Search This Blog

Tuesday, 1 November 2022

UMENIFUNGULIA DUNIA - 3

 








Simulizi : Umenifungulia Dunia

Sehemu Ya Tatu (3)





Kifupi hata nae alikuwa na kesi nae, alivyoona majibu ya Salama akajua kuwa anaweza kumueleza kinachomsumbua bila kuleta madhara. Hivyo kukataa kwake wala hakukumsumbua Anisa.

Vinywaji vilikwisha, muhudumu hakuonekana kabisa eneo lile,

Anisa akiwa ndio mwenyeji akalazimika yeye kunyanyuka kwenda kaunta, uso kwa uso na Mwinyi. Bila kujiuliza, Mwinyi akamvuta mkono Anisa aliekuwa amekunja sura akigeuza njia baada ya kumuona Mwinyi.

Moyoni Mwinyi alijihoji ni kipi kilichomkasirisha Anisa ikiwa ni yeye ndio alieingilia penzi la watu tena akiwa anajua.

“Samahani Anisa naomba kuongea nawe kwa dakika 3 tafadhali,”

“Sina muda,” bado Mwinyi aliendelea kumshika mkono hadi Anisa aipotoa sauti ya kero

“Niache bwana, we vipi?” hakumuacha, aliendeea tu kumshikilia

“Anisa sikuazimishi kuongea nami, bali ninaomba unisikilize shida yangu, hata usiponijibu, sawa ila tu niwe nimekwambia,” aliomboleza Mwinyi

“Haya sema haraka haraka, kuna mtu ananisubiri kule kwenye bembea,”

Mwinyi alishukuru kwa kupata nafasi ile na kiukweli aliitumia vema kumuomba msamaha kwa yale yaliyotokea siku iliyopita na pia akamuomba amsaidie kumuombea msamaha kwa Side mpenzi wake na pia Ramlat na mama yao.

“Umeona hao tu ndio uliowakosea? Salama je hastahili...” Mwinyi ambae muda wote huo alikuwa bado amemshika mkono, akamuachia na kumzuia Anisa asiendelee kuongea, akasema

“Hapana hapana Anisa, nampenda sana Salama na hata sijui nitampata wapi binti wa watu kwani sijui yupo katika hali gani?”

“Nyoo! Wakati unafanya madudu yako uikuwa unategemea nini? Halafu kwanini hujatulia wakati una mwanamke mzuri kuliko wote uliotembea nao? Huoni ni kumdhalilisha? Hata kama ningekuwa mie ndio Salama, nisingekusamehe baradhuli mkubwa we!”

“Sawa tu Anisa, unaweza kusema tu chochote ambacho moyo

wako unakiona kipo sahihi, lakini moyoni mwako hata wewe unajua,”

“Mi najua nini?” Mwinyi akamkumbusha jinsi ambavyo yeye Anisa alivyomtega na kumuingiza kwenye anga zake

Akamweleza kuwa hata wale wengine wote kila mmoja alimuingiza kwenye anga zake kwa style tofauti. Kama alivyoshindwa kukwepa vituko vyake, pia kwa wale wengine, pia alikwama kabisa.

“Hata hivyo Anisa, najutia yote nliiyoyatenda, naomba wewe uwe wa kwanza kunisamehe tafadhali,” akapiga magoti mbele ya Anisa.

Kauli za Mwinyi zilimuingia sana Anisa na kumwambia yeye binafsi amekubali kumsamehe, ila kwa wengine hajui itakuwaje, maana hawezi kuisemea mioyo yao. Pande zote mbili pale Nyati Pub, yaani ndani ya Bar na kule kwenye bembea, kila mtu alikuwa akimsubiri mwenzie.

Salama aikuwa akimsubiri Anisa, Mgasi nae alikuwa akimsubiri Mwinyi. Kama walioambiana vile, Mwinyi na Salama kila mmoja akanyanyuka pale alipokuwepo ili kwenda kujua ni kipi kimemsibu Yule aliekwenda nae.

Mtu wa kwanza kuwaona alikuwa ni Mgasi akawasogelea pale walipokuwa wamekumbatiana. Waliachiana baada ya kumuona Mgasi akiwakaribia. Mwinyi akamtambulisha Mgasi kwa Anisa kama rafikie. Wakasalimiana na kufurahi kukutana kwa mara ya kwanza.

Anisa akamuomba Mwinyi palepale aende sehemu fulani na ndani ya dakika 5 atakuwa amerejea. Mwinyi akamuelekeza sehemu walipo na kumwambia awakute pale. Anisa akajibu poa na kuinama kuchukua makopo ya soda aliyokuwa ameweka chini.

Wakati Anisa kainama bado, Mgasi akambinya Mwinyi na kumnong’oneza

“Enhee Mwinyi, usigeuke kihasara hasara, tulia hivyo hivyo kile kifaa

bubu nilichokwambia kinakuja hukuhuku,” akatikisa kichwa na kusubiri bila kugeuka, Anisa ndio akaanza kuondoka. hatua moja mbele akamuona Salama.

Aishtuka sana Anisa, maana hakutegemea kumuona Salama pale, akamuuliza vipi mbona yupo kule?

“Nimeona umechelewa na simu yako ina missed calls 3,” sauti Mwinyi aliitambua, uzalendo ukamshinda, akageuka na kumuona Salama aliekuwa busy na maongezi na Anisa.

“Ha! Salama...” Mwinyi aliita huku akimsogelea, Mgasi alishangaa, hata huyu anamjua?

Anisa nae alipopewa simu, kutokana na kuchanganyikiwa kwa kumuona Salama kwa ghafla, akajikuta ameipokea simu na kuiweka mfukoni kwenye jeanz aiyokuwa ameivaa bila hata kuangalia ni nani aliepiga.

Sauti ilimshitua Salama, nae hakutegemea kukutana na mtu anaemjua pande zile. Akamuona Mwinyi akimkaribia, yeye Salama akapeleka

macho kwa Anisa na kumuuliza

“Kwa hiyo ndio umenileta kunikutanisha na huyu Mzandiki eti Anisa?” Anisa alikuwa akikanusha kwa kichwa tu, maana alishindwa kabisa kunyanyua sauti yake, Mwinyi akamsogeea Salama na kumpigia magoti.

Sasa ndio mshangao wa Mgasi ukawa hadharani, akakubali kweli Mwinyi ni fundi kwa hawa viumbe, alikuwa akimsikia tu Salama, kumbe ni bomba kiasi hiki? Jamaa yangu ana haki ya kuchanganyikiwa.

Kwa kushirikiana Mwinyi, Mgasi na Anisa, hasa baada ya Mwinyi kuelezea chanzo cha tukio ile, ambacho Salama alikiri kuwa na taarifa hizo kupitia kwa Mwinyi aliekuwa akimueeza matukio mengi yaliyokuwa yakitokea.

Walijitahidi sana kumshawishi Salama kumsamehe Mwinyi kupitia kipengele hicho. Bado ikawa haitoshi kumrudisha kuwa mpenzi wake, walifanikiwa kumshawishi amsamehe tu.

Hivyo akaagwa kimapenzi japo msamaha amepewa, lakini kwa

mapenzi akaambiwa asahau.

Katika maisha yake ya kimapenzi, Mwinyi hakuwahi kumlilia msichana yoyote, ila kwa siku hiyo akiwa amepiga magoti, amekumbatia miguu ya Salama, alimwaga machozi hadharani, akamtazama usoni Salama na kumuuliza

“Sasa huo ni msamaha gani Salama? Kumbuka nami ni binadamu wala si Malaika, hivyo ninatenda makosa na ninapaswa kusamehewa, mbona wanitesa Salama? Nisamehe!”

Salama aijitahidi kumsukuma lakini alishindwa, Mwinyi akamwambia kama hamtaki, basi ni heri amchome tu kisu cha moyo ili afe kabisa na atoweke Duniani.

Ukali wa maneno ya Mwinyi, uliulainisha moyo wa Salama. Nae chozi likamdondoka.

Akamnyanyua Mwinyi na kukumbatiana wakitokwa machozi, Salama akamwambia Mwinyi kuwa amemsamehe bila sharti lolote. Wakaondoka pale walipokuwa hadi kwenye meza waliokuwa wamekaa Mgasi na Mwinyi.

Walikaa pae hadi saa 3 usiku kisha ndio wakaondoka kuelekea katika nyumba mpya anayokaa Mwinyi palepale maeneo ya National ambapo ni njia ya kuelekea Bachu anapokaa Anisa. Hawakukaa sana, wakaaga. Salama aliahidi kwenda siku ifuatayo, wakakiss kisha wakaondoka Anisa akiwa kwenye usukani.

Muda wote Anisa ndani ya gari alikuwa kimya, japo alishiriki kuwapatanisha lakini hakupenda jambo hilo kutokea. Hiyo ndio sababu iliyomfanya akonde ghafla na kuwa mdogo mdogo.

Wakati wakirejea nyumbani, Anisa ndio akakumbuka kuwa kuna missed calls kwenye simu yake, zilikua ni za Side, akampigia. Side alipokea hali ya kuwa akilia, aipomuuliza tatizo, akamjibu kuwa mama yao amefariki ghafla saa 1 jioni kwa presha

Anisa alishindwa kuendesha gari na kuipaki pembeni, akamjulisha Salama juu ya ile simu aliyopiga, akabaki na mshangao, ila kwa kiasi Fulani yeye alibaki na nguvu wakabadiishana na Anisa, Salama akashika usukani, akaelekezwa hadi msibani.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Walikaa sana na Anisa aliekua akilia kwa majonzi sana, hadi usiku mnene kisha wakarudi kwao, wakiwa njiani ndio wakampigia simu Mwinyi kumpa taarifa za msiba ule. Aisikitika sana ila alipotoa wazo la kwenda msibani wote walimpinga vibaya sana kwa usalama wake.

“Tena Mwinyi kibaya Zaidi Salome nae kalazwa hospitali kwa kujaribu kutoa mimba yako, hivyo mumewe japo wamehama tangu mchana, lakini najua atakuwepo msibani lazima, kwa ajili ya kukusaka wewe, maana bado ana hasira sana na wewe,” Aliongea Anisa kama taarifa tu, kisha Salama akamuomba simu na kuongezea

“Unaona matokeo ya matendo yako Mwinyi?” Aliuliza Salama kwa sauti ya amani kabisa.

Kulikuwa hakuna jawabu zaidi ya majuto tu, nao wakalielewa hilo, walikuwa wakipokezana simu. Sasa akaichukua Anisa na kumtoa shaka Mwinyi. Alimpoza na kumwambia awe makini sana kwa sasa.

Simu akamrejeshea Salama ambae alimuaga na kumwambia kesho wakitoka mazishini jioni, wataelekea huko kwake, awasubiri wala asitoke, akakubali haraka haraka na kuahidi kuwepo, wakaagana, kulikuwa hakuna kiss, walisha changanyikiwa.

Usiku wa pili mfululizo ukawa ni mgumu kwa Mwinyi, ikamlazimu tena kumwamsha Mgasi kwa simu na kumueleza kila kilichotokea

“Mgasi ndugu yangu najuta mwenzio, sitokaa nikasahau siku hizi mbili za mateso makubwa kwangu, naapa kwa Mungu mmoja, mimi sintorudia tena” Mgasi akamtuliza na kumpa moyo, pia akamuasa kuwa makini na akamshauri kesho aombe ruhusa kazini asiende. Wakakubaliana hivyo na kukata simu wakalala.

Mazishi yalifanyika kama ilivyo pangwa na baada tu ya mazishi

watu wakatawanyika, muda huo Mwinyi na Salama ndio waliutumia kwenda kwa Mwinyi. Bahati yao ilikuwa njema, maana walimkuta na Mgasi kulekule. Waliwakarimu vizuri sana.

Mwinyi bado alikuwa na hamu ya kutaka kujua sababu iliyopelekea kifo cha Mama Ramlat, Anisa ndio akamueeza baada ya yeye kuondoka, Salome nae akatoka kwenda hospitali ili kujaribu kuichomoa ile mimba, nyuma huko mumewe akaja na gari na kuhamisha kila kitu cha ndani.

Kule hospitali, dakatari akashindwa kuichomoa na hali ya Salome ikawa si njema. Nesi mmoja kati ya wale waliopo pale hospitali, ambae yeye aionekana kupinga tangu awali kufanyika kwa zoezi lile pale hospitali, akavujisha siri. Hivyo daktari akakamatwa na kuswekwa lupango.

Hivyo askari wakaelekea nyumbani kwake kumtafuta mumewe Salome ambae hawakumkuta

“Ilikuwa ni bahati tuseme, ila sijui kama ni nzuri au mbaya, jamaa hakuwepo maana tayari aikuwa ameisha ondoka na gari, mama akaanza kuhojiwa kawaida tu na askari, si ndio presha ikampanda? Hasa pale Side alipoitwa na kukataa kuja kwa kusema wayamalize wenyewe” alimaliza Anisa kuhadithia.

“Mwinyi unazibeba lawama kwa kiasi kikubwa sana wewe kwa jamii

nzima inayojua suala hilo, lakini mi binafsi lawama nazishusha kwa Side, kwanini akatae wakati alipoitwa?”



Mwinyi alielewa sasa chanzo ni nini, alibaki kusikitika bila kujua ni nini cha kufanya, moyoni aliona kama anahusika kwa kiasi kikubwa juu ya kifo cha Mama Ramlat, lakini alijipa moyo kuwa muhusika mkuu atakuwa ni Side kwa kuwa alikataa kuja wakati alipoitwa na ndio amepelekea kifo cha mama yake.

Walikaa hadi muda wa Magharibi ndio Anisa akaomba ruhusa arudi kwao, Mgasi nae akaungana nae kwa kutegemea lift pale. Wakawaruhusu na kuwashindikiza hadi garini, dereva akiwa ni Anisa, Mgasi akakaa kushoto.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Safari iianza kimyakimya kia mmoja akiwa ana yake kichwani mwake, Mgasi alikuwa anashindwa kabisa kuisoma bahati aliyokuwa nayo Mwinyi, aliamini Mwinyi ni mtu mwenye bahati sana ya kupendwa, ila aliona kabisa kuwa, huyo mpendwaji ndio hayupo. Aliguna tu ndani ya nafsi yake.

Wakati yeye akiwaza hayo, Anisa aikuwa na siri kubwa sana moyoni mwake, siri ilioutesa moyo wake aikuwa hajaitoa bado, alitamani sana kuisema, lakini alijizuia, maana hakumuona wa kumwambia lakini sasa ilikuwa ikimtesa sana, aliazimia sasa kuitoa, alihofu kama ataendeea kuificha, ipo siku itamuumbua.

Sasa alitamani awe huru kabisa na ili itimie hilo, ni lazima siri ile aitoe, naam iwe si siri tena, ni lazima mtu mwingine ajue, sasa mtu huyo ni nani? Hapa ndio palipomuumiza kichwa, aipogeuka kushoto akamuona Mgasi kama mtu alie mbali na fikra zake, hakujiuliza mara mbili, akaona huyu ndio mtu anaemfaa. Anafaa kabisa kuijua siri ile na hapo atakuwa amepata tiba ya kile kinachomsumbua.

Akasimamisha gari pembeni bila kumwambia lolote Mgasi. Na kuegamia Sterling. Mgasi akishangaa na kuhoji kulikoni? Anisa akanyanyua kichwa na kumuomba amsikilize, akapunguza sauti ya radio ya gari na kumtaka amtunzie siri atakayompa.

Mgasi akatikisa kichwa na kuketi vizuri garini na kumsikiliza kwa umakini. Anisa akafunguka, hakika aliongea kwelikweli, tangu kumjua Mwinyi kupitia Ramlat hadi yeye Anisa kujilengesha na kufanya nae mapenzi kwenye gari.

Tayari yale wala haya kumshangaza maana alikuwa akiyajua kwa kuhadithiwa na Mwinyi

“Mgasi kile kliikuwa ni kitendo kibaya sana kwangu, kwani ilikuwa ni kuwasaliti ndugu wawili kwa mtu mmoja na kwa wakati mmoja, nilimsaliti rafiki yangu Ramlat na mpenzi wangu Side na hata kwa upande wake Mwinyi ilikuwa ni kumsaliti Salama, japo yeye siwezi kumlaumu, maana nilimtega” Mgasi akabaki na mshangao, kumbe alijua ni makosa sasa kwanini alitenda?

“Kibaya zaidi kaka yangu, nimetokea kumpenda sana Mwinyi..” Alimkatiza Mgasi kwa swali la mshangao.

“Nini?” Hii haikumfanya Anisa abadili msimamo wake, bali akahoji kwa kujiamini

“Mgasi, sijui hapa utanisaidiaje?” Mgasi akashusha pumzi kwa nguvu na kuuliza

“Anisa, Side je?” bila hata ya kujifikiria Anisa akajibu kama kwamba ni mtu ambae alikuwa na jibu tayari.

“Achana nae huyo, hana tena nafasi kwangu, hebu tumzungumzie Mwinyi, ndio alietukutanisha mie nawe”

Mwinyi akaomba poo kwanza, akataka muda wa kufikiri ii amshauri nini afanye au nini aache, Anisa alishukuru, maana aliona kama mzigo wake tayari ameisha utua. Wakapeana namba za simu kisha wakaondoka hadi kwa Mgasi akashuka garini na Anisa akaelekea kwao akiwa na amani kiasi fulani kwa kuutua mzigo ule.

Anisa alipofika kwao akawaambia kuwa Salama ameonana na mjomba wake ambae alipoteza mawasiliano nae na leo wamekutana msibani kwenye kikao, kumbe hata nao wana uhusiano na kina Ramlat. Hivyo ndivyo walipanga akifika kwao adanganye. Wazee wake wakaridhika, hasa pale siku yapili alipokuja kuaga na kubeba mizigo yake.

Salama alikaa kwa Mwinyi kwa muda wa siku 3 na kurejea jijini Mwanza kuendelea na maisha yake akimuasa Mwinyi kutokufanya kosa lolote lile. Mwinyi akaahidi hivyo, tena ni kwa dhati kabisa toka moyoni.

Mgasi alishindwa kabisa kutoa ushirikiano wowote kwa Anisa, kila mara alimwambia subiri. Anisa alitokea kumwamini sana Mgasi, hivyo aliendelea tu kusubiri akitegemea huenda Mgasi hajapata nafasi ya kukaa na Mwinyi na kuongelea juu ya jambo hilo.

Wiki moja baadae, Anisa alikwenda kwa Mwinyi na gari huku akilia na kumwambia kwamba ile ilikuwa ni siku ya tatu Ramlat hajaonekana kwao, wamemtafuta kila sehemu hawajafanikiwa kumpata. Ndugu, jamaa na marafiki wote hawajui ni wapi alipo, na kinachowaumiza sana ni hali ya ujauzito aliyonayo.

Mawazo yakamvaa tena Mwinyi, bado aliendelea kuamini yeye ndio chanzo cha maumivu yale yote kwa wengine, alijua kuwa matatizo yote yale kuanzia kifo cha Mama Ramlat hadi kutoonekana kwa Ramlat, yeye ndio muhusika namba moja.

Side alimpigia simu Anisa na kumuuliza wapi alipo, Anisa akamwambia yupo njiani anatoka Cheyo anaelekea nyumbani kwao, Side akamwambia muda ule yupo Polisi, lakini nae anarejea nyumbani, atakapofika kwao anaomba waonane, Anisa akamkubalia na kumwambia atakwenda.

Akiwa bado ametawaliwa na mawazo kedekede, Mwinyi simu yake ikaita, namba ilikuwa ni ngeni na tena ni ya mezani. Aiipokea kwa kujiamini na kujuishwa kuwa pale ni kituo cha polisi kati, anahitajika mara moja na kuombwa kufika kwa mahojiano mafupi. Alishindwa kuhoji lolote, akaitika tu kwa heshima kukubali.

Baada ya simu kukatwa upande wa pili, alitaka kukimbia. Ila kwa ushauri wa Anisa akamwambia atamsimamia yeye kwa kila kitu, wakaondoka kuelekea kituoni kwenda kuhojiwa akiwa hajiamini kabisa.

Walimpigia simu Mgasi na kumuomba afike kituoni akiwa na kitambulisho, waliamini inawezekana akang’ang’aniwa hadi apatiwe dhamana. Mgasi hakukataa, akawaahidi baada ya muda mchache watakuwa pamoja nae.

Mwinyi alikiri kuwa yeye ni muhusika wa mimba ile na hadi muda ule mawasiliano na Ramlat hakuna, hivyo hata sasa hajui ni wapi anaweza kuwa Ramlat amekwenda, askari walimuelewa na kumtaka ajidhamini mwenyewe ila muda wowote watakaomuhitaji afike kituoni bila kukosa.

Akatoka nje na kuwakuta Anisa na Mgasi wamesimama pembeni ya gari wakimsubiri, aliwaona na kuwasogelea, wakaingia garini na safari yao ikaishia nyumbani kwa Mwinyi. Waliagiza chakula cha mchana na kula palepale nyumbani huku wakitazama TV Hadi Mwinyi aipomkumbusha Anisa juu ya wito wa Side.

Anisa akanyanyuka na kuwaaga, Mwinyi akamshindikiza hadi nje. Kule nje Anisa akajitutumua na kumuuliza Mwinyi kama amepata ujumbe wake toka kwa Mgasi

“Ujumbe gani Anisa?” aliuiza Mwinyi huku akimtazama machoni

“Ujumbe wowote tu unaonihusu mie toka kwa Mgasi?”

Mwinyi akakataa na Anisa akamwambia basi akirudi ndani aende akamuulize, kisha akaingia garini na kuwasha gari akaondoka

akimuacha Mwinyi akimtazama anavyoendesha gari kwa kasi.

Mawasiliano kati ya Mwinyi na Salama yakaendelea kwa kasi sana. Wakati huohuo tayari Mgasi aliisha fikisha salamu za Anisa kwa Mwinyi, Mwinyi hakuzipa nafasi kabisa. Hali ile ilisababisha Anisa ajiapize kumpata Mwinyi awe wake jumla jumla, kitu ambacho kiikuwa ni kigumu mno.

Baada ya taabu nyingi na mashaka mazito, Anisa alifanikiwa kumtia Mwinyi mikononi mwake kwa ahadi ya kuwa penzi lao itakuwa ni la kificho. Waliibana kweli, Mgasi alijuishwa kila kitu na Mwinyi mwenyewe

Mgasi alijaribu sana kumkanya Mwinyi, lakini hakumsikia kabisa. Huku nako upendo wa Salama kwa Mwinyi ukawa umerejea kabisa kama awali, alijitahidi kumtembelea kila alipopata nafasi kwa miezi mitatu tangu kutokea tukio lile.

Matukio yale yalikuwa yakimuumiza sana Mgasi kutokana na uzuri wa Salama na matendo anayofanyiwa, ilimkera sana. Aliendelea kumuonya Mwinyi juu ya tabia hiyo, lakini haikusaidia.

Siku moja usiku akavunja ukimya, akamueleza Salama kila kitu kinachoendelea kati ya Mwinyi na Anisa. Salama hakuamini kabisa akahisi kuna kitu hapa au wanataka kugombanishwa. Kilichomchanganya zadi ni ile hali ya Mgasi kutangaza nia.

Alimbadilikia na kumtukana kweli kweli na kumuonya kutorudia tena kumpigia simu na kumpa maneno ya kijinga kama yale. Mgasi akacheka na kumwambia

“Naomba Jumamosi ijayo uje ghafla bila ya kutoa taarifa na uingie kwa Mwinyi jioni, utakayoyaona huko usinitaje, sawa?”

“Siwezi kufanya kitu cha kipumbavu kama hicho, chukua hamsini zako na kama vipi wewe nipotezee” akasonya na kukata simu

Mwinyi akaitazama simu yake na kucheka.. kukatika simu ile ndio kukampa nafasi nzuri Salama kutafakari juu ya yale aliyoambiwa na Mgasi. Alifikiria kwa undani akaamua ni heri afanyie uchunguzi yale yasemwayo.

Moyoni aliendelea kujiambia mwenyewe...

“Ikiwa si kweli, nitamtukana sana Mgasi na nitamueleza mwinyi kwamba hana rafiki, aachane nae mara moja” akataka kulala, nafsi ikaendelea kujiuliza..

“Na je ikiwa ni kweli nami ndio tayari nimeisha mtukana kaka wa watu, nitafanya nini? Si itakuwa ni aibu kwangu?”

Akapanga kufanya kama alivyoshauriwa na Mgasi na kusema iwapo atakuta si kweli, ataonekana kaenda kumuona mpenzi wake, na ikiwa ni kweli, basi siku hiyohiyo ndio itakuwa Mwisho wa penzi lao hapohapo

“Safari hii nikimfumania, sitasikiliza la mtu yeyote, hata washuke Malaika wa peponi, sitakubali, na ole wake Mgasi iwe uongo..” akavuta shuka akalala.

Zaidi ya miezi mitatu sasa tangu Ramlat atoweke, hakuna ajuae yupo wapi. Nyumbani kwao pamegeuka kuwa ni nyumba ya ndugu zao tu, maana hata Side nae ameisha ondoka na kuelekea anapopajua mwenyewe, familia imesambaratika kabisa.

Mwinyi siku hiyo akiwa na Anisa alimwambia kuwa anatamani kumuona Ramlat, Anisa akamwambia hata nae ana hamu sana ya kumuona wifi yake wa zamani ambae kwa sasa ni kama mke mwenzake, wakaanza kucheka wenyewe wamejiachia chumbani.

Hakuna aliekuwa akijua ni nini kilichokuwa kinafuatia mbele yao. Walikuwa pamoja tangu asubuhi na wakati huo Salama alikuwa ameondoka Mwanza kuelekea Tabora bila kumwambia mtu yoyote.

Saa 6 mchana Salama aliwasili Tabora mjini kwa basi la Unique. Akafikia Bachu Guest jirani na kwa kina Anisa ila hakufika hata kuwasalimia, alipanga ataenda siku ifuatayo kama mambo yatakuwa ni shwari.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Jioni akakodi pikipiki iliompeleka moja kwa moja hadi National kwa Mwinyi. Aifika na kulipia, kisha akasogea. Nje ya nyumba aliweza kuiona gari ya Anisa. Hakushtuka maana anajua kuwepo pale Anisa si tatizo, bali tatizo aliliona mara tu alipoingia ndani na kukuta nguo ya kike katika sofa.

Nguo hiyo aliiona mara tu alipofungua mlango mkubwa wa barabarani ambao uikuwa haujafungwa bali ulirudishwa tu, akaitazama kwa mbali akiwa amesimama bado pale mlangoni na kuamua kuisogelea aione.

Aliichukua na kuiangalia kama anaijua, hakuweza kuitambua.

Akaitupa chini na kuelekea chumbani akiwa na tahadhari.

Alipoukaribia akajiuliza kama aufungue ama agonge. Akaamua

kuchungulia kwenye Tundu la funguo pale mlangoni. Aliweza kuona kilichokuwa kikiendelea mle chumbani.

Alisogea pembeni na kuanza kutembea huku na kule akiwa haamini kama ni kweli anachokiona ama anaota. Akaigiza vidole vyake kichwani mwake kwenye nywele zake zilivyokuwa zimetengenezwa vizuri, akazivuruga vuruga kwa hasira

Roho ilimuuma sana, aishindwa kufanya chochote, akaegamia ukuta akilia kawa sauti ya chini na kurudi kukaa kwenye sofa kivivu kabisa huku akilia kwa kusalitiwa. Akapata ujasiri na kunyanyuka kwenda kufungua mlango.

Mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani, akaupiga ngumi huku akilia kwa sauti ya kawaida sana na kuuegemea akikaa kwa kutereza ukutani mikono ikiwa kichwani. Ndani wakashtuka, Mwinyi akaja na kufungua mlango akiwa na jazba ni nani anagonga mlango kwa nguvu kiasi kile.

Kabla hajatoka akaitwa na Anisa na kumkiss, akamrudisha kitandani kisha yeye ndio akachukua khanga yake na kujifunga kifuani, akaenda mlangoni na kuufungua, alichokiona Anisa alitamani afe palepale.





**********



Kitambo sana Joy amepotezana na Victor hawajaonana, maana ni tangu Salama alipoachana na Victor, Victor nae akahamia Kahama. Siku hiyo wakiwa ugenini Shinyanga bila kutegemea walionana

Walifurahi sana kuonana tena ugenini wakati kila mmoja akiwa na mishemishe zake. Waliongea kwa takriban dakika 5 hivi na kupeana namba bila kumuongelea Salama, mwisho ndio Victor akataka kujua alipo Salama. Joy akamwambia kuwa Salama yupo tu.

“Vipi ameisha olewa?”

“Hapana bado yupoyupo, anakusubiri wewe, ama mwenzie umeisha oa?” alichomeka Joy

“Dada Joy mimi sijamuona wa kumuoa zaidi ya Salama. Ni yeye pekee ndie niwezae kumuoa, tofauti na hapo, siwezi kumuoa mwanamke yoyote dada Joy” Joy akishangaa

“He! We Victor kwanini sasa?”

“Dada Joy nimejaribu kukaa na wanawake wa3 tangu niipoachana na Salama lakini mwisho wake nimetengana nao wote, naamini hawakunipenda kwa dhati bali kuna kitu Fulani walikifuata kwangu,”

“Sijakuelewa kaka Victor,”

“Ni kwamba, mimi kwa sasa nina kila kitu kinachotakiwa kuwa nacho mwanadamu mwenye maisha ya kawaida, namaanisha nina gari, nyumba, sehemu za biashara, kazi nzuri na mfano huo, lakini kuna kitu kimoja tu nakikosa, furaha...”

“Sasa unakosaje furaha ikiwa nzwe una kila kitu?” aliuliza Joy huku akimtazama

“Furaha inatakiwa itoke kwenye moyo wenye upendo, upendo unaanzia nyumbani kwa mke mwenye mapenzi ya dhati, sasa huyu ndio nimemtafuta kwa muda mrefu sana nia sijafanikiwa kumpata” aiongea Victor kwa hisia kali.

“Victor bado hujatafuta, lakini kwani una haraka gani? Fanya subira kaka yangu,”

“Dada Joy, umri ni kitu kinachokwenda, nimetafuta sana mwanamke atakaenifaa, wapi dada yangu na kila nikiangukia mapenzini, naambulia maumivu tu, ndio maana ninamkumbuka sana Salama, Salama ni kila kitu kwangu, Joy nikutanishe nae tafadhali,”

Huruma ilimuingia Joy na kuahidi kumkutanisha nae midhali tayari ana namba yake, siku chache zijazo atawakutanishahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Ila Victor jambo la msingi zaidi ni kuwa hewani muda wote,”

“Usijali, simu yangu siizimi hata nikiwa kanisani, muda wowote dada yangu we nipigie tu,”

“Poa!” wakaagana, Joy akapanda Taxi kwenda kwenye mishemishe zake na Victor akaingia ndani ya gari lake nae akaelekea kwenye shughuli zake.

Mtu wa kwanza kutoka chumbani alikuwa ni Anisa, alipomuona Salama hakuamini, alitetemeka nusura ya Khanga aliyojifunga imuanguke, Salama alinyanyua shingo na kumtazama Anisa bila kumsemesha lolote, bali alisimama na kuzidi kumtazama kwa ghadhabu, ni kama alitamani kumrukia.

Jicho Salama aliomkata Anisa, lilimsababisha arudi nyuma hatua kadhaa, kitu kilichomshitua Mwinyi na kuuliza kulikoni? Huku akinyanyuka kitandani. Salama aliweza kuzidhibiti hasira zake alizonazo na kushusha pumzi kisha akasema neno moja tu...

“Samahani!” kisha akageuka na kutoka kasi. Mwinyi aliweza

kumuona Salama akimalizikia mlangoni kuelekea nje.

Alihisi kuchanganyikiwa akatoka mbio kifua wazi kumkimbiza, lakini wakati yeye akifungua mlango aliweza kumuona Salama

akisimamisha pikipiki, akapanda na kutokomea mbele huko.

Mwinyi akapagawa kabisa, Anisa ndio haisemeki, wakaketi sofani wakiwa pamoja lakini kifikra, waikuwa mbalimbali kama umbali wa Mbingu na Ardhi kila mmoja akili yake ilikuwa mbali sana, wakati akili ya Mwinyi ikiwa inawaza hiki, na ile ya Anisa ilikuwa ikiwaza kile, hawakuwaza kitu kimoja.

Walijiona ni wakosefu sana na kujutia matendo yao japo kwa muda ule haikusaidia. Kimya kiliwatawala kwa muda mfupi kabla ya kuvunjwa na Anisa aliemwambia Mwinyi amrejeshe kwao. Mwinyi aligoma kabisa kutoka ndani ya nyumba ile kwa siku ile Anisa nae akamwambia Mwinyi kuwa, hawezi kuendesha gari muda ule, kwani amepoteza uwezo wake na akilazimisha atasababisha ajali. Mwinyi hakuhangaika hata kumjibu, alikaa kimya tu maana akili yake wala haikuwa pale.

Salama huku akilia kwa majuto, alimuelekeza dereva wa pikipiki hadi kule Guest alipofikia, akamlipa na kuingia ndani. Alijifungia mlango wake chumbani na kuanza kutafakari juu ya kile aichokiona ni kweli ama ni ndoto. Alisikitika sana na kujilaumu sana juu ya kile kitendo chake cha kumtukana Mgasi.

Kama si Mgasi kumueleza juu ya uwepo wa jambo lile daima Salama asingejua, maana mara kwa mara alikuwa akiwasiliana na Anisa kama vile wifi yake, akaamua ampigie simu Mgasi.

Aliitafuta sana namba ya Mgasi ili ampigie simu na kumuomba radhi kwa maneno makali aliyo mwambia, lakini hakufanikiwa kuipata.

Maana tangu siku ile ya ugomvi wao wa kwenye simu aliifuta, sio kwa bahati mbaya, bali alikusudia. Leo alikuwa akijilaumu kwanini aliifuta, hakuwa na jinsi tena, akakubali matokeo.

Muafaka baina ya Anisa na Mwinyi ukapatikana, Anisa akaamua kuacha gari pale na kuahidi kulifuata siku ifuatayo, Mwinyi wala hakukubali wala kukataa, alikuwa kama sanamu, kichwani aliamini kabisa sasa Salama ndio kwaheri. hatompata tena. Anisa akamuaga na kutoka bila kuitikiwa.

Upweke mkubwa ulioandamana na Majuto, ulimvaa Mwinyi, akachukua simu yake na kumpigia simu Mgasi kumuelezea yote yaiyotokea pale. Masikini.. hakujua kuwa yule ndio sterling wa picha lote.

Mgasi alimsikiliza tu muda wote bila kumjibu lolote, Mwinyi akaanza kulalamika kuwa Mgasi siku hizi hamjali, Mgasi akahoji

“Unataka nifanyeje Mwinyi?”

“Nataka unishauri nifanye nini?”

“Leo unahisi ushauri wangu unaweza ukafaa?”

“Kha! Mgasi.. lini ushauri wako ulikuwa haufai?”

“Kumbuka nilikushauri hapo awali juu ya jambo hili, lakini ukakataa na kuona ushauri wangu haufai, ukaona kama vile ninatamani utapeli wako, leo yapo wapi?” ilikuwa ni mwendo wamaswali tu mwanzo mwisho na hakukuwa na mtu wa kujibu.

“Kweli nilikosea, lakini yale yameisha pita, nisaidie kwa hili Mgasi.”

“Nikusaidie kivipi sasa?”

“Vyovyote vile ili jambo hili likae sawa Please..!” aliomboleza sana Mwinyi na Mgasi akamjibu kiufupi tu;

“Sasa sina msaada wowote ndugu yangu,” hawakuweza kufikia muafaka. Maana tayari Mgasi alikuwa na malengo yake kwa Salama.

Waliposhindwa kufikia muafaka Mgasi na Mwinyi, akatumia fursa ile kumpigia simu Salama. Nae kwa kuwa alikuwa ameisha futa namba yake ya simu, alishindwa kumtambua hadi alipojitambulisha mwenyewe

“Oh! Samahani kaka yangu kwa yote yaliyotokea huko nyuma, niikua nikijua ule ni uzushi tu, ila sasa naomba radhi sana”

“Usijali Salama na nimefurahi umeona mimi si muongo” Mgasi

akaanza kujitengenezea njia

“Ni kweli na ninashukuru sana kwa msaada wako”

“No! Noo Salama, ni mapenzi yangu makubwa kwako ndio yaliyoniongoza mie kufanya vile, upo wapi kwa sasa?”

Salama palepale akajiongeza, kauli ile ya Mgasi ilipokuwa inaelekea, ikamfanya agundue kuwa bado jamaa anamtaka kimapenzi, hapohapo akamrusha.

“Nipo ndani ya gari naelekea Mwanza muda huu, ila nitalala Nzega,”

“Ha Salama! Acha roho mbaya, mbona haraka hivyo? Kweli hata hatutafutani? Au tumekuudhi wote?” maneno ya Mwinyi yalionesha kabisa kukata tamaa.

“Hapana kaka yangu, ila nisamehe kwa hilo”

“Sawa, sasa nina ombi lakini usinichukulie tofauti”

“Mh! Nakusikiliza,”

“Unajua kila mtu duniani ameumbwa na tabia yake, kuna walio na tamaa na walio wakinaifu, pia kuna wenye mapenzi na kuna makatili, na mfano huo...” Salama akamkatisha

“Sawa Mgasi, lakini umesema una ombi, mbona imekuwa ni habari?”

“Ok! Ni hivi Salama, nakupenda, naomba uwe Mpenzi wangu,

nakuhaki...” akamuwahi.

“Subiri, maneno uyasemayo ni haki yako kuyaongea, ila hapa si mahala pake, huwezi kupiga makofi kilioni japo una haki ya kufanya hivyo popote, tafadhali, tafuta muda na siku nyingine, nipo kwenye usafiri wa jumuia hapa, siwezi kuzungumzia hilo, samahani kaka” akakata simu na kuitupia kitandani

Asubuhi ya siku iliyofuata, Mgasi alimfuata Mwinyi na kwenda kazini kwao, maana wote wanafanya kazi sehemu moja. Wakati huo ndio Salama alikuwa yupo barabarani akirejea jijini Mwanza, Anisa alikuwa amepitia gari lake kwa Mwinyi na kuelekea chuo cha Utumishi alipokuwa akisoma.

Maisha yakaendelea pasina mawasiliano yoyote baina ya Mwinyi na Salama, bali penzi kati ya Anisa na Mwinyi likazidi kuchanua na kushika kasi, haikuwa siri tena sasa ikawa ni dhahiri, suala la Anisa kuwa na mpenzi wazazi wake nalo hawakuliafiki.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Kimbembe kikaanzia hapo, mtoto anapenda, wazazi hawataki, mchakato wa kuwatenganisha ukaanza taratibu. Wazazi hawakutaka kutumia nguvu sana kwa mtotot wao hasa ukizingatia kuwa ndio mtoto wao pekee walie nae pale japo wengine wapo, ila ni mbali nao, hivyo hawakutaka kumuudhi ndio maana hata gari wamempa atumie.

Siku moja Joy akiwa amekaa nje kibarazani kwake peke yake akiwa hana hili wala lile, simu yake ikaita. Alikuwa ni Victor akimsalimia na kutaka kujua kama Joy ameisha onana na Salama. Pia kama ujumbe wake atakuwa ameufikisha na majibu yake yakoje

Joy alimwambia kuwa hawajaonana na Salama ila ujumbe tayari ameisha ufikisha.

“Enhe, ameupokeaje?”

“Katika hali ya kawaida tu, waa hakuonyesha hali yoyote tofauti”

“Kwa maana hiyo Joy, Salama hanipendi tena?”

“Anasema hataki kabisa suala la mahusiano, kwa sasa ameelekeza akili zake kwenye biashara”

“Kweli Joy umeshindwa kabisa kumuelezea hisia zangu?”

“Nimejaribu Victor, lakini Salama ana msimamo thabiti katika mambo anayo yaamua”

“Hapana dada Joy, naomba namba yake,” aliomba Victor.

“Mh! Hilo ndio gumu zaidi, labda nimpe yeye namba yako kisha

nimwambie akupigie,”

“Dada Joy, yeye hawezi kunipigia maana hana shida nami, bali mimi ndio nina shida nae”





“Usihofu Victor, nitamuita nyumbani na kumbembeleza akupigie na nina yakini atakupigia” Japo hakuwa ameridhika, akakubali na kumuambia anamtegema yeye juu ya kufanikisha jambo lile. Hivyo ndivyo walivyomaliza mazungumzo yao ya

siku ile na kila mmoja akashika hamsini zake.



KUKUTANA NA KIKWAZO.



Mwanzo ilkuwa ni siri, hasa ukzingatia watoto wa kike wa kiarabu kuwa na mahusiano kabla ya ndoa ni jambo gumu sana tofauti na mataifa mengine kama vile yale ya Ulaya.

Penzi la Anisa na Mwinyi polepole likaanza kuwa ni dhahiri, watu wa nje ya kwao na Anisa ndio walioanza kuliona hilo na kulipeleka mbele ya familia ya kina Anisa, mwanzo alikataa kabisa na kukana kuwa anasingiziwa.

Muda uliongea hata hivyo, baadae ikawa si siri tena, wazazi walipiga hadi wakahisi wataua, motto wao ndio kwanza kama kaoneshwa njia sahihi tofauti na ya awali kuwa ilimpoteza.

Familia ya Anisa ilijaribu tena sasa kukaa na Anisa na kumwambia juu ya wao kutoutaka uhusiano baina yake na Mwinyi, lakini kwa mara nyingine tenaAnisa hakuelewa. Walijitahidi kwa kila hali kumshawishi aachane nae, hawakufanikiwa, mwisho wakajidai wamekubali matokeo, wakamruhusu awe nae.

Ile ilikuwa ni danganya toto, Anisa hakuelewa masikini kuwa wazazi wake wanamcheza shere, akawakumbatia na kuwabusu kuwa makini. Mama yake akamwambia amlete Mwinyi nyumbani ili nao waweze kumtambua rasmi.

Wala haikuwa kazi ngumu kwa Anisa, ila alijiuliza, je Mwinyi atakubali? Akajipa moyo kuwa atajitahidi kumshawishi hadi atakubali. Akaenda ndani na kumpigia simu Mwinyi na kuongea nae, Kama alivyohisi, Mwinyi aligoma, lakini baadae akakubali.

Siku iliyofuata, mida ya jioni Mwinyi alikubali kwenda kwa kina Anisa. Alipokaribia, akampigia simu Anisa akamfuata na kumkaribisha ndani. Akiwa ni mwenye furaha tele, Anisa alimtambulisha Mwinyi kwa wazazi wake na kuwaambia atawapenda zaidi wazazi wake na kuahidi kuzidisha upendo juu yao kwa sababu wameonesha kumjali.

Wazazi walitabasamu na kumwambia Anisa awapishe kidogo waongee na Mwinyi. Anisa alinyanyuka na kwenda alipo Mwinyi na kupiga magoti hali ya kuwa mikono kaiweka kwenye mapaja ya Mwinyi na kumwambia kwa sauti ya chini

“Mpenzi jisikie huru, hawa ni wazazi wako pia, kama unavyoongea na baba na mama Mwinyi, hata hawa ongea nao hivyo hivyo.. Nakupenda Mwinyi” Mwinyi hakuwa akijiamini sana pale ndani ya nyumba, hasa baada ya Anisa kumaliza kuongea nae na kuondoka.

Kitendo cha kuwapa mgongo tu Anisa, sura za wazazi wake wote wawili ziibadilika na kuwakutoka kwenye hali ya tabasamu zilipokuwa wakati wameingia na kuwa za hasira na chuki iliyojionyesha waziwazi.

Mwinyi aiingia hofu na kuanza kujuta ndani ya nafsi yake na kujikuta akijilaumu ni kwa nini alikubali kuja. Baba Anisa akaanza kuzungumza kwa jazba

“wewe ndio kidume unaetuharibia binti yetu si ndio?”

“Hapana wazee”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Hapana nini? Umefanya Anisa abadilike kwa ajili yako, hasikii lolote kwa sisi wazazi wake, hapiki humu ndani wala kuosha vyombo anavyotumia, na hii yote ni kwa ajili yako wewe, sasa…” maneno haya aliyaongea mama Anisa, akini hata hivyo alikatishwa na baba Anisa alieonekana kama nae ana mengi sana ya kuongea

“Unasikia wewe kimburu, kuanzia leo sitaki kukusikia tena katika mdomo wa mwanangu wala kukuona nae popote, tambua chochote kitakachompata mtoto wangu wewe utakuwa ni muhusika namba moja na baada ya ahapo usije kunilaumu kwa litakalo kutokea iwapo utaendelea kuwa pamoja na Anisa, fahamu kuwa mimi huwa sina huruma kwa viumbe wasiokua na uelewa,” alimaliza Baba Anisa na kudakiwa na mkewe

“Tena huyu anaonekana ni jeuri, si unamuona hata hilo lisura

lake” kauli ile ya Mama Anisa ilimuumiza sana Mwinyi, akanyanyua ulimi wake

“Lakini wazazi wangu...”

“Wee! Nani mzazi wako hapa? Loh! Mimi siwezi kuzaa ngedere!” jazba sasa ikampanda Mwinyi kutokana na kauli ile ya Mama Anisa, akahamaki na kusema

“Sasa wazee naona heshima yangu imeshindana na hekima yenu, inaonekana mmeniita ili kunidhalilisha ndani ya nyumba yenu, tambueni mimi sipo tayari kwa hilo,”

Baba Anisa akasimama na kumtaka Mwinyi anyamaze kabla hajamuitia Polisi, hapo sasa akawa kama vile ndio kawasha moto kwenye mitungi ya gesi

“Huwezi kuniita Ngedere nikanyamaza eti kwa kutegemea Polisi, kule ni usalama wa raia na mali zao, nami ni raia. Halafu we mzee kumbuka mimi ni wa hapahapa, wewe si wa kuja tu. yaani unitishie amani kwenye nchi yangu? Siwezi kuruhusu hali hiyo itokee Abadan Nguruwe nyie!” jazba ya Mwinyi ilikuwa ipo juu sana.

Kelele za ukumbini zikamfanya hata Anisa aliekuwa jikoni akipika chakula cha jioni atoke na kusogea kule zinapotoka kelele zile na kukuta baba yake na mpenzi wake wakijibizana kwa kelele na wote wakiwa kwenye jazba ya hali ya juu.

Alipojitokeza tu, mama yake akamuwahi kwa kumwambia

“We mi nilikwambia haya majitu meusi hayana adabu, limetuita sisi Nguruwe, hebu litazame sasa linavyomkaripia baba yako” baba Anisa akamsogelea Anisa na kumwambia

“Haya mtoe haraka huyu Nyani wako nje kabla sijamuitia kelele za wizi hapa akachomwa moto,”

Anisa alikuwa njia panda haelewi kama Mwinyi ametenda kweli ama anasingiziwa, akaamua ni heri aepushe shari, asiwe upande wowote kwa muda ule, hadi atakapokaa nao kila upande ndio atachagua ule utakao kuwa upo sahihi ndio aushikilie.

Akapiga hatua kumsogelea Mwinyi aliekuwa amefura kwa

hasira, walipotazamana tu, macho yao yaipokutana, midomo ya Mwinyi ikafunguka

“Usijaribu kunisogelea hata kwa hatua moja bata we! Si umenileta kwenu kuja kunidhailisha eenh? Ipo siku mtajutia hizi kauli zenu Nguruwe nyie” jazba ilikuwa juu sana, akaendelea huku akionesha ishara ya kuondoka

“Nyie ndio bado mnaishi katika karne ile ya wapumbavu wachache wanao amini weupe ni deal, tambueni nyie weupe ungekuwa deal, wajapan wasingehangaika kutengeneza Super black, mi ninakwenda ila ninasema, bahati yenu sana nipo ndani kwenu ila siku nyingine mkijaribu..” akasonya na kutoka akibamiza mlango.

Kutoka kwake kulimuweka Anisa katika wakati mgumu sana, alibaki hajielewi, amfuate Mwinyi au abaki na wazazi wake, akakumbuka kauli ya Mwinyi

“Usijaribu kunisogelea hata kwa hatua moja..” na kwa hali aliyokuwa nayo Mwinyi pale, Anisa akatepeta na kumuacha Mwinyi apotelee mbele yeye akimtazama tu bila kufanya lolote

Aliwageukia wazazi wake na kuwaona kila mmoja ana la kwake kichwani, akawauliza kwa sauti ya unyonge sana lakini yenye kumaanisha hasa, ilimaanisha kutaka kujua undani wa vurugu zile.

“Baba na mama, kuna nini kimeendelea nilipotoka?”

“Toka hapa, nenda jikoni huko, unatuletea waswahili hapa!” jibu hilo iitoka kwa mama yake halikumridhisha kabisa, akaanza kuhisi kuwa tatizo litakuwa upande wa wazazi wake yeye wala halipo kwa Mwinyi.

Nae akagoma kuondoka hadi mama yake alipomlazimisha na kuondoka nae akiwa amemshika mkono huku akilia hadi jikoni aipokuwa akipika

“Mtu uliemleta hana heshima hata kidogo, ametaka kumpiga baba yako,” mama Anisa alimuongopea mwanae, Anisa akaguna na kuuliza

“Kisa nini?” Swali lilikuwa ni la msingi sana lakini likatoa jibu la

uongo

“Abuy wako alipo muuliza kuhusu mpango alio nao kwako, akasema kwa sasa hana mpango wowote nawe zaidi ya kuwa ni mpenzi wake basi,”

“Hapana mama umemsingizia, Mwinyi hawezi kusema hivyo!” Alikataa Anisa kwa ishara zote

“Kwa hiyo mimi nasema uongo eti,”

“Si hivyo, ila hicho unachokisema umekiongezea mama, yawezekana alijibu tofauti na mlivyotaka nyinyi, lakini sio kama hivyo ulivyoniambia,”

“Wewe ulikuwepo?”

“Mama mimi sikuwepo lakini Mwinyi mimi ninamjua vizuri mama yangu, anajiheshimu sana na anaheshimu wengine pia,”

“Sasa nasema hivi, hatumtaki mswahili humu ndani, full stop!”

“Sawa, nae hamtaki yoyote humu ndani zaidi yangu mie,”

“Nyamaza mpuuzi wee, huna adabu eti? Unajibizana nami? Umekuwa sasa eenh?”

“Haya tu! Mimi nitafanyaje na wakati sina haki? Ipo siku nami nitapata nafasi ya kuwa na maamuzi yangu binafsi,” Aliongea Anisa kwa huzuni kutoka ndani kabisa ya moyo.

“Labda ukiwa kwa mumeo huko, sio hapa kwetu” aliongezea Mama yake huku akimtazama mwanae.





“Sawa mama, basi niacheni mimi niolewe na huyu nimpendae ama mnamkataa kwa sababu ni Mswahili?” kabla hata Mama yake hajajibu akamsogelea na kumwambia kwa sauti ya upole.

“Lakini mama yangu jamii yote iliyotuzunguka hapa ni waswahili, tupo nao kila siku kwenye shida na raha tunasaidiana, iweje tubaguane kwenye suala la ndoa na mapenzi mama yangu?” Maneno yale yalimgusa sana mama Anisa, lakini akajidai kama hayaoni umuhimu wake, akamkaripia tena kwa dhihakihttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Unampenda sana huyo mswahili eenh? Sasa hapa hatakiwi, wewe utaolewa na mtoto wa Mzee Salum wa Shinyanga, basi sina tena mjadala nawe, wewe utaolewa upende ama lah” mam

akaanza kuondoka kule jikoni akielekea sebuleni.

“Samahani mama, kama hamtaki chaguo langu mie ninae olewa, hakika nami sitakubali chaguo lenu, tambua Mama hilo halitowezekana,” Mama alikuwa amefika mlangoni, akasimama na kumtazama Anisa kisha akasema

“Anhaa! Wewe si ni jeuri? Dawa yake ni kiburi, sasa tutaona ni yupi mzazi na yupi ni mtoto,” Akafyonza na kutoka.

Anisa akabaki jikoni peke yake, akakaa chini na kuanza kulia alitamani sana kukamilisha ndoto za kuwa na Mwinyi, lakini utofauti wa damu zao ulionekana kuwa ni tatizo kubwa kabisa katika kukamilisha ndoto zake Anisa, akaanza kulia peke yake.

**********







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog