Search This Blog

Tuesday 1 November 2022

KILIO CHA NAFSI - 5

 





    Simulizi : Kilio Cha Nafsi

    Sehemu Ya Tano (5)





    Dereva yule akatoka nje na kumuacha Dk.Samweli akiendelea kumhudumia mama yake ambae alikuwa ameanza kuyafumbua macho yake na kutazama japo kwa shida sana.

    “Sa..Samweliii uliku..uuuwa wapi mwanangu?” aliongea kwa taabu sana mara baada ya kukaa vizuri.

    “Mama mimi nipo usijali tulia kwanza usiwe na wasiwasi,” alisema kwa huzuni sana huku akimyanyua mama yake aliyekuwa amelala chini na kumkalisha huku mgongo akiwa ameugemeza kwenye kocho sebuleni hapo.

    “Samahani Mama naomba unisaidie elfu hamsini.”

    Hakupenda kufanya kitendo hicho ila hakuwa na jinsi maana hakuwa na pesa yeyote na dereva tax alikuwa akisubili pesa yake.

    “Monica kamchukulie kwenye droo ya kitanda chumbani kwangu.”



    Monica msichana wa ndani ambae ndiye alikuwa amemfungulia geti Dk. Samweli alinyanyuka na kuelekea chumbani, dakika tatu alirejea na pesa na kumkabidhi Dk. Samweli aliyezipeka kwa dereva.

    “Hebu nieleze nini kilitoke kwako mara baada ya wewe kuondoka nyumbani?” Mama yake alianzisha mazungumzo mara baada ya Dk. Samweli kurudi.

    “Mama ni habari ndefu sana.”

    “Ipi?”

    Dk. Samweli alimsimulia kila kitu kilichomtokea hali iliyomsikitisha sana Mama yake.

    “Tulikutafuta sana na habari tulizozipata zilikuwa mbaya tulielezwa ulikufa.”

    “Mimi?”

    “ Ndiyo. Taarifa hizo zilipelekea baba yako kupoteza maisha.”

    Dk. Samweli aliumizwa sana na taarifa za kifo cha baba yake alilia sana lakini hakuwa na jinsi na siku iliyofuta aliomba apelekwa sehemu aliyokuwa amezikwa baba yake. Huko nako alizidisha kilio na kuwafanya watu wote waliokuwa eneo hilo nao kulia utadhani ilikuwa siku ya msiba.Moyo wake uliumia sana aliamini bila yeye kuondoka nyumbani hapo kwa muda mrefu baba yake asingeweza kuyapoteza maisha yake.

    “Mama nisamehe sana.”

    “Kwali lipi?”

    “Mimi ndiye chanzo cha kifo cha baba yangu laiti nisingeondoka baba yangu angekuwa hai,”akazungumza huku macho yake yakiendelea kutoa machozi mfano wa mtoto mdogo aliliaye nyonyo kwa mama yake.

    “Hapana sio wewe!”

    “Kumbe nani?”

    “Ni wakati wake ulikuwa umewadia tambua kila nafsi itaonja mauti huna sababu ya kujilaumu, kama kufa angekufa tu hata ungekuwepo na huu sio muda wa kujilaumu yaliyopita si ndwele tungange yajayo,”akamwambia huku akimpiga piga kifua chake kumfariji.

    “Kweli?”

    “Ndio tumuombee tu hicho ndicho cha muhimu sana na si kulia tumia muda wako kumuombea sana baba?”

    “Ahsante mama,”akamkumbatia mama yake kwa hisia ya hali ya juu sana akiwa ameyauma meno yake kwa uchungu.



    Hawakukaa sana makaburini huko dakika arobani na tano zilitosha kwa wao kuwa eneo hilo, wakarejea nyumbani kwao wakiwa na moyo wa maumivu sana lakini hwakuwa na jinsi lililokuwa limetokea halikuweza kubadilishwa.



    “Mama nitaenda kutafuta kazi vyeti vyangu ninavyo yaliyopita yashapita acha nikatafute kazi kesho kama nitaamka salama.”

    “Na kwa ndugu zako hutoenda?”

    “Nitaenda mara baada ya kumaliza mihangaiko yangu maadamu wameshafahamu.”

    Huo ndio uamuzi aliouchukua Dk. Samweli aliamka mapema sana na kuelekea Muhimbili hospitali aliyokuwa akifanyia kazi kabla ya kuondoka, kila mtu aliyekuwa akimfahamu alishanga sana kumuona wengine walitoa machozi ya furaha ya kuungana na rafiki yao.

    “Mbona nafasi yako ipo huna haja ya kuomba kazi tena serikali bado inakutambua wewe kesho njoo kazini?”

    “Kweli Dk. Godfrey?”

    “Ndiyo.”

    “Siami.”

    “Amini.”

    “Vipi Dk. Rose yupo?”

    “Yupo ni mke wa mtu mbona ama ushasahau?.”

    “Aaaah! Basi nilitaka kujua tu kama yupo ni rafiki yangu wa damu tumetoka mbali.”

    “Ni kweli ila uliichezea bahati Dokta.”

    “Hapana sikumpenda na sina haja ya kujilaumu, siangalii ya nyuma naitazama kesho.”

    “Huo ndiyo uwanaume.”



    Ilikuwani furaha sana kwa Dk. Samweli kitendo cha kupata kazi kilimfurahisha sana alifanya kazi kwa bidii sana na kwa kujituma kama zamani, ubize wa kazi ulipelekea kuanza kumsaha Naomi pole pole ila hakutaka tena kuwa na msichana maishani mwake, aliamini siku moja Naomi angerejea na alikuwa tayari kumsamehe kwani alikuwa bado anampenda sana.

    “Dk. Samweli kuna mgonjwa anataka kuonana na wewe?”

    “Mimi?”

    “Ndiyo kwani wewe siyo Dk. Samweli?”

    “Aaaah! Rose ni mimi. Okay naomba umruhusu aingie.”

    “Hawezi kutembea kama hutojali ambatana nami.”

    “Sawa,” alikifunga kitabu alichokuwa akikisoma kisha alivua koti lake la kazi na kuongozana na Dk. Rose.

    “Yule pale kitanda cha mwisho.” Dk.Rose alimuonesha mara baada ya kufika ndani ya chumba alichokuwa amelazwa mgonjwa aliyekuwa akimhitaji Dk.Samweli.

    Alinyosha moja kwa moja hadi kitandani hapo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mmmmh!”Akaguna huku macho yake akiwa ameyatumbua kwa mtu aliyekuwa amelala juu ya kitanda.

    “Nisamehe Samweli na…na..hita…ji.. msamaha… wak..oo..kabla ya..kif..o ch.angu.”Akazungumza mgonjwa huyo ambae alikuwa katika hali mbaya sana huku akibubujikwa na machozi.

    ***







    Zilikuwa ni pesa nyingi sana kwa Naomi alibaki akizitumbulia macho kana kwamba alikuwa bado hajawahi kuziona toka azaliwe, kitendo alichomfanyia Sharifu alikisifia sana. Alianza kuzihesabu taratibu huku akizipanga kwa ustadi wa hali ya juu.

    “Milioni saba kweli huyu alikuwa boya atawezaje kutembea na pesa zote hizi?” Aliwaza peke yake na kunyanyuka alitembea hadi dirishani akalifunga mara baada ya kuhisi alikuwa akitazamwa kisha alizichukua zile pesa na kuzificha chini ya begi lake sura yake ikiwa na tabasamu muda wote.



    “Hapa simtafuti mtu mimi nakula bata simtaki Davis wala Deus waende nina pesa kwanza watanipa nini na isitoshe waume za watu,”akazungumza huku akijitupa juu ya godoro lake na kulala chali mkononi akiwa na simu yake hakuwa na usingizi hata kidogo kazi iliyokuwa mbele yake ilikuwa ni kuperuzi tu ndani ya mtandoa hadi majira ya saa kumi na mbili ndipo alipoamu kujilaza akachukuliwa na usingizi alikuja kushtuka majira ya saa nne asubu tena kwa kugongewa.



    “Nani?”

    “Halima hapa wewe kahaba unalala mpaka mida hii unategemea nani akufanyie usafi.”

    Binti wa mama mwenye nyumba akazungumza kwa nyodo akijitikisa tikisa utadhani alikuwa akizungumza na mtu ana kwa ana.

    “Halima safisha nitakulipa bhana.”

    “Nini unapesa gani wewe hadi unilipe wakati hata kodi yenyewe unahongwa kula kwetu hujielewa amsha mbavu zako na uje utufanyie usafi bibie.”

    “Unataka bei gani,”Naomi akazungumza akiwa bado amejilaza juu ya godoro lake macho akiwa ameyafunga kutokana na usingizi ulikokuwa ukimsumbua sana.

    “Elfu kumi.”

    “Poa safisha nakulipa.”

    “Weeeee! Kazi na dawa oooooh!Mkono kwa mkono.”



    Naomi hakutaka kuzunguza alichokifanya ni kujilazimisha kuamka na kuchomoa noti mbili za elfu kumi kumi na kumtupia Halima mara baada ya kuufungua mlango wake.

    “Mmmh!Wewe! ”Halima akashtushwa sana na kitendo hicho hata kuinama kuziokota zile pesa akashidwa akabaki akimtazama Naomi aliyekuwa amevaa kinguo kifupi sana akiuacha mwili wake ukiwa wazi kwa asilimia kubwa.

    “Hapo unasafisha zamu yangu yote na ole wako uje unisumbue tena nakuzibua,”

    “Walaaaa..shoga-angu.”

    Akaainama haraka- haraka na kuziokota zile pesa kisha akaondoka eneo hilo akiwa anachekelea chekelea kitendo cha kupata elfu ishirini asubuhi hiyo bila hata kufanya kazi kilimfurahisha sana.

    “Hapa naelekea kariakoo nikachukue madela yangu mawili watanikoma mtaani,”akazungumza huku akiendelea kutembea kuelekea ndani kwao, akafika na kupitiliza chumbani kwake alikokwenda kuzihifadhi zile pesa na kutoka nje kwa lengo la kufanya usafi.



    Naomi hakutaka tena kuendelea na kazi yake zaidi ya kutumia pesa kama kawaida japo alikuwa akiumia sana kumkosa Davis mwanaume aliyetokea kumpenda sana lakini hakuwa na jinsi alizidi kujikaza kwa muda wa wiki moja wiki ya pili alimtafuta yeye mwenyewe.

    Mapenzi kama ugonjwa alijikuta akirudiana tena na Davis ambaye alikuwa mume wa mtu walitumia pesa kama watoto wa vigogo huku Davis akitengeneza mazingira ya kumuibia pesa zote. Siku moja Naomi alipokuwa ametoka kidogo Davis alichukua pesa zote na kutokomea.



    “Nini ina..aaamaana pe..pe..pesaa nazo hakuna?”Akazungumza huku akiwa amesimama na mikono yake akiwa imekishikilia kichwa chake mara baada ya kugundua ukosefu wa Davis chumbani humo, pesa nazo hazikuonekana hata senti tano hapo ndipo alipozidi kuchanganyikiwa sana, mapigo ya moyo wake yakaanza kwenda kasi ya ajabu sana taratibu akakaa chini mara baada ya mwili wake kuishiwa nguvu kope zake zikilowa kwa machozi na kilio cha chini chini ikaanza kuchukua nafasi yake.



    “Inamana Davis ananifanyia hivi mimi?....Sasa kosa langu ni lipi daaaah…ila poa cha kuiba hakidumu naye ataibiwa,”akajitahidi kujifariji mwenyewe huku moyoni akidhamiria kumtafuta mwanaume huyo kwa udi na uvumba.

    “Poa niliziiba acha nami niibiwe mimi bado ninalipa nitapata zingine.”

    Jioni hiyo hiyo akatoka na kuelekea kazini kwake kama kawaida huko hakuwa na huruma hata kidogo kila mwanaume aliyejirengesha kazi yake ilikuwa ni kuwaibia tu, roho wa kulipiza kisasi kutokana na kitendo alichofanyiwa na Davis ilikuwa bado ikimsumbua sana, aliwaona wanaume wote sawa na hakuwa na huruma hata kidogo.

    Mwaka wa tatu wa yeye kufanya kazi ya kuuza mwili wake alianza kudhoofika mwili wake ukapungua kwa kiasi kikubwa hata wanaume waliokuwa wakimkibilia siku za nyuma nao wakatoweka, siku zingine alirudi nyumbani kwake akiwa hajabahatisha kupata hata mteja mmoja.

    “Hivi tatizo ni nini?”

    “La nini kwani?” Mwenzake akamuuliza akiwa anakunywa konyangi mara baada ya wao kutoka viwanja.

    “Si… sipati wateja kama zamaini.”

    “Hii! Wewe hata hujioni ulivyoisha shoga-angu kule hakukufai tena wewe badilisha eneo umeharibika sana Naomi huvutii kama zamaini.”

    “Itabidi nifanye hivyo maana duu.”

    “Ndio hivyo mwenzagu upepo unapobadilika nawe lazima ubadilike la sivyo utakula nini itabidi urudi kijijini.”

    “Mimi sina kijijini nikifa nazikwa hapa hapa.”



    Huo ndio uamzi aliouchukua kuazia siku ya pili yake akawa anakwenda sehemu za chini kabisa zile za kusimama barabarani ama eneo la makaburi huko alikuwa akipata wateja wa bei ya chini sana, mwanzo ilikuwa ni ngumu sana kuzoea kiasi kidogo cha pesa.

    “Hivi huku wateja wenyewe ndio hawa?”Akamuuliza msichana mwenzake aliyekuwa amesimama kando kidogo na kuuegemeza mgongo wake kwenye mti.

    “Eeeeh!Tena wa kugombani ukikaa kimya na kujiona mzuri sana hupati mteja tambua biashara mtangazo.”

    “Hilo nalifahamu. Ila nimetatizwa na pesa wanazotoa.”

    “Wewe ulikuwa ukipata bei gani mwenzagu maana unamaswali mfano hakuna.”

    “Laki, elfu 50 na ikiwa ndogo elfu 30.”

    .”Sasa huku buku tano hata mbili bila kusahau pesa ya mlinzi nayo mia tano unabaki na buku nne na nusu kama umelipwa buku tano ukikubali mbili unabaki na buku jero upo?”

    “Mmh!Nimepatikana.”

    “Tena si kidogo,”akamjibu akiwa anamtazama kwa macho ya dharau sana akiwa ameibinua midomo yake iliyokuwa imekolezewa rangi nyekundu na kufanania na mkundu wa nyani.

    Mwilini mwake alivaa viguo vifupi sana kiguo cha juu kilikuwa cha mikono mifupi kikiuruhusu kuuacha mgongo na mabega yake wazi huku shingo akiivalisha cheni kubwa sana, upande wa chini alikuwa amevaa kisketi kifupi kilichokuwa kimechanua kwa chini lakini kiliishia katikati ya mapaja yake na kuyaacha yakiwa wazi kabisa.Chini nako alivaa kiatu kifupi na mguu mmoja alikuwa ameuvalisha kibagili kidogo cha shaba alimarufu kama kikuku.



    Aliendelea kufanya kazi ile kwa muda wa miezi saba hali ikabadilika na akawa akipata homa za mara kwa mara zikawa hazikatiki mwilini mwake, mwanzo hakuijali sana hali hiyo aliendelea na kazi kama kawaida, akiiziba na vodonge mbalimbali na hata muda mwingine alikuwa akibwia dozi za maralia bila kupima lakini homa hizo hazikukata hata kidogo. Udhoofu wa mwili ulipelekea hata huko nako wateja wakawa wanamkimbia kabisa,kwa macho ya kawaida tu Naomi alionekana mgongwa kabisa, siku zinigine akawa haendi kufanya kazi yake hiyo.

    “Sasa Naomi kama hutaki kwenda hospitali naomba utoke chumbani humu tumechoka kuuguza sisi siyo madaktari.”

    “Kwani nani mwenye chumba?”

    “Wewe ila tambua leo ni siku ya sita hujaenda kazini sisi tumekuwa wa kukulisha kukufulia nguo kisa chumba chako kapime yawezekana maralia.”

    “Sina pesa.”

    “Mimi nitakupa na nitakupeleka hata sasa hivi wewe cheki ulivyokonda mwili wote umeota mapele mwenzetu kapime yawezekana miwaya.”

    “Kweli shoga-angu bora uwahi mapema tu.” Aliongea msichana mmoja kati ya watatu waliokuwa wakiishi chumba kimoja na Naomi.Kiasi maneno yao yalianza kumuingia Naomi alijikuta akikubali kupelekwa hospitali na majibu yalipotoka alikuwa ameambukizwa virusi vya ugonjwa wa ukimwi. Alilia sana hakuamini kama kweli daktari aliyekuwa akitegemewa kuwa mkombozi wa watanzani leo alikuwa ameambukizwa virusi hivyo.

    “Sasa unalilia nini? Wewe usikubali kufa peke yako cha msingi ni kuanza kutumia dawa mpema ili ujenge shavu kisha unaingia kazini na ulivyo mzuri lazima utaondoka na wengi.”



    “Hapana niliyofanya yamenitosha acha nife haya ni malipo niyomfanyia Samweli sijui yuko wapi, niliuchezea moyo wake nimemharibia mipango yake,” aliongea huku akizidi kulia kama mtoto mdogo. Majuto ni mjukuu muda huo akaanza kujutia kile alichokuwa amemfanyia mwanaume huyo.



    “Hujui unajiumiza shauri yako sisi tunaenda kazini kama vipi kesho.”

    Marafiki zake waliondoka bila kujali kama rafiki yao mkuwa alikuwa akihitaji ushauri na faraja ya hali ya juu. Wao walichokijali ni upataji wa pesa.

    “Nitaondoka kwenda kumtafuta Dk.Samweli …nitaondoka na nitaondoka liwalo na liwe bado nampenda na hata yeye naamini ananipenda,”akazungumza huku akijitahidi kusimama na kufanikiwa kusimama japo kwa taabu sana akatoka nje na kuelekea bafuni alikooga kisha akarejea ndani kuvaa na baada ya dakika saba akatoka kwa lengo la kwanda kumtafuta Dk.Samweli.







    Ulikuwa ni uamzi wa ajabu sana hata yeye mwenyewe hakuwa na uhakika kama kweli angeweza kuona na mtu huyo na kukubaliwa kile alichokuwa akienda kukizungumza. Hakuwa na uhakika kama Dk.Samweli angekubali kuiona sura yake na kuzungumza naye neno hata moja la karibu.Mawazo mengi yaliendelea kupita ndani ya kichwa chake na kuweka barabara kubwa la maswali ambayo alikuwa akijiuliza yeye mwenyewe na baadhi ya mengine aliweza kuyapatia majibu peke yake lakini mengine hakuweza kuyapatia ufumbuzi wa aina yeyote. Akatoka bafuni akiwa anatetemeka mwili mzima kutokana na baridi kali alilokuwa akilihisi japo hakukuwa na hali ya ubaridi ila yeye mwili wake haukukatika kuvamiwa na baridi kila siku mara baada ya kukwaa maradhi hayo ambayo yalikuwa yakimuumiza sana.



    Mwendo wake ulikuwa wa polepole sana alijikuta akitumia dakika kama saba kuufikia mlango wa chumba chake akaingia kwa kujilazimisha na kukaa kwanza juu ya godoro lake ambalo lilikuwa liko chini kabisa, akili yake ikamtuma kuitafuta albamu yake akajitahidi kunyanyuka na kujivuta hadi kunako begi lake aina ya Omega akalifungua na kuupeleka mkono wake chini kabisa alipoutoa akatoka na albamu hiyo.

    “Mmmmh!”Akashusha pumzi ndefu na yenye maumivi ndani yake kumbukumbu ya siku aliyonunuliwa hiyo albamu ikapita ndani ya kichwa chake akamuona jinsi Dk. Samweli alipomletea akiwa ameifunga ndani ya kiboksi kidogo huku pembeni yake kukiwa na kiboksi kingine kilichokuwa na pete ndani yake.

    “Naomi leo nataka nikufanyie kitu ambacho hutakuja kukisahamu maishani mwako.”

    “Kipi hicho baby,”akazungumza huku akisimama eneo alilokuwa amekaa na kutembea kueleka usawa aliokuwa amesimama Dk.Samweli akiwa na zawaidi yake mkononi akafika na kumkumbatia kisha akamshushia mvua ya mabusu usoni mwake bila kujali macho ya wazazi wa Samweli ambao walikuwa sebuleni hapo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Yatosha mpenzi…yatosha mama punguza mashamsham,”akazungumza huku akimtoa Naomi mwilini mwake na kumuongoza hadi kwenye kochi akamkalisha na yeye akapiga magoti mbele yake kisha akalifungua lile boksi na kuitoa pete, akauchuka mkono wa Naomi na kidole chake cha kati akakivisha pete hiyo ambayo ilikuwa ya madini aina ya dhahabu kabla ya kuubusu.

    “Leo umekuwa mchumba wangu rasimi naomba uutunze uchumba huo siku zako zote,”akazungumza huku akikumbatia na wazazi wake wakapiga makofi kufurahia kitendo alichokifanya kijana wao.Wote wakitoa machozi ya furaha.

    “Nitakupenda sana na milele yot…..,”alipofika hapo akashindwa kuvumilia akajikuta akilia sana huku akiwa ameikubatia ile albamu akiiomba msamaha kana kwamba ile ndo alikuwa Dk.Samweli.

    ****



    Yalikuwa ni maumivu makali sana ambayo hakuwahi kuyasikia siku zote taswila ya mambo yote waliyofanya siku hiyo ikarejea upya akamuona Dk.Samweli akimtania na kumchekelea akimbeba juu juu na kumbwaga kitandani kabla ya kumlalia akimuahidi mambo mengi sana na yenye tumaini ndani. Ooooh!Akajiona mjinga sana na mkosefu chini ya jua na hadi juu ya jua.

    “Kw…a..kwaa.kaaaa.waakwwwwaaawema wo..teeee huo..nimemfanyia hivi ..da..daaaaa,”akazugumza huku akilia sana na kamasi nyepesi nyepesi zikichuruzika ndani ya vitundu vyake vya pua. Hata hamu ya kuifungua ile albam ikapotea kabisa ikabidi alirudishe pahala pake na kusimama kisha akatafuta nguo aliyoona inafaa kuusitri mwili wake, akaivaa na kutoka ndani ya chumba chake akiwa na dhamira madhubuti ya kumpata Dk.Samweli popote pale yeye alichota kutoka kwake ni kumuomba msamaha japo hakuamini kama angeweza kusamehewa ila alijipa tumanini yeye mwenye.



    “Nitaondoka kwenda kumtafuta Dk.Samweli …nitaondoka na nitaondoka liwalo na liwe bado nampenda na hata yeye naamini ananipenda,” akazidi kuzungumza peke yake huku akizidi kutembea kueleka kitua cha daladala cha majimatitu.

    Dakika kadhaa akawa amefika eneo hilo na bahati ikawa yake akalikuta daladala likiwa halijajaza akajitoma ndani na kutulia siti ya nyuma kabisa akiwa kimya. Njia nzima alikuwa akimsihi Mungu wake kutenda miujiza huko alikokuwa akienda, muda mwingine alikuwa akikata tamaa mwenyewe na kujiona kama asingeweza kusamehewa na mwanaume huyo.



    Masaa mawili ndiyo aliyotumia kufika bunju akashuka na kuanza kutembea taratibu kuelekea nyumbani kwa akina Samweli, kadiri alivyokuwa akitetemba ndivyo mapigo ya moyo wake yalivyozidi kuongezeka, macho yake yalipoliona geti la nyumba ile ndivyo alivyozidi kuogopa zaidi.

    “Au niache tu,”akawaza peke yake akiwa amesimama mita chake kufika getini hapo.

    “Aaaah!Maji nishavulia nguo lazima niyaoge nahitaji msamaha kabla ya kifo changu nafahamu nitakufa tena kwa muda mfupi sana,”akayapuuzia mawazo yake na kuanza kutembea tena.Akafika na kugonga geti kisha akasubili kama dakika tano akagonga tena na tena lakini hakupata msaada wowote.

    “Ama nimekosea nini?”Akajiuliza huku akirudi nyuma kidogo ili kuichunguza nyumba hiyo.

    “Lakini ni hapa hapa hata sijakosea nii,”akajikuta akinyamaza mara baada ya geti kufunguliwa kwa nguvu na msichana mwembamba akasimama mlangoni hapo akimtazama kwa macho makali sana na yenye kuuliza unafanya nini hapo.

    “Nikusaidie nini?”

    “Habari yako dada?”Akamsalimia kwa unyenyekevu huku akitembea kumfuata mlangoni hapo.

    “Habari yangu wewe haikuhusu sema shida yako haraka nina kazi za kufanya,”Monica kama kawaida yake akamfyatulia maneno bila kuyachuja na kuyapima uzito wake.

    “Okay namuuliza Dk.Samweli.”

    “Wa nini?”

    “Nina shida naye.”

    “Haishi hapa umekosea nyumba uwe na jioni njema,”akasema huku akilifunga geti lakini Naomi akawa amewahi na kulizuia.

    “Sikia naomba unisikilize mimi ni rafiki yake wa miaka mingi sana nataka kuonana naye.”

    “Nimekwambia hayupo,”akamjibu huku akimsukuma na kulifunga geti kisha karudi ndani akimuacha Naomi nje akiwa amedondoka na kuumia mguu wake wa kulia.



    Alijisikia vibaya sana akabaki eneo hilo akilia polepole kisha akajikokota na kurudi kwake akiwa amepondeka pondeka moyo wake na kulani mtu aliyemuingiza katika kazi ya ukahaba, lawama zote akamtupia Stella.



    Siku zikazidi kukatika huku akiendela kuumia kwa mawazo na kila sika akazidi kukonda na kutisha kwa asilimia mia.

    “Ila wewe Naomi mbona unatumiza vichwa vyetu?”

    “Eti ujue hata mimi nilikuwa na mawazo kama yako umeniwahi tu shoga-agu,”mwenzake akadakia aliyekuwa akiutazama uso wake na kipande cha kioo ambacho alikuwa amekishikiria mkono wake wa kushoto huku mkono mwingine ukiwa unaubinya binya uso wake kuviondoa vipele vidogo dogo ambavyo vilikuwa vimetapaka usoni mwake majira ya saa saba mchana mara baada ya wao kumaliza kupata chakula cha mchana.

    “Kawanini?”Akawauliza kwa sauti ya chini kabisa tena ikiwa inatoka kwa wasiwasi.

    “Wewe huioni hali yako?Shoga tunaogopa kufiwa humu ndani tumekuambia utumie dawa hutaki ona unavyotisha Naomi mpenzi,”akasema akiwa anamtazama machoni mwake na kuikatisha kazi yake ya upangaji wa nguo ndani ya begi lake dogo.

    “Kwani nikianza kutumia dawa naweza pona kweli?”

    “Ndio unachotakiwa wewe ni kwenda hospitali huko utapata maelezo ya kila kitu sio kulala na kula, kitanda siyo dawa Naomi naumia sana,” Noela kati ya wasichana waliokuwa wakifanya kazi haramu ya kuuza mwili akamweleza moyoni akiwa anaumizwa na hali ya Naomi. Na ni huyo huyo aliyejitolea kumpeleka Naomi kucheki afya yake.

    “Kweli?”

    “Ndio unapona kabisa kama uko tayari mimi nitakupeleka kesho omba Mungu leo nikapate pesa nyingi kesho asubuhi tu tunaondoka.”

    “Nitashukuru sana na iwe hivyo,”akamshukuru mwenzake akinyosha mkono lakini Noel hakuupokea akaendelea na kazi yake.

    Noela hakuwa kama wenzake wawili alijaliwa moyo wa huruma sana kwa kila mtu hakuwa radhi kumuacha Naomi ashinde njaa hata siku moja wema aliowahi kumfanyia kipindi cha nyuma ulizidi kuishi ndani ya akili yake.Kile kidogo alichokuwa akikipata alikuwa radhi kugawana naye, alijitahidi kumtunza kwa pesa zake alizokuwa akizipata, alimununua chakula cha kuisaidia afya yake na kata kumfulia nguo.



    Kuanzia hapo akili yake ikafokasi namna ya kuzipata pesa za kumsaidia rafiki yake akanza kuwaza ni wapi angeanzia ila kajipa tumaini la kufanikiwa.

    “Hapana natakiwa nilipe fadhira kwa wema alionifanyia asingekuwa yeye nadhani ningekuwa nimeshakufa?”Akawaza ndani ya akili yake huku akianza kuukumbuka wema aliofanyiwa na Naomi.



    ****



    Ulikuwa ni usiku wa saa nane na dakika kumi na saba siku ya ijumaa siku mabayo mwanzo wa mapumziko ama kwa jina maarufu hufahamika kama mwanzo wa weekend. Siku hiyo ilikuwa ya shangwe sana ndani ya jiji la Dar es salaam, toka siku ya jumatatu wakazi wa mji huo wapenda muziki walikuwa wakiisubili siku hiyo kwa hamu ya hali ya juu sana.

    Kila sehemu iliyokuwa na kikundi cha watu mazungumzo yake yalikuwa juu ya siku huyo, neno Fiesta halikukatika midomoni mwao utadhani lilikuwa mswaki kwao. Siku hizo pia wafanyabiashara wa nguo waliweza kuuza sana kwani vijana wapenda kwenda na wakati hawakuwa nyuma kulandalanda madukani kutafuta mavazi nadhifu yatakayoendana na usiku huo wa Fiesta ambao waliupachika jina la Night shangwe Fiesta.



    Amsha amsha hiyo ilikuwa kichukua nafasi ndani ya Club ya Dar live, club maarufu sana ndani ya jiji hilo hakuna mkazi yeyote asiyeifahamu club hiyo ambayo iko maneno ya mbagala Zakhemu karibu kabisa na benki ya Nmb tawi la Temeke.



    Amsha amsha hiyo ilianza kuchukua nafasi kuazia majira ya saa kumi na mbili ambapo madijei machachari katika kucharaza nyaya za miziki hawakuwa nyuma kuzikonga nyoyo za wahudhuliaji waliokuwa wamejitokeza eneo hilo.

    Wasani wachanga nao walipewa nafasi ya kuonyesha makali yao na kuufanya usiku huo kuwa shangwe ya aina yake.Miongoni mwa wasanii hoa alikuwepo Pablo na Molto ambao walikuwa wakitisha na ngoma zao mpya kabisa masikioni mwa vijana wengi kila mtu alitamani kuwaona vijana hao.

    “Mmmh huyo nani kweli?”Noela akamuuliza mmoja wa kijana aliyekuwa amesimama karibu yake.

    “Pablo huyo mwanangu sana kitambo namkubali kinyama Diamond analala kwa dogo,”akamjibu huku akimpamba Pablo kwa maneno yenye asali ndani yake.

    “Wapi hafiki kwa Molito yule babu kubwa kwanza anafahamu kile anachokifanya.”Wakazidi kubishana bishana kama dakika mbili kisha Noela akatoka enoe hilo na kusogea pembeni lakini akajikuta akikutana na mtu aliyekuwa hatazamii kutana naye kabisa, akachanganyikiwa na kuanza kuondoka lakini haikuwa bahati yake akaungukia mikononi mwa mtu huyo na kulamba ngumi ya pua kabla ya kudondoka.



    Macho yake hayakuamini kama kweli yalikuwa yamemuona mtu huyo ambaye hakutengemea kumuona maishani mwake, akajihisi labda alikuwa ameona vibaya lakini haikuwa hivyo kwani hata alipojaribu kuyapikicha macho yake ukweli ukabaki ni ule ule kuwa hayakumdanganya. Akabaki amepigwa bubuwazi kama sekunde arobani na tano akimtazama mtu huyo ambaye naye alikuwa akimtazama kwa macho makali sana. Sekunde ya hamsini na mbili Noela akageuka haraka sana kwa lengo la kukimbia lakini akajikuta akiangukia mikononi mwa mtu huyo ambaye alikuwa na mikono mikubwa na yenye nguvu za ajabu kupita maelezo.



    Naiach…”

    Hakuimalizia sentensi yake uso wake ukapokea ngumi ya ajabu sana iliyomfanya kuhisi kizunguzungu na idadi kadhaa ya nyota mbele ya macho yake akaweweseka na kumpalamia mmoja wa vijana waliokuwa eneo hilo lakini naye akamrudisha kwa mtu huyo.

    “Ulijua sitakukamata?”Akazugumza kwa kitetemeshi cha hali ya juu mwili wake wote ukitetemeka kwa hasira za ajabu hata waliokuwa eneo hili wakamshanga.

    “Nisa..aa…mehee ..tafadhuliii,” akazugumza kwa taabu tena kwa kuyaharibu maneno yake mara baada ya mdomo wake kutwangwa ngumi kali sana iliyopelekea jino lake moja kung’oka papo hapo na kudondoka chini.

    “Utanitambua na utanitambua leo zako malaya mkubwa wewe,”akasema huku akianza kumvuta kumtoa na kutoka nje ya club hiyo hakuna mtu aliyejali ugomvi huo kila mtu alikuwa na yake.



    “Nisa..samehee tafadhali Juma ni shetani tu alinipitia nisamehe mpenzi wangu,”Noela akazidi kujitetea lakini maneno yake hayakumuingia hata kidogo mwanamume huyo yeye alichokuwa akikijali ni kulipiza kisasi kwa ubaya aliokuwa amewahi kumfanyia siku za nyuma.

    “Kwanini ulifaanyia hivyo wewe kahaba?”

    “Ha..ahapana niini….,”Maneno yake yakazuiwa na makofi makali ya mgongoni kwake n a kuvitiwa ndani ya gari aina ya Noah akiwa amefungwa kitambaa machoni gari hilo likatoka eneo hilo kwa mwendo wa kasi sana. Njia nzima Noela alikuwa akilia sana na kumuomba msamaha mwanaume huyo lakini haikusaidia chochote.

    “Nifungue macho tafadhi kwanini unanitesa hivyo.”

    “Wewe ulivyonifanyia ulifikiria nini yaani sina msamaha hata kidogo pumua pumzi zako za mwisho na usali sala zako pia huna muda mrefu wa kuendelea kuishi dunia, kila kitu unachokifanya ni cha mwisho kabisa,”akazidi kuzungumza huku akiendelea kuliendesha gari hilo kuelekea Kongowe sehemu aliyokuwa na shamaba lake kubwa la mazo mbalimabali.

    “Honey umeona hilo gari?”

    “Lipi?”

    “Si hiyo Noah nyeusi,”Naomi akazungumza huku aliisonta gari hiyo iliyowapita kwa kasi ya ajabu mita chache mara baada ya kuwapita kwa kasi ya ajabu sana hata Naomi akaogopa yeye mwenyewe japo hakufahamu gari hilo lilikuwa na nini ndani yake lakini moyo wake ulijawa na wasiwasi.

    “Tulifatile,”akazungumza huku akimzuia Davis kutembea mara baada ya kusimama mbele yake.

    “Unamfahamu Naomi?”

    “Hapana ila nahisi kama kunakibaya kinaenda kufanyika tambua huku ni porini na ni nadra sana kupita magari usiku huu hilo gari linaenda wapi, kuna siku mwenzetu alikutwa ameuawa na watu wasiojulika huku huku porini hapana mimi nalifutilia hakuna usalama kabisa,”akazungumza kwa hisia za hali ya juu kabia na kuanza kuondoka eneo hilo akikimbia kimbia na kufanya kisketi chake kifupi kipande juu.

    “Poa wewe nenda lolote litakalokupata kivyo.”

    “Poa wewe huna hata roho wa huruma kumbe mbaya sana.”

    “Mia,”akamjibu na kuendelea na safari yake bila kufikiria kama Naomi angeenda kupata matatizo huko alikokuwa akienda.

    Naomi hakutaka kurudi nyuma moyo wake ulimwambia kuwa kulikuwa na tukio baya ndani ya gari hilo.kumbukumbu ya mwanamke mwenzao aliyekuwa akifanya kazi za kuuza mwili kama yeye aliyekutwa ameuwa huku ilikuwa bado ikiendelea kuisumbua akili yake.

    “Hakuna usalama kabisa na lazima gari hilo linaenda kwenye lile shamba sasa cha kufanya napita njia hii ya mkato.”

    Hakuta kupoteza muda akakatisha njia ya mkato na njia iliyokuwa nyepesi sana dakika kumi akawa amefika sehemu hilo.

    “Si nimesema lazima kuna kibaya Munguuuuu daaaaa!” Akazungumza kimoyo moyo mara baada ya macho yake kushuhudia mwanaume huyo akimsurubu Noela kwa vipigo vya mbwa mwizi na kumrushia maneno makali sana na ya lawama ya hali ya juu.

    “Sasa nakuchoma moto kabisa acha nikupeleke huku,”akamwambia huku akianza kumvuta kichwa chini miguu juu kuelekea upande uliokuwa na vichaka vingi sana na huko huko ndiko Noami alikuwa amejificha,hatua kama tano za kumfikia Naomi ndipo alipomtupia Noela.

    “Kaa hapo nikalete petrol leo zako wewe si uliniacha hai sasa kibao kimekugeukia,”akazungumza huku akimpiga teke la mbavu teke ambalo halikumfanya Noela kushtua wala kijitikisa tayari alikuwa ameshapoteza fahamu muda mfupi kabla ya kutupiwa eneo hilo.Maneno haya yakamuuma sana Naomi na kuanza kutetemeka mwili mzima.



    “Hapana natakiwa kumsaidia huyu ni binadamu mwenzangu noooo!”Akawaza na kuanza kuny’ata kwa tahadhali kuelekea eneo hilo, akafika na kumnyanyua juu juu kisha akaanza kutokomea naye akiwa anatetemeka sana tetemeko la hofu ya kukamatwa hakufahamu kama angeweza kumkwepa mwanaume huyo ambae alionekana kuwa na roho ya kikatiri sana kwa Noela, alikimbia kama mita kumi tu akawa amechoka sana na kulemewa na uzito wa mtu huyo ikabidi amshushe taratibu na kumlaza. Akatumia mafunzo mafupi aliyokuwa ameyapata kule chuo ya kumuhudumia mtu aliyekuwa amepoteza fahamu alichokifanya ni kumfungua mdomo wake akawa nampulizia pumzi huku mkono wake wa kulia akikikandamiza kifua chake taratibu bila kuyajali maneno ya mwanaume aliyekuwa akiyafyatua mara baada ya kumkosa Noela eneo alilomuacha.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Dakika kumi na tano za yeye kumpatia huduma hiyo Noela alikohoa hapo ndipo Naomi alipozidi kupata nguvu za kuendelea kumsaidia.

    “Poa nitakukamata tu nafahamu hujafa ila siku nyingine hutopona,”akayasikia maneno ya mwanaume huyo na dakika mbili akaona mwanga wa taa za gari likiondoka akashuska pumzi ndefu na kujiona mshindi wa ajabu sana.

    Macho yake hayakuwa nyuma kumtazama Noela kila sekunde alitamani afumbue macho ili aweze kumuona lakini haikuwa hivyo Noela aliendelea kuyafumba macho yake na kufanania na mtu aliyekuwa amelala.

    “Mungu ahsante hapa nimeponesha sasa nitamtoa je huku na usiku nao unazidi kuingia,”akazungumza peke yake akiwa amesimama wima na mikono yake ikiwa imekishika kiuno akitafakuri namna ya kutoka eneo hilo.

    “Hapa nambemba hadi barabarani nikifika huko natafahamu cha kufanya.”

    Hivyo ndivyo ilivyokuwa akamnayua juu juu japo kwa shida sana maana Noela alikuwa mnene zaidi yake lakini ajikuta akiweza kumbeba kitu ambacho hata yeye mwenyewe alikuwa akikishangaa sana, uwepo wa giza tororo shambani humu nao ulichangia kwa kiasi kikubwa Naomi kumuokoa Noela kila mita kadhaa alikuwa akimtua na kupumzika kisha anamnyanyua na kuendelea na safari dakika arobani na tisa ndizo alizoweza kufika eneo lililokuwa na wapita njia wengi sana.



    “Dada unaenda?”Mmoja wa vijana waliokuwa wamekaa juu ya pikipiki akasema mara baada ya kumuona Naomi akitembea kwa haraka sana kuwafuata eneo hilo.

    “Ndio naomba unifuate huku.”

    Kijana huyo akawasha pikipiki yake na kuigeuza kuelekea upande aliokuwa akielekea Naomi mita kadhaa akasimamisha pikipiki yake na kutembea hadi eneo alilokuwa amesimama Naomi.

    “Vipi huyu?”Akamuuliza kwa mshangao wa hali ya juu mara baada ya kumuoana Noela akiwa ametapakaa uchafu mwili mzima na kingine kilichomshtua ni mavazi yao.

    “Hana tatizo naomba tumpakie.”

    “Lakini..lakini hii hatari huyu mtu mzima kweli?”

    “Ndio.Umeambiwa kafa acha uchoro basi.”

    “Poa unaelekea wapi na una bei gani?”

    “Majimatitu na elfu kumi.”

    “Mmmmh!Elf kumi wewe siwezi tambua hapa nabeba kesi akinifia njiani bila elfu thelathini siendi.”

    “Kakaaa!Mbona huna huruma oky nakupa ishirini.”

    “Ongeza elfu tano.”

    Naomi akajifikiriaa kama dakika kadhaa kila akakubaliana na kijana huyo.Wote kwa pamoja wakasaidizana kumnyanya kutoka eneo alilokuwa amelala na kumpakiza juu ya pikipiki katika yao na safari ikaanza.

    Siku ya pili yake majira ya saa nne asubuhi Noela alishtuka na kujikuta akiwa amelala juu ya kitanda huku baadhi ya sehemu zake za mwili zikiwa zimefungwa bandeji, kwanza aliwaza sana ni kwa namna gani aliweza kufika eneo hilo lakini kabla ya kupata jawabu sahihi mlango ulifunguliwa na Naomi akaingia akiwa na mfuko mkononi.

    “Wao umeamka bora nilikuwa nawaza sana unajisikia?” Akamuuliza akiwa anakaa pembeni yake uso wake wote ukipabwa na sura ya furaha sana.

    “Viz..,”akashindwa kuzungumza vizuri mara baada ya mdomo wake kuhisi maumivu makali sana ambayo hakufahamu yalikotokea.

    “Pole tulia kwanza na ondoa hofu mamy kila kitu kipo sawa pumzika kwa amani,”akamwambia na kumuacha apumzike ndani ya siku tano hali ya Noela ilitegemaa na siku hiyo ndipo alipoamua kumsimulia Naomi kisa cha yeye kutekwa na mwanaume huyo.



    ***



    Naomi alikuwa na shauku ya hali ya juu sana kufahamu ni kipi kilikuwa kimemtokea Noela mpaka akajikuta anaingia katika hatali ya kutaka kuyapoteza maisha yake.



    “Usijali mama yangu je unaweza kunieleza kipi kilisababisha yule mwanaume akakufanyia ubaya ule je unamfahamu?”Naomi akamuliza huku akiketi pembeni yake mkono wake wa kushoto akiwa ameshikilia kikombe cha plastiki mara baada ya kumaliza kumpatia uji Noela na kumkalisha juu ya kitanda mgongo akiwa ameuegemeza ukutani majira ya saa tano asubuhi.

    “Ndio namfahamu kwani ulimuona?”

    “Hapana Noela sikuiona sura yake ilikuwa usiku sana.”

    “Kwani wewe ulikuwa unatoka wapi majira hayo mpaka ukatuona samahani kwa swali lakini,”akazungumza huku akimtazama usoni kwa macho ya kutaka kufahamu kabisa.

    “Noela siku hiyo si unakumbuka ilikuwa Fiesta?”

    “Ndio.”

    “Sasa mchana yake tulikuwa pwani na shemji lako jioni yake tukaja na gari na bahati mbaya gari likaharibika hivyo watu wote ikatulazimu kutembea kwa miguu, na njiani majira ya saa mbili ndo gari hilo likatupita kwa kasi ya ajabu hata sijui kwanini moyo ulinituma kulifuatilia nilijikuta tu nafanya hivyo.”

    “Mmmmh!Mwanamke jasiri sana wewe sijui nitakulipa nini.”

    “Usiwaze mpenzi leo kwako kesho kwangu ondoa hofu.”

    “Na hizi huduma nani alinisaidia? Ulinipeleka hospitali?”

    “Mimi mwenyewe dokta nimekuhudumia na nimeuza kitanda changu nadhani jioni kitachuliwa na mwenyewe.”

    “Weweeee!”Noela akashangazwa sana na maneno ya Naomi bila kusahau matendo yake.

    “Usikonde.”

    “Acha nikwambie mama yangu yule mwanaume anaitwa Juma aliwahi kuwa bwana angu kwa muda mrefu sana siku moja nilimfanyia mbaya mara baada ya yeye kunisaliti na kutembea na mdogo wangu wa damu nilipanga mpango kwa kumvamia nyumbani kwake na kumpola kila kitu kisha nikampiga na risasi ya kifua nikidhani alikufa kumbe alipona,”akatoa maelezo huku uso wake akiwa ameuinamisha na kuitazama sakafu kwa aibu ya hali ya juu.

    “Wewe Noela!”

    “Ndo hivyo Naomi huo ndo ukweli ndo maana alikuwa na hasira sana na mimi na hasira yake bado inaishi milele.”

    “Pole sana.”

    Wakayamaliza mazungumzo yao yaliyokuwa mafupi kupita kiasi kwa kumbatiana na kuahidia kusaidizana kwa kila kitu.

    Noela akashusha pumzi ndefu mara baada ya kutoka katika kumbukumbu hiyo na kuigeuza shingo yake kuelekea upande aliokuwa amelala Naomi akiugulia kwa maumivu makali sana, akamtazama kwa dakika mbili kisha akajifuta macho yake mara baada ya kutokwa na machozi.

    “Nitakusaidia Naomi,”akazungumza ndani ya nafsi yake na kuimalizia kazi yake ya upangaji wa nguo,kisha akatoka nje kwa lengo la kujiandaa kwa ajili ya kwenda kazini japo siku zote haikuwa kawaida yake kuondoka mapema nyumbani lakini siku hiyo akili yake ilikuwa imevurugwa kwa asilimia mia, hakupenda kumuona Naomi akipoteza maisha yake wakati uwezo wa kumsaidia alikuwa nao.

    “Kama aliweza kuuza kitanda chake kwa ajili yangu mimi na kukubali kuishi na mimi hata akaninunulia hili jino mimi ndo nishindwe kulipa fadhira? Nitakuwa mjing sana, “ akaendelea kuwaza peke yake na hata muda mwingine alikuwa akizungumza peke yake mfano wa mtu aliyekuwa amechanganyikiwa.



    Alichofanya siku hiyo ni kutumia akili zaidi ya siku zingine ili tu aweze kupata pesa za kumsaidia rafiki yake Naomi.Alikuwa tayari kutapeli na hata kuwaibia wasichana wenzake pesa na simu zao, siku hiyo ilikuwa vurugu sana sehemu aliyokuwa akijitafutia ridhiki hakukubali kutoka na pesa kidogo alihakikisha anakamilisha malengo yake aliyokuwa amejiwekea kichawani mwake.

    “Naomi !Naomi amka uone,”akamuita Naomi mara mbili mara baada ya kurejea kutoka kazini kwake majira ya saa kumi usiku.

    “Ku..na …nini?”

    “Amkaa mpenzi amkaaa kitu hiki hapa mbona umepona labda ukatae wewe kwenda hospitali,” akazungumza huku akimtupia noti nyingi sana za elfu kumi kumi juu ya kifua chake, kifua alichokuwa amekilaza chali na macho yake kulitazama dari, kwa kujikakamu sana Naomi kajitahidi kuamka na kukaa juu ya godoro hilo mwili wote ukiwa unamtetemeka kwa baridi la usiku huo.

    “Naomi unapona mpenzi na hakuna atakayeamini kama wewe ndiye ulikuwa na umekondeana na kuwa mfupa hata hao wanaokusema watakukoma hizi zote zako Naomi.”

    “Wewe umetoa wapi pesa hizo?”

    “Ilikuwa lazima nipate Naomi siwezi kesho asubuhi hospitali nakupeleka,”akamwambia huku akimsaidia kukaa vizuri kwa kumuwekea mto nyuma ya mgongo wake.

    “Ahsante sana Noela sijui cha kukulipa mpenzi wangu.”

    “Mie ndo natakiwa kukushukuru vipi kahaba mwenzetu kesharudi?”

    “Hata sifahamu sijamsikia tokea saa moja nilipolala sijashtuka itakuwa bado hajarudi.”

    “Mmmmh!Kina roho mbaya sana kile sikipendi kichoyo na kibinafsi hakifai.”

    “Aaaah!Noela usiwe na roho hivyo achana naye hakulishi nakushukuru sana.”

    “Poa mamy acha nikusaidie kukulaza mimi naenda kuoga kwanza,”

    “Haya.”



    Majira ya saa kumi na mbili na dakaka saba Naomi na Noela walikuwa ndani ya daladala la kuelekea mbagala rangi tatu ambalo lilikuwa likifanya safari zake kati ya Chamanzi na mbagala baada ya kufika mbagala wakawa webadili na kupanda la kuelekea Tandika wakiwa na lengo la kuishia ndani na hospitali ya wilaya ya Temeke.



    “Hapo sawa sasa mbona umepona mama.”

    “Aise kweli Noela! Nikipona nitafurahi sana,”akamjibu huku akikanyanga ngazi ya kwanza ya kuingia ndani ya hospitali hiyo walifika mapokezi na kujiandisha kisha wakapewa utaratibu na kusubili kuonana na dokta.



    “Kwanini unataka kuanza kutumia dawa za Arv nani kakwambia?”Dk.Husein akamuliza mara baada ya wao kuingia ndani ya chumba hicho na kutoa maelezo.

    “Ndio kinga za mwili wangu ziko chini sana.”

    “Umejuaje?”

    “Nishawahi kupima dokta na seli ziko chini sana.”

    “Ziko ngapi kama kweli unafahamu.”

    “Nina CD4 250 ambazo ni lazima nianze kutumia dawa,”Naomi akamjibu kwa kujiamini huku akimkazia macho ya kumwambia naomba unipe dawa hizo mara moja ungefahamu ninavyoumia hata usingenichelewesha.



    Dk.Husein akamtazama Naomi kwanza kabla ya kumwabia chochote na kukitikisa kichwa chake.

    “Okay nani atakayekusimamia kipindi unaanza dozi ya Arv?”

    “Mimi hapa Dokta,”Noela akajibu haraka haraka kana kwamba yeye ndiye alikuwa mgonjwa ama aliulizwa yeye mwenyewe.

    “Haina shida ni kweli unatakiwa uanze dawa haraka iwezekanavyo maana hata majibu yangu yameonyesha hivyo ila huna CD4 250 ziko kama 310 ambazo sio mbaya sana ukizingatia dawa utaishi muda mrefu sana, unachotakiwa ni kuzingatia dozi na kuitumia katika muda sahihi jitahidi kula na kushiba kabla ya kumeza dawa punguza mawazo yasiyo na ulazima kazi ngumu za kutumia nguvu na kede wa kede natumai utazingatia.”

    “Ndio dokta,” Naomi akaitikia huku macho yake yakilengwa lengwa na machozi moyo wake ulimuuma sana kuyasikia maneno hayo alitamani angekuwa yeye ndiye daktari.

    “Sina wa kumlaumi najilaumu mimi mwenyewe,”akawaza na kuyafuta machozi yaliyokuwa yakiyalowanisha mashavu yake.



    Hivyo ndivyo ilivyokuwa Naomi akawa ameannza kupata matibabu ya Arv yanayofahamika kwa jila la kitalamu kama Antiretroviral Therapy. Miezi mitatau ya yeye kutumia dawa hizo mwili wake ulianza kubadilika na kunenepa kama mwanzo hata akawa na nguvu za kufanya kazi zake yeye mwenyewe akawa na uwezo wa kutembea na kufanya mazoezi kama mwanzo.

    “Shoga ona ulivyonawili sasa hivi hata siamini kama ni wewe.”

    “Umeona hata siamini kama ni mimi daaah! Nilikuwa nimekata tama kabisa,”akamjibu Naomi.

    “Hata usikate tamaa ushapona mimi nipo nitakuwa na wewe bega kwa bega hadi mwisho wako ama wangu.”

    “Ahsante sana,”akamshukuru huku akitandaza mikono yake na kumkubatia Noela kwa nguvu zake zote moyoni akiwa na furaha ya ajabu sana.

    “Sasa best mimi najiachia kazini kama vipi saa kumi usitoke.”



    “Sitoki wangu.”

    “Poa.”

    Wakaangana na Noela akaelekea viwanja huku nyuma Naomi akabaki peke yake ndani ya chumba chake kwani hata yule msichana mwanzao naye alikuwa ameshaondoka. Siku hiyo hakupika zaidi ya kununua chipsi na kula kisha akajitupia kitandani kulala majira saa nane usiku ghafla akasikia mtu akigonga mlango kwa funjo huku akipiga kelele za ajabu kitendo kilichomshtua san Naomi.

    “Nani wewe?”Akaiuliza ile sauti huku moyo wake ukienda kwa kasi ya ajabu.

    “Fungua… fungua… Naomi… funguaa… mama fungua…Noe..Noel…..,”akashindwa kuzungumza vizuri kutokana kilio alichokuwa akikitoa, Naomi akakosa nguvu za kwenda kuufungua mlango huo na kubaki akitetemeka asifahamu nini kilikuwa kimetoke huko.

    ****

    Mapigo ya moyo wa Naomi yalikuwa yakienda kwa kasi ya ajabu mara moja hakufahamu ni kipi msichana huyo kilikuwa kikimpigisha kelele za ajabu kiasi hicho na kelele zenye kuushtua moyo wake mwili wote ukakosa nguvu na kubaki amesimama katika ya chumba huku mapigo ya moyo wake yakienda kwa kasi ya ajabu asifahamu ni vipi angeweza kuyatuliza.

    “Naomiiii!”Sauti ile ikasikika tena safari hii iliita kwa ukali kidogo huku ikiambatana na ugongwaji wa malango.

    “Shadia nini mbona hivyoo?”

    “Noela …No..Naomi hayupooooo,”akazidi kuongea huku akiendela kulia tena kilio cha sauti ya juu hali iliyopelekea hata badhi ya wapangaji wenzao kushtuka na masikio yao kuyaelekezea upande sauti hiyo ilikokuwa ikitokea.

    “Kafanyaje?”

    “Fungua tafadhali.”



    Naomi hakuwa na jinsi zaidi ya kuanza kupiga hatua kuelekea mlangoni nakuufungu huku akiwa na wasiwasi ya hali ya juu sana.

    “Niambe nini kimetokea?”

    “Noela.”

    “Kafanyanje ?”

    “Noela jamani…Noela…,”akamwambia huku akisimama wima na kumfuata pale mlangoni akamkumbatia kwa nguvu sana macho yake yakitoa machozi kupita maelezo. Naomi hakuelewa ni kipi kilikuwa kimemtokea kwa mtu huyo alichokifanya ni kujitoa mwilini mwake na kumshika mkono kisha akamvuta hadi ndani ya chmba chao.



    “Nieleze mpenzi kunanini,”akazungumza huku akimkalisha juu ya kochi na yeye kukaa pembeni yake mkono wake mmoja akaupitisha juu ya mabega ya Shadia uso wake ukawa unamtazma kwa umakini sana.

    “Noela hatupo naye.”

    “Heeee!”Akatamka neno hilo huku akisimama kwa haraka ya ajabu neno hatupo naye tayari alikuwa ameshafahamu lina maana gani.

    “Una..nataka..kunia…sikia Shadia mimi siyo mtani wako na usipende kuleta utani okaya hebu sema…mmmh sema,”akayatamka maeneno hayo akimsogelea karibu yaka na kupiga magoti mbele yake mikono yote ikiwa inatetemeka sana.

    “Kweli…hayaup ooo.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Wewe nyosha maelezo so Noela amefariki?”

    “Ndioooooo,”akamjibu huku akiachia kilio cha juu na chenye maumivu ndani yake Naomi alibaki amekishikilia kichwa chake asiamini kile masikio yake yalichokisikia akaona kama ulikuwa uongo.

    “Nahitaji ukweli wako unasikia?”Akazungumza kwa ukali huku akimsogelea na kuikaba kwa nguvu shingo yake mwili wote ukitetemeka kwa hasira ya hali ya juu.

    “Ukweli…ukweli..upiiiiii..Noela akapigwa risasi ya kichwa na Jumaaaaa.”

    “Mamaaaaaaa!”Naomi akapiga ukulele wa juu kisha akatulia na kuyatumbua macho yake akiwa amesimama wima na dakika ya tatu ya yeye kuwa katika hali hiyo akadondoka chini kama mzingo na kutulia kitendo kilichomshtua sana Shadia aliyekuwa bado akiendelea kulia.



    Lakini ghafla akanyamaza na kumfuata Naomi sehemu aliyokuwa amedondoke.

    “Naomi..Naomi…,”akamutia kama mara mbili huku akimtikisa tikisa lakini Naomi hakushtuka wala kuyafumbua macho yake. Haraka-haraka akachukua kitenge kilichokuwa kimetundikwa juu ya kamba na kuanza kumpulizia kwa haraka sana, hakutaka kuona marafiki zake wakipoteza maisha siku moja. Dakika tano za yeye kufanya kitendo hicho Naomi akashtuka huku akiwa analia sana Shadia akabaki katika wakati mgumu wa kumtuliza Naomi. Haikuwa rahisi lakini alifanikiwa.

    “Ilikuwaje Shadia?”Naomi akamuuliza mara baada ya kutulia.

    “Juma ndiye akamuua Noela kamvamia pale kijiweni na kumpiga risasi mbili za kichwa akafa papo hapo na kujeruhi wengine wawili.’

    “Kweli amekufa?”

    “Ndio Naomi amini,,”akamjibu huku akilia kilio kilipelekea na Naomi naye kuunganisha wote wakawa wanabadilishana sauti mfano wa wanakwaya kanisania walipohakikisha wameridhika na kilio wakanyamza na kufarijiana lakini kwa upande wa Naomi alijiona mkosefu sana na akawa amepoteza tumaini la kushi tena. Siku iliyofuata walielekea hospitali ya Mwananyamala ili kujihakisha kama kweli Noela alikuwa amefariki.Naomi hakuamini lakini hakuwa na jinsi akalia na kulia mpaka basi.

    “Tumanini langu ulikuwa wewe sijui nitaishije.”

    “Utaishi tu.”

    “Mmh!”



    ***

    Wiki mbili baadaye.



    Mara baada ya kifo cha Noela maisha ya Naomi yakawa magumu kupita kiasi hakuwa na pesa ya kujikimu kwa chakula na baadhi ya mahitaji Shadia hakuwa na huruma hata kidogo ile chuki yake ikazidi kuongezeka na kumfanya Naomi aanze kutoka tena.

    Ufanyaji wa kazi hiyo ukawa kama chachu kwa ugonjwa wake ambao ulizidi kuzishambulia seli zake sekunde baada ya sekunde hakuwa tena mtu wa kuzingatia matumizi ya dozi kama mwanzo kilio na majonzi ya kila aina mwili wake ukaanza kudhofika kama zamani na kuyachukiza macho ya watu.



    “We Naomi hivi wewe unajionaje na hiyo hali yako mbovu na mbaya kuja kusimama huku?”

    “Sasa wewe hali yangu inakuhusu nini?”

    “Weeee!Tena usitujibu hivyo wewe ni maiti inayotembea na unasambaza virusi bila huruma hata kidogo sikia wewe muda wako ulishapita kasubili kifo nyumbani,”msichana aliyekuwa akifahamika kwa jina la Magreti na mbabe kupita wote kijiweni hapo akamtemea cheche Naomi bila kujali kama maneno yake hayo yalikuwa mwiba mkali ndani ya moyo wake.

    “Lakini..si…,”

    “Mmh!Usizungumze chochote kabisaaa…kaa kimya na utusikilize,”mwingine akamsodoa huku wakianza kumzunguka na kumuweka katikati wakamtapikia maneno yasiyokuwa na idadi, wengine wakimsongola kwa vidole vyao wakimcheka na kumtema kadiri walivyoweza.

    “Na sitaki kesho nikuone hapaaa,”Magreti akamalizia maneno yake na kumsukuma Naomi akaweweseka lakini hakuanguka akawatazama kwa macho yenye maumivu ndani yake kisha akaanza kuondoka akilia ndani ya nafsi yake.

    “Nastahili kuyapata haya.”



    Safari yake ilikuwa ya maumivu njia nzima alilia na kujutia uamuzi wake akawalani wote waliosababisha yeye kuwa hivyo hadi anafika chumbani kwake alikuwa bado analia hakuwa na hamu ya kufanya chochote zaidi ya kujitupia kitandani akalala kifundifudi shuka lake akaufunika uso wake akilia sana.

    “Wewe toka muda ule unalia tu?”

    “Haikuhusu niacheni mnasikia!”

    Hahahahaha!Mwaka wako utajiju.”

    “Shadiaaaa…kwanini unakuwa na roho ya kikatili kiasi hicho?”

    “Babuuu weeee raha apate yeye kero siye akuuuu.”



    Hayo ndiyo yalikuwa maisha ya Naomi na marafiki zake ambao walikuwa wawili Shadia aliyekaribishwa chumbani hapo na Noela huku naye akimkaribisha rafiki yake Mwajuma msichana aliyekuwa na miaka kumi na sita tu ila alikubuhu katika kazi ya uuzaji wa mwili wake hakuna sehemu ya Dar es salaam aliyokuwa haifahamu. Japo familia yake ilikuwa na hali nzuri ya maisha lakini alibadilika na kuwa mtukutu kupita maelezo,akiwa na umri wa miaka kumi na nne tu alitoroka nyumbani kwao mkoani Rukwa na kukimbilia jijini Dar es salaam akiwa na marafiki zake wawili ambao walikamatwa wiki nne mara baada ya kuukanyanga mjio huo na kurudishwa kwao lakini Mwajuma akafanya ujanja wa kujifichaficha na kuendelea kuishi mjini humo kwa maisha ya kuunga unga hadi siku aliyokutana na Shadia aliyemsimulia kila kitu naye roho wa huruma akachukua nafasi yake na kuamua kumshirikisha Naomi ambaye ndiye alikuwa mwenye chumba.Naomi hakukata alimkaribisha wakawa wanaishi wote chumbani humo.

    “Mtatoka humu mkinizingua niacheni.”

    “Mwaya mimi sikusumbui mpenzi,”Mwajuma akajifanya kujitetea lakini moyoni alikuwa akimcheka Naomi na kumsodoa kwa kila kitu

    Upande wa Naomi alibaki akilia na kuilaumu akili yake alimchukia sana Stella kwani bila yeye aliamini hayo yote yasingemtokea.

    Alishi kwa upweke ndani ya wiki tatu hakula na kushiba zaidi ya kulia mawazo na upweke ulipelekea afya yake kuporomoka kwa asilimia kubwa sana hali iliyopelekea marafiki zake kumpeleka hospitali ya wilaya ya Temeke huko alilazwa kwa muda wa wiki moja kisha alipewa ruhusa ya kwenda kutibiwa hospitali ya taifa Muhimbili mara baada ya afya yake kuzidi kuwa mbaya.



    Muhimbili ilikuwa ni zaidi ya ugonjwa aliokuwa nao aliumia kila alipoifikiria ilikuwa ni hospitali iliyoyaokoa maisha yake kwa miaka kadhaa iliyokuwa imepita.Ilikuwa ni hospitali iliyowahi kumpitisha katika maisha mazuri na yenye uhakika wa ushindi, laiti angeitumia nafasi adimu aliyoipata kwa sasa hivi angekuwa miongoni mwa madaktari waliokuwa wakifanya kazi hospitalini hapo.



    Machozi hayakukatika machoni mwake kumbukumbu yote ilikuwa imerejea picha ya Dk.Samweli haikukatika akilini mwake.

    “Kwanini wamenileta hapa na mbaya zaidi kwenye hichi chumba,”akazungumza peke yake huku akiendelea kulia muda mfupi mara baada ya kufikishwa ndani ya wodi ya watu waliokuwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi.



    “Bibi mbona unalia?”Mmoja wa wagonjwa aliyekuwa amelala kado ya kitanda chake kamuuliza huku akimtazama machoni.

    “Mmmmh!Leo hii mimi naitwa bibi aaaah!Kweli dunia imeniponza,”akawaza ndani ya moyo wake akikizidisha kilio chake.

    “Wewe hutakiwi kulia kiasi hicho wote hao wanaumwa wew ndo unayeumwa peke yako?”Nesi akamfyatulia maneno huku akiendelea kumhudumia.

    “Hapana.”

    “Sasa nini?”

    “Aaaah!Naomba unisaidie kitu kimoja kama hutojali,”akayafuta machozi yake na kuyapanguza machozi na kujikaza kiume.

    “Kipi?”

    Naaa…naaomba ukaniiii…tafutie..naniii…ana…,”akashindwa kuzungumza vizuri mara baada ya mlango wa chumba hicho kufunguliwa na mtu ambae hakutegemea kumuona akaingia moyo wake ukaanza kudunda kwa kasi ya ajabu huku akitetemeka sana na asijue nini cha kuzungumzwa endapo angeulizwa maswali na mtu huyo.







    Macho yake hayakuamini kile kilichoona aliona ni kama macho yake yalikuwa yakimdanganya akayafumba kwanza kidogo na kumtazama tena mtu huyo huku mapigo ya moyo wake yakizidi kuongezeka.

    Akabaki akimtazama mtu huyo bila kupata jibu la kipi angeenda kukizungumza endapo angeongeleshwa.

    “Huyu amekuja lini?” Akauliza mtu huyo huku macho yake yakimtazama Nesi aliyekuwa akiendele kumhudumia Naomi ambae macho yake yalikuwa kwa mtu huyo.

    “Si ni Dk.Rose huyu,”Naomi akajiuliza peke yake huku akiendelea kumtazama mwanamke huyo ambae alikuwa hajamfahamu kabisa japo muda mwingine walikuwa wakikutanisha macho lakini ukweli ulikuwa Dk.Rose hakuwa amemfahamu Naomi.

    “Ana kama siku mbili hapa ila leo ndo kaletwa humu,” akamwambia huku akisitisha kazi yake na kumtazama mwanamke huyo kwa macho yake makubwa kiasi.

    “Okay ni walewale?”

    “Ndio.”

    “Basi sawa,”akamjibu huku akianza kutembea na kwenda katika kitanda cha jirani yake na kile alichokuwa amelazwa Naomi.

    Akashusha pumzi ndefu sana kisha macho yake yakaendelea kumtazama Dk.Rose mwanamke aliyewahi kumpokonya mtu wake aliyekuwa akimpenda sana.

    “Ni bora nisingekutana na yeye tu hivi akifahamu kama mimi ni Naomi atanifikiriaje?”Akawaza na kuwazua ila akajipa moyo wa kutaka kuzungumza na mwanamke huyo, lakini kabla ya kuzungumza kile alichokuwa nacho Dk.Rose akaondoka ndani ya wodi hiyo akimuacha Naomi akiwa na shauku la kutaka kuzungumza naye.

    “Hi..vi..huyu..dak..tari..atarudi…tena?”Akamuuliza mgonjwa mwenzake maneno yake akiyakata kata kutokana na kukwaruza kwaruza kutokana na kulia sana.

    “Ndiyo atakuja ila si sasa hivi nadhani mchana ama jioni vipi unamfahamu?”

    “Ndio. Alikuwa rafiki yangu.”

    “Aaaah!Sawa shoga yangu atakuja.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Moyo wa Naomi ukawa na sahauku la kumuona tena Dk.Rose aliamini kumuona yeye uwezekana wa kukutana na Dk.Samweli ulikuwepo tena wa asilimia kubwa, hivyo akawa macho kutazama kila aliyekuwa akiingia ndani ya chumba hicho ambaacho miaka ya nyuma aliwahi pia kulazwa humo kabla ya kubadilishwa na kuwa chumba cha waathilika wenye virusi vya ukimwi na mbaya zaidi kitanda kilikuwa ni kile kile, toka dakika hiyo akawa anatoa machozi bila kikomo.

    Majira ya saa saba mchana mlango ukafunguliwa tena hapo macho yake yakawa kule mlangoni ili aone ni nani aliyekuwa akiingia ndani ya chumba hicho.

    “Ni yeye lazima nimtafute la sivyo nitakufa kabla ya kuonana na Dk.Samweli,”akawaza mara baada ya kumuona akiingia ndani ya chumba hicho hakuwa na papala hivyo ikabidi asubili hadi atakapofikia kitanda chake.

    “Ooooh!Naomi ni wewe ninayekufahamu?”Akamuliza huku akimshangaa sana kwani hakuamini kama alikuwa ni yeye akabaki akimtazama msichana huyo mkononi akiwa na faili la mgonjwa huyo ambae aliwahi kumpokonya mpenzi wake.

    “Ndio ni mimi.”

    “Mmmmh!”Akaguna na kukitikisa kichwa chake asiamini kama alikuwa ni msichana huyo ambae alikuwa mazuri kupita maelezo.

    “Samahani Dokta unaweza kunisaidia kitu,” akaongea kwa taratibu kwani mwili wake wote ulikuwa unamuuma.

    “Kipi Naomi?”Dk. Rose akamuuliza huko moyo wake ukijawa na huruma sana kwa msichana huyo japo aliwahi kumchukia sana Naomi lakini kwa wakati huo hakuwa na kinyongo naye kabisa aliona hayo ndiyo yalikuwa malipo ya kumpokonya mwanaume aliyekuwa ameutesa moyo wake kwa muda mrefu.

    “Namuulizia Dk. Samweli mrefu kiasi mnene na maji ya kunde je bado yuko hapa?”

    “Nani yako?”Akamuuliza kwa makusudi kabisa kwani alikuwa akimfahamu kila kitu kichokuwa kimewahi kutokea huko nyuma.

    “Aliwahi kuwa rafiki yangu…naomba unisadie kama kunauwezekano.”

    Dk. Rose hakuongea chochote zaidi ya kuendelea na jukumu lake la kumpima huku moyo ukimuuma sana kila alipomkumbuka Dk. Samweli aliumia sana japo tayari alikuwa mke wa mtu ila penzi lake kwa Dk. Samweli lilikuwa halijafa.

    Alitoka wodini humo akiwa anahuzunika sana muda mwingine alitamani asifikishe ujumbe kwa mhusika ila alista hivyo akawa ameongoza moja kwa moja ofisini kwa Dk.Samweli na hiyo ndo ikawa mara ya kwanza kwa yeye kuzungumza na Dk.Samweli.



    ****



    Ulikuwa ni mshtuko wa hali ya juu sana macho yake hayakuamini kama siku moja yangekuja kuona kitu kama hicho. Alihisi mapigo ya moyo yakifanya kazi yake zaidi ya uwezo wake alibaki amemtazama mwanamke aliyekuwa amelala kitandani akiwa amekondeana kupita maelezo.

    Ule uzuri wake uliokuwa ukiwatingisha wanaume wengi sasa haukuonekana alibaki mifupa mitupu.

    “Samweli..nisamehe kabla…ya..ki..fo..cha..ngu,” akazungumza kwa taabu sana mara baada ya kumuona mwanaume huyo akiwa amesimama akiwa haelewi kile kilichokuwa mbele yake.Macho yake yaliyokuwa ndani yakimtazama Dk. Samweli kwa wasiwasi.

    “Naomiii!”

    “A..beee.”

    “Kwanini ulinifanyia hivyo?”Alimuuliza kwa sauti ya juu iliyopelekea hata baadhi ya wagonjwa waliokuwa wamelazwa wodi moja na Naomi kuzigeuza shingo zao. Mwili wake wote ukianza kuvimba kwa hasira.



    “Naju..a..ni..liku..te..nda .. sa.na..ila..ninahitaj…iii…msa..maha..wako..kabla…y..aaa..kuuufff…,”hakuweza kumalizia sentensi yake mara alianza kutapatapa kitandani hapo akikinyanyua kifua chake juu na kukishusha chini kwa haraka haraka Dk. Samweli hakuamini kile kilichokuwa kikitokea alibaki amesimama wima asijue cha kufanya.



    “Samweli huoni anavyofanya?” Sauti ya Dk. Rose ndiyo iliyomshtua kutoka katika mawazo alipoyatupa macho yake kitandani kwa Naomi alikaribishwa na macho yakiwa juu mdomo ukiwa wazi.

    “Naomi…Naomiiii,” alimuita huku akimtikisa tikisa.

    Lakini Naomi hakushtuka wala kuongea chochote macho yake yakaendelea kuwa juu.

    “Oooh!Nooo!”Akayazungumza maneno hayo ambayo yalikuwa mawili tu huku akianza kutoka ndani ya chumba hicho akikimbia mfano wa mtu aliyekuwa ameugua ukichaa wa ghafla sana, alihisi kama yuko ndotoni kumbe haikuwa ndoto kiu ya kutaka kumuuliza maswali Naomi kabla ya kifo chake tayari alikuwa ameshapokonywa hakuweza kuyazuia machozi kutiririka mashavuni mwake kila alipoyakumbuka mambo waliyowahi kufanya na Naomi moyo wake ulimuuma sana.

    “Samweli!Samweli kunanini?”Mmoja wa mfanyakazi mwenzake akamuuliza mara baada ya kukutana naye na kumshika mkono.

    “Naomii…Naomi..Dokta …Naomi…moyo wanguu mieeee,”akazungumza huku akilia machozi na kukishika kifua chake mfano wa mtoto mdogo.

    “Twende,”akamshika mkono na kumrudisha ndani ya chumba hicho huko nako mambo yalikuwa ni kama mwamzo hakuweza kumtazama Naomi ambae sasa alikuwa ameshafunikwa na shuka jeupe na kitanda chake kikizungushiwa mfano wa pazia ambalo lilikuwa limefungwa kwenye chuma na lenye nguo ya kijani.Picha ya haraka haraka akawa amegundua kuwa Naomi alikuwa ameshafairiki.



    Hakuwa na nguvu za kuendelea kubaki wodini humo zaidi ya kutoka na kuelekea ofisini kwake huku akilia sana, alifika na kukaa juu ya kiti chake kisha uso wake aliulaza juu ya meza kubwa iliyokuwa mbele yake. Neno Naomi halikukatika mdomoni mwake moyo wake bado ulikuwa na mapenzi ya dhati kwa Naomi japo alikuwa mtu mzima wa miaka thelathini na nane bila kuwa na mtoto hilo hakulijali yeye alichokuwa akikijali ni uwepo wa Naomi maishani mwake.



    “Nitaku..pata..wapi Naomiiii… kwanini umeondoka kipindi nilichokuwa nakuhitajiii…rudi Naomi njooo mpenzi nishakusamehee,“ aliongea peke yake maneno yenye uchungu sana na maumivu makali kupita maelezo.

    “Samweli hutakiwi kukufuru kiasi hicho yote muachie Mungu.”

    “Dokta inaumaaa… inaumaaa… Naomi nilimpenda sana…yeye ndiye aliyenionesha maisha ya mapenzi yeye ndiye aliyestahili kuwa mke wangu… sijali alichonifanyia..nishasamehe…ninampendaaa Naomi.”

    “Nafahamu Doktar ila jikaze wewe ni mwanaume tena mwanume aliyekamilika Naomi ameshaenda pinga moyo konde,” Dk. Godfery Gerevas aliyekuwa rafiki yake mkubwa sana toka akiwa mwanafunzi alizidi kumbembeleza huku mikono yake ikiupiga piga mgongo wake. Alimpenda Dk. Samweli kama mtoto wake japo yeye kwa wakati huo alikuwa mtu mzima sana lakini urafiki wao ulikuwa unazidi kuchanua.



    Dakika tatu za rafiki yake kuingia ndani ya ofisi yake akasimama wimi akiwa amebadilika uso wake na mkono wake akiwa ameukunja ngumi kali sana Dk.Godfrey kuona hali hiyo naye akasimama huku akiwa na wasiwasi moyoni mwake macho yake yakimtazama rafiki yake ambae alikuwa anaanza kupiga hatua za kumfuata naye kuona hivyo akaanza kurudi nyuma akitetemeka mwili mzima.



    Itaendelea….



    KILIO CHA NAFSI-24

    Na:Teddy Andrew.

    Email.modelteddy4@gmail.com

    Ilikotoka…..



    Dakika tatu za rafiki yake kuingia ndani ya ofisi yake akasimama wimi akiwa amebadilika uso wake na mkono wake akiwa ameukunja ngumi kali sana Dk.Godfrey kuona hali hiyo naye akasimama huku akiwa na wasiwasi moyoni mwake macho yake yakimtazama rafiki yake ambae alikuwa anaanza kupiga hatua za kumfuata naye kuona hivyo akaanza kurudi nyuma akitetemeka mwili mzima

    SONGA NAYO.





    Muonekano wa Dk.Samweli ulizidi kumtesa sana Dk.Godfrey toka amfahamu kijana huyo hakuwahi kumuona katika hali hiyo hata siku moja, alikuwa mpole sana na mcheshi kwa kila mtu hata kama alikuwa amekwazika suruhisho lake lilikuwa ni kilio tu kitendo cha kubadilika na kuvimba mwili wake wote kwa hasira kilimtisha sana.

    Akazidi kupiga hatua za kurudi nyuma huku akiwa tayari kwa kukimbia endapo lolote lingeweza kutokea.

    “Mmmmh!Huyu kijana kumbe yuko hivi?”Akawaza peke yake akiendelea kurudi nyuma bahati mbaya akaufikia mlango na alipojaribu kuufungua mlago ulikuwa umejifunga hakufahamu ni wakati gani mlango huo ulijifunga na ni nani alikuwa ameufunga na ni saa ngapi.Hakukumbuka kama ni yeye alikifanya kitendo hicho mara baada ya kuingia katika chuma hicho akihofia watu wengi kujanzana ndani ya ofisi hiyo.

    “Usinifanyie ubaya Samweli.”

    Dk.Samweli hakumjibu chochote zaidi ya kuendelea kutiririkwa na machozi akatembea hadi dirishanai na kusimama eneo hilo akiendelea kulia sana.

    “Pole Samweli kazi ya mola haina makosa piga moyo konde,”taratibu akaanza kutembea akimfuata eneo hilo akafika na kumuwekea mikono yake begani kazi yake ikawa ni kuupiga piga mgongo huo alipoona ametulia akamrudisha kwenye kiti chake na kumkalisha.



    “Nahitaji kuona mwili wa mke wangu,” akaongea huku akisimama wima.

    “Tulia kwanza kwa sasa huwezi.”

    “Hapana nitatulia endapo nitamuona Naomi wangu.”

    “Sawa nitakupeleka je na hili kovu la nini?” Alimuuliza huku akilisonta kovu lililokuwa kidoleni kwake.



    “Ofuuh!”Alishusha pumzi ndefu kisha aliketi kumbukubu ya siku waliyofanyiana kiapo na Naomi cha kuchanjiana damu ilirejea mara moja.

    “Hivi kweli unanipenda Naomi?”

    “Ndiyo tena sana nipo tayari kufanya chochote ili uamini kuwa nakupenda,”aliongea Naomi huku akimlegezea macho.

    “Je upo tayari kuuganisha damu na mimi?”

    “Ndiyo hata sasa hivi.”

    Papo hapo Dk. Samweli akauchukua mkono wa Naomi na kuung’ata kwa nguvu hali iliyopelekea eneo hilo kutoboka na damu kutoka nje alipohakiksha amekamilisha zoezi hilo naye alifanya vivyo hivyo kisha damu zao waliziunganisha kama ishara ya penzi lao.

    “Mimi na wewe milele mpaka kufa.”

    “Nami pia,” alijibu Dk. Samweli huku akimkubatia Naomi kwa hisia kali sana macho yao hayakusita kutoa machozi ya furaha.

    “Hakuna kitu Dokta niliumia kipindi niko Napel nilipokuwa na hali ya ukichaa.”

    “Kweli?”

    “Ndiyo kwanini nikudanganye.”

    “Okay sawa njoo nikupeleke.”

    Walitoka ofisini humo na kuelekea sehemu ya kuhifadhia maiti alimarufu kama mwochari kabla ya kuingia ndani ya chumba hicho walizungumza na mlinzi na kupelekwa sehemu ya mwili wa Naomi ulipokuwa umehifadhiwa. Alitumia kama dakika arobaini na tano kuutazama mwili huo huku akilia sana muda mwingine alitamani na yeye kufa kila alipomtazama Naomi aliyekuwa amefumba macho na kukata kauli ndipo uchungu ulipozidi.

    “Yatosha tuondoke.”

    “Hapana nitalala na Naomi humu humu.”

    “Samweli hutakiwi kufanya hivyo tafadhali nielewe.”

    “Nampenda Naomi nampenda sana siweziiii…niacheni nilale na mke wangu huyu ni wangu tuu,”akasema huku akipiga kelele za juu sana.

    “Hapana kaka humu hakufai si sehemu sahihi ya wewe kulala,”mlinzi wa eneo hilo naye akamwambia akijaribu kumshika mkono ili amtoe eneo hilo lakini hakuweza kufanikiwa kwani Dk.Samweli alikuwa na nguvu sana.

    “Hakufai kaka.”

    “Pana faaaa…mbona yeye yuko humu?Nami nitalala na mke wangu,”akajitoa mikononi mwa mlinzi huyo na kukimbia hadi kwenye kabati alilokuwa limewekwa mwili wa Naomi akalifungua na kuanza kuubusu mwili huo bila kujali kama angeweza kupata madhara yeyote.Dk.Godfrey kuona hivyo naye akakimbilia eneo hilo na kumtoa kwa nguvu zake zote akisaidizana na mlinzi huyo.

    Ilikuwa ni shughuli pevu kumtoa ndani ya chumba hicho lakini waliweza kufanikiwa na kumpeleka moja kwa moja ndani gari lake na kuondoka hospitalini hapo akiacha ameweka histori kwa watu waliokuwa wamelishuhudia tukio hilo.

    Wapo waliomhurumia sana na hata kutoa machozi na wapo waliomcheka na kumuona mjinga sana.



    ****



    Siku tatu mbele mwili Naomi ulizikwa ndani ya makaburi ya wilaya ya Kindoni kitu ambacho Dk. Samweli hakukiamini hata kidogo lakini hakuwa na jinsi ilibidi ayapokee matokea hayo. Wiki nzima alishinda chumbani kwake akilia na kutazama picha za Naomi hali iliyokuwa ikiwaumiza sana ndugu zake mama yake alikonda kwa mawazo.

    “Saweli.”

    “Naamu kaka.”

    “Unavyofanya hivyo utamsababishia matatizo makubwa mama,”Kaka yake mkubwa aliyekuwa akifahamika kwa jina la Erick aliongea mara baada ya kuingia chumbani kwa mdogo wake na kumkuta akiendelea kulia.

    “Erick naumia sana.”

    “Nafahamu ila huna jinsi unatakiwa unyamaze wewe ni mwanaume hutakiwi kuwa hivyo.”

    “Nitawezaje kumsahau labda?”

    “Jichanganye na marafiki zako fanya mazoezi kama mwanzo hizo picha za Naomi hutakiwi kuwa nazo tena hebu jiangalie una miaka mingapi mdogo wangu badilika.”

    “Siyo rahisi kama unavyofikiria nitamlilia Naomi mpaka mwisho wa uhai wangu.”

    “Tambua utamuua na mama huyo ndiye aliyebaki jicho letu sote.”



    Kaka yake alijitahidi kumshauri sana na hatimae alikubaliana na ushauri wa ndugu yake huyo na kitu kilichomfanya akubali ushauri ni mama yake hakupenda kumuumiza mama yake. Mwaka uliofuata alibahatika kumpata msichana aliyetokea kumsahaurisha maumivu ya Naomi kwa kiasi kikubwa sana. Mapenzi yao yalianza kama mchezo mchezo lakini mwisho wa siku walifunga ndoa na kuishi pamoja.

    “Ujue sijaziona siku zangu kama miezi miwili,” Teddy aliongea huku akimtazama Dk. Samweli machoni.

    “Usiniambie kuwa ni mjamzito!”

    “Sina uhakika ila naomba kesho unipeleke nikapime.”

    “Ukapime wapi wakati Daktari unae ndani vipimo vya mimba ninavyo utanikumbusha kesho asubuhi nikupime kwa mkojo wa asubuhi.”

    “Sawa.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walilala kwa furaha huku wakiingojea asubuhi ifike mapema.

    “Kweli Saweli nina ujauzito.”

    “Ahsante sana Teddy umeirejesha furaha yangu iliyokuwa imepotea kwa miaka mingi sana naahidi kukupenda sana.”

    “Nami pia.”

    Walikumbatiana na kupigana mabusu kana kwamba ilikuwa mara yao ya kwanza kukutana mabusu hayao yalipelekea hadi kujikuta wakitupiaana kitandani na kilichotokea hapo hakiandikiki.



    MWISHO.

0 comments:

Post a Comment

Blog