Search This Blog

Sunday, 20 November 2022

KASRI YA MWINYI FUAD - 4

 

    Simulizi : Kasri Ya Mwinyi Fuad

    Sehemu Ya Nne (4)







    “Na hebu usindike huo mlango!” Fuad aliamuru lakini si kwa hamaki kama kawaida yake.



    Baada ya kuusindika mlango Kijakazi alikwenda mpaka penye pembe ya kitanda alipolala Fuad na kusimama hapo.



    “Kaa! Kaa! Usiogope,” Fuad alimwambia Kijakazi.



    Kijakazi alikaa pembeni mwa kitanda kwa hadhari kubwa huku akiupakata mguu wa Fuad uliokuwa ndani ya gamba la chokaa. Alianza kuukanda na kuutikisatikisa.



    “Hivyo hivyo!” Fuad alisema kwa sauti ya chini.



    Kijakazi aliukanda na kuutikisa mguu wa Fuad kama mama anapombembeleza mtoto wake. Kijakazi alijiona amefanikiwa pakubwa kuitwa na Fuad kuja kumkanda mguu. Fursa kama hii hakuipata tokea alipokatazwa kumbeba Fuad na Bi. Maimuna wakati Fuad alipokuwa bado mdogo. Kijakazi aliukumbatia mguu wa Fuad huku furaha imemjaa moyoni. Aliona kama anambembeleza mtoto na huku mtoto huyo anapata usingizi kidogo kidogo.



    Kijakazi aliukanda mguu wa Fuad kama alivyoweza. Alijikusanya nyuma akawa mdogo mwisho wa uwezo wake.



    “Ah! Kijakazi” Fuad alianza kusema kwa sauti ya mtu aliyekuwa akiona raha kwa kukandwa, “Tokea leo wewe ndiye utakayekuwa mwuguzaji wa mguu wangu. Wewe ni bora kuliko daktari yo yote yule; wewe cdie ulicnilea nilipokuwa mdogo,” Fuad alisema huku Kijakazi amelikumbatia guu lake.



    “Hayo ni kweli Bwana,” Kijakazi alijibu mbio mbio huku machozi yanammiminika kwa huruma aliyokuwa nayo kwa Bwana wake. “Muni nimekulea tokea udogo wako na ilikuwa ni mimi tu niliyeweza kukunyamazisha wakati unapoanza kulia, hapana mtu yo yote aliyeweza kufanya hivyo; hata mama yako Bi. Maimuna alikuwa akishindwa kukunyamazisha. Ulikuwa kitoto kizuri,” Kijakazi aliendelea kusema.



    “Haya Kijakazi, wewe ni mtumishi wangu mtiifu. Nyimbo gani vile ulikuwa ukiniimbia nilipokuwa mdogo?” Fuad alimwuliza Kijakazi.



    “Hebu niimbie kidogo,” Fuad alimwomba Kijakazi.



    Kijakazi alipata furaha kubwa kuambiwa maneno kama yale na Fuad, hakupala hata siku moja kuambiwa maneno kama yale. Alihisi kazi yake ya utiifu kwa Bwana wake ilikuwa si ya bure kwani Bwana leo amcfurahi naye, na kumwambia kwamba ni mtumishi mtiifu. Alipata furaha isiyokuwa na mfano.



    “Bwana! Sijui kama nitaweza kuimba kama nilivyokuwa nikikuimbia!” Kijakazi alijibu huku akiogopa, bado ameupakata mguu wa Fuad.



    Mara Kijakazi alianza kuimba kwa sauti yakc nenc yenye kukwaruza kama debe bovu na Fuad alionyesha kufurahi. Kijakazi aliona kama anaota kwa furaha aliyokuwa nayo. Aliendelea kuimba:



    Lala mtoto tala, katika kitanda lala,

    baba ni mtukufu, mama ni mtukufu,

    Lala mtoto lala, katika kitanda lala...

    “Funga mdomo wako!” mara Fuad upole aliokuwa nao ulimwisha. “Sauti kama ng’ombe! Unatikiri huo ndio wimbo uliokuwa uldniimbia?” Kwa hamaki Fuad aliuliza.



    “Huu ndio ule wimbo Bwana! Huu ndio wimbo uliokuwa ukiutaka kila siku! Huu ndio wimbo niliokuwa nikikuimbia; ndio uliokuwa mzuri kuliko zote, nina hakika nasema kweli!” Kijakazi alijibu huku akitetemeka kwa hofu kwa kumkera Bwana na pia akiogopa asije akamtonesha mguu wake kwa kutetemeka kwake.



    “Sitaki kusikiliza sauti yako mbovu! Hufai pesa moja! Washenzi wale wananikera na wewe huwezi kuniliwaza hata kwa kuimba tu! Toka hapa! Mungu akulaanini nyote!” Fuad alipiga kelele huku akitaka kuinuka lakini alishindwa.



    “Itanibidi niondoke Bwana?” Kijakazi aliuiiza kwa hofu akijihisi amefanya makosa makubwa.



    “Ondoka! Toka nenda zako!” Fuad alipiga kelele.



    Kijakazi aliulaza mguu wa Fuad uliokuwa na maumivu juu ya kitanda kwa hadhari kubwa halafu akasimama.



    “Haya toka hapa nenda kawape ng’ombe maji! Upesi” Fuad alisema.



    Kijakazi alitoka chumbani mle mbio huku akishusha pumzi.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Kijakazi alikwenda bandani kwa ng’ombe na kuwapa maji kama alivyoamrishwa na Fuad.



    “Ah! N’nastahili haya!” Kijakazi alisema peke yake huku anawapa maji ng’ombe. Alihisi anastahili yale kwa kutaka makubwa.



    Hazikupita siku nyingi, Fuad alimwita tena Kijakazi chumbani. Mara hii Fuad alikuwa amekaa juu ya kitarida huku ameegemea mto uliokuwa nyuma ya mabega yakc. Kijakazi, kama mara ya kwanza, alikwenda na kuketi pembeni mwa kitanda huku akiunyanyua mguu wa Fuad kwa hadhari kubwa na kuuweka taratibu juu ya mapaja yake. Kijakazi alimtazama Fuad kwa macho makali kama kwamba ndiyo kwanza amwone.



    Kijakazi alikuwa ameupakata mguu wa Fuad anaukanda na mara Fuad alianza kumsaili.



    “Hebu niambie Kijakazi,” alianza, “unaionaje dunia ya leo? Unayaonaje haya mambo mapya ya siku hizi?”



    Kijakazi hakujua nini la kujibu kwani yeye hakuwa na lo lote alilolijua. Aliogopa hata kusema asije akafurushwa kama mara ya kwanza. Alijibabaisha na kujidai kumkanda Fuad mguu huku akiimba:



    “Lala mtoto lala; lala mtoto lala ...”

    “Ebo! Mimi nasema na wewe, unaniona kama mwenda wazimu? Nakuuliza haya mambo unayapenda au huyapendi?” Kwa hamaki Fuad aliuliza tena.



    “N-n-nayapenda Bwana! Nashukuru kwa yote!” Kijakazi alijibu.



    “Unasemaje?” Fuad alimkodolea macho Kijakazi “Wewe unawapenda wale wahuni wale! Washenzi wale! Wezi! Wajinga! Unayapenda mambo wanayoyafanya makafiri wale? Oh! Hivyo na wewe pia uko pamoja nao?” Fuad alitoa maneno kwa hamaki kubwa.



    Kijakazi alibabaika; hakujua aseme nini kwani alikuwa hata hakufahamu aliulizwa nini na Fuad. Hakuyaelewa hayo mambo mapya aliyoulizwa na Fuad. Kichwa kilimduru na mara alisema.



    “Sijui unakusudia nini Bwana! Mimi mambo haya siyaelewi!”



    Kijakazi khofu ilimshika; alikuwa akitetemeka.



    “Naona sasa wewe ushakuwa unashirikiana nao wale, eh? Sikujua kama nilikuwa mkimlea nyoka ndani ya nyumba yangu!’’ Fuad alipiga kelele.



    “Ah! Bwana wangu! Mimi nimemtumikia baba yako kwa utiifu kabisa na nitakutumikia wewe vile vile kikomo cha uwezo wangu.” Kijakazi alisema huku akila viapo.



    Mara Fuad alikunja matao ya chini na kuanza kuzungumza na Kijakazi kwa upole, “sikiliza Kijakazi, sherti ujue kama sisi tunakuona kama wewe m mmoja wetu ndani ya nyumba hii, wewe ni kama bibi yangu, ni sawa sawa na ye yote katika ukoo wangu. Wewe wakati wote ulikuwa mtumisbi mtiifu. Kijakazi sherti ufahamu kwamba wewe ni kama mzee wangu kwani wewe ndiye uliyenilea. Nakuahidi kwamba utakapofariki nitakufanyia mazishi makubwa yasiyowahi kufanywa hapa Koani, nami nakwambia wazi wazi kama wewe umekuwa kama mama yangu wa pili.”



    Kijakazi alikuwa ameshughulika kuukanda mguu wa Fuad huku akimsikiliza kwa makini.



    Fuad aliendelea na manemo yake na kusema, “Lakini sikiliza Kijakazi, hawa washenzi hawa, mijitu hii siku hizi imekuwa kama mizimwi. Ati hivi vijitu vifukara katika kijiji hiki vimejikusanya na ati vinajidai vinataka kuanzisha kilimo cha pamoja na kuishi kijamaa! Unafikiri vijitu hivi, visivyojua kitu, vinaweza kufanya kitu cho chote. Wao kila wakija hapa wananiletea haban za kutaka kulichukua shamba langu. ati nijiunge pamoja na vijitu vile. Wao hawaelewi jambo moja; wanafikiri wanauhodari kuliko mimi Fuad, Fuad bin Malik.”



    Fuad aliendelea kuropoka, akiutukana na kuufanyia stihizai mpango wa ujamaa na serikali ya mapinduzi.



    Alisita kidogo na kutikisa kichwa akaendelea kusema:



    “Sikiliza Kijakazi: mimi nakwambia yote haya kwa sababu nakuamim. Tena kitu kimoja; napenda kukutahadharisha na Mkongwe. Tafadhali siku hizi usichanganyike naye. Usichanganyike naye hata kidogo kwani yeye amekwisha tutoka na karibu namwona atatukimbia hapa nyumbani. Siku hizi amezidi, hafanyi kazi, amekuwa mvivu kama kunguni na amekuwa mjeuri. Hana adabu tena. Juzi nilimwita na mara alinitolea ujuvi; lakini mwache aondoke. Atakapoondoka itakubidi wewe Kijakazi ufanye kazi zaidi.”



    Kijakazi aliyasikia maneno ya Fuad kwa mbali na wakati Fuad alipokuwa akisema Kijakazi hakuamini kwamba maneno hayo alikuwa akiambiwa yeye. Kijakazi alianza kujiuliza.



    “Amesema nini vile? Mimi ni sawa sawa na mama yake wa pili? Vipi vile? Mimi ni sawa sawa na yo yote ndani ya nyumba hii. Oh! Bwana amenambia maneno mazuri leo, haijambo kazi yangu si ya bure. Sasa nitafanya kazi zaidi ili bwana afurahi na m’mi zaidi.”



    Kijakazi aliendelea kumkanda mguu Fuad mpaka akapata usingizi na baada ya hapo aliulaza mguu huo taralibu juu ya kitanda. Alitoka nje na kuufunga mlango akamwacha Fuad amelala.



    Siku ya pili ilifika na Kijakazi alitamani aitwe na Fuad kwenda kumkanda mguu ili amsikie akisema kuwa amekuwa kama mama yake wa pili. Maneno haya yalimpa Kijakazi furaha maalum. Lakini siku ile ilipita, kesho ikapita, leo ilikuwa jana, na jana ikawa juzi, na taratibu siku zilipita bila ya Kijakazi kuitwa tena kwenda kuuguza mguu wa Fuad.



    Kijakazi alikuwa amejinyosha juu ya kitanda cha mayowe na ghafla Mkongwe akaingia chumbani kwake. Kwa namna Mkongwe alivyoingia ilikuwa dhahiri alikuwa na kitu muhimu alichotaka kumwambia Kijakazi. Mkongwe alikuwa amechukua kifurushi chepesi mkononi mwake.



    “Nimekuja kukuaga Kijakazi. Nimekata shauri kuacha kazi na kesho asubuhi naondoka hapa. Nimechoka kutumwa na kusumbuliwa na Fuad. Mtu huyu hana wema wala ihsani. Hata fadhila na mtovu wa adabu. Roho yangu imechoka, nakwenda zangu.”



    “Unakwenda wapi mwanangu? Umekaa hapa huna wasiwasi wo wote. Unataka kwenda wapi?” Kijakazi aliuliza.



    “Sina wasiwasi? N’na wasiwasi, tena wasiwasi mkubwa.”



    “Wasiwasi gani ulio nao, mwanangu?”



    “Naujua mwenyewe,” Mkongwe alijibu.



    Pale pale Kijakazi aliyakumbuka maneno ya Fuad aliyomwambia kuhusu Mkongwe kama sasa amekuwa haaminiki na anaweza kuondoka saa yo yote ile. Aliyaona maneno ya Fuad yote ni ya kweli, sio kuhusu Mkongwc tu bali yote aliyoambiwa na Fuad kuhusu wale watu na mipango yao mipya.



    Kijakazi alimkodolea macho Mkongwe na kumtazama na, mara alimwambia, “Mkongwe, nakuomba usiondoke; usiwafuate wale wabaya!”



    “Nani hao walo wabaya?” Mkongwe aliuliza.



    “Wale watu wanaokuja hapa kila wakati kumkera Bwana!”



    “Wale?” Mkongwe alisema, “Wale watu wazuri sana, tena nawaombea dua Mungu awasaidie katika wanayotaka kuyafanya. Nani aliyekwambia kama wale ni watu wabaya?”



    “Bwana. Bwana Fuad, ameniambia kuwa wale ni wahuni, wezi na makafiri.”



    “Wale si wezi si wahuni. Wale ni watu na heshima zao, tena wana heshima kuliko huyo Fuad wako. Fuad ndiye mwizi, mwizi wa nguvu za watu, mtovu wa adabu tena hana heshima hata kidogo. Katuweka hapa anatutuma kama ng’ombe na hatuna lo lote tunalolipata kutoka kwake!” Mkongwe alisema huku hamaki zimemjaa.



    “Oh! Mkongwe unasema hivyo mwanangu? Unamwita Bwana hivyo?”



    “Ndiyo namwita mwizi, mtovu wa adabu, hana wema wala ihsani. Na wewe Kijakazi utakuja kukubaliana na mimi siku moja kama utakuwa bai!”



    “Basi unanikimbia Mkongwe mwanangu? Sasa kazi zote zitanielemea mimi; nitakuwa sina wa kunisaidia,” Kijakazi alisema huku akipumua kama mtu aliyekimbia masafa marefu. Mara Kijakazi alianza kusema tena kumnasihi Mkongwe:



    “Lakini, Mkongwe, unaelewa unalolifanya? Umefikiri vizuri kabla ya kukata shauri ya kuacha kazi? Nakwambia, Mkongwe. halafu utakuja kujuta na kama unavyojua, majuto mjukuu. Inakupasa ufikiri vizuri kwani halafu utakuja taka kurejea na Bwana hatokukubali tena.”



    “Nani? Mimi, nirejee tena hapa kwa mnyonyaji huyu anayetutesa bila ya hata kutuonea huruma? Nastahabu kufa na njaa kuliko kurejea hapa. Mimi nimeshafikiri barabara na nimeshaamua kwenda kujiunga na wenzangu katika shamba la ushirika. Nitakwenda huko kuishi kijamaa pamoja na wakulima wenzangu. Huko mambo ni mazuri kabisa. Huko wana ng’ombe kiasi ya hamsini na mpaka hivi sasa wanawake walioko huko hawatoshi kwa kazi za ufugaji. Kuna kuku, kuna mbuzi; shamba hilo ninalokwambia ni zuri sana,” Mkongwe alimweleza Kijakazi.



    “Shamba hilo ni zuri kuliko la Bwana?”



    “Eh, Kijakazi shoga! Bwana wako hana shamba tena. Wewe uko wapi siku zote hizi?”



    “Na hao ng’ombe wote wa nani?”



    “Ni wa kila mtu aliye mfanyakazi wa shamba hilo.”



    “Lakini vipi ng’ombe hao wanaweza kuwa wa watu wote? Vipi kila nunoja ataweza kuyajua maziwa yake?”



    Mkongwe alikaa vizuri akiona huu sasa ndio wakati wa kumfahamisha Kijakazi.



    “Hebu sasa Kijakazi nisikilize vizuri,” Mkongwe alianza. “Maziwa yote hutiwa ndani ya madebe na kupelekwa madukani kwa ajili ya kuuzwa. Pesa zinazopatikana hugawiwa kwa mujibu wa kazi aliyofanya kila mmoja katika shamba hilo na zinazobakia hutengwa na kuwekwa katika mfuko wa akiba wa shamba hilo. Mpango huu huu ndio unaofuatwa kuhusu mazao mengine kama vile mpunga, muhogo na kadhalika. Ukifanya kazi zaidi unapata pesa zaidi; umefahamu?”



    Kwa wakati ule Mkongwe alijihisi kama ni mwalimu anayemfahamisha mwanafunzi jambo ambalo hakupata kulisikia. Kijakazi alishangazwa na maneno ya Mkongwe kwani yale yalikuwa lu mengine mapya ambayo hakupata kuyasikia katika maisha yake.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    “Nani mkubwa huko? Nani kama Bwana Fuad?”



    “Sikiliza Kijakazi; wewe umekwishazoea kila wakati uwe unachungwa na kuamrishwa. Wewe unataka kila wakati awepo mtu na fimbo nyuma yako huku anakupigia makelele kaina mnyama asiye na thamani.” Mkongwe alimweeleza Kijakazi huku akimsogelea karibu.



    “Sikiliza Mkongwe mwanangu, hayo ndiyo majaaliwa yangu. Kuna wengine Bwana Mungu amewajaalia na kuwatukuza mabwana wakubwa na wengine amewajaalia umasikini. Lazima ufahamu Mkongwe kama kila mtu na majaaliwa yake. Hivi ndivyo ulivyo ulimwengu.”



    “Hivyo sivyo ulimwengu wa leo ulivyo,” Mkongwe alisema kama kutaka kumsuta Kijakazi.



    “Sivyo?”



    “Sivyo,” alijibu Mkongwe. “Ni kweli hivi sasa kuna matajiri na masikini lakini nakuahidi kwamba matajiri hawataendelea kuwa matajiri na masikini hawatakufa masikini. Mambo yamebadilika,” Mkongwe alisema.



    “Kayabadilisha nani?” Kijakazi aliuliza kama kutaka kufanya stihizai.



    Kwa hamaki Mkongwe alijibu, “Watu! Watu wenyewe ndio. walioyabadilisha. Wale unaowaona wakija na kuondoka hapa pamoja na wenziwao wengi ndio waliyoyabadilisha mambo!”



    “Sikiliza mtoto; hutobadilisha kitu cho chote kwa kunipigia makelele. Jitulize na useme taratibu,” Kijakazi alimwambia Mkongwe huku akiwa na hofu Fuad asiyasikie waliyokuwa wakizungumza.



    Mkongwe, ambaye alijawa na hamasa, alianza tena kuzungumza kwa sauti ya chini. Alihisi kwamba alifanya makosa kumpigia makelele Kijakazi wakati wajibu wake ulikuwa m kumfahamisha kwa utaratibu mpaka aelewe.



    “Kijakazi! Najua kwamba wewe unamwogopa Fuad. Najua kuwa wewe m mtumishi wake mtiifu, tena mtiifu wa kutolewa mfano...”



    “Ah! Kweli?” Kijakazi aliukunjua uso kwa furaha kwa kuambiwa vile na Mkongwe.



    “Wacha upumbavu wako unisikilize ninavyokwambia!” Mkongwe alihamaki tena na kumpigia makelele Kijakazi.



    “Ninajua kuwa Fuad anakuamini sana wewe na siku hizi anakwita chumbani kwake ukamwuguze. Pia najua kakwambia usishirikiane na mimi. Ndiyo maana siku hizi unanikimbia kama shetani anavyoukimbia Msahafu. Lakini Kijakazi jifikirie nawe. Kwa nini ufanyisbwe kazi kama punda kwa pesa mbili tu?”



    “Siyo suala la pesa shoga yangu!”



    “Nini basi?”



    “Ni utiifu wa kazi tu,”



    “Utiifu wa kazi! Utiifu kwa nani? Kwa bakhili yule, mtu ambaye anaweza kuitafuna hata shahamu yake mwenyewe? Mimi siwezi tcna kuvumilia mateso yake.”



    “Mkongwe mwanangu,” Kijakazi alianza kusema huku akimpiga piga bega Mkongwe, “hili ni jambo usiloweza kulielewa. Mimi si kama nipo hapa kwa ajili ya Bwana Fuad tu bali kwa kila kilichomo ndani ya shamba lake. Mama yangu amemaliza maisha yake hapa na mimi nimedhamir’a kufuata unyanyo wa mama yangu. Mimi nipo hapa kwa yote yaliyopo hapa; Bwana Fuad, kuku wake, ng’ombe wake na kila kilichomo ndani ya shamba hili mimi nakipenda. Nimeazimia kutum’ka hapa mpaka kufa kwangu.”



    Mkongwe alinyamaza kimya. Alitaka kumwuliza Kijakazi kama huyo Bwana wake alipata kumnunulia ijapokuwa gwanda la kaniki lakini hata hivyo alinyamaza kimya akijua kwamba maneno aliyoyasema Kijakazi yalitoka ndani ya moyo wake na kwamba hilo ni jambo linalopasa kuheshimiwa. Lakini hata hivyo hakuacha kuzipinga fikra za kipumbavu za Kijakazi, fikra za kitumwa, utumishi wa upofu, utumishi unaomdhalil’sha binaadamu.



    Kwa sauti ya chini Mkongwe alianza tena kumweleza Kijakazi.



    “Kijakazi! Wewe kweli ni mtiifu na katika maisha yangu sijapata kumwona mtu mtiifu kukushinda wewe. Lakini kuna faida gani kumtii mtu huyu. Wewe umepoteza maisha yako yote katika shamba hili na bado huna cho chote cha kuonyesha ulichopata kutokana na jasho lako. Shamba hili limekunyonya nguvu na damu na kukuunguza kama taa inavyounguza mafuta. Shamba hil’ limekuvunja miguu yako na baada ya miaka yote hiyo ya kazi na utiifu kvva Fuad huna hata kipande cha kaniki cha kujitanda. Ni kweli shamba la Fuad ni kubwa na zuri. Laldni hata ukuti mmoja katika shamba hili si wako wewe. Hakuna cho chote kilicho chako. Wewe mwenyewe hujimiliki. Binaadamu unamilikiwa na mwenye shamba kama anavyomiliki kuku na ng’ombe. Hata hao kuku na ng’ombe wana afadhali kuliko wewe kwani wao walau hupata chakula oha kutosha. Wewe hupati chakula cha kukutosha. Habidhi yule hakuthamini wewe hata kidogo. Hata mimi nilikuwa nikiishi haijambo kidogo kuliko wewe. Kwa muda mrefu watu wote hapa wamekuwa wakikuepuka kwa kuchelea usije ukamwambia Fuad yale waliyokuwa wakizungumza. Lakini sasa unaelewa kila kitu, sikuweza kukuficha tena yaliyokuwemo ndani ya kifua changu. Mimi ninaondoka hapa.”



    Kijakazi alikuwa na wasiwasi alipokuwa akizungumza na Mkongwe. Alihisi kama Bwana wake aliyasikia yote yaliyosemwa na Mkongwe. Alimtumbulia macho Mkongwe na ghafla akaanza kulia.



    “Mkongwe! Mkongwe! Tafadhali nyamaza upuuzi wako na niondokee mbele ya macho yangu. Tafadhali ondoka uende zako. Wewe huwezi hata kunionea huruma!” Kijakazi alipiga kelele huku machozi yakimmiminika.



    “Kijakazi shoga yangu, tafadhali nyamaza kulia. Usilie namna hiyo, mimi sikukwambia jambo lo lote lililo baya; tafadhali nyamaza kulia namna hiyo. kwani ukiendelea utaweza kuniliza na mimi. Basi naondoka nenda zangu takini nakuomba ukipata nafasi uje unitembelee siku moja na tutazungumza zaidi habari hizi,” Mkongwe alisema.



    Pale pale alitoka chumbani kwa Kijakazi na hakungojea tena siku ya pili ifike kama alivyokusudia mwenyewe. Alichukua kile kifurushi alichokifunga na bila ya kumuaga mtu ye yote isipokuwa Kijakazi alishika njia kulikimbia na kulihama shamba la Fuad. Alimwacha Kijakazi kwikwi imemshika kwa namna alivyokuwa akilia.



    Siku nzima ile Kijakazi alifanya kazi huku akiwa na majonzi makubwa. Mkongwe amemtukania Bwana wake; amemwita mwizi, hana adabu, bakhili na sifa nyingi nyingine mbaya. Kwa Kijakazi Fuad alikuwa m mtu aliyetimilia; hakuna mwenye heshima na adabu kumshinda yeye, hakuna mzuri wa kumshinda yeye; hana dosari hata kidogo. Na tazama leo, Mkongwe amekuja kumchamba mbele yake.



    “Sitomsahau mtoto yule. Ama kweli watoto wa siku hizi hawana adabu!” Kijakazi alisema peke yake.



    Kijakazi alifanya kazi hii na ile. Mara kwa mara alijipitisha mbele ya chumba cha Fuad ili apate kuitwa asifiwe kwa utiifu wake, lakini hakuitwa tena. Fuad alikuwa amepata nafuu kidogo na lile gamba la chokaa lilikwisha tolewa mguuni mwake.



    Mara moja, Kijakazi alipokuwa akijipitisha hapo, Fuad alimwita.



    “Kijakazi! Njoo hapa!”



    Kijakazi alisita kidogo, amefurahi, ile fursa aliyokuwa akiitaka kwa muda mrefu sasa ameipata. Alitabasamu lakini punde alimpigia makelele na kumsitua.



    “Unacheka nini? Jambo gani linalokuchekesha? Nakwambia njoo hapa!”



    Fuad alikuwa amekwisha kuyasahau yote yale aliyomwambia siku ile alipokuwa ameupakata mguu wake mgonjwa. Si mama yake wa’ pili tena. Wala si sawa na yeyote yule ndani ya nyumba ile. Ni Kijakazi tu kama kawai. da.



    “Yuko wapi Mkongwe?”



    Kijakazi alitaka kujibu kwamba amekwenda zake lakini alikuwa na hofu ya kujibu hivyo asije akaambiwa na yeye alikuwa akishirikiana naye kwani alikwisha onywa asifanye hivyo.



    “Sijui Bwana!”



    “Hujui? Ebo! Nenda kamtafute aje kunisafishia viatu vyangul” Fuad aliamuru kwa makolele kama kawaida yake.



    “Sijui nitamwona wapi, Bwana!”



    “Hujui utamwona wapi? Neoda kamtafute mpaka umwone!”



    Sasa Kijakazi alifikwa na kazi kubwa. Kazi ya kumtafuta Mkongwe ambaye alikuwa na hakika hayupo tena shambani mwa Fuad. Hakujua alikokwendea na alilolijua ni kwamba amekwenda kujiunga na wale ambao Fuad anawaita wahuni. Kijakazi alikuwa na hofu ya kumwambia Fuad hivyo kwani pindi akimwambia basi lazima atakabiliwa na swali la “ulijuaje isipokuwa na wewe unashirikiana nao?” Wasiwasi ulimjaa wala hakujua la kufanya.



    Alihangaika kumtafuta kwenye kila pembe ya shamba la Fuad huku akijua hakika hawezi kumwona.



    Baada ya muda mrefu Kijakazi alirejea kwa Fuad akamkuta amekaa ukumbini.



    “Sikumwona Bwana!”



    “Hukumwona? Ng’ombe we! Nimekwambia usirejee hapa mpaka umwone!”



    “Lakini, Bwana......”



    “Lakini, lakini, lakini nini?”



    “Lakini, Bwana, nimemtafuta kila pahala sikumwona!”



    “Umekwenda kibandani kwake?”



    “Nimekwenda kila pahala, Bwana! Hakuna pembe ya shamba hili niliyoibakisha, lakini sikumwona!”



    “Ahaa! Hukumwona sio? Mwachilie mbali! Lazima amekimbia hapa na mimi nitakwenda kumwona baba yake. Mzee Sharwan, nimuhadithie kila kitu,” Fuad alisema, lakini sasa kwa sauti ya chini.



    “Umari je, umemwona po pote?”



    “Umari nimemwacha kule bondeni anapalilia mpunga,” Kijakazi alijibu.



    “Nenda kamwite basi!”



    Kijakazi alikuwa amechoka lakini, ndio yumo katika utiifu; kumtii Bwana wake. Bila ya kupoteza wakati alikwenda mpaka kule alikokuwa Umari.



    Alimkuta Umari ameshughulika, tumbo wazi. anapalilia mpunga.



    “Umari, Bwana anakwita.”http://pseudepigraphas.blogspot.com/



    Umari aliinuka na kujiuyosha, kijasho kinamtoka. Ali mtazama Kijakazi na halafu akatikisa kichwa.



    “Kwani Kijakazi hunioni kama mimi nina kazi mkononi?” Umari aliuliza.



    “Nimemwambia kuwa unapalilia mpunga lakini kanituma nije nikwite,” Kijakazi alijibu.



    “Nenda kamwambie sitaki,” Umari alisema.



    “Ah! Mimi sitoweza kumjibu hivyo!” Kijakazi alisema.



    “Usiogope, Kijakazi, nenda kamwambie hivyo hivyo. Usimwogope yule, Kijakazi: wakati wake umekwisha, na sote hapa tunangojea siku ifike tuondoke. Labda utabakia wewe peke yako hapa, Kijakazi.” Umari alisema huku akitabasamu,



    Mbio, Kijakazi alirudi na alipofika alimkuta Fuad amekaa pale pale ukumbini.



    “Yuko wapi?” Fuad aliuliza kwa hamaki.



    “Anasema... anasema...” Kijakazi hakuweza kusema kama alivyoambiwa.



    “Anasema nini?” Fuad aliuliza huku amesimama baada ya kuondoka kwa ghafla juu ya kiti alichokuwa amekalia. “Anasema nini?”



    “Arasema hataki!” Kwa khofu Kijakazi alijibu.



    “Hataki? Anathubutu. kujibu hivyo? Mwachilie mbali; leo ndio mwisho wake ndani ya shamba hili.”



    “Basi, wewe Kijakazi nenda ukafanye kazi zako na huyo Umari akija tutaonana mimi na yeye.”



    Kwa hakika Fuad mwenyewe alikwisha kuelewa kwamba siku zake zimekwisha ila alijikaza kisabuni tu. Kila mmoja katika watanyakazi wake alikwisha yajua hayo isipokuwa Kijakazi.



    Kijakazi aliendelea na kazi zake tangu asubuhi mpaka magharibi. Usiku ulipofika alijitia chumbani mwake na kujinyosha. Alijitupa na kulala chali, macho yake yakiangalia boriti za dari. Taa ya kibatari iliyokuwamo humo ilitoa mwangaza mdogo uliomwezesha kuona bali duni ya maisha yake lakini haukutosha kumwonyesha jinsi gani atokane nayo. Zlimjia fikra nafflna kwa namna na katika jambo lililozidi kumharibu akili yake lilikuwa ni mazungumzo yake na Mkongwe. Alijaribu kujikurupusha ili zimtoke fikra alizokuwa nazo lakini hakuweza.



    Hata usingizi ulimruka. Alijihisi kama mtu aliyefikwa na msiba mkubwa. Mazungumzo ya Mkongwe yalimchafua moyo wake. Alihisi Mkongwe anataka kumfarakanisha na Bwana wake mpenzi Fuad.



    Aligaragara, mara ageuze ubavu huu mara ubavu ule lakini usingizi hakuupata kamwe. Mara zilimjia fikra za Fuad. Alifikiri jinsi alivyokuwa ameupakata mguu wake huku akizungumza naye taratibu. Hakupara kusemeshwa taratibu na Fuad hata siku moja isipokuwa siku ile aliyomwita akamwuguze. Lakini sasa hata mawazo haya hayakuweza kumletea Kijakazi furaha kwani pale pale zilimjia fikra za jinsi alivyotukanwa kabla hata’ hajawahi kuimba ule wimbo aliotakiwa na Fuad auimbe.



    Mara aliyasikia kichwani mwake maneno aliyoambiwa na Umari, “Usimwogope yule, zake” zimekwisha.” Aliyafikiri maneno haya lakini kwake yeye havakuwa na maana yo yote. Hakufahamu Umari alikusudia nini.



    Baada ya kufurukuta huku na huku kwa muda mrefu usingizi ulimchukua. Katika huo usingizi alitoa ndoto ya ajabu. Aliota anamnyonyesha mtote mchanga na mtoto huyo alikuwa akizivuta chuchu zake kwa nguvu kwa ajili ya njaa aliyokuwa nayo. Kijakazi alishindwa kuvuta pumzi kwa namna mtoto huyo alivyokuwa akizivuta chuchu zake. Mwisho Kijakazi aliweza kumgandua mtoto huyo kifuani na kupata nafasi ya kuvuta pumzi. Mara ndoto ilibadilika na badala ya kitoto kile kilichokuwa kikinyonya aliuona uso wa bwana shamba unamulika; amemsimamia mbele yake anampigia kelele. Kijakazi alishtuka na kuzindukana.



    Kijakazi aliamka mapema na kama kawaida yake alisafisha uwanja, akawalisha ng’ombe na kuwapa maji. Alifanya kazi zake zote. Baada ya kumaliza, alikusanya taka akazitia ndani ya debe na kulichukua debe hilo kwenda kulimwaga.



    Wakati anapita mbele ya nyumba ya Fuad na pipa lake la taka kichwani, Fuad alichungulia dirishani pa mara alimwona na kumpigia makelele, “Kijakazi! We Kijakazi! Njoo!”



    Bila ya kufikiri, Kijakazi alitua pipa la taka alilokuwa amelichukua na kukimbilia chumbani kwa Fuad. Hakujua anakwenda kuambiwa nini tena la kheri au shari.



    Alimkuta Fuad amelala kitandani.



    “Njoo univue viatu!” Fuad aliamrisha.”



    Kijakazi alikaa pembeni ya kitanda na mara Fuad alintupa mguu wake juu ya mapaja yake. Fuad alikuwa amekula amevimbiwa hata hawezi kufurukuta. Kijakazi aliweza kuona namna gani Fuad alikuwa anahisi joto kwa namna uso wake ulivyomwiva.



    “Fanya upesi na wacha kunipotezea wakati wangu!” Fuad aliamuru.



    Kwa mara ya kwanza katika maisha yake, Kijakazi alimwangalia Fuad kwa karibu. Macho ya Fuad yalikuwa yamedidimia ndani ya uso wake na matone ya majasho yanang’aa juu ya kipaji chake. Kijakazi alikuwa akimvua viatu Fuad na wakati huo ilimjia huruma kubwa kumhurumia Bwana wake, Fuad mpenzi. Alimhisi kama ni mateka asiyekuwa na silaha. Hapo hapo Fuad alichukuliwa na usingizi na Kijakazi alimvua viatu taratibu ili asije akamwamsha. Hapo hapo Kijakazi ilimjia fikra nyingine na kufikiri labda kuna mtu anamhadaa. Alijiuliza moyoni, “Nani hasa anayejaribu kunihadaa? Nani? Nani hasa?” Na baada ya hapo mara kwa mara Kijakazi aHkuwa anajiuliza swali hili. Kulikuwa kumekwisha pambazuka, lakini Fuad hakuinuka kitandani ijapokuwa alikuwa yu macho. Hewa nzuri ya upepo wa umande uliokuwa ukivuma alfajiri ulimtia uvivu Fuad na kumfanya abakie hapo hapo kitandani akiwa amejifunika shuka.



    Hakuwa na raha ya moyo hata kidogo licha ya kuwa kila alichokitaka katika raha za maisha aliweza kukipata. Pesa alikuwa nazo, tena nyingi, lakini maisha hakujua yanaendea wapi. Kila alilotaka kulifanya aliona silo. Khofu na wasiwasi vilimjaa moyooi.



    Alihisi mambo yamebadilika. Heshima aliyokuwa akipewa ilikuwa inapungua, kwani hata Umari naye huitwa na kuthubutu kujibu “staki”. Aliiona dunia imempa kisogo na mambo yamembadilikia.



    Fuad alikuwa amejinyosha hapo kitandani fikra namna kwa namna zikimjia kichwani mwake. Alifikiri labda mambo huenda yakabadilika. Alijigeuza huku na huku pale kitandani alipokuwa amejinyosha na mara alisikia sauti ya mtu ikiita kutoka nje, “Hodi! Hodi!”



    “Karibu!” Fuad aliruka kutoka pale kitandani kidogo aanguke. Alijizoazoa na kujifunga sbuka aliyokuwa ameivaa kiunoni uzuri, na bila ya hata kunawa uso Fuad alitoka nje kwenda kumsikiliza aliyebisha hodi.



    Hapana aliyewahi kujibu. Mara Fuad alifika mlangoni huku akijipangusa tongo zilizokuwa zimemjaa machoni.



    “Je, kumezidi nini tena; mbooa leo asubuhi na mapema?” Fuad aliuliza.



    ‘Tumekuja tunataka kuonana na wewe mara moja, alijibu mmoja katika wale vijana.



    Wote wanne walikuwa wamevaa mashati na suruali, viatu virefu vya mpira na makofia makubwa ya ukuli. Walikuwa wamechukua vijiti vifupi vilivyochongwa katika ocha moja na kamba ndefu iliyozongwazongwa. Walikuwa ni watu wapya ambao Fuad hakupata kuwaona - sio wale waliokuja kila siku. Hata hivyo alihisi kuwa hata wao ni katika kundi la wale wale wanaokuja kumkera kila mara.



    “Piteni ndani. Karibuni ukumbini; lakini tafadhalini nisubirini kidogo nikajitie maji, “ Fuad aliwaambia wageni wake ambao hakujua walilolijia.



    “Hapana kitu, fanya kazi zako kwa utulivu. Sisi tutakusubiri hapa nje.”



    “La! Kwa nini mkae nje? Piteni ndani. Karibuni... nyumba, nyumba yenu,” Fuad alisema.



    Bila ya kupoteza wakati katika kujadiliana ama waingie au wasiingie, wote waliingia ndani na walifululiza moja kwa moja mpaka ukumbini. Walikaa juu ya makochi mazuri yaliyokuwamo ukumbini hapo na kila mmoja katika wao alianza kutazama huku na huku baada ya Fuad kwenda msalani. Walishangazwa na mapambo waliyoyaona ukumbini hapo na mara mmoja katika wao alisema kwa sauti ya kunong’ona, “Hadi amestarehe kijana huyu!”



    Hakuna aliyejibu katika wale wenzake, walinyamaza kimya wakitazamana macho. Walikaa kwa kituo hapana aliyekuwa na wasi wasi, wote wanamngojea Fuad kwa hamu kubwa.



    Fuad alifanya haja zake zote na alipomaliza aliingia chumbani na kuvalia nguo zake. Baada ya kumaliza alikuja pale ukumbini ili kuwasikiliza wageni wake na kujua nini lililowaleta pale



    “Naam, mnasemaje?” Fuad aliuliza huku wasi wasi umemwingia.



    “Sisi ni watumishi wa Idara ya Ugawaji wa Ardhi,” alisema mmoja katika wale wageni wa Fuad.



    Fuad roho ilimpiga na moyo ukaanza kumwenda mbio. Aliona sasa kweli imedhihiri.



    “Idara ya Ugawaji wa Ardhi?” Fuad aliuliza, macho yamemtoka.



    “Ndiyo”.



    “Ehe! Mna shida gani n’nayoweza kukusaidieni?” Fuad aliuliza, uso umemwiva, midomo inamcheza.



    “Tunataka utuonyeshe mipaka ya shamba lako,” alisema yule mtu.



    “Kwani mna...” Fuad alitaka kusema kwa hamaki. Kabla hajamaliza aliyotaka kuyasema alikuja matao ya chini na kuzizuia hamaki zake za “hayati Bwana”.



    “Mipaka ya shamba langu siyo?” Fuad aliuliza.



    “Ndiyo,” alijibu yale kijana.



    “Kaskazini limepakana oa shamba la Ruwehi, kusini nashambala...”



    Kabla hajamaliza yule mtu alimkatiza maneno yake “Sisi hatutald maelezo, tunataka ukatuonyeshe wewe mwenyewe.”



    “He! Itakuwa kazi kubwa, kazi ya kutwa; pengine hata tusiimalize,” Fuad alisema.



    Tunajua.”



    Fuad aliinama chini na kufikiri. Hakujua la kufanya Mara aliinua kichwa na kusema, “Basi nisubirini kidogo.”

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Aliingia ndani bila ya hata kuwa na haja yo yote na mara akatoka nje.



    “Haya twendeni.”



    Safari ya kwenda kukagua mipaka ya shamba la Fuad ilianza; nayo ilikuwa ndefu. Walikwenda kaskazini na kusini, mashariki na magharibi huku wakipima kila sehemu waliyokuwa wakiikagua kwa kamba zao. Baada ya kila marefu waliyoyataka walichomeka kijiti katika vile vijiti walivyokuwa navyo. Fuad alikuwa amechoka taabani, anakwenda aldpepesuka kama mtu aliyekunywa chupa nzima ya tende. Hakupata maishani mwake kwenda masafa marefu kwa miguu kama siku ile. Hapana aliyekula kitu isipokuwa matunda mbali mbali waliyoyaangua kutoka kwenye miti ya matunda iliyokuwa shambani mle.



    Huku nyuma Kijakazi alijawa oa wasi wasi. Kutwa nzima hakumwona bwana wake wala hakujua ameendea wapi. Alitaagatanga kila pembe lakini hakufanikiwa kumwona bwana wake mpenzi Mwishowe aliangukia kibandani kwa Umari ambaye siku ile alikuwa hakwenda kazini kupiga majalbe.



    “Umari mwanangu! Hukumwona Fuad?”



    Umari aliyekuwa amekaa juu ya kigogo cha mnazi nje ya kibanda chake alimtazama Kijakazi kwa jicho la humma kama kutaka kumwambia “masikini roho yako.”



    “Kwani unamtafutia nini? Umari aliuliza.



    “Leo kutwa sijamwona; sijui amefikwa na masahiba gani!” Kijakazi alijibu na kuuliza huku akionyesha ni mtu mwenye wasi wasi mkubwa.



    “Mimi pia sijamwona; sijui yuko wapi?” alisema Umari.



    “Masikini! Sijui yuko wapi tena? Anajitabisha ilhali mguu wake hata haujapona uzuri” alisema Kijakazi.



    Hapo hapo Kijakazi aliondoka na kuendelea na msako wake wa kumtafuta Fuad.



    Umari hakushughulishwa na cho chote. Alikuwa amekwisha pata fununu kwamba shamba la Fuad karibu litachukuliwa lakini hakujua lini. Yeye alikuwa anangojea siku ifike tu.



    Fuad na wageni wake waliendelea kulipima shamba mpaka jua lilipokuchwa. Kazi yote ilimalizika magharibi na. baada ya kumaliza wakaanza safari ya kurejea nyumbani kwa Fuad. Lilikuwa shamba kubwa lililojaa miti ya kila aina. Baada ya masafa marefu walifika nyumbani kwa Fuad na hapo mmoja katika wale watu alimwomba Fuad wazungumze kidogo.



    Kijakazi alikuwa amekaa nje ya nyumba ya Fuad amejikunja lakini unyonge wote ulimwisha alipomwona Fuad anarejea. Alifurahi kama vile anavyofurahi mtoto mchanga anapomwona baba yake baada ya kutomwona kwa muda mrefu. Alitabasamu na kushusha pumzi



    “Si bora tukenda ukumbini kwa mazungumzo yetu?” Fuad alitoa shauri.



    “Haya, po pote pale ni sawa.”



    Waliingia ukumbini na kukaa juu ya makochi. Wote walikuwa wamechoka lakini Fuad alikuwa amechoka zaidi.



    Mara Fuad alipiga makelele na kumwita Kijakazi, “Kijakazi!”



    “Bee!” Kijakazi aliitika mbio mbio.



    “Hebu tuletee maji ya kunywa.”



    Haikuchukua muda mara Kijakazi aliingia ndani na jagi la maji pamoja na gilasi. Aliviweka vitu hivyo juu ya meza iliyokuwapo katikati ya ukumbi buo na bapo hapo alitoka nje.



    “Yule ni nani?” aliuliza mmoja wa wale watu.



    “Yule ni mzee wangu. Yupo hapa siku nyingi tokea uhai wa marehemu baba yangu,” Fuad alijibu.



    “Alaa!” alisema yule mtu.



    Kila aliyetaka kunywa maji alijitilia mwenyewe ndani ya gilasi na kunywa. Fuad alikaa juu ya kiti akiwa amechoka sana hata hakuweza kujiinua.



    “Naam, sasa mnasemaje?” Fuad aliuliza.



    “Sisi hatuna maneno mengi. Jambo tunalotaka kukwambia ni kwamba hili shamba tumekwisha lipima na sasa litakuwa ni mali ya serikali na tutawagawia wale wakulima wasiokuwa na ardhi, lakini ilivyokuwa na wewe ni mtu vile vile na unahitaji kuendesha maisha yako basi tutakukatia eka tatu katika sehemu yo yote ile unayotaka mwenyewe na sehemu hiyo itakuwa yako wewe.



    Fuad alishtuka, roho ilimruka na alikaribia kuzimia. Hakuwa na la kusema, kabaki kushangaa, kinywa wazi. Machozi yalianza kumlengalenga lakini ilimbidi ajizuie kulia Mara alianza kusema kwa unyonge. “Hivyo nd’o mnaninyang’anya shamba langu?”



    “Ala! Kwani hawakuja watu kukwambia habari ya sheria ya ardhi iliyopasishwa na serikali ya kimapinduzi?” aliuliza mmoja katika wale watu.



    “Ah Walikuja, lakini...”



    Fuad hakuwa na la kusema. Alikuwa hata hajui analolisema wala analolifanya.



    “Lakini nini?” aliuliza yule mtu.



    “Lakini hili ni shamba langu, haki yangu mwenyewe nimerithi kwa marehemu baba yangu!”



    “Kama tulivyokwambia, sisi ni wajumbe tu na mjumbe hauawi. Maneno yotu nd’o kama tulivyokwisha kukwambia. Kama una malalamiko yo yote unaweza kufika makao makuu ya onsi yetu huko mjini.”



    “Ah haya bwana, mimi sina la kusema. Fanyeni mna. vyotaka,” Fuad alisema shingo upande na mnyonge kabisa.



    Pale pale wale watu walitoka na kumwacha Puad amekaa pale ukumbini. Alibakia pale pale juu ya kiti amepigwa na bumbuazi hajui la kulifanya. Hamaki zilikuwa zimemjaa lakini alizidiwa nguvu. Usiku ulikuwa umekwisha ingia na Fuad aliwasha karabai na baadaye akarejea pale pale alipokuwa amekaa juu ya kiti.



    Kijakazi ambaye alikuwa amekaa pale palenjeya nyumba aliingia ndani kwenda kumwangalia Fuad baada ya kumwona kimya kwa muda mrefu. Alinyatia kidogo pale ukumbini, na alipochungulia ndani humo alimwona Fuad amelala usingizi juu ya kiti. Huruma za moyo zilimjaa na aliweza kubaini mara moja kwamba watu wale walikuja kumkera Bwana wake. Alikwenda mpaka karibu yake akapiga magoti chini na kuanza kumvua viatu vilivyokuwa vimechafuka kwa dongo jekundu.



    Mara Fuad alizindukana na kumsukumia teke Kijakazi.



    “Unafanya nini hapa? Nani kakwita? Tokea lini ukathubutu kuingia ndani humu bila ya kuitwa. nyama mkubwa wel” Fuad alipiga makelele.



    Kijakazi alianguka chini vibaya kidogo kichwa chake akipige sakafuni. Alijiburura nyuma na kuegemea ukuta huku amejikunyata kama mtu aliyeshikwa na baridi kali.



    “Nisamehe, Bwana! Nisamehe! Kweli nimefanya makosa lakini nilikuona umechoka nikahisi bora nikuvue viatu upate kupumzika uzuri!” Kijakazi alisema huku sauti yake imejaa kitetemeshi kwa khofu aliyokuwa nayo.



    “Haya ondoka hapa kabla sijakuvunja kichwa chako; upesi niondokee mbele ya macho yangu, kisirani mkubwa we!” Fuad alipiga kelele, amekwisha pata mnyonge wake wa kummalizia hasira zake.



    Kijakazi alijizoazoa na kwa haraka akatoka nje moja kwa moja mpaka kwenye kile kijichumba chake nyuma ya banda la ng’ombe na kujitupa chini.



    “Ah! Mtoto huyul Sina n’nalolifanya likawa na kheri?’’ Kijakazi alijiuliza. “Lakini haidhuru,...”



    Huku nyuma hasira zilimzidi Fuad akawa anapiga makelele kama mwenda wazimu.



    “Eka tatu, eka tatu, eka tatu zitanitosha nim mimi? Sina haja nazo; na wapate wao. madhalimu wakubwa! Wallahi! Wallahi, nitasoma halbadiri. Haidhuru, waache wachukue shamba langu, na wapate wao, lakini watapukutika mmoja mmoja. Hawajui kama marehemu baba alilizindika shamba hili? Waache wote watatokomea!” Fuad aliendelea na makelele huku akitoka pale ukumbini na kuelekea chumbani kwake.



    Kwa namna alivyochoka, Fuad alishindwa hata kuvua nguo. Alivua viatu tu ambavyo alikataa kuvuliwa na Kijakazi, akajitupa kitandani na moja kwa moja usingizi ukamchukua.



    Asubuhi Fuad al’amka tafran. Alitamani aridhi ipasuke aingie, shamba limeshakwenda, shamba lake zuri alilorithi kutoka kwa baba yake, marehemu Bwana Malik. Laiti kama angaliweza, basi angelitia moto lote. Lakini jambo hilo hakuweza kulifanya. Ijapokuwa alikuwa akijidai kuonyesha uhodari anapokuwa peke yake, ukweli wa mambo m kwamba Fuad alikuwa na hofu kubwa na serikali ya kimapinduzi. Hakuweza kupinga sheria hata moja katika sheria zilizokuwa zikitangazwa na serikali ya kimapinduzi ijapokuwa hakupendezewa wala kukubaliana na sheria yo yote katika sheria hizo. Uhodari wake wote ilikuwa ni kuisubu serikali ya kimapinduzi wakati anapokuwa peke yake pamoja na wale waliokuwa mabwana shamba kama veye ambao walikuwa wakija kumtembelea mara kwa mara.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Siku kadhaa zilipita na hata Kijakazi na upumbavu wake wote sasa aliweza kuhisi kama pana mabadiliko fulani yaliyotokea pahala pale. Aliwaona watu namna kwa namna wakija shambani hapo; watu ambao hapo zamani hakupata kuwaona, wakija wakilima au kuokota nazi bila ya mtu ye yote kuwaambia kitu cho chote.



    Umari naye pia alipatiwa eka tatu katika shamba lile alilotumika maisha yake yote na sasa alikwenda kondeni wakati alipotaka yeye mwenyewe tu. Fuad hakuwa na amri tena kwa ye yote katika shamba lile. Hakushughulika na cho chote. Mahanda ya ng’ombe na ya kuku yalikuwa yakibomoka anayatazama macho tu wala hachukui taabu ya kuyatengeneza.



    Alikuwa hamwulizi mtu ye yote anayekuja shambani pale. Sasa safari za mjini zilikuwa hazimwishi.



    Kijakazi hakuweza kukaa na ujinga wake na aliona bora aulize ili apate kuyajua. Hapana ye yote ambaye angeliweza knmwuliza akamweleza kwa kituo isipokuwa Umari. Kwa hiyo ilipofika jioni wakati watu washarejea makondeni, alijiburura kidogo mpaka kibandani kwa Umari.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog