akimwambia,“Nyamaza, usituletee ujinga humu ndani”Muda huo huo wazazi wao nao waliwasili kwahiyo waliona Erick alivyomzaba vibao Daima, basi Daima alikaa chini na kuanza kulia huku akisema kuwa nyumba yote ile yani Erick, Erica na Vaileth wamemchangia na kuanza kumpiga, baba Angel hakutaka kusikiliza zaidi kwani muda ule ule alimwambia Vaileth akalete nguo zote za Daima, basi Daima alianza kuomba msamaha pale kuwa abaki,“Hapana huwezi kubaki hapa ,si salama tena kwako kwa hali yako hiyo. Usituletee balaa”“Naomba mnisikilize basi”“Tukusikilize nini, kama wamekuchangia wote na kukupiga si balaa hilo!! Sitaki matatizo mimi”Vaileth alileta zile nguo za Daima na muda huo huo baba Angel alimchukua Daima na kuondoka nae kwani aliamini kuwa Daima anapafahamu kwao kwahiyo atamuonyesha tu, hakutaka kwenda na mke wake kwani aliona ni vyema kwa mke wake kukaa na mtoto wao mdogo ambaye wamemuacha muda kidogo.Basi mama Angel alibaki pale na kuanza kuuliza vizuri ambapo Erica alimuelezea jinsi Daima alivyokuwa akitukana,“Sitaji hayo matusi mama maana na mimi nitakuwa nimetukana, ila hafai kabisa huyu mtu”Basi walikuwa wakiongea tu pale huku mama Angel akimngoja mumewe arudi kwanza ndipo waweze kwenda kulala.Baba Angel aliondoka na Daima huku akimtaka amuelekeze wanapoishi, basi Daima alienda nae na kumuelekeza sehemu nyingine kabisa, na walipofika alidai sio hapo na kumuelekeza sehemu nyingine na muda ule ulikuwa ni usiku yani hadi baba Angel alichukia sana na kuanza kumfokea,“Una matatizo gani wewe binti, kwanini uananizungusha hivi mtu mzima kama mimi? Hebu acha ujinga huko nionyeshe kwenu nikupeleke la sivyo nakuacha popote”Daima akamuelekeza sehemu nyingine baba Angel, walienda na kufika hiyo sehemu, kisha Daima alimuonyesha nyumba ambayo wanatakiwa kuingia, basi wakashuka kwenye gari maana baba Angel alitaka amkabidhi huyu binti kwa wazazi wake kabisa.Kabla ya kuingia kwenye hiyo nyumba, baba Angel alishtuka kidogo kwani mbele ya ile nyumba paliandikwa pembezoni yake, ‘LODGE’Baba Angel alishtuka sana na kumuangalia Daima kwa hasira,“Yani wewe mjinga unanileta Lodge?”Baba Angel kwa hasira akamnasa kibao Daima, muda huo Daima alianza kupiga kelele nyingi,“Ananibaka, ananibaka”Watu wa karibu walifika eneo lile na kuanza kumshangaa baba Angel. Kabla ya kuingia kwenye hiyo nyumba, baba Angel alishtuka kidogo kwani mbele ya ile nyumba paliandikwa pembezoni yake, ‘LODGE’Baba Angel alishtuka sana na kumuangalia Daima kwa hasira,“Yani wewe mjinga unanileta Lodge?”Baba Angel kwa hasira akamnasa kibao Daima, muda huo Daima alianza kupiga kelele nyingi,“Ananibaka, ananibaka”Watu wa karibu walifika eneo lile na kuanza kumshangaa baba Angel.Kwakweli kwa muda huo baba Angel hakujua cha kufanya na aliona kuna wananchi wengine wakija na gadhabu huko akaona isiwe shida, ilibidi afanye maamuzi ya haraka kichwani maana aliona hapo kujitetea itashindikana, muda ule ule aliingia kwenye gari na kuondoa gari lake kwahiyo alimuacha Daima akiwa pale pale na wale watu huku baadhi yao wakirushia mawe gari la baba Angel, ila alifanikiwa kuondoka kabisa eneo hilo.Daima ndio alibaki pale na wale watu huku akilia na kusema kuwa yule baba alimkuta njiani na kumpa lifti halafu alikuwa akimlazimisha kufanya nae mambo machafu, kwahiyo walimuhurumia sana, halafu msamaria mwema mmoja akajitokeza ili kwa usiku huo Daima aweze kulala kwake halafu kesho yake ndio aweze kurudi nyumbani kwao.Basi yule mama alienda na Daima nyumbani kwake, ila Daima alionekana kulia tu,“Nyamaza binti, cha kushukuru ni kuwa hakuweza kukubaka. Yani wanaume ni wajinga jamani. Sasa mbaba mtu mzima vile atake kwenda kulala na wewe kitoto kidogo? Wewe si sawa tu na binti zake jamani! Mbona haya mashikolo mageni”Mama mwingine akamuuliza Daima,“Kwahiyo yule baba humjui? Na usiku huu ulitoka wapi binti?”Daima alikuwa akilia na kuanza kuwaelezea,“Yani mimi nina mikosi sana, kuna nyumba ya ndugu yangu Fulani nilikuwa nakaa, basi mtoto wake wa kiume akanitaka kimapenzi nikamwambia mimi siwezi maana wewe ni ndugu yangu. Akachukia na kusema maneno ya uongo kwa wazazi wake, ndipo waliposema usiku huu huu nirudishwe kwetu, sikuwa na tatizo maana kwetu kupo. Nikapanda kwenye gari na yule kijana, akanipeleka mahali na kunitupa huko halafu yeye akaondoka yani nikakosa uelekeo, ndio akaja huyu baba na kusema kuwa atanisaidia, basi nikapanda kwenye gari yake ila ndio hivyo akawa anataka kunibaka ndani ya gari, nikamuomba tutafute chumba kwani nilijua akitafuta chumbva naweza pata msaada kwa wananchi. Tukafika pale, ndio akanishika mkono na kunilazimisha kuingia nikawa nakataa ndio akaninasa kibao, ikabidi nipige kelele”Daima alikuwa akiwaonyesha alama ya kibao kwenye shavu lake, na kweli alitokwa na alama kwani baba Angel alimzaba kwa hasira sana, basi wale wamama walimuhurumia sana Daima na kulaani vikali vitendo vya wanaume huku wakisema,“Yani wanaume ni wanyama, hawafgai kabisa wana roho mbaya sana, hebu ona binti mdogo hivi kafanyiwa unyama na wanaume”“Nikwambie wanaume ni viumbe hatari sana, tunaishi nao tu duniani ila wanaume jamani, ptuuuuu. Siwataki hata kidogo”Basi walimbembeleza Daima pale na kumtaka kwenda kulala tu kwa muda huo huku wakimuahidi kuwa kesho yake watamsaidia kumpeleka kwa wazazi wake, Daima alitulia tu ila alielewa madhara ya uongo alioutengeneza pale.Baba Angel alirudi nyumbani kwake usiku sana, tena alirudi huku akionekana kama akili yake ikikosa mawasiliano vile, alimkuta mkewe tu ndio yupo kumsubiri, alivyorudi mama Angel alifurahi kwa uwepo wake na kwenda nae moja kwa moja chumbani huku akimpa pole na kumuuliza kilichomfanya na kumchelewesha vile,“Wazazi wa Daima walikuwa wakigoma kumchukua mke wao nini?”“Yani bora hata ningefika kwa hao wazazi wa Daima kuliko alichonifanyia huyo Daima”“Kakufanyaje tena?”“Jamani, kanizungusha mji wote kila mahali tukifika sio hapo kwetu, ananionyesha pengine, hadi nikachukia sasa, akanipeleka ehemu moja hivi kumbe ni Lodge, khaaaa kushuka kwenye gari naona lodge nikachukia sana, na kumnasa kofi Daima, weee asianza kupiga kelele kuwa nataka kumbaka, watu wakajaa, siunjaua wananchi tena wanione na mtoto mdogo kama Daima wangenielewa wapi, niliamua tu kufanyua akili ya haraka haraka hata sikuongea kitu zaidi ya kupanda kwenye gari na kuondoka, wananchi wale walipiga mawe gari langu lakini sikujali, kwakweli huyo Daima sitaki hata kumuona na hapa nyumbani kwangu asije tena mtajuana mambo yenu na huyo mtoto wenu wenyewe, mtajua wewe na dada yako mtakachokifanya kwa huyo Daima kwakweli nimeshindwa, khaaaa huyu mtoto hapana aiseee”“Dah! Pole sana mume wangu, pole kwa hayo yaliyokupata, bora ningempeleka mwenyewe. Mtoto mjinga sana huyo jamani loh! Sikutegemea kama angefanya kitu cha namna hiyo”Mama Angel aliamua kutumia muda huo kumtuliza mume wake, kwani alitambua wazi kuwa mambo hayo yamemchanganya sana mumewe, basi akamtuliza pale hadi mwishowe wakaamua kulala tu.Leo wakiwa shuleni, karibia na muda wa kutoka, siku hii hakukuwa na masomo mengi kwahiyo wanafunzi walikuwa wakiongea ongea tu, basi kwa muda huo Erick alikaa na Elly huku wakizungumza kwani siku hizi hawakuwa na zile tofauti zao hata kidogo na walikuwa wakiongea vizuri tu.Elly alijikuta akimuelezea Erick kuhusu kile kitendo cha mjomba wao kusema kuwa yeye ni mwanae,“Duh!! Inawezekana ikawa kweli Elly, kwani wewe unaonaje?”“Sijui, ila mwenye ukweli ni mama maana mama ndio pekee anayejua baba halisi wa mtoto”“Ila mama yako anasemaje?”“Nimejaribu kumdadisi sana hataki kuniambia ukweli, anachokisema yeye ni kuwa yule mtu sio baba yangu”“Sikia Elly nikwambie kitu, yule mama ni mama yako ila ana mambo mengi sana ya ajabu huwezi kuyajua ila mama yako ana mambo mengi sana ya ajabu. Ukiona moyo wako unamkubali baba huyo basi ujue ni kweli ni baba yako, kwani kwa kipindi kifupi tu nilichomfahamu mama yako nimegundua kuwa ni mtu anayeweza kukazania ukweli kuwa uongo na uongo kuwa ukweli, yani utakuta anakazania kabisa, hata ugomvi wangu na yeye ni sababu ya swala lake la kunizushia maneno ya uongo, siku hizi mbona kaacha mwenyewe, kwa kifupi Elly kuwa makini sana na mama yako. Wewe mkazanie huyo kuwa ni baba yako na ipo siku atakwambia ukweli tu”“Tena baba mwenyewe anaonekana kuwa na upendo sana, kwakweli huwa napenda sana kuwa na baba, nimekosa mapenzi ya baba kabisa. Mama angekubali hata angeniruhusu nikakae kule na baba ila mama yangu namfahamu mwenyewe”Wakati wanaendelea kuongea pale, alifika Sarah na kumtaka Elly kuwa waondoke wote,“Elly si unajua leo ni Ijumaa!! Inabidi uende nami nyumbani kwetu ili tukawe huko”Erick akamwambia Elly,“Ningekuwa mimi ningeenda kutumia huu muda wa mwisho wa wiki kukaa na baba yangu”Sarah alimuangalia Erick na kumwambia,“Mbona una wivu sana wewe! Kwahiyo nikiwa na Elly roho inakuuma sana? Pole eeeh! Ulikataa bahati, pole sana”Sarah akamshika mkono Elly, na kwakweli Elly hakubisha kwani bado elimu yake ilimtegemea mama yake Sarah, basi aliondoka nae. Na Sarah aliamua kuondoka nae muda ule kwavile hakutaka kupanda nae kwenye gari la shule ndiomana akafanya vile, Erick nae akaamua siku hii asipande usafiri bali moja kwa moja amfate Erica tu shuleni kwao na waweze kurudi wote nyumbani.Mama Angel leo aliamua kwenda moja kwa moja kumuangalia tena Derrick kuwa anaendeleaje, basi alienda kumuangalia na kumkuta Derrick akiwa mzima kabisa, na muda huo alimkuta akimwagilia bustani ya mboga mboga,“Oooh kaka yangu umemaua kulima mboga mboga?”“Yani nimeona ni vyema nijishughulishe kidogo maana kukaa tu hakuna faida yoyote ile nitakayoipata ukizingatia nimepona. Ila nimemkumbuka sana mtoto Elly”“Usijali, nitakuja nae tena tu”“Yule ni mtoto wangu, nina watoto wawili mimi, na yule ni mmoja wapo”“Ila yule sio mtoto wa Oliva au Manka, ni mtoto wa Sia yule”“Kheeee yule Sia chizi?”“Kheee kumbe unamjua? Ndio huyo huyo”“Aaaah yule mjinga, inawezekana hata aliiba mtoto. Bora mngenitajia mama mwingine ila kwa yule Sia yule, hapana aisee yule mwanamke hana mtoto nina uhakika asilimia mia moja kuwa Elly ni mtoto wangu, huyo Sia tukimbana atatueleza ukweli ila Elly ni mtoto wangu”Mama Angel hakuwa na cha zaidi cha kuongea na Derrick, basi alimuaga tu kwa muda huo na kuondoka zake.Akiwa njiani alikutana na mama Sarah na kumsimamisha huku akianza kuongea nae,“Sikia Manka, tunataka kuja kwako ili tujadiliane vizuri kuhusu mtoto Sarah”“Kheee una wazimu nini wewe, ujadiliane na nani kuhusu Sarah?”“Tunataka kujua ukweli wa mtoto huyu, kama ni wa mzee Jimmy, Erick au Derrick”“Mjinga sana wewe, mimi ndio mama mzazi wa Sarah, na mimi ndio mwenye uwezo wa kuwaambia kuwa yule mtoto ni wa nani. Ningetaka hayo basi ningekuja mwenyewe huko kwenu ili tujadiliane nanyi, ila sina haja mfahamu chochote kile”“Unajua acha kichaa weee mwanamke, ulisema wazi kuwa Sarah anampenda Erick na unajua wazi kama Sarah na Erick wakiwa pamoja ni shida sababu ni ndugu hata iweje, ikiwa Sarah ni mtoto wa mzee Jimmy, wa Erick au Derrick bado ni tatizo kwani ni ndugu, tunahitaji kujadiliana ili watoto watambuane kuwa ni ndugu na waujue ukweli halisi wa mambo”“Hayo mambo hayakuhusu, kwanza sidhani kama nina muda mchafu wa kukaa na kujadiliana na wewe kuhusu huo ujinga”Mama Sarah aliondoka zake, basi mama Angel aliona ni vyema kwa muda huo aende moja kwa moja kwa wifi yake Tumaini ili kuongea nae kuhusu hilo swala, yeye alitamani hilo swala liishe ili yote yawe peupe kabisa.Basi alifika kwa Tumaini na kumkuta na kumueleza yale yaliyojiri kwa siku hiyo, akamueleza pia alivyokutana na mama Sarah na walivyozungumza,“Yule mtoto kuna utata maana hata Derrick anasema mtoto wa mama Sarah ni wake”“Kheeee kuna wanawake wa ajabu sana duniani, mtoto mmoja ana mababa watatu! Duh sio haki kwakweli, kuna wanawake hawajitambui. Huyo mama Sarah ni hajitambui kwakweli”“Sasa tutafanya nini?”“Nenda kamwambie Erick kuwa Jumapili tunaenda huko kwa mama Sarah, yani yule mwanamke atake au asitake lazima tujadiliane nae kuhusu hili, asituchezee kabisa, na kama Sarah sio wetu basi atuweke wazi, kuliko kusema watoto wanapendana halafu watoto hao ni ndugu ana maana gani? Kwahiyo anataka ndugu watembeleane? Asituletee matatizo sie”Mama Angel akakubaliana na Tumaini kuwa Jumapili wataenda kwa mama Sarah kujadiliana nae kuhusu hilo swala.Erick kama alivyopanga, moja kwa moja alienda kwenye shule anayosoma Erica kwahiyo aliondoka na Erica bila kupanda basi la shule, waliongozana kurudi nyumbani huku wakiongea mambo mbalimbali,“Eeeeh uliahidi kuninunulia karata Erick, nahitaji karata”Basi Erick alipitia dukani na kumnunulia dada yake karata, basi pale dukani kuna watu walisikika wakisema,“Siku hizi kuna mambo ya ajabu sana, watoto wadogo utakuta washaanza kupendana yani hapo kamununulia karata ili amuhonge”Mwingine akacheka na kusema,“Kheee hadi kwa karata jamani, mabinti hawana thamani siku hizi”Yale maneno waliyasikia vizuri sana, cha kustaajabu, Erick alimuacha Erica pale na kusogea kwa wale waliokuwa wakiongea na kumpiga ngumi yule aliyesema kuwa mabinti hawana thamani siku hizi, na mzozo ulianzia pale maana huyu alikuwa ni mama mtu mzima halafu Erick katumia nguvu kufanya vile, yule mama alianza kumsema Erick na wote pale walianza kumshambulia kwa maneno,“Una laana wewe, utampigaje mtu mkubwa hivi, huyu si kama mama yako tu! Mitoto ya siku hizi mpaka mara nyingine unawaza kuifanya supu ujinywee zako unenepe, sio kuzaa watoto punguani kama huyu”“Unavuta bangi au?”Wale wamama wakaambizana kuwa wamchangie Erick ili wamfundishe adabu basi walianza kumzoga zoga pale, yani Erica alikuwa akilia tu na kumuombea msamaha kaka yake, ila muda huo wakati wale wanawake wamesema wamchangie, Erick alikuwa katikati yao na wala hakuonyesha kuwa anaogopa chochote kile, basi Erica alienda pale katikati na kuana kumsihisi kaka yake,“Waombe msamaha tuondoke”“Siwaombi msamaha, kwani walichokuwa wakikisema ni kizuri, waache wanipige tu halafu ndio watajua kuwa mimi ni mtu wa aina gani”Kuna baadhi ya wanawake waliogopa na kuna wegine walitaka kumuadhibu ili kile kiburi chake kiishe kabisa, cha kushangaza kati yao hakuna aliayeanza kumpiga Erick bali walikuwa wamemzingira tu huku wakimpa maneno mbalimbali,“Unajivunia huo urefu, wenzio wanajivunia akili sio urefu”“Wazazi wako wana mikosi kwa kukuleta mtoto kama wewe, hufai duniani wala akhera”Ila kuna mama alitokea pale na kuwaomba wale wamama wamsamehe tu Erick, na kumtoa pale katikati ya wale wamama na kumtaka aopndoke, kwahiyo Erick aliondoka na dada yake.Yule mama aliwaambia,“Jamani wamama wenzangu, hawa watoto wa siku hizi maradhi kibao yamewajaa, usikute ni kifo chake, unajaribu kumpiga unashangaa yupo chini amekufa, halafu inaanza kesi ya mauwaji tutakimbiana hapa mjue, hebu muecheni tu. Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu, naomba tusimfunze sisi wanawake, ila tuache wanaume wenzie ndio wamfundishe”Wale wamama waliongea sana ila hakuna hata mmoja aliyejua ni kwanini walishindwa kumpiga yule kijana yani walibakia tu kumtupia maneno lakini hakuna aliyeweza kumpiga, na hakuna aliyejua ni kwanini yule kijana alionyesha kujiamini sana kupita chochote kile.Mama Daima alichukia sana kwa yale maelezo aliyopewa na Daima, maana wale wamama walimrudisha kwao tu na kusema kuwa alitaka kubakwa, sasa walipoondoka ndipo Daima alipomwambia mama yake kuwa aliyetaka kumbaka alikuwa ni baba Angel na kumfanya mama yake achukie sana kwa hilo.Mida ya jioni, mama Daima aliondoka nyumbani kwake, akaenda moja kwa moja nyumbani kwa mama Angel na kumkuta mama Angel amakaa na mwanae Erica kwenye kibaraza maana Erica alitaka kumuhadisia mama yake ya siku hiyo kuhusu Erick, ila yule mama alivyofika pale bila hata salamu alianza kusema mambo ambayo ameyatunza kwenye moyo wake, kwanza alifunga kibwebwe na kuanza kusema,“Hata kama mwanangu ni muhuni sio kwa hili mlilotaka kumfanyia, yani kijana wako atake kumbaka na mumeo nae atake kumbaka”“Kheee wewe mama una akili lakini, si uulize sio unakuja kupaniki tu”“Niulize kitu gani? Mnatabia mbaya sana nyinyi, huyo mumeo kakosa wanawake wote wanaojiuza huko hadi atake kumbaka binti yangu, tuseme wewe humtoshelezi mumeo mpaka atake kumbaka binti yangu? Mnachefua sana, wewe na tabia zako chafu nimekusitiri tu, umetembea na ukoomzima wa mume wangu ila unadhani hatujui kwa kukaa kimya kukusitiri tu maana tunaona tukisema tutakuabisha sana mjinga wewe. Kumbe hata hujifikirii hata kidogo, hujui baya wala hujui vibaya, mwanamke mbaya wewe na mchafu loh!”“Umemaliza?”‘Sijamaliza bado”Akaendelea kuongea, basi mama Angel alimuangalia Erica na kumtuma,“Kalete maji ya kunywa ndani”Erica alienda na muda kidogo alikuja na maji, basi mama Angel akamwambia mama Daiam,“Najua utakuwa unaishiwa na pumzi sababu ya kuongea sana, maji hayo hapo utakuwa unashushia kidogo kidogo”“Puanguani nini wewe, aliyesema anataka maji ya kunywa nani? Nakueleza tabia mbaya za mumeo unajifanya huelewi”“Ungekuja kuuliza kistaarabu ningekujibu”Basi mama Angel akamvuta mkono Erica na kuingia nae ndani kwahiyo walimuacha mama Daima anaongea pake yake pale nje.Kwakweli mama Daima alichukia sana na kuendelea kusema maneno machafu pale, muda huu Erick mdogo alikuwa nyuma ya nyumba yao, aliposikia zile kelele za mama Daima alisogea karibu, basi mama Daima kumuona Erick akamsogelea na kumkunja huku akisema,“Eeeeh tena ndio wewe wewe uliyetaka kubaka mwanangu”Akaanza kumwambia maneno yake ambayo yalimchukiza sana Erick, na yule mama hakujua hasira alizonazo Erick ila alishtukia tu akipewa ngumi hiyo ambayo ilimpeleka hadi chini, kiasi kwamba alianza kutoka damu mdomoni, halafu Erick hata hakujali aliingia ndani, yani mama Daima aliona ile nyumba ina magaida, kwa muda huo aliamua kuondoka huku akijifunika mdomo wake ambao ulikuwa ukitoa damu.Usiku huu wakati baba Angel yupo ndani na mkewe alielezewa kuhusu mama Daima kwenda pale na kuanza kutukana, yani kitu ambacho mama Angel hakukijua ni kuwa mama Daima alipigwa ngumi na Erick, muda wakati anamuhadithia mumewe, simu yake ilianza kuita na kupokea allikuwa ni baba Daima,“Kwakweli sijapenda kwa kitendo mlichomfanyia mke wangu”“Kitendo gani”“Mke wangu kaja huko kwa ustaarabu kuwaeleza kuhusu alichokisema binti yetu, kweli mlichokifanya kwa mwanetu mnaona kipo sawa?”“Sikia baba Daima, angekuja kwa ustaarabu mbona tungeelewana, sasa mkeo kaja na matusi”“Ndio mumpige ngumi ya mdomo hadi mke wangu kuanza kutokwa na damu mdomoni”“Kheee mwenye uwezo wa kumpiga ngumi mkeo hadi damu ni nani?”“Unajifanya hujui, si huyo kijana wako humo ndani. Huyo jambazi mnayemfuga humo ndani”“Khaaa jamani, hapana aiseee, Erick hawezi kufanya hivyo”“Muulize akwambie alichomfanya mke wangu, mtoto wako ana roho mbaya sana huyo. Halafu kwanini mmefanya hivi kwa binti yangu mjue tunaheshimiana sana!”Mama Angel aliamua kumueleza kilichojiri hadi baba Angel kumuacha pale na kuondoka zake,“Haya wale wananchi wangeamua kumpiga mume wangu na kumdhuru, si ingekuwa ni tatizo kubwa sana. Kwakweli huyo binti yako hafai na usipokuwa makini unaweza hata kugombana na baadhi ya majirani kwa uongo wake”“Ulishindwa nini kumueleza mke wangu mambo hayo?”“Muulize mkeo jinsi alivyokuja kwangu, muulize akamwambie maneno aliyoyasema’Basi baba Daima alikata ile simu na muda ule alianza kuongea na mumewe,“Jamani inawezekana kweli kwa Erick kufanya hivyo?”“Hata mimi nashangaa kwakweli, inawezekana Erica anajua ngoja nikamuulize maana kama Erica anajua ataniambia ukweli zaidi kuliko Erick”Basi mama Angel moja kwa moja alienda chumbani kwa Erica ambaye alificha karata zake baada ya mama yake kuingia,“Umeficha nini Erica?”“Hakuna kitu nimeficha mama”“Yani wewe mtoto wewe, hebu niambie jana tulivyoingia ndani na mimi nikaenda chumbani nini kilitokea? Yule mama aliyekuwa akiongea aliondoka muda gani?”“Mimi nilikuwa sebelni mama, Erick alikuwa nje, basi nikasikia kama yule mama anaongea na Erick halafu nikachungulia na kuona yule mama kamkunja Erick ila muda ule ule Erick alimsindika ngumi hiyo yule mama hadi alianguka chini na damu zilikuwa zikimtoka yani alipoinuka alikimbia na kuondoka zake”“Mbona hukuniita sasa”“Mmmh Erick angechukia zaidi, ila unadhani hilo tukio ni la kwanza kufanywa na Erick? Leo leo kafanya balaa huko njiani”“Balaa gani?”Erica hakumueleza mama yake kuwa walienda kununua karata, bali alisema kuwa Erick alienda kumnunulia juisi, basi akamwambia maneno waliyokuwa wakiongea wale wamama na Erick kwenda kumpiga mama mmoja wapo, na jinsi ilivyokuwa, kwakweli mama Angel alishangaa sana na kusema,“Hapana aiseee, Erick wangu hawezi kufanya hivyo”“Usikatae mama, ndio kafanya hivyo huyo Erick wako hata usimkatalie”Mama Angel akakumbuka pia Sia alivyolalamika kuwa kapigwa sana na Erick hadi mbavu zilimuuma kipindi hiko, ila bado mama Angel aliona hiyo ni ngumu sana kwa mwanae.Basi akaondoka na kumuacha Erica alale halafu akaenda kwa mumewe na kumuelezea hayo,“Mmmh itabidi kesho niongee na kijana wangu, asije kuleta balaa bure, huo ubondia kautoa wapi?”“Kautoa kwako, maana nawe mkorofi”“Hapana sijafikia huko”“Ila cha kurithi kinazidi”“Hata kama, sio kawaida hii kuna tatizo kwa mtoto wetu lazima tujue kuwa tatizo ni kitu gani”Basi wakaongea na muda huo kuamua tu kulala.Jumamosi ya leo, Steve anaongea na mtoto Paul kuwa waende kwenye matembezi naye, kwakweli Steve alijikuta akipatana sana na mtoto huyu, yani alipatana nae kupita maelezo ya kawaida, alikuwa kama mwanae kabisa, ana alifanya mambo yote pamoja nae, kitendo kile kilimfanya madam Oliva kuhisi furaha sana moyoni mwake.Basi muda ulipofika Steve pamoja na Paul walijiandaa na kwenda kwenye matembezi ambapo walienda sehemu mbalimbali yani Steve aliona fahari kwake kutambulisha kuwa Paul ni mtoto wake.Katika kwenda sehemu mbalimbali ndipo alipoamua kwenda na Paul nyumbani kwao, na hapo walimkuta mamake Steve akifanya tu shughuli zake, kwakweli alishangaa sana kuwaona na kuwakaribisha, basi waliongea ongea pale ila huyu mama aliashindwa kujivunga na kusema,“Steve, huyu mtoto unajua kuwa umefanana nae sana!”“Hata mimi nimeona, duniani wawili wawili”“Au ndio yule wa kipindi kile!”Steve alicheka na kumwambia mama yake,“Huyu ni mwanangu, kutoka kwa Oliva”Mama Steve alishtuka kidogo, na kumvuta mkono Steve na kwenda kuongea nae pembeni,“Inamaana hujaanza leo na huyo Oliva, mna muda mrefu eeeh!”Steve alicheka, na mama yake aliendelea kuongea,“Sema ukweli mwanangu, naona wazi kuwa huyu ni mjukuu wangu kabisa”Steve aliamua kumdanganya mama yake kuwa ni kweli alikuwa na madam Oliva tangu zamani na wamezaa pamoja huyo mtoto Paul, kwakweli mama Steve alifurahi sana na kumwambia Steve kuwa siku zote alikuwa akimpinga madam Oliva ila kwa hilo anamkubali kwa mikoni miwili.Basi mama Steve akamfata Paul na kumkumbatia huku akimwambia,“Karibu nyumbani mjukuu wangu”Kisha mama Steve alienda kukamata kuku nje, na kuanza kumuandaa kwani alitaka kumfurahisha mjukuu wake, yani alikuwa na furaha sana kuona mtoto wake ana mtoto kweli.Paul naye alifurahi sana, ila kitu ambacho Paul hakukielewa ni kuhusu Steve kama ni baba yake kweli au ni baba yake kwavile anaishi na mama yake, yani hapo ndio hakuelewa kabisa.Mama Steve alimaliza kuandaa ile kuku na kuiweka mezani ili wote waweze kula, basi Steve alishangaa tu pale kuwa na ile kuku ya kuchomwa, halafu kuna mchuzi wa samaki na wali, akauliza,“Mbona mama hiyo kuku umemuwekea Paul peke yake?”“Ndio ni ya mjukuu wangu, nataka ale afurahi na yeye kwa uwepo wa bibi yake”Basi Steve akacheka tu na kuendelea kula kile chakula kilichoandaliwa na mama yake.Baba Angel alienda zake kiwandani leo na alienda na Erick basi walipomaliza mambo yote, aliamua kwa siku hiyo kwenda na Erick kwenye moja ya mgahawa ili kuweza kuzungumza nae,“Mwanangu nimesikia habari zako, umeanza lini ubondia?”“Ubondia baba! Kivipi?”“Si nasikia kila anayekuchokoza huko unampiga tu utakavyo”“Oooh baba, naomba unisamehe”“Unajiamini vipi kupambana na watu wote, umesahau kuwa wewe ulichapwa na madam Oliva fimbo moja na ukazimia?”“Nakumbuka baba, ila sijui kwanini siku hizi yani nikishikwa na hasira najiona kuwa na nguvu za ajabu sana”“Mmmh, utakuwa na tatizo mwanangu, nadhani utakuwa na mapepo”“Hapana baba, sina mapepo mimi wala nini. Huwa watu wakinikera ndio nakuwa hivyo”Baba Angel aliamua kuzungumza na mwanae namna ya kuheshimu watu wote, na madhara ya kugombana na watu, alimuelekeza vingi ili mwanae aweze kuacha hiyo tabia maana hata yeye binafsi hakuelewa kuwa tabia hiyo mtoto wake kaitoa wapi.Walielewana kisha kufanya safari ya kurudi nyumbani.Usiku wa siku hiyo, mama Angel alikumbuka kumwambia mumewe kile ambacho alijadiliana na Tumaini kuhusu mama Sarah,“Kwahiyo ndio kesaho tukazungumze na huyo mwanamke”“Ndio, bora mambo haya kuyaweka sawa, huyu mwanamke ni vyema gtumfate wote ili atwambie ukweli, kumbuka alimwambia Tumaini kuwa hata mzee Jimmy hamfahamu kabisa, kwahiyo tunatakiwa kuwa makini na maneno yake”“Sawa nimekuelewa mke wangu, kwahiyo kesho tutampitia Tumaini na kuondoka nae kwa pamoja, nimekuelewa vizuri sana”Kisha mama Angel alimuuliza mumewe kama aliongea na mtoto wao Erick, na mumewe alimueleza ambacho aliongea nae, muda kidogo ilipigwa simu kutoka kwa baba Daima na akalalamika kuwa mkewe kalazwa anaumwa juu ya ngumu aliyopewa na Erick.Kwakweli hawakutaka kufikiria sana kuhusu hilo.Jumapili kama walivyopanga, walijiandaa vizuri kabisa na kumpitia Tumaini kisha kufanya safari ya kuelekea nyumbani kwa mama Sarah.Walifika pale na kukaribishwa ndani ila waliambiwa kuwa mama Sarah hayupo kwani aliyewakaribisha alikuwa ni Siku yani mdada wa kazi wa mama Sarah, siku hii mama Sarah hakurudi toka ameondoka jana yake jioni, halafu Elly nae leo aliondoka asubuhi asubuhi kwenda Kanisani kwahiyo pale alibaki Siku na Sarah tu. Ikabidi waulizie uwepo wa Sarah,“Sarah yupo ndani kalala, analalamika tumbo linamuuma sana”Mama Angel alijikuta akijiwa na moyo wa huruma tu, kwani huwa akisikia mtoto anaumwa anasikia kuteseka sana moyoni, basi akahitaji kwenda kumuona.Ikabidi yeye na Tumaini huku wakiongozana na Siku wakaenda hadi chumbani kwa Sarah na kumkuta amekaa huku akilalamika tumbo, walipoingia tu alianza kutapika, wakati wanamuhamisha ili wamfute yale matapishi walikuta kuna damu nyingi sana zinamtoka. Mama Angel alijikuta akijiwa na moyo wa huruma tu, kwani huwa akisikia mtoto anaumwa anasikia kuteseka sana moyoni, basi akahitaji kwenda kumuona.Ikabidi yeye na Tumaini huku wakiongozana na Siku wakaenda hadi chumbani kwa Sarah na kumkuta amekaa huku akilalamika tumbo, walipoingia tu alianza kutapika, wakati wanamuhamisha ili wamfute yale matapishi walikuta kuna damu nyingi sana zinamtoka.Hapo wakaona kuwa huyu mtoto anahitaji tiba ya haraka sana, kwahiyo ilibidi mama Angel aanze kumuandaa kwaajili ya kwenda nae hospitali, yani Sarah hata hakuwa na maelezo yanayoeleweka juu ya hali yake.Wakatoka nae na moja kwa moja kuanza nae safari ya kwenda hospitali, Siku alibaki nyumbani huku akiwaangalia tu maana alihitaji kubaki na kuangalia nyumba kwani alijua wazi kama mama yao angerudi na kutokuwakuta wote ingekuwa balaa.Baada tu ya wale kuondoka, ndipo Elly aliporudi nyumbani na kumkuta Siku yupo nje anafua, alienda ndani kumuangalia Sarah aliyemuacha mgonjwa ila hakumkuta, ikabidi arudi nje kumuuliza Siku aliyekuwa anafua,“Yuko wapi Sarah?”“Oooh Sarah ni mgonjwa, yani anaumwa sana kwahiyo walikuja hapa wale wakina mama Erick ndio wamempeleka hospitali”“Alizidiwa sana au?”“Aaaah si unajua wale wana viherehere sana, mama si ameondoka kamuacha Sarah anaumwa hapa wala hakuwa na tatizo kwani alijua lazima atapona tu, ila wao sasa na viherehere vyao yani wamemchukua na kumpeleka hospitali”“Sasa hata hujui ni hospitali gani wamempeleka, wasiporudi nae je?”“Kwani kwao hapafahamiki? Tutaenda nyumbani kwao, waache wahangaike nae huko, watamrudisha tu”Basi Elly akatamani kujua kuwa Sarah alikuwa akisumbuliwa na nini, ila kwa muda huo njaa nayo ilikuwa ikimsumbua maana aliondoka bila ya kula chochote, akamwambia Siku,“Si chai ipo eeeh! Ngoja nikakoroge ninywe”Muda huo huo Siku aliacha kufua na kumwambia Elly kuwa anaenda kumuandalia chai, basi moja kwa moja aliingia nae ndani, na kumuandalia chai kweli ambapo Elly alikunywa na kujihisi vizuri, baada ya hapo Siku alimletea Elly juisi na kumtaka ashushie kwa ile chai aliyokunywa,“Mmmh nimeshiba sana”“Aaaah kwetu kukataa mtu kitu alichokuandalia ni vibaya kabisa, naomba unywe hata kidogo”Basi Elly alichukua ile glasi na kunywa kidogo ila baada ya kunywa tu alijihisi kulewa yani kama mtu aliyekunywa pombe, basi Siku alifunga milango na kumchukua Elly kwenda nae chumbani kwake, na kuanza kumpapasa, na kuweza kulala nae sababu tu Elly hakujielewa na ile hali ya kuwa kama amelewa.Yani Elly alivyokuja kurejewa na fahamu zake aliumia sana kwenye moyo wake kwani hakutegemea kufanya kile kitu na Siku,“Kwanini umenifanyia hivi dada?”“Nilikuwa nakutamani sana Elly kwa muda wote, yani kila siku nilikuwa nakutamani sana. Nashukuru leo nimepata nafasi, huu ni mwanzo najua sasa utakubali kwa hiyari yako”Elly alichukia sana, na kutoka mule chumbani kwa Siku na kwenda chumbani kwake huku akiwa amechukia sana.Wakina mama Angel walifika hospitali wakiwa na Sarah na moja kwa moja alipelekwa kwenye matibabu, basi walitulia huku wakisikilizia kuwa itakuwaje. Mama Angel aliamua kumpigia simu mama Sarah ila ile simu iliita sana hadi kukatika yani hakuna cha maana alichokipata.Baba Angel akasema,“Haya mambo ndio huwa siyapendi, kweli mama wa mtoto anaondoka na kuacha mtoto wake anaumwa jamani”“Labda alijua anaumwa kidogo”“Kidogo, hakumuangalia vizuri, kwa zile damu zilizomtoka inaonyesha ni muda mrefu tatizo lilianza”Waliongea kidogo pale huku baba Angel akifatilia hali ya yule mtoto Sarah, badae daktari alikuja na kuhitaji mzazi wa yule mtoto, sababu wale ndio walimpeleka na kudai kuwa ni ndugu wanaoishi na yule mtoto ilibidi tu awaambie kinachomsumbua yule mtoto,“Ni hivi jamani, inaonekana mtoto alikuwa na mimba changa sasa imetoka”Wote wakashangaa sana, mama Angel aliuliza,“Jamani, mtoto mdogo kama Sarah anatoa wapi mimba?”Tumaini akadakia na kusema,“Kila siku huwa nasema sana kuhusu malezi mabovu, kwani Daima kapata vipi ile mimba aliyoipata? Watoto wa siku hizi wana mambo sana”Basi daktari akaondoka kuendelea na huduma kwa yule mtoto kwani ilibidi wamsafishe, kwakweli baba Angel aliwaambia,“Jamani, mimi naondoka mtaniambia yatakayojiri. Sitaki habari za watoto wasiojielewa kama huyo”Baba Angel aliondoka zake na kumuacha pale Tumanini na mama Angel, ila muda kidogo Tumaini nae aliondoka zake na kumuacha pale mama Angel, yani mama Angel alishindwa kuondoka bila ya kuruhusiwa kuondoka na Sarah, kwahiyo hakutaka kuondoka kabisa.Tumaini akiwa njiani akielekea nyumbani kwake, ndipo alipokutana na mama Sarah, alimsimamisha na kuanza kuongea nae,“Kheee unajua nilikuwa sikujui kabisa mambo yako, kumbe wewe mwanamke ni mbaya kiasi hiki”“Kwani nimefanyeje?”“Unawezaje kuondoka na kumuacha mwanao mgonjwa ndani au ulikuwa ukijua ni kitu gani kinamsumbua mwanao?”“Kwahiyo ulikuwa nyumbani kwangu?”“Ndio, tulikuwa na kikao na wewe kwani tulikuwa tukihitaji kujua ukweli kuhusu mtoto Sarah, ila hatujakukuta na kumkuta mtoto akiumwa vile nyumbani kwako”“Kheee jamani, Sarah alikuwa anaumwa tumbo tu wakati naondoka. Siwaelewi imekuwaje?”“Imekuwaje kuhusu nini? Mwanao katoa mimba huko”“Katoa mimba? Hiyo mimba Sarah aitoe wapi? Mbona mnataka kuchekesha walionuna”“Ndio hivyo, nenda hospitali huko kamfate mwanao. Umemkuta Erica hana roho mbaya na ndio kabaki na mwanao hospitali, nenda kamuangalie huko. Nilikusema sana kwa malezi mabaya unayompa Sarah, nadhani umeona matunda yake sasa”Tumaini akamuelekeza tu hospitali aliyolazwa Sarah na kuachana nae pale.Walipomaliza kumuhudumia Sarah na kila kitu ndio wakampa ruhusa mama Angel aweze kurudi nae nyumbani, daktari aliongea tu na mama Angel kiasi kidogo pale,“Mpeni mtoto elimu stahiki, kumbe alikuwa mjamzito halafu akaenda kuchoma sindano ya uzazi wa mpango, imeenda kuharibu ile mimba na ndiomana kaumwa sana, hebu muwe makini sana na hawa watoto wenu, mtawapoteza mjue.”Basi akapewa na dawa zitakazoweza kumsaidia kwa kipindi hiko, mama Angel akaondoka sasa na Sarah yani alikuwa akimuangalia bila ya kummaliza kwakeli, basi akawa anaondoka nae huku akiendesha gari na kumuuliza baadhi ya maswali,“Kwanza Sarah ulipata vipi hiyo mimba?”Sarah alikuwa kimya tu huku akiinama chini, mama Angel alipumua kidogo na kumuuliza tena,“Na ilikuwaje hadi ukaenda kuchoma sindano ya uzazi wa mpango?”Bado Sarah alikuwa kimya tu, basi mama Angel akamwambia,“Utaniambia vizuri ukiwa vizuri, nakuhurumia sana, wewe Sarah bado ni mtoto mdogo sana”Basi walifika nyumbani kwakina Sarah na Sarah kuingia ndani na moja kwa moja mama Angel alimpeleka Sarah chumbani ili aweze kupumzika, ila wakati anatoka tu chumbani kwake alikutana na mama Sarah ambaye ndio alikuwa ametoka kufika,“Yani nimetoka hadi kwenye ile hospitali mliyoenda nikaambiwa kuwa mmetoka, kwanza nakushukuru kwa hili ulilolifanya kwani mwanangu anaumwa nini?”“Yani unakaa na mwanao kweli hujui tatizo lake? Mwanao alikuwa ni majamzito, kaenda kuchoma sindano ya uzazi wa mpango sijui basi ile sindano imeenda kuharibu ile mimba na kumfanya aumwe sana, na hiyo hali imefanya apoteze damu nyingi sana. Anatakiwa kula vizuri na kuna dawa nimemuachia hapo ambazo walimuandikia”“Oooh nashukuru sana, sikutegemea kama ungefanya kitu cha namna hii, asante sana Erica”“Usijali, watoto hawa ni wa kwetu sote. Ila dokta kasisitiza sana juu ya malezi tunayowapa watoto, tunatakiwa kuwa makini sana”“Asante”Basi mama Angel alimuaga na kuondoka zake, kwakweli hata yeye alishangaa mno kuona jinsi mama Sarah alivyokuwa mpole kwa siku hiyo.Moja kwa moja mama Sarah alienda chumbani kwa mwanae na kumuangalia, basi alikaa karibu yake na kumuuliza,“Mwanangu kwani hiyo mimba umepataje?”“Sijui hata nimepataje”“Nani alikupeleka kwenda kuchoma hiyo sindano ya uzazi wa mpango?”“Sijui mama, nimechoka sana. Hali yangu sio nzuri kabisa, kwasasa nahitaji kupumzika”“Pole sana mwanangu, Mungu atakusaidia utapona tu”Kisha mama Sarah alitoka na kumtaka Siku amuandalie chakula Sarah ili aweze kwenda kumlisha kikiwa tayari. Siku hii mama Sarah hata hakujua kama ataweza kutoka kwa ile hali ya mtoto wake.Mama Angel alirudi nyumbani kwake wakati hata giza limeanza kuingia na kumkuta mumewe akiwa amejilaza tu kwa muda huo, basi alienda kuoga na kurudi kuongea na mume wake,“Ila mume wangu jamani, ndio kuniacha mwenyewe hospitali”“Kiukweli huwa sipendi ujinga wa watoto wa kike kamavile kwakweli, mtoto anabeba mimba kwa umri mdogo vile! Na kwanini imetoka sasa?”“Sijui alikuwa na mimba halafu akaenda kuchoma sindano ya uzazi wa mpango”“Aaaargh katoto kana tabia mbaya hadi kamewaza kwenda kuchoma sindano ya uzazi wa mpango jamani!! Si umri wakina Erica yule aarrgh!”“Unajua watoto tusiwalaumu sana vitu vingine hawajui”“Hawajui wapi? Mtoto anajua kabisa nitapata mimba ndio kaenda kuchoma sindano ya uzazi wa mpango ili asipate na aendelee kufanya kwa raha zake, naye ni mtoto huyo? Hata sitaki tena awe karibu na watoto wangu maana atawafundisha tabia mbaya”“Aaaah usiseme hivyo mume wangu, mimi nina uhakika Sarah hajapata mtu wa kuongea nae na kumuelewesha vizuri kwani nina hakika angeeleweshwa vizuri basi yote haya yasingetokea”“Aeleweshwe nini na mtoto kashapata utamu wa tunda?”Mama Angel alicheka tu, kisha baba Angel akauliza tena,“Je umemuuliza nani muhusika wa hiyo mimba iliyotoka? Umemuuliza ni nani aliyempeleka kwenda kuchoma hiyo sindano ya uzazi wa mpango?”“Nimemuuliza kabaki kimya tu, anaona aibu ila nasubiri apone vizuri nitamuuliza”“Utamuuliza nini sasa? Si ndio wakina Daima hao? Toto limefata tabia mbaya ya mama yake lile aaargh”Baba Angel alionekana kutokupenda kabisa lile jambo ambalo Sarah amelitenda kwahiyo kwa muda huo aliamua kulala tu wala hakutaka matatizo mengine.Kulipokucha, Baba Angel alijiandaa na kwenda kazini kama kawaida na wakina Erica walienda shuleni kwahiyo pale nyumbani alibaki tu mama Angel, Vaileth na Ester kama kawaida.Basi mama Angel alianza kumsimulia Vaileth kitu ambacho kimejiri kwa Sarah,“Yani nimeumia sana kwa mtoto mdogo kama Sarah kupata ujauzito loh! Halafu kaenda kutumia sindano ya uzazi wa mpango jamani”“Sasa nani kampa Sarah mimba?”“Anataka kusema basi!! Sijui imekuwaje, yani mimi nina wasiwasi sana yasije kuwa mambo kama ya Daima”“Jamani”“Roho imeniuma sana, huwa namuona Sarah kama mtoto wangu, huwa namuona Sarah kama ninavyomuona Erica tu. Nimeumia sana”“Kweli ni mdogo sana, kaanza mapenzi basi ndiomana akapata hiyo mimba, hadi imetoka dah!”Mara mlango ulifunguliwa na aliyefungua mlango alikuwa ni Erica, basi mama yake alimuuliza kilichomfanya arudi mapema vile,“Tumbo mama linaniuma sana”Mama Angel akashtuka maana hofu ikamjaa kuwa isijekuwa mambo yale yale ya Sarah, basi alienda nae mwanae chumbani na kumuuliza vizuri,“Ni tumbo gani linakuuma mwanangu”“Tumbo la kikubwa mama”Hapo mama Angel alielewa vizuri kabisa kitu kinachomsumbua mtoto wake.Baada ya muda Erica alimfata Vaileth ambae kwa muda huu alikuwa chumbani kwake na kuanza kumuuliza,“Ni nani mliyekuwa mnamzungumzia kuwa katoa mimba?”“Ni Sarah huyo, yani kumbe mtoto mdogo ana mambo ya ajabu”“Kheee Sarah kaanza mambo ya wanaume!! KWahiyo naye kapata mimba kama Daima?”“Ndio ila imetoka, yani Sarah kafanya mchezo wa ajabu sana”“Kheee kumbe!!”Basi Erica aliridhika kwa muda kuipata habari hiyo maana alishindwa hata kupumzika kidogo bila kujua kilichokuwa kikizungumziwa na mama yake pamoja na Vaileth pale sebleni, kwahiyo alivyojua aliweza kuridhika na moyo wake sasa.Baba Angel akiwa ofisini kwake leo alitembelewa na Sia, na kushangaa ila alimkaribisha na kumuuliza,“Ndio ushapata jibu la utafiti wako juu ya aliniwekea sumu?”Kidogo Sia alijiuma uma na kusema,“Hiko sio kilichonileta ila kilichonileta ni swala lingine kabisa”“Swala gani?”“Hivi kwanza unajua kama Erica amewahi kuwa na mahusiano na Derrick? Ni ndugu yake ila amewahi kuwa na mahusiano nae”“Hayo hayanihusu kabisa, kinachonihusu sasa ni kuwa Erica ni mke wangu halafu Derrick ni shemeji yangu”“Duh!! Yani wewe Erick ni wa ajabu sana”“Sema lingine ulilokuja nalo”“Ni kuhusu mtoto Elly”“Eeeeh una story mpya kuhusu Elly au kitu gani? Hebu sema ukweli kuwa Elly ni mtoto uliyezaa na Derrick”“Hapana, mimi sijazaa na Derrick. Ngoja leo nikwambie ukweli”“Haya, niambie nakusikiliza”“Mimi kiukweli kabisa nilizaa na Steve yani huo ndio ukweli halisi”Baba Angel alicheka kwanza na kusema,“Ila wewe mwanamke jamani dah!! Nakusikiliza vizuri sana, na ulivyokuwa umekazana kuwa umezaa na mimi ni nini?”“Sikiliza basi, ni hivi mimi siku nimeenda kujifungua nilienda kabla hata ya muda ila mwanangu alikuwa vizuri tu, sema hakuzaliwa kwa uzito ule uliotakiwa, basi ikapewa yule mtoto ila alikuwa akilia sanaalipokuwa kwangu. Baba yako mzee Jimmy alikuja kuongea nami, yani aliongea na mimi kabla sijajifungua na akaongea na mimi baada ya kujifungua, alipanga nami mpango wa kubadilisha mtoto wangu na mtoto wa Erica, nilikubali sababu ya shida yangu ya hela, mtoto alipofika miezi mitatu kasoro ndipo mzee Jimmy alipowabadilisha, kwamaana hiyo Elly ni mtoto wa Erica halafu Erick ni mtoto wangu ndiomana nilikuwa nakukazania kuwa nimezaa na wewe kwani nilijua hata mwanangu akipimwa damu atakutwa ni mwanao kweli yani Elly. Ila baada ya sokomoko hili la kusema kuwa Elly ni mtoto wa Derrick basi kuna uhakika kabisa kuwa Erica aliendelea na Derrick kwahiyo Elly na Erica mdogo wote ni watoto wa Derrick maana mtoto wangu mimi ni Elly”“Uwiii sijakuelewa hata jambo moja ulilonieleza Sia”“Hujanielewa kivipi? Ushahidi pia ninao kuwa mimi na baba yako tulibadilisha watoto”“Mlibadilisha wakiwa na umri gani?”“Miezi mitatu kasoro”“Mbona wanangu walipomaliza mwezi tu niliondoka nao na mama yao tukaenda Afrika kusini na tulirudi huko baada ya miaka mitatu, unajua sikuelewi kabisa”“Nitakuletea ushahidi basi, mimi sio chizi kusema kila siku kuwa Erick ni mtoto wangu. Ila ndio hivyo mkeo alikusaliti huyo ndiomana imekuwa hivyo”“Nenda tu Sia, ila mke wangu awe alinisaliti au hakunisaliti bado nitampenda hadi mwisho wa maisha yangu”“Duh!! Ni mzima kweli wewe?”“Ni mzima kabisa, nilishasema hata nimfumanie hapo mke wangu basi nitamsamehe maana nampenda sana”“Mmmmh!! Shukuru Mungu mkeo hana hayo mambo siku hizi”“Ndiomana nimemuoa kwnai najua sio mwanamke wa kutangatanga tangu zamani”“Sio wa kutangatanga wapi, angetembea na ukoo mzima huyo! Unamtetea tu”“Alikuwa akitafuta penzi la kweli ila mke wangu katulia sana na nina mpenda sana, hakuna kinachoweza kututengenisha”“Ngoja nikapekue vizuri ule ushahidi nikuletee”Sia aliamua kuondoka zake maana aliona hakuna ushirikiano wowote kwa baba Angel ila alimuahidi kumletea ushahidi kwa yale aliyoyasema.Baba Angel siku hii baada ya maneno ya Sia, aliamua kupitia dukani kumnunulia mkewe zawadi, kwnai yale maneno ya Sia yalimuingia sikio la kushoto na kutokea sikio la kulia, alienda moja kwa moja kwenye duka ambalo huwa ananunua na leo alimkuta baba Emma na kufurahi kwani alijua kuwa atamchagulia kitu ambacho mke wake atakipenda sana.Alipofika pale tu baba Emma alimuonyesha zawadi ya kumpelekea mke wake,“Leo mpelekee tu hiki kikoi nina uhakika atakipenda sana”“Mmmh atapenda kikoi mke wangu kweli!”“Kweli atakipenda sana, ni kizuri hiki hakuna mwanamke ambaye atakiona na kukichukia”Basi baba Angel alimchukulia mkewe kile kikoi na moja kwa moja kurudi zake nyumbani kwa mke wake.Leo alipofika tu ndani moja kwa moja alimuonyesha mke wake ile zawadi aliyomchukulia, kwakweli mama Angel alifurahi sana na kumwambia mume wake,“Ulijuaje kama nataka kikoi jamani mume wangu? Kweli wewe ni kiboko yangu. Nimependa sana hiki kikoi mume wangu, asante sana.”Muda wote mama Angel alikuwa akikitazama tu kile kikoi ilionyesha ni jinsi gani amekipenda kile kikoi.Usiku wa siku hii, Erica alienda moja kwa moja chumbani kwa kaka yake Erick na kuanza kuongea nae kuhusu kile alichosikia kuhusu Sarah,“Umesikia hayo yaliyopo huko”“Mmmh umeanza Erica, mambo gani hayo?”“Kumbe Sarah alikuwa na mimba kwahiyo imetoka”“Mmmh alikuwa na mimba!! Jamani, Sarah kapata wapi mimba?”“Kapata wapi? Kwani wewe hujui mimba inapatikanaje?”Erick alimuangalia nduguye bila ya kumjibu kitu na kuamua kuanza kumueleza mambo mengine,“Hivi zile karata siku hizi unacheza mwenyewe? Leo nije tucheze wote?”“Hapana, leo sichezi karata”“Kwanini?”“Subiri baada ya siku tatu ndio nitacheza karata”“Kwanini?”“Siri yangu, usiku mwema”Kisha Erica aliondoka zake na kumuacha Erick pale akimshangaa tu na kujiuliza kwanini Erica kasema vile kuhusu kucheza karata mpaka baada ya siku tatu, hakumuelewa kwakweli.Leo Erick alipokuwa shuleni aliamua kumuuliza Elly kuhusu Sarah kwani ni kweli hakuonekana shuleni, basi alikaa nae na kuanza kumuuliza,“Vipi Sarah anaendeleaje?”“Kheee mbona umeniuliza mimi!”“Nasikia anaumwa, na wewe ulisema kuwa upo nae karibu”“Ndio anaumwa, ila twende ukamuone sio kuniuliza uliza maana hilo sio jukumu langu”“Duh!! Basi tutaenda badae baada ya masomo”Walirudi darasani na kuendelea na masomo kama kawaida, ila vipindi vilivyoisha, Elly alimkumbusha tena Erick swala la kwenda kumuona Sarah, ni kweli Erick alikubali na moja kwa moja kuondoka na Elly kuelekea nyumbani kwakina Sarah.Walipofika, walimkuta Sarah yupo chumbani, basi Siku alienda kumuita na kumwamnbia kuwa,“Erick kaja kukuona”“Oooh mwambie aje kuniona chumbani”Ikabidi Siku ampelekee ujumbe ule Erick, na muda ule Erick na Elly waliingia pamoja chumbani kwa Sarah ila Sarah aliomba kuzungumza na Erick kwahiyo alihitaji Elly asubirie kwanza, na Elly alifanya vile basi Erick alianza kuzungumza nae,“Kwani ni kitu gani kinakusumbua Sarah?”“Najua mama yako ameshakwambia”“Kaniambia kuhusu nini?”“Kuwa nilikuwa na mimba na hiyo mimba imetoka”Erick akashtuka kidogo maana hizi habari alizipata kwa Erica ila hakuziamini moja kwa moja, ila muhusika alipomuhakikishia alishangaa sana na kumuuliza kwa makini,“Sarah unazungumzia nini?”“Kwani hujanisikia au hujanielewa? Ndio kama ulivyoambiwa kuwa nilipata mimba na imetoka”“Ulipataje mimba Sarah?”“Kwani mimba inapatikanaje?”Sarah alianza kucheka tena alicheka sana na kusema,“Erick usiniambie hujui hata mimba inapatikanaje?”“Wewe ni mtoto mdogo sana Sarah! Unajua kama ulichokifanya sio sawa kabisa”“Sio sawa kitu gani, kuna mtu ambaye huwa hafanyi mapenzi?”Erick aliona ni vyema abadilishe mada na kuanza mada zingine kwahiyo alianza kumpa pole tu maana aliona kama angeendelea na mada ile basi ingekuwa ni ngumu sana kuelewana na Sarah,“Pole sana Sarah”“Ila haya yote umeyataka wewe Erick”“Kivipi sasa?”“Wewe ndio chanzo cha mimi kupata mimba na wewe ndio chanzo cha mimi kuchoma sindano na mwisho wa siku ile mimba ikatoka kabisa”“Unaongelea nini wewe? Unadhani mimi naweza kufanya huo upuuzi? Kwanza hiyo kwangu ni dhambi”“Dhambi unaijua wewe! Yani hata usijitetee kwa lolote, maana wewe ndio chanzo cha kila kitu”“Duh!! Kwaheri”Erick hakuweza kukaa zaidi, basi aliinuka na kutoka kabisa, aliwaaga na kuondoka zake kwani hata hakumuelewa Sarah na wala hakutaka kumuelewa. Muda huu aliingia Elly chumbani kwa Sarah na kuanza kuongea nae,“Ulikuwa unaongea nini na Erick?”“Nilikuwa namwambia ukweli kuwa mimi nilikuwa na mimba na imetoka ndio alikuwa akishangaa kuwa mimba nimeitoa wapi, yani huyu Erick huwa anaongea kama sio mwanaume vile”“Mmmh usiseme hivyo, mimi naogopa mama akijua ukweli maana atanifukuza hapa”“Kwa usalama wako nishakwambia usiondoke kabisa mahali hapa yani endelea kuishi hapa hapa sababu ukiondoka tu basi niotasema ukweli wa mambo ulivyo”“Mmmmh hata nikiwepo, ukikazaniwa na mama yako hutonitaja!”“Subiri wakikazana kuniuliza kuna kitu nitakifanya, tulia tu”“Mmmh kitu gani Sarah?”“Wewe tulia tu, utaona itakavyokuwa”Basi Elly alimuangalia tu Sarah bila ya kusema kitu kingine chochote kile.Erick alirudi nyumbani kwao, na mtu wa kwanza kumuuliza kwanini kachelewa alikuwa ni Erica,“Mbona leo umechelewa sana Erick, ulipita wapi?”“Khaaa Erica nawe, nilipita kumuangalia Sarah”Mama Angel akasikia na kumuuliza Erick vizuri,“Eeeeh Sarah anaendeleaje?”“Anaendelea vizuri mama”“Unajua anachoumwa?”“Hapana, kasema homa tu”Erick aliogopa kusema kwani aliona hayo mambo kama ya kikubwa sana kuongelewa na yeye, basi mamake nae hakumuhoji zaidi.Usiku wa leo mama Angel aliongea na mume wake kuhusu mtoto Sarah yani alijikuta akitamani sana kujua ukweli wa kuhusu mtoto huyu,“Kwakweli mume wangu natamani sana kujua vingi kuhusu Sarah”“Kwanini au kwavile umesikia kuwa ni shangazi yako?”“Yani sijui kwanini? Natamani kujua vingi, halafu roho inaniuma sana kuona kaharibikiwa, najua tukiujua ukweli basi tutaweza kumlea na tutakuwa na uhuru nae tofauti na sasa ambavyo mama yake kamshikilia”“Fatilia kwanza ujue ni nani alimpa mimba nadhani ndio mengine utayafahamu”“Yani huyo mjinga wa kumdanganya Sara nikimjua dah sijui hata nitamfanya nini jamani!! Yule mtoto nampenda sana, hata sijui kwanini mama yake katokea kuwa Manka jamani, yani mimi yule Manka huwa sivutiwi nae kabisa haswaa yale maneno yake ya kujiona ni bora kushinda wengine. Sijui kwanini mtoto bora kama Sarah kumpata mama kama Manka”“Ndio mama yake sasa, utafanya nini wewe?”“Ila kesho nitaenda, najua Sarah nikiongea nae vizuri ataniambia mengi sana, natamani sana Sarah akae katika mstari ulionyooka”“Haya, mimi hata sijishughulishi kwa hilo”Baba Angel hakutaka kujifanya anashughulika sana na mambo yale kwani mkewe alimfahamu vizuri sana kuwa atamgeuka tu na kusema anashughulika vile sababu ya mama Sarah, kwahiyo yeye akajiepusha kabisa.Basi moja kwa moja waliamua kulala tu kwa muda huo.Leo Mama Sarah alikaa nje na mwanae huku akiongea nae mawili matatu kuhusu kile kilichomtokea,“Eti mwanangu Sarah niambie jamani, nani muhusika wa yote hayo? Nafanya hivi kwaajili yako mwanangu”“Kwani unataka kumfanya nini huyo muhusika mama?”“Hakuna kitu ila nataka nikufundishe, najua Sarah mwanangu huelewi vizuri kuhusu mapenzi ndiomana imefikia hatua ya kufanya hivyo, sasa watu wote wamejua kuwa mimi sio mleaji mzuri ni bora ningekugundua mimi mwenyewe kuliko lile kundi lililokugundua kuhusu hili, hadi napata aibu”“Sasa mama, niache kuona mimi aibu uone wewe mama yangu jamani!!”Muda huo alifika mama Angel na kuwakuta pale nje, basi aliwasalimia pale na kuungana nao pale nje huku akimpa pole Sarah kwa yale yaliyomkuta na kumuuliza,“Kwanza Sarah ni nani aliyekwambia kuhusu kwenda kuchoma sindano ya uzazi wa mpango?”“Tulifundishwa shuleni njia za kuzuia mimba, na mchumba angu hakutaka nipate mimba kwa kipindi hiki wakati nasoma ndio tukashauriana nikachome sindano”Mama Angel alipumua kwanza maana alikuwa kama haelewi vile, alimuangalia vizuri Sarah na kumuuliza,“Kwani Sarah unamchumba?”“Ndio ninaye na wote mnamfahamu”Mama Angel na mama Sarah waliangaliana na kujikuta wakiuliza kwa pamoja,“Nani huyo?”Sarah alicheka na kusema,“Ni Erick”Yani mama Angel alihisi kama moyo wake ukipasuka kusikia kuwa mwanae ndio muhusika wa matendo yale. Mama Angel alipumua kwanza maana alikuwa kama haelewi vile, alimuangalia vizuri Sarah na kumuuliza,“Kwani Sarah unamchumba?”“Ndio ninaye na wote mnamfahamu”Mama Angel na mama Sarah waliangaliana na kujikuta wakiuliza kwa pamoja,“Nani huyo?”Sarah alicheka na kusema,“Ni Erick”Yani mama Angel alihisi kama moyo wake ukipasuka kusikia kuwa mwanae ndio muhusika wa matendo yale.Alimuangalia vizuri Sarah na kumuuliza tena,“Huyo Erick ni Erick mwanangu mimi au ni yupi?”“Ndio huyo huyo”“Kwahiyo ndio aliyekupa mimba, na ndio aliyekushauri kuhusu uzazi wa mpango?”“Ndio, na hata jana kaja kuniona”Halafu Sarah akainuka zake na kwenda ndani, kwahiyo alimuacha mama yake pale na mama Angel wakitazamana bila ya jibu, ni mama Sarah ndiye aliyeanza kuongea,“Mbona makubwa haya, unajua Erick na Sarah ni ndugu!”“Ni kosa lako Manka, kwanini hukutaka mtoto aujue ukweli? Hebu ona mambo kama haya kweli! Yani haijalishi Sarah ni mtoto wa mzee Jimmy au Derrick bado ni ndugu kwa Erick maana aaaarghh hata sijui nisemeje”“Ila mwanao ana tabia mbaya jamani, kujifanya mpole vile kumbe kaanza mambo mabaya. Haya Manka hajui kulea mtoto, na wewe je umeleaje huyo wako?”“Sikia nikwambie, hii ni ajali tu kama ajali zingine ila hata hivyo bado hainiingii akilini kabisa, mwanangu Erick namfahamu vizuri sana, hawezi kufanya kitu cha namna hii, kwanza Erick alikuwa akimuheshimu sana Sarah”“Watoto wa kiume ni wa kuwakatalia basi!! Hebu nenda kaongee vizuri na kijana wako, mimi hizi habari zimenichanganya kwakweli, halafu tujue cha kufanya maana Erick na Sarah ni ndugu”Mama Angel pia alihisi kama akili yake kwa muda huo haifanyi kazi vizuri, basi aliamua kuaga na kuondoka zake.Leo usiku wakati baba Angel katoka kazini, mkewe aliamua kuongea nae chumbani kuhusu vile Sarah alivyosema, ila baba Angel alicheka kidogo hadi mkewe akamuuliza,“Sasa unacheka nini? Ni habari ya kuchekesha hiyo?”“Hapana, ila nimetambua kuwa mwanangu ni mwanaume rijali”“Khaaa sikutegemea kama utafurahia huu ujinga baba Angel jamani, huu ni urijali au ujinga? Kwahiyo umefurahi kwa mtoto kurithi tabia mbaya kama hii? Halafu kaa ukijua kuwa Erick na Sarah ni ndugu”“Hapana mke wangu sijafurahia kiivyo, ila nilichocheka ni kuwa alichokifanya Sarah ni sawa na alichokifanya Daima, yani hapo ni wazi kuwa Erick kasingiziwa”“Kasingiziwa vipi wakati hata wewe ndio ilikuwa tabia yako hii!”“Ni kweli mimi sikuwa kijana safi hata kidogo tena nilikuwa msumbufu sana, natakiwa nisishangae sana kuhusu kijana wangu kuwa hivyo maana nitaishia kusema tu amerithi kwangu ila nakataa hiyo kitu asilimia mia moja kwa kijana wangu Erick, nakataa kabisa mwanangu hajafanya hiko kitu hata kidogo. Huyo Sarah kafanya kitu kama alichokifanya Daima tu, ila huyo Sarah sijajua lengo lake nini ila mwanangu Erick hawezi kufanya kitu cha namna hiyo”“Mmmh ila mimi nitamuuliza tu Erick, na hivi kesho ni mapumziko basi nitamuuliza Erick”Baba Angel wala hakubisha sana alimuacha mkewe afanye vile atakavyotaka.Kulipokucha leo, Erick na Erica walitoka nje na kuanza kufanya usafi wa nyumba yao, walisafisha ndani na kisha kwenda kusafisha nje ya nyumba yao, wakati Erick akikatakata maua, Erica alikuwa akikusanya yale majani ya maua na kuyaweka sehemu moja, muda huu baba yao alitoka nje na kuwakuta watoto wake wakiendelea na ile kazi kwakweli alifurahi sana na kuwaambia,“Kwakweli watoto wangu mnajituma sana, hadi nahisi fahari kuwa nanyi, leo jioni nikirudi mjiandae maana nitaenda nanyi kutembea kidogo”Erick na Erica walifurahi na kumuitikia baba yao, kisha baba yao pale aliwaaga na kuondoka zake, kwakweli alikuwa akijihisi ufahari sana kupata watoto wanaopenda kujituma kama wale.Mama Angel nae alitoka nje kabisa muda huu na kukuta ndio wamemalizia ule usafi waliokuwa wakifanya,“Oooh watoto wangu mmefanya kazi kubwa sana, nitamuita yule kijana aje tu kuyabeba hayo matakataka akayatupe, kwakweli watoto wangu mananifurahisha sana. Ila mkitoka kunywa chai nina maongezi kidogo na wewe Erick”Erick aliitikia tu ila hakujua kuwa ni maongezi gani ambayo mama yake alikuwa nayo juu yake, basi waliingia ndani na moja kwa moja kwenda kuoga maana hata kuoga walikuwa hawajaoga, walipomaliza ndio walienda kunywa chai huku Erica akimwambia Erick,“Natamani na mimi nikasikilize hayo maongezi ya wewe na mama”“Khaaaa Erica jamani, unajua una mambo ya ajabu sana, sasa maongezi ya kwangu halafu unataka ukayasikilize kweli!!”“Ndio, natamani kujua ni kitu gani yani roho inaniuma kweli kwa kutokujua. Basi nikuombe kitu Erick ukishaongea na mama naomba unihadithie ni kitu gani”“Haya, baba si kasema tutaenda kutembea? Basi nitakuhadithia huko”Yani Erica alitamani sana mama yao aseme hayo maongezi na yeye akayasikilize kuwa yanahusu nini.Erick alipomaliza kunywa chai moja kwa moja alimfata mama yake ili aweze kuongea nae, ila mama Angel alimtambua mwanae vizuri, alimwambia asubiri kwanza atamuita mwenyewe, alitaka kwanza chai aliyokunywa imshuke maana hasira za mwanae alizitambua fika zilivyo, haswaaa kitu cha kusingiziwa huwa hapendi kabisa.Kwenye mida ya mchana, mama Angel alimuita Erick kwenye bustani yao na kuanza kuzungumza nae kuhusu madai ya Sarah,“Kwanza mwanangu samahani, ile juzi ulienda kumuona Sarah kwanini?”“Mmmh mama! Ni vile niliambiwa Sarah anaumwa, nilimuuliza Elly akasema kwanini nisiende kumuona ndio nikaenda kumuona”“Unajua anaumwa nini Sarah?”“Mimi sijui mama”“Hajakwambia chochote?”“Mmmmh hajaniambia”“Basi Sarah alikuwa mjamzito na hiyo mimba imetoka”Erick alijifanya kushtuka kwani hakutaka kumuonyesha mama yake kuwa anafahamu hizo habari, basi mama Angel aliendelea kusema,“Mimba ya Sarah imetoka sababu alienda kuchoma sindano ya uzazi wa mpango. Nilienda jana kumuuliza vizuri kuwa ni nani aliyempeleka kuchoma sindano ya uzazi wa mpango na ni nani muhusika wa mimba iliyotoka, akakutaja wewe”Hapa ndio Erick alishtuka zaidi na kumuuliza kwa makini mama yake,“Kanitaja mimi?”“Ndio, mwanangu Erick naomba uniambie ukweli unajua mimi ni mama yako. Niambie ukweli tafadhari usinifiche”“Mama, nakwambia ukweli wa moyo wangu. Mimi sijawahi kufanya hayo mambo kabisa, na hata hivyo nakumbuka uliniambia kuwa Sarah ni ndugu yangu, nawezaje kufanya huo ujinga nae!”“Nimekuelewa mwanangu hata usijifikirie vibaya wala nini, nimekuelewa vizuri sana mwanangu. Naomba usifikirie vibaya, nilitaka tu ukweli na ushanipa ukweli, naomba usifikirie kuhusu hilo”Kisha mama Angel aliachana na Erick kwani hakutaka kumlazimisha zaidi mtoto wake kwa kitu alichokataa kabisa kukifahamu. Kisha mama Angel aliamua kwenda kuendelea na mambo yake mengine.Mama Sarah alijiandaa na kuondoka nyumbani kwake, maana alipanga kukutana na Rahim ili aweze kuongea nae kuhusu ya nyumbani kwake,“Mwanangu Sarah nikuletee nini?”“Hapana mama, hata sitaki chochote”“Mmmh mwanangu jamani!!”“Labda chokleti”Basi akaagana nae na kuondoka zake, moja kwa moja alienda kukutana na Rahim kama ambavyo alipanga kukutana nae na kuanza kuongea nae,“Yani binti yangu ana matatizo, sijui alipata mimba halafu akaenda kuchoma sindano ya uzazi wa mpango na ile mimba ikatoka”“Ila watoto wa siku hizi wabunifu”“Ubunifu wao nini sasa?”“Hajataka shida, kaenda kujichomea sindano na mimba ikatoka, hapo katumia elfu mbili au elfu tatu maana alivyozidiwa mmeshughulika nae wenyewe”“Sio ubunifu ule ni ujinga”“Kwahiyo binti yako mjinga?”“Ndio ni mjinga, ni kweli zile sindano zina uwezo mkubwa sana wa kutoa mimba ila mara nyingine ile mimba inaweza isotoke na kukupa shida sana na ukazaa mtoto asiyeeleweka mwanzo wala mwisho, au mara nyingine mimba ikatoka na kukusababishia matatizo makubwa sana. Ndiomana ni vyema mtu kwenda hospitali na kutumia njia nzuri ambazo madaktari wanatumia katika kutoa mimba”“Kwahiyo unasapoti utoaji wa mimba?”“Hapana, sisapoti hata kidogo. Kwanza roho inaniuma sana kuhusu mwanangu, tumempana kasema mimba kapewa na Erick”“Erick yupi?”Mama Sarah akaanza kumueleza Rahim kuhusu huyo Erick bila ya kujua kuwa Rahim anaielewa hiyo familia vizuri sana, basi Rahim akasema,“Unachukua uamuzi gani?”“Sijui nifanyeje sasa”“Nipeleke nikaongee na binti yako, nataka niongee nae kama baba anavyoongea na mwanae”Mama Sarah aliona kuwa ni sawa, basi akakubaliana nae na kuondoka mahali hapo kuelekea moja kwa moja nyumbani kwa mama Sarah.Jioni hii ya leo, baba Angel alivyorudi nyumbani tu aliwataka watoto wake wajiandae kwaajili ya kwenda kutembea nao kwa muda huo.Walijiandaa na kutoka na baba yao, moja kwa moja walienda ufukweni na kuanza kufurahi huku kwahiyo Erick na Erica walikuwa wakirushiana rushiana maji, muda huu baba Angel akamuona Steve akiwa ameongozana na kijana mwingine, basi aliwasogelea na kuwasalimia, ambapo Steve alimtambulisha yule kijana kwa baba Angel,“Huyu anaitwa Paul, ni mtoto wa madam Oliva”Basi baba Angel alisalimiana na mtoto yule pale na kuongea mawili matatu, kisha alimvuta Steve kwa pembeni na kumuuliza,“Kwani madam Oliva ulizaa nae?”“Hapana”“Mbona huyu mtoto ni wewe mtupu?”“Duniani wawili wawili, hata mimi huwa sielewi ni kwanini nimefanana hivi na huyu mtoto”“Steve sikia nikwambie kitu hiki, huyu ni mtoto wako, yani ni mtoto wako kabisa napata hisi a hizo kuwa huyu Paul ni mtoto wako”“Khaaa jamani, mimi na Oliva tumefahamiana rasmi mwaka huu, sasa tutoe wapi mtoto mkubwa hivi! Ila mimi mwenyewe huwa namuangalia sana huyu mtoto na huwa namuona kama mwanangu mzazi kabisa, yani najiona ni wazi kuwa mimi ni baba Paul”“Duh!! Kwlei dunia ina mambo hii, yani mtoto kakuranda kila kitu, Steve chunguza vizuri ila huyu ni mwanao”“Sasa nichunguze nini? Mama halali wa huyu mtoto sijawa nae kwa kipindi hiko, nimekuwa nae kwa kipindi hiki, je huyo itawezekanaje kuwa mwanangu?”Baba Angel hakutaka kuongea zaidi ila bado alihisi kwa upana zaidi kuwa yule mtoto ni mtoto wa Steve. Waliongea kidogo pale na kuagana, halafu baba Angel aliwafata watoto wake ambao walikuwa wakichezea chezea maji na kuwataka kwa muda huo waweze kwenda kula sasa.Mama Sarah alifika na Rahim nyumbani kwake, na kumkuta Sarah yupo tu nyumbani kama alivyomkuta, kisha Rahim alitaka kutoka nje ya nyumba na kuzungumza na yule mtoto, ambapo ilikuwa hivyo alitoka nae na kuanza kuzungumza nae,“Unajua madhara ya kutoa mimba?”“Sijui sema mimi sikupanga kutoa mimba yani imetokea tu bahati mbaya, sikupanga kitu cha namna hiyo”“Ila ulipanga kubeba mimba?”“Hapana sikupanga, mimi bado mdogo mimi ni mwanafunzi”“Unasikitisha Sarah, unajua wewe ni binti mdogo sana. Huwa mambo ya kijinga namna hiyo yanafanywa na mabinti walioshindikana kwa wazazi wao, unakuta binti hajulikani popote wala lolote ndio hufikia hiyo hatua. Haya ni nani kidume aliyekudanganya yote hayo?”“Ni Erick”Rahim alimuangalia vizuri Sarah na kumuuliza tena,“Ni nani?”“Ni Erick”Rahim akamuangalia tena na kumwambia,“Hebu Sarah niangalie machoni”Sarah akafanya hivyo kwa muda na kushusha macho yak echini, Rahim akashtuka kidogo na kusema,“Basi, nakusihi tu upende masomo achana na mambo ya mapenzi yatakuharibu akili yako”Rahim aliinuka na kumuita mama Sarah kisha akamwambia,“Kuna kitu nimekigundua kuhusu binti yako”“Kitu gani hiko?”“Aaaah sijui hata nikwambiaje, ila kuna kitu sielewi sijui ni hisia zangu sijui ni nini?”“Kitu gani?”“Nimewahi kumuona binti mmoja mwenye macho kama Sarah miaka mingi iliyopita, sitaki kumuongelea binti huyo kwasasa, ila kuna tatizo kwa binti yako. Kaa nae vizuri, mfundishe kama mama, binti yako ni muelewa sana muelekeze vizuri atakuelewa”“Unajua sikuelewi Rahim, kwani ni kitu gani umegundua kwa Sarah”“Aaaah unajua mimi nina mahusiano na wewe!! Si vizuri kwakweli”“Si vizuri nini? Sikuelewi”“Ila naomba namba ya huyo mamake Erick”Mama Sarah alimpatia Rahim namba ila bado hakumuelewa, Rahim aliaga na kuondoka na kumuacha mama Sarah akiwa haelewi chochote kile kilichoongelewa na Rahim, alienda kumuuliza binti yake moja kwa moja kitu ambacho alikuwa akizungumza na Rahim ila Sarah alimueleza tu vitu vya kawaida hata alishangaa ni kwanini Rahim kasema vile.Wakati baba Angel na watoto wake wanarudi nyumbani, walikutana njiani na Sia, na yule Sia ndio aliliona gari la baba Angel kwani alilisimamisha ikabidi baba Angel ashuke kumsikiliza kuwa anasemaje,“Yale niliyokwambia umeyafanyia kazi?”“Yapi hayo?”“Kuhusu Elly na Derrick na kuhusu Erick na mimi”Baba Angel akakumbuka kitu na kujikuta akiunganisha matukio,“Tena umenikumbusha kitu, hivi si ulisema kuwa wewe ulibadilishana na baba yangu watoto?”“Ndio, na alinilipa kufanya hivyo. Sikutaka ila umasikini ndipo umepelekea haya”“Kwahiyo hujui mwanao alipo?”“Sijui kivipi wakati mwanangu ni Erick!”“Erick sio mwanao, yani nakataa kabisa. Ila tusiandikie mate wakati wino upo. Mimi nitakupelekea wewe na Erick hospitali mkapime damu, najitolea kulipa kila kitu halafu tukipata majibu ndio utajua kuwa mtoto wako yuko wapi”“Mmmmh unamaanisha nini?”“Unajua katika maisha kuna ujinga mtu unaufanya ila hufikirii kuwa ujinga huo utakufanya nini badae, unaona sawa tu kufanya ujinga ulioufanya, mimi nina kuhakikishia kabisa Erick sio mtoto wako”“Mmmmh!! Haya nipo tayari kwenda kupima nae”“Kwenye ukweli, uongo hujitenga. Kesho tutaondoka wote ila usimwambie chochote Erick kuwa tunaenda kupima nini, tutamchukua tu damu halafu nitakuita nawe uchukuliwe damu, ikipimwa ndio nadhani utaweza kujiongeza sasa kuwa mwanao yuko wapi? Uache tamaa za kijinga, umasikini usiwe chanzo cha ujinga, kwaheri”Baba Angel alimuacha Sia akijiuliza vitu vingi sana bila ya jibu lolote lile.Usiku wa leo, baba Angel anaamua kuongea na mama Angel kuhusu kuonana kwake na Steve akiwa ameongozana na mtoto Paul,“Yani yule mtoto ni moja kwa moja ni mtoto wa Steve, niliwahi kumuuliza Steve aliniambia kuwa yeye mtoto aliyezaa na Sia tu ndio aliamini kuwa ni mtoto wake. Sijawahi kuongea na Oliva ila napata hisia kuwa yule ndio mtoto wa Steve”“Mmmmh mbona makubwa haya”Halafu baba Angel alimuelezea mama Angel vile ambavyo Sia alimsimulia na jinsi alivyomwambia,“Unajua Sia anakazana bado kusema Erick ni mwanae, mimi najua tu kuwa sio ukweli. Naenda kuvunja nae mzizi wa fitini kwa kupima damu yake na damu ya Erick kesho”“Bora iwe hivyo maana anakera sana yule”“Ila mimi nina hisia mbaya sana toka nimuone Steve na yule mtoto, nahisi yule mtoto wa madam Oliva ndio mtoto wa Sia na Steve”“Kheeee basi itakuwa Elly ni mtoto wa madam Oliva na Derrick, ila imekuwaje hiyo?”“Kumbe madam Oliva alizaa na Derrick?”“Ndio hivyo”“Basi itakuwa ni kweli maana kwa maelezo ya Sia ni kuwa alibadilisha watoto, kwahiyo kuna uwezekano mkubwa sana kuwa hao watoto walibadilishana”“Mmmmh inawezekanaje?”“Nasikia baba yangu ndio alifanya huo mchezo mzima, sijui ni kwanini alifanya hivyo, au baada ya kukosa mtoto wangu ndio akafanya hivyo sielewi, kuna siri kubwa sana kwa huyu mzee”“Inatakiwa basi tumtafute bi.Aisha atakuwa anafahamu mambo mengi sana”Mara simu ya mama Angel ilianza kuita, ikabidi aipokee simu ile na kuanza kuongea nayo,“Rahim anaongea hapa”“Kheee unataka nini?”“Sikia, hebu jifunze kulea watoto basi unaachiaje watoto hadi wanaenda kupena mimba? Umewezaje kutokumfunza vyema huyo Erick mdogo?”“Hapana, mwanangu si muhusika wa mambo hayo”“Unamkatalia ulikuwa nae? Au unagtembea nae kila mahali?”“Hapana, namfahamu vyema mwanangu, hana tabia hiyo”“Hivi Erica unawezaje kukataa hilo, ikiwa baba na mama mmeoana ila wote mnafanana tabia, watoto je watakuwaje eeeh!”“Kwani wewe shida yako nini, nishakwambia mwanangu hahusiki. Nakata simu sasa hivi”“Hapana, usikate simu hata mimi najua kuwa mwano hahusiki na kitu chochote ila naomba nikupe kazi ndogo”“Kazi gani?”“Nenda kazungumze na Sarah, halafu ukiwa unaongea nae muangalie kwenye macho yake ndio utagundua ukweli wake na uongo wake”“Kwahiyo wewe umeongea nae?”“Nimekupa hiyo kazi, nilikuwa nakutisha tu kuhusu mwanao, namfahamu vizuri sana mwanao Erick, ni rafiki yangu mzuri tu naelewa wazi kuwa hawezi kutenda jambo hili. Kuna watoto hata ukiwaangalia unawahisi wanaweza kufanya lolote ila sio kwa mtoto kama Erick, mchunguze Sarah na utaweza kufahamu mambo mengi sana”“Haya nitafanya hivyo asante”Alikata simu ila kwa muda huu hakumueleza mumewe kitu alichokuwa akiongea wala baba Angel nae hakumuuliza mkewe kitu alichokuwa akikiongea kwenye simu.Kulipokucha tu, wanafanya mambo yao mengine na kuamua kwenda Kanisani ila Vaileth anadai kuwa hayupo kwenye hali nzuri kwa siku hiyo, kwahiyo wote wanaondoke na yeye anabaki mwenyewe.Muda kidogo tu alifika Junior pale nyumbani na kufurahi sana,“Kwanza nimefurahi kwa yule jini kisirani kuondoka”“Mjinga sana yule binti”“Halafu unajua ubaya alioufanya? Kamsingizia baba kuwa anataka kumbaka”“Khaaaa mjinga sana yule Daima”Basi wakainuka na kwenda chumbani, ila Vaileth akakumbuka kuwa bado hajafunga milango, ndio akarudi sebleni ile anataka kufunga tu mlango akaingia mama Junior, ikabidi asalimiane nae pale na mama Junior akakaa pale sebleni,“Yani sijakuta mtu eeeh!”“Hawapo ndio wote wameenda Kanisani”“Hawa watu nao kujifanya wanapenda sana Ibada hadi kero jamani, ila nitawasubiri hapa mpaka warudi”Vaileth alitulia kimya kwani aliona ni jinsi gani swala lake linaharibika kwa muda huo, akakaa nae kidogo tu na kumwambia,“Mama, samahani nataka niende kuoga”“Kheee kumbe hujaoga? Mbona umejipodoa kabisa?”Vaileth akajichekesha kidogo na kusema,“Mwanamke kupendeza mama, si huwa mnasema hivyo sio nionekane mchafu tu muda wote”“Mimi sikujua kama hujaoga, haya nenda kaoge”Vaileth alienda chumbani kwake na kufunga mlango, na kuongea kidogo na Junior,“Mama yako kaja Junior, balaa leo na kasema haondoki hadi warudi”“Duh huyu mama nae sijui ana matatizo gani, sasa anataka nini tena?”“Hapa nimekuja tu nimemdanganya kuwa naenda kuoga”“Haya, itabidi leo tukaoge wote yani kashaniharibia tayari huyu mama”Junior hakupenda kabisa kwa uwepo wa mama yake mahali hapo kwa wakati huo.Leo Sarah alimgomea Elly kutoka kabisa kwahiyo Elly alibaki na Sarah nyumbani tu kwa siku hiyo, na walikaa nje pamoja huku wakiongea ongea,“Unajua mimi nilishazoea kwa mama kwenda kwenye Ibada”“Sasa unaenda kufanya nini kwenye Ibada na hizi dhambi tulizofanya?”“Mmmh dhambi gani?”“Inamaana hujui? Uzinzi ni dhambi halafu sisi tumefanya uzinzi, nimepata mimba nje ya ndoa, nayo ni dhambi. Tumeenda pamoja kuchoma sindano ya uzazi wa mpango na kusababisha mimba itoke kwahiyo tumefanya dhambi ya mauaji maana kutoa mimba ni uuaji, halafu tumesema uongo”“Mmmh uongo gani tena?”“Mimi nilimwambia mama Erick kuwa Erick ndio muhusika wa kila kitu”Yani Elly hadi alihisi kupaliwa kabisa na kumwambia Sarah,“Mbona unanizidishia dhambi jamani, huo uongo mimi nimeusema muda gani?”“Mimi na wewe tumekuwa mwili mmoja, kwahiyo nikisema mimi uongo ni sawa na umesema wewe”“Duh!!Sijategemea kusikia neno kama hilo”“Ndio hivyo, mimi na wewe si tutaoana eti!!”“Duh!! Sarah!”Elly alihisi tena kukohoa na akaamua kwenda ndani kuchukua maji ya kunywa.Ibada ilipoisha, walitoka ila mama Angel alihitaji kwenda kumuona Sarah kwani alitaka atomize ile azma ya kuongea nae kwa siku hiyo, kwahiyo aliwataka wale warudi nyumbani na mtoto, baba Angel aliongea nae kidogo tu,“Nitarudi nao na kutoka kidogo na Erick kwa ile niliyokwambia jana”“Oooh nakumbuka vizuri, haya mimi ngoja iende”Mama Angel aliwaacha wale wameondoka kurudi nyumbani halafu yeye alianza safari ya kwenda kwa mama Sarah kama alivyopanga.Mama Angel alivyofika alimkuta Sarah pale nje na moja kwa moja kwenda kuongea nae, na alipomuuliza kuhusu aliyempa mimba bado alikazana kuwa ni Erick,“Una uhakika na hilo Sarah? Mbona Erick kakataa kabisa?”“Anakataa tu ila ndio yeye”“Hebu niangalie machoni Sarah”Basi alianza kutazamana na Sarah, na alipomuangalia vizuri alishtuka pia, na kumwambia,“Unajua Sarah tumefanana sana macho, yani tumefanana sana, sikugundua jambo hili ndio nagundua leo. Hupendi kutazama machoni Sraah sababu unaongea uongo, ila kaa ukijua kuwa wewe na huyo Erick ni ndugu”“Mmmh ndugu kivipi?”“Sarah, mimi ni shangazi yako. Yani hapa hakuna ubishi hata kidogo, kwa mfanano huu! Mimi ni shangazi yako Sarah, usimwambie ukweli mama yako ila nitakuja kukuchukua na kukupeleka kwa baba yako. Niambie ukweli Sarah, nani muhusika wa yote”“Ni Erick”Sarah akainuka na kwenda ndani kwani hakutaka kuongea sana, basi Sarah alivyoenda ndani ikabidi mama Angel nae ainuke ili aondoke ila nyuma aliitwa,“Mama Erica”Mama Angel alisimama na kugeuka nyuma, akamuona aliyemuita kuwa ni Elly, kisha alimsogelea mama Angel na kumkumbatia kisha akamwambia,“Naomba msamaha, naomba niokolewe kwenye dhambi hii”“Dhambi gani?”“Sio Erick aliyehusika, ni mimi”Mama Angel alimuangalia Elly na kumshangaa Mama Angel alisimama na kugeuka nyuma, akamuona aliyemuita kuwa ni Elly, kisha alimsogelea mama Angel na kumkumbatia kisha akamwambia,“Naomba msamaha, naomba niokolewe kwenye dhambi hii”“Dhambi gani?”“Sio Erick aliyehusika, ni mimi”Mama Angel alimuangalia Elly na kumshangaa.Kwakweli mama Angel alipenda kuongea zaidi na Elly, alimuomba asogee nae mahali ili waweze kuongea, nae Elly alikubali kwani alitaka kuisafisha dhamira yake.Walipanda pamoja kwenye gari ya mama Angel na kuelekea sehemu ambayo kuna mgahawa kisha walishuka hapo kwani mama Angel alitaka kumsikiliza vizuri Elly,“Eeeeh nieleze sasa, maana hata sijakuelewa, kwahiyo muhusika ni wewe?”“Ndio ni mimi, namaanisha kuwa ni mimi ndiye nilimpa mimba Sarah, na ni mimi ndiye niliyeenda na Sarah mpaka kwenye kituo ambacho alichoma sindano ya uzazi wa mpango”“Kheee hebu nielezee vizuri kwanza, ilikuwaje hadi ikawa hivyo Elly?”“Sijui nikwambiaje yani, ila kwa kifupi ni umasikini ndio umesababisha haya”“Hebu nielezee vizuri Elly?”Yani Elly hakumficha kitu chochote, alianza kumueleza mama Angel toka siku ya kwanza ambayo alianza kushawishiwa na Sarah na hadi walipoenda kuchoma sindano,“Mimi sikujua kama ana mimba, na tulinunua hadi kipimo cha mimba ila nilikuwa naogopa kweli kama akipima na kugundulika kuwa ana mimba itakuwaje? Siku ile uliyonikuta na kwenda nami hospitali kule ndio siku ile niliyoenda na Sarah kumsindikiza kwaajili ya kuchoma sindano na alisema kuwa tukifika kule niseme kuwa mimi ni mdogo wake ili yeye anaonekane mkubwa”“Duh! Yani nimesikitika sana, unajua kitu gani?”“Nini?”“Wewe na Sarah ni ndugu”Elly akashtuka ila aliikataa ile kauli,“Haiwezekani”“Ndio hivyo Elly usikatae, yule Derrick wa siku ile ndio baba yenu”“Mmmh haiwezekani, sijui kama yule anaweza kuwa baba yangu, mbona mama amekataa jambo hilo”“Tulia bado nafanya utafiti ila nitakuja na jibu zuri tu, sasa kuna kitu Elly. Ukiendelea kukaa kule lazima Sarah ataendelea kukusumbua”“Tena sio Sarah peke yake, bali hata yule mdada wao wa kazi ananisumbua sana”“Kheee hadi yule Siku anakusumbua?”“Ndio, nimewahi kulala nae mara moja”Mama Angel akaona hili ni tatizo tena ni tatizo sana, basi alimuomba kitu Elly,“Naomba turudi wote nyumbani kwangu, naomba ukaishi kwangu kwanza”“Mmmh naogopa maana mamake Sarah ndio anayenisomesha mimi”“Hata mimi ninao uwezo wa kukusomesha Elly kuliko hiyo fedheha unayoipata, nakuomba ukubali. Halafu kesho tutaenda wote kwa yule baba wa siku ile pamoja na Sarah, tutaenda kumfata”“Kwahiyo kesho nisiende shule?”“Ndio kwa kesho itabidi tu usiende shule, najisikia kuweka sawa haya mambo kwanza, nimeumia sana moyo kwa hayo maelezo yako Elly, kama mama nimeumia sana”Elly alikubali kuondoka nae, kwahiyo kwa muda huo yeye na Elly waliondoka kuelekea nyumbani kwake.Mama Angel alipofika nyumbani kwake, anamkuta dada yake yuko pale akimsubiria yani siku hii mama Junior alijipanga kuwa hatoki kwenda popote pale mpaka aweze kuonana na mama Angel, basi moja kwa moja alimuacha Elly pale na kwenda na dada yake kwenye bustani kwaajili ya kuongea,“Eeeeh dada yangu nini tena kimetokea?”“Nimefatwa na wazazi wa Daima, nasikia mmemtimua Daima hapa nyumbani, basi mama yake kaja na kuongea maneno machafu sana”“Dada, huyo Daima hafai hata kidogo”Mama Angel alimuelezea yale matukio machache ya Daima ambayo yalimkera sana na kufanya wamtoe pale nyumbani,“Kaenda kusema kuwa mume wangu alitaka kumbaka! Mwanangu Erick alitaka kumbaka! Mtoto mwehu kabisa yule”“Kheee makubwa, mna haki ya kumfukuza kama ni hivyo, yani mama yake kaja kunitukana sana nyumbani”“Yule nae anahangaika tu, mimi pia kaja kunitukana hatari, mtu kashindwa kulea mtoto halafu anataka kutusumbua akili zetu tu. Akatulie huko na mtoto wake. Nimemwambia asubiri huyo mtoto wake ajifungue ili tukampime huyo mtoto kama kweli ni damu yetu”Basi waliongea mengi, ndipo mama Junior aliuliza pia kuhusu mama Angel kufika na Elly pale,“Hivi yule si mtoto wa Sia yule! Imekuwaje hadi umekuja nae kwako?”“Dada, ni historia ndefu nikikueleza hata hatutaelewana”“Niambie hata kwa kifupi tu”Mama Angel alimueleza tu kuhusu Sarah kupata mimba na jinsi Elly alivyokuja kumwambia,“Halafu sasa dada kuna hatihati kuwa huyu Elly na huyo Sarah ni watoto wa Derrick”“Kheee kwahiyo ni shangazi zetu? Halafu wametembeleana?”“Ndio hivyo, yani sijui tufanyeje maana hii ni aibu sana”“Mmmmh!!”Mama Junior alishindwa kuendelea kuongea mengine ila kidogo ile habari ilimshtua, akaongea kidogo na mama Angel na kuamua kumuaga tu kwa muda ule na kuondoka zake.Moja kwa moja kwa siku hiyo, Elly alipelekwa chumbani kwa Erick ili kulala nae, ila Erick hakupenda kabisa kulala na Elly,“Aaaah mama lakini jamani”“Lakini nini Erick? Lala nae kwa leo tu, halafu kesho Vaileth akikifanyia usafi kile chumba kingine atahamia huko, ila kwa leo lala nae usiwe mbishi mwanangu”Akakubali tu ila kishingo upande.Ila usiku wa siku hiyo walijikuta wakiongea mambo mengi sana na Erick,“Kwanza Erick pole, sikujua ujue kama Sarah anasingizia kuwa muhusika ni wewe!”“Ndio mama alikuja kuniuliza, nikamwambia mbona sijui chochote”“Muhusika ni mimi”“Kheee kwahiyo Elly ulilala na Sarah?”“Ndio, alinilazimisha na nikajikuta tu inakuwa hivyo ila nilijihisi vibaya sana. Mama yako kanionea huruma leo ndiomana kanichukua ili nije nikae huku kwanza”“Mama ana roho nzuri ndio, ila Elly nawe kwahiyo ulikubali kabisa kulala na mwanamke?”“Sikia Erick, yale mambo hayana ujanja, akikuwekea na zile video wewe mwenyewe utajikuta tu umefanya”“Mmmmh, sitaki kujua. Usiku mwema”Basi kila mmoja alilala huku kageukia upande wake, kwakweli siku hii Elly aliweza kulala vizuri kwani siku zote alizokuwa akiishi kwakina Sarah alikuwa akiishi kwa uoga maana kama hajagongewa na Sarah basi lazima atagongewa na Siku.Leo asubuhi ndipo mama Sarah alipogundua kuwa Elly hayupo nyumbani kwake, basi akashangaa sana na kuuliza,“Kwani jana Elly alienda kwao?”“Hapana mama, jana alikuja mama Erick basi Elly ndio akaondoka nae”“Kheee kwanini? Halafu Elly ni mpuuzi sana yule, umasikini wake unafanya awe kero sana, yani kila atakayesema twende basi na yeye yumo tu. Naenda kumfata”“Si atakuwa kaenda shule”“Kaenda shule ya wapi wakati hata sare za shule kaziacha huku, mjinga yule mtoto”Basi mama Sarah alijiandaa na kuondoka, pale nyumbani alibaki Sarah akiwa na Siku, basi Siku alianza kumuuliza Sarah,“Hivi ulijijuaje kuwa una mimba?”“Hata sikujua kama nina mimba, mimi nilienda tu kuchoma sindano, tena kipimo cha kupimia mimba ninacho huku chumbani, kipo kabatini kwangu pale”“Kwahiyo hukukitumia”“Ndio sijakitumia wala nini”“Unampenda Elly eeeh!!”“Sijui, niliyempenda ni Erick ila nikajikuta nipo na Elly hata sijui imekuwaje, kuna muda namuona Elly hana amani kabisa hadi namuonea huruma”“Ila Sarah umeanza mapema sana hayo mambo, ungesubiri hata umalize kidato cha nne”“Ila najikaza tu yani, yale maumivu ya kusafishwa uwiiii yanauma jamani, hadi nilikuwa nahisi roho inatoka. Unajua hata kuongea na Elly najikaza tu hata sitaki tena ule mchezo, nitakufa mimi kabla ya siku zangu”Siku akawa anacheka tu, na kuamua kwenda kuendelea na kufanya shughuli za pale.Mama Angel alijiandaa muda huu na kutoka na Elly kama ambavyo alipanga kwa siku hii kuwa atatoka nae, kwahiyo mtoto alimuachia Vaileth kama kawaida, basi alivyoondoka na Elly moja kwa moja alienda nyumbani kwa mama Sarah, na kuongea na Sarah pale ili akubali waende pamoja, na kweli Sarah hakukataa wala nini alijiandaa na kuondoka nao.Kitu ambacho mama Angel hakumwambia Sarah kwa muda huo ni kuwa amegundua kuwa Erick hana kosa, kwahiyo mama Angel alimuacha Sarah aendelee kuamini vile vile kuwa mama Angel bado haujui ukweli wakati anajua kila kitu.Mama Angel alienda na watoto wale moja kwa moja hadi nyumbani kwakina Derrick ambaye kwa muda huu walimkuta akimwagilia mboga, basi aliwakaribisha vizuri sana na muda huo huo akamwambia mama Angel,“Naona umeniletea na mtoto wangu mwingine?”“Ndio, huyu anaitwa Sarah”“Ona alivyofanana na wewe hayo macho, ulishindwa kutambua kuwa hii ni damu yetu Erica? Huyu ni mtoto wangu, huyu ni wa kwetu”Sarah alikuwa akishangaa sana, halafu Derrick alisogea karibu na Sarah na kumwambia,“Sarah, mimi ni baba yako”“Hapana, mama aliniambia kuwa baba yangu alishakufa”“Hapana Sarah, nipo hai ni mimi baba yako”Sarah akaona anachanganyiwa mada tu hapa maana hakuelewa kitu, basi alimuomba mama Angel warudi tu nyumbani kwa muda huo maana alijikuta kutokumuelewa kabisa huyu aliyesema ni baba yake.Junior alipata upenyo muda huu ambapo familia nzima ilikuwa imetoka, kwahiyo alijiandaa vizuri kabisa kwaajili ya kuondoka na kurudi shuleni.Basi aliagana na Vaileth pale na kuagana nae, wakati anatoka getini ndio akakutana na mama Sarah,“Kheee Junior, ndio unafanya nini hapa? Ndio unaishi hapa?”“Ndio, ni kwa mama yangu mdogo”“Sasa huu muda ndio unaenda shule au unaenda wapi? Mbona umechelewa kama ni shule?”“Aaah siendi shule, kuna mahali tu naenda”“Kumbe Junior wewe ni mdogo eeh!”Junior akacheka tu na kuondoka, kisha mama Sarah alienda ndani na moja kwa moja kuanza kumuuliza Vaileth ambaye alisema kuwa wametoka,“Huyu mwanamke ni mjinga sana, atamchukuaje Elly? Kwanini amchukue Elly? Yani kanikera sana”Basi akainuka na kuondoka zake, kwakweli Vaileth muda huu aliweza kupumua maana toka jana alikuwa akiishi kwa mashaka tu kuwa ikigundulika kuwa Junior yupo chumbani tena chumbani kwake ingekuwaje? Yani alikosa raha kwa siku ya jana, kwahiyo hapa ilikuwa kidogo ni afadhari kwake.Muda kidogo simu yake ya mkononi ilianza kuita, basi akaichukua na kuipokea,“Mimi dada yako Prisca, mbona umetutupa hivyo Nyanda?”“Hapana ila si mnajua baada ya yale masokomoko yenu nawezaje kuaga kila mara kusema nakuja huko kwenu?”“Hata kama, ila sisi tutaendelea kuwa ndugu zako tu, nitakuja kukusalimia siku isiyo na jina”“Mmmh na wewe!”Prisca alikata ile simu ila kiukweli Vaileth hakuhitaji tena ndugu zake wawe wanapatikana eneo lile.Mama Sarah, muda ameondoka pale, ni moja kwa moja alienda kwenye kazi ya Sia ila hakumkuta wala nini, ikabidi aende nyumbani kwake tu, ambapo alimkuta akishughulika na kuweka vitu safi, basi alianza kuongea nae,“Unajua Erica kamchukua Elly na kwenda nae nyumbani kwake?”“Kisa nini?”“Ndio kamchukua, mimi nataka kumkazania ili amrudishe mtoto”“Mkazanie kweli, kamchukua kwa misingi gani sasa?”“Ndio hapo pa kumshangaa, badae nitakupigia simu kama kamrudisha au la”Sia alikubaliana nae, na kwa muda huo mama Sarah aliondoka zake ili arudi nyumbani kwake, njiani alikutana na Rahim, maana mama Sarah alikuwa yupo kutembea kwa miguu tu,“Mbona upo kama umechanganyikiwa?”“Unajua ile jana, kumbe mama Angel sijui alienda nyumbani kwangu halafu kamchukua yule kijana ninayemlea mimi”“Kaenda nae wapi?”“Nasikia kaenda nae nyumbani kwake”“Kwani tatizo lako ni nini? Si atamrudisha tu”“Hata kama, ila atamchukuaje bila ridhaa yangu? Yule mtoto ni kama mwanangu kabisa”“Basi punguza hasira, naomba nimuombee msamaha”“Hebu niondolee balaa mie”“Naona umevurugwa, panda kwenye gari nikurudishe nyumbani kwako”Mama Sarah alipanda na moja kwa moja, Rahim alimpeleka mama Sarah nyumbani kwake na kuachana nae hapo sababu alikuwa na mambo mengine ya kufanya.Siku alivyobaki mwenyewe nyumbani kuna jambo alijiuliza sana, alijiuliza kuhusu yeye na kile kitendo cha kulala na Elly,“Siku ile nilikuwa katika siku za hatari, na kama Elly aliweza kumpa mimba Sarah, atashindwa vipi na kwangu?”Ikabidi aende akachukue kipimo alichoambiwa na Sarah na moja kwa moja kwenda kujipima huku akihofia kiasi majibu ya kile kipimo.Basi alitulia kwa muda na kuangalia yale majibu, akajikuta ni majmzito na kusema kwa nguvu,“Mungu wangu, nitafanyaje mimi!”Mlango uligongwa, ikabidi aweke kile kipimo haraka haraka na kwenda kufungua ule mlango, aliyeingia alikuwa ni mama sarah huku akilalamika kuwa hajawapata na akiongea sana.“Yani mjinga yule sijamkuta na mtoto”“Kheee pole mama”Basi mama Sarah aliamua kwenda kupumzika kwanza.Muda kidogo alifatwa na Siku kuwa kuna mgeni, alipotoka mgeni mwenyewe alikuwa ni mama Angel, basi akaenda kuongea nae amsikia kuwa siku hiyo kaja na jipya gani,“Eeeh unasemaje?”“Naomba tukaongee nje kidogo”Kisha wakatoka nje kwaajili ya kwenda kufanya mazungumzo, basi mama Angel alianza kumwambia,“Ni wakati sasa mtoto anatakiwa kuujua ukweli Manka, mimi nimeujua ukweli ila mtoto naye anatakiwa kuujua ukweli”“Ukweli upi?”“Kuwa baba yake ni Derrick”“Khaaaa kumbe ndio mjinga kiasi hiko wewe, umemchukua mtoto hapa kumbe kumueleza sijui baba yake nani, hayo mambo yanakuhusu ndugu yangu? Mbona huwa wanadamu mnapenda kujitia kazi jamani!”“Hapana, mimi ni ndugu wa Derrick kumbuka, nionapo damu ya kaka yangu lazima nishtuke”“Mambo mengine huwa unayaacha kama yalivyo, nikijisikia kuwaambia nitawaambia, hata hivyo huyu Sarah sio mtoto wa Derrick”“Unajua unakataa ukweli hadi nafsi inakusuta masikini ya Mungu jamani, eeeeh kwanini unakataa ukweli kiasi hiko?”“Hapana cha ukweli wala nini”“Haya, sina mengi ya kusema ila kitu kingine Elly naondoka nae”“Kivipi?”“Kama mama, njoo nyumbani kwangu nikueleze kuhusu Elly, ni mtoto mdogo huyu, sio wakati wa kumsumbua na kumchanganya akili huu”Mama Sarah hakutaka hiko kitu kabisa, ila muda anataka kwenda ndanbi kumzuia Elly, alikuta Elly kashabeba nguo zake zote na kuweka kwenye gari ya mama Angel, kisha mama Angel kwenda kwenye gari nankuondoa gari.Baba Angel akiwa anakaribia kufunga ofisi yake, anafatwa na mgeni na mgeni huyo ni Sia basi anaanza kuongea nae, ambapo Sia anamtolea makaratasi ya ushahidi kuwa alibadilisha watoto,“Hivi Sia una akili kweli wewe?”“Akili ninazo ndio, na ndiomana nimetunza huu ushahidi hadi leo, nisingekuwa na akili kwa hakika nisingeweza kutunza huu ushahidi”“Pole sana, hivi unajua kama unaweza kufungwa na ushahidi wako, maana ulicghokifanya kisheria ninkosa tena umefanya makusudi kabisa, ni kosa kubwa sana tena la jinai”“Sasa mambo hayo ya makosa yanatokea wapi Erick wakati wewe mwenyewe umeniambia nikuletee ushahidi”Basi baba Angel aliupitia vizuri ule ushahidi, ni kweli kulikuwa na mwaniko wa baba yake ukionyesha kuwa ameidhinisha wale watoto wabadilishwe, yani mtoto wa Sia alelewe na mama Angel halafu wa mama Angel alelewe na Sia,“Khaaa jamani, baba yangu hakuwa mtu mzuri kabisa, sasa kama alifanya hivi alikuwa na lengo gani haswaa?”“Sijui, nadhani ni yeye ndio anajua dhamira ya alichokifanya”“Ila mbona kipindi mnabadilisha watoto sikuwepo nchini?”“Erick usibishe, teknolojia ina mambo mengi sana. Ila hebu jaribu kuangalia kwenye ufanano wako wewe na Erick, mtoto gani jamani hufanani nae hata kucha eeeh! Halafu unasimama kabisa kwa sauti kuwa yule ni mtoto wako. Hebu amka Erick, yule sio mwanao”“Mbona na huyo Elly sijafanana nae pia?”“Sia akacheka na kusema,‘Utafanana nae vipi sasa wakati ni mtoto wa Derrick? Pale huna chako labda ulichoambulia ni yule mtoto wa mwisho, ulikuwa unawatoa sana mabinti mimba basi ndio mshahara wako huo maana mshahara wa dhambi ni mauti”“Koma wewe, mimi nilikuwa nawatoa mabinti mimba? Hivi mtu angesema anabaki na mimba yake ningempeleka kwa daktari kutoa? Si wao wenyewe nikiwaambia kuwa sitaki mimba basi wanasema tupeleke tukutoa, mimi nimemshawishi mwanamke kutoa mimba muda gani? Ni upuuzi wao na nujinga wao wenyewe”Sia alicheka na kusema,“Waseme tu vibaya ila Erick kuna siku utalia tena kilio cha mbwa kachoka nakwambia, kuna siku utalia sana. Hao watoto utawalilia sana. Mkeo kakufanyia vizuri sana kwenda kuzaa na nduguye kisha wewe ndio umelea”“Ila una maneno sana Sia, naomba tu siku ya kuchukua majibu twende wote kuchukua ili hapo aeleweke kama kweli Erick ni mtoto wako. Nimeanza kupima nawe makusudi yani vbbipimo vikionyesha hivyo basi kila neno uliloliongea Sia nitaliamini kwa asilimia mia moja”“Haya, majibu yakitoka njoo unichukua ila nina uhakika kuwa Erick ni mwanangu, na wewe huna chako maana Elly ni mtoto wa Erica na Derrick. Halafu kukuonyesha kuwa mkeo hataki mtoto wake awe mbali, kamchukua na kwenda kuishi nae nyumbani kwako pale”Sia alicheka na kuinuka kisha kuondoka zake. Baba Angel alimuangalia ila aliweka kazi zake vizuri na yeye kwenda nyumbvani moja kwa moja.Leo usiku, baba Angel aliamua kumuuliza mkewe kuhusu uwepo wa Elly hapo maana hakuongea nae vizuri kuhusu Elly kuwepo pale,“Eeeeh imekuwaje kwa huyu Elly kuwepo hapa maana hata hujanishirikisha”“Ni kweli nimefanya kosa”Baba Angel moyo wake ukafanya paa, yani alijua mama Angel anafunguka na kusema ukweli kuwa kazaa na Derrick, ila bado alijipa moyo na kuendelea kumsikiliza,“Ila vipi mume wangu, mbona kama huna amani”“Aaaah hamna kitu”“Naomba unisamehe maana sikukwambia jana, nimechukua tu majukumu ya kumleta huyu mtoto hapa bila ya kukushirikisha baba mwenye nyumba naomba unisamehe sana. Ila ngoja nikusimulie kisa kilichofanya nimelete humu ndani huyu mtoto”Mama Angel alianza kumsimulia vile ambavyo ilivyokuwa wakati alipoenda kumuuliza Sarah tena na jinsi Elly alivyoenda na kumwambia ukweli na kueleza maisha anayoishi, kwakweli hata baba Angel alimuhurumia sana na moyo ulimuuma sana,“Yani kuna wanawake ni wapumbavu kabisa”“Kwanini?”“Hivi mwanamke anayezaa mtoto kwa uchungu anawezaje kulipwa hela na kukubali mtoto abadilishwe?”“Yani hapo ndio namshangaa Sia, huyu Elly atakuwa ni mtoto wa madam Oliva, na sijui mtu unaanzaje kumwambia ukweli halisi ulivyo, kwakweli Sia sio mtu mzuri kabisa, yule mwanamke hafai kuigwa na jamii”“Wa kumuiga yule atakuwa chizi na yeye, yani mtu ukubali mtoto abadilishwe sababu ya hela, haya sasa huyo Elly anamshindwa kulea kila siku hadi anaenda kumuingiza mtoto kwenye matatizo kama hayo, hebu ona nina uhakika Elly hatokuja kusahau hiko kitu cha wanawake kumlazimisha kulala nae, nina uhakika kitamuuma siku zote za maisha yake, halafu kumbe yule mjinga alimbadilisha”Basi walijikuta kwa siku hii wakijadiliana tu matatizo ya Sia katika maisha yake mwenyewe.Kulipokucha, leo Sarah anaenda shule, kwahiyo moja kwa moja anaenda darasani na kuendelea na masomo ila muda wa mapumziko anaamua kwenda kumuona Erick na Elly, anamfuata Elly ila hampati na anakutana na Erick na kuanza kuongea nae,“Yani wewe binti una dhambi sana, hivi kunisingizia mimi ndio muhusika wa ujinga wako ndio nini?”“Aaaah nisamehe Erick, nimefanya hivyo sababu nakupenda”“Akili mbovu kabisa, ushaambiwa kuwa mimi ni ndugu yako unachonipenda haswaa unanipendea kitu gani eeeh!!”“Nakupenda tuwe wapenzi”“Toka lini ndugu wakawa wapenzi? Umeanza kuchanganyikiwa Sarah eeeh!! Muone vile, na una bahati ukweli umejulikana, maana bila ukweli kujulikana nahisi ungejuta kunifahamu nakwambia”“Ukweli upi umejulikana”“Kuwa muhusika ni Elly”Kwakweli hapo Sarah alijihisi aibu kuona kumbe mambo yapo wazi kabisa, aliamua hadi kuachana na Erick na kurudi zake darasani kwao tu.Siku alikuwa nyumbani akiwaza kuwa itakuwaje na yeye na ile mimba ya Elly, aliwaza kuwa atafanya kitu gani na ile mimba hakujielewa kabisa, akakumbuka tukio ambalo alilifanya Sarah ni la kwenda kuchoma sindano ya uzazi wa mpango.Basi aliondoka pale nyumbani kwao na kufunga milango vizuri kabisa hadi hospitali kwaajili ya kuchoma sindano ya uzazi wa mpango.Ni kweli alivypofika na kuongea nao kidogo tu, waliweza kumuamini na kumchoma ile sindano na kumpa ratiba ya sindano zingine, basi Siku alirudi moja kwa moja nyumbani huku akijisemea,“Sarah imejulikana sababu Sarah ni mtoto ila mimi ni mambo ya kimya kimya yani hakuna kitu kitakachojulikana, nitavumilia tu kwenye kila kitu”Alijipa moyo haswaa juu ya jambo lile, muda kidogo alifika pale nyumbani mama Sarah akiwa ameongozana na Rahim, basi waliingia ndani na kuanza kuongea ongea huku Rahim akimwambia mama Sarah,“Binti yangu anayeitwa Samia ni mjanja sana, huwezi kukuta anadanganywa na kihjana wa aina yoyote maana nishamfundisha kila kitu yule”“Hongera sana, kwahiyo hakubali wanaume?”“Awakubali wa kazi gani? Nimemfundisha mambo mengi sana yule mwanangu”Kisha mama Sarah na Rahim walienda chumbani moja kwa moja na kujifungia huko.Ikawa ndio kama Rahim amefika maana alikaa hapo kwa siku kama tatu, yani hakuna kuondoka yuko hapo hapo kwa mama Sarah.Siku hii baba Angel alipokuwa ofisini kwake alipigiwa simu kuwa aende kuchukua majibu ya vipimo, basi moja kwa moja aliamua kumpitia Sia ili kwenda nae kufata hayo majibu.Basi alimpitia kwenye biashara yake na kuondoka nae hadi kwenye ile hospitali, na walipewa majibu ambapo baba Angel alitaka Sia ayafungue kwanza na kuyasoma mwenyewe.Basi Sia aliyafungua yale majibu ila muda kidogo Sia alianguka na kuzimia Basi alimpitia kwenye biashara yake na kuondoka nae hadi kwenye ile hospitali, na walipewa majibu ambapo baba Angel alitaka Sia ayafungue kwanza na kuyasoma mwenyewe.Basi Sia aliyafungua yale majibu ila muda kidogo Sia alianguka na kuzimia.Baba Angel badala ya kumsaidia Sia kwa ile hali ya kuzimia, alianza kumcheka hadi daktari alimuuliza,“Mbona unacheka badala ya kumpa huduma ya kwanza?”“Nimpe huduma ya kanza ya kazi gani? Mwache atazinduka mwenyewe, mambo mengine binadamu huwa tunayataka wenyewe tu”Ikabidi yule daktari ndio amshughulikie Sia maana kwenye kile chumba cha daktari walikuwa watatu yani Sia, baba Angel pamoja na yule daktari.Basi Sia aliweza kuinuka na kukaa, ila swali la kwanza aliloulizwa na baba Angel,“Sasa ni kitu gani kilichofanya uzimie?”Sia alianza kulia tena alilia sana, hadi baba Angel alimshangaa maana hakuwahi kumuona Sia akilia kwa namna ile, kwahiyo aliamua tu kumbembeleza,“Hebu nyamaza, na wewe usilete ujinga”Ikabidi baba Angel amuage yule daktari na kutoka na Sia hadi kwenye gari lake huku akimbembeleza,“Hebu nyamaza Sia, unajua ukilia hutopata jibu kabisa”“Sasa mwanangu yuko wapi kama Erick sio mwanangu!”“Unajua mambo mengine huwa mtu unafanya ila kufikiria, hivi kweli kabisa tubadilishiwe mtoto wa miezi mitatu tusigundue? Inakujia akilini kweli hiyo? Nishawahi kusikia watoto wanaobadilishwa kipindi cha kuzaliwa ila mtoto anabadilishwa akiwa na miezi miwili au mitatu, nani ambaye hatogundua huo ujinga?”“Yani hapa sielewi, mzee Jimmy nilielewana nae vizuri na pesa alinipatia”“Basi mzee Jimmy alikupiga chana la macho, pole sana. Usikute mchezo alikufanyia mwenyewe ila usikate tamaa, ilimradi ukweli umejulikana basi mwanao halasi nae atafahamika tu”“Roho inaniuma sana, siku zote huwa najua kuwa Erick ndio mwanangu, sasa nitampata wapi mwanangu mimi jamani!! Roho inaniuma sana”Basi baba Angel akamchokoza kidogo na kumwambia,“Wewe si mchunguzi wa mambo na mpelelezi, basi peleleza ili ujue mwanao halali yuko wapi”“Halafu Erick hebu niache kwanza”“Nikuache nini? Yani hapo tamaa imekuponza, yani Erick sio mwanao wala Elly sio mwanao, yani mzee Jimmy kakufanyia mchezo sio wa nchi hii. Ngoja nikurudishe kwako ukashushe presha”Baba Angel alikuwa akicheka sana huku akiendesha gari kuelekea nyumbani kwa Sia, ila kwakweli Sia alikuwa na mawazo sana yani hakuamini kile kilichotokea kabisa, hadi alihisi labda daktari kambadilishia majibu. Basi baba Angel akamuuliza tena Sia,“Ila na wewe ulianzaje kufikiria swala la kukubali kubadilisha mtoto?”“Yani umasikini huu, acha tu Erick hapa sijielewi kabisa. Sijui mwanangu yuko wapi?”Aliinama tena akilia, basi baba Angel alikuwa akicheka tu huku akiendelea kumrudisha kwake. Walifika nyumbani kwa Sia, kisha wakashuka pale halafu baba Angel akamwambia Sia,“Nitakuwa naendelea kukuita Sia tu mpaka pale mtoto wako atakapogundulika kuwa ni nani ndio nitaanza kukuita mama Fulani”“Unanipa uchungu sana ukisema hivyo Erick, watu walizoea kuniita mama Elly”“Kwani hukujua kama Elly sio mtoto wako? Si unaujua ukweli, yani kitu ambacho ulikuwa hujui ni kuhusu Erick tu. Jitahidi umjue mtoto wako wa ukweli. Yani usipofanya hivyo utalia tu ndugu yangu”“Siku zote nilijua Elly ni mtoto wako ndiomana nilimpenda sana Elly”“Kwahiyo hutompenda tena baada ya leo?”“Hapana, nitaendelea kumpenda tu, kwani nimemlea kwa siku zote hizi na hakuna kasoro hata moja niliyomuonyesha kama sio mwanangu”“Ila wewe mwanamke dah umejua kutuendesha akili zetu jamani hadi kutukosesha raha ila leo Mungu kakuumbua haswaa”“Jamani hata kunihurumia Erick!”“Nani akuhurumie sasa kwa huo ujinga wako ulioufanya? Hivi unafikiri kipindi kile wakati ukikazana kuwa Elly ni mwanangu na mfano ingekuwa kweli mmebadilisha mwanangu, tungepima na kukuta ni mwanangu, hivi ningeelewekaje kwa mke wangu? Wewe mjinga umejua sana kuichanganya akili yangu na akili ya familia yangu. Kila siku mama alikuwa akinisema vibaya na kunishutumu, dah wewe jamani. Umepigwa kofi na Mungu, mwanamke mjinga sana wewe”Baba Angel alimuacha hapo Sia na kuondoka zake, kwakweli Sia aliingia ndani huku akiwa na mawazo sana.Baba Angel alirudi nyumbani kwake, na kumkuta mke wake akiwa chumbani kwa muda huo. Basi aliamua kwenda kumpa habari za Sia, kwakweli mama Angel alicheka sana kwa kuambiwa vile,“Kwahiyo kwa kipindi chote hiki aliamini kuwa Erick ni mtoto wake?”“Ndio, aliamini kuwa Erick ni wake yani hadi kazimia na hayo majibu”“Mjinga yule, tumezoea kuona wanaume ndio wakipima DNA maana wengi wanasingiziwa watoto ila mama mjinga kama yule kazaa mtoto na kumbadilisha halafu anaanza kuhangaika kutafuta mtoto wake wa ukweli, yani ni mjinga sana yule”“Mwenzio anadai umasikini ndio ulimfanya akubali kufanya hivyo”“Mjinga sana huyo binadamu, yani mwanamke ubebe mimba kwa tabu, uzae kwa uchungu halafu upate nguvu ya kubadilisha mtoto eti kwa kisingizio cha umasikini jamani loh. Umasikini gani huu unaosemwa na huyu kiumbe jamani!”“Ndio hapo sasa, hivi itakuwaje kama mtoto wa madam Oliva akawa ndio mtoto wa Sia?”“Mmmh haiwezekani hiyo kitu, inamaana madam Oliva alibadilishiwa mtoto? Na wa madam Oliva atakuwa nani sasa?”“Si ulisema mwenyewe kuwa madam Oliva alizaa na Derrick, basi inawezekana mtoto wa madam Oliva akawa Elly”“Mmmmh jamani, mbona vitu vingine ni ngumu kumeza? Mzee Jimmy alifanya hayo kwa maana ipi jamani”“Sijui, tunasema tu hapa ila hatuna uhakika, hakuna mwenye uhakika kama yule mtoto wa madam Oliva ni wa Sia, na wala hatuna uhakika na Elly ila tunakisia tu”“Ngoja, nitamtafuta madam Oliva niongee nae kuhusu uzazi wake, nina uhakika nitagundua mambo mengi sana baada ya kuongea nae. Ila kama ni kweli sijui huyu mzee Jimmy nimuweke kwenye kundi gani jamani, ni baba yako Erick, ni baba mkwe wangu kweli ila kwa mambo kama haya sijui alikuwa akifikiria nini”“Ila usimseme vibaya baba yangu, kumbuka ni mzazi wangu”“Yamewakuta wenzio ndiomana unasema hivyo ila yakikukuta na wewe sidhani kama utasema hivyo”“Erica, baba yangu hawezi kunitenda hivyo. Ana maovu yake ila sidhani kama anaweza kunitenda hivyo kwakweli. Tupeleleze tu ukweli wa mambo ili kugundua mambo yalivyo, kwa hili simsifu baba yangu kuwa katenda jambo zuri ila sidhani kama anaweza kunitenda mimi?”“Sawa, kesho si Jumamosi!! Basi nitamtafuta madam Oliva ili niweze kuongea nae maana najua atanipa tu ushirikiano ukizingatia nishawahi kuongea nae kuhusu mtoto wake na Derrick”“Sasa utaongea nae nini? Utamwambia kuwa unahisi mtoto wake sio wake? Utamwambia kuwa unahisi kabadilishiwa mtoto sababu mtoto kafanana na Steve? Labda alizaa nae huyo Steve utajuaje?”“Siwezi kumuuliza hivyo, ila najua tu nitakavyoongea nae. Nitamuuliza tu aalipo, halafu nitaenda kukutana nae na nitaongea nae mengi tu na hapo nitapata baadhi ya mambo”Basi wakaongea mengi sana na kwa muda huo sababu usiku nao uliingia waliamua tu kulala moja kwa moja.Leo palipokucha tu, Erica moja kwa moja alienda chumbani kwa Erick ambapo ndio alimkuta anaamka basi alianza kuongea nae,“Mwenzio leo nimeota”“Kheee umeanza tena mambo yako ya kuota?”“Ndio, nimeota kuwa mimba ya Daima imetoka”“Kheee Erica umeanza tena, hebu acha kuombea watu mabaya”“Kwani nimeomba mabaya jamani! Mimi huyo Daima ananihusu nini eeeh!! Nimeota tu kuwa mimba yake imetoka”“Haya, twende tukafanye usafi tunaoufanyaga”“Hivi unajua hata kulala vizuri leo sijalala vizuri yani macho mazito hapa ila nimeamka tu”“Sasa kwanini hukulala vizuri?”“Sababu ya ndoto hiyo, yani nilikuwa nalala nashtuka, nakuwa macho kwa muda, nikilala tena inanijia”“Aaaah yani wewe jamani, jitahidi basi tukafanye usafi kwanza ndio utaenda kulala”“Mmmh kwa leo, ngoja nikaoge kwanza ili nipate nguvu na nipendeze ndio nikafanye usafi”“Khaaa yani usafi na kupendeze, ila Erica una vituko sana jamani. Haya na mimi ngoja nioge”Basi Erica alirudi chumbani kwake na kwenda kuoga, alipomaliza tu alisikia kuna kelele ya mtu sebleni akilala mika basi aliavaa haraka haraka na kwenda kuangalia huyo mtu ni nani.Alishangaa kukuta yule mtu ni mama Daima ambaye alikuwa akiongea hovyo hovyo,“Yuko wapi mama yenu?”Mama Angel nae alitoka ndani, na mama Daima alianza kusema yake,“Naona sasa utakuwa na furaha kwenye moyo wako maana mimba ya mwanangu imetoka”“Ila wewe mwanamke una wazimu jamani, mimi na wewe nani atakayekuwa na furaha kwa hilo? Si ulikuwa ukiona aibu wewe kwa binti yako mdogo kupata mimba? Haya imetoka nenda mkasherekee leo”Mama Angel alisogea kwenye kabati na kutoa hela halafu akasogea kwa mama Daima,“Chukua hiyo elfu ishirini ukanunue kuku mumpikie mzazi supu”“Mjinga wewe eeeh!”“Ulitaka nikwambie nini sasa?”Mama Angel alirudi zake ndani, basi mama Daima kwa hasira alirusha ile elfu ishirini na kuondoka zake, yani Erica ndio aliiokota ile hela na moja kwa moja kwenda kwa mama yake na kumwambia,“Mama, yule mama kairusha hii hela”“Ichukue nimekupa”Erica alifurahi sana na kutoka nayo, muda huu hata Erick alikuwa katoka na wakatoka nae kuelekea nje kwenye usafi, basi Erick alianza kuongea,“Nimeshangaa sana kusikia zile kelele za mama Daima, kumbe kweli mimba ya Daima imetoka?”“Ndio, si nilikwambia nimeota?”“Naona umeanza kuota kama zile ndoto zako za kipindi kile wakati upo mdogo. Ulikuwa unaota ndoto za kweli, naona ndio na hii imetokea”“Unajua mimi huwa sioti mara kwa mara ila mara nyingi nikiota basi inakuwa kweli hiyo kitu”Muda kidogo pale nje alitoka Elly maana kwa kipindi hiko nae alikuwa akiishi hapo kwa mama Angel ila alikuwa amepewa chumba kingine cha kulala.Alipofika pale nje aliwasalimia Erica na Erick kisha aliwaomba kitu,“Jamani, nawaomba jambo moja mnisindikize leo”“Jambo gani?”“Naomba mnisindikize nyumbani kwakina Sarah, anaomba tukamuone. Nawaomba sana twende wote”Walikubali ila walipanga kumaliza kwanza usafi wa pale nje ambapo walianza kusafisha.Mama Angel aliwasiliana na madam Oliva ili aweze kukutana nae, yani aliona ni vyema kwa yeye kufanya jambo hilo kwa siku hiyo, basi aliongea nae kwenye simu,“Naweza kukutana nawe madam, nina shida sana na wewe”“Inawezekana ndio, njoo karibu na saluni yangu”“Hebu nielekeze, nakuja muda sio mrefu”Madam Oliva alimuelekeza, na kweli mama Angel aliondoka pale na kwenda kukutana na madam Oliva ambapo walienda kwenye eneo la karibu na pale ambapo kulikuwa na bustani na waliuza vinywaji, watu wengi walipenda kukaa hapo na kuzungumza, kwahiyo walikaa pale na kuanza kuzungumza,“Kwanza madam samahani kwa kukushtukiza, ila kwakweli nahitaji kuzungumza na wewe”“Hamna usiwe na shaka”“Kwanza nilifurahi sana kumuona mwanao”“Kheee ulimuona wapi? Mbona hajawahi kusema kama alikutana na wewe?”“Hapana, waliwahi kukutana na mume wangu. Halafu kuna siku njiani tuliwaona ndio mume wangu akanionyesha ila hatukusalimiana nao”“Oooh sawa, nimekuelewa”“Samahani mwenzangu, mimi nakumbuka wakati najifungua wale mapacha wangu jamani nilikuwa na hali mbaya siku ile hata sikufikiria kama baada ya uzazi ule ningeweza kuzaa tena. Hebu fikiria nilikuwa naishi nyumbani halafu mume wangu kasafiri kama jana yake, alisema angerudi asubuhi yake ila akapata dharula hakuweza kurudi, jamani nilikuwa na hali mbaya, niliumwa ule uchungu hakuna mfano jamani, akaja baba mkwe wangu ndio akanisaidia hadi kunipeleka hospitali. Ila kitu ambacho sikutegemea ni kufanyiwa operesheni, nilijua ningezaa kawaida ila nilifanyiwa operesheni na kukaa nusu kaputi mwenzangu ila nashukuru Mungu alifika mama yangu kwa wakati na kupewa watoto wangu. Wewe ulijifungulia hospitali gani?”Madam Oliva alimtajia hospitali ambayo alijifungulia na kufanya mama Angel ashtuke kiasi kwani ndio hospitali ile ile aliyojifungulia Sia, na ndio hospitali ile ile aliyopelekwa yeye ila hakuonana na wote hao maana hospitali yenyewe ilikuwa ni kubwa, basi mama Angel akamuuliza tena,“Ulijifungua kawaida au kwa kisu”“Mmmh kwa kisu mwenzangu, mimba yangu ilikuwa na matatizo kidogo”“Matatizo gani?”“Ni hivi, nilijifungua kabla ya wakati kutokana na matatizo niliyokuwa nayo, ilibidi tu nifanyiwe operesheni kuokoa mtoto wangu na mimi mwenyewe, kuna kiasi nawashukuru sana pale ila kuna kipindi walikuja kunikera sana”“Kivipi?”“Yani mimi nilijifungua njiti, kwahiyo mtoto alikuwa bado hospitali kwa ule uangalizi wa karibu. Jamani ilipokaribia mimi kumchukua mwanangu ili niende nae nyumbani, eti nikapewa taarifa kuwa mtoto amepotea, hapo sikutaka kuwaelewa kabisa, nilichanganyikiwa jamani asikwambie mtu, nakumbuka hadi nilienda polisi na kufungua kesi nikiishtaki ile hospitali. Yani walinifanyia mambo ya kijinga sana, nilikuwa nalia kila siku, ndio siku hiyo wakaniletea mtoto wangu eti kumbe walimbadilisha hospitali maana hali yake ilibadilika, ni Mungu tu ndio anayejua jinsi moyo wangu ulivyoumia baada ya kupotelewa na mwanangu. Jamani ile hospitali toka wanikabidhi mwanangu siitaki tena, kwanza niliposikia imefungiwa na serikali nikafurahi sana maana inatakiwa kuchunguzwa ile, sio kwa mchezo mchafu ule waliotaka kunifanyia. Sijui walitaka kumuuza mtoto wangu wale wajinga? Dah!!”Kidogo kuna picha mama Angel aliipata kwenye kichwa chake, basi alimuuliza madam Oliva,“Ila una uhakika kuwa mtoto waliyekupa alikuwa ni mtoto wako?”Madam Oliva alitulia kimya kwa muda kidogo, basi mama Angel akamwambia,“Samahani kwa swali hili, sijakuuliza kwa nia mbaya”“Naelewa, ila mimi sijui kwakweli. Nilipewa na kushukuru Mungu kwa kumpata mwanangu, nimemlea kipindi chote hiki na sijapata tatizo lolote lile, naamini ni mwanangu”Mama Angel akapumua kidogo, kisha madam Oliva akamuuliza,“Niambie kwani ni kitu gani umeniitia?”“Mmmmh samahani, kitu nilichokuitia ni kukuuliza kama uliwahi kuwa na mahusiano na Steve kabla ya kumpata mtoto wako wa kwanza”“Hapana, Steve mimi nimefahamiana nae mwaka jana, yani ndio ilikuwa mara ya kwanza wakati tumeanza mahusiano yetu”“Ooooh sawa, yani mwanao kafanana sana na Steve”“Duniani wawili wawili, namshukuru Mungu kwa Steve na mwanangu kufanana. Najua watapendana sana, na hiyo ni sababu tosha ya mimi kukubali kwa moyo mweupe kuolewa na Steve”“Sawa, nitakuwepo kusapoti harusi yenu. Nafurahi sana kuongea nawe kwa siku ya leo, naona nikuache uendelee na shughuli zingine ila nitakapokuomba tena tuzungumze basi usisite ndugu yangu”Wakafurahi pale, ila kiukweli madam Oliva bado hakufikiria mantiki ya mama Angel kuomba kuongea nae ikiwa waliyoyaongea yalikuwa ni ya kawaida tu kwake.Erick, Elly na Erica walijiandaa kwaajili ya kuondoka, ila gari walilotaka kutumia Erick aligundua kuwa halina mafuta ya kutosha, ila kwake hilo halikuwa tatizo sana, aliondoka na wenzie na kupitia kituo cha mafuta ambacho baba yake huwa mara nyingine anaweka mafuta kwa bili na kuwaambia hapo wamuwekee mafuta. Nao walifanya vile, ila yule mdada wa kwenye kituo cha mafuta alimuita Erick pembeni kidogo na kuongea nae,“Erick, siku nyingine ukija hapa ulizia Rose basi mimi nitakuja na kukuwekea mafuta”“Oooh sawa, hakuna tatizo”“Ila ungenipa na namba zako Erick”Sababu Erick hakuwa na simu, basi alimpa namba ya simu ya mezani ya nyumbani kwao na kuagana nae.Moja kwa moja walienda kwakina Sarah, na walimkuta Sarah sebleni ambae aliwakaribisha vizuri tu ila hakupenda kwa kumuona Erick na Elly pamoja na Erica kufika pale kwapamoja, alikaa nao kidogo sebleni akiongea nao ila Erica alionekana kusinzia na mwisho wa siku alilala kabisa pale kwenye kochi, muda huo Sarah alimuomba Erick na Elly akaongee nao nje kidogo, walitoka na kuanza mazungumzo,“Sijapenda mmekuja wote, ila nimefurahi mmefika ili niweze kuzungumza ya moyoni. Kwanza kabisa Erick naomba unisamehe maana ukweli utakuwa umeujua ndiomana Elly ameondoka kwetu. Halafu kitendo cha Elly kuondoka kwetu sijafurahishwa nacho kabisa kwani inaonekana kama mimi nakulazimisha kufanya mambo mengine”“Aaaah Sarah hujanielewa tu, ila hapa kwenu nimeondoka kwasababu nyingi sana”“Haya niambie ni sababu gani iliyokufanya ukimbie nyumbani kwetu, je mama yangu ni tatizo kwako? Nimekufichia aibu kwa mama, na hata akigundua basi nitamueleza ukweli wote bila hata ya kumficha”“Aaaah Sarah jamani acha maneno kama hayo, haya sasa tunaongelea nini kwa wakati huu?”Mara walishangaa kumuona Erica akitoka pale nje huku akiwa anathema, wote kwa pamoja walimuuliza,“Tatizo nini Erica?”“Nimeota vibaya sana?”“Umeota nini?”Erica alinyamaza kimya kidogo na kusema,“Sijui kama nilichoota ni cha kweli ila naomba mnisamehe kama kitawakwaza, sema nahitaji kusema ili kama ni kweli basi huyu mtu apone”“Sema basi, umeota kitu gani?”“Samahanini, mimi simfahamu vizuri huyu dada wa kazi humu ndani, ila nimekaa pale kwenye kochi nikasinzia nikajiwa na ndoto kuwa yule dada alikuwa mjamzito”Wote waliangaliana, tena Elly ndio akashtuka zaidi maana alianza kuhisi vibaya muda huo, alihisi huenda hata Sarah akajua kuwa alitembea na huyo dada, ila Sarah alimuuliza Erica,“Mmmh Erica, sasa tumsaidiaje maana unasema hiyo ndoto unatusimulia ili tuweze kumsaidia”“Nimeota kuwa hiyo mimba imetoka, sema inatoka vipande vipande na inamsumbua sana, yani anaumwa. Nimeota kuwa huyu mdada apelekwe hospitali maana akikawia anaweza kupoteza maisha maana anazidi kupoteza damu”“Mmmh Erica wewe jamani, tuko nae hapa siku zote hatujui hayo”“Mimi sijui ila nimeota tu”Basi Erick alikumbuka yale ya kutoka mimba ya Daima, aliamua kumwambia Sarah kuwa akamuulize huyo dada yake,“Ngoja nikamuulize ila siku tatu hizi kapooza sana, hayupo kama zamani. Mara nyingi anakimbilia chumbani, sikujua tatizo ni nini”“Aaaah sasa nilivyoota mimi kuwa anaumwa sana, ana hali mbaya sana”Basi Sarah aliamua kwenda kumuangalia Siku, na kweli alikuwa yupo chumbani, Sarah aliingia na kumkuta akigalagala chini kuwa anaumwa sana,“Tatizo ni nini dada?”“Sijui mdogo wangu, naumwa sana”“Umeanza lini kuumwa?”“Toka juzi ila leo imezidi, naumwa sana Sarah. Naumwa mimi, nadhani nitakufa mimi”Sarah alisikia harufu ya damu mule chumbani na kugundua maneno ya Erica kuwa huenda ikawa kweli maana inaonyesha huyu dada ametokwa na damu nyingi sana, basi aliwaomba wakina Erick na kuanza kumkongoja na kuingia nae kwenye gari na kwenda nae hospitali.Walifika hospitali walitakiwa waandike kadi na vipimo vya awali, yani Erica alijikuta ile elfu ishirini ikimtoka maana kwa pale walipokuwepo hakuna hata aliyekuwa na pesa ya kufanya chochote kile.Kisha Sarah alimpigia simu mama yake ili kumpa taarifa ya pale hospitali,“Tupo hospitali mama”“Kwani kuna nini?”Sarah alimsimulia mama yake kile walichoambiwa na Erica na mpaka kumpeleka pale hospitali, basi mama Sarah aliahidi kwenda pale hospitali ili kuona kinachoendelea ni kitu gani.Walikaa pembeni wakijadiliana maana hakuna aliyejua tatizo linalomsumbua ni nini, ila Sarah akasema,“Mmmh inaonekana wewe ni noma sana Erica, khaaa nimekuogopa kwakweli. Inakuwaje unaota ndoto zinazotokea?”“Hata mimi sijui kabisa inakuwaje ila hizi ndoto huwa zinanijia mara nyingi tu, na kama ni ndoto ya kusema hapo basi nasema hapo hapo. Kuna kipindi niliacha kuota ndoto za namna hii ila nashangaa kwa jana zimeanza tena”“Ila ni vizuri maana huyu dada angeendelea kuugulia ndani tu, halafu mimi sijaenda kutoa pesa sijui leo ingekuwaje bila ya wewe kuwa na hela”Mama Sarah alifika mahali pale na kwenda moja kwa moja kuongea na daktari, na kuelewana nae kuwa wamfanyie kila kitu maana gharama zote atazilipa mwenyewe, halafu akarudi kuongea na hawa vijana wake. Ila alipomuona Erick alichukia sana kwani bado alikuwa na ile dhana kuwa Erick ndio kaharibu fikra za Sarah, alisogea na kumzaba vibao Erick.Kitu ambacho mama Sarah hakukijua ni kuwa Erick ni mtu ambaye huwa na hasira sana, wakati anamzaba vile vibao, Erick alikuwa akikunja ngumi yake kwaajili ya kumpiga nayo mama Sarah, yani ni Erica ndio alimuona na kumuwahi Erick ule mkono huku akimsihi waondoke,“Nakuomba Erick twende nyumbani, nakuomba sana”Mama Sarah nae aligundua hili kwani alimuona Erick usoni akiwa hadi amesimamisha mishipa ya sura, kwahiyo aliamua kusogea nyuma kabisa na kwenda mbali nao. Erick alimuangalia Erica, ila kwa leo alimsikiliza na moja kwa moja kwenda kwenye gari, basi Erica na Elly walimfata nyuma na kuondoka nae ila wakiwa kwenye gari Erick alikuwa haongei kitu, yani alikuwa akiendesha gari huku machozi yakimtoka maana bado alikuwa na hasira, hadi Erica alimuomba Erick aweke gari pembeni na kuanza kuongea nae,“Sasa Erick ndugu yangu, hasira za nini kiasi hiko jamani eeeh!! Naomba ufurahi na mimi basi, yule mmama si tumeshamuacha pale? Nakuomba Erick shusha hasira zako”Basi Erica alifanya kazi ya kumfuta yale machozi, yani hata Elly aliweza kugundua ni kiasi gani Erick alikuwa ni mtu mwenye hasira sana.Basi mama Sarah alimsogelea mwanae na kuongea nae kuhusu ugonjwa wa Siku na zile hasira za Erick, ila alianza kuongea nae kuhusu hasira za Erick,“Kwahiyo mwanangu Sarah kabisa ndio ukampenda mtu kama huyu?”“Kwani ana tatizo gani mama?”“Khaaa mwanaume wa hasira hivyo hafai kabisa mwanangu, mbona unaweza kulia na mtu kama huyo jamani. Unawezaje kuishi na mtu kama huyo? Hebu fikiria mimi kumnasa kibao tu kabadilisha ile sura yake, mishipa imemtoka usoni balaa halafu kakunja na ngumi, khaaa huyu Erick hapana aiseee hata hafanani na babake jamani”“Unamfahamu vizuri yule baba yake mama? Labda nae alikuwa vile ujanani?”“Namfahamu vizuri sana, ana hasira ila sio za namna ile kabisa. Yule Erick nimemfananisha na mkaka mmoja hivi, loh alikuwa akichukia unaweza kulia, ila nasikia kaoa mke mpole sana, ndio inavyotakiwa kwa mtu mwenye hasira kiasi hiki, aaah hafai huyu mtoto tena hafai kabisa”“Mmmmh mama”“Haya tuachane na hayo, huyu dada yako nae mtu mzima kwenda kufanya mambo ya kitoto kama uliyoyafanya wewe ndio nini?”“Mambo gani mama?”“Kumbe lilipata mimba halafu nalo likaenda kuchoma sindano ya uzazi wa mpango, si kunitia gharama tu jamani, leo hatotoka huyu ndio atabaki hapa hapa hospitali nasikia kapoteza damu nyingi sana huyu mjinga kabisa. Anataka anifie ndani halafu mimi jopate lawama kwa ndugu! Hii ndio shida ya msichana wa kazi kukuzoea sana basi anakupanda hadi kichwani kama huyu alivyofanya kwangu”“Kwahiyo mama utamrudisha kwao”“Mmmmh nimemzoea sana, halafu nilishasema nitaishi nae hadi atakapooelewa, unajua huyu Siku ni mtoto wa ndugu yangu kabisa!! Ndiomana huwa namuamini sana ila kumbe akili zake ni finyu kama zako”Basi mama Sarah alienda tena kuongea na daktari kisha aliamua kurudi nyumbani tu na Sarah maana waliambiwa kuwa Siku anatakiwa kubaki pale hospitali kwaajili ya kumuangalia kwa karibu zaidi.Kufika nyumbani ndio mama Sarah alichoka, aliingia jikoni na kukuta vyombo havikuoshwa wala nini,“Khaaa huyu mjinga kumbe hakuosha vyombo jamani, hili sufurua si limepikiwa tambi juzi loh!”“Kumbe tangu juzi alikuwa akiumwa mama”“Kheee basi na humu ndani hakuna usafi uliofanyika, jamani kuwa na kazi nyingi napo loh!! Hata sijagundua hiki kitu, mlikula nini sasa jana?”“Aaaah mimi nilimuagiza yule dereva wa bodaboda atuletee chips ile jioni maana nilikuwa na njaa halafu dada alisema anaona uvivu kupika”“Khaaa ndio masahani ya chips haya hapa, mweeeh jamani uchafu gani huu lakini! Na leo nimechoka sana wala siwezi kufanya chochote, twende tu mahali tukale huko halafu nitajua cha kufanya nikirudi”Ikabidi wajiandae kwa muda huo na kwenda kula kwenye mgahawa.Leo usiku, mama Angel aliamua kumueleza baba Angel kile ambacho amezungumza na madam Oliva, hapo ndio baba Angel nae alipata picha na kusema,“Oooh hapo kuna uwezekano mkubwa sana kuwa madam Oliva alibadilishiwa mtoto, nina hisi tulichokuwa tunahisi ni kweli kuwa Elly ni mtoto wa madam Oliva halafu yule mtoto wa madam Oliva ni mtoto wa Sia”“Haya mambo jamani, ila mzee Jimmy kwanini afanye kitu cha namna hiyo? Kwani ana ugomvi gani na madam Oliva mpaka ambadilishie mtoto?”“Mmmh hapo sijui kitu, ila kwakweli kama baba yangu kafanya hiko kitu ni mbaya sana. Kesho nahitaji kwenda kaburini kwa baba mara moja”“Mmmmh unaenda kufanya nini? Twende wote basi”“Hapana, wewe nenda Kanisani na watoto halafu mimi nitaenda huko. Kuna vitu nahitaji kuwauliza wale walinzi wa lile eneo, yani kuna kitu kinanijia kichwani”“Kitu gani?”“Nitakwambia nikirudi, ila baba yangu kama alifanya hivyo kwa kudhamiria kwakweli hakufanya sawa kabisa”Basi waliamua tu kulala kwa muda huo.Kulipokucha tu, asubuhi na mapema, baba Angel alijiandaa na kuondoka zake kuelekea kwenye eneo ambalo kulikuwa na kaburi la mzee Jimmy, maana yule mzee alizikwa kwenye eneo lake mwenyewe.Basi baba Angel alifika pale, na kusogea karibu na kaburi la baba yake ila gafla alishikwa bega, alipogeuka nyuma alishangaa sana kumuona bi.Aisha, basi bila hata salamu alimuuliza jambo moja kwanza,“Nilipanga kuja kuongea na wewe, ila nilipokuona na Sia nikaishiwa nguvu kabisa ya kuja kukuona. Sia ashakwambia yaliyomkuta?’“Kaniambia ndio, kuwa mtoto aliyefikiria ni wake, kakuta sio wake tena. Ila sijashangaa sana”“Kwanini?”“Kwani mzee Jimmy alikuwa na uwezo wa kufanya chochote alichojisikia na yote aliyafanya akiwa na maana nayo thabiti kabisa”“Sasa alikuwa na maana gani kufanya kitu cha namna hiyo?”“Unashangaa hayo tu, je ukigundua alichokufanya wewe kwa watoto wako utafanyaje?”Baba Angel alimuangalia vizuri huyu bibi yani alikuwa kama hajamsikia vizuri Basi baba Angel alifika pale, na kusogea karibu na kaburi la baba yake ila gafla alishikwa bega, alipogeuka nyuma alishangaa sana kumuona bi.Aisha, basi bila hata salamu alimuuliza jambo moja kwanza,“Nilipanga kuja kuongea na wewe, ila nilipokuona na Sia nikaishiwa nguvu kabisa ya kuja kukuona. Sia ashakwambia yaliyomkuta?’“Kaniambia ndio, kuwa mtoto aliyefikiria ni wake, kakuta sio wake tena. Ila sijashangaa sana”“Kwanini?”“Kwani mzee Jimmy alikuwa na uwezo wa kufanya chochote alichojisikia na yote aliyafanya akiwa na maana nayo thabiti kabisa”“Sasa alikuwa na maana gani kufanya kitu cha namna hiyo?”“Unashangaa hayo tu, je ukigundua alichokufanya wewe kwa watoto wako utafanyaje?”Baba Angel alimuangalia vizuri huyu bibi yani alikuwa kama hajamsikia vizuri vile.Ikabidi baba Angel amuulize tena,“Unasemaje?”“Kwani hujanisikia Erick? Ukigundua alichofanya baba yako kwa watoto wako utafanyaje?”“Kwani kafanya kitu gani?”“Niliwahi kumdokezea mke wako, na nilimwambia kuwa asifike huku mwenyewe, ila nina haraka kidogo. Tuondoke kwanza eneo hili na nitakwambia kwa kifupi tu”Kwakweli baba Angel alijikuta akitamani kufahamu ni kitu gani haswaa ambacho kimeendelea kwa familia yake, akaondoka na huyu bibi. Akapanda nae kwenye gari na kwenda kwenye eneo moja ambalo palikuwa na mgahawa na kuagiza vinywaji halafu wakaanza kuongea, basi bi.Aisha akamwambia,“Hebu kunywa kwanza hiko kinywaji maana tunaweza kuondoka hapa na hujanywa hata kidogo”Baba Angel alihisi hata moyo wake kwenda mbio sana, akamuangalia huyu bibi na kumwambia,“Naomba ieleze”“Kunywa kwanza hiko kinywaji chako”Baba Angel alikunywa kidogo na kuanza kumsikiliza huyu bibi,“Kwanza kabisa, mimi na baba yako tumefahamiana kwenye harusi yako, nilialikwa na mtu mmoja hivi. Basi nikafahamina na baba yako, katika maongezi ya mimi na yeye tuligunduana kuwa wote ni waathirika, basi aliniambia kuwa kama nipo tayari anioe, nikakubali na tulifunga ndoa bomani. Kama ujuavyo, babako hakuwahi kuoa kwahiyo mimi ndio nilikuwa mke wake wa kwanza. Niliishi na baba yako ila niligundua vitu vingi sana, ngoja nikwambie baadhi ya vitu hivyo. Hebu kunywa kwanza kinywaji chako ushushie na pumzi ndefu”Kwakweli baba Angel aliona huyu bibi akizidi kumchanganya tu kwani yeye alihitaji kugundua ukweli, aliamua kunywa kile kinywaji ili kumridhisha yule bibi,“Ni hivi, kuna mwanamke alikuwa akiitwa Ester, mwanamke huyu alipendwa sana sana na baba yako, yani hiyo ndio ilikuwa ndoto yake, ila hakuweza kuwa na mwanamke huyu na mpaka mwisho hakuweza. Ila baba yako alitokea kumpenda sana mwanamke mwingine, na huyu si mwingine bali ni mke wako Erica, yani alitamani kufanya chochote kwaajili ya mke wako Erica, ile harusi yenu ameigharamikia sio sababu yako ila ni sababu ya mke wako Erica, yani alimpenda sna. Na usifikiri baada ya wewe kuoanana Erica basi baba yako aliacha kumfatilia Erica! Hapana, yani ndio alikuwa akimfatilia sana, ila mkeo najua hajawahi kukwambia haya sababu hakutaka ujihisi vibaya kwa baba yako. Kuna siku hata alitaka kumbaka, najua mkeo hajawahi kukueleza jambo hili”Baba Angel alipumua kidogo huku akiendelea kumsikiliza bi.Aisha,“Sasa ule upendo wa kumpenda Erica na kumuona yupo na wewe ulimuumiza sana, na alipanga kufanya kitu cha kukufanya wewe ujute na hata Erica ajute katika maisha yake”“Kitu gani hiko?”“Upo tayari kukisikia?”“Ndio nipo tayari”“Haya, kunywa tena kinywaji chako”Kwakweli baba Angel alikuwa hamuelewi kabisa huyu bibi aliona kama anamchanganyia mada tu, basi akamwambia,“Naomba uniambie tu, hizo habari za kusema kila muda ninywe kinywaji nashindwa kukuelewa kabisa”“Ila wewe ni mbishi sana hata baba yako aliwahi kunilalamikia sababu hiyo, hivyo basi sitokwambia yote”Baba Angel alikuwa akitamani hata kumzaba vibao huyu bibi ili aongee haraka ila alitakiwa tu kuwa mpole na kumsikiliza,“Ni hivi, ni kweli kabisa baba yako alibadilisha watoto na mpango wake ulikuwa ni kubadilisha mtoto wa mke wako pamoja na mtoto wa Sia, ila sijui nini kilitokea hapo maana hata yeye alilalamika kuwa kuna kitu kimekwama katika mipango yake, kwahiyo sijui kipi kilifanikiwa na kipi kilikwama. Ila uhakika nilionao ni kuwa kuna sindano ya ajabu sana walichomwa watoto wako mapacha wakiwa wachanga kabisa”“Unamaanisha Erica na Erick?”“Kwani una watoto wengine mapacha zaidi ya hao?”“Ni hao tu, inamaana kuna sindano aliwachoma wanangu baada ya kushindwa kuwabadilisha?”“Kuhusu kuwabadilisha nisikuhakikishie maana sina uhakika sana kama alishindwa ila tu alilalamika kuwa hajafanya vile alivyotaka. Kitu cha kusikia kuwa ameenda kuwachoma sindano watoto wako, niliumia sana na ndio ugomvi wa mimi na yeye ulipoanza”“Kwahiyo hizo sindano aliwachoma za nini na ilikuwa ni kipindi gani?”“Sikia, mtafute yule daktari wa ile hospitali. Yule daktari mkubwa yule mwenye jina kama la baba yako, anaitwa dokta Jimmy, ndio anayeweza kukueleza kuhusu hiyo sindano”“Duh!! Niambie vyote ili nijue cha kufanya”“Nenda kafanyie kazi hilo ndio unitafute, sio ukiniona na Sia unadhani mimi ni msaliti, hata Sia sio msaliti wako ila baba yako ndio alikuwa msaliti wako”Yani baba Angel hata hakutaka kuongea zaidi, kwani kwa muda huo huo, alimuaga yule bi.Aisha na kuondoka zake kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwake.Tumaini leo alivyotoka tu kwenye Ibada, moja kwa moja alienda nyumbani kwa mama Sarah kwani alihisi kuwa kuna mengi ya yeye kuzungumza na huyu mwanamke, basi alifika pale na kumkuta mama Sarah nje ya nyumba huku akiosha vyombo,“Kheeee naona mwanamke kujituma”“Kujituma wapi? Mdada wangu wa kazi anaumwa, kwahiyo hii shughuli imeniangukia mwenyewe”“Ila na nyie mnayataka, mpo wangapi ndani hadi umeosha vyombo vingi hivi!!”“Mmmh toka majuzi hivi vyombo ndiomana unaviona vingi na hapa ndio namalizia, vilikuwa vingi sana. Nimechokaje hapa”“Pole sana, ndio umama huo. Jikaze tu”“Yani acha tu, umeona nguo zilivyojaa kwenye kamba hizo! Nilikuwa nafua ndiomana nimechoka sana”“Duh pole, kwahiyo umezifua leo?”“Ndio, asubuhi nimeamkia hizo nguo ujue, nilipomaliza ndio nikasafisha ndani halafu muda huu ndio naosha vyombo, nimechokaje hapa”“Kwani Sarah hayupo?”“Yupo ndani, saizi nadhani atakuwa anaangalia muvi”“Kheeee hivi wewe ukoje? Si Sarah angeosha hivyo vyombo!”“Weeee Sarah aoshe vyombo!! Hajawahi si atavitoa na mafuta!”“Nalea watoto kijinga ila wewe mwenzangu umezidi, mtoto hata kuosha chombo hajui! Hapana hayo sio malezi kabisa, unamuharibu mtoto sio kumpenda. Nilikusema siku ile, haya tukaja mtoto alipata mimba sijui kachoma sindano ya uzazi wa mpango, unafikiri hayo mambo kayajulia wapi Sarah? Unafikiri ni wapi amepata ushawishi? Hayo masimu unayomuachia hayo”Tumaini siku ile ilikuwa kama amepanga kumsema mama Sarah maana alimsema sana kwa ulezi mbaya wa mtoto wake.Baada ya yale mambo sasa ndio Tumaini alikuwa akiongea nae vizuri,“Hebu niweke wazi, Sarah ni mtoto wa nani?”“Ngoja nikwambie ukweli, Sarah ni mtoto wa mzee Jimmy”“Aaaah acha uongo wako bhana, baba nilikuwa namtambua vizuri, baba alikuwa na matatizo ya kizazi. Kama ulimsingizia sawa, mimi nipo hapa kutaka kujua tu kama mtoto ni wa Erick na sio vinginevyo”“Mtoto ni wa mzee Jimmy, kama unabisha sawa ila huyu ni mtoto wake”“Kwahiyo wewe ulizaa na baba yetu?”“Ndio, na huyu ndio mtoto mwenyewe”“Haya nimekuelewa, unaweza kunipa mdogo wangu nikamlee kwa wiki mbili tu!”“Hata siku mbili siwezi kukupatia, mimi niliapa kwa mzee Jimmy, kuwa sitokuja kumtesa huyu mtoto, sitokuja kumpiga wala kumfanya chochote. Baba yake alipenda kumuona huyu mtoto kama yai na ndio niliapa kumlea hivyo Sarah”Kwakweli yale maneno bado hayakumuingia akili kabisa Tumaini, aliondoka lakini alijihisi wazi kutokuelewa chochote kile.Leo Sia anaenda moja kwa moja nyumbani kwa mama Angel maana na yeye alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, basi aliongea pale na mama Angel kidogo na kumwambia,“Naomba niitie Elly hata niongee nae kidogo tu”Mama Angel aliamua kumuita Elly ambapo Sia alitoka nae nje na kuanza kuongea nae,“Elly mwanangu, tatizo nini hadi umeondoka kule kwenye msaada?”“Hata hawa wameahidi kunisaidia mama”“Na mbona hujarudi nyumbani? Naomba kwa leo twende nyumbani tu mwanangu”Elly alimuangalia mama yake ambaye alionyesha sura ya huruma sana kwa siku hiyo, kwahiyo ilibidi tu akubali na moja kwa moja kwenda kumuaga mama Angel kuwa anaondoka na mama yake mara moja.Wala mama Angel hakumkatalia jambo hilo, basi Elly aliondoka na mama yake huyu, wakiwa njiani Sia alianza kumuuliza mwanae,“Hivi mwanangu kwa mfano akatokea mtu na kukwambia huyu sio mama yako mzazi, ni amekulea tu lakini sio mama yako mzazi utafanyaje?”“Kwanza nitamshangaa sana halafu nitaona amechanganyikiwa huyo mtu”“Sasa utafanyaje? Utanikataa kuwa sio mama yako tena au utafanyaje?”“Mama, haiwezekani kitu kama hiko. Wewe ndio mama yangu, hakuna kitu cha kusema wewe sio mama yangu”Basi Sia alitamani amwambie ukweli ila aliogopa kwani huyu mtoto alishamzoea sana kama mwanae wa kumzaa tu.Usiku wa leo, baba Angel alikuwa na mawazo sana, alifikiria sana vile alivyoongea na bi.Aisha, basi alimsimulia mkewe kila kitu ambacho mama Angel anashangaa kiasi kwani huyu bibi alishawahi kumuelezea. Basi baba Angel akamuuliza mkewe,“Ni kweli baba yangu aliwahi kutaka kukubaka?”“Ndio ni kweli”“Na mbona hukuniambia?”“Mmmh sikutaka kukugombanisha na baba yako”“Hebu nidokezee ilikuwaje maana hata sijaelewa kabisa”“Nikiwa na mimba kubwa sana ya hawa mapacha, nakumbuka siku hiyo baba yako alikupigia simu kuwa twende kumsalimia, ila tulivyofika pale tu akakutuma wewe kwenye ofisi gani sijui. Kwahiyo ndani nilibaki mimi na yeye tu maana mkewe alikuwa katoka kidogo, sijui alikuwa akitafuta nini chumbani, akaniita ili nikamsaidie, sikujiuliza sana nilienda, uwiii mzee Jimmy alibamiza mlango na kutaka kuniingilia kimwili kwanguvu tena bila kujali mimba niliyobeba, nakumbuka yule mkewe bi.Aisha ndio alikuja kunisaidia ili mzee Jimmy asinibake”“Ila kwanini hukuniambia jamani Erica?”“Sikuweza kwakweli kukwambia chochote kile, ningewagombanisha mapema sana, nami sikutaka kitu cha namna hiyo”“Nasikia baba yangu alikuwa akikusumbua sana. Unajua yani vitu vingine nafikiria na kukosa jibu kabisa, baba nae anaumia kabisa moyo wake kwa kukuona mimi na wewe kweli? Yani kuna vitu nafikiria na kuvikosea jibu kabisa”“Kwanza kule kwenye kaburi, yule bibi alinikataza kabisa yani kuwa nisiende peke yangu. Kwahiyo kuna makubwa tu yapo hapo katikati”Kiukweli mama Angel alikuwa akiongea tu ila aliona kuna kila sababu ya kuchunguza mambo yote yale, waliamua kulala tu kwa muda huo.Asubuhi ya leo kulipokucha, mama Sarah alichelewa kumuamsha mwanae kwaajili ya kwenda shule na kumwambia,“Oooooh kumbe Siku huwa anafanya kazi kubwa sana humu ndani, hivi kweli Sarah umeshindwa kuamka mwenyewe na kuwahi shule mwanangu?”“Aaaah mama, sijui imekuwaje ila nitaenda tu hakuna tatizo”Sarah alienda kujiandaa na kuchukua hela kwa mama yake maana alisema kuwa atatumia usafiri wa kukodi siku hiyo ili aweze kuwahi shule.Ila Sarah alipoondoka pale hakwenda shule wala nini, moja kwa moja alienda nyumbani kwa mama Erica ambapo alimkuta amejiandaa anataka kutoka ila alipomuona alimshangaa klidogo,“Kumbe Sarah?”“Eeeeh ndio mimi”Basi mama Angel akasalimiana nae pale na kukaa nae kidogo huku akimuuliza kilichompeleka kwa muda ule,“Naomba unisamehe kwa yote, labda unaujua ukweli au huujui ila naomba unisamehe nipo kwako kukiri”“Nini tena?”Mama Angel alitoka nae nje na kwenda nae kwenye bustani yao ili aweze kuwa huru katika kuelezea yanayomsibu, basi Sarah alimueleza kila kitu mpaka swala la yeye kuanza kutembea na Elly, yani hakuacha kitu chochote,“Kwanini ulikuwa ukifanya hivyo sasa Sarah?”“Kiukweli, nilijikuta nikimpenda sana Erick, yani sana na kila nilipomwambia hakuonekana kunielewa kabisa. Mama alinifunza kuwa nikimpenda mtu basi nimwambie moja kwa moja, na mimi nilimpenda sana nikajikuta nikimwambia ila Erick hakutaka. Sasa simu yangu hii nina marafiki wengi sana, wakubwa kwa wadogo, kuna siku walinitumia video zilinisisimua sana na wakanielekeza zinapopatikana kwenye mitandao, na hata mikanda yake wakaniletea, nilikuwa nikiangalia nasisimka sana. Kuna kipindi nikaanza na mimi kutamani kufanya kamavile wanavyofanya kwenye video ila tatizo ni kuwa sina ukaribu na watoto wa kiume. Mama alipomleta Elly nyumbani nilifurahi sana, naye nilimuonyesha hizi video na kujikuta tukiwa wote”Kwakweli mama Angel alisikitika sana, na kumuhurumia Sarah kisha akamwambia,“Pole sana binti yangu maana huwa nakuona wewe kama mwanangu kabisa vile, pole sana. Ila Elly ni ndugu yako hata Erick ni ndugu yako, usinibishie maana huu ndio ukweli, mama yako hataki tu kukwambia ukweli ila huu ndio ukweli mwanangu. Hebu niambie kwasasa unajihisije?”“Yani mama, sijui nikwambiaje, ni kama nimeathirika hivi na hizi video, siwezi kulala bila kuziangalia, halafu muda mwingi natamani Elly awe karibu yangu hata nifanye nae tu ndio niridhike na moyo wangu. Kwakweli nipo kwenye wakati mgumu sana, dada hayupo imefanya leo nichelewe kwenda shule maana nimechelewa kuamka, nilimwambia mama kuwa nitaenda ila nimekuja huku, nikiamini unaweza kunisaidia maana akili yangu haipo sawa, hata unaniambia Elly ni ndugu yangu sikuelewi kwa chochote wala kwa lolote”“Dah pole sana”Mama Angel alifikiria kidogo, ingawa alikuwa na safari zingine ila aliona ni bora ampeleke mtoto huyo kwenye maombi, akamkumbuka yule mama aliyekuwa akifanya maombi basi alimwambia Sarah kwa muda huo waondoke na waelekee huko.Leo baba Angel akiwa ofisini anajikuta akiwa na mawazo mengi sana, anahitaji kumpata huyo dokta Jimmy kwa haraka zaidi, alijiuliza mno kuwa atampata vipi huyu dokta ikiwa hana mawasiliano nae yoyote.Akaona ni vyema aende kwenye ile hospitali, ingawa imefungwa, alihisi huenda akapata hata mtu akampatia mawasiliano ya yule daktari.Alifunga kazi zake na kuondoka kwa muda huo, alikuwa akiendesha gari huku akiwa na mawazo sana,“Kama baba aliwapiga sindano wanangu zilikuwa za dawa gani na waliwachoma kwanini? Au alisema wachomwe ili iweje, kitu gani baba amekiandaa kwaajili ya kizazi changu?”Alikuwa akijiuliza sana huku akiendesha gari lake.Alifika kwenye ile hospitali na kweli mazingira yalikuwa kimya kabisa kwani hospitali ile ilifungwa kwahiyo vitu vilibaki baki tu na kulikuwa na walinzi wachache tu, aliingia kwenye eneo hilo huku akitembea tembea na akiongea mwenyewe, kuna mtu ndio alimshtua na alikuwa ni mlinzi wa eneo hilo,“Vipi mzee wangu”“Aaaah salama tu, samahani hivi hii hospitali ilifungwa kwa sababu gani?“Oooh kuna kipindi hii hospitali ilipata sifa mbaya sana ya kubadilisha watoto”Moyo wa baba Angel alihisi ukiripuka kabisa, na kumuuliza kwa makini,“Kwahiyo hii hospitali ishafanya michezo hiyo sana?”“Hapana, ila hii sifa mbaya ya kipindi kimoja tu imefanya hospitali ifungwe hii, kuna baba Fulani hivi ndio kaishtaki hii hospitali, ana watoto wawili wakaona wale watoto wana tabia tofauti na zao, wakaamua kupima nao vinasaba, wale watoto hawakufanana na baba wala mama basi walichukia sana na kuishtaki hii hospitali na wanadai watoto wao hadi leo”“Duh!! Kwanini sasa hii hospitali walifanya hivyo?”“Mmmh sijui kwanini walifanya vile, ila hiyo sifa mbaya imefanya hospitali ifungwe hii. Sijui kama kuna mengine ila mimi najua hilo tu.”“Kwahiyo hii hospitali mtu akizalia hapa lazima abadilishiwe mtoto?”“Hapana, nadhani ni hao tu maana hakuna wengine walioishtaki hii hospitali.”“Je naweza kupata mawasiliano ya yule mmiliki wa hii hospitali, dokta Jimmy”“Mmmh huyo dokta sijui kajificha wapi maana kesi ya watoto ipo mahakamani na anatakiwa kusema ukweli halisi wa wazazi wa wale watoto”“Duh hatari ipo, kwahiyo hata haijulikani atapatikana wapi?”“Ndio hivyo haijulikani kabisa”Basi baba Angel alimwambia yule mlinzi kuwa ataenda tena mahali pale, na kuamua kuondoka tu.Ila alijiuliza sana na kukosa jib utu,“Inawezekana hao waligundua ila wengine bado hawajagundua kama kuna mchezo ulikuwa ukifanyika? Sasa baba yangu kafanya yote haya kwa watu wasio na hatia kweli!! Halafu kawadunga sindano watoto wangu loh kwa kosa gani jamani dah!! Nakosa hata jibu, kwa muda huu ngoja tu nirudi nyumbani kwangu”Basi baba Angel aliamua kurudi tu nyumbani kwake kwani aliona kama akili yake haisomi kabisa, na vile alivyoambiwa na mlinzi ndio kabisa yani akazidi kuingiwa na mashaka na hospitali ile.Mama Angel alifika kule kwa yule mwanamaombi Ester, walimkuta na kumsalimia pale na kuanza kuongea nae, ila yule bi.Ester alimuuliza mama Angel,“Kumbe ulikuwa na mtoto mwingine?”Mama Angel hakuelewa lile swali, alijua kamuuliza kuhusu mtoto wake mdogo,“Ndio nina mtoto mwingine anaitwa Ester, hatukukwambia eti eeeh!!”“Hapana huyo mmeniambia, nakuuliza huyu”“Mmmh hapana, huyu ni mtoto wa rafiki yangu. Mtoto huyu anaitwa Sarah”“Ila umefanana nae sana, yani kama mama na mwana vile”Mama Angel alimuangalia Sarah na kutabasamu, kisha akasema,“Sijui ni kwanini kuna watu wanafananisha macho yangu na macho ya huyu binti”“Ni kweli mmefanana haswa kwenye paji la uso, yani huyu kama sio mwanao basi ni mtoto wa ndugu yako wa damu”“Ni kweli, ni mtoto wa kaka yangu ambaye tumechangiana nae baba”Basi Sarah akamuangalia na kumuuliza,“Kwahiyo baba yangu ni kaka yako?”“Ndiomana nakwambia vipo vingi Sarah huvijui, kwanza huoni ajabu kwa watu wengi wakituona mimi na wewe wanasema tunafanana? Damu nzito kuliko maji binti yangu”Bi.Ester hakuwaelewa vingine, ila aliwauliza tu tatizo lililowapeleka pale, ambapo mama Angel alimueleza bila kificho chochote kiel,“Kwakweli nahitaji huyu binti akombolewe, maana nimetazama na kuona hapa silaha ni maombi tu hakuna namna nyingine”“Basi tutashirikiana kwenye hayo maombi, ila inatakiwa na huyu mtoto akatae hiyo hali, yani uikatae kabisa ili iondoke kwako. Wewe bado mdogo sana, kwanini uwe hivyo? Inatakiwa ukatae”Basi yule bibi alianza kuwasomea maandiko kwanza na kuanza nao maombi.Erica leo aliweza kuongea na rafiki yake Samia, ambapo Samia alimuelezea Erica kuhusu tabia ya baba yake,“Yani baba yangu ana tabia mbaya jamani, unaweza kuzimia”“Kafanyaje tena”“Hajalala nyumbani siku tatu, mama kalalamika sana. Yani yule baba ashukuru kumuoa mama yetu msomi la sivyo angemdhalilisha yule”“Hivi baba yako anafananaje?”“Unataka kumfahamu? Leo tukitoka shule, nitakupitisha kwenye biashara yake utamuona”Basi Erica alikubali na kweli baada ya kutoka shule tu, hakupanda usafiri ambao huwa anapanda bali moja kwa moja alienda na Samia ili akamuonyeshe baba yake.Walivyofika, Erica alishangaa,“Kumbe Samia, huyu ndio baba yako!”“Kwani unamfahamu?”“Ndio, ashawahi kunipa hela mara nyingi tu”Rahim akawasogelea pale na kuwasalimia, kisha alianza kuongea nao,“Leo umefata nini huku Samia?”“Nilikuwa nakuja kumuonyesha huyu rafiki yangu akufahamu”“Kheee kumbe huyu ni rafiki yako!! Nimefurahi kutambua hilo, haya Erica hajambo mama yako?”“Hajambo”“Haya, twendeni kwenye gari nimrudishe Erica halafu na wewe nikupeleke nyumbani”Wakapanda kwenye ya Rahim kisha safari ya kwenda kwakina Erica ikaanza, ila njiani kuna gari ilipita na Rahim alionyeshea ishara ile gari isimame ambapo ilisimama na muhusika alishuka, alikuwa ni mtu ambaye wanamfahamu, akamwambia,“Si unaenda nyumbani kwangu?”“Ndio”“Naomba uende na binti yangu halafu mimi nimpeleke huyu”Halafu Rahim akamwambia Samia ashuke ili aondoke na huyo mtu, kwakweli moyo wa Erica ulidunda kiasi kwani alishikwa na uoga, Samia akashuka na kumuaga rafiki yake halafu Rahim akamwambia Erica,“Haya, Erica njoo ukae hii siti ya mbele hapa”Ilibidi Erica akakae pale mbele huku akiwa na uoga sana kwani hakujua kama atakuwa salama kweli, ila ule uoga aliokuwa nao Erica, basi Rahim alimuona vizuri sana.Akawa akiendesha gari huku akimuuliza,“Mbona unaonekana kuogopa sana, huniamini?”Erica akawa kimya tu, ndipo Rahim alipomuuliza tena,“Unadhani nitakubaka?”Erica alikaa kimya, basi Rahim akacheka na kusema,“Siwezi kufanya hivyo, wewe ni kama binti yangu. Yani wewe nakuona kama Samia, ngoja leo nikuibie siri nikido ila usimwambie Samia. Ni hivi, mimi nilikuwa nampenda sana mama yako, tena sio nilikuwa maana hadi leo bado nampenda sana ila baba yenu kanipiku kuwa naye”Hapa ndio kidogo Erica alianza kuongea,“Kwahiyo mama Samia humpendi?”“Aaaah hapana, nampenda ila mama yako nampenda zaidi yani, yeye ndio mwanamke wa maisha yangu kwakweli”“Ila mama anapendwa sana na baba”“Natambua hilo, ila hata mimi ninampenda. Kwani wewe unafikiri nampenda vipi?”Walikuwa wameshafika kwakina Erica, yani Erica alifungua haraka haraka mlango wa lile gari na kushuka, muda huo mama Angel nae ndio alikuwa anaingia maana kwanza alimrudisha Sarah nyumbani kwao, kwahiyo kitendo cha kuona Rahim akimrudisha Erica moyo wake ulifanya paaa, alihisi kama moyo wake kupasuka, alimvuta mkono Erica na kuingia nae ndani,“Wewe mtoto, nani aliyekutuma uongozane na yule mtu?”“Kwani kuna tatizo gani mama?”“Alikuwa anakwambiaje?”Erica alimsimulia mama yake kile ambacho alikuwa akizungumza na Rahim, basi mama Angel aliingia nae tu ndani bila ya kusema chochote ila kiukweli habari hiyo ilimuumiza sana.Sia alikuwa ni kama mwanamke aliyechanganyikiwa kwakweli, kilichokuwa kikimuumiza akili ni kujua mwanae halisi ni nani, yani alikuwa akiumia sana roho.Siku hii alienda Kanisani na kushinda huko siku nzima ingawa haikuwa siku ya Ibada, wakati anatoka huko alikuwa yupo njiani akiongea mwenyewe tu maana alikuwa kama mtu asiyejielewa vile, kuna mtu alimshika bega na kumshtua,“Una matatizo gani mbona unaongea peke yako?”Katika hali ya kuchanganyikiwa ilikuwa ngumu kwa yeye hata kugundua kuwa anaongea na nani, alianza tu kumwambia,“Niliyekuwa nafikiria ni mwanangu kumbe sio mwanangu, niliyelea sio mwanangu sijui mwanangu yuko wapi. Kama amekufa basi wanionyeshe hata kaburi lake”“Nani hao?”“Nilifikiria Erick ni mwanangu kumbe sio mwanangu, nimemlea Elly nae sio mwanangu, sijui mwanangu yuko wapi”“Unajua unayeongea nae lakini?”Sia akamuangalia kwa makini, na kushtuka sana pale pale alianguka na kuzimia. Katika hali ya kuchanganyikiwa ilikuwa ngumu kwa yeye hata kugundua kuwa anaongea na nani, alianza tu kumwambia,“Niliyekuwa nafikiria ni mwanangu kumbe sio mwanangu, niliyelea sio mwanangu sijui mwanangu yuko wapi. Kama amekufa basi wanionyeshe hata kaburi lake”“Nani hao?”“Nilifikiria Erick ni mwanangu kumbe sio mwanangu, nimemlea Elly nae sio mwanangu, sijui mwanangu yuko wapi”“Unajua unayeongea nae lakini?”Sia akamuangalia kwa makini, na kushtuka sana pale pale alianguka na kuzimia.Muda kidogo akazinduka tena na kumuangalia yule mtu, akasema kwa mshangao,“Kumbe ni Elly!!”Akazimia tena, kwakweli Elly hakumuelewa kabisa mama yake hata yale maneno yake hakuyaelewa pia, ikabidi tu kwa wakati huo aombe usaidizi kwa watu ili waweze kumsaidia arudi na mama yake nyumbani.Basi kuna mtu alikuwa na gari, ndio gari hilo Elly alilisimamisha na moja kwa moja yule mtu alimsaidia Elly pamoja na mama yake, alimuuliza,“Nikupeleke nae hospitali au?”“Hapana, nirudishe nae nyumbani tu, nadhani mama yangu kuna mambo yamemchanganya tu ila atakuwa sawa”Basi Elly alianza kumuelekeza yule mtu mpaka walipofika kwao, ila mama yake alizinduka kwa muda huu huku akijaribu kuvuta matukio vizuri, wakati wanashuka ilibidi wamshukuru yule mtu aliyewasaidia, ndipo Sia aliposhtuka sana kumuona yule mtu,“Kheeee Juma!!”“Kumbe ni wewe, nimekusaidia wewe mwehu!”Elly bado alikuwa akishangaa tu, muda ule ule Sia alikimbilia ndani na kujifungia mlango, yani Elly hakuelewa ikabidi aulize,“Kwani kuna tatizo gani? Umetusaidia kwani tatizo ni nini?”“Namfahamu vizuri sana huyo mama yako, ni mwehu huyo. Muulize vizuri anafahamiana vipi na mimi? Na ningejua kuwa ni yeye kaanguka kwa hakika nisingemsaidia”Huyu baba hakumuona vizuri mwanzoni sababu ni watu ndio walimuinua na kumpakiza kwenye gari, kwahiyo wakati amezinduka na kushuka ndiop wakagunduana, yani Juma hakuongea zaidi ila akarudi kwenye gari yake na kumwambia Elly,“Mpe ujumbe kuwa siku yake ipo nitamkamata tu na uchizi wake”Kisha Juma akaondoka zake, kwakweli bado Elly hakuelewa kabisa na kwenda ndani kumgongea mlango mama yake,“Mama, nifungulie mimi ni Elly”“Ameondoka yule mtu?”“Ameondoka ndio”Basi Sia alifungua mlango kisha Elly aliingia ndani, ila jambo la kwanza kabisa Elly alimuuliza mama yake,“Kwani mimi sio mwanao?”Sia alishikwa na kigugumizi na kujikuta akishindwa hata kueleza, wakati Elly alipokazana kumuuliza lile swali alijikuta akianza kulia tu, na muda ule ilikuwa ni usiku, ikabidi Elly aache kumuuliza mama yake lile swali na kuongea kile ambacho watakula kwa usiku huo,“Haya mama, ni usiku tayari na leo hata haieleweki, tutakula nini sasa?”“Ngoja nikatafute mkate mwanangu”“Hapana, ngoja nikanunue mwenyewe”Basi Sia alimpa Elly hela ambapo Elly aliondoka muda huo na kwenda dukani, Sia alichukua simu yake na moja kwa moja kumpigia baba Angel simu na kuanza kuongea nae,“Naona nakaribia kuwa chizi”“Sio unakaribia, wewe ni chizi kabisa tena chizi fresh”“Jamani, usiseme hivyo. Najua Elly akijua ukweli hatonikubali tena, hata huyo mtoto wangu wa ukweli najua hawezi kunikubali”“Hiyo inaitwa utavuna ulichokipanda, tamaa zingine ni mbaya sana. Yani haya yamekutokea puani. Mara nyingi chizi huwa hajioni kama ni chizi bali huona wenzie kuwa machizi, ila mpaka umeanza kujitambua kuwa ni chizi basi uchizi umeana kukukolea. Sia unavuna ulichokipanda, na bado”“Jamani, badala unitie moyo kweli unaniambia maneno gani?”“Toka lini mtu mwenye akili timamu ukamtia moyo chizi? Kwaheri”Simu ile ilikatika, Sia alijiinamia chini huku akianza kujuta yote ambayo amewahi kuyafanya katika maisha yake, na kusema,“Kweli kila kitu kina gharama zake, ila hiki changu kinagharama kubwa sana, sijui nitafanyaje jamani!”Sia alikuwa akiwaza mwenyewe bila ya kupata jibu la mawazo yake aliyokuwa nayo.Mama Angel akiwa na mumewe nyumbani muda baada ya mumewe kutoka kuongea na Sia, alianza kumueleza kuhusu alichokuwa akikisema Sia,“Au Elly kaujua ukweli?”“Sijui, yule mwanamke ni chizi yani hakuna mtoto atakayemkubali na uchizi wake. Hivi unadhani Elly agundue ukweli kuwa mama yake mzazi ni madam Oliva, atamkumbuka huyo chizi?”“Tena jinsi madam Oliva alivyo ataamua tu moja kwa moja kuwa amlee Elly na amlee na huyo mwanae”“Sasa tutafanyaje kumkutanisha madam Oliva na Elly?”“Mmmh sijui tufanyaje, ila mzee Jimmy mbona kaleta makubwa sana?”“Ni baba yangu ila sikutegemea kwa haya aliyoyafanya kwangu, naamini dada yangu Tumaini akisikia haya atachukia sana.”“Ila kumbuka Tumaini alimpenda sana baba yenu, sidhani kama anaweza kuamini vitu hivyo”“Kweli usemayo, kwa Tumaini kuamini kidogo itakuwa ni ngumu sana. Ila najua ataamini tu mambo ya baba yake, najua nikimbana vizuri yule bi.Aisha atanieleza mengi sana naona kuna mengi mno yaliyojificha kwa baba yangu mzee Jimmy, na sijui alikuwa na maana gani. Ila kinachonifikirisha kwasasa, ni sindano gani aliwachoma wanangu? Na aliwachoma kwaajili ya nini?”Hapo hata mama Angel hakuwa na cha kuongea kabisa maana kila akifikiria mambo hayo aliona yanazidi kuwa magumu.Waliamua tu kulala kwa muda huo, ila kabla ya kulala mama Angel alimwambia mwanae kuwa anahitaji kumuona Erica kwanza,“Kwanini? Kwani kafanyaje?”“Mmmh kuna kitu naona hakipo sawa kwa huyu mtoto kwa siku hizi”“Ooooh mimi sijui, wewe ndio mama utakuwa unaelewa fika mwenendo wa watoto. Nenda kamuangalie tu”Mama Angel alitoka na moja kwa moja kwenda chumbani kwa Erica ila alimkuta akicheza karata ambapo Erica alizificha zile karata baada ya kumuona mama yake, mama Angel alitikisa kichwa tu na kusema,“Erica, unadhani unaweza kunificha? Nimekuona vizuri sana ukicheza karata na wala leo siji kwaajili ya karata zako. Ila mwanangu una matatizo gani?”“Kwanini mama?”“Unajua sikukuelewa kabisa na yule mtu uliyeongozana nae, alikuwa na maana gani yule? Kwakweli leo sijapenda kabisa, kama mama yako nimechukia sana, ingawa umenieleza ila sijapenda”“Nisamehe mama”“Umeanza kama dada yako Angel kukimbilia msamaha kila unaposemwa ili akusemae asikuseme sana, kwakweli leo umenikera sana. Usirudie tena jambo hilo, ukitoka shule ni moja kwa moja nyumbani hakuna kupita popote pale. Haya leo mbona unacheza karata mwenyewe! Si huwa unacheza na Erick wewe!”“Kasema leo kachoka sana”“Wewe hujachoka na huo umbea wako wa kwenda kuchunguza hadi baba wa Samia ni nani? Haya umepata faida gani, nakukataza kila siku huo umbea ila husikii lolote, umbea huo utakuponza mwanangu naomba uache”“Haya mama”“Na muda huu ulale, sio uendelee kucheza karata”Erica alimuitikia mama yake, kisha mama yake aliinuka na kwenda chumbani kwake kulala.Kwakweli mama Sara hakupendezewa kabisa na tabia ya mwanae kutoka na kwenda kwa mama Angel na kupelekana kwenye maombi,“Kwahiyo mlienda kwenye maombi kufanya nini?”“Alienda kuniombea”“Yani mwanamke anajishauwa sana yule, simpendi kama nini”“Aaaah mama jamani, usiseme hivyo, si majuzi tu ulikuwa ukimsifia kwa kuniokoa mimi, halafu leo unasema humpendi! Mama ukiendelea kumchukia yule mama basi mimi nitahama hapa nyumbani”“Kheee utahamia wapi?”“Kule kule kwa mama Erick”“Unadhani atakupenda?”“Tena atanipenda sana, yule mama ana upendo sana. Na huwa ananihudumia mimi kama mwanae, halafu nikwambie kitu mama”“Niambie”“Kila mahali tunapopita na yule mama, watu wengi wanamuuliza kama mimi ni mwanae kabisa, ila mama nadhani kuna undugu wa damu kati yangu mimi na yule mama, ni vile tu hutaki kuniambia ukweli ila ukweli utajulikana tu”“Unataka ukweli? Unajua ni mtu gani ambaye yule mama anadai kuwa wewe ni mtoto wa huyo ndugu yake? Ukimjua kwa hakika hutokubali kuwa ni baba yako. Hebu nisikilize mimi mama yako, kufanana duniani ni kawaida ila kwa kifupi ni kuwa huna undugu wowote na yule mama”“Mmmmh”Sarah hakuongea zaidi, aliamua tu kumuaga mama yake usiku mwema, na kuamua kulala kwa muda huo.Leo kulipokucha, asubuhi na mapema baba Angel alijiandaa na kutoka ila mama Angel leo aliamua tu kubaki nyumbani maana aliona ni vyema aende kesho yake kuzungukia mambo yake maana bado alihitaji kufahamu ukweli halisi wa mambo ulivyo.Basi kwa muda huo alianza kufanya kazi zake tu za hapa na pale kwenye nyumba yake.Ila kwenye mida ya mchana, kuna mgeni alifika pale kwake na mgeni huyo alikuwa ni baba Daima, ambaye alitaka kuongea na mama Angel kwahiyo alienda nae bustanini kuzungumza nae,“Kwanza kabla ya yote napenda niombe msamaha kwa niaba ya mke wangu maana amekiri wazi kwangu kwamba alikuja kwako na kusema maneno mabaya juu yako, naomba umsamehe sana mke wangu”“Nishamsamehe ila kiukweli sikupenda kabisa hiyo tabia aliyoifanya kwangu”“Aaaah ni wivu ulimsumbua tu, unajua nini baada ya kugundua kuwa wewe ndio Erica niliyekuwa nakutaja ndio akawa vile naomba umsamehe tu”“Hakuna shida”“Ila unajua nini, nafikiria kama mapenzi yetu yasingeingia dosari inamaana kuwa kwasasa tungekuwa tukiishi pamoja. Unajua nini Erica, mimi na wewe tuliumbwa tuwe pamoja ila dunia hii na mambo yake ndio tukatenganishwa”Mama Angel alicheka tu na kusema,“Achana na habari hizo bhana, kwasasa kila mtu yupo kwenye maisha yake na familia yake”“Unajua yule rafiki yako Dora hakuwa mtu mzuri kabisa, nakumbuka siku nimetoka rumande akaanza kuniambia maneno machafu kuwa sina hadhi ya kuwa na wewe, niliumia sana moyo. Ila usikute alisema kweli maana Erica ndoto yako ilikuwa ni kuolewa na mwanaume tajiri na ndiye uliyempata, nadhani moyo wako umeridhika sasa”“Usiseme mwanaume tajiri ndiye niliyekuwa namtaka, hapana. Kwanza kuhusu hela kila mtu anapenda hela, nilichokuwa nataka mimi ni penzi la dhati, nilichoka kuumia na ndio nikawa nahitaji penzi la dhati”“Sasa mimi nilikuwa na tatizo gani? Je sikuwa na penzi la dhati kwako?”“Babuu, hayo yameshapita na unaelewa wazi ni kitu gani kilitokea baina yetu”“Kwahiyo huyu mumeo hukumpendea pesa wewe?”“Nilianza kumpenda kabla hata ya kuwa na pesa, na kama ningehitaji mwanaume wa pesa basi ningekazana na Rahim maana kwa kipindi hiko ndio alikuwa na pesa zaidi”Muda kidogo baba Angel kumbe alikuwa amerudi, na alipoambiwa kuwa mkewe kuna mtu anaongea nae kwenye bustani ikabidi aende na kumuona, kwakweli hakupenda kwani huwa hapendi kuona mkewe akitumia muda mrefu kuongea na mwanaume, na hapo alijua lazima katumia muda mrefu, na alipoenda tu baba Daima aliaga na kuondoka zake, ilibidi mama Angel amwambie tu mumewe kuwa huyo alienda kwa lengo la kumuombea msamaha mkewe.Baba Angel alipoingia ndani, alihitaji chakula kwa muda huo, kwahiyo ilibidi mama Angel amuandalie chakula alichopika mumewe, ambaye alianza kula kile chakula huku akiongea ongea mambo mbalimbali,“Nina hamu sana ya kuonana na huyo dokta Jimmy”“Tutamuona tu, hakuna marefu yasiyo na ncha”“Ila unaweza kuhisi kuwa ni dawa gani aliyowapa watoto wetu?”“Nashindwa hata kuhisi kwani mimi naona Erica na Erick wapo sawa kabisa, au wewe unaona kuna tatizo lolote kwao?”“Hapana, hata mimi naona wapo kawaida tu ila huwezi jua labda ni dawa ambazo zitaanza kufanya kazi badae”“Mfano ndio tukajua ni dawa gani na watoto washatumia tutafanyaje?”“Aaaah itakuwa rahisi tukijua, hata tatizo likitokea tutajua ni kitu gani cha kufanya”Waliongea pale na baba Angel alipomaliza kula, moja kwa moja walienda chumbani ila baada ya muda kidogo tu simu ya mama Angel iliita na alipopokea akakuta anayempigia ni mama Sarah,“Hivi sijapenda kabisa, au unafikiri huyu Sarah ni damu yenu?”“Kwani tatizo liko wapi nikimsaidia Sarah?”“Umetumwa? Sitaki mazoea na wewe”Mama Sarah alikata simu, ila mama Angel hakutaka hata kujiumiza kichwa kwa jambo hilo kabisa.Usiku wa siku hiyo, moja kwa moja waliamua kulala tu kwani hawakuwa na mambo mengi ya kufanya kwa siku hii.Ila palipokucha tu kama kawaida baba Angel aliondoka, ila kwa muda huu huu mama Angel alipigiwa simu na ndugu yake Derrick akimuomba aende nyumbani kwao ili wapate kuzungumza kwani alitaka wazungumze kuhusu mtoto Elly na Sarah.Mama Angel alijiandaa kisha kama kawaida, kumuachia Vaileth mtoto na kuondoka zake.Vaileth alihisi kuwa hana hali ya kawaida kabisa, alijihisi sana huenda akawa mjamzito, akili nyingine ikawaza kuwa atafanyaje kama ni mimba ya Junior,“Mmmmh na hivi Junior anasoma jamani, hivi nitafanyaje mimi? Si ndio nitafukuzwa hapa jamani, nitaelekea wapi? Hivi familia yangu itakubali kupata watoto wawili na wababa wasioeleweka? Si ndio nitatukanwa sana mimi!”Aliamua kwa muda huo kumpigia simu Junior ili aende wapate kuongea, ukizingatia watu wote hawakuwepo pale nyumbani, na kweli baada ya muda mfupi tu Junior alifika mahali na moja kwa moja kwenda ndani kuzungumza na Vaielh,“Mbona umekuja kwa haraka sana, yani nikasema na hivi ni siku ya shule na hatujapanga basi nikajua utachelewa sana”“Aaaah Ijumaa leo, hakuna tatizo. Ndiomana nimewahi kuja. Haya niambie mpenzi wangu, umenikumbuka eeeh!”“Nimekukumbuka ndio ila kuna kubwa zaidi”“Kubwa gani?”“Nina mimba”Junior alishtuka kidogo na kufikiria kwa muda, ndipo Vaileth alipomuuliza,“Mbona umeshtuka hivyo?”“Aaaah sio kwa ubaya, ila nimeshtuka tu, si unajua tena bado nasoma na wewe hapa unafanya kazi, yani hapo ndio naona ni tatizo kubwa sana.”“Sasa tufanyeje?”“Hakuna namna hapo ni kutoa tu”Vaileth alishtuka sana baada ya kusikia ile kauli toka kwa Junior na kusema,“Itakuwa Junior hunipendi wewe, inakuwaje utoe kauli kuwa mimi nikatoe mimba kweli? Nitatoaje mimba? Bora hata ungesema kitu kingine”“Hapana Vai, usinielewe vibaya wala nini. Nakupenda tena sana ila nimejaribu kufikiria mambo mengi sana. Ukiangalia mimi bado nasoma, na wewe upo hapa kikazi tu, ni nani atakayekubali kulea mdada wa kazi mwenye mimba? Lazima utafukuzwa na sitokuona tena, halafu itakuwa tatizo kwangu ambaye bado nasoma, naomba tuitoe tu hiyo mimba”“Junior sikuelewi, kwanza unajua madhara ya kutoa mimba au? Nikifa mimi itakuwaje? Halafu kitu kingine ni kuwa mtoto ni baraka, je hupendi kuzaa na mimi?”“Napenda sana, ila tutafanyaje na maisha haya? Sina msaada wowote kwako kusema kuwa nitaweza kulea mtoto wakati hata mimi nahitaji kulelewa”Hapo Vaileth alijiona kuwa na mtihani mzito sana, kwanza hakutegemea kabisa kama itafikia hapo kwenye hali hiyo, alifikiria kwa muda na kumwambia Junior,“Sawa, naomba hela ya kwenda kuitoa hii mimba sababu lazima niende hospitali na niongee na daktari na hapa sidhani kama itakuwa chini ya laki mbili”“Zile hela za kipindi kile ziko wapi?”“Usinichanganye Junior, hela gani lakini? Si umesema nikatoe mimba, basi unipatie pesa ya kufanya hivyo”“Basi usijali, ngoja niende kwa mama najua kesho tu nitakuletea hiyo hela hata usijali”“Poa”Kiukweli Vaileth hakuwa na furaha kabisa kama ambavyo siku zote huwa na furaha, alihisi maisha yake kubadilika kwa muda mfupi tu huu.Junior moja kwa moja alienda nyumbani kwa mama yake, na kweli alimkuta akifanya tu mambo yake mengine na kumsalimia pale,“Kheee Junior, huu muda unatakiwa kuwa shuleni, imekuwaje umekuja nyumbani?”“Ni kweli natakiwa kuwa shuleni ila kuna tatizo mama”“Tatizo gani?”“Ni hivi mama, sisi tumeambiwa tuanze kujiandaa kwa mitihani ya kidato cha sita”“Kheee Junior, muanze kujiandaa na mitihani kabla hata ya kuingia kidato cha sit?”“Mama unafikiri siku zinachelewa basi!! Bado miezi michache tu nitakuwa kidato cha sita, kwa kifupi hii ni tofauti na ada, kila mwanafunzi anatakiwa kutoa laki tatu kwaajili ya hiyo”“Kheee nilijua tu kuwa hapa kinachotakiwa ni hela, maneno mengi kumbe unahitaji hela, mara nyingine Junior kuwa na huruma na mimi, sina kazi mama yako ujue”“Ila mama, kwani wewe kutokuwa na kazi ni kosa langu? Sijakukalisha nyumbani mama yangu, mwanao mimi sio mgonjwa kusema kwamba uliacha kazi ili uniangalie muda wote, Mungu kakusaidia kunipata mtoto mwenye afya tela na nguvu halafu unasema huna kazi, je ni sababu yangu?”“Kwahiyo ni nini?”“Hayo ni maamuzi yako mama, kuna wanawake huko tunawaona hawajasoma ila wana kazi zao za kufanya, wapo walioamua kuwa mama lishe, wapo wanaopika vitumbua, wanatengeneza batiki, sabuni, wengine wamesoma na wengine hawajasoma ila wanatafuta kazi za kuwaingizia kipato. Sasa mama yangu wewe ni mzima kabisa, umeumbwa vizuri, una mikono miwili mizima, miguu miwili mizima na macho mawili mazima halafu umesoma mpaka chuo kikuu, na upo hapa kuniambia kuwa unajua sina kazi mwanangu, hivi inaingia akilini hiyo kitu mama!”Mama Junior alifikiria kidogo na kusema,“Mtoto mjinga sana wewe, kwahiyo yote hayo yanakutoka sababu nimeshindwa kukupa hiyo laki tatu? Na sikupi sasa, nitakuja mwenyewe huko shuleni kwenu na kuwalipa mwenyewe walimu”“Hayo ndio maneno, ila sio kuniambia kuwa huna kazi, sasa mimi unataka nifanyeje mama? Subiri nimalize shule nami nitafute cha kufanya ndio nianze kukulea mama yangu. Ni bora uniambie mwanangu kwasasa sina hela nitakuelewa ila wimbo wa kuniambia huna kazi huwa siulewi kabisa, swala la hela sio lazima uwe na kazi, kuna watu hawana kazi ila hela wanazo, ila ambaye hana kazi na hana hela kaamua tu. Kuna watu wana kazi lakini hawana hela, au hela zina matumizi mengi, ila maswala ya kuniambia sina kazi sijui kama nitayasikiliza tena. Toka nipo mdogo una usemi huo huo wa sina kazi, nimechoka mama na usemi huo”“Kheee yani Junior, yote hayo yanakutoka kisa hela tu jamani!! Umesahau hasara ya laki mbili uliyoiweka kwangu mjinga wewe, halafu huna hata aibu unakazana kusema maneno mbalimbali. Sikia nikwambie, sitaki kufanya kazi ndiomana sina kazi, nadhani utakuwa umeridhika sasa, niondokee hapa rudi shuleni, maswala ya kuniomba hela zisizokuwa na kichwa wala miguu siyataki”Junior alimuangalia mama yake bila ya kusema chochote maana kwa muda huo alikuwa akiwaza tu kuwa atafanya kitu gani na ile mimba ya Vaileth, yani maneno mengi yalimtoka kwa mama yake sababu ya ile mimba ya Vaileth.Aliondoka hapo huku akiwaza cha kufanya, moja kwa moja alienda ofisini kwa baba yake mlezi ili aongee nae kuhusu hilo swala.“Kheee Junior, umekuja kufanya nini ofisini kwangu leo?”“Nina shida”“Shida gani?”Junior alimuelezea vile ambavyo aliongea na mama yake, basi Deo alimuangalia na kumwambia,“Sina hiyo hela mimi”“kwani nyie mnafanya nini juu yangu? Nahitaji kusoma ili niweze kujitegemea ila mambo kama haya mnanikatalia, mna nia gani na mimi?”“Kwani unaoishi nao hawawezi kukusaidia? Mfate baba mdogo wako Erick akupe hiyo hela”“Sikia baba, yule ni babangu mdogo na wewe ndio baba yangu, yule bamdogo ananisomesha, siwezi kukazana na kumuomba kila kitu wakati wazazi wangu mpo”“Katika kuomba kuna utaratibu wake, sio unaibuka tu unataka hela basi tukugaie, sikia Junior laki tatu sio elfu kumi kijana, ni laki tatu hiyo umeisema, mtu unaweza kununua hata bati kadhaa za kuezekea nyumba”“Sasa nisipowaomba nyie nikamuombe nani?”“Utajua mwenyewe”“Dah!! Sijui kwanini, hujawahi kunipenda hata kidogo jamani, sijui sababu sio baba yangu mzazi, ila umenilea na ninakuheshimu sana. Hilo sio jibu la kunipa mimi kama mzazi, ungeniambia vizuri sio nitajijua mwenyewe, ila asante sana.”Junior akainuka, yani alikuwa na mawazo sana na hata hakuelewa cha kufanya kwa muda huo, aliamua tu kurudi shuleni kwao huku akifikiria kingine cha kufanya.Jioni ya leo, mama Angel alirudi toka sehemu aliyokuwa ameelekea, kwa kiasi Fulani alikuwa amechoka sana, basi akaanza kuongea na Vaileth kuhusu mambo yaliyoendelea hapo nyumbani.“Vipi habari a hapa? Hajasumbua leo Ester?”“Hapana, leo alikuwa kimya tu”Basi mama Angel akaenda chumbani ambako mwanae alikuwa amelala, sema kwa muda huu mama Angel alijihisi kuchoka sana kutokana na mizinguko ya siku hii.Alikuwa akipekua kitu kwenye kabati lake na ikaanguka picha ya Angel alipokuwa mtoto, basi mama Angel aliishika ile picha huku akitabasamu na kusema,“Mwanangu Angel, nakumbuka kipindi ulipokuwa mtoto, ulikuwa ukinifurahisha sana, muda mwingi ulitumia kuwa na mimi ila siku hizi hakuna kabisa mambo ya kuwa karibu na mama”Muda kidogo baba Angel nae alikuwa kawasili, basi mama Angel akaongea na mumewe,“Nimemkumbuka Angel jamani, nimemkumbuka sana”“Hata salamu mke wangu!”Mama Angel alicheka kidogo na kuanza kusalimia mumewe, basi baba Angel akasema,“Karibu shule itafungwa, atarudi nyumbani kwa kipindi hiki sio kama ile likizo aliyokaa kwa bibi yake. Atarudi nyumbani moja kwa moja, hakuna tatizo”“Ila miaka inaenda sana, nakumbuka kipindi hiko tukiishi mimi, wewe na Angel tu hata hatukufikiria kama tutakuwa na watoto wengine jamani, ila Angel ni maisha yangu ujue”“Naelewa ndio, na Angel ndiye aliyetuunganisha tena mimi na wewe. Najua bila kuzaa wewe, ungeendelea tu kushikwa akili na wengine na kukuumiza tu moyo wako maana hawakufahamu vizuri kama mimi ninavyokufahamu na akili zako”Mama Angel alicheka tu, ila ni kweli mumewe alimfahamu sana ndiomana aliweza kuishi nae kwa muda mrefu sana.Usiku wa siku hiyo, Vaileth alikaa chumbani kwake huku akiwaza sana kuwa afanye kitu gani, hakupata jibu kabisa, aliwaza kuhusu ile mimba ila uhakika wa kweli kuwa ana mimba hakuwa nao. Akakumbuka njia ya kupima mimba aliyoambiwa na bibi yake, akasema kuwa ataifanya kesho yake asubuhi maana mkojo wa asubuhi ulikuwa rahisi sana kukufanya ugundue kuwa una ujauzito au la.Muda huu aliamua kulala ila alikuwa na mawazo mengi sana hadi alihisi usingizi kutowe, palipokucha tu alienda jikoni na kuchukua chumvi na vikopo vyake, kisha alienda tena chumbani kwake na kupima ule mkojo wake, kwakweli alishtuka sana kwani ilionyesha wazi kuwa ni mjamzito, alianza kuwaza ni kitu gani afanye, huku wazo la kutoa ile mimba likichukua nafasi kubwa sana.Mara akasikia mlango wake ukigongwa na kumfanya apatwe na hofu kiasi, akaenda kumwaga ile mikojo yake na kutupa kabisa ule ushahidi maana hakutaka hata mtu kumuhisi vibaya, basi alienda kufungua mlango wake na kukuta aliyekuwa anagonga ni Erica ambapo moja kwa Erica aliingia chumbani kwa Vaileth na kumwambia,“Dada samahani, tukae kidogo tuongee kuna kitu nataka kukwambia”Vaileth alikaa nae kitandani na kuanza kumsikiliza Erica huku akimuangalia kwa makini,“Eeeh niambie”“Nimeota kuwa wewe una mimba”Vaileth alishtuka sana, na kushindwa hata kuongea, ila Erica aliendelea kusema,“Tena nimeota kuwa hiyo mimba unataka kwenda kuitoa”Yani Vaileth ndioT alihisi kuchanganyikiwa kabisa kwa muda huo. Mara akasikia mlango wake ukigongwa na kumfanya apatwe na hofu kiasi, akaenda kumwaga ile mikojo yake na kutupa kabisa ule ushahidi maana hakutaka hata mtu kumuhisi vibaya, basi alienda kufungua mlango wake na kukuta aliyekuwa anagonga ni Erica ambapo moja kwa Erica aliingia chumbani kwa Vaileth na kumwambia,“Dada samahani, tukae kidogo tuongee kuna kitu nataka kukwambia”Vaileth alikaa nae kitandani na kuanza kumsikiliza Erica huku akimuangalia kwa makini,“Eeeh niambie”“Nimeota kuwa wewe una mimba”Vaileth alishtuka sana, na kushindwa hata kuongea, ila Erica aliendelea kusema,“Tena nimeota kuwa hiyo mimba unataka kwenda kuitoa”Yani Vaileth ndio alihisi kuchanganyikiwa kabisa kwa muda huo.Vaileth alinyamaza kimya bila ya kusema chochote, kisha Erica akaendelea kuongea na kumwambia Vaileth,“Sikia dada, unajua kama kutoa mimba kuna madhara sana. Sio vizuri kutoa mimba, bora uvumilie uweze kuzaa uwe na mtoto wako”Muda huu Vaileth alijikaza na kumuuliza Erica,“Umepata wapi hiyo habari kuwa mimi ni mjamzito na ninataka kutoa mimba?”“Nimepata hiyo habari kwenye ndoto, nimeota kuwa una mimba na unataka kuitoa”“Una uhakika gani?”“Kama unanibishia basi nikamwambia mama ili twende wote hospitali kupima, nina uhakika na ndoto zangu”“Erica jamani usifanye hivyo tafadhari, nakuomba usimwambie chochote mama.”“Ukitaka nisiseme niahidi kuwa hiyo mimba hutoitoa”“Nakuahidi Erica, sitotoa mimba hii wala nini, nitailea hadi nitakapozaa ila usiseme Erica, nitafukuzwa kazi mimi, na kwetu maisha ni shida sana”“Naelewa, kweli mimi ni mbea sana na huwa nawashwa kukaa bila kusema ila niruhusu nimwambie mtu mmoja tu ambaye namuamini kuwa yeye anaweza kukaa na jambo moyoni na hatolisema kwa yoyote”Vaileth akaogopa kidogo, na kumuuliza Erica kwa uoga,“Nani huyo?”“Ni Erick, niruhusu nimwambie tu Erick yani nitakuwa sawa nikimpata hata mmoja wa kumwambia hili na sitosema popote tena”Hapa kidogo Vaileth alipumua kwani kweli Erick hakuwa na tabia za umbea kabisa, yani huwa hata kumuuliza muhusika tu hamuulizi kabisa, basi akakubali na kusema,“Hakuna tatizo, naamini Erick hawezi kusema. Ila nakuomba usimwambie yoyote yule mwingine, sina maisha yoyote mimi, hii kazi ndio tegemeo langu”“Sawa, nimekuelewa”Ilisikika sauti ya mama Angel akimuita Vaileth, ilibidi pale Vaileth aachane na Erica na kwenda kumsikiliza mama Angel anasema kitu gani.Wakati huo Erica nae aliondoka na kwenda kufanya kazi zingine za pale ndani kwao, moja kwa moja alienda chumbani kwa Erick ili akafanye nae kazi ila alimkuta kwa muda huo Erick akijiandaa,“Kheee unaenda wapi kwani?”“Naenda na baba kiwandani”“Aaaah sawa”Erica alitoka zake na kumuacha Erick akimalizia kujiandaa pale.Siku ya leo, nyumbani kwa madam Oliva alikuwepo Paul na Steve tu, walikuwa nje wakijishughulisha na vitu mbalimbali, basi Steve alimuuliza Paul,“Vipi shuleni maendeleo yakoje?”Ndipo Paul alipokumbuka kuwa kuna barua alipewa jana yake kuwa awapatie wazazi wake, waweze kwenda shule siku hii ya Jumamosi kwenda kuongea na mwalimu wa paul. Basi Paul akaenda kumletea Steve ile barua ambapo baada ya muda kidogo Steve aliamua kumpia simu madam Oliva ili ampe ule ujumbe,“Kuna barua, Paul kanipatia hapa kuwa wazazi wake tunahitajika shuleni”“Kheeee huyo Paul kafanyaje tena huko shuleni?”“Sijui, inabidi kwenda”“Sawa, si upo nae hapo nyumbani. Basi nenda nae huko shuleni, mimi nikiwahi pia nitafika hapo hakuna tatizo”Basi Steve alijiandaa vizuri kabisa kwaajili ya kuondoka na Paul kwenda nae huko shuleni walikoitwa.Kisha Steve na Paul waliongozana kwenda huko shuleni ambapo Paul anasoma, wakati wanafika tu pale na madam Oliva alikuwa kashafika kwahiyo ilibidi tu wote kwa pamoja waende ofisini ila mwalimu mmoja alipowaona akaropoka,“Kheee huyu Paul kumbe baba yake yupo? Anavyosemaga kila siku hana baba!!”Wote wakaangaliana na kuguna tu, kisha madam Oliva akasema,“Jamani walimu wenzangu, hebu acheni hiyo tabia mnadhalilisha taaluma yetu”Basi wakabaki wanatazamana maana hawakujua kama mamake Paul ni mwalimu pia.Moja kwa moja walienda kuzungumza na mwalimu aliyewaita, ambapo mwalimu alimtaka Paul kuwasubiri wazazi wake nje kwanza, halafu Paul alivyotoka ndio alikaa vizuri ofisini na wazazi wa Paul na kuanza kuzungumza,“Kwanza kabisa sikujua kama babake Paul yupo, nilijua ni ana mama tu kwani siku zote huwa anasema baba yake hayupo”Madam Oliva alijibu kwa kujibalaguza pale,“Babake yupo”“Hata mimi naona aisee, basi kesi imeisha tayari ngoja niongee sasa”“Eeeeh tunakusikiliza”“Paul, nimemkuta mara nyingi tu akiwasimulia wenzie kuhusu ubaya wa mababa, yani kila mara anawaambia wenzie kuwa wababa ni watu wabaya sana, wanatelekeza watoto wao hata hawana habari kuwa mtoto anakula nini au anavaa nini, yani yeye huwa anasifia tu kuhusu mama yake, ila anasema mama yake ana mawazo sana sababu hana baba wa kuwa nae. Mimi kama mwalimu niliumia sana, kuna siku mwanangu alikuja nyumbani, anasoma hapa ni rafiki wa Paul, aliniambia mama naomba tumpe Paul baba yetu hata mara moja akae nae, alisema Paul anatia huruma sana sababu baba yake sio binadamu wa kawaida. Nikashtuka sana, halafu siku hizi huwa namuona Paul anakuwa na mawazo muda wote, utakuta amekaa darasani kajiinamia chini akiwaza sana, ndiomana nikaamua nimuite mzazi wake ili nikwambie na ujue cha kufanya”Kisha alimwangalia Steve na kumwambia,“Jamani, nyie wababa hebu acheni roho mbaya hizo. Mpaka mtoto anafiki hivi kweli!! Cheki ulivyomfananisha jamani, halafu umemuacha anahangaika bila baba, ni bora ijulikane umekufa kuliko upo hai halafu humjali mtoto”“Nimekusikia mwalimu”Steve hakutaka kuongea sana, mwalimu aliongea pale na kuagana nao, kwakweli kwa upande mwingine Steve alijihisi vibaya, katika hisia zake alihisi kabisa kuwa Paul ni mwanae wa kumzaa ila kwanini inakuwa vile? Hakuelewa kabisa.Madam Oliva nae alijihisi vibaya sana, walitoka na kuondoka na Paul kurudi nae nyumbani ila hawakuongea kitu chochote kile, kisha walivyofika nyumbani madam Oliva alienda chumbani na kuanza kuzungumza na Steve,“Tufanyeje sasa?”“Inavyoonyesha mlisha Paul sumu mbaya sana kuhusu wababa”“Ni kweli, sababu ya hasira nilizokuwa nazo juu ya baba yake, alinitenda vibaya sana”“Hata kama, ila si vizuri kumlisha mtoto sumu mbaya kiasi hiki. Yani mtoto ajue kuwa alikataliwa na baba yake, sijui hapendwi. Najua Paul anachowaza sasa ni kitu gani! Ni hivi, anafikiria ukaribu uliokuwepo kati yangu na yake, anafikiria kuwa je mimi ndiye baba yake? Anafikiria jinsi mama yake ulivyomwambia kuhusu baba yake ndiomana anakuwa na mwazo sana. Na maneno ukishatamka hayarudishiki mdomoni yani ni kama maji yakimwagika vile, sasa hapa cha kufikiria tu kuwa tutafanyaje na huyu mtoto”Madam Oliva akapumua kwanza na kusema,“Unajua hadi nahisi kuchanganyikiwa mmmh!! Ila mtoto amekuwa kwasasa, sijui kama atanielewa nikimbadilishia maneno. Unajua mimi nilikuwa na kidonda moyoni, ndiomana muda wote nilipokuwa naongea na mwanangu nilikuwa namwambia ubaya wa baba yake tena bila kujali kuwa kuna wanaume wengine wanawapenda sana watoto wao wala nini, nilikuwa naumia sana, hebu fikiria toka nina mimba mtu hataki kuniona na mimba ameikataa, nimejifungua bado akanikataa, kwakweli nilikuwa kwenye wakati mgumu sana ndiomana nimejikuta nikimwambia maneno yote hayo Paul wangu jamani”“Hasira hasara, umejenga kitu kibaya sana kwa Paul. Na bora ni mtoto wa kiume pia, ila angekuwa ni mtoto wa kike, angekuwa muda wote anawaza mabaya tu kwa wababa. Nitajitahidi kuongea nae, nitajitahidi kuwa nae karibu ili aweze kuhisi uwepo wa baba katika maisha yake.”Madam Oliva alimsihi tu baba Angel amsaidie jambo hilo maana yeye alihisi kutokuweza kabisa kumuelewesha tena mwanae kuhusu wababa.Baba Angel akiwa kiwandani na Erick baada ya kazi za hapa na pale, alifika Juma ambaye alibahatisha tu siku hiyo na kuwakuta kwakweli alifurahi sana na kuanza kuongea nao,“Kwanza nimefurahi mno kuwaona mpo pamoja”Kisha Juma alimuomba kidogo baba Angel kuongea nae, kwahiyo walimuacha Erick aendelee na kazi zingine,“Hivi ndugu yangu mbona huwa hutaki kunielewa kuhusu kipaji cha huyu mtoto? Hebu nipatie niwe nae japo kwa wiki moyo na mimi akanisaidie kazi yangu”“Hivi akili yako ni nzima kweli Juma? Yani mimi nikakupatie kijana wangu kweli!!”“Kwani kuna tatizo gani jamani eeeh! Mambo mengine kusaidiana, sawa isiwe wiki moja, naomba hata kwa siku moja tu.”“Kwa hutojali, twende wote hilo eneo la tukio”“Hakuna tatizo, hayo ndio maswala ya kuongea sasa kuliko kubaniana riziki”“Kwahiyo mtoto wangu ndio ridhiki yako?”“Sinamaana hiyo, ila nina maana kuwa mwanao atafungua na kunionyesha njia vizuri kwenye biashara yangu kwani nimeshaona uelewa wake ulivyo”“Sawa nimekuelewa kwa hilo”Basi wakaongea pale, na kisha Juma alimuaga baba Angel na moja kwa moja baba Angel alirudi ofisini kwake kumalizia kazi na kijana wake, alipomaliza ndipo walipoenda dukani kwani baba Angel hakuwa ametembelea duka kwa siku nyingi kidogo.Basi walimkuta Rama pale akiendelea na kazi zake vizuri kabisa, ila baba Angel wakati akiongea nae Rama alimwambia jambo ambalo lilitukia mahali hapop,“Kuna mwanamke Fulani alikuja hapa, alilia sana kwa muda mrefu halafu akaondoka”“Mmmmh mwanamke gani huyo?”“Alisema anaitwa Sia”Baba Angel akacheka na kumwambia Rama,“Huyo mwanamke huwa akili zake zinaenda na kurudi, usijaribu kumsikiliza anachokisema”Waliongea kidogo pale huku wakipitia baadhi ya bidhaa za pale, ila Rama alikumbuka kitu na kusema,“Alisema kuwa Jumapili baada ya kutoka Kanisani atakuja tena hapa”Baba Angel alielewa vizuri akili za Sia zilivyo basi akasema kuwa kesho yake na yeye ataenda tena baada ya kutoka Kanisani.Baba Angel na Erick walirudi nyumbani kwa siku hiyo wakati muda kidogo umeenda hivyobasi walifikia kupata chakula cha jioni tu moja kwa moja, baada ya hapo kila mmoja alienda moja kwa moja kwenye chumba chake.Baba Angel alimueleza mke wake kuhusu walipoenda leo na Erick na kila kitu kilichotokea, ila hakukumbuka kumwambia kuhusu Juma kuhitaji siku moja Erick afike kwenye biashara zake.Alimueleza tu jinsi walivyoenda dukani na jinsi alivyoambiwa na Rama kuwa Sia alikuwa mahali pale,“Kheee sasa alifata nini dukani na kilio juu”“Yule mwanamke ni chizi, ila nasikia Kesho anaenda tena, hakuna shida nitaenda pale ili nimuulize vizuri tatizo lake ni nini”“Mjinga sana, sasa pale angepata msaada gani?”“Sikia nikwambie kidogo malengo ya yule mwanamke yalivyokuwa, ni hivi aliamini kuwa kabadilishana mtoto na wewe, kwamaana hiyo aliamini Erick ni mwanae halafu Elly ni mwanetu, ndiomana alikuwa akisema ile biashara ni ya mwanae, akimaanisha kuwa kama tukimpa Erick ni sawa sababu ni mwanae, na kama Elly tungegundua badae basi lazima tungempa mali zetu ambapo Elly asingeweza kumtupa mwanamke aliyemlea kwa siku zote. Ila kwasasa akili yake kama imegonga mwamba, sababu Erick sio mwanae, na ile kitendo cha kumwambia kuwa unahisi Elly ni mtoto wa Derrick ndio anapata mawazo sana, sababu kazi ya Derrick aliitambua na siku zote alikuwa akiitoa kasoro, kwahiyo lazima achanganyikiwe sana”Mama Angel alicheka sana na kusema,“Yani yule ana akili ndogo sijapata kuona, halafu yule tusipokuwa makini ataokota makopo, ingawa nahisi kuwa yule mtoto wa madam Oliva atakuwa ni mwanae”“Unadhani madam Oliva atakubali? Ni ngumu ujue”Walijadiliana ila hawakupata jibu na kufanya wapate mawazo tu ya kuendelea kuchunguza.Erica alimfata Erick chumbani kwake kwa muda huu na kuanza kuongea nae, kwanza alimpa pole kwa mizunguko,“Ila nina usingizi sana Erica”“Ni kweli una usingizi hata mimi naona ila nisipokwambia hili nitaumwa mimi”“Nini tena Erica jamani!”Erick alikuwa akiuliza huku akisinzia tu, basi Erica alitaka kumwambia ila akakumbuka kitu,“Mmmmh haya ndio yale yale, najiropokea kumbe mama ananisikiliza”Akainuka na kwenda kufunga mlango vizuri, na kurudi kitandani kwa Erick, ila bado Erick alikuwa amelala basi moja kwa moja alienda na kuosha mkono wake na kushika maji kiasi kisha alienda na kumnawisha Erick usoni na kufanya Erick ashtuke tu,“Jamani Erica kwanini lakini?”“Mimi sitaweza kulala na hili, nisikilize tafadhari”Basi Erick ilimbidi tu akae ila kiukweli alikuwa na usingizi sana ingawa aliamua kumsikiliza Erica, ambapo Erica alianza kumwambia,“Nimeota kuwa dada Vai ana mimba na anataka kuitoa hiyo mimba”“Aaaah sawa”Kisha Erick akajilaza tena, na kumfanya Erica amtingishe pale kitandani kwani alikuwa akihitaji kusikilizwa,“Erica nakuomba nisaidie jambo moja tu”“Jambo gani?”“Naomba tulale, lala tu hapa kitandani kwangu ulale na mimi kwa leo halafu nikishtuka wakati usingizi umeisha ndio uanze kuniambia yote unayohitaji kuniambia, nakuomba dada yangu, nakuomba Erica”Erick alikuwa akiongea kwa usingizi kabisa, basi Erica alikubali na kulala pembeni ya nduguye.Kulipokucha, Erick ndio alikuwa wa kwanza kuamka, basi alimuamsha Erica kwani alikumbuka kile alichokuwa akimsumbua usiku,“Erica, Erica, amka uniambie sasa”Erica aliamka na kufikisha macho, ila hakusema kitu chochote bali aliinuka gafla kama mtu aliyepatwa na kitu sio cha kawaida halafu akaondoka mule chumbani kwa Erick, kwakweli hata Erick hakumuelewa dada yake.Junior bado alikuwa na uhitaji wa kupata pesa ya kuweza kumpatia Vaileth ili aende kutoa ile mimba aliyokuwa nayo, kwavile kwa baba yake mlezi ilishindikana na kwa mama yake ilishindikana basi siku hiyo alijiandaa na kutoka shuleni halafu moja kwa moja alienda nyumbani kwa Linah.Alifika nyumbani kwa Linah na kumkuta muda huo akinywa chai,“Ooooh nilijua tu kuwa utarudi”“Naomba unisamehe”“Yani hata usijali, nilijua tu kuwa utarudi ila kipindi hiki nitakupa sheria za kuwa na mimi”“Sawa, nipo tayari kwa lolote lile. Nimepatwa matatizo na sina pa kukimbilia, nimekukumbuka wewe tu ndio msaada wangu”“Una tatizo gani”“Kuna mwanafunzi mwenzangu nilikuwa natumia simu yake, bahati mbaya njiani nikaibiwa na vibaka. Sasa mwenyewe anadai simu yake”“Khaaa ulikuwa ukiongea na nani?”“Na mama, halafu mama kakataa katakata kunikabidhi pesa nikamnunulie yule mwanafunzi simu yake”“Kwani wewe simu yako iko wapi?”“Mimi sina simu, iliharibika”“Hebu kaa chini kwanza nikupe masharti yangu”Junior alikuwa mpole kabisa akisikiliza masharti ya huyu mama,“Safari hii ukivunja masharti yangu sidhani kama tutaelewana kwakweli, yani ole wako ukiuke masharti yangu. Kwanza hakuna kutoka shule bila ruhusa yangu, ni mimi tu mwenye uwezo wa kukutoa shule na kukupeleka nitakapo, kila muda nikikupigia simu unatakiwa kupokea simu yangu haijalishi kitu chochote, ole wako nikufumanie na mwanamke, nadhani utataja jina langu la utoto. Haya, hiyo simu uliyoibiwa inauzwaje?”“Laki mbili na elfu hamsini”“Oooh tutaenda wote dukani kuinunua”Junior hakuwa na usemi kwani hakutaka kuongea sana, kuepuka swala la yeye kuonekana ni muongo. Basi siku hiyo alishinda na huyu mama kwa muda mwingi sana ila kuna simu iliingia kwa huyu mama na baada ya hii simu huyu mama akachukua pochi yake na kumkabidhi Junior laki nne kisha akamwambia,“Lete kwanza kitambulisho chako cha shule”Junior alimkabidhi yule mama kitambulisho chake halafu huyu mama akamwambia tena,“Nenda tu kanunue hiyo simu maana haitawezekana kuendelea kuwa hapa na haitawezekana kuondoka wote, ila nitakuja shuleni kwenu kukukabidhi hiki kitambulisho. Hela itakayobaki kanunue simu yako ila hakikisha unanipigia ukirudi tu shuleni”Junior aliitikia na kwa wakati huo aliondoka mahali pale, safari yake ilikuwa ni kuelekea moja kwa moja nyumbani kwa mamake mdogo yani mama Angel.Kama kawaida walijiandaa wote na kwenda kwenye Ibada, ila Vaileth alibaki nyumbani maana huwa anapata sababu kila ifikapo siku hiyo kwani alitaka pia kuwasiliana na Junior kwa siku hiyo.Walivyoondoka, ndipo alipoanza kumtafuta Junior, yani alimpigia sana simu Junior bila ya mafanikio yoyote, alijiuliza maswali mengi sana kuwa kwanini Junior anafanya vile,“Aliniahidi jana kuniletea pesa, ila jana imepita kimya, leo tena hata simu hapokei, sijui ana mpango gani na mimi! Ila Erica nae kaniambia nisitoe hii mimba, hivi mimi nitakuwa ni mgeni wa nani ikiwa wakigundua kuwa nina mimba humu ndani?”Aliwaza sana na kukosa jibu, basi alianza kujifanyia tu kazi zake ambazo zimebakia hapo na mwishoe akaenda kulala kwani alikuwa amechoka kiasi.Kwenye mida ya mchana, mama Angel na familia yake walirudi na kumkuta Vaileth pale basi alianza kuongea nae mawili matatu,“Mbona baba hajarudi?”“Aaaah kapitia kwenye biashara huko, tena nimekumbuka Vai, jioni utaenda buchani kununua maini”“Sawa mama, hakuna tatizo”“Unikumbushe basi maana mimi naweza nikasahau”Basi walikuwa wakiongea pale huku mama Angel akionekana kupiga simu zake mbali mbali na kuwasiliana na watu wake, ila bado Vaileth alikuwa na mawazo sana kuhusu junior kuwa ni kwanini hapokei simu zake halafu hajaonekana ile jana kama alivyomuahidi.Junior alifika nyumbani kwa mama Angel na kuingia ndani ambapo alimkuta na kuanza kumsalimia pale,“Kheee umeamua kurudi leo?”“Nimewakumbuka ndio, nikaona nije kuwasalimia”“Karibu, hapa ni nyumbani”“Asante mamdogo ila njaa inaniuma, Vaileth yuko wapi?”“Kuwa na adabu wewe, yule ni kama dada yako. Sema dada Vai sio kumuita Vaileth kamavile ni mtu unayelingana nae”“Samahani mamdogo sijui mimi nimezoeaje, ila hata wakina Erick huwa hawaniiti kaka Junior labda ndiomana”“Hawakuiti sababu ya tabia zako, rekebisha tabia kwanza uheshimiwe”“Sawa, dada Vai yuko wapi?”“Nimemtuma, kuna mahali ameenda, ila kama njaa inakuuma ngoja nikuitie Erica akupe chakula”Basi mama Angel alimuita Erica pale ampe Junior chakula, halafu yeye akaenda zake ndani. Wakati huo Junior nae moja kwa moja alienda chumbani kwa Vaileth na kuandika ujumbe kisha akamuachia zile hela akiwa amezifunga kwenye karatasi, akaweka kwenye droo halafu akatoka nje, moja kwa moja alienda mezani ambako ndio kuliandaliwa chakula na Erica na kuanza kula kile chakula ila alikula kwa kiasi kidogo sana, kwani kiukweli alishashiba toka kule kwa Linah alipokula.Baada ya kumaliza kula, aliinuka na kumuaga Erica kuwa anaondoka,“Kheee humsubirii dada Vai?”“Aaaah nina haraka sana, akija msalimie”Halafu Junior aliondoka zake, basi Erica alimuangalia na kujisemea,“Ndiomana watu huwa wanasema kuwa wanaume wana tabia mbaya sana, kashampa mimba mwenzie, saivi anajifanya hata hawezi kumngoja kidogo tu amsalimie jamani. Ila Mungu atamsaidia dada Vai”Kisha Erica aliendelea na mambo yake mengine.Vaileth akiwa anataka kurudi kutoka alipokuwa ametumwa na mama Angel, njiani alikutana na Sia ambaye alimsimamisha Vaileth na kuanza kuongea nae,“Unakumbuka kuna siku nilikuja pale kwenu na kukwambia kuwa inawezekana Erick akawa mtoto wangu sababu nilicheza mchezo wa kubadilisha watoto, unakumbuka?”“Nakumbuka ndio”“Basi, Erick sio mtoto wangu ndio vipimo vilivyoonyesha hivyo na wala Elly sio mtoto wangu”“Duh!! Kwahiyo vipimo vimeonyesha kuwa Elly sio mtoto wako?”“Hapana, sijapima na Elly, kutokana na haya yaliyopo, kuna uwezekano mkubwa sana wa Elly kutokuwa mtoto wangu. Tamaa imeniponza mimi, hapa nilipo najuta tu hata sijui cha kufanya kwakweli”“Aaaah pole sana”“Asante, nishauri cha kufanya basi. Namtafuta mwanangu halisi”“Unadhani hata akikufahamu atakukubali? Akija kujua kuwa ulimbadilisha sababu ya pesa atakukubali? Sijui lakini, ila ulichofanya hakikuwa sawa kabisa”“Umetoka kununua nini?”“Maini”“Aaaah ya Erick eeeh! Maana huwa anapenda sana rosti ya maini na chapati. Naomba nifate”Sia alimshika Vaileth mkono hadi kwenye banda lake na kutoka na mfuko kisha akampa Vaileth na kumwambia,“Hizo ni chapati nne, leo asubuhi zilibaki, naomba mtakapomuwekea Erick chakula usiku basi umuwekee na chapati moja kati ya hizo. Ipashe tu na uiweke. Huwa sipiki Jumapili, yani huwa sifungui biashara yangu ila leo nimefungua sio kwa kutaka bali kuna vitu vinanisumbua sana. Naomba unisaidie kwa hilo”“Kheee kwanza unamuongelea Erick yupi? Yule mdogo?”“Hapana, namuongelea baba Angel. Naomba unifanyie hivyo. Humu sijaweka dawa wala kitu chochote, hakuna kibaya nilichoweka humu, ila najua akila atanikumbuka japo kwa kiasi tu na anaweza hata kufikiria kunisaidia juu ya hili linalonitatiza, nisaidie Vaileth nakuomba”Vaileth alimuangalia sana na kumuona anatia huruma kwakweli, kwahiyo alichukua zile chapati na kurudi nazo nyumbani.Muda wa chakula cha usiku, ni kweli kabisa leo kwa mama Angel zilipikwa chapati na rosti la maini, basi Vaileth aliogopa kufanya kama alivyoagizwa na Sia badala yake zile chapati za Sia alijiwekea yeye mwenyewe kwenye sahani yake ili kama kuna madhara yoyote basi yampate yeye, ila walipokaa mezani kuanza kula, baba Angel alivuta ile sahani ya Vaileth na kumwambia aweke chapati zingine kwenye sahani nyingine maana zile atazila yeye, basi baba Angel alianza kuzila zile chapati, muda huu mama Angel alikuwa chumbani na mtoto wake mdogo akimnyonyesha maana alianza kulia muda kidogo tu baada ya wao kukaa mezani kwahiyo aliinuka na kwenda kumnyonyesha.Basi Vaileth alikuwa akimuangalia tu baba Angel akila zile chapati, ila baba Angel alishtuka kidogo na kuuliza,“Nani kapika hizi chapati?”Vaileth akajibu kwa uoga sana,“Mimi ndio nimepika”“Nani aliyekutuma ulete chapati zilizopikwa na Sia humu ndani?”Kwakweli Vaileth alitetemeka kwani hakutambua kama ingefahamika kuwa zile chapati ni za kutoka kwa Sia. Basi Vaileth alikuwa akimuangalia tu baba Angel akila zile chapati, ila baba Angel alishtuka kidogo na kuuliza,“Nani kapika hizi chapati?”Vaileth akajibu kwa uoga sana,“Mimi ndio nimepika”“Nani aliyekutuma ulete chapati zilizopikwa na Sia humu ndani?”Kwakweli Vaileth alitetemeka kwani hakutambua kama ingefahamika kuwa zile chapati ni za kutoka kwa Sia.Baba Angel aliacha kula na kuinuka zake kuelekea chumbani, basi Erica alimuangalia Vaileth na kumuuliza,“Dada, chapati za Sia kivipi?”“Sijui”“Hebu nipe nizionje”Vaileth alimsogezea ile sahani Erica, ambaye alionja kidogo na kusema,“Mbona nzuri tu”“Hata mimi nashangaa kwanini baba kazikataa”“Ila hujazipika wewe eeeh! Si ungeniambia nije nikusaidie!”Vaileth aliinama chini tu, kwani alishindwa hata kujibu, basi Erica alimsogezea na Erick zile chapati huku akimwambia,“Hebu zionje na wewe”“Hilo jina la mtengenezaji tu, limezhaniochefua unadhani naweza kuendelea kula? Ngoja na mimi niondoke zangu”Erick nae aliinuka na kuelekea chumbani, kwahiyo pale walibaki Vaileth na Erica tu ambapo Erica alimuuliza Vaileth,“Kwani dada imekuwaje? Umetoa wapi chapati za huyo Sia? Kwanza Sia ndio nani?”“Ni mama yake Elly”“Khaaa jamani, ndio nyumba nzima hawamtaki yule mama jamani, wakati huo huo huwa tunaishi na Elly hapa ndani!! Ngoja mimi nile hizi chapati na nione kama zitanidhuru”Erica na Vaileth walikula kisha kila mmoja kuelekea chumbani kwake.Erica alipokuwa yupo chumbani kwake tu, alifika kaka yake na kumwambia Erica,“Mimi nina njaa sana”“Si ukale zile chapati”“Hapana Erica, naomba ukanisongee ugali”“Kheee umenifanya kama mkeo”Halafu Erica akainuka, kwakweli Erick alimuangalia tu na kushindwa kusema chochote kile ila aliinuka tu na kwenda sebleni halafu chakula kilipoiva Erica alimuita ili aweze kula, basi Erick alienda mezani na kula ule ugali ambao ulisongwa na Erica kisha akainuka na moja kwa moja alienda tena chumbani kwa Erica ambaye kwa muda huu alikuwa akijiandaa kulala,“Asante kwa chakula Erica ila sijapenda ulivyoniambia”“Nilivyokwambia nini?”“Kuwa mimi nakufanya kama mke wangu, nitawezaje kukufanya mke wangu wakati wewe ni dada yangu?”“Kwani dada na kaka hawaoani?”“Hakuna kitu kama hiko, kwanza ni laana”“Haya yaishe, umeshiba!”“Ndio nimeshiba”“Basi nenda chumbani kwako ukalale”Kwakweli Erick alishindwa kumuelewa Erica toka asubuhi ya siku hiyo alionekana tofauti sana ukilinganisha na siku zote.Vaileth akiwa amelala na mawazo mengi sana yakitawala kichwa chake, akachukua simu yake tena na kumpigia Junior, aliona hiyo sababu ni usiku basi Junior angepokea mapema simu yake, ila haikuwa hivyo kwani simu iliita sana hadi kukatika, kwakweli alikata tamaa ila kuna ujumbe mfupi uliingia kwenye simu yake,“Vai mpenzi, najua unajiuliza kwanini nipo kimya na pengine unahisi ni makusudi au ni kitu gani, ila mimi nilikuwa nikitafuta pesa na yote haya nafanya sababu ya hiyo pesa. Angalia ndani ya droo ya kwenye kabati lako hapo, kuna karatasi nimeviringisha utaliona hapo. Ukifanikisha utaniambia, nipo sehemu mbaya kwasasa, siwezi kuongea na simu”Vaileth alijiuliza sana kuwa hiyo sehemu mbaya ni sehemu mbaya ipi wakati anajua kuwa Junior ni yupo shule, halafu shule yao wapo huru sana kiasi kwamba huwa anaongea nae kwenye usimu hasa usiku kama huo.Basi aliweka simu pembeni na kwenda kuangalia kwenye droo kweli alikuta kama Junior alivyomwambia, alihesabu ile hela na kuona Junior alimuwekea laki tatu. Akafurahi sana na kuona kuwa Junior anampenda kweli,“Aaaah, sasa nimeamini kuwa Junior ananipenda sana. Sasa sijui niendelee na wazo la mimi na Junior yani wazo la kutoa mimba au nikazane na wazo la Erica kuwa nisitoe mimba? Ngoja niangalie madhara yake kwa yote mawili ili kama madhara makubwa niyaepuke. Kwanza kabisa, wakijua kama nina mimba kuna uwezekano mkubwa wa mimi kukosa kazi, ila kuna uwezekano mkubwa wa mimi kutetewa na Erica, nikitoa mimba basi Erica atanisemea na kuna uwezekano mkubwa wa mimi kufukuzwa kazi, ila si nakataa tu kuwa sikuwa na mimba! Mmmmh sijui ipi ni njia bora kwangu!”Aliwaza kiasi na kuamua tu kulala kwa muda huo maana hakutaka kuwaza sana.Kulipokucha tu, mama Angel ilibidi akampikie chakula cha asubuhi mume wake kwani alikuja kugundua ile asubuhi kuwa hakula kile chakula walichopika usiku, na alimuona mumewe kuwa kaamka akiwa na njaa, basi alimuandalia chakula na kwenda nae mezani ili aweze kula, basi baba Angel alikaa mezani na kuanza kula kile chakula alichoandaliwa na mkewe,“Mbona usiku hukula mume wangu?”“Umejuaje kama sikula?”“Unajua nilikuangalia ule usiku tulivyokuwa tumelala nikahisi tu hukula chakula, vipi hukupenda chapati?”“Aaaah sikuzitaka kwa jana”Baba Angel hakutaka kumwambia mke wangu kuwa katambua zile chapati za jana ni za kutoka kwa Sia, kwani anajua lazima mkewe atachukia sana na kumfokea Vaileth, ingawa na yeye alitaka kujua ni kwanini Sia amempa zile chapati mdada wao wa kazi.Basi alikula pale na kuongea mambo mengine na mke wake.Kisha baba Angel alijiandaa na kuondoka zake, ambapo moja kwa moja alienda kwenye biashara ya Sia kwani alitaka kujua kwanini kafanya vile.Alimkuta Sia akiwa makini na kazi zake za pale, ila Sia alipomuona baba Angel aliacha kazi zake na kumfata kuongea nae,“Wewe kwanini umeweka chapati zako kwangu?”“Ooooh nashukuru sana, kwani umezila na kugundua kuwa zimetoka kwangu”“Mjinga wewe, umenilaza na njaa jana. Sikutaka tu kumwambia ukweli mke wangu maana angemgombeza bure yule msichana wa kazi”“Kwanza naomba unisamehe, sikuwa na nia mbaya ila nilijua ukizila zile chapati basi utanikumbuka na kuja kama hivi kuongea nami. Unadhani naweza kukuwekea dawa kwenye chapati? Hapana, ila nilitaka tu unikumbuke na uje kuniona kama hivi. Unajua sikutaka kufika nyumbani kwako ndiomana nimefanya hivi”“Haya ulikuwa na shida gani?”Sia akamsogeza pembeni zaidi baba Angel na kuanza kuongea nae,“Ni hivi, unajua mimi nipo kama nimechanganyikiwa hivi najiona kabisa siku hizi nipo kama kichaa, kuna siku nilishinda Kanisani ila nilipotoka nilikuwa naongea peke yangu, nikashikwa bega na kuropoka kila kitu kumbe nimeongea mbele ya Elly, kiukweli Elly hanielewi kabisa ndiomana hata hajaondoka tena nyumbani, anahisi mama yake nina matatizo. Yani akili yangu imeharibika kweli, na ninakubali kuwa nina matatizo kweli, ila jana wakati nimetoka kununua bidhaa za kupika, nilipita mahali na kumuona dokta aliyenibadilishia mtoto”Hapo ndio baba Angel akashtuka kidogo na kumuuliza,“Dokta gani?”“Ni dokta Jimmy maana ndio alihusika na kunibadilishia mimi, alilipwa pia na mzee Jimmy. Ila ni kwavile sikuwa na usafiri na wala hela ya kumfatilia, sababu nilikuwa nishanunua bidhaa ila nisingenunua bidhaa ningemfatilia ili aniambie ukweli kuwa mwanangu yuko wapi”“Kumbe dokta Jimmy ndio alifanya mchezo huo?”“Ndio, tena yeye ndio alikuwa akinihakikishia kuwa mtoto tumebadilisha na mtoto wa Erica, kiukweli nimemlea Elly sijawahi kumlea vibaya hata mara moja, sina pesa ndio ila sijawahi kumlea vibaya Elly”“Asante kwa ujumbe huo, maana nina muhitaji sana huyo dokta, nikimpata nitafurahi kwakweli. Nahitaji kuongea nae, haya jambo lingine ulilotaka kuniambia?”“Nilitaka kukuona tu, ili niridhike na moyo wangu, hivi kweli Erick ungekuwa bega kwa bega na mimi kipindi kile haya yote yangetokea? Nina uhakika kusingekuwa na kitu kama hiki”Baba Angel alimuaga pale na kuondoka zake, ila ujumbe kuwa dokta Jimmy yupo, aliupenda kwani aliona itakuwa ni rahisi zaidi kumfatilia dokta huyo.Mama Angel akiwa yupo nyumbani kwake, alikuwa akijiandaa kwa muda huo na yeye aweze kutoka ila alifika pale Elly na kufanya aongee nae, Elly alimsalimia pale mama Angel na kuanza kuongea nae,“Hujaenda shule leo Elly?”“Sina raha ya kuwa shule kabisa, sina amani wala sina furaha”“Tatizo ni nini kwani Elly?”“Nimekaa na kutafakari siku zote hizi ila sina raha, nilimsikia wazi mama akiongea kuwa mimi sio mtoto wake. Roho inaniuma, inamaana aliniokota au kitu gani? Je wazazi wangu wako wapi? Na yule uliyenipeleka anayesema yeye ni baba yangu ni nani? Nimechanganyikiwa nahitaji kujua”Mama Angel akapumua kidogo, basi alimwambia Elly amsubirie pale sebleni halafu yeye alienda chumbani moja kwa moja kumpigia simu madam Oliva kwani alitaka amkutanishe na Elly halafu aone itakuwaje maana alikuwa akiamini damu ni nzito. Alimpigia na kuanza kuongea nae,“Madam Oliva, upo wapi leo?”“Nilikuwa shuleni, ila muda sio mrefu nitakuwa kwenye saluni yangu”“Aaaah basi nakuja huko kwenye saluni yako”Basi mama Angel alikata ile simu na moja kwa moja alienda kuongea na Elly pale na kumtaka waende mahali, basi Elly alikubali yani kwa kipindi hiko hata shule alikuwa akiiona chungu yani hadi mama Angel alikuwa akimuhurumia sana.Basi walifika mpaka kwenye saluni ya madam Oliva ambapo naye ndio alikuwa anafika, basi mama Angel alimsogeza Elly pale kwa madam Oliva na kumtambulisha,“Huyu anaitwa Elly ni mtoto wa ndugu yangu”“Ooooh sawa, nashukuru kumfahamu”Kisha mama Angel akamwambia Elly akamsubiri kwenye gari yake ambapo Elly alifanya hivyo, halafu mama Angel alianza kuongea na madam Oliva sasa,“Unapomuona huyu Elly unahisi anafanana na nani?”“Mmmmh nimemfananisha na Derrick ujue, yani kafanana na Derrick kweli tena!!”Mama Angel akapumua kidogo na kusema,“Hujakosea, ni kweli yule Elly ni mtoto wa Derrick”“Aaaah ndio mtoto aliyezaa na Manka eeeh!! Au alizaa na mwanamke mwingine tena?”Mama Angel alikaa kimya kwa muda kwani alikuwa akitafuta la kuongea pale, kisha akamwambia kitu,“Unajua nini, ile hospitali ambayo wewe ulijifungua ndio hospitali niliyojifungua mimi”“Halafu nasikia imefungwa eti, ila sijui kwasababu gani?”“Baba Angel alienda pale, na kuambiwa kuwa ile hospitali imefungwa sababu kuna watu hao wanadai kuwa walibadilishiwa watoto pale hospitali, kwahiyo wanahitaji kufahamu watoto wao halisi, halafu yule daktari kashindwa kuwaonyesha watoto halisi wa wale watu, halafu sijui kuna skendo zipi zingine zimefanya ile hospitali kufungwa”“Mmmmmh mbona unanitisha? Ile hospitali walikuwa wanabadilisha watoto?”“Ndio, nilivyosikia hivyo”“Hivi kweli nije kusikia kuwa Paul wangu sio mtoto wangu wa kumzaa jamani? Wanaume ndio wanasingiziwaga watoto, kumbe na wanawake tunabadilishiwa watoto! Ila haiwezekani, Paul ni mwanangu”“Sijakwambia Paul sio mwanao ila ile hospitali inatakiwa kufanya uchunguzi wa hali ya juu, wote tuliozalia pale inatakiwa tujitathimini”“Kwani wewe huwa unahisi watoto wako sio wako?”“Mmmmh hapana, wale ni watoto wangu”“Sasa tuchunguze nini? Mimi hata naogopa kuchunguza. Nipate habari kuwa Paul sio mwanangu, hapana kwakweli sitaweza kuifanyia kazi hiyo habari. Nampenda sana mwanangu”Mama Angel akapumua tena kidogo, ila hakutaka kuongea zaidi, basi alimuaga na kudai kuwa alienda pale kumsalimia tu.Aliondoka moja kwa moja kwenda kwenye gari lake na pale alimkuta Elly amekaa tu huku kajiinamia, basi akaondoka nae mahali hapo na moja kwa moja alienda nae kwa Derrick kwani alijua ni wazi kule Elly ataweza kujihisi vizuri, ila kitu ambacho hakuelewa ni kwanini hata madam Oliva hajaonyesha tofauti yoyote ya kutamani hata kuwa karibu na Elly.Basi walifika nyumbani kwakina Derrick, kwakweli siku hizi Derrick alikuwa kabadilika sana, kwani muda wote utamkuta akijishughulisha tu na kazi mbalimbali, alifurahi sana kuona mama Angel kampelekea tena mwanae, basi akamuomba jambo moja mama Angel,“Naomba leo uniache na huyu kijana, naomba uniache nae niongee nae halafu kuna kitu nitakwambia”“Hakuna tatizo, ngoja nimuulize Elly mwenyewe kama yupo tayari”Mama Angel alimuuliza Elly, kiukweli Elly alikuwa akihitaji mtu wa kuongea nae kwa ukaribu zaidi kwahiyo alikubali kwa haraka sana kukaa hapo na kushinda na Derrick. Basi mama Angel akampatia tu pesa kidogo Elly kuwa akihitaji kurudi basi atakuwa na nauli kabisa, kisha mama Angel aliondoka zake na kurudi nyumbani kwake kwa muda huo.Mama Angel kabla hajarudi nyumbani kwake, aliamua kwanza kupitia ofisini kwake maana hakwenda kwa siku kadhaa kidogo, basi alipitia na kuangalia mambo ya pale yanaendaje kisha alipomaliza aliamua kuondoka zake, ila wakati anatoka ofisini kwake tu, alikutana na rafiki yake Dora na kuanza kusalimiana nae ambapo waliingia tena ofisini na kuongea mawili matatu,“Kheee siku hizi hushikiki ndugu yangu yani hupatikani kabisa”“Jamani mbona nipo ndugu yangu”“Sasa ndugu yangu, kuna siku nimemuona binti mmoja uwiiii umefanana nae jamani, kweli duniani wawili wawili”Mama Angel alicheka na kuuliza,“Nani huyo?”“Sijui anaitwa nani, ila yote tisa kumi jana nimemuona tena yule mwanamke wa kuitwa Manka, yani yule anajidai na mali za mzee Jimmy ujue”“Mmmh!!”“Ndio hivyo, mzee Jimmy mpuuzi alimpenda sana yule mwanamke sijui alimpendea nini ila nahisi kuna mambo ambayo mzee Jimmy alikuwa akiyafanya halafu yule mwanamke anayafahamu vizuri. Hivi unamfahamu kwanza huyo Manka?”“Mmmmh simfahamu, ndio kwanza nilikusikia wewe”Mama Angel aliamua kujibalaguza,“Ni hivi, ni mweupe peee peee, yani ule weupe umefanya awe mzuri sana. Kwakweli Manka ni mzuri ila bado mimi ni mzuri zaidi”Dora alicheka na mama Angel alicheka pia, kisha Dora aliendelea kuongea,“Kuna gari nimemuona analiendesha, kwakweli yule mwanamke kachukua mali nyingi sana za mzee Jimmy. Ila nadhani Manka alikuwa haelewi akili za mzee Jimmy zilivyo, yule mzee hawezi kukufanyia kitu ambacho badae hutokuja kukijutia, yani lazima anakufanyia mazuri halafu na majuto anakuandalia”“Mmmh kama yapi? Sasa majuto gani atampa huyo Manka? Ukiangalia mzee Jimmy alishakufa, na kama mali kashampa huyo Manka!”“Nakwambia hivi, mzee Jimmy ni baba mkwe wako ila hufahamu vitu vingi sana vya yule mzee. Kwanza lile zee ndio lilinipa mimi ukimwi halafu anasingizia mimi ndio nilimpa ukimwi, mzee ana mipango yule. Amekufa ndio ila aliowaacha huku nyuma sijui tu, ila yule Manka atakuwa anajua vizuri sana maana alikuwa karibu sana na mzee Jimmy”“Itabidi tumfatilie huyo Manka vizuri ili tujue mambo ya mzee Jimmy, usikute kuna mengi nyuma ya pazia”Mama Angel aliongea na Dora pale, hadi waliagana na kuondoka, ambapo mama Angel alimpeleka Dora hadi mahali karibu na kwake halafu yeye akaondoka zake, yani mama Angel kuna jambo jipya liliingia kwenye akili yake kuwa mama Sarah anafahamu vitu vingi sana vya mzee Jimmy ila hakujua kama mwanamke huyu anaweza kukaa chini na kuwaambia chochote kile.Erica aliporudi kutoka shuleni leo, moja kwa moja alienda kumsaidia kazi mbalimbali za mule ndani kwao Vaileth huku akimuuliza,“Ila dada kwanini jana ukaenda kuchukua chapati kwa yule mwanamke jamani! Si ungesema nikusaidie kupika?”“Ila zingine nilipika”“Humu ndani unajua watu wake vizirani, baba kagoma, Erick nae akagoma hadi kuja kuniambia nikamsongee ugali”“Ila upo vizuri sana Erica, una roho nzuri sana wewe mtoto”Kuna mgeni walisikia amefika pale kwao wakiwa jikoni, basi Erica alitoka na kwenda kumsikiliza huyo mgeni, akakuta ni Rahim yani baba yake Samia, basi alimsalimia na kumsahngaa,“Kheee mbona umekuja kwetu?”“Kwani vibaya mimi kuja kwenu?”“Hapana”“Nimekuja kumuulizia Samia, amefika huku”Erica alishangaa kwa yule baba kumuulizia Samia kwa muda ule wakati Samia anamsimuliaga mambo yote ya yule baba, kwahiyo Erica alibaki akimuangalia kwa muda tu, mara mama Angel nae alitoka ndani, kwakweli mama Angel alipomuona Rahim pale kwanza hakupenda pili alishtuka kiasi na kumtaka Erica akaendelee na kazi zingine kisha alitoka nje na Rahim,“Umefata nini nyumbani kwangu?”“Nimekuja kumuulizia binti yangu Samia”“Khaaa jamani, lini Samia wako kaja huku kwa muda huu! Hebu nenda kamfatilia huko, halafu giza linakaribia kuingia”“Kiukweli sio Samia aliyenileta hapa, ila nilitaka tu kukuona”“Unajua wewe una wazimu eeeh!! Akili zako kuna muda zinaenda na kurudi. Jichunguze. Kwaheri”Mama Angel alitaka kurudi ndani ila Rahim alimvuta, na wakati huu alimvuta karibu na kumkumbatia, baba Angel alikuwa nae ameingia na alichukia sana akasogea pale na kumsukuma Rahim chini, kumbe muda ule Erica alikuwa akichungulia dirishani kwahiyo alikuwa akiona kinachoendelea.Rahim aliinuka pale chini na kutikisa kihwa tu halafu akamwambia baba Angel,“Dawa yako inachemka sijui sura yako utaificha wapi? Siku zote mwanaume wa kwanza kuzaa na huyo mwanamke basi huyo ndio mumewe, nakuhurumia sana kuchukua mizigo usiyoijua”Baba Angel alichukia sana na kutaka kumfata Rahim ila mke wake alimshika na kumsihi waende ndani, wakati huo Rahim alisogea getini na kutoka nje na kuondoka kabisa.Mama Angel aliingia na mumewe ndani hadi chumbani ili kumshusha zile hasira,“Hizi huyu Rahim ananitakia nini mimi na familia yangu?”“Naomba uachane nae tu mume wangu, asituumize kichwa huyu kabisa, tuwaze mambo mengine tu”“Eti mtu wa kwanza kuzaa na huyo mwanamke ndio mumewe, kwahiyo yeye ni mume wa wanawake wangapi maana wengi kawazalisha, akili mbovu kabisa yule mtu jamani!! Sijui kama kuna siku ugomvi wangu na ugomvi wa Rahim utakuja kuisha”“Naamini mambo yataisha haya na kila kitu kitakuwa sawa”Mama Angel alijitahidi pale kushusha hasira za mume wake kwani alionekana kuchukia sana kwa muda huo.Mama Angel alihitaji kujua kuwa Erica alikuwa akiongea nini mwanzoni na Rahim, basi alimfata Erica chumbani kwake, na kumkuta kajiinamia tu basi akamfata na kumuuliza,“Tatizo nini mwanangu, mbona umejiinamia tu?”Kabla ya kujibu, Erica alimuuliza swali mama yake,“Mama, hivi Erick kachukua hasira za baba eeeh!”“Kwanini umeniuliza hivyo?”“Kuna siku tulikuwa njiani na Erick ila aliwasikia wamama Fulani wakitusema vibaya, basi Erick alienda kumpiga ngumi moja mama yule, halafu hataki kuondoka yani anataka kupambana nao wote, kuna siku nyingine kwa mama Sarah, wakati mama Sarah akimsema vibaya, uwiii Erick alitaka kumpiga ngumi mama Sarah hadi nikamzuia. Nimemuona baba leo akimsukuma baba Samia kwa hasira, kumbe hasira za Erick ni za baba?”“Eeeh ndio, kafata hasira za baba yako. Ila na wewe Erica ni mbea jamani, kuchungulia nje ndio nini? Yani mtoto mbea wewe sijapata kuona”“Ila mama, kwani umbea huu nimerithi wapi?”“Sijui wewe na Mungu wako maana kwetu wala kwa baba yenu hakuna wambea kama wewe”“Mmmh mama au mimi sio mtoto wenu?”Erica alisema hivyo huku akiinama chini inaonekana ni kitu kilichoanza kumsumbua akili, basi mama yake alimuangalia vizuri na kuanza kuhisi kuwa labda zile mada za kubadilisha watoto basi moja kwa moja zimemfikia Erica, ukizingatia ni mbea sana, basi mama Angel akamuuliza Erica,“Kwanini umesema hivyo?”“Sijui mama, sijui ila kama sijarithi tabia zenu huenda mimi sio mtoto wenu”“Erica, najua ni umbea wako ndio umepelekea kuanza kusema hayo. Najua huwa unasikia mimi na baba yako tukizungumzia kuhusu watoto waliobadilishwa hospitali, ila hii haihusiani kabisa na nyie watoto wangu. Kwani wewe unajiona ni tofauti?”“Sijui mama, ila Erick kafanana na baba hasira, ila mimi umbea nimefanana na nani?”“Sikia Erica, sio kila kitu utafanana na wazazi. Hebu fikiria ni watu wangapi wakikuona wanasema kuwa wewe ni mwanangu! Hata ambao hawajui kuwa mama yako ni mimi ila watakwambia wazi kuwa mama yako ni Erica eeeh! Sababu mimi na wewe tumefanana, na tumefanana vitu vingi sana, mfano kwenye kupika unafikiri umerithi kwanani kupenda kupika? Umerithi kwangu, huo umbea umerithi kwa mjomba wako mmoja hivi ni mbea sana, kuna siku nitakuonyesha pacha wako Erica”Kisha mama Angel akasogea na kumkumbatia mwanae, akajua zile habari ambazo huwa anaongea na mumewe basi zimefika kwa mbea wake mashuhuri wa mule ndani, basi aliongea nae kidogo tu, mwisho wa siku hata hakumuuliza kuhusu alichokuwa akiongea na Rahim zaidi ya kumuaga tu usiku mwema na kuachana nae.Mama Angel aliporudi chumbani kwa mumewe, aliamua kumueleza kile alichozungumza na Dora siku hiyo kuhusu Manka,“Inamaana Manka atakuwa anafahamu vitu vingi sana vya baba yangu?”“Ndio, yani hapo ni wazi kabisa kuwa Manka anafahamu vitu vingi sana kuhusu mzee Jimmy”“Sasa tutawezaje kupata ukweli toka kwa Manka?”“Hapo ndio pagumu ila kama tukiamua basi tutaweza tu kugundua ukweli wa mambo ulivyo”Basi baba Angel alimgusia pia na swala la Sia kumuona dokta Jimmy,“Ila yule Sia ni chizi sema tukimtumia kwa hili tutaweza kufanikiwa, yani kama tukimwambia Sia afatilie kuhusu dokta Jimmy anaweza yule na uchizi wake”“Ni kweli, ila kesho nitaenda tena pale hospitali kuna kitu nimefikiria”Baba Angel aliongea na mke wake kuhusu mipango yake na kwa muda huo waliamua tu kulala.Kulipokucha baba Angel alijiandaa na kuondoka ile asubuhi na mapema kabisa maana alisema atapitia kwanza ofisini kwake halafu ndio ataenda kwenye ile hospitali kufatilia.Mama Angel akiwa nyumbani kwake kwa muda huo, alitembelewa na wifi yake Tumaini basi alisalimiana nae na kuanza kuongea nae pale,“Nikwambia mambo yaliyopo nyumbani kwa mama Sarah”“Mambo gani tena?”“Yule Sarah si ndio tulihangaika nae kipindi kile kwa kuchoma sindano ya uzazi wa mpango wakati ni mjamzito hadi mimba ikatoka”“Ndio, ila kwasasa anaendelea vizuri”“Ndio, ila yule mdada wao wa kazi nae kaenda kuchoma sindano ya uzazi wa mpango wakati ana mimba basi imemsumbua alilazwa na mimba imetoka”Mama Angel alikumbuka mambo ambayo Elly alimwambia, basi moja kwa moja alipata jibu hapo kuwa Elly ndio muhusika wa ile mimba ya huyo dada wa Sarah pia. Ila alibaki kushangaa tu,“Nani aliyewaambia kuwa kutoa mimba ji kuchoma sindano ya uzazi wa mpango? Wajinga hao watakufa wanajiona, huyo mdada mtu mzima nae anafanya mambo kama mtoto”“Ndio hapo sasa, yani hata hajaona shida wala nini. Watoto wa siku hizi jamani, hapana kwakweli, haya yote tisa kumi ni mdada wangu wa kazi”“Kafanyaje tena?”Muda huu Vaileth alikuwa akimletea glasi ya juisi huyu shangazi yao wakina Erica, basi Tumaini alikuwa akimwambia mama Angel,“Msichana wangu wa kazi ana mimba”Vaileth aliangusha glasi na kufanya ile glasi ivunjike, basi wakamshangaa pale na Tumaini ndio akaanza kuongea pale,“Wewe vipi, inaonyesha hii habari imekushtua au na wewe una mimba?”Vaileth alikuwa kimya tu kama akimshangaa Tumaini, halafu Tumaini akasema,“Itakuwa una mimba wewe, usije ukatuletea mambo ya Daima hapa kuwa mimba ya Junior!”Yani Vaileth alijihisi kupatwa na baridi gafla kwenye mwili wake na kuanza kutetemeka. Vaileth aliangusha glasi na kufanya ile glasi ivunjike, basi wakamshangaa pale na Tumaini ndio akaanza kuongea pale,“Wewe vipi, inaonyesha hii habari imekushtua au na wewe una mimba?”Vaileth alikuwa kimya tu kama akimshangaa Tumaini, halafu Tumaini akasema,“Itakuwa una mimba wewe, usije ukatuletea mambo ya Daima hapa kuwa mimba ya Junior!”Yani Vaileth alijihisi kupatwa na baridi gafla kwenye mwili wake na kuanza kutetemeka.Mama Angel nae alimuangalia kwa makini Vaileth na kumuuliza,“Una nini wewe? Una mimba kweli au?”Vaileth akajibu kwa uoga,“Hapana mama, sina mimba”“Mbona hii mada inaonekana imekugusa sana”“Nisamehe mama”Kisha Vaileth akaenda kuleta tambara na kufuta pale alipoangusha glasi, basi Tumaini akamwambia mama Angel,“Atakumalizia glasi zako huyu, kama ana mimba ondoa haraka asikuletee usiku”“Na hiyo mimba anaitoa wapi?”“Jamani, kwani mimba inatoka wapi? Si inatoka kwa wanaume”“Unajua najiuliza hao wanaume Vai atakutana nao muda gani?”“Wewe hujamuwekea gunzi huyu, unavyomtuma sokoni? Ukiwa haupo unadhani inakuwaje? Jitahidi ukampime mimba”“Kwahiyo niende nae hospitali eeeh!!”“Njoo na kile kikopo cha kupimia mwambie aweke mkojo wake, halafu uende ukapime. Asituletee ujinga sisi”“Umenitisha, basi itabidi tufanye muda huu huu”“Ndio, hawa wadada wa kazi wana siri nyingi sana. Halafu mwishowe anakuletea mabaa na mimba zao, yani ukigundua ana mimba ni nyumbani kwao moja kwa moja hakuna kumchekea wala nini. Usifanye masikhara na kulea mwanamke mjamzito”“Naelewa, ila sidhani kama Vaileth anaweza kuwa na mimba”“Usimkatalie wala nini, hawaaminiki hawa viumbe ujue”“Sasa tufanyeje?”“Ni kuchukua hatua muda huu huu, huyu msichana akapimwe mimba”“Ila hiko kikopo cha kuchukua mkojo na kwenda nao hospitali nitakipata wapi?”“Ngoja kwanza”Tumaini alianza kupekua mkoba wake na kutoa kikopo ambacho huwa kinatumiwa hospitali kupima haja ndogo,“Chukua hiki hapa, nenda kampe aweke mkojo wake humu asitutanie kabisa. Tena tutaenda wote huko hospitali kupima”Basi mama Angel alichukua kile kikopo na kumpelekea Vaileth ili aweke haja ndogo mule.Wakati Tumaini yupo sebleni, muda kidogo alirudi Erica kutoka shule na kumsalimia pale,“Mbona mapema leo?”“Naumwa tumbo shangazi”“Wewe nawe sijui una chango jamani, kukua ndio kuumwa kila leo ukiona mambo jamani!!”Mama Angel alitoka nae alimkuta Erica pale akilalamika kuhusu kuumwa na tumbo,“Oooh ndiomana umewahi kurudi mwanangu, halafu si kuna zile dawa ulipewa wewe!! Hilo tumbo limekuanza tena! Pole mwanangu, nenda kapumzike kwanza halagfu nikupashie maji moto nije nikukande kidogo mwanangu”“Asante mama”Basi Erica aliondoka na kuwaacha wakiendelea na mazungumzo mengine.Moja kwa moja Erica alienda chumbani kwa Vaileth na kuikingia ila akamkuta Vaileth kajiinamia tu, akilia, kwakweli huruma ilimjaa kwani hakupenda kumuona akilia haswaa kutokana na ile hali ya ujauzito aliyokuwa nayo, alimshika bega na kumwambia,“Nini shida dada Vai?”“Nimeambiwa nitoe mkojo ili wakanipime mimba, naogopa mimi maana ikigundulika ndio kazi sina tena”“Lete hicho kikopo”Halafu Erica alienda nacho chooni na kuweka haja ndogo yake halafu akampelekea vaileth kile kikopo halafu yeye alirudi chumbani kwake, kwakweli Vaileth hakuamini kile kitu aliona kama ni muujiza hivi.Muda kidogo alifika mama Angel akidai ule mkojo ambapo Vaileth alimpatia halafu mama Angel alitoka nao kwenda sebleni ila Vaileth hakuwa na hofu yoyote tena maana kilichotendeka alikielewa vizuri sana.Mama Angel alipokuwa sebleni anamwambia wifi yake,“Mkojo huu hapa, ila sasa nitaondokaje na kumuacha huyu mtoto anayeumwa? Sijui wifi utaniendea”“Hakuna tatizo, naenda tu hapo duka la madawa kupima”Basi muda huo huo Tumaini aliondoka na kile kikopo ili wajue kama Vaileth ana mimba kweli au la.Basi mama Angel alibaki pale na kumuita Vaileth na kuanza kuongea nae,“Hebu Vaileth niambie ukweli, una mimba kweli?”“Hapana mama sina mimba”“Usiniaibishe Vai, unajua nimempa wifi yangu akapime huku nina mashaka sana moyoni. Naomba iwe kweli maana hii aibu siitaki kwakweli”“Kweli mama, sina mimba”“Haya, kaendelee na kazi zako zingine”Basi mama Angel alienda chumbani ila akapigiwa simu na Derrick muda huo huo, akapokea na kuanza kuongea ne,“Ndio Derrick, ni nini tena?”“Kuna kitu nimegundua kuhusu huyu Elly”“Mmmh kitu gani hiko?”“Huyu Elly ni mtoto wangu tena ni mwanangu kabisa, ila kila nikijaribu kumuangalia naona haendani kabisa na Oliva, sijui labda kuna mwanamke mwingine nilizaa nae, si unajua ujana tena. Kwahiyo huyo Sia anasema mamake Elly ni nani?”“Mmmh huyo Sia hata hajui kwakweli, basi wewe hebu jaribu kupitia wanawake wote ambao uliwahi kuwa nao na pengine mmoja wapo ndio atakuwa mama wa Elly”“Inawezekana, ila huyu ni mwanangu nina uhakika asilimia moja. Na mlivyosema hana baba basi ndio nimepata jibu wazi kuwa huyu ni mwanangu. Piga ua galagaza ila huyu ni mwanangu kabisa”Mama Angel alikuwa akicheka tu ila akasema,“Kama sio wa Oliva atakuwa wa nani maana kuna uhakika wa asilimia zote kuwa mtoto anayelelewa na Oliva ni mtoto wa Sia ila tu hatujamwambia kwani uchizi wake tunaujua na hatujui ni kitu gani kitatokea, kwahiyo Elly yuko wapi?”“Kaondoka jana jioni kwenda kwa huyo mama yake Sia”“Ila hujamwambia chochote kama Sia sio mama yake?”“Hapana sijamwambia, ila tu nazidi kumsisitiza kuwa mimi ni baba yake ili asinichukie wala nini”“Basi tutaongea vizuri, ila jaribu kuweka macho karibu kwa huyo mtoto ili uweze kugundua mama wa huyo mtoto ni nani”“Nitafanya hivyo”“Loh na wewe Derrick ulizidi jamani, hebu ona unavyohangaika! Yani wewe loh!”Basi waliongea pale na kukata ile simu ambapo mama Angel aliamua kuendelea na mambo mengine tu.Ila mama Angel alipigiwa simu na wifi yake na kwenda kuonana nae mahali kuhusu majibu ya Vaileth.Baba Angel alipotoka kwenye kazi zake, moja kwa moja anaongoza kwenye ile hospitali ili ajaribu kuchunguza zaidi, basi alifika na kuanza kuongea na walinzi,“Jamani, mimi nina shida sana na huyu dokta Jimmy, mnavyoniambia hamna mawasiliano yake mnazidi kuniachangaya”“Ni kweli hatuna mawasiliano yake kabisa”Mara baba Angel alishangaa mahali pale akifika madam Oliva, basi alianza kusalimiana nae pale na kuulizana kwa mshangao kuwa wote wanafanya nini pale, basi madam Oliva alianza kujieleza,“Mimi nina shida na dokta Jimmy kwakweli, nahitaji aniambie ukweli tu kuhusu mtoto wangu, je mtoto aliyenipa ni wangu au sio wangu? Kila siku nazidi kupatwa na mawazo tu juu mambo ambayo huwa naongea na mkeo. Na wewe je umekuja kufanya nini?”“Dah!! Mimi ni mambo mengi, unajua mke wangu nae alijifungulia hapa, nataka tu kujua ni kitu gani aliwafanya wanangu wakati wadogo, sababu nasikia kuna sindano aliwachoma”“Kheee huyu dokta, kumbe ana makubwa kiasi hiko. Haya tutampataje sasa?”Baba Angel na madam Oliva walijadiliana kwa muda kidogo na kisha madam Oliva akasema kitu,“Nina uhakika kwa asilimia kubwa hawa walinzi watakuwa wanajua huyu dokta alipoa”“Wanasema hawajui”Madam Oliva aliwauliza pia, na walimjibu vile vile ambavyo walimjibu baba Angel, basi madam Oliva akawaambia,“Sikieni, ni nani aliyewaajiri kulinda hapa na ni nani anayewalipa mishahara yenu?”“Mdogo wake dokta Jimmy”“Ni nani huyo?”Wale walinzi walitoa zile namba za mdogo wake dokta Jimmy na kuwaambia kuwa wamtafute huyo ndio atawajulisha, kwa muda huo walimpigia simu ila iliita sana hadi ilikatika, basi wakapanga kumpigia tena kwa muda mwingine, kisha baba Angel na madam Oliva waliagana na kila mmoja kuondoka zake.Kwakweli baba Angel alikuwa na mawazo sana, hivyobasi moja kwa moja alienda nyumbani kwake, na alipofika hakumkuta mke wake maana alikuwa kwa muda huo ametoka.Akaagiza chakula tu, ambapo Vaileth alimuwekea chakula na alijitahidi na kula kile chakula huku akijiuliza baadhi ya vitu kwenye kichwa chake.Baba Angel aliamua kwenda kujilaza kwa muda huo, ila muda kidogo mkewe alirudi na kuanza kuongea nae,“Ulienda kwenye kazi leo?”“Haoana, ila Tumaini alikuja hapa”Basi mama Angel alianza kumueleza mumewe kuhusu hofu ya Tumaini ya kusema kuwa Vaileth ni mjamzito,“Ila yale majibu aliyoniitia ni kwamba Vai hana mimba, nimeshukuru sana kwakweli. Maana sipati picha ambavyo Tumaini angenisema”“Oooh dada yangu nae muda mwingine, anajijuaga mwenyewe”“Haya yote tisa, kumi ni kuwa kule aliponiita Tumaini kuna jambo jipya nimeedna kukutana nalo”“Jambo gani hilo?”“Unamkumbuka Moses? Yule Moses aliyekuwa akiuza duka lako kipindi kile? Yule Moses ambaye mimi nilijua ndio mmliki halali wa lile duka lako mpaka akampenda Angel na kufanya Angel awe balozi wa duka lako unamkumbuka?”“Namkumbuka ndio, alikuwa ni muaminifu sana yule mtu”“Unajua yuko wapi siku hizi?”“Hilo sijui maana sijawasiliana nae siku nyingi sana toka kipindi kile alivyoondoka wala sijawasiliana nae tena”“Jamani, leo nimemuona. Moses kawa Moses kweli, kwanza kanenepa sana, nimumuona kwenye gari nzuri ya gharama anatembelea, inaonyesha Moses ana maisha mazuri sana kwasasa, sikuweza kuongea nae maana anaonekana alikuwa na haraka, kabadilika hatari”“Yeye alikuona?”“Hapana, yani alikuwa na haraka huyo. Jamani Moses kabadilika, na nisingemkumbuka bila Tumaini kunikumbusha jamani, Moses kawa Moses kweli. Ana mali nyingi, pesa nyingi. Gari aliyokuwa nayo ni zile gari nzuri za gharama”“Kama ya pesa ngapi?”“Mmmh ile gari kama milioni mia tano”“Duh!! Kweli huyo katoka kimaisha, kapata wapi hela yote hiyo?”“Duniani kuna mambo unajua vitu vingine sio vizuri kuviwaza ila mtu unaviwaza na kuona mmmh kuna kitu katikati. Hebu fikiria jambo Fulani, lile duka lako ni Moses ndio alikuwa amelishikilia vilivyo yani hakuna kilichokuwa kinafanyika bila yeye. Halafu kumbuka kuwa lile duka ulilifunga na kuacha biashara ile baada ya Moses kuondoka pale, hapo akili kichwani mwako”“Si unajua tuliibiwa pale”“Mmmmh mume wangu, ukifikiria zaidi utayaona mambo ya Derrick ujue kwenye hili!!”Baba Angel aliwaza kiasi na kuona ataumia kichwa zaidi, basi alibadili mada na kuanza kuongea mengine na mke wake.Basi Vaileth akiwa anamalizia zile kazi za Usiku, alifika mama Angel na kumwambia kuhusu majibu ya ile mimba yake,“Kwanza Vai, nakushukuru kwa kuwa msichana bora kwangu. Yani nilijua kweli u mjamzito, oooh nimefurahi sana Vaileth”“Nashukuru kwa kuniamini mama”Basi mama Angel alimuaga Vaileth na kuondoka zake, ambapo moja kwa moja Vaileth alienda chumbani kwa Erica ili akamshukuru kwa kile alichomfanyia, ila alipofika kabla hajaingia alikuta mlango wa Erica haujafungwa vizuri basi alisimama na kuangalia kinachotendeka, ambapo alimuona Erick akimpa huduma Erica yani alikuwa akimkanda tumbo lile lililokuwa linamuuma, basi Vaileth aliangalia sana na kujisemea,“Hawa watoto mbona wana mambo ya ajabu sana, mapacha gani hawa wanafanya hivi. Yani kama wapenzi vile mmmh!!”Aliendelea kuwaangalia ila mwishowe aligonga na kukaribishwa ndani, aliingia na kuwasalimia pale huku akisema anataka kuongea na Erica,“Unataka kuniambia nini kwani? Niambie tu”“Nataka niongee na wewe peke yako”Erica alicheka kidogo na kusema,“Unamuogopa Erick? Unamuogopa bure tu maana hata ukiniambia peke yangu basi nitaenda kumwambia tu”Erica alicheka tena, yani inamaana kuwa umbea wake alishaukubali kwa asilimia zote, ni kweli Vaileth aliona hata akimwambia Erica peke yake basi ile habari lazima moja kwa moja itafika kwa Erick, basi alimwambia,“Asante sana kw akuniokoa siku ya leo”“Usinishukuru mimi, mshukuru Mungu aliyenirudisha nyumbani kwani aliniotesha kuwa leo siri itabumbuluka ndiomana nilivyofika tu nilianza kuja chumbani kwako”Vaileth alimuangalia Erick na Erica kwa aibu ila bado aliendelea kumshukuru Erica kisha Erica akamwambia,“Ninachotaka ni huyo mtoto azaliwe, halafu sisi tutalea. Si mtoto wa ndugu yetu, kwahiyo ni damu yetu. Si eti Erick tutalea eeeh!”“Ndio tutalea”Vaileth aliwashukuru tu pale kwa aibu na kuondoka zake maana alihisi kuaibika sana kwa wakati huo.Siku ya leo, kuna jambo linamjia sana kichwani anaona ni vyema kama akipanga safari na kwenda kuongea na mama Sarah, basi alijiandaa na kuondoka nyumbani kwake moja kwa moja kuelekea kwa mama Sarah.Mama Angel alipofika pale tu alimkuta mama Sarah akiendelea na mambo yake mengine kwani kwa siku hiyo alipanga kutoka jioni ndiomana hadi muda huo alikuwepo nyumbani kwake.Mama Sarah alipomuona alimkaribisha vizuri tu ila alitoka nae nje na kumwambia,“Najua lazima kuna mada umekuja kuongea nami, haya tuongee hapa nje”“Asante, kuna mambo nahitaji kukuuliza ili niyajue”“Mambo gani tena hayo? Kuhusu baba mzazi wa Sarah au kitu gani?”“Hapana, siwezi kuuliza kuhusu baba wa Sarah wakati inajulikana wazi, huyu Sarah ni mtoto wa nani. Ila ninachotaka kuuliza ni kuhusu mzee Jimmy”“Unataka kusikia nini kuhusu mzee Jimmy?”“Nahitaji kujua ukweli tu, ni kitu gani kipo kati yako na mzee Jimmy!”“Hivi una wazimu wewe? Mzee Jimmy alikuwa kwangu kama Erick alivyo kwako nadhani unanielewa kwa hilo. Nadhani pia unanielea nikisema kuwa mzee Jimmy ni baba wa Sarah”“Usibadilishe mada Manka, kuna vitu vingi mzee Jimmy alivifanya ambavyo sio sahihi kwakweli, lazima wewe unaelewa mambo mengi sana yaliyofanywa na mzee Jimmy kabla ya umauti wake. Naomba uniambie”“Hivi Erica unachekesha sana, naanzaje mimi kukwambia kuhusu mzee Jimmy, kabisa mimi nikwambie wewe jamani!! NI mzima kweli wewe? Ni hivi, kwanza mrudishe Elly hapa kwangu ndio uongee huo utumbo wako”“Huyo Elly anarudi vipi kwako? Unajua ni kwanini kaondoka?”“Nitajuaje ikiwa wewe ndio umemchukua bila ruhusa yangu”“Kwanza tambua Elly na Sarah ni mtu na dada yake maana wote ni watoto wa Derrick”“Kama mtu na dada yake kuna ubaya gani wakiishi nyumba moja? Si ndio undugu wao utajengeka zaidi”Mama Angel alimuangalia mama Sarah kwa hasira kidogo na kumjibu,“Huo undugu utajengwa vipi, ikiwa watoto wanatamaniana? Unajua kama mimba ya Sarah iliyotoka ni mimba ya Elly?”Mama Sarah alishangaa sana kwani kitu hiki hakukijua kabisa, siku zote alikuwa akimuhisi vibaya Erick sasa kuambiwa kuwa ni Elly alishangaa sana.“Kumbe ni Elly, haya nashukuru kufahamu. Mama Angel naomba uondoke nyumbani kwangu”Mama Angel hakuongea zaidi, kwani aliamua kuondoka tu kwa muda huo kuelekea nyumbani kwake.Mama Angel alipokuwa njiani aliona kuwa mama Sarah anaweza kwenda kumfanyia fujo Sia, kwahiyo aliona ni vyema kwenda kumwambia Sia ukweli, ila alijilaumua sana kuwa kwanini kamwambia mama Sarah ukweli ulivyo.Moja kwa moja mama Angel alienda kwenye biashara ya Sia na kuanza kuongea nae,“Kheee kwahiyo Elly alimpa mimba Sarah?”“Ndio hivyo”“Kweli Elly sio mtoto wangu, ni lazima atakuwa mtoto wa huyo huyo asiyejielewa Derrick. Haiwezekani mwanangu akawa Elly halafu akafanya ujinga namna hiyo kwa jinsi ninavyomfundisha kuhusu kuwa mtoto mwema halafu akafanye huo ujinga jamani!!”“Hapana, yule kalazimishwa tu na huyo Sarah wala sio kosa lake, ndiomana nilivyoenda aliniomba niondoke nae”“Kheee hako kaSarah nako kahuni kama mama yake, kweli mtoto wa nyoka ni nyoka tu. Ila na wewe ulifata nini kwa mama Sarah?”“Nilihitaji kuongea nae kwani yeye anafahamu vitu vingi sana kuhusu mzee Jimmy”“Aaaah kumbe!!”Mama Angel alimueleza Sia kwa kifupi tu kuhusu mama Sarah na mzee Jimmy, ila Sia alishaelewa kwa haraka sana, kisha mama Angel akamwambia tena,“Usimfokee Elly, ila ujue jinsi ya kumlinda ili huyo Manka asiweze kufanya chochote kwa Elly maana ana hasira sana yule mwanamke. Halafu wewe ingawa Elly sio mwanao ila kumbuka umemlea Elly kwa kila hali akijua kuwa wewe ndiye mama yake basi kuwa nae kwa makini sana hata akija kuujua ukweli bado aendelee kukuthamini kama ambavyo anakuthamini sasa”“Nimeelewa, siwezi kumtupa Elly kwakweli”Basi mama Angel aliamua kuondoka tu kwa muda huo na kumuacha Sia pale.Muda ule ule Sia aliondoka na moja kwa moja kwenda ofisini kwa baba Angel, kwani yeye huwa akifikiria kitu anahisi ni rahisi zaidi kusaidiwa na baba Angel kuliko mtu mwingine yoyote.Alimkuta pale na kuanza kuongea nae,“Erick kuna kitu nataka kukwambia”“Kitu gani hiko?”Sia alianza kumueleza kile ambacho aliongea na mama Angel kwa siku hiyo, kisha alimwambia baba Angel,“Unajua kwanini nimekwambia yote haya?”“Ili nikuone wewe na mke wangu mnapatana siku hizi”“Hapana sio sababu hiyo, unajua mimi sio mbaya wa Erica wala nini. Mapenzi yangu kwako ndio yalikuwa kitu kibaya kwa Erica. Ila tuachane na hayo, nimekueleza yale kwasababu kubwa moja, kama mama Sarah yani Manka ndiye anayefahamu vitu vingi kumuhusu mzee Jimmy, basi njia pekee ya kupata siri hizo ni kwa kupitia wewe”“Mmmmh kwa kupitia mimi kivipi?”“Yani wewe ndio uwe karibu na mama Sarah, wewe nio umuulize kwa hakika atakwambia ukweli wa kila kitu na atakuweka wazi kwa kila kitu klabisa”“Mmmh!”“Ni kweli sababu aliwahi kukupenda”“Hiyo sio sababu, aliwahi kunipenda ndio, ila sio kwasasa ambapo kila mtu ana masisha yake. Ila nitajaribu kumdadisi”“Ila nimekumbuka kitu, naomba unisamehe sana kwa kuchelewa kukwambia kuhusu jambo hili, ni hivi kuhusu wewe kuwekewe sumu ni huyo huyo Manka ndio muhusika mkuu ila usinitaje kama nimesema”“Unaongelea nini? Sikuelewi”“Kipindi kile ulipopewa sumu, nilifatilia na kugundua kuwa ile sumu uliipata kwenye matunda ambayo ulipewa na huyo mama anayewauzia matunda nje hapo, ila yule mama sio kwamba yeye ndio alikuwekea sumu! Hapana, yule mama alitumwa na huyo Manka kukupa yale matunda ambayo yalikuwa na sumu tayari. Nilipokuwa nachunguza, ndipo Manka mwenyewe akanibamba na kunipa onyo kali sana kuwa nisifatilie maisha yake, ukizingatia yeye ndio anamsomesha mtoto wangu, basi sikuwa na namna yoyote ya kutenda zaidi ya kukubaliana na hali halisi tu ya kutokufatilia maisha yake, na niliogopa kuja kukwambia ukweli. Ila kuwa nae makini sana”“Duh!! Kumbe Manka alifikia hatua hiyo! Sikufikiria kwakweli, huyo mama nae muuza matunda aliwezaje kukubali matunda kwa mtu na kuniletea mimi!!”“Aliahidiwa hela ya mtaji ndiomana alifanya vile, unajua sisi masikini huwa tunajikuta tunatenda vitu vingine na kuja kujutia badae”“Umasikini gani wa kuniwekea sumu? Ningekufa je! Ndio angesema umasikini wake umeniua au? Kwanza masikini unawajua vizuri au? Mfano kama wewe, mambo mengine huwa unayataka mwenyewe, hivi Sia uambiwe jambo kama hilo uje kunitendea mimi sababu umeahidiwa hela hiyo ni sawa kweli? Mwishowe usingizie umasikini! Umeauza mtoto umesingizia umasikini, halafu kwasasa unataka kuniambia kumuwekea mtu sumu ni umasikini kweli!!”“Hapana mimi siwezi kuweka sumu, hata kama nina shida kiasi gani siwezi kufanya hivyo, hata yule mama nina uhakika asilimia zote hakujua kama ni sumu. Yani kuna kitu kingine mtu unaamua kusema kuwa hizi shida zinimalize ila sio nifikie hatua ya kutoa uhai wa mtu sababu ya pesa, hiyo ni tamaa tu, mtu awe na pesa au asiwe nazo ila akiingiwa na tamaa ya hivyo basi atafanya tu”“Na kwasasa uache kusingizia umasikini basi, lini umekwama kwenye biashara ukaniambia nikaacha kukusaidia? Mimi nipo vizuri sana ila huwa sipendi tu uchizi wako ambao ukiuanzisha hadi zimamoto waje kuuzima. Kitu kingine nakushukuru kwa uchunguzi wako. Nakupa kazi nyingine, ukimuona dokta Jimmy popote pale naomba umfatilie hadi tumpate kwani ana mengi sana ya kujibu, licha ya kubadilisha watoto ila kuna mengi anatakiwa kujibu”“Sawa, hakuna tatizo”Baba Angel leo alimpa na hela kidogo Sia, ambapo Sia alifuirahi sana na kumuaga halafu akaondoka zake ambapo cha kwanza kabisa alienda kwa yule mama muuza matunda ingawa aliwahi kukatazwa na mama Sarah.Alimkuta pale yule bibi akiendelea na mambo yake na kumsalimia pale kisha alianza kuongea nae,“Vipi ulishapewa mtaji?”“Mmmh ndugu yangu, yamenishinda”“Kwanini?”“Kuna siku yule tajiri alikuja na chakula kizuri sana alisema nimpelekee bosi Erick, nikamwambia kuwa bosi Erick siku hizi hata matunda yangu hali, akaniambia kuwa bosi akiona kile chakula atakipenda na kukila tena nisiondoke hadi amalize kula. Kisha akanipa laki moja ya kufanya hivyo, mmmh niliogopa yani kazi ya kupeleka chakula tu ndio anipe laki moja! Nikamwambia kuwa siwezi kufanya vile, alichukia na wala hakuniambia kitu zaidi zaidi aliondoka na hela yake na chakula chake”“Duh! Pole sana, yani mabosi wana mambo sana”Basi Sia alimuaga yule mama ila pale alipata kitu kuwa bado mama Sarah anaendelea kumfatilia baba Angel, ila tu hakujua ni kwasababu ipi.Usiku wa siku hii, mama Angel alikuwa akiongea na mume wake kuhusu yaliyojiri yani vile alivyoenda kwa mama Sarah kwahiyo aliongea nae vitu vilivyotokea pale, kisha baba Angel alimwambia ushauri aliopewa na Sia na jinsi Sia alivyomwambia kuhusu mama Sarah na kufanya mama Angel ashtuke kiasi,“Mmmh hata usimfatilie, kumbe ni yeye aliyetaka kukuwekea sumu?”“Ndio, yani Sia kanihakikishia kila kitu”Muda kidogo simu ya baba Angel ilianza kuita, kuangalia mpigaji ni madam Oliva ila alipokea tu hivyo hivyo,“Samahani kwa kukupigia usiku huu”“Bila samahani, nini tatizo madam”“Kuna mlinzi niliongea nae, nilimwambia kuwa mdogo wake dokta Jimmy akienda anipe taarifa, anasema kuwa kaongea nae huyo mdogo wake dokta Jimmy kasema anaenda kesho. Kwahiyo kama inawezekana twende kesho”“Sawa hakuna tatizo, itabidi kesho twende”Baba Angel aliongea na mke wake kuhusu jambo hilo, mama Angel aliona ni vyema kwa mume wake kufanya vile na alimsapoti kwa jambo lile.Leo baba Angel alijiandaa na kuwasiliana na madam Oliva kisha alimpitia na kuondoka pamoja nae kuelekea kwenye ile hospitali.Na kweli waliwakuta walinzi, na huyo mdogo wake dokta Jimmy anaonekana nae alifika ile asubuhi maana huwa sio mkaaji wa eneo lile.Basi wakina baba Angel walionyeshwa tu na kumsogelea ambapo huyo mdogo wake dokta Jimmy alikuwa kawapa mgongo kwa muda huo, basi walimsalimia pale ambapo aligeuka na kuwatazama ila baba Angel na yule mdogo wake dokta Jimmy walishangaana kwani ni watu wanaofahamiana. Basi wakina baba Angel walionyeshwa tu na kumsogelea ambapo huyo mdogo wake dokta Jimmy alikuwa kawapa mgongo kwa muda huo, basi walimsalimia pale ambapo aligeuka na kuwatazama ila baba Angel na yule mdogo wake dokta Jimmy walishangaana kwani ni watu wanaofahamiana.Baba Angel ndio alianza kutamka jina la yule mdogo wa dokta Jimmy kwa mshangao,“Moses ni wewe!!”Moses nae alionekana kumshangaa baba Angel kwani hakutegemea kumuona kwa wakati ule mahali pale, basi madam Oliva alimuuliza baba Angel,“Kumbe unafahamiana nae?”“Ndio, namfahamu vizuri sana huyu mtu”Baba Angel aliendelea tena kuongea na Moses,“Za siku Moses”“Nzuri tu”“Naomba tuongee kidogo”“Nina haraka sana kwa muda huu”Yani Moses alisema vile huku akielekea kwenye gari yake na kupanda na kuondoka, huku madam Oliva na baba Angel wakiwa pale wakimshangaa,“Sasa anamaana gani?”“Nadhani hakutegemea kukuona mahali hapa, ndiomana unamuona hivyo. Ngojea tumuulize vizuri yule mlinzi”Basi walimuita tena yule mlinzi na kumuuliza,“Kwani unafahamu anapoishi?”“Hapana, huwa sijui anaishi wapi na hakuna anayejua anapoishi kati yetu”“Mmmh! Na huwa anaondoka kwa haraka hivi?”“Hata nashangaa kaondoka bila hata ya kutuaga maana sio kawaida yake kabisa, huwa akija lazima aende kwenye ile ofisi ya dokta ambayo yeye ndio ana funguo zake na huwa sijui anaenda kufanya nini maana sisi tunalinda tu”“Hivi ni kweli hii hospitali imefungwa na serikali au ni kitu gani? Ndio wasije kuikagua kweli?”“Sisi hatujui ila ndio tulivyoambiwa kuwa imefungwa na serikali”“Mmmmh hapa kuna siri kubwa sana tena sana”Basi madam Oliva alimvuta pembeni baba Angel na kumuuliza,“Kwahiyo huyu kijana unamfahamu vizuri sana?”“Tena sana, ila kwasasa kanenepa sana. Huyu kijana alikuwa akiuza duka langu moja hivi lilikuwa ni kubwa sana, nadhani kwasasa ndio lingekuwa duka pekee kubwa sana hapa nchini kwa vifaa na vitu vya watoto maana lilikuwa na bidhaa nzuri na kufanya wengi walipende, kule kote ninakofungua maduka kwasasa, nanusanusa tu ila ile ndio ilikuwa biashara yangu kubwa sana”“Kwahiyo imekuwaje? Ulifunga au imekuawaje?”“Ni historia ndefu kidogo, kwanza ile biashara kwa asilimia zote ilikuwa ikifanywa na huyu kijana, yani kama hujui hata unaweza sema ni duka lake sababu nilimuamini sana kwenye biashara yangu ile, na ilikuwa na faida haswaaa kwani tulikuwa na wateja wengi. Mwanangu Angel wakati mdogo ndio alikuwa balozi wa duka langu lile, sasa badae mke wangu alivyojifungua na kupatwa matatizo mbalimbali, niliamua kwenda nae Afrika kusini kwaajili ya matibabu, basi nilisafiri na familia yote yani mimi, mke wangu na watoto wetu wote na tulikaa huko kwa miaka mitatau huku biashara yangu kubwa ikiendeshwa na Moses kwani huwa hata nikiwa mbali basi yeye anaendesha biashara yangu vizuri kabisa. Nakumbuka tulivyorudi nchini na kuanza maisha hapa tena, ndio hapo tatizo lilianza kwani biashara ile ilianza kuyumba sana na baba alinilaumua kuwa nimefanya uzembe, kuondoka na kuacha biashara, moses aliandika barua ya kuacha kazi na kuondoka zake, sikuwa na usimamizi mzuri kwakweli. Baada ya Moses kuondoka, wiki moja nilishusha mzigo mpya kwa kutumia akiba yangu nyingine ili duka nilisimamie mwenyewe, ila duka lilivamiwa na majambazi ambao walikomba kila kitu yani unajua kila kitu! Ni kila kitu hadi taa, duka lilibaki jeupe kama halijawahi kuwa na kitu. Ndio toka kipindi hiko niliacha hiyo biashara na sikuonana tena na huyu jamaa hadi leo, fikiria toka wakina Angel wadogo hadi leo! Ni muda mrefu sana umepita”“Ni kweli ni muda mrefu sana, ila hakuna mtu mliyekuwa mnamshuku kwa wizi huo?”“Nimshuku nani ikiwa hadi walinzi wangu waliuwawa? Yani kwasasa ndio unaona nakuwa na duka la kawaida tu kama lile, ila duka langu hilo lilikuwa ni kubwa sana, nilikuwa nafanya biashara ya jumla na rejareja”“Ooooh pole sana kwakweli, wezi huwa wanajua kurudisha mtu maendeleo nyuma. Pole sana”Wakaongea kiasi pale na kuamua kuondoka ambapo baba Angel alimpitisha hadi shuleni maana madam Oliva alikuwa akienda shuleni kwa wakati huo, basi madam Oliva akamuuliza,“Ushuki kuja kusalimia mwanao?”“Aaah Erick!! Atashtuka akiniona kwa muda huu, acha niende ofisini tu”Basi waliagana oale, halafu baba Angel aliondoka zake.Njiani, baba Angel aliwaza kuwa aende kwa Sia, kwahiyo moja kwa moja aliongoza mpaka kwenye biashara ya Sia ambapo alimkuta pale akiendelea na biashara yake basi akaongea nae,“Kwakweli Sia kwa uchunguzi nakukubali sana, nakuomba fanya juu chini uweze kuchunguza kuhusu dokta Jimmy. Halafu unajua kitu kingine nilichogundua?”“Kitu gani?”“Unamkumbuka yule Moses aliyekuwa anauza duka langu kipindi kile, lile duka langu kubwa la vitu vya watoto”“Oooh lile duka ulilomfanya Angel kuwa balozi?”“Ndio lile lile, sasa kumbe Moses ndio mdogo wake na dokta Jimmy na kwasasa Moses ndio mtu pekee anayejua dokta Jimmy alipo”“Kheee umejuaje Erick?”Baba Angel alimueleza Sia vile alivyoweza kugundua kuhusu Moses, na jinsi alivyoondoka upesi upesi pale hospitali,“Mmmmh huyo itakuwa ana siri kubwa sana ila ndiomana mimi sijawahi kumuamini huyo kiumbe jamani! Kumbe ni ndugu yake dokta Jimmy!!”“Ndio, ni ndugu yake kabisa. Nasikia ni ndugu yake wa damu”“Sasa unanifungua ufahamu wangu kidogo, ndio naanza kuelewa zile hisia zangu. Unajua Erick, usikute ule wizi wa duka lako ni Moses ndio alihusika!!”“Hapana jamani, biashara na Moses nilianza nae miaka mingi sana, kweli kwa muda ule ndio aamue kuniibia? Haiwezekani”“Sisemi sana ila nahisi hivyo, ila kitu kingine yule Moses sasa naelewa ni kwanini niliwahi kumkuta mara kadhaa akiwa na mzee Jimmy”“Naona unataka kuniletea mada zingine sasa, kumbuka baba yangu hayupo halafu mnavyomuongelea kila mara sio picha nzuri”“Ila kumbuka yote haya mimi nahangaika nayo sababu ya baba yako, yani Erick huwezi kukwepa maovu ya baba yako aliyoyafanya kipindi cha uhai wake. Mimi nitamfatilia huyo dokta Jimmy ila natakiwa niwe na pesa, kwasasa sina hela za kutosha”Baba Angel hakutaka pesa ndio zikwamishe kile anachotaka yeye kufahamu, hivhobasi akampa Sia laki tatu ili zimsaidie na kumwambia kuwa atamuongeza zingine bila kujali kuwa akigundua kuhusu dokta Jimmy itakuwa ni msaada na kwake pia. Kisha baba Angel alimuaga pale na kwenda ofisini kwake.Mama Angel akiwa nyumbani kwake, leo alipigiwa simu na mama yake na kuanza kuongea nae,“Kheee nyie watoto wabaya, hivi kweli Erica ndio wakukaa kipindi chote hiki bila kuja kuniona kweli!!”“Mama, naomba unisamehe bure. Kesho nitafanya juu chini nitakuja kukuona na Ester”“Hapo nitafurahi sana nikimuona mjukuu wangu, najua amekuwa sana kwasasa”Basi alimaliza kuongea na mama yake, kisha alimuita Vaileth na kumuuliza,“Hivi ndugu zako huwa hawakuulizi pia kuhusu kwenda kuwasalimia?”“Na yale mambo ya kipindi kile, si unaona hata kuja wanakuja kiuoga, wala hata hawasemi chochote”Wakawa wanaongea pale, muda kidogo Erica alirudi kutoka shuleni na kuwasalimia pale kisha alimuomba mama yake kuwa ana mazungumzo nae, mama Angel alijua tu kuwa Erica atakuwa amerudi na maneno yake ya umbea kwahiyo anatafuta pa kuyafikisha, basi mama Angel moja kwa moja alienda chumbani kwa Erica na kumsikiliza,“Mama, hivi kweli mimi ni mtoto wako?”“Hivi wewe mtoto una wazimu au kitu gani? Swali gani hilo unaniuliza sijui mara ya ngapi leo! Si nilishakujibu wewe, unaniletea kichaa eeeh!”“Sasa mama, nimetoa wapi umbea?”“Sitaki ujinga, umbea ni tabia kama tabia zingine, hiyo ni tabia yako haina kurithi hiyo. Umeipata mwenyewe, jifunze tu kuirekebisha maana umbea sio mzuri, ipo siku utasutwa hadi ukosee njia”Erica alipumua na kumuuliza tena mama yake,“Mama, wakati mimi na Erick tumezaliwa, tulikuwa na alama gani wakati wadogo? Au mimi nilikuwa na alama gani?”“Alama kivipi?”“Kuna kidude mwilini mwangu sikielewi mama”“Kidude gani?”Erica aliondoa shati lake na kuinua mkono juu ambapo chini ya mkono wake wa kushoto yani kwenye sehemu karibu na kikwapa mama Angel aliona kuna kakinundu,“Kheee tuseme kile kinundu kimerudi tena!!”“Ndio, sikipendi mama, nimerithi kwa nani?”“Sijui, hayo ni matatizo tu. Inatakiwa tujue tiba ili utibiwe, hayo mengine matatizo tu. Sio kila jambo ni kurithi. Nakumbuka tulikikata kipindi kile hospitali, sikujua kama kitarudi tena. Nitakupeleka tena hospitali”Mama Angel aliona Erica hana maneno ya maana basi aliamua kuondoka tu chumbani kwa Erica kwa muda huo.Usiku wa leo, baba Angel aliamua kumueleza mkewe kuhusu mambo yaliyojiri kwenye hospitali ambayo alienda kwaajili ya kumfatilia huyo mdogo wake dokta Jimmy,“Kheee kumbe Moses! Umemuona alivyonenepa eeeh!”“Nimemuona, kabadilika sana hajataka hata kuongea na mimi”“Basi ukweli wote anaujua, yani yeye ndio wa kumshikilia nadhani pia hakutegemea kama angekutana na wewe”“Hakutegemea kabisa, ila kabadilika sana kwanza sijategemea pia kama Moses angegoma kuongea na mimi kwa kisingizio kuwa ana kazi nyingi!!”“Ila ndio wanadamu walivyo mume wangu”Waliongea sana pale, hadi kwa siku hiyo walichelewa kulala kwakweli.Kulipokucha, ni mtoto ndio aliwaamsha baada ya kuanza kulia, ikabidi baba Angel ajiandae na kwenda ofisini.Mama Angel nae aliamka na kumuandaa mwanae ili aende kumuona mama yake kama ambavyo alimuahidi.Basi alipomaliza alienda kujiandaa alienda kumuaga Vaileth,“Leo, naondoka na mtoto maana naenda kwa bibi yake”“Kheee kwahiyo mama, leo kurudi jioni?”“Ndio, ni jioni kabisa ndio nitarudi. Basi upike vile vile kama kawaida ila hawa wakitoka shule wakute chakula”“Sawa mama, hakuna tatizo”Basi mama Angel alitoka na kuondoka zake, ila siku hiyo alitoka na dereva kwani asingeweza kuendesha mwenyewe na mtoto mkononi.Vaileth alishukuru kuona wote pale nyumbani wameondoka, basi alimpigia simu Junior, ambaye alimuahidi kufika kama kawaida, kisha yeye aliendelea na kazi mbalimbali za hapa na pale.Na kweli baada ya muda tu Junior alifika na kuanza kuongea na Vaileth,“Unajua nilikuwa nakujaribisha tu kama utafika, Junior jamani huwa unasoma muda gani?”“Aaaah nasoma, halafu leo si Ijumaa”“Inamaana muda wote huwa upo na simu?”“Yani hujui tu Vai ukinipigiaga simu jinsi akili yangu inavyopoteza uelekeo, kwanza niambie ushatoa mimba? Ushatumia uzazi wa mpango?”“Vyote tayari”“Oooh kwahiyo ni kujiachia tu kwasasa? Ndiomana watu huwa wanasema kuwa wanawake wakubwa wana akili sana, na hizi ndio akili sasa”“Akili kutoa mimba Junior?”“Hapana, sio akili kutoa mimba ila akili yako ni kwamba unawaza mambo ya mbali, mfano mimi bado nasoma, je ukizaa mtloto itakuwaje? Hapa ndani wakigundua kuwa una mimba si watakufukuza? Na je mimi si nitachukiwa sana hapa nyumbani? Kwahiyo kwa kitendo chako cha kutoa umenifurahisha sana”Vaileth alipumua kiasi na kumuangalia huyu Junior kwa makini, na kuona hapa huyu kijana yupo kwake kwaajili ya starehe tu na si vinginevyo. Kwahiyo aliona ni vyema aishi kwa akili. Basi Junior alisema aende kuoga kwanza, kwahiyo alienda kuoga na muda huo huo Vaileth alishika simu ya Junior ambapo ujumbe uliingia kutoka kwa jina lililoandokwa ‘Mama Linah’Ujumbe ulisema,“Junior mpenzi, ulisema nikutumie kiasi gani?”Vaileth akafikiria kidogo na kumjibu,“Naomba nitumie laki sita mpenzi”“Nitume zote kwenye simu yako au nitume kwenye namba uliyosema unadaiwa?”Vaileth akafikiria tena na kumwambia,“Tuma laki tani kwenye ile namba halafu laki moja kwenye namba yangu, ngoja nikutumie namba ya kutuma na jina kamili ili usikosee”Basi muda ule ule Vaileth alimtumia mule namba yake na jina lake, ambapo baada ya muda kidogo kuna ujumbe kwenye simu yake kuwa amepokea laki tano uliingia, halafu yule mama alituma ujumbe mwingine,“Natumaini umepata, hata huyo mdai wako amepata”“Ndio nashukuru sana, kanipigia simu muda huu huu”“Basi muda sio mrefu nitakufata halafu nitakurudisha shule Jumapili jioni, sawa mume wangu mpendwa!”“Hakuna tatizo mke wangu”Basi Vaileth alifuta zile jumbe zote na kuweka pembeni simu ya Junior, hata Junior alipotoka kuoga alienda nae sebleni ili aweze kula chakula maana alimuandalia na kuongea nae vizuri kabisa, kisha baada ya kula aliamua kuongea nae kidogo,“Hivi Junior ni kweli unanipenda?”“Ndio, nakupenda sana, tena sana”“Sawa, je huna wanawake wengine?”“Ila wanawake jamani, huwa hamjiamini kabisa, sijui kwanini lakini. Mimi nakupenda wewe, sasa mwingine wa kazi gani? Sina haja na mwanamke mwingine mimi”“Sawa nimekuelewa, sasa tunaongea sana leo. Twende tukajipumzishe kidogo”“Hapana, leo sijisikii kwakweli nilikuita tu nikuone”“Aaaargh ndio mambo gani hayo lakini Vai?”“Kweli tena, sijisikii kabisa leo”Mara simu ya Junior ilianza kuita na aliipokea, na kuongea nae kwa kifupi tu kisha akainuka na kumwambia Vailet,“Natakiwa shuleni mara moja, ngoja niende tutawasiliana”Kisha Junior alisogea karibu na Vaileth na kumbusu halafu akaondoka zake, yani Vaileth alimuangalia kwa hasira sana huyu Junior ila akawa za kitu,“Hivi kweli kabisa niendelee kukaa na mimba ya Junior kwa akili kama hizi alizokuwa nazo kweli jamani!! Natamani kwenda kuitoa hii mimba, sijui nifanyeje?”Akawaza, akaona sana akaona bora atamtafute nduguye Prisca na kumuuliza baadhi ya mambo,“Prisca ndugu yangu, kuna jambo nataka nikuulize”“jambo gani tena?”“Hivi kipindi kile nilikusikia ukiongea na bibi kuwa mtu ukipata mimba halafu hiyo mimba huitaki, sasa ukitaka itoke unafanyaje?”“Mmmmh Nyanda usiniambie kuwa una mimba? Ni mimba ya huyo baba mwenye nyumb? Unatoaje mimba ya tajiri hivyo?”“Hapana, sina mimba ila kuna mtu nataka kumsaidia ndio ana mimba”“Mmmmh mtu gani huyo?”“Niambie kwanza halafu nitakwambia ni mtu gani”“Nitafute usiku nikuelekeze vizuri, ila kama ni wewe pia uniweke wazi”Basi Vaileth alikubaliana nae kuwa atamtafuta usiku ili aweze kuongea nae kuhusu jambo hilo.Mama Angel alifika nyumbani kwa mama yake, kwakweli mama yake alifurahi sana kumuona mtoto wake maana ni siku nyingi sana hakukutana nae, kwahiyo walifurahiana pale na kukaa pamoja huku wakiongea mambo mbalimbali,“Yani Angel huwa naenda kumuona hadi anasema mama na baba ndio kama wamenitupa huku maana hata hawaji kuniona”“Mama, tumepanga likizo ndefu ndio tutamrudisha nyumbani, si unajua yule mtoto alivyojua kuchanganya vichwa vyetu yule, yani mpaka nilikuwa najihisi kupata ugonjwa wa moyo. Kwanza natamani hata akae huko huko hadi amalize shule kabisa, mambo yake na Samir mimi hata siyawezi. Ila wale masister sasa wanawachunga wale watoto hata ujinga haiwezekani”“Ni kweli, ile shule ni nzuri sana. Ila Angel alikuwa anaelekea pabaya, nadhani kapata macho juu juu kama baba yake, ila tabia sio yako kabisa”“Mmmh jamani mama”“Ndio, naona Erica ndio kachukua tabia yako maana hana mambo ya ajabu yule”“Ila umbea ni moto, katoto ni kambea hadi shetani anaogopa sijui umbea ule kaupata wapi”Bibi Angel alicheka sana, tena sana na kuanza kuongea na mama Angel,“Sikia nikwambie, babu wa baba yenu yani baba yake mzazi na babu yenu. Jamani yule babu alikuwa ni mbea hadi basi, Mungu amrehemu tu huko alipo ila alikuwa ni mbea hakuna mfano. Halafu ubaya ni mmoja, alikuwa na mtindo wa kuota mambo ya ukweli, yani yeye utakuta anaota kitu kilichopo, akishaota sasa anakueleza kila kitu, na aliyekaribu anamwambia, yani siri yako peupeee, yule babu nasikia watoto wake karibia wote waliachana na waume zao na wengine waliachana na wake zao maana yule babu alikuwa noma. Unapanga kitu mwenzio kashakiota, ukija anakuumbua mwanzo mwisho. Vipi Erica kapona na ndoto?”“Zamani ndio alikuwa na mtindo huo, ila kwasasa ameacha”“Kheee basi yule babu, alikuwa na nundu Fulani kwenye kwapa, yani hadi wajukuu zake wanampa ushauri kuwa apelekwe kukatwa ila anakataa na kusema kuwa lile nundu ndio linamfanya aote siri za watu”“Kheee!!”Mama Angel kidogo akashtuka na kumwambia mama yake,“Hata Erica ana kinundu Fulani kwenye kwapa, tuliwahi kumkata wakati yupo mdogo ila jana kaniopnyesha kile kinundu kimerudi tena”“Duh!! Hebu mfatilie Erica vizuri”“Ila mama mbona hata Derrick ni mbea ila huwa hasemi kama anaota?”“Derrick ni mbea kweli, ila pia ni muongo ndiomana hata kazi ya utapeli aliiweza, kwanza anaendeleaje?”Ndipo mama Angel alipoanza kumueleza mama yake hadi mambo ya mtoto Elly aliyekuwa kwa Sia kuwa ni mtoto wa Derrick, kwakweli bibi Angel alishangaa sana na alipoambiwa kuwa jambo hilo lilifanywa na mzee Jimmy alishangaa zaidi na kusema,“Yani yule mzee akili zake anazijua mwenyewe, nilitaka nishangae kafa tu na kuacha salama mambo yote!! Nilijua lazima kuna ujinga atakuwa amefanya. Umenikumbusha kitu, kuna siku alisema kuwa ipo siku hata akifa wewe Erica utaenda kwenye kaburi lake na kulia sana”“Kheee mzee ana wazimu huyo eeeh!!”“Ni kweli ana wazimu tena haswaa, ila maneno yake yalishakufa nae kashashindwa yule”Waliamua kubadilisha mada na kuanza kuongea vitu vingine kwa wakati huo, kwani waliona mada za mzee Jimmy zingewachanganya akili.Ila muda wakati mama Angel anakaribia kuondoka ndipo alipogundua kuwa simu yake haina muda wa maongezi,“Unajua nini mama? Nilimwambia dereva nitampigia muda wa kuondoka aje anichukue, ila muda wa maongezi kumbe sina”“Kheee na mimi sina yangu haina muda wa maongezi pia”“Basi ngoja nikanunue vocha”Mama Angel alimuacha pale mama yake na yeye kuondoka zake kuelekea dukani kwani kwa muda huo mtoto wake mdogo alikuwa amelala.Mama Angel, alipotoka nje ya nyumba yao alishangaa kuona kuna gari imesimama hapo, alijiuliza sana kuwa ile gari ni ya nani ila hakuelewa kuwa ni ya nani kwa muda huo, basi aliamua kuachana nao na kuendelea na safari ila alisikia sauti ikimuita,“Erica”Akasimama na kugeuka nyuma, alishangaa kumuona Rahim, ambapo Rahim alimsogelea na kuanza kuongea nae,“Mambo vipi Erica?”“Kilichokuleta huku kwetu leo ni nini?”“Hata mimi sijui ni kitu gani? Nilikaa nyumbani kwangu ila nikajisikia tu kuwa kuja huku kwenu nikuone”“Kweli akili yako haina akili kabisa, yani kipindi kile nina mtoto mdogo hapa, ulishindwa hata kuja kumtazama mtoto wako mwenyewe, halafu kwasasa unajifanya una hamu sana ya kuja kuniona mimi!!”Kisha mama Angel alikuwa akiendelea kwenda dukani huku Rahim akimfata nyuma na kuongea nae,“Zilikuwa ni akili za ujana zile, kwasasa nimejua thamani yako. Yani nina hamu kweli ya kuishi nawe pamoja na mtoto wetu Angel, natamani kweli watoto wote ulionao ingekuwa umezaa na mimi”Mama Angel alifika dukani na kununua vocha kisha kuanza kurudi nyumbani, basi Rahim aliendelea kuongea tu,“Unajua nini Erica, mimi bado nakupenda tena nakupenda sana”Mama Angel alisimama na kumwambia Rahim,“Hebu nisikilize Rahim tena nisikilize kwa makini sana, mimi nimeolewa kwasasa na nina maisha yangu, na wewe umeoa na una maisha yako. Unatakiwa kumuheshimu mke wako kama mimi ninavyomuheshimu mume wangu. Nampenda sana Erick, ndiye mwanaume aliyefuta machozi yangu, mwanaume aliyeondoa aibu yangu, mwanaume aliyenifanya nijione mwanamke kati ya wanawake, mwanaume aliyefanya wengi wanaotuona kutamani mapenzi yetu na kuniona kuwa mimi ni mwanamke mwenye bahati sana. Kweli nina bahati sana kumpata Erick kwenye maisha yangu, nampenda sana kupita chochote”“Dah! Umeamua kunimaliza kabisa leo kwa maneno yako. Huwezi jua siri za ndani ya nyuma, nyumba zinja siri kubwa sana Erica. Nikikueleza ya mke wangu kwa hakika utachoka kutasikiliza kabisa. Ila hakuna tatizo, najua ni jinsi gani unapendana na Erick ila ukweli utabaki pale kuwa na mimi nakupenda sana wewe”Mama Angel akafikiria kitu na kukumbuka jambo, basi alimwambia Rahim,“Kama kweli unanipenda au ulikuwa na upendo wa dhati juu yangu naomba ufanye jambo moja kwaajili yangu”“Jambo gani hilo?”“Najua kwasasa una mahusiano na mwanamke aitwaye Manka, ila kuna jambo kubwa sana kuhusu huyo Manka. Alikuwa yupo karibu sana na baba mkwe wangu aliyeitwa mzee Jimmy, nadhani unamfahamu vizuri sana. Naomba umchunguze huyu mwanamke ujue yeye na mzee Jimmy ni kitu gani kimejificha”“Eeeeh baada ya kazi hiyo ndio nitakupata?”“Halafu wewe una kichaa kweli, hivi unajisahaulisha kuwa umeathirika au kitu gani!”Kisha mama Angel aliingia ndani kwao na kumuacha Rahim pale nje kwani alihitaji kumpigia dereva wao simu ili aweze kwenda kumchukua.Mama Sarah, toka siku ameujua ukweli alisikia roho kumuuma sana, na kwavile siku hizo Elly hakurudi nyumbani kwake basi akaona ni vyema akamfate shuleni kwao.Alienda mpaka shuleni na kumuita Elly, ambaye alienda kumsikiliza kisha alimwambia kuwa anahitaji kuondoka nae, kwakweli Elly alishindwa kukataa kwani ni huyu mama ndiyo anayemtegemea kwenye elimu yake.Aliondoka nae huku mama Sarah akiongea nae kwenye gari,“Ulianza lini mchezo mchafu Elly?”“Mchezo gani?”“Unajifanya hujui au? Mchezo wa kuwapa wanawake mimba”Elly alikaa kimya kwani aliogopa kiasi, kisha mama Sarah aliendelea kumwambia,“Nadhani hunijui vizuri, mimi ni mwanamke mwenye huruma sana pia ni mwanamke mwenye roho mbaya sana, nimekereka mno kusikia kuwa wewe ndio kidume ambaye umempa mimba binti yangu. Yani nikusomeshe, mama yako ategemee pesa yangu, mle chakula changu halafu uje kumfanyia vibaya binti yangu? Sijapenda hata kidogo”Elly alikuwa akitetemeka tu bila kujua cha kujitetea wala kujua kitu chochote cha kufanya, basi moja kwa moja mama Sarah alienda nae mahali Elly na kumkabidhi kwa mtu akimtaka mtu huyo amuadhibu Elly atakavyo ambapo yule mtu alianza kwa kumchapa viboko visivyokuwa na idadi, yani Elly alikuwa akilia sana huku akilaani vikali umasikini uliokuwepo kati yake na mama yake.Yule mtu alipomchapa sana Elly alimuuliza mama Sarah,“Adhabu zingine sijui kama utapenda kuona nitakavyompatia! Niruhusu niende nae kule mtoni nikamuadhibu vizuri”“Sawa hakuna tatizo”Mama Sarah alikaa pembeni ya gari yake huku amekunja sana sura yake na akifurahia vile Elly alivyoenda kuadhibiwa, akatoa na kinywaji kabisa kwenye gari lake na kuanza kunywa taratibu. Ila baada ya muda mfupi tu, yule kijana aliyekuwa akimuadhibu Elly, alikuja mbio hadi kwa mama Sarah na kumwambia,“Mama, kuna kitu sio cha kawaida nimekiona kwa huyu kijana”Mama Sarah alishtuka kuwa ni kitu gani hiko. Mama Sarah alikaa pembeni ya gari yake huku amekunja sana sura yake na akifurahia vile Elly alivyoenda kuadhibiwa, akatoa na kinywaji kabisa kwenye gari lake na kuanza kunywa taratibu. Ila baada ya muda mfupi tu, yule kijana aliyekuwa akimuadhibu Elly, alikuja mbio hadi kwa mama Sarah na kumwambia,“Mama, kuna kitu sio cha kawaida nimekiona kwa huyu kijana”Mama Sarah alishtuka kuwa ni kitu gani hiko.Basi mama Sarah ilibidi aongozane na yule kijana, ambapo Elly alikuwa chini huku akivuja damu nyingi kwa kipigo alichokipata kwa yule kijana, basi mama Sarah akaanza kumfokea yule kijana,“Imekuwaje umpige mpaka aanze kuvuja damu hivyo?”Kisha mama Sarah alijikuta akijiwa na huruma ya hali ya juu, na kwenda pale chini alipokuwa Elly, kisha yule kijana alimwambia,“Kilichonishangaza sio hizo damu nyingi zilizomtoka, ila angalia mbele ya hizo damu”Mama Sarah alipoangalia aliona kuwa hizo damu za Elly, zimeenda kuzunguka kwenye mti ambao umeandikwa kwa kukwanguliwa jina ‘Manka’ kwakweli mama Sarah alishtuka sana, hakujua ile inamaanisha nini, ila alimuomba yule kijana wasaidiane kumchukua Elly na kumpeleka hospitali.Walimbeba na kumkimbiza kwenye gari, kisha kumpeleka hospitali. Huko mama Sarah hakusema kama wamempiga ila aliongea na daktari tu amuhudumie maana yeye kamsaidia, akampa pesa yule daktari ambapo alianza tu kumuhudumia Elly bila kutaka kujua kama waliompeleka hospitali ndio waliompiga.Kwakweli mama Sarah alikuwa haelewi kitu, na muda nao ulikuwa umeenda sana kwa siku hiyo, yani alizunguka zunguka pale hospitali na aliumia sana moyo wake.Aliondoka pale hospitali kwenye mida ya saa tano usiku na kurudi nyumbani kwake huku akiwa na mawazo sana haswaa ni kwanini jina lake limechorwa kwenye ule mti!! Yani hapo ndio hakuelewa kabisa.Mama Sarah alipoingia ndani kwake na kwenda kuoga tu, akafatwa na Sarah ambaye alimsubiria mama yake amalize kuoga kisha akamuuliza,“Mama, mbona siku hizi sikuelewi!”“Kwanini mwanangu?”“Yani huwa muda mwingine unaonekana ukiwa na mawazo sana, unaonekana huna raha. Siku hizi unaenda sana kwenye mikesha yani huwa sielewi, na yote kwa yote leo ndio sijakuelewa kabisa, kwanza umechelewa kurudi halafu umerudi ukiwa na hofu kubwa”“Hebu kwanza niambie ukweli, ni kweli Elly alikubaka hadi ukapata mimba ile?”“Hapana Elly hajanibaka mimi, ila mimi ndio nilitaka kuwa nae, yani kwa tatizo hili wala sio kosa la Elly kabisa”Mama Sarah alipumua kiasi kwa muda maana alihisi kama mawazo yake kukatika, kisha Sarah akamuuliza,“Nani kakwambia kuwa Elly alinibaka?”“Hapana, hakuna kitu mwanangu”Basi mama Sarah aliamua kuagana na binti yake tu kwani aliona kwa muda huo akili yake kutokufanya kazi kabisa.Vaileth kama ambavyo aliwasiliana na ndugu yake, basi alimtafuta tena kwa usiku ule na kuanza kuongea nae ili kujua cha kufanya kuweza kuitoa ile mimba aliyokuwa nayo. Basi alianza kuwasiliana nae,“Eeeh Prisca niambie ile dawa sasa”“Kwanza niambie ukweli ili nikupe dawa ya uhakika”“Basi tuache masikhara, ni kweli mimi ndio nina mimba ila ni mimba ya mlinzi”“Oooh hiyo toa haraka sana, haifai hata kulea hiyo mimba”“Haya, nakusikiliza hiyo dawa”“Kuna dawa za aina mbili, kuna moja ni uhakika yani lazima itoke na kuna nyingine ni bahatinasibu, unahitaji ipi?”“Niambie hiyo ya uhakika ndio ninayoihitaji”“Sasa hiyo unatakiwa kuifanya mchana halafu wakati watu wote hawapo, inawezekana?”“Inawezekana ndio”“Kuna yale majani mekundu, nadhani unayakumbuka yale sijui kama huko yapo au nikuletee?”“Mmmmh ngoja niangalie maana huyu mama kapanda maua mengi sana, nitayaangalia kesho, nikipata nifanyeje?”“Yani unatakiwa hiyo dawa wakati unaichemsha asiione mtu halafu unainywa taratibu, ngoja nikutumie ujumbe wa vitu vya kuchanganyia humo. Ni chungu ila mambo fasta tu”“Sawa sawa, nitumie huo ujumbe”Kwakweli Vaileth alikuwa na hamu sana ya kufanikisha lile jambo ili ajihisi sawa kabisa kwani mambo ya Junior yalimchosha sana.Kulipokucha, mama Sarah alishtuliwa na sauti ya mwanae ambaye alimuuliza mama yake,“Mama Elly yuko wapi?”“Kwanini unaniuliza hivyo?”“Mama, mamake Elly kanipigia simu kuwa Elly hayupo nyumbani kwao na amejaribu kuulizia kote alipodhani yupo ila kaambiwa kuwa hayupo. Je Elly yuko wapi mama?”“Naomba leo nikamtafute huyo Elly halafu nitakupa jibu mwanangu, nenda shule tu halafu nitafanyia kazi jambo hilo”“Ona sasa mama, umesahau hata kama leo sio siku ya shule, leo ni Jumamosi ujue!”“Oooh samahani mwanangu, labda kuchanganyikiwa tu. Nitamtafuta usijali, vipi leo utashinda siku nzima nyumbani?”“Hapana, nitaenda kwa mama mkubwa kumsalimia nimemkumbuka sana”“Sawa, kamsalimie sana”Mama Sarah kwa muda huo, alijiandaa na kuondoka zake na safari yake ya kwanza ni hospitali kumuangalia Elly ambaye bado hakuwa na hali nzuri kutokana na kile kipigo alichokipata, basi mama Sarah alimuomba daktari ajitahidi sana katika kumpa huduma zote huyo Elly, kisha akamuachia hela nyingine. Na kwa wakati huo aliondoka moja kwa moja na kwenda mpaka kwenye biashara ya Sia ili kuweza kuongea nae kuhusu Elly, alimkuta kwenye biashara na kumuita pembeni na kuanza kuongea nae,“Ndugu yangu, mama mwenzangu naomba tuongee jambo hili”“Yani kabla ya hilo jambo, sipo sawa kabisa ujue, mwanangu Elly hajulikani alipo, nimeenda hadi shule kumuulizia ingawa leo sio siku ya shule, cha kushangaza nimeambiwa na mlinzi wa pale kuwa jana aliondoka na wewe. Niambie kwanza yuko wapi mwanangu Elly?”“Ndio hilo jambo nililokuwa nataka kuongea na wewe, ni hivi Elly anaumwa na yupo hospitali”Sia alishtuka sana na kuuliza kwa makini,“Anaumwa nini tena?”“Tulia kwanza, usiwe na papara utajua tu ukweli”Mara mama Sarah alipigiwa simu na daktari na kupewa ujumbe kuwa Elly anahitaji damu kwani katokwa na damu nyingi sana, kwahiyo ikabidi mama Sarah amwambie Sia waende nae hospitali kwa muda huo.Kwakweli Sia alikubali kwani kwa siku hiyo hata hakuwa akifanya biashara kama siku zote kwani alikuwa akiwaza kuwa mtoto Elly yuko wapi.Leo, baba Angel aliona ni vyema kwenda ofisini kwake kwani alikuwa na mambo mengi ya kufanya huko ofisini, pia aliona kuna umuhimu wa mtu kwenda kiwandani basi alimuomba Erick aende ambapo Erick aliomba kwenda na Erica huko kiwandani, kwahiyo walijiandaa na kwenda kiwandani, halafu baba Angel nae ndipo alipoondoka na moja kwa moja kwenda ofisini kwake. Kwahiyo nyumbani alibaki tu mama Angel pamoja na Vaileth, basi mama Angel alianza kuongea na Vaileth,“Hivi Vai, nasikia huko kwenu watoto huwa wanatembea haraka sana, huwa mnawafanya nini?”Vaileth alicheka kidogo na kusema,“Ni bibi zetu hao ndio wanadawa za kimila hatari, yani mtoto ili atembee haraka huwa wanamchanjia na mavi ya panya”“Kheee Vai, mavi ya panya tena!!”“Ndio, kule panya ni wengi sana, si unajua kijijini tena, tofauti na hapa kwako hata mende tu kumpata ni adimu”Mama Angel alicheka na kusema,“Naogopa mende mimi balaa jamani, yani ndiomana huwa nawaita wale wa kupulizia dawa kwenye chemba za vyoo ili nisiwapate hao mende kabisa, nawaogopa sana. Ila mimi hayo mambo ya kumchanja mwanangu na mavi ya panya mmmh siyawezi”Vaileth akacheka na kusema,“Hata ukitaka mtoto aongee upese dawa ipo”“Mmmh nyie nadhani mna dawa hata ya kutolea mimba nyie”Vaileth alicheka kiasi na kuomba akaendelee na kazi zingine huku akitamani sana mama Angel aweze kuondoka kwa siku hiyo ili yeye aweze kufanya dawa zake alizoambiwa na ndugu yake Prisca.Baba Angel akiwa ofisini, siku ya leo alimuita yule mama muuza matunda ili kuongea nae kuhusu kile alichokuwa ameambiwa na Sia maana hata alishindwa kuamini vizuri, basi alimuita ofisini kwake na kuanza kuongea nae,“Mama, unakumbuka matunda ya mwisho kunipatia mimi?”“Nakumbuka ndio”“Uliyatoa wapi yale matunda? Na unajua kwanini siku hizi sili matunda yako?”“Hapana sijui ni kwanini huli, ila yale matunda kiukweli kabisa kuna mama aliniletea ili nikupatie na aliniambia kuwa atanisaidia kuniongezea mtaji na alisema wewe ni rafiki yake sana ila hakutaka ujue kama ni yeye amekupatia yale matunda”“Ila kwanini hukujiuliza kabla ya kuniletea mama yangu? Unajua ungeniua?”Yule mama alikuwa kimya kwa muda huku akitoa macho yake, kisha baba Angel aliendelea kuongea,“Kwenye yale matunda kulikuwa na sumu, kwani baada ya kula tu nilirudi nyumbani nikiwa na hali mbaya. Mke wangu aliniwahisha hospitali na kufanya niweze kupata matibabu haraka ila bila ya hivyo ningekufa mimi”“Aaaaah naomba unisamehe baba yangu”Huyu mama alipiga magoti huku akimsihi baba Angel amsamehe na machozi yakimtoka, huku akisema,“Tamaa hii jamani, tamaa ya pesa ndio iliyoniponza. Naomba unisamehe sana, nilitaka kutanua biashara yangu, hata sikujua kama kuna kibaya kwenye yale matunda”Baba Angel alimuinua pale na kuendelea kuongea nae,“Ila huyo mwanamke hakukwambia lengo lake kwangu ni nini?”“Hakuniambia, na kama ningejua basi kwa hakika nisingethubutu kukupatia yale matunda. Naomba unisamehe sana”“Haya, amekupatia hiyo hela ya kuongeza mtaji wako?”“Hapana, mwanzoni alikuwa anakuja mara kwa mara ila kuna siku alikuja na chakula na kutaka nikuletee kile chakula, akanipatia laki moja kwa kazi hiyo, hapo nilishtuka na kukataa kwani sio kitu cha kawaida kusema nikuletee chakula halafu anipe laki moja ya kazi hiyo, nilivyokataa ndio akaondoka na hakurudi tena”“Duh!! Kuna kitu umenifungua, huyo mama yukoje?”“Ni mweupe sana, ana mwili kiasi, pia ni mrefu. Halafu ni mzuri, hata sikumtegemea kama anaweza kufanya kitu kama hiko”“Asante kwa taarifa hiyo, nashukuru. Basi hiyo ndio sababu ya mimi kutokula matunda yako tena”Huyu mama alikazana kumuomba baba Angel msamaha ila baba Angel alimwambia kuwa ameshamsamehe na kufanya huyu mama aweze kwenda kuendelea na kazi zake zingine.Mchana wa siku hiyo, mama Angel alipigiwa simu na kudai kuwa inabidi aondoke kwa muda huo, basi alimuaga Vaileth na kumuachia mtoto kama kawaida.Kwa Vaileth lile swala la mama Angel kuondoka lilikuwa ni swala la muhimu sana kwake, kwani alipoondoka tu, ndipo na yeye alipoanza kufanya ile dawa ambayo alielekezwa na Prisca kuona kama itafanya kazi mapema kama alivyoambiwa, alienda kutafuta na kupata majani aliyoambiwa, alichanganya vyote alivyoambiwa maana vyote vilikuwepo kule ndani, kisha alibandika jikoni na kuanza kuchemsha.Wakati yupo jikoni, alishangaa kuna mgeni ameingia ndani na moja kwa moja kuingia kule jikoni, ambapo alishtuka sana kwani hakumtegemea mgeni huyu kwa wakati huu, alimuangalia kwa mshtuko,“Kheee Sarah!”“Ndio ni mimi, unapika nini dada?”Kabla hata Vaileth hajamjibu, tayari Sarah alishasogelea hadi lile sufuria ambalo lilikuwa jikoni likichemka ile dawa na kumfanya Vaileth achukie sana ila hakuwa na cha kufanya kwa Sarah, na yeye Sarah alishangaa sana kumuona Vaileth kachukia kwa namna ile,“Kwani tatizo nini dada mbona unaonekana umechukia?”“Hakuna kitu”Basi Vaileth aliipua ile dawa maana hata hakuona umuhimu tena wa kuendelea kuichemsha ile dawa maana ishakosewa masharti tayari, basi akatoka na Sarah mpaka sebleni na kumuuliza,“Kwani tatizo lako nini Sarah?”“Mbona unaniuliza kwa ukali hivyo?”“Nisamehe, samahani nimekuuliza tu kuwa tatizo ni nini?”“Leo, nimeenda kwa mamangu mkubwa kumsalimia na lengo langu siku ya leo nimalizie huko ila nimemkuta Junior”Kidogo hii habari ilimshtua Vaileth na kumfanya aulize vizuri zaidi kwani aliweza kupata picha kuwa huyo mtu atakuwa ndio mama Linah,“Duh! Huyo mamako mkubwa anaitwa nani?”“Jina lake halisi anaitwa Linah”“Duh! Kwahiyo ndio umemkuta Junior huko?”“Ndio, tena hana hata habari nilitaka nije nimwambie mama hapa”“Mmmh usimwambie hiko kitu atachukia sana”Mara mama Angel nae alikuwa amerudi muda huo na kuuliza kwa makini kuwa ni kitu gani ambacho anatakiwa kufichwa na Sarah, ni hapo hapo Sarah aliporopoka kuwa Junior yupo kwa mamake mkubwa na kumfanya mama Angel achukie sana huku akifikiria kitu cha kufanya ili kumtoa Junior kwa huyo Linah.Baba Angel akiwa anaendelea na kazi zake pale ofisini alipigiwa simu na mke wake na kuambiwa ule ujumbe kuwa Junior yupo kwa Linaha alichukia sana na kwa muda huo huo aliamua kwenda nyumbani kwake, kisha alipofika kwake tu aliomba kuondoka na Sarah ili kwenda kuonyeshwa nyumbani kwa Linah, kwahiyo Sarah aliondoka na baba Angel na moja kwa moja kwenda nae nyumbani kwa mamake mkubwa.Basi baba Angel, alisimamisha gari na kumtaka Sarah amsubiri kwenye gari lake halafu yeye ndio alishuka kwenda kumfata Linah ambaye alionekana nje ya nyumba yake kwa muda huo.Baba Angel alimsogelea pale karibu na kumsalimia kisha akamwambia,“Naomba niitie Junior”Linah alienda ndani na kumuita Junior, kisha baba Angel aliondoka na Junior kwenda nae kwenye gari lake, yani hata Linah hakusema jambo lolote lile kuwakatalia kuwa wasiondoke wala nini.Moja kwa moja baba Angel aliondoa gari lake hadi nyumbani kwakina Sarah ambako alimuacha Sarah huko halafu yeye alienda nyumbani kwake.Mama Sarah na Sia walipofika hospitali, moja kwa moja mama Sarah aliongea na Sia ili waweze kuona kama anaweza kumchangia Elly damu, kwakweli Sia alikubali tu na daktari muda ule ule aliamua kumpima damu Sia aone kama ataweza kumchangia mtoto wake, ila cha kushangaza damu ya Sia haikuendana na damu ya Elly, ikabidi watafute njia nyingine, ndipo mama Sarah alipouliza kama yeye ataweza kumchangia,“Kama inawezekana basi mimi nitolewe damu nimchangie”Basi walienda kumpima na kukuta damu yake inaendana na Elly, ikabidi atolewe yeye damu na aende kuongezewa Elly.Basi mama Sarah alikaa na Sia kwa muda huu na kumuuliza swali,“Inawezekanaje mama na mtoto msiendane damu?”“Inawezekana ndio, labda karithi kwa baba yake?”“Oooh kweli lakini usemayo, inawezekana hiyo kitu. Ila nashukuru nimeweza kumtolea damu Elly natumai atakuwa mzima kabisa”“Ila hujaniambia kuwa alifanya nini?”“Unajua nini kuna mahali nilienda kumuonyesha Elly ila alikazana kusema kuwa anataka kurudi nyumbani basi nikamruhusu kuwa arudi, cha kushangaza sasa wakati anarudi sijui vijana gani huko wakampiga sana, kwa bahati nzuri nami ilirudi eneo lile ndio nikamuokoa”“Ooooh jamani, mtoto wangu mpendwa dah! Nimeumia sana”“Pole, ila atapona kabisa”Basi walikaa kaa kidogo na kisha mama Sarah alimlazimisha Sia kuhusu kumrudisha nyumbani kwake kwa muda huo kwani muda ulikuwa umeenda sana.Baba Angel alifika na Junior nyumbani kwake moja kwa moja yani alikuwa na hasira kiasi kwamba alishindwa hata kuongea na Junior kuhusu jambo lolote, basi mama Angel ndio aliamua kwenda kuongea na Junior,“Hivi wewe mtoto una nini lakini? Yani unaacha kuwa shule kweli unaenda kwa huyo mwanamke mtu mzima? Unajua umuhimu wa elimu wewe!”“Nisamehe mamdogo”“Unadhani hiyo nisamehe yako inasaidia kitu gani? Hiyo nisamehe yako ndio inaenda kukufaurisha mitihani au kitu gani? Hebu niambie ukweli kwanza ni kitu gani kinakufanya hadi unakazana kuwa kwa huyo mwanamke?”“Nisamehe mamdogo, sitarudia tena”“Ulisema hivi hivi mwanzoni na kitu gani umefanya sasa? Yani Junior tunahangaika kukusomesha halafu unaenda kufanya ujinga kweli!! Sijapenda kabisa kabisa, kesho nitakupeleka mwenyewe shule mjinga sana wewe”Mama Angel hata hakufurahishwa na majibu yale ya Junior ya kutokusema ukweli, ila alipotoka kuongea nae hapo aliamua kumpigia simu dada yake ili kumueleza jambo lililotokea, kwakweli mama Junior alichukia sana na kuahidi kuwa kesho ataenda pale nyumbani ili na yeye amseme pia mtoto wake na wampeleke wote shuleni kwao,“Kwakweli huyu Junior kanikera sana, yani hata nimejikuta kutokujua cha kufanya kwakweli. Hivi hilo jinga litamaliza shule kweli jamani!”“Tumuombe tu Mungu kwakweli, maana karudi kwa yule yule mwanamama tuliyegombana nae jamani dah!! Nimechukia sana”Basi mama Angel aliongea na dada yake pale na kukata simu.Usiku wa siku hii, Erica kabla ya kulala alienda moja kwa mona chumbani kwa Erick na kuanza kuongea nae,“Hivi yule tuliyekutana nae leo umemuelewa?”Erick alifikiria kidogo kwani alishasahau ni mtu gani ambaye walikutana nae kwa siku hiyo, kisha alimuuliza Erica,“Yupi huyo?”“Si yule aliyekuwa akitushangaa pale njiani”“Oooooh nimemkumbuka, yule aliyesema kuwa hatuna adabu eeeh!”“Ndio, hivi kwanini watu wakituona mimi na wewe wanatuhisi tofauti? Yani kwanini huwa hawahisi kuwa sisi ni ndugu na wanahisi sisi ni wapenzi?”“Nadhani ni sababu ya kile kiapo ambacho tulisema kuwa mimi na wewe tusiwe na marafiki wengine”“Basi inabidi tukavunje hiko kiapo au unasemaje?”Erick alibaki kimya kwa muda kidogo mpaka Erica alimshtua na kumwambia tena,“Inabidi tukavunje hiko kiapo”“Kwakweli sipo tayari kwa hilo, sitaki kuona ukizungukwa na marafiki kama Bahati na Abdu kwahiyo siwezi kuvunja hiko kiapo kwakweli”Erick alionyesha hadi kunyong’onyea wakati Erica akimkazania kuvunja kile kiapo, basi ilibidi Erica atoe ushauri kuwa wacheze karata, halafu Erica akaenda kuchukua karata chumbani kwake na kurudi kuanza kucheza na Erick na kama kawaida walicheza hadi usiku sana na mwishowe walijikuta wakipatwa na usingizi tu mule mule ndani kwa Erick.Junior alipatwa na aibu sana, kwahiyo aliona ni vyema kumuomba msamaha hata Vaileth maana aliona ni wazi kuwa amemkera kila mtu mule ndani, basi alitoka chumbani kwake na kwenda kugonga chumbani kwa Vaileth ila hakufunguliwa mlango, basi alirudi chumbani kwake na kuanza kumtafuta Vaileth kwa njia ya ujumbe mfupi maana simu alimpigia sana ila Vaileth hakupokea simu za Junior kabisa, akamtumia ujumbe,“Vaileth mpenzi wangu kwanini lakini umekuwa hivyo?”“Mjinga wewe tena usinizoee kabisa”“Ndio yamekuwa hayo kweli? Umesahau kila nilichokifanya kwaajili yako?”“Usinibabaishe huko, ni kipi ulichofanya kwangu chenye umaana zaidi ya uhuni wako tu!!”“Hujui tu Vaileth ni kwanini nimekutwa na yule mama, nilikuwa na shida na pesa mimi kwaajili ya kutoa ile mimba yako, sikuwa na pengine pa kupata pesa zaidi ya kwa yule mama”“Mjinga wewe, ulishindwa vipi kusema gtulee tu!”“Sasa tutaleaje Vai wakati bado nasoma?”“Usinizoee, endelea na kusoma kwako”Muda huu Vaileth alizima na simu kabisa kwani zile jumbe kwa Junior zilikuwa haziendi tena kwa Vaileth, kwakweli Junior alijihisi vibaya sana na kusema,“Haya ndio matatizo ya wanawake, yani mtu namsaidia mwenyewe halafu anaona kamavile nimefanya makusudi, mjinga kweli huyu mwanamke. Aaaargh hawa wanawake wananichanganya akili mno, ningejua ningemuacha na mimba yake ajijue nayo mwenyewe”Alichukia na kuamua kulala tu kwa muda huo.Mama Angel aliamka mapema sana kwa siku hii sababu ya kuamka kwa mtoto wake mdogo, basi alianza kushughulika nae pale, muda kidogo baba Angel nae aliamka kutokana na kelele za yule mtoto,“Oooh mume wangu pole jamani, endelea kupumzika”Mama Angel alitoka na yule mtoto kwani alitaka amuandalie maziwa, basi moja kwa moja alienda nae chumbani kwa Erica ili Erica amshike mdogo wake ila alishangaa kutokumuona,“Kheee mapema yote hii haka katoto kameenda wapi jamani!”Akapata wazo la kwenda kumuangalia chumbani kwa Erick na kweli alimkuta kalala huko akiwa hana hata habari na karata zao zikiwa pembeni, yani mama yake alimshtua pale na kufanya hata Erick ashtuke pia,“Hivi nyinyi kwanini mnapenda kucheza karata hadi usiku sana, mna matatizo gani? Au ndio midawa mliyopewa kuwa mchzage karata!”Erica na Erick walishangaa maana hawakuwa wakijua kuhusu hiyo mada ya dawa, basi Erica alimuuliza mama yake,“Dawa gani mama?”“Mnajiona mpo sawa? Watu gani nyie mnacheza karata hadi usiku halafu mnajikuta mmelala, mimi sijawahi kuona hili jambo kwakweli, sijapata kujua kama nyie watoto mtakuwa wajinga kiasi hiki. Haya Erica mshike mdogo wako”Alimpa mtoto Erica na kutoka zake, basi Erica alikaa na yule mtoto, na wakati huo hata Erick alikuwa ameamka na kukaa kwahiyo walianza kuongea,“Dawa gani anazozisema mama kuwa tumekunywa?”“Mmmh hata sijui, ila kwanini tukicheza pamoja karata basi tunacheza hadi usiku sana na mwishowe tunajikuta tumelala yani kama hatujalala chumbani kwako basi tutalala huku kwangu kwanini?”“Hata sielewi pia, tunatakiwa kujua ni dawa gani zinazosemwa na mama”Kisha Erica aliinuka na yule mdogo wake hadi sebleni huku akijiuliza kuhusu dawa alizoambiwa na mama yake.Ila alipokaa pale sebleni na mtoto alijikuta akisinzia na kujiwa na ndoto ambapo alikuja kushtuliwa na mama yake,“Yani Erica umeshika mtoto huku umelala jamani!!”“Nisamehe mama, ila nimeota”“Umeota nini?”“Nimeota kuwa jana kaka Junior mlienda kumfata na kumkuta kwa yule mama wa siku ile, halafu nimeota ulirudi na kumsema sana Junior”Mama Angel alishtuka kidogo, kwani wakaina Erica waliporudi hawakujua chochote kilichoendelea kwani muda huo hata Junior alikuwa amelala, basi akaanza kukumbuka kitu alichoambiwa na mama yake kuhusu huyu mtoto wake, basi alimsogelea karibu na kumuuliza,“Umeota nini kingine?”“Nimeota Junior akipewa hela na yule mama, yani Junior anamfata yule mama sababu ya pesa zake”Muda huu Junior nae alikuwa akitoka chumbani, kwahiyo alijikuta akisimama tu kwenye ngazi huku akimsikiliza Erica alivyokuwa akifunguka kuhusu mahusiano yake na yule mmama.Leo mama Sarah alifikiria sana jambo na aliona ni vyema kama akienda kwenye ilea lama ya jina lake kugundua ukweli, kwani alitaka kujua imekuwaje jina lake kuwepo sehemu ile, basi alijiandaa na kuondoka pale nyumbani kwake.Moja kwa moja alienda kwenye ule msitu mdogo na kwenda karibu na mto ule mdogo ili kujua ni kitu gani kilitokea, ila alikuta kuna mtu amesimama karibu na ule mti akiuangalia basi mama Sarah alishtuka na kumsalimia yule mtu, ambapo yule mtu aligeuka na kumfanya mama Sarah ashtuke sana kwani hakutegemea kumuona mahali hapo, mtu huyu alikuwa ni Derrick. Moja kwa moja alienda kwenye ule msitu mdogo na kwenda karibu na mto ule mdogo ili kujua ni kitu gani kilitokea, ila alikuta kuna mtu amesimama karibu na ule mti akiuangalia basi mama Sarah alishtuka na kumsalimia yule mtu, ambapo yule mtu aligeuka na kumfanya mama Sarah ashtuke sana kwani hakutegemea kumuona mahali hapo, mtu huyu alikuwa ni Derrick.Mama Sarah alimshangaa sana na kusema kwa mshangao,“Derrick!!”“Ndio, ni mimi. Derrick nipo hapa, nimefurahi kukuona, umekuja kufanya nini hapa?”“Kwani wewe unafanya nini hapa?”“Si unaona huu mti unajina lako!”“Kwahiyo kama una jina langu?”“Nakumbuka siku niliyoandika jina hili ni siku nilipogundua kuwa Elly ni mtoto wangu halafu sio mtoto niliyezaa na Oliva, niliwaza sana kuwa itakuwa nimezaa na nani Elly maana nina hisia asilimia zote kuwa ni mtoto wangu. Ila nilikuja na kuandika jina lako kwenye mti hapa, kuna kitu kiliniambia kuwa kama ikitokea damu ya Elly ikazunguka mti huu basi huyu ndio atakuwa mama mzazi wa Elly, na pia Elly atahitaji damu sababu damu yake imetoka halafu huyu mama atamuongezea damu. Sijui hilo jambo litatokea lini, ila nimekuja leo na kuona mti umezungukwa na damu iliyoganda sijui ndio ya Elly au ni nini”Mama Sarah alipumua kwanza kwasababu kama alikosa usemi hivi, alijikuta akikaa pale chini kabisa na kumuuliza Derrick,“Umejuaje kuwa vyote hivyo vimetokea?”“Kwahiyo ndio ilivyokuwa? Elly ni mwanao Manka, ni furaha sana kugundua hilo”“Hebu nisikie tena unisikie kwa makini. Mimi sio mwanaume kusema nilimpa mwanamke mimba akazaa huko halafu sijui kuhusu mtoto ndio nije kugundua badae, ila mimi ni mwanamke niliyebeba mimba kwa miezi tisa kamili, nikashikwa na uchungu na kwenda kuzaa. Katika maisha yangu sijawahi kuzaa mtoto mwingine zaidi ya Sarah tu, ndio mtoto niliyezaa, nikamnyonyesha, nikamlea na nimemkuza, sikuelewi unavyoniambia kuwa Elly ni mwanaungu, unasema hivyo kwa vigezo gani?Mbona Elly ni mtoto wa Sia na Erick!!”“Sikia nikwambie, labda kama Sia hajakwambia ukweli, ni hivi yule mtoto sio wa Sia hata yeye mwenyewe hakujua wazazi wa yule mtoto, ila Mungu ni mwaminifu, kamleta kwangu kwanza na kunifanya nimtambue kuwa ni mtoto wangu, na sasa nimetambua kuwa nimezaa na wewe”“Loh!! Kwakweli unanichanganya yani sikuelewi hata kidogo kabisa, unanichanganya haswaaa”“Sijui ni kitu gani kipi, ila nina uhakika kuwa wewe ndio mama mzazi wa Elly”“Na Sarah je?”“Huenda ulipata mapacha, labda hospitali waliiba mtoto mmoja”“Uwiii mbona nitakuwa nimeumbuka mimi!”“Umeumbuka kivipi?”Mama Sarah hakujibu, kwani moja kwa moja alirudi kwenye gari lake na kupanda kisha alijisemea,“Nimezaaje mapacha bila kujua? Inamaana mwanangu mmoja walimuiba? Kama ni hivyo inamaana Sarah alitembea na kaka yake wa damu? Oooh nimeumbuka mimi jamani, watoto wangu kweli watembeleane? Inamaana mimi nimemuadhibu kiasi kile mwanangu? Nahisi kuchanganyikiwa kwakweli”Alihisi akili yake kutokuwa sawa kabisa, hivyobasi moja kwa moja alienda kwenye hoteli moja na kukodi chumba kisha aliagiza pombe humo na kuanza kuzinywa, alichukua simu kwa muda huo na kumpigia dokta ambaye alihusika na kujifungua kwake,“Eti dokta, inawezekana mimi nilijifungua mapacha?”“Inawezekana ndio”“Kivipi? Niambie ukweli, nilijifungua mapacha eeeh! Wa kike na wa kiume?”Huyu dokta alikata simu na kumfanya mama Sarah akili yake iwe mbovu kabisa kwa wakati huo, basi aliagiza vinywaji na kunywa sana kama mtu aliyechanganyikiwa kabisa.Mama Angel leo anaamua kukaa na Erica kwani aliona anatakiwa kuongea vitu vingi sana na huyu mtoto kwani hakumuelewa ndoto aliyosema ameiota,“Erica mwanangu, huwa unaota nini na nini?”“Naota mambo mengi tu”“Mfano”“Kabla hamjapata ukweli kuhusu kutoka kwa mimba ya Daima niliota kuwa mimba hiyo imetoka”“Kheee mbona huwa husemi sasa?”“Vingi huwa namwambia Erick”“Mwanangu, naomba unieleze mambo yote ambayo huwa unaota kuhusiana na familia hii”Mama Angel alitaka kufahamu hiko kilichopo kwenye akili ya mwanae, ila Erica hakutaka kusema kwani angeweka wazi kuhusu mimba ya Vaileth na kumfanya Vaileth kuwa vibaya.Muda kidogo alifika mama Junior kama ambavyo walipanga ile jana yake, alimuita mwanae na kumsema sana kuhusu lile jambo ambalo amelifanya,“Mwanangu hakuna faida yoyote utakayopata kwa kufanya huo ujinga, zaidi zaidi unanidhalilisha mama yako na kufanya nizidi kutukanwa na baba yako. Kwanini lakini unafanya hivi mwanangu?”“Nisamehe mama”“Kuna muda hata hawa wanaokusomesha watachoka na kukuacha ukihangaika na maisha tu, kwakweli sijapenda kabisa”Kisha mama Angel nae alijiandaa na kuondoka pale nyumbani wakiwa wameongozana na Junior kwa lengo la kumrudisha shuleni.Kwahiyo nyumbani alibaki tu Vaileth pamoja na Erica na kuanza kuongea mambo mawili matatu yaliyopo pale, kwanza Vaileth alianza kwa kumshukuru Erica,“Kwanza nashukuru sana kwa kuendelea kunifichia siri yangu”“Lakini masharti ya hii siri yangu si unayajua?”“Ndio, nayajua”“Na mbona jana ulitaka kujaribu kuitoa hiyo mimba sababu wakati unachemsha dawa alikuja Sarah hapa nyumbani”“Khiiii ila wewe Erica sio mtu wa kawaida kabisa dah!! NImekutoa kwenye kundi la watu wa kawaida”“Hapana mimi ni wa kawaida sana, sema huwa naota hayo mambo yote ninayokwambia”“Sitarudia tena kutoa mimba, wala sitoitoa. Nitabaki nayo tu hii mimba na nitazaa ingawa nina mawazo sana kuwa nitaleaje?”“Utalea kama jinsi utakavyozaa, usiitoe hiyo mimba kabisa”Yani Erica alikuwa akiongea huku akimaanisha kitu alichokuwa akikiongea.Muda kidogo simu yao ya mezani ilikuwa ikiita, basi Erica alienda kupokea na kufurahi sana kwani alikuwa ni dada yake,“Jamani dada Angel nimekukumbuka sana, wote nyumbani tumekukumbuka sana. Sijui tutakuona lini?”“Mtaniona tu hata msijali, nampigia simu baba hapokei”“Yupo Kanisani umesahau leo ni lini?”“Kheee baba nae, siku hizi anachelewa kutoka namna hii. Akirudi nyumbani mwambie anipigie”Erica alifurahi sana kuongea na Angel kwa siku hiyo, basi aliagana nae huku akiwa na furaha sana.Siaalipotoka kanisani kwa siku ya leo, moja kwa moja alienda hospitali kumuona Elly kwani alijikuta akimkumbuka sana mwanae huyu ukizingatia alishazoea kuishi nae.Alipofika hospitali, kabla ya kwenda kumuona Elly kuna mtu alimuona na kumgundua, mtu huyu alikuwa ni dokta Jimmy, basi Sia aliamua kutumia muda huo kuanza kumfatilia dokta Jimmy hata hakuendelea tena na swala la kumuangalia mtoto pale hospitali.Dokta huyu alionekana na haraka sana kwani alipanda gari lake na kuondoka, muda huo Sia nae aliita bodaboda na kumtaka wamfatilie dokta yule hadi alipokuwa akielekea, ni kweli walimfatilia na moja kwa moja waliingia kwenye hoteli ambapo Sia alishuka na kuanza kumfatilia, ila kuna chumba alimuona akiingia ila yeye hakuweza kuingia ingawa alitamani kuingia humo. Ila alijibanza mahali na kuona dokta akitoka, na kuna mwanamke aliyefunga mlango ambapo Sia alimtambua vizuri sana yule mwanamke, basi moja kwa moja alimuacha yule dokta aondoke halafu yeye alienda hadi kugonga pale ambapo yule mwanamke alimfunbgulia mlango na Sia aliingia moja kwa moja ndani, kwakweli huyu mwanamke alimshangaa kidogo ila Sia alimwambia,“Bila shaka unaweza ukawa unanikumbuka kuwa mimi ni nani?”“Mmmh hapana”“Mimi naitwa Sia, niliwahi kuwa mpenzi wa boss wa mume wako”“Unamaanisha Erick?”“Ndio huyo huyo, kumbe boss wa mume wako unamfahamu eeeh!! Kuna nini kinachoendelea kati yako na huyu aliyetoka yani dokta Jimmy?”“Mmmh ni shemeji yangu huyu”“Unajua kama anatafutwa na watu wengi sana kutokana na aliyoyafanya?”“Mimi sijui kitu”“Na mbona unaishi hotelini inamaana siku hizi mna utajiri wa kuishi maisha haya?”“Kheee ndio maswali gani hayo umeniuliza?”“Mumeo yuko wapi? Hivi unajua nakuuliza maswali ya msingi sana”“Ila mimi nilimwambia Moses, haya mambo nilijua tu siku moja itakuwa tatizo”“Nadhani unaelewa ninachoweza kufanya, basi nisikilize ni hivi, naomba namba za dokta Jimmy ila usimwambie kama tumeonana mimi na wewe na wala usimwambie kama nimechukua namba kwako”Huyu mwanamke alikuwa akimtambua Sia vizuri kabisa ingawa mwanzoni alidai kuwa hamtambui Sia, basi muda huo huo alitaja namba za dokta Jimmy na kumfanya Sia aondoke akiwa amepata mawasiliano ya dokta huyo.Moja kwa moja alirudi kwa yule dereva na kumtaka ampeleke tu nyumbani kwake, kwakweli huku walipoenda ilikuwa ni mbali sana, na kiukweli dereva alifanya kazi kubwa ya kufatilia na kupoteza muda kwenye eneo moja.Walifika nyumbani kwa Sia ambapo tayari kulikuwa na giza, Sia alimuuliza yule wa bodaboda kuwa amlipe pesa ngapi,“Hapa labda laki moja na elfu hamsini”“Duh! Kama nilikodi kosta kumbe bodaboda”“Sasa unadhani ni pesa ngapi? Nimefanya kazi kubwa sana, jumlisha na mafuta yangu”“Ila kumbuka wakati tunarudi nilitoa elfu ishirini ukajaza mafuta pale”“Ndio, ila mafuta niliyotumia wakati wa kwenda je? Tena mimi nimekuhurumia kufanya kazi yako bila ya maswali mengi”Sia aliamua kwenda tu kutoa hiyo hela kwani alijua wazi kama akimwambia baba Angel basi atapata hela zaidi ya hiyo.Aliamua tu kupumzika kwa muda huo, maana alikuwa kachoka na ule upepo wa pikipiki katika kumfatilia dokta Jimmy.Usiku wa leo, mama Angel anakaa na mumewe chumbani na kuanza kuzungumza kuhusu habari za Erica na ndoto alizosema huwa anaota, ni hapo baba Angel alipokumbuka ujumbe aliopewa na Erica kuwa amtafute, basi moja kwa moja baba Angel alimpigia simu mwalimu mlezi wa pale na kuuliza kama kwa muda huo ataweza kuongea na Angel,“Ooooh Angel kwa muda huu! Wamelala, labda umpigie simu kesho”“Basi nitajitahidi na kuja mwenyewe huko ili nimuone”Basi alikata simu kisha baba Angel akamwambia mke wake,“Ngoja kesho niache mambo yote niende kumtazama Angel kwanza, itakuwa katukumbuka sana. Dah sijui shule anamaliza lini maana hata mimi nimemkumbuka sana”Waliongea sana na baba Angel alipanga kuwa asubuhi na mapema wakati wakina Erica wakienda shuleni na yeye ndio aondoke na kwenda moja kwa moja kwenye shule ya wakina Angel ili kuweza kumsalimia.Ila katika ile mada ya kuhusu Erica, baba Angel akasema jambo,“Ila mke wangu kama mtoto wetu huwa anaota mambo ya ukweli, inatakiwa tumshirikishe kwenye vitu vingi. Inawezekana hata haya tunayohangaika nayo ikawa yeye akapata jibu mapema, tunapomshirikisha ndio atapata mwanga”“Mmmh tumshirikishe kuwa walichomwa sindani! Mbona hapo pagumu sana mume wangu!”“Hapo pagumu kweli, na hakuna namna ila cha muhimu ni kumuuliza mara kwa mara ili tujue ni kitu gani ambacho huyu mtoto huwa anakiota kwani itasaidia kwasisi kufahamu yanayoendelea juu yake”Basi waliongea na kuamua kulala tu kwa muda huo.Kulipokucha, baba Angel aliamka na kuanza kujiandaa ili kwenda kumsalimia mtoto wao ila mama Angel nae akaona ni vyema aongozane na mume wake na kumwambia,“Twende wote kwakweli, mbona na mimi nimejikuta nikitaka kwenda kumsalimia”“Sawa, hakuna tatizo lolote”Mama Angel alianza kujiandaa, wakati huu baba Angel alitoka kabisa sebleni kumsubiria mke wake.Akiwa pale sebleni alimuona Erica akiwa ametoka na sare za shule, akamsalimia pale basi baba Angel alimuuliza,“Wewe mbona umechelewa hivi!! Si gari la shule litakuwa limekuacha?”“Ni kweli nimechelewa hata hilo gari limeondoka, ila baba naomba usiende leo kumuona dada Angel”“Kwanini unasema hivyo?”“Nimeota vibaya, nimeota kuwa wewe na mama mkienda huko leo mtapata ajali”Baba Angel alishtuka kidogo na kumuangalia kwa makini binti yake, kisha akamuuliza,“Umejuaje kama naenda na mama yako?”“Sijui ila nimeota tu kuwa unaenda na mama”“Duh!! Wewe mtoto hapana kwakweli”“Sasa nimeota baba ndiomana nimeshindwa hata kuondoka bila ya kuwaambia hiko kitu”Mama Angel alitoka ndani akiwa kamaliza kujiandaa, ila na yeye alishtushwa na ile taarifa ya Erica, basi mama Angel alimuuliza zaidi,“Yani Erica umeona sisi tukipata ajali?”“Ndio mama, nimeota. Mara nyingine sioni sura kwenye ndoto ila naelewa inaponielekeza”“Duh! Kwahiyo umeota tukienda huko tuitapata ajali?”“Ndio, tena katika hiyo ajali wewe mama utaumia sana, haswaa mkono wako wa kulia yani hadi mfupa utateguka”“Duh!!”“Sijui ni wapi anasoma dada Angel ila nimeota kuwa hiyo ajali mnapata kwenye njiapanda ya karibu na shule ya wakina dada Angel”“Duh!! Basi mwanangu, kweli kuna njiapanda pale. Hatuendi tena tumeahirisha, ngoja nimwambie dereva tu akupeleke shule”Kisha Erica alitoka nje kwani baba Angel aliwasiliana na dereva kwenye simu, baba Angel na mama Angel walibaki wakitazamana tu yani hiyo safari waliihairisha kabisa yani kilichoendelea hata kwenda kazini pia baba Angel alihairisha yani akaona ni vyema kwa siku hiyo kubaki tu nyumbani bila kwenda popote pale.Mama Sarah anaamka akiwa hotelini na kukumbuka kuwa jana yake hakurudi kabisa nyumbani kwake, nasi aliinuka na kuoga kabisa kisha akaenda moja kwa moja hospitali kumuangalia Elly, na kweli alimkuta akiendelea vizuri basi aliongea na daktari ambaye alimpa ruhusa na kumfanya mama Sarah kuamua kwenda nae nyumbani kwake.Yani walipanda kwenye gari la mama Sarah ila Elly hakuwa na amani kabisa yani alijiona kama anaenda kutupwa tena, ila mule kwenye gari mama Sarah alianza kuongea nae,“Elly naona huna amani kabisa kuwa nami karibu, hebu naomba usahau yote yaliyopita na tunaenda kuanza maisha mapya, utasoma na kufurahi kama zamani”Elly aliitikia tu kwa kichwa ila alikuwa akiogopa hata kuongea kutokana na kipigo alichokipata hapo kabla.Basi moja kwa moja wanenda hadi nyumbani kwa mama Sarah na kufika pale ambapo mama Sarah anampeleka Elly moja kwa moja chumbani huku kichwani akijiwa na dhana kuwa huenda Elly akawa ni pacha wa Sarah.Anamngoja Sarah arudi jioni, na anapofika tu anaanza kuongea nae,“Sarah, nakuomba mwanangu huyu Elly umuheshimu kama kaka yako kabisa”“Lakini mama, Elly sio kaka yangu”Mama Sarah alitokwa na machozi na kumwambia binti yake,“Kuna mambo mtu huwezi kuyaelewa na utaona kama wanaoyaongea wapo kupiga kelele tu, ila kiukweli wewe na Ellu ni ndugu tena ndugu wa damu”“Kwahiyo yule wa siku ile ndio baba yetu?”“Yupi huyo?”“Mama Erick alitupeleka kw ambaba mmoja hivi, mimi na Elly na kudai kuwa yule ni baba yetu ila mimi sikubali hilo swala kabisa. Najua baba yangu alishakufa, usiniambie vingine mama sijui kama naweza kukuelewa”“Na wala sina haja ya kukwambia vingine na sijasema kuwa huyo sijui nani ndio baba hyako hapana, ila nimesema kuwa Elly ni ndugu yako. Muheshimu kama kaka yako”“Ila nimempenda mama”“Usiniletee wazimu huo Sarah, nimekwambia muheshimu Elly kama kaka yako”“Hapana mama, nampenda Elly na siwezi kusahau nilichokuwa nimefanya nae”“Hivi wewe mtoto una wzimu au kitu gani?”“Hapana mama, siwezi kukuelewa kwa wewe kuniambia kuwa Elly ni ndugu yangu ikiwa nishafanya nae vingi, nishamtunuku usichana wangu”Mama Sarah alijikuta akichukia sana, kwa mara ya kwanza alijikuta akimnasa kibao mwanae na kumfanya Sarah akimbilie chumbani kwake akilia, kwakweli mama Sarah alijikuta tu akifanya vile ingawa hajawahi kumpiga Sarah toka alipokuwa mdogo kwani alimpenda sana mtoto huyu na alimuona kama ndio maisha yake, Ila kwa siku hiyo hata yeye alikaa chini na kujishangaa kwa muda kwa kitendo chake cha kumpiga Sarah wakati hajawahi kufanya hivyo hata mara moja.Alitoka chumbani kwake na kwenda mlangoni kwa Sarah na kumgongea ila Sarah hakufungua mlango wala hakusema chochote kile na kumfanya mama Sarah apatwe na uchungu sana moyoni mwake.Sia alienda moja kwa moja ofisini kwa baba Angel ili amueleze yale yaliyojiri ila hakumkuta, ikabidi aende nyumbani kwa baba Angel ili hata kama akimkuta mama Angel amwambie yale mambo maana aliona ni sawa pia kufanya huvyo.Alifika nyumbani kwa mama Angel na kuingia ndani ambapo alimkuta Vaileth na kumuuliza,“Yuko wapi mama mwenye nyumba?”“Yupo kule kwenye bustani na baba”Basi Sia alienda moja kwa moja walipo, na kweli aliwaona kwenye bustani, roho ilimuuma ila hakutaka kuwaza hayo kwa muda huo, aliwasalimia pale na kuanza kuwaeleza kile ambacho alikutana nacho, kwakweli baba Angel alifurahi sana na kumpongeza Sia,“Kuna muda huwa upo vizuri sana Sia, unaweza kutupeleka kwenye hiyo hoteli?”“Ndio, napakumbuka vizuri sana”Mama Angel akachangia hapa,“Mmmh mnadhani tutawakuta tena!! Hivyo lazima yule atakuwa amewaambia na wamehama, hebu tuanze na hiyo namba kupiga”“Tumieni simu yangu maana kuna laini yangu ipo tu huwa haijulikani kirahisi kuwa ni yangu”Basi baba Angel alifanya hivyo na kuchukua simu ya Sia, kisha akapiga ile namba ambapo baada ya muda kidogo tu simu ilipoita ilipokelewa,“Hallow, nani mwenzangu?”“Nina shida na wewe dokta”“Kwani wewe ni nani?”“Tuonane kwanza ndio utajua mimi ni nani”“Kama hujitambulishi kwaheri”Ile simu ilikatwa muda ule ule, baba Angel alipojaribu kupiga tena ile simu haikupokelewa basi waliangaliana pale na kuanza kujadiliana,“Lazima kuna kitu kikubwa sana, ila nakuamini Sia huwezi kuacha kumfatilia huyu hadi tujue vingi zaidi”“Ninachohitaji kufahamu ni sehemu wanayoishi kwani nikifahamu hapo itakuwa ni rahisi zaidi kumpata”Walijaribu kupanga mambo kadhaa kisha Sia aliondoka zake na kurudi nyumbani kwani baba Angel alimuahidi kumpelekea pesa nyingine kwaajili ya kazi yake ya uchunguzi.Baada ya Sia kuondoka, ndipo mama Angel alipomwambia mume wake,“Unajua kwanini nimekataa tusiende huko kuwatafuta?”“Kwanini?”“Naogopa ndoto ya Erica, mmmh tusijepata ajali kweli bure”“Mmmh mke wangu, umeanza kuishi kwa hofu sasa. Kweli kuna kutoka hapa mmmh!!”Walijikuta wote wakicheka kwa pamoja maana kwa wakati huo wote walijikuta wakitawaliwa na hofu.Usiku huu mama Sarah akiwa chumbani kwake akiwaza jinsi ambavyo hapati ushirikiano mzuri na mwanae, muda huo huo alipigiwa simu na Rahim na kuanza kuongea nae,“Sijakusikia kwa siku hizi mbili tatu, upo sawa kweli!!”“Nipo sawa tu”“Nakuja nyumbani kwako, niandalie chakula”Mama Sarah alimkubalia tu, kwani kwa kiasi Fulani aliona kuwa ile kwake ni jambo jema ukizingatia alikuwa na mawazo mengi sana ambayo yalikuwa yakichanganya akili yake kwa kipindi hiko, basi moja kwa moja aliinuka na kwenda jikoni kupika ila alipika tu ilimradi maana hata hakuwa na furaha ya kufanya hivyo.Kweli baada ya muda kidogo Rahim alifika tena akiwa na begi la mgongoni, basi mama Sarah alimkaribisha vizuri kabisa na Rahim aliomba kupewa chakula alichodai kuwa aandaliwe, alitengewa na kula kile chakula na baada ya hapo alienda chumbani na mama Sarah kwani muda ulikuwa umeenda sana, halafu akatoa vinywaji kwenye begi alilokuwa amebeba,“Oooh halafu sikukuuliza kuwa umebeba nini humo?”“Ni nguo na hii mizinga mitatu tu”“Kheee hii si pombe kali? Unakunywaga pombe Rahim?”“Kwanini nisinywe? Nimemkosea nini Mungu hadi nisinywe pombe!”Mama Sarah alicheka na kwenda kuchukua glasi kisha yeye na Rahim walianza kunywa huku wakiongea kuhusu zile nguo ambazo Rahim amezibeba,“Na nguo hizi za nini?”“Nimepanga kuja kukaa huku wiki mbili kwa safari hii”“Duh!! Ya sasa kali”“Ni kali kweli, nimeamua kujitoa muhanga kwako maana nakupenda sana”Basi walikunywa sana zile pombe, na mpaka wakajikuta wamelewa na kulala pamoja.Kulipokucha asubuhi, mama Sarah alikuwa akijiangalia vizuri na kuwa kama mtu anayejuta kitu Fulani, basi Rahim alimuuliza,“Nini mawazo tena mpenzi?”“Unajua hatujatumia kinga usiku?”“Kinga ya nini? Unahofia kupata mimba au kitu gani?”“Kinga ni bora maana tunajitenga na ukimwi pia”“Inamaana siku zote hizi huniamini jamani au nini? Hivi inawezekanaje mtu kama mimi kupata ukimwi? Wapo wa kupata ukimwi jamani Manka na sio mtu kama mimi”“Ila na mimi je unaniamini vipi?”“Nakuamini, ikiwa unakumbuka kinga muda wote inamaana upo vizuri na unajiamini, basi unatakiwa uniamini na mimi kama na mimi ninavyokuamini wewe”Mama Sarah alitulia tu ila kiukweli alikuwa na mawazo sana, kwani kwa upande wake alikuwa ameweka kinga ni jambo la muhimu sana kutokana na mtu mmoja aliyemuamini sana halafu akakuta ameathirika, basi toka hapo alianza kutumia kinga tu, mpaka siku hii aliyosahau kutumia kinga sababu ya kulewa sana na Rahim.Siku ya leo, mama Angel alipatwa na ugeni ambao hakuutaraia kwakweli maana alifika rafiki yake wa chuo, ila hakujua kama angefika kwa siku hiyo,“Kheee jamani Fetty, karibu sana”Basi walikumbatiana pale na kufurahia huku Fetty akimwambia mama Angel,“Naona leo timu nzima ipo nyumbani!”“Si unajua tena!! Leo ni sikukuu ya kitaifa!!”“Najua maana na wanangu wapo nyumbani ila watoto wale jamani, Mungu anisaidie tu”“Vipi tena?”“Kuna kale kanaitwa Abdi dah huyu mtoto ni pasua kichwa hatari, leo ndio nimejua maana ana ugomvi na kaka yake Bahati wa muda mrefu sana”“Ugomvi gani?”“Kumbe wanamgombania binti yako Erica”Mama Angel alishangaa sana na kuuliza kwa mshangao,“Kheee wanamgombania Erica? Kivipi?”“hata mimi sikuwaelewa kwakweli, ila wanamgombea binti yako, kila siku huwa wanagombana yani leo ndio nimejua chanzo cha ugomvi wao”“Kwani ndio uliozaa na Bahati hao?”“Nizae nae wapi? Yule nae si ndio mzazi mashuhuru! Ana watoto kila kona yani, huyo Abdi ni mtoto wa mdogo wake Nasma ambaye anaitwa Siwema, na huyo Bahati ndio mtoto wa Siwema, hapo sikutajii timu nyingine aliyoniwekea pale nyumbani. Mwanaume hafai yule namvumilia tu, kwani ni mimi ndio nimembadilisha tabia yake mbovu”“Sasa umegundua vipi kuwa wanamgombania Erica wangu?”“Leo wakati natoka, nilimuaga baba yao pale ndipo kila mmoja alisema mtaa ninaoelekea ni mtaa anaokaa Erica wake, nilipowadadisi ndio nikagundua ni mwanao ndio anatajwa. Ila mimi nimepitia tu hapa ingawa haikuwa safari yangu ya leo”“Kwani ulikuwa unaenda wapi?”“Sio naenda wapi! Nimetoka kumuangalia rafiki yangu mmoja huko amepata ajali na ameumia sana hadi huruma jamani”“Kheee jamani, lini tena?”“Jana hiyo, kaumia sana yani”“Kwani alikuwa akienda wapi jamani! Pole yake kwakweli”“Kuna mtoto wao anasoma, sasa walipanga kwenda kumuona mtoto wao shuleni ila mumewe akapata dharula kwahiyo hakwenda, ndio akaenda huyo rafiki yangu jamani, kaumia sana hadi huruma”Mama Angel aliuliza tena,“Ni shule gani hiyo aliyokuwa anaenda?”Fetty alimtajia na kumfanya mama Angel ashangae sana kwani ndio shule anayosoma Angel pia, kisha akamuuliza tena,“Kwahiyo ajali kapata maeneo gani?”“Yani nasikia karibu na hiyo shule kuna njiapanda, basi ndio hapo hapo kapata ajali hiyo na kuumia sana”Mama Angel alishangaa sana kwani ni kitu hiki hiki waliambiwa jana yake na Erica. Fetty alimtajia na kumfanya mama Angel ashangae sana kwani ndio shule anayosoma Angel pia, kisha akamuuliza tena,“Kwahiyo ajali kapata maeneo gani?”“Yani nasikia karibu na hiyo shule kuna njiapanda, basi ndio hapo hapo kapata ajali hiyo na kuumia sana”Mama Angel alishangaa sana kwani ni kitu hiki hiki waliambiwa jana yake na Erica.Basi mama Angel aliyasikiliza maelezo ya Fetty kwa makini ila alikuwa akitafakari vitu vingi sana, na hakuweza kusema zaidi kwani alihisi yale maelezo kumchanganya, basi alimuuliza tena Fetty,“Huyo rafiki yako huwa anaishi huku? Maana sijawahi kukusikia kuwa unaenda kumuona rafiki yako huku”“Hapana haishi huku wala nini, ila kutokana na ile ajali imebidi arudi kwa dada yake mkubwa ambaye ndio kama mama yao kwahiyo ndio anamuhudumia kwa yale majeraha”“Hospitali je?”“Walienda ndipo walipotoka walirudi moja kwa moja huku ndiomana mimi kuja kumuona imebidi nije huku”“Hapo nimekuelewa”Baada ya muda kidogo, Fetty aliaga na kuondoka zake, na moja kwa moja mama Angel alienda kuongea na mumewe ili kumpa hiyo habari,“Mmmh umesikia hii?”“Nini tena?”Mama Angel alimsimulia kila kitu ambacho Fetty amesema na kufanya baba Angel ashangae pia, alimuuliza mkewe,“Kwani Erica alituambiaje jana?”“Alisema sisi ndio tutapata ajali halafu mimi nataumia sana, eneo alilolitaja Erica ndio lile lile ambalo rafiki wa Fetty kapatia ajali”“Dah!! Unajua mwanetu anaanza kuwa mtabiri sasa?”“Kivipi?”“Maana katabiri vile ambavyo ilivyo ila katuokoa maana hiyo ajali ingekuwa ya kwetu ila ndio imeenda kwa huyo”“Dah! Unajua mume wangu umefikiria mbali sana! Mimi sikufikiria huko”“Ulifikiriaje?”“Yani moyo ulianza kunienda mbio wakati Fetty ananisimulia, nakumbuka Erica kasema kuwa kaota sisi wazazi wake tukienda huko tutapata ajali, basi Fetty alivyosema vile nikaanza kuwaza au sisi sio wazazi wa Erica!!”Baba Angel alimuangalia mkewe na kumuuliza kwa mshangao,“Kwanini sasa umewaza hivyo?”“Weee na hayo matimbwilitimbwili ya dokta Jimmy ya kubadilisha watoto lazima vitu vingine vinipe mshtuko mkubwa sana”“Walibadilisha watoto wa wengine ila sio watoto wetu sisi, kwanza hebu muangalie Erica au huwa humuangalii vizuri yule mtoto mke wangu? Mtoto umefanana nae yule jamani kila kitu hadi kupika, kasoro yenu ni kuwa Erica ana maneno mengi ila vingi umefanana nae, yani hata mimi ningekuwa simjui Erica basi ningemuona lazima ningesema ni mtoto wako”“Ila kweli, kwa asilimia mia moja Erica ni mwanangu. Unajua mambo ya hiyo ndoto ya ajali ndio yamenishtua”“Ila mke wangu unachekesha, kipindi kile Sia amekazana kusema Erick ni mwanae, ulikuwa ukipinga vikali hadi mishipa ya ufahamu inakusimama ila sasa hivi ndio unaanza kuwa na mashaka mwenye kuhusu Erica jamani!!”“Hapana mume wangu, kuna mambo Erica anayo huwa yananishangaza sana. Erica anaweza kuwa na kitu halafu asiniambie mimi mama yake, akaenda kumwambia Vai huko au hata Sia akikutana nae njiani anamwambia kuliko kuniambia mimi”“Aaaah usitake kujisahaulisha huko, kila siku nilikuwa nikikusikia ukimkemea mtoto kuwa asikuletee umbea wake, nilikuwa namuona anavyoondoka amenyong’onyea, ila alikuwa anajitahidi kuja kukwambia na mara nyingi ulikuwa ukimfokea, kwani unadhani na yeye hasomi alama za nyakati? Anajua hupendi umbea na yeye na umbea ndio damu damu, ndiomana hakwambii ila wewe ndio umesababisha yote hayo mke wangu”Mama Angel alianza kukumbuka na kuona ni kweli kuwa huwa anamfokea sana mtoto wake kuhusu kumletea habari za umbea, basi aliongea pale na mumewe na kuahidi kuwa atabadilika ili kuwa karibu tena na mwanae na aweze kujua vitu vingi alivyonavyo Erica.Usiku wa leo, Erica alitoka chumbani kwake na moja kwa moja alienda chumbani kwa Vaileth na kuanza kuongea nae,“Dada Vai, hivi karibuni ushawahi kuongea na yule ndugu yako mchawi?”“Kheee ndugu yangu mchawi? Kivipi?”“Si yule dada yako, sijui anaitwa nani?”“Aaaah Prisca, ndio nimewasiliana nae”“Basi nimeota amekuja, kakuletea dawa kuwa unywe uweze kutoa mimba ila hiyo dawa kama ukiinywa itakutoa hiyo mimba na kizazi”Vaileth alishtuka sana na kumuuliza Erica,“Ila watoto wa siku hizi mnajua vitu vingi eeeh!”“Ndio, ila kwani mimba ni jambo jipya sana kusema mtu kama mimi nisijue?”Vaileth hakusema kitu zaidi, basi Erica alimuaga na kuondoka zake.Vaileth alilala huku akiwaza sana, kuwa huyu Erica huyu ana makusudi gani na maisha yake? Yani aliona kama mimba hii ni kikwazo kikubwa sana kwenye maisha yake, na kuwaza kuwa atafanyaje pale tumbo litakapokuwa limetangulia mbele? Aliwaza bila ya jibu na kujitahidi kulala tu kwa muda huo.Kulipokucha, Vaileth aliamka na kufanya shughuli za hapa na pale, ila kwa kipindi hiki alikuwa akichoka haraka sana kutokana na ile mimba aliyokuwa nayo, kwahiyo alifanya kazi nyingi kwa uvivu sana.Muda kidogo, mama Angel nae alitoka siku hii na kumuacha Vaileth na mtoto kama kawaida,“Ila leo nitawahi kurudi tofauti na siku zote”“Sawa mama, hakuna tatizo”Basi mama Angel aliondoka zake na kumuacha pale Vaileth.Baada ya masaa machache kuna mgeni alifika pale, na mgeni huyo alikuwa ni Prisca yani dada wa Vaileth, basi alivyofika tu alianza kumsema mdogo wake,“Ila na wewe Nyanda ulianzaje kutembea na mlinzi jamani!”“Sijui ila si unajua mapenzi ni upofu”“Upofu wapi? Ujinga huo, unaacha kutembea na mwenye nyumba unaenda kutembea na mlinzi loh!! Najua dawa ya siku ile ilishindikana, chukua hii ni kiboko kabisa ndani ya muda mfupi kitu kitakuwa tayari”“Oooh asante, ila dada ondoka tu sitaki huyu mwenye nyumba akukute hapa”Kwahiyo ilibidi Prisca aondoke tu kwa muda huo na kumuacha Nyanda akifikiria kuhusu ile dawa kama ainywe au la, huku akikumbuka maneno ya Erica ya kumpa onyo.Muda wa mapumziko kama kawaida, Erica na rafiki yake Samia walikaa na kuanza kusema kwanza watu wa shuleni kwao, kisha kuanza kuongelea kuhusu familia zao, ila Samia ndio alikuwa na mtindo wa kumuelezea Erica kuhusu baba yake nyumbani,“Jamani, baba kasafiri”“Kheee kumbe kasafiri baba yenu?”“Ndio, kidogo maneno yamepungua. Nadhani mama yangu alichoka ndiomana alianza kuongea yani ni kweli kabisa wanaume ni watu wasiofaa”“Hadi wewe Samia unawajua wanaume?”“Sikia nikwambie, mimi nina yule kaka yangu yani na yeye ni balaa, kuna wadada pale wa kutosha wanakuja kumlilia kaka, inamaana wote wale kawadanganya”Basi walijikuta wakiwajadili watu wote kwa muda ule, mpaka waliporudi tena madarasani na kutangaziwa kuwa wanakaribia kujiandaa kwaajili ya mitihani walishukuru sana kwani kutokana na kile kidato walichopo basi hata likizo zile ndogo ndogo walishindwa kukaa nyumbani kwani walitakiwa kuwa shule tu muda wote.Ila muda wa kutoka shule siku hiyo, Samia alimshawishi Erica kuwa wasitumie gari la shule, badala yake, waende kupanda daladala ya kurudi nyumbani. Walikubaliana kufanya hivyo.Daladala walilopanda, kuna mtu akamshika bega Erica alipogeuka akakutana na Daima na kuanza kuongea nae,“Kheee umetoka wapi Daima?”“Nimetoka hospitali”“Unaumwa nini?”“Kiukweli sina hali nzuri, unajua ile mimba yangu ilitoka, basi toka kipindi hiko nimekuwa nikipata matatizo mengi sana, mpaka leo nimetoka hospitali naumwa”“Pole sana Daima”Kisha Daima alianza kuuliza kuhusu habari za Junior na kumfanya hata Erica amshangae kwasababu kwa mambo yale hakufikiria kabia kama huyu Daima angepata ujasiri wa kumuuliza Erica kuhusu Junior.Basi wakati wapo mule kwenye daladala, kuna mkaka mmoja alipanda pia, ni Daima ndio aliwatonya Samia na Erica,“Kheee mmemuona yule kijana alivyo mzuri?”Samia nae alimuangalia kwa makini na kusema,“Kheee jamani ni mzuri sijapata kuona mimi”Erica alikuwa akiwaangalia tu, sababu mambo kama hayo yeye hakuwa nayo, basi walifika stendi ya kushuka ambapo alikuwa akishuka Erica, na yule kaka nae alishuka na kufanya Daima na Samia washuke pia pale stendi huku kila mmoja akimsakizia mwenzie kwenda kumuuliza kitu yule mkaka ila Erica aliona ule ni ujinga na kuamua kuondoka zake kuelekea nyumbani kwao huku akimuacha Samia na Daima wakimfatilia yule mkaka.Mama Angel moja kwa moja alifika nyumbani kwakina Derrick na kuanza kuongea nae maana siku hii Derrick alimuita tena ili kuongea nae,“Najua uliniuliza sana kuwa naelewa kitu gani kuhusu Elly”“Eeeh niambie”“Ninachoelewa ni kuwa Elly ni mtoto wangu, na kwasasa nimeelewa kuwa mtoto Elly nimezaa na Manka”Mama Angel alishangaa kidogo na kumuuliza vizuri Derrick,“Sasa, huyo Manka si umezaa nae mtoto wa kuitwa Sarah? Au yule Sarah si mwanao?”“Yule ni mwanangu pia?”“Umezaa na nani sasa? Kama Elly unasema kuwa umezaa na Manka, je Sarah umezaa na nani maana ndio mtoto wa Manka tunayemtambua!”“Kwakweli sijui ila ninachojua ni kimoja tu kuwa Elly ni mwanangu ambaye nimezaa na Manka”“Mmmh au Manka alizaa mapacha ila mtoto mmoja akaibiwa? Ila mbona hiyo habari naona inazidi kuchanganya akili”“kwanini?”Mama Angel alimwambia ukweli Derrick kwa kilichotokea baina ya Sarah na Elly, kwakweli Derrick alijihisi vibaya sana hata moyo wake ulimuuma, na kukaa chini kabisa huku akisema,“Sikutegemea kama yale makosa yangu ndio Mungu angeniadhibu kiasi hiki!”“Makosa yako gani tena!!”“Umesahau kuwa mimi nilikulazimisha wewe! Nadhani imejirudi tena kwa watoto, hii ni laana kwakweli, ila si tulifanyiwa tambiko?”“Ila nadhani kama ni laana basi imesababishwa na mdomo wako huo mchafu maana kila uliyekutana nae ulimueleza kama mimi na wewe tuliwahi kuwa na mahusiano bila kujali hata kama mimi na wewe ni ndugu!!”“Usiseme hivyo Erica!”“Yani hapo ndio ujijadili wewe mwenyewe na roho yako, watoto ndio wameshatembeleana, itakuwa unavuna ulichokipanda, na unaambiwa huyo Sarah anampenda Elly balaa, kwahiyo kazi kwako”Mama Angel alimuaga Derrick na kumuacha Derrick pale akiwa na mawazo sana.Usiku wa leo, Rahim alikuwa amekaa ndani na mama Sarah na kuanza kuongea nae kwani kwa hizo siku chache tu aliweza kugundua kuwa huyu mwanamke kwa kipini hiko hakuwa sawa kabisa. Basi alimuuliza,“Kwani tatizo nini Mank? Inaonhyesha haupo sawa kabisa kipenzi”“Ngoja nikwambie kitu labda utanielewa, mfano uwe na watoto wawili yani watoto wako mwenyewe halafu kwa bahati mbaya umkute mtoto wako kalala na huyo nduguye na wamepeana mimba”“Duh!! Ni ndugu yako yamemtokea hayo?”“Hapana, nijibu kwanza ungefanyeje?”“Najua hilo jambo haliwezekani kwangu, yani watoto wangu wajazane mimba kweli!! Haiwezekani, kwanza nina damu kali mimi haiwezi kuwa hiyo kitu”“Mmmh hongera zako”“Basi, niambie tatizo ni nini?”“Ni hivi, Sarah ni binti yangu kabisa. Ila sikujua kama nilizaa mapacha, kuna kijana nilimleta na kuishi nae hapa nyumbani kwangu kumbe ndio pacha wa Sarah, basiSarah alitembea na huyo kijanahadi wakapeana mimba”“Duh!! Wewe hujui kama ulizaa mapacha?”“Sijui, sababu mimi nilizimia baada ya kujifungua”“Duh!! Wanawake mna kazi kumbe. Ila daktari aliyekuzalisha unamfahamu vizuri?”“Ndio namfahamu na hadi huwa nawasiliana nae”“Basi huyo ndio wa kumshikilia akwambie ukweli, maana yeye ndio anajua kama alikuzalisha mapacha na atakuwa anajua ukweli halisi wa watoto wako. Kwani wewe umejuaje kama huyo mwingine ni pacha wa huyo?”“Aaaah ni historia ndefu”“Sawa, basi naomba kesho tukamfate huyo daktari ili atuambie ukweli, sipendi kuona ukiwa na mawazo kiasi hiko kipenzi”Basi mama Sarah alikubaliana na Rahim kuwa kesho yake wamtafute yule dokta na waweze kuongea nae vizuri.Kesho yake kama ambavyo mama Sarah alipanga na Rahim, alimpigia simu dokta wake na kupanga kukutana nae mahali.Kisha aliondoka na Rahim kwenda kukutana na yule dokta waliyepanga kukutana nae, walifika na kukuta dokta ameshafika basi Mama Sarah alimtambulisha pale,“Dokta samahani, huyu ni mume wangu mtarajiwa anaitwa Rahim. Halafu Rahim huyu ni daktari aliyenizalisha, anaitwa dokta Jimmy”Basi dokta Jimmy na Rahim walifahamiana pale na kukaa kuanza kuongea, kisha mama Sarah alianza kuongea,“Najua umeshangaa sana kwa mimi kuja na mtu leo katika kuonana na wewe, usiwe na wasiwasi nae. Ni hivi nimepata mkanganyiko sana juu ya uzazo wangu, dokta niambie ukweli sasa, ni kweli nilizaa mapacha? Kama ulivyoniambia kwenye simu?”“Kwani kwenye simu nilikwambiaje?”“Nilikuuliza dokta, kuwa mimi nilizaa mapacha, ukanijibu kuwa nilizaa mapacha, ndio nipo hapa nikitaka ukweli”“Aaaah Manka jamani, hivi uzae mapacha kweli halafu mimi nikwambie ni mtoto mmoja!! Inamaana siipendi kazi yangu au kitu gani? Halafu inamaana huyo mtoto mwingine nimempeleka wapi?”Mama Sarah alipumua kidogo na kumuuliza tena,“Unajua kuna mtloto kajitokeza na kusema kuwa ni mtoto wangu, mimi ni mwanamke siwezi kusingiziwa mtoto. Katika maisha yangu nimezaa mara moja tu. Iweje niwe na mtoto Sarah halafu atokee na mtoto mwingine aseme kuwa ni mtoto wangu?”“Kwani imekuwaje kwanza? Niambie ukweli maana sikuelewi”Basi mama Sarah alianza kumueleza huyu dokta kuhusu tukio la Elly na jinsi alivyokutana na Derrick, basi dokta alimuangalia kwa makini sana mama Sarah na kumuuliza,“Kwani wewe huyo Sarah ulizaa na marehemu mzee Jimmy au ulizaa na nani? Sikuelewi ujue, unawezaje kusema sijui Derrick ndio baba wa mtoto sijui ikaenda ikarudi yani hadi sikuelewi, ulizaa na nani Manka, hebu niweke wazi”Hapo mama Sarah alinyamaza kwa muda kidogo na kumfanya huyu dokta aongee tena,“Mnajua nyie wanawake mna mambo ya ajabu sana, nadhani hayo mambo ya ajabu hata nyinyi wenyewe huwa yanawapa mashaka sana. Sasa wewe siku zote unasema mtoto ni wa mzee Jimmy, hadi anakufa mzee wa watu anajua kuwa amezaa na wewe, halafu wewe unaniambia habari za Derrick, vipi wewe ni mzima kweli kichwani! Umezaa na nani? Mzee Jimmy au Derrick!”“Basi yaishe”Mama Sarah alimgeukia Rahim na kumtaka waondoke tu, kwahiyo waliondoka zao kwa muda huo na kurudi nyumbani.Samia na Erica wakati wanatoka shule siku ya leo, Samia alianza kumueleza Erica kuhusu yule mkaka waliyekuwa wamemfata jana yake,“Erica, yule makaka wa jana ni noma”“Mmmh umeanza hivyo!! Ndiomana mama yangu huwa hapendi nipande daladala sababu ya mambo kama haya haya”“Hujui tu Erica, hivi umemuona vizuri yule mkaka? Kwanza ni mtanashati sijapata kuona”“Kheee kwahiyo kwasasa, huoni tena uzuri wa Erick!”“Erick sio kitu kwa yule mkaka, ila ana maringo huyo hapana jamani, hivi mkaka unamuuliza unaitwa nani halafu anakuangalia bila ya kukujibu, yani anaondoka zake bila hata ya habari kuwa umemuuliza chochote”Basi Erica alicheka sana kwa lile aliloambiwa na Samia, kisha akamwambia Samia,“Hamuwezi kujua jamani, usikute kaka wa watu ni kiziwi ndiomana imekuwa hivyo!!”“Mmmh halafu Erica umeongea kitu jamani, kweli usikute ni kiziwi, sie tumekazana kusema ana maringo halafu kumbe mkaka wa watu ni kiziwi”Muda huo Samia alicheka sana na kusema tena,“Mimi na yule Daima tulibaki tukimshangaa yule mkaka tu, maana hajatujibu hata jambo moja, kumbe mkaka wa watu ni kiziwi loh!! Mkaka mzuri vile anakuwa kiziwi jamani! Kweli hujafa hujaumbika”Basi waliingia kwenye gari ya shule na kuelekea makwao, muda Erica aliposhuka tu nyumbani kwako alimkuta kijana bahati yupo nje ya geti lao huku kashika mfuko mkononi na kumfanya Erica aulize,“Umebeba nini?”“Ni zawadi yako Erica, nimekulea”Erica alichukua ule mfuko na kuangalia kwa makini na kuona ni viatu, alitabasamu na kumwambia bahati,“Asante sana, ila kwanini umeniletea zawadi hii?”“Nimejisikia tu kufanya hivi Erica, kwani vibaya jamani?”“Hapana hakuna ubaya”Erica alimkaribisha ndani kwao Bahati ila Bahati alikataa na kuaga kisha akaondoka zake, na kufanya Erica aingie ndani kwao.Ila Erica alipoingia tu kwenye mlango wao wa kuingia sebleni alimkuta mama yake amekaa sebleni na kitu cha kwanza kabisa mama Angel alimuuliza Erica,“Umebeba nini kwenye huo mfuko?”“Ni viatu mama”“Umevituoa wapi? Hebu tuvione?”Erica alimpa mamake ule mfuko ambapo mama Angel alitoa vile viatu na kuviangalia halafu akasema,“Ni vizuri ila umevitoa wapi Erica?”“Mama, nimekutana na Bahati hapo nje ya geti ndio amenipa kasema ni zawadi yangu”“Aaaah kumbe!! Hebu viache kwangu, nenda kabadili sare za shule huko”“Aaaah mama, hata kuniacha nivijaribishe kidogo?”“Huo ujinga sitaki kusikia Erica, naomba uende zako ndani. Mimi naelewa ni kwanini nimevichukua hivi viatu, na mambo ya kupokea pokea zawadi kwa wanaume sitaki kusikia kabisa”Muda huu Erick nae alirudi kutoka shule na kumkuta mama yake akimsema Erica, basi aliipenda ile mada pia kwani mama yao alimwambia Erick,“Nakuomba Erick uwe mlinzi wa huyu ndugu yako, kwakweli hii tabia ya kupokea pokea zawadi kwa wanaume sijui kaitoa wapi jamani!”“Basi atakuwa kapewa hiyo zawadi na yule wa kuitwa Bahati!”“Umejuaje mwanangu?”“Nilimuona jana akijitapa, ila Erica huwa hasikii nilishamwambia kuwa asiwe karibu na hao watu ila hasikii kitu”“Wewe Erica wewe, hebu nisikilize kwa makini mama yako. Maswala ya marafiki wa ajabu ajabu sitaki kabisa, rafiki yako ni Erick tu nimemaliza”Erica hakuongea neno zaidi kwa mama yake, kwani muda huo huo aliondoka zake kuelekea chumbani kwake, hata Erick alielekea chumbani kwake pia. Mama Angel akainuka tu na vile viatu kisha akaenda chumbani na kumpigia simu rafiki yake Fetty,“Kesho nakuja nyumbani kwako, naomba nikutane na huyo kijana wako wa kuitwa Bahati”“Mume wangu au?”“Hapana, huyo Bahati mdogo”“Kuna nini kwani?”“Hapana, hakuna kitu ila nahitaji tu kuonana nae tafadhari”Basi waliongea kidogo na kukata ile simu, huku mama Angel akifikiria kuwa kesho yake aende huko kwa Fetty maana aliona ni vyema kama akiongea moja kwa moja na huyu kijana.Usiku wa siku hii mama Angel na mumewe walianza kuongea ambapo baba Angel alimueleza mkewe kuhusu mambo yanavyoendelea maana bado alikuwa akichunguza yale yaliyotokea na yanayoendelea, muda huo kuna simu ilianza kuita kwa mama Angel basi aliipokea maana aliyepiga alikuwa ni mama Derrick, akaanza kuongea nae,“Erica mwanangu, nduguyo Derrick sijui ana matatizo gani yani muda wote anaongea peke yake, sijui tutamsaidiaje”“Duh hatari hiyo mama, ngoja niwasiliane na dada Mage, atawatafuta Kesho anaweza akaja”Basi alikata ile simu na kwa muda ule, alimtafuta dadake mage hewani na kumtaarifu tu kuwa awasiliane na familia ya wakina Derrick alijua kuwa itakuwa rahisi kwani alihisi Derrick atamueleza kinachomsumbua ila mama Angel alielewa wazi kuwa kinachomsumbua Derrick ni lile swala la kugundua kuwa watoto wake yani Sarah na Elly wametembea pamoja.Basi mama Angel aliendelea na maongezi mengine na mume wake kwani hakutaka kumwambia kuhusu mambo hayo ya ndugu yake.Waliamua kulala tu kwa muda huo, kwani ilikuwa ni usiku sana.Kulipokucha tu, baba Angel alijiandaa na kuondoka zake ila aliongea na mke wake jambo ambalo anahitaji kufanya kwa siku hiyo,“Nataka leo niende na Sia kwenye ile hoteli aliyompata mke wa Moses”“Ila na sisi ni wazembe jamabi, toka tumepewa ujumbe ndio tunakumbuka leo dah!!”“Ndio hivyo mke wangu, mambo mengi sana ila leo ni siku nzuri”Mama Angel alikubali swala hilo, basi muda kidogo baba Angel aliondoka nyumbani kwake na kuelekea kwanza ofisini kwake.Mama Angel, leo alienda nyumbani kwa rafiki yake Fetty kama ambavyo alipanga jana yake kuwa ataenda, kwahiyo alibeba na ule mfuko wa viatu na kwenda nao hadi kwa Fetty, alifika pale na kumkuta rafiki yake na kuanza kuongea nae,“Bora umekuja kweli, nataka kujua tatizo ni nini rafiki yangu?”Mama Angel alimtolea vile viatu ambavyo Bahati alimpa Erica na kusema,“Yani huyo Bahati ndio kaanza kumuhonga binti yangu jamani!”“Kheee jamani, viatu vizuri hivyo, nadhani kanunua bei hivi, ila kwanini kampelekea mwanao?”“Sijui yani hebu niitie”Fetty alianza kumuita Bahati, kisha Bahati aliitikia kuwa anaenda, ila muda huu Fetty alichukua vile viatu na kutaka kuvijaribisha maana alivipenda ila kabla hajavijaribu alisikia sauti ya Bahati ikimwambia,“Mama, nakuomba usijaribu hivyo viatu”Kisha Bahati akakimbia pale na kuchukua vile viatu, kwakweli mama Angel na Fetty walishangaa sana. Fetty alianza kumuita Bahati, kisha Bahati aliitikia kuwa anaenda, ila muda huu Fetty alichukua vile viatu na kutaka kuvijaribisha maana alivipenda ila kabla hajavijaribu alisikia sauti ya Bahati ikimwambia,“Mama, nakuomba usijaribu hivyo viatu”Kisha Bahati akakimbia pale na kuchukua vile viatu, kwakweli mama Angel na Fetty walishangaa sana.Fetty alijaribu kumuuliza pale Bahati,“Wewe mtoto una matatizo gani? Kwani hivyo viatu vina nini?”Bahati hakujibu zaidi ya kuweka vile viatu vizuri na kuondoka navyo, Fetty alimuangalia mama Angel na kumwambia,“Haya ndio matatizo ambayo nakumbana nayo kwakweli kwa hawa watoto, wamechukua tabia za mama zao huko wananisumbua balaa”“Kheee pole sana, bora wangechukua tabia za baba yao”“Yani wangechukua tabia ya baba yao naona ingekuwa heri kwangu, kwanza baba yao ni mpole, ni mwenye huruma, halafu ni mtu wa kujishusha na kusikiliza ushauri, sasa hawa watoto wapo masikio waruwaru kama antena za chuma”Mama Angel akacheka kidogo na kusema,“Yani nacheka kama mazuri, ila kwakweli huyu mtoto kaonyesha dharau za hali ya juu”“Bora hili shoga yangu, navumilia mengi ujue usione hivyo, huyu Bahati ndio ana kiburi hatari, hivyo mara nyingi namtimua hapa aende kwa mama yake. Ukija kwa upande wa huyo Abdi nae kila leo kazua jipya huko mtaani, ila Bahati akiwepo ndio anamtuliza Abdi maana Abdi akiwa hapa ndio anajifanya kidume wa familia, mitoto ya laana hii inasumbua hatari”“Pole mwaya, ila bado huyu mtoto kaaacha maswali kichwani mwanangu, ni kwanini kampa mwanangu zawadi ya viatu? Halafu kwanini kakukatalia wewe usijaribu, isije ikawa ndio mambo ya waganga!”Fetty alicheka kidogo na kusema,“Itakuwa mambo ya babu wa Bagamoyo hayo, yale mambo ya Dora na rafiki yake Sia”“Ila mtoto mdogo hivi mambo ya waganga ya nini?”“Weeee uliza kwanza, mama wa huyu mtoto ni kupuliza madawa kwa waganga kila leo. Babu yake huyu mtloto alifia kwa mganga sababu ya ushirikina, huyo mamake hajaacha ushirikina hadi leo ingawa anajua wazi kuwa haumsaidii, hajua kama nyumba yangu naifanyia dua kila leo, hayo madawa yake yanagonga mwamba hapa, yani mamake huyu anafanya biashara Fulani hivi ila kwa ndumba, yani ningekuwa sio mtu wa ibada kwa hakika ningeshaachana na mume wangu. Si unajua kipindi kile nimekuja kukulalamikia kuhusu mume wangu kuwa ameanza kukutaja wewe tena, yani haeleweki wala nini hadi na mimi nilihisi kuchanganyikiwa nikawa naenda hotelini huko na kukaa hadi usiku ndio narudi nyumbani kwangu, ila sasa nilikutana na yule mama wa kuitwa Ester yule ambaye huwa anawafanyia maombezi, nilijikuta nikiongea nae kuhusu mume wangu, alinishauri mambo mazuri sana, alisema hakuna kinachoshindikana kwa Mungu, kila kitu ni kuomba maana kama mpaka nimefunga nae ndoa na ninaishi nae hadi leo basi niamini kuwa ni mume wangu, nisikubali shetani anitenganishe nae, ukizingatia nampenda. Basi yale maneno yake yaliniingia sana, tulikutana tu njiani ndio kuongea yote hayo, basi nilivyorudi nyumbani nikasema sasa nabadilika, nilianza kufanya ibada upya. Kuna siku nilichukua pesa na kwenda kutoa msaada kwa watoto yatima, yani nilifanya vile kama sadaka kwangu yani nilitoa sadaka kwaajili ya mume wangu, kisha tukafanya dua na wale watoto, mbona mume wangu alianza kubadilika mwenyewe, hadi sasa kabadilika kabisa. Kwakweli mume ndani ukimuona kabadilika sio na wewe unaota pembe na kubadilika ili umkomeshe, huwezi jua anapitia kitu gani ndiomana kabadilika, cha muhimu ni kufanya maombi tu”“Ooooh kweli uminiambia kitu kikubwa sana, hata mimi yule mama huwa ananifundisha mambo mengi sana, namshukuru Mungu kwa maombi ninayofanya kwaajili ya mume wangu inasaidia kwa yeye kutokutamani wanawake wengine”“Ila wanawake tulioolewa tuna nini lakini, yani tumeacha hata kuzungumza yaliyotukutanisha na kuanza kuzungumza kuhusu waume zetu, dah wanaume wanatutoa akili hawa”Mama Angel alicheka sana, maana kweli waliacha mada zao na kuanza kuzungumza kuhusu waume zao. Basi waliongea sana na Fetty aliahidi kumsemea Bahati kwa baba yake maana hakurudi tena hadi mama Angel aliaga na kuondoka zake.Mama Angel akiwa kwenye gari lake, kuna mtu alimuona na kuamua kusimamisha gari kisha kushuka na kumfata alimshika bega ambapo yule mtu aligeuka na alikuwa ni mke wa Moses, basi mama Angel alimsalimia pale ila yule mwanamke aliitikia ile salamu kwa uoga kiasi, basi mama Angel akamuuliza,“Hajambo mumeo?”“Hajambo”“Unajua nini, kuna mambo mtu huwezi kuyaficha milele kuna kipindi lazima yatakuwa wazi tu”“Ila mimi sijamtuma kufanya hayo, usinifikirie vibaya”Mama Angel alimshangaa mwanamke huyu kwa kuanza kujishuku, basi alimuangalia kwa makini na kumuuliza,“Kwnai wewe ulimtuma kufanya nini sasa mpaka kafanya kinyume?”“Sikia, mimi ni mwanamke tu. Mimi nimeolewa tu wala sina sauti katika ndoa yangu, ni mwanaume ndio anaamua cha kufanya. Nadhani Sia kakwambia kuwa kaniona na yule dokta, yule ni shemeji yangu nawezaje kumkwepa? Ila sikumtuma mimi Moses kufanya kazi na baba wa Erick ila hatukufikiria kama baba wa Erick atakuwa na jambo lolote baya”“Ngoja nikuulize swali, mfano umelea mtoto wako vizuri kabisa halafu unakuja kupata habari kuwa yule mtoto sio wako ila alibadilishwa hospitali, kama wewe ungejisikiaje?”“Mmmh sijui, ila kwanini umeniuliza hivyo?”“Kamuulize mume wako, kwakweli huu mlioufanya kwa kushirikiana na huyo dokta wenu sijui shemeji yako sio uungwana kabisa wala sio utu. Kwakweli Mungu anawaangalia tu kwa jambo hili”“Unasema? Yani watoto wako walibadilishwa?”“Sio watoto wangu, ila kila aliyezalia ile hospitali ya kijinga kabadilishiwa mtoto, sijui kwanini wamefanya huo mchezo jamani!! Na mumeo ameshiriki kwenye hujuma hiyo”Mke wa Moses alikaa kimya kwa muda kwani hakuelewa kuwa ajibu kitu gani kwa muda ule, ila aliamua kuondoka tu hata mama Angel alipomuita tena hakuitikia na kumfanya mama Angel ahisi pale kuna namna zaidi, basi alirudi kwenye gari lake na kuendelea kurudi nyumbani kwake.Leo mume wa Fetty alivyorudi tu, aliamua kumueleza kuhusu mtoto wao Bahati na jinsi alivyompokonya vile viatu,“Mmmh, unahisi nini mke wangu?”“Nihisi nini hapo zaidi ya ndumba? Hiyo ni ndumba hakuna ubishi ni ndumba hiyo”Basi baba Bahati aliamua kumuita mwanae pale mbele ya mama yake mlezi na kuanza kumuuliza kuhusu hivyo viatu,“Haya wewe mtoto usiyejielewa yani unajifanya umekua sasa hadi umefikia uwezo wa kumuhonga kitu mwanamke, haya kwanini ulimpelekea viatu huyo Erica?”Huyu Bahati kidogo alikuwa akimuogopa baba yake maana alikuwa mkali, aliona akichekea hawa watoto wake basi watafanya ujinga sana ukizingatia walikuwa na ujinga mwingi nyumbani, basi Bahati alianza kwa kumuomba msamaha,“Naomba unisamehe baba, ila mimi sikuwa na nia mbaya, nilimpelekea vile viatu kama zawadi tu”“Alikwambia kuwa anahitaji zawadi ya viatu?”“Hapana, ila siku ya kwanza kufahamiana nae yule ilikuwa ni siku ambayo alikuwa akiulizia bei ya kiatu”“Yani nyie watoto hata sijui hizo tabia mmerithi kwa nani, halafu Bahati sikukufikiria ujue, nilijua huo ujinga anafanya ndugu yako Abdi tu. Huyu Abdi si ndio alifanya niitwe shuleni kwa kutaka kumbaka huyo huyo Erica, halafu leo hii na wewe huyo kiguu na njia kwenda kupeleka viatu kwa Erica. Kama mnajiona mmekuwa basi muhame nyumbani kwangu mkajitegemee huko sio kuniletea ujinga tu hapa, mnadhani mnafundisha nini wenzenu?”“Nisamehe baba”“Haya, na hivyo viatu uliweka nini maana hata mama yako umegoma asijaribishe”“Sijaweka kitu baba”“Usikatae wakati mamako anapenda sana ushirikina, labda kashakupa madawa ya kukufanya uweze kumpata huyo Erica, kwakweli leo umenichefua sana. Niambie umeweka nini kwenye viatu”“Kweli baba sijaweka kitu”Baba Abhati aliona kuwa anadanganywa na mtoto wake, basi aliinuka na kuvua mkanda wake huku akimshika mwanae, yani hapo Bahati alijua wazi kipigo kitakachomuangukia hapo sio cha kawaida, ilibidi amwambie baba yake ukweli,“Baba usinipige, ngoja nikwambie ukweli ulivyo”“Haya niambie na usinifiche chochote maana ukinificha nitajua”“Siku moja mama alinikuta nikiwa na mawazo, aliniuliza ni nini, niliamua kumwambia ukweli kuwa kuna binti anaitwa Erica nampenda sana, basi mama akaniambia kuwa nisijali. Aliniuliza tu, Erica anapenda nini kama zawadi, nikamwambia anapenda viatu, aliniuliza tu namba ngapi anavaa nikamtajia, basi kesho yake mama akaniletea vile viatu akasema nikampe Erica na atakapoenda kuvivaa atanipenda sana ila sijui ni sababu ya nini na mimi sijaweka chochote ndiomana nilimkataza hapa mama asivivae vile viatu asije akanipenda yeye”Yani hadi baba Bahati alijikuta tu akicheka na kusikitika, kisha kumtimua mwanae na kumwambia kuwa akamrudishie mamake vile viatu,“Na umwambie kuwa baba kaujua ukweli wote”Fetty alidakia,“Nilijua tu, maana yule mwanamama haaminiki kabisa, ila mimi siruhusu avirudishe kwanza, mwambie avilete”Basi Bahati akaambiwa avilete ilibidi akavichukue na kuwapelekea, moja kwa moja Fetty alivichukua na kutoka navyo nje kisha akavimwagia mafuta ya taa na kuvichoma moto, kisha akamwambia bahati,“Mwambie mama yako, mama kule nyumbani kachoma moto vile viatu, najua atakuja tu akipata hiyo habari”Bahati hakuongea neno zaidi zaidi ya kuondoka tu, ila kiukweli Fetty na mume wake walisikitika kuona mtoto mdogo kama Bahati kaanza kufundishwa vitu vya kupendwa na mwanamke.Basi usiku wa leo, mama Angel anaamua kumuelezea mumewe alivyoenda kwa Fetty maana anamwambia na jinsi Erica alivyopewa viatu, na jinsi alivyokutana na mke wa Moses,“Naona kuna mengi sana nyuma ya pazia ambayo hatuyajui maana ni ngumu kutaona kwa macho ya kawaida”“Ni kweli mke wangu kuna mengi sana, kuna muda nawaza hata sijui cha kufanya, unajua hata kule tulipoenda na Sia hatujawakuta tena!!”“Nilijua tu lazima watakimbia, halafu leo nilivyomuona mke wa Moses nikasahau kama na wewe ulipanga kwenda kumtafuta, ila ningekuwa mtekaji ningemteka yule mwanamke maana najua ana mambo ya mumewe aliyoyafanya, na sasa nazidi kupata picha kuwa Moses ndio alihusika kwenye wizi wa duka lako”“Mmmmh ila kwanini Moses afanye hivyo? Mbona siku zote hakufanya hivyo?”“Sijui ila nina hisia mbaya kwakweli, kama Moses ameweza kushirikiana na huyu dokta aliyeharibu maisha ya watu wengi, je anashindwa kushirikiana na wabaya katika kuharibu biashara yako? Halafu nadhani walijua utafilisika maana ndio biashara uliyokuwa unaitegemea sana”“Na kweli niliyumba si masikhara, isingekuwa mke wangu upo vizuri basi kipindi kile ndio ningekuwa naumbuka jamani, nakumbuka mama hakuwepo, halafu baba aligoma kabisa kunisaidia, yani niliyumba hatari. Ila mke wangu kwakweli Mungu akuzidishie yani wewe ni mwanamke kweli uliyeumbwa kwaajili yangu, kumbe kuna wajinga wakila tu pesa na kuhisi wananikomesha”“Umekubaliana na usemi wangu eeeh kuwa Moses kahusika?”“Hapana, sijasema hivyo”Mara simu ya mama Angel ilianza kuita, na aliyekuwa akipiga alikuwa ni Fetty basi mama Angel alipokea simu ile na kuanza kuongea nayo ambapo Fetty alimueleza yale yaliyojiri yote wakati Bahati alipoulizwa na baba yake,“Kheee makubwa, kwahiyo karudi na huyo mama yake?”“Arudi wapi? Nadhani kamsimulia na kumfanya ashikwe aibu, yani yule mwanamke sijui ataacha lini ushirikina. Na bora umegundua mapema”Kwakweli mama Angel alishangaa sana na kuagana na Fetty, kisha alimsimulia kiasi mume wake na kusema,“Ngoja nikamueleze na huyo Erica”“Jamani, kuna mambo duniani. Ila usisahau kesho kama tutaenda wote kiwandani, si unajua ndio ile Jumamosi tuliyopanga?”“Naelewa, hakuna tatizo”Basi mama Angel aliongea kidogo na mume wake pale kisha kuinuka na kwenda chumbani kwa binti yake.Muda huu Erica alikuwa chumbani kwake ila alitaka kutoa karata zake ili aanze kucheza maana alikuwa amechukia jana yake kwa Erick kusaidiana na mama yake kumsema, kwahiyo hakutaka hata kwenda kucheza zile karata na Erick kwa muda huo wala nini.Ila kabla hajazitoa, aliingia mama yake na kumfanya ashtuke,“Mbona umeshtuka sana?”“Aaaah hapana mama, hamna kitu”“Nilijua tu bado hujalala na hivi leo ni Ijumaa nahisi unawaza kucheza karata tu hapo”Erica aliinama tu na kuangalia chini, basi mama yake alianza kumpa habari za Bahati jinsi alivyoambiwa na Fetty,“Unaona mwanangu, kumbe walikuwekea dawa, ungejikuta taratibu unaanza kumpenda huyo Bahati”“kwahiyo mama, hiyo dawa ndio kama ile ambayo dada Vaileth alipewa na ndugu zake kwaajili ya baba”“Aaaah wewe nawe unaleta habari gani, mimi nakwambia mengine halafu wewe unaleta habari zingine, nakueleza mambo ya huyo mleta viatu wako Bahati”“Basi mama nimekusikia, nashukuru kwa kuniponya maana nisingejua ningevaa tu vile viatu”“Haya mwanangu, ila safari nyingine jitahidi uwe makini sana na hayo mambo mwanangu, sitaki kukupoteza kizembe. Muombe Mungu kila utokapo na uingiapo, ukiwa shuleni muombe Mungu, ukitoka shule muombe Mungu, jitahidi kufanya sala kila muda”“Sawa mama”Basi mama Angel alimuaga mwanae na kuondoka zake kwa muda huo, kwakweli Erica nae aliacha kucheza karata kwa muda huo na kuzibeba hadi chumbani kwa Erick ambapo alimkuta ndio anajiandaa kulala basi alimshtua na kumtaka wakae na wacheze karata, ingawa Erick alikuwa amechoka ila alishindwa kumkatalia Erica kucheza nae karata, ambapo wakati wakicheza karata ndipo Erica akamsimulia kuhusu alichoambiwa na mama yake kuhusu vile viatuambavyo aliletewa na Bahati,“Kheee kumbe ndio ilikuwa hivyo?”“Ndio, eti ili nimpende jamani!! Duniani kuna mambo ya ajabu”“Ila na wewe kwanini ulichukua viatu vyake kama humpendi?”“Mimi simpendi kweli jamani”“Haya unampenda nani?”“Mimi nakupenda wewe”Erick alitabasamu na kumwambia,“Ila mimi ni ndugu yako?”“Kwani ndugu hawaruhusiwi kupendana jamani Erick?”“Aaaah kumbe unasemea upendo wa ndugu”“Wewe ulijua ni upendo upi?”“Hukuna kitu, tucheze tu karata”Basi waliendelea kucheza karata, na mwisho wa siku kama kawaida walijikuta wakiwa wamelala pamoja kwenye kitanda cha Erick.Kulipokucha, Erica ndio alikuwa wa kwanza kuamka na muda kidogo Erick nae aliamka ila Erica alimuangalia Erick na kushtuka kisha alimuuliza kwa mshangao,“Nini hiko kimetuna hapo mbele ya kaptula yako?”Erick aliona aibu kiasi na kuchukua shuka kujifunika huku akimjibu Erica,“Ndio huwa hivi kila asubuhi”“Mmmh mbona sijawahi kukuona?”“Labda leo ndio umeniangalia”“Hebu nionyeshe, yani vua nguo nione imekuwaje hadi kukatuna”Erick alicheka tu na kutokujibu chochote,“Kisha aliinuka na kutaka kama kuvua kaptula yake”Gafla ikasikika sauti ya mama Angel akimuita Erica, kwahiyo kwa haraka Erica alitoka mule chumbani kwa Erick na kukimbilia ambapo mama yake kamuita.“Erica, mimi na baba yenu tunatoka muda sio mrefu kwahiyo make mumuangalie mtoto. Leo zamu yenu sio kumuachia Vaileth tu”“Sawa mama”Basi moja kwa moja Erica alienda chumbani kwake kwaajili ya kuoga na kuondoa uchovu wa usiku.Basi mama Angel na baba Angel wanafika kiwandani na kuanza kufanya mambo mbalimbali ya pale kiwandani, ila baada ya muda kidogo anafika pale rafiki wa baba Angel ambaye ni Juma kisha Juma anamuita baba Angel na kuongea nae,“Ndugu yangu, tulipanga vizuri kabisa ila kwanini umenigeuka hivyo?”“Nini tena?”“Nilikuomba twende wote na kijana wako kwenye ile kazi yangu ila ukanigomea, kwakweli ulichonifanyia sio kizuri”“Hivi ni kosa langu au kosa lako Juma? Ni lini ulisema kuwa twende leo?”“Nilikupigia simu sana ila simu zangu hukupokea na wala hukujisumbua kunipigia tena. Sijapenda kabisa ndugu yangu”“Naomba unisamehe tu yani kichwa hiki kina mambo mengi sana, naomba siku unayopanga uje nyumbani moja kwa moja halafu tutaenda huku kwenye biashara yako”“Nitampata Erick?”“Utampata ndio, hata shule tutamfata. Mimi mwenyewe nimekuruhusu kuhusu hilo”Basi Juma aliongea kidogo tu na kuaga pale na kuondoka zake, kisha baba Angel alirudi ofisini na kuendelea na mambo mengine na mke wake, ila muda kidogo yule mteja ambaye huwa wanamuita mwarabu alifika pale kwenye ofisi ya baba Angel kuagiza mzigo kama kawaida yake, ila mama Angel alipomuona huyu mzee alishtuka kidogo ingawa aliongea nae mawili matatu,“Oooh wewe ndio mama wa yule mtoto mrembo wa kuitwa Erica!”Mama Angel akatabasamu kidogo na kusema,“Ndio, mimi ndiye mama yake”“Nimependa sana yule mtoto anavyoongea, nilimuomba siku anikutanishe na ndugu zake wengine, alinionyesha tu yule kijana mzuri Erick, halafu alisema ana dada yake anaitwa Angel na mdogo wake anaitwa Ester”“Kheee kumbe alikutajia wote!”“Ndio, yupo vizuri sana yule binti kwakweli, halafu ana akili sana. Natamani kumuona dada yake huyo Angel najua nae atakuwa ni mzuri sana kama yeye”“Karibu sana, tutakukaribisha nyumbani kwetu”Waliongea ongea pale na yule mzee kisha yule mzee aliweka oda yake na moja kwa moja kuaga mahali pale na kuondoka.Wakati mama Angel na baba Angel wanaondoka, njiani mama Angel alimwambia mume wake,“Ila yule mzee jamani kafanana na Rahim ujue!”“Yule mwarabu?”“Ndio, nahisi ni ndugu wa Rahim na huenda ni baba yake”“Mmmmh!”“Ndio, mimi simfahamu baba yake Rahim inawezekana akwa yule, sijaongea sana na baba yake ila nahisi maana Rahim alishawahi kunieleza kuwa baba yake ni mkarimu sana na yule mzee ndio yupo hivyo, anaonekana kuwa mkarimu sana”“Duh!! Inawezekana lakini”“Halafu yule mzee anataka kumuona Angel”“Kheee kamjuaje Angel?”“Si huyo mwanao chaumbea Erica, amemtajia orodha nzima ya watu kwenye familia hadi Ester”“Kheeee kweli mwanangu yupo kwenye viwango vingine vya umbea”“Ni kweli kabisa, yule ni kiwango yani umbea wake kungekuwa na shule ya umbea ukimpeleka akasome utakuta amekuwa mwalimu wao”Baba Angel alicheka sana maana pia hakutegemea kama binti yake Angel aliweza kupiga Stori na huyo baba hadi kufikia hatua ya kumtajia orodha ya watu kwenye familia yao.Leo madam Oliva anafikiwa na mgeni wa muda mrefu ambaye ni rafiki yake, kwahiyo anafurahi sana kufika pale na kuanza kumwambia madam Oliva,“Natumai leo nimemkuta mtoto wako!”“Ndio, mwanangu yupo leo siku hizi nakaa nae”Basi madam Oliva anamuita Paule ambaye alifika kwa haraka na kuanza kumtambulisha kwa rafiki yake huyu,“Mwanangu mwenyewe ndio huyu anaitwa Paul, halafu Paul huyu ni rafiki yangu ni mwalimu pia anaitwa mama Yusra”Basi Paul anamsalimia pale na kumfanya huyu mama amsifie sana kuwa Paul anaonekana ni kijana mpole,“Yani inaonyesha Paul ni mpole sana, hongera kwa hilo madam”“Asante”Kisha madam Oliva alimruhusu Paul kuendelea na kazi zake, muda kidogo anafika Steve ambapo madam Oliva alimtambulisha pia kwa rafiki yake huyu na kufurahi pale huku wakiongea mambo mbalimbali.Wakati wakiondoka, ndipo mama Yusra alipomuuliza rafiki yake,“Hivi nakumbuka si ulisema babake Paul alimtelekeza mtoto?”“Ndio, wanaume wana mambo ya ajabu sana. Tunawavulia basi tu”“Kwahiyo umeamua kurudiana nae?”“Nirudiane nae wapi? Huo ujinga siwezi kuufanya hata nikiwa nimekufa, yani siwezi kufanya kitu kama hiko kabisa, yule mwanaume sitaki hata kumuona kwenye uso wangu”“Mmmh ila mbona ndio umenitambulisha pale kwako”“Kivipi?”“Kwani yule Steve si ndio babake Paul?”“Hapana, yule sio”“Acha masikhara bhana madam, yule ndio baba wa mtoto wako, hata chizi huwezi kumdanganya, mtoto kafanana kila kitu na yule baba”Madam Oliva alishindwa hata kutia neno pale, moja kwa moja alimsindikiza rafiki yake hadi alipopanda basi.Wakati anarudi alijiuliza sana kwanini inakuwa hivyo? Hakupata jibu kabisa, wazo la mama Angel kuwa huenda alibadilishiwa mtoto linaanza kufanya kazi kwenye akili yake, basi anaona ni vyema aanze kumchunguza Steve ili ajue kama kuna mwanamke Steve alizaa nae ili aweze kupata ukweli.Ilipita kama wiki, ndipo mama Sarah alikuwa huru kwani kwa siku hiyo Rahim aliondoka yani siku ambazo Rahim alikuwepo alishindwa kufanya chochote sababu muda mwingi Rahim alionekana kumfatilia kwa mambo yote anayoyafanya.Basi kwa siku hiyo aliamua kumpigia simu dokta Jimmy na kuanza kuongea nae,“Ila dokta Jimmy, kwanini ulianza kuniambia vile mbele ya yule mtu?”“Mtu gani?”“Yule niliyekuja naye na nikakutambulisha kuwa ni mume wangu mtarajiwa”“Mume mtarajiwa wakati yule ni moto”“Moto? Moto kivipi?”“Yule jamaa sio mzima, au na wewe ni moto?”“Sikuelewi dokta, unazungumzia nini kwani?”“Sikia nikwambie, mara kadhaa nimewahi kumuona yule jamaa hospitali moja hivi akifata vidonge vya ARV”“Unaongelea nini kwani? Ni vidonge gani?”“Uko wapi wewe hujui ARV? Wa wapi wewe jamani? Hujui mtu akianza kunywa hivyo vidonge kapatwa na nini?”“Sielewi kweli, hebu nieleweshe”“Kwa kifupi yule jamaa yako ni muathirika, ana ukimwi”“Unasemaje?”Yani mama Sarah aliona hata simu ya moto, alijikuta tu akiikata ile simu yani aliiona haifai. Ila baada ya muda kidogo alipigiwa tena simu na dokta Jimmy,“Basi tukutane ili tuweze kuzungumza, nitakushauri cha kufanya usijali hata kama umekutana nae kimwili”“Utanishauri nini? Jamani si ndio nitakuwa nimeubeba mimi!!”“Sikia Manka, usipaniki wala nini. Tukutane halafu huyo jamaa itakuwa amekufanyia makusudi, ila atajuta kutufahamu, tulia tu Manka najua unanijua vizuri, siwezi kuacha uteketee. Halafu tutaongea vizuri na kuhusu yale madai yako”Mama Sarah aliitikia tu ila kiukweli hakuwa na furaha yoyote ile.Sia kama kawaida yake katika harakati za kumfatilia dokta Jimmy, kwa bahati anamuona mahali na kuanza kumfatilia kwa karibu zaidi, mara dokta akamuona mzee Jimmy kasimama mahali anaongea na simu,“Ndio, tukutane kule kwenye kaburi la mzee kama baada ya masaa matatu maana mimi ndio naondoka huku muda sio mrefu”Yani moja kwa moja Sia akahisi tu kaburi linalosemwa ni kaburi la mzee Jimmy, yani muda huo alihisi kama akili yake ikipaa kwani aliondoka hapo na kumpigia simu baba Angel na kuomba akutane nae mahali ambapo muda mfupi tu walikutana hapo na baba Angel,“Muda sio mrefu nimemsikia dokta Jimmy akiwasiliana na mtu kuwa wakutane kwenye kaburi la mzee Jimmy, kama inawezekana twende muda huu huko huko”“Basi ngoja niende huko, ila wewe Sia ubaki”“Mmmh hapana, twende tu wote hata sijui usalama wa huko, naomba twende wote”“Usalama gani kwani kuna vita?”“Mtu akifikia hatua ya kubadilisha watoto ni sawa na vita hiyo, sio wa kumuamini mtu huyo, twende wote tu”“Kwahiyo wewe ndio unakuwa kama bodyguard wangu!!”Baba Angel alicheka kiasi kisha aliingia kwenye gari na Sia na kuondoka kuanza safari ya kuelekea kwenye kaburi la mzee Jimmy.Kwenda kwenye kaburi la mzee Jimmy kulikuwa na mwendo kiasi, kwahiyo baba Angel ilibidi aongeze mwendo ili aweze kufika kama wale walivyopanga baada ya masaa matatu, walifika na kusimamisha gari pembeni kwanza kisha walishuka na kuanza kuelekea kwenye eneo la lile kaburi.Kabla hawajafika kabisa walimuona dokta Jimmy na mama Sarah ndio wamesimama pale kwenye kaburi wakiongea, yani pale baba Angel ndio alipoamini vingi alivyosikia kuhusu mama Sarah Kabla hawajafika kabisa walimuona dokta Jimmy na mama Sarah ndio wamesimama pale kwenye kaburi wakiongea, yani pale baba Angel ndio alipoamini vingi alivyosikia kuhusu mama Sarah.Kwakweli baba Angel alipaniki sana kwa muda ule na kumwambia Sia,“Kwakweli mimi naenda pale ili waniambie mbivu na mbichi”Baba Angel akataka kwenda ila Sia alimzuia na kumwambia,“Hapana Erick usiende, tujibanze tu na kuangalia kinachoendelea, huwezi jua kuwa wale watu wana ajenda gani!”“Sio ajenda gani, hebu kumbuka yule dokta kafanya mambo mangapi? Halafu yule Manka kama mjinga kabisa, anawezaje kushirikiana na mtu kama yule!”“Ni kweli kabisa usemayo, ila tusisonge popote, tusimame hapahapa tuendelea kuchunguza”“Kwakweli uchunguzi usio na majibu huwa siuwezi kwakweli, siku zote hizi nipo tu makini na uchunguzi hata mambo mengine sifanyi, yani hapa natakiwa kupata jibu au kuacha haya mambo kama yalivyo. Natakiwa nionane nao kabisa ili nijue mbivu na mbichi”Baba Angel alikuwa bado akihitaji kwenda ila bado Sia alimzuia kwa kumshika mkono, baba Angel ilibidi amsukume Sia pembeni na moja kwa moja kwenda waliposimama dokta Jimmy na mama Sarah hata wao walimshangaa kwani hawakutegemea kumuona, basi baba Angel akasema,“Bora nimewakuta, niambie ukweli dokta kuhusu watoto wetu uliwafanya nini?”“Kwani wewe unataka kitu gani? Kama kilichotokea tayari kilishatokea huwezi kubadilisha chochote, unataka nini kwani?”Baba Angel alijikuta akijawa na hasira sana kwa lile jibu la dokta, basi moja kwa moja alimkunja dokta na kumpiga ngumi moja ya sura na kufanya yule dokta hata aanguke chini, mama Sarah alijaribu kumtoa baba Angel pale na kumwambia,“Ondoka wewe, unataka kujitafutia matatizo”“Matatizo gani? Na wewe usinijibu muuwaji mkubwa wewe”Muda ule ule baba Angel alimnasa kibao mama Sarah maana alijikuta akikumbuka yale mambo ya yeye kuwekewa sumu, kwakweli mama Sarah alichukia sana na kusema,“Nadhani Erick hunijui vizuri mimi, hivi kweli wa kunizaba kibao wewe!!”Erick hakumsikiliza ila alimkunja dokta Jimmy na kumwambia,“Leo sikuachii hadi umeniambia ukweli wa kila kitu”Sia alikuwa yupo kule kule kwa mbali akiangalia kila kinachoendelea, gafla aliona kama mama Sarah akitoa ishara kwa mtu, vile Sia alipokuwa akiangalia vizuri ilia one ni mtu gani aliyepewa ishara alishtuka kumuona kashika bastola halafu kailengesha kwenye kichwa cha baba Angel, kwakweli kwa muda ule ule Sia alisema kwa nguvu sana,“Erick, inamaaaaaa….”Kisha akageuka upande aliokuwepo baba Angel, muda ule ule alishangaa kuona baba Angel akiwa chini huku damu zikimtoka, yani hapo Sia alihisi kama moyo wake unalipuka hivi na kuanza kupiga kelele za kuomba msaada sasa,“Tunakufaaaa, tusaidieni….”Na kwavile Sia alikuwa na sauti kali, zile kelele zilifanya hata dokta Jimmy na mama Sarah wakimbie halafu Sia alienda eneo lile huku baadhi ya wananchi nao wakisogea mahali pale.Kwakweli baba Angel alikuwa akitokwa na damu nyingi sana, kwahiyo ilibidi wasiulizane pale kuwa imekuwaje zaidi ya kuanza kumpa huduma ya kwanza baba Angel ambaye walipomuangalia vizuri ilionyesha kapigwa risasi kadhaa miguuni, basi wale wananchi walijitahidi kuweza kumbeba hadi kwenye gari yake kisha kijana mmoja ndio alijitoa kwaajili ya kuendesha na kuwapeleka hospitali.Mama Angel akiwa nyumbani kwake, leo aliona ni vyema akatoka kidogo na kwenda kuangalia kinachoendelea kwenye ofisi yake, ila alipofika tu ofisini alikutana na mwanamke mmoja ambaye alimsalimia kwakweli mama Angel alimshangaa kiasi ingawa alikuwa akimtambua mwanamke huyo, basi alisimama na kuongea nae kidogo ila yule mwanamke alimuomba wakae eneo kidogo na apate kuzungumza nae, ikabidi mama Angel akubali na walikaa eneo ambalo sio mbali na ofisi ya mama Angel kisha yule mwanamke alianza kumwambia,“Unajua sikuwa najua unapoishi wala unapofanyia kazi, ila nikajaribu kukuangalia mtandaoni na kugundua ofisi yako hii ilipo basi nikaamua kuja kwa haraka ili kukwambia hili”“Niambie tu”“Ingawa najua mume wangu hataki kabisa swala hili niseme ingawa nilimwambia kuwa nitasema”“Yani Moses hataki? Niambie tu ni kitu gani?”“Nisikilize kwa makini, ni hivi Moses ndiye aliyesababisha hadi duka la mumeo likaibiwa kila kitu”Mama Angel alishtuka kiasi na kuendelea kumsikiliza huyu mama ambaye ni mke wa Moses na aliendelea kueleza,“Usishtuke tu kuhusu hilo, ila shtuka hili. Mume wangu hakujiamulia tu kufanya vile, ila aliombwa na mkwe wako kufanya vile”“Kheeee babake Erick!!”“Ndio, mzee Jimmy. Yeye ndio alimuomba Moses kumuibia mumeo kwa lengo kuwa mumeo atachanganyikiwa kabisa baada ya ule wizi na atafilisika na kuomba msaada tena kwake”Mama Angel alipumua kidogo na kusema,“Kheee makubwa, eeeh ikawaje tena?”“Mimi nilimkataza Moses kukubali ila mume wangu hakutaka kuelewa ni kwavile aliahidiwa pesa nyingi sana na yule mzee ila ndio baada hapo tulianza kuwa watumwa wa mzee yule yani tulifanya kitu ambacho alikitaka yeye”“Duh!! Niambie tu hata usiogope”“Kama una kumbukumbu nzuri, kuna siku mumeo alivamiwa akiwa kwenye gari na aliibiwa kila kitu na kurudi nyumbani kwa miguu”Mama Angel alikumbuka hilo tukio ambalo huwa hata halikumbushi maana huwa linamtia uchungu sana na kuendelea kumsikiliza huyu mwanamke tu kuhusu kitu anachokizungumzia,“Sasa pale ni vijana ambao walitumwa na Moses, na aliagizwa na mzee Jimmy kufanya vile. Nakumbuka mliamua kwenda kuishi kwa mzee Jimmy ila mliishi kidogo na wewe kumshawishi mumeo kuondoka, kisha akaondoka na kurudi kwenu. Pale ndipo mlipomchanganya mzee Jimmy maana sijui ilikuwaje mkauza ile nyumba yenu na kwenda mbali bila kumwambia yoyote yule kati ya ndugu zenu. Pale ndio palikuwa pagumu sana kwa mzee Jimmy, sijui hata mlifikiria nini hadi kufanya yote yale ila ndipo mlipomchanganya mzee Jimmy, hamjui tu ni jinsi gani mliweza kumchanganya baada ya pale na aliumia sana roho. Sikujua ni kwanini mzee Jimmy alikuwa akifanya vile kwa mwanae mpendwa ila badae alisema kuwa alitaka siku Erick aende kumpigia magoti na kulia kwa maisha kumshinda ila haikuwa hivyo, sijui ni kwanini alitaka kuombwa msamaha na Erick sielewi kabisa. Je unajua kilichosababisha kifo chwa mzee Jimmy?”“Kitu gani hiko?”“Ukikijua utashangaa sana maana kifo cha mzee Jimmy kimemfika baada ya maisha yenu kubadilika kabisa na kuanza maisha mapya, kwanza hakutegemea kabisa. Kuna siku alikuja na kucheza na wajukuu zake nyumbani kwako, ila kuna jambo alifanyiwa na yule mtoto wako mdogo wa kike na jambo lile lilimsababishia kifo chake”Mama Angel alishangaa sana,“Unamaanisha Erica? Alifanyiwa nini na Erica? Maana ndio alikuwa mtoto wangu mdogo wa kike kwa kipindi kile”“Ndio huyo huyo Erica, kuna jambo la ajabu sana alimfanyia babu yake na jambo hilo lilimsababishia kifo chake, sijui kama mwanao anaweza kukumbuka ila unaweza kumuuliza”“Kheee hebu niambie ni jambo gani maana sijui chochote kile, yani hapa ni kama unaniamsha toka usingizini, hakuna ninachoelewa”Yule mke wa Moses, alivuta pumzi kiasi kwanza huku akitaka kuanza kumueleza mama Angel sasa,“Ilikuwa, siku ya mwisho kwa mzee Jimmy kuja nyumbani kwako kabla ya kufikwa na umauti wake, sasa……!!”Mara simu ya mama Angel ilianza kuita hata mama Angel aliogopa maana kwa muda ule alihisi kama kapigwa ganzi mwilini vile, akifikiria ni kwanini baba mkwe wake awe katili kwao kiasi kile hakupata jibu kabisa, basi alimuomba samahani kidogo mke wa Moses na kupokea ile simu ambapo alikuwa akipigiwa na Sia, alipoanza kuongea nayo tu mke wa Moses nae aliinuka na kuondoka zake kwani naye ilionyesha simu yake kuita.Kwakweli mama Angel alishtuka sana kuambiwa kuwa mumewe yupo hospitali, akiwa hoi kabisa, yani mama Angel alihisi kupagawa kwa muda ule, hata hakufatilia tena mke wa Moses kaenda wapi, bali alikuwa akihangaika namna ya kumfikia mumewe kwenye hospitali aliyopelekwa.Moja kwa moja mama Angel anaendesha gari lake kama mtu aliyechanganyikiwa vile kwaajili ya kumuwahi mumewe hospitali.Mama Angel alifika hospitali wakati giza likiwa tayari limeanza kuingia, moja kwa moja alienda kuulizia kuhusu mumewe na kupelekwa alipo mumewe kwakweli alimuona mumewe akiwa na hali mbaya sana hata aliomba wampe uhamisho wa hospitali ili aende na mumewe kwenye hospitali kubwa ingawa pale napo walianza kumuhudumia ila alijikuta kutokuamini maana tayari alihisi kuchanganyikiwa kabisa.Hata hivyo alikuta pale hospitali napo ndio walianza kumuandikia ruhusa ya kupata huduma kwenye hospitali kubwa zaidi, basi moja kwa moja walipanda kwenye gari la wagonjwa pamoja na mgonjwa wao, kwa wakati huo alikuwepo mama Angel na Sia kwenye lile gari yani mama Angel alimpigia simu tu dereva wake ili aende kwenye ile hospitali kuchukua gari zao ambazo zipo kule.Walifika kwenye hospitali kubwa, na baba Angel alipelekwa moja kwa moja kwenye chumba maalum ili madaktari waweze kumuhudumia.Kwakweli mama Angel alikuwa nje hajielewi kabisa, alimuangalia Sia na kumuuliza,“Kwani imekuwaje?”Sia alimueleza kila kitu yani hakuacha jambo lolote lile katika maelezo yake, ila kiukweli mama Angel hata hakuwa akielewa vizuri kwa muda huo maana akili yake ilikuwa kwa mumewe tu.Walikaa pale hospitali hadi asubuhi yani mama Angel alishindwa hata kuwasiliana na familia yake kwa jinsi alivyochanganyikiwa kuhusu mume wake.Wakina Erica nyumbani walishangaa sana kwa kutokupata mawasiliano yoyote toka kwa wazazi wao, kiasi kwamba hawakuweza hata kwenda shule kwa siku ya leo maana hawakujua kitu chochote kile kinachoendelea, ukizingatia usiku kucha, Erica ndio alikuwa akimbembeleza mdogo wake. Muda mwingi walikuwa wakimpigia simu mama yao kwa kutumia ile simu ya mezani alikuwa hapokei simu yao. Basi ile asubuhi ndio walimuona dereva wao akiwa kaongozana na mtu mwingine wakileta gari za wazazi wao, ilibidi Erica awafate kuwauliza,“Hata hivyo tungekuja kuwaambia”“Kuna tatizo gani kwani?”“Nasikia mzee kapatwa na matatizo, hata sisi hatujamuona bado, tumeenda tu kuchukua hizi gari halafu ndio twende hospitali waliyo”“Ni wapi huko? Naomba twende wote”“Hapana Erica, bakini tu nyumbani”Erica alisononeka na wale madereva waliondoka zao, moja kwa moja Erica aliingia ndani na kuanza kuwaeleza wenzie,“Inasemekana wazazi wetu wamepatwa na matatizo”Erick akamuuliza Erica,“Hujaota Erica ni matatizo gani wameyapata?”“Ningeotaje wakati usiku mzima nilikuwa macho nikimbembeleza mtoto”“Oooh pole, nadhani ni zamu yetu sasa nenda tu kapumzike”Muda uke, Erick alimchukua mtoto ila muda kidogo mtoto nae alilala na kumfanya hata Erica kwenda kulala kwa amani sasa kwani alikuwa na usingizi wa kutosha tu.Muda kidogo, Erica alishtuka na kwenda moja kwa moja kwa Erick na kumwambia,“Nimeota baba yupo hospitali, eti alipigwa risasi”Erick alishtuka sana kusikia vile, ila baada ya muda kidogo mama yao nae alirudi nyumbani na walimfata kumuuliza vizuri, ambapo aliwaambia vile ambavyo Erica alisema kuwa baba Angel kapigwa risasi,“Jamani baba yetu, hali yake ikoje kwasasa?”“Mungu atusaidie kwakweli apone kabisa, naamini Mungu ni mwema na baba atapona kabisa ila tuzidi kumuombea baba jamani, haya matatizo sio madogo ni makubwa haya wanangu”Kisha mama Angel alienda ndani sasa kuoga na kumchukulia mumewe baadhi ya vitu ili ampelekee kule hospitali, baada ya muda mama Angel alitoka tena ila muda huu ilibidi aondoke na watoto na wao waweze kwenda kumuona baba yao hospitali.Walifika hospitali na kwenda kumuona, kwakweli bado hali yake haikuwa sawa, ila waliendelea kumuomba Mungu tu. Muda kidogo alifika pale hospitali ni rafiki wa baba Angel ambaye alikuwa ni Juma, maana alipata habari baada ya kumpigia simu mama Angel.Basi aliwakuta pale na kuanza kuongea na mama Angel,“Ilikuwaje kwani hadi Erick akapigwa na risasi?”“Hata naelewa basi!! Yani sielewi kitu”“Unajua nashangaa sana kuona Erick ana maadui wa kufikia hatua hiyo”“Maadui anao ndio maana aliwahi hata kuwekewa sumu kwenye chakula”“Duh!! Sikutegemea, kumbe!! Nadhani ni mambo ya biashara haya, dah sikufikiria kabisa kama jambo kama hili litampata Erick, wamefanikiwa kumtoa risasi lakini!”“Ndio, wamemtoa moja ila wanasema bado moja, kuna operesheni nyingine watamfanyia kumtoa hiyo risasi”“Dah nimesikitika sana”Basi Juma alikaa kidogo pale hospitali, na muda wa kuondoka mama Angel alimuomba aweze kurudi na watoto wake nyumbani, kwahiyo Juma aliongozana nao na kuwarudisha nyumbani kwao.Baada ya hapo Juma aliomba wasaa wa kukaa na Erick mdogo na kuanza kuzungumza nae, walienda kukaa kwenye bustani,“Sasa Erick, baba yako amepatwa na matatizo. Hapo ndio unatakiwa kuelewa ni kwanini Mungu alikuumba mwanaume katika familia hii, unatakiwa kusimama kiume, unatakiw akuonekana kwenye mstari wa mbele kuhakikisha baba yako anakuwa sawa. Biashara zake nyingi zitasimama kama wewe hutoweza kuziendesha, kumbuka itamchukua baba yako muda mrefu sana kuwa sawa kabisa, sisemi kuwa hatopona hapana, ila itachukua muda mrefu sana kwa baba yako kupona kabisa, unatakiwa kuwa makini. Simamia vyema biashara za baba yako,“Ila mimi nakaribia kufanya mitihani”“Nakwambia kuwa ndio hapa ule usemi wa wanaume tumeumbwa mateso hutimia, huwezi kusongesha biashara za baba yako kama usipokubaliana na hayo mateso. Najua kuwa baba yako anapenda usome kwa bidii na ufike mbali, mimi nakwambia kuwa soma huku ukisimamia biashara za baba yako kwa bidii, yupo hospitali na atahitaji matibabu pale tena matibabu ya hali ya juu na yatahitaji pesa, bila kukazana basi hamtoingiza pesa yoyote na kila kitu kitashindikana katika maisha yenu hapa nyumbani. Unatakiwa kuwa makini sana, nadhani unanielewa Erick”“Nakuelewa ndio”“Sitokuacha, nitakuwa nakusaidia kwenye kila kitu, najua unajua ni jinsi gani ninavyokupenda na ninavyopenda ubunifu wako na kazi zako. Nitakusaidia na kukupeleka sehemu mbalimbali ili kukuza biashara ya baba yako”Erick aliitikia tu kwani aliyokuwa akielezwa yalikuwa na ukweli mtupu kwani lazima gharama kubwa zitatumika kwaajili ya baba yao hospitali, kwahiyo alijiona kwa muda huo kuwa anatakiwa kushughulika kwa hali na mali kwaajili ya kusaidia familia yake.Basi Juma alimuaga na kumwambia kuwa atilie maanani aliyomwambia kisha aliondoka zake.Familia ya baba Angel ilikuwa kwenye wakati mgumu sana kwasasa, kwani muda mwingi mama Angel alionekana kushinda hospitali kwaajili ya mumewe kiasi kwamba hata mtoto wao mdogo Ester ilibidi tu aachishwe ziwa, muda mwingi Erica mdogo alikuwa nyumbani kushinda na mtoto halafu Erick nae alikuwa na swala moja la kwenda shule na kwenda kufatilia biashara za baba yake, na wakati huo huo kumfundisha Erica vitu vingine ambavyo utakuta amevikosa shuleni sababu ya muda mwingi kuwa nyumbani akimlea mdogo wake, kwahiyo alikuwa haendi shule kwa siku zingine yani kwa kipindi hiko hata kitu kucheza karata alikiacha kwa muda kwani alijikuta akipatwa na mambo mengi na akipata wasaa wa kulala alikuwa akilala sana.Siku hiyo Erick kama kawaida, alienda shule na alipotoka shuleni alienda moja kwa moja kiwandani kwa baba yake ili kuendelea kusimamia vyema biashara za baba yake, basi siku hii alifika yule mteja wao mkubwa sana yule mwarabu na kuanza kuongea nae,“Niambie kijana Erick, sijawasiliana na baba yako kwa siku nyingi, kwani kasafiri?”“Hapana, hajasafiri ila baba yangu amepatwa na matatizo”“Kheee, matatizo gani tena?”Erick alimwambia tu kwa kifupi huyu mwarabu na kumfanya ashtuke sana,“Ni majambazi walimvamia au kitu gani? Yani imekuwaje hadi akapigwa risasi?”“Itakuwa ni majambazi walimvamia maana alienda kutembelea kaburi la babu yetu”Yule mwarabu alisikitika sana na kuomba kupelekwa huko hospitali siku ya kesho yake ili aweze kumuona huyo mgonjwa maana ni mtu aliyemfahamu vizuri.Basi waliagana nae na kupanga kukutana nae kesho yake asubuhi ili waende hospitali.Kesho yake kama walivyopanga, yule Mwarabu alikutana na Erick na moja kwa moja kwenda hospitali ambapo walimkuta pale mama Angel na kwenda kumuona baba Angel ambaye bado hali yake haikuwa nzuri, basi yule Mwarabu akauliza vizuri,“Wamemtoa risasi zote lakini?”“Wanasema bado moja”“Ngoja niongee nao ili tufanye utaratibu wa kumuhamishia hospitali nyingine, kuna hospitali nzuri sana huko na wanaweza kufanya hili”Yule mwarabu alienda kuongea na daktari, ila huyu mzee ni mtu anayefahamika sana na anafahamiana na watu wengi kwahiyo iliwezekana kwa kila alichokisema na siku hiyo hiyo baba Angel alihamishwa kwenye hospitali nyingine, na huko alipewa huduma kwa siku hiyo hiyo na kutolewa ile risasi iliyobaki.Kwakweli mama Angel alimshukuru sana huyu mwarabu na alifurahi kufahamiana nae, yani kwa kipindi hiki mama Angel hata hakufatilia ni wakina nani wamempiga mumewe na risasi, je wako wapi kwani yeye alichokuwa akifatilia ni kimoja tu kujua hali ya mumewe inaendeleaje maana ndio ilikuwa ikimpa shida.Ila baada ya ile huduma ambayo baba Angel aliipata, taratibu alionekana kuanza kuwa sawa kwani alikuwa akiweza hata kukaa na kuongea mawili matatu na mke wake, na hilo lilikuwa ni jambo la furaha sana kw amama Angel.Mama Angel siku hii aligundua jambo kuwa watoto wake wanapata shida kwenye masomo yao kwani muda mwingi wamejikuta na mambo mengi kama yeye,“Oooh jamani, hata wewe Erica huwa huendi shule?”“Huwa siendi kama mtoto akisumbua sana”“Kheee hapana mwanangu, huyu Ester nitakuwa namuhudumia mwenyewe kuanzia sasa. Baba yenu anaonyesha matumaini. Namshukuru sana yule Mwarabu, kwakweli katupeleka kwenyehospitali kubwa, na siku sio nyingi baba yenu ataruhusiwa ila tu hatoweza kutembea kama zamani kwanza, atakuwa akitembea kile kiti cha matairi.”“Dah! Namuhurumia sana baba”“Ila yote haya yataisha tu, Erica naomba kesho uanze kwenda shule vizuri kama zamani na hata Erick nitamwambia hili. Msome watoto wengi, tutafanya tu haya mengine.”Erica alikubaliana na mama yake, na kweli kuanzia kesho yake walianza kwenda shule kama kawaida kwani mama yao afadhari alikuwa akipata muda wa kulala na mwanae mdogo nyumbani tofauti na kipindi wakati akilala hospitali sababu ya hali ya mumewe ambayo ilikuwa mbaya, ila kwa kipindi hiko hali ya mumewe ilimridhisha na kumfanya aweze hata kulala nyumbani na mtoto wao mdogo.Siku hiyo ndio ilikuwa furaha sana nyumbani kwa mama Angel kwani baba Angel aliruhusiwa kutoka hospitali na kurudishwa nyumbani, kwahiyo walikuwepo pale nyumbani na kufurahi sana huku wakiongea mambo mengi mengi, kwa wakati huo alikuwepo pale mama mzazi wa mama Angel, ndugu zao wengine, pamoja na mama mzazi wa baba Angel, na Tumaini pia alikuwepo pale kwani walifurahi kwa kiasi Fulani kwa baba Angel kuruhusiwa kutoka hospitali.Basi baba Angel aliongea kiasi na mama yake mzazi na mama mkwe wake,“Mama zangu, naomba kwasasa Angel asifahamu chochote ambacho kimenitokea, najua ni kwa kiasi gani swala hili limewazorotesha wanangu hawa kimasomo, nisingependa Angel nae apate simanzi, hivyobasi akiwa likizo muwe mnamuacha huko huko kwenu yani sitaki aelewe chochote kile, mwambieni nataka kuonana nae hadi atakapomaliza shule”“Sawa hakuna tatizo, na hivi Angel anavyokupenda nadhani ni wazi kabisa atashindwa hata kufanya mitihani”“Naelewa, hapa nyumbani tu huyu Erick na Erica naona wamekonda sana, najua ni sababu ya mawazo ila nitaongea nao pia ili wasome kwa amani”Basi mama yake akauliza,“Ila Erick ni kitu gani haswaaa kilitokea maana nashindwa kuelewa”“Mama, ukimpata Sia atakueleza mengi sana maana ni yeye ndiye nilikuwa nae siku ya tukio”“Usiniambie kuwa yule mwanamke alianza tena matatizo yake!”“Hapana mama, siku hizi Sia kawa mtu mzuri kabisa hana matatizo wala nini. Tena naweza kusema kuwa amenisaidia sana, kwani yeye ndiye aliyemuona aliyekuwa akitaka kunipiga risasi na kuwahi kuwa niiname, sasa yule mpiga risasi aliamua kunilengesha nitakapoinama na kufanya zile risasi zinipate miguuni kisha nikaanguka, inaonesha alilenga kunipiga kichwani ila baada ya sauti ya Sia kuwa niiname ndio yeye akaamua kunipiga miguuni akijua ningeinama”Walipumua kiasi,“Duh!! Kwahiyo dhamira hapo ilikuwa ni kukuua?”“Kwakweli sijui hata kidogo, ila mama nimewahi kuwekewa hata sumu kwenye chakula. Nadhani ni watu wenye mpango wa kuniua kwa muda mrefu”“Kheee nahitaji kuwafahamu”“Hapana mama, usijiingize kwenye matatizo”Aliongea nao pale ila kiukweli hawakuridhika wala nini, na muda wa kuondoka mahali pale ndipo Sia nae alipofika kwenda kumuona baba Angel maana alikuwa akienda mara kwa mara hospitali, basi alivyowasalimia pale ndio mama mzazi wa baba Angel aliamua kuondoka na Sia ili aweze kumsimulia vizuri.Waliondoka nae na kuongea nae, kwakwlei Sia hakuwa na sababu ya kuficha jambo lolote, yani alieleza kila kitu toka mwanzo alivyopanga na mzee Jimmy kubadilisha watoto,“Kheee ndioma ulikuwa umekazana kusema umezaa na mwanangu sababu ulijua akipima damu atakuta ni mwanae sababu mlimbadilisha?”“Ndio, yani nilikuwa najua hivyo ila sijui yule mzee alinichezea mchezo gani ila hakuwa mtu mzuri kabisa”“Unajua umenishangaza sana, yani kwanini aligeuka na kuwa mbogo kiasi hiko? Yani abadilishe watoto ili iweje? Kumbe ndiomana alipoona Erica anakaribia kujifungua basi akaona ampeleke Erick mbali, aaaah kweli mume nilipata jamani, yani anafanya kitu kama hiko kwa mtoto wake mwenyewe!! Na aliyempiga Erick risasi ni nani?”“Nilimuona kwa macho yangu wala siwezi kumsingizia, alikuwa ni Moses”Huyu bibi alishangaa sana kwani huyo Moses alimfahamu vizuri sana na kusema,“Haiwezekani, yani Moses ndio kawa mnyama kiaski hiko kwa Erick jamani!! Inaonyesha kuna mengi huwa yanaendelea kwenye kaburi la mzee Jimmy eeeh!”“Ndio mama, ni mengi sana yanaendelea”“Basi sikia, wala msifatilie tena jambo hilo yani msijisumbue tena. Kila kitu niachieni mimi. Usinione hivi, hata huyo mzee Jimmy alikuwa akiniogopa maana nikiamua langu basi naamua tu. Kama niliweza kusimama mwenyewe kama mwanamke na kufanya vyote nilivyovifanya basi naamini hakuna kitu kinachonishinda. Sia nbiachieni mimi na kila kitu kitakuwa wazi hapa mbele yenu, yani ukweli utapatikana tu”“Oooh asante mama, yani hivi hata sijui mtoto wangu wa kweli ni yupi”“Aaaah usiniambie hilo, maana huo ni ujinga wako. Uliona wapi mwanamke uzae kwa uchungu halafu ukubali kwa hiyari yako kubadilisha mtoto na kuchukua mtoto wa mwenzio? Ukiulizwa wako alikuwa na matatizo unajibu hapana, yani njaa na shida zikufanye ufanye ujinga namna hiyo!! Huo ni ujinga hata sio umasikini bali ni ujinga, kuna wanawake utakuta hawajiwezi kabisa ila wanakazana kulea watoto wao katika hali yoyote ile na wanawapenda hatari, halafu wewe upate nguvu ya kubadilisha mwanao kwa hiyari halafu upo kulalamika ni pesa!! Huo ni ujinga, labda useme kuwa mzee Jimmy alikuroga”Sia hakuweza kuongeza neno lolote kwa huyu mama zaidi zaidi alikubaliana nae tu kwa kile ambacho alikiongea.Miezi ilipita na mimba ya Vaileth ilizidi kukua, sema ilikuwa ngumu kugundulika na mama Angel kwani muda mwingi alijifunga kwa khanga kifuani halafu mama Angel nae alikuwa na majukumu mengi ukizingatia mumewe alikuwa bado akitembelea kiti cha matairi kwa kipindi hiko maana miguu bado haikuwa sawa.Basi Vaileth alikuwa akitumia kila namna kuweza kuficha ile mimba yake, alipoona anakaribia mwishoni alianza kumuomba mama Angel ruhusa ili akasalimie kwao,“Vai jamani utaondokaje katika kipindi hiki? Yani hapa nahitaji msaidizi wa hali na mali. Unajua kabisa nina matatizo, utaondokaje, yani sitaki kukukosa hata kwa siku moja. Naomba univumilie Vaileth, kwenu utaenda tu hakuna tatizo binti yangu”Vaileth aliogopa kumwambia ukweli mama Angel kuwa ana mimba kubwa kabisa, kwahiyo aliamua kuendelea kuvumia tu ile hali.Siku hiyo usiku, alihisi kushikwa na uchungu wa hali ya juu ila alikuwa akijikaza, yani alikuwa akiugulia sana chumbani kwake na akaona akifanya ujinga basi anaweza kujikuta hata akijifungulia pale pale nyumbani.Aliandaa nguo zake na kubeba begi lake ili ikiwezekana awahi hospitali kujifungua na moja kwa moja aende nyumbani kwao maana hakutaka kujilikana na mimba ile ndiomana muda wote alivaa nguo kubwa kubwa na kujifunga khanga kifuani, na kwavile hakuwa na tumbo kubwa sana kwa ile mimba kwahiyo ilikuwa sio rahisi kumgundua kwani alijitahidi kwa kila hali isionekane. Basi alitoka sebleni na kumuomba mama Angel ruhusa kwa mara nyingine,“Mama, nahitaji kwenda kuwasalimia nyumbani”“Mbona unaongea huku umekunja sura Vai? Una tatizo gani kwani?”Vaileth aliinama chini akiugulia maumivu ya uzazi aliyokuwa akiyapata, alisema kwa kutazama chini,“Naomba niruhusu mama”Mama Angel alimsogelea karibu, na muda ule Vaileth alishindwa kusimama tena, alijikuta tu akikaa huku damu na maji zikimuanguka miguuni. Vaileth aliinama chini akiugulia maumivu ya uzazi aliyokuwa akiyapata, alisema kwa kutazama chini,“Naomba niruhusu mama”Mama Angel alimsogelea karibu, na muda ule Vaileth alishindwa kusimama tena, alijikuta tu akikaa huku damu na maji zikimuanguka miguuni.Hapo ndio mama Angel alipohisi wazi kuwa Vaileth alikuwa ni mjamzito ila muda ule haukuwa muda mzuri wa kuanza kumuhoji maswali kwani alikuwa kwenye hali mbaya tayari, mama Angel alimuita tu dereva na kisha kumsaidia Vaileth kupanda kwenye gari halafu kumpeleka hospitali yani alikuwa akimshangaa sana kwa Vaileth kujificha kwa siku zote hizo kumbe alikuwa ni mjamzito.Walipofika hospitali tu, yani ile kupokelewa Vaileth alijifungua na moja kwa moja kumkumbiza leba, kwahiyo mama Angel alibaki akiandikisha tu, yani hakuna jambo alilokuwa akilielewa kwa muda ule, kisha mama Angel alipomaliza kuandikisha ilibidi aondoke ili arudi nyumbani kuweka mazingira sawa ukizingatia aliondoka kwa haraka tu kumuwaisha Vaileth hospitali.Yani njiani alikuwa na mawazo sana huku akijiuliza maswali mengi,“Huyu Vaileth jamani kwanini kanifanyia hivi!! Haya si ndio mambo aliyokuwa akiyasema Tumaini mweeeh jamani huyu mtoto kaniweza kwakweli, sijui hata nitafanyeje na hapa nina majukumu hatari sijui nitafanyeje jamani”Mama Angel aliwaza sana maana alihisi huduma zote kumuelemea kwa muda huo, basi alifika nyumbani kwake moja kwa moja, alipoingia getini tu akamuona Erica na kumuuliza,“Wewe usharudi shule? Ila afadhari maana hata sikujua nianzie wapi”“Nimerudi mama sababu ya dada Vaileth”“Usiniambie na hilo umeota?”“Ndio, nimeota kuwa kajifungua”“Kheee, haya kajifungua mtoto gani?”“Wa kiume”“Khaaaa, wewe mtoto hapana jamani kama mfalme njozi, haya twende ndani ili nimpikie chakula mgonjwa”“Aaaah nimempigia mamkubwa simu, kashakuja yupo jikoni kupika”“Khaaaaa”Basi mama Angel aliingia ndani hadi jikoni, ambapo alimkuta dada yake yani mama Junior akishughulika na zile kazi za pale,“Khaaaa dada, kwani huyu Erica kakwambiaje?”“Huyu mtoto jamani loh!! Unajua kanifata nyumbani, kasema nije nikusaidie kuna matatizo, nimetoka huko hai hai maana nimeogopa matatizo ya shemeji tena. Kufika hapa ndio ananiambia kuwa Vaileth kajifungua kwahiyo mimi nimpikie, kwanza kanichosha nimeona nisiongee kwanza, nipike tu. Hiyo na wewe mdogo wangu unawezaje kuishi na bingti wa kazi mwenye mimba katika nyumba yako? Sasa atakusaidia nini? Atakuwa msaada gani kwako jamani!”“Acha tu dada, unadhani nilijua basi! Hata sikujua chochote yani mimi sikujua kitu kama vaileth ana mimba. Unajua majukumu yangu ya sasa, mume wangu bado ni mgonjwa, mambo kibao yameniandama yani hapa ndio naujua ugumu wa maisha ulivyo. Kwa kifupi nachanganyikiwa yani, huyo Ester mwenyewe saivi amekua kingangari maana kunyonya aliacha kipindi kile kile, ila Mungu ni mwema maana mtoto anatembea vizuri tu na kula vizuri. Leo sasa si ndio nikakutana na hili balaa la Vaileth, jamani mikosi ikiamua kukuandama inakuandama hadi akili ikukae sawa”“Ila mdogo wangu kuwa makini sana, huyu binti akirudi aende kwa huyo muhusika”“Nitakachomuhurumia hapa ni kusubiri tu mwanae akatike kitovu basi, nimruhusu kwenda kwao maana nikimtoa sasa sitakuwa nikimfanyia mazuri. Kumbe alikuwa akifanya kazi zote za humu na mimba yake dah nimeshangaa sana”“Ila subiri, nitakwambia cha kufanya wanaona wewe ni mpole mdogo wangu”Basi walikaa pale na kupika na kumsaidia mdogo wake kazi zingine, ila mama Junior alipigiwa simu na mume wake, kwahiyo ilibidi amuage mdogo wake na kuondoka maana kazi karibia zote pale walishafanya.Mama Angel muda huu aliondoka na moja kwa moja kwenda zake hospitali kwaajili ya kumuona Vaileth na kumkuta akiwa na hali nzuri, akaongea nae kidogo pale,“Pole na hongera ila bado sijamaliza maneno yangu kwako”“Asante mama”“Wamelikupa uji eeeh!”“Ndio, walinipa uji na maandazi”“Hii hospitali ipo vizuri sana, ngoja nikaongee na daktari aweze kunipa ruhusa tuondoke maana naona upo sawa”Basi mama Angel alienda kuongea na daktari, ili ampe ruhusa. Kwa muda huo alikutana na yule daktari rafiki yake yani dokta Maimuna basi alianza kuongea nae pale,“Mimi sina tatizo na wewe mama Angel ila nina tatizo na yule mume wako, sikujua kama ni mumeo yule”“Ila amepatwa na matatizo, alipigwa risasi miguuni yani hawezi kutembea kwasasa, anatembelea kiti cha matairi tu. Huyu aliyejifungua ni mdada wangu wa kazi, yani naona nitashindwa hizi safari za kuja hospitali ndiomana nikaja kumuombea ruhusa maana naona yupo sawa”“Weeee Erick alipigwa risasi na nani?”“Watu wabaya tu”“Jamani, hata kwa mambo yote ambayo Erick amenitenda bado siwezi kufikia hiyo roho mbaya ya kumpiga risasi au kumtumia watu wafanye hivyo. Erick hana roho mbaya kiasi hiko mpaka apate maadui wa hivyo, kwakweli nimeingiwa imani na hilo swala jamani dah!!”“Ndio hivyo ndugu yangu”“Nitamuandikia ruhusa huyu mdada wako halafu tutawasiliana kesho maana nitakuja kumuona Erick mara moja”“Nashukuru sana dokta Maimuna”Basi waliongea kiasi na yule daktari alienda kumuangalia kwanza Vaileth na kisha kumuandikia ruhusa mama Angel ilia pate kuondoka nae.Kwahiyo mama Angel sasa aliondoka na Vaileth na kurudi nae nyumbani kwake.Walifika nyumbani na kukuta Erica ameandaa mazingira mazuri kabisa chumbani kwa Vaileth kwaajili ya kukaa na mtoto yani alisafisha kila kitu, kwakweli kwa uchapakazi aliokuwa nao huyu mtoto ilimfanya mamake amsifie sana,“Kwahili mwanangu hongera sana, yani dada yako Angel sasa uwiiii nisingekuta kafanya chochote na uvivu wake”“Ila mama tumemkumbuka Angel”“Atarudi tu, akishamaliza kabisa shule atarudi, sijataka achanganye masomo yake na hii hali ya baba yenu kwasasa”Basi mama Angel alienda kumkanda Vaileth kwanza na kuoga, kisha kumpatia tena chakula, halafu alimuacha na mtoto wake chumbani.Kwakweli Vaileth alijikuta akitokwa na machozi tu kwa huduma ile aliyopewa na mama Angel maana alimajali kama ni mwanae kabisa, alimpatia huduma zote muhimu, Vaileth alijihisi uchungu kwakweli kwa namna moja au nyingine.Ila bado alijisemea kuwa swala hilo ataendelea kulifanya kuwa siri kabisa kwani hakutaka kueleza kwa uwazi kuwa yule mtoto ni wa Junior, alitaka adanganye tu maana aliona kusema ukweli atasababisha tatizo kubwa sana.Basi mama Angel aliongea na mumewe chumbani kuhusu Vaileth,“Yani balaa zimetupata mume wangu, na hii purukushani sijui itakuwaje”“Ila hata hukuweza kumuhisi kuwa ni mjamzito!”“Yani huwezi amini, Tumaini alisema hili jambo na nilimktalia katakata kuwa Vaileth ni mjamzito halafu na yeye Vaileth sijui akanifanyia mchezo gani maana kumpima nikakuta kweli hana mimba kumbe mimba anayo jamani!! Wasichana wa kazi hawa mambo yao loh!!”“Ila ni nani muhusika wa hiyo mimba?”“Sijamuuliza, ila umeniambia jambo jema itabidi nimuulize ila nimechoka hatari, nitaongea nae kesho tu”“Pole mke wangu jamani”Yani baba Angel alikuwa akimuhurumia sana mkewe, haswaa kwa siku kama hiyo alizidi kumuhurumia maana mambo yote yalimuelemea pale nyumbani kwao.Yani siku hii mama Angel alilala kama mzigo yani hadi alikuwa akikoroma kwa uchovu wa siku hiyo.Kulipokucha tu, alishukuru sababu ilikuwa ni Jumamosi, kwahiyo wakina Erica walikuwa nyumbani na waliweza kumsaidia baadhi ya kazi, ambapo kwa asubuhi ile tu Erick alienda zake kiwandani yani kwa kipindi hiki familia ilikuwa ikijishughulisha sana na hata hapakuwa na muda wa kupumzika.Kwenye mida ya mchana wa siku hii, mama Angel aliamua kwenda kuzungumza na Vaileth ambapo alihitaji kujua baba wa mtoto ni nani,“Eeeeh vai, huyo baba mtoto ni nani?”“Nisamehe mama, kuna kijana mmoja ila alikataa mimba”Vaileth aliinama chini na kutoa machozi, kisha mama Angel akamuuliza,“Kwani Vaileth wewe si una mtoto huko kijijini kwenu?”“Ndio nina mtoto”“Imekuwaje upate mtu mwingine wa kukudanganya na kukujaza tena mimba bila ya ndoa? Unajua nini, mtu uking’atwa na nyoka basi ukiona jani lazima ushtuke, sasa wewe mwenzetu vipi eeeh! Yani upate mtoto wa kwanza asiye na baba halafu uje uzae mtoto wa pili asiye na baba, akili zako ni timamu kweli? Haya una mpango gani?”“mama, naomba tu unisaidie kwa siku chache halafu nitaenda kumpeleka mtoto kwa wazazi wangu”“Sababu wazazi wako ndio kituo cha kulelea watoto wasiokuwa na baba? Hebu muda mwingine muwe na akili nyie mabinti, hivi mnajua kama mnatuvuruga akili wazazi? Yani huwa tunachanganyikiwa, uzae mtoto wa kwanza nyumbani na baba asiyeeleweka, tunasema hili ni kosa ila ni kosa la kwanza labda mtu hajajua kadanganywa kwenye mapenzi. Ila bila hata ya kufikiria unapata tena nguvu ya kubeba mimba nyingine na kuzaa mtoto mwingine na unawaza kuwapelekea wazazi wako watunze, halafu inakuwaje? Unarudi tena kufanya kazi hapa kwangu ili upate mimba nyingine na uwapelekee wazazi wakatunze mtoto!!”Vaileth alikaa kimya na kuinama chini huku machozi yakimtoka kwani ni kweli alikuwa amefanya kosa, basi mama Angel akamwambia tena,“Vai, mimi ni mpole sana tena nina huruma sana ila katika maisha yangu ujinga sipendi. Ninapofanya ujinga mara moja huwa namuomba Mungu nisirudie tena huo ujinga, ni kweli sisi wanawake kuna muda tuna ujinga unatusumbua kichwani ila ni kumuomba Mungu ili huu ujinga ututoke. Vai, nitakapokuja kukuuliza tena kuhusu huyo mwanaume basi uwe na taarifa kamili zake, kama hataki tutaenda kupima damu na mtoto, yani naomba siku nitakayokuuliza tena uwe na jibu kamili juu ya huyo mjinga aliyekuambukiza ujinga binti mpole na mstaarabu kama wewe”Kisha mama Angel aliinuka na kuondoka zake, kwakweli yale maneno yalimuingia sana Vaileth, alijihisi vibaya ila muda mwingine aliona mama Angel kamwambia maneno ya ukweli kwani alichokifanya ni ujinga kweli.Mama Angel muda huu alipotoka tu alikutana na Erica ambaye alimuuliza mama yake,“Kwani mama unataka kumfukuza dada Vai?”“Nitamfukuza ndio, ujinga gani huu alioufanya? Hata wewe ukipata mimba nitakufukuza”“Kheee mimi nikipata mimba? Nikipataje?”“Aaaah usinichanganye Erica”“Ila mama, kabla hujafikia swala la kumfukuza dada Vai, naomba ukumbuke yale mazuri aliyoyafanya kwenye familia yetu”“Siwezi kumfukuza ila namtishia tu ili akae sawa”Mama Angel aliondoka zake na kuendelea na mambo mengine.Jioni ya siku hiyo ndipo dokta Maimuna alipowasiliana na mama Angel, kisha aliweza kufika pale nyumbani kwa mama Angel ili kuonana na baba Angel, kwakweli alipofika pale na kumuona baba Angel hata yeye alijikuta tu akimuhurumia na hata kile kinyongo alichokuwa nacho juu yake kikaisha, aliakaa nae chini na kuanza kuzungumza nae,“Ilikuwaje lakini?”“Hata mimi sielewi yani ila ndio hivi”“Aaaah pole sana, hapa kwasasa kinachotakiwa ni mazoezi kwasana halafu kuna dawa Fulani hivi ni nzuri kwakweli nitakuletea ili uwe unatumia naimani utapona kabisa na kuwa kama zamani”“Nashukuru sana”“Nitaongea na mke wako, halafu nitakuwa nakuja kila asubuhi kukufanyisha zoezi Fulani hivi, ni zuri kwaajili ya kurudisha miguu katika hali yake, yani alivyoniambia mke wako nilijikuta nikisikitika sana”“Ndio hivi, hujafa hujaumbika kwahiyo tupo tu katika maisha haya”“Nitakuwa najitahidi, siku ninazopata muda nitakuwa nakuja kukupa hilo zoezi, yani kila nikipata muda nitakuwa nakuja”“Aaah sikutegemea kwakweli, una roho nzuri sana Maimuna”“Unanielewa vizuri sana, hata kama nikiwa na roho mbaya bado sitohitaji baya likufike. Nakumbuka siku ile uliyoletwa umepewa sumu niligoma kukuhudumia ila nilikuwa naumia sana moyoni, yale matendo yako yalinijia kwa kasi sana kichwani, ila bado asingetokea wa kukuhudumia basi ningekuhudumia tu. Sina roho mbaya kiasi hiko cha kumtoa mtu uhai”Waliongea pale, kisha dokta Maimuna kwenda kuongea na mama Angel pia kuhusu hiyo huduma kwani alikuwa akimuhabarisha ila mama Angel hakukataa kwani kwa wakati huo alichokuwa akikihitaji ni uzima wa mume wake tu na si vinginevyo na ndiomana alishirikiana na yeyote aliyesema kuwa atamsaidia kwa mumewe.Usiku wa leo madam Oliva anazungumza na teve kuhusu kwenda kumuona baba Angel maana hata wao lile tukio lilikuwa kubwa sana,“Yani kwakweli ni jambo kubwa sana kwa mtu mzima kama Erick kukalishwa chini sababu ya wajinga wasiopenda maendeleo yake, inauma sana. Kesho naomba twende wote familia nzima kumuona”“Unamaana twende na Paul?”“ndio, twende na Paul kumuona baba Angel yani najua kuwa atafurahi sana kutuona”Basi waliongea mambo mengi mno kwa usiku ule, ila muda kidogo madam Oliva alipigiwa simu na namba ngeni ambayo hakuijua mwanzoni na kuipokea huku akijiuliza kuwa ni nani, alipopokea tu alimuuliza,“Nani wewe?”“Mbona umepokea simu kwa uoga kiasi hiko?”“Hapana, ila nauliza wewe ni nani?”“Unaongea na dokta Jimmy hapa”“Kheee dokta Jimmy? Eeeh niambie ukweli”“Kwanza nilitaka kukuuliza, huwa unaenda pale hospitali kwangu kuniulizia ili iweje?”“Nilikuwa nataka kujua ukweli, hivi mliyenipa ni mtoto wangu au kitu gani?”“Unajua wewe mwanamke usilete kichaa chako eeeh!! Sikia, wewe mwenyewe ulitaka hadi kushtaki watu pale kwa madai kuwa mtoto wako amepotea, tuliacha shughuli zote kwa muda na kukutafutia mtoto wako, ambaye ni uzembe wako mwenyewe ndiomana alipotea. Tukampata na kukukabidhi, unaacha kushukuru kwa kazi tuliyoifanya eti upo kuulizia kama ni mwanao tulikupa au la! Ni kitu gani kinakufanya useme kuwa huyo si mwanao? Umempi DNA au ni kitu gani?”“Hapana, nilikuwa nauliza tu”“Halafu acha kuniwekea sifa mbaya, nitakuchafua. Kuna mwenzio mmoja naye anajifanya kujua sana, kaniwekea sifa mbaya eti nimebadilisha watoto wake hospitali. Mungu si Athumani, kapata ajali huko yupo kuuguza majeraha. Hebu fanya mambo yako, vitu vingine mtapata laana bure”Ile simu ilikatika, basi madam Oliva alibaki kushangaa tu ile simu sababu hakuitegemea wala nini kwa muda ule yani hakufikiria kama angepata ujumbe kama ule, hakuweza hata kumsimulia vizuri Steve zaidi ya kuamua kulala tu kwa muda huo.Leo, Sia alikuwa akiwaza mambo mengi sana haswaa mambo ya kuhusu mama Sarah, alikuwa ashaenda nyumbani kwa mama Sarah mara kadhaa ila alikuta nyumba imefungwa, basi leo aliamua kwenda tena, alihisi kama anahitaji kuongea na mama Sarah,“Mimi ni muoga ndio, ila nikiamua basi huyu mwanamke nitaongea nae tu. Haiwezekani, nakumbuka vizuri kuwa ni yeye ndiye aliyetoa amri ya kupigwa kwa Erick, halafu ni Moses ndiye aliyemshuti Erick, nadhani bado nahitaji kuufahamu ukweli.”Basi alijiandaa na kuondoka nyumbani kwake, moja kwa moja alienda nyumbani kwa mama Sarah, sababu aliona siku ile ni Jumapili basi alihisi kuwa anaweza kumpata nyumbani kwake.Ila alipofika pale alikuta mlango umefungwa na kila kitu kikiwa kimya kabisa, ilionyesha ni kwa muda mrefu sana hakuna mtu aliyeonekana kuishi katika nyumba ile.Alizunguka ile nyumba huku akiangalia huku na huku, wakati anataka kuondoka ndio alipokutana na dada wa mama Sarah yani alikutana na Linah na kuanza kusalimiana nae pale kisha kuongea nae,“Wewe unajua alipo mama Sarah?”“Nijue wapi? Yani sijui imekuwaje hadi kaondoka bila hata kututaarifu ndugu zake”“Kheee hadi ndugu zake hajawaambia kumbe!!”“Hajatuambia ndio, hatujui lolote lile”“Duh!! Basi hatari”Sia hakutaka kuongea zaidi kwani alimuaga Linah na kuondoka muda huo ila badae alikumbuka kuwa anatakiwa kwenda kumuangalia baba Nagel kwanza, basi aliamua kuongoza kwa baba Angel tu.Sia alipofika kwa baba Angel, alipoingia tu getini alimuona Paul akiwa amekaa kwenye kibaraza na Erica, kwakweli alijikuta akimuangalia sana mtoto huyu hata alipowasogelea alikuwa akimuangalia sana na kuwasalimia pale, kisha alimuuliza Erica,“Samahani, huyu ni ndugu yenu?”“Hapana, huyu ni mtoto wa madam Oliva anaitwa Paul”“Aaaah”Basi Sia alimuangalia Paul kwa muda mrefu kidogo hata Paul alimshangaa ila muda kidogo Sia aliingia ndani ili kusalimia waliopo mule ndani na kweli aliwakuta wote wamekaa tu na kuwasalimia pale, ila muda kidogo madam Oliva nae aliaga kuondoka na familia yake kwahiyo walimuita Paul ili awaage pia kwani madam Oliva hakupenda kukaa karibu sana na Sia.Basi Paul alifika ndani na kushikana nao mkono wa kwaheri, wakati Sia ameshikana mkono na Paul alijihisi kitu kingine kabisa, yani alijikuta kama akitokwa na machozi kwenye macho yake kiasi kwamba aliamua tu kumkumbatia Paul kwa muda huo, mama Angel na baba Angel walielewa ila wengine walibaki kushangaa kwa muda.Baada ya tukio hilo, madam Oliva na familia yake wakaondoka, ila Sia alimuita mama Angel pembeni na kuanza kuongea nae,“Unajua nini ndugu yangu sijui nini kimenitokea, wakati namshika yuele mtoto mikononi nilihisi damu mwilini ikinikimbia, nilihisi machozi yakinitoka na hadi nikajikuta nikimkumbatia, msinihisi vibaya”“Kwanza niambie umehisi nini?”“Sijui, ila nimehisi kama nimemuona mtoto wangu wa halali”Mama Angel alimuangalia kwa muda na kutamani hata kumweleza kilichopo ila alisita kwa muda na kumuuliza,“Je unahisi kuwa Elly ni mtoto wa madam Oliva halafu mtoto wa madam Oliva ndio wako?”“Mmmmh sijui kwakweli, ila inawezekana Elly akawa mtoto wa madam Oliva maana mbona Elly mpole kama yule madam”“Aliyekwambia yule madam ni mpole nani?”“Ila Elly angekuwa wa madam Oliva, basi angehisi kitu kwa siku zote hizi ambazo yupo shule anasoma kwa huyu madam. Sijui lakini, ila natamani kumuona mwanangu mimi”“Pole sana”Kisha Sia aliamua kumueleza mama Angel kuhusu swala la mama Sarah kutokuonekana kabisa, na vile vile kwa maelezo yale aliweza kumkumbusha tukio la baba Angel kupigwa risasi,“Dah!! Huwa sisahau hilo tukio kabisa, ila naamini mume wangu atapona tu”“Ni kweli atapona, nitaendelea kufatilia mambo mbalimbali na tutajua tu mbivu na mbichi hakuna tatizo juu ya hilo”Sia aliongea kidogo na kuamua kuaga tu ili kurudi zake nyumbani kwake.Basi kesho yake, alifika dokta Maimuna mapema kabisa na kumpatia baba Angel dawa alizoahidi kumletea kisha kuanza kumfanyisha baadhi ya mazoezi,“Usijali Erick, utakaa sawa tu”Kwakweli baba Angel alishukuru sana, na hii ikawa ndio mtindo wa huyu dokta mara kwa mara kwenda kumpa baba Angel mazoezi kwaajili ya kumuweka sawa.Siku hiyo baba Angel aliamua kumuuliza dokta Maimuna,“Ila Maimuna, unajua nini kwanini umeamua kujitoa hivi kwaajili yangu?”“Kuna siku utagundua kwanini nimefanya hivi baada ya yote yale”“Mmmh Maimuna, niambie ukweli”“Ukweli utauopata pindi ukitembea kabisa, yani ukishapona ndio itakuwa furaha yangu na hapo nitaweza kukwambia ukweli kuwa kwanini nafanya hivi”Kisha dokta Maimuna akamuita mama Angel na kuanza kumuelekeza baadhi ya vitu vya kufanya, huku akimwambia,“Mimi natarajia kusafiri kesho, ila huyu asibaki bila mazoezi yani haya mazoezi yafanyike kwake mara kwa mara ili aweze kufunguka na kuwa mzima kabisa yani. Nitakuelekeza baadhi ili usiache kumfanyia, halafu nikirudi tutaangalia hali yake, natumai atakuwa akiendelea vizuri”“Nashukuru sana kwakweli, kwahiyo wewe unaenda wapi?”“Kuna mahali huko naenda, yani kuna tukio Fulani lilitokea. Kuna mtu alikufa na nilikuwepo kule, na tuliweza kumfanyia uchunguzi yule marehemu ambaye ilionyesha wazi kuwa ameuwawa, niliwaambia kuwa nipo tayari kutoa ushahidi basi ndio ninaenda huko kesho. Ila sio hiko tu kinachonipeleka bali kuna kazi pia ambayo naenda kuifanya huko”“Oooh sawa, kwakweli Mungu akutangulie. Una moyo wa kipekee sana, Mungu akuzidishie dokta Maimuna”Aliongea kiasi pale na kuagana nao.Usiku wa leo, baba Angel na mama Angel walianza kuongea baadhi ya mambo ambayo yametokea,“Unajua yule dokta alivyosema anaenda kuchunguza kuhusu kifo sijui kutoa ushahidi ndio nimekumbuka kitu”“Kitu gani?”“Kabla ya ile habari kuwa wewe umepiga risasi, nilifatwa na mtu ofisini kwangu ambaye alikuwa ni mke wa Moses. Nilienda kuongea nae kwenye mgahawa wa karibu na ofisini pale, na aliniambia mambo mengi sana”“Mambo gani hayo mke wangu?”“Najua hata wewe yatakushangaza haya mambo”“Niambie tu”Mama Angel alianza kumueleza kuhusu ujumbe aliopewa na mke wa Moses kuhusu biashara yake ile, yani baba Angel alishangaa sana kwakweli, pia alimwambia kuhusu kifo cha mzee Jimmy,“Hapo kwenye kifo ndio alinichanganya kwakweli, sijui kivipi Erica alisababisha kifo cha babu yake”“Hebu kamuite atuambie maana hata mimi nimehisi kuchanganywa na hizo habari sasa”Ikabidi mama Angel ainuke na kwenda kumuita Erica, ambapo moja kwa moja alienda nae chumbani kule na kumtaka akae kwenye kiti na kuanza kumuuliza, basi baba Angel alianza kumwambia,“Mwanangu usiogope tumekuita wala usianze kufikiria mambo mengine, tumekuita kwa uzuri tu. Unamkumbuka babu yako yani baba yangu mimi?”“Ndio namkumbuka, si wewe baba umepigwa risasi ulipoenda kutembelea kaburi la baba!!”“Oooh kweli una kumbukumbu nzuri, je unakumbuka siku ya mwisho babu yako kuja hapa kabla ya kushikwa na umauti wake?”“Nakumbuka ndio”Wazazi wake wakapumua kidogo na kumuuliza kwa pamoja,“Ulimfanya nini”“Nilimfanya nini kivipi? Mbona sikumfanya kitu”Baba Angel ikabidi abadilishe swali,“Yani ni kitu gani unakumbuka kutokea kati yako wewe na babu yako ile siku ya mwisho kufika mahali hapa”“Mmmmh hakuna kilichotokea baba”“Au ni nini uliongea nae, yani kuna kitu nahitaji kufahamu mwanangu ndiomana nimekuuliza”“Ninachokumbuka ni hivi, babu alifika siku ile na alikuja moja kwa moja sebleni na kutusalimia na tuliongea nae kiasi tu, kisha aliondoka na kwenda kukaa kwenye bustani. Nakumbuka siku hiyo kuna sinema Fulani ilikuwa ikionyeshwa kwenye tv, kulikuwa na mtoto anacheza na babu yake nikajikuta nimeipenda sana ila sisi babu yetu hakuwa vile, basi moja kwa moja nilienda kwenye bustani na kumvizia babu ila nilimkuta akiongea na simu, sijui alikuwa akiongea nayo nini ila nilichogundua ni kuwa babu hatupendi, basi nilienda mbele yake babu na kumwambia babu sikupendi, aliniuliza kwanini? Nilimwambia sikupendi, sikuweza kuizuia chuki yangu mbele ya macho yake, nakumbuka nilirudia hilo neno kama mara tano hivi halafu niliondoka kwa kukimbia, nisameheni wazazi wangu ila mimi nilimwambia ukweli wa moyo wangu, sikuwahi kumpenda babu toka siku namtambua kuwa ni babu yetu”Baba Angel na mama Angel walitazamana kwa muda kidogo bila ya kusema neno ila badae walimruhusu Erica aende kulala tu kwa muda huo, basi Erica akaondoka na wenyewe wakaongea kidogo.“Hivi umemuelewa mtoto?”“Unajua mimi huwa simuelewi huyu Erica kabisa, kwanza kana mambo ya ajabu sana. Mtoto kama huyu alianza kumchukia babu yake toka siku ya kwanza kwasababu gani?”“Mke wangu, kumbuka huyu Erica huwa anaota inawezekana amewahi kuota matukio ya baba yangu ndiomana alijikuta kutokumpenda toka siku ya kwanza, tusimlaumu sana. Ila najiuliza kama hilo neno la sikupendi ndio lililomfanya baba afe? Mmmh!”Walijadiliana pale ila hakuna jibu walilolipata.Kesho yake mapema kabisa, mama Junior alienda tena pale kwa mdogo wake kumuangalia baba Angel pamoja na kumuangalia Vaileth aliyejifungua maana hata siku ile hakuweza kumsubiri.Basi alifika na kumkuta mama Angel pale,“Pole mdogo wangu, pole kwa mambo mengi ya hapa kwako. Vipi huyo mzazi hajaenda kwao tu!”“Hapana, nipo nae, nimeona bora mtoto achangamke kwanza”“Basi ngoja nikamuone kidogo”Basi wakaongozana hadi chumbani kwa Vaileth ambapo alikuwa akimyonyesha mtoto, na aliwasalimia alipowaona, basi alipomaliza kumnyonyesha mtoto alimpa mama Junior ili amshike kidogo ila mama Junior alipomtazama yule mtoto alishtuka sana na kusema,“Kheee mbona huyu mtoto kafanana sana na Junior!!”Mama Angel nae akamuangalia vizuri na kuona kuwa ni kweli yule mtoto kafanana sana na Junior. Basi wakaongozana hadi chumbani kwa Vaileth ambapo alikuwa akimyonyesha mtoto, na aliwasalimia alipowaona, basi alipomaliza kumnyonyesha mtoto alimpa mama Junior ili amshike kidogo ila mama Junior alipomtazama yule mtoto alishtuka sana na kusema,“Kheee mbona huyu mtoto kafanana sana na Junior!!”Mama Angel nae akamuangalia vizuri na kuona kuwa ni kweli yule mtoto kafanana sana na Junior.Mama Angel alikaa kabisa na kumuangalia Vaileth kisha akamwambia,“Eeeh Vaileth hebu sema ukweli mtoto ni wa nani?”Mama Junior akasema,“Aseme mtoto wa nani wakati ni chata ya Junior hii!! Atuthibitishie tu ukweli kuwa mtoto ni wa Junior”Kwakweli Vaileth aliona aibu sana, ila kwavile walimuuliza sana ilibidi tu akubali,“Ni kweli mtoto ni wa Junior”Alikuwa akiongea huku ameinamia chini, mama Angel akasikitika kiasi na kusema,“Yani Vaileth, binti mwerevu kweli unadanganywa na Junior? Halafu ulikuwa hutaki kusema ukweli kwanini? Je ningekufukuza wakati baba wa mtoto ni mwanetu? Kwanini ulikuwa hutaki kusema ukweli?”“Nilikuwa naona aibu”Mama Junior akasema,“Ndio lazima uone aibu maana Junior ni mdogo kwako, wewe ndio wa kumfundisha Junior”Mama Angel akasema,“Ni kweli Junior ni mdogo kiumri kwa Vai ila Junior ni mkubwa sana kuliko hata huyu Vai, maana Junior anahangaika na wamama watu wazima wenye umri mkubwa kushinda hata wewe mama yake, sembuse haka kavaileth!! Tena usikute Junior alimbaka huyu. Eti Vai, ulibakwa na Junior au ulikubaliana nae?”Vaileth alikuwa akihisi aibu sana yani alihisi aibu kupitiliza,“Hajanibaka”“Kwahiyo ulikubaliana nae? Vitu vingine vinachekesha na kusikitisha, kwahiyo Junior akakupa maneno matamu kuwa nitakuoa hata usijali na kukufanya wewe umuamini kabisa, bila kujali kuwa Junior ni kavulana kadogo kanakochipukia”Mama Junior akaongezea,“Yani Junior akakuoe wewe!! Khaaa jamani haya mashikolo mageni, yani wewe ukaolewe na Junior!! Siku ile mmekuja nyumbani kwangu kumbe ndio mmekuja kutambulishana loh!!”“Tena Daima alituambia humu ndani kuwa Junior na Vai kuna kitu kinaendelea tukamkatalia binti wa watu na kumuona chizi, kumbe ni kweli. Nashangaa sana kwakweli”Vaileth alikuwa ameinama chini tu kwa muda huo huku machozi yakimtiririka, basi mama Angel alijiwa na imani kiasi na kumwambia,“Vai, nyamaza yani hata usilie kitu. Naelewa uliyopitia au unayoyapitia, ila umekosea sana maana tayari umezaa mtoto wa kwanza nyumbani, ulitakiwa kuwa makini sana hata kabla ya kuamua kuzaa tena. Kwakweli mnatufanya wazazi tupate aibu kwasana. Ila hilo swala la Junior niachie, kama alipanga kukuoa wala hiyo ndoto yako usiitoe kichwani mwako”Basi mama Angel alimtoa dada yake pale na kwenda nae kuongea nae.Mama Junior alimuuliza mama Angel kwa makini sana kwani hakumuelewa kwa ile kauli yake,“Unajua kuwa sijakuelewa, ulikuwa unamaanisha nini? Kwahiyo Junior atamuoa Vaileth?”“Dada, naomba uniachie hili swala mimi. Natambua maumivu aliyonayo yule binti, kafanya makosa ndio ila mara nyingine mapenzi yanatufanya tusione vya mbele, thamani ya yule binti imeshuka. Ni kweli ana mtoto ila ni binti aliyetulia sana, nina uhakika bila Junior basi huyu Vaileth yasingempata haya yaliyompata. Mwache tu Junior aserebuke huko, ajiachie na kujidai ila akirudi kuna mke wake huku hata asitake kunitania”“Mmmh Erica jamani, unajua yule Vai ni mkubwa kwa Junior”“Huyo Junior angeona Vai mkubwa basi asingemtongoza, kaona ni rika lake na atamuoa tu”Mama Junior alimuangalia sana mdogo wake, ingawa hata na yeye alichoshwa na tabia za mwanae ila bado ilikuwa ngumu sana kwa yeye kukubali kuwa mwanae Junior amuoe Vaileth.Waliongea kiasi pale ila mama Junior inaonyesha hakufurahi wala nini kwa lile swala, basi alimsaidia baadhi ya kazi pale mdogo wake halafu mama Junior akaondoka zake ila njiani akakutana na Linah ambaye alimuita mama Junior,“Niambie mama mkwe”“Mama mkwe!!”“Unajifanya hujui kama wewe ni mkwe wangu kwa Junior au!! Junior ni mwanao halafu mimi ni mume wangu”“Ila jamani, hivi huna watoto kweli wewe! Kwanini kumfanyia hivyo mwanangu?”“Hata watoto wangu wote wamekubali kuwa Junior ni baba yao sasa sijui wewe ni nani wa kupinga na kukataa hilo. Unatakiwa kukubali tu kuwa mimi ndio mkwe wako”Mama Junior alimuangalia sana Linah na kushindwa hata kumjibu kwa muda ule, kisha aliamua tu kuondoka zake huku akiona bora hata ya Vaileth kuliko huyo mkwe wake mama mtru mzima Linah.Erica leo akiwa anatoka shule, alishukia njiani na kuanza kutembea kuelekea nyumbani kwao ila mbele yake kuna mtu alimuona, huyu mtu alikuwa ni kijana ambaye aliwahi kumuona kabla, alijaribu kutafuta kumbukumbu na kugundua kuwa yule kijana alimuona kwenye daladala kidha Daima na Samia walishuka kumfatilia na ambapo hakuwajibu kitu, basi Erica alijisemea,“Si ndio huyu kaka kiziwi”Akapita karibu sana, akagongana macho na yule kijana, basi Erica akasimama kumsalimia ili atambue kama kweli yule kijana ni kiziwi,“Mambo vipi?”“Poa, unanifahamu?”“Hapana sikufahamu ila nimeona umeniangalia ndio nilitaka nikuulize na mimi unanifahamu?”“Hapana, mimi naitwa Emmanuel. Je wewe unaitwa nani?”“Mimi naitwa Erica”“Ooooh jina zuri sana, unaishi wapi Erica”Erica alimuonyesha kwa kidole tu, kisha huyu Emmanuel akampa Erica mawasiliano yake ili wapate kuwasiliana,“Nadhani ninahitaji muda zaidi wa kuongea na wewe”“Sawa hakuna tatizo”Basi Erica aliagana nae na kuondoka zake, ila alianza kuhisi huenda huyu kijana anahitaji kumtongoza, ila kitu ambacho hakuelewa ni kwanini huyu kija a hakuitikia salamu za Daima na Samia hadi walihisi ni kiziwi ila leo kaongea vizuri kabisa na Erica,“Mmmh au sio mwenyewe? Hapana ndio mwenyewe yule yule, namkumbuka vizuri sana”Erica kwa muda huo aliongoza tu moja kwa moja na kurudi nyumbani kwao ambapo alianza kufanya shughuli za pale kwao maana kwa siku hizi alikuwa akirudi tu basi anaanza shughuli za nyumbani.Usiku wa leo, Erica alienda kuongea na Erick maana siku hizi huwa hawaongei mara nyingi ila leo alijikuta akitamani sana kumueleza Erick kuhusu kijana aliyekutana nae,“Jamani Erick kuna kijana tulijua mwanzoni ni kiziwi na bubu ila leo kaniongelesha”“Ni kijana gani na kwanini mlimuhisi ni kiziwi na bubu?”Erica alianza kumueleza ilivyokuwa hadi wakamuhisi hivyo yule kijana kuwa ni kiziwi na bubu,“Aaaah kumbe alifatwa na hao vichaa, sasa huyo Samia na huyo Daima lazima mtu mwenye akili zake timamu asiwasikilize kabisa, ila huyo kijana ana shida gani na wewe?”“Sijui ila kasema atahitaji kuongea nami zaidi”“Nipatie namba zake”Erica alimpa Erick lile karatasi la namba ambapo Erick alilichanachana lile karatasi na kumwambia Erica,“Hakuna kuwasiliana nae, kumbuka hata mama kasema nikulinde kwa kadiri niwezavyo, nami nasema kuwa hakuna kuwasiliana nae”“Ila kwanini Erick unakuwa hivyo jamani!! Unajua kuna wakati huwa sikuelewi, hebu niambie kitu gani unachoptaka kwangu”“khaaaa usiniulize swali kama hilo mimi usije kunitendesha dhambi bure, ni usiku sasa unaweza kwenda kulala au umekumbuka karata leo!”Erica hakujibu kitu kwani alichukia na moja kwa moja kuondoka zake na kwenda kulala.Palipokucha, leo ilikuwa ni siku ya mapumziko kwahiyo hawakwenda shule, Erick aliona ni vyema kama akienda kumuamsha Erica maana jana yake aliondoka akiwa amechukia.Basi moja kwa moja Erick alienda hadi chumbani kwa Erica, ila alimkuta amelala vibaya, yani kalala huku nguo imemfunuka, yani Erick alijikuta akimtazama kwa muda kisha alienda na kumfunika na shuka na hapo Erica alishtuka toka usingizini,“Kheee Erick umekuja muda gani humu chumbani kwangu?”“Muda sio mrefu, nilikuja kukuamsha”“Umejiona kwanza hapo mbele?”Erick aliinama kujiangalia, yani aliona aibu na kuondoka mule chumbani kwa Erica ila Erica alibaki akicheka tu kwa muda ule sababu yeye alihisi kama ni kichekesho kile.Moja kwa moja Erica aliinuka na kwenda kuoga kisha alienda kumsalimia baba yake, maana kwa siku hizo ndio ilikuwa tabia yake kwa kila asubuhi kwenda kumsalimia baba yae.Ila leo alivyoenda kumsalimia baba yake akamuuliza,“Hivi Erica hakuna kingine ulichofanya kwa babu yako zaidi ya kumwambia kuwa humpendi?”“Mmmh sikumbuki baba”“Na ulivyomwambia kuwa humpendi ilikuwaje?”“Nilimuona ameinama kwa muda kidogo na kuniangalia, halafu aliniuliza unasemaje Erica, nilimjibu sikupendi Babu basi sikuongea nae tena kwani niliondoka muda ule ule. Nisamehe baba ila kiukweli sikumoenda babu”“Ila hujanipa sababu, kwanini humpendi?”“Sababu yeye hakutupenda”“Kivipi? Ulijuaje kama yeye hakutupenda?”“Kwanza toka siku ya kwanza mnanitambulisha kwa babu sikumpenda, kuna siku niliota kuwa anataka kukuua. Nakumbuka ndio kesho yake akaja, kwahiyo ile filamu nilivyoiona, niliipenda kuona yule mtoto anacheza na babu yake, ila kwanini babu yetu alitaka kukuua? Ndio hapo nilimfata na kumsikia akiongea na simu ambayo sikumbuki ila ninachokumbuka ni kumfata na kumwambia kuwa simpendi”“Mmmmh, wewe unaaminije kuwa alitaka kuniua? Unajua yule ni baba yangu kama nyie mlivyo kwangu, kanilea, kanisomesha na vyote kanifanyia, ni baba yangu ambaye ananipenda sana, utasemaje hakuwa akinipenda na alitaka kuniua?”“Sijui baba, mimi niliota tu kuwa anataka kukuua”“Je mimi naweza kuwaua ninyi? Huoni kama hiyo ilikuwa ni ndoto tu!”“Ni ndoto tu ila matukio niliyoota yalikuwa ni yale yale”“Kivipi?”“Niliota kuwa babu amekuja vizuri kabisa hapa nyumbani, kisha akatusalimia na kwenda kwenye bustani ambapo aliongea na simu halafu sisi tulikuwa tukiangalia sinema halafu wewe ulikuwa kazini, ila ulivyorudi tu babu akakuita kwenye bustani na kukupulizia dawa usoni ambapo ukaanguka na kwenda kulazwa hospitali na ukafa. Ila kitendo cha mimi kwenda kuongea na babu kule kwenye bustani ni kama kilimfanya ajue kuwa ni kitu gani kinaendelea, unaweza usinielewe baba ila ndio ilivyokuwa. Sikuwa na nia mbaya kumwambia babu kuwa simpendi”“Hivi ulimjua lakini kama neno lako sikupendi lingemaliza maisha ya babu yako?”“Hapana sikujua, kwani babu amekufa kwasababu hiyo?”“Sasa ni sababu gani iliyomuua babu yako?”“Ni dawa aliyotaka kukupulizia wewe, alijipulizia mwenyewe na kufa”“Mmmmh Erica jamani, babu yako aliondoka hapa akiwa mzima kabisa, utasemaje alijiwekea dawa?”“Huwezi kunielewa, babu hajajiwekea dawa hapa, ila aliweka dawa baada ya kufika nyumbani kwake”Kwakweli baba Angel bado hakumuelewa kabisa huyu mtoto wake na wala hakufikiri kama anaweza kumuelewa kwani aliona anachoongea kama hakihusiani vile na kifo cha baba yake, bado alikuwa na maswali mengi sana baba Angel kuhusu kifo cha mzee Jimmy toka mkewe kamuambia kuwa kifo cha mzee Jimmy kilisababishwa na Erica mdogo, basi akajisemea,“Hapa watakaokuwa wanajua ni wafuasi wa mzee Jimmy tu maana huyu Erica nae hata sidhani kama anajielewa kwa kitu anachokisema”Basi baba Angel alikaa tu pale kwenye kiti chake huku akitafakari mambo mbalimbali, kwanza kuhusu ndoto aliyoisema Erica kuwa baba yake alitaka kumuua aliikataa kabisa kwani aliona ni jambo lisilowezekana wala nini.Mama Angel kama ambavyo alielekezwa na dokta Maimuna, basi muda huu alienda kufanyisha zoezi mume wake kama kawaida, na alipomaliza alikaa chini na kuongea nae,“Sijawahi kufikiria katika maisha yetu hata mara moja kuwa kuna siku itakuwa hivi!!”“Je ushawahi kufikiria kuwa kuna siku utabaki mjane”“Jamani Erick naomba usiseme maneno hayo, naomba usiseme kabisa. Unanimaliza nguvu, naomba nitangulie mimi kufa kabla yako”“Jamani mke wangu hapo unakosea, unajua sisi wanaume hatuwezi majukumu mazito ya familia ndiomana huwa tunakufa mapema, usiniombee kuniacha mke wangu maana nitakuwa kwenye wakati mgumu sana”“Mungu atusaidie ili tuzeeke pamoja”“Sasa hayo ndio maneno mke wangu, ili tulee pamoja familia yetu hii maana bado wanatuhitaji. Naamini nitainuka na nitatembea kabisa kama zamani”Basi mama Angel alikuwa akitabasamu pale huku akiongea na mume wake, mara kuna simu iliingia kwenye simu ya mama Angel, alipoiangalia aliona namba ngeni ila aliipokea na kuanza kuongea nayo,“Pole sana Erica”“Kwani nani wewe?”“Mimi ni Manka, pole sana”“Kheeee Manka? Yani unajua wewe umefanya jambo la ajabu sana, kweli kumpiga risasi Erick kwa kosa gani?”“Hapana, si mii niliyempiga na wala sijasema kuwa apigwe. Huwezi ukaniamini ila si mimi”“Kama uliweza kumuwekea sumu Erick unashindwa vipi kusema apigwe risasi?”“Hata sumu si mimi niliyemuwekea, aliyempiga risasi ndio anajua kila kitu”“Moses!!”“Ndio Moses, mimi siwezi kufanya hivyo unajua. Ni kweli nina roho mbaya ila siwezi kufanya hivyo”“Na umewezaje kushirikiana na watu wanaomfanyia hivyo Erick kama wewe huna nia mbaya kwake?”“Hayo sio niliyokupigia simu, ila nilichopiga simu ni kuuliza hali ya Erick anaendeleaje kwasasa?”Mama Angel alipatwa hata na hasira kwakweli, alijikuta akijibu kwa hasira tu,“Alikufa”Kisha akakata ile simu, na kuanza kumueleza mumewe kuhusu aliyepiga, kwakweli hata baba Angel alimsifu mkewe kwa kumjibu kuwa alikufa,“Hilo ndio lilikuwa lengo lao kuniua, sasa ananiulizia naendeleaje wakati waliniua!! Huyo mwanamke ni mjinga sana sijapata kuona dah!!”Basi mama Angel aliamua kwa muda huo kumrudisha mumewe ndani baada ya yale mazoezi ya asubuhi ambayo alimfanyia.Kwenye mida ya mchana, mama Junior alifika tena pale kwa mama Angel ila leo alibeba na zawadi za mtoto yani hata mama Angel alifurahi kuona vile kwani ilionyesha kuwa kwa muda huo dada yake alikuwa amekubaliana na hali halisi kuwa yule mtoto wa Vaileth ni mjukuu wao,“Naona umejiongeza sasa dada!”“Nisijiongeze mchezo!! Mwenzio si nilikutana na yule mtu mzima jamani, akaanza kuniita mama mkwe tena anasema intake nisitake yeye ni mkwe wangu tu”“Kheee yule Linah!!”“Ndio huyo huyo, yani nilichukia kweli kwa ile kauli yake”“Khaaa halafu ana wazimu yule mmama jamani. Ila lazima tufanye jambo tu kuwa Junior amuoe Vaileth”“Hata mimi nipo tayari kwa hilo kuliko yule mtu mzima kunizidi mimi kuniita mama mkwe dah nilijihisi vibaya sana”Mama Angel alicheka kidogo,“Yani nacheka kama mazuri, ila huyu Junior huyu dah!! Kwakweli katushinda tabia huyu mtoto”Basi mama Junior, moja kwa moja alienda chumbani kwa Vaileth na kumshika mtoto kisha kumpa Vaileth zile zawadi ambazo alimbebea mtoto, kwakweli Vaileth alifurahi na kumshukuru sana kwa jambo lile.Kisha mama Junior alianza kuongea nae,“Eeeeh niambie kwanza, utaweza kuishi na mwanangu?”Vaileth alijibu kwa uoga uoga,“Nitaweza”Mama Angel nae aliingia muda ule mule ndani na kuwakuta wakiulizana hivyo, basi akasema,“Asiweze kuishi nae kwanini? Mtu kaweza kulala nae na kupata mimba, ndio atashindwa kuishi nae kweli!!”“Mmmh Erica siku hizi umekuwa mjanja mdogo wangu yani unaongea kijanja janja, halafu sikutegemea kama unaweza kukubali Junior kuishi na huyu mwanamke”“Dada, huyu Vaileth ni mwanamke mwenzetu, najua unaelewa ambavyo anajisikia kwa hili alilolipitia. Muache apate faraja kidogo, Vaileth usijali huyo Junior atakuoa tu, ilimradi amekuzalisha basi atakuoa tu”Kiukweli Vaileth alitabasamu na kufurahi sana kwenye moyo wake kwani hakutegemea kama wale wamama wawili wangekuwa upande wake.Kuna kitu Sia alikuwa akikiwaza sana, haswaaa kuhusu mtoto wa madam Oliva, yani alikuwa na hisia zote kuwa huenda yule mtoto akawa mtoto wake maana hakuona kama kule kufanana na yule mtoto ni kwa kawaida.Basi leo, aliamua kwenda kwa madam Oliva sababu alikuwa akipafahamu hakupata shida kwenda pale ila alijisihi kwanza moyo wake kuwa anatakiwa kuwa mstaarabu na sio kukurupuka kama alivyofanya kwa Erick wakati anang’ang’ania kuwa ni mwanae.Moja kwa moja alienda nyumbani kwa madam Oliva, ila muda huu hakumkuta madam Oliva na hata Steve alikuwa amelala kwa muda huu kwahiyo ni yule yule mtoto Paul ndiye aliyemkaribisha na kuongea nae kiasi,“Kwani kaenda wapi mama yako?”“Kwenye biashara zake, mama yangu ni mwanamke shupavu. Anapenda kujishughulisha na mambo mengi, hapendi mimi nipate shida”“Na baba yako je?”“Mmmh huwa simuelewi, ila nampenda. Sema simuelewi kabisa, muda wote anashinda nyumbani na kufanya kazi za nyumbani na kulala, sijui kama wanaume wote wapo kama baba”Sia akagundua kuwa anachofanya Steve hakikuwa sahihi mbele ya macho ya mtoto kwani alikuwa akijifunza kile kitu ambacho hakikuwa na maana, basi Sia alimwambia,“Kwani baba yako hajawahi kufanya kazi?”“Mimi sijui maana baba mwenyewe nimemjua ukubwani hivi. Ila mimi nakumbuka wakati naishi kwa bibi, ni bibi ndio utamkuta muda wote nyumbani na akiondoka sana basi yupo kwenye bustani yake ila babu alikuwa akipenda kujishughulisha, na ukimkuta nyumbani basi atakuwa akisoma vitabu. Nakumbuka hata kwa mama mkubwa nilipoishi ndio ilikuwa balaa huwezi kumkuta baba mkubwa akishinda nyumbani muda wote. Ila toka nimekuja hapa, ni mama ndio anahangaika ila baba muda mwingi tunafanya nae shughuli za nyumbani hapa halafu na kwenda kulala”“Sawa, unaweza kuniitia baba yako kidogo niongee nae na nimuage maana nitakuja siku nyingine”Ni kweli Paul aliinuka na kwenda kumuita Steve, yani Steve alivyotoka na kumkuta Sia kiukweli alichukia kiasi ila aliamua kutoka nae nje kabisa ili aondoke,“Umefata nini nyumbani kwangu Sia?”“Sijaja kwa lengo baya wala sijaja kwa ugomvi, nimekuja kwa mema tu. Nashukuru umenitoa nje ili niweze kuongea hili”“Lipi hilo?”“Steve, najua unaishi vizuri na huyu madam, najua kama madam anajiweza maana ana biashara zake na kazi yake. Ila kuna muda mwanaume unatakiwa kuwa mwanaume, hebu simama kwenye nafasi yako Steve, hili ndio jambo hata ndugu zako waliweza kukutoa kwangu, ni mwanaume gani wewe unashindwa kusimama kwenye nafasi yako?”“Kivipi?”“Laiti ungemsikia yule mtoto alivyokuwa akisema, nadhani akili yako ingekukaa sawa”“Alikuwa anasemaje?”Sia alimwambia kwa kifupi tu na kumuongezea,“Sasa unatakiwa kujishughulisha, usitegemee kulishwa na kulelewa na mwanamke kwa kila kitu. Unatakiwa kusimama kama mwanaume. Acha ujinga Steve”“Nimekusikia, ila nini kilichokuleta!”“Nitakwambia tu kilichonileta nikija tena, mtunze sana Paul ni mtoto mwenye akili ambaye kagundua kuwa mwanaume hufai kukaa nyumbani na kulala lala kama mwanamke, wenzio huko hata kama hawana shughuli za kufanya wanashika vitabu au magazeti wanajisomea, sio kulala tu na hakuna ulichofanya. Hayo ni mambo ya kike, mwanaume analala sababu kachoka, katoka kufanya kazi ngumu huko amechoka na kuamua kujilaza mchana, sio unakuwa kama mwanamke unaamka asubuhi na kufanya kazi za nyumbani halafu kulala. Kusaidiana kupo hatukatai ila sio ndio unakuwa kama mwanamke jamani unatia aibu”Sia hakuongeza neno la zaidi kwani muda huo huo tu akaondoka zake.Leo Erick alienda kiwandani kwa babake kama kawaida kwani kwa siku hizi ni yeye ndiye aliyekuwa akienda huku kuangalia shughuli zinaendaje, basi akiwa pale kiwandani alienda pale Juma ambaye ni rafiki wa baba yake na kuanza kuongea na Erick,“Unajua kabla baba yako hajapata matatizo, ni mengi sana nilipanga nae. Moja wapo ni kuongozana na wewe katika biashara yangu Fulani hivi”“Biashara gani hiyo?”“Ni vyema kama kesho tukienda wote ili ukaone hiyo biashara nina uhakika utafanya vizuri sana kwenye biashara hiyo”“Mmmmh ila Kesho nitaenda kwenye Ibada”“Oooh ila inatakiwa twende asubuhi kabisa maana tukichelewa itakuwa tatizo, inatakiwa twende asubuhi. Jitahidi twende asubuhi, halafu baba yako usimwambie kwani nataka ujumbe aupate baada ya sisi kurudi”Erick alikubali tu ingawa alikuwa akiona kama hilo swala ni gumu kwake kwani kufanya kitu bila kumshirikisha baba yake aliona ni ngumu sana, basi aliongea nae vizuri na kwa muda huo walipanga na Juma kuwasiliana sababu Erick alikuwa na simu ndogo kwa siku hizo ili kuweza kuwasiliana na wateja tofauti wa baba yake.Kisha Juma alimuaga pale na kuondoka zake, Erick alipomaliza kazi zake za pale moja kwa moja alirudi nyumbani kwao tu.Kulipokucha, Erick alipigiwa simu mapema sana na Juma kuwa ajiandae na waweze kuondoka zao, basi aliamka na kujiandaa vizuri kabisa, ila aliwaza sana kwa kitendo cha yeye kuondoka na Juma bila ya kumwambia ukweli baba yake!! Akaona si jambo jema, basi kabla ya kuondoka ikabidi amfate baba yao na kumwambia,“Baba, jana kiwandani alikuja yule rafiki yako na kusema kuwa mlikuwa na mipango mingi sana kabla, alikuwa akiomba leo niende nae kwenye biashara yake”“Mmmh, mbona hajanipigia simu kuniambia sasa?”Erick aliamua kumpigia simu Juma na kumpa aongee na baba yake, kwakweli Juma alishindwa kuficha tena na kuonyesha tu ni wazi kuwa alihitaji kutoka na Erick.Basi baba Angel alimkubalia tu, ila kishingo upande.Moja kwa moja Erick alitoka na alikuwa akisubiriwa na Juma, nje ya nyumba yao ambapo aliondoka nae, na walipoelekea palikuwa mbali sana yani safari ilitumia kama masaa matatu hivi, mpaka Erick aliuliza,“Mbona mbali hivi?”“Huwa tunawekeza mbali, maana vitu vingine kuwekeza mjini havifai”Walifika mpaka sehemu ambayo kulikuwa na shamba kubwa sana ambalo lilikuwa limejaa miti mingi, basi Juma akamwambia Erick,“Siku nyingi nilitamani uje huku, niitamani sana Erick, kwakweli leo nimefurahi”“Kwahiyo hapa unajishughulisha na nini?”“Hapa nimepanda miti, ila nilipokuwa nataka ufike kwanza ni huku”Waliongozana hadi mwishoni mwa lile shamba ambapo palikuwa na nyumba halafu palikuwa na jiwe kubwa mbele yake. Moja kwa moja Juma alisogea eneo lile pamoja na Erick na kumwambia Erick,“Hii ni sehemu ambayo babu yangu aliwahi kuishi zamani sana, alipapenda sana hapa ndiomana niliamua kupaendeleza kwa kuweka shamba langu maeneo haya. Naomba tukae hapa”Basi Juma alikaa kwenye lile jiwe na kumtaka Erick nae akae ambapo Erick alikaa pale halafu Juma alianza kumwambia,“Hapa tulipokaa ni kaburi la babu yangu”Erick alishtuka sana maana hakuelewa ni kwanini Juma kaamua kumpeleka kwenye kaburi la babu yake na kumketisha juu yake. Basi Juma alikaa kwenye lile jiwe na kumtaka Erick nae akae ambapo Erick alikaa pale halafu Juma alianza kumwambia,“Hapa tulipokaa ni kaburi la babu yangu”Erick alishtuka sana maana hakuelewa ni kwanini Juma kaamua kumpeleka kwenye kaburi la babu yake na kumketisha juu yake.Erick alimuangalia sana huyu Juma na kumuuliza,“Una maana gani kunileta huku?”“Sababu wewe ni damu yangu”“Damu yako? Kivipi?”“Erick, ngoja leo nikwambie ukweli. Siku zote ambazo huwa nakuona, huwa nakuona kama mwanangu kabisa yani. Nahisi wewe ni mwanangu kwa namna yoyote ile”“Kwahiyo mimi sio mtoto wa baba?”“Sijasema hivyo, ila kuna vitu vinaendana kati yangu na yako, unaona huyu aliyepo kwenye kaburi hili, ndio alikuwa na tabia kama zako Erick, alikuwa na akili kama wewe, na alikuwa na mambo kama yako. Siku aliyopigwa alizimia kama wewe ulivyozimia shuleni, ndiomana nilipopata habari ya lile tukio nilishtuka sana na kuzidi kukuweka karibu”Erick aliinuka kwanza na kumuuliza Juma,“Ni nani aliyekupa taarifa kuhusu kuzimia kwangu?”“Nilipewa taarifa na mwalimu wako, kuna mwalimu pale shuleni nimemuweka kwaajili ya kukufatilia wewe tu, kiukweli Erick nahisi wazi kuwa wewe ni damu yangu”“Hapana, mimi siamini hilo kwani baba yangu namjua wazi kuwa ni nani”“Sijakataa kuhusu huyo unayemjua ila nina hisia hizo kuwa wewe ni mwanangu”“Naomba niondoke, naomba kurudi nyumbani”Juma aliinuka pia na kumwambia Erick,“Kabla ya kuondoka, naomba twende kwanza kidogo ukaangalie nyumba ya babu yangu”Kwakweli bado Erick alishindwa kumuelewa Juma, ingawa alianza kumfata tu alipokuwa akielekea ila walipofika mlangoni, Erick alirudi nyuma na kugeuka kisha alianza kukimbia ili kutoka katika eneo hilo, hata Juma alipomuita hakumuitikia kabisa kwani alihitaji kwenda nyumbani kwao.Juma alimfatilia kwa nyuma ila Erick hakusimama na kitu kilichoendelea kumchanganya Juma ni kuwa Erick alikuwa na mbio sana na kumfanya azidi kumuona kama babu yake ambaye alikuwa na mbio sana.Ilibidi tu Juma arudi kwenye gari na kupanda kisha kuanza kumfatilia Erick, alivyomfikia akamwambia,“Erick, basi nipo tayari turudi nyumbani tu, usiniogope”“Usinifanye chochote kibaya”“Siwezi kukufanya kitu kibaya Erick, naomba unisamehe kwa kukupeleka kwenye kaburi la babu yangu”Erick alikubali tu kupanda ila kishingo upande, na walikuwa kama wakiondoka na Juma kwani walianza kwenda kwenye barabara waliyotokea wakati wakienda huko shambani.Ila kabla ya kufika mbali, Juma alisimama na kumwambia Erick,“Hapo mbele kuna kisima, hiko kisima kilijengwa na babu yangu. Naomba tushuke tu ukatie baraka kwenye hiko kisima, nakuomba Erick, nakuomba sana”Erick alikuwa akimshangaa sana Juma, kwakweli alishindwa kumuelewa kabisa kwa yale mambo ambayo yaliendelea, kisha alishuka nae tu mpaka karibu na hiko kisima, kisha Erick akamuuliza,“Kwahiyo natakiwa kufanyeje?”“Sema tu, kuwa unakitia baraka kwenye hiki kisima ili mjukuu wa kwanza wa mzee Nguvumali aweze kufaidika. Maana babu yangu aliitwa mzee Nguvumali na mimi ndio nilikuwa mjukuu wake wa kwanza, sisi hatukuwa kwenye ukoo mkubwa sana, hata hivyo ndugu zetu ni wachache sana”Erick alikubali tu na kusema,“Nakitia baraka hiki kisima ili mjukuu wa kwanza wa mzee Nguvumali aweze kufaidika”Yani Juma alimshukuru sana Erick kwa lile jambo, kisha alipanda nae kwenye gari sasa kwa safari ya kumrudisha kwao huku akimsisitiza kuwa asiseme chochote kilichotokea huko kwa baba yake,“Kwanini nisimwambie?”“Baba yako atajisikia vibaya kama akipata maneno kama hayo, naomba usimwambie lolote”Erick alimuitikia tu ili aweze kurudi nyumbani kwao, basi moja kwa moja alirudi nae nyumbani kwao.Walipofika nyumbani kwa baba Angel, ilikuwa ni usiku tayari, ambapo Juma alisogea kwa baba Angel na kumwambia,“Nimemrudisha kijana wako, nashukuru sana kwa kukubali niende nae siku ya leo”“Sawa usijali”Basi Juma aliaga na kuondoka, ila kwakweli baba Angel alitamani sana kujua kuwa ni mahali gani Juma alienda na kijana wake, basi alimuita Erick na kumuuliza, kwakweli Erick alishindwa kumueleza yale mambo yote yaliyotokea kule, ila tu alimwambia kuhusu kisima ambacho Juma alimwambia kuwa akitie baraka,“Yani kakuchukua hapa ili ukatie baraka kwenye kisima!!”“Ndio, ila ni mbali sana ndiomana tumechelewa hata kurudi”“Pole sana mwanangu”Mama Angel nae alienda karibu na kusema,“Nilijua tu kuwa huyu Juma ni mshirikina, sasa hayo mambo ya kutia baraka kwenye visima yanaanzia wapi?”“Hapo hata mimi sijaelewa mke wangu”“Yule Juma ni mshirikina, yani ni mshirikina kabisa ndiomana kwa siku nyingi tu alikuwa akikazana kuwa aende na Erick kwenye biashara zake, kumbe kwenye kisima chake, si angesema ukweli tu!!”Walijadiliana pale, ila hakuna mtu aliyekuwa na ukweli kati yao kwani ni Juma pekee ndiye aliyeelewa ni kwanini alifanya kitu cha namna ile.Usiku wa leo, wakati Erick amelala alibaki akiweweseka tu, yani lile tukio zima la kupelekwa na Juma kule lilikuwa likimjia kwenye kichwa chake na kujikuta kila mara akishtuka na kushindwa hata kulala vizuri, mara nyingine akijiuliza,“Sijui kwanini nilikubali kwenda nae! Mbona sina raha kabisa mimi!!”Alijaribu tena kulala ila alishindwa na kuendelea kuweweseka tu, na hapo aliona hawezi kuendelea kulala peke yake kwani aliinuka na moja kwa moja kwenda chumbani kwa Erica ambaye kwa muda huo alikuwa amelala.Basi Erick alienda kulala pembeni mwa Erica kwani kule chumbani kwake alikosa usingizi na alihisi pengine akilala pembeni ya mtu basi ataweza kulala, na kweli alipojilaza tu pembeni ya Erica alijikuta akijiwa na usingizi mzito kabisa na kulala hapo hadi asubuhi.Kulipokucha, Erica ndio alikuwa wa kwanza kuamka na alishtuka sana kumuona Erick pembeni yake sababu hakumtegemea kwa muda huo, basi alimshtua pia na kumuita,“Erick, Erick”Erick alishtuka pia huku akiwa na usingizi bado, basi Erica akamuuliza,“Ni muda gani umekuja chumbani kwangu?”“Usiku wakati nimekosa usingizi”“Unajua nilichoota Erick?”“Umeota nini?”“Aaaah sitaki kukwambia, ila kwanini umekuja na kulala pembeni yangu Erick jamani!! Unajua mimi ni dada yako!”“Najua ndio, kwani dada na kaka hawawezi kulala pamoja?”“Hapana, sijasema hivyo. Uswahilini huko, kwenye shida ya makazi, utakuta baba na mama wana chumba na sebule, basi kule chumbani wanalala wao halafu sebleni wamepatenga na wanalala humo watoto wa kike kwa wakiume, ila ni uswahilini na washazoea hivyo ila binafsi siyaamini maisha yao”“Unaongelea nini Erica?”“Sijui, nahisi nimeongea tu”Erick alimuangalia vizuri Erica, ila aliona utofauti kwenye sura ya Erica kwa siku ya leo, kila siku huwa anamuona ila leo alimuona na utofauti, hadi Erica alimuuliza,“Mbona unaniangalia sana?”“Unajua kuna kitu nadhangaa, mbona leo umekuwa mzuri zaidi Erica?”“Erick, naomba utoke chumbani kwangu”Erica alimfukuza Erick baada ya ile kauli, hata Erick alishangaa maana yeye alimwambia kile ambacho amekiona kwa muda huo, ila Erick hakubisha na kuamua kutoka tu mule chumbani kwa Erica.Mama Angel akiwa anaongea na mumewe baada ya mazoezi, alikuta simu yake ilipigwa sana na aliyekuwa akimpigia alikuwa ni Sia, basi aliamua kumpigia na kugundua kuwa simu yake ilikuwa imeisha vocha, basi mama Angel alimuita Erica maana hii siku ilikuwa ni siku ya mapumziko ya kiserikali kwahiyo Erica alikuwa nyumbani, basi alifika pale na alimuagiza akamnunulie vocha ili aweze kuweka na kuzungumza na huyo Sia.Basi Erica aliondoka pale kwao na moja kwa moja kuelekea dukani, alivyonunua tu vocha akakutana dukani na yule Emmanuel ambaye walihisi mwanzoni kuwa alikuwa kiziwi, basi yule Emmanuel alimsalimia Erica, ila Erica kwa siku ya leo hakuacha kumuuliza lile swali,“Unajua kuna siku rafiki zangu walikuona kwenye daldala, na vile ulishuka nasi tulishuka, wakakufata nyuma na kukusalimia ila hukuitikia, walikuongelesha ila hukuongea hadi tulihisi huenda ulikuwa kiziwi”“Ni kipindi gani hiko?”“Ni miezi mingi imepita, kama utaweza kukumbuka kwa mbali ni hivi alikufata mdada mmoja aliyekuwa kajitanda halafu mwingine alikuwa kichwa wazi, walikusalimia ila hukuitikia”“Oooh naweza kukumbuka kidogo, unajua mimi nina matatizo na kipindi hiko ndio matatizo yalinizidia kwani mama yangu alikuwa kwenye hali mbaya sana sababu alipata ajali ila kwasasa anaendelea vyema, kwakweli nilikuwa nimechanganyikiwa. Inawezekana niliwaona vizuri ila sikuwatilia maanani. Unaishi wapi wewe? Na mbona hukunitafuta tangu siku ile?”“Aaah nilipoteza namba zako, ila mimi siishi mbali na hapa”“Kama hutojali, basi naomba nipafahamu nyumbani kwenu”Erica hakuona tatizo lolote, na kuanza kuongozana na huyu Emmanuel hadi nyumbani kwao, ila walipofika getini kabla hata ya kuingia ndani, Emmanuel alipigiwa simu na kusema kuwa ataenda siku nyingine, basi aliagana tu na Erica pale kisha Emmanuele alimuandikia tena Erica namba yake ya simu ili aweze kuwasiliana nae, halafu Erica aliingia ndani kwao kumpelekea mama yake ile vocha.Mama Angel muda ule ule alipoweka tu hiyo vocha, alimpigia simu Sia maana alihisi lazima kuna jambo la muhimu anahitaji kuambiwa na Sia,“Nilikupigia sana simu ila hukupokea, sijui tatizo nini?”“Hakuna tatizo ila nilikuwa mbali tu na simu, niambie shida yako”“Sikia, leo ni siku ya mapumziko ila nilienda shuleni kwakina Elly maana kuna mtu kaniambia kuwa maeneo ya kule yapo vizuri kwa biashara, si unajua mimi natafuta riziki, basi nikaenda kuangalia na kule kama inawezekana kufanya biashara kule, basi nikamuona mama Sarah akiwa ameongozana na Moses wakiingia kwenye ile shule”“Unamaanisha Manka?”“Ndio huyo huyo, mimi nimezoea kumuita hivyo mama Sarah”“Eeeeh walikuwa wakifanya nini?”“Hapo ndio sijui ila kuna mtu niliongea nae akasema kuwa ile shule ni ya mtoto Sarah, yani ndio shule aliyopewa na baba yake, kwaamana hiyo ile ni shule ya mzee Jimmy”“Oooh niliwahi kusikia hiko kitu, kwahiyo kwasasa wanafika kwa kujificha?”“Nadhani sababu ya hilo tukio ambalo wamelifanya, ila nikajaribu kuwafatilia bhana, huwezi amini muda si mrefu mama Sarah alikuja kwenye biashara yangu hadi nimefunga kwa leo na kurudi tu nyumbani kwangu”“Mmmh alikuwa anasemaje sasa?”“Jamani, huyu mwanamke sijui huwa anagundua vipi kama namfatilia, amekuja kunipa onyo hilo balaa. Hata nimejivika ujasiri na kuanza kusema, kweli nina moyo wa chuma ila nimepewa onyo kabambe”“Pole sana, kwahiyo hataki umfatilie!”“Ndio, kasema ole wangu niendelee kumfatilia nitaiona dunia chungu. Umbea umeniishia Erica, naacha umbea rasmi”“Pole sana, utaacha umbea wakati bado mwanao wa ukweli hujamjua!”“Simjui na wakati huo huo sitaki Elly ajue kama mimi sio mama yake wa ukweli, haya mambo yananitesa hadi najiona kuisha tu kwa siku hizi, yani nakonda sana”mama Angel aliongea ongea na Sia kidogo kisha kuagana nae, na kumsimulia mumewe kuhusu Sia kuonana na mama Sarah, kwakweli baba Angel alitamani apone haraka kwani aliona kuwa kuna vitu vingi sana ambavyo bado anahitaji kuvifanya.Usiku wa leo, Erick alienda tena chumbani kwa Erica kwani hakumuelewa sababu ya Erica kumfukuza toka chumbani kwake, basi alimkuta amejiinamia tu, akamuita na kuanza kuongea nae,“Erica, kwanini ulinifukuza asubuhi?”“Mmmmh naomba unisamehe tu maana sikutarajia wala nini”“Ila hujaniambia kwanini ulinifukuza”“Nikuulize kitu Erick?”“Niulize tu”“Katika maisha yako ni kitu gani unapenda yani nini unapenda kukipata zaidi katika maisha yako?”“Napenda furaha, yani furaha ndio jambo la kwanza katika maisha yangu. Huwa namuomba sana Mungu ili familia yetu iweze kuishi na furaha kama zamani, huwa naomba baba apone, apate nguvu na tuishi vizuri kama zamani”“Roho huwa inakuuma eeeh ukimuona baba katika hali ile!”“Ndio, naumia sana. Unajua baba anatupenda sana, yani sisi hata tukiumwa kichwa unaona ni jinsi gani baba anavyohangaika. Kwakweli Mungu atusaidie baba yetu apone, nahitaji awe mzima kama zamani”“Sawa, nikuombe kitu?”“Niombe tu”“Naomba simu yako nimpigie yule kaka wa siku ile”“Mmmh Erica jamani, kwani huyo kaka anauhusiano gani na hiki tunachokiongea kwasasa? Yani huyo kaka anahusika na nini?”“Hivi si unapenda furaha Erick? Nina uhakika unapenda kuona nami nikifurahi, naomba simu yako kwa leo tu halafu nikimaliza kuongea nayo nitakwambia”Erick hakukataa na kwenda kuchukua simu yake moja kwa moja na kumletea Erica, ambaye alichukua tena namba za Emmanuel na kumpigia, basi simu iliita na muda kidogo ilipokelewa,“Hallo, Emmanuel unaongea na Erica hapa”“Aaaah mimi sio Emmanuel mimi ni Emmanah”“Kheee Emmanah!! Mbona nilikutana na Emmanuel ndio akaniambia kuwa hii ni namba yake”“Ni kweli ni namba yake, ila ametoka na kuniachia simu yake. Mimi ni pacha wake”“Kheee kumbe, mpo mapacha!!”“Ndio, akirudi nitamwambia akupigie”“Sawa, kwaheri”Basi Erica aliikata ile simu na kumuangalia Erick kisha alimwambia,“Kumbe huyo Emmanuel ana pacha wake wa kuitwa Emmanah”“Sawa, sasa wewe ulikuwa unampigia simu wa nini?”“Yani kwa jinsi nilivyoongea na huyu Emmanuel nimeona ni mtu wa dini, nikasema nimpigie ili tushirikiane nae kwenye maombi yani mimi, wewe na yeye ili tumuombee baba yetu”“Hapo umesema vizuri, ila tusimsahau na Elly”“Sawa sawa hakuna tatizo”“Haya sasa niambie kwanini ulinifukuza?”“Unataka kulala tena chumbani kwangu na leo? Karibu”Erick alimuangalia sana Erica na kuona kuwa Erica hakutaka tu kumwambia ukweli wa kwanini alimfukuza, basi aliongea nae tena kidogo na kuamua kuondoka zake.Kesho yake, baada ya Erick kutoka shule, aliona ile namba ya Emmanuel ikiingia kwenye simu yake, basi Erick aliikata ile simu kwani hakutaka huyu mtu aongee na ndugu yake mara kwa mara, alijikuta akisema,“Simuamini huyu mtu”Kisha moja kwa moja alirudi nyumbani kwao na baada ya mambo ya hapa na pale alimfata baba yake na kuongea nae maana aliambiwa kuwa anaitwa na baba yake, kisha baba yake alianza kumuuliza,“Kwani siku ile na yule rafiki yangu Juma mlienda kufanya nini?”“Hakuna kitu baba zaidi ya vile nilivyokwambia kwani vipi?”“Amenipigia simu huku akiniambia kuna mambo mazuri yanakuja sababu ya ile safari mliyoenda, matunda yameonekana”“Kheee kivipi?”“Hata mimi sijamuelewa, ila amesema atakuja maana kwasasa kuna vitu vimemfanya awe busy sana katika sehemu ile mliyoenda”“Basi sijui kwakweli maana nakumbuka aliniambia nibariki kisima tu basi, na hakuna kazi yoyote ambayo mimi na yeye tuliifanya”“Haya mwanangu, basi”Erica nae alikuwa ametoka shule, na moja kwa moja alienda chumbani kwa baba yake ambapo baba yake alikuwa akiongea na Erick basi alimsalimia pale na kumwambia Erick,“Mwambie tu ukweli kuwa ulienda nae kwenye kaburi la babu yake kwanza”Erick alimuangalia Erica kwa muda na kumshangaa kwani hakufikiria kama kile kitu basi kingejulikana kwa Erica, basi baba Angel alimuangalia mwanae na kumuuliza,“Niambie Erick, mlienda kwenye kaburi la babu yake kufanya nini?”Kwakweli hapa Erick alishindwa kabisa kumficha baba yake kwani aliamua tu kwa muda huo kumueleza kila kitu ambacho kilitokea wakati yeye alivyoondoka na Juma kwa siku ile, baba Angel alibaki kushangaa tu huku akijiuliza kuwa rafiki yake alikuwa na maana gani kufanya vile.Kisha baba Angel alimruhusu Erick kuondoka tu na Erica maana aliona hana cha ziada cha kuongea nao, basi Erick alimfata Erica na kumuuliza,“Inamaana na haya nayo uliota?”“Ndio, niliota toka umeondoka siku ile na yule mbaba”“Kwahiyo vingi huwa unaviota kuhusu familia yetu? Je kuhusu baba kwenda kupigwa risasi uliota pia ila hukusema?”“Sio vyote ninavyoviota maana mambo mengine huwa sioti”“Hapo sawa”Yani Erick alikuwa akimuuliza kwa makini ili kugundua kama anaweza kuota kuhusu simu ya Emmanuel ambayo aliikata, kwahiyo aliposikia kuwa vingine huwa haoti basi aliweza kuendelea na mambo yake mengine kwa amani.Baada ya wiki mbili, dokta Maimuna alirudi na moja kwa moja alienda nyumbani kwa mama Angel kwani alitaka kuangalia maendeleo ya baba Angel na siku hiyo alifika na magongo ya kutembelea ili waanze na magongo na taratibu iwe kwa baba Angel kuweza kutembea kabisa.Alifika na magongo pale na kumpa baba Angel mazoezi ya kutembelea hayo magongo, haikuwa shida sana kwa baba Angel kutokana na yale mazoezi ambayo walikuwa wakimpatia hapo kabla kwahiyo aliweza kwa haraka sana.Ile kitu ilikuwa ni furaha kubwa sana kwa baba Angel na mama Angel pia, basi walikaa na kuanza kuongea na dokta Maimuna kuhusu maendeleo ya hali ya baba Angel,“Kwakweli kwasasa nina matumaini kuwa Erick utarudi kwenye hali yako ya kawaida, Mungu ni mwema atakusaidia tu”“Asante sana dokta”“Mshukuru sana mke wako maana naona alikuwa vizuri sana kwenye kukupa zoezi, nilivyomuelekeza ndio alivyokuwa akifanya”“Ndiomana nampenda huyu mwanamke, kichwa chake chepesi sana na yupo vizuri ndiomana kanizalia watoto wazuri”Hapo inaonekana dokta Maimuna hakupenda kwani alikuwa akitabasamu mwanzoni na kuacha kabisa kutabasamu na muda sio mrefu aliaga na kuondoka zake, basi mama Angel alikaa na mumewe na kumsema kiasi,“Ila baba Angel na wewe mambo mengine unayataka, huyu mwanamke kajitolea kwa kila hali kukuhudumia, ila kumwambia unanipenda sana ujue umeumiza moyo wake kwani na yeye alikupenda kabla”“Khaaa kwahiyo kachukia kwasababu hiyo! Ila sijamwambia uongo, ni kweli nakupenda sana, kwanza ni mzuri halafu ni mwelewa, yani mimi huwa natamani kila ninayekutana nae basi nimweleze ni kiasi gani nakupenda wewe”“Duh! Haya nashukuru kwa upendo wako huo, ila mume wangu uwe unajistahi muda mwingine”“Aaaah wewe Erica umeniroga wewe, ona najiropokea tu. Ila ongeza tu dozi mama niwe mwehu kabisa maana nakupenda sana”Baba Angel alikuwa akiongea huku akicheka na kumfanya mke wake nae acheke.Siku hii ya Jumamosi, alifika Juma pale nyumbani kwa baba Angel kumsalimia na kumpatia habari aliyokuwa nayo, basi baba Angel alipomuona alimkaribisha tu huku magongo yake yakiwa pembeni,“Kheee unatembelea magongo sasa hivi!! Kwakweli Mungu ni mwema, utapona kabisa Erick”“Asante”Kisha Juma alitoa mfuko na kumkabidhi baba Angel, ambapo alifungua mfuko ule na kuona kuna kama vipande vitatu vya dhahabu, kwakweli baba Angel alishangaa sana na kumuuliza,“Nini hii?”“Ni utajiri huu Erick”“Umepata wapi haya?”“Sio haya tu, bali nilipata na mengine nimeenda kuuza, kwahiyo nina pesa za kutosha kwasasa, nikasema nisiwe mchoyo wa fadhila na kuamua kukuletea haya”“Hebu nieleweshe nielewe”“Ni hivi, siku ile nimeondoka na Erick mdogo. Nilitaka kwenda nae kwenye kaburi la babu yangu na ndio tulifanya hivyo, kwani nilihitaji kupata baraka za babu kupitia Erick, nakumbuka niliwahi kusikia kuwa pale ambapo babu alichimba kisima kuna dhahabu na hakuna mtu anayejua. Basi nilipopita na Erick nilimwambia aweke baraka mahali pale, huwezi amini nimechimba dhahabu pale na nimepaziba kabisa, nimekuletea tu hizi chache kama asante, na ukipona basi nitakupa eneo na wewe pale uweze kuchimba”“Mmmh mbona sikuelewi, kuna mahali pa kuchimba dhahabu kweli hapa mjini?”“Huwezi kuelewa Erick, ila Mungu ni wa ajabu sana. Sitaki kutangaza kwani najua serikali itaninyang’anya mali yangu”Kisha Juma akainuka na kumuaga baba Angel na kumuachia ule mfuko wa dhahabu, kwa muda ule mama Angel hakuwepo pia kwani alikuwa ametoka kidogo.Erick, akiwa anatoka kiwandani kwa baba yake, moja kwa moja alienda dukani kwa baba yake kwani alihitaji kujua kila biashara ya baba yake inaendeleaje.Akiwa dukani siku ya leo, kuna baba mmoja alifika pale dukani na kusalimiana nae ambapo yule baba alimwambia Erick,“Kama nakufahamu vile, nahisi kama kuna mahali nimewahi kukuona”Erick alivuta kumbukumbu vizuri kiasi na kumkumbuka huyu baba,“Ndio nimekukumbuka pia”“Eeeeh ni wapi tulionana?”“Kuna siku mimi na baba tulikuja dukani kwako kwaajili ya kumchukulia zawadi mama, halafu wewe na yule mama mwingine mlichagua zawadi tofauti tofauti mkasema tumpelekee mama, nami nikamshauri baba achukue zote ilia one mama ataipenda ipi”“Khaaa kweli una kumbukumbu sana kijana, hujambo lakini”Basi Erick alianza kumsalimia vizuri yule baba pale, ambapo alijitambulisha kwa jina la baba Emma, kwani Erick alikuwa hafahamu jina la huyu baba vizuri,“Halafu baba yako sijamuona kwa siku nyingi, kwani yumko wapi siku hizi?”“Baba alipata matatizo”“Nini tena?”“Alivamiwa na majambazi, wakampiga risasi za miguuni kwahiyo yupo nyumbani hawezi kutembea”“Khaaa jamani, mbona mambo mapya haya loh! Sikutegemea kabisa, naomba twende wote nikamuone tu”Erick alikubali, na muda huo huo kuondoka na baba Emma kuelekea nyumbani kwao.Walipofika, moja kwa moja Erick alimkaribisha baba Emma pale nyumbani kwao, muda huo mama Angel nae alikuwepo sebleni na mume wake, ila alipoona mlango unafunguliwa alibaki kuangalia ili kuona ni nani anaingia, alishangaa sana kuona Erick kaongozana na yule baba ambaye alikuwa anafahamiana nae vizuri sana. Walipofika, moja kwa moja Erick alimkaribisha baba Emma pale nyumbani kwao, muda huo mama Angel nae alikuwepo sebleni na mume wake, ila alipoona mlango unafunguliwa alibaki kuangalia ili kuona ni nani anaingia, alishangaa sana kuona Erick kaongozana na yule baba ambaye alikuwa anafahamiana nae vizuri sana.Baba Emma na mama Angel walitazamana kwa muda, kisha baba Emma alisogea karibu na kumkumbatia mama Angel kisha kuanza kusalimiana nae ambapo mama Angel alijitoa pembeni kidogo ili asimkasirishe mume wake, walianza kuongea na baba Emma,“Za siku Erica! Kumbe unaishi hapa”Kisha baba Emma alimuangalia baba Angel na kumpa pole,“Pole sana, nimekutana na kijana wako huyu ndio nikamuuliza akasema ulivamiwa na majambazi, dah pole sana kwakweli”“Asante ndugu yangu, kumbe unafahamiana na mke wangu eeeh!!”“Ndio, niliwahi kufahamiana nae kitambo. Nafurahi sana kugundua kuwa huyu ndio mkeo, hongera sana ndugu yangu, kwakweli hapa umepata mke. Hongera sana”baba Angel alitabasamu na kuendelea na maongezi mengine,“Amekukuta wapi huyu?”“Aaah nimekutana nae kwenye duka la vifaa vya watoto maana mke wangu kajifungua”“Oooh hongera sana, mpe hongera zake. Ndio mtoto wako wa ngapi huyo?”“Wa tatu, ni wakike anaitwa Emmanuela”“Oooh hongera sana ndugu yangu”Basi waliongea pale na kuagana kwani kwa muda huo baba Emma aliaga na kuondoka zake.Muda huu baba Angel aliingia chumbani ila alihitaji maelezo kwa mke wake kuwa kamfahamu vipi baba Emma yani ni nani katika maisha yake kwani bado alikuwa akijiuliza maswali mengi sana sababu akikumbuka zawadi alizokuwa anaenda kumnunulia mkewe kwa baba Emma siku zote ni huyu baba ndio alimchagulia mama Angel zawadi, kwahiyo leo alishangaa sana kuona huyu mtu anafahamiana na mke wake tena inaonyesha wanafahamiana vizuri sana, basi alimuuliza,“Mke wangu naomba unieleze kuwa huyu mtu mmefahamiana nae vipi, unajua nimeshangaa sana jinsi mlivyojuana, naomba niambie ukweli ili niweze kuelewa”mama Angel alipumua kidogo na kuanza kumueleza mume wake,“Ni hivi, huyo uliyesema ni baba Emma, namfahamu kwa jina la John. Nilikutana nae miaka ya nyuma sana wakati nimemaliza kidato cha tano, nakumbuka nilikuwa narudi likizo ndio nikakutana nae kwenye zile basi kubwa za mkoani na tuliongea mengi sana, ila kitu alichonipatia kilikuwa ni ukumbusho mkubwa sana kwangu, alinipa zawadi ya simu, yani nilifurahi sana ukizingatia simu nilikuwa na uhitaji nayo sana”Baba Angel akamkatisha kidogo,“Kwahiyo alikuwa ni mpenzi wako!! Si ndio”“Nisikilize kwanza mume wangu, ni kweli nilianza mahusiano na John ila katika mahusiano yetu hatukufanikiwa kuwa pamoja kimwili kabisa, kwanza tulikuwa wote tunasoma halafu tulipotezana kimawasiliano”“Ulimpenda sana?”“Mmmh mume wangu jamani, katika maisha yangu hakuna mwanaume yoyote ninayempenda zaidi yako, najua unatambua hilo. Najua unatambua ni jinsi gani nakupenda ila huyu John ni mmoja katika mapito yangu kama wewe ulivyopita kwakina Sia, inamaana ulikuwa unawapenda sana au ndio unawapenda sana kuliko mimi!!”“Hapana, mimi nimekuuliza hivi kwa maana yangu. Unajua nini, huyu jamaa ndio mwenye lile duka la nguo na kila siku nikikuletea zawadi basi huwa nimezotoa dukani kwa huyu kijana na huwa ananichagulia yeye, kwa hakika huwa unazifurahia sana na kuzipenda sana, ushawahi hadi kuniambia kuwa siku hizi nakuchagulia zawadi nzuri sana. Kuna siku nilienda na Erick dukani kwa huyu jamaa, kisha yeye na mkewe wakachagua zawadi tofauti, Erick alisema nikuletee zote hapa nyumbani ila bado ulichagua ile ya huyu jamaa bila kujua kuwa nachukua kwake zawadi. Nakumbuka siku nyingine nilikuchukulia viatu, huyu jamaa sikumkuta bali nilimkuta mke wake ndio alinichagulia vile viatu, vilivyofika hapa nilitaka tutoke ukiwa umevaa vile viatu ila ulidai vinakubana na kukuumiza miguu na hadi leo hujawahi kuvaa tena vile viatu, ndiomana nimekuuliza mke wangu, huyu John ndio ulimpenda sana”“Unajua hadi nashangaa na kujikuta nikikosa kabisa cha kuongea, yani sina kabisa cha kuongea. Mimi sio kwamba nilimpenda sana John, kwakweli hilo siwezi kukubali. Ila ninachokumbuka kuwa John ndio mwanaume wa kwanza mimi kuanza nae mahusiano ila hata hivyo sijawahi kulala nae, kingine John ni mwanaume wa kwanza kunipa mimi zawadi ambayo nilikuwa na uhitaji nayo kwa kipindi hiko na niliipenda, ila kusema kuwa John nilimpenda sana hapana mume wangu. John kwangu ni wa kawaida tu, labda kitu ambacho hufahamu ni kuwa John ni mdogo wake Rahim”“Mdogo wake Rahim!! Kivipi?”“Hata mimi mwanzoni sikujua kama ni ndugu, ila mama yao ana watoto wawili tu yani John na Rahim ila baba zao ni tofauti yani Rahim ana baba yake halafu John pia ana baba yake. Na ndio yule mama aliponigundua alisema kuwa mimi ni malaya sababu nimetembea na watoto wake wote”“Aaaah kumbe ndio ilikuwa hivyo, ila bado najiuliza kwanini huyo John akikuchagulia zawadi ndio unapenda?”“Hilo sijui mume wangu, hata sijui ni kwanini yani utakuwa unaniuliza tu na hata sielewi chochote kile”Ilibidi baba Angel aache kumbana mkewe kwa maswali na kuanza kupanga mazoezi yatakayoendelea kesho yake.Basi kila siku iliyoendelea mama Angel aliendelea kumfanyisha mazoezi mume wake ili aweze kuwa sawa kabisa maana alitamani sana kuona siku ikifika ambayo mumewe atainuka na kutembea kabisa kama zamani.Siku hiyo baada ya mazoezi walikaa wakiongea,“Unajua mke wangu nimechoka hii hali, yani nimechoka kabisa, nachoka sana kufanya mazoezi na kuzunguka na magongo, natamani siku moja Mungu aniinue niweze kusimama na kutembea tena”“Mungu ni mwema mume wangu, naamini kuwa utapona kabisa, uzima upo njiani mwako”“Asante ila hivi ni kitu gani kimetokea kwa dokta Maimuna maana ni wiki ya pili sasa hajaja wala hajapiga simu”“Halafu sio kawaida ujue, maana toka aondoke siku ile ndio imekuwa basi tena. Nakumbuka siku anasafiri alituaga vizuri kabisa na wakati yupo safarini alikuwa akitupigia simu na kuulizia kuhusu maendeleo yako, na amerudi tu moja kwa moja alikuja, tuseme kasafiri tena au ni nini!”“Hata angesafiri tena ni lazima angetuaga tu, sijui alichukizwa na nini”“Mmmh na wewe mume wangu usitake kusahau hapa, nilikwambia yale maneno yako ya kunisifia sana mimi inawezekana kuwa sababu kubwa sana ya kumchukiza”“Sasa na yeye si amwambie mumewe amsifie huko!! Mambo mengine ni ya ajabu hata kufikiria, tulikuwa vizuri tu hapa, sasa nisisifie ninachokipenda kwasababu ipi?”“Hata kama unasifia angalia na mazingira na pia angalia moyo wa mtu mwingine, ngoja nikupe mfano, tuseme mimi nimeolewa na mwanaume mwingine na wewe huwa unanipenda sana ila sijaolewa nawe nimeolewa na huyo mwingine. Halafu tunakutana naanza kukwambia kuhusu ninavyompenda mume wangu, unajua lazima uumie sababu ulinipenda sana. Ni heri tuongee mada zingine ila kumsifia umpendae mbele ya mtu aliyekupenda sana sio vizuri, labda kama yule mtu kakusumbua ila sio vizuri”“Hapo nimekuelewa mke wangu, ni kweli inauma hasa pale umeoa au kuolewa na mtu ambaye hakuwa wa ndoto zako halafu unakutana na yule uliyekuwa unamuwazia sana anakwambia kuwa anampenda sana aliyemuoa au kuolewa nae, ni kweli inauma ni heri kuzungumza mada zingine. Ila kwa lile alilolisema siku ile ndio lilipelekea mimi kusifia kuwa wewe ni mwanamke wa kipekee sana na ninakupenda sana, sikufanya kwa ubaya kabisa ila nilifanya vile kutokana na kile ambacho yeye alikisema mwanzo”“Nimekuelewa pia mume wangu”“Leo utapenda kula nini ili nikupikie upendacho, haya mavyakula ya kupangiwa nayo ushakula sana jamani, leo tubadili”“Sijala pilau siku nyingi sana, natamani ningekula pilau leo”Mama Angel alitabasamu na moja kwa moja kwenda jikoni ili kuanza mapishi.Wakati mama Angel yupo tu jikoni, alifika Erica muda huo na kumfanya mama yake amuulize,“Mbona leo umewahi sana kurudi shule?”“Tumetolewa mapema mama, halafu leo ni Ijumaa”“Oooh hapo nimeelewa, haya bora umerudi. Najihisi uchovu balaa, baba yako leo anahitaji kula pilau, nina uhakika utapika ya kumfanya baba yako ajilambe. Unataka kupika pilau nini maana ndio hapa nilikuwa nafikiria tu nipike pilau nini!”Erica alitabasamu na kumwambia mama yake,“Naomba nipike pilau kuku”“Mmmh kwa kupenda vitu vizuri tu mwanangu hujambo, haya jiko lako hilo kama kuna cha kukusaidia utaniambia”Sababu Erica alishatoa sare zake za shule, moja kwa moja alianza kupika pale jikoni kama alivyoagizwa na mama yake.Alivyomaliza Erica, muda anaandaa kile chakula ndio muda ambao Erick nae alikuwa amerudi shule, ila kwa harufu ya kile chakula akasema,“Naomba kabla hata ya kwenda kubadili hizi sare, nile kwanza hiko chakula maana sio kwa kunukia huku”Erica alitabasamu na kufurahi tu, ila Erick alienda kubadili sare kwanza maana alijua akikaa vile kula ingekuwa balaa kwa mama yake.Basi Erica alimpakulia baba yake chakula na kumpelekea, ambapo baba yake alimwambia“Erica mwanangu asante sana, haya kaa uombee hiki chakula”“Nimeombea jikoni baba”“Aaaah sawa, ombea na hapa”Basi Erica aliombea tena kile chakula na baba yake kuanza kula, yani mama Angel aliingia ndani na kukuta mumewe ndio akila kile chakula na kukisifia sana,“Mke wangu, yani kwa hiki chakula ni hakika huyu Erica umejizaa mwenyewe jamani. Aaaah mtoto mdogo anafanya mambo makubwa kiasi hiki!! Ni ajabu sana”“Ndiomana nilipoona tu amerudi nikamsakizia apike mwenyewe, unajua kwenye mapishi Angel sio sana ila kimbembe kipo hapa kwa Erica, hata mimi kanizidi”“Aaaah mtoto ana balaa huyu, yani mahari yake kwa hakika naozesha kwa milioni ishirini hapa”Mama Angel alicheka sana na kumwambia mumewe,“Sasa itakuwa kuozesha au kumuuza hapo!!”“Kheee hiyo ni mahari, unauzaje mtoto kwa milioni ishirini!! Thamani ya mwanangu ni kubwa sana, hata kwa bilioni tano siwezi kumuuza mwanangu, hiyo ni mahari yani sitaki mwanaume wa kumuoa Erica awe ngonjwa ngojwa, nahitaji awe ni mwanaume mwenye wadhifa na pesa yake”Mama Angel alicheka sana jinsi baba Angel alivyomsifia binti yake, yani alikula kile chakula huku akisifia muda wote, mpaka pale Erica alipoenda kutoa vyombo bado alikuwa akisifia na kumshukuru sana huyu binti yake kwa kupika chakula kitamu. Baada ya Erica kuondoka, baba Angel alianza kumwambia mke wake,“Yani mimi ni baba mwenye bahati, kwakweli sisi ni wazazi wenye bahati sana. Hawa mapacha wetu wawili, ni watoto ambao wamebadili maisha yetu kwa kiasi kikubwa sana, angalia Erica ni mtoto msikivu, mpole, mcheshi na mpishi mzuri sana, tukiacha sifa ya umbea aliyonayo bado Erica anabaki kuwa binti mzuri na bora katika maisha yetu. Tunakuja kwa Erick sasa, ni kijana mwerevu, mpole na msikivu. Naumwa siwezi kwenda kazini wala kutembelea biashara zangu ila Erick anafanya yote hayo yeye mwenyewe, nabaki tu kupigiwa simu kuwa kila kitu kinaenda vizuri na wengine wakinisifia sana kuwa nimepata mtoto haswaa ambaye anaonekana kubadilisha maisha yangu kwa kiasi kikubwa. Tukitoa hasira na kisirani cha Erick ila bado anabaki kuwa kijana bora sana katika maisha yetu. Hawa mapacha najivunia sana kuwa nao”“Kweli mume wangu, yani huwa nikikumbuka kuanzia siku niliyopata mimba ya hawa watoto, misukosuko tuliyoipata, halafu leo tupo nao tukiwa na furaha tele huwa nafurahi sana moyoni. Kwakweli hii ni dhahabu safi katika maisha yetu”Siku hii baba Angel na mama Angel walijikuta wakisifia sana uwepo wa Erica na Erick katika maisha yao.Usiku wa leo, Erica akiwa chumbani kwake, aliwaza pia kuhusu Emmanuel na kuona kuwa anahitaji kuzungumza na mtu huyu, moja kwa moja aliamua kwenda chumbani kwa Erick ili amuombe simu aweze kumpigia Emmanuel.“Erick naomba simu ili nimpigie yule Emmanuele tena maana mbona hajanitafuta hadi leo?”“Sikia nikwambie kitu Erica, kuna kitu tufanye halafu nitakupa simu uongee na huyo Erick utakavyo”“Kitu gani hiko?”“Kalete karata”Basi moja kwa moja Erica alienda kuleta karata, na kumpatia Erick, basi Erick alimtaka waanze kucheza karata na kumwambia,“Ukinifunga goli tano za karata basi nakupa simu unaenda kulala nayo kabisa chumbani kwako na unaongea na yeyote utakaye”“Ila na wewe Erick, umeanza masharti kama mganga wa kienyeji”“Mmmh Erica, mambo ya mganga wa kienyeji umeyajulia wapi wewe?”“Si huwa naona kwenye sinema, halafu hata Samia huwa ananihadithia sana. Alishawahi kuniambia kuwa, wao wangekuwa na baba mwingine. Mama yao aliwahi kuwasimulia kuwa kuna mwanaume alipendana nae sana ila yule mwanaume alirogwa na mwanamke mwingine, basi mama yao ndio akaamua kuanza na baba yao wanayeishi nae sasa, kwahiyo mambo ya waganga yapo nayajua”“Duh!! Wewe ni noma”Pale walianza na maongezi mengine, ambapo Erica alikumbushia pia maongezi ambayo baba yao alikuwa akiongea na mama yao maana alikuwa akisikiliza vizuri maongezi yale,“Erica jamani, kumbe ulikuwa ukiwasikiliza?”“Ndio, si walikuwa wakiongea pale sebleni nisisikilize kwanini? Nimemkosea nini Mungu hadi nisisikilize?”Yani Erick alicheka tu, na kuendelea kucheza karata ila walicheza sana karata hata Erica alisahau mambo ya kupiga simu kwa Emmanuel na ile ilikuwa ni furaha kwa Erick maana alitaka kumgelesha Erica kuhusu hayo mawasiliano yake.Basi walicheza sana karata na mwisho wa siku kama kawaida walijikuta wakilala hoi pamoja pale kitandani.Kulipokucha, mama Angel alitoka chumbani kwake na kuelekea chumbani kwa Erick kwani alikuwa akitaka kumuagiza ofisini kwa baba Angel kwa siku hii, kwahiyo moja kwa moja alienda chumbani kwa Erick, alipoingia ndani alishangaa sana kuona Erica na Erick na leo wamelala pamoja, basi aliwaamsha na kuwaambia,“Yani nyie bado tu hii tabia yenu ya kulala pamoja inaendelea?”Hawakujibu kitu zaidi ya kumsalimia na kufikicha macho tu, kisha mama Angel aliendelea kuwasema,“Nyie mmekuwa wakubwa sasa, sio wadogo tena kama zamani. Kwasasa, wewe Erick umekuwa na wewe Erica umekuwa haifai kulala pamoja kabisa. Mnajua madhara yake?”“Hatujui mama?”“Nyie ni ndugu, sasa mnawezaje kulala pamoja na ukubwa huu!! Haya mkilala hapo halafu Erick ukakosea na kumshika dadako ziwa unadhani itakuwaje?”“Kwani kuna ubaya mama? Si itakuwa bahati mbaya hiyo?”“Hebu achene ujinga, bahati mbaya kumshika ziwa dada yako!! Sitaki huu ujinga wa kukuta mmelala pamoja tena, nyie ni wakubwa kwasasa, mmelala udogoni ila sio kwasasa. Nadhani tumeelewana, haya Erica nenda chumbani kwako huko”Basi muda ule, Erica aliinuka na kwenda chumbani kwake halafu mama Angel alibaaki kumuagiza Erick ofisini kwa baba yake,“Leo naomba uende ofisini kwa baba yako, halafu ukienda pale ofisini unatakiwa kupitia mikataba ya watu watatu, jitahidi upitie kwa makini mwanangu”“Sawa mama, hakuna tatizo”Basi mama Angel aliondoka zake na kumuacha pale Erick ajiandae kwenda huko ofisini.Mama Angel alirudi kwa mume wake moja kwa moja na kumwambia,“Kwakweli leo hawa watoto wamenichukiza sana”“Wmefanyaje?”“Eti nimewakuta wamelala pamoja hawana hata habari”“Kivipi?”“Yani Erick na Erica nimewakuta wamelala pamoja chumbani kwa Erick na hawana hata habari”“Walikuwa wanafanya kitu gani kibaya?”“Hakuna, walikuwa wamelala tu”“Sasa umechukia nini mke wangu?”“Unaona ni kawaida kwa watoto wakubwa vile kulala pamoja? Unajua yule ni mtoto wa kike na wa kiume?”“Kwnai unahisi nini kitatokea wakilala pamoja mke wangu?”“Sijui ila sipendi halafu nahisi wanaweza hata kutamaniana na kutuletea balaa sie”“Kheee jamani, ndugu watamaniane tena kweli mke wangu!! Au yale niliyokuwa nasikia ni kweli, kuhusu wewe na Derrick!”Hapo mama Angel aliamua kubadilia mada kwani huwa hapendi kuzungumzia kilichotokea kati yake na Derrick.Erick akiwa ofisini mule kwa baba yake, alichukua ile mikataba na kuanza kuipoitia maana ameshakuja mara kadhaa hapa ofisini ila huwa hakai kwa muda mrefu sana, mara nyingi anafika kwa kuagizwa na baba yake, basi wakati akipitia mkataba wa mwisho, kuna mtu aligonga ule mlango wa ofisini, alimruhusu kuingia na alimuona kuwa ni mwanamke wa makamo ambaye alikuwa amebeba sahani ambayo imefunikwa juu kwa lailoni nyeupe yenye kuonekana, kwenye sahani hiyo kulikuwa na matunda, basi yule bibi alifika na kukaa karibu na kumsalimia Erick kisha akasema,“NBilijua boss Erick amekuja”“Hapana, mimi ni mtoto wake”“Mmmh sijawahi kukuona kabla, ila umefanana sana na binti yangu”“Binti yako? Kivipi?”“Wewe utakuwa ni mjukuu wangu tu lazima”“Sikuelewi, mjukuu wako kivipi?”“Umefanana sana na binti yangu, halafu binti yangu hajabahatika kupata mtoto, kwakweli wewe ni mjukuu wangu kabisa. Unaitwa nani?”“Naitwa Erick”“Wow na wewe ni Erick kumbe!! Nimekupenda bure mjukuu wangu, naomba uwe mjukuu wangu kweli, mimi ni bibi yako, naitwa mama Juli”“Kheee haya sawa”“Niite bibi, nitaridhika sana, unajua sijawahi kukuangalia ila leo nimekuona vizuri sana, kwa hakika unafanana sana na binti yangu. Karibu matunda”Yule bibi alimuachia Erick yale matunda aliyokuwa ameyabeba, kisha Erick aliweka yale matunda pembeni na kuendelea na kazi yake.Alipomaliza moja kwa moja aliondoka pale ofisini na kuelekea dukani kwa baba yake, alibeba na yale matunda maana hakutaka kuyala kabisa akihofia mambo aliyoambiwa ya kula kula hovyo kuwa sio mazuri.Alifika pale dukani na moja kwa moja kuanza kufatilia mambo yanayoendelea pale dukani na kuangalia vitu mbalimbali, ila alipotaka kuondoka tu alitokea Juma pale dukani na kuanza kuongea na Erick,“Kumbe umekuja huku leo! Kwakweli baba yako lazima ajivunie sana kwa kumpata kijana kama wewe, yani wewe ni kijana wa tofauti sana”“Asante”Erick alikuwa akielekea kwenye gari lake ambalo alienda nalo, ila alipofungua mlango wa gari, Juma aliweza kuona yale matunda ambayo Erick aliyaweka karibu na kioo, basi Juma alimwambia Erick,“Dah nimeona hayo matunda nimejikuta nikiyatamani jamani, unaweza kunipatia kidogo”Erick alichukua yote na kumpatia kwani kiukweli hata hakuyataka yale matunda, basi Juma aliyapokea na pale pale alianza kula huku akimuongelesha Erick, ila alipokula tunda la kwanza tu alishtuka sana na kumwambia Erick,“Kweli wewe ni mwanangu, nimeamini sasa”“Hivi huwa unamaanisha nini? Unajua huwa sikuelewi, yani yule sio baba yangu?”“Hapana, sina maana hiyo ila kuna kitu nahisi unajua ladha ninayoipata kwenye haya matunda? Kuna siku nitakwambia. Ila sijakwambia kuwa Erick sio baba yako, hapana. Maana hata mimi nikiwa baba yako, je nimezaa na nani? Sijawahi kuwa na mahusiano na mama yako. Nadhani unaelewa ila mimi huwanakupenda yani napenda hata ungekuwa kijana wangu, ipo siku nitakwambia ladha niliyoipata kwenye haya matunda”Erick hakutaka kufikiria sana kwani muda ule ule aliaga na kuondoka zake.Baba Angel, muda huu alitamani sana kupata maziwa yale ambayo huwa yanauzwa kwenye pakti, kwahiyo kwa muda huo waliamua kumuagiza Erica ili aende akawanunulie hayo maziwa.Erica alipotoka tu kununua maziwa, alikutana njiani na Emmanuel ambaye alikuwa ameongozana na pacha wake Emmanah, kwahiyo pale pale aliamua kumtambulisha Emmanah kwa Erica kwahiyo walifahamiana pale na kufurahiana, kisha Erica aliwaambia jambo moja,“Jamani, mwenzenu baba yangu naumwa miguu yani nashuhudiwa kwenye moyo wangu kuwa nikifanya maombi pamoja nanyi, basi baba yangu atapona, kwahiyo nawaomba kama hamtojali basi twende wote nyumbani kwetu ili tufanye pamoja maombi kwaajili ya baba yangu”Yani Emmanuel alijikuta akimfurahia sana Erica na kumuitikia kwa haraka,“Kwakweli upo vizuri sana, nimefurahi kukutana na binti unayependa maombi kiasi hiko, na mwenye imani kubwa hivyo. Basi naomba hayo maombi tufanye siku ya kesho maana leo kuna mahali tulikuwa tunaenda”“Sawa, hakuna tatizo. Mtakuja muda gani nyumbani?”“Kwenye saa kumi jioni tutakuja huko nyumbani kwenu, hakuna tatizo”“Sawa, nimefurahi sana kunikubalia jambo hili. Mbona Emmanah huongei kitu?”“Aaah mimi nimekubali tu”“Inaonyesha wewe sio muongeaji eeeh!”Emmanuel akasema,“Sio nini!! Weee anasoma mazingira kwanza, huyu anaongea kinanda nyuma”Wote walicheka tu, kisha Erica aliagana nao hawa na moja kwa moja alienda nyumbani kwao kumpelekea baba yake yale maziwa aliyokuwa amembebea.Alifika nyumbani na moja kwa moja kumuwekea baba yake yale maziwa kwenye kikombe kisha kumpatia ambapo alianza kuyanywa yale maziwa huku akiyafurahia, Erica alitaka kuondoka ila baba yake alimtaka akae pale waweze kuongea nae ambapo Erica alikaa,“Unajua nini! Nakumbuka zamani, ulikuwa na mtindo wa kuja na kunielezea kila kitu ila siku hizi umebadilika mwanangu au ndio ukubwa!”Erica alitabasamu tu na kusema,“Mbona nipo kawaida baba”“Haya niambie mwanangu, hebu nielezee na mimi mambo ambayo huwa unayaota.”“Mmmh mengine nasahau baba”“Sasa, ngoja nikuombe kitu. Kwasasa ukiota tu basi kesho yake hakikisha unanihadithia kila kitu kuhusu hiyo ndoto uliyoota, au utashindwa kufanya hivyo?”“Nitaweza baba”“Ndio uweze kama ambavyo unapenda kucheza karata maana nasikia wewe bila karata basi siku yako sio nzuri”“Hapana baba, huwa nacheza tu kujifurahisha”Basi baba Angel kwa siku ya leo aliongea mambo mengi sana na Erica maana alikuwa akitamani kwa muda mrefu sana kuweza kuzungumza na binti yake.Usiku wa leo kama kawaida, Erica anaenda tena chumbani kwa Erick na kumkuta ndio anajiandaa na kulala, basi Erick anamwambia“Ila mama si amekataza wewe kulala huku?”“Kakataza kulala ila hajasema nisiwe nakuja huku, hata hivyo baba kasema hakuna ubaya maana hata yeye alikuwa akilala chumbani kwa dada yake hata alipokuwa mkubwa kabisa”“Aaaah kumbe ni kawaida”“Ni kawaida ndio, mama alichukia sababu hapendi karata, kwahiyo kitendo cha kuopna karata karibu yetu kilimfanya aongee sana utadhani kitu gani. Ila kuna muda yale maneno yake yana maana”“Kwanini?”“Kwakweli, kwasasa tumekua wakubwa, kuna vitu kwenye mwili wako hata sivielewi jamani huwa natamani kuviona hasa hiko ambacho huwa kinatuna hapo”Erick alijitazama na kucheka, kisha Erica akaendelea kuongea,“Tubadilishe mada, kilichonileta ni kuwa leo nimekutana na huyo Emmanuel na pacha wake Emmanah”Hapa Erick alijihisi aibu kidogo ukizingatia alimkatalia simu ila ameweza kukutana nao, yani hapo alijihisi vibaya, na kumuuliza tu kwa upole,“Ulikutana nao wapi?”Erica alimueleza kisha alimuomba,“Nakuomba kesho tushiriki maombi na watu hawa kwaajili ya baba yetu, moyo wangu unanishuhudia kuwa kama tukifanya hivi basi baba atapona”“Mmmh haya, mimi nakubali. Kwahiyo tutamuombea baba humu ndani? Kwanza nahisi baba atacheka tu, maana sisi na kuombea wapi na wapi?”“Ni kweli baba atacheka, mama nae atacheka na tutawavunja imani bure ila kinachotakiwa ni sisi kuwa na imani thabiti kuwa baba atapona tu. Nimefikiria na kuona kuwa wale wakina Emmanuel wakifika basi tutaenda nao kule kwenye bustani na kufanya maombi kule”“Mmmh tukiomba kule mbali halafu baba yupo ndani atapona kweli?”“Kila kitu ni imani Erick, kuna watu wapo Marekani ila anamuombea mtu wa Tanzania na anapona, yote ni sababu ya imani. Unaambiwa imani inaweza kuhamisha milima, kwahiyo tuamini tu kuwa atapona hata bila ya chochote, ila sisi tutashirikiana na kuomba kwa kumaanisha”“Kwahiyo tutamwambia ajiandae”“Ajiandae kufanya nini sasa? Sisi tutabeba mzigo wote, na tutajitolea kwaajili ya hili, nimewaomba sana wale wakina Emmanuel na wamekubali kwa moyo wote, kwahiyo nao wamekuwa na imani juu ya hili. Naomba nawe uwe na imani”Erick alikubali tu na kisha waliagana halafu Erica alirudi chumbani kwake kulala.Jumapili ile kama kawaida ya ile familia, wachache walienda kwenye ibada maana kwa kipindi hiko ilikuwa ni ngumu sana kwa familia nzima kuondoka mahali hapo, na hata wakiondoka walikuwa wanawahi kurudi.Kwenye mida ya saa kumi jioni, kama ambavyo walikubaliana ni kweli Emmanuel na Emmanah walifika na aliyewapokea alikuwa ni Erica ambaye moja kwa moja alienda nao kwenye bustani yao na kumuita Erick, kisha walisalimiana pale na moja kwa moja Erica alianza kusema,“Jamani, kama nilivyoongea nanyi, hili jambo tunaenda kulifanya kwa imani. Sisi sio wachungaji wala viongozi wa dini, sisi ni watu wa kawaida kabisa, ila nina imani kuwa tukifanya jambo hili kwa imani basi litafanikiwa tu. Naamini nanyi mnaamini kama mimi ninavyoamini”“Ndio tunaamini”“Basi tushikane mikono na tufanye maombi huku tukiamini kuwa Mungu atatenda kwa baba yetu”Basi walishikana mikono na kuanza maombi mahali pale.Muda huu baba Angel na mama Angel walikuwa wamekaa sebleni huku wakiongea ongea kuhusu mambo mbalimbali,“Unajua ule mkataba wa mwisho Erick anasema amekuta una matatizo sana”“Upi huo?”“Ule wa mwisho kusainiwa”“Kheee haiwezekani jamani, wananifanyia ujinga sababu naumwa ila naamini muda utafika na mimi nitainuka tena na kutembea kama zamani bila maumivu yoyote huku nikifanya shughuli zangu zote”“Mungu ni mwema, tuwe na imani”Mara gafla baba Angel aliinuka na kuanza kutembea, kwakweli lile jambo lilikuwa ni la kustaajabisha sana machoni pa mama Angel. Mara gafla baba Angel aliinuka na kuanza kutembea, kwakweli lile jambo lilikuwa ni la kustaajabisha sana machoni pa mama Angel.Baba Angel aliongea kwa furaha huku akitembea tembea,“Jamani natembea, kweli Mungu katenda miujiza kwangu, kwasasa natembea”Mama Angel nae aliongea kwa furaha sana,“Mungu ni mwema sana, mume wangu umepata uponyaji. Oooh Mungu ashukuriwe kwakweli”Yani baba Angel alikuwa na furaha ya ajabu, yani ile furaha aliyokuwa nayo ilimfanya moja kwa moja aende chumbani kumpigia simu mama yake maana aliona ndio wa muhimu kwanza kabla ya yote, ila mkewe alimfata nyuma na kumwambia,“Kabla ya yote mume wangu tunatakiwa kumshukuru Mungu maana ni Mungu tu ametenda haya”“Sawa mke wangu, nina furaha sana ujue”Kisha mama Angel aliingia kwenye maombi ya kumshukuru Mungu kwaajili ya uponyaji kwa mumewe, ila tu hawakujua kama Erick na Erick waliita wenzao kwaajili ya maombi hayo pia.Baada ya yale maombi sasa, ndipo baba Angel alipompigia simu mama yake ambaye nae alifurahi sana kwa kupewa taarifa na mwane kuwa amepona kabisa mguu,“Jamani Erick, huwezi amini nilivyofurahi. Naomba nije tufanye tafrija fupi hata tule wote chakula cha mchana hapo kwako”“Hakuna shida mama”“Alika na baadhi ya watu wako wa karibu, unajua nina furaha sana yani siamini kabisa hiki ninachokisikia”“Ukiniona ndio utaamini zaidi mama yangu maana mimi ni mzima wa afya kabisa sasa”“Kwakweli Mungu ni mwema sana”Basi baba Angel alimaliza kuongea na mama yake, na muda huo akampigia dada yake yani alikuwa na furaha sana juu ya kupona kwake, basi akaanza kuongea na mkewe,“Yani kesho tu naenda ofisini, unajua sina maumivu yoyote yale niliyokuwa nayasikia. Huu uponyaji ni wa viwango vingine, siamini mimi nimebaki nastaajabu”“Mungu anaweza yote mume wangu, kesho tutaenda wote basi huko ofisini”“Ila kwa daladala, yani nina furaha hata natamani nitembee kutoka hapa hadi ofisini”Mama Angel alifurahi tu kwani aliweza kuiona furaha ya mume wake kwa wakati huo, akamwambia,“Sikia mume wangu, kesho tutaondoka wote hakuna tatizo tutaondoka wote kwa daladala kama usemavyo halafu mimi nitarudi nyumbani na badae nitakuja kukufata na gari lakini”“Aaaah hapo sawa, ila nina furaha sana jamani khaaa kweli natembea mimi!! Au na leo tutoke mke wangu?”“Jamani mume wangu, labda tuzunguke nyumba ila sio kutoka jamani!! Najua furaha yako mume wangu”Ile wazo la kuzunguka nyumba, baba Angel aliliafiki na muda huo huo wakainuka ili watoke nje na watembee kuzunguka nyumba yao.Muda huu Erica alikuwa akiwashukuru sana wakina Emmanuel kwa kuungana nao kwaajili ya kumuombea baba yao, kwahiyo walianza kuongea ongea pale kawaida ambapo sasa Erica alitaka kuwakaribisha ndani kwao ili waweze kusalimia wazazi wao ila muda ule ule Emmanuel alipigiwa simu, na alipomaliza kuongea nayo alimuangalia Emmanah na kumwambia,“Mama huyo anatupigia, kasema twende haraka sana”Basi wakawaangalia wakina Erica pale na kuwaomba ruhusa tu ili waweze kuwahi kwao, hawakuweza kuwakatalia na kuanza kuondoka nao ila walipokaribia getini Erica akasema,“Ila mama na baba walikuwa hapo sebleni tu, twendeni basi mkawasalimie”Waliongozana pamoja hadi sebleni ila wazazi wao hawakuwepo, Erica alimuuliza Vaileth ambaye alionekana kuingia jikoni muda ule,“Eti dada, mama na baba wako wapi?”“Sijui, mimi sijawakuta hapa”Basi Emmanuele akasema,“Tutawasalimia siku nyingine”Ilibidi tu wakubaliane nao na kuwasindikiza huku wakiongea ongea, basi Emmanah akasema,“Mtatupa taarifa sasa ya jinsi ilivyokuwa”“Sawa hakuna tatizo”“Namba ya simu je? Ngojeni niwape namba yangu ili kama mkikosa ya Emmanuel mnipigie mimi”Emmanah alianza kutaja namba yake, ambapo Erick alitoa simu yake na kuandika ile namba iliyokuwa ikitajwa na Emmanah, basi baada ya kuwasindikiza kidogo waliagana nao huku wakipanga siku nyingine kwenda na pia kuwakaribisha wakina Erica nyumbani kwao ili na wao wapate kufahamu wanapoishi.“Asanteni sana, ipo siku tutafika huko hakuna tatizo”Waliagana pale, halafu wakina Erica walirudi nyumbani kwao.Erica na Erick walipoingia tu wanamuona baba yao anatokezea na mama yao huku wakiwa na furaha sana kwani baba yao anawapa ushuhuda na watoto wake kuwa amepona, hilo jambo linawafurahisha sana Erica na Erick ingawa hawakumwambia baba yao kuwa walikuwa wakifanya maombi ili apone ila walifurahi sana kwa jambo lile, na moja kwa moja Erick alivyoingia ndani kwake tu alianza na ile namba ya Emmanah sababu ndio ilikuwa juu na kuwapa ushuhuda wa baba yao kuwa amepona,“Jamani, baba Amepona na kwasasa antembea vizuri kabisa”“Oooh hiyo ni habari njema sana, kwakweli Mungu ni mwema”“Tumefurahi sana, asanteni sana”Erick alivyomaliza kuongea na simu, Erica nae alikuwepo pale chumbani kwa Erick na kuendelea na furaha yake,“Umewaambia eeeh!!”“Ndio, wamefurahi sana pia, kweli kila kitu ni imani. Nimefurahi sana, wewe Erica ni mtu mwingine kabisa”“kwanini?”“Ulifikiria nini kwanza kabla ya haya yaliyotokea?”“Nilikumbuka ya kwamba kila kitu kinafanyika kwa imani, basi siku niliyokutana na Emmanuel nikawaza kuwa hatuwezi kuungana nae na kufanya pamoja maombi? Nilipowaona tena njiani na pacha wake ndio ikabidi niwaombe tena na tumefanikiwa kwa hili”“Aaaah hongera sana, je wazazi hatutawaambia hili lilolofanyika”“Wala tusiwaambie ila watajua tu, yani wewe tulia halafu utaona, baba na mama watajua wenyewe na wao ndio watatuambia sisi”Basi Erick hakuwa na cha ziada cha kuongezea maana alikuwa na furaha, kisha kila mmoja sasa alielekea kwenda kufanya mambo mengine.Usiku huu wakati Erick akijiandaa kulala, kuna ujumbe uliingia kwenye simu yake ukitoka kwenye ile namba ambayo Emmanah alisema ni yake,“Mambo vipi Erick? Ni Emmanah hapa, baba anaendeleaje?”“Kwakweli anaendelea vizuri tunamshukuru Mungu kwa hili, tumekula nae vizuri na wameenda vizuri kulala”“Oooh hiyo ni habari njema, kwakweli nimefurahi sana. Mungu ni mwema”“Amen”“Ila zaidi ya yote nimefurahi sana kukufahamu”“Hata mimi nimefurahi kukufahamu pia”“Basi tuwe tunawasiliana Erick, nimejikuta napenda sana kuwasiliana na wewe. Nimekufahamu leo ila nimefurahi sana kukufahamu, nadhani Mungu alikuwa na lengo jema kutukutanisha. Naweza kukupigia simu muda huu?”“Piga tu hakuna tatizo”Basi baada ya muda kidogo simu ya Erick iliita ambapo aliipokea ile simu na kuanza kusikilizana nayo, sauti ya Emmanah ilikuwa kwa chini sana kiasi kwamba lazima amsikilize kwa makini sana,“Unajua nataka kulala muda huu, ila nikajisemea kuwa nikupigie simu kwanza. Au nimefanya vibaya?”“Hapana, halafu sikujua kama wewe ni muongeaji mzuri hivyo kumbe wewe ni muongeaji!! Nakumbuka ulikuwa unakaa kimya muda wote”“Mimi huwa mara nyingi hadi mtu nimzoee sana, ila mimi ni muongeaji mzuri tu. Hata kukutafuta wewe, nimejitahidi sana kwani huwa naogopa kuwasiliana na watu wengi, yani mtu pekee ambaye huwa nawasiliana nae ni Emmanuel tu sababu ndio ananifahamu vizuri mimi”“Aaaah sawa nimekuelewa, usiku mwema”“Kheee mbona haraka hivyo, unaniaga kabla hata sijakuaga jamani!! Mimi bado nataka tuongee”Erick alishangaa kidogo kwani hakuona kama ana mazongezi ya ziada ya kuongea na huyu Emmanah ila aliongea nae hivyo hivyo kuhusu mambo mbalimbali hadi alijikuta akichelewa sana kulala, na iliwezekana pale simu ya Emmanah ilipoisha muda wa maongezi, yani Erick alishukuru kwakeli na kuamua kulala ila muda ulikuwa umeenda maana ilikuwa ni saa nane usiku.Kulipokucha kama kawaida, Erick aliamka na kujiandaa kwaajili ya kwenda shule ila alikuwa na usingizi kiasi kwani alichelewa sana kulala, basi hivyo hivyo alijitajidi na kwenda shule.Baba Angel kama ambavyo aliongea na mke wake leo, walijiandaa vizuri kabisa na moja kwa moja kuondoka kwenda kupanda daladala na kwenda kwenye ofisi ya baba Angel kama ambavyo walipanga, kwakweli baba Angel alikuwa na furaha sana kwa siku hii na kuongea mambo mengi sana na mke wake,“Yani natembea huku siamini kama ni mimi niliyekaa chini miezi mingapi sijui, siamini kabisa”“Amini tu, Mungu ni mwema halafu mahafali ya Angel yanakaribia”“Oooh wow, nimebata na bahati ya kwenda kuudhuria na mahafali ya binti yangu kipenzi. Hii ni furaha sana kwangu. Ila tunastahili pongezi kwakweli, mtoto anamaliza kidato cha sita sasa tumekuza sana”“Na kweli tumekuza, mwingine amemaliza na kutupatia zawadi ya ujukuu. Jamani Junior mambo yake!!”“Hivi bado hamjamwambia ukweli eeeh!!”“Tumesema hatumwambii lolote, mwache tu amalize vizuri mitihani yake, halafu akirudi hapa nyumbani tumpatie zawadi yake ya kumaliza kidato cha sita, naamini atapendezewa na hii zawadi ya mtoto au ndio ataanza kuruka futi mia kama kawaida yenu wanaume”Baba Angel alicheka na kusema,“Hawezi kukataa bhana, kwanza mtoto kafanana nae halafu kila kitu kipo wazi”“Nimesema na atake asitake atamuoa huyo huyo Vaileth hata asitutanie. Kale kabinti huwa nakahurumia sana ujue, kwanza ana mtoto tayari ambaye haeleweki baba maana baba wa mtoto alishakimbia majukumu yake, halafu apeleke mtoto mwingine kwao ambaye baba haeleweki jamani!! Aaaah sio nzuri, mimba yenyewe kapatia kwetu, yani Junior atake asitake ataoa tu huyu mwanamke”Baba Angel alicheka tu na kusema,“Najua ukiamua umeamua, yani Junior kama alijua kwa huyu Vai atapita kama kwa Daima alivyopita basi kakosea namba maana naona mama mwenye nyumba umecharuka, hutaki ujinga kabisa. Ila kweli yule binti wa watu ni mpole, na akionekana anazaa zaa hovyo watampa sifa mbaya ya umalaya wakati binti katulia tu. Msumbufu ni kijana wetu, ila dada yako amekubali kuhusu hilo?”Leo ndio mama Angel alimsimulia mumewe kuhusu mama Junior alivyokutana na Linah, yani baba Angel alicheka na kusikitika kwani mambo aliyokuwa anayafanya Linah yalimsikitisha kwakweli.Basi walifika ofisini na baada ya muda kidogo mama Angel alimuacha mumewe pale ofisini halafu yeye akaondoka zake kurudi nyumbani kama ambavyo walikuwa wamepanga kufanya hivyo.Basi baba Angel alipokelewa vyema tu pale na wafanyakazi wake, ambao walionekana kufurahi sana kwa bosi wao kurudi tena kazini kama zamani, kisha baba Angel alianza kupitia faili zake ofisini kwake kwanza maana ni muda mrefu hajafika humo.Muda kidogo, alienda yule bibi muuza matunda na kufurahi sana kumuona baba Angel kisha alimsalimia na kumwmabia,“Nilikuja na kumkuta kijana wako, nilijua ni wewe upo kumbe ni yeye. Hongera sana, una kijana mchapakazi sana nimempenda”“Asante”“Ila kijana wako kafanana sana na mwanangu”“Mmmh kafanana na mwanao tena!! Mwanao gani?”“Mimi nina mtoto anaitwa Juli, kwasasa ni mtu mzima ila mwanangu yule hajabahatika kuwa na mtoto. Mara nyingi anabeba mimba zinatoka, utakuta anajifungua ila watoto bahati mbaya, yani mwanao kafanana na mwanangu hadi raha. Nilimwambia hata siku aliyokuja hapa kuwa kafanana sana na mwanangu, nikamuomba nimuite mjukuu wangu”“Duniani wawili wawili”“Ni kweli kabisa, duniani wawili wawili”“Kwani huyo mwanao yuko wapi kwasasa?”“Unafikiri ana maisha mazuri basi!! Yani yupo yupo tu. Yupo huko mkoani anafanya kazi sijui kwenye shirika gani, yule nae alijikatia tamaa ya maisha kabisa, huwa anasema anatafuta hela ya kula tu basi maana atafute hela nyingi ya nini wakati hana wa kumuachia urithi!! Mwanangu kajikatia tamaa yule, yupo yupo tu”Kwa muda huu baba Angel alikuwa na kazi nyingi sana, basi akamwambia huyu bibi kuwa wataongea habari zile kwa siku zingine maana alikuwa na kazi nyingi sana,“Ila bado nakupa hongera, kama kijana umepata, kwanza ana heshima halafu ni mchapakazi kama wewe”“Haya, nashukuru”Yule bibi aliinuka huku akimuangalia sana baba Angel ambaye aliendelea na shughuli zake tu, yani baba Angel toka ile mikasa ya kupewa sumu basi alijikuta hapendi kutumia muda mrefu sana kuongea na huyu bibi ukizingatia alimuamini sana ila bibi huyu aliweza kurubuniwa kirahisi kabisa na mama Sarah.Mama Angel akiwa njiani akielekea nyumbani kwake, maana aliposhuka kwenye daldala aliamua kutembea tu kuelekea nyumbani kwake, ila kuna mtu alimuita na kumsalimia, alipomuangalia mtu huyo alimkuta ni Elly, ikabidi asimame na kuanza kuongea nae,“Mbona siku hizi huji nyumbani Elly? Hujui kama mimi ni shangazi yako!!”“Tatizo hampo wazi kwangu, siambiwi vizuri, ni shangazi yangu sababu yule anayesema ni baba yangu ni ndugu yako, sasa mbona mama anakataa kumfahamu baba yangu?”“Ukikua zaidi utaelewa Elly, hiyo ni kawaida kwa wanawake wengi sana, ila kaa ukijua kuwa mimi ni shangazi yako na yule ni baba yako”“Haya nashukuru, ila nafurahi kukuona leo ili nikupe huuu ujumbe”“Eeeh ujumbe gani huo?”“Ni hivi, jana nilipigiwa simu na Sarah, alidai kuwa anahitaji sana kuongea na wewe ila hakuwa na mawasiliano yako”“Mmmh nipe namba zake tafadhari”Elly alimpa mama Angel namba zile za Sarah, kisha mama Angel alimsihi Elly kwenda tena kuwatembelea kisha alimwambia na habari ya baba Angel kupona,“Mwambie mama yako kuwa baba Angel amepona na kwasasa anatembea vizuri tu”“Aaaah hiyo ni habari njema sana, nitampa huo ujumbe. Asante sana”basi mama Angel aliagana na Elly na moja kwa moja yeye kuelekea nyumbani kwake.Mama Angel alipofika tu nyumbani kwake, muda huo huo aliamua kumpigia simu Sarah kwa ile namba aliyopewa na Elly ili aweze kuzungumza nae, muda mfupi ile simu ilipokelewa na mama Angel kuanza kujitambulisha kama ambavyo Sarah alimzoea kumuita,“Mama Erick anaongea hapa, hujambo Sarah!”“Nafurahi sana umenitafuta, nimechoka kuishi na mama”“Tatizo ni nini kwani Sarah?”Sarah aliongea huku akilia,“Natamani kumtoroka mama ila sijui nitakapoelekea”“Aaaah usiseme hivyo Sarah wakati hapa nyumbani kwangu papo, unaweza kuja hapa. Kwani mko wapi na mama yako kwasasa?”“Siwezi kutaja maana mama akinisikia hata kwa bahati mbaya atachukia sana, kwa kifupi mama yangu kabadilika sana yani simuelewi kabisa mambo yake”“Sasa sikia Sarah, naomba uje tu moja kwa moja huku nyumbani. Hata ukipata usafiri mwambie huyo mtu akulete halafu mimi nitamlipa, jitahidi ufanye hivyo”“Sawa nashukuru sana”Mama Angel alijua wazi kuna tatizo kubwa sana lipo kati ya Sarah na mama yake, ingawa alijua wazi kuwa ile ya yeye kumchukua Sarah itakuwa tatizo kwa mama Sarah ila bado alihitaji kufanya hivyo maana moyo wa imani ulimfikia kila alipoongea na Sarah na kuona ile hali ya kilio cha Sarah.Mama Angel kama alivyopanga, jioni yake anaenda ofisini kwa mumewe na kumchukua na kurudi nae nyumbani huku wakiwa na tabasamu, leo walipofika nyumbani tu walimkuta Sia yupo pale maana alipopata taarifa kuwa baba Angel amepona aliamua kwenda kumuona tu, kwahiyo waliongea ongea pale kisha waliagana nae.Usiku ule, mama Angel aliongea na mumewe kuhusu Sarah, na baba Angel alikubali vizuri kabisa,“Ni bora aje hapa tuishi nae maana najua hata huyo Manka atafika tu hapa na tutajua mipango yake yote”“Ndio, itakuwa rahisi sana kufahamu mengi yahusuyo kwa Manka”Basi waliongea mambo mengi sana, na toka siku hiyo mama Angel ndio alikuwa akifanya jukumu la kumsindikiza mumewe kazini maana alikuwa haamini kwa mume wake kwenda mwenyewe.Siku hiyo, mama Junior alifika tena nyumbani kwa mama Angel kwa lengo la kumuona mjukuu wake, alivyofika pale alimkuta tu Vaileth na mtoto wake pamoja na Ester yani mtoto mdogo wa mama Angel, basi aliuliza pale,“Baba Angel na mama Angel wameenda hospitali nini mbona hawapo leo?”“Hamna, mama kamsindikiza baba kazini”“Oooh kumbe kaanza kwenda na kazini, Mungu amsaidie shemeji yangu apone kabisa”“Mbona ameshapona tayari, anatembea vizuri kabisa kwasasa”Mama Junior alishangaa sababu alikuwa hajui halafu mdogo wake hakumwambia habari hiyo dada yake, basi akamchukua mjukuu wake na kumuangalia huku akizidi kumuona kuwa kafanana na Junior,“Jamani huyu mtoto kila siku anazidi kuwa Junior mtupu, hivi mmempa jina gani?”“Mama wa humu ndani kasema tumuite Joseph, jina la babu yake”“Oooh hilo ni zuri sana, jina la kipenzi baba yangu. Mungu amrehemu, sijui Erica kafikiria nini jamani dah!! Nimefurahi sana kusikia hivyo. Ngoja nimlee vya kutosha baba yangu mie”Vaileth alikuwa akitabasamu, muda huu Ester alikuwa chini akila chakula hata mama Junior alipenda kwakweli kwani Ester alikuwa akila vizuri sana,“Hadi raha, kumbe Ester anakula mwenyewe!! Kweli wewe ni dada mlezi mzuri wa watoto ndiomana mdogo wangu hataki kukuondoa hapa kwake. Upo vizuri sana”Vaileth alitabasamu tu na waliendelea kuongea mambo mengi na mama Junior ambaye kwasasa alikuwa ni mama mkwe wake.Basi mama Junior aliamua kumuaga Vaileth na kuondoka zake maana kuna mahali alikuwa akihitajika,“Nitampigia simu badae mama yenu, nikisahau basi naomba umkumbushe anipigie. Au akirudi tu mwambie anipigie”“Sawa mama, hakuna tatizo”Kisha mama Junior akaondoka zake kuelekea alipokuwa anatakiwa kupitia kabla ya kurudi nyumbani kwake.Mama Junior akiwa njiani, akashikwa bega, kugeuka akamuona Linah ambaye alimsalimia,“Habari mama mkwe”“Hebu jiheshimu basi, mimi siwezi kuwa mama mkwe wako”“Huwezi kivipi wakati nipo na mwanao!”“Hivi chukua nafasi yangu, yani wewe uwe mimi halafu mimi niwe wewe ungekubali?”“Kwanini nikatae ikiwa watu wanapendana? Upendo wa kweli hauangalii umri bali ni ule upendo wa dhati kutoka moyoni, kwakweli mimi na Junior tunapendana sana hilo huwezi kupinga hata ufanyeje hapa Junior habanduki”“Dah! Hujielewi ndugu yangu”“Na sijielewi kweli ujue, haya tuachane na hayo. Jiandae kupokea ujukuu maana kwasasa nina mimba ya Junior”“Unasemaje!!”“Hujanisikia au hujanielewa? Jiandae kupokea ujukuu maana nina ujauzito wa Junior, kwa kifupi Junior ndio baba wa mwanangu mtarajiwa”Yani mama Junior alihisi hata kichefuchefu kuongea na huyu mtu, kwani aliondoka tu bila ya kusema chochote na kumuacha Linah akiwa anacheka sana.Mama Angel leo mumewe alivyorudi nyumbani, ilibidi waongee tena kuhusu habari ya Sarah,“Hivi kwani umewasiliana nae tena?”“Ndio, leo nimewasiliana nae tena, kasema atakuja tu. Alikuwa na mitihani kaona bora amalizie kabisa ndio aje”“Aaaah hapo nimemuelewa, kwahiyo uhakika wa yeye kuja upo ila hajataka kusema alipo mama yake?”“Yani hilo kakataa kabisa, sijui ni nini ila najua Manka anajificha sababu ya haya mambo aliyokufanyia wewe nadhani anahisi tunaweza kumfungulia kesi”“Ila kunikalisha nyumbani mwaka mzima, kweli nina haki ya kuwafungulia keshi hawa watu jamani, wamerudisha nyuma vitu vyangu vingi sana. Ila sasa Mungu alivyomwema, yani kila kitu Erick amekifanya kwenye mstari ingawa alikuwa akisoma. Kila siku nitashukuru kwa kumpata mtoto huyu katika maisha yangu”“Hivi Erick kafata akili zako au akili zangu?”Baba Angel akacheka na kusema,“Kafata akili zangu yule”“Mmmh ila asifate matendo yako”“Kwanini sasa?”“Unaona matendo yako yalikuwa sawa?”“Lakini si nimebadilika!”“Erick umebadilika na maombi wewe, muda mwingi nilikuwa nakesha kwa maombi ili mume wangu usitamani hovyo wanawake wengine na hadi leo unahisi kamavile nimekuroga, mimi nilikuwa namuomba Mungu ubadilike. Unadhani bila maombi nyie wanaume mnawezekana”“Aaaah jamani mke wangu unaanza kunifananisha mimi na hao wanaume wengine wasiokuwa na akili? Kuna wanawake wanakesha makanisani, wanalia hadi jasho ila mwanaume habadiliki wala nini, utakuta ni anakunywa pombe hadi anazima na bado anabadili wanawake kama nguo, na mwanamke anaomba hadi anapata homa, kwahiyo ukikuta mwanaume kabadilika basi naye amechagua kubadilika. Ila hata hivyo nashukuru mke wangu maana maombi yako yameniokoa kwa vingi”Mama Angel alicheka na kusema,“Unamkumbuka Bahati alivyokuwa akinisumbua mimi hadi sina amani wala raha nikimuona, basi Fetty kamfanyia maombi yule, katoa na sadaka kwaajili yake, Bahati katulia tuli wala ahangaiki tena nadhani huwa hanitamani tena mimi, kwahiyo hata kama unapenda kubadilika ila maombi nayo yanasaidia sana maana bila maombi nyie wanaume mnavutwa sana mara mwingine akufanyie dawa, mwingine akufanyie uchawi kwahiyo lazima tuombe”“Hata mimi huwa naomba sana Mungu akulinde mke wangu”Wakawa wanacheka tu huku wakiendelea na maongezi yao.Usiku wa leo, Erick akiwa chumbani kwake akijiandaa kulala muda kidogo aliingia Erica mule ndani na kuanza kuongea nae maana alikuwa akisikia wazazi wake wakiongea kuhusu habari za Sarah,“Nasikia Sarah anakuja hapa nyumbani kuishi na sisi”“Umesikia wapi habari hizo?”“Nimesikia baba na mama wakiongea kuhusu hiyo kitu”“Mmmmh hujaacha tu mambo yako”“Naomba simu yako mara moja Erick”Erica aliamua kubadili mada na kumuomba Erick simu yake, ila alipoichukua tu muda huo huo kuna ujumbe uliingia kutoka kwa Emmanah,“Nakupenda sana Erick”Erica alimuangalia sana Erick na kumfanya Erick amuulize,“Tatizo nini Erica?”Erica nae alijibu kama ujumbe wa kwenye simu ulivyoingia,“Nakupenda sana Erick” Erica aliamua kubadili mada na kumuomba Erick simu yake, ila alipoichukua tu muda huo huo kuna ujumbe uliingia kutoka kwa Emmanah,“Nakupenda sana Erick”Erica alimuangalia sana Erick na kumfanya Erick amuulize,“Tatizo nini Erica?”Erica nae alijibu kama ujumbe wa kwenye simu ulivyoingia,“Nakupenda sana Erick”Kwakweli Erick alihisi moyo wake kuripuka kwa muda huo, sio kwamba hajawahi kusikia hili neno akiambiwa na Erica ila leo lilionekana kutoka kwa tofauti sana yani tofauti na siku zingine zote, Erick alimuuliza tena Erica,“Unasemaje Erica?”Erica nae alirudia ujumbe ule ule wa kwenye simu,“Nakupenda sana Erick”Yani Erick alimfata Erica karibu na kumkumbatia sana, yani hata Erica alikuwa akishangaa sababu hakutegemea kuwa baada ya kusema vile angemfanya Erick kuwa na furaha sana.Yani Erick alimkumbatia Erica kwa muda mrefu sana huku akimwambia,“Erica nakupenda sana pacha wangu, tena sana nakupenda naomba unipende hivyo hivyo”Erick alianza kumbusu Erica, ila Erica alimsukumia pembeni na kumwambia,“Weee mjinga unadhani ni mimi ndio nimekwambia kuwa nakupenda sana!”Hapo Erick alikaa kimya kwa muda, kisha Erica alimpa Erick simu yake na kumwambia,“Chukua huo upuuzi wako”Halafu Erica alitoka na kuondoka zake kuelekea chumbani kwake.Ndipo Erick alipochukua simu yake na kuangalia vizuri na kuona ule ujumbe ulikuwa umetoka kwa Emmanah, yani alishindwa hata kujibu ule ujumbe kwani muda huo huo aliweka simu pembeni na kuamua tu kujilaza kwani hakutaka hata kuwasiliana na Emmanah.Erick alipoamka asubuhi ya leo, cha kwanza kabisa aliona ni vyema kwenda chumbani kwa Erica kwani aliona ana kila sababu za kumuomba Erica msamaha ukizingatia ni kweli amemkosea, basi aliingia na kumkuta Erica amejiinamia tu na kusalimia pale huku akimwambia,“Erica naomba unisamehe, nisamehe sana sikujua chochote ila naomba unisamehe”“Ila kwanini unaomba msamaha?”“Sikujua kama kuna ujumbe toka kwa Emmanah kwenye simu yangu, naomba unisamehe sana”“Kwani kukiwa na ujumbe toka kwa Emmanah ndio unapaswa kuniomba msamaha? Huyo Emmanah si atakuwa wifi yangu au ni vipi?”Erica aliongea huku akitazama chini, Erick nae alipumua kiasi na kumwambia Erica,“Hapana hawezi kuwa, sijui nikwambiaje Erica ila naogopa kusema. Sijui hata naanzaje kukueleza”Erica alimuangalia Erick na kumwambia,“Nadhani tunahitaji tupate mahali na tuweze kuzungumza kwa upana zaidi, au unasemaje?”“Ni kweli, nina mengi ya kusema ila huwa nashindwa maana mdomo wangu unakuwa mzito sana”“Twende ufukweni, na huko tutazungumza mengi. Leo ni Jumamosi, tukiwaomba ruhusa wazazi wetu watakubali tu ukizingatia ni siku nyingi hatujaenda kutembea”“Sawa ni kweli, ngoja nikaongee na baba nadhani atanielewa”“Ngoja mimi nitamwambia mama hata usijali, najua kwenye kujieleza sio mzuri sana wewe. Naomba tukifika huko uwe huru niambie chochote kile unachohisi nami nitakwambia”Erick alikubali tu maana kiukweli alihitaji kuongea mambo mengi sana na Erica.Mama Junior akiwa nyumbani kwake akiendelea na shughuli zake, kuna simu iliingia kwake na moja kwa moja aliipokea na kuanza kuongea nayo,“Habari mama mkwe”“Nani wewe?”“Kheee, mimi ni mkweo Linah au una wakwe wangapi?”“Khaaaa hivi wewe mmama huchoki? Kwanza nani kakupa namba yangu?”Linah alisikika akicheka, na kusema,“Kabisa unajikakamua kuuliza swali kama hilo kweli!! Namba nimepewa na mume wangu kasema leo nikusalimie mama yake, unajua kuwa nipo nae huku!”“Nitolee balaa mie”“Nadhani huniamini”Mara ilisikika sauti ya Linah ikiita,“Junior mume wangu hebu njoo mara moja”Halafu ikasika sauti ya Junior,“Nipo hapa kipenzi changu”“Kuna mtu naongea nae hapa halafu haamini kuwa tupo wote, hebu mwambie ni jinsi gani unanipenda”Mara Junior akasema,“Nampenda sana Linah, nipo tayari kufa kwaajili yake”Halafu Linah akaongea kwenye simu,“Nadhani umesikia mwenyewe, mtoto ndio kashaganda, chezea mimi eeeh!! Hapa haambiliki wala hasikii anatamani kunioa hata leo, nasubiri tu amalize mitihani yote tutangaze ndoa. Najua utatuandalia zawadi nzuri sana”Mama Junior alihisi hasira sana na kukata ile simu, yani hata kazi aliyokuwa akifanya aliiacha na kukaa chini huku machozi yakimtoka na kujisemea,“Huyu huyu Junior nilimzaa mimi kweli au ana mama mwingine? Yani limeacha kujiandaa vyema kwa mitihani akiwa shuleni limeenda kwa mwanamke kweli!!”Muda huo huo akaamua kumpigia simu mdogo wake mama Angel ili kumwambia jambo lile angalau apumue kidogo,“Kwakweli mdogo wangu huyu Junior ananikosesha raha kabisa, sina amani mimi”“Sikia kitu dada, hata usipaniki wala nini. Tunatakiwa kufanya kitu pamoja”“Kitu gani hiko?”“Njoo nyumbani tuongee, nakwambia huyo Junior na huyo mama yake watakoma tu, hapa ni ndoa ya Junior na Vaileth, hiyo ndoa ya Junior na huyo bibi yake Linah hatuikubali wala hatuielewi hapa. Asitupande kichwani huyu mtoto”Basi alikata simu na kuanza kujiandaa ili kwenda kwa mdogo wake kuongea nae.Erica alimfata mama yake na kumuomba ruhusa ili yeye na Erick waweze kwenda kutembea ufukweni, cha kushangaza ni jinsi mama Angel alivyokubali kuwa waende tu hata muda huo,“Najua watoto wangu mmekaa sana nyumbani, mimi nawaruhusu kabisa na hela nitawapa. Nenda kamwambie Erick ajiandae mwende mkatembee huko ufukweni”Erica aliondoka akifurahi sana ila mama Angel alifurahi zaidi na kusema,“Afadhari jamani, sijui wamejuaje hawa watoto kwenda kutembea yani hapa angekuja dadangu tungeanza kujibana bana kuongea kwa kuhofia umbea wa Erica ila kwasasa ni huru kabisa tutapanga kila kitu hapa hapa nyumbani. Yani hawa na hela nawapa kabisa wakajaze mafuta kwenye gari waende huko wakazurule wee watakavyo”Baada ya muda Erick na Erica walikuwa tayari wameshajiandaa na kumfata mama yao ambaye aliwapatia pesa akasema waende kutumia na kuweka mafuta kwenye gari,“Hata hivyo najua kama wanangu mmefanya kazi kubwa sana, najua baba yenu angekuwepo hapa basi angetaka hata kuwaongezea pesa, ila natumaini hii ninayowapa itawatosha”Walimshukuru sana mama yao pale ambapo aliongezea,“Kama mkipungukiwa na hela basi Erick nipigie ili niwatumie nyingine kwenye simu”“Aaaah hii inatosha mama, mbona nyingi tu”“Haya, nawatakia matembezi mema”Basi Erick na Erica waliondoka zao, kisha mama Angel alimuita Vaileth kwanza na kuanza kuongea nae,“Vaileth mwanangu, sijawahi kukuuliza hili maana huwa tunaongea tu. Upo tayari kuolewa na Junior?”“Ndio mama nipo tayari”“Aaaah sawa kama ni hivyo basi kazi itakuwa rahisi sana hii”“Kazi gani kwani?”“Wewe tulia tu, subiri ndoa mwanangu”Vaileth alitabasamu tu kwani ile ilikuwa ni habari nzuri sana kwake.Erica na Erick walifika kwenye ufukwe waliohitaji kuwa na kutafuta mahali ambapo walikaa huku wamenunua vitu vitu vya kutafuna na kuanza maongezi yao, ambapo Erica ndio alianza kuongea,“Leo, Erick naomba utoe dukuduku lako lote la moyoni najua una mengi sana na usijisumbue kunificha lolote lile, nieleze kila kitu unachohisi kwenye moyo wako”“Hadi naogopa kujieleza”“Usiogope nileze ukweli ili nami nikwambie ukweli”“Ni hivi Erica, mimi najua kama wewe ni dada yangu tena ni pacha wangu ila tatizo lililopo ninapatwa na hisia tofauti sana juu yako yani najikuta nikitamani uwe mpenzi wangu wakati ni kitu ambacho hakiwezekani. Kuna siku niliwahi kukwambia kuwa mimi sitakuja kuoa katika maisha yangu sababu ninayempenda siwezi kumfanya awe mke wangu kwani ni dada yangu ambaye ndio wewe. Sijui nikueleze vipi Erica ila ndio hivyo, jana uliponiambia ile kauli kuwa unanipenda sana nilihisi kuchanganyikiwa kabisa, mwili wote nilihisi ukionyesha hisia za mapenzi juu yako. Ndiomana asubuhi nimekuja kukuomba msamaha kwani najua wazi kuwa nitakuwa nimekukwaza Erica, nisamehe sana”“Usijali kuhusu habari za msamaha, nimeshukuru kwa kuniambia ukweli. Ipo hivi, sijui ni nini ambacho huwa kinakuja katika akili yangu yani huwa najikuta nikikupenda sana kiasi kwamba sitaki mwanamke yoyote awe karibu na wewe, nikiona kuwa mwanamke anaanza kujisogeza kwako huwa naumia sana, ila swala linabaki kwanini inakuwa hivi wakati sisi ni ndugu? Yani huwezi amini ile jana baada ya ujumbe wa Emmanah nilijikuta nikikosa usingizi na kuanza kulia, hadi nilikuwa sijielewi, na kilichoniliza zaidi nikikumbuka ni ile hali uliyonikumbatia nayo ilizidi kunipa hisia ndiomana nilikutoa pembeni, kwakweli Erick sielewi pia”“Dah!! Mimi huwa naumia sana nikiona kuna vijana wanakufatilia. Ni kweli nilimkatia simu Emmanuel kwa kuhisi kwamba atakuhitaji kumbe haikuwa hivyo, yani yote hii ni sababu naumia sana juu yako Erica, sijui tatizo ni nini?”“Hapo kwenye tatizo ni nini ndio pa kujadili, mimi na wewe ni ndugu tena ni mapacha. Inawezekana kwa ndugu kujikuta katika mapenzi ila kama hawafahamiani kuwa ni ndugu, utakuta wamegundua badae sana ila tofauti na mimi na wewe, tumekuwa pamoja, tunajuana kuwa ni ndugu tena ni mapacha, kwanini tuwe na hisia za kimapenzi kati yetu?”“Sijui, ila mimi nakupenda sana. Hadi huwa najiuliza ni kwanini hairuhusiwi kwa ndugu kuwa pamoja kwenye mahusiano”“Sio hiruhusiwi ila ni heshima tu, ukiangalia hapa duniani binadamu wote ni ndugu kwahiyo ndugu hawawezi kuwa wapenzi sababu ya heshima tu na kuangalia mipaka ya undugu na mahusiano ya kimapenzi. Ila kwa mimi na wewe ni kesi nyingine, huwa nahisi kuna jambo ambalo sio sawa kati yetu”“Erica huwa unaota mambo mengi sana, je umewahi kuota chochote kuhusu sisi?”“Huwezi amini, katika ndoto zangu zote sijawahi kuota kuhusu mimi na wewe, natamani sana kujua ni kitu gani kimefanyika baina ya mimi na wewe hadi tunajikuta kwenye hali kama hii. Kwanini unitamani mimi wakati unajua wazi kuwa mimi ni dada yako!! Na kwanini mimi nikutamani wewe wakati najua wazi kuwa wewe ni kaka yangu! Hapa ndio kwenye tatizo, na ninashikwa na wivu balaa pale ninapokuona upo na mwanamke mwingine”“Sasa tunafanyaje Erica kwa hili?”“Tunatakiwa kuchunguza”“Ila nakuomba usiwe na mwanaume mwingine”“Dah!! Kweli hapa ni tatizo, tunaweza kuona ni kawaida ila ni tatizo na tusipoangalia tutafanya hata wazazi wetu watuchukie sana. Sikia Erick tusionyeshe chochote kwa yeyote, tuwe tu kawaida huku tukichunguza. Najua siku nitawabana mama na baba nao wataongea ukweli kuhusu jamabo hili maana imezidi sasa”Kwa maongezi haya, ilifanya moyo wa Erica na Erick kuwa huru sasa maana kila mmoja aliongea ukweli wa kile anachokihisi katika moyo wake na kuomba pale kuwa kila mmona ajitahidi kutokuumiza hisia za mwingine huku wakiendelea na uchunguzi maana Erica aliona kuwa jambo lile linahitaji kufanyiwa uchunguzi ukizingatia si rahisi kwa ndugu tena mapacha wa damu kujikuta kwa pamoja wameingiwa na hisia za mapenzi.Mama Junior alifika nyumbani kwa mama Angel na kuanza kuongea na mdogo wake, ambapo mama Angel alimwambia kwanza mama Junior kuhusu mpango alioufanya kuhusu Junior,“Sasa dada kwa hayo mambo ya Junior tunatakiwa kufanya juu chini amuoe Vaileth”“Atamuoaje sasa maana nina uhakika yule Linah akijua ni lazima atavuruga tu”“Sikia dada, mimi na wewe ndio tutaenda kwakina Vaileth kujitambulisha na mambo ya mahari tutashirikiana na kutoa. Kisha siku Junior anarudi nyumbani tu inakuwa ndio siku yake ya harusi, yani tutafatilia wanamaliza lini mitihani na kwenda kumchukua ili afunge ndoa na mwenzie”“Vaileth kakubali lakini?”“Unadhani anakataaje na mtoto kashazalishwa!!”“Sawa, je mila za kwakina Vaileth sio nyingi za kutusumbua?”“Hamna cha kutusumbua wala nini, kwanza tutaongea na Vaileth ili aongee na kwao waweze mupunguza masharti na iwe kwetu rahisi kwenye kumuozesha Junior. Yani Junior, atake ataoa na asipotaka ataoa”“Ila ni vyema kuwa na msimamo hivyo, yule mama kanichefua sana jamani, hadi nilikosa amani kabisa kabisa”“Ngoja tumuite Vaileth tunakamilisha kila kitu hapa”Mama Angel alimuita Vaileth pale na kuanza kuongea nae kuhusu sheria za kwao ambapo mwanaume akaitaka kuoa kwao ni kitu gani kinafanyika. Vaileth alianza kuwaeleza pale kisha mama Angel akamwambia,“Hatutaki haya mambo kuyavuta sana, tunahitaji yaende haraka haraka ili tuweze kufanya shughuli kwa wakati. Natumaini inawezekana kwenye kwa haraka, si unajua kwenu kulivyo mbali?”“Kwetu ni mbali ndio, ila mnaweza kwenda kwa kupitia shangazi, halafu mimi nitawapigia simu kule nyumbani kwetu. Siku ya mahali tu ndio ikaenda kule kwetu.”“Haya kwa shangazi yako sio mbali, tuandalie barua ya uchumba hapo tumpelekee leo leo halafu ongea nao huko wapange mahari upesi ili tuweze kwenda kutoa mahari hii wiki inayoanza tu.”Kwakweli Vaileth alifurahi sana kusikia jambo lile, na moja kwa moja alienda kuandaa barua ya uchumba kwa niaba ya Junior ambaye bado alikuwepo shuleni.Alipomaliza kuandaa ile barua, Vaileth aliwapelekea na kuwaelekeza kwa shangazi yake na kuwapa mawasiliano yake.Waliisoma na waliona ni jinsi gani Vaileth ameweza kujiongeza kwenye ile barua, kisha muda huo huo mama Angel alienda kujiandaa vizuri na kutoka kuelekea kwa shangazi yake Vaileth.Mama Angel na mama Junior walibahatika kufika nyumbani kwa shangazi wa Vaileth ambaye aliwakaribisha vizuri tu sababu alishapigiwa simu na Vaileth, kwa muda huu shangazi alijisahaulisha yote ambayo yaliwahi kutokea kuhusu yeye kwenye nyumba ya mama Angel wakati amepeleka dawa zake pale.Basi alianza kuongea nao kuhusu taratibu zote za kwao na kila kitu kuanza kujitambulisha basi waliongea nae tu wafanye haraka kisha waliamua kuaga na kuondoka zao ila ile habari ilikuwa ni nzuri sana kwa shangazi wa Vaileth yani aliwasindikiza huku akiwa na furaha kubwa sana.Basi mama Angel na mama Junior waliongozana, wakiwa kwenye gari walianza kuongea kuhusu hilo swala walilolianzisha,“Hivi wakishataja mahari itakuwaje?”“Itakuwaje vipi dada? Tutalipa tu”“Sasa wakitaja kubwa sana?”“Wataje kubwa sana kwa misingi ipi? Kwanza kumbuka hawajui kama binti yao ana mtoto maana nishaongea na Vaileth kuwa hilo swala afanye siri kwanza kama alivyofanya kwetu, najua wazazi wa kiafrika wataanza kudai faini ya mtoto”“Sasa itakuwaje kwenda kutoa mahari? Huyo Vai si tutaenda nae?”“Twende nae wapi? Hao wazazi wake wana shida balaa, nadhani huwajui tu. Tukienda kutoa mahari utaona watakavyofurahi, yani hapa ni kumpanga Vaileth tu na kumuweka kwenye mstari. Anataka kuolewa, anajua kabisa mwanaume ni mwanafunzi, hiyo mahari kubwa anakubaliana na kwao kwa misingi ipi? Nitaongea nae na nitampangia kabisa mahari ya kusema kwao, hapa kwenyewe tumetoka kwenye matatizo, hizo hela nyingi tunaziotoa wapi? Mambo mengine watatafuta na mumewe wakiwa ndani ya nyumba yao. Sisi tutafanya kwa upande wetu na kupumzika”“Hapo nimekuelewa mdogo wangu”Njiani mama Junior alishuka maana alitaka tu kuonganisha kwenda kwao.Mama Angel alivyofika getini ndipo akakutana na Sarah naye akiwa anashuka kwenye gari ambalo lilimleta, basi mama Angel alishuka na kumfanya Sarah kumuona, kwakweli Sarah alimkimbilia huku akilia na kumkumbatia sana mama Angel, basi alimbembeleza pale na kuongea nae mawili matatu, kisha alitakiwa kumlipa yule dereva aliyemleta Sarah,“Unamdai pesa ngapi?”“Ni elfu laki moja mama”“Duh!! Sarah umetokea wapi jamani!! Inaonekana ni mbali sana eeeh!! Ila sio tatizo, twende ndani nikamletee hela yake”basi mama Angel aliingia ndani na Sarah kisha alitoka na kumpatia yule dereva hela yake na kurudi ndani.Mama Angel alianza maongezi na Sarah sasa kuhusu alipotoka ila Sarah alikuwa akilia tu,“Siku nilipomsikia mama akiongea kwenye simu na kusema kuwa wamempiga risasi baba Erick nilijikuta nikiumia sana moyo wangu, kwanini mama kafanya kitu cha namna hii? Ingawa kwenye ile simu alikuwa anasema kuwa hataki iwe vile ilivyokuwa ila ndio ilishatokea tayari”“Pole sana, yani mama yako sijui huwa anawaza kitu gani, kwakweli akili ya mama yako ina matatizo sana”“Sijaweza kuendelea kukaa nae, nimeamua kuondoka nyumbani, nitarudi kama akija tu kuomba msamaha mahali hapa”Ila Sarah alionekana ana mengi sana ya kuzungumza ila muda huo alikuwa na hasira sana kiasi kwamba alikuwa hazungumzi vizuri, basi mama Angel ilibidi amuandalie tu kile chumba ambacho walikuwa wamemuandalia Elly aweze kupumzika mule na aweze kulala kwenye kile chumba.Erick na Erica waliamua kurudi nyumbani muda huu ila walipanga pamoja mambo mengi sana ikiwa ni pamoja na kutokutiana kwenye tamaa maana hakuna aliyekuwa akijua kuna tatizo gani kati yao, na pia hawakutaka kuumizana moyo maana kila mmoja kajua ni tatizo gani linamsumbua mwingine.Erick alimuahidi Erica kuwa atamtafutia zawadi,“Naomba uikubali zawadi yangu, kesho nitatoka kwenda kule dukani kwetu. Nitakujia na zawadi natumaini utaipenda”“Hiyo zawadi inamaana ipo tayari au ni kitu gani? Umeiongea tu muda huu au ipo?”“Hamna, ni kesho ndio nitaitafuta, haipo wala nini ila kesho nitainunua na kuja nayo”“Haya nimekumbuka kitu ni kuhusu Sarah, akija nyumbani kweli je!”“Hakuna tatizo Erica, yote nadhani tumemaliza, kwani kuna tatizo? Kumbuka Sarah nae ni ndugu yetu, mama alisema”“Nakumbuka, halafu Sarah nae alikuwa akikutaka, mweeeeh ukoo una nini huu? Kuna tatizo lazima”“Ni kweli, halafu Sarah na Elly wakapeana mimba na wote ni ndugu zetu”“Mmmmh kweli kuna tatizo mahali, ila mimi na wewe isifikie huko”“Haiwezi kufikia sababu kila kitu tumekiweka wazi baina yenu, ni swala tu la kutafuta tatizo lipo wapi. Ila sijui kwanini wanazuia mahusiano ya kimapenzi baina ya ndugu!”Erica alicheka sana na kisha kuendelea na mada nyingine, ila aliuliza jambo,“Ila wana haki ya kuzuia, unajua haileti maana eti, maana mtoto atakuwaje ikiwa wazazi ni ndugu? Hili ni pepo tunatakiwa kulikataa kabisa”Waliendelea na mazungumzo mengine hadi walipofika nyumbani na walipofika tu walimkuta Sarah maana muda huo alikuwa akila chakula, walimpokea vizuri tu na kumkaribisha vizuri.Leo Erica hakuwa na tatizo lolote lile kwa Sarah, hata Sarah aliweza kugundua kuwa Erica amebadilika kwa kipindi hiki.Usiku wa siku hii, Sarah alienda chumbani kwa Erica na kumuomba walale pamoja ingawa anajua kwa siku za nyuma haikuwezekana hiyo kitu ila kwa leo Erica alikubali tu na walilala wote hadi asubuhi bila ya tatizo lolote lile.Kulipokucha tu, ni Erica ndio alimwambia Sarah,“Leo si tutaenda Kanisani eeeh!!”“Aaaah kumbe ni siku ya ibada leo!! Tutaenda basi”“Hadi hujui kama leo ni Jumapili!! Kweli kuna tatizo kwako”“Yani kwenye familia yetu hakuna Jumapili wala Ijumaa”“Kumbe!! Ila nilisikia wewe hupendi Ibada”“Hapana, ila ni malezi niliyopewa na mama hatuna kawaida ya kwenda Kanisani. Ila mimi sina nguo za kuvaa huko ibadani maana mavazi yangu nayajua mwenyewe”“Usijali, utavaa za kwangu mbona miili yetu inaendana tu”Basi waliongea kidogo na kuanza kujiandaa, kisha waliweza kuondoka kwa pamoja na kuelekea huko kwenye ibada.Erick alipotoka tu, moja kwa moja alienda dukani kwa baba yake ili kuangalia ile biashara ya duka inaendaje, alifika pale na kufanikisha yote ambayo alitakiwa yeye ndio ayafanikishe, kisha alitaka kuondoka ila kabla ya kuondoka alifika Juma mahali pale na kumsalimia kisha kuanza kuongea nae, ambapo Juma alimchukua Erick pembeni na kumuuliza,“Samahani Erick, yale matunda ya siku ile uliyatoa wapi?”“Kwanini unaniuliza hivyo? Yalikuwa na tatizo kwani?”“Hapana ila yamenikumbusha mbali sana, nakumbuka miaka ya nyuma alikuwepo mama yangu ambaye alikuwa akinitengenezea matunda kwa kunichanganyia vile na alisema kuwa kile ni kitu kilichopendwa sana na babu yangu. Kwakweli Erick nazidi kupata ushahidi kuwa wewe ni damu yangu”“Unahisi nimetengeneza mimi yale matunda?”“Ndio, niliambiwa kuwa wewe huwa huli kitu hovyo, kwahiyo ninahisi kwa asilimia zote kuwa ni wewe ndiye uliyetengeneza yale matunda”“Hapana, yale matunda nimepewa na bibi mmoja hivi yupo kule kwenye ofisi ya baba. Labda kama yule bibi ndio mama yako”“Aaaah kwa bahati mbaya mama yangu alishakufa siku nyingi sana”“Basi yule bibi utakuwa na undugu nae sababu ni yeye ndio aliyenipa yale matunda, lazi ma atakuwa ndugu yako tu ndiomana umehisi hivyo”Juma alifikiria kiasi na kusema,“Unachokisema kinauwezekano ila bado nahisi kuna kitu hapa, kwanini hayo matunda ni wewe ndio unipatie mimi! Nishaenda ofisini kwa baba yako mara nyingi tu, sijawahi kuonana na huyo bibi na hata mara moja hajawahi kuleta matunda hayo mule ofisini kwa baba yako. Lazima kuna kitu ndiomana umeniletea wewe, unaona kama huyo bibi amekupa ila kulikuwa na lengo madhubuti kuniletea ujumbe mimi”“Ujumbe gani sasa?”“Kuwa wewe ni damu yangu”“Unajua unanikumbusha mwanamama mmoja hivi ambaye alinisumbua sana kipindi cha nyuma akidai kuwa mimi ni mtoto wake, yule mama aliniharibu sana kisaikolojia maana mimi nawaamini wazazi wangu kuwa ndio pekee wanaohusika na mimi na si vinginevyo. Nadhani na wewe unataka kuniletea mada mpya, ila unadhani itaniumiza kichwa hiyo? Yani ni hivi uliyoyasema ndio nayaacha hapa hapa dukani, wewe unashindwa kujitafakari, mimi niwe damu yako kwa misingi ipi? Mbona nalelewa kwingine na sio kulelewa na wewe? Msinisumbue jamani, kama una lingine sema lakini maswala ya kusema mimi ni damu yako sitaki kutasikia”“Sijakwambia kwa ubaya Erick”“Cha kukusaidia ni kuwa nenda ofisini kwa baba yangu utampata bibi mtengeneza matunda halafu ndio uulizane nae undugu wenu, usinihusishe mimi. Wazazi wangu ni Erick na Erica nimemaliza”Erick alienda kupanda gari na kuondoka zake, kwakweli Juma alimuangalia bila kummaliza na kuzidi kuona kiburi cha wazi cha mtoto huyo kilivyokuwa.Leo Sia alivyorudi nyumbani kwake tu, baada ya muda kidogo alitokea mama Sarah na kuanza kuongea nae,“Wewe Sia umempeleka wapi mwanangu Sarah?”“Sarah!! Jamani, mtoto mwenyewe sina hata mazoea naye, nimpeleke wapi mie?”“Unajua huwa nakuangalia sana wewe, ila hujui kuwa mimi ni mtu wa aina gani? Hujui ni kitu gani naweza kufanya kwako”“Unazungumzia kuhusu nini? Unataka kunitishia maisha?”“Utishiwe maisha kwa lipi? Wewe ni kiumbe mdogo sana yani hata mtu hawezi kutumia muda mwingi na wewe”“Sikia nikwambie Manka, leo nakuita kwa jina lako. Mimi ni mbea sana hilo sikatai, katika maisha yangu kitu pekee ninachokiogopa ni umasikini ila sio kifo, kwa kifupi mimi siogopi kufa kwahiyo kama unanitishia maisha umekosea kwa hilo”“Ninaongea kingine unajibu kingine, kweli huna akili wewe. Haya na huyo Elly yuko wapi? Ushamueleza ukweli kuwa wewe sio mama yake ila ni tamaa zako ndio zilikufanya umbadilishe na mwanao wa kweli?”Hapo Sia alipunguza sauti kwanza kwani katika kitu ambacho hakukitamani kukiona ni swala la Elly kujua ukweli kuwa yule sio mama yake mzazi, basi alianza kuongea na mama Sarah taratibu,“nakuomba ndugu yangu tukaongee sehemu nyingine”“Nini sasa tuongelee sehemu nyingine? Elly, Elly , Elly”Mama Sarah alianza kuita jina la Elly na baada ya muda tu Elly alitoka ndani, na kusogea pale walipo kisha mama Sarah akamwambia Elly,“Huyu unayeishi nae sio mama yako mzazi, kwa tamaa zake alikubadilisha na mtoto wake ili mwanae aishi maisha ya kitajiri”Elly alimuangalia mama yake kwa makini sana huku akiendelea kusikiliza maneno ya mama Sarah. Mama Sarah alianza kuita jina la Elly na baada ya muda tu Elly alitoka ndani, na kusogea pale walipo kisha mama Sarah akamwambia Elly,“Huyu unayeishi nae sio mama yako mzazi, kwa tamaa zake alikubadilisha na mtoto wake ili mwanae aishi maisha ya kitajiri”Elly alimuangalia mama yake kwa makini sana huku akiendelea kusikiliza maneno ya mama Sarah.Mama Sarah aliendelea kuongea,“Najua Elly hujui ukweli, ila ukweli wa mambo ni kuwa huyu unayemuona ni mama yako, huyu unayemuita ni mama yako, sio mama yako mzazi, yani yeye kwa tamaa zake aliamua kukubadilisha wewe na mtoto wake wa halali ili amwanae alelewe kwenye maisha ya kitajiri, na usimuone hivyo mama yako anaumbuka kila siku”Sia alikuwa ameinama chini huku akilia maana ni aibu sana kwake na hakutaka kitu hiko kiwe wazi kwa Elly kwa namna hiyo ukizingatia ukweli wa kuhusu Elly bado umeuwa ni kitendawili kigumu sana kwake.Alikuwa akilia huku mama Sarah akiendelea kuongea,“Huyo mama yako, alikuwa akidhani Erick ndio mtoto aliyembadilisha, yani yale maisha anayoyapata Erick alikuwa anataka mwanae ndio ayapate, muulize imekuwaje? Mambo ya Erick yameishia wapi? Muulize kwa makini akwambie imekuwaje? Huyo mama yako hafai, unamuona anakupenda ila hana cha upendo wowote na wewe alikuwa na maana yake. Kwa leo nimemaliza ila ukitaka ukweli zaidi nitafute, huwa sipendi uongo, siku zote ukweli humweka mtu huru”Mama Sarah aliondoka zake na kumuacha pale Sia akiwa analia huku Elly akiwa na hasira sana, basi Elly alimfata Sia na kusema,“Mama, naomba uniambie ukweli. Naomba usinifiche, kipindi kile umezimia sikuelewa kabisa mambo haya, yani sikuelewa kabisa. Nilijua umechanganyikiwa, ila nilikusikia kabisa ukisema kuwa Elly sio mwanangu na Erick sio mwanangu, nahitaji uniambie ukweli mama, kwanini imekuwa hivi? Usinidanganye mama, tafadhari naomba uniambie ukweli mama”Sia alikuwa akilia tu, huku akiwaza ukweli atakaoenda kusema ni ukweli ambao utamfanya Elly asimsamehe kabisa, ila atafanyaje kama kila kitu kipo wazi mbele yake? Alikuwa akilia huku akisema,“Elly mwanangu, naomba unisamehe”“Sio muda wa kuniomba msamaha huu, niambie ukweli. Nahitaji ukweli toka kwenye minywa chako”“Ni kweli mwanangu kuwa wewe sio mwanangu wa kumzaa”“Unasemaje mama? Ilikuwaje ukawa na mimi? Ndio hizo tamaa alizozisema huyu mama? Ulitaka mwanao aishi maisha mazuri halafu mimi niishi vibaya?”“Sikia Elly, sikupanga iwe hivi naomba unisamehe”“Nimekwambia kuwa huu sio muda wa kuniomba msamaha ila ni muda wa kunielezea kwanini ulinibadilisha?”“Nililazimishwa Elly”“Kwa hakika sikupendi, sikupendi kabisa. Siamini kama mama yangu ungenitenda hivi”Elly aliinuka kwa hasira na kuondoka zake, yani kile kitendo kilimfanya Sia alie sana hata akakumbuka vifo vya wazazi wake, akakumbuka enzi za ujana wake, akakumbuka vitu vingi sana ambavyo vilitokea katika maisha yake, akakumbuka jinsi baba yake alivyokufa na kusema kuwa Erick ndio mwanaume anayepaswa kumuoa yeye, akakumbuka pia mama yake alivyokufa na kusema vilevile, akakumbuka jinsi Erick alivyokuwa kwa Erica, akakumbuka jinsi alivyoshawishika kwenda kwa mganga wa kienyeji, akakumbuka siku aliyompelekea Erick tunda halafu likarushwa nje ya geti, akakumbuka jinsi alivyomkuta Steve akila lile tunda, na jinsi alivyoanza kuishi na Steve hadi kufikia hatua ya kuoana, akakumbuka jinsi alivyoshawishiwa na mzee Jimmy kuhusu kubadili mtoto na jinsi Steve alivyomkimbia kwani mtoto alikuwa haeleweki, jinsi Erick anavyomkataa kila siku. Alijikuta akilia sana na kuona dunia imemuelemea, aliona dunia ni mbaya sana kwa upande wake, yani alilia hadi alilala pale pale nje huku akilia tu.Yani Elly hakufikiria hata kama muda umeenda sana, alikuwa na mawazo sana, hakuwa na raha ya maisha kabisa, aliona kama kaonewa na maisha alijiuliza maswali mengi sana,“Sasa mimi wazazi wangu wako wapi?”Hapo akili ikamtuma kuwa moja kwa moja aende kwa yule mtu ambaye huwa anadai ni baba yake yani aende kwa Derrick maana aliona wazi kuwa akili yake haifanyi kazi kwa muda huo.Basi alienda moja kwa moja kwa Derrick na kugonga mlango, yani Derrick alitoka huku akishangaa tu kwani hakutegemea kumuona Elly kwa muda ule, basi alimkaribisha na kuanza kuongea nae,“Karibu Elly, tatizo ni nini kwani?”Elly alikuwa akilia tu, ikabidi Serrick amkumbatie na kumuuliza kwa karibu kuwa tatizo ni kitu gani,“Nahitaji kuwajua wazazi wangu, nahitaji kumfahamu mama na baba yangu. Nahitaji kujua mimi ni uzao wa nani?”“Nyamaza kwanza Elly na tuweze kuongea vizuri”“Roho inaniuma sana, niliyemtegemea siku zote, niliyemuamini siku zote, niliyempenda kwa moyo wote leo nimegungua kuwa sio mama yangu mzazi, alinibadilisha tu ili sijui mwanae aishi maisha mazuri, nimeumia sana moyo. Mimi sikuwa na haja ya maisha mazuri ila ninahaja ya kutambua wazazi wangu”“Pole sana Elly, nilijua siku ukitambua hayo utaumia sana”“Inamaana unajua?”“Najua sababu najua kuwa wewe ni mwanangu ila sijawahi kuwa na mahusiano na yule mama yako, kwahiyo moja kwa moja nikaelewa kuwa kuna namna imefanyika maana wewe ni mwanangu”“Imekuwaje sasa? Kwanini imekuwa hivi? Mama yangu mimi ni nani?”“Sikia nikwambie, mara nyingine unaweza kulaumu kila unayemuona mbele sababu ya kitu kilichotokea, ila tunatakiwa kuyakubali makosa halafu kujifunza kutokana na makosa. Kwa namna moja au nyingine hata mimi pia sijihesabii kuwa baba bora. Kuna wanawake zangu wawili tu ndio ambao nina uhakika walikuwa na mimba zangu, kuna mmoja anaitwa Oliva na mwingine anaitwa Manka, ila kiukweli sikuwa na uwezo wa kulea wote wawili katika ile hali ya mimba zao, ikanifanya nimkatae Oliva, ila Manka nae akanikimbia toka hapo hakuna niliyejua yuko wapi hata walivyojifungua sikuwa najua chochote kile, nilipokutana na mmoja wao nilidai mtoto wangu ila wote waligoma kuzaa na mimi, nilikuwa naumia sana moyo maana naamini kuwa watoto wangu wapo ila wote wanakataa kuzaa na mimi. Ila Mungu mwema akanifahamisha kuwa wewe ni mwanangu kwa njia ya tofauti sana, ile njia ya ugonjwa wangu ilinifanya kwa urahisi zaidi nitambue kuwa wewe ni mwanangu”“Haya, mama yangu ni nani sasa?”“Hapo bado nina ukakasi lakini nahisi wazi kuwa mama yako ni Manka”“Manka? Ndio nani?”“Yule mnamuita mama Sarah sijui”“Aaaah hapana, sitaki kusikia, yule hawezi kuwa mama yangu. Sitaki kusikia hiyo habari, yule mama alinitesa sana alinipiga hadi nilipoteza fahamu halafu mnasema ni mama yangu? Hapana sitaki hata kidogo, sitaki yule mwanamke awe mama yangu”“Nisamehe mimi mwanangu ila huo ndio ukweli”“Inamaana Sarah ni ndugu yangu?”“Ndio ni ndugu yako”“Hapana, sitaki jamani, sitaki kukubali hiko kitu kabisa. Mbona ndio nimezidi kuchanganyikiwa jamani”“Hebu tulia kwanza Elly, kesho tutajitahidi twende kwa mama yako aliyekulea, kwani najua utakuwa umeondoka kwa hasira sana na yule mama anafahamu vitu vingi sana, hutakiwi kumchukia kiasi hiko. Kweli sio mazi wako ila ni mlezi wako”Elly aliitikia tu kwa shingo upande, basi Derrick aliandaa mazingira ili waweze kulala na Elly kwa siku hiyo maana Elly alionekana kutokuwa sawa kabisa.Leo wakati Erica kalala, basi Sarah alimfata tena na kumtaka walale pamoja kisha walianza kuongea mambo mbalimbali ambapo Erica alimuuliza Sarah kuwa ilikuwaje hadi akajikuta akilala na Elly,“Mmmh sijui ni nini, itakuwa ni huu ujana halafu hisia nazo zilinishika sana”“Kivipi?”“Sikia, mimi nilikuwa nampenda sana Erick kabla sijajua kuwa Erick ni ndugu yangu, nilitamani siku moja niweze kulala nae, ndio nikaamua kulala na Elly”“Ilikuwaje kwanza niambie”“Elly alikuwa akikataa kabisa jambo hilo, ila nilimuoshesha video za mapenzi”“Kheee video za mapenzi ndio zipi hizo?”“Zipo kwenye simu yangu, yani mwanaume na mwanamke wanavyofanya, tulipoangalia zile video basi tulijikuta tukifanya. Hujawahi kuziona?”“Nizionee wapi?Mimi sina simu”“Basi nitakuonyesha, kwenye simu yangu zipo hizo video, yani ukiangalia lazima utajikuta ukiingiwa na tamaa na ndivyo ilivyokuwa mimi na Elly. Unataka kuziona?”“Mmmh naogopa kuziona, usinionyeshe kwa leo”“Sio mbaya lakini, zingine mbaya ila kwenye simu ninazo nzuri yani ukiziona lazima uzipende, Halafu shule si zimefungwa? Ngoja nikuonyeshe kwa hakika utazipenda, ni nzuri sana. Basi nikajikuta hivyo. Ila unafikiri najutia kufanya kile kitendo na Elly?”“Kheee hujutii?”“Ndio sijuitii maana mimi ni mwanamke na Elly ni mwanaume”“Lakini Elly pia ni ndugu yetu”“Muda mwingine naumia sana roho kila nikifikiria hilo jambo, ila sasa lilishatokea nitafanyaje?”“Ukimuona Elly je utafanya nae tena?”“Hapana, kwasasa siwezi hata kumsumbua siwezi maana Elly ni ndugu yangu”Kisha Sarah alichukua simu yake na kuanza kumfungulia Erica zile video, ila wakati video inaanza kuonyesha tu mule ndani kwa Erica aliingia mama yao,“Kheee nilijua mmeshalala kumbe bado?”Erica aliweka ile simu pembeni na kuanza kumsikiliza mama yao,“Aaaah tulikuwa tunaongea mama”“Sawa, nilitaka kuongea kidogo nawe Sarah. Maana kesho ni siku ya shule, inakuwaje kuhusu shule, au nikaongee na walimu?”“Hapana mama, shule mbona tumefunga”“Kheee kumbe mshafunga! Sina khabari mimi, kwahiyo na nyie wakina Erica mmefunga?”“Ndio mama”Mama Angel alimuona kama Erica akikazana kuficha ile simu, na huwa anajua wazi kama mwanae anamficha kitu ni lazima sio kizuri basi alimuuliza kwa ukali kwani anajua Erica ni muoga kwahiyo akiulizwa kwa ukali lazima aseme ukweli,“Unaficha nini wewe eeeh! Hebu nionyeshe”Erica alitoa ile simu na kumpa mama yake, kisha mama Angel akaamuuliza Sarah,“Hii ni simu yako eeeh!!”“Ndio”“Simu kubwa hivi ndio ulikuwa unatumia wewe!”“Ndio, mama alisema ndio nzuri”“Haya mlikuwa mnafanya nini?”Erica akajibu,“Sarah alitaka kunionyesha video za mapenzi”Mama Angel alishtuka sana na kumuangalia Sarah kisha akamwambia amuonyeshe yeye hizo video, yani Sarah alizifungua kwa uoga kisha mama Angel akawaambia,“Haya laleni hapo, kwa leo Sarah naomba niende na hii simu yako”Sarah hakubisha wala nini na kufanya mama Angel atoke mule ndani kwa watoto huku akisikitika sana.Sarah akamwambia Erica,“Kwanini umemwambia ukweli? Atachukia sana halafu atanichukia mimi. Zile video ni za tabia mbaya, huwa wakubwa wengi hawapendi kujua kama watoto wanaangalia”“Sikuwa na cha kufanya, tulale tu Sarah”Yani Sarah alikubali kulala huku akiwa na mawazo sana na ile simu yake ambayo mama Angel ameichukua.Moja kwa moja mama Angel alienda na ile simu hadi kwa mume wake, maana ulikuwa ni muda wa kulala na mumewe alikuwa kashalala ila alimuamsha na kuanza kumuonyesha,“Hebu ona video ambazo watoto wanakazana kuziangalia”Baba Angel na mama Angel waliangalia kwa kifupi tu na kusikitika kisha mama Angel akasema,“Huwa naonekana mshamba sana kwa kutokumkabidhi mtoto wangu simu, ila haya ndio mambo ninayoyaepuka. Kuna umri wa kumpa mtoto simu, haya Sarah akili zake hadi zimeraruka sababu ya mambo kama haya, hebu fikiria mtoto akiangalia mavideo haya kwa siku nzima hiyo akili yake inakuwaje? Lazima atakuwa anawaza ujinga na ndiomana hata kaweza kumlaghai Elly kuwa nae kimapenzi”“Nimesikitika sana, sikufikiria kama mtoto kama Sarah anaweza kuwa na video hizi kwenye simu”“Yani mimi nilihisi hata damu kuniruka wakati wananionyesha, yani ndio nimewakuta wanataka kuonyeshana na Erica huu ujinga. Mtoto mdogo kama Sarah unampa hii simu kubwa ya nini? Haya ndio madhara yake, unahitaji kuwasiliana nae tu, kwani simu za mawasiliano tu hazipo? Napo ni tatizo maana hawa watoto kushawishika ni rahisi sana. Hata kama akiwa anawasiliana na wewe, basi mzazi jitahidi usiku uwe unachukua ile simu ya mwanao na kuikagua na ikiwezekana uwe unamkabidhi kwa muda unaoona unamfaaa. Watoto wetu hawa wana akili mbovu sana. Ndio utakuta wengine hata kusoma hawasomi muda wote wapo kwenye mitandao ya kijamii, yani mtoto mmoja anakuwa na akaunti kibao kwenye mitandao, ukifatilia yupo kidato cha kwanza, cha pili sijui cha tatu au cha nne, mwingine utakuta ndio yupo shule ya msingi kabisa, halafu mzazi hata hushtuki jamani dah!! Haya mambo haya, mtoto aharibike kwa bahati mbaya ila sio kwa makusudi sababu mzazi umeshindwa kumuangalia vyema. Malezi ya Manka kwa huyu mtoto yalilenga kumuhatribu kwa asilimia zote, nimeumia sana”“Basi jitahidi kukaa nae na kumuelewesha, naona Sarah ni mtoto muelewa sana, nina uhakika atakuelewa tu. Hizi video sio nzuri kwake na zina muharibu ubongo wake, ataacha kufikiria ya maana atakazana kufikiria watu wanavyofanya humu”Kwakweli baba Angel na mama Angel walisikitika sana, ila mama Angel alipanga kuongea vizuri sana na Sarah kwa kesho yake ili aweze kujaribu kumuweka kwenye mstari.Elly na Derrick walijiandaa na kuondoka kwa muda ule kuelekea nyumbani kwa Sia kwani Derrick alijua wazi kuwa kuna mengi kwa wao kuzungumza na Sia, basi walifika nyumbani kwa Sia na kumkuta amelala tu nje ya nyumba, Elly alikumbuka wazi kuwa mama yake ndio sehemu aliyomuacha tangu jana wakati ameondoka eneo hilo kwa hasira, alijikuta tu huruma ikimjia moyoni na kwenda pale kumuinua,“Mama jamani, nini tatizo?”Sia aliinuka, alipomuona Elly alifurahi sana na kumkumbatia huku akilia na kumwambia,“Nisamehe Elly, tafadhari usiniache nao,ba unisamehe”“Naomba unyamaze kwanza”“Sina raha mimi, najua nimefanya makosa makubwa sana ila wewe Elly ni kama mwanangu, wewe ndio wa kunifuta machozi yangu, naomba Elly nihurumie mama yako”Basi Derrick nae alisogea pale na kusaidiana na Elly kumuingiza Sia ndani huku akimtaka Sia kwenda kuoga na aweze kupata nguvu, Sia alikubali kufanya hivyo ambapo Elly aliamua kwenda kumpikia mama yake uji ili aweze kunywa na kupata nguvu.Sia alimaliza kuoga na kwenda kuongea nao, ila hata kunywa ule uji kwa muda ule hakuweza kabisa kwani alijikuta akiwa hana hamu ya kula chakula chochote kile kwa muda ule, ingawa Elly alimuwekea ule uji aweze kunywa ila bado hakuweza kunywa, basi Elly alimbembeleza pale,“Mama , kunywa kidogo utaumwa”“Hata nikinywa nitaumwa tu, najutia vingi sana katika maisha yangu. Naomba unisamehe”“Usijali mimi nimekusamehe ila niambie ni kwanini ulifanya hivyo!”“Ngoja niwaambie ukweli halisi ulivyokuwa”Derrick na Elly walianza kumsikiliza kwa makini,“Mimi, maisha yangu hayakuwa maisha mazuri sana, mimi na wazazi wangu tumeishi maisha ya kawaida kabisa. Nilikuwa na mpenzi au naweza kusema mchumba sababu alijulikana na wazazi wangu, huyu aliitwa Erick, nilimpenda sana na nusu ya maisha yangu alikuwa nayo yeye. Nikiongea sana nitaonekana mwehu zaidi ya hapa ila kwa kifupi nilimpenda. Badae Erick alipata mwanamke mwingine na kunikataa, hapo niliumia sana, nikamdanganya kuwa nina mimba yake ila bado alikataa, ndipo nilipopata mchumba mwingine ambaye alinipa ujauzito kweli ila kwavile nilimpenda Erick ikabidi nimsingizie kuwa ile mimba ni yake. Ila alikataa ikabidi niende kwa wazazi wake, ndio hapo nilipoanza kushirikiana na baba yake Erick yani mzee Jimmy, aliniambia kweli unayesema ni mjukuu wangu, nikazidi kuongopa maana nilikuwa na maisha ya shida, nilichokuwa nataka ni kupata tu msaada kutoka kwake na kweli alikuwa akinisaidia sana kipindi chote cha mimba ila aliniambia jambo moja kuwa nikijifungua atanibadilishia mtoto alinaimbia kuwa mimi nitalea mtoto wa Erick halafu wakina Erick watalea mtoto wangu, sikukataa kwakweli. Nilienda kujifungua kabla hata ya tarehe yangu kufika, nilifanyiwa operesheni, na kweli nilijifungua vizuri na kukabidhiwa mtoto. Nilijua kuwa sijapewa mtoto wangu maana ndio makubaliano yetu yalivyokuwa ila yule mtoto alikuwa akilia sana hadi binafsi nilikuwa nikiumia moyo kwa kuchukua mtoto wa mtu mwingine. Mtoto alivyofikisha miezi mitatu kasoro, ndipo mzee Jimmy aliniita tena na kusema kuwa walisahau kumbadilisha mtoto, kwahiyo kwa siku hiyo ndio walikuwa wanataka kumbadilisha mtoto, nililia sana sababu mtoto yule nilishaanza kumzoea, nilimuweka hadi alama kwenye paja lake la kushoto. Ila kwavile mzee Jimmy aliniambia hivyo na matunzo yote nilikuwa napata kwake sikuweza kukataa ingawa niliumia moyo sababu mtoto nilishamzoea, ndipo aliponikabidhi wewe. Niliondoka nawe kurudi na wewe nyumbani nikitambua kabisa kuwa wewe sio mwanangu ila nilipiga moyo maana sikuwa na cha kufanya kwa kipindi hiko. Naomba unisamehe sana Elly kwa hilo, nakumbuka kitendo cha kukuleta wewe hapa hata mume wangu nikagombana nae kwani hakunitaka tena, na hapo ndipo tupoachana kabisa na jukumu lote la kukulea lilikuwa juu yangu, ila haikuwa tatizo sana sababu mzee Jimmy alikuwa akinisaidia kwa kiasi kikubwa sana ndiomana bado nilikuwa na matumaini kuwa mzee Jimmy amenipa mjukuu wake wa ukweli maana huduma zote alikuwa akinipatia na nilikuwa nikiishi vizuri tu. Mambo yalibadilika baada ya mzee Jimmy kufa, sikuwa na msaada wowote ila bado niliweza kupambana kwa kila hali ili kukulea wewe katika maisha mema na mazuri. Elly nilikuwa najizuia mimi kula vizuri na kuvaa vizuri ili wewe usome shule nzuri hali ya kuwa ninajua wazi kuwa wewe sio mwanangu wa damu, nimejitahidi kupambana kw akila hali kwaajili yako. Najutia makosa yangu Elly, naomba usinihukumu kwa kuniacha, nipe hukumu nyingine”Sia alienda kwa Elly na kumpigia magoti ili amsamehe, ila Elly alimuinua na kumuuliza,“Kwahiyo mimi wazazi wangu ni wakina nani? Mama yangu ni nani?”“Hata mimi sijui Elly, yule mzee alinidanganya, sijui kwakweli. Nilichezewa mchezo pia, naomba unisamehe sana”Elly alipumua kwanza na kuona hapo hakuna hata cha maana kitakachoongeleka ukizingatia muda wote huyu Sia alionekana kulia tu, basi Derrick alisema,“Huyu Elly ni mtoto wangu, nina uhakika hii ni damu yangu na mama yake Elly ni lazima atakuwa Manka tu sababu nilizaa nae”Hapo kidogo Sia alinyamaza kimya, na kusema,“Basi huyu Manka atakuwa kachezewa mchezo na mzee Jimmy pia, na inawezekana kabisa mama mzazi wa Elly akawa Manka ndiomana hata hospitali siku ile ni yeye ndiye aliyeweza kumuongezea damu Elly”Kisha Sia alieza ilivyokuwa, naye Elly alieleza tukio alilofanyiwa na mama Sarah na kuendelea kukataa kuwa yule hawezi kuwa mama yake, yani kwa Elly aliona ni bora abaki na huyo mama bandia yani Sia kuliko huyo aliyeambiwa kuwa ni mama yake mzazi, hakutaka kabisa kutambua jambo hilo.Siku hii ilikuwa ni siku ya kusuluhisha na kuweka mambo sawa maana akili ya Sia ilionekana kuanza kuvuka mipaka.Leo mama Erica anaenda kuongea na Vaileth ambapo wanapanga mambo mbalimbali kuhusu mahari yake na kumuuliza maana alihitaji iwe haraka ili mambo yaende kama walivyopanga,“Nimeongea nao, washapanga mahari”“Eeeh wamesema pesa ngapi?”“Wamesema laki tano ya mahari, halafu vitenge viwili, shuka mbili, blanketi mbili na kuku yani Jogoo na tetea”“Kheee mahari zenu mapaka kuku?”“Ndio mila za kwetu zilivyo, sema siku hizi vitu vingi vya mila vimepunguzwa”“Kesho nitaenda mjini kutafuta hayo mashuka, blanketi na vitenge halafu kesho kutwa kijijini kwenu kupeleka hiyo mahari”“Ila kuku ni wa muhimu mama”“Aaaah hamna shida, hiyo hiyo kesho kutwa tutanunua hao kuku, kukaa nao ndani huku balaa, ngoja hiyo hiyo kesho kutwa tununue. Ila kuku ni wa nini? Jamani mila zingine nazo, ila mila zenu rahisi maana wengine ungesikia mbuzi, sijui kondoo, mara ng’ombe, maisha yenyewe haya magumu, ukitaja mahari ngumu hivyo unamfukuza mume, utasikia mahari milioni nne, jamani kwa maisha haya ya sasa hivi, huyu wa kutoa milioni nne nani? Wapo lakini ni wateso tu, atakutolea milioni nne halafu ndani mtakula mauzauza sababu umeyataka, ila nashukuru kwa kuongea vyema na wazazi wako maana wametupangia mahari ambayo inawezekana”“Niliongea nao, hata hivyo mmewasaidia sana wazazi wangu, nao wanakumbuka fadhila zenu kwao. Hivi watakuwepo kwenye harusi?”“Sikia mwanangu, haya mambo nahitaji tuyafanye haraka kidogo, yani harusi ikiisha tu tunarudi kufurahi hapa nyumbani halafu tunapanga siku ya kwenda kufanya sherehe huko kijijini kwenu. Si unajua mambo ya sherehe yalivyo na gharama, kuyapanga haraka hivi ni ngumu, itatutoka hela hadi tuzimie, ukizingatia tumetoka kwenye matatizo. Au hupendi harusi bila sherehe?”“Hapana mama, mbona ni nzuri tu”“Ndio, tutapika hapa nyumbani. Mtaenda Kanisani kufunga ndoa na kurudi hapa huku mashamsham yakifanyika hapa hapa nyumbani”“Sawa mama, asante”Mama Angel alifurahi pia, na alimtaarifu dada yake kuwa ajiandae keshokutwa kwaajili ya safari ya kwenda kijijini kwakina Vaileth kwani alihitaji yale mambo kuyafamya kwa haraka sana.Kwa siku hizi, Erica alikuwa akifanya kazi ya kumfundisha Sarah baadhi ya kazi za nyumbani ila Sarah alikuwa akilalamika kuchoka sana ukizingatia hakuzoea kufanya kazi za namna hii.“Yani nachoka mno”“Taratibu utazoea tu, wewe ni mwanamke Sarah kwahiyo lazima ujishughulishe kwenye kazi zote”“Huwa unapika chakula kitamu sana Erica”“Ipo siku na wewe utapika chakula kitamu pia maana utazoea tu”“Yani mama yangu, sijui kwanini hakunizoesha haya mambo jamani”“Pole ila utazoea tu”“Naona mama yupo busy sana atanipa simu yangu kweli!! Maana toka alivyoichukua hajaongea na mimi chochote, naona kila siku anatoka”“Kuna mambo nadhani anayafatilia ila usiwe na mashaka atakupa tu, nadhani anataka kwanza aongee na wewe”Basi Erica alikuwa akijaribu kumfundisha Sarah mambo mbalimbali kama kuosha vyombo, na kupika baadhi ya vyakula kwahiyo kwa kipindi hiki ni yeye na Sarah ndio walikuwa wakikaa jikoni kwa sana, kitu kile kilimfanya Sarah kutokufikiria sana simu yake kwani muda mwingi walikuwa na kazi za kufanya.Leo mama Angel aliongea na dada yake mama Junior asubuhi na mapema na kwenda kukutana kisha kuanza safari yao ya kwenda kijijini kwakina Vaileth, basi njiani wakaongea,“Mwenzangu inahitajika kuku tetea na jogoo ndio mila ya kwao”“Sasa tutafanyeje?”“Tukifika kule kwao tukanunue”“Halafu vipi kuhusu mshenga? Unajua haya mambo tumefanya kienyeji sana, najua hiyo familia ya Vaileth lazima watatushangaa sana”Hapo mama Angel aliona wazi kuwa wamekosea, ila walishaingia kwenye kijiji cha wakina Vaileth, aliwaza kidogo mama Angel na kumwambia mama Junior kuwa wakienda kununua kuku wajaribu kuongea na mtu kama anaweza kuwa mshenga wao.Na kweli walifika mahali na kumkuta mtu akiuza kuku, alikuwa ni baba kidogo wa makamo, na kwa muda huo alikuwa amebaki na kuku wawili tu, yani huyo tetea na Jogoo, mama Angel aliongea nae na kununua wale kuku, ila pia aliamua kuongea na huyu baba ili awe mshenga wao, walijaribu kumuelewesha na kumwambia kuwa watamlipa, mwisho wa siku yule baba alikubali na muda ule ule aliwaomba wampeleke kwake ili ajiandae na aweze kwenda nao.Wakampeleka, akajiandaa na kwenda nao kwakina Vaileth.Walipokelewa vizuri kabisa, na walifanya kila kitu cha kulipa mahari na mama Angel kuahidi kuwa ataenda na Vaileth na huyo mchumba ambaye anatarajia kumuoa Vaileth, pia alijaribu kuelezea ni kwanini wameamua kufanya haraka vile,“Vijana wamependana, na kijana wetu ndio anamaliza kidato cha sita, tumeona bora tufanye haraka maana hawa vijana wasije kutuletea matatizo. Ukizingatia hawa watoto wa kiume kubadili mawazo ni wepese sana”“Tunashukuru sana kwa kufanya hivyo”Waliongea mengi sana na wazazi wa Vaileth, mwisho wa siku waliamua kuagana nao kwani wao walikuwa wakirudi sehemu ya mbali sana ukizingatia mjini na pale kijijini kwakina Vaileth ni mbali mno, na walibahatika kufika mapema sababu ya usafiri binafsi.Kisha waliondoka na mshenga wao, huku wakiongea ongea kwenye gari, yule mshenga aliuliza,“Kwani mlitoka muda gani mjini maana naona mmewahi!”“Tulitoka saa kumi alfajiri ndiomana tulisema hata kuku tutanunua huku huku”“Ila kweli mlidhamiria”Basi walivyokuwa wanampeleka yule mshenga kwake, ndio walibahatika kuangalia na mazingira, kuna nyumba nzuri sana ilionekana mahali pale, ikabidi mama Angel amuulize yule baba,“Samahani, unajua nimeishangaa sana ile nyumba, ni nzuri mno. Inaonyesha mwenye nyumba ni tajiri sana”“Na kweli ni tajiri, hata sijui kwanini kaamua kuja kuishi huku, anaitwa dokta Jimmy”Hapo mama Angel alishangaa kiasi, alipotazama vizuri aliona kuna gari imesimama nje ya geti la ile nyumba na mara alitoka dokta Jimmy kwenye lile gari. Basi walivyokuwa wanampeleka yule mshenga kwake, ndio walibahatika kuangalia na mazingira, kuna nyumba nzuri sana ilionekana mahali pale, ikabidi mama Angel amuulize yule baba,“Samahani, unajua nimeishangaa sana ile nyumba, ni nzuri mno. Inaonyesha mwenye nyumba ni tajiri sana”“Na kweli ni tajiri, hata sijui kwanini kaamua kuja kuishi huku, anaitwa dokta Jimmy”Hapo mama Angel alishangaa kiasi, alipotazama vizuri aliona kuna gari imesimama nje ya geti la ile nyumba na mara alitoka dokta Jimmy kwenye lile gari.Mama Angel aliangalia kwa makini na kupumua huku akitaka kwenda kumfatilia ila dada yake alimzuia kwani aliona kuwa lile ni tatizo, na kumtaka wampeleke yule baba kwake kwanza na mama Junior hakutaka yule baba ahisi chochote kile, kwahiyo mama Angel aliendelea na safari huku akisikiliza maelezo kutoka kwa yule baba ambapo mama Junior alimuuliza yule baba,“Kwahiyo huyo dokta huwa anawasaidia eeeh!”“Ndio, kwa kiasi huwa anatusaidia kama mtu umepata dharula anakusaidia ila anasema aliamua tu kupumzika kwenye kazi yake ya udaktari”“Aaaah ila kwanini aliamua kujenga huku?”“Sijui kwakweli yani tulimshangaa mwanzoni ila kwasasa tumemzoea”Basi walimfikisha huyu mzee Mussa nyumbani kwake, kisha waliagana nae na wao kuondoka zao.Wakiwa kwenye gari, mama Junior alianza kumwambia mdogo wake kuhusu ubaya wa yeye kutaka kwenda kwa yule dokta,“Unajua nini Erica, kumbuka kuwa yule alifanya mumeo akae nyumbani mwaka mzima, halafu leo umfate bila kujipanga na lolote? Mnatakiwa mjipange”“Nakumbuka mamake Erick alisema kuwa atashughulikia swala hili”“Basi ni kitendo cha kuwasiliana nae tu.”“Itabidi tufanye hivyo”“Yani mdogo wangu wakati nakuona ukiwa na hisia za kutaka kwenda kwa yule dokta nilijawa na hofu moyoni, unadhani kitendo mlichotuhadithia walichomfanya shemeji hatukukielewa? Walikuwa na lengo la kumuua, halafu muda huu uende tu na kujipeleka pale! Tushukuru tumeshajua anapoishi kwahiyo ni rahisi zaidi kwetu”Mama Angel alikubaliana na maneno ya dada yake kwani aliona wazi kuwa dada yake anaongea ukweli mtupu.Mama Angel aliingia nyumbani kwake akiwa kachoka sana, moja kwa moja alienda kuoga yani hata chakula alikula akiwa amechoka kwahiyo alikula kidogo tu. Vaileth alimpa pole pale na kuongea nae kidogo tu,“Usijali, nitakuja tuongee chumbani kwako. Ngoja nimalizie’Mama Angel alipomaliza kula, moja kwa moja alienda chumbani kwa Vaileth na kumueleza jinsi safari ya kule kwao ilivyokuwa na kumwambia kuhusu mipango mingine ya harusi,“Kesho kutwa jiandae maana tutaenda kutafuta shela litakalokufaa”Vaileth alizidi kuwa na furaha maana harusi ilikuwa inanoga,“Asante sana mama, kwakweli nazidi kupata furaha yani siamini kama harusi yangu inaenda kufanikiwa”“Usijali, kila kitu kinaenda katika mstari, haya mambo nahitaji tufanye haraka kidogo maana akili za vijana hawa haswaaa akili za Junior, tusije kujilaumu badae bure”“Kwahiyo mama, na ndoa umeshaandikisha?”“Baba yenu kaandikisha ndio, kaongea na Mchungaji kwahiyo ndoa itafungwa tu. Tutafunga siku ya kawaida tu, yani sitaki kuchelewesha mambo ni kumchukua Junior kurudi kenye ndoa”Vaileth alifurahi sana, kisha mama Angel alimuuliza swali jingine,“Samahani Vaileth, unamfahamu dokta Jimmy?”“Dokta Jimmy!! Yule mwenye jingo zuri sana kijijini kwetu!”“Ndio huyo huyo, umemfahamu tokea lini?”“Ni muda tu nimemfahamu, yule dokta ni tajiri sana, ana pesa na mali nyingi. Ni ngumu kumuona, watu huwa wanamfata wakiwa na shida na huwa anasaidia watu wengi sana”“Aaaah kumbe!! Yupo vizuri eeeh!”“Ndio yupo vizuri, ila watoto wake wana maringo sana”“Ana watoto wangapi?”“Wawili, halafu anawapenda sana”“Ooooh sawa, niliona mjengo wake, basi tutaendelea kuongea mwanangu”Basi mama Angel akamuaga Vaileth pale usiku mwema na moja kwa moja kwenda chumbani kwake.Mama Angel alipoingia chumbani kwake, alikuta mume wake ameshalala, ila alimuamsha ili kumpa ile habari ya dokta Jimmy, alimueleza kuhusu kumuona kwake dokta Jimmy na vile alivyoongea na Vaileth kuhusu dokta Jimmy,“Kumbe ni kitambo kahamia huko eeeh!!”“Ndio inavyoonyesha hivyo, ni kitambo yupo kule. Wanafahamu hadi watoto wake”“Sasa hiyo ni vizuri tumefahamu anapoishi, kweli nimeamini katika maisha kila kitu kina sababu, hakuna kinachotendeka kwa bahati mbaya, yani kila kitu kinasababu tu. Mmeenda huko kwakina Vaileth tumeweza kujua mtu tuliyemtafuta kwa muda kumbe yupo anaishi huko, basi hiyo ni rahisi kwetu. Safari yenu haikuishia kwenye mahari tu, bali imezaa na matunda mengine”“Dada Bite akaniambia ni kheri tuwasiliane na mama yako maana ndio alisema atalifatilia jambo hili”“Hapo sawa, tutawasiliana nae tu na yeye atakuwa kapata mwanga, najua mama anatamani sana kujua ni kitu gani kilikuwa kikifanywa na mzee Jimmy”Ila baba Angel na mama Angel walifurahi kupafahamu mahali anapopatikana dokta Jimmy, kisha baba Angel alimuuliza mkewe kuhusu mipango ya harusi,“Nilitaka Junior akichukuliwa ni moja kwa moja Kanisani kufunga ndoa”“Aaaah mke wangu, sikia Junior tutamchukua siku moja kabla, tuongee nae hapa tumkanye halafu kesho yake ndio atafunga ndoa. Uende kumchukua siku hiyo hiyo ukute lile jimama lake lishamnyakua hata tusijue pa kuanzia hapo!! Yule tutamchukua tumkanye itoshavyo halafu kesho yake ndio ndoa inafanyika, yani hakuna kumpa uhuru wa kuaga marafiki wala wakina nani, ni moja kwa moja anaingia kwenye ndoa, bila kufanya hivi yule mtoto atatukanyaga hadi kichwani”Mama Angel aliona sawa kabisa kuhusu swala hilo kwani kwa kiasi kikubwa sana alikuwa amechoshwa na matendo ya huyu kijana.Kulipokucha tu, leo baba Angel alitoka ila mama Angel alinaki kwani aliona ni vyema kwa siku hii akipumzika nyumbani ukizingatia siku karibia zote kashafanya mizunguko mingi sana, kwahiyo aliona ni vyema akiitumia siku hii kupumzika tu.Ndipo alipopigiwa simu na Derrick na kupewa ile taarifa kuwa Elly ameshaujua ukweli,“Kwahiyo mama yake Elly ni nani?”“Ni Manka, si nilishakwambia”“Ila Manka, ana mtoto wa kuitwa Sarah, inamaana Sarah sio mtoto wa Manka au Sarah na Elly ni mapacha?”“Mimi sijui ila ninachojua ni kuwa Elly ni mtoto wa Manka ingawa Elly hamtaki Manka kabisa nasikia Manka alimpiga sana Elly hadi Elly akalazwa, basi Elly hamtaki kabisa Manka”“Duh!! Kumbe kuna makubwa”“Ndio, Elly kaujua ukweli ila anasema ni bora aendelee kuwa karibu na mama aliyemzoea kuliko kuwa karibu na Manka”Mama Angel alisikitika kiasi, kisha aliagana na Derrick na kuendelea na shughuli zake zingine.Mama Angel akiwa ametulia kwa muda huu, ndipo Sarah anaamua kumfata ili aongee nae kuhusu simu yake maana hakumrudishia toka ile siku aliyoichukua,“Mama, samahani hujanirudishia ile simu hadi leo”“Oooh nimekumbuka, hebu tuongee kwanza”Mama Angel aliinuka na kumuongoza Sarah hadi kwenye sebule yao nyingine na kuanza kuongea nae, kwanza mama Angel alimwambia,“Naomba kwa muda huu tuongee kama marafiki halafu ndio tutakuja kuongea kama mama na mtoto. Upo tayari kuwa rafiki yangu kwa muda huu?”“Nipo tayari ndio”“Haya rafiki, naomba uniambie ni kitu gani unajihisi ukiangalia zile video? Kumbuka mimi ni rafiki yako, kuwa huru usimdanganye rafiki yako eeeh!”Sarah akapumua kidogo na kusema,“Mimi napenda tu halafu huwa najihisi raha kuziangalia”“Raha gani ambayo huwa unahihisi wewe?”“Sijui, basi tu najihisi raha”“Kwa mara ya kwanza uliona wapi hizo video?”“Kwenye simu ya mama”Mama Angel akapumua kidogo na kumuuliza tena Sarah,“Kwahiyo mama yako kwenye simu yake ndio alikuwa na video za aina hiyo?”“Ndio tena zilikuwa nyingi tu, nilikuwa namuomba mama simu yake nicheze game halafu nikikuta hizo video naanza kuangalia. Sababu ya kumuomba mara kwa mara nicheze game ndio akaamua kuninunulia simu yangu”“Eeeh na kwenye simu yako ulizipataje?”“Sasa mama alipochukua simu yake na kuninunulia simu, ndipo nilipojiunga na mitandao ya kijamii, siku hiyo nikiwa naperuzi instagram niliona ukitaka video za kikubwa nifollow, nikamfollow, nikakuta kuna mahali kaweka namba tulipie halafu anatuunga kwenye group la kuona video za kikubwa, basi nikajiunga humo na humo ndio nikagundua sehemu nyingi zinapopatikana hizi video”Mama Angel alisikitika kiasi na kumuuliza tena,“Hebu niambie ukweli Sarah, lazima hizi video ndio zilifanya ukalala na Elly, uongo?”“Ni kweli, kila nilipoziangalia nilitamani sana kujaribu kufanya kile kinachofanywa ila sikujua kama naweza kujaribu na nani, ndipo mama alipomleta Elly niliona ni vyema kujaribu nae, nilimuonyesha hizo video akapenda basi tukajikuta tunafanya”Mama Angel alipumua na kuanza kumfundisha Sarah sasa ili awe mtoto mzuri na aweze kurudi kwenye maadili,“Najua ni ngumu sana kukuelewesha, ila mimi nitajitahidi kukuelewesha kama mwanangu. Sarah wewe bado mdogo, hapo ulipo una ndoto nyingi sana za maisha, sio ndoto za kutazama haya mavideo ya ngono hakuna kitu chochote kitakachokuwa msaada kwako kwa kutazama hizi video zaidi ya kuathirika kisaikolojia tu, kwamba ukizikosa uone kama kuna kitu muhimu sana kimepungua kwako katika maisha. Mimi nitakuwa sambamba na wewe Sarah kuhakikisha kuwa unarudi kwenye mstari, najua wewe ni mtoto mzuri, bado hujawa katika kiwango cha kuropoka na kujibu watu vibaya, kwahiyo tutaenda pamoja tu. Kwasasa naomba uniachie simu yako, nakuomba mwanangu. Halafu kadri ninavyokufundisha ndivyo nitakavyokuja kukuachia simu, kuwa na simu sio mbaya ila ubaya ni kile unachofanya na simu, mbona kuna mambo mengi tu ya kujifunza hata humo kwenye mitandao ya kijamii? Unaweza kujifunza mapishi, afya, kilimo, ujasiliamali yani kuna vitu vingi tu vya kujifunza na vyenye manufaa kwako. Vingine sio muhimu sana kwasababu vipo kwetu na vitakuja kwetu kwa hali ya uhalisia, kwahiyo mwanangu nitajitahidi walau kila siku nipate muda wa kuzungumza na wewe. Ila naamini hujakwazika?”“Hapana sijakwazika”Sarah alikuwa akimpenda sana huyu mama, alikuwa akipenda sana jinsi huyu mama alivyoongea kwa upendo alitamani hata siku itokee kuwa kalala na kuamka na kuambiwa kuwa huyu mama ndiye mama yake mzazi, yani alijikuta akimpenda sana na kumsikiliza kwa kila kitu alichokuwa akimfundisha.Leo Erick alipotoka tu kiwandani aliwasiliana na baba yake na moja kwa moja baba yake alimwambia kuwa aende ofisini kwake, kwahiyo Erick alienda ofisini kwa baba yake, na alipoingia pale walianza kujadiliana kuhusu faili lile ambalo alilikuta kuwa lina makosa.Muda kidogo alifika yule bibi wa matunda mule ofisini na kuwasalimia kisha kuanza kuongea nao,“Nawaona leo baba na mwana, yani hadi raha”Baba Angel alitabasamu tu na kumkaribisha huyu bibi, kisha huyu bibi akasema,“Yani boss Erick, huyu kijana wako kafanana sana na binti yangu tena sana”“Kheee, duniani wawili wawili”Muda kidogo alifika Juma yani rafiki wa baba Angel pale ofisini, ni hapohapo Erick alipomwambia yule bibi,“Mwanao mwingine huyo hapo”Alikuwa akimuonyesha Juma kwa yule bibi, basi Juma na yule bibi waliangaliana kwa muda kiasi kisha wakachukuzana na yule bibi nje kwaajili ya maongezi, basi baba Angel alimuangalia mwanae na kumuuliza,“Imekuwaje umemwambia huyu rafiki yangu kuwa yule ni mama yake?”“Kuna siku nimekuja hapa, akaja huyu bibi na kukazana kuwa nimefanana sana na mwanae sijui niwe mjukuu wake, aliongea sana, basi akanipa na matunda ila sikula. Nilipoenda dukani nikakutana na huyu baba ambaye aliyataka yale matunda na kukazana kusema kuwa kweli mimi ni damu yake. Nadhani sijakwambia baba, huyu huwa anasema mimi ni damu yake. Alikula yale matunda na kukazana kusema mimi ni damu yake, maana yale matunda ndivyo ambavyo babuyake alikuwa anapenda. Basi leo ndio akutane na mama yake”“Dah! Wewe mwanangu una balaa, duh sikufikiria hiko kitu. Ila nitamuuliza huyu rafiki yangu, kwanini anasema kuwa wewe ni damu yake ana maana gani?Sijaongea nae toka kipindi cha kukupeleka sijui kwenye kaburi la babu yake, ila nitaongea nae tu. Ngoja arudi”Ila mpaka jioni wanatoka, Juma hakurudi tena pale ofisini. Ikabidi tu waondoke na kurudi nyumbani kwao.Walipofika nyumbani, leo baba Angel aliongea na mke wake kuhusu swala la Juma na kuhusu Erick,“Ila hawa watu wana matatizo gani lakini! Kamaliza Sia, kaanza Juma, hivi nae alibeba mimba kuzaa au kitu gani?”“Usinichekeshe mke wangu jamani, hata usiumie kichwa na hawa watu wala nini, sisi tufikirie mambo yetu ya maendeleo tu. Nitajua mimi, nitaongea tu na Juma hakuna tatizo”Basi walimaliza yale maongezi na kuendelea na mambo mengine.Leo, mama Angel mapema kabisa alichukuzana na Vaileth ili kwenda kujaribu gauni la harusi kama ambavyo alipanga nae, kwahiyo kwa muda ule mchache walimuacha mtoto kwa Erica.Basi mama Angel alipokuwa na Vaileth wakichagua nguo ya harusi na kujaribisha ndipo alipokutana na rafiki yake Dora,“Kheee kwenye duka la nguo za harusi tena! Mara ya pili au?”“Hapana, ni binti yangu wa kazi ndio anaolewa”“Kheee hongera sana, umeishi vizuri na binti wa kazi hadi anaolewa nyumbani kwako! Hongera sana, harusi lini sasa?”“Ni alhamisi hii ndio harusi yenyewe, karibu sana”“Asante sana, nitakuja basi. Sijui nije nyumbani kwako au kanisani?”Mama Angel alimuelekeza Kanisa hilo lilipo ili moja kwa moja afike hapo kanisani,“Muda ni saa tisa alasiri”“Basi nitakuja, yani nisingekutana na wewe najua haya mambo yangekuwa kimya kimya, loh mambo yako Erica jamani loh!”Basi walicheka tu pale huku mama Angel akimuomba msamaha kidogo rafiki yake maana kwa kipindi hiko alikuwa na mambo mengi sana kwahiyo alisahau kuwapa taarifa rafiki zake wengine hawa wakati kulikuwa na umuhimu sana wa kumwambia mtu kama Dora.Siku ya leo baba Angel alipokuwa ofisini kuna simu iliingia kwake, alipoiangalia ilikuwa ni namba ya mwalimu wa Angel, basi aliipokea simu ile na kuanza kuongea nayo,“Ndio, mwalimu niambie”“Wakina Angel wanamaliza mtihani leo, alikuwa anauloza utakuja kumchukua leo?”“Aaaah atakuja bibi yake kumfata kesho maana mimi bado nipo huku mjini na sikujua kama mitihani wanamaliza leo. Kwani na mambo ya mahafali si mlisema tusubiri”“Ndio, yani lengo la binti yako ni kuwa anataka kusherekea na wenzie leo jioni kumaliza mtihani, sasa kuna mchango wamekubaliana kutoa ndiomana aliniuliza kuwa nimuulizie kwako ili ajue kama atasherekea na wenzie”“Kwani huo mchango ni pesa ngapi?”“Wamekubaliana kuchangia elfu hamsini kila mmoja”“Nakutumia mwalimu, halafu mwambia bibi yake atakuja kesho kumfata”“Sawa”Muda kidogo, baba Angel alimtumia huyu mwalimu wa Angel hiyo hela aliyoambiwa kwani huyu baba huwa hapendi mtoto wake asononeke.Baada ya muda kidogo, baba Angel akakumbuka kitu kuwa lazima Junior nae ndio anamaliza mitihani siku hiyo, basi akawaza kuwa aende kumuwahi huko shule maana alihofia pia kwa Junior kuchukuliwa na Linah.Baba Angel alimaliza kazi zake mapema kabisa na kuondoka pale kuelekea shuleni kwakina Junior, moja kwa moja alienda kwa mwalimu kuongea nae,“Madam, naomba Junior akimaliza mitihani tu niondoke nae”“Kheee huyu Junior leo jamani, na mamake mdogo nae kaja kumfata kasema akimaliza mitihani tu anamuhitaji aondoke nae”“Mamake mdogo yupi huyo?”Yule madam alimuonyesha baba Angel gari ambalo alikuwepo huyo aliyekuwa anamsubiria Junior, basi baba Angel alienda hadi kwenye lile gari, alishangaa sana kumuona Linah ndio ambaye alikuwa akimsubiria Junior, basi baba Angel alimshtua na kumwambia,“Linah jamani, umeshindwa hata kuwa na aibu hata kwa mbali? Haya Junior nani yako?”Linah hakujibu kitu ila aliona aibu, basi alifunga vioo vya gari lake na kuondoka zake.Baba Angel alimsubiri Junior pale pale shuleni kwao, na alipomaliza tu mitihani akamchukua na kuondoka nae huku akimsema sana kwa vitendo anavyovifanya,“Yani Junior kweli unaacha masoma na kuondoka na yule mama? Dah basi tu, tutaongea nyumbani”Moja kwa moja baba Angel alienda nyumbani muda huo na Junior.Walivyofika nyumbani tu, mama Angel alifurahi sana kwa baba Angel kurudi na Junior, aliinuka na kumshika mkono Junior,“Shikamoo mamdogo”“Twende ukachukue shikamoo yako na wewe ili kama ni chakula uweze kushiba muda huu”Mama Angel alimshika mkono Junior hadi chumbani kwa Vaileth ambapo Vaileth alikuwa akinyonyesha mtoto yani Junior alibaki kistaajabu maana hakufikiria kile kitu kabisa, basi mama Angel alimkalisha chini Junior na kumwambia,“Umemuona mtoto wako?”Junior alizidi kushangaa huku akitetemeka, basi mama Angel akamwambia tena,“Unatetemeka nini sasa? Kwani ulipopanda mahindi ulitegemea kuvuna nini? Ila hongera kwa kuitwa baba na ujiandae kwa harusi”Hapo ndio Junior akashtuka kiasi,“Harusi!!”“Ndio harusi, wewe unaenda kumuoa Vai. Usifikirie ni siku nyingi bado, ila ni kesho kutwa hapo”“Kheee sijawahi kuona harusi ya hivyo”“Ndio uione sasa, nenda kaoge uje huku kumshika mtoto na kuongea na mwenzio. Nimemaliza, jiandae sasa”Yani Junior alishindwa hata cha kusema, na kuinuka kama alivyoambiwa kuwa akaoge kwanza.Junior alioga huku akijifikiria sana, aliona kama akili yake haisomi vile yani hakuna alichokuwa anaelewa hata kimoja.Alipomaliza, moja kwa moja alienda chumbani kwa Vaileth maana alikuwa na maswali mengi sana na hakusema asubirie kuvizia usiku lazima tu afanye vile inavyotakiwa.Basi alienda na kumkuta Vaileth akiwa anakunja nguo za mtoto, alifika pale na kupumua kidogo kisha alimwomba msamaha Vaileth kwani alijua wazi kuwa anapaswa kumwomba msamaha,“Naomba unisamehe Vai, nisamehe kwa yote. Nisamehe kwa kushawishi kutoa mimba, nisamehe kwa kukata mawasiliano na wewe, naomba unisamehe sana. Kwakweli nimefanya hiki kitu bila ya kujifikiria, nisamehe sana Vaileth”“Nimeshakusamehe”“Naomba nimshike mtoto”Vaileth alimtoa mtoto kitandani na kumpa Junior huku akimwambia,“Anaitwa Joseph”“Oooh jina la babu, kapewa na nani?”“Bibi yake mdogo”“Aaaah halafu naomba unieleweshe hayo mambo ya harusi kesho kutwa”“Ni hivi mama amwshaenda kujitambulisha kwetu, kashatoa mahari na walishaandikisha ndoa. Kwahiyo kesho kutwa tunaoana”“Ila kwanini wamefanya hivyo bila ya kunishirikisha muhusika?”“Kwani hutaki kunioa Junior?”“Hapana, nina lengo jema tu ila kwanini hawajanishirikisha? Hapo ndio walipokosea ila sijachukia”Kisha Vaileth akamtolea gauni la harusi ambalo lilikuwa kabatini na kumfanya Junior aamini wazi kuwa ndoa inafungwa kweli, alitabasamu tu ila alikuwa na mawazo mengi sana.Baada ya hapo Junior alirudi chumbani kwake, ila muda ule ule alitumiwa ujumbe na Linah,“Junior mpenzi wangu, nilifika kukuchukua leo kama ahadi yetu ilivyokuwa kuwa ukimaliza mitihani tu basi utakuja kukaa kwangu mwezi mzima. Babako mdogo kajifanya kuja kuniwahi hapo shuleni, kwahiyo Junior fanya kitu tuonane”Junior alisoma ule ujumbe mara mbilimbili na bila ya kujibu chochote, kisha akaamua kulala tu.Leo mapema kabisa, Sia akiwa nyumbani kwake alifatwa tena na mama Sarah ambapo mama huyu alianza kuongea nae,“Mwanangu yuko wapi?”“Hivi kweli kabisa unatoka huko na kuja kumuulizia Sarah hapa, una akili kweli wewe?? Unaamini kabisa kuwa Sarah ni mwanao?”“Ndio, Sarah ni mwanangu”“Pole sana, ulihisi mchezo ule mzee Jimmy kanichezea peke yangu, kwa taarifa yako mtoto wako ni Elly, wala Sarah sio mwanao”“Haiwezekani”“Haiwezekani nini? Nenda kapime huko, kapime na Elly na Sarah halafu mtafutie Sarah wazazi wake kama mimi nilivyotafuta wazazi wa Elly na kugundua kuwa mmoja wapo ni wewe usiyejielewa”“Unaongea au unatapika? Hujui kama mimi nilijitolea kumsomesha mtoto wangu?”“Umejitolea kumsomesha mtoto wako pia maana Elly ni damu yako, nilitaka nishangae yani mzee Jimmy akuache tu na amani wewe bila ya kukufanyia mchezo!!! Kitu hiko hakiwezekani, pole sana, huyo ndio mzee Jimmy bhana”Sia alikuwa akicheka tu ila jambo lile lilimpa mawazo sana mama Sarah kiasi kwamba hakuweza tena kuendelea kuongea na Sia maana muda huo huo aliamua kuondoka zake.Wakati baba Angel kaenda mjini na Junior, mama Angel aliwaita wakina Erica na kuwapa taarifa juu ya harusi ya kesho. Kidogo ilikuwa ni taarifa ya kushtukiza maana hawakujua kama kuna mipango ya harusi, basi Erica alimlaumu sana mama yake kwa kutowaambia mapema,“Ila mama umefanya vibaya, kwanini hujatuambia mapema tufanye maandalizi?”“Maandalizi ya nini sasa Erica? Ni harusi ya haraka hii, wala hakuna sherehe wala nini, tutapika tu hapa nyumbani na kula kama familia. Sherehe kubwa itaandaliwa na itafanyika kijijini kwakina Vaileth, huko ndio tutajipanga ila sio kwasasa”“Haya, na kuhusu hiyo kesho ndio tumejipangaje? Chakula gani tutapika, vitu gani vitakuwepo?”“Tutapika tu pilau, na vinywaji vitakuwepo maana baba atapita kuvichukua na Junior, halafu Erick nae nilimuagiza kuna vitu apitie kwahiyo akitoka tu kiwandani atapitia kwenda kuvichukua”“Mama jamani, tupike na tambi za nyama ya kusaga”“Ila tambi sijanunua labda nikuagize ukanunue hapo madukani”Basi mama Angel alimuagiza Erica, na muda mfupi tu Erica alitoka kwenda kununua tambi alizoagizwa.Wakati Erica anarudi, alikutana na Emmanuel, basi alimsalimia pale na kumualika kwenye harusi ya kesho yake kwani aliona kuwa na wao wana umuhimu wa kwenda.“Jitahidi uje na Emmanah, tuanzie Kanisani”“Sawa ingawa gafla mno”“Hata sisi wenyewe tumeshtukizwa tu, naomba mjitahidi”Aliagana nae na kurudi nyumbani.Siku hii usiku walikuwa wakifanya maandalizi tu ya harusi ya kesho, walicheza na kufurahi pamoja.Siku ya harusi ilifika, kwakweli Vaileth alipendeza sana ingawa ilikuwa ni harusi ya fasta fasta ila alipendeza sana.Familia yote ya mama Angel ilikuwepo hapo kushuhudia hiyo harusi, basi taratibu zote zikafanyika kama kawaida.Wakati mchungaji aliposema,“Kuna mtu yeyote mwenye pingamizi hapa?”Sauti ikasikika toka mlangoni,“Mimi hapa nina pingamizi”Mtu huyu alikuwa akija mbele na watu wote waligeuka kumuangalia, kwakweli mama Angel ndio alishangaa sana kwani huyu mtu alikuwa ni Linah. Wakati mchungaji aliposema,“Kuna mtu yeyote mwenye pingamizi hapa?”Sauti ikasikika toka mlangoni,“Mimi hapa nina pingamizi”Mtu huyu alikuwa akija mbele na watu wote waligeuka kumuangalia, kwakweli mama Angel ndio alishangaa sana kwani huyu mtu alikuwa ni Linah.Kila mtu alikuwa akimshangaa kwa waliomfahamu na wasiomfahamu, ila Linah hakuona aibu na kusogea moja kwa moja mbele hadi kwa mchungaji, kwakweli Junior alibaki kushangaa tu hata mtu aliyempa taarifa Linah hakumtambua kwakweli, basi mchungaji akamuuliza,“Una pingamizi gani mama kwa hawa mahurusi”“Haiwezekani ndoa ikafungwa maana mimi nina mimba yake”“Mimba ya nani huyo? Unamsema huyu kijana?”“Ndio, huyo bwana harusi mimi nina mimba yake”Kila mmoja alibaki kushangaa, baba Angel alisogea mbele pia hata mama Angel na wakubwa wengine huku baba Angel akimlazimisha Linah kutoa nje maana pale anajiaibisha mwenyewe tu, ila Linah aliongea kwa ukali,“Na wewe Erick naomba uniache, tena niache kabisa. Huyu Junior ataoa vipi wakati mimi na yeye tumeishi nae kama mke na mume kwa kipindi chote hiki na hapa nilipo nina mimba yake”“Hivi Linah unaijua sheria wewe?”“Sheria gani? Sheria ya mimi kupewa mimba halafu nifurahie? Siijui”Mchungaji aliamua kuhairisha kwanza ili wale wenye mashtaka yao wakayamalize ofisini, na alitoa nusu saa tu kuwa kama haitawezekana kumaliza hiyo tofauti basi ndoa haitafuingwa na itahairishwa maana kunatakuwa na kasoro, kwakweli Vaileth aliinama akilia ni mama Angel ndio alimchukua pembeni akimbembeleza huku baba Angel akimwambia Erick akae na Junior wakati yeye anaenda ofisini ili huyo mwanamke aache hizo lawama zake.Basi mama Angel alikuwa akimbembeleza Vaileth,“Ni mkosi gani huu nilionao mama? Kwani kosa langu mimi ni nini? Nimekosea wapi nijue jamani? Kwanini imekuwa hivi”“Hakuna ulipokosea, achana na huyu mtu mzima asiyekuwa na akili”Kisha mama Angel alimuita mama Junior akae na Vaileth ili yeye akajaribu kuzungumza ofisini huko na wajue jinsi ya kufikia muafaka, wengine walibaki tu wakijadiliana na kushangaa kwani yale mambo yalikuwa ni ya ajabu halafu ni ya aibu kubwa sana.Mama Angel alienda ambapo mumewe alikuwa akizungumza na Linah huku akitamani hata kumzaba vibao maana inaonyesha Linah alikuwa akimjibu baba Angel majibu mabaya,“Sikia Erick huna cha kunibabaisha ujue, kwahiyo utaenda kufungua mashataka kuwa Linah alikuwa anambaka Junior? Toka lini mwanamke akambaka mwanaume? Hiyo kitu inapatikana wapi? Huyo Junior mtoto? Kashavuka miaka kumi na nane inamaana kuwa ni mtu mzima ndiomana hata nyie mmepata nguvu ya kuja kumfungisha ndoa. Sasa na mimi haki yangu iko wapi na niliishi na Junior kinyumba hadi kanipa mimba?”“Yani wewe Linah unaongea utadhani ni mtu wa wapi sijui, Junior ni mdogo sana kwako. Junior ni sawa tu na mtoto wako hata wa tano huko, hivi huoni hata mchungaji kakushangaa kusema unapinga ndoa kisa una mimba? Mtu gani mwenye mimba ya mtoto wewe?”“Uliona wapi mtoto akaweza kumpatia mwanamke ujauzito? Junior ni mwanaume aliyebalehe na ndiomana kanipatia mimi mimba. Na huo uwezo wa kumbaka Junior mimi nautoa wapi? Mnajijua kabisa wanaume mlivyo kuwa hakuna kinachowezekana bila ya mashine zenu kusimama, haya mimi nitaweza wapi kufanya hilo kama sio Junior kwa mapenzi yake na tamaa zake, kwanza Junior amekula vingi sana vyangu, lazima anioe, mimi ni mtu mzima ndio ila sina mume na mume wangu ni Junior. Kwahiyo msinichanganye kabisa, angejiona mtoto basi asingekuwa na mimi”“Si kwasababu ulikuwa ukimlazimisha”“Msinichekeshe mimi, toka lini mwanaume akalazimishwa? Msitake niwatusi hapa”Linah aligoma kabisa kumaliza ule utata, basi Mchungaji aliwaita ofisini kwake na kuanza kuongea nao tena,“Bado dakika tano, hamjafika muafaka?”Linah alijibu kwa kujiamini kabisa,“Hatuwezi kufika muafaka, Mchungaji najua kuwa wewe ni mtumishi wa Mungu, angalia jambo hili kwa undani. Huyo Junior nimemsomesha na kumlea kama mume wangu mtarajiwa, na tulipanga kuoana kabisa hadi mimba nikabeba sababu najua mume yupo. Mchungaji unataka nitoe mimba yani niue kiumbe cha Mungu?”Mchungaji alisikitika na kusema,“Unajua siku hizi mna mambo ya ajabu sana, yani kuna vitu vya ajabu ambavyo mtu huwezi hata kufikiria kama vinaweza kutokea. Ngoja nikuulize kwanza, una miaka mingapi mama”“Miaka yangu ya nini Mchungaji? Mimi ninachotaka ni mume wangu”“Aaaaah yani kuna mambo mengine hata kujadili hayana maana kabisa”Mara pale kwenye ofisi ya mchungaji aliingia Dora na kufanya wamuangalie kwanza maana alichelewa na kuanza kusema bila kusalimia,“Nimeaingia Kanisani nikaona mambo hayaeleweki na watu wametoka nje, nikaamua kuuliza ndio naambiwa sijui kuna mwanamke anasema kuwa ana mimba ya Junior, kwahiyo ndoa haiwezi kufangwa. Kwani yuko wapi huyo mwanamke?”Maana aliona wote pale ni watu wazima halafu ni watu anaowafahamu, mama Angel akamwambia akimuonyeshea Linah,“Huyu mwanamama hapo ndio mwenye mimba ya Junior”Dora alihamaki kwa sauti,“Linah!! Kheee unawezaje kubeba mimba ya mtoto wa binamu yako?”Wote wakashangaa na kumuangalia kwa makini Dora, huku Linah akimuuliza Dora,“Unamaanisha nini?”“Kwani hujui kama Junior ni mtoto wa marehemu James?”Hapa Linah alijikuta akiinuka ila walimshika mkono na kumuuliza,“Unaenda wapi sasa? Bado unamtaka Junior?”“Niacheni mie”Linah alitoka nje ambapo alifatwa na Dora na kusimama mahali huku wakiongea, wakati huo baba Angel alimuomba tu mchungaji waweze kwenda kumaliza swala la ile ndoa ya Junior na Vaileth, na Mchungaji alikubali maana muda haukupita sana, ingawa muda aliosema ulipitiliza ila kutokana na ile kesi aliamua tu kuendelea na lile swala.Dora alisimama nje na Linah akiongea nae, ambapo Linah alimuomba Dora wakaongelee kwenye gari yake,“Nahisi kama presha inapanda na kushuka, siwezi kusimama hapa. Twende tu ndani ya gari tukaongee”Basi walienda kwenye gari na Linah alimuuliza tena Dorah,“Hebu niambie ukweli Dorah,yani huyu Junior ni mtoto wa James?”“Ndio, ni mtoto wa James, tena mtoto wa ndoa kabisa. Kama unamkumbuka yule mke wake wa kwanza ndio alizaa nae huyo mtoto”“Kheee yule mke wake wa kuita Bite?”“Ndio huyo huyo, kwani hujawahi kumuona mamake Junior?”“Mmmmh jamani, nagombanaga nae kila siku, sikujua kitu kama ni yeye. Kabadilika sana mbona, wakati anaolewa na James hakuwa vile, alikuwa mwanamke mwembamba Fulani halafu alikuwa akijipenda sana, yani kawa tofauti sana yani sikuhisi kabisa kama Junior ni mtoto wa James, wewe nakufahamu sababu unatufahamu vizuri sana ndugu wa James. Ila mbona hii aibu jamani nitaweka wapi sura yangu?”“Kwahiyo ni kweli una mimba ya Junior?”Linah aliinama kwa muda kabla ya kujibu, ilionyesha kwa muda huo alikuwa kakumbwa na aibu sana,“Yani na utu uzima huu, nimeamua kubeba mimba ya katoto Junior, kumbe ni mtoto wangu kabisa loh!! Nikikumbuka James tulivyokuwa tukipatana halafu mimi nikatembee na mtoto wake kweli!! Aaaah nimechanganyikiwa mimi”“Kheee pole sana, sijui utafanya kitu gani ila ndio hivyo, Junior ni mtoto wa James. Na ulijuaje kama yeye anaoa?”“Yani ni hivi, nina ndugu yangu mmoja hivi nadhani unamfahamu vizuri tu na yeye, anaitwa mama Emma, mwenye wale mapacha wawili Emmanuel na Emmanah ndio nilipoenda kwake jana nikakuta Emmanuel akimwambia Emmanah kuhusu hii harusi, niliuliza kwa makini sana na niliwaomba kuwa wasije kabisa siku ya leo, nikawadanganya na kuwapa pesa za kutumia leo nadhani hawajafika maana nilikuwa najua kitu ninachotaka kufanya leo ila dah nimeaibika jamani hata sikutegemea kabisa”“Huyo mama Emma ni Neema au?”“Ndio ni yule Neema”“Kheee ukoo huu jamani, sasa imekuwaje hao wakina Emmanuel wamefahamiana na hawa? Kheee jamani, haya ndugu yangu, wifi yangu ndio hivyo. Naona harusi imeisha maana nasikia vigelegele tu”“Naomba niende, nahisi kuchanganyikiwa kabisa”Basi Dora alishuka na kuagana nae, kisha yeye alirudi kwenye shamrashamra za harusi.Dora anakuta kweli ndio wanatoka, na moja kwa moja walirudi nyumbani kama ambavyo walipanga, na kufurahi pale kama familia, kupiga picha na kula chakula na ilipendeza haswaa, basi walipokuwa wakiongea ongea baada ya chakula ndipo Dora alipoenda pembeni kuongea na mama Angel,“Hili wazo la kufanyia sherehe nyumbani umelitoa wapi? Mmeacha hata kukodi ukumbi?”“Mmmmh inatakiwa mtu utambue mfuko wako kwa kipindi hiko, kwasasa mimi na mume wangu hatuko vizuri kivile, kumbuka amekaa akiuguza miguu mwaka mzima hapa nyumbani, kwahiyo tusingekuwa na hela kama zamani. Hata hapa tunashukuru Mungu, ila tunajipanga kwenda kufanya sherehe kwenye kijiji cha huyu binti”“Ila ni wazo zuri pia kufanyia nyumbani maana mmepunguza gharama nyingi tu, watu hawajui huwa wanadhani kufunga ndoa ni lazima ufanye sherehe kubwa. Nakumbuka mimi na James tulivyoona, tulirudi tu nyumbani na kula chakula chetu na kufurahi tu kinyumbani nyumbani ila ndoa ilifungwa kihalali kabisa”“Ndio hivyo, ila hebu niambie vizuri, yule Linah umemfahamu vipi na undugu na James upo vipi mbona hakumfahamu dada yangu?”“Yani Linah na James ni mtu na binamu yake, mtoto wa shangazi yake, na walipatana mno, mamake James, Linah anamuita shangazi, na Linah na James walikuwa wakipatana sana ila inaonyesha Linah alikuwa hawatembelei sana James na Bite, ila dada yako muulize kwa makini, kwanini ndugu wa James walikuwa hawamtembelei, na yeye alikuwa hawatembelei kwanini? Hapo ndio kwenye utata, ila James na Linah ni ndugu kabisa kwahiyo Junior ni mtoto wake pia ndiomana umeona Linah amehamaki”“Ila Linah kapata wapi taarifa ya ndoa?”“Anasema kapata kwa Emmanuel na Emmanah, ni watoto wadogo sijui wameambiwa na nani ila ndio taarifa kaipata huko”Waliongea ongea kiasi ila sababu muda nao ulikuwa umeenda ilibidi Dora aage na kuahidi kwenda tena, ila kabla ya yote alimuuliza mama Angel,“Kwahiyo hawa maharusi wamefunga ndoa, wataenda kuishi wapi au ndio mtakaa nao humu ndani?”“Tutaishi nao tu maana bado hatujajipanga sehemu watakayoenda kuishi, nakwambia ndugu yangu mambo yamekuwa haraka haya, halafu kwasasa sipo vizuri kivile”Dora alimuelewa rafiki yake na kuagana tena halafu akaondoka zake.Kulipokucha, kila mmoja aliamka na uchovu wa shughuli ya jana, basi walikuwa wakifanya tu shughuli mbalimbali za pale nyumbani kwao, ila baba Angel alitoka na kwenda kazini kwani alitaka kufululiza na kazi kwa kipindi hiko.Mama Angel alimuita Erica maana alijua wazi Erica ndio anajuana na hao wakina Emmanuel, na alipomuuliza ni kweli Erica alikubali kufahamiana nao.“Nashangaa jana hawakuja”“Yule mtu mzima aliyekuja kuvuruga ndoa ya Junior jana ni ndugu yao kumbe!! Ila mimi nahitaji kitu kimoja Erica”“Kitu gani hiko mama?”“Nahitaji kuwafahamu zaidi hawa watu, nahitaji kuwafahamu huyu Emmanuel na Emmanah sijui kwanini ila nahitaji kuwafahamu”Erica alikubali kumletea mama yake watu hao maana walikuwa ni rafiki zake, kisha Erica aliendelea na mambo mengine ambapo alienda kuongea na Sarah ambaye kwa muda huu alionekana kajiinamia tu,“Sarah, tatizo ni nini?”“Nimekumbuka simu yangu, mama hataki kunipatia”“Usijali, mama atakupa tu”“Ila mimi nataka kucheza game jamani, nimeumia moyoni jamani, sijui kwanini mama ameing’ang’ania! Mbona mama yangu huwa hana tatizo kabisa na mimi kutumia simu?”“Ngoja nitaongea na mama Sarah, ila usiwe na mawazo hivyo. Twende tukamwagilie maua”“Kheee hapa kwenu kazi haziishi jamani!! Nishakumbuka nyumbani tayari”Sarah aliinuka tu na Erica, hata alishangaa kuona Erica anapata wapi nguvu ya kufanya kazi kila mara, maana Erica alikuwa akifanya karibia kila kazi na mara chache sana ukimkuta analalamika kuwa amechoka maana muda mwingi huwa hasemi kama amechoka.Usiku wa siku hii, wakati Erica na Sarah wakiwa chumbani maana siku hizi Sarah alikuwa akilala na Erica toka siku aliyomuomba kulala nae hakuondoka tena na wala hakugombana nae tena, basi muda ule alifika Erick mule chumbani na kumwambia Erica,“Leo ndio nimekuletea ile zawadi niliyokuahidi”“Kheee toka siku ile jamani Erick!!”“Ndio, nisamehe lakini ila naomba uipokee”Erick alitoa zawadi ya viatu ambapo Erica alivijaribu vikampendeza sana, basi alikuwa akitembea tembea navyo kama kujiangalia, Erick akamwambia,“Erica, tunajua kama una mguu mzuri na nilijua tu kuwa lazima hivi viatu vitakupendeza”Sarah akauliza,“Inamaana mimi nina mguu mbaya?”“Mmmh hapana Sarah, unaanzaje kuwa na miguu mibaya wewe?”Basi Sarah akataka naye kujaribisha vile viatu, alivyovivaa tu miguuni vilimtosha vizuri sana na vilimpendeza na kumfanya Erick aseme,“Dah ndio vimekupendeza kiasi hiko!!”Erica alichukia kiasi na kusema,“Kwahiyo mimi havikunipendeza?”“Hapana sijasema hivyo ila ni kwavile tu sikujua kama na Sarah nae vingemtosha, ila wewe vilikupendeza zaidi”“Mmmh ndio mnasifiana mapacha eeeh!! Haya bhana, tusiokuwa na pacha wetu tunalo”Sarah alivivua vile viatu na kuviweka pembeni kisha alijilaza, inaonyesha hakupenda kile kitu, basi Erick aliamua kuondoka tu kwa muda ule kwenda chumbani kwake.Habari za kuhusu mtoto zilikuwa zimemchanganya sana mama Sarah, kwakweli hakuelewa kabisa, aliamua kwenda hotelini na kuagiza pombe ambazo alikunywa sana huku akiongea hovyo hovyo tu maana alihisi kama akili yake kuvurugika, alichukua tena simu na kuongea nayo,“Naomba dokta Jimmy niambie ukweli kuhusu watoto wangu”“Ukweli upi? Na watoto wako kivipi? Mwanao si mmoja tu, mtoto wako ni Sarah”“Wewe na mzee Jimmy mmenifanyia mchezo nyie, yani dokta umesahau yote niliyokuwa nashirikiana na wewe halafu leo unashindwa kuniambia ukweli wa mlichonitenda wewe na yule mzee asiokuwa na aibu wala staha”“Aaaah maliza pombe zako halafu ndio unipigie simu, naona unaropokwa tu”Simu ilikatika, kwakweli mama Sarah hakuwa kwenye hali nzuri kwani muda mwingi alijikuta akilia tu, ila muda kidogo alitokea Rahim na moja kwa moja alimsaidia mama Sarah na kwenda nae moja ya vyumba kwenye hoteli hiyo kwani mama Sarah alikuwa amelewa sana na alikuwa akilia, basi alimsaidia mule chumbani na kujaribu kuongea nae katika hali ile ile ya pombe,“Kwani wewe Manka una matatizo gani? Unazungumzia watoto gani?”“Sielewi, kumbe Sarah sio mtoto wangu, sijui kweli aio au nilizaa mapacha hata sielewi, wajinga wawili dokta Jimmy na mzee Jimmy walishirikiana katika kunifanyia hujuma hiyo”“Pole sana, ila si nasikia kuwa wewe ulimpiga risasi Erick?”“Mimi!! Hapana sio mimi, ni Moses huyo ndio alimpiga Erick, yani Moses kanituma vitu vingi sana, yeye ndio alinituma nimuwekee Erick sumu kwani kwa muda mrefu na siku nyingi sana tulijua kuwa Erick alishakufa ila baada ya kugundua uwepo wake ndio mambo yalianza upya”“Duh!! Kahiyo mlivyogundua yupo hai ndio mkapata kiwewe cha kumuua? Nani aliwaambia kuwa Erick amekufa?”“Sijui, ila baada ya msiba tu wa baba yake ilianza kusambaa habari hiyo kuwa amekufa. Ila sikuaiamini sana na ndiomana sijashangaa kumuona, ila mimi sina nia ya kumuua Erick wala nini na siwezi kumuua, jamani mimi”Alianza tena kulia kiasi kwamba hata Rahim alikuwa hamuelewi, ila alilala nae hadi asubuhi.Kulipokucha, mama Sarah alionekana kurudiwa na akili zake na alianza kuuliza baadhi ya mambo maana hakuwa na kumbukumbu na kile kilichotokea jana yake.“Ila Rahim naomba kwa muda huu twende kule nyumbani kwangu, nahitaji kurudi kule. Nimeanza kuwa mwehu, bora nirudi kule tu”“Sawa hakuna tatizo”Walioga na kwenda kunywa supu, kisha kuondoka mahali hapo ila Rahim kuna vitu vingi sana alikuwa akimsoma mama Sarah bila ya mama Sarah kujua kitu chochote kile.Mama Angel akiwa anajiandaa na kutoka kwa siku hii maana alikuwa akihitaji kutoka kidogo, ila muda ule alifika Dora na kuanza kuongea nae,“Kheee mama Angel kumbe unataka kutoka, naomba tuongee kidogo”“Basi twende tuongee kule kwenye bustani”Basi waliongozana wote kwenda kwenye bustani na kuanza kuongea,“Unajua nini Erica, kuna jambo nimelifikiria sana na limeniumiza akili haswaaa”“Jambo gani hilo?”“Sasa kuna maana gani ya vijana kuoana na kuzidi kuishi humu ndani na nyie, maana maisha ya ndoa inapendeza mkienda kuishi wenyewe kwanza bila ya wazazi. Sasa hawa ndio wameoana nini? Junior kahamia chumbani kwa Vaileth au Vaileth kahamia chumbani kwa Junior?”“Mmmmh hapana, yani Junior analala kwenye chumba chake kilekile halafu Vaileth analala kwenye chumba chake na mtoto”“Basi hao wameoana kwaajili ya vyeti tu, hakuna maana ya ndoa hapo. Inatakiwa waanze maisha ya wawili tu”“Nafikiria jambo hilo pia, kuna mambo nakamilisha. Kama leo nilikuwa nataka kutoka maana kuna dalali nimeongea nae ili akanionyeshe vyumba vya kupanga, nataka tuwapangie chumba na waanze maisha humo. Yani ni sababu tu ya hela inasumbua kwasasa ila nilitaka niwaweke mahali pazuri na wafurahie maisha ya ndoa”“Oooh kumbe nimekuja kwa wakati muafaka kabisa!! Sasa naomba unikubalie jambo hili Erica”“Jambo gani?”“Ile nyumba ambayo James alikuwa akiishi zamani na mke wake, unakumbuka kuwa alipanga?”“Nakumbuka ndio”“Badae alinunua ile nyumba, kwahiyo ile nyumba ni mali ya James. Kulikuwa na wapangaji pale, ni wiki iyopita tu wamemaliza kodi yao na kuhama, kuna dalali alikuwa akishughulikia mpangaji mpya pale. Ila jana kapata mpangaji mpya, nimeenda hadi pale ili anilipe hela, nimejikuta nimepatwa na mawazo sana kufika pale, nikajiona sitokuwa na akili timamu kama nikipokea ile hela, kwahiyo yule mpangaji nimemkatalia na nimemuweka kijana jana anifanyie marekebisho pale. Naomba ukubali ili Junior akaishi pale, ile nyumba ni mali yake, naomba apate haki yake tafadhari na tutakaa chini ili tujue namna ya kugawa mali za James. Kila siku roho huwa inaniuma sana nikifikiria haya mambo, nisamehe kama nimekosea ila nakuomba unikubalie kwa hili”Mama Angel alipumua kidogo na kumwambia Dora,“Mimi siwezi kukataa kwani ile nyumba ndio ambayo Junior kazaliwa mule, kwahiyo wewe kuikabidhi kwa Junior ni jambo la maana tu umefanya. Mimi nimekubali kwa roho nyeupe, basi pesa ambayo tulitaka kumpangia nyumba tumnunulie vitu vya ndani ili waweze kuanza maisha”“Sawa, na mimi kwenye hela hiyo nitaongezea milioni moja. Halafu jana, niliweza kwenda ofisini kule alipokuwa akifanyia James zamani, niliwaambia kuwa swala la Junior kuoa, wamelalamika sana na kusema kwanini hatujatangaza ili wamchangie mtoto wao. Kwahiyo basi, wamepanga kuchanga na kumtunza kijana wao, nadhani tutapanga nao siku maalum ili tuweze kuwatunza vijana wetu”“Kweli Dora umekuwa wa tofauti sana kwa kipindi hiki, mimi nimekubali kabisa hakuna tatizo lolote lile”Dora na mama Angel waliongea mambo mengi sana na kukubaliana, kisha Dora aliaga kuwa anaondoka ila akasema,“Nimekumbuka jambo mama Angel, jamani kile chakula cha juzi alipika nani?”“Mambo ya Erica hayo”“Vile vyakula vyote alipika Erica?”“Ndio, tulimsaidia mambo machache tu ila Erica ndio alipika kila kitu. Ndiomana hata kanisani hakuja, yani mambo mengi alisimuliwa tu”“Kheee mwanao jamani ni taifa jingine, inabidi mfungue hoteli yenu maana sio kwa chakula kile khaaa mtoto mdogo kama Erica ndio anapika chakula kitamu vile!! Kwahiyo vitu vya kupika vyote alipanga yeye?”“Ndio, yani mimi nimemsaidia kidogo tu kama kuchambua mchele, kumenya menya vitunguu halafu vingine alisaidiwa na Erick maana na yeye anapenda sana kumsaidia dada yake na shughuli za jiko”“Kweli hao mapacha, huwa napenda sana wanavyopendana, toka wadogo ukimuudhi mmoja basi balaa unalo, nakumbuka vizuri mambo yao. Kwakweli watoto umepata Erica, ila fata nilichokwambia mfungue hoteli au fungueni sehemu ya mapishi yani muwe mnakodiwa kupika kwenye masherehe huko, aaaah nimependa sana”“Haya na leo kabla ya kuondoka twende ukale alichopika, maana kapika ndizi nyama”Basi Dora alienda kula kwanza, alisifia sana kile chakula maana kilikuwa na ladha sana, basi aliaga tena na kuondoka zake.Baba Angel alipomaliza kazi zake, alifunga ofisi na kuondoka zake ila alipokuwa njiani alikutana na Juma na kumsimamisha huku akianza kuongea nae,“Hivi toka siku ile hatujaonana ndugu yangu, hivi imekuwaje kwanza? Ni kitu gani kipo kati yako na yule mama Juli?”“Unajua kuna kitu cha ajabu sana nimekigundua ambachop sikukitarajia”“Kitu gani hiko?”“Unajua mimi, mama yangu alikufa na kuniacha mdogo sana, baba akaoa tena na huyo mama alizaa mtoto mmoja tu ndio huyo Juli sijui yupo wapi siku hizi ila familia ilitengana kidogo baada ya baba kufa. Kwahiyo yule mama ni mama yangu wa kambo, yani mke wa baba”“Kheee kweli milima haikutani, binadamu hukutana umemjuaje sasa?”“Ni hivi, siku moja Erick alinipa matunda, jinsi yale matunda yalivyokuwa ni kwamba babu yangu mimi alipenda vile kwenye matunda na kunigfanya moja kwa moja nihisi kuwa Erick anahusika na ukoo wangu kwa asilimia mia moja. Nilijua Erick ndio katengeneza yale matunda, ila ndio kaja kunikutanisha na huyu mama, kumbe ni mke wa baba kwahiyo na yeye alikuwepo kwa babu pale, ndiomana anamtindo ule wa kuweka matunda”“Ila kwanini huwa unahisi Erick anakaa kwenye ukoo wako? Ni kipi kinachokufanya uhisi kuwa Erick ni mtoto wako?”“Yani ni hivi, kuna matendo Fulani ya Erick yanafanana na babu yangu. Kuna kipindi babu yangu alipigwa na kuzimia, ila alipotoka hapo alikuwa na nguvu za ajabu halafu alikuwa na hasira sana nasikia alikuwa akimpiga kila mtu, nimekuwa nikimfatilia Erick kwa muda mrefu sana, nisamehe kwa hili. Kwanza kabisa nilihisi Erick ni mtoto niliyezaa na baby, yani nimeanza kumfatilia Erick hata wewe hujui kama namfatilia. Mimi Erick aivyochapwa na kuzimia, nilikuwa wa kwanza kupewa taarifa maana kulikuwa na mwalimu pale shuleni kwanina Erick ambaye nilimwambia amfatilie Erick na kila kinachompata aniambie kwahiyo ilikuwa wa kwanza mimi kupewa taarifa. Erick ana akili sana, kitu hiki kinanifanya nimfananishe na babu yangu, hata nimewahi kumshawishi mara kadhaa kuwa aache shule kwani najua akili zake ni zaidi na kukaa darasani”“kwahiyo huyo Erick umezaa na nani? Unajua unanichanganya wakati najua wazi kuwa Erick ni mwanangu, ulizaa na mke wangu?”“Hapana, nilidhani nimezaa na baby ila huyu baby niliwahi kukutana nae, aaah kumbe haitwi baby ni jina la uongo alinipa. Mwanamke ni muongo yule hakuna mfano, nilimkuta akilia peke yake akilalamika kuwa maisha yamemtenda. Namuuliza kuwa mwanangu yuko wapi, analalamika kuwa hata yeye hajui mwanae yuko wapi, aaaah wanawake wengine huwa tunazaa nao tu, kumbe ni wajinga”Baba Angel alipumua tu maana hata hakuelewa vizuri, alimuangalia Juma na kumuuliza tena,“Kwahiyo Erick sio mtoto wako?”“Kwasasa nina haki ya kusema sio mwanangu, sikujua kama Mungu alitaka nifahamu maisha ya mama yangu wa kambo yalivyo na maisha ya ndugu yangu Juli. Natakiwa nimtafute ili arudi kwenye mstari, kwahiyo Erick alikuwa kama daraja la mimi kufahamu kuhusu ndugu yangu”“Na huyo baby?”“Mjinga yule, Mungu amempiga kofi. Nimemkuta kalewa, analia hovyop tu, nikamuacha hapo. Kwaheri ndugu yangu.Basi baba Angel aliamua tu kuondoka zake kwa muda huo na kurudi nyumbani kwake.Usiku wa leo, mama Angel na baba Angel walijadiliana habari za Juma kuhusu kijana wao Erick,“Kheee kumbe ndio ilikuwa hivyo?”“Ndio mke wangu, yani nimemshangaa sana”Mara simu ya mama Angel ilianza kuita, baba Angel alimuangalia mkewe na kumuuliza,“Nani huyo anapiga usiku huu?”“Mmmh hata sijui”“Hebu pokea”Mama Angel alipokea ile simu na kusikia sauti ya Rahim,“Rahim hapa anaongea, toka nje mara moja nina ujumbe wako”“Kheee usiku huu!!”“Ndio, ni ujumbe wa muhimu sana kuhusu familia yako”Mama Angel na baba Angel walitazamana kwa mshangao kwanza. Mama Angel alipokea ile simu na kusikia sauti ya Rahim,“Rahim hapa anaongea, toka nje mara moja nina ujumbe wako”“Kheee usiku huu!!”“Ndio, ni ujumbe wa muhimu sana kuhusu familia yako”Mama Angel na baba Angel walitazamana kwa mshangao kwanza.Kisha mama Angel akamwambia mume wake,“Niende nikamsikilize?”“Ukamsikilize ili iweje?”“Kasema ni jambo la muhimu sana, linahusu familia yetu”“Saa ngapi saa hizi?”Mama Angel aliangalia muda na kujibu,“Saa sita kasoro”“Hivi kweli saa sita kasoro usiku, mke wa mtu atoke kwenda kuongea na mwanaume aliyezaa nae nje eti huyo mwanaume ana jambo la maana, inakuingia akilini kweli!”“Kheee yamekuwa hayo”“Hata kama sio mwanaume uliyezaa nae, inawezekana vipi kwa mke wa mtu kutoka usiku na kwenda kuzungumza na mwanaume nje eti kuna jambo la muhimu!”“Samahani mume wangu, ila ingependeza zaidi kama tungeenda wote”“Wapi huko? Kuonana na Rahim kwa usiku huu, ili iweje? Mke wangu hebu tulia, nakupenda sana kama jambo la maana angetuambia mapema au asubiri hadi kesho au atume ujumbe basi ila kutoka nje muda huu nakataa kabisa”“Ila huwezi jua mume wangu, anataka kuongelea kuhusu familia yetu”“Erica sikia mke wangu, kwanza nimekukumbuka sana. Huu sio muda muafaka wa kwenda kuongea na watu nje, njoo tufanye yetu, mambo ya kuongea na watu tuyaache”Basi kwa muda huo, mama Angel alitoa kabisa wazo la kuonana na Rahim na kuwa na mume wake.Simu ya mama Angel iliita sana ila haikupokelewa tena na badala yake baba Angel aliizima kabisa maana aliona ni usumbufu.Leo, Sia alipotoka Ibadani tu moja kwa moja alienda kwa mama Angel kwani aliona anatakiwa kuongea nae mambo mengi tu ambayo hajaongea nae.Alipofika ndio akagundua pia na swala la Vaileth kuolewa na Junior, basi aliongea nae pale,“Hongera sana, hiyo ni bahati ujue maana wanawake wengi wanaililia”“Asante sana”“Kuna wanawake huko wenye elimu zao na kazi zao ila wapo tu, hajatokea hata yule wa dada naomba tukaishi wote, achilia kupata ndoa. Kwakweli ukibahatika kupata ndoa ni swala la kushukuru sana. Hongera kwa hilo, sijui mama Angel yupo”“Yupo ndio”Vaileth alienda kumuitia mama Angel ambapo alitoka na kwenda kuongea nae kwenye bustani kwani alijua wazi kuwa Sia huwa ana mambo mengi sana, kwanza Sia alimueleza kuhusu mama Sarah na tuhuma za mtoto,“Kheee basi Sarah yupo hapa kwangu”“Aaaah kumbe!! Ila sijamuacha, nimemsema pia, anadhani Sarah mtoto wake!! Thubutu, mtoto wake ni Elly”“Kheee kwahiyo Sarah ni wa nani? Nilihisi huenda kazaa mapacha!”“Mapacha wapi? Hakuna cha mapacha wala nini, yule kajifungua mtoto mmoja tu ambaye ni Elly, pale mzee Jimmy kampiga changa la macho pia na yeye, huyo Sarah hata sio mwanae, mtoto hafanani nae hata ukucha”“Mmmmh kwahiyo Sarah wa nani?”“Mimi sijui, ila muulize Derrick anaweza kujua Sarah ni mtoto wa nani kama alivyojua kuhusu Elly”“Wanawake aliozaa nao Derrick ni Oliva na Manka, ila hata mara moja Oliva hajawahi kushtuka kuhusu Sarah, halafu ni mwalimu wake pia, yani hajawahi hata mara moja, kama ni mwanae lazima angeshtuka”“Mmmh kuna kitu naanza kufunuka, kwamaana hiyo, yule mtoto aliyepo kwa yule madam sio mtoto wake pia? Na yeye alijifungulia hospitali gani?”“Ile ile ya majanga ya mzee Jimmy”“Mmmh inawezekana yule ndio akawa mwanangu, jamani huyu mzee Jimmy alikuwa na maana gani lakini? Sasa Sarah ni mtoto wa nani kama Oliva sio mtoto wake?”“Mimi sielewi”“Haya mambo yalivyo unaweza kushangaa hata wewe Erica na Erick wote sio watoto wako sijui utafanyaje”“Weeee ushindwe, wale ni watoto wangu, nina uhakika nao kabisa”“Nimetania tu, ila kale kasarah umefanana fanana nacho”“Nahisi ni mtoto wa Derrick maana Derrick ni ndugu yangu, ndiomana damu yangu na damu ya Sarah zimeendana”“Kwahiyo unataka kusimamia huo msimamo kuwa Manka alijifungua mapacha?”“Sijui, ila inawezekana”“Kheee kazi ipi, ila jana usiku kuna mahali nilipita nikamuona Makna na Rahim”“Mmmmh!! Walikuwa wakifanya nini?”“Sijui maana sijafatilia, umbea nauogopa siku hizi. Ngoja niende, nilileta hayo tu”Sia hakukaa sana kwani muda huo huo aliondoka ila hapo alishapata uhakika kuwa mtoto aliyepo kwa madam Oliva ni mtoto wake wa damu.Usiku wa leo, moja kwa moja Erica alienda chumbani kwa Erick na kuanza kuongea nae,“Jamani kwakweli nimekumiss sana, yani naona kama kuna kitu kimepungua kwangu, hakuna tena uhuru wa kuongea kama tuliokuwa nao zamani sababu ya Sarah”“Ila hukuipenda zawadi yangu jamani Erica!”“Sijaipenda wapi wakati Sarah ameng’ang’ania vile viatu”“Basi nitakununulia vingine”“Haya, nimekufata tucheze karata”Erick hakukataa kwani ni muda mrefu hakucheza na dada yake, kwahiyo aliona ni sawa tu kwa siku hiyo kucheza nae karata, basi walianza kucheza zile karata ila kwa leo Erick alikuwa akimuachia Erica kushinda tu muda wote mpaka Erica akamuuliza,“Kwanini leo hushindi wewe Erick?”“Nina usingizi”“Mmmh haya, ngoja nikuache ulale”“Hapana, naomba leo ulale pembeni yangu kama unavyolala na Sarah”“Mama katukataza lakini?”“Najua ndio, ila nakuomba Erica leo tu ulale humu chumbani kwangu”“Sawa, hakuna tatizo”Basi Erica alilala pembeni ya Erick, ila kwenye saa nane ya usiku walisikia mlango ukifunguliwa wote wawili walishtuka ila aliyeingia alikuwa ni Sarah, basi walimwambia kwa mshangao,“Sarah!!”“Ndio, utaniacha vipi nilale mwenyewe wakati wewe umekuja kulala huku! Labda kama tulale wote huku”Basi Erica aliinuka pale kitandani na kumshika mkono Sarah na kwenda nae chumbani kulala kwani alijua wakiendelea kuongea pale, huenda mama yao angetoka, walifika chumbani na kulala tu.Kulipokucha, Erica alianza kuongea na Sarah,“Kwani wewe ulikuwa ukifikiria kitu gani kwa mimi kulala chumbani kwa Erick?”“Hapana sikufikiria chochote ila kwanini uniache mimi nilale mwenyewe? Hapo ndio pagumu Erica, wala hata sikufikiria chochote kibaya”“Haya sawa, leo tutaenda kwenye biashara ya mama Elly uone jinsi ambavyo huwa anapika”“Sawa, hakuna tatizo”Walikubaliana vizuri pale na kuendelea na mambo mengine.Asubuhi ya leo, wakati Sia anatoka kununua mahitaji yake, alikutana njiani na Rahim ambapo ni Rahim ndio alisimamisha gari na kumuita Sia,“Wewe cha umbea”Sia alishtuka kuitwa cha umbea, basi alipomuangalia alimtambua na kwenda kumsikiliza ambapo kitu cha kwanza alimuuliza,“Kwanini umeniita cha umbea?”“Nimepata taarifa zako kuwa wewe ni mbea sana na unapenda kufatilia mambo ya watu”“Mmmh!! Haya niambie ulichoniitia”“Najua kama uliniona nilipokuwa na Manka”Sia akashtuka na kumfanya Rahim amshushue,“Usijifanye kushtuka, au hukuelewa kama ningekuona au ni kitu gani?”“Hamna kitu”“Nilienda kwa huyo Erica ili kumwambia ukweli maana aliniambia nimfatilie Manka kama kweli ninampenda”“Eeeeh!!”“Umeshtuka sababu hujui, ni hivi mimi nimewahi kuwa na mahusiano na Erica najua kama hilo unalifahamu hadi tukabahatika kumpata mtoto Angel, najua pia unafahamu hilo. Ila ambacho hujui ni kuwa mimi hadi leo bado nampenda Erica tena ninampenda sana, bila mambo ya ujana kunisonga basi Erica ndio angekuwa mke wangu, nadhani sasa umepata umbea mwingine wa kukuongezea siku za kufanya umbea wako”Sia alikuwa kimya tu, kisha Rahim aliendelea kuongea,“Sikia nikwambie kitu, hata yule Manka hakujua kama Erick kamuoa Erica, anasema siku aliyojua ni siku ambayo alimfata mwane nyumbani kwa Erica, ndio hapo alikutana nae kwa mara ya kwanza na kufahamiana, ila alikuwa akijua kuwa Erica kaolewa na mtu mwingine kabisa tofauti na Erick. Kitu kilichokuwepo ni kuwa ule ukoo ambao Erica kaolewa humo, najua alikubali kuolewa na Erick sijui ni sababu ya pesa au ni sababu ya nini maana kama pesa hata mimi nilikuwa nayo, sio nilikuwa tu hata kwasasa ninayo, mimi nimezaliwa kwenye hela na nimekulia kwenye hela tofauti na Erick. Sijui ni nini kilimfanya akubali kuolewa na Erick ila yule baba yake Erick alikuwa ni zaidi ya mafia, mzee alikuwa na roho mbaya sana yule. Laiti Erica angejua kitu alichopanga yule mzee ukumbini kukifanya! Mimi mwenyewe sikujua ingawa nilikuwepo pale ukumbini ila nasikia yule mzee alibabaishwa na mama mmoja ambaye saivi unaweza kumuita bibi maana umri ushaenda, anaitwa bi.Aisha, huyu amebahatika kujua vitu vingi sana vya mzee Jimmy. Nilitaka kumwambia Erica mambo mengi sana zaidi ya haya ila sababu ya kiburi chake hakutaka kunisikiliza kitu, namuacha tu na ujinga wake na mume wake, au unataka nikueleze wewe!”“Ndio niambie”“Cheki ulivyotegesha masikio vizuri, unadhani naweza kukwambia wewe! Nilataka nionane na Erica mwenyewe nimueleze ujinga wa baba mkwe wake, ukikutana na Erica mwambie nina mengi sana ya kuongea nae, mimi sitamtafuta ila yeye anitafute mimi. Afanye kabla mambo hayajaharibika, maana akigundua kilichofanyika kwa hao mapacha wake anaweza akalia machozi ya damu. Ongea nae mwambie afanye hima kabla mambo hayajaharibika, ataumbuka na sijui ataweka wapi sura yake kwa hiyo aibu ambayo ataletewa na wale mapacha wake, watoto wamekuwa wale, asipokazana kwasasa, atalia na sijui atajificha wapi”“Mmmmh!! Kwani ni kitu gani kipo kati ya Erick na Erica?”“Kuna jambo kubwa sana limetengenezwa na yule mzee kwa wale watoto, hilo bomu likilipuka sijui huyo baba mtu na mama mtu wataweka wapi sura zao maana itakuwa ni aibu kubwa sana kwao. Haya sio kwa Manka, nimeyapata kwa mwenyewe dokta Jimmy ambaye ni muhusika wa mambo yote. Roho imeniuma kama mzazi halafu ukizingatia nampenda sana Erica, najua angekuwa mke wangu kwahiyo roho inaniuma mimi. Mwambie anitafute haraka sana”Kisha Rahim akapanda kwenye gari yake na kuondoka zake, Sia alisimama kwa muda bila ya kuelewa kitu chochote kile.Basi aliamua kurudi kwenye mgahawa wake kwanza ilia pike pike na badae aende kwa mama Angel kuongea nae kuhusu hiyo habari.Mama Angel alitoka maana alipigiwa simu na Dora ili wakaangalie maendeleo ya nyumba ya James maana alikuwa akiitengeneza kwanza kabla ya kuikabidhi mikononi mwa Junior.Kisha Erica alimwambia Sarah sasa kuwa wanaweza kutoka kwenda kule alipomwambia kwenye mgahawa wa mama Elly.Basi moja kwa moja walienda kwenye ule mgahawa wa mama Elly na kumkuta pale akiwahudumia wateja wake, alipowaona aliwafata karibu na kusema,“Wewe Erica umemleta Sarah huku hujui kama anatafutwa na mama yake?”“Kheee kwahiyo haruhusiwi kutembea?”“Hapana sio hivyo ila mama yake anamtafuta”“Aaaah mimi nilimleta tu aone mgahawa wako au Sarah umewahi kuja hapa? Lakini kama umewahi kuja basi umesahau”“Ila kabla hamjaondoka, hebu subiri kwanza”Sia alienda kuandika ujumbe kwenye karatasi na kuuweka kwenye bahasha kisha akamwambia Erica kuwa ampagtie mama yake ule ujumbe,“Oooh sawa, sasa si ndio mama atajua kama tulikuja huku, kwanini usimpigie simu?”“Nimejaribu ila sijampata hewani”“Duh!! Sawa basi nitampatia”Kisha Sia alimwambia Sarah kuwa aonje chakula ambacho yeye anakipika ila Sarah na Erica waligoma huku wakidai kuwa wameshiba sana, kisha wakamuaga na kuondoka zao. Njiani Sarah akasema,“Ila huyu mama Elly anajikaza tu, sema anaonekana ana shida sana”“Ni kweli ana shida, ni baba ndio huwa ana msaidia, mwanzoni nilikuwa namuona ni mtu mbaya sana ila badae niliona hana tatizo lolote lile. Sijui ilikuwaje maana Erick alikuwa hampendi huyu mama hata kumsikia”“Duh!! Erick nae ana matatizo sana yule, najua utamwambia sababu ni pacha wako ila ana matatizo sanba yule”Njiani walikutana na Emmanuel ambaye alikuwa ameongozana na Emmanah, ndipo Erica alipoanza kuongea nao,“Halafu nyie kwanini hamkutaka kuja kuhudhuria sherehe”“Mama mkubwa alitukataza, ndiomana hatukuja”“Basi, kesho naomba mje nyumbani kwetu”Emmanah akauliza swali,“Hivi wewe Erica, si Erick ndio pacha wako? Na huyu ni nani?”“Aaaah huyu ni ndugu yangu anaitwa Sarah”“Yani mlivyoongozana kama mapacha vile”Erica alicheka, hata Sarah nae alicheka na kusema,“Unajua mimi hata kuna watu huwa wananifananisha na mama yao na hawa, kipindi hiko sijui kama ni ndugu zangu ila kwasasa sina shida sababu ni ndugu zangu”“Erick sasa, kawapita urefu maana nyie ni wafupi”“Hapana, sisi sio wafupi ila sisi sio warefu. Jamani watu wafupi ni wafupi sana, yani sisi sio warefu kama Erick ila sisi sio wafupi. Ila ni sawa na wewe na huyu Emmanuel maana yeye mrefu na wewe sio mrefu”Wote wakacheka tu, na Erica aliendelea kuwasisitiza kuwa wasikose kwenda nyumbani kwao kwa siku ya kesho kama alivyoongea nao. Kisha waliagana pale.Mama Angel akiwa na Dora kuangalia ile nyumba, alifurahi sana kwani Dora aliweka karibia kila kitu kilichohitajika katika ile nyumba,“Kwakweli hapa Dora umefanya kazi kubwa sana”“Asante, nashukuru kwa hiyo sifa”“Itabidi hii hela nyingine tuwapatie wenyewe kwaajili ya maisha”“Ila kwa tabia ya Junior ilivyo ndugu yangu, wanaweza kutumbua hiyo hela yote na maisha kuwashinda ingawa wana nyumba. Sikia kitu, kule ofisini kwa babake Junior nako wamesema wanachanga. Vitu hivi nimenunua mimi pamoja na yule aliyekuwa mshirika wa James kwenye kazi zao, naweza sema alikuwa ni bosi wa James, kwahiyo hapo lazima tufikirie kitu wanachoweza kufanya wakina Junior ili kuboresha maisha bila ya hivyo basi hata vitu vya ndani humu Junior atauza vyote, sijui akili mbovu kaitoa wapi yule, yani babake hata hakuwa na akili mbovu kiasi kile”“Ila hata huko ofisini nawapongeza sana, ni ofisi chache sana ambazo muhusika anakufa ila bado wanakumbuka fadhila zake na kusaidia kizazi chake, ni ofisi chache sana, nawapongeza kwakweli”“Yani james licha ya yale mauzauza yake ya uhuni ila alikuwa ni mtu wa watu sana, pale ofisini kila mtu ukimuuliza atakwambia kuwa ana historia ya kusaidiwa na James, mwingine utasikia James aliokoa maisha ya mama yangu, mwingine James alinitoa gerezani mimi, ningekuwa jela bila yeye. Kama huyu aliyenunua vitu vyote humu ndani huwa anaongea sana, sijui alifanya madudu gani, akahukumiwa kifungo cha miaka thelathini na tatu jela au dhamana ya shilingi milioni ishirini na nane, unaambiwa alijua lazima afie gerezani ila James alitoa hela hiyo na rafiki yake kuwa huru, kwakweli James alikuwa akisaidia sana kipindi alipokuwa na hela, starehe alifanya sana ila na misaada alitoa sana ndiomana wanakumbuka watoto wake”“Duh!! Kweli lakini, James alikuwa na moyo wa kusaidia, namkumbuka vizuri isingekuwa kunitaka sababu ya tamaa yake basi siku zote angebaki kuwa shemeji bora kwangu”“Haya, tujadiliane sasa cha kufanya na Junior”“Naona ni vyema nikamuulize Vaileth kuwa anaweza kufanya biashara gani, halafu tufungue biashara ambayo itasimamiwa na Vaileth ili waweze kusonga mbale kimaisha.”“Oooh hiyo nzuri, halafu mimi nitajaribu kuongea nao pale ofisini kwa baba yake ili kama inawezekana wamtafutie Junior kazi yoyote pale, maana akiwa busy itapunguza usumbufu wake na kuhangaika”Waliongea mengi sana na kupatana juu ya hilo, kisha waliagana na kuanza kuondoka ambapo mama Angel alikuwa akielekea nyumbani kwake ila njiani alikutana na rafiki yake Johari ambapo alisimamisha gari na kusalimiana pale kisha Johari alimuuliza,“Hivi mume wangu kaja huko kwenu hivi karibuni?”“Hapana, kwani vipi?”“Kwakweli haeleweki, kuna mambo anayafanya nyumbani haeleweki kabisa, utamkuta kasimama kasema aaargh Erick, huwa simuelewi kwakweli”“Mmmh!! Hebu mfatilie kwa makini, mbona ni ajabu?”“Unajua namshangaa, bora nimekutana nawe nimeweza kukuuliza, yani huwa simuelewi kwakweli kuwa ana maana gani kufanya vile”Waliongea kidogo tu na kuagana.Yani Erica alipokuwa nyumbani alijikuta akiwa na hamu sana ya kujua kile ambacho kimeandikwa kwenye ile barua na Sia, ila alishindwa kuichungulia sababu karibia muda mwingi alikuwa karibu na Sarah, kitu kile kilimfanya ashindwe kusoma.Mama Angel aliporudi moja kwa moja aliamua kumpelekea ile barua ambapo mama Angel aliiweka na kwenda kuoga kwanza, kisha alienda kuongea kidogo na Vaileth ili ajue jinsi inavyoendelea hapo nyumbani kwani kwa siku hizo walimkatalia Junior kutoka walimwambia mtu akitoka kuoa kuna siku ambazo anatakiwa kukaa ndani kwahiyo lazima atomize siku hizo,“Eeeh Vaileth, hapa nyumbani mnaendeleaje? Junior hasumbui kweli?”“Hapana mama, hasumbui na tunaishi vizuri tu”“Haya, ukikaa nae vizuri hebu jadiliana nae kuwa ni kitu gani anapenda. Kumbuka kwasasa, wewe na yeye ni mke na mume, wewe hutoendelea kufanya kazi hapa bali mtaishi pamoja, ila kabla ya kuishi pamoja sisi kama wazazi tunahitaji kuwaandalia nyie mazingira ya kuwawezesha kuishi pamoja kwa amani. Hebu nikuulize wewe, katika maisha yako kitu gani unapenda kufanya?”“Mmmh mama, mimi sijasoma maana niliishia kidato cha pili tu na kupata mimba, kwahiyo sijui nitafanya kazi gani”“Hamna Vai, mambop ya kufanya bado yapo haijalishi umesoma au hujasoma, katika maisha makosa huwa yanatomkea, ila yanapotokea ni muda wa kujifunza kutokana na makosa ili usiweze kuyarudia tena, kwahiyo usijali, kitu gani ulikuwa ukipenda kufanya?”“Mmmh mimi nimewahi kutamani kushona nguo”“Oooh kwahiyo unahitaji kujua cherehani?”“Ndio mama”“Sawa, ni vizuri kama ni hivyo, kwahiyo wewe ni kujifunza cherehani na kukununulia tu vifaa kisha uanze kazi ya kushona! Basi hakuna tatizo, tutafanikisha tu hilo swala”“Kwakweli mama hata huwa sijui niseme kitu gani kwa jinsi ambavyo unanisaida, kwakweli unanifanya kama binti yako kabisa”“Usijali, wewe ni binti yangu. Napenda uishi kwa amani, sijawahi kugombana na wewe, hujawahi kunijibu vibaya, kukiwa na kosa nitakufokea na utanielewa, halafu nakupenda sababu wewe ni mwepesi wa kuomba msamaha, kwahiyo naishi nawe kama binti yangu, sijakuona na kasoro yoyote sijui tabia mbaya, sijui manini huko, upo vizuri sana Vaileth, usijali yani usiniogope kabisa uwe unaniambia kila kitu halafu tutajua jinsi ya kusaidiana”“Sawa mama, nashukuru sana”“Hekima na nidhamu uliyonayo ndio silaha kubwa sana kwako na ndio kitu kinachofanya upendwe na kila mtu”Basi mama Angel alimuacha Vaileth pale na moja kwa moja kwenda chumbani kwake kuendelea na mambo mengine.Wakati wa kulala, mama Angel alimueleza baba Angel kuhusu alichokifanya Dora kwaajili ya wakina Junior,“Kumbe kuna kipindi Dora uwa anakuwa na akili eeeh!!”“Siku hizi Dora kawa vizuri sana”Mama Angel akakumbuka ile barua aliyopewa na Erica na kuamua kuichukua muda ule na kuisoma, kisha kumpa mumewe,“Hii barua, wakina Erica wanasema kuwa wameitoa kwa Sia, anasema eti niwasiliane na Rahim mmmh!!”“Huyo Rahim kaonana muda gani na Sia?”“Mimi sijui kwakweli, nadhani wenyewe ndio wanajua. Je vipi, nimpigie huyo Rahim?”“Hakuna kumpigia usiku huu, kwanza anachofahamu yeye ni kitu gani mpaka kutaka kutafutwa mwenyewe? Mimi sitaki kabisa, kwanza huwa simuamini huyo Rahim”“Mmmh ila anasema ni mambo ya familia yetu”“Hata kama, siku akikupigi simu mwambie aje kuongea na mimi maana mimi ndio baba wa familia kwahiyo ndio mwenye familia, kila kilichopo hapa kipo chini yangu. Mwanaume huwa anaitwa nani katika viungo vya mwili!”“Kichwa”“Eeeeh mimi ndio kichwa, kwahiyo natakiwa niongoze familia nzima, kichwa ndio kinaonyehsa cha kufanya halafgu vingine vinafatia, mwambie Rahim aje kuongea na mimi na si vinginevyo”“Sawa mume wangu, nimekuelewa”“Tulale tu, hayo mambo ya Rahim huwa sitaki hata kuyasikia”Basi waliamua tu kulala kwa muda huo.Baba Angel alipoenda ofisini kwa siku ya leo, alipigiwa simu na mwalimu wa Angel akipewa taarifa kuwa siku ya Jumamosi ndio siku ambayo shule imepanga kuwepo kwa mahafali ya wanafunzi wao,“Wanafunzi wetu wote tutawaaga hapa kwenye kiwanja cha shule yetu, ndiomana hawakuondoka. Karibuni sana”“Sawa mwalimu tutakuja tu huko hakuna tatizo”Basi baba Angel aliagana na mwalimu na kuanza kufikiria pale vitu vya kununua kwaajili ya zawadi ya Angel, ila muda sio mrefu alifika yule bibi ambaye huwa anauza matunda, baba Angel alifurahi kumuona ili amuulize maswali yake ambayo alikuwa ameyaandaa kwake, ila yule bibi ndio alianza kuongea,“Kwanza ninakushukuru sana bosi kwa kunikutanisha na kijana wangu Juma”“Oooh nashukuru, ila kuna maswali kadhaa nilitaka kukuuliza”“Niulize tu”Mara simu ya yule bibi ilianza kuita, na kumfanya yule bibi aombe samahani kwanza kwa baba Angel,“Samahani, ni binti yangu Juli ndio anapiga”Basi yule bibi alipokea na kuongea nayo kwa muda, kisha alimtaka baba Angel kuweza kusalimiana na huyo Juli, baba Angel alichukua simu na kusalimiana nae ila ile sauti ilikuwa kama sauti anayoifahamu na kuamua kuuliza,“Mbona sauti yako kama naifahamu?”“Hata mimi sauti yako kama naifahamu, wewe sio Erick kweli? Uliniambia mkeo anaitwa Erica na binti yako mkubwa anaitwa Angel!”“Oooh kumbe wewe ni Juli yule uliyekuwa ukinifanyia usafi!!”“Ndio mimi bhana”Walianza kuongea mengi tu, kisha kuagana na baba Angel alimtazama mama Juli na kumwambia vile ambavyo anafahamiana na binti yake,“Kuna kipindi nilikuwa mkoa Fulani huko, halafu huyu Juli ndio alikuwa akinifanyia usafi kwenye chumba changu. Nimefurahi sana kufahamu kuwa wewe ndio mama mzazi wa Juli”Basi walichekeana pale na kuongea mengi sana hata baba Angel alisahau mambo ya kumuuliza maswali yule mama.Baba Angel aliporudi alimwambia mkewe juu ya mahafali ya binti yao Angel, basi mama Angel aliona ni vyema kuanza maandalizi ya zawadi ya kumpatia binti yao,“Ila hivi Angel tumpe zawadi gani afurahi?”“Mmmmh sijui, maana Angel mara nyingine huwa haeleweki tofauti na huyo Erica”“Ni kweli, Erica ni mtoto wa tofauti sana. Kwa kifupi Erica ni mtoto mzuri tukitoa tu hilo swala lake la umbea”“Ila muulize Erica, tumnunulie zawadi gani dada yake halafu Erica atasema, najua zawadi ambayo Erica atamchagulia Angel ni lazima Angel ataipenda maana Angel huwa anampenda sana Erica”“Kweli kabisa usemayo”Walijadiliana mambo mengi sana.Kulipokucha, mama Angel aliamua kwenda kuongea na Erica kama ambavyo baba Angel alimuagiza, basi alimwambia,“Mwanangu, Jumamosi ni mahafali ya dada yako. Tumnunulie zawadi gani, tumefikiria hatuajua”“Mmmh sijui ila ningekuwa mimi ningependa mninunulie zawadi ambayo inanikaa mwili mzima yani nikitoka navaa zawadi zenu tupu”Mama Angel alicheka na kumuuliza,“Zawadi gani hiyo?”“Yani, kuanzia nguo ya ndani hadi kiatu na mkoba, nadhani mmenielewa”“Duh!!”“Kwahiyo hujapenda mama?”“Hapana, ni sawa tu hakuna tatizo”Basi mama Angel alipoondoka hapo aliwasiliana na mume wake na kwenda kufanya hiyo kitu pamoja hadi waliporidhika na kuongeza zawadi zao nyingine.Siku ya mahafali, baba Angel aliondoka na mama Angel tu kuelekea shuleni kwakina Angel kwaajili ya mahafali, walifika pale na walikuta watu wamejaa sana tu ila kila wazazi walipofika walipewa namba za viti kwahiyo kila mzazi alikuwa na namba yake ya kiti cha kukaa.“Baba Angel na mama Angel, namba zenu ni hizi nne na tano”Wakapokea zile namba na moja kwa moja kwenda kukaa kwenye zile siti zenye namba zao, ila mama Angel alipotazama pembeni alishtuka kidogo kwani pembeni yao walikaa watu wanaowafahamu vizuri tu, mama Angel akamshtua mumewe ambaye nae alishangaa kuona pembeni yao wamekaa Rahim na dokta Maimuna. Wakapokea zile namba na moja kwa moja kwenda kukaa kwenye zile siti zenye namba zao, ila mama Angel alipotazama pembeni alishtuka kidogo kwani pembeni yao walikaa watu wanaowafahamu vizuri tu, mama Angel akamshtua mumewe ambaye nae alishangaa kuona pembeni yao wamekaa Rahim na dokta Maimuna.Baba Angel anamuuliza mke wake,“Hii inamaana gani?”“Hata mimi sielewi”“Inamaana Rahim kajua kama leo ni mahafali ya Angel au ni kitu gani?”“Sielewi kwakweli, unajua nabaki kushangaa tu. Hata hivyo angejuaje kama Angel anasoma shule hii na ikiwa tumejitahidi kumficha tuwezavyo!”“Itakuwa umemwambia wewe Erica”“Hapana, siwezi kufanya hivyo, na kwanini nifanye hivyo? Hapana kwakweli”Basi baba Angel alimuomba mama Angel waondoke eneo lile maana hakutaka kukaa pamoja na wale watu, ila Rahim na mkewe dokta Maimuna hata hawakuwaona baba Angel na mama Angel maana walikuwa wanachezea simu zao tu, yani kila mmoja alikuwa makini na simu yake.Basi baba Angel na mama Angel wakaenda kuomba nafasi nyingine na kubadilishana na wazazi wengine, ambapo walikaa na kuendelea kutazama kile kinachoendelea pale mbele,“Ila natamani tu hii mahafali iishe turudi nyumbani, nimeboreka kwakweli kumuona Rahim”“Hata mimi nimeboreka sana”Mara wakamsikia mwalimu akitangaza,“Kuna wanafunzi wawili wameandaliwa kwaajili ya kusoma lisala, mmoja kutoka shule ya wasichana na mwingine kutoka shule ya wavulana”Basi mama Angel na baba Angel walitazamana, na walipoangalia vizuri ndio walijua kuwa kuna wanafunzi wa kiume na wa kike,“Kheee kumbe wamefanya mahafali ya shule mbili!!”“Naona, nilijua ni moja tu”Kisha mwalimu akatangaza kwenu,“Naomba niwakaribishe hawa wanafunzi, Angel Erick atasoma risala ya shule ya wasichana na Samir Rahim atasoma risala ya shule ya wavulana”Hapa mama Angel na baba Angel waliangaliana kwa mshangao, ila walipowaangalia hawa watoto wao vizuri ndio walibaki kushangaa tu,“Kumbe yule Samir kamfata Angel hadi huku!! Kwahiyo walisoma shule zinazohusiana!! Kheeee watoto hawa jamani!!”“Unajua mpaka muda huu nashangaa, nimejitahidi kwa kila hali kumficha Angel kuhusu shule ambayo anaenda kusoma, ili asimwambie Samir, sijui imekuwaje tena wamesoma shule zinazokaribiana!!”Yani baba Angel na mama Angel walijikuta wakiongea tu kiasi kwamba hata ile risala iliyosomwa na vijana wao hawakuisikiliza kwani walikuwa kwenye mshangao tu kwa muda huo.Basi ratiba zingine ziliendelea kama kawaida, hadi muda ya kugawa vyeti na zawadi uliwadia ila bado mama Angel na baba Angel walikuwa wakiongea tu na kustaajabu yale yanayotukia mahali pale.Muda wa chakula, ndipo Rahim nae alipowaona baba Angel na mama Angel na kuwafata, kisha aliwasalimia na kusema,“Kumbe Angel mlimleta shule hii? Au Angel niliyemsikia sio mwenyewe!”Walikuwa kimya kwa muda, kisha mama Angel alimuuliza,“Kwani wewe umekuja kufanya nini hapa?”“Kijana wangu Samir, kahitimu pia kidato cha sita, shule ya wavulana. Tumeambiwa wote tuje hapa maana mahafali inafanywa moja tu kwa wote”“Kheeee kwahiyo Samir ni mwanao?”“Ndio, ni mwanangu kwani unamfahamu?”Mama Angel alibaki kimya kwa muda kidogo na kujidai kuwa hamfahamu Samir, basi Rahim akamwambia mama Angel,“Hata hivyo nina maongezi na wewe”Baba Angel alimuangalia Rahim na kumwambia,“Huu sio muda wa maongezi”Kisha akamvuta mkewe mkono na kwenda kukaa nae sehemu nyingine huku wakiendelea kupata chakula, ila kiukweli mama Angel alijikuta akipata mawazo ya gafla, kwani hapo ndio akatambua wazi kuwa Angel na Samir ni ndugu, kitendo kile kilimpa mawazo zaidi kwani anajua ni jinsi gani Angel na huyo Samir wanavyofatana fatana, maana hata kuwa hapo kwenye hiyo shule karibu hakujua kuwa imekuwaje.“Mbona mke wangu unaonekana kuwa na mawazo?”“Aaaah hapana sina mawazo wala nini”“Upo sawa kweli?”“Ndio nipo sawa hata usiwe na wasiwasi na mimi”Basi waliendelea kula, na kisha kuwa karibu na binti yao na kumpongeza, ila baba Angel hakutaka kupoteza muda kwani aliona mahafali imeisha basi akamtaka Angel na mama yake aondoke nao ili kama kusherekea wakamalizie nyumbani, Angel alikubali tu ila aliwaomba kwanza akaage rafiki zake.Wazazi wake walikubali ila walikuwa wakimuangalia anayemuaga, ambapo moja kwa moja Angel alienda alipo Samir na kuagana nae, kisha kukumbatiana nae, kwakweli mama Angel alisikitika tu.Angel alirudi na moja kwa moja walipanda nae kwenye gari na safari ya kurudi nyumbani ilianza.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment