Search This Blog

Tuesday 1 November 2022

ZEE LA NYWILA - 1

 






IMEANDIKWA NA : ABYAS MZIGUA



*********************************************************************************



Simulizi : Zee La Nywila
Sehemu Ya Kwanza (1)


 MJ MOTEL, Ndivyo kilivyosomeka kibao kilichokuwepo juu ya jengo hilo la wazi. Jengo lililogawanywa pande mbili, sehemu ya kwanza ikiwa ni mgahawa, ambapo watu hujipatia aina mbalimbali za vyakula. Sehemu ya pili, kumewekwa karakana ndogo, marekebisho ya magari binafsi yakifanyika eneo hilo. Ni eneo lililobuniwa vizuri hasa.



Ubunifu na ubora wa huduma zipatikanazo mahala hapo, ndivyo vilivyowavuta kijana Patrick na swahibaye Harrison. Walileta gari lao lifanyiwe marekebisho, wakaamua wapate chakula cha mchana kabisa. Chakula kilisindikizwa na mazungumzo ya chinichini yaliyowachota vilivyo, kiasi cha kutohisi uwepo wa runinga kubwa iliyokuwepo mbele yao.

Patrick akionekana ndiye muongozaji wa mazungumzo, alitawala kikao hiki. Huku Harrison akibaki kuitikia tu. Hakumpuuza! Laa hasha!, ila yeye aliongea akachoka, vyakuongea bado havikuwa vimekwisha, ikamhiyari amuachie Patrick, ama Patty, kama alivyozoea kumuita.

Achana na unadhifu wa mavazi waliyovaa, vyakula vya bei kali walivyoagiza; vinaakisi hali 'jayyid' ya uchumi waliyokuwa nayo.

"Nashindwa kutambua la kufanya Patty, I lost the game!" Harrison alilalamika, akakunja sura yake yenye rangi ya kahawia, akamaliza kwa kugugumia 'glass' ya kinywaji walichoagiza.

"Hujapoteza kitu my friend, trust me!" Patrick alitoa tabasamu hafifu, lilioambatana na matumaini yenye uchangamfu.

"Unanishaurije? Nibet tena?" Harrison aliuliza, macho yake yakielekea usoni kwa Patrick, kusubiri jibu. Anamuamini mno rafiki yake--Chochote wanachoshauriana hutekelezwa.

"Noop! Kwa sasa acha kwanza. Kuna kitu…"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

" Habari zenu maboss? Gari yetu iko tayari. Kama hamtojali, ningeomba funguo ili nikaisogeze mahali pazuri!" Kabla ya Patrick kumaliza alichokuwa akiongea, mazungumzo yalikatishwa na kijana aliyevaa fulana nyekundu, nyuma ikikozwa na maneno MJ MOTEL, yaliyo katika rangi nyeupe.

Harrison hakujibu kitu, alimpatia funguo. Si mara ya kwanza kwake kufika eneo hilo, aliwaamini wafanyakazi wa hapo. Hawakuwa na mikono mirefu kwa wateja, wala majibu ya hovyo, yale ya reja reja.



Baada ya kupatiwa funguo, yule kijana akaenda zake.

Tofauti na alivyotegemea, Harrison alitaraji punde tu baada ya kutoa funguo, Patrick angeendelea na kuzungumza. Badala yake, kimya kiliendelea kutawala. Ndipo ilibidi amgeukie...

" Oy Patty! Patty! Wewe Patty! Wewe!"

"Enh! Naam, unasema?" Patrick alikurupuka, mithili ya anayetokea usingizini. Muda wote huo, tangu yule kijana alipokuja, mpaka alipoondoka, alimtizama sana.

" Yes! Yes! Yes!" Patrick alifurahia huku akigonga meza iliyo mbele yao.

"Mbona unanichanganya Patrick? Sikuelewi ndugu yangu." Harrison aliingiwa na kitendawili cha ghafla.

"Huwezi kunielewa Harry! Ila ukinielewa, nakuahidi utakuwa tajiri namba moja nchini!"

" Hahahah! Hebu acha masihara yako bwana. Fanya tuondoke ili…." Harrison alihisi Patrick kaanza masihara yake, ni kawaida yao kutaniana. Ila walinena wanenaji; Si kila siku ni Jumapili. Leo hiyo Patrick alikuwa akimaanisha,alimshika Harrison mkono…

"Hebu kaa Harrison! Umemuona yule kijana?" Patrick aliuliza.

" Yupi?", Harrison naye aliuliza, huku akivuta kiti chake nyuma kidogo na kuketi kwa mara nyingine.

"Huyu aliyekuja kuchukua funguo."

" Kafanya nini?" Bado Harrison hakuelewa alichotaka kumaanisha Patrick.

"Vizuri! Unajua nini Harrison, umri kwa sasa wewe umeshakwenda! Yatupasa tutumie mpango mwingine," Patrick alijibu.

"Mpango gani?" Harrison aliuliza, akizidisha umakini kusikiliza kile anachohitaji kuambiwa.

Patrick alimeza funda jepesi la mate, akaendelea kuzungumza, ndiyo kawaida yake, hachokagi kuongea huyu.

"Tunatakiwa tumtumie! Hakuna mchezo tutakaoshindwa. Hakika nakwambia."

"Tumtumie vipi?" Harrison alihoji, akiwa hamuelewi Patrick mpaka sasa--nini anataka kuzungumza.

" Umeona muonekano wake? Rangi yake je?, Hebu cheki mwili ule! Sikia Harrison, hii kazi niachie Mimi. Nitakupa majibu."



Harrison alikubali, anamuamini sana Patrick, nahisi kuliko mtu yeyote mwingine hapa duniani. Na hii imetokana na kamari ya picha za uchi wanazocheza kwa pamoja.



Usishangae! Ndiyo, ni kamari ya picha za uchi. Usitumie nguvu kubwa sana kuelewa. Usijali, nitakueleza yote.



Baada ya kutoka, waliipitia gari yao. Tofauti na walivyokuja, safari hii Patrick alibaki pale pale katika mgahawa, hawakuondoka wote. Aliingia katika juhudi za kumtafuta yule kijana waliyemuona.





Ilikuwa ni "tafuta n'kuone" iliyodumu kwa takribani robo saa, bila mafanikio. Uamuzi aliouchukua ni kujaribu kumuulizia. Ghafla akaingiwa walakini, Atamtafutaje mtu asiyefahamu jinale wala ukoo? Akawaza, akafikiria, akapata jibu.



"Habari yako kaka?" Alimfuata mfanyakazi mmojawapo, aliyeoneka anashughulishwa na akifanyacho. Kiasi cha kumjibu Patrick bila ya kumtizama...



"Salama,"



"Samahani ndugu, kuna mtu namtafuta!" Patrick akaenda moja kwa moja kwenye shida yake.



Kimya kifupi kikatawala, Patrick akisubiri kuulizwa "nani?", naye kijana akingoja aelezwe anayetafutwa ni " nani?".

Patrick alielewa hilo, akatangulia kueleza kabla ya kuulizwa…



"Ni jamaa fulani hivi, mrefu kidogo, mweusi lakini si sana. Tatizo, jina lake simfahamu."



"Nishamfahamu, anaitwa ABUU huyo. Sisi tumezoea kumuita SUKARI YAO!" Jamaa tayari alishamfahamu, mtu ambaye Patrick anamuulizia.



"Hahahaha! Sukari yao?" Patrick alijichekesha huku akiingizia swali, swali lililobeba tone la uchunguzi. Alitaka apate uhakika, Hii SUKARI YAO ina maana ile ile aijuayo yeye ama?.



"Ndiyo! Wateja wengi wa kike wanaokuja hapa, wengi wao - HUTULILIA namba yake wakishamwona." Jamaa akafunguka kila kitu.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Yes! Huyu ndiye mtu ninayemtafuta Aisee!" Patrick alijisemea, mwanga wa kufanikiwa kile akitafutacho ulianza kuchomoza ndani mwake. Hesabu zake alizopiga, tayari zilishatoa majibu, hata bila ya kuingizwa kikokotozini.



"Hahahahah! Hatari sana hiyo. Vipi, naweza nikampata hivi sasa?" Patrick alijechekesha kidogo, kisha aliuliza.



"Daah! Ameshaondoka, muda wake wa kazi ulishakwisha,"



"Anhaa! Kumbe hapa mnaingia kwa zamu?, kwa hiyo kesho nije muda gani, ambao kuna uwezekano wa kumkuta?"



"Muda wowote, kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa nane boss!"



"Saa nane mchana?"



"Ndiyo,"



"Nashkuru sana ndugu yangu, hii utapata soda kidogo," Patrick alimshukuru, akatoa shilingi 10,000 kumpatia yule jamaa. Naye hakutaka kuleta maringo, ya kuyakuta mambo yapo kwenye ukingo,kwa kusikitika; uanze kuitesa shingo. Aliipokea ile pesa na kumshukuru pia.



Patrick aliondoka, aliendelea na pilika zake za siku hiyo. Shabaha kubwa akiwa anaielekezea siku inayofuata. Ampate Abuu ama SUKARI YAO, Kama alivyopata utambulisho wa awali.



***

Kulikuchwa kisha kukakucha tena.

Ni saa tano asubuhi, ndani ya MJ MOTEL.

ABUU, kijana nadhifu wa mavazi, mzuri wa sura na umbo "mumtazi". alikuwa katika shughuli yake ya kusogeza magari, baada ya kufanyiwa huduma za kiufundi.



Abuu ni kijana msomi, mwenye shahada yake ya uwalimu wa kiingereza na kiswahili. Ugumu wa maisha na ukosefu wa ajira usiokwisha, haukutaka kabisa mtaani kum'bakisha, akaacha kusubiri aje kufundisha, magari akaanza jifunza kuendesha.



Alijifunza udereva ndani ya miezi mitatu, ukiongezea utaalamu mkubwa wa lugha alionao, haraka alipata kazi punde baada ya kuleta CV yake katika kampuni hii, inayosimamia MJ MOTEL.



Kazi aliyopata hapa, Ni kupanga magari katika mpangilio mzuri yakishafanyiwa huduma stahiki. Ni kazi rahisi, ila ni ngumu kwa wingi wa magari yanayokuja eneo hili.

Huyo ndiye Abuu kwa ufupi, utazidi kumfahamu vizuri mbeleni.



" Kaka, kuna mgeni wako!," Wakati Abuu anaendelea na shughuli zake, aliletewa taarifa hii.



"Mara ngapi nikwambie lakini? Waambie sipo! Ni hivii, SII-POOO!," Abuu alijibu na kutoa msisitizo, kuonesha msimamo wa kile anachokizungumza.



"Siyo mwanamke! Ni mwanaume," Mleta taarifa aliongezea.



Baada yakusikia hivyo, akapoa kidogo.



Huwa hataki kusikia kabisa kuhusu mgeni wa kike. Wengi wao wakija, humtani wawe nae katika mahusiano, wapo wanaomtongoza, wapo wanaomhonga na wapo wanaotamani walau tu wapige naye picha. Abuu ni kijana mzuri aisee, nikikwambia mzuri, namaanisha mzuri!.

Si kwamba hakuna msichana aliyevutiwa naye, miongoni mwa hao wamwindao. Hapana! Wapo kama utitiri.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Tatizo, ni historia chafu iliyomkumba Abuu katika maisha yake, chafu!.

Miaka mitatu iliyopita aliwahi kuwa katika mahusiano.

Ukiacha yale ya Sharkhur Khan na Kajol, ya kwao yalikuwa mahusiano bora kabisa kuwahi kutokea katika sayari hii.



Abuu alimpenda Almasi, Almasi alimpenda Abuu. Almasi ni msichana wa kitajiri, babaye akiwa balozi wa Tanzania nchini Uturuki, aliingia katika dimbwi la mahaba na mwana-utanashati Abuu.



Upendo, uaminifu na malengo. Vyote viliinea vinywani mwao, wakaitana mume na mke, kila mmoja akamkubalia mwenzake, akampa kilichopo kati ya mapaja yake. Hatimaye, Muumba alijaalia yake, tumboni mtoto akachukua nafasi yake.



Yote hayo yanatokea, baba mtu huko Ubalozini, hafahamu ya Musa wala Firauni. Busara za kizigua zinasemaga…

"Njia pekee ya kufanya jambo lisijulikane hapa duniani, Ni kutolifanya!". Habari zikamfikia huko huko Uturuki.



Ni nani anayependa bintiye achezewe? Ni nani anayependa bintiye abebe mimba ya kijana masikini? Ni nani?. Halikuwa jingine, zaidi ya Salamu za adhabu kutumwa kwa Abuu, na zikamfikia.



Walitumwa vijana, wakavamia nyumbani kwao usiku. Anapoishi yeye na mama yake pekee, Baada ya babaye kufariki kabla ya Abuu kuzaliwa.

Hawakuacha mtu! Walimpiga yeye na mama yake, hawakuwa na huruma wala busara. Na onyo juu wakaliacha...

" Huyu Almasi muone kama UKOMA mjinga Wewe!".



Kidonda cha moyo, kilizidi vya mwilini. Mama yake alipata maumivu makali, mwili mzima ukapooza, Almasi mawasiliano naye akapoteza, alihisi walimwengu wote wanam'beza, HATOPENDA TENA akajiapiza.

………



"Yuko meza namba ngapi?," Baada ya kutajiwa mgeni amsubiriaye ni wa kiume, akaulizia alipo.



"Meza namba 32, kavaa fulani ya bluu na kadeti nyeupe, mfupi hivi kidogo. Ameagiza Maji tu," Kijana aliyeleta taarifa, alizitoa kiukamilifu kisha akaondoka.



Hakuhitaji kuchelewesha Wakati, alijiweka sawa na kuitikia wito wa mtu asiyemfahamu.

Baada ya mazungumzo marefu, akarudi! Alikuwa katika dimbwi la mawazo, haikwenda yoyote kazi siku hiyo. Akawahi kuondoka,hata kabla ya muda kufika.



Akiwa katika daladala, maongezi yake na aliyeonana naye, yakawa yanarejea rejea kichwani mwake. Alikuwa ameongea na Patrick…



"Unalipwa laki tano kwa mwezi? Basi sisi tutakulipa kila wiki milioni moja. Na hiyo ni ya kuanzia tu!," Hayo yalikuwa ni maneno ya Patrick, yalimzungumka kichwani mwake, hakuwahi kutegemea kabisa kuja kupata pesa ya namna hiyo maishani, aliitamani mno kazi yenye ujira mkubwa kiasi hiko, leo hii kaipata. Huo ufanywaji wake sasa!



Aliendelea kurudisha maneno ya Patrick kichwani….

"Kazi yenyewe rahisi tu, ni KUPATA PICHA ZA UTUPU ya msichana tutakayekuagiza sisi. Ukiachana na mshahara huo wa wiki, kila utakapokamilisha kazi moja, utapata milioni 15,"



Naam, hiyo ndiyo KAMARI YA PICHA ZA UTUPU mpenzi msomaji, niliahidi nitakueleza. Acha niitimize…



Ni kamari isiyojulikana na watu wengi duniani, yawezekana hata wewe huifahamu, ila ni moja ya haramu zenye pesa nyingi duniani. Iko hivi; Wafanyabiashara wawili, wanawekeana dau. Mmojawao anapendekeza msichana. Tena anachaguliwa yule mwenye heshima yake na adabu katika jamii. Kisha, zinawekwa siku za mchezo kukamilika.

Atakayepata picha ya msichana huyo akiwa mtupu, atabeba pesa zote! Ila kwa masharti.



Picha hiyo isiwe ya kuhaririwa (edited), msichana kwenye picha anatakiwa awe hajafungwa. Aonekane kapiga picha hiyo kwa hiyari na matakwa yake.

Na ndiyo maana, wengi wao wanaanzisha mahusiano na wasichana hawa, ndani ya muda mchache wanawarubuni wafanye nao ngono, huku akihakikisha picha ya msichana huyo akiwa mtupu, inapatikana. Hiyo ndiyo NUDE PICTURES BETTING (Kamari ya picha za utupu), mchezo haramu wenye kuingiza pesa zaidi duniani.



….

Mpaka usiku unaingia, Abuu bado alikuwa katika bahari ya maamuzi, akubali au akatae. Aliwaza sana! Hakuweza hata kula siku hiyo.



Taratibu, alichomoa kijikadi katika mfuko wake wa suruali, maneno machache aliyotolewa na Patrick yakarejea tena…



"Business card hii, ukipata maaumuzi yoyote. Naomba unipigie leo usiku, nikiona kimya mpaka kesho, sitakutafuta tena!"



Aliitazama sana kadi ile, akatoa simu yake ya mkononi. Akaanza kuinakili namba ile. Kama hajamiliza, akahisi sauti inamwambia;

"Achana na ufuska wa aina hiyo Abuu!", haraka akazifuta, akairudisha kadi mfukoni, simu yake akaitupa kitandani.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Aliinuka, akavua Shati kwa joto Kali aliloanza kulihisi humu ndani, alitoka na kwenda chumbani cha pili. Humo alimkuta mamaye akiwa kalala, kutwa kucha mama yake ni wa kulala tu. Kapooza! Hana lolote awezalo kulifanya.

"Sikia, Wewe ifanye hiyo kazi. Ukishafikisha milioni 50 za kumpeleka mama India, unaachana nayo,". Sauti nyingine, yenye ushawishi hasi, ikapenya bongoni mwake.



Akajikuta anarudi chumbani mwake, alichomoa kadi mfukoni na kuanza kuzinakili zile namba kwa mara nyingine.

Huku akifahamu fika; hiyari na mukhtari vyote viko mabegani mwake.

Ila hakujua kuwa, anataka kufanya ibada ndani ya jumba la kishetani. Hakutambua hilo!

_____

"Hellow!" Baada ya muito wa sekunde kadhaa, simu ikapokelewa, si mwingine aliyepokea ila ni Patrick.



"Hellow! Abuu hapa nazungumza," Alijitambulisha.



"Ndiyo SUKARI YAO! Nipe mrejesho," Patrick alijitia kuuliza, huku akitambua fika! Sumu Kali aliyomtemea Abuu lazima ingefanya kazi.



Ni kweli, halikuwa jingine zaidi ya kukubali kwa Abuu kufanya kazi ile. Kazi isiyojali ubinadamu wala ubin'hawa, itakayomlazimu kuruka kila upande ingawa hana mbawa, isiyojali utu wala kitu usawa, itakayomfanya asiwe mgonjwa ila akameza dawa.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Vizuri, vizuri sana! Naomba nipe dakika kumi Kisha nitakupigia!". Patrick alizungumza kwa sauti iliyojaa furaha na shauku, kisha simu ikakatwa.



Haraka, Patrick muda huo huo,alimpigia Harrison. Alimpa taarifa zote kuhusu mpango wao. Hesabu, tathmini, mashauriano na hitimisho vyote vikawa vimechukua nafasi baina yao.



Huku kwa Abuu, miale ya majuto ikigonga kwa mbali mtimani mwake, ikishindana na kiza kikali cha matumaini ayaonayo akiianza kazi hii mpya, iliyo mbele yake.

Sekunde zilipita, dakika kumi zikawa robo saa. Aloanza kuingiwa na wasiwasi, kila muda aliitazama simu yake, akaitazama tena na kuishusha chini. Punde! Alishtushwa na mtetemo wa simu aliyotoka kuishika muda si mrefu, alikuwa ni Patrick.



" Sasa Abuu, Jiandae! Kesho asubuhi tutafanya utaratibu, unaenda Ufilipino!," Baada ya kuipokea tu, Patrick alizungumza.



Ganzi ya moyo ikamkumba, hakuelewa kipi anachoambiwa na Patrick, akahisi hajamsikia vizuri…



"Unasema?," Abuu aliuliza, huku akibonyeza kwenye simu yake-sehemu palipoandikwa "loudspeaker" ili asikie vizuri.



"Jiandae, Kesho utasafiri kwenda Ufilipino," Patrick alirudia bila kusita.



"Ufilipino! Mbona imekuwa ghafla mno? Na hatukukubaliana suala hili," Abuu aliongea kwa sauti ya kati, haikuwa ya juu sana wala ya chini, ila ilisheheni ukakasi wa ufokaji.



" Abuu, tutazungumza vizuri hiyo hiyo kesho," Patrick akajaribu kumtuliza.



"Hapana! Tusifanyiane hivyo kiongozi. Kama ni masuala ya kusafirishana, mie sitaki!" Abuu alimuonesha msimamo wake.



"Kwani nini unahofia Abuu? Tutataweka mkataba kati yetu. Mkataba utaonesha tumepeleka kukusomesha, hii italinda usalama wako," Patrick akamuelezea kwa uchache kumpunguza jazba.



Naam! Hii kauli kidogo ilituliza "shukuru-shakara" za Abuu, akapoa, akaingiwa na matumaini. Ila, akakumbuka jambo; Mama yake, mboni yake, lulu ya maisha yake- atabaki na nani? Nani atamuangalia na kumhudumia?.



"Lakini Patrick! Si unakumbuka nilikwambia kuwa nina mama ambaye ni mgonjwa?," Abuu aliuliza tena, wakati huu ilikuwa ni kwa sauti ya chini, iliyopoa na yenye adabu.



"Nakumbuka! Na kila kitu kipo sawa. Mama yako tutamtunza na kumhudumia kwa kipindi chote. Mpaka utakaporejea!".

Huyo ndiye Patrick, Harrison anapenda kumuita " Patty MASTER PLAN", akipanga jambo huwa linakwenda likifuata ramani aliyoichorea.



Patrick ndiye mtu wa kwanza kabisa kumshauri Harrison kuingia katika kamari hii haramu, ndiye aliyemshauri kuacha biashara za migodini na badala yake pesa kuziwekeza katika umalu'uni huu.

Faida ya haraka na kubwa aliyoanza kuipata Harrison, ilimfanya kumuamini Patrick, kwa chochote kile. Ikafikia kuwa kama ndugu wa damu, mtu na kaka yake.

……….



Asubuhi ilifika, utaratibu ukafanyika, hatimaye ulikamilika. Tayari kwa safari ya Abuu kutoka Tanzania kwenda nchini Ufilipino.

Huko alitakiwa akaishi kwa takribani mwaka mmoja, akafanyiwe ukarabati. Ndiyo, ukarabati!. Anaenda kujengwa upya kwa kila kitu, akirudi ni kazi tu.



Ilimchukua takribani masaa kumi na dakika kadhaa, kufika jijini Manila, nchini Ufilipino. Hapo akachukua ndege nyingine kuelekea kisiwani Palamacan. Tofauti kabisa na kibali chake kisemavyo, kuwa ataelekea chuo kikuu cha - Ateneo de Manila, kilichopo hapo hapo jijini Manila.



Ni umbali wa lisaa limoja mpaka kufika kisiwani huko. Kisiwa chenye mvuto wa aina yake, chenye mzunguko wa mchanga mweupe pande zote. Huku hoteli kubwa ya kifahari, ya Amanpulo resort - ikinogesha umaarufu wake. Na hapo ndipo Abuu aliwekewa kambi yake.

Inasadikika, kugharimu takribani dola 1220, kulala kwa usiku mmoja ndani ya hoteli hii.

Muda aliofika Abuu, ulikuwa ni usiku tayari, ilimlazimu kula chakula na kulala, safari ilimchosha kwa kiasi chake.



Asubuhi na mapepa, programu maalumu ilianza. Alipokea mgeni kutoka Nigeria, akimletea vitabu sita, vilivyobora kabisa - vinavyozungumzia "SAIKOLOJIA YA WANAWAKE".

Ndivyo ratiba ilivyosema; Miezi mitatu ya mwanzo, alitakiwa awasome wanawake, awajue wanawake. Alitakiwa ajue; Kipi wanapenda kipi hawapendi, vipi wanafurahi vipi wanahuzunika. Kiufupi, alijifunza na kuwafahamu wanawake, zaidi ya wanawake wenyewe wanavyojifahamu.

Miezi mitatu ilikatika, kurasa za vitabu vyote hivyo alizimaliza.



Ikafuata miezi mitatu mingine.

Katika miezi hii, alitakiwa ajifunze kuwa mwanaume na si mvulana. Akatafutiwa mtaalamu.

Alimfundisha vyote; wanaume wanazungumzaje, wanatembeaje, wanavaaje, wanakulaje, wanachekaje, wanaliaje, yani kila kitu!. Akawa mwanaume halisi.



Ikafuata miezi mitatu mingine,

Hii ilikuwa miezi ya utongozaji. Si unajifanya unajua kutongoza? Hebu acha wewe! Hujui kitu nakwambia. Kuna watu wamebobea. Na Ndiyo Abuu akatafutiwa mmojawapo.

Alimfunza mbinu zote, za kila aina. Vipi unatongoza harusini? Ufukweni, nyumbani, hotelini, maktabani, Na hata katika nyumba za ibada. Alifunzwa kutongoza mwalimu, daktari, mwanasiasa, mwanafunzi na hata mke wa mtu. Vyote alifundishwa Abuu, akafundishika.



Miezi mitatu ya mwisho, ili mwaka mmoja ukamilike, ilikuwa ni mazoezi ya ngono. Yeah! Alijifunza jinsi ya kushughulika!

Wanawake wanatofautiana, basi hata namna za kuwashughulikia zinatofautiana. Akaletwa mkufunzi wa kike.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Darasa likaanza, likaendelea, likanoga na hatimaye majaribio yakafanyika; mkufunzi na mwanafunzi, wote wakaweka maamuzi, Kitanda kukifanyia upuuzi.

Hakuna wa kulaumiwa, Abuu alishaelewa sana somo, mwalimu alishamuelewa sana msomaji.



…..

Muda wa Abuu kurudi nchini ukafika. Akajiandaa, na safari ilianza kurejea nyumbani, nchini Tanzania.



Alifikia katika hoteli, usiku huo huo kukawa na kikao cha watu watatu; Harrison, Patrick na Abuu. Ukiwaona, waweza sema - Abuu yuko na wafanyakazi wake wawili. Kwa namna alivyopendeza na kuvutia. Ni haki yake! Si tayari kashafundishwa kuwa mwanaume? Yes, Acha apendeze bwana.



"Enhee SUKARI YAO, hebu niambie unataka ukaishi eneo gani hapa nchini?," Patrick aliuliza, huku akiwa ameshika kalamu na kijidaftari kikiwa mbele yake. Tayari kwa kuandika vitu muhimu.



Abuu akatoa tabasamu hafifu la kiume, kisha akazungumza kistaarabu na kwa madaha;

"Kwanza, hilo jina la SUKARI YAO lifute. Mie mpaka sasa passwords za wasichana wote ninazo, hakuna nitakayetongoza akatae. So niiteni, Mr. Password!,"



"Hahaha! Hilo jina ni kwa kiingereza, kwa kiswahili je?" Harrison alicheka Kisha akauliza swali la kizushi.



Kwakuwa ni mwalimu mzuri wa kiswahili, anakifahamu vizuri, Abuu akajibu kiufupi;

"ZEE LA NYWILA!".



" Hahahah!"

Wote kwa pamoja wakacheka, wakagonga glass zao za vinywaji, maongezi mengine yakaendelea.

Huku nyuso za Harrison na Patrick zikijaa tumaini zito.

Walakini, wangalijua kisima walichochimba ndicho watatumbukia, katu karibu wasingekisogelea!.

_____

Kama makubaliano yalivyokuwa; Akirudi nchini, ni kazi tu. Uwekezaji mkubwa walioufanya Patrick na Harrison ulihitajika urejeshe faida. Tena si faida tu, faida kubwa zaidi.



Akiwa ndani ya hoteli aliyopangishiwa, akisubiri utaratibu wa nyumba aliyoahidiwa kupatiwa ukamilike; Alijilaza chali kitandani, hajavaa fulana wala shati; namaanisha "kifua wazi".

Kumbukumbu na fikra zake zilikuwa zipo katika ngono na wanawake tu.



Abuu huyu si yule aliyeondoka nchini mwaka mmoja uliopita. Siye Abuu yule aliyekuwa anaitwa na wasichana awakatae, siye kabisa!

Huyu ni Abuu mpya, huyu ni Abuu " ZEE LA NYWILA".

Hajui kitu kupenda kamwe!.

Hata aje msichana mzuri kiasi gani, atamlaghai, atamchezea kisha anampotezea.



Mpaka sasa, wiki mbili tu tangu aripoti nchini baada ya kutoka Ufilipino, ameshapita na wasichana "kumi kidogo". Usiniulize amewezaje kukutana nao, amewezaje kuwatongoza, amewezaje kuwashiwishi mpaka "akawananiliu", hilo Usiniulize! Wewe elewa tu; huyu ni ZEE LA NYWILA.



Idadi yote hiyo ya wasichana, kazi bado haikuanza; Twaweza sema - Alikuwa anapasha tumbo joto tu. Leo ndiyo siku ya kuanza amali zake.

Na hapa, alikuwa amejilaza kusubiria ujumbe alioahidiwa na Patrick. Kuhusiana na "mission" yake ya kwanza.



Naam, hazikupita dakika nyingi, ujumbe katika kompyuta yake mpakato uliingia. Ingawa ulimshtusha, hakutegemea kabisa,ila ndiyo ishakuwa kazi kwake - kuwajibika kulimuelemea.



Kabla hakujakuchwa, bi'maana siku hiyo hiyo , Abuu alitakiwa asafiri kuelekea nchini Afrika kusini. Huko kuna mtoto wa kiongozi mkubwa tu, ambaye yupo mapumzikoni. Umri wake ni miaka 24, anasoma katika chuo kikuu cha Rwanda.

Kwa upande wa uraia, msichana huyu amechanganya mataifa. Mamaye ni Mrundi (Raia wa Rwanda) na baba yake ni Mtanzania.

Anazungumza lugha moja tu! Kiingereza.

Picha yake ya "utupu" ilihitajika, Na malipo ya kazi hii - Ilikuwa ni milioni 25 kwa Abuu.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Utaratibu wa safari na kila kitu ulifanyika, Kwa kutumia shirika la "AIR NAMIBIA", Abuu alitumia masaa matatu na dakika ishirini na tano, kuwasili jijini Johannesburg - Afrika Kusini.

Hapo ilimhitaji apande ndege nyingine, wakati huo ni saa nane na robo mchana.

Mpaka anafika jijini Port Elizabeth, tayari ni takribani saa kumi na moja.



Hakutaka kulaza damu, moja kwa moja alifikia katika hoteli inayosadikika msichana huyo amepanga chumba .

Si kwingine! Ni mahali safi, tulivu na yenye upepo mwanana wa bahari, hii ni SINGA LODGE. Yenye hadhi ya nyota nne, takibani mwendo wa dakika mbili tu kwa gari, kuufikia ufukwe wa HOBIE (HOBIE BEACH). Panavutia sana kiukweli.

Na hivi, ndivyo vitu avipendavyo Abuu.



ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog