Search This Blog

Tuesday, 1 November 2022

PENZI AMA KABURI - 4

 






Simulizi : Penzi Ama Kaburi

Sehemu Ya Nne (4)





“Na unasomea nini?”

“Nasomea mambo ya kijamii...kama una matatizo ya kimapenzi, naweza kukusaidia,” alisema jamaa huyo huku akimwangalia Shadya, wakaanza kucheka.

“Ooh!”



“Yeah! Nina kurasa zangu zangu zinaitwa Mapenzi na Mahusiano, unaweza kuingia Facebook, Instagram, zipo huko,” alisema jamaa huyo.



“Sawa!”

Shadya akabaki kimya kwa sekunde kadhaa, alimwangalia jamaa huyo, kwa jinsi alivyoonekana tu, kweli alionekana kufahamu kuhusu mapenzi, mtoa ushauri mkubwa tu.



Kitu alichokuwa akihitaji kipindi hicho ni ushauri wa kimapenzi tu. Akili yake ilivurugika, mapenzi juu ya Gibson yalimuumiza kupita kawaida.



Alihisi kama alikuwa akikosea, inawezekana mwanaume huyo alihitaji mapenzi ya namna hii lakini yeye alipeleka mapenzi ya namna ile.



Wanaume walikuwa tofauti, kulikuwa na wengine waliwapenda wanawake wa hivi wengine wa vile, inawezekana mapenzi aliyokuwa akimpa Ngwali si yale ambayo mtu kama Gibson alitakiwa kupewa na ndiyo maana mwanaume huyo alionekana kubadilika.



“Ila nyie wanaume!” alisema Shadya.

“Tumefanyaje?” aliuliza jamaa huyo.

“Mnafanana!”



“Hahaha! Huwa hatufanani!”

“Kweli tena! Yaani sijui sisi watoto wa kike mnatuchukulia vipi!” alisema Shadya.



“Unamaanisha nini?”

“Hivi mnataka mpewe nini mpaka mjue mtu fulani anawapenda?” aliuliza.

“Inategemea! Wengine ukionyesha kutujali tu, tunajua unatupenda!” alijibu.

“Sasa mwanaume unamfanyia vyote hivyo na bado hakujali! Tatizo huwa ni nini?” aliuliza Shadya.



“Kwanza kwa jina naitwa Alex!” alijitambulisha jamaa huyo.

“Hahaha! Aya Alex niambie!”

“Cha kwanza ni lazima ujue sisi wanaume hatujakamilika, hakuna mwanaume mwenye sifa zote za uanaume bora,” alisema Alex.



“Sawa!”

Inapotokea hivyo, ni lazima wewe mwanamke utumie muda wako kututengeneza sisi. Inawezekana mimi sipendi kutabasamu, muda wote nataka niwe cool, ni lazima wewe uwe mtu wa kutengeneza tabasamu kwangu,” alisema Alex.

“Sawa!”





“Wanawake huwa wanahitaji kupetiwapetiwa ila wanaume wanahitaji hilo kwa asilimia kubwa zaidi ya wanawake, unalijua hilo?” aliuliza Alex.

“Unamaanisha nini?”



“Mwanaume ni shupavu, mtu imara ila jua kuna kipindi moyo wake huvunjikavunjika na hivyo huwa anahitaji kukumbatiwa, kutiwa moyo, mnachokosea nyie wanawake mnataka kutufanya wanaume tujione makomandoo, hapana, huwa tunaumia kama nyie, tuna hisia mno, tunahitaji sana kupetiwapetiwa na nyie,” alisema Alex.

“Nakusikiliza!”

“Ushawahi kumpetipeti mpenzi wako?” aliuliza.



“Hapana! Lakini huwa si tunafanya mapenzi!”

“Shadya, kufanya mapenzi huwa haitoshi. Ngoja nikuulize swali!” alisema.

“Uliza.”



“Siku ina saa ngapi?”

“Ishirini na nne!”

“Huwa mnafanya mapenzi kwa saa ngapi kwa siku?”



“Kama moja ama mbili!”

“Sawa! Tufanye mbili. Baada ya kutoa hayo masaa mawili yanabaki mangapi?”

“Ishirini na mbili!”

“Huwa mnafanya nini kwenye hayo yaliyobaki?”



“Daah!”

“Nisikilize Shadya, upendo si kufanya ngono tu, ngono huwa na asilimia 2.007 kwenye uhusiano wa kimapenzi. Kwenye saa zilizobaki ndipo ambapo unatakiwa kumuonyesha kwamba unamjali, unamthamini na kumsikiliza,” alisema.

“Ooh! Kumbe!”



“Hivi ushawahi kumtoa out mpenzi wako?”

“Hapana!”

“Yeye alishawahi kukutoa?”

“Yaap!”



“Kwa nini wewe hujawahi kumtoa out? Unadhani mwanaume ndiye mwenye wajibu wa kukutoa out? Shadya, mwanaume hupenda kufanyiwa vitu ambavyo hatarajii kufanyiwa kwenye maisha yake.



Hebu mfuate mpenzi wako, mwambie leo nataka nikutoe out, tukale, ufurahi, mnunulie zawadi, tatizo nyie wanawake ndiyo mnataka kufanyiwa kila kitu nyie kwa kuhisi wanaume ndiyo wenye wajibu huo, ndiyo maana wengi hukimbia baada ya kufanya mapenzi na nyie,” alisema Alex huku akimwangalia msichana huyo.



“Aiseeee!”

“Inafika kipindi mwanaume anajiuliza...hivi mbali na ngono, msichana ana kitu gani cha kuofa kwangu? Akiangalia ni kweli hakuna, ni kwa sababu hujawahi kumpelekea zawadi, kumtoa out, kumfanyia mambo mengine ambayo anakufanyia, sasa wengi wakishaona hivyo, wanakimbia zao, mwisho mnaanza kulalamika nyie,” alisema Alex.



“Sasa unataka nifanye nini?”

“Umeuliza swali zuri sana....” alisema Alex, hapohapo akaanza kutoa tabasamu pana usoni mwake.

.

.



“Sasa unataka nifanye nini?”

“Umeuliza swali zuri sana....” alisema Alex, hapohapo akaanza kutoa tabasamu pana usoni mwake.



Alex alikuwa mshauri mzuri wa mahusiano, aliwasaidia watu wengi na katika kipindi hicho alijiwekea uhakika kwamba ni lazima kwa ushauri ambao angeutoa kwa msichana huyo, mwisho wa siku angeweza kubadilika kabisa.

Waliendelea kuzungumza kwa pamoja, walifurahi na wakati mwingine walikuwa wakigongesheana mikono kumaanisha walikuwa wakikubaliana kwenye kila kitu.



Shadya alikuwa msichana wa Kipemba, mzuri, mwenye mvuto wa kila aina, yaani kama ingemtia machoni mwake kwa siku moja tu basi ungekiri kwamba kwenye maisha yako utakuwa umewahi kumuona mwanamke mzuri, pengine kuliko wote uliowahi kuwaona.



Alex alizungumza naye lakini akili yake haikuwa hapo, Shadya alimchanganya na ndiyo maana hata ushauri wa kimapenzi aliokuwa akimpa msichana huyo ulimfanya kuonekana kama mwanaume fulani aliyekuwa akijua kupenda, yaani mwanamke ambaye alikuwa akitoka naye kimapenzi wakati huo inawezekana alikuwa mwenye bahati kuliko wanawake wote katika dunia hii.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Mawazo ya Shadya kwa Gibson yalipotea kwa muda, kwanza alikuwa makini na huyo Alex ambaye alikuwa akiongea kwa mbwembwe nyingi mbele yake.



Baada ya dakika kadhaa, safari ikaanza na kueleka huko walipokuwa wakielekea. Kitu kimoja ambacho kilikuja kichwani mwa Alex ni kuchukua namba ya msichana huyo, ikiwezekana, siku moja ajaribu bahati yake.



“Ila atakubali?” alijiuliza kimyakimya.

“Hawezi kukataa! Yaani ushauri wote huu niliompa akatae? Mh! Haiwezekani, ngoja nijaribu!” alijisemea Alex, hapohapo akamwambia Shadya kuhusu namba yake.

“Wewe namba ya nini?”

“Nataka nikafungie maandazi!” alijibu na kutoa tabasamu. Shadya akaanza kucheka.



“Una vituko wewe mwanaume!”

“Ila sikushindi wewe, yaani mpaka leo hujui namba ni ya kazi gani!” alisema Alex, wote wakacheka tena.







Kwa jinsi alivyokuwa akizungumza, utani aliokuwa amemletea na mambo mengine, Shadya hakutaka kukataa kutoa namba yake, haraka sana akampa mwanaume huyo na hata alipoteremka maeneo ya huko Mwenge tayari kwa kwenda Sinza, tayari Alex alijisemea ilikuwa ni lazima amchukue msichana huyo.



Shadya akachukua bodaboda na kuanza kumpeleka katika mgahawa wa Napoleon uliokuwa Sinza Kumekucha. Mawazo juu ya Gibson yakaanza kujirudia tena kichwani mwake.



Mwanaume huyo alimchanganya, ilifika kipindi kama alianza kuwachukia wanaume wote waliokuwa wakipita mbele yake lakini kuna kipindi alijiona kufanya hivyo ulikuwa ni utoto mkubwa.



Hakuchukua muda akafika hapo, akateremka na kuelekea huko. Gibson hakuwepo, akampigia simu na kumwambia tayari alifika, hivyo akaambiwa asubiri.

Akatafuta sehemu na kukaa, akaagiza juisi na kuanza kunywa taratibu.



Moyo wake kipindi cha nyuma uliamini kabisa huyo Gibson ndiye ambaye angekuwa mwanaume wake wa kufa na kuzikana na ndiyo maana aliamua kuanza kumpotezea Ngwali kumbe hakuwa mwanaume sahihi.



Alimpenda mtu huyo, alikuwa tayari kufanya kitu chochote kile lakini si kumkosa. Aliendelea kusubiri mpaka baada ya dakika kama kumi hivi, Gibson akafika mahali hapo, akasimama na kumkumbatia.



“Unanukia vizuri!” alimwambia mwanaume huyo.

“Ahsante sana,” alijibu Gibson huku akimwangalia Shadya.

Msichana huyo akajisikia raha, hakuamini kama hatimaye alikuwa mbele ya mwanaume huyo, mtu aliyeamini alikuwa akimpenda kuliko yeyote katika dunia hii.



Alitamani kumwambia Gibson maneno yote matamu na mazuri ili aone ni kwa jinsi gani alikuwa akimpenda lakini alishindwa kumwambia hayo kwa kuwa alihitaji kusikia msimamo wake.

“Mbona umebadilika sana?” aliuliza Shadya.



“Nimekuwaje mpenzi?” aliuliza Gibson.

Shadya akaanza kulalamika kama mara ya kwanza. Gibson alikuwa kimya, siku hiyo hakutakiwa kumuonea huruma Shadya, kama angejifanya kuwa baba huruma ilimaanisha angeharibu mambo kwa Paula kwani msichana huyo angemng’ang’ania mwanzo mwisho, ilikuwa ni lazima ajivike sura ya nyani.

“Nipo bize sana!” alisema Gibson.

“Hata kwa mpenzi wako?”





“Shadya! Maisha yananichanganya sana. Unajua unapokosa pesa wakati mwingine mpaka mapenzi huyafikirii kabisa,” alisema Gibson maneno yaliyouchoma moyo wa Shadya vilivyo, lakini akatoa tabasamu kama aliridhika na maneno hayo.



“Oh! Pole kwa ubize mpenzi! Naomba uniambie kitu kimoja,” alisema Shadya.

“Kitu gani?”

“Kuhusu msimamo wako!”

“Upi?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Juu yangu! Ni kwamba tunaendelea kuwa wapenzi ama basi?” aliuliza msichana huyo.



Hakutaka kujishtukia kuuliza swali hilo, kama mwanamke ilikuwa ni lazima aujue msimamo wake, kama angeona aibu kuuliza maswali hayo ilimaanisha hakuwa siriazi na maisha yake.



Ni kweli alimpenda mno Gibson lakini muda huo ulikuwa ni wakati wa kujua ukweli wake, kama kweli alihitaji kuendelea kuwa naye ama la!”

Shadya unajua na...”



“Gibson! Usirukeruke! Ninahitaji kuujua msimamo wako! Wewe ni mwanaume, niambie ukweli, sihitaji kupoteza muda kwa mwanaume ambaye sina nafasi kwake, sipendi kuumizwa, sipendi kulia, ninahitaji nijue msimamo wako!” alisema Shadya, kwa jinsi alivyokuwa akizungumza, ni kama mwanaume aliyekuwa akimwambia mwanamke.



“Naomba muda nijifikirie!”

“Gibson! Hilo ni jibu tosha kwamba sina nafasi kwako, huwezi ukahitaji muda wa kujifikiria juu yangu na wakati unajua mimi ni mpenzi wako. Mapenzi yameshuka, nashukuru kuna mambo nimejifunza kwako,” alisema Shadya huku akionekana kutia huruma.

Ghafla meseji ikaingia kwake. Ilikuwa ni ya Alex.



“Namba yangu huyo,” ujumbe ulisomeka, akausoma, hapohapo akaujibu.

“Nashukuru! Naomba nikuulize swali, nijibu haraka sana.



Kama mwanaume ameniumiza, nikiwa naongea naye, natakiwa nifanye nini ili naye achanganyikiwe?” aliandika, baada ya sekunde kama thelathini ukajibiwa.

“Kill him with your smile!” (muue kwa tabasamu lako) uliandika ujumbe kutoka kwa Alex.



“Sawa!” akaujibu.

“Tena muonyeshe kama hujaumia, yaani kuwa poa, hata kama unalia moyoni.”

“Nimekuelewa!”



Muda wote huo Gibson alikuwa kimya, alimwangalia Shadya ambaye alionekana kuwa bize kidogo na simu yake, alipouinua uso wake, ulitawaliwa na tabasamu pana.





Gibson akashtuka, hakutarajia kuliona tabasamu hilo usoni mwa msichana huyo, alimuuliza maswali yaliyoonyesha kwamba siku hiyo ungekuwa mwisho wa uhusiano wao, alikuwa na uhakika alipendwa, lile tabasamu lilishindwa kumpa majibu sahihi, kama alikuwa akifanya hivyo, inamaanisha alifurahia ama?

“Gibson! Endelea na maisha yako baba!” alisema Shadya kwa tabasamu pana.



“Shadya!”

“Nimekupa nafasi! Unajua hakuna muda wa kulazimishana mapenzi. Mwanamke natakiwa kupendwa, kupetiwapetiwa, hakuna mwanamke anayependa kuona mpenzi wake akiwa bize, yaani bize hata huna dakika na mimi! Naomba niondoke! Najisikia furaha nafsini mwangu,” alisema msichana huyo, uso wake ulikuwa na tabasamu pana kupita kawaida.



“Shadyaaaaaa.....wait......”

Msichana huyo hakujali, akaita bodaboda, akapanda na kuondoka zake. Gibson alibaki akiiangalia bodaboda ile, alitegemea baada ya kuachana na msichana huyo angelia, angehuzunika, angekasirika lakini ndiyo kwanza alimuacha huku akiwa na tabasamu pana moyoni mwake.



Akachanganyikiwa!

Alipokuwa kwenye bodaboda hapo ndipo Shadya alipoanza kulia, moyo wake ulichoma mno, hakuamini kilichokuwa kimetokea. Alihisi akiwa na maumivu makali moyoni mwake kupita kawaida.

Aliingia pupa kwa Gibson, akamvua nguo zake kisha kumuacha.



Hapo ndipo akasikia maumivu makali ya kutengana na mtu na wakati mwingine alihisi kabisa mauamivu hayohayo ndiyo ambayo aliyasikia Ngwali kila alipokuwa akimtafuta kwa lengo la kuzungumza naye.



Akapelekwa mpaka chuo, akateremka, bodaboda alishangaa kumuona akiwa analia, hakutaka kuuliza, akachukua pesa yake na kuondoka.



Shadya alijikaza mpaka chumbani kwake, akapanda kitandani na kuanza kulia kwa maumivu makali kama mtu aliyefiwa na mtu muhimu katika maisha yake.



Hakuamini kama kweli alichana na Gibson baada ya kumuona mwanaume huyo haeleweki hata kidogo. Kipindi hicho alihitaji sana kubembelezwa, alifikiria mtu sahihi wa kumbembeleza, akahisi kaka yake, Rahim alifaa lakini akagundua hakuwa mtu sahihi.



Mtu wa mwisho kabisa kuja akilini mwake akawa Alex, aliamini kwa jinsi alivyokuwa mshauri mzuri basi angeweza kumliwaza kwa maneno matamu na kumwambia ni kitu gani alitakiwa kufanya.



Akachukua simu yake na kumpigia, ikapokelewa na kuanza kuzungumza naye. Alimwambia ukweli kwamba aliachana na mpenzi wake, ilimuuma mno moyoni mwake, alikuwa na maumivu kupita kawaida.



“Pole sana! Ila mwanaume amekuacha wewe?” aliuliza Alex kwenye simu huku akionekana kushangaa.

“Ndiyo!”

“Kuna wanaume wapumbavu sana! Kumbe mpaka karne hii kuna wanaume wajinga kiasi hiki! Mungu wangu!” alisema Alex.





“Kwa nini unasema hivyo?”

“Yaani mwanaume amekuacha wewe?”

“Ndiyo!”

“Ni ujinga ulioje? Pole sana. So nikusaidie nini?”

“Nahitaji nikuone! Tuzungumze mengi, unishauri ya kunishauri!”

“Basi haina shida.



Nakuja,” alisema kijana huyo na kukata simu, kidogo sana Shadya akajisikia ahueni, ila bado moyo wake ulikuwa na maumivu makali ya Gibson, yaani mwanaume huyo alimuumiza vilivyo.

.

.



Kulikuwa na mambo magumu sana duniani, mambo ambayo hata kama ungetumia muda mrefu kiasi gani usingeweza kufanikisha. Kulikuwa na wanawake wagumu duniani ambao hata kama ungetumia maneno laini usingeweza kuwatia mikononi mwako.



Hiyo haikuwa kwa Shadya, alionekana kuwa msichana mwepesi kwa Alex kwa sababu tayari moyo wake ulijeruhiwa na kipindi hicho alikuwa akihitaji sana faraja kutoka kwa mwanaume yeyote yule.



Ndani ya bajaji aliyopanda kijana huyo alikuwa akifikiria mambo mengi, kwanza uzuri wa msichana huyo, jinsi alivyovutia na kuonekana kuwa msichana wa tofauti kabisa, lakini pia akaanza kufikiria njia mbalimbali ambazo angetumia kumnasa Shadya, aliamini angefanikiwa katika hilo.



“Mtoto wa Kimanga! Wallahi huyu simuachi,” alijisemea.

Haikuchukua muda akafika mahali alipokuwa Shadya na kuanza kuzungumza naye. Kwa kumwangalia tu machoni hakuonekana kuwa sawa hata kidogo, aliumizwa, macho yake yalikuwa mekundu kwa sababu alitumia muda mwingi kulia kuliko hata kutabasamu.



Alex aliligundua hilo, kitu cha kwanza alichokifanya ni kuonyesha sura ya majonzi mno, alionyesha kuumizwa kwa kilichotokea kwa kuwa naye mwenyewe alikuwa akihitaji sana kuwa na msichana huyo mrembo.



“Yaani kuna mwanaume anaweza kukuumiza namna hii?” aliuliza Alex, miongoni mwa watu walioonekana kuumizwa na kile kilichokuwa kikiendelea kwa Shadya, alionekana kuwa wa kwanza.

“Ila kawaida tu! Wanaume mpo hivyo!” alisema msichana huyo.



“Hapana! Usitufananishe sisi wengine na wapumbavu kama hao. Hivi inakuwaje mpaka unamuumiza mwanamke kiasi hiki? Machozi ya mwanamke ni laana, akiamua kupiga goti na kulia kwa ajili yako, laana zote za mababu zitakufuata wewe,” alisema Alex, kwa jinsi alivyokuwa akizungumza, naye alionekana kuwa kama alikuwa upande wa Shadya.



“Nyie wanaume nyie! Hata Gibson alisema hivyohivyo!” alisema Shadya.

“Kuna kitu unakosea sana Shadya!” alisema Alex, akaanza saundi zake kama kawaida.

“Kitu gani?”







“Kwa nini ulitokea kumwamini huyo fala haraka sana?” aliuliza, ili kumpata msichana yeyote duniani kwanza ni lazima utengeneze uadui na mtu aliyemuumiza, yaani aone kama na wewe umeanza kumchukia kumbe hakuna lolote.



“Unamuita fala tena!”

“Kila mwanaume anayediriki kumuumiza mwanamke yeyote kwangu ni fala tu! Haiwezekani umuumize mtoto wa kike namna hii, kila wakati awe analia kwa ajili yako, kama humtaki, kwa nini ulimfuata?” aliuliza huku uso wake ukiendelea kuwa vilevile, unafiki mwanzo mwisho.



“Kwa sababu alipata alichokitaka!”

“Kuna wanaume wangapi wanapata wanachokitaka lakini mwisho wa siku wanaamua kutulia na watu hao? Shdaya, nikwambie ukweli tu, hakuna kitu ambacho kimeniumiza mno kama wewe kuumizwa na huyo jamaa. Hebu naomba namba yake kwanza,” alisema Alex.



“Wewe ya nini?”

“Naomba tu!”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Unataka umtukane!”

“Wewe naomba Shadya! Kuna mambo mengi ya kuvumilia, kuna wapuuzi wengi sana ambao tunaweza kuwavumilia lakini si wapuuzi kama hawa! Inaniumiza sana kwa sababu sijawahi kumuona hata baba yangu akimuumiza mama, kwa nini huyu pimbi mmoja afanye hivi?” alisema Alex.



“Lakini si una....”

“Usimtetetee...naomba namba yake!” alisema Shadya.

“Kwa namba siwezi kukupa!”

“Bado unampenda?”

“Hapana! Simuhitaji!”

“Basi naomba namba yake!”

“Haiwezekani! Sitaki kuona ukimtukana, siwezi,” alisema Shadya.



Mpaka hapo Alex alijiona kuwa mshindi, hakuamini kama alifanikiwa kwa kiasi kikubwa namna hiyo. Mwanamke anahitaji kutetewa kwa vyovyote vile, kwa kitendo cha kuhitaji namba ya Gibson kwa lengo la kujifanya kutaka kumtukana kisa tu alimuumiza Shadya, msichana huyo tayari aliona kama alikuwa upande wake.



Akakataa kumpa, Alex hakutaka kujali, alichomwambia ni kwamba alihitaji kukaa naye, wazungumze mambo mengi na kumsahaulisha kwa yale yaliyotokea.



Hilo halikuwa tatizo, Shadya akakubaliana naye na hivyo kuondoka na kuelekea katika Ufukwe wa Kunduchi.

Walipofika huko wakatafuta sehemu nzuri pembeni ya boti iliyopakiwa na kutulia hapo. Wakaanza kuzungumza mambo mengi yaliyotokea katika maisha yao.







Kama kawaida Gibson hakutakiwa kuwa mkweli kwa lolote lile, ilikuwa ni lazima kumfanya msichana huyo ajue alikuwa hana kosa, ajifanye kabisa alikuwa mtu mwema kuliko wanaume wote katika dunia hii.



“Ila unaposema sisi wanaume wote tupo hivi huwa unakosea sana,” alisema Alex.

“Kwa sababu gani?”



“Niliwahi kuwa na uhusiano na msichana mmoja aitwaye Upendo. Nilimpenda sana, nilimpa kila kitu alichokuwa akikihitaji katika maisha yake. Huwa ninapokuwa na msichana ninapenda mno kujitoa kwa kila hali ili awe na furaha,” alisema, kama kawaida alikuwa akitunga kauongo fulani kazuri sana.



“Ikawaje?”

“Yaani sijui nisemeje. Baada ya siku kadhaa, nikawa nimeamua kumnunulia zawadi fulani hivi, nikaenda kumpelekea nyumbani kwake. Akaipokea, nikamwambia ninataka tutoke kidogo kwa ajili ya dinner, akakubali hivyo akaenda kuoga,” alisema huku Shadya akisikiliza kwa makini kabisa.



“Ikawaje?”

“Sasa alipokuwa bafuni nikasikia simu yake imelia kama kuna ujumbe, si unajua hizi touch, meseji ikapop up pale juu, nilichokisoma, niliumia sana,” alisema Gibson, kwanza akanyamaza, akaangalia chini halafu akatingisha kichwa chake kuonyesha kuumizwa.



“Ikawaje?”

“Hawa wanawake hawa! Dah!”

“Ikawaje?”

“Tuishie hapo!”

“Hapana! Hebu niambie! Ujumbe ulisemaje?” aliuliza Shadya.



Kitu muhimu alichokifanya kijana huyo ni kuuchukua utulivu wa Shadya, alihitaji kumuweka katika hali ambayo ingemfanya kuwa makini sana kumfutilia kwa kile alichokuwa akikizungumza na kukiweka akilini mwake.



“Kuna jamaa alikuwa akidate nae, alimtumia meseji kumsifia jinsi walivyofanya ngono usiku uliopita. Unajua nilisikia maumivu ambayo sikuwahi kuyasikia,” alijibu Alex.



“Jamani poleeee...”

“Nashukuru! Ila ndiyo maisha! Kuumizwa ni kawaida, huwezi kuwa kwenye furaha kila siku na ndiyo maana uliponiambia kuhusu ishu yako, ilinigusa sana, imeniumiza mno na ndiyo maana nilihitaji namba ya jamaa ili nimtukane,” alisema, akaunganisha matukio.



Mpaka kufikia hapo tayari Shadya akahisi huyo alikuwa mwenzake, upande mmoja kumbe haikuwa hivyo, kama walivyokuwa wanaume wa vyuo vikuu, nae alitaka kupata alichokihitaji na kuondoka zake.



Walikaa na kuzungumza mambo mengi, ilipofika jioni, wakaingia baharini kuogelea, walifurahia mno na walipomaliza, wakaondoka ufukweni hapo kurudi chuoni.



Wakawa pamoja kwa mawazo na kupeana ushauri wa mambo mengi kuhusu mapenzi. Kwa jinsi walivyokuwa karibu, Shadya akaanza kuhisi kwamba kwa mwanaume aliyekuwa akimtafuta katika maisha yake alikuwa huyo Alex kwani alikuwa na kila sifa.



Kwanza mpole, mcheshi, mkarimu na hata alipokuwa akiongea aliongea kwa huruma nzito kama padri aliyekuwa akihubiri kanisani.



Alihitaji kuiteka akili ya msichana huyo hivyo kwenye kila neno alilokuwa akilizungumza, kitu cha kwanza kabisa lilikuwa ni kuwaponda wanaume ambao hawakuwa waaminifu, kwake walionekana kama wavunja amani nchini Tanzania.

.

.



. “Hii ni mimba yako!” ilisikika sauti ya msichana mmoja kwenye simu.

“Yangu! Yangu kivipi yaani?” alisikika mwanaume naye akiuliza.



“Hivi unajifanya umesahau!”

“Ndiyo unikumbushe!”

“Siku ile nilikwambiaje?”

“Ndiyo nikumbushe! Siku gani?”

“Tulipofanya mapenzi!”



“Sikumbuki Angelina! Hebu nikumbushe!”

“Nilikwambia nipo kwenye siku zangu za hatari, ukatafute mpira, halafu ukaniambiaje?” aliuliza msichana huyo.

“Daah!”



“Alex! Yaani umenipa mimba halafu unataka kukataa kwamba hii si mimba yako! Nimesema sikubali!” alisikika msichana huyo.



“Hebu naomba tuonane kwanza!”

“Si unajifanya kukataa! Sasa subiri!”

“Rose! Usiwe mkali kwanza, hebu tuonane! Mimba ishu ndogo tu!” alisema Alex.



Alikuwa akizungumza kwa simu, alipigiwa na msichana Rose ambaye alikuwa mpenzi wake na kwenda pembeni kuongea naye huku akimwambia Shadya asubiri kidogo.



Alipomaliza kuongea, akamrudia msichana huyo na kumwambia alipigiwa simu na kuambiwa mama yake hakuwa na hali nzuri, hivyo alitakiwa kwenda kumuona.



Kwa kuwa Shadya alikuwa rafiki yake, akaomba kwenda naye lakini akakataa kwa kuleta visingizo vingi mpaka akakubalika na kwenda huko peke yake.



Njiani alikuwa na mawazo tele, alimfikiria huyo Rose.



Alikuwa msichana wake, aliyekuwa akimtumia kama chombo cha starehe, kila alipokuwa na hamu ya kufanya mapenzi, wanawake wote walipokuwa wakimzingua, msaada wake wa mwisho alikuwa huyo Rose.



Alimtumia alivyotaka na siku ya mwisho kufanya naye mapenzi alimwambia kabisa kwamba alikuwa kwenye siku zake za hatari na hakuwa amechoma sindano za kuzuia mimba ila Alex akamshawishi na hatimaye kulala naye.



Akampa mimba na ndipo hapo alikuwa akipewa taarifa. Alitaka kuruka lakini mwisho akaamua kukubaliana naye hivyo kutaka kuonana.



Alichohitaji si kukubaliana na mimba hiyo ila alichohitaji hasa kilikuwa ni kumshawishi na hatimaye akubali kuitoa. Hakuwa tayari kuwa na mtoto, ni kweli alitembea na wanawake wengi lakini suala la kuwa na mtoto aliliweka kando kabisa.

Hakuchukua dakika nyingi akafika kwa Rose na kuanza kuzungumza naye.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Alimwambia vilevile kwamba alikuwa na mimba hivyo alihitaji kupata ushauri ni kitu gani walitakiwa kufanya.

“Inabidi itolewe!” alisema Alex, yaani aliongea simpo sana kama alikuwa akimsalimia mtu.



“Unasemaje?”

“Sasa Rose, wewe upo tayari kuitwa mama?” aliuliza.

“Hapana!”

“Sasa unadhani ni kitu gani tunatakiwa kufanya! Inabidi itolewe tu!” alisema Alex.



“Ila naogopa!”

“Kwani wewe ni wa kwanza mpenzi? Kuna wanawake zaidi ya milioni mia tano wametoa mimba, tena wengine mpaka tano, lakini ni wazima wa afya tele, tena baada ya kuolewa, wakaja kuzaa tena,” alisema alex.



Rose alibaki kimya akimsikiliza mwanaume huyo aliyekuwa na maneno mengi ya ushawishi. Aliongea sana na hatimaye wakakubaliana kwamba mimba ilitakiwa kutolewa.



“Ila mimi siwajui wanaotoa mimba!”

“Usijali! Nitawasiliana na madaktari ninaowafahamu!” alisema Alex, kichwani mwake kukaja madaktari kama watano hivi, wote hao aliwahi kuwatumia katika suala nyeti kama hilo, tena kwa mafanikio makubwa.

.





Muda huo Alex alikuwa bize na Shadya, hakutaka kusikia la mwanamke mwingine. Kulikuwa na kitu alikihitaji na aliona kabisa mara baada ya kukipata, asingeendelea kuwa naye.



Alimjali msichana huyo, alimsikiliza na kumuheshimu, alimuonyesha mapenzi yote ambayo mwanamke alitakiwa kuonyeshwa, aliaminiwa kwa kuwa alionekana kama alikuwa mkweli kwa kile alichokuwa akikifanya kumbe haikuwa hivyo.



Japokuwa mara nyingi Shadya aliteswa na mawazo juu ya Gibson lakini baada ya wiki moja ya ukaribu na Alex akaanza kumsahau mwanaume huyo, taratibu akaanza kumtoka moyoni mwake.

Akawa na furaha tele, kwa jinsi Gibson alivyokuwa hakuamini kabisa kama kuna siku naye angeweza kubadilika.



Mpaka kipindi hicho Gibson hakutaka kumwambia jambo lolote lile kuhusu mapenzi, aliuandaa moyo wa msichana huyo, kwenye kitu ambacho hakutakiwa kumfanyia basi la kwanza lilikuwa ni kumtongoza.



Yaani alihitaji wajikute tu wakifanya mapenzi, alihitaji hilo kwa kuwa alikuwa na maana yake kubwa, yaani hata likitokea la kutokea, awe na la kujitetea, amuulize kwani nilishawahi kukwambia nakupenda?



Kila siku walikuwa pamoja, waliendelea na maisha yao. Moyo wake ulijeruhiwa kwa ajili ya mapenzi lakini badala ya kujiweka pembeni, avute pumzi lakini hakutaka kuelewa kabisa.



Lile jiji la Dar es Salaam ambalo alionywa sana ajitenge nalo kwani kulikuwa na wanaume waliokuwa na kila aina ya saundi ya kumtokea msichana, likamchukua, kila aliyekuja mbele yake alionekana kama ana mapenzi ya kweli kumbe haikuwa hivyo kabisa.



“Wewe ni mzuri sana,” alisema Alex, hayo yalikuwa maneno aliyoyarudia kila siku, na kila alipokuwa akiyatamka, Shadya aliachia tabasamu pana.



Hakuwahi kumwambia alikuwa akimpenda hata mara moja, yeye kazi yake ilikuwa ni kuusifia uzuri wake, macho yake, ngozi yake na mambo mengine mwilini mwake.

Ilipofika wiki ya pili baada ya kuonana na kuongea hapo ndipo mambo mengine yakaanza kuibuka.



Kila walipokuwa wakikaa darasani, Alex alitumia muda wake kupitisha mikono yake kwenye mapaja ya msichana huyo na kuanza kuyachezea.



Kwa Shadya hapakuwa na tatizo lolote, angeweza vipi kumzuia mwanaume ambaye alimwambia alikuwa mzuri kama malaika? Hivyo akamwachia afanye lolote alitakalo.



“Unakwenda wapi huko?” aliuliza Shadya, mkono wa Alex ulianza mapajani, sasa ukawa unahama na kwenda juu.

“Subiri kwanza!” alisema Alex, Shadya akaangalia huku na kule darasani, hamukuwa na watu wengi, tena wale wachache kila mmoja alikuwa bize na mpenzi wake.



“Hebu panua miguu kidogo!” alisema Alex, cha kushangaza, Shadya akafanya hivyo.



Mkono ukaenda mpaka katikati ya mapaja na kutulia hapo kwa dakika kadhaa. Shadya alibaki akiugumia kwa raha ya kipekee, mkono ule uliweza kutalii vizuri maeneo hayo.



Zoezi hilo lilichukua kwa dakika tano nzima na baada ya hapo Alex akamwambia waende sehemu kupumzika, na kwa kuwa Shadya akawa hajiwezi, akakubaliana naye, wakaondoka na kwenda kuchukua chumba katika lodge moja iliyokuwa nje ya chuo hicho.



Hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Shadya kulala na Alex, walifanya ngono kuanzia majira ya saa kumi na moja mpaka saa tatu usiku, tena hawakuishia hapo, wakalala wote mpaka asubuhi.



Moyo wake ukafunguliwa kwa mwanaume huyo. Japokuwa Alex alikuwa na mademu wengi kutoka sehemu mbalimbali lakini aliweza kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha Shadya hagundui ilo.



Msichana huyo akamwamini Alex, yaani kwake hapakuwa na mwanaume mwaminifu kama huyo. Wakawa pamoja, Alex akatambulishwa kwa Rahim.

Ndugu yake huyo alimshangaa dada yake lakini akakubaliana naye kwa kuwa mambo ya mapenzi hakutakiwa kabisa kuyaingilia.



Moyo wa Shadya ukawa na furaha tele, hakukuwa na kitu kilichompa raha na furaha ya moyo kama kuwa na mwanaume huyo aliyejua kumuhendo mwanamke kama alivyokuwa akifanya.



“Nitataka niishi na wewe maisha yangu yote!” alisema Shadya huku akimwangalia Alex.

“Hakuna shida. Nakuahidi hakutokuwa na mwanamke mwingine zaidi yako!” alisema Alex.



Mapenzi hayo yaliendelea mpaka mwaka wa kwanza chuo ulipokwisha na hivyo vyuo kufungwa. Shadya na Rahim wakarudi Ilala ambapo walikaa siku moja na iliyofuata kuondoka kuelekea Unguja.

Alipofika, bandarini kulikuwa na ndugu zao wachache na Ngwali ambao walikuja kuwapokea.



Shadya hakutegemea kumuona mwanaume huyo mahali hapo, alishtuka kwani alitoka kabisa moyoni mwake na hakumfikiria hata mara moja.

Wakapokelewa, wakasalimiana na kuondoka mahali hapo. Njiani, Ngwali alikuwa kimya, moyo wake ulikuwa na furaha kumuona mpenzi wake lakini kwa jinsi alivyokuwa, alihisi kabisa kulikuwa na tatizo.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Alitamani kuuliza lakini alishindwa. Moyo wake ulimuuma mno, alihisi mpenzi wake alibadilika na inawezekana kabisa alimpa mwanaume mwingine huko Dar alipokwenda.

“Ila niliongea naye na kuniambia hawezi!” alijisemea.







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog