Simulizi : Umenifungulia Dunia
Sehemu Ya Nne (4)
Baada ya kukuru kakara nyingi na kelele na taabu za kutosha, hatimae Victor alifanikiwa kumrejesha Salama mikononi mwake kwa msaada mkubwa wa Joy. Victor hakutaka tena kuchelewa, haraka haraka alikwenda kuwaona wazazi wa Salama na kukaa nao meza moja hadi walipomalizana.
Haikuwa hata na wiki moja mbele akamvalisha pete ya uchumba na kumfungulia biashara palepale Mwanza maeneo ya Liberty. Joy nae haikuwa haba, alinufaika kidogo kwa kulifanikisha lile.
Mgasi nae alikuwa hajakata tamaa ya kumpata Salama, aliendelea kuwasiliana nae na kuchombeza vilevile, sasa hiki ndio kipindi ambacho Salama akamueleza Mgasi ukweli kuwa sasa tayari yeye ni mchumba wa mtu. Akamuomba tu asimsumbue tena.
Ilikuwa ni ngumu sana kwa yeye kuelewa, lakini kwa kuwa ni mtu mkubwa na pia ana akili timamu, ilifika hatua akakubali matokeo, siku hiyo aliyokubali kushindwa, ndio siku ambayo Mgasi alimpigia simu Mwinyi na kumuuliza alipo.
Walipanga wakutane nyumbani kwa Mwinyi siku ileile jioni mara wakitoka kazini, maana siku hiyo Mgasi hakwenda. Walipokutana Mgasi alimueleza Mwinyi kila kitu kinachoendelea kwa Salama, bila kumweleza juu ya kumtokea
Mwinyi alishangaa sana kusikia Mgasi ana mawasiliano na Salama, Mgasi alicheka tu akashika simu yake.
“Sasa kaka naomba basi namba yake ya simu?” aliomba Mwinyi
“Aaah, Mwinyi hapana bhana, utamuharibia, we si aliisha kupa nafasi ukaichezea? Sasa acha atulie na alie nae, mi sitakupa namba”
“Ah sawa kaka, siku zote mwenye bahati mbaya, ni sawa na kusema hana bahati kabisa”
“Unamaanisha nini?” aiuliza Mgasi huku akimtazama Mwinyi
“Hata wewe umekuwa wa kunitenga Mgasi? Siamini ndugu yangu” Mwinyi aliongea kwa huruma sana huku mkono ukiwa shingoni upande wakushoto, huruma ikamuingia Mgasi
“Nakupa namba kwa masharti”
“Mh” Mwinyi aliitika huku akibadili pozi la kukaa, sasa akakiegamia kiti alichokalia kama vile hataki tena, Mgasi akaendelea
“Usimpigie simu asubuhi sana, wala usiku na hata wakati wa chakula cha mchana, sawa?”
“Kuna linguine?” Aijibu Mwinyi kwa njia ya swali, Mwinyi akamjibu
“Usiongelee suala la mapenzi nae, upo tayari?” huku akitabasamu akajibu
“Nipo tayari” Mgasi akachukua simu ya Mwinyi na kuiandika namba ya Salama na akamuomba amuahidi atatii masharti yale.
Juhudi za Anisa kumtia tena mikononi Mwinyi zilionekana kuishia ukingoni. Mwinyi hakupenda kudharauliwa kabisa yaani hata kwa utani, aliamini japo hakuwa na pesa ya kutosha kushindana nao, lakini pesa ya kula tu haikumsumbua.
Kila mara aipopigiwa simu na Anisa, aliikata na hata alipoipokea kwa bahati mbaya aidha kwa kutokujua namba, maana wakati mwingine Anisa alibadili namba maksudi ilimradi tu Mwinyi apokee na kuongea nae, lakini kila alipopokea na kugundua kuwa anae ongea
nae ni Anisa, alikata simu palepale.
Ujumbe wa simu aliotuma haukujibiwa na hata alipokwenda kwa Mwinyi mara kadhaa aikuta mlango umefungwa. Ila kuna mara moja ilikuwa ni asubuhi na mapema aliukuta mlango ukiwa wazi na alipojaribu kuingia ndani alifukuzwa kama mwizi. Kwa aina ileile Mwinyi alivyofukuzwa kwao.
Mara nyingine alikwenda jioni na kukuta mlango ukiwa umerudishwa tu. Aiingia na kumkuta Mwinyi yupo Sitting room kiwa na msichana mwingine. Wala Mwinyi hakushughulishwa nae, kila Anisa alipotaka kumsemesha, Mwinyi aijidai yupo ‘busy’ na mpenzi wake.
Alinyanyuka Mwinyi na kuingia chumbani kwake na mpenzi wake akimuacha Anisa pale kwenye masofa. Alikaa pale hadi usiku bila Mwinyi kutoka chumbani kwake. Hakuwa na la kufanya zaidi ya kuondoka na kurejea kwao akiwa hana amani kabisa.
Kabla hajaondoka alichukua Counter book kutoka kwenye mkoba wake wa chuo na kuchana karatasi kisha akaandika ujumbe uliosema
“Kwanza nashukuru sana kwa kuweza kuniruhusu kuingia ndani na kukaa hapa ambapo ni muda sasa sijaingia na kuketi hivi. Lakini hilo sio lililonileta. Mwinyi, naomba usinihukumu kwa kosa lisilokuwa langu, kwanini unaniadhibu kwa kosa lisilonihusu?
Tafadhali kumbuka, hata mimi nina moyo, tena sio wa chuma bali ni wa nyama kama wa kwako. Moyo wangu unapotendewa sio, unaumia pia, kwanini unaniumiza moyo wangu? Mwinyi mimi nimekusamehe yote uliyonifanyia nyuma.
Ni mengi tu nayakumbuka kama vile kunifukuza kwako, kunikatia simu na hata hili la leo... najua ni ghadhabu tu, nami natumia fursa hii kukuomba msamaha japo ninaamini sina kosa. Ninatambua waliokukosea ni wazazi wangu, nawe unajua hilo basi naomba kutumia muda huu kuwaombea msamaha, nawaombea radhi wazazi wangu, ninaamini hawajui ni kiasi gani mtoto wao nakupenda!
Sijakata tamaa, nitarudi tena siku nyingine, nakupenda sana Mwinyi, sijawahi penda kama hivi nilivyokupenda wewe,” Anisa akawa amemaliza barua yake.
Alipotoka pale akaelekea moja kwa moja kwa Mgasi na kumueleza kila lililotokea muda mchache uliopita. Mgasi akaahidi kumsaidia kwa kuongea na Mwinyi.
Akamwambia Anisa afanye kila analoweza, siku ya Jumamosi mchana waweze kuonana maeneo ya mnadani Ipuli. Anisa akatabasamu na kutikisa kichwa akifurahi, aliamini sasa inawezekana suala la kukutanishwa na Mpenzi wake.
**********
Kasi ya penzi la Salama na Victor ilikuwa ni kubwa sana, muda wote walikuwa pamoja. Victor alimzuia Salama kufanya chochote ila tu kukaa dukani pale maeneo ya Liberty jijini Mwanza.
Siku ya Ijumaa mchana, Salama akiwa dukani anaongea na mteja wake aliekuwa ametokea Ukerewe kufuata mzigo waJumla, simu yake ikaita.
Namba hakuitambua, ila hilo haikumpa taabu, maana tayari yeye aliisha kuwa ni mfanya biashara, hivyo suala la namba yake kusambaa wala halikumsumbua.
Alipokea na kusalimiana na Mpigaji, sauti ilikuja kichwani moja kwa moja, ghadhabu ilimpanda akajitahidi kuidhibiti. Waliongea kawaida tu kwa kuulizana habari za masiku. Hakika upande wa Mwinyi alikuwa anaona fahari sana kuongea na Salama.
Waliagana kwa ahadi ya kuzidi kuwasiliana japo Salama hakutaka kabisa kitu hicho kiendelee, maana tayari kichwani mwake aliisha mfuta Mwinyi. Upande wa Mwinyi alipata nafuu
Ama tuseme ahueni na kuamini ule ni mwanzo mzuri kwake.
Jumamosi ilifika, Mwinyi na Mgasi wakatoka kuelekea mnadani maeneo ya Ipuli, hakumwambia juu ya miadi ya kukutana na Anisa maeneo hayo.
Kule waliagiza vinywaji na nyama choma. Ghafla wakaiona gari ya Anisa ikiwasili, mtu wa kwanza kuiona alikuwa ni Mwinyi, akamuonyesha Mgasi.
Mgasi alinyanyuka na kwenda kumfungulia mlango Anisa na kumleta pale mezani. Anisa alifika pale mezani na kumsalimia Mwinyi, hata hakuitika bali alinyanyua kinywaji chake na kubugia.
Aipokishusha mezani akasema huku akimnyooshea kidole Anisa lakini akimtazama Mgasi
“Mgasi ungejua walichonifanyia huyu na wazazi wake na wakati hawa ni watu wakuja tu, hata usinge mshobokea, hafai kabisa huyu” Muda wote huo bado Anisa alikuwa amesimama, Mgasi akamvutia kiti na kumtaka akae.
Anisa alikaa akiwa hajiamini.kiukweli kabisa Mwinyi hakuwa akimtamani kabisa Anisa, hasa kwa dharau kubwa sana waliomuonesha wazazi wake Anisa.
Hakutaka hata kumuona, lakini kwa uwepo wa Mgasi pale alifanikiwa kuwaweka bila kugombana. Mgasi alimtazama Mwinyi, ambae muda wote alikuwa akitazama pembeni bila kumuangalia Anisa hata mara moja.
Mgasi akamsemesha
“Mgasi, najua unaona kosa alilokufanyia Anisa ni kubwa sana?”
“Kupita Dunia na ni nzito kuliko vilivyomo vyote,” kisha akaendelea huku akimtazama Mgasi
“Hivi kama ni wewe utafurahi kuitwa Ngedere? Utafurahi kunyanyaswa kwenye ardhi ambayo babu yako aliikomboa kwa taabu na dhiki kubwa na manyanyaso?” akatulia na kuangalia kiatu chake baada ya kuhisi kuna mdudu anamtembelea, aliporidhika na kuhona hakuna chochote kibaya, akaendelea kuongea
“Tena inavyosemwa hata watu hawahawa walishiriki kuwanyanyasa wazazi wetu ambao katka historia tunasoma, leo tena aje aninyanyase na mie? Si utakuwa ni upumbavu huo? Nmimi sipo tayari. Unakumbuka wazee wetu tuliwaona wajinga sana kutawaliwa na watu wachache, vipi leo mimi nidharauliwe na popo hawa?” aliuliza kwa uchungu, huku akimkata jicho baya kabisa Anisa.
Mgasi akagundua kuwa, busara ilihitajika, akamtuliza Mwinyi
“Najua inauma na inakera sana, sasa labda nikuulize Mwinyi, ni nani alikuita Ngedere?”
“Muulize huyo anajua ni kina nani waliniita jina hilo,” huku akimnyooshea kidole Anisa.
“Sasa nimuulize yeye kwani ndie aliesema maneno haya usemayo rafiki yangu?” Mgasi alikuwa anajaribu kumuweka sawa kidogo Mwinyi na kumfanya amsafishe Anisa.
“Si yeye, ila huyu alitumwa kuniita na kunipeleka kwao ili mimi niende kutukanwa na kudhalilishwa, yaani sitamani hata kumsikia licha ya kumuona,” akageukia upande wa pili.
“Aaanh Mwinyi hapo sasa unakosea, mbona unaongozwa na hisia?” Mwinyi hakujibu bali alitoa simu na kuanza kubofya bofya. Mgasi akatikisa kichwa na kumgeukia Anisa
“Anisa ilikuwaje ukamchukua Mwinyi na kumpeleka kwenu akatukanwe?” aliuliza kama mtu anaetaka kuwapambanisha
“Hapana Mgasi, mi siwezi kufanya hivyo, wazazi waliniambia wanataka kumuona mkwe wao, ndio sababu mie nikampeleka, ninaapa kwa Mungu mimi ninampenda sana Mwinyi”
Ikasikika sauti ya Mwinyi ikisonya kisha akaongezea
“Tangu lini kukawa na mapenzi kati ya binaadamu na Ngedere? Labda ni kwa ajili ya kumfuga tu... Yaani hujui tu we mwarabu koko, nawachukia nyie hadi maua yenu, Pumbavu.” akasonya tena na kugeuka upande wa pili.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sio tu Anisa alieuona ugumu wa jambo lile, bali hata Mgasi akachoka kabisa, ila akakomaa na kumshika mkono Mwinyi, akamwambia
“Mwinyi nina hakika kabisa kuwa hata wewe umewahi kufanya
makosa na ukasamehewa, uongo?” aliuliza Mgasi kwa sauti tulivu mno yenye hekima kubwa ndani yake.
“Ah! Binadamu yoyote ni lazima akosee”
“Sasa basi alie mbora ni Yule anaegundua kuwa alichokifanya ni kosa, kisha akaomba msamaha, nasema uongo?”
“Acha siasa bhana, kusamehe si ni hiari ya aliekosewa?” aijibu Mwinyi kwa kebehi.
“Upo sawa kabisa, lakini tambua mbora zaidi ni Yule alieombwa msamaha na akasamehe”
“Kwa hiyo mtu utakuwa unafanya makusudi kumkosea mtu kwa kutegemea msamaha eti?”
“Sio hivyo, bahati mbaya hutokea tu kama ajali, haina muda ndugu yangu! Mwinyi samahani, hebu msikilize asemacho Anisa, mbona unamuadhibu kwa kosa lisiomstahili?”
Mwinyi alifikiri kwa sekunde kadhaa na kumtazama Anisa, kisha akamwambia aseme kilichompeleka pale. Mbele ya watu waliokuwepo pale mnadani, walikuwa ni watu wengi sana, lakini Anisa akanyanyuka kwenye kiti chake na kupiga magoti mbele ya Mwinyi na kumuomba msamaha.
Mwinyi hakuwa na huruma hata chembe! Akamjibu
“Nimekusamehe, nyanyuka uende,” akageukia upande w pili. Kauli ile ilimchanganya hata Mgasi, sio Anisa peke yake ambae sasa machozi yalionekana yakimlenga kabisa
“Kha! Mwinyi ndio nini sasa? Acha kuwa na kisasi kama mwanamke wewe, unataka ufanyiwe nini sasa ili yaishe? Unakera mno na wewe” hata Mgasi sasa alihamaki.
Jibu la Mwinyi ndio likamzidishia hasira hasa aliposema
“Nataka nipigane nao hawa wote tena palepale kwao ndio nitaridhika na hasira zangu zitaisha,” wakamshangaa
“Mwinyi umechanganyikiwa?” Mgasi aliuliza huku akimshangaa
“Ndio” akamjibu huku akijiegemeza kwenye kiti, Mgasi akaona sasa ni kweli rafiki yake kachanganyikiwa. Kawa sio Mwinyi Yule anaemjua. Ikabidi yeye sasa awe mpole ili waweze kufikia muafaka.
Akaanza kumpa nasaha za aina mbalimbali na kumkumbusha jinsi jitihada alizozifanya Anisa mara ya kwanza wanapoonana na Salama wakati yeye alikuwa ameisha likoroga. Akamkumbusha ni kiasi gani Anisa alipambana na hadi kufanikisha kumrudisha Salama mikononi mwake.
Mwinyi alilainika na kumpa mkono Anisa aliekuwa amepiga magoti bado akamnyanyua na kumwambia aketi kwenye kiti alichokuwa amekaa awali.
Anisa alikuwa ni kama mtu asieamini hivi. Alikuwa anataka kusema kitu lakini alikuwa akishindwa kukisema.
Mgasi aliekuwa Mwenyekiti wa kikao kile cha dharula, akaliona hilo kwa Anisa, akamwambia kama kuna kitu anataka kuongea, basi atumie muda ule kuongea. Mwanzo alikuwa akionekana kumuogopa Mwinyi, lakini Mgasi alimtoa shaka.
Hiyo ndio nafasi aliokuwa akiihitaji, akaitumia vema kwa kumuhakikishia Mwinyi kuwa anampenda Mwinyi peke yake. Kumbe hilo lilikuwa ni tatizo kwake, maana baada ya Mwinyi kujua kuwa Anisa anampenda kiasi kikubwa, akaweka kikwazo
“Anisa mimi nitakusamehe kabisa kwa roho nyeupe na kurudi kuwa wapenzi kama zamani iwapo tu utakuwa tayari kwa nitakayo mimi, sawa?” Mgasi sasa alikuwa akiwatazama tu, masikini Anisa bila hata kufikiria, akakubali sharti asilolijua.
“Muda huu baba yako na mama yako wapo wapi?” ilikuwa ni saa 12 jioni
“Wapo nyumbani, muda huu hupenda kukaa nje kwenye bustani,” Anisa alikuwa mpole sana muda ule.
“Nakupa sharti langu sasa ambalo tayari umeisha likubali si ndio?” akakubali tena bila kufikiria.
“Muda wowote nitakao kuhitaji nataka nikupate, ni hilo tu”
“Mwinyi mimi nakubali, lakini isiwe usiku wala muda ambao nitakuwa na wazazi nyumbani”
“Iwapo Anisa utashindwa sharti langu hili moja, mimi nafikiri
utakuwa umeshindwa wewe mwenyewe” Hakika sharti liikuwa ni gumu mno. Lilikuwa ni kama sharti la kukomoana. Mwinyi alijua kile anachokifanya bali wale wengine hawakujua chochote kilichokuwa ndani ya akili ya Mwinyi.
Anisa alikosa jibu na hata akili yake ilishindwa kumsaidia. Mgasi alipokutanisha jicho na Anisa, akaona jicho la kuomba msaada, akajaribu kumtetea
“Mwinyi acha kumuwekea vikwazo, kumbuka huyu anaishi na wazazi
Wake,”
“Mgasi, labda kwanza nikupe hongera, kazi aliyokuwa amekutuma Anisa, umeimaliza kitambo, tena kwa mafanikio, huu ni mkataba mpya tumeingia sisi nawe ukiwa kama shahidi, mkataba ambao aliukubali hapo awali, kwa hiyo kama sasa ameamua kubadilika, nami nitafanya hivyo pia,”
“Mh! Haya bhana, hili sasa limekuwa ni penzi la kisasi, twendeni tuondoke,” alisema Mgasi huku akinyanyuka.
Wakaigia garini Mwinyi akapanga dereva atakua Mgasi, nao wapenzi watakaa nyuma na safari ielekee moja kwa moja kwa kina Anisa. Mgasi akatekeleza, hadi mbele ya nyumba, mlango ulikuwa umefungwa, lakini gari iliposimama mlango ukafunguliwa.
Mgasi alishuka garini na kuvuka upande wa pili wa barabara, Anisa akafuatia kushuka na Mwinyi akashuka upande wa pili na kumuita Anisa aliekuwa ameanza kuingia ndani ya gari mbele upande wa dereva.
Mlangoni mwa nyumba yao aLisimama Mama yake, anamuogopa lakini si sana. Kilichomfanya asimjali mama yake ni ile ahadi waliyopeana muda mchache uliopita, akatoka garini, mlango wa gari ukiwa umewatenganisha, Mwinyi akamuuliza Anisa
“Unanipenda Anisa?”
“Kuliko sana na unajua hilo,”
“Ok! Nakupenda pia, naomba unikiss mdomoni,” Ulikuwa ni mtihani mgumu sana kwa Anisa kufanya kitendo kile mbele ya Mgasi na mama yake tena na watu wengine wakishuhudia.
Lakini kwa kuwa anampenda kutoka moyoni, akambusu kama alivyotaka Mwinyi, wakatazamana na kuagana, Anisa akaingia garini na Mwinyi akamfungia mlango, wapita njia wakapiga mbinja kwa kitendo kile, Mwinyi akavuka barabara kumfuata Mgasi.
Mama Anisa alishuhudia kila kitu alichokifanya mwanae, tangu wamefika hadi sasa ameingia garini, kwa hasira aliingia ndani na kubamiza mlango, na hicho hasa ndio Mwinyi alichokuwa amejipanga, kuwaumiza nao kupitia mtoto wao.
Mgasi akamuuliza kwanini amefanya kitendo kile mbele ya mama
Yake na Anisa.
“Wale wanatudharau sana sisi waswahili kwa sababu ya rangi zao, sasa nataka niwaonyeshe mie ni nani, mbona hapa bado wangu? Wale wataomba poo wenyewe,”
“Kwa kweli watanyooka! Haya bhana, kwa picha la leo, mie sina swali,” wakaanza kuondoka.
Siku kadhaa mbele, saa 12 jioni Mwinyi akampigia simu Anisa na kumwambia atoke nje waongee kidogo. Anisa akatokea mlango wa uwani wakati wazazi wake wakiwa sebuleni wakitazama TV. Pale nje kweli aimkuta Mwinyi pembezoni mwa ukuta wa nyumba yao pia aliweza kumuona Mgasi kwa mbali.
Walisaimiana kwa kukumbatiana na Anisa akaomba asikae sana maana baba yake akijua kuwa yeye hayupo ndani, atampiga sana.
“Unajua siku ile mama alifoka sana? Nusura anipige. Bahati tu baba hakuwepo, lakini hata hivyo nimenyang’anywa gari”
“Ha! Kwanini?” Mwinyi alishangaa utadhani gari alinunua yeye kwa ajili ya mpenzi wake.
“Kwa sababu mama alimuona Mgasi akishuka upande wa dereva, akasema gari ikiwa inaendeshwa na kila mtu itawahi kuharibika,”
“Pole mpenzi wangu, ipo siku haya yataisha,”
“Lini Mwinyi wangu?”
“Siku ambayo wewe utaamua, maana kila kitu kipo mikononi mwako,”
“Kivipi Mwinyi, mbona sikuelewi?”
“Tuliache hilo kwa sasa, kesho tutaliongelea zaidi. Nitakuijia saa 10 jioni. Leo nimekuletea zawadi mpenzi wangu,”
“Woow! Zawadi gani?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Subiri kisura wangu, mbona una haraka hivyo?” Mwinyi akatoa makopo ma3 ya bia na kumpa mawili Anisa.
Moja akalifungua na kunywa kidogo kisha akampa Anisa na kuyachukua yale yasiofunguliwa. Anisa alikuwa bado amesimama akishangaa na kusubiri zawadi yake. Akaona anaambiwa anywe pombe. Mshangao wake ukawa mkubwa
“Khaa Mwinyi! Acha utani wa hivyo, mimi leo sinywi pombe bwana,”
“Kumbe hunipendi, pombe yenyewe ya kopo, tena moja tu hutaki?”
“Sio kama sitaki, mi ninywe pombe hapa nyumbani? Naomba kwa hili
unisamehe,”
“Kwani umefanya kosa gani mpenzi wangu?” Mwinyi alimshawishi kwa kila lugha anayoijua hadi Anisa akakubali kuonja.
Hatimae kopo moja likaisha huku akilalamika ni chungu. Kwa mbali Mgasi alikuwa akishuhudia, akatikisa kichwa kwa masikitiko ila hakuwa na cha kufanya. Mwinyi akambusu Anisa na kumpa kopo lingine na kumwambia aingie nazo ndani atakunywa asubuhi maana tayari iliisha ingia usiku.
Anisa aligoma tena, kwa mapenzi makubwa na kupitia kile kinywaji kimoja alicho kunywa, Mwinyi alikuwa akimchezea chezea sehemu za mwili na huku akimlaghai hadi akakubali kuichukua na kuingia nayo ndani.
Akaichukua na kuificha kwenye kitambaa chake cha kichwani na kuelekea ndani kwa ahadi ya kukutana mchana wa siku ifuatayo. Mwinyi akambusu na kuanza kuondoka na Anisa akaingia ndani kwao.
Mwinyi alipofika kwa Mgasi alimkuta akitabasamu, wakagonga mikono yao huku wakiongea
“Twende zetu mie nimemaliza kazi niliyoipanga kwa leo,” Mgasi akatazama saa yake na kusema
“Dah! We ni nouma.. tangu saa 12 hadi saa hizi ndugu?”
“Mbona hii ya leo ni cha mdoli kaka? Subiri mchezo wa kesho, ndio balaa kabisa!”
“Tayari ujue kuwa umeishauza kesi kule ndani?”
“Na hio ndio hasa lengo langu, nachotaka ni kupotea amani kabisa ndani ya nyumba ile kama sio kuvurugika kabisa,”
“Kwanini sasa jamaa yangu? Huoni kuwa imetosha?” alimuuliza Mgasi huku akitaka kusimama
“Mh! Bado sana inatakiwa wao wenyewe wakubali kuwa mimi ni mtoto wa Kinyamwezi, mtoto wa kibongo, a.k.a wa hapa hapa,” huku
akijipiga kifuani kwa fahari
“Haya bhana, mimi nasubiri matokeo, maana kwa hali halisi mimi nimeshindwa kukushawishi wewe kuachana na jambo hilo,”
“Naam kaka, kwa hili ninaomba uniachie mwenyewe, sipendi kabisa
wewe uingie matatizoni,”
“Lakini hata sijui akili ya kutenda mambo haya unaitoa wapi, maana ni kama mtu aliejipanga kwa muda mrefu sana,”
“Hapana kaka, majaribu hutuongezea maarifa ingawa yanatuumiza.”
“Ni kweli hali hiyo hutupelekea kutumia akili zetu za ziada kunaweza kutufariji na kutupa wasaa wa kutafuta muafaka juu ya kile kinacho tukwaza,” wakiwa wamesimama nje ya nyumba ya Mgasi wakaagana.
Mwinyi aliita pikipiki iliokuwa ikipita na kuelekea kwake akiwa amemuahidi Mgasi kuwa watakutana kazini siku ifuatayo ambayo pia ni siku ya kuendeleza mapambano baina yake na wakwe zake, yaani wazazi wake na Anisa.
Saa nne asubuhi Mwinyi akiwa kazini, akapokea ujumbe wa simu toka kwa Anisa ukimjulisha kwamba alipigwa sana usiku uliopita ila akamwambia kuwa maelezo zaidi atampatia watakapo onana mchana lakini pia akamjulisha juu ya suala la yeye kunyang’anywa simu na mama yake.
Alisikitika sana kwa suala la Anisa kupigwa, bali alifurahi kuona ujumbe wake unafika japo ni kwa njia ya maumivu jwa mpenzi wake Anisa, ila zaidi ya yote aliamini lile alilolipanga kichwani mwake litatimia.
Alichokuwa akikisubiri sasa, ni muda tu muafaka wa yeye kukutana na Anisa ili aweze kumpa taarifa zote kamili tangu kilichojiri baada ya yeye kuingia kwao. Ni hicho tu ndio alikitamani.
Maandalizi ya ndoa kati ya Salama na Victor yalizidi kupamba moto, karibu kila kitu kilikamilishwa ni siku tu ndio iliokuwa ikisubiriwa na watu wengi kwa hamu kubwa, takriban ni wiki moja tu iliokuwa imesalia kabala ya tukio lenyewe kukamilishwa.
Si Mwinyi wala Mgasi aliekuwa akimpata Salama, hakuna aliempata kwa namba yake ya mkononi na lakini hawakujua ni kwanini na kibaya zaidi hawakuwa na namba ya mtu mwingine yeyote wa kuweza kumuuliza.
Kama walivyokubaiana, mchana wa siku ile Mwinyi akiwa ameisha toka kazini kwake, kakaa chumbani akimsubiri Anisa. Haikuchukua
muda mrefu, Anisa akawa amewasili pae kwenye pikipiki, maarufu
kama bodaboda.
Mwinyi akampokea Anisa kwa mapenzi makubwa sana hadi Anisa akajiona kama Malaika na hali hana hata hadhi ya kuwa Malikia
“Mwinyi unajua kupenda, kwanin umenikatili kwa muda mrefu?” akamvuta Mwinyi na kuangaiana nae usoni kisha akaendelea
“Na kama ungeendelea kunipotezea, haki ya mama mimi ningejiua,”
“Pole mpenzi wangu, yale yameisha na ninaamini haitajirudia, uongo?”
“Kabisa mwanaume, nambie sasa,” Anisa akamsukuma Mwinyi kwenye sofa na kumkalia juu
“Hebu niambie kuhusu jana, ilikuwaje?”
“Mpenzi wangu, hukuwepo Mwinyi... Dah!” Anisa alianza kuongea huku akimchezea kidevu Mwinyi aliekuwa akimtazama.
“Ama jana nimepigika mie, hee… nimepigwa vibaya sana,” Mwinyi akahoji kizushi
“Kwa sababu gani sasa mrembo wangu?” huku nae akimchezea Nywele zake za kimanga
“Unajua baada ya kuingia ndani, nilijiona jasiri sana hata baba aliponisimamisha, nikampita tu, mbele nikakutana na Mama akanizuia kuingia chumbani...” hapa akacheka mwenyewe kwani sasa alikuwa akijiona ni mpumbavu kwa kitendo chake kile, kisha akaendelea
“Katika purukushani si ndio pombe yangu ikaanguka? He he heeee... hapana kabisa nami nimekuwa na majanga jamani!” Mwinyi nae huku akitabasamu, akampiga kikofi cha mapenzi shavuni, Anisa hakujali, akaendelea
“Hapo ndio pakachimbika Mpenzi wangu, tena na hivi nilikuwa tayari nimeisha onja, wakasikia harufu, halafu mwenzao hata sijali, nilikuwa nipo tayari kwa lolote, nikawa nasema kuwaambia kama mmenichoka si mnifukuze?” Mwinyi sasa nae akacheka na kusema
“Uifikiri wao hawana akili eti? Wakufukuze ili uje kwangu?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kama ulikuwepo vile, Baba akasema hivyo hivyo, mama alikasirika hadi akalia, kitu kilichopelekea baba nae kupata hasira zaidi, hapo sasa ndio ainidundaje! We acha tu,”
“Enhe, ikawaje tena?”
“Baba wakati ananipiga akataka nimlete kwako, nikagoma na
kumtaka aniue tu, siwezi kumleta kwako, hivyo nikawajibu kwamba sipajui unpokaa, wakachukua simu wakupigie wakashindwa
kuitambua namba yako, maana sijai Save kwenye simu,”
“Dah! Ulicheza kweli,” alimwambia huku akimbusu kwenye paji la uso
“Lazima, si nipo na Striker,” wakaanza kutaniana
“Hongera,”
Ghafla Anisa akabadilika na kuwa katika hali ya kawaida, utani akaweka pembeni, akamnyanyua shingo Mwinyi na kumwambia
“Mwinyi mimi nafanya yote haya kwa sababu ninakupenda, kila siku ninakosana na wazazi wangu kwa ajili yako, tafadhali usije kunitenda, nitaumia hadi kufa,”
“Amini sitakutenda waa sitakutenga,” Anisa alifurahi kwa kauli ile na kuanza kucheza na kuruka hapa na pale wakiwa na amani tele.
Walikuja kushtuka saa nne usiku, Anisa akakurupuka na kwenda kuoga, aliporudi kutoka bafuni, alionekana kuwa na woga kiasi kikubwa sana, kwa mara nyingine, Mwinyi akamlaghai Anisa na kumtaka alale pale kwake.
“Hapana, hapana... Siwezi kulala nje ya nyumbani, acha niende najua nitapigwa, ila niwepo nyumbani,” akaisogelea Dressing table ili kujipaka mafuta na kujiweka safi zaidi kabla hajaondoka
“Ngoja, ngoja Anisa,” Mwinyi akamdaka mkono na kanga aliyokuwa amevaa ikadondoka. Unafikiri ni nini kilichotokea? Yes! Upo sawa kabisa!”
Kuja kushtuka ni saa 9 alfajiri. Anisa akataka kuondoka muda huohuo, Mwinyi akamtisha sana na kwa ule woga wa kike, akakubali kuumaliza usiku pale, historia ikajiandika, kwa mara ya kwanza, Anisa kalala nje ya nyumba yao
Saa 12 asubuhi, Anisa akarejea kwao akiwa ameshindikizwa na Mwinyi, akiwa na woga mkubwa akaingia getini kwao ambapo alipakuta pakiwa wazi kwani msaidizi wao tayari alikuwa yupo nje akifanya usafi wa uwanja.
Alipoona Anisa tayari kaingia ndani, yeye taratibu akapotelea zake mbele akiwa ni mwenye furaha tele, maana tayari alihisi kuna balaa kubwa atakuwa tayari amelianzisha na hasa hilo ndilo alilokuwa akilihitaji.
Zilipita siku mbili bila mawasiliano yoyote kati ya Anisa na Mwinyi, Mwnyi hakuumia na ukimya ule, lakini kwa Anisa ilikuwa ni zaidi ya mateso. Siku ya 3 bila hata kujarajia, Mwinyi akiwa na Mgasi bila kutarajia wala hodi kugongwa, akaingia Anisa.
Alikuwa amedhoofu sana na alitia huruma, wote walimuonea huruma hata kabla hajasema lolote, akanyanyua mdomo na kusema
“Ah! Mwinyi mpenzi wangu, nimekuona tena,” Mwinyi akazinduka na kusimama akiwa ameshika mto mkononi, hakuwa Anisa Yule wa kila siku, huyu Anisa wa leo alidhoofu sana na alionekana kabisa kutokuwa na furaha.
Akautupa mto chini na kumkumbatia Anisa, aliekuwa akilia huku akisema
“Niikukukmbuka sana, lakini sina mawasiliano, wameninyang’anya gari, wamechukua simu na sasa wamenizuia kutoka, sina furaha maishani, nakosa amani moyoni hadi ninapokuwa nawe Mwinyi nipo katika wakati mgumu sana mpenzi wangu, na sababu yote ni kukupenda wewe, naomba usinitenge Mwinyi wangu,”
Maneno hayo yalimuingia Mwinyi barabara na kwa mara ya kwanza akahisi uchungu, walikuwa bado wamesimama na kukumbatiana. Mwinyi akamnyanyua sura Anisa na kumfuta machozi, akampoza na kumwambia
“Anisa, nakuahidi nitakuwa nawe bega kwa bega katika kipindi hiki chote kigumu kwako, usitegemee tena maumivu, bali tegemea faraja na raha tupu, njoo tukae hpa mpenzi wangu,”
Akamketisha taratibu sofani kisha akambusu, ndio Anisa akapata akii ya kumuona Mgasi aliekuwa amekaa sofa lingine amekumbatia mto kifuani. Wakasalimiana kwa bashasha.
Mgasi alikua mnyonge sana hasa kutokana na kauli zile za Anisa, alipojaribu kumpa pole Anisa, alishangaa kuona kuwa Anisa amekuwa jasiri sana tofauti na awali, Anisa alitabasamu na kusema
“Shem wangu Mgasi, hizi ni adhabu za mapenzi, ni kawaida sana kutokea kwenye mapenzi,” Mgasi akishangaa sana ni wapi kautoa huu ujasiri Anisa. Akatikisa kichwa kukubali, akiwa hajiamini, alipaswa kukubali ama kusikitika.
Anisa akamgeukia Mwinyi aliekuwa kushoto kwake kakaa, pasina
kumwambia kitu, akaingiza mkono wake ndani ya mkoba aliokuja nao na kutoa kitita cha pesa, kisha akasema
“Shika hii pesa, kazi yake nitakwambia baadae, acha mie nirejee nyumbani kwanza, maana nimetoroka kupitia mlango wa nyuma wakishtuka kama mie sipo, nikirudi sasa ndio wataniuwa kabisa,” Mwinyi akapokea kile kitita na kubaki kakishikilia, akapata akili ya
kuhoji wakati tayari Anisa kaisha simama
“Subiri Anisa, hebu niambie kuhusu...”
“Mwinyi nachelewa niache niende, nitakwambia hata baadae, hebu nipe simu yako hiyo ndogo ambayo haina WhatsApp,”
Mwinyi hakuelewa ni kipi alichokuwa akikimaanisha Anisa kwani alikuwa hajiamini kutokana na kuwa na mawasiliano na mademu wengi, lakini akampa kama aivyotaka. Anisa akaichukua na kutoa line ya Mwinyi akamrudishia kisha akaaga huku akiweka simu ile mkobani.
“Mwinyi sasa nafikiri utakuwa umenielewa namaanisha nini, mimi sina mawasiiano nawe, pia sina muda wa kutoka kwenda kununua simu na hata nikipata muda nitaonekana, na hapo nitakuwa nimetengeneza tatizo linguine,”
“Ok! Nimekupata mpenzi wangu, umeeleweka vema habibty wangu, mimi nitamaliza kila kitu,”
Anisa akambusu Mwinyi na kumuaga Mgasi kisha akatoka kwa kasi ya radi huruma ikawingia sana, wakabaki na masikitiko ambayo hayakuwa na msaada wowote. Walipokumbuka pesa, wakazitolea macho
Mgasi akazichukua na kuzihesabu, zilikuwa ni pesa taslimu shilingi Milioni moja ya Kitanzania. Mgasi akamkabidhi Mwinyi pesa ile, Mwinyi akaropoka
“Sasa ndio muda muafaka wa kula kuku, bata na samaki kwa pamoja,”
“Acha wewe! Mtazame kwanza… we sasa hivi umemuahidi nini Anisa?” Mwinyi akabaki kimya kama hajielewi, Mgasi akaendelea
“Umemuahidi faraja na raha kwa kipindi hiki kigiumu kwake, sasa inakuwaje tena unaingiwa na tamaa kwa pesa ambayo hata hujajua ni ya nini?”
“Dah! Hapo tena mi sijui nikoje. Sasa Mhasibu wangu tunafanyeje?”
“Tulia umsikilize Anisa, huwezi kujua ana maana gani kuleta pesa hii kwako”
“Eti eeeh? Poa kaka umeeleweka vizuri, sasa suala la kwanza itakuwa ni simu”
“Hilo ndio umenena la maana, kama vipi twende zetu!”
**********
ANISA ANATOROKA KWAO.
Saa moja jioni simu ya Mwinyi ikaita, namba ilikuwa ni ngeni kabisa, japo alitegemea kupokea simu ya Anisa, lakini hakuamini kama itakuwa ndio ile hasa ukizingatia muda ule, yeye alijua itakuwa kwenye usiku mnene.
Akapokea simu ile na aliepiga wala hakuhitaji kujitambulisha, alimtambulisha, alimtambua barabara. Baada ya salamu Mwinyi akataka kujua kama Anisa alifika salama kwao. Akamwambia kuwa alifika salama ndio.
“Lakini kwa mujibu wa mama, walijuwa kama nimetoka na kuna mtu kawaambia kuwa ameniona maeneo ya National, eneo ambalo wanatambua kuwa wewe unaishi,”
“Enhe, sasa ikawaje?”
“Bado hakuna kilichoendelea, maana Mzee bado hajarudi na kwa nilivyo sikia wapo pande hizo wanakutafuta, kuwa makini mpenzi wangu,”
“Usijali Anisa, nashukuru sana kwa taarifa,”
“Huna haja ya kushukuru, nakupenda sana Mwinyi, lazima nikujuishe kila baya inalotaka kukufika ikiwa ninalijua ili uliepuke.”
“Ahsante! Vipi kuhusu juzi asubuhi, mbona hujanieleza?”
Alimkumbushia siku ile aliyoingia kwao alfajiri kutoka kwake, akacheka Anisa ilikuwa ni cheko ya huzuni, na kusema kwa huzuni
“E bwana ni nouma, nilipofika pale nikakuta geti lipo wazi, nikaingia ndani, si uliona?”
“Ndio pale nilikuona.”
“Basi ile nashika tu kitasa cha mlango mkubwa, Abui huyu hapa, akasema hapohapo ulipo simama. Umetoka wapi? Mpenzi wangu sikuwa na jibu, sio kwamba jibu lilikuwa halipo, hapana bali wa kulitamka ndio hakuwepo japo alieulizwa alikuwa yupo ambae ni mimi,”
Ukimya wa Anisa mbele ya baba yake ikawa ni kama dalili ya kiburi, hivyo alimpiga sana, maana alikuwa akijua kabisa kuwa Anisa katoka kwa Mwinyi, kijana ambae wao wala hawamtaki hata kumsikia licha ya
kumuona.
“Nimepigika siku hiyo, we acha tu. Baba akasema sasa amenichoka hivyo nisubiri uamuzi wake, sasa ukija kuchanganya na hili la leo, uuuwwi.. sijui akirudi itakuwaje?”
“Mh! Mpenzi wangu unateseka sana kwa ajili yangu, mimi nakupenda sana lakini pia najali mno maisha yako, kwanini tusisitishe hili penzi letu..” akamkatisha kwa sauti ya ghadhabu
“Mwinyi... Mwinyi... nawe tayari umenichoka? Sema tu wala usiogope,” nae akamkatisha
“Hapana Anisa, natetea amani yako na maumivu ya kila siku kwenye mwili wako,”
“Maumivu haya ya Mwili ni nafuu kwa sababu yanaonekana na ni ya muda mfupi tu, tofauti na maumivu ya moyo ni ya milele na kibaya zaidi hayaonekani kwa macho ya kawaida,”
“Sasa hali hii itaendelea hadi lini mwanamke wangu?”
“Hadi siku watakayoniruhusu kufunga ndoa nawe, hata kama itachukua miaka dahari kwenye adhabu ya kipigo, kwangu sawa,”
“Kweli Anisa?” aliuliza Mwinyi kwa mshangao
“Hadi leo bado hujaamini msimamo wangu Mwinyi?”
“Nakuamini sana, ila nashangaa huu ujasiri wewe umeutoa wapi siku za karibuni,”
“Nataka niwaoneshe kuwa kila mtu ana haki zake kwa wenzake, wawe ni wazazi ama mtu mwingine yeyote,”
“Sawa, nimekubaliana nawe, sasa vipi kuhusu zile pesa?”
“Ngoja, nasikia kama kuna nyayo zinakuja huku kwangu kisha zimekata ghafla, subiri...”
Anisa akanyanyua mto na kuiweka simu kisha akasogea mlangoni na kuufungua akiwa ameshika mafuta mkononi, akamuona mama yake akipotelea chumba kingine, akafunga mlango na kuirejea simu yake.
“Hellow, tuendelee mpenzi wangu,”
“Upo wapi muda huu?”
“Nipo chumbani nimejifungia, sitaki kufanya chochote hadi wakubaliane na matakwa yangu,”
“Hawawezi hao Anisa, hawataki Mswahili nakwambia,”
“Swadakta hubby, wao hawamtaki mswahili, nae mswahili hawataki, ila huyo mswahili mie ninamtaka naye pia ananitaka, ama nasema uongo mpenzi wangu?”
“Upo sawa Habibt wangu, lakini huoni kuwa wanaweza kujidai wamekubali ili waniingize mtegoni kama awali?”
“Mtego upi?”
“Wa kushindwa mwenyewe,”
“Kivipi? Sijakuelewa hapo Mwinyi...”
“Nafika kwenu wananiambia mahari ya kununua Fuso mbili,” Anisa akacheka kwanza
“Hilo haliwezekani, kidini mahari anapanga mwanamke anaeolewa sasa vipi wataje wao?”
“Lakini tambua wazazi wako hawapo kidini, wapo kidunia zaidi, ingekuwa wapo kidini mbona wasingenitukana vile?”
“Basi Mwinyi, hebu ile tuliache, mie tayari nimepanga suala la mahari yangu kwa kuangalia uwezo wako, sijakurupuka, sawa? Ama nikutajie?”
“Ngoja nibahatishe...”
“Sawa jaribu,”
“Milioni tano,” alijibu Mwinyi akiamini ni pesa ndogo anataja.
“Umekosea, kumbe unazo wewe,”
“Sina mie. Labda laki 5,”
“Hapana umeshuka sana,”
“Basi Milioni 3,”
“Umepanda,”
“Ah basi nitajie wewe mwenyewe,”
“Jaribu mara ya mwisho,”
“Milioni moja,”
“Bado, umekosea,”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nimekubali kuwa siwezi, nakupa mji,”
Utani ukachukua nafasi na kujikuta wamejisahau kabisa kuwa wapo kwenye maongezi nyeti na yanayobeba mustakbali wa penzi lao.
Anisa alisahau taabu zake
“Nataka Arusha, nimiliki mbuga za wanyama!”
“Nakuongeza na Manyara, ili umiliki na mgodi wa Tanzanite!” wakacheka wote kwa sauti ya juu kama vile hakuna tatizo, kisha
“Sawa, shilingi za kitanzania Milioni mbili tu,”
“He! Anisa, mie sina uwezo huo ati,”
“Ndio sababu nikakuletea zile pesa mchana, nipo kimaandalizi zaidi, sasa nafikiri hakuna swali, ama kuna cha ziada?”
“Lipo moja tu la mwisho.”
“Lipi? Uliza ujibiwe,”
“Umeniletea milioni moja si ndio?”
“Haswaa, timamu kabisa,”
“Hivyo nalazimika nami kuongeza moja ili kutimiza mbili si ndivyo?”
“Hapana sio hivyo” Anisa aliongea kwa shauku na kuendelea
“Utafanya kitu kimoja, acha nikufundishe...”
“Utatanguliza milioni moja hiyo uliyo nayo na kuahidi baada ya wiki mbili ama mwezi utamalizia zingine zilizobakia,”
“Milioni kwa mwezi mmoja mie nitaitoa wapi mpenzi wangu?”
“Subiri basi, mi leo ndio Sterling, we utakuwa ni tairi sawa?” wakacheka tu kisha akaendelea
“Ukishatoa mahari huwa anapewa anaeolewa, lakini najua hawatonipa zote, watakata kama laki mbili ama tatu, zile watakazonipa nitakurejeshea wewe laki 5 uzilete tena, we unapaswa kutafuta laki 5 kwa mwezi huu, sawa?”
“Duh! Nimekusoma mama mipango.” wakacheka wote.
“Tena basi ukikwama kuipata ya kumalizia, utakapokuja kuleta hiyo ya mara ya pili, unakuja kabisa na tarehe kabisa ya ndoa isiwe mbali sana na unatoa ahadi ya kumaliza deni la mahari tukiwa ndani ya ndoa, najua sasa nimeeleweka?”
“Sina swali.” Anisa aikuwa na amani sana muda huu, alitamani wasimalize maongezi.
“Nami naomba kuwasilisha, nimeimaliza hoja yangu” wakaendelea kufurahi wenyewe
“Mama umetisha,” Mwinyi alimpongeza.
“Baba unapendwa wewe,” Anisa nae akachombeza.
Waliendelea kuzungumza hadi mlango wa chumbani kwa Anisa ulipogongwa na hapo ndio wakaagana kwa ahadi ya kuwasiliana wakati ujao tena pale tu Anisa atakapokua anapiga yeye.
Zikiwa zimesalia siku 3 tu kufikia ndoa ya Salama na Victor, hiyo ilikuwa ni siku ya Jumatano, katika beach moja tamu sana jijini Mwanza iitwayo ‘Shafeeq’ kulikuwa na Sendoff ya Salama. Ilikuwa ni ya watu wachache lakini waliojipanga vema.
Salma Cone iliandaa chakula na vinywaji kule, pia waliokwenda kule kwa kadi maalum walibeba zawadi za kutosha. Sherehe iikuwa ni fupi lakini ilifana mno na zawadi zilikuwa ni nyingi na za kuvutia sana
Salama alipendeza mno Victor nae alivutia kweli kweli, muda wote walikuwa wametabasamu na wapambe wao nao walikuwa hawatulii sehemu moja, walikuwa wakiranda kila sehemu kule na huko.
Walifurahi hadi muda wao wa kuondoka pale ulipowadia, Salama na watu wake wakaelekea kwao wakati Victor na kundi lake nao wakaelekea kwenye kumbi za starehe kwenda kumalizia siku yao iiyokuwa imeanza vizuri na walitaka iishe vizuri pia.
*
Saa 12 asubuhi, Mwinyi alikuwa akimgongea mlango Mgasi ambae hadi muda ule alikuwa bado amelala. Kiuvivu Mgasi akanyanyuka na kufungua mlango, alishangaa kumuona jamaa yake pale akiwa na kibegi mgongoni tena asubuhi vile.
Kama mtu aliekuwa akijua kuwa kuna maswali yataanza muda sio mrefu akaanza yeye kuongea
“Jamaa yangu nimekupigia sana simu hupatikani”
“Ni kweli, kuna jamaa alikuwa akinisumbua usiku jana, nikaamua kuizima simu” wakaanza kuingia ndani Mgasi akiwa mbele na Mwinyi akimfuatia.
Wakaketi sofani na Mgasi akionyesha kabisa shauku ya kutaka kujua ni kipi hasa kinachoendelea kwa Mwinyi ambae alikuwa na kibegi mgongoni na kipi kimemfanya atoke mapema kiasi kile nyumbani kwake na kumleta pale
“Ndugu yangu, sijui nianzie wapi na aniishie wapi?”
“Mwinyi vipi? Anza mwanzo na uishie mwisho ili nikuelewe,”
“Sawa, acha nianzie jana tangu kuachana nawe kule duka la simu, kwenye majira ya saa moja usiku, Anisa alinipigia simu...” hapa pia akamueleza yote waliyoongea ili kumuweka sawa
“Saa sita usiku akanipigia simu, safari hii alikuwa akilia, masikini mtoto wa watu, anateseka kwa ajili ya mapenzi...” Mgasi hakusema neno, akawa anamtazama tu
“Akaniambia baba yake alimuita usiku ule na kumtukana sana na hata kutishia kumfukuza, yeye akadai kuwa alikuwa tayari kwa hilo, ila anasema kilichomshtua ni kauli ya baba yake aiyoitoa mbele yake kuwa wamenitafuta mie na kunikosa, tena nina bahati sana maana alipanga kunipa kesi, tena kesi mbaya.”
“Kwani walikutafutia wapi?” aliuliza Mgasi.
“Walikuja National, wakapotea nnapokaa ndio wakarudi hadi kwa Anisa usiku uleule. Kwa kuwa walikuwa na askari wakatumika kumtishaAnisa ili awaelekeze ninapokaa, kwani mie ni mtu mbaya sana, sasa kwa usalama wake yeye Anisa na familia yake ni heri awaonyeshe, kwa vitisho na ule woga wa kike, akawaelekeza, lakini nao inaonekana hawakuwa na vibali maalum, maana ilikuwa ni saa 5 usiku, wakapanga waje leo asubuhi na mapema wanikamate na kunipa kesi,” Mgasi akaguna tu na kumtaka aendelee
“Wakamuuliza kama ana namba zangu za simu, akawajibu hana simu kwa sasa, kupitia jibu hilo akawa amewatoa woga wa kuwasiliana nami,”
“Dah hapo alipatia, picha ikaendeleaje sasa?”
“Kabla hawajaondoka wakamuuliza ni wapi alipokuwepo mchana wa siku ile? Akawajibu kuwa alikuja kwangu na bahati mbaya akanikosa na alipojaribu kuniulizia akaambiwa sipo kwa takriban siku mbili sasa,” huku Mgasi akijiweka vizuri kitini akampongeza Anisa
“Safi sana, msichana ana akili sana huyu, mh.. hebu endelea,” Mwinyi akaendelea
“Iiwavunja nguvu kiasi Fulani, lakini wakaahidi kunifuatilia asubuhi na mapema. Wakaacha na maagizo kuwa wamzuie kabisa Anisa asitoke siku nzima ifuatayo ili asije kuharibu mipango yao,” Mwinyi aionekana kama amemaliza, lakini Mgasi alitaka kujua zaidi
“Hao nao maziro kabisa, mwisho ikawaje?”
“Ndio akaniamuru nifanye mpango wakuondoka mapema sana, niende sehemu nikajipange kisha nimjulishe yeye atakuja kuishi nami. Nikamwambia sina pesa, akaniambia niitumie ile Milioni alioniletea kwa ajii ya posa. Huo ndio mkasa mzima ndugu yangu”
“Kwa hiyo mpango mzima?” aiuliza Mgasi kutaka kujua nini mpango wa Mwinyi
“Mimi mbele,” akasema huku akimkabidhi funguo za nyumba yake
“Wapi sasa?”
“Kwanza Mwanza, kisha mchakato ukiisha nitakujuisha,”
“Tupo pamoja, kuwa makini zaidi dogo,” akampa matumain kwa kumuita jina lile.
“Poa mie naondoa jeshi la mtu mmoja,”
Wakakumbatiana kisha walipoachiana wakagonga tano na Mwinyi akatoka ndani kuelekea stand ya mkoa kutafuta basi la kuelekea Mwanza akimuacha Mgasi akiwa amesimama kwa nje ya mlango wake akimtazama jamaa yake akipotelea maeneo ya game.
**********
Hawakuweza kuwasiliana Anisa na Mwinyi hadi siku ya Ijumaa asubuhi wakati Anisa alipopiga simu na kumwambia anataka kumfuata alipo.Mwinyi alishangaa, maana alikuwa bado hajajipanga kama walivyokubaliana awali.
“Mimi nipo Mwanza, kwani vipi Anisa?”
“Sawa, mi nipo Nzega kwa sasa, sikuwa na mwelekeo, nikifika Shinyanga nitakujulisha”
“Sawa!” Mwinyi akaitikia pasina kujua ni nini Anisa alikuwa akikimaanisha
Sammer jamaa yake Mwinyi aikuwa akimiliki gari aina ya RAV 4 nyekundu ambayo muda mrefu alikuwa akiitumia pale jijini Mwanza, hata walipokuwa wakiwasiliana, Mwinyi alikuwa yupo na gari ile pamoja na jamaa yake Sammer.
Walipoondoka Shinyanga waliendelea kuwasiliana hadi waipofika Hungumalwa, Mwinyi alikuwa tayari amewasha gari kutoka mabatini alipokuwepo na kuanza kujisogeza Nyegezi. Hivyo alipowasili Anisa kituo kikuu cha mabasi cha Nyegezi, nao walikuwa wapo tayari wanamsubiri.
Walimpokea na kuondoka nae hadi maeneo ya Ghana ambapo Mwinyi alikuwa amepanga chumba pale kwenye hotel iitwayo Smart, waliamua kukaa huku ili kukwepa mjuano na watu ambao walihisi huenda wakiwaona watatoa taarifa.
Hawakutoka siku hiyo nzima japo Sammer aliwaachia gari kwa ajili ya matembezi. Usiku waliposikia njaa ndio wakatoka kwa ajili ya kwenda kula. Lakini kabla hawajatoka Mwinyi akawa akimuhoji baadhi ya maswali mawii matatu.
Alimuuliza sababu ya safari ile ya ghafla, badala ya kujibu, Anisa akahoji iwapo Mwinyi hakuipenda. Ili kuepusha shari, Mwinyi akamwambia basi yaishe. Ndio Anisa akajibu sasa
“Najua Mwinyi kuwa nilikwambia ujipange, akini ningesema niendelee kusubiri wewe ujipange, kwa lililokuwa litokee mbele yetu, basi ndoto zetu za kuwa pamoja kama hivi, zingebaki kuwa ndoto na daima yetu sie yasingetimia,”
“Kwanini unasema hivyo Anisa?”
“Jana walivyokuja kwako na kukukosa, abui alirudi na hasira sana, akampigia simu Mzee Salum Nassor wa Shinyanga akimuuliza suala lile la ndoa, nikamsikia baba akimdanganya kuwa kuna posa nyingi anazikataa, sasa kama wao bado hawapo tayari kwa siku chache zijazo, basi waruhusu wazee warudishe mahari ili niolewe sehemu nyingine, wee...”
Hapo Umyy akamuwekea Mwinyi kidole mdomoni, walikuwa kitandani, chini amelala Mwinyi kichalichali na Anisa akiwa kwa juu, Mwinyi kifua wazi Anisa kajifunga kanga kwapani
“Hukuwepo wewe, Yule Mzee wa Shinyanga akaomba apewe siku 3 tu wafanye kikao cha dharula, bado baba akakataa, akasema kesho tu anataka jibu, ambalo ina maana ilikuwa ni jana, kweli wakaleta jibu kuwa, tarehe 15 ya mwezi ujao, ndio iwe ni siku ya ndoa na mama akaja kunifuata ili kuniambia akiwa na furaha usoni, akitegemea nami nitafurahi. Basi palepale nikamwambia naomba mniache niolewe na Mwinyi, akageuka mbogo, nikawa mpole nikiamini muda ule sio muafaka kuongea nao, nikapanga nitaongea nao usiku wakiwa wametulia. He kabla sijaongea nao si nikasikia wakitangaza vikao? Nikaona alaa! Msinitanie nyie, hamnijui vizuri sio? nikazama chumbani kwa Mama, nikachukua pesa kwenye draw na kuja nazo chumbani kwangu, leo asubuhi wakati wao bado wamelala nikatoroka, ndio sababu nipo hapa.” Alimaliza kuhadithia Anisa.
“Mh! Kazi kwelikweli, haya karibu katika maisha mapya,”
“Ahsante najua kuwa bado hujajipanga kisawasawa, ama?”
“Ni kweli, hata nyumba sijapata, lakini tutakwenda kuongea na dalali ili kesho tupate nyumba nzima ama unasemaje mchumba?” aliuliza Mwinyi akimchumu mdomoni
“Sawa tusubiri hiyo kesho iongee,” kisha Anisa akanyanyuka kuelekea dirishani kutazama mandhari ya eneo la Ghana.
Jioni ya siku ile kwa kutumia namba mpya kabisa, Anisa akaongea na msaidizi wao, akamuuliza juuyakile kinacho endelea pale kwao
“Wamekutafuta sana, wamekwenda kila sehemu, Polisi hadi Hospitali na hata kwa Yule nani sijui...” akasahau jina, Anisa akamuuliza
“Nani?”
“Yule wanaesema ndio bwana wako,”
“Enhe!” akahoji kwa shauku
“Wakadai ndio amekutorosha,”
“Ikawaje?”
“We wakakukosa na huyo kijana pia wakamkosa, wakamkamata mtu mwingine waliemkuta, hadi sasa hawajamuachia,” kama mtu aliehisi swali inaofuatia, Anisa akamuwahi yeye
“Sasa kama kuna kitu kitatokea, we nitumie sms kwenye namba hii, mie nipo sehemu moja hapahapa Tabora nimejificha peke yangu hadi wakubali, nikirudi nitakupa zawadi, sawa?”
“Haya unitumie muda wa hewani,”
“Sawa nitakutumia,” kisha akakata simu na kuanza kujadili
“Mwinyi penzi letu sisi linawatia matatizoni watu wengine, tena watu wasiohusika kabisa, ona sasa Mgasi yupo ndani,” Mwinyi akanyanyuka kitandani alipokuwa amekaa na kusimama ukutani akiwa ameweka mikono kifuani
“Hata sijui nifanyeje? Sisi tunakula maisha na asie husika anateseka,” akashusha pumzi.
Akatoa simu mfukoni na kumpigia Mgasi, akawa wala hapatikani, ikabidi awapigie ndugu zake, bahati mzuri wakamwambia tayari wamemtoa nje kwa dhamana na kutakiwa kuripoti kituoni kila siku hadi atakapoonekana huyo binti ama yeye atakapo jisalimisha kituo chochote cha Polisi.
Mwinyi aliomba kuongea na Mgasi, ajabu Mgasi alipopewa simu, akaongea taratibu sana na hata alipopewa pole na Mwinyi, alimwambia asijali kabisa. Lakini nae akataka kujua kama wapo Salama. Mwinyi akamwambia kuwa wapo salama kabisa na ili kumuhakikishia, akampa simu aongee naAnisa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hawakuongea sana, ila akawaahidi ataongea nao usiku, maana muda ule sio muafaka kwa wao kuweza kuongea mambo muhimu kama yale bado wakaendelea kumpa pole na kumuomba kama vipi warudi. Akawaambia wataongea usiku.
Saa 3 usiku, Mwinyi akampigia simu Mgasi na kuweka sauti ya njewakati akiongea nae ili Anisa nae asikie
“Walikuja askari wawili mie nikiwepo pale kwako wakikutafuta, nikawaambia una siku tatu sasa haupo mkoani. Wakanilazimisha niseme ulipo,nikawajibu kuwa umekwenda Dodoma. Wakaongea na baba yake Anisa na kuamua niende nao kituoni ii tukaandike maelezo. Kwa sababu nilikuwa nikijiamini nikaondoka nao hadi kituoni, huko
tulipofika si wakanigeuzia kibao rafiki yangu?”
“Enhee, wakasemaje?” aliuiza Mwinyi kwa Shauku
“Wakaniambia nimeshiriki kumtorosha Binti yao aitwae Anisa. Basi mimi nikakana simjui. Kosa hilo wakaniambia ni la kwanza, la pili wakasema ni kumficha mtuhumiwa namba 1 ambae ni wewe, nikawaambia nina siku 3 sijakuona, sasa nitakufichaje mtu nisiemuona?”
“lilikuwa ni swali gumu sana,”
“Basi bwana kwa ubabe tu wakanitupa ndani tangu saa 5 asubuhi ile hadi muda ule uliopiga simu ndio niikuwa nimetoka kwa dhamana,”
“Dah! Pole sana jamaa yangu, mimi kwa sasa nafikiria kuja ili tu niweze kukutoa kwenye majanga yasiyokuhusu,”
“Acha wendawazimu wewe, huoni utakuwa umekamiisha hisia za wale askari na wazazi wa Anisa ambao hadi muda huu wanatapatapa
hawajui cha kufanya?”
“Sasa nikufanyie nini kwa wema wako kaka?”
“Unapaswa kumlinda Anisa kwa hali yoyote na kwa gharama yoyote, mimi nipo nanyi hadi dakika ya mwisho, sijui unanielewa?”
“Nashukuru kaka, nimekuelewa, upo wapi muda huu?”
“Nipo hapa kwako, nitakuwepo kila siku na muda wote ambao sitakuwepo kazini, nitakuwa hapa ili wajue kwamba siwaogopi”
“Kama vipi nikutumie pesa ili upakie vitu hivyo...” akamkatiha palepale
“Ah aha! Noma hiyo haifai, watafuatilia, tusubiri hadi hili jambo lipungue uzito kwa sasa kisha baadae tutajua cha kufanya, kwani nyie huko mmejipangaje?”
“Kesho tunatafuta nyumba na baada ya hapo kitakacho fuatia mie nitakujulisha kila hatua. Lakini ninakuonea huruma sana ndugu yangu kwa majanga nilio kuingiza bila kutarajia,”
“Usikonde wangu ndio maisha haya,” walimaaliza maongezi yao na kisha wakapanga kuwasiliana tena kutakapokuwa na habari mpya.
Anisa na Mwinyi sasa wakapata nafasi ya kujadiliana, Mwinyi ndio alifungua mjadala kwa kumzungumzia Mgasi
“Sikutegemea kama Mgasi ni jasiri kiasi hiki na sikudhani hata siku moja kama ananijali hivi, sijui nimlipe nini jamaa yangu huyu?” Anisa aikosa la kuchangia akabaki kimya tu
Njaa sasa ilikuwa ikiwauma, japo walikuwa wameahirisha kutoka,l akini sasa ikawalazimu kutoka ili kwenda kutafuta chakula. Wakaona sehemu ya karibu ni Villa Park, kwa Mwinyi haikuwa ni sehemu ngeni, ila kwa Anisa ilikuwa ndio mara yake ya kwanza kuwa sehemu kama ile, palimvutia sana.
Walitafuta sehemu nzuri ya kukaa wakiwa wameshikana mikono, walipoipata Mwinyi akamketisha chini Anisa kwenye kiti kisha yeye akaelekea Counter ya nje kuweka order japo wahusika waikuwa wakipita huku na kule.
Anisa akiwa mezani peke yake, akamuona mtu ambae wala hakumtegemea kabisa kumuona maeneo yale, hata yule nae alimuona Anisa, pia nae hakutegemea kumuona eneo lile, akishangaa na kwenda pale mezani akiwa na furaha.
Anisa alisimama wakakumbatiana na hapo ndio Mwinyi akatokea na kuona Anisa akiwa amekumbatiana na Mtu ambae hakumtambua, akajiuliza ni nani amemjua Anisa huku na hadi wanakumbatiana, akakosa jibu na kuamua kusogea.
“Balaa gani hili? Sasa hii leo si ni aibu?” aliwaza Mwinyi baada ya kumuona Fardos ambae alikuwa ni mpenzi wake wakati akiishi Mwanza
Alijibanza karibu na pale waipokaa kwa dakikika chache akitegemea Fardos ataondoka, lakini ikatimia dakika 5 bila Fardos kuonesha dalili yoyote ya kuondoka, ilikuwa ikionesha kwamba, mazungumzo yao yalikuwa ni mazito sana.
Mwinyi akajiongeza na kutoa simu, akapiga namba fulani na kuongea nayo
“Mambo vipi Far?”
“Poa tu za kunitenga?”
“Sio hivyo, upo pande zipi?”
“Nipo Villa, we upo wapi? Tabora?”
“Hapana nipo Mwanza, tena Villa,”
“Wee! Kweli? Sehemu gani?” Aliuliza Far kwa shauku
“Njoo geti kuu kama unaelekea The Kiss nakusubiri, usichelewe”
“Nakuja sasa hivi,” Fardos akanyanyuka na kumtaka Anisa watoke nje kwenda kumuona shemeji yake maana nae pia ni mtu wa Tabora bila kumtajia jina.
“Haiwezekani mie kuondoka hapa, si unajua nipo na mpenzi na ameniacha nikiwa nimekaa hapa? We mfuate huyo jamaa mi utanikuta hapahapa,”
“Poa usiondoke lakini mpenzi” akainama na kumbusu midomoni.
“Ondoa shaka,” kisha Fardos akatoka eneo lile na kuelekea nje alipo Mwinyi.
Mwinyi alipomuona Fardos anatoka, yeye akafanya haraka na kuelekea nje pale alipomuelekeza kuwa yupo na kukaa akimsubiri. Walifurahi kuonana, Mwinyi akamrudisha ndani tena na kumvutia kiti baada ya kufika kwenye meza tupu
“Ngoja tukae pande hizi kuna mtu niamsubiri eneo hili tumepanga tukutane,” Mwinyi alikua kama vile haeleweki, akaendelea kuongea
“Nakuagizia kinywaji, usitoke hapa, kuna mtu anakuja hapa,”
“Lakini Mwinyi kuna ndugu yangu yupo hapa katoka Tabora na amekaa peke yake, si ni bora niende nikakae nae kule alipo?” akawa akimuonesha kwa kidole.
“Ngoja nirudi, twende wote ili tusije kupotezana,” Mwinyi akanyanyuka mara baada ya vinywaji kuteremka mezani na kuvilipia.
“Sawa, usichelewe basi Mwinyi jamani,” Mwinyi akasimama na kumbusu Fardos kisha akatokomea kule alipo Anisa.
Alipofika mezani kwa Anisa, akamuhamisha kwa kusingizia taa, wakasogea mbele huko gizani, kisha akaanza kumuhoji maswali
“Kuna mtu niliona unawasiliana nae, unamfahamu?”
“Ndio, anaitwa Fardos, ni ndugu yangu wa Shinyanga ila kwa sasa yeye anaishi huku,”
“Anafahamiana na wazazi wako? Namaanisha kimawasiiano anaweza kuwasiiana nao?”
“Sana tu! Hata akija Tabora hufikia nyumbani,” alijibu kwa kujiamini
“Dah! Umemwambia ni kwanini upo huku?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hapana nimemwambia kuwa nimekuja matembezi tu,” alianza kupoteza kujiamini
“Umemjulisha tulipofikia?” Mwinyi aiendelea kukandamiza maswali kwa Anisa
“Ndio nimemwambia, kwani vipi? Mbona maswali mengi?”
“Tayari umefanya kosa kubwa sana, namba yako ya simu umempa?”
“Hapana!” sasa Anisa nae akajibu kifupi
“Dah! Afadhali hilo moja umecheza vizuri na kama vipi tutampoteza,”
Bado Anisa alikua njia panda, hakuwa ameelewa lolote, Mwinyi akatoa simu na kuizima kabisa baada ya kukaa, kisha walikula kwa haraka japo hawakupanga hivyo, na walipomaliza kula na kulipa, wakatokea mlango wa nyuma ulipo uwanja wa soka wa CCM Kirumba, wakaondoka.
**********
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment