Search This Blog

Tuesday 1 November 2022

PENZI LA MZOA TAKATAKA - 2






Simulizi : Penzi La Mzoa Takataka 
Sehemu Ya Pili (2)




Kitanda cha Mazoea kilionekana kidogo, alijigalagaza huku na kule ilihali mawazo yake yote yakimfikiria Nyogoso. Moyo wake ulimuhitaji sasa, vile vile macho yake yakawa na shauku ya kutaka kumuona kwa mara nyingine tena, safari hiyo akiwa katika hali ya usafi. Hakupata picha atakuwa kidume wa aina gani endapo ikitokea akiwa ndani ya mavazi mazuri na nadhifu pia. Mara baada kuwaza kwa muda mrefu alishusha pumzi ndefu kwa mara nyingine tena kisha akatuliza akili yake, pole pole usingizi ulimjia na mwishowe alisinzia kabisa.

Kesho yake asubuhi palipo pambazuka,jiji la Dar es salaam lilionekana kuwa na hali ya hewa ya mawingu. Hali ya hewa hiyo iliweza kupelekea wakazi wengi wa jiji hilo kuamini kuwa muda wote wote mvua itanyesha.. "Umeamkaje kaka?.." Jaluo alimsabahi Nyogoso.

"Nimeamka salama tu, sijui wewe"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Mimi pia nimeamka salama. Naam! Tayari kumekucha vipi utaweza kwenda kazini?.."

"Ndio naweza, mimi ni mwanaume. Na huu ndio wakati pekee wa kugangamala ili nifike malengo ingawa Kuna changamoto ngumu" Akajibu Nyogoso kwa sauti ya upole, iliyopenya vema masikoni mwa Jaluo. Jaluo akashusha pumzi ndefu kwanza kisha akasema "Ni kweli,ila dhamila pekee ni kupambana pasipo kuangalia changamoto. Lakini pia bro, yakupasa kuwa makini sana katika mizunguko yako. Mfano jana mshukuru binti yule aliyekusaidia, la sivyo ungekufa. Amini ni wasichana wachache sana karne hii wenye moyo kama yule binti. Wasichana wengi wa karne hii wamejaa nyodo na dharau pia kana kwamba wanatembea angani aidha wao hawaendi msalani. Hebu tuachane na hayo, ngoja mimi niwahi kabla mvui haijaanza kunyesha si unaona hali ilivyo angani?"

"Ndio naona kaka, tangulia nipo nyuma. Na pia kila siku mtu hujifunza kutokana na makosa. Kwahiyo kosa nililofanya jana sitegemei kulirudia siku nyingine" Akaongea Nyogoso. Jaluo akaachia tabasamu kisha akaondoka zake akimuacha Nyogoso akiwa bado anasafa kwa maumivu. Upande wa pili nyumbani kwa kina Mazoea,anaonekana mama Mazoea akibisha hodi chumbani kwa Mazoea. Mama huyo akagonga mlango mara ya kwanza huku akilitaja jina la binti yake, akarudi mara ya pili kisha kumaliza mara ya tatu. Mlango ukafunguliwa.

"Mazoea mwanangu, mpaka muda huu bado umelala?.." Akaongea mama Mazoea akimwambia binti yake ambaye siku hiyo amechelewa kuamka tofauti na siku nyingine. Mazoea akiwa ndani ya khanga moja aliyojifunga kifuani ikimstili mpaka kiunoni akapiga kwanza mwayo huku akinyoosha kisha akasema." Jana nilichelewa kulala mama. Shkamooo"

"Malakhabaa,haya jiandae uende shule kumekucha sasa" Akaongeza kusema mama Mazoea halafu akarejea chumbani kwake. Macho ya Mazoea yanatazama saa ya ukutani. Anashtuka kukuta imetimu saa moja kasoro robo. Haraka anaingia bafani kuoga,kwa muda wa dakika tano anarejea chumbani. Anavaa nguo haraka haraka kisha safari ya kuelekea shule inanzia hapo. Ni mwanzafunzi wa chuo kikuu Dar es salaam. Ni mrembo madhubuti mwenye ngozi nyororo yenye rangi asilia ya kiafrica. Mrefu kiasi, kinywa chake kilivutia sana kwa mwanya mdogo uliupo meno ya juuu. Mazoea binti ambaye alisifika kwa ulivu wake, sio shule wala mtaani anakoishi. Mbali na wazazi wake kuwa na pesa, ila binti huyo katu hakuonyesha nyodo kwa wasio na kitu. Palipo stahili msaada alisaidia kwa kadili ya uwezo wake. Walimu na wanafunzi walimpenda sana, uwezo wake darasani ndio kabisaa ukampatia umaarufu chuoni kote. Lakini siku hiyo inakuwa siku ya tofauti kwa Mazoea, taswira ya mzoa takataka Nyogoso ilimjia mara mbili mbili kichwani mwake hali ambayo inamfanya kuwa tofauti na kabisa na namna alivyozoeleka.

Na pindi Mazoea yupo katika hali hiyo, kwingeneko anaonekana Nyogoso akiwa mtaani anatembea kwa kuchechemea shauli ya kipigo kikali alichokipata siku ya jana. Alipita nyumba moja baada ya nyingine akiulizia takataka, hatimaye zinafika nyumba kumi pasipo kuambulia hata msigo wa shilingi mia mbili. "Haaah! Kweli hii ni zaidi ya shida" Alisema Nyogoso wakati huo anajifuta jasho la mnyonge katika paji uso wake. Kiu na njaa vikilindima tumboni mwake, mfukoni hakuwa na hata senti ya kunulia japo kitumbua, kwani hata zile fedha alizopewa na Mazoea alipokonywa siku ile ile na vibaka waliomkaba wakati anarejea maskani. Anajikuna anashindwa afanye nini, aamue lipi aache lipi. Hakika aliyakumbuka maneno ya mama yake aliyomuasa kabla hajachukuwa uamuzi wake. Pumzi ndefu anashusha huku akitazama namna jua kali la utosi lilivyokuwa likiangaza jiji la Dar es salaam. Machozi yakamtoka Nyogoso, muda akiwa amejibanza kwenye moja ya nyumba aliyopendelea kutafuta takataka. Lakini wakati yupo kwenye dimbwi kubwa la mawazo, usingizi ukampatia ila punde akastuka baada kumwagiwa maji yenye shombo ya samaki. Nyogoso anakarupuka kutoka usingizini kisha anamtazama mtu huyo aliyemwagia maji ya shombo. Anaishia kusikitika tu, hakutaka kuongea neno lolote na mtu huyo zaidi ya kujitazama namna maji hayo yalivyomchamfua. Ni mwanamke mnene, ngozi yake inaonekana imechakazwa na mikorogo. Mama huyo anamtazama Nyogoso kwa jicho pembe akingojea ni kipi atakacho amua mzoa takataka Nyogoso baada kumwagiwa maji hayo ya shombo. Alipoona Nyogoso hajaongea wala kumfanya kitendo chochote, akatema mate chini kisha akarudi ndani.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Huu ni uonevu ulio kidhili, ni kwanini hawa walicho nacho huwadharau wasio kuwa nacho? Kosa gani nililofanya? Na nikwanini hujiasahau kuwa kuna leo na kesho?.." Anajiuliza Nyogoso huku akizinusa nguo zake ambazo kwa muda huo tayari zinatoa harufu ya shombo. Punde si punde anasikia sauti ikimwambia kwa ukali." Oya ondoka hapa kabla sijakufanya kitu kibaya, mtu gani unatoa harufu kama gari taka?.. " Sauti hiyo inamshtua Nyogoso, anainua uso wake kumtazma mtu aliyemwambia hivyo. Ni kijana mdogo wa makamo, kando alisemama na yule mwanamke aliyemwagia Nyogoso maji ya shombo. Mwanamke huyo analilalia bega la kijana huyo aliyemtaka Nyogoso aondoke mahali hapo. Nyogoso anaondoka kichwa chini wakati huo huo akasindikizwa na sauti ikisema "Nisikuone tena unasogelea nyumba hii, mbwa koko wewe". Sauti hiyo inatoka kinywani mwa yule mwanamke mnene aliyemwagia Nyogoso maji ya shombo. Ni tusi ambalo lilimuumiza sana mzoa takataka Nyogoso, ila hakuhitaji kujibizana naye zaidi ya kuishia kwenye vichochoro kuendelea na shuguli yake ya kutafuta takataka majumbani. Lakini bado anaambulia patupu kwa mara nyingine tena,na hivyo anaamua kujitosa majalalani kutafuta chakula chochote kilicho tupwa. Siku hiyo inakuwa siku mbaya upande wake, hakuweza kupata hata kipolo kilicho tupwa, alichoka sana wakati huo jua la Dar es salaam likizidi kuwa kali kana kwamba limeshuka sentimita kadhaa. Masaa yalivyozidi kwenda ndivyo Nyogoso alivyozidi kukosa nguvu, njaa na kiu kali vinamnyong'onyesha kitendo ambacho kinamfanya kuushiwa nguvu ya kwenda jalala lingine kutafuta kitoweo. Alipoangukia ndio hapo hapo. Anakosa nguvu ya kujinyanyua. Akanyoosha mkono juu ishara ya kuomba msaada kwani muda huo hakuwa na uwezo wa kupasa sauti. Alihema haraka haraka huku kijasho chembamba kikimtoka ilihali macho yake yakiona ukungu na kwa mbali mbele yake anapata kumuona bibi kizee akiwa na mkongojo akizipiga hatua pole pole kuja mahali hapo jalalani alipoangukia..





Akiwa chini alistaajabu sana kumuona bibi kizee huyo aliyekutwa akitembea kuja mahali hapo alipoangukia, kwenye wingi wa takataka kunako jalala. Bibi huyo alikuwa na mkongojo huku akionekana katika mavazi meupe. Nyogoso aliogopa sana, alitamani kukimbia lakini nguvu hizo hakuwa nazo. Woga ulimjaa ilihali kijasho chembamba nacho kikimtoka kuanzia kichwani mpaka kwenye nyayo za miguu yake. Akiwa katika hali hiyo, punde akapoteza fahamu. Akazinduka baada ya lisaali moja akistuliwa na manyunyu ya mvua ya mpito. Mapigo ya moyo wake yalienda kasi, kwa mbali alimkumbuka bibi kizee yule aliyemuona kabla hajapoteza fahamu ni mara tu akili yake ilivyorudi katika hali ya kawaida. Muda huo huo alimuona mama ntilie akiwa na ndoo kichwani akijongea katika jalala hilo alilopo. Ndoo hiyo aliyobeba mama ntilie huyo ndani ilikuwa imesheheni makombo ya vyakula mchanganyiko na ukoko. Alitembea kwa umakini kabisa katika shehena hiyo ya uchafu jalalani,macho yake yakagoda pale alipolala Nyogoso lakini aliishia kusikitika tu na wala hakuweza kushuhulika naye kwani alijua dhahili shahili ni mwendawazimu aliyejipumzisha. Hivyo alimwaga makombo hayo ya vyakula kisha akaondoka zake huku moyoni akijisemea "Kweli kichaa ni kichaa tu. Yani maeneo mazuri kaona hayafai akaamua kuja kutulia jalalani. Duuh! Ama kweli bora ukose mali ila sio akili" Alihitimisha kwa nahau mama ntilie huyo. Pasipo kujua kuwa aliyemuona jalalani sio mwendawazimu bali ni mtu mwenye akili zake.

Baada mama ntilie huyo kuishia zake,Nyogoso alishusha pumzi ndefu, macho yake yakitazma pale yalipomwagwa makombo. Punde akajikaza kisabuni kusogelea eneo hilo, hatimaye akapafikia. Aliyala kwa pupa makombo hayo kana kwamba alikuwa na njaa ya siku saba. Alipotosheka akalala chali huku paji la uso wake akitazama angani namna mawingu yalivyokuwa yakipishana. Hakutaka kuondoka alitulia kwa muda wa dakika tano kisha akanyanyuka akaendelea na safari yake kwenda asiko kujua sababu hakuwa mwenye ji wa jiji la Dar es salaam.



**********



Katika mitaa ya magomeni, Nyogoso aliingia. Wakati alipokuwa anatembea ghafla alikutana na Jaluo, kijana muokota makopo ambaye ni mtu anayeishi naye maskani. Jaluo alikuwa amebeba mzigo mkubwa kichwani,mzigo ambao ulimstua Nyogoso ambapo akajikuta akisikitika ilihali akizipiga hatua kusogelea. Alipo mkaribia akasema.

"Habari yako ndugu yangu" Ni salamu ambayo Nyogoso aliitoa huku kinywa chake kikiwa na tabasamu bashasha. Jaluo aliposika sauti hiyo hakuitikia zaidi alimjibu "Fanya kazi kijana salamu maskani.." Jibu hilo lilimshangaza Nyogoso, akajikuta akibaki mdomo wazi akishindwa kuelewa kwanini mtu wake wa karibu amemjibu hivyo kana kwamba hawafahamiani.

"Ni kwanini amenijibu hivi kama hanifahamu? Au uchovu? Doh ama kweli mjini njoo na peke yako, tabia na vingine utakumbana navyo huku huku" Alijisemea hivyo Nyogoso wakati huo Jaluo akiwa ameshatokomea zake na mzigo wake wa makopo ilihali Nyogoso akimsindikiza kwa macho lakini mwishowe alishusha pumzi ndefu kisha akaambaa na moja ya mitaa Magomeni. Alipokuwa anatembea, mbele yake anaona gunia likipeperushwa na upepo. Haraka sana aliukanyaga akautia mbavuni akajongea kando ya mtaa huo kisha akaketi chini kufikiria kazi ipi afanye mbali na hiyo ya kuzoa takataka ambayo upende wake ni kama inamuwea changamoto.

"Ooh Mungu wangu. Nyogoso hakika nimepatikana! Dunia naiona chungu. Hivi kweli ni mimi ambaye nilikuwa navuna zaidi ya magunia saba ya mahindi nyumbani? Ni mimi mkulima hodari Baliadi? Ona thamani yangu iko wapi sasa? Nimekuwa kama kichaa Nyogoso" Alijisemea Nyogoso ndani ya nafsi yake. Pumzi ndefu akashusha kisha akaendelea kuipa akili yake kutafakri uamuzi upo utakao kuwa sahihi kwake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Kazi hii imekuwa na kila aina ya changamoto vile vile ni ngumu sana. Naona bora nimfuate ndugu yangu Jaluo kwenye kazi ya kuzoa takataka. Lakini inasemekana kazi hii ni rahisi sana mtu mzima mwenye akili zake timamu kugeuka kichaa. Sipati picha katika maisha yangu. Hapana acha nibaki huku huku nina imani nitapata nauli ya kunirudisha nyumbani. Aah nimepakumbuka Baliadi.. " Baada kuwaza na kuwazua hatimaye aliona bora aendelee kufanya kazi hiyo hiyo ya kuzoa takataka japo inavikwazo vingi sana. Pindi hayo yaliyokuwa yakiendelea kwa Nyogoso upande mwingine Mazoea alizidi kukosa amani ndani ya moyo wake. Alijikuta tayari akili yake ikimfikiria mzoa takataka Nyogoso, na mara kwa mara alikuwa akimjengea picha kichwani pindi atakapo mtia kwenye himaya yake na kumsafisha kwa kumvisha nguo za bei ghalama bila kusahau cheni na saa za bei ghali. Mawazo hayo yalimfanya kushusha kuachia tabasamu huku akikutupa kando kitabu alichopenda kujisomea lakini pia akiisogeza mbali kabisa Laptop yake vile vile akidiliki kuvunja ratiba ya kujisomea aidha kulala mapema. Taswira ya Nyogoso ilitawala fikra zake kiasi kwamba Mazoea huyu si yule wa zamaani aliyekuwa hafikirii mapenzi ingawa hakuwachikia wanaume. Moyoni alikosa raha kabisa mwisho aliamua kufunga kwa maombi ili Mungu amsaidie aweze kukutana na kijana huyo aliye uteka moyo wake. Wakati Mazoea akiwa kwenye hali hiyo ya kutamani penzi la Nyogoso, Nyogoso yeye hakujua kama binti yule aliyemsaidia kutoka kwenye mikono ya wale vijana waliokuwa wakimpiga kwa kosa la kutupa takataka hivyo ametokea kumpenda. Na kuhakikisha hilo jambo hatimaye binti huyo alifika eneo lile alilopigiwa Nyogoso. Alipaki gari yake ndani kidogo ya mtaa huo kisha akashuka akazipiga hatua kuingia ndani kabisa. Hatua kadhaa mbele aliona kundi la vijana wakipiga zogo. Mazoea aliwasalimu vijana hao kisha akasema "Kuna mkaka mmoja hivi mzoa takataka huwa anapita hapa?.."

"Yupi huyo dada sababu wazoa takataka wapo wengi sana?.." Aliuliza mmoja ya vijana hao. Mazoea aliposika swali hilo alikaa kimya huku akijaribu kuvuta kumbukumbu muonekano wa Nyogoso. Kwa mbali alinasa kumbukumbu hiyo, hivyo akamuelezea. Ni kijana mmoja tu ndiye aliyemfahambuka kati ya hao aliowakuta ambao walikuwa vijana wasio pungua watano. Punde naye alielezea muonekano zaidi alionao mzoa takataka Nyogoso kitendo ambacho kiliwapelekea na hao wengine kumfahamu. Mazoea alifurahia sana.

"Eenhe vipi ni ndugu yako?.." Aliulizwa Mazoea. Mazoea akacheka cheko la madaha kisha akasema "Ammmh!ndio ni kaka yangu. Kwahiyo nitafurahi sana endapo kama mtanisaidia kumpata vile vile nitawazawadia laki tano.."

"Laki tano?.." Walishtuka vijana hao huku wakitazamana. Mazoea akajibu "Yes ila kwanza chukueni hii Elfu hamsini mgawane hela ya maji,na hii ni namba yangu ya simu mtanitaarifu kitakacho jili"

"Dada kwanza tunashuru sana.. Na kwa dau hili ulilotaja, nakuhakikishia haki ya Mungu huyu mtu tutamtafuta kila konaaaa kudadadeki". Aliongea moja ya vijana hao akionyesha kupagawishwa na zawadi aliyoahidi mrembo Mazoea binti wa kitajiri. Ni maneno ambayo yalimtia matuamini Mazoea, hatimaye aliwaaaga vijana hao kisha akazipiga hatua za malingo kurudi mahali ilipo gari yake. Hakika ni msichana mzuri sana aliyevutia vema machoni,kiasi kwamba hao vijana walimsindikiza kwa macho wakitazama namna alivyojazia nyuma....hakika walibaki midomo wazi. Wanamama wa mtaa huo wa uswahilini hawakusita kumchungulia wakiwa wamesimama kwenye vizingiti vya milango ya nyumba zao huku kila mmoja akizungumza lake ndani ya nafsi yake. "Ahahahah hah.. Aloooooh.." vicheko vya umbea navyo kutoka kwa vibinti vya uswazi vilisikika vyema hakika Mazoea aliacha zahma kubwa mtaa huo.. !





Rasmi Nyogoso anakuwa mzoa takataka ambaye aliweza kujizolea umaarufu mkubwa sana katika mitaa iliyokuwa akipendelea kupita mara kwa mara., sifa ya uaminifu na kumuheshimu kila mja ndio sababu pekee iliyomfanya kujizolea umaarufu huo. Hakuwa mtu wa kuiba kitu chochote kwenye nyumba ya mtu, kigezo ambacho hakikuwepo kwa wazoa takataka wengine ambao wengi wao walisifika kwa wizi. Wakati mzoa takataka akizidi kuwa nguli kwenye kazi yake hiyo ya kuzoa takataka majumbani mwa watu, kwingeneko mrembo Mazoea alizidi kukosa raha, moyo wake ulimpenda vilivyo kijana huyo kiasi kwamba siku mpaka siku alionekana kuwa mnyonge kiasi kwamba wazazi wake wakawa na sitomfahamu juu yake. Asubuhi moja baba Mazoea akimwambia mkewe "Mama Mazoea, hebu kaa na binti yako umuulize anasumbuliwa na nini sababu Mazoea hayupo kama zamani, yaani kabadilika kabisa.."

"Haswaah! Hujakosea mume wangu. Hata mimi naanza kumtilia shaka. Au tayari kaanza kujihusisha kwenye mapenzi?." Alidakika mama Mazoea.

"Mmmh Hapana siwezi kukubalina na hilo" baba Mazoea alikataa.

"Sasa ananini? Kwa sababu kila kitu anapata. Labda ngoja akirudi kutoka chuo nitakaa naye nitamuuliza kipi kinacho msibu. Mtoto mwenyewe mmoja kwahiyo si vizuri kumruhusu ateseke ikingali wazazi wake tupo hai na pesa ipo ya kutosha" Tabasamu bashasha lilionekana usoni mwa baba Mazoea baada kusikia maneno hayo ya mkewe, alinyanyuka kutoka kwenye sofa akamkumatia akambusu. Alipojing'atua kwenye kifua cha mkewe akazipiga hatua kuelekea nje ambako palikuwa na gari aina ya Randcruse, lakini kabla hajaifikia gari hiyo alijipapasa mfukoni akatikisa kichwa na punde akarejea ndani ambapo napo alikutana na mkewe akiwa ameshika funguo ya gari mkononi.

"Mmh leo kweli unaharaka mume wangu" kwa sauti ya mahaba ingali macho akiwa ameyalegeza mama Mazoea alimwambia mumewe. Baba Mazoea akamkonyeza kitendo ambacho kilipelekea wote kujikuta katika jangwa la tabasamu bashasha lililojaa upendo ndani yake hali ambayo iliamsha hisia ndani ya miili yao licha ya kwamba tayari miaka yao imesonga ila bado walionekana kila mmoja kutaka kutaka kukumbushia ufundi wa kucheza katika uwanja mdogo kabisa wa futi tano kwa sita.

"Ahahahah hahaha. Hebu acha utani bwana nipe funguo niondoke" Aliongea baba Mazoea.

"Mmh staki" Alitania mama Mazoea jambo ambalo liliwapekea kukimbizana huku na kule ingwa mwishowe mama Mazoea alimpatia mumewe funguo hiyo ya gari kisha akamuasa kuwa makini barabani.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Usijali mke wangu nitakuwa makini. Na pia usisahau kuzungumza na mwanao" Alijibu baba Mazoea wakati huo akiendesha gari pole pole kutoka ndani ya geti.



*********

Upande mwingine alionekana Nyogoso akiwa amebeba mzigo mkubwa wa takataka began, mzigo ambao ulikuwa ukitiririsha maji machafu yaliyokuwa yakitoa harufu mbaya. Jua kali yapata saa saba mchana Nyogoso alizipiga hatua kuelekea mahali lilipo jalala, jalala lilikuwa mbali sana hivyo ilimlazimu Nyogoso kutua mzigo wake chini ili apumzike kisha ndipo aendelee na safari ya kuelekea jalalani kuzitupa takataka alizopata.

"Daah! Hii tabu mpaka lini? Sasa najuta maamuzi yangu. Ni heri ningemsikiliza mama yangu wala maisha haya yasingekuwa juu yangu..Laah! Ama kweli asuyesikia la mkuu, huvunjika guuu" Akiwa ameshika tama, kijasho chembamba kikimshuka usoni huku nguo alizovaa nazo zikitoa harufu mbaya, alijisemea maneno hayo maneno hayo Nyogoso. Punde akajifuta jasho la mnyonge kwa kutumia shati lake kukuu ambayo kila pande ilichakaa michirizi ya maji machafu. Alishusha pumzi ndefu huku akilini akizidi kujutia kuingia jijini Dar es salaam, jiji lenye kila aina ya maisha,jiji lenye kila aina ya starehe. Jiji ambalo wakuja anaweza kulowea na kujikuta akisahau kijijini alikozaliwa pindi maisha yanapomnyookea. Ila upande wake Nyogoso ikawa ikawa bahati mbaya, alijikuta akiingia katika mazingira ambayo hakuwahi kuyafikiria.

Majuto yakabaki kuwa mjukuu kwa mzoa takataka Nyogoso. Baada kupumzika kwa kitambo hatimaye alisimama akajinyoosha huku akipiga mwayo kisha akainamama chini kuunyanyua mzigo wake wa takataka na kuutupia begani tayari kwa safari ya kuelekea mahali lilipo jalala lakini mzigo huo ulimsumbua sana, alihangaika pasipo kufanikiwa. Mara kadhaa alimponyoka na kuanguka chini.

Wakati Nyogoso alipokuwa alihangaika kujitwisha mzigo wa takataka, kwa mbali alionekana Mzoaea akiwa na jopo la marafiki zake ambapo wote kwa pamoja walionekana kujongea mahali alipo Nyogoso ambaye kwa muda huo bado alikuwa akijitahidi kujitwisha mzigo huo wa takataka. Mazoea na wenzake walikuwa wakipiga zogo huku wakicheka mara kwa mara ingawa gumzo ikiwa ni Mzoaea kutembea kwa miguu kwani ilikuwa nadra sana binti huyo kumuona kupanda daladala aidha kutembea kwa miguu pindi atokapo chuo au kwenye matembezi ya kawaida. Lakini siku hiyo Mazoea alikuwa sambamba na marafiki zake wakitoka chuo kwa kutembea na miguu kuelekea nyumbani huku moyoni akiamini kuwa mbinu hiyo inaweza kumsaidia kumuona mzoa takataka kipenzi cha moyo wake pasipo kujali kazi anayofanya. Hivyo akiwa na marafiki zake walizidi kujongea mpaka mahali aliposimama Nyogoso na mzigo wake wa takataka. Walipomkaribia zaidi marafiki zake Mazoea waliziba pua zao kukwepa harufu mbaya iliyotoka kwenye mzigo wa takataka. Ila hali hiyo ikawa tofauti kwa mrembo Mazoea. Moyo wake ulistuka baada kumuona kwa mara nyingine tena Nyogoso. Mapigo yake ya moyo yakamuenda mbio huku machozi ya furaha yakimtoka katika mboni za macho yake ambayo muda huo yalikuwa yakimtazama Nyogoso mzoa takataka. Marafiki zake walipigwa huku wakishindwa kuelewa kinacho mliza Mazoea ambapo wote kwa pamoja wakatazama na kisha kuishia kuguna.

"Ni macho yangu au ni ndoto?.." Alijiuliza Mazoea ndani ya nafsi yake wakati huo uso wake ukichakazwa na machozi ya furaha..



Machozi ya Mazoea yaliwashangaza sana marafiki zake aliokuwa nao wakati huo, wakishindwa kuelewa ni kipi hasa kinacho mliza Mazoea. Lakini wakati marafiki hao wakiwa na sintofahamu kuhusu mwenzao muda huo Mazoea akamsogelea Nyogoso, alipomkaribia akamsalimu kwa sauti nyororo iliyopenya vema kwenye ngoma ya masikio ya mzoa takataka. Nyogoso alistisha zoezi la kuendelea kuhangaika kujitwisha mzigo wake, kumbukumbu ikamjia akapata kumkumbuka kuwa mrembo huyo aliwahi kumuokoa kwenye sakata lile la kupigwa na vijana wa mjini kwa kosa la kutelekeza mzigo wa takataka kwenye makazi ya watu.

"Habari za siku nyingi.." Aliongea Mazoea kwa tabasamu bashasha huku akijinyoosha nyoosha vidole vyake. Nyogoso alijifuta jasho kisha akaitikia "Salama tu. Vipi hali yako?.."

"Mimi pia mzima" Alijibu Mazoea wakati huo akifikiria mbali, akajihisi tayari mzoa takataka yupo katika himaya yake, jambo ambalo lilimpelekea kujawa na furaha muda wote huku tabasamu nalo likitamalaki kinywani mwake. Ni kitendo ambacho kiliwakera sana marafiki zake ambapo mwishowe waliamua kuondoka wakimuacha Mazoea akiwa sambamba na mzoa takataka,kila mmoja alimshangaa kwa jicho la tatau ilihali wakistaajabishwa na kile kitendo cha Mazoea kububujikwa machozi pindi alipomuona mzoa takataka. Marafiki hao walienda mbali kabisa kwa kumuhisi Mazoea kuwa huwenda kampenda Nyogoso.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Mimi na nadhani itakuwa hivyo, na kama ni kweli basi litakuwa jambo la kushangaza sana. Yani urembo wote ule ampende mzoa takataka, kichaa, teja hohe hahe asiye na mbele wala nyuma?.." Alisema mmoja kati ya marafiki zake Mazoea,muda huo huo mwingine akasikika akisema." Muda utaongea, ngoja tuvute subira tuone kipi kitaendelea.. ".

Wakati marafiki hao wakiendelea kumjadili Mazoea, kwingeneko Mazoea aliishia kumtazama Nyogoso pasipo kuongea nenk lolote. Aliogopa kumtamkia ukweli uliopo ndani ya moyo wake, alijikuta mdomo wake ukiwa mzito kutamka kitendo ambacho kilimfanya Nyogoso kumshangaa na ndipo alipomuliza kipi kinacho msibu "Vipi kunatatizo?.." swali hilo Nyogoso alimuuliza Mazoea kwa taharuki ya hali ya juu.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog