Search This Blog

Tuesday, 1 November 2022

SIPASWI KUSAMEHEWA - 4

 








Simulizi : Sipaswi Kusamehe

Sehemu Ya Nne (4)







“Mikono inaposhindwa kumgusa mtu labda kutokana na umbali ama sababu nyingine yeyote, kitu pekee ambacho kinaweza kumgusa ni moyo na hata kumkumbatia bila kujali umbali, Esmile upo sana moyoni mwangu na sitegemei kukutoa, labda wewe ufanye kitendo hicho cha kikatili,” alijitetea Mam.

“Usitegemee kabisa jambo hilo kutoka kwangu Mam, ninaamini mimi ndio nitakuwa mtu wa mwisho kulivunja pendo letu,” waliongea mambo mengi kunakshi penzi lao na mwisho wakaagana kwa ahadi ya kuwasiliana siku ifuatayo.

Usiku huo akajiweka sawa Esmile, akafikiri kwanza, maana yeye huamini mno kauli za mwanzo za wazee ambazo zilikuwa na mafunzo makubwa, alikumbuka kauli moja isemayo

“Fikiri kabla ya kutenda,” ndio nae sasa aliketi chini na kufikiri, afanye hivyo akili yake inavyomtuma ama aipotezee?

Asubuhi na mapema Esmile akawaaga wazazi wake na kuwaambia anaelekea Tanga mara moja ila hajui atarudi lini, bali akiisha fika na kujua kile kinachompeleka huko, atawasiliana nao na kuwajulisha anaweza kurudi baada ya muda gani.

“Inaweza kuzidi siku 3?” aliuliza mama yake.

“Hapana haiwezi kuzidi siku 3mama yangu,” akaondoka na kwenda Ubungo. Akapanda gari kuelekea Tanga bila hata kumtaarifu Mam, Saa 6 mchana alikuwa jijini Tanga. Akatafuta mgahawa na kupata kitu kwa ajili ya kukaza tumbo.

Saa 8 mchana, Esmile alimpigia simu Mam na kumuuliza alipo, akajibu yupo Tanga, Esmile akacheka na kusema

“Najua upo Tanga, Tanga ni kubwa sana, sehemu gani?”

“Aaah, Makorora kwa bibi, kwani vipi?”

“Hapana nataka kujua, maana waswahili walisema abiria chunga mzigo wako” alitania Esmile Mam akacheka kwa sauti na kuchombeza

“Anhaa, kumbe mi mzigo eti? Poa bwana, mzigo gani uaongea?” wakataniana kidogo, kisha akamuuliza hapo Makorora kwa bibi yake pakoje, kabla hajamjibu, Mam akamuuliza anapaulizia pa nini

“Mam acha mambo yako, kwani hujui kazi yangu? Wakati mwingine mi hufika bandari ya Tanga, ndio sababu nataka kupajua kwa bibi ili nikifika siku yoyote niweze kumtembelea, ama si sawa?”

“Eh makubwa, yaishe,” akamuelekeza na kumuuliza ana mpango wa kwenda huko lini, akamjibu kuwa leo leo atakuwa Tanga. Mam akacheka na kumkaribisha akijua ni sehemu ya matani yao.

“Naruhusiwa kufika kwa bibi?”

“Yah, why not? Utapokelewa kwa mikono 6” Bado Mam aliendelea kutania tu. Esmile akacheka na kusema itakuwa ngumu kidogo kufika kwa bibi. Mam akamwambia iwapo atafika Tanga, nae akiwa kule, asipofika kwa bibi yake, wala asimtafute, Esmile alisema hataenda ng’o…

“Poa, hapo ndio utaujua msimamo wangu, nitaliweka penzi pembeni,”

“Labda uutoe moyo, nilivyo kushika hivyo? Utaanzaje kunipotezea?” Walicheka kwa pamoja na kuendelea kutaniana kwa muda kidogo kisha wakaagana.

Muda wote waliokuwa wakitaniana, Esmile alikuwa ndani ya Jiji la Tanga akitalii kwenye mitaa mbalimbali hadi saa 11 jioni alipoita Taxi na kumuelekeza sehemu anayotaka kwenda. Walifika kule na kuachana, Esmile akaelekea mlangoni.

Sehemu yenyewe ilikua ni nyumbani kwa bibi yake Mam. Alifanya Surprise, hakutaka hata kumpigia simu. Akasimama mbele ya nyumba alio elekezwa na kujisemea moyoni ikiwa sio hii basi pale watamuelekeza. Maana nyumba zile zilikuwa zimefanana mno.

Baada ya kugonga mara moja tu lakini kwa nguvu, aliweza kusikia akikaribishwa na baada ya sekunde kadhaa alikuja binti mdogo kiasi kufungua, alikuwa ni binti mwenye heshima kubwa, akamkaribisha ndani na kuketi kwenye kiti, kisha pasi na kumuuliza, akamletea maji ya kunywa, Esmile alishangaa kuletewa maji hata kabla hajaomba, lakini utaratibu ule ila ulimvutia sana japo ulikuwa ni mgeni kwake.

Alipokea maji yale na kunywa kidogo, alipomaliza kunywa maji na kuweka glasi juu ya meza ndio wakasalimiana kwa kituo na binti yule, akamuulizia Mam, akaambiwa wapo jirani kuna hina ya harusi, Esmile akatoa simu ili ampigie, binti akamwambia haina hata haja maana wote wameziacha simu zao pale ndani zikiwa kwenye chaji.

“Ujue umeme ulikatika hapa kwetu Tanga tangu jana usiku na leo ndio umerudi alasiri hii na kama unavyojua simu hizi za Android zinavyokula charge, hivyo wameamua kuziacha kwenye charge,” aliongezea binti huyo ili kumfanya Esmile asijiulize maswali mengi.

Alipojaribu kumtuma akamuite akaambiwa itakuwa ngumu kwa sababu yeye hawezi kumuacha mgeni asiyemjua ndani peke yake, hivyo binti yule alimuomba Esmil kuvumilia tu hadi watakaporudi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Wanategemea kurudi saa ngapi?” alihoji Esmile.

“Haina uhakika ni muda gani lakini hawatochukua muda mrefu sana, we wala usihofu mgeni, karibu sana na jisikie upo nyumbani.”

Esmile alimuelewa binti yule akawa mpole. Aliendea kukaa naye na kupiga nae stori za hapa na pale ili kuusogeza muda mbele ambao kwa hakika Esmile alikuwa akiona kama vile muda umesimama.

Upande wa Yule binti yeye alikuwa akiona kama kwamba muda unayoyoma sana, maana kuna mengi alitakiwa kuwa nafanya muda ule lakini yalikwamishwa na kutokuwepo kwa Mam na bibi yake.

Kule aliko Mam nayo mambo yakanoga hivyo wakajisahau hata kurudi nyumbani kwa wakati, ikawa stori moja baada ya nyingine.

“Binti, huchukua muda gani hadi shughuli kama hizi kuisha? Nahic muda si rafiki tena kwa mimi kuendelea kuwepo hapa,” aliongea Esmile huku akitazama saa ya kwenye simu yake.

“Ni kweli kwa leo wamechelewa, lakini huenda wamepatwa na udhuru Fulani, nahisi itakuwa ndio sababu ya kuwachelewesha,”

“Unaweza kunielekeza hiyo nyumba yenyewe yenye shughuli ili niende nikaulizie na ikiwezekana waniitie?”

“Hapana kaka1 huko kuna mambo ya kike matupu, si vizuri kwa mwanaume kufika, kwa mila na tamaduni zetu za huku Pwani, hutakiwi kufika hapo,”

Kwa mara nyingine tena, Esmile alimuelewa yule binti na kushindwa kumshawishi juu ya kumuonesha nyumba ambayo ina sherehe inayo Endelea.

Ilipofika saa moja kasoro Esmile uzalendo ukamshinda, sasa ikabidi aage, binti alijitahidi sana kumbembeleza abaki, lakini Esmile akamueleza kuwa muda si rafiki na sasa hauruhusu tena kwa yeye kuendelea kuwa pale, na kwa kuwa kesho atakuwa bado yupo Tanga, atakuja tena, suala la Msingi ni kumsalimia Mam atakapokuja.

Binti akamruhusu kwa unyonge, kitu ambacho kilizidi kumshangaza Esmile, maana hawajuani, ila moyoni akajiongeza, ndio maana wanasema mapenzi yalizaliwa Tanga, wana upendo sana sana watu wa kule.

Wakati Esmile ameshika kitasa cha mlango ili atoke, nje nako kulisikika sauti za watu waliokuwa wakigonga mlango huo huo, Esmile akarudi nyuma ili kumpisha mwenyeji ndio afungue mlango

Esmile alirudi nyuma kidogo na kumuacha binti afungue mlango, ghafla binti akasema huku akimtazama Esmile akiwa na tabasamu usoni

“Ndio hao wamerudi, lazima itakuwa ni wao tu wamerudi.”

Akashika kitasa cha mlango na kuufungua, na Mam ndiyo alikuwa mtu wa kwanza kuingia ndani, hakuamini macho yake, akafumbua midomo kwa mshangao na kusema

“Haaa Esmile!” huku akiwa ameziba midomo kwa mikono yake yote miwili, kisha akamrukia kifuani na kumkaribisha tena, akashindwa kumkatalia Mam, akarudi kuketi huku bibi akiwa anawatazama tu kisha nae akaingia baada ya wao kuingia.

Mam akamtambulisha Esmile kwa bibi yake kama jirani yao kule Dar, amefika kikazi pale Tanga kisha akamtambulisha Esmile kuwa yule ni bibi yake mzaa baba na ndio Mam mwenyewe, wakacheka na wakaketi wao wawili, Bibi na binti wakaondoka pale na kuwaachia nafasi wawili hao wapate kuongea yao.

Hawakuongea kwa muda mrefu sana maana muda ulikuwa umeisha kimbia sana. Esmile aliaga baada ya bibi kuja na hata bibi alipomkaribisha chakula, bado esmile alikikataa na kutoa ahadi ya kuja kula siku nyingine atakayojaaliwa.

“Bibi mimi huja hapa Tanga mara nyingi sana, lakini hapo awali nilikuwa sipafahamu, ila sasa bibi yangu utanichoka tu…” alisema Esmile huku akinyanyuka.

Wakaagana na kuchomoka akishindikizwa na Mam hadi nje aliposimamisha pikipiki iliyomchukua hadi hotelini alipofikia.

Aliporejea hotelini baada ya kuoga na kuwasha TV, akachukua simu yake ya mkononi na kumpigia Mam. Kwanza walizungumza yao na hapa ndio Esmile alipotumia kumuuliza ni kwanini aliondoka katika mazingira yale.

Mam akamuomba asizungumzie suala lile kwa wakati ule kwani ni sawa na kutia chumvi kwenye kidonda kibichi.

“Mam milele kama kidonda kisipopata tiba muafaka, hakiwezi kupona, tena hii karne tuliyonayo sasa si ile karne iliopita, karne ya kutegemea kudra ya Mungu ili mambo yako yaende sawa, karne yetu sisi ni lazma tupambane Mam,”

“Ni kweli lakini si unajua kuwa kila kitu kina muda? Muda wa kutafuta tiba utakapowadia, ninaamini nitafanya hivyo,”

“Acha kujidanganya wewe! Muda huo ndio huu sasa, tunapaswa kutafuta tiba juu ya tatizo linalokusumbua,” Esmile alimlazimisha sana Mam amueleze tatizo alilonalo. Bado Mam hakuwa tayari, lakini baada ya kumfanyia laghai kidogo kwa vichekesho kiasi na serious kidogo, hapo sasa hakuwa na jinsi ikabidi aseme ukweli.

Alimwambia kwamba siku hiyo ndiyo alimuona mbaya wake ambae amekuwa akimtafuta kwa muda mrefu.

Nafsi ya Esmile ikapiga mshindo alitamani kutaka kujua ukweli zaidi kwamba mtu huyo ni nani na alimuona wapi? Maana hadi wakati huo hakujua chochote, lakini akampa pole na kukatisha stori hiyo akaamuliza atakuwa Tanga kwa muda gani.

Esmile akamwambia hana sababu ya kuendelea kuwepo kule, maana alichokifuata ni faraja kutoka kwake, kwa kuwa tayari ameipata, inamlazimu kurejea kazini siku ifuatayo.

“Sasa mbona umemuahidi bibi utakuja kula siku moja?”

“Yap! Nimeahidi hivyo wala sikatai lakini sijasema siku yenyewe kama ni kesho,”

“Ah! Mtoto wa Kiswahili wee…, mi nitakuweza wapi baba? Haya umeshinda wewe,” Esmile akacheka kutokana na kauli ya Mam.





“Sawa, niambie sasa ni lini utarudi Dar ili niendelee kuwa pamoja nawe tena Mpenzi wangu karibu yangu, ubavuni mwangu?”

“Sijajua ni lini hadi nitakapoketi chini na kutulia ndio nitapanga iwe lini, lakini kwa sasa bado,” alijibu Mam kwa kujiamini kabisa.

“Sidhani kama itazidi siku mbili mbele my love,”

“Siku ngapi? Unacheza wewe! Nimekuja juzi tu hapa!”

“Ina maana hizo siku mbili hazitoshi tu Mam?”

Mam nae akamuambia Esmile kuwa baada ya wiki mbili ndio atakuwa Dar, tena iwapo tu mambo yake baadhi yatakamilika kwa wakati. Alishangaa Esmile na akaonesha dalili kuwa hjaridhika maana Esmile hakuona sababu ya Mam kuendelea kukaa Tanga muda wote huo.

“Bado unataka kukaa Tanga kufanya nini sasa?” aliuliza Esmile kwa mshangao.

“He! Huku pia si ni nyumbani kwetu pia? Ujue bibi yangu anahitaji kusaidiwa pia,” alijitetea Mam akimtumia bibi yake kama kinga.

Sasa ikawa ni utata, Mam anataka kuendelea kuwepo Tanga, Esmile anataka Mam arejee Dar haraka. Hapakutosha hadi simu zao zilipokatika kwa kuishiwa salio, na bado Esmile akashindwa kupata usingizi.

Kilichosababisha kutokulala ni kwa kufikiri mbaya wa Mam ni nani? Na kwanini aonekane siku muhimu kama ile ambayo yeye alimvisha pete? Pale kwao palikuwa na wanaume wasiozidi watano waliohuhuria shughuli ile, akajitoa yeye na baba yake ambao walifanya jumla ya wanaume wote kuwa saba.

Ndio akaanza kujiuliza sasa ni yupi kati ya hao watano waliosalia aliyemtenda mpenzi wake kitendo kile cha kinyama. Hatimaye usingizi ukamchukua bila kupata muafaka wa jambo lile.

Asubuhi baada ya kunywa chai na kuweka salio, alimpigia Mam na kumuuliza siku halisi sasa ya kurudi Dar, maana siku iliopita walishindwa kufikia muafaka, leo Mam alimuahidi atarejea baada ya wiki moja. Wakaagana na Esmile akaelekea stendi tayari kurudi Dar.

Baada ya kufika Dar akataka kufanya papara ya kutaka kumjua aliembaka Mam, lakini kupitia masomo aliyochukua akaanza kupita hatua kwa hatua, maana alihisi akifanya haraka, itakuwa ni sawa na kumdhalilisha, kwani kuna watu watano anaowashuku yeye, kati yao mmoja ndiye aliembaka ambaye bado yeye hajamjua Sasa kama ataamua kumuuliza kila mmoja wao, ni sawa na kumhalilisha Mam.

Akiwa katikati ya lindi la mawazo, baba yake aliingia na kumsemesha, Esmile hakumsikia hadi alipoingia na kuketi jirani nae, na kumuuliza kile kinachomsibu. Mwanzo Esmile alikataa kutoa ushirikiano. Baba yake akamwambia kuwa yeye ni mtoto wa kiume na hana wa kumwambia kinachomtatiza zaidi ya yeye baba yake, ambae ndio yeye, asihofu, aseme tu kinahomsumbua.

Nasaha hizo zilimlainisha Esmile na kumtamkia baba yake kuwa kilichomsababishia safari ile ya Tanga ni Mam, akamueleza hali halisi bila kuficha chochote, hadi sababu ya Mam kulia pale kwa kumuona mtu aliembaka. Mzee Hanson alishtuka sana.



Mzee Hanson alishtuka sana, kwani bado ana mzimu unaomtafuna taratibu na tena kimya kimya, mzimu wa mwanafunzi wa kike! Binti aliekuwa akisoma Zanaki bado unamsumbua, lakini hakuhisi kama ndio huyo Mam, lakini historia zao zilishabihiana, akatamani kumuona…

Hivyo akamwambia ajitahidi mara arudipo Mam toka huko Tanga, amlete yeye aongee nae kama mzazi anaamini watafikia muafaka tu, kwani penye wazee hakiharibiki kitu.

Esmile alitabasamu na kumwambia mzazi wake kuwa anajivunia sana kuwa na mzazi huyo, akamkumbatia na kumshukuru na kuahidi kufanya hivyo.

Siku hazigandi Mam akatua Dar, Esmile ndie aliekwenda kumpokea na kumpeleka hadi nyumbani kwao na kumuacha pasina kuzungumza jambo lolote lile zaidi ya story za kawaida tu.

Siku kadhaa mbele Esmile akamwambia anataka aende nae nyumbani kwao akaongee na baba yake, ajabu Esmile alipomgusia tu juu ya la kukutana na baba yake, Mam alikuja juu vibaya sana na kuanza kulia huku akisema hawezi kwenda na hataki.

Esmile hakumuelewa na baada ya kumbembeleza kwa muda mrefu, Mam alikubali na kumwambia Esmile ategemee lolote baada ya mkutano ule, japo hakumuelewa nini ana maanisha, lakini akakubali.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Alimchukua na kwenda naye kwao, walifika na kumkuta Mzee Hanson, Esmile akamuomba baba yake watoke nje kwenye bustani kisha akamfuata Mam na kumpeleka kwenye Bustan pia, akaendea vinywaji kwa ajili yao.

Sura aliyoionyesha Mam kwa Mzee Hanson ilitosha kabisa kumkumbusha kila kilichotokea miaka kadhaa iliopita, badala ya kuzungumzia suala hilo, ikabidi Mzee Hanson atumie muda huo kumuomba radhi Mam, kitu ambacho kilimfanya Mam kuangusha kilio.

Kilio kile kilimshitua Esmile, akataka kusogea. Ila akajizuia kwani alitegemea jambo kama hilo kwani sasa anamtambua vizuri Mpenzi wake, jinsi alivyo Mam inapofika kwenye suala lile.

Kwa kuwa alikuwa amewapisha waongeehakupaswa kusogea hadi aitwe, hivyo hakujua zaidi ni kipi kinachomliza, maana angejua au angekuwepo pale kwenye kile kikao cha dharula, sijui nini kingetokea.

Mam akamwambia Mzee Hanson moja kwa moja kwamba hajamsamehe, wala hajafikiria kumsamehe na milele hatomsamehe kwani hana mpango wa kumsamehe.

Akashusha pumzi Mzee Hanson kwa nguvu baada ya kushtushwa na maneno ya Mam ambayo yalionekana yanatoka chini kabisa ya uvungu wa moyo. Kutokana na jinsi alivyo onyesha Mam, Mzee akakata tamaa mapema ya kupata msamaha. Basi akamuomba Mam aachane na Esmile, kwa kuwa ameshindwa kumsamehe yeye. Mam akageuka mbogo na kumwambia asimpangie lolote kwani chochote anachokisema yeye anakichukia, hata kama ni sahihi, ajue kabisa yeye hawezi kukifanya, hivyo awaache tu walivyo na ajue ipo tu siku atalipiza kisasi.

Hapo akanyanyuka na kuelekea ndani akimuacha Mzee Hanson mwenye mawazo kedekede, mara kajishika kichwa, mara katembea tembea hapa na pale, mara kasimama. Alikuwa wala hajielewi.

Esmile na mama yake wakampokea Mam aliyekuwa anabubujikwa machozi mashavuni, japo alijitahidi kuficha kwa kuyafuta mara kwa mara, lakini ilionesha kabisa kuwa alikuwa akilia.

Mama Esmile alikuwa hajui kinachoendelea, akahoji lakini hakujibiwa, akatoka na kwenda kumuuliza mumewe, kule napo alimkuta amekuwa mbogo mara tu baada ya kumuuliza swali la kwanini Mam analia? Akashindwa kuelewa ni nini hasa kinachoendelea.

Wakiwa wamesimama baba na mama, wakawaona Esmile na Mam kwa mbele wakitoka, tena bila ya kuaga, Mam akiwa mbele na Esmile akimfuatia kwa nyuma kama mtu ambae anabembeleza, wazazi wakatazamana kama wanao ulizana, vipi?

Hapo ndio Mzee Hanson akamwambia mkewe kiufupi tu kuwa Mam alibakwa kitambo, sasa ile hali imemuathiri kisaikolojia. Wazo la kwanza la Mama Esmile lilikuwa ni kupima, Mama akahoji

“Vipi alishaenda kupima?” Ajabu swali lile likamfanya Mzee Hanson apanic na kamtaka mkewe anyamaze. Kashangaa tu mama wa watu na kujiuliza kuna nini? Mbona Mzee Hanson amekuwa vile na tena kwa ghafla?

Kumbe mwenzake alikuwa mbali hasa alipokumbuka juu ya kumbaka Mam, tena bila Condom, na hali akijua kuwa yeye ni muathirika, ikawa ni kizaazaa, akafikiria mbali zaidi juu ya suala la mwanae Esmile kuachana na Mam linavyoweza kuwa gumu.

Inaonekana kabisa ni kiasi gani wanapendana hawa watoto, lakini nikisema suala hili niliache tu bila kuwatenganisha hawa wana, basi ni wazi kwamba mwanangu nae anaikanyaga miwaya. Hiyo ilikuwa ni sehemu ya mawazo ya Mzee Hanson.

Hakika alikuwa na mawazo mengi sana aliwaza na kujiuliliza maswali mengi kama Esmile na Mam wameshafanya mapenzi na alijiuliza kama Mam atakuwa aliathirika itakuwaje?

‘Je itakuwa ni sahihi kwa familia nzima kufa kwa Ukimwi?’ jibu likawa ni hapana, mawazo yalitimba kichwani kwa Mzee Hanson ambae hakuwa tayari hilo litokee, hivyo kwa gharama yoyote akapanga kuwatenganisha.

Wakiwa garini kuelekea Kigogo, Esmile alimuuliza wamefikia muafaka gani, Mam alimtazama Esmile kwa jicho la huzuni, sababu ikiwa ni huruma, kwani kulikuwa hakuna muafaka wowote na katu hauwezi kupatikana, maana mtendaji wa kile kitendo ni mzee wake.

Akajilazimisha na kumwambia wameongea japo hawajafikia muafaka, ila siku za usoni watafikia muafaka.

Usiku haukuwa wa kawaida kwa Mzee Hanson, aliteseka sana, kilichomtesa si usingizi, bali ni kule kumbaka msichana ambae sasa ametaka kuwa mkwewe. Na kilichomtesa zaidi ni pale alipohisi amemuambukiza Ukimwi, aliumia sana.

Kwa Esmile, usiku ule pia ulikuwa ni mrefu mno, nae alikuwa akijiuliza kama Mam alipima baada ya kubakwa ama lah, lakini akahofu kumuumiza Mam kwa swali hilo, maana tayari waliachana siku hiyo akiwa na majonzi tele, akajipanga kumuuliza siku za mbele.

Asubuhi Mzee Hanson aliamka na wazo moja tu la kuhakikisha anawatenganisha kwa namna yoyote ile, akaanza kusuka mipango, kila mpango alioufikiria aliona wazi kwamba unagonga mwamba, akakata tamaa.

Lakini wakati anafunga mlango wa gari lake ili kwenda kwenye suala la kazi zake, ghafla akapata wazo jipya, wazo ambalo ambalo alimini kwamba halitashindikana…







Aliwatafuta watu na kupanga kwa ajili ya kuwavamia Esmile na Mam na jambo alilotaka ni kuhakikisha Mam anauawa. Akawakodi majambazi kwa ahadi nono ya pesa, nao wakapanga mitego yao tayari tayari kwa ajili ya utekelezaji wa hiyo kazi.

Walikuwa wakiwawinda Mam na Esmile, takriban wiki mzima, Esmile na mwenendo wake wote lakini pia Mam na nyendo zake. Waliweza kugundua kwamba njia tahisi zaidi ni pale wanapokuwa pamoja, kwani Mam baada ya kutoka shule, hatoki tena baada ya kuingia kwao hadi atoke tena kwenda shule.

Lakini Esmile pekee ndio mtu aliekuwa akionekana kumtoa kwao wakati wowote, hivyo nao wakaona nafasi ya kufanya yao ni hiyo.

Siku moja usiku wakati Esmile akimrudisha Mam, gari yao ikatekwa kwa kuwekwa mawe kwenye kona kali na gari ikapinduka wakati Esmile akijitahidi kuyakwepa, Mam aliekuwa ni mlengwa, kwa bahati mbaya hakuwa amefunga mkanda kama ujuavyo wakina dada wakiwa kwenye magari na wapenzi wao hujisahau kabisa.

Aliumia vibaya sana sehemu za begani na kichwani na kupoteza fahamu palepale ila Esmile hakuumia sana ila nae alipoteza fahamu, majambazi wale walishindwa kuumalizia Mam kwa kuwa sekunde chache baada ya ajali watu walifika kwenye eneo hilo kwa lengo la kutoa msaada na wengine kuwahi vyao kama ujuavyo panapotokea ajali.

Lakini wote waliwahishwa hospitalini kwa matibabu zaidi.

Ajali ile ndiyo iliyoutambulisha uchumba wa Mam na Esmile upande wa pili, yaani nyumbani kwa kina Mam.

Japo kwa malezi ya Mam yalivyokuwa, ilikuwa ni kesi kubwa sana kwa motto wao kuwa na mahusiano nje ya ndoa, lakini kwa muda ule isingewezekana kulizungumzia hilo kwa kuwa hali za wajeruhiwa hazikuwa nzuri.

Hata familia zilikuwa kitu kimoja lakini mzee Hanson alikuwa na yake moyoni, ama kweli moyo wa mtu ni kichaka. Mzee Hanson kwa kutaka kuwatenganisha kwa lazima, akajiweka karibu zaidi na familia ya kina Mam akawa busy na hata akafika nyumbani kwa kina Mam.

Alikaa nao kwa masaa kadhaa kisha akaondoka, wakiwa wanatoka, akamuomba Mzee Mahmoud waongee kidogo faragha, Mzee Mahmoud alipotaka kurudi ndani, akamwambia kwamba maongezi yao ni nyetu na watayafanyia ndani ya gari.

Waliingia na kuanza maongezi yao na Mzee Hanson alichokitaka ni kujua mazingira nayoishi mzee mwenzie na family yake, ili aweze kuitokomeza vile ambavyo akili yake ilijipanga.

Jambo la kwanza ambalo akili yake ilimuagiza kulifanya ni kuitoa familia ile kutoka katika mazingira ambayo Esmile anayajua. Na kwa kuanzia tu akamshauri wampeleke Mam nje ya nchi kwa matibabu zaidi, maana alichelewa kurejea katika hali yake ya kawaida.

Mzee Mahmoud alipinga hilo kwa kusema yeye hana pesa, Mzee Hanson akatabasamu na kusema hilo ni juu yake, hapo mzee mwenzie hakukataa hakuwa na uwezo wa kukataa tena.

Mzee Hanson aliandaa mipango ya kumpeleka Mam Nairobi kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi na kichwani mwake alijieleza kuwa gharama za kumtibu Mam na kila ambacho anatumia katika jambo lile bado havijafikia thamani ya motto wake wa pekee.

“Naweza kutumia hata mali zote ilimradi tu Esmile asije kuingia ndani ya mahusiano na Mam, maana hadi sasa sina imani nae huyu binti,” hiyo ilikuwa ni sehemu ya mawazo ya Mzee Mahmoud.

Wakati Mam yuko kule nje kwa matibabu zaidi, Dar es Salaam hali ya hewa ilibadilika ghafla na mvua kubwa zikaanza kunyesha kunyesha mfululizo.

Hali ya jiji la Dar na mvua inaponyesha, inakuwa ni adha kubwa. Familia ya Mam ambayo ilikuwa ikiishi Kigogo, haikuwahi kufikiwa na maji ya mafuriko hata mara moja, ila mara hii maji yalikuwa mengi sana.

Kwa kuwa Mzee Hanson na baba yake Mam walikuwa wamefahamiana na wanazungumza vizuri, Baba Mam akamueleza mzee mwenzie juu ya tatizo lililowapata.

Hakuwa na lengo la kuomba msaada, lah hasha! Ilikuwa ni kwa nia njema tu ya kumpa taarifa na kuzugumza tu ili kunogesha maongezi na kuvuta muda, lakini Mzee Hanson alitumia nafasi hiyo hiyo kufanya yake.

Aliingiza wema usiotarajiwa, akawashauri wahame eneo lile kwa kipindi hiki na kujitolea kumpeleka kwenye nyumba yake iliyopo Msasani kwa muda wakati akifanya mipango ya kuwatafutia nyumba ya kudumu.

Wakati hayo yakiendelea, Mam aliekuwa Nairobi akiwa ameongozana na Mama yake, Mzee Mahmoud na familia yake waliobakia Dar wakahamia Msasani, kwenye nyumba ambayo Mzee Hanson aliwapa kama sehemu ya kujishikiza wakati akitafuta nyumba kwa ajili yao.

Huku nyuma Esmile ambaye alionekana kuwa hakuumia sana hali yake nae ikabadilika akaanza kuugua sana huku akilalamika maumivu ya ndani ya kifua. Mzee Hanson sasa nae akaanza kujutia kitendo chake alichokifanya.

Ikalazimu sasa Esmile kwenda kutibiwa Afrika Kusini, hapa wakaandamana wote, baba, mama na mtoto. Ndani ya wiki moja hhakukuwa na mawasiliano yoyote kati ya Mam na Esmile na hakuna aliyejua nini kinaendelea kwa mwenzie kwa kuwa wote walikuwa hospitalini na walikuwa wamezimia.

Esmile alipokuwa akiuliza kuhusu Mam, aliambia Mam yuko salama lakini alishangaa kwanini hajamuona hospitali? hadi waliposafiri kwenda Afrika Kusini, hakuwahi kumtia machoni.

Mam naye alipopata nafuu akauliza kuhusu Esmile akaambia yuko salama kabisa. ila upande huu kidogo ukawa ni mkweli, ukamwambia Esmile alipelekwa Afrika Kusini kuchekiwa afya yake kwa kuwa anahisi maumivu sehemu za kifuani.

Siku zikapita na wote wakarejea, Mam akiwa ni mtu wa kwanza kurejea Jijini Dar na Esmile na familia yake ikafuatia wakarejea Dar, hali sasa kwa wote ilikuwa ni nzuri tu sana.

Alishangaa mno Esmile, badala ya kwenda kwao Tabata wanaenda Upanga, anajua kwamba wana nyumba huko, lakini kwanini waende huko wakati huu na si Tabata? Akatulia kimya kwa wakati ule hakuoji lolote.

Kitendo cha kuingia ndani kikazusha maswali kibao toka kwa Esmile kwenda kwa wazazi wake, kwanza alitaka kujua alipo Mam, bado walimzungusha tu, kwani wao walikuwa na furaha hasa baada ya mtoto wao kupata matibabu na kitu kikubwa zaidi ni yale majibu ya vipimo vya HIV ambayo walimuomba daktari ampime bila yeye kujua yaliyokuwa yameonesha kuwa Esmile hajaathirika.



Mzee Hanson ndie aliefurahi zaidi, alimshikashika kichwani na kumwambia wataongea baadae, apumzike kwanza. Esmile hakukubali, alinyanyuka na kuwaaga wazazi wake kuwa anakwenda kwa Mam, baba yake akamwambia akae kwanza chini waongee kidogo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Akiwa ni mwenye wasiwasi tele alikaa na kuwauliza kama kuna tatizo? Wakatazamana, kisha akaendelea kuwaambia ni heri wamwambie.

“Unajua baada tu ya ile ajali, kuna mengi sana yametokea hapa katikati kwa sababu ulikuwa mgonjwa, tulishindwa kukwambia, ukweli wenyewe ni huu…” Esmile akamkatisha

“Baba usiniambie kama Mam amefariki kutokana na ajali ile please…”

“Hapana mwanangu, ila aliumia sana kuliko wewe, mlikimbizwa hospitali wote. Hali yake ikawa mbaya zaidi, hivyo wazazi wake wakaamua kumuhamisha hospitali, tukaafikiana kwenda kumtibu nje ya nchi, hivyo nami nikawaongeza kiasi cha pesa kwa ajili ya matibabu wakaondoka,”

“Wakaenda hospitali gani?”

“Walikwenda Nairobi, mwanzo niliwasiliana nao ila baadae tulipokwenda Afrika Kusini, nikapoteza mawasiliano nao,” Esmile akashusha pumzi kwa nguvu na kuuliza tena..

“Kwa hiyo baba hujamtuma hata mtu aende kwao ili kujua anaendeleaje?”

“Ni jana tu kabla hatujaondoka Afrika Kusini, nilimtuma kijana lakini hakuwakuta hivyo tuvute subira tupumzike kwanza kesho tutaanza kuwatafuta…”

Esmile aliinama na kuweka mikono yote mashavuni huku akiwaza

‘huenda Mam amekwenda Tanga kwa bibi yake na hata kama asipokuwepo huko, bibi atajua kila kitu kuhusu mjukuu wake’

Kama mtu aliyezinduka kutoka kwenye usingizi mzito, akauliza ilipo simu yake, akaambiwa ilipotea siku ya ajali

“Siku ya tukio lile Esmile, simu, pesa ulizokuwa nazo na baadhi ya vitu vingine, viliibwa na vibaka, hatukuweza kupata chochote zaidi ya kumshukuru Mungu kwa kuwakuta nyinyi hospitali,”

Alizidi kuchanganyikiwa akalegea na kujisemea moyoni kuwa ni heri wangeiba kila kitu hata gari ila wakamuachia simu yake tu, kwani mle kuna namba nyingi za muhimu na zaidi zingine zilikuwa za watu wa karibu na Mam.

“Ningepata namba ya bibi au Rahel angeniambia kama Mam ni mzima ama amekufa, na iwapo amekufa, lipo wapi kaburi lake na kama ni mzima yupo wapi,”

Mzee Hanson alimtuliza na kumwambia asiwe na wasiwasi, moyoni alijua anachokifanya, mzee alikuwa ni zaidi ya Jasusi, alijua jinsi ya kujipanga na alifanikiwa kwa sehemu kubwa.

Na akamwambia kuna simu mpya wamemnunulia, itamsaidia kwa mawasiliano, akashukuru na kuuliza swali lignine, kwanini wamehama Tabata.

Hili halikuwa ni swali kwa Mzee Hanson, maana alikuwa amejiandaa, akamjibu kwamba nyumba ile ya Tabata wameamua kuikarabati ili waipangishe, kwani kama ana kumbukumbu nzuri, Mam anadai alimuona mtu aliembaka, kwa hiyo wamefanya vile ili siku akimpata Mam asifike kule tena bali wamuweke mbali na eneo lile

“Ama unaonaje Esmile?”

“Ah baba yangu, kwangu yote mi ni sawa, mi nina hamu ya kumuona Mam tu basi”

“Usijali mwanangu, utamuona tu Mam…” sasa jibu la mwisho lilitolewa na mama yake

“Sawa mama, ila mimi ndio naanza sasa kumtafuta, tutaonana baadae,” lakini kabla hajatoka, akaingia chumbani kwake.

Chumba kilikuwa kama kipya maana hakukuwa na vitu vyake muhimu, alipotoka kuuliza akaambiwa havijafunguliwa kwenye maboksi, akachoka na kuamua kuahirisha safari na kujichimbia chumbani.







Simu yake ilikuwa ni mpya na line mpya tena ikiwa na mtandao mwingine, kwa kuwa jioni ilifika akaona haitawezekana kwa yeye kwenda kuomba ku ‘renew’ line yake ya mwanzo. Hivyo akaitumia simu hiyo usiku huo kuperuzi mitandao ya kijamii.

Alikuta salam nyingi za pole kutoka kwa marafiki zake kwenye ukurasa wake wa Face book, Instagram na Twitter alifanya kazi ya kuwajibu na kuwajulisha hali yake na pia kuwataarifu kwamba amesharejea Dar es Salaam.

Wiki mzima sasa tangu Esmile awe katika hali nzuri, alijitahidi kumtafuta Mam kila sehemu aliyoijua, kwa simu na kwa gari. Alifika hadi nyumbani kwa Rahel, ajabu Rahel akashangaa kusikia walipata ajali hadi Mam kuwa taabani, kwa hali hiyo hakupata msaada wowote, ikabakia sehemu moja tu…Tanga!

Ndio sehemu pekee ambayo alikuwa ameibakisha kwenda! Sasa akalazimika kupanga safari ya Tanga, nyumbani kwa bibi yake Mam ndio eneo aliloamini kwamba atapata msaada wowowte anao uhitaji.

“Hata kama bibi akiniuliza ni kipi ambacho nina mpango na mjukuu wake? Nitamwambia nipo tayari kufunga ndoa nae hata sasa,” alijipanga kabisa kabla hajafika eneo la tukio na hata safari hajaianza.

Akaomba ruhusa ya siku tatu kazini ambazo alipewa bila kipingamizi wakiamini bado anaumwa anahitaji mapumziko, maana yeye huwa ni mtendaji mzuri sana kazini. Akarejea kwao na kumuaga mama yake kuwa anaeleka Tanga kwa Bibi yake Mam.

Haikuwa ajabu kwa Esmile kusafiri, lakini safari hii mama yake hakuiafiki, akamshauri amsubiri baba yake.

Mshangao aliouonyesha Esmile ulimfanya hata mama yake aone aibu, akasema

“Mama, leo safari ya hapa Tanga hadi nimsubiri baba, wakati huwa naenda sehemu mbalimbali bila kusubiri ridhaa yake, humjulisha kwa simu, tena wakati mwingine huenda nje ya nchi kwa kuwapigia simu tu kuwa nipo safarini, inakuwaje leo nakuaga ana kwa ana unaniambia nimsubiri baba arudi, sasa mama unamaanisha baba afanyeje?”

“Ni vile wewe bado hujapona sawasawa ndio maana nasema hivi,”

Esmile akamsogelea na kumwambia asiwe na shaka, atafika salama na hatochelewa, siku mbili tu atakuwa amerejea, akalazimika kumruhusu, Esmile akambusu mama yake na kuondoka bila mzigo wowote.

Aliwasili Tanga saa12 jioni na kuelekea hotelini moja kwa moja. Alikaa hadi saa 2 usiku kisha akatoka kuelekea kwa bi Maryam. Tayari aliisha fika Tanga zaidi ya mara tatu, hakuwa mgeni tena, alipajua vizuri nyumbani.

Nje ya nyumba alikuta watu kadhaa wakiwa wamekaa wanapata chakula cha usiku. Mkao ule ulimshitua, alipoteremka toka kwenye Taxi, tena bila hata kumlipa dereva, akaelekea moja kwa moja kundini.

Alikaribishwa na Mzee Mahmoud, kisha akawasalimia na kwenda kukaa jirani na Mzee Mahmoud na kusalimiana nae tena, wakaulizana hali zao, kisha Esmile akamuuliza kuna kitu gani hapo.

“Kwani wewe umetoka wapi?” Alishangaa Mzee Mahmoud. Ikabidi Esmile ajitambulishe maana Mzee Magmoud alikuwa akimsikia tu.

“Ok samahani, nilijua una taarifa tayari…”

“Hapana sina taarifa zozote mzee…” Esmile alikuwa akijibu haraka haraka ili ajue kuna nini pale. Aliwaza huenda Mam amefariki, maana dalili zote zilionyesha kuwa pana msiba pale, ghafla akasikia.

“Kaka samahani… nikusubiri au vipi?” Alikuwa ni dereva Taxi, Esmile akakumbuka kuwa hajalipa

“Ooh nisamehe bure ndugu yangu,” Akanyanyuka na kumlipa kisha akakaa

“Eh hapa pametokea tatizo, mama yangu mzazi, yaani Bi Maryam, alifariki jana jioni na leo mchana tumemzika,” akampa pole ya kufiwa na kuketi kwa dakika kadhaa akibadilishana mawazo.

Baada ya dakika kadhaa, akaomba kuonana na Mam pamoja na Mama yake kwa ajili ya kuwapa pole, akatumwa mtu kwenda kuwaita pembeni mwa nyumba, wakajitokeza Mam na Mama yake.

Mam hakuamini walipomuona Esmile pale, akamuita kwa sauti huku akimsogelea na hapo ndio mama yake akamjua kuwa Yule ndio Esmile japo alimuona wakati wakiwa hospitali.

Sasa ndio mama Mam alimkaribisha na kusalimiana nae huku wote wakipeana pole, ila Mam alipomsogelea alilia sana kiasi hata Esmile akahisi nae anaweza kulia. Walifanikiwa kumtuliza baadaye Esmile aliaga kuwa atakuja siku ifuatayo kwa maongezi zaidi.

Kitanda kikawa ni kikubwa sana kwa Esmile usiku ule, maana alianza kupata picha kwanini mama yake alimzuia kwenda Tanga, kumbe alikuwa anajua kinachoendelea huko. Akashangaa na kutikisa kichwa, akajilaza na kuvuta shuka akaanza kuutafuta usingizi.

Alipoamka akawasiliana na wazazi wake na kuwaahidi kurejea siku ile jioni. Wakamuuliza kama ameonana na familia ya kina Mam, akawaambia kweli kuwa ameonana nao wote ila hakuweza kuongea na Mam maana alikuwa akilia kwa huzuni sana, hivyo atakwenda kumuona asubuhi ile kabla ya kuanza safari ta kurejea Dar.

Aliwaeleza wazi kuwa atakwenda ili kujua msimamo wake Mam kama bado yupo tayari wafunge ndoa ama lah. Kauli ile iliwaweka wazazi wake katika hali ngumu sana hasa baba yake. Mama Esmile aliliona hilo, akamuuliza mwenzie kulikoni? Ikamlazimu sasa kumwambia kweli mkewe, akamweleza kuwa amejaribu kuwatenganisha kwa kila njia ila imeshindikana, maana hajapata mafanikio yoyote.

“Mume wangu sijakuelewa, unaposema kila njia imeshindikana, kwani ulitumia njia gani?” akawa muwazi kwa njia zote alizotumia, mama akashtuka na kuuliza kwa jazba

“Kwanini hukumwambia tu kuwa hutaki awe na Mam hadi ukatumia njia za kikatili hivyo?”

“Kimya na wewe nae, kwani hujui kuwa yule binti alibakwa? Sasa unajua matokeo ya tukio lile? Kama aliambukizwa Ukimwi je?” akasonya kwa hasira.

Mama Esmile akapoa, baba nae akatulia, wote sasa wakashusha jazba zao na kuongea kwa kituo na kufikia muafaka kwa kusema Mam na Esmile wanapendana kwa dhati, hakuna wa kuweza kuwatenganisha, ni heri tu Esmile atakaporejea, wawashauri waende kupima na matokeo ndio yataamua kuhusu ndoa.

Hadi pale familia ilikuwa inatambua kuwa Esmile yeye ni mzima, hajaathirika. Maana walimpima alipokuwa hospitali huko Afrika Kusini, tatizo likawa kwa Mam pekee.

Muda huo wao wakiwa na mawazo lukuki, Esmile alikwenda na kuongea na Mam na kufikia muafaka kuwa, baada ya wiki mbili, familia nzima ya Mzee Mahmoud itarejea Dar, na huko ndio watakaa na kupanga kila kitu. Akaaga ili aondoke, akashindikizwa na Mam hadi nje, Mam akaanza kulia tena.

Esmile akambembeleza na kumtaka amueleze sababu inayomliza, Mam akamwambia anahisi kwenye swala hili kuna kikwazo. Hakumulewa, akamtazama kisha wote wakakutanisha macho.

“Esmile, kikwazo ni baba yako, simpendi nae pia hanipendi, na usiniulize sababu, kwani anaijua yeye,” Esmile akabaki kapigwa na butwaa, maana hiki kilikuwa ni kitu kipya kwake, hakuweza hata kukihisi, akamtaka Mam amuachie yeye suala lile.

Mam akamtazama Esmile na kumwambia...

“Nakupenda sana Esmile, ila nasikitika kuwa pendo langu kwako limeingia dosari kubwa sana, hata watu walionikosea, leo tena wananichukia?” akaendelea kulia. Wale waliokuwa mbali walijua ni majonzi ya kifo cha bibi yake ndio yanayomtoa machozi, kumbe ni mapenzi ndio yanayomliza binti.

Esmile alirejea Dar akiwa na mawazo mengi sana, lakkini hakudikiria kuwa mzee waKe ndiyo anahusika na tukio la kumbaka Mam. aliwaza kwamba pengine baba yake anamchukia Mam kwa sababu labda alibakwa au anaonekana muhuni muhuni au anatoka familia masikini tofauti na familia yao.

Siku tatu baada ya Esmile kufika Dar. Wazazi wake walimuita na kumketisha chini, kwanza walimwambia kuhusu Ukimwi na madhara yake. Halikuwa jambo geni kwake, aliutambua vema masuala hayo kwani tangu akiwa shule alikuwa mshiriki mzuri kwenye klabu za masuala ya Afya hivyo ajifahamu kuhusu Ukimwi na athari zake kwa mtu binafsi, familia na Taifa kwa ujumla..

Wazazi wake walizungumza mambo mengi ya maisha na mahusiano, walitoa mifano mingi na kwa kweli walitumia njia ndefu sana kutaka kufikisha ujumbe mzito waliokuwa nao kwa Esmile ambaye hadi wakati huo hakuwahi kuhisi wala kufikiria kwamba wazazi wake wote wana siri kubwa mno ambayo hakuwahi kuisikia.

Walimueleza juu ya masuala ya urithi na mali wanzomiliki na namna ambayo wanataka aishi kwa amani na awe na mke bora ambaye hatoharatisha maisha yake kwa namna yoyote ile. Aliwasikiliza na kuwalewa lakini kipengele cha kuwa na mke bora kikajirudia rudia akilini mwa Esmile na ikabidi aulize

“Mnamaanisha nini mnnaposema mke bora ambaye hatoharatisha maisha yangu?”

Mzee Hanson alikuwa mstari wa mbele kulizungumzia hilo…

“Shida yetu ni kuona kwamba mali hizi unaziendelea na familia yako inakuja kuishi kwa furaha… tungependa usijiingize kwenye hatari kwa kuwa na watu ambao status zao kuhusu Ukimwi zinatoa mashaka,” alisema…

Hata hivyo Mzee Hanson alishindwa kwenda moja kwa moja kumueleza Esmile hisia zake juu ya Mam, lakini aliendelea kumwambia juu ya kutaka awe na mke bora na familia nzuri na ndoto zake juu ya kumuona mwanae akiishi maisha mazuri zaidi.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/





Kuliibuka mvutano huku Esmile akiwa haelewi lengo hasa na kikao kile kisicho rasmi cha yeye na wazazi wake. Alihoji juu ya nini wanamaanisha, alikuwa mkali mno na kuwaleza kwamba yeye mtu anayejitambua na anajipangia maisha yake sasa.

Kuona hivyo, Mzee Hanson ikabidi afunguke zaidi na safari hii alikuwa serious sana kuliko ilivyokuwa hapo kwenye maongezi ya mwanzo ikabidi amueleze Esmile kitu ambacho hakifahamu na hakuwahi kukidhania katika familia yake hasa kwa Baba na Mama yake anaowapenda.

Akamueleza juu ya yeye na Mama yake kuwa wanaishi na virusi vya Ukimwi kwa miaka 10 sasa, hakuwa na jinsi isipokuwa kupasua jipu tu! Habari hizi zilimpa mshtuko mkubwa sana Esmile. Mstuko huu haukuwa wa kawaida, alihisi kuchanganyikiwa alihisi kupiga makelele.

Mzee Hanson aliendelea kumueleza zaidi…

“Sikia Esmile, ndio sababu sisi tumaamua kukuweka wazi juu ya jambo hili wewe ukiwa kama mtoto wetu wa pekee, sisi tayari tulifanya kosa, hatupo tayari kuona nawe unafanya kosa hilo hilo tena,” alipomaliza, mama akadakia

“Maana tulichukua ahadi ya kukulinda kwa gharama yoyote…” aliongea mama yake na kumfanya Esmile atikise kichwa kuonesha anakubaliana nao.

“Nafikiri unatambua kuwa Mam alibakwa, hilo si jambo la msingi sana hasa ukizingatia unampenda sana kiasi cha kutotambua lolote…”

“Ndio baba”

“Sawa, sasa jambo la maana ni moja tu mwanangu, usije thubutu kufanya nae mapenzi kabla hamjapima, sawa Esmile?”

“Nimekusikia Mzee wangu!”

Kama alivyoahidi, Mam, walikuja Dar na kukutana na Esmile lakini Mam akagoma kabisa kufika kwao, jambo lile lilimuumiza sana Esmile hadi akakumbuka kauli ya Mam aliyoitoa siku za nyuma. Aliporudi nyumbani akamvaa baba yake juu ya suala lile.

Mapigo ya moyo ya Mzee Hanson yakapiga mshindo, lakini utu uzima dawa

“Ni kweli Esmile, Mam anadai alibakwa, lakini ukimweleza suala la kupima hataki, ndio nikamwambia simpendi hadi atakapokubali kupima, hiyo yote ni katika kukulinda wewe mwanangu wa pekee!”

Ilikuwa ni sababu ya msingi sana aliyoitoa Mzee, Esmile akaridhika nayo na hata hakuwa na sababu ya kuibishia, akasimama upande ule wa baba yake pasina kujua kuwa kuna siri nyuma ya pazia. Maana hata mara moja Mam hajawahi kukataa suala la kupima na wala Mzee hajawahi kumwambia.

Esmile akajitoa muhanga hadi kwa Mam na kumwambia kuwa baba yake anasema yamkwisha yale na leo anamuomba waonane nyumbani. Mam akagoma kwenda. Esmile alitumia kila lugha anayoijua lakini wapi, mtu kagoma. Mwisho akapata wazo la kumpigia simu mama yake na kumwambia yupo na Mam, bado hataki kuja nyumbani.

Mama Esmile akaongea na kumshawishi kwa muda mrefu ndio Mam akakubali kwa shingo upande. Wakaondoka muda uleule na kwenda huko. Walikaa hadi jioni wakiwa na amani tele. Mwisho akamuuliza mkwewe kama kweli wanampenda.

“Sote tunakupenda sana na tunatamani hata sasa uje kuishi nasi humu ndani na ndio sababu nimekuita Mam, kama mtakuwa wazima kesho, napenda mwende mkapime afya zenu ili tuanze mipango ya harusi, unaonaje Mam?”



“Mi sina tatizo Mama namsikiliza tu Esmile,”

Esmile akaisikia mwenyewe kauli ya Mam na hapo ndio ulipoanzia mzozo, maana yeye alikuwa hajiamini kabisa, alipoambiwa siku yenyewe ya kupima ni kesho, akatoa visingizio kibao, mara ooh kesho atakuwa kazini, mara eti hajajiandaa. Wakamuuliza anatakaje? Akaomba wakutane Jumamosi asubuhi.

Maongezi aliyofanya na jamaa zake yakamtia moyo na kukubali kwenda kupima. Usiku uleule akampigia simu Mam na kumwambia wakutane asubuhi ya siku ifuatayo ili waende wakapime.

Mam kama alivyojibu awali, yeye wala hakuwa na tatizo, tatizo lilikuwa kwake, wakaagana na kila mmoja akavuta shuka na kuanza kuutafuta usingizi.

Siku ikafika, wakachukuana ndani ya gari ya Esmile hadi kituo cha afya, wakiwa njiani Mam alitamani aina moja ya biscuit ambazo zilikuwa zikiuzwa na mpita njia waliekutana nae kwa bahati tu, akamuomba Esmile asimame na kumrudia.

Walipofika eneo alilokuwa amefika, Mam akamsemesha na kutaka kujua bei, Esmile akatoa pesa na kumpa Mam, baada ya kununua, chenji yote Esmile akamwambia akae nayo watapitia mahindi ya kuchoma.

“Si unajua mahindi ya kuchoma barabarani yalivyo matamu? Yanazidi hata yale ya kuchoma nyumbani!”

“Toka hapa sasa ndio mahindi ya elfu tisa nzima? Sasa itakuwa tunatengeneza kande,” huku akifunua pochi yake, Mam akaweka pesa ya chenji na kumtazama Mpenzi wake. Walitawaliwa na furaha sana muda wote na hiyo ndio ilikuwa aina ya maisha wanayoishi wapendanao wale wawili.

Waliwasili kituo cha afya na kuulizia utaratibu wa kile kilichowapeleka hapo, wakaelekezwa na kuketi kwenye foleni kusubiri muda wao ufike. Naam zamu yao ikawadia, wakachuliwa damu, na kuambiwa waketi nje ili kusubiri majibu.

Kabla ya kupokea majibu, walikuwa taratibu wakizitafuna biskuti zao walizonunua njiani, Esmile alimuuliza Mam itakuwaje kama majibu yatatoka na kukutwa yeye ameathirika, atakubali na kuendelea nae? Mam akacheka na kumtania Mpenzi wake;

“We nikae na muathirika wa nini? Mi nakubwaga tu, tena mchana kweupee” akacheka Mam na kusababisha Esmile atabasamu, kabla hata hajakanusha kauli yake Mam, maana aliitoa kwa mazingira ya utani, wakaitwa majina ili kuingia ndani.

Mshauri nasaha akakaa nao na kuwashauri mambo mengi, mwisho baada ya kuridhika kuwa amewajenga kiasi cha kutosha, akawauliza majibu yao watayapokea kwa mtindo gani?

Wakakubaliana kila mmoja apokee majibu ya mwenzie, alianza Esmile kupokea majibu ya Mam na hakutaka kuyafungua, maana alimuamini sana na upande wake yeye akachukua majibu ya Esmile na kuyafungua. Mam akambusu Esmile aliekuwa amefumba macho na hakumwambia chochote.

Ukimya ule ukasababisha Esmile afumbue macho na kumwambia Mam

“Niambie basi mchumba, ama nipe mwenyewe nisome, naona we unachelewa sana,” wakawa kama ni watu wanaonyang’anyana ile karatasi.

Mam akatabasamu na kukataa, akaifungua tena na kuisoma, akamkumbatia Esmile na kumpa hongera na kumwambia licha ya virusi vya Ukimwi, hana hata ugonjwa wowote wa zinaa.

Wakakumbatiana na kubusu midomo yao, bado Esmile alikua akitetemeka kwa kukosa kujiamini, matokeo yale yalikuwa ni kama anahisi amedanganywa na Mam, akachukua karatasi lakini Mam akamwambia hatampa hadi nae ampe majibu yake.

Ni kweli yeye nae alikuwa na majibu ya Mam ambayo hajayafungua. Akaanza kufungua, kwani ilikuwa ni zamu ya Esmile kumwambia Mam matokeo ya vipimo vyake, Mam alikuwa akijiamini sana na hata Esmile pia alikuwa akimwamini mno Mam hadi akamwambia Mam kuwa si muhimu sana kusoma.

Mam akang’ang’ania kuwa ni lazima tu wayaone, maana kama ilikuwa ni kutaka yake peke yake, wasingepimwa wote.

Esmile akakubali yaishe, akaitoa mfukoni ile karatasi ambayo alikuwa ameikunja kunja na sasa taratibu akaanza kuikunjua, kisha akaisoma, akapigwa na butwaa, akashangaa na kukaa chini kajishika kichwa

“Vipi Esmile?” Aliuliza Mam kwa shauku.

“Ah, Mam imekuwaje?” Mam akanyakuwa ile karatasi na kuitazama kwa umakini, alipoiachia akajishika kichwa na kuanza kulia, akachomoka mbio. Muda huo Esmile alikuwa amejiinamia chini akiwa haamini yale majibu, akijiuliza kichwani kama vipimo vile ni sahihi

Aliponyanyua sura, masikini..! Alimuona Mam akikimbilia barabarani, hakika alichanganyikiwa, hakuwa ametegemea kabisa jibu la aina ile. Pamoja na ushauri wote wa mshauri nasaha, bado haikumsaidia Mam kupata ujasiri wa kukubali matokeo mabaya, kwani alijiamini kupita kiasi, hadi kufanya hata yale aliyokuwa akiyasema mshauri wala hakuyapa nafasi, kwani alijua kwamba haiwezi kutokea kuwa yeye ni muathirika.

Kasi yake na kutokuwa makini kidogo msababishie ajali, kwani wakati akivuka barabara bila ya tahadhari yoyote, ghafla ilitoka pikipiki na kumkosa Mam akajibamiza kwenye gari, Esmile akaanza kumkimbiza huku akimuita arudi.

“Maam simama… Maam rudii... Please mpenzi rudi!” kelele zile hazikusababisha Mam kurudi wala kusimama, kifupi hakusimama wala hakurudi bali alisimamisha Taxi na kuingia pasina hata kujua analekea wapi.

Esmile alirudia gari yake na kuanza kumfukuzia. Aliweza kuionaTaxi iliyombeba ikikatiza mitaa. Gari mbili tu kumfikia, taa zikamruhusu Mam kupita wakati Esmile zikamzuia, akakata tama, lakini alimini atafika nyumbani kwao salama kwa kuwa yupo kwenye usafiri.

Akajaribu kumtafuta hewani, simu iliita tu, ilipokatika haikupatikana tena, nyumbani kwao hakufika, kila sehemu waliyotegemea anaweza kuwepo, Mam hakuwepo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Majuto yakamvaa Esmile, kwanini hakujiongeza kuchukua bodaboda ambayo angeitumia kumfikia Mam kwa haraka zaidi tofauti na gari? Akajiona ni mkosaji mno, lakini mwenyewe akajipa moyo kwamba pale akili wala haikuwa yake.

Familia zote mbili zilihangaika kumtafuta bila mafanikio, siku iliyokuwa ni ya furaha, sasa ikawa ni ya majonzi, huzuni ilitawala kwenye mioyo yao huku majonzi yakizivaa nyuso zao. Hadi usiku unapotea kuingia asubuhi ya siku nyingine, hakukuwa na fununu yoyote.

Kwa nafsi yake ilivyo, Esmile alihisi kabisa Mam atakuwa amekwenda kujiua, hasa akikumbuka kipindi kile ambacho alimuokoa kwani hali ilikuwa ni katika mazingira kama hayahaya.

Ukapita usiku wa kwanza pasina watu wote kujua ni wapi mam atakuwa amelala, lakini ilikuwa ni vigumu kujua, maana uondokaji wake wala haukuacha chochote cha kuwaonyesha njia.





Simu za ushirikiano baina ya pande zile mbili ziliendelea kuwa ni za mara kwa mara, Esmile akawauliza kama Mam hajaenda Tanga? Wakamwambia Tanga hajaenda na kule kwa sasa hawezi kukaa kwani aliekuwa akimfuata ni bibi yake ambae tayari ameisha fariki.

Wakaketi chini sasa kusubiri kudra ya Mungu na au uamuzi wa Mam mwenyewe kama ataamua kujitokeza hadharani ama kama ni kujidhuru basi wasubiri matokeo.



**********



Jumapili mchana chakula kikiwa mezani, Esmile ameketi na wazazi wake wanakula, simu yake ikaita, kwa uvivu akaitoa na kuitazama, akashtuka na kusema kwa sauti kama vile anawaambia wazazi wake “He! Mam…” wote wakaacha kula na kumsogelea Esmile. Kama kawaida, Mam alikuwa akilia akamwambia Esmile hata kabla ya salamu.

“Nakupenda sana Esmile, lakini tangu jana nimelizika rasmi penzi letu. Naomba usinitafute wala usiwasumbue wazazi wangu, nipo Morogoro naelekea sehemu nisiyoijua, kwaheri ya kuonana,”

Jamani bila hata ya kutoa nafasi kwa Esmile, Mam akakata simu na kuzima kabisa simu, walipojaribu kumpigia akawa hapatikani tena. Kama mtu aliechanganyikiwa Esmile akasema peke yake

“Mam amefanya haraka sana, leo mi nilirudi kule kituoni kujua kama walikosea vipimo, daktari akanijibu kwamba kitu kile huwa kipo na ndio maana mtu anapaswa kupima mara tatu kabla ya kuikubali hali halisi aliyonayo,” kauli ya Esmile haikusaidia lolote wala kufanya Mam arudi.

Wazazi wake walimpa moyo na kumtaka akaze nafsi huenda kuna kheri ndani yake jambo la muhimu ni yeye kujipanga upya.

Hapo kwenye kujipanga upya, ndio Esmile akaamua ajipange kimasomo zaidi ili kukamilisha ndoto yake, akaamua kuchukua shahada ya uzamivu (masters) ya Sheria katika chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT) kilichopo Malimbe, jijini Mwanza.

Huko ndio sehemu ambayo aliamini anaweza kuwa vile atakavyo yeye, akaandaa barua yake ya maombi na kutuma akiwa ameambatanisha na mahitaji yote yanayotakiwa.

Jumatatu akaitumia kwa kuandika barua ya kuacha kazi na kuiwakilisha jioni wakati wakitoka, barua ilikuwa na notisi ya mwezi mmoja. Huzuni ilitawala, majonzi yaliwavaa wafanyakazi wote kwa kujua kuwa wanapoteza jembe lao la ukweli, walijitahidi kuongea nae ili abadili uamuzi, haikuwezekana.

Uamuzi wake ulikuwa ni uamuzi wa mwisho, wala hakukuwa na yoyote wa kuupinga, hata mzee wake nae hakumpinga bali alimtaka kujituma zaidi ili kufikia nukta ya ndoto zake.

Kutokana na kuungwa mkono na familia yake, basi michakato yake ikaanza kwa kasi huku akienda kazini na kukabidhi majukumu aliyokuwa nayo taratibu akivutia siku za kuachia ngazi.

Siku kadhaa mbele alikwenda kuiaga familia ya Mzee Mahmoud, ambayo kwa sasa ilikuwa ikitambua ni wapi alipo Mam, japo waligoma na kusema hawajui ni wapi alipo.

Esmile aliliona hilo kupitia hisia zake, lakini kwa kuwa hakuwa na hakika, akatulia tu na hivyo aliwaomba atakapowasiliana nao, siku yoyote wamwambie kwamba bado anampenda sana na siku yoyote yeye atampokea watakapokutana.

Aliamua kwenda kukaa mbali na familia yake na mazingira yote aliyoyazoea alitaka kubadili kila kitu hadi mfumo mzima wa maisha yake, alitamani kuwa mpya, alitaka awe Esmile mwingine.

Wazazi wa Mam walisikitika sana kutokana na maamuzi yake, tayari walikuwa wamemzoea, lakini waliahidi kufikisha salam hizo, wakaagana na Esmile akatoka na kuingia garini, akarejea kwao na baada ya siku chache mbele akaondoka kwenda kujiunga na chuo huko Mwanza.





Masomo yakaanza kuchanganya, ikakatika miezi minne bila mawasiliano yoyote na Mam, hii ilimfanya azidi kujikita kwenye masomo yake.

Mwaka ulikatika, ikabaki miezi sita tu ya kuhitimu shahada yake ya pili ambayo aliisomea kwa miezi 18, akasikia juu ya baba yake kuvamiwa na watu Fulani ambao walimteka yeye tu na kutokuchukua chochote katika vile alivyokuwa navyo.

Hali ile ilimchanganya mno Esmile na kumfanya ayumbe kidogo, maana hadi siku ya tatu mama yake alikuwa haelewi kinacho Endelea juu ya kutoweka kwa mumewe ilhali kila kitu hadi simu yake vikiwa vipo salama ndani ya gari.

Ikalazimika apange safari ya kuelekea Dar siku ya pili. Usiku akaongea na mama yake na kumtaarifu juu ya suala hilo, lakini alipopiga simu yake ikaita kwa muito mmoja tu na kupokelewa. Aliepokea simu ile alikuwa ni mwanaume.

Mapigo ya moyo yalimlipuka na hofu ilimjaa ghafla, akataka kuongeza sauti lakini shock ikamfanya apoteze umakini na kujikuta amekata simu ile na kushusha pumzi kwa nguvu.

Kabla hajaamua kupiga tena, safari hii ikaita simu yake, akaipokea na kunyamaza, aliepiga akasalimia na sasa Esmile aliweza kuitambua sauti kuwa ilikuwa ni ya baba yake.

Kwa shauku kubwa akataka kuongea mambo mengi kwa wakati mmoja, lakini akajikuta akiishia kuuliza maswali machache tu kwa mzazi wake

“Baba ni mzima kweli?” alimjibu kuwa yeye yupo salama kabisa na hana tatizo lolote.

“Baba mimi sikuelewi unaposema upo salama kabisa na hali hujaonekena nyumbani kwa siku tatu bila taarifa yoyote japo wewe ni mzazi na ni mtu mkubwa unaejielewa, lakini sidhani kama ulikuwa sehemu salama,”

“Ni kweli mwanangu, Sikuwa sehemu salama, lakini kwa kuwa nimerudi salama, mengine yote utayajua tu hivi karibuni, vipi masomo yako?” Mzee akaamua kumrusha mwanae.

Esmile akashusha pumzi za kukata tama, aliona kabisa kuwa kina kitu baba yake anajaribu kumficha, nae akamjibu kifupi tu kuwa anaendelea vizuri na kumuaga.

“Huenda alikuwa kwa mchepuko wake bhana, mambo mengine si ya kuuliza sana, kwa kuwa amerejea salama basi mengine atayajua mwenyewe,” hivyo ndivyo alivyojipa moyo Esmile na kuiua rasmi safari yake.

Akili akairudisha darasani, alikuwa amedhamiria na pia anajua kuwa ni nini anataka, hivyo kila muda wake mchache alioutumia pale chuo, basi aliutumia kwa umakini wa hali ya juu.

Akiwa amebakiza miezi miwili kumaliza masomo yake, akapokea taarifa za kifo cha ghafla cha baba yake Mzee Hanson ambaye alikutwa amekufa ndani ya gari lake kwa kuchomwa na visu kadhaa kifuani.

Kilipewa jina la ghafla kwa kuwa aliondoka nyumbani akiwa yupo safi kabisa na muda mchache sana mbele ndio akakutwa ameuawa.

Sasa ilikuwa ni lazima aende kwenye mazishi ya baba yake, baba ambae alikuwa ni zaidi ya rafiki kwake.

Alihudhuria mazishi na baada ya kukamilisha hatua zote za mazishi, ikafuatia mambo ya Polisi, aliitwa kituo kikuu cha Polisi ili kufanya mahojiano na Msimamizi wa kesi. Aliowakuta askari watatu kwenye kile chumba alichoingia.

Wote walikuwa na mavazi ya kiraia isipokuwa mmoja tu ambae alionekana ni askari asiekuwa na cheo chochote, baada ya muda tu nae akatoka na kuwaacha wawili ambao walimpa pole kwa kufiwa na mzazi wake kisha wakaanza mahojiano nae.

Walimuuliza juu ya kufahamu chochote juu ya mauaji yale lakini akakataa na kusema hatambui lolote na pia hakuwepo kabisa eneo la Jiji la Dar.

“Huenda kama ningekuwepo, ningeweza kujua juu ya tukio hili kutokana na kuwa na ukaribu na mzee wangu kwa kipindi kile nilichokuwepo Dar kabla ya kwenda chuo”

“Sasa ni kipi kilichomfanya abadilike na kushindwa kukujulisha mambo yake baada ya kuwa wewe upo chuo?” alihoji askari mmoja wa kike hukua kimtazama Esmile kwa makini, akitaka kujua kama kuna uongo wowote ambao anaufikiriahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Nahisi ni kwa sababu ya kutaka kunipunguzia majukumu, alitamani sana nimalize chuo nikiwa sina majukumu zaidi, akanipa uhuru wa kutosha,” alijibu kwa kujiamini.

Aliuliza ni hatua gani ambayo wamefikia kwa sasa? Walimjibu kuwa

“Kwa kuanzia upelelezi, tumewakamata wafanya biashara wenziwe wawili kwa hisia za kudhaniwa kuhusika na kifo kile, na muonekano wake ni mzuri, huenda wakatufikisha kwenye shina,”

“Unataka kunihakikishia Mkuu kwamba wahusika watapatikana?”

“Wahalifu tutawatia tu nguvuni, ila si kwa jitihada zetu binafsi bali pia ni kwa msaada wa raia wema ambao tuna hakika wamesambaa kila sehemu,”

Alitikisa kichwa Esmile kuonesha kuwa amemuelewa na kumuuliza kama nae binafsi anaruhusiwa kufanya uchunguzi binafsi.

“Sheria za nchi yetu haziruhusu jambo hilo kufanyika ndani ya ardhi yetu, ila kwa kibali maalum, kwa kuwa umehoji name nitakuelekeza ni wapi uende, ukikidhi vigezo vya nchi ilivyoweka, utaruhusiwa,” alimaliza askari na kufunga jalada ambalo alikuwa akiliandika na kunyanyuka.

Walitoka nje wakiwa wameongozana watu watatu na kufika mapokezi, Yule askari wa kika akabaki na Esmile akatoka nje akiwa na Yule Mpelelezi na kuanza kumuhoji maswali machache juu ya vigezo vinavyotakiwa.

“Esmile, kama hata vigezo huvijui, itakuwaje sasa uombe nafasi hiyo?” alimjibu kwa mtindo wa swali.

“Hapana Inspekta, najua baadhi tu ila nataka kujiridhisha tu,”

“Kipi unachokijua wewe mfano?” hapa walikuwa wakitembea taratibu kuvuka eneo la Polisi

“Kwa kuwa mimi ni mtaalamu wa fani Fulani, basi napaswa kujisajili kwenye chama chenye watu wenye fani yangu, mfano wakandarasi wana chama chao, wanasheria tuna chama chetu, je nipo sahihi?”

“Naam upo sahihi!”

“Basi napaswa kujisajili kwenye chama cha Wapelelezi wa kujitegemea, kama sijakosea,” aliuliza Esmile na kumfanya askari amshike mkono kama kwamba anamsimamisha asizidi kwenda mbele zaidi

“Naam ni sawa, sasa swali ni hili, je tayari umejisajili? Una muda gani toka ujisajili?”

“Hapana, mimi sijajisajili kwenye chama hicho hadi sasa kwa kuwa bado nipo chuo,”

“Basi kwa hilo moja tu hujatimiza vigezo. Nakushauri tu kuliamini jeshi lako la Polisi, kwani hadi sasa tumepata mwanga mzuri tu wa wauaji, imebaki kufanya shambulio ili kuwakamata,”

“Kwa hiyo Inspekta hao mlio wakamata wanahusika na mauaji hayo?”

“Yap kwa kiasi kikubwa walipanga shambulio hilo ambalo linahusianana tukio lile la kwanza la kutekwa kwa mzazi wako,” sasa alielewa vema na kuwaombea wafanikiwe juu ya kuwatia nguvuni kisha akamuaga na kuondoka.

Nyumbani kulikuwa bado kuna watu wengi tu, akamfuata mama yake na kumueleza juu ya maelezo yaliyotoka Polisi, mama yake akamwambia kuwa si kweli kuwa wazee wale waliokamatwa wanahusika, wale hawahusiki hata chembe,

“Ni kweli atakuwa ameuawa na wafanyabiashara wenzie, lakini nina hakika wala si wao hao waliokamatwa, itakuwa ni wengine kabisa japo alifanya nao biashara, ila kuna kitu kikaingia kati,”

“Ni kina nani hao mama? Inaonekana wewe unajua mengi mno lakini unanificha hata mimi, mama mimi ni mwanao wa pekee, unapaswa kunijuza lolote.”

“Hapana mwanangu, hizi ni hisia zangu tu ndio maana hata Polisi mimi sijawaeleza, kwani kila kitu kinataka ushahidi,” alijitetea mama mtu.

Alimuelewa mama yake na kumwambia kuna wakati anatakiwa akiwa na wasiwasi wowote awaeleze wanausalama, huenda wasiwasi wake ukawa na ukweli ndani yake na ukawafungulia njia.

“Kwa hiyo unanishauri niwaambie?”

“Ah basi achana na jambo hilo, unaweza kuwapelekea habari hiyo ikazusha mapya, nitalishughulikia mwenyewe baada ya kumaliza masomo yangu, kwani nimebakiza muda mchache sana,” walimaliza maongezi yao na Esmile akatoka.

Alikaa kule kwa wiki moja tu Jijini Dar na kurudi chuoni kufanya maandalizi ya mitihani yake ya mwisho.

Kutokana na kujiandaa vizuri, mitihani kake haikuwa migumu ingawa kwa hakika alifanya mitihani hiyo akiwa na mapigo makuu mwili moyoni mwake... Pigo la kuondokewa na baba yake kipenzi lakini pia na kumkosa mtu aliyempenda maishani mwake Mam.

Baada ya mitihani na kuwasilisha utafiti wake kama ilivyo ada kwa wasomi wa kada hizo. Akarudi Dar akiwa na lengo la kufanya mambo matatu likiwepo la kumtafuta muuaji wa baba yake.

Jambo la pili lilikuwa ni kumtafuta Mam popote pale alipo ili aweze kumuonesha aliembaka ili nae pia amburuze kortini, haijalishi Mam atakuwa kwenye hali gani, lakini tu yeye awe ametimiza ahadi yake.

Na jambo la mwisho alilolipanga lilikuwa ni kufungua kampuni ya binafsi ya uwakili, hakutaka kuajiriwa kabisa, aliamini anaweza na atakapokwama, alijua atakimbilia wapi.

Katika maazimio yake yote matatu, lile la mwisho, yaani la kufungua kampuni lilikuwa ndio jepesi zaidi na aliamini ndio linaweza kufungua njia zote kwani atakuwa na ofisi.

Hapa kwenye kufungua uwakili alijua ni vigumu mno kuliweka jina juu,

“Kupambana na majina makubwa yaliyopo hapa mjini ni shida sasa inapaswa kutumia akili ya ziada, lah sivyo mtu unaweza ukajikuta unaua ofisi yako na kwenda kuajiriwa kwa mtu,” aliwaza hivyo.

Akili yake ikamtuma afikiri ni nini cha kufanya, akafikiri sana lakini hakujua afanyeje, akaliweka wazo hilo pembeni na kuanza kulimaliza kwanza la usajili wa kampuni.

Aliwafuata wazoefu na kuomba msaada pale alipokwama, akatumia pesa ambayo mzazi wake aliiacha kwa ajili ya mambo ya kiofisi na moja ya nyumba zao kwa ajili ya ofisi ya kudumu, hakutaka kujiumiza kwa kuchukua ofisi kubwa katikati ya Jiji.

Baada ya kukamilisha usajili na pia ofisi yake, kampuni yake akaiita kwa jina la ‘The Chambers,’ akatoa nafasi za kazi kwa watu sita ambao yeye aliamini kwamba watamtosha sana, pindi wakihitajika zaidi basi atatoa tena nafasi nyingine.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Suala likabaki ni vipi ajiweke vizuri mjini? Hilo ndio jambo ambalo lilimla kichwa, lakini kwa kuwa alikuwa amedhamiria kufanya jambo hilo, alizidi kuumiza kichwa chake.

Muda wa usiku siku moja, akiwa anatazama taarifa ya habari, akaona tukio likitangazwa juu ya kijana mmoja ambae alifungwa kwa suala ambalo aliona lilikuwa na uwezo wa kumuweka huru.

Hapo ndio akapata wazo, akaiona fursa. Akapanga kusafisha jina kwa kusaidia watu ambao hawana uwezo wa kujisimamia kwenye kesi zao, lakini je wangapi hadi aweze kujiweka vizuri mjini?

Alijiuliza na kuamua kufanya kazi na watu wawili waliofungwa kwa makosa yanayoweza kumuweka mtu huru.





**********





ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog