekeleza adhima yake ya kujiua, dondoka hiyo ikapelekea yeye kupoteza fahamu.



****

Alihisi maumivu makali sana ndani ya moyo wake maumivu aliyokuwa nayo aliyafahamu yeye mwenyewe laiti angepata mtu wa kumgawia maumivu hayo angeweza kumpatia yeyote aliyekuwa akihitaji kumsaidia lakini haikuwa hivyo aliendelea kukaa na maumivu yake kama kawaida, akiwa anazungumza peke yake mbele ya uso wa kioo mkono wake wa kulia ukishikili bastola ambayo mdomo wake ulikuwa ameuelekezea kichwani mwake tayari kwa kuyafupisha mmaisha yake ghafla akaanza kuzungumza na picha iliyokuwa kwenye mkono wake mwingine, maumivu, machungu na hasira ikapelekea macho yake kukosa uwezo wa kuona vizuri na kupokea hali ya usingizi ghafla akadondoka chini na kupoteza fahamu.

Udonokaji wa fahamu ulimuchukua muda mrefu sana kupata msaada kwani chumba chake alikuwa amekifunga kwa ndani hivyo ndugu zake walipata wakati mgumu sana kuuvunja malango huo na kumpeleka hospitali.

“Kwanini mwanagu najitesa kiasi hicho?”Mama yake akazungumza akiwa amekaa juu ya kochi siku nne mara baada ya Dk.Samweli kutoka hospitali.

“Mama kwanini ananifanyia hivi mimi?”

“Una uhakika na hicho unachokizungumza?”

“Ndiyo mama nimezungumza na rafiki yangu pia nilifanya mazungumzo na wakuu wa chuo wote wanasema hayupo chuoni.”

“Dk. Samweli sina uhakika na hicho unachokizungumza na hutakiwi kuyaruhusu mawazo mabaya yaitawale akili yako, usijibebeshe mzingo mkubwa wakati huna uhakika na hilo.”

“Mama nina uhakika Alex hawezi kunidanganya ni mtu wa karibu sana namuani.”

“Sawa lakini fanya uchunguzi kwanza mimi nipo tayari kukusaidi kwa lolote ila nakuomba usilie wewe ni mwanaume jikaze.”

“Mama kosa langu ni lipi? Nimemvumilia vya kutosha ni mwanaume gani anageweza kufanya haya kwa msichana, ni nani atakayeweza kumvumilia ona leo nina miaka thelethini na tatu sina mtoto na tegemeo langu la kupata mtoto ni yeye nitauficha wapi uso wangu mama,” Dk. Samweli aliongea huku akizidi kulia muda mwingine alimkubuka Rose msichana aliyetokea kumpenda kwa asilimia kubwa na alimbembeleza kwa kipndi kirefu.

“Samweli tabua kulia siyo njia sahihi ya wewe kulitatua tatizo lililopo mbele yako, kinachotakiwa ni kuujuwa ukwel naomba ufatilie usafiri wa wewe kwenda huko.”

“Aya.” Aliitikia kisha alinyanyuka kivivu na kuingia ndani kitu cha kwanza kukifanya ni kumtafuta Naomi lakini hakupatikana hapo ndipo alipozidi kuyaamini maneno ya Alex na kuumia sana, kila sekunde macho yake yalitoa machozi.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Siku iliyofuta alifuatilia usafiri wa yeye kwenda nchini Mrekani na baada ya siku tano alisafiri, alifika nchini humo majira ya saa kumi na moja majira ya huko, hakutaka kweda kokote zaidi ya kuelekea moja kwa moja chuoni hapo.Majibu aliyoyapokea ni yale yale ya Naomi kutokuwepo chuoni hapo kwa muda wa miezi tisa kitu kilichozidi kumuumiza sana hakuweza kuyazuia machozi yaliyokuwa yakitiririka na kulowanisha mashavu yake taswila ya mambo waliyowahi kuyafanya nyuma na msichana huyo ilianza kuisumbua akili yake kwa mara nyingine.

“Nashukuru sana mkuu,”akamshukuru mmoja wa walimu waliokuwa wakifanya kazi chuoni hapo kwa lugha ya kingereza.

“Kwani unalia Samweli?”

“Ha..hapana ni ..ni…ni….,”akashindwa kuzungumza mara baada ya moyo wake kuzidiwa maumivu, japo hakupenda kuyaonyesha machozi yake mbele za watu lakini kipindi hicho kila mtu aliyaona machozi yake ambayo hayakuwa na siri tena.

“Hapana lakini unalia, okay sawa pole nakutakia jioni njema,”akazungumza na kuondoka eneo hilo akimuacha Dk.Samweli akiwa amesimama kinyonge sana kope zake zikiendelea kulowana kwa machozi, muda mwingine alitamani muujiza utokee aweze kumuona Naomi na hayo yabaki kama ndoto tu lakini haikuwa hivyo yale yaliyokuwa yakitokea yalikuwa ni kweli kabisa.



Taratibu akairuhusu miguu yake na kutoka eneo hilo akitembea kwa unyonge mfano wa mtu aliyekuwa ametoka katika ugonjwa wa muda mrefu sana, hadi anafika sendi ya mabasi yaliyokuwa yakielekea mjini sehemu aliyokuwa akitegemee kwenda kulala mikono yake ilikuwa kichwani kama mtu aliyekuwa amejitwisha kitu flani.



Dakika tatu za yeye kuwa eneo hilo basi lilifika na kuingia ndani yake mara baada ya kufanya malipo kabla ya basi kufika, safari yake ikaishi katikati ya jiji la nchi hiyo akasuka na kuchuka tax iliyompeleka ndani ya hoteli kubwa sana akalipia na kuzama chumbani asihitaji kitu chochote zaidi ya kulia na kuitazama picha ya Naomi.



Usiku mzima aliiutumia kulia na kumlaani Naomi alijilaumu kuupoteza muda wake kwa kumpenda msichana huyo aliyemsaidia kwa zaidi ya asilima mia.

“Nitamfuta Napel.”

Hilo ndilo jibu aliloona ni sahihi alivuta shuka na kujifunika ili kuulazimisha usingizi lakini haukuonekana, hadi kunapambazuka hakuweza kupata hata lepe la usingizi. Saa moja sabuhi aliamka na kuelekea bafuni kisha alitoka na kuelekea idara ya anga ya nchi hiyo kwa lengo la kupata tiketi ya kuelekea Napel. Ilikuwa kama bahati aliweza kupata nafasi ya ndani ya ndege toka shirika la Quatar ndege iliyokuwa ikiondoka saa sita mchana majira ya huko.

“Acha nikamtafute Alex anieleze ni mji gani?” Akajiuliza huku akizidi kutembea kwa mwendo wa kasi sana,kulia tena aliacha na tumaini la yeye kumpata Naomi lilikuwa limeanza kuonekana moyoni mwake aliamini kufika Napel uwezekano wa yeye kumpata ulikuwa kwa asilimia mia kabisa kwani pesa alikuwa nazo tena za kutosha, hakufahamu ni kwanini moyo wake ulikuwa ukimpenda msichana huyo na alikuwa radhi kabisa kumsamehe kwa asilimia mia kabisa aliamini kosa moja halifukuzi mke pia hilo hilo moja haliwezi kuyafuta tisini na tisa mema aliyokuwa amewahi kufanyiwa na Naomi.



Alitoka ofisini humo na kuelekea ofisini kwa Alex aliyekuwa mtanzania lakini alikuwa akiishi nchini humo.

“Ni mji wa Jankpur ni magharibi mwa nchi hiyo,”akazungumza huku akiendelea kumchorea ramani.

“Ulisema anaitwa nani?”

“Naija ni mtu mzima kabisa na ninasikia ni mtu maarufu huwezi kumkosa ukimuulizia tena acha nikupatie na picha yake,”akampatia ramani hiyo kisha akamtumia picha yake kupitia mtandao wa WhatsApp moyoni akimhurumia sana rafiki yake aliyewahi kusoma naye chuo kimoja na kutokea kuwa marafiki wa kudumu kabisa.

“Ahsante sana.”

“Karibu tena.”



Waliagana kisha Dk. Samweli alitoka ndani ya ofisi hiyo akiwa na hasira sana dhidi ya mwanamke huyo aliyemvurugia maisha yake, safari yake iliishia ndani ya hoteli aliyokuwa amefikia siku ya jana alichukua kila kitu kilichokuwa chake kisha alielekea uwanja wa ndege kwa safari yake ya kuelekea Napel. Akitazamia kumkamata Naomi na kumrejesha Tanzania.







Ilikuwa ni safari ya machungu sana moyoni mwa Dk. Samweli kila alichokifikiria kukifanya kwa mwanamke huyo kilionekana hakifai aliwaza na kuwazua lakini hakupata adhabu sahihi kwa Naija.Mara kwa mara alikuwa akifungua kibegi chake kidogo na kuitoa picha ya Naija pamoja na ya Naomi na kuwatazama watu hao kwa sura mbili tofauti, kisha anairudisha na alipopata mwasha wa kufanya hivyo anafanya tena, kitendo kilichokuwa kikimshangaza hata abiria aliyekuwa amekaa kiti cha pembeni.



Picha ya Naomi alipoitazama sura ya upendo ilionekana usoni mwake na hata moyoni pia alikuwa na sura yenye huruma ya hali ya juu akatamani hata atokee wakati huo huo amchukue na kumrejesha Tanzania mara moja, sura ya pili ilikuwa mbaya sana na yenye muonekano wenye machungu yaliyochanganyikana na hasira za waziwazi muda mwingine aliweza kututumuka na kuvimba kwa hasira mithili ya unga wa maandazi ambao ulikuwa tayari kwa uchomwaji wa maadazi, alikuwa akiyauma meno yake kwa maumivu makali ndani ya kifua chake na kuipiga ngumi picha hiyo hadi anaingia nchini humo alikuwa hajapata jibu sahihi la kumfanyia mwanamke huyo.Alishuka na kutoka ndani ya uwanja huo mara baada ya kukamilisha taratibu zote zilizokuwa zikihitajika eneo hilo.

“Nipeleke Jankpur.”

“Jankpur?”

“Ndiyo.”

“Ni mbali sana kwa tax nakuomba ukachukue garimoshi,” dereva tax alimueleza Dk. Samweli mara baada ya kutajiwa eneo akimtazama kwa macho yenye maswali mengi sana tena yenye kuhitaji majibu ya haraka-haraka kwa wakati huo lakini haukuwa muda fasaha wa yeye kufanya hivyo.

“Nisaidie kitu kimoja?”Akasema huku macho yake akiyaangaza pande zote za dunia kana kwamba alikuwa akitafuta kitu!Kweli akili yake yote ilikuwa kwa Naomi na Naija.

“Kipi?”

“Nielekeze kituo cha gari hilo.”

“Ooooh! Mita chache kutoka hapa nyosha na barabara hii kwa mbele utakuta ofisi zake kuna kibao hapo kinajieleza ingia humo na ukate tiketi kisha unaisubili.”

“Nashukuru sana.”

“Karibu sana.”

Samweli hakuta kupoteza muda aliondoka eneo hilo akifuata maelezo aliyokuwa ameelekezwa na mwanaume huyo raia wa nchi hiyo, alitembea kwa mwendo wa haraka sana hadi eneo hilo lililokuwa na idadi kubwa ya watu ambao wengi wao walikuwa wakisubiri usafiri huo.

Nusu saa ya yeye kufika eneo hilo garimoshi ilifika Dk. Samweli alikuwa mtu wa kumi kuingia ndani ya treni hiyo, alitafuta siti iliyoyavutia macho yake aliketi na kutulia.Ulikuwa ni mwendo wa masaa manne kuingia mjini humo. Mji uliokuwa mzuri japo ulikuwa ni usiku wa saa sita lakini uzuri wake haukuweza kufichika.

“Nitalala hapa hapa.”

Alitafuta eneo ndani ya kituo cha garimoshi hilo na kukaa hakuta kutafuta hoteli aliona kufanya hivyo ilikuwa ni kujipotezea muda.Siku ya pili yake alianza kuzunguka mtaani kumtafuta Naomi na Naija lakini hakuweza kumpata yeyote akarejea eneo la stesheni ya treni hiyo akiwa amechoka sana.

“Kaka unamfahamu mtu huyu?”

“Mmmmh!Hapana simfahamu,”akajibu kwa mkato kijana aliyekuwa amejitwika tenga lenye bidhaa mbalimbali ambazo alikuwa akiziuza kwa wasafiri waliokuwa wakitoka mjini humo na kuingia humo.

“Lakini mwenyeji sana mtu huyu?”

“Kaka simfahamu siko hapa kwa ajili ya kumfahamu mtu mimi nimetumwa pesa,”akazungumza huku akianza kuondoka eneo hilo na kumuacha Dk.Samweli akiwa ameganda eneo hilo hana cha kufanya, akafyonza kidogo na kuupigiza mguu wake chini kwa hasira kisha akaanza kutembea tembea ndani ya stesheni hiyo akimtazama kila mtu ili kuona kama alikuwa Naomi ama Naija lakini hadi usiku unaingia hakuweza kumuona mtu yeyote , akatafuta eneo sahihi aliloona linamfaa na kuuruhusu ubavu wake kulala eneo hilo.Saa kumi na moja asubuhi majira ya huko akadamka na kuanza kuzunguka kila kona ya kituo hicho lakini wapi alijitahidi kuwaonesha watu picha za watu hao napo hakuweza kuwapata.

“Nitafanya nini sasa?”Akajiuliza peke yake siku nne toka aanze kumtafuta mpenzi wake Naomi, tumaini la yeye kumpata likaanza kufifia taratibu kadiri siku zilivyokuwa zikiendelea kuongezeka.

“Au niingie katika makasino? Lakini nitampata?” Akapata jibu la wapi angeanzia tena lakini nafsi ya pili ikampinga ila akaipuuzia na usiku huo huo wa siku ya nne akaanza kutembea sehemu mbalimbali za starehe lakini nako wapi Naomi wala Naija hakupatikana hata kidogo.

“Sikati tamaa hata kidogo nitamtafuta mpaka apatikane siweziiii….seweziiii nasema lazima.”



Alijikuta akitumia miezi miwili kumtafuta Naomi aliyeamini kuwa alikuwa nchini humo lakini haikuwa hivyo Naomi alikuwa Tanzania kwa muda wa miezi mitatu bila kutoa taarifa kwa ndugu yeyote wa Dk. Samweli. Ilikuwa ni aibu sana kwake kuuoneha uso wake mbele ya watu waliyomfanyia mema toka utoto wake.

“Shitiii!” Alipiga ngumi aridhini mara baada ya kutoka katika kumbukumbu ya maisha yake, alinyanyuka na kusimama wima kama mwanajeshi vitani kumbukumbu ya matukio ya nyuma ilikuwa imeiharibu akili yake kwa asilimia mia.



****

Naomi mara baada ya kufika Tanzania hakuwa na sehemu ya kuishi zaidi ya kuishi na Stella msichana aliyemuingiza ndani ya biashara ya ngono bila kujali hali ya maisha aliyowahi kuyapitia.Mwanzo waliishi maisha ya kifahari sana kutokana na pesa walizokuwa wametoka nazo Napel hawakujishughulisha na kazi yeyote zaidi ya kutumia pesa kila siku, kutembea sehemu mbalimbali za starehe nyakati za usiku huku wakiteketeza pesa. Miezi mitano ya wao kuishi kwa raha akiba waliyokuwa nayo ilikwisha hivyo wakawa watu wa kuomba omba kwa wanaume waliokuwa wakijichekesha kwao. Buguruni nzima walifahamika kila kona jina la Stella na Naomi lilijulikana.

“Sikia Naomi mimi nataka nirudi nyumbani maisha ya hapa mjini yamenishinda.”

“Kwanini?”

“Sasa wewe unaona haya ni maisha? Nimechoka kuishi kwa kuuza mwili wangu kila mtu angalie usawa wake, nitaenda kuomba msamaha kwa wazazi wangu naimani watanipokea”

“Umeniharibia maisha yangu ndiyo unanikimbia? Yako wapi maneno yako uliyokuwa ukiyatamka? Uko wapi urafiki wako wa dhati ulioniahidi?” Naomi aliongea kwa hasira kali sana, hakuamini kama kweli Stella rafiki aliyemchukulia kama ndugu yake leo alikuwa amembadilikia alitamani kulia lakini hakuweza hata chipsi alizokuwa akila aliziona chungu, aliiruhusu akili yake kukumbuka maisha mazuri aliyoyapata kutoka kwa Dk. Samweli aliumia sana.

“Wewe nani alikuharibia maisha? Nilikushika? Ulikuwa mtu mzima na akili yako ujinga wako babue na mimi kesho nasepa kodi imebaki wiki moja utajua cha kufanya.”

“Sawa utalipiwa.”

“Nilipiwe mara ngapi? Ujinga wako.” Aliongea kisha alisimama na kutoka nje hakujali kama maneno hayo yalikuwa mwiba mkali ndani ya mtima wa Naomi.

“Nilifanya nini mimi?Yako wapi maneno niliyomweleza Dk.Samweli matendo yake mema nimemlipa ubaya nitaanzanje kumtazama tena?”Akazungumza peke yake akiwa analia kwa kwikwi alitamani sana kwenda kuzungumza na Dk.Samweli aliyeamini kuwa yupo nchini lakini alijionea aibu mwenyewe, nafsi yake ilimsunta sana na kujiona mkosefu mbele za Samweli na Mungu wake, akajiona hastahili masamaha wa aina yeyote na adhabu yake ilikuwa hiyo hiyo ya kutanga tanga. Akatumia muda mrefu sana kuwaza na kulia lakini hakupata jawabu sahihi la kipi angefanya.

“Mimi ndo hivyo wenzio kesho home shoga-angu tutaonana kama Mungu akipenda.”

“Lakini stel….”

“Aaaah!Mama kama unaongea pumba sitaki ongea point upo!”Akamkatiza kwa ukali huku akiendelea kujipodoa tayari kwa kuelekea kijiweni kuongezea pesa ya nauli, Naomi akakosa cha zungumza zaidi ya kukiinamisha kichwa chake katikati ya mapaja yake akilia taratibu alimuona Stella ni mwanamke mkatiri sana na mbaya kwa wanawake wote duniani alimuona hafai hata kidogo na nyoka mwenye sumu kali.

“Oya zungumza mie naharaka.”

“Nenda tu mimi sina cha kuzungumza.”

“Sasa kinachokuliza ni nini?Kamlilie Naija ama akili yako sote tuna makosa unaponilani mimi na kunihukumu bila kuingalia nafsi yako na akili yako unategemea nini?”

“Sasa Stella siyameishaaaa nenda,”akasema huku akinyanyuka eneo alilokuwa amekaa na kutembea kinyonge hadi dirishani akasimama na kuyatazama maadhari ya nje ambayo halikuwa si pendwa kwa afya za binadamu.

“Huku nako kunanuka mtaro puuuuh!” Akatoka eneo hilo na kurudi juu ya godoro kwa lengo la kuusaka usingizi lakini hakufanikiwa kuupata hadi saa nne Stella aliorejea akiwa amelewa chakali.



Siku iliyofuata kweli Stella alielekea kwao mkoani Morogoro sehemu moja inayaofahamika kwa jina la Dakawa akimuacha Naomi hana mbele wala nyuma japo hakuwa na uhakika wa yeye kusamehewa na wazazi wake lakini alijipa tumaini la yeye kupokea msamaha huo

“Hapa nitafahamu cha kufanya acha aondoke,”akawaza Naomi akiwa anamsaidia rafiki yake kutoa mizigo yake nje tayari kwa kuondoka.



****

Jijini Dar es salaam maisha ya Naomi yalikuwa ya kubabaisha sana hakuwa na kazi yeyote zaidi ya kuirudia kazi yake ya zamani, kila siku jioni alijipamba na kuelekea sehemu zenye starehe huko hakukosa mwanaume wa kumnunulia chakula na hata kumlipia chumba, siku tano za Stella kuondoka Naomi alibahatika kupata mwanaume aliyekuwa akifahamika kwa jina la Davis. Davis alimpenda sana Naomi hata alidiriki kumpangishia chumba kingine huko mbagala majimatitu. Mwanzo waliishi kama wanandoa lakini miezi kadha Davis alibadilika akawa mtu wa kulala nje, mkorofi sana na pindi Naomi alipodiriki kumuuliza zawadi yake ilikuwa makofi ama matusi.

“Hapa ni kujitafutia changu huyu boya atanisumbua,” aliwaza usiku mmoja mara baada ya kumaliza kula mihogo mikavu akiwa peke yake ndani ya chumba chake

Mawazo yake ya usiku aliyatekeleza mara moja usiku huo huo alijiandaa na kutoka kwa kuwa alikuwa mwenyeji wa jiji hilo hakukosa sehemu ya kwenda huko alibahatika kupata mwanaume maana uzuri na umbo lake vilikuwa mtaji tosha vya yeye kupata alichokuwa amekidhamiria. Maisha ya Naomi yakawa ya namna hiyo mchana anashinda geto na usiku viwanja.

****



Maisha ya Dk. Samweli yalianza kubadilika kila siku hakuwa mtu aliyejijali kama mwanzo aliishi mtaani na hata kulala kokote usiku ulipomkuta, hakuwa yule aliyeheshimika kwa ushupavu wa kazi yake ya udaktari ndani ya nchi yake, aliishi kwa kuomba omba kila siku huku akiendela kumtafuta Naomi na Naija kila siku alizidi kuwa kichekesho mbele ya macho ya watu hakuwa na mtu aliyekuwa karibu yake kila mtu alimtenga kutokana na muonekano wake wa mwili uliokuwa mchafu kupita maelezo hata ukiambiwa kuwa yule alikuwa kichaa huwezi ukakataa.

Aliishi maisha ya upweke sana kila alipomfikiria mwanamke aliyeuteka moyo wake alizidi kuchanganyikiwa sumu ya mapenzi ilikuwa inamtesa kwa asilimia kubwa. Miezi tisa ya yeye kuishi nchini humo ilimfanya awekituko kwa kila mtu, jina la Naomi halikufutika mdomoni mwake.Alimtaja kila sekunde mithili ya wimbo mzuri unapotoka na kupendwa na watu huwa haukatiki ndani ya mioyo yao.

Hakuwa na sehemu ya kulala zaidi ya kulala chini ya daraja laiti kama ungelezwa kuwa alikuwa msomi tena wa elimu ya juu usingeweza kuamini. Siku moja alipokuwa akizurula zurula alibahatika kukutana na Naija kwanza hakuamini alibaki akimtazama kwa macho ya hasira sana kisha alianza kumfutilia hadi alipohakikisha amepaona alipokuwa akiishi.

“Naenda kuua wote kisha na mimi najiua siwezi… siwezi…. mimi,” alisema peke yake huku akitafuta sehemu ya kujikinga kwani mvua ilikuwa imeanza kunyesha.

“Nasubili mvua ikate tu namfuta atanikoma,” alisema peke yake na kukaa chini ya mti mkubwa ili kujikinga na maji ya mvua. Zaidi ya masaa mawili mvua hiyo iliendelea kunyesha huku ikiambana na baridi kali sana hali iliyopelekea Dk. Samweli kutetemeke kwa baridi kali.

“Namfuta huko huko,” aliwaza na kunyanyuka eneo hilo akiwa amelowa chapa chapa moyoni alidhamiria kumungamiza, alitembea kwa tahadhari ya hali ya juu sana maana mtaa huo ulikuwa maarufu kwa makazi ya vibaka na wauza madawa ya kulevya.

“Hivi kwa mfano nikifika nianzeje kumuua?”Akazungumza huku akiutazama mkono wake wa kushoto ambao alikuwa ameukunja ngumi akiuzungusha zungusha hewani asiamini kama siku hivyo alikuwa amempata adui yake wa muda mrefu.Kabla ya kuingia ndani ya kijumba hicho alisimama kwanza nje akitafakari ni jinsi gani angemvamia machozi yaliyokuwa yamechanganyikana na maji hayakuwa nyuma kutona ndani ya macho yake na kuzilowanisha kope zake lakini hayakuonekana kutokana na maji ya mvua iliyokuwa ikinyesha kwa wakati huo. Ile simama yake ya muda mrefu pale nje ikapelekea macho ya Naija kumuona yeye na kuanza kumpigia kelele ya hofu kutokana na muonekanao wa Dk.Sawmeli.



Upigwaji wa kelele hizo ndio uliochochea yeye kuanza kuingia ndani lakini kwa bahati mabaya hakuweza kumfanya chochote Naija mara baada ya Naija kuwaita vijana waliokuja kumchukua na kumpeleka kwenye mti na kumfuka kisha waliondoka siku ile kabla ya kuokolewa.



****



Kila kitu kilikuwa kimeharibika kwa upande wa Dk. Samweli hivyo aliamua maisha yake yaishie vivyo hivyo aliendelea kusimama eneo hilo mara baada ya kuyakumbukia maisha yake.

“Nishapoteza kila kitu acha niwe kichaa tu nitalala majalalani na kula kokote hadi siku nitakapokufa ila sitakuja nimuamini tena mwanamke,”akazungumza huku macho yake yakiitazama mbingu ambayo ilikuwa imepambwa kwa mbaramwezi na nyote nzuri zilizokuwa zikitoa mwanga mzuri sana na wenye kuyapendeza macho yake kwa wakati huo, lakini moyo wake haukuwa na furaha hata kidogo.

Huo ndio uamuzi aliouchukua na kuanzia dakika hiyo Dk. Samweli akawa mtu wa kulala kokote kuishi majalalani na kokote, upweke na ukosefu wa mtu wa kumshauri ulimpelekea yeye kuwa kichaa kabisa hakukumbuka wapi alikotoka zaidi ya kuyafurahia maisha hayo ya ukichaa.

Miaka miwili ya yeye kuishi maisha hayo ya kichaa alibahatika kuchukuliwa na shirika la kuhudumia wangonjwa wenye matatizo ya akili la nchini humo aliishi kambini hapo kwa muda wa miezi sita akipata huduma na tiba ili kuirejesha akili yake.

“Mimi si ni Samweli?” Alimuuliza nesi mara baada ya kumaliza kupewa dawa asubuhi moja.

“Unasema?” Naye akamuuliza kwa lugha ya kingereza maana Dk. Samweli alikuwa ameongea lugha ya kiswahili ambayo ilikuwa ngeni masikioni mwa nesi huyo. Aliyeshangazwa na lugha hiyo.

“Naitwa Dk. Samweli.”

“Wewe ni Dokta?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Ndiyo. Hapa nimefikaje?”

Nesi hakumjibu chochote zaidi ya kumchukua na kumpeleka ofisini kwa Dokta kisha alitoa maelezo yote na kuondoka.

“Unaitwa nani?” Dk. Kumar Shah mzee kiasi mwenye mvi nyingi kichwani kwake alimuuliza mara baada ya yeye kukaa kwenye kiti kilichkuwa kimetazamana na cha kwake, nyuso zao zikawa zinatazama.

“Dk. Samweli.”

“Doktar? Unatibu nini na wewe ni raia wa wapi?”

“Magonjwa ya moyo(Cardiovascula desease) na ni raia wa Tanzania.”

“Ulifikaje hapa?” Dk.Samweli akaanza kukikuna kichwa kichwa chake kama dakika moja na kuutoa mkono kichwani mwake kisha akamtazama machoni mzee huyo ambae alikuwa kivifuatilia vitendo vyote alivyokuwa akivifanya mtu huyo.

“Niambie ulifikaje?”

“Sielewi ila namtafutaaaaaa…nani nani… nimemsahau.”

“Okay Cardiovascula desease ni nini?”Ikabidi amuulize swali hilo ili aone kama kweli akili yake ilikuwa imeanza kutegemaa.

“Ni aina ya magonjwa ya moyo.”

“Kama?”

“Hypertension.”

“Ni nini hicho?”

“Ni ugonjwa wa kupanda kwa shindikizo la damu ambalo tunaweza tukaliita kama high blood pressure, pia kuna magonjwa kama Coronary heat desease huu ni ugonjwa wa moyo ambao mafuta yanaganda ndani ya ateri koronari na kusababisha ateri hizo kuziba kabisa,”akazungumza kwa kujiami huku akirusha rusha mikono yake hewani maana midadi ilikuwa imeanza kumpanda na hata alijikuta akiisahau hali yake aliyokuwa nayo. Majibu ya Dk,Samweli yakamuacha hoi Daktari huyo na kuwa na shauku ya kufahamu kipi kilipelekea yeye kuwa katika hali hiyo, moyo wake ukaumizwa sana na hali aliyokuwa nayo hakuamini kama mtu huyo aliyekuwa akiidharaulika na kuonekana hafai mbele za wanapel wote kumbe alikuwa na elimu na ujuzi wa hali ya juu ambao hata ungeweza kuwasaidi wao, ooooh!Akamuone huruma na kumsikitikia sana.



“Dokta unaweza ukanieleza kipi kilikufanya mpaka ukawa hivi,”akamuuliza huku akitoa miwani yake ya macho na kuiweka juu ya meza kubwa iliyokuwa mbele yake akaufuta uso wake na macho yake yakamtazama Dk,Samweli aliyekuwa kimya kabisa akitafakari kipi kilipelekea yeye kuwa hapo.

“Sina kumbukumbu yeyote kwa sasa,”akamjibu kwa mkato na kuyafumba macho yake yaliyokuwa yamekondeana kupita maelezo alipokuja kuyafumbua kope zake zilikuwa zimelowana na machozi kitendo kilichomshtua sana Dk.Kumar Shal.

“Huatakiwi kulia nieleze nitakusaidia.”

“Sina kumbukumbu kwa sasa nipeni muda wa kufikiria kwanza.”



Daktari huyo hakuwa na jinsi ikabidi amruhusu kutoka ndani ya chumba chake na kumkabidhi kwa Daktari mwenzake aliyempa jukumu la kumtembeza sehemu mabalimabi za jengo hilo akimuuliza maswali tofauti tofauti ili kujidhihirishia kuwa alikuwa amepona kabisa tatizo lake la ukichaa, siku tatu za yeye kuzungushwa zilimfanya akili yake kukumbuka kila kitu na kuomba kuonana na Dk.Kumar shal.







“Karibu sana Dk.Samweli,”akamkaribisha mara baada ya yeye kuingia ndani ya chumba cha ofisi yake akitabasamu tabasamu lakini kwa upande wa Dk.Samweli hakuthubutu kuyatoa meno yake nje.

“Unatatizo?” Akamuliza akiwa amesimama na mikono yake ikiwa imeshika meza kwa juu hali iliyoufanya mgongo wake kuinama kidogo. Kabla ya Dk.Samweli kuzungumza chochote alianza kulia na kumfanya mwenyeji wake kupata wakati mgumu sana kwani siku hiyo alidhamiria kusikia mengi kutoka kwa Dk.Samweli.



Ulikuwa ni wakati mgumu sana kwa Dk.Samweli kuzungumza kile alichokuwa akikifahamu,kila kitu kilikuwa kimerejea ndani ya ubongo wake na kumfanya moyo wake kuumizwa sana na matendo aliyokuwa amefanyiwa na mpenzi wake Naomi msichana aliyempenda kwa moyo wake wote kwa nguvu zake zote na kwa akili zake zote.Upendo huo ukawa mwiba mkali ndani ya moyo huo aliouponda ponda bila huruma.



Kuzungumza alitamani ila alikosa ni wapi angeweza kuanzia kila alipopanga kupaanza alipaona hapafai hata kidogo, aliendelea kuwa katika hali hiyo ya ukimya sana akiwa ameyauma meno yake kwa nguvu sana na kuifanya sura yake kukunjamana kwa mistari- mistari.



“Tafadhali siti,” Dk. Kumar shal akazungumza tena akiitoa mikono yake juu ya meza na mkono wake wa kulia akakisonta kiti ambacho Dk.Samweli alitakiwa akikalie, maneno yake yakawa yamepita kushoto kabisa kwa Dk.Samweli ndo kwanza alizidi kututumuka na kuzidi kumtisha hata yeye. Ikabidi amuache kwanza kama muda wa dakika tano ndipo alipokubali kukaa yeye mwenyewe na kuiinamisha shingo yake, kichwa akakilaza juu ya meza akili yake ikipitisha tukio moja baada ya jingine, akaliona tabasamu la Naomi, akayaona maneno yake na kuvisikia vicheko vyake hapo ndipo alipochanganyikiwa zaidi na kuipiga meza kwa ngumi kali sana kisha akakinyayua kichwa chake tayari macho yake yalikuwa yakitoa machozi kama mtoto mdogo na kuambatana na kamasi nyepesi nyepesi ndani ya matundu yake ya pua.



“Tulia…tulia kwanza tulia hutakiwi kutumia nguvu na hasira.”

“Naumia sana naumia hujui tu ninavyoumia doktaaaaaaa,”akazungumza huku akizidi kulia tena kilio cha sauti kama mtoto mdogo na kumfanya daktari mwenzake kunyanyuka eneo alilokuwa amekaa na kutembea hadi kwa Samweli akasimama mgogoni mwake na kuanza kuupiga piga mgongo wake moyo wake ukiumizwa sana na hali ya Dk.Samweli.Haikuwa kazi nyepesi sana na rahisi kumtuliza Dk.Samweli kwani alijikuta akitumia dakika hamsini na mbili za kumuweka katika hali nzuri na hata kukubali kuzungumza kila kitu kilichokuwa kimemsibu.



“Utanieleza?”

“Ndiyo niko tayari,”akazungumza huku akikohoa kikohozi kikavu cha kuliweka koo lake sawa kwani lilikuwa limeanza kukwama kwama.

“Karibu kama hutojali,”akasema huku akijiweka sawa kwa kusikiliza kile kilichokuwa kikienda kuzungumzwa.



Ikabidi Dk. Samweli amsimulie kila kitu hali iliyomsikitisha sana Dk. Kumar Shal, alijihisi kama yeye aliyefanyiwa unyama huo.



‘Je upo tayari kuwa naye?”

“Ndio hata sasa hivi nahisi bado nampenda sana Naomi,”akazungumza huku akikimanisha kile alichokizungumza.

“Basi ni sawa mimi siwezi kukushauri chochote dhidi ya huyo mwanamke wewe ndiye mwamzi mkuu na wa mwisho.”

“Ahsante sana,”akashukuru huku akiunyosha mkono wake wa kulia na Dk.Kumar Shal akaupoke na kuufumbata vyema kisha akautingisha tingisha ishara ya kukubaliana kile alichokizungumza mwenzake.

“Labda tukusaidie nini?”

“Nataka kurudi nyumbani kama itawezekana huo ndio masaada tosha kwenu.”

“Kingine hakuna?”

“Hapana kubwa kuliko yote ni hayo nikifika huko nitafahamu wapi pa kumpatia mke wangu.”

“Basi tutalishughulikia hilo haraka iwezekanavyo.”

“Nitashuru sana.”



Alitoka ofisini humo akiwa haamini kama kweli alikuwa kichaa wa miaka miwili hata alipoutazama mwili wake ulivyokuwa umedhoofika aliumia sana, ila hakuwa na jinsi ilibidi yakubali yote yaliyotokea. Baada ya mwezi mmoja alisafirishwa hadi Tanzania mara baada ya habari yake kuifikia ofisi ya balozi wa Tanzania nchini humo.

Hakuamini kama kweli alikuwa anaenda kuikanyanga aridhi ya nchini kwake, mara baada ya muda mrefu kupita, hakuwa na mawasiliano yeyote.



“Ahsante Mungu kwa kunirejesha tena nyumbani salama,” aliongea mara baada ya kutoka ndani ya uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere, alisimama kwa muda kuyatazama mazingira ya Tanzania kisha aliendelea na safari yake.

“Nipeleke Bunju.”

“Poa,” alijibu dereva tax huku akimfungulia mlango Dk. Samweli kisha na yeye alizunguka upande wa pili na kuwasha gari safari ilianza. Njia nzima hakuna aliyemuongelesha mwanzake hadi anafikishwa mtaani kwao hakuwa amefungua kinywa chake.

“Nisubili nikakuletea pesa yako.”

“Poa fanya fasta.”

Dk. Samweli alipiga hatua kulikaribia geti lililokuwa chakavu kiasi huku mapigo ya moyo wake yakienda kasi, hakuwa na tumaini kama kweli nyumba hiyo ilikuwa bado ya wazazi wake wakiendelea kuishi hapo kutokana na uchakavu wake.

“Nakujaa”

Sauti ya msichana ilisikika mara baada ya Dk. Samweli kugonga geti hilo.

“Nikusaidie nini?”

“Aaah! Nawaulizia wenyewe sijui nimewakuta?”

“Wenyewe wapi?,” Msichana mwembamba kiasi aliongea kwa nyodo huku akimtazama Dk. Samweli kuanzia juu hadi chini kwa macho ya dharau.

“Namuulizia mama Samweli?”

“Una ahadi naye?”

“Hapana… ila ninataka kuonana naye naomba unisaidie tafadhali.”

“Subiri nikuitie,” alimjibu na kulifunga geti dakika saba alisikia nyayo za watu zikielekea getini hapo.



“Mamaaaaaa….maaaaa!” Hakuamini kama kweli mwanamke aliyekuwa amesimama mbele yake alikuwa mama yake, japo alikuwa mtu mzima lakini sura yake ilibaki ile ile.

“Samwelii ulik…” hakuweza kuongea alijikuta akidondoka chini kama mzigo puuuh!Mbele ya macho ya Dk.Samweli aliyekuwa na shauku kubwa sana ya kuzungumza na mama yake akabaki amesimama wima asifahamu kile kilichokuwa kimetokea, dakika mbili ndipo aliposhtuka mara baada ya ngoma za masikio yake kuzibuliwa na sauti ya msichana yule aliyemfungulia geti akilia sana.

“Hebu nipishe,”akazungumza huku akimsukuma kutoka eneo alilokuwa amelala mama yake akiwa haelewi kipi kilikuwa kinaendelea, achuchumaa na kuupeleka mkono wake wa kulia kifuani kwa mama yake,na kujikuta akishtuka sana macho yake yakamtazama yule msichana na walipoyagonganisha akatoa chozi asiuamini mkono wake.



Ulikuwa ni mshtuko wa hali ya juu sana.Mama Samweli hakuamini kama siku moja angekuja kumuona mwanae akiwa mzima kabisa, aliona kama ulikuwa ni mzimu na hakuwa yeye mshtuko huo ukapelekea mapigo ya moyo wake kuongezeka na kufanya macho kuhisi hali ya usingizi singizi huku mwili wake wote ukiishiwa nguvu na kujikuta akidondoka chini kama mzingo puuuh!Hapo hapo akatulia akiwaacha Dk.Samweli na msichana yule wakiwa hawaelewi kile kilichokuwa kimetokea kwani kilikuwa ni kitendo cha ghafla sana.



“Mamaa,”Msichana yule akapiga kelele za juu sana zilizompelekea Dk.Samweli kushtuka kutoka katika hali ya sintofahamu iliyokuwa imemvaa ghafla akapiga hatua hadi sehemu aliyokuwa ameangukia mama yake na kumtoa masichana yule ambae alionekana kama kikwazo kwake, taratibu akachuchumaa akiwa amechuchumaa mkono wake wa kulia akauweka kifuani kwa mama yake kama dakika mbili kisha akautoa na kumtazama msichana yule kwa macho asiyoyaelewa, macho yake yalipogongana msichana yule akazidisha kilio na kumfanya Dk.Samweli kutokuamini kile alichokutana nacho.







“Wewe umemua mama kwanini wewe kichaa umefanya hivi,”akazungumza msichana yule huku akimpiga Dk.Samweli mgongoni na vigumi vyake vya kike ambavyo havikuwa chochote kwa mwanaume huyo.

Japo alikuwa akipigwa pigwa vigumi hivyo lakini akili yake haikuwa kwa msichana huyo yeye alichokuwa akikiangalia ni uhai wa mama yake tu.

“Tokaaa.”

“Nani atoke hebu kaa mbali na mimi niache,”akamkalipia msichana yule macho yake tu yalikuwa yakionesha kile alichokuwa akikizungumza, taratibu msichana yule akasimama pembeni akiwa ameikusanya mikono yake kwa mbele moyo ukiwa unakwenda kwa kasi ya ajabu, huku akili yake ikianza kuwaza mawazo mabaya juu ya mama Samweli aliyekuwa ametulia tu chini asifahamu kile kilichokuwa kikiendelea kwa wakati huo.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Kwa mikono yake miwili akaufungua mdomo wa mama yake na kukipeleka kinywa chake kwanye mdomo huo akaanza kumpulizia pumzi huku akikikandamiza kifua chake polepole bila kupumzika alipohakikisha ameanza kupumua alivua shati lake na kuanza kumpulizia hewa.



“Oyaa mshikaji unanichel….,”Dereva tax akazungumza huku akilisukuma geti na kuingia ndani lakini aliyakatisha maneno yake mara baada ya kuikuta hali hiyo, akabaki amesimama asijue cha kufanya.

“Mshikaji naomba unisaidie kumpeleka ndani.”

“Poa usijali,”akapiga hatua hadi eneo alipokuwa amelala mama yake Samweli akiwa anapumua kwa mbali kidogo ila hali yake ilikuwa imeanza kutegemaa.

“Sasa niko hapo nje nakusubili.”

“Haina shida”





ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog