Search This Blog

Tuesday, 1 November 2022

UMENIFUNGULIA DUNIA - 2

 








Simulizi : Umenifungulia Dunia

Sehemu Ya Pili (2)







Akampigia simu mama yake na kumueleza kile alichokiona kwa macho yake. Kumbe muda ule Mwinyi na Ramlat walikosa vyumba pale na kutokea mlango wa nyuma wakahamia sehemu nyingine wakati huohuo Side amekaa makini nje ya guest akimsubiri mama yake waje

wafumanie.

Mama akatoka akiwa na jazba tele, kwanza akifikiri ni kwanini achanganywe na mwanae kwa mwanaume mmoja na pia kwanini mwana ajiingize kwenye mapenzi wakati huu akiwa masomoni badala ya kutumia muda mrefu kwa ajili ya kusoma. Kwa hakika Mama mwenye nyumba alikuwa hajiamini kama akiwakuta, hivyo akamchukua Salome na kwenda nae, laiti wangejua..

Hakika Mwinyi ni mchafu sana kitabia, maana wale viumbe wawili waliochukuana, hawakujuana kama wote wameisha fanya ngono na mtu yuleyule wanakwenda kumfumania. Salome upande wake alitaka kuhakikisha tu kama ni kweli Mwinyi anatoka na Ramlat ama ni uzushi. Waliwasili Guest na kumkuta Side anawasubiri palepale nje.

Akawaongoza kuingia ndani moja kwa moja hadi mapokezi. Walifika na kujitambulisha kuwa wao ni wageni wa Bwana Mwinyi na mkewe Ramlat, muda sio mrefu uliopita walikubaliana watakutana pale. Mhudumu akafungua kitabu na kutafuta majina yale, akayakosa. Akawauliza kama kuna jina lingine wanalijua huenda wakawa wamelitumia.

Wakasema hakuna maana hata mtoto hawana, akawaambia wawapigie simu, Side akajibu haipatikani simu yao. Akawauliza muonekano wao, wakamulza, muhuumu akasema watu wale hawapo pale. Side hakuiafiki kabisa kauli ya yule muhudumu, akahisi kuna mazingira ya watu wale kufichwa. Muhudumu akawajibu pia yawezekana maana hakuna hotel yoyote duniani ambayo mtu atakuja na kutaka kuingia chumbani kwa mteja bila kuwa na ahadi nae

Mama akatoka nje na kumuacha Salome akiwa amsimama, Side akawa anaendelea kuonga na Muhuumu akimwambia kuwa wao wana ahadi nae, Muhudumu akajitetea kuwa pale kwake hana taarifa hiyo, hivyo wafanye njia nyingin ya kuwasiliana nao, wakatoka nje na

kumkuta Mama Ramlat akiongea na simu.

Mama Ramlat alikuwa hewani akiongea na mwanae ambae alimwambia kuwa muda ule yupo kwa wifi yake, mpenzi wa kaka yake aitwae Anisa. Moyo wa Mama ukatulia, jazba ikapungua na kumwambia Ramlat asitoke pale hadi yeye atakapofika. Bado Side hakuamini mchezo uliochezwa pale, Salome akasema yeye anatangulia nyumbani, Side nae akasema yeye ataendelea kuwepo pale kwa muda.

Kumbe baada ya kukosa chumba pale, walihamia guest nyingine ya karibu na palepale na kuanza kula ujana. Hapakuwa mbali sana na kwa Anisa ambapo alisema yeye yupo, Ramlat akanyanyuka haraka haraka na hata hakuhitaji kusema anaenda wapi, maana Mwinyi alisikia kila kitu.

Ramlat akatokea upande wa Bar na kutokomea kwa Anisa kwa mwendo

wa haraka na kumuacha Mwinyi akiwa amebaki peke yake, na hapo ndio Mwinyi huwa hafanyi kosa, si unakumbuka alihokifanya TAI 5 huko Mwanza? Na hapa baada ya kuona kabaki peke yake, akampigia simu Salome na kumuelekeza alipo ili amfuate.

Salome aliruka kimanga na kumwambia ashindwe na alegee, Mwinyi akacheka na kusababisha hata Salome acheke na kukata simu. Hakuwa na cha kufanya tena pale, akaamua ni heri ampigie simu Salama kumjulia hali, maana alikuwa ana kama siku nzima bila kuwasiliana nae. Waliongea kwa shauku na bashasha tele.

Anisa, rafiki wa Ramlat, pia ndio mpenzi wa Side, ambae aliunganishiwa na Ramlat na kutokea kuwa ni wapenzi wa ukweli. Japo alikuwa ni binti wa kiarabu, lakini alikuwa ni chakaramu hasa, hakutulia hata robo. Ujio wa Ramlat kwa muda ule aliutilia shaka, na kumbe ni kweli, alikuwa sahihi.

Mwinyi akampigia simu Mama Ramlat baada ya maongezi yake na Salama kuisha. Akamulekeza ili waende wakafurahi ile jioni walioiona kuwa ni njema kwao. Japo ni jimama lakini Mwinyi alilizimia kwa mambo lililokuwa likimfanyia. Mama Ramlat akamuahidi kuelekea huko mara tu akitoka sehemu kumuona mtu fulani

Ramlat akamuelezea kila kitu na kwanini yupo pale, Anisa alishangaa sana, maana wao wamezoea kumuita Ramlat kama ‘Mgumu wa eneo’ sasa imekuwaje kanasa kwa mtu ambae alikuwa akimtaja kama sio mzima? Hakika hapo hapo Anisa nae akajikuta kaisha changanywa na Mwinyi

“Lakini Ramlat we si ulikuwa hutaki mambo haya? Imekuwaje tena?” alidadisi Anisa.

“Mh! Mwenzangu.. we acha tu. kwa Mwinyi mwenzangu sijielewi wala

sijitambui, na haki ya Mungu siku nikimuona na Mwanamke, nitamuua,” aliongea Ramlat akiwa makini kabisa

Anisa akacheka kinafiki ila akawa nae sasa anatamani kujua ni nini hasa kilichompagawisha, akaanza kujipanga ili kumpanga Mwinyi kwenye mikono yake.. akiwa yeye anafikiria hivyo, Mama Ramlat akawa amefika pale na kuwakuta Ramlat na Anisa wamejaa pale kama maji baharin

Aliwasalimia na kumuomba Ramlat waongee faragha kidogo, kabla hawajaongea simu yake ikaita, alikuwa ni Mwinyi, mama Ramlat hakuongea sana bali alisema kumwambia asiondoke amsubiri palepale yeye atakwenda muda ule yupo njiani. Akamjulisha kuwa akizidi kuchelewa, hatamkuta, ataondoka.

Wakati huohuo Anisa akautumia upenyo wa Ramlat kuitwa na mamae nje kwa kukagua simu yake ili aibe namba ya Mwinyi. Hakuijuwa na alitegemea haitakuwa na jina la Mwinyi, sasa alichofanya ni kufungua sehemu ya namba zilizopigwa na kuhukua ile namba ya mwisho, kasha

akaiandika kwake.

Namba ile aliikuta kule kwa jina la ‘My Preciouos’ aliamini ndio namba anayoitafuta kwa sababu mbili. Moja ni kuwa wakati Fulani wakiwa wanapiga soga, Ramlat aliongea na Mwinyi, hilo lilimfanya aamini kabisa ile ni namba halisi ya Mwinyi. Na sababu ya pili katika kuhakiki, akaenda kwenye sent item.

Kule napo aliikuta namba ile ikiwa imetumiwa sms ikiwa na jina la Mwinyi ndani yake, akaridhia na kujiridhisha kuwa hajakosea.

Huko nje mama akamuuliza mwanae juu ya uhusiano wake na Mwinyi, Ramlat alikataa katakata na hata kumponda na ilhali yeye mwenyewe ukweli anao moyoni. Mama akafurahi na kumpa nasaha fupi akimuasa juu ya masomo na umuhimu wake.

Kisha akamtaka kuwahi kurudi nyumbani mapema tena mua uleule ili akawahi kufanya kazi za nyumbani, kwani yeye kuna sehemu anaenda ameitwa na atachelewa kurudi. Wakarejea ndani na kuaga kisha kila mmoja akashika hamsini zake.

Akiwa anatazama mpira wa miguu palepale guest, Ramlat akampigia simu na kumueleza yaliyojiri na kutumia nafasi ile kumuomba arejee nyumbani kwani atakuwa peke yake.

Mwinyi akamuhakikishia ndani ya nusu saa atakuwa nyumbani. Mwinyi akatazama saa na kuona muda unakwenda pasina mama Ramlat kufika, ila kabla hajafanya uamuzi wowote, mtu mzima jimama ikaingia. Ah! Hata kwani ilichukua muda? Wakaanza kujiachia kwa

raha zao.

Katikati ya sherehe msg ikaingia ikisema ‘Usije kaka amerudi, nipo nae hapa nyumbani’ akaona Yes, full shangwe... Akazima simu na kuendelea kufanya yake na Mama Ramlat. Pale nyumbani Ramlat na Side ukazuka ugomvi mkubwa sana, Side aliendelea kumtuhumu Ramlat juu ya kuwa na uhusiano na Mwinyi

Mwanzo Ramlat alikana kwa nguvu zake zote, ila kutokana na kubanwa sana na Side, akamjibu kwa jazba kaka yake

“Hata kama ni kweli wewe inakuhusu nini? Utanioa wewe? Mahitaji yangu yote utanitimizia wewe?” kauli ile ya Ramlat aliekuwa amekasirika, ikawahamisha kutoka kwenye ugomvi wa maneno hadi kufikia matusi na hatimae ikawa ni makofi kwa Ramlat.

Baada ya kutoa kipigo kwa dada yake, Side akatoka na kwenda kijiweni kwake. Akiwa pale akamuona Mwinyi akiwa anarejea nyumbani kutoka anapopajua yeye, Side akamsimamisha kwa nia njema tu na kumuhoji juu ya uhusiano alionao na dada yake. Pia alitaka kujua kama Mwinyi anajua kama Ramlat ni mwanafunzi.

Mwinyi alikiri kujua kuwa Ramlat ni mwanafunzi ila akakana kuwa na uhusiano nae. Side alitikisa kichwa na kumueleza Mwinyi juu ya kile alichokiona ilikuwa ni aibu moyoni. Lakini mdomoni aliendelea kukataa vilevile.

Mama alirejea nyumbani nusu saa baada ya Mwinyi na kuwahiwa na mpangaji wake wa kike alieshuhudia ugomvi ule na yote yaliyotokea muda uliopita, akampasha habari zote, mwanzo mwisho. Ghafla Mwinyi akatokea pale uwani na kuelekea chooni, alionyesha kabisa kutokujiamini.

Kutokana na mzunguko uliokuwepo, akahisi kabisa kikao kile kilikuwa kikimzungumzia yeye, maana aliona na Ramlat anasogea pale, kwa mbali tu aliweza kusikia Ramlat akimshitaki Side kwa mama yake

Alipotoka maliwatoni, akawapita bila hata kuwasemesha wala kuwatazama usoni lakini pia hata wale waliokuwepo pale uwani walijiona ni wajinga japo ilikuwa ni siri ya kila mmoja moyoni mwake, wakasambaa kimyakimya wakielekea vyumbani mwao, Mwinyi nae akaingia chumbani kwake.

Mama mwenye nyumba alionekana ni mtu mwenye furaha sana usoni na hata moyoni pia kwani kabla Mwinyi hajatoka, alimuita na kujidai anamuonesha bill ya maji kumbe alikuwa akitamani kuwa nae karibu.

Mapenzi ya Ramlat kwa Mwinyi sasa yalikuwa ni ya dhati hivyo akawa ni msumbufu. Mara chache chache akawa anatoka na kwenda kujivinjari sehemu mbalimbali. Siku moja wakiwa kitandani, Ramlat akamwambia kuwa tayari yeye amenasa ujauzito. Mwinyi akajua ni utani tu, hapo tayari wakiwa na mahusiano ya takriban miezi miwili na kidogo.

Usiku mnene akiwa amelala, akapokea sms ya kuomba kupigiwa. Namba ilikuwa ni ngeni kabisa, akaenda hewani, kumbe alikua ni Anisa, Mwinyi aikuwa akimjua kwa kutambulishwa kama rafiki wa Ramlat na baadae Ramlat akamtambulisha kama Anisa ni mpenzi wa Side.

Anisa aliomba kuonana na Mwinyi siku ifuatayo huko maeneo ya Cheo Club kwa maongezi muhimu, Mwinyi akaomba adokezwe kidogo, lakini Anisa alikataa katakata na kumwambia avute tu Subra hadi siku ifuatayo wataongea kiurefu na kwa mapana

Mwinyi alishindwa kulala, hakika alihisi itakuwa ni tatizo lilelile alilolisikia jioni toka kwa Side na wale waliokuwa pae uwani, akajua huyu sasa amesikia nae na anataka kujua. Akili ilikataa kbisa lakini akajifikiria na kuamua kupuuzia tu hadi

muda waliopanga utakapo fika na ataenda kushuhudia ni kipi kitaendelea, akavuta shuka akalala.

Saa 10 jioni Mwinyi tayari alikuwa ameisha fika maeneo yale husika kama walivyoahidiana na Anisa kuwa wakutane sehemu ile. Sasa ikawa anamsubiri Anisa atokee kwani hakuwa na amani hata kidogo.

Hakukawia sana akaingia sehemu ile ya ahadi akiwa na gari ndogo aina ya IST . walisalimiana, ajabu ndani ya dakika zile 10 za mwanzo tu, Anisa alikuwa amekunywa bia kopo zima na hali yeye alikana kuwa hajawahi kunywa pombe.

Mwinyi alipotaka kujua sababu ya kuitwa pale akaaswa asubiri kwanza na asiwe na pupa. Wakaendelea kukata bia, zilipoanza kuwakolea zaidi, Anisa akamuomba Mwinyi amshindikize chooni, kwa kuwa wote walikua pombe, wakanyanyuana na kuelekea choo cha wanawake bila kujali vyoo vimetenganishwa, wanaume peke yao na wanawake peke yao.

Mlangoni, tena mlango ukiwa wazi, kwenye vyoo vya wanawake, ndio Mwinyi aipoishia na kumsubiri Anisa pale, mwanamke akidhamiria kitu.. hatari sana! Akavua nguo na kuchuchumaa akimuacha Mwinyi akiona kila kitu kilichopo kwenye mwili wake mweupe wa Kimanga.



http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Mwinyi roho ikamfika mbali, tamaa ikamuingia lakini akajizuia, akamnyanyua huku akimsaidia kuvaa suruali na kumshikashika hapa na pale, hatimae ndimi zao zikakutana, hawakutengana hadi pale waliposikia kuna mtu akielekea upande ule waliopo.

Kutoka pale hawakukaa tena, walienda Counter na kulipa bili yao na kuondoka, Anisa alijidai kama hawezi kuendesha kutokana na kuzidiwa na kilevi, hivyo ikamlazimu Mwinyi ashike usukani, kitu ambacho Anisa alikua akikihitaji.

Walikwenda na barabara ya Boma hadi karibu na uwanja wa shule ya Msingi Mwenge na kupaki gari pembeni, muda wote huo Anisa alikua akimchokoza Mwinyi aliekuwa akiamini Anisa kalewa, kumbe walaaa, hakuwa amelewa hata kidogo bali alikuwa na lake lengo.

Alifanikiwa kumshawishi Mwinyi na kuweza kufanya nae mapenzi garini kwa msaada wa giza nene la usiku lililokuwepo nje na kutawala anga lote. Walifanya yao na kupongezana kwa utundu wao huku Anisa akijisifia kwa kumwambia Mwinyi kuwa sasa amejua ni kwanini Ramlat anampenda sana.

Mwinyi hakusema kitu bali alicheka tu na kumtaka Anisa waondoke pale warudi makwao maana usiku unazidi kuliwa na watachelewa kulala. Walibadilishana viti, Mwinyi akaenda cha abiria na Anisa akasogea kwa dereva, wakaondoka.Njiani ndio Mwinyi akamuuliza Anisa imekuwaje leo ametoka usiku? Akacheka na kumwambia ni mjini hapa.

Akavuta draw ya Dashboard na kutoa kadi ya mwaliko wa sherehe na kumpa Mwinyi. Aliisoma na kutikisa kichwa na kuirejesha mahala pake, wakawa wamewasili jirani na pale anapokaa Mwinyi, wakaewana amuache hapohapo, waka kiss na kisha akatoka na kuelekea kwake kulala.

Wiki moja baadae Salome alimfuata Mwinyi na kumwambia kuwa yeye ni mjamzito ametoka kupima muda uleule, na amegunduika ana mimba. Mwinyi akaikana

“Wewe mwanamke huna aibu eti una mimba yangu... Mi nawe tume sex mara moja tu,”

“Sasa Mwinyi ulitaka iwe mara ngapi? Kwani shambani mbegu hupandwa mara ngapi kabla ya kuota? Mi nilikuwa nakuona una akili kumbe wee ni Ziro?” aliongea Salome kwa jazba.

“Hayo ni yako wewe,” Mwinyi akajibu huku akiondoka.

Hakuweza kupata muda zaidi wa kujadili na kichwa chake, akapanga siku ifuatayo asubuhi na mapema ampe pesa aende akaitoe mimba ile ili awe huru na amani kabla mumewe hajarejea.

Wazo ile lilipita bila kupingwa kichwani mwake.

Nyumba kwa nje ilikuwa imepoa kupita kiasi hadi Mwinyi

akaamini nani hakuna mtu, ila alipoingia ndani, alisikia sauti ikilia kwa kuomboleza

“Nisamehe kaka nitakwambia...” Sauti aliitambua lakini wala haikumshughulisha maana hata hakujua chanzo cha kelele zile ni nini. Akaingia chumbani kwake ikiwa ni saa 11 jioni.

Simu yake iliita nae akapokea na kusalimiana na mpigaji, alikuwa ni mama Ramlat akihitaji waonane baadae, kifupi alimwambia kama yupo ndani basi asitoke. Hakuwa na wasiwasi akamjibu kuwa yeye yupo ndani na hatotoka kwa siku ile tena.

Pamoja na kauli ile, akaamua kumpigia simu dalali kumtafutia nyumba sehemu nyingine maana pale tayari aliisha anza kuona hapamfai, alihofu ipo siku mambo yataharibika na kuwa hadharani hatimae watu watachinjana bure.

Bahati ilikuwa upande wake, simu ikapokelewa na dalali akamwambia

kuna chumba mjini palepale maeneo ya Kanyenye, akadai anataka viwili, navyo akaambiwa vinapatikana hapo hapo maeneo ya Bachu, wakapanga siku ifuatayo asubuhi waende wakavione.

Saa 1 usiku Mama Ramlat akazama chumbani kwa Mwinyi pasina mtu yeyote Yule kumuona, alionekana kuwa ni mtu mwenye majonzi tele, Mwinyi akambana na kumtaka amueleze kwanini yupo vile, Mama Ramlat aliguna na kutikisa kichwa, kisha akasema

“Ramlat amegundulika kuwa na mimba ya mwezi mmoja na nusu,” moyo wa Mwinyi ukapiga mshindo. Mama Ramlat akaendelea

“Na kibaya zaidi hataki kumtaja muhusika ni nani...” Mwinyi akakaa na kukosa la kuchangia, ila akamuuliza kama wamemuhoji kwa umakini.

“Ndio amegoma, na ole wake nimjue huyo aliemuharibia masomo yake mwanangu, atanijua mimi ni nani,” Akili ya Mwinyi ikaganda, Mama Ramlat alipoendelea kumsemesha

ilikuwa ni kama anaeongea peke yake.

Ili kuzuga na kutaka kujua zaidi kinachoendelea, akahoji swali la kizushi kuwa ni kwanini hawamtishi ili amtaje muhusika? Mama Ramlat akajibu kuwa, sio tu kumtisha, bali kaka yake amempiga kabisa lakini

bado alishikilia msimamo wake uleule wa kutokumtaja.

Mama Ramlat akaendelea kumfahamisha Mwinyi kuwa walivyoendelea kumtisha kwa kumwambia kuwa watamtimua pale nyumbani iwapo hatamtaja muhusika moja kwa moja hapo ndio akamtaja kaka yake kuwa ndio aliempa mimba ile.

Mwinyi akajidai kushtuka kinafiki na kuuliza huku amemkazia macho Mama Ramlat

“Inawezekana ikawa ni kweli?”

“Hapana si kweli, aliamua tu kutaja vile ili kuzidi kutuchanganya na kufanya tuuache wakati tunafikiria nini kifuatie”

Wakaachana na mada ile huku Mwinyi akijipa Moyo kuwa kesho atajitahidi kuweka mambo yote sawa mapema kabla Hayajawa mabaya zaidi yaani atoe pesa kwa wanawake wale wote wawili ili wakatoe zile mimba na kesho hiyo hiyo yeye ahame kwenye nyumba ile ili kukwepa majanga ambayo yanaonekana kumsogelea kwa kasi.

Akiwa bado yupo na jimama chumbani mwake, Salama akapiga simu na kumuuliza alipo. Kwa kuwa Salama yupo mbali, hakutaka kumdanganya, ila alishangazwa na swali lile, kabla hajamueleza kama yupo wapi, akamuuliza yeye kwanza inakuwaje anamuulizia alipo na wakati yeye yupo mkoa mwingine mbali kabisa?

Salama akamwambia kuna mtu alimtuma kwake kama Suprise akini kwa bahati mbaya kapotea. Mwinyi akamwambia ampe namba yake ili akikaribia pae amtafute. Salama akakataa na kutaka aelekezwe yeye nae atamuelekeza mwenyewe, akaamua kumlaghai Mwinyi

“Unajua ni aibu sana kumwambia mtu kuwa hupajui kwa mpenzi wako,” Mwinyi akakubali yaishe, akamuelekeza kwa umakini na kukata simu.

Wakaendelea kufanya yao na mama Ramlat. Kwa mbaali wakasikia sauti ikimkaribisha mtu, sauti iliomkaribisha mgeni ilikuwa ni sauti ya Salome, mpangaji mwenzie, hii Mwinyi aliitambua. Mama Ramlat nae aliitambua ile sauti nyingine, ilikuwa ni sauti ya mpangaji wake, yaani mume wa Salome, akamwambia Mwinyi huyo alieingia ndio mume wa Salome, naamini wewe hujawahi kumuona.

Mwinyi alitikisa kiichwa kukubali Moyoni laishukuru kwa kuamini sasa anaweza kuwa amepunguza mzigo mmoja wa kero na usumbufu, hakuweza kuona tatizo lingine lolote, alitazama faida tu upande wake bila kuangalia hasara kwa upande wa pili.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Walikuwa wamelaliana vifuani wakiongea kwa mapenzi ya hali ya juu, mlango wa Mwinyi ukagongwa, akaenda kuufungua akijua ni mtu aliekuja kuleta mzigo wake toka kwa Salama, kumbe haikuwa hivyo, alimkuta Side ndio amesimama mlangoni, alishtuka sana na kuhisi mambo yameharibika, huenda Ramlat kaisha tibua.

Lakini kumbe wala! Ulikuwa ni wasiwasi wake tu, Side akamsalimia kwa bashasha na kumwambia nje kuna mgeni wake anamsubiri

“Ni msichana anasema ni mchumba wako, amegoma kuingia hapa ndani,”

Wakati Side akiongea hayo, Ramlat alikuwa yupo pembeni akisikia kila kitu. Mwinyi akahisi kuna kamchezo Salama kamchezea. Akashika simu kumpigia. Kabla hata hajapiga simu mlango waSalome ukafunguliwa na Salome akatoka akilia huku mume wake akiwa yupo nyumba na mkanda mkononi, hadi pale walipo Mwinyi na Side.

Kama maigizo vile, Salama akaingia na kwenda kumrukia Mwinyi shingoni kwa furaha. Salama hakupata mapokezi aliyostahili wala yale mapokezi aliyoyategemea, maana amezoea kupokelewa kwa aina tofauti kila siku za furaha pekee, sio majonzi

Akishangaa kumuona Mwinyi anazidi kuwa mpole, maana anamjua jamaa alivyo, Side akapumbaa, Salama akishangaa, Salome akapigwa na butwaa na mume wa Salome akabaki amebung’aa, wote walishindwa kuamini kwanini mgeni hapokelewi.

Akili ya Mwinyi ilisimama, akahisi kizunguzungu na kushindwa cha kufanya hasa baada ya kusikia Sauti ya Salama ikimuuliza yeye

“Mpenzi, hujafurahia kuniona?” na hata kabla Mwinyi hajajibu, Salama akawa akigeuka kulia na kushoto kuwatazama watu waliopo pale. Akamuona mume wa Salome na kumshangaa, mume wa Salome akamuuiza yeye Salama sasa

“We umekuja kufanya nini hapa?” yaani kama watu wanaojuana kitaambo, swali lile pia halikuwa na jibu maana karibu kila mtu pale alikuwa hajielewi.





Kama mtu angeweza kusoma mawazo yao pale, hata sijui angejifunza nini! Maana kila mmoja alikuwa na lake akilini mwake, Mwinyi aliwaza aibu ya kufumaniwa, mpangaji alihisi talaka, mume aikuwa na hasira ya kusalitiwa, Ramlat alikuwa na jazba ya kudanganywa na Mwinyi, Salama bado alikuwa hajielewi elewi.

Ni Side pekee alieweza kuweka wazi fikra zake na kuuliza huku akimtazama Mwinyi

“Kaka mbona mgeni hapokelewi mzigo wala kukaribishwa ndani?” hapo tena jibu likawa hakuna, ikalazimu sasa Side amuombe Mwinyi amkaribishe mgeni ndani. Mwinyi akawa anasitasita.

Akapeleka mkono kwenye begi ili alishike, lakini kabla hajaligusa, wakasikia

“Wewe bwana mdogo unajidai ni kidume sana eti? Mume wa Salome alimuuliza Mwinyi huku akimkusanya Singland kifuani,

Mwinyi akajikakamua na kuuliza

“Kwani vipi kaka?” Jamaa akapandisha munkari

“We mpumbavu nini? unajidai hujui sio? Yaani unampa mimba mke wangu, nakuuliza nawe unajidai kuniuliza ‘kwani vipi’ unajua uchungu wa mke wewe?” Mwinyi hakujibu

“Sasa leo mimi nitakufundisha adabu” akatupa ngumi mbili za haraka haraka zilizompata Mwinyi sawasawa na kumfanya kulelengeta.

Kauli ie ya Jamaa ilisikika na wote hivyo kumfanya Ramlat kukaa chini, Salama akashika kichwa, Side akaingilia kati na kuwatenganisha, maana palikuwa na kila dalili ya Mwinyi ndio kuumizwa. Maana hakuwa na hata nguvu ya kusogea, achana na kurusha ngumi.

Side kwa kusaidiana na jamaa yake wakawatenganisha na kumpeleka

Mwinyi hadi mlangoni kwake na kumtaka aingie ndani ili kuepusha shari zaidi, siku ya aibu.., ni aibu tu hata ufanyeje.

Mwinyi aligoma kuingia ndani ila Side kwa kushirikiana na jamaa yake walifanikiwa kumuingiza ndani. Sasa walichokiona humo ndani Side na Jamaa yake ndio aibu yenyewe. Ama kweli siku zote mwisho wa ubaya ni aibu. Side aishangaa kwa sauti ya juu

“Ha! Mama, hapa ndio kwa Bi Fatma?” wote wakasahau ugomvi wao na kuingia ndani akitangulia Salama, akifuatia Salome na mumewe na mwisho akaingia Ramlat.

Kile kitendo cha kuingia ndani tu na kumuona mama yake, Ramlat akazimia, hiyo iitokea baada ya kumkuta mama yake akionyesha dalili zote za kuonyesha yeye na Mwinyi wana mahusiano, wakamtoa nje na kuanza kumpepea huku wakimpa huduma ya kwanza.

Side hakuwa na papara, alionyesha uanaume hasa, akatoa simu na kuita gari ili wampeleke Ramlat hospitali iwapo hali itachelewa kurudi katika ubora wake kwa wakati. Kichwani mwake alihisi itakuwa ni mshituko tu alioupata baada ya

kuona tukio lile na hakuwa na hisia zingine zozote

Haikumchukua muda mrefu akazinduka, Mwinyi na wengine wote walikuwa wametoka chumbani wakiwa wamemzunguka Ramlat ila Mwinyi yeye alikuwa akizunguka huku na kule bila mwelekeo wowote.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Ramlat aliposhtuka na kuona watu wengi hakuchelewa kupata kumbukumbu hasa pale alipomuona Mwinyi na kuangusha kilio huku akisema

“Mwinyi umefanya nini sasa? Mimi umenipa mimba na kumbe hata mama nae ni mpenzi wako? Eeh Mungu, ni aibu gani hii?”

Watu wote wakasahau ya kwao yanayowasibu na wote kuguna kwa sauti moja ‘Haa’ kama walio ambiana. Na mlango nao ukafunguliwa kwa kasi, Anisa akaingia na kuhoji kuna nini.

Siku ya leo ilikuwa ni siku ambayo haikuwa na majibu kwa maswali yote yanayoulizwa, sasa busara ilimuishia Side, akachomoka na kumvaa Mwinyi mzima mzima. Alimpiga ngumi moja ya begani, alikuwa hawezi kujitetea kwa lolote siku hiyo.

Mume wa Salome aliona hili, akasogea na kumzuia Side kwa kusaidiana na Anisa aliefika punde na hakuelewa kilichokuwa kikiendelea. Waliwatenganisha na kisha Anisa akatoka nje na Side aliekuwa akitokwa na machozi ya hasira.

Salama nae kwa hasira akabeba begi ake na kutaka kuondoka, Mume

wa Salome akamzuia na kumsihi asubiri asiondoke kwanza, kisha akamwambia Mwinyi

“We Mwinyi nilikuamini sana na kukuchukulia kama mdogo wangu, kumbe ni nyoka, tena wewe ni Ibilisi kabisa,” Akamgeukia Salama na kumwambia

“Wakati nimefika ndani kitu cha kwanza kukiona ni hiki cheti cha maabara nikakichukua na kukisoma, dah! Nilishtuka mno, sasa nikishangaa kuona cheti kinaonesha mke wangu ni mjamzito wa mwezi mmoja na hali mie sikuwepo kwa miezi miwili, sikuamini kabisa,” akamtazama Salome

“Kipigo ndio kimemfanya huyu malaya amtaje huyu mbwa,” sasa aikuwa akimtazama Mwinyi kwa jicho la ghadhabu na kisha kuendelea

“Sasa kuanzia leo mimi nakubinafsishia huyu Nguruwe mwenzio, mtaishi pamoja, nawatakia maisha mema Kenge nyie!”

Jamaa akasema huku akimsukuma mkewe aliekuwa akilia huku akiomba msamaha, Side na Anisa nao wakawa wanaingia, Salama chozi la hasira linamtoka, Mwinyi kajikunyata tu chini hana la kufanya

Side aliyasikia maneno ya Mume wa Salome, nae akaendeleza

“Mi siwezi kumuacha hivihivi huyu changudoa wa kiume, nitamburuza kortini ili aweze kujua thamani ya watoto wa shule” akamgeukia mama yake na kumwambia

“Mama kwa aibu uliotupa leo, nalazimika kukwambia kwamba, tangu sasa nahama rasmi ndani ya nyumba hii, baki wewe na mwanao, nawatakia maisha mema,”

Side kabla hajatoka, mama yake akamdaka mkono, akautupa huko. Kwa bahati tena akamdaka mguu na kumbembeleza huku akilia na kumtaka asiondoke, Side hakukubali na aliendelea kushikilia msimamo wake uleule.

Upande wa Salome na mumewe nako hali haikuwa shwari, alipokuwa akitaka kuondoka alimsukuma mkewe na kujigonga ukutani na kupoteza fahamu, chumba kikageuka wodi, baadhi ya majiran wa karibu wakaanza kusogea taratibu kama ilivyo ada huko uswahilini.

Salama akaanza kutoka pale nyumbani, Mwinyi akahisi kama kuna sauti ikimwambia asiruhusu hali ile imtokee, hali ya Salama kuondoka! Akapata ujasiri na kumfuata ili apate kumzuia, akasimama mbele yake na kupiga magoti akimuomba asiondoke.

Alichokifanya Salama ni kumtandika kofi la maana sana Mwinyi na kumtukana pia kadri alivyoweza. Mwinyi alikuwa ni bwege kweli siku ile. Alikuwa ni mdogo mdogo siku ile, pamoja na Salama kumuita kila jina baya na kumtukana kila aina ya tusi, lakini bado aliendelea kumpigia magoti akimsihi asimuache.

Wazee wawili wa kiume na mmoja wa kike wenye busara zao

wakaingilia kati na kuwaketisha chini wote. Ina maana ikawa ni kikao cha dharula, wakaulizwa tatizo ni nini hadi pale pamekuwa hapatoshi? Salama, Side na mume wa Joy, Kila mtu akataka aanze kusema yeye.

Nafasi akapewa Mama Ramlat ndio aanze kuongea, kwa aibu alishindwa kuongea lolote, hivyo bahati ikaangukia kwa Side, akaelezea kila kitu kilichomuhusu Ramlat

“Ilifikia hatua wazee wangu, mimi namuuliza Ramlat mbele ya Mama kuwa mimba hii ni ya nani? Ramlat ananitaja mie, iikuwa shida yake ni kunipa aibu kwa sababu nilikuwa nikimchunga sana kwa faida yake nae alikua hataki. Kwa hiyo basi...” akamalizia kwa kuweka wazi msimamo wake.

Akawaambia wazee kuwa ni lazima ampeleke Mwinyi mahakamani ili kutoa somo kwa wakware wengine wanaopenda kuwaharibia wanafunzi masomo yao. Na anahama pale nyumbani kwao ili kuikwepa aibu kubwa iliyompata

Mtu wa pili kuongea aikuwa ni mume wa Salome, yeye alianza wa kusema kuwa alimpigia simu mkewe juzi na hakuwa hewani siku nzima, jana akampigia tena, simu iliita sana lakini haikupokelewa, akapata wasiwasi na ndio sababu akapanga safari ya dharula kurejea nyumbani.

“Nikiwa garini nikakutana na huyu binti... (huku akimuonesha kwa kidole Salama) ila hilo tuliache, nilipofika hapa nyumbani mke wangu aliponiona akashtuka, mimi nikajiuliza vipi, mbona sio kawaida hali hii?” akajisachi kitu Fulani kisha akaendelea

“Kutokana na kumkumbuka sana mke wangu, nikamsogelea na kumkumbatia. Ile kumkaribia tu, nikashtukia tumbo lake, si unajua mkeo ni mkeo tu, hata kama awe na mabadiliko kiasi gani we lazima ujue” wazee wakatikisa vichwa kukubali na ili kumpa nafasi ya kuendelea

“Ajabu ya Mungu, hata kabla sijamuachia nikakiona hiki cheti...” jamaa akatoa cheti cha daktari kilichoonyesha majibu ya kuwa mke wake ni

mjamzito na kuwapa wazee wakitazame

Wazee wakashika vichwa, baada ya kujua kuwa tayari Mwinyi kaisha wapachika mimba wale wasichana wawili. Yaani Salome, mke wa jamaa na Ramlat pia, hapo ilifichwa juu ya Mama Ramlat kuwa na uhusiano na Mwinyi, liibaki kuwa ni siri ya walewale waliomo ndani ya nyumba ile. Kisha Salama akapewa nae nafasi ya kuongea.

Hapo ndio walichoka kabisa hasa pale Salama alipowaambia yeye ni mchumba wa Mwinyi na yupo nae kwa zaidi ya mwaka sasa na amekuwa akimjali kwa kipindi chote japo wapo mbalimbali, yeye akiwa anaishi Mwanza.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Anisa aliekuwa nyuma ya wakati, sasa nae akawa amelielewa somo, alishangaa uzuri wa Salama, akamtazama Mwinyi na kutikisa kichwa, Salama akaendelea

“Hadi wakati anahamia hapa miezi mitatu iliyopita alinijulisha na pia alinieleza kuhusu kero za kinadada hawa wawii japo hakunionesha, lakini nimeweza kuwatambua kutokana na maelezo yao”

Mzee mmoja akamuuliza alichukua uamuzi gani baada ya yeye kujulishwa kero zile, Salama akajibu kwamba alimwambia atulie na asisikiize sana maneno ya kinadada

“Sasa ameamua kunidhalilisha..(akamtazama Mwinyi) nakuchukia sana” kisha akamsonya na kugeuka pembeni, Mwinyi akasimama na kumsogelea akimuomba msamaha, bado Salama hakutaka hata kumuangalia

Akanyanyuka na kutaka kuondoka zake, wazee wakamzuia na kumuomba amsamehe mchumba wake, maana alikuwa kaisha mwambia ukweli tangu awali.

“Kwa kweli kama ingekuwa ni hawa kinadada peke yao, mi

ningemsamehe, ila na huyu mama tena.. Hapana! Kwa sasa simpendi kabisa Mwinyi, namchukia mwanaume baradhuli mkubwa! Mxchs”





Sasa ndio wazee wakashtuka na kujua kuwa pamoja na wale mabinti wawili, pia Mwinyi alikuwa na uhusiano na Mama Ramlat. Bibi aliekuwepo pale akamuuliza Salama ilikuwaje hata akaweza kufika pale? Maana alionekana kama kaja bila taarifa.

Salama alikiri ni kweli alifika pale bila taarifa kwani pale ni kwake

“Siku niliyopanga kuja huku sikumwambia Mwinyi juu ya safari yangu, maana kila mara huwa ninamwambia, sasa awamu hii nikataka nimshitukize nikiamini atafurahi. Hivyo nilimuomba anielekeze, nae alifanya hivyo akiamini kuna mtu ninataka amletee mzigo...” akameza mate na kuendelea

“Sasa nikiwa Stand leo asubuhi kwa safari ya kuja huku, nikakutana na bwana huyo hapo...” akamnyooshea kidole mume wa Salome

“Kwanza hata nae namshangaa kujidai kusema eti anamuacha mke wake kwa Mwinyi, wakati yeye alijitahidi sana kunitongoza kwa kila neno tamu na ahadi kemkem tangu mwanzo wa safari, na hilo umemwambia mkeo? (huku akimtazama mume wa Salome) we bwana mi si nina kuuliza?”

Wote wakageuka na kumuangalia mume wa Salome, hata Salome alionekana kupata nguvu kidogo na mumewe alionekana kumtazama Saome kwa jicho la chinichini. Salama akaendelea kuwapa kisa

“hakika huyu bwana nilimkatalia kwa kulinda heshima ya Mwinyi ambae sikujua kama huku ananisaliti, dah! Yaani nyinyi wanaume.. sina hamu,” alimaliza Salama na kuweka mikono shavuni.

“Lakini hujamaliza binti, nini kilifuatia baada ya kufika hapa Tabora mjini?” Aliuliza Anisa ambae alikuwa na shauku nae ya kutaka kujua kilichofuatia

“Unasikia dada yangu, baada tu ya kufika stand kuu, huyu

bwana akaniambia kuwa yeye ni mwenyeji n anaka maeneo ya huku, sikutaka kuongozana nae yeye akachukua bodaboda nami nikachukua Taxi, kwani mimi si mwenyeji. Nikamuelekeza dereva alienileta hadi hapa na kukutana na kisanga hiki…” Salama kamalizia kwa msonyo mkali.

Hapo sasa hata wale waliokuwa hawajaelewa kwanini Salama yupo pale, sasa walielewa, Anisa alinyanyuka na kwenda kumpa pole Ramlat na kumnyanyua. Kuna kitu wote wale wawili, yaani Anisa na Ramlat walitaka kuongea ila walijizuia.

Anisa alimtazama Mwinyi kwa jicho la chuki japo wote hawakujua ni

kwanini alimtazama vile, zaidi ya kufikiri kuwa ameungana nao kwa ajii ya kitendo chake cha kuzini na wanawake wale kwa wakati mmoja, kumbe nae alikuwa na yake yanayomsibu ila tu alijizuia tu kuyaongea tu.

Wazee wakaomba wayaache yote yae kwa usiku ule na kesho asubuhi wayazungumze huenda wakapata muafaka na kuyamaliza. Ramlat akatoka hadi chumbani kwake akilia. Kutokana na busara za wazee wale na maneno ya SalamaMume wa Salome alimchukua mkewe japo kwa shingo upande na kuingia ndani kwao.

Side na mama yake wakaelekea ndani kwao pia, ila Side aligoma kabisa kulala pale akasema ni heri akalale guest usiku ule mmoja na siku ifuatayo ana hakika tu atapata nyumba kwa madalali

Wakabaki Mwinyi na Salama pekee, Anisa tayari alikuwa kaenda ndani na Ramlat. Salama alikuwa na hasira vibaya, kwa dharau akamtazama Mwinyi na kushika begi lake na kuanza kutoka. Mwinyi hakuwa na uwezo hata kidogo wa kumzuia asiondoke.

Nae akaingia chumbani mwake na kuanza kutafakari jinsi siku ile ilivyokuwa ni mbaya hadi kufikia kujuta kwa yote yaliyotokea, alitamani iwe ni ndoto, lakini haikuwezekana kuwa ndoto, maana ile ilikuwa ni hali halisi.

Wakati Salama akitoka, getini alipishana na Anisa akiingia, hakuna aliemsemesha mwenzie, walitazamana tu. Anisa alijua yule Salama ni nani, lakini Salama hakumjua binti Yule ni nani hata jina pia.

Moja kwa moja Anisa aliingia hadi chumbani kwa Mwinyi, tena hata bila ya hodi na kurudisha mlango, aliamini hakuna tatizo lolote kwa muda ule, maana kila mtu tayari alikuwa na majanga yake, hakuna wa kushughulika na ya mwenzake

Anisa ambae siku zote Mwinyi alikuwa akimchukulia kama mtaratibu sana, leo alitoa makucha yake. Kwa sauti ya polepole lakini ya hamaki, akaanza kumsimanga

“Nimekuona shujaa wa kiume, wewe ndio mwanaume wa shoka, ulianza mama, ukaja mtoto, ukafuatia jirani na mwisho wifi yao, hongera sana kidume, haya sasa mwisho wake je? Aibu tupu! Loh... mtu wewe sijui u mchafu kiasi gani? Nimekuchukia, sitamani hata kukuona,” Anisa alisema na kusonya.

Mwinyi hakusema kitu, alikuwa akimtazama tu, maana alimshangaa, kwani wote aliowataja pale yeye wala hakuwa akiwapenda. Naweza kusema hakuna hata mmoja ambae alikua ana chembe ya upendo, labda Ramlat pekee. Anisa alipomaliza kumwaga sumu yake akatoka na kubamiza mlango.

Side baada ya kugoma kulala pale nyumbani kwao, alitoka hadi nje ilipo gari ya Anisa ili kumsubiri Anisa alieingia ndani, lengo ikiwa ni kwenda nae akamuache guest aupitishe usiku ule mbali na kwao ambapo sasa alipaona ni kama najisi.

Akiwa pae nje anamsubiri Anisa, ndio akatokea Salama akiburuta begi lake. Side akamsogelea na kumuhoji anapoelekea. Salama hakuwa na jibu zaidi ya kusema kuwa hakuna kingine atakacho zaidi ya kufika guest yoyote itakayokuwa jirani na stand ya mabasi ili alale hadi siku ifuatayo arejee Mwanza.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Kichwani mwanaume akajiongeza… ‘Yes nafasi si ndio hii? Ndege Tausi huyoo kavunjika bawa, hawezi kuruka, ni wa kukamata tu na kuchinja, siwezi kumuacha mtoto mzuri kama huyu akalale guest peke yake.’

Hayo ni baadhi tu ya mawazo yaliyopita kichwani kwa Side, alifika mbali zaidi kwa kufikiria kuwa ile ndio nafasi ya yeye kulipiza kisasi ili Mwinyi ajue nae ni kiasi gani aliumia kwa kitendo chake alichokitenda.

Salama akaona hapati jibu akamshitua Side kwa kumuita

“Kaka vipi? Hakuna guest unayoifahamu maeneo ya stand?”

“Ah samahani Aunt, ngoja Anisa aje nitakupeleka Guest nzuri mno wala usihofu, nina mawazo mengi sana samahani bi dada.”

“Pole sana na wala usijali kaka yangu, hayakuti wanyama hayo, yote haya yapo kwa ajili yetu wana adamu,” aliongea Salama akitazama saa yake ya mkononi.

Anisa akatokea na kukuta Salama na Side wanaongea pembeni ya gari lake, moyo ukamlipuka, japo anamwamini Side.., lakini uzuri wa Salama ukamnyima amani, akawahoji vipi? Side akamueleza hali halisi juu ya Salama kutaka guest.

Akawa ameelewa lengo la mkutano wao ule, kisha akamuuliza nae vipi? Side nae akamjibu kuwa hatolala pale. Kengele ya tahadhari ikalia kichwani kwa Anisa, akamuuiza Side atapenda kulala guest gani, Side nae akawa mjanja

“Jambo la kwanza Salama ndio apate pa kulala maana yeye ndio mgeni, mimi nitafuatia, uongo Salama?” kabla hajajibu, Anisa akadakia

“Ok! Hio sio tatizo, niachieni mimi mambo yote, Side ingiza basi mzigo wa Salama garini,”

Wakaingia garini na kuondoka. Anisa aliipeperusha vibaya kabisa ndoto ya Side kumpata Salama sio tu kwa siku ile, bali kwa kipindi chote atakacho kuwepo Tabora kama ataendelea kuwepo.

“Side tutakuacha pale Classic hotel nami na Salama tutaendelea mbele,” kabla Side hajajibu

“Aunt Salama pole sana kwa uliyopambana nayo leo na kama hutajali mimi ninaomba leo ukalale nyumbani kwetu, tafadhali usikatae,”

“Nashukuru sana dada Anisa, sikutegemea kukutana na kitu kama hiki, kwa hakika kimeniumiza sana,”

“Pole, pole sana dada Salama,”

“Ahsante, ila dada Anisa, suala la kulala kwenu mimi naomba unisamehe,”

“Kwanini Salama?” Aliuliza huku akimtazama kwa mshangao

“Huoni kuwa ni usumbufu dada yangu?”

“Ha! Salama kwani tunakubeba mgongoni? Acha mambo ya ajabu wewe.”

Wakati Salama akionyesha kukataa ofa ya Anisa, Side alikuwa yupo upande wake japo hakutaka kujionesha. Mwishoni akakubai kulala kwa Anisa na hivyo ndivyo ndoto ya Side ya kumpata Salama ikawa imeishia njiani.

Walifika Guest na Side akashuka na kuagana nao, alitamani kuchukua hata namba, lakini angeiombaje na Anisa yupo? Akawa mpole, akamkiss Anisa na kuachana nao wao wakiekea kwa kina Anisa nae akaingia guest.

Safari ikaishia ndani kwa kina Anisa. Mapokezi yalikuwa si haba kifupi yalikuwa ni mazuri. Alitambulishwa ka wazazi wa Anisa kama rafiki kipenzi na ndio ametoka kumpokea na gari huko stand mpya akitokea Mwanza ambapo ndipo anapoishi.

Anisa aliwadanganya wazazi wake kuwa Yule ni rafiki yake waliokutana kwenye mtandao, yeye ameanza kuja na kuna wakati na yeye atapaswa kwenda kumtembelea Mwanza. Wazazi wa Anisa waimkaribisha vizuri sana na kumsihi ajione kama vile yupo nyumbani kwao. aliwashukuru.

Ajabu hadi muda ule Salama alikuwa hajajua huyu Anisa ni nani, maana hajapata muda wa kutambulishwa japo walikutana kule kwa Mwinyi. Walipokuwa wakila chakula cha usiku, Salama akamuuliza yeye ni nani. Anisa akamjibu kuwa wataongea zaidi siku ifuatayo, leo apumzishe tu akili yake mapema.





Baada ya hatua zote muhimu kama kula na kuoga, Salama akaonyeshwa chumba nadhifu na kizuri, akaingia kulala. Hakika pamoja na kero zote laizozipata siku ile, huwezi amini usingizi ulimpitia mapema sana, na wala hakuwa akigeuka geuka mara kule mara huku, liionyesha kuwa alichoka sana.

Usiku uikuwa ni mfupi sana kwa Salama lakini ulikuwa ni mrefu mno kwa Mwinyi. Aijaribu kumpigia simu Salama ili apate kujua ni wapi alipo na kama yupo Salama, jibu likawa halipatikani alijuta ni kwanini

hakufuatilia mapema na kujua ni wapi alipoelekea Salama usiku ule

Usalama wa mpenzi wake Salama, ulimfanya apoteze amani hata ile kidogo aliyokuwa nayo, akaamua kumpigia simu rafiki yake aitwae Mgasi na kumueleza yote yaliyojiri tangu jioni ya siku ile hadi muda ule.

Mgasi hakuwa na cha kumshauri bali ni kumpa mawazo tofauti, huo ndio msaada pekee alioweza kumpa na kumwambia nyumba ile anatakiwa atoke haraka iwezekanavyo, wazo lile Mwinyi wala hakulipinga, akaliunga mkono

Bila ya kujai muda ilikuwa ni usiku mnene, akampigia simu dalali na kumwambia afanye kila awezalo ampatie nyumba nzima na sio chumba tena, na iwe ni haraka. Dalali akamuhakikishia kumpatia atakacho kabla ya saa tatu asubuhi.

“Nipitie muda huo ili twende ukaione nyumba yenyewe muda huo, ipo maeneo ya National,”

Mwinyi akapata ahueni na kumpigia simu Mgasi na kumwambia ajitahidi kesho saa moja asubuhi aende pale stand ya zamani akachukue Fuso na aelewane nae kabisa kwa ajili ya kuhama toka Bachu hadi National.

Mgasi akishangaa na kumuuiza Mwinyi kama hatoipenda hiyo nyumba au akiikuta labda tayari imepangishwa je? Mwinyi

akamwambia pale alipo tayari amejipanga kivingine.

“Kivipi Mwinyi? Mbona sikuelewi?”

“Mgasi utanielewa tu, tatizo lako wewe una haraka, hebu fanya nilichokwambia kwanza,”

Asubuhi palikucha vizuri kabisa, Anisa aianza kuamka na kwenda kumtazama mgeni wake, akamkuta bado kalala, akamuacha na kwenda kurekebisha mambo Fulani. Mambo ya chai na maji moto ya kuoga. Baada ya muda nae akaamka na kutoka.

Walikutana Sitting room, walisaimiana kwa kukumbatiana kwa furaha.baba yake Anisa alitabasamu kutokana na muonekano wa wale mabinti, muonekano wa kuwa na mapenzi ya kisichana. Waiandaa kia kitu na baada ya kukamilisha kila kinachopaswa kufanywa kabla ya kufungua kinywa.

Sasa ndio wakakaa mezani kupata istaftah. Chai ilikua nzuri sana, sio kwa sababu ilipikwa kwa ustadi, bali pia ilinywewa na watu zaidi ya wawii kwa wakati mmoja, hata wazazi wa Anisa walionekana kuvutiwa na chai ile. Mama Anisa akavunja ukimya

“Naona umelala kwelikweli, mchoko utakuwa umepungua,”

“Sio umepungua mama, umeisha kabisa, nafikiria mwingine sasa!”

“Mwingine? Nini ama sijakuelewa?” Baba Anisa akauliza kwa mshangao, kikombe mkononi.

“Ah! Baba si unajua barabara yenu hapa kati ya Tabora na Nzega ilivyo mbovu? Sasa leo tena si nitafika Mwanza hoi?”

“Ha! Salama, unataka kuondoka leo hii?” Anisa aliuliza kwa shauku huku wote wakimtazama Salama

“Ndio Anisa, nikae kufanya nini sasa hapa rafiki yangu?”

“Haiwezekani Salama, ulikuja Tabora kupumzisha akili, hivyo inabidi...”

“Hapana Anisa, wewe unajua kila kitu, acha tu mimi niende,”

“Kwa hilo Salama utanisamehe, siwezi kukuruhusu uondoke leo wala kesho, nipe angalau wiki moja tu ya kukaa nawe!”

Baba Anisa akamuunga mkono mwanae kwa kutikisa kichwa

“Ha Anisa, wiki? Utakuwa unatania wewe!”

Mjadala ulikuwa mrefu sana na kwa msaada wa wazazi wa Anisa, wakafanikiwa kumshawishi Salama abaki Tabora kwa siku tatu, sasa akiwa ni mgeni wa Anisa, sio tena mgeni wa Mwinyi.

Sababu iliyowafanya hata wazazi wake waombe Salama aendelee kuwepo ni ile furaha walio muona nayo mtoto wao tangu usiku uliopita alipowasili pamoja na Salama. Hawakujua ni kwa nini, lakini walitamani hali ile iwe ni kila siku.

Swali hilohilo ungelielekeza kwa Anisa, hakika angekosa jibu kabisa, maana yeye lengo la kumchukua Salama ilikuwa ni kumuepusha na Side ambae alionekana tayari ameisha mtamani, ajabu kufika nae pale

nyumbani ametamani tu aendelee kuwepo.



MGASI ANAMSALITI MWINYI.



Saa moja na nusu asubuhi, tayari Fuso iikuwa imepaki mlangoni kwa Mama Ramlat, Mwinyi kwa kusaidiana na Mgasi na wapagazi watatu wakawa wakipakia vitu garini. Hakuna hata mmoja aliewasemesha, wote waliona na kukaa kimya na kurudi vyumbani mwao.

Mume wa Salome kumbe nae tayari aliisha toka asubuhi na mapema akimuacha mkewe ndani na kumwambia atakaporudi asimkute, abebe chochote atakacho hata kama ni chumba kizima, kitu ambacho Salome hakuwa tayari, alikuwa bado akimpenda mumewe japo alimsaliti.

Kule chumbani Salome alichungulia tu dirishani vitu vikitolewa, alitamani kujua ni wapi Mwinyi anahamia, lakini ilikuwa ni vigumu sana kumuuliza, kwani nyumba nzima kila mtu alikuwa anamuonea aibu mwenzie, hivyo alibaki anaungulia ndani kimya kimya.

Kutokuwepo na amani ndani ya nyumba ile kukasababisha hata Mwinyi akose mtu wa kumuaga baada ya kufungasha virago vyake. Kimya kimya akaacha funguo palepale kwenye kitasa na kuingia garini, safari ikaanza hadi kwa Dalali aliewapeleka hadi National.

Walifika pae ilipo nyumba na kwa bahati nzuri ikamvutia, wakafanya maongezi na mwenye nyumba kwa mtandao, wakateremsha vitu na kuvipanga, nyumba yenyewe ilikuwa bado ni mpya, ndio kwanza mafundi wamemaliza kuijenga

Kufikia mchana wakawa wamemaliza mchakato wao na kuketi sasa ili kupumzika. Mgasi ndio akapata wasaa wa kumuuliza Mwinyi ingekuwaje kama wangekosa nyumba ile nao tayari wamepakia vitu garini. Mwinyi akamjibu huku akitabasamu

“Nilidhamiria kwenda kuviacha vitu vyote nyumbani iwapo ningekosa nyumba hii na hata nyingine yoyote kuliko kulala nyumba ile japo kwa usiku mwingine mmoja tu,” Mgasi aliridhika na kumuaga Mwinyi kuwa watawasiliana baadae na kurejea kwake.

Mwinyi akautumia muda huo kwa kujipumzisha, akachapa usingizi kwa takriban masaa mawili hadi alipoamshwa na muito wa simu yake. Alikuwa ni Mgasi akimuuliza wanaenda wapi jioni ya siku ile? Mwinyi

akamwambia ni heri waende NYATI PUB wakapate bia moja moja.

Wakakubaliana wakutane pale saa 11 jioni bila kukosa. Mwinyi wala yeye hakutakiwa kutumia usafiri, maana ni karibu na kwake, Mgasi ndio aiazimika kupanda Daladala hadi huko kwenye miadi yao.

Alasiri Anisa akamtoa Salama kwa matembezi ya jioni. Nia ya Anisa ilikuwa ni kumueleza siri Fulani iliyokuwa ikimuumiza moyoni tangu usiku uliopita, na ndio sababu hasa iliyomfanya amng’ang’anie na kumzuia asiondoke na pia ndio sababu ya kumtoa jioni ile ili wakaongee

Mwinyi wakiwa na Mgasi wanakata maji ya rangi ya mende, Mgasi akatoka na kuelekea upande wa pili ili kuagiza nyama choma, hapo akamuona demu bomba sana, akamtamani, akamsogelea na kumsemesha, hakujibiwa lolote, akarejea ndani na kumwambia Mwinyi juu ya mrembo huyo aliemuona.

Mbiombio hadi kwa Mwinyi na kumuita kwa jina la Fundi, naam, ni fundi hasa Mwinyi kwa kina dada ni hatari mno.

“Fundi mshikaji wangu ni nouma, kuna demu nimemuona, ni mkali kweli kweli, we bwana si mchezo, lakini bubu”

“Yupo wapi? Halafu wewe usidanganyike, huenda ni mavazi tu yale yamekaa mahali pake,”

“Hamna wewe, unafikiri we unaweza kumfananisha na nani Yule sijui… Ramlat? Wapi... huyu ni kifaa, tatizo ni bubu!” aliongea Mgasi kwa msisitizo.

“Bubu kivipi? Kwani ulirusha kete?”

“Eenh, hakujibu hata salamu zaidi ya kubinua midomo yake,”

Wakati wao wakimzungumzia binti ambae Mgasi amemuona, Anisa nae alikuwa akizungumza na Salama kwa kituo, muda ule ndio aliutumia kwa kujitambuisha yeye ni nani, maana aliamini kabisa kwamba Salama hamjui. Hivyo alimwambia yeye ni nani na kivipi anamtambua Mwinyi.

Hakutaka kuulizia uhusiano uliopo kati yao, yaani kati ya Salama na Mwinyi, maana tayari aliisha usikia.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Salama kuna baadhi ya mambo watu hawapaswi kuyaigilia, likiwemo suala la mapenzi, nasema uongo?” Anisa alimuuliza kimtego ili aweze kujua kama wapo nae pamoja.

“Ni kweli Anisa, maana wapendanao wakikosana kwa sababu ya mtu fuani, kisha baadae wakaelewana, huwa ni aibu kwa mtu Yule.”

“Sawa kabisa. Ila kwa suala la jana Shosti, sihitaji ruhsa yako kuliingilia, bali najua ni kiasi gani Mwinyi amekukosea, lakini unapaswa kumsamehe dada Salama,”

“Kamwe haitotokea, mbona mimi tayari nimeisha mfuta kichwani mwangu dada Anisa?”

“Kwanini imekuwa ni haraka hivyo Dada Salama?”

Hakupata kile alichokuwa akikihitaji Anisa, pamoja na jitihada zake zote za kumshawishi, lakini aligonga mwamba na hatimae Anisa akakubali kushindwa, maana hata nae alikuwa akijiuliza ni kwanini anatafuta suluhu yao wakati hajatumwa na yeyote?

Salama aijiuliza kama Anisa katumwa na Mwinyi? Lakini nae akashindwa kumuuliza. Akabaki kafa na tai shingoni. Kumbe nia ya Anisa, haikuwa kuwapatanisha, bali alitaka kupima maji kabla hajadumkia.









ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog