Search This Blog

Tuesday, 1 November 2022

MY CLASSMATE - 2






Simulizi : My Classmate

Sehemu Ya Pili (2)





Mauaji ya aina ileile kama yaliyotokea Arusha.

Katika Chuo kikuu cha St Augustine cha huko jijini Mwanza kuna mwanafunzi aliuwawa kikatili.

Alikuwa anatoka kujisomea usiku akielelekea Hosteli.Alinyang'anywa njiani roho yake !



Maiti yake iliokotwa asubuhi katika uwanja wa mpira wa chuo ikiwa haitamaniki !

Ngozi iliokotwa upande wa goli la kaskazini.Kiwiliwili kisicho na ngozi kiliokotwa karibu na goli la kusini.



Yalikuwa mauaji ya kinyama sana !Yaliowaacha na uwoga mkubwa sana wanafunzi wa Chuo hiko kikubwa jijini Mwanza.



Mwanafunzi huyo alikuwa ni mtoto wa waziri wa ujenzi Mheshimiwa Karimu Nduguga.Polisi wa Mwanza nao wakalipata hekaheka kama ilivyokuwa kwa wenzao wa Arusha,wa kumsaka muuaji huyo asiye na huruma !



Lakini hawakumpata na wala hawakukaribia kumpata.!



Ndipo hali ya hatari ikatangazwa nchi nzima na Waziri wa wa mambo ya Ndani ya nchi,Mheshimiwa Frank Chali.Ilitolewa tahadhari hasa kwa watoto wa viongozi wakuu wa chama na Serikali.



Watoto wa vigogo wakawa wanalindwa hasa.Huku doria za Polisi zikishamiri Tanzania mzima.



"Mimi na Raiya tuliendelea kusota selo.Sasa tulihamishiwa Gereza kuu Arusha.Ilikuwa kwa usalama wetu kama Polisi walivyosema.Wiki mbili zilipita maisha yetu yakiwa selo.



Nakumbuka ilikuwa siku ya jumatatu asubuhi.Ya wiki ya tatu tangu nihamishiwe Magereza.Nilitolewa selo na kupelekwa Katika chumba cha mahojiano cha Gereza lile.Siku hii nilihojiwa na mtu mpya.Hakuwa wa gereza la Arusha.Maana wengi nilikuwa nawafahamu sasa.



"Unaitwa nani?"

"Naitwa Abdul Ramadhani"

"Niambie kwa kifupi unavyolielewa sakata hili?"

Nilimsimulia kila kitu tangu safari yangu ya kutoka Bagamoyo hadi nilivyofika Arusha.

"Unajua Kwa nini umewekwa ndani? "

"Ndio"

"Kwanini?"

"Kwa ajiri ya usalama wangu."

"Sasa mimi nataka nikutoe nje Abdul"

"Ati !"

"Ndio nataka uisaidie Polisi ukiwa nje"

"Nahofia usalama wangu,wataniua vibaya"

"Usiwe na shaka.Utakuwa na mimi kila hatua utakayopiga, mimi naitwa Daniel Mwaseba!!!"



Nilistuka sana kusikia jina hilo. Hakuna Mtanzania ambaye alikuwa halijui jina la Daniel Mwaseba .



Alikuwa mpelelezi namba moja Tanzania.Alikuwa mtu hatari kuliko hatari yenyewe. Alishawahi kuliokoa Taifa hili katika matatizo makubwa sana.Aliliokoa kutoka katika hila mbaya za maadui zetu.Alikuwa kijana makini,mpiganaji,mzalendo wa kweli kwa nchi yake.



Kuja kwa Daniel Mwaseba kwenye kesi hii nikajua mambo yamefikia pagumu.Mbele ya Daniel nilikuwa radhi nitolewe.Niliamini nitakuwa salama.Nilikubali.Tulitoka gerezani tukiwa tumefuatana na Daniel Mwaseba.



Nilijisikia fahari kufuatana na Daniel.Njiani nilikuwa namuuliza hili na lile.Yeye alikuwa anajibu kwa mkato tu.Daniel alikuwa ananipekeka Kijenge juu.Kwenye nyumba niliyopangiwa na jeshi la Polisi kuishi kwa muda.Hosteli haikuwa sehemu salama kwangu tena.



Tulishuka kwenye gari ya Daniel tukiwa sambamba.Tulikuwa tunakatisha barabara ili tuingie katika nyumba niliyopangiwa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Wakati tukiwa katikati ya barabara gari dogo aina ya Noah nyeusi ilikuja kwa kasi kwa lengo la kutaka kutugonga.Mimi nililiona lakini sikuwa na jinsi ya kufanya.Lilitukaribia sana.Kwa kasi ile nilijua lazima tugongwe !. lazima tufe mimi na Daniel Mwaseba.Kilikuwa kifo dhahiri mbele yetu.. !







Kilikuwa kifo dhahiri mbele yetu..! Ghafla nilijikuta nimerudi nyuma kwa haraka sana !



Gari lilipita sentimita chache sana na pale tuliposimama na Daniel.Kilikuwa ni kitendo cha haraka sana !



Sikuelewa nimerudi vipi nyuma kwa kasi ile.Nikamwangalia Daniel Mwaseba alikuwa anatabasamu,hana wasiwasi wowote.Huwezi jua kama kilitukosa kifo sikunde chache zilizopita .



"Mwanzo mzuri" Nilimsikia akinong'ona mwenyewe.

"Hivi limetukosaje lile Gari ?.Halafu alidhamiria kutugonga kwa makusudi !."

"Nilikuvuta mkono"



Alijibu jibu fupi na kunishika mkono tukarejea kwenye gari yake.Kwa hakika Daniel Mwaseba Alikuwa mtu wa ajabu sana !



Kwenye gari hakuongea neno.Alikuwa kimya makini na usukani huku akipiga mluzi.Akiimba wimbo nisiouelewa.Lakini akiangalia kwenye vioo vya pembeni vya gari kila mara.



"Hivi kitu gani cha siri alichowahi kukwambia Mayasa?" Ghafla Daniel aliniuliza swali huku akiwa anaangalia mbele.

"Hakuna kitu cha siri alichowahi nambia Mayasa"

"Una uhakika Abdul ?.Nakuuliza hili kwa ajiri ya maisha yako.Kuficha hakukusaidii"

"Kweli kaka Daniel.Hakuna siri yoyote aliyowahi nambia Mayasa."



Safari yetu ilishia kituo kikuu cha Polisi Arusha.Tulikaa kaunta pamoja na Daniel na askari mwengine.

Mara simu ya mezani ya pale kaunta ikaita.



"Hallo "

"Napiga toka Magereza Arusha"

"Ehh nambie Afande"

"Kuna tatizo hapa Magereza"

"Tatizo gani Afande ?"

"Yule mwanamke aliyewekwa mahabusu kwa ajiri ya usalama wake amefariki!!!"

"Nani ?"

"Raiya"

"Unasemaa !"

"Ameuwawa Afande"

"Natuma askari sasa hivi"

"Sawa"



Yule askari alituambia taarifa ya kifo aliyoipokea.Ilikuwa ni taarifa ya kifo cha Raiya, iliyonistua sana.Nilimwona mpaka Daniel akistuka.Lilikuwa pigo la ghafla na la kushangaza sana.



Mtu kufariki akiwa mikononi mwa askari siyo tatizo sana.Lakini mtu kuuwawa mikononi wa askari ilikuwa ni tatizo kubwa sana.Ndani ya Gereza lenye ulinzi mkali kama la Arusha.Yalikuwa maajabu!



Tulifuatana na Daniel kuelekea Magereza.Daniel hakutaka kuniacha hata sekunde moja.Alijua lazima wauaji watataka kuniua na mimi.Kwa vyovyote walikuwa wanataka kupoteza ushahidi kwa kuuwa.



Daniel alijua kwa kunitumia mimi ndipo atakapowatia mkononi kwa urahisi wauaji.Alinitumia kama chambo.Alijua kwa vyovyote nitakuwa nawindwa niuwawe !



Tuliwasiri Magereza majira ya saa nne asubuhi.Tulikuta hali ya gereza ikiwa shwari na vikundi vidogovidogo vya askari.Tulienda moja kwa moja kwa mkuu wa Gereza.



Niliuona mstuko wa wazi usoni kwa mkuu wa Gereza baada ya kumuona Daniel. Nadhani alikuwa anamjua kabla,na hakutegemea kama atakuwa pale.Alitukaribisha kwa heshima.Mimi nikibaki kuwa mtazamaji na msikilizaji.

Baada ya salamu Daniel alianza kuuliza.



"Ilikuwaje mkuu"

"Mnamo mida ya saa tatu asubuhi alikuja mtu.Alidai yeye ni ndugu na Raiya.Baada ya kumkagua askari walimruhusu aingie.Hakuwa na kitu chochote cha hatari.Baada ya kama dakika nne aliaga na marehemu alirudi selo.Lakini baadae askari walipoenda kwenye selo yake walimkuta ameuwawa !."

"Marehemu alipomuona huyo mtu alionesha dalili yoyote ya kumtambua?"

"Siwezi kujibia hilo ngoja tumwite askari aliyekuwa zamu"



Mkuu wa Gereza alimpigia Simu huyo askari.Baada ya kumaliza wakaendelea na maongezi yao

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Kwanini mnahisi huyo mgeni ndiye anahusika Katika mauaji."

"Marehemu hakuongea na mtu mwengine yeyote baada ya yule mgeni kuondoka"



Baada ya maelezo hayo yule askari aliyepigiwa simu na mkuu wa Gereza alikuja alikuja.Alisema hakuwa makini kuchunguza kama mgeni na marehemu walikuwa wanajuana ama lah.Yeye aliwakutanisha tu na kuondoka.Bila kutafiti chochote !



Tuliongazana na mkuu wa magereza pamoja na Daniel kwenda kuuangalia mwili wa marehemu Raiya.Ilikuwa ni picha mbaya sana ambayo haitafutika kichwani kwangu hadi leo.Picha mbaya ilioje kumkuta binadamu unayemfahamu kachunwa ngozi mithili ya Ng'ombe !



Nilikuwa namchukia sana Raiya lakini siku ile nilitoa machozi kwa ajili yake.Nilimuonea huruma sana.Nilijua kapitia maumivu makali sana akiwa anaipigania roho yake.Mwili usio na ngozi uliwekwa hapa.Na ngozi iliyokusanywa iliwekwa pale...!



Hali ilikuwa ya kutisha sana.Hakuna aliyeongea kwa zile dakika tano tukizokaa katika chumba.Nilimwangalia Daniel usoni.Alikuwa anatabasamu bila wasiwasi wowote..!



Tulirudi ofisini kwa mkuu wa Gereza.Sasa nikaigundua tabia moja ya Daniel.Huwa anatabasamu kila mambo yanapokuwa magumu.

Daniel alikuwa anatabasamu mbele ya maiti ya Raiya iliyouwawa kinyama.



"Nimemuona mkuu.Ni aina ya mauaji sawa na ya Mayasa.Sawa na ya mtoto wa waziri aliyeuwawa kule Mwanza.Itakuwa ni kundi moja kama siyo muuaji mmoja.Lakini awe mtu kiwe kikundi nitahakikisha hafanyi mauaji mengine ya raia wema !"

Alisema kwa uchungu mkubwa Daniel.



Tuliondoka pale Magereza tukiacha mwili wa marehemu Raiya ukipakiwa Kwenye gari kupelekwa hospitali.



Nilikuwa mwenye majonzi sana.Watu wawili waliojitolea kunisaidia kwa hali na mali walikuwa wamefariki kwa tofauti ya masaa machache sana.Ni mkosi gani huu !



Njiani nilimuona Daniel Mwaseba akitabasamu.Nikajua kuna kitu kakiona.Tena cha hatari !



"Tunafuatwa"

Nilimsikia akisema kwa sauti ndogo.



Ama zetu,

Ama zao ! "



Tuliifuata njia iliyokuwa inaelekea Moshi mjini kutokea Arusha.Mimi roho inanidunda.Daniel hana wasiwasi hata kidogo.Akiendelea na mluzi wake.Niliangalia kwenye kioo cha pembeni nami nikaona.Gari tatu nyeusi aina ya Noah zilikuwa zinatufuata kwa kasi kubwa !.



Daniel alikuwa makini na usukani.Alipofika Tengeru alikata kulia.Tukawa tunaelekea barabara ya vumbi iliyokuwa inaelekea chuo cha Maendeleo ya jamii Tengeru.Zilikuwa mbio kali sana kwenye barabara ya vumbi.Jamaa walianza kurusha risasi.Daniel alikuwa dereva makini.Alihakikisha hatudhuriki na risasi zile.Na hatukudhurika !



Daniel aliingiza gari ndani ya Chuo cha Tengeru. Sikutegemea kama ataiingiiza gari chuoni kwa kasi ile.Mimi nilidhani atakata kulia njia inayoelekwa chuo cha Sayansi cha Nelson Mandela. Haikuwa hivyo lakini.



Ilikuwa patashika ndani ya Chuo cha Tengeru.

Tulikuta wanachuo wengi wapo nje.Baada ya kufunga breki kali ! Tulishuka haraka haraka na kujichanganya na kundi la wanachuo waliokuwa wanaelekea kunywa chai mgahawani.Tuliziona zile Noah tatu nazo zikifunga breki kali .Vumbi lilitimka.Baadhi ya wanafunzi wa kike wakipiga kelele za uwoga,wa kiume walikuwa wanashangilia.Bila kujua nini kinatokea .



Walishuka jumla ya watu kumi na tano toka katika Noah zile tatu.Wote na bunduki mkononi.Mimi na Daniel tulikuwa tushaingia mgahawani.Lakini tuliona kila kilichokuwa kinafanyika pale nje karibu na geti ya kuingilia chuoni.Wanafunzi walianza kukimbia hovyo.



Jamaa moja alipiga risasi tatu hewani. Sasa lilikuwa vurumai.Wanafunzi walikimbia hovyo huku wakipiga kelele za taharuki.Wakajigawa wale majamaa.Watano walielekea madarasani.Wawili walienda maktaba.Watatu walienda uelekeo wa ofisi za walimu.watatu wengine walielekea vimbwetani na wawili walikuwa wanakuja mgahawani tulikokuwa sisi..!





Wauaji watatu wengine walikuwa wanaenda vimbwetani na wawili walikuwa wanakuja Mgahawani tulipokuwa sisi..!



Daniel aliinuka pale kwenye meza akaenda kujificha nyuma ya mlango wa Mgahawa ule.Mimi aliniacha palepale mezani pamoja na wale wanafunzi. Hali ya hofu ilitawala ndani ya mgahawa.Wote tuliwashuhudia watu wale wawili wakija Mgahawani na silaha zao mkononi.Wanafunzi walikuwa na hofu kubwa,wanalia kimya kimya.



Wale watu waliingia Mgahawani kwa umakini mkubwa sana.Mimi Nilikuwa nasubiri hatua atakayoichukua Daniel kule nyuma ya mlango.Nilikuwa na imani nae sana.Akaingia wa kwanza.Akaingia wa pili.Wote wakiwa na bunduki zao mkononi,aina ya SMG.



Ghafla yule jamaa mmoja alidondoka chini.Watu wote tulistuka mule Mgahawani.

Nikamwangalia Daniel kule nyuma ya mlango alikojificha.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Mdomo wa bastola yake ulikuwa unafuka moshi.Nikajua bastola ya Daniel imetumika.Na ilikuwa imefungwa kiwambo cha kuzuia sauti.Na bila shaka risasi imetua mgongoni kwa yule jamaa.



Nilimwona yule jamaa mwengine akibabaika sana.Hakujua nini kimempata mwenzie?.

Mgahawa sasa ulikuwa kimya.Kila mtu alitulia kusubiri hatma ya roho yake.Yule jambazi mwengine aligeuka nyuma kuangalia kule mlangoni.Alikutana nayo!.Alipigwa risasi ya utosini.Damu chache ziliwarukia baadhi ya wanafunzi waliokuwa karibu naye.Nae alielekea kuzimu bila ya kuaga.



Sasa Daniel alitoka kule mlangoni.Akazivuta zile maiti mbili na kwenda kuzificha nyuma ya mlango.Hakuwa na wasiwasi kabisa !Alikuwa kama anavuta magunia ya mkaa.



"Wanafunzi wote laleni chini haraka.Atakayejifanya mjuaji tu shauri yake !!"

Daniel alisema huku na yeye akilala chini. Tulitulia shwari.



Baada ya kama dakika kumi sauti za mlango zilisikika tena.Mimi nilimchungulia nikiwa nimelala pale chini.Alikuwa jambazi aliyevaa sawa na wale wenzake.Suti nzuri nyeusi na shati jeupe ndani.Na bunduki iliyotayari kuuwa wakati wowote itakapoamrishwa.



Huyu aliingia bila umakini wowote.Bila shaka alitegemea Uwepo wa wenzake mule ndani.Hivyo yeye hakuwa makini sana.

" Chugaaa"alianza kuita.

"Naam"Aliitikiwa.

Daniel aliitikia ule wito huku akinyanyuka alipokuwa amelala.Jamaa aliashangaa sana.Akiwa Kwenye mshangao Daniel aliachia risasi iliyozama katika tumbo la yule jamaa.Alikufa na mshangao wake usoni!



Daniel aliivuta ile maiti tena na kwenda kuiweka nyuma ya mlango nayo.Ulikuwa ni mchezo hatari sana lakini Daniel aliucheza bila uwoga wowote! Kosa moja lingesababisha kifo !



Wanafunzi wengi walikuwa wameshajikojolea pale sakafuni kwa uwoga.Mimi sasa kidogo nilianza kuwa mzoefu.Mzoefu wa kuona maiti.Mzoefu wa kuona watu wakiuwawa.Nilianza kuupenda pia mchezo huu.



Watu wote tulikuwa tumeikumbatia sakafu kasoro Daniel pekee.Alikuwa amesimama akiangalia kule nje.



Simu moja ya wale marehemu ilikuwa inaita kule nyuma ya mlango.Daniel alienda kuipokea.

" Chuga hapa"

"Yah,waje wawili"



Nikaelewa Daniel alijitambulisha kuwa yeye ni Chuga.Na kuomba watu wawili waje mgahawani.Hawakuchelewa!



Walikuja haraka sana.Wakati Daniel akiwa bado yupo kule nyuma ya mlango.Alikoenda kupokea simu.

Wauaji waliingia ndani huku wakimwacha Daniel kule nyuma ya mlango.Hawakufikiria kabisa kama kuna hatari !



Mimi jicho langu lipo kwa Daniel kuona atafanya nini ?.Nilimuona akijishika kiuno.Alitoka na visu viwili.Kimoja amekishika kwa mkono wa kulia na kingine mkono wa kushoto.

Alivirusha vyote kwa mpigo na kwa nguvu visu vile kuelekea kwa wale majamaa.Vyote vilitua shingoni.Kila mmoja na chake.Walienda chini kama mizoga.

Nilimuona Daniel akitabasamu.



Majambazi watano sasa alikuwa kawamaliza kimya kimya mule Mgahawani.



Mara nililiona kundi la Wauaji wote kumi waliobaki likija Mgahawani wakiwa wanakimbia.Bila shaka walihisi kuna kitu cha hatari ..!



Bila shaka walihisi kuna kitu cha hatari...!



Sasa ilikuwa hatari zaidi.Mimi nilianza kutetemeka mwili mzima kwa hofu.Nilimwangalia Daniel kule Nyuma ya mlango,nilimshangaa hakuwa na hofu kabisa mwanaume yule !.Kwa hakika Daniel hakuwa binadamu wa kawaida.Kila hatari inavyomkaribia yeye anazidi kuwa mtulivu na tabasamu lisiloisha usoni.



Wale jamaa waliingia ndani ya mgahawa.Pale nyuma ya mlango sasa Daniel Alikuwa ameshika bastola mbili mkononi.Ndani ya nusu dakika watu wote kumi walikuwa chini.Wote walikuwa wameuwawa na Daniel.



Wanafunzi wote walisimama na kumpa mkono wa pongezi Daniel.Alikuwa shujaa kwao.Alikuwa shujaa zaidi kwangu.Walimuhusudu sana,nilimuhusudu zaidi !



Tulitoka eneo la Chuo huku Daniel akiwapigia simu Polisi waje kutoa maiti zile.Sisi tulielekea moja Kwa moja kituo cha Polisi Arusha.



**************

Katika nyumba moja iliyopo mtaa wa Mikocheni,Dar es salaam.Kulikuwa na kikao.Kikao kilihusisha watu watano.Wanajeshi wanne wenye vyeo vikubwa jeshini na raia mmoja wa kawaida.Wanajeshi wale walikuwa wana vyeo vikubwa sana jeshini.Walikuwa wanajadiri mpango wao walioupa jina la Angamizo.Lengo la Mpango huu ni kuwaangamiza watoto wote wa viongozi wa Tanzania.Ili kusafisha njia kwa Mpango wa Angamizo!



Katika kikao kile mtu mmoja tu ndiye ambaye hakuwa mwanajeshi.Mumewe Raiya.Salehe.Yeye ndiye aliyesababisha siri za mpango huu zivuje Kwa mtu asiyehusika.Kwa bahati mbaya lakini siri za mpango huu wa Angamizo zilimfikia Raiya.



Ilikuwa siku ya ijumaa.Mumewe Raiya alichelewa kurudi nyumbani.Raiya alijisikia mchomvu sana.Alichukua laptop ya mumewe ili apoteze mawazo .Kipindi hiko Raiya alikuwa na wakati ngumu sana katika ndoa yake.Mumewe alikuwa bize sana. Vikao visivyoisha hadi saa tisa ya usiku.Kutokana na ubize huo Raiya akahisi anasalitiwa.Kumbe Hakuwa anasalitiwa.Mumewe alikuwa bize na Mpango haramu ulioitwa Angamizo !



Hakuwa anampa haki yake ya ndoa mkewe.Alibadirika kabisa.Muda mwingi alikaa peke yake kutafuta tulizo la nafsi.



Siku moja akiwa anachezea laptop ya mumewe.Ndani ya laptop ya mumewe Raiya aliliona faili liliandikwa Siri.Akalifungua bila wasiwasi wowote.Ndani ya faili hilo ndimo alikuta mambo yaliyomtisha sana.Mpango wa Angamizo ulipangwa utekelezwe baada ya miaka miwili.Ulikuwa Mpango hatari ulioratibiwa na watu hatari sana !



Siku alipoliona faili lile lenye siri toka Kwenye laptop ya mumewe kesho yake ndipo alipokutana na Abdul.Akiwa anatoka Bagamoyo.

Na kuaanzisha uhusiano haramu.Ulikuwa uhusiano haramu Lakini ulioleta faida kubwa kwa Taifa baadae.



Siku zilivyosonga mbele Salehe alihisi mabadiliko toka kwa mkewe.Akahisi huenda anatoka nje ya ndoa yao.Anamsaliti!

Siku zote alikuwa anamlalamikia kuhusu suala la unyumba.Lakini Sasa alikuwa halalamiki tena.Akaanza kumchunguza.Na zaidi Raiya akaanza kumuogopa sana mumewe.Salehe akachunguza.Akagundua kila walichokuwa wanafanya na Abdul.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Mbaya zaidi Salehe aligundua pia kuwa Raiya amegundua mpango wao wa Angamizo!.Na akajua kwa vyovyote Raiya lazima atamsimulia mtu wake wa karibu.Ambaye ni Abdul.



Sasa Salehe alianza kumfatilia Raiya kwa kila hatua aliyopiga.Siku Aliyomuaga kuwa anakwenda Arusha alimkubaria lakini hakumwacha peke yake. Alimfatilia!



Ndipo alipogundua kwa kina kila kitu kuhusu uhusiano wetu na kuamua kutuangamiza wote kwa sumu kali na hatari iitwayo Proxine...!



Ndani ya kikao kile ilikuwa ni kutupiana lawama.Wanajeshi wote wanne walikuwa wanamtupia lawama Salehe.Kwa kuweka rehani Mpango wao hataruki !.

Salehe alijitetea sana.Lakini hakueleweka kabisa.Wakati wanaendelea na mazungumzo simu ya Salehe iliita.



"Halo"

"Bon,Arusha"

"Nambie Bon"

'Mambo mabaya sana"

"Kuna nini tena"

"Tumepoteza wapiganaji kumi na tano leo"

"Unasema!!!"

"Ndio hivyo Salehe,kumi na tano wameuwawa"

"Sisi tumefanikiwa lakini"

"Tumefanikiwa nusu"

"Nusu kivipi"

"Tumemuua mkeo lakini yule Jamaa bado"

"Kwanini Bon..hadi sasa anapumua?"

"Ni msumbufu sana kaka"

"Inamaana ni yeye ndio aliyewauwa wapiganaji wetu kumi na tano"

"Ndio Salehe.Ni hatari yule mtu"

"Nakuja na Avira na Avast kwa ndege ya jioni,kummaliza"

"Itakuwa poa kaka"



Hali ilikuwa tete ndani ya kundi hili lenye Mpango wa Angamizo.



Jioni ya siku ile Salehe akiongozana na Avast na Avira walikuwa wanaelekea jijini Arusha.Kwa kazi moja tu.Kuhakikisha Abdul anauwawa.



Avast na Avira walikuwa wauaji hatari.Wauaji wanaojua aina zote za mauaji.Walikuwa makomandoo toka Marekani walioletwa kwa ajili ya kuleta Angamizo nchini Tanzania.



Ni hawa wauaji wanaotumia sumu hatari ya Proxine kuwaua watu kinyama.Asubuhi ya leo walikuwa Arusha kutekeleza kifo cha Raiya akiwa gerezani.Na sasa wanarudi tena Arusha kukatisha maisha ya Abdul.



Hawakuwahi kushindwa wanapoamua kuuwa mtu.Walikuwa makini kwa kazi yao.



Walitua jijini Arusha saa moja kamili usiku.Walipanga asubuhi ndio waanze kazi yao ya kumsaka Abdul.Hawakuwa na wasiwasi hata kidogo.Walikuwa na uhakika hata kama askari wote Arusha watakaa nje ya kituo cha Polisi alikokuwemo Abdul.Walikuwa na mbinu na hila zote za kijasusi.Waliamini watamuua tu!

Walijiamini.

Waliaminiwa!



Daniel Mwaseba alimwacha Abdul amemfungia katika chumba cha siri pale Polisi.Hakukuwa na Polisi wa kawaida aliyekuwa anakijua chumba kile.Zaidi ya RPC wa Arusha na OCD.Kilikuwa chumba kinachotumiwa kwa nadra sana.Tena kwa sababu maalum.



Yeye Daniel alienda kufanya kazi.Aliyanasa maongezi ya Kwenye simu kati ya Bon na Salehe kutoka Kwa rafiki yake aliyekuwa anafanya kazi katika kampuni ya simu waliyotumia Bon na Salehe kuwasiliana.Alihisi kuna kitu kutoka kwa mumewe Raiya.Hivyo aliongea na rafiki yake anase na kurekodi simu zote za Salehe kwa kifaa kiitwacho telemax.Hivyo alisikia simu zote zilizoingia na kutoka katika simu ya Salehe.Ikiwemo simu aliyopiga Bon kwenda kwa Salehe.



Na Daniel sasa alikuwa uwanja wa ndege wa Arusha akiwasubiri wageni wake..!





Daniel aliwasubiri wageni wake..!



Daniel aliiona ndege waliyopanda Salehe,Avast na Avira ikitua pale uwanja wa ndege wa Arusha.



Aliwaona watu wale watatu wakishuka kwa kujiamini sana.Macho ya Daniel yalikuwa makini sana na wale majamaa mawili,Avast na Avira.Macho yake yalimwambia hawakuwa watu wa kawaida !



Aliwaona walivyoshuka kwenye ndege na kupanda kwenye gari aina ya Noah nyeusi.Sawa na zile alizofukuzana nazo asubuhi.Aliifuata nyuma Noah ile akiwa na pikipiki yake.



Avast na Avira hawakuwa watu wa kawaida.Huwa wanaweka tahadhari kabla ya jambo halijatokea.Leo walivyoshuka tu kwenye gari walihisi watafuatwa.Walikuwa

makini sana!



Wakati Daniel akiwafata akina Avast na Avira kutoka uwanja wa ndege kina Avast walikuwa makini sana na magari yaliyokuwa nyuma yao.



Baadae kidogo waliitilia shaka pikipiki iliyokuwa inawafata nyuma.Wakawa wanasubiri muda muafaka wamtie mikononi mfuatiliaji.Wakawa wanaendesha gari taratibu wakiipigia hesabu ile pikipiki.



Walikuwa na sumu yao hatari ya Proxine.Tayari kwa kuitumia muda wowote itakapobidi.Msafara uliwafikisha kwenye mzunguko wa Azimio la Arusha wakielekea stendi kuu.Walipofika mbele kidogo Daniel alibadili njia.Hakuwafata tena.



Wakati wao wakinyoosha yeye alikata kulia njia iliyokuwa inaelekea uwanja wa mpira wa Shekhe Amri Abeid.Alipofika usawa wa geti la uwanja akasimama.



Mule ndani ya gari walishangaa ile pikipiki wakiyoitilia shaka imepotea ghafla.Wakawa wanaangaza huku na huko hawakuiona ile pikipiki.



Walipofika mbele kidogo walisimamisha gari yao.Daniel sasa alikuwa anatembea kwa miguu. Aliwaona jinsi maadui zake walivyobabaika.Akagundua walishajua kuwa wanafuatwa.Akajipongeza kwa uamuzi wake wa kuchepuka.



Kina avast walijifanya kutengeneza gari yao.Salehe aliingia uvunguni wakati Avast Na Avira walikuwa wanaangazaangaza huku na kule kumtafuta mwendesha pikipiki.Dereva Alikuwa ametulia tuli kwenye usukani.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Mbinu wakizozitumia kina Avast Daniel alikuwa ndio Mwalimu wa mbinu hizo.Alijificha kwenye mti mmoja akisubiri wafanye kosa lolote,awaadhibu !



Alikaa robo saa.Kosa halikutokea.Avast na Avira hawakuwa watu wa kufanya makosa kizembe.Walikuwa watu wanaoijua kazi yao.Baada ya robo saa walipanda kwenye Gari yao na kuondoka.



Daniel aliachana nao.Akijua ipo siku watakutana tu !



Alirudi nyumbani kwake mtaa wa maji ya chai kwa kutumia pikipiki yake.Siku nzima hakulala.Alikuwa anafikiria ni kitu gani wanachotaka kufanya watu wale.Hakupata jibu.



Asubuhi na mapema alienda kituoni.Alimkuta askari mmoja yupo kaunta.Alikaa na kuongea nae pale kaunta.



Saa moja na nusu asubuhi alikuja mgeni alijitambulisha kama ndugu wa Abdul.



Daniel kumuona tu mtu yule alimtambua.Alikuwa mmoja ya watu watatu aliowafatilia usiku wa jana yake usiku.Daniel alitabasamu !



"Habari Afande"

"Nzuri vipi hali yako?"

"Kwema,kuna ndugu yangu nimekuja kumwangalia"

"Anaitwa nani ?"

"Abdul"

"Unatokea wapi ?"

"Bagamoyo"

"Sawa"

Jamaa alionesha tabasamu la matumaini kwa mbali.

Aliyekuwa anaongea na na yule polisi ni Avira.Komandoo toka Marekani.Daniel akiwa pembeni alikuwa anamwangalia huku anatabasamu. Alimkumbuka vizuri sana!



Daniel aliomba kuongozana na yule mtu kumpeleka kwa Abdul.



Sasa waliongozana na Avira kwenda kumwangalia Abdul.



"Nilikuwa nimefungiwa kwenye chumba cha siri.Kilikuwa chumba chenye kila kitu ndani yake.Nilipewa na msichana mmoja aliyekuwa ananisaidia kazi ndogo ndogo mule ndani.



Nikaona mlango ukifunguliwa.Ilikuwa saa mbili asubuhi.Akaingia Daniel na mtu mwengine nisiyemfahamu.Walikuwa wanakuja kama marafiki wa kawaida.Yule mtu alinyoosha mkono ili tusalimiane na mimi.Nilisikia ukelele toka kwa Daniel akinikataza kushikana mkono na yule mtu .Nilirudisha mkono wangu kwa haraka wakati yule mtu akizidi kuuleta kwangu.Daniel Mwaseba alirusha teke lililoupiga mkono wa yule jamaa.Ukaanza mpambano sasa !



Yule jamaa alirusha ngumi mbili zilizopanguliwa na Daniel kwa ustadi mkubwa.Akarusha teke moja maridadi lililompata Daniel kwenye mbavu.

Alikuwa anataka kutoa kitu mfukoni Daniel alimzuia kwa kungfu kali ya mkononi.



Jamaa kwa ghadhabu alirusha kichwa kilichokwepwa na Daniel.Hadi hapo Daniel hakufanya shambulio lolote zaidi ya lile la kuzuia mkono wa yule jamaa usigusane na wangu.Na lakuzuia asitoe kitu mfukoni yule jamaa.



Jamaa alirusha ngumi mbili zilizompata Daniel usoni.Daniel alijishika uso.Jamaa alitaka kutoa kitu mfukoni Daniel alimzuia kwa teke kali lililompata barabara mkononi.



Jamaa Sasa alikuwa na hofu.Alisimama na kumpiga kofi la nguvu Daniel ,Daniel alikwepa.Jamaa alirusha Kofi lengine Daniel akakwepa tena.



Sasa Ulikuwa mwendo wa makofi kutoka kwa yule Jamaa na Daniel alifanikiwa kuyakwepa yote.Sasa jamaa akaanza kulia.Alijaribu kuingiza mkono mfukoni Daniel alimzuia kwa kumpiga ngumi kali ya uso !



Jamaa alisimama. Ghafla akaanza kuumuka !.Mimi macho yalinitoka pima!.Ngozi ya yule jamaa ilikuwa inavuka !.Lilikuwa tukio la kusikitisha sana.Tukuo la kuogofya sana.Jamaa ngozi yake ilikuwa inashuka chini taratibu.Alikufa kifo kinachofanana na cha Mayasa !.Alikufa kifo kinachofanana na cha Raiya ! . alikufa kifo kinachofanaa na cha afande John.Yule jamaa alivuka ngozi !http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Kumbe yule jamaa alishika ile dawa inayoitwa Proxine pale alipotaka kunisalimia mimi kwa mkono.Na alivyokuwa anataka kutoa kitu mfukoni alikuwa anataka kutoa dawa nyingine ili ajipake dawa kuzuia madhara ya ile dawa.Lakini alichelewa.Daniel alikuwa anamzuia kwa pigo kila alipotaka kuitoa dawa hiyo.Alijua atakufa.Ndomana alianza kulia kabla.Siku zote mshahara wa dhambi ni mauti !









ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog