Search This Blog

Thursday 24 November 2022

NGUVU YA MAPENZI - 5

 

    Simulizi : Nguvu Ya Mapenzi

    Sehemu Ya Tano (5)







    Wakiwa kwenye gari, mama Angel aliamua kumuuliza binti yake kuhusu Samir maana hakuelewa,

    “Angel imekuwaje umeenda kusoma na Samir shule za karibu, ulimwambia?”

    “Hapana mama, ila nadhani Mungu kuna kitu kaweka kati yangu na Samir”

    “Kivipi?”

    “Mimi na Samir tunapendana sana”

    “Weee mtoto, huogopi kusema hivyo? Ndio shuleni mmejifunza hivyo?”

    “Hapana mama, ila tumejifunza kujiamini, kwasasa najiamini na ninapenda kusimamia imani yangu”

    “Imani ipi hiyo?”

    “Kuwa nampenda sana Samir”

    “Uwiiii hizi shule jamani, ndio tumeenda kusomesha mtoto hivi kweli!! Yani Angel huna hata uoga kuwa unaongea na mama yako!”

    “Ila mama jamani, mimi ni binti mkubwa sasa, kumbuka nina miaka kumi na nane”

    “Miaka kumi na nane ndio mkubwa Angel jamani!! Mimi na umama wangu huu lakini kuna mambo siwezi kumwambia mama yangu, ila naona wewe upo huru kabisa huna mashaka yoyote, amakweli tumesomesha mmmh! Kwahiyo ukamwambia Samir shule uliyopo?”

    “Hapana mama, kwanza mimi nakuja shuleni sina kabisa mawasiliano na Samir, yani nilikuwa siwasiliani nae kabisa. Ila sikuhiyo tulikutanishwa shule yao na shule yetu kwenye marumbano ya hoja, pale ndio nikaonana na Samir kwa mara nyingine. Kwakweli nilifurahi sana na nimesoma kwa amani sana kwa kipindi chote hiki kwa kugundua kuwa Samir hayupo mbali na mimi”

    “Duh!! Nimechoka kwakweli, kichwa kinaniuma, nitakuhoji kwa muda mwingine”

    Mama Angel alichoka kwa majibu ya mtoto wake, yani kwa kipindi hiki Angel alionekana kujiamini kupita maelezo ya kawaida ndiomana alikuwa akimjibu mama yake bila uoga wowote wakati ingekuwa zamani basi angebaki kulia tu na kutetemeka.

    Yani hapo hawakuzungumza tena hadi wanaingia

    nyumbani.Wanafika na moja kwa moja kushuka kwenye gari, huku wakina Erica wakitoka ndani na kwenda kumlaki Angel huku wakimfurahia sana na kufanya iwe ni furaha kubwa pale nyumbani kwao kwa siku hiyo.Hapo ndio akapewa na taarifa mbalimbali kuwa Vaileth na Junior wameoana hata wana mtoto tayari, alibaki tu kushangaa ila aliwapongeza sana, yani ilikuwa ni furaha, wakiwa sebleni, baba Angel alifatwa na mlinzi kuwa kuna mgeni wake nje, ikabidi baba Angel atoke kwenda kuzungumza na huyo mgeni, akakuta kuwa huyo mgeni ni Rahim na kumuuliza,“Umefata nini?”“Nimekuja kumpongeza mwanangu, kwani kuna ubaya?”“Mtoto hakutambui Rahim, kila kitu huwa kinaenda ngazi kwa ngazi, subiri mtoto aambiwe ukweli ndio utakuwa huru kumpongeza kwa wakati wowote”“Lini mwanangu ataambiwa ukweli? Hata mimi natamani sana kuwa karibu na mwanangu, pale shuleni nimejaribu hata kwenda kumpa mkono ila amekataa kupokea mkono wangu, yani angel ana maringo kama ya mama yake jamani”“Sawa nimekusikia ila huu sio muda muafaka wa kuongelea hilo swala”“Haya naomba tuongee kuhusu watoto wako”“Watoto wangu wamefanyaje?”“Usiwe mkali wewe, wanao watapeana mimba”Baba Angel alicheka sana na kumwambia Rahim,“Unafikiri mimi ndio nilizaa hovyo hovyo kama wewe, maana wewe kila mwanamke uliona uchomeke mbegu zake ndio uzae nae, sasa wewe ndio watoto wako watapeana mimba na sio watoto wangu, maana mimi wangu wote wametoka kwenye familia moja”“Yani Erick, unajua ulikuwa rafiki yangu mkubwa sana wewe. Hivi bila kulazimisha vidada vya watu kutoa mimba ungekuwa na watoto wangapi wewe? Nadhani ungefungua shule yako kabisa ambapo wangekuwa wanasoma watoto wako tu, unaniona mimi muhuni sababu nina watoto wengi, mimi sijawahi kuwatoa wanawake mimba ndiomana nina watoto wengi sio wewe. Halafu nataka kuongea nawe mambo mengine halafu wewe unaongelea vitu vingine sijui vya kuzaa hovyo, mambo yameingilianaje hapo?Utajijua mwenyewe na familia yako”Kisha Rahim aliondoka zake na kufanya baba Angel nae arudi tu ndani na kuendelea kufurahi na familia yake.Leo muda wa kulala, Erica alienda kulala chumbani kwa dada yake kwani alimkumbuka sana ukizingatia ni kipindi kirefu alikuwa yupo shule.“Dada jamani, nakumbuka kile kipindi ambacho wewe ulikuwa ukituambia sisi kuwa wewe ndiwe mama yetu”“Ndio, mimi ni mama yenu maana mimi ni dada yenu wa kwanza”“Eeeeh nipe habari za shule?”“Kabla ya yote, nasikia siku hizi umekuwa mpishi hodari sana, nasikia unapika hadi watu wanajing’ata”“Nani kakwambia dada?”“Huko bibi yako anakusifia kila kukicha, kwakweli mdogo wangu umekuwa noma”Erica alicheka na kusema,“Jamani dada!”“Ndio, basi kesho naomba unitengenezee keki ili niwapongeze Vaileth na Junior kwa kuoana, najua na mimi ya kwangu itakuwa nzuri balaa”“Ya kwako na nani dada?”“Nani mwingine zaidi ya Samir? Nampenda sana Samir naye ananipenda sana, mapenzi matamu ni kupendana. Asikudanganye mtu mdogo wangu, yani kupendana ni raha sana”“Hongera sana dada”“Asante na wewe ukikua utampata unayependana nae kama mimi nilivyompaya Samir”“Mmmmh nishampata tayari”“Niambie mdogo wangu, ni nani huyo?”“Utamfahamu tu, jina lake linaanzia na E kama langu”“Kheee umeanza kuchukua mtu kwa kufanana nae herufi ya jina!! Cha muhimu ni kupendana tu”Erica alitabasamu tu na kuendelea na maongezi mengi sana na dada yake.Kulipokucha, moja kwa moja Angel alienda kwa mama yake na kumuomba mama yake amnunulie simu,“Ulisema nikiwa mkubwa ndio nitamiliki simu, naomba ninunulie simu mama”“Usijali, hakuna tatizo. Simu yako ipo tu. Kwani unashida gani Angel?”“nataka kuwasiliana na Samir”“Tafadhari Angel usinitajie tena hilo jina hapa, nisije kufanya kitu kibaya, nakuomba sana usinitajie hilo jina”Mama Angel alienda chumbani kwake, alijiuliza moyo wake na kuona kuwa anachotenda kumficha Angel sio kitendo sahihi ukizingatia Angel na huyo Samir wamependana, basi alijisemea,“Nadhani ni wakati wa Angel kuutambua ukweli wa mambo kama baba yake mzazi ni Rahim, anatakiwa ajue kuwa huyo Samir ni ndugu yake maana ni mtoto wa baba mmoja. Asiniletee mambo ya mimi na Derrick bure!!”Akawaza kwa muda kidogo ila bado hakujua ni jinsi gani aanze kumweleza mwane kuhusu ukweli halisi wa baba yake mzazi, alitambua kuwa mwanae anatakiwa kujua ukweli ila huo ukweli anausemaje? Hapo ndio palikuwa pagumu kwake, akajisemea tena,“Inabidi nitafute wataalamu wa saikolojia ili wanishauri ni kitu gani naweza fanya ili binti yangu aufahamu ukweli kabla ya kuibua mengine”Alifikiria sana ila aliamua tu kuendelea na mambo mengine.Mchana wa siku hiyo, Erica alishaandaa keki aliyoambiwa na dada yake, kisha kuweka mezani halafu Angel aliwaita Vaileth na Junior, ili kwa pamoja wakate keki na kula ili kusherekea na kuwapongeza kwa ndoa yao.Wakati wanafurahi pale, ndipo alipofika mgeni mahali hapo, mgeni huyo alikuwa ni Daima, ambapo aliuliza kwa makini,“Kuna nini hapa?”Alijibiwa na Erica bila ya kuficha kitu chochote kile,“Tunampongeza Junior na Vaileth kwa hatua yao ya kufunga ndoa na kupata mtoto wao wa kwanza wa kiume”Kwakweli Daima alihamaki kwa hasira sana,“Kumbe ni kweli ndiomana ulikuwa hunitaki hapa wewe mtu mzima Vai”Vaileth akajua tu pale lazima matusi yataanza kumtiririka Daima, hivyobasi aliamua tu kwenda chumbani, ikabidi Erick ndio amtoe nje Daima, ila Daima hakubisha na kutoka nae hadi nje ya geti kabisa kisha akamwambia,“Naomba uondoke Daima”Ila Daima alimuangalia Erick na kumwambia,“Unajua sikuwahi kukuangalia vizuri ila leo nimekuangalia vizuri”“Kivipi?”“Kheee wewe kijana ni mzuri sana, yani leo ndio nimeuona uzuri wako”“Kheee nenda zako bhana”“Kwenda naenda ndio ila wewe ni mzuri sana, sio kama Junior, yani huyo mtu mzima atajuta tu kuolewa na Junior. Ila wewe ni mzuri sana, unafaa kuwa mume wa mtu”Daima alitaka kumsogelea Erick ili ambusu ila muda huu, Erica alitoka ndani na kumvuta Erick kwa nyuma kisha akaingia nae ndani na kumuacha Daima akiwa mwenyewe pale nje, ambapo aliamua kuondoka tu kwa muda huo.Erica aliingia ndani na Erick huku akimsema kwa kitendo cha kumsikiliza Daima,“Ulikuwa ukimsikiliza wa nini yule lakini? Watu wengine sio wa kuwasikiliza kabisa, au alikuchanganya kukwambia anakupenda?”“Hapana hajaniambia hivyo”Mara simu ya Erick iliita kwa muda huo, akapokea ni baba yake ambaye alikuwa akipiga na alimuita mahali kuwa aende kwa muda huo. Basi alimweleza tu Erica pale kuwa anaenda kuonana na baba yao, basi Erica akamwambia,“Naomba twende wote”“Mmmh Erica, kaniita mimi lakini”“Ndio kakuita wewe, najua kama leo sio siku ya kazi, kuna jambo ambalo baba kakuitia, naomba twende wote”“Sawa hakuna tatizo”Basi sababu walikuwa tayari, walienda tu kumuaga Angel na kuondoka zao, kwahiyo hata mama yao aliyekuwa chumbani hawakumwambia kuwa wanaenda wapi.Moja kwa moja Erick alipofika sehemu ambayo baba yake kamuita, walienda na Erica na kumfanya baba yao ashangae kidogo,“Kheee mmekuja wote?”“Ndio, Erica kataka kuja pia”“Kuna rafiki yangu alisema kuwa anahitaji kukufahamu ndiomana nimekuita hapa”Muda kidogo yule rafiki wa baba Angel alifika, na alipoona wale watoto wapo wote alisema,“Bila shaka hawa ndio Erick na Erica?”“Ndio, umewaona eeeh!! Nilimwambia Erick aje mwenyewe ila na Erica akaja pia”“Na nilijua tu kuwa lazima wangekuja wote”Baba Angel alimuangalia rafiki yake kwa makini na kumuuliza,“Umejuaje?”“Aaaah hawa watoto wanapendana sana, nilijua tu kuwa lazima wangekuja wote”Baba Angel alitabasamu kidogo na kusema,“Ni mapacha hawa, lazima wapendane”“Ila upendo wao ni zaidi ya unavyofikiria wewe”Hii kauli baba Angel hakuielewa maana bado alijiuliza huyu rafiki yake kahisi nini kuwa hawa watoto watakuja wote? Kauli ya kupendana kupita na anavyofikiria yeye hakuielewa kwani kuna sehemu nyingi tu ambazo Erica na Erick hawaendi pamoja, basi aliwatambulisha pale na kuachana na ile mada asiyoielewa,“Jamani huyu ni rafiki yangu mkubwa sana, anaitwa Mr.Noah”Basi Erica na Erick walipena mikono na Mr.Noah na kisha kukaa pamoja ambapo waliagiza chakula na kuanza kula huku yule Mr.Noah akiwauliza Erick na Erica maswali kadhaa wakati wa kula chakula huku akionekana kuwaangalia sana watoto hawa kanakwamba kuna kitu kingine ambacho alihitaji kuongea halafu hakukiongea.Walipomaliza, walijiandaa kwaajili ya kuondoka ambapo baba Angel alienda kupanda kwenye gari na watoto wake sababu yeye hakwenda na gari kwahiyo alichomuitia Erick kitu kingine ni kile kwenda pale na usafiri ili waweze kuondoka vizuri.Usiku wa leo, Erica alimfata Erick chumbani kwake na kuanza kuongea nae kuhusu yule rafiki wa baba yao,“Hivi yule rafiki wa baba umeweza kumuelewa kweli?”“Sijamuelewa hata nimebaki kumshangaa tu”“Anamaanisha nini kusema upendo wetu ni tofauti na baba anvyofikiria, au kaona kama tunapendana kwa namna tofauti?”“kaonaje na yeye katufahamu leo”“Mmmh sijui, usikute anatufahamu tangia zamani. Ila hii hali ya mimi na wewe kupendana zaidi imekuwa kubwa kwenye ukubwa wetu huu, kwahiyo yule sijamuelewa kabisa”“Nadhani kuna kitu anajua kuhusu mimi na wewe, sijui ni kitu gani ila aaargh sijui ni kwanini jamani, mara nyingine najihisi hata kulia, kwanini nikupende hivi dada yangu? Ninakuwa na wivu na wewe, najikuta nikitamani unifanyie vitu vingi sana, najikuta nikitamani mimi niwe mpenzi wako na tuishi kama wapenzi wanavyoishi”“Pole sana, mimi sasa ndio nimejikuta nikitamani hata Junior na Vaileth walivyoona iwe ni mimi na wewe”“Aaaaarggh sisi ni ndugu ujue, kwanini lakini? Na kwanini wanazuia ndugu kuwa pamoja? Sitaki kukupoteza Erica na sitaki uwe na mwanaume mwingine, sijui nitafanyaje nikigundua”Erica alihema kwa nguvu maana hakuwa na jibu kwani ni kweli hata yeye alijikuta akimpenda sana Erick kila siku inavyoenda ndivyo anavyozidi kumpenda.Erick alimsogelea Erica na kumkumbatia, kwakwlei Erica alihisi akisisimka mwili mzima na kumtoa Erick pembeni,“Mmmmh hapana, naogopa mimi naogopa”Erica alitoka mule chumbani kwa Erick, basi Erick alikaa kitandani kwake na kujiinamia huku machozi yakimtoka na kujiuliza,“Kwanini kila siku zinavyozidi kusonga mbele ndio hamu yangu ya kuwa na Erica inazidi? Kwanini Erica ni ndugu yangu? Nampenda sana, aaaarghh nadhani tutatengwa na ukoo, kwanini macho yangu yasitamani wasichana wengine yakaenda kumtamani Erica kweli!!! Aaaargggh”Erisk alijikuta tu akitokwa na machozi, na mwisho wa siku aliamua tu kulala kwa muda huo maana hata angewaza sana bado asingepata jibu la mawazo yake.Kulipokucha, baba Angel na mama Angel waliongea kuhusu Vaileth na Junior kuhamia kwenye hiyo nyumba ambayo Dora anataka kumzawadia Junior kama urithi wa kutoka kwa baba yake, ila mama Angel anaona kabla ya hilo watimize kwanza ahadi yao ya kufanya sherehe ndogo kijijini kwakina Vaileth ili kuwawezesha wazazi wa Vaileth nao kufurahi na binti yao,“Ila mke wangu, sasa hivi unavyojua pesa imekuwa tatizo kidogo kwetu”“Hakuna tatizo, yani hii namwambia Dora halafu utaona mambo yatakavyoenda, mbona ofisini kwa marehemu James wanachanga, hata wao walitaka kumfanyia sherehe kidogo Junior, basi tutawaomba tufanyie huko kijijini, halafu huko gharama haitakuwa shida, si unajua kijijini watu hata hawana makuu, raha ya sherehe wao ni wale na kunywa sio kama hapa mjini tulivyo na makuu, tunaweka hata vingine visivyokuwa na maana utakuta watu wanaviacha”Baba Angel akacheka kidogo tu ila jukumu hilo aliona ni vyema kumuachia mke wake maana aliona akilibeba yeye basi litamshinda mara moja.Baba Angel aliondoka zake kwenda ofisini, halafu mama Angel alimtafuta Dora na kuongea nae kuhusu hilo swala la sherehe ambapo Dora aliona hilo swala lipo sawa kabisa,“Halafu uliongea na yule binti kitu anachoweza kufanya?”“Ndio niliongea nae, alisema kuwa anaweza kufanya cherehani, ameomba kwenda kusomea hayo mambo ya kushona”“Oooh hiyo haina kazi, najua utamsimamia, ili awe anashona halafu tumfungulie mahali ambapo atauza hata na vitambaa, vitenge na khanga huku akiwa fundi mwenyewe itamlipa sana hiyo”“Kumbe Dora noma sana wewe, kuna muda unakuwa na akili timamu haswaaa”Dora alicheka sana, na kupanga mipango mbalimbali haswaaa mipango ya kufanya sherehe nyumbani kwakina Vaileth.Usiku wa leo, mama Angel alimueleza taarifa zote mumewe kuhusu hiyo sherehe na kila kitu alichoongea na Dora,“Naona kaamua”“Roho imemsuta, unajua alifanya vibaya, Junior ni mtoto halali kabisa wa James tena ni mtoto wa ndoa, sema tu mambo hapo kati yalitokea na kufanya baba na mama yake watengane, ila hilo haliwezi kukosesha Junior kupata haki zake. Ila mbaya mwingine ni yule shemeji Deo, yani ni mwanasheria ila hakutaka kujishughulisha na chochote kuhusu mali za Junior. Ila muache ataumbuka tu kwasasa, maana atashangaa kuona Junior amesharudi kwenye nyumba ya baba yake”“Halafu hata kwenye harusi hakuja”“Ndio hakuja, alimwambia mkewe kuwa mnajisumbua na huyo Junior, kwanza mnajipa mizigo maana mtahudumia watu watatu, Junior, mke wake na mtoto, akasema mtajuta sana. Badala mumkanye mtoto ndio mnahalalisha zinaa yake kwa kumfanyia harusi, mambo ya harusi mngemuacha agangamale nayo mwenyewe. Yani sijui kwanini Deo ana roho mbaya kiasi hiki, hampendi Junior hadi Junior mwenyewe anajua kama babake wa kambo hampendi”“Yule nae sijui vipi, kama huyu Junior kuharibika hata na wao wamechangia kwa kiasi kikubwa sana. Mtoto hana uangalizi, kazi ya mama ni kulalamika tu na kusema mtoto amemshindwa tabia, yani Mungu amsaidie tu Junior aweze kupata akili ya maisha”“Naamini Vaileth atamuweka sawa, kwani ni binti ambaye akili yake ipo vizuri, Vai atashughulika na Junior ndiomana nimefanya juu chini waoane tu.”Wakajadiliana pale na kuamua tu kulala.Siku hizi Dora na mama Angel walikuwa wakishirikiana vilivyo kuhakikisha kuwa sherehe kwenye kijiji cha wakina Vaileth inafanyika, na itakuwa nzuri tu, kwahiyo walifanikiowa kuweka kila kitu sawa na kushirikiana vyema na upande ule wa ndugu wa Vaileth katika maandalizi, kwanza na wao walifurahi sana, haswaa mama yake Vaileth ambaye a,ishajikatia tamaa ya binti yake kuolewa, kwahiyo ile ilikuwa ni furaha nyingine baada ya ile furaha ya kwanza ya mahari kupita.Siku moja kabla ya shughuli, ilibidi mama Angel akaongee na mama mzazi wa Vaileth ili amwambie ukwlei kuhusu vaileth kuwa na mtoto maana walikuwa hawajui,“Mama samahani, hatukuwaambia mwanzoni, ni hivi mtoto wenu Vaileth amezaa na kijana wetu”“Oooh kumbe!! Ila kwanini hamkusema”“Tuliogopa faini”“Sasa faini tuwapige ya nini wakati mtoto mwenyewe alishazalia nyumbani tayari, tushindwe kumpiga faini aliyetuachia kuanzia mimba hapa kulea hadi mtoto halafu tuje kuwapiga faini nyie kweli!! Hilo ni jambo la kheri, tena tunashukuru sana mmetuambia, ni furaha sana kwetu kwani ni matunda mema”Basi mama Angel alishukuru kwa yule mama kukubali tu bila ya tatizo lolote lile.Siku ya sherehe, waliondoka familia nzima, mapema kabisa ili wawahi kule kijijini na pia waweze kuwahi kurudi, kwakweli ilikuwa ni furaha na shamra shamra nyingi tu.Wakati sherehe ikiendelea, mama Angel alifatwa na mama Vaileth na kumwambia,“Samahani mwanangu, kuna wazee pale wanahitaji maelezo pia uliyonipa mimi kuhusu Vaileth kuwa na mtoto”Mama Angel hakuona tatizo, na moja kwa moja aliondoka na yule mama Vaileth ili kuwafuata wale wazee, ila kabla hajawafikia mama Angel alishikwa bega nyuma, alipogeuka alikutana macho kwa macho na dokta Jimmy. Wakati sherehe ikiendelea, mama Angel alifatwa na mama Vaileth na kumwambia,“Samahani mwanangu, kuna wazee pale wanahitaji maelezo pia uliyonipa mimi kuhusu Vaileth kuwa na mtoto”Mama Angel hakuona tatizo, na moja kwa moja aliondoka na yule mama Vaileth ili kuwafuata wale wazee, ila kabla hajawafikia mama Angel alishikwa bega nyuma, alipogeuka alikutana macho kwa macho na dokta Jimmy.Mama Angel alishtuka sana ila dokta Jimmy alimwambia kuwa asishtuke halafu akamuomba yule mama aliyekuwa ameongozana na mama Angel kuwa azungumze nae kidogo, yule mama hakukataa kwani yule dokta ni mtu ambaye aliheshimika sana pale kijijini.Dokta Jimmy alisogea pembeni na mama Angel, kwakweli mama Angel alimfata tu na kujishangaa maana hakuwahi kufikiria kama siku akikutana na dokta Jimmy wazi kabisa atafanyaje nae.Ila alivyozidi kusogea nae alimuuliza,“Tatizo nini kwani?”“Nisikilize Erica, kule na yule mama unaenda wapi?”“Tatizo liko wapi? Unahisi naenda nae wapi?”“Kijiji hiki unakifahamu vizuri Erica?”“Hapana sikifahamu vizuri ila ninachojua ni kuwa hawa watu ni wakarimu sana”“Mzee Mussa ndio ambaye alikuwa mshenga wenu, niliwahi kukutana nae na alinieleza kuhusu wewe, aliponiambia tu moja kwa moja nilitambua kuwa ni wewe. Swala la nyie kuja kuoa huku sio baya ila swala la nyie kuja kufanya sherehe huku ndio baya na msipokuwa makini litawagharimu sana”“Sikuelewi”“Kwani, muda huu yule mama kakuitia nini?”Mama Angel aliamua tu kumwambia ukweli bila kujali kuwa huyu ni adui yao au la,“Sasa hujawaambia kwani kuwa binti ana mtoto?”“Nimeongea na mama yake kasema haina tatizo hilo ni swala la baraka ila sijajua kwanini leo kasema kuwa nikazungumze na wazee”“Basi wale wazee watawaletea mlolongo usiotakiwa, na utajutia nakwambia, aiseee itawagharimu tena haswaaa, mimi nawajua wale wazee, yule mama hana tatizo ila wale wazee. Mimi ni kweli sio mtu mwema kwako, ila uliyopitia yanatosha, hakuna sababu ya kupitia mengine kwa wema wako ulioufanya kwa binti huyu. Mama wa huyu binti hana tatizo, hana tatizo kabisa, ni mtu mzuri, tatizo lipo kwa hao wazee waliokuita. Yani ukirudi nyumbani mwambie binti kuwa uliitwa na wazee, kwanza atatetemeka sana akisikia hivyo. Wale wazee wanaogopewa sana, na hivi hujaenda watafanya jambo”“Kheee sasa nifanyeje?”“Cha kufanya, nenda kakusanye familia yako hadi huyo binti na mtoto na mumewe, jifanye kama unaenda kuongea nae, zungukeni kwenye magari yenu muondoke hata msijisumbue kurudi wala nini kwa muda huu. Mimi nitaongea na yule mzee ambaye ni mshenga wenu ataenda kuwaombea ruhusa kuwa mmepatwa na dharula mmeondoka. Najua hata mlipokuja kutoa mahari hamkukutana na wale wazee”“Hatukukutana nao ndio”“Wale sio ndugu ila ni wazee wa kimila, wana mambo mabaya sana. Sio wa kuwaaga, nakuhurumia wewe na familia yako, ondoka muda huu na hivi umefanya sherehe wanajua wewe ni tajiri”Kidogo mama Angel alishikwa na uoga, na hapo aliamua kufanya kamavile dokta Jimmy alivyomwambia, alivuta familia yake na kuondoka nayo huku akimwambia mumewe kuwa pale sio pazuri, wanatakiwa kuondoka halafu wanatakiwa wawahi ili wafike mjini mapema. Kwahiyo waliondoka bila wenyeji kujua maana hata Vaileth hakuaga, zaidi ya kuitwa kama kwa maongezi na kupandishwa kwenye gari, hapo ilikuwa ni safari tu ya kuondoka kurudi nyumbani.Mama Angel alikuwa na mashaka sana ukizingatia alibeba familia yake yote na kwenda nayo huko, hakuelewa wala hakuwa na raha dhidi ya kile kitu kilichopo.Walifika nyumbani wakiwa na uchovu kiasi, ila wote waliuliza ni kwanini wameondoka gafla vile ila mama Angel aliwaambia ni kwaajili waweze kuwahi, kwa upande mwingine alishukuru hawakwenda kule na wafanyakazi wa baba yake na Junior ambao walisema wataandaa tafrija fupi tu ya kumpongeza yule kijana, ila kule kijijini waliona kuwa ni mbali. Yani mama Angel hata kumuuliza Vaileth kwa siku hiyo alishindwa kabisa yani alikuwa hadi anatetemeka na kuamua tu kwenda kulala maana hata mumewe hakumwambia ukweli.Kulipokucha, kitu cha kwanza kabisa, mama Angel alienda chumbani kwa Vaileth na kumtaka Vaileth kuongea nae,“Samahani Vaileth, eti kwenu kuna mila gani?”“Kivipi?”“Mimi, niliongea na mama yako kuhusu wewe kupata mtoto, mamako hakuwa na tatizo lolote lile na alibariki tu lile swala. Ila toka tumefika jana kwenye ile sherehe nikashangaa tukiendelea na sherehe ila hakuna aliyeuliza mtoto wa Vaileth yuko wapi au mlete mtoto tumshike, hata wakati mtoto upo nae pale mbela, ila sikushangaa sana. Sema mama yako alikuja kuniita na kuniambia kuwa wazee wa kimila wanataka kuongea na mimi kuhusu swala la wewe kuwa na mtoto”Vaileth alishtuka na kumuuliza mama Angel,“Ulienda kuongea nao?”“Hapana sikwenda, kuna mtu akanitonya kuwa niondoke na nisiende kuwasikiliza hao wazee wa kimila”“Aaaarrrgh wale wazee wana mambo ya ajabu sana, sijui nani atakuwa kawaambia kuhusu shefrehe nyumbani kwetu. Ndiomana mimi wakati tumefika toka mwanzo nilimuachia mtoto akae na Erica tu hadi pale alipomleta ili anyonye, nawajua wale wazee yani lazima wamemsumbua mama ndiomana kakuita”“Huwa wanataka nini?”“Yani wale wazeee ungeenda kuwasikiliza, wangekutajia faini ya kulipa kwa kitendo cha mimi kuzaa kwanza kabla ya ndoa, halafu wana mtindo wa kuangalia uwezo wako kwahiyo wanakutajia faini kulingana na uwezo wako. Na hivi waliona tumeenda na magari basi hapo lazima wanajua ni matajiri kwahiyo wangetaja faini ndefu, ukikataa kulipa wanakwamisha safari yani unashangaa tu pale kijijini huwezi kuondoka, yani mnekuwepo pale na kuwaachia chochote mlichokuwa nacho, halafu wanawapa shida sana kwenye safari. Sikujua kama wale wazee wamerudi tena kijijini kwetu. Kuna kipindi waliondoka”“Duh!! Kwahiyo ningewasikiliza ingekuwa balaa, kwahiyo wangenitajia ngapi?”“Huwa wanataja wale, wakiona mtu ana gari wanaanza kutaja milioni ishirini”Mama Angel alishtuka sana,“Kheee jamani, hiyo hela ya mtaji kabisa wa biashara kubwa tu”“Ndio hivyo, pole mama. Ashukuriwe huyo aliyekwambia mapema”“Kwanini mama yako nae asiniambie?”“Sijui ila najua pia hakupenda ila hakuwa na namna, ngoja nimpigie”Muda huu Vaileth alimpigia simu mama yake na aliweka sauti kubwa na kuanza kumsalimia pale, ambapo mama yake alimuuliza,“Mlifika salama jana?”“Ndio mama tulifika salama, ila mama kulikuwa na tatizo gani?”“Mmmmh si wale wazee jamani, mimi niliwaita wajomba zako na kuwaambia ukweli, sijui mjomba wako gani na kiherehere chake kaenda kuwaambia wale wazee wa mila, nikashindwa kufanya chochote kile. Nakumbuka hata mwanangu ulisema kuwa mahari tusipange kubwa ila wale wazee wa mila najua lengo lao lilikuwa ni kuwaumiza wageni wetu”“Sasa mama, kwanini usingetutaarifu mapema”“Jamani mwanangu, kwani siipendi familia yangu kuendelea kuishi huku!! Hii sehemu ni nzuri, ardhi inarutuba, tunakula na kuishi, nilivyoona vile niliamua kuongea na yule mshenga wao nikamueleza kuhusu wale wazee wa kimila, basi yule mshenga wao nae aliogopa jambo kulibeba yeye kama yeye, basi akasema kuna yule dokta mkubwa aliwahi kuongea nae na anaonekana kufahamiana na watu hao, akasema ataenda kumwambia, kwahiyo hata wakati naondoka na mama yako halafu dokta akamuita sikuwa na tatizo sana, ukizingatia karibia nilikuwa nafika nae kwa wazee wa kimila, kwahiyo wote waliona jinsi alivyoitwa na yule dokta. Si unajua yule dokta anavyooogopewa hapa kijijini, basi ndio ikawa rahisi, hata mlipoondoka na mshenga kuja kusema mmepata tatizo, na wenyewe walihisi mambo mbalimbali ila nani wa kumshikilia kasema? Watamshikilia yule dokta watamuweza yule? Nisamehe sana mwanangu, ila hawa wazee hata sikutaka wafike, ndiomana umeona hata sijafurahia ujio wenu, hata sijataka kumshika mjukuu wangu, yani hawa wazee hapana kwakweli. Nisamehe sana mwanangu”Basi Vaileth alimaliza kuongea na mama yake na kukata ile simu huku akimuangalia mama Angel ambaye alipumua tu na kusema,“Kweli duniani kuna mambo jamani, sikutegemea kama kuna sehemu kuna hayo mambo ya ajabu kama huko kijijini kwenu”“Wenye mambo ya ajabu ni wale wazee ila wengine wapo salama tu”“Au ndioama yule mwanaume wa mwanzo alikimbia kwa mambo kama haya?”“Hapana, kipindi kile wale wazee wa kimila walikuwa vijiji vingine, wanazunguka wale sio kwamba wapo kijiji kimoja, wale ni watu wa kuzunguka. Sio watru wazuri”“Duh!! Nimefahamu vitu vingi, mmmh sikutegemea kwakweli. Nilihisi mwili wote kusisimka”Basi mama Angel alimaliza pale na kumuacha Vaileth huku akirudi chumbani kwake sasa ambapo mumewe alikuwepo tu amekaa kitandani huku akisoma gazeti, alianza kumwambia yale na kumfanya ashangae sana kwani ni kitu ambacho hata yeye hakukitegemea kabisa na aliona ni cha ajabu,“Yani dokta Jimmy ambaye ndiye adui yetu namba moja halafu yeye ndio amekuwa msaada wetu!”“Ndio hapo”“Ila licha ya hayo, ila nahisi kuna mengi katikati hapo”“Kama yapi mume wangu?”“Nahisi dokta Jimmy hataki twende tena kule kijijini kumfatilia, kwahiyo ameshatutisha tayari na hatuwei kwenda tena maana tuna uoga”“Ila mume wangu licha ya hivyo ametusaidia sana”“Hata kama, bado sio mtu wa kumuamini dokta Jimmy, wala sio mtu wa kumshukuru kwani bado mabaya yake yanaendelea kucheza katika maisha yetu. Yeye na hao wazee wa kimila ni wako sawasawa, halafu hao wazee nadhani hawajawahi kukutana na watu wabishi, hivi nianze tu kutoa milioni ishirini mimi!! Labda sio mimi Erick”Baba Angel alitabasamu tu, mama Angel alijua utata wa mumewe, alijua pale lazima lingezuka la kuzuka maana baba Angel asingekubali kutoa hiyo hela.Leo, Angel aliamua kumfata mdogo wake Erick na kumukmba simu yake kwani alihitaji kuwasiliana na Samir ukizingatia hakuasiliana nae kwa muda kwani simu hakuwa nayo, ile simu yake ilikuwa kwa bibi yake.Erick alimpatia simu, kisha Angel akaenda kuwasiliana nae, na kukubaliana nae kuwa Samir ataenda pale kwakina Angel siku hiyo.Na kweli jioni yake, Samir alienda pale nyumbani kwakina Angel na kukaa na angel kwenye bustani huku akizungumza nae, kile kitendo mama Angel hakupendezea nacho kabisa, akaanza kijisemea,“Wale ni ndugu, haya ni mambo ya ajabu kwakweli, inatakiwa Angel aufahamu ukweli. Lini nitamwambia ukweli Angel?”Hapo ndio palikuwa na utata kwa upande wake, basi aliishia kuwaangalia tu ambapo Angel na Samir waliendelea na maongezi yao bila wasiwasi wowote ule.“Unajua Angel kitendo cha sisi kukosa mawasiliano kinaniumiza sana”“Ni kweli, hata mimi naumia ila nitaipata tu ile simu yangu au niende kwa bibi nikaichukue?”“Nikupeleke kesho basi, mwambie bibi yako kuwa umekuwa mkubwa na unamaamuzi yako”“Unadhini siku hizi hata mama namuogopa? Hakuna kitu kama hiko, kwasasa hata mama simuogopi wala nini, namwambia ukweli tu na yeye, ananielewa vizuri, nimeona uoga wetu ndio utakaovunja mapenzi yetu wakati Mungu anahitaji sana tuwe pamoja. Hebu angalia ni vikwazo vingapi tumepitia ila bado Mungu anatuweka pamoja”“Kwakweli naamini hayo usemayo kuwa Mungu anataka gtuwe pamoja, kwahiyo wazazi lazima wakubaliane na matakwa yetu.”“Vipi lakini wewe wazazi wako?”“Aaaah mimi kwa mama yangu yupo sawa tu, ila baba sijawahi kumwambia wala nini, sema mama aliwaka tu kipindi kile cha mdogo wangu ila kwasasa naona yupo sawa tu, sababu nilikaa nae na kuongea nae na kumweleza ni jinsi gani nakupenda, basi alinielewa”“Kwa upande wangu msumbufu ni mama, ila baba najua nikiongea nae ni mwelewe na atanielewa kwa haraka sana, nikiona mama haeleweki basi nitamwambia baba. Sisi hatuwezi kuwa mbalimbali kwani tunapendana”Wakaongea mengi sana pale, ni mpaka Samir alipoamua kuondoka na kuondoka zake.Mama Angel alimuita Angel na kuanza kuongea nae,“Ila Angel mwanangu una nini lakini wewe?”“Kwanini mama?”“Si nilishakueleza kuwa huyu Samir simtaki na wala hakufai mwanangu, kwanini unakuwa hivyo lakini?”“Mama, naomba unisikilize, mimi Angel ni binti mkubwa sasa, kama mzazi unatakiwa ukubali maamuzi yangu maana nimeyapima na kuona kuwa yanafaa, mama nampenda sana Samir, na yeye ananipenda sana, usitake kutuvuruga na kufanya tuachane, mimi na Samir tunapendana sana”“Ni kweli mwanangu ila wewe na Samir hamfai kuwa pamoja”“Kivipi mama, na kwanini hatufai kuwa pamoja ilihali tunapendana sana”Mama Angel akapumua kidogo na kusema,“Angel mwanangu, subiri umalize chuo ndio uanze hayo mambo ya mapenzi”“Mama, kwani kuna muda ambao mtu anastahili kuanza kupenda? Mama Samir nampenda kweli tena, naomba tu mama niache niwe na Samir yani ukiniachanisha nae unanipa wakati mgumu sana. Naona wazi sitaweza kwenda mbele”Ilionekana wazi kuwa mama Angel anashindwa cha kusema dhidi ya Angel na Samir, yani alijikuta akijiuma uma tu na kuachana na mtoto wake huku akifikiria vitu vingi sana.Baada ya Samir kuondoka tu, ndio muda ambao Emmanuele na Emmanah waliwasili, na kumfanya Erica kwenda kumuita mama yao ili aweze kufahamiana na hao watu maana mama Angel alisema kuwa anahitaji kuwafahamu zaidi, kwahiyo Erica alifanya kila juhudi wale waweze kufika pale kwao.Basi mama angel aliwakaribisha ndani kwake na kuwafurahia sana huku akiongea nao mambo mengi sana kwa wakati huo,“Wazazi hawajambo”“Hawajambo kabisa”“Nimefurahi sana kuwafahu, kwa leo naomba tule chakula kwa pamoja kama hamtojali, tafadharini msikatae jamani”Wote walitabasamu tu, na kwavile kwa siku hiyo mama Angel alikuwa amepika mapema, basi aliweka chakula na wote wakaenda mezani na kuanza kula kile chakula, kwakweli mama Angel alijikuta habandui macho yake kwa Emmanuel na Emmanah maana alijikuta akiwapenda sana wale watoto, vile walivyokuwa wakiongea ndio alizidi kuwapenda maana walionekana ni watoto wacheshi sana, kama alivyompenda Sarah basi ndivyo alivyowapenda na hawa watoto.Walimaliza pale kula na kumshukuru, kisha alirudi kukaa nao sebleni ambapo kwa muda huo aliwaita watoto wake wote, kuanzia Angel, Junior, Vaileth, Sarah, Erick, Erica pamoja na wale Emmanuel na Emmanah na kusema,“Jamani, kwasasa huyu Emmanuel na Emmanah nao ni ndugu zetu naomba tuwatambue kama ndugu zetu”Wote walitabasamu na kufurahi tu huku maongezi mengine yakiendelea, hata Emmanuel na Emmanah walipoaga ni mama Angel ndio alijitoa kuwasindikiza watoto hawa maana alijikuta akiwapenda sana, njiani aliwaambia shauku yake ya kutaka kuwatambua wazazi wao,“Natamani sana niwafahamu wazazi wenu, natamani sana kwakweli. Nahisi tu watakuwa ndugu zangu kwa namna moja au nyingine, maana naona damu yangu na damu zenu ikipatana sana”“Haman tatizo, utawatambua tu wazazi wetu, hata sisi tumekupenda sana”“Msiache kuja kunitembelea mara kwa mara, si mnaona watoto wangu pale nyumbani eeeh!! Pale kuna mmoja anaitwa Elly hayupo pale, na Ester amelala, nyie wote ni watoto wangu, nawapenda sana”Emmanuel na Emmanah walitabasamu pia kwani waliweza kuona jinsi huyu mama alivyokuwa na moyo wa kipekee maana aliwapenda waziwazi bila kujificha kwa namna moja au nyingine, alionyesha wazi upenzo wake kwao.Basi waliagana nae na kuondoka zao kuelekea nyumbani kwao.Usiku wa siku hiyo, Erica alienda chumbani kwa dada yake na kumkuta kajiinamia tu, basi alikaa na kuongea nae huku akimuuliza kuwa tatizo ni kitu gani,“Kwani vipi dada?”“Mapenzi mdogo wangu, sijui kwanini mama hataki niwe na Samir ilihali ninampenda sana halafu na yeye ananipenda sana”“Hivi dada, mapenzi ni mpaka mpendane?”“Ndio, kupendana ndio raha ya mapenzi, yani umpende mwenzio halafu na yeye akupende wewe, hapo ndio raha ya mapenzi ilipo. Huyo uliyemtaja siku ile ni nani?”“Aaaah nitakwambia tu dada”“Au ndio huyu uliyemleta leo? Ni huyu Emmanuel?”Erica alicheka na kusema,“Hapana dada, yule ni rafiki yangu tu si unaona mama ameshatambulisha kuwa ni ndugu, yupo nimpendaye”“Mmmh si uniambie dada yako”“Nitakwambia tu dada”“Halafu mama jamani kila mtu ni ndugu yetu yani na yeye anaanza kama wale mama wakubwa maana wale kila kijana nitakayesimama nae wakinikuta nae tu basi wanaleta sera za kusema ni ndugu yangu, jamani ukoo gani huu wenye ndugu kila kona? Kwakweli mimi kwa Samir hata sikubali, awe ndugu yangu au asiwe ndugu yangu siwezi kuachana nae kamwe. Mama kila siku anaongeza ukoo, rafiki zetu wote ni ndugu zake, anadhani itakuwaje kwetu”“Ila dada, si hairuhusiwi kwa ndugu kuwa na mahusiano?”“Unadhani ndio wakisema Samir ni ndugu yangu nitaachana nae! Thubutu, siachani nae hata kidogo kwanza duniani wote ni ndugu maana wote tumetoka kwenye uzao wa adamu na Eva”“Aaaah kumbe, kweli ukifikiria hilo utapata jibu kuwa wote ni ndugu, kwahiyo swala la kuoana ndugu ni swala la kawaida, maana najiuliza kwani Adam na Eva ndio walikuwa wanadamu wa kwanza, haya sasa watoto wao walioana na wakina nani kama sio wenyewe kwa wenyewe?”Angel na mdogo wake walicheka na kusema,“Ni kweli hapo mdogo wangu, lazima walioana wenyewe kwa wenyewe, kwahiyo maswala ya kusema ndugu siwezi kukubali kuvunja mahusiano kwa kisingizio cha undugu”Basi Erica alijadiliana vitu vingi na dada yake kwa usiku ule, kisha alimuacha mule chumbani kwake na kumuaga usiku mwema halafu yeye akaenda moja kwa moja chumbani kwa Erick ambapo alimkuta amejiinamia tu kwa wakati huo,“Kheee Erick, nilijua umelala”“Hapana, nina mawazo mengi sana Erica”“Nini tena?”“Unajua bado nafikiria ni kwanini mimi nakupenda kiasi hiki?”“Pole, ila nilikuwa naongea na dada angel muda mfupi tu uliopita anasema kuwa sio tatizo kwa ndugu kupendana na kuanza kuwa wapenzi sababu hapa duniani wote ni ndugu”“Kivipi?”“Hebu fikiria Adam na Eva, waliumbwa peke yao na kuzaa watoto je wale watoto wao walioa wakina nani kama sio kuoana na dada zao ili kukuza kizazi?”“Mmmh Erica, umefika hadi kwenye uumbaji?”“Ndio, au tuseme ile dhana kuwa binadamu wa kwanza alikuwa nyani ni ya kweli? Kwahiyo kulikuwa na ukoo wa Adam na Eva halafu ukoo wa manyani, ndio watoto wa Adam na Eva wakaoa kutoka kwenye ukoo wa manyani?”Hapa Erick alicheka sana, na Erica nae alicheka ila gafla walijikuta wakiangaliana kwa muda mrefu kidogo na kusogeleana, kila mmoja alianza kumbusu mwenzie, ila Erica alishtuka na kuinuka na kusema,“Hapana Erick, sisi ni ndugu”“Kumbuka umetoka kusema hapa kuwa ndugu si vibaya kupendana”“Ni kweli ila hatutakiwi kupendana kupitiliza”“Kwahiyo unatafuta ukoo wa manyani ndio uupende kupitiliza?”Hapa wote walianza kucheka tena, kisha Erica aliamua tu kumuaga kaka yake na moja kwa moja kwenda chumbani kwake ila alimkuta Sarah amekaa tu, inamaana na yeye hakulala toka alipoondoka,“Kheee Sarah hukulala kumbe!!”“Kila siku unaniacha mwenyewe chumbani Erica, sio vizuri. Ningeenda kile chumba alichosema mama ila kulala bila simu siwezi, basi ongea na mama anipatie simu yangu niweze kulala nayo na kuichezea”“Pole Sarah, nitaongea nae kwa hakika atakupatia tu hata usijali. Pole sana”“Asante, sina raha mimi wala sina furaha. Ni kweli nimeondoka kwa mama yangu ila angalau ningewasiliana nae hata kidogo tu, nimemkumbuka pia”Ni kweli Sarah alionekana kumkumbuka mama yake, ila Erica alielewa kuwa yote ile ni sababu mama Angel amekuwa akimbana Sarah sana mule ndani kwao kiasi kwamba Sarah kajiona kuwa hana uhuru tena wa kufanya chochote haswaa uhuru wa kuchezea simu yake, basi Erica alimbembeleza pale kisha wakaamua kulala tu.Baba Angel leo akiwa tu ofisini kwake, anapigiwa simu na rafiki yake Mr.Noah, na hapo anamuelekeza ofisini kwake ambapo rafiki yake huyo anaenda na kumkaribisha kisha kuanz akuongea nae,“Karibu sana, hapa ndio ofisini kwangu, ila hii ofisi nilikaa mwaka mzima bila kuikanyaga sababu ya matatizo yaliyonipata”“Duh pole sana, kwahiyo nani alikuwa akisimamia biashara yako sasa na kazi yako?”“Namshukuru Mungu nimepata kijana mwenye akili na kujituma, yani mwanangu Erick yupo vizuri sana, ni yeye ndio alikuwa akisimamia kila kitu, kuanzia biashara yangu na kila kitu hadi hapa kazini”“Oooh hongera kwa hili, kwahiyo mwanao yule anaweza kushinda asubuhi hadi jioni hapa?”“Ndio, ila mara nyingi sana huwa anashinda kiwandani, yani kiwanda changu kimeendelea sababu yake, kwa jinsi nilivyoumwa vile, kile kiwanda kingekufa ila Erick kawa mtoto wa ajabu sana katika maisha yangu maana kasimamia kile kiwanda hadi ndio imekuwa biashara kubwa sana kwangu sababu ndio inaniingizia hela nzuri zaidi”“Hivi mwanao huwa anakula chakula gani akishinda ofisini au huko kiwandani”“Mmmh mwanangu yule ni mtihani mkubwa sana, alikuwa anaweza kushinda asubuhi hadi jioni bila kula chakula chochote kile eti hadi arudi nyumbani kula. Nilipiga nae kelele hadi nilikoma, ila badae nikaona kumbe kitu rahisi ni kumtuma Erica yani yule dada yake awe anampelekea chakula, basi akipelekewa chakula na Erica anakula ila asipopelekewa hali wala nini”“Mmmh nilijua tu, watoto wako wale wanapendana sana”“Ila sikuelewi, kwnai kupendana kwao na hayo maswali yako kuna husiana vipi?”“Kuna siku utanielewa kuwa hao watoto kwanini nasema wanapendana sana, huoni kama maswali ninayokuuliza kuhusu hao watoto! Hayakupi maswali pia kwenye kichwa chako?”“Napata maswali pia lakini sikuelewi”“Basi kaa ukijua kuwa watoto wako wanapendana sana”“Ila kama wanapendana ni vizuri maana upendo ndio kila kitu katika maisha”“Kweli kabisa, siku moja jaribu kusema kuwa unahitaji kusafiri na Erick halafu utakaa nae wiki nzima huko unapohitaji kwenda nae, halafu sikiliza atakachokisema Erica baada ya wewe kusema hivyo”“Mmmmh unajua sikuelewi”“Kuna siku utanielewa, ila sina mengi sana kwa leo. Nilitaka tu kufahamu ofisi yako basi na si vinginevyo”Mr.Noah alimuaga baba Angel na kuondoka zake, kwakweli baba Angel alibaki na baadhi ya maswali kichwani mwake.Usiku wa siku hii, baba Angel alimueleza mke wake kile ambacho aliongea na rafiki yake ofisini kwake kuhusu watoto wake,“Unajua sijaweza kumuelewa kwakweli, yani amekazana muda wote kuongea kuhusu watoto wetu mapacha kuwa wanapendana sana, yani sijaweza kumuelewa”“Na yeye ana mambo ya ajabu, kwahiyo anataka watoto wachukiane? Ndugu wanachukianaje jamani! Mbona kuna watu wana mambo ya ajabu loh!!”“Nimemshangaa sana kwa hilo, yani nimeona ni mtu wa ajabu kushangaa hilo jambo, sababu ndugu watachukianaje? Ndugu ni lazima kupendana”“Huyo nae sijui ana mambo gani, yani hii familia jamani, likitoka hili linaingia lile khaa jamani!!”Baba Angel alikumbuka kitu kingine,“Halafu kesho natakiwa kwenda kwenye ofisi za yule mwarabu, kasema anataka mzigo nimpelekee mwenyewe halafu ana maongezi na mimi, sijui anataka kuongea nini na mimi”“Itakuwa ni mambo ya biashara tu hayo maana nasikia yule ni mfanyabiashara mkubwa sana”“Ndio, halafu anajuana na watu wengi ndiomana hata swala la kuumwa kwangu kaweza kulifanya vizuri sana”Waliongea mengi tu, na kuamua kulala kwani muda nao ulikuwa umeenda.Leo baba Angel kama ambavyo aliahidiana na yule mwarabu, basi alichukua mzigo ambao yule mwarabu aliutaka na kumfikishia moja kwa moja kwenye ofisi zake, kisha akampigia simu,“Oooh Erick umekuja, njoo tu kwenye ofisi yangu hii ya chini nipo na kijana wangu huku”“Sawa, nakuja hamna shida”“Ndio njoo, umfahamu na kijana wangu”Basi baba Angel moja kwa moja alienda kwenye ofisi aliyoelekezwa na mwarabu, ila alipofika pale ofisini alimuona kuna baba mwingine amekaa na yule mwarabu, alipomwangalia vizuri yule mtu aligundua kuwa yule ni Rahimu Basi baba Angel moja kwa moja alienda kwenye ofisi aliyoelekezwa na mwarabu, ila alipofika pale ofisini alimuona kuna baba mwingine amekaa na yule mwarabu, alipomwangalia vizuri yule mtu aligundua kuwa yule ni Rahim.Baba Angel alishangaa kwa muda, ila yule mwarabu alipomuona alimuita karibu na kusema,“Sogea hapa karibu kijana wangu”Kisha yule mwarabu alianza kumtambulisha baba Angel kwa Rahim,“Huyu ni kijana wangu, ndio mtoto wangu wa kwanza anaitwa Rahim, halafu Rahim huyu ni kijana wangu pia ndio ambapo kiwandani kwake nachukua sana bidhaa kama unakumbuka ni kile kiwanda ulichonionyesha kipindi kile”Kisha Rahim na baba Angel wakapeana mikono, ila baba Angel alielewa kuwa Rahim ndio alimuonyesha yule mwarabu kile kiwanda chake na kufanya awe mteja mzuri kwao.Ila wakati wakipeana mikono, Rahim akasema kwa baba yake,“Ila huyu ni rafiki yangu mkubwa sana”“Aaaah kumbe”“Ndio, kipindi kile nipo Marekani ndio nilikuwa nae. Ni rafiki yangu sana huyu, anaitwa Erick”“Kweli inaonyesha mnafahamiana, ndiomana ulikazana kuniambia kuwa kile kiwanda kina bidhaa nzuri sana kumbe ulikuwa ukijuana vizuri na rafiki yako eeeh!! Ila hata hivyo ni kweli kuna bidhaa nzuri, hongera sana kijana”“Asante sana”Kisha Rahim akaamua kumuacha baba yake aweze kuongea na baba Angel maana hakujua ni kitu gani anataka kuongea nae, ila alimwambia baba Angel,“Kabla hujaondoka naomba tuongee ndugu yangu, nitakuwa ofisi zile za juu nishtue tu”“Sawa hakuna tatizo”Rahim akaondoka na kumuacha baba Angel na yule mwarabu, ambapo cha kwanza kabisa yule mwarabu alianzakumsifia mtoto wake,“Huyu kijana wangu yupo vizuri, ila tatizo lake uhuni, aaaarrgh mtoto kanisumbua huyu, najua unamjua sababu ni rafiki yako, mama yake alikuwa akimkatalia sana, hata kipindi nimemtafutia mwanamke aoe, bado mama yake alikuwa akikataa kuwa sio muhuni hadi pale wanawake zake walipoanza harakati za kubwaga watoto kwa bibi yao yani mama yake, kwakweli mimi nilikataa kabisa kuletewa watoto wa ajabu ajabu”“Kwani mama yake Rahim huishi naye?”“Aaaah sisi mila zetu zipo tofauti kidogo na kipindi kile zilikuwa kali sana, ni kweli nilizaa nae ila kumuoa ilishindikana kabisa kwani nyumbani walikataa na kutaka nioe mtu mwenye asili yangu, ndio sababu ikafanya nisiweze kumuoa na kutengana nae, yani tofauti ni asili tu na si kingine.”“Ooooh mna mila kali”“Eeeeh ndio kwetu kulivyo, ila siku hizi wanaoana tu ila napo ni kwa kulazimisha maana hairuhusiwi. Huyu Rahim mke wake wa kwanza nilimtafutia mimi mwenyewe, mwanamke aliyetulia, alikuwa ni mzuri tena alichanganya, lakini huyu kijana wangu sasa uwiiii alikuwa akimpiga sana na kumuacha mtoto wa watu na maalama kila kona, mwishowe wakashindwa kuishi wote. Ila nimepata shida maana mimi ndio niliingia dhamana ya kuoa yule mwanamke kwa niaba ya huyu mwanangu. Tuachane na hayo, tujadili nilichokuitia huku sasa”“Sawa, nakusikiliza mzee”“Yule kijana wako wa kuitwa Erick, kuna siku nimeongea nae kwakweli yule mtoto anaonekana kuwa na akili sana, kwakweli nimempenda kupita maelezo ya kawaida. Sasa nilikuwa naomba kitu moja, nipe ruhusa ya kufanya kazi na kijana wako kwa wiki moja tu halafu tutaongea zaidi”“Aaaah sawa, hilo halina shida, nitaongea nae natumaini atakubali tu”“Basi ongea nae juu ya hilo, kuna vitu nahitaji anaielekeze na anisaidie, kijana wako anaonekana kuwa vizuri sana. Kwakweli nimependa sana jinsi alivyo na akili ya tofauti, nitafurahi sana nikifanya nae kazi”“Hakuna tatizo juu ya hilo mzee wangu”Kisha waliongea mengi pale na kupanga mambo mbalimbali ya kuweza kumshawishi huyo Erick mdogo ili akubali kwenda kufanya kazi kwa huyo mwarabu japo kwa hiyo wiki moja.Basi mwarabu alimaliza kuongea na baba Angel, na baba Angel akamuaga ila akamkumbusha kuhusu Rahim kuwa alihitaji kuongea nae pia,“Ngoja nimshtue kwenye simu”Huyu baba Alimpigia simu Rahim kisha baba Angel alitoka na kwenda kukutana na Rahim kwneye ofisi nyingine ilia pate kuongea nae.Rahim alimkaribisha baba Angel kwenye ile ofisi ambapo walikuwa wawili tu na kuanza kuongea nae alichotaka kuongea nae, ila kabla ya yote baba Angel alimshukuru kwanza kwaajili ya kumtambulisha baba yake kwenye biashara yake,“Nashukuru sana Rahim, sikujua kama ungefanya kitu kama hiki”“Sina ugomvi na wewe, najua ugomvi wetu mkubwa huwa upo kwenye mapenzi sababu wote tumempenda mwanamke mmoja ila bado sio sababu ya mimi kugombana na wewe kila mara. Mara nyingi huwa nipo na pombe kichwani ndiomana nakujibu vibaya na kugombana na wewe ila sio kwa akili zangu timamu. Usijali kuhusu hilo, kumbuka kabla ya yote tumewahi kuwa marafiki wazuri sana, na tukiambiana kila kitu, kwahiyo bado nakumbuka mazuri tuliyotenda pamoja”“Oooh sawa, ni vizuri sana”“Sasa nilichokuitia ni kuhusu Angel”Baba Angel akashtuka kidogo na kumsikiliza Rahim ambapo Rahim aliendelea kuongea,“Yule binti kawa mkubwa kwasasa, nakumbuka pale shuleni hata nilivyomfata kumsalimia alinikwepa. Kama mzazi iliniuma sana ile kitu, na jinsi Angel alivyokaribu na wewe nikaumia zaidi, nakuomba jambo moja mwanaume mwenzangu, naomba Angel atambue ukweli, naomba Angel anitambue baba yake halisi na anipokee kama baba yake halisi, yani Angel ajue kama mimi ni mwanae”Baba Angel akapumua kidogo na kusema,“Dah, ila hilo swala ni gumu sana kuongea mimi”“Najua ni ngumu sababu Angel amekuzoea sana, siku zote anajua kuwa wewe ni baba yake, hana wazo kuwa kuna kiumbe sijui baba mwingine wa kuitwa Rahim, naomba fanya lolote ili Angel atambue uwepo wangu”“Labda niongee na mama yake ndio amwambie”“Sijui kama atakubali ila najua wewe ni mwanaume pekee unayeweza kumshawishi Erica kuongea na mwanae ukweli wa mambo yote”“Ila Rahim, unajua una makosa sana, kipindi kile niliweka utaratibu mzuri tu wa mtoto kuweza kukutambua wewe kama baba yake ila wewe ukataka kufanya mambo mengine”“Sikatai, ni kweli nilifanya makosa yani hilo nakiri kabisa, nisamehe na Mungu anisamehe. Kweli ni mara nyingi sana nilitaka kumbaka Erica, sababu bado nilikuwa na mapenzi nae, nilijilaumu sana kuoa mwanamke ambaye hakuwa chaguo langu sababu yule alikuwa chaguo la baba, na mimi nilikubali tu kwa kutumiwa picha zake, niliporudi nikawa nae yeye, huwa najiona mjinga sana kumuacha mwanamke kama Erica ambaye kwa kipindi kile alikuwa tayari kwa chochote kile kwaajili ya mtoto ila mimi nilikuwa mjinga sana. Naomba hayo yaishe, ila naomba ongea na Erica amwambie ukweli Angel, amueleze kuwa mimi ni baba yake halisi ili Angel anithamini na kuniamini”“Sawa, nitajaribu kuongea nae kuhusu hilo kwani Angel kawa mkubwa kwasasa anatakiwa kujua ukweli”“Asante sana Erick, nashukuru sana kwa hilo yani utakuwa umenisaidia kwa kiasi kikubwa sana, natamani sana mtoto wangu anifahamu”Basi baba Angel aliagana na Rahim kisha yeye kuondoka zake na kurudi nyumbani kwake huku kichwa chake kikiwa na mawazo mengi sana.Usiku wa leo, wakati baba Angel yupo chumbani na mke wangu akaamua kumueleza lile swala la kukutana na mwarabu ya kuwa Rahim ni mtoto wa yule mwarabu na kitu ambacho Rahim kakifanya kumjulisha yule mwarabu kuhusu bidhaa zao,“Mmmh Rahim huyo ndio kamfahamisha yule mwarabu kiwanda chetu!”“Ndio, ni yeye. Mwarabu mwenyewe kasema hilo”“Basi Rahim huwa anajichetua tu, kumbe mara nyingine anajielewa. Tunamshukuru kwa hilo”“Ila kuna jambo lingine”“Lipi hilo?”Baba Angel aliamua kumwambia mama Angel kuhusu kile ambacho Rahim amekisema kuhusu kutambulishwa kwa Angel, basi mama Angel akasema,“Kheee ndiomana kumbe kumtambulisha baba yake kiwanda chetu ili tuweze kumfahamisha kuhusu Angel! Aaaargh alivyokuwa akifanya ujinga hakujua kama kuna siku itabidi amfahamu Angel kwa undani zaidi?”“Kaomba msamaha, ila mke wangu ni kweli ana haki ya kufahamiana na mtoto wake”“Mimi simtambui Rahim, ninachojua ni kuwa Angel ni mtoto wako”“Ila mama Angel twende mbele na kurudi nyuma, wakati unamwambia Rahim kuwa una ujauzito wake alikataa?”“Hapana”“Kipindi cha mimba alikuwa hakuhudumii?”“Hapana, alikuwa akinihudumia vizuri tu hata akanipangia chumba maana niliogopa kurudi nyumbani na mimba, mama algundua siku ya mwisho mimi kwenda kujifungua”“Ila unajua kuwa kuna mabinti wanabeba mimba na kukataliwa pindi anapomwambia mwanaume tu kuwa nina ujauzito wako?”“Najua”“Wewe chanzo cha Rahim kuacha kuhudumia mtoto na mengine ni kitu gani?”“Kwakweli sijui, ila nakumbuka kila nikimwambia njoo kwetu anasema nitakuja nitakuja, halafu toka nilipojifungua ndipo Rahim alipoanza kupunguza matumizi kwangu kanakwamba hakumtaka tena mtoto. Hata nimwambie kitu gani hakuwa na muda wa kunisaidia kabisa, nakumbuka niliongea na dada zangu wakaniambia kama mwanaume ana pesa, muombe basi hela ya mtaji ili angalau upate cha kujishikisha uweze kulea mtoto wako, kwakweli hela Rahim alikuwa nayo wala sio hela ya kubabaisha, nikamuomba hela ya mtaji. Nakiri kwamba nilimuomba hela kubwa ila hakutakiwa kunijibu kitu ambacho alinijibu”“Ulimuomba pesa ngapi?”“Nakumbuka wazi, nilimuomba milioni kumi na tano ili nifungue biashara ya kuuza vitu vya watoto. Ni bora Rahim angenijibu kiustaarabu kuwa sina hiyo pesa au mimi nina kiasi kadhaa kwahiyo fikiria biashara nyingine, ila hapana alianza kunikejeli alinitusi sana, niliumia sana moyo wangu hadi akasema nimemfanya yeye ndio tegemeo langu na familia yangu kwasababu sisi ni masikini, akaniambia badala nimuombe elfu kumi ya mtaji eti namuomba milioni kumi na tano, nafikiri pesa inaokotwa, yani alinijibu kwa kejeli sana. Toka hapo ikawa ndio kama nimemfukuza kwani hakutaka tena kuwasiliana na mimi, hakutaka kujua habari za mtoto wala kumsaidia mtoto. Nilikuwa nalia tu, kumbuka ndio nilitoka kumaliza chuo, sikuwa na kazi wala chochote cha kuniingizia pesa, niliona maisha mabaya sana, nikikaa kidogo mama ananisema sana kuwa mimi ni mjinga kwa kuzaa mtoto asiye na baba. Yote aliyoyafanya Rahim sikuhesabia kama ni kosa ila swala la kutokutaka kumuona mtoto liliniuma sana, hakuwa na mpango wa kuja kujionyesha kwetu na wala kusema kuwa Angel ni mwanae. Nakumbuka hadi nilimwambia Rahim kama kikwazo ni dini basi mimi nipo radhi kubadilisha dini ili tulee mtoto pamoja, ila Rahim alinikataa kabisa. Unadhani ningefanya nini? Kumpeleka mtoto kwa baba asiyemtaka kweli?”Baba Angel alipumua kidogo na kuongea tena na mke wake,“Hilo kweli ni kosa, tena kosa kubwa tu alilolifanya ila nadhani ni upepo mchafu ambao ulimpitia kiasi cha kukataa kufahamishwa vizuri kwa mtoto aliyemuhudumia toka tumboni. Ila mimi kama mwanaume najua ni jinsi gani wanaume tulivyo na makosa, nakuomba mke wangu shusha moyo na upunguze presha, mwambie Angel ukweli wa mambo ili amjue baba yake halisi”“Kwani umechoka kumlea Angel?”“Hapana sijasema hivyo ila Angel ana haki pia ya kujua ukweli, yani yeye ndio atakuwa na maamuzi ya mwisho ila muweke wazi aufahamu ukweli”“Dah!! Hiyo kitu naiona ni ngumu sana kwangu”“Jitahidi mke wangu”“Nitajaribu, ila sijui kama nitaweza kwakweli”Kwa siku hiyo mama Angel alijihisi hata kutokupata usingizi kabisa, alikuwa akigeuka huku na huko akiwaza jinsi ambavyo Angel atachukulia hilo swala la kuambiwa ukweli halisi wa maisha yake.Siku hii, mama Angel baada ya kazi za hapa na pale alimwambia Angel kuwa anahitaji kutoka nae sababu ana maongezi nae, hakufikiria kama lile jambo anaweza kuongea na Angel pale nyumbani.Basi alitoka na Angel moja kwa moja alienda nae ufukweni na kuanza kuongea nae,“Mwanangu Angel, leo nataka kukwambia ukweli”“Ukweli gani huo mama?”“Nisikilize kwa makini”Angel alitulia na kumskiliza mama yake,“Katika maisha yangu, kuna mwanaume mmoja nilikutana nae, niliamini ananipenda sana kwani alikuwa akionyesha mapenzi ya kweli kwangu na hata pesa alikuwa akinipatia, ila nikaja kupata ujauzito wake hapo ndio palianza kuwa na utata. Baada ya kujifungua alikataa kabisa kuja nyumbani kwetu na kufanya nitukanwe sana, nidharauliwe na kuitwa malaya kuwa niliyezaa nae simfahamu, nililia sana ila ni kosa kweli nilifanya kukubali kuzaa na mwanaume ambaye sifahamu hata nyumbani kwao. Nilikuwa nawasiliana nae na ananijibu vibaya sana, na mwisho wa siku alikata kabisa mawasiliano na mimi. Kwakweli niliona dunia ikinishurutisha sana na kunikosesha furaha kabisa kwani muda mwingi nilikuwa nikilia na kumshika mwanangu aliyekuwa akijaa machozi yangu, ila Mungu mwema akatokea mwanaume mwingine na kunipenda sana, huyu mwanaume akasema kuwa yupo tayari kumlea mtoto wangu na kumpa jina lake ni kweli kamlea kwa mapenzi yote, ila sasa kajitokeza yule mwanaume wa kwanza anamtaka mtoto wake”Hapo mama Angel alinyamaza kwanza na kuinama chini huku machozi yakimtoka, Angel alimuangalia mama yake na kumuuliza,“Unamaanisha huyo mtoto ni mimi? Unamaanisha baba sio baba yangu?”Mama Angel alikuwa akilia na kusema,“Nina uchungu mwanangu Angel nina uchungu sana, sikujua kama kuna siku kama ya leo itatokea katika maisha yangu. Nilifanya makosa sana, naomba unisamehe mwanangu”“Sijakuelewa mama, naomba unieleweshe”“Mwanangu, Erick sio baba yao mzazi. Baba yako mzazi anaitwa Rahim”“Hapana mama, sitaki kusikia jambo kama hilo”“Huo ndio ukweli mwanangu”“Yani baba sio baba yangu! Hapana mama sitaki, sitaki kusikia hivyo”Angel aliinuka na kuziba masikio kwa mkono halafu alianz akukimbilia baharini, hapo mama Angel akaona ni jambo lingine linataka kutokea, yani aliinuka na kumkimbia Angel, alipotaka kufika kwenye maji alimdaka kwa nguvu na kurudi nae nyuma ila Angel alisema,“Ni heri nife kuliko kuniambia kuwa baba sio baba yangu”“Jamani Angel mwanangu kwanini lakini, nisikilize kwanza”Kwa muda huu mama Angel hakutaka kumuacha Angel mwenyewe, zaidi zaidi alimchukua hadi kwenye gari na kumpandisha huko, kisha naye akapanda na kumwambia,“Mwanangu Angel jamani hebu jaribu kunielewa mama yako, nina maana thabiti kukueleza sasa”“Sitaki kukuelewa na sitakaa nikuelewe juu ya hilo, ninachojua mimi ni kuwa baba ni baba yangu na si vinginevyo”Mama Angel alijaribu kuongea ila kwa muda huu Angel hakumjibu chochote kile mama yake, yani alikaa kimya tu ilibidi mama Angel arudi nyumbani tu na mtoto wake.Walipofika nyumbani, moja kwa moja Angel alienda chumbani kwake na kujifungia, kwakweli mama Angel hakujua cha kusema, aliingia chumbani kwake pia na kuchukua simu yake kisha akampigia dada yake mkubwa aitwaye Mage,“Dada, leo nimemwambia Angel ukweli kuhusu uwepo wa baba yake”“Oooh wow, hapo ndio umeonyesha ukomavu wa akili maana mtoto ana haki ya kumjua baba yake mzazi haijalishi ni kipi kilitokea kati yako na baba yake ila kumtambua baba yake ni haki yake”“Ila Angel amechukia sana na hataki kukubali ukweli, muda huu kajifungia tu chumbani”“Muache tu hata usiwe na mashaka nae, muache atulize akili yake maana huko chumbani atafikiria na kujua umuhimu wa kitu ulichomwambia. Unajua Angel anaelekea pabaya kweli maana nishawahi kumkuta mara kadhaa tu na kaka zake, maana nawatambua wale watoto kuwa ni watoto wa Rahim, si picha nzuri kwa dada na kaka kutembeleana, umefanya jambo zuri mdogo wangu”“Kwahiyo nimuache tu kwasasa?”“Ndio, muache mwenyewe maana hapo ndio mawazo yake yatakuwa kwa upana zaidi”Basi mama Angel aliongea ongea na dada yake na kukata simu, hata mumewe aliporudi usiku hakumwambia kama amemwambia Angel ukweli halisi wa maisha yake badala yake alianza kuongea nae mambo mengine kabisa.Asubuhi ya leo wakati Sia akielekea kwenye biashara yake, njiani alikutana na Rahim na kuanza kusalimiana nae huku wakiongea machache,“Unajua Erica hakutaka kabisa kukutana nami wala kuongea nami kuhusu jambo lolote lile ila nilikuwa na mambo ya maana sana kumuambia”“Mambo gani hayo maana ulinidokeza ila hukuniambia”“Nilitaka kumueleza kuhusu wale mapacha wake yani Erick na Erica”“Ni kitu gani?”“Kwa kifupi wale watoto wanapendana tena wanapendana sana”“Mmmh kivipi? Ni mapacha wale kwahiyo wana haki ya kupendana”“Ni kweli wana haki ya kupendana ila wanavyopendana wale ni kwa namna tofauti”“Kivipi?”“Wale watoto ni mapacha ila wanatamani kuwa wapenzi”“Mmmh kwanini sasa?”“Ndio hiko nilitaka kuzungumza na Erica ila hajataka kunisikiliza kabisa nadhani alishauriana ujinga na mume wake, ila watajutia badae. Nilikutana na Erick ila sikumwambia haya sababu pia hata mimi nina yangu kuhusu mtoto wangu”“Yapi hayo?”“Nataka Angel afahamu ukweli kuwa mimi ni baba yake mzazi, anipende na kuniheshimu kama anavyompenda na kumuheshimu Erick”“Ni kweli ila hilo jambo linahitaji muda, sio rahisi kwa mtoto kuhamisha mapenzi yake toka kwa mtu anayependa na aliyemzoea kuja kwa mtu ambaye ni mgeni kwake”“Ila mimi ni baba yake, basi anipende kama anavyompenda Erick”“Pia si rahisi kukupa wewe na Erick upendo sawa, kumbuka Erick anampenda sana yule mtoto na amemfanya kama mtoto wake, kwahiyo ni ngumu sana kwa Angel kuhamisha majeshi yake ya upendo kuja kwako kwa urahisi namna hiyo”“Kwahiyo nini kifanyike?”“Unatakiwa kuwa mpole tu kwa mtoto, huo upendo hauwezi kuja kwa haraka. Mtoto lazima wewe umuonyeshe upendo na ukaribu kwanza ndipo na yeye atajifunza kukupenda hata kwa kidogo, kwakweli Erick yule ni wa viwango vingine, anajua sana kucheza nafasi yake kama mwanaume. Kwahiyo na wewe cheza nafasi yako vizuri”Rahim aliona aagane tu na Sia na kuondoka zake kwa muda ule.Mama Angel alitaka kuwasiliana na mtu kwa muda ule, ila aligundua kuwa hakuwa na muda wa maongezi hivyobasi akaamua kumtuma Erica kwenda kumnunulie vocha, kama kawaida Erica aliondoka na kwenda dukani kununua vocha ila njiani wakati anarudi alikutana na Sia, basi Sia alisalimiana nae na kuanza kuongea nae pale,“Erica, bora nimekuona leo. Naomba nikuulize maswali machache tu, upo tayari?”“Ndio niulize”“Eti unampenda vipi Erick?”“Kivipi?”“Yani nasikia unampenda Erick kama mpenzi wako”Erica alishtuka kidogo baada ya ile kauli ya Sia na alikaa kimya kwa muda, kisha Sia alimwambia tena,“Mbona upo kimya Erica? Hebu niambie ili nijue jinsi ya kukusaidia”“Sio nipo kimya ila nakushangaa tu, mimi nimpende kimapenzi kaka yangu kweli! Unachoniuliza umeambiwa na nani? Hujui kama yule ni pacha wangu? Kwahiyo watu kuongozana pamoja mara zote ndio wanapendana kimapenzi? Kwenye dunia hii wenye haki ya kupendana ni wapenzi tu? Ndugu hawawezi kupendana?”“Sijui kama umenielewa Erica, hata mimi sikuelewa wakati naambiwa hivyo mwanzoni ila nilitaka kukusaidia ndiomana nimekuuliza”“Aliyekwambia ni mbea, maana hiko kitu hakipo. Mimi na kaka yangu hatuwezi kupendana kwa namna hiyo maana sisi ni ndugu, aliyekwambia mwamabie kuwa mimi nina mchumba wangu anaitwa Emmanuel na Erick ana mchumba wake anaitwa Emmanah, nimemaliza”Hapo Sia aliamua kukaa kimya tu na kuagana na Erica kisha Erica akarudi kwao na kumpa mama yake ile vocha ili aweze kuwasiliana.Mama Angel muda huo aliamua kupiga ile simu sababu alikuwa akitaka kuwasiliana na mama Junior, basi alimpigia simu muda huo na kuanza kuongea nae,“Dada, nitakuita ili tuweze kukutana sababu watoto hawa tunataka kuwapeleka kwao”“Kivipi? Umewapangia nyumba kwani?”“Sasa dada unafikiri hawa nitaishi nao milele? Ni mke na mume hawa kumbuka, yani wewe na shemeji huko hata hamjifikirii kuhusu hawa watoto?”“Mimi sijui, unajua sina kazi ndiomana nipo nipo tu ila ningekuwa na kazi labda ningejua jinsi ya kuwasaidia watoto wangu”“Usijali, jiandae mwisho wa wiki hii tuwapeleke watoto sehemu watakayoenda kuanzisha maisha yao. Kwahiyo usijali”Mama Junior alikubali tu kwa hali ile na kuanza kufikiria mambo mengine.Erica alimfata Erick chumbani kwake ili kuweza kumwambia habari aliyoambiwa na Sia alivyokutana nae njiani, basi alimweleza kila kitu na kumfanya Erick ashangae pia,“Kaambiwa na nani maneno hayo?”“Sijui ila nimemziba kidomodomo kwa kumwambia kuwa mimi nina mchumba wangu wa kuitwa Emmanuel na wewe unae wa kuitwa Emmanah”“Khaaa inamaana wewe unampenda kweli Emmanuel?”“Hapana, nimesema tu ili kumkata yule mwanamke kidomodomo maana mimi nakupenda wewe”“Ila mimi na wewe ni ndugu si ndio msemo wako huo? Tutawezaje kuwa pamoja Erica?”“Sijui ila ninachojua ni kuwa tunapendana tu, ila kwani uongo? Mimi na wewe ni ndugu kweli”“Ndio tena ni mapacha, ila kwanini tunapendana?”“Sijui Erick, yani mimi ukiniuliza swali la namna hiyo kwakweli sina jibu la kukujibu kabisa kwani naona tu tunapendana na sijui kwanini tunapendana”“Unaweza kuhisi hali hii itaisha lini?”“Sijui”“Ila mimi najua hii hali itaishije?”“Mmmh niambie sasa?”“Kesho, muda wa kulala njoo chumbani kwangu halafu nitaongea na wewe jinsi ya kumaliza hii hali”“Mmmh Erick!! Si uniambie tu”“Nitakwambia kesho. Hivi Sarah kwasasa analala chumbani kwake eeeh!!”“Ndio, siku nyingine analala chumbani kwake na siku nyingine analala chumbani kwangu”Basi Erica alimuaga kaka yake kisha yeye aliondoka zake na kwenda chumbani kwake kulala ambapo kwa siku hiyo Sarah alikuwa kalala chumbani kwa Erica.Kulipokucha tu, Sarah alianza kuongea na Erica,“Unajua dada Angel sijamuona toka juzi akitoka na kula au kuongea nasi, hivi tatizo litakuwa ni nini?”“Ila kweli usemayo, sijui ana tatizo gani. Ngoja niende kumwambia mama usikute hajui”Erica aliondoka na moja kwa moja kwenda chumbani kwa mama yake.Muda huu Erica alimkuta baba yake ndio anataka kutoka ila muda ule ule alimwambia mama yake,“Mama, unajua dada Angel toka juzi hatoki nje kula!”Hapo mama Angel alishtuka kidogo na kumtaka Erica kuondoka ili aongee na mume wake, halafu mama Angel alianza kumwambia baba Angel,“Chonde chonde naomba ukaongee na Angel, nilimwambia ukweli na amechukia sana”“Kivipi?”“Nilimwambia ukweli kuwa baba yake ni Rahim”“Lini hiyo mbona hukunishirikisha?”“Nisamehe mume wangu, toka siku uliyosema, basi nilifikiria na juzi kumwambia ukweli Angel. Naomba unisamehe, sasa kusikia kuwa hatoki nje kabisa nimeogopa sana, nakuomba mume wangu nenda kaongee na Angel”“Ila mama Angel una masikhara ujue, yani mtoto jana nzima hajatoka hata hujaulizia?”“Nilijua katoka, yani sijafatilia swala hilo hata kidogo”Basi baba Angel akatoka chumbani kwake na moja kwa moja alifika chumbani kwa Angel na kugonga maana Angel alikuwa kafunga malngo, aligonga sana bila kufunguliwa, ilibidi aseme,“Angel mwanangu, naomba unifungulie, mimi ni baba yako”Muda mfupi Angel alifungua ule mlango na kumkumbatia baba yake huku akibubujikwa na machozi, basi baba Angel alimbembeleza pale na kwenda kukaa nae humo chumbani ili kuongea nae,“Mwanangu umejifungia mlango, huli chakula tatizo ni nini?”“Naomba kwanza niambie ukweli, wewe ni baba yangu au sio baba yangu?”Baba Angel alipumua kidogo na kusema,“Mimi ni baba yako Angel, kwani tatizo ni nini?”“Kwahiyo mama alikuwa akinidanganya eeeh!”“Sikia Angel mwanangu, naomba kwanza utulivu wako halafu tutaongea vizuri”“Sitaki cha kusikia kuwa wewe sio baba yangu”“Mimi ni baba yako, hakuna mahali niliposema mimi sio baba yako. Umewahi kusikia hilo toka kwangu?”“Hapana baba”“Basi tulia, inuka hapo twende wote tukale. Leo sitoenda hata kazini ili nikae na wewe siku nzima”Angel alifurahi sana, kisha aliinuka na baba yake, na kwenda nae mezani kula chakula.Kwakweli siku hii baba Angel hakwenda tena popote maana alikuwa na binti yake tu huku akiongea nae mambo mbalimbali na sio swala la baba tena.Usiku wa leo, karibia na muda wa kulala, Erica alitoka chumbani kwake na kwenda cumbani kwa Erick kama ambavyo walipanga jana yake.Alivyoingia tu alifunga mlango ila muda huo huo Erick alitoka bafuni kuoga na alipomuona Erica alifungua taulo lake na kuanza kujifuta maji, kile kitendo kilimfanya Erica atake kukimbia ila Erick alimsogelea na kumshika mkono. Alivyoingia tu alifunga mlango ila muda huo huo Erick alitoka bafuni kuoga na alipomuona Erica alifungua taulo lake na kuanza kujifuta maji, kile kitendo kilimfanya Erica atake kukimbia ila Erick alimsogelea na kumshika mkono.Erick alimuuliza Erica,“Unakimbilia wapi sasa Erica?”“Nataka kutoka humu chumbani”“Kwani unafikiria ni kitu gani?”“Sijui, kwani ni nini?”“Hebu vua nguo kwanza halafu uone ni nini”Erica akamshangaa sana Erick na kumwambia,“Kheee nivue nguo? Erick unataka kufanya kitu gani?”“Hapana, sitaki kufanya chochote ila nimekumbuka wakati wadogo tulikuwa tukioga pamoja na tukivaa pamoja, wala hakuna mtu aliyekuwa akimuogopa menzie”“Hebu vaa taulo kwanza halafu ndio tuendelee kuongea”Erick alichukua taulo na kujifunga, kisha Erica akamwambia,“Vaa na kaptula ndio tuongee vizuri”Erick alivaa ile kaptula na kumuangalia Erica ambaye alisema,“Usiniangalie hivyo, haya niambie sasa ulikuwa ukitaka nini kati yangu na yako?”“Sikia Erica, hata mimi sijui ni kwanini hakupenda au ni kwanini tunapendana, nilitaka mimi nibaki mtupu na wewe ubaki mtupu halafu tulale pamoja tuone nini kitatokea kati yetu”Hapo Erica kidogo alinyamaza kimya kwa muda mpaka Erick alipomshtua tena,“Erica, kwani vipi?”“Sijui”“Umekubali? Tuvue nguo halafu usiku wa leo tulale wote tuone nini kitatokea”“Unahisi kitatokea nini?”“Sijui, kwani kila siku tukilala pamoja kinatokea nini?”“Hakitokei kitu”“Ndio, nahisi hakitatokea kitu. Tulale tu pamoja halafu asubuhi kila mmoja atavaa nguo zake”“Mfano kikitokea kitu je?”“Kitu gani?”Erica alikuwa kimya tena, basi Erick alimsogelea karibu na kumuuliza,“Upo tayari tujaribu kufanya hivi tuone kitatokea nini? Ngoja nifunge mlango na funguo ili mama asije kutufata kama kawaida yake”Basi Erick akasogea mlangoni, ila wakati akitaka kufunga mlango kuna mtu akaingia na huyo mtu alikuwa ni Sarah, ambaye moja kwa moja alimfata Erica alipokuwa amesimama na kumwambia,“Erica, naomba tukalale wote, nashindwa kulala peke yangu”Erica alikuwa kimya tu akimuangalia, kisha Sarah alimuuliza Erica,“Mbona moyo wako unaenda mbio kiasi hiko?”Sarah hakuongea tena ila alimshika mkono Erica na moja kwa moja kwenda nae chumbani kwao kwaajili ya kulala, halafu alipokaa nae alimuuliza tena,“Erica kuna nini? Sijamuelewa Erick wala wewe sijakuelewa kwani kuna nini?”“Hamna kitu”Erica alijilaza tu pale kitandani ila siku hii ilikuwa tofauti sana kwa Erica kwani usiku wote alijikuta akifikiria tu maumbile ya Erick.Kulipokucha tu, Sarah alitoka chumbani na moja kwa moja kwenda chumbani kwa Angel na kuanza kuongea nae,“Sijui kwanini huwa sina mtindo wa kuja kuongea nawe, labda sababu muda mwingi nakuona unapenda kuwa peke yako peke yako”“Usijali, unakaribishwa tu muda wote kuja kuongea na mimi”“Mimi huwa napenda sana kuongea na Erica, mara nyingi nakuwa nae hata kulala huwa nalala nae. Ila kilichotokea jana sasa”“Kitu gani?”“Mara nyingi, huwa kama sijamuona Erica kwa muda mrefu shumbani najua lazima yupo kwa Erick na kweli nikienda namkuta huko, sasa jana nimemkuta tena”“Aaah, ikawaje sasa?”“Nimewakuta katika hali sio ya kawaida”“Hali gani?”“Kwanza Erick alishtuka sana kuniona, halafu Erica alikuwa akihema kwa haraka sana nadhani walitaka kufanya kitu kibaya”“Kitu gani?”“Sijui ila nimewashangaa tu”“Nikuulize kitu?”“Niulize dada”“Ushawahi kupata sifa ya umbea yani ushawahi kukutana na watu wakakwambia kuwa wewe ni mbea?”“Mmmmh!! Hapana kwakweli, sijawahi kuitwa mbea mimi”“Basi kwa mara ya kwanza mimi ndio nitakuita mbea maana ulichokuja kunieleza ni umbea, sasa Erick na Erica wapange kufanya kitu gani? Na kuhusu kuwa pamoja, wale toka watoto ndio wapo vile, hata kuwatenganisha vyumba ni mama ndio alifanya kazi ya ziada maana hawakutaka kutengana, walikuwa wakipenda kula pamoja, kuoga pamoja na kulala pamoja kwahiyo mimi hata sishangai kuhusu hiko ulichokisema, wale ni kawaida yao kuwa sana karibu”“Oooh basi yaishe dada”“Yameisha ndio ila acha umbea, umbea sio mzuri na umbea haufai mtoto wa kike”Basi Sarah aliamua kuondoka kwani kwa muda huo alihisi aibu ukizingatia aliyekuwa akimsalimia ndio huyo kajifanya ahusiki.Kisha moja kwa moja Sarah alimfata mama Angel, aliamua kuongea nae kuhusu simu yake kwani hakutaka tena kumpa hiyo habari ya Erica na Erick ukizingatia ameshashushuliwa na Angel,“Mama samahani, nilikuwa na uhitaji na simu yangu”“Naona umeugua kwa kukosa simu yako kwa muda?”“Kiukweli sina raha kabisa yani, natamani sana kuipata simu yangu ili niweze kuwasiliana na watu mbalimbali kama ambavyo nilikuwa nikifanya”“Sawa nitakuletea ila kuwa makini, yale mavideo yako usiyaangalie”“Sawa mama”Baada ya muda mama Angel alienda kumkabidhi Sarah ile simu na kumfanya Sarah afurahi sana, moja kwa moja alienda nayo chumbani na kumpigia Elly sababu ndio mtu aliyetaka kuwasiliana nae kwa muda mrefu sana, alimsalimia na kuongea nae,“Mama yangu hakuja huko kwenu kuniulizia?”“Kwakweli mama yako kanitafutia balaa”“Mmmh balaa gani hilo?”“Anasema kuwa ninayeishi nae sio mama yangu mzazi, kwakweli nimeshangaa sana. Kulikuwa na balaa hapa Sarah, uko wapi kwani?”“Mimi nipo kwakina Erick”“Bado una mpango wako ule wa kumtaka Erick?”“Hapana, halafu huwezi amini, siku hizi wala simtaki Erick kama mwanzoni, toka nimeambiwa kuwa ni ndugu yangu basi simtaki tena, hivi huwa unanikumbuka kweli?”“Kwanini nisikukumbuke wakati wewe ni dada yangu jamani!! Halafu kitu kingine ni kuhusu yule baba, anaomba uje kumtembelea hata kidogo tu ili aongee na wewe”“Baba yupi huyo?”“Yule wa siku ile ambaye tuliambiwa mimi na wewe kuwa ni baba yetu”“Ila dunia hii jamani loh!! Mtu kila siku unabadilishiwa wazazi tu, mimi namjua baba yangu aliyekufa tu, huyo mwingine simtambui ila nitakuja kumtembelea”“Basi kesho twende”Sarah alikubaliana na Elly sehemu ya kukutana ili kesho yake waweze kwenda kumtembelea Derrick ambaye inasemekana kuwa ni baba yao mzazi.Usiku wa leo, Sarah akiwa chumbani na Erica akainuka na kufunga mlango kabisa halafu anamwambia Erica,“Sasa nataka kukuonyesha zile video maana mama ameshanipa simu yangu”Erica alitamani sana kuziona, basi akamsubiria Sarah azifungue, ila Sarah aligundua kuwa mama Angel alifuta zile video zote na kusema,“Aaaah kafuta zote, ila nina rafiki yangu huyo ngoja nimpigie anitumie”Sarah alipiga simu na kumwambia huyo rafiki yake amtumie, kisha alikuwa akingoja amtumie huku akiongea na Erica,“Yani huyu ni noma, yeye lazima awe na hizo video”“Nani huyo?”“Ni rafiki yangu anaitwa Abdi”“Abdi? Unamjua?”“Na wewe unamjua? Mimi Andi ni rafiki yangu sana”Sarah alimuelezea Erica kuhusu Abdi anayemfahamu yeye na hapo Erica akatambua wazi kuwa ndio Abdi yule yule ambaye yeye anamfahamu, basi muda kidogo Abdi alikuwa ametuma zile video ambapo Sarah alifungua ya kwanza na kumuonyesha Erica, kwakweli Erica alishtuka na kuuliza,“Ndio manini wanafanya haya?”Sarah alicheka sana na kusema,“Acha ushamba Erica, hayo ndio mapenzi. Ndio chanzo cha mimi kupata mimba ya Elly”“Duh!!”“Ila usiogope, njia za kuzuia mimba zipo nyingi tu ukitaka nitakuelekeza”“Mmmh hapana, Sarah usinionyeshe tena hizi video naogopa mimi”Erica aliweka simu ya Sarah pembeni na kuamua kulala, ila siku hiyo ndio mawazo yalimzidi zaidi kwani kila muda alihisi zile video zikimjia kichwani na alihisi maumbile ya Erick yakimjia kichwani pia.Leo Sia, moja kwa moja anaenda ofisinbi kwa baba Angel kwani alijikuta akitamani sana kumwambia baba Angel kuhusu ujumbe aliopewa na Rahim kuhusu wale mapacha wa baba Angel, ila aliona ni lazima aonekane ni mbea zaidi.Alifika hadi ofisini kwa baba Angel na kumkuta na kazi zake, basi alimsalimia na kuanz akuongea nae,“Kuna kitu nataka kukwambia”“Kitu gani hiko?”“Mmmh!! Wachunguze vizuri watoto wako”“Kivipi? Niwachunguze watoto wangu gani?”“Erick na Erica naomba uwachunguze”“Kivipi? Ushakuja na umbea wako tena eeeh!! Unataka kusema wale watoto sio damu yangu au kitu gani maana wewe kuna muda huwa unajianzia tu, sijui unapata faida gani ukisema maneno kama hayo. Haya niwachunguze nini?”“Umefika mbali Erick maana mimi nilitaka kuongelea kitu kingine kabisa”“Kitu cha kuongelea, ushaanza na mada ya kusema nichunguze watoto wangu, unataka kuongelea nini? Unataka kusema wale mapacha sio wangfu, haya, watoto wangu wako wapi kama wale sio wangu? Semeni lingine ila kuhusu watoto sio wangu hapo nitaanza kuwa mswahili”“Jamani Erick dah!! Sijui hata kama umejua nataka kuzungumzia nini, ngoja niondoke maana hutaki kunisikiliza”“Ondoka ndio”Kwakweli Sia hata alishindwa kuongea chochote baada ya kumuona baba Angel kabadilika hata sura juu ya watoto wake, hakuwa na namna yoyote zaidi ya kuondoka tu kwa muda huo.Sia akiwa njiani, alikutana tena na Rahim, ambaye alimsimamisha Sia na kuanza kuongea nae, Rahim alianza kusema,“Unajua kadri ninavyokuwa karibu na Manka, napata upenyo wa kuwa karibu na yule dokta wenu dokta Jimmy, kwakweli Erica hataki tu kunisikiliza sababu yeye anawaza mambo mengine ila angenisikiliza angeweza kuokoa mambo mengi sana”“Kwahiyo umeshindwa njia yoyote ya kuzungumza nae?”“Njia gani sasa? Kwasasa nikimpigia simu yangu anakata, nimeenda hadi kwao siku hiyo hawajataka kuonana na mimi. Jamani wale watoto wao wanatakana, hayo mambo yamefika pagumu kwasasa, watalia jamani, huyo Erick na Erica watalia, halafu watasema kumbe Rahim alitaka kutuambia toka mwanzo, ila watakuwa wamechelewa”“Sasa ni kitu gani kinafanya wale watoto watakane”“Kila kitu ni mchezo wa babu yao, huyo baba mzazi wa Erick. Ila mimi napenda sana kuwasema nyie mabinti, huo mtindo wenu wa kuvamia vamia maukoo na kuolewa nayo mtakuja kulia na kusaga meno. Yani hii kitu hawawezi kuiepuka kama hao wazazi hawajaamka kwasasa, watoto wanatakana wale, wanapenda kufa mtu, yani kila mmoja yupo tayari kufa kwaajili ya mwenzie, upendo wao ni mkubwa sana. Siku ukikutana na yule Erick au Erica muulize tu swali la mtego kuwa nani afe kati yao ikitokea hivyo kama hawajakujibu wanataka wote wawili wafe, yani hawawezi hata kuwa na mahusiano tufauti na wao sababu wanapendana sana”“Duh!!”“Endelea kushangaa tu, ila wewe tulia tulia na uangalie jinsi mchezo unavyoenda, yule binti akishajaa tumbo ndio wale wazazi akili zitawakaa sawa”Kwa hapo Rahim aliachana tena na Sia na kuondoka zake.Elly alifika na Sarah nyumbani kwakina Derrick na yeye aliwapokea vizuri sana na kuwakaribisha kisha alianza kuongea nao, ambapo Sarah alimuuliza,“Ila unasema kuwa mimi ni mwanao, je ni mwanao kivipi? Maana mimi nina baba yangu ambaye alishakufa”“Sarah ulidanganywa kuhusu baba yako ila baba yako mzazi ni mimi”“Hapana, siamini kuwa wewe ni baba yangu mzazi maana mama hajawahi kuniambia hilo”“Hajawahi ndio, ila mimi ni baba yako mzazi”“Hapana kwakweli, hiko kitu nitapinga hadi naingia kaburini. Wewe sio baba yangu mzazi, hivi unajua jinsi baba alivyokuwa akinipenda? Yani mali zote ambazo mama anajivunia ni mimi nimepewa na baba yangu”“Ni kweli ila mama yako alifanya hivyo sababu ya mali na si vinginevyo, mimi ni baba yako Sarah”Pale Derrick alijaribu kumshawishi Sarah sana ila bado ilikuwa ngumu kwa Sarah kushawishika kuwa yule ni baba yake, basi wakaongea ongea kidogo na kuamua kuondoka ambapo Sarah aliongozana tena na Elly na kumuuliza maswali Elly,“Kwani huyu mbaba ana undugu gani na mamake Erick?”“Huyu na yule mama ni mtu na kaka yake kabisa, wamechangia baba kasoro mama tofauti”“Kwa maana hiyo hata mimi na wewe tumechangia baba kasoro mama?”“Aaaah Sarah dunia ina mambo sana hii, unajua kama yule ninayeishi nae sio mama yangu halisi?”Sarah alishtuka na kumuuliza tena Elly,“Kwahiyo mama yako ni nani?”“Nikikwambia waliyeniambia nadhani utachoka na huwezi kukubali kama ambavyo mimi sijaweza kukubali”Mara kidogo kuna mtu alitokea na kuwasalimia, alikuwa ni mama wa makamo ambaye anaenda kama kwenye ubibi basi aliwauliza,“Samahanini, kuna mwanamke mmoja niliwahi kuonana nae zamani sana, nadhani kwasasa atakuwa ni mama mtu mzima tu. ANaitwa Erica, mtakuwa na undugu nae eeeh!!”Elly na Sarah walitazama na kuitikia kuwa wanamfahamu, kisha yule bibi akasema tena,“Yani kama wewe binti ndio umefanana nae balaa, ila hata huyu kijana kafanana nae pia. Msalimieni sana”“Sawa, tumwambie nani anamsalimia?”“Mwambieni mama mkwe wake wa zamani anamsalimia sana”Elly na Sarah waliangaliana tena ila waliitikia tu na kuendelea na safari yao, ila Sarah akasema,“Unajua naanza kuamini kuwa mimi nina undugu na mama Erick maana huyu sio wa kwanza, ni wengi nikikutana nao huwa wananifananisha mimi na mama Erick, nina hakika kuwa yule mama kwa namna yoyote ile lazima atakuwa ni ndugu yangu tu ndiomana nampenda sana”“Basi ndio ujue kuwa yule kweli ni baba yetu”“Mmmh kwa hapo nina mashaka kidogo, ila mmmh sijui labda siku mama anihakikishie”Waliongozana na moja kwa moja Elly alimfikisha Sarah na kuagana nae maana yeye hata hakuingia kabisa ndani.Mama Angel leo jioni aliwasiliana na dada yake ili aweze kukutana nae, kisha aliongea na wakina Junior kuhusu swala la kutoka nao kesho na kuwapeleka kwenye makazi yao, kwahiyo walifurahi ingawa kwa upande mwingine waliumia kidogo sababu walishazoea kuishi hapo nyumbani. Mama Angel aliwataka mapema kabisa wajiandae kwaajili ya kuondoka naye kuelekea huko kwao.Basi siku hiyo, kwa pamoja walikula wote chakula cha usiku kwaajili ya kuwaaga wakina Junior maana tayari alishawaambia kuwa kesho yake atawapeleka huko.Basi walikula na kufurahi huku wakiongea mambo mengi sana na usiku ulipoingia wote waliamua kwenda tu kulala.Kulipokucha, kama ambavyo mama Angel alihitaji wajiandae, basi aliwachukua na mizigi yao kisha kuanza safari ya kwenda alipowaambia kuwa wanaenda kwa siku hiyo.Moja kwa moja, walimpitia kwanza mama Junior na kuondoka nae kuelekea ambapo walipokuwa wakielekea.Kufika kule, walimkuta Dora ameshafika na walishuka pale, kwakweli mama Junior alishangaa sana, yani mpaka wanaingia ndani ya nyumba ile bado alikuwa akishangaa kwakweli, kisha wakina Junior walikabidhiwa pale huku Dora akimwambia Junior,“Karibu hapa ni nyumbani kwako, hii ni nyumba ambayo wewe Junior ulizaliwa humu, baba yako mzazi na mama yako walikuwa wakiishi humu”Junior alikuwa akishangaa tu, yani mama Junior alijikuta akianza kulia maana hakuelewa kabisa kile kitu, ilibidi mama Angel akae nae na kumuelekeza dhumuni la Dora kufanya vile, kwakwlei alifurahi sana kwa mwanae Junior kurudi kwenye nyumba ambayo alizaliwa humo,“Kwahiyo umewapangia tena hii nyumba?”“Hapana, James aliinunua kabisa hii nyumba. Nilichokifanya mimi ni kuikarabati na kuirudisha kwa muhusika”“Oooh asante sana Dora, yani sikufikiria kabisa jambo kama hili, nashukuru sana”Mama Juior alimkumbatia Dora na hapo walianza kuongea mengi kwani ilikuwa ni furaha kubwa sana kwa mama Junior, hata Junior nba Vaileth walibaki kustaajabu tu huku wakionyeshwa mazingira ya nyumba ile huku Junior akiambiwa vitu mbalimbali kuhusu uwepo wa nyumba ile ambao hakuujua sababu kipindi kile alikuwa ni mtoto mdogo.Angel aliona siku hii ni siku nzuri kwa yeye kuweza kuonana na Samir ukizingatia wote kwenye familia yake hawakuwepo, basi aliomba simu kwa Sarah na kumpigia simu Samir kuwa aende kwao, na kweli muda sio mrefu Samir alifika, na muda ule walibaki tu Angel, Erica, Sarah na Ester maana wengine wote walitoka kutokana na majukumu ya siku hiyo.Angel alimkaribisha Samir na kwenda kukaa nae kwenye bustani yao huku wakiongea ongea,“Mfano wazazi wako wakija je itakuwaje?”“Sipendi kujificha ujue, yani wazazi wangu wajue wazi ni jinsi gani nakupenda na huwa nawaambia wazi kuwa nakupenda sana”“Kweli Angel umeamua ila nadhani tungekaa chumbani na kuongea ingekuwa vizuri zaidi kuliko hapa nje”“Mmmh kwahiyo twende chumbani?”“Ndio, twende tukaongee chumbani ndio vizuri”“Sawa, ila ngoja nikuulize kitu. Kwa mfano ukaja kuambiwa kuwa baba unayeishi nae sio baba yako utafanyaje?”“Mmmh mimi jamani sijui ila baba yangu nagombana nae kila siku, sipatani nae kwa matendo yake anayomfanyia mama, najua hata mama anamvumilia tu sababu yetu, ila isingekuwa sisi basi mama hata asingeweza kumvumilia baba maana baba yetu ana mambo ya ajabu sana”“Na wewe badae utakuwa kama hivyo?”“Hapana, mimi nitakuwa kama baba yako sababu huwa naambiwa sifa zake na yule mdogo wangu Samia, nasikia baba yenu anampenda sana mama yenu, nasikia anawapenda sana watoto wake, na mimi nahitaji kuwa kama baba yako”“Wow, baba yangu kweli ana upendo sana”“Sawa, Angel twende chumbani tukaongee vizuri, ni mengi nataka kuongea na wewe ila nashindwa kuongea nawe hapa nje. Halafu nafasi kama hii juu yetu ni nadra sana kupatikana Angel”Angel alipofikiria aliona ni kweli kuwa nafasi ya yeye kuongea na Samir na ndogo sana, basi aliamua kwenda nae chumbani kwake huku akipanga siku ya kwenda kwa bibi yake ili kuchukua simu yake ambayo upo huko kwa bibi yake.Baba Angel akiwa anakaribia kutoka ofisini kwake, siku ya leo akafatwa na rafiki yake Juma kwahiyo alitoka na kwenda nae nje ili kuzungumza nae mawili matatu, ila kuna jambo Juma alimueleza baba Angel ambalo lilimshangaza kidogo,“Yani nimeamua kukutafuta ili niongee na wewe”“Kitu gani hiko?”“Uliwezaje kulea vyema mtoto wa mke wako hadi akajua kuwa wewe ndiye baba yake?”Baba Angel alicheka na kumuuliza,“Wewe umejuaje kama yule si mwanangu?”“Dunia haina siri, mtu anatakunyima chakula na sio maneno ndugu yangu. Kuna mtu alimtonya mke wangu, hata hivyo mtoto hafanani na wewe Erick hata kidogo yule, ila mwenzetu upo katika viwango vingine, ndiomana nimekuuliza umewezaje kulea mtoto wa mke wako hadi kujulikana kuwa ni mtoto wako?”“Nilimpenda mke wangu, nikapenda na uzao wake, toka siku ya kwanza nilimchukulia yule mtoto kama mtoto wangu wa damu, kwahiyo hakuna kitu kilichonifanya nimlee mtoto yule vizuri kama swala la kumchukulia kama mtoto wangu wa damu”“Hongera sana kwa hilo, maana sisi wengine sijui vipi hatukuweza jambo hilo. Mke wangu alikuwa mapepe sana, unalea mtoto huku na majukumu yote unafanya halafu yeye anaenda kukutana na baba wa mtoto wake, nikamwambia mke wangu, tumpeleke mtoto kwa baba yake, ndio hapo mtoto akaenda kwa baba yake na mimi na mke wangu tukaanza maisha mengine”“Oooh, kwanini umeniambia yote hayo?”“Jamani, kale katoto kalipata mimba sijui kalipewa na nani huko, kakatimuliwa na baba yake na kuja kukimbilia kwa mama yake yani pale ninapoishi na mama yake, kwakweli nilikaonea huruma na tukalea hiyo mimba hadi kakajifungua vizuri kabisa, mtoto ni mkubwa sasa ana miaka minne, huwa sisemi tu jambo hili. Ila leo nimemuuliza kama baba mwenye mtoto ni nani yani mwanaume aliyempa mimba ni nani! Jamani katoto kale kamenitusi hadi nimehisi kizunguzungu, nimeona nikikapiga nitakaumiza, kwakweli nimekosa hata raha ndiomana nikaja kwako rafiki yangu ili unipe ushauri juu ya hili”“Duh pole sana ndugu yangu, kumbe una mitihani kiasi hiko!”“Yani acha tu, nina mitihani hadi nahisi kuchanganyikiwa hapa. Naomba unishauri chochote tu ili nami niridhike jamani.”“Ngoja kwanza, niongee na mke wangu ili ashauriane na mwenzie na mjue cha kufanya na mtoto wenu huyo. Kwasasa sina ushauri kwakweli”“Sawa, nadhani hata kupitia kwa mkeo napo sio jambo baya, itanisaidia kwakweli, labda aongee na mwenzie yani mimi nimeshindwa maana chochote nitakachofanya yule mtoto ataona nambagua”Basi waliongea kidogo na kisha kila mmoja kuondoka zake na kuelekea nyumbani kwake.Usiku wa leo, baba Angel alikuwa akimueleze mkewe kuhusu alichoongea na Juma, mkewe alikubali kumtafuta rafiki yake ili aongee nae maana aliona kuna umuhimu wa yeye kufanya hivyo,“Nitaongea nae tu hakuna tatizo, ila habari njema ni kuwa wakina Junior wamefurahi sana kwenye makazi yao mapya”“Na mamake kasemaje?”“Amefurahi sana kwakweli, nadhani alikuwa akiwaza sana maisha ya mwanae ila kwasasa kafurahi, mimi nitakuwa naenda kuwatembelea mara kwa mara ili kujua maendeleo yao. Halafu kuna mahali nimemtafutia Vaileth atakuwa anaenda kujifunza maswala ya ushonaji, ngoja kwanza mtoto akue kue”“Oooh hapo sawa mke wangu”Mara simu ya baba Angel ilianza kuita, alipoiangalia aliona namba ya yule mwarabu, alishangaa sana na kusema,“Huyu mwarabu ananipigia leo usiku kuna nini?”“Pokea umsikie”baba Angel alipokea ile simu na kuanza kuongea nayo,“Mr.Erick, kesho nitakuja kwako hapo mapema kabisa kumchukua Erick mdogo, kuna mahali nahitaji kwenda nae, kwenye kile kiwanda nilichokwambia”“Oooh sawa nimekuelewa hakuna tatizo”Basi yule mwarabu alikata simu kisha mama Angel akamuuliza mume wake,“Kwani huyo mwarabu na Erick huwa wanafanya kazi gani? Maana naona kama wiki yote hii Erick alikuwa akienda kwenye kazi ya huyo mwarabu”“Aaaah huyu mwarabu kuna biashara zake alipenda Erick amuelekeze, halafu pia kuna kiwanda chake kimoja hivi niliongea nae, aliniomba Erick afike pale kwa siku moja ili amuelekeze baadhi ya mambo”“Ila mume wangu unaona ni sawa kwa watu kumtumia hivi mtoto wetu? Hivi huyu Erick atakumbuka masomo kweli? Naona kama itaenda enda hela zitaanza kumtawala, lini nimemuona Sarah kavaa viatu vya gharama sana, nimemuuliza kavitoa wapi, kasema kanunuliwa na Erick, naona kama Erick ameanza kutawaliwa na hela”“Hapana mke wangu, Erick ni kijana mwenye akili sana na anajitambua sana, kwahiyo hata tusiwe na hofu naye, shule ikifunguliwa basi atakazana na masomo na bila shaka atamaliza vizuri maana ana akili”Waliongea kiasi ila mama Angel anaonekana hakuridhika kabisa na lile swala la Erick kufanya kazi na mwarabu.Asubuhi na mapema, Angel alitoka nje na kuanza kufanya usafi, kisha Erica na Sarah nao walitoka pia ila wakiwa sebleni pale kuna mtu aligonga mlango na Angel ndio alienda kufungua na kumkaribisha, mtu huyu alikuwa ni yule mfanyabiashara maarufu wa kuitwa mwarabu, basi walimsalimia pale ila huyu mfanya biashara hakuitikia kwanza zile salamu za wale mabinti.Kwa muda kidogo yule mwarabu alimtazama Angel na kusema,“Bila shaka wewe ni mjukuu wangu! Bila shaka wala kupepesa macho, wewe ni mtu wa ukoo wangu”Baba Angel nao na mama Angel walikuwa wametoka ndani ila hii kauli iliwafanya wajikute wamesimama gafla. Kwa muda kidogo yule mwarabu alimtazama Angel na kusema,“Bila shaka wewe ni mjukuu wangu! Bila shaka wala kupepesa macho, wewe ni mtu wa ukoo wangu”Baba Angel nao na mama Angel walikuwa wametoka ndani ila hii kauli iliwafanya wajikute wamesimama gafla.Yule mwarabu aliendelea kusisitiza pale kuwa Angel ni mjukuu wake, akasema,“Mbona mnanishangaa? Wewe binti ni mjukuu wangu kabisa yani, sijawahi kuwagundua wajukuu wangu haraka kama nilivyokugundua wewe”Baba Angel aliamua kusogea maana aliona huyu mwarabu anaharibu tu kwa muda huo, Angel alitoka pale na kukimbilia chumbani kwake, basi baba Angel alitoka kidogo nje na mwarabu ili kuongea nae ila mwarabu ndiye aliyeongea,“Erick, kwakweli nahitaji kuongea na wewe kwa upana zaidi kuhusu huyo binti, nahisi kabisa ni damu yangu. Huyo binti ni mjukuu wangu”“Sawa sawa, tutaongea vizuri hakuna tatizo juu ya hilo”“Kwa muda huu naomba niitie Erick mdogo niende nae huko maana inatakiwa tuwahi ndiomana nimemfata mwenyewe”Basi baba Angel anamuita Erick mdogo na Erick anatoka akiwa kajiandaa sababu baba yake alimwambia juu ya hilo, kwahiyo moja kwa moja Erick anaondoka na yule mwarabu.Baada ya kuondoka tu, mama Angel alimfata baba Angel na kuongea nae,“Mmmmh kaongee na binti yako huko, si unajua alivyo kisirani basi atakuwa kashachukia kuambiwa na huyu mwarabu kuwa ni babu yake ndiomana kaenda kujifungia chumbani kwake”“Ngoja nikaongee nae”Baba Angel aliondoka zake na kuekea chumbani kwa binti yake ambapo aligonga na kuamua tu kufungua mlango ambapo Angel hakuwa ameufunga kwa funguo, alimkuta Angel akilia, basi alimsogelea na kuanza kuongea nae,“Angel mwanangu tatizo ni nini?”“Najua babu zangu wote walishakufa, huyu simtambui naomba baba uniambie kuwa si babu yangu”“Hebu Angel tulia kwanza, tulia nikwambie. Kwani tatizo lako haswa ni nini?”“Mimi nakujua wewe tu baba, wewe ndio baba yangu sitaki kusikia kuwa mimi nina bab mwingine”“Sasa kwani ukiwa na baba mwingine Angel ni tatizo?”“Kwani baba hunipendi?”“Hapana, nakupenda sana binti yangu”“Sasa kwanini uruhusu mimi niwe na baba mwingine? Kwanini baba mwingine aje katika maisha yangu? Mimi nakutambua wewe tu”Baba Angel akapumua kidogo na kuona wazi kuwa lile ni tatizo, ila je nani wa kulaumiwa kwa lile tatizo? Ni mama Angel, baba Angel au Rahim? Hapo hakujua kwakweli yani alijikuta akikosa hata jibu la kusema kuhusu kumsaidia Angel, aliishia tu kumbembeleza na kumuhakikishia kuwa yeye ndiye baba yake halisi,“Kwani baba si uliniambia hizi nywele nimefanana na bibi yako?”“Ndio, bibi yangu alikuwa na nywele ndefu hata baadhi ya watu walimuita mwarabu”Hapo Angel alitulia kidogo kuona kuwa kuna mtu kafanana nae kwenye ukoo wa baba yake, na hiko ndio kitu pekee ambacho huwa kinamfanya Angel afarijike maana huwa akiambiwa tu kafanana na huyo bibi alikuwa akijihisi amani sana.Mwarabu alifika kwenye kiwanda chake na Erick, ambapo alianza kumuonyesha baadhi ya sehemu na vitu ambavyo kile kiwanda kinatengeneza, kuna mahali kwenye kile kiwanda kipo chini ya usimamizi ya mwanamke ambapo huyu mwanamke Erick alikuwa hapendi kukutana nae sababu alimsumbua hata walipokuwa dukani kwa yule mwarabu ila alimkuta tena kwenye hiko kiwanda akiwa ndio msimamizi wa sehemu hiyo,“Unamkumbuka huyu eeeh!! Huyu wa kuitwa Zaby”“Namkumbuka ndio”“Haya, kwasasa nitakuacha nae hapa ili umuelekeze baadhi ya vitu halafu mimi nitaondoka na kurudi badae, nitakuchukua mimi mwenyewe na kukurudisha kwenu”Erick aliitikia tu, na yule mwarabu kweli aliondoka kwa muda ule, na sehemu ile kumuacha Erick pamoja na yule Zaby, basi Zaby alianza kumuelekeza,“Hii sehemu tunatengeneza haswaa nguo za ndani za wanawake za kuvaa kwenye tupu yao”Zaby alianza kumuonyesha Erick baadhi ya nguo za ndani na jinsi ya kutengeneza, huku akimwambia kuwa wameambiwa yeye atawaonyesha cha kufanya zaidi, basi waliwatembelea wote wanaotengeneza pale kwenye mashine, kisha Zaby alienda ofisini na Erick ili Erick aweze kuandika baadi ya mambo, na kweli Erick alikaa na kuanza kuandika andika, yule Zaby alizunguka kwa nyuma ya Erick na kumshika mabega na kuwa kama akimkanda kanda yale mabega,“Niache bhana”“Erick una nini lakini? Mbona ni mshamba hivyo wewe”“Ndio, niache na ushamba wangu”“Sawa, ila ngoja nikuonyeshe kitu”Mara Zaby alienda mbele ya Erick na kumwambia,“Unafahamu tupu ya mwanamke?”Erick alinyamaza tu, na muda ule ule yule Zaby alifungua nguo yake na kumwambia Erick,“Hii nguo ya ndani pia imetengenezwa hapa, ngoja niivue uone tupu ya mwanamke”Erick aliinama chini na kujilaza kwenye meza kabisa kwani hakutaka kuonyeshwa alichotaka kuonyeshwa na Zaby, mwishowe aliona hata kuinama haitasaidia bali aliinuka na kutoka nje ya ofisi na kuona ni bora aende kuandika kule kule kwenye mashine ambako kuna watu wengi wakitenda kazi, kwahiyo alielekea kule kule kwenye mashine.Mchana wa siku hii Angel alienda kukaa bustanini ambapo Erica na Sarah walimfata na kuanza kuongea nae mambo mbalimbali, ambapo Sarah alimuuliza Angel,“Eti dada, nini maana ya mapenzi?”“Mmmh na nyie mna mambo sana, mnataka kujua maana ya mapenzi! Na wewe Erica unataka kujua?”“Mmmh ndio, ningependa nijue”“Mapenzi ni kumpenda anayekupenda”Erica akauliza kitu,“Je mapenzi ni kuangalia video za watu wanaofanya mapenzi?”Angel alishtuka na kumuangalia vizuri Erica, kisha akamuuliza,“Ni video gani mnazizungumzia?”“Ni video za wakubwa, zipo kwenye simu ya Sarah”“Kheee Sarah ndio huwa unaangalia hizo video?”Erica akajibu tena,“Tena, aliangalia na Elly hadi wakapeana mimba”Angel alishangaa sana na kuwaangalia kwa makini, kisha akasema,“Mnajua nyie bado wadogo sana? Mimi tu wala sithubutu kuangalia hizo video, eeeh Sarah ulijisikiaje ulivyo nanii na huyo Elly?”Sarah akapumua kidogo na kumuangalia Angel kwa aibu kidogo huku akiogopa kusema na kumfanya Angel amuulize tena,“Niambie Sarah ulijisikiaje?”“Kwani wewe dada hujawahi kujaribu?”“Mmmh naogopa, nasikia kuna maumivu”“Mmmh hamna, ni kidogo tu ndio maumivu”“Halafu inaendeleaje?”“Sijui ila nitakuonyesha video”Erica akadakia na kusema,“Mimi hizo video sitaki kuonyeshwa”“Sawa hakuna tatizo, leo Sarah njoo ulale chumbani kwangu”“Sawa dada, kwakweli nitafurahi sana kupata mtu wa kukubaliana nami kwa hizi video maana zingine ni nzuri”“Mmmh!”Erica aliguna na kuinuka zake kwani aliona zile mada kumuendea kushoto kabisa kwa wakati ule, basi moja kwa moja Erica alienda kufanya kazi zake zingine.Usiku wa leo wakati Erica anataka kulala tu, muda sio mrefu chumbani kwake aliingia Erick na kumfanya Erica ashtuke kidogo na kumkaribisha,“Karibu Erick”“Oooh umenikaribisha leo, hadi nimejihisi furaha”Basi Erick alienda kukaa kitandani kwa Erica na kuanza kumwambia,“Erica, ndugu yangu, pacha wangu, mpendwa wangu naweza kukuita pia mpenzi wangu. Kuna jambo nahitaji kuongea na wewe, maana uliniambia niwe huru kuongea nawe”“Niambie tu hakuna tatizo Erick”“Ni hivi, kule kwenye kazi za yule mwarabu ambako huwa naenda, huwa nakutana na mdada mmoja anaitwa Zaby, kwakweli yule mdada huwa ananiweka kwenye majaribu sana, na leo ndio kaniongezea majaribu”“Kivipi?”“Yani, kunai le wiki nilikuwa naenda kwenye duka la yule mwarabu basi huyo mdada alikuwa akinifata sana, mara aanze kunipapasa kwakweli ananipa majaribu na kunikosesha amani, nikimkemea hata hanisikii kabisa. Sasa leo ofisini kaja kuvua nguo mbele yangu, nimejihisi vinaya sana na kutoka mule ofisini”Erica alipumua na kumpa pole Erick,“Pole sana kaka yangu”“Asante, sijui nawezaje kuendelea kuishi na yule kiumbe kwenye ile ofisi”“Dah!! Pole sana hata sijui nikusaidiaje”“Cha kunisaidia kipo”“Kipi hiko?”“Inatakiwa mimi na wewe tulale pamoja tukiwa watupu kabisa”“Mmmh isiwe nyumbani basi maana itakuwa balaa, hawatafikiria kama hatuna lengo baya au unasemaje?”“Ni sawa isiwe nyumbani, kwahiyo tuombe ruhusa siku twende hotelini au unasemaje? Tuwaambie kuwa tunaenda kutembea, mimi na wewe tu kama siku ile tulivyoenda ufukweni”“Aaaah hapo sawa, ila tutafanya nini humo?”“Itajulikana tu humo humo tukiwa pamoja”“Sawa, nenda kalale basi”Erick alimuangalia Erica, kisha alimsogelea na kumbusu kwenye paji la uso kisha alimuaga na kuondoka, ila Erica alibaki tu ameduwaa kwa muda kidogo yani siku hiyo pia alilala huku akijifikiria vile hadi alijiuliza,“Kwani ni mara ya kwanza Erick kunibusu? Hapana, kwanini leo imekuwa tofauti na siku zote?”Alikosa jibu kabisa ila aliamua tu kulala kwa muda huo.Baba Angel akiwa ofisini kwake, alipigiwa simu na mwarabu kisha alimuelekeza ofisi yake ilipo ambapo yule mwarabu alienda ofisini kwa baba Angel na kumkuta pale, alianza kuongea nae,“Hongera sana, sikuwahi kufika kwenye ofisi yako, ila una ofisi nzuri sana, na ipo kwenye mpangilio mzuri, nimependa watu uliowaweka mapokezi ila mbona ni wamama watu wazima sana?”“Aaaah ni mke wangu huyo ndio aliamua vile, alisema ofisi zinazoweka vijana ni kwaajili ya kuvutia wateja, ila hapa hatupo kwenye mvuto ni tupo kwenye kazi tu, wateja wetu ni wa kwenye mitandao, kwahiyo naona hakuna tatizo kuwa na watu wazima hapa”“Ila mkeo ana akili, kaona mabinti wasijekukuungiza majaribuni mume wake, maana mabinti wengine nao kama wametumwa vile. Kuna kamoja nimekafukuza kazi pale kwenye ofisi zangu, kalikuwa kana mambo ya ajabu sana, huwa nawaambia watu waje kwa maadili kazini, ila yeye kila siku anavaa vimini tena vimini haswaa halafu akifika ofisini kwangu ni lazima ainame hata kama hana sababu ya kufanya hivyo, juzi nikamwambia mjinga wewe na kazi huna kuanzia leo, kila siku kuniweka kwenye majaribu tu”Baba Angel alicheka sana, na kuendelea kuongea,“Yani hapa ukikuta wanawake basi ni wamama wa makamo, ila ninachowapendea wapo vizuri sana kwenye kazi. Hata kipindi naumwa walijitahidi kumpa mwanangu ushirikiano mzuri sana, kwakweli mke wangu anataka mtu akiomba kazi hapa basi usahili amfanyie yeye, mke wangu nimemzoea mwenyewe, kule kiwandani tumeajiri wanaume tu, anasema kama kuna mwanamke anahitaji basi lazima amuone yeye kwanza”“Aaaah mke wako atakuwa na wivu sana”Mwarabu alicheka kiasi, muda kidogo alikuja yule bibi wa matunda na kuwaletea matunda pale, ila alipokuwa akiwasalimia yule mwarabu alimwambia,“Hivi wewe si ushawahi kufanya kazi nyumbani kwangu ukiwa na mtoto mdogo kipindi kile?”“Ni kweli ni mimi, sikujua kama ungenikumbuka”“Sura yako haibadiliki, yani sura ipo vile vile”Walisalimiana pale na kuongea mawili matatu kisha yule bibi alitoka, na mwarabu aliongea tena na baba Angel,“Kweli umeajiri watu wazima hapa, hadi huyu mwanamke! Ni siku nyingi sana aliwahi kufanya kazi kwangu”“Aaaah huyu sijamwajiri, ni mama ambaye huwa anatusambazia matunda”Ila baba Angel leo alishangaa pia maana hata hakumwambia huyu bibi alete matunda ila huyu bibi alileta matunda kwa baba Angel, kisha mwarabu alianza kueleza azma yake ya kufika siku hiyo,“Nahitaji kujua ukweli kuhusu yule mtoto wa jana”“kivipi?”“Erick sikia, nina uhakika asilimia mia moja kuwa yule ni mjukuu wangu, yani haiwezekani kupinga hiyo, naomba uniambie ukweli tu”“Sawa, je ni mjukuu wako kwa mtoto wako yupi?”“Mimi sijui ila nahisi ni mjukuu wangu tu”“Basi, nenda kamuulize vizuri mwanao Rahim, muulize kuwa imekuwaje na yeye atakujibu kuwa imekuwaje ukiniuliza mimi hakutakuwa na jibu zuri”“Ila ungeniambia wewe ingekuwa vizuri zaidi”“Najua ila itapendeza zaidi akikwambia Rahim”“Kesho nitajitahidi nikutane na kijana wangu nimuulize hayo maswala”Sababu muda nao ulikuwa umeenda ikabidi yule mwarabu amuage baba Angel, naye baba Angel muda kidogo tu alitoka ili kuondoka ila moja kwa moja alienda kwa yule bibi muuza matunda na kumuuliza,“Mbona sijakuagiza matunda leo ila ukaniletea?”“Nilitaka yule mwarabu anione”Baba Angel alicheka sana na kuondoka zake.Usiku wa siku hiyo, baba Angel alimweleza mkewe jinsi mwarabu alivyofika kuongea nae ofisini kwake,“Nimemwambia akamuulize mwanae”“Yani angekuja kuniuliza mimi mwenyewe hata asingejisumbua kumuuliza huyo mwanae”“Ila mwanae ndio atampa jibu zuri”“Kesho nimepanga kwenda kumtembelea Junior na Vaileth ili kuona maendeleo ya ndoa yao maana Junior haaminiki ujue, yani Junior huwa namuamini robo robo”“Ni kweli Junior haaminiki na utakuwa umefanya jambo jema sana kwenda kuwaangalia ni jinsi gani wanavyoishi na kuendelea na maisha yao ya ndoa.”Walipanga mambo mengi na kuamua tu kulala kwa muda huo, ila simu ya mama Angel ilianza kuita kabla hata ya kulala vizuri ikabidi mama Angel aipokee na kuanz akuongea nayo,“Unaongea na Manka hapa”“Kheee Manka!!”“Nakuuliza, mwanangu Sarah yupo kwako?”“Kama ungetaka kujua yupo kwangu au hayupo kwangu ungekuja nyumbani kwangu na sio kuniuliza kwenye simu”“Erica, mimi na wewe hatuna ugomvi na wala hatujawahi kugombana, ninavyomuulizia Sarah nina maana yangu kubwa sana, Sarah ni mwanangu na Sarah ndio maisha yangu na kwa kifupi siwezi kuishi pali na Sarah nimevumilia lakini nimeshindwa”“Ni usiku huu Manka, ukimtaka mwanao njoo nyumbani sio tuongee kwenye simu”“Haya nitakuja kesho kutwa maana nipo mbali”Halafu Manka alikata ile simu na kumfanya mama Nagel amuangalia mumewe kwa makini na kusema,“Jamani, unajua huyu mwanamke kaanza kuwa chizi, hivi mtoto utamuuliziaje usiku huu? Siku zote hizi alikuwa wapi kuja kumuulizia Sarah hapa? Kwanza sina amani kwa Sarah kurudi kwenye himaya yake maana huyu mwanamke kwenye kulea ni ziro kabisa”“Ila utamkataliaje mtoto wake?”“Aaaah sijui, ila hajui kulea mtoto kabisa. Mimi natamani Sarah nimlee mwenyewe maana naona hapa kwangu kabadilika vitu vingi sana”Muda huo waliamua kulala tu kwani muda nao ulikuwa umeenda sana.Kulipokucha kama kawaida baba Angel alitoka zake, mama Angel nae alijiandaa na muda huo huo kutoka zake kuelekea nyumbani kwa Junior na Vaileth.Angel alimuomba Sarah simu yake na kumpigia Samir ili aende kumchukua aweze kwenda nae kwa bibi yake kuchukua simu yake ambayo bado ilikuwa kwa bibi yake.Basi baada ya muda kidogo tu, Samir alifika kwahiyo Angel aliondoka na Samir na pale nyumbani kuwaacha wadogo zake tu.Samir na Angel walikuwa wakiongea mambo mengi sana walipokuwa njiani,“Hivi uliwaza kweli kama kuna siku itatokea kama hivi mimi na wewe kuongozana wote njiani?”“Mmmh ni ngumu kwakweli, ila nilikuwa naamini maana ni kweli nakupenda sana Angel”“Je kwa bibi tutaingia wote?”“Uwiiii kwa yule bibi yako alivyokuwa na mdomo, akituona wote itakuwa balaa. Kwahiyo mimi nitakusubiri mahali ili ukitoka tu tuwe pamoja”“Niambie ni wapi utakapo nisubiria maana yule bibi huwa anajishauwa utasikia anataka kunisindikiza”“Mbona dawa yake ndogo, mwambie bibi nakuonea huruma na utu uzima huo, najua tu miguu itakuuma kwenda nami mpaka barabarani. Ngoja niite bodaboda”“Mmmh kwa yule bibi alivyo, utasikia na mimi nataka kufanya zoezi, nitembee tembee hadi stendi”“Basi mwambie kuwa umechoka kutembea na utakodi bodaboda, halafu mimi na wewe tutakutana pamoja”“Halafu tutaenda kuongea wapi?”“Kuna kitu nikuombe leo Angel”“Niambie tu”“Naomba leo tukaongee hotelini, yani ukitoka tu kwa bibi yako tutakodi bajaji na moja kwa moja tutaenda nayo hotelini kule kidogo nje ya mji halafu hatutaongea sehemu ya wazi bali tutakodi chumba na kuongea humo”“Mmmmh hiko chumba utakodi wewe!!”“Ndio, kwnai tatizo liko wapi Angel hata usiwe na wasiwasi”Na kweli waliongozana hadi kwa bibi wa Angel ambapo Angel alienda moja kwa moja kwa bibi yake ambaye alifurahi kumuona na kumsifia kuwa amekuwa,“Kwakweli mjukuu wangu umekuwa mkubwa sasa, yani mwanadada mkubwa kabisa, najiona kuzeeka zaidi”“Bibi bhana, kumbuka Junior ana mtoto”“Kwani Junior tupu, umesahau watoto wa mamako mkubwa Mage, yani mimi nishazeeka jamani. Haya karibu”“Bibi, nimemaliza shule nahitaji ile simu”“Umekubaliana na mama yako hivyo au?”Angel alijaribu kumwambia maneno bibi yake ya kumbembeleza ili ampatie ile simu, kwahiyo bibi yake ilibidi tu akaitoe ile simu na kumkabidhi Angel ambaye alifurahi sana, na muda kidogo akamuaga bibi yake,“Khaaa mbona mapema hivi, hutaki hata kusubiri chakula?”“Bibi, nimetoka nyumbani nimeshiba sana halafu nimemwambia mama kuwa sitachelewa kurudi”Yani Angel alitumia maneno yote ya kumshawishi bibi yake na mwisho wa siku bibi yake mwenyewe alikubali na kumpa ruhusa Angel ya kuondoka, ambapo Angel aligoma kabisa kusindikizwa na bibi yake kisha akatoka na moja kwa moja alienda kukutana na Samir na kuondoka zao kuelekea kwenye hoteli waliyopanga kuwa wataenda kwa siku hiyo.Leo, Elly alienda nyumbani kwa mama Angel yani yeye hakutaka tu kuonana na wengine pale, kwahiyo siku hiyo wakati Erica na Sarah wamemwambia kuwa wamebaki wenyewe aliamua kwenda pale na kuongea nao mambo mbalimbali, ambapo kama kawada Elly alianza kulalamika kuhusu wazazi, aliamua kuwaeleza Erica na Sarah ukweli,“Hivi unajua kuwa mimi yule ninayeishi naye sio mama yangu mzazi!”Erica na Sarah walishtuka na kumuuliza vizuri,“Kivipi?”“Siku zote nilikuwa nikiishi na mama na nilijua ni mama yangu mzazi, ila swala la mimi kugundua baba yangu ni nani ndilo ambalo lilianza utata, na hapo nikaja kutajiwa mama yangu kuwa mwanamke mwingine kabisa ambaye sifikirii kuwa anaweza kuwa mama yangu”“Kwahiyo umeambiwa mama yako ni nani?”“Eti mama yako Sarah ndio mama yangu”Hapo Sarah alishtuka sana kwani hakuelewa ukizingatia anachojua ni kuwa kwa mama yake yeye ni mtoto wa pekee ilibidi amuulize vizuri Elly kuhusu tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa, alipotajiwa ndio alichoka zaidi kwani ndio tarehe ile ile, ila Erica alisema,“Mbona hata mimi na Erick tumezaliwa tarehe hiyo hiyo!”“Sasa inamaanisha mimi na Elly ni mapacha?”Erica alijibu,“Inawezekana”Sarah aliinama chini na Elly nae aliinama chini, ndipo Erica aliposema,“Uwiii halafu mkapeana mimba, toka lini mapacha wakapeana mimba? Mtakuwa na laana nyie”Elly na Sarah wote walikuwa kimya kwa muda, ila Erica akasema tena,“Inawezekanaje lakini? Imekuwaje mlelewe sehemu tofauti tofauti? Mnajua hairuhusiwi kwa ndugu kuwa na mahusiano? Yani nyie ni laana”Sarah akapumua kidogo na kupiga magoti kwa Elly huku akimwambia,“Naomba unisamehe Elly, sio kwamba nakubali kama sisi ni mapacha hapana, ila hata kama sio mapacha bado sisi tuna undugu halafu ni mimi ndio nilikuingiza kwenye dhambi hii naomba unisamehe Elly”Kwa muda huo Sarah na Elly wote walijikuta wakianza kulia na kujutia kile ambacho kimefanywa kati yao.Mama Angel alipofika nyumbani kwakina Junior, alifurahi jambo moja kumkuta dada yake yupo kule kwa wale watoto na kuanza kuongea nae,“Dada nimefurahi sana kukukuta, ni leo ndio umefika?”“Hapana, nipo hapa toka juzi, tabia za mtoto wangu nazijua lazima niwe nae karibu, nimemuomba hadi mume wangu ruhusa, nitakaa huku kwa wiki nzima”“Oooh vizuri sana dada, ila ulikutaje?”“Unajua Junior alianza habari zake za kutoka na kurudi usiku wa manane ila nipo hapa nimemdhibiti, nataka afanye mambo ya maana sio afikirie ujinga ujinga wa kwenda kuzunguka huko na wanawake”“Umefanya jambo la maana sana, sababu hata mimi nilikuwa nafikiria jambo hili”Waliongea vitu vingi sana, ila mama Angel hakutaka kukaa sana mahali pale na kuamua kumuaga dada yake tu pamoja na Vaileth na Junior.Wakati mama Angel anarudi, njiani alikuta na Rahim ambaye alifurahi sana kukutana na mama Angel kisha akamwambia,“Ingawa baba yangu kaniambia kuwa leo ana maongezi na mimi, ila nimefurahi sana kukuona wewe, nina mengi ya kuzungumza na wewe. Naomba usikatae maana haya ninayotaka kuzungumza na wewe ni ya muhimu sana, naomba tutafute mahali tuweze kuzungumza haya”Mama Angel alifikiria kidogo, akaona pengine Rahim ana jambo la muhimu sana la kuweza kuzungumza nae kwahiyo aliona ni vyema kufanya mazungumzo nae, maana hakutaka kufikiria katazo la mume wake kwa muda huo.Basi waliondoka na kwenda mahali na kukaa hapo kisha kuanza mazungumzo,“Niambie cha maana Rahim, usinianzie mambo yasiyoeleweka”“Sina mambo yasiyoeleweka, hapa nataka tuongee kuhusu mapacha wako yani Erick na Erica”“Mmmh wamefanyaje tena watoto wangu?”“Kuna tatizo kubwa sana kati ya wale watoto”“Lipi hilo?”Rahim alikaa vizuri na kutaka kuanza kumuelezea mama Angel, ila kabla hajaanza kumuelezea alishtuka sana kiasi hata mama Angel alishtuka pia na kugeuka sehemu ambayo Rahim alikuwa akiangalia, hapo alimuona Angel akiwa ameongozana na Samir huku wameshikana mikono. Rahim alikaa vizuri na kutaka kuanza kumuelezea mama Angel, ila kabla hajaanza kumuelezea alishtuka sana kiasi hata mama Angel alishtuka pia na kugeuka sehemu ambayo Rahim alikuwa akiangalia, hapo alimuona Angel akiwa ameongozana na Samir huku wameshikana mikono.Mama Angel alishtuka sana, na kufanya ainuke ambapo nae Rahim aliinuka na kutaka kuwafata wale watoto wao, ila gafla kuna upepo unapita kati yao kwa muda na kufanya wajifikiche macho, kitendo kile kilifanya Angel na Samir kupotea mbele ya macho yao na kufanya Rahim na mama Angel waangaliane kwa mshangao, huku Rahim akisema,“Unaona haya mambo Erica? Wote wale ni watoto wangu! Hasira zako za kutokutaka mtoto aufahamu ukweli ndio umeniletea mambo kama haya, wameenda wapi wale watoto?”“Mimi sijui, unanilaumu bure Rahim, mimi sijui kitu”“Hujui kitu wapi? Unajua kila kitu wewe”“Rahim, utanilaumu bure tu, ni kweli huyo Samir kaanza kumfatilia Angel kwa muda mrefu sana ila siku zote nimekuwa nikipinga mahusiano kati yao hadi kumpeleka mwanangu kwenye shule ile ya mbali ila bado nikaja kwenye mahafali na kuwakuta”“Ulishindwa nini kuniambia mapema?”“Sikujua mimi kama Samir ni mwanao pia”“Mara ngapi nimekwambia kuwa Angel awajue ndugu zake? Mara ngapi Erica nimekuomba juu ya jambo hili? Nitaweka wapi sura yangu mimi? Nataka kurekebisha nyumba ya mwenzangu wakati na ya kwangu inateketea! Hebu niambie cha kufanya kwasasa?”“Sijui mimi nahisi kuchanganyikiwa hapa”Rahim alichukua simu yake na kumpigia Samir simu ila simu iliita hadi kukatika yani haikupokelewa kabisa, basi alimuuliza mama Angel,“Naomba namba ya Angel nimpigie”“Angel hana simu”“Aaaargggh nilikuwa nakusifia siku zote ila sikuwahi kufikiria kuwa wewe ni mwanamke mshamba kiasi hiki, mtoto mkubwa kama Angel asiwe na simu kweli!! Aaaarrgh, nitafutie wanangu Erica na ole wako chochote kibaya kitokee kwao”“Usinitishe baba, tena usinitishe kabisa, ungejua kama ni wanao wanatakiwa kuwa karibu basi toka zamani ungejiheshimu na kuheshimu wengine. Ulinifanyia visanga vyako wakati mtoto mdogo hadi nikambadilisha jina sababu ya ujinga wako. Haya, Erick akakupa ruhusa ili mtoto akuzoee ukataka kunibaka, ulitaka tukubebe mgongoni au ndio ujue namna ya kulea mtoto? Mara ngapi umenitukana na kumtukana huyo Erick bila kujali kitu, wala hukujali kuwa mimi ni mwanamke ambaye uliniacha kwa aibu nikalea mtoto mwenyewe, ila usivyokuwa na haya ukanitukana na kuniita malaya, nakumbuka vizuri usidhani sikumbuki, mtoto kafanana kila kitu na wewe hata mtu baki akimuona hapingi kuwa ni mwanao ila wewe ukathubutu kusema huenda hata mtoto sio wako, eti nimempata kwenye umalaya, hivi unafikiri hiyo kauli inanitoka kichwani kwangu? Nakumbuka vizuri, yani Rahim uliniona mimi kama takataka ya kutupwa, leo unanikoromea na kunipa vitisho eti nitafutie wanangu, baba niache tena uniache kabisa, kama kulia nishalia sana, kama kumkanya huyo mtoto nishamkanya sana, usinichefue mie”“Yani unavyoongea utadhani hakuna kitu kibaya kilichotokea hapa, hebu tutafute watoto hayo mambo yaliyopita tuyaache”“Hiyo kazi ya kutafuta watoto nakuachia wewe, kwaheri”Mama Angel aliondoka zake kwa muda huo hata hakutaka kuangalia nyuma wala nini na kumuacha pale Rahim akijiuliza maswali mengi sana.Rahim alikaa chini kwanza huku akijiuliza kuwa wale watoto ataanza kuwakuta wapi, alijisemea,“Yani wanawake ni watu wa ajabu sana, yeye ndio mwenye makosa halafu yeye ndio wa kwanza kulalamika hapa, hata kama mimi nina makosa ila yeye hakupaswa kumficha mtoto kuhusu ukweli halisi wa mimi baba yake, hata sijui naanzia wapi kuwatafuta, ila huyu Samir huyu nadhani hanijui vizuri”Ila akaona ni vyema arudi nyumbani kwake ili aongee na mke wake waweze kumtafuta Samir kwanza.Mama Angel alifika nyumbani kwake akiwa amejichokea kwa kiasi Fulani siku hiyo kutokana na aliyoyaona, basi moja kwa moja alimuita Sarah na Erica na kuwauliza kuhusu Angel kuwa ameenda wapi, ndipo Sarah aliposema,“Aliniomba simu yangu kuwasiliana na yule mchumba wake, halafu alisema kuwa anenda sijui kwa bibi”“Aaaah jamani!!”Mama Angel alienda chumbani kwake na moja kwa moja kumpigia mama yake simu ambaye alisema kweli Angel alienda na alichukua simu yake akisema kuwa kaagiziwa na yeye, yani mama Angel alisikitika sana ila hakumwambia ukweli mama yake na kuagana nae tu, alijiuliza mno kuwa atampata wapi huyo Angel! Aliwaza sana na kukosa jibu, ila alijipa imani kuwa Angel atarejea tu nyumbani.Mpaka baba Angel anarudi nyumbani, bado Angel hakuwasili na kumfanya mama Angel aongee na mumewe juu ya swala hilo,“Kheee kwahiyo ulimuona Angel na huyo Samir kabisa?”“Ndio, yani ni upepo tu ndio umetupoteza. Kwahiyo Angel hadi muda huu yupo na yule kijana, kuan usalama kweli hapo?”“Asilimia kubwa hakuna usalama ila tunatakiwa kuwa wapole kwasasa ili tuweze kumpata Angel”“Tatizo tunampataje? Yani hadi nimechanganyikiwa”“Nipatie namba ya simu ya huyo Samir!”Mama Angel alimpatia namba aliyoitoa kwa Sarah ambapo hata kwake iliita tu bila ya kupokelewa, basi baba Angel nae aliipiga kwa muda kidogo ila haikupokelewa, na kufanya watazamane wasijue cha kufanya kwa muda huo,“Sasa tutafanyaje mume wangu, kwanini Angel kaamua kunidhalilisha hivi?”“Ni ujana tu unamsumbua mke wangu, halafu wamejua wazi kuwa mmewaona ndiomana hawapokei simu. Angel anajua jinsi ulivyomkali, yani hapo anajua kipigo atakachokipata toka kwako, mbona atamsahau huyo Samir muda huo huo. Nakuona mke wangu jinsi ulivyofura kwa hasira ila inatakiwa tuwe wapole kwanza ili kuweka mambo sawa”“Hii ni aibu mume wangu, tena aibu kubwa sana. Tunafanyaje sasa?”“Ngoja niwatumie ujumbe, inatakiwa tuwe wapole tu kwasasa mke wangu ili huyu mtoto arudi nyumbani”Basi baba Angel akaandika ujumbe na kuutuma kwenye namba ya Samir,“Samir, najua upo na mwanangu kipenzi Angel, mimi baba yake nampenda sana na ninatambua ni jinsi gani wewe na yeye mnapendana. Ila inatakiwa kuwepo na utaratibu wa nyie kutambulika vizuri kwetu ili muwe huru kabisa, mimi sina kipingamizi chochote juu ya mapenzi yenu. Naomba mpatie simu mwanangu Angel niongee nae japo kidogo tu, nimemkumbuka sana na ninaumia sana juu yake, natamani kusikia sauti yake ili roho yangu itulie kuwa mwanangu yupo salama”Kisha baada ya nusu saa, baba Angel alipiga ile simu ambayo iliita kama mara mbili na kupokelewa, kisha baba Angel alianza kuongea nayo,“Unaendeleaje mwanangu Angel?”“Naomba unisamehe baba”“Sina tatizo mimi, ila nahitaji kujua hali yako”“Nipo salama baba, sijapenda kufanya hivi ila naogopa kurudi nyumbani”“Naelewa mwanangu, ila mimi baba yako ninakuhakikishia kuwa kuna usalama kabisa nyumbani, hakuna mtu yoyote wa kukubugudhi wala nini, mimi kama mzazi nahitaji kupata heshima, sio jambo zuri kwa mtoto wa kike kama wewe kulala nje ya himaya ya wazazi wake. Nakuhitaji nyumbani mwanangu. Niambie ulipo nije kukufata”“Mmmmh baba, naogopa mama atanipiga”“Hapana, wala mama yako hawezi kukupiga. Niambie ulipo Angel mwanangu kipenzi, mimi nitakuja kukufata. Nimekwambia nilipo mimi hakuna yoyote wa kukudhuru, sina nia mbaya kwako wala kwa huyo Samir, tena nitakuwa namkaribisha vizuri sana nyumbani kwangu”“Basi baba nitakutumia ujumbe wa mahali nilipo”“Sawa, nitumie sasa hivi mwanangu maana nishajiandaa hapa, nakuja kukufata malkia wangu”Kisha simu ilikatwa, halafu mama Angel alimuangalia mume wake na kumwambia,“Yani mtoto kafanya ushetani kiasi hiko halafu unakazana kumbembeleza!! Akirudi hapa, kwakweli leo lazima nimfundishe adabu”“Nani kakwambia kuwa ni fimbo pekee ndio zinafundisha mtoto adabu? Muulize mamangu mkubwa yule aliyenilea, muulize alinipiga mara ngapi ila niliweza kuelewa? Alikuwa hadi akilia yule ninapofukuzwa shule, fimbo hazifundishi mtoto mke wangu, mimi nitaenda kumfata, tafadhari usimpige Angel niachie hiyo kazi mwenyewe kama huwezi kumfundisha kwa mdomo nitamfundisha mwenyewe”Muda kidogo ujumbe uliingia kisha baba Angel alitoka muda ule ule kwenda kumfata Angel.Kwakweli mama Angel alitulia kwa muda na kutafakari sana huku akijisemea,“Yani sijui damu ya Erick na Angel zimeendaje, yani hawa watu wanapatana sana. Nakumbuka Angel wakati mdogo analilia simu anaongee na Erick, hajui kuongea ila nikimuwekea simu anatulia tuli, sijui Erick alikuwa akimwambia nini mtoto, ndio anambembeleza hivi hata akiwa na makosa!! Kwakweli Angel ana haki ya kumpenda huyu, baba zetu sisi, leo angepigwa hadi meno ya mbele yangemtoka.”Mama Angel akapumua kidogo na kuamua kutulia ili kusikilizia kuwa mwanae amefika.Baada ya masaa kadhaa, baba Angel aliwasili nyumbani na binti yake ambapo moja kwa moja Angel alienda chumbani kwake kulala kisha baba Angel alirudi chumbani na kumsihi mke wake kuwa walale tu kwa muda huoyani hakutaka mkewe aende kumsema Angel kwa muda huo wala nini.Kulipoucha asubuhi, baba Angel leo hakwenda popote, alitulia nyumbani na familia yake huku akiwataka watoto wake wampikie chakula ambacho anakipenda yeye ili aweze kula na kufurahi, kwahiyo walikazana kupika, muda huu wa asubuhi Erica alikuwa akipika chapati huku Angel alikuwa akitengeneza supu kwaajili ya baba yao, halafu Sarah alikuwa akichemsha maziwa basi walikuwa wakiongea mambo mengi jikoni, basi Angel akamuuliza Sarah,“Kwahiyo Sarah ulikuwa hujui kupika?”“Ndio, nilikuwa sijui kabisa, yani hizi ni juhudi za Erica, yeye kanifundisha mambo mengi na sasa nimejikuta naweza kupika baadhi ya vitu”Erica akachekesha pale,“Eti alikuwa hawezi kukaanga hata mayai”Angel alimcheka sana Sarah na baada ya hapo waliandaa kile chakula, ila siku hiyo ile asubuhi asubuhi alifika mgeni nyumbani kwao ambaye alikuwa ni Elly kwahiyo walijumuika nae mezani katika kula kile chakula cha asubuhi.Kwakweli, mama Angel bado alikuwa na kinyongo na binti yake kiasi kwamba hata hakuweza kwenda kukaa nao mezani na kunywa nao chai, moja kwa moja alitoka nje ya nyumba na kujifanya akifanya usafi nje ya nyumba yao, mara kidogo alifika mgeni na mgeni huyo alikuwa ni Manka, mama Angel alimkaribisha pale na kuanza kuongea nae,“Karibu Manka”“Sijaja kukaa sana, nimekuja kumuulizia mwanangu Sarah”“Tena uzuri wapo wote, yani Sarah na Elly”“Hivi na wewe unaamini kuwa Elly ni mwanangu?”“Kama Sarah na Elly wamezaliwa siku moja, hospitali moja, halafu wewe ndio uliyeweza kumchangia damu Elly, kwanini nisiamini kuwa Sarah na Elly ni watoto wako?”“Inamaana mzee Jimmy alimchukua mtoto wangu mmoja na kumgawa?”“Tatizo ulikuwa karibu na mzee Jimmy ila ambacho hukujua ni kile ambacho mzee Jimmy anaweza kutenda kwa watati wowote ule, yule mzee ni mafia kama ulikuwa hujui naomba nikujuze, kwahiyo hiko kitu anaweza kabisa kukitenda tena kwa upana zaidi”“Ila sidhani kama nilijifungua mapacha mimi?”“Utafahamu vipi na walikupiga nusu kaputi, usikatae ndugu yangu. Haya tuseme basi ulijifungua mmoja, ila Elly ndio mwanao na yule uliyemlea miaka nenda, miaka rudi sio mwanao”Hapo Manka alinyamaza kidogo, na kumuangalia vizuri mama Angel kisha akamwambia,“Unamaanisha Sarah!”“Ndio, Elly ni mwanao ila Sarah sio mwanao”“Haiwezekani, nasema haiwezekani kabisa”“Basi, kubali kuwa ulijifungua mapacha”Manka alikaa chini kwanza akiwa kama mtu anayetafakari jambo, kisha aliinuka na kuondoka bila hata kumuaga mama Angel yani alijihisi kuchanganyikiwa kabisa.Leo, moja kwa moja Sia aliamua kwenda kwa madam Oliva sababu alifikiria mambo mengi sana kuhusu yule mtoto wa madam Oliva yani Paul.Alivyofika pale siku ya leo, alimkuta Paul yupo mwenyewe ndani ya nyumba yani leo madam Oliva alitokana pia Steve alitoka basi alianza kuongea na Paul.“Unajua wewe umefanana sana na mwanangu aliyepotea miaka mingi iliyopita”“Mmmh kwahiyo una mtoto ambaye alipotea?”“Ndio, akiwa na miezi mitatu kasoro, niliumia sana kupotea kwa mwanangu. Nakumbuka kuna alama nilimuweka”“Hiyo alama ulimuweka klabla ya kupotea? Ulijua kama atapotea?”“Hapana, ila nilimuweka alama tu akiwa mdogo kabisa, alipopotea niliumia sana. Nilimuweka alama pembeni ya paja la mguu wa kushoto”Paul alimuangalia na kumuuliza,“Alama gani?”“Nilimuweka alama ya herufi S, nadhani kwasasa itakuwa ni ndogo sana katika mwili wake maana nilimuweka ilea lama akiwa mdogo”“Mmmh ulimuweka na kitu gani?”Hapo Sia alinyamaza kimya kwa muda na kuendelea kusisitiza kuwa aliweka hiyo alama,“Lengo langu ilikuwa ni kupata kumtambua kwa haraka pindi akipotea”“Ulikuwa unajua kama atapotea?”“Hapana, ila kuna kipindi watoto walikuwa wakipotea sana ndiomana nikafanya vile”“Ila unajua hata mimi nina alama hapo unaposema, tena alama yenyewe huwa nikiiangalia sana naona kama herufi S”Hapo Sia akapumua kidogo kwani akazidi kupata uhakika kuwa yule ndio mtoto wake kabisa, basi alimwambia“Unajua inawezekana kuwa wewe ndio mwanangu?”“Ukimaanisha kuwa mama aliniiba?”“Hapana, sina maana hiyo kabisa, ila huwezi jua wala walimbadilishia mtoto hospitali”“Unataka kusema kuwa wewe ni mama yangu?”“Sikulazimishi kuamini hilo, ila mimi niliona vyema nije kukwambia hili maana naona kuwa unafanana na mwanangu aliyepotea miaka ya nyuma iliyopita”Paul alikaa kimya kwa muda, na kufanya hata Sia kumuaga na kuondoka zake kwahiyo alimuacha ajifikirie mwenyewe tu bila ya yeye kusema chochote kile.Jioni hii mama Angel baada ya kuongea kwa muda na mumewe, aliamua kumfata mwanae chumbani na kuongea nae,“Unajua kwanini leo sijaweza kula siku nzima mwanangu?”“Hapana sijui mama”“Sababu ya matendo yako, kwakweli Angel umeniumiza sana. Kama mama nimeumia sana”“Nisamehe sana mama, naomba unisamehe”“Usione nimekaa kimya ukafikiri napenda hiki ulichokifanya. Haya naomba tuongee kirafiki, ni nini kimetokea kati yako jana na Samir?”“Nisamehe mama”“Sio nisamehe, nimeomba uniambie kilichotokea, mimi ni rafiki yako kwasasa”“Hakuna kilichotokea mama”“Una uhakika?”“Ndio, nina uhakika mama hakuna kilichotokea kati yetu”“Kuwa makini sana Angel. Mimi ni mama yako na unaniaibisha sana, unanikosesha raha, amani na furaha, unanifanya niwe na hudhuni sana. Naomba hiki kitu kisijirudie tena, ila napenda ujue kuwa Samir ni ndugu yako”“Aaaah sawa mama nimekuelewa”Mama Angel alifurahi kwa mwanae kumuitikia haraka vile ila hakujua ni kwanini mwanae kamuitikia haraka kiasi kile, basi aliongea nae kidogo tu na kuondoka zake, ila Angel alijisemea,“Yani hawa jamani, mtu mmoja unaambiwa kila mtu ni ndugu yako, yani naona dalili ya kupata ndugu dunia nzima, ila nitawafurahisha”Kisha akaendelea na mambo yake mengine.Usiku wa leo, wakati Erick akitaka kulala alipigiwa simu na Zaby, basi alipokea simu ile na kuanza kuongea nayo,“Erick upo wapi muda huu?”“Ndio nataka kulala”“Umevaa nini hapo?”“Kivipi?”“Kheee wewe Erick vipi lakini, una matatizo gani yani unajibu kama vile sio mwanaume. Hivi yote ambayo huwa nafanya kwako hunielewi au kiburi”“Kukuelewa nini?”“Mimi nakupenda sana Erick, nahitaji uwe mpenzi wangu”Erick alikaa kimya kisha Zaby akamwambia tena,“Naomba kwa usiku wa leo tufanye ngono kwa njia ya simu”Erick alikata ile simu, kisha Zaby aliendelea kumpigia kwa muda kidogo, Erick aliacha simu chumbani kwake na moja kwa moja kwenda chumbani kwa Erica ambaye alikuwa akijiandaa kulala pia, kisha Erick akamwambia,“Naomba kwa usiku wa leo nilale pembeni yako Erica”“Kheee kivipi? Si tulishakubaliana?”“Ndio, ila kuna kitu sitaki kulala mwenyewe chumbani kwangu”Muda huo huo alifika na Sarah, alisikia Erick akisema anaomba kulala humo na kusema,“Kama Erick unakataliwa na Erica kulala humu chumbani kwake basi twende ukalale chumbani kwangu”Erica alimuangalia Sarah na kumwambia,“Yani wewe Sarah, laana za Elly hujazimaliza halafu unataka tena laana za Erick, una nini lakini wewe? Hujui kama Erick ni ndugu yako!”“Najua, kwani kuna ubaya gani ninaotaka kuutenda? Si Erick kasema leo anashindwa kulala mwenyewe ndiomana mimi nimemwambia tukalale wote, kwani tatizo ni nini? Basi wote watatu tulale humu humu”Walikubaliana, kisha wote watatu wakalala kitandani kwa Erica.Kulipokucha, wote watatu walichelewa sana leo kuamka, kiasi kwamba mama Angel alienda moja kwa moja chumbani kwa Erick ila hakumkuta na kwenda chumbani kwa Erica na kukuta Erica, Erick na Samir wote wamelala pamoja tena wakiwa hawana habari kabisa, kwakweli mama Angel alitikisa kichwa chake na kushangaa sana, kisha aliwaamsha,“Hivi na wewe Erick, kuja kulala na wasichana ndio nini mwanangu jamani? Hebu amka hapo, uende chumbani kwako”Erick aliinuka na kuona hata aibu, moja kwa moja alielekea chumbani kwake, mama Angel aliwakaripia Erica na Sarah kisha kutoka zake na kwenda kumfata mumewe kumueleza,“Nimekuta wote watatu wamelala pamoja, Erica, Erick na Sarah”“Kwahiyo ule ugonjwa aliokuwa akiusema Sia kuwa Erica na Erick wanapendana sana ndio umehamia kwa Sarah pia!”“Alisema ugonjwa gani?”“Eti alisema watoto wetu wanapendana sana, upendo usio wa kawaida kabisa, nikamwambia wale ni ndugu tena ni haki yao kupendana. Akadai kuwa tuwachunguze, sasa tuwachunguze kitu gani!”“Yule Sia nae huwa haponi kichaa chake kile, nadhani bado akili yake haifanyi kazi vizuri, ila hawa watoto leo wamenishangaza sana, kulala wote watatu halafu wamepitiliza hata muda wa kuamka. Au kwavile leo Erick haendi popote pale?”“Itakuwa ni sababu pia, ila leo pia nitakuwepo hapa nyumbani”Basi mama Angel na baba Angel waliendelea na mambo yake mengine.Leo ni siku ambayo mwarabu alipata muda wa kuweza kuongea na mwanae Rahim, maana alimuita na kuanza kuongea nae kuhusu Angel,“Rahim, niambie ukweli kuhusu Angel”“Oooh baba kumbe umemjua Angel! Ni mtoto wangu yule, ni mtoto wangu kabisa”“Ni kwanini hafahamiki kwenye ukoo?”“Kwakweli baba, nakiri wazi kuwa nimefanya jambo ambalo sio sawa kabisa, nilikuwa na yule mwanamke na kumfanyia mambo mengi ya ajabu sababu ya ujana ulionisumbua. Kwa kipindi kile, mimi nilikuwa napendwa sana na wanawake, na walikuwa wakinipa pesa, nilikuwa nikipewa pesa na wanawake nami ndio nampa Erica yani mamake Angel, ila badae kuna mmoja aliiteka kabisa akili yangu basi nilijikuta kutokumpenda tena Erica, na vile ulivyonitafutia mchumba ndio kabisa sikumtaka tena”“Ila mwanangu hilo sio tatizo, ila tatizo ni kuwa kwanini hukumuweka wazi mtoto kwa siku zote hizi?”“Walinificha, yani Erick na Erica walikuwa wakimficha yule mtoto kwangu”“Ungeomba usaidizi hata kwa sisi watu wazima tungekusaidia, yani ulichofanya sio sawa kabisa mwanangu”Basi Rahim alimueleza baba yake na lile tukio la kumkuta Angel na Samir na kumfanya baba yake ashangae zaidi,“Hiyo ni laana ujue, inawezekana vipi kaka na dada kufanya hivyo?”“Sielewi mpaka muda huu baba, yani lile toto nimetamani hata kulitupa ila limetetewa na mama yake. Toto jinga lile kama mama yake”“Hata wewe ni mjinga, kukataa mtoto uliyezaa mwenyewe nao ni ujingahuo, kwahiyo usimseme tu huyo wakati hata wewe ni mjinga tena mjinga namba moja kabisa. Hapa cha muhimu ni kujua cha kufanya na watoto hawa”“tutafanyaje sasa baba?”“Kesho, twende tukamfate huyo Angel, na aambiwe mbele ya mama yake kuwa sisi ni ukoo wake natumaini ataelewa kisha tumchukue akafahamu ndugu zake wote”Wakaelewana kufanya hivyo kisha kila mmoja kuondoka zake.Jioni ya siku hii, Sia alikutana na Manka na kuanza kuzungumza nae kuhusu watoto wao, ambapo Sia alimwambia Manka,“Ngoja nikwambie kitu, yule mwanamke wa kuitwa Oliva, na yeye alijifungulia hospitali ile ile ya majanga, na hivi nikwambiavyo ni kuwa yule mtoto aliyenaye ndio mwanangu”“Kheee na mwanae yeye yuko wapi?”“Inawezekana mwanae akawa Sarah”“Hebu nenda huko, haya mambo yanawezekanaje? Mbona haieleweki?”“Inaeleweka vizuri kabisa, labda kama hutaki kuelewa kitu cha namna hii ila inaeleweka vizuri kabisa, mzee Jimmy alifanya jambo kubwa sana kwa watoto wetu. Mimi nilipewa Elly kumlea ambaye ni mwanao, Oliva alikuwa akimlea Paul ambaye ni mwanangu halafu wewe umemlea Sarah ambaye ni mtoto wa Oliva”“Haiwezekani hiyo kitu, unajua kwanini?”“Kwanini?”“Ngoja nikwambie kitu leo, ili uweze kujua kuwa hiyo kitu haiwezekani”“Haya niambie”“Ni hivi, mimi nilikuwa na mahusiano na mzee Jimmy, wakati huo nina mahusiano na Derrick. Mzee Jimmy alinihitaji mimi nilale na Erick ili niweze kuzaa na Erick, sijui alikuwa na lengo gani juu ya hilo, basi tulimnyeshwa pombe sana Erick na mimi nikaenda kulala nae”Hapo Sia alishtuka kidogo na kumuuliza vizuri Manka,“Ni kweli ulilala na Erick?”“Aaaah hiyo ni siri yangu, ila nilipotoka hapo nilienda kulala na mzee Jimmy ila kipindi hiko nilikuwa tayari nina mimba na nilikubali kufanya vile ili kumsingizia mzee Jimmy mtoto sababu ana mali aweze kumtunza mtoto wangu. Nilipomwambia nina mimba, hakusema hata kidogo kuwa ni mimba ya Erick ila alisema kuwa ni mimba yake na alifurahi sana juu ya hilo. Yani hadi najifungua, mzee Jimmy alikuwa akiamini kuwa Sarah ni mtloto wake, tena alimpa jina la mamake mzazi, alimuita Sarah basi ndio jina hilo amekuwa nalo hadi sasa, kwahiyo mzee Jimmy aliamini kuwa Sarah ni mtoto wake, iweje ambadilishe?”“Sasa jiulize, iweje Elly awe mtoto wako? Cha kukusaidia tu nenda kapime damu na Elly, ila hakuna haja ya kupima mbona inaonyesha wazi kuwa Elly ni mwanao? Unakataa vipi Manka? Kubali au kata, mzee Jimmy kakufanyia mchezo labda sio mimi ninayekwambia haya, nenda kamshikilie huyo dokta Jimmy vizuri akwambie ukweli nimemaliza”Sia aliondoka zake, na muda huo Manka nae aliondoka zake huku akiwa na mawazo sana na moja kwa moja aliona ni vyema amfate dokta Jimmy.Usiku wa leo, wakati baba Angel akijiandaa kwaajili ya kulala alipigiwa simu na mama yake na kuamua kupokea simu ile,“Pole mwanangu kwa mimi kupiga usiku huu ila nakuomba kesho asubuhi twende pamoja hadi kwenye kaburi la mzee Jimmy”“Kuna nini mama?”“Kuna jambo la muhimu sana, kuna mtu kaniambia, inapaswa twende ili tuonane na huyo mtu”“Ni nani huyo?”“Ni mlinzi wa pale, kuna jambo huwa linaendelea kwenye kaburi la baba yako yule. Nahitaji twende kwani kuna mambo mengi yamuhusuyo mzee Jimmy nimeyatambua”“Sawa mama”Basi ile simu ilikatika kisha mama Angel alimuuliza mumewe ambaye alimjibu kitu ambacho kilikuwa kinazungumzwa mahali hapo, basi mama Angel akamwambia,“Mmmh jamani mimi huko kaburini kwa huyo mzee huwa napata hofu sana katika moyo wangu, yani nakosa raha na amani kabisa”“Usijali mke wangu, nitakuwa salama kabisa”“Haya, tufanye yetu basi maana nishaanza kuigopa siku ya kesho”Baba Angel alitabasamu ila upande mwingine aliipenda ile kauli ya mke wake.Asubuhi na mapema, baba Angel alitoka na kukutana na mama yake kisha safari yao ilikuwa moja kwa moja kwenye kwenye kaburi la mzee Jimmy huku wakiongea mambo mengi sana njiani.Walipofika pale, walisogea hadi kwenye kaburi ila walishangaa sana kumuona mwanamke akigalagala juu ya lile kaburi huku akilia sana......... Walipofika pale, walisogea hadi kwenye kaburi ila walishangaa sana kumuona mwanamke akigalagala juu ya lile kaburi huku akilia sana.Mama mzazi wa Erick, alisogea pale karibu na kaburi na kumuangalia kwa makini yule mwanamke, ndipo Erick alipogundua kuwa yule mwanamke alikuwa ni Manka, basi wakamkalisha na wao walikaa pale pale juu ya kaburi la mzee Jimmy na kumuuliza vizuri huyu mama,“Tatizo ni nini Manka?”“Sikujua kama mzee Jimmy ni mtu mbaya kiasi hiki”“Kivipi?”“Yani, wakunibadilishia mtoto mimi kweli?”Baba Angel na mama yake walitazamana kwa muda, ambapo baba Angel alimpa maelezo mafupi mama yake kuhusu mtoto aliyenaye Manka, kisha alimuuliza,“Inamaana Sarah sio mwanao?”Manka alilia sana na kusema,“Sarah sio mwanangu jamani, mwanangu ni Elly mimi, sitaki kukubali hiki kitu”Baba Angel alishangaa kwakweli na kumuuliza,“Kwahiyo wazazi wa Sarah wako wapi?”“Ooooh niacheni jamani mimi, Sarah binti yangu kipenzi, kwanini mzee Jimmy kanitenda hivi mimi, nimemkosea kitu gani? Kwanini anifanyie hivi jamani?”“Dah!! Pole sana”“Kwakweli, huu mzee ipo siku mimi nitamfukua na kumzika tena sio kwa jambo hili alilonifanyia mimi”Kisha Manka akainuka na kuondoka zake, na kufanya baba Angel na mama yake kuangaliana kwa muda kisha mamake baba Angel akasema,“Yani huyu Jimmy akili zake sijui zikoje, mambo yake ya kujaribu vitu ndio yalifanya nimkimbie, hata nisiweze kuishi nae, Mungu anawapa pesa na vichaa wanatusumbua tu duniani kama huyu mzee, hela ilimchanganya sana huyu. Sasa kumbadilishia mwenzie mtoto ndio nini?”“Mama, sio huyo tu yani baba kabadilishia wengi sana watoto hata sijui alikuwa na maana gani au alikuwa akitaka kitu gani toka kwenye hilo jaribio lake”“Duh!! Hiyo hatari sana, haya twende kwa yule mlizni tuongee nae”Basi moja kwa moja walienda kwa mlinzi wa eneo hilo ambaye aliwaona fika wakiongea na Manka pale ila alikuwa akiwaangalia tu, kwahiyo walivyomfata na kusalimiana nae, baba Angel alianza kumuuliza,“Yule mwanamke aliyekuja unamfahamu vizuri lakini?”“Ndio namfahamu, hata leo namshangaa kuja kulia na kugalagala pale kwenye kaburi labda kamkumbuka sana mzee”“Alikuwa akija mara kwa mara?”“Ndio, alikuwa anakuja na binti yake mmoja hivi, utakuta wanaleta maua na mishumaa kuzunguka kaburi la mzee ila leo nimeshangaa kwa kitendo chake kuja kulia, tena mwanzoni alikuwa akilia kwa nguvu kama mtu aliyefiwa”Basi mamake baba Angel alianza kuongea na yule mlinzi sasa,“Eeeeh ile simu uliyonikurupua nayo jana, na kusema kuwa nije huku ulikuwa unamaana gani?”“Unajua watu ambao huwa wanakuja huku kwenye kaburi la mzee mara nyingi ni watu walewale yani hata sura zao nimezizoea, ila jana kuna mtu amekuja wa tofauti sana, alikuwa amevaa miwani”“Hukumuuliza?”“Nilimfata, nikamuuliza kuwa yeye ni nani?”“Akasema kuwa yeye ni rafiki mkubwa sana wa mtoto wa mzee Jimmy, ambaye ktoto huyo anaitwa Erick”Baba Angel akamuangalia kwa makini na kumuuliza,“Nani huyo?”“Sijui, hakunitajia jina lake ila alisema kuwa yeye ni rafiki yako mkubwa sana, pia alisema kuwa kuna siri kubwa sana ipo kwenye familia yako”Baba Angel akashtuka hapa na kuamuangalia kwa makini huyu mlinzi kisha akamuuliza,“Siri gani hiyo?”“Alisema kuwa nikwambie umtafute dokta Jimmy, umwambie kuwa umeujua ukweli, ni bora yeye akueleze ilivyokuwa maana ukweli umeujua. Kasema dokta Jimmy atakuelezea ilivyo halafu yeye atakuja kumalizia”“Mmmh sielewi”Mamake akaingilia kati na kusema,“Hapo inatakiwa tu uelewe mwanangu, hakuna ya sielewi ukaeleweka wala nini, yani unatakiwa uelewe tu mwanangu”“Kwahiyo tufanyaje mama”“Ni kumtafuta huyo dokta Jimmy, hakuna namna ni kumtafuta tu”“Sawa, itabidi nifanye hivyo”Waliongea na yule kisha waliamua kumuaga ambapo baba Angel aliamua kumpeleka kwanza mama yake sehemu aliyofikia kisha yeye ndio kufanya safari ya kurudi nyumbani kwake.Mama Junior akiwa nyumbani kwa Junior huku amembeba mjukuu wake, alisikia simu yake ikiita ila alipoletewa ilikuwa tayari imeshakatika na kumuomba Junior ampatie simu yake ili aweze kupiga,“Ni baba yako ndio alikuwa akipiga, naomba tu simu yako nimpigie”Basi Junior alimuachia mama yake pale simu halafu yeye alienda zake dukani kwa muda huo, mama Junior alipiga kwa mumewe ila mumewe alimwambia,“Nipe kama nusu saa mama Junior, nitakupigia mwenyewe”Simu ilikatika, muda ule ule kuna ujumbe uliingia kwenye simu ya Junior, mamake aliposoma mtumaji aliona jina Daima, na kushangaa sana kuwa mwanae bado anaendeleza mawasiliano na Daima, basi akafungua ule ujumbe na kuusoma,“Safari hii Junior, uje na kinga. Maswala ya kupata mimba tena halafu nionekane malaya sitaki”Kisha ukaingia ujumbe mwingine toka kwa huyo huyo Daima,“Mbona hilo nalijua wazi kabisa kuwa huyo mtu mzima humpendi wamekulazimisha tu kumuoa, yani mara nyingine wazazi wana mambo ya ajabu sana, unaweza hata kuwawekea sumu na kuwamaliza kabisa”Mama Junior alisikitika sana, kuna ujumbe mwingine ukaingia kutoka kwa huyo huyo Daima,“Nakupenda pia Junior, wewe ndio mwanaume wa maisha yangu”Yani mama Junior aliumia sana moyo wake, hakutaka fanya kitu kwanza zaidi ya kufuta zile jumbe zote, kisha akamuita Vaileth na kuanza kuzungumza nae,“Eti Vai mwanangu, ni jinsi gani unampenda Junior?”“Nampenda sana, yani nampenda sana”“Kwa asilimia ngapi unampenda?”“Sijui ila kwa asilimia zote nampenda Junior, kiasi kwamba sitaki kumkosa katika maisha yangu”“Kwasasa mnashirikiana nae vizuri tu kama mke na mume?”Hapo kidogo Vaileth aliona aibu ila alijibu,“Ndio”Basi mama Junior alimkabidhi Vaileth mtoto kisha aliinuka na kumsubiria mwanae arudi, yani alimsubiria nje ya nyumba kabisa. Aliporudi tu, mama Junior alimzaba kofi na kumuuliza,“Vaileth unampenda au humpendi?”“Mbona nampenda mama?”Huku Junior akiugulia lile kofi alilozibuliwa na mama yake,“Unampenda na Daima je?”Junior akajiuma uma, kisha mama yake akamwambia,“Junior ukiniletea ujinga wako wewe mtoto, utafanya nikupige wakati una familia tayari, naomba ujinga uache Junior, nimemaliza”Kisha Junior alichukua simu yake na kurudi nayo ndani tu moja kwa moja.Kama ambavyo mwarabu na Rahim walipanga, basi siku hii moja kwa moja walienda nyumbani kwa mama Angel ili kuweza kuongea vizuri na Angel na kama ikiwezekana wamchukue Angel aweze kutambulikana na ndugu zake wengine.Mama Angel alipowaona tu alitoka nje kwenda kuzungumza nao,“Eeeeh niwasaidie nini?”Mwarabu alimuangalia mama Angel na kumwambia,“Kheee mwanamke mkavu wewe loh!! Yani umekuja hapa kabisa, niwasaidie nini kwani hujui shida yetu? Shida iliyotulea hapa ni mtoto, namuhitaji Angel akawatambue ndugu zake, mimi ndio babu yake nimesema”“Aaaah sawa”Mama Angel hakuwakatalia kwani muda huo huo alienda ndani na kumuita Angel ambaye alitoka nje na kuwakuta wale watu na kuwasalimia, kisha mama Angel akawaambia,“Angel mwenyewe huyo hapo”“Mtambulishe sasa mtoto sio kusema kuwa Angel mwenyewe huyo hapo, kwani wanawake kwanini mnakuwa na visirani kiasi hiko!! Ukimtambulisha utapungukiwa na nini?”Mama Angel alimuangalia mwanae na kumwambia,“Angel, huyu ndio baba yako mzazi anaitwa Rahim na huyu ndio babu yako yani baba yake na huyu Rahim”“Mama, sikuelewi”“Hunbielewi nini sasa na wakati nilikwambia kila kitu”“Ndio uliniambia ila mama sikuelewi kwakweli, mimi nishasema sina mababa wawili. Baba yangu ni mmoja tu na yeye anaitwa Erick, haya mengine sitaki kuyajua”Kisha Angel alikimbilia ndani, mwarabu alimuangalia mama Angel na kumwambia,“Umemfundisha vitu gani mtoto? Lazima umemfundisha mambo yasiyokuwa mazuri, nyie wanawake mna nini lakini, Mungu anawaona kwa haya mnayoyafanya kwa watoto”“Hata mwanaume unapomkana mtoto kumbuka kuwa Mungu anaona maana si vizuri kukana damu yako”“Haya, hayo yameisha, mtoto umemwambia nini hadi atutaki kabisa?”“Sina jibu”Mwarabu hakuwa na sababu ya kuendelea kuwa hapo na kumtaka kijana wake tu waondoke kwa wakati huo.Baba Angel akiwa amechoka kutokana na kwenda kutembelea kaburi la mzee Jimmy, na vile jinsi walivyomkuta Manka akiomboleza kwenye kaburi, alitaka moja kwa moja alale ila Mama Angel alimua kumueleza kuhusu ujio wa mwarabu na Rahim na jinsi Angel alivyofanya kiasi cha wakina Rahim kuhisi kuwa amemfundisha vibaya mtoto wake,“Yani huyu Angel ni balaa ujue, ndio kaondoka kabisa, mtoto ana dharau huyu sijapata kuona”“Kwahiyo tufanyeje mke wangu?”“Sielewi kwakweli, ila huyu mtoto ni mtihani halafu wakina Rahim wanataka kumtambulisha kwa ndugu zake. Hili ni tatizo kwakweli maana mtoto haujui ukweli toka siku nyingi, hili ni tatizo kwakweli”“Basi kosa ni lako kwa kumficha mtoto, mama Angel kwakweli kichwa changu kina mambo mengi sana kwasasa, yani sijui kama nitaweza kuendelea kufikiria hayo ya wakina Rahim kwakweli. Nadhani nifanye yangu kwanza halafu ndio nifikirie hayo ya wakina Rahim”Kwa muda huo baba Angel aliamua tu kulala.Kulipokucha tu, Angel ndio alikuwa wa kwanza kugonga mlango wa wazazi wake, kisha alimuomba baba yake aweze kuzungumza nae, basi baba yake alitoka na moja kwa moja kwenda nae kwenye sebule yao nyingine ili kuzungumza nae,“Niambie Angel”“Bado kuna utata kuhusu maisha yangu, mimi ni mwanao au sio mwanao”“Kwani ni kitu gani unataka kufahamu Angel?”“Nataka kufahamu ukweli”“Upo tayari kwaajili ya kuubeba ukweli?”“Ndio baba”“Ipo hivi, mimi nilikupenda sana, na nilimpenda mama yako, niliamua kumuoa ili wewe ubaki kuwa mtoto wangu milele”“Kwahiyo mimi sio mtoto wako baba?”“Hapana, sijasema hivyo”Yani baba Angel alikuwa akiona hili swali ni gumu sana ingawa kwa wakati huo alielewa wazi kuwa yeye ndio anayetakiwa kutoa ukweli kwa Angel dhidi ya baba yake ila kila anapojaribu kumwambia, aliona ulimi wake kuwa mzito sana, alijiona wazi akishindwa kuzungumza kuhusu swala hilo kabisa, yani alikosa amani katika moyo wake.Basi alimpooza tu pale Angel na kumuhakikishia kuwa yeye ndiye baba yake mzazi kisha akarudi chumbani kwake na kuongea na mke wake,“Roho inanisuta sana kung’amg’ania uongo kuwa ukweli kwa Angel ila nawezaje kumweleza Angel ukweli ikiwa hautaki huo ukweli?”“Hapo ni pagumu ila kwa nilichomweleza ni wazi Angel amefahamu ukweli halisi ila hataki tu kukubaliana na ukweli. Acha muda utasema na atakubaliana tu na ukweli halisi, na hivi Rahim ana watoto kama mchanga, nahisi Angel atachukia sana kuwafahamu hao ndugu zake”“Dah!! Ngoja niondoke, leo nitaenda ofisini ila kesho nitaenda kumfata huyo dokta Jimmy ili niweze kuongea nae vizuri”Baba Angel alijiandaa na kuondoka zake kwenda kazini.Muda mfupi tu, mama Angel alipigiwa simu na Manka na kuanza kuongea nae, yani Manka alikuwa akiongea huku akilia,“Tatizo nini Manka?”“Unajua mzee Jimmy ni mzee mpuuzi katika wote chini ya jua”“Kivipi?”“Unajua kama Sarah sio mtoto wangu halafu Elly ndio mtoto wangu”“Kheee nani kakwambia? Na Sarah ni mtoto wa nani?”“Wakina Erick hawajakueleza au? Nimejikuta jana nikiomboleza juu ya kaburi la mzee Jimmy, yani sina raha hata kidogo, hivi mimi nafanyeje? Nishamzoea Sarah mimi”“Kwahiyo Sarah ni mtoto wa nani?”“Sijui, yani sijui ni mtoto wa nani naomba hilo fatilieni wenyewe maana huyo mtoto kafanana na ukoo wenu, kwakweli mzee Jimmy alaaniwe huko huko kaburini alipo”Kisha Manka alikata ile simu na kumuacha mama Angel akiwa na swali moja tu kichwani kuwa Sarah ni mtoto wa nani.Baba Angel akiwa ofisini leo alifuatwa na Sia, ambaye moja kwa moja alianza kuongea nae kuhusu alichogundua kuhusu uwepo wa mtoto wake,“Yani nimechunguza kwa makini na kugundua kuwa yule mtoto aliyekuwa kwa madam Oliva ndio mtoto wangu”“Kheee umejuaje?”“Unajua toka siku ya kwanza namfahamu yule mtoto nilihisi kuna kitu kinahitaji mimi nimfahamu vizuri zaidi yule mtoto, nimemfatilia vizuri na nimegundua kuwa ni mwanangu”“Ndio, umepata uhakika gani kuwa ni mwanao yani ni kitu gani hicho kimekujulisha?”“Wakati nilipokuwa na mtoto yule wakati mchanga, nilimuweka alama kwenye paja lake la mguu wa kushoto, niliandika herufi S kwani mzee Jimmy nilijua wazi anambadilisha baada ya kusema kuwa hakuweza kumbadilisha akiwa mchanga, basi nikakubali ambadilishe ila nilijua wazi kuwa ilea lama itafanya nimtambue mwanangu hata hapo badae, ila nilikuwa najua ni Erick yule mdogo. Sema yule Paul nimemkuta nayo hiyo alama, kwahiyo yule ni mtoto wangu kabisa”“Duh!! Kwahiyo madam Oliva mwanae atakuwa nani?”“Nina wasiwasi kuwa atakuwa Sarah yani Elly ni mtoto wa Manka, halafu Sarah ni mtoto wa madam Oliva halafu mtoto wangu ni yule Paul”“Mmmh inawezekana lakini, ila kuukubali ukweli huo ndio shida. Unadhani Sarah anaweza kukubali? Au huyo Paul anaweza kukubali? Huyo Elly mwenyewe kwasasa anamsikiliza Derrick tu hata hataki kukubali huo ukweli kuwa yeye ni mtoto wa Manka”“Ataukataa ukweli ila ukweli utabaki kuwa ukweli siku zote, nampenda sana Elly ila sio mtoto wangu. Huwa nikiwa nae karibu kwa kipindi hiki, huwa najaribu kumuelezea ili mwisho wa siku aweze kumkubali Manka kama mama yake mzazi”Basi aliongea nae na kuagana nae ambapo Sia aliondoka moja kwa moja na kuelekea kwenye mgahawa wake, ila njiani alikutana na Manka ambaye alianza kumlalamikia kitu kilekile kuwa Elly ndio mwanae na Sarah sio mwanae,“Pole sana Manka, ulimuamini sana huyo mzee ila nilikwambia mimi kuwa huyo mzee hafai, natumaini dokta Jimmy ameamua kukueleza ukweli?”“Ndio, ingawa hadi muda huu hajaniambia mzazi wa Sarah anasema kuwa hata yeye hamjui mzazi wa Sarah ni mzee Jimmy mwenyewe ndio anatambua. Roho inaniuma sana, mimi nampenda sana mtoto wangu Sarah”“Pole sana”“Ngoja niende kunywa wee, najua baada ya hapo akili yangu itanikaa sawa”“Kwa mawazo hayo halafu unaenda kujiongezea na pombe!! Duh”Sia aliachana na Manka kisha yeye akaenda zake kwenye biashara yake maana ukweli wa kuhusu mwanae alishaupata ingawa tu hakujua kama mwanae anaweza kumkubali, sema akiwa kwenye mgahawa wake akajikuta akijiwa na wazo lingine kwahiyo alihitaji kufanya kitu kingine kwa muda ule.Madam Oliva alkuwa akiumwa umwa kipindi hiki, basi aliamua kwenda hospitali huku akiwa ameongozana na Steve, kufika kule hospitali walimpima na kumpa majibu kuwa ni mjamzito, ile ilikuwa ni furaha kubwa sana kwake, yani aliona kama muujiza sababu hakutarajia kuzaa tena kwa kipindi hiko.Basi waliondoka hapo huku wakiwa na furaha sana, basi madam Oliva akamwambia Steve,“Sasa, nadhani ni wakati muafaka wa mimi na wewe kufunga pingu za maisha”“Ndio hata isingekuwa hivyo bado mimi na wewe tungeoana tu. Ila unaonaje muda huu twende nyumbani kwetu”Basi wakakubaliana, kisha muda huo huo moja kwa moja madam Oliva na Steve walienda nyumbani kwakina Steve na huko walimkuta mama yake na Steve, kabla ya yote Steve alimpa taarifa mama yake kuhusu ujauzito wa madam Oliva na kumfanya mama yake afurahi sana na kusema,“Mbona hamuoani nyie jamani, kitu gani kinawakwamisha kufunga ndoa?”Hapa madam Oliva alicheka yani huyu mama aliongea kamavile sio yeye ambaye alikuwa akipinga mahusiano kati ya madam Oliva na Steve.Walikaa pale na kuongea sana kisha kuamua kuondoka ila njiani walikutana na Sia ambaye alionekana pia akielekea nyumbani kwa mamake Steve, ilibidi Steve amuulize kwa mshangao,“Sia, unaenda wapi? Mbona kama unaelekea kwetu?”.“Hiyo ndio salamu Steve?”“Aaaah samahani, za saa hizi!”“Nazijua mwenyewe, saa hizi naelekea kwenu”“Kufanya nini?”“Mamako hakuniamini mimi kama kweli nimezaa na wewe, nataka kwenda kumthibitishia hilo”“Unaongelea nini wewe?”“Kwa kifupi ni kuwa yule Elly sio mwanangu kwahiyo mlikuwa na haki ya kumkataa sababu hamkujua ukweli, ila mtoto wangu halisi nimemtambua”“Mwanao halisi ni nani?”“Subiri nikaongee na mama yako Steve halafu atakwambia ukweli wote”Sia aliwaacha pale na kuondoka, ila hata wao waliamua kuondoka tu maana waliona kufatilia maneno ya Sia ni kuumiza akili zao tu.Usiku wa leo baba Angel alikuwa kwa makini akisikiliza maelekezo ya mke wake kuhusu mahali anapoishi dokta Jimmy sababu alitaka moja kwa moja aende nyumbani kwa dokta Jimmy kwaajili ya kuonana nae, waliongea na kuwahi kulala kwa siku hiyo ili aweze kuwahi kuamka kwenda ukizingatia palikuwa na umbali kidogo.Kulipokucha tu, mapema kabisa baba Angel aliondoka nyumbani kwake kuelekea nyumbani kwa dokta Jimmy.Alipofika kwa dokta Jimmy aligonga na kukaribishwa ndani na mwanamke aliyejitambulisha kwake kuwa ndio mke wa dokta Jimmy,“Samahani, sijui naweza kumpata dokta Jimmy?”“Hapana, hayupo labda uwasiliane nae tu”“Naomba namba zake basi”“Hapana, ngoja nimpigie kwenye simu yangu”Kisha mke wa dokta Jimmy alipiga simu na kuongea nayo kisha kumpa baba Angel aongee nayo ambapo alijitambulisha kwanza kwa dokta Jimmy, kisha alimwambia,“Nahitaji kuonana nawe dokta Jimmy”“Unataka kunikamatisha au kitu gani?”“Hapana kuna kitu nataka kuzungumza na wewe kuhusu wale watoto wangu”“Kitu gani?”“Nimejua kila kitu, ninachohitaji ni uthibitisho tu”Dokta Jimmy alicheka kisha akasema,Kabla ya yote sikia nikwambie kitu, upo tayari kukifanya?”“Ndio, nipo tayari”“Ngoja nakutumia ujumbe kwenye simu yako halafu uende ukafanye kama nitakavyokwambia halafu mimi na wewe ndio tutaongea”“Sawa, nasubiri ujumbe wako”Kisha dokta Jimmy alikata simu na kumfanya baba Angel apumue kiasi huku akingoja ujumbe toka kwa dokta Jimmy ili ajue ni kitu gani cha kufanya.Jioni ya leo, Erica alikuwa amkaa kwenye bustani mwenyewe tu, muda mfupi alienda Erick eneo lile na kuanza kuongea nae,“Kheeee leo umewahi kurudi?”“Ndio, yule dada ananisumbua sana Erica”“Anataka nini kwani?”“Sijui ila anahitaji niwe mpenzi wake”“Mwehu huyo mwanamke eeeh!!”“Ni mwehu kweli, hata kesho siendi ila kuna kitu nilikuwa nahitaji tukifanye kesho"“Kitu gani hiko?”“Nataka kesho ndio twende tukatembee sehemu Fulani hivi ila ipo mbali kidogo”“halafu tutalala huko huko?”“Hapana, jioni tunarudi”“Sasa tunaagaje?”“Mmmmh ngoja nifikirie”Mara alifika pale baba yao na kuanza kuongea nao,“Kumbe mpo pamoja huku?”“Ndio baba”“Basi kuna jambo nataka mnisaidie nyie wawili wote”“Jambo gani hilo?”“Natake kesho muende kule kwa babu yenu, kuna kitu cha kufanya nitawaelekeza kwa njia ya simu mkifika huko”Erica na Erick walitazamana na kumuuliza baba yao,“Ni lazima twende wote wawili?”“Ndio, kuna karatasi za kutafuta na inatakiwa kutafutwa na nyie wawili”Erick na Erica walitazamana ila mwisho wa siku walikubali tu, na hapo waliona mpango wao wa kwenda kwenye matembezi umekufa.Basi kila mmoja aliamua kwenda kujiandaa tu kwaajili ya safari ya kesho sababu kwa babu yao palikuwa mbali kidogo kutoka kwao.Usiku huo wakati baba Angel akipanga mipango na mke wake ndani, alishtuliwa na simu kutoka kwa namba ngeni na kupokea simu ile, sauti ilisikika ni ya mwanamke akilia,“Erick naomba unisaidie”“Wewe ni nani?”“Mimi ni Linah”“Una tatizo gani?”“Nilikuwa natoa mimba ila sijui imekuwaje muda huu damu imenitoka nyingi sana, naomba msaada wako”Kisha Linah alikata simu na muda huo baba Angel alitaka kujiandaa ili akamsaidie Linah ila mke wake akamkataza na kumwambia,“Hakuna kwenda popote”“Ila inaonyesha anahitaji msaada wa haraka sana”“Jamani Erick nimesema hakuna kwenda popote, hivi inakuingia akilini kweli? Mtu eti alikuwa akitoa mimba, sijui damu imemtoka nyingi sana, hiovi mwanamke mtu mzima kama Linah bado anatoa mimba kwa njia ya kienyeji?”“Kwahiyo ulitaka atoe kwa njia gani?”“Baba Angel. Tuisirefushe mada hapa, kila mtu anajua kama kitendo cha kutoa mimba si halali, hata huko hospitali hufanywa na madaktari kwa kificho kwani ni kitendo kisichoruhusiwa. Kwa binti mdogo mtu unaweza sema ni ujana unamsumbua, ila kwa mama mzima kama Linah kweli? Hapana jamani, siwezi kukubali uende”“Labda katoa sababu ya aibu ya kugundua kuwa Junior ni mwanae”“Nakwambia hivi baba Angel, hakuna kwenda popote, hayo mambo unayonieleza wala siyaelewi”“Ila sijasema kama nataka kwenda”“Haya tulale”Basi kwa muda huo waliamua kulala tu.Asubuhi na mapema, walishtuliwa na mlio wa simu ya baba Angel ambapo aliichukua na kupokea ila aliyepiga alikuwa ni Manka na alikuwa akilia sana huku akisema,“Dada yangu Linah amekufa”Baba Angel alishtuka sana na kushangaa. Asubuhi na mapema, walishtuliwa na mlio wa simu ya baba Angel ambapo aliichukua na kupokea ila aliyepiga alikuwa ni Manka na alikuwa akilia sana huku akisema,“Dada yangu Linah amekufa”Baba Angel alishtuka sana na kushangaa.Mama Angel alimuangalia kwa makini na kumuuliza,“Kwani kuna nini?”“Nasikia Linah amekufa”“Kheeee mbona makubwa haya, imekuwaje tena?”“Ukitaka kujua imekuwaje jiandae hapo twdende huko msibani ili tujue kilichotokea maana hata mimi hii habari imenishtua”“Mmmmh!”Mama Angel alijiandaa, kisha baba Angel akajiandaa pia, kwahiyo walipokuwa wakitoka waliwaambia wakina Erick wasiende popote tena kwani wao wanatoka, kisha wakaondoka zao.Nyumbani walibaki wakina Erick tu wakijiuliza kuwa kuna kitu gani,“Kwani nini kimetokea?”“Mmmh hata sijui”Muda kidogo, alifika pale mama Sarah na kumuita mwanae ambaye alitoka ndani na kumkuta mama yake akiwa amejaa machozi, kisha mama Sarah alisogea na kumkumbatia Sarah huku akimwambia,“Mwanangu, mamako mkubwa amekufa”“Nani mama, yupi? Mamkubwa Linah?”“Ndio mwanangu, mamako mkubwa Linah amekufa”Sarah alihisi kama kuchomwa na kitu katika moyo wake kwani ilikuwa ni habari ya gafla sana kwake, alilia sana na hapo kuamua kuondoka na mama yake ili kuelekea msibani na kujua kitu kitakachoendelea.Nyumbani alibaki Angel na wadogo zake, ambapo bibi yao alipiga simu na moja kwa moja alipokea Angel ile simu,“Mama yenu yupo?”“Hamna, ametoka bibi”“Katoka na mtoto?”“Hapana, Ester yupo”“Basi nikuombe kitu”“Niambie bibi ni kitu gani?”“Naomba uje na Ester, mlete Ester nyumbani kwangu hapa. Jitahidi ufanye hivyo Angel”“Sawa bibi”Kisha Angel aliandaa chai na kunywa, halafu kumlisha vizuri Ester na kumuomba dereva wao ili awapeleke yeye na Ester kwa bibi yao.Basi Erica akauliza,“Kwahiyo ndio unaniacha mwenyewe!!”“Mwenyewe kivipi? Si upo na Erick tatizo liko wapi?”“Basi tuondoke wote, mimi, wewe, Ester na Erick”“Halafu hapa nyumbani abaki nani? Kumbuka mama hajui kitu, halafu yeye na baba wameondoka tu, jitahidi hapa nyumbani ubaki na Erick, usiende popote Erica, angalieni hata sinema jamani”Kisha Angel alimchukua Ester na kuondoka nae, kwahiyo pale nyumbani walimuacha Erick na Erica tu.Baba Angel na mama Angel, wakiwa kule nyumbani kwa Linah, ndio wakapata taarifa vizuri sasa kutoka kwa mdada wa kazi wa Linah,“Kwani ilikuwaje?”“Mama, aliniambia nimweleze mtu mmoja tu”“Mtu gani huyo?”“Alisema anaitwa Erick”Basi mama Angel na baba Angel waliangaliana kwa muda kisha mama Angel alisogea pembeni halafu baba Angel alimwambia yule mdada wa kazi,“Mimi ndio Erick”“Mama alikuwa akiumwa sana kwa siku nzima ya jana, hali yake ilikuwa mbaya, aliamua kupiga simu kwa mtu aliyeitwa Erick alisema kuwa mtu huyo akifika anaweza kuokoa maisha yake. Alikataa wote kumpeleka hospitali hadi huyo Erick afike, na hakutaka tumueleze mtu yoyote hadi afike Erick. Tulikaa kama lisaa bila huyo Erick kufika, mama akaomba karatasi na peni aliandika ujumbe na kunipatia mimi, kisha alisema huo ujumbe usisomwe na mtu yoyote yule zaidi ya Erick, nilipoenda kuhifadhi ule ujumbe chumbani kwangu, niliporudi nikamkuta tayari mama ameshaaga dunia”Yule mdada wa kazi alianza kulia, ikabidi baba Angel amnyamazishe, huku akimuomba ampatie ule ujumbe, basi yule dada alienda kutafuta ule ujumbe, ila muda kidogo pale alifika mama Sarah akiwa ameongozana na Sarah sasa sababu ndiye mtu aliyeona ataweza kumfariji kwa wakati huo wa kuondokewa na dada yake mpendwa.Ila mama Sarah alimsogelea Erick na kuanza kumpiga kama vibao huku akilalamika na kulia,“Utatumaliza ukoo wote mjinga wewe”“Kwani nimefanyaje Manka jamani!”“Mjinga wewe, dada yangu nasikia alikuwa akihitaji sana msaada wako, ila ulivyo na roho mbaya umeshindwa hata kuja kumsaidia kweli! Mbaya sana wewe”Hapo mama Angel alisogea maana hakuelewa ile hali ila mumewe alisogea nae pembeni na kumueleza kwa kifupi, na kufanya mama Angel ashtuke,“Mmmh kwahiyo hizi lawama za kifo cha Linah sasa zinataka kunihangukia mimi? Wazima wa akili kweli hawa? Mimi ndio nilimwambia atembee na mwane, mimi ndio nilimshauri kutoa mimba? Nilichofanya ni kumzuia mume wangu kwaajili ya ndoa yetu, nina upendo na mume wangu, kwani Linah ana ndugu wangapi kwanini asiwapigie wote hao simu aje kumpigia mume wangu? Jamani, sitaki hizi lawama kabisa, nahisi kuchanganyikiwa, ngoja niende kwa mama yangu”Mama Angel hakutaka hata kusikia kitu kwa muda huo kwani alipanda kwenye gari na moja kwa moja alifanya safari ya kwenda kwa mama yake.Erick na Erica walikuwa wenyewe ndani kwao, walipokunywa chai tu waliambizana waende sebule nyingine ya nyumba yao,“Twende kule Erica tukaangalie muvi”“Zile alizokuwa akileta Samia?”“Ndio, tukiangalia hapa haipendezi, tufanye kama kipindi kile kwa kuangalia kwa kificho, kipindi kile wakati tunaangalia na Junior”“Sawa twende tu”Kisha waliinuka na kwenda kwenye sebule nyingine ya nyumba yao na kuanza kuongea ambapo Erick alimuuliza Erica,“Hivi imekuwaje? Jana mimi na wewe tulipanga kwenda sehemu ya mbali ambapo sehemu hiyo tungekuwa wawili tu ila leo eti tumeachwa wawili tu humu ndani, hii umeielewa kweli Erica?”“Kwakweli nimeshindwa kuelewa kabisa, ni kwanini tumeachwa wawili tu”“Mmmh au wanataka tujaribu”“Tujaribu nini sasa?”“Ile tuliyopanga siku ile ya wote wawili kubaki watupu kabisa”“Mmmmh!!”Erica alijihisi moyo kwenda mbio sana kisha Erick akamwambia,“Ngoja nikafunge mlango wa chini”Yani Erica alikuwa akihema sana kwa muda kidogo, kisha Erick alirudi toka kwenye kufunga mlango na kumwambia Erica sasa,“Kuna kitu tufanye kwanza”“Kitu gani?”“Twende kuoga pamoja”“Yani mimi na wewe?”“Ndio, kwani tatizo nini? Mbona zamani tulikuwa tukifanya hivi? Ni mara ngapi tumeoga wote, ni mara ngapi tumelala wote?”“Ila kweli, kwani kuna nini kitatokea?”“Sijui, ila kikitokea chochote itakuwa ni siri yetu maana humu ndani tupo wawili tu”Wakaongozana muda huu, hadi chumbani kwa Erick kisha kila mmoja alitoa nguo na kwenda kuoga pamoja, ila walipotoka kuoga kila mmoja alijikuta akishikwa na matamanio zaidi kwa kumtazama mwenzie kiasi kwamba hadi wote wawili walipatwa na aibu kubwa sana, Erica alijiziba uso kwa aibu, Erick alimsogelea na kumkumbatia na kufanya Erica aongee kwa sauti ya kutetemeka,“Unataka kufanya nini Erick?”“Sijui”Walijikuta kwa pamoja wakikumbatiana kwa nguvu sana.Angel akiwa na mdogo wake, walifika moja kwa moja kwa bibi yao na kumkuta bibi yao akiwa na mgeni mwingine pale, basi bibi yao alifurahi sana na kuwakaribisha, huku akianza kuwatambulisha kwa yule mgeni,“Huyu ni bibi yenu pia, anaitwa Ester, nimekuita na mtoto ili aweze kumuona wajina wake”“Aaaah sawa”Basi alimasalimia pale na kuanza kuongea mambo mbalimbali ya kuhusu shule na kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea, basi Angel alimuacha pale Ester kwa bibi yake na yule mgeni halafu yeye aliaga kuwa anaenda dukani, bibi yake alimkubalia tu.Angel alitoka nje na kwenda kukutana na Samir ambaye alikuwa ameshampigia simu toka anatoka kwao, kwahiyo Samir moja kwa moja alienda pale kwa bibi yake Angel. Walisimama nje na kuanza kuongea,“Yani nilipopata nafasi tu ya kutoka nyumbani nikaona cha kwanza kabisa nikutafute wewe Samir, kwakweli nimekumiss sana”“Mimi zaidi Angel, huwa muda wote nakuwaza”“Eeeeh kwanza ikawaje siku ile, maana hata hatukuongea vizuri, kwenu ilikuwaje?”“Sio ilikuwaje tu ila kwetu ni balaa, baba yangu hataki kusikia kabisa habari za mimi kuwa na wewe, nasikia alirudi nyumbani na kufoka sana. Mama alinipigia simu akasema nisirudi kabisa nyumbani, basi toka siku ile nakaa kwa mjomba, yani nyumbani kwetu ni balaa, hapakaliki, nasikia baba kamwambia mama kuwa hataki kuniona.”“Ila baba yako nae loh!! Anataka nini kwani?”“Sijui mwenyewe, sijui anafikiria nini. Kanisema sana, eti anahofia wewe utapata mimba yangu, halafu cha kushangaza eti baba yangu ameanza kusema wewe ni mwanae eti, mimi na wewe ni ndugu”“Khaaaa!! Baba yako anaitwa nani kwani?”“Anaitwa Rahim”“Khaaa mimi sio mwanae kabisa, asiniletee balaa. Sikia Samir, siku hizi pale nyumbani kwetu huwa wanatoka toka sana, kiasi kwamba nahisi nitabaki peke yangu pale nyumbani”“Naomba siku ya kubaki mwenyewe uniite”“Mbona umewahi! Ndio nilikuwa nataka kukwambia hivyo hivyo”Kuna gari waliiona kwa mbali inakuja, Samir alishtuka na kumwambia Angel,“Sio gari ya mama yako ile?”Angel alipoangalia aliona kuwa ndio yenyewe, basi Samir muda huo huo akazunguka kidogo na kuondoka, halafu Angel akaingia ndani na kutoa vyombo vichafu nje na kuanza kuviosha.Muda kidogo tu mama yake aliingia ndani na kumuuliza bila hata salamu,“Angel, umekuja kufanya nini huku? Na mbona niliona mtu kama wewe umesimama na mwanaume nje?”“Aaaah ni bibi kaniita nimlete Ester mdogo, halafu sijaenda nje mama. Nilenda dukani tu, na sasa nimeona nimsaidie bibi kuosha vyombo maana bibi hana msichana wa kazi kwasasa”“Mmmmh ila wewe mtoto!!”Kisha mama Angel aliingia ndani na kufurahi sana kumuona yule mama wa kuitwa Ester, basi aliwasalimia pale na kuanza kuongea nao, ambapo bibi Angel alianza kwa kuomba msamaha kwanza,“Kwanza mwanangu nisamehe kwa kumwambia Angel aje bila ruhusa yako, hii ni kutokana na kupiga simu yako bila ya kupokelewa, basi nikaona ni vyema nimwambie Angel aje maana ni mkubwa sasa”“Ni kweli, amekuwa mkubwa kwasasa”“Ila mtoto Ester jamani, ni mpole hadi raha, yani mtoto sio mlizi kabisa”“Ni kweli mama, huyu sio mlizi, ukimuona analia ujue njaa, halafu usimuone kimya huwa ana mtindo wa kusoma mazingira. Kama unamkumbuka vizuri Angel alipokuwa mdogo basi ndio kama huyu Ester, yani yeye anasoma mazingira halafu anaweza kuja kukuumbua badae. Kuna siku nilimficha kitu baba yao, nilitaka kumuonyesha kwa kumshtukiza tu, kheee kumbe Ester kaniona nilipoficha, yani baba yao aliporudi tu akawa wa kwanza kumtolea na kumpatia”Wote wakacheka kisha bibi Angel alisema,“Kaanza mapema umbea wa Erica jamani. Sijamuulizia mjukuu wangu bingwa wa kupika anaendeleaje?”“Hajambo, naona nyumbani atakuwa kabaki na kaka yake tu”Yule Ester mkubwa akasema,“Halafu hao watoto hamjawahi kuwaleta kwangu jamani, muwalete siku moja wajukuu zangu”“Usijali mama tutawaleta, nilikuwa nangoja wamalize shule ndio nianze kuzunguka nao”Waliongea mengi sana pale, kisha yule mama ambaye aliitwa Ester pia aliondoka kwa muda huo, ni Angel ndio aling’ang’ania kumsindikiza yule mama, kwahiyo mama yake na bibi yake waliishia njiani, kisha Angel ndio alimsindikiza hadi kituoni huku wakiongea mambo mbalimbali.“Umeokoka Angel!”“Mmmh nimeokoka lakini kidogo”“Kwanini?”“Wokovu mgumu, masharti yake magumu”“Nani kakwambia hivyo Angel? Siku njoo nyumbani kwangu tuongee vizuri, mwambie mama akuelekeze”“Sawa hakuna tatizo”Yule mama alipanda basi na kuondoka kisha Angel alimpigia tena simu Samir ambaye hakuwa mbali, halafu alianza kuongozana nae kurudi kwa bibi yake,“Kwani mama yako kaja kufata nini?”“Najua basi!! Sijui kitu gani kimemleta huyu, mama ana machale balaa”“Na huyu mgeni ndio alikuwa ndani kwenu?”“Ndio, ananiambia niokoke”Samir alicheka sana na kusema,“Ili nikukose, wanaokokaga waliozeeka kama yeye”Wote wakacheka sana na kufurahi kwa muda huo, kisha Samir alimsindikiza Angel hadi kwa bibi yake huku wakipanga kuwasiliana vizuri kwa siku zijazo kwani Angel alisikia sikia kuhusu safari ya Erick na Erica kwahiyo akawa na uhakika siku wakiondoka hao basi hapo kwao kutakuwa hakuna mtu mwingine zaidi yake.Mama Angel alimueleza mama yake kuhusu tukio la Linah na jinsi walivyopata ujumbe kuhusu kifo cha Linah,“kwahiyo ndio wanalaumu hapo mama, sasa kosa langu ni nini hapo?”“kwani nani kasema kuwa ni kosa lako?”“Baba Angel huyo, anadai kuwa nisingemkataza basi huyo Linah angepona, nawezaje kumkubali mume wangu aende kumsaidia usiku mwanamke aliyewahi kuwa na mahusiano nae jamani!”“Huo ujinga hata mimi niliukataa hata kipindi nipo na baba yenu, naita ni ujinga huo tena ni ujinga kabisa, ni mume wangu halafu akatoe msaada kwa mtu usiku ambaye aliwahi kuwa na mahusiano nae, tena huyo mtu ana ndugu zake. Kuna uhakika gani? Akienda kule na kukumbushiana je na ruhusa umetoa wewe mwenyewe!”“Aaaah ila mama nimefikiria kitu”“Kitu gani?”“Kwanini ile usiku nisingemwambia mume wangu twende wote!”“Kweli ni jambo jema hilo ulilofikiri, ila mwanangu naomba usijihukumu kwa hilo. Kitu kimeshatokea, huwezi jua ni kwanini imekuwa hivi, kila kitu katika maisha kina sababu zake”Bibi Angel na mama Angel waliendelea kupeana moyo pale, na kisha Angel aliporudi ilibidi wajiandae kwaajili ya kurudi nyumbani maana na muda nao ulikuwa umeenda.Walipokuwa kwenye gari na Angel wakati wa kurudi, njiani alimuoa rafiki yake Johari ndipo alikumbuka pia ujumbe ambao aliwahi kupewa na mumewe ila hakuufanyia kazi kwa kumtafuta Johari wala nini, ilibidi asimamishe gari na kushuka kisha alianza kuongea na Johari kidogo,“Wapi unaenda muda huu Johari?”“Narudi nyumbani kwangu yani kwa mume wangu, nimetoka huko kwetu”“Salama lakini?”“Salama wapi ndugu yangu! Si unakumbuka mtoto wa kwanza mimi nilizaa na yule mwalimu wa nidhamu, unakumbuka lakini?”“Nakumbuka ndio”“Unajua kwanini hakunioa?”“Kwanini?”“Mwalimu mjinga yule, alinidanganya mimi kumbe alikuwa na mke wake, kipindi yupo na mimi yule mkewe alikuwa safarini tena alikuwa kwenye likizo ya uzazi huko kwao halafu ndio akanidanganya mimi na kuzaa na mimi jamani. Yani watu wengine hadi kichefuchefu. Haya sasa unajua kilichotokea?”“Nini kimetokea?”“Yule mwalimu alidai mtoto wake alee mwenyewe, basi sikugoma ikabidi tumruhusu tu amlee, na kweli kamlea sasa kidato cha pili toto likapata mimba, mweeeh yule mwanaume kamtimua mtoto nyumbani kwake, basi akaja kwangu analia, kama kawaida wamama ndio tunabeba madhaifu yote, nakwambia nikaongea na mume wangu na yeye hakuwa na hiyana, tumelea mtoto kwa kipindi chote hiki wala hakuna nini wala nini. Sasa kuna siku mume wangu kamuuliza baba wa yule mtoto ni nani maana mtoto ameshakuwa mkubwa, kheee jamani kumbe akaanza kumktukana mume wangu, nasikia alimtukana sana, ila nilikuwa mbali kwenye biashara zangu sikujua hilo na wala mume wangu hakuniambia. Sasa juzi ndio kuna mtu kaniambia kuwa alimuona mwanangu njiani na kijana, basi niliporudi nilimwambia mume wangu kuwa tumuulize, ndipo mume wangu alipokataa na kunieleza hayo yaliyopita, ila sikuamini kabisa. Jana nilimlazimisha tena mume wangu amuulize, loh alianza kumporomoshea matusi mume wangu hatari, sijawahi kumpiga yule mtoto ila jana nilimpiga sana na leo nimemleta kwa bibi yake yeye na mwanae, hata mimi nimemchoka”“Duh!! Sasa bibi yake atamuweza? Na kwanini sisi wazazi tukishindwa huwa watoto tunawatupia kwa mabibi kama wenyewe ndio wenye makosa?”“Ndugu yangu, sina cha kufanya sasa, unadhani mwanangu ataishi na nani ikiwa anamuudhi mtu anayutuhudumia ndani ya nyumba? Babake hamtaki tena sababu ya ujinga wake, je ni nani atakayemuweza? Nadhani ujinga huu kaupata kwa baba yake”“Pole sana ndugu yangu, nadhani tutaongea vizuri kesho maana nitakuja nyumbani kwako”“Sawa sawa hakuna tatizo, karibu sana”Kisha mama Angel aliagana na rafiki yake halafu yeye alirudi kwenye gari na kuendelea na safari yao ya kurudi nyumbani kwao.Baba Angel akiwa kule msibani, aliendelea kumfatilia yule mdada wa kazi ili ampatie ule ujumbe ambao alipewa na marehemu, ila huyu binti kidogo alikuwa akihangaika kwahiyo hakutoa lile karatasi kwa muda muafaka.Baba Angel aliendelea kusubiria, muda huu aliitwa tena na Manka na kisha Manka akampatia simu na kumwambia aongee nayo,“Dokta Jimmy anaongea hapa, mbona hatujakutana leo?”“Aaaah sababu ulisema kwanza watoto waende kule”“Ndio, watoto waende kule halafu mimi na wewe tukutane”“Tulipata taarifa ya msiba kwahiyo ikawa ngumu kwa mimi kukutafuta hata watoto niliwazuia”“Aliyekufa ni nani yako?”“Ni rafiki yangu”“Yani rafiki tu ndio anakufanya uache kufatilia mambo ya msingi? Hujui umuhimu wa mimi na wewe kukutana? Kama hujui ni kwanini ulinitafuta? Si usingenitafuta”“Naomba unisamehe sana ndugu yangu, yani sikujua kama haya yatatokea, sikujua kabisa”“Unafiwa na rafiki unashindwa kufika kwenye mambo ya muhimu, kwani usingeenda huko msibani leo ungepungukiwa na nini? Haya, mmeshazika”“Hapana bado”“Kesho nitafute, ila kabla ya kunitafuta hakikisha wale watoto wameenda kule kwa babu yao”“Sawa, hakuna tatizo”Ile simu ilikatika, baba Angel alijiuliza, inamaana dokta Jimmy hafahamu kwamba aliyekufa ni ndugu yake Manka mpaka kuuliza vile? Baba Angel alishangaa sana ila hakutaka kuanza kufatilia ile karatasi maana huyu msichana wa kazi nae alionekana kumzungusha tu mpakagiza liliingia akiwa pale, basi moja kwa moja aliamuaga mama Sarah pamoja na Sarah na kuondoka zake kuelekea nyumbani kwake.Mama Angel akiwa na Angel na Ester ambaye alikuwa amelala kwa muda huo waliwasili nyumbani kwao.Moja kwa moja waliingia ndani na kumkuta Erica akiandaa chakula mezani huku akisaidiana na Erick, basi mama yao alifurahi huku akisema,“Leo mmeachwa watoto wa kazi, nilijua tu kila kitu nitakikuta sawa”Angel akasema,“Mmmmh jamani mama, kwani mimi sio mtoto wa kazi?”“Aaaah sijasema kwa ubaya ila nimewasifia tu wadogo zako, huwa najua akiwepo Erica nyumbani na Erick huwa akiharibiki kitu. Vipi baba yenu amesharudi?”“Bado mama hajarudi”Mama Angel alichukia sana kusikia kuwa bado mumewe hajarudi, aliamua kumpigia simu ambapo mumewe alidai kuwa yupo njiani kurudi nyumbani, na kweli baada ya muda mfupi tu baba Angel aliwasili nyumbani, na hivyobasi wote walikaa mezani na kuanza kula huku kama kawaida wakisifia chakula kilichopikwa na Erica,“Lakini leo mama tumepika wote wawili, yani mimi na Erick”“Kheee Erick nae kapika nini?”“Kapika mama”Erick nae akasema kuwa amepika pia basi mama yao aliwasifia wote wawili, kisha walipomaliza kula ndipo baba yao alipowaita na kuongea nao kuhusu kwenda kwa babu yao,“Sasa mjiandae kesho ndio mtaenda kwa babu yenu, si mnajua kulivyo mali? Kwahiyo mjiandae mapema halafu dereva atawapeleka”“Sawa baba”“Mkifika, mimi nitawaambia kitu cha kwanza cha kufanya pale kwa babu yenu”“Hakuna tatizo baba”Kisha baba Angel aliwatakia wanae usiku mwema halafu yeye alienda moja kwa moja chumbani kwake.Wakiwa chumbani baba Angel alimwambia mke wake kuhusu alichoongea na dokta Jimmy na alichoenda kuwaambia watoto kuwa kesho wajiandae,“Ila huyu dokta Jimmy ana nini na watoto wangu lakini? Kwanini anataka waende huko kwa babu yao?”“Mimi na wewe hatujui kuna nini ila tunahitaji kuufahamu ukweli ndiomana nimekubali tu kuwa waende na mimi nitaenda kuzungumza nae ili tujue kisa na mkasa”“Mmmmh yani najikuta kutokumuamini amini huyo dokta jamani, hebu angalia hiyo simu unayosema umeongea nae akilalamika kwanini umeenda kwenye msiba bila kukutana nae, inamaana hajui kama dada wa Manka amekufa?”“Mke wangu, nimejiuliza swali kama hilo pia. Labda sababu yeye ni daktari, kazoea kuona maiti mara kwa mara kwahiyo kwake kifo ni kitu cha kawaida”“Hata kama, tunawaona madaktari wangapi ikitokea msiba wa karibu na wao wanashtuka? Yani huyo amenishangaza kwakweli, ila sitaki tena kuwa kikwazo kwa hili, nenda kakutane nae tu ingawa mimi simuamini”“Usijali kitu mke wangu, kila kitu kitaenda sawa, hakuna kitakacho haribika”“Sawa, mimi nakubaliana tu na wewe mume wangu ila kesho nitatoka, nitaenda kwa rafiki yangu Johari kuongea nae”“Aaaah kuhusu maswala ya mtoto wake eeeh!!”“Ndio, nitaenda kuongea nae kuhusu hilo”“Sawa, hapa nyumbani atabaki Angel peke yake?”“Aaaah kwani Angel anaogopa nini hapa? Hata hivyo, Ester yupo kwahiyo sioni kama ni tatizo”“Basi sawa, nimekuelewa”Kisha kwa muda huo waliamua tu kulala kwaajili ya kujiandaa kwa mambo ya kesho.Erica akiwa anajiandaa kulala, chumbani kwake aliingia Erick na kuanza kuongea na Erica ambapo Erica alikaa na kumsikiliza,“Naomba unisamehe kwa mchana wa leo”“Ila hakuna kibaya kilichotokea kati yetu”“Hakuna ndio ila dah sijui nisemeje”“Usijali wala nini”Kisha Erick aliinuka na kwenda chumbani kwake, basi Erica alianza kufikiria kuhusu kilichotokea mchana,“Mmmmh ni nini kilitaka kutokea kile? Mimi na Erick tulikumbatiana tukiwa watupu kabisa, nashukuru Mungu niliweza kumtoa Erick mwilini mwangu na kukimbia, ila kama ningebaki ni kitu gani kingetokea kwani? Mbona mwili wangu nilihisi ukipokea mabadiliko ya hali ya juu?”Alikuwa akijiuliza sana bila ya jibu, kitu hicho kilimfanya muda wote akumbuke jinsi alivyokumbatiana na Erick chumbani huku wakiwa watupu kabisa.Kulipokucha tu, Erica alijiandaa na baada ya hapo alitoka nje na kumkuta Erick nae kajiandaa kisha wakaenda kwenye gari ambapo dereva nae alikuwa tayari na kuanza safari ya kwenda huko kwa babu yao.Baba Angel nae alijiandaa na kumpigia simu dokta Jimmy ambaye alimjulisha mahali pa kukutana ambako hapakuwa mbali sana na kule walipoenda watoto wake, basi moja kwa moja baba Angel alienda kukutana na dokta Jimmy ambapo alimpata na kusalimiana nae kisha kuongea mawili matatu halafu dokta jimmy akamwambia,“Washaenda watoto?”“Ndio, nadhani watakuwa wanakaribia kufika maana hapa sio mbali na kule halafu wenyewe waliondoka mapema zaidi”“Aaaah sasa wapigie simu halafu nipe niongee nao”Baba Angel alipiga simu kwa Erick ambapo muda ule ule Erick alipokea ile simu,“Mmeshafika?”“Ndio tumefika muda sio mrefu baba”“Basi, msikilizeni huyu awape maelekezo cha kufanya:”Basi baba Angel alimkabidhi simu dokta Jimmy ambapo alianza kuongea nayo,“Sikia, nenda moja kwa moja kwa mlinzi hapo mwambia akupe funguo, halafu mkiingia ndani kuna funguo kwenye kabati ya hapo sebleni ichukueni hiyo funguo mwende nayo hadi chumba cha mwisho hiko ndio kilikuwa chumba cha babu yenu. Kisha mkiingia humo ndani, mtakuta kuna CD imewekwa juu ya deki, chukueni CD hiyo muiweke kwenye deki halafu muwashe hiyo Tv. Angalieni kama nusu saa halafu ndio mtapiga simu”“Sawa tumekuelewa”Kisha walikata simu halafu dokta Jimmy alikaa na baba Angel sasa akiongea nae mambo mengine huku akimwambia wasubiri hiyo nusu saa ipite.Erick na Erica walifanya kama ambavyo walielekezwa, na walipoingia ndani waliona jinsi nyumba ile ilivyosafi kwamaana kuwa huwa inafanyiwa usafi mara kwa mara ingawa mwenye nyumba amekufa.Walienda moja kwa moja hadi chumbani na kufanya kamavile walivyoelekezwa, basi ile video ilianza kuonyesha ambapo walimuona mdada na mkaka ambao walikuwa ni vijana yani rika kama lao, halafu mule kwenye video ilisikika sauti ya mtu kama akiwaelekeza cha kufanya, waliona yule mkaka na mdada wakianza kushikana shikana na mwishowe wakavua nguo zote. Walienda moja kwa moja hadi chumbani na kufanya kamavile walivyoelekezwa, basi ile video ilianza kuonyesha ambapo walimuona mdada na mkaka ambao walikuwa ni vijana yani rika kama lao, halafu mule kwenye video ilisikika sauti ya mtu kama akiwaelekeza cha kufanya, waliona yule mkaka na mdada wakianza kushikana shikana na mwishowe wakavua nguo zote.Kisha Erick akamwambia Erica kuwa wafanye kamavile ambavyo wanafanya kwenye ile video, basi Erica akamwambia Erick,“Unaona kuwa ni sawa kwa sisi kufanya vile Erick?”“Sijui, labda tujaribu mbona kama wanafurahia wale! Hebu na mimi jaribu kunifanyia kama yule dada anavyomfanyia yule kaka!”“Mmmmh Erick jamani!”“Jaribu Erica, mbona naona itakuwa ni raha sana”Erica akainama na kuanza kufanya kamavile wanavyoangalia kitendo ambacho kilimchanganya sana Erick na kumfanya apige kelele huku akisema,“Mungu wangu Erica, sijawahi kuona kitu cha namna hii”Kitu kile kilifanya Erick atoe ute ute na kumfanya Erica aruke pembeni na kusema,“Ndio nini sasa Erick?”Erick alikaa kimya kwa muda huku akijitathimini na baada ya muda akasema,“Nahisi raha sana Erica, natamani hii raha uipate na wewe pia”“Aaaah ila mimi naogopa”“Unaogopa nini? Naomba basi nikufanyie kama huyo mkaka anavyomfanyia huyo mdada”“Hapana Erick”Basi waliwaangalia tena wale wa kwenye video na kuona kwa muda huu staili yao imebadilika huku wakionekana kufurahia sana kufanya vile wanavyofanya, Erick alimuangalia Erica na kumwambia,“Sasa bado kufanya kama vile”Kisha Erick alimkumbatia Erica na kumuangusha kitandani ila kabla Erick hajafanya chochote, Erica alimwambia Erick,“Huu ni mtego Erick”“Mtego kivipi? Tufanye Erica jamani!”“Huu ni mtego, tumechunguliana inatosha”“Hapana, haitoshi erica naomba jamani nashindwa kuvumilia kikweli naumia sana hapa, nahisi hadi misuli inaniuma”“Kwahiyo tufanye nini ili hiyo misuli iache kuuma?”“Basi naomba nifanyie kama mwanzo”Erica hakubisha na alifanya vile, kisha alipoona tena ute aliinuka na kuzima ile video kisha alikimbilia bafuni na nguo zake.Alijifungia mule bafuni na kumwambia Erick,“Naomba uvae nguo zako Erick, nitakwambia kwanini ukishamaliza kuvaa”Basi Erick akaona bora aende kwenye bafu lingine na kujisafisha ili na yeye avae nguo vizuri.Baba Angel akiwa anaangalia saa yake, aliona kama muda umeenda sana, basi akamwambia dokta Jimmy,“Kwasasa ni karibia lisaa linapita”Dokta Jimmy alicheka sana na kumuangalia baba Angel kisha akamwambia,“Unajua ni kwanini hawajapiga?”“Eeeeh kwanini?”“Muda huu watoto wako wapo kuzini, itakuwa wapo kukumbatiana kwa shughuli nzito waliyopeana”“Kivipi? Sikuelewi”“Hebu nisikilize kwa makini sana nikueleweshe Erick”“Nieleweshe tu nakusikiliza”“Ni hivi, baba yako yani mzee Jimmy alikuwa akimpenda sana mke wako uliyemuoa yani Erica, alikuwa akimpenda sana tena sana na alikuwa tayari kufanya chochote juu yake huyo mwanamke. Kuna siku huyo mkeo akiwa mjamzito wa hao mapacha wako, alimjibu vibaya sana baba yako, unaweza kumuuliza na atakwambia kama anakumbuka. Kitu hiko kilimkera sana mzee Jimmy, alikuja na kunilalamikia, akasema kuwa lazima mkeo amkomeshe, alisema kuwa lazima mkeo amlee mtoto ambaye sio wake, na mpango wa baba yako ulikuwa ni kubadilisha watoto, tulitaka kumbadilisha mtoto wa mkeo na mtoto wa Sia, na ndio mpango ulivyokuwa ila badae wakati mimba ya mkeo imefikia ukingoni ndio wazo likabadilika kwani kuna mtaalamu mmoja hivi alisema kuwa anadawa ambayo akiwawekea watu wakati wadogo basi watu hao wataanza kuingiwa na hisia za kimapenzi wakiwa wakubwa, ndipo baba yako aliposema kuwa dawa zile tujaribu kwa watoto wako na sio kuwabadilisha tena. Mkeo alijifungua, kuna kitu kilitokea kabla hata ya kuwachoma sindano, alikuja mama mzazi wa mke wako na kusema kuwa aonyeshwe watoto ambao mwanae alijifungua, basi ilibidi akaonyeshwe na wazo la kuwabadilisha likafa muda ule ule, tukaendelea na wazo la sindano tu. Basi baada ya muda tuliwachoma zile sindano ambazo ni wazi zinaanza kufanya kazi vizuri baada ya watoto kufikia umri wa balehe. Nilichofanya leo ni kujaribu kuhusu zile dawa kuwa zimefanya kazi au la maana watoto wako wale mapacha wapo kutamaniana kimapenzi kwa muda mrefu sana, kwahiyo ule mkanda niliowaambia waweke ni mkanda wa ngono wa kuweza kuwahamasisha na wao kufanya ngono na mpaka muda huu wameshafanya ndiomana unaona simu haijapigwa halafu…..”Baba Angel aliinuka kwa hasira na kusema,“Stooop, nakwambia nyamaza dokta Jimmy, ni ujinga gani huu kunitendea kwa watoto wangu, watoto ambao mke wangu kabeba mimba kwa shida na kuwazaa kwa uchungu halafu nyie mmenda kunifanyia ufedhuli huu kweli! Wanangu wakishafanya mapenzi nyie mnapata raha gani? Wanangu wakipeana mimba kwenu ni furaha gani?”Kwa mara ya kwanza baba Angel alijikuta akiongea huku akibubujikwa na machozi ya nguvu, alikuwa akilia kwa hasira sana, alijiona kama kabeba kitu katika moyo wake, alijikuta akiwa na hasira kiasi kwamba alitamani hata amchukue dokta Jimmy na kumponda ponda, basi akaanza kuondoka na dokta Jimmy akamuuliza,“Unaenda wapi sasa?”“Nawafata wanangu”“Unajisumbua, kama bikra washavunjana hao. Njoo tujadili cha kufanya”“Mjinga wewe achana na mimi”“Unajifanya una hasira sana na mwanao, na huyo Erica mdogo akipata hiyo mimba mlee, sijui mtoto wake atawaitaje, masikini jamani mnatia huruma”Dokta Jimmy alikuwa akiongea huku akicheka na kutikisa kichwa, kwakweli baba Angel alizidi kupandwa na hasira kwani kwa muda huo mawazo yake yote ilikuwa ni juu ya wanae, alikuwa akitembea huku machozi yakimtoka na kuingia kwenye gari yake ila dokta Jimmy aliingia pia na kumwambia,“Erick, naomba niruhusu nikuendeshe tu twende eneo la tukio, bado nakuhurumia. Najua uchungu ulionao ila kosa sio langu ni kosa la baba yako”Baba Angel hakujibu kitu, kwahiyo dokta Jimmy alianza kuendesha na kuelekea nyumbani kwa mzee Jimmy.Dokta Jimmy na baba Angel walipofika pale hata hawakuuliza kwa walinzi kuwa imekuwaje moja kwa moja waliingia hadi chumbani kwa mzee Jimmy ila Erick na Erica hawakuwepo na kumfanya baba Angel azidi kupatwa na mawazo alijaribu kuwaita lakini hawakuitika, basi dokta Jimmy aliwasha ile CD maana bado ilikuwa kwenye deki, na ilianza kuonyesha, huku dokta Jimmy akicheka alimwambia baba Angel,“Angalia hata kitanda, kilikuwa kimetandikwa hiki ujue, halafu sikiliza harufu ya hiki chumbakwa mbali utasikia kama harufu ya shahawa”Kile kitu kilizidi kumchanganya baba Angel, kisha dokta Jimmy alimwambia tena baba Angel,“Naona bado huamini, twende ukaone”Kisha baba Angel akiwa anatikisa kichwa na machozi ya hasira yakimtoka alifatana na dokta Jimmy hadi kwenye chumba kingine ambacho kulikuwa na Tv kisha dokta Jimmy akawasha na kusema,“Kuna CCTV camera tumefunga kwenye chumba cha mzee wako, nataka ujionee mwenyewe”Baba Angel akaona pale Erick na Erica wakivua nguo, kisha akamuona Erica akiinama kwenye maungo ya Erick, kwakweli baba Angel alishikwa na hasira ya gafla na kuvunja ile Tv, kisha alimgeukia dokta Jimmy na kuanza kumkaba hadi dokta Jimmy alianguka chini na kupoteza fahamu halafu baba Angel akatoka mule akiwa na hasira zaidi hata mlinzi alipomuuliza,“Mzee kuna nini kwani?”Alimpiga ngumi moja ya sura kiasi kwamba yule mlinzi alianguka chini na damu kuanza kumtoka puani, mlinzi wa pili alitaka kukimbia ila baba Angel akamuuliza,“Wewe mjinga, watoto wangu waku wapi?”“Sijui mzee ila walitoka gafla na kuondoka”Baba Angel alianza kumsogelea yule mlinzi ila yule mlizni alikimbia haraka haraka na kutoka nje kwani alimuogopa baba Angel ambaye alionekana kubadilika sura kabisa. Baba Angel alirudi kwenye gari lake na kuondoka nalo, alivyofika njiani alilisimamisha pembeni na kujikuta akilia sana, yanbi alilia kama mtu aliyefiwa vile, kwanza hakuelewa watoto wake watakuwa wapi baada ya kitendo kama kile, hakuelewa ni kwanini baba yake kaamua kumuumiza kiasi kile, hakuelewa ataweka sura yake wapi baada ya Erica kuonekana kuwa ana mimba ya Erick, yani alijikuta anawaza hata vitu visivyokuwepo, hata aliwaza huenda watoto wake wamejidhuru baada ya yale, yani alilia sana na kukosa raha kabisa.Siku ya leo ilikuwa ni nzuri sana kwa upande wa Angel kwani ni siku ambayo alibaki mwenyewe tu na Ester, hivyobasi aliamua kumpigia simu Samir ambaye hakuchukua muda mrefu na kufika pale kwakina Angel, halafu alianza kuongea nae,“Naona hii ndio siku ile uliyoniambia Angel”“Ndio, ni hii”“Sikia nikwambie kitu Angel”“Kitu gani”“Wanakazana kusema kuwa mimi na wewe ni ndugu ila hili mimi nimelipinga au mwenzangu umelikubali?”“Hata mimi nimelipinga”“Sasa inabidi tufanye kitu kudumisha mapenzi yetu na ili kuonyesha kuwa tunapingana na mawazo yao”“Kitu gani Samir?”“Inatakiwa tufanye mapenzi Angel, kwanini kila siku tunaahirisha? Kumbuka ulisema siku kama hii ndio itakuwa nzuri kwa mimi na wewe kuwa pamoja”“Sawa, hakuna tatizo. Ngoja mtoto alale basi”Muda huu Angel alimbembeleza mdogo wao ambaye hakuchukua muda mrefu sana akapitiwa na usingizi na kulala, basi Angel akamlaza kwenye kochi halafu yeye na Samir moja kwa moja walienda chumbani.Kama walivyopanga, walienda kutimiza adhma yao tu waliyokuwa wakiitaka kwa siku zote, kitendo kile kilimfurahisha sana Samir na kumshukuru sana Angel,“Nafurahi sana mimi kuwa mwanaume wa kwanza kwako”“Mmmmh!! Mimi naona aibu”“Aibu ya nini Angel wakati mimi ndio mumeo”Hapo Angel alifurahi na wote wawili kuanza kucheza cheza mule chumbani kisha wote wawili walilala pamoja mule mule chumbani kwa Angel.Mama Angel kama ambavyo alipanga kwa siku hii, moja kwa moja alienda kwa rafiki yake Johari maana alishapanga kwenda kuzungumza nae, basi alimkuta pale na kuanza kuongea nae kuhusu mambo yaliyopo baina yake na mtoto wake,“Johari kuwa makini sana, mtoto atafanya ugombane na mumeo huyu”“Ndiomana nimemrudisha kwetu maana alikuwa akitaka kuniletea balaa”Muda huu alifika Juma yani mume wa Johari na kuanza kumsalimia mama Angel, na kama kawaida ya Juma alianza kumuulizia Erick kwanza kama kawaida yake,“Vipi Erick hajambo? Anaendeleaje na pacha wake?”Mama Angel alihisi moyo wake ukifanya paaa, na kuema,“Jamani, mbona moyo umeniuma gafla”Johari alimuangalia na kumuuliza,“Kivipi? Kwani kuna tatizo?”“Hapana, kila kitu nimeacha kikiwa salama kabisa ila najiona gafla sina raha tena, nahisi kama sijui moyo wangu umefanyeje”“Oooh pole sana ndugu yangu”Basi Johari akaenda kumletea maji ambapo mama Angel alikunywa kidogo tu ila bado hakujisikia vizuri maana bado moyo wake ulikuwa ukimuuma sana na muda huo kuamua kumpigia simu mume wake ambapo simu ya mume wake iliita tu bila ya kupokelewa, basi walianza kuongea nae taratibu na kumpooza kuwa hakuna baya lililotokea,“Unajua kuna kipindi moyo huwa unashtuka tu, kwahiyo usijali mama Angel, hakuna baya kati yako”“Ila najihisi kupumzika, yani nimejikuta tu gafla nikiwa sina raha tena, hapa nilipo nahisi kama kichwa changu kimeingiliwa na kitu”“Pole sana”Johari aliona ni vyema kama rafiki yake akipumzika basi alimtafutia chumba cha wageni pale kwake ili aweze kupumzika ila napo bado alikuwa anajihisi vibaya na kuamua kuaga kabisa ili aende kwake, basi Juma alijitolea kumpeka hadi nyumbani kwake.Mama Angel alipofika nyumbani kwake, Juma alimuaga halafu moja kwa moja yeye aliingia ndani na kuona pako kimya sana, akajua Angel na mtoto lazima watakuwa wamelala chumbani kwa Angel, kwahiyo moja kwa moja mama Angel alienda chumbani kwa Angel, alipofungua mlango tu alitamani hata kupiga yowe,“Angel!! Angel!! Angel!! Nakuita mara tatu mwanangu, ndio uchafu gani huu umekuja kunifanyia Angel jamani, kwanini Angel?”Samir na Angel waliinuka huku Samir akivaa haraka haraka na kutaka kuondoka, ila kabla ya kutoka mama Angel alimshika mkono Samir na kumwambia,“Wewe mjinga, baba yako hajakueleza kuwa Angel ni nani yao au kiburi?”Samir alikaa kimya tu, kisha mama Angel alimzaba vibao mfululizo Samir na kufanya Angel asogee karibu ila mama yake aache kumpiga Angel, kitendo hiko kilimkera sana mama Angel na muda huo alimuacha Samir na kuanza kumpiga Angel ambapo Samir alikimbia, kwahiyo mama Angel alibaki akimpiga Angel kwa hasira,“Mjinga wewe, nimekulea kwa shida, nikakupeleka hadi shule za masister ili uwe na maadili halafu bila aibu unaenda kuleta mwanaume kulala nae nyumbani kwangu! Halafu mwanaume mwenyewe ni kaka yako, mjinga sana wewe”Mama Angel aliendelea kumpiga Angel kwa hasira huku akihisi kama kitu kikimkaa kwenye moyo wake maana alikuwa na hasira sana tena hasira zilizopitiliza.Ila gafla walisikia sauti ya Samir ikisema,“Moto, moto huku jamani moto”Hapo mama Angel alimuacha Angel na kushuka chini huku wakimkuta Samir kamkumbatia mtoto Ester halafu mlinzi wao akijaribu kuuzima ule moto ambao ulitapakaa jikoni yani ilikuwa ni kitu cha ajabu sana, ikabidi Angel amchukue mdogo wake halafu Samir alianza kusaidiana na yule mlinzi katika kuuzima ule moto sababu nyumba yao ilikuwa na vifaa maalumu vya kuzumia moto, na Samir aliweza kuvitumia kwahiyo ikasaidia swala lile la kuzima moto.Mama Angel alijikuta akiishiwa na nguvu, alikaa chini tu huku machozi yakimtoka kwa mfululizo yani hakuamini kile kilichotokea.Angel alimuuliza Samir,“Kwani imekuwaje?”“Wakati nakimbia, nilipofika sebleni nilikumbuka kuwa mtoto ulimlaza kwenye kochi ila sikumuona na kuona moshi ukitokea maeneo yale, basi niliamua kwenda yani Mungu tu amesaidia, nilimuona mtoto huyu akiwa katikati ya moto halafu kashika kiberiti”Mama Angel alisisimka sana, alijihisi kukosa amani katika moyo wake na kujikuta akiangua kilio cha nguvu maana kwa siku hii ndio angekuwa kampoteza mtoto wake Ester kwasababu ya hasira alizokuwa nazo, basi mama Angel aliinuka na kwenda chumbani kwake ambapo alilia sana, kisha Angel na Samir pamoja na yule mlinzi walisaidiana kuweka baadhi ya vitu sawa huku Angel kambeba mdogo wake mgongoni.Mama Angel alitoka chumbani kwake wakati giza limeshaingia tayari, alifika sebleni moja kwa moja na kumkuta Angel amejiinamia tu kisha akamuuliza,“Baba amerudi?”“Bado hajarudi”“Erick na Erica?”“Bado hawajarudi”“Ooooh Mungu wangu, ni nini hiki jamani? Siwezi mimi, naomba Mungu nirudishie familia yangu, siwezi mimi”Alijikuta akitoa tena machozi, kitu kilichokuwa kikimchanganya ni ile hali ya kuwapigia simu na kutokupokea, yani alihisi kuchanganyikiwa kabisa.Walikaa kwa muda pale sebleni na Angel ila bado ndugu zao hawakurejea, kwenye mida ya saa tatu usiku ndipo Erick na Erica waliporudi na kufanya mama yao afurahi kwani alikuwa na uhakika na mumewe sasa kuwa atarudi, ila baada ya salamu ilibidi Erick na Erica kila mmoja kwenda chumbani kwake kuoga.Basi mama Angel aliendelea kusubiri pale, hata Angel alipoinuka na kwenda kulala bado yeye aliendelea kusubiri, kwenye mida ya saa sita kasoro usiku ndipo baba Angel aliporudi nyumbani kwake, kwakweli mama Angel alifurahi sana ambapo moja kwa moja walienda chumbani na baba Angel cha kwanza kabisa aliuliza,“Erick na Erica wapo ndani?”“Ndio, wapo ndani mume wangu”“Oooh asante Mungu”Kisha baba Angel alienda kuoga kwanza na mkewe alimuuliza kuwa akamuandalie chakula gani maana hata hamu ya kupika toka litokee seke seke la moto haikuwepo mule ndani,“Nikuendalie chakula gani mume wangu?”“Sina hata hamu ya kula”“Kwani tatizo ni nini mume wangu”“Sijui kama nikikuelezea utaweza kuvumilia”“Nieleze tu hakuna tatizo”“Ooooh hapana niache nilale kwanza”Baba Angel hata hakutaka kuongea na moja kwa moja alilala kwanza.Usiku huu Erick alienda chumbani kwa Erica na kuanza kuongea nae kwa yale yaliyotokea baina yao siku hiyo, alianza kwa kumuomba msamaha,“Naomba unisamehe sana Erica, nisamehe sana hata sijui ni kitu gani huwa kinaingia katika akili yangu. Naomba unisamehe sana”“Usijali Erick, mimi bado najiuliza kuna nini kati yetu?”“Sijui, ila nakushukuru sana Erica maana siku zote umekuwa mstari wa mbele kutuepusha katika kutenda haya ingawa leo ilibaki kidogo tu tuangukie kwenye hayo mambo”“Ila Erick umeona? Umegundua kitu?”“Kitu gani?”“Kumbuka muda ambao mimi na wewe tulipokuwa kule wakati tunataka kufanya yale mambo, unakumbuka lakini?”“Nakumbuka ndio, ila ulininanii vizuri Erica, nilijihisi kama napaa vile”“Acha maneno yako Erick, sikia kwanza umeona hapa nyumbani imetokea ajali ya moto? Nasikia bado kidogo Ester angeungua, tungemkosa mdogo wetu kwa ujinga wetu”“Dah!! Kwani ilikuwaje?”“Wewe ukishatenda dhambi huwa hata hutaki kusikiliza yaliyotokea, nasikia leo jikoni kumewaka moto, bado kidogo tu Ester angeungua, ameokolewa tu. Yani kulikuwa na balaa”“Kheee kwahiyo hilo balaa ndio tumesababisha sisi?”“Sijui, nahisi ni hivyo kuwa ni sisi ndio tumesababisha. Ila kama kule tulikuwa tumewekewa mtego itakuwaje?”“Haitakuwa kitu, kwani tumefanya kitu gani kibaya?”“Kile nilichokufanyia ni kizuri? Erick tumekosea sana maana sisi ni ndugu ujue, sisi ni mapacha”“Naelewa hilo Erica, ila sio kosa langu na pia sio kosa lako kwani nahisi hata wewe unahamu kubwa ya kuwa na mimi kimapenzi”“Mmmh ishia hapo, usiku mwema na urudi chumbani kwako”Erick aliondoka na kwenda chumbani kwake, basi Erica alikaa kwanza kitandani na kuanza kufikiria yale matukio yaliyotokea baina yake na Erick.Akakumbuka muda alipoingia bafuni na kumuomba Erick avae nguo, ambapo alipotoka alimuomba Erick waondoke waende ufukweni kupunguza mawazo, akakumbuka jinsi Erick alivyolalamika kuwa anahisi kuwa na hali mbaya basi akakumbuka alivyotumia muda mrefu kuweza kumbadilisha Erick mawazo, basi akajisemea,“Kwanini lakini? Kwanini inakuwa hivi? Kama mimi na Erick ni mapacha, sasa kwanini tunatamaniana? Na kwanini iwe hivi kati yangu na Erick”Aliwaza Erica kwa muda mrefu sana bila ya jibu la aina yoyote ile na kuamua tu kulala kwa muda huo.Asubuhi na mapema, Erica alienda chumbani kwa Erick na kumuamsha kisha akaanza kumueleza kila kitu kilichotokea hapo kwao hadi mama yake alivyowafumania Angel na Samir, Erick alimuangalia dada yake na kumuuliza,“Yote hayo umeyaona ndotoni?”“Ndio, na hadi moto ulivyoanza. Ni kuwa, Ester alikuwa amelala sebleni kwenye kochi, alipoamka akainuka na moja kwa moja alienda jikoni na kuanza kuchezea vitu vilivyokuwepo jikoni. Kama unakumbuka kuna chupa ya mafuta ya taa ililetwa ndani na baba, sasa ile chupa ilikuwa jikoni, basi Ester aliichezea na kuifungua ile chupa basi mafuta yalimwagika pale, kisha akaanza kuchezea kiberiti na mwisho wa siku wa siku akafanikiwa kuwasha, yani moto umewaka halafu Ester wala hakushtuka. Bila yule Samir ingekuwa balaa kwa siku ya jana. Kwahiyo chanzo cha moto ni Angel na Samir”“Aaaah ila wewe Erica ni noma kwenye maswala ya ndoto, kila kitu unaota. Hivi huwa unafanyeje hadi unaota?”“Hata sijui ila huwa najikuta tu nikiota”“Je hujawahi kuota kuhusu mimi na wewe? Hujawahi kuota kuhusu safari ya jana? Hujawahi kuota kinachoendelea kati yangu na yako?”“Mmmmh Erick hata mimi mwenyewe sielewi ni kwanini sijawahi kuota baina yangu na yako, nilichowahi kuota nikikwambia hata wewe kitakuacha mdomo wazi”“Kitu gani hiko?”Muda huu baba Angel aliingia humu chumbani kwa Erick bila hata ya hodi na kumkuta Erick na Erica wamekaa kitandani wakiwa hawana hata habari yani wakiongea tu mambo yao, kiukweli baba Angel alijihisi vibaya sana kuwaona pamoja, upande mwingine alitamani kuwafokea ila upande mwingine aliona kuwa wale watoto hawakuwa na makosa, basi aliwaangalia tu ambao nao walishtuka na kumsalimia kwa pamoja, kisha kabla ya kuwaitikia salamu aliwauliza,“Mnafanya nini pamoja?”“Hamna kitu baba, ni Erica alikuwa akinisimulia ndoto aliyoota jana”“Ndoto gani?”Erica ilibidi aanze kumsimulia baba yake kutokana na jinsi alivyoota, ndio pale hata baba Angel alipogundua kuwa mkewe alitaka kumueleza kuhusu jambo hilo pia ila yeye alifanya haraka kwenda kumuona Erick kwanza, basi alimuuliza Erica,“Kwani jana wakati panaungua ulikuwepo?”“Hapana, tuliporudi tu tukakuta hivyo ila usiku ndio nikaota”Baba Angel alitamani pia kuwauliza kuhusu kilichotokea kati yao kwa siku ya jana ila alijikuta akishindwa kuwauliza yani alibaki kuwaangalia tu halafu akamuomba Erica atoke ili aongee na Erick.Basi baba Angel alipobaki na Erick alianza kumuuliza,“Mwanangu umewahi kulala na mwanamke?”Erick alishtuka sana hili swali kutoka kwa baba yake na kujibu,“Hapana baba”“Umewahi kufanya mapenzi?”Erick alishangaa tena na kujibu hapana, kisha baba Angel alimuuliza tena,“Je jana ulifanya mapenzi?”Hapa Erick alishtuka zaidi na kumuuliza baba yake,“Kwanini unaniuliza hivyo baba?”“Aaaah basi tu”Kisha baba Angel akatoka mule chumbani kwa Erick, kiukweli baba Angel alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa kabisa yani hakujielewa hata kitu gani anaongelea kabisa.Usiku wa leo, baba Angel aliamua tu kumueleza ukweli mke wake maana aliona kuendelea kuumia kwa swala hilo ni hatari katika maisha yake, yani wala hata hakujali jinsi mkewe aivyomsimulia kuhusu Angel na Samir,“Jamani mume wangu unaonekana hata hujali, unajua Angel na Samir ni mtu na dada yake? Wote ni watoto wa Rahim”“Hebu tulia mama Angel, ukisikia ya kwetu huku nahisi utatamani ardhi ipasuke uingie”“Ya kwetu ipi hiyo?”“Ushawahi kusikia watoto wa baba mmoja na mama mmoja wamepeana mimba?”“Mmmmh, hebu niambie vizuri baba Angel”“Ni hivi Erick na Erica sio watoto tena”“Kivipi?”Baba Angel alimsimulia tu mama Angel kwa kifupi na kuhusu video waliyoikuta ya Erick na Erica, mama Angel alijikuta akipiga yowe na kutaka kuinuka kwenda kuwauliza vizuri watoto wake ila baba Angel alimzuia kwanza na kumwambia,“Mke wangu swala hili hata sio la kwenda nalo kichwa kichwa, tutakosa yote”“Kivipi?”Mama Angel aliinama chini kwani alikuwa haelewi kitu kwa muda huo, hata hakujua cha kufanya, alichukua simu yake hata hakuelewa anataka kumpigia nani ila muda huo huo kuna ujumbe ukaingia kwenye simu yake, aliufungua na kuusoma,“Mumeo ameua. Mama Angel aliinama chini kwani alikuwa haelewi kitu kwa muda huo, hata hakujua cha kufanya, alichukua simu yake hata hakuelewa anataka kumpigia nani ila muda huo huo kuna ujumbe ukaingia kwenye simu yake, aliufungua na kuusoma,“Mumeo ameua”Mama Angel alimuangalia mumewe kwa uoga, kiasi kwamba hata baba Angel alihisi kuwa kuna kitu sio sawa na kuchukua ile simu kwa mkewe kisha alisoma huo ujumbe, na baada ya hapo mama Angel alimuuliza,“Eeeeh mume wangu umemuua nani?”“Mimi sijui maana sijui kama niliowashughulikia walikufa”“Ulishughulikia wakina nani?”Baba Angel alimuuleza mkewe kwa kifupi jinsi alivyomkaba dokta Jimmy, na jinsi alivyompiga ngumu mlinzi kisha akasema,“Kwakwekli Mungu anisamehe tu ila nilikuwa na bhasira sana, huo ujumbe sio nani kautuma. Natumaini yule mlinzi hakufa maana sio kosa lake, na kama amekufa basi nitajilaumu sana mimi sababu yeye nimempiga kwa hasira ila huo ujumbe napenda uwe wa kumuhusu dojkta Jimmy yani waseme ndio amekufa. Siku ya mazishi naenda pale na panga langu yani maiti yake naikata na kichwa kabisa”Mama Angel alimuangalia kwa makini mumewe ila kwa lile lililokuwepo alielewa ni kwanini mumewe anaongea kwa hasira kiasi kile, ndio na yeye sasa alianza kuingiwa na akili sawa kwani alishtuka kitu na kujisemea,“Inamaana kweli mwanangu Erick na Erica wamefanya mapenzi!!”“Sasa unafikiri mimi ningejianzia tu kuchukia? Mama Angel mimi nina hasira sana, naongea lakini sina raha kumbuka jinsi tulivyojitahidi kulea watoto wetu, katika maadili na njia za kumpendeza Mungu ila ni nini hiki? Eti kuna mjinga mmoja alikuwa akifanya majaribio kwa watoto wetu? Alikuwa akinikomesha mimi kwa damu yangu? Kwakweli nina hasira sana”Muda huo baba Angel alioneka hata kusahau kama kitendo kile kimefanywa na baba yake mzazi, kwajinsi alivyokuwa akiongea na kumuita mjinga mmoja.Basi baba Angel alichukua simu na kumpigia mama yake mzazi, ila muda ule mama Angel nae aliinuka kumbe alienda chumbani kwa Erica kwani huwa anajua kama mwanae huyu huwa anapenda kusema ukweli ingawa hakuwa na uhakika kama hilo angelisema ukweli pia.Baba Angel moja kwa moja alimpigia simu mama yake na kuanza kuongea nae kwani kwa muda huo alishikwa tena na hasira kwa ule ujumbe kuwa amemuua mtu,“Mama, nakuomba mama yangu jitahidi uwezavyo tuonane maana mtoto wako nipo kwenye hali mbaya sana. Nahisi utanikosa”“Tatizo ni nini Erick?”“Mama, sina wa kumweleza hii aibu iliyonifika. Naomba mama yangu uje, nabaki kutangatanga na moyo tu”“Naona kweli haupo sawa, mimi sipo mbali sana ila nimefikia hotelini. Kama utaweza mwanangu kuja hotelini kwa muda huu ni sawa hakuna tatizo, njoo tuonane ili tuweze kuongea”“Sawa mama hakuna tatizo, nakuja huko sasa hivi”Kisha baba Angel alianza kujiandaa bila kujali kuwa ule ni usiku, kwavile anaijua hoteli ambayo mama yake anapenda kufikia kwahiyo alifanya tu upesi upesi ili aondoke na kuelekea huko kwa mama yake.Mama Angel alienda moja kwa moja chumbani kwa Erica na kumkuta Erica kajiinamia tu, kwanza moyo wake ulifanya paaa, ila alimsogelea binti yake na kukaa nae karibu,“Unajua ni saa tano usiku hii Erica, mbona hujalala mwanangu?”“Sina usingizi tu mama”“Pole sana mwanangu, tatizo ni nini hadi umekosa usingizi?”“Sijui mama”“Nisikilize Erica, mambo mengi sana huwa unapenda kuniambia na mengine huniambia hata kabla hayajatokea, na mengine hata yakitokea basi huniambie. Najua kuna kipindi nilikuwa nakusema sana kuhusu wewe kuniambia ukweli na kukasababisha ukaacha kuniambia mambo ya muhimu kiasi kwamba ukawa mkubwa bila ya kuniambia ila mwanangu nilikuomba msamaha na ukaanza kuniambia tena. Mbona hili hujaniambia?”“Lipi hilo mama?”“Wewe na kaka yako mlifanya nini kwenye nyumba ya babu yako?”Mama Angel aliuliza hilo swali kwa binti yake huku midomo yake ikimtetemeka, na Erica alishtuka na kuanza kumjibu mama yake kwa uoga,“Nisamehe mama”“Msamaha wangu ni pale wewe utakapoamua kunieleza ukweli, mimi ni mama yako na usinifiche chochote niambie ukweli halisi”“Ni aibu mama”“Kitu gani hiko cha aibu Erica eeeh!! Mwanangu wewe ni binti shupavu na mimi naelewa hilo kuwa wewe ni binti shupavu na huwa unasema dhahiri kuwa huogopi chochote, na siku zote hupenda kueleza ukweli. Niambie ukweli mwanangu”“Mmmh mama, naomba unisamehe”“Sawa, ila unajua kuwa ukweli humuweka mtu huru? Niambie ukweli mama, nakuomba mwanangu”“Niahidi kuwa hutonipiga!”Mama Angel akapumua kidogo na kumuahidi mwanae kuwa hatompiga, basi Erica alianza kumuelezea,“Mama samahani, hata sikujua kama itakuwa hivi. Tunaona aibu mbele yenu na mbele ya macho ya baba, hata kuongea nae tunajikaa tu ila tunaona aibu hata sijui imekuwaje na sijui nianzie wapi kuelezea”“Anzia popote unapoona panafaa kuanzia, hata ukianzia hapo kwa babu yenu ni sawa”“Tulifika kwa baba mama, tukapewa maelekezo kuwa tuingie kwenye chumba cha babu na tuweke CD iliyopo kwenye video, kisha tukaanza kuangalia. Kiukweli ile video haikuwa nzuri mama, na haikuwa nzuri kwa umri wetu ila tuliangalia siwezi kukana hilo mama. Kwenye ile video walikuwa wakitenda matendo ya ngono ambayo huwa unatukataza hata video za kawaida tukiangalia ndani ikionekana mwanamke na mwanaume kitandani huwa mama unapeleka mbele sehemu hiyo ila kwenye ile video walikuwa watupu kabisa, na sisi tulivua nguo pia”Mama Angel akapumua na kuendelea kusikiliza yani alihisi akitetemeka hadi masikio kwa muda huo,“Eeeeh ikawaje?”“Kile kitu cha mbele ya Erick kiliinuka juu na kuonyesha kama mishipa imesimama, niliogopa kiasi ila kwenye video kuna kitu kilionekana kwanza ndio Erick aliponiambia mimi nimfanyie kamavile kwenye video, ndipo nilipoinama na kunanii nanii yake”Mama Angel alishtuka kwanza na kumuuliza erica,“Erica mwanangu hebu nyoosha maelezo yako hapo, kunanii nanii yake ndio nini?”“Nilianza kumnyonya mama halafu…..!”Mama Angel alijikuta akiinuka na kumwambia Erica,“Nyamaza mwanangu”Akatoka na kurudi chumbani kwake, aliinama na kulia sana, yani alilia sana akajua pale ni kitu gani kilitokea baina ya watoto wake, alimuita baba Angel pale ila hakumuona basi alilia sana tena sana yani alijikuta akikosa raha ya maisha kabisa, alilia kwa muda mrefu sana kwani alielewa baada ya ile kitu lazima Erick na Erica waliharibiana tu.Baba Angel alifika hotelini alipofikia mama yake na moja kwa moja alienda kwenye chumba ambacho mama yake anapenda kufikia, aligonga ila aliyefungua hiko chumba hakuwa mama yake kama ambavyo alizoea bali alikuwa ni mwanamke ambapo baba Angel alimshangaa kwa muda ila yule mwanamke alitabasamu na kumuangalia na kusema,“Erick jamani!! Umenikumbuka lakini? Siamini kama nimekuona tena leo”Mara mlango mwingine ulifunguliwa ndipo mama yake alipotoka na kumfata baba Angel kisha akamvuta na kumwambia,“Wewe imefika chumba hiki leo”Alimvuta hadi kwenye chumba alichofikia yani baba Angel bado alikuwa ameduwaa kama mtu aliyepigwa na ganzi vile.Kisha baba Angel alipelekwa kwenye chumba ambacho mama yake alikuwa amefikia humo, basi alimkalisha kwenye kiti na kuanza kuongea nae,“Wewe Erick una matatizo gani wewe? Yani hata kuuliza nimefikia chumba gani hakuna unfanya kukariri tu, haya niambie uzima upo lakini!”“Upo mama ila nina matatizo”“Kweli una matatizo maana kama umepigwa na shoti ya umeme vile, hata hueleweki, hebu nieleze kinachokusibu mwanangu”Baba Angel hakusubiri muda kupita kwani alianza kumueleza mama yake kila kitu kuanzia alipoanza kumtafuta dokta Jimmy hadi alipopanga nae kuhusu watoto wake mpaka dokta Jimmy alivyomsimulia na kile alichokikuta kwa watoto wake, yani baba Angel alimaliza kusimulia huku machozi yakimtoka hadi mama yake aliamua kuanza kumbembeleza,“Kwakweli mwanangu umeumia, hadi kukuona ukilia hivyo!! Kwa hakika umeumia, ila ni kweli hii kitu inaumiza, hivi huyu mzee Jimmy ni kwanini alikuwa na akili mbovu kiasi hiki jamani! Hapa ndio naanza kuwaelewa wale wa kusema kuwa tuwapime akili watu kabla ya kuzaa nao, jamani huyu mzee Jimmy kumbe alikuwa na akili mbovu kiasi hiki!! Nisamehe mwanangu kwa kitendo changu cha kuzaa na mtu mwenye akili mbovu kama mzee Jimmy”Kisha huyu bibi alipumua kidogo na kuendelea kuongea,“Unajua nini mwanangu?”“Niambie mama”“Kwa jinsi hali ilivyo, kwanza kabisa tuepuke aibu namba moja, twende tukampime Erica mimba ili tujue cha kufanya maana hii ndio itakuwa aibu kubwa kwetu”“Kwahiyo tukikuta ana mimba twende tukamtoe mama?”“Ndio, unadhani aibu hii tutaiepukaje?”“Mama, tatizo haliepukwi kwa kuongeza tatizo. Mama nadhani kuna mambo ambayo kijana wako niliyatenda mwanzo ila ulikuwa huyajui, mama nishafanya dhambi hizo za kupeleka wadada kwenda kutoa mimba na mara zote Mungu aliacha salama kwani nilirudi nao salama ila kitendo cha kumtoa mimba binti yangu inaweza kuwa ni adhabu kwangu huwezi jua maana binti yangu anaweza kupoteza damu nyingi sana na kupoteza maisha”“Kheee mwanangu, tunampeleka hospitali anatolewa kitaalamu”“Mama, kutoa mimba haina fomula. Unaweza shangaa mtu katolewa hospitali na kupoteza uhai vile vile ndiomana hiki ni kitendo hatarishi. Kuna mwenzetu amekufa sababu ya kutoa mimba, siwezi kukubali binti yangu atoe mimba”“Ila upo tayari kupambana na hiyo aibu ya mimba ya Erica?”Baba Angel aliinama kwanza maana hakuwa na jibu, kisha mama yake akasema tena,“Halafu mwanangu hilo swala la dokta Jimmy kwasasa niachie, naona huyo dokta hajielewi kama baba yako”Ndipo baba Angel alikumbuka na ule ujumbe ambao mkewe alitumiwa kwenye simu, basi aliamua kumueleza mama yake kuhusu kile alichosoma na jinsi alivyofanya kwa dokta Jimmy na mlinzi, hapo mama yake alipumua kidogo na kusema,“Erick, naomba nikuombe kitu mwanangu”“Kitu gani mama?”“Kwa leo, naomba ulale hapa mwanangu halafu kesho tutafikiria cha kufanya”Mama yake aliamua kumlazimisha kufanya vile, kwahiyo aliamua kukubaliana na mama yake na kulala hapo kwani kile chumba alichochukuwa mama yake kilikuwa ni kikubwa, na mama yake alikataa kuchukua chumba kingine kwahiyo alimlazimisha baba Angel alale kwenye kochi pale sebleni halafu yeye alienda kulala chumbani maana kilikuwa ni chumba kikubwa chenye sehemu mbili yani chumba na sebule.Mama Angel alilia pale na kulala pale pale alipokuwa, yani ni Ester tu ndio aliyemshtua na kulikuwa kumekucha tayari maana ilikuwa ni saa kumi na mbili alfajiri, basi aliamka, akamuona Ester kashika karatasi yenye maneno, basi mama Angel akaichukua na kuisoma akagundua ni ujumbe uliachwa na mume wake akimueleza kuwa ameenda hotelini kuonana na mama yake, basi hapo mama Angel ndio akaelewa ni kwanini hakumuona mume wake.Muda kidogo mlango wa mama Angel uligongwa na aliyeingia alikuwa ni Erica ambaye alimsalimia mama yake na kumwambia,“Mama, kuna wageni nje wanamuulizia baba”Mama Angel akashtuka kidogo na kuamua kutoka ili kwenda kuongea nao.Alifika hadi nje na kuwakuta pale, ambapo wale wageni walijitambulisha,“Sisi ni maafisa usalama, tumekuja kumchukua ndugu Erick ili kwenda nae kituone kwaajili ya mahojiano”Mama Angel akashtuka kwanza na kuwaambia kuwa mumewe hayupo, ila wale maafisa usalama hawakuamini ile kauli ya mama Angel basi wakamwambia,“Naomba uturuhusu tuingie ndani na kukagua nyumba yako”“Mmmmh hebu subiri kwanza”Mama Angel akamuomba Erica akamletee simu yake ambapo alipofika nayo tu aliwaambia wale maofisa,“Jamani kabla sijawaruhusu kufanya hivyo, kuna mtu naomba nimpigie kwanza simu”“Ujue unatuchelewesha mama, kama mumeo yupo mwambie aje hapa tuondoke nae au tuachie tukakague ili tujihakikishie kama kweli hayupo”“Nawaomba dakika tano tu niwasiliane na huyu mtu”Kisha mama Angel alipiga simu moja kwa moja kwa shemeji yake na kumueleza kama watu wa usalama wamefika pale wanamtafuta mumewe ambaye hayupo ila wanataka kukagua nyumba ili kujihakikishia kuwa hayupo kweli, basi shemeji yake alimwambia vitu vinavyotakiwa kabla ya nyumba kukaguliwa kisha mama Angel alivyokata simu aliwaambia wale maofisa wamuonyeshe hivyo vitu alivyoambiwa,“Hivi mama unautambuzi vizuri au hutambui?”“Natambua vizuri ndiomana kabla ya kukubali niliamua kumpigia mwanasheria simu ili nijue cha kufanya, maana mimi sheria siijui vizuri”“Unawezaje kuwakatalia polisi kukagua nyumba yako?”“Sijakataa ila naomba kuonyeshwa barua inayoruhusu nyie kukagua nyumba yangu”“Hivi hujui kama kuna vitu huwa ni vya dharula kama jambo hili? Tunahitaji kukagua nyumba ili kujiridhisha”“Nitaruhusu endapo na mimi nikijiridhisha kuhusu nyinyi”“Unawajua polisi vizuri wewe?”Mama Angel alikaa kimya, kisha wakasema tena,“Inaonyesha una kiburi sana wewe mwanamke, unawezaje kuwakatalia polisi kufanya kazi yao?”“Sijakataa ila nahitaji kibali ili niweze kujiridhisha, nimeambiwa mnionyeshe vitambulisho vyenu kwanza mmegoma kunionyesha, barua ya kuwaruhusu nyie kukagua nyumba yangu napo mmegoma, je mwenye matatizo hapo ni mimi au ni nyie?”“Aaaah sasa na wewe kesi yako inakuja”Yule mmoja akamuitwa mwenzie aliyekuwepo kwenye gari,“Afande Petro hebu lete pingu tumfunge huyu mama tumchukue kwa niaba ya mumewe”Muda huo huo mama Angel aliingia ndani na kumtaka mlinzi afunge geti halafu yeye alikimbilia ndani kwake na kumpigia tena simu shemeji yake,“Shemeji eti walitaka kunikamata mimi”“Wakukamate kwa kosa lipi?”“Sijui, nimewaambia wanionyeshe vitambulisho vyao wamegoma”“Mmmmh shemeji sio mapolisi hao, mnatakiwa kuwa makini sana. Watu wakija kwako na kujitambulisha kuwa ni watu wa usalama, wakupe vitambulisho vyao kwanza uvisome ili ujihakikishie kuwa ni wenyewe, vinginevyo hao sio itakuwa ni matapeli wa mjini tu”Mama Angel alihisi moyo kwenda mbio yani hadi kuanza kufatiliwa na matapeli wa mjini tena alihisi baridi kwenye mwili wake.Leo Junior alitaka kwenda kwenye msiba wa Linah ila mama yake sababu kamzuia kutoka ikawa ni ngumu sana kwake ingawa alitumiwa jumbe nyingi sana za kifo cha Linah,“Ila mama si vizuri kutokwenda kwenye msiba wake”“Mjinga wewe, bora useme unaenda sehemu nyingine ila sio kwenye msiba wa huyo mtu”Junior aliamua kujigelesha pale na kudai kutokwenda tena, ila kuna muda aliwaaga kuwa anaenda dukani kisha aliongoza moja kwa moja hadi nyumbani kwa Linah ambapo alikuta watu wamejaa kwenye ule msiba, basi alisogea karibu na mwanamama mmoja alimsogelea Junior na kumkumbatia huku akilia kwa kutaja shemeji shemeji na kufanya waliokuwepo pale kushangaa tu, kisha alipomaliza alianza kumueleza kwa kifupi,“Kwani imekuwaje?”“Sijui hata imekuwaje? Linaha hakuniambia ukweli mimi, mwisho wa siku nimekuja kupata taarifa tu kuwa amekufa, ila ngoja nikuibie siri maana hii tunajua wachache sana, inasemekana Linah alikuwa akitoa mimba”Junior alishtuka na kusema,“Inamaana alikuwa na mimba kweli?”“Ndio, ulidhani hawezi kushika mimba au? Ulipomuona ni mtu mzima ukahisi hawezi kuzaa tena! Linah alikupenda kweli na alitaka mfike mbali ndiomana aliamua kuzaa na wewe, sijui nini kimempata hadi kutoa mimba hiyo, au ile kasumba ya kusema umeoa Junior! Hivi umeoa kweli au?”Kuna mtu alisogea karibu yao na kumuuliza Junior,“Hivi wewe sio mtoto wa marehemu James kweli?”“Ndio ni mimi, naitwa Junior”“Kheee Junior kumbe ndio umekuwa mkubwa hivi jamani!!”Yule mtu alimkumbatia Junior na kumwambia,“Mimi ni babako mdogo, yani kumbe Linah alikuwa akikufahamu halafu wala hakutuambia”Ndipo yule rafiki wa Linah na Junior wakashtuka kisha rafiki wa Linah akauliza,“Kwani huyu ni nani yenu?”“Huyu ni mtoto wa kaka yangu James, yule marehemu yani ukimuangalia kwa mbali kama James vile, cheki alivyofanana nae jamani!”“Kwani Linah na huyo James ni nani na nani?”“Linah ni mtoto wa shangazi yetu, halafu Linah alipatana sana na James naona ndio sababu ya yeye kuwa karibu na mtoto wa James kuliko sisi ambao tulimuona huyu mtoto akiwa mdogo kabisa. Jamani Junior umekuwa sana, mama yako yuko wapi? Anajua kama kuna msiba wa wifi yake huku au hajui?”Junior alibaki kimya akijiuma uma tu maana hata yeye alikuwa anashangaa tu kusikia kuwa Linah alikuwa ni ndugu yake, kwahiyo alikuwa na mahusiano na shangazi yake, hapo hata yule rafiki wa Linah aliweza kuelewa ni kwanini Linah alichanganyikiwa hadi kufikia hatua ya kutoa ile mimba ambayo imechukua uhai wake”Junior alibaki kushangaa tu ila hakuwa na namna zaidi ya kuulizia ratiba ya mazishi maana msiba huu aliusikia muda hata akajua pengine wameshazika ila hadi siku hiyo wala hawakuwa wamezika, akamuuliza yule rafiki wa Linah kuwa mazishi ni lini,“Wanasema kuwa mazishi ni kesho, ndio tupo kusubiria hapa ili ratiba kamili ipatikane”“Aaaah sawa”Kisha yule baba alimshika mkono Junior ili kwenda kumtambulisha kwa ndugu wengine, kwakweli yule rafiki wa Linah alibaki kustaajabu tu,“Huyu hakuwa akimfahamu Junior ila nahisi alifahamu tu kuwa kaka yake alikuwa na mtoto wa kuitwa Junior, na alipomuona tu kamtambua kuwa kafanana na ndugu yake, iweje Linah alishindwa kutambua hili? Kwanini lakini? Uwiiii, rafiki yangu jamani”Alifikiria na kukosa jibu kisha akaamua kuendelea na mambo mengine tu.Baba Angel kule hotelini, alitaka kuondoka mapema sana ila mama yake alimzuia hadi wapate kifungua kinywa kwahiyo walishuka chini na kuagiza kifungua kinywa huku wakila na kuongea mambo mbalimbali, ila alifika yule mwanamke ambaye usiku wake baba Angel alikosea mlango, basi yule mwanamke alifika na kuwasalimia kisha aliomba kuongea kidogo na baba Angel ambapo mama yake aliwapisha na kukaa meza ya pili,“Inamaana Erick hujanitambua hata kidogo? Halafu mbona upo hivyo kama mtu aliyechanganyikiwa na maisha?”“Acha tu”“Tatizo ni nini?”“Hakuna tatizo”“Haya niambie hujanikumbuka tu!”“Kweli kabisa sikukumbuki”“Kuna kipindi ulikuwa Afrika Kusini, na ulikutana na mimi kwenye kasino, hapo tukazioeana na kupendana, tulianza mawasiliano na kuwa karibu. Tulipiga picha mbalimbali pamoja na uliahidi kunioa”Kisha yule mwanamke alitoa baadhi ya picha alizokuwa nazo kwenye mkoba, zilikuwa kama picha tatu na kumpa baba Angel ambapo alipoziangalia tu alielewa na kusema,“Khaaa kumbe Jack!”“Ndio ni mimi, hata nimeshangaa kunisahau Erick jamani utadhani tuligombana!”“Mbona umebadilika? Umenenepa sana kwasasa”“Ukubwa huu Erick, saivi nimekuwa mmama ila bado huwa nakukumbuka sana. Niliporudi hapa nchini kitu cha kwanza nilikumbuka kuweka hizi picha katika mkoba wangu maana huwa nakukumbuka sana nikiziangalia, Erick bado nakupenda sana”Baba Angel alitabasamu tu na kusema,“Aaaah acha hizo Jack, kila mtu ana familia yake kwasasa. Nina mke na watoto wa kutosha tu”“Ila unajua kama mimi na wewe tuna mtoto pia?”“Mmmmmh Jack!”“Ndio, kipindi kile ulipoondoka uliniacha na ujauzito Erick, sikutaka kukwambia tu kwani nilielewa kile kisirani chako cha kuwatoa wanawake mimba. Niliitunza ile mimba na sasa nina mtoto mkubwa kabisa ambaye ni mtoto wa mimi na wewe”“Mmmmh!!”“Usigune ila kubali tu siku umuone mtoto wako, nilikupenda kwa dhati. Niliitunza mimba na nikamtunza mtoto ingawa haukuwa pamoja nami, ila imani yangu ni kuwa dunia ni duara, nilijua ipo siku tu mimi na wewe tutakutana ndiomana sijaweza muzitupa hata hizi picha. Erick, mimi na wewe tuna mtoto mkubwa tu wa kiume”Baba Angel alizidi kustaajabu yani alikuwa haelewi kitu kwa muda huo, hapo kengele ya hatari ikalia kichwani mwake kuwa kilichotokea kwa Rahim na watoto wake basi kinaweza kutokea na kwake pia, ni kweli alifanya makosa ila ilikuwa kipindi cha ujana, basi alimuangalia huyu Jack na kumwambia,“Nimekuelewa, ila itakuwa vyema kama ukija kunitambulisha mwanangu ili nimtambulishe kwa ndugu zake aweze kufahamiana nao. Halafu naomba nitakulipa gharama zako, najua siwezi kukulipa kwa kiasi kikubwa ulichokifanya kwa mwanangu ila nitakupa hata hela ya kufutia machozi, naomba unitambulishe kwa huyo mwanangu tu.”“Sawa, hakuna tatizo nitakutambulisha ila ningependa kujua anuani ya unapoishi, namba yako ya simu ili tuendelee mawasiliano baina yetu”Baba Angel aliamua kumpa kadi yake ya mawasiliano, kwakweli muda huu baba Angel alikuwa haelewi kitu chochote aliona kama kuzidi kuchanganywa tu maana hata hakujua ni jinsi ataweza kumueleza mkewe kuhusu huyo mtoto ambaye hawakujua kama yupo, ila kama Jack alielewa vile na kumuuliza baba Angel,“Inaonyesha unamuogopa mke wako eeeh!!”“Aaaah hapana”“Erick utakuwa mwanaume gani wewe wa kumuogopa mkeo? Yani ushindwe kumtambulisha mwanao kwa uhuru sababu ya mkeo? Tena hata usimwambie ila hiyo siku iwe ni mshtukizo tu kwake”“Mmmmh nampenda sana mke wangu”“Huo ndio ujinga wa baadhi ya wanaume, muda wote kukazana nampenda sana mke wangu, mwishowe maji yanakufika shingoni unashindwa cha kufanya. Wanaume kama wewe ndio wale ambao mnasikiliza kila kitu toka kwa wake zenu, yani mkeo akikukataza kufanya kitu basi hufanyi, unakuwa sio mwanaume kwakweli, unatakiwa kusimama kiume kwenye kila eneo. Mkeo yupo chini yako, sio swala la kumsikiliza mwanamke muda wote”Baba Angel hakutaka kuendelea kuongea na huyu mwanamke maana huwa hapendi mtu akitoa tafsiri mbaya juu ya mke wake, kwahiyo aliamua kumuaga na moja kwa moja alimfata mama yake na kumuaga kisha aliondoka zake kuelekea nyumbani kwake.Baba Angel alirudi nyumbani kwake na kumkuta mkewe kajifungia tu chumbani, basi alimgongea na kufunguliwa kisha alipoingia alimuelezea jinsi mama yake alivyomueleza kuhusu watoto wao, kisha mkewe nae alimwambia kuhusu polisi feki waliofika hapo nyumbani kwao, kisha akamuuliza,“Hujapata taarifa yoyote kwani mume wangu?”“Hakuna taarifa yoyote niliyoipata zaidi ya kutumiwa ujumbe kuwa kesho ni mazishi ya Linah”“Kheee walikuwa hawajazika tu hadi leo?”“Ndio na wamesema kuwa nisikose”“Huu ndio ujinga nisioupenda, usikose kwani wewe ndio Mchungaji wa kuongoza sala kwenye huo msiba au kitu gani? Baba Angel, hakuna kwenda popote”“Mmmh na wewe mama Angel, unajua kuna vitu unakataza bila hata kufikiria. Ule ni msiba lazima tushiriki, huo ndio ujamii”“Hivi mambo yaliyokupata, unatakiwa kukaa chini na kutafakari sio kuanza kuhangaika baba Angel, naomba unisikilize kwa hili. Kama pole utaenda kuwapa, hapo ulipo hata hujui ni nani aliyekupa shutuma za kuua na hata hujui ni nani aliyekufa”“Ninachojua ni kuwa hakuna niliyemuua, na kama dokta Jimmy amekufa basi natamani niende kwenye msiba wake nikamkate kichwa. Kiukweli mama Angel sipo sawa mimi, acha tu nikashiriki mambo mengine ya kijamii ili niweze kuwaza vitu vipya”Mama Angel alishindwa hata namna ya kuendelea kumshawishi mumewe kuwa asiende huko kwenye mazishi ya Linah.Usiku wa leo, Junior alimueleza ukweli mama yake kuwa alienda kwenye msiba wa Linah na kumueleza kitu alichoenda kukutana nacho huko, mama Junior alishangaa sana kwani hakutegemea na ndugu yake mama Angel hakumueleza ukweli kuhusu undugu wa Linah na Junio basi alishangaa pale,“Ndio hivyo mama, yule bamdogo alienda kunufahamisha kwa ndugu wengine pale”“Duh!! Jamani, mbona sijui mambo haya”“Ndio hivyo mama”Ila ambacho Junior hakumwambia mama yake ni ile hali ya kusema kuwa Linah alikuwa akitoa mimba, maana aliona ni swala la aibu.Usiku huu mama Junior alijikuta akifikiria tu kuhusu swala hili, kulipokucha alijiandaa mapema kabisa na moja kwa moja kwenda nyumbani kwa mama Angel ambapo alipishana na baba Angel ndio alikuwa akitoka kwa muda huo, basi aliasalimiana nae na yeye kuingia ndani.Baba Angel alifika msibani na kukuta watu pale kama kawaida na wengine walikuwa wakiongezeka kwaajili ya mazishi ya Linah.Basi baba Angel aliitwa na Manka ambaye alimuuliza,“Mbona umekuja peke yako? Mke wako yuko wapi? Tuseme hakumfahamu Linah?”“Aaaah mimi nipo kumuwakilisha hata yeye pia”“Erick,angalia nyuma yako”Baba Angel aligeuka na kukutana uso kwa uso na watu wawili waliovalia sare za polisi, wakiwa wameshika pingu na kumsogelea kisha walimfunga zile pingu na kumwambia kuwa yupo chini ya ulinzi. Baba Angel aligeuka na kukutana uso kwa uso na watu wawili waliovalia sare za polisi, wakiwa wameshika pingu na kumsogelea kisha walimfunga zile pingu na kumwambia kuwa yupo chini ya ulinzi.Baba Angel alishangaa sana, ila Manka alimuangalia na kuanza kucheka kisha alimuuliza kwa kejeli,“Kwani umefanya nini Erick?”“Hata mimi sijui”Basi baba Angel aliwauliza wale maaskari,“Kwani nimefanya nini?”“Inamaana hujui kama umeua?”“Nimemuua nani sasa?”“Utajua huko huko mbele ya safari”Basi Manka alicheka tena na kumuuliza baba Angel,“Na utanashati wako huo kumbe muuwaji eeeh! Hebu niambie uliuaje Erick”Kwakweli baba Angel alikuwa akishangaa tu, jinsi alivyokamwatwa na jinsi wale maaskari walivyoacha apewe maneno na Manka, ambapo Manka aliendelea kuongea,“Erick, sikia nikwambie. Unaijua kesi ya mauwaji vizuri? Yani ukiwa na kesi ya mauwaji basi ujue, kifungo chake ni maisha yako yote. Sasa kaa huko gerezani halafu uone huyo mwanamke unayejifanya unampenda sana kama hatoolewa na mwanaume mwingine”Manka alicheka tena na kusema,“Yani nakwambia utakuwa na maumivu sijui aina ngapi katika maisha yako, mapacha wako wamepeana mimba, kumbuka ni damu yako ile eeeh!! Mkeo alikuwa akimcheka Sarah wangu na kuniona sijui kulea, haya kiko wapi sasa kwa yeye anayejua kulea? Mbona watoto aliowaaa mwenyewe wameweza kupeana mimba? Tena watoto mapacha, ni aibu kubwa sana sijui suira zenu mtaziweka wapi kwenye jamii, lakini hakuna shida maana sura yako utaiweka gerezani. Haya maumivu ya kusalitiwa na baba yako mzazi, maumivu ya kufanya hasira na kuua, maumivu ya mkeo kuolewa na mwanaume mwingine. Halafu unajua mkeo ataolewa na nani? Hahaha ataolewa na dokta Jimmy”Hapo baba Angel alishikwa na hasira zaidi na kutamani kumpiga Manka ingawa kafungwa pingu kwani alijikuta akimkata mtama na kumfanya Manka aanguke chini, basi wale maaskari wakamshikilia vilivyo baba Angel, halafu Manka akamwambi,“Umechukia eeeh!! Ulihisi umemuua dokta Jimmy, kwa taarifa yako umemuua yule mlinzi wenu asiyekuwa na hatia, na subiria kifungo chako cha maisha halafu mkeo ataolewa na dokta Jimmy, nitakuletea picha za harusi yao huko huko gerezani utakapokuwa. Mjinga wewe, upo chini ya sheria halafu unanipiga, acha niongee yote ya moyoni. Naomba nikwambie kwamba, sikupendi Erick na sijawahi kukupenda mjinga wewe, muda wote kujifanya unampenda sana Erica, tuone kama ataenda na wewe gerezani”Halafu Manka alimsogelea tena baba Angel pale alipokuwa ameshikiliwa na wale maaskari halafu akamnasa baba Angel vibao kadhaa na kusema,“Vingine nitakuja kukumalizia unapopelekwa rumande, mjinga wewe. Hebu mtoeni hapa asijekuharibu mambo ya msiba bure. Nina machungu ila kukamatwa kwako, kwangu ni furaha sana. Mpelekeni huko mjinga huyu, nilikuwa nakuhimiza kuja ili ukamatwe na tumefanikisha hili oooh asante Mungu”Wale maaskari walimshika baba Angel na kumburuza hadi kwenye gari ambalo walienda nalo pale na kumpakia kisha kuondoka nae katika eneo lile.Mama Junior alikaa na mdogo wake huku wakizungumza mambo mbalimbali ambapo mama Angel alimueleza vile ambavyo aliambiwa na Dora kuhusu undugu wa Linah na James, na hapo alimuuliza dada yake juu ya swali ambalo Dora alimuuliza,“Eeeeh dada ni kwanini mlikuwa hamuwatembelei ndugu zake James na wala ndugu zake kuja pale kwako kwanini?”“Mmmmh mdogo wangu sijui nikwambiaje”“Niambie tu dada”“Ni hivi, kiukweli mimi zamani sijui nilikuwaje, nilikuwa na kinyaa sana kiasi kwamba ndugu wa James wengi walikuwa hawanipendi, halafu mume wangu alifanya mimi nijione ni bora kuliko mwanamke yoyote duniani, wanawake wengi wanaolewa wakiwa hawana bikra ila mimi nilikuwa mwanamke bikra na tena sikuwa na mahusiano na mwanaume yoyote kabla ya James. Mume wangu alikuwa akinipenda sana, nikisema hiki sitaki basi alikitoa kwangu. Mimi si kwamba nilikuwa sipendi wageni ila walikuwa wakiniona mimi wanadhani najivuna sana, ila ni sababu ya malezi tu ambayo nililelewa, nakumbuka kuna kipindi kulikuwa na msiba kwakina James, tulienda msibani ila huwezi amini pale kwakina James sikunywa hata maji yani sijui nilikuwa naonaje, nikiwa na njaa namwambia James twende hotelini tukale, alinitambua nilivyo kwahiyo alikuwa hakatai, kuanzia asubuhi hadi usiku tunakula cha hotelini kwahiyo kwenye msiba nilikuwepo tu, halafu kitu kingine mimi nilikuwa mvivu sana kiasi kwamba pale msibani hakuna kazi niliyokuwa naifanya na hata kulala ilibidi mimi na watoto wengine wa ndugu zao tukalale chumbani, sikuweza kulala kwenye majumuiko. Kumbe kile kitu kiliwakera sana ndugu wa James, na hapo walimwambia James mimi ni marufuku kukanyaga kwao na wala wao hawatakuja kukanyaga kwa James. Haikuwa tatizo sana kwangu kwani sikufikiria kama kwao nitaenda tena, na kweli sijaenda hadi tulivyoachana na James. Ila kitendo cha mimi kukaa nyumbani kimenifanya niwe nibadilike, nianze kuishi vyema na jamii inayonizunguka, niache kinyaa na majivuno, kwasasa uliza wifi yangu yoyote kwa Deo kama kuna mmoja atakwambia kuwa mimi najivuna! Na wote huwa wanakuja kwangu na mimi naenda kwao, kwakweli nilichokuwa nafanya ni kibaya sana”“Ndiomana kwasasa ukaweza kuzoa watoto wote wa mumeo na kulea mwenyewe!”“Ndio, ninawalea sitaki tena kuwa kama vile nilivyokuwa. Sio tabia njema kabisa, mama alikuwa mkali ila sijui kwanini mimi nilikuwa mvivu jamani loh!”Basi mama Angel akamshauri dada yake kuwa wapange siku waende kwenye familia ya James ukizingatia familia hii dada yake hajaonana nayo toka kipindi hiko cha nyuma. Ni wachache sana waliomuona Junior wakati mdogo ndiomana wengi hawakumjua kama ni mtoto wa James.Muda kidogo mama Junior alipigiwa simu kuwa aende mahali, basi akaongea na mdogo wake pale,“Erick si anipeleke na gari tu huko ninapoenda?”Ikabidi mama Angel amuite Erick ila hapo ndio akagundua kuwa Erick hakuwepo na ilisemeka na kuwa alitoka mapema kabisa kabla hata baba yake hajatoka,“Kheee kaenda wapi? Mbona hajaniaga?”“Hakuna aliyemuaga huku ndani mama, ila wote tumeshangaa tu hayupo”“Khaaaa jamani, mambo gani haya sasa?”Mama Angel hakuelewa, kwahiyo kwa muda huo alijikuta akianza kufikiria kuwa mwanae yuko wapi, ikabidi tu mama Junior aondoke mwenyewe maana aliona tayari mdogo wake kashaanza mambo mengine ya kumtafuta Erick.Yani mama Angel kwa muda huo alijaribu hata kuwapigia simu watu wa karibu na Erick ili ajue kama wapo pamoja nae ila wote hawakujua Erick alipo.Erick siku hii aliondoka kwao mapema sana, kumbe alikuwa akisubiri baba yake atoke na alianza kumfatilia, na alifika nae hadi kule kwenye msiba kisha baba yake alivyochukuliwa na wale maaskari naye Erick alikuwa nyuma yao akiwafatilia ila yeye alikuwa na pikipiki maana ndio aliyotoka nayo nyumbani kwao.Alimfatilia baba yake ila alichoshangaa Erick ni kuwa baba yake hakupelekwa kwenye kituo cha polisi ila moja kwa moja baba yake alipelekwa kwenye ile nyumba ya babu yake. Ndipo hapo akili ya haraka ikamcheza Erick na kumfanya kuweka pikipiki pembeni kisha kuanza kusogea pale karibu na kwa babu yake.Alipofika pale, alichungulia na kumkuta dokta Jimmy kasimama pembeni halafu kuna mtu amelazwa chini huku baba Angel akiamriwa amkabe yule mtu aliyelazwa chini, baba Angel aliambiwa,“Unachotakiwa kufanya kwasasa ni kumkaba huyo mtu kama ulivyonikaba mimi”“Mbona siwaelewi!”“Usiwe mbishi”Baba Angel alishtukia akipewa ngumi ya mgongo na kupiga magoti mbele ya yule mtu, kisha yule aliyevalia nguo za kiaskari mmoja wapo alimfungua baba Angel zile pingu ili aweze kumkaba yule mtu.Erick hakuelewa ni kwanini wanafanya vile ila muda ule ule Erick alisogea kati yao na kufyatua risasi juu na kusema,“Wote mikono juu”Kilikuwa ni kitendo cha haraka na hakuna alieyekitarajia kwa muda ule, waliacha kila kitu na kupandisha mikono juu, hakuna aliyeweza kuelewa kwa haraka kuwa Erick ametoa wapi ile risasi, kisha Erick alimuamuru baba yake atoke nje ya pale, ila mtu mmoja pale aliamua kujitoa muhanga na kumshika baba Angel, yani yule mtu alishtukia akipigwa teke la maana sana na Erick hadi aliangukia pembeni kisha Erick alimfata nyuma baba yake hadi kwenye bodaboda yake na kupanda naye kisha kuondoka kwenye eneo lile.Kwakweli ilikuwa ni jambo la haraka sana kiasi kwamba hakuna hata mmoja aliyeelewa kuwa kuna kitu kama kile kinaweza kutendeka pale, ukizingatia baba Angel sio mtu wa mapigano wala sio mtu wa kutunza silaha ndani ya nyumba yake.Kila mmoja alishangaa kuwa ile risasi yule Erick mdogo kaitoa wapi, na lile teke alilompiga nalo yule mtu kajifunzia wapi? Kila mmoja pale alibaki kustaajabu kwa kile kilichofanywa na Erick mahali pale.Baba Angel alimuomba Erick wapiti kwenye hoteli ya karibu kwanza kwani alitaka kupiga simu nyumbani kwake kwanza kwa usalama wa familia yake, kwahiyo walifanya hivyo na kukodi chumba pale, kitu cha kwanza baba Angel alimpigia mke wake kuwa asiwe na wasiwasi naye wala Erick halafu alimpigia simu mlinzi wao ili asimkaribishe yoyote hapo nyumbani kwake. Kingine aliona vyema amtafute shemeji yake na kumwambia kwa kifupi tu ili shemeji yake ajue jinsi gani ataisaidia familia yake sababu mambo mengi ya sheria anayafahamu.Baba Angel alitulia kwa muda kimya huku akitafakari, aliinua kichwa na kumuangalia Erick ambaye bado inaonyesha akiwa na hasira hadi mishipa ya fahamu ikiwa imemsimama, kisha baba Angel alimwambia mwanae,“Asante kwa kuniokoa mwanangu, asante sana sijui hata wale watu walitaka nini na ili iwe ini sielewi mpaka muda huu nahisi tu kutetemeka mwili mzima”“Pole sana baba”“Ila ulijuaje mwanangu kuwa kuna matatizo hadi ukaja kunisaidia?”“Mimi sikujua kitu, ila kuna muda jana usiku alikuja Erica chumbani kwangu akasema alikuwa akipita karibu na chumba chenu akakusikia wewe na mama mkiongea kuhusu kwenda mahali ambapo mama alikuwa akikukataza kwenda ila wewe ulikuwa ukikazana kuwa utaenda tu, ila badae Erica aliniambia anapata hisia mbaya sana juu ya sehemu unayotaka kwenda, anaona wazi si salama. Mara nyingi huwa napenda kuyaamini mawazo ya Erica ila nilijipanga bila yeye kujua, nilitaka kujua ni kitu gani kitaendelea kwako. Huwezi amini, mimi nimetoka asubuhi kabla hujatoka wewe, nilienda kufata ile pikipiki gereji ila nilikuta bado haijatengemaa vizuri basi nikakodi nyingine, nilikukuja karibu na nyumbani nikikuvizia utoke nianze kukufatilia, nilijua nikikwambia twende pamoja ungekataa”Baba Angel alipumua kidogo na kumuuliza,“Na hiyo bastola umeitoa wapi?”“Kwanza, hii bastola sikujua hata kama ina risasi. Siku tumeenda kwa babu, kuna chumba mimi nilienda kuvaa nguo na ndipo nilipoiona hii bastola nikaificha hata Erica sikumwambia, na nilimwambia Erica twende ufukweni ili nikapunguze mawazo ila tulivyofika kule, kuna muda Erica alienda kujisaidia basi kuna mahali nilichimba na kuificha kule kule, sema kule watu huwa hawaendi mara kwa mara. Leo nilivyochukua ile pikipiki, kitu cha kwanza ni kwenda hadi ufukweni kufata bastola na kurudi kukuvizia wewe”“Sasa bastola ulichukua ya nini?”“Sijui ila nilikuwa nasema endapo kukitokea dharula”“Duh!! Unajua umeniokoa mwanangu, ila mengi nimeshangaa ujasiri huo na nguvu hizo umezitoa wapi?”“Sijui, labda sababu napenda sana kuangalia muvi za kivita”Baba Angel alimuangalia mwanae bila hata ya kummaliza maana ni mambo mengi sana alijikuta akijiuliza juu ya mwanae, kiukweli alimchanganya sana yani kuna vitu alikuwa havielewi kabisa ingawa ile kuokolewa na mwanae ilikuwa ni njema.Mama Junior akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake maana alishatoka kule alikokuwa akienda, akakutana na mama Daima na kusalimiana nae pale, basi alimuaga na kutaka kuondoka ila mama Daima alimshika mkono na kumwambia,“Ila unajua wewe ni mwanamke mwenzangu hata kama huna mtoto wa kike ila ulitakiwa kuwa na huruma kwa mtoto wa mwanamke mwenzio”“Kwani nimefanyeje?”“Kumbe nia yenu ilikuwa ni kumfanya Junior amuoe yule msichana wa kazi wa ndugu yako, uliona Junior akimuoa Daima basi Daima atafaidi sana au kitu gani?”“Jamani, yametokea wapi hayo?”“Nakuuliza mama mwenzangu, yani mmemlazimisha Junior aoe ili kunikomesha mimi au kumkomesha huyo Daima? Kumbuka ulichofanya kwa mwanangu kitafatilia hata wajukuu zako.”“kheeee usione nimenyamaza ukadhani napenda, kwani una matatizo gani wewe! Huyo Daima hajakwambia ukweli kuwa alimsingizia shemeji yangu anataka kumbaka hadi aksababisha watu wengi kujaa na kutaka kumpiga shemeji! Hajakwambia huyo Daima wako?”“haya tuachane na hayo, hivi unajua kuwa Daima ni mjamzito tena?”“Mmmh!!”“Guna tu ila Daima ana mimba nyingine ya Junior”Mama Junior alisikitika kwanza ka kusema,“Hivi watoto wa kike ni nani aliyewaroga jamani hata awahurumie kidogo, huyo Daima hajui kama Junior ni mume wa mtu kwasasa? Mbona kujitafutia tu matatizo jamani, mambo mengine yanasononesha na kusikitisha. Hiyo habari umeichukuliaje mama yake?”“Aaaarggh!!”Mama Daima hata hakuongea zaidi kwani muda huo huo aliondoka zake na mama Junior kwenda nyumbani kwake kwanza.Baba Angel na mwanae Erick walifika nyumbani kwao wakati tayari usiku umeshaingia, basi waliingia ndani na kusalimia wale waliopo nyumbani kwao. Muda huo huo simu ya baba Angel ilianza kuita maana alikuwa nayo mfukoni tu, basi akaichukua na kupokea na kukuta mpigaji ni Sia, basi alianza kuongea nae,“Kuna muda Fulani nilifika nyumbani kwako, nikaona kuna vijana kama watatu halafu kila mmoja alikuwa na pikipiki na walikaa nje ya nyumba yako kamavile kuna kitu walikuwa wanavizia”“Mmmh!!”“Sikuondoka hadi walipoondoka, walikaa pale nje kama masaa mawili hivi sijui ni kitu gani walikuwa wakivizia hapo nyumbani kwako”“Sijui, hivi hujaenda kwenye msiba wa Linah yule ndugu wa Manka?”“Aaaaah ule msiba nilienda mara moja tu, nilipoona haueleweki sikwenda tena kwenye ule msiba, yani pale katika msiba kuna watu wana mipango isiyoeleweka mwanzo wala mwisho. Nasikia jana wamezika”“Kakwambia Manka?”“Ndio, tena kanipigia simu huku akicheka kuwa wameshazika hata sikumuelewa mtu umefiwa halafu unacheka. Ule msiba sijauelewa kabisa, ila Erick kuna kitu nataka nikwambie”“Kitu gani?”“Kuwa makini sana na yule mwanamke, sio mtu mzuri kwako. Kuna siku nilimkuta na mtu huyo, yani mipango waliyokuwa wakipanga nikikwambia unaweza kupatwa na kichaa, nitakutafuta ili tuongee vizuri zaidi”Kisha Sia alikata simu halafu baba Angel aliinuka moja kwa moja na kwenda chumbani kwake.Baba Angel alimsimulia mke wake kuanzia mwanzo wa tukio hadi mwisho, na kumfanya mama Angel ashangae sana na kuogopa,“Lakini nilikukataza mume wangu?”“Nakumbuka, majuto ni mjukuu. Sijui ingekuwaje kwasasa na sijui walitaka nini”“Nadhani walitaka kupata ushahidi ili uhukumiwe na mahakama moja kwa moja, hawakutaka kukuhukumu wao ila walitaka uhukumiwe na mahakama”“Simpendi yule dokta Jimmy simpendi kabisa, ila simpendi zaidi Manka, ni mwanamke mbaya sana. Kanifanyia kitu kibaya ambacho sikukitegemea”“Pole mume wangu, huwa tunamsema Erica kwa umbea kumbe kuna mahali umbea wake utatusaidia”“Ila mke wangu swala la watoto wetu kuwa pamoja kimapenzi umefikia nalo wapi?”“Baba Angel naomba hayo maswala tusizungumze kabisa maana nahisi kupatwa na uchizi jamani, nawapenda sana watoto wangu ila kila nikifikiria hayo nahisi kuchanganyikiwa. Ila mume wangu, tufanye swala moja unajua wakija kutukamata na bastola humu ndani itakuwa balaa sana!!”“Naelewa, ila Erick sio mjinga kiasi cha kukaa na bastola humu ndani”“Sasa ataiweka wapi? Yani hiyo ni kesi nyingine, hatuna kibali cha kumiliki hiyo kitu, ila duh Erick kajifunzia wapi hayo? Hadi naogopa yani nahisi kusisimka mwili mzima”Waliongea siku hii yani waliongea sana, walijikuta wakiongea hadi panakucha maana ilikuwa ni siku ya ajabu sana kwao.Sia, leo aliamua kwenda tena kwa mama yake Steve maana siku ile yule mama alipishana na Sia kwahiyo alitoka muda ule ule ambao Sia aliingia.Leo alimkuta na kuanza kuongea nae,“Kwanza mama naomba mnisamehe sana, kipindi cha nyuma nilikuwa kama nimepumbazwa”“Eeeeh kilichokuleta?”“Ni hivi mama, ni kweli mtoto yule niliyekuwa namlea hakuwa mtoto wa Steve”“Nilijua tu, ulizaa na mwanaume mwingine halafu kuja kumdanganya mwanangu”“Sio hivyo mama, ni kwamba yule mtoto hakuwa wa Steve wala hakuwa mtoto wangu ila yule wa mwanzo uchangani niliyempa jina Steve ndio alikuwa mtoto wetu kweli”“Sikuelewi”“Ni hivi mama, yani mimi nilimlea mtoto vizuri kabisa, ila siku nampeleka kliniki wakaniambia kuwa mtoto amepotea, basi nilipewa mtoto mwingine nimlee, sikutaka kurudi bila mtoto ndio nikamkubali yule na kuanza kumlea”“Hivi unadhani hayo maelezo yako kuna mtu yanaweza kumuingia katika akili yake? Haya ikawaje sasa?”“Mtoto wangu nimejua alipo kwasasa”“Yuko wapi?”“Mtoto wangu ni yule Paulo anayeishi na Steve na yule mke wake”“Hivi una akili timamu wewe? Yule ni mtoto ambaye Steve alizaa na yule mwanamke ila alituficha tu”“Mama, naomba nisiongee sana. Ila siku muulize yule Oliva ukweli kuhusu yule mtoto halafu atakujibu na ndio hapo utagundua kuwa yule ni mtoto niliyezaa na Steve, si unamuona anavyofanana na Steve?”“Yani nilifikiri umepona kichaa kumbe kila kukicha ndio kinazaliwa upya, pole sana. Umeanza hadi kudai watoto wa wenzio, bila shaka utaanza kudai na wazazi wa wenzio maana unapoelekea sio penyewe. Pole sana binbti, wewe sio wa kufokewa ni wa kuonewa huruma tu”“Sitaongea sana ila nitaongea kwa vitendo nanyi mtanielewa, maana yule ni mtoto wangu kabisa”Sia aliona huyu mama hamsikilizi kabisa kwahiyo aliamua tu kuondoka kwa muda ule, alikuwa akitembea huku akiwaza cha kufanya.Aliwaza vitu vingi sana, alitamani cha kwanza kabisa ampate mtoto wa madam Oliva kwani alihisi kuwa akimpata mtoto wa madam Oliva itakuwa rahisi kwa yeye kuaminika na maneno yake, akajiuliza,“Je mtoto wa madam Oliva ni Sarah? Mmmmh nahisi Sarah ni mtoto wa madam Oliva, ila yule Sarah si anasoma shule anayofundisha madam Oliva, inamaana yule madam hajamgundua kuwa yule ni mtoto wake? Mmmh”Alivyokuwa akitembea kuelekea stendi, akakutana na Manka akiwa kaongozana na Sarah ilibidi asalimiane nao ambapo Manka alimchukua pembeni Sia na kuanza kuongea nae,“Mtoto ananisumbua huyu balaa, yani anachong’ang’ania yeye ni kwenda kuishi nyumbani kwa Erick na Erica, sijui nifanyeje na huyu mtoto unajua nashindwa kukubali ukweli kuwa huyu mtoto sio wangu!!”“Ndio sio wako huyo, huyo ni mtoto wa Oliva”“Haiwezekani, Oliva ni adui yangu, sidhani kama ningelea mtoto wake. Unajua nashindwa kukubali kabisa, kwanza sifikirii swala kuwa mzee Jimmy aliweza kunibadilishia mimi mtoto”“Ila dokta Jimmy si amekuthibitishia hilo? Hata nashangaa unazidi kujitia uchizi, mimi ni chizi ndio ila mwenzangu uchizi wako umezidi. Huyo unayeona rafiki yako wa damu kakuthibitishia kabisa kuwa mtoto umebadilishiwa”“Una uhakika gani?”“Kilichokupeleka kwenye kaburi la mzee Jimmy na kukufanya ulie kwa uchungu ni kitu gani? Si baada ya kugundua kuwa ni kweli umebadilishiwa mtoto? Ila kwasasa unajifanya hukubali wala kuamini ukweli, ipo siku huyo mzee Jimmy atatamka pale pale kaburini kuwa alikubadilishia mtoto ndio akili itakukaa sawa”Manka alikaa kimya kwa muda kidogo na kumtazama Sia, kisha alimwambia,“Unajua kilichotokea jana?”“Kipi hiko?”“Kwasasa, Erick yupo rumande maana anatuhumiwa kumuua mlinzi wa nyumba ya baba yake”“Kakamatwa lini?”“Jana”“Pole sana, nimeongea usiku na Erick ni mzima wa afya njema. Aliyekwambia Erick amekamatwa nani? Na hiyo ndio habari ya kukufurahisha?”Manka alijaribu kumuelezea kwa ufupi Sia kuhusu kilichotokea siku ya jana, na jinsi alivyoongea na dokta Jimmy ambaye alimuhakikishia kuwa baba Angel yupo rumande, basi Sia alimuangalia Manka na kumwambia,“Pole sana, hao ndio unaamini wanakupenda na kusaidiana nao. Hata una msiba wa dada yako ila unacheka kwaajili ya Erick, hao wamekudanganya, waambie wakwambie ukweli, ningekuwa ni wewe ningeachana na mambo ya dokta Jimmy na ningeenda kumueleza kila kitu Erick kuhusu mipango ya dokta Jimmy, pengine tukakomboka wote. Yani wewe huyo mtu kakufanyia ufedhuli ila bado unashirikiana nae, aaaah bora Mungu akunyime mali lakini sio akili”“Kheee leo hii wewe umekuwa na akili kunizidi mimi wakati kila mtu anakuona ni chizi namba moja”“Mimi chizi ndio, nimemuona mwanao anaondoka na wala sijakwambia”Manka akaangalia sehemu aliyomuacha Sarah ni kweli hakumuona Sarah kwenye eneo hilo, katika vitu ambavyo vilijua kumchanganya Manka vizuri ni kitendo cha mtoto wake Sarah kupotea, basi hapo alihisi hata akili yake kumruka kabisa na muda huo huo kuondoka hapo na kuanza kumuangalia Sarah ili aone mahali ambapo Sarah ameelekea.Sia aliondoka ila hata yeye alishangaa jinsi alivyojiamini siku hii na jinsi alivyoweza kumjibu Manka ambaye siku zote alikuwa akimuogopa sana, ila leo aliona kajitoa ufahamu kabisa maana alimjibu bila kujali lolote.Moja kwa moja, Sia alirudi nyumbani kwake ila alipokuwa akikaribia nyumbani kwake alimuona madam Oliva akiwa kwenye gari yake, alipoangalia vizuri aliona madam Oliva kama amepanda na Sarah kwenye lile gari, Sia akapumua kidogo na kusema,“Inamaana Oliva kampata mwanae sasa! Sijui ni mwanae kweli au la mmmh!!”Aliangalia gari la madam Oliva hadi lilipoishia kisha yeye akaenda kuingia nyumbani kwake na kuanza shughuli zake huku akifikiria kama ni kweli madam Oliva ni mama mzazi wa Sarah.Usiku wa siku hii, baba Angel na mama Angel walikuwa wakipanga mambo mbalimbali chumbani kwao maana kwa siku hii hakuna mtu ambaye alitoka nje ya nyumba yao ukizingatia kwa yale ambayo yalikwisha kutokea kwao, kwahiyo waliamua kuwa makini sana.“Kwahiyo mke wangu tutakaa nyumbani hadi lini?”“Hapana, ila tulikuwa tukiangalia upepo, sema kingine ni kutoa taarifa polisi ili iwe rahisi kwetu”“Kweli kabisa, kesho nitaenda basi ofisini kwa shemeji yangu najua hata siku ile kuna kitu alifanya ila yule inabidi awe anakumbushwa kwa mambo mengi”“Sawa, ila cha kwanza ni kutoa taarifa polisi ili iwe rahisi”Walipanga mipango mingi sana kwa siku hii pia.Kwa hizi siku baba Angel hakutaka kujishughulisha na mambo mengine na kulikuwa na ulinzi mkali nyumbani kwake kwani tayari alishatoa taarifa kuhusu watu wanaomfatilia, na aliweza kugundua ukweli kuwa hajafanya kosa lolote la kuua ila wale watu walihitaji kumtafutia ushahidi, hakuna aliposema kuwa Erick ndio amemuokoa zaidi ya kumwambia mke wake tu maana alijua lazima itaanza kupelelezwa kuwa Erick alitoa wapi ile silaha aliyokuwa nayo.Angel alilalamika kuwa anaumwa sana na hata hakuwa na hali nzuri kabisa, ikabidi mama Angel amchukue na kwenda nae hospitali.Walipofika, moja kwa moja alichukuliwa vipimo ila majibu yale yalimfanya mama Angel ahisi hata kuzimia maana aliambiwa kuwa Angel ni mjamzito. Walipofika, moja kwa moja alichukuliwa vipimo ila majibu yale yalimfanya mama Angel ahisi hata kuzimia maana aliambiwa kuwa Angel ni mjamzito.Mama Angel alimuuliza daktari kwa hamaki,“Una uhakika kuwa mwanangu ni mjamzito?”“Ndio, mtoto ni mjamzito huyu”Mama Angel alimuangalia Angel na kumuuliza,“Unajijua kama wewe ni mjamzito?”Angel alikaa kimya tu kiasi cha kumfanya mama yake achukie zaidi ila daktari pale alijaribu kumpa ushauri kidogo, sema mama Angel hakuelewa kitu kwakweli na alikuwa hakubaliani na ile hali iliyotokea.Basi akainuka na Angel kuelekea nae nyumbani huku akiwa kimya tu, moja kwa moja alimshika Angel mkono hadi chumbani kwake kisha akamkalisha na kuanza kuongea nae,“Kwahiyo Angel, hiyo mimba ni ya nani? Ya Samir?”Angel aliitikia kwa kichwa tu na kumfanya mama yake azidi kupatwa na hasira, akainuka na kumzabua kofi kisha akamwambia,“Mtoto mjinga sana wewe, nimekutambulisha baba yako, nimekwambia wazi kuwa huyo Samir ni ndugu yako ila ukaja kunidhalilisha kwa kulala na huyo Samir kwenye nyumba yangu halafu umepewa na mimba na huyo Samir ambaye ni kaka yako. Mbona Angel umekuwa mjinga kiasi hiko wewe!!”Angel alikuwa kimya tu huku ameinama, mama Angel akaendelea kuongea kwa hasira,“Jamani sijawahi kuwa na akili mbovu kama za kwako, kupata mwanaume na kumleta nyumbani kwetu tena chumbani kwangu halafu kulala nae humo!! Sijawahi kufanya huo ujinga, umetoa wapi hiyo akili wewe?”Mama Angel alichukua simu na kumpigia mume wake,“Baba Angel, asubuhi si niliondoka kumpeleka Angel hospitali sababu ya kujihisi vibaya, sasa majibu ni kuwa ana mimba”“Ana mimba!!”“Ndio, tena mimba ya huyo huyo mwendawazimu mwenzie Samir. Ongea na Rahim maana mimi hata sijui cha kufanya muda huu”Mama Angel alikata simu na kumuangalia tena binti yake kisha alikaa na kuongea nae kwanza,“Nadhani umefanya mambo sababu hujui historia halisi ya mama yako, hujui ni kwanini mimi nimekuwa na hasira sana ya wewe kukimbilia mapenzi. Binti yangu Angel wewe ni mzuri sana tena sana ila uzuri wako huo utaenda kuharibiwa na hiyo mimba uliyoibeba, baada ya hapo utasikia kwenye mabomba kuhusu swala la kuolewa maana hata huyo Samir hatoweza kukuoa. Licha ya kuwa ni ndugu yako ila ni hulka ya wanaume kuwapa wanawake mimba na kukimbia majukumu. Utalia na hiyo mimba, utakumbuka maneno yangu siku zote ya kukukanya wewe. Usifikirie Junior alipanga kumuoa Vaileth ila ni mimi ndio nilishikilia bango ili Junior amuoe Vaileth, nilimuhurumia sana maana soko lake la ndoa ndio lilizidi kushuka zaidi, sasa wewe mwanangu utafanyaje? Mbona umeenda kujitafutia mkosi na laana tu mwanangu jamani!”“Nisamehe mama”“Saizi ndio unakumbuka neno nisamehe ila najua hiyo nisamehe utaiomba maradufu zaidi ya hapa, ngoja nikwambie kwa kifupi tu. Baba yako mzazi huyo Rahim alijifanya kunipenda sana, hakuna mwanamke kama mimi duniani, alifanya nijione wa pekee alinipa chochote nitakacho, nikajitoa kwake kwa kila hali, nikapata mimba yake, ila bado hakuacha kunihudumia ila hakutaka kunitambulisha kwao wala hakutaka kuniona tena, hadi nimejifungua bado hakutaka kuniona, hapo ndio alianza kunifanyia kejeli na karaha akiwa huko huko mbali, yani hataki kuniona na bado ananipa maneno ya kashfa, nilinihisi vibaya, aligoma kuja kujionyesha kwetu na kufikia hatua ya mimi kutukanwa kuwa simjui baba wa mtoto. Nilihudhunika sana, sikuwa na raha nilikuwa nalia kila siku. Alisitisha huduma, kuwa na mimba hutoona tabu sana, balaa huanza zaidi ukijifungua ingawa wengine balaa huanza toka wakiwa na mimba. Sasa malezi ya mtoto mwenyewe utaona nanga inapaa, maisha yetu sisi yalikuwa ya kawaida tu, vingi tulikuwa tukimtegemea mama yetu, yani mamako mkubwa mama Junior ndio alikuwa akinipa msaada sana na mumewe maana kipindi hiko walikuwa na pesa ila kiukweli kwa upande wangu maisha yalikuwa magumu sana. Kipindi kibaya ni pale dada zangu waliponishauri niombe hela ya mtaji nami nikamuomba kweli Rahim, alinipa jibu hilo ambalo liliumiza sana moyo wangu, ni bora angesema sina hiyo pesa kuliko jibu alilonipa. Mwanangu, mapenzi ni matamu sana mkiwa mnaruka ruka hivyo ila ukianza kulea mtoto ndipo utakapoona uchungu wa mapenzi. Tena usiombe ukimbiwe ukiwa na mimba hivyo, na swala la wewe kukimbiwa lipo wazi ukizingatia Samir ni ndugu yako, nakuhurumia sana mwanangu. Ulidhani unatukomesha ila umejikomesha mwenyewe, maana ni wewe ndio utapigwa na maisha na utapambana mwenyewe na maisha yako, utajijua mwenyewe cha kumueleza mtoto wako kuwa baba yako wewe ni kaka yangu nilikuwa nawakomesha wazazi. Yani kila kitu ni juu yako, hujanikomesha mimi wala baba yako maana siku zote kakulea kwa upendo kama mwanae kabisa na hakuna siku uliyoona tofauti ila ulivyomjinga ukaamua kutukomesha, ungesubiri ndoa basi ndio ufanye huo ujinga wako ila kwasasa utajutia nakwambia. Nitaongea tena badae”Mama Angel aliinuka na kwenda chumbani kwake maana alikuwa akijihisi hasira sana kwa muda huo.Baba Angel baada ya ile simu ya mke wake, aliamua kumpigia simu Rahim na kuomba kukutana nae kwa siku hiyo ili aweze kuzungumza nae kuhusu swala hilo na wajue cha kufanya.Walifika walipoahidiana na kukaa hapo kuanza kuzungumza, ambapo baba Angel alimwambia Rahim kuhusu simu aliyopokea kutoka kwa mkewe kuwa Angel ana mimba ya Samir, kwakweli Rahim alichukia sana na kusema,“Nilijua tu haya mambo ndiomana nikawahi mapema kuwa mniruhusu nitamtambulishe mwanangu kwa ndugu zake, ona sasa ni kitu gani hiki?”“Rahim, usitoe lawama zisizokuwa na msingi wala nini kwa wakati huu, unajua toka mwanzo ilikuwaje. Usimlaumu yoyote, tuongee tu hapa tujue cha kufanya”“Sababu umegundua watoto wako wale mapacha wana mahusiano basi unataka na watoto wangu wawe hivyo, kwanini lakini Erick?”“Nimekwambia usinipe lawama Rahim, tujadiliane kitu cha kufanya hapa. Mimi sina kosa maana mtoto tumemlea vizuri katika mstari ulionyooka”“Ndio kulea mtoto vizuri huko? Mlijifanya watu wa dini kiko wapi sasa? Mtoto kapata mimba kabla hata ya ndoa, hivi unajua kulea vizuri wewe? Mtoto wa kike anatakiwa kujiheshimu mpaka ndoa, au ndio anajiachia kama mama yake? Ndio shida ya kuzaa na wanawake matahira”“Rahim, usitake tugombane muda huu. Kama huna cha kujadiliana na mimi kuhusu mtoto ni sawa ila sio kuanza maneno yako ya kashfa kwa mke wangu”“Hapa sijui kama kuna cha kujadiliana kwakweli, nahisi kuchanganyikiwa tu hapa, kwanza naanza na huyu Samir atanieleza vizuri ujinga wake huo halafu ndio nitajua cha kufanya. Kesho nitakuja huko nyumbani kwako”“Haya mambo ni makubwa sio ya kuchukulia juu juu kiasi hiko”“Sitaki hata kukusikiliza Erick, kwaheri”Rahim aliinuka na kuondoka zake, basi baba Angel hakuwa na namna zaidi ya kuondoka zake tu, ila siku hii aliamua kwanza kwenda kwenye duka lake.Basi alifika pale na kumkuta Rama kama kawaida, ila leo Rama alianza kuongea nae kwani ni muda mrefu sana baba Angel hakwenda huku dukani,“Bosi, kuna baba mmoja aliwahi kuja hapa dukani”“Alikuwa anasemaje? Ni baba gani huyo?”“Mimi namuamini sana Mwenyezi Mungu, pia naamini kuwa mtoa riziki ni Mwenyezi Mungu, kwakweli sikuweza kukufanyia hii hujuma ingawa waliniahidi faida kubwa sana”“Hujuma gani tena?”“Waliniambia kuwa tufanye mpango wa kufilisi hili duka, niondoe hawa walinzi uliowaweka halafu watume watu kama majambazi waje kuvamia siku ambayo utashusha mzigo mpya ili tuweke hasara kwako na wakaniahidi kunipa mimi pesa mara mbili ya mtaji wa hili duka. Nadhani ni watu ambao wanakufahamu vizuri sana kwani wanajua kuwa mimi naelewa siku ya kufika mzigo mpya, walitaka niwaambie ila nikawaambia sijui kitu. Kwakweli mzigo ule ulishuka hapa mwezi uliopita, niliogopa sana kwani nilihisi wanaweza hata kunivamia kweli, ndiomana nimeamua kuongeza ulinzi, naomba msamaha sababu sikukutaarifu mapema”“Aaaaah Rama, hakuna sababu ya kuniomba msamaha, nakushukuru sana Rama. Nakushukuru sana, nshukuru una hofu ya Mungu, nashukuru sana. Asante Rama”“Usijali bosi wangu, mimi naridhika na hiki ninachopata, najua kama Mungu atapenda niwe sehemu nyingine basi ataniweka ila sio kwa kutoa hujuma kwa mtu mwingine”“Yani Rama sijui nikwambie nini nashukuru sana, huhyo baba alikuwaje?”Rama alianza kumueleza pale na moja kwa moja baba Angel alielewa kuwa yule mtu alikuwa ni ni Moses, yani hata alishindwa kumuelewa huyu mtu kwakweli kiasi cha kumfatilia yeye kama hivyo wakati aliishi nae vizuri kabisa kama ndugu yake.Aliongea na Rama pale, kisha kuagana nae na kurudi nyumbani kwake.Usiku wa leo, Angel anaamua kumpigia simu Samir ili kuongea nae kuhusu ile mimba aliyokuwa nayo, ila simu inaita sana bila ya kupokelewa hadi Angel anashangaa kuwa ni kitu gani kimetokea kwa Samir, basi alimpigia kwa mara tatu hizi ndipo Samir alipokea ile simu ya Angel na kuanza kuongea nae,“Mbona ulikuwa hupokei simu yangu Samir?”“Aaaah kuna tatizo Angel ndiomana ikawa hivi”“Tatizo gani?”“Aaaah acha tu, niambie sasa”“Samir, mimi nina mimba”“Duh!! Angel itakuwaje sasa?”“Itakuwaje kivipi wakati nimekwambia nina mimba”“Sikia Angel, unakumbuka siku ile tuliyolala pamoja?”“Nakumbuka ndio”“Je tuliongelea swala la mimba?”“Hapana”“Ndiomana nashangaa na kukuuliza inakuwaje maana mimi na wewe hatujapanga chochote kuhusu mimba”“Ila si ulisema utanioa Samir?”“Hivi umeuona moto uliowaka Angel? Baba yangu amekuwa mbogo, yani ninavyokwambia muda huu nimejifungia chumbani kwa mjomba, hali ni mbaya, baba anataka hata kuniua. Nakuomba Angel, usiseme kuwa hiyo mimba ni yangu”“Kheee una wazimu wewe au? Nisiseme mimba ni yako? Kwahiyo nimejipa mwenyewe hii mimba au kitu gani? Sikuelewi ujue”“Naelewa jinsi unavyosikia Angel, nakuomba sana hali si shwari kwasasa. Usiseme kuwa mimba ni yangu, yani mimi sielewi hapa, sielewi kabisa. Angel naomba unisamehe sana kwa hili ila mimi nitakukana kwakweli”Halafu Samir alikata ile simu na kumfanya Angel kutokuelewa kitu chochote, hapo ndio alianza kujiwa na maneno ya mama yake kuwa mtu anaweza kukuachia ujauzito na badae kukukana kuwa ile mimba sio yake, alijihisi vibaya na kuanza kulia, alilia sana na mwishowe alijikuta akilala chini ya sakafu huku akilia, hapo aliona kila alichoambiwa na mama yake kikianza kuonekana mapema kabisa.Baba Angel na mama Angel walianza kuongea kuhusu cha kufanya na binti yao, kisha baba Angel akamwambia mkewe,“Ila mimi naona kama tumeharakisha sana kumwambia Rahim?”“Hapana, anatakiwa ajue, ni vyema ingekuwa ni mimba ya mtu mwingine ila sio mimba ya kijana wake”Muda huo huo kuna ujumbe uliingia kwenye simu ya mama Angel, alipoangalia aliona ni namba ya Rahim, basi akafungua ule ujumbe na kuusoma,“Mkishamaliza ya mwanangu, mwende mkampime na huyo Erica wenu mimba pia. Kesho nakuja kumchukua mwanangu”Mama Angel alitazamana na mumewe na kumwambia kuhusu ule ujumbe, kisha mumewe akasema,“Nilikwambia mke wangu kuwa tumeharakisha kuhusu hili jambo. Akili za Rahim nadhani unazijua vizuri sana zilivyo, huyu mtoto ni kweli kafanya makosa ila haitakiwi kumburuza kwa kiasi hiki maana hata sisi wazazi tuna makosa pia”“Sasa tutafanyaje?”“Kesho asubuhi nitaondoka na Angel, nitampeleka kwa mama yangu kule ila sitamwambia ukweli kuwa Angel ni mjamzito na hata Angel nitamwambia afiche hilo huku sisi tukijipanga cha kufanya”“Halafu wewe ndio umefuga ubovu kwa huyu mtoto, umefanya Angel afanye ujinga kwa kujiamini sana kwani muda wote anaamini kuwa baba yake upo na utamtetea”“Nilisema toka mwanzo, nitampenda Angel, nitamlinda na kumthamini, nitakuwa nae bega kwa bega, nitakuwa kama baba yake. Nimemlea mwenyewe na kaharibika kwenye mikono yangu mwenyewe, natakiwa nijue cha kufanya, sitoamuacha Angel aende kuadhibiwa na mtu asiyejua uchungu wa Angel, mimi mlezi ndio naujua uchungu wa Angel, najua ni wapi nimepita nae hadi kumfikisha alipo. Mama Angel niache tu nifanye nitakavyo, kama Angel kaharibika kwenye mikono yangu basi niache nifanye kile ninachoona sahihi kwasasa, haiwezekani Rahim aje kumchukua mtoto kwa wakati huu, tutaongea kwanza tujue jinsi ya kusuluhisha haya ndio atakuwa na nafasi ya kuzungumza na mtoto”Mama Angel hakutaka kumbishia sana mume wake, ila alichopanga kwa muda huo ni kuwa pakikucha aende na Erica hospitali kwaajili ya kumpima ujauzito.Kulivyokucha, mama Angel alimchukua Erica na kwenda nae hospitali kama alivyopanga kwenda nae, ila walipima na kukuta Erica hana mimba, basi mama Angel aliridhika na kurudi nyumbani ambapo muda huu Angel na baba yake waliondoka pamoja na Erick, kwahiyo ambavyo hakuwakuta nyumbani alijua ni lazima tu wameondoka na mtoto mdogo Ester.Basi Erica aliamua kumuuliza mama yake,“Ila mama, kwanini uliamua kwenda kunipima mimba?”“Mmmmh Erica naomba unisikilize mwanangu, kitu ambacho mlifanya wewe na kaka yako sio kitu kizuri kabisa, na msirudie tena maana mtatutia aibu wazazi wenu”“Ila mama sijafanya kitu na Erick”“Hebu kwenda huko, watu mmechunguliana na kuachana watupu kabisa halafu unasema hamjafanya kitu? Mimi usinione naongea hapa, naongea huku nina maumivu sana najikaza tu. Kwanza najiuliza maswali mengi tu bila ya majibu, aliyekufundisha kufanya kile ulichomfanyia kaka yako ni nani?”“Ni kwenye video mama, halafu….”“Weeee hebu nyamaza huko, hivi unaona ni kitendo kizuri hiko hata kuweza kunielezea kwa uhuru kabisa? Hawa wanawapaga dawa na machizi, wameniharibia kabisa watoto mweeeh!!”Mama Angel alimtaka Erica kwenda kuandaa chakula tu, kisha yeye alienda zake ndani kwake.Baba Angel wakati anaondoka na Angel, walienda na kumuacha Erick kiwandani kisha baba Angel alifanya safari ya kwenda na Angel kwa bibi yake huku Angel akiwa amempakata mdogo wake Ester kwa muda huo,“Sasa baba wakati wa kurudi huyu Ester atashikwa na nani?”“Aaaah huyu nitamfunga kwenye kiti chake, hakuna tatizo”“Halafu baba, huko nitaenda kuishi kwa muda gani?”“Mpaka pale tatizo litakapoisha”“Baba, kwanini unanipenda sana? Mama hanipendi, ananionyesha baba mwingine ila wewe baba hujawahi kunionyesha mama mwingine, unanipenda sana baba yangu.”“Usijali, ila usimwambie bibi ukweli kuhusu swala lako la kuwa na mimba”Walifika hadi kwa bibi Angel ambapo baba Angel alimuacha Angel mahali hapo na kuondoka na Ester, kwahiyo alimpigia tu mama yake simu ili kumpa taarifa kuwa kamuacha Angel pale nyumbani kwake.Basi baba Angel alikuwa akirudi na Ester, ila alipomuangalia huyu mtoto aligundua kuwa muda huu atakuwa na njaa na ukizingatia kule kwa bibi yake ni safari ndefu, aliamua kupitia kwenye hoteli moja na kusimama pale kwaajili aweze kumuagizia Ester hata mtori ampe halafu ndio aendelee na safari ya kurudi nae, na yeye aweze kula chochote kile kitakachopatikana.Akiwa pale hotelini na mtoto wake, ndipo alipomuona tena Jack ambaye alienda na kumsalimia,“Kheee Erick, unalea mwenyewe!! Mkeo yuko wapi?”“Aaaah kuna mahali nilienda na mtoto, ndiomana muda huu nimeamua nipite nae hapa niweze kumlisha”“Tena vizuri nimekuona tena, huwezi amini napiga simu zako sizipati hewani, swala lililokuwepo hapa ni wewe kumuona mwanao”Yule Jack aliinuka, na pale mtori ulifika na baba Angel alianza kumlisha mtoto wake.Baada ya muda, Jack alirudi akiwa ameongozana na kijana mkubwa kabisa na kumwambia baba Angel,“Huyu hapa kijana wako”Baba Angel alishtuka kwanza na kumwambia Jack,“Khaaa mbona mtoto kafanana na Rahim?”Hapo hata Jack alishtuka pia,“Rahim? Ndio nani?”“Kuna rafiki yangu mmoja anaitwa Rahim, inamaana Jack humfahamu huyo Rahim? Yani huyu mtoto ni Rahim mtupu, nikikuletea hapa huwezi kubisha hata kidogo, huyu ni mtoto wake”“Wewe Erick una wazimu au ni kitu gani? Huyo Rahim simfahamu mimi, huyu ni mtoto nimezaa na wewe”“Kwani mimi nimekataa? Ila naomba siku nikukutanishe na huyo Rahim halafu wewe mwenyewe utasema ukweli kuhusu baba wa mtoto”Hata kijana yule alichukia kwani aliinuka na kuondoka zake, basi Jack alimsonya baba Angel na kumfata mtoto wake na kumfanya baba Angel aongee mwenyewe,“Yani ndio huyu mwanamke alitaka kunigombanisha na mke wangu, azae na Rahim huko halafu aniletee mtoto mimi. Anajifanya Rahim hamfahamu loh!! Aende zake huko, akinitafuta nitampeleka kwa Rahim, kajiongezea mtoto mwingine wa kiume. Huyu Rahim loh!! Hapana kwakweli”Baba Angel aliendelea kumlisha mwane, alipomaliza, Jack alimfata tena na kumpa baba Angel namba zake za simu kisha akamwambia,“Namba zangu hizo, ukipenda nitafute usipopenda potezea”Halafu Jack akaondoka zake, zile namba baba Angel akaziweka vizuri na kuondoka zake moja kwa moja alielekea kwenye gari lake na kwenda nyumbani kwake.Kwakweli mama Junior hili swala la Junior na Daima lilikuwa likimuumiza sana kichwa, kwahiyo jioni ya leo aliamua kumuita mwanae Junior na kuongea nae kuhusu Daima ukizingatia ukweli ni kuwa aliona ujumbe wa Daima kwenye simu ya junior,“Hivi wewe Junior mwanangu unataka nini lakini? Yote yanayotokea hayakufunzi akili? Huyu mwanamke anakupenda ila wewe masikio na macho juu juu kwenda kuwatafuta tena wakina Daima, una nini lakini?”“Hamna kitu mama”“Haya, kwanini unaenda kukutana tena na Daima hadi umempa tena mimba?”Junior alimshangaa mama yake na kusema,“Mama, sijakutana na Daima tangu nimeoa”“Mjinga wewe, na mimba aliyobeba ya nani?”“Kwani Daima ana mimba? Mimi sijui kama Daima ana mimba”“Unanifanya mimi mtoto eeeh!! Hebu mpigie hapo Daima nisikie, na uweke sauti kubwa na uongee nae maongezi ya kawaida ili nijue kama kweli hamjaonana toka ufunge ndoa”Junior alipiga simu na kuweka sauti kubwa ili mama yake apate kusikia,“Daima, niambie Daima”“Nimekumiss tu Junior”“Hivi hatujaonana siku nyingi eeeh!!”“Ndio, halafu tuliongea vizuri siku ile nikakutumia ujumbe ila hukujibu”“Ujumbe gani?”“Mjinga wewe, sijui mke wako anakukataza kuongea na simu loh!! Mjinga sana wewe”“Usijali, tutaonana tu. Ila kuna mtu kaniambia kuwa una mimba”“Mimba? Nani ana mimba? Hiyo mimba nibebe ya nani? Mimi nangoja wewe ndio unipe mimba nyingine”Basi Junior alikata ile simu na kumuangalia mama yake ila mama yake akamwambia,“Niondolee upuuzi wako mimi, unaongea ujinga hata hufikirii kama ni mbele ya mama yako”“Ila mama, kosa langu hapo ni nini?”“Hebu nenda weee, usinichanganye mie”Junior aliachana na mama yake tu na kwenda kufanya mambo mengine.Kwa zile siku chache tu ambazo Sarah ameishi na madam Oliva, aliweza kuzoeana vizuri sana na Paul, na aliweza kugundua kuwa Paul anampenda ila yeye alikuwa akijigelesha juu ya Paul yani hakutaka kuonyesha kuwa na yeye kavutiwa nae.Kwa upande mwingine aliona kuendelea kuishi hapo kwa madam Oliva kunaweza kupelekea yeye akaangukia kwenye mapenzi na Paul na hakutaka jambo hilo litokee, hakutaka kufanya kosa tena alilofanya na Elly.Basi ule usiku aliamua kuongea na madam Oliva kuhusu yeye kurudi kwa mama Angel,“Samahani madam, mimi kabla ya mama yangu kunichukua nilikuwa nikiishi kwa mama Erick, nitafurahi nikienda kuishi tena huko”“Unampenda sana mama Erick eeeh!!”“Ndio nampenda sana”“Halafu umefanana nae balaa, kamavile wewe ni mwanae”“Watu wengi wakiniona huwa wananifananisha nae, ila yeye mama Erick husema mimi ni mtoto wa ndugu yake Derrick”Hapo madam Oliva alishangaa kidogo, kitu ambacho huyu madam alikuwa hajui ni kuwa Manka ndio mama wa Sarah, alikuwa hajui kuwa Manka ndio anahusika pia na ile shule anayofundisha yeye, alichokuwa akijua ni kuwa baba mzazi wa Sarah alishakufa na alikuwa ni tajiri sana, basi alimuangalia vizuri Sarah na kumuuliza,“Kwani wewe, mama yako ni nani?”“Mama yangu anaitwa Manka”Hapa madam Oliva alishtuka pia, alimuangalia Sarah vizuri na kusema,“Mbona hufanani nae, unaonekana kuwa mtoto mpole, mcheshi na msikivu, huyo Manka hufanani nae hata kidogo. Kwahiyo kuhusu ile shule na mama yako nae anasimamia?”“Ndio, mama anasimamia pia ile shule ila tu huwa anaenda pale mara chache chache sana, nadhani wengi hawamfahamu kama anahusika pale. Mama aliacha nifahamike mimi sababu mimi ndio mmiliki wa ile shule”“Mmmmh!!”Madam Oliva alipumua kwanza na kumuuliza tena Sarah,“Unataka kwenda lini huko kwa mama Erick?”“Hata kesho”“Basi kesho nitakupeleka hakuna tatizo”Sarah alikubaliana na madam Oliva kuwa kesho yake atampeleka kwa mama Angel.Usiku huu ndipo mama Angel anaamua kumwambia mumewe kuhusu kitu ambacho Rahim amefika kusema akiwa pale kwao,“Yani Rahim kaja hapa na amefoka hatari, kasema anatupa siku mbili tu na Angel awe hapa au tumpeleke kule kwake”“Khaaa ana wazimu huyo Rahim au kitu gani? Kwanza yeye ni baba mzazi tu ila hajui malezi yoyote aliyoyapata Angel, aache nipambane mwenyewe na Angel wangu. Kama aibu hata mimi nimepata aibu vilevile ila najaribu kuangalia swala hili tunalichukuliaje na sio swala la kuanza kuropoka tu bila kufikiria. Asinitishie hata kidogo”“Yani alivyokuja amechukia, kwa hakika mume wangu usingeweza hata kumjibu yani alikuwa na hasira hatari”“Pole sana, huyo Rahim nitashughulika nae mwenyewe. Halafu kitu kingine mke wangu tujue kuwa tuna mtoto bondia maana toka siku ile namvulia kofia Erick, kwahiyo hakuna wa kuja kubabaisha hii familia”Mama Angel akaguna tu, basi ujumbe uliingia kwenye simu ya mama Angel, alipoangalia aliona ni namba ya Sia basi akafungua na kuusoma,“Kesho nitakuja, kuna jambo nataka kuwaambia. Mwambie mumeo asiondoke, maana nahitaji niwakute wote”Mama Angel alipomaliza kuusoma akamwambia mumewe,“Ujumbe wako huu!”“Aaaah huyu nae, mimi kesho kuna sehemu ya muhimu sana natakiwa kuwepo. Nitamngoja hadi saa mbili, nispomuona naondoka zangu, huo ujumbe nitaukuta kwako”Kwa muda huo waliamua tu kulala.Leo madam Oliva alijiandaa pamoja na Sarah na Paul maana alitaka kujua ni wapi ambapo Sarah anapelekwa, basi waliondoka kwa pamoja na kuanza kuelekea kwa mama Angel.Walifika, muda huu mama Angel alikuwepo kwenye kibaraza cha nyumba yao amekaa tu, kwahiyo alivyowaona aliwakaribisha pale ila hata yeye alishangaa kidogo kwani hakujua kama Sarah angekuwa kwa madam Oliva.Muda kidogo aliingia Sia, ambaye alisogea karibu yao, aliwaangalia kwa muda bila salamu na kusema,“Bora Oliva umejiongeza kwa kuniletea mwanangu Paul halafu wewe ubaki na mwanao Sarah”Madam Oliva alimuangalia akimshangaa kwakweli. Muda kidogo aliingia Sia, ambaye alisogea karibu yao, aliwaangalia kwa muda bila salamu na kusema,“Bora Oliva umejiongeza kwa kuniletea mwanangu Paul halafu wewe ubaki na mwanao Sarah”Madam Oliva alimuangalia akimshangaa kwakweli.Sia akamwambia,“Mbona unashangaa Oliva? Kwani hujui kama Sarah ni mtoto wako?”“Sikuelewi”“Ni hivi, watoto walibadilishwa wakati wadogo kwahiyo wewe ukapewa mtoto wangu, halafu mimi nikapewa mtoto wa Manka, halafu Manka akapewa mtoto wako amlee”“Haiwezekani”“Haiwezekani kivipi? Hujazaa na Steve wewe ila mimi ndio nimezaa na Steve, hivi huwa hujishtukii kwa kila mtu kusema kuwa mtoto wako kafanana na Steve? Huyo ni mtoto wangu, ukatae ukubali ila ukweli ndio huo, halafu wewe mtoto wako ni Sarah”“Una wazimu wewe au? Umeyatoa wapi hayo maneno?”“Kamuulize dokta Jimmy maana ndio aliyebadilisha hawa watoto”Madam Oliva akapumua kwanza na kusema,“Yani dokta Jimmy alishiriki kufanya hiko kwangu? Ananijua vizuri huyu dokta, huwa sipendi ujinga mimi. Haiwezekani”“Ndio imewezekana sasa, ukweli ndio huo”Paul hakuweza kuvumilia kwani alitoka nje ikabidi madam Oliva nae amfate mtoto wake Paul maana hata yeye hakuweza kuelewa kabisa yanayosemwa na Sia.Basi pale, mama Angel alimuuliza Sia,“Ila Sia una uhakika na hayo maneno yako?”“Ndio nina uhakika”Sarah akauliza pia,“Inamaana mama sio mama yangu?”“Ndio, sio mama yako. Mama yako mzazi ni yule madam aliyeondoka”“Jamani!! Haiwezekani”Sarah alimfata mama Angel na kumkumbatia kisha akamuuliza,“Kwanini mimi sikulelewa na mama yangu mzazi? Kwanini hivi lakini, hivi inawezekana kweli?”Mama Angel alimbembeleza kidogo Sarah maana aliona mtoto huyu akiumia sana bila tatizo, basi aliamua kwenda na Sarah chumbani kwake ili kujaribu kuongea nae kabisa, kitendo kile kilimfanya Sia ahisi kudharauliwa kwahiyo akaamua kuondoka zake.Madam Oliva alifika nyumbani na kijana wake na kuanza kuongea nae, ambapo Paul alimweleza pia mama yake kuhusu alama aliyoambiwa na yule mwanamke, na kumuuliza mama yake,“Mama, je ni kweli yule ndio mama yangu halisi?”“Mwanangu, hata mimi sijui ukweli ila nitahakikisha mpaka naupata ukweli halisi, pole mwanangu”“Ila mama, kwani inakuwaje hadi mtu anabadilisha mtoto? Je ni kweli mimi nimebadilishwa?”“Mwanangu, sijui kitu”“Naumia mama”“Naelewa na mimi ndio ninayeumia zaidi usijali mtoto wangu, ukweli utajulikana tu. Nikipata ukweli sitoona shida kukwambia mtoto wangu. Siku zote nimekulea na kukupenda na bado naendelea kukupenda”Madam Oliva aliingia chumbani kwake na kumpigia simu baba Angel kwa wakati huu,“Unajua kipindi kile tulikuwa tukimfatilia dokta Jimmy ila sikujua kama kuna mambo kama haya”“Mambo gani?”“Sia kaniambia kuwa dokta Jimmy alinibadilishia mtoto, eti mwanangu ni Sarah halafu mwanae ni Paul. Jamani nasema haiwezekani kabisa”“Duh!! Pole sana ila tukikutana itakuwa vizuri zaidi”“Nakuja ofisini kwako muda sio mrefu”Basi madam Oliva aliondoka muda ule ule na kumuaga tu mtoto wake kisha moja kwa moja alienda ofisini kwa baba Angel.Alipofika alimkuta baba Angel akiendelea na kazi zake kama kawaida, basi alimsalimia na kuanza kuongea nae kuanzia pale alipokutana na Sia,“Pole sana madam”“Asante, ila kilichonifanya nije ni kukuuliza kuhusu dokta Jimmy umeweza kufahamu nyumbani kwake?”“Ndio napafahamu”“Nielekeze ili niende”“Mmmmh peke yako? Yule dokta ni mwehu yule usije pata matatizo bure”“Sijali kitu chochote, yule dokta ananielewa mimi ni nani katika maisha yake na ataniambia ukweli tu. Tulia, nielekeze halafu nitaenda”Baba Angel alimuelekeza na kumshauri kuwa kama akitaka kwenda basi aende kesho yake maana muda tayari ulikuwa umeenda halafu anapoishi yule dokta ni mbali.Baada ya maelekezo, madam Oliva alimuaga baba Angel na kuondoka zake.Usiku wa leo, madam Oliva aliamua kumsimulia Steve kuhusu kile kilichotokea siku hiyo kwani kilikuwa bado kinamuumiza kichwa,“Huyo Sia anasema kuwa Paul ni mtoto wake”“Ooooh ndio maneno niliyotoka kuyapata kwa mama, nasikia Sia alienda tena kwa mama yangu na kusema kuwa Paul ni mtoto wake. Kwani mke wangu ilikuwaje?”“Mimi sijui ila huyo dokta Jimmy najua atanieleza ukweli”“Ila unahisi vipi? Hebu jaribu kunisimulia kwa ufupi kuhusu uzazi wako kwa Paul”“Mimi nilijifungua kabla ya wakati. Kwa maana hiyo nilizaa mtoto njiti kwahiyo alikuwa hospitali kwaajili ya uangalizi maalum, ila sasa kilichotokea kuna kipindi mtoto wangu alipotea na hapo ikawa tatizo, ndipo ugomvi wangu na dokta Jimmy ulipoanza hadi nikamfungulia mashtaka, ndipo alipokuja kuniletea Paul na kusema ndio mtoto wangu kapatikana, eti kuna mama aliondoka na mwanangu ila wamejitahidi na kumrudisha kwangu. Kwahiyo hapo ndio nashindwa kuelewa, sijui ni kweli nilibadilishiwa au la”“Kwahiyo inawezekana yule Sarah ndio akawa mtoto wako halisi?”“Hapana, na hilo nakataa pia kwani nakumbuka mtoto wangu alikuwa njiti ila alikuwa ni wa kiume, iweje leo niambiwe wa kike ndio mwanangu? Hilo halipo na hata haiwezekani kabisa, yani labda kama ni kweli basi mtoto wangu yupo sehemu nyingine ila Sarah ni mtoto wa yule yule Manka ingawa haendani nae.”“Dah!! Haya mambo hayaeleweki kwakweli, na huyo Sia anavyojua kushupalia jambo sipati picha, yani alivyoenda kushupalia kwa mama yangu hatari. Kwahiyo kwa huyo dokta unataka kwenda kesho”“Ndio, kesho nitaenda”“Basi tutaenda wote mke wangu”Madam Oliva alikubali jambo hilo kwani alichokuwa akitaka ni kuongea na dokta Jimmy tu ili aweze kujua ukweli.Leo mapema kabisa, madam Oliva aliondoka na Steve kuelekea nyumbani kwa dokta Jimmy, na walifika huko na kumkuta dokta Jimmy akimwagilia bustani, ni kitu ambacho dokta Jimmy hakukitarajia kwahiyo alishtuka tu kumuona madam Oliva,“Kheee Oliva?”“Ndio ni mimi, sitaki maelezo yoyote yale Jimmy, kwa muda huu nataka ukweli kuhusu mtoto wangu”“Ukweli upi?”“Usijifanye hujui dokta, mwanangu mimi yuko wapi? Umenipa mtoto wa mwingine halafu ukanidanganya kuwa ni mwanangu, yuko wapi mtoto wangu?”“Nimekuelewa Oliva, basi twende tukakae pale ili tuweze kuzungumza hayo”Dokta Jimmy alikuwa akiongoza sehemu ya kukaa, yani dokta Jimmy alikuwa ni mpole sana kiasi kwamba hata Steve alimshangaa huyu dokta maana huwa anasikia sifa zake kuwa ni mkorofi, ila alishangaa kumuona amekuwa mpole vile kwa madam Oliva.Walifika kwenye mahali kulikowekwa viti pale nje ya nyumba ya dokta na kukaa kisha dokta alianza kusema,“Hata salamu oliva?”“Hivi naanzaje kukusalimia eeeh!! Nakusalimiaje kiumbe mwenye roho mbaya kama wewe”“Unajua Oliva siwezi kukutendea ubaya!”“Usingeweza basi usingefanya ubaya juu yangu, ungenipatia mtoto wangu halisi nimlee mwenyewe, sio leo natukanwa na kudhalilishwa, nakuja kuambiwa kuwa mwanangu halisi ni Sarah sijui mtoto wa Manka, kwanini lakini umefanya hivi dokta Jimmy?”“Nisikilize Oliva, nani kakwambia kuwa mwanao ni Sarah? Unakumbuka kuwa mtoto wako alikuwa ni mtoto wa kiume au umesahau?”“Nakumbuka ndio, kama mliweza kumpa Manka mtoto wa kike akalea ikiwa alijifungua mtoto wa kiume ndio mnashindwa kufanya na kwangu? Nimekushangaa sana, nasikia unajuana vizuri sana na huyo Manka, laity ungejua Manka yupo vipi kwangu basi usingenifanyia hivi dokta Jimmy”“Kwanza naomba unisamehe Oliva, ila leo nitakwambia ukweli ingawa sikupanga kuusema leo”“Ndio niambie, na mwanangu halisi yuko wapi?”“Mwanao halisi yupo, yupo sehemu nzuri tu hata usijali”“Niambie bhana, naona kama unanibabaisha tu”“Sikia nianze kukwambia Oliva kitu kilichokuwepo, naomba unisikilize kwa makini”“Nakusikiliza, niambie”“Siku uliyojifungua wewe ni siku ambayo alijifungua mwanamke Fulani hivi ambaye nae alijifungua mtoto njiti kama wewe, ila yeye alikimbia hospitali, watoto wale wawili tulikuwa tukiwalea kwa hali zote ambazo zilikuwepo pale hospitali. Na tuligundua kuwa mmoja kati ya wale watoto ana upeo mpana sana, nilijua ni mwanao nikampenda sana. Ila kuna kitu kilitokea hapo kati mtoto mmoja kati ya wale wawili akaibiwa na hakuwepo kabisa pale hospitali, tukapata mawazo sana, basi nikaamua mwanao kumuweka alama ili asiibiwe. Ila kuna siku ndio mambo yaliharibika kabisa na mwanao pia akaibiwa, ndipo ulipoanza purukushani ya kutaka mtoto wako, hakukuwa na namna zaidi ya kukupa yule mtoto wa yule mwanamke chizi sababu yule mtoto alishamlea na tukaamini kuwa yupo katika mazingira mazuri wakati tunaendelea kumtafuta mtoto wako. Basi ukachukua yule mtoto ila siku zingine sasa ndio tukampata mtoto wako halisi, nami nikaamua kumtunza ila nilijua tunkuwa siku moja utaujua ukweli kuhusu mtoto wako. Hakuna baya ulilowahi kunitendea, kwahiyo hakuna kibaya nilichomtenda mtoto wako, tumemlea kwa upendo wote, na watu wote wanaonizunguka wanajua kuwa ni mtoto wangu mimi.”“Yuko wapi huyo mtoto?”“Ngoja nikamuite ila usije kumwambia kuwa wewe ni mama yake kwa gafla hivyo, najua mimi nitakavyomuandaa kisaikolojia na atakukubali tu. Namleta ili akusalimie na umuone, sitaki umtie mawazo kwasasa, najua jinsi ya kumwambia. Nimeamua kukwambia ukweli Oliva maana sina sababu ya kukuficha, sina ugomvi wowote na wewe Oliva”Kisha dokta Jimmy aliinuka na kwenda kumuita huyo mtoto.Steve alimuangalia madam Oliva ambaye alikuwa ameonekana kujawa na hasira sana, kisha alimwambia,“Unajisikiaje kumpokea mtoto wako halisi?”“Sijui yani, akili yangu hata haipo hapa kabisa, nahisi kama kupagawa vile”Baada ya muda kidogo, dokta Jimmy alifika na kijana ambapo alimwambia madam Oliva,“Kijana wangu huyu anaitwa Jimmy”Madam Oliva alimuangalia sana yule mtoto ambaye alikuwa ni mfanano halisi wa Derrick, yani hakuna ambaye angemuona huyu mtoto halafu angebisha kuwa si mtoto wa Derrick, yani madam Oliva alijisikia uchungu sana katika moyo wake, aliinuka na kumzaba kibao dokta Jimmy kisha akamwambia,“Mjinga sana wewe, halafu umempa na mjina wako usiokuwa na maana yoyote. Sikupendi wewe dokta”Pale dokta Jimmy alimwambia kijana wake Jimmy kuwa aondoke na kuwapisha ila madam Oliva alikazana kusema kuwa anataka kuondoka na mwanae,“Oliva, sikia nikwambia nimesema kuwa kila kitu tutakifanya kwa mpangilio, sio swala jepesi kumueleza kijana mkubwa kama Jimmy kwa haraka haraka hivyo kuwa huyu ndio mama yako. Mimi nitaongea na huyu kijana na nitakuja kukukabidhi kwani tatizo liko wapi?”“Nipe niondoke nae”“Nitakuletea Oliva, na pia nakuahidi kuwa kwa hili basi bnipo tayari kumwambia kila niliyemkosea ukweli halisi. Hata mimi roho imeniuma sana kwa hiki nilichokifanya, sijapenda kwakweli, naomba unisamehe sana”“Mjinga sana wewe, unaomba msamaha wakati umefanya makusudi”“Sio makusudi Oliva, kumbuka mtoto alipotea halafu wewe ulikuwa ukimuhitaji mtoto wako, sikuwa na la kufanya zaidi ya kukupa mtoto ambaye angekuridhisha wewe na moyo wako. Halafu alipopatikana, sikuweza uja kukwambia maana ningekuchanganya ndiomana niliamua kumlea mwenyewe, nisamehe sana kwa hili Oliva”Kwakweli madam Oliva alichukia sana na kumuuliza tena dokta Jimmy,“Kwahiyo lini utakuja kunikabidhi mtoto wangu?”“Nitakuja kumleta hata mwisho wa mwezi huu lakini nahitaji kwanza kumuandaa kisaikolojia”Kisha madam Oliva aliinuka na kufatwa nyuma na Steve kisha kuondoka.Wakiwa kwenye gari wakati wa kurudi, Steve alianza kuongea na madam Oliva,“Kwa habari nilizowahi kusikia kuhusu huyu dokta ni kuwa ana roho mbaya sana, ila mbona leo amekuwa tofauti? Halafu mbona anaonekana kukuogopa sana wewe?”“Unajua sijaweza kuamini kama huyu mjinga angeweza kunifanyia mimi kitu cha namna hii jamani, unajua huyu dokta kapata huo udokta wake kwa msaada wa baba yangu”“Kivipi?”“Baba yangu alikuwa anatambulika sana serikalini, kwahiyo aliweza kumuombea msaada wa kwenda kusoma nchi za nje, yule dokta Jimmy kwao walikuwa hawana lolote lile, yani baba yangu ndio kamfanya aweze kusoma huo udokta na kumaliza, hata hospitali ile alipata msaada mkubwa kwa baba yangu enzi za uhai wake, halafu leo hii ameenda kunifganyia unyama kama huu kweli? Nahisi baba yangu huko alipo anatokwa na machozi ya damu loh huyu dokta Jimmy kanichefua hatari”Hadi madam Oliva alifungua kioo na kutema mate, yani alikuwa na hasira kupita maelezo yoyote yale. Kwahiyo waliendelea na safari tu ya kurudi nyumbani kwao kwa muda huo.Usiku wa leo, baba Angel alikuwa akimuelezea mke wake kuhusu Angel maana yeye ndio anaepata taarifa kuhusu Angel sababu yupo kwa mama yake,“Yani mama kanipigia simu anasema Angel analala lala hatari, hivi mke wangu kumbe kweli Angel ana mimba eeeh!”“Sasa ulidhani nakutania au kitu gani baba Angel, mimi nikutanie au nikudanganye ili nifaidike na nini? Siwezi kufanya hivyo mume wangu, Angel nimeenda nae hospitali mwenyewe na tumepima na kumkuta na ujauzito, na kaniambia kwa mdomo wake mwenyewe kuwa ni mimba ya Samir”“Ila mama Angel, inabidi tujitafakari, hivi tumekosea wapi katika kumlea huyu mtoto? Mbona nahisi malezi yote tumempatia, upendo wote tulimpatia ni kwanini imekuwa hivi?”“Hata mimi sielewi mume wangu, ila tusilaumiane, kama malezi yote tumempa Angel basi ni akili yake mbovu tu. Sijui karithi kwa baba yake loh!!”“Yani nimejiuliza mke wangu nilipopigiwa simu na mama balaa, sijui kitu gani kimetokea kwa mtoto wetu Angel, sielewi mpaka muda huu kuwa Angel kapatwa na nini”Mara simu ya baba Angel ilianza kuita muda huo, basi alipokea na kuisikiliza,“Dokta Jimmy anaongea hapa”“Unashida gani wewe mjinga?”“Nahitaji kuongea na wewe Erick, nahitaji kukwambia ukweli”“Ukweli upi? Sitaki kuongea na wewe, achana na mimi kabisa”“Nataka kukwambia kilichowekwa kwa watoto wako na jinsi ya kuwaokoa maana bado kuwaokoa kwasasa, ukumbuke wameanza kwahiyo kitakachoendelea ni kuwa wataendelea na mchezo ule ule waliouona, ukizingatia washapata radha yake”“Mjinga sana wewe dokta, usiniambie kitu, sikuelewi chochote. Ila jua kuwa dawa yako inachemka, unanifanyia ujinga, halafu bado bila aibu unataka kunitegeshea kesi, hivi bila mwanangu Erick kwasasa si ningekuwa ndani kwa uongo wenu nyie!”“Eeeeh tena umenikumbusha jambo, nahitaji kuongea nawe kuhusu huyo Erick, kuna sehemu tumpeleke yani huyo mtoto atakuwa hatari hapo badae na ataingiza hela za kutosha”“Nimekwambia sitaki hata ushauri wako hata kidogo, dokta Jimmy hebu fanya mambo yako”Baba Angel alikata ile simu, kiukweli hakutaka kuongea na dokta Jimmy kabisa hata kuonana nae hakutaka hilo jambo, kila alipomfikiria aliona kupatwa na hasira zaidi.Hata aliacha maongezi na mke wake muda huo na kumtaka waweze kulala tu kwani alizidi kupatwa na hasira zaidi katika akili yake .Siku ya leo, Angel anaambiw ana bibi yake kuwa ajiandae waweze kwenda kutembea nae kidogo kwani bibi anakumbuka jinsi alivyokuwa akiishi na Angel hapo kabla.Angel anakubali tu na kwenda na bibi yake kutembea, walipofika kule kiliagizwa chakula pale ili waweze kula ila Angel aligoma na kudanganya kwa bibi yake kuwa ameshiba sana,“Jamani Angel, umekula muda gani nyumbani wakati tumeondoka wote bila ya wewe kula chakula chochote?”Muda kidogo alifika mr.Peter ambaye ni rafiki wa bibi huyu na kukaa karibu yao, ila bibi alivyoinuka tu kwenda msalani, yule mr.Peter alimwambia Angel,“Wewe Angel, ni mjamzito wewe!”“Hapana, mimi sina mimba”“Unajua mimi ni mtu mzima, halafu niliwahi kusomea udaktari ila niliishia kati. Wewe Angel usinibishie, mimi huwa nikiangalia tu mtu mwenye mimba hata ya mwezi mmoja namtambua, wewe Angel ni mjamzito, haya mtoto mdogo hivyo umeanza kuzini hadi mimba!! Au ni kitu gani hiko?”“Hapana, sina mimba”“Ulidanganywa nini na mwanaume? Alikudanganya na hela? Mbona wazazi wako wapo vizuri kwenye swala zima la hela Angel? Alikudanya na simu? Mbona nilikununulia simu ya gharama sana? Alikudanganya na upendo? Mbona wazazi wako wanakupenda sana? Alikudanganya kitu gani huyo mwanaume Angel? Ameahidi kukuoa? Wapi imeandikwa uolewe baada ya kuzaa? Uzao mzuri ni ule wa ndani ya ndo, hata mimi nimeshikwa na uchungu juu yako, yani jinsi bibi yako anavyokupenda na anavyoongea kuhusu maisha unayoyapata wewe, jinsi nilivyoongea na mama yako siku ile, dah Angel imekuwaje umebeba mimba mapema hivi? Hujui mimba inapatikanaje? Ulibakwa au ni kitu gani? Unajua wewe ni binti mzuri sana, ungejituliza ungempata mume bora katika maisha yako”Bibi Angel alirudi na hapo Angel hakuweza kuendelea kukaa na kudai kuwa anajihisi vibaya, hata kuongea hakuongea chochote hadi wanarudi nyumbani, yani Angel alijifungia chumbani na kujiwa na yale maneno ambayo mama yake aliongea juu yake alijihisi maumivu sana yani aliwaza vitu vingi mno na aliumia sana katika moyo wake na kujiona kuwa alichokifanya hakikuwa sawa kabisa, aliwaza na kujisemea,“Kwa hakika nimewakosea sana wazazi wangu, ni kweli wamenilea vizuri, mama amejitahidi sana kunilea na kumuondoa Samir mbele yangu, baba nae kafanya jitihada zote hata kunipeleka shule ya mbali, sijui ni kitu gani kimeniingia mimi Angel. Siku zote nimejilinda ila siku moja tu imefanya iondoe thamani yangu nzima, ni aibu kwangu na kwa familia yangu”Alijikuta akilia kwa muda huku akijutia sana, kitu kingine kilichomuumiza ni vile baba yake ambavyo anampenda sana, basi kwa muda huo aliamua kumuandikia Samir ujumbe wake kuhusu ile mimba,“Samir, tufanyeje na hii mimba niliyonayo?”“Sijui Angel yani hata mimi sielewi”“Je utanioa Samir?”“Nitakuoa vipi Angel wakati baba kasema wewe ni dada yangu”“Samir, yamekuwa hayo? Si ulisema hujali chochote wewe jamani, leo unaniambia kitu cha namna hiyo Samir kweli? Kwakweli mimi najiona nimekosa furaha na thamani ya maisha kabisa”“Usiseme hivyo Angel”“Unategemea niseme nini ikiwa ninayekupenda unasema huwezi kunioa, na bila kusahau kuwa wewe ndio uliyenishawishi mimi hadi tukafanya na sasa mimi ni mjamzito”“Angel, vitu vingine huwa nasema tu. Ila kiukweli mimi nahitaji kukuoa kabisa, huwezi amini sikai kwa baba, nipo kwa mjomba ila baba alikuja kunifanyia fujo na sasa nipo kwa mjomba mwingine. Angel nakupenda sana hata sijui kwanini umekuwa ndugu yangu”“Kwahiyo hitimisho lako kwangu ni nini?”“Sijui, ila nitakachoamua mimi Angel sijui kama kitakuwa kizuri”“Kitu gani?”“Tulia tu”Hapo Angel alimtumia ujumbe mwingine Samir bila kujibiwa na kumfanya ajihisi vibaya zaidi, alijua tu kinachofuata ni Samir kumuacha yeye moja kwa moja, basi Angel alilia sana na kuamua kumuandikia ujumbe baba yake kwani aliona baba yake ndio atampa faraja kidogo, alilia sana na kuamua kulala.Baba Angel alipoamka asubuhi kabisa, kitu cha kwanza ilikuwa ni kuchukua simu yake ambapo alikutana na ujumbe wa Angel,“Baba nisamehe sana, nimekosa mimi, sina raha mimi, sijui nifanyeje, huyo Samir hanitaki tena na sijui cha kufanya. Nisaidie baba yangu, nisamehe sana”Baba Angel alimsomea mke wake ambaye alisema pia,“Huyu mtoto mwehu, mbona mimi hajaniandikia huo ujinga wake! Kiukweli huyu Angel katudhalilisha sana, na anapenda kukwambia wewe ujinga wake sababu anajua kuwa wewe unamtetea na ujinga anaoufanya”“Usiseme hivyo mama Angel”Basi baba Angel alienda kujiandaa, sababu alitaka kutoka ila alichokuwa akitaka kufanya kwa siku hiyo ni kupita kwa mama yake ili kuongea na Angel sababu alijua kuwa Angel anahitaji kuongea nae kwa kipindi hiko.Baba Angel wakati anatoka tu nje alikutana na Rahim ambaye alikuwa amefura kwa hasira, kisha Rahim akasema,“Kwakweli katika siku zote leo nimechukia zaidi na ninaenda kutenda dhambi kwa mtoto wangu mwenyewe”Kisha Rahim akaondoka, kwakweli baba Angel hakumuelewa kabisa na kuamua kumfata ambapo walienda moja kwa moja hadi nyumbani kwa Rahim kisha Rahim alimuita Samir ambaye kwa muda huo alikuwa nyumbani kwake, muda kidogo Samir alitoka ndani kwao ila alikuwa akijiamini sana kupita siku zote ambazo alikuwa na uoga, kisha Rahim alimuuliza,“Jana umenitumia ujumbe gani wewe mjinga?”“Nimekwambia naenda kumuoa Angel”“Mjinga wewe”Rahim alimkaba Samir, kisha alitoa kisu kwenye mkanda wake wa suruali na kutaka kumchoma nacho Samir.Muda kidogo aliingia Sia, ambaye alisogea karibu yao, aliwaangalia kwa muda bila salamu na kusema,“Bora Oliva umejiongeza kwa kuniletea mwanangu Paul halafu wewe ubaki na mwanao Sarah”Madam Oliva alimuangalia akimshangaa kwakweli.Sia akamwambia,“Mbona unashangaa Oliva? Kwani hujui kama Sarah ni mtoto wako?”“Sikuelewi”“Ni hivi, watoto walibadilishwa wakati wadogo kwahiyo wewe ukapewa mtoto wangu, halafu mimi nikapewa mtoto wa Manka, halafu Manka akapewa mtoto wako amlee”“Haiwezekani”“Haiwezekani kivipi? Hujazaa na Steve wewe ila mimi ndio nimezaa na Steve, hivi huwa hujishtukii kwa kila mtu kusema kuwa mtoto wako kafanana na Steve? Huyo ni mtoto wangu, ukatae ukubali ila ukweli ndio huo, halafu wewe mtoto wako ni Sarah”“Una wazimu wewe au? Umeyatoa wapi hayo maneno?”“Kamuulize dokta Jimmy maana ndio aliyebadilisha hawa watoto”Madam Oliva akapumua kwanza na kusema,“Yani dokta Jimmy alishiriki kufanya hiko kwangu? Ananijua vizuri huyu dokta, huwa sipendi ujinga mimi. Haiwezekani”“Ndio imewezekana sasa, ukweli ndio huo”Paul hakuweza kuvumilia kwani alitoka nje ikabidi madam Oliva nae amfate mtoto wake Paul maana hata yeye hakuweza kuelewa kabisa yanayosemwa na Sia.Basi pale, mama Angel alimuuliza Sia,“Ila Sia una uhakika na hayo maneno yako?”“Ndio nina uhakika”Sarah akauliza pia,“Inamaana mama sio mama yangu?”“Ndio, sio mama yako. Mama yako mzazi ni yule madam aliyeondoka”“Jamani!! Haiwezekani”Sarah alimfata mama Angel na kumkumbatia kisha akamuuliza,“Kwanini mimi sikulelewa na mama yangu mzazi? Kwanini hivi lakini, hivi inawezekana kweli?”Mama Angel alimbembeleza kidogo Sarah maana aliona mtoto huyu akiumia sana bila tatizo, basi aliamua kwenda na Sarah chumbani kwake ili kujaribu kuongea nae kabisa, kitendo kile kilimfanya Sia ahisi kudharauliwa kwahiyo akaamua kuondoka zake.Madam Oliva alifika nyumbani na kijana wake na kuanza kuongea nae, ambapo Paul alimweleza pia mama yake kuhusu alama aliyoambiwa na yule mwanamke, na kumuuliza mama yake,“Mama, je ni kweli yule ndio mama yangu halisi?”“Mwanangu, hata mimi sijui ukweli ila nitahakikisha mpaka naupata ukweli halisi, pole mwanangu”“Ila mama, kwani inakuwaje hadi mtu anabadilisha mtoto? Je ni kweli mimi nimebadilishwa?”“Mwanangu, sijui kitu”“Naumia mama”“Naelewa na mimi ndio ninayeumia zaidi usijali mtoto wangu, ukweli utajulikana tu. Nikipata ukweli sitoona shida kukwambia mtoto wangu. Siku zote nimekulea na kukupenda na bado naendelea kukupenda”Madam Oliva aliingia chumbani kwake na kumpigia simu baba Angel kwa wakati huu,“Unajua kipindi kile tulikuwa tukimfatilia dokta Jimmy ila sikujua kama kuna mambo kama haya”“Mambo gani?”“Sia kaniambia kuwa dokta Jimmy alinibadilishia mtoto, eti mwanangu ni Sarah halafu mwanae ni Paul. Jamani nasema haiwezekani kabisa”“Duh!! Pole sana ila tukikutana itakuwa vizuri zaidi”“Nakuja ofisini kwako muda sio mrefu”Basi madam Oliva aliondoka muda ule ule na kumuaga tu mtoto wake kisha moja kwa moja alienda ofisini kwa baba Angel.Alipofika alimkuta baba Angel akiendelea na kazi zake kama kawaida, basi alimsalimia na kuanza kuongea nae kuanzia pale alipokutana na Sia,“Pole sana madam”“Asante, ila kilichonifanya nije ni kukuuliza kuhusu dokta Jimmy umeweza kufahamu nyumbani kwake?”“Ndio napafahamu”“Nielekeze ili niende”“Mmmmh peke yako? Yule dokta ni mwehu yule usije pata matatizo bure”“Sijali kitu chochote, yule dokta ananielewa mimi ni nani katika maisha yake na ataniambia ukweli tu. Tulia, nielekeze halafu nitaenda”Baba Angel alimuelekeza na kumshauri kuwa kama akitaka kwenda basi aende kesho yake maana muda tayari ulikuwa umeenda halafu anapoishi yule dokta ni mbali.Baada ya maelekezo, madam Oliva alimuaga baba Angel na kuondoka zake.Usiku wa leo, madam Oliva aliamua kumsimulia Steve kuhusu kile kilichotokea siku hiyo kwani kilikuwa bado kinamuumiza kichwa,“Huyo Sia anasema kuwa Paul ni mtoto wake”“Ooooh ndio maneno niliyotoka kuyapata kwa mama, nasikia Sia alienda tena kwa mama yangu na kusema kuwa Paul ni mtoto wake. Kwani mke wangu ilikuwaje?”“Mimi sijui ila huyo dokta Jimmy najua atanieleza ukweli”“Ila unahisi vipi? Hebu jaribu kunisimulia kwa ufupi kuhusu uzazi wako kwa Paul”“Mimi nilijifungua kabla ya wakati. Kwa maana hiyo nilizaa mtoto njiti kwahiyo alikuwa hospitali kwaajili ya uangalizi maalum, ila sasa kilichotokea kuna kipindi mtoto wangu alipotea na hapo ikawa tatizo, ndipo ugomvi wangu na dokta Jimmy ulipoanza hadi nikamfungulia mashtaka, ndipo alipokuja kuniletea Paul na kusema ndio mtoto wangu kapatikana, eti kuna mama aliondoka na mwanangu ila wamejitahidi na kumrudisha kwangu. Kwahiyo hapo ndio nashindwa kuelewa, sijui ni kweli nilibadilishiwa au la”“Kwahiyo inawezekana yule Sarah ndio akawa mtoto wako halisi?”“Hapana, na hilo nakataa pia kwani nakumbuka mtoto wangu alikuwa njiti ila alikuwa ni wa kiume, iweje leo niambiwe wa kike ndio mwanangu? Hilo halipo na hata haiwezekani kabisa, yani labda kama ni kweli basi mtoto wangu yupo sehemu nyingine ila Sarah ni mtoto wa yule yule Manka ingawa haendani nae.”“Dah!! Haya mambo hayaeleweki kwakweli, na huyo Sia anavyojua kushupalia jambo sipati picha, yani alivyoenda kushupalia kwa mama yangu hatari. Kwahiyo kwa huyo dokta unataka kwenda kesho”“Ndio, kesho nitaenda”“Basi tutaenda wote mke wangu”Madam Oliva alikubali jambo hilo kwani alichokuwa akitaka ni kuongea na dokta Jimmy tu ili aweze kujua ukweli.Leo mapema kabisa, madam Oliva aliondoka na Steve kuelekea nyumbani kwa dokta Jimmy, na walifika huko na kumkuta dokta Jimmy akimwagilia bustani, ni kitu ambacho dokta Jimmy hakukitarajia kwahiyo alishtuka tu kumuona madam Oliva,“Kheee Oliva?”“Ndio ni mimi, sitaki maelezo yoyote yale Jimmy, kwa muda huu nataka ukweli kuhusu mtoto wangu”“Ukweli upi?”“Usijifanye hujui dokta, mwanangu mimi yuko wapi? Umenipa mtoto wa mwingine halafu ukanidanganya kuwa ni mwanangu, yuko wapi mtoto wangu?”“Nimekuelewa Oliva, basi twende tukakae pale ili tuweze kuzungumza hayo”Dokta Jimmy alikuwa akiongoza sehemu ya kukaa, yani dokta Jimmy alikuwa ni mpole sana kiasi kwamba hata Steve alimshangaa huyu dokta maana huwa anasikia sifa zake kuwa ni mkorofi, ila alishangaa kumuona amekuwa mpole vile kwa madam Oliva.Walifika kwenye mahali kulikowekwa viti pale nje ya nyumba ya dokta na kukaa kisha dokta alianza kusema,“Hata salamu oliva?”“Hivi naanzaje kukusalimia eeeh!! Nakusalimiaje kiumbe mwenye roho mbaya kama wewe”“Unajua Oliva siwezi kukutendea ubaya!”“Usingeweza basi usingefanya ubaya juu yangu, ungenipatia mtoto wangu halisi nimlee mwenyewe, sio leo natukanwa na kudhalilishwa, nakuja kuambiwa kuwa mwanangu halisi ni Sarah sijui mtoto wa Manka, kwanini lakini umefanya hivi dokta Jimmy?”“Nisikilize Oliva, nani kakwambia kuwa mwanao ni Sarah? Unakumbuka kuwa mtoto wako alikuwa ni mtoto wa kiume au umesahau?”“Nakumbuka ndio, kama mliweza kumpa Manka mtoto wa kike akalea ikiwa alijifungua mtoto wa kiume ndio mnashindwa kufanya na kwangu? Nimekushangaa sana, nasikia unajuana vizuri sana na huyo Manka, laity ungejua Manka yupo vipi kwangu basi usingenifanyia hivi dokta Jimmy”“Kwanza naomba unisamehe Oliva, ila leo nitakwambia ukweli ingawa sikupanga kuusema leo”“Ndio niambie, na mwanangu halisi yuko wapi?”“Mwanao halisi yupo, yupo sehemu nzuri tu hata usijali”“Niambie bhana, naona kama unanibabaisha tu”“Sikia nianze kukwambia Oliva kitu kilichokuwepo, naomba unisikilize kwa makini”“Nakusikiliza, niambie”“Siku uliyojifungua wewe ni siku ambayo alijifungua mwanamke Fulani hivi ambaye nae alijifungua mtoto njiti kama wewe, ila yeye alikimbia hospitali, watoto wale wawili tulikuwa tukiwalea kwa hali zote ambazo zilikuwepo pale hospitali. Na tuligundua kuwa mmoja kati ya wale watoto ana upeo mpana sana, nilijua ni mwanao nikampenda sana. Ila kuna kitu kilitokea hapo kati mtoto mmoja kati ya wale wawili akaibiwa na hakuwepo kabisa pale hospitali, tukapata mawazo sana, basi nikaamua mwanao kumuweka alama ili asiibiwe. Ila kuna siku ndio mambo yaliharibika kabisa na mwanao pia akaibiwa, ndipo ulipoanza purukushani ya kutaka mtoto wako, hakukuwa na namna zaidi ya kukupa yule mtoto wa yule mwanamke chizi sababu yule mtoto alishamlea na tukaamini kuwa yupo katika mazingira mazuri wakati tunaendelea kumtafuta mtoto wako. Basi ukachukua yule mtoto ila siku zingine sasa ndio tukampata mtoto wako halisi, nami nikaamua kumtunza ila nilijua tunkuwa siku moja utaujua ukweli kuhusu mtoto wako. Hakuna baya ulilowahi kunitendea, kwahiyo hakuna kibaya nilichomtenda mtoto wako, tumemlea kwa upendo wote, na watu wote wanaonizunguka wanajua kuwa ni mtoto wangu mimi.”“Yuko wapi huyo mtoto?”“Ngoja nikamuite ila usije kumwambia kuwa wewe ni mama yake kwa gafla hivyo, najua mimi nitakavyomuandaa kisaikolojia na atakukubali tu. Namleta ili akusalimie na umuone, sitaki umtie mawazo kwasasa, najua jinsi ya kumwambia. Nimeamua kukwambia ukweli Oliva maana sina sababu ya kukuficha, sina ugomvi wowote na wewe Oliva”Kisha dokta Jimmy aliinuka na kwenda kumuita huyo mtoto.Steve alimuangalia madam Oliva ambaye alikuwa ameonekana kujawa na hasira sana, kisha alimwambia,“Unajisikiaje kumpokea mtoto wako halisi?”“Sijui yani, akili yangu hata haipo hapa kabisa, nahisi kama kupagawa vile”Baada ya muda kidogo, dokta Jimmy alifika na kijana ambapo alimwambia madam Oliva,“Kijana wangu huyu anaitwa Jimmy”Madam Oliva alimuangalia sana yule mtoto ambaye alikuwa ni mfanano halisi wa Derrick, yani hakuna ambaye angemuona huyu mtoto halafu angebisha kuwa si mtoto wa Derrick, yani madam Oliva alijisikia uchungu sana katika moyo wake, aliinuka na kumzaba kibao dokta Jimmy kisha akamwambia,“Mjinga sana wewe, halafu umempa na mjina wako usiokuwa na maana yoyote. Sikupendi wewe dokta”Pale dokta Jimmy alimwambia kijana wake Jimmy kuwa aondoke na kuwapisha ila madam Oliva alikazana kusema kuwa anataka kuondoka na mwanae,“Oliva, sikia nikwambia nimesema kuwa kila kitu tutakifanya kwa mpangilio, sio swala jepesi kumueleza kijana mkubwa kama Jimmy kwa haraka haraka hivyo kuwa huyu ndio mama yako. Mimi nitaongea na huyu kijana na nitakuja kukukabidhi kwani tatizo liko wapi?”“Nipe niondoke nae”“Nitakuletea Oliva, na pia nakuahidi kuwa kwa hili basi bnipo tayari kumwambia kila niliyemkosea ukweli halisi. Hata mimi roho imeniuma sana kwa hiki nilichokifanya, sijapenda kwakweli, naomba unisamehe sana”“Mjinga sana wewe, unaomba msamaha wakati umefanya makusudi”“Sio makusudi Oliva, kumbuka mtoto alipotea halafu wewe ulikuwa ukimuhitaji mtoto wako, sikuwa na la kufanya zaidi ya kukupa mtoto ambaye angekuridhisha wewe na moyo wako. Halafu alipopatikana, sikuweza uja kukwambia maana ningekuchanganya ndiomana niliamua kumlea mwenyewe, nisamehe sana kwa hili Oliva”Kwakweli madam Oliva alichukia sana na kumuuliza tena dokta Jimmy,“Kwahiyo lini utakuja kunikabidhi mtoto wangu?”“Nitakuja kumleta hata mwisho wa mwezi huu lakini nahitaji kwanza kumuandaa kisaikolojia”Kisha madam Oliva aliinuka na kufatwa nyuma na Steve kisha kuondoka.Wakiwa kwenye gari wakati wa kurudi, Steve alianza kuongea na madam Oliva,“Kwa habari nilizowahi kusikia kuhusu huyu dokta ni kuwa ana roho mbaya sana, ila mbona leo amekuwa tofauti? Halafu mbona anaonekana kukuogopa sana wewe?”“Unajua sijaweza kuamini kama huyu mjinga angeweza kunifanyia mimi kitu cha namna hii jamani, unajua huyu dokta kapata huo udokta wake kwa msaada wa baba yangu”“Kivipi?”“Baba yangu alikuwa anatambulika sana serikalini, kwahiyo aliweza kumuombea msaada wa kwenda kusoma nchi za nje, yule dokta Jimmy kwao walikuwa hawana lolote lile, yani baba yangu ndio kamfanya aweze kusoma huo udokta na kumaliza, hata hospitali ile alipata msaada mkubwa kwa baba yangu enzi za uhai wake, halafu leo hii ameenda kunifganyia unyama kama huu kweli? Nahisi baba yangu huko alipo anatokwa na machozi ya damu loh huyu dokta Jimmy kanichefua hatari”Hadi madam Oliva alifungua kioo na kutema mate, yani alikuwa na hasira kupita maelezo yoyote yale. Kwahiyo waliendelea na safari tu ya kurudi nyumbani kwao kwa muda huo.Usiku wa leo, baba Angel alikuwa akimuelezea mke wake kuhusu Angel maana yeye ndio anaepata taarifa kuhusu Angel sababu yupo kwa mama yake,“Yani mama kanipigia simu anasema Angel analala lala hatari, hivi mke wangu kumbe kweli Angel ana mimba eeeh!”“Sasa ulidhani nakutania au kitu gani baba Angel, mimi nikutanie au nikudanganye ili nifaidike na nini? Siwezi kufanya hivyo mume wangu, Angel nimeenda nae hospitali mwenyewe na tumepima na kumkuta na ujauzito, na kaniambia kwa mdomo wake mwenyewe kuwa ni mimba ya Samir”“Ila mama Angel, inabidi tujitafakari, hivi tumekosea wapi katika kumlea huyu mtoto? Mbona nahisi malezi yote tumempatia, upendo wote tulimpatia ni kwanini imekuwa hivi?”“Hata mimi sielewi mume wangu, ila tusilaumiane, kama malezi yote tumempa Angel basi ni akili yake mbovu tu. Sijui karithi kwa baba yake loh!!”“Yani nimejiuliza mke wangu nilipopigiwa simu na mama balaa, sijui kitu gani kimetokea kwa mtoto wetu Angel, sielewi mpaka muda huu kuwa Angel kapatwa na nini”Mara simu ya baba Angel ilianza kuita muda huo, basi alipokea na kuisikiliza,“Dokta Jimmy anaongea hapa”“Unashida gani wewe mjinga?”“Nahitaji kuongea na wewe Erick, nahitaji kukwambia ukweli”“Ukweli upi? Sitaki kuongea na wewe, achana na mimi kabisa”“Nataka kukwambia kilichowekwa kwa watoto wako na jinsi ya kuwaokoa maana bado kuwaokoa kwasasa, ukumbuke wameanza kwahiyo kitakachoendelea ni kuwa wataendelea na mchezo ule ule waliouona, ukizingatia washapata radha yake”“Mjinga sana wewe dokta, usiniambie kitu, sikuelewi chochote. Ila jua kuwa dawa yako inachemka, unanifanyia ujinga, halafu bado bila aibu unataka kunitegeshea kesi, hivi bila mwanangu Erick kwasasa si ningekuwa ndani kwa uongo wenu nyie!”“Eeeeh tena umenikumbusha jambo, nahitaji kuongea nawe kuhusu huyo Erick, kuna sehemu tumpeleke yani huyo mtoto atakuwa hatari hapo badae na ataingiza hela za kutosha”“Nimekwambia sitaki hata ushauri wako hata kidogo, dokta Jimmy hebu fanya mambo yako”Baba Angel alikata ile simu, kiukweli hakutaka kuongea na dokta Jimmy kabisa hata kuonana nae hakutaka hilo jambo, kila alipomfikiria aliona kupatwa na hasira zaidi.Hata aliacha maongezi na mke wake muda huo na kumtaka waweze kulala tu kwani alizidi kupatwa na hasira zaidi katika akili yake .Siku ya leo, Angel anaambiw ana bibi yake kuwa ajiandae waweze kwenda kutembea nae kidogo kwani bibi anakumbuka jinsi alivyokuwa akiishi na Angel hapo kabla.Angel anakubali tu na kwenda na bibi yake kutembea, walipofika kule kiliagizwa chakula pale ili waweze kula ila Angel aligoma na kudanganya kwa bibi yake kuwa ameshiba sana,“Jamani Angel, umekula muda gani nyumbani wakati tumeondoka wote bila ya wewe kula chakula chochote?”Muda kidogo alifika mr.Peter ambaye ni rafiki wa bibi huyu na kukaa karibu yao, ila bibi alivyoinuka tu kwenda msalani, yule mr.Peter alimwambia Angel,“Wewe Angel, ni mjamzito wewe!”“Hapana, mimi sina mimba”“Unajua mimi ni mtu mzima, halafu niliwahi kusomea udaktari ila niliishia kati. Wewe Angel usinibishie, mimi huwa nikiangalia tu mtu mwenye mimba hata ya mwezi mmoja namtambua, wewe Angel ni mjamzito, haya mtoto mdogo hivyo umeanza kuzini hadi mimba!! Au ni kitu gani hiko?”“Hapana, sina mimba”“Ulidanganywa nini na mwanaume? Alikudanganya na hela? Mbona wazazi wako wapo vizuri kwenye swala zima la hela Angel? Alikudanya na simu? Mbona nilikununulia simu ya gharama sana? Alikudanganya na upendo? Mbona wazazi wako wanakupenda sana? Alikudanganya kitu gani huyo mwanaume Angel? Ameahidi kukuoa? Wapi imeandikwa uolewe baada ya kuzaa? Uzao mzuri ni ule wa ndani ya ndo, hata mimi nimeshikwa na uchungu juu yako, yani jinsi bibi yako anavyokupenda na anavyoongea kuhusu maisha unayoyapata wewe, jinsi nilivyoongea na mama yako siku ile, dah Angel imekuwaje umebeba mimba mapema hivi? Hujui mimba inapatikanaje? Ulibakwa au ni kitu gani? Unajua wewe ni binti mzuri sana, ungejituliza ungempata mume bora katika maisha yako”Bibi Angel alirudi na hapo Angel hakuweza kuendelea kukaa na kudai kuwa anajihisi vibaya, hata kuongea hakuongea chochote hadi wanarudi nyumbani, yani Angel alijifungia chumbani na kujiwa na yale maneno ambayo mama yake aliongea juu yake alijihisi maumivu sana yani aliwaza vitu vingi mno na aliumia sana katika moyo wake na kujiona kuwa alichokifanya hakikuwa sawa kabisa, aliwaza na kujisemea,“Kwa hakika nimewakosea sana wazazi wangu, ni kweli wamenilea vizuri, mama amejitahidi sana kunilea na kumuondoa Samir mbele yangu, baba nae kafanya jitihada zote hata kunipeleka shule ya mbali, sijui ni kitu gani kimeniingia mimi Angel. Siku zote nimejilinda ila siku moja tu imefanya iondoe thamani yangu nzima, ni aibu kwangu na kwa familia yangu”Alijikuta akilia kwa muda huku akijutia sana, kitu kingine kilichomuumiza ni vile baba yake ambavyo anampenda sana, basi kwa muda huo aliamua kumuandikia Samir ujumbe wake kuhusu ile mimba,“Samir, tufanyeje na hii mimba niliyonayo?”“Sijui Angel yani hata mimi sielewi”“Je utanioa Samir?”“Nitakuoa vipi Angel wakati baba kasema wewe ni dada yangu”“Samir, yamekuwa hayo? Si ulisema hujali chochote wewe jamani, leo unaniambia kitu cha namna hiyo Samir kweli? Kwakweli mimi najiona nimekosa furaha na thamani ya maisha kabisa”“Usiseme hivyo Angel”“Unategemea niseme nini ikiwa ninayekupenda unasema huwezi kunioa, na bila kusahau kuwa wewe ndio uliyenishawishi mimi hadi tukafanya na sasa mimi ni mjamzito”“Angel, vitu vingine huwa nasema tu. Ila kiukweli mimi nahitaji kukuoa kabisa, huwezi amini sikai kwa baba, nipo kwa mjomba ila baba alikuja kunifanyia fujo na sasa nipo kwa mjomba mwingine. Angel nakupenda sana hata sijui kwanini umekuwa ndugu yangu”“Kwahiyo hitimisho lako kwangu ni nini?”“Sijui, ila nitakachoamua mimi Angel sijui kama kitakuwa kizuri”“Kitu gani?”“Tulia tu”Hapo Angel alimtumia ujumbe mwingine Samir bila kujibiwa na kumfanya ajihisi vibaya zaidi, alijua tu kinachofuata ni Samir kumuacha yeye moja kwa moja, basi Angel alilia sana na kuamua kumuandikia ujumbe baba yake kwani aliona baba yake ndio atampa faraja kidogo, alilia sana na kuamua kulala.Baba Angel alipoamka asubuhi kabisa, kitu cha kwanza ilikuwa ni kuchukua simu yake ambapo alikutana na ujumbe wa Angel,“Baba nisamehe sana, nimekosa mimi, sina raha mimi, sijui nifanyeje, huyo Samir hanitaki tena na sijui cha kufanya. Nisaidie baba yangu, nisamehe sana”Baba Angel alimsomea mke wake ambaye alisema pia,“Huyu mtoto mwehu, mbona mimi hajaniandikia huo ujinga wake! Kiukweli huyu Angel katudhalilisha sana, na anapenda kukwambia wewe ujinga wake sababu anajua kuwa wewe unamtetea na ujinga anaoufanya”“Usiseme hivyo mama Angel”Basi baba Angel alienda kujiandaa, sababu alitaka kutoka ila alichokuwa akitaka kufanya kwa siku hiyo ni kupita kwa mama yake ili kuongea na Angel sababu alijua kuwa Angel anahitaji kuongea nae kwa kipindi hiko.Baba Angel wakati anatoka tu nje alikutana na Rahim ambaye alikuwa amefura kwa hasira, kisha Rahim akasema,“Kwakweli katika siku zote leo nimechukia zaidi na ninaenda kutenda dhambi kwa mtoto wangu mwenyewe”Kisha Rahim akaondoka, kwakweli baba Angel hakumuelewa kabisa na kuamua kumfata ambapo walienda moja kwa moja hadi nyumbani kwa Rahim kisha Rahim alimuita Samir ambaye kwa muda huo alikuwa nyumbani kwake, muda kidogo Samir alitoka ndani kwao ila alikuwa akijiamini sana kupita siku zote ambazo alikuwa na uoga, kisha Rahim alimuuliza,“Jana umenitumia ujumbe gani wewe mjinga?”“Nimekwambia naenda kumuoa Angel”“Mjinga wewe”Rahim alimkaba Samir, kisha alitoa kisu kwenye mkanda wake wa suruali na kutaka kumchoma nacho Samir. Kisha Rahim akaondoka, kwakweli baba Angel hakumuelewa kabisa na kuamua kumfata ambapo walienda moja kwa moja hadi nyumbani kwa Rahim kisha Rahim alimuita Samir ambaye kwa muda huo alikuwa nyumbani kwake, muda kidogo Samir alitoka ndani kwao ila alikuwa akijiamini sana kupita siku zote ambazo alikuwa na uoga, kisha Rahim alimuuliza,“Jana umenitumia ujumbe gani wewe mjinga?”“Nimekwambia naenda kumuoa Angel”“Mjinga wewe”Rahim alimkaba Samir, kisha alitoa kisu kwenye mkanda wake wa suruali na kutaka kumchoma nacho Samir.Baba Angel alienda kumdaka Rahim na kumuangushia pembeni ambapo Samir aliinuka pale alipokuwa ameangushwa na baba yake, kisha baba Angel alimshika Samir mkono na kuondoka nae ambapo moja kwa moja alienda nae nyumbani kwake.Kwakweli mama Angel alipomuona Samir ameenda nyumbani kwake alijikuta aking’aka kwa hasira,“Sitaki kumuona huyu kiumbe nyumbani kwangu”“Aaaah mama Angel, usiwe hivyo nakuomba. Tutaongea vizuri”“Tutaongea vizuri nini? Sitaki kumuona huyo kiumbe kwenye nyumba yangu”Baba Angel alimwambia Samir aingie ndani, halafu yeye alienda chumbani na mke wake ili kumuelewesha,“Mke wangu, kuwa mpole kwanza”“Niwe mpole nini sasa? Amemfanyia vibaya sana binti yetu”“Naelewa ila sio wa kuhukumiwa kufa”“Kuhukumiwa kufa? Kivipi?”“Rahim alitaka kumchoma kisu ujue”“Ndio ungemuacha amchome, si mwanae?”“Kwahiyo hata akitaka kumchoma kisu Angel na amchome tu sababu ni mwanae! Mara nyingine ufikirie kwanza kabla ya kuongea, huyu Samir sio kama amembaka Angel, si walikubaliana au ni kitu gani? Kwanini tumuhukumu yeye tu!! Kama kuhukumu basi tuwahukumu wote wawili, hakuna sababu ya kumfanya vibaya huyu kijana, mwache akae hapa nyumbani kwa muda kwanza halafu nitafikiria pa kumpeleka. Mama Angel, acha hasira na jazba chukulia mfano huyu Samir ndio angekuwa kijana wako sasa ungejihisije?”“Tatizo lako wewe unajifanya una huruma sana?”“Kiasi sio sana, panapotakiwa kuonewa huruma basi lazima nitakuwa na huruma napo”Mama Angel hakutaka kuongea zaidi ila hakupenda kabisa kitendo cha mumewe kumchukua Samir hapo nyumbani kwao, kisha mama Angel alimuuliza mumewe,“Kwahiyo atakaa hapa kwa muda gani?”“Mpaka pale tutakapoona mambo yapo sawa”“Mmmmh!!”Baba Angel hata hakujali sana bali aliondoka ili aweze kuzungumza na Samir.Baba Angel alimuita Samir na kwenda nae kwenye bustani na kuzungumza nae kuhusu Angel na kuhusu kile kinachoendelea,“Kwani wewe Samir umemtumia ujumbe gani baba yako?”“Nilimtumia kuwa nahitaji kumuoa Angel”“Kwanini sasa umemtumia ujumbe huo?”“Sababu Angel analalamika kila muda kuwa mimi nilikuwa kumdanganya ila mimi sikuwa nikimdanganya Angel maana ninampenda kweli”“Je, hujaambiwa na baba yako kuwa Angel ni ndugu yako?”“Yani baba yangu kila leo anatutambulisha mtoto mpya nadhani hadi sasa haijuilikani idadi kamili ya watoto wake, halafu ndio aseme mimi dada yangu Angel? Hilo nimekataa”“Sikia Samir nikwambie kitu, Angel ni dada yako yani hili lipo wazi kabisa kuwa Angel ni dada yako na ulitakiwa kuwa makina nae vizuri sana”“Nilikuwa tayari nishampenda na yeye alikuwa tayari ananipenda, yani sijui kama naweza kuvumilia kwa kumuangalia Angel akiwa na mwanaume mwingine”Baba Angel alisikitika na kumuuliza tena,“Unahisi kwanini mimi nimekusaidia?”“Ni sababu ya moyo wa huruma uliokuwa nao, hata Angel aliuwahi kuniambia hivi. Nakumbuka nilimwambia kuwa natamani ungekuwa ni baba yangu mzazi, kwanza una moyo wa huruma na pili ni mwerewa”“Basi naomba nikuombe kitu”“Niambie tu”“Naomba kwasasa muone Angel kama dada yako, muone kamavile umezaliwa nae tumbo moja yani baba na mama mmoja. Wakati mimi najaribu kuweka mambo sawa, tulia nirekebishe kwanza halafu nijue hatma yako na hatma ya mwanangu Angel”Samir hakumbishia kabisa baba Angel kwani huyu baba Alionekana kuwa na roho ya tofauti sana.Usiku huu mama Angel hakuridhika na kuanza kumlalamikia mume wake kuhusu kumruhusu Samir kuishi hapo kwao,“Kwakweli baba Angel nashindwa kukuelewa jamani, umewezaje kufanya kitu cha namna hii?”“Kwani tatizo ni nini mke wangu?”“Kwahiyo huoni tatizo kabisa hapa, yani mtu kampa binti yetu mimba halafu unamchukua huyo mtu na kumkaribisha ndani kwetu jamani!!”“Hivi mama Nagel nilikuuliza asubuhi, kwani huyu Samir alimbaka Angel? Ni wapi ulipowakuta pamoja? Si uliwakuta wamelala wote! Ingekuwa nyumba yetu ya hovyohovyo basi tungesema Samir alikuja na kumshawishi Angel, ila ni wazi kuwa Angel alimuita Samir kwa matakwa yake mwenyewe. Kwanini utake kumuhukumu huyu kijana?”“Najua huna uchungu, sababu Angel sio mtoto wako”“Mama Angel, usitake tugombane sababu ya ujinga. Lini nimesema vibaya juu ya Angel? Nilimpenda na bado ninampenda kama mzazi wake, pia najaribu kuokoa hili jahazi, haya hayo mambo ya kusema nafanya hivi sababu Angel sio mtoto wangu yanatoka wapi? Uliona wapi mwanaume ambaye anaishi na mtoto sio wake na anajua ila akampenda kama ambavyo mimi nampenda Angel? Nimemuandikisha mali zangu Angel ila nikijua wazi kuwa sio damu yangu, unawezaje kusema kuwa nafanya hivi sababu Angel sio mwanangu? Mimi najaribu kuangalia hali halisi ilivyo na jinsi ya kufanya ili tuweze kutatua hili”“Kwahiyo kulitatua ni kumchukua muhalifu na kumkalisha ndani ya nyumba?”Mara simu ya baba Angel ilianza kuita, ambapo baba Angel aliichukua na kuanza kuongea nayo, moja kwa moja alijua wazi anayeongea na Rahim sababu alianza kwa kumtusi tena alimtusi sana huku akimsema vibaya,“Unajua Rahim, hebu kuwa na heshima basi”“Heshima unaijua wewe? Kilichokufanya kumchukua huyo Samir ni kitu gani?”“Nisingeweza kuvumilia wewe umpige Samir au umuue mbele yangu, kwa kosa gani alilolifanya?”“Kwahiyo huoni kama kosa la kumpa mimba Angel ni kosa kubwa sana?”“Yani wewe huyu Samir ni mwanao au sio mwanao?”“Toto linamaudhi sana hilo hujui tu, mimi nalifundisha halafu linaniambia intake au nisitake lazima yeye amuoe Angel”“Sasa sio swala la kuchukia hivyo, ni kweli Samir kampa mimba Angel ila wote wawili wana makosa hapa.Na pia sisi wazazi tuna makosa pia maana watoto hawakujua ukweli mapema”“Weee makosa unayo mwenyewe, toto hilo kabla halijaharibu mambo nimeliambia kuwa Angel ni dada yake, halafu limeenda kufanya ujinga. Limenitia aibu sana, sasa huyo mtoto wao ataniita mimi nani?”“Atakuita babu, hebu acha maneno mengi sana Rahim, nisikilize kwanza, acha kuropoka utafikiri una matatizo ya kinywa. Angel ni mtoto wetu na Samir ni mtoto wetu, tunatakiwa kukaa chini na kuyazungumza haya na sio kufanya hasira tu”“Huna uchungu na Angel wewe, ndiomana ulikuwa unamtaka”“Khaaa yani mimi nilikuwa namtaka Angel!! Ndio shukrani yako hii kwangu?”“Shukrani gani nikupe mjinga kama wewe usiyejua kulea, mapenzi gani ya baba na mtoto hayo unayompa Angel kiasi hata baba yake mzazi hamtaki? Na usikute hiyo mimba wewe na Samir mmeshirikiana ndiomana unamtetea”Baba Angel alichukia sana na kuamua kukata simu na kuizima kabisa, kwa muda huu hakutaka hata kuzungumza na mke wake kwani aliamua tu kulala basi kwani na muda ulishaenda.Asubuhi na mapema, baba Angel anaondoka nyumbani kwake na kuelekea ofisini kama kawaida, alipanga kwenda kumuona Angel ila alijikuta akiahirisha tu ile safari kwa siku hiyo.Mama Angel alitoka ndani muda huu na kukuta mezani wapo watu watatu wakinywa chai, Erica, Sarah na Samir yani Erick alikuwa ameondoka.Basi mama Angel aliwafata karibu na kusema,“Aliyewaambia make karibu na huyu ni nani?”Erica alijibu na kusema,“Hamna mtu mama ila baba katutambulisha kuwa huyu tumtambue kama kaka yetu”“Kaka yenu wa wapi huyo ni mbakaji, halafu wewe Samir usiniletee ujinga kwneye nyumba yangu kabisa, kaa mbali na watoto wangu usije ukawabaka bure”Samir alinyong’onyea sana na kutaka kuinuka ila Erica alimshika mkono kuwa akae, basi mama yao aliondoka na Erica akamwambia Samir,“Usichukie, sijui ni kitu gani kimemkumba mama, huwa hayupo hivi. Ukimzoea utampenda, hana roho mbaya kiasi hiki mama yetu”Sarah nae akaongezea,“Ni kweli hana roho mbaya, ukimzoea utampenda tu, itakuwa kuna upepo mchafu umempitia. Jisikie huru”Basi jambo lile lilimfanya Samir sasa akae vizuri bila kujali kuwa ni maneno gani mama Angel ametoka kuyasema muda mfupi uliopita, alikunywa chai na wakina Erica pale na walipomaliza walikaa nae na kuanza kuzungumza nae, hadi Samir alijikuta akifurahia maana aliwaona hawa wawili kuwa ni wacheshi sana, ukizingatia Sarah alipenda sana kuongea ndio kitu kilichomfanya Samir afurahi zaidi halafu Erica nae alikuwa ni mtu wa kumzoea mtu mwingine haraka zaidi.Baba Angel akiwa ofisini kwake akiendelea na mambo yake, ndipo kwa muda huu alipofika madam Oliva mule ofisini kwa baba Angel na kuanza kuongea nae kuhusu aliyoyapata kwa dokta Jimmy.Alikaa na kumuelezea kila kitu ambacho kimetokea,“Kheee kwahiyo dokta Jimmy ana mtoto wako?”“Ndio, mjinga yule kampa mwanangu mjina wake jamani, nimechukia sana”“Pole sana, kwahiyo anasemaje huyo dokta feki”“Anasema kuwa yupo tayari kumueleza kila mtu kila kitu kilichotokea.”“Vipi kuhusu wazazi wa Sarah?”“Hajaniweka wazi ila nina uhakika asilimia mia moja kuwa Sarah sio mtoto wa Manka, lazima kuna namna ilifanyika na dokta Jimmy anajua kila kitu sema alichofanya ni kumdanganya”“Dokta Jimmy alinipigia simu kuwa anataka kuniambia ukweli kuhusu watoto wangu”“Ungekutana nae kumsikiliza, lazima lipo la maana analotaka kuongea na wewe maana kwa jinsi nilivyomsema lazima anataka kukwambia ukweli tu”“Basi huo ukweli napenda uwepo na wewe ndio auseme maana siwezi kuusikiliza peke yangu, haaminiki yule dokta”“Pole sana, basi tutaenda wote. Muulize ni wapi anahitaji kuonana na wewe ili aseme ukweli halafu tutaenda wote”“Sawa ngoja nimpigie muda huu nimuulize alipo”Baba Angel alichukua simu na kumpigia dokta Jimmy ambapo baada ya muda kidogo tu dokta Jimmy alipokea simu ile na kuanza kuongea nae,“Erick, upo tayari kuongea na mimi?”“Ndio nipo tayari”“Chagua sehemu ambayo tutaweza kuzungumza”“Sijui, hata nyumbani kwangu”“Hapana, ni vizuri ikiwa kwenye kaburi la mzee Jimmy maana haya mambo ni yeye ndio aliyoyafanya”“Duh!! Kwahiyo lini tutazungumza hayo?”“Nipe wiki moja, ni vizuri ukija wewe na mke wako maana nina mengi ya kuongea nanyi wawili”“Sawa, nimekubali”Ile simu ilikatika, kisha baba Angel aliongea na madam Oliva,“Natumaini umesikia, kwahiyo tutaenda wote eeeh!”“Ndio, usijali, tutaenda wote, najua ni wapi pa kumkomeshea dokta Jimmy hadi atasema ukweli”Basi madam Oliva aliagana na baba Angel pale halafu akaondoka zake kwa muda huo.Erick alipotoka kiwandani, moja kwa moja aliamua kupitia kwenye duka la baba yake, na alipofika alimuona mtu pale dukani akizungumza na Rama, alipata hisia mbaya kuhusu yule mtu. Ila hakutaka kujitokeza kati yao, badala yake yule mtu alivyoondoka ndipo Erick alipoamua kumfatilia na aliweza kumfatilia hadi nyumbani kwake huyo mtu, kisha alimfata wakati akitaka kuingia ndani, yule mtu alishangaa sana kumuona yule kijana, halafu Erick alimsogelea huyu baba na kumkaba kisha akamuuliza,“Ulienda kufanya nini pale dukani?”“Wapi tena jamani wapi?”“Mjinga wewe hujui ulipotoka au? Kwanza unaitwa nani?”“Naitwa Moses”“Haya, pale dukani ulienda kufanya nini?”Moses alimuangalia huyu Erick ambaye ni kijana mdogo ila muda ule alionekana kujawa na misuli katika mwili wake, alionekana kuwa na nguvu sana tena ngu za ajabu mno.Basi kwa wasiwasi Moses alijikuta akijielezea,“Aaaah mimi nilienda kununua bidhaa pale”Erick alimshushia ngumi moja ya shavu kiasi cha kumfanya Moses damu zianze kumtoka mdomoni, na hapo Moses alianza kumuogopa zaidi huyu Erick, basi akamwambia kwa woga,“Naomba unisamehe sana”Erick alimpiga mtama Moses na kumuangusha chini, basi Moses alianza kusema,“Mimi ni sawa na umri kama baba yako”“Unamjua baba yangu wewe?”“Aaaah hapana lakini wewe ni kama kijana wangu”“Sasa sikia nikwambie kitu, leo iwe mwisho na mwanzo wa wewe kwenda dukani kwangu tena, lile ni duka langu kama ulikuwa hujui. Nasema hivi, leo iwe mwanzo na mwisho, kama hujupendi jua nitakupa ukilema, mimi sitakuua bali nitakupa ukilema ili ukae ndani bila kutembea. Jina langu ni Erick, na mali zozote za mtu anayeitwa Erick uzione kama ukoma. Mjinga wewe umefanana na yule mjinga mwenzio”Kisha Erick alimpiga teke Moses ambaye alijikuta akiangukia karibu na geti lake halafu Erick akaondoka zake kwa muda huo.Kwakweli Moses hakuelewa kitu chochote, alihisi akili yake kutokupata nafuu kabisa.Erick alipotoka hapo alipitia tena dukani ambapo Rama alikuwa tayari kashafunga kisha Erick alirudi nyumbani kwao ambapo alimkuta mama yake akiwa na mashaka maana Erick amechelewa sana kurudi kwa siku hii.“Jamani mwanangu, mbona umechelewa hivi?”“Nilipita dukani mama”“Ulikuwa unasubiri wafunge duka au?”“Ndio mama”“Siku nyingine uwe unasema, yani hapa umenifanya roho iwe juu juu hatari”Basi mama Angel alimuandalia mwanae chakula ambapo Erick alikula kidogo kile chakula ili kumridhisha mama yake na kisha kwenda chumbani kwake kupumzika maana bado alikuwa na hasira kiasi ila mama Angel hakuweza kwa haraka kumgundua mtoto wake kwani hajawahi kumuona vizuri akiwa amepandisha hasira.Erick alipokuwa chumbani kwake tu, muda kidogo alienda Erica na kumwambia,“Nimesikia kuwa umerudi, mbona leo umechelewa sana? Halafu unaonekana umefura kwa hasira, hivi umeweza kula kweli leo?”“Nimekula ndio”“Hapana Erick, mimi nakufahamu vizuri sana. Niambie tatizo ni nini pacha wangu?”“Niite mpenzi wangu ndio nikwambie”Erica alimpiga kibao kidogo mgongoni Erick ili asiendelee na utani ule, ila Erick alicheka tu kwa kile kibao kisha Erica alimwambia,“Najua sasa ni kwanini umesema hivyo?”“Kwanini?”“Ushakorofisha huko, yani hapo akili ishakuruka”“Hata nahisi kuwa sitaweza kulala peke yangu leo, tunaweza kulala wote Erica?”“Kwa yale maswahibu yaliyotokea hadi mama ananishika na kwenda kunipima mimba halafu tulale wote!! Hapana Erick, jikaze ulale mwenyewe tu, au njoo chumbani tulale pamoja yani mimi, wewe na Sarah”Erick alikubali hilo pia maana alijiona kuwa na hasira sana na hakuhisi kama angeweza kulala mwenyewe kwa hasira zile alizokuwa nazo.Kulipokucha kwa siku ya leo, baba Angel aliongea na mkewe kwa kifupi tu kuhusu alichoongea na madam Oliva maana usiku wake hakumwambia kitu kisha akamwambia kuwa kesho ataenda kumuona Angel.“Kwahiyo tutaenda wote kwa huyo dokta Jimmy?”“Ndio, inabidi twende wote, kwahiyo inabidi twende wote tukamsikilize”“Sawa nimekuelewa, ngoja nikawaamshe wakina Erica waje kufanya usafi”Baba Angel aliondoka zake, halafu mama Angel moja kwa moja alienda chumbani kwakina Erica na kukuta wamelala wote watatu, kwakweli alisikitika sana yani zile dawa ambazo mzee Jimmy aliwapa watoto hawa bado hakuzielewa, inamaana hapo asingekuwepo Sarah basi wangekuwa wamelala watu wawili tu ambao ni tatizo zaidi.Basi mama Angel aliwaamsha pale ambapo moja kwa moja Erick aliinuka na kuelekea chumbani kwake huku mama yake akisikitika tu, halafu akawaambia wakina Erica wakafanye usafi.Mama Angel alitoka nje ya nyumba na kumkuta Samir akipalilia maua ya pale nyumbani kwao, basi alimuangalia na kumsogelea ambapo Samir alimsalimia mama Angel, naye aliitikia kisha alianza kumuuliza Samir,“Umemfahamu kipindi gani baba yako Rahim?”“Nikiwa na miaka mitano, wakati huo mdogo wangu alikuwa na mwaka mmoja”“Yani ilikuwaje? Mama yako alikuzaa kabla ya ndoa?”“Ndio, mimi nilizaliwa nje ya ndoa hata mdogo wangu ni hivyo hivyo ila badae baba aliamua kumuoa mama, na hapo tukawa watoto wa familia moja”“Mamako anampenda sana baba yako eeeh!!”“Eeeeh anampenda ila mama huwa anasema baba alimtendea kitu kibaya sana, huwa hataki kukisema ila najua ni kitu kibaya sana. Sitaki kitokee kwenye familia yangu pia”“Swala la wewe kuwa na Angel, mama yako analichukuliaje?”“Tatizo mama yangu muda wote yupo kwenye kazi, ila mama yangu hajachukia kabisa mimi kuwa na Angel. Mwanzoni alichukia baada ya kujua kuwa Angel anaitwa Angel Erick, ila badae alivyogundua kuwa Angel ni mtoto wa baba alifurahi na yeye ndio aliniambia kuwa nikaishi kwa mjomba na kunipa baraka zote, kabla sijamtumia ujumbe baba kuwa nahitaji kumuoa Angel, ni mama aliniambia kuwa baba asinibabaishe natakiwa kusimamia msimamo wangu”“Mmmmh!! Mama yao hajafikiria madhara ya wewe kufunga ndoa na dada yako?”“Mama anasema sio mbaya, yani mama kabariki hili swala kwa baraka zote ni baba tu ndio ataki”Hapo mama Angel akaelewa wazi lazima kuna tatizo kati ya Rahim na mke wake ndiomana mke wa Rahim anaona kawaida, labda anataka kumkomesha mumewe bila kujali athari watakazozipata watoto. Ila siku hii mama Angel hakuongea vibaya na Samir, hata Samir alimshangaa jinsi huyu mama alivyobadilika gafla vile.Baba Angel akiwa ofisini kwake huku akiendelea na kazi zake, muda huu anapigiwa simu na namba ngeni na kuipokea,“Ni Moses anaongea hapa”“Unasemaje Moses”“Kwakweli hapa ninavyoongea na wewe nipo kitandani, mbavu zote zinaniuma yani naumwa sana”“Mmmmh!!”Baba Angel aliguna tu sababu kwa kpindi hiko Moses alikuwa ni adui yake namba moja ukizingatia kwa mambo ambayo Moses ameyafanya na jinsi alivyoambiwa na Rama, basi Moses aliendelea kuongea,“Kwakweli Erick sijui ulimtuma kijana wako anifatilie sijui ni kitu gani, ila kanifatilia jana halafu kanipiga sana. Hivi yule mtoto ni mtu au ni mzimu?”“Unamuongelea nani?”“Namuongelea Erick, yani nimepigwa mimi jana na kijana wako hatari. Kanipiga sana, hapa taya linauma, na mgongo unauma, mbavu zote zinaniuma, nilitaka nikupigia simu siku ya jana ila sikuweza maana nilikuwa na hali mbaya sana”“Mmmmh mwanangu ndio kafanya hivyo!!”“Ndio, yani kanipiga sana. Inamaana hujui kitu? Erick, kwani mwanao umeenda kumfundisha kareti au kitu gani? Umemfundisha mtoto wako ubondia? Mbona amekuwa hivi? Dah kanipiga sana”Baba Angel hakusema kitu maana hata kutoa pole alishindwa ukizingatia akikumbuka jinsi Moses alivyompiga risasi zile zilizomfanya asifanye chochote kwa mwaka mzima, basi alimsikiliza tu mpaka Moses alipokata simu.Kisha baba Angel alijiuliza juu ya mtoto wake Erick,“Katoa wapi hizo nguvu Erick? Hata kile kitendo chake cha kuniokoa mimi kilinishangaza sana maana nilimuona mwanangu akiwa amebadilika na mwili wake wote ukijaa misuli kama mtu wa mazoezi mazito, katoa wapi hizo nguvu?”Baba Angel akapanga kuwa akirudi nyumbani aende kumuuliza mwanae vizuri, ila muda huo akapigiwa simu na mama yake na kupokea ile simu,“Erick, kwakweli Angel anaumwa, kajifungia ndani hataki kutoka nikimuita anasema anayemtaka ni baba yake tu. Kwahiyo anakutaka wewe”“Kheee toka lini mama?”“Toka juzi alivyoingia ndani basi hajatoka tena, jana kutwa nzima hajatoka. Leo pia, nimeshindwa kuvumilia ndiomana nimekupigia, hebu uje upesi”Hapo baba Angel aliacha kila kitu, maana huwa akisikia Angel anaumwa anaona kama akili yake ikimruka, yeye alijikuta akiwa na uchungu zaidi na Angel kuliko mtu yoyote yule.Aliacha kila kitu na muda huo huo alitoka na kupanda gari lake na kuelekea nyumbani kwao kwaajili ya mtoto wake Angel.Baba Angel alipofika, alimkuta mama yake akiwa amekaa na kusema kuwa aende sasa akaongee na binti yake ili afungue mlango.Baba Angel alisogea hadi chumba anacholala Angel na kumuita,“Angel mwanangu, naomba ufungue mlango”Angel alifungua ule mlango, baba Angel alipomtazama chini aliona kuna damu inamchirizika Angel miguuni. Angel alifungua ule mlango, baba Angel alipomtazama chini aliona kuna damu inamchirizika Angel miguuni.Baba Angel alimuwahi binti yake na kutoka nae nje ambapo alienda kumpakiza kwenye gari na kuondoka nae huku akimwambia mama yake kuwa atampigia simu, moja kwa moja baba Angel alimpeleka Angel hospitali ambapo aliwekwa kwenye matibabu halafu baba Angel alikuwa akimsubiria huku ajiuliza mambo mengi sana,“Sijui ndio mimba imetoka au sijui ni kitu gani?”Alikosa jibu kwakweli na kuendelea kusubiri, muda kidogo alipigiwa simu na mke wake ambaye alikuwa na maagizo kwake,“Baba Angel unaporudi naomba upitie pale….!”Baba Angel aliamua amkatishe maongezi kwanza kwa kumwambia kuwa sio kwamba atarudimuda huo,“Mama Angel, sipo karibu nipo mbali kidogo kwahiyo nitachelewa kurudi”“Uko wapi kwani?”“Nikirudi nitakwambia mke wangu”“Niambie bhana, tatizo nini kwani?”“Ila usipaniki”“Sawa, niambie tu”“Nipo na Angel hospitali hajisikii vizuri kidogo”“Tatizo nini tena?”“Nkirudi naye nitakwambia”Baba Angel alikata ile simu na kumfata daktari maana alikuwa ameitwa naye, basi alivyofika daktari akamwambia,“Huyu binti alikuwa ni mjamzito, sasa mimba yake imetoka”“Oooh asante Mungu”“Kheee yani kitendo cha kutoka mimba unashukuru?”“Dokta, kulikuwa na mgogoro kuhusu hiyo mimba balaa, huyo ni binti yangu ila nashukuru kama mimba imetoka maana tulikuwa na mawazo sana”“Kivipi?”“Mara nyingine kuna vitu vingine ni Mungu tu anaviiruhusu ili kuepuka baadhi ya migogoro, nashukuru kama mimba imetoka yenyewe kuliko binti yangu angepatwa na matatizo mengine”“Mmmh!! Ila ngoja nikushauri kitu kuhusu hawa watoto wa kike”Huyu dokta alimshauri pale baba Angel, kisha alimwandikia dawa za kutumia Angel na kumpa ruhusa kuwa anaweza kuondoka nae.Kwakweli muda ulikuwa umeenda ila baba Angel muda ule ule aliondoka na mwanae kuelekea nyumbani kwake.Angel alianza kuongea kwenye gari kwa uchungu akimwambia baba yake,“Nisamehe baba, sijui kwanini inanitokea hivi mimi”“Pole mwanangu”“Hakuna kitu ambacho nimekosa kwenu kama wazazi wangu, mnanipa mapenzi ya kweli, hakuna shida ninayopata halafu nisisaidiwe, hakuna kitu ninachotaka ambacho hamkunipatia wazazi wangu hata nashangaa ni kwanini nimewatenda hivi. Nisamehe baba yangu, najua ni jinsi gani nimekudharaulisha”“Usijali mwanangu, ngoja tufike nyumbani upumzike tu halafu tutaongea kwesho”Bibi Angel nae alipiga simu ili kujua hali ya mjukuu wake maana aliona kimya kimezidi, basi baba Angel alimwambia kuwa mtoto anaendelea vizuri na wanaenda nyumbani ambapo bibi Angel aliahidi kwenda kumuona huko huko nyumbani kwao.Baba Angel na Angel waliingia saa sita usiku pale nyumbani kwao, mama Angel alikuwepo maana toka aambiwe kuwa wapo hospitali alikuwa na mashaka sana na hali ya mtoto wake, ila walivyofika baada ya salamu, baba Angel alimuomba mama Angel kuwa Angel apumzike kwanza na kama kuongea nae basi aongee nae kesho yake, ni kweli mama Angel hakubidha na kumuacha binti yake aende kupumzika.Ila walipokuwa ndani mama Angel aliamua kumuuliza mumewe ili amwambia kiundani zaidi ambapo alimweleza kuhusu kutoka kwa mimba ya Angel, yani mama Angel alifurahi sana na kumwambia mumewe,“Yani nimefurahi sana kusikia hivyo, basi kesho naomba huyu kijana Samir arudi kwao maana hapa hapa tena atampa Angel mimba nyingine maana ni rahisi zaidi”“Ila mke wangu kumbuka kuwa mtoto hachungwi, ni swala la kumfundisha mtoto tabia njema ili aweze kuishi vizuri. Hatuwezi kumchunga Angel, akiamua ataonana tu na huyo Samir hata asipokuwa hapa nyumbani. Wote wawili, Angel na Samir wanahitaji Elimu wale ili waweze kujichunga na kujitunza wenyewe wakati tukiendelea kufatilia swala la undugu wao”“Ila mume wangu, kinga ni bora kuliko tiba, tuliwahi tatizo mapema kwa kumuondoa huyu Samir hapa nyumbani, tukichekelea tu jambo hili kwa hakika tutalia sana maana mambo yatakuwa magumu zaidi”“Tutaongea kesho asubuhi mke wangu, kwasasa acha nipumzike”Waliamua kulala kwa muda huo, na palipokucha tu, alijiandaa baba Angel na kwenda kumuita Samir ili kuweza kuongea nae maana aliona ni vyema kuongea nae kwanza.Mama Angel nae ile mapema kabisa, alienda chumbani kwa Angel kuongea nae ambapo Angel alipiga magoti na kumuomba msamaha mama yake,“Naomba unisamehe mama”Mama Angel alimuinua na kumuuliza,“Kwahiyo kwasasa hutorudia huo ujinga tena?”“Sirudii mama, nimekoma na sirudii tena nakuahidi mama nitakuwa binti mzuri kwasasa”“Ukimuona Samir utafanyaje? Bado una wazo la kuoana na Samir?”Hapo Angel alikaa kimya kwa muda, ambapo mama Angel alimuuliza tena,“Ukimuona Samir utafanyaje?”“Hamna kitu mama”“Hebu kaa chini nikwambie Angel”Angel alikaa na kumsikiliza mama yake,“Mimi nilipobeba mimba yako, nilikuwa najificha kwanza ili nisionekane kama nina mimba, nilimaliza chuo ila niliogopa kurudi nyumbani maana mama angenigundua na mimba ilikuwa ni kubwa tayari, niliongea na baba yako ambapo alinitumia pesa za kupanga chumba, nikawa naishi mwenywe. Asikudanganye mtu mwanangu, mimba ya kulea mwenyewe tena kisirisiri inaumiza sana moyo, nakumbuka muda mwingi nilikuwa najiinamia na kulia sana chumbani kiasi kwamba sikuwa nakula vizuri wala nini. Mama Akatonywa na rafiki yangu, kuja kuniona ndio nilikuwa na hali mbaya, nikawahishwa hospitali na kwenda kujifungua wewe, mama yangu akawa ndio kila kitu kwangu, yeye ndio alikuwa wa kunihurumia na kunisaidia, sikuona sura wala jicho la baba yako. Nilirudi nyumbani tukakuficha ndani maana kila mmoja anaogopa ile aibu tutakayoipata ya kusema mimi nimezaa, ikiwa nilihesabika kama mtoto mwema mtaani, mtoto niliyependa masomo na dini, aibu ile ilikuwa maradufu pale baba yako alipogoma kuja kujitambulisha kwetu, alipogoma kuja kukuona mtoto wake, nilikuwa naumia kila siku, nalia sana na kumuomba Mungu anisaidie, yani kuna mwanaume nilitaka kuolewa nae, sio kwamba nilimpenda hapana, ila alinipenda sana, ila kwavile alitaka kunioa nikawa tayari kwa hilo ili kuificha aibu yangu, nilijua nitajifunza kumpenda ndani ya ndoa ila ndugu zake nao walipogundua nina mtoto wa kiarabu waligoma nisiolewe nae, na walinipa maneno ya kashfa sana, unaweza kuelewa ni jinsi gani machozi yalikuwa ndio rafiki yangu kwa kipindi hiko. Ndipo alipotokea huyu baba yako, aliyenipenda kwa dhati na alikuwa tayari kwa chochote kile juu yangu japo tulipigwa vita ila alinioa na kunionyesha mapenzi ya dhati kwangu na kwa mwanangu hadi kesho bado anatupenda sana. Tukakulea katika maadili mema na kukuepusha ili usitende ubaya, ila Angel ukaenda kubeba mimba kabla ya ndoa na mbaya zaidi umeenda kuzaa na kijana niliyekukataza kuwa naye. Unaweza kuelewa ni jinsi gani umeweza kumfedheesha na kumsononesha baba yako, unaweza kuelewa jinsi gani huyu baba anayetupenda anasononeka baada ya sisi kumlipa kwa kumfanyia mabaya badala ya mema, sijui unanielewa mwanangu?”Mama Angel alimuangalia Angel ambapo Angel alikuwa amejawa na machozi kwenye sura yake, yani Angel alikuwa akilia sana kiasi kwamba hakuweza kunyamaza kiurahisi, Angel alionekana kujutia vitu vingi sana, basi mama Angel ilibidi ambembeleze, kisha Angel alimuuliza mama yake,“Mama kwanini hukuniambia haya mapema?”“Sikutaka kukuchanganya mtoto wangu, sikutaka kukuchanganya na masomo yako, kwani siku zote unajua na kuamini kuwa huyu ni baba yako mzazi, nikajua wazi ikiwa nitakwambia kuwa kuwa mwingine ni lazima nitakuwa nimekuchanganya sana binti yangu”“Mama, nahitaji kutubu zaidi kwa baba. Ananipenda sana, kwanini mimi nimefanya hivi? Baba mzazi hakunitaka ila huyu alinipenda na bado ananipenda, ananihurumia, ananiangalia, kwanini lakini huyu hakuwa baba yangu mzazi?”“Hilo ni kosa langu mwanangu, hata mimi nilitamani sana kama huyu angekuwa ni baba yako mzazi yani ingekuwa ni nzuri sana, ila mwanangu hakuna kilichoharibika maana huyu anakupenda kwenye kiwango kile kile”“Mama, namuomba baba ili niweze kumuomba msamaha tena, mama naomba niitie baba yangu”Angel alikuwa akilia sana, na alionekana kukosa amani kabisa kwa muda huo, basi mama Angel aliinuka na kwenda kumuita baba Angel ambaye alikuwa bado akiongea na Samir, kisha alimwambia kuwa Angel anahitaji kuongea nae, ambapo baba Angel alimalizana na Samir pale na kwenda chumbani kwa Angel huku mama Angel akimfata kwa nyuma.Baba Angel alipoingia pale, Angel alianguka kwenye miguu ya baba yake huku akilia sana na kuomba msamaha kwa kile kitendo alichokuwa amekifanya, ila baba Angel alimnyanyua na kumkumbatia ingawa Angel alikuwa akilia sana,“Nyamaza mwanangu, mimi nilishakusamehe mbona toka siku ile”“Najua baba, najua sababu unanipenda sana. Nisamehe baba yangu kwa kutokuthamini upendo wako kwangu, naomba unisamehe sana”“Usijali, na Samir yupo hapa nyumbani kwani baba yake alitaka kumuua kwa kitendo hiko ila mwanangu nakuomba sana muone Samir kama kaka yako”“Ila mimi simtambui yule baba”“Sikia Angel, wewe ni mwanangu. Naomba Samir mchukulie kama mwanangu pia, mchukulie Samir kuwa mimi ni baba yake na umuheshimu kama kaka yako kutoka kwenye uzao wangu”Angel alimuitikia baba yake, kisha baba Angel aliwaaga pale kwani kuna mahali alikuwa akienda kwa muda huo.Baba Angel akiwa ofisini kwake, alifikiwa na mgeni ambaye alikuwa ni Sia, alimkaribisha na kuanza kuongea nae,“Kheee Erick hata kuniuliza kilichonileta nyumbani kwako siku ile?”“Usinilaumu yani nina mambo mengi hatari, kichwa kimoja lakini kinabeba vitu vingi sana hadi nahisi kupagawa”“Mmmmh pole sana, kwakweli nakupa pole. Unajua kuna vitu vingine vikiwa vinatokea katika maisha unajiuliza ni kwanini vimetokea ila badae unakuja kujua ni kwanini vile vitu vimetokea”“Unamaanisha nini?”Simu ya baba Angel ilianza kuita kwa muda huo na mpigaji ilikuwa ni ile namba ya Moses, basi baba Angel alipokea na kuongea nae,“Hapa ninapoongea na wewe taya inaniuma na mbavu zote zinaniuma, kwani kijana wako ni mwalimu wa karate?”“Khaaaa!! Ila Moses usiendelee kunishangaza, uliniambia kuwa umepigwa na Erick halafu nikashangaa pia, halafu muda huu unaniuliza kama mwanangu ni mwalimu wa karete, mimi na karete wapi na wapi?”“Hapana yani unajua kanipiga sana, kijana mdogo kama yule wa kunipiga hivi!! Tena alikuwa akijitapa kuwa hakuna chochote anachoogopa na kusema kwamba nisimbabaishe”“Mmmmh hayo mambo ni makubwa, ngoja nikupe pole labda utapona. Pole sana”Kisha baba Angel alikata simu, ambapo Sia nae alimuuliza maana yale maongezi aliyasikia pia,“Kapigwa na Erick huyo?”“Ndio anasema kapigwa na Erick”“Yule mtoto wako sio, yani yule mtoto wako sio kabisa, siku aliyonipiga mimi hadi nilihisi kuwa naenda kukata roho, jamani mwanao hafai. Yule mtoto namuogopa hadi leo, huwa siongei kitu mbele yake, yani mwanao Erica yupo vizuri ni mtu wa watu ila yule ni moto wa kuotea mbali”“Unajua hata mimi nashangaa kwa habari hizi”“Hebu mtafute dokta Jimmy muulize ni kitu gani alifanya kwa Erick”Basi muda huo huo baba Angel alimpigia simu dokta Jimmy ambaye alipokea na kuanza kuongea nae,“Hivi ni kitu gani kilifanyika kwa mwanangu Erick maana nasikia kawa bondia sana siku hizi?”“Katoka kuniambia Moses kuhusu hiko kitu, anaumwa sana nasikia kapigwa na Erick, halafu yule ambaye alipigwa teke na Erick siku ile ni ameumwa wiki nzima. Nimejaribu kutafakari sana sijui ni sababu Erick alipewa dawa nyingi wakati mtoto!”“Dawa nyingi!! Kivipi?”“Si nilikwambia kuwa wale mapacha wako walichomwa sindano wakati wadogo! Yule wa kiume tulimpa dawa nyingi sana ili awe wa kwanza kumshawishi mwenzie sababu watoto wa kiume huwa wanawahi kupatwa na hamu”“Mjinga wewe, kumbe ndio mlichokifanya!! Wajinga sana nyie”“Sio kosa langu Erick, nisamehe sana”“Toka hapa, mjinga wewe na ngoja awakomeshe wenyewe na ujinga wenu”Baba Angel alikata ile simu ambapo Sia alikuwa makini kabisa akisikiliza na kusema,“Itakuwa kweli, hawakuelewa mambo ya hizo dawa, ni lazima zimemuathiri Erick. Ndiomana yupo vile”“Tuachane na hayo, niambie kilichokuleta”Muda huu, baba Angel hata hakuwa na hamu ya mazungumzo wala nini kwahiyo alikuwa akiongea kwa kujilazimisha tu, basi Sia alianza kumwambia,“Ni hivi, kuna kitu nimegundua kuhusu jambo Fulani”“Ni kitu gani hiko?”“Ni hivi, nilienda kule kwenye duka lenu na kumkuta Moses kule, moja kwa moja nilihisi kuwa Moses ana mpango usiokuwa wenyewe kuhusu lile duka lako. Nilijaribu kufatilia na nilionana na mke wa Moses na kusema kuwa yeye hataki kushiriki kwenye hiyo dhambi ambayo mumewe anataka kuitenda, nasikia siku ya jana ndio alipanga iwe siku ya kuvamia duka lako, ingawa Rama kakataa ila alitaka kutumia nguvu na ndiomana nilikuja siku ile ili nikupe huo ujumbe mapema kabisa”“Asante sana kwa ujumbe, mambo yalikuwa mengi yakafanya nishindwe kufatilia ila huyo Moses kakomeshwa, kwa kipigo alichopata toka kwa Erick sidhani kama ataendelea na huo mpango tena maana sijasikia chochote, nikitoa kazini leo nitaenda kupita na dukani kwangu kuona kuna kitu gani kinaendelea kule”“Aaaah sawa, halafu nisaidie jambo moja. Nisaidie niweze kuishi na mwanangu Paul hata kidogo”“Sio rahisi hivyo, kumbuka mtoto hajakuzoea kabisa kwahiyo inatakiwa ufanye taratibu”“Nifanye vipi ili anizoee?”“Kwasasa jifunze kuwa karibu na madam Oliva ili uweze kuwa karibu na mtoto wako, na hapo anaweza kukubali kuja kuishi na wewe hata kidogo”“Ila mbona Elly amekubali kirahisi kuwa karibu na baba yake Derrick, ila mama yake ndio hamtaki”“Inategemea Elly na Derrick walikutana katika mazingira gani, ila kama nilivyokwambia kuwa unatakiw akuanza kuwa karibu na madam Oliva kwanza kabla ya yote ili ujenge ukaribu na mtoto. Yule madam ni mwelewa sana, ukiwa nae karibu utapenda zaidi”Basi Sia aliamua kumuaga baba Angel na kuondoka zake.Baba Angel muda huu alipotoka, moja kwa moja alipitia dukani kwake ili kuangalia maendeleo, alipakuta pako vizuri kabisa hapakuwa na tatizo lolote lile, na kumfanya afurahi sana ila alimuuliza kama hata jana hapakuwa na tatizo,“Jana ilikuwaje lakini? Palikuwa shwari kabisa?”“Ndio palikuwa shwari ila kuna muda alikuja yule kijana wako yani yule Erick, basi alikuwa kama anakagua kagua nje ya duka, akamuona kijana Fulani anachungulia, kwakweli alimrusha na teke hilo, yule kijana aliangukia kule barabarani, ilikuwa bado kidogo tu yule kijana agongwe na gari”Baba Angel akapumua na kushangaa sana kwani kama alikuwa haelewi na kuuliza vizuri,“Alikuwa akichungulia wapi?”“Alikuwa akichungulia hapo mbele, yani kila aliyeona tukio lile alishangaa sana. Lilikuwa ni tukio la ajabu”“Ila alipona huyo mtu?”“Ndio, aliinuka na kuanza kukimbia hata kila mtu alimshangaa ila kijana wako ni kiboko”Muda mfupi alifika Juma pale dukani na kuanza kuongea na baba Angel kuhusu Erick.Usiku wa leo baba Angel aliamua kumueleza mke wake kuhusu Erick, vile alivyoambiwa kwenye simu na Moses na vile Sia alivyomwambia na jinsi alivyoambiwa na dokta Jimmy na mambo aliyoyakuta dukani, basi mama Angel akafurahi na kusema,“Afadhali kuna bondia kwenye nyumba yangu”“Kumbe umefurahia mke wangu!”“Ndio, wangekuwa wametuibia wale wajinga, tena Erick awe anawapa kipigo cha hali ya juu. Natamani Erick akutane na huyo dokta Jimmy halafu ampe kipigo kilichoenda shule yani huyo dokta Jimmy atakuwa na heshima na adabu. Ila mume wangu haya mambo ya Erick na Erica tunayamalizaje? Maana kwasasa tumekazana na mambo ya Angel na Samir tu”“Naelewa mke wangu kuhusu Erick na Erica, yani hadi kichwa kinachanganya nikiwafikiria hawa watoto na sijui jinsi ya kuwanusuru”“Halafu nimegundua kitu”“Kitu gani?”“Inawezekana Erick akimaliza hayo mapambano yako huwa anajikuta akitamani sana kulala na Erica maana siku ile nilimkuta kalala chumbani kwakina Erica huku pembeni yake kuna Erica na Sarah”“Duh!! Mke wangu, hii hatari ujeue, yani mtu unafikiria hadi akili inaacha kufanya kazi. Kwanza hatuna uhakika kama siku ile walitoka salama kweli maana vitendo vyote walishafanya aarrghh huwa sitaki hata kuwaza mambo hayo maana hasira huzidi kwenye akili yangu aaargh”“Pole mume wangu, ila tunapofikiria maswala mengine basi tufikirie pia na hili la watoto wetu mapacha maana hatuna cha kufanya dhidi yao”“Tuache hayo kwanza, tukienda kuongea na dokta Jimmy nina uhakika tutajua vitu vingi sana, yeye ndio atatuambia cha kufanya. Sema cha muhimu kwasasa ni kutokuwapa nafasi Erick na Erica wawe pamoja kwa moda mrefu”Baba Angel aliamua kulala maana aliona kama akili yake ikigoma kuendelea kuwaza.Leo baba Angel alitaka tu kukaa nyumbani kwake bila ya kwenda popote pale, ila akapigiwa simu na Jack ambaye alimuuliza baba Angel nyumbani kwake ili aweze kwenda,“Hapana, usije kwangu niambie ulipo nije”“Sawa, ila unachonifanyia Erick sio kizuri, Mungu anakuona kwakweli”“Sikia Jack, niambie ulipo halafu nitakuja. Unanihisi vibaya, ila niambie ulipo”“Sawa, njoo tuongee vizuri”“Na mtoto upo naye?”“Ndio nipo naye”“Sawa nakuja”Basi baba Angel alijiandaa na kumuaga mke wake kuwa anaenda kwenye kazi, kisha akaondoka pale nyumbani ila mke wake hata hakumuuliza sana.Basi baba Angel njiani akampigia simu Rahim kuwa akutane nae ili aende mahali kuzungumza nae, na kweli Rahim hakuwa mbali sana na eneo alilokuwepo baba Angel kwahiyo alimwambia kuwa anaenda kuonana nae.Baba Angel alifika pale alipo Jack na kuanza kuongea nae ambapo Jack alimlalamikia sana kwa kitendo chake cha kukataa mtoto,“Unajua Erick unanisikitisha, unamkataa mtoto wetu kweli? Unajua shida niliyoipata kwa huyu mtoto hadi unafikia hatua ya kumkataa?”“Naomba unisamehe kwanza, yuko wapi mtoto?”Jack alimpigia simu na mwanae alifika pale na kumsalimia baba Angel, muda kidogo Rahim nae alifika eneo lile, ambapo baba Angel alimkaribisha pale ila Jack na Rahim hata hawakuwa watu wanaofahamiana kwani walisalimiana juu juu tu, ila Rahim alipomuona yule mtoto akasema,“Jamani, hii kopi yangu imetokea wapi?”Jack alikaa kimya akimuangalia Rahim na baba Angel na kumuuliza baba Angel,“Ni ndugu yako huyo?”“Hapana ni rafiki yangu, umeona jinsi alivyofanana na mwanao?”Jack alimwambia mwanae aondoke tena eneo lile, ambapo mwanae aliondoka halafu Jack akamuuliza Rahim,“Samahani kaka, eti mimi na wewe tunafahamiana?”“Hapana, ndio kwanza nakuona leo”“Ni hivi, yule mtoto ni mtoto wangu na nimezaa na huyu mtu hapa ila anasema mtoto kafanana na wewe, inakuwaje na mimi nimezaa na yeye? Kwakweli hakuna kitu ninachoelewa hapa, hebu jiulizeni zaidi ya urafiki mlionao nyie sio ndugu?”Baba Angel na Rahim waliangaliana na kusema kwa pamoja,“Kheee ndugu tena!!!”Kisha Rahim akasema,“Inawezekana hiyo ikawa kweli, maana huyu jamaa mke wake ana nyoto ya kutembea na watu wa ukoo wangu tu. Kwahiyo inawezekana mimi na yeye tukawa ndugu”“Acha maneno yako Rahim”“Aaaah hebu jiulize na wewe, simjui huyu mwanamke, sijawahi kumuona kabisa iweje mtoto wake afanane na mimi!! Na anadai kuwa mtoto ni wako, hata kama duniani ni wawili wawili ili ule mfanano umezidi jamani, yani hadi nilipomuona mtoto ni wazi kuwa nimejiona mimi mtupu. Erick, itakuwa mimi na wewe ni ndugu hebu tuchunguze hili, halafu mkeo ana nyoto kubwa sana ya kutembea na ukoo wangu”Hakuna kitu ambacho baba Angel alikuwa hakipendi kama kitu cha kumsema vinaya mke wake, kiasi kwamba aliona yale mazungumzo magumu sana kwake. Basi aliamua kuyakatisha kwa kusema,“Jack, naomba tumalize utata wa jambo hili, mimi nipo tayari kupima DNA na mtoto wako, kama ikikubali basi nitamkubali kuwa ni wangu hakuna tatizo juu ya hilo”“Sawa, mimi nina uhakika kuwa ni mwanao. Na vipimo vitathibitisha hilo, umeniletea huyu mtu simjui kabisa, labda nimuite shemeji”“Ila na wewe, siku zote hukuona kama mtoto hafanani na mimi?”“Mimi sikujua, nilijua kwenye ukoo wenu ndio mpo vile. Nakumbuka kuna mwaka Fulani nilikuwa nikiingia facebook nakuona umejirusha wewe na mtoto wako mmoja wa kike ambaye sura yote kafanana na mwanangu”Baba Angel alicheka kidogo na kutikisa kichwa, alihisi kamavile kuna mchezo anafanyiwa baina ya Rahim na Jack, waliongea kidogo tu halafu baba Angel aliaga na kuamua kuondoka zake.Rahim hakuondoka kwa muda huo na alitaka kuongea zaidi na Jack ila Jack aliinuka na kumuaga pia,“Mmmh hutaki tuongee kidogo”“Tuongee kuhusu nini? Mimi sio muongeaji sana, Erick ananifahamu vizuri”“Mbona unanyodo sana, umeolewa kweli wewe!!”“Niolewe ili nigundue nini?”“Mmmmh”Rahim aliishia kuguna na kumuacha huyu Jack aendelee na mambo yake mengine.Baba Angel alifika nyumbani kwake ila getini alikutana na mama yake ambaye nae alikuwa amefika kwaajili ya kumuona mjukuu wake, basi alisalimiana nae pale na kumkaribisha ndani.Walipofika mlango wa kuingia ndani, Samir alikuwa kafungua mlango akitoka basi bibi Angel alishtuka sana kumuona Samir na kumuuliza baba Angel kwa mshangao,“Ni nani huyu!?” Walipofika mlango wa kuingia ndani, Samir alikuwa kafungua mlango akitoka basi bibi Angel alishtuka sana kumuona Samir na kumuuliza baba Angel kwa mshangao,“Ni nani huyu!?”Baba Angel alimshangaa pia mama yake na kumuuliza,“Kwani unamfahamu mama?”“Hapana, ila ni nani?”“Aaaah historia ndefu mama, nitakwambia tu karibu ndani”Bibi Angel aliingia ndani ila jicho lake halikuganduka kwa Samir kwani alijikuta akimuangalia sana na kabla ya yote alitaka kutambulishwa kwa Samir kwanza kuwa ni nani, ikabidi baba Angel amuulize mama yake kuwa anafikiria ni kitu gani.“Kwani mama unafikiria ni nani maana uleshtuka sana na bado unamuangalia?”Bibi Angel alikuwa akiongea kiutaratibu na mwanae sasa,“Weee mbona huyu kijana kafanana sana na baba yako! Yani kipindi cha ujana wao ndio alikuwa hivi hivi, yani huyu ni mzee Jimmy mtupu”“Mmmmh mama!”“Ndio, hamjawahi kuona picha za baba yenu za ujana wake? Alikuwa hivi hivi, yani kila kitu khaaa, hebu niambie ni nani?”Baba Angel alipumua kidogo, akakumbuka mambo ya mtoto wa Jack, akakumbuka jinsi Rahim alivyosema huenda yeye na Rahim wana undugu, basi akafikiria kidogo na kusema, hapana kisha akamuuliza mama yake,“Mama,kwani mzee Jimmy alikuwa na mtoto mwingine?”“Mmmh yule baba yenu alikuwa na matatizo ya kizazi haswaaa, awe na mtoto mdogo hivyo!! Mimi nilijua huenda ukasema kuwa huyo ni mtoto wako, ulizaa huko nje maana nyie watoto wa kiume mna mambo sana, mwanamke akiolewa ajue tu kuna siku mambo yataripuka yani muda wote awe tayari kwa chochote. Kwahiyo huyo kijana ni mtoto wa nani?”“Ni mtoto wa rafiki yangu mama”Bibi Angel akaomba kutoka nje kidogo na baba Angel, kisha alienda nae moja kwa moja kwenye bustani ambapo bibi Angel alimuuliza baba Angel,“Hebu niambie ukweli mwanangu, huyu mtoto sio damu yako kweli?”“Mmmh sijui mama”“Naomba kamuulize vizuri mama wa huyu mtoto, hamfahamiani kweli?”“Aaaah mama, huyo mamake niliwahi kuwa na mahusiano nae zamani”“Inawezekana ikawa ni damu yako ila alikuficha maana sisi wanawake tunamatatizo sana ikiwa mwanaume kakuudhi, mara nyingi unaamua kumfanya mtoto ni wako peke yako sababu baba yake alikuumiza sana. Hebu muulize vizuri ila nina uhakika asilimia mia moja kuwa hii ni damu yako, ingekuwa mzee Jimmy alikuwa na uwezo wa kuzaa tena baada ya wewe basi ningesema huyu ni mtoto wake ila mzee Jimmy alipata matatizo ya kizazi, halafu usifikirie ni mtloto wa mdogo wake mzee Jimmy labda ndio kamzaa huyo mtoto hapana, mzee Jimmy kwao alizaliwa peke yake ndiomana alikuwa na mali nyingi sana kwani ukoo mzima walikuwa wakimthamini yeye, na babu yao alikuwa ni mwenye pesa nyingi kwenye kijiji chao, kwahiyo alimtoa mjukuu wake kule na kumpa mali nyingi sana. Kwahiyo, nina uhakika asilimia mia moja kuwa hii ni damu yako”Yani baba Angel alipumua ila alijiona kuwa na mawazo zaidi, maana kama Samir ni damu yake, je ataweza vipi kuliweka sawa swala hilo? Na je ni kivipi ikiwa yeye na mamake Samir waliachana sababu ya yeye kumsababishia yule mwanamke mimba itoke!! Alijikuta akikaa kimya kwa muda huku akimtazama mama yake ambaye alimwambia tena,“Ukoo wenu sio mkubwa, kusanya vitoto vyako, bile mwenyewe katika mstari. Kwangu upo peke yako, kwa baba yako mpo wawili tu, kusanya hao ndio ndugu zenu wa badae. Nimemaliza, ila yule ni mjukuu wangu”Kisha bibi Angel akauliza alipo Angel ili akamsalimie, yani baba Angel alimpeleka mama yake huku akiwa na mawazo sana juu ya kile ambacho mama yake amekiongea kwake kwa muda huo.Basi baba Angel alirudi sebleni huku akimuangalia sana Samir, yani kwa muda huu alimuangalia sana hakuweza hata kummaliza, alijiuliza maswali mengi sana kuwa kama kweli Samir ni mtoto wake ila hakupata jibu la moja kwa moja.Basi bibi Angel alipotoka alimtaka mwanae amsindikize kidogo, ingawa alikuwa na gari ila alitaka mwanae amwendeshe kidogo ambapo baba Angel alitoka kumsindikiza mama yake.Wakiwa kwenye gari, bibi Angel alirudia tena yale maneno yake,“Wakati wa kutoka tena nimemuangalia sana yule kijana, aaaah yule ni mwanao lazima ni mwanao Erick”“Mmmh ila mama, siku ya kwanza nakutana na yule kijana nilimfananisha sana na jamaa fulani hivi”“Acha kujidanganya Erick, labda kama unajifananisha nae mwenyewe, yule mtoto ni damu yako.”Baba Angel alikaa kimya ila mama yake aliendelea kuongea,“Jumamosi nitakuuliza kama tayari ushaongea na mama wa mtoto, akigoma nenda kapime damu na mtoto yule maana ni damu yako”Yani baba Angel alishindwa kuongea kwakweli na kukaa kimya tu, mpaka pale mama yake aliporidhika basi yeye alishuka na kurudi nyumbani kwake ambapo tayari ilikuwa ni usiku.Mama Angel alimuuliza mumewe kitu ambacho mama yake alishangaa kumuona Samir,“Alishangaa sana halafu alikuwa kama anakunong’oneza kitu, mara ukatoka nae nje ni kitu gani hiko”“Aaaah mama alikuwa kiuliza ugonjwa wa Angel, mbona alishaacha kumshangaa Samir yani yeye alichokuwa akishangaa ni kuwa yule kijana anafanya nini hapa nyumbani kwetu. Nilipomwambia ni mtoto wa rafiki yangu akaridhika”“Aaaah kumbe!! Eeeeh umemwambia Angel alikuwa akiumwa nini?”“Hivi mama Angel, mwanzoni kabisa nilipomuona Samir nilikwambia namfananisha na nani?”“Mmmmh hata hukuniambia ila ulisema kuwa kuna mtu anafanana nae tena ulisema mtu huyo namfahamu ila hukuniambia hadi leo kuhusu huyo mtu”“Aaaah nilifikiri nilimtaja?”“Hapana, ni nani uliyekuwa ukimfananisha na Samir?”“Aaaah ni Rahim”“Rahim wapi? Yule mtoto hata hafanani na Rahim sijui na yeye kachomekewa”Halafu mama Angel alianza kucheka ambapo baba Angel akamuuliza,“Kama wewe ulivyonichomekea Angel?”“Mmmh jamani yamekuwa hayo tena!! Wewe si ulimkubali Angel ilihali unafahamu kila kitu!! Tuachane na hayo mume wangu, tujadili maswala ya watoto”“Eeeeh Angel anaendeleaje”“Hajambo kabisa, anaendelea vizuri”Baba Angel hakutaka kuongea sana kwa muda huo kwani aliona akili yake kama imevurugika hivi, kwahiyo aliamua tu kulala.Leo baba Angel alimuita Samir mapema kabisa kwenye bustani yao na kuanza kuongea nae,“Eti Samir, huwa baba yako unamuonaje yule?”“Sijawahi kumuelewa tangu nilipokuwa mtoto, sijui kama ni baba yangu yule”“Kwa mfano mama yako akakutambulisha baba yako mwingine utafanyaje?”“Nitafurahi tu, maana yule baba hata huwa simuelewi”“Jiandae, kuna mahali nataka kwenda na wewe”Basi Samir alijiandaa kisha alitoka na baba Angel na moja kwa moja baba Angel alienda na Samir nyumbani kwa Tumaini, wakati huo alikuwa amemtumia ujumbe Tumaini kuwa amuangalie sana huyu kijana ambaye anaenda nae nyumbani kwake.Walipofika ni kweli Tumaini nae aliguna na kuwasalimia pale kisha alimvuta nje kaka yake na kumuuliza,“Erick, ndio matunda yako yameanza kuonekana nini?”“Kivipi?”“Unafikiri mchezo!! Wale wanawake wote uliokuwa ukiwapa mimba kipindi kile na kuwatoa, wapo ambao walitunza”“Kwanini unasema hivyo?”“Hii damu yetu hii, umekuja kunionyesha shangazi yangu eeeh!!”“Aaaah sio hivyo, unaona kafanana na nani huyo mtoto?”“Kuna picha za baba akiwa mvulana mdogo yani hivyo hivyo kama huyo kijana. Siku nikienda kule nyumbani nitaenda kuzipekua, Erick kwakweli una damu kali mdogo wangu”“Hivi hujawahi kumuona huyu kijana eeeh!!”“Sijui kama nimewahi kumuona, nahisi sijawahi kumuona ila nimefurahi kumjua. Kumbe tuna kijana mkubwa hivi, nilijua Erick ndio mkubwa pekee”“Aaaah Tumaini acha zako bhana”“Halafu sikukwambia, jana kuna maeneo nilikuwepo halafu akapita Erick nikasikia wanasema duh yule kijana ni hatari sana, mwengine akasema anacheza kungfuu huyo, duh sikusema kitu maana hawakujua kama wanayemuongelea ni damu yangu”“Mmmh dada, mambo ya Erick yaache kwanza. Nilimleta huyu kijana umuone basi”“Nimemuona na nimemkubali kuwa ni wa kwetu”Hapo baba Angel hakuwa na usemi zaidi basi walirudi ndani ambapo Tumaini alienda kuwaandalia chakula ili waweze kula pale nyumbani kwake.Walipoanza kula tu, simu ya baba Angel iliita ikabidi atoke nje na kuipokea maana aliyekuwa akipiga ni Jack,“Samahani Erick, naona kila siku hatuelewani. Ni hivi, mtoto huyu kuna binti alimpa mimba, yule binti kajifungua leo, ile familia wanahitaji twende kujitambulisha. Ndiomana siku zote hizi nilikuwa nakukazania ili ujue kuwa mtoto wako anahitaji kutambua kwamba ana baba yake”Baba Angel akapumua kidogo na kusema,“Nimekuelewa Jack, mmepanga kwenda lini?”“Wiki ijayo”“Sawa hakuna tatizo, tutaenda wote. Nishtue tu siku ikifika”Basi baba Angel alikata ile simu na kurudi ndani kuendelea kula, na baada ya muda waliondoka zao.Jioni ya leo, Angel alitoka na kwenda kukaa kwenye bustani yao ambapo Erica nae alienda kukaa nae karibu na kuongea nae,“Unaendeleaje dada?”“Sarah yuko wapi?”“Amelala, ila nimekuuliza unaendeleaje?”“Kwani nilikuwa naumwa?”“Ndio, si ulikuwa na mimba wewe imetoka!”“Mama amekwambia?”“Hapana”“Ila umepata wapi hiyo habari?”“Nimeota”“Umeanza mambo yako ya ndoto, haya hiyo mimba ni ya nani ilikuwa?”“Nimeota kuwa ulipata mimba ya Samir, siku ile mliyosababisha moto. Halafu baada ya kugundua, baba na mama wakakukimbizia kwa bibi ambapo kuna siku hukula na ukikuwa ukilia sana, ukahisi kizunguzungu na kuanguka hakuna aliyejua, ulizinduka ukiwa mwenyewe chumbani, bibi akakuuliza ukasema uitiwe baba ndio baba akaitwa ukapelekwa hospitali na kukuta mimba imetoka”“Kheee nimekuvulia kofia wewe mtoto jamani, hebu niambie kwenye ndoto zako unaona mimi nitaolewa na nani?”“Niliwahi kuota kuwa wewe unaolewa na huyo huyo Samir ila kuna utata mkubwa sana ulitokea maana kila mtu alikuwa akipinga kuoana kwenu na wakidai kuwa nyie ni kama ndugu”“Ni kama!! Kwahiyo sisi sio ndugu?”“Sijui kitu, nakueleza vile nilivyoota”“Wewe Erica, unapata wapi uwezo wa kuota vitu vyote hivyo?”“Hata mimi sijui, kuna ndoto zingine hata kusema huwa naogopa maana zinakuwa na makubwa ndani yake”“Kama ndoto gani?”“Kama ndoto ya kuhusu mimi na Erick”“Eeeeh wewe na Erick mmefanyaje?”“Ipo siku nitakwambia ila sio leo. Sema pole sana dada yangu, haya ni mapito tu, kuna muda utazoea na kusahau kama kuna kitu cha namna hii kimepita katika maisha yako”“Wewe bado mdogo ila mara nyingine una maneno ya busara sana. Yani Sarah ndio mvivu kama mimi jamani, hebu kamuamshe”Basi Erica alienda ndani kumuamsha Sarah ambaye aliamka na kutoka na Erica hadi kwenye bustani, halafu Angel alimwambia Sarah“Yani wewe unapenda kulala jamani, utapata wapi muda wa uwaza maendeleo? Muda wa kuwaza mahali pa kupatia pesa?”“Kwanini niwaze vyote hivyo dada?”“Kwanini?”“Mimi kwetu ni mtoto wa pekee, baba yangu aliniachia mali nyingi sana, hapa unavyoniona nina nyumba tatu, nina mashamba makubwa matatu, nina ile shule kubwa sana. Baba yangu alikuwa akinipenda sana, na hakutaka nipate shida duniani, namshukuru mama kwa kunitafutia baba kama yule”“Mama yako akiviuza je?”“Angeviuza wakati nipo mdogo ila sio kwasasa hivi nikiwa mkubwa hivi, mama hana kiburi cha kufanya chochote bila ridhaa yangu. Ila kwa jinsi ninavyowapenda Erick na Erica basi najitolea kugawana nao mashamba yangu yani kila mmoja atachukua moja moja”“Kheee na mimi je dada mkubwa?”“Wewe nitakupa nyumba”Walicheka pale, walijua ni maongezi tu ya kumaliza siku yani hakuna aliyetilia maanani yale yote yaliyokuwa yakizungumzwa mahali pale.Usiku wa leo, Erick akiwa chumbani kwake alifatwa na Erica ambaye alianza kuongea nae, kwanza alimuita“Erick”Erick akageuka maana alikuwa akiangalia sehemu nyingine, kisha akasema,“Erica umenishtua sana yani sijui nimehisi vipi”“Pole sana, leo ulikuwa wapi?”“Aaaah kwanini umeuliza hivyo? Mbona siku zote huniulizi?”“Aaaah nimekuuliza leo tu”“Kama kawaida nilikuwa kiwandani”“Umemfanya nini yule meneja wa pale kiwandani?”“Mmmh!! Umeanza mambo yako hivyo Erica!! Sijamfanya kitu ila nimempa onyo basi”“Duh!! Ila Erick mambo yako ni hatari sana”“Kwahiyo siku hizi unaniogopa Erica?”“Hapana, ila watu wanakuogopa Erick”“Achana nao Erica, njoo ukae hapa karibu tuongee ya maana basi”Erica alisogea karibu na kukaa kitandani pamoja na kaka yake ambapo Erick alikaa kimya kwa muda bila kuongea chochote na kumfanya Erica amuulize,“Mbona huongei kitu sasa?”“Sijui ni nini, nashangaa siku hizi ukiwa karibu yangu nashindwa kukwambia chochote kile Erica, sijui tatizo ni nini”“Pole”“Je unaweza kunifanyia tena kama siku ile?”Erica alihisi kusisimka mwili mzima na kuinuka kisha akamuacha kaka yake mule chumbani mwenyewe kwani hakutaka tena kutenda kile kile alichokitenda na kaka yake.Kulivyokucha, mama Angel alimtaka mumewe anywe chai kwanza kabla ya kwenda ofisini, basi walikaa mezani na kuanza kuzungumza,“Hivi yule dokta Jimmy si mlipanga kukutana baba Angel, ungemkumbusha kabisa ili tujue ni wapi tutakutana nae”“Nitamuuliza ila lazima twende na madam Oliva maana yule dokta haaminiki ujue, asije kutufanyia kitu mbaya”Erick alikuwa akipita ila mama yake alimuita ili nae anywe chai kwanza,“Si unaenda kiwandani mwanangu!!”“Ndio mama”“Njoo unywe chai kwanza halafu ndio utaenda huko”Basi Erick alikaa pale na kunywa chai huku baba Angel na mama Angel wakiendelea kuongea ambapo mama Angel alisema,“Simpendi dokta Jimmy”Baba Angel akadakia,“Nadhani hunifikii mimi mke wangu, ningekuwa na uwezo wa kumfanya chochote dah basi tu. Ila muache atupe siri kwanza”“Najua unachuki nae sana ila anagalia usitende dhambi”Waliongea pale, kisha baba Angel aliondoka zake, halafu Erick nae aliondoka zake kuelekea kiwandani.Baba Angel akiwa ofisini kwake kwa siku ya leo, alifuatwa na yule bibi muuza matunda ambaye huwa siku zote yupo hapo akiuza matunda yake, basi aliingia ofisini kwa baba Angel na kumwambia,“Leo, nimekuletea zawadi”“Kheee zawadi gani?”Bibi alitoka nje na kumkaribisha mgeni aliyeambatana nae na kumwambia baba Angel,“Haya sasa, Juli huyu hapa”Baba Angel alifurahi kiasi na kusalimiana na yule Juli huku akiongea nae mambo mbalimbali,“Yani kumbe Juli, siku zote hizi nipo na mama yako mzazi hapa”“Unajua nilishangaa sana siku ile wakati naongea nawe kwenye simu kwa kupitia simu ya mama. Ndiomana nimerudi nikamwambia mama cha kwanza kabisa naomba unipeleke kwa boss Erick ili nikamsalimie”“Oooh vizuri sana, nafurahi kusikia hivi”Muda kidogo alifika mgeni mwingine kwenye ofisi ya baba Angel, mgeni huyu alikuwa ni Juma ambaye alifika na kuwasalimia kisha kuanza kuongea pale,“Yani dunia ina mambo yaliyojificha sana, mimi sikujua kama kuna ndugu yangu huyu. Nafurahi kukufahamu Juli”Walipongezana pale, kisha Juli alihitaji kupafahamu nyumbani kwa baba Angel sababu aliwahi kuongea na mke wake,“Nahitaji kumfahamu na yeye anifahamu maana kipindi kile alinihisi vibaya sana”“Sawa, basi nikitoka tu ofisini hapa tutaenda wote nyumbani kwangu”Kisha Juli na mama yake walitoka kwanza kumsaidia mama yake kuweka matunda vizuri kwanza, halafu baba Angel alibaki pale na Juma huku wakiongea,“Unajua Erick ni bondia sana”“Umeanza Juma”“Kweli, nilimshuhudia pale dukani kwako akimpiga mtu mmoja dah!! Erick ni bondia, ana nguvu ambazo niliwahi kusikia kuwa babu yangu anazo”“Kwahiyo bado una wazo kuwa Erick ana husiana na wewe!!”“Hapana, nimesema tu. Siwezi sema nahusiana na Erick maana mimi sijawahi kuwa na mke wako hata mara moja”“Haya, ngoja nimalize kazi kwanza”Baba Angel alimaliza kazi zake na moja kwa moja kuondoka na Juma, pamoja na Juli na mama yake kuelekea nyumbani kwake.Muda huu Erick alikuwa dukani kwa baba yake ambapo alikuwa akiongea na Rama kuhusu kilichoendelea baada ya siku ile,“Kitu gani kilitokea? Wale watu walirudi tena?”“Hapana, sikuwaona wala nini”Muda kidogo kuna mteja alifika pale dukani kwa baba Angel na kuanza kuulizia baadhi ya vitu, ila Erick alimfata huyu mtu na kumuuliza,“Jina lako nani?”“Kwani unanijua?”“Nakujua ndio, unaitwa nani?”Huyu mtu alihofia kidogo na kutoka mule dukani kwa kasi halafu akaondoka zake, ila kitu ambacho hakukifahamu ni kuwa Erick alikuwa akimfatilia kwa nyuma, alipofika tu nyumbani kwake alishangaa nuona Erick nae amefika basi huyu mtu aliogopa hata kutoka ndani ya gari lake, ila Erick alisogea karibu na gari la huyu mtu na kuvuta mlango ambao ulifunguka na kumtoa huyu mtu nje, akamkaba na kumuuliza tena,“Ni nani wewe?”“Aaaah, mimi ni dokta”“Dokta huna jina?”“Naitwa dokta Jimmy”“Huwa nasikia baba akikutaja taja sana sijui umemfanyia nini na siku ile ambayo baba alitekwa ni wewe nilikukuta lile eneo la tukio”Kisha Erick alimpa ngumi ya mdomo dokta Jimmy kiasi cha kumfanya kuanza kutoa damu mdomoni ila Erick hakujali kitu chochote kile zaidi ya kumshindilia ngumi nyingine, halafu akamwambia,“Maswala ya wewe kufatilia familia yangu sitaki kabisa kusikia, nikiona baba akilalamika tena kuhusu wewe utanitambua mjinga mmoja wewe”Kisha Erick alimpiga mtama dokta Jimmy na kumfanya aanguke chini halafu alienda na kumpiga teke ambalo lilienda kumuangusha karibu na getini kwake. Halafu Erick akaenda kupanda pikipiki yake na kuondoka maana kwa kipindi hiko alikuwa akitumia zaidi usafairi wa pikipiki.Usiku wa leo, baba Angel anapigiwa simu na Jack ambapo anapokea na kuanza kuongea nae,“Tutaenda kumuona kesho, kwahiyo sio Jumamosi bali ni kesho”“Sawa hakuna tatizo, utaniambia muda na mahali pa kuelekea”“Nakutumia kwenye ujumbe”Muda kidogo ujumbe ulitumwa ambapo baba Angel aliusoma na kufuta ujumbe ule kwani hakutaka mkewe aone ule ujumbe wa kwenye ile simu. Kisha aliendelea na maongezi mengine na mke wake,“Kwahiyo yule wa leo ndio alikuwa Juli yule aliyekuwa akikufanyia usafi?”“Ndio, ni yule, ndiomana siku ile nilikwambia mke wangu usiwe na mashaka, huyu ni mama mwenye heshima zake. Ndiomana na yeye ametaka kuja kukusalimia”“Yule Juma nae ana kiherehere, sasa kilichomleta na yeye ni kitu gani?”“Unajua yule ni ndugu yake!! Yani ni ndugu yake kabisa, kwahiyo usishangae kwa yeye kuja pamoja nao wale”“Sasa mbona alikuwa na haraka sana ya kuwaharakisha wenzie kuondoka?”“Aaaah yule Juma mzoee tu hata usiwe na shaka nae”Waliongea ongea kupoteza muda tu kwa usiku ule.Muda huu baba Angel alijiandaa, kisha akaondoka nyumbani kwake na kumpigia simu Rahim huku akimwambia mahali pa kukutana, yani bado alikuwa na imani kuwa yule mtoto ni mtoto wa Rahim.Wakakutana na kisha kukutana na Jack na mtoto wake halafu wakaanza kuondoka, Rahim aliamua kuuliza,“Kwani tunaenda wapi?”“Huyu kijana kazalisha bhana, ndio tunaenda kumuona mtoto kama wazazi”“Kheee na mimi ndio nimewekwa kwenye kundi la wazazi?”“Ndio kwani kuna ubaya, hebu ona mtoto ulivyofanana nae Rahim yani ni wewe mtupu”“Halafu huyu kijana hata hamjanitajia anaitwa nani”Jack aliyekuwa kimya tu, akasema“Anaitwa Derrick”Baba Angel akashtuka kidogo maana hakujua jina la huyu mtoto, akamuuliza kwa makini Jack,“Anaitwa nani?”“Anaitwa Derrick, nilimpa jina ili aendane na wewe. Kwahiyo ni Derrick Erick”“Duh!”Baba Angel alipumua tu na walifika mahali walipokuwa wanaenda, ila muda wote huyu kijana Derrick alikuwa kimya kabisa, inaonyesha hata yeye hakuwaelewa hawa watu maana aliambiwa mmoja ni baba yake ila hakuona huyu mtu akijali lolote.Walipoingia kwenye hiyo nyumba ndipo Rahim alipopatwa na mshtuko, mara kuna mama alitoka ndani ya ile nyumba na kusogea karibu na Rahim kisha akamnasa kibao yani kila mtu alikuwa akishangaa kwanini huyu mama kamnasa kibao Rahim. Walipoingia kwenye hiyo nyumba ndipo Rahim alipopatwa na mshtuko, mara kuna mama alitoka ndani ya ile nyumba na kusogea karibu na Rahim kisha akamnasa kibao yani kila mtu alikuwa akishangaa kwanini huyu mama kamnasa kibao Rahim.Kisha yule mama alianza kumwambia Rahim,“Mjaa laana wewe, ulimkimbia mwanangu toka akiwa na mimba haya leo nini kimekuleta?”“Dah!! Nisamehe”“Nani akusamehe? Mjinga sana wewe, umekuja kufanya nini? Ndio umekuja kumuona mjukuu wako? Na mjukuu mwenyewe alivyokufanana ni balaa”Basi huyu mama alimshika mkono Rahim na kumuingiza ndani na hawa wengine walibaki kushangaa tu kuwa ni kitu gani kinaendelea.Moja kwa moja Rahim aliingizwa ndani ambapo palikuwa na binti amepakata mtoto mchanga akimnyonyesha, huyu mama alimwambia Rahim“Haya sasa, umemuona binti yako na mjukuu wako!! Maana huyu binti hujawahi kumuona toka mama yake akiwa na mimba ya miezi sita, ukakimbia mazima, haya muone sasa”Rahim alibaki kutoa mimacho tu, huyu mama aliangalia wale waliokuja na Rahim na kumtambua Erick,“Kheee Erick!! Mbona leo makubwa haya, unanikumbuka mimi lakini? Umekuwa mbaba siku hizi!”“Nakukumbuka ndio, wewe si mama mdogo wa Sia”“Oooh kweli unanikumbuka jamani, umemtoa wapi huyu kiumbe mjinga aliyekimbia mtoto wake!! Mwanaume mjinga sana huyu, hivi mtu unawezaje kukimbia mtoto wako eeeh!! Haya angalia sasa hadi linaona aibu”Sasa ilibidi Erick aulize vizuri,“Kwahiyo, huyu kijana ndio amezaa na huyu binti”Akimuonyeshea Derrick, hapo yule mama akamuangalia na Derrick pia maana hakuwahi kumuona, basi alihamaki na kusema,“Kheee mbona kijana mwenyewe kafanana na huyu mjinga Rahim? Inamaana watoto wa Rahim mmetembeleana na kuzaa!”Huyu mama alipiga makofi na kucheka kisha akakaa chini na kusema,“Dunia ndogo hii, huwa watu mnaona dunia ni kubwa sana huenda mkajificha na maovu yenu ila hii dunia ni ndogo sana. Ona kilichotokea sasa, watoto wa baba mmoja mjinga wameenda kuzaa na kuendeleza kizazi, na mimi nawaambia hivi wajukuu zangu mmepata baraka zote kutoka kwangu, mtaoana tu hakuna cha ndugu wala nini, hii ndio dawa ya wanaume wakware”Kwakweli Rahim alikuwa kimya tu ni kama mtu aliyepigwa na bumbuwazi yani alikuwa ni kama anashangaa kila kitu kinachoongelewa, kisha yule mama akaongea tena,“Yani Rahim limekushuka shuu, umekuwa mdogo kama piritoni hapo ulipo mbele huchezi na nyuma hutikisiki, ulikuwa unanikera nikikukumbuka wewe mjaa laana loh!! Nasema hivi mjukuu wangu hata mahari sitaki, semeni tu lini mnaenda kuanza kuishi pamoja. Liacheni libaba lenu hili lililojaa laana mpaka kwenye unyayo, mjinga sana wewe, hodari kuwaambia wanawake wakuzalie halafu hodari kwa kukimbia watoto.”Yani kwa ufupi hata walishindwa kufanya mazungumzo yoyote pale, Rahim alimshika mkono baba Angel na kutoka nae nje ili waweze kujadiliana maana hakuelewa kabisa,“Unajua hapa nilipo sielewi kitu?”“Kwani huyu mama unamjua kweli?”“Ndio, niliwahi kuwa na mahusiano na binti yake, nakumbuka vizuri nilimuacha akiwa mjamzito”“Kheee basi shughuli ipo”“Ila huwezi amini, Erica ndio alifanya mimi nimuache huyu mwanamke”“Halafu na Erica mwenyewe ulimuacha akiwa na mimba, nahisi una aleji na wanawake wenye mimba wewe”“Lakini yule mama sio muelewa, kaniparamia tu kuwa yule ni mtoto wangu pia. Mmmmh au kweli yule kijana ni mtoto wangu!! Naanza kupata mashaka, inabidi mniruhusu nikapime na yule kijana, ila kama wote ni watoto wangu nitafanyaje? Mbona kichwa kinaniuma jamani. Ya Angel na Samir hayajaisha halafu linaibuka hili lingine uwiiii mimi jamani nitajificha wapi. Naondoka Erick”Rahim alimuacha baba Angel pale na kuondoka zake maana alihisi akili yake kutokuwa sawa kabisa kwa muda huo, baba Angel nae alijikuta akikosa maamuzi sahihi na kutaka kuondoka ila aliamua kumuita Jack kwanza na kuongea nae pale nje,“Samahani Jack, mimi naomba niende”“kwahiyo unaniacha peke yangu na mtoto!!”“Hivi Jack, hukusikia kile kilichokuwa kinaendelea au kitu gani?”“Nimesikia vizuri, alikuwa akisemwa yule mwenzio kwani ni wewe uliyekuwa unasemwa? Ukweli wa mtoto tunao mimi na wewe”“Hapana, ukweli unao wewe. Si unaona hata yule mama alipomuona kijana wako Derrick kashtuka na kusema ni mtoto wa Rahim, ni wazi kuwa mwanao kafanana sana na Rahim. Hebu jaribu kuchunguza hili”“Nichunguze kitu gani wakati mimi najua kuwa baba wa mtoto ni wewe!!”“Basi Jack, naomba uniruhusu niondoke halafu kesho tutaonana na tutaongea vizuri, sawa”Jack hakuitikia ila alimuangalia tu baba Angel ambaye aliondoka zake kwa muda huo.Baba Angel alipotoka pale moja kwa moja alipitia kiwandani na kuanza kukagua maana ni muda mrefu hakuja kwenye kiwanda chake, mara nyingi alikuwa ofisini kwake kwahiyo huku kiwandani ni Erick tu ndio alikuwa anakuja.Basi alitembelea na kwenda kuongea na meneja wa kiwanda chake yani Yuda, alimkuta mkononi kafunga hogo yani mkono unaning’inia tu, ikabidi baba Angel amuulize,“Tatizo nini Yuda?”“Kwani hujaambiwa?”“Niambiwe na nani?”“Shughuli ya Erick hii”“Kheee Erick!! Ilikuwaje tena?”“Dah!! Sina hata cha kusema, ila bora hapa ofisini uwe unakuja mwenyewe, zamani tulikuwa tunaona Erick mpole sana kumbe ni tofauti hakuwa mpole wala nini. Humo kiwandani wafanyakazi wote hao wanamuogopa Erick balaa”“Kwani ilikuwaje?”“Aaaah mimi sijui ila alinikunja mkono tu na kusema ananipa onyo, yani mkono umeniuma sana, nimeenda hospitali ndio nimefungwa hilo hogo”“Duh!! Pole sana. Kwakweli sikuwa nafahamu hayo kabisa”“Yani mwanao siku asipokuja basi wafanyakazi wote hapa huhisi kufanya sherehe, mwanao ni mkali hatari”“Ila naona kiwanda kimeendelea, ufanisi wa kazi umeongezeka”“Ni kweli, Erick hataki masikhara kabisa, mtu akiharibu kumwambia sitaki kukuona kazini kesho kwake ni kawaida, kwahiyo wafanyakazi wengi wamekuwa makini. Kwa hilo nampongeza sana ila apunguze ukali wake”Baba Angel aliahidi pale kuwa atazungumza na kijana wake, kisha alivyoondoka hapo moja kwa moja alienda dukani kwake napo kuangalia kuwa kuna nini kinaendelea katika duka lake.Basi alivyofika kule alimkuta Rama na kumuuliza maendeleo ya pale,“Bosi, jana kuna mteja alikuja hapa na alikuwa akiulizia bidhaa vizuri tu. Mara alitokea Erick na kumfata yule mteja huku akimuuliza kuwa anaitwa nani, yule mteja naona aliogopa na kuamua kuondoka ila Erick alimfatilia na pikipiki yake, sijui ni kitu gani kilitokea huko ila Erick hakurudi tena hapa”“Khaaa sasa Erick kavuka mipaka sasa, ubondia hadi kwa wateja jamani!”“Ndio hivyo bosi, na sijui kwanini Erick hakumtaka yule mteja. Mbona wengine huwa anawahudumia mwenyewe na huwa wanampenda sana na kumuulizia kila wanapokuja ila nashangaa sana kwa mteja wa jana”Baba Angel hakutaka kuongea sana ila aliona kuwa kuna ulazima wa yeye kuongea vizuri na Erick maana aliona kuwa amevuka mipaka. Kwahiyo aliondoka hapo dukani na kuelekea nyumbani kwake.Baba Angel alifika nyumbani kwake wakati giza tayari lilikuwa limeshatanda, ila alivyofika tu moja kwa moja alihitaji kuongea na Erick, kwahiyo aliulizia kuwa Erick yuko wapi,“Khaaaa mbona Juma alikuja kumfata Erick muda ule ule ulipoondoka wewe”“Kheee kaenda nae wapi? Mbona hajaniambia?”“Nikajua mliongea maana jana mlikuwa wote, kwahiyo Juma aliondoka na Erick na bado Erick hajarudi hapa nyumbani”“Duh!! Na Samir je?”“Samir aliondoka pia, alisema anaenda kwa mama yake”“Aaaah mbona hajaniaga na yeye!!”“Unadhani mtoto wa mwenzio ni sawa na mtoto wako!! Yeye anajichukulia maamuzi yake mwenyewe, nadhani mimi kaniaga sababu nilikuwa hapa nyumbani”“Aaaah sawa hakuna tatizo, kama mama yake na baba yake wamepatana basi sawa”“Hivi yule dokta Maimuna anajua kweli kama sisi ndio wazazi wa Angel?”“Sidhani kama anajua, kumbuka hata sisi tumejua baada ya kuwaona kwenye mahafali, kwahiyo sidhani kama anajua”Basi wakaacha ile mada na kuendelea na mambo mengine, hadi baba Angel aliamua kulala bado Erick alikuwa hajarudi, ilibidi mama yake tu ndio amsubiri kwanza arudi nyumbani.Erick alifika nyumbani kwenye mida ya saa tano usiku, kwakweli mama yake hakupenda na alimsema kwa tabia hiyo,“Sijapenda kabisa Erick, siku hizi umefanya kama mazoea ya kunirudia usiku kwanini lakini?”“Nisamehe mama”“Huangalii muda huko unapokuwa? Unafanya roho yangu iwe juu juu muda wote, yani sijapenda kabisa kabisa, halafu mtu mwenyewe uliyeondoka nae ni Juma, kumbe hata ruhusa kwa baba yako hajaomba. Hiyo tabia isijirudie tena”“Sawa mama”Basi moja kwa moja Erick alipitiliza chumbani kwake, alioga na kulala ila muda kidogo Erica alienda chumbani kwa Erick na sahani ya chakula kisha akamuamsha na kumtaka ale,“Umejuaje kama sijala Erica?”“Najua tu kama hujala, mama kakusema na wewe hupendi kusemwa. Una hasira za karibu sana Erick, ila mimi nakuomba ule hiki chakula nilichokuletea”Basi Erick alikaa na kaunza kula kile chakula huku akiongea na dada yake,“Mlienda wapi leo Erick?”“Aaaah yule jamaa unajua ananipelekaga kwenye vitu vya hatari sana”“Vitu gani?”“Tulienda huko kwenye mizinga ya nyuki eti kumsaidia kupakua asali”“Mmmh nyuki hawajakuuma kweli?”“Wala hawajaniuma, nilikuwa naogopa ila nikajipa ujasiri tu, kisha akanielekeza cha kufanya basi nikawa nafanya nae”“Hukuogopa kweli!! Nyuki naogopa mimi”“Hamna hata hawafanyi kitu, tutapanga siku twende pamoja”“Sawa Erick”Erick aliendelea kula ila kuna muda alikuwa akiona uvivu kubeba kijiko na kula chakula, basi Erica akajitolea kumlisha kwa muda huo kwani alikuwa akijua wazi kuwa kaka yake hajashiba kile chakula, muda kidogo akaingia baba yao mule chumbani kwa Erick na kumkuta Erica ndio akimlisha Erick chakula, kiukweli baba Angel alichukia sana na kuwauliza,“Ndio mambo gani hayo?”“Erick amechoka kubeba kijiko baba, ndio namsaidia kumlisha”“Huyo wa kumpiga kila mtu ndio achoke kubeba kijiko tu! Nyie watoto jamani, msitutie simanzi wazazi wenu, kumbuka tunawapenda sana. Hii imezidi sasa ila nitajua tu cha kufanya, haya Erica nenda chumbani kwako.”Ikabidi Erica aache kumlisha Erick na kuondoka zake kisha baba Angel alimwambia Erick,“Kesho nina maongezi na wewe”halafu baba Angel alitoka zake na kurudi chumbani kwake tu kwa muda huo.Baba Angel alimwambia mkewe ndani,“Ni bora tu ningeendelea kulala kuliko niliyoenda kuyashuhudia huko”“Yapi tena hayo?”“Nimekuta Erica akimlisha chakula Erick, jamani hawa watoto kwasasa wamevuka mipaka. Hivi hawakufanya kweli hawa?”“Mmmmh inawezekana wamefanya, labda tunafuga viwapenzi humu ndani, aibu yetu ni kubwa mno.”“Sasa tufanyaje mama Angel?”“Mmmh sijui yani watoto wananipa mawazo hawa hatari”“Unaonaje tukimtafutia Erica shule ya bweni huko awe harudi hapa nyumbani maana naona hii ya kurudi inampa kiburi sana”“Mmmmh hiyo ya bweni si ndio atarudi na akili kama za dada yake Angel, maana karudi na msemo wake tumefundishwa kujiamini, yani mitoto isiyojua kutafakari ni shida tupu”“Basi, ngoja tufikirie mambo mengine, maana naona akili yangu haifanyi kazi vizuri kabisa”Baba Angel aliamua kulala tena kwa muda huo, ila muda kidogo alikuwa akipigiwa simu, alipoangalia aliona ni Jack ndio aliyekuwa akipiga ile simu basi alikuwa akiikata na mwisho wa siku akaizima kabisa maana ulikuwa ni usiku na hakutaka mkewe amfikirie vibaya.Asubuhi na mapema, baba Angel kama alivyopanga alimuita Erick ili aongee nae kuhusu swala lake la kupiga hadi wateja na swala la kupiga Yuda,“Erick mwanangu, nimeenda jana kiwandani nimemkuta Yuda ana hogo, tatizo ni nini kwani? Kwaniniumempiga?”“Baba, yule Yuda alikuwa na mtindo mchafu, alikuwa akitoa bidhaa kwa njia za panya na kwenda kuziuza huko. Sasa nilipomgundua ndio nikampa onyo”“Kwahiyo pale umempa onyo!!”“Ndio, sijampiga yule, nimempa onyo tu”“Duh!! Ila Erick sijapenda, unapiga hadi wateja”“Mteja gani baba?”“Juzi dukani, nasikia umemtisha sana mteja”Simu ya baba Angel ilianza kuita muda ule kwahiyo baba Angel aliacha kuongea na Erick kwanza na kupokea ile simu na kuanza kuongea nayo maana aliyekuwa akipiga alikuwa ni madam Oliva,“Hivi unakumbuka kuwa ni leo ndio tulipanga kuonana na dokta Jimmy!”“Oooh umenikumbusha, yani nilishasahau, ngoja nimtafute nijue pa kukutana nae.”“Pa kukutana nae wapi? Huyo dokta Jimmy yupo hoi nyumbani kwake”“Anaumwa nini tena?”“Nimempigia simu anasema kuwa kuna mtu kampiga sana, kwahiyo hali yake sio nzuri hata ongea yake ni ya shida”“Duh!! Na yeye kapata kiboko yake kumbe!! Ila ni jambo la muhimu sana kuongea nae”“Ndio hivyo haiwezekani ila yeye anasisitiza kuusema ukweli wote, nadhani tu tupange siku twende kwake ili tukaongee nae pale pale wala huo ugonjwa usiwe kisongizio”Basi madam Oliva alikata ile simu halafu baba Angel alitabasamu kidogo maana kusikia kuwa dokta Jimmy kuna mtu kampiga kwake ilikuwa amani, ukizingatia alijikuta huyu dokta hampendi tu kwa yale aliyomtendea. Kisha baba Angel akauangali Erick na kumuuliza tena,“Eeeeh hatujamalizana, kwanini umpige mteja”Erick alimsimulia baba yake ilivyokuwa hadi alivyomfata huyo mteja, yani baba Angel alijikuta baada ya maelezo haya akifurahi sana, hata hakumuuliza swala lingine Erick ila moja kwa moja alienda kwa mke wake na kuongea nae,“Hatimaye zile dawa walizozifanya kwa watoto wetu zimeenda kuwarudi wenyewe”“Kivipi?”“Nasikia Erick kampa kichapo dokta Jimmy kiasi kwamba dokta Jimmy hawezi kwenda popote pale, anaongea kwa shida tu. Hakuna siku niliyofurahi kama leo, nilikuwa nahitaji sana dokta Jimmy aingie kwenye anga za Erick na hatimaye kaingia na kapata kichapo chake. Kumbe yeye ndio alikuwa mteja”“Mmmh alikuwa mteja kweli au alikuwa na mambo yake!! Mbona bora jamani, simpendi yule baba hatari”Baba Angel alicheka tu na kwenda kujiandaa kwaajili ya kutoka tu kwa muda huo.Baba Angel alienda moja kwa moja ofisini kwake kwa muda huo ila alipofika tu alianza kupigiwa tena simu na Jack,“Kwani uko wapi baba Derrick”“Duh!! Nishakuwa baba Derrick tayari”“Acha masikhara jamani, sasa unadhani nimezaa na nani mimi? Unajua unanichanganya sana Erick jamani!!”“Basi yaishe, nipo ofisini kwangu muda huu”“Ila kwanini unanifanyia hivi Erick? Kwanini lakini, simu zangu unakata, hutaki kuongea na mimi unachonifanyia sio kizuri kabisa. Naomba nielekeze ofisini kwako basi ili niweze kuja tuzungumze”“Sawa nakuelekeza, huwezi potea maana sio mbali wala nini”“Sawa, hakuna shida nasubiri”Basi baba Angel akamtumia Jack maelekezo ya ilipo ofisi yake kisha aliendelea na kazi zake.Ila mpaka muda baba Angel anamaliza kazi zake hakuweza kumuona Jack wala nini, akaamua kumpigia simu mwenyewe ili aongee nae,“Mimi ndio nataka kuondoka Jack, au utakuja kesho?”“Kesho utakuwepo ofisini?”“Hapana, kesho nitakuwepo nyumbani labda uje kesho kutwa”“Basi nielekeze nyumbani kwako”“Aaaaah hiyo ni ngumu Jack, unajua mke wangu hajui kitu chochote kuhusu mimi na wewe!”“Ila ndio anapaswa kujua hivyo, una nini lakini Erick jamani. Tena nyumbani kwako ndio itakuwa vizuri ili nimlete Derrick aonane na ndugu zake”“Aaaah Jack, sikia basi, tutawasiliana tu kesho halafu mimi kesho kutwa nitakufata mwenyewe tuongee”“Kwani kuna nini nikija nyumbani kwako Erick?”“Sio kwasasa Jack, nakuomba sana utakuja siku nyingine. Mimi na wewe tutaongea Jumatatu”Baba Angel alikata ile simu na kupumua kidogo huku akisema,“Huyu mwanamke anataka kuniletea balaa huyu, anataka kukumbusha mambo ya zamani yaliyopita, namshangaa kuzidi kukazana kuwa mtoto ni wangu wakati picha halisi ya yule mtoto inaonekana kuwa ni mtoto wa Rahim. Au ananichezea mchezo huyu na Rahim wana lengo la kugombanisha ndoa yangu!”Baba Angel aliamua kufunga kazi na kuondoka zake kwa muda huo kuelekea nyumbani kwake.Erick, leo alikuwepo tu nyumbani na dada zake akiongea nao kuhusu vitu mbalimbali maana leo ilionyesha kuwa ana furaha tofauti na siku zingine, hata Angel alimuuliza Erick,“Mbona leo una furaha sana?”Sarah akasema,“Huyu anatakiwa kuwa na furaha siku zote maana amezungukwa na wadada, anakosaje furaha? Na sasa nimeongezeka na mimi?”Angel alimuuliza Sarah,“Yale mashetani yako ya kumtaka Erick umeyaacha eeeh!!”“Aaaah nitamtaka vipi wakati nijua ukweli kuwa ni ndugu yangu!! Sina sababu ya kuendelea kumtaka ndugu yangu. Ila jamani tuongee ukweli, Erick ni mzuri jamani halafu ana mwili wa kiume”“Mmmmh na wewe Sarah una mambo, kwani kuna wanaume wana mwili wa kike?”“Ndio, wapo wengine wamelegea sana”“Mfano kama nani?”Erick aliamua kuwabadilishia stori, yani siku hii walionekana kuwa na furaha sana. Hata mama Angel alipowaangalia alihisi raha moyoni mwake kwani siku zote alikuwa akitamani kuona watoto wake wakiwa na furaha, hasa alikuwa akipenda kuona wakipatana sana na Sarah maana hata Sarah alimuweka kama moja ya familia yake, kwahiyo ile hali aliifurahia sana.Muda kidogo alifika mgeni ambaye alikuwa ni Sia, basi mama Angel aliamua kwenda kuongea nae ili kujua ni kitu gani kimemleta pale kwake,“Eeeeh Sia, niambie”“Nimekutana na Manka”“Eeeh anasemaje?”“Unajua Manka ni kama amechanganyikiwa kwasasa eeeh!! Hajielewi kabisa yule mwanamke, bado anakazana kuwa Sarah ni mwanae pia wakati Sarah ni mtoto wa Oliva”“Ila na wewe muda mwingine umezidi, kama siku ile ulichokifanya hata sijakipenda, mtu gani umemkuta tu hapa madam basi kuropoka ndio moto, yani wewe mambo yako jamani unajijuaga mwenyewe”Mara simu ya Sia ilianza kuita na hapo baada ya Sia kuongea nayo tu akamuaga mama Angel na kuondoka zake.Usiku wa siku hii baba Angel na mama Angel walikuwa chumbani wakijadili kuhusu kesho yake,“Mmmh kesho twende Kanisani mume wangu, unajua hatujaenda siku nyingi!!”“Halafu kweli mke wangu, hatujaenda siku nyingi kweli sijui siku hizi tumepatwa na kitu gani”“Watoto leo walikuwa wamepatana sana hadi raha, nimefurahi kwa wanangu kuongea vizuri na Sarah”“Aaaaah yule mtoto yupo vizuri, mwanzoni hakufundishwa vizuri tu. Saivi nimemuona amekuwa na adabu sana”Walijikuta wakiongea mengi tu kwa siku hii na kuamua kulala.Kulipokucha tu, mapema kabisa baba Angel alipata ujumbe kwenye simu yake na kuamua kuusoma, ujumbe ule ulitoka kwa Jack ukisema,“Jana, nilikuja ofisini kwako nimekufatilia hadi nyumbani kwako. Nashukuru sana nimepafahamu nyumbani kwako kwahiyo nitarajie kwa siku yoyote na muda wowote kuja hapo, mwambie kabisa mke wako kuhusu uwepo wangu”Baba Angel alishtuka kidogo na kutoka nje kisha akampigia simu Jack ambaye alipokea na kuanza kuongea nae,“Una nini lakini Jack? Wewe ni mwanamke muelewa, kwanini unataka kufanya ujinga wa namna hiyo?”“Huu sio ujinga, kwanini hutaki mkeo ajue ukweli? Kwanini unaficha Erick? Mimi nitaendelea kumficha huyu mtoto hadi lini?”“Naomba tukutane tuongee Jack”Jack akakata ile simu, baba Angel akafikiria kwa muda kidogo kama kweli amwambie mkewe kuhusu swala lile, yani hakuelewa hapo.Baba Angel alirudi chumbani ambapo mke wake alikuwa akijiandaa kwaajili ya kwenda kwenye Ibada, kisha baba Angel alikaa kwanza ambapo mkewe alimuuliza,“Tatizo ni nini mume wangu? Jiandae basi twende”“Unafikiri najisikia! Yani sijui leo nipoje”“Sio leo upoje, kwasasa huwa sikuelewi maana kuna simu Fulani hivi huwa unaongea nayo kwa siri halafu ukimaliza kuongea nayo huwa sikuelewi kabisa, huwa sikuulizi tu ila najua wazi kuwa haupo sawa, tatizo ni kitu gani”“Basi njoo tukae ili tuweze kuzungumza kuhusu hili jambo”Mama Angel alikaa ila baba Angel alimwambia mama Angel kuwa wakanywe chai kwanza halafu ndio waongee vizuri kuhusu hilo analotaka kumwambia, kwakweli mama Angel alimshangaa sana mumewe.Leo mamake Samir yani dokta Maimuna alijiandaa na Samir kwani alitaka mwanae ampeleke huko kwa wazazi wa Angel ambapo ndio alikuwa akiishi huko, Samir alikubali. Kisha na mama yake waliondoka kwao na kuanza safari ya kwenda kwakina Angel.Samir na mama yake walifika pale ila mama yake alishangaa kidogo maana pale alikuwa akipafahamu vizuri sana, ila hakuongea kitu chochote kile na moja kwa moja wakagonga geti na kuingia ndani.Na hapo walifika kugonga mlango wa ndani hodi, alitoka Erica na kuwafungulia ila wakati wanaingia tu ndipo Jack nae alipofika mahali pale na mtoto wake Derrick. Samir na mama yake walifika pale ila mama yake alishangaa kidogo maana pale alikuwa akipafahamu vizuri sana, ila hakuongea kitu chochote kile na moja kwa moja wakagonga geti na kuingia ndani.Na hapo walifika kugonga mlango wa ndani hodi, alitoka Erica na kuwafungulia ila wakati wanaingia tu ndipo Jack nae alipofika mahali pale na mtoto wake Derrick.Kisha Maimuna na Jack walitazamana kwa muda kidogo ambapo Jack alimwambia Maimuna,“Wewe si ndio dokta Maimuna!!”“Ndio ni mimi”Basi Maimuna na Jack walikumbatiana pale, muda huo Erica nae alikuwa anaendelea kuwakaribisha kiasi kwamba baba yake na mama yake walikuwa wakishangaa kuwa huyu Erica anawakaribisha wakina nani, baba Angel akainuka kwenda kuangalia kuwa ni kitu gani kinaendelea, alipomuona Jack na Maimuna moyo wake ulifanya paaa, na kilichomshtua zaidi ni kumuona Jack maana hakutegemea kama Jack angefika pale kwao, basi alitoka nje kwa haraka ili aweze kuongea nao ila mkewe nae alikuwa ametoka pia.Kwahiyo hakuwa na namna zaidi ya kuwakaribisha tu, ila baba Angel alijua wazi kuwa lazima hapo kitanuka tu na hakutaka watoto wasikie, kwahiyo aliwaomba hawa wakaongee kwenye bustani ambapo Mimuna aliuliza,“Kwani unajua kilichotuleta? Yani mfano mimi unajua ni kitu gani kimenileta?”“Hapana, ila twendeni tukaongee pale maana hata nimeshangaa kuwa mnafahamiana”Waliongozana tu mpaka kwenye bustani, muda huo wote mama Angel alikuwa akishangaa tu kwani hakuelewa chochote kile kilichokuwa kikiendelea.Wakina Samir pamoja na yule Derrick ilibidi tu waingie ndani na kukaa pale sebleni pamoja na wenzao wengine, huku Derrick akijitambulisha kwao hawa halafu na wao wakijatambulisha majina yao kwake,“Nashukuru kuwafahamu”Basi Samir akamwambia Derrick,“Dah!! Umefanana sana na baba yangu, yani baba yangu ni kopi yako kabisa”Angel nae akadakia,“Kumbe na wewe umeona eeeh!! Kafanana sana na baba yako, halafu na yule ndugu yako Muddy kafanana nae sana.”Derrick alicheka tu jinsi alivyofananishwa na watu wale kisha akawaambia,“Huyo mnayemsema nimeonana nae na kila mtu ananifananisha nae, mwanzoni nilikuwa simjui basi watu wengi walikuwa wakisema kuwa nafanana na Rahim nilibaki kuwashangaa tu ila kwasasa nimemjua na kweli nina fanana nae”Samir akamuuliza,“Au ni ndugu yetu wewe, maana mimi ni mtoto wa Rahim!”“Aaaah, baba yangu mimi anaitwa Erick”Wote ndani walishtuka na kumuangalia vizuri, pale alikuwepo na Sarah ambaye alishangaa kwa sauti na kusema,“Kheeee, mbona wewe kama mwarabu!!”Kisha Sarah akajijibu mwenyewe,“Ila hata dada Angel nae ni mwarabu.”Samir akasema,“Watoto wababa wote ni waarabu kasoro mimi tu”Ndipo Erica alipouliza,“Kwani da Angel ni mtoto wa baba yako pia?”Angel aliamua kubadilisha mada na kuwauliza wanapenda sinema gani ili waweze kuangalia kwa muda huo kuliko kuongelea yale waliyokuwa wakiongelea maana hakuona kama yana umuhimu kwa muda ule.Walipofika kwenye bustani mama Angel aliwakaribisha pale ila alihitaji utambulisho hasa kwa Jack maana hakumfahamu, baba Angel aliomba kuwa akaongee pembeni kidogo na Jack ila Jack aligoma na kusema,“Pembeni tukatafute nini Erick? Hukuamini kama nitakuja nyumbani kwako au nini? Sina nia ya kuharibu familia yako ila nina nia ya mwanangu kuwatambua ndugu zake”Hapo baba Angel aliamua kuwa mpole tu, kisha alimuuliza Maimuna,“Na wewe dokta!”“Mimi nilikuja hapa na mwanangu Samir, nia yangu ni kuangalia sehemu aliyokuwa anaishi, nimeshangaa kukuta kuwa alikuwa anaishi hapa. Kumbe yule Angel niliyekuwa namsikia ndio mtoto wa Rahim!!”Mama Angel alijibu tu kwa taratibu,“Ndio”“Kumbe mlizaa na mume wangu, mbona ulikuwa ukificha jambo hili mama Angel! Siku zote ulikuwa rafiki yangu mkubwa sana, ila nilishangaa siku uliyomuona mume wangu pale hospitali ukapotea kimoja.”Halafu dokta Maimuna akamuangalia Jack na kumuuliza,“Mwanao yuko wapi?”“Si ndio yule niliyekuwa nimeongozana nae! Nadhani yupo kule kunisubiria, huyu ndio mwanaume niliyezaa nae”Kwakweli mama Angel alikuwa haelewi kitu kwa muda huo, alikuwa akimuangalia tu mume wake ambapo baba Angel aliamua kusema,“Sikia Jack, umechukua uamuzi wa haraka sana kufika nyumbani kwangu, kwanza sijajiridhisha kuwa yule ni mwanangu. Dokta Maimuna, wewe ni daktari, nenda kamthaminishe yule mtoto vizuri uone kama kafanana na mimi. Mtoto kafanana na Rahim kwa kila kitu halafu uje nyumbani kwangu na kusema kuwa ni mwanangu! Nilikwambia tuongee kwanza Jack ila ukawa mbishi, hivi unadhani kwa stahili hii ndio kitu gani utakuwa umefanya sasa?”Dokta Maimuna alipumua kidogo kwanza, na kuwaangalia ambapo mama Angel aliuliza,“Mnajua siwaelewi, hebu nielewesheni”“Ni hivi, mimi nilikuwa na mahusiano na Erick kipindi yupo Afrika kusini na aliniacha na ujauzito halafu akaja huku, nilizaa mtoto na kumlea mwenyewe, na sasa mtoto amekua anamuhitaji baba yake, ndio nimemleta”Mama Angel alimuangalia vizuri huyu dada, alijikuta akikumbuka kipindi akiwa chuo aliwahi fatwa na Tumaini na kuambiwa kuwa baba Angel yani Erick anamchumba Afrika Kusini na amepanga kumuoa mchumba wake huyo, kisha alimuonyesha picha, alimkumbuka vilivyo ingawa kwa kipindi hiki alikuwa kanenepa nenepa ila sura yake haikubadilika sana, alimtazama na kumtazama baba Angel kisha akamuuliza,“Ndio huyu mwanamke ambaye nilikuwa naonyeshwa picha zake na Tumaini?”“Mke wangu, hayo tutazungumza wenyewe, ngoja tumalize haya kwanza”Jack alijibu,“Ndio ni mimi, nilikuwa nawasiliana mara kwa mara na huyo wifi yangu Tumaini, kwanza anafahamu wazi kuwa mimi nina mtoto wa ndugu yake”Mama Angel alipumua kwanza na kuamua kukaa kimya kwa muda, kisha baba Angel akasema,“Tumekusikia, ila mbona mtoto hajafanana na mimi? Siwezi kumkubali mpaka pale nitakapopima nae vinasaba”Hapo dokta Maimuna aliyekuwa kainama tu alikohoa kwanza na kufanya washtuke kidogo kisha akasema,“Jamani sijui nisemaje, sijui kama naweza kueleweka, sijui kama manaweza kunielewa. Naomba nisamehewe kwanza”“Kwanini”“Sikutegemea kama kuna siku kama hii itatokea katika maisha yangu, ila nilitegemea kuwa kuna siku nitasema ukweli kabla sijaingia kaburini, naomba mnisamehe sana”“Kwani tatizo ni nini Maimuna?”“Naomba unisamehe sana Jack, nisamehe dah sikutegemea jambo kama hili”“Jambo gani?”“Kwanza sikujua kama umezaa na Erick, sikujua kabisa, huyu ni mwanaume niliyekuwa namchukia maisha yangu yote. Nakumbuka stori za mimi na wewe hatujawahi kuwaongelea kuhusu wanaume waliotuzalisha maana walikuwa ni wabaya kwetu, ila naomba unisamehe Jack”“Kwani ni kitu gani?”“Naomba tu niseme ingawa sikutegemea kama nitasema siku ya leo ila pia sitegemei kwa mtu mzuri kama Jack kuumbuka kwa makosa yangu”“Sema nikusikie Maimuna”“Niliwahi kuwa na mahusiano na Erick hapo kabla, ila alinifanyia kitu kibaya sana, nilipata mimba ya kwanza akasababisha ikatoka, nikapata mimba ya pili napo akaniletea ujinga wake wa machungwa na mimba yangu ikatoka. Nikamchukia sana Erick, yeye pamoja na wanaume wengine nikajikuta nayachukia mapenzi kupita maelezo, ila akaja mwanaume mmoja wa kuitwa Rahim ambaye alionyesha kunipenda sana tena sana, nakumbuka kipindi hiko nilikuwa nipo kwenye mafunzo ya vitendo. Rahim akanipa mimba na kuniacha kwenye mataa, aaah nilichukia sana, nikiwa na mimba yangu nikamfumania Rahim na wanawake mara tano, nilikosa amani ya moyo, sikumpenda hata kidogo, nikahisi kama moyo wangu umeingia donge zito, huwezi amini nilikuwa natamani hata mimba itoke, sikufikiria kama nitampenda mtoto ambaye nitakuwa nimezaa na Rahim. Nikaitwa na mjomba wangu mmoja ana hospitali Afrika Kusini kwani aliambiwa kuwa nina msongo wa mawazo, alisema niende kule ili akili yangu ikae sawa, na nifanye kazi pale kwenye hospitali yake na kweli nilikuwa pale na kufahamiana na Jack. Huyu Jack alikuwa akija mara kwa mara pale hospitali na nilikuwa naongea nae sana, na yeye alikuwa akisema jinsi mwanaume alivyomtenda ila hakusema kama ana hasira nae, sema nilihisi tu kuwa atakuwa na hasira nae. Siku ambayo Jack aliletwa akiwa na uchungu mkali, ni mimi niliyempokea hospitali na kumpeleka leba, ila na mimi nilishikwa na uchungu muda ule na kupelekwa chumba kingine kwaajili ya kusaidiwa, kweli sikukawia kujifungua ila muda niliojifungua ndio muda aliojifungua Jack, watoto wetu walikuwa wakihudumiwa na dokta mmoja wa kuitwa Samir, nilijikongoja na kumfata kwenye sehemu ya watoto kumbuka nilikuwa ni mtu wa pale kwahiyo nilikuwa na kibali cha kuingia popote, nilipofika nilimng’ang’ania dokta Samir anipe mtoto wangu, basi alinipa ila mimi nilimkazania yule wa Jack kwani nilijua wazi sababu yule mtoto simjui uhalisia wake basi nitamlea kiukweli kweli, na mwanangu alelewe vizuri na Jack ambaye anaonekana bado ana mapenzi na baba mtoto wake. Hata dokta Samir alinishangaa sana ila nilimtunuku kwa kumoa mwanangu jina lake”Baba Angel akamkatisha kidogo dokta Maimuna na kumwambia,“Inamaana Samir ndio mtoto wa Jack, halafu mtoto wa Jack ndio mtoto wako”“Ndio, naomba mnisamehe sana”Baba Angel alipumua kwanza maana kama hakuelewa kitu vile, kwakweli Jack alikuwa akishangaa sana huku akimuangalia dokta Maimuna na kumwambia,“Sikuelewi”Mama Angel nae akadakia,“Yani mimi ndio sielewi chochote kinachozungumzwa hapa, kwahiyo Samir ni mtoto wako Erick? Kila siku unasema kuna mtu unamfananisha nae kumbe ni mwanao!!”“Aaaah mke wangu tutaongea vizuri, ngoja tumalize hili kwanza.”Kwa busara baba Angel aliona ni vyema hapo wamuache dokta Maimuna na Jack waongee wenyewe na wakubaliane wenyewe sababu wao ndio wahusika wakuu wa watoto wao na ndio wanajua ni kitu gani kilichotokea.Baba Angel alienda pembeni na mke wake huku akiongea nae kwa taratibu,“Natumaini mke wangu utanielewa”“Sio nitakuelewa, nishakuelewa ila sijui kwanini Tumaini kanificha kuhusu hili”“Sio wewe tu hata mimi nilikuwa sijui, nadhani hakutaka kuweka mgogoro baina yetu. Mengine tutaongea vizuri zaidi tukiwa chumbani, ngoja wayaweke sawa wenyewe”“Kwahiyo, Samir ni mtoto wako?”“Tutaongea vizuri”“Mmmmh makubwa haya, dunia ina mambo sio ya kitoto duh!!”“Usijali mke wangu tutaongea tu”“Ila bado najiuliza, kwahiyo Rahim alimuoa dokta Maimuna huku akiamini kuwa Samir ni mtoto wake!!”Basi Dokta Maimuna aliwaita kuwa kashamaliza kuyapanga na Jack, walirudi pale na kusikilizana nao, baba Angel aliwauliza,“Mmefikia muafaka?”“Ndio, mwanangu mimi ni mtoto wa Jack, na mtoto wangu ndio mtoto wenu na Jack. Kwamaana hiyo Samir ni mtoto wako na Jack. Nimemuelewesha Jack, sikumchukua kwa ubaya Samir, nimejitahidi kumpa mapenzi yote na kumlea kama mama kwani najua wazi kuwa hata mwanangu nae anapendwa vizuri na kulelewa vizuri. Kama shule nzuri Samir nimempeleka na mapenzi yote nilimpatia kama mama, hata mkimuuliza Samir atawaambia kwanza nina uhakika hawezi kuamini kama mimi sio mama yake mzazi”Mama Angel aliuliza,“Ila ngoja nikuulize dokta, ulipata ujasiri gani wa kuchukua mtoto wa mwenzio na kulea wewe halafu kuacha mtoto wako kwa mwenzio, yani ulijiamini nini? Na siku zote Rahim alijua kuwa Samir ni mtoto wake? Kwani wewe na Rahim mlioana kwa kipindi gani?”“Sidhani kama maswali yako hayo ni muda muafaka wa kuyajibu, kumbuka mtoto wa kwanza nimezaa na Rahim, nimembadili bila ya yeye kujua, alivyorudi badae alirudisha mapenzi kwangu na kumuhudumia mtoto ingawa alikuwa na mke wake, ila hapo nilizaa nae mtoto wa pili ndipo alipoamua kumuacha mkewe na kunioa mimi, sijawahi kumwambia ukweli kuhusu Samir, siku zote anajua kuwa mtoto ni wa kwake, ila mtoto sio wake nilimbadilisha. Sikumjua baba wa Samir kuwa ni wewe, nadhani ningemjua nisingeweza kumuiba wala nini. Nisameheni kwa hiki kilichotokea. Haya tuzungumze yangu, ila sijui kama kunahitajika maelezo maana mambo yamegeuka zaidi ukizingatia huyo Angel ni mtoto wa Rahim ila kalelewa na wewe Erick, wakati huo Samir ni mtoto wako ila kalelewa na Rahim, hapo sijui nini kitatendeka. Ila kwa ushauri wangu, naomba jambo hili nilichukue kisaikolojia, sio jambo la kukurupuka kuwaambia watoto, nitajua jinsi nitakavyoongea na Samir na nina uhakika atanielewa ila sijui kama atakubali kuniacha mimi, halafu Jack utaongea na mtoto wako ila cha muhimu usimwambie kuwa mimi simpendi, mwambie nilikosea, nitakwambia jinsi ya kumwambia ili aweze kuelewa, halafu mimi na wewe Jack tutakutana na watoto wetu na tutaongea nao vizuri kabisa. Kwahiyo kazi ni kwako Erick kumkubali mwanao, na huyo Rahim nitaenda kuongea nae na kumuelewesha pia kuhusu huyu mtoto wake wa ukweli. Naomba kwa leo yaishie hapa, Jack nenda na Derrick kama ulivyokuja nae na mimi naondoka na Samir kama nilivyokuja nae, halafu tutakutana tena, tusiongee chochote hapa tutachafua tu hali ya hewa”Waliweza kumuelewa huyu dokta Maimuna, na walikubaliana nae vizuri kabisa kwahiyo kwa muda huo waliweza kila mmoja kuondoka na mwanae na kusema kuwa wataenda kuongea vizuri wakiwa nyumbani kwao.Baba Angel na mama Angel kwa siku ya leo bado hawakuwa sawa kabisa, baba Angel alimuomba mke wake kuwa watoke kidogo kwaajili ya mazungumzo yani waende mbali kidogo kama walivyokuwa wakifanya kipindi cha katikati, kwani aliweza kuona ni jinsi gani mke wake alivyokosa amani juu ya jambo lile jambo.Mama Angel na baba Angel walitoka na kwenda kwaajili ya maongezi, kwahiyo moja kwa moja walienda kwenye hoteli na kuagiza vinywaji huku wakinywa, baba Angel alimuomba msamaha tena mke wake,“Naomba msamaha kwa hili lililotokea, natumai umenielewa mke wangu”“Hakuna tatizo nimekuelewa mbona. Hivi mimi nishindwe kukuelewa kwa hili kweli!! Ulinikubali mimi nikiwa na mtoto wa mwanaume mwingine, halafu mimi nisindwe kukuelewa wewe kuwa na mtoto mwingine nje wakati tabia yako ya mwanzo naijua fika ilivyokuwa. Mtoto angekuwa mdogo hapo sawa, ningekuuliza imekuwaje mume wangu hadi ukaenda kuzaa na mwanamke mwingine ndani ya ndoa yetu? Ila mtoto ni mkubwa yule, naulizaje sasa? Nimekubali kwa mikono miwili kuwa ni mtoto wetu na tutaishi nae tu hakuna tatizo”“Nimefurahi kusikia hivyo mke wangu, unajua nini ni mama ndio alinishtua kuhusu Samir, baada ya kusema kafanana sana na mzee Jimmy enzi za ujana wake, mama alisisitiza nimfatilie Samir ili nijue ukweli wake maana mama alihisi kuwa Samir ni mtoto wangu kabisa”“Aaaah kumbe ndio siku ile!”“Ndio, yani ile siku mama alinikazania sana nimueleze ukweli kuhusu Samir, hata nilipomwambia kuwa ni mtoto wa rafiki yangu, bado hakunielewa kabisa”“Haya, sasa utaenda kumuelewesha, najua atafurahi. Hatimaye tumeongeza mtoto mwingine wa kiume maana tulikuwa na Erick pekee ila bado natumaini kuwa Erick atabaki kuwa mtoto wako wa pekee au nakosea?”“Ni kweli, nampenda mwanangu Erick na nitawapenda wote pia. Sasa ngoja nikwambie jambo lingine”Baba Angel alimuelezea mke wake kuhusu ile safari ambayo alienda na Rahim na kukutana na yule binti aliyezalishwa na yule kijana Derrick, mama Angel alishtuka sana na kusema,“Kheee huyo Rahim kama alichangayikiwa juu ya Samir na Angel basi kwasasa ndio atachanganyikiwa maradufu, duh mbona ni hatari sana”“Ni hatari kweli, ila hata kwetu hakuna usalama mke wangu. Kumbuka Angel ni mwanangu halafu Samir ni mwanangu pia na wale watoto wanapendana kama na wao walipewa dawa aliyopewa Erick na Erica dah!! Sijui hata tunafanyeje?”“Na nijuavyo akili zao wale, wakijua ukweli tu basi tujue ndio mimba ya pili ipo mlangoni, inatakiwa tufanye juhudi za mapema kunusuru hili jambo. Mimi ndio hata sielewi, nikiwafikiria Erick na Erica ndio napata kichaa kabisa yani”“Mmmh turudi nyumbani mke wangu, hakuna ninachoelewa hapa kwa muda huu kwakweli”Waliongea kidogo kisha kuinuka na kurudi nyumbani tu.Kulivyokucha siku ya leo, baba Angel alienda zake ofisini kwake kama kawaida na kuanza kazi zake ila muda kidogo alifika pale Erick akiwa na sare za shule na kuanza kuongea nae,“Erick, leo vipi mbona upo hapa muda huu na sio shuleni?”“Aaaah baba kuna jambo nataka tuongee”“Jambo gani hilo?”“Unajua leo shuleni, asubuhi kabisa kaja yule sijui mamake Sarah, yule ambaye alikuwa akija na Sarah kipindi kile”“Eeeh alikuwa akitaka nini?”“Aliniita ofisini na kuanz akuongea na mimi, tulibaki wawili tu yani mimi na yeye”“Alikuwa anasemaje sasa?”“Ameniambia kuwa, katika maisha yake hakuwahi kufikiria jambo ambalo limetokea kwake. Anasema alikuwa akiamini kuwa Sarah ni mwanae ila kaambiwa kuwa mwanae ni Elly na kapewa uhakika, anasema kwamba bado anajipa moyo kuwa Sarah ni mtoto wake yani anaamini kuwa alijifungua watoto mapacha sababu mpaka leo haijulikani wazazi wa Sarah wako wapi, ila kaniuliza swali moja ambalo nilishindwa kumjibu kwakweli”“Swali gani?”“Kaniuliza kuwa ikitokea mimi na Sarah ni mapacha je mimi nitafanyaje? Yani kama Erica sio pacha wangu, sijamuelewa ana maanisha nini? Kwani Sarah ni mtoto wa nani na kwanini imekuwa hivi?”Baba Angel alipumua kwanza kwani hapa aliona ni pagumu sana kwake kisha akasema,“Huyo mwanamke lazima atakuwa na wazimu tu sio bure, nyie wote ni watoto wangu yani wewe na Erica”“Na Sarah je? Maana mama huwa anasema kuwa Sarah ni mwanae!”“Ndio huwa anasema hivyo sababu Sarah ni mtoto wa mjomba wenu Derrick, kwahiyo kama ni mtoto wa kaka yake basi na yeye ni mtoto wake pia. Usijali maneno ya huyo mama, ni amechanganyikiwa”“Basi Sarah mama yake ni nani?”“Huyo huyo mama Sarah ndio mama yake na Sarah, achana na hayo mwanangu. Ndio kimekutoa shule hiko?”“Ndio baba, yani nimejikuta nakosa amani kabisa. Nampenda sana dada yangu Erica”Baba Angel akaguna na kuinuka kisha akamwambia Erick,“Nikurudishe shule mwanangu, achana na hayo mambo”“Hapana, siwezi kurudi tena shule muda huu, acha tu niende kiwandani”“Basi twende wote”Baba Angel alikamilisha kazi zake pale na kuondoka na kijana wake kuelekea nae kiwandani.Baba Angel na Erick walifika kiwandani na kuanza kufanya kazi mbali mbali za pale kiwandani huku wakipitia mafaili mbalimbali, kwakweli baba Angel alikuwa akipenda utendaji kazi wa mtoto wake, kwani vitu vingi vilienda kwenye mstari hapo kiwandani sababu ya Erick, na waliweza kuingiza faida kubwa sababu ya ufanisi wa kazi wa Erick.Ilipofika jioni, simu ya baba Angel iliita, alipoangalia aliona ni dokta Jimmy anapiga basi akatoka nayo nje ya ofisi na kupokea,“Ndio nakusikia”“Nakuomba kitu kimoja Erick”“Kitu gani?”“Naomba fanya mpango ili mwanao Erick aweze kulala na pacha wake”“Una kichaa nini wewe!!”“Ili tumuokoe huyo mtoto bila ya hivyo ni hatari, hujui tu alichokifanya leo”“Kwani kafanyaje tena?”“Erick naomba unisikie, tiba ya ubondia wa mwanao ni kulala na dada yake tu, hapo tutakuwa tumemaliza kazi ila hivi ni kazi bure, mwanao hafai huyo”“Kwani kafanyaje?”“Mwanao ataua watu huyo ujue, nakuomba ukubaliane nami ili tuweze kumnusuru mtoto wako”“Nitolee ujinga mie, siwezi kukubali huo uchafu hata kidogo”Kisha baba Angel alikata simu bila hata kujua kuwa ni kitu gani cha ajabu kimefanywa na Erick siku hiyo ila baba Angel hapo alipumua kidogo kwani aliweza kujua kuwa siku ile Erick hakulala kimapenzi na Erica.Jioni ya leo, Junior aliamua kutoka na mke wake Vaileth kwaajili ya matembezi, yani toka wafunge ndoa ndio siku hiyo ambayo waliamua kutoka kwa pamoja, kwahiyo walienda kuangalia mazingira mengine na kuongea pamoja huko, mtoto aliachwa na bibi ambaye alikuwepo tu nyumbani kwa Junior kwa siku hiyo, walitafuta mahali kwenye bustani nzuri na kukaa kwaajili ya maongezi,“Ila Junior umejua kusumbua akili yangu wewe dah!! Hadi leo huwa siamini kama tumeoana, hata huwa siamini kama unanipenda”“Aaaah mimi nakupenda Vai, achana na yale mambo ya utoto”“Ila huo utoto sijuiutakuisha lini?”“Kwanini?”“Haya, tupo pamoja hapa ila macho yako yapo kule unaangalia nini Junior?”Junior alikaa kimya kwa muda na kumjibu mke wake,“Mbona hakuna kitu ninachoangalia”“Acha masikhara yako Junior, nimekuona vizuri ukiangalia kule, sijui unatazama kitu gani. Yule mwanamke kageuka mgongo tuila macho yote yamekutoka kwake”“Aaaah sijui unaweza kunielewa Vai, yani ni kawaida ya wanaume kupepesa macho ila mimi na wewe tupo pamoja, hata mimi sijui nilikuwa naangalia nini”Vaileth akageuka tena kuangalia mahali ambapo Junior alikuwa akiangalia ila macho yake yaligongana na macho ya Daima, kwahiyo kwa muda wote Junior alikuwa akitazamana na Daima, kile kitendo kilimkera sana Vaileth na kumfanya ainuke kwa hasira,“Unaenda wapi sasa mke wangu?”“Naenda nyumbani”“Kwahiyo unaenda nyumbani na kuniacha mimi hapa!! Haya, nenda tu”Vaileth alimuangalia Junior na kuamua kukaa ila kiukweli ile tabia ya Junior kwa siku hiyo hakuipenda kabisa, muda kidogo walipokaa Daima alisogea kuwasalimia akiwa ameongozana na kijana mwingine, Junior alipomuangalia yule kijana akagundua kuwa ni ndugu yake yule James. Vaileth alimuangalia Junior na kuamua kukaa ila kiukweli ile tabia ya Junior kwa siku hiyo hakuipenda kabisa, muda kidogo walipokaa Daima alisogea kuwasalimia akiwa ameongozana na kijana mwingine, Junior alipomuangalia yule kijana akagundua kuwa ni ndugu yake yule James.Yani pale Junior alibadili muonekano wake kwakweli, halafu Daima na James wakaka pale ambapo Daima alimtambulisha James kwa Junior,“Huyu ni mchumba wangu anaitwa James”“Mjinga wewe, huyu ni ndugu yangu”“Kumbe ni ndugu yako!! Napo sio mbaya sana maana kumbe sijaenda mbali na ukoo wako”“Wewe mwanamke una kichaa au kitu gani?”James ilibidi aingilie kati na kuuliza,“Mbona Junior imeonekana kupaniki sana, huyu uliyenaye ni nani?”“Huyu ni mke wangu”“Kheee mmefunga ndoa kabisa?”“Ndio ni mke wangu wa ndoa”“Jamani, ndio kimya kimya ndugu yangu. Kweli hatupendani loh!! Ila sisi ni ndugu Junior, yani uwe unakumbuka hili muda wote”“Aaaah ilikuwa haraka ila huyu mwanamke uliyenaye hafai”Daima alikuwa akicheka tu na kusema,“Sasa sifai nini?”“Aliwahi kuwa na mimi huyu”“Kwani nikiwahi kuwa na wewe ndio nini? Wewe ni mume wa mtu sasa, na mimi nipo na James ambaye ni mume wangu mtarajiwa kwani tatizo ni nini?”Junior alimuangalia Vaileth na kumtaka kuwa waondoke mahali hapo maana alijiona akizidi kupatwa na hasira, kwani hakutegemea kama hapo wangekutana na Daima, ila kabla ya kuondoka walibadilishana tena mawasiliano na James maana hata iweze bado wao ni ndugu tu.Baba Angel na Erick, walimaliza mambo yao na kuanza kurudi nyumbani ila baba Angel hakumuuliza chochote mwanae juu ya kitu gani amekufanya kama ambavyo dokta Jimmy alisema.Wakiwa njiani, gari yao ilisimamishwa na aliyesimamisha alikuwa ni Juma ambaye alishuka kwenye gari yake na kwenda kuongea nao,“Yani hapa ndio nilikuwa nakuja huko kiwandani, ila nimekutana nanyi njiani, bora nimewawahi”“Ndio, kuna tatizo gani Juma”“Kuna kitu naombva, naomba kesho Erick ukanisaidie kule kwenye mizinga yangu ya nyuki ili tupakue asali”“Kheee hao nyuki wapo vizuri, tayari asali nyingine!!”“Hata mazingira yangu yapo vizuri, nakuomba sana Erick. Ila kama tungepata na kijana mwingine ingependeza zaidi”“Sawa nimekuelewa”Kisha wakaamuaga Juma pale na baba Angel alianza kuondoka na mwanae huku akimuuliza,“Kwahiyo kesho huendi shule Erick?”“Nitaenda tu baba, usiwe na mashaka na mimi. Nina akili za kuzaliwa”“Kweli naona ila elimu nayo ni muhimu sana”“Kwanza nashukuru nimalize shule, yani nimechoka kusoma hatari”“Ila Erick ulikuwa unapenda shule wewe, sijui shetani gani limekukumba tena. Usiwe kama mimi baba yako, ilibidi nijiendeleze shule kidogo nikiwa hivi mkubwa maana mimi niliacha shule nikiwa kidato cha pili”“Kheee kwanini sasa baba? Mlishindwa ada au kitu gani? Mbona babu anaonekana kuwa alikuwa na mali nyingi toka siku nyingi!”“Acha tu mwanangu, mapenzi kwa mamako yaliniponza mimi baba yako. Nilikuwa nampenda sana, tena sana muda wote nilikuwa darasani namuwaza, yeye, ila nilipomwambia alinitolea nje, niliumia sana. Na hivyo niliamua kufanya kwa vitendo, ikawa tatizo bhana kuna kirafiki chake Fulani huwa anaongea nacho hadi leo si kikapeleka umbea kwa bibi yenu, akaja shule kufoka tukafukuzwa shule. Nilikuwa naishi na mamdogo, alichoka kwa utukutu wangu wa kunihamisha shule kila siku, alisema hanipeleki tena shule, basi nikaanza kuishi mitaani, hapo ujue wala sikuwa namfahamu baba yangu wala nini, kumbe mama na baba waligombana wakati mimi mdogo kwahiyo mimi nikaishi na mama na kuwajua ndugu wa mama tu. Siku hiyo katika mahangaiko yangu si nikaenda kuomba kazi mahali kumbe ndio kwa baba yangu, kwanza aliponiona tu alishtuka huwezi amini hiyo siku ndio ikabadilisha maisha yangu. Ila mmmh sijui kwanini nakwambia yote haya!”“Ni vizuri umeniambia baba ili nami nijue mapenzi yanafanyaje kazi”“Aaaah ila wewe acha bhana tabia ya kumpenda dada yako, yule ni pacha wako ujue”Hapo Erick alikaa kimya kwanza kwani haya maneno ya mwisho yalimuingia baba yake, alijikuta akimuuliza kuhusu kitu kingine,“Huyo rafiki wa mama aliyekuwa mbea ni nani?”“Ni mke wa Juma, yani mke wa Juma ni rafiki mzuri sana wa mama yako ila alikuwa ni mbea sana yule mwanamke”“Aaaaah kwahiyo alisababisha wewe na mama msiweze kuwa pamoja kwa wakati?”“Ndio, yani yeye ndio chanzo hadi mimi nikaacha shule yani mambo mbalimbali ila Mungu ni mwema tumesahau hayo”“Aaaah hujasahau baba, ungesahau usingekumbuka kuyasema”“Si tunayasema tu kupoteza siku”“Unajidanganya baba, hata hujayasahau”Baba Angel alicheka tu, muda huo walikuwa wamefika nyumbani kwao kwahiyo waliingia ndani tu moja kwa moja.Kwakweli hii kitu aliyoifanya Junior leo, haikumpendeza kabisa Vaileth aliweza kuhisi kuwa bado Junior alikuwa na mapenzi na Daima, kwahiyo aliondoka nae bila ya kuongea chochote kile hadi walipofika nyumbani kwao.Wakati wa kulala, Vaileth alishindwa kuvumilia na kuamua kumuuliza Junior kuhusu Daima,“Kama ulikuwa ukimpenda Daima, ni kwanini ulimkana wakati amekuja na mimba hadi ukasababisha balaa kwake?”“Hivi unaona Daima ni mwanamke anayejielewa? Sikuwa na namna zaidi ya kumkana tu”“Kwahiyo kati ya mimi na Daima ungeambiwa uchague basi ungemuoa Daima au?”Junior alicheka na kusema,“Ila Vai mke wangu, maswali mengine unauliza wakati jibu unalo”“Jibu lipi hilo, niambie basi, ungemuoa Daima au?”“Kwani hapa nimemuoa nani? Si inamaana nakupenda wewe au ni nini?”Simu ya Junior ilianza kuita ambapo aliipokea na mpigaji alikuwa Erick, yule ndugu yake mtoto wa baba Angel,“Niambie Erick”“Kesho unaenda wapi kaka?”“Hapana, nipo nyumbani tu”“Kuna kazi, nataka tukaifanye wote”“Oooh, vizuri sana. Basi utaniambia pa kukutana”Junior alikata ile simu na kumuangalia mke wake na kumwambia,“Ila Erick yupo vizuri sana, yani huwa ananikumbuka sana kaka yake”“Haya vizuri”Vaileth aliamua kulala tu kwa muda huo, hata Junior nae aliamua kulala.Leo kama ambavyo Erick alipanga na Junior, aliweza kukutana nae na moja kwa moja kwenda shambani kwa Juma kwaajili ya kumsaidia kuhusu ile mizinga,“Oooh Erick kumbe umekuja na kijana”“Ndio nimekuja nae, nilikuonea huruma jana uliponipigia na kusema kuwa itabidi uje na mke wako”“Hata hivyo nimekuja nae, ila ni muoga sana hataki hata kupaka dawa ili tuingie yani anaogopa nyuki balaa”“Aaaah yuko wapi nikamsalimie”Juma akamuongoza hadi alipo mke wake ambapo Erick alimsalimia yule mke wa Juma kisha Juma alianza kupanga nao jinsi ya kufanya kazi siku hiyo.Wakajiandaa na wote wakaingia kwenye kazi, muda huo mke wa Juma alikuwepo tu sehemu ya nje akiangalia angalia kwani yeye alikuwa akiogopa sana nyuki.Wakati wakiendelea na kazi, Juma alishangaa tu gafla hamuoni tena Erick, ikanidi amuulize Junior kuwa Erick amekwenda wapi,“Yuko wapi tena Erick?”“Sijui katoka kaenda wapi”Juma aliamua kumuangalia Erick kuwa kaenda wapi, katika kumtafuta tafuta akamuona Erick amemshika mke wake mkono huku akiongozana nae, kwakweli Juma hakuelewa kuwa Erick anaenda wapi na mke wake yule, akawaita ila kitu cha kustaajabusha eneo lile walitokea nyuki wengi sana na kumvamia mke wa Juma, kwakweli kitendo kile kilimstaajabisha sana Juma ikabidi akimbie eneo lile na kwenda kumuokoa mke wake kutoka kwa wale nyuki ila kitu cha kwanza alijikuta akishikwa na hasira sana kwani alihisi kuwa lazima Erick amefanya kile kitu kwa kudhamiria kabisa, basi aliposogea pale na kumtoa mkewe kwa wale nyuki maana yeye alikuwa akijua kitu cha kufanya ukizingatia ameshafuga sana nyuki. Basi akamsogelea Erick na kumnasa kibao, hapo ndio aliharibu akili ya Erick kabisa na hata hakutegemea kama Erick angefanya kitu cha namna ile alichokifanya pale.Erick alirudi nyumbani kwao kama kawaida, na kwenda moja kwa moja kuoga alipotoka tu alikuta ndio wapo kula kwahiyo na yeye aliungana nao mezani kwaajili ya kupata kile chakula cha usiku, basi pale mambo yalikuwa yakizungumzwa mbalimbali huku wakiendelea kula ila hakuna mahali hata sehemu moja ambayo Erick alisema jambo lolote.Alipomaliza kula tu moja kwa moja alirudi chumbani kwake, baada ya muda mfupi Erica alienda chumbani kwa Erick na kuanza kumuuliza maana alimuona hana raha kabisa,“Tatizo nini Erick, au umechukia kwa mama kukukataza jana kulala chumbani kwetu?”“Aaaah hamna klitu”“Najua kama ulichukia Erick, ila unajua kama mama ana mashaka sana na sisi yani mama hatuamini kabisa, anahisi kuna kitu sio cha kawaida ambacho tutakifanya tukiwa pamoja”“Aaaah huwa sipendi wanifikirie vibaya, ni kweli nina hisia nyingi sana na wewe Erica, ila nashukuru Mungu amekupa upeo mkubwa sana maana bila ya hivyo basi tungekuwa tumetenda zaidi ya kile tulichokifanya. Naomba unisamehe tu, ila mama huwa hajui ni kwanini napenda kulala karibu yako Erica”“Najua kuwa ulikosa amani, basi leo najitolea mimi kuja kulala humu chumbani kwako. Kwa leo tutalala wote Erick”“Nitafurahia sana, asante kwa hilo”Basi Erica hakutoka kweli mule chumbani kwa Erick kwani alilala pembeni yake na wote wakashikwa na usingizi kwa muda huo.Baba Angel akiwa na mkewe chumbani wakiwa wanajiandaa kwaajili ya kulala, muda kidogo simu ya baba Angel iliita na kumfanya aipokee simu ile kwani mpigaji alikuwa ni Juma kwahiyo alitaka kusikia kuwa tatizo ni kitu gani,“Yani hapa tulipo ndugu yangu tupo hospitali”“Kheee vipi tena?”“Alichotufanya Erick ni Mungu tu ndio anajua”“Kwani kafanyaje?”“Njoo utuone, hapa nimebakisha sauti tu ya kuongea kwakweli, mtoto huyo hapana, kuanzia leo hata simtaki tena”Baba Angel alishangaa sana, hata mama Angel alishtuka kwakweli na kuulizia vizuri ambapo alipewa yale maelezo ambayo baba Angel alipewa na Juma, walijikuta wakitazamana,“Kwani imekuwaje tena?”“Hata sijui”“Twende tukamuulize Erick”Walijikuta wakiinuka kwa pamoja hadi chumbani kwa Erick, walipofungua mlango waliona Erick amelala na Erica kwenye kitanda kimoja tena wakiwa hawana habari sema hakuna lolote baya walilokuwa wakifanya, ni kila mmoja alilala kivbyake na uzuri walikuwa wamevaa nguo zao za kulali, ila mama Angel alitaka kumtimua Erica ambapo mumewe alimsuia na kurudi tu chumbani kwa muda huo na kuanza kuongea,“Kwanini umenikataza nisimuamshe Erica, wakitenda dhambi je?”“Hiyo dhambi wakitaka kuitenda wataitenda tu, kwani sehemu zote tunaenda nao pamoja? Wakiamua mbona tumeisha, hata tusitake kufatilia sana mke wangu tutalia tu, sema tujue jinsi ya kuweza kumdhibiti Erick”“Sasa atakuwa amefanya mambo gani?”“Sijui, unajua hata kuhusu mambo aliyosema dokta Jimmy sijafatilia wala nini yani, kesho mapema tutaenda hospitali kumuona huyo Juma. Tena hata tusimuulize Erick ila tutakuja kuongea nae baada ya kutoka hospitali”Mama Angel alikubali ila kishingo upande kwani alilala huku mawazo yake yote yakiwa juu ya watoto wake maana hakuelewa kabisa kitu ambacho kingetokea baina yao.Kulivyokucha tu, mapema kabisa baba Angel na mama Angel walijiandaa na kwenda hospitali ambapo Juma alikuwa kalazwa na mkewe, na kweli waliwakuta wana hali mbaya kiasi, basi walisogea na kuanza kuongea na Juma,“Imekuwaje kwani?”“Mtoto wako kanifanyia fujo jana sikutegemea kabisa”“Kwani kafanyaje?”“Kwanza kamchukua mke wangu, sijui kampeleka sehemu yenye nyuki, anajua mwenyewe alichokifanya maana wale nyuki walianza kumshambulia mke wangu, na hapo ikawa ni hatari nami nikawasambaratisha maana nishafuga nyuki sana naelewa, ila nilichukia maana mke wangu aliakuwa kaumia, basi nikamzaba Erick kibao, jamani sitaki kusema ilivyokuwa, hapa nilipo hakuna rangi ambayo nimeacha bila kuiona kwakweli, nimepigwa na Erick mimi tena nilikuwa sijielewi kabisa, bila yule ndugu yake aliyekuja naye basi mimi ningekuwa marehemu. Mwanao hafai kabisa tena hafai”“Dah!! Pole sana”Baba Angel na mama Angel walisikitika, kisha walienda kumuona na mke wa Juma yani Johari na kusikitika pia, basi waliongea kidogo tu pale na Juma na kukubaliana nae kuwa watakuwa wakienda kuwaangalia mara kwa mara na wataenda kuongea na mtoto wao.Baba Angel na mama Angel waliporudi nyumbani waliambiwa kuwa wakina Erick wameenda shuleni kwahiyo wakasema kuwa watamuuliza tu siku akipumzika nyumbani.Siku hii baba Angel akiwa ofisini kwake, alifatwa na madam Oliva na kumkaribisha na kuanza kuongea nae,“Kheee kumbe kuna baraka inakuja eeeh!!”Madam Oliva akacheka tu maana tumbo lilikuwa limetangulia mbele kabisa, kisha madam Oliva akasema,“Yani nikizaa mtoto wa kiume tena, siwezi hata kwa bahati mbaya kumpa jina Erick”“Kwanini?”“Yani majina ya Erick nyie ni watu wa ajabu sana”“Kivipi?”“Unajua mwanao kafanya maajabu sana shuleni, na sasa ana wiki nzima hajakanyaga kabisa shuleni halafu wewe Erick mwenzie hata kuulizia kuwa imekuwaje hakuna, unajua mwanao yupo darasa gumu kabisa kwasasa”Baba Angel alipumua kwanza na kumuuliza vizuri madam Oliva,“Sikuelewi madam”“Sikuwepo kazini, unajua siku hizi sio mara kwa mara mimi kwenda shuleni, nasikia alifika siku hiyo mamake Sarah yule Manka ambaye ndio mmliki wa pili wa ile shule, sasa sijui akaenda kuongea na Erick ofisini unaambiwa kila mtu alishangaa kusikia yule mama akipiga kelele, walipoenda walimkuta akipokea kichapo toka kwa Erick, na kila mwalimu aliyeingilia naye alipigwa vibaya sana, hata walinzi walijaribu kumkamata nao walipigwa vilevile, kwakweli Erick hafai halafu wewe hata hujaja shuleni wala nini, huna haja ya kufahamu maendeleo ya mtoto wako wala nini. Tulitamani kumshtaki ila kila mtu anamuhurumia maana Erick bado ni kijana mdogo, mwanao ameanza kuvuta bhangi?”“Unajua bado nashangaa”“Twende shuleni ndio ukashangae vizuri zaidi”Basi baba Angel aliamua kufunga kazi tu na moja kwa moja kuondoka na madam Oliva kuelekea nae shuleni ili kujua kisa na mkasa.Walifika pale shuleni na moja kwa moja baba Angel alifika ofisini na walimu wote wa pale walianza kumsimulia baba Angel kila ambacho mtoto wake amekifanya, kwakweli alistaajabu na kuuliza,“Chanzo ni nini kwani?”“Sidhani kama kuna anayetambua chanzo ni nini? Alifika bosi wetu hapa na kuhitaji kuongea na Erick, waliingia kwenye ofisi hiyo kwaajili ya maongezi, baada ya muda mfupi tu tulimsikia yule bosi akipiga kelele, yani kila aliyeenda kuzuia alipewa kichapo cha hali ya juu, hata walinzi walipigwa jamani, kwakweli huyu Erick hafai na alituacha hapa na kuondoka, toka siku hiyo Erick hajafika tena shule hadi leo”Hapo baba Angel akakumbuka vizuri jinsi ambavyo Erick alienda ofisini kwake na ilikuwa mapema sana, akakumbuka jinsi maelezo ya Erick ambavyo yalikuwa hayana mashiko wala nini ila hakuwa na cha kufanya kwa muda ule zaidi ya kuwasikiliza walimu tu,“Sisi kama shule tunahitaji kumfukuza shule huyu mtoto Erick, hatuwezi kuishi na mwanafunzi wa dizaini hii”“Jamani nawaomba walimu, msimfute shule mtoto wangu, kumbukeni huu ndio mwaka wake wa mwisho, naomba tu aweze kumaliza shule hapa salama”“Njia nyingine ni kuwa, mtoto wako hatotakiwa shuleni hadi siku ya mtihani wa mwisho, kama umeafikiana na hilo tukubaliane hapa”“Dah!! Mwanangu atakosa masomo, si atafeli huo mtihani jamani!! Naomba mmuhurumie mwanangu”“Hatuwezi fuga mabondia hapa shuleni, na hiyo njia ya pili ni tumekupendelea maana kilichopo ni kumfukuza shule kabisa. Na hiyo njia ya pili itafanikiwa endepo Erick akikubali kuja kuomba msamaha hapa shuleni”Baba Angel akafikiria kwa muda na kuona wazi kuwa anatakiwa kumshawishi mtoto wake kuja kuomba msamaha mahali hapo, kwahiyo alikubaliana na walimu kuwa atampeleka Erick kwenda kuomba msamaha, aliamini kuwa walimu wanaweza kumfikiria adhabu nyingine Erick maana aliona swala hili kidogo litaathiri mwenendo wa Erick shuleni.Basi walipomaliza pale, baba Angel aliondoka huku ameongozana na madam Oliva ambapo madam Oliva alimuuliza,“Kwani Erick amekuwaje tena? Mbona alikuwa mtoto mzuri tu, ni kitu gani kipo kati yake?”“Hata najua basi madam! Yani pale nilikuwa nashangaa tu, jinsi Erick alivyokuwa muoga halafu leo hii naambiwa kafanya kitu cha namna hiyo, kwakweli nimebaki nimeduwaa tu”“Nakumbuka mimi niliwahi sababisha matatizo kwa Erick, ila sikutegemea kabisa, nilimchapa fimbo moja tu halafu akazimia yani hapo ilikuwa ni mwisho kwa mimi kupiga watoto. Nakumbuka hadi Erick kazinduka na kuendelea na masomo alikuwa ni mtoto mzuri tu, huwezi mkuta hata akibishana na mwanafunzi mwenzie shuleni hata sijui ni mdudu gani kamkumba Erick jamani dah!”“Yani ambavyo huelewi madam na sisi ni hivyo hivyo”Ila baba Angel alijikuta akitamani kumueleza madam Oliva kuhusu dokta Jimmy alichokifanya kwa Erick na Erica wakati wadogo akajikuta akisita tu na kutokumwambia chochote kile, hadi wanaagana hakuongea nae chochote kuhusu hilo jambo.Usiku wa leo, baba Angel alimsimulia mke wake kuhusu kile alichokifanya Erikc shuleni, kwakweli waliamua kumuita kwa pamoja chumbani kwao ili waweze kuongea nae maana waliona kuzidi kukaa kimya ni kuendelea kufanya tatizo liwe kubwa zaidi.Erick alienda chumbani kwa wazazi wake ambapo walimkalisha na kuanza kuongea nae, baba Angel alimuuliza kwanza,“Erick, mara ya mwisho wewe kwenda shule ilikuwa ni lini?”“Siku ile niliyokuja mapema ofisini kwako”“Kwanini hukwenda tena shule Erick?”“Baba sikia, nilikuwa shule siku ile kama kawaida, alikuja yule mama wa kuitwa Manka au mama Sarah akaniita nami nilitii na kwenda kuongea nae. Alichokuwa akiniambia ofisini sasa, kwanza aliongelea kuhusu Sarah, sijui Sarah sio mwanae sijui anahisi Sarah ni mtoto wa familia yetu ila akajijibu mwenyewe kuwa haiwezekani kwani mimi na Erica tulikuwa ni sehemu ya mtego, nikamuuliza mtego kivipi ndipo aliponiambia kuwa mimi nimepewa dawa ili nimtake dada yangu Erica kimapenzi, na pale nitakapofanya mapenzi na dada yangu basi ndio undugu wetu utakuwa umekwisha, nilimuuliza kwanini ilifanyika hivyo, akasema ili kuwakomesha wazazi wetu, halafu akasema kuwa wewe baba ni malaya sana, hapo ndio alinikera zaidi. Akamalizia kwa kusema mimi nimepewa dawa nitembee na dada yangu ili nisirithi umalaya wa baba. Nasema wazi nilichukia mno, nilijikuta nikipandwa na hasira za ajabu na hapo ndio nikafanya fujo pale shuleni ila haikuwa lengo langu wala haikuwa dhamitra yangu, niliogopa kuwaambia kwani najua wazi mngechukia sana, ila najua hadi mmeniuliza ni lazima mmejua ukweli”Baba Angel na mama Angel walipumua kwanza maana haya mambo kwao yalikuwa makubwa sana, kisha mama Angel alimuuliza Erick,“Kwahiyo wewe ni kweli huwa unapatwa na hisia kwa ndugu yako Erica?”Hapa Erick alijibu kwa kichwa kumaanisha kuwa ni kweli, baba Angel na mama Angel walipumua tena na kumtaka mtoto wao kwenda kulala ila kabla ya kuondoka baba Angel alimwambia Erick,“Basi Erick nakuomba jambo moja tu, naomba twende wote shule ukawaombe msamaha walimu ili uweze kufanya mtihani wa mwisho, halafu tutatafuta twisheni ya wewe kupata masomo yaliyokupita shuleni, sijui umeielewa hiyo?”“Nimekuelewa baba, hakuna tatizo”Kisha wakamruhusu Erick kuondoka kwa muda huo.Baba Angel na mama Angel waliangaliana kwa muda bila ya kusema chochote halafu mama Angel akasema,“Kwahiyo hawa watu kitendo cha kufahamu udhaifu wa watoto wetu imekuwa tatizo jamani? Kwanini dah!! Sielewi kwakweli”“Je unaona kampiga kihalali au kakosea?”“Ila yule Manka nae amezidi mdomo acha apate adabu kidogo, kumbuka amejaribu kukuua mara mbili yule kiumbe, mwache tu akomeshwe kwasasa”Wakaikatisha mada hiyo na kuamua tu kulala.Kulivyokucha, baba Angel alimwambia mkewe kitu ambacho alifikiria kwa wakati huo,“Mke wangu, hivi kwanini tusiende kwa dokta Jimmy tu. Nina hakika kipo ambacho anacho cha kuongea na sisi”“Hapo sawa mume wangu, twende lini sasa?”“Leo yani muda huu, jiandae twende”Mama Angel alijiandaa kwa muda huo kisha yeye na mume wake waliondoka hapo kwao na moja kwa moja kuanza safari ya kuelekea kwa dokta Jimmy.Walipofika tu kwa dokta Jimmy, kuna mtu walimuona akitoka kwenye nyumba ya dokta Jimmy na kufanya washtuke sana kwani ni mtu ambaye walimfahamu na hawakufikiria kama ana ukaribu wowote na dokta Jimmy. Walipofika tu kwa dokta Jimmy, kuna mtu walimuona akitoka kwenye nyumba ya dokta Jimmy na kufanya washtuke sana kwani ni mtu ambaye walimfahamu na hawakufikiria kama ana ukaribu wowote na dokta Jimmy.Baba Angel alienda kuweka gari pembeni kwa haraka ili kumuwahi yule mtu waweze kumuuliza vizuri, ila yule mtu nae aliingia kwenye gari yake na kuondoka zake, mama Angel na baba Angel wakatazamana, kisha baba Angel akamuuliza mkewe,“Huyu baba Emma kafata nini huku kwa dokta Jimmy?”“Mmmmh hata sijui”“Au wana undugu?”“Sidhani kabisa kuhusu hilo, ila huwezi jua maana hawa shemeji yao ni dokta pia kumbuka hilo, ila sijui kwakweli. Sema nimeshangaa sana”“Kama mimi, hili jambo limenishangaza haswa yani, mpaka muda huu sielewi kitu”Basi wakashauriana kiasi kisha wakashuka kwenye gari na kuelekea ndani kwa dokta Jimmy ambapo waligonga lile geti na kufunguliwa kisha kuingia ndani na kumuulizia dokta Jimmy,“Hapana, dokta ametoka”“Ametoka? Si alisema anaumwa?”“Ndio, hali yake bado sio nzuri na ameenda hospitali kwaajili ya matibabu zaidi”“Kheee kwahiyo hayupo”“Ndio hayupo”Baba Angel alichukua simu yake na kuanza kumpigia dokta Jimmy ila simu iliita sana bila ya kupokelewa, basi ilibidi tu waage na kuondoka.Walipotoka kwenye lile geti, waliona kuna gari ya kukodi imemleta mtu pale, walisimama na kuangalia wakaona huyo mtu anayeshuka alikuwa ni Manka huku akiwa na majeraha, ila Manka nae alipowaona alionekana kuchukia sana na kuwafata karibu akiwaambia,“Mnaona mtoto wenu alichonitenda?”Na kweli Manka alionekana kuwa na majeraha kwenye mwili wake, hasa usoni ingawa ni majeraha ambayo yalionyesha kuanza kupona, kisha Manka akasema,“Mimi Manka, nitahakikisha mtoto wenu anaenda jela kwa hili alilonifanyia”“Pole sana”“Pole haitoshi, wala pole sio msaada kwangu. Nilikuwa na dada yangu Linah mimi yani nilikuwa nikipata tatizo lolote ni yeye ambaye ananisaidia, sasa amekufa halafu mtoto wangu naye mmemchukua maana najua tu kuwa yupo kwenu. Ila hiki mnachonifanyia ipo siku kitawarudi”“Kwani kosa letu ni nini Manka?”“Kosa lenu ni kuzaa mtoto mwenye roho ya kigaidi, halafu wewe Erick uende ukafate barua ya marehemu Linah alikuachia huko hadi leo hujaifata. Kwaherini”Halafu Manka aliingia nyumbani kwa dokta Jimmy kwahiyo walijikuta wakimuangalia kwa muda tu pale, halafu wakarudi kwenye gari yao.Waliongea kwa muda kuhusu cha kufanya ila waliona vyema kwa muda huo warudi tu nyumbani kwao.Angel na wadogo zake leo walikuwa nyumbani ambapo Sarah na Erica ndio waliingia jikoni na kupika siku hii maana Sarah bado alikuwa kwenye kujifunza kupika.Wakati wanaandaa chakula mezani, alifika shangazi yao na kumsalimia pale kisha kumkaribisha mezani ambapo alikaa nao na kula nao, leo hata Erick alikuwepo nyumbani kwahiyo na yeye alikuwa akila tu. Shangazi yao aliwauliza kuhusu wazazi wao ambapo walisema kuwa wametoka,“Kheee jamani hata leo Jumamosi wametoka!”“Tena wametoka asubuhi kabisa”Basi waliendelea kula huku shangazi yao akisifia baadhi ya vitu kwenye chakula kile,“Hizi tambi kapika nani?”“Mambo ya Erica hayo shangazi”“Ooooh tamu sana, ila Erica leo hujaunga vizuri haya maini”Angel alicheka na kusema,“Ni mambo ya Sarah hayo”Tumaini alicheka, aliangalia yale maini akajikuta akikumbuka mbali sana, muda ule ule Erica akasema,“Msishangae jamani kuona nyanya zimesimama peke yake, Sarah anajifunza kupika”Wote walikuwa wakicheka, Tumaini aliangalia kwa makini jinsi ile mboga ilivyokuwa yani alijikuta akicheka kisha akamuangalia Sarah na kumwambia,“Usijali mtoto mzuri ipo siku utaweza kupika na utapika vizuri kama Erica, hata utasahau kama ilikuwepo siku ambayo ulipika nyanya zikiwa zimesimama dede huku vitunguu vikielea”Walicheka tena huku wakiendelea kula kile chakula.Kabla ya kumaliza, Tumaini alipigiwa simu na kwenda nje kuipokea ile simu na kuwaacha pale ndani ambapo baada ya kumaliza tu waliweza kutoa vyombo huku Angel akisema kuwa wajiandae kutengeneza chakula kingine cha usiku, Erick akasema,“Ila apike Erica”“Mmmh wewe nawe, kama humu ndani kuna mpishi mmoja tu!! Cha usiku nitapika mimi na Sarah”Muda kidogo shangazi yao alirudi ndani na kumuita Erick pambeni kuongea nae kwanza,“Mwanangu Erick, kuna mahali naomba unisindikize”“Wapi huko shangazi?”“Unajua wamenishtua tu, sikujua kama nitaenda leo, ingekuwa Jumatatu ni bora ningeenda na mjomba wako ila sehemu yenyewe siwezi kwenda mwenyewe na wamepanga kunidhulumu wale, nisipoenda leo itakuwa balaa”“Sawa, shangazi ngoja nikajiandae basi”Erick alienda ndani kujiandaa na baada ya muda alitoka na shangazi yake ili waweze kuondoka, basi nje Tumaini alianza kuwaza,“Mmmh sijui tukakodi bajaji maana si unajua kama sijaja hata na gari”“Usijali shangazi, twende kwa pikipiki”Basi Erick alienda kuitoa pikipiki yao na kupanda na shangazi yake kisha kuondoka kwa maelekezo ya shangazi yake kuhusu mahali wanapoelekea.Walifika sehemu ambayo ndio shangazi mtu alikuwa akielekea, basi akamwambia Erick kuwa sio mbali kutoka pale, ila ilibidi awasiliane na mtu kwanza, aliwasiliana nae na yule mtu alifika pale alipokuwa Tumaini na Erick, yule mama alimwambia Tumaini,“Kheee ulivyosema lazima nije na kijana wa kiume nilijua unakuja na baunsa, kumbe upo na kijana wa shule kabisa”“Ndio, ila mwanaume ni mwanaume. Najua peke yangu watanizingua wale ila wakiona mwanaume wataogopa”“Ila wamejipanga hao, hadi huruma, yani leo roho imeniuma hadi nimeamua kukuita, bila aibu wanagawana tu vipande vya shamba lako, halafu wapo wengi sana. Ila nitambulishe kwa mwanao huyo, ndio wa kwanza nini!!”“Aaaah si unajua mimi sina mtoto wa kiume, ila huyu ni mtoto wa kaka yangu kabisa, kwahiyo hii ni damu yangu, anaitwa Erick”“Kheee kumbe, na mimi naitwa mama Erick”“Mmmmh wewe nawe kila leo kumbadilisha mtoto wako majina, ukiniona na Leah hapa utajifanya mama Leah”Walicheka tu na kuendelea na safari wakati huo Tumaini na huyu mama walikuwa wakitembea huku Erick akiwafata nyumba taratibu na pikipiki yake.Walifika eneo la shamba ambapo Erick sasa aliweka pikipiki pembeni na kuanza kuwafata wale waliokuwa wakimegeana sehemu, walifika pale na Tumaini akawauliza,“Jamani mbona mnamega shamba langu bila ya kunishirikisha?”“Sikia mama, serikali imeamuru watu wenye mashamba makubwa yapunguzwe”“Mbona sijasikia hilo tangazo?”“Sio lazima usikie, kwahiyo sisi tupo kazini”Tumaini aliangalia na aliona wazi kuwa hakuna cha kufanya, alimuangalia yule mwenzio na kumwmabia,“Sasa nifanyeje?”“Hao, labda uwape pesa si unaona wapo na migambo, yani kwenye shamba lako wamejipanga haswaa, bora hata mashamba mengine walikuwa wachache, na muhusika akija na mwanaume wanaweza kuelewana nae, ila wewe na hako kakijana kako sijui katakusaidia nini”“Kwahiyo hela ngapi?”“Muite pembeni huyo umuulize”Basi akamuita yule aliyekuwa akiongea nae ili amuulize vizuri kama ni pesa awape pesa ngapi,“Mimi nakuombeni kitu kimoja, mngeniachia shamba langu mbona nalishughulikia vizuri tu”Yule mama mwingine akasema,“Nilisikia serikali ikisema walioacha mashamba kama mapori ndio wanyang’anywe ila huyu ndugu yangu anajitahidi kwakweli, analifanyia usafi hili shamba kila mara ndiomana mnaona ni safi na mmeweza kupima”“Hili shamba pia ni moja kati ya mashamba yanayopaswa kugawiwa kwa wananchi”Basi Tumaini akasema,“Kwani mnataka pesa ngapi ili niwape muweze kuachia shamba langu?”“Sijui wenzangu watasemaje, ngoja nikajadiliane nao”Akasogea kidogo kwa wenzie na kurudi kuwapa ujumbe,“Wamesema maana huu ujumbe ni wa serikali kwahiyo wakipuuza ni kama wanajitafutia matatizo, ila wamesema kama ukiwapa milioni mbili basi wataahirisha zoezi”Yule mama pamoja na Tumaini walishtuka kwa pamoja,“Milioni mbili!!”“Jamani hili shamba nilinunua au nilipewa bure!”“Mama, hatupo kwenye mabishano hapa, kama hutaki basi hili shamba litakatwa vipande na kuuzwa kwa wananchi wengine wenye uhitaji wa viwanja”Halafu yule baba akaelekea kule kwa wenzie na kuendelea kupima, yani Tumaini alihisi kuchanganyikiwa na kumuangalia mwenzie na kuuliza tena,“Nifanyeje mama Kulwa jamani!!”“Nina uhakika kama wangekuwa wachache halafu ungekuwa na mwanaume mkubwa wale mbona wangeacha eneo lako maana hakuna tatizo, hujawahi kuacha pori hapa, halafu kitu kingine hiyo milioni mbili ni kubwa sana jamani loh!! Si hata ukaanze kununua tofali hapa, hata kama mtu una pesa sio kununua shamba moja mara mbili mbili”“Yani nakumbuka miaka hiyo ya nyumba hili shamba loto ndio nilinunua kwa hiyo bei halafu leo hii niitoe tena kunusuru kwa hawa wazulumaji jamani, bora hata ningekuja na mume wangu”Wakati huo Erick alikuwa tu pembeni akitathimini lile eneo la shamba maana lilikuwa ni kubwa halafu lilivutia, ila alipomuangalia shangazi yake alimuona kuwa hayupo kawaida na kusogea karibu kumuuliza ambapo Tumaini aliamua kumueleza ukweli wa kila kitu, ila hapo alishangaa gafla kuona Erick akibadilika halafu alienda kuwafata wale watu kwenye lile eneo na kutoa amri moja tu kwao, walipobisha aliwapa kipigo hiko hadi Tumaini alijikuta akishika kichw ana kutokutaka kutazama tena, yani aliangalia chini tu maana hakuamini kile kilichokuwa kinatokea.Ndani ya dakika tano palikuwa kimya kabisa pale shambani yani hapakuwa na kelele ya mtu yeyote maana wale watu wote hawakuonekana kabisa.Kisha Erick alirudi kwa shangazi yake na kumuuliza,“Kuna lingine?”“Mmmh hapana shangazi”“Je hiyo milioni mbili ya kuwapa hawa ulikuwa nayo?”“Yani mwanangu, hapa nilikuwa na mawazo hatari hata sikujua cha kufanya, yani nilikuwa nataka kwenda kujaribu kuongea na mjomba wako.”“Haya shangazi, nilikuwa nakwambiaje. Nenda tafuta hizo hela uje ujenge hata chumba kimoja hapa hawataweza kuvamia tena”Tumaini na yule mama walimuangalia kwa makini Erick ambaye alikuwa akielekea kwenye bodaboda yake kwa ishara kuwa alitaka waondoke, basi Tumaini akainuka na kuanza kufatana nae, alimuaga yule mama na kuondoka akiwa na Erick yani Tumaini hakuelewa kitu chochote kwakweli.Njiani alimuomba tu Erick amfikishe yeye nyumbani kwake halafu ndio Erick arudi kwao.Tumaini alianza kumsimulia mumewe kuhusu kitu alichokifanya Erick kwakweli hata mumewe alishangaa jambo hilo,“Erick katoa wapi hizo nguvu?”“Hata najua basi, yani nimebaki kushangaa hadi niliinamisha kichwa chini kwa uoga, yani Erick alikuwa kama wale wakaka wa kwenye sinema za kivita”“Duh!! Katoa wapi hayo mapambano Erick?”“Hata najua basi!! Yani nilibaki kushangaa tu na kustaajabu kwakweli, yani Erick sio mtu wa kawaida nakwambia”Mara kidogo simu ya Tumaini iliita, aliangalia na kukuta yule rafiki yake mama Kulwa ndio alikuwa akipiga, akapokea na kuongea nae,“Kheee huyo kijana wako nimemfananisha na babu mmoja kijijini kwetu, yani huyo babu alikuwa ni tishio”“Babu gani?”“Kuna huyo babu ilikuwa ni balaa, babu alikuwa na nguvu huyo akianza kupiga anachakaza kabisa, kwakweli nimemuogopa tena sana. Nimemuogopa kabisa”“Yani mimi nimebaki mdomo wazi hadi muda huu sielewi ujue, sijawahi sikia kama mtoto wa kaka yangu yupo hivi, sijawahi sikia kabisa hayo mambo. Nimeshangaa kama wewe tu ulivyoshangaa”“Tutaongea vizuri ukija tena huku”Kisha yule mama alikata simu na hapo mume wa Tumaini alimwambia kuwa apige simu kwa baba Angel ili kuuliza vizuri kuhusu Erick“Usikute wamemuweka kwenye shule ya ubondia”“Mmmh inawezekana”Tumaini alimpigia simu moja kwa moja mdogo wake na kumueleza hayo ambaye alishangaa pia ila hakushangaa sana kwani tabia ya Erick kwa siku hizo aliifahamu vizuri sana.Mama Angel na baba Angel baada ya kuambiwa yale na Tumaini, waliona leo pia wapime kuhusu mtoto wao, je ataenda kulala kwakina Erica au atalala peke yake? Na kama akilala peke yake ni kitu gani kitatokea? Walitaka kutambua jambo hilo kwanza.Basi muda wa kulala, mama Angel alienda kumchungulia Erick chumbani kwake na kweli hakumkuta na moja kwa moja alijua lazima Erick kalala chumbani kwakina Erica, basi mama Angel nae alienda kwakina Erica na kweli alimkuta Erick kalala na siku hii hata Sarah hakuwepo inamaana Sarah alilala kwenye chumba chake, basi mama Angel alimuamsha Erick pale,“Weee inaka upesi, nenda kalale chumbani kwako huko. Usiniletee balaa mie”Erick aliinuka na kwenda kulala chumbani kwake, kisha mama Angel alirudi chumbani kwake lakini kwa siku hii walijikuta siku nzima wakitumia kumchungulia Erick chumbani kwake ni kitu gani huwa kinatokea.Walichoona ni kuwa Erick hakulala kabisa alikuwa akijigeuza geuza tu, kumbe Erick akitoka kupambana huko halafu akalala mwenyewe basi huwa anakosa usingizi kabisa yani kila walipoenda kuchungulia walimkuta Erick akiwa macho .Kulivyokucha, mama Angel na baba Angel walijadiliana,“Jamani huyu mtoto unajua hajalala usiku mzima!”“Hii inaonekana itakuwa kawaida yake, ndiomana huwa anataka kulala na Erica”“Mmmmh kwanini inakuwa hivi lakini?”“Yani hapa, lazima tupate tiba ya tatizo la kijana wetu maana naona tatizo linakuwa kila siku, yani kila siku tatizo ni kubwa zaidi”“Yani hapa ni huyo huyo dokta Jimmy ndio tumshikilie maana hapa hakuna cha kufanya kama hatujajua dawa ya tatizo”“Dawa aliyosema dokta Jimmy si mimi wala si wewe unayeweza kuikubali, maana dokta Jimmy anataka mimi na wewe tukubali Erick na Erica walale pamoja kimapenzi, hivi kweli waliwapa watoto wetu dawa kwa lengo la kutuumiza!! Hivi binadamu wapoje jamani”“Dah!! Mume wangu, naomba leo twende kanisani, siku hizi tunasahau sana kusali labda ndiomana tunapatwa na majanga kila siku, twende kwenye ibada leo”“Sawa, umesema jambo jema, tutaenda familia nzima”“Ngoja nikaandae chai ili tule kwa pamoja twende”Mama Angel alienda kuandaa chai na aliita watoto wake wote pamoja huku wakinywa chai na akiwaambia kuhusu kwenda Kanisani, akasema Sarah,“Ila mimi huwa sina nguo za kwenda nazo Kanisani”Erica akamwambia Sarah,“Na wewe, si utavaa zangu, siku zote unavaa za kwangu tatizo lako ni nini?”“Hivi kumbe mnavaliana eeeh!!”“Ndio, miili yetu inaendana halafu hadi viatu tunavaliana”“Kumbe!! Basi vizuri hivyo, Sarah utavaa nguo za Erica”Mama Angel alimtazama Erick ambaye ndiye pekee ambaye hakuongea wala kucheka pale mezani na alionekana akila kwa taratibu sana kuliko siku zote, mama Angel alimuangalia na kumuuliza,“Na wewe vipi mwenzetu?”Kabla Erick hajajibu rara kuna sauti ilisikika nje kwa nguvu na walipoisikiliza kwa makini mama Angel na baba Angel walijua moja kwa moja kuwa ile sauti ilikuwa ni sauti ya Rahim,“Wewe wa kuitwa Erick unayejiita baba Angel kuja hapa nje upesi”Baba Angel alishangaa kwakweli na kutoka nje, ila ile kitu ilifanya wote pale mezani kuanz akuinuka na kutoka nje ili wajue kuwa kuna kitu gani kinaendelea.Rahim alikuwa amesimama kwa hasira huku amemshika mkono Samir, basi baba Angel alipotoka tu akamwambia,“Wewe baba Angel feki nipe Angel wangu na umchukue Samir wako”“Rahim, hebu twende pembeni kuongea, unaongea vitu visivyo na maana unawafaidisha watoto tu”“Nawafaidisha kitu gani? Wanatakiwa kujua ukweli, nyie watoto, huyu Samir ni kaka yenu yani ni mtoto ambaye baba yenu kazaa na mwanamke mwingine halafu huyo Angel ni mwanangu mimi, yani mimi nilizaa na mama yenu kabla ya huyu baba yenu”Hapo baba Angel alishikwa na hasira sana basi alijikuta akimsogelea Rahim na kumnasa kibao cha nguvu sana, kile kibao kilimfanya Rahim amtumie Samir kwa pembeni maana alikuwa na hasira sana kwa yale aliyoambiwa ukizingatia kamlea sana Samir bila kujua kuwa analea mtoto wa baba Angel kama ambavyo baba Angel amelea mtoto wake.Rahim alimvamia baba Angel na kumpa mtama ambao ulimuangusha chini baba Angel ila kabla hajaanza kumshambulia, Rahim alishtukia akikabwa na kuinuliwa juu juu yani kile kitendo kila mtu alikishangaa sana, kitendo hiko kilifanywa na Erick, yani kila mtu alibaki akishangaa, hapo mama Angel alijikuta akijiwa na huruma ya Rahim alivyokunjwa na Erick, basi alisogea karibu ili kumzuia Erick ila alishangaa akisukumwa vibaya sana na Erick yani hapo mtoto wao alikuwa amebadilika kabisa, mlinzi wao nae alisogelea alimpa ngumi moja na kumfanya aanguke huko na kupoteza fahamu, yani kwa jinsi alivyokuwa amemkaba Rahim ni wazi alikuwa akitaka kummaliza kabisa, baba Angel aliona ile ni balaa, basi alijaribu kusogea karibu ila alipoona Erick akitaka kumpiga hadi yeye akaogopa na kurudi nyuma, hapo akili ya haraka ikamjia na kwenda kumvuta Erica ambaye alikuwa pamoja na wakina Angel wakimshugulikia mama yao ambaye ameanguka, baba Angel alimuomba Erica,“Nakuomba nenda kamzuie kaka yako, ataua yule”Erica akaenda mbele kabisa, ila bado Erick hakumuachia Rahim wala nini kiasi cha kumfanya Rahim kutokwa na jasho jingi sana, basi Erica akili yake ikacheza haraka na kwenda nyuma ya Erick na kumkumbatia, muda huo huo Erick alimuacha Rahim chini ambaye alianguka na kupoteza fahamu kabisa, basi Erica alimpeleka moja kwa moja Erick ndani na alimpa glasi moja ya maji, kisha aliongozana nae mpaka chumbani kwake, yani Erica hakutaka kuongea na Erick kwa muda huo wala nini zaidi ya kumtaka alale na kupumzika tu, kwakweli Erick alikuwa na hasira sana ila baada ya kukaa kidogo na Erica aliweza kulala na hapo ndio Erica alitoka sasa.Kila mtu pale nje alikuwa haelewi kwakweli, ilibidi tu baba Angel na Samir wamkimbizie Rahim hospitali maana tayari waliona kuwa hali yake sio nzuri kutokana na kule kukabwa sana na Erick.Mama Angel alikuwa amekaa na Angel, Sarah na Erica ambapo Angel aliuliza,“Kwani Erick ana tatizo gani jamani?”“Mmmmh sijui, labda muulizeni Erica mtu wa ndoto ndio atakuwa anajua”Erica akasema,“Siku nyingine Erick huwa anaweza kujizuia hasira zake ila leo toka asubuhi anaonekana kuwa alikuwa na hasira sana, itakuwa kuna kitu hakipo sawa kwake toka usiku”Yani siku hii hata walisahau kama walipanga kwenda kwenye Ibada maana walihisi kila kitu kimevurugika kabisa, walihisi mambo yameenda ndivyo sivyo, walijadiliana sana ila hawakufikia muafaka wa majadiliano yao.Moja kwa moja mama Angel alienda chumbani kwake huku akijiuliza sana,“Hivi huyu Erick ndio hizo sindano au kuna kitu kingine kati yake? Mbona amekuwa wa ajabu kiasi hiki!! Tutapata kesi sisi kama hatujachukua hatua kwa haraka sana”Mama Angel akawaza kitu kingine ambacho walimzuia Erick kulala chumbani kwa Erica, waliwaza pengine ndio hasira zile maana inaonekana wazi hakuna mtu aliyekuwa akimsikiliza wakati kwa kawaida Erick aliwaogopa sana wazazi wake, ila hapo walimshangaa kwakweli maana Erick aliwabadilikia hadi wao.Mama Angel aliamua kujilaza maana alihisi mgongo wake kuuma kwa kile kitendo cha Erick kumsukuma, pale alivyojilaza alipitiwa na usingizi kabisa.Baba Angel alirudi nyumbani kwake na moja kwa moja kwenda chumbani kuongea na mke wake,“Kwanza anaendeleaje huyu mtu?”“Anaendelea vizuri, tumekutana na Maimuna pale kasema atakuja kutueleza vizuri ilivyokuwa ila ametaka nimuache pale na familia yake”“Ila mambo naona kama yanazidi kuwa magumu, hivi ulitegemea kweli kama Erick angenisukuma hivi au angekutishia wewe kukupiga?”“Unajua sielewi, kila nikifikiria lile tukio nahisi kuchanganyikiwa”“Mume wangu, kiukweli tunahitaji msaada, tena msaada wa nguvu. Hebu jaribu tena kumpigia dokta Jimmy”Baba Angel alimpigia dokta Jimmy simu ambapo mud aule ule ile simu ilipokelewa na dokta Jimmy,“Ndio Erick, tena afadhali umenipigia maana nilitaka kukupigia muda sio mrefu”“Eeeeh dokta nakusikiliza”“Nasikia mlikuja kwangu ila mkanikosa, naomba kesho fanya juu chini mje tafadhari maana hili jambo ni lazima tulichukulie hatua kwasasa”“Jambo gani tena?”“Si jambo la watoto wenu hao, naomba mje”“Sawa tutakuja”Walikata simu, ila waliona ni vyema kwenda ili kujua mbivu na mbichi, juu ya kitu kinachoendelea kati yao na kati ya watoto wao.Muda kidogo ule mlango wa chumbani uligongwa, walipomkaribisha mgongaji aliingia Erick yani baba Angel na mama Angel walitazamana, ila Erick alifika na kuwaomba msamaha wazazi wake,“Baba na mama naomba mnisamehe sana, hata sijui ilikuwaje. Naomba mnisamehe sana”“Usijali, tumekuelewa. Kuwa na amani tu Erick”Baba Angel na mama Angel hawakutaka kuongea mengi sana wala kumuuliza maswali mengi Erick.Leo mapema kabisa, baba Angel na mama Angel walijiandaa kwa pamoja na kuondoka kuelekea nyumbani kwa dokta Jimmy.Walipofika moja kwa moja walikaribishwa ndani ambapo dokta Jimmy walimkuta amekaa kwenye bustani yake, kwahiyo walimfata alipo na kuanza kuongea nae kuhusu kinachoendelea, dokta Jimmy alianza kuwaambia,“Hivi mnajua kama watoto wenu wale wanatakiwa kuwa na mwenzao!”Mama Angel na baba Angel walishangaa na kuuliza,“Mwenzao kivipi?”“Nadhani hamnielewi, ila kabla ya yote kuna kitu kikubwa sana ambacho hamfahamu kuhusu watoto wenu”Baba Angel na mama Angel walishtuka na kumuangalia kwa makini dokta Jimmy Walipofika moja kwa moja walikaribishwa ndani ambapo dokta Jimmy walimkuta amekaa kwenye bustani yake, kwahiyo walimfata alipo na kuanza kuongea nae kuhusu kinachoendelea, dokta Jimmy alianza kuwaambia,“Hivi mnajua kama watoto wenu wale wanatakiwa kuwa na mwenzao!”Mama Angel na baba Angel walishangaa na kuuliza,“Mwenzao kivipi?”“Nadhani hamnielewi, ila kabla ya yote kuna kitu kikubwa sana ambacho hamfahamu kuhusu watoto wenu”Baba Angel na mama Angel walishtuka na kumuangalia kwa makini dokta Jimmy.Kisha baba Angel alimuuliza,“Kipi ambacho hatufahamu ikiwa kuhusu dawa tunafahamu?”“Lipo ambalo hamfahamu, sio kuhusu dawa tu ila kuna jambo ambalo hamfahamu”“Tuambie ni jambo gani?”“Ngoja nimuite huyu mtu kwanza, hajui kitu ila nahitaji nae ajue”Dokta Jimmy aliinuka na kwenda kumuita mtu huyo ambaye alikuwa ni Manka, alifika pale na kuwasalimia maana hakujua kama wamekuja hapo nyumbani kwa dokta Jimmy, kisha dokta Jimmy akauliza,“Kwani Sarah yuko wapi Manka?”“Yupo kwa hao japo, hao ndio wananiharibia mtoto wangu”“Samahani, Manka. Hawa hawamuharibu mtoto wako maana yule ni mtoto wao”Manka pamoja na mama Angel na baba Angel walibaki wakishangaa na kumuuliza kwa pamoja dokta Jimmy,“Kivipi?”“Yule Sarah ni mtoto wenu wewe Erica na Erick”Baba Angel na mama Angel waliangaliana kwa muda na kuuliza,“Inamaana Erica na Erick sio watoto wetu? Au kuna mmoja kati yao sio mtoto wetu?”Manka nae alimuuliza dokta Jimmy,“Unazungumzia kitu gani dokta? Sikuelewi ujue!”“Naomba mnisikilize kwa makini, msiyaingilie haya maelezo ili nisikosee kuwaelezea, nisikilizeni kwa makini sana”“Mmmh!!”Walijikuta wote watatu wakiguna, kisha dokta Jimmy alianza kuelezea,“Ni hivi, mzee Jimmy alikuwa na mahusiano na Manka, na kwa hakika alimpenda sana ila sehemu ambayo hakumuelewa Manka ni pale Manka alipodai kuwa ana mimba yake wakati mzee Jimmy anakumbuka wazi kuwa siku zote alilala na Manka kwa kutumia kinga, ila hakukataa kwani Manka alikazana kuhusu jambo hilo. Kuna siku mzee Jimmy alimuwekea mtego Manka, na hapo alitambua ukweli halisi wa mtoto wa Manka wakati huo Manka akiwa na mimba kubwa sana, kwakweli mzee Jimmy alichukia mno, ingawa alijua wazi kuwa mimba si yake ila alichukia zaidi kumjua muhusika wa ile mimba. Tulikuwa na mpango na mzee Jimmy wa kubadilisha watoto yani tulitaka mtoto wa Sia tumbadilishe na mtoto wa Erica ila hapo kuna mtu alituletea dawa ndipo mzee Jimmy aliona hiyo dawa itakuwa ni bora zaidi kwani Erica na Erick mtaumia moyo sana pale watoto wenu watakapotakana kimapenzi, roho yake ilikuwa ikiumia sana kwa kile kitendo cha Erick kutomsikiliza na kuamua kumuoa Erica, na swala la Erica kumkataa lilimuumiza sana alijikuta akiumia sana moyo wake na ndiomana alifikia hili swala la kumbadilishia Erica mtoto. Wakati Erica anakaribia kujifungua, mzee Jimmy aliamua kumtuma mbali Erick ili asiweze kushuhudia kile tulichokuwa tunataka kukifanya. Erica alipoletwa hospitali moja kwa moja tulimpeleka kwenye operesheni ila ukweli ni kwamba Erica alijifungua mapacha watatu badala ya wawili, na hapo mmoja alikuwa wa kiume na mwingine alikuwa wa kike, hapo kidogo hata sisi tulipagawa ila akili ya mzee Jimmy ilikuwa ikifanya kazi haraka kupita maelezo kwani muda huo hata Manka nae alikuwa kajifungua ila alijifungua mtoto wa kiume, yani akili ya mzee Jimmy ilimtoa yule mtoto wa kiume wa Manka na kumuweka pembeni halafu tukamchukua mtoto mmoja wa Erica ingawa ni wa kike tukamuweka kwa Manka, ili Erica asijue chochote kile, ukizingatia alishaambiwa kuwa ana mapacha wa kike na wa kiume tumboni. Basi kilichofanyika pale ni kuwaweka watoto alama na kwenda kuwaweka sehemu ya watoto ambapo baada ya muda mfupi alifika mama yake mzazi na Erica akitaka kuona wajukuu zake, ilibidi tu tumuonyeshe basi muda ule mzee Jimmy akasema kuwa kitakachoendelea ni ule mpango wetu wa sindano tu, ndio tulipowarudisha tukawadunga sindano zetu basi, alipozinduka Erica tukamkabidhi mtoto wake, wakati huo mtoto wa Manka yupo mafichoni. Yule mtoto nilimlea mwenyewe pamoja na mtoto wa Oliva, ila nilikuja kumkabidhi Sia wakati mtoto ana miezi mitatu kasoro hivi maana mzee Jimmy alikuwa akimuhudumia pia Sia sababu alibeba mtoto wa Manka, na alimpa Manka mtoto wa Erica ili mali zote atakazoziandikisha kwa mtoto basi zirudi kwenye familia yake. Naomba mnisamehe na pia mumsamehe mzee Jimmy, ila Sarah ni mtoto wenu pia”Kiukweli Manka alikuwa ameinama huku akilia tu wakati huo baba Angel na mama Angel walikuwa wakishangaa maana hii habari iliwashangaza sana, yani baba Angel alijiuliza sana dhumuni la baba yake bado hakupata jibu kabisa, kisha Manka alianza kumwambia dokta jimmy,“Yani siku zote unanichekea kumbe kuna ujinga wewe na mzee Jimmy mmenifanyia dah!! Kwanini lakini jamani!”“Nisamehe Manka, ila na wewe ulizidi kumdanganya yule mzee mtoto wa kwake wakati sio wa kwake, yule mzee mwenzio hata hakuwa na uwezo wa kuzalisha tena ndiomana alikugundua mapema tu kuwa kuna mahali umebeba ile mimba basi akaanza kukufatilia”Baba Angel akamuuliza dokta Jimmy,“Bado kwetu hujamaliza, kwahiyo ndio Erica na Erick mkawachoma sindano?”“Ndio, tena Erick tulimchoma mbili ila yeye iwe rahisi zaidi kumpenda dada yake, na kwa nguvu ya ile sindano tuliamnini kama Erick akimshawishi kidogo dada yake basi wangefanya maana inafanya kazi pia kwenye mwili wa Erica”“Dah!! Mna dhambi sana nyie watu, sasa kwanini jamani, kwanini lakini eeeh!!”“Sio mimi ila ni mzee wako, alikuwa na lengo la kuwakomesha”“Ila amekomesha na ukoo wake, kwakweli nimechukia sana. Halafu unasema sio kosa lako wakati wewe usingekubali najua isingewezekana maana baba huo utaalamu wa kuchoma sindano autoe wapi? Wewe ni mbaya sana dokta Jimmy, wewe na baba yangu ni mashetani”“Tusamehe bure Erick, ila njia pekee ya kumuokoa mwanao na huo ubondia wake ni kuhakikisha kuwa hao mapacha wawili wanalala pamoja kimapenzi”“Wewe dokta hebu nitolee huo upuuzi wako mie, mmefanya ujinga halafu unaendelea kutuambia ujinga”“Sio ujinga Erick, ni tiba kwaajili ya watoto wako”Mama Angel aliyekuwa amekaa kimya kidogo, aliinuka kwa muda huo na kumzaba kibao dokta Jimmy kisha akasema,“Ni mjinga sana wewe daktari, kwakweli hapa nilipo nina hasira sana na wewe”Kisha mama Angel alimzaba kibao cha pili na kusema,“Hiko ni kibao cha kukumbusha yale uliyonitendea, hivi kabla ya kufanya hayo mlijaribu kufikiria maumivu tutakayoyapata kwenye mioyo yetu? Kwanza nimekereka sana kwanini mtoto wangu mumchukue wakati mdogo?”Dokta Jimmy akajieleza kwa kifupi,“Mwanao alichukuliwa ili kuandikishwa kiurahisi mali za babu yake”Mama Angel alimzaba kibao kingine yule dokta na kusema,“Kwani asingepewa hizo mali angekufa? Hizi ni binadamu gani nyie ambao mlikosa utu kabisa, ni viumbe gani nyie?”Mama Angel alijikuta akipandwa na hasira sana, hivyo kuanza kumkaba dokta Jimmy yani ni baba Angel tu ndio aliyemtoa na kuondoka na mke wake kwani kwa muda ule wote walikuwa na hasira na dokta Jimmy.Manka alibaki pale akilia kama mtu aliyefiwa kabisa, alilia sana alijikuta akikumbuka msiba wa dada yake vizuri, alilia akikumbuka maneno ya dada yake, yalikuwa yakimjia kichwani kwake,“Manka, usidhani hao wanakupenda, hao ni wanafki na hawakupendi wala nini. Ipo siku utakumbuka maneno yangu kuwa hao hawakupendi, haiwezekani watu wanaokupenda wanakuwa kwako kwaajili ya maslahi yao tu na kukutuma kufanya kazi zao za ajabu ajabu, hawakupendi hao, ipo siku utaniambia”Manka alijikuta akipaza sauti na kusema,“Uko wapi Linah, uko wapi dada yangu? Leo imefika ile siku uliyosema kuwa nitaumbuka basi ndio leo nimeumbuka mimi Manka, yule mtoto niliyekuwa naringia kila mahali sio mtoto wangu, mtoto ambaye niliteseka katika kulea, mtoto ambaye niliogopa hata kumuangushia kofi langu, nakuja kugundua sio mtoto wangu. Naumia mimi kushinda nilivyokuwa nahisi mwanzo kuwa nilizaa mapacha ila kwasasa maumivu yangu ni maradufu, yule aliyelelewa maisha ya kimasikini hadi nikaamua kumsaidia na bado nikamuadhibu kwa kutembea na mwanangu kumbe ndio mwanangu”Manka alilia kama mtoto mdogo, hata huyu dokta Jimmy hakuweza kumbembeleza, maana kila aliposogea Manka alijibu kwa ukali,“Niache, shetabi mkubwa wewe. Toka mbele yangu shetani”Ni wazi kuwa Manka alikuwa na hasira sana, yani leo alilia kushinda siku aliyolia kwenye kaburi la mzee Jimmy, alijikuta akisema,“Kwanini lakini mzee Jimmy umenifanyia hivi? Si bora ungekataa tu kuwa mtoto wako simtaki halafu ungeniacha na mwanangu ningejua jinsi ya kumlea, sasa mwanangu wa ukweli hanitaki na huyu wa uongo hanitaki pia”Yani kelele alizokuwa akipiga Manka hadi watu walianza kuzunguka nyumba ya dokta Jimmy huku wakitaka kuingia na kujua kuna nini, basi dokta Jimmy kwa haraka haraka alienda kuchukua dawa na kumpulizia Manka ambaye alianguka chini na kupoteza fahamu, kisha akambeba na kumpeleka ndani ya nyumba kabisa.Mama Angel alijikuta akishindwa hata kuongea kitu, alikuwa tu akifikiria toka siku ya kwanza kukutana na Sarah na jinsi alivyoona yeye na Sarah wameendana damu, akakumbuka zawadi ambayo Sarah alimletea wakati katoka kujifungua, akakumbuka ucheshi wa Sarah, akajikuta machozi yakimtoka kila alipokumbuka jinsi Sarah alivyomshawishi Elly ambaye ni binamu yake kutembea nae, mama Angel alijikuta akipatwa na maumivu kwa hilo, aliona ni vyema angelea mwenyewe watoto wake wote. Akawaza pia kuhusu dawa ambayo wameambiwa kuwa mtoto wake Erick na Erica wamepewa, alijikuta akizidi kuumia moyo maana anaambiwa suluhisho ni Erick na Erica kulala pamoja kimapenzi, moyo wake unavuja machozi haelewi kabisa, anaanza kuhisi laana ya yeye kulala na ndugu yake yani Derrick ndio ambayo imerudi kwa watoto yani mtoto wake kulala na mtoto wa Derrick halafu matukio yamefanana kwa kiasi Fulani kwani Sarah nae alipata mimba ya Elly na kuitoa kwa njia ya kujizuia kupata mimba, alijikuta akisema,“Hii ni laana”Alianza tena kulia kwa sauti, ilibidi baba Angel apaki gari pembeni na kuanza kumbembeleza mke wake,“Laana ya nini mke wangu? Haya mambo yaache tu tutagundua ufumbuzia juu ya kitu cha kufanya, usiumie moyo mke wangu, hata mimi naumia vile vile ila Mungu ni mwema hata hapa bado anatupigania”“Roho inaniuma Erick, kwanini lakini kwanini mzee Jimmy anifanyie haya? Ni sababu ya ile milioni kumi au kuna lingine? Ile hela yote aliichukua Dora hata mzee Jimmy anatambua hilo ila kwanini anifanyie hivi, kaniumiza sana tena sana”“Pole mke wangu, mimi na wewe wote tumeumia yani hujaumia peke yako, cha msingi ni kumuomba Mungu atupe subira na busara ili tujue cha kufanya maana akili zetu zimefika mwisho kabisa kwenye swala la kufikiria kuhusu haya mambo”Baba Angel alijitahidi kumnyamazisha mke wake, yani hata yeye alikuwa na uchungu ila alitakiwa kupooza uchungu wake ili waweze kufika nyumbani salama, mama Angel sasa ilikuwa kama leo kapata uthibitisho maana siku zote alipokuwa akisikia kuwa watoto walipewa dawa, aliona kama masikhara, sasa leo aliona kumbe ni kweli kuna tatizo kubwa sana juu ya watoto wake.Njia nzima alikuwa akilia tu, yani hakuwa na amani mama Angel kabisa.Wakiwa nyumbani siku hii, Angel na wadogo zake waliamua tu kula kwa muda huo kwani waliona wazazi wao wamekawia kuja, walikula huku akiongea kidogo ambapo Angel alimuuliza Sarah,“Hivi huwa unamkumbuka mama yako Sarah?”“Ndio huwa namkumbuka sana tu, yule ni mama yangu na siwezi kupingana na hilo. Akijirekesbisha basi mimi nitaenda kuishi nae, ila kiukweli natamani kama mama yenu ndio angekuwa mama yangu, ningefurahi sana”“Aaaah usijali, mama ana upendo, huwa anapenda watu wote yani yeye ndio kazaliwa hivyo kwa upendo”Muda kidogo mama Angel na baba Angel waliingia yani mama Angel alishindwa kujizuia kabisa kwani moja kwa moja alienda kumfata Sarah alipo na kumkumbatia huku akilia tena alilia sana hata watoto wake wote walimshangaa mama yao, alimshika na kusema,“Nakumbuka maneno ya marehemu baba yangu siku anakata roho akiwa mikononi mwangu aliniambia nichunge sana maana binadamu ni wabaya, anaweza akakuchekea machoni kumbe moyo I anakupalia makaa.”Akakumbuka jinsi mzee Jimmy alivyojitolea kugharamia harusi yake na mume wake, yani mzee Jimmy aligharamia kila kitu kwenye ile sherehe na kweli ilifana, yani mama Angel hakufikiria kama kuna siku ambayo mzee Jimmy angetenda jambo kama lile, licha ya mabaya ambayo mzee Jimmy alikuwa akiyafanya ila hakufikiria kama angefanya kitu cha namna ile. Alimkumbatia sana Sarah na kumwambia,“karibu nyumbani mwanangu, hapa ni nyumba ni kwenu. Mimi na mama yako kabisa na hawa ni ndugu zako kabisa”Alimfata Erick na Erica na kuwavuta kwa pamoja kisha akawakumbatia na kusema,“Naomba mumpokee Sarah ni ndugu yenu kabisa”Akamvuta na Angel huku akisema yale maneno tena, kwakweli ilikuwa ni kitu cha kustaajabisha kwa upande wa watoto ila walikuwa wakiitikia tu huku wakimuangalia mama yao maana walishindwa cha kusema wala kufanya kwa muda huo.Mama Angel aliporidhika ndipo alipoenda nyumbani kwake kumalizia machungu yake sasa.Angel na wadogo zake walikuwa wakishangaa pale ila mara Erica akawaambia,“Ndio, Sarah ni pacha wangu”Angel alimuangalia na kumuuliza,“Kivipi?”“Tulizaliwa watatu ila Sarah walimuiba, hii kitu imenijia mara kadhaa ila nilikuwa siiielewi na sasa nimepata kuielewa”“Kheee kwahiyo Sarah….!! Hata sielewi mwenzenu, haya Sarah karibu kwenye familia yetu. Haya mambo ya kuiba watoto mmmh”Kisha walitoa vyombo pale na wote kwa pamoja kuelekea vyumbani kwani kila mmoja alikuwa na mawazo yake, haswa Sarah hakuna kitu ambacho alielewa kwa wakati ule ndiomana alikuwa akishangaa tu.Usiku huu baba Angel alijaribu kuongea na mke wake ili akimtaka waweze kwenda kula chakula maana alionekana kutokuwa sawa kabisa, basi alianza kuongea nae,“Kwanza kabisa mke wangu ni jambo la kumshukuru Mungu kuweza kuwafahamu watoto wetu wote”“Na kuhusu swala la Erick na Erica?”“Hili ni tatizo ila sio tatizo sana sababu tumejua ukweli na tutaweza kukabiliana nao, ni kujua tu jinsi ya kukabialiana nao”“Au tuwaambie ukweli Erick na Erica kuwa walipewa dawa wakati wadogo!”“Mmmh sijui kama itakuwa sahihi ila ikiwezekana inabidi tu tuwaambie ukweli maana najua hata wao wanashangaa ile hali waliyokuwa nayo, nina uhakika hata wao inawachanganya sana. Ni ngumu kwa kaka na dada kushikwa na hisia za kimapenzi kama wao, basi moja kwa moja hapa inatakiwa waujue ukweli ila tutapanga namna ya kuwaambia ukweli huo”“Tusubiri wafanye mitihani basi”“Hapo ni sawa mke wangu, ila kwa muda huu naomba twende kula chakula kwa pamoja halafu ndio tutakuja kulala, kumbuka toka mapema tupo kwa yule mjinga Jimmy, yani yule ni sawa tu na dokta feki jamani hadi kero kumfahamu”Mama Angel aliinuka na moja kwa moja kwenda na mumewe sebleni na kuandaa chakula kisha kuanza kula, kidogo mlinzi wao aliwagongea mlango basi walimfungulia na kuongea nae,“Vipi tatizo nini?”“Yani bosi mbavu zinaniuma sana”“Kheeee imekuwaje tena!! Nakumbuka Erick alikupiga ngumi usoni”“Aaaah mama, Erick hafai yani sio mtu wa kawaida kabisa. Leo alikuwa akipita getini nikamwambia Erick ulinipiga sana hadi nilipatwa na kizunguzungu, jamani baada ya kumwambia hayo sikuamini kwani alinipiga ngumi moja kwenye mbavu zangu hapa hadi muda huu zinaniuma”“Khaaa huyu Erick kafikia pabaya jamani”Ila baba Angel na mama Angel hawakutaka kuongea mengi sana kwani kwa muda huo huo walimuahidi yule mlinzi kuwa kesho watampa pesa za kuweza kwenda kuangalia hali yake ya afya.Siku ya leo, mama Angel aliamua kuwaita wanae wote maana aliona ni vyema kuweka sawa kuhusu swala la Sarah kuwa ni ndugu yao ili watoto wake wasijiulize sana kuhusu jambo hilo, basi alianza kuongea nao,“Jamani watoto wangu, najua jana mmenishangaa sana ila hata mimi hii kitu ilinishangaza ndiomana nilijikuta kama nimepagawa vile, mimi mama yenu wakati wa kujifungua uzao wa pili kumbe nilijifungua mapacha watatu ambapo sikutambua hili wala nini, nilijua tu ni wawili yani huyu Erica na Erick kumbe ilikuwa ni watatu, nasikia babu yenu ndiye aliyempeleka pacha mmoja na kumbadilisha na mtoto halisi wa Manka ambaye ndio mnamtambua kama mama yake Sarah, kitendo kile kilifanya Sarah akulie kule na ni yeye ndiye aliyempa jina Sarah, ni jina la mama yake mzazi, kwahiyo Sarah kapewa jina la nyanya yake. Hivyobasi naomba mumtambue Sarah kama ndugu yenu, najua kwako Sarah ni ngumj sana ila ndio hivi ilivyokuwa”Sarah akauliza,“Na mama yangu yule anayajua haya? Yuko wapi kwasasa? Na mwanae halisi ni nani?”“Mtoto halisi wa mama yako ni Elly ambaye ni binamu yenu halafu mamako amejua kila kitu, hata yeye hii habari imemchanganya sana”“Ningependa nimuone najua atakuwa amelia sana”“Usijali Sarah, nitakupeleka alipo maana ndiye aliyekulea na kukufikisha hapo ulipo”“Inamaana yule niliyeonyeshwa kwenye picha kuwa ndio baba yangu ni babu yangu?? Inamaana lile kaburi tunaliendaga na mama kumtembelea baba ni la babu na ndiye aliyefanya yote haya?”“Ndio ni yeye”“Ila mama aliniambia kuwa baba alinipenda sana, unajua sielewi eeh yani sielewi kabisa”Mama Angel aliamua kukaa pembeni na Sarah ili kuweza kumuelewesha kilichopo, ni kweli siku zote Sarah alitamani kuwa mtoto kabisa wa mama Angel ila hakufikiria kama itakuwa kwa namna hiyo.Mama Angel alipoongea kidogo na Sarah aliamua kumpigia Manka simu kwanza ili Manka aweze kuongea na binti yake, ila ile simu iliita tu bila ya kupokelewa yani hapakuwa na matumaini yoyote ya kupokelewa kwa ile simu ilibidi mama Angel aache tu na kumuahidi Sarah kuwa wataenda kumtembelea.Wakati huo alifika Sia akiwa ameongozana na Elly, kwahiyo walimkaribisha tu.Dokta Maimuna aliwasiliana na Jack kuwa ampeleke yule Derrick mdogo nyumbani kwake, ili waweze kuongea nae kidogo.Basi Jack alijiandaa na Derrick na kuondoka nae wakielekea nyumbani kwa Rahim.Walifika pale, ila Rahim bado alikuwa kitandani kutokana na kipigo alichopata kutoka kwa Erick, basi Rahim alikiwa hajiwezi kabisa.Dokta Maimuna aliomba kidogo Jack ampe nafasi ili aweze kuongea na Derrick, ambapo Jack hakubisha na kuwaach kwaajili ya maongezi, basi walianza kuongea pale ambapo dokta Maimuna alimwambia Derrick,“Ni hivi, wewe ni mtoto wangu na wala mamako sikujua mambo haya, unajua tena hizi hospitali nazo kumbe walituchanganyia watoto, mimi wakanipa mtoto wa mamako halafu mamako wakampa mtoto wangu ambaye ndio wewe”Derrick alimuangalia na kumwambia,“Sikuelewi”“Kwani mama yako hajakwambia?”“Kaniambia ila na yeye sijaweza kumuelewa”Basi dokta Maimuna pale aliamua kutumia njia mbalimbali ili kufanya Derrick aelewe ujumbe ila ni kwa kiasi kidogo sana Derrick aliweza kuelewa.Ilibidi dokta Maimuna akamuomba Jack kuwa wajaribu kupanga siku hizi wawe wanakaa karibu na watoto wao wa ukweli yani yeye Jack awe karibu na Samir halafu Derrick awe karibu na yeye dokta Maimuna,“Mmmh sijui kama Derrick ataweza, unajua huyu mtoto hajazoea na hajawahi kuishi na mtu mwingine tofauti na mimi!”Hapo dokta Maimuna alimtazama kwa makini na kutaka kuleta maelezo mengine, ila muda kidogo mahali pale alifika mkwe wa dokta Maimuna yani baba mzazi wa Rahim yani yule Mwarabu, mtu wa kwanza kumuona alikuwa ni Derrick mdogo kwakweli yule mwarabu alijikuta akisimama kama dakika kumi bila kuongea huku akimshangaa tu Derrick.Baba Angel leo alipotoka ofisini tu, basi moja kwa moja aliamua kupitia kule alipokuwa akiishi marehemu Linah kwaajili ya ile barua.Alifika na kumkuta yule msichana wa kazi ambaye baada ya salamu tu alienda kumletea baba Angel ile barua ambaye aliifungua na kuanza kuisoma palepale ila ule mstari wa kwanza ulimshtua na kumfanya aache kuisoma ile barua. Alifika na kumkuta yule msichana wa kazi ambaye baada ya salamu tu alienda kumletea baba Angel ile barua ambaye aliifungua na kuanza kuisoma palepale ila ule mstari wa kwanza ulimshtua na kumfanya aache kuisoma ile barua.Kisha baba Angel alianza kuangalia mara mbili mbili na kumuita yule mdada wa kazi akamuuliza,“Unauhakika hii barua imeandikwa na marehemu Linah?”“Ndio, na hakuna aliyeiona yani wewe ndio wa kwanza kuifungua, nisingekiuka kile ambacho alikisema, niliishi nae kama mama yangu mzazi”“Aaaah sawa, hakuna tatizo. Kwaheri”Baba Angel aliiweka ile barua na kwenda kuisoma nyumbani kwake.Alipofika nyumbani kwake alienda kuoga na kumuomba jambo mkewe kuwa anhitaji utulivu kiasi kwahiyo alienda kwenye sebule yao nyingine na kuifungua ile barua na kuanza kuisoma, nayo ilianza,“Najua tu hii barua umeipokea na kuanza kuisoma mbele za watu wakati mimi nataka uisome sehemu iliyotulia”Baba Angel akapumua na kuanza kuisoma tena ile barua kwa makini zaidi,“Erick, nilikupenda sana na hili siwezi kubisha maana nilikupenda halafu niliamini kuwa wewe utakuja kuwa mume wangu, niliamini katika nguvu nilizokuwa nazo kiasi kwamba niliweza kupambana na wanawake wengi uliokuwa nao, kwa kipindi hiko ni mwanamke wako mmoja tu ambaye alinishinda kwenye mapambano naye alikuwa ni Sia, sio kwamba alinishinda kwa ubavu hapana maana ubavu huo hakuwa nao na kama ningeamua basi ningemchakaza kwa dakika ingawa nguvu alikuwa nazo. Ila hakuna mtu aliyekuwa na maneno ya karaha kama Sia, alikuwa na maneno ya kukera na yale ya kuumiza moyo kiasi kwamba ukitaka kumpiga unajikuta umeishia njiani maana hujui ni wapi uanzie kugombana na Sia, alikuwa na mtindo wa kuuma na kupuliza. Ni yeye alinishinda ila niliamini kama hujamuoa yeye basi utanioa mimi. Siku nakutana na Sia akaniambia wazi kuwa umeoa, tena umeoa mwanamke mwingine kabisa ambaye niliwahi kutaka kumpiga pia, niliumia moyo ila niliacha maisha yaendelee. Nilipoachana na wewe niliwahi kuwa na mausihano kadhaa ila mahusiano yale hayakuzaa matunda kwani wanaume wote walikuwa ni waongo na hawakuwa na mapenzi ya kweli, ndipo nilipompata kijana Junior, sikufikiria kama ningeweza kuwa na mahusiano na mtoto mdogo kama Junior, ila kuna siku nilienda disko kujirusha na ndio huko nilipokutana na Junior kwa mara ya kwanza, kila nilipokuwa nikicheza alikuja nyuma yangu na tukacheza wote, baada ya hapo tulikunywa sana pombe, muda wa kuondoka sikuweza hata kuendesha gari langu sababu ya ulevi, basi Junior akaamua kunirudisha nyumbani kwangu, ila Junior hakuondoka bali nililala nae hadi asubuhi, ni akili za pombe ndio zilinituma kufanya vile ila baada ya hapo ndio mapenzi yangu kwa Junior yalipozaliwa, nilimpenda, nilimjali na kumthamini, kikubwa zaidi kila nilipomuhitaji alikuja kuwa na mimi. Ndiomana alipogeuka nilikuwa tayari kutumia nguvu ili kumrudisha Junior mikononi mwanangu, roho imeniuma sana baada ya kujua kuwa Junior alikuwa ni mtoto wa ndugu yangu James, huyu James nilikuwa napatana nae sana, na tena amenisaidia vitu vingi sana, sikutegemea kabisa kama mimi ningechukua maamuzi ya kutembea na mwanae tena kumpenda kupita kiasi yani kupita maneno. Ni kweli nilibahatika kupata mimba ya Junior katika umri mkubwa huu, niliamua kumzalia mwanaume niliyempenda kwa dhati ila nilipogundua kuwa ni mwanangu niliona aibu sana sikujua pa kuiweka sura yangu, na ndio wazo la kutoa mimba liliponijia kichwani. Niliamua kunywa dawa za kutoa mimba, na kuna mahali walinishauri kitu cha kufanya, sikutaka kwenda hospitali kwasababu zangu mwenyewe ambazo hata nikifa nitakufa nazo moyoni mwangu. Damu ni nyingi sana zimenitoka siku zote hizi hadi mara ya mwisho nilikupigia simu ila hadi muda huu hujatokea Erick nadhani utapata tu ujumbe kuwa Linah amekufa, kwa upande Fulani habari ya kifo changu itafurahisha sana familia yako. Ila kuna jambo kubwa sana ambalo limejificha katika familia yako pia, sio kila kitu mtu utajua, vingine huwezi kuvijua, yani kuna jambo zito mno. Mchunguze vizuri binti yako Erica utagundua kuwa naongelea nini, nilikutana mara kadhaa na huyo mtoto ila niliweza kumsoma, mchunguze vizuri kijana wako Erick utagundua, na utakapogundua hayo yatakuumiza sana, utakosa raha na amani katika moyo wako ila itakubidi kuukubali ukweli halisi wa kinachoendelea. Erick, ni wazi nilikupenda sana, yote niliyokuwa nafanya kwako chukulia tu ni kama changamoto za maisha, ni kama changamoto ulizozipata kwa Sia ila najua mtu huyu kwasasa amekuwa mtu wa karibu kwako na unaongea nae vizuri. Hata nikifa usiache kuja kutembelea kaburi langu mara kwa mara, nadhani nitakuwa nafurahi huko nilipo kwa kukuona ukinijali hata kama nimekufa. Ila narudia jambo hili, wachunguze vizuri watoto wako hawa, kuna jambo kubwa sana limejificha kati yao, kuna kitu kikubwa sana kati ya watoto wako hawa wawili namaanisha huyo Erick na Erica, Ila kuna rafiki yako dokta usisahau kumtafuta kwaajili ya watoto wako hawa halafu kitu kikubwa jihadhari sana na mwanao Erick kula ndizi, kuna kitu kiliwekwa kwa kupitia ndizi mbivu kwa yeye, kwaheri”Ile barua iliisha na baba Angel alipumua huku akiiangalia mara mbili mbili huku akijiuliza maswali kadhaa,“Anamzungumzia rafiki yangu dokta yupi? Nina marafiki wengi ni madokta lakini sio dokta Jimmy maana hajawahi kuwa rafiki yangu na kwamwe hatokuwa rafiki yangu. Na matatizo ya watoto wangu anazungumzia matatizo ya sindano au kuna mengine tena? Mmmh bora angekuwa hai ningemuuliza vizuri”Baba Angel aliikunja ile barua na moja kwa moja kwenda kuiweka chumbani kwake.Usiku wa leo wakati baba Angel na mama Angel wapo chumbani wakiongea, simu ya baba Angel iliita na yeye aliipokea simu ile ambapo mpigaji alikuwa ni Jack, basi alianza kuongea nae,“Leo, nilienda nyumbani kwa Maimuna, alikuja baba mzazi na yule mwanaume na kusema kuwa Derrick ni mjukuu wake. Ulikuwa na haki ya kukataa kufanana na Derrick ila sio kosa langu maana mimi nilikuwa najua wazi niliyezaa nae ni wewe”“Natambua hilo, usiku mwema”Baba Angel alikata ile simu kwani hakutaka kuweka nae mazungumzo marefu sana ukizingatia ni usiku, ila baada ya hapo mama Angel alimwambia,“Ni Jack huyo!!”“Aaaah msumbufu tu huyu”“Hapana sio msumbufu, alikuwa akikupa ujumbe”“Ujumbe gani usiku!! Huu ni muda wa kulala”“Baba Angel, ungekuwa unathamini muda wa kulala basi ungekuwa unazima simu usiku ila siku zote simu yako ndio ya kupokea jumbe na simu zisizoeleweka usiku”“Aaaaah mke wangu jamani, unajua kwanini huwa naacha simu hewani, ni sababu ya biashara zangu, naweza tafutwa na mtu hata usiku mnene. Ila nimekuelewa maana kwa siku hizi nitakuwa nazima”“Haya ni lini watu wa maana wamekutafuta usiku wa manane tuongee ukweli baba Angel, kipindi kile alikuwa ni Sia tena huyu alikuwa akisumbua hata saa nane usiku, akaja madam Oliva, mara Manka, mimi natunza tu akiba, mara Linah kazidiwa usiku eti wa kwanza kumtafuta ni wewe yani kaacha ndugu zake wote huko kaja kukutafuta wewe, na siku hizi ni huyu Jack yani yeye huwa muda wote sijui hana muda ila usiku tena muda wa kulala ndio anachukua simu yake na kukupigia. Baba Angel kama kweli hizi kero huzipendi basi nakushauri uzime simu, mara nyingi tu simu yangu huwa naizima na ukiikuta hewani basi ni bahati mbaya au wewe haupo nyumbani ila mara nyingi nazima simu usiku”“Nimekuelewa mke wangu”Muda huo baba Angel alichukua simu yake kwaajili ya kuizima ila alikutana na ujumbe wa Jack,“Yani Erick ni wa kunikatia simu kweli!! Kumbuka mimi na wewe iwazazi, haijalishi kitu gani ila mtoto wetu amepatikana, halafu kikubwa ni kuwa mimi na wewe tuonyeshe mapenzi kwa mtoto wetu ingawa hatujamlea toka mtoto. Kesho nakuja ofisini kwako”Baba Angel akazima ile simu na kumtaka mke wake kuwa walale tu kwa muda huo.Kulipokucha kama kawaida, baba Angel alijiandaa na kuondoka zake kuelekea kwenye kazi yake, muda kidogo pale nyumbani kwao alifika Sia akiwa ameongozana na Elly, walisalimiana pale na mama Angel ambaye alimuuliza Sia,“Jamani, leo ni siku ya shule, huyo Elly vipi mbona hajaenda shule”“Aaaah kasimamishwa huyu, wamesema aende siku ya mitihani”“Duh!! Hatari jamani, kisa cha kusimamishwa?”“Si yule mama yake alienda na kutaka kupatana nae, huyu na yeye kiburi sijui kakitoa wapi jamani, si kamfanyia fujo yule mama, basi uamuzi wa shule umemsimamisha”“Yani Manka kakubali mtoto wake asimamishwe?”“Unajua bado yule haamini kama huyu ni mwanae”“Mambo ya lini hayo?”“Mbona ana kama wiki mbili huyu haendi shule”Mama Angel alipumua kidogo akajua hapo ni wazi kabla Manka hajapata ukweli halisi kuwa Elly ndio mwanae kabisa, yani kwa pale alikuwa na uhakika lazima Manka bado yupo kwenye maombolezo maana kilio walichomuacha nacho ilikuwa kama kufiwa na mtoto wake.Basi waliongea kidogo ambapo Elly alienda ndani kuongea na Sarah ambaye alikuwepo tu nyumbani pamoja na Angel kwa kipindi hiko.Kidogo mama Angel alipigiwa simu na dada yake kuwa aende, basi hakuwa na namna zaidi ya kumuaga tu Sia ambapo Sia aliomba asogezwe tu kwenye mgahawa wake ili aendelee na biashara.Mama Angel alijiandaa na moja kwa moja kutoka pamoja na Sia, kisha alimuacha Sia kwenye mgahawa wake ila wakati anaondoka tu alimuona baba Emma na kaumua kusimamisha gari kisha alishuka kumfuata kwani bado alihitaji sana kujua kuwa baba Emma alienda kufanya nini nyumbani kwa dokta Jimmy.Alimsogelea na kumsalimia pale kisha kuanza kuongea nae,“Yani John nilivyokuona moyo ukashtuka sana”“Kheee kwanini umeshtuka hivyo sasa?”“Acha tu, ni hivi kuna kitu nataka kukuuliza”“Kitu gani hiko?”“Unamfahamu dokta Jimmy?”“Aaaah yule dokta mpuuzi sana, simpendi hata kidogo”Hapa ndio mama Angel alikuwa akipasubiria kwani alitaka kujua kuwa dokta Jimmy kamfanya kitu gani huyu baba Emma, akamuuliza kwa makini sasa,“Ni kitu gani?”“Kwani wewe unamfahamu vipi huyo dokta?”Hapa mama Angel aliamua kufunguka kwanza ili huyu baba Emma afunguke pia,“Yani huyu dokta kanifanyia kitu cha ajabu sana, mimi nilijifungua kwenye hospitali yake kumbe nilijifungua mapacha watatu halafu yeye akanipa wawili, mtoto mwingine kampa mtu baki amlee yani nimechukia sana”“Sasa huyo mtoto wenu watatu mmempata?”“Ndio, Mungu ni mwema mtoto alikuwa akiteswa na yule mama akaja kwetu tu kuomba msaada ila sasa kila kitu mtoto kafanana na sisi yani kumbe yule mjinga katuaibia mtoto wetu jamani. Kuchunguza ndio tumejua ukweli”“Dah!! Hongereni kwa kumpa mtoto wenu, dokta mwehu sana yule, mke wangu alijifungua kwake pia, ila sasa kilichotokea tumekuja kugundua kuwa wale watoto wote sio wa kwetu yani watoto ukipima nao majibu yanagoma ila ndio tumeshalea mpaka sasa na watoto wanajua sisi ndio wazazi wao wa ukweli, sijui kwanini huyu dokta kaamua kutufanyia hivi jamani. Halafu kila nikimfata kuhusu watoto wangu ananikimbia maana nilihitaji kujua ukweli wa watoto wangu wako wapi? Kwanini imekuwa hivi!”“Khaaaa kwahiyo mkeo alijifungua mapacha sio!”“Ndio, ni Emmanuel na Emmanah ndio watoto wangu ila kumbe sio damu yangu ukweli, ningehisi mke wangu kachepuka ila wote tulienda kupima, yule dokta anaweza sambaratisha familia za watu jamani. Hata sijui watoto wangu wa ukweli wapo wapi, ingawa hata wale nawapenda ila ningependa kujua na wanangu wa kweli wako wapi?”“Aaaah pole sana jamani”“Asante, yani acha tu nina hasira na yule dokta hatari. Amefanya hata nitembee huku naongea peke yangu”“Pole sana”Mama Angel aliagana na baba Emma ila pale pale mama Angel alibadili safari yake na kuelekea ofisini kwa mumewe ili kwenda kumpa hiyo habari ya baba Emma.Baba Angel akiwa ofisini huku akiendelea na shughuli zake, alishasahau ujumbe wa Jack kuwa siku hii angefika ofisini kwake, basi muda huo alishangaa tu kumuona Jack akiingia pale ofisini basi alimshangaa,“Kheee Jack!!”“Unashangaa nini sasa Erick? Hukunitarajia? Si nilikwambia kuwa leo nitakuja ofisini kwako”“Haya karibu”Ila Jack hakukaa, alisimama tu huku akimuangalia baba Angel ambaye alimuuliza,“Mbona hujakaa?”“Kwani nikiongea nawe huku nimesimama utakufa au nitakufa?”“Hapana Jack, haya niambie kilichokuleta”“Sijui nikwambie”“Ni nini hiko, niambie tu”“Hebu simama kwanza”Baba Angel hata hakujiuliza mara mbili kwani alisimama muda ule ule, halafu Jack akamwambia,“Toka hapo kwenye meza yani simama pembeni”“Ila nina kazi hapa jack, huu ni muda wa kazi”“Najua kama una kazi, ila na mimi pia ni kazi”“Kheee kivipi?”“Sogea nikuonyeshe”Baba Angel hakujiuliza pia na kusogea, kisha Jack alimsogelea baba Angel na kumkumbatia kwa nguvu sana huku akimwambia,“Nimekumiss sana mpenzi wangu, kwakweli nimeshindwa kuvumilia nimeshindwa jamani. Nakupenda sana Erick”Kisha Jack alianza kumbusubusu Erick, ila mlango wa ofisini ukafunguliwa na aliyeingia alikuwa ni mama Angel ambaye alishangaa sana na kusema,“Khaaa jamani baba Angel kweli!! Ndio kinachofanyika ofisini hiki”Mama Angel alisema kwa sauti kubwa kiasi, ikabidi baba Angel kujitoa kwa Jack na kwenda kumnyamazisha ili asipayuke sana,“Tupo ofisini mke wangu”“Kama ungekuwa unaiheshimu ofisi ungetaka kufanya uchafu ofisini!”“Taratibu mke wangu, nisikilize kwanza”“Nikusikilize nini?”Kisha mama Angel alimuangalia Jack na kumwambia,“Ondoka”“Hapana, siwezi kuondoka. Mimi pia nina haki ya kuongea na huyu maana ni baba wa mwanangu”Mama Angel alimuangalia baba Angel na kumwambia,“Nilijua kile kipindi cha ujinga kimepita, kweli bado kinaendelea Erick!!”“Hapana mke wangu”“Ondoa huyu mwanamke kwanza ndio nitaweza kuongea neno”baba Angel alimuangalia Jack na kumtaka kuwa aondoke,“Jack nakuomba ondoka”“Aaaah jamani Erick hatujamaliza kujadilia”“Hatuna cha kujadili mimi na wewe”“Ila kumbuka wewe ni mzazi mwenzangu!”“Ndio mimi ni mzazi mwenzio ila mimi nina mke wangu, naiheshimu ndoa yangu”“Huu ndio ujinga wa ndoa, hebu ipitishwe sheria jamani ili mwanaume mmoja aweze kuoa wanawake wengi atakavyo na hawa wanaotusumbua sijui mume wangu, mume wangu wafunge kidomodomo”“Hata ikipitishwa hiyo sheria bado haiwezi kunifanya mimi nisiwe na mke mmoja tu, ndio maisha niliyochagua haya na maisha ni kuchagua. Naomba jack uondoke”Basi Jack alimuangalia mama Angel kwa muda kidogo na kuondoka zake, muda huu mama Angel alikaa kwenye kiti pale ofisini huku amejiinamia kwani alihisi uchungu tu katika moyo wake, mumewe alijaribu kumtuliza pale ila alirudia kauli yake,“Nilijua enzi za ujinga zimepita Erick, kumbe bado zinaendelea!!”“Mke wangu, nitakueleza vizuri, natumaini utanielewa”“Tutaongea nyumbani”Mama Angel aliinuka na kuondoka zake maana hakutaka hata kuweka maneno mengi mahali pale kwa muda ule.Moja kwa moja mama Angel alienda kwa dada yake Mage ambaye ndio alikuwa amemuita kwa siku hii, alijifanya kufukia yote yale aliyoyaona ofisini kwa mume wake na kufika kwa dada yake kwaajili ya kuitikia wito, basi dada yake alianza kuongea nae,“Bora umekuja nikajua hutokuja!”“Hamna dada, lazima ningefika hata kwa kuchelewa. Niambie dada yangu”“Kaa chini kwanza”Basi mama Angel alikaa halafu dada yake aliagiza soda ambapo alianza kunywa na dada yake huku dada yake akimuuliza swali la kwanza,“Hivi ndoa yako unaipenda?”Hapa mama Angel alishtuka sana na kumjibu dada yake,“Naipenda ndio”“Nikajua na wewe kama Bite kwenye ile ndoa yake ya kwanza, ingawa James alikuwa muhuni ila Bite nae alikuwa mzembe, yani ile ndoa ilikufa kizembe sana, Bite hakuwa mwanamke mpambanaji, na hata ya sasa asipokuwa makini itakufa maana nasikia kahamia kwa mwanae kabisa”“Eeeh yupo kulea mjukuu”“Kwani huyo Junior na mkewe wangeshindwa kulea? Kamuacha mumewe kule halafu yeye yupo kulea mjukuu, ni akili au matope? Bite sio kusema ni mtu mzima sana kiasi kwamba anaacha ndoa yake na kukimbilia wajukuu, si mwanae tu kamuwahi kumpa ubibi, lakini Bite anatakiwa kukaa chini na kuitunza ile ndoa, halafu ndoa yenyewe hajazaa hata mtoto pale ukimwambia utasikia oooh huyu mwanaume ana watoto wengi sana, sawa ana watoto wengi ila umezaa nae? Kwani wewe una watoto wangapi? Utasikia mmoja, sasa si uongeze mwingine, oooh mwanaume ana watoto wengi sana yani yule Bite ile ndoa itakata roho siku sio nyingi asipojirekebisha.”“Sasa dada si ungemwelimisha”“Najitahidi ila yule huwa anajijua mwenyewe, ila ngoja nikwambie nilichokuitia”“Eeeeh dada”“Uwe makini sana na sehemu ambazo mumeo anaenda, yani mumeo anaenda hotelini unamuacha aende peke yake halafu anakwenda na wanawake kweli!!”“Lini tena hiyo dada?”“Kwa macho yangu nilimshuhudia mumeo akiwa hotelini na mwanamke”Mama Angel aliuliza vizuri na kugundua kuwa huyo mwanamke alikuwa ni yule yule Jack, alijikuta akichukia maradufu yani hadi anamuaga dada yake alikuwa tayari ameshachukia vya kutosha.Aliondoka, akiwa njiani alimuona Juma akiwa anaingia duka la madawa, basi alisimama na kumsalimia,“Acha tu Erica, alichonitenda mtoto wenu ni Mungu tu ndio anayejua”“Pole sana ndugu yangu, ila rafiki yangu Johari anaendeleaje”“Kidogo afadhari ingawa ana maumivu kiasi, kuna dawa ndio nilikuwa nanunua hapa”Mama Angel alimuhurumia kweli kwa kiasi Fulani halafu aliagana nae.Baba Angel alivyotoka kazini alikuwa akijiwa kichwani na ile barua ya Linah, halafu jambo kubwa lilikuwa likimjia kwenye kipengelea cha mwisho kuwa ajihadhari sana kwa watoto wake hawa mapacha kula ndizi mbivu haswaa Erick, ila alihitaji kujua kuna nini kwenye ndizi mbivu kwa watoto wake wakati watoto wake wanapenda na ilikuwa ni kawaida kwao kuzila, ni kipindi hiko tu ndio hawajala siku nyingi, alipitia kwenye genge na kuchukua za kutosha tu kisha akaenda nazo nyumbani kwake.Alifika na kuwakuta watoto wake wakila, siku hii walikuwa wakila wali, basi aliwaambia watoto wake kuwa amewaletea matunda ya ndizi mbivu, yani siku hii baba Angel hata watoto wake walimshangaa kwani alienda kuziosha na kuwawekea mezani ili wale ila alivyoziweka mezani tu ni Erick ndio alikuwa wa kwanza kuchukua ila Erica alimshika mkono Erick kama kumkataza na kumfanya baba Angel aulize,“Kwanini unamkataza?”“Aaaah atakula nyingi maana naona yeye ndio kakimbilia”“Hapana, nimeleta nyingi sana, mle watoto wangu mfurahi”Swala lile lilimfanya Erick aweke wali pembeni na kuchukua sahani nyingine kisha akamenya ndizi za kutosha na kuzila pale, yani baba Angel alikuwa amesimama tu akiwaangalia watoto wake wala hakuna aliyekuwa amemuelewa kwa wakati ule kuwa kwanini imekuwa hivyo kwa baba yao, Erica alikula moja tu na kumfanya baba yake amuulize,“Ndio ulikuwa unamkatalia mwenzio kumbe wewe huzipendi wala nini!”Erica alicheka na kusema,“Humu ndani wapenda ndizi ni Angel na Erick, ndio wanapenda sana ndiomana nimemkataza Erick sababu nilijua atamaliza kumbe zipo nyingi”Basi kwa muda huo baba Angel ndio alienda chumbani kwake.Usiku wa leo, kiukweli kabisa mama Angel hakutaka kuongea na mumewe kuhusu baba Emma ila aliongea nae kuhusu Jack, alitaka kujua kitu gani ambacho mumewe huwa anazungumza na Jack.Baba Angel hakumficha, alimueleza wazi kuhusu kitu kilichotokea baina yake na Jack kwa siku hiyo ili mke wake asiwe na mashaka nae,“Kuna ujumbe nataka kukupa ila ujumbe huo nitakupa kesho”“Sawa, hakuna tatizo mke wangu”Badae mama Angel alifikiria kidogo na kuona ni vyema tu kumueleza mume wake, basi alimwambia kuhusu kukutana na baba Emma na kuhusu mapecha wa baba Emma,“Kheee sio watoto wake kivipi?”“Sijui anasema kuwa dokta Jimmy alimbadilishia”“Mmmh isije kuwa na wa kwetu walibadilishwa!”“Hapana baba Angel, utaanzaje kuwa na mashaka kuhusu hilo? Kwanza kumbuka dhumuni la baba yako labda kama katika watu wake kuna waliomsaliti ila kumbuka mipango ya baba yako ilikuwa ni kati yake na dokta Jimmy na kidogo Moses ambaye siku zote anataka kukuua, halafu kuhusu watoto yani mimi nimekubali kabisa kuwa Sarah ni wa kwetu sababu angalia nilivyofanana nae, halafu angalia Erica na Sarah mwanzoni sijui ilikuwaje tukashindwa kuwafanananisha watoto hawa, tumekuja kugundua kuwa hadi nguo wanavaliana, yani Erica na Sarah ni mapacha, haya tukija upande wa Erick, zile hasira amerithi kwako ila yeye zimezidi sababu ya dawa alizokuwa nazo”Muda ule ule baba Angel alikumbuka ujumbe toka kwenye barua iliyoachwa na marehemu Linah kuwa achunguze vizuri watoto wake na akigundua ataumia sana, akajikuta akiwa na hamu ya kuanza kuwachunguza sasa ila hakutaka kumwambia mke wake sema alipanga kuwachunguza watoto wake ili awatambue vizuri, ukizingatia alishaona wakila zile ndizi mbivu alizowapelekea.Basi mke wake alivyolala tu, yeye aliamua kuwanyatia watoto wake ili ajue kuna kipi kilichopo.Alianza kwenda chumbani kwa Erick, ila alisikia kama Erick akiongea kwa sauti ya kunong’ona, akamsikia aliyekuwa akiongea nae alikuwa ni Erica,“Ila mimi Erick nilikuwa nakukataza kula zile ndizi”“Ila nazipenda Erica, ningefanyaje?”“Pole sana, mimi sina msaada kwa leo”“Nakuomba Erica nisaidie, nina hali mbaya mwenzio”Baba Angel alijaribu kuchungulia akamkuta Erick amevua nguo zote yani yupo mtupu kabisa na alionekana kumtaka Erica afanye kitu cha kumsaidia kwa maumbile yake, kwakweli baba Angel alijihisi vibaya sana, yani alihisi kama dunia ipasuke aingie, hakutaka kuona Erica na Erick wangefanya nini au Erica angemsaidiaje Erick yani hiki kitu hakukitaka kabisa, ikabidi baba Angel aingie tu mule chumbani kwa Erick ambapo Erick alishtuka sana na kujifunuka na nguo, kwakweli kile kitendo kilikuwa ni cha aibu sana kwao, baba Angel hakuwafokea ila aliwauliza,“Nifanye kitu gani kuwasaidia watoto wangu?”Erica alimwambia baba yake,“Naomba tuambie ukweli baba”Baba Angel alipumua kidogo na kuamua tu kuwaambia,“Wanangu najua kuwa sio kosa lenu ila nawaomba mjinusuru kwa laana hii wangu, ni hivi kuna mtu anaitwa dokta Jimmy kwa kushirikiana na baba yangu waliamua kuwachoma sindano ili mkikua muwe mnapendana na muweze kufanya mapenzi na kutuumiza wazazi wenu. Naomba msifanye chochote, mimi na mama yenu tunajitahidi kumaliza hili tatizo”Hapo Erica alitoka nje ambapo Erick alibaki na baba yake ila hakuongea chochote kile kwa muda huo, baba Angel aliendelea kuongea ila Erick hakumjibu kitu, basi aliamua kumuacha alale halafu yeye alirudi chumbani kwake.Mapema kabisa, baba Angel aliamka na kwenda kumuangalia Erick ila hakumkuta mule chumbani kwake, kidogo akaanza kuhisi Erick atakuwa ametoka, basi akaenda getini kumuuliza mlinzi naye alimwambia,“Mapema kabisa leo, Erick aliondoka eneo hili”Baba Angel aliguna ila kengele ya hatari ikalia kichwani mwake, hapo aliwaza tu lazima dokta Jimmy hatokuwa na bahati siku hiyo.Basi alienda kujiandaa haraka na kutaka kumfatilia Erick ila kabla ya yote alimpigia simu dokta Jimmy na kumtaka akimbie nyumbani kwake,“Mwanangu Erick kajua ukweli, halafu nyumbani kaondoka asubuhi sana. Kwahiyo sijui kama atakuacha salama akikukuta, ondoka haraka sana”Kisha baba Angel alipanda gari lake na kuondoka kuelekea nyumbani kwa dokta Jimmy.Alipokuwa anakaribia kufika, kuna mahali alikuta watu wengi wamejaa na wengine wamejeruhiwa kiasi, basi aliweka gari pembeni na kwenda kuuliza kuwa kuna nini,“Kuna kijana sijui katokea wapi yule kijana alikuwa kwenye pikipiki, unaona lile gari (Baba Angel alionyeshwa gari ambalo lilikuwa limebonyea kidogo) Lile ni gari la dokta, sasa yule kijana kaligonga lile gari likasimama, kaenda kumshusha dokta na kumuinua juu juu kisha kumtupa chini yani kila aliyeingilia alipigwa ndio hao unawaona wapo chini hapo”Baba Angel aliamua kuuliza kwanza hali ya dokta maana moja kwa moja alijua tu huyo ni dokta Jimmy,“Na dokta yuko wapi?”“Weeee huyo dokta ndio hatamaniki, ana hali mbaya sana, nadhani ni yule chini ya gari amezungukwa na watu”Baba Angel alisogea pale na kukuta wote waliokuwepo pale wakilia, alipojaribu kumuangalia huyo dokta alipo pale chini aliona pametapakaa damu tupu. Baba Angel aliamua kuuliza kwanza hali ya dokta maana moja kwa moja alijua tu huyo ni dokta Jimmy,“Na dokta yuko wapi?”“Weeee huyo dokta ndio hatamaniki, ana hali mbaya sana, nadhani ni yule chini ya gari amezungukwa na watu”Baba Angel alisogea pale na kukuta wote waliokuwepo pale wakilia, alipojaribu kumuangalia huyo dokta alipo pale chini aliona pametapakaa damu tupu.Pale pale akili ya baba Angel ikafanya kazi haraka na kujua kuwa lazima Erick atakuwa amemuua dokta Jimmy, hata hakutaka ushahidi bali alirudi kwenye gari lake na kuanza safari ya kurudi nyumbani, njiani alimpigia simu mke wake,“Nakuomba mke wangu, Erick akirudi hapo nyumbani nakuomba umsihi kwa namna yoyote ile asitoke hapo nyumbani, hii sasa ni kali zaidi, tutampoteza mtoto huyo. Nakuomba sana sana”Baba Angel aliondoa gari yake huku akiwaza vitu mbalimbali katika kichwa chake, alijua ile lazima ni kesi kubwa sana, na mwanae akishikwa basi ni kifungo cha maisha bila mjadala wa aina yoyote ile.Kiukweli baba Angel alikuwa akiendesha gari huku akiwa na uoga sana kwenye moyo wake.Baba Angel alifika nyumbani kwake, cha kwanza kabisa aliulizia kuhusu Erick na kuambiwa kuwa Erick yupo chumbani amelala, basi alimuangalia mke wake na kumwambia,“Mama Angel, huko mtoto wetu ameua kwahiyo cha kufanya kwasasa wote tuondoke hapa, twendeni kwa mama yangu kwanza, najua nitakachoongea nae ila tuondoke hapa kwanza halafu tukifika huko nitajua cha kufanya”“Kaua nani kwani?”“Taratibu mke wangu, huko dokta Jimmy ni kwisha habari yake, Erick ameshafanya yake”Yani mama Angel alikuwa kama kachanganyikiwa ila mumewe alimpa moyo na kumtaka wajiandae kwa haraka na baada ya kumaliza waliita watoto wao wote ambao hawakuelewa kwa haraka ila walibeba nguo chache na kupakia kwenye gari kisha kuanza safari, baba Angel aliwaambia tu kuwa wanaenda kumsalimia bibi yao,“Baba, kumbuka shule tunakaribia kuanza mitihani!”“Sio tatizo, ila leo twende kwanza kumsalimia bibi”Basi baba Angel aliondoa gari lile ila mlinzi aliagwa kuwa wanaenda kwenye matembezi tu, ingawa aliona kuwa muda umeenda tayari.Baba Angel na familia yake walifika kwa mama yake, basi moja kwa moja alienda kwa mama yake na kumueleza kwa kifupi tu,“Mama, naomba mimi na familia yangu kwasasa tuishi hapa kwako maana huyu Erick kashafanya yake”“Kafanyaje tena?”“Yani kuna uwezekano mkubwa wa Erick kuwa amemuua dokta Jimmy maana alienda kupambana nae akiwa na kasira sana”Ila huyu bibi badala ya kusikitika alionekana kufurahi na kusema,“Kama kamuua ni afadhari jamani, sikuona sababu ya yule dokta mtenda maovu kuendelea kuvuta hewa ya ulimwengu huu”“Kheee mama, ila kuua ni dhambi”“Ila alichokufanyia sio dhambi? Hiyo huruma ya hivyo imekuanza lini Erick?”Baba Angel alikaa kimya kwani bado alikuwa akijadili kitu na ubongo wake yani alijiona kuwa hayupo sawa kabisa.Usiku wa siku hiyo, walipewa vyumba pale kwa bibi Angel ambapo ilibidi Angel alale na wadogo zake halafu Erick ndio alale mwenyewe ila kwa siku hiyo ni baba Angel mwenyewe ndio aliruhusu Erick akalale na dada zake, ila Angel aligoma,“Aaaah baba, Erick mtoto wa kiume huyu halafu aanze kulala na sisi wanawake kweli!”“Aaaah basi, Sarah na Erica mtaenda kulala na Erick”Yani hakutaka kuweka nafasi kwa Erica na Erick pekee ingawa anajua wazi angewaambia wangekubali, ila hakutaka jambo baya litokee kati yao ndiomana akamuweka Sarah kuwa alale nao.Usiku ule, Erica aliweza tu kugundua kuwa Erick hayupo sawa kabisa, kwahiyo badala ya kulala alijikuta akimuhoji maswali mengi,“Erick wewe kuna kubwa ulilolifanya zaidi ya hilo baba analolijua. Kwani umefanya nini tena?”Erick alikuwa kimya tu, na Erica akaendelea kuongea,“Haya, kuna kusoma tena hapa!! Kumbuka tulikaribia kufanya mitihani, itakuwaje tena? Mitihani ndio basi!!”“Erica, naomba uache nilale tu kwani naona akili yangu haipo sawa”“Unadhani nipo kukulaumu kwa ulichokifanya? Kama ni wao waliweka dawa na kukufanya uwe kama mcheza mieleka basi wanastahili kupata kipigo cha dawa walizoweka, ila kwenye kuua ndio pagumu Erick”Erick alikaa kimya, Erica alimuangalia na kumuona kama Erick anataka kupandisha hasira mpya, basi ikabidi aanze kumbembeleza kaka yake kwani alijua hapo hawezi kumpiga yeye ila kuna jambo angefanya hata kwenda nje na kumpiga yeye atakayemuona kwasababu ya hasira alizokuwa nazo.Yani siku hii Erica alijitolea kulala na kaka yake huku amemkumbatia, wakati Sarah amelala pembeni yao maana yeye alikuwa haelewi kitu chochote kinachoendelea yani alikuwa akishangaa tu, hata walivyohamishwa bado alikuwa haelewi sababu ya kuhama kwao ilikuwa ni kitu gani.Kulipokucha tu, mapema kabisa baba Angel alijiandaa na kutoka pale kwa mama yake ambapo moja kwa moja alienda nyumbani kwake.Ila kabla hajafika nyumbani kwake alimuona Jack akitaka kupanda kwenye pikipiki, basi akamsimamisha na kumwambia apande kwenye gari lake na kuanza kuongea nae,“Kheee ulikuwa wapi Erick?”“Aaaah mambo tu yamechanganya, ndio umetoka kwangu?”“Ndio, nilikuwa nataka kuja kukuaga maana kesho nasafiri kwenda zangu Afrika kusini”“Unaenda na Derrick?”“Hapana, nitamuacha sababu Maimuna kaniomba halafu ukizingatia yule mwanamke aliyezaa na Derrick, tunasubiri ili ikiwezekana Derrick na Samir waje kidogo na wao kule, niweze kuishi kidogo na mwanangu Samir, sema natakiwa kuondoka kesho ndiomana sijaweza kukaa zaidi hapa”“Dah!!”Kisha jack akamwambia baba Angel,“Ila huko nyumbani kwako nimekutana na askari watatu wakiongea na mlinzi wako”Hapo baba Angel alishtuka sana, akajua ndio mamabo yamekucha sasa, akageuza gari na kumuuliza Jack yani alikuwa hata hajielewi kabisa kwa muda huo,“Hao askari walikuwa wanataka nini?”“Mbona umegeuza gari haraka Erick?”“Dah!! Nina matatizo, niambie hao askari walikuwa wanataka nini?”“Nasikia kijana wako, kuna mtu kaenda kumnyonga nyumbani kwake, unajua sijaamini eeeh!! Ila kuna kesi na pale wanahisi huenda mmekimbia”“Ooooh Mungu wangu, naomba nikuombe kitu Jack”“Kitu gani?”“Naomba unavyosafiri kesho uende na kijana wangu Erick, nakuomba chondechonde nakuomba”“Kwani kuna nini?”“Nitakuelezea kila kitu Jack, ila nakuomba nahitaji kumuokoa mwanangu”“Ana hati ya kusafiria?”“Anayo ndio, mimi watoto wangu wote wanazo hati za kusafiria na huwa ikiisha muda basi mimi mwenyewe ndio naenda kui-renew tena”“Pole sana, ila niambie kwanza ni kitu gani?”Baba Angel alienda mahali na kuweka gari kisha kuanza kumueleza Jack kwa kifupi yani baba Angel alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa hata Jack alitambua jambo hili sema alikubali kumsaidia kwa lile hjambo linalomkabili,“Usijali Erick, Munguatusaidie tu tuweze kutoka na mwanao hapa nchini halafu nitakufundisha kitu na mwanao ataonekana hana hatia hapo badae, usijali kitu. Kuna watu wengi sana mimi najuana nao”Baba Angel alishukuru sana kwa hilo, basi kwa muda huo aliondoka na Jack kwenda kufanya mipango na taratibu za tiketi ya Erick.Kwakweli mama Angel alikuwepo pale nyumbani ila nae alikuwa haelewi kitu, kwa siku hii aliona ni vyema kumkataza kabisa mwanae kwenda sehemu yoyote ile, alimuomba sana kuwa atulie tu nyumbani,“Nakuomba mwanangu Erick, tulia nyumbani. Najua kama walichotutenda sio sawa ila mwanangu tulia, usiogope kitu”Baada ya muda, baba Angel alirudi nyumbani na kumtaka Erick ajiandae kwaajili ya safari ya kwenda Afrika kusini pamoja na yule Jack, hapo mama Angel alipinga kidogo,“Kheee aende na Jack tena!!”“Mke wangu, hii ni kwa usalama wa mtoto wetu, ataozea jela huyu”“Mmmmh lakini nani mwenye ushahidi juu ya hilo, na hakuna tunachojua kuwa dokta Jimmy kweli amekufa”“Mke wangu, unaambiwa huko nyumbani kwetu walienda mapolisi leo, bora tuwahi mapema haya mambo, kinga ni bora kuliko tiba”“Ila ndio aende na Jack jamani!! Simuamini yule mwanamke”“Hapana, yule Jack hana roho mbaya kama unavyomfikiria, ni mtu mwenye roho nzuri sana na ana utu sana, siku kaa na yule Derrick halafu atakwambia jinsi alivyo Jack”Mara simu ya baba Angel ilianza kuita, kuangalia akaona mpigaji ni Manka, basi baba Angel akaipokea na kuanza kuongea nayo,“Erick, hivi unajua alichosababisha mwanao huku?”“Kipi hiko?”“Mimi nilikuja nyumbani kwa Moses, tulikuwa tunaongea kwani kuna vitu nilikuwa namlaumu sana Moses, ila gafla alitokea Erick na kumkaba Moses, yani kamuua Moses mbele ya macho yangu. Kwahiyo mwanao kaua, yuko wapi kwani?”“Kheeee, makubwa hayo. Hata mimi sijui kwakweli alipo mwanangu maana hayupo nyumbani ana wiki sasa”“Kheeee, basi mwanao kaua hivyo”Baba Angel alikata ile simu na kumuangalia Erick kisha akamuuliza,“Kumbe sio dokta Jimmy pekee Erick umemuua hadi Moses?”“Nisamehe baba ila nilishindwa kuthibiti hasira zangu”“Ilikuwaje kwani?”“Mimi nilipotoka kugombana na yule dokta, niliamua kwenda kwa huyo Moses ili nimwambie ukweli wa nilichofanya kwa ndugu yake maana nilishajua kuwa ni ndugu. Nikafika na kumkuta na yule mnamuita Manka sijui, nilisikia wakiongea na nilifatilia yale maongezi yao kwani yule Manka alikuwa akiongea kwa sauti huku akilia ndipo nilipopatwa na hasira na kumkaba”“Duh!! Kwani walikuwa wakiongea nini?”“Yule mama alilalamika kuwa mara kadhaa yule Moses kamtuma kuja kukuua wewe, akamwambia kuwa amekudhulumu mali zako ila bado hajatosheka na kumtuma mara kadhaa akumalize, na bado akakupiga risasi miguuni, anasema kuwa kamtilia ubaya hadi yeye kwa kufanywa kazi za kutumikishwa wakati kafichwa ukweli wa mtoto kuwa sio wa kwake, kwa kufupi yule mama alikuwa akilalamika, ndio hapo nikajua ukweli kuwa ni yeye aliyekufanya ukae mwaka mzima bila kufanya kazi yoyote, nilishikwa na hasira na kumkaba, sijielewi baba, kwakweli sijielewi kabisa. Hizi nguvu nyingi natoa wapi sijielewi”Kiukweli baba Angel alimuhurumia sana kijana wake na hapo hata mama Angel alikubali kuwa Erick asafiri tu na Jack maana aliona hapo litaibuka kubwa zaidi ya wanaloliona na kulisikia.Usiku wa siku hii waliitumia kama familia kwaajili ya kumuaga Erick, ila baba Angel alikuwa na mashaka sana kuwa kama mwanae wamemtangaza basi itakuwa ni ngumu sana kuweza kutoroka hapo nchini, Erica alimuangalia baba yake na kumuuliza,“Baba, una mashaka na safari ya Erick?”“Kiukweli sina raha kabisa”“Hapana kuwa na amani tu, ataondoka salama”Basi Erick kusikia vile, alimvuta Erica pembeni na kuongea nae,“Ila je nitaweza kuishi bila kukuona wewe kabisa kwa siku zote?”“Kwani umeambiwa kuwa hutoniona siku zote? Kuna siku utaniona tu hata usijali, nenda tu huko kwa usalama wako Erick. Mimi mwenyewe binafsi sitaki upatwe na matatizo yoyote yale”“Sawa nimekuelewa, ila nitakukumbuka sana”“Najua hilo Erick, ila jiokoe kwanza kwa haya yaliyopo”Basi wakarudi na kula kwa pamoja na kuagana nae maana kesho yake ndio alikuwa akianza safari yake, kwa siku hii Sarah na Erica walilala nae pamoja tena.Muda wa safari tu ulipofika, baba Angel aliondoka na Erick mpaka uwanja wa ndege na kukutana huko na Jack, kisha akaongea na Jack pale jinsi ya kumsaidia mtoto wake ambapo kuna namba za mtu wa kumsaidia ambazo Jack alimpa kisha muda ulipofika moja kwa moja Jack na Erick walimuaga vizuri baba Angel na wenyewe wakaondoka.Baba Angel alikaa pale akiangalia angalia na muda ulipofika aliamua kuondoka ambapo moja kwa moja alienda kukutana na mtu ambaye alipewa namba na Jack, basi alikutana na yule mtu ambaye aliwasiliana nae, basi yule mtu alimsalimia baba Angel na kujitambulisha jina lake,“Mimi naitwa Ayubu au baba Yusra, karibu sana”“Asante, mimi naitwa Erick au baba Angel. Nashukuru sana kukufahamu”“Jack alinieleza mambo mengi tu kuhusu yanayokusibu”Kidogo simu ya yule Ayubu ilianza kuita, basi baada ya kuongea nayo ndio akamuangalia baba Angel na kumwambia,“Oooh kuna jirani yangu mahali Fulani nasikia ameuwawa, leo wamenikumbuka na wanahitaji nifanye uchunguzi wa hiyo kesi ili mtuhumiwa akamatwe”“Ooooh sasa itakuwaje?”“Hapo pagumu kidogo, ila unaonaje twende nyumbani kwangu ili ukapafahamu”Baba Angel alikubali na kwenda pamoja na huyu Ayubu ili apafahamu nyumbani kwake.Kufika nyumbani kwa Ayubu alishangaa kuona binti wa Ayubu akimfahamu yeye vizuri sana,“Nakufahamu ndio, wewe si baba yake Angel!!”“Ooooh kumbe unamfahamu Angel?”“Ndio namfahamu nilisoma nae yule”“Aaaah, nafurahi kujua hilo. Nitamwambia basi”Kisha baba Angel aliagana pale na Ayubu huku wakitegemea tena kuonana kwani Ayubu ndio alikuwa anataka kwenda kwenye huo msiba.Baba Angel alirudi nyumbani kwake lakini moja kwa moja alijua wazi kuwa yule Ayubu ameitiwa msiba wa Moses ila hakutaka kumuonyesha mshangao mapema, alitaka tu akimaliza hayo mambo ndio aweze kuongea nae.Usiku wa siku ile baba Angel alipigiwa simu na Ayubu kisha kuanza kuongea nae,“Jirani yangu anaitwa Moses, mazingira ya kesi yake yanafanana na ambayo amenielezea Jack, je ndio kesi ambayo mwanao anahusika”“Mmmmh tuonane kwanza ili tuongee vizuri”“Usijali, nataka niweke sawa haya mambo, kama ni yeye niambie ili nijue jinsi nitakavyowajibu kuhusu ushahidi wangu”“Ngoja basi nimuulize vizuri halafu nitakujulisha”Baba Angel alikata ile simu huku akiwaza kwa muda na kuamua kumpigia Jack ila kwa muda huo Jack hakupatikana hewani, aliamua kumtafuta kwenye mtandao wa kijamii na kumpata kisha akamuuliza,“Yule Ayubu kaniuliza swali ambalo ni kweli kabisa muhusika ni Erick, je nikubali? Haiwezi kuwa tatizo badae yani labda watumie kama ushahidi?”“Hapana usijali, yule ni ndugu yangu kabisa hawezi kukufanyia kitu kibaya, nishamueleza kuhusu mimi na wewe, hawezi kufanya ubaya, wewe mueleze tu kila kitu naye atajua namna ya kukuepusha na hilo janga”Ndipo baba Angel alipopata ujasiri wa kuwasiliana tena na yule mtu na kumwambia kuwa mwanae ni kweli ingawa hana uhakika kama kahusika kwa asilimia mia moja,“Basi ngoja nitajua jinsi ya kufanya, usijali kitu chochote. Kuwa na amani tu”Basi baba Angel alikata ile simu, ila kiukweli hakuwa na raha kabisa yani mambo hyote alikuwa akiyafanya ilimradi tu.Wakati mitihani ilipokaribia, ilibidi baba Angel ampeleke Erica akaishi kwa dada yake yaani Tumaini ili iwe rahisi maana kule kwa mama yake ni mbali sana, ingekuwa ngumu kwa Erica kwenda shule na kufanya mtihani.Basi waliongea kidogo pale na dada yake,“Hayo mambo yataishia wapi?”“Sijui dada yangu kwakweli ila Mungu anisaidie tu”Kisha baba Angel aliondoka kwa dada yake, ila njiani alikutana na Sia na kuanza kuongea nae kwani anajua fika kuwa Sia anafahamu vitu vingi sana, kwanza Sia alianza kumuuliza baba Angel,“mbona hewani hupatikani?”“Simu yangu ilipotea”“Halafu nyumbani kwako hampo familia nzima!”“Aaaah matatizo tu, nipe khabari maana najua wewe huwa hupitwi”“Na kweli sipitwi, nilikutana na Manka, yupo kama mtu aliyechanganyikiwa vile. Nasikia Moses amekufa, halafu mke wa Moses nae kachanganyikiwa sana”“Duh!! Dokta Jimmy anaendeleaje maana simpati hewani”“Huyo ndio hajulikani kabisa, ni wa kufa leo au kesho, hali yake ni mbaya sana kupita maelezo ya kawaida”“Duh!!”Hapa baba Angel ndio aligundua kuwa Erick hakumuua siku ile dokta Jimmy bali ameenda kummaliza Moses na shahidi wa mambo yote yale ni Manka tu ndiomana yupo kama kachanganyikiwa basi baba Angel aliona ni vyema kuongea na Manka pia huku akisaidiana na Ayubu katika kumsafisha mwanae.Baada ya miezi miwili, baba Angel alimtafuta Manka ambaye alikuwa kama watu waliopungukiwa na akili, hata yeye mwenyewe binafsi alimuhurumia sana, ila alikaa chini na kuongea nae,“Unajua sina amani, sina furaha moyoni, siwezi kuishi tena na Sarah maana kawapenda sana halafu pia siwezi kuishi na Elly, najihisi vibaya sana katika moyo wangu. Natamani ingetokea kitu moja kikubwa kifanyike hata niweze kuishi pamoja na wanangu hata niwe nawaona tu”“Usijali, lazima tuhakikishe kuwa tutafanya kitu. Ngoja nikuulize, kesi ya kifo cha Moses imeishia wapi?”“Ni wazi aliyeua ni mwanao, ila ulichokifanya Erick unakijua mwenyewe, leo hii inasemekana kuwa Moses kajiua mwenyewe, halafu dokta Jimmy alipata ajali eti ajali ndio imemuweka kitandani hadi umauti!!”“Khaaa dokta Jimmy amekufa?”“Ndio, dokta Jimmy amekufa, tumetoka kumzika kama wiki mbili zilizopita, hakuna mwenye amani ya moyo kabisa.”“Yule mtoto ambaye dokta Jimmy alikuwa akimlea, yule wa madam Oliva kaishia wapi?”“Yule mtoto kachukuliwa na Oliva mwenyewe, kwanza unajua kama huyo Oliva alishajifungua tayari!!”“Kumbe!!”“Ndio, amepata mtoto wa kike, na yule mtoto wake ameenda kuishi nae. Yule mtoto anaitwa Jimmy. Ila mimi na yule anaitwa Sia ndio hatuna bahati kwakweli, mimi sijui naishia wapi najiona kabisa nimefikia ukingoni”“Pole sana”“Kuna shamba kubwa sana, Sarah alipewa na mzee Jimmy ila Sarah hajawahi kuliona shamba hilo, siwezi kumdhurumu, nashukuru nimekutana nawe twende nikakuonyeshe shamba hilo”Baba Angel alikubali tu na muda huo huo waliondoka na kuelekea kwenye hilo shamba huku wakiongea vitu mbalimbali,“Ila kwanini ulitaka kuniua Manka?”“Nisamehe ila nilikuwa natumwa tu kufanya vile, nilijua hawa watu niko nao pamoja kumbe wananing’onga na kunicheka”Walifika kwenye lile shamba na baba Angel alipata kuliona, kwakweli lilikuwa kubwa sana na kumfanya baba Angel afikirie kitu cha kufanya na lile shamba.Aliongea nae kidogo tu na kuahidi kumtafuta tena.Baba Angel, leo alihama na familia yake kutoka kwenye nyumba ya mama yake maana kulikuwa na nyumba yake nyingine ambayo ndio aliimalizia kuijenga, basi walifurahi na kwa pamoja waliondoka na kuhamia huko, ila sehemu waliyohamia walikuta na baba Emma nae na familia yake ndio wamehamia sehemu hiyo hiyo.Basi siku hiyo alikutana nae huku baba Emma akilalamika,“Yani yule dokta Jimmy amekufa bila mimi kujua ukweli wa watoto wangu walipo!! Roho inaniuma sana”“Pole sana, ila Mungu akitaka ukweli uujue basi utaujua tu maana hakuna marefu yasiyokuwa na ncha”“Ila naumia sana, huyu dokta Jimmy nitamchukia hadi naingia kaburini”Baba Angel alijaribu kumpa moyo pale kisha kuendelea kuwa majirani wazuri pale kwao.Baba Angel aliamua kutimiza lile wazo la Jack na kuamua pia kuishi sehemu moja Derrick na Samir maana alijenga sehemu nyingine ya kuweza kuishi hawa watoto wa kiume ili pale pale maeneo ya nyumbani kwake. Alifanya hivi ili asiwe nao mbali na hawa ukizingatia Jack ndio alikuwa akiishi na Erick.Pia baba Angel alimwambia mama Sarah arudi kwenye nyumba yake ambapo mara moja moja Sarah alikuwa akimtembelea maana bado ni mlezi wake ila mama Sarah alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa haswaa kwa swala la Elly kutokumkubali huku akizamia kwa baba yake Derrick.Miaka mitano inapita na kufanya waanze kusahau yale machungu ambayo yalitokea baina yao, leo ilikuwa ni siku ya furaha sana kwenye familia yao kwani ilikuwa ni siku ambayo Erick alirudi kutoka Afrika Kusini akiwa ameongozana na Jack, yani ilikuwa ni furaha sana kwa familia hii na wote walikuwepo nyumbani kwaajili ya kumkaribisha Erick tena katika maisha yao.Siku hii Angel alikaa na Samir na kuanza kuongea nae,“Angel, sikia nikwambie kitu yani mimi naona kabisa sitaweza bila wewe kuwa mke wangu. Ila nafasi ya mimi na wewe kufunga ndoa ipo wazi kabisa, sababu wewe ni mtoto wa Rahim na mimi ni mtoto wa Erick, mama zetu ni tofauti kabisa, je kwanini tusiweze kuoana?”“Mmmmh ngoja tumuombe baba, anaweza akakubali”Walijipanga na siku hii Angel aliweka ombi hili kwa baba yake kuwa anaomba yeye na Samir wafunge ndoa,“Hapana haiwezekani Angel”“Baba, inamaana mimi sitaolewa miaka yote maana mtu ninayempenda ni Samir halafu hakuna kizuizi kati yangu na Samir, kwanini isiwezekane?”“Ngoja nikajadiliane hayo maswala na mama yenu”Baada ya shughuli ya siku ile baba Angel alienda kumwambia mama Angel kuhusu watoto wao ila mama Angel alikubali kiurahisi kabisa, kisha kesho yake wakamtaka Angel na Samir waende kuongea na Rahim kuhusu swala lao la hiyo ndoa.Angel alimuomba Erick aweze kumsindikiza katika kumpa ujumbe Rahim juu ya ndoa yake na Samir maana Samir aliogopa kwenda kusema ukizingatia alikuwa akimuogopa sana Rahim toka siku aliyotaka kumuua.Angel alikutana njiani na Rahim na kuanza kumwambia kuhusu dhamira yake,“Naomba mimi na Samir tuweze kufunga ndoa, nampenda na yeye ananipenda”“Haiwezekani, aibu niliyoipata kwa Derrick inatosha msije kuniletea na nyie aibu”“Aibu kivipi? Baba kule amekubali ukizingatia mimi na Samir sio ndugu”“Nitolee balaa Angel, Samir nimemlea kama yeye haoni undugu wenu basi alete masikhara kwangu nitamfanyia kitu kibaya asiweze kusahau maisha yote”Mara Erick akamwambia Rahim,“Unasemaje wewe?”Rahim alimuangalia Erick na kumuona kabadilika sura huku mishipa ikiwa imemsimama yani Rahim aliogopa sana alikumbuka siku aliyokabwa na Erick, kwahiyo kwa kujihami akajikuta akianza kukimbia, ila kwa bahati mbaya hakuangalia upande wa pili wakati anavuka barabara kwa kukimbia hadi akagongwa na gari. Rahim alimuangalia Erick na kumuona kabadilika sura huku mishipa ikiwa imemsimama yani Rahim aliogopa sana alikumbuka siku aliyokabwa na Erick, kwahiyo kwa kujihami akajikuta akianza kukimbia, ila kwa bahati mbaya hakuangalia upande wa pili wakati anavuka barabara kwa kukimbia hadi akagongwa na gari.Kilikuwa ni kitendo cha gafla sana, ikabidi Angel na Erick wasogee pale alipokuwa Rahim na kuomba msaada wa kupelekwa hospitali ila haikuchukua muda kwani majibu yalipatikana pale pale kuwa Rahim ameaga dunia, basi Angel alianza kupigia simu watu mbalimbalikuwapa ile taarifa huku akimwambia Erick,“Na wewe umezidi na misuli yako, kwa stahili hii jamani si utaua wengi wewe!”“Aaaah sikutaka ila sikupenda ile kauli yake”“Hata kama, uwe unajitahidi kujizuia, Erick umerudi jana tu halafu leo umezua balaa jamani loh!!”Wakaenda nyumbani ambapo baba Angel na mama Angel walielezewa na Angel ilivyokuwa na moja kwa moja walijua kuwa uoga wa Rahim kwa Erick ndio umesababisha yote yale ila hawakuwa na cha kufanya maana tayari msiba ulishatokea.Ikawa ni majonzi ya kifo cha Rahim lakini kilichosababishwa na Erick, huku ikisemekana kuwa ni ajali ndio iliyomuua Rahim, hapo walilia sana hasa watoto wa Rahim na baba Angel kuzidi kuona madhara yaliyopo kwa Erick, kiukweli hakujua cha kufanya na Erick.Siku ya mazishi ya Rahim, na Manka alikuwepo kwahiyo baada ya mazishi tu baba Angel aliamua kwenda kuongea na Manka kuhusu Erick, alikuwa akihisi huenda hata dokta Jimmy alikuwa amemuachia siri ya kufanya Erick apate nafuu, ila Manka alimwambia kuwa dawa ni moja tu yani Erick alale na Erica ndio nguvu za Erick zitakuwa sawa, kwakweli baba Angel bado roho ilimuuma sana kwa kuweza kufikiria jinsi Erick na Erica walale kimapenzi wakati ni watoto wake wote wawili.Ila wakati anataka kuondoka, Manka alimpa ujumbe ambao alipewa na Sarah,“Sarah kaniambia kuwa kapata mchumba, atakuja kukutambulisha ili aolewe”“Kheee watoto wa siku hizi wanawahi”“Mwache awahi tu, huyu mtoto alianza mapepe mapema sana, bora tu aolewe ila mimi najitolea kuishi nao yeye na mchumba wake nyumbani kwangu”“Kama wakiamua kuishi kwao je?”“Basi nitahamia huko, mimi ni mpweke sana. Halafu ngoja nikwambie kitu kingine ambacho hujui kuhusu mimi”“Kitu gani hiko?”“Mimi ni mwathirika”Hili baba Angel alilijua vizuri kabisa maana huyu alitembea na Rahim ambaye alishaathirika kitambo sana ila tu alijifanya kushangaa kanakwamba hakujua kitu,“Oooh pole na hongera kwa ujasiri wako wa kusema, kuwa muathirika sio mwisho wa maisha, bado unanafasi kubwa sana ya kusonga mbele”“Asante ila najua aliyeniambukiza”“Nani huyo?”“Huyu huyu marehemu Rahim, alijifanya ananipenda kumbe yupo kwaajili ya kunipa maradhi tu, ila Mungu alivyosasa ona yeye kafa kwa ajali tena ya kujitakia mwenyewe maana alikuwa anakimbilia wapi sijui”“Mmmmh haya yaishe, tutaonana tena siku nyingine”Siku hizi Manka alikuwa mpole sana, kwanza alionekana kama mtu ambaye akili zake hazifanyi kazi vizuri na hakuona tatizo kuongea lolote na sehemu yoyote ile.Baba Angel alirudi nyumbani kwake huku akikuna kichwa chake kwa mawazo aliyokuwa nayo, basi aliongea na mke wake kile ambacho aliambiwa na Manka,“Unajua Manka anasema tatizo la Erick linaweza kumalizwa na Erica tu”“Hivi kwa mfano tukamtafutia Erick msichana mwingine itakuwaje?”“Mmmh unatafuta balaa mama Angel, tutamsafirisha wapi tena akiharibu? Anaweza kuua huyu mtoto ujue. Tujifunze kutokana na makosa”“Sasa itakuwaje? Tutakubali watoto wetu walale pamoja kimapenzi?”“Aaaah hiyo ngumu ila ngoja tutafakari”Waliamua tu kulala kwa muda huo.Kulivyokucha tu, Sarah aliwafata na kuwapa taarifa kuwa anataka kwenda kumtambulisha mchumba wake kwao, walikubali tu hawakuwa na pingamizi juu ya hilo.Kisha baba Angel alienda kumfata Erick ambaye hana siku nyimgi toka arudi, aliongea nae kirafiki tu amsikie majibu yake,“Erick, hebu niambie kitu. Leo ndugu yako Sarah amesema kuwa analeta mchumba wake kumtambulisha, je wa kwako utamleta lini?”“Kwani na Erica kashamleta wa kwake?”“Hapana”“Nitamleta pindi Erica akimleta mtu”Baba Angel aliitikia tu ila alijaribu kusoma kitu na kwenda kuongea na mke wake kisha wakapanga mpango.Kwenye mida ya jioni, Sarah alileta mchumba wake nyumbani kwao na walimkaribisha vizuri sana, huyu alikuwa ni mtoto aliyelelewa na madam Oliva, ila ni mtoto wa Sia na Steve yani Paul.Baba Angel na mama Angel hawakuwa na pingamizi kabisa juu ya mapenzi ya hawa watu.Kisha baada ya Paul kuondoka, baba Angel aliondoka pia ili kwenda kujaribu kile anachoona kinafaa zaidi, alienda hadi nyumbani kwa Bahati na Fetty na kuongea nao juu ya kijana wao Bahati aje kwake kujitambulisha kama mchumba wa Erica, alimuahidi kumlipa ila hakumwambia kwanini anataka iwe hivyo, hilo lilikuwa swala rahisi sana kwa Bahati mdogo kwani alikubali kiurahisi ukizingatia anampenda sana Erica.Baba Angel alipomaliza hapo alirudi nyumbani na kumpa ule ujumbe mke wake, ambaye aliafikiana nae na wakapanga kesho yake kuwa wampange Erica aweze kukubali wakati Bahati anaenda kujitambulisha maana hawakutaka kuchelewesha mambo.Halafu wakapanga lingine sasa,“Hili likifanikiwa tu, basi moja kwa moja tutaenda kuongea na baba Emma ili tumchukue yule Emmanah awe na Erick au unasemaje?”“Hapo sawa kabisa baba Angel, yani yule Emmanah umelenga haswaaa, tujitahidi Erick aweze kumkubali kwakweli”Basi walipanga mpango wao kwa namna hiyo.Kulipokucha tu, mama Angel akamuita Erica na kumpanga ila Erica alikuwa akipinga vikali kuhusu swala hilo,“Kwanini mmefikia huko mama?”“Tunataka kumuokoa kaka yako”“Nadhani mnataka kumuangamiza, mnajua madhara ya hiko mnachokitaka?”“Usiwe mkaidi Erica, naomba ukubali”Erica alikubali lakini kishingo upande.Jioni ya siku hii, alikuja Bahari kama mchumba wa Erica yani alikuja kujitambulisha na baba Angel aliwaita watoto wake wote ili wamshuhudie mchumba wa Erica, basi baba Angel alianza kutoa ule utambulisho, kitu cha kushangaza Erick aliinuka huku akiwa na gadhabu kali sana, alimkunja Bahati na kumtwika ngumi ambayo ilimpeleka Bahati chini yani ilibidi tu Erica ndio aende kuingilia kati ila Bahati alikuwa na hali mbaya sana ikabidi wamkimbizie hospitali kwa tiba ya haraka yani kila kitu hapo nyumbani kwao kilivurugika.Wakati baba Angel yupo hospitali kwaajili ya matibabu ya Bahati, ndipo alipokutana na mke wa Moses ambaye alidai kuwa mwanae yupo hapo hospitali pia,“Kheee pole sana, kafanyaje kwani?”“Kapata ajali, kapoteza damu nyingi sana yani sijui nifanyeje na anatakiwa kuongezwa damu”Baba Angel alijitolea kufanya hivyo, ila walienda kumchukua damu yake na kukuta na damu ya yule kijana haziendani, ila mara baba Emma nae alionekana pale akisema kachanganyikiwa maana mwanae kapata ajali pia na anatakiwa kuongezwa damu ila yeye haendani nae damu yake, ila daktari akawaita wote wawili maana kila mmoja damu ilionekana kuonda kwa mwingine, yani baba Emma alifanana damu na mtoto wa Moses halafu baba Angel alifanana damu na Emmanuel, basi waliwaongezea damu na watoto wakendelea vizuri.Ikawa kila wanapoenda hospitali wanakutana, huku wakina Bahati na mkewe Fetty nao wakienda kumtazama mtoto wao.Siku hii, Erica alimuita baba yake na mama yake na kuanza kuongea nao,“Kwani baba na mama tatizo lenu ni nini?”“Tatizo letu ni kuwa tunaogopa wewe na Erick kuwa pamoja kimapenzi, ndiomana tunafanya jitihada zote kuweza kuweka mambo sawa”“Ila kabla hamjaendelea na hiso jitihada zenu, nakuomba baba nenda kamtafute yule rafiki yako dokta Noah mwambie akwambie ukweli”Baba Angel alishangaa sana ila alikubali kufanya vile, na kweli siku ile ile aliamua kumtafuta dokta Noah na kuanza kuongea nae, hata dokta Noah alimshangaa baba Angel na kumuuliza,“Nani kakwambia kuwa mimi nina ukweli?”“Binti yangu Erica”“Dah!! Ila naogopa”“Hapana, niambie tu.”“Ngoja nitapanga siku nitakuita mahali utakutana na wengine, na hapo nitasema ukweli ila mnilinde maana sina cha kufanya”“Nitakulinda, nahitaji tu ukweli”Baba Angel alimuahidi dokta Noah kuwa atamlinda maana alimwambia kuwa atausema ukweli wote ulivyo.Siku hiyo dokta Noah alimuita baba Angel na mama Angel, walijiandaa na kwenda alipowaita ila walishangaa sana kufika kule kumkuta baba Emma, mama Emma, mke wa Moses pamoja na Juli, kisha dokta Noah alianza kuongea,“Samahani sana kwa hiki nitakachowaambia”“Bila samahani, sisi tutakusikiliza”“Miaka ya nyumba iliyopita wakati Erica akiwa mjamzito, nilimsikia mkwe wake na dokta mwenzangu wakipanga mipango mibaya juu ya wale watoto, kwanza walipanga mipango ya kuwabadilisha na badae walipanga mipango ya kuwachoma sindano, roho iliniuma sana kwani nilijua wazi hao watoto wakiwa wakubwa watakuwa ni mwiba kwa wazazi wao. Naomba mnisamhe hiki ambacho nitakachowaambia, kuna huyu dada anaitwa Juli, enzi hizo alikuwa na maisha magumu sana na alikuwa akitaka atoe mimba, ila badae alipanga akijifungua atupe mtoto, ila alijifungua watoto mapacha mmoja wakike na mwingine wa kiume, nilimuomba asiwatupe, nikaenda kuwahifadhi na ndipo muda naenda kuwahifadhi nilikuta Erica ameshajifungua wale watoto wake, ila alijifungua mapacha watatu tofauti na tulivyojua mwanzo, yani hata sikufikiria mara mbili bali nilimbadili yule mtoto wa kiume na mtoto wa Erica muda huo huo. Ila sikutaka mtoto wa Erick aende kuishi maisha ya shida, na hivyo nikawaweka pembeni na kupewa mgonjwa wa kujifungua ambaye alikuwa ni wewe Neema, kiukweli hukujifungua mapacha ila ulijifungua mtoto mmoja, nami nikamchukua mtoto wako na kukuwekea wale wawili ambapo mmoja ni mtoto wa Juli na mwingine ni mtoto wa Erica, nikaondoka na mtoto wako ambaye sikutaka apate shida pia, basi mke wa Moses alipojifungua nikamuongezea na mtoto mwingine ambapo na yeye alionekana kuwa kajifungua mapacha, hii kitu imenitesa kwa miaka yote hii. Niliandika hadi kwenye Kitabu changu cha kumbukumbu, kila siku nilitamani kusema ukweli ila niliogopa. Nilijua kuwa wote mngenichukia, sikufanya kwa nia mbaya ila kitendo changu cha kubadilisha mtoto wa Erica ndio kimezaa yote haya. Naomba mnisamehe sana”Baba Angel alipumua kiasi na kumuuliza,“Inamaana hata dokta Jimmy na mzee Jimmy hawajui hiki ulichokifanya?”“Hakuna aliyekuwa anajua zaidi yangu”“Yani kumbe wengine wanabadilisha huku watoto na wewe unabadilisha huku, mnajua nyie mnaweza fanya wazazi wakawa machizi!”“Nisamehe Erick, ila nilifanya kwaajili ya kukomboa kizazi chako”“Kwahiyo Erick sio mwanangu?”“Ndio, Erick na Emmanah ni mapacha, ni watoto wa Juli ambaye alishindwa kuwalea”“Duh!!”Baba Emma nae aliuliza vizuri,“Kwahiyo na mimi mwanangu ni nani?”“Ni mtoto wa Moses, anaitwa Abraham ndio mtoto wako wewe”Mke wa Moses nae alikuwa akishangaa na kuuliza,“Kwahiyo sikujifungua mapacha?”“Ndio, ulijifungua mtoto mmoja tu”“Ile hospitali ndiomana mnapenda kutufanyia upasuaji kumbe mnayenu mnayoyajua nyie”“Ishafungwa ile hospitali kwa ujinga wao”“Naomba mnisamehe maana nilitaka kuokoa watoto wa Erick”“Aaaah hata kama, ila kwanini uingilie na kubadilisha watoto wa wengine? Hapo ndio sijakupenda”Basi mama Angel alimuangalia Juli na kumuuliza,“Na wewe kulikoni kutaka kutupa watoto? Ulizaa na nani kwanza?”“jamani maisha dah!! Najua hata hivyo watoto wenyewe hawawezi kunikubali. Nilizaa na mtu mmoja anaitwa Yuda”“Khaaa alipokea kichapo toka kwa Erick huyo loh!! Ni halali yake kumbe, alikataa mimba eeeh!!”“Ndio alikataa ndio chanzo cha mimi kuanza kutangatanga”Ila wote walijikuta wakimjadili vibaya dokta Noah, kasoro baba Angel, mama Angel na Juli. Ila sababu dokta Noah alisema ukweli baba Angel aliamua kuchukua hatua pale pale na kurudi nyumbani kwake huku akiruhusu Erica na Erick kuwa pamoja maana aliona Erick atazidi kuharibu na kuharibikiwa.Ila Erica bado alishikilia msimamo wake ule ule kuwa hakuna kitu mpaka ndoa ifanyike, kwakweli hili swala lilikuwa ni jambo la aibu kwa baba Angel ila alikubaliana nao wote kufunga ndoa na kufanya sherehe ya kifamilia.Na kweli walifunga ndoa na kufanya sherehe ya kifamilia, yani baba Angel alikuwa akiona aibu sana ila siku aliyofunga ndoa Angel na Samir, ndio siku aliyofunga ndoa Sarah na Paul halafu Erica na Erick nao walifunga ndoa siku hiyo. Baba Angel hakutaka wengi wajue, ila habari ilimfikia Sia ambaye alifika na kuongea na baba Angel,“Unajua kuna vitu mtu unaweza kuvizuia weee ukajikuta unashindwa ila badae mapenzi yakachukua nafasi yake, unaamini kuwa mapenzi yana nguvu sana?”“Ndio ninaamini, hata kwa madam Oliva na Steve ilikuwa hivi hivi, tulijua ni dawa tu kumbe na mapenzi nayo yalikuwa na nguvu zake hadi mtu kajikuta anatengeneza dawa”“Umeona kwa watoto, umewalea siku zote katika misingi ya dini sijui ikawaje ukateleza kumbe nguvu ya mapenzi inataka kuchukua nafasi yake”Baba Angel akacheka na kumwambia Sia,“Mjinga wewe, saivi na mke wangu tunarudi tena kwenye maombi”“Mungu hakutaka mumsumbue kwa maombi yenu ya kuombea watoto watengane wakati kuna nguvu ya mapenzi kati yao”“Mjinga sana wewe”“Ila tuache masikhara Erick, kwakweli mapenzi yana nguvu”Baba Angel alicheka tu, ila zile sherehe zilipoisha aliwapatia wote watoto wake nyumba za kuishi halafu yeye nyumbani kwake alibakia na mke wake pamoja na mtoto wao Ester.Leo, baba Angel alienda kumtembelea Erick pamoja na Erica huku akiwa ameongozana na dokta Noah, ambapo alikaa na kuongea nao ukweli wote ila ilikuwa ni ajabu sana kwani Erick hakuchukia kama siku zote jinsi anavyofanya ila tu alimpongeza huyu dokta kwa kile alichokifanya kwao, huku akimsifia sana Erica,“Licha ya dawa tulizopewa ila bado Erica ni mwanamke jasiri sana, kwani ameweza kunitoa katika hali hii mara nyingi sana. Kwakweli Erica anahaki ya kupewa sifa ya kuwa mke mwema”Basi baba Angel alimuuliza mwanae kwa masikhara,“Eti Erick, mapenzi yana nguvu?”“Ndio baba yana nguvu sana, yani wao walipanga vile halafu mapenzi yakapanga vingine. Unafikiri kwanini huyu dokta alitubadilisha! Ni sababu ya nguvu ya mapenzi, hakubadilisha kwa akili yake ila nguvu ya mapenzi ilimsukuma, alihisi uchungu kwa rafiki yake kufanyiwa fedheha”“Ila bado Erick utabaki kuwa mwanangu wa pekee”“Hata wewe baba utabaki kuwa baba yangu wa pekee”Erick na baba Angel walikumbatiana pale.

    MWISHO


0 comments:

Post a Comment

Blog