Search This Blog

Tuesday, 1 November 2022

NAUZA BIKIRA YANGU - 2

 






Simulizi : Nauza Bikira Yangu
Sehemu Ya Pili (2)




Mshtuko alioupata haukuwa wa kawaida, Jasho likimtiririka angali bape sebuleni kuna kiyoyozi kinachotoa baridi isiyoweza kuruhusu mwili wa binadamu yeyote kutokwa na jasho, Akiwa haamini

macho yake kwa kiumbe kilichosimama mbele ya sebule yake ya kifahari, ni mgeni wa ajabu, Mgeni ambaye hakumtegemea katika maisha yake. Ni mgeni ambaye ameibuka katika kipindi ambacho si sahihi. Kwa tabasamu la kutengeneza huku akimkumbatia moyo wake ukiwa na chuki. Akimshika mkono kwa furaha ya kutengeneza na kumuonyesha njia ya kutoka kwa kutumia mlango wa pili katika jumba lile, tayari walikua wakifuata njia ya kuelekea katika msitu wa Trotoro msitu ulio pembezoni mwa jumba la Lord Brown, Huku wakiongea kwa furaha kama watu waliopotezana kwa muda mrefu.

"Ni muda mrefu sana, Mimi ni wiki ya pili tokea nitoke Gerezani kwa msamaha wa Rais, Na ni jana tu ndo nimeingia kwenye hili jiji la Pona"

Jackson Dudu aliongea kwa furaha huku akimuangalia Lord Brown kwa Furaha.

"Pole sana Rafiki yangu, Na karibu Pona"

Lord Brown alimjibu Dudu huku akimuangalia kwa Tabasamu la kuchonga.

"Nashukuru, Hivi unajua yule mkuu wa Gereza, Rweineni alifariki"

Hakuna kauli ilikua mbaya katika mazungumzo yao kama kauli ya kumkumbusha Lord Brown kuhusu Rweineni, Hakutegemea kukumbushwa mtu huyo kwa wakati huo. Siri aliyoificha kifuani kwake kwa muda mrefu huku akitumia gharama kubwa kuficha tatizo lake kwa kuua watu sasa siri hiyo ilionekana kutaka kuvuka mipaka ya kifua chake. Tayari mtu wa siku nyingi aliyemuokoa na kifo kule Gerezani yupo Uraiani na anasiri inayohusu maisha yake.

"Nataka nikupe zawadi rafiki yangu"

Lord Brown aliongea kwa upole walipofika karibu na shimo.

"Nitashukuru sana"

Dudu alijibu kwa shauku.

"Najua ulinisaidia sana kule Gerezani, Na bila wewe ungekuta nimekufa sasa nenda katika lile shimo utaona sanduku lenye Fedha chukua nilikuhifadhia kama shukrani"

Dudu alipiga hatua kwa furaha kusogelea lile shimo, Macho yake yakatua juu ya jeneza lililo wazi kwa mshtuko akageuka na kukutana na Bastola aina ya C 56G yenye kiwambo cha kuzuia Sauti {Voice Broof} Risasi zisizopungua sita zilisambaratisha ubongo wake na kudondokea ndani ya lile shimo, Kwa mwendo wa haraka Lord Brown alikua akirudishia udongo katika lile shimo bila kugundua kama kuna kamera zilikua zikirekido tukio zima. Baada ya kumaliza akapanda mti na kuondoka zake huku akijipongeza kwa tabasamu akiamini amefanikiwa kuficha siri.

Abas akiwa na mpira wa maji tayari alikua akitekeleza wajibu wake wa kila mara wa kunyeshea miti katika msitu ule. Mti mpya uliopandwa muda mfupi uliashiria tayari Camera zimepata tukio jipya. Akiangalia huku na huko kama hakuna mtu anayemuona Abas akaanza kupanda mti ili achukue Kamera iliyokua karibu na eneo lile aliopa. Wakati mkono unafikia ile kamera Ghafla akasikia Sauti ya Lord Brown ikimuita kwa hasira.

"Abass!!!!"

**** ****

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Siri waliyopewa na Abas ilitengeneza mwanga mkubwa sana katika njia ya kuitawala nchi ya jamuhuri ya watu wa Kolo, Tayari mpira walikua nao kilichosalia ni jinsi ya kumalizia. Vikao vilikua haviishi kwa viongozi wa chama cha The Revolution, Mikakati ya kuhakikisha wanamnasa Lord Brown katika tukio la ushoga ilikua ikisukwa kwa ufundi na umakini sana. Abas kutokea katika kipindi hicho ilikua kama Mungu kamtuma malaika wake aje kuonyesha maovu ya Tajiri huyo. Imani kubwa iliyojijenga kwa wananchi dhidi ya Lord Brown ilikua ikiwatesa katika kipindi cha awali, Sasa walikua Tayari wana silaha, Silaha kubwa ya kummaliza Mpinzani wao.

"Mimi napendekeza ushahidi ukikamilika tukiwa nao mkononi, Tumuite tumuonyeshe kisha tumpe masharti ya kujiuzulu kugombea Urais"

Salomenyo Chaloo alitoa wazo lililopingwa vikali na Paul Bona.

"Sasa kama unapinga toa wazo lako, Tufanye nini?"

Salomenyo alimuuliza Paul Bona swali.

"Mimi nachopendekeza tutafute njia ya kuwahakikishia wananchi vitendo vinavyofanywa na Lord Brown na mikakati ya jinsi ya kuwaambia ifanywe mapema iwezekanavyo"

Paul Bona alitoa wazo lake ambalo lilizua mjadala mrefu mwisho wa siku maamuzi yakatoka wakae na kusubiri ushahidi kukamilika, Huku kwa sehemu kubwa wakimtegemea Abas.



Mshtuko alioupata abas baada ya kusikia jina lake likitajwa ulipelekea ajiachie juu ya ule mti na kudondoka chini.

"Si nilisema hamruhusiwi kugusa matunda katika msitu wangu"

Lord Brown aliongea kwa ukali huku akimfuata Abas, Mlio wa simu toka katika mfuko wa suruali yake ndio ulimfanya akasimama na kusikiliza simu kisha akakata na kumuangalia Abas kwa hasira.

"Usije ukarudia Tena, na hiyo miti wacha utaanza kunyeshea tena keshokutwa"

Lord Brown aliongea na kugeuka kisha akarudi alipotokea huku Akifuata nyuma kwa woga.

Trii triiii riii

Simu ya Abas ilikua ikiita alipofika tu getini, Akaitoa kwa hofu na kuiweka sikioni.

"Vipi bado hujafanikiwa?"

Sauti toka upande wa pili wa simu iliuliza.

"Sikia mambo bado si mazuri kuweni wavumilivu"

Abas alijibu kwa sauti ya chini huku akiwa na wasiwasi.



**** ****



Hali ya kampeni katika nchi Jamuhuri ya watu wa Kolo ilikua imepamba moto, Vyama vikuu viwili vya Democracy Movement na The Revolution vilikua vikipambana vikali huku vyama vingine vinavyofuata vikijikongoja mkiani, Watafiti wa masuala ya uchaguzi kutoka nchi za magharibi walikua wamekwishatoa matokeo ya kitafiti yanayoonyesha Lord Brown ndiye anayeongoza kwa asilimia sabini na moja wakati mpinzani wake Elibariki chalambo akiwa na asilimia ishirini na tano huku asilimia nne zilizosalia zikiwa vyama vilivyobakia. Matokeo hayo yalionyesha hali mbayaa kwa chama cha The Revolution wakati hali hiyo ikiwa tete viongozi wa chama hicho hawakuonekana na wasiwasi hali iliyozidisha hofu kwa chama cha Democracy Movement na kuongeza nguvu ya ushawishi. Misaada aliyokua akiitoa Lord Brown kwa vikundi mbalimbali vya kijamii huku ahadi kibao zikiwa zinafuatana kwa karibu zaidi ziliwachanganya wananchi na kuwafanya wazibe masikio wasisikie sera za mgombea yeyote zaidi ya Lord Brown.



Mfumo wa uchaguzi wa nchi hiyo ndio uliowapelekea wagombea ubunge wa kila jimbo kufanya kazi kubwa ya kumtangaza na kumuombea kura rais wao kwa kuwa rais anayepita atapita na Wabunge wake wote.

Katika mkutano mkubwa kati ya mikutano mikubwa ya chama cha Democracy Movement Lord Brown akiwa kasimama jukwaani akipungia mkono wananchi, kelele za shangwe zilikua zikisikikaa, Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliokua wakifuatilia kwa makini kampeni za nchi hiyo walikua wakihangaika kuhakikisha wanapata habari katika tukio hilo. Lord Brown akiwa anaongea Ghafla hali ya kutetemeka ikamkumba akashukuru na kurudi kuketi huku hali ile ikizidi kumtesa. Katibu wa chama alikua jukwaani akimwaga sera ambazo Lord Brown hazikumsaidia chochote kwa wakati huo. Akiteta jambo na mmoja wa wasimamizi wa kampeni zake, Lord Brown anasimama na kuelekea kwenye gari na gari linaondoka kwa mwendo wa kasi kuelekea katika Jumba lake la kifahari. Akishuka katika gari kwa mwendo wa haraka na kuingia ndani.

" Ruza kuna kazi nataka ukanisaidie kule msituni Jiandae"

Lord Brown alimwambia Kijana wake wa kazi aliyemkuta pale sebuleni akifuta thamani za pale ndani.

"Sawa Boss"

Lord Brown akaingia kwenye moja ya chumba kati ya vyumba vilivyo ndani ya jumba lile baada ya muda mfupi alitoka akiwa kavaa taulo na tisheti nyepesi na kumkuta Ruza akimsubiri, Safari ya kuelekea Katika msitu ikaanza. Wakafika msituni pembeni ya shimo linaloonekana limechimbwa muda mrefu kidogo.

"Ruza kuna kazi nataka ufanye nitakupa pesa unayotaka na kazi hii nataka iwe siri"

Lord Brown alimwambia Ruza huku akiwa kalegeza macho.

Ruza tokea amjue boss wake hajawahi kumuona hata siku moja akiongea kwa upole kama siku hiyo.

"Usijali boss nitaifanya kwa usahihi na sitomwambia mtu"

Ruza alijibu kwa kujiamini.

"Nataka uniingilie kinyume na maumbile, Nimevutiwa nawe naomba uniridhishe"

Huku akimshika shika Ruza kifuani Lord Brown alikua keshalegea huku akizidi kutetemeka na muda huo alikua akitaka atimiziwe hitaji lake, Ruza akitetemeka kwa woga alijikuta tayari zipu ya suruali yake imekwishafunguliwa na Lord Brown na suruali ilikua ikielekea kupishana na magoti. Bila kuridhia tayari Ruza alikua akifanya kile alichoambiwa na boss wake yule. Baada ya kumaliza bila kutarajia Risasi mbili zilibusu paji la uso la Ruza na kudondokea ndani ya shimo na tayari Lord Brown alikua akirudishia Udongo kwa haraka kisha akapanda mti juu yake na kutabasamu kasha akaondoka taratibu.



**** ****

Hakuna aliyekua akiamini kile walichokua wakikishuhudia mbele ya macho yao katika Tv kubwa iliyounganishwa na kamera ndogo, Risasi zilizokua zikisambaratisha kichwa cha Dudu na kuangukia katika shimo zndizo ziliwaacha midomo wazi viongozi wa chama cha the Revolution, video ya pili ndiyo iliwaduwaza zaidi baada ya kushuhudia Lord Brown rais mtarajiwa akifanyiwa kitendo cha kishoga na kijana mdogo na kisha kumtoa uhai wake. Hakuna aliyetaka kuamini kile anachokiona kitendo kilichopelekea kurudisha nyuma video zile na kuangalia mara kwa mara. Tayari ushindi ulikua mezani kwao wakiwa na furaha walikumbatiana huku wakimpongeza Abas kwa kazi kubwa aliyoifanya.

"Sasa huyu firauni amekwisha"

Mr. Ngwali aliongea kwa sauti iliyopokewa na vicheko kutoka kwa viongozi wengine.

"Mimi nina wazo litakalowabadilisha wananchi"

Rosemary aliinuka katika kiti chake na kuzungumza.

"Wiki ijayo si ndio mdhalo wa mwisho wa wagombea Urais, na siku hiyo asilimia kubwa ya wananchi watakua wanatazama mdahalo huo, Mimi naona hiyo ndiyo nafasi ya kubadili fikra za wananchi kwani baada ya hapo ni uchaguzi, sasa chakufanya hapa tunae Abdallah na Deogratias wao wanamiliki Tv na zitaonyesha mdahalo huo. Sasa wakati mdahalo unaanza kabla ya Chalambo kuzungumza wakati wananchi wana shauku ya kumuona Lord Brown turushe video hii japo inavipande vibaya kwa watoto kuona ila tuwe tayari Tv za hawa wenzetu kufungiwa ila ujumbe ufike na chalambo akiwa Rais Zitafunguliwa"

Wajumbe walipihwa na butwaa kwa wzo ambalo hawakutegemea kama litatolewa na mwanamke.

"Yees Good idea"

Deogratias alijibu huku akipiga makofi yaliyopokewa na viongozi wengine.

"Ila nina wazo, Suala la mawasiliano ni pana sana na tv zitakua nyingi na ingekua bora kama tv zote zingeonyesha tukio hili zisiwe zetu tu na sababu waves tunapokea toka Tv ya taifa itakua ngumu sisi kujipenyeza mnaonaje tukatafuta mtu wa kufanya kazi ya ku lob matangazo kwa muda na tv zote zikaonyesha kile tunachotaka"

Deogratias alitoa wazo lililopita bila kupingwa na muafaka ukatolewa kazi ifanyike haraka.



**** ****http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Virus ndilo jina alilokua akiitwa na kila mtu katikati ya mtaa wa Suez, Ni kijana aliyekulia katika maisha ya kimasikini, Utundu wake wa kutengeneza vifaa vya umeme na mawasiliano ulimfanya ajulikane na kila mtu, Elimu yake ya msingi haikutomfanya kushindwa kutambua baadhi ya maneno ya kingereza kama Network, internate, Browse, Wifi, Connect na hata disconect. Akipata umaarufu baada ya kuanza kutengeneza simu alikua akipokea simu nyingi na kuzitengeneza. Virus za alizua gumzo kubwa mtaani kwao baada ya kufungua Redio yake ya chumbani kwake akaanza rusha matangazo yaliyokua yanaingiliana katika mawimbi ya redio nyingine na kusababisha watu kusikia kile anachotangaza yeye. Mamlaka ya mawasiliano ya nchi ya Kolo walimkamata na kumtoza faini kubwa ambayo iliigharimu familia yake kuuza nyumba na kumkomboa mtoto wao aliyekua akiteseka mahabusu. Habari iliyomuhusu Virus ilichapishwa kama makala katika Gazeti la Mtanzania gazeti linalotoka nchini Tanzania na kusomwa kwa wingi na wananchi wa jamuhuri ya Kolo. Ni makala iliyobeba kichwa cha habari "KICHWA CHA AJABU KILICHOFUNGUA REDIO CHENYE UWEZO WA KUFUNGUA TV CHAOZEA MTAANI" Ni makala yenye mshiko sana ambayo iliandikwa na muandishi mahiri wa Makala nchini Tanzania Anold Sway. Makala hii ndiyo iliyomvuta Mr. Ngwali na kutamani kufahamiana na Virus.



Tayari kazi ya kuingilia mawimbi ya video ya Tv zote na kurusha video wanayoihitaji ilikua mikononi mwa Virus ambayo kwake ilikua ni kazi sahisi sana. Kwa kutumia Sacket ya simu na waya wa AV wa kamera tayari mafanikio yalishaonekana kwa kujaribu kuingiza sauti katika Tv ya Taifa. Akiwa Busy katika chumba cha siri tayari Virus alikua akisubiri muda ufike ili aweze kumuanika Lord Brown mbele ya Tv za wananchi.





Ilikua ni gumzo kila pembe ya nchi ya jamuhuri ya watu wa Kolo, Hakuna ambaye alikua hazungumzii jambo hilo, Kuanzia watoto hadi wazee ndilo lilikua jambo kubwa lililopamba hadi vyombo vya habari kwa wakati huo, Shirika la Real Social lililopata ruzuku ya kutoa elimu ya uchaguzi na uraia ndani ya nchi hiyo lilikua limetangaza kufunga Projector n luninga katika kila kata ili kutoa fursa kwa wananchi kuweza kuona uwezo wa wagombea wao kujieleza na kujibu maswali. Nia ya shirika hilo ni kuwza kutoa fursa kwa wananchi kuchagua kiongozi atakaekua bora kwa miaka minne ya kipindi chake cha kuongoza. Muda ulikua ukisogea taratibu kama mwendo wa konono huku wananchi sehemu mbalimbali wakiwa wanajisogeza katika viwanja vya kata kwa ajili ya kuangalia mdahalo mkubwa wa mwisho unaohusisha wagombea wa Urais wa vyama vyote vinne wakijibu maswali na kujieleza kwa wananchi huku wakipewa fursa ya kuomba ridhaa ya kuongoza kwa wananchi ambao ndio wanamamlaka ya kuchagua nani awe rais wa nchi hiyo.

Saa kumi na mbili kamili jioni ilipotimia tayari watu walikua mbele ya luninga zao wakisubiri robo saa ijayo kuweza kuona wagombea wao. Mapenzi makubwa dhidi ya Lord Brown kwa wananchi walioko mjini mpaka vijijini hayakuweza kujificha yalionekana dhahiri kwa wingi wa watu waliovalia sare za chama cha Democracy Movement, Mbali na sare wengingine walibeba mabango yenye ujumbe mbalimbali za kumuunga mkono Lord Brown na wengine wakiwa na picha kubwa za Lord Brrown huku nyimbo za kumtukuza zikiimbwa kwa furaha. Mtangazaji maarufu wa luninga nchini Kolo mwenye uzoefu wa kufanya mahojiano na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa, Si Mwingine ni Jenifa Priva au maarufu kama Jane akiwa kavaa suti nzuri ya kike ya rangi ya kijivu iliyomkaa vyema alitokeza katika luninga na kusababisha wananchi waliokua wakipiga kelele za kuhamasisha kunyamaza kimya kwa ajili ya kusikia kinachozungumzwa.

“Karibuni katika usiku wa Mwisho wa kampeni na usiku wa mwisho wa kuwasikia wagombea wa kiti cha Urais, Na tuna wagombe wanne kutoka ktika vyama vinne vilivyoomba ridhaa ya kusimamisha mgombea wa nafasi ya yo urais ambavyo ni New Democracy, The Revolution, Youth Republican na Democracy Movement. Na wagombea wote wako tayari kwa ajilili ya kuanza kwa mdahalo”

Jane alimaliza na pazia kubwa likafunguka wakaonekana wagombea wanne wamekaa vyema katika viti wakionekana na tabasamu, Mchanganya picha za video alichanganya picha ya Lord Brown iliyopigwa kwa ukaribu iliyopelekea kujaa katika uso wa luninga ambapo kitendo hicho kiliamsha kelele za kushangilia kutoka kwa wananchi waliokua hwaambiwi wala hawasikii kuhusu Lord Brown huku wakimuita mkombozi wao.

**** ****

Jina la Dudu lilishtua jeshi la Polisi la nchi ya Jamuhuri ya watu wa Kolo, Kitendo cha jina la Dudu kuwa mmoja wa wafungwa waliopata msamaha wa Rais kilifanya kamati maalumu ya jeshi la polisi iliyoongozwa na Inspekta George Iron kukutana kwa dharura, Kikao kilidumu zaidi ya saa nane na mwishowe mamuzi yakatoka mpelelezi maarufu Michael Sabuni apewe jukumu la kufuatilia nyendo za Dudu tokea anatoka Gerezani ili kuweza kugundua kama bado mtandao wake wa genge la uhalifu kama unafanya kazi. Historia ya matukio aliyofanya kipindi cha nyuma ililitisha jeshi la polisi mpaka kupelekea kuamua kumfuatilia Dudu ili asije akaleta madhara na kuchafua utendaji wa jeshi hilo ukizingatia kuna vuguvugu la uchaguzi linaendelea ndani ya nchi hiyo.

Michael akiwa kava miwani ya jua yenye Lensi zilizounganishwa na waya wa mawasiliano wenye kuvuta picha ya mbali na kuhifadhi wave za video na sauti katika memory card ndogo iliyo ndani ya mkono wa miwani ile. Wakati Dudu akishangaa Picha ya Lord Brown, Michael alikua hatua chache akifuatilia kila anchokifanya. Ndani ya Bus liitwalo Polepole Trans katika siti ya pili kutoka mwisho alikua kakaa Dudu huku macho yake yakitazama luninga iliyo ndani ya basi hilo lililokua likielekea jijini Pona. Filmu ya Anold Schwarzeniger iitwayo Comando ilikua imemteka vilivyo. Dudu akifuatilia kila tukio katika filamu ile. Michael akiwa kakaa kiti cha pembeni ya Dudu huku akitafuna Big G huku macho yake yakiperuzi gazeti la udaku la Fichua huku akimuangalia Dudu kila kitendo cha tofauti anachofanya. Mwisho wa Michael kumuona Dudu ilikua ni pale Dudu alipoingia ndani y Geti kubwa la kasri ya Lord Brown anzia hapo hakumuona tena wala kusikia habari zake. Jithada zake za kusubiri kama atatoka ziligonga mwamba na alipotumia njia za kichunguzi kuweza kujua kama yupo ndani ya jumba hilo hazikuzaa matunda baada ya kuambulia jibu hakuna mtu kama huyo. Majibu hayo yalimuumiza kichwa Michael na kuamua kuanza kufuatilia Kasri la Lord Brown ili kubaini kama kuna mlango wa ziada ambao mtu yeyote anaweza kutumia kutokea lakini hakufanikiwa kupata jibu tena. Msimamo wa Mkuu wake wa kazi Inspekta George Iron katika Ripoti ya kazi ulizidi kumuumiza kichwa na kumuweka Michael katika wakati mgumu, ripoti isiyo na maelezo, Ripoti yenye mtokeo yaliyoambatana na kukamawa kwa muhalifu ndiyo alikua akiitaka mkuu wake wa kazi. Michael lijikuta akiongea mwenyewe.

“Dah sasa kazi ndo imeanza”

**** ****

Akiwa kavaa kanzu na kofia kichwani huku akiwa makini kumtazama kila mgombea huku akiwa anaandika vitu kadhaa katia kitabu chake kidogo, Si mwingine ni mpelelezi Michael aliyekua kakaa siti ya nyuma upande ambao walikua wamekaa wageni waalikwa na waandishi wa habari wa magazeti. Jane akiwa na tabasamu alisimama na kuanza kutambulisha Wagombea huku akitoa utaratibu utakaofuatwa siku hiyo.

“Naomba nimtambulishe kwenu Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha New Democracy Ndugu Liberatus Mfunjo”

Jane alifanya utambulisho ulioambatana na Mgombea kusimama na kupunga mkono.

“Naomba nimtambulishe kwenu Mgombea mwingine wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha the Revolution Ndugu Elibariki Chalambo”

Chalambo alisimama na kupunga mkono makofi mchache toka kwa wananchi waliokua wakitazama mdahalo ule kupitia luninga na Projector yalisikika.

“Sasa naomba nimtambulishe kwenu Mgombea Urais kwa Tiketi ya Chama cha Youth Republican, Kijana mdogo Ndugu Derick Ngonyaye”

Derrick alisimama na kupunga mkono kasha akakaa

“Naomba nimtambulishe mgombea wa kiti cha Urais aliyesalia kwa tiketi ya chama cha Democracy Movement Ndugu Lord Brown”

Lord Brown akasimama na kupunga mkono kitendo kilichoamsha shangwe na kelele kwa wananchi waliokua wakitazama kupitia luninga huku wakimuita Rais mkombozi.

“Sasa kutokana na utaratibu tutatoa nafasi kwa wagombea kutoa sababu ya wao kuomba Ridhaa ya kuongoza nchi na kisha nafasi hiyo itaambatana na swali toka kwa mwananchi, Kwa kuwa katika utambulisho tulianza na Ndugu Liberatus Mfunjo, Naomba wakati huu tuanze mwisho naomba nimlete kwenu Ndugu Lord Brown.”

Lord Brown alisimama na kuelekea sehemu maalumu kilipo kipaza sauti huku kelele zikiwa zimezidi huko mtaani kwa wananchi waliokua wakitazama kupitia luninga. Miale ya kamera za waandishi wahabari ilikua ikishindana kummulika Lord Brown. Akiwa kapambwa na Tabasamu Lord Brown akalegeza koo kwa kutoa kikohozi kidogo.

**** ****

Virus akiwa katika chumba cha siri ndani ya nyumba ya Deogratias, Mitambo yake ikiwa tayari huku akishuhudia kila kinachoendelea kupitia Tv ndogo iliyounganishwa na kamera ndogo iliyo mezani huku kompyuta ndogo mpakato ikiwa pembeni na waya uliotoka katika simu kuu kuu na kuingia moja kwa moja katika ile kompyuta. Macho yake yaitua kwa Lord Brown aliyekua kasimama mbele huku akijiandaa kuongea. Virus akiandika maandishi makubwa katika kompyuta yaliyosomeka “HUYU NDIYE RAIS TUNAYEMTAKA” Akabonye kitufe cha simu kuruhusu ile simu kuwaka ili kuweza kuunganisha mawimbi yaweze kuingilina. Mara mlio wa tahadhari kutoka kattika ile imu ukasikika na kutokea maandishi juu ya kioo cha ile simu “BATERY LOW” kisha simu ikazima kitendo ch Virus kuona maandishi yale kilimchanganya na kuashiria kuwa kazi inayotakiwa kufanywa haitowezekana na aliambiwa ahakikishe anafanya kabla Lord Brown hajaanza kuongea. Kitendo cha Lord Brown kuanza kujitambulisha kilimchanganya Mr. Ngwali na viongozi wengine wa chama cha The Revolution kwa kutoona kile walichotegemea kwa akati ule kupitia Luninga zilizotundikwa ndani ya studio zile. Mr. Ngwali kwa kutumia simu yake ya Mkononi akaamua kupiga namba ya Virus iliy katika ile simu inayotumika kuingilia mawimbi ya video akakutana na jibu lililomchanganya.

“Mtumiaji wa simu unayempigia hapatikani kwa sasa, Tafadhali jaribu tena baadae”

**** ****

Hakuna mtu aliyekua anatetemeka na aliyekua anaonekana mwenye hofu kama Abass muda wote aliokua akiangalia Luninga alikua akitetemeka huku akionekana mpole kuliko kawaida, Tukio linalofuata aliliona kama sinema ktika ubongo wake, Wakati Lord Brown akiwa anasogelea kipaza sauti na ukichanganya a kelele za watu vilimchnganya na kumfanya chuki iongezeke dhidi ya Lord Brown. Alikua akiangalia watu pale uwanjani huku akitbasamu tabasamu la uchungu, tabasamu la huruma kwa wananchi wale wasiojua chochote kuhusu Lord Brown. Alijikuta akizungumza mwenyewe moyoni huku akijipatia majibu ya kuiridhisha nafsi yake.

Baada ya kikohozi kidogo Lord Brown alianza kwa kutazama pande zote za ukumbi wa studio ile uliojaa watu wengi huku akifurahiwa na Miale ya Mwanga wa kamera za waandishi wa habari iliyokua ikimmulika kila upande.

“Kwanza napenda kumshukuru Mungu kwa kuweza kutuwezesha kufika siku ya leo, Pili naomba nichukue nafasi hii kuwapa pole wale wote waliopoteza ndugu zao katika mazingira mbalimbali katika kupigania maisha”

Lord Brown alinyamaza na kusababisha makofi na kelele za ng makofi na kelele za nguvu kutoka kwa wattu waliokua pale ndani, Huko nje kwa wanaanchi ndio ilikua balaa. Wakati hayo yanaendelea hali ilikua mbaya kwa viongozi wa The Revolution, Mpaka kufika wakati huo video waliyotegemea ingeonekana ilikua haijaonekana na kutokupatikana kwa Virus katika simu ndicho kitu kilichowachanganya zaidi. Uamuzi wa kuelekea kule walipomuacha Virus ndio ulikua sahihi kwa wakati huo. Mr. Ngwali jasho lkiwa linmtiririka angali kulikua na kiyoyozi kilichokua kikifanya kazi vyema ndani ya ukumbi ule, Alisimama kwa mwendo wa haraka na kutoka nje ya ukumbi ule kuelekea eneo la kupaki magari na kuingia ndani ya gari lake na kutoa Gari kuelekea barabarani. Mrundikano wa magari na watu waliokua wakiangalia Luninga kubwa iliyofunga karibu na barabara kuu ulimfanya kuishiwa nguvu na kujikuta akijiegemeza kwenye usukani huku akiwa kakata tamaa.

**** ****

Baada ya kelele kwisha Lord Brown alianza kuzungumza kwa upole huku wananchi wakimsikiliza kwa furaha kwa kauli za matumaini alizotoa Lord Brown.

“Kitu kilichonisukuma kuomba Ridhaa ya kuongoza nchi hii ni kutokana na hali ya nchi hii, Kiukweli halini mbaya na nimeona ni ngumukusaidia mtu moja mmoja uwezo wangu ni mdogo, Naamini mkinipa ridhaa ya kuongoza nchi hii nitaweza kufoa fungua milango ya mafanikio kwa wananchi walio vijijini na mijini kwa kutoa fursa za ajira kw vijana, Mikopo yenye masharti nafuu kwa kina mama na huduma bora za afya kwa watu wote na kutoa kipaumbele kwa wazee, wakina mama na watoto”

Kitendo cha simu kuishiwa na chaji kilimchanganya Virus na kuishiwa na nguvu, Kila batter alilokua akijaribu katika ile simu lilikua ni tofauti na ile simu. Muda ulionekana kukimbia kuliko kawaida na kumfanya Virus kujiona ni mjinga kwa kutojaribu vifaa vyake mapema, Wazo aliloona la msingi kwa wakati huo ni kujaribu njia nyingine ambayo inaweza kuwasha simu ile, Tayari chaja ya simu aina ya nikia iliku imekatwa kichwa na waya mbili za kupitsha moto ziliku zimechomwa katika njia ya kpiitishia Moto katika simu ile, Kwa haraka kama yupo katika mashinano ya kukimbizana na muda. Chaji ilikua katika soketi ya umeme na kubonyeza kitufe cha kuruhusu moto kupita katika ile chaji.Kitendo cha Simu kuonyesha mwanga mweupe na ishara ya batter kuchaji ilibadili sura ya Virus na kuonekana mwenye Furaha. http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Simu ilikua imekwisha washwa na tayari alikua ameruhusu maandishi aliyoandika kwenye kompyuta yake ndogo kwenda hewani. Maandishi makuwa yaliyoonekana mbele ya Luninga yaliyosomeka.

“HUYU NDIYE RAIS TUNAYEMTAKA” maandishi yale yalimshtua Mr. Ngwali na kutoa macho huku akitazama kwa makini kupitia kioo cha mbele cha gari yake macho yakitua katika luninga kubwa iliyo pembezoni mwa barabara huku akishuhudia watu wengi wakitazama tukio lile. Mara picha ya Lord Brown akiwa kaongozana na Dudu katika msitu wake ulio pembeni ya nyumba yake. Sauti ya Lord Brown wakati anaongea na Dudu na kisha kumwambia aelekee katika lile shimo ilisikika barabara na risasi zikisambaratisha ubongo wa Dudu na mpaka alipomaliza kufukia shimo lile na kupanda mti juu yake. Ngwali alishuhudia wananchi wakipigwa na butwaa mara maandishi mengine yakajaa mbele ya Luninga. “CHAGUA LORD BOWN KWA VITENDO HIVI” kisha akaonekana Lord Brown kava taulo na singlend akiwa kaongozana na kijana aliyevaa nguo a nyeupe. Mazungumzo ya Lord Brown na Yule kijana yalivunja uaminifu wa wananchi kwake na hasira zikawaka katika vifua vyao na kuanza kupiga kelele za kulaani.

Wakati hali hiyo ikiendelea Mpelelezi Michael Sabuni alikua akiwasiliana na Polisi ili wafike katika hilo na kumuweka Lord Brown chini ya ulinzi, Tayari alikua amekwishakamilisha kazi nzito iliyokua mbele yake huku yeye akiwa shahidi namba moja ambye alishuhudia Dudu akiingia ndni ya Kasri la Lord Brown na hakutoka tena. Lord Brown alichanganyikiwa na asijue cha kufanya Tayari waandishi wa habri walikua wakipiga picha kwa kila kitendo kilichoendelea. Tukio la kuingiliwa kinyume lilifungua mtazamo mpya kwa wananchi na dhabu ya Risasi kwa kijana Yule iliamsha hasira zaidi ndani ya dakika chache Tayari Wananchi walikua nje ya Studio za Televisheni ya taifa huku wakichoma Moto picha za Lord Brown wakiimba nyimbo za kutaka auawe. Nguvu za ziada zilibidi kutumika na Jeshi la polisi huku Lord brown akiwa chini ya Ulinzi mkali wa polisi kama mtuhumia wa mauji ya watu wawili.



**** ****

Maandamano makubwa ya kushinikiza Lord Brown anyongwe yaliibuka nchi nzima huku kundi kubwa la Raia wakiharibu mali za Lord Brown na mpaka wakti huo Tayri kasri lake lilikua limekwisha vamiwa na wananchi na Kazi za kufukua Mashimo yaliyoonekana kama yamepandwa miti na Tayari maiti za watu zaidi ya hamsini ambao ni vijana wadogo zilikua zimetolewa ndani ya Mashimo hayo. Kulingana na Sheria n kanuni za katiba ya Jamuhuri ya watu wa Kolo inayotengua haki ya mgombea kugombea iwapo atahusishwa na kesi ya jinai. Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo ilimuengua Lord Brown kugombea nafasi hiyo na kuipa nafasi mahakama kuweza kufanya maamuzi juu ya kesi inayomkabili. Huo ndio ukawa mwisho wa Lord Brown katika nchi hiyo na uchaguzi uliofuata ulimpitisha Ndugu Elibariki Chalambo kuwa rais wa jamuhuri ya watu wa Kolo na Wabunge wake wote. Katika miezi miwili ya mwanzo tayari Chalambo alikua keshajenga imani kubwa kwa wananchi wake huku akifanya uteuzi katika sekta mbalimbali za serikali. Suala kubwa lililokua likimuumiza kichwa ni jinsi gani ataunda baraza la mawaziri la serikali yake, Chalambo akiwa na mke wake Tclee katika ikulu ya Kolo walikua wakipata chakula cha jioni siku hiyo Chalambo alionekana kufikiria kitu Fulani kichwani mwake.

“Vipi mume wangu una shida gani mbona kama hauko sawa?”

Tclee alimuuliza mume wake huku akimuangalia usoni kwa umakini

“Ah usijali mke wangu kuna mambo yananichnganya si unajua ugeni wa huu uongozi”

Chalambo alimjibu mke wake huku akiendelea kula.

“Mumu wangu kumbuka mimi ni First Lady wan chi hii na unapaswa kunishirikisha kama naweza kukushauri”

Tclee alijibu huku akiacha kula na kumsogelea mume wake huku akimpapasa mgongoni.

“Ndio maana nakupenda sana mke wangu, Una akili sana, Najivunia kuwa na mke kama wewe”

Chalambo alimjibu mkewe huku akimshukuru kwa busu lililochoma papi cha mkewe kwa joto la kiume.

“Tatizo ni kuhusu wale watu walioniweka hapa, Wanataka niwachague kuwa mawaziri bila kujali uwezo wao katika hizo nafasi nahofia utendaji mbovu katika serikali yangu, Ukizingatia ahadi nilizotoa kwenye kampeni ni kubwa sana na sina budi kujitahidi zitekelezeke”

Chalambo alimwambia mkewe huku akionekana mwenye huzuni.

“Mume wangu unamkumbuka Mfalme suleimani wa kwenye Biblia?”

“Ndio kwani ana nini?”

“Je unakumbuka hadithi ya wale wanawake wawili waliokua wanagombania motto mfu na aliye hai”



“Ndio nakumbuka”

“Unakumbuka busara alizotumia Suleiman kuhakikisha anatenda haki kwa tukio lile”

Chalambo alinyamaza bila kujibu huku akimuangalia mke wake.

“Mbona umenyamaza je, Unakumbuka?”

“Ndio nakumbuka”

“Sasa nwe inakupasa uangalie pale ilipo haki bila kujali ni nani anadhulumu au kudhulumiwa, Kumbuka sasa wewe ni Rais tatizo lolote likitokea katika nchi utanyooshewa wewe vidole. Ni vyema kuwa na msimamo katika kila jambo na kwa sasa unaangaliwa na kila jicho, Ukigeuka kushoto wako Umoja wa mataifa, Kulia wako wananchi, Mbele yako wamesimama Umoja wa Africa na nyuma yako wamesimama wapinzani wako na kila mmoja anaangalia wapi utapindisha ili wapate cha kuongea, Simamia maamuzi yako mume wako, Umesahau wewe ni mwanaume”

Maneno ya Tcle yalimchoma Chalambo na kumuangalia mke wake huku akiwa haamini kile alichozungumza kitendo kilichopelekea kumkubatia kwa muda mrefu huku akimshukuru na kushukuru kwa mungu kwa kumpa mke mzuri na mwenye akili.

**** ***

Kikao cha siri cha viongozi wa The Revolution kilikaa zaidi ya masaa tisa huku malumbano yakiwa makubwa, N malumbano yakugombea madaraka ya katika wizara mbalimbali. Matajiri tisa wa L9 walikua wakimshinikiza Rais Chalambo kukubaliana na maamuzi yao. Moyo wa kizalendo wa Rais Chalambo ulipingana na maamuzi yale na kuzua mtafaruku mkubwa uliopelekea Rais Chalambo kutoka katika mkutano ule na kuwaacha matajiri wale peke yao.

Akiwa mwenye Hasira Mr. Ngwali ambaye kwa wakati huo alikua kateuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi wa nch hiyo alisimama na kutoa kauli iliyopokewa bila kupingwa.

“Huyu kijana hajui gharama tulizotumia kumuweka hapo alipo, Kwa kuwa mimi ni mkuu wa Majeshi,Tunapindua nchi iwe chini ya utawala wa kijeshi usiku wa leo na Mimi ndiye nitakua Rais na kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa”

**** ****



Maamuzi ya kuondoka katika kikao na kuwaacha Matajiri tisa wa L9 waliomuweka katika kiti cha urais yalimuumiza Chalambo wakati yupo njiani kuelekea ikulu, Amri ya kugwuzwa kwa gari ilipokewa na Dereva na tayari alikua anarudi katika kile kikao, Kiza cha matatizo ya mbeleni iwapo hatokubaliana na watu wale kilizidi kutawala mbele yake na tayari nafsi yake iliridhia kukubaliana na kile wanachotaka japokua upande wa pili nafsi ilikua ukimsuta ni kutokana na kauli za mke wake mpendwa Tclee.

"Nipo tayari kwa hilo mnalolitaka"

Ni sauti kavu iliyojaa ukakamavu huku akidhihirisha kile anachomaanisha. Makofi yaliibuka huku nyuso za matajiri wale zikipambwa ba tabasamu na tayari mgawanyo wa madaraka katika serikali ya Jamuhuri ya watu wa Kolo katika baraza la mawaziri ukipangwa kuhusisha matajiri wale katika wizara mbalimbali.



Baada ya makubaliano kufikiwa Siku iliyofuata Rais Chalambo alitangaza baraza lake la mawaziri huku akitoa mikakati ya kiutendaji kwa mawaziri wakati wa sherehe za kula kiapo cha utii chini ya katiba ya Jamuhuri ya watu wa Kolo. Hapo ndipo utawala wa kupangiwa ulipoanza huku matajiri wale wakitumia nyadhifa zao kurudisha mali walizopoteza katika kampeni na kujirundikia shehena ya mali katika benki mbalimbali nje ya nchi. Ubinafsishwaji holela wa viwanda na umilikwaji wa mali za umma ulifanywa bila mpangilio na Rais hakua na kauli mbele ya Matajiri wale.



Hali ilikua mbaya sana katika nchi ya Kolo, Huduma hafifu za kujamii zilididimiza uchumi wa nchi hiyo huku dhiki na njaa vikiongezeka maradufu, Kilio cha wananchi kilizidi huku wakilalamikia ukame na ugumu wa maisha. Matatizo hayakupungua huku maandamano ya mara kwa mara yakiibuka kila pande ya nchi hiyo. Kitendo kilichopelekea Rais Chalambo kuamua kuchukua maamuzi magumu yatakayogharimu maisha yake bila kujali kundi dogo la watu wanaomuendesha. Mkakati ulio kichwani mwake, Mkakati wa kuikomboa nchi chini ya Ukoloni wa wazawa, mi mkakati wa siku mpya ya uhuru wa nchi hiyo. Akilihutubia taifa na kuahidi kipindi cha siku tisini cha kutatua matatizo ya wananchi huku akiahidi kufanya mabadiliko makubwa ya serikali yake na kuondoa vikwazo vyote vinavyokwamisha harakati zake huku akionya wakati wa mafisadi kuwa ndani ya serikali umefikia. Kauli hiyo haikua na mantiki mbele ya L9 na waliamini ni maneno ya kisiasa kutoka kwa Rais Chalambo yenye lengo la kupooza kelele za wananchi dhidi yake.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Hapo ndipo siku tisini zilipotimia katika siku ya kutimiza miaka ishirini na moja ya uhuru wa Jamuhuri ya Watu wa Kolo na maamuzi yaliyo ndani ya kichwa cha Rais Chalambo yakapita na mwishowe Kiza cha milele kikatawala mbele ya macho ya Rais Chalambo na Mkewe Teclee na kwa maumivu kutoka katika mdomo ya Bunduki aliyobeba mwanadada Chiku. na Adhabu hiyohiyo ikawakabili L9 na mpaka wakati huo tayari nchi ilikua chini ya utawala wa kijeshi na Rais akiwa ni Koblo Chiku.



**** ****

hiku akiwa ndani ya ikulu ya Jamuhuri ya watu wa kolo alijikuta akipekua kila mahali huku akiwa kakamata bunduki yake aina ya SMG mkononi, Karatasi ya majina mbalimbali ilikua katika droo iliyo kwenye meza ya Rais, Jina la Abdul Azeez likiwa ni jina la kwanza huku likimtambulisha kama Waziri mkuu wa nchi hiyo, Hofu ikatanda na kugundua kuwa huyo atakua anajua siri ya ya kutaka kuteuliwa kuuwa waziri mkuu, Mawazo ya kumuua abdul azeez ndiyo yalikua yanaranda randa kichwani kwake. Akitoa Radio Call mfukoni na kuzungusha kitufe upande wa kushoto tayari Amri ya kuuawa kwa tajiri maarufu nchini humo si mwingine ni abdul azeez ilikua imetolewa.



**** ****

Kitendo cha Kukabiliwa na machafuko kwa nchi ya Kolo kilipokelewa kwa hisia tofauti ndani y nchi ya The African, Baada ya kushindwa kwa mbinu yao ya kupandikia Rais wao, Gia ya kusaidia kuokoa amani ya nchi ya Kolo kwa kutuma kikosi cha wanajeshi kupambana na waasi walioitek nchi chini ya Jeshi ikiwa inaongozwa na Koplo Chiku. Ndege za kivita zilivamia anga la nchi hiyo huku ndege nyingine zikitua katika ardhi ya nchi hiyo na kushusha vikosi vya wanajeshi. Jeshi la nchi hiyo linaloongozwa na Koblo Chiku liliingia vitani kukabiliana na Jeshi la The African waliopigana kwa mwamvuli wa ukombozi huku wakitumia ndege zao za kivita kusomba madini ya Gramnet. Chiku akiwa anaongoza kikosi cha anga tayari likua ndani ya ndege ya kivita akitumia mbinu za kijeshi kushusha ndege za kivita. Mabomu yalidondoshwa ovyo na kuua maelfu ya raia huku kundi kubwa la watoto wazee na wakina mama wakiathirika. Tayari katika njia ielekeayo nchi za jirani makundi makubwa ya Raia walikua wakikimbia nchi yao. Mchafuko yaliyoikumba nchi ya Jamuhuri ya watu wa Kolo yaliathiri sana na kusababisha mamia ya wananchi kuikibia nchi yao, Makundi makubwa ya wananchi wakiwa wamebeba mizigo yako vichwani, Wakiwa wamechoshwa kwa safari ndefu ya kuikimbia nchi yao, Tayari walikua katika msitu mkubwa wa Iranto msitu wenye simba wengi ambao umepakana na barabara kubwa inayoelekea mashariki mwa nchi ya Tanzania. Msichana mwenye umri wa miaka ishirini akiwa biguu peku bila viatu, Gauni lake lililochafuka na kuchanika kwa kuchanwa na vichaka vilivyozunguka msitu huo. Akiwa amekata tamaa bila kujua anapoelekea alikua ni mmoja kati ya watu waliokua wakiikimbia nchi ya Kolo. MAbomu yaliyokua yakidondoka na kuzalisha milipuko mikubwa ndicho kitu kilichomuongeza mwendo bini yule na kukatiza katikati ya vichaka akiwa anatafuta usalama wa kufika sehemu iliyo salama zaidi.



Vikosi vya wanajeshi wa Jeshi la Jmuhuri ya Kolo vilikua vimeweka kambi katikati ya msitu wa Iranto, Denis Chama ndiye alikua mkuu wa kikosi kile cha nchi kavu, Roho yake mbaya na uwezo wa kupambana katika vit vya nchi kavu ndicho kitu pekee kilichopelekea kukabidhiwa kikosi hicho, Wanajeshi wote walikua wakimuogopa kwa jinsi alivyokuwa mkatili. Akiwa ndani ya hema lake Huku akisubiri utekelezwaji wa kuletewa mwanamke mmoja kati ya wanajeshi wanawake walio katika kambi hiyo. Starehe ya kuwalazimisha wanawake kufanya ngono ndiyo alikua akiipenda sana. Wakati akisubiri anasikia hatua za mtu akipita pembeni ya hema lake, Kwa mwendo wa haraka huku bunduki yake ikiwa mkononi tayari kwa kukabiliana na Adui macho yake yanatua kwa binti mbichi aliye katika harakati za kuokoa maisha yake. Umbo lenye mvuto la bini yule lilimuhamasisha chama kutaka kumaliza haja zake kwa yule binti. Kama wafanyavyo watekaji tayari yule binti alikua kazibwa mdomo na kuingizwa kwenye tenti na nguo zake zikiwa zimechanwa mpaka chupi binti alikua akilia huku akijificha.

"Unaitwa nani"

Chama alimuuliza yule binti huku akiwa anavaa kondom

"Naitwa Tusmo"

Yule msichana alijibu huku akitetemeka

"Ok kuwa huru nataka unipe penzi halafu nitakuacha"

Chama alimwambia yule msichana huku akimsogelea kwa uchu

"Mimi sijawahi, naomba nisamehe"

Tusmo alijibu huku akisogea nyuma

"Hujawahi nini wewe?"

Chama alimjibu kwa dhihaki huku akiweka silaha pembeni

"Mimi bado ni bikira"

Tusmo alijibu kwa sauti ya chini

"Wewe Ni Bikiraaaaa!!!!"



Hakuna kitu ambacho alikua akiomba Mungu wake kila siku kama kumaliza chuo, Ndoto yake iliyo ndani ya Moyo wake ilikua ikimsukuma na kutamani ndege kutua katika uwanja wa JK Nyerere haraka ili mboni za macho yake ziweze kumuona yule ambaye hajaonana nae kwa muda mrefu. Sauti laini ya muhudumu wa ndege ya Gulf Air iliyokua ikitokea australia ilipenya katika masikio na kupokewa na kope za macho zilizobeba nyusi ndefu kufunguka na kuruhusu mboni ya rangi ya brown ya jicho la mtoto wa tajiri mkubwa jijini Dar es salaam kuweza kutazama. Mikono ikitekeleza maagizo kutoka kwa muhudumu yule tayari mkanda ukawa umepita katika mwili wake na kujiegemeza vizuri katika kiti chake tayari ndege kugusa ardhi ya jiji la dar es salaam.

akiwa kavaa shati la rangi hudhurungi lenye mikono mirefu, Suruali ya jeans ya kibuluu ilimfanya azidi kupendeza. Mkononi akiwa kashika ua rose la rangi nyekundu macho yake yalikua yakitazama mlango wa kutokea abiria katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu JK yerere, Macho yake yakagongana na Msichana mrembo akisukuma kitoroli chenye begi juu yake, Sauti ya shauku ikamtoka na kumstua yule binti.

"Neelam"

Neelam aliacha kile kitoroli na kukimbia akamkumbatia yule kijana

"Rajiv"

Walikumbtiana kwa muda kisha wakaachiana kila mmoja akimuangalia mwenzake kwa shauku.

"mai tume mis karathaho meri jaan rajiv" {Nimekumiss sana Rajiv}

Neelam alimwambia Rajiv huku akimuangalia machoni

"mai be mis kar raha ho jan a dea Neelam" {Pia mimi nimekumiss sana Neelam}

Rajiv alimjibu huku akimpa ua na kumsika mkono na kuelekea mahali ambapo wazazi wa Neelam walikua wamesimama. Kwa furaha Neelam akamrukia baba yake huku akimbusu shavuni.

"Kaise ho mai tik hu papaa" {Habari ako baba}

"Mai tik hu Neelam" {Nzuri sana Neelam}

Neelam akamgeukia mama yake huku kizidisha tabasamu

"Kaise mai tik hu maa" {Habari yako mama}

"Mai tik u" {Nzuri sana}

Mama yake akamkumbatia Neelam na kuelekea kwenye gari huku Rajiv akiwa kabeba begi.



**** ****



Denis Chama Hakuamini kile alichosikia kwenye masikio yake, Kwa wog akirudi nyuma na kumfungulia mlango wa tent Tusmo atoke nje, Tusmo hakuamini kama ni yeye anaambiwa atoke nje, Kwa tahadhari Tusmo alitoka nje na kukutana na wanajeshi watano wakiwa na silaha mkononi huku zimemuelekea yeye.

“Hapana msimdhuru”

Chama alitoa Amri iliyopokewa na wale wanajeshi kwa utii, Wakashusha silaha zao chini.

“Mpeni ulinzi huyu binti mpaka nje ya huu msitu kisha mumuache aende zake”

Chama alitoa maagizo yaliyopokelewa kwa utekelezaji na wale wanajeshi, Tusmo akiwa mbele huku wanajeshi watano wakiwa wanamlinda kwa nyuma. Chama akiwaangalia huku wakipotelea katikati ya miti mingi. Kutokana na mila ya kabila la wa kurdi kabila ambalo ni la kina Chama mwanamke ambaye ameweza fikisha umri zaidi ya miaka kumi na sita na bado ni bikira yeye ni malaika na mwnaume napaswa kumueshimu sana. Kitendo cha chama kugundua Tusmo ni bikira kilimstua sana na kujitolea kumpa watu wa kumsindikiza ili asidhurike na wanyama wakali walio katika lile pori. Tusmo akitembea kwa woga huku wanajeshi wakimfuata kwa nyuma wakiwa makini kwa chochote kinachoweza kutokea, Baada ya kutembea mwendo mrefu kwa takribani saa tatu Tusmo alianza kuchoka akaelekea chini ya mti mkubwa na kuketi chin yake. Wale wanajeshi walisimama mita chache huku wakivuta sigara, Tusmo akiwa mwenye wasiwasi huku akiwa kabana miguu ishara ya kubanwa na mkojo. mandhari ya kogofya yaliyo katika msitu ule yalimfanya kusindwa kwenda pembeni hata hatua moja. Maamuzi magumu ya kukojoa pale alipo ndiyo yalipita katika ubongo wake na kujikuta amekwisavua nguo na kuanza kukojoa. Macho ya mwanajesi mmoja yalitua juu ya mapaja ya rangi ya shaba ya binti mwenye mchanganyiko wa rangi ya kisomali na ki pwani. Muhemko wa ngono ukamkumba na kujikuta ameweka silaha yake pembeni kwa mwendo wa kunyata tayari alikua keshamfiki Tusmo. Sauti kali ya woga toka kwa Tusmo iliwashtua wanajeshi wengine wakaweka silaha zao tayari, Walichokiona hawakuamini, Msichana aliyenona akiwa hana nguo tayari mwenzao alikua kesamvua kwa nguvu, Wakiwa wamekubaliana kufanya ngono kwa zamu kwa kumlazimisha yule binti. Silaha zao zikiwa pembeni huku suruali zao zikiwa magotini mwanajeshi wa kwanza akiwa anamsogelea Tusmo huku Tusmo akirudi nyuma kwa woga atua zake zikaishia kwenye mti aliojigonga kwa nyuma na kujikuta yule mwanajeshi akiwa tayari mbele yake na mikono yake ikiwa inapapasa kiuno chake.



**** ****

Ilikua ni majonzi kwa mara nyingine ni baada ya Neelam kurudi toka Suleni australia huku akitegemea kupata muda mwingi wa kukaa na mpenzi wake Rajiv Roshan lakini ikawa Tofauti, Mapenzi liyokuwa nayo kwa Rajiv kutokana na uhusiano ulioko kati yake na binti ke Neelam Mzee Pandya mfanyabiashara na tajiri Mkubwa nchini Tanzania aliamua kumtafutia Rajiv kazi nzuri itakayomfanya aishi vizuri na mtoto wake piindi muda utakapofika watakapooana. Tayari Rjiv alikua kapata kazi katika sirika la kuhudumia wakimbizi la umoja wa mataifa kama mtunza kumbukumbu na afisa mawasiliano katika kambi ya wakimbizi iliyopo Jijini Mwanza, Kwa Heshima aliyokua nayo mzee pandya hakukua na muda wa kufanya usaili na Rajiv alitakiwa kuwasili kituo chake cha kazi na kuanza kazi.

Neelam akiwa uwanja wa ndege mchozi yakimtoka hakuridhika Rajiv kumuacha mwenyewe na yeye kwenda jijini mwanza.

“Mai tum se pyar karta hu Rajiv” {Nakupenda Rajiv}

Neelam alimwambia Rajiv huku akilia, Rajiv akiwa kamkumbatia kwa nguvu kwa sauti ya chini alimjibu Neelam masikioni

“Mai bi tum se pyar karta hu Neelam” {Nakupenda pia Neelam}

Neelam huku akilia alimkumbatia kwa nguvu Rajiv huku wakiahidiana mambo mengi.

“Rajiv Tum muj se shadi karoge?” {Rajiv utanioa?}

Neelam uvumilivu ulimsinda na kujikuta akiuliza swali lililotoka moj kwa moja katikati ya moyo wake, Rajiv kwa kujiamini alijikuta akimjibu Neelam kwa sauti kubwa.

“Hai mai eelam” {Ndio Neelam}http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Jibu lile lilimfanya mzee Pandya kutabasamu na kuwasogelea.

“I like your relationship, I will ask our Guru to protect you” {Napenda mahusiano yenu, Nitmuomba Mungu wetu awalinde}

Mzee Pandya aliwaambia wanae kisha wakaachiana Rajiv akaingia ndani ya uwanja wa ndege huku akimuacha Neelam akiugulia kwa maumivu. Kitendo cha kuiona ndege ikipotelea angani kilimuumiza sana Neelam na kumpelekea azidise kulia huku akiwaachia wazazi wake kazi kubwa ya kumbembeleza.



“I love you Rajiiiiiv” {Nakupenda Rajiiiiv}

Neelam alitamka kwa sauti kubwa mapaka watu waliokua wamesimama ple uwanja wa ndege wakamuangalia kitendo kilichopelekea baba yake kumshika na kumpeleka katika gari kwa nguvu.





ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog