Search This Blog

Thursday 24 November 2022

NGUVU YA MAPENZI - 3

 


    Simulizi : Nguvu Ya Mapenzi

    Sehemu Ya Tatu (3)





     Sara alijikuta akimpa tu mama Angel ile picha ya marehemu baba yake, ila mama Angel alipoiangalia ile picha alionekana kushangaa sana kwani ni mtu aliyemfahamu vizuri kabisa.

    Mama Angel alimuangalia Sarah kwa makini sana na kumuuliza,

    “Kwahiyo huyu ndio marehemu baba yako?”

    “Ndio, ni marehemu baba yangu”

    “Umewahi kumuona?”

    “Sijawahi, mama aliniambia kuwa alikufa pindi tu nilipozaliwa”

    “Mmmmh!”

    “Mbona unaguna mama? Ila baba yangu alinipenda sana kwani mama anasema kuwa hata hii nyumba baba aliijenga kwaajili yangu hata kabla sijazaliwa, na biashara nyingi za familia ni yeye aliziweka kwaajili yangu yani hakutaka mimi nipate shida, natamani sana angekuwepo baba yangu maana alinipenda sana”

    Mama Angel akamuangalia kwa makini Sarah na kumtaka muda huo waende nae hospitali tu huku akili yake ikiwaza vitu vingi sana kutokana na ile picha aliyoiona.

    Basi waliondoka na Sarah kuelekea hospitali ambapo alichukuliwa vipimo na kugundulika kuwa ana malaria, kwahiyo alipewa dawa na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

    Basi mama Angel na Erick wakamrudisha Sarah nyumbani kwao ambapo alikuwepo msichana wa kazi tu akiishi nae sababu mama yake hakuwepo, ila mama Angel alitamani sana waondoke na Sarah ili akamuhudumie kwani aliona kuwa Sarah anahitaji kupata huduma ya karibu zaidi, sema Erick akamzuia mama yake,

    “Ila mama, utamchukuaje Sarah bila ruhusa ya mama yake? Ungempata mama yake hewani basi ungeongea nae kwanza ila sio kujichukulia tu maamuzi”

    “Basi mwanangu nimekuelewa”

    Kisha mama Angel alimuuliza yule msichana wa kazi wakina Sarah kama ataweza kukaa na mgonjwa vizuri,

    “Nitakaa nae tu mama, hakuna tatizo”

    “Nitajitahidi kesho mchana nije kumuona pia hali yake inaendeleaje”

    “Sawa, nashukuru sana”

    Basi mama Angel na Erick ikabidi wage pale kwakina Sarah na kuondoka zao, basi wakiwa kwenye gari Erick akamuuliza mama yake,

    “Mbona mama ile picha ya marehemu baba yake Sarah imekushtua sana?”

    “Unajua ni mtu ninayemfahamu sana, sijui hata nikwambiaje ila kwa kifupi Sarah ni ndugu yenu”

    “Mmmh
    mama, ndugu yetu kivipi?”“Kama ile picha aliyonionyesha ni kweli basi elewa kuwa Sarah ni ndugu yenu”Erick alishangaa na kumuangalia mama yake bila ya kummaliza, kisha akamwambia,“Ndiomana ulikuwa uking’ang’ania tukamuuguze nyumbani!”“Hapana hiyo sio sababu ila tu nilitaka kuwa nae karibu sababu ni mgonjwa”“Hapana mama nadhani ni sababu unahitaji kujua zaidi kuhusu baba yake Sarah, ila ni marehemu kumbuka”“Ndio ni marehemu kwani mimi nimesema yuko hai! Hebu endesha gari na wewe, hivi unajua muda umeenda sana na tangu tuondoke nyumbani hatujarudi mpaka muda huu, sijui mwanangu kaliaje huko jamani”“Atakuwa Amelia sana ila Erica yupo atambembeleza”“Unamuamini sana Erica eeeh! Ndiomana ulitaka kuja kumuombea niwe nampa mia tano! Hebu elewa jambo moja, yule ni mtoto wa kike, naogopa kumzoesha hela”Hapo Erick hakuongea neno lolote zaidi ya kuendelea kuendesha gari tu.Erica alikuwepo nyumbani akimbembeleza mdogo wake tu, ni kweli siku hii mama yao alichelewa sana kwenye hiyo safari aliyoenda na Erick, basi Erica akawa anamuuliza Vaileth,“Kwani walienda wapi?”“Nilisikia kuwa wameenda kumuona Sarah”“Kafanyeje huyo Sarah?”“Nasikia anaumwa”“Ila mama nae jamani loh! Mtoto analia hivi”“Ngoja nikubebeshe labda atatulia”Basi Vaileth alimbebesha Erica yule mtoto, na kweli alivyombeba mgongoni alitulia na alionyesha kubembelezeka hata kulala alianza kulala sasa, na alivyotulia vizuri, Erica aliweza kukaa na kuangalia Tv.Muda kidogo mama Angel na Erick walirudi na kumkuta Erica akiwa kambeba mtoto mgongoni,“Oooh Erica mwanangu, kweli umekuwa mama. Pole eeeh!”Kisha mama Angel akamchukua mtoto na kwenda nae chumbani, halafu Erick akaenda pia chumbani kwake ambapo alipakuta pamepangwa vizuri kabisa, akaenda kuoga kwanza ili akale maana hakula chochote kile toka ameondoka na mama yake, basi alienda kula na kumkuta Erica akiwa pale mezani,“Nilikuwa nakusubiri tu, nikasema usipotoka basi nakuja kukufata mwenyewe humo chumbani kwako maana mmeondoka bila kula”“Ni kweli, na nilikuwa nahisi njaa hatari ila nilikuwa navumilia tu”“Anaendeleaje huyo Sarah”“Tulimpeleka hospitali, tumemkuta ana malaria.”Basi Erick alikuwa anakula, kisha mama yao nae anaenda kula, basi anakula pale huku akiongea ongea nae ila alikuwa na mawazo sana huku akitamani kumwambia mume wake kuhusu alichokipata kwakina Sarah.Mama Angel alipomaliza tu kula alienda chumbani na kujilaza huku akifikiria mambo kadhaa, akachukua simu yake na kumpigia mume wake ili ampe ujumbe, simu ile ikapokelewa ila mumewe aliongea katika hali ya usingizi sana,“Kumbe ushalala mume wangu?”“Muda umeenda huu mama Angel”“Haya usiku mwema”Basi akakata simu na kuanza kufikiria mambo kadhaa, kwanza kuhusu Sarah na yule aliyemuona kwenye picha,“Hivi inawezekana kweli marehemu mzee Jimmy akawa ndio baba mzazi wa Sarah!! Mmmh natakiwa kuonana na mama Sarah ili nimuulize vizuri. Ila si mpaka mwisho wakina Erick walisema kuwa baba yao ana matatizo ya uzazi!! Anaweza kuwa na mtoto kweli halafu watoto wake wasijue? Halafu kwanini Sarah aseme baba yake kafa baada ya yeye kuzaliwa, jamani mbona mzee Jimmy kaacha hata wajukuu wake wamekuwa kuwa, maana nakumbuka kifo chake wakina Erica walikuwa darasa la tano! Inakuwaje Sarah awe kabla hajazaliwa? Mmmh!”Alichoka sana kufikiri ila alishangaa siku hiyo akiwa hana usingizi hata kidogo, aliamua kuchukua simu ya mwanae Angel ile iliyopasuka kioo, aliiwasha nayo ikawaka, na moja kwa moja alifungua data na kuingia kwenye facebook ya mtoto wake ili aangalie alikuwa akiwasiliana na nani, ila aliona mtu ambaye mwanae aliwasiliana nae sana alikuwa ni Samir, tena sio kwa kutumia facebook maana inaonyesha walitumia ujumbe wa kawaida kwa sana kwenye mawasiliano yao. Basi alikuwa akiangalia tu taarifa mbalimbali za kwenye mtandao, ndipo alipoona mtu kaandika ujumbe, unaosema,“Jamani mwenzenu simuelewi mume wangu, akiwa yupo nyumbani ataniita majina yote mazuri, mara mke wangu, mara mpenzi yani hadi huwa Napata raha sana, ila akiwa mbali sasa balaa nikimpigia simu muda wowote hata usiku wakati amelala utasikia ananiita mama Fulani, yani haniiti mke wangu kama nyumbani”Mama Angel akapumua kidogo, na kuangalia wachangiaji walichosema,“Ukiona hivyo ujue unaibiwa, mumeo anaogopa kukuita mke wangu maana mchepuko atajua kama ana mke, kumbuka sio michepuko yote wanaojuaga kuwa huyu mtu kaoa au ana mke, wengine hawajui kwahiyo anazidi kumficha”“Tena mimi wangu utakuta unampigia anajifanya amelala kumbe anachepuka, jamani wanaume hawa Mungu atusaidie tu”“Pole sana, hapo jua tu kuna watu wanakusaidia”“Tena mwingine akiona unamsumbua usiku anaamua kuzima na simu kabisa, yamenikuta hayo. Poleni wanawake wenzangu”Mama Angel alihisi tumbo lake kuunguruma kwa muda huo kwani akizingatia ni muda mfupi tu katoka kumpigia mume wake simu na alionyesha kuwa amelala halafu hakumuita mke wangu kama siku zote bali alimuita mama Angel, basi alijikuta akishikwa na wivu na kuchukua tena simu ili kumpigia, jibu lililokuja,“Mtumiaji unayempigia hapatikani kwasasa, tafadhari jaribu tena badae”Yani hapo ndio alihisi kuibiwa kabisa, na usingizi ndio ukakata kabisa alijikuta akishindwa kulala hadi panakucha yani hakuwa na usingizi hata kidogo.Kwenye mida ya saa mbili asubuhi, mama Angel aliamua kumpigia tena simu mume wake ambaye kwa muda huo alipokea na kuanza kuongea nae,“Mume wangu, ilikuwaje ukazima simu yako?”“Yani jana nilichoka sana halafu simu kumbe iliisha chaji kwahiyo ikajizima yenyewe, samahani mama Angel”“Na hiyo mama Angel vipi? Mbona sikuelewi?”“Jamani mke wangu, hunielewi nini tena?”Hapo mama Angel alitabasamu kiasi na kumwambia,“Unajua mara nyingine napata mashaka, vile ukishindwa kuongea nami kwenye simu!”“Mashaka ya nini tena mke wangu jamani!! Siku zote hizi hujanizoea tu eeeh!! Nawezaje kufanya ujinga kwako? Usiniwazie tofauti mke wangu, tujenge maisha yet utu. Vipi watoto lakini wanaendeleaje?”“Wapo salama tu, ila kuna jambo nahitaji tuongee ukirudi mume wangu maana nadhani kwasasa wala hatutoelewana”Sababu mumewe alikuwa anawahi kwenye shughuli zake za huko, ikabidi waagane tu maana hakukuwa na namna tena.Mchana wa siku hiyo, mama Angel aliamua kwenda kumuona tena Sarah, na alipofika alimkuta Sarah anatapika na kupata habari kuwa alitapika sana hata asubuhi ya siku hiyo, basi alimsaidia pale na kukaa nae ndani kwa muda, kisha akamuomba yule msichana wa kazi ili amruhusu yeye kuondoka na Sarah,“Naomba uniruhusu niende na Sarah ili nikamuuguze nyumbani kwangu”“Mmmh hapana mama, siwezi kukubali maana watanisema sana ukizingatia nimeachiwa mimi dhamana ya kumuangalia Sarah”“Ila anaumwa sana, eti Sarah unasemaje kuhusu mimi kukuchukua ukaugulie nyumbani kwangu eeeh!”“Nipo tayari, hapa dada hata haniangalii vizuri”Basi dada yake akamuangalia na kusema,“Jamani Sarah, kweli sikuangalii vizuri mimi!”“Sina maana hiyo, ila nikienda kwa huyu mama nitapata nafuu kwa haraka sana, kumbuka mama yangu hayupo na mimi napenda kuwa karibu na mama, halafu mama yangu hayupo unadhani ni nani anaweza kunipa mapenzi ya mama zaidi ya huyu aliyejitolea? Mimi nawafahamu ni watu wenye roho nzuri, nipe ruhusa tu niende dada Siku”“Mmmh jamani sijui yani”Mama Angel ikabidi amtoe uoga,“Sikia Siku, tutaenda wote hadi nyumbani kwangu ambapo atabaki Sarah ili nimuhudumie kwa ukaribu, yani wewe upafahamu nyumbani kwangu ili usiendelee kuwa na mashaka nami”Basi Siku akakubali na kuenda kumuandalia Sarah nguo chache kisha kuondoka nao mapaka nyumbani kwa mama Angel.Walifika pale, walikaribishwa vizuri kabisa na Vaileth kisha baada ya muda kidogo Siku aliondoka tu kurudi kule nyumbani kwa mama Sarah.Leo Erick anawahi kutoka shule sababu alishaomba ruhusa kwa mwalimu wake, hivyobasi alivyoondoka tu moja kwa moja alienda kwenye duka la baba yake, na kuanza kuangalia vizuri ila wakati yupo pale dukani alifika yule rafiki wa Steve yani yeye alienda kwaajili ya kumtembelea rafiki yake maana siku zote alifika na kukuta duka limefungwa, basi alivyomkuta Erick ndio alianza kuongea nae,“Steve ni rafiki yangu sana”“Aaaah, basi Steve kapata kazi sehemu nyingine. Na hapa tunatafuta mtu”“Jamani hata mimi nafaa jamani, sina kazi mimi”“Unaitwa nani kwani?”“Naitwa Rama”“Oooh ila majina ya Rama, naona wengi ni wastaarabu. Basi fanya hivi, kesho nitakuja hapa dukani niletee wadhifa wako yani cheti chako, barua ya serikali ya mtaa wako na barua yako ya maombi ya kazi, nitaipitisha ili Jumatatu uanze kazi”“Dah! Nashukuru sana, yani sasa hivi naenda kufanya hivyo vitu. Yani mimi nahangaika tu siku zote hizi sina kazi”“Basi ndio umepata kazi, ila kuwa muaminifu kama jina lako”“Hata hivyo mimi ni muaminifu kweli, hivyo vitu hata leo leo ningevileta”“Ila naona muda umeenda, nitachelewa nyumbani. Jitahidi iwe kesho halafu ndio nitakuonyesha na vitu ndani tunafanyeje”“Asante sana”Kisha Rama akaondoka muda huo ili kwenda kushughulikia vitu hivyo.Erick aliangalia angalia vizuri kwenye lile duka na wale walinzi ambao baba yake aliwaweka, kisha akataka kuondoka basi wakati anatembea ili aite bodaboda aondeke nayo, alishangaa akishikwa bega, alipogeuka alikuwa ni Sia amemshika bega, Erick akachukia sana na kusema,“Ni wewe kimama tena!!”“Najua Erick unanichukia sana, ila ungepata kuona nafsi yangu jinsi gani napata faraja hata kuongea nawe tu, ungenielewa”“Unataka nikuelewe kuhusu nini? Kuwa wale ninaoishi nao sio wazazi wangu? Na wewe ndiye mama yangu au nini?”“Bado una mambo hayo tu Erick jamani, achana na mambo hayo ya mwaka jana, zama zimebadilika hizi. Ni hivi Erick, endelea kuwaheshimu na kuwasikiliza wazazi wako ila na mimi usinichukie kiasi hiko, nipende na kunijali, sio kosa langu mimi kufanya yote haya ninayoyafanya, ipo siku utanielewa ni kwanini nafanya haya niyafanyayo, naomba unisamehe sana”“Achana na mimi bhana”“Nitaachana nawe ila niambie kuwa umenisamehe, Erick sitaki kuwa kikwazo katika mafanikio yako ila nataka kuwa chachu ya wewe kufanikiwa zaidi, achana na yote yaliyopita Erick mwanangu”“Hapo ndio unaponikera, nani mwanao?”“Mtoto wa mwenzio ni wako, kwahiyo wewe ni kama mwanangu. Nakuona wewe ni kama Elly, usinichukie Erick”“Kwaheri”Erick alishaita bodaboda na kupanda kisha aliondoka nayo sababu tu hakutaka kuendelea kumsikiliza Sia.Basi Erick anarudi hadi nyumbani kwao, ila alipofika tu sababu ya uchovu ni moja kwa moja alienda chumbani kwake na kujilaza, yani leo alisahau hata kwenda kula au kuvua sare za shule kwani alihisi kichwa chake kuchoka sana.Muda huu mama Angel alikuwa sebleni pamoja na Erica sababu Sarah alikuwa amelala, ila Erica alikuwa akimlalamikia mama yake,“Yani mama ndio kumuweka Sarah nilale nae kweli?”“Kwani kuna ubaya gani jamani! Sarah ni mgonjwa unataka alale peke yake, akizidiwa je!”“Ila mama, aaargh jamani”Erica akaondoka na kwenda tena chumbani kwake, muda kidogo alifika Junior na mama Angel kumshangaa,“Kheee Junior, umerudi tena!”“Mamdogo, leo ni mwisho wa wiki, nitaenda tena shule Jumatatu”“Sasa hiyo ni shule ya bweni au ni shule ya kutwa?”“Jamani mamdogo, yani wanafunzi wote wa karibu wameondoka leo, ni wale wa mbali tu ndio wamebaki, halafu na mimi nibaki kweli wakati naishi karibu hapa”“Haya, nimekuelewa”Kisha Junior moja kwa moja alienda jikoni kwani alijua huko lazima atamuona Vaileth na kweli alimkuta akiwa ndio anamalizia kupika, basi akaenda nyuma yake na kumbusu halafu akamwambia,“Unajua siwezi kukaa shule kwa siku nyingi zaidi maana mawazo yangu yote ni juu yako”Vaileth alitabasamu tu, mara ikasikika sauti ya mama Angel,“Vai, hiko chakula bado tu!”“Ndio namalizia mama”Mama Angel tayari alishafika jikoni na kumuuliza Junior,“Na wewe Junior, kituo cha kwanza jikoni kuna nini?”“Ni njaa mamdogo, nahisi njaa sana”“Khaaa wanafunzi wa bweni jamani mna vituko sana, haya Vai andaa hiko chakula ili wote wapate kuja kula”Kisha Junior akatoka, na mama Angel akatoka pia kwenda kumchukua Sarah chumbani ili aweze kula chakula.Alijua Erica atamkuta chumbani pia ila Erica hakuwepo mule chumbani, basi alikaa na Sarah na kumwambia,“Twende basi ukajaribishe kula chakula nilichokuandalia”“Mmmh hata sijisikii kula”“Hapana Sarah, ule japo kidogo upate nguvu binti yangu”Mama Angel akatoka na kwenda kumletea chakula Sarah na kuanza kujaribu kumlisha pale ni kweli alikula, tena alikula vizuri tu na baada ya kushiba sasa aliongea nae kidogo na kumruhusu apumzike halafu yeye akatoka na kuondoka zake, hakuwa na tatizo na wanae kwani alijua ni lazima wangeshuka na kula chakula tu.Erica aliamua kwenda chumbani kwa Erick ili kumuelezea, ila alimkuta akiwa amelala tena bado hajavua hata sare za shule, basi alimshtua na Erick aliamka,“Wewe Erick, nini tena?”“Dah!! Nimechoka sana jamani”“Kwahiyo hata kula hujala jamani, halafu sikujua maana ningekuja kukuamsha muda sana”Basi Erick ndio aliinuka na kuanza kubadili zile sare za shule,“Khee unabadili nguo hata huniambii nikupishe?”“Sasa unipishe kitu gani? Kuna kipi hukijui katika mwili wangu”Erica alicheka tu na kuinuka, kisha akamwambia,“Utanikuta sebleni”Basi Erick alienda kuoga na baadae alishuka kwenda kula chakula na baada ya hapo aliongozana tena na Erica kwenda chumbani kwake, basi Erica alianza kumwambia,“Mama, anaupendeleo sana”“Kafanyaje kwani?”“Mama kamleta Sarah hapa nyumbani”“Mmmh kamleta Sarah?”“Ndio, kumbe hujui! Basi mama kaja na Sarah leo, ila anavyomjali huyo Sarah tofauti na sisi, yani Sarah kaenda kulishwa chakula sababu anaumwa halafu kamuweka nilale nae mimi”“Unasema kweli mama kamleta Sarah hapa nyumbani? Kakubaliana na mama yake kweli?”“Sijui ila ndio Sarah yupo hapa nyumbani, kwakweli mimi siwezi hata kwenda kulala huko chumbani bora nikalale sebleni tu”“Aaaah jamani usifanye hivyo”“Mimi sikubali, mama angetaka aneomba ushauri kwanza kwangu mwenye chumba sio kujiamulia tu mwenyewe na maamuzi yake”Kisha Erica akainuka na kusema,“Usiku mwema”“Kwahiyo ndio unaenda kulala sebleni?”“Ndio, siwezi kwenda kulala chumbani kwangu”“Hapana usiende kulala sebleni, tafadhari baki humu chumbani tulale wote”Erica nae aliona ni jambo jema, kwahiyo alibaki humo chumbani kwa Erick na muda huo wakalala wote.Kulipokucha, mama Angel alienda kumuangalia Sarah ajue hali yake ila alimkuta ameanza kupona maana hata nuru usoni mwake ili onekana, basi alimsalimia pale na kuongea nae kidogo,“Eeeh unajisikiaje, unaendeleaje?”“Naendelea vizuri mama”“Vipi huyu Erica ameshaamka nini”“Sijui, kwani Erica huwa analala humu?”“Ndio, huwa analala humu”“Basi sikumuona maana nililala mwenyewe tu kama nyumbani”“Kwahiyo nyumbani kwenu napo umezoea kulala mwenyewe eeeh!”“Ndio, mama huwa anasema mimi ni mlalavi yani nalala vibaya kwahiyo nisilale na mtu, huwa nalala mwenyewe tu”“Oooh basi sawa, labda Erica kajiongeza. Asubuhi hii nikuandalie nini?”“Mmmh labda supu ya kuku na chapati”“Sawa, hakuna tatizo”Basi mama Angel alienda jikoni na kuandaa hiko chakula mwenyewe, yani Erica alimkuta mama yake akiandaa hiko chakula,“Ndio chakula chetu hiko leo mama?”“Cha mgonjwa hiki, si unajua Sarah anaumwa?”“Najua ila na mimi nitakula hiko hiko unachomuandalia Sarah”Mama Angel hakusema neno maana alimtambua wazi mtoto wake huyu kwa ubishi, basi alimuita Vaileth tu na kumtaka aandae supu ya nyumba nzima ili wote wapate kunywa supu hiyo.Mida ya saa nne asubuhi, Erick alijiandaa na kumuaga mama yake ila kwa muda ule Erica nae aling’ang’ania aondoke na Erick maana hakutaka kukaa hapo nyumbani wala nini.Basi mama yake alimruhusu tu bila kujua kuwa Erica amechukia uwepo wa Sarah pale nyumbani kwao.Baada ya kuondoka tu, ni Vaileth ndio alienda kumwambia ukweli,“Unajua nini mama, mwenzio Erica kachukia uwepo wa Sarah”“Jamani haka katoto sijui nani kakafunza roho mbaya mweeeh!”Kisha mama Angel alienda kuongea na Sarah ambaye bado alikuwa chumbani na alitoka kuoga tu kwa muda huo,“Unajionaje hali kwa muda huu Sarah?”“Nimepona, maana hata nimeweza kuoga. Ila kwanini Erick hajaweza kuja hata kuniona huku chumbani!”“Kheee hakuja kukuona! Nadhani sababu ya majukumu yake, ila atawahi kurudi na atakuja kukuona”“Sawa, ila mama mbona ulishangaa sana kuona picha ya marehemu baba yangu?”“Aaaah kuna mtu nimemfananisha nae, hivi huko kwenye kaburi la baba yako mmeanza kwenda lini?”“Toka mwaka juzi, huwa tunaenda mara kwa mara na mama na kufanya usafi kwenye kaburi la baba”“Huyo baba yako aliitwa nani?”“Mama, aliniambia kuwa baba anaitwa Jimmy”Hapo kidogo mama Angel akashtuka na kuhisi pengine kuna ukweli ila bado ilimchukua ngumu sana kuamini, akamuuliza baadhi ya maswali Sarah na mwisho wa siku aliamua kutoka nae sebleni ili wakae waangalie hata vipindi mbalimbali kwenye luninga.Siku akiwa anafanya kazi zake, mara alifika pale mama mkubwa wa Sarah yani dada yake na mama Sarah, na alienda pale kwa lengo la kumuona Sarah, kwakweli aliogopa sana ukizingatia katoa ruhusa ya Sarah kwenda kuhudumiwa pengine,“Haya Saraha yuko wapi?”Siku alikuwa akitetemeka kwani alimjua huyu alivyo mkali,“Nisamehe mama”“Nikusamehe kitu gani? Yuko wapi Sarah?”Ikabidi amueleze ukweli wote wa jinsi ilivyokuwa hadi kufikia hatua ya kumpa Sarah ruhusa,“Hivi wewe Siku una akili kweli, hata kama umeshindwa kumuuguza mtoto si ungenipigia simu hata mimi nije nimchukue jamani! Ila ni vyema alijitokeza huyo msamalia mwema, yani wewe huna maana kabisa, mdogo wangu anakuhudumia bure, anakupa kila kitu halafu unashindwa kumuuguza mtoto wake kweli!! Shwain, haya nipeleke huko kwa msamalia mwema”Ilibidi Siku ampeleke huyu dada wa mama Sarah hadi nyumbani kwa mama Angel, walifika pale na kuingia ndani ambapo walipogonga mlango wa sebleni ni mama Angel ndio alienda kufungua mlango ili awakaribishe ila mama Angel alishangaa baada ya kumsikia yule mgeni akisema,“Kumbe ni wewe Erica, sikupendi”Halafu yule mgeni akamnasa kibao mama Angel.Sara alijikuta akimpa tu mama Angel ile picha ya marehemu baba yake, ila mama Angel alipoiangalia ile picha alionekana kushangaa sana kwani ni mtu aliyemfahamu vizuri kabisa.Mama Angel alimuangalia Sarah kwa makini sana na kumuuliza,“Kwahiyo huyu ndio marehemu baba yako?”“Ndio, ni marehemu baba yangu”“Umewahi kumuona?”“Sijawahi, mama aliniambia kuwa alikufa pindi tu nilipozaliwa”“Mmmmh!”“Mbona unaguna mama? Ila baba yangu alinipenda sana kwani mama anasema kuwa hata hii nyumba baba aliijenga kwaajili yangu hata kabla sijazaliwa, na biashara nyingi za familia ni yeye aliziweka kwaajili yangu yani hakutaka mimi nipate shida, natamani sana angekuwepo baba yangu maana alinipenda sana”Mama Angel akamuangalia kwa makini Sarah na kumtaka muda huo waende nae hospitali tu huku akili yake ikiwaza vitu vingi sana kutokana na ile picha aliyoiona.Basi waliondoka na Sarah kuelekea hospitali ambapo alichukuliwa vipimo na kugundulika kuwa ana malaria, kwahiyo alipewa dawa na kuruhusiwa kurudi nyumbani.Basi mama Angel na Erick wakamrudisha Sarah nyumbani kwao ambapo alikuwepo msichana wa kazi tu akiishi nae sababu mama yake hakuwepo, ila mama Angel alitamani sana waondoke na Sarah ili akamuhudumie kwani aliona kuwa Sarah anahitaji kupata huduma ya karibu zaidi, sema Erick akamzuia mama yake,“Ila mama, utamchukuaje Sarah bila ruhusa ya mama yake? Ungempata mama yake hewani basi ungeongea nae kwanza ila sio kujichukulia tu maamuzi”“Basi mwanangu nimekuelewa”Kisha mama Angel alimuuliza yule msichana wa kazi wakina Sarah kama ataweza kukaa na mgonjwa vizuri,“Nitakaa nae tu mama, hakuna tatizo”“Nitajitahidi kesho mchana nije kumuona pia hali yake inaendeleaje”“Sawa, nashukuru sana”Basi mama Angel na Erick ikabidi wage pale kwakina Sarah na kuondoka zao, basi wakiwa kwenye gari Erick akamuuliza mama yake,“Mbona mama ile picha ya marehemu baba yake Sarah imekushtua sana?”“Unajua ni mtu ninayemfahamu sana, sijui hata nikwambiaje ila kwa kifupi Sarah ni ndugu yenu”“Mmmh mama, ndugu yetu kivipi?”“Kama ile picha aliyonionyesha ni kweli basi elewa kuwa Sarah ni ndugu yenu”Erick alishangaa na kumuangalia mama yake bila ya kummaliza, kisha akamwambia,“Ndiomana ulikuwa uking’ang’ania tukamuuguze nyumbani!”“Hapana hiyo sio sababu ila tu nilitaka kuwa nae karibu sababu ni mgonjwa”“Hapana mama nadhani ni sababu unahitaji kujua zaidi kuhusu baba yake Sarah, ila ni marehemu kumbuka”“Ndio ni marehemu kwani mimi nimesema yuko hai! Hebu endesha gari na wewe, hivi unajua muda umeenda sana na tangu tuondoke nyumbani hatujarudi mpaka muda huu, sijui mwanangu kaliaje huko jamani”“Atakuwa Amelia sana ila Erica yupo atambembeleza”“Unamuamini sana Erica eeeh! Ndiomana ulitaka kuja kumuombea niwe nampa mia tano! Hebu elewa jambo moja, yule ni mtoto wa kike, naogopa kumzoesha hela”Hapo Erick hakuongea neno lolote zaidi ya kuendelea kuendesha gari tu.Erica alikuwepo nyumbani akimbembeleza mdogo wake tu, ni kweli siku hii mama yao alichelewa sana kwenye hiyo safari aliyoenda na Erick, basi Erica akawa anamuuliza Vaileth,“Kwani walienda wapi?”“Nilisikia kuwa wameenda kumuona Sarah”“Kafanyeje huyo Sarah?”“Nasikia anaumwa”“Ila mama nae jamani loh! Mtoto analia hivi”“Ngoja nikubebeshe labda atatulia”Basi Vaileth alimbebesha Erica yule mtoto, na kweli alivyombeba mgongoni alitulia na alionyesha kubembelezeka hata kulala alianza kulala sasa, na alivyotulia vizuri, Erica aliweza kukaa na kuangalia Tv.Muda kidogo mama Angel na Erick walirudi na kumkuta Erica akiwa kambeba mtoto mgongoni,“Oooh Erica mwanangu, kweli umekuwa mama. Pole eeeh!”Kisha mama Angel akamchukua mtoto na kwenda nae chumbani, halafu Erick akaenda pia chumbani kwake ambapo alipakuta pamepangwa vizuri kabisa, akaenda kuoga kwanza ili akale maana hakula chochote kile toka ameondoka na mama yake, basi alienda kula na kumkuta Erica akiwa pale mezani,“Nilikuwa nakusubiri tu, nikasema usipotoka basi nakuja kukufata mwenyewe humo chumbani kwako maana mmeondoka bila kula”“Ni kweli, na nilikuwa nahisi njaa hatari ila nilikuwa navumilia tu”“Anaendeleaje huyo Sarah”“Tulimpeleka hospitali, tumemkuta ana malaria.”Basi Erick alikuwa anakula, kisha mama yao nae anaenda kula, basi anakula pale huku akiongea ongea nae ila alikuwa na mawazo sana huku akitamani kumwambia mume wake kuhusu alichokipata kwakina Sarah.Mama Angel alipomaliza tu kula alienda chumbani na kujilaza huku akifikiria mambo kadhaa, akachukua simu yake na kumpigia mume wake ili ampe ujumbe, simu ile ikapokelewa ila mumewe aliongea katika hali ya usingizi sana,“Kumbe ushalala mume wangu?”“Muda umeenda huu mama Angel”“Haya usiku mwema”Basi akakata simu na kuanza kufikiria mambo kadhaa, kwanza kuhusu Sarah na yule aliyemuona kwenye picha,“Hivi inawezekana kweli marehemu mzee Jimmy akawa ndio baba mzazi wa Sarah!! Mmmh natakiwa kuonana na mama Sarah ili nimuulize vizuri. Ila si mpaka mwisho wakina Erick walisema kuwa baba yao ana matatizo ya uzazi!! Anaweza kuwa na mtoto kweli halafu watoto wake wasijue? Halafu kwanini Sarah aseme baba yake kafa baada ya yeye kuzaliwa, jamani mbona mzee Jimmy kaacha hata wajukuu wake wamekuwa kuwa, maana nakumbuka kifo chake wakina Erica walikuwa darasa la tano! Inakuwaje Sarah awe kabla hajazaliwa? Mmmh!”Alichoka sana kufikiri ila alishangaa siku hiyo akiwa hana usingizi hata kidogo, aliamua kuchukua simu ya mwanae Angel ile iliyopasuka kioo, aliiwasha nayo ikawaka, na moja kwa moja alifungua data na kuingia kwenye facebook ya mtoto wake ili aangalie alikuwa akiwasiliana na nani, ila aliona mtu ambaye mwanae aliwasiliana nae sana alikuwa ni Samir, tena sio kwa kutumia facebook maana inaonyesha walitumia ujumbe wa kawaida kwa sana kwenye mawasiliano yao. Basi alikuwa akiangalia tu taarifa mbalimbali za kwenye mtandao, ndipo alipoona mtu kaandika ujumbe, unaosema,“Jamani mwenzenu simuelewi mume wangu, akiwa yupo nyumbani ataniita majina yote mazuri, mara mke wangu, mara mpenzi yani hadi huwa Napata raha sana, ila akiwa mbali sasa balaa nikimpigia simu muda wowote hata usiku wakati amelala utasikia ananiita mama Fulani, yani haniiti mke wangu kama nyumbani”Mama Angel akapumua kidogo, na kuangalia wachangiaji walichosema,“Ukiona hivyo ujue unaibiwa, mumeo anaogopa kukuita mke wangu maana mchepuko atajua kama ana mke, kumbuka sio michepuko yote wanaojuaga kuwa huyu mtu kaoa au ana mke, wengine hawajui kwahiyo anazidi kumficha”“Tena mimi wangu utakuta unampigia anajifanya amelala kumbe anachepuka, jamani wanaume hawa Mungu atusaidie tu”“Pole sana, hapo jua tu kuna watu wanakusaidia”“Tena mwingine akiona unamsumbua usiku anaamua kuzima na simu kabisa, yamenikuta hayo. Poleni wanawake wenzangu”Mama Angel alihisi tumbo lake kuunguruma kwa muda huo kwani akizingatia ni muda mfupi tu katoka kumpigia mume wake simu na alionyesha kuwa amelala halafu hakumuita mke wangu kama siku zote bali alimuita mama Angel, basi alijikuta akishikwa na wivu na kuchukua tena simu ili kumpigia, jibu lililokuja,“Mtumiaji unayempigia hapatikani kwasasa, tafadhari jaribu tena badae”Yani hapo ndio alihisi kuibiwa kabisa, na usingizi ndio ukakata kabisa alijikuta akishindwa kulala hadi panakucha yani hakuwa na usingizi hata kidogo.Kwenye mida ya saa mbili asubuhi, mama Angel aliamua kumpigia tena simu mume wake ambaye kwa muda huo alipokea na kuanza kuongea nae,“Mume wangu, ilikuwaje ukazima simu yako?”“Yani jana nilichoka sana halafu simu kumbe iliisha chaji kwahiyo ikajizima yenyewe, samahani mama Angel”“Na hiyo mama Angel vipi? Mbona sikuelewi?”“Jamani mke wangu, hunielewi nini tena?”Hapo mama Angel alitabasamu kiasi na kumwambia,“Unajua mara nyingine napata mashaka, vile ukishindwa kuongea nami kwenye simu!”“Mashaka ya nini tena mke wangu jamani!! Siku zote hizi hujanizoea tu eeeh!! Nawezaje kufanya ujinga kwako? Usiniwazie tofauti mke wangu, tujenge maisha yet utu. Vipi watoto lakini wanaendeleaje?”“Wapo salama tu, ila kuna jambo nahitaji tuongee ukirudi mume wangu maana nadhani kwasasa wala hatutoelewana”Sababu mumewe alikuwa anawahi kwenye shughuli zake za huko, ikabidi waagane tu maana hakukuwa na namna tena.Mchana wa siku hiyo, mama Angel aliamua kwenda kumuona tena Sarah, na alipofika alimkuta Sarah anatapika na kupata habari kuwa alitapika sana hata asubuhi ya siku hiyo, basi alimsaidia pale na kukaa nae ndani kwa muda, kisha akamuomba yule msichana wa kazi ili amruhusu yeye kuondoka na Sarah,“Naomba uniruhusu niende na Sarah ili nikamuuguze nyumbani kwangu”“Mmmh hapana mama, siwezi kukubali maana watanisema sana ukizingatia nimeachiwa mimi dhamana ya kumuangalia Sarah”“Ila anaumwa sana, eti Sarah unasemaje kuhusu mimi kukuchukua ukaugulie nyumbani kwangu eeeh!”“Nipo tayari, hapa dada hata haniangalii vizuri”Basi dada yake akamuangalia na kusema,“Jamani Sarah, kweli sikuangalii vizuri mimi!”“Sina maana hiyo, ila nikienda kwa huyu mama nitapata nafuu kwa haraka sana, kumbuka mama yangu hayupo na mimi napenda kuwa karibu na mama, halafu mama yangu hayupo unadhani ni nani anaweza kunipa mapenzi ya mama zaidi ya huyu aliyejitolea? Mimi nawafahamu ni watu wenye roho nzuri, nipe ruhusa tu niende dada Siku”“Mmmh jamani sijui yani”Mama Angel ikabidi amtoe uoga,“Sikia Siku, tutaenda wote hadi nyumbani kwangu ambapo atabaki Sarah ili nimuhudumie kwa ukaribu, yani wewe upafahamu nyumbani kwangu ili usiendelee kuwa na mashaka nami”Basi Siku akakubali na kuenda kumuandalia Sarah nguo chache kisha kuondoka nao mapaka nyumbani kwa mama Angel.Walifika pale, walikaribishwa vizuri kabisa na Vaileth kisha baada ya muda kidogo Siku aliondoka tu kurudi kule nyumbani kwa mama Sarah.Leo Erick anawahi kutoka shule sababu alishaomba ruhusa kwa mwalimu wake, hivyobasi alivyoondoka tu moja kwa moja alienda kwenye duka la baba yake, na kuanza kuangalia vizuri ila wakati yupo pale dukani alifika yule rafiki wa Steve yani yeye alienda kwaajili ya kumtembelea rafiki yake maana siku zote alifika na kukuta duka limefungwa, basi alivyomkuta Erick ndio alianza kuongea nae,“Steve ni rafiki yangu sana”“Aaaah, basi Steve kapata kazi sehemu nyingine. Na hapa tunatafuta mtu”“Jamani hata mimi nafaa jamani, sina kazi mimi”“Unaitwa nani kwani?”“Naitwa Rama”“Oooh ila majina ya Rama, naona wengi ni wastaarabu. Basi fanya hivi, kesho nitakuja hapa dukani niletee wadhifa wako yani cheti chako, barua ya serikali ya mtaa wako na barua yako ya maombi ya kazi, nitaipitisha ili Jumatatu uanze kazi”“Dah! Nashukuru sana, yani sasa hivi naenda kufanya hivyo vitu. Yani mimi nahangaika tu siku zote hizi sina kazi”“Basi ndio umepata kazi, ila kuwa muaminifu kama jina lako”“Hata hivyo mimi ni muaminifu kweli, hivyo vitu hata leo leo ningevileta”“Ila naona muda umeenda, nitachelewa nyumbani. Jitahidi iwe kesho halafu ndio nitakuonyesha na vitu ndani tunafanyeje”“Asante sana”Kisha Rama akaondoka muda huo ili kwenda kushughulikia vitu hivyo.Erick aliangalia angalia vizuri kwenye lile duka na wale walinzi ambao baba yake aliwaweka, kisha akataka kuondoka basi wakati anatembea ili aite bodaboda aondeke nayo, alishangaa akishikwa bega, alipogeuka alikuwa ni Sia amemshika bega, Erick akachukia sana na kusema,“Ni wewe kimama tena!!”“Najua Erick unanichukia sana, ila ungepata kuona nafsi yangu jinsi gani napata faraja hata kuongea nawe tu, ungenielewa”“Unataka nikuelewe kuhusu nini? Kuwa wale ninaoishi nao sio wazazi wangu? Na wewe ndiye mama yangu au nini?”“Bado una mambo hayo tu Erick jamani, achana na mambo hayo ya mwaka jana, zama zimebadilika hizi. Ni hivi Erick, endelea kuwaheshimu na kuwasikiliza wazazi wako ila na mimi usinichukie kiasi hiko, nipende na kunijali, sio kosa langu mimi kufanya yote haya ninayoyafanya, ipo siku utanielewa ni kwanini nafanya haya niyafanyayo, naomba unisamehe sana”“Achana na mimi bhana”“Nitaachana nawe ila niambie kuwa umenisamehe, Erick sitaki kuwa kikwazo katika mafanikio yako ila nataka kuwa chachu ya wewe kufanikiwa zaidi, achana na yote yaliyopita Erick mwanangu”“Hapo ndio unaponikera, nani mwanao?”“Mtoto wa mwenzio ni wako, kwahiyo wewe ni kama mwanangu. Nakuona wewe ni kama Elly, usinichukie Erick”“Kwaheri”Erick alishaita bodaboda na kupanda kisha aliondoka nayo sababu tu hakutaka kuendelea kumsikiliza Sia.Basi Erick anarudi hadi nyumbani kwao, ila alipofika tu sababu ya uchovu ni moja kwa moja alienda chumbani kwake na kujilaza, yani leo alisahau hata kwenda kula au kuvua sare za shule kwani alihisi kichwa chake kuchoka sana.Muda huu mama Angel alikuwa sebleni pamoja na Erica sababu Sarah alikuwa amelala, ila Erica alikuwa akimlalamikia mama yake,“Yani mama ndio kumuweka Sarah nilale nae kweli?”“Kwani kuna ubaya gani jamani! Sarah ni mgonjwa unataka alale peke yake, akizidiwa je!”“Ila mama, aaargh jamani”Erica akaondoka na kwenda tena chumbani kwake, muda kidogo alifika Junior na mama Angel kumshangaa,“Kheee Junior, umerudi tena!”“Mamdogo, leo ni mwisho wa wiki, nitaenda tena shule Jumatatu”“Sasa hiyo ni shule ya bweni au ni shule ya kutwa?”“Jamani mamdogo, yani wanafunzi wote wa karibu wameondoka leo, ni wale wa mbali tu ndio wamebaki, halafu na mimi nibaki kweli wakati naishi karibu hapa”“Haya, nimekuelewa”Kisha Junior moja kwa moja alienda jikoni kwani alijua huko lazima atamuona Vaileth na kweli alimkuta akiwa ndio anamalizia kupika, basi akaenda nyuma yake na kumbusu halafu akamwambia,“Unajua siwezi kukaa shule kwa siku nyingi zaidi maana mawazo yangu yote ni juu yako”Vaileth alitabasamu tu, mara ikasikika sauti ya mama Angel,“Vai, hiko chakula bado tu!”“Ndio namalizia mama”Mama Angel tayari alishafika jikoni na kumuuliza Junior,“Na wewe Junior, kituo cha kwanza jikoni kuna nini?”“Ni njaa mamdogo, nahisi njaa sana”“Khaaa wanafunzi wa bweni jamani mna vituko sana, haya Vai andaa hiko chakula ili wote wapate kuja kula”Kisha Junior akatoka, na mama Angel akatoka pia kwenda kumchukua Sarah chumbani ili aweze kula chakula.Alijua Erica atamkuta chumbani pia ila Erica hakuwepo mule chumbani, basi alikaa na Sarah na kumwambia,“Twende basi ukajaribishe kula chakula nilichokuandalia”“Mmmh hata sijisikii kula”“Hapana Sarah, ule japo kidogo upate nguvu binti yangu”Mama Angel akatoka na kwenda kumletea chakula Sarah na kuanza kujaribu kumlisha pale ni kweli alikula, tena alikula vizuri tu na baada ya kushiba sasa aliongea nae kidogo na kumruhusu apumzike halafu yeye akatoka na kuondoka zake, hakuwa na tatizo na wanae kwani alijua ni lazima wangeshuka na kula chakula tu.Erica aliamua kwenda chumbani kwa Erick ili kumuelezea, ila alimkuta akiwa amelala tena bado hajavua hata sare za shule, basi alimshtua na Erick aliamka,“Wewe Erick, nini tena?”“Dah!! Nimechoka sana jamani”“Kwahiyo hata kula hujala jamani, halafu sikujua maana ningekuja kukuamsha muda sana”Basi Erick ndio aliinuka na kuanza kubadili zile sare za shule,“Khee unabadili nguo hata huniambii nikupishe?”“Sasa unipishe kitu gani? Kuna kipi hukijui katika mwili wangu”Erica alicheka tu na kuinuka, kisha akamwambia,“Utanikuta sebleni”Basi Erick alienda kuoga na baadae alishuka kwenda kula chakula na baada ya hapo aliongozana tena na Erica kwenda chumbani kwake, basi Erica alianza kumwambia,“Mama, anaupendeleo sana”“Kafanyaje kwani?”“Mama kamleta Sarah hapa nyumbani”“Mmmh kamleta Sarah?”“Ndio, kumbe hujui! Basi mama kaja na Sarah leo, ila anavyomjali huyo Sarah tofauti na sisi, yani Sarah kaenda kulishwa chakula sababu anaumwa halafu kamuweka nilale nae mimi”“Unasema kweli mama kamleta Sarah hapa nyumbani? Kakubaliana na mama yake kweli?”“Sijui ila ndio Sarah yupo hapa nyumbani, kwakweli mimi siwezi hata kwenda kulala huko chumbani bora nikalale sebleni tu”“Aaaah jamani usifanye hivyo”“Mimi sikubali, mama angetaka aneomba ushauri kwanza kwangu mwenye chumba sio kujiamulia tu mwenyewe na maamuzi yake”Kisha Erica akainuka na kusema,“Usiku mwema”“Kwahiyo ndio unaenda kulala sebleni?”“Ndio, siwezi kwenda kulala chumbani kwangu”“Hapana usiende kulala sebleni, tafadhari baki humu chumbani tulale wote”Erica nae aliona ni jambo jema, kwahiyo alibaki humo chumbani kwa Erick na muda huo wakalala wote.Kulipokucha, mama Angel alienda kumuangalia Sarah ajue hali yake ila alimkuta ameanza kupona maana hata nuru usoni mwake ili onekana, basi alimsalimia pale na kuongea nae kidogo,“Eeeh unajisikiaje, unaendeleaje?”“Naendelea vizuri mama”“Vipi huyu Erica ameshaamka nini”“Sijui, kwani Erica huwa analala humu?”“Ndio, huwa analala humu”“Basi sikumuona maana nililala mwenyewe tu kama nyumbani”“Kwahiyo nyumbani kwenu napo umezoea kulala mwenyewe eeeh!”“Ndio, mama huwa anasema mimi ni mlalavi yani nalala vibaya kwahiyo nisilale na mtu, huwa nalala mwenyewe tu”“Oooh basi sawa, labda Erica kajiongeza. Asubuhi hii nikuandalie nini?”“Mmmh labda supu ya kuku na chapati”“Sawa, hakuna tatizo”Basi mama Angel alienda jikoni na kuandaa hiko chakula mwenyewe, yani Erica alimkuta mama yake akiandaa hiko chakula,“Ndio chakula chetu hiko leo mama?”“Cha mgonjwa hiki, si unajua Sarah anaumwa?”“Najua ila na mimi nitakula hiko hiko unachomuandalia Sarah”Mama Angel hakusema neno maana alimtambua wazi mtoto wake huyu kwa ubishi, basi alimuita Vaileth tu na kumtaka aandae supu ya nyumba nzima ili wote wapate kunywa supu hiyo.Mida ya saa nne asubuhi, Erick alijiandaa na kumuaga mama yake ila kwa muda ule Erica nae aling’ang’ania aondoke na Erick maana hakutaka kukaa hapo nyumbani wala nini.Basi mama yake alimruhusu tu bila kujua kuwa Erica amechukia uwepo wa Sarah pale nyumbani kwao.Baada ya kuondoka tu, ni Vaileth ndio alienda kumwambia ukweli,“Unajua nini mama, mwenzio Erica kachukia uwepo wa Sarah”“Jamani haka katoto sijui nani kakafunza roho mbaya mweeeh!”Kisha mama Angel alienda kuongea na Sarah ambaye bado alikuwa chumbani na alitoka kuoga tu kwa muda huo,“Unajionaje hali kwa muda huu Sarah?”“Nimepona, maana hata nimeweza kuoga. Ila kwanini Erick hajaweza kuja hata kuniona huku chumbani!”“Kheee hakuja kukuona! Nadhani sababu ya majukumu yake, ila atawahi kurudi na atakuja kukuona”“Sawa, ila mama mbona ulishangaa sana kuona picha ya marehemu baba yangu?”“Aaaah kuna mtu nimemfananisha nae, hivi huko kwenye kaburi la baba yako mmeanza kwenda lini?”“Toka mwaka juzi, huwa tunaenda mara kwa mara na mama na kufanya usafi kwenye kaburi la baba”“Huyo baba yako aliitwa nani?”“Mama, aliniambia kuwa baba anaitwa Jimmy”Hapo kidogo mama Angel akashtuka na kuhisi pengine kuna ukweli ila bado ilimchukua ngumu sana kuamini, akamuuliza baadhi ya maswali Sarah na mwisho wa siku aliamua kutoka nae sebleni ili wakae waangalie hata vipindi mbalimbali kwenye luninga.Siku akiwa anafanya kazi zake, mara alifika pale mama mkubwa wa Sarah yani dada yake na mama Sarah, na alienda pale kwa lengo la kumuona Sarah, kwakweli aliogopa sana ukizingatia katoa ruhusa ya Sarah kwenda kuhudumiwa pengine,“Haya Saraha yuko wapi?”Siku alikuwa akitetemeka kwani alimjua huyu alivyo mkali,“Nisamehe mama”“Nikusamehe kitu gani? Yuko wapi Sarah?”Ikabidi amueleze ukweli wote wa jinsi ilivyokuwa hadi kufikia hatua ya kumpa Sarah ruhusa,“Hivi wewe Siku una akili kweli, hata kama umeshindwa kumuuguza mtoto si ungenipigia simu hata mimi nije nimchukue jamani! Ila ni vyema alijitokeza huyo msamalia mwema, yani wewe huna maana kabisa, mdogo wangu anakuhudumia bure, anakupa kila kitu halafu unashindwa kumuuguza mtoto wake kweli!! Shwain, haya nipeleke huko kwa msamalia mwema”Ilibidi Siku ampeleke huyu dada wa mama Sarah hadi nyumbani kwa mama Angel, walifika pale na kuingia ndani ambapo walipogonga mlango wa sebleni ni mama Angel ndio alienda kufungua mlango ili awakaribishe ila mama Angel alishangaa baada ya kumsikia yule mgeni akisema,“Kumbe ni wewe Erica, sikupendi”Halafu yule mgeni akamnasa kibao mama Angel. Ilibidi Siku ampeleke huyu dada wa mama Sarah hadi nyumbani kwa mama Angel, walifika pale na kuingia ndani ambapo walipogonga mlango wa sebleni ni mama Angel ndio alienda kufungua mlango ili awakaribishe ila mama Angel alishangaa baada ya kumsikia yule mgeni akisema,“Kumbe ni wewe Erica, sikupendi”Halafu yule mgeni akamnasa kibao mama Angel.Kwakweli mama Angel alimshangaa sana, huku akimuangalia kwa makini huyu mwanamke ambaye alionekana kuwa na gadhabu sana, basi mama Angel alimuuliza,“Kwani tatizo nini dada?”Yule mama aliongea huku akibana pua na kuiga alichoongea mama Angel,“Kwani tatizo nini dada? Hivi una akili wewe mwanamke, yani unaweza hata kuthubutu kumchukua mtoto wa dada yangu umlee na hiyo roho yako mbaya! Muone vile, sikupendi kabisa”“Nimefanyaje? Sikuelewi?”“Hunielewi eeeh!! Sio wewe uliyekuwa ukishangaa shangaa pindi ukifika ofisini kwa Erick! Sio wewe ambaye kipindi kile nilitaka kukuraluwa halafu ukatetewa na Sia!!”Huyu mama akacheka kwanza na kusema,“Mimi ndio Linah, haya huyo Sia kikowapi? Kaolewa na Erick au kaishia wapi? Sikupendi wewe”Mama Angel akajaribu kuvuta kumbukumbu ila kumbukumbu zake ziligonga mwamba kabisa, akaona kuwa anatakiwa kutumia busara tu kwa muda huo maana hakumuelewa kabisa huyu mtu anamaanisha nini.Basi alirudi sebleni na kukaa ambapo wale nao waliingia, kisha yule mama alienda kumshika mkono Sarah ili aondoke nae, ila Sarah aligoma,“Mimi sitaki kuondoka”“Kheee una wazimu wewe au kitu gani? Sasa hutaki kuondoka, ni kwenu hapa?”“Sio kwetu ila naridhika nikikaa hapa, hata nimepata amani ya moyo na nimeanza kupona, nitarudi kesho”Yule mama akamuangalia mama Angel na kumuuliza,“Umemfanya nini mtoto wangu wewe Erica na uchawi wako?”Mama Angel alikuwa nyumbani kwake ila alinyamaza kimya kabisa na alishindwa kusema jambo lolote kwani hakumuelewa huyu mtu kabisa.Huyu mwanamke alionekana yupo kwa shari mahali hapo na kwenda kumbeba Sarah kinguvu na kutoka nae nje halafu alimwambia mama Angel,“Mimi na wewe hatujamalizana, kama siku ndio kwanza imeanza na nitahakikisha unanikumbuka vizuri, mjinga sana wewe mwanamke”Halafu akatoka na kuondoka akiwa na Sarah pamoja na yule msichana Siku maana yule msichana hakuongea neno lolote lile zaidi ya kufanya vile alivyo amriwa tu.Mama Angel kwakweli alipumua kidogo na kuinuka kwenda chumbani kwake maana yale yalikuwa maswahibu kwake, alijaribu kuwaza sana bila hata ya kupata jibu, alijiuliza sana lakini hakupata jibu,“Linah! Linah ndio nani mbona simkumbuki jamani! Nimewahi kuonana nae wapi?”Akakumbuka pia huyu msichana kamtaja Sia, hapo akaona kuna ulazima wa kumtafuta Sia ili aweze kujua huyu mwanamke ni nani kabla hajamrudia tena maana kwa ule muda mchache hakumuelewa kabisa.Leo alichukua simu yake na kumpigia Sia, kitendo ambacho hajawahi kukifanya kutokana na akili ya Sia,“Kheee leo Erica umenipigia! Kweli maajabu, kuna nini tena jamani?”“Nina maongezi na wewe”“Oooh nije kwako? Nakuja sasa hivi, utamwambia basi mlinzi aniruhusu niingie”Muda ule ule Sia alikata simu yani hakusikiliza maelezo mengine wala nini inaonyesha alifurahi kusikia kuwa mama Angel ana mazungumzo nae.Basi mama Angel akajiweka sawa na kusema,“Najua si jambo jema kuzungumza na Sia ila kwa hili natakiwa kuzungumza nae tu, natakiwa nimtambue huyu mwanamke mapema, maana simkumbuki kwa lolote lile jamani”Baada ya muda mfupi tu alipokea simu toka kwa mlinzi akiulizwa kuwa amruhusu Sia nae alisema amruhusu basi alitoka nje na kukutana na Sia na moja kwa moja alienda nae kwenye bustani yake kuzungumza nae,“Najua utashangaa sana kwanini nimekuita”“Kweli nashangaa hadi muda huu bado nashangaa, upendo ulionionyesha leo ni mkubwa”“Kheee jamani wewe mwanamke, hivi huna mashaka kuwa nitakudhuru?”“Wapo wakuwa na mashaka nao ila sio mtu kama wewe, nikiitwa na yule Oliva lazima ningeomba usaidizi wa kusindikizwa, ila wewe hapana jamani huwezi kunidhuru. Niambie tu ulichoniitia hata hivyo mimi sio adui yako kabisa, ila adui yako ni mapenzi”“Mapenzi ndio adui yangu!! Khaaa tuachane na habari hizo kwanza, kuna kitu nataka nikuulize”“Kitu gani?”Mama Angel alimueleza kwa kifupi tu kuhusu mtu aliyekuja hapo nyumbani kwake na kusema anaitwa Linah, hakumuelezea tu kuhusu Sarah kuwa alienda kumchukua au nini ila alimuelezea kile alichotaka kufahamu kuhusu Linah,“Unajua nimejaribu kumkumbuka ila simkumbuki kabisa, sema kasema kuwa alitaka sijui kuniburuza ofisini ila nikaokolewa na wewe”“Kheee yani kumbe yule Linah mkorofi ndio kapajua hapa kwako!! Mbona pole sana”“Eeeeh nielekeze vizuri”“Kipindi cha zamani hapo, wakati mwanao Angel akiwa mdogo sijui ulitumwa na Erick kuja ofisini kumchukulia Angel bima ya afya, ila yule secretary akasema subiri, na mara akaja Linah na kukusukuma, ni kidogo tu ungebamiza kichwa hiko ila kwa bahati nilitokea nyuma yako na kukudaka”Hilo tukio mama Angel aliaweza kulikumbuka na kusema,“Aaaah kumbe!! Ndio yule mdada alikuwa baunsa?”“Ndio huyo huyo, na ni baunsa kweli yani, siku ile nisingetokea kukutetea lazima ungerudi kwenu na ngeu, maana yule pale ofisini kote walikuwa wanamuhenya”“Sasa nimekumbuka, ila mimi kosa langu nini kwani hadi leo?”“Kosa lako si kumchukua Erick! Kwani hujui ni kwanini tunakuchukia jamani? Ni sababu ya Erick tu, yani Erick ndio tatizo wa yote haya”“Hebu leo tuongee vizuri kwanza, maana hadi sijamuelewa huyu Linah kabisa”“Ngoja nikueleze kwa kifupi, na miaka hiyo ya nyuma niliwahi kukwambia, ni hivi Erick hakuna rangi ya mwanamke aliyoiacha, aliyejichubua kidogo, aliyejichubua sana, aliyekuwa hasilia wote kapita nao, mwembamba, mnene, mrefu, mfupi, saizi ya kati wote kapita nao yani Erick hakuna mwanamke aliyeacha, sema wengine tulikuwa tukimvumilia tu huku tukijipa moyo kuwa ipo siku atatuoa, kama mimi na wengi waliamini nitaolewa na Erick ila haikuwa hivyo”Sia akapumua kidogo na kuendelea,“Sasa kuhusu Linah, pale ofisini mwanamke ambaye alitembea na Erick halafu alikuwa na nguvu sana na wote ofisini walimuogopa alikuwa ni Linah, yani yeye ndio kila mtu pale ofisini alikuwa akimuogopa kasoro mimi ambaye wengi walihisi ndio nitakuwa mke halali wa Erick, kama kuhusu mimba, Erick kashatutoa sana mimba, kiukweli Erick unamuona mstaarabu tu kwasasa ila kama watoto naye angekuwa na kijiji chake kwasasa, ila katoa wanawake wengi sana mimba, na wengi walikuwa wakikubali maana alikuwa anasema ukiendelea na hiyo mimba naachana na wewe, basi tukajikuta tunakuwa watumwa kwa Erick. Yani ilikuwa unamkuta na Kitabu chake kidogo kina tarehe za siku za wanawake zake kama ni siku zake vile, yeye hadi anakukumbusha ukachome sindano za majira. Kwakweli Erick alikuwa akijijali yeye na hisia zake tu, sasa kilichotokea ni kwamba, baada ya sakata lako kila mtu pale ofisini alikuwa hakufagilii wala nini, ila kuna jambo baya sana lilitokea maana Erick alirudi na kutufukuza wote kazi, yani wote na akaajili watu wengine kwahiyo watu wengi walikosa kazi sababu yako akiwepo na huyo Linah, na hadi anaondoka pale kazini alisema nikija kumkamata huyo Erica nahisi atanitambua vizuri”“Duh jamani, sasa mimi nahusika na nini hapo?”“Wewe huhusiki ila ni kwamba mtu anakuwa na kinyongo tu na kuhisi kuwa wewe ndio chanzo, ila una pesa Erica, basi usibabaishwe na huyo Linah, halafu mumeo akirudi hebu mwambie akae sawa na wanawake wote aliowapitia ili ajue kaacha doa gani”“Duh!”“Usishangae, haya mambo ndio yalivyo, unajua mara nyingine mtu unafanya jambo katika maisha ila hujui madhara yake sema badae yanapokutokea puani ndio uanjua kuwa ulichokuwa unafanya hakikuwa sawa. Katika wanawake wote wa Erick basi mimi ndio nilikuwa namba moja maana nilijulikana na familia yake nzima, mama yake, baba yake, huyo dada yake Tumaini ndio alikuwa rafiki yangu mkubwa sana na anajua ni mangapi nimepitia kwa mdogo wake, ni kweli natenda mambo ya karaha ila huyo Tumaini hawezi kusema sana kwani anajua ni mangapi nimepitia, huyo Erick pia ataishia kunipiga tu ila hawezi kunifanyia kitu kibaya maana ingawa kwa ubaya wangu ninaoufanya ila bado kuna mazuri yangu ambayo akiyafikiria moyo wake unamsuta sana”“Mmmh!”“Usigune Erica, kumbuka Erick alikuwa ni mlevi sana anaweza akajitapikia balaa basi mimi nitamtoa nguo na kuanza kuzifua na kusafisha pote alipotapika, kuna siku alitapikia gari yake nilifanya usafi kwenye gari ila kamavile hakutapika kabisa, kwakweli nilikuwa najitoa sana kwa Erick nikiamini kuwa yeye ndio atakuja kuwa mume wangu na nitaishi nae kwa furaha na amani”Mama Angel akaona hapo ataletewa stori zingine kabisa, basi aliamua kumkatisha Sia kwa kumshukuru kwa kumuelezea kuhusu Linah kisha akamuaga,“Kheee jamani ndio hata kwenda ndani kwako kula hakuna!”“Mimi sikukuita uje kula ila nilikuita kwasababu hiyo”Ila mama Angel alijua wazi kuwa Sia alikuwa akipenda sana pesa basi alienda ndani na kumtolea pesa kidogo na kumpa, basi Sia akatabasamu na kuondoka zake, kisha mama Angel akaenda zake ndani sasa.Erick alikuwa na Erica kwenye lile duka la baba yao, na muda kidogo yule Rama alifika na vile vitu alivyokuwa ameagiziwa na Erick,“Oooh ndio umeniletea wasifu wako eeeh!”“Ndio, kama ulivyoniagiza jana”Basi Erick alifungua ile bahasha na kupitia pitia, basi Rama alikuwa akimuangalia Erica jinsi alivyokuwa akiangalia angalia vitu pale dukani, akamuuliza Erick,“Samahani, ndio shemeji yule nini!”“Mmmh kivipi?”“Yani yule ndio mtu wako? Yani mpenzi wako?”Erick akacheka kwanza na kumwambia,“Hey, sababu nasimamia duka hapa ndio unaniona mkubwa, jamani mimi bado mdogo sina hayo mambo kabisa. Yule ni mdogo wangu, ni pacha wangu, mimi na yeye tumezaliwa mapacha”“Aaaah naomba unisamehe”Kisha Erick akamuita Erica karibu na kuanza kumtambulisha kwa Rama,“Si unaona hata majina yetu yanavyoendana? Sababu sisi ni mapacha”“Nisamehe, ila kwenu ni wazuri sana, maana huyu pacha wako ni mzuri sana”Erick alishika ule wasifu wa yule kaka na kumwambia kuwa Jumatatu aende kuanza kazi, ila yule kaka akamwambia,“Hata kesho naweza kuanza tu hakuna tatizo”“Sawa, basi kesho njoo uanze kazi, kila kitu nitakuonyesha leo. Halafu kesho nitapitia kidogo kukuangalia”Basi akaanza kumuelekeza vitu pale dukani na kuweka vizuri kila kitu, na walipomaliza Erick alitaka kufunga tu duka maana alikubaliana na Rama kuanza kesho ila Rama akamwambvia,“Hapana, ngoja tu leo niimalizie hapa ili hata wateja wajue kuwa duka limerudi sasa na litakuwa wazi siku zote”“Oooh sawa, sasa watakaokusaidia kuuza, maana Steve alikuwa na wadada wawili humu dukani, yeye ndio anajua alikowapata maana sisi tulikuwa tunamtambua yeye. Na kitu kingine hao watu wewe ndio unajua cha kufanya nao, kwahiyo kama utataka wale wa Steve sawa, au kama utatafuta wengine napo sawa, ila tu biashara isonge mbele. Ukiwatafuta nitakuja kuwakagua pia”Rama aliitikia tu maana hakuwa na namna zaidi ya kumuheshimu mtu huyu ingawa alikuwa mdogo kwake ila alikuwa na pesa za kumfanya yeye amuheshimu sana tu.Basi Erick alipomaliza aliondoka na Erica kwenda nae kiwandani.Walifika kiwandani nankutembea nae sehemu mbalimbali kisha Erick alienda ofisini sasa kufanya kazi za pale ambazo zipo ila muda huo Erica alikuwa akizunguka zunguka tu nje ya kiwanda kile, na mara akakutana na yule baba aliyekutana nae siku ile ya uzinduzi ambaye alimpa pesa na kadi ya mawasiliano,“Erica hujambo!”Erica akashtuka kidogo na kumuitikia,“Sijambo shikamoo”“Leo hapa kiwandani umekuja tena na mama yako?”“Hapana, nimekuja na kaka”“Oooh unanikumbuka vizuri, siku ile nilikupa pesa na kadi yangu ya mawasiliano”Erica aliitikia kwa kichwa tu kuwa anamkumbuka, kisha yule baba akasema tena,“Mbona hukunitafuta au zile pesa hazikukutosha?”“Kheee, mimi pesa za nini zile? Nilimpa mama hela zote na ile kadi”“Wa wapi wewe mtoto eeeh! Mbona wa ajabu hivyo, kwani huna matumizi ya pesa? Una simu?”“Hapana sina simu”“Basi mimi nitakununulia simu nzuri sana, unajua wewe ni binti mzuri sana”Erica akatabasamu, basi yule baba akasema,“Khaaa kumbe wewe katoto umerithi hadi dimpozi za mama yako, hakika wewe ni mrembo sana. Yani ndio nyie ambao mmezaliwa mkazalika, wewe mtoto ni mzuri sana, unavutia sipati picha ukiwa mkubwa huko utakuwaje? Ila kiukweli nimevutiwa sana na wewe”Erica alikaa kimya sasa maana hata hakujua ni kitu gani ajibu kwa huyu mtu aliyekuwa akimsifia kiasi huki, basi yule baba akatoa pesa zingine na kumapa Erica ila Erica alikataa zile pesa,“Chukua tu, mama mwambie kuwa anko Rahim ndio kanipa hizi hela, unafikiri atagomba! Yani atafurahi tu”“Hapana, mimi sina matumizi ya hela”“Wewe mtoto mbona wa ajabu sana, huna matumizi ya hela kivipi? Kwanza dada yako Angel yuko wapi?”“Yupo shule, anasoma boarding”“Kheee ndio wamemkumbizia huko mwanangu!”“Mwanao!!”Mara alifika pale Erick na kumuita,“Erica”Basi akageuka na kumuaga yule baba na kumfata Erick,“Nani yule, na ulikuwa unaongea nae nini?”“Si yule wa siku ile, alikuwa ananipa tena hela ila nimekataa”“Haya, twende tukakae wote ofisini yani wewe mambo yako hata sijui huwa unafikiria nini”Moja kwa moja Erica aliongozana na Erick hadi ofisini na kumuacha yule baba akiwa amesimama tu pale nje ya ile ofisi na alisimama pale kwa muda kidogo kisha akaondoka zake.Erica na Erick walimaliza na kutoka ofisini kurudi nyumbani kwao, walipokuwa kwenye gari Erica alilalamika kuhusu Sarah,“Jamani mimi na leo nitalala sebleni”“Hapana utalala chumbani kwangu, usiwaze kulala sebleni wakati chumbani kwangu papo”“Sawa, hakuna tatizo. Kheee kaka hebu angalia yule ni nani?”Ilibidi Erick asimamishe gari pembeni, na walimuona mjomba wao Erick akiwa amezingirwa na vijana kama kumi hivi huku wengine wakisogea, basi ilibidi washuke kwenye gari na kufata karibu ili wajue tatizo ni kitu gani,“Jamani kuna nini?”“Nyie watoto mtatusaidia nini hata mnauliza kuna nini?”Ila Derrick alipoona hawa watoto wa dada yake aliwasogelea karibu na kuanza kuwaomba msaada,“Nisaidieni wangu, nahadhirika leo”“Kwani tatizo ni nini?”“Wananidai laki moja”Yani Erick kwakweli hakuona kama ni jambo jema kwa mjomba wao kudhalilika sababu ya laki moja, basi kwa bahati alikuwa nayo kwenye gari ikabidi atoe na waondoke pale na mjomba wao, huku wale watu wakidai siku hiyo wangemfunza adabu, Erick aliondoa gari lile na kumuuliza,“Kwani mjomba tatizo ni nini? Kwanini udhalilike kiasi hiko, mbona nasikia wewe umesoma sana tu”“Ni kweli mwanangu, yani hata mimi sielewi, sijui nina laana sijui ni kitu gani. Ila nashukuru sana mmenisaidia maana leo hata sijui ningefanyeje jamani”Basi kuna mahali akafika na kuhitaji wamshushe na kuwaomba hata nauli, basi Erick akatoa elfu kumi na kumpatia mjomba wao nauli na kuagana nae.Ila wakati Erick anaendelea kuendesha ile gari akagundua kuwa mafuta yalikuwa yameisha na kumwambia dada yake,“Aaaah siku makini, unajua mafuta haya hayawezi kutufikisha nyumbani, ngoja tupitie pale kituo cha mafuta tuweze kuongeza mafuta”“Bora umekumbuka maana linetuzimikia katikati ya barabara ndio balaa”Basi walipita kwenye kituo cha mafuta na kuweka gari yao ili ijazwe mafuta, kisha mama wa makamo ndio alifika dirishani na kuwauliza,“Ya pesa ngapi?”“Ya elfu arobaini”Basi yule mama aliwatilia mafuta na baada ya hapo kuwadai hela, ila cha kushangaza Erick hakuwa na pesa yoyote ile yani alijipekua ila hakuwa na pesa kabisa, Erica alimuuliza,“Kwani imekuwaje?”“Unajua sielewi kabisa hata sielewi imekuwaje ila pesa hakuna”Yule mama alisikia akaona hawa watamkimbia basi akawahi kuingiza mkono wake kwenye gari na kuchukua funguo, kisha akawaambia,“Nipeni pesa yangu ndio muondoke hapa”Basi Erick akaamua kumsihi yule mama,“Sikia mama, naomba turuhusu halafu mimi nitakuletea hiyo hela yako”“Unachekesha sana, hivi nyie vijana wa siku hizi mkoje eeh! Mnacheza na kazi za watu sio, umekuja na gari zuri sijui umeaizma wapi, umekuja na kimwanamke chako, kwahiyo ukataka kukionyesha kuwa una hela, weka mafuta ya elfu arobaini halafu hela yenyewe huna, sichezi hapa, nina watoto wakubwa kushinda nyie, nipeni hela yangu ndio muondoke kabla sijawaitia watu hapa”Erick alimuangalia Erica, ikabidi washuke tu kwenye gari ili wajadiliane pembeni, basi Erica akasema,“Basi tumpigie simu mama au baba”“Tutawapigia na nini? Mimi huwa sina simu toka mama alivyotupokonya, nikiwa ofisini basi nawasiliana nao kwa simu ya ofisi, ila sasa tupo njiani tutafanyaje jamani!”“Kwanza imekuwaje huna hela? Yani imekuwaje tuseme tuwekewe mafuta bila hela?”“Sijui kama unaweza kunielewa, ni hivi wakati natoka nyumbani nilikuwa na laki moja kwenye gari maana baba aliniambia kuwa niwe natembea na pesa kiasi ili likitokea tatizo niweze kupata ufumbuzi, sasa na kule kiwandani kuna laki tatu nimetoka nayo leo maana hatukuifanyia mahesabu na ilikuwepo pale maana wanunuzi wetu wengi wanalipia kwa kutumia hundi. Nilipanga na meneja wa pale kuwa kesho nitaenda tuifanyie mahesabu kwahiyo nikaondoka nayo na niliiweka kwenye wallet, tulivyofika pale ambapo mjomba alizingirwa na lile tatizo la laki moja, nikaona isiwe kesi ndio nikatoa ile laki moja ya kwenye gari na kuwapa wale halafu tukaondoka na mjomba, sasa wakati mjomba anashuka alivyokuwa anaomba nauli ndio nikamtolea elfu kumi kwenye wallet na kumpa, ila nashangaa hapa sina kitu kwenye wallet, ni tupu kabisa, hakuna hata mia”“Duh!! Sasa ni kitu gani hiki?”“Yani sielewi, ukisikia kuumbuka ndio leo jamani, sijui tutapata wapi msaada”Yule mama alikuwa akiwafata mara kwa mara na kuwaambia maneno ya karaha, yani wakawaza cha kufanya pale hadi basi, kisha Erica akasema,“Au tufanyeje, tukodi bodaboda halafu mmoja wetu aende nyumbani kuchukua hela”“Umewaza vyema ila itatugharimu sana”“Najua ila ni bora kuliko aibu na dhahma hii”“Lakini nani ataenda nyumbani na nani atabaki hapa?”“Mimi hapa naweza kubaki tu”“Hapana, siwezi kuruhusu ubaki tu hapa au uende mwenyewe nyumbani na bodaboda”“Kwanini sasa?”Mara Erick alimuona kama mtu anayemfahamu, basi alimfata na kumsalimia, alikuwa ni Juma ambaye alikuwa akipita hapo kwenye kituo cha mafuta,“Kheee Erick, nimefurahi sana kukuona.”“Samahani baba, nilikuwa na shida. Unaweza kutuazima elfu arobaini”“Ya nini kwani?”Erick alimsimulia kifupi tu kuwa wanadaiwa hela ya mafuta hapo, walikwenda kujaza mafuta bila kuangalia pesa kama ipo, kwakweli Juma aliamua kumpa Erick hiyo hela maana huwa anampenda sana huyu mtoto, basi Erick alimshukuru pale na kwenda kumlipa yule mama ambaye alitoa funguo kwa masimango pia,“Ndio muache tabia hii jamani, hiki kituo cha mafuta sio cha baba yenu”Basi walimshukuru tena yule Juma na kuagana nae ambapo sasa walielekea nyumbani.Mama Angel alishangaa sana kwa jinsi watoto wake walivyochelewa kurudi ila walimsimulia kila tukio mama yao,“Kheee jamani, mlianzaje kumpa hela mjomba yenu?”“Sasa tungefanyaje mama? Alikuwa na matatizo”“Ni kweli yule ni mjomba wenu ila ana matatizo sana, mjomba wenu ni tapeli kwahiyo hizo hela ni yeye kazichukua kimazingaombwe”“Kwahiyo si kweli kwamba wale walikuwa wakimdai laki moj?”“Inawezekana ikawa kweli ila tapeli siku zote hana shukrani, sasa nyie mmemsaidia kwa upendo halafu yeye kawatapeli jamani, poleni sana wanangu”Ila mama Angel hakupenda kabisa kile kitendo ambacho kimefanywa na Derrick.Yani Erica na Erick hakuna hata mmoja aliyeulizia habari za Sarah kuwa yuko wapi wala nini, zaidi zaidi walienda kula na moja kwa moja kwenda kulala ambapo Erica alienda kwanza chumbani kwake, na vile hakumkuta Sarah ndio akafurahi na kulala humo kwa furaha.Usiku wa leo, kama kawaida Junior alikuwa amelala chumbani kwaVaileth huku wakiongea mambo mbalimbali,“Hivi kweli Junior utanioa?”“Ndio, nitakuoa Vai. Niamini, nimedhamiria kuwa na wewe”“HIvi kweli umeacha kabisa kufikiria wanawake zako wengine?”“Wa kazi gani sasa wakati wewe upo”Mara kuna ujumbe uliingia kwenye simu ya Junior, ila Vaileth aliomba ausome huo ujumbe, na Junior alimpa bila tatizo,“Hellow Junior, mbona umenipotezea hivi? Natuma ujumbe hunijibu, nakupigia simu hupokei, kwanini unanifanyia hivi Junior?”Basi Vaileth alimuangalia Junior na kutabasamu kwani alitambua kuwa kwasasa Junior anampenda kiasi cha kusahau wanawake zake wengine wote.Kulipokucha, mama Angel alikuwa kaamka na kuwataka wote mule ndani wajiandae kwaajili ya kwenda ibadani, na kweli wote walijiandaa kwa siku hii hadi Vaileth maana alitaka kuondoka na watu wote.Basi mama Angel alipokuwa akitoka ndani, alishangaa kumuona yule Linah akiingia getini kwake, inamaana siku hii alirudi tena, halafu alikuwa kaongozana na mwanamama mwingine mwenye mwili mkubwa zaidi hadi mama Angel alishikwa na uoga kiasi, ila walipomsogelea tu kabla hawajaongea chochote, wakina Junior nao walitoka ndani na kusogea pale ila cha kushangaza yule Linah alipomuona Junior alishangaa sana na kusema,“Junior!! Kheee unaishi hapa!” Basi mama Angel alipokuwa akitoka ndani, alishangaa kumuona yule Linah akiingia getini kwake, inamaana siku hii alirudi tena, halafu alikuwa kaongozana na mwanamama mwingine mwenye mwili mkubwa zaidi hadi mama Angel alishikwa na uoga kiasi, ila walipomsogelea tu kabla hawajaongea chochote, wakina Junior nao walitoka ndani na kusogea pale ila cha kushangaza yule Linah alipomuona Junior alishangaa sana na kusema,“Junior!! Kheee unaishi hapa!”Junior alikaa kimya tu, ila huyu mama alisogea na kumshika Junior mkono halafu akatoka nae nje ya geti kabisa huku yule mmama mwingine akimfata kwa nyuma, kwakweli hii hali ilikuwa inamshangaza mama Angel hadi akakosa cha kusema kwa muda huo, alibaki anashangaa tu basi Erica akasema,“Mama unashangaa hivyo unajua yule mwanamke ni nani?”“Mmmh! Inamaana wewe unamjua? Ni nani?”“Mmmh sitaki kusema hapa nitaonekana mbea”Muda huo Vaileth alienda ndani maana alihisi kutokuelewa kabisa, kwahiyo pale alibaki Erica na mama yake maana Erick alisogea kule getini alikopelekwa Junior, basi mama Angel alimuuliza vizuri,“Ni nani kwani?”“Yule mama ni mwanamke wa Junior”Mama Angel alishangaa sana hadi alihisi akili yake kugoma kufanya kazi,“Yani Junior akawe na mahusiano na mwanamke mtu mzima vile kushinda hata mama yake!!”“Ndio hivyo”“Hebu mshike mtoto nenda nae ndani”Kisha mama Angel alienda moja kwa moja nje ili ajue ni kitu gani wale wanawake wameenda kuongea na Junior, alipofika nje aliwaona wale wanawake wakiingia kwenye bajaji na Junior wakiondoka nae, kwakweli alishangaa zaidi na kumuuliza Erick ambaye nae alisimama akiwashangaa,“Umeelewa kitu gani mwanangu?”“Sielewi kitu, nimesikia tu yule mama analalamika kwa Junior kuwa kwanini anapiga simu halafu Junior hapokei, sijui anatuma jumbe ila hazijibiwi na Junior ndio wakambeba na kuondoka nae”“Kheee makubwa haya”Mama Angel alirudi ndani hata Erick nae alirudi ndani ila kiukweli kwa muda huo hakuwa tena na hamu hata ya kwenda ibadani kwani alihisi akili yake kuvurugika vilivyo, kuna muda alijipa moyo kuwa Junior angerejea tu ila badae akaona hapana anatakiwa kujitoa muhanga na kwenda kumfatilia Junior, hivyo alimuomba mwanae Erick waende pamoja kwahiyo hapakuwa tena na safari ya ibadani,“Ila mama tutaenda kuwafata wapi?”“Yule mwanamke ni mama mkubwa wa Sarah, kwahiyo twende kwakina Sarah ndio tutajua pa kuwapata”Basi Erick alikubali kwahiyo mama Angel alienda kubadili nguo kisha akawaaga wakina Erica na kuondoka na Erick.Vaileth alimfata Erica na kumuuliza vizuri maana alihisi lazima kuna jambo Erica anatambua kuhusu wale wanawake,“Erica naomba uniambie ukweli, kumbuka mimi ni mwanamke mwenzio”“Ila humu ndani si huwa mnaniita mimi kambea?”“Hapana, mimi sijawahi kukusema vibaya kwa hiyo tabia yako, nakuomba Erica uniambie ukweli”“Ni hivi, yule mmama aliwahi kuwa na mahusiano na Junior”Yani hata Vaileth mwenyewe alishangaa sana na kuuliza,“Kheee mmama wote yule?”“Nakumbuka nishawahi kukwambia kuwa Junior aliwahi kuwa na mahusiano na wamama wakubwa kushinda hata mama yake, basi ndio kama vile”“Jamani Junior, kwanini lakini?”“Kwanza ungetakiw akushangaa kwa Junior kukufata wewe, maana ni kijana mdogo ila kakufata wewe na anajifanya anakupenda sana kuliko chochote kile. Jiulize kwanza wewe Junior umempita umri gani? Na alipata wapi ujasiri wa kukufata wewe?”“Mmmh Erica unaongea kama na wewe ni mtu mzima? Inaonekana unatambua mengi sana”“Ndio, sababu mimi ni mbea na umbea wangu unafanya nitambue mambo mengi sana, na vingine hata huwezi kudhani na unaweza kujiuliza kuwa huyo mama nimemjuaje? Ila mimi namjua huyo mama na nilionyeshwa na huyo huyo Junior”“Kheeee!!”“Kwa kifupi, Junior anapenda kuwa na mahusiano na wanawake waliomzidi umri, sijui ni kwanini ila ndio tabia yake, hata baadhi ya watu waliniambia hivyo kuwa Junior anatembea na wanawake wakubwa sana. Naona kukupata wewe imekuwa furaha kwake, yani wewe unajiona mkubwa ila Junior anaona kamavile upo sawa nae. Ila jitafakari kama Junior anakufaa”Yale maneno yalimuingia Vaielth kwenye akili yake, na kujikuta akiinuka pale sebleni na moja kwa moja kwenda chumbani kwake.Mama Angel na Erick walifika nyumbani kwakina Sarah na hawakumkuta mtu yoyote, nyumba tu ilikuwa imefungwa, yani hapo ndio mama Angel hakuelewa kabisa, basi hakuwa na namna zaidi ya kumwambia mwanae warudi nyumbani tu kwani alitaka kwenda kufikiria zaidi kitu cha kufanya.Wakiwa njiani, alimuona Sia ameongozana na mtoto wake Elly basi mama Angel alimwambia Erick asimamishe gari kisha akashuka na kumuita Sia ambapo Sia alifika na kumsalimia, Elly nae akamsalimia mama Angel,“Shikamoo”Sia akadakia na kumwambia Elly,“Shikamoo nani? Sema shikamoo mama”Basi Elly akarudia tena,“Shikamoo mama”Mama Angel aliitikia tu kwani hakutaka kufanya mabishano yoyote na Sia kwa muda huo, kisha akamvuta pembeni na kumwambia yale yaliyojiri kwani alimtambua fika Sia kuwa ni mtu wa matukio mbalimbali,“Samahani, kwanza nashukuru kukuona. Nyumbani kwangu kumetokea tatizo”“Tatizo gani?”Mama Angel akamsimulia jinsi Linah na mwenzie walivyokuja na jinsi alivyoambiwa na Erica na jinsi walivyoondoka na Junior hapo kwake, basi Sia akasikitika na kusema,“Naona kwasasa unauona umuhimu wangu Erica, mimi ni kama maji usiponinywa basi utanioga tu”Erica hakutia neno hapo maana alikuwa akihitaji msaada kwaajili ya Junior, kisha Sia akaongea tena,“Ipo hivi, kwa habari ambazo nimezisikia, Linah ana stress bora hata zangu afadhari, kiukweli huyu Erick huyu katutianuchizi haswaa, yani nasikia Linah aliona kuwa wanaume wakubwa hakuna mwenye mapenzi ya kweli ndio hapo alipoanza kutembea na vivulana vidogo. Namshukuru Mungu sijafikia huko maana ni kujidhalilisha, kwahiyo inawezekana kabisa kuwa alikuwa na mahusiano na Junior ukizingatia Junior ni kavulana kahuna sana, kamerithi kwa baba yake kale, ila uhuni utamtesa kama huyo babake mdogo Erick. Ila mimi nitakusaidia na Junior atarudi nyumbani”“Nashukuru sana ndugu yangu”“Kheee makubwa, nimekuwa ndugu yako leo, yani mimi adui yako namba moja leo nimekuwa ndugu!! Kweli maisha yanabadilika”“Tuachane na hayo yaliyopita bhana, unajua nimeshangaa sana kwa Junior kuwa na mahusiano na mmama mkubwa vile!”Sia akacheka na kusema,“Ama kweli inachekesha na kuhuzunisha kwa wakati mmoja, mwanamke anatembea na baba halafu miaka ijayo anakuja kutembea na mtoto jamani maisha haya. Ila hata Erick alikuwa hivyo, alikuwa anatembea na wadada wakubwa kwa wadogo, usimshangae sana Junior”“Mmmmh! Hayo mambo yalishapita ndugu yangu”Ila kwa stahili hii naamini kuna siku utakubali Erick anioe mimi na wewe yani wote tuishi pamoja, yani mimi kinachonitesa ni mapenzi, kilichoondoa akili yangu ni mapenzi. Nimejaribu sana kumtoa Erick katika akili zangu, fikra zangu na mawazo yangu lakini nashindwa kabisa, muda wote nakumbuka mapenzi yake, nakumbuka alivyokuwa akinijali, nakumbuka alivyokuwa akinibembeleza, licha ya maudhi machache aliyokuwa nayo Erick ila ni mwanaume ambaye anajua sana kupenda, kila muda namuwaza Erick”Mama Angel alipumua tu ila hakusema neno lolote lile, zaidi zaidi aliagana nae,“Natumaini utanifanyia hiyo kazi, asante sana”“Usijali ila kitu kimoja tu ningetaka kutoka kwako, uwe unaniruhusu hata nije nyumbani kwako kumsalimia Erick, tafadhali msinifanyie kama mlivyomfanyia Rahim kutokumuona kabisa mwanae na hadi sasa hajui anafananaje, nipeni ruhusa ya kuja kumsalimia Erick”“Hapo ndio mimi na wewe hatuelewani, hebu kuwa muwazi, kwahiyo Erick ni mwanao na Elly ni mwanangu? Na imekuwaje hiyo?”“Sijui jinsi ya kukueleza ila Erick ni mwanangu na Elly ni mwanangu pia”“Yani kama binadamu ana akili tatu basi wewe imebaki moja tu ya kukuongoza kwenye mambo madogo madogo, hebu sikia kwanza, nilibeba mimba, nilienda hospitali nikiwa na mume wangu kupima, nikagundulika nimebeba mapacha tena wa kike na wa kiume. Nilijifungua ingawa kwa operesheni lakini salama kabisa na nilikabidhiwa watoto wangu na ndio hao nawalea hadi sasa. Nakumbuka wewe ulibeba mimba ya mtoto mmoja, haya iweje una mtoto wako na bado unang’ang’ania mtoto wangu?”“Ipo siku Erica utaitambua akili yangu vizuri, ila ukipaniki utajitesa na kujisumbua mwenyewe. Hata mimi kuna vitu vingine sielewi, najua kwamba Erick ni mwanangu ila sijui ni kwanini ananichukia maana nahisi huyo mtoto akiambiwa mtu wa kwanza kumuua duniani ataanza na mimi. Hivi kwanza hamumuoni kwamba hafanani na nyie ndani kwenu, mtoto ana roho mbaya huyo kama mkaanga sumu, mtoto ana akili mbovu huyo kupita maelezo, mpe malezi yote, msomeshe dini zote ila hapo utagonga mwamba, najua siku moja utakuja kunililia kuhusu huyo mtoto, utasema kuwa nilikwambia na maneno yangu yatatimia”“Ushindwe na ulegee”Kisha mama Angel aliondoka zake na kurudi kwenye gari ila Erick hakushuka kabisa hata kumsalimia huyu mama ndio kwanza alimuuliza mama yake,“Kwani mama ulikuwa unaongea nini na yule mmama?”“Aaaah kuna mambo nilikuwa namwambia”“Simpendi kabisa, yani simpendi”“Naelewa ni kwanini humpendi ila usimjali maneno yake maana huyu mwanamke ni watu waliochanganyikiwa na maisha. Hata usimjali kitu”Basi wakaendelea na safari na kurudi nyumbani.Mama Angel alienda moja kwa moja chumbani kwake kupumzika kwani aliona akili yake ikigonga mwamba, alifikiria kuhusu Junior bila ya jibu kisha alianza kufikiria kuhusu maneno ya Sia na kujisemea,“Yule mwanamke ni mgonjwa tena ni mgonjwa sana, huwezi kukazana kusema mtoto ni wako halafu unamuombea mabaya muda wote, hakuna mzazi anayemuombea mabaya mwanae. Nadhani kuna kitu anataka kukijenga kwetu, anataka tumchukie mtoto wetu halafu mwishowe tujutie kwa kitendo hiko. Sasa maneno yake yameingia kulia na kutokea kushoto, nitampenda Erick na yeye ndio atakayeangalia dada zake”Basi wakati akifikiria hayo, akapigiwa simu na huyo huyo Sia, ikabidi apokee na kuanza kuongea nayo,“Nimefanikiwa kufika nyumbani kwa Linah, ni kweli kabisa yupo na Junior na analalamika kuwa Junior kampotezea, eti huwa anampigia simu halafu hapokei anamtumia ujumbe halafu hamjibu. Kwakweli hata mimi imeniuma kwa mtoto mdogo kama Junior kuwekwa kinyumba na hili zee, sijapenda kabisa. Sasa nitajitahidi Junior nirudi nae leo, sema sasa tafuta pa kumpeleka maana hili limama litamfata tena”“Sawa hakuna tatizo”Basi akakata ile simu na kuanza kufikiria kwa muda huo kuwa Junior akirudi tu basi arudi shuleni tu kwa siku hiyo.Na kweli jioni ya siku hiyo Junior aliletwa na Sia, kiukweli Junior alikuwa mpole sana kiasi cha kushindwa kuongea lolote, mama Angel akamwambia,“Kajiandae nikupeleke shule, muda huu huu”Junior hakubisha zaidi ya kwenda kujiandaa, halafu Sia alitoka nje kwenda kuongea na mama Angel,“Nashukuru sana kwa kazi uliyofanya ya kunirejeshea mwanangu”“Usijali, ingawa nimepambana, na nimetumia uongo wa hali ya juu najua Linah akijua atachukia sana ila mimi kunipata hawezi”Ikabidi mama Angel ampe tu pesa kidogo Sia kama shukrani kwake, kisha Sia akaondoka halafu mama Angel alimfata Junior na kumtaka waondoke nae ampeleke shule, yani Junior hakuweza kubisha wala kupinga kutokana na mambo yaliyotokea siku hiyo.Basi wakati wanatoka mama Angel alimwambia mlinzi wake kutokuruhusu tena watu asiowafahamu ndani kwake,“Natumai umenielewa, kama wale walioingia asubuhi, tafadhari usiruhusu tena watu kama wale”“Sawa mama nimekuelewa”Basi mama Angel akaondoka na Junior kuelekea shuleni kwakina Junior.Wakiwa kwenye gari alimsema sana,“Kwakweli Junior unatia aibu, kijana mdogo kama wewe kwenda kuhangaika na wamama walioshindikana kiasi kile jamani!”“Nisamehe mamdogo”“Sio nisamehe, kwakweli umenikera sana. Na hayo maswala yako ya kurudi rudi nyumbani siyataki hata kidogo, nikikuta umerudi tu bila sababu tutagombana Junior, nadhani umenielewa”“Nimekuelewa mamdogo”“Loh unachefua kabisa, mmama wote yule. Ptuuu mtoto mchafu wewe aaarrghhh yani sijui hata cha kukufanya, ukasome tu mjinga wewe. Umenichefua sana”Basi alimfikisha Junior shuleni na kumuacha hapo kisha yeye akawa anarudi, ila njiani kuna mtu alimuona na kumfananisha na mtu ambaye aliwahi kusoma nae ila hakusimamisha gari kumsalimia kwani mtu huyo alionekana kuwa na haraka sana.Moja kwa moja mama Angel alirudi nyumbani kwake akiwa amechoka na mambo ya Junior kwa siku hiyo, muda kidogo alipigiwa simu na mume wake,“Nasikia umeanza kushirikiana na Sia”“Mmmh kushirikiana nae kivipi?”“Kwani umeongea nae nini leo na kitu gani kakusaidia?”“Mume wangu, ngoja niingie chumbani nikusimulie ilivyokuwa”Basi mama Angel alienda moja kwa moja chumbani kwake, na kuanza kuongea na mume wake sasa, ambapo alimueleza mlolongo mzima, kuanzia habari za Sarah hadi mambo ya Linah,“Hadi masikio yanauma kusikiliza hayo mambo, unajua sijaelewa kituhata kimoja ulichoniambia. Ni kwamba baba yangu alikuwa na mtoto mwingine? Yani Sarah ni mtoto wa baba yangu?”“Sijui mimi, ila ndio picha niliyoikuta nyumbani kwakina Sarah”“Dah!! Hiyo habari sidhani kama ina ukweli wowote, baba yangu alikuwa na matatizo ya uzazi, na kwenye kaburi lake mbona kuna watu ambao tuliwaweka kwaajili ya kufanya usafi na kuangalia na hawajawahi kutuambia kama wamewahi kuwaona hao watu. Hapo kuna kitu mke wangu, kwa hayo mambo naomba hata huyo mtoto Sarah uwe mbali nae kwa muda kwanza maana nashindwa kuelewa kabisa”“Na habari ya huyo Linah ambaye alikuwa mwanamke wako, ndio alikuja ili kunipiga na mwenzie sijui, ila ndio hivyo wamemkuta Junior ambaye alikuwa akitembea nae”“Hiyo ndio sijaielewa hata kidogo, nina hakika huyo Linah kwasasa ni mtu mzima wa kutosha tu, hivi akatembee na Junior kweli!! Mbona dunia ina mambo kiasi hiki”“Kwahiyo wewe hujashangaa swala la huyo mwanamke kutaka kunipiga ila umeshangaa swala la yeye kutembea na Junior?”“Yote nimeshangaa mke wangu, ila kwasasa nitaongeza ulinzi hapo nyumbani, watu wa kijinga jinga wasiwe wanafika kabisa hapo”“Haya sasa, lingine ni kuhusu huyo shemeji yako Derrick unayemtetea siku zote, ni hivi kawatapeli watoto wako laki nne”“Sikuelewi”Mama Angel akamuelezea vile ambavyo yeye alielezewa na watoto wake,“Ila mbona kama ndio hivyo kafikia hatua mbaya sana huyo Derrick, halafu kwa mtindo huo inamaana Derrick anatumia chumaulete eeeh!! Maana sio kwa kuvuta hela kwa aina hiyo”“Ndio hivyo, mimi nilikwambia wazi kuwa Derrick sio mtu mzuri, haya sasa hii hela utailipa wewe”“Khaaaa mama Angel lakini dah!! Utafikiri akaunti zangu huzijui? Nenda katoe hela kwangu uweke hapo ilipopotea”“Ila nimeona vyema kukwambia”“Ni vizuri kuniambia ila nakuamini mke wangu, tena nakuamini sana. Na ninahangaika kwaajili yenu yani wewe na watoto wetu kwahiyo vitu vyangu, pesa zangu na kila kitu changu kipo juu yenu”Mama Angel aliongea na mumewe na badae kuagana nae kwaajili ya kulala, ila alipomaliza kuongea na mumewe alikaa na kujitafakari,“Hivi wanaume kama huyu Erick wapo kweli duniani, yani mara nyingine anaongea na mimi naona kama naota vile. Ni kweli nimeolewa na mwanaume mwenye upendo kiasi hiki!! Hii ni bahati kwangu, inapaswa mimi kumshukuru Mungu. Jumapili ijayo nitaandaa sadaka ya shukrani kwaajili ya mume wangu, nitamshukuru Mungu kwa kunipatia huyu mume katika maisha yangu.”Kisha mama Angel akaamua kulala tu kwa muda huo, ila wakati amelala kuna wazo lilimjia yani alijikuta akitamani kuujua ukweli kuhusu Sarah kuwa mtoto wa mzee Jimmy, yani alijikuta tu akitamani kutambua hayo. Basi akaona ni vyema kesho yake aende kutembelea kaburi la mzee Jimmy ambaye alikuwa ni baba mkwe wake.Vaileth alienda kulala ila hakuwa na raha kabisa, alijikuta akikaa tu chumbani na kulia kwa muda mrefu sana, alijiona kuwa na mkosi, alijiona kukosa bahati kabisa, aliwaza ni kitu gani afanye ila alikosa jibu kabisa kuwa ni nini afanye, wakati analia na kuumia, simu yake iliita na alipoangalia aliona ni Junior anapiga, kwakweli hakutaka kupokea ila moyo ulikuwa unamuuma sana na kuamua kupokea ile simu,“Naomba unisamehe mpenzi wangu Vaileth, najua ni jinsi gani umeumia na ni jinsi gani nimekukera”“Kwakweli Junior naomba tuachane tu, yani kila mtu apite na mambo yake, kwakweli siwezi kuendelea na wewe”“Kwa kosa gani nililolifanya? Yule mama simtaki kabisa ila huwa anatumia mabavu muda wote, tatizo mamdogo nae hana nguvu hivi kweli anamuacha mwanamke baunsa vile anitoe tu jamani! Yule mama ndio ule ujumbe uliousoma usiku uliopita akilalamika kuwa sipokei simu zake, na alichonifanya aliponichukua ni Mungu tu anajua, sitakwambia kwasasa ila ipo siku nitakwambia. Kuna yule mama huwa tunamchukia sana hapo nyumbani ila ndiye aliyenisaidia, kwakweli yule mama ana mbinu za ajabu sana hata nilishangaa kama nitaweza kupona kwenye mikono ya yule mama maana usiku wa leo sijui ningekuwaje mimi Junior. Sirudii tena upuuzi wa namna hii, naomba unisamehe Vaileth”“Nimekusamehe ila sikutaki tena Junior”“Nimeambiwa nisirudi hovyo hapo nyumbani ila kwaajili yako nitarudi tu, siwezi kuishi bila wewe Vaileth. Nisamehe tafadhari”Mara mlango wa Vaileth uligongwa, alishtuka sana na kuweka simu mbali, na kwenda kufungua tena mgongaji alikuwa ni mama Angel,“Kheee usiku huu unaongea na simu Vai, ndio umeanza kudanganywa tena na wanaume eeeh! Kuwa makini sana siku hizi magonjwa mengi na unaweza kudhani unapata wa maana kumbe unaangukia kwenye mikono ya wazee”Vaileth aliangalia chini tu kwa aibu, kisha mama Angel akamwambia,“Kesho itabidi uamke asubuhi sana sababu kuna mahali nataka kwenda kwahiyo nitaenda mapema ili niwahi kurudi maana kule ni mbali sana, kwahiyo utaamka asubuhi kwaajili ya kukaa vizuri na mtoto”“Sawa mama”Kisha mama Angel aliondoka na kurudi kulala.Ila ni tofauti na jinsi ambavyo walipanga kwani kesho yake mama Angel alijikuta akiamka saa mbili asubuhi na sio kama alivyopanga, basi aliamka na uchovu kiasi na kwenda moja kwa moja jikoni kumfokea Vaileth,“Jamani, wewe hata kuniamsha?”“Niesamehe mama, hata mimi nilipitiliza yani nimeamka wakati wakina Erick wanaondoka”“Khaaa huu usingizi gani jamani loh! Sasa nitafanyeje? Itabidi niende kesho halafu nitamwambia Erick ndio aniamshe”Basi wakakubaliana pale kuwa aende kesho yake.Leo Erick alipomaliza masomo yake kama kawadia alienda kushtuliwa na madam Oliva ili waende kiwandani yani madam Oliva nae ilionyesha kuwa maeneo ya kule kiwandani ameyapenda maana kila siku alikuwa akitaka kumsindikiza Erick.Basi alienda hadi kiwandani na moja kwa moja Erick alivyoingia kiwandani pale nje alibaki madam Oliva huku akiangaza angaza mazingira ya pale, alishikwa bega na kushtuka kiasi, alipogeuka alikuta ni baba wa siku ile yule Rahim, basi alianza kuongea nae,“Oooh madam, ulishangaa sijakupigia simu eeeh!”“Ndio, hujanitafuta”“Aaaah yani sijui vipi, nilikuwa natamani sana kukutafutaila nikajua utakuwa upo na jamaa yako na hawezi kufurahi akisikia kuna mwanaume mwingine amekupigia simu”Madam Oliva alitabasamu tu, kisha Rahim aliendelea kuongea,“Una mtoto madam?”“Ndio ninaye mmoja”“Wa kike au wa kiume”“Ni wa kiume”“Hupendi kuwa na mtoto wa kike?”“Napenda ila naona kama umri umepita”“Aaaah umri umepita wapi, mbona wewe bado kijana mdogo yani bado unadai wewe. Sikia sasa, una mpango gani na huyo jamaa yako?”“Tuna mpango wa kuoana”“Oooh vizuri sana, nafurahi kusikia hivyo. Sikia madam, nahitaji ukiwa na muda wako wa ziada nitafute mimi kuna mambo ya muhimu sana nataka kuongea na wewe”Kisha Rahim akatoa pesa na kadi yake ya mawasiliano na kumkabidhi madam Oliva huku akitabasamu, basi madam Oliva alipokea na kuagana na Rahim, baada ya kuondoka alijisemea,“Jamani wanaume wa namna hii walikuwa wapi kipindi cha ubinti wangu? Mwanaume hata hufahamiani nae vizuri anakuhonga kweli! Mwanaume mzuri, shombeshombe, mrefu, ana mwili mzuri halafu hakufahamu vizuri lakini ana kuhonga mweeeh walikuwa wapi enzi zangu hawa! Hivi akinitongoza kama huyu namkataaje kwa mfano? Yani hapo mambo ya Steve mbona yatasahaulika kabisa, kwanza hana kazi yule namlea na kumlisha mwenyewe. Nilitongozwa na huyu ajue namuacha kwenye mataa na ujinga wake”Madam Oliva alikuwa akijisemea huku akitabasamu, yani alionekana kuwa na furaha sana.Erick alipotoka aliondoka nae mpaka kwao na kumuacha karibia na njia ya kwao halafu yeye akaenda nyumbani kwake.Kisha Erick moja kwa moja akaenda kwao ila akakutana getini na Sia, kwakweli Erick hakumpenda kabisa huyu mama, basi Sia alipomuona Erick alitabasamu na kufurahi sana kisha akamsogelea ili amkumbatie ila Erick alimsukuma hadi chini, yani Sia alianguka ila alisonya na kusema,“Liangalie vile, toto lina roho mbaya kama mkaanga sumu”Ila Erick hakumjali wala nini zaidi zaidi aliingia ndani kwao, basi Sia aliinuka huku akijikung’uta na kulalamika sana halafu akaondoka zake.Usiku wa leo, mama Angel alimuomba Erick amuamshe asubuhi ili aweze kuondoka kwani alijua akipanga yeye mwenyewe tena itakuwa mambo kama ya jana yake.Basi wakakubaliana muda ambao atamuamsha na kweli palivyokucha tu Erick alienda kumuamsha mama yake ambapo aliamka na kuanza kujiandaa halafu alienda kumuamsha Vaileth ili aweze kubaki vizuri na mtoto.Alipomaliza kujiandaa, alimuaga Vaielth na kuondoka zake, kwakweli ilikuwa ni safari ndefu kiasi maana alitumia kama masaa sita hivi kufika kwenye kaburi la mzee Jimmy, alisogea pale kwenye kaburi, ni kweli palikuwa pamesafishwa vizuri na palikuwa pamewekwa maua na mishumaa hata yeye mwenyewe akasema,“Lazima kuna wa ziada wanaofanya haya licha la yule mlinzi”Mara akashikwa bega, na kusikia sauti ikimuita,“Erica”Alishtuka sana kwani hakutegemea kwa muda huo kumpata mtu aliyemfahamu yeye kwa jina lake la Erica. Alipomaliza kujiandaa, alimuaga Vaielth na kuondoka zake, kwakweli ilikuwa ni safari ndefu kiasi maana alitumia kama masaa sita hivi kufika kwenye kaburi la mzee Jimmy, alisogea pale kwenye kaburi, ni kweli palikuwa pamesafishwa vizuri na palikuwa pamewekwa maua na mishumaa hata yeye mwenyewe akasema,“Lazima kuna wa ziada wanaofanya haya licha la yule mlinzi”Mara akashikwa bega, na kusikia sauti ikimuita,“Erica”Alishtuka sana kwani hakutegemea kwa muda huo kumpata mtu aliyemfahamu yeye kwa jina lake la Erica.Basi mama Angel aligeuka na kukutana na bi.Aisha, ni mwanamke ambaye alionana nae kwa kipindi kirefu sana ila alimfahamu kutokana na maneno yake ya busara, alimsalimia kisha bi.Aisha akamuuliza,“Unanikumbuka lakini?”“Nakukumbuka ndio, wewe ni bi.Aisha”“Wow, vizuri sana, nilijua utakuwa umesnisahau maana mimi na wewe mara ya kwanza kufahamiana ilikuwa ni siku ya harusi yako, na baada ya hapo tukawa karibu kiasi hadi kipindi nilipoondoka kwa mzee Jimmy ndio ikawa mwisho kuonana”“Nakumbuka ndio”“Umekuja huku Erica, kuangalia kaburi la mkwe wako!! Kwakweli Hongera sana maana una moyo wa kipekee mno”“Asante, lakini hakuna sababu ya mimi kushindwa kuja kutembelea kaburi la baba mkwe, ni kwamba hatukupanga tu kufanya hivi ndiomana”“Pole sana, kwa ujinga wote aliokufanyia mzee Jimmy, ila bado umepata nguvu ya kusema hakuna chochote”“Ujinga gani?”“Inamaana hujui alichokifanya kwako? Ndio sababu hata mimi ya kutokuendelea tena kuishi naye, sitaki kusema mengi ila utayajua yote”“Ujinga gani, tafadhali mama niambie ni kitu gani”“Sijui kama ni hivi ambavyo nilimsikia akiongea na yule daktari, kwanza watoto wako wanaendeleaje? Nauliza kwa wale mapacha?”“Wanendelea vizuri tu, kwani ni kitu gani?”Hapo mama Angel alishgtuka zaidi na kutamani kujua kuwa ni kitu gani,“Sijui nikwambie nini Erica, ila kuna siku nilikuwa nyumbani kwa mzee Jimmy, alikuwa na rafiki yake mmoja ambaye alikuwa ni daktari, alikuwa akiongea nae kuwa ukiaribia kujifungua basi ampe kazi Erick yani aondoke kabisa ili swala zima la kujifungua alisimamie yeye, halafu kuna sindano sijui za aina gani aliongea na yule daktari kuwa awachome hao mapacha wako pindi watakapozaliwa tu, halafu nilisikia kuwa hizo sindano zitawasumbua sana watoto wako kiasi kwamba utahitaji msaada wake, na nia yake ni kukukomesha wewe. Kwakweli nilisogea pale na kumzaba mzee Jimmy kibao kwani kila nikikumbuka jinsi mtu unavyobeba mimba kwa shida, na kuzaa kwa shida halafu mtu ana mpango wa kuchoma sindano zisizofaa watoto wako ili tu kukutesa, sikupenda kabisa nilijikuta nikilia kwa uchungu na kumuuliza kwanini anataka kukufanyia roho mbaya kiasi kile, ila hakunijibu kitu halafu ulipokaribia kujifungua ni kweli alimuondoa Erick, nilipatwa na wazo baya sana na pale nilipoamua kuondoka kwa mzee Jimmy maana sikutaka kuendelea kushuhudia mambo kama yake. Huwa mara nyingi nakuja huku kaburini yani nawaza kuwa naweza kufa na siri hii bila ya wewe kujua ukweli. Ila kweli watoto wako wanaendelea vizuri”Mama Angel akapumua kidogo na kujibu,“Wanaendelea vizuri ndio”“Umewachunguza? Labda dawa aliyowapa inafanya kazi taratibu, naogopa sana mimi, naogopa kwakweli.”“Ila siwaoni kama wana tatizo lolote, sababu nawaona ni kawaida kabisa”“Pole sana Erica, hivi unakumbuka ajali uliyoipata pindi ukiwa unakaribia kujifungua na ndipo ukawaishwa hospitali?”Mama Angel akakumbuka kidogo, ni kweli ilikuwa ni ajali mbaya sana kwake yani ilibakia kidogo tu angeweza kupoteza hata maisha, akajibu,“Nakumbuka ndio, huwa siwezi kusahau lile tukio maana dereva wangu alikufa”“Basi ile ajali ilipangwa na mzee Jimmy”“Jamani kwanini lakini aliamua kunifanyia hivi!! Kwani kosa langu ni nini, hakujua kama akiniumiza mimi basi anamuumiza mtoto wake?”“Hilo mzee Jimmy hakujali, huyu mzee kafa na laana nyingi sana, nikikueleza mambo mengi aliyoyafanya juu yako unaweza ukahisi moyo wako kuvuja damu hata ukatamani kufukua kaburi lake upigepige mifupa yake, Mzee Jimmy hakuwa mtu mzuri kwako kabisa, alisimamia harusi yenu ila alikuwa na mambo yako, nikikwambia kitu alichokipanga hata unaweza kulia hapa”“Unajua mama unanitisha sana, kuna mwanamke mmoja alikuwa na mahusiano na Erick, yule mwanamke kaibuka kipindi hiki na kudai kuwa pacha mmoja sio mtoto wangu, kuwa ni mtoto wake, yani hadi alimwambia hivyo mwanangu na alimchanganya sana, mpaka mwanangu anakuwa na mawazo mno”“Hebu tulia, tuliza akili, kama unalea watoto wako na hakuna tatizo lolote uliloliona huenda mambo ya mzee Jimmy hayakufanikiwa. Ila huyo asikufanye ukose raha ya maisha inawezekana yupo kwenye kiapo cha kukutesa na mzee Jimmy, yani hiyo inawezekana kabisa ni mambo ya kukutesa kisaikolojia wewe na familia yako. Kama watoto wako ni wazima wa afya basi achana na dhana yake kuwa mtoto sio wako, sasa mtoto sio wako kivipi wakati ulijifungua mapacha?”“Ndio hapo huwa nashangaa sana mama”Bi.Aisha alijaribu kumwambia mama Angel maneno ya busara ili aweze kufanya vizuri, alimshauri pia,“Nakuomba huku kuja kutembelea kaburi la mzee Jimmy uwe unakuja na Erick au Tumaini, usije mwenyewe maana huyu mzee haaminiki hata kidogo, ni kweli amekufa ila kaacha watu gani nyuma yake? Kumbuka mwanadamu anaweza kukuangamiza sababu ya pesa, je kawaachia pesa ngapi ya kufanya ujinga? Ni kweli amekufa ila ahadi walizoahidiana bado zinaishi. Kwa muda huu nakuomba tu ugeuze na uondoke maana hata mimi binafsi siwezi kuridhika kukuacha wewe huku kwenye kaburi la mzee Jimmy”Mama Angel alisikia mausia ya huyu mama, hivyobasi aliamua kuagana nae na kuondoka zake.Vaileth akiwa nyumbani na mtoto, alishangaa tu kuona Junior amefika mahali pale,“Kheee Junior si untakiwa kuwa shule wewe!!”“Ni kweli natakiwa kuwa shule ila sijihisi kabisa kukaa shuleni ilihali hujanisamehe Vaileth”“Hapana, mimi siwezi tena kuwa na wewe Junior”Basi Vaileth aliinuka na kwenda kumlaza mtoto kwenye kitanda chake pale sebleni maana alikuwa amelala, kwahiyo alimlaza pale ili iwe rahisi kwake kumsikia pindi atakapoamka.Alipomlaza tu, nyuma yake alienda Junior na kuanza kumpapasa huku akijaribu kumpa maneno matamu, yani Vaileth alishindwa hata kusema chochote kile na kujikuta na yeye akimpa sapoti Junior na moja kwa moja walienda chumbani na kulala huko.Hapa sebleni alifika mama Junior kwa muda huo, alishangaa kumkuta mtoto kalazwa pale, basi alijaribu kuita ila hakuitikiwa,“Wenyewe! Mama Angel, Vaileth. Kheee humu ndani leo hakuna mtu zaidi ya huyu mtoto mdogo Ester jamani eeeh!!”Basi mtoto nae alianza kulia, ikabidi amchukue na kuanza kumbembeleza, akataka kwa muda huo ampigie simu mama Angel ili kumpa hiyo taarifa, ila kabla hajapiga ndipo Vaileth alitoka ndani na kwenda pale sebleni,“Kheee wewe Vaileth nakuita muda wote huitiki ulikuwa wapi?”“Nilikuwa naoga mama, nisamehe”“Mjinga wewe, halafu umemlaza mtoto hapa sebleni akiibiwa je?”“Nilijua haiwezi kuwa hivyo sababu kuna mlinzi getini”“Mjinga sana wewe, usirudie hiki kitu tena, yuko wapi mama Angel?”“Kuna mahali kaenda asubuhi sana ila kasema ni mbali na atachelewa kurudi”“Jamani aaargh. Ngoja niende chooni kwanza”Basi mama Junior akainuka na kwenda chooni, muda huo Junior nae alitoka taratibu na kumbusu Vaileth halafu akaondoka ili mama yake asimuone na asitambue kuwa alifika mahali hapo.Junior alivyofika getini alimshukuru sana yule mlinzi,“Asante sana kwa ujumbe ulionipa leo kuwa mamdogo hayupo, nashukuru sana wewe ni rafiki wa kweli. Naomba wote wakina Erick wasijue kama leo nilirudi hapa”Kisha akampa mlinzi elfu kumi halafu akamuaga na kuondoka zake akielekea shuleni.Njiani alikutana na Sarah pamoja na mama yake, basi Sarah akambulisha Junior kwa mama yake ila mama yake akasema,“Namfahamu huyu mbona”Junior aliona aibu tu na kuangalia chini, kisha mama Sarah akamwambia Junior,“Wewe bado ni kijana mdogo sana, zingatia masomo yako achana na watu wazima utalia. Nimepata habari zako achana na watu wazima nakwambia. Yule ni dada yangu namjua vizuri, wewe ni mtoto mdogo sana Junior”Basi Junior akawaaga pale na kuondoka zake maana aliona huyu mama atazungumza mengi kwani alishawahi kumuona mara kadhaa akiwa na Linah.Njiani mama Angel alijiuliza sana, kuwa alienda kwenye kaburi la mzee Jimmy kufanya nini sasa ikiwa hakufanya chochote zaidi ya kukutana na bi.Aisha tu!! Pia alijiuliza kuhusu swala la watoto wake kuchomwa sindano, alijiuliza sana ni sindano ya nini na je alikuwa na lengo gani kufanya hivyo? Ila kilichompa tumaini ni kuona kuwa watoto wake hawana tatizo lolote lile maana aliona wapo kawaida na wanaishi kawaida kabisa, basi alikuwa akiendesha gari huku akiwaza mambo mengi sana.Alipokuwa anakaribia nyumbani kwake, ilikuwa ni jioni kabisa, hata giza kwa mbali lilianza kuonekana, ila alimuona Sia na kusimamisha gari lake kisha akashuka na kumuita,“Sia”Sia alisogea karibu na kumsikiliza, kisha akamsalimia na kumuuliza,“Umetoka wapi muda huu Erica? Mumeo hayupo na bado unanyonyesha, au Junior kakorofisha tena?”“Hapana, ila nilienda kwenye kaburi la mzee Jimmy”Sia akashtuka kidogo na kumuuliza,“Umepata nini huko?”“Nimegundua vitu vingi sana, hivi Sia mzee Jimmy alikulipa kiasi gani cha kuisumbua akili yangu?”“Mmmh jamani, sijalipwa na mzee Jimmy mimi”“Haya ni kipi kinakufanya uwe unasema Erick ni mtoto wako?”“Kheee muda gani nimesema hivyo kuhusu Erick jamani!! Ni mtoto wangu tokea lini?”“Khaaa kumbe wewe ni mwezi mchanga, kwaheri”Mama Angel alirudi kwenye gari yake na kuondoka zake, yani alikuwa akishangaa gafla jinsi Sia alivyobadilisha maana ya kitu ambacho kila siku anakiongelea, kuwa Erick ni mwanae halafu siku hii kakataa kabisa, kwakweli mama Angel alishangaa sana na kusikitika.Kwanza alijiuliza sana, maana angekuwa na mtu angesema Sia anakataa sababu ya yule mtu ila alikuwa mwenyewe na Sia amekataa katakata kwamba hajwahi kusema hivyo, yani aliondoa gari huku akisikitika sana.Mama Angel aliingia nyumbani kwake kwenye mida ya saa moja maana ilikuwa ni safari ndefu na alichoka sana, basi moja kwa moja alienda kuoga tu na kurudi kula, kisha Vaileth alimweleza kuhusu ujio wa mama Junior,“Alikuja hapa mama Junior, ila amekaa sana alipoona hurudi akaamua kuondoka”“Jamani dada yangu masikini, kanikuta na mambo mengi leo hatari, nitawasiliana nae hakuna tatizo. Ila umeshinda salama na mtoto!! Naona kalala muda huu”“Ndio, nimeshinda nae salama, na alivyorudi Erica basi imekuwa rahisi zaidi maana Erica anajua sana kubembeleza mtoto yani kama amewahi kuwa na mtoto vile”“Mwanamke yule, mwanangu ni mwanamke kamili maana naona vitu vyote vifanywavyo na mwanamke basi Erica anavimudu”Basi mama Angel alipomaliza kula, aliinuka na kupitia chumbani kwa Erick ili kumuangalia kama yupo macho basi azungumze nae kidogo kuhusu kiwandani, ila alipoingia chumbani kwake alimkuta yupo hoi kabisa huku akiwa na makaratasi ya mahesabu pembeni yake, mama Angel alisikitika kiasi,“Masikini mwanangu jamani, tunampa mzigo mkubwa sana kushinda umri wake hebu ona alivyochoka hapo!”Na kweli Erick hakuwa hata na habari, basi akamuacha kwanza na kusema kuwa kesho atawahi kuamka ili aongee nae kwanza kwani alipanga kumwambia kuwa awe anapumzika siku zingine yani sio kila siku awe anaenda kiwandani.Kisha mama Angel alienda zake kulala tu kwa muda huo, ila kabla usingizi haujampitia vizuri simu yake iliita alipoiangalia aliona ni mumewe anapiga, basi akaipokea simu ile,“Erica, nasikia leo ulienda kwenye kaburi la marehemu baba, kwanini umeenda bila ya kuniambia?”“Samahani mume wangu, ila kuna kitu nilitaka kugundua ukweli, nilitaka kujua kama kweli Sarah na mama yake wanaenda kule kaburini mara kwa mara”“Na ukweli huo ungeupata wapi?”“Kwa wale walinzi”“Haya, wamekwambia chochote?”“Sijaongea nao sababu nilikutana na bi.Aisha yule mmama aliyeamua kuishi na baba yako kipindi kile ambacho baba yako alilalamika kuwa ni mpweke”“Na mkazungumza vitu gani?”“Vitu vingi sana ila kikubwa kaniambia kuwa nisiwe naenda kule mwenyewe, kasema niende na wewe au na Tumaini, sijui ni kwanini ila kasema hivyo tena akanitaka niondoke muda huo huo kwahiyo hata kaburini sikusogea zaidi ya kuondoka tu. Nisamehe sana mume wangu”“Haya, nimekusamehe. Ila kuna jambo mke wangu nataka unisaidie sijui utaweza”“Jambo gani?”“Nataka kesho uende ofisini kwangu, kuna faili nitakuelekeza uniangalizie, nataka uniangalizie wewe. Sijui utaweza?”“Nitaweza ndio, hakuna tatizo”Basi alikubaliana na mume wake na moja kwa moja kuamua kulala tu kwa muda huo.Siku hii Erick alienda shuleni kama kawaida ila Sarah nae alifika siku ya leo maana alisema kuwa anaendelea vizuri, basi muda wa mapumziko moja kwa moja Sarah alimfata Erick na kuanza kuongea nae,“Ila Erick tabia mbaya, kweli kabisa nimekuja kuishi kwenu hata kupata moyo tu wakuja kuniona!!”“Nilikuwa na mambo mengi sana”“Nikwambie kitu ninachotamani kwasasa?”“Kitu gani?”“Natamani kubeba mimba yako”Erick alishtuka sana, na kusema,“Hivi Sarah una wazimu au ni kitu gani? Ni malezi gani wewe uliyolelewa”“Kwanini?”“Huoni kama haupo sawa na mtoto wa kiafrika, hivi utasema unatamani kubeba mimba yangu kwa umri huo!! Na bado unasoma, hivi unafikiria maisha yako ya baadae?”“Unajua niliwahi kuongea na mama yangu, aliniambia kuwa kuna mambo ukifikiria maisha yako ya badae basi huwezi kuyafanya ila mambo hayo yanafanya maisha yako ya badae kuwa bora na imara zaidi”“Kama mambo gani?”“Mama, huwa ananiambia kuwa hakuwa na mpango wa kunizaa mimi kabisa. Ukizingatia alikuwa bado hajaolewa na hakujua ni kipindi gani angeolewa, na aliniambia fika kuwa alijua wazi baba yangu asingeweza kumuoa yeye, nilimuuliza kwanini akasema kuwa ataniambia tu. Ila kuna mtu alimshawishi kuzaa na baba, na baada ya kubeba mimba yangu basi maisha yake yalibadilika moja kwa moja, akaanzishiwa biashara, akafunguliwa miradi mbalimbali na ile nyumba tunayoishi ya kisasa ni matokeo ya kunizaa mimi, kwahiyo maisha ya mama yangu yamebadilika baada ya kupata ushawishi wa kunizaa mimi”“Sikuelewi, ngoja nikwambie kitu Sarah. Kwasasa zingatia masomo, kama mapenzi yapo tu. Yalikuwepo na yataendelea kuwepo”“Yani furaha yangu itatimia pindi nikibeba ujauzito wako”Yani Erick alimuangalia bila kummaliza, kwa bahati nzuri kengele ya darasani ililia basi ikabidi wote waingie tu darasani.Mama Angel alienda ofisini kwa mume wake na kufanya yote ambayo mume wake alimuelekeza, na alipomaliza aliweka vizuri na kuondoka kwani alikuwa ameacha mtoto wake nyumbani.Ila wakati anatoka tu kwa muda huo, akakutana na mtu nje ya ofisi ila ni mtu ambaye anafahamiana nae, basi alisimama na kusalimiana nae,“Oooh leo nimefurahi sana kukuona Erica”“Haya, vizuri ila mimi nataka kuwahi”“Subiri kwanza nikwambie kitu, mwanangu anaumwa”“Pole sana”“Mbona huniulizi anaumwa nini?”“Eeeeh anaumwa nini?”“Ngoja nikwambie, unajua sijui ni kitu gani kipindi kile mimi na wewe tulipandikiza kati yetu, nakumbuka nilikupenda sana kiasi cha kuanza hata kupagawa sababu ya kukupenda wewe. Sasa nina mwanangu ambaye kachukua jina langu, anaitwa Bahati na yeye, sijui alionana wapi na mtoto wako Erica, basi mwanangu anaugua sana moyo wake maana anampenda sana mwanao Erica, halafu hata mwanao anaonekana kumuelewa mwanangu”“Bahati, hebu acha ujinga wako, usitake kuharibu watoto. Hivi watu wengine mnaleaje watoto wenu lakini? Mimi watoto wangu kwa umri ule huwezi kusikia akikwambia natamani mtu, sijui nataka kuwa na mpenzi sijui nini na nini, hivi wenzangu ujasiri huo wa kufundisha watoto wenu ujinga mmeutoa wapi? Nina uhakika hao watoto wako watakuwa wamefundishwa huo ujinga kwa mama zao maana Fetty hawezi kubaliana na hayo mambo. Mkanye mwanao, tena akimuona mahali mwanangu basi iwe kama muhalifu kaona kituo cha polisi, kwaheri”Mama Angel aliingia kwenye gari na kuondoka zake.Basi alivyofika tu nyumbani kwake, akapigiwa simu na rafiki yake Fetty,“Ndugu yangu yani huwezi amini yaliyonipata leo”“yapi tena hayo?”“Jamani si nimekutana na Derrick, basi nikafurahi mwenyewe sababu hatujaonana siku nyingi, basi nikakumbatiana nae pale, jamani kuja kuangalia pochi yangu kulikuwa na elfu sitini yote haipo basi hata sielewi kama nimeibiwa na Derrick au kitu gani”“Duh pole sana ndugu yangu, ngoja nitafatilia ili nijue kama ni Derrick”Alishindwa kumtaja moja kwa moja ingawa tabia ya Derrick ilianza kumkera sasa maana alitapeli hadi watu wa karibu, basi akajisemea,“Yani huyu Derrick kawa mbaya jamani, anatapeli kila mtu”Vaileth akasogea na kumwambia,“Kuwa makini mama ili asije akakutapeli hata wewe”“Weee amtapeli nani? Hawezi kunitapeli mimi maana nina akili zangu timamu”“Hata hao anaowatapeli mama wanaakili zao timamu, yani yeye akija anajua mtu kama wewe akutapeli vipi ni kuwa nae makini tu”Basi mama Angel aliachana na Vaileth pale na kwenda chumbani kwake tu kupumzika muda huo.Ila baada ya muda aliwaza kuwa bora siku hiyo hiyo angemaliza na swala la yeye kuchukua hela kwenye akaunti ya mume wake kwaajili ya kulipa ile ambayo ilitapeliwa na Derrick, kwahiyo akaona ni vyema aondoke muda huo kuichukua ili Erick akirudi amkabidhi hela hiyo.Basi alimpigia simu mume wake kumpa hiyo taarifa,“Ndio, nataka kwenda leo kuchukua ile hela mume wangu”“Ila si nilishakurubhusu jamani mke wangu, hata usijali”Basi wakati anaongea na mumewe kwenye simu alisikia sauti ya pili kama ikimuuta mumewe,“Erick, njoo tujadiliane kuhusu hiyo simu”Basi mama Angel akaguna na kusema,“Mbona hiyo sauti ya kike?”“Mke wangu jamani, tusiishi hivyo kwakutokuaminiana jamani, hapa huwa wananitania tu kuwa mke wangu ananichunga sana, ndiomana umemsikia huyo mama akisema hivyo”Basi mama Angel aliridhika na kuagana na mumewe.Baada ya hapo alijiandaa kwaajili ya kwenda kwenye ATM kutoa hiyo pesa ili amkabidhi Erick.Kama kawaida Erick alienda kiwandani akiwa na madam Oliva, basi moja kwa moja alienda kiwandani huku madam Oliva akiwa nje ya kiwanda kama kawaida, basi Erick alishughulika mule kiwandani basi kama kawaida pale nje alipokuwa madam Oliva, alipita Rahim na kuanza kuongea nae,“Mbona hata kunipigia simu hakuna ile usiku?”“Aaaah niliona nikupigie muda wa mchana”“Una wasiwasi gani kwani tunaongea kuhusu nini? Kuwa huru nipigie muda wowote ule. Halafu nikuombe tu jambo huna muda tuweze kuonana na kuongea vizuri mwisho wa wiki hii?”“Muda ninao”Ila leo Erick aliwahi kutoka kiwandani na kumkuta madam Oliva amesimama na Rahim, basi Erick alijikuta akichukia tu maana toka siku ambayo alipewa maelezo kuwa yule alimpa hela Erica basi alijikuta akiwa na hasira nae sana, kiasi alisogea pale bila ya kumsalimia, madam Oliva alimfokea,“Erick, tabia ya wapi hiyo ya kutokusalimia?”Rahim akauliza,“Na huyu anaitwa Erick?”“Ndio, anaitwa Erica”“Ni mtoto wa Erick na Erica?”“Ndio, unawafahamu kumbe?”“Ila jamani kuna watu wanapenda kugelezea sana, yani yule Erick kaona kuna mtoto kapewa jina kama langu basi na yeye akaamua kumpa mwanae jina lake, wanachekesha sana hawa watu. Haya wewe kijana mbona unaonekana una kiburi sana?”Erick alikaa kimya tu bila ya kusema chochote kile,“Mmmh sijawahi kuona mtoto mwenye kiburi hivi jamani ila nikiamua nitakunyoosha mjinga wewe”Erick alimwambia madam Oliva,“Madam naomba twende nyumbani”“Erick mbona hivyo? Mbona unaonekana kuwa na hasira sana?”Erick hakumjibu hata mwalimu wake, ila cha kushangaza, Erick aliondoka pale na moja kwa moja kuchukua pikipiki na kwenda nayo nyumbani kwao yani hata hakufatilia chochote kile, yani madam Oliva na Rahim walibaki kumshangaa tu, ila madam Oliva akamwambia Rahim,“Ila usijali kuhusu huyu mtoto, mimi ni mwalimu wake wa nidhamu na nitamnyoosha, siku zote huwa namuona ni mtoto mwenye heshima sana ila sijawahi kufikiria kama ana kiburi kiasi hiki!!”Kisha madam Oliva aliagana pia na Rahim kwani hakuipenda kabisa tabia ambayo imeonyeshwa na Erick.Mama Angel alikuwa muda huo ndio amerudi nyumbani baada ya kutoka Atm kuchukua hiyo pesa, basi alivyokuwa anataka tu kuingia getini kwake akashtuliwa na Derrick maana muda huo hakutembea na gari sababu aliona achukue tu usafiri wa haraka kwenda na kurudi, basi alisimamishwa na Derrick na kusimama na kuanza kuongea nae,“Muda huu kweli nyumbani kwangu jamani!!”“Halafu nilikuwa napita tu, sema nikakuona nikasema sio vizuri nisije kukusalimia”Mara simu ya Derrick iliita kidogo na kukata, kisha akaitoa mfukoni na kutoa karatasi la vocha basi akasema,“Oooh dada, samahani naomba nisaidie shilingi mia hapo nikwangulie hii vocha, yani huyu mtu ananisaka sana, halafu simu yangu imeisha hela, nilinunua hii vocha na kuiweka maana sikuwa na cha kukwangulia”Mama Angel hakuona tatizo la kumpa Derrick shilingi mia akwangulie vocha, basi alimpa na muda ule ule Derrick alimuaga ila mama Angel alimuuliza,“Kheee wewe kama ulikuwa na lengo kweli la kunisalimia mbona hutaki kwenda kusalimia watoto wangu? Au unaogopa utapeli wako ulioufanya kwao?”Ila Derrick hakusema neno na alianza kuondoka, mama Angel alishtuka pia na kujiuliza,“Hivi hajanitapeli na mimi kweli!!”Akaangalia kule alipomtolea mia na kukuta hana hela yoyote ile.Ila Derrick hakusema neno na alianza kuondoka, mama Angel alishtuka pia na kujiuliza,“Hivi hajanitapeli na mimi kweli!!”Akaangalia kule alipomtolea mia na kukuta hana hela yoyote ile, kwakweli alishangaa sana basi alianza kumuita Derrick ila Derrick hakuitika wala nini, ndipo alipoamua kumkimbilia ila mbele kidogo Derrick alipanda pikipiki na kuondoka zake, kwakweli mama Angel alichoka kabisa, hakuwa na namna zaidi ya kuingia tu getini, alifika ebleni na kupumua kwa nguvu sana hata Vaileth alifika na kumuuliza,“Vipi mama? Ni salama?”“Yani leo ndio nimeamini ule msemo usemao lisemwalo lipo na kama halipo basi linakuja, yani huwezi amini, leo leo nimekutana na Derrick hapo nje ya geti na amenitapeli jamani!! Huyu Derrick ni mzima kweli dah!”“Pole mama, amekutapeli vipi?”“Sikia nikwambie, ndio kwanza nimerudi kutoka ATM nikakutana na Derrick hapo getini akidai alikuwa anapita ila kaona vyema asogee kunisalimia, mara simu yake ikaita mara moja na kukatika yani kama mpigaji alikuwa akimbeep vile, mara akatoa vocha na kuniomba mia haraka haraka akwangulie vocha, yani sikuwa na wazo kwamba anaweza kunitapeli kwa kutumia ile mia jamani, nikaitoa na kumpa, kakwangulia pale na kuanza kuondoka, nikamuuliza mbona anaondoka bila kuingia ndani kusalimia wanangu? Nikamuuliza au unaona aibu sababu umewatapeli, ila hakunijibu kitu nikashtuka na kuangalia kwenye mkoba, kwakweli hela zote hazipo yani Derrick kanilamba pesa yote hivi hivi yani. Sielewi ni kitu gani hiki jamani!”“Mama, huyo sio tapeli pekee bali anatumia pia chumaulete”“Kheee chumaulete tena!! Ndio inakuwaje hiyo naisikiaga tu”“Yani mtu anakuja kukuomba hata hamsini na ukimpa tu basi hela zako zote anavuta, nakumbuka kuna kipindi nilikuwa nauza duka la mjomba, sasa mambo ya chumaulete yakakazana hatari, yani mtu unauza, anatokea mteja huyo anataka kitu halafu hela yake unatakiwa kumpa chenji basi ukimpa tu utakuta kakomba hela zote”“Kheee sasa si hasara hiyo? Sasa mlifanyaje?”“Ni kweli ni hasara tena hasara kubwa sana, ila pale kijijini tuligundua kitu. Yani tuligundua nguvu ya mkaa kwa chumaulete, yani ikawa kila mtu anaweka kipande cha mkaa kwenye droo ya pesa au kwenye pochi ya kuhifadhia pesa, basi chumaulete akija hawezi kuvuta zile hela sababu ya nguvu ya mkaa”“Mmmmh yani mkaa tu!! Sasa mkaa ndio una nguvu gani?”“Sijui, ila ni mambo ya imani haya mama. Ila huwezi amini ni kweli ukiweka mkaa kwenye hela zako basi huyo chumaulete hawezi kuvuta pesa zako, yani walizidi ilifikia kipindi mtu unatembea na kipande cha mkaa hata kwenye mfuko wa sketi yako au suruali yako maana chumaulete unaweza kukutana nae popote pale, na mara nyingine ukamsaidia kwani unaweza kujua kuwa ana tatizo kweli kumbe mwenzio yupo kazini, basi mkaa ndio ilikuwa komesha yao”“Kwakweli tabia ya Derrick imeniogopesha, nitaanza na mimi kutembea na mkaa jamani!! Ila huyu Derrick dawa yake inachemka jamani, haiwezekani asumbue kiasi hiki”Basi mama Angel aliinuka zake na kwenda chumbani ila hilo swala la yeye kutambeliwa na Derrick aliona akimwambia mumewe atamcheka kwahiyo aliona vyema kukaa nalo kimya bila kusema lolote lile kwa mumewe.Leo usiku, Erick alikuwa amechoka kiasi kwahiyo baada ya kula tu alienda kulala. Muda huu Erica nae alitoka chumbani kwake na moja kwa moja kwenda chumbani kwa Erick sababu kuna jambo alitaka kumueleza, ila alipofika alimuona Erick akiota huku akiweweseka na kutaja jina la Erica,“Jamani Erica, aaaah Erica”Erica akamshtua pale kaka yake,“Kheee wewe unalala hadi unaota na kuongea, haya ni kitu gani hiko hadi unitaje ndotoni?”Erick alikaa huku akiwa kimya kwa muda maana alikuwa akitafakari ndoto yake, basi Erica alimshtua tena na kumuuliza,“Ulikuwa unaota kuhusu nini?”“Mmmh acha tu Erica ni ndoto tu hata sijui ni kuhusu nini!”“Unajua sijawahi kuona ukiota ndoto hadi unaongea namna hiyo, ila nitakachokwambia si ndio uataota unaongea hadi asubuhi”“Kitu gani hiko Erica, niambie tafadhari”“Hata sikwambii”Kisha Erica akainuka na moja kwa moja kutoka kwenye kile chumba cha kaka yake, basi Erick alibaki kumuangalia tu na kujiuliza kuwa anataka kumwambia kitu gani ila hakupata jibu ya kitu hiko.Kulipokucha Erick alienda shuleni kama kawaida, ila alipopanda kwenye gari tu alikaa na Sarah ambapo Sarah alionekana kufurahi sana,“Siku hizi sikupati kwenda shule wala kurudi, una mambo mengi sana Erick”“Ni kweli nina mambo mengi”“Ila wewe ni mwanaume uliyetulia sana, shuleni kuna wasichana wengi mno ila Erick hujaonyesha kuvutiwa hata na mmoja wapo jamani! Ila mimi nakuahidi kujitunza hadi pale utakaponizawadia”“Halafu Sarah kuna kitu hujui kati yetu”“Kitu gani?”“Mama aliniambia kuwa inawezekana mimi na wewe ni ndugu kwahiyo kuna uwezekano wa asilimia tisini kuwa wewe ni ndugu yangu”“Hapana haiwezekani kabisa, siwezi kuwa ndugu na mwanaume nimpendaye namna hii, hivi Erick unajua ni jinsi gani nakupenda lakini”“Tupo kwenye gari la shule Sarah, hebu jiheshimu na maneno yako basi”Walifika shuleni na moja kwa moja Erick alienda darasani ila aliitwa na madam Oliva, kwahiyo ilibidi aende kumsikiliza, kwakweli leo madam Oliva hakumchekea kama siku zote anavyofanyaga, alirudisha ukali wake ule aliokuwa nao kabla hajamfahamu baba wa Erick na kuanza kumpenda, basi Erick alivyokuwa pale huyu madam alimuamuru kupiga magoti, ilibidi Erick apige magoti tu kisha madam Oliva alimuuliza,“Unajua kwanini nimekupigisha magoti?”“Sijui”“Sasa mbona umepiga?”“Ningekataa ungesema nina kiburi ndiomana nimepiga magoti kama ulivyosema”“Ni kweli una kiburi Erick, mbona hukuwa hivyo wewe!! Ulikuwa kijana mtulivu na mwenye heshima, ila kwasasa umekuwaje? Ni kitu gani kimekukumba Erick?”Erick alikaa kimya tu, kisha madam Oliva aliendelea kuongea,“Sasa nakupa onyo la mwisho, kwakweli ukionyesha tabia kama ile tena utaniona mbaya kabisa, sipendi watoto wasiokuwa na nidhamu. Haya inuka nenda darasani”“Asante”Kisha Erick aliinuka na kwenda zake darasani, ila siku hii alivyotoka shule aligoma kwenda kiwandani yani yeye hakutaka kwenda tena na madam Oliva kwahiyo akamdanganya tu kuwa siku hiyo mama yake alimwambia kuwa asiende kwahiyo kwa siku hiyo moja kwa moja alirudi nyumbani kwao.Mama Angel alipomuona Erick mapema siku hiyo akajua sababu hakumpatia ile pesa ambayo alitapeliwa na Derrick, basi alianza kumuuliza mwanae,“Mbona leo hujaenda?”“Basi tu mama”“Ila hata hivyo nilitaka kuja kuongea na wewe kuwa uwe unaangalia na siku za kwenda sio kila siku kila siku maana utashindwa kufanya vizuri kwenye masomo yako”“Nimekuelewa mama, ila mimi kuna kitu sikipendi”“Kitu gani?”“Kila siku ninapoenda kiwandani basi madam Oliva anaambatana na mimi, kwakweli sitaki haya mambo kabisa mama. Niwe naenda mwenyewe tu”“Mmmh yule madam nae kiherehere kweli yani, sikia basi dereva atakuwa anakuja kukuchukua, ila siku za kwenda kiwandani iwe Jumatatu, Jumatano na Ijumaa napo sio unakaa kwa muda mrefu, yani jitahidi usitumie muda mrefu sana kiwandani”“Sawa mama, nimekuelewa mama yangu”Kisha Erick akaenda zake ndani, basi mama Angel akajijadili kuwa kwanini huyo madam Oliva ameanza pia kumfatilia mtoto wake,“Jamani hawa watu loh! Wameanza tena kumfatilia mwanangu jamani! Sijui vipi”Basi baada ya muda kidogo Erica nae alirudi kutoka shule, na alivyofika tu alianza kumsimulia mama yake,“Yani mama leo wakati tunarudi tukiwa kwenye basi la shule, njiani nilimuona anko Derrick, uwiii kuna mtu kamtapeli maana yule mtu alikuwa akimlalamikia sana. Ila mama hivi hamjapata tu cha kufanya na huyo anko?”“Tufanye kitu gani?”“Ngoja mama, nitamuwekea mtego halafu nyie mtajua cha kufanya”“Mmmh Erica mtego!! Sasa mtego gani utakuwa nao wewe?”Erica alicheka tu na kwenda zake ndani kubadili sare za shule.Muda wa kulala ulipofika, mama Angel moja kwa moja alienda zake kulala ila kabla ya kulala alipigiwa simu na Sia, basi akaipokea simu ile,“Mambo vipi Erica?”“Salama tu”“Hivi mumeo unajua alipo na anafanya nini?”“Mmmh yupo kikazi kwani vipi?”“Kuna mwanamke nasikia umewahi kusoma nae, ilikuwa kipindi mpo shule wewe na Erick, huyo dada aliitwa Manka, unamkumbuka?”“Mmmmh Manka? Oooh nimemkumbuka, alikuwa ni mweupe sana”“Ndio, sasa nasikia yule amewahi kuwa na mahusiano na Erick”“Unazungumzia nini wewe?”“Basi nakwambia kuwa huyo Erick yupo na Manka kwasasa, wanakula raha yani hakuna cha kazi wala nini. Hivi wewe hushtuki eeeh! Sio kawaida ya Erick kusafiri muda mrefu hivi na kukuacha mkewe, kwanza kakuacha ili iweje? Mwenzio kakuzalisha ili yeye apate upenyo wa kuwa pamoja na Manka”“Kiukweli sikuelewi kabisa”“Sikia nikwambie, siku moja mdadisi huyo rafiki yako Jofari kuhusu Manka na Erick”“Kheee unamfahamu hadi Johari!”“Ndio namfahamu, sasa unadhani huyo Manka ningemfahamu vipi? Huna mashaka ndugu yangu eeeh? Ni kweli una rangi nzuri ila mwenzio Manka ni mweupe, na asilimia kubwa ya wanaume wanapenda wanawake weupe sana, najua wewe sio mweusi yani siwezi kukuweka kwenye weusi ila mwenzio Manka ni mweupe peee, na yale macho yake ya gololi, unadhani Erick anaweza kupindua pale?”“Usinichanganye mie”Mama Angel aliikata ile simu kwani aliona Sia akimchanganya tu kwa muda huo, basi alivyokata simu akaanza kumkumbuka vizuri huyo Manka,“Mmmh hivi huyu Manka si ndio kipindi kile tunasoma alisema kuwa ana mahusiano na Erick hadi mimi nikaogopa kuwa pamoja na Erick! Mmmh Johari si ndio alikuja kunipa maneno kuwa Erick yupo na Manka hadi wamepelekana kutoa mimba jamani! Ila mbona Erick hajawahi kugusi hata mara moja kuwa aliwahi kuwa na mahusiano na Manka?”Akainuka na moja kwa moja akasogea kwenye kioo na kujiangalia kisha akasema,“Mimi sio mbaya, hivi huyu Sia ana wazimu wa kusema Manka ni mzuri sana sababu ni mweupe sana? Kwani nani kasema kuwa weupe ndio uzuri? Asinibabaishe mie nishindwe kulala kwa amani nianze kuwaza mambo yasiyokuwa na kichwa wala miguu”Kisha aliamua moja kwa moja kulala, yani kwa muda huo hata mume wake hakumpigia simu wala nini kwani aliona maneno ya Sia ni kumuweka roho juu juu tu.Siku hii mama Angel alikaa nyumbani kwake akiwa amejichokea kiasi kidogo, kwahiyo alijikuta akijiwa na usingizi tu kwenye kochi, mida ya mchana akafikiwana mgeni na kushtuliwa pale na Vaileth basi akaamka na kumkuta huyo mgeni ni Juma, basi alimkaribisha vizuri sana na moja kwa moja Juma alianza kuulizia maendeleo ya Erick,“Anaendeleaje kijana wetu Erick?”“Yupo salama kabisa, ameenda shule”“Na kiwandani huwa anaenda?”“Ndio, ila nimemwambia awe anaenda mara moja moja, ili athiathiri masomo yake”“Oooh ni vizuri, ila shemeji naomba nikuulize swali la kizushi”“Uliza tu”“Hivi kwa mtoto Erick hukuchepuka kweli? Mmmh mbona nahisi kama sio damu ya Erick hii”“Kheee ndio swali gani hilo sasa? Nampenda mume wangu na tangia niingie kwenye hii ndoa basi huko unakoita kuchepuka hakuna nafasi katika maisha yangu yote. Kwahiyo unataka kusema mtoto Erick sijazaa na mume wangu? Kumbuka wapo mapacha, kwahiyo hii pacha nilichepuka eeeh!”“Aaaah shemeji, mimi nimeuliza tu”“Haya, basi nilichepuka na wewe”“Jamani shemeji ndio yamekuwa hayo? Unajua mimi sio kwamba sikufahamu wewe, nakufahamu vizuri sana, hata mtoto wa kwanza sio wa jamaa, hilo nafahamu”“Kheee umetumwa wewe au?”“Sio kutumwa, mimi nakufahamu vizuri Erica, kama uliweza kutembea na shemeji yako yani mume wa dada yako ndio utashindwa kuchepuka kwenye ndoa yako?”“Naomba uende mjinga wewe, naona huna jambo la kuongea na mimi. Kama ningekuwa hivyo usemavyo si hata wewe ningekukubali, mjinag wewe. Toka nyumbani kwangu”Mama Angel alichukizwa na kujikuta akimfukuza tu, basi Juma alianza kumuomba msamaha na kusema kuwa ni utani,“Nisamehe jamani shemeji yangu, sikujua kama una hasira kiasi hiki, naomba unisamehe”“Naomba uende tu kwa amani, tusiharibiane siku tafadhari”Basi Juma alkamuaga mama Angel na kuondoka zake.Siku hii ya Ijumaa pia Erick hakutaka kwenda kiwandani na madam Oliva, basi alikaa hadi mwisho huku akipanga aende kwanza kwao halafu kama akiweza basi kwa siku hiyo abadili tu nguo na kwenda kiwandani sababu siku hii waliwahi kutoka shule, ila walivyopanda kwenye gari la shule kurudi nyumbani, leo Erick hakukaa siti moja na Sarah, ila Erick alivyofika kwao na kushuka ni hapo ambapo Sarah nae alishuka.Basi wakiwa pale nje ya geti, Erick alimuuliza Sarah,“Mbona umeshuka sasa?”“Kiukweli nimemkumbuka mama yako, nahitaji kumsalimia tu ndio nirudi nyumbani”“Kheee makubwa, ila kama nilivyokwambia kuwa mimi na wewe ni ndugu”“Hilo kwangu sijali ila ninachojali ni kuwa nakupenda sana”Erick hakubishana nae, basi moja kwa moja aliingia nae ndani kwao, na kumuacha sebleni akiwa na mama yake, basi Sarah alikuwa akiongea na mama Angel,“Yani nimejikuta nimekukumbuka sana, basi nimeona leo nije nikusalimie mara moja tu halafu niende nyumbani”“Oooh nashukuru sana kwa kunikumbuka”“Ila mimi sio mkaaji sana mama”“Oooh basi, Erick atakurudisha hakuna tatizo”Na muda kidogo Erick alitoka ndani maana alitaka kwenda kiwandani, ila alipofika tu sebleni kabla hajamwambia mama yake lengo lake la kutaka kwenda kiwandani, aliambiwa na mama yake kuwa ampeleke Sarah nyumbani kwao,“Hakikisha unamfikisha ndio unarudi, natumai unanielewa mwanangu”Ilibidi Erick amuitikie tu mama yake na hata hakumwambia lengo lake kwani alijua wazi kuwa anaweza akachelewa na kushindwa kwenda kiwandani sababu kwakina Sarah na kiwandani zilikuwa ni sehemu mbili tofauti na zilikuwa mbalimbali.Basi akatoka na Sarah na kuondoka nae kwenda nae nyumbani kwao, basi Sarah akawa akimuuliza,“Ila mbona siku hizi Erick kama unanikwepa hivi, unajua sijui tatizo ni nini?”“Hakuna tatizo”Walifika nyumbani kwakina Sarah, basi Erick alimtaka Sarah ashuke ila Sarah alitaka kushuka nae kwanza ikabidi ashuke nae na kwenda nae ndani kwake, amabpo cha kwanza Erick aliulizia alipo mama yake Sarah,“Kwani mama yako bado hajarudi?”“Alirudi ila jana kasafiri tena, ila safari hii hatokawia kurudi”“Aaaah sawa, basi mimi naenda”“Unaenda wapi tena Erick? Naomba twende wote chumbani kwangu mara moja”Erick aliogopa na kuinuka, kisha akatoka nje ambapo Sarah alimfata na kumuuliza,“Kwani Erick wewe sio mwanaume?”“Mimi sio mwanaume ndio maana mimi bado ni mdogo, kwahiyo mimi ni mvulana”“kheee wawapi wewe lakini, mbona unakuwa mshamba hivyo?”“Acha niendelee na ushamba wangu”“haya, nikusubiri hadi miaka mingapi? Nikusubiri hadi umalize kidato cha nne?”Sarah alikuwa akiongea na Erick huku kalegeza macho haswaa, yani kwa muda ule ilibidi tu Erick amuage na moja kwa moja alienda kupanda gari na kuondoka, badala ya kwenda kiwandani, ni moja kwa moja alienda kwenye duka lao ambapo alimuweka Rama kuuza lile duka.Alipofika pale dukani alimkuta Rama akiangalia simu yake, na kugundua kuwa Rama alikuwa akiangalia mtandao wa facebook huku akisikitika, basi Erick alimuuliza,“Sasa unasikitika nini?”“Kuna huyu mtu nimemuona huku, yani nasikitika haswaa”“Mtu gani?”Rama akamuonyesha Erick ile picha, katika picha ile kulikuw ana binti mdogo tu halafu kasimama na mbaba, ila yule mbaba Erick alimfahamu, ila alimuuliza Rama ni kitu gani kinamsikitisha haswaa,“Mbona ni picha ya kawaida, ila kwanini umesikitika hivyo?”“Ni picha ya kawaida ndio ila huyu baba lazima atakuwa na mahusiano na huyu binti aliyepiga nae picha”“Kwanini?”“Huyu baba namjua vizuri, aliwahi kuwa shemeji yangu ila ni muhuni hatari, na umuonapo hapo kaathirika tayari, yani yeye anajivunia uzuri wake na pesa yake, kampa dada yangu ukimwi huyu baba, halafu hana aibu hata kidogo anatembea na wasichana wadogo kwa wakubwa, ndiomana nasikitika sana kwani namsikitikia huyu binti”Erick alimuuliza ilia pate uhakika wa anachokihisi, alimuuliza,“Kwani huyo baba anaitwa nani?”“Anaitwa Rahim, nasikia kwasasa kaoa mke daktari tena mkewe nasikia ni mpole sana, ametulia ni mwanamke mwenye stara na heshima zake. Anaitwa Maimuna, ni mwanamke mpenda dini na anayeheshimu watu wote ila dada huyu hajapata bahati kabisa ya kuolewa na hiki kimeo yani namuhurumia sana. Hii picha ya kawaida ila kwa tabia za huyu mwanaume hata sio kawaida hapa lazima kuna kitu kinaendekea”“Duh! Kumbe”Basi Erick aliendelea na mambo mengine pale dukani ila kwa taswira ya haraka haraka ni kuwa huyu Rahim anamtaka pia Erica maana haikuwa kawaida kwa jinsi ambavyo kila akimuona Erica kutaka kumpatia pesa.Erick alipomaliza alirudi tu nyumbani kwao, na siku hii alikaa na mama yake na kumueleza tu kwa kifupi kuhusu huyo Rahim, yani vile alivyotaka kumpa Erica pesa, na jinsi anavyokuwa akiongea na madam Oliva, na jinsi alivyoambiwa na Rama, basi mama yake na hivi huwa anamchukia Rahim ndio akachukia maradufu na kumwambia mwanae,“Tena Erick kuwa makini sana mwanangu, bora umemgundua, naomba ukae mbali na mtu huyo, hata kumsalimia usimsalimie hivyo hivyo, sitaki kabisa uwe karibu naye, ni mtu mbaya sana huyo”“Sawa mama nimekuelewa, hata mimi nilihisi kuwa si mtu mzuri kabisa, kwajinsi ambavyo huwa anaongea na Erica, nikahisi kuwa yule sio mtu mzuri kwenye maisha yetu kabisa”Erick akakubaliana na mama yake kuwa awe anamkwepa Rahim kabisa na hata kumsalimia asiwe anamsalimia, mama Angel alifanya hivi sababu alihofia ikiwa Rahim atapata ukaribu na Erick, basi atamwambia ukweli kuhusu Angel na yeye hakutaka hilo.Muda wa kulala ulipofika kila mmoja alienda kulala na siku hiyo asubuhi na mapema Erick aliamka na kujiandaa halafu akaenda kiwandani sababu hakuenda kwa siku zote hizi akaona ni vyema aende siku hiyo.Jumatatu ilipofika, kama kawiada Erick alikuwa shule na alivyomaliza masomo tu, madam Oliva alimuita ili waende nae kiwandani, Erick alikuwa akikataa ila madam Oliva akamlazimisha sana, ikabidi Erick akubali tu maana hakuwa na namna tena.Waliondoka na madam Oliva hadi kiwandani, na kama kawaida wakati Erick ameenda kufanya kazi, huyu madam alibaki nje na baada ya muda pale nje alifika Rahim na kuanza kuongea nae,“Aaaah madam na wewe ni mzushi sana, tumekubaliana vizuri kabisa kuwa tutakutana mwisho wa wiki hii, sasa mbona umezingua?”“Dah!! Naomba unisamehe bure, ni kweli tulipanga kukutana ila mume wangu mtarajiwa alinibana haswaa hakutaka nitoke hata kidogo. Leo sikupanga kuja huku ila nikasema ngoja nije ili niweze kuonana na wewe na kuongea na wewe”“Yani umeniangusha sana, huwa najua walimu sio waongo, ila wewe umenidanganya, yani nimesubiri simu yako hadi nikahisi kuchanganyikiwa”“Nisamehe tafadhari”“Haya, tutakutana lini tena na tutakutana wapi? Hapa sio mahali pazuri kwa mimi na wewe kukutana, inatakiwa tupate sehemu nzuri ili tuzungumze kwa upana zaidi, ni wapi tutakutana sasa?”“Mmmh sijui, popote tu utakapopenda”“Nielekeze shule unayofundisha ili siku nije nikuchukue muda wa kutoka halafu twende mahali tukayajenge”Madam Oliva alianza kumuelekeza Rahim ili afahamu shule anayofundisha, muda kidogo Erick nae alitoka kiwandani na alitaka waende nyumbani.Ila alipofika pale na kumuona Rahim kama kawaida hakumsalimia wala nini, basi madam Oliva alichukia sana na Rahim akamwambia madam,“Si mwalimu wa nidhamu wewe!! Ndio mnavyowafundisha hivi shuleni kudharau wakubwa?”Erick hakusema chochote ila aliondoka, na kama kawaida aliita pikipiki na kuondoka nayo kwenda nyumbani kwao.Erick aliingia nyumbani kwao na wala hakusema kitu chochote cha siku hiyo zaidi ya kufanya mambo mengine tu ambayo huwa anayafanya siku zote hadi muda wa kulala na moja kwa moja kwenda kulala.Kulipokucha tu alijiandaa na kwenda shuleni kama kawaida.Erick alipofika tu shuleni aliitwa na madam Oliva, na kwenda kisha madam Oliva akamwambi,“Natumaini unaelewa ni kitu gani umefanya”Erick alikaa kimya tu, kwani hakuwa muongeaji wa sana, na tabia hii ilifanya wengi kumuona kuwa ana kiburi, kisha madam Oliva alisema tena,“Ila wewe Erick una kiburi sana, si nilikuonya wewe ila jana umeenda kurudia kitendo kilekile, halafu kuna habari nyingine nimesikia kuwa una mahusiano ya kimapenzi na Sarah, nadhani ndio kitu kinachochangia kukufanya uwe na kiburi kiasi hiko. Hivi hujui mambo kama hayo yanakatazwa shuleni? Yani mimi huwa nakutetea sababu naelewana na wazazi wako, ila hakuna atakayeweza kufurahi akisikia mambo kama haya. Leo nitakuchapa fimbo tatu, ila jirekebishe, kwanza uwe na adabu na pia umuone Sarah kama dada yako, mambo ya kusikia tena una mahusiano nae sitaki kuyasikia. Haya inuka nikuchape”katika vitu ambavyo Erick alikuwa havipendi ni kuchapwa viboko, ni sababu nyumbani kwao sio mtoto mbishi kwahiyo hata viboko hajawahi kuchapwa na mama yake wala na baba yake.Kwahiyo swala la kuambiwa kuwa achapwe viboko lilikuwa gumu sana kwake, basi akamwambia madam Oliva,“Madam nina ombi moja”“Ombi gani hilo”“Kabla ya kunichapa viboko naomba uniruhusu nimuite mama yangu nae asikie mashtaka haya halafu akuruhusu kunichapa”“Unasemaje wewe! Mjinga kabisa”Madam Oliva aliinuka kwa hasira na kumcharaza fimbo moja ya nguvu sana Erick, ila kitendo kile kilimfanya Erick aanguke na kupoteza fahamu. Madam Oliva aliinuka kwa hasira na kumcharaza fimbo moja ya nguvu sana Erick, ila kitendo kile kilimfanya Erick aanguke na kupoteza fahamu.Hapo madam Oliva akashikwa na wasiwasi sana, basi akaanza kumpatia Erick huduma ya kwanza, na baadhi ya walimu walienda kumsaidia, ila walipoona kuwa hazinduki ikabidi wampeleke hospitali.Madam Oliva alijieleza kuwa mtoto kaanguka tu mwenyewe, aliogopa kusema kamchapa maana alijua kama akipatwa na matatizo itakuwa ni tatizo kubwa zaidi, basi yule daktari akawaambia kuwa wamuite mzazi wa yule mtoto, ilibidi tu madam Oliva ampigie simu mama Angel na kumuelekeza hospitali waliyokuwepo ili afike.Kwakweli madam Oliva alihisi yupo kwenye wakati mgumu sana, huwa anaadhibu watoto ila ilikuwa tofauti kwa huyo mtoto, wakati amekaa na mawazo akapigiwa simu na Rahim, ilibidi aende nayo pembeni kuongea nayo,“Vipi madam, nimepita hapa karibu na shule yenu, nije kukusalimia?”“Dah nina matatizo mwenzio, nipo hospitali kwasasa”“Hospitali? Unafanya nini tena? Nielekeze ni hospitali gani nije”Madam Oliva alimuelekeza vizuri kabisa ila hakuwa na amani katika moyo wake hata kidogo kwani alijua wazi ukweli ukigundulika basi itakuwa ni tatizo kubwa sana kwake, yani alikuwa akifanya maombi yote ili Erick azinduke tu.Kwakweli mama Angel toka amepata ile simu kuwa aende hospitali alihisi kuchanganyikiwa kabisa, hakujielewa maana hakujua huko hospitali kuna tatizo gani.Basi alimuacha mtoto kwa Vaileth na kuondoka zake hadi huko hospitali, kwanza alimkuta madam Oliva akiwa nje kasimama na Rahim, akapatwa na hasira kuona madam Oliva kamuitia Rahim akataka kuondoka, ila madam Oliva akamkimbilia bila kujua kuwa anataka kuondoka sababu ya Rahim,“Mama Angel mbona kama unataka kuondoka? Ni Erick amelazwa”Hapo moyo wa mama Angel ulilia paaa, yani alihisi kama kapewa habari gani vile, na kutaka kuonyeshwa mwanae, basi moja kwa moja alipelekwa kwa daktari ambaye alianza kuongea nae,“Samahani, mwanao ana tatizo la kuanguka?”“Ninachotaka ni kumuona mwanangu, niambieni ukweli nini kimetokea kwa mwanangu? Naomba mniambie”“Inasemekana mwanao alianguka gafla shuleni, na bado tunampatia huduma ila tumekuita ili tuweze kupata historia ya ugonjwa”“Hakuna historia hiyo kwa mwanangu wala kwenye ukoo wetu hakuna kitu cha namna hiyo, nionyeshe Erick tafadhari”Basi moja kwa moja daktari akampeleka mama Angel katika chumba alicholazwa Erick, pale mama Angel alimsogelea mwanae na kumshika mkono yani alijikuta tu akitokwa na machozi mengi kama maji, ila muda huo huo Erick nae alifumbua macho na kusema,“Nakupenda sana mama”Kwakweli mama Angel alifurahi sana na kumkumbatia mwanae huku akisema,“Asante Mungu, asnte Mungu, asante Mungu”Yani ndio kauli aliyokuwa akiitamka, ila madaktari walijaribu kumpima Erick na kugundua kuwa hana tatizo lolote lile.Kwahiyo walimpa ruhusa huku wakimtaka aende siku nyingine kwaajili ya uchunguzi, muda huu ndio daktari na mama Angel waliangaliana na kukuta ni watu wanaofahamiana,“Kheee kumbe ni wewe Erica”“Ndio ni mimi, unajua hata sikufikiria pia kuwa ni wewe”“Nakumbuka kipindi kile ulikuwa bado binti mdogo, saivi umekuwa ila sura yako haipotei yani bado umzuri vile vile”Mama Angel aliona bora aagane nae tu huyu daktari ili asije kuzungumza mengine bure mbele ya mtoto, basi akaagana nae na kuondoka.Pale nje bado madam Oliva alikuwa kasimama na Rahim, yani hata hakujua kuwa mtoto kazinduka, ila alivyowaona alitaka kuwafata ila mama Angel aliongozana haraka na Erick na kupanda gari ili kuelekea nyumbani kwao.Madam Oliva akiwa amesimama pale na Rahim akasema,“Simuelewi mbona kachukia hivyo au mwanae kamwambia ukweli”“Kwani ukweli ni nini?”“Ni hivi, nilikuwa nimechukizwa sana na tabia yake ya jana, basi leo nikaamua kumuadhibu tena nilimchapa fimbvo moja tu ndio akaanguka na kupoteza fahamu, sasa sielewi tatizo ni nini. Ila nimekoma mimi, unadhani nitarudia tena kuchapa mtoto wa mtu! Kamwe sirudii mimi, yani nilikuwa naiona rumande inakuja jamani”“Aaaah pole ila usingefungwa wala nini?”“Mmmh unasemaje? Unadhani mtoto angekufa huyu kuna ambaye angeniamini kuwa ni bahati mbaya?”“Najua Erica angekusamehe”“Kheeee sio kwa watoto wake, yani yule mwanamke chezea vyote ila sio watoto wake na wala sio mume wake. Kumbe unamjua eeeh!”“Namfahamu ndio, tuachane nae tuongee yetu. Vipi sasa twende tukayajenge”“Yani leo sipo vizuri, akili yangu imevurugika kabisa, sina amani sina raha, hapa kwenyewe narudi kazini tu nachukua ruhusa na kwenda nyumbani kwangu, yani siwezi kwenda popote, nilikuwa naongea na wewe hapa kuendelea kujipa moyo tu na matuamaini ila ungeingia katika moyo wangu na kuona hali yake ilivyokuwa basi ungenielewa nasema kuhusu kitu gani. Tutaenda kuzungumza vizuri siku nyingine”Na alipomaliza kusema hayo, aliamua tu kuagana na Rahim na kurudi zake shuleni kwanza kuchukua ruhusa ila Rahim hakupenda maana siku hiyo alitaka apate muda mzuri wa kuongea nae.Mama Angel akiwa kwenye gari na mwanae akamuuliza,“Erick sio kawaida ujue, usione nimeondoka tu na wewe hospitali bila kuuliza vizuri, lazima kuna tatizo mwanangu. Niambie tatizo ni nini? Imekuwaje hadi uanguke?”“Mama, kwakweli sikumbuki vizuri ila mara ya mwisho nakumbuka ni madam alinichapa fimbo”Mama Angel alisimamisha gari na kuliweka pembeni kwanza, halafu akamuuliza mwanae kwa makini,“Alikuchapa fimbo? Kisa nini?”Erick alimuelezea mama yake jinsi ilivyokuwa hadi madam Oliva akamchapa fimbo,“Aaaargh ningejua mapema jamani, ngoja”Kisha mama Angel akageuza gari na moja kwa moja kwenda hadi shuleni kwakina Erick, na moja kwa moja alienda kwenye ofisi ya mwalimu mkuu kumlalamikia,“Shule zipo nyingi, ila mzazi nimeamua kugharamikia kumleta mwanangu hapa ilia je kupata elimu bora, sio aje kupata fimbo, haya leo mlimchapa mwanangu akazimia, na siku mkiniulia kabisa mtoto?”“Mama Erick, naomba upunguze jazba”“Sio nipunguze jazba, kwakweli siwezi kukubaliana na hali kama hii kabisa, natupa hela zangu nyingi sana hapa shuleni, nimeishi na mwanangu kwa miaka yote hii, hana kiburi, sio jeuri wala sio mbishi, sijawahi kumchapa hata kumpiga kibao sijawahi, halafu leo unaenda kumchapa mwanangu tena bila hata ya kuniuliza mzazi wake jamani!!”“Tusamehe bure mama Erick, kwanza mimi sielewi kitu ni nini kimetokea kwani?”“Muulize huyo mwalimu wako madam Oliva”“Oooh amekuja hapa muda sio mrefu kuchukua ruhusa, kasema hajisikii kukaa ofisini kwa siku ya leo”“Basi ndio huyo kanichapia mwanangu hadi kazimia, nahisi mwanangu hayupo sawa kabisa. Kumbuka natoa pesa nyingi kwa elimu ya mwanangu halafu mnataka kuniulia mwanangu kweli!”“Naomba utusamehe bure mama Erick, huyo madam Oliva nitaongea nae vizuri”“Nitawafungulia kesi mimi maana ushahidi upo”Huyu mkuu wa shule aliamua kuendelea kumbembeleza mpaka pale mama Angel aliporidhika na kuondoka na mwanae, ila wakati wanarudi nyumbani ndani ya gari tu akampigia simu mume wake, hadi Erick aliomba tu gari aendeshe yeye maana aliona mama yake ataleta balaa bure.Basi akamuacha Erick aendeshe huku yeye akiongea na mume wake,“Sasa huyo Oliva ametaka kutuulia mtoto leo”“Kafanyaje?”“kampiga mtoto hadi kazimia, hivi nimetoka hospitali na ndio naenda nyumbani na Erick, yani sijapenda kabisa tabia aliyoifanya madam Oliva”“Sawa, mke wangu nashukuru kwa taarifa”Kisha baba Angel alikata simu, ambacho mama Angel hakufahamu ni kuwa baba Angel ndio alichukia zaidi yake, yani alichukia mno, alitamani hata huyo madam Oliva angekuwa karibu yake kwa muda huo.Madam Oliva alirudi nyumbani kwake ila bado alikuwa na mawazo kiasi, basi alikaa na Steve ambapo Steve alimuuliza tatizo ni nini, aliishia tu kumwambia,“Wewe acha tu”Muda kidogo simu yake ya mkononi ikaita, kuangalia akaona mpigaji ni baba Angel, yani hapo akapatwa na mashaka makubwa sana, ila aliipokea ile simu ambapo baba Angel alianza kumwambia maneno yake aliyojisikia kuyasema kwa muda ule,“Sijapenda kabisa, unataka kuniulia mwanangu? Hivi unajua kama mtoto wa kiume ninaye mmoja tu!! Hivi unajua kama yule ndio mtoto wa kuwaangalia dada zake, unataka kumuua ili mimi nibakiwe na nini?”“Naomba unisamehe, haikuwa kusudio langu, naomba unisamehe sana, yani mimi nilikuwa tu nataka kumfunza adabu ila ikawa vile”“Umfunze adabu kwa lipi alilokukosea?”“Sikia nikwambia, huwa naenda na mwanao kiwandani, ila kule nilikuwana na baba mmoja anaitwa Rahim na tulikuwa tunaongea maswala ya biashara, ila mwanao huwa akinikuta na yule baba huwa hamsalimii kabisa na nikimuuliza ananiangalia kwa dharau na kuondoka zake, sasa leo nikasema ngoja nimchape kiboko ili ajifunze heshima, jamani fimbo moja tu hata sijui imekuwaje hadi kuwa vile”“Mjinga wewe, kwanza aliyekwambia uwe unaenda kiwandani na mwanangu ni nani? Halafu kitu kingine, wewe si ndio ulikuwa ukililia kuolewa wewe na kusema kuwa unataka kuolewa na Steve, haya huyo uliyekutana nae unayezungumza nae kuhusu biashara wa nini? Utakufa na ukimwi wewe, tamaa zitakuponza, umesoma lakini kajinga. Mwenzio ana ukimwi yule anafanya kazi ya kuusambaza tu, usije kumuua Steve wa watu bure kwa ujinga wako, umemtundika midawa hata kutoka hawezi halafu unataka kumletea na maradhi. Mjinga kweli wewe”Madam Oliva alikaa kimya kwa muda kisha akasema tena,“Nasamehe tafadhari”Halafu baba Angel alikata ile simu, Steve alimuangalia madam Oliva na kumuuliza kuwa anaomba masamaha wa kitu gani, ikabidi madam Oliva amsimulie kila kitu jinsi ilivyokuwa kwa siku hiyo.Steve alishangaa kwa muda ila akasema,“Dah iliwahi kunitokea hiyo siku moja wakati nikiwa mvulana mdogo, kuna mtu alinikorofisha basi nikamzaba kibao, uwiii si akaanguka na kupoteza fahamu yani nilihisi kuchanganyikiwa, mpaka alipokuja mama yake, ndio akazinduka, ndio mama yake akaniambia kuwa mwanae huw ahapigwi. Yani toka siku hiyo nilikuwa naogopa kupiga watu hovyo balaa”“Ooooh pole, basi ndio yaliyonipata leo”Kisha madam Oliva aliinuka na kwenda chumbani basi alifikiria kwa muda maneno ambayo baba Angel alimwambia mwishoni kuwa Rahim ameathirika, akajiangalia kwa muda na kusema,“Hivi baada ya miaka yote hii kujitunza, nije kupata ukimwi kizembe namna hii dah!”Akapumua kwa muda na kuamua kujilaza tu kwa muda huo.Muda huu mama Angel akiwa nyumbani huku Erick akiwa ameenda kupumzika, mara akapata ugeni na mgeni huyo alikuwa ni Sia, sababu alimruhusu siku ile basi mlinzi hakuwa akimkatalia tena kuingia ndani, na yeye akaongea nae kawaida tu ili kujua shida yake,“Nimekuja kumuona Erick”“Ili iweje?”“Nasikia alizimia, na mimi kama mama nina wajibu wa kujua kuwa mwanangu anaendeleaje?”“Dah! Yani wewe sijapata kuona mimi, huwa nakutafakari sana ila nakosa jibu kabisa. Anaendelea vizuri. Una lingine”“Ndio lipo, mwanao Elly anakusalimia”“Naona umeamua kuja kuniachanganya muda huu, hebu Sia acha kunitia kichaa, niliyonayo kichwani yananitosha. Naomba utoke”Sia hata hakubishana leo kwani muda huo huo aliofukuzwa, alijiongeza na kuondoka zake.Alipoondoka, mama Angel alipumua kiasi yani aliona ni afadhari kaondoka, ila baada tu ya kuondoka, alisogea Vaileth mahali pale na kumuuliza mama Angel,“Samahani mama, kwani huyu mwanamke huwa anakuja kwako mara kwa mara kufanya nini?”“Aaaah achana nae huyu”“Mmmh kama namfahamu”Mama Angel akashtuka kidogo na kumuuliza kwa makini,“Unamfahamu? Kivipi?”“Ila sina uhakika kuwa ni yeye”“Niambie tu unavyomuhisi”“Ni hivi, mimi nina babu yangu ni mganga wa jadi, sema siku hizi sina mawasiliano nae ya karibu sana kutokana na dawa aliyokuwa anataka kunifanyia nami nikaikataa hiyo dawa. Nakumbuka kipindi nikiwa mdogo huyu mwanamke nimewahi kumuona mara kadhaa kwa babu, inasemekana alikuwa akichukua dawa ya kumdhibiti mwanaume ila dawa sijui ilikosewa ikaenda kwa mwanaume mwingine, na hilo swala likamsumbua sana, huwa nahisi kama ni yeye vile, najua hanikumbuki ila mimi namuhisi”“Huyo babu yako yuko wapi?”“Anaishi Bagamoyo”“Oooh sawa, nitafatilia tu kujua kuwa ni yeye au wanamsingizia. Ngoja nikuulize na wewe, inamaana kipindi kile ndugu zako ndio walichukua dawa kwa huyo mganga?”“Hapana, mganga yule walimpata hapahapa mjini, hata nilikuwa simfahamu hadi siku waliyonipeleka”“Ila Vai unaonaje kuhusu maswala ya uganga?”“Mmmh hata sielewi, ila mimi uganga kiukweli siupendi. Naomba nikaendelee na kazi zingine”Vaileth aliona ataulizwa maswali mengine ambayo atashindwa kujieleza, kwahiyo aliamua kwenda jikoni na mama Angel alimruhusu kufanya hivyo.Usiku wa leo, Erica anaamua kwenda chumbani kwa Erick maana kama hakuelewa vile wakati mama yake akizungumza, akamfatya ili aujue ukweli,“Kwani leo kimetokea nini Erick?”Erick alimsimulia jinsi ilivyokuwa, ila katika maelezo ya Erick hakuna hata sehemu moja aliposema kuwa sababu za kupigwa na madam Oliva zimehusishwa pia na swala la yeye kuwa na mahusiano na Sarah. Yani alikuwa akielezea tu kutokumsalimia Rahim,“Kale kamadam jamani loh! Yani angaejua huyo mtu asivyopendwa kwetu nahisi angeelewa ni kwnaini hujamsalimia”“Ndio hivyo, yani akanipiga kiboko hiko ila nashangaa ni kwanini nimezimia kwa fimbo moja tu!”“Ila na yeye kwanini kakuchapa? Na hospitali nao wamesema kwanini umezimia?”“Hawajasema tatizo ni nini ila nadhani tatizo ni kuchapwa, ila kwanini nizimie baada ya kuchapwa kiboko kimoja tu! Ni kweli sijawahi kuchapwa na mama wala na baba ila sijafikiria kuwa naweza kuwa na tatizo nikichapwa mimi. Nitachunguza tu na kujua kuwa tatizo ni nini”“Mimi nitakusaidia kuchunguza, hata usijali. Ila leo nitalala humu humu chumbani kwako ili usije kuzimia tena bure, lazima nikuangalie”Erick alicheka sana, ila hakusema neno lolote lile, kwani hata yeye alifurahi kwa swala la Erica kulala chumbani kwake.Siku hii, mapema kabisa Vaileth alikuwa ameshaamka ila aligundua kuwa Erick na Erica hawakuamka kwenda shuleni, moja kwa moja alienda chumbani kwa Erica aligonga ila hakuitikiwa, akafungua mlango na kukuta Erica hayupo humo, basi akaenda chumbani kwa Erick aligonga ila hakuitikiwa, akafungua mlango na kukuta Erick na Erica wamelala tena wakiwa hawana habari kabisa, alisikitika huku akiwaangalia mara mbilimbili na kusema,“Hawa si kaka na dada hawa? Tena mapacha, maajabu haya jamani, ndio ulalaji gani huu?”Akafikicha macho yake vizuri na kuwasogelea kisha aliwashtua, kwakweli walishtuka sana toka usingizini, halafu Vaileth alimuuliza Erica,“Mbona umelala humu leo? Na vipi huendi shule?”“kwani saa ngapi saa hizi?”“Saa moja na nusu hii”“Kheeee!”Kisha Erica alimuangalia Erick na kumuuliza,“Kwahiyo igtakuwaje, na wewe hutoenda shule?”“Tushachelewa, haiwezekani kwenda shule, nitaenda kiwandani tu leo”“Basi tutaenda wote kiwandani, ngoja nikajiandae”Erica aliinuka, yani Vaileth aliwaangalia sana wala hawakuonekana kuwa na wasiwasi wa aina yoyote ile kila kitu kwao ilikuwa ni kawaida kabisa, basi Vaileth nae alitoka mule chumbani ila alikuwa akitafakari sana huku akijisemea,“Mmmh haya ni malezi mabovu, watoto wa Kiswahili ukawalee kizungu ndio madhara yake haya, yani watoto wanalala pamoja kama sio dada na kaka vile mmh!!”Kisha akaenda jikoni kuandaa chai.Erisk alishaenda kuongea na mama yake kuhusu kwenda kiwandani kwa siku hiyo, basi walipomaliza kujiandaa na Erica walienda kunywa chai na kumuaga mama yao kisha kwenda kiwandani, basi mama Angel alikuwa amekaa huku akimbembeleza mwanae mdogo, Vaileth alienda karibu yake na kumuuliza,“Mama, mbona hujamwambia Erica aende shule basi?”“Wamechelewa kuamka, watoto wale mapacha wana mambo yakufanana ndiomana hata huwa sijiumizi kichwa changu”“Hivi Erick na Erica umeanza kuwatenga chumba wakiwa na umri gani?”“Yani nyumba ambayo nilikuwa naishi mwanzoni, nilipenda watoto wangu wote walale pamoja na walikuwa wanalala pamoja, ila badae Angel alisema kuwa Erick ni mtoto wa kiume na atawachungulia, basi tulipohamia hapa nikawahamisha kila mtu na chumba chake, ila ilikuwa ni ngumu sana kwa Erick na Erica kulala kwenye vyumba vyao, yani kama hujamkuta Erick kwenye chumba cha Erica basi utamkuta Erica kwenye chumba cha Erick hadi nikaanza kuwafanyia ukali, kidogo ikasaidia ila baba yao hakupenda ukali ninaoufanya kwa watoto, yani ni wao wenyewe ndio walivyoona wamekuwa basi ndio hivyo kila mmoja analala kivyake”“Halafu jana nilisikia ukisema kuwa Erick alipigwa shuleni hadi akazimia, kwahiyo huyo mwalimu alimpiga hovyohovyo?’“Alimpiga fimbo moja”“Hujawahi kumchapa Erick?”“Nimchape kwa kosa gani? Yani humu ndani kwangu hakuna watu waoga kama watoto wangu, ni waoga balaa, tena Angel ile ukishika fimbo tu basi utaona chozi na kuomba msamaha balaa, kuhusu Erick ndio kabisa, sijawahi kumpiga hata kibao, huwa nafoka tu ila sijawahi kuwapiga”“Wanaraha kukupata wewe, jamani mama yangu uwiii hata akikuita hukuitika sababu hukusikia, utashtukia tu mkong’oto huo wa nguvu hadi unasahau jina lako, jamani kuna wamama wanapiga haswaaa, ila nadhani wewe sio mpigaji ndiomana hata Angel huwa anakusumbua sana”“Niliwahi kumpiga Angel siku ile, ambayo nilijifungia nae chumbani, ila nilikuwa nalia sana. Yani mimi kumuadhibu mtoto siwezi jamani, sijui kwanini ila siwezi, nitawafundisha vyote ila sio viboko”Vaileth alimuangalia tu ila hakusema neno lingine lolote lile, kisha akaenda kufanya mambo mengine.Mchana wa siku hiyo, alifika mgeni pale nyumbani kwa mama Angel, alifika Juma na kumkuta mama Angel na kuanza kuongea nae,“Unajua kilichonileta?”“Kipi hicho, mimi nitajuaje? Nimekuwa mfalme njozi?”“Una majibu sana, ila nimekuja kumuona Erick anaendeleaje? Nimepata habari zake za kuzimia”“Kheee jamani, hiyo habari ndio imeenea kiasi hiko?”“Hakuna kitu kinaweza kumpata Erick halafu mimi nisijue”“Kwakuwa wewe ni nani kwa Erick? Wewe ndio mzazi wake au kitu gani?”“Hapana, ila hujui tu jinsi ninavyomfatilia huyu mtoto kwa karibu. Na huwa namwambia hata rafiki yangu Erick kuwa kapata mtoto haswaa, yani ni mtoto ambaye anatakiwa kumtumia katika biashara zake, unajua Erick ni kijana mwenye akili sana. Msimpoteze kwa kumuweka shuleni”“Unamaana gani?”“kama hayo yaliyotokea, basi muachisheni shule halafu muache akae kiwandani kwa mwezi mmoja tu makini uone kama hamjafungua kiwanda kingine, na mtanishukuru sana. Huyo mtoto ni kichwa kingine kabisa”“Haya sawa, ngoja nikuulize je wewe unafaidika na nini kumfatilia hivyo Erick?”“Hata mimi mwenyewe sijui nafaidika na nini ila natamani kumfatilia kwa karibu sana, natamani kumfahamu vizuri, natamani kujua mengi kuhusu yeye. Mnisamehe bure tu ila nataka kumfahamu Erick zaidi”“Kheee makubwa jamani! Hapa ndio uchawi unapoanzia, yani uache kufatilia watoto wako ufatilie mwanangu kweli? Usione kama watoto wako wana akili, uone akili za mwanangu kweli?”“Usinifikirie vibaya, wakati ujenzi unaendelea niliwahi kufika pale kiwandani na kukutana na vijana wenu wawili. Junior na Erick, ila kwanini nilikuja hadi kumwambia rafiki yangu kuhusu Erick? Ni kutokana na vile nilivyokuwa nikiongea nae, niliweza kumsoma kuwa ni mtoto mwenye kipawa cha ajabu sana, ni mtoto mwenye akili kubwa sana. Natamani muone kile ambacho mimi nakiona kwa Erick ila sijui kwanini hamuoni hili jamani dah! Kwahiyo yuko wapi leo?”“Kaenda kiwandani”“Basi naenda huko, niongee nae japo kidogo tu”Muda huo huo Juma akaondoka zake, ila mama Angel alimuangalia na kujiuliza sana kuwa kwanini huyu anaonekana kutaka kumjua zaidi Erick yani hapo hakumuelewa kabisa.Siku ya leo kwenye madam Oliva anadatwa shuleni na Rahim, kwakweli alishangaa ujio wake na kwenda kuongea nae,“Mmmh madam, najua saivi ni muda wa kupata chakula cha mchana, naomba leo twende tukapate wote chakula cha mchana”Madam Oliva hakuona kama ni tatizo, ilimradi ni chakula cha mchana basi alikubali na moja kwa moja kupanda kwenye gari ya Rahim na kwenda nae kwenye moja ya hoteli ambapo kila mmoja aliagiza chakula alichokitaka na kuanza kula, basi Rahim alianza kuongea nae,“Katika maisha yangu sikuwa naelewa neno kupenda lina maana gani, yani nilikuwa nashangaa tu wale wanaosema nimependa sana hadi nimeachwa nahisi kuchanganyikiwa, yani nilikuwa nawashangaa mno. Unajua kwanini? Naomba leo nikueleze kidogo tu kuhusu maisha yangu”Moja kwa moja madam Oliva akajua hapo ndio muda ambao Rahim anahitaji kumtongoza, yani alielewa kuwa Rahim atasema hakuwahi kupenda ila kampenda yeye, kwahiyo alitegesha masikio yake kumsikiliza kwa makini sana,“Nakusikiliza Rahim”“Kwanza mimi nimeishi sana Marekani, mimi nilikuwa natongozwa sana na wanawake, na walikuwa wakinipa pesa ili nitembee nao, sikuwa napenda kabisa yani nilikuwa natembea nao ilimradi tu. Sikukaukiwa na hela mimi maana kwetu kulikuwa ni sehemu yenye hela na wanawake zangu wengi walikuwa ni wenye hela na walikuwa wakinipa wenyewe. Siku moja nikiwa nimerudi nyumbani, nilimkuta binti mmoja ambaye nilitambulishwa, kiukweli nilipomuona moyo wangu ulidunda sana na kujikuta nikitamani kuwa nae karibu. Njia pekee ya kumvuta yule mwanamke ilikuwa kwakutumia pesa, ila baada ya muda niliona moyo wangu kuanza kumuhitaji sana, basi nikamshawishi kulala nae kwakujua kuwa hamu yangu kwake itaisha, ni kweli nililala nae na nilimfaidi haswaaa, halafu katika siku hizo hizo akabeba mimba yangu ila niliamua kumpotezea taratibu, na kumpa vigezo vigumu ili aachane na mimi, kiukweli alikuwa akiumia sana tena sana kwa niliyokuwa namfanyia, ila imani yangu iliniambia kuwa mwanamke nikimzalisha ni ngumu sana kuniacha, kwahiyo nilijua ni wazi kuwa hawezi kuniacha kwa vyovyote vile. Ila huwezi amini yule dada aliolewa na mtoto wangu akampa jamaa mwingine, ila cha kushangaza sasa kila muda najikuta nikizidi kumpenda huyu mwanamke yani nampenda sana ingawa tayari ni mke wa mtu”Madam Oliva alikaa kimya tu akimuangalia, halafu alishangaa kushtuliwa na swali hili,“Hivi mama yake na yule kijana Erick anaishi wapi? Unapafahamu?”“Napafahamu ndio”“Naomba unipeleke”Madam Oliva alimuangalia ila hakumuhoji zaidi ya kukubali kumpeleka kwani hata yeye alijua atapata muda wa kuongea na mama Angel kuhusu Erick.Basi aliinuka na kuondoka na Rahim kuelekea kwa mama Angel.Walifika kwa mama Angel na mlinzi aliwafungulia geti na kuwakaribisha, basi waliingia ndani na muda huo mama Angel alikuwa ametoka nje ila Rahim alipomuona mama Angel alimkimbilia na kumkumbatia. Walifika kwa mama Angel na mlinzi aliwafungulia geti na kuwakaribisha, basi waliingia ndani na muda huo mama Angel alikuwa ametoka nje ila Rahim alipomuona mama Angel alimkimbilia na kumkumbatia.Mama Angel alimtoa Rahim katika mwili wake ila Rahim hakutoka kwani alikuwa amemkumbatia kwa nguvu sana, yani lile tukio lilimshangaza, madam Oliva, Vaileth na hata mlinzi maana wote muda huo walikuwa hapo nje.Basi mama Angel alipopata upenyo wa kuondoka kwenye mikono ya Rahim, yani alijikuta muda huo akikimbilia ndani kwake, yani hakutaka kuongea chochote kile, alikimbilia chumbani moja kwa moja na kufunga mlango huku akihofia kuwa huenda Rahim akawaeleza kitu pale nje, ila aliogopa kutoka tena nje ya nyumba yake.Ila pale nje napo, Rahim alipoona mama Angel kakimbilia ndani, alimgeukia madam Oliva na kumtaka waondoke bila hata kuongea chochote kile.Yani madam Oliva alishangaa tu na kumfata kwa nyuma, basi akaondoka nae, ambapo moja kwa moja Rahim alimrudisha madam Oliva kwenye ile shule anayofundisha, ila madam Oliva akamuuliza,“Kuna nini kinaendelea? Sijakuelewa?”“Kusoma hujui, hata picha nayo huoni? Ila asante sana, nashukuru kupafahamu mahali pale, asante sana”Kisha Rahim hakutaka kuongea zaidi na kumtaka tu madam Oliva ashuke ambapo alishuka halafu yeye aliondoka zake kuelekea nyumbani kwake.Mama Angel alikuwa bado ndani, ila aliona ni vyema ampigie simu mlinzi ili amuondoe mtu huyo, ila mlinzi alimwambia kuwa kashaondoka, basi mama Angel alipumua kiasi na kukaa chini kisha akajisemea,“Kwani huyu Rahim anataka nini katika maisha yangu? Kwanini haniachi niishi kwa amani kwenye ndoa yangu?”Mama Angel akakumbuka baadhi ya mambo ambayo yamewahi kutokea kipindi cha nyuma sababu ya Rahim, akajikuta akitaka kutoa machozi ila akajikaza na kusema,“Nilishasema na kuapa kuwa sitokuja kulia tena sababu ya huyu mtu, nilishalia nilishateseka, nilishadharaulika, nilishasemwa vibaya, imetosha sasa, sitalia tena, na siku zote Angel atabaki kuwa Angel Erick”Akainuka na kutaka kutoka ila alijihisi kama ananuka harufu ya Rahim, yani alienda kuoga muda huo na kubadilisha nguo, kisha akatoka na kwenda sebleni, basi Vaileth alipomuona akamwambia,“Kheee mama ushabadilisha nguo?”“Sio kubadilisha nguo tu bali nimeoga kabisa”“Kwani yule ni nani mama?”“Sio kila kitu unapaswa kukifahamu Vai, ila naweza tu kuongea na wewe kwa mambo machache kama funzo katika maisha yako. Hebu njoo ukae hapa karibu yangu”Vaileth alienda kukaa, kisha mama Angel alimuuliza,“Najua kuwa una mtoto mmoja, je mtoto huyu ulimzaa kwa kipindi gani, na ulikuwa na malengo gani wakati unamzaa mtoto huyu? Ulipanga au ilikuwaje? Na je baba wa mtoto yuko wapi?”“Mama, sijui kama sijawahi kukueleza. Ila mimi nilibeba mimba nikiwa shuleni, ilikuwa ni bahati mbaya na nilijihisi vibaya sana, kwani sikuweza hata kufanya mtihani wa kumaliza kidato cha nne. Mwanaume aliyenipa mimba alinidanganya kuwa atanioa, ila alikimbia kipindi tu nina ujauzito, maisha yangu yameharibika na mambo yangu mengi yameharibika sababu yake, ila nikapata habari kuwa kaoa mwanamke mwingine, niliumia sana mama ila sikuwa na jinsi zaidi ya kuacha maisha yaendelee tu”“Je unaweza kuwa nae tena?”“Hapana siwezi kabisa”“Je hajawahi kuhitaji tena mtoto wake?”“Ni hivi yule mwanaume mwanzoni ndugu zangu walimtafuta na kumtaka alipe faini ili amkomboe mtoto ila aligoma na kusema kuwa mtoto sio wa kwake, niliumia sana, ila nilijipa moyo tu. Sasa yule mwanaume kaoa, na wameishi na mkewe hawajabahatika kupata mtoto, ndio yule mwanaume alikuja kwetu ili amtoroshe mwanangu wakalee na mke wake, basi tulipogundua ndio tukampeleka mwanangu kwa bibi yangu, kwahiyo mtoto yupo kwa bibi kwasasa na yule mwanaume hapajui kwa bibi”“Mfano akaja na kukubembeleza mrudiane, akuoe na mlee mtoto upo tayari?”“Siwezi mama, ni kweli nina shida bado ila siwezi, acha tu nihangaike na shida zangu, yule mwanaume kanipa dharau za kutosha sana, kanipa mimba shuleni ila bado kaniita kuwa mimi ni mwanamke mpumbavu sababu nimebeba mimba shuleni na kushindwa kumaliza shule, yani kasahau kuwa yeye ndio kanifanyia huo upumbavu ila akanitukana mimi, kwakweli siwezi yani siwezi kabisa, acha tu nihangaike, akitaka afate sheria za kwetu na mimi niridhie”“Sawa, nimekuelewa. Haya kaendelee na kazi zako”Vaileth aliinuka na kwenda kuendelea na kazi zake, wakati huo mama Angel alikuwa tu pale akitafakari baadhi ya mambo na kuingiwa na chuki zaidi na madam Oliva, kwani alianza kumuona ni nuksi katika maisha yake.Muda huu Erick alikuwa kamaliza mambo ya kiwandani, na alitaka kuondoka yeye pamoja na Erica ila kabla hawajaondoka, alifika pale Juma na moja kwa moja kwenda ofisini kuongea na Erick wakati huo Erica alibaki akiangalia tu bidhaa mbalimbali, basi aliongea nae vizuri sana maana huwa hana ugomvi nae kabisa,“Vipi Erick, unaonaje kazi za hapa?”“Salama tu, naendelea nazo vizuri”“Kwanza pole, nilisikia ambacho kilikupata jana”“Asante, ila hata sijaelewa ni kwanini imekuwa vile”“Usijali, ngoja nikuhadithie jambo. Nilikuwa na babu yangu mimi, alikuwa ni mkorofi sana yani usimkorofishe kidogo, yeye lazima atakubutua, siku moja alikutana na mkorofi mwenzie, basi wakabishana pale, yule mwenzie akachukua bakora na kumtandika babu fimbo tatu za kichwa, uwiii babu yangu nasikia alianguka na kupoteza fahamu, walihangaika nae, siku tatu bila ya kuzinduka, yule mtu alishikiliwa na kijiji kwani walihisi huenda babu akawa amekufa, ila alipozinduka kitu cha kwanza kabisa nasikia babu aliulizia alipo mama yake, basi mama yake alifika na babu alifurahi na kumkumbatia mama yake, ila kutoka hapo sasa babu akawa moto wa kuotea mbali. Kuna siku nitakuja kukwambia babu yangu alivyokuwa tokea pale”“Mmmmh! Unamaanisha nini sasa, yani na mimi ndio nitakuwa kama babu yako?”“Sina maana hiyo, ila nilikuwa nakupa mfano tu ili usijihisi vibaya ukadhani kuwa una kasoro au wewe ni binadamu wa kwanza kukumbwa na majanga kama hayo, hiyo ni kawaida tu na huw ainawakumbuka watu mbalimbali ila tu uwe imara, nikuhakikishie jambo hakuna atakayekuweza tena”“Unamaanisha nini?”“Tuachane na hayo, ngoja nikuulize jamabo. Je unayapenda maisha ya shule?”“Napenda ndio, maana napenda kusoma, nahitaji kufika mbali zaidi kielimu ili nitimize malengo”“Unadhani kuwa malengo yako yatatimia wewe kwa kusoma?”“Ndio”“Sikia nikwambie, katika maisha cha muhimu ni kujua kusoma, kuandika na hesabu yani kujumlisha, kutoa, kugawanya, kuzidisha, hivyo ndio vitu vya muhimu katika maisha. Vingine ni nyongeza tu, vinatuchosha akili zetu, kuna vitu mnafundishwa shuleni hata kazini hamvifanyi, ngoja nikuulize tu mfano upo hapa kiwandani je hesabu za magazijuto na kutafuta kipenyo kuna mahali umezitumia?”“Hapana”“Huoni kuwa ni kuchoshana tu akili, yani kuna vitu vipo kwaajili ya kukuchosha akili tu, haya huku sekondari nako ndio kutakuvuruga, utajifunza katika historia kuwa binadamu wa kwanza alikuwa nyani, je kuna swala la unyani kwenye biashara? Zaidi zaidi utakaa na watu wa dini huko na kuanza kubishana nao, wewe utasema binadamu wa kwanza nyani na mwenzio anasema Adam na Hawa, yani kuchoshana akili tu.”“Kwahiyo unamaanisha nini?”“Namaanisha kwamba, kwasasa kuwa makini huku kutakutoa kimaisha. Nipo tayari kukusaidia, kuna jambo nataka kufanya na wewe hata baba yako akiligundua ni lazima atafurahi sana”“Kwahiyo niache shule?”“Mmmh ngoja nitakuja kukwambia ninachofikiria, ila usiache kuja kiwandani kuangalia mambo yanaendaje. Jumamosi hii naomba nikupeleke mahali kama hautojali”“Ni wapi huko?”“Ni mahali pazuri, na huko ndipo akili yako itapanuka zaidi na kukufanya utende mambo makubwa zaidi kupita hata umri wako, kila mtu atatambua uwepo wako Erick. Kubali twende wote Jumamosi hii”Muda huu Erica nae aliingia mule ofisini kwahiyo Juma alikatisha yale maongezi na kuagana na Erick huku akimwmabia kuwa ataenda kumtembelea siku nyingine.Basi Juma akaondoka, halafu Erick nae akaondoka na Erica, wakiwa kwenye gari Erica aliuliza,“Kwani anataka mwende wapi Jumamosi?”“Mmmh sijui”“Usikubali Erick, sina imani na huko anapotaka kukupeleka, naomba ukatae”“Ila sijakubalia”“Nikiona Jumamosi unajiandaa kwenda basi namwambia mama, nakuomba usiende Erick”“Mmmh na wewe jamani, siendi popote mimi. Sasa unamwambia mama wa nini? Kwani nimekubali kwenda jamani! Siendi wala nini”Walirudi moja kwa moja nyumbani kwao kwa muda huo.Walimkuta mama yao yupo sebleni tu, basi wakamsalimia. Baada ya hapo mama Angel aliinuka na kwenda chumbani ila Erica alimfata nyuma na kuanza kuongea nae,“Mama, tulipokuwa kiwandani alikuja yule rafiki wa baba. Sijui anaitwa nani yule”“Juma”“Eeeh huyo huyo Juma”“Alikuja kufanya nini?”“Sijui ila alienda ofisini kuongea na Erick, mimi nilikuwa nje ila moyo nikahisi unaniuma sana nikajikuta natamani kujua ni kitu gani wanachozungumza, basi nikaenda na kuingia mule ofisini, nikamkuta yule baba anamwambia Erick kuwa Jumamosi hii ampeleke mahali ambapo ataenda kupata nguvu zaidi na kuwa tofauti na wanadamu wengine”Mama Angel alishtuka kidogo na kumuangalia Erica kwa makini, kisha akamuuliza,“Unasemaje?”“Ndio hivyo mama ila alivyoniona mimi aliaga na kuondoka, nimemsema Erick kuwa asikubali kwenda hiyo safari, mimi sina imani na hiyo sehemu ingawa sijui ni wapi”“Dah asante mwanangu, kulikuwa na sababu kubwa sana Mungu akakuumba jinsi ulivyo, nashukuru sana”Kisha mama Angel alitoka na moja kwa moja kwenda chumbani kwa Erick kumuuliza, mara nyingi Erick kitu kikiwa wazi huwa hakifichi tena, basi alimueleza mama yake mambo yote ambayo alizungumza na Juma, kisha mama yake akamwambia,“Erick, nakuomba mwanangu usiwe karibu na yule Juma sio mtu mzuri kwako. Kwanza anataka nini kwako hadi hataki usome? Hataki ufike mbali kielimu? Elewa kuwa hana lengo zuri na wewe. Haya nenda ukale, usiku mwema mwanangu”Mama Angel alitoka ila akili yake kwa muda huo haikuwa mahali hapo kabisa kwani alijikuta akiwa na mawazo sana.Usiku wa leo mama Angel aliamua kumpigia simu mume wake, kwani aliona ni vyema kumwambia jambo kama lile kwani aliona ni vyema mumewe akatambua yaliyotokea hapo nyumbani,“Kwanza kabisa kuna hii habari ya Juma jamani, huyu rafiki yako ana nini lakini na mtoto wetu?”“kafanyaje kwani?”Mama Angel akamsimulia vile alivyosimuliwa na watoto, basi baba Angel alichukia sana na kusema,“Dah! Kwanini kawa hivyo! Unajua Juma ni rafiki yangu mkubwa sana na hakuwa na mambo hayo kabisa, sijui kaingiliwa na kitu gani jamani. Ila jitahidi mke wangu asiwe karibu na watoto huyo, yani nahisi kama kumkataza kabisa Erick asiwe anaenda kiwandani awe tu makini na masomo”“Nilikwambia mume wangu mapema kabisa, ila ukasema ni vizuri kumfundisha mtoto mapema, umeona sasa eeeh!”“Nimeona mke wangu, mwambie Erick asiende kwasasa kiwandani atakuwa anenda kwa zile siku ambazo mimi tu nitakuwa namwambia aende”“Sawa, jambo lingine mume wangu, mwenzangu leo si madam Oliva kaniletea mapya”“Nini tena?”“Huwezi amini, kamleta Rahim hapa nyumbani kwangu”“Aaaarrgh hiko ndio kitu kimenichefua kuliko vitu vyote, tutaongea kesho mke wangu, ngoja akili yangu ikae sawa kiasi”Baba Angel alikata simu yani hata hakutaka kujua kuwa Rahim alifanya nini alivyofika hapo kwake ila tu kitendo cha kuambiwa kuwa Rahim alienda kilikuwa kimeshamchefua tayari.Muda ule ule mama Angel aliinuka na kwenda chumbani kwa Erick, ambapo alimkuta Erica yupo humo akiongea na Erick basi alimuuliza,“Kheee Erica hujaenda kulala tu!!”“Nilikuwa namshauri Erick hapa kuhusu kutokwenda na yule mbaba, halafu nilikuwa namwambia ni kwanini nimekueleza ukweli”“Yani nilijua mtakuwa mmeshalala watoto wangu, sasa ngoja niongee na wewe Erick”“Kwahiyo mimi nitoke mama?”“Hapana baki tu”Basi Erica alifurahi sana kuambiwa abaki kwani alitamani sana kusikia kuwa ni kitu gani ambacho mama yao anataka kumwambia Erick,“Ni hivi mwanangu, nimeongea na baba yako kasema kuwa kwasasa usiende tena kiwandani, utakuwa unaenda tu pale atakaposema yeye kuwa uende”Erica akadakia,“Kwanini mama? Sababu ya yule mbaba?”“Ndio, sitaki tena awe nae karibu, maana anamshauri ujinga, anamshauri aache shule na kufanya biashara. Jamani baba yenu anahangaika kwasababu yenu, yani hizi biashara zote kafungua kwaajili yenu halafu leo mmuangushe kweli!! Baba yenu anahitaji msome, anahitaji mpate elimu bora ndiomana anahangaika kuwapeleka kwenye shule nzuri mtakazo, hebu kumbuka Erick ulipomlalamikia baba yako kuhusu kuhama shule, angalia alivyofanya haraka kukuhamisha, sababu anataka usome bila manung’uniko, baba yenu anahitaji msome, na elimu ndio urithi bora kwenu, hata pesa na biashara vikipotea, angalau kichwani kuna kitu cha kuwasaidia, tafadhari usisikilize mawazo ya huyo mtu mwanangu”Erica akadakia,“Itakuwa yeye hajasoma nini?”“Yeye kasoma, pale alipo ana diploma halafu anataka mwanangu aache shule kidato cha pili yani ni mwehu kweli yule. Kusoma ni zaidi ya kupata kazi na zaidi ya kuwa na pesa, maana akili yako inakuwa inafanya kazi vizuri. Pesa bila elimu ni sawa na bure, hebu msome, natumai Erick umenielewa”“Nimekuelewa mama, kwahiyo kiwandani ni mpaka baba aseme?”Erica akadakia na kusema,“Ndio, halafu mama yani baba akisema kuwa Erick siku hiyo aende kiwandani itabidi niende nae, maana hata mimi simuamini kabisa yule baba”“Ni sawa mwanangu, umesema vymea. Haya Erick, nimepisha swala hili, siku yoyote ya kwenda kiwandani hakikisha kuwa unaenda na Erica, yani huyu ndio atakuwa mlinzi wako, haijalishi ni mtoto wa kike au ni nini ila ndio atakuwa mlinzi wako, natumaini nimeeleweka”“Umeeleweka mama, nitakuwa nafanya hivyo hata mimi siwezi kuwaangusha wazazi wangu. Baba huwa ananiambia kuwa mimi ndiye nitakayekuwa nasimamia biashara na kuwaangalia dada zangu, basi bila elimu sitaweza kufanya mambo kama haya, natakiwa kupata elimu ya kutosha, na kitu kingine kama nikianza kwenda na Erica kiwandani itasaidia sana, kwani tutaanza kufanya kazi pamoja, na mwisho wa siku sio mimi tu nitakayesimamia biashara ila wote tutasimamia maana najua hata dada Angel atakubali swala la kufanya biashara pamoja”“Hapo sawa”Kisha mama Angel alimtaka Erica akalale, halafu na yeye aliinuka kwenda kulala huku moyo wake ukiwa na amani kwa kuongea hayo na watoto wake.Siku hii watoto walienda shule kama kawaida, ila Erick leo hakupanda basi la shule, kwahiyo alimuomba tu dereva wao ampeleke shule. Alifika na kuingia darasani ila alifatwa na Sarah na kuanza kuongea nae,“Erick sijakuona jana nini tatizo? Hata juzi sijakuona, halafu leo hujapanda basi la shule”“Nakuomba ukae mbali nami Sarah”“Kwanini?”“Hivi unajua kuwa juzi nimechapwa na madam Oliva kwasababu yako”“Kheee kwasababu yangu?”“Ndio, nilichapwa hadi nikazimia”“Kheee kumbe mwanafunzi aliyezimia ni wewe Erick! Yani madam Oliva anakupiga wewe hadi unazimia kwasababu yangu?”“Ndio, kasema asinione tena karibu na wewe”“Aaaah tulia, dawa ya huyo madam inachemka, amekaa hapa shuleni kwa muda mrefu na kupendwa na wengi ila kwasasa kapoteza sifa yake na atajutia sana tu”“Kivipi?”“Subiri, utaona tu”Sarah aliinuka na kuondoka zake, kwahiyo Erick alibaki akimtazama tu bila ya kummaliza.Madam Oliva, siku hii alimuita Erick ili aongee nae kuhusu kwenda kiwandani ila Erick aligoma na kusema kuwa hatoenda,“Baba, kaniambia kuwa nisiwe naenda, nitaenda kwa zile siku anazozisema yeye tu”“Kheee mnaharibu biashara lakini ujue”“Wapo watu wakusimamia, huwa naenda tu mimi ila watu wapo”“Ila wewe mtoto ni mbishi, hata sijui walikupata kwa kipindi gani? Hivi na wazazi wako huwa unawabishia kiasi hiki au?”“Madam, nimekwambia siendi tena kiwandani hayo maswala ya ubishi ni yako. Hakuna mzazi wangu niliyewahi kumbishia kitu chochote kile”Basi Erick akaondoka, kwakweli madam Oliva hakupenda kabisa ila hakuweza tena kumuadhibu Erick, muda huu aliamua tu kurudi nyumbani kwake.Leo hakutembea na usafiri wake, basi njiani alikutana na Sia ambaye alianza kumuongelesha kwa kutikisa kichwa,“Yani wewe madam una mambo ya ajabu sana, umpende A utegeshe dawa, umpate B halafu unajifanya ndio umezama kwa huyo B”“Kwani tatizo lako ni nini?”“Tatizo langu analijua, muulize mimi ni nani kwake? Yeye ni baba wa mtoto wangu”“Kheee makubwa, mbona mwenyewe hajawahi kuniambia mambo kama hayo?”“Atakwambia muda gani na umemfanya bwege? Hivi unajisikiaje kumfuga mwanaume ndani kwako? Yani badala ya yeye kuwa mwanaume basi wewe ndio unakuwa mwanaume, yani yeye akae ndani tu ukirudi akupikie, wewe ule na kutundika miguu juu. Unajisikiaje madam? Kumbuka ni mtoto wa mwanamke mwenzio yule, hebu mwache Steve asimame kwenye nafasi yake kama mwanaume na afanye vile wanaume wengine wafanyavyo”“Unajua huwa sikuelewi kabisa, unataka nini Sia?”“Nimekwambia muache Steve asimame kwenye nafasi yake, acha kumfuga namna hiyo jamani, na yeye anahaki ya kutambua ukweli wa maisha, yani ataendelea hivyo hadi lini? Mpunguzie dozi bhana mtoto wa watu”Kisha Sia akaondoka zake, ila hakusema chochote kuhusu kupigwa kwa Erick inaonekana hakujua kama ni madam Oliva ndiye aliyempiga Erick.Madam Oliva alifika kwake akiwa amechoka kiasi na kukaa sebleni, ila Steve alikuwepo na alikuwa ameshapika na kuandaa chakula basi madam Oliva akacheka na kukumbuka yale maneno ya Sia, kisha akamuangalia Steve na kumwambia,“Nimeambiwa nikupunguzie dozi”“Dozi gani?”“Eti sio kawaida kwa mwanaume kukaa nyumbani na kufanya kazi za mwanamke”“Aaaah achana nao bhana, mimi nimeridhika na nitakuhudumia mke wangu”Madam Oliva alitikisa kichwa tu, ila alihisi lazima kuna kitu hakipo sawa kwa Steve maana alikuwa akishinda nyumbani tu labda amwambia siku kuwa watoke ila bila ya hivyo alishinda nyumbani tu na alifanya kazi zote za nyumbani pale kama kupika, kufua, kusafisha nyumba hata kuosha vyombo.Usiku wa siku hiyo madam Oliva alipigiwa simu na Erick, basi aliipokea na kuanza kuongea nae,“Hivi wewe mwanamke una kichaa au kitu gani?”“Kwanini lakini, kwanini upeleke watu wa ajabu ajabu nyumbani kwangu? Nadhani hunijui, nishakuona ukiifatilia sana familia yangu ila nitakukomesha”“Kheee jamani, sikuelewi ujue”Ile simu ilikatika na kumfanya madam Oliva abaki kuwa na maswali maana hakufikiria kama kile kitu ni cha kuchukia kiasi kile.Basi Steve alikuwa akimuuliza pale imekuwaje,“Yani hata nikikueleza huwezi kuelewa, ila leo nimekutana na Sia anadai kuwa wewe na yeye mna mtoto”“Yule mwanamke ni kichaa ujue, nimelea mimba, nimehudumia kila kitu, ila kumbe mtoto mwenyewe ana mababa sijui wangapi, mara aseme mtoto wangu, mara wa Erick, mara sijui wa nani huko, mara nikute kuna jamaa anamdai mtoto, halafu mtoto mwenyewe, wakati mchanga lkaletwa mwingine na baada ya siku chache kaletwa mwingine na kubadilishwa jina, kwakweli yule mwanamke huwa haeleweki hata kidogo”“Kheee imekuwaje, inawezekanaje kwanza? Mbona ni tofauti sana?”“Ndio hivyo, yule mwanamke anajijua mwenyewe na anajua mwenyewe ni kitu gani alifanya mpaka imekuwa hivi ilivyukuwa. Twende tukalale tu mke wangu, achana na mambo hayo”Basi madam Oliva alielekea tu kulala bila kuwaza mengine katika akili yake.Leo Erick alipoenda shuleni, alifatwa tena na Sarah darasani na kuanza kuongea nae,“Erick, tayari nishampa funzo madam Oliva”“Funzo gani?”“Utaona tu, hii shule ni ya baba yangu na ilijengwa kwaajili yangu, inaendeshwa kwaajili yangu halafu atokee mtu wa kunifanyia vitu visivyoeleweka kweli!”“Kumbe shule hii ni mali yako?”“Ndio, mimi sio mtu wa mchezo mchezo Erick, nakupenda sio sababu ya mali zenu hapana, yani nakupenda tu, kama mali basi niameachiwa za kutosha na baba halafu kumbuka kuwa mimi ni mtoto pekee kwa mama yangu”“Je huyo baba yako hakuwa na watoto wengine?”“Mama kasema hata kwa baba mimi ni mtoto pekee ndiomana kaniachia hizi mali zote”“Hongera sana”“Asante, hakuna wa kukatisha mahusiano yetu Erick. Acha sisi tupendane na mwisho wa siku tuje tuishi pamoja kwa furaha”Erick alitabasamu tu kwani alijua wazi kuwa hawezi kumpenda Sarah hata iweje kwani alikuwa akimuona kawaida tu, basi Sarah aliamua sasa kwenda darasani kwake.Kuna ujumbe madam Oliva aliupata kwa siku hiyo alihisi akili yake kuchanganyikana kabisa, basi akabeba mkoba wake na kuondoka, njiani akakutana tena na Sia ambaye alimuuliza,“Mbona leo upo kama umechanganyikiwa”“Nina haki ya kuchanganyikiwa kwakweli, nimefanya kazi kwenye ile shule kwa miaka mingi sana. Halafu leo kwasababu za kijinga tu eti nimesimamishwa kazi, yani huyu Erick huyu!”“Erick yupi?”“Si kale katoto kenye roho mbaya”“Kheee Erick amenza kufanya roho mbaya hadi kwa watu baki jamani! Ngoja leo nitaenda huko naona Erica hamfunzi vizuri adabu huyu mtoto”Yani Sia hakuuliza imekuwaje wala nini zaidi zaidi akapanga hivyo tu, basi moja kwa moja alienda nyumbani kwake.Siku hii Elly aliwahi kurudi kisha Sia alimwambia Elly amsindikize mahali,“Wapi mama?”“Kuna mahali nataka kwenda kumuonyesha mtu mmoja asiyejua kulea watoto ajue ni jinsi gani watoto wanapaswa kulelewa”“Kheee haya mama”Basi Elly alijianmdaa vizuri na kuondoka na mama yake.Muda huu Erick alikuwa amerudi nyumbani kwao, ila mama Angel alimtuma sababu alihitaji vocha na simu yake haikuwa na hela,“Kaninunulie vocha mwanangu, nitakaa ndani ya geti kusubiria”“Kheee mama ndani ya geti? Kwani si naleta tu!”“Nina haraka nayo sana”Basi Erick aliondoka na kwenda dukani, wakati anarudi kufika tu getini akamuona Sia, kiukweli hakupenda kumuona wala nini, basi Sia akasogea ili amuongeleshe ila kabla hajasema neno lolote, Erick alimsukuma Sia na kumuangusha chini, kitendo kile kilimkera sana Elly na hapo hapo alijikuta akimvaa Erick na kuanza kupigana nae. Basi Erick aliondoka na kwenda dukani, wakati anarudi kufika tu getini akamuona Sia, kiukweli hakupenda kumuona wala nini, basi Sia akasogea ili amuongeleshe ila kabla hajasema neno lolote, Erick alimsukuma Sia na kumuangusha chini, kitendo kile kilimkera sana Elly na hapo hapo alijikuta akimvaa Erick na kuanza kupigana nae.Mama Angel alisikia kile kishindo cha Sia kuanguka, kwahiyo alitoka nje kwa haraka kujua ni nani anaanguka ndipo alipokutana Elly akimpiga Erick kwani Erick hakuwa mtu wa kupigana kwahiyo alikuwa amesimama tu, basi mama Angel alienda na kumsukuma Elly kisha akamnasa kibao na kumwambia kwa ukali,“Unawezaje kupigana na mtu ambaye hapigani na wewe?”Kisha mama Angel alimuangalia Sia, halafu akamsogelea na kumnasa kibao na kumwambia,“Chezea vyote na sio watoto wangu”Mama Angel akamshika mkono Erick na kuingia nae ndani, kwahiyo pale nje alibaki tu Elly na mama yake, ambapo waliangalia kisha Elly akamwambia mama yake,“Yani mama umeshindwa kabisa kunitetea kwa yule mama?”“Sasa mwanangu hata mimi mwenyewe nimeshindwa kujitetea maana nilikuwa namshangaa tu yule mwanamke, baada aulize chanzo ni kitu gani anavamia tu watu na kuwachapa makofi, ila ipo siku atajutia jambo hili”“Utamfanyaje mama?”“Si unajua huwa mama yako hakuna kitu kinachonishinda, basi subiri tu utaona picha lenyewe litakavyoenda, anamuona huyu Erick kama dhahabu ila atalia kilio mbuzi kachoka”Kisha Sia akaondoka na mtoto wake muda huo.Mama Angel nae akiwa ndani alimfokea Erick,“Na wewe unakuwa kama mzembe jamani, unaachaje mtu akupige namna ile?”“Mama, mimi huwa sipendi ukorofi na hujanifundisha hivyo”“Oooh sawa, hata hivyo nimeogopa sana jamani, ungezimia na pale mwanangu je!”“Jamani mama, inamaana mimi nitakuwa nazimia hata nikiguswa kidogo tu!!”“Sina maana hiyo mwanangu, haya nipe hiyo vocha”Erick aliangalia vizuri na kugundua kuwa hiyo vocha ameiangusha nje ya geti lao, akamwambia mama yake,“Dah! Nadhani pale wakati yule ananitingisha na vocha ilianguka pale, ngoja nikaifate mama”“Hapana, kaa hapo naenda kuifata mwenyewe”Mama Angel aliinuka na kutoka, basi alipotoka tu nje ya geti wakati anaangalia ile vocha na kuinama ili aiokote, alishangaa kuna mtu kainama pia na kushika mkono wake, kwahiyo alipoinuka aligongana nae macho kwa macho mtu huyo alikuwa ni Rahim,“Kheee Rahim!”“Ndio ni mimi, nipo hapa kipenzi changu. Mwanamke wa roho yangu”“Kwenda zako huko”Mama Angel aliinuka sasa, ila Rahim alimwambia,“Kumbuka mimi ndiye mwanaume wa kwanza kabisa kukupa heshima wewe ya kuwa mama, halafu unapokumbuka mabaya yangu basi jaribu kukumbuka na mazuri yangu. Wanawake wangapi huwa wanapewa mimba na kutelekezwa kabisa yani mwanaume hata hajali kuwa una kiumbe chake, ila mimi wakati umeniambia kuwa una mimba yangu, nilikutumia pesa ya kupanga chumba na kununua kila kitu ndani na bado nilikuwa nakujali kwa kukutumia pesa kila mara, hata ulipojifungua bado nilikuwa nakujali Erica, ila tatizo lako wewe ni kukazana kuwa lazima nikuoe ndio ikawa tatizo kwangu sababu kwa kipindi hiko sikuwa na maamuzi sahihi ila ukiniambia kwasasa Erica nakuoa tu tena bila ya kipingamizi”“Unajua usitake kuniletea uchizi hapa, jisahaulishe tu mambo yako, ni kweli ulikuwa ukinitumia pesa ila ulisahau jambo moja tu kuwa utu ni bora kuliko kitu. Nimekaa mimi, nimedhalilishwa mimi, nimechekwa mimi, nimeitwa majina yote mabaya sababu tu ya kumbeba Angel, na bado baba wa mtoto nikikwambia kitu unanijibu vibaya, hivi ulikuwa unawaza hata kwa mbali ni uchungu gani niliokuwa naupata kwa yale majibu yako? Naomba Rahim niache kwa amani, niache niishi vyema na familia yangu”“Na mimi kamwe sitokuacha kwa amani, yani hilo sahau kabisa, tena nikome nakwambia”“Bado, nitakuja tena”Rahim alimsogelea mama Angel na kumbusu kwenye paji la uso, lile tukio lilikuwa la haraka kidogo kwahiyo hata mama Angel hakujipanga nalo, ila muda huo huo aliamua tu kuingia ndani halafu Rahim nae alirudi kwenye gari yake, kumbe kwa muda huo Tumaini nae alikuja akija hapo kwa mama Angel ila alipoona vile alijibanza mahali, kwahiyo Rahim aliporudi kwenye gari tu alimfata na kumuuliza,“Kuna nini kinaendelea kati yako na Erica?”“Kwani wewe ni nani?”“Mimi ni wifi yake”“Oooh ni dada yake Erick, yule ulikuwa bonge kipindi kile unakula kila kitu, ila saivi umekuwa mmama na mwili umekupendeza, sio kipindi kile, binti ila bonge shavu hilo utafikiri…”Tumaini alimkatisha na kumuuliza,“Kwani wewe ni nani?”“Sijui unijui au kiburi tu au umenisahau? Au nimezidi kuwa mtanashati, maana kila siku nazidi kuchanganya macho ya wanawake, usikute na wewe umeanza kuchanganyikiwa na mimi”“Vipi wewe?”“Mimi naitwa Rahim, mimi ndio mwanaume wa kwanza kabisa kuwa na Erica, mimi ndio nilimfundisha Erica nini maana ya mapenzi, mimi ndio nilimfanya awe mama kwa umri ule, mimi ndiye niliyemfanya, apate mtoto mzuri hadi kuchukuliwa na makampuni mbalimbali kwa matangazo. Mimi ni mzuri na ninajivunia hilo”“Mbona unajisifia kama mwanamke?”“Ukitaka kujua uanaume wangu tafadhari twende chumbani”“Mjinga wewe”Tumaini akaondoka zake, na wala hakuingia tena kwa mama Angel, naye Rahim akaondoka zake pia.Tumaini alivyofika tu nyumbani kwake, alimpigia simu mdogo wake na kumueleza kile alichokikuta kwenye nyumba yake,“Kiukweli nimeshindwa hata kuingia, usidhani nakuharibia ndoa ila nakwambia ukweli halisi.”“Nimekuelewa na wala siwezi hisi kuwa unaniharibia ndoa, sababu najua jinsi gani Erica anavyonipenda, hakuna kiumbe yoyote wa kukatisha mbele yake halafu akanisahau mimi”“Na alivyombusu je?”“Itakuwa ni bahati mbaya, Tumaini hujaingia kwenye moyo wa Erica wewe. Yule hata umchane chane, basi damu yake itaanguka chini na kuandika Erick”“Mmmh siwawezi”“Na hakuna anayetuweza hata mmoja, mimi na Erica tunapendana, kwahiyo hakuna kiumbe yoyote wa kukatisha kwenye penzi letu. Kama kuna mwanamke alinikosa mimi kwa kipindi kile basi asitegemee kunipata kwa kipindi hiki, na kama kuna mwanaume alimkosa Erica kwa kipindi kile asitegemee kumpata kwa kipindi hiki, namuamini sana mke wangu na kumthamini”“Haya basi yaishe, mbea mimi kukuletea huo ujumbe”“Hujafanya vibaya kuniambia ila tu nilikuwa nakusahihisha kuwa huyo jamaa hawezi kuharibu penzi langu na Erica sababu sisi tuna nguvu iliyopo ndani ya mioyo yetu”Tumaini hakuwa na la kuongeza zaidi ya kumuaga tu kaka yake, ila mumewe alikuwepo siku hii basi alimsikia kwenye yale maongezi na kumuuliza vizuri, na yeye alianza kumuelezea kuaznia mwanzo hadi jinsi alivyojibiwa na Erick,“Kheee huyo Rahim bado tu anamfataga mdogo wangu?”“Kumbe unamfahamu”“Namfahamu ndio, ila Erick hajakosea ni kweli kabisa ukimchana Erica basi damu yake itaanguka chini na kuandika Erick. Kwakweli mdogo wangu ni amependa tena kapitiliza, hakuna hata mmoja wa kumbabaisha”“Mmmh ila wanavutia na mapenzi yao, hivi na wewe unanipenda hivyo kweli mimi!”“Kwani ushawahi kunifumania?”“Sijawahi? Ila ndio kusema huna wanawake wa nje?”“Mwanaume yoyote ambaye hujawahi kumfumania jua kuwa huyo anakupenda sana, kama mwanaume ana wanawake nje ila anamficha mkewe yani anafanya juu chini mkewe asijue basi huyo mwanaume anaupendo wa dhati na mkewe, na hataki mke wake atambue kitu cha namna hiyo. Kwahiyo ukiishi na mwanaume bila kumfumania, acha kumuwazia mawazo potofu maana anakupenda sana kiasi hawezi fanya ujinga mbele yako”“Kwahiyo wewe una wanawake wengine huko eeeh!”“Hapana sina maana hiyo ila nilikuwa nakuelekeza tu, wanawake wengine mimi wanini jamani wakati nakupenda wewe mke wangu! Tumetoka mbali Tumaini, acha kunihisia vibaya, jua mumeo nakupenda sana na hakuna wa kukuzidi”Hapo Tumaini alifurahi sana na kutabasamu kwa furaha aliyokuwa nayo, maana kitu ambacho kilikuwa kinamfanya achukie mapenzi ni ile hali ya kusalitiana.Mama Angel aliongea na simu kwa muda mrefu sana maana alikuwa akiongea na dada yake Mage, kwahiyo aliongea nae kwa muda mrefu sana, na alipomaliza kuongea alisinzia kwa muda huo.Alishtuka usiku sana, basi akachukua simu yake na kuona kuwa siku hii hakumtafuta mume wake hewani, ikabidi ampigie simu muda huo, simu iliita sana ikakatika, basi akapiga tena na mumewe akapokea ila akiwa katika hali ya usingizi,“Mke wangu mbona usiku huu!”“Aaah nimekukumbuka tu mume wangu, usiku mwema”Basi mama Angel aliridhika kwa muda huo na kukata ile simu kisha na yeye akalala sasa.Asubuhi kulivyokucha tu baada ya wakina Erick kwenda shuleni, muda kidogo alifika mgeni na mgeni huyo alikuwa ni madam Oliva, alimshangaa kwa kwenda ila alimkaribisha kwanza na kumwambia,“Baada ya kunipigia mwanangu hadi kuzimia, na kuniletea mgeni wa maajabu, leo umekuja bila aibu?”“Kwanza naomba unisamehe, sikuwa na lengo la kumchapa Erick azimie, nilimchapa fimbo moja tu hata nashangaa alizimia sijui tatizo ni nini? Na nyie wazazi mna makosa, kwanini msingesema tangu mwanzo kuwa mtoto wenu ni mgonjwa? Yani na nyie pia mna matatizo, ila naomba unisamehe sana”“Nimekusamehe ila kama mwanangu angepatwa na matatizo zaidi sidhani kama ningesikiliza huo msamaha wako”“Asante, na pia nisamehe kwa kumleta yule mgeni, sikujua kama mna ugomvi wenu, nilijua ni kawaida tu ndiomana nikamleta. Naomba unisamehe na hilo pia”“Nimekusamehe, haya sema kilichokuleta”“Ni hivi, nilimchapa Erick siku ile kwa makosa mawili, moja la kutokumsalimia yule baba ila sikuelewa kumbe mna ugomvi wenu, na la pili kuwa na mahusiano ya kimapenzi shuleni wakati mapenzi shuleni yamekatazwa”“Unamaana gani? Yani mwanangu ana mwanamke shuleni?”“Ndio, ana mahusiano na Sarah”“Mmmh hainiingii akilini hiyo”“Ndio hivyi, Erick ana mahusiano ya kimapenzi na Sarah, na nilimsema pia siku ile kuwa azingatie masomo bado mdogo mapenzi yatampoteza. Sasa kilichotokea, Sarah kafikisha maneno kwenye uongozi wa shule na mimi nimesimamishwa kazi”“Sikuelewi, yani usimamishwe kazi kwa maneno ya mwanafunzi! Uache kusimamishwa sababu ya kumpiga Erick ila usimamishwe sababu ya Sarah!”“Ndio, unajua Sarah ile ni shule ya marehemu baba yake, kwahiyo kamuachia mali nyingi sana Sarah, yani Sarah anajivunia sana, yule mtoto hachapwi wala hafanywi kitu chochote, mama yake mwenyewe anamlea yule mtoto kama Mungu mtu nakwambia”“Mmmh!!”“Jinsi unavyomuona Sarah, hawezi kufua hata nguo yake ya ndani ila walimu tukiongea tunaonekana kuwa tunapiga kelele, kwahiyo nimesimamishwa kazi. Kilichonileta hapa, ingawa nimesimamishwa kazi ila bado Erick ni kama mwanangu lazima nimuhurumie, ongea nae mwambie mapenzi na shule ni vitu viwili tofauti yani yeye akazane tu na masomo wala asiangalie mapenzi yatampoteza”Mama Angel akapumua kidogo na kusema,“Haya nimekusikia ingawa nimeshangaa sana”“Ndio hivyo, kuwa makini na mtoto wako. Mfunze yaliyomema bado mdogo sana, ndio kwanza kidato cha pili”“Nimekusikia mwalimu nakuahidi kuwa nitaongea nae, ila nikiweza pia nitaenda kuongea na uongozi wa pale shuleni, na hata nitaongea na Sarah na wewe utarudi shuleni kama kawaida kwani najua Sarah ni muelewa yani ni mtoto wa kumuelewesha tu”“Nashukuru kwa hilo”Leo madam Oliva wala hakuongea mengine zaidi ya hayo, kisha akaaga na kuondoka zake.Erica alitoka shule kabla ya kaka yake, kwahiyo alimkuta mama yao na kumsalimia pale, ambapo mama yao alimuuliza,“Jipya la shuleni leo?”“Mmmh hakuna jipya mama, ila njiani nimemuona mama yake Samia”“Wewe unamfahamu mama yake Samia?”“Hapana, ila alisimamisha gari ya shule na Samia akashuka akisema ni mama yake”“Kwahiyo ni hilo tu leo mwanangu? Niambie kama kuna lingine”“Mmmh lingine sina uhakika nalo”“Lipi hilo?”“Yule mnayemsemaga Samir Samir kuwa anamsumbua dada Angel nahisi ni kaka yake Samia”“Mmmh!! Samir na Samia wana undugu?”“Ndio mama, maana hata Samia huwa anamtajataja, halafu tabia za Samia na tabia za huyo Samir kama zinafanana”“Tabia gani hizo?”“Mmmh mama jamani, leo unanikaba na maswali hadi nashindwa kujieleza”“Kheee makubwa, Erica wewe ndio ushindwe kujieleza kweli!! Hapana haiwezekani hiyo kabisa, hebu niambie ukweli”“Ni hivi mama, huwa nawasikia kuwa Samir anamsumbua dada Angel mara kwa mara, na imetokea kuwa Samia anamsumbua Erick mara kwa mara na leo kanipa….. Aaah mama hakuna kitu”“Mjinga wewe, yani habari umenianzishia halafu unataka kuikatisha hebu nipe alichokupa”Erica alitoa barua nyingine aliyopewa na Samia kuwa amletee Erick, kisha mama yake akamtaka akabadili nguo tu kwa muda huo, basi Erica akaondoka zake ila alitaka kujua hitimisho la yeye kuikabidhi ile barua kwa mama yao.Muda huu Erick alikuwa chumbani kwake, basi mama yake alimfata na kuanza kuongea nae,“Erick mwanangu ni kitu gani kinaendelea shuleni?”“Hakuna kitu mama”“Ni nini kinaendelea kati yako na Sarah?”“Mmmh hakuna kitu mama”“Nimepata habari kuwa una mahusiano na Sarah, mwanangu mahusiano na shule ni mbaya sana. Je ni kweli una mahusiano nae?”“Hapana mama, ila ngoja nikwambie ukweli, ni kwamba Sarah aliniambia kuwa ananipenda sana ila nilimwambia kuwa siwezi kuwa nae”“Kheee watoto wa siku hizi jamani, mna mambo sana sijapata kufikiria kama mna mambo kiasi hiki. Sikia mwanangu nikwambie jambo, kata hivyo hivyo usijihusishe na mapenzi kabisa, zingatia masomo, wazazi wenu tunahitaji msome na mfike mbali kielimu ila mkiendekeza mapenzi mtaishia njiani. Hivi kesho si Ijumaa!! Naomba mwambie Sarah aje hapa nyumbani, nina maongezi naye halafu nitaongea nanyi wote ili muwe kitu kimoja”“Sawa mama”“Ila zingatia, yoyote anayekufata kwa habari za mapenzi usikubali”Kisha mama Angel aliinuka na kwenda chumbani kwake, ila baada ya muda mfupi tu alifatwa na Erica ambaye alimuuliza mama yake,“Mbona hujamwambia Erick kuhusu barua ya Samia niliyokupa?”“Una uhakika gani kuwa sijamwambia?”“Nilikaa pale mlangoni kwake wakati ukiongea nae, nilikuwa nasikiliza”Ilibidi mama Angel acheke na kusema,“Dah!! Hivi huo umbea wa hivyo Erica umeutoa wapi jamani kheee yani mtoto mbea sijapata kuona, kwahiyo uliupoona naenda kuongea na Erick basi na wewe ukanyata ili usikilize hayo maongezi, loh! Hebu nenda kalale huko”Basi Erica aliondoka zake, na muda huo mama Angel alimpigia simu mumewe na kumueleza hayo ya watoto wake,“Jamani huyu Erick kaanza kuwa kama Erick wewe, kurithisha watoto majina nako ni balaa”“Kawaje kwani?”“Anatongozwa na watoto wa kike, ila tofauti ya wewe na yeye ni moja tu. Mwenzio hawakubali”“Kwani mimi nilikuwa nawakubali?”“Ndio, tusizungumze hayo maana utachukia bure. Sasa huyu Erica jamani ni mbea yani kama mtoto wa Sia”Mama Angel alikuwa akiongea huku akicheka sana, basi mumewe akasema,“Mmmh usimuite mtoto kama mtoto wa Sia, yule Sia sio mzima kwenye akili yule na hafai hata kuwa mama yani hata yule Elly namuhurumia kwakweli”“Haya mume wangu, ila unarudi lini? Nimekukumbuka mwenzio, sina raha ujue na sijazoea kuishi mbali na wewe, yani nahisi kama kuna kitu kimepungua katika maisha yangu”“Hata mimi nimekukumbuka sana mke wangu ila nitakaporudi kwa hakika utafurahi sana, kwani nitakuja kivingine wala hatutohangaika tena kufanya kazi muda wote bali tutafanya kwa afya kwa tu”“Sawa nakusubiri”“Nisubiri tu, unajua ni jinsi gani nakupenda mke wangu”Hapo mama Angel alikuwa anahisi amani sana moyoni mwake kila alipoambiwa na mumewe kuwa anapendwa, ni mara kwa mara mumewe alisema hivi ila kwa mama Angel mara zote aliona kama ni kitu cha muhimu sana katika maisha yake.Asubuhi ya leo mama Angel aliona ajitahidi yeye mwenyewe kwenda kiwandani ilia one ni kitu gani kinachoendelea, basi alijiandaa na kuondoka zake.Alipofika pale kiwandani kwakweli alishangaa kwani kila mfanyakazi aliendelea na mambo yao tu kwani msimamizi wao alichelewa kufika, mama Angel alichukia na kumfata mlinzi,“Hivi hapa huwa wanafika muda gani? Yani huyo msimamizi anakuja muda gani?”“Mara nyingi anafika saa tatu au saa nne”“Kwahiyo muda huo ndio hawa wafanyakazi wanaanza kufanya majukumu yao?”“Ndio, sababu hawawezi kufanya chochote bila kuelekezwa cha kufanya”“Hivi kiwanda kitaendelea kweli kwa mambo kama haya jamani!”“Unajua mwanzoni wakati Erick anakuja kila siku kidogo ilikuwa afadhali na walikuwa wakifanya kazi kwa bidii ingawa wanachelewa ila wanahakikisha hadi muda Erick anafika basi wanakuwa wametimiza malengo ya Erick. Unajua Erick ana hasira sana, kuna mfanyakazi Fulani alimfukuza kazi hapa bila hata kumsikiliza vizuri, ila asipokuja ndio kama hivi”“Aaaah jamani, majitu mazima haya ndio yakasimamiwe na Erick kweli!! Ngoja aje huyo kiongozi wao nimpe habari, na kila siku asubuhi nitakuwa nakuja mwenyewe, huu ni ujinga, kiwanda hakiwezi kuendelea kwa ujinga huu”Mama Angel alienda kukaa pembeni kwanza akimsubiria kiongozi wa hapo afike, na baada ya muda alifika, ila kwakweli hakutegemea ujio wa mama Angel kwahiyo aliogopa kiasi, kisha mama Angel alimpa masharti anayoyataka pale nakumwambia kuwa atakuwa anaenda kila asubuhi kuangalia vile walivyofanya,“Kumbe kuna umuhimu sana wa kuja Erick mahali hapa! Sasa tumeweka wafanyakazi wa kazi hgani? Mbona kutaka kurudishana nyuma jamani! Naomba ratiba izingatiwe, sitaki hiki kiwe kiwanda cha kwanza na cha mwisho, nataka maendeleo kutoka hapa, msiniletee ujinga mimi.”Kisha mama Angel alienda nae yule kiongozi ndani ya kiwanda na kukagua vizuri mambo yanavyoendelea pale, alikagua kila kitu na aliporidhika na mahesabu ndio aliondoka muda ule.Kwakweli alivyoondoka yule kiongozi alipumua kidogo na kumfata mlinzi,“Wewe lazima kuna kitu umemwambia huyu mama”“Nimwambie nini mimi? Sina undugu nae, siwezi kumwambia chochote”“Ila huyu mama mzuri sema anaonekana kuwa na roho mbaya sana, yani hacheki wala nini. Nadhani ndio kamlandisha yule mwanae Erick maana kale katoto kagumu hatari, siku ile laki tatu tu sababu haikuwa na mahesabu ya kueleweka akaondoka nayo, yani katoto kale ni balaa. Ila ngoja tupige kazi”“Ndio bosi, ni kheri kuendelea na kazi maana ndio zinazotufanya tucheke hizi”“Usiniite bosi bhana, mabosi wenye viwanda vyao. Niite jina langu tu”“Sawa Yuda”“Eeeeh hapo sawa”Kisha alienda kuendelea na kazi kama kawaida ila kwa siku hiyo aliweza kutambua ukali wa mama Angel.Siku hii mapema kabisa, Erica na Erick walienda shuleni, wakati Erick yupo shuleni alifatwa na Sarah kama kawaida na yeye alimpa ujumbe wa kuonana na mama yake.“Jamani, mama mkwe kanikumbuka eeeh!”Erick alikuwa kimya tu maana hakuwa na cha kumjibu kwa muda huo, halafu Sarah aliendelea kuongea,“Hivi unajua ni kiasi gani nakupenda Erick?”“Tuachane na mambo hayo jamani Sarah, kuna vitu vya muhimu vya kujadili na sio mapenzi”“Ila mimi nakwambia ukweli kuwa nakupenda sana, siku moja nitaenda na wewe kwenye kaburi la baba yangu, najua atafurahi kuona binti yake nimepevuka na kufikia hatua ya kupenda”Erick aliamua kwenda darasani tu kwani maongezi ya Srah hayakumvutia hata kidogo.Walipotoka shule, leo kama ambavyo walipanga ni kuwa Sarah alishuka na Erick na moja kwa moja kwenda naye ndani kwao na alimkuta mama yao yupo ndani na alionekana muda sio mrefu katoka kufika mahali hapo, basi mama Angel alimkaribisha na kuanza kuongea nae kama mama, alimfundisha kwa kiasi maswala ya madhara ya mapenzi shuleni na jinsi mwanamke unavyokuwa ukimtongoza mwanaume,“Ipo hivi binti yangu, mtoto wa kike unapomtongoza mwanaume kwanza kabisa unadharaulika, hakuna mwanaume anayependa kutongozwa na mwanamke. Unaishusha heshima yako, kama mwanaume anakupenda mwache aje akwambie mwenyewe, umejifunzia wapi kumueleza mwanaume mambo kama hayo?”“Mama, mimi sijakurupuka kufanya hivi ni kutokana na malezi ambayo mama amenipa. Huwa ananiambia kuwa nikimpenda mtu ni bora kuwa muwazi, kumueleza mtu huyo mapema kuwa nampenda ili awe anajua kuliko kuishia kumuonyesha kama nampenda tu, inatakiwa ajue kwani itamfanya yule mtu apate urahisi wa kuwa na mimi kwani ataona ni jinsi gani nimejivika ujasiri wa kumueleza ukweli kuwa nampenda sana”“Muulize vizuri mama yako alikuwa akikufundisha hayo kwa misingi ipi maana sifikirii kama mama yako alikuwa na hiyo nia ambayo wewe unaisema. Ngoja nikwambie kitu kingine, kuhusu Erick. Kwanza kabisa ile picha ya baba yako kama unakumbuka nilishtuka sana nilipoiangalia, na kama yule ndio baba yako basi wewe na wakina Erick ni ndugu sababu yule ni babu yao”Sarah alishtuka sana na kusema,“Hapana, baba yangu alikuwa ni mtu wa nje na hakuwa na ndugu hapa nchini”“Ngoja nisiongee mengi zaidi, kesho ni Jumamozi naomba niletee mama yako ili niongee nae, Natumai amerudi”“Ndio, amerudi jana”“Basi kesho naomba uje nae niongee nae kwani najua nikiongea nae atanielewa zaidi na yeye kukuelekeza itakiwa vizuri zaidi”“Sawa nitamwambia tu”“Sawa, ila weka akilini mwako kuwa mtoto wa kike kumtongoza mwanaume hiyo haifai kabisa, unaondoa thamani yako kama mwanamke, yani hutaonekana kabisa, unatakiwa kuwa makini kwa yote uyafanyayo. Sarah wewe ni binti mzuri sana, Mungu atakujaalia na utapata mume mzuri mwenye moyo wa upendo. Mimi nakupenda ndiomana nimekuita na kukueleza haya, nakupenda sana sijui kwanini ila nakupenda na sipendi upotee kabisa, napenda uje kuwa mwanamke bora hapo badae, uwe ni mwanamke wa kuigwa na wengine. Natumaini Sarah unanielewa ninayoyasema”“Ndio nimekuelewa”Sarah aliamua kuaga kwani lile swala la kuambiwa kuwa ana undugu na Erick hakulipenda kabisa, na bado akajiapia kuwa hata kama ana undugu na Erick bado hakutaka kuacha kumpenda kama mpenzi wake.Kisha mama Angel alimtaka Erick kumsindikiza Sarah nyumbani kwao, ila Erica nae alitokezea na kusema kuwa na yeye anaenda ikabidi waende wote wawili kumsindikiza Sarah.Walifika nyumbani kwakina Sarah na kukaribishwa vizuri kabisa, mama Sarah alionekana kufurahi sana kwa yeye kumuona Erick na kusema,“Umekuja tena!! Nimefurahi sana Erick, karibuni nyumbani kwangu”Walimsalimia pale ila hakutaka kukaa sana na kuamua kuaga muda huo na kuondoka zao.Basi Sarah alienda na mama yake chumbani na kumuelezea kuhusu kuitwa kwake na mama Angel,“Kaniambia kuwa anataka kuongea na wewe”“Mmmh kuhusu nini lakini? Kwani ananifahamu?”“Hakufahamu ila amesema kuna mambo anahitaji kuongea na wewe kuhusu mimi”“Mmmh umefanya nini tena huko Sarah mtoto wangu jamani!”“Sijafanya kitu mama, si unanifahamu vizuri huwa sina ugomvi na mtu yoyote yule”“Nakuelewa mwanangu, hakuna tatizo. Kesho jioni tutaenda wote”Sarah alikubaliana na mama yake kuwa wataenda kesho yake jioni.Erick na Erica wakati wanarudi kwenye gari, Erick alimuuliza,“Mbona leo umekazana kuwa na wewe unataka kumsindikiza Sarah?”“Ni hivi, nishasema kuanzia sasa nitaanza kukulinda, nishasema kiwandani tutaenda wote, na ukiwa unaenda mahali basi tutaenda wote hakuna tatizo”Njiani wakamuona Elly na mama yake, basi Erica akasema,“Simamisha nimsalimie Elly”“Kumbe hujui? Elly alitaka kupigana na mimi, Elly ni mkorofi”“Kheee mbona haonekani, karithi kwa mama yake basi maana hata mama yake ni mkorofi kumbe hadi wakina Samia wanamjua”“Kheee wewe nawe una habari zote, wanamjua vipi?”“Nasikia huwa anafatilia familia yao balaa ila mama yao ndio huwa namtimua kwani hataki kufatiliwa nae, nasikia mama yao na wakina Samia hapendi marafiki kabisa. Halafu nimekumbuka jana Samia alinipa barua yako ila mama kaichukua”“Mmmh mama kajuaje?”“Aliniuliza na mimi nilimwambia ukweli maana sikuweza kumficha”“Ila wewe…. Ngoja nisiseme sana”Basi walirudi moja kwa moja nyumbani kwao na walimkuta mama yao akiendelea na mambo mengine tu.Usiku ule kila mmoja alilala kwa usalama kabisa, kulivyokucha, mama Angel aliamka na kumtaka Erick ajiandae ili aende nae kiwandani kwa asubuhi ile, basi moja kwa moja walienda kiwandani ila siku hii walikuta wafanyakazi wamefika mapema sana na wameanza kufanya kazi zao mbalimbali, basi mama Angel alimtaka Erick amuelekeze yeye ambacho huwa anafanya, kwani alitaka afahamu ili aanze kusimamia yeye mwenyewe na mwanae awe makini na masomo.Jioni ya siku hii, Sarah aliongozana na mama yake hadi nyumbani kwa mama Angel kwani alitaka kufahamu kitu ambacho huyo mama alimuitia, ila walifika na kutokumkuta, hata Sarah akashangaa imekuwaje hawajamkuta wakati jana yake alimsisitiza kuwa aende na mama yake.Kwa kawaida mama Sarah huwa hapendi kupoteza muda sehemu moja, basi muda ule ule ambavyo hawajamkuta muhusika akaamua kumwambia mwanae kuwa waondoke, kwahiyo waliwaaga tu wakina Vaileth, ila wakati wanataka kutoka ndio muda huo huo mama Angel na Erick walikuwa wamerudi, kwakweli mama Sarah alipomuona mama Angel alishangaa na kusema,“Kumbe ni Erica!!” Kwa kawaida mama Sarah huwa hapendi kupoteza muda sehemu moja, basi muda ule ule ambavyo hawajamkuta muhusika akaamua kumwambia mwanae kuwa waondoke, kwahiyo waliwaaga tu wakina Vaileth, ila wakati wanataka kutoka ndio muda huo huo mama Angel na Erick walikuwa wamerudi, kwakweli mama Sarah alipomuona mama Angel alishangaa na kusema,“Kumbe ni Erica!!”Mama Angel alimshangaa kwa muda kidogo yani alikuwa kama amemsahau, kisha mama Sarah akamwambia mama Angel,“Tuseme hunikumbuki mimi! Hunikumbuki kuwa tumesoma wote? Unajua wewe hubadiliki”Mama Angel aliposikia kuwa tumesoma wote akajua lazima litazuka la kuzuka hapo, kwani ana mashaka sana na watu ambao amesoma nao basi akamvuta mkono mama Sarah na kwenda nae pembeni kuzungumza nae, halafu akamuuliza,“Hebu nikumbushe?”“Mimi ni Manka, tuseme umenisahau?”“Oooh ni Manka, umenenepa ndiomana nimekusahau. Kwahiyo wewe ndio mamake Sarah?”“Ndio ni mimi, Sarah ni binti yangu wa pekee”“Sawa, ngoja tuongee kidogo”Mama Angel alisogea na mama Sarah hadi kwenye bustani, kisha alikaa nae kwenye viti vya hapo na kuanza kumuuliza maswali,“Hebu niambie ukweli, Sarah ni mtoto wa nani?”Mama Sarah akashtuka sana na kumuuliza,“Kwanini umeuliza hivyo? Uliwahi kuongea na Johari hivi karibuni?”“Kuongea nae kuhusu nini? Hakuna chochote nilichoongea na Johari ila nimekuuliza tu”“Sikia kwanza nikwambie kitu, kwanza kabisa sikujua kama ni wewe ndiye uliolewa na Erick yani sikujua chochote kabisa, ni mpaka nilipokutana na Johari na akanieleza kuwa uliolewa na Erick hata sikuwa najua”“Imekuwaje? Erick anaingiaje hapa? Kwani Erick ndio baba wa Sarah?”Mama Sarah akashtuka tena huku akijibu kwa wasiwasi kidogo,“Hapana sio Erick”“Basi baba wa Sarah ni nani?”“Kwanza niambie kwanini unataka kumjua baba wa Sarah?”“Ni hivi, kipindi Sarah anaumwa nilikuja nyumbani kwako nakukuta akiangalia picha, aliniambia kuwa ni picha ya baba yake mzazi, nikataka kuiona, kwakweli niliona ni mtu ninayemfahamu, ndiomana nimehitaji kuongea na wewe je kweli mzee Jimmy ndio baba wa Sarah?”“Sasa unataka ukweli gani hapo?”“Na kwanini umwambie Sarah kuwa baba yake hakuwa na mtoto mwingine zaidi yake na umwambie kuwa baba yake hakuwa na ndugu?”“Ndio nakiri kumwambia hivyo, ila ni sababu tu sikutaka mtu yoyote kunifatilia. Kwani wewe unamfahamu mzee Jimmy kama nani?”“Yule ni mkwe wangu, mimi ni mke wa Erick na mzee Jimmy ni baba mzazi wa Erick”Mama Sarah alionekana kushangaa sana kwani jambo hili yeye hakulifahamu kabisa,“Kheee inamaana mzee Jimmy na Erick ni ndugu?”“Ndio, ni mtu na mtoto wake. Ndiomana nikashangaa sana kuona ile picha halafu Erick hajui chochote, mzee Jimmy alikuwa na watoto, mzee Jimmy alikuwa na ndugu ila sijui ni kitu gani ulipanga kuhusu mzee Jimmy na wewe”Mama Sarah alionekana kuinama kwa muda na kufuta machozi, ambapo mama Angel alimuuliza kwa ukaribu zaidi,“Kwanini unalia?”“Sijui hata nikwambie kwanini nalia, ila najuta mimi”“Unajuta nini?”“Ngoja nikwambie jambo moja ambalo hulijui wala hujawahi kulihisi”“Niambie”“Nakumbuka wakati tunasoma, mimi nilikuwa ni binti niliyesiwa kwa urembo shuleni, ni wengi walinisifia na wanaume wengi walinitaka kimapenzi, ila alipofika Erick pale shuleni nilijikuta nikivutiwa nae sana. Basi niligundua kuwa Erick anakuhitaji wewe sikupenda, ila nikatumia ule udhaifu wako wa ukimya kusema kuwa Erick ananitaka, na kwa msaada wa Johari hakika tuliweza kukusambaratisha wewe na Erick kipindi tupo shuleni. Nakiri wazi baada ya kumaliza shule pale, niliwahi kukutana na Erick na kuanza mahusiano nae, ila siku zote aliniambia wazi kuwa anakupenda sana sema niliamini ipo siku angenipenda na mimi kwani niliamini kuwa mimi ni mweupe na mzuri kushinda wewe, ila haikuwa hivyo, nilibeba mimba ya kwanza, Erick alikazana hadi ile mimba nikaitoa, nilibeba mimba ya pili nayo ikawa vilevile. Ikafikia kipindi Erick akanikataa kabisa akidai kuwa kampata mpenzi wa moyo wake ila bado sikukata tamaa, na ndio kuna kipindi wakati namfatilia Erick nikakutana na huyu mzee Jimmy, hata sikujua kuwa ni baba wa Erick ila nilipanga nae vitu vingi sana”Mama Sarah akainama tena na kulia, basi mama Angel akasogea karibu yake na kumbembeleza huku akimuuliza kwa makini,“Ndio ukazaa na mzee Jimmy?”“Sijui, yani sijui ila kwa kifupi tu nilitembea na mzee Jimmy na nilitembea na Erick ila usiniulize kuhusu Sarah ni mtoto wa nani”Mama Angel akapumua kiasi, akamuangalia mama Sarah bila ya kummaliza, yani alikaa kimya kidogo bila ya kujua cha kuongea kisha akasema,“Je mzee Jimmy alitambua kuwa ulishawahi kuwa na mahusiano na Erick?”“Ndio alijua, ila kuna kitu kilitokea hapo katikati kabla ya kuzaliwa Sarah! Hapana jamani mzee Jimmy hawezi kuwa baba wa Erick”Mama Sarah aliinama huku akilia, basi mama Angel aliendelea kumbembeleza ili amweleze ukweli,“Kulia hakutakusaidia bali ukweli ndio utakuweka huru, niambie ukweli. Mimi sitachukia, hata kama kuna kitu kilitokea kati yako na Erick bado siwezi kuchukia kwani ni mambo ya zamani”“Erica, sipo sawa. Siku nikiwa sawa nitakuja kuongea nawe vizuri sana, yani sikufikiria haya, nitakutafuta”Mama Sarah aliinuka na kwenda kumfata mwanae kisha akaondoka nae, yani mama Angel alibaki akimshangaa tu na kuingia zake ndani.Mama Angel alienda chumbani kwake huku akijiuliza maswali kadhaa bila ya majibu ya aina yoyote,“Huyu Manka anamaanisha nini? Mbona Erick hajawahi kutaja hata mara moja kuwa alikuwa na mahusiano na Manka! Nadhani alichofanyiwa Manka na mzee jimmy ni kile alichokuwa akitaka kunifanyia mimi, yani alitaka kutembea na mimi wakati nipo na Erick, yule mzee ana wazimu sana, ingawa marehemu huwa hasemwi vibaya ila mzee Jimmy hapana jamani, kwahiyo Sarah ni mtoto wa mzee Jimmy! Nina uhakika hawezi kuwa wa Erick, ila mmmh usikute Manka nae kazaa huko ila kambebesha mzee Jimmy sababu aligundua kuwa ana pesa, ila haya mambo jamani kama sielewi elewi hivi loh!”Mama Angel aliamua kwenda kuoga tu kwa muda huo, ila alipotoka alikuta simu yake inaita na kuichukua ili kuongea nayo, alikuta ni mumewe anapiga, basi akaona pia ni muda wa kumuuliza mumewe,“Aaaah mke wangu mbona nimepiga sana?”“Nilikuwa kuoga, ngoja nikuulize kitu. Kumbe uliwahi kuwa na mahusiano na Manka?”“Aaaah nani kakwambia hayo maneno?”“Hii dunia ni ndogo sana mume wangu, hakuna kitu unaweza fanya kisijulikane”“Naomba unisikilize mke wangu, mpenzi wangu, kipenzi cha roho yangu naomba unisikilize kwa makini. Mambo yote mimi na wewe tutayazungumza vizuri nikirudi, naomba na namuomba Mungu asije kuibuka shetani wa kukuchanganya hiyo akili yako. Nakuomba mke wangu tena nakuomba sana, kwasasa usisikilize maneno ya mtu yoyote yule, subiri nirudi halafu tutaongea kwa kina na tutajua cha kufanya ila naomba neno lolote la mtu lisiingie kwenye akili yako”“Jamani, yote hayo yanatoka wapi? Mimi nimekuuliza tu”“Kwani mke wangu sikujui vizuri wewe!! Nakujua vizuri sana, kitu kidogo kama hiki kinaweza kuanza kukuliza mke wangu, naomba usisikilize maneno ya mtu yoyote, mimi ndiye mwenye kauli na ndio inafaa kunisikiliza. Natumaini umenielewa mke wangu, tafadhari usisikilize chochote”Kisha baba Angel akambadilishia mkewe mada, ambapo waliongea hadi alipokata simu, kwakweli mama Angel alijiuliza, kwanini mumewe kawahi kusema kuwa asisikilize ya watu,“Mmmh au kuna ukweli? Ila ngoja nisijiumize moyo mie, nimsubiri tu mwenyewe akirudi atanieleza vizuri”Mama Angel nae kwa muda huo aliamua kulala tu.Kulipokucha, wakina Erick walijiandaa na kwenda Ibadani ila siku hii walienda Erick na Erica tu maana mama yao alibaki nyumbani hata Vaileth nae alibaki nyumbani ila Vaileth akamwambia mama Angel,“Mama, ni wiki ya tatu hii hujaenda Ibadani!”“Mmmh halafu kweli eeeh!”“Ndio ni kweli mama, najua huwa unapenda sana Ibada hata sijui nini kimekupata”“Mmmh ngoja niende basi, ila mimi jamani mtoto ananipa uvivu sana”“Mimi nipo nyumbani mama, unaweza kuniachia tu”“Na wewe hutaki kwenda Ibadani?”“Mimi nitaenda wiki ijayo mama”Mama Angel hakujiuliza sana zaidi zaidi alienda kujiandaa na kuondoka zake kwenda Ibadani, baada ya muda mfupi tu pale nyumbani alifika Junior, kumbe Vaileth alikuwa akimbembeleza mama Angel aende Ibadani ili yeye apate muda mzuri wa kuwa na Junior, basi Junior akaanza nae,“Unajua nilivyopokea simu yako usiku nikajua ni wazi umenimiss sana, hadi kutaka nije?”“Yani sijui nisemeje, kila muda toka jana nakuwaza tu. Nimejitahidi kujizuia wapi jamani! Nakuhitaji Junior, yani leo najikuta nakuhitaji sana”Basi moja kwa moja Junior na Vaileth walienda chumbani kufanya mambo yao, na walikaa huko hadi ule muda walipoona ni karibia na walioenda kwenye Ibada wanarudi.“Dah! Ila Vai natamani kama leo ningelala hapahapa ila siwezi sababu sitaki mama mdogo agundue chochote kati yetu”“Hata mimi sitaki agundue ila nimeridhika sasa, kwakweli nilikuwa na hali mbaya sana, nilitamani uje jana ila Erica cha umbea ndio tulikuwa nae hapa nyumbani, nikaona yule atasema tu. Anaweza asiseme yote ila la wewe kuja akasema tu”Basi Junior akajiandaa na kula kabisa kisha kuondoka zake kurudi shuleni kwao.Erick na Erica wakiwa wanarudi huku wameambatana na mama yao, na dereva muda huo alikuwa ni Erick, basi njiani walimuona Derrick akiwa amezingirwa na watu halafu kama kuna mabishano vile, basi Erica akamwambia mama yao,“Mama, sio anko Derrick yule?”Mama Angel alimuangalia vizuri na kujithibitisha kuwa ni yeye,“Ndio ni yeye, sijui kakumbwa na nini?”“Itakuwa watu wanaomdai wale”“Mmmmh!!”“Kwanini tusiende kumsaidia?”Erick akasema,“Kheee Erica hukumbuki kama ndio huyu alifanya tutukanwe sana pale kwenye kituo cha mafuta sababu alikomba hela zote!”Mama Angel nae akasema,“Jamani eeeh ingawa tumetoka kusali ila kwa Derrick hapana jamani, yani pale hata haijulikani ni kweli au ndio njia ya utapeli. Huyu mjomba wenu, sikuwaambia sijui, alinikuta getini siku hiyo na kuniomba shilingi mia ili akwangulie vocha, niliona jambo la kawaida tu, ila kufumba na kufumbua hela zote nilizochukua zilikuwa zimeisha. Erick naona umepunguza mwendo, hebu endesha turudi nyumbani, hivi Derrick mnamfahamu vizuri au mnamsikia tu.”Erick aliongeza mwendo na moja kwa moja kwenda nyumbani tu, na walimkuta Vaileth ndio kwanza kaanza kupika chakula alichoambiwa aandae, yani yeye alipika chakula cha upesi cha kula Junior tu, halafu kile alichoambiwa aandae muda huo ndio alikuwa anakiandaa, basi mama Angel alimkuta ndio anaandaa,“Kheee wewe Vaileth, muda wote ulikuwa unafanya nini?”“Mtoto mama, leo Ester kasumbua kweli”“Nimekuelewa, haya Erica kamsaidie basi”Vaileth alipumua kwani alijua Erica akienda kumsaidia ndio atapumzika kabisa ukizingatia Erica alipenda sana kupika.Baada ya muda chakula kilikuwa tayari na walikaa kwaajili ya kula huku wakiongea mambo mbalimbali na ule utamu wa kile chakula.“Oooh mwanangu Erica, kila siku unazidi kunifurahisha juu ya upishi wako, hakika wewe ni mwanamke kamili”Basi Vaileth akaongea leo,“Ni kweli Erica yupo vizuri sana, ila unaweza kushangaa anaolewa halafu mumewe anaenda kuhangaika na wanawake wengine wakati mkewe wanajua kupika hivi”Mama Angel alimuuliza Vaileth,“Unamaana gani Vai?”Maana yeye alihisi anasemwa yeye na mume wake, basi Vaileth aliamua kumuomba msamaha tu.Jioni ya siku hiyo wakati mama Angel katulia zake, alipokea simu kutoka kwa dada yake Mage, basi dada yake alianza kumwambia,“Ni hivi nasikia Derrick kapigwa na kuumizwa vibaya sana, kwahiyo yupo hospitali kwasasa”“Kheee, mambo hayo yametokea wapi?”Mage alimtajia na kumfanya mama Angel kushangaa zaidi kwani kumbe pale walipomuona Derrick kazingirwa ndio hapo ambapo alikuwa anapigwa, kwahiyo alishangaa sana, basi alimuuliza tu dada yake mahali ambapo Derrick amelazwa basi maana ile ilikuwa ni habari mbaya kidogo ukiacha yale matendo ya Derrick ya siku zote.Muda huu mama Angel alimua tu kulala kwani hakutaka kichwa chake kuendelea kufikiria mambo kama hayo ya kumkosesha usingizi tu.Kulipokucha tu, mama Angel alijiandaa na kwenda hospitali kwanza kumuona Derrick kwani hata akikataa bado ni ndugu yake wa damu.Alifika hospitali, alimkuta pale mama mzazi wa Derrick ambaye alifurahi kumuona mama Angel,“Siamini Erica umekuja kumuona kaka yako!”“Ndio nimekuja mama, yani huyu ni kaka yangu haijalishi ni kipi kimewahi kupita kati yetu ila bado ni kaka yangu”“Nafurahi kuona ulimsamehe, ila ana hali mbaya sana”Basi mama Angel alisogea kumuangalia na kweli Derrick alikuwa na hali mbaya sana, yani alionekana kupigwa sana, basi alikaa pale na mama Derrick huku wakiongea,“Ila Derrick atapona tu”“Natumaini atapona, jana nilikuwepo hapa na yule dada yenu mkubwa Mage. Kwakweli huyu amekuwa ni msaada mkubwa sana kwangu, toka Derrick akiwa mdogo hadi leo, mshikilieni sana huyu dada yenu. Ameondoka usiku sana jana, tulikubaliana leo ataleta chakula cha mchana”“Oooh sawa, basi na mimi nitajitahidi nije tena jioni ule muda wa kuangalia wagonjwa”Basi wakaongea pale, na muda wa kuangalia wagonjwa uliisha kwahiyo walitoka nje ambapo mama Derrick hakutaka hata kuondoka zaidi ya kumsindikiza kidogo tu mama Angel,“Basi jioni mama nitakuja kumuona”“Sawa hakuna tatizo, Mungu amsaidie mwanangu apone jamani”“Atapona tu, Mungu ni mwaminifu”Kisha mama Angel alipanda kwenye gari akielekea kiwandani kwani ndio alikuwa na lengo hilo kwanza kwa muda huo, ingawa mumewe hakujua kama mkewe kaanza ratiba za kwenda kufatilia kiwanda ila mama Angel aliamua kufanya hivi kwaajili ya usalama wa mali zao na kiwanda chao, alijua angemwambia mumewe asingekubali ukizingatia mtoto wao bado ni mdogo.Moja kwa moja mama Angel alienda kiwandani na kukuta walifika na kuanza kufanya kazi, kwahiyo ule msisitizo wa siku ile inaonyesha uliwafanya sasa kuzingatia muda wa kwenda kazini na kufanya kazi kwa ufasaha zaidi, basi alimuita yule kiongozi wa pale na kuongea nae,“Yuda, kama kuna kitu chochote kinatakiwa au kuna mapungufu yoyote tafadhari kwasasa muwe mnaniambia mimi”“Sawa mama”“Ile Jumamosi nilifanya mahesabu na Erick, na alinielekeza mambo mbalimbali. Sasa nahitaji kufanya mahesabu na wewe pia, usinione hivi ni mwanamke ila mahesabu kichwani kwangu yapi vizuri sana”Mama Angel alikuwa akimwambia hivi ili kama kumpa tahadhari kwanza kuwa mahesabu anatakayomfanyia yawe halisia maana hata yeye anaelewa mahesabu yalivyo, basi Yuda alienda na mama Angel ofisini na kuanza kuonyeshana na kumuelekeza mahesabu, alimfanyia mahesabu yote kisha mama Angel alimuuliza,“Kuna laki mbili hapa imepelea na kuna laki tatu inazunguka tu, hizi hela ni vipi?”“Aaaah mama, hiyo laki tatu ndio ile ambayo Erick aliondoka nayo siku ile”“Haya, na hii laki mbili?”“Aaaah hii aaah hebu subiri kidogo mama”Yuda aliondoka na kwenda kuongea na baadhi ya wafanyakazi, kwahiyo mama Angel alikaa pale akisubiri majibu.Basi Yuda aliita pale wafanyakazi kama watatu wa pale kiwandani na kuanza kuongea nao,“Jamani huyu mama ni hatari, hafai kabisa bora hata bosi Erick arudi, huyu mama ni nuksi kushinda hata mtoto wake. Unajua kagundua kuhusu ile laki mbili!! Huwezi amini kaanza na mimi mahesabu ya tangia tumeanza kiwanda”“Duh!! Ndiomana mmetumia muda mrefu sana?”“Ndio, hata cha mchana sijala sababu ya kuelekezana nae jamani, yani mama anauliza hadi mia imeenda wapi, haka kamama sijui kabila gani jamani! Mtu ana hela lakini hela ndogo ndogo anataka kuzichunguza hadi basi. Tujipange sasa, hiyo laki mbili tuseme nini?”“Halafu tutaipata wapi tena?”“Mshahara ukitoka mwisho wa mwezi huu, tuchangishane tuilipe hiyo hela ya watu ila saivi niambieni cha kusema ili iwe rahisi kumtuliza”“Sikia Yuda, mwambie kuwa kuna sehemu tuliagiza mzigo ila wamezingua na wamesema wataturudishia hela. Mdanganye kuwa tulisikia wanauza kwa bei nzuri ndiomana tukaagiza”“Mmmh akiniuliza wapi itakuwaje?”“Mmmh tafuta maneno na wewe, weka hata uongo hapo. Mwambie tushaandikishiana mwisho wa mwezi huu hela hiyo inalipwa”“Sijui kama atanielewa jamani dah! Mama ni mtata huyu hatari”Basi Yuda akaenda kuongea nae kama alivyokubaliana na wenzie,“Haya hayo maandishi kuwa mnalipana mwisho wa mwezi huu yakowapi?”“Oooh nimesahau nyumbani mama ila kesho nitakuja nayo”Mama Angel alisikitika kidogo, kisha alimsisitiza kuwa kesho yake angehitaji kuyaona hayo maandishi, kisha mama Angel alizunguka kiwandani pale na alipomaliza aliondoka zake na kupata wazo kuwa aende kwanza kutembelea na lile duka lao maana hakujua chochote kinachoendelea ukizingatia Erick aliongea nae juu juu tu.Basi alienda katika lile duka na kumkuta Rama, ambapo naye alimuuliza mahesabu ya pale kisha Rama alianza kumuonyesha na kumuelekeza ilivyo, mama Angel kuja kushtukia ni usiku ushaingia, hakwenda hospitali wala nini na alikuwa amechoka sana, hata kula chakula alikuwa hajala, basi kwa muda huo moja kwa moja alirudi nyumbani kwake tu.Kwakweli siku hii mama Angel alichoka sana, hakushinda na mwanae, alishinda kwenye biashara tu, basi alienda kuoga na kula chakula, kisha muda huo Erick alienda kuongea na mama yao,“Mama, ulienda kiwandani leo?”“Ndio nilienda mwanangu, nimechokaje jamani maana nilikuwa nafanya mahesabu na yule Yuda”“Uligundua upotevu wa laki mbili?”“Kheee kumbe na wewe ulijua? Mbona hukusema sasa?”“Sikusema ndio ila niligundua muda tu, tatizo wale huwa wananiona mimi mtoto sana ndiomana sikuwauliza”“Ila mwanangu unatakiwa ujiamini maana ile ni mali ya baba yenu, mkishindwa kuisimamia ni nani ambaye angeisimamia?”“Ndiomaana zile laki tatu niliamua kuondoka nazo mama”“Nimekuelewa mwanangu, ila unatakiwa kutetea mali ya baba yako kwa nguvu zako zote, watapoteza laki mbili, kesho milioni, kesho kutwa mtaji mzima na kiwanda kitafungwa, inatakiwa kuwa makini sana”“Sawa mama”Basi mama Angel alifurahi kwa kuona kuwa mwanae ana akili sana, muda huu aliinuka na kwenda chumbani huko aliamua kumpigia simu Tumaini ili kumpa taarifa kuhusu kuumwa kwa Derrick,“Jamani, nini kimempata tena?”“Nasikia kapigwa sana, kuna watu kakutana nao wamempiga sana”“Au aliwafanyia kama alivyonifanyia mimi?”“Mmmh sijui ila kapigwa sana na kwasasa yupo hoi hospitali”“Dah! Itabidi kesho nijitahidi niende kumuona”“Hata mimi kesho nitaenda tena, ila ndio hivyo Derrick hana hali nzuri kabisa”Tumaini alishukuru kwa taarifa, na kwa muda huo mama Angel aliamua tu kulala kwani alikuwa amechoka kwa kiasi Fulani.Kulipokucha tu, mama Angel alipokea simu kutoka kwa dada yake Mage,“Ila Erica una tabia mbaya wewe, jana jioni umeahidi kwenda kumuona mgonjwa ila hujaenda”“Ni majukumu dada yalinibana”“Basi jitahidi leo, na jitahidi umuandalie mgonjwa chakula atakachokula usiku, muandalie tu mtori au chakula chochote kilaini”“Sawa dada nimekuelewa”Mama Angel alikata ile simu, ila kiukweli leo alikuwa amechoka na alitaka kutumia muda kidogo kuwa na mtoto wake kwahiyo aliona ni vyema asienda kiwandani kwa siku hii, anajua tu kule sababu hawajui lazima wajishughulishe kwani watahisi muda wowote ule ataenda.Basi akaona ni vyema kwenda kutafuta vya kupika kwaajili ya kumpelekea mgonjwa jioni hospitali.Kwenye mida ya saa tatu asubuhi, mama Angel aliondoka nyumbani kwake na kwenda sokoni, alipomaliza tu kununua mahitaji yake akakutana na Sia,“Kheee kumbe na wewe huwa unakuja sokoni!”“Jamani, kwani mimi nina nini cha kufanya nisije sokoni?”“Aaah nimekuuliza tu, vipi mume amesharudi?”“Bado”“Huna wasiwasi? Unaibiwa huko, shauri yako nakwambia, wanaume wenyewe hata hawaaminiki hawa haswaa kwa mwanaume kama Erick unamuamini vipi? Yani kama hujaletewa binti mwenye mimba nyumbani kwako sijui”“Nitolee balaa mie”Mama Angel aliondoka zake na moja kwa moja kuelekea nyumbani kwake.Muda huu Tumaini alikuwa anatoka nyumbani kwake, ila alifika mgeni pale nyumbani na mgeni huyo alikuwa ni mama Sarah,“Kheee mama Sarah, karibu ila mimi nilikuwa natoka”“Jamani, nilikuwa nina maongezi na wewe. Unaenda wapi kwani?”“Mmmh kuna kijana nilisoma nae, sasa nasikia kapigwa sana na amelazwa hospitali, ndio naenda kumuona, yani nasikia yupo kwenye hali mbaya sana”“Kheee, basi twende wote”“Hakuna tatizo”Basi Tumaini aliondoka na mama Sarah na moja kwa moja walienda hospitali huko, kisha walienda kwenye wodi aliyolazwa Derrick, hadi pale kitandani ilikuwa ni wodi ya mgonjwa mmoja mmoja, kwahiyo kwa muda huo alikuwepo Derrick na mama yake ambaye naye alifika kumuona mwanae, basi wakafika na kumpa pole ila mama Sarah alishtuka kidogo na kuuliza,“Jamani huyu sio Derrick huyu!!”“Ndio mwenyewe, kumbe unamfahamu?”Mara mama Angel nae alifika pale kumuona mgonjwa, ila mama Sarah alishtuka na kumuangalia mama Angel kisha akamuuliza,“Erica!! Inamaana unamfahamu huyu Derrick?”“Ndio, ni kaka yangu wa damu” Mara mama Angel nae alifika pale kumuona mgonjwa, ila mama Sarah alishtuka na kumuangalia mama Angel kisha akamuuliza,“Erica!! Inamaana unamfahamu huyu Derrick?”“Ndio, ni kaka yangu wa damu”Mara mama Sarah akaonekana kama mtu aliye na kizunguzungu na kutaka kama kuanguka ni Tumaini ndio alimdaka kwa haraka.Wote walimshangaa kuwa ana matatizo gani, mama Angel alimshika mkono na kutoka naye nje akamuuliza,“Tatizo nini Manka?”Mama Sarah alipumua kisha akasema,“Acha tu kama ilivyo, utamwambia mama Leah nimeondoka. Kwaheri”Kisha mama Sarah aliondoka zake, kwakweli mama Angel alimshangaa sana na kurudi wodini ambapo Tumaini alimuuliza vizuri,“Kwani imekuwaje?”“hata sijui, kaniaga tu na kuondoka”Mama Derrick akasema kuwa,“Au na yeye katapeliwa na mwanangu jamani, yani huyu Derrick dah!!”“Usiwaze hayo mama, kwasasa tusifikirie utapeli wa Derrick ila tufikirie namna ya kupona kwa Derrick.”Waliongea kidogo pale kisha waliaga ambapo walipotoka nje, Tumaini alimuuliza mama Angel,“Inamaana Derrick ni tapeli!! Inamaana siku ile alinitapeli eeeh! Ndiomana nilihisi hivyo”“Ni kweli ni tapeli ila nadhani anatumia dawa maana sio hali ya kawaida, utashangaa anakuazima tu hela ndogo na ukimpatia utakuta amekomba hela zote za kwenye mkoba wako”“Aaaah kumbe, halafu kitu kingine hebu tuongee kikubwa, yule shoga yule yani mama Sarah nakumbuka aliwahi kuniambia kuwa anafahamiana na wewe, sema namba yake ndio akaichukua Derrick. Ila leo nimeshangaa sijui mlishaonana? Halafu kuna nini kinaendelea kati yake na Derrick?”“Mmmh hata sijui”“Hajakwambia chochote kwani ulivyotoka nae nje?”“Si nilikwambia pale, hakuna alichoniambia zaidi ya kuniaga tu”“Oooh nilijua unanificha sababu ya mama yake Derrick pale, au Derrick ndio baba mzazi wa Sarah?”“Mmmh! Kwani unamfahamu vizuri yule mwanamke?”“Namfahamu kiasi tu sio kivile, ila huwa haongei habari za kuwa na mume wala baba yake Sarah, ndiomana nimehisi hivi, labda hakutegemea kukutana nae, hebu fatilia usikute Sarah ni shangazi yako!!”Halafu Tumaini akaagana na mama Angel ambapo muda huu mama Angel moja kwa moja aliondoka na kurudi nyumbani kwake, na yeye alikuwa akijiuliza tu bila ya kupata jibu.Mama Angel aliwakuta wanae muda huu wanakula, basi na yeye alienda kujimwagia na kujumuika nao, kisha akawaambia hali ya mgonjwa,“Jamani wanangu sikuwaambia ni hivi, mjomba wenu Derrick kalazwa, hospitali kumbe siku ile tulipomuona akapatwa majanga pale, nasikia walimpiga sana. Nimetoka kumuona leo hospitali anaendelea vizuri”“Oooh masikini jamani, ndiomana nilikuwa nasema tukamsaidie ila wewe mama na Erick mlikataa na kusema kuwa tusimsaidie atatutapeli, niliona yale mazingira sio rafiki kwake. Ila bora anaendelea vizuri, Mungu amsaidie apone”“Mmmh leo Erica naona una huruma sana”“Ndio mama, yule ni mjomba wetu, lazima niwe na huruma naye”Muda huu Erick hakuongea jambo lolote lile, walimaliza kula na kila mmoja alienda chumbani kwake, ila Erica moja kwa moja alienda chumbani kwa Erick na kuanza kuongea nae,“Mbona hujasema chochote kuhusu mjomba kulazwa”“Sasa ulitaka niseme nini jamani!”“Hata utoe pole kwa mama , kwani yule ni kaka yake mama”“Ila katutapeli laki tatu”“Kumbuka kuna watu kawatapeli hela nyingi kuliko hizo, ila kapatwa na matatizo unatakiwa kuwa na huruma naye”“Mimi sina huruma naye labda mpaka atakapoacha utapeli wake”“Mmmh wewe nawe, halafu ngoja nikuulize, hivi siku ile alivyokuja Sarah na mama yake ulimuelewa mama yake Sarah na mama?”“Sikuwaelewa ila inaonyesha kuwa ni watu wanaofahamiana ndiomana mama anasema kuwa Sarah ni ndugu yetu”“Ila habari ya Sarah kuwa ndugu yetu nimeipenda sana”“Kwanini?”“Sababu ataacha kukusumbua wewe, toka lini ndugu wakawa wapenzi? Hakuna mila za kihivyo, mimi sitaki Sarah awe mpenzi wako, kwahiyo kama ni ndugu yetu ni afadhali sana yani”Erick alikaa kimya tu, kisha Erica alimuuliza,“Kwani hujapenda kwa Sarah kuwa ndugu yetu?”“Vyote kwangu sawa tu, awe ni ndugu yetu, au asiwe ndugu yetu ila bado mimi siwezi kuwa na mahusiano naye”“Kwahiyo utakuwa na mahusiano na nani? Au utamkubali Samia?”“Hakuna, kwani umesahau kiapo chetu Erica hadi unaniuliza maswali kama hayo? Leo nimechoka halafu nina usingizi sana, muda sio mrefu nalala”Erica ilibidi amuage kaka yake na kuondoka zake kuelekea chumbani kwake kulala.Mama Angel alijikuta akiwaza kuhusu mama Sarah, alijiuliza maswali mengi sana bila ya majibu,“Kwanini ashtuke vile na kutaka kuzimia? Je Derrick ni nani katika maisha yake au alikuwa na mahusiano na Derrick? Je Sarah ni mtoto wa nani? Wa mzee Jimmy, wa Erick au Derrick? Ila hawezi kuwa wa Erick bhana, hilo nakataa maana angeniambia mapema tu. Ila ni wa nani? Au ndio mtoto ambaye Derrick huwa anamsema? Sielewi jamani, kuna nini kati ya Manka na Derrick, au kipindi anampenda sana Erick akakutana na Derrick akamdanganya kama alivyonidanganya mimi? Mmmmh!!”Mama Angel aliwaza sana bila hata ya jibu lolote na kuamua kulala, ila alishtuliwa na simu kutoka kwa mume wake na kuamua kupokea ile simu,“Kumbe Derrick kalazwa? Ndio Tumaini kanipigia simu kuniambia leo, mke wangu umeshindwa kuniambia kweli?”“Nisamehe mume wangu jamani, sijui hata nimeghafilika vipi ila ndio hivyo kalazwa”“Una mawazo gani Erica? Sio hali ya kawaida, kwanza jana kutwa nzima hatujawasiliana na leo nisingekutafuta basi inamaana ingepita bila ya sisi kuwasiliana, tatizo ni nini mke wangu?”“Hakuna tatizo”“Nimekwambia kuwa habari za wakina Manka, sijui wakina nani zisikupe presha mke wangu, yote nikirudi tutazungumza kwakina, nakuomba usiwe na mawazo kwasababu hiyo”“Sina mawazo yoyote hata usijali kuhusu mimi mume wangu”Basi wakaongea mengi kwa usiku ule, kisha kuagana na mama Angel kuamua kulala sasa kwa uzuri zaidi.Leo Erick alivyoenda shuleni tu alifatwa na Sarah ambaye alianza kuongea nae,“Erick, mbona unaonekana kunikwepa sana?”“Sikukwepi, ila Sarah hivi unajua kama sisi ni ndugu?”“Hilo nishalikataa kabisa, siwezi kuwa na undugu na wewe Erick, ninachojua ni kimoja tu kuwa nakupenda sana”“Duh!”Muda wa kipindi ulianza kwahiyo ikabidi Sarah aende darasani, kwahiyo Erick alibaki huku akishangaa tu maana hakumuelewa Sarah kwakweli.Basi waliendelea na masomo kama kawaida, ila siku hiyo mchana Erick alifatwa darasani kuwa anaitwa halafu alitoka na moja kwa moja kwenda ofisini kwa walimu na kukuta ni Sia yuko pale ambapo Sia aliwaomba walimu nafasi kidogo aweze kuzungumza na Erick maana alijitambulisha yeye kama mama mdogo wa Erick, kwanza kabisa Erick aliulizwa,“Je unamfahamu huyu? Ni mamako mdogo?”Erick aliitikia tu maana angekataa basi siku hii angemfanya Sia aumbuke sana, basi akatoka nae nje na kwenda kuzungumza nae,“Kwanza kabisa asante Erick, nilijua utanikana”“Hapana, nazijua akili zako ndiomana nimekubali, ushindwi kuangua kilio ofisini”Leo Sia alicheka kiasi na kumwambia Erick,“Kilichonileta hapa ni kitu kimoja, nimeona bora nije shule nikwambie hili, ni hivi nasikia kuna mwanaume anaitwa Juma anapenda sana kukufatilia. Tafadhari Erick kaa mbali na mtu huyu maana si mtu mzuri kwako”“Kivipi?”“Ipo siku nitakaa na wewe na kuongea nawe vizuri zaidi ila yule mtu si mtu mzuri kwako”“Kwahiyo kwasasa hujaja na hoja kusema kuwa wewe ni mama yangu?”“Siku zote uongo hujitenga na ukweli, na kitu kama ni ukweli basis i kulazimisha maana kuna kipindi kitajidhihirisha chenyewe. Kuna upendo ambao watu wanaita ni upendo wa asili, je huna upendo huo juu yangu? Kama unao basi mimi ni mama yako, ila kama huna huo upendo juu yangu basi mimi si mama yako, ila hata kama mimi si mama yako bado ninajukumu la kukulinda na kukutunza, nakuomba uwe mbali kabisa na Juma. Sikujua mapema kuwa anakufatilia ila sasa imejua”“Umejuaje?”“Yule Juma ana mke wake, na yule mke wake ni rafiki yangu mkubwa na ni rafiki wa mama yako pia. Nimejikuta nikimpenda na kuongea nae mambo mengi sana, kwahiyo kuwa makini sana na Juma, jiepushe nae na ikiwezekana ukimuona mkimbie kabisa. Yangu ni hayo tu, sina mengine wala sina la ziada, kwaheri”Sia alienda ofisini na kuwashukuru walimu kwa kumruhusu kuongea na Erick halafu aliondoka zake, kwakweli Erick alikuwa akishangaa tu kwanza alishangaa jinsi huyu Sia alivyoongea kiustaarabu siku ya leo, basi alikuwa akienda darasani huku akisema,“Ingawa kaongea na mimi kiustaarabu ila hiki kimama sikipendi jamani, yani sikipendi kabisa”Akaenda zake darasani na kuendelea na masomo yake kama kawaida.Mama Angel akiwa kiwandani leo, bado alitaka maelezo ya ile laki mbili, basi Yuda aliileta ile laki mbili na kumkabidhi huku akisema kuwa yule mtu amemlipa, haikuwa kweli ila Yuda alikopa ile hela mahali ili aweze kumlipa huyu mama na kuepuka lawama,“Oooh kumbe wameleta, basin i vizuri kumbe ni waaminifu”“Halafu Erick mtoto atakuja lini tena kiwandani?”“Atakuja tu ila mwanangu nimeona bora akazanie masomo kwanza kwani ndio ya muhimu kuliko vitu vyote”“Unaonekana unapenda shule eeeh!”“Ndio napenda sana, napenda watoto wangu wawe wasomi wa kimataifa”Waliendelea kufanya kazi huku mama Angel akipita kukagua kagua eneo lake, muda kidogo wakati anajiandaa kutoka, mule ofisini alifika mgeni na mgeni huyo alikuwa ni Juma kwani alijua kuwa siku hiyo angemkuta humo ofisini, ila alimkuta mama Angel, ikabidi tu akae na kuanza kuzungumza nae,“Halafu sikutegemea kama ningekukuta wewe”“Ndio umenikuta sasa, karibu”“Asante, ila si una mtoto mdogo wewe huoni kama ukija huku unamkosesha mtoto haki yake?”“Yani uzuri ni kuwa mtoto wangu amezoea kila kitu, kwahiyo anakunywa maziwa analala, na sio msumbufu hadi wakati narudi”“Hata kama ila mtoto anahitaji jasho la mama kwa ukaribu sana”“Aaaah hayo mambo ilikuwa zamani, ila kwasasa wanawake tumeamka”“Sawa, sikupingi. Yuko wapi Erick?”“Yupo shule, unadhani atakuwa wapi?”“Yani alikopigwa hadi akazimia bado umemrudisha tena! Nina mashaka na wewe, ni mzazi wa aina gani usiye na huruma na mtoto wako?”“Sikuelewi”“Hivi umeshindwa kufikiria kweli, ni bora hata ungemuahamisha shule, kuliko kumrudisha shule hiyo hiyo. Hata hivyo hiki sio kilichonileta”“Haya sema kilichokuleta”“Ni hivi, nilipanga na Erick kuwa Jumamosi ningekuja kumchukua ili twende mahali ila nilishindwa, basi namuomba Jumamosi hii, tena ni vizuri nimekukuta na wewe mama yake, naomba ruhusa kwako”“Haiwezekani, siwezi kumrudusu mwanangu kwenda sehemu nisiyoijua”“Kumbe tatizo ni wewe kutokupajua tu!! Basi naomba twende wote siku hiyo, tafadhari nakuomba. Natumaini utatendea kazi ombi langu, kwaheri”Juma aliinuka na kuondoka yani hakutaka hata kusikia jibu la mama Angel kama kakubali au kakataa ila yeye alihakikisha tu kuwa ameshamwambia na kama anataka na yeye aongozane nao.Mama Angel alirudi nyumbani kwake muda huu akiwa amejichokea kiasi Fulani, baada ya kuoga na kula alienda kuongea na Erick kuhusu Juma,“Nakuomba mwanangu jambo moja, najua nilikwambia ila narudia tena naomba mwanangu usiwe karibu na Juma, hata akufate wapi mkwepe, naona sio mtu mzuri kweko”“Halafu leo mama, alikuja yule mwanamke nisiyempendaga shuleni”“Nani huyo? Sia?”“Ndio huyo huyo”Mama Angel akachukia hapo na kuuliza kwa makini kuwa ni kitu gani Sia alimwambia mtoto wake, ila Erick alimwambia vile ambavyo alizungumza na Sia mpaka mama Angel alishangaa na kusema,“Yani Sia ndio kaja kukwambia hayo maneno! Huo urafiki wa Sia na mke wa Juma umeanza lini hadi waambiane kila kitu jamani! Mmmmh unajua mtu unaweza kuzungukwa hapa hapa bila hata kujijua wala kutambua kuwa ni kitu gani kinachokusumbua kumbe ni mtu wako wa karibu. Haya mwanangu hata kama huwa unamchukia ila hilo alilokwambia ni bora zaidi, tafadhali kaa mbali na Juma”Kisha akamuaga mwanae na moja kwa moja kwenda chumbani kwake, na huko alimpigia simu mumewe na kumwambia tu habari za Juma, ila hakumwambia kuwa alienda kiwandani kwani hakutaka mumewe ajue kuwa huwa anaenda kiwandani,Huyu Juma ana wazimu eeeh! Kwahiyo alikuja tena hapo nyumbani?”“Ndio alikuja”“Sijui kaingiliwa na nini jamani na huyo Juma, anaacha kufatilia watoto wake anakazana kufatilia watoto wa wenzake”“Tuachane na hayo, jamani mume wangu unarudi lini? Nimekukumbuka sana ujue”“Nitarudi tu mke wangu usijali ila siku ya kurudi sitakwambia maana nataka nikushtukize tu”“Ushaniambia tayari maana mshtukizo hata mtu haambiwi kabisa, huwa inatokea tu”Baba Angel akacheka, na kuongea zaidi kidogo na mke wake kisha waliagana na kulala huku mama Angel anawaza kukikucha tu aende kwanza kiwandani maana alitakuwa kwasasa anataka kujua kila kitu.Basi kulivyokucha, alijiandaa kwaajili ya kutoka ila muda ule ule alifika mama Junior, na kumfanya mama Angel ashangae maana ni asubuhi sana, basi alienda kukaa nae kwenye sebule yao nyingine na kuongea nae maana pale ndio kwanza Vaileth alikuwa akifanya usafi,“Kheee dada mbona asubuhi asubuhi?”“kwani na wewe hii asubuhi yote unaenda wapi?”“Naenda kazini dada”“Kivipi? Hebu nieleweshe vizuri”Mama Angel alimwambia kuwa huwa anaenda kiwandani kuangalia jinsi kiwanda kinavyofanya kazi, na kufatilia wafanyakazi wa pale, na hata alimuelezea toka kaanza kufatilia ni makosa mangapi kayagundua,“Ni vizuri sana sio vibaya ila huwa unaondoka muda gani na kurudi muda gani?”“Asubuhi halafu narudi jioni”“Aaaah Erica hebu wacha ujinga, una mtoto mdogo wewe ujue!! Sikia, unachofanya sio kibaya ila panga muda wako vizuri uwe unawahi kurudi kumnyonyesha mtoto na kukaa nae karibu, jamani unafanya kama wale wanawake ambao hawana waume kwahiyo wanapambana wenyewe ili watoto wale, ndio huwa wanafanya kazi muda wote hata muda wa kulea watoto haupo, unadhani Erick akisikia hili atafurahi? Hawezi kufurahi hata kidogo, amehangaika, ameteseka ili mke wake na watoto mtulie, amehitaji mtoto ili utulie nyumbani kulea mtoto ila wewe ndio kama biashara umeanza leo jamani Erica eeeh! Usiwe hivyo jamani mdogo wangu”“Haya nimekuelewa, asubuhi yote hii ya nini?”“Jana bhana, kuna binti kaja kunililia usiku mwenzangu ana mimba ya Junior”Mama Angel alishtuka sana na kumuangalia dada yake,“Kheee sasa umeamua nini?”“Niamue nini zaidi ya kumshauri akatoe”“Hapana dada usifanye hivyo, unajua kutoa mimba ni sawa na dhambi ya kuua tu. Muache azae mtoto wake”“Unakumbuka kipindi chako nini?”“Nakumbuka ndio, muacheni azae, wala hata usimtoe hiyo mimba. Kwanza wewe mwenyewe una kitoto kimoja tu halafu ndio uanze kutoa mimba za wakwe zako kweli? Muache azae tu”“Haya, ila kuna mengine”“Yapi hayo?”“Kuhusu shemeji yako jamani, si kuna kimwanamke alikipata huko sijui wapi ndio kikawa kinamsumbua akili, hadi nilikuja siku ile ili nikueleze dukuduku langu, ila sasa akili ikacheza, siku hiyo kachelewa kurudi nikamuanzishia kilio kama cha msiba, yani nilikumbuka msiba wa baba kabisa, kwani amerudia tena kuwasiliana na yule mwanamke mbele yangu! Kwani kachelewa tena kurudi!!”“Mmmh dada, kwa kilio tu au kuna mengine ulimfanyia?”“Ukiona mumeo anakusumbua niambie nikueleze, ila ndio hivyo Deo saibvi katulia ila sitaki tena kukaa nyumbani, nataka kuanza kazi kwakweli nimechoka kukaa nyumbani, kwahiyo natafuta kazi”“Hilo la kutafuta kazi ni wazo zuri dada, tena kuna rafiki yake baba Angel nitakuunganisha nae, hukusema tu mapema ila kwasasa usijali mambo ni moto. Ila bado hujaniambia mbona umekuja asubuhi sana?”“Nilijua sitokukuta, maana mara nyingi tu napoiga simu naambiwa kuwa umeondoka”“Huwa unapiga ya mezani wewe, ila hata hivyo Derrick kalazwa, sijui umepata habari au dada Mage alisahau kukwambia?”Mama Junior alishangaa kidogo, na kusema kuwa siku hiyo itabidi waende wote kumuona Derrick maana hata wafanyeje bado ni ndugu yao tu.Tumaini akiwa anaelekea katika shughuli zake, akakutana njiani na Dora na kuanza kuongea nae na kumpa taarifa kuhusu kulazwa kwa Derrick,“Jamani masikini, kafanyaje tena?”“Kumbe hujui? Derrick alikuwa ni tapeli ila dada yake yani Erica alikuwa akimfichia siri”“Ila unajua kuna kitu huwa sielewi”“Kitu gani?”“Ni kuhusu Derrick na Erica, kwahiyo wale ni ndugu kabisa?”“Ndio ndugu, baba mmoja wale”“Unajua nini?”“Nini?”“Kipindi tupo chuo, kuna kipindi Fulani Erica alikuwa anatembea na Derrick, si unajua Erica alikuwa ni rafiki yangu sana ila tukaja kugombana badae kwa mambo madogo tu, basi Erica alikuwa anatembea na Derrick”“Mmmh kwahiyo alikuwa ni mpenzi wake kabisa?”“Ndio, alikuwa nae sasa nashangaa kusikia kuwa ni ndugu”“Ila Erica anaonekana kuwa mpole sana, sidhani kama alitembea nae”“Weeee ana upole gani yule! Niulize mimi listi ya wanaume aliotembea nao, ninaowajua tu ni wengi hatari, kuna kijamaa kilikuwa kinaitwa Babuu katembea nacho, kilikuwa kimasikini hatari ila Erica ndio alikufa alioza, mwenzio Erica katembea na George na aliachwa na George sababu hakuwa bikra”“Mmmh unajua George na Erick ni ndugu kwa upande wa mama yake Erick huko!”“Kheee basi hekaheka za Erica sio za nchi hii, kuna kipindi alijikuta kagonganisha ndugu watatu yule na wote katembea nao, huyo Derrick unayesema ni ndugu yake katembea nae, halafu kuna jamaa nadhani unamjua siku ya harusi ya Erick na Erica aliongea maneno mengi kiasi, yule jamaa anaitwa Bahati, kwasasa anaishi na Fetty basi yule Erica katembea nae, usimuone vile huwa kuna mambo namtetea tu. Ni kweli ni mpole ila kwenye swala la uhuni na yeye alikuwa muhuni”“Kumbe!! Ndiomana alipatana na wewe, nikamshangaa msichana mpole vile kuwa na urafiki na wewe! Bora hata Fetty kidogo hakuwa na makuu chuoni ila wewe mmmh nilishangaa sana”“Siku zote mwizi anatembea na mwizi mwenzie, ila kwasasa nimeokoka hayo mambo nimeacha jamani hata umbea huu sikutakiwa kukwambia, eeeh Mungu nisamehe”Tumaini alicheka sana na kumuuliza,“Ila hiyo listi ya wanaume wa Erica uliijuaje?”“Mmmh unajua mimi nina dhambi nyingi jamani, namshukuru Mungu ni mwaminifu na anasamehe, la sivyo mimi nisengesamehewa jamani. Unajua nilikuwa namuonea sana huruma Erica akilia kuhusu mapenzi halafu hivi vidume vikijidai vyenyewe kwa kuumiza moyo wa Erica, yani siku niliyogundua nimeatirika basi nilimfata mmoja baada ya mwingine na kutembea nae, yani kila aliyemuumiza Erica nami nilihakikisha namuumiza na ukimwi”“Ndiomana ukaamua kumuambukiza na baba yangu! Mwanamke mbaya wewe hata hufai”“Mmmh tuachane na habari hizo Tumaini ila baba yako ndio aliniambukiza mimi. Nisamehe kwa hilo”“Mbaya wewe na sidhani kama dhambi zote umesamehewa, hata huo ulokole wako nina mashaka nao. Kajinga kweli wewe”Dora akaona yataanza marumbano pale bure, kwahiyo akaamua kuagana na Tumaini tu ila aliahidi kuwa ataenda kumsalimia Derrick pia.Baada ya Dora kuondoka, kwakweli Tumaini alijiuliza sana,“Kumbe watu wanatoka mbali eeeh! Ndiomana Erica alipata yule mtoto wa kiarabu kumbe na yeye alikuwa na mambo sana”Basi akachukua simu yake na kumtumia mdogo wake ujumbe,“Habari Erick, nasikia Erica kabla ya kukutana na wewe alishatembea na wanaume zaidi ya watano”Muda kidogo akapokea ujumbe kwa Erick,“Hata angetembea na dunia nzima bado ningempenda tu tena sana.”Kisha akapiga simu ambapo Tumaini akapokea,“Ila dada yangu kwani una matatizo gani? Ulisikia kuwa mwanamke akiwa ametembea na wanaume wengi haolewi wapi? Si ilimradi apate anayependana nae tu”“Kheee yameisha basi, mimi nilikuwa nasema tu”“Unajua kuna muda huwa sikuelewi, unampenda Erica ila unaniambia maneno kama haya, unataka niachane nae au ni kitu gani? Dada yangu nakuomba umuheshimu mke wangu, nampenda sana na unalijua hilo, mimi Erica nampenda hata niambiwe wale watoto wote sio wangu kazaa na wanaume wengine huko bado nitampenda na watoto nitawapenda yani usijisumbue kupata habari huko na kuniambia”“Basi yameisha wala sitokwambia tena mambo kama haya”“Halafu hizo tabia za umbea sijui umezitoa wapi? Utakuwa unaongea sana na Sia wewe ndiomana, naomba usiniletee tena umbea wa kuhusu mke wangu, nampenda jinsi alivyo na huwezi jua nimempendea nini”“Nimekuelewa Erick, hata mimi nampenda Erica yani hata sijui naanzaje kukuletea umbea wa aina hii, naomba unisamehe”“Kila siku na mke wangu tunajiuliza Erica mdogo katoa wapi umbea kumbe katoa kwako, naomba usiniambie tena habari za hivi, tuwe tunaongea mambo mengine tu”“Nisamehe, nimekuelewa”Tumaini alikata simu na kupumua kiasi kisha akasema,“Kweli mapenzi ya kweli yapo, kuna muda hadi nahisi Erick karogwa jamani, si kwa kupenda huku mmmh! Ila hata mimi mume wangu ananipenda jamani, niache wivu loh!”Akaendelea na safari yake ya kwenda kwenye shughuli zake.Mama Angel alimuomba dada yake wapiti kwanza kiwandani halafu ndio waende hospitali maana hakutaka siku hiyo aipitishe bila kwenda kuangalia shughuli za kiwanda zimekwendaje.Basi walienda hadi kiwandani, kwa mara ya kwanza mama Junior aliweza kuona kile kiwanda kilivyo,“Jamani mdogo wangu, mmejitahidi sana”“Asante”Basi mama Junior alikuwa akitembelea tembelea maeneo baadhi ya kile kiwanda, kisha akatoka nje na kuanza kutembelea maeneo ya nje ya kile kiwanda, ila mara alipita mmama wa makamona kumsimamisha mama Junior kisha akamuuliza,“Wewe si mama yake na Junior?”“Ndio ni mimi”Yule mama akamnasa kibao mama Junior, ila mama Junior nae huwa hapendi kuonewa kwahiyo alimnasa pia kibao yule mama.Mara mama Angel nae alifika pale kumuona mgonjwa, ila mama Sarah alishtuka na kumuangalia mama Angel kisha akamuuliza,“Erica!! Inamaana unamfahamu huyu Derrick?”“Ndio, ni kaka yangu wa damu”Mara mama Sarah akaonekana kama mtu aliye na kizunguzungu na kutaka kama kuanguka ni Tumaini ndio alimdaka kwa haraka.Wote walimshangaa kuwa ana matatizo gani, mama Angel alimshika mkono na kutoka naye nje akamuuliza,“Tatizo nini Manka?”Mama Sarah alipumua kisha akasema,“Acha tu kama ilivyo, utamwambia mama Leah nimeondoka. Kwaheri”Kisha mama Sarah aliondoka zake, kwakweli mama Angel alimshangaa sana na kurudi wodini ambapo Tumaini alimuuliza vizuri,“Kwani imekuwaje?”“hata sijui, kaniaga tu na kuondoka”Mama Derrick akasema kuwa,“Au na yeye katapeliwa na mwanangu jamani, yani huyu Derrick dah!!”“Usiwaze hayo mama, kwasasa tusifikirie utapeli wa Derrick ila tufikirie namna ya kupona kwa Derrick.”Waliongea kidogo pale kisha waliaga ambapo walipotoka nje, Tumaini alimuuliza mama Angel,“Inamaana Derrick ni tapeli!! Inamaana siku ile alinitapeli eeeh! Ndiomana nilihisi hivyo”“Ni kweli ni tapeli ila nadhani anatumia dawa maana sio hali ya kawaida, utashangaa anakuazima tu hela ndogo na ukimpatia utakuta amekomba hela zote za kwenye mkoba wako”“Aaaah kumbe, halafu kitu kingine hebu tuongee kikubwa, yule shoga yule yani mama Sarah nakumbuka aliwahi kuniambia kuwa anafahamiana na wewe, sema namba yake ndio akaichukua Derrick. Ila leo nimeshangaa sijui mlishaonana? Halafu kuna nini kinaendelea kati yake na Derrick?”“Mmmh hata sijui”“Hajakwambia chochote kwani ulivyotoka nae nje?”“Si nilikwambia pale, hakuna alichoniambia zaidi ya kuniaga tu”“Oooh nilijua unanificha sababu ya mama yake Derrick pale, au Derrick ndio baba mzazi wa Sarah?”“Mmmh! Kwani unamfahamu vizuri yule mwanamke?”“Namfahamu kiasi tu sio kivile, ila huwa haongei habari za kuwa na mume wala baba yake Sarah, ndiomana nimehisi hivi, labda hakutegemea kukutana nae, hebu fatilia usikute Sarah ni shangazi yako!!”Halafu Tumaini akaagana na mama Angel ambapo muda huu mama Angel moja kwa moja aliondoka na kurudi nyumbani kwake, na yeye alikuwa akijiuliza tu bila ya kupata jibu.Mama Angel aliwakuta wanae muda huu wanakula, basi na yeye alienda kujimwagia na kujumuika nao, kisha akawaambia hali ya mgonjwa,“Jamani wanangu sikuwaambia ni hivi, mjomba wenu Derrick kalazwa, hospitali kumbe siku ile tulipomuona akapatwa majanga pale, nasikia walimpiga sana. Nimetoka kumuona leo hospitali anaendelea vizuri”“Oooh masikini jamani, ndiomana nilikuwa nasema tukamsaidie ila wewe mama na Erick mlikataa na kusema kuwa tusimsaidie atatutapeli, niliona yale mazingira sio rafiki kwake. Ila bora anaendelea vizuri, Mungu amsaidie apone”“Mmmh leo Erica naona una huruma sana”“Ndio mama, yule ni mjomba wetu, lazima niwe na huruma naye”Muda huu Erick hakuongea jambo lolote lile, walimaliza kula na kila mmoja alienda chumbani kwake, ila Erica moja kwa moja alienda chumbani kwa Erick na kuanza kuongea nae,“Mbona hujasema chochote kuhusu mjomba kulazwa”“Sasa ulitaka niseme nini jamani!”“Hata utoe pole kwa mama , kwani yule ni kaka yake mama”“Ila katutapeli laki tatu”“Kumbuka kuna watu kawatapeli hela nyingi kuliko hizo, ila kapatwa na matatizo unatakiwa kuwa na huruma naye”“Mimi sina huruma naye labda mpaka atakapoacha utapeli wake”“Mmmh wewe nawe, halafu ngoja nikuulize, hivi siku ile alivyokuja Sarah na mama yake ulimuelewa mama yake Sarah na mama?”“Sikuwaelewa ila inaonyesha kuwa ni watu wanaofahamiana ndiomana mama anasema kuwa Sarah ni ndugu yetu”“Ila habari ya Sarah kuwa ndugu yetu nimeipenda sana”“Kwanini?”“Sababu ataacha kukusumbua wewe, toka lini ndugu wakawa wapenzi? Hakuna mila za kihivyo, mimi sitaki Sarah awe mpenzi wako, kwahiyo kama ni ndugu yetu ni afadhali sana yani”Erick alikaa kimya tu, kisha Erica alimuuliza,“Kwani hujapenda kwa Sarah kuwa ndugu yetu?”“Vyote kwangu sawa tu, awe ni ndugu yetu, au asiwe ndugu yetu ila bado mimi siwezi kuwa na mahusiano naye”“Kwahiyo utakuwa na mahusiano na nani? Au utamkubali Samia?”“Hakuna, kwani umesahau kiapo chetu Erica hadi unaniuliza maswali kama hayo? Leo nimechoka halafu nina usingizi sana, muda sio mrefu nalala”Erica ilibidi amuage kaka yake na kuondoka zake kuelekea chumbani kwake kulala.Mama Angel alijikuta akiwaza kuhusu mama Sarah, alijiuliza maswali mengi sana bila ya majibu,“Kwanini ashtuke vile na kutaka kuzimia? Je Derrick ni nani katika maisha yake au alikuwa na mahusiano na Derrick? Je Sarah ni mtoto wa nani? Wa mzee Jimmy, wa Erick au Derrick? Ila hawezi kuwa wa Erick bhana, hilo nakataa maana angeniambia mapema tu. Ila ni wa nani? Au ndio mtoto ambaye Derrick huwa anamsema? Sielewi jamani, kuna nini kati ya Manka na Derrick, au kipindi anampenda sana Erick akakutana na Derrick akamdanganya kama alivyonidanganya mimi? Mmmmh!!”Mama Angel aliwaza sana bila hata ya jibu lolote na kuamua kulala, ila alishtuliwa na simu kutoka kwa mume wake na kuamua kupokea ile simu,“Kumbe Derrick kalazwa? Ndio Tumaini kanipigia simu kuniambia leo, mke wangu umeshindwa kuniambia kweli?”“Nisamehe mume wangu jamani, sijui hata nimeghafilika vipi ila ndio hivyo kalazwa”“Una mawazo gani Erica? Sio hali ya kawaida, kwanza jana kutwa nzima hatujawasiliana na leo nisingekutafuta basi inamaana ingepita bila ya sisi kuwasiliana, tatizo ni nini mke wangu?”“Hakuna tatizo”“Nimekwambia kuwa habari za wakina Manka, sijui wakina nani zisikupe presha mke wangu, yote nikirudi tutazungumza kwakina, nakuomba usiwe na mawazo kwasababu hiyo”“Sina mawazo yoyote hata usijali kuhusu mimi mume wangu”Basi wakaongea mengi kwa usiku ule, kisha kuagana na mama Angel kuamua kulala sasa kwa uzuri zaidi.Leo Erick alivyoenda shuleni tu alifatwa na Sarah ambaye alianza kuongea nae,“Erick, mbona unaonekana kunikwepa sana?”“Sikukwepi, ila Sarah hivi unajua kama sisi ni ndugu?”“Hilo nishalikataa kabisa, siwezi kuwa na undugu na wewe Erick, ninachojua ni kimoja tu kuwa nakupenda sana”“Duh!”Muda wa kipindi ulianza kwahiyo ikabidi Sarah aende darasani, kwahiyo Erick alibaki huku akishangaa tu maana hakumuelewa Sarah kwakweli.Basi waliendelea na masomo kama kawaida, ila siku hiyo mchana Erick alifatwa darasani kuwa anaitwa halafu alitoka na moja kwa moja kwenda ofisini kwa walimu na kukuta ni Sia yuko pale ambapo Sia aliwaomba walimu nafasi kidogo aweze kuzungumza na Erick maana alijitambulisha yeye kama mama mdogo wa Erick, kwanza kabisa Erick aliulizwa,“Je unamfahamu huyu? Ni mamako mdogo?”Erick aliitikia tu maana angekataa basi siku hii angemfanya Sia aumbuke sana, basi akatoka nae nje na kwenda kuzungumza nae,“Kwanza kabisa asante Erick, nilijua utanikana”“Hapana, nazijua akili zako ndiomana nimekubali, ushindwi kuangua kilio ofisini”Leo Sia alicheka kiasi na kumwambia Erick,“Kilichonileta hapa ni kitu kimoja, nimeona bora nije shule nikwambie hili, ni hivi nasikia kuna mwanaume anaitwa Juma anapenda sana kukufatilia. Tafadhari Erick kaa mbali na mtu huyu maana si mtu mzuri kwako”“Kivipi?”“Ipo siku nitakaa na wewe na kuongea nawe vizuri zaidi ila yule mtu si mtu mzuri kwako”“Kwahiyo kwasasa hujaja na hoja kusema kuwa wewe ni mama yangu?”“Siku zote uongo hujitenga na ukweli, na kitu kama ni ukweli basis i kulazimisha maana kuna kipindi kitajidhihirisha chenyewe. Kuna upendo ambao watu wanaita ni upendo wa asili, je huna upendo huo juu yangu? Kama unao basi mimi ni mama yako, ila kama huna huo upendo juu yangu basi mimi si mama yako, ila hata kama mimi si mama yako bado ninajukumu la kukulinda na kukutunza, nakuomba uwe mbali kabisa na Juma. Sikujua mapema kuwa anakufatilia ila sasa imejua”“Umejuaje?”“Yule Juma ana mke wake, na yule mke wake ni rafiki yangu mkubwa na ni rafiki wa mama yako pia. Nimejikuta nikimpenda na kuongea nae mambo mengi sana, kwahiyo kuwa makini sana na Juma, jiepushe nae na ikiwezekana ukimuona mkimbie kabisa. Yangu ni hayo tu, sina mengine wala sina la ziada, kwaheri”Sia alienda ofisini na kuwashukuru walimu kwa kumruhusu kuongea na Erick halafu aliondoka zake, kwakweli Erick alikuwa akishangaa tu kwanza alishangaa jinsi huyu Sia alivyoongea kiustaarabu siku ya leo, basi alikuwa akienda darasani huku akisema,“Ingawa kaongea na mimi kiustaarabu ila hiki kimama sikipendi jamani, yani sikipendi kabisa”Akaenda zake darasani na kuendelea na masomo yake kama kawaida.Mama Angel akiwa kiwandani leo, bado alitaka maelezo ya ile laki mbili, basi Yuda aliileta ile laki mbili na kumkabidhi huku akisema kuwa yule mtu amemlipa, haikuwa kweli ila Yuda alikopa ile hela mahali ili aweze kumlipa huyu mama na kuepuka lawama,“Oooh kumbe wameleta, basin i vizuri kumbe ni waaminifu”“Halafu Erick mtoto atakuja lini tena kiwandani?”“Atakuja tu ila mwanangu nimeona bora akazanie masomo kwanza kwani ndio ya muhimu kuliko vitu vyote”“Unaonekana unapenda shule eeeh!”“Ndio napenda sana, napenda watoto wangu wawe wasomi wa kimataifa”Waliendelea kufanya kazi huku mama Angel akipita kukagua kagua eneo lake, muda kidogo wakati anajiandaa kutoka, mule ofisini alifika mgeni na mgeni huyo alikuwa ni Juma kwani alijua kuwa siku hiyo angemkuta humo ofisini, ila alimkuta mama Angel, ikabidi tu akae na kuanza kuzungumza nae,“Halafu sikutegemea kama ningekukuta wewe”“Ndio umenikuta sasa, karibu”“Asante, ila si una mtoto mdogo wewe huoni kama ukija huku unamkosesha mtoto haki yake?”“Yani uzuri ni kuwa mtoto wangu amezoea kila kitu, kwahiyo anakunywa maziwa analala, na sio msumbufu hadi wakati narudi”“Hata kama ila mtoto anahitaji jasho la mama kwa ukaribu sana”“Aaaah hayo mambo ilikuwa zamani, ila kwasasa wanawake tumeamka”“Sawa, sikupingi. Yuko wapi Erick?”“Yupo shule, unadhani atakuwa wapi?”“Yani alikopigwa hadi akazimia bado umemrudisha tena! Nina mashaka na wewe, ni mzazi wa aina gani usiye na huruma na mtoto wako?”“Sikuelewi”“Hivi umeshindwa kufikiria kweli, ni bora hata ungemuahamisha shule, kuliko kumrudisha shule hiyo hiyo. Hata hivyo hiki sio kilichonileta”“Haya sema kilichokuleta”“Ni hivi, nilipanga na Erick kuwa Jumamosi ningekuja kumchukua ili twende mahali ila nilishindwa, basi namuomba Jumamosi hii, tena ni vizuri nimekukuta na wewe mama yake, naomba ruhusa kwako”“Haiwezekani, siwezi kumrudusu mwanangu kwenda sehemu nisiyoijua”“Kumbe tatizo ni wewe kutokupajua tu!! Basi naomba twende wote siku hiyo, tafadhari nakuomba. Natumaini utatendea kazi ombi langu, kwaheri”Juma aliinuka na kuondoka yani hakutaka hata kusikia jibu la mama Angel kama kakubali au kakataa ila yeye alihakikisha tu kuwa ameshamwambia na kama anataka na yeye aongozane nao.Mama Angel alirudi nyumbani kwake muda huu akiwa amejichokea kiasi Fulani, baada ya kuoga na kula alienda kuongea na Erick kuhusu Juma,“Nakuomba mwanangu jambo moja, najua nilikwambia ila narudia tena naomba mwanangu usiwe karibu na Juma, hata akufate wapi mkwepe, naona sio mtu mzuri kweko”“Halafu leo mama, alikuja yule mwanamke nisiyempendaga shuleni”“Nani huyo? Sia?”“Ndio huyo huyo”Mama Angel akachukia hapo na kuuliza kwa makini kuwa ni kitu gani Sia alimwambia mtoto wake, ila Erick alimwambia vile ambavyo alizungumza na Sia mpaka mama Angel alishangaa na kusema,“Yani Sia ndio kaja kukwambia hayo maneno! Huo urafiki wa Sia na mke wa Juma umeanza lini hadi waambiane kila kitu jamani! Mmmmh unajua mtu unaweza kuzungukwa hapa hapa bila hata kujijua wala kutambua kuwa ni kitu gani kinachokusumbua kumbe ni mtu wako wa karibu. Haya mwanangu hata kama huwa unamchukia ila hilo alilokwambia ni bora zaidi, tafadhali kaa mbali na Juma”Kisha akamuaga mwanae na moja kwa moja kwenda chumbani kwake, na huko alimpigia simu mumewe na kumwambia tu habari za Juma, ila hakumwambia kuwa alienda kiwandani kwani hakutaka mumewe ajue kuwa huwa anaenda kiwandani,Huyu Juma ana wazimu eeeh! Kwahiyo alikuja tena hapo nyumbani?”“Ndio alikuja”“Sijui kaingiliwa na nini jamani na huyo Juma, anaacha kufatilia watoto wake anakazana kufatilia watoto wa wenzake”“Tuachane na hayo, jamani mume wangu unarudi lini? Nimekukumbuka sana ujue”“Nitarudi tu mke wangu usijali ila siku ya kurudi sitakwambia maana nataka nikushtukize tu”“Ushaniambia tayari maana mshtukizo hata mtu haambiwi kabisa, huwa inatokea tu”Baba Angel akacheka, na kuongea zaidi kidogo na mke wake kisha waliagana na kulala huku mama Angel anawaza kukikucha tu aende kwanza kiwandani maana alitakuwa kwasasa anataka kujua kila kitu.Basi kulivyokucha, alijiandaa kwaajili ya kutoka ila muda ule ule alifika mama Junior, na kumfanya mama Angel ashangae maana ni asubuhi sana, basi alienda kukaa nae kwenye sebule yao nyingine na kuongea nae maana pale ndio kwanza Vaileth alikuwa akifanya usafi,“Kheee dada mbona asubuhi asubuhi?”“kwani na wewe hii asubuhi yote unaenda wapi?”“Naenda kazini dada”“Kivipi? Hebu nieleweshe vizuri”Mama Angel alimwambia kuwa huwa anaenda kiwandani kuangalia jinsi kiwanda kinavyofanya kazi, na kufatilia wafanyakazi wa pale, na hata alimuelezea toka kaanza kufatilia ni makosa mangapi kayagundua,“Ni vizuri sana sio vibaya ila huwa unaondoka muda gani na kurudi muda gani?”“Asubuhi halafu narudi jioni”“Aaaah Erica hebu wacha ujinga, una mtoto mdogo wewe ujue!! Sikia, unachofanya sio kibaya ila panga muda wako vizuri uwe unawahi kurudi kumnyonyesha mtoto na kukaa nae karibu, jamani unafanya kama wale wanawake ambao hawana waume kwahiyo wanapambana wenyewe ili watoto wale, ndio huwa wanafanya kazi muda wote hata muda wa kulea watoto haupo, unadhani Erick akisikia hili atafurahi? Hawezi kufurahi hata kidogo, amehangaika, ameteseka ili mke wake na watoto mtulie, amehitaji mtoto ili utulie nyumbani kulea mtoto ila wewe ndio kama biashara umeanza leo jamani Erica eeeh! Usiwe hivyo jamani mdogo wangu”“Haya nimekuelewa, asubuhi yote hii ya nini?”“Jana bhana, kuna binti kaja kunililia usiku mwenzangu ana mimba ya Junior”Mama Angel alishtuka sana na kumuangalia dada yake,“Kheee sasa umeamua nini?”“Niamue nini zaidi ya kumshauri akatoe”“Hapana dada usifanye hivyo, unajua kutoa mimba ni sawa na dhambi ya kuua tu. Muache azae mtoto wake”“Unakumbuka kipindi chako nini?”“Nakumbuka ndio, muacheni azae, wala hata usimtoe hiyo mimba. Kwanza wewe mwenyewe una kitoto kimoja tu halafu ndio uanze kutoa mimba za wakwe zako kweli? Muache azae tu”“Haya, ila kuna mengine”“Yapi hayo?”“Kuhusu shemeji yako jamani, si kuna kimwanamke alikipata huko sijui wapi ndio kikawa kinamsumbua akili, hadi nilikuja siku ile ili nikueleze dukuduku langu, ila sasa akili ikacheza, siku hiyo kachelewa kurudi nikamuanzishia kilio kama cha msiba, yani nilikumbuka msiba wa baba kabisa, kwani amerudia tena kuwasiliana na yule mwanamke mbele yangu! Kwani kachelewa tena kurudi!!”“Mmmh dada, kwa kilio tu au kuna mengine ulimfanyia?”“Ukiona mumeo anakusumbua niambie nikueleze, ila ndio hivyo Deo saibvi katulia ila sitaki tena kukaa nyumbani, nataka kuanza kazi kwakweli nimechoka kukaa nyumbani, kwahiyo natafuta kazi”“Hilo la kutafuta kazi ni wazo zuri dada, tena kuna rafiki yake baba Angel nitakuunganisha nae, hukusema tu mapema ila kwasasa usijali mambo ni moto. Ila bado hujaniambia mbona umekuja asubuhi sana?”“Nilijua sitokukuta, maana mara nyingi tu napoiga simu naambiwa kuwa umeondoka”“Huwa unapiga ya mezani wewe, ila hata hivyo Derrick kalazwa, sijui umepata habari au dada Mage alisahau kukwambia?”Mama Junior alishangaa kidogo, na kusema kuwa siku hiyo itabidi waende wote kumuona Derrick maana hata wafanyeje bado ni ndugu yao tu.Tumaini akiwa anaelekea katika shughuli zake, akakutana njiani na Dora na kuanza kuongea nae na kumpa taarifa kuhusu kulazwa kwa Derrick,“Jamani masikini, kafanyaje tena?”“Kumbe hujui? Derrick alikuwa ni tapeli ila dada yake yani Erica alikuwa akimfichia siri”“Ila unajua kuna kitu huwa sielewi”“Kitu gani?”“Ni kuhusu Derrick na Erica, kwahiyo wale ni ndugu kabisa?”“Ndio ndugu, baba mmoja wale”“Unajua nini?”“Nini?”“Kipindi tupo chuo, kuna kipindi Fulani Erica alikuwa anatembea na Derrick, si unajua Erica alikuwa ni rafiki yangu sana ila tukaja kugombana badae kwa mambo madogo tu, basi Erica alikuwa anatembea na Derrick”“Mmmh kwahiyo alikuwa ni mpenzi wake kabisa?”“Ndio, alikuwa nae sasa nashangaa kusikia kuwa ni ndugu”“Ila Erica anaonekana kuwa mpole sana, sidhani kama alitembea nae”“Weeee ana upole gani yule! Niulize mimi listi ya wanaume aliotembea nao, ninaowajua tu ni wengi hatari, kuna kijamaa kilikuwa kinaitwa Babuu katembea nacho, kilikuwa kimasikini hatari ila Erica ndio alikufa alioza, mwenzio Erica katembea na George na aliachwa na George sababu hakuwa bikra”“Mmmh unajua George na Erick ni ndugu kwa upande wa mama yake Erick huko!”“Kheee basi hekaheka za Erica sio za nchi hii, kuna kipindi alijikuta kagonganisha ndugu watatu yule na wote katembea nao, huyo Derrick unayesema ni ndugu yake katembea nae, halafu kuna jamaa nadhani unamjua siku ya harusi ya Erick na Erica aliongea maneno mengi kiasi, yule jamaa anaitwa Bahati, kwasasa anaishi na Fetty basi yule Erica katembea nae, usimuone vile huwa kuna mambo namtetea tu. Ni kweli ni mpole ila kwenye swala la uhuni na yeye alikuwa muhuni”“Kumbe!! Ndiomana alipatana na wewe, nikamshangaa msichana mpole vile kuwa na urafiki na wewe! Bora hata Fetty kidogo hakuwa na makuu chuoni ila wewe mmmh nilishangaa sana”“Siku zote mwizi anatembea na mwizi mwenzie, ila kwasasa nimeokoka hayo mambo nimeacha jamani hata umbea huu sikutakiwa kukwambia, eeeh Mungu nisamehe”Tumaini alicheka sana na kumuuliza,“Ila hiyo listi ya wanaume wa Erica uliijuaje?”“Mmmh unajua mimi nina dhambi nyingi jamani, namshukuru Mungu ni mwaminifu na anasamehe, la sivyo mimi nisengesamehewa jamani. Unajua nilikuwa namuonea sana huruma Erica akilia kuhusu mapenzi halafu hivi vidume vikijidai vyenyewe kwa kuumiza moyo wa Erica, yani siku niliyogundua nimeatirika basi nilimfata mmoja baada ya mwingine na kutembea nae, yani kila aliyemuumiza Erica nami nilihakikisha namuumiza na ukimwi”“Ndiomana ukaamua kumuambukiza na baba yangu! Mwanamke mbaya wewe hata hufai”“Mmmh tuachane na habari hizo Tumaini ila baba yako ndio aliniambukiza mimi. Nisamehe kwa hilo”“Mbaya wewe na sidhani kama dhambi zote umesamehewa, hata huo ulokole wako nina mashaka nao. Kajinga kweli wewe”Dora akaona yataanza marumbano pale bure, kwahiyo akaamua kuagana na Tumaini tu ila aliahidi kuwa ataenda kumsalimia Derrick pia.Baada ya Dora kuondoka, kwakweli Tumaini alijiuliza sana,“Kumbe watu wanatoka mbali eeeh! Ndiomana Erica alipata yule mtoto wa kiarabu kumbe na yeye alikuwa na mambo sana”Basi akachukua simu yake na kumtumia mdogo wake ujumbe,“Habari Erick, nasikia Erica kabla ya kukutana na wewe alishatembea na wanaume zaidi ya watano”Muda kidogo akapokea ujumbe kwa Erick,“Hata angetembea na dunia nzima bado ningempenda tu tena sana.”Kisha akapiga simu ambapo Tumaini akapokea,“Ila dada yangu kwani una matatizo gani? Ulisikia kuwa mwanamke akiwa ametembea na wanaume wengi haolewi wapi? Si ilimradi apate anayependana nae tu”“Kheee yameisha basi, mimi nilikuwa nasema tu”“Unajua kuna muda huwa sikuelewi, unampenda Erica ila unaniambia maneno kama haya, unataka niachane nae au ni kitu gani? Dada yangu nakuomba umuheshimu mke wangu, nampenda sana na unalijua hilo, mimi Erica nampenda hata niambiwe wale watoto wote sio wangu kazaa na wanaume wengine huko bado nitampenda na watoto nitawapenda yani usijisumbue kupata habari huko na kuniambia”“Basi yameisha wala sitokwambia tena mambo kama haya”“Halafu hizo tabia za umbea sijui umezitoa wapi? Utakuwa unaongea sana na Sia wewe ndiomana, naomba usiniletee tena umbea wa kuhusu mke wangu, nampenda jinsi alivyo na huwezi jua nimempendea nini”“Nimekuelewa Erick, hata mimi nampenda Erica yani hata sijui naanzaje kukuletea umbea wa aina hii, naomba unisamehe”“Kila siku na mke wangu tunajiuliza Erica mdogo katoa wapi umbea kumbe katoa kwako, naomba usiniambie tena habari za hivi, tuwe tunaongea mambo mengine tu”“Nisamehe, nimekuelewa”Tumaini alikata simu na kupumua kiasi kisha akasema,“Kweli mapenzi ya kweli yapo, kuna muda hadi nahisi Erick karogwa jamani, si kwa kupenda huku mmmh! Ila hata mimi mume wangu ananipenda jamani, niache wivu loh!”Akaendelea na safari yake ya kwenda kwenye shughuli zake.Mama Angel alimuomba dada yake wapiti kwanza kiwandani halafu ndio waende hospitali maana hakutaka siku hiyo aipitishe bila kwenda kuangalia shughuli za kiwanda zimekwendaje.Basi walienda hadi kiwandani, kwa mara ya kwanza mama Junior aliweza kuona kile kiwanda kilivyo,“Jamani mdogo wangu, mmejitahidi sana”“Asante”Basi mama Junior alikuwa akitembelea tembelea maeneo baadhi ya kile kiwanda, kisha akatoka nje na kuanza kutembelea maeneo ya nje ya kile kiwanda, ila mara alipita mmama wa makamona kumsimamisha mama Junior kisha akamuuliza,“Wewe si mama yake na Junior?”“Ndio ni mimi”Yule mama akamnasa kibao mama Junior, ila mama Junior nae huwa hapendi kuonewa kwahiyo alimnasa pia kibao yule mama. Basi mama Junior alikuwa akitembelea tembelea maeneo baadhi ya kile kiwanda, kisha akatoka nje na kuanza kutembelea maeneo ya nje ya kile kiwanda, ila mara alipita mmama wa makamo na kumsimamisha mama Junior kisha akamuuliza,“Wewe si mama yake na Junior?”“Ndio ni mimi”Yule mama akamnasa kibao mama Junior, ila mama Junior nae huwa hapendi kuonewa kwahiyo alimnasa pia kibao yule mama. na pale pale alijikuta yeye na yule mama wakianza kupigana vibao hadi alipotokea Rahim na kuwaamulia maana wote wawili alikuwa akiwafahamu.Rahim aliwauliza pale,“Kwani mna matatizo gani nyie?”Mama Junior akaongea,“Hata namshangaa huyu mwanamke, simjui, hanijui halafu kanivamia tu na kuanza kunipiga vibao”Rahim alimuangalia yule mwanamke na kumuuliza,“Weee Linah, kwani tatizo ni nini?”“Mwambie huyo mwanamke akamuulize mtoto wake Linah ni nani?”“Khee makubwa, mtoto wangu aanze kufahamiana na watu wazima kama wewe!”Mama Angel nae alifatwa na mlinzi kwahiyo alitoka pale nje kuangalia kuna nini na kumkuta Rahim ndio yupo kati akiwaamulia watu hawa, basi mama Angel akasema kwa msahangao,“Kheee ni wewe tena!!”Mama Junior akamuuliza,“Kwani unamfahamu?”“Dada, dunia ina makubwa hii unaweza kuzimia mambo mengine ukiyajua, eti huyu mtu mzima na ukubwa wake alikuwa na mahusiano na Junior”Yani pale Rahim nae aliuliza,“Kwani huyo Junior ana umri gani?”Linah aliondoka huku akisonya tu, na mama Angel akamwambia Rahim,“Junior na Angel wamepishana mwaka mmoja tu”“Khaaa, huyu Linah mbona katia aibu hivyo?”Rahim aliwaacha pale mama Junior na mama Angel halafu yeye alimfata Linah alipoelekea.Basi mama Junior alimuomba tu ndugu yake waondoke muda huo maana alihisi akili yake kutokuwa sawa kabisa, basi mama Angel alienda kukamilisha kazi kidogo na kuondoka na ndugu yake ambapo moja kwa moja alienda nae kwenye mgahawa na kuagiza chakula pale huku wakiongea kidogo, basi mama Junior akauliza tena,“Inamaana yule mwanamke mtu mzima ndio alikuwa akitembea na Junior?”“Ndio! Sasa dada unashangaa nini wakati wewe mwenyewe uliwahi kusema kuwa Junior anatembea na wamama wakubwa”“Yani nilikuwa najua ni wale wanawake wa kumzidi miaka kumi au kumi na mbili, kumbe anatembea na wanawake wanaoweza kumzaa kabisa jamani eeeh!! Sasa yule si Junior ni kama mtoto wake watatu au wanne, ana nini huyu Junior lakini jamani!”“Usijali dada, Junior tutamdhibiti tu na atakaa sawa kama watoto wengine, kwasasa nimempiga marufuku hata kurudi nyumbani, nimemwambia akae shuleni huko na akazane na masomo, hakuna cha mwisho wa wiki wala nini, sitaki ujinga wa kurudi nyumbani kabisa, naona akiwa nyumbani ndio anawaza ujinga zaidi”“Yani Junior jamani dah!! Sasa mama mkubwa vile kweli, halafu halina adabu linafika na kuanza kuninasa vibao, nikasema huyu hajui kichaa changu nikaanza kumnasa vibao pia, yani yule mwarabu koko wako asingetokea basi mimi na yule mwanamke tungechapana pale”Mama Angel alicheka na kusema,“Jamani dada eti mwarabu koko!”“Ndio ni mwarabu koko yule, yani hajali chochote hata kuja kuamulia naona kajitoa kweli. Halafu huku kafata nini au kajua kuwa unakuja huku siku hizi!!”“Hapana, ila nyumbani kwao sio mbali na hapa yani kwao kabisa. Hivi dada asingetokea yule kweli mngepigana?”“Naona Erica unanisahau, jamani mimi huwa sitaki ujinga, anianzae nammaliza, yani sitaki ujinga kabisa, na hata ule mwili wake usingenitisha tungepigana vizuri kabisa pale, mimi ni mpole sana ila huwa sipendi mtu anitanie. Unadhani ndio kama wewe, ambaye unapigwa halafu unaangalia tu yani Erica dah sijui umerithi wapi huo upole”Basi wakaongea kidogo na kupanga kwenda hospitali kumuona mgonjwa kama ambavyo walipanga.Moja kwa moja, Rahim alimfata Linah na kuanza kuongea nae akiwa njiani tu,“Najua ulipata aibu ndiomana ukaondoka, ila kama unajua ni kitu cha aibu uliwezaje kuwa na mahusiano na mtoto mdogo hivyo!!”“Sijui yani, sijui ni kuchanganyikiwa yani sijui halafu najikuta nikimpenda hatari”“Kwani huyo mtoto ana nini cha ziada ambacho watu wazima hatuna?”“Mmmh Rahim niache mie, hivi asiyejua kuwa umeathirika ni nani? Labda mgeni na wewe, naomba uniache tu tafadhari, uliniumiza vya kutosha. Nikajua nitafurahia maisha na huyu mtoto ila naye kumbe mama yake anakataa mapenzi yetu”“Haya ni lini umesikia kuwa nimeathirika? Ukimwi sio mwisho wa maisha, si unaniona bado nadundika, watakufa hao wasiumwa na mimi nitaendelea kubaki na uzima wangu. Ukimwi sio kifo, ila ukimwi ni ugonjwa ambao unakufanya binadamu ujifunze kula vizuri na kuishi vizuri. Pole kwa kuhangaika na watoto wadogo huku ukijua hilo ndio suluhisho la mapenzi, kwanza mwanangu hajambo?”“Mjinga wewe, mwanao siku hizi anaendesha bajaji, usiniulize tena ukimuhitaji haswaa nitafute sio kukutana njiani na kuniuliza ujinga”Linah aliondoka zake, ila Rahim alimuangalia na kutikisa kichwa huku akisema,“Hawa wanawake huwa wanachekesha sana, si kipindi kile aling’ang’ania kuwa mtoto anaweza kumtunza mwenyewe bila msaada wangu, haya imekuwaje sasa mtoto anaendesha bajaji? Wanawake ni watu wapuuzi sana, ila mwanangu atanitafuta tu, hiyo bajaji ikimchosha atakuja kunitafuta”Kisha akaondoka zake na yeye kuendelea na mambo yake mengine.Erick leo aliwahi kurudi nyumbani tofauti na siku zingine na alimkuta Vaileth akiwa amesinzia tu sebleni, kisha alipoingia Erick alishtuka na kumuuliza,“Imekuwaje leo mapema hivi?”“Kichwa kinanigonga sana ndio nikaomba ruhusa na kuondoka zangu, ndiomana nimewahi kurudi”“Pole sana, ila itakuwa una mawazo mengi sana. Sijui huwa unawaza vitu gani ila nakuona kuwa una mawazo mengi sana, cha kufanya uwe unakunywa maji mengi ndio yatakusaidia kutengeneza kichwa vizuri”“Eti eeeh! Asante kwa ushauri wako, ngoja nikapumzike kidogo”Erick alikuwa akiondoka ila ile simu ya mezani nyumbani kwao ilianza kuita na muda huo Vaileth alimuomba Erick apokee mwenyewe ile simu, moja kwa moja Erick alienda kupokea ile simu na kweli mpigaji alikuwa ni Srah,“Jamani Erick nini shida? Nimesikia kuwa umeondoka unaumwa?”“Ndio, ni kichwa”“Pole sana, nikitoka tu shule nakuja kukuona jamani, pole sana”Halafu ile simu ilikatika kisha Erick aliinuka na moja kwa moja kwenda chumbani kwake.Ila baada ya kama nusu saa hivi, mara alifika Sarah mahali pale inaonyesha na yeye aliomba ruhusa hata hakungoja watoke,Alifika na kumuuliza Vaileth kuwa Erick yuko wapi,“Ameenda chumbani kwake kulala”“Chumba chake kiko wapi?”“Ukipandisha hapo, mlango utakaotizamana nao upite halafu ingia chumba kinachofatia ndio cha Erick”“Asante”Vaileth hakutaka kufatilia sana kwani aliona kuwa Sarah kwa kipindi hiko alikuwa akiishi hapo kama mwanafamilia.Sarah alipoingia alimkuta Erick amelala, akaona akimuamsha atamsumbua, basi na yeye alienda kujilaza pembeni yake.Mama Angel na mama Junior walifika hospitali kwaajili ya kumuona Derrick, kwakweli leo kidogo maendeleo ya Derrick yalionekana kwani aliweza hata kufumbua macho yake, basi walimtazama pale na kuanza kumuuliza mama yake,“Ila kwasasa anakula vizuri mama?”“Namshukuru Mwenyezi Mungu kwakweli, kwasasa Derrick anaendelea vizuri”“Mchana wa leo aliletewa chakula na dada Mage?”“Hapana, Mage alimletea asubuhi, na cha jioni hii kimetoka nyumbani kwangu ila mchana alileta yule mwanamke ambaye siku ile alitaka kuanguka halafu akadakwa na wifi yako”Mama Angel aliguna kwani alielewa kuwa huyo mwanamke ni nani, alielewa kuwa ni Manka, ila hakuelewa kuna nini kinaendelea kati ya Manka na Derrick, basi aliitikia tu na kuendelea kuuliza habari zingine za ndugu yao.Muda kidogo alifika Dora nae kwenda kumuona mgonjwa yule, kwakweli mama Junior hakupenda kumuona Dora kabisa ila Dora alimsalimia mama Junior na kuwasalimia wote mahali hapo kisha akaomba mara moja akazungumze nje na mama Junior huku mama Angel akiwa shahidi kwani alimtambua jinsi mama Junior alivyokuwa na hasira, kwahiyo hakutaka kuanza nae shari.Walimuaga mama Derrick pale na kutoka nje kwenda kuzungumza,“Kwanza kabisa dada yangu samahani, najua mimi na wewe hatujapata muda mzuri wa kukaa na kuongea na pengine unanichukia bure tu hujui ni nini kipo kati yangu, sijui unanielewa?”“Wewe endelea tu”“Kwasasa nimeokoka, najitahidi kuacha maovu ambayo nilikuwa nayafanya nyuma”“Unachekesha wewe, unacheza na wokovu, mtu kama wewe unaokokaje?”Mama Angel akamkatisha dada yake,“Dada, msikilize kwanza”“Ni hivi, kipindi kile ni kweli nilifanya makosa, nakiri wazi nilienda kwa mganga na kuchukua dawa za kumteka James, ila kilichonifanya nifanye vile ni kimoja tu. Siku tumetoka mimi, Erica na James, basi James akanifanya ninywe sana pombe, hata Erica alipoondoka alimuahidi kuwa atanirudisha nyumbani ila haikuwa hivyo, badala yake alinipeleka kwenye chumba na kuniingilia kimwili tena mbele na nyuma, halafu akanitupa njiani, kiukweli niliumia sana tena sana, nakumbuka nilimfungulia kesi ila alishinda sababu ya pesa zake, na akawa akinikana kila sehemu kuwa hajawahi kuwa na mimi na sio yeye aliyenifanyia mimi vile, ukizingatia ile kesi alishinda, hujui tu ni jinsi gani niliumia moyoni mwanangu. Ni kweli mimi nilikuwa nahangaika na wanaume ila sikuwa najiuza mimi kwamba unikute nimejisimamisha barabarani ili waninunue hapana, ila nilikuwa na wale walionitaka tu. Halafu kitu kingine ni kuwa hakuna nilichokuwa naogopa kama kufanya mapenzi kinyume na maumbile, nilikuwa naogopa sana, halafu James alinifanyia unyama kama huu. Niliumia sana, ndipo nilipokuwa sawa nikasema James lazima nimfundishe funzo, ndipo nilipoenda kwa mganga kuchukua dawa na kumpatia James, na hapo ndipo alipoanza kunipenda hatari. Sasa ulipomuacha hakuwa na namna zaidi ya kunioa mimi tu. Unajua miaka ilipopita James alirudia tabia yake ya umalaya, yani ile tabia ipo kwenye damu yake jamani ndiomana naomba kila siku ili mwanangu Jesca asije akarithi tabia yangu wala ya baba yake, nahitaji mwanangu awe mtoto mwema kama watoto wengine. Ni marafiki wa James ndio walionikazania kuwa nishikilie mali zote ndiomana imekuwa hivi, naomba unisamehe sana tafadhari, halafu kitu kingine ambacho hujui ni kuwa James alikufa akiwa guest na mwanamke, naomba ukiwa unaomba kata hiko kitu kwa mtoto wako yani asijekuwa kama hivyo. Nisamehe dada yangu, hii hali ya kutangatanga na maisha ndio inafanya watu tuache utu kwakweli, nipo tayari kukaa chini ili tuwagawie watoto wote mali sawa kwa sawa, maana yupo na yule James, yule mtoto ambaye James alizaa na mdada wako wa kazi, naomba tuzingatie hilo pia”Mama Junior akapumua kidogo na kusema,“Kumbe kuna wakati huwa unaweza kuongea kwa busara namna hiyo?”“Nimebadilika mimi, nazidi kumuomba Mungu anibadilishe zaidi kuna tabia naomba azitoe kabisa katika maisha yangu ili nibaki safi”“Khee makubwa, ila nimekuelewa nadhani tutakaa kuongea vizuri kwa mama Angel, tupange tu siku ya kufanya hivyo”Basi wakapanga siku ya kuonana tena na kuagana kwa muda huo, kisha mama Nagel alimrudisha dada yake nyumbani kwake moja kwa moja halafu yeye kuondoka zake kuelekea nyumbani kwake pia.Erica nae alipotoka shuleni tu, kitu cha kwanza leo ilikuwa ni kumuulizia Erick maana kuna habari alikuwa nayo, alimuuliza Vaileth,“Eti dada, Erick amesharudi?”“Ndio muda tu tena anaumwa”Basi Erica hata hakusikiliza maelezo mengine kwani moja kwa moja alienda chumbani kwa Erick, akamuona Erick amelala huku Sarah yuko pembeni yake, yani Erica alijikuta akijawa na hasira sana na kitu pekee alichowaza muda huo ni kwenda chooni na kuchukua maji kisha kuja kuwamwagia pale kitandani Erick na Sarah, kwakweli walishtuka sana na wa kwanza kushtuka alikuwa ni Sarah ambaye aliuliza,“Nani katumwagia maji?”Srick nae alishtuka kumuona Sarah yuko pale kitandani na kuuliza,“Sarah umefika muda gani?”“Muda tu Erick, nilipomaliza kuongea na wewe tu niliomba ruhusa na kuondoka”Erica alikuwa akiwaangalia tu, basi Erick akamuuliza,“Kwahiyo Erica ndio umetumwagia maji!”“Ndio, umesahau ahadi yetu Erick!”Basi Erick ukizingatia alikuwa anaumwa na yale maji aliyomwagiwa na Erica alijikuta akianza kutetemeka na hakuweza kulala tena pale kitandani kwani kulikuwa kumelowa, basi huruma ikamshika Erica ilibidi amsaidie kumtoa pale na kumpeleka chumbani kwake, basi Sarah akataka naye aingie ila Erica alimzuia,“Kwani una nini wewe? Utanikatazaje kumuona kaka yako!”“Sitaki ndio”“Au unamtaka kaka yako!”Erica alimnasa kibao Sarah kwa maneno haya, ila Vaileth alisikia ule mzozo mwanzoni kabisa kwahiyo alienda kuingilia, wakati Sarah akitaka kumrudishia Erica, tayari Vaileth alikuwa pale kuwaamulia na kuwaachanisha ambapo alimtaka Sarah aondoke tu, kwakweli Sarah aliondoka ila alikuwa na hasira sana kwa muda huo na kusema kuna siku atamkomesha Erica.Mama Angel aliporudi nyumbani kwake tu alipewa taarifa kuhusu kuumwa kwa Erick,“Kheee jamani, kumbe mwanangu anaumwa”Basi akataka kwenda moja kwa moja chumbani kwa Erick ila Erica alimwambia kuwa yupo chumbani kwake, mama Angel hata hakuuliza sababu zaidi ya moja kwa moja kwenda huko chumbani kwa Erica ili kumuangalia Erick na kweli alimkuta anaumwa sana na muda huo alikuwa akitetemeka kabisa, basi alimchukua na kumbembeleza pale ili aende nae kwanza hospitali, kwahiyo aliondoka nyumbani akiwa yeye na Erica kwani yeye alikaa kuendesha gari huku Erica akiwa amekaa na Erick hadi hospitali kwahiyo nyumbani alibaki tu Vaileth na mtoto Ester.Mama Angel alivyofika hospitali, moja kwa moja alimpeleka Erick kwa daktari halafu Erica alibaki nje tu.Muda kidogo simu ya mama Angel ilikuwa ikiita na Erica ndio alikuwa na ile simu kwahiyo alipokea muda huo huo,“Hallow”“Mama yupo kwa daktari na Erick”“Kheee kuna nini kwani?”“Erick anaumwa”“Khaaa jamani, ndiomana moyo wangu unaumia. Niambie ni wapi nije sasa hivi”“Kwani wewe nani?”“Nielekeze nije”“Mimi sijui ni hospitali gani hii, mama ndio anajua”Halafu Erica alikata simu na kuangalia ile namba ila ilikuwa ni namba tu bila jina, basi hakujali kitu na kuendelea kukaa pale akisubiri mama yake atoke ili amuulize vizuri.Ila muda kidogo simu nyingine ikaita ila sasa hivi aliyepiga alikuwa ni madam Oliva, ila Erica hakutaka tena kupokea simu kwani alijua wazi mama yake akimkuta kapokea zake nyingi basi atachukia.Vaileth akiwa na mtoto nyumbani, kuna mgeni alifika na mgeni huyo alikuwa ni Sia kwa kipindi hiko Sia alikuwa hazuiliwi kwenda pale kwahiyo mlinzi alikuwa akimruhusu tu.Basi alifika pale na kumuuliza Vaileth kuwa Erick kapelekwa hospitali gani,“Mmmh sijui maana mama wakati anaondoka hajasema kuwa anampeleka hospitali gani, ila umejuaje kama anaumwa?”“Nilimpigia simu mama yenu ila ilipokelewa na Erica mdogo ambaye akaniambia kuwa wapo hospitali ila hakusema ni hospitali gani, ndiomana nimekuja hapa moja kwa moja”“Hata mimi sijui ila naomba nikuulize swali mama yangu maana wewe ni mkubwa kwangu kwahiyo ni kama mama tu”“Uliza tu, ila sina mtoto mkubwa kama wewe”“Haya sawa, ila kwanini unapenda sana kufatilia hii familia haswaa unapenda sana kumfatilia Erick kwanini?”“Ngoja nikujibu tu kwa kifupi, katika maisha mtu huwa unapitia mambo mengi sana ambayo unaweza kuwa huyapendi ila inabidi uyapitie sababu ya kitu Fulani, kwa kifupi ni kuwa Erick ni mwanangu”“Mmmh mwanao? Kivipi?”“Ni mwanangu wa kumzaa”“Kheee makubwa, inamaana sio mtoto wa hii familia au ni kitu gani?”“Sijui, yani sijui hata nikuelezeje. Ngoja nikwambie tena, mimi nilipanga na mtu kubadilisha mtoto wakati najifungua, ila sijui ilikuwaje maana mtoto walisahau kumbadilisha ila nadhani sababu Mungu alitaka kidogo mtoto wangu anuse jasho langu, basi mtoto akiwa na miezi mitatu kasoro akabadilishwa ndio hapo nilipewa mtoto wa huyu mama yenu nimlee na yeye alipewa mtoto wangu”“Mmmh!!”“Ila usimwambie mama yenu habari hii, yani Erick katolewa kwenye mikono yangu akiwa na miezi mitatu kasoro ndio nikaletewa Elly nimlee. Kipindi hiko Erick nilimpa jina la Steve ila alivyoletwa huku alibadilishwa hadi jina ili nisimfahamu ila siku zote damu yako ni damu yako tu”“Kwahiyo wewe hukutamani kuwa na mtoto wako mwenyewe?”“Sikia, tulipanga abadilishwe kipindi akizaliwa tu na nilijua hivyo maana wakati namchukua sikujua kama ni mtoto wangu kumbe ndio wangu ila alikuwa ni mlizi sana, yani alikuwa analia mno na kunifanya nikeshe usiku, kuna muda mwingine nilikuwa namuacha alie tu bila kuhangaika nae, ila wakaja kuniambia kuwa hawakuweza kumbadilisha wakati mdogo sijui mama Angel alizimia wakati wa kujifungua na bibi mtu alikuja kung’ang’ania watoto wapimwe kwanza, kwahiyo wakati mtoto ana miezi mitatu kasoro ndio wakaniomba ili wakambadilishe, mimi nikiwa nyumbani nikaletewa mtoto mwingine hapo nikaambiwa kazi imeisha. Sikujua kama na yeye nitampenda maana ni wazi sio wangu ila alikuwa tofauti sana alikuwa mtulivu sio mliaji hovyo yani nimemlea Elly kwa raha sana ndiomana nampenda sana”“Inamaana mama anajua kuhusu hilo?”“Hajui kitu ndiomana nakwambia kuwa usimwambie, yani siku Erick akikubali nitakuonyesha hadi alama ambayo nilimuweka kabla hajaondolewa katika mikono yangu, hiyo alama nilimuweka kwenye makalio. Akikubali basi ataonyesha, nimemlea mwanangu kwa mwezi miwili sio kwamba sijamlea”“Ila kwanini ulikubali abadilishwe?”“Usiombe umasikini ukutawale katika maisha, yani yote hii ni umasikini uliokithiri. Ila kitu kimoja tu ambacho nafanya sawa ni kuhakikisha kuwa Elly namlea katika misingi na maadili mazuri, sina pesa ila Elly anasoma shule nzuri na sitaki apate shida kwani najua hata mwanangu huku analelewa vizuri. Najua ipo siku Erick atanikubali ila hata asiponikubali basi niwe napata japo nafasi ya kumuona tu”Kwakweli Vaileth alipumua tu maana hakuelewa kabisa, ila alitamani kujua kwa undani zaidi kuhusu maneno ya yule mwanamke, yani aliona ni ngumu sana kwa mtoto kubadilishwa hata kwa mwezi mmoja halafu mwenye mtoto asigundue chochote.Kwenye mida ya saa tano usiku, walirudi kutoka hospitali na kumkuta Sia pale nyumbani kwao akitaka kujua hali ya Erick ila mama Angel hakupenda kabisa na kumtimua huku akimwambia kama anahitaji kujua chochote kuhusu Erick basi aende kesho yake, kwa kipindi hiko Sia hakuwa mbishi kabisa kwani kwa muda huo huo aliotimuliwa aliondoka zake.Mama Angel alimpeleka Erick chumbani kwake na kugundua kuwa kitanda cha Erick kina maji na kuuliza imekuwaje, basi Erica alitaka kujielezea ila Erick alisema,“Nilikuwa na kiu, nikamuagiza Erica aniletee maji, ila alivyonipa mkono ukaniteleza na kile kikombe kikaangukia kitandani”“Kheee basi, ukalale kwa Angel?”“Hapana mama, bora nilale kwa Erica”Mama Angel hakusema neno na moja kwa moja alimpeleka mwanae chumbani kwa Erica na ile ilikuwa ni furaha kubwa sana kwa Erica, kwanza kutetewa na Erick na pia kwa mama yao kukubali Erick kwenda kulala kwake.Kwa muda huo mama Angel alikuwa amechoka sana, alienda kuoga na kumchukua mwanae, huku akiwaza kwa muda jinsi ambavyo hampi haki inavyotakiwa mtoto huyo maana kutwa kucha anahangaika tu na kumuacha mtoto na mdada wake wa kazi, alikuwa amechoka na muda huo akaamua kulala tu.Kulipokucha alienda kumuangalia Erick ila alimkuta Erica nae akigoma kwenda shule sababu Erick anaumwa ila akaona ni vyema amlazimishe na hivyo Erica akajiandaa na kwenda shule.Basi Erica alivyoondoka alitoka zake sebleni huku akilalamika,“Yani Erica leo ameniletea akili mbovu sana, asiende shule sababu Erick anaumwa kweli!! Khaaaa jamani, mimi kwangu utaenda tu sijali huo upacha wala nini, hakuna maswala ya akiumwa mmoja eti mnaumwa wote, nilimuachia siku ile basi akajua na leo nitamuachia, kajinga kweli haka”Basi Vaileth akaona ni muda muafaka wa kumuuliza mama Angel maswali yake kwani hata yeye hakuelewa yale maneno ya Sia,“Mama, unajua siku zote anajiuliza hivi Erick na Erica ni mapacha au ni watoto waliofatana?”“Kheee jamani Vaileth siku zote upo ndani humu na hujui kama Erick na Erica ni mapacha? Kama ni watoto waliofatana nimewaza vipi kuwazaa hivyo walivyo? Ingeonekana kidogo wamepishana sio hivyo wako sawa kabisa”“Samahani mama kwa maswali haya, uliwazaa kwa kawaida au kwa kisu?”“Kwa kisu yani, halafu damu zilinitoka nyingi sana, nilizimia na kuzimia, nakuja kukabidhiwa watoto siamini macho yangu kuona wanangu wakiwa wazuri na nyuso za furaha ila kile kidonda kilinitesa sana ndiomana sikuwa na hamu tena ya kuzaa”“Kheee pole sana mama, uzazi wako wote ni kisu au hao tu?”“Jamani, huoni Ester nimejifungua kawaida? Sijui ni sababu ni mmoja, ila wapo wanaozaa mapacha kawaida tu ila mimi walikuwa wanene sana”“Ila kuhudumia mapacha ni kazi sana, ulikuwa na msichana wa kazi mama?”“Hapana, hapakuwa na msichana wa kazi kwangu, yani kidonda kilinisumbua. Kipindi najifungua baba yenu hakuwepo kwahiyo aliyenipeleka hospitali ni baba mkwe wangu ila nilipojifungua nilirudi nyumbani, baada ya wiki mbili mume wangu alirudi ila sababu kidonda kilikuwa kikinisumbua sana ilibidi awakatie watoto hati ya kusafiria na tukaondoka nao wote kwenda Afrika Kusini kwaajili ya matibabu yangu, yani watoto tulisafiri nao wakiwa na wiki tatu tu. Ila tulikaa sana huko, tulirudi na watoto wakiwa wakubwa kabisa”“Kheee kwahiyo mlisafiri na Angel?”“Ndio maana na yeye alikuwa ni mdogo kwa kipindi hiko, basi kule watoto wangu waliishi vizuri sana, na nilipata huduma nzuri sana, huwezi amini kila kitu alikuwa akifanya mume wangu, yani tumeishi hivyo kwa maisha yote. Ila nilipopona nilikuwa nafanya mwenyewe na tumaishi huko kwa miaka kama mitatu yani tumerudi watoto wakiwa wakubwa kabisa na walizoea maisha ya kule ila walikuja kuzoea na huku. Kwakweli toka uzazi ule sikufikiria kama nitakuja kuzaa tena”“Ila hawakuwa walizi sana watoto wako?”“Halafu hawa watoto kama walijua hali ya mama yao vile, hawakuwa walizi hata kidogo, wakishiba tu wanalala hoi yani hawakuwa na tatizo kabisa”Vaileth akapumua tu, yani toka hapo hakuelewa ila aliweza kuhisi kuwa Sia ana matatizo kidogo kwenye kichwa chake ndiomana kaweza kumwambia maneno kama yale, hakujua ni kitu gani kilimsumbua Sia ila hakuhisi kama Sia ni mzima kichwani.Muda huu mama Angel alitoka nje na Erick akimwambia kidogo wapate mwanga wa asubuhi, kwahiyo walikaa kwenye kibaraza chao, muda kidogo tu alifika madam Oliva kwakweli huyu madam alifurahi sana kwa siku hiyo kumkuta mama Angel nyumbani kwake, ila kabla hajaongea chochote alifika Sia ambaye alienda pale kumuona Erick ila alivyomkuta madam Oliva alichukia sana na kumuuliza,“Umefata nini hapa?”Madam Oliva alibaki kumuangalia tu kwani alimshangaa kumuuliza hivyo wakati nyumbani pale sio kwake, basi Sia akasema tena,“Au Steve kakutuma uje kumuangalia mtoto wake?”Madam Oliva alishangaa na kuuliza,“Mtoto wake?” Madam Oliva alibaki kumuangalia tu kwani alimshangaa kumuuliza hivyo wakati nyumbani pale sio kwake, basi Sia akasema tena,“Au Steve kakutuma uje kumuangalia mtoto wake?”Madam Oliva alishangaa na kuuliza,“Mtoto wake?”Sia akajibu kwa haraka,“Ndio, Erick ni mtoto wa Steve”Mama Angel alimuangalia na kumuuliza,“Hivi wewe Sia, leo umekunywa dawa zako za mwezi mchanga? Naona kile kichaa chako kinaanza tena. Mlinzi njoo unitolee huyu kiumbe tafadhari”Basi mlinzi alifika na kumtoa Sia, ila Erick nae aliamua kwenda ndani kwani kwa kawaida huwa hampendi huyu mama kabisa.Basi pale nje alibaki mama Angel na madam Oliva ambapo madam Oliva naye alikaa chini pale kibarazani na kuanza kuongea na mama Angel, kwanza kabisa alianza kuongea kuhusu Sia,“Hivi yule mwanamke ana wazimu au ni kitu gani? Mtoto gani anaemsema ni wa Steve?”“Achana na yule mwanamke, ni mwezi mchanga yule”“Na kwanini unamchekea? Nadhani ingekuwa mimi wala asingekanyaga nyumbani kwangu maana muda wote ni kuongea mambo yasiyoeleweka tu kuhusu wewe”“Nishamzoea tayari, achana nae tu”“Sijui baba Erick alikwambia au alisahau! Ni hivi kuna siku nilikuona na rafiki yako nikaja kukusalimia, nia yangu ni kuhakikisha kuwa yule rafiki yako ndio yule ninayemdhania au la, nikakuta ni yeye. Yani yule rafiki yako nilimkuta akiongea na huyu Sia na wakipanga mambo mbalimbali na pale nikasema yule sio rafiki mzuri kwako kwani siku zote huwa hata huyu Sia naona sio mzuri kwako”“Kheee leo naona unafunguka sana madam, haya niambie ujio wako”“Ujio wangu ni kutaka ukaniombee msamaha shuleni, najua wewe ukiniombea msamaha basi nitarudishwa kazini. Natamani sana kurudi kwenye kazi yangu maana mimi kufundisha kupo kwenye damu, nisaidie nisije nikawa chizi mie”“Sawa hakuna tatizo, nitaenda na kuongea na uongozi wa shule”“Asante sana, hizi siku zote nilikuwa nahitaji kuja kuzungumza na wewe kuhusu hilo swala ila kila nikija sikukuti yani leo ndio nimekubahatisha”“Nina mgonjwa mwenzio, kaka yangu kalazwa, alipigwa huko basi yupo hospitali”“Jamani masikini dah! Kalazwa wapi?”Mama Angel alimueleza, basi madam Oliva alimuomba siku mama Angel akiwa anaenda awasiliane nae ili aweze kwenda nae,“Yani nimejikuta tu naingiwa na imani jamani, utaniambia basi twende wote kumuona”“Sawa hakuna tatizo nitakushtua”madam Oliva alimuachia tena mama Angel namba zake kisha akamuaga na kuondoka zake kuelekea nyumbani kwake.Leo Erica akiwa shuleni, muda wa mapumziko alikaa pembeni akiongea na rafiki yake Samia ambapo Samia alianza kumuhadithia mambo ya nyumbani kwao,“Mmmh leo mama na baba bado kidogo tu wapigane”“Duh!! Kisa nini?”“Sijui imekuwaje ila nimewasikia asubuhi wakizozana, mama akilalamika kwa baba, yani wewe mwanaume umelala kweli unawewesika unaanza kutaja wanawake zako kweli? Sijui Erica jamani umenikera kweli leo. Niliguna kusikia jina lako, kweli baba yangu alale akiweweseka akitaja jina lako!!”Kisha Samia alikuwa anacheke kidogo, basi Erica akamwambia,“Itakuwa ni Erica mwingine maana hilo jina ni la watu wengi sana. Ila jamani nyumbani kwetu hata mara moja sijawahi kumsikia mama akigombana na baba”“Itakuwa labda wanajificha huko, hata mimi sikuwahi kuwasikia ila leo ndio nimesikia wakizozana hivyo yani kidogo tu wangepigana ila mama alitoka maana alikuwa anaenda kazini. Unajua kama mama yangu ni daktari?”“Aaaah kumbe!! Kwahiyo nyumbani kwenu hamna hata shida!”“Ndio, ila mkali huyo balaa. Siku ile aliipata barua aliyonijibu Erick jamani nilipigwa na mama hadi nikazimia, akaniambia hataki tena kusikia nikija jina la Erick pale nyumbani kwetu. Kwanza barua Erick umempa?”“Nilimpa ndio kwani ilikuwa inahusu nini?”“Nilimuandikia jinsi mama alivyonichapa, jamani mama yangu ana hasira sana hadi basi. Ila mimi nampenda Erick sijui nifannyeje?”“Kama umekatazwa na mama yako naomba uache, wazazi wana busara zaidi na akikukataza kitu basi ameona kasoro yake”“Kwahiyo Erick ana kasoro?”Kengele ya darasani ililia na wote wakarejea kwenye darasa ili kuendelea na vipindi.Madam Oliva alivyofika kwake kama kawaida alimkuta Steve akifanya kazi za nyumbani basi alimwambia aache ili amuelezee yaliyojiri siku hiyo,“Ila kabla ya yote, hivi Steve watu wakija hapa nyumbani na kukuta wewe unafanya kazi za hapa watanielewaje? Na mbaya zaidi akija mwanangu jamani sijui itakuwaje?”“Hivi mwanao mkubwa eeeh!”“Ndio ni mkubwa, yupo kwa mama yangu ndio anaishi huko na kusoma huko. Subiri siku aje hapa, ni mkubwa mwanangu”“Aaaah ila usijali haya mbona mambo madogo tu, ni mwende wa kumuelewesha, mwanao ni wa kike au wa kiume”“Ni wa kiume, anaitwa Paul”“Sawa hakuna tatizo, kwanza atajifunza kupitia mimi kuwa atakapokuwa na mke anapaswa kumsaidia kwa namna yoyote ile”Madam Oliva alicheka kisha akaendelea kumwambia kuhusu alipoenda,“Nashukuru kwa kunisisitiza kuwa niende kuonana na mama Erick, unajua sikudhani kama yule mama ana moyo wa huruma kiasi kile na sikujua kama ni muongeaji mzuri vile, yani tumeongea nae vizuri na amekubali kabisa kwenda kuongea na uongozi wa shule”“Yule mama huwa hana tatizo, tena huwezi amini anaweza akaenda kesho tu”“Jamani dah!! Yule Sia ni mwehu kweli ametaka hata kuniharibia siku pale”“Kivipi?”Madam Oliva alimsimulia kuhusu alichokuwa akikisema Sia pale nyumbani kwa mama Angel,“Oooh achana na chizi yule, yani yule mwanamke hana akili nzuri kwakweli. Sikia nikwambie, ni kweli alipata mimba na alisema kuwa ni mimba yangu na nikawa nae bega kwa bega ila mara aseme ile mimba ni ya Erick mkubwa yule bosi wangu, nikimkomalia anasema kuwa mimba ni yangu yani mwanamke haeleweki yule hata kidogo. Kwanza hakushikwa na uchungu wala nini na walichukuzana na nani huko akaenda hospitali na kurudi na mtoto na kusema kuwa kajifungua kwa njia ya operesheni, sikubisha kwani sijui uzazi wa mwisho unakuaje, na nilimsifu kwa ujasiri aliokuwa nao, nikawaataarifu ndugu zangu alikuja hadi mama yangu na tulikaa nae kama wiki mbili pamoja na mtoto ila mtoto alikuwa akilia sana sijui ilikuwa ni nini ila alikuwa akilia sana na yeye kama alikuwa akisita kumnyonyesha hivi yani anamnyonyesha mtoto kwa machale hadi mama alikuwa akimsema kwanini anafanya anayoyafanya kwa mtoto, alimpa jina Steve huyo mtoto, na mara nyingi alikuwa akihudumiwa na mama yangu ila hata mama alimlaumu ni kwanini alifanyiwa upasuaji akasema anaogopa maumivu ya kuzaa kawaida na pia anaogopa kuharibika maungio yake ya siri, kwakweli mama yangu alimsema sana. Basi mama aliondoka na tukaendelea kuwa pale nyumbani na huduma zote mtoto nilikuwa nikimpatia, tena yeye kama alikuwa sijui anamfanyaje mtoto maana akiwa na mimi mtoto halii wala nini na nilikuwa nampa maziwa ya ng’ombe maana mara nyingi alikuwa hamnyonyeshi sijui alikuwa na tatizo gani. Baada ya mwezi alirudi siku hiyo maana alikuwa akitoka toka ingawa kuna mtoto mdogo nyumbani ambaye hata arobaini hajafikisha, yani yule mwanamke sijui alikuwa akitoa wapi nguvu ya kuzurula jamani. Siku hiyo alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, nilimshangaa kuanza kumpenda mtoto na kumlea vizuri hata kumnyonyesha alianza kumnyonyesha vizuri tena kwa wakati hata kile kilio mtoto alipunguza ikawa afadhari. Nakumbuka yule mtoto akiwa kitu kama na miezi miwili na wiki kama tatu hivi, alitoka na kudai anaenda kliniki na mtoto, kurudi jamani karudi na mtoto mwingine sio yule tena, hapo ndio ugomvi wa mimi na yeye ulipoanza, hadi nikamuita mama na dada, nao walipoona walishangaa na kusema sio yule mtoto wetu wa mwanzo, tukamwambia kuwa tunahitaji mtoto ila hakuwa na jibu zaidi ya kusema msinibabaishe hata yule hakuwa mtoto wako, kwakweli niliumia sana. Akambadilisha jina mtoto na kumuita Elly, hapo ndio nikajua dhahiri kuwa mtoto kabadilishwa, yani niliamua kuondoka na sikutaka tena kuishi nae kwakweli”“Kheee makubwa jamani, sasa mtu utawezaje kufanya kitu cha namna hiyo? Yani kawezaje kubadilisha mtoto wake wa kuzaa mwenyewe na amebadilishana na nani?”“Ukweli anaujua mwenyewe, ndiomana mimi huwa namuita chizi, hata sitaki kumsikiliza maneno yake, na hata usimfatilie pia”Kisha Steve aliona ni vyema akaendelea na kazi zake ili ajishughulishe shughulishe kidogo.Erica aliporudi tu kutoka shule, kitu cha kwanza alianza kumsimulia mama yake aliyosimuliwa na Samia wakiwa shuleni, yani alimtafuta mama yake hadi kumfata chumbani na kuanza kumsimulia,“Mama, kumbe Samia alipigwa na mama yake hadi kuzimia baada ya mama yake kuona jina la Erick. Halafu baba yake Samia sijui kaweweseka huko wakati wa kulala kataja Erica, ugomvi kati ya baba yake na mama yake”“Sikuelewi kabisa, unazungumzia nini kwani?”“Mama, kwani ulisoma vizuri ile barua ambayo Samia alimuandikia Erick ile niliyokupa?”Mama Angel akakumbuka kuwa ile barua aliisoma juu kwa juu wala hakuitilia maanani na alisoma ile mistari ya juu tu ambayo Samia alieleza ni jinsi gani anampenda Erick, basi mama Angel akachukua tena ile barua ili kuisoma sasa, muda huo Erica katulia pembeni akisikiliza mama yake atamwambiaje, ila mama yake alimuangalia na kumkaripia,“Hivi wewe Erica ukoje lakini? Hata sare za shule hujavua upo makini kusikiliza ni nini nitasema, hebu toka hapa niondolee ujinga wako mie. Yani wewe na huyo Samia inaonekana mpo sawasawa, basi siri zote za hapa Samia atakuwa anazijua, yani wewe loh!”Basi Erica aliondoka tu huku amenyong’onyea.Kisha moja kwa moja alienda chumbani kwake na kumkuta bado Erick amelala humo, alifurahi sana na kumsalimia pale,“Kumbe hujarudishwa chumbani kwako?”“Nadhani mama kajisahau, ila yale maji yatakuwa yamekauka”“mmmh bila kuanika godoro? Ila bora wasiwe wameanika tu ili uendelee kulala huku huku. Haya ngoja niende chumbani kwako nikabadilishe nguo”Erick alicheka tu, wakati Erica ametoka na nguo kwenda kubadilisha na yeye alitoka na kumfuata nyuma hadi chumbani kwake, ambapo Erica ndio alibadilisha na kujiandaa kwenda kuoga,“Mmmh Erick jamani umekuja kufanya nini?”“Khaaa kwani wewe unaogopa nini kwangu? Kipi unachonificha? Mimi nimeondoka kule chumbani kwako ili urudi kule, na muda huo walimuona Vaileth akirudisha godoro la Erick kumbe lilitolewa nje kuanikwa na wao hawakutambua hadi wakati analirudisha ndio wakagundua kuwa godoro lilitolewa kitandani, basi Vaileth alimuuliza Erica,“Mbona upo na taulo huku?”“Nilitaka nikaoge sababu Erick alikuwa chumbani kwangu”Kisha Erica akabeba nguo zake na kuelekea chumbani kwake, wakati huo Vaileth aliweka tu godoro na kutoka zake, ila Erick hakulala zaidi alikaa tu pembeni kwenye kiti kilichokuwa pale chumbani kwake.Usiku wa leo mama Angel kama kawaida aliwasiliana na mume wake maana ilishakuwa ndio taratibu yao,“Mke wangu, kuna jambo moja zuri sana nataka nikirudi tulifanye”“Jambo gani hilo?”“Tutaongea nikirudi”Mara ikasikika sauti ya kike ikiita ‘Erick’ mama Angel akashtuka na kumuuliza mumewe,“Sauti ya nani hiyo?”“Aaaah mke wangu wasiwasi wa nini? Ngoja nikupe uongee nae”Basi mama Angel alianza kuongea na yule mtu wa kwenye simu,“Habari, naitwa Juli”“Haya Juli usiku huu unafanya nini na mume wangu?”“Hapana sifanyia nae kitu chochote, ila aliniita kwaajili ya kufanya usafi kwenye chumba chake, ila nimemaliza ndio nimekuja kumuita kuwa nimemaliza”“Haya, mpe simu niongee nae”Basi baba Angel akapewa tena ile simu ambapo mama Angel akapumua kwanza na kuongea nae,“Mume wangu kweli usafi usiku jamani eeeh! Na kwanini usafi afanye mwanamke huko?”“Mke wangu, muda mwingi nakuwa busy, ni usiku huu ndio nimepata muda. Nikamwambia anisafishie chumba na nilikuwa hapa nje namsubiri amalize ndio ameniita kuwa kamaliza”“Inamaana huyo ni mfanyakazi, inakuwaje akuite kwa jina yani hana heshima kiasi hiko?”“Ni mtu mzima mke wangu, alikuwa ananiita baba ila nikamwambia uwe unaniita tu jina langu la Erick”“Mmmh mbona ana sauti nyororo sana?”“Ni sauti yake tu ila haifikii uzuri wa sauti yako mke wangu, naomba ujiamini kuwa upo peke yako katika maisha yangu. Nakupenda sana Erica wangu”Wakaongea ongea pale na mwishowe mama Angel aliamua tu kulala kwa muda huo.Kulipokucha, mama Angel alifanya mambo mengine kisha alijiandaa na kutoka kwani moja kwa moja alitaka kwenda kwanza shuleni kwakina Erick ili kuongea na uongozi kuhusu madam Oliva halafu ndio aende kiwandani.Alifika shuleni kwakina Erick, na moja kwa moja alienda kuongea na uongozi wa pale shuleni. Basi alikutana na muhusika wa pale na kuanza kuongea nae huku akiomba mwalimu Oliva asamehewe,“Aaaah ni ngumu sana mama”“Kwanini wakati tatizo lilikuwa ni mwanangu kuzimia? Nimeamua kumsamehe maana amekiri kutokurudia tena”“Tatizo sio tu kuzimia kwa mwanao, ila yule mwalimu kakorofishana na Sarah”“Kwani Sarah ndio nani?”“Sarah ndio mmiliki halali wa hii shule”“Huyo Sarah na yeye ni mwanafunzi?”“Ndio anasoma, yupo kidato cha tatu”“Oooh kumbe Sarah, naomba kuongea nae kama hutojali”Basi mama Angel alienda kuitiwa Sarah na kukaa nae mahali kuzungumza nae,“Sarah kwanini umemchukia madam Oliva?”“Sijapenda alivyompiga Erick, kwanini ampige vile eti sababu ya Erick kuwa na mimi!”“Ila Sarah nilikufundisha nini kwani? Nilikufundisha kutojihusisha na maswala ya mapenzi, jithamini mwanamke, halafu kitu kingine kumbuka yule madam ana watoto kama wewe na wanamtegemea, kasimamishwa kazi atakula nini na watoto wake, naomba umuhurumie kwa hilo”“Akimpiga tena Erick je!”“Hawezi kumpiga, kapata fundisho na kaniahidi kuwa hatorudia tena. Naamini ilikuwa ni makosa, kwani yule madam huwa anachapa watu shuleni?”“Hapana, hata nilishangaa kwanini alimchapa Erick”“Basi ni bahati mbaya na anajutia, nina hakika hatorudia tena jambo kama hilo. Muhurumie Sarah tafadhali”“Kwasababu yako nitamsamehe sababu mimi nakupenda sana wewe”Sarah alimsogelea mama Angel na kumkumbatia kisha Sarah alienda kuongea na uongozi wa pale shuleni, na walikuwa wakimsikiliza mtoto huyu kupita maelezo ya kawaida, yani hata sheria zingine zitavunjwa sababu ya kumsikiliza tu mtoto huyu.Basi mama Nagel alivyotoka pale aliaga na kuondoka zake kwani leo alitaka kwenda moja kwa moja kiwandani.Mama Angel alifika kiwandani na kufatilia mambo ya kiwanda na kukuta yapo sawa, tofauti na siku zilizopita ambapo alikuta vimeo vingi vingi.Basi aliongea na Yuda na kukubaliana nae vitu vingi,“Ila leo sikai sana hapa kwani nataka kurudi nyumbani kwaajili ya kumuangalia mwanangu, halafu Erick nae anaumwa”“Jamani, kumbe Erick anaumwa dah! Mpe pole sana”“Haya nashukuru”Kisha mama Angel akaaga pale ili aondoke, ila alipotoka nje kabla hajaingia kwenye gari maana siku hiyo aliliacha nje ya geti, kuna mtu alifika nyuma yake na kumsalimia, basi akageuka na mtu huyo alikuwa ni Rahim,“Kheee Rahim!!”“Ndio ni mimi, nadhani hukutegemea kuniona kwa muda huu”Mama Angel alinyamaza tu, kisha Rahim aliongea tena,“Dah! Hivi wewe mwanamke ulinipa vitu gani jamani? Kama kuna dawa ulinipa tafadhari naomba hiyo dawa iishe mara moja, unajua sio kitu cha kawaida kabisa, nilioa nikaacha, nikaoa tena, halafu nikaoa tena yani nikawa na wanawake wawili ila wote nikawaacha, sikujua nifanye kitu gani yani sikujielewa kabisa. Ikabidi nikamfate mwanamke ambaye hajaolewa na nilimzalisha watoto wawili kabla ya ndoa, halafu ni mwanamke msomi, nikaona yeye nitaweza kudumu naye, ni kweli nilimuoa na tumeishi vizuri kwasababu kubwa moja. Unataka kujua ni sababu gani?”“Sababu gani?”“Sababu mimi na yeye hatuingiliani mambo yetu, yani simu yake ni yake na simu yangu ni yangu, hakuna mtu anayeshika simu ya mwenzie na tunaishi vizuri tu na huwa hatuulizani maswali ya kijinga sijui nimesikia una mwanamke sijui una mwanaume, hakuna kitu kama hiko. Kwanza ni msomi halafu ni mwanamke anayejiamini sana halafu ana akili, tatizo ni moja tu yupo busy sana, unajua mke wangu ni daktari yani yeye na kazi kazi na yeye, unaweza usimuone hata siku mbili au hata tatu anasema kazi zimemtinga, ila ndio maisha tunayoishi na hatujawahi kugombana. Sema juzi usiku kuamkia asubuhi ndio mara ya kwanza kwenye ndoa yetu kuzozana na chanzo cha ugomvi ni mimi kulala huku nikiweweseka na kutaja jina lako, yani mke wangu hajapenda kwakweli tena hajapenda kabisa, yani kalalamika hadi nimemuonea huruma. Huyu mwanamke ananipenda sana na sitaki kumpoteza kabisa, ila kwanini akili yangu inatawaliwa na uwepo wako Erica? Tafadhari niokoe”“Kheee una wazimu, sasa mimi nakuokoaje?”“Nadhani ukikubali kulala na mimi kwa mara ya mwisho tena mara moja tu itakuwa ndio njia ya kuniokoa maana nitaweza kukusahau na kufanya maisha mengine”Mama Angel alimsonya na kuingia kwenye gari yake kisha kuelekea nyumbani kwake maana aliona huyu mtu anamchanganya tu akili yake kwa wakati huo.Sarah aliwahi kutoka shule kwani alitaka kwenda kumuona Erick kabla ya Erica kutoka shuleni na kumfanyia fujo kama za siku ile, na kweli aliweza kufika kwa muda mzuri nyumbani kwakina Erick na kulikuwa kimya sana kwani alikuwepo tu Erick na Vaileth pamoja na mtoto, alimkuta Erick yupo nje kwao kwenye bustani kwahiyo alienda huko kwaajili ya kuzungumza nae,“Erick jamani nimekukumbuka sana ujue”“Hakuna tatizo, Jumatatu nitakuwepo shuleni”“Nakupenda yani nimemsamehe madam Oliva kwaajili yako kwahiyo atarudishwa shuleni, je upo tayari?”“Ndio, sina tatizo juu ya hilo”“Erick, nifanye nini ili ujue kuwa nakupenda?”“Jamani Sarah kwanini unakuwa sio muelewa kiasi hiko jamani! Sisi bado ni wadogo, kwakweli mimi najiona ni kijana mdogo sana kuingia katika mahusiano ya kimapenzi.”“Sasa Erick una udogo gani jamani!! Mbona ni mkubwa wewe, au bado hujabalehe?”Erick alinyanyuka na kusema kuwa ni muda wake wa kunywa dawa kwahiyo alifatana na Sarah kwenda ndani ila haukuwa muda wake wa kunywa dawa wala nini sema tu hakutaka tena yale maswali.Muda kidogo mama Angel nae aliwasili pale nyumbani na kumkuta Sarah yuko pale, basi akamwambia,“Oooh Sarah umekuja kumuona ndugu yako!”Sarah akaitikia tu maana alishindwa hata kumkatalia mama Angel aliyoyasema, hata mama Angel alitambua hilo kisha akamuangalia Sarah na kumwambia,“Yule ambaye unaonyeshwa kwenye picha kuwa ni baba yako basi ndio babu yao kabisa kabisa na wakina Erick kwahiyo wewe ni shangazi yao”“Duh!! Haiwezekani”“Ndio hivyo, labda kama mama yako atakuonyesha baba yako mwingine ila yule ni babu wa wakina Erick”Bapo Sarah alihisi kama kuvurugwa maana siku zote huwa kama haelewi elewi undugu wake na Erick upo vipi ila hapo alipata kidogo uelewa na akaamua kuaga muda huo huo na kuondoka zake.Usiku wa siku hiyo kama kawaida mama Angel alichukua simu yake na kumpigia mume wake ila siku hiyo alipata jibu kuwa namba ya mume wake haipatikani, na kuanza kuhisi tofauti ila badae akakumbuka maneno aliyokuwa anaongea Rahim kuhusu mke wake, kuwa anajiamini basi alijisemea na yeye,“Kama mke wa Rahim ambaye anajua wazi kuwa mumewe ni muhuni hafai ila anajiamini, kwanini mimi nisijiamini? Natakiwa nijiamini pia kwani Erick ananipenda sana”Basi akaondoa hofu moyoni mwake na moja kwa moja kulala tu.Kulipokucha alifanya kazi zake kidogo za nyumbani, siku hizi hakutaka kuonekana kiwandani kwa kila siku, alichagua siku zake za kwenda ilia pate na muda mzuri wa kukaa na familia yake basi aliona pia siku hiyo ni vizuri kwa yeye kwenda kumtembelea Derrick hospitali, basi akawasiliana na madam Oliva ili amwambia na madam Oliva alifurahi na kusema kuwa yupo tayari na muda huo atafika hapo kwa mama Angel ili waondoke pamoja.Muda ulivyofika, madam Oliva alipiga simu kuwa yupo nje na mama Angel alitoka ili kuondoka nae, ila pale nje alitokea pia Sia ambaye alikuwa akitikisa kichwa na kusema,“Eti leo mmekuwa marafiki, khaaa dunia bila unafki haiwezekani”Ila hakuna aliyetaka kumsikiliza kwani walijua kumsikiliza Sia basin i kuharibu siku yao yote, kwahiyo waliondoka tu bila kumjibu.Mama Angel na madam Oliva waliongozana kwa muda huo na moja kwa moja walienda hospitali aliyolazwa Derrick, ila walipokuwa wanaingia wodini simu ya madam Oliva ikaita kwahiyo ikabidi atoke nje kuisikiliza, basi mama Angel ndio alisoge pale kwa mgonjwa na alimkuta pale mama Derrick pamoja na dada yake Mage maana ndio walikuwa wakienda mara kwa mara, ila hata Derrick alikuwa kafumbua macho huku kamuegemea mama yake tu, kwahiyo mama Angel alikuwa akiulizia hali ya Derrick,“Tunamshukuru Mungu saivi anaendelea vizuri kama hivi anaangalia na anakula vizuri tu tofauti na mwanzo”“Yule mwanamke alikuja tena? Yule ambaye alitaka kuzimia”“Yule alikuja jana, ila leo hajaja kabisa toka asubuhi”“Oooh sawa ila cha muhimu anaendelea vizuri”“Ndio, bado kuongea tu”Basi madam Oliva alimaliza kuongea na simu na kuingia sasa mule wodini na moja kwa moja kwenda kwa mgonjwa yule, ila alipomuona alishangaa sana na kusema,“Derrick!!”Naye Derrick kwa mara ya kwanza toka aumwe alisema,“Oliva!!”Basi wote pale wakashangaa kuona watu hawa wanafahamiana.Madam Oliva alibaki kumuangalia tu kwani alimshangaa kumuuliza hivyo wakati nyumbani pale sio kwake, basi Sia akasema tena,“Au Steve kakutuma uje kumuangalia mtoto wake?”Madam Oliva alishangaa na kuuliza,“Mtoto wake?”Sia akajibu kwa haraka,“Ndio, Erick ni mtoto wa Steve”Mama Angel alimuangalia na kumuuliza,“Hivi wewe Sia, leo umekunywa dawa zako za mwezi mchanga? Naona kile kichaa chako kinaanza tena. Mlinzi njoo unitolee huyu kiumbe tafadhari”Basi mlinzi alifika na kumtoa Sia, ila Erick nae aliamua kwenda ndani kwani kwa kawaida huwa hampendi huyu mama kabisa.Basi pale nje alibaki mama Angel na madam Oliva ambapo madam Oliva naye alikaa chini pale kibarazani na kuanza kuongea na mama Angel, kwanza kabisa alianza kuongea kuhusu Sia,“Hivi yule mwanamke ana wazimu au ni kitu gani? Mtoto gani anaemsema ni wa Steve?”“Achana na yule mwanamke, ni mwezi mchanga yule”“Na kwanini unamchekea? Nadhani ingekuwa mimi wala asingekanyaga nyumbani kwangu maana muda wote ni kuongea mambo yasiyoeleweka tu kuhusu wewe”“Nishamzoea tayari, achana nae tu”“Sijui baba Erick alikwambia au alisahau! Ni hivi kuna siku nilikuona na rafiki yako nikaja kukusalimia, nia yangu ni kuhakikisha kuwa yule rafiki yako ndio yule ninayemdhania au la, nikakuta ni yeye. Yani yule rafiki yako nilimkuta akiongea na huyu Sia na wakipanga mambo mbalimbali na pale nikasema yule sio rafiki mzuri kwako kwani siku zote huwa hata huyu Sia naona sio mzuri kwako”“Kheee leo naona unafunguka sana madam, haya niambie ujio wako”“Ujio wangu ni kutaka ukaniombee msamaha shuleni, najua wewe ukiniombea msamaha basi nitarudishwa kazini. Natamani sana kurudi kwenye kazi yangu maana mimi kufundisha kupo kwenye damu, nisaidie nisije nikawa chizi mie”“Sawa hakuna tatizo, nitaenda na kuongea na uongozi wa shule”“Asante sana, hizi siku zote nilikuwa nahitaji kuja kuzungumza na wewe kuhusu hilo swala ila kila nikija sikukuti yani leo ndio nimekubahatisha”“Nina mgonjwa mwenzio, kaka yangu kalazwa, alipigwa huko basi yupo hospitali”“Jamani masikini dah! Kalazwa wapi?”Mama Angel alimueleza, basi madam Oliva alimuomba siku mama Angel akiwa anaenda awasiliane nae ili aweze kwenda nae,“Yani nimejikuta tu naingiwa na imani jamani, utaniambia basi twende wote kumuona”“Sawa hakuna tatizo nitakushtua”madam Oliva alimuachia tena mama Angel namba zake kisha akamuaga na kuondoka zake kuelekea nyumbani kwake.Leo Erica akiwa shuleni, muda wa mapumziko alikaa pembeni akiongea na rafiki yake Samia ambapo Samia alianza kumuhadithia mambo ya nyumbani kwao,“Mmmh leo mama na baba bado kidogo tu wapigane”“Duh!! Kisa nini?”“Sijui imekuwaje ila nimewasikia asubuhi wakizozana, mama akilalamika kwa baba, yani wewe mwanaume umelala kweli unawewesika unaanza kutaja wanawake zako kweli? Sijui Erica jamani umenikera kweli leo. Niliguna kusikia jina lako, kweli baba yangu alale akiweweseka akitaja jina lako!!”Kisha Samia alikuwa anacheke kidogo, basi Erica akamwambia,“Itakuwa ni Erica mwingine maana hilo jina ni la watu wengi sana. Ila jamani nyumbani kwetu hata mara moja sijawahi kumsikia mama akigombana na baba”“Itakuwa labda wanajificha huko, hata mimi sikuwahi kuwasikia ila leo ndio nimesikia wakizozana hivyo yani kidogo tu wangepigana ila mama alitoka maana alikuwa anaenda kazini. Unajua kama mama yangu ni daktari?”“Aaaah kumbe!! Kwahiyo nyumbani kwenu hamna hata shida!”“Ndio, ila mkali huyo balaa. Siku ile aliipata barua aliyonijibu Erick jamani nilipigwa na mama hadi nikazimia, akaniambia hataki tena kusikia nikija jina la Erick pale nyumbani kwetu. Kwanza barua Erick umempa?”“Nilimpa ndio kwani ilikuwa inahusu nini?”“Nilimuandikia jinsi mama alivyonichapa, jamani mama yangu ana hasira sana hadi basi. Ila mimi nampenda Erick sijui nifannyeje?”“Kama umekatazwa na mama yako naomba uache, wazazi wana busara zaidi na akikukataza kitu basi ameona kasoro yake”“Kwahiyo Erick ana kasoro?”Kengele ya darasani ililia na wote wakarejea kwenye darasa ili kuendelea na vipindi.Madam Oliva alivyofika kwake kama kawaida alimkuta Steve akifanya kazi za nyumbani basi alimwambia aache ili amuelezee yaliyojiri siku hiyo,“Ila kabla ya yote, hivi Steve watu wakija hapa nyumbani na kukuta wewe unafanya kazi za hapa watanielewaje? Na mbaya zaidi akija mwanangu jamani sijui itakuwaje?”“Hivi mwanao mkubwa eeeh!”“Ndio ni mkubwa, yupo kwa mama yangu ndio anaishi huko na kusoma huko. Subiri siku aje hapa, ni mkubwa mwanangu”“Aaaah ila usijali haya mbona mambo madogo tu, ni mwende wa kumuelewesha, mwanao ni wa kike au wa kiume”“Ni wa kiume, anaitwa Paul”“Sawa hakuna tatizo, kwanza atajifunza kupitia mimi kuwa atakapokuwa na mke anapaswa kumsaidia kwa namna yoyote ile”Madam Oliva alicheka kisha akaendelea kumwambia kuhusu alipoenda,“Nashukuru kwa kunisisitiza kuwa niende kuonana na mama Erick, unajua sikudhani kama yule mama ana moyo wa huruma kiasi kile na sikujua kama ni muongeaji mzuri vile, yani tumeongea nae vizuri na amekubali kabisa kwenda kuongea na uongozi wa shule”“Yule mama huwa hana tatizo, tena huwezi amini anaweza akaenda kesho tu”“Jamani dah!! Yule Sia ni mwehu kweli ametaka hata kuniharibia siku pale”“Kivipi?”Madam Oliva alimsimulia kuhusu alichokuwa akikisema Sia pale nyumbani kwa mama Angel,“Oooh achana na chizi yule, yani yule mwanamke hana akili nzuri kwakweli. Sikia nikwambie, ni kweli alipata mimba na alisema kuwa ni mimba yangu na nikawa nae bega kwa bega ila mara aseme ile mimba ni ya Erick mkubwa yule bosi wangu, nikimkomalia anasema kuwa mimba ni yangu yani mwanamke haeleweki yule hata kidogo. Kwanza hakushikwa na uchungu wala nini na walichukuzana na nani huko akaenda hospitali na kurudi na mtoto na kusema kuwa kajifungua kwa njia ya operesheni, sikubisha kwani sijui uzazi wa mwisho unakuaje, na nilimsifu kwa ujasiri aliokuwa nao, nikawaataarifu ndugu zangu alikuja hadi mama yangu na tulikaa nae kama wiki mbili pamoja na mtoto ila mtoto alikuwa akilia sana sijui ilikuwa ni nini ila alikuwa akilia sana na yeye kama alikuwa akisita kumnyonyesha hivi yani anamnyonyesha mtoto kwa machale hadi mama alikuwa akimsema kwanini anafanya anayoyafanya kwa mtoto, alimpa jina Steve huyo mtoto, na mara nyingi alikuwa akihudumiwa na mama yangu ila hata mama alimlaumu ni kwanini alifanyiwa upasuaji akasema anaogopa maumivu ya kuzaa kawaida na pia anaogopa kuharibika maungio yake ya siri, kwakweli mama yangu alimsema sana. Basi mama aliondoka na tukaendelea kuwa pale nyumbani na huduma zote mtoto nilikuwa nikimpatia, tena yeye kama alikuwa sijui anamfanyaje mtoto maana akiwa na mimi mtoto halii wala nini na nilikuwa nampa maziwa ya ng’ombe maana mara nyingi alikuwa hamnyonyeshi sijui alikuwa na tatizo gani. Baada ya mwezi alirudi siku hiyo maana alikuwa akitoka toka ingawa kuna mtoto mdogo nyumbani ambaye hata arobaini hajafikisha, yani yule mwanamke sijui alikuwa akitoa wapi nguvu ya kuzurula jamani. Siku hiyo alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, nilimshangaa kuanza kumpenda mtoto na kumlea vizuri hata kumnyonyesha alianza kumnyonyesha vizuri tena kwa wakati hata kile kilio mtoto alipunguza ikawa afadhari. Nakumbuka yule mtoto akiwa kitu kama na miezi miwili na wiki kama tatu hivi, alitoka na kudai anaenda kliniki na mtoto, kurudi jamani karudi na mtoto mwingine sio yule tena, hapo ndio ugomvi wa mimi na yeye ulipoanza, hadi nikamuita mama na dada, nao walipoona walishangaa na kusema sio yule mtoto wetu wa mwanzo, tukamwambia kuwa tunahitaji mtoto ila hakuwa na jibu zaidi ya kusema msinibabaishe hata yule hakuwa mtoto wako, kwakweli niliumia sana. Akambadilisha jina mtoto na kumuita Elly, hapo ndio nikajua dhahiri kuwa mtoto kabadilishwa, yani niliamua kuondoka na sikutaka tena kuishi nae kwakweli”“Kheee makubwa jamani, sasa mtu utawezaje kufanya kitu cha namna hiyo? Yani kawezaje kubadilisha mtoto wake wa kuzaa mwenyewe na amebadilishana na nani?”“Ukweli anaujua mwenyewe, ndiomana mimi huwa namuita chizi, hata sitaki kumsikiliza maneno yake, na hata usimfatilie pia”Kisha Steve aliona ni vyema akaendelea na kazi zake ili ajishughulishe shughulishe kidogo.Erica aliporudi tu kutoka shule, kitu cha kwanza alianza kumsimulia mama yake aliyosimuliwa na Samia wakiwa shuleni, yani alimtafuta mama yake hadi kumfata chumbani na kuanza kumsimulia,“Mama, kumbe Samia alipigwa na mama yake hadi kuzimia baada ya mama yake kuona jina la Erick. Halafu baba yake Samia sijui kaweweseka huko wakati wa kulala kataja Erica, ugomvi kati ya baba yake na mama yake”“Sikuelewi kabisa, unazungumzia nini kwani?”“Mama, kwani ulisoma vizuri ile barua ambayo Samia alimuandikia Erick ile niliyokupa?”Mama Angel akakumbuka kuwa ile barua aliisoma juu kwa juu wala hakuitilia maanani na alisoma ile mistari ya juu tu ambayo Samia alieleza ni jinsi gani anampenda Erick, basi mama Angel akachukua tena ile barua ili kuisoma sasa, muda huo Erica katulia pembeni akisikiliza mama yake atamwambiaje, ila mama yake alimuangalia na kumkaripia,“Hivi wewe Erica ukoje lakini? Hata sare za shule hujavua upo makini kusikiliza ni nini nitasema, hebu toka hapa niondolee ujinga wako mie. Yani wewe na huyo Samia inaonekana mpo sawasawa, basi siri zote za hapa Samia atakuwa anazijua, yani wewe loh!”Basi Erica aliondoka tu huku amenyong’onyea.Kisha moja kwa moja alienda chumbani kwake na kumkuta bado Erick amelala humo, alifurahi sana na kumsalimia pale,“Kumbe hujarudishwa chumbani kwako?”“Nadhani mama kajisahau, ila yale maji yatakuwa yamekauka”“mmmh bila kuanika godoro? Ila bora wasiwe wameanika tu ili uendelee kulala huku huku. Haya ngoja niende chumbani kwako nikabadilishe nguo”Erick alicheka tu, wakati Erica ametoka na nguo kwenda kubadilisha na yeye alitoka na kumfuata nyuma hadi chumbani kwake, ambapo Erica ndio alibadilisha na kujiandaa kwenda kuoga,“Mmmh Erick jamani umekuja kufanya nini?”“Khaaa kwani wewe unaogopa nini kwangu? Kipi unachonificha? Mimi nimeondoka kule chumbani kwako ili urudi kule, na muda huo walimuona Vaileth akirudisha godoro la Erick kumbe lilitolewa nje kuanikwa na wao hawakutambua hadi wakati analirudisha ndio wakagundua kuwa godoro lilitolewa kitandani, basi Vaileth alimuuliza Erica,“Mbona upo na taulo huku?”“Nilitaka nikaoge sababu Erick alikuwa chumbani kwangu”Kisha Erica akabeba nguo zake na kuelekea chumbani kwake, wakati huo Vaileth aliweka tu godoro na kutoka zake, ila Erick hakulala zaidi alikaa tu pembeni kwenye kiti kilichokuwa pale chumbani kwake.Usiku wa leo mama Angel kama kawaida aliwasiliana na mume wake maana ilishakuwa ndio taratibu yao,“Mke wangu, kuna jambo moja zuri sana nataka nikirudi tulifanye”“Jambo gani hilo?”“Tutaongea nikirudi”Mara ikasikika sauti ya kike ikiita ‘Erick’ mama Angel akashtuka na kumuuliza mumewe,“Sauti ya nani hiyo?”“Aaaah mke wangu wasiwasi wa nini? Ngoja nikupe uongee nae”Basi mama Angel alianza kuongea na yule mtu wa kwenye simu,“Habari, naitwa Juli”“Haya Juli usiku huu unafanya nini na mume wangu?”“Hapana sifanyia nae kitu chochote, ila aliniita kwaajili ya kufanya usafi kwenye chumba chake, ila nimemaliza ndio nimekuja kumuita kuwa nimemaliza”“Haya, mpe simu niongee nae”Basi baba Angel akapewa tena ile simu ambapo mama Angel akapumua kwanza na kuongea nae,“Mume wangu kweli usafi usiku jamani eeeh! Na kwanini usafi afanye mwanamke huko?”“Mke wangu, muda mwingi nakuwa busy, ni usiku huu ndio nimepata muda. Nikamwambia anisafishie chumba na nilikuwa hapa nje namsubiri amalize ndio ameniita kuwa kamaliza”“Inamaana huyo ni mfanyakazi, inakuwaje akuite kwa jina yani hana heshima kiasi hiko?”“Ni mtu mzima mke wangu, alikuwa ananiita baba ila nikamwambia uwe unaniita tu jina langu la Erick”“Mmmh mbona ana sauti nyororo sana?”“Ni sauti yake tu ila haifikii uzuri wa sauti yako mke wangu, naomba ujiamini kuwa upo peke yako katika maisha yangu. Nakupenda sana Erica wangu”Wakaongea ongea pale na mwishowe mama Angel aliamua tu kulala kwa muda huo.Kulipokucha, mama Angel alifanya mambo mengine kisha alijiandaa na kutoka kwani moja kwa moja alitaka kwenda kwanza shuleni kwakina Erick ili kuongea na uongozi kuhusu madam Oliva halafu ndio aende kiwandani.Alifika shuleni kwakina Erick, na moja kwa moja alienda kuongea na uongozi wa pale shuleni. Basi alikutana na muhusika wa pale na kuanza kuongea nae huku akiomba mwalimu Oliva asamehewe,“Aaaah ni ngumu sana mama”“Kwanini wakati tatizo lilikuwa ni mwanangu kuzimia? Nimeamua kumsamehe maana amekiri kutokurudia tena”“Tatizo sio tu kuzimia kwa mwanao, ila yule mwalimu kakorofishana na Sarah”“Kwani Sarah ndio nani?”“Sarah ndio mmiliki halali wa hii shule”“Huyo Sarah na yeye ni mwanafunzi?”“Ndio anasoma, yupo kidato cha tatu”“Oooh kumbe Sarah, naomba kuongea nae kama hutojali”Basi mama Angel alienda kuitiwa Sarah na kukaa nae mahali kuzungumza nae,“Sarah kwanini umemchukia madam Oliva?”“Sijapenda alivyompiga Erick, kwanini ampige vile eti sababu ya Erick kuwa na mimi!”“Ila Sarah nilikufundisha nini kwani? Nilikufundisha kutojihusisha na maswala ya mapenzi, jithamini mwanamke, halafu kitu kingine kumbuka yule madam ana watoto kama wewe na wanamtegemea, kasimamishwa kazi atakula nini na watoto wake, naomba umuhurumie kwa hilo”“Akimpiga tena Erick je!”“Hawezi kumpiga, kapata fundisho na kaniahidi kuwa hatorudia tena. Naamini ilikuwa ni makosa, kwani yule madam huwa anachapa watu shuleni?”“Hapana, hata nilishangaa kwanini alimchapa Erick”“Basi ni bahati mbaya na anajutia, nina hakika hatorudia tena jambo kama hilo. Muhurumie Sarah tafadhali”“Kwasababu yako nitamsamehe sababu mimi nakupenda sana wewe”Sarah alimsogelea mama Angel na kumkumbatia kisha Sarah alienda kuongea na uongozi wa pale shuleni, na walikuwa wakimsikiliza mtoto huyu kupita maelezo ya kawaida, yani hata sheria zingine zitavunjwa sababu ya kumsikiliza tu mtoto huyu.Basi mama Nagel alivyotoka pale aliaga na kuondoka zake kwani leo alitaka kwenda moja kwa moja kiwandani.Mama Angel alifika kiwandani na kufatilia mambo ya kiwanda na kukuta yapo sawa, tofauti na siku zilizopita ambapo alikuta vimeo vingi vingi.Basi aliongea na Yuda na kukubaliana nae vitu vingi,“Ila leo sikai sana hapa kwani nataka kurudi nyumbani kwaajili ya kumuangalia mwanangu, halafu Erick nae anaumwa”“Jamani, kumbe Erick anaumwa dah! Mpe pole sana”“Haya nashukuru”Kisha mama Angel akaaga pale ili aondoke, ila alipotoka nje kabla hajaingia kwenye gari maana siku hiyo aliliacha nje ya geti, kuna mtu alifika nyuma yake na kumsalimia, basi akageuka na mtu huyo alikuwa ni Rahim,“Kheee Rahim!!”“Ndio ni mimi, nadhani hukutegemea kuniona kwa muda huu”Mama Angel alinyamaza tu, kisha Rahim aliongea tena,“Dah! Hivi wewe mwanamke ulinipa vitu gani jamani? Kama kuna dawa ulinipa tafadhari naomba hiyo dawa iishe mara moja, unajua sio kitu cha kawaida kabisa, nilioa nikaacha, nikaoa tena, halafu nikaoa tena yani nikawa na wanawake wawili ila wote nikawaacha, sikujua nifanye kitu gani yani sikujielewa kabisa. Ikabidi nikamfate mwanamke ambaye hajaolewa na nilimzalisha watoto wawili kabla ya ndoa, halafu ni mwanamke msomi, nikaona yeye nitaweza kudumu naye, ni kweli nilimuoa na tumeishi vizuri kwasababu kubwa moja. Unataka kujua ni sababu gani?”“Sababu gani?”“Sababu mimi na yeye hatuingiliani mambo yetu, yani simu yake ni yake na simu yangu ni yangu, hakuna mtu anayeshika simu ya mwenzie na tunaishi vizuri tu na huwa hatuulizani maswali ya kijinga sijui nimesikia una mwanamke sijui una mwanaume, hakuna kitu kama hiko. Kwanza ni msomi halafu ni mwanamke anayejiamini sana halafu ana akili, tatizo ni moja tu yupo busy sana, unajua mke wangu ni daktari yani yeye na kazi kazi na yeye, unaweza usimuone hata siku mbili au hata tatu anasema kazi zimemtinga, ila ndio maisha tunayoishi na hatujawahi kugombana. Sema juzi usiku kuamkia asubuhi ndio mara ya kwanza kwenye ndoa yetu kuzozana na chanzo cha ugomvi ni mimi kulala huku nikiweweseka na kutaja jina lako, yani mke wangu hajapenda kwakweli tena hajapenda kabisa, yani kalalamika hadi nimemuonea huruma. Huyu mwanamke ananipenda sana na sitaki kumpoteza kabisa, ila kwanini akili yangu inatawaliwa na uwepo wako Erica? Tafadhari niokoe”“Kheee una wazimu, sasa mimi nakuokoaje?”“Nadhani ukikubali kulala na mimi kwa mara ya mwisho tena mara moja tu itakuwa ndio njia ya kuniokoa maana nitaweza kukusahau na kufanya maisha mengine”Mama Angel alimsonya na kuingia kwenye gari yake kisha kuelekea nyumbani kwake maana aliona huyu mtu anamchanganya tu akili yake kwa wakati huo.Sarah aliwahi kutoka shule kwani alitaka kwenda kumuona Erick kabla ya Erica kutoka shuleni na kumfanyia fujo kama za siku ile, na kweli aliweza kufika kwa muda mzuri nyumbani kwakina Erick na kulikuwa kimya sana kwani alikuwepo tu Erick na Vaileth pamoja na mtoto, alimkuta Erick yupo nje kwao kwenye bustani kwahiyo alienda huko kwaajili ya kuzungumza nae,“Erick jamani nimekukumbuka sana ujue”“Hakuna tatizo, Jumatatu nitakuwepo shuleni”“Nakupenda yani nimemsamehe madam Oliva kwaajili yako kwahiyo atarudishwa shuleni, je upo tayari?”“Ndio, sina tatizo juu ya hilo”“Erick, nifanye nini ili ujue kuwa nakupenda?”“Jamani Sarah kwanini unakuwa sio muelewa kiasi hiko jamani! Sisi bado ni wadogo, kwakweli mimi najiona ni kijana mdogo sana kuingia katika mahusiano ya kimapenzi.”“Sasa Erick una udogo gani jamani!! Mbona ni mkubwa wewe, au bado hujabalehe?”Erick alinyanyuka na kusema kuwa ni muda wake wa kunywa dawa kwahiyo alifatana na Sarah kwenda ndani ila haukuwa muda wake wa kunywa dawa wala nini sema tu hakutaka tena yale maswali.Muda kidogo mama Angel nae aliwasili pale nyumbani na kumkuta Sarah yuko pale, basi akamwambia,“Oooh Sarah umekuja kumuona ndugu yako!”Sarah akaitikia tu maana alishindwa hata kumkatalia mama Angel aliyoyasema, hata mama Angel alitambua hilo kisha akamuangalia Sarah na kumwambia,“Yule ambaye unaonyeshwa kwenye picha kuwa ni baba yako basi ndio babu yao kabisa kabisa na wakina Erick kwahiyo wewe ni shangazi yao”“Duh!! Haiwezekani”“Ndio hivyo, labda kama mama yako atakuonyesha baba yako mwingine ila yule ni babu wa wakina Erick”Bapo Sarah alihisi kama kuvurugwa maana siku zote huwa kama haelewi elewi undugu wake na Erick upo vipi ila hapo alipata kidogo uelewa na akaamua kuaga muda huo huo na kuondoka zake.Usiku wa siku hiyo kama kawaida mama Angel alichukua simu yake na kumpigia mume wake ila siku hiyo alipata jibu kuwa namba ya mume wake haipatikani, na kuanza kuhisi tofauti ila badae akakumbuka maneno aliyokuwa anaongea Rahim kuhusu mke wake, kuwa anajiamini basi alijisemea na yeye,“Kama mke wa Rahim ambaye anajua wazi kuwa mumewe ni muhuni hafai ila anajiamini, kwanini mimi nisijiamini? Natakiwa nijiamini pia kwani Erick ananipenda sana”Basi akaondoa hofu moyoni mwake na moja kwa moja kulala tu.Kulipokucha alifanya kazi zake kidogo za nyumbani, siku hizi hakutaka kuonekana kiwandani kwa kila siku, alichagua siku zake za kwenda ilia pate na muda mzuri wa kukaa na familia yake basi aliona pia siku hiyo ni vizuri kwa yeye kwenda kumtembelea Derrick hospitali, basi akawasiliana na madam Oliva ili amwambia na madam Oliva alifurahi na kusema kuwa yupo tayari na muda huo atafika hapo kwa mama Angel ili waondoke pamoja.Muda ulivyofika, madam Oliva alipiga simu kuwa yupo nje na mama Angel alitoka ili kuondoka nae, ila pale nje alitokea pia Sia ambaye alikuwa akitikisa kichwa na kusema,“Eti leo mmekuwa marafiki, khaaa dunia bila unafki haiwezekani”Ila hakuna aliyetaka kumsikiliza kwani walijua kumsikiliza Sia basin i kuharibu siku yao yote, kwahiyo waliondoka tu bila kumjibu.Mama Angel na madam Oliva waliongozana kwa muda huo na moja kwa moja walienda hospitali aliyolazwa Derrick, ila walipokuwa wanaingia wodini simu ya madam Oliva ikaita kwahiyo ikabidi atoke nje kuisikiliza, basi mama Angel ndio alisoge pale kwa mgonjwa na alimkuta pale mama Derrick pamoja na dada yake Mage maana ndio walikuwa wakienda mara kwa mara, ila hata Derrick alikuwa kafumbua macho huku kamuegemea mama yake tu, kwahiyo mama Angel alikuwa akiulizia hali ya Derrick,“Tunamshukuru Mungu saivi anaendelea vizuri kama hivi anaangalia na anakula vizuri tu tofauti na mwanzo”“Yule mwanamke alikuja tena? Yule ambaye alitaka kuzimia”“Yule alikuja jana, ila leo hajaja kabisa toka asubuhi”“Oooh sawa ila cha muhimu anaendelea vizuri”“Ndio, bado kuongea tu”Basi madam Oliva alimaliza kuongea na simu na kuingia sasa mule wodini na moja kwa moja kwenda kwa mgonjwa yule, ila alipomuona alishangaa sana na kusema,“Derrick!!”Naye Derrick kwa mara ya kwanza toka aumwe alisema,“Oliva!!”Basi wote pale wakashangaa kuona watu hawa wanafahamiana. Basi madam Oliva alimaliza kuongea na simu na kuingia sasa mule wodini na moja kwa moja kwenda kwa mgonjwa yule, ila alipomuona alishangaa sana na kusema,“Derrick!!”Naye Derrick kwa mara ya kwanza toka aumwe alisema,“Oliva!!”Basi wote pale wakashangaa kuona watu hawa wanafahamiana.Ila Derrick alivyosema hivyo alizimia na kufanya wazidi kushangaa zaidi kwahiyo ilibidi akaitwa daktari halafu mama Angel atoke na madam Oliva nje yani alihisi tu kuna kitu, basi moja kwa moja alienda nae kwenye gari na kupanda kisha kukaa halafu mama Angel alianza kumuuliza,“Umemjua vipi Derrick?”“Mwanaume mpuuzi sana yule hata najuta kumfahamu”“Kwanini?”“Unajua mimi nina mtoto anaitwa Paul, kiukweli baba wa Paul ni huyu mwehu simpendi hata kidogo”“Kheee kumbe umezaa nae! Ulikuwa na mahusiano nae! Kakufanyaje tena hadi humpendi?”“Jinga sana hili janaume, yani huyu ndiye mwanaume aliyefanya niyachukie mapenzi hadi sasa nipo kutangatanga tu na kuhangukia kwakina Steve wasiokuwa na hatia yoyote ile”“Dah! Pole hata sikujua yani, pole sana ila yote Mungu ni mwema na anamakusudi yake kukuleta huku na mimi kwani imekuwa vyema kumgundua kuwa yupo baba wa mwanao”“Hata sikutaka kujua kama yupo huyu mwehu yani, maana nilishaamua kumlea mwanangu mwenyewe kuwa hana baba basi kuliko kulea mtoto na hilo chizi, nimechefukwa kumuona hatari, huwa sisahau hata herufi za jina lake”“Dah!! Pole sana, ila wanaume wana mambo sana jamani, mpaka mtu unaweza kuwa chizi ila niambie tatizo ni nini maana mimi siwezi kukulaumu kwa chochote”“Nitakwambia ila naomba tutoke kwanza eneo hili maana nazidi kuchefukwa”Mama Angel alitaka kujua kwa undani zaidi kuwa Derrick aliwahi kumfanya nini madam Oliva, basi akaamua kumfatilia na kufanya atakacho kwahiyo kwa muda huo waliwasha gari na kuondoka maeneo hayo ya hospitali tena bila hata kuangalia hali ya mgonjwa tena kwani hawakuingia tena wodini, basi moja kwa moja mama Angel alienda na Oliva hotelini na kuagiza vinywaji huku akimsikiliza kwa makini,“Kwahiyo umenileta hadi huku usikie tu!”“Sio kwa ubaya maana Derrick ni kaka yangu kabisa, mimi na yeye tumeshea baba”“Oooh hapo nimekuelewa, leo ngoja nitoe dukuduku langu juu ya huyu mtu na nitakueleza kwa upana zaidi”“Nieleze tu madam hata usijali kitu, wanaume nawajua pia”“Aaaah huwajui wewe, unayeishi kwa furaha na kupendwa hivyo na mume wako unasema kuwa wanaume unawajua!! Hapana mama Erick huwajui wanaume wewe, bado kabisa hujapata uchungu wa wanaume, kuna watu tumechefukwa na wanaume hata tulikuwa tukiona suruali unajua ndio wale wale wanapita”“Mmmmh jamani, ila hata kuna wanaume wengine wamechefukwa na wanawake kama sisi tulivyochefukwa nao”“Jamani mama Erick usijiweke kwenye kundi letu la kuwasema wanaume wakati kuna mwanaume anayekupenda kufa na kupona halafu useme wanaume wote sawa kweli!! Hapana, hata mimi kwasasa nimegundua kuwa kuna wanaume tofauti tofauti kutokana na mazingira waliyokulia na malezi yao waliyopewa”“Ni kweli, nakusikiliza madam”“Ila ngoja nikueleze kwa kifupi maana nikikueleza yote kwa hakika hatutomaliza hapa, ngoja nikueleze tu ujinga wa huyu ndugu yako”“Sawa, mimi nakusikiliza kwa makini sana”“Ni hivi, nilianza mahusiano na Derrick, kipindi niko chuo ila mimi kwetu ilikuwa kuna kajiuwezo kidogo kwahiyo wazazi walikuwa wakinipatia pesa, yani hatukuwa na shida moja kwa moja halafu mimi nilikuwa napata mkopo chuo na boom kama kawaida. Basi nilianza mahusiano na Derrick jamani kipindi hiko sina uelewa vizuri na mahusiano kila kitu nahisi ni kupendwa, basi Derrick alinilalamikia kuwa kwao kuna shida halafu yeye hajapata mkopo ila sababu nilimpenda niliweza kumvumilia na alisema akimaliza chuo tutaoana kwani ana lengo zuri na mimi, yani niliona ananipenda sana kwani muda wote Derrick alikuwa akiniambia maneno matamu. Ila vocha ni kwangu yani mimi ndio wa kumtumia vocha sababu yeye hana hela, nikipata ile hela ya kujikumu basi naigawa nusu kwa nusu yani nachukua mimi na kumpa Derrick, niliamini ya kuwa yeye ndio mume wangu na siwezi kumuomba hela wakati najua hana hela, na siwezi kumnyima hela anayoniomba kwani ndio mume wangu mtarajiwa nikimnyima naweka picha gani kwaajili ya maisha yetu ya badae? Tena haikutosha, mara zote nikienda kumtembelea anadai nimpelekee zawadi basi najikakamua na kubeba zawadi kwaajili yake, nikipewa hela nyumbani bado na yeye atataka basi nampa yani ilifikia kipindi mimi nabaki sina hela kwaajili yake yani yeye afurahi. Nakumbuka akiwa kaishiwa tu basi atakuja chuoni kwetu na kuhitaji nimpatie pesa nami nitakopa popote ili nimpe yeye, halafu hakuna mwanaume anayependa ngono kama Derrick yani kama karogezewa kwenye ngono, kwahiyo alinitumia vilivyo yani nilikuwa kama mke wake.Balaa lilipoanza ni pale nipopata mimba jamani! Yani hii lilikuwa ni balaa zaidi kwanza kabisa Derrick alikataa ile mimba, nikajua ni sababu ya kipato nikaongea nae kuwa akubali tu nami najua jinsi nitakavyowapanga nyumbani na watatusaidia kulea ila alikuwa mkavu kabisa na kudai mimba yangu nimeipata kutoka kwa wanaume wengine. Siku moja niliumia sana yani bado kidogo niende kutoa mimba, nilimkuta Derrick na mdada mmoja mweupe sana wakiwa na mahusiano jamani siku ile Derrick aliniambia maneno machafu sana kuwa sina hadhi ya kuwa nae, hawezi kutembea na mwanamke mweusi wakati weupe wapo, alidai kuwa mimi ni mbaya sana kwahiyo yupo na mwanamke mzuri na wa kisasa, yani hiyo kaongea mbele yangu nikiwa nimesimama huku nikiwaangalia na huyo mwanamke wake na mimba yangu imeenda mbela, roho iliniuma sana, wala Derrick hakujali hali yangu zaidi ya kuniambia maneno ya karaha tu, niliumia sana nilirudi kwangu na kulia sana maana nilikuwa nimepanga kwa kipindi hiko kwa aibu ya ile mimba, nakumbuka nililia mno nikatamani kwenda kutoa ile mimba ila daktari aliniambia ni bora nivumilie na kuzaa tu. Basi ikawa ni maumivu kila siku kwangu maana Derrick alikuwa akinipigia simu kwa makusudi huku akiniambia weee malaya, bado tu hujamzaa huyo malaya mwenzio, nilikuwa naumia sana, sikujua ni kitu gani nilichomkera Derrick hadi kunifanyia hivi, nakumbuka nilienda kujifungua kabla ya muda na mtoto alitoka njiti kwahiyo akawa hospitali akihudumiwa tu, ila badae sijui ilikuwaje pale hospitali mtoto wangu alipotea kwenye mazingira ya kutatanisha!! Kiukwlei niliumia sana na nikawa nafatilia mara kwa mara, wakati nipo na mimba ile nilitamani kutoa ila nilipomuona mwanangu sikutaka aondoke kwenye mikono yangu. Baada ya miezi michache ndio mtoto wangu akapatikana baada ya kuwaambia kuwa nitawafungulia kesi ila yule mtoto sikutaka kuamini moja kwa moja kuwa ni wangu kwahiyo nilienda kupima nae damu kwanza, nilipojihakikisha kuwa ni wangu ndipo nikaondoka nae na kurudi nae kwetu, wote walifurahi ambavyo sikutegemea kabisa maana alikuwa amekuwa kwa kipindi hiko, na kalikuwa kanalia sana sijui sababu ya kukazaa njiti, ila baada ya siku chache alianza kutulia, na baba yangu alimpa jina lake la Paul, kwahiyo mtoto yule anaishi kwetu huwa hata mama yangu hataki niende nae mbali. Hayo ndio mambo aliyonifanyia huyo mwehu Derrick, simpendi hata kidogo jamani”Mama Angel akapumua kidogo na kumwambia madam Oliva,“Kwakweli nimekuelewa madam, tena nimekuelewa sana. Kwakweli pole sana madam, yani kumbe Derrick ndio alikufanyia ujinga wa kiasi hiko!! Pole sana, sikushangai kwa kumchukia yani jitu lilikuwa linakuombha hela, umelihudumia halafu limeenda kukufanyia ujinga hivyo dah!! Kweli inauma sana”“Ndio hivyo, sina hamu nae kabisa yani. Ananichefua huyo mtu, kwanza kachelewesha maendeleao yangu kwakweli sababu nilikuwa namuhudumia yeye na utahira wake”Mama Angel aliweza kugundua ni kiasi gani madam Oliva alivyokuwa na hasira na Derrick, basi kwa muda huo alimbadilishia tu mada kisha waliamua kuondoka ambapo kwa siku hiyo mama Angel alimpeleka madam Oliva hadi nyumbani kwake na kuagana nae halafu yeye ndio akaondoka na kurudi nyumbani kwake.Leo haikuwa siku ya shule, kwahiyo Erica alikuwa nyumbani tu pamoja na kaka yake, basi alimuuliza Erick kuwa atapenda kula chakula gani maana kajitoa kumpikia,“Utakula chakula gani Erick? Nataka nikupikie mwenyewe leo”“Ila muda umeenda sana Erica, ninachokitamani mimi hapa kitakuchukua muda kwakweli”“Ni kitu gani hiko?”“Natamani sana kula keki, yani nimeitamani mno”“Ila mama najua angekununulia, ila mimi nitapika kwaajili yako nitapika hata kidogo. Ngoja nichukue hela kwa dada nikanunue vitu ambavyo havipo nije kupika”Erica alienda kuangalia na kugundua kuwa blueband ndio hakun kwaajili ya kupika hiyo keki, basi moja kwa moja alienda kuongea na Vaileth ili ampatie pesa,“Dada, naomba hela kidogo nikanunue blueband”“Kwani unataka kupika nini Erica?”“Nataka kupika keki maana Erick kasema anataka kula keki leo”“Kheee unajua kupika keki wewe?”“Najua ndio ila najua kiasi kidogo na sijawahi kupika hata mara moja ila mahitaji yake nayajua”“Duh! Mimi sijui kwetu hayo mambo hayapo”Kisha alimpatia pesa na moja kwa moja Erica alitoka na kwenda dukani kununua hiyo blueband, ila aliponunua tu alikutana na Elly pale dukani na kufurahi sana kumuona kisha kuanza kuongea nae,“Jamani Elly nimekukumbuka sana maana wewe huwa nakuona kama ndugu yangu vile”“Hata mimi nimekukumbuka sana Erica, yani kiukweli huwa nakuona kama ndugu yangu wa damu kabisa yani. Ila tu kwavile sina uhuru wa kuja sana nyumbani kwenu, mamako alinikuta nataka kupigana na Erick basi akachukia sana”“Msamehe bure mama yangu, unajua Erick ni dhaifu ndiomana mama anakuwa mkali sana kwa Erick. Ila bora nimekutana na wewe, Erick anaumwa halafu kasema anataka kula keki ndio nimetoka dukani hapo kununua blueband ili nikatengeneze ila sina utaalamu wa kutengeneza keki sana, nimefurahi kukuona ili uniambie tu maana najua lazima mama yako huwa anatengeneza”“Ni kweli mama huwa anatengeneza, kwenye biashara yake sio mbali na hapa, twende nikupeleke ili akuelekeze”Basi Erica aliongozana na Elly hadi kwenye biashara ya mama yake, yani Sia alipowaona pamoja alitabasamu na kusema,“Ni pale hata watu wafanyaje ila mapacha wataendelea tu kuwa mapacha, nafurahi kuwaona pamoja. Naamini nguvu iliyowaunganisha tumboni ndio ambayo inaendelea kuwaunganisha duniani hata watu wafanye vipi fitina”Si Erica wala Elly ambaye alimuelewa mama huyu, ila Elly hakutaka kusema mengi zaidi ya kumuuliza mama yake tu namna ambavyo keki zinatengenezwa sababu Erica anataka kwenda kumtengenezea Erick, yani Sia alifurahi sana na kuanza kumuelekeza Erica pale namna ya kupika keki na mahitaji yote muhimu,“Kheee bora umenielekeza jamani, najua tu mahitaji yake ila hapo kwenye vipimo lazima ningekosea tu”“Ila vya kukorogea keki vipo kwenu?”“Vipo ndio, zamani mama alikuwa anapika ila siku hizi wala hata hajishughulishi na mambo hayo”“Oooh ndiomana baba yenu anahangaika sana siku hizi, ni lazima mama yenu kapoteza ladha aliyokuwa nayo mwanzo”“Kivipi?”“Tuachane na hayo, ngoja nikuulize Erick anaendeleaje?”“Anaendelea vizuri”“Ila Erica huwa ukimuona Elly unamuonaje na Erick unamuonaje?”“Mmmh Erick ni pacha wangu na nina mpenda sana, ila Elly namuona pia kama kaka yangu sababu ana moyo wa upendo na ana heshima”“Na wewe Elly huwa unamuona vipi Erica?”“Namuona kama dada yangu na ninampenda sana”Sia alitabasamu na kufurahi sana kwani ile kwake ilikuwa ni furaha kubwa kugundua kuwa hawa watoto wameelewana, kisha Sia aliamua kumuandikia kabisa Erica namna ya kupika keki ili asisahau aliyomuelekeza, halafu akamkabidhi ile karatasi na kumwambia,“Nakupenda sana wewe binti, kwanza una upendo halafu unaelewa na unajua kumsikiliza mtu. Msalimie sana Erick, hapa ndio kwenye biashara yangu muda wowote ukijisikia njoo hapa unisalimie”Basi wakaagana na Elly aliamua kumsindikiza kidogo tu, ila alipokaribia kwao alirudi.Kabla Erica hajafika kuingia kabisa kwao, alikutana na Bahati kwa mara nyingine ambapo ni kitambo sana hawakuonana, basi alisimama na kusalimiana nae, naye Bahati alimwambia Erica,“Yani wewe sidhani kama familia yako huwa wananuna, jamani upo vizuri sana, ni mcheshi na unaelewa kuishi na mtu wa aina yoyote ile. Kwakweli mimi huwa nakupenda sana”Erica alikuwa akicheka tu na kufurahi kwani kwake ilikuwa ni habari ya furaha ile na ukizingatia hakuwa mtoto wa kununanuna, na hivi alipenda umbea kwahiyo kwake kununa hakukuwa na nafasi ili aweze kupata habari azitakazo kwa urahisi.“karibu kwetu, mimi nawahi nyumbani”“Sijui kama nitaruhusiwa kuingia kwenye hilo geti, ila kwaheri sema kila siku tambua kuwa nakupenda sana”Erica aliondoka zake na kuingia ndani kwao hata Vaileth alimshangaa sana kuchelewa kwa siku hiyo ila kwavile mama yao alikuwa hajarudi hakuweza kumsema sana, na moja kwa moja Erica alianza kufanya mapishi ya ile keki.Mama Angel wakati anarudi nyumbani kwake, njiani alikutana na Dora kwahiyo alisimama kumsalimia kwanza,“Umetoka wapi muda huu Dora?”“Yani mama alinituma nikaongee na Steve maana mama anahitaji Steve arudi nyumbani, nashukuru nimeenda na sijamkuta huyo Oliva sijui, ila moyo umenisuta sana nikaona hata nisijisumbue kusema chochote basi nikamwambia nimeenda kumsalimia tu. Nimechoka kuingilia mapenzi ya watu, yawe ya dawa sijui nini watajijua wenyewe, mbona mimi sikuingiliwa na James? Nimechoka kwakweli”“Umefanya jambo la maana, waache waishi wenyewe, kama ni dawa jua kuwa zitaisha siku moja kisha Steve atakuwa huru, ni swala tu la kuendelea kumuombea ila sio kumtoa kinguvu”“Na wewe umetoka wapi?”“Nimetoka kumpeleka madam Oliva nyumbani kwake maana nilikuwa nae leo”“Oooh ndiomana Sia aliniambia kuwa wewe umeanza urafiki na huyo Oliva, kuwa makini ndugu yangu, kuwa makini na ndoa yako. Wengine sisi ni wajane hatuna tatizo tunaweka urafiki na mtu yoyote tu ila wewe una mume, naomba uwe makini sana, hawa wanawake hawaaminiki hata kidogo”“Nimekusikia ila huyo Sia nae ni mnafki sana, sitaki kumuongelea kwasasa, kwaheri”Basi akaagana na Dora pale na kuondoka zake, ila mama Angel aliona kuwa kuna umuhimu wa yeye kuongea na Sia kwani aliona kama Sia kaanza hivyo basi hashindwi kukutana na kila mtu wa karibu wa mama Angel na kuongea nao kuhusu shutuma zake za mtoto.Wakati mama Angel anakaribia kufika nyumbani kwake, ndipo alipomuona Sia kwahiyo akasimama na kumsalimia pale kisha kuongea nae,“Sikia Sia, unajua mimi huo uchizi wako siupendi kabisa, kila siku ukija kwangu unasema Erick ni mwanao hivi unataka watu watuonaje au watuelewe vipi lakini?”“Sina nia mbaya, ila nia yangu nyingine ni kuwaweka karibu na mwanangu Elly maana ile ni damu yako, na hujui tu ni jinsi gani Elly na Erica wanavyopendana sababu ndio mapacha halisi”“Unamaana kuwa Erick ulimbadilisha na Elly? Kivipi, hivi unajua kama mimi na wewe hatujajifungulia hospitali moja?”“Ila tumejifungua siku moja, na wote kwa kisu kwahiyo usikatae”“Hiyo sio sababu najua Erick na Erica ni watoto wangu”“Laiti ungemuona Erica leo alivyokuja hapa kwenye mgahawa wangu alikuwa vipi na Elly ndio ungetambua ukweli kuwa Erica na Elly ni mapacha na ndio ungetambua kuwa Erick sio mtoto wako”“Ok, tumalize utata. Nipo tayari kwenda na wewe, Erick na Elly hospitali ili tukapime damu, siku hizi vipimo vipo kwahiyo usinichanganye akili yangu”“Hapo kwenye vipimo umeenda sehemu nyingine, mimi sijasema habari za kupima ila nimeongea kwa uhalisia. Kusoma hujui hata picha huoni jamani!”“Tumalize utata, basi nipe Elly nikapime nae”“Kwenye maswala ya vipimo siko tayari ila ndio nimeongea hivyo”“Kama kupima hutaki basi na mimi sitaki kuendelea kusikia huo upuuzi wako, niache na familia yangu nikae nayo kwa amani”“Sawa, ila mwanao Erica ana akili sana. Ungekuwa na akili kama mtoto wako Erica basi ungenielewa mapema sana”“Mjinga wewe”Mama Angel aliingia kwenye gari lake na kurudi nyumbani kwake kwani aliona huyu mtu anaichosha tu akili yake.Mama Angel alipofika nyumbani kwake ndio muda huu aliwakuta wakina Erica wakila ile keki ambayo Erica kaitengeneza, basi alionja kipande kimoja tu na kwenda chumbani kwake kubadili nguo na kuoga.Alipomaliza ndipo alipoiwaza tena ile keki ya Erica,“Mmmh hii keki wamenunua wapi hawa jamani, mbona tamu hivi. Ngoja nikawaulize”Ila kabla alipokea ujumbe kwenye simu yake, alipoangalia ni ujumbe kutoka kwa Sia,“Mwanao Erica ana heshima sana ndiomana kwa busara zangu nikamuelekeza kupika keki vizuri ili mwanangu Erick apate ladha nzuri”Mama Angel alisonya na kusema,“Yani kufahamiana na watu wasiokuwa na akili ni kazi sana, kakazana kuwa Erick ni mtoto wake, twende tukapime damu basi hataki, yani anaona sifa sijui kuongea ugonjwa wake muda wote. Mwehu kweli huyu, ila Erica naye alianzaje kwenda kumuuliza huyu mwehu kuhusu kupika keki jamani dah!”Mama Angel akatoka moja kwa moja na kwenda kuuliza kuwa ile keki wameiotoa wapi, ila Erica alimsimulia mama yake mwanzo hadi mwisho wa yeye kuipika ile keki, hadi alivyokutana na Elly na ambavyo Elly alivyompeleka kwa mama yake akamuelekeza, yani alimueleza kila kitu kiasi kwamba mama Angel hakuwa na swali lingine kwa mtoto wake huyu kwani alishamueleza kila kitu basi alimchukua tu mtoto mdogo Ester na kwenda nae chumbani huku akisema,“Ni kweli Erica ni mbea ila namshukuru Mungu mtoto wangu huyu sio muongo, yani yeye huwa anaeleza kila kitu jinsi kilivyo, sema tu hawezi kunyamaza ndio tatizo lake”Basi alienda hadi chumbani kwake na kwa muda huo aliamua kumpigia simu kwanza mume wake maana hata kuhusu kuumwa kwa Erick hakumpa taarifa hiyo, kwahiyo akamwambia tu,“Anaendeleaje kwasasa?”“Yupo vizuri”“Naomba niongee nae”Basi mama Angel akatoka na kumpelekea Erick simu ili aongee na baba yake, kwahiyo alimuacha hapo akiwa anaongea na simu huku yeye akirudi chumbani na kushughulika na Ester.Na kweli Erick aliongea pale na baba yake na kupata faraja zaidi, basi alipomaliza kuongea na ile simu ilikatika halafu Erick aliinuka ili ampelekee mama yake ile simu ila muda huo huo kuna ujumbe uliingia kwenye ile simu na kuwa juu ya simu ile ambapo Erick alijikuta akiusoma tu,“Msalimie sana mwanangu Erick, usikatae ukweli kwani Erick ni mwanangu hata ufanyeje atabaki kuwa mwanangu tu. By, Sia”Yani Erick alijikuta akichukia sana kusoma ule ujumbe, alijikuta akifungua vizuri na kuufuta kabisa kwani hakuupenda na wala hakujali kama mama yake atauliza halafu alimrudishia mama yake ile simu.Erick alienda chumbani kwake akiwaza kwanini yule mama anakazana kusema kuwa yeye ni mtoto wake, yani akajikuta akiwa na hasira sana,“Inawezekanaje nilelewe kwingine halafu niwe mtoto wa mtu mwingine? Inamaana mama na baba sio wazazi wangu? Inamaana Angel na Erica sio ndugu zangu? Hapana jamani, hawa ni ndugu zangu tu, ni kwanini huyu mama anapenda kuichanganya akili yangu? Simpendi kabisa”Muda huu Erica nae alienda chumbani kwa kaka yake na kuanza kuongea nae ambapo Erick alimuuliza,“Nimekusikia kuwa ulienda kwa mama Elly sijui akakuelekeza kupika keki, je huyu mama anapatikana wapi?”“Unataka nikupeleke?”“Ndio ila mama asijue kama umenipeleka”“Basi Kesho wakati wa kwenda Kanisani nikupeleke”Erick alikubali na hata hakutaka kuongea mambo mengi sana kwa siku hii, kwani moja kwa moja aliagana na Erica tu na yeye kulala kwa muda huo.Jumapili hii, kweli kabisa Erica na Erick walitoka wenyewe kwenda kwenye Ibada, na walipotoka huko Erica alipitia kwenye mgahawa wa mama Elly na kumuonyesha ila mara zote mama Elly huwa hafungui mgahawa siku ya Jumapili kwahiyo mgahawa ule ulikuwa umefungwa tu,“Ila kwanini Erick umetaka kupafahamu?”“Basi tu, nimetaka tu kupafahamu”Basi walirudi nyumbani moja kwa moja, ila Jumapili hii mama Angel hakwenda kwenye Ibada badala yake alikuwa tu nyumbani na aliandaa chakula kwaajili ya wanae siku hiyo, na waliporudi tu waliweza kula chakula ambacho mama yao alikiandaa, muda mwingi Erick alionekana kuwa na mawazo ila walijua ni sababu ya kule kuumwa kumbe kichwa chake kilikuwa kimevurugwa na mambo ya Sia.Leo jioni mama Angel akiwa ametulia nyumbani kwake kwenye bustani, kuna ujumbe uliingia kwenye simu yake kutoka tena kwa Sia, basi mama Angel alichukia na kuamua kumpigia simu,“Hivi wewe mwanamke una matatizo gani lakini? Nimekwambia kama huyo Erick unang’ang’ania ni mwanao tukapime damu basi sio kuletea maneno yasiyokuwa na mwanzo wala mwisho, unanikera sana Sia hujui tu”Kumbe Erick alikuwa akielekea bustanini pia kwahiyo alivyofika pale alimpokonya mama yake simu na kuanza kusikiliza yeye ambapo alisikia sauti ya Sia ikicheka na kusema,“Unajua Erica usinichekeshe, hivi huoni kama huhyo mtoto hamjafanana nae hata kidogo. Nyie leeni tu lakini mnayemlea ni mtoto wangu, mwanamke una roho mbaya wewe yani unanikataza hata kuja kumuona mwanangu? Subiri tu, huyo Erick bado anakua, siku hiyo wakati ubongo wake umefunguka vizuri kuhusu mimi ndipo mtamuona akiwakimbia hapo nyumbani na kuja kwangu maana huyo ni mwanangu”Erick akakata ile simu bila ya kuongea chochote halafu akamrudishia mama yake yani mama Angel alishindwa hata kusema kitu kwa muda kidogo hadi pale Erick alipokuwa akiondoka na kumfata nyuma na kumwambia,“Mwanangu nakuomba upuuzie maneno ya huyu mwanamke tafadhari, naomba usiyajali kabisa”“Mama naona kichwa kinaniuma tu ila kiukweli maneno yake yamenichosha anafanya hata nisiishi kwa amani jamani!”“Usijali mwanangu, haijalishi chochote kile maana sisi tutabaki kuwa wazazi wako milele mwanangu, usiwe na mashaka”Erick aliondoka zake ila alikuwa na hasira sana.Usiku wa siku hiyo Erick hakulala kabisa maana alikuwa akimuwaza huyo huyo Sia tu ukizingatia alijikuta akiwa na hasira sana juu yake, basi usingizi haukumpata kabisa yani.Kulipokucha tu Erick alijiandaa kwenda shuleni kama kawaida na kweli alienda shule ila kwenye mida ya saa tatu aliaga na kusema bado hajisikii vizuri kwa siku hiyo kwahiyo alipewa ruhusa tu.Moja kwa moja Erick alienda kwenye mgahawa wa Sia, kwakweli Sia alipomuona alifurahi sana na kwenda kumlaki ila Erick alimkunja Sia na kumpiga ngumi ya sura ambayo ilimpeleka Sia hadi chini. Kulipokucha tu Erick alijiandaa kwenda shuleni kama kawaida na kweli alienda shule ila kwenye mida ya saa tatu aliaga na kusema bado hajisikii vizuri kwa siku hiyo kwahiyo alipewa ruhusa tu.Moja kwa moja Erick alienda kwenye mgahawa wa Sia, kwakweli Sia alipomuona alifurahi sana na kwenda kumlaki ila Erick alimkunja Sia na kumpiga ngumi ya sura ambayo ilimpeleka Sia hadi chini.Kisha Erick alimnyanyua tena Sia na kumpa ngumi nyingine ambayo ilimuangusha Sia tena chini na kumtoa damu mdomoni, halafu Erica alianza kumpiga Sia mateke pale chini tena alimpiga yasiyokuwa na idadi huku sura ya Erick ikionekana ni sura yenye hasira sana ikabidi Sia ndio amuombe msamaha kwa haraka,“Naomba unisamehe Erick, nisamehe sana, kwani kosa langu ni nini jamani? Naomba unisamehe”Kuna watu walisogea ili kuingilia ugomvi ule ila Sia aliwakataza watu wale, alijitahidi kuinuka pale chini na kumuuliza tena Erick,“Kwani tatizo langu ni nini?”“Sitaki unifatilie maisha yangu, naomba maisha yangu uyaache kama yalivyo, sitaki unifatilie kwa lolote”“Kwani nimekufatilia wapi tena baba?”“Maswala ya kumuandikia mama yangu ujumbe sitaki, nakwambia iwe mwanzo na mwisho, sitaki tena huo ujinga”“Nisamehe haitojirudia tena”“Nadhani hunijui vizuri, nina hasira sana mimi kwahiyo usitake nikufanyie kitu kibaya, nitakufanyia kitu ambacho hutokisahau hadi siku unayoenda kaburini, naomba uniache kama nilivyo, niache na maisha yangu”“Sawa baba nakuacha na wala sitakufatilia tena kwa lolote lile. Naomba unisamehe sana”Kisha Erick akaondoka zake, yani siku hiyo hakutembea na usafiri wala nini na alionekana kumpania tu Sia kwa siku hiyo.Erick alipoondoka Sia alirudi kwenye mgahawa na kukaa, kuna mfanyakazi wake alienda kumuuliza,“Kwani tatizo ni kitu gani mama?”“Acha tu, unajua kuna mimba zingine mtu ukipata unawaza kutoa toa basi ndio mimba ya huyu mtoto yani naona yale mambo ya kutoa mimba ndio yamejirudia”“Kwani ni mwanao huyo?”“Ndio ni mwanangu ila anampenda mtu mwingine kabisa ambaye sio mzazi wake wala nini, mtoto huyu ndio hasikii hatambui kwa mtu huyo halafu mama yake ananiona kama takataka jamani loh!”“Pole sana, ilikuwaje kwani mtoto wako hadi asikusikilize wewe halafu aende kumsikiliza mtu mwingine? Kwani karogwa au umempa malezi mabaya maana bado ni kijana mdogo kuacha kumsikiliza mama yake kweli!”Hapo Sia aliona mlolongo mrefu sana halafu alikuwa na maumivu na ile ngumi ya mdomo aliyopewa na Erick kwahiyo aliamua kumwambia huyu mfanyakazi wake amletee tu mahesabu maana yeye anaenda nyumbani kupumzika, kisha alichukua mkoba wake na kuondoka maana hakuwa katika hali nzuri kabisa.Muda huu Erick hakwenda kwao, kwani hakutaka mama yake ajue kama siku hiyo aliwahi kutoka shule na alipitia sehemu nyingine, kwahiyo moja kwa moja alienda kwenye duka la baba yake ambalo alimuweka Rama ili kuangalia maendeleo ya duka hilo maana hakwenda kwa siku nyingi kidogo.Alifika pale dukani na kukutana na Rama, kwakweli Rama alikuwa akimuheshimu sana mtoto huyu ingawa kiumri alikuwa ni mdogo sana kwake ila alimuheshimu sana, basi alimsalimia pale na kuanza kuulizana mambo ya pale dukani ila walipomaliza kuna kitu Rama alikigundua kuhusu Erick na kumuuliza,“Samahani bosi Erick, unaonekana kuwa na hasira sana leo”“Dah! Usiniite bosi, unajua kama mimi ni mdogo sana kwako lakini? Hela zisifanye heshima ishuke, unaniheshimu ndio, pia natakiwa kukuheshimu, una umri mkubwa tu kama baba yangu, na kwetu tuna pesa ila sio swala la wewe kuniita bosi, utanikweza sana na kufanya nisisonge mbele”“Oooh sawa Erick, tatizo ni nini kwani?”“Kuna mtu kaniuzi sana, sijui nikoje, huwa najaribu kuzuia hasira zangu ila najikuta siwezi yani huwa nina hasira sana, na afadhari nimemkuta na kumpiga kidogo ndio hasira zimepungua pungua”“Duh pole sana, ila usifikirie mtu wa hivyo upo peke yako. Mfano mimi ni mtu mzuri sana, nacheka, nafurahi naongea vizuri na kila mtu ila kitu cha kusingiziwa jamani huwa sikipendi hatari, yani hakuna kitu kinaniuma kama kusingiziwa maneno. Wewe ni mtoto mdogo ila kadri unavyokuwa utagundua jinsi maneno ya kusingiziwa yanavyouma, mimi nina mke na watoto ila kuna kipindi nikasingiziwa kuwa nimetembea na mdogo wa mke wangu, dah niliumia sana na ile habari ilitambaa hatari ila nilijitahidi kuidhibiti kwa niwezavyo. Kwahiyo usijishangae kuwa na hasira ni jambo ambalo huwa linamkuta yoyote pindi akifanyiwa asichokipenda”“Nimekuelewa, ila nafanyaje kushusha hasira hizi hadi nafikiria kurudi nyumbani maana sitaki mama anione nikiwa na hasira kiasi hiki”“Kunywa maji mengi, utaona tu hasira zinapungua zenyewe, unajua maji ni uhai katika maisha yetu. Tunapokuwa na hasira basi kuna kitu kinakaa kitika moyo hapa kinapanda hadi kooni, unahisi kimekukaba sana, sasa kunywa maji mengi kushusha hiyo hasira, ngoja nikakuchukulie”Basi Rama alienda kumchukulie Erick chupa za maji na kumletea pale basi alikuwa akinywa huku wakiendelea na mazungumzo mengine.Kwakweli leo Sia hakuwa na raha kabisa, alikaa nyumbani kwake akiwaza sana na kujiuliza maswali mengi mno,“Hivi Erick ni mtoto wangu kweli? Hapana jamani, hata kama mtoto hamjui mama yake halisi hata kama ni mtoto wa kuokotwa hivi anakosa kuwa na upendo halisi jamani! Yani Erick hana upendo na mimi hata kwa mbali, au kwavile nilimlea kipindi akiwa analia sana? Jamani mbona Erick kawa hivi dah! Nadhani sio mwanangu labda kuna kitu kingine kilifanyika ila yule Erick sidhani kama ni mwanangu, na nikikubali kupima damu na ikajulikana sio wangu basi anaweza kuninyonga yule maana mtoto anaonekana kuwa na roho mbaya sana yule”Kisha Sia akachukua simu yake na kumpigia baba Angel ambaye kwa muda ule ule alipokea ile simu, kisha Sia alijitambulisha na kuanza kuongea nae kwani alijua wazi kuwa namba yake haipo kwenye simu ya baba Angel ukizingatia yule baba Angel huwa hamkubali pia, basi alianza kuongea nae,“Samahani Erick kukupigia simu, hata sikupanga kukupigia ila imenibidi nikupigie”“Una shida gani?”“Kwanza jua kuwa mwanao Erick kanipiga sana leo, hata nahisi kuna baadhi ya meno yangu hayatakuwa sawa”“Aaaah acha masikhara jamani, yani Erick akupige!! Kwasababu gani lakini hebu acha zako”“Kweli nakwambia, yani Erick leo kaja kwenye mgahawa wangu na kunipiga, kuna ujumbe nilimtumia mkeo sasa sijui kamuonyesha Erick basi ndio Erick kachukia na kuja kwenye mgahawa wangu kwakweli kanipa kipigo cha hali ya juu hapa nilipo taya yote ya mdomo inaniuma, mbavu zote zinaniuma maana kanipiga sana mateke jamani”“Haya, pole sana”“Ila kitu nilichokupigia simu ni kwamba, kuanzia leo huyo Erick sio mtoto wangu na simtambui kabisa, ni mtoto wenu. SIkuzaa bondia mimi, sikuzaa mtoto asijielewa mimi, kwahiyo sitaki tena kusikia habari zake”“Kwani nani huwa anakupa habari za Erick? Mpigie anayekupa habari za Erick mwambie kuwa hutaki kusikia habari zake na sio mimi”“Sawa ila nimekupigia tu utambue kuwa simtaki tena Erick na sio mwanangu, mtoto ana laana yule”“Ushindwe na ulegee, laana unayo wewe na sio mwanangu. Ujinga wa kusema mwanangu ana laana sitaki kuusikia kabisa, kwaheri”Baba Angel alikata ile simu, kisha Sia nae aliamua kupumzika kwa muda huo kwani alikuwa na maumivu ya kile kipigo alichopokea toka kwa Erick, mpaka Elly anarudi kutoka shule alimkuta mama yake na hali mbaya, alimuuliza ila Sia hakumwambia ukweli kwani alijua lazima Elly akamfanyie fujo Erick, kwahiyo alimwambia tu kuwa alivamiwa na vibaka siku hiyo na walimpiga sana ndiomana amekuwa na hali ile mbaya, kwakweli Elly alimuhurumia mama yake na kuanza kumuhudumia kwa muda huo.Usiku wa leo, mama Angel alikuwa katulia ndani yani akiwa hana habari yoyote, basi alipigiwa simu na mumewe na kuanza kuulizwa,“Watoto nyumbani wanaendeleaje? Vipi Erick hali yake?”“Anaendelea vizuri, hata shule leo alienda. Na watoto wote wako salama, maana walisharudi na sasa wapo vyumbani kwao”“Leo chizi Sia alinipigia, akasema kuwa Erick ameenda kwenye mgahawa wake na amempiga sana, kweli Sia ni chizi”“Dah ni chizi kweli yule mwanamke, jamani Erick anaweza kufanya ujinga wa namna hiyo?”“Ndio hapo pa kumshangaa, eti Erick kampiga sana hadi taya inamuuma, sijui mbavu zinamuuma. Na kasema kuanzia leo hataki kusikia swala lolote la kusema kuwa Erick ni mtoto wake, eti hamtaki tena”“Kwani nani anamtaka? Atuondolee balaa sie”Basi aliongea nae pale na kuagana nae, kisha mama Angel aliamua kwenda kulala tu kwa muda huo.Kulipokucha kwa siku hiyo mama Angel alifanya mambo yake na kwenye mchana wa siku hiyo aliamua kwenda kiwandani maana jana yake hakwenda.Basi alifika pale na kukuta kupo salama kabisa, alimuita tu Yuda na kuongea nae vizuri,“Vipi soko lakini?”“Lipo vizuri, ila kuna jamaa mmoja hivi anapenda sana kuagiza bidhaa zetu hapa, ila kasema anatamani sana apelekewe bidhaa hizi na Erick”“Kheee anamfahamu Erick?”“Ndio, kuna siku aliwahi kuja ofisini na kuongea nae, kwahiyo anatamani sana aonane nae tena”“Basi nitaangalia uwezekano wa hilo jambo hakuna tatizo lolote”Basi alifatilia kila kitu na muda ule ule aliaga na kuondoka kwani pia alitaka kwenda hospitali kumuangalia Derrick.Basi aliondoka hapo na moja kwa moja kwenda hospitali kumuangalia Derrick, alifika pale siku ile alimkuta mama Derrick, dada yake Mage, pamoja na mama Junior, basi alifika na kusalimia pale ila hali ya Derrick kwa kipindi hiko ilionekana kutengemaa, alivyomsalimia ni kwamba Derrick alitaka kuongea nae kwa ukaribu zaidi,“Samahani Erica, naomba uje tena na yule Oliva maana nina maongezi nae”“Weee huyo Oliva hawezi kukubali jamani maana unajua kila kitu chako alishanieleza”“Duh! Alishakwambia?”“Ndio, tena kila kitu ulichomfanyia. Ingawa unaumwa jamani ila sikupenda kwakweli, wewe sio wa kufanya hivyo Derrick umekuwa na roho mbaya hadi shetani anaogopa jamani.”“Ila nahitaji sana kuongea nae, naomba mwambie kuwa nahitaji sana kuongea nae hata sio mambo hayo ila kuna mambo ya msingi sana nataka kuongea nae”“Sijui, nitajaribu ila sidhani kama atakubali usijipe moyo na usijipe asilimia zote. Nitaangalia uwezekano huo”“Sawa, nitashukuru”Basi waliongea ongea pale, kisha mama Angel pamoja na dada yake mama Junior waliondoka kwa pamoja huku wakiongea,“Kheee dada, toka huyu Derrick adundwe ndio umekuja leo?”“Hata hivyo nimekuja basi tu baada ya kusemwa sana na Mage ila hata sikutaka kuja kumuona huyu mjinga”“Alikufanyia nini tena?”“Kuna siku nilikuwa na laki tano ambayo mume wangu aliniambia niipeleke mahali, jamani si ndio likaja hili jinga likanitapeli ile laki tano yote, dah! Ugomvi mkubwa na mume wangu hadi kuanza na wanawake wengine si sababu ya hiyo laki tano yani ndoa yangu ilikuwa na hali mbaya sababu yake, jamani Deo alichukia sana kuhusu laki tano yake, ndipo kukatoweka maelewano kabisa, je napata wapi nguvu ya kuja kuliona hili chizi? Ndiomana sikutaka hata kuja, bila Mage nisingekuja kwakweli”“Oooh pole sana dada yangu, kwakweli Derrick tabia zake ni ngumu na hazivumiliki, anatutoa moyo wa kuja kumuona kwakweli ndiomana hata mimi siku nyingine nakuja na siku nyingine siji wala nini. Unajua Derrick huyu aliwatapeli wanangu laki moja, halafu akawatapeli laki tatu, jumla laki nne, halafu bila aibu alikuja na kunitapeli mimi laki tatu, kwa kifupi tu huyu Derrick ni sababu ni ndugu yetu ndiomana tunakuja kumuona vinginevyo hakuna mwenye hiyo habari naye kabisa”“Tena mtu unaweza shangaa unakufa halafu anayekulilia ni mamako mzazi tu sababu wote wamekuchoka, yani Derrick asipojiangalia atazikwa na jiji jamani maana hakuna hata ndugu yake anayemtaka, hebu ona hakuna mtoto wa mama yake hata mmoja aliyekuja kumuona. Mjinga sana huyu”Basi aliongea na dada yake na kupanda nae kwenye gari huku safari ikielekea ya kumpeleka dada yake nyumbani kwake tu halafu ndio yeye arudi kwake.Leo wakati Erica akitoka shule, kufika njiani gari yao ya shule ilipata hitilafu kwahiyo dereva alishuka kwaajili ya kuitengeneza na baadhi ya wanafunzi walishuka akiwemo Erica mwenyewe maana pale ilikuwa sio mbali na mgahawa wa mama Elly, basi moja kwa moja Erica alienda kumsalimia mama Elly ambapo alimkuta tu amekaa pembeni pale, basi alimsalimia na kuanza kuongea nae,“Mbona leo mama Elly umepoa sana?”“Mwanangu, wewe una roho ya tofauti sana, kwakweli wewe una huruma na upendo na una busara. Leo sikutaka hata kuja ofisini hapa ila nimekuja muda sio mrefu ili kuangalia biashara yangu imeendaje, yani alichonifanyia kaka yako ni Mungu tu anaju”“Ni nani na amekufanyia nini?”“Ni Erick, jana amekuja hapa na kunipiga sana yani kanipiga ngumi usoni na mateke ya kutosha tu, hapa nilipo mbavu zote zinauma, taya za mdomo zinauma, yani sina raha kabisa, kwakweli Erick alichonifanyia sio ustaarabu”“Kheee kwanini sasa?”“Anajua mwenyewe sababu zake, sijataka hata kumwambia Elly ukweli maana najua lazima angechukia ila Erica yule kaka yako kuwa nae makini sana maana ana roho mbaya sana tena roho ya kiuaji ila usiseme kama nimekwambia hivi maana kaahidi kuja kuniua”“Kheee jamani, mbona sielewi!”“Ndio hivyo”Mara Elly alitokea ambapo mama Elly aliamua kubadilisha mada, basi Erica alienda kumuaga dereva wao halafu yeye alisindikizwa na Elly tu kurudi nyumbani kwao.Basi wakiwa wanaondoka, alimuuliza tu,“Kwani mama yako anaumwa nini?”“Naelewa basi!! Ila analalamika mbavu zinamuuma sana, namuonea huruma sana mama yangu maana anahangaika sana halafu homa kama hivyo inamoata jamani.”“Mpe pole sana, najua hela itakuwa inawasumbua sana kwasasa ila msijali mimi nitajaribu kufanya kitu cha kuwasaidia”“Oooh asante sana Erica, kwakweli utakuwa umefanya kitu kikubwa sana katika maisha yetu”Basi Elly alimfikisha Erica kwao na kuagana nae ambapo Erica aliingia ndani kwao tu kwa muda huo.Muda mama Angel akiwa anarudi nyumbani kwake sasa ndio alikutana na madam Oliva njiani, basi akasimamisha gari na kuanza kuongea nae kuhusu swala la Derrick kutaka kuongea tena na yeye,“Mmmh labda Ijumaa maana hizi siku za karibuni nina mambo mengi sana”“Sawa hakuna tatizo, basi Ijumaa nitakushtua ili twende kumuona”Hakuongea nae sana kwani muda ule ule waliagana na kila mmoja alienda sehemu yake, ambapo mama Angel aliamua kuendelea na safari yake ya kurudi nyumbani kwake.Alikuwa amechoka kiasi, aliamua kwenda kuoga na kurudi kukaa na mtoto wake sasa, kisha alianza kumuuliza Vaileth jinsi anavyokaa,“Eeeeh Vai, mtoto huwa hasumbui?”“Hapana mama, huwa hasumbui”“Mwezi ujao nataka rasmi nianze shughuli zangu zote yani, unajua nikikaa kulea tu basi mambo mengi yatalala yani kuanzia kesho nitasimama imara kufanya mambo yangu yakae sawa.”Basi Vaileth alimsikiliza kidogo tu na kuondoka zake, ila mama Angel hakutaka kufatilia pia, aliona bora kwa muda huo aende kulala na mwanae tu, ila alipoingia chumbani tu alifatwa na Erica ambapo Erica alianza kuongea na mama yake,“Mama, hivi unajua kama Erick siku hizi kawa bondia?”“Kivipi?”Erica alianza kumuhadithia kile ambacho aliambiwa na mama Elly, basi mama yake akamwambia,“Erica usitake kunikera mwanangu, hebu fanya mambo mengine ya maana, achana na vitu vya kijinga kabisa, sitaki ufatilie tena mambo ya huyo mama. Hebu fanya mambo yako, achana na ujinga huo wa kuongea na huyo mwanamke, sitaki tena kusikia huo upuuzi Erica”Basi Erica alitoka chumbani kwa mama yake na kuondoka zake, kwakweli mama Angel hakutaka kusikia habari yoyote kuhusu Sia ndiomana alimtimua mwanae.Siku hii mama Angel alijiandaa kama kawaida na kwenda kiwandani kwake, basi alifanya shughuli zote za kiwanda na kuwahi kuondoka, ila nje alikutana na Rahim ambapo Rahim huyu alimsimamisha na kuanza kuongea nae,“Erica, leo naomba unisikilize wala sitaongea na wewe maneno ya karaha”“Haya sema unataka nini?”“Naomba kitu kimoja tu, nahitaji mwanangu Angel anifahamu, nahitaji afahamu ndugu zake, nina watoto wengi wakubwa kwa wadogo, naogopa isije kuwa balaa badae kwa watoto wangu kuoana”“Si ulisema mtoto akikua atakutafuta mwenyewe wewe! Imekuwaje leo?”“Hapana Erica, kuna muda mtu unasema kit utu ila badae roho yako inauma kwa kile ulichokisema, nakuomba sana, nakuomba Angel anifahamu baba yake. Nipo tayari kulipa kila kitu ambacho Erick amemuhudumia binti yangu Angel”Mama Angel alimuangalia bila kumjibu kitu chochote halafu aliondoka zake na muda huo moja kwa moja alielekea nyumbani kwake.Alishangaa siku hii kufika nyumbani alipoambiwa na Erica kuwa amerudi shule sababu anajihisi vibaya,“Nini tena mwanangu?”“Tumbo linaniuma mama”“Kheee nyie watoto jamani, ndio mmeanza majanga haya kila siku tena!!”Basi mama Angel akampatia mwanae dawa za maumivu, akasubiri kama tumbo litaendelea kumuuma basi ampeleke hospitali ila Erica hakulalamika tena tumbo ila hata mama Angel hakujua ukweli kama Erica alirudi sababu ya kuumwa tumbo tu au alikuwa na mambo mengine ila hakufatilia.Kesho yake Erica alienda shule kama kawaida, na siku zote alienda kama kawaida yani lile tumbo lililalamikiwa siku moja tu na wala hakulalamika tena.Siku hii mama Angel akiwa anatoka kwenye mambo yake, alimuona Sia njiani, akaamua kusimama ili na yeye amuulize kuhusu kupigwa na Erick, basi alisimamisha gari na kumuita ambapo Sia akasema,“Nilitaka nishangae hiyo roho mbaya umeanza lini kiasi cha kutokutaka kuniona wakati unajua nimepokea kipigo toka kwa mwanao!”“Ushaanza lawama jamani, mimi nakuuliza tu unaendeleaje na ilikuwaje maana hata sielewi ni kitu gani kinaendelea kwakweli”Basi Sia alianza kumueleza jinsi Erick alivyoenda na kumpiga na maneno aliyoyaongea, kisha Sia akamwambia mama Angel,“Naomba leo nikwambie ukweli wa kwanini nakazana kusema kuwa Erick ni mwanangu”“Eeeeh niambie huo ukweli niusikie, huenda nikakuelewa kuliko kila siku kuanza kutupiana maneno”“Ipo hivi, mzee Jimmy aliongea na mimi kuwa anataka kubadilisha watoto yani mtoto wangu akupe wewe na mtoto wako anipe mimi, nilimuuliza kwanini alisema kuna kitu anataka kugundua, akanilipa na hela nyingi sana, sababu ya shida zangu nikakubali tu. Sijui siku uliyopelekwa hospitali ni siku ambayo na mimi niliitwa hospitali yani nilifanyiwa operesheni bila ya kuwa na dalili zozote za kujifungua ilimradi tu mtoto atoke, na kweli nilijifungua ila nikamsikia mzee Jimmy akilalamika kuwa umejifungua watoto wa kike tupu, sijui alikuwa akinichanganya akili sijui ni kitu gani, maana alisema yeye hitaji lake ni mtoto wa kiume ndio ana kazi nae, ila nikashangaa nimeletewa mtoto wa kiume, basi nilirudi nae nyumbani kwangu nikijua ni mtoto wako ila yule mtoto alikuwa akilia sana. Ila alivyofika miaezi kama mitatu hivi mzee Jimmy akaniambia kuwa kipindi kile hawakubadilisha maana sijui alienda pale hospitali mama yako na akang’ang’ania awashike wajukuu wake mwenyewe, kwahiyo alisema anataka kubadilisha kwa kipindi hiko, nilimuuliza si utagundua maana mtoto wangu ni wa kiume na wako ni wa kike? Akasema alikosea kuangalia kumbe watoto wako mmoja wa kiume na mwingine ni wa kike, basi tulienda hospitali na mwanangu alichukuliwa baada ya muda nikaletewa mtoto ambaye niliambiwa ni mtoto wako, yani chanzo cha ugomvi wangu na Steve pia ni kuhusu mtoto kuwa kwanini mtoto wa mwanzoni alikuwa ni tofauti na mtoto wa pili? Ndio hapo alipochukia na kuondoka ila sikujali sababu nilikuwa na pesa. Baada ya siku chache mzee Jimmy alisema mmesafiri na kwenda Afrika kusini na watoto wenu, aliniambia nitafurahi sana kwani mwanangu atakuwa na maisha mazuri sana, na jina la Elly kwa mwanangu ni yeye ndiye aliyelitoa alisema sababu ni mjukuu wake, ila anahitaji Elly akikua afanye kisasi kwenu sababu mtamkataa. Sasa baada ya kifo cha mzee Jimmy, roho ilikuwa inaniuma sana, nilitamani Elly awajue wazazi wake halisi na Erick anijue mzazi wake halisi, ndiomana kila siku nasema kuwa Erick ni mwanangu”“Oooh leo nimekuelewa Sia na nimekuelewa vizuri sana tena sana, ila hapo nadhani kuna kitu kimejificha. Sidhani kama mzee Jimmy alikuwa na lengo la kunikomesha mimi maana aliyekukomesha ni wewe tena kakukomesha vibaya sababu hata huwezi jua mtoto wako wa kweli yuko wapi na huyo Elly ni mtoto wa nani, ila kitu kingine usikute Elly ndio mtoto wako halisi”“Kwanini?”“Ni hivi, mimi nilivyojifungua kwa kisu sikuwa katika hali nzuri, kiasi kwamba Erick alikuwa akinihurumia sana na kuona kuwa nahitaji matibabu ya hali ya juu, watoto wakiwa hawajatimiza hata mwezi tulisafiri nao kwenda nje kwaajili ya matibabu na tulikaa huko kwa miaka kama mitatu hivi, haya huyo Erick kabadilishwa muda gani? Hebu jitafakari tena kuna kitu mzee Jimmy alikuficha, yani marehemu huwa asemwi vibaya ila naweza kumsema vibaya yule mzee Jimmy, mzee ni mpuuzi sana yule dah! Ndiomana sikuwahi kumpenda ingawa alikuwa ni mkwe wangu. Ngoja tu niwahi nyumbani kwangu”Mama Angel aliamua kumuaga Sia na kuondoka zake kwenda nyumbani kwake yani hata hakumsikiliza zaidi.Siku ya Ijumaa kama ambavyo mama Angel alipanga na madam Oliva, basi moja kwa moja alimfata ili waende nae hospitali na yeye alikubali kweli kwenda hospitali kumuona huyo Derrick.Walivyofika hospitali walikuta hata Derrick karuhusiwa siku hiyo kwahiyo ndio wanajiandaa kwaajili ya kuondoka, ila muda kidogo alifika mama Sarah ambapo alipofika tu madam Oliva alionekana kuchukizwa sana kumuona mama Sarah, kiasi kwamba alimsogelea kwa hasira na kumkunja yani pale hospitali wote walikuwa wakishangaa tu lile swala. Walivyofika hospitali walikuta hata Derrick karuhusiwa siku hiyo kwahiyo ndio wanajiandaa kwaajili ya kuondoka, ila muda kidogo alifika mama Sarah ambapo alipofika tu madam Oliva alionekana kuchukizwa sana kumuona mama Sarah, kiasi kwamba alimsogelea kwa hasira na kumkunja yani pale hospitali wote walikuwa wakishangaa tu lile swala.Mama Angel akakumbuka kitu na kwenda karibu na kuwaachanisha kisha alimvuta madam Oliva pembeni na kumwambia,“Madam, wewe ni mwalimu tafadhari usijiondolee sifa yako kwa hizi fedheha, ni aibu kubwa sana kwa mwalimu kama wewe kuonekana kupigana na mtu au kurushiana maneno na mtu njiani”Basi madam Oliva alipumua kidogo na kusema,“Kwaheri, siwezi kukaa tena hapa hospitali”Ila mama Nagel alielewa na kumruhusu tu aondoke kwani madam Oliva alishamsimulia kila kitu kwahiyo muda huo alikuwa ameunganisha matukio tu.Derrick nae alishangaa kumuona mama Sarah kwani hakumuona kabla sababu mama Sarah alifika kipindi Derrick akiwa hoi kabisa na tangu kapata unafuu hakufika tena hadi siku hii ndio alionekana tena kwenda kumsalimia, basi Derrick akamwambia mama Sarah,“Manka, wewe mwanamke ni mjinga sana umekuja kufanya nini hapa?”Wote wakamuangalia kisha mama yake akamkataza na kumwambia,“Laiti ungejua kuwa mwanamke huyu alijitolea kukuhudumia wala usingemsema”“Kwani niliomba msaada wake? Hamjui tu huyu mwanamke ana akili mbovu kiasi gani, hamjui tu nawaambia”Basi mama Sarah hakutaka kuongea mengi na kutaka kuondoka zake, ila Derrick alisema anahitaji kuongea na mwanamke huyo ambapo walitoka nje, kisha kupanda kwenye gari na safari ikafanyika hadi nyumbani kwakina Derrick, na huko walitoa upenyo kidogo wa mama Sarah kuongea na Derrick,“Samahani Manka, mtoto wangu yuko wapi?”“Samahani Derrick, huujui ukweli tu”“Ukweli upi?”“Hukuzaa na mimi, kiukweli sina mtoto wako”“Sikuelewi Manka, najua wazi ile mimba ilikuwa ni yangu ila mtoto wangu ulienda na kumpa baba mwingine sababu ni tajiri na mimi ni masikini ukaona sifai, ila Manka nina kila sababu ya kumfahamu mtoto wangu na pia kuna kila sababu ya mtoto wangu kunifahamu mimi. Unajua kwanini nimepigwa sana?”“Sijui?”“Sababu mimi ni tapeli, unajua kwanini mimi ni tapeli?”“Sijui”“Sababu yako Manka, nimejaribu kufanya kazi tofauti tofauti ila bado malengo yangu ya kuwa tajiri hayakutimia, pale waliponifukuza kazi ndio wakaitibua kabisa akili yangu kwani malengo yangu ni kuwa tajiri ili nikikutana na wewe uone kweli Derrick amebadilika, nasema wazi kuwa wewe Manka ndio sababu ya kunifanya mimi niwe tapeli, kwakweli Manka ni asilimia kubwa sana umechangia katika kuharibu maisha yangu. Nadhani unamkumbuka yule mwanamke aliyekukunja pale hospitali, nina uhakika unamkumbuka sana tu”“Namkumbuka ndio”“Yule mwanamke alinipenda sana ila nilimuacha kwaajili yako Manka, ila wewe ukanifanyia mambo ya ajabu sana kwa kwenda kuuza mtoto kwa mwanaume mwingine, kwakweli sikupenda kabisa ulichofanya wala nini”“Unanilaumu bure tu, unaacha kujilaumu kuhangaika kwako na wanawake unakazana kunilaumu mimi, kuna kitu nilichokuwa nahitaji kwako kwa kipindi hiko, ukikaa chini na kutafakari utakijua, ila sijaja kukuona ili unipe lawama zako, kwaheri”Manka aliinuka na kutoka nje ambapo aliwaaga na wakina mama Angel ila mama Angel alimfata mama Sarah ili amuulize vizuri, alimuuliza,“Inamaana Sarah ni mtoto wa Derrick?”“Hapana, ila baba wa Sarah hakuhusu”Mama Sarah hakuangalia hata nyuma alivyolitoa jibu hilo kwani moja kwa moja aliondoka zake, basi mama Angel alibaki akimshangaa tu kwa muda kidogo kisha akarudi tena nyumbani kwakina Derrick ila hakutaka kukaa sana aliongea kidogo tu na kusema anahitaji kuongea kidogo na Derrick pia ili amuage.Mama Angel aliingia kuongea na Derrick kwa muda huo, basi alimuuliza swali la kwanza kabisa,“Huyu Manka ndiye mwanamke uliyezaa nae?”“Ndio ni yeye, ila mtoto kamkabidhi mwanaume mwingine”“Dah pole sana, ila usijali nitafatilia jambo hili. Na vipi kuhusu mtoto wa Oliva, wewe ndiye baba au?”“Mimi ndiye baba wa mtoto wa Oliva, ila sijui ni utoto sijui ni kitu gani, unajua kipindi kile sikuwa na kazi yoyote, bora yako hata ulikuwa ukifanya kazi kwa shemeji yako halafu akaja Erick na kukukomboa tofauti na mimi nilikuwa na shida sana, nikaona nikichukua majukumu ya kulea mtoto itakula kwangu, wakati huo Manka nae akisema ana mimba yangu basi ikabidi Oliva nimtoe sadaka, ila sikupenda ni umasikini tu”“Duh!! Huu umasikini ungekuwa una sauti basi ungeongea maana watu mnafnaya mambo ya kijinga halafu mnasingizia umasikini, kubali tu ulifanya makosa na sio kusingizia umasikini. Mimi nitajaribu kupoteza muda wangu na kwenda kuongea na Manka pia kwenda kuongea na Oliva”“Dah!! Utakuwa umenisaidia sana, nataka wanangu watambue uwepo wangu”Basi mama Angel kwa muda huo aliamua kumuaga na kuwaaga wote kwenda zake nyumbani kwake kama kawaida.Alipofika alikuta watoto wake wote wameenda kulala, basi alimuuliza Vaileth,“Mbona wanalala mapema sana hawa viumbe wangu?”“Sijui ila namuona Erica kama hizi siku za karibuni kabadilika kiasi, tofauti na ambavyo huwa akirudi shule anaanza kueleza habari mbalimbali ila toka siku ile karibu akiumwa na tumbo basi amekuwa akirudi tu anaishia huko huko chumbani kwake, akitoka ni kula kidogo na kurudi chumbani kwake, bora hata Erick, ila hata Erick kaniambia kuwa Erica alimfukuza chumbani kwake wakati akitaka kwenda kumuuliza tatizo linalomfanya awe mpole kiasi hiko”“Kheee anamfukuza hadi kaka yake?”“Ndio, sijui ana tatizo gani”“Jamani huu ubusy nao loh!! Nakosa hata muda wa kukaa na watoto kuuliza tatizo ni nini, hebu nikamuangalie kwanza”Basi mama Angel moja kwa moja alienda chumbani kwa Erica na kumuamsha kisha kumuuliza kitu gani kinachomsumbua ila Erica alijibu kuwa hana tatizo lolote na yupo sawa kabisa tu, basi mama Angel alimuacha pale mwanae na moja kwa moja kwenda chumbani kwake kujipumzisha.Basi muda kidogo akapigiwa simu na rafiki yake Johari na kuanza kuongea nae,“Kwakweli nakushukuru sana shoga yangu kule uliponipeleka, nimeweza kufungua mawazo yangu na sasa natengeneza vitu vyangu mwenyewe na kuvisambaza”“Oooh hongera sana, hiyo ni habari njema kwakweli”“Nakwambia shoga sasa hivi na mimi nitakuwa juu kabisa ya kinara, yani sasa hivi nitakufikia ila tutakuwa na sifa tofauti maana wewe ni hela za mumeo lakini mimi ni hela zangu nilizozitolea jasho”“Jamani Johari hata mimi nachakarika sio kujikalia tu nyumbani”“Uchakarike wapi? Wenzio tulizaa tukaacha na kupumzika huku tukiwaza vya kufanya, sasa wewe bado unazaa kweli kuna kuchakarika hapo? Kila utakapokuwa maziwa tu yanakuchuruzika”“Hayo mambo yalikuwa kwa mama zetu sio karne hii ndugu yangu, hakuna mwanamke wa kujibweteka. Watu na watoto migongoni wanachakarika sembuse mimi”Basi wakaongea pale na kuagana, ila mama Aliwaza kitu kuhusu ofisi yake ambayo hakwenda kwa kitambo kidogo, akaona bora kesho yake ajitahidi aende kuangalia ofisi yake inaendeleaje nayo, hakutaka kujibweteka ndiomana alikuwa akichakarika.Kulipokucha tu, mama Angel alijiandaa moja kwa moja na kwenda kiwandani kwani alishapanga siku hii aende kiwandani halafu akaangalie na ofisi yake ipo katika hali gani, kwahiyo alivyomaliza shughuli za kiwanda moja kwa moja aliamua kwenda kwenye ofisi yake ili kuangalia mambo yanaendaje kwenye ofisi yake, basi alifika pale na wafanyakazi wake walifurahi sana kisha aliingia ofisini na kuanza kuangalia kazi zake moja baada ya nyingine, alitumia muda mrefu kidogo, kiasi kwamba alipanga siku hiyo awahi kurudi nyumbani kwake ukizingatia ni Jumamosi lakini hakuweza kufanya hivyo kwani alikuta kazi nyingi zikiwa zinamsubiria, kwahiyo aliendelea nazo tu kwa muda huo.Muda kidogo alipigiwa simu na mume wake na kupokea ile simu,“Uko wapi mama Angel?”“Oooh sikukwambia mume wangu, nimekuja mara moja kwenye ofisi yangu huku”“Mama Angel, mimi kukuagiza mara moja ofisini kwangu sikuwa na maana kuwa muda wote unatakiwa kuwa ofisini, hebu tenga muda vizuri mke wangu, kuna watoto pale wanahitaji malezi yako ya karibu sana, na kuna mtoto mdogo Ester anahitaji maziwa yako muda wote, kweli kumuacha mtoto mdogo vile muda wote jamani mke wangu!”“Nisamehe sikukwambia ila Ester nilimkamulia maziwa”“Jamani mke wangu kwanini lakini? Wanawake ambao waume zao hawajiwezi wahangaike halafu na wewe uhangaike kweli jamani dah!”“Nisamehe mume wangu”“Oooh yani katika vitu vyote basi ni swala la kuomba msamaha, jamani Erica nakusifu kwa hilo ni rahisi sana kwako kuomba msamaha bila ya kujali uzito wa tatizo wala nini. Hivi unajua kinachoendelea kwa Erica mdogo!”“Kitu gani hiko?”“Unaona sasa, hata mwanao anasumbuliwa na kitu gani hujui sababu unakosa muda wa kuongea nae kama mama umuelekeze mema yanayotakiwa. Ni hivi kumbe Erica kakua, yani kamfata Sia ndio ambaye anampa maelekezo ya kufanya kitu gani na kitu gani ila wazazi hatujui chochote. Mke wangu naomba muda huu funga hizo kazi zako, rudi nyumbani waangalie watoto wangu, nahitaji watoto wetu wapate malezi bora”Mama Angel akapumua, kwanza kidogo habari ya Erica ilimchanganya, basi aliagana na mumewe na kufunga kazi halafu akaondoka muda ule ule.Mama Angel alikuwa njiani akifikiria sana, kuwa mwanae amekuwa halafu kashindwa kumwambia yeye na kwenda kumwambia Sia!! Kwakweli hapa alishangaa sana, alipokuwa anakaribia nyumbani kwake alikutana na Sia njiani, basi akasimamisha gari ili amuulize vizuri,“Yani mwanangu kakua kaja kukwambia wewe?”“Usishangae, siku zote mtoto huangalia sehemu ambayo ataweza kupata msaada kwa urahisi zaidi”“Kwahiyo kwako ndio sehemu ya urahisi kwake kupata msaada kuliko mimi mama yake?”“Sijui, ila nadhani kuna kitu huelewi kuhusu mwanao, anapenda sana kusikilizwa, anapenda sana kupewa kipaumbele na sio kuachwa nyuma nyuma, aliniambia kuwa akikwambia chochote huwa unamshushua sana ndiomana ameogopa kukwambia hili. Kwa kifupi ni kuwa mwanao kakua, mimi kama mzazi nimetumia muda wangu vizuri tu katika kumuelekeza swala zima la ukuaji na swala zima la kujistiri, kwakweli aliondoka akiwa na furaha na uelewa wa hali ya juu”“Haya asante”Mama Angel alirudi kwenye gari na kuanza kuelekea nyumbani kwake.Wakati amefika nyumbani kwake, kuna mtu alimkuta ndio anatoka, mtu huyo alikuwa ni wifi yake Tumaini, basi alishuka kwaajili ya kumsalimia pale, wakaongea mawili matatu,“Mbona mapema sana wifi yangu?”“Unajua nimekuja muda sana huku nyumbani kwako ila hukuwepo na nilijua leo nitakukuta nyumbani”“Ni kweli ungenikuta ila sijui hata nikueleze vipi, majukumu haya ndugu yangu”“Mmmh na wewe jamani, hayo majukumu ni majukumu yapi? Kusimamia watu nayo ni majukumu, mbona kutaka kujitia kazi ambazo zinakuzidi nguvu jamani! Mtoto unamuacha na Vai kila siku, kuwa na msichana wa kazi imekuwa tatizo? Tena wakati mwingine unaondoka asubuhi sana na kurudi usiku, sio siri wifi yangu jirekebishe, hatukatai watu tunakuwa na majukumu ila wakati mwingine tunatakiwa kuwa makini na majukumu yetu tunayoyafanya, wewe ni mama na unatakiwa kuwa makini sana katika ulezi wako”“Nimekuelewa wifi yangu ila nipo makini”“Wapi ndugu yangu? Makini!! Ungeshindwa kujua kuwa mtoto wangu kwasasa amekuwa mkubwa kweli?”“Unajua Erica huwa nazungumza nae mambo mengi sana kiasi hata sielewi ni kwanini hajaniambia kuhusu hilo swala jamani, unaweza kunilaumu bure tu lakini mtoto mwenyewe ndio tatizo”“Hapana na wewe kutokuwa makini, kwanza kwa kipindi chote hiki si ungekuwa ukijitafuti mwanangu bado tu kukua, mwanangu bado tu. Kuna watoto wanakua wakiwa darasa la sita, wengine la saba ila Erica kachelewa kiasi ingawa hajachelewa sana ila ungekuwa unajiuliza kama mama, na mtu kama Erica ungekuwa umemfundisha baadhi ya mambo kiasi kwamba angeona na kukufata wewe moja kwa moja. Unajua shuleni wanajifunza mengi sana, basi yeye kashajua mambo mbalimbali ndiomana alivyoona kaona bora akamwambie mama anayemsikiliza. Halafu kitu kimoja ambacho hujui kuhusu Sia, yani yeye akijua mtu huyu anapenda sana kusikilizwa basi atajifanya kumnyenyekea na kuwa nae karibu kiasi kwamba mtu huyo lazima awe anaenda kwake tu sababu ananyenyekewa sana, humsomi mwanao, unaacha mpaka machizi wajue kuhusu mwanao”“Nisamehe wifi yangu tafadhari”Aliamua kuagana nae maana Tumaini alisema kuwa ana haraka kwahiyo aliagana nae na yeye kuingia ndani kwake.Mama Angel alipoingia ndani tu, moja kwa moja alienda chumbani kwa Erica ambapo hakumkuta chumbani kwa muda huo na kutoka kumuuliza Vaileth,“Kwani Erica yuko wapi?”“Oooh yupo kule bustanini na Erick”Basi mama Angel akatoka na kwenda bustanini na kukuta kweli Erica na Erick wamekaa ila walivyokaa kama watu ambao sio ndugu kabisa, halafu kama maadui vile kwani walikaa mbalimbali, basi alipofika aliwasalimia pale na kuwaauliza kwanini wamekaa vile mbalimbali, Erick alimjibu mama yao,“Mama, sijui kwanini jamani ila Erica anafanya kazi ya kunikwepa tu sijui hata tatizo ni kitu gani, nilimfata chumbani kwake ili niongee nae ndio akaja huku, nimemfata napo ananikwepa”“Sawa, naomba niongee kidogo na Erica, wewe nenda tu ndani Erick”Basi Erick aliondoka na mama Angel alisogea karibu na mwanae na kuanza kuongea nae, kwanza alianza kumuelekeza kuhusu ukuaji na pia alimuelekeza kuhusu swala zima la kujiweka katika usafi, kisha kuanza kumuuliza,“Mwanangu kwanini lakini hukuniambia kama umekua?”“Niliogopa mama”“Uliogopa nini sasa?”“Ungesema nimeanza umbea tena maana ulisema nisikuletee tena maneno ya umbea”Ilibidi mama Angel afanye kazi ya kumuelimisha mtoto wake kuwa kwanini alisema vile na kuzidi kumuelekeza mtoto wake jinsi ya kuishi vyema na wazazi,“Yani mzazi ndio mtu wa kwanza wa kujua chochote kinachoendelea katika maisha yako, haya ni kwanini unamkwepa hivyo Erick?”“Yule mama kaniambia kuwa, nikiwa kwenye hali hii natakiwa kuwakwepa kabisa wanaume, sababu ukikaa nao karibu watagundua ndiomana namkwepa Erick”“Dah! Mwanangu unahitaji kupata somo la ziada kwakweli ili uweze kuielewa hiyo hali uliyokuwa nayo, ila usijali tupo pamoja”Kisha mama Angel alianza kumuelekeza mwanae namna ya kuendenda katika hali kama ile na jinsi ya kuishi na watu wote, na alimfundisha kutambua kuwa ile ni hali ya kawaida tu sema inahitaji usafi tu ili kuepuka harufu mbaya, na pia kuepuka magonjwa mbalimbali maana mtu ukiwa msafi ni ngumu kupatwa na magonjwa mengine kwahiyo kuna baadhi ya magonjwa yanaepukika kwa usafi tu”“Sawa mama, nimekuelewa”Basi mama Angel alimtoa hofu yoyote ambayo Erica alikuwa nayo, kisha ndio akaenda ndani sasa kufanya mambo yake mengine.Usiku wa leo, Erick alienda tena kuongea na Erica ili ajue ni kwanini Erica alikuwa akimkwepa sana kwa kipindi hiko, alimkuta muda huo akiandaa nguo ya kuvaa kesho yake, basi alianza kuongea nae,“Kwanini Erica ulikuwa unanikwepa? Kwanini ulikuwa ukinifukuza humu chumbani kwako?”“Samahani Erick, naomba unisamehe bure, ila sikuwa najihisi vizuri”“Yani ulishindwa kuniambia kama unaumwa? Ni mara ngapi unaniambia mambo yako Erica halafu ushindwe tu kuniambia kuwa unaumwa!”“Sio ugonjwa kama ugonjwa ila nilikuwa naumwa ukubwa”“Kheee ukubwa ndio nini?”“Kama hujui potezea”“Mmmh ndio kubunja ungo nini!”“Toka zako bhana, mimi sipendi mtu aniambie hivyo”“Basi sirudii tena, ila unaendeleaje kwasasa?”“Naendelea vizuri tu, natafuta nguo ya kuvaa kesho kwenye ibada, njoo unisaidie basi”Moja kwa moja Erick alimsaidia Erica kuchagua nguo ya kuvaa, na nguo aliyomchagulia ni ile ambayo aliwahi kumnunulia kwani alipenda tena kumuona katika nguo hiyo, kwahiyo walikubaliana kuwa kesho yake atavaa nguo ile, na muda ule Erick aliondoka na kurudi chumbani kwake.Kulipokucha kama kawaida walijiandaa vizuri kabisa na kwenda Kanisani, siku hii waliondoka wote pale nyumbani hata Vaileth aliondoka pia kwahiyo hakuna mtu ambaye alibaki nyumbani kwa muda huu.Ila leo ibadani kila mtu alikaa sehemu yake, muda kidogo Erica aliinuka ili kwenda maliwatoni, ila muda mwingi Erick alikuwa akimuangalia Erica kwahiyo alikuwa kama anaangalia muda alioinuka na muda atakaorudi.Erica moja kwa moja alienda maliwatoni, ila wakati anatoka kufika njiani tu kuna mtu alimshtua na kumsimamisha, alipogeuka mtu huyu alikuwa ni Bahati, basi alianza kusalimiana nae,“Kheee unafanya nini hapa kanisani?”“Huwezi amini, nimekaa kwetu nimejikuta nakufikiria sana, basi nikasema leo nije tu hapa angalau nikuone. Kidogo moyo wangu umeridhika”“Oooh sawa, basi mimi naenda”“Hapana, usiende, naomba tuongee kidogo”Basi Bahati akamvuta mkono Erica na kutoka nae pale kwenye eneo la kanisa kidogo na kuanza kuongea nae,“Unajua nakupenda sana, nahitaji uwe mpenzi wangu”“Kheee jamani, mimi haya mambo sijazoea kabisa, ni maneno gani unaniambia hayo?”“Nahitaji uwe mpenzi wangu Erica, nakupenda sana”Muda huo huo alitokea Erick mahali pale maana alikuwa akimtafuta Erica baada ya kuona kachelewa kurejea ndani ya Kanisa, basi alifika na kumshika mkono yani hakuongea kitu chochote zaidi ya kwenda nae tena Kanisani tu kwa muda huo.Wakati wanarudi nyumbani, mama Angel alimuona madam Oliva kwahiyo aliwaacha watoto wake kwenye gari waendelee na safari ya kurudi nyumbani halafu yeye akashuka na kumfata madam Oliva,“Oooh bora nimekuona hapa muda huu”“Kuna mahali nimetoka, halafu kuna kitu nilikuwa nasubiria hapa”“Najua hatukupata muda mzuri wa kuongea ile juzi, naomba tusogee kidogo pale kwenye mgahawa naomba muda wako kidogo tuzungumze”Madam Oliva alikubali na moja kwa moja walienda kwenye mgahawa wa hapo karibu na kukaa huku wakianza kuzungumza,“Kwanza kabla ya yote, kuna kitu nilihisi siku ile. Nadhani yule ndio mwanamke aliyeharibu penzi lako na Derrick, je nipo sawa?”“Ni sawa kabisa”“Ila kwasasa una maisha yako, umelea mwanao nina hakika umesamehe hayo yaliyopita, ila jamani kwanini ulimkunja tena?”“Mama Erick, yani yule mwanamke alinitenda vibaya sana. Kwanza kawa mpole ila alikuwa na nyodo sana yule mwanamke”“Haya tuachane na habari zake, vipi Derrick anaweza kumuona mtoto wake?”“Yule ni mwanangu na sio mtoto wa Derrick, mtoto yule anatumia jina la mbele la babu yake yani baba yangu, anaitwa Paul Paul, kiukweli huyo Derrick sitambui kama nilizaa nae katika maisha yangu ila ninachotambua ni kuwa kuna msumbufu mmoja nilikutana nae katika maisha, sina muda nae kabisa na simtaki tena”“Naelewa kabisa kuhusu hilo, ila kuna umuhimu wa mtoto kumfahamu baba yake”“Mama Erick hebu jaribu kidogo kukaa nafasi yangu. Eeeeh nimekumbuka kitu, yule Rahim aliniambia kuwa amezaa na wewe, nina uhakika mtoto aliyezungumziwa ni Angel, je anamfahamu baba yake? Ingekuwa anamfahamu, je Rahim angekuwa analalamika hadi leo kuhusu Angel? Wanawake tunapitia mengi sana ndiomana kuna muda tunafanya maamuzi magumu hata kuyafikiria, kwakweli mimi niache tu na furaha yangu ila Derrick asahau kabisa kama kuna mtoto yoyote alizaa na mimi”Mama Angel alipumua kidogo kwani yale maneno yalimuingia vilivyo ukizingatia ni kweli yeye hataki hata kidogo Angel afahamiane na baba yake, yani yupo radhi Angel asimfahamu baba yake maisha yote, sababu tu ya mambo ambayo bado anayakumbuka katika akili yake kuwa ni mabaya na hakupaswa kutendewa na Rahim ila yeye mwenyewe alikuwa kumbembeleza mwenzie ampeleke mtoto kwa baba yake, ila maneno ya sasa yalimuingia kwenye kichwa vilivyo na kuamua kuacha kwanza, alimwambia“Madam, hata sikulazimishi wala nini nilikuwa naongea tu. Najua alifanya makosa sana juu ya hilo, kutelekeza mtoto wake jamani! Kwakweli hajafanya vizuri kabisa”“Ndio hivyo, kwasasa nataka kuandaa harusi yangu na Steve, nahitaji mimi na Steve tuanze kuishi rasmi kama mke na mume”“Ila naomba nikushauri kitu”“Kitu gani?”“Kwanza kabisa mtafutie shughuli ya kufanya, si vizuri mwanaume kushinda nyumbani siku nzima kufanya shughuli za mwanamke, afanye kama kusaidia ila sio ndio kusema inakuwa kazi yake moja kwa moja. Msaidie kwa hilo ndugu yangu”Haya maneno yalimuingia madam Oliva na kuahidi kuwa atayafanyia kazi, basi waliagana na kuondoka zake.Mama Angel aliona ni vyema kama siku hiyo hiyo akiitumia pia kuonana na mama Sarah ili kuongea nae kuhusu mtoto wa Derrick, basi akachukua bodaboda pale na moja kwa moja kuelekea nyumbani kwa mama Sarah.Alimkuta mama Sarah yupo nje akimwagilia maua yake, basi alimsogelea na kumsalimia, kisha kumuomba kidogo waongee,“Mama Sarah, nina maongezi na wewe kidogo tu. Nakuomba kidogo tukae mahali tuweze kuzungumza”“Kuzungumza kuhusu nini?”“Mmmh kuhusu baba mzazi wa Sarah”“Wewe anakuhusu nini huyo baba mzazi wa Sarah?”“Nataka kufahamu ukweli”“Ukweli upi?”“Je baba mzazi wa Sarah ni Derrick?”“Hapana, baba mzazi wa Sarah ni mume wako”Mama Angel alijikuta akipumua tu kwa nguvu maana kama kitu kiligonga kwenye moyo wake. Alimkuta mama Sarah yupo nje akimwagilia maua yake, basi alimsogelea na kumsalimia, kisha kumuomba kidogo waongee,“Mama Sarah, nina maongezi na wewe kidogo tu. Nakuomba kidogo tukae mahali tuweze kuzungumza”“Kuzungumza kuhusu nini?”“Mmmh kuhusu baba mzazi wa Sarah”“Wewe anakuhusu nini huyo baba mzazi wa Sarah?”“Nataka kufahamu ukweli”“Ukweli upi?”“Je baba mzazi wa Sarah ni Derrick?”“Hapana, baba mzazi wa Sarah ni mume wako”Mama Angel alijikuta akipumua tu kwa nguvu maana kama kitu kiligonga kwenye moyo wake.Mama Angel alimuangalia tena mama Sarah na kumuuliza tena,“Unasema Sarah ni mtoto wa nani?”“Inamaana hujanisikia au? Sarah ni mtoto wa mume wako, Sarahni mtoto wa Erick, unataka nini lingine nikujibu?”Mama Angel akapumua tena na kumuuliza mama Sarah tena,“Hivi wewe si ndio umemuonyesha Sarah kuwa baba yake ni mzee Jimmy? Halafu saa hizi unasema ni mtoto wa Erick, wakati huo huo inasemekana kuwa ni mtoto wa Derrick. Lipi ni lipi?”“Mimi ndio mama mzazi wa Sarah, na hao wanaume wote watatu nimetembea nao, na mimi ndiye ninayejua ukweli halisi wa Sarah. Ukweli ni kuwa huyu ni mtoto wa Erick, nimemaliza. Kama imekuuma chukua chupa saga halafu meza vipande vyake”Mama Angel alikaa kimya kwa muda halafu mama Sarah aliendelea kuongea,“Kwanza wewe sio wa kushangaa kuhusu mimi na Erick, mbona mahusiano naye nilianza kitambo sana, kwani mimba ngapi za Erick nilizotoa? Yani wewe unaongea kama unatapika tu, hata hukutakiwa kufata ushahidi kwangu. Jiongeze tu huyu ni mtoto wa Erick ndiomana anakupenda na wewe unampenda, ndiomana akikuletea vitu unafurahi sababu damu ya Erick unayempenda ipo ndani yake, na mimi nampenda sababu nampenda Erick na kumpenda siachi wala usijidanganye kusema kuwa nimemuacha Erick, maana nikikutana nae lazima nikumbushie enzi”Safari hii mama Angel hakujibu kitu wala hakusema neno zaidi ya yeye kuondoka zake tu, aliondoka moja kwa moja na kwenda kusimamisha bodaboda na kuelekea nayo nyumbani kwake kwani alichoka mwili na roho kwakweli.Mama Angel alifika nyumbani kwake na kuwakuta wanakula, walimkaribisha mama yao nae alienda kujumuika nao kula ila alionekana kuwa na hasira sana, ilibidi Erica amuulize mama yake,“Mbona mama unaonekana haupo sawa?”“Ni kweli sipo sawa mwanangu, matatizo tu ya dunia”“Nini mama?”“Aaaaah msijali kitu”Kisha mama Angel alikula kidogo tu na kuondoka zake kuelekea chumbani na kwenda kuoga maana siku hii alitangulia kula kabla ya kuoga, ila akiwa chumbani kwake, leo kwa mara ya kwanza alifatwa na Erick mdogo ambaye alienda kumuuliza mama yake kuwa tatizo ni kitu gani kumbe hata yeye aliona tofauti ya mama yake ukilinganisha na siku zote,“Kwani mama tatizo ni nini? Unaonekana huna raha, yani kama una dukuduku moyoni tatizo ni nini?”“Kuna mtu nilienda kuongea nae leo ila alichonijibu sijapendezewa kabisa”“Mtu gani na alikujibu nini mama?”“Yani mama Sarah ana tabia mbaya, najuta kumfahamu yule mwanamke, kanichefua kabisa”“Mmmh kafanyaje kwani mama?”“Wewe bado mdogo Erick, kuna mambo hutakiwi kuyatambua kwasasa, kwahiyo neneda kalale tu”“Lakini mama….”Simu ya mama Angel ilianza kuita, na aliyekuwa akipiga ni mume wake, ilibidi Erick atoke na kumuacha mama yake akipokea ile simu na kuanza kuongea nayo;“Kheee mke wangu mbona leo unaongea kama mgonjwa?”“Dah! Nilienda kuongea na Manka bhana aka….”Mumewe akamkatisha na kumwambia,“Tafadhari usiniambie alichokwambia Manka maana sitaki hata kukisikia ila mke wangu tafadhari naomba uwe na amani katika moyo wako, acha kuwaza vitu tofauti ambavyo havipo kabisa. Unababaishwa na maneno ya Manka ya kazi gani hayo? Muone Manka ni mjinga kama wajinga wengine, umeweza kupotezea maneno ya Sia, ndio maneno ya Manka yatakuumiza kichwa kweli mke wangu! Hebu achana nayo, hata hivyo mimi karibia narudi kwahiyo usijali kitu”Kidogo mama Angel akawa na furaha na kuongea vizuri na mume wake kwa wakati huo.Kama kawaida siku hii, Erick na Erica walienda shuleni. Basi Erica alipokuwa shuleni akaanza kuongea na rafiki yake Samia maana Samia alipenda sana kumuelezea Erica mambo ya nyumbani kwao, na alipomaliza akamuuliza,“Hivi mamako na babako huwa hawagombani kweli?”“Mmmh sijawahi kuwasikia hata siku moja wakigombana, kwa kifupi baba yangu na mama yangu wanapenda sana”“Kheee mama yenu atakuwa na raha sana, nasikia mwanamke akipendwa ni raha sana”“Mmmh Samia?”“Kweli nakwambia, mke wa kwanza wa baba nasikia hakupendwa na baba hata kidogo, alikuwa anapigwa huyo hadi huruma, jana nilienda kwa bibi ndio nikayajua haya. Ndiomana mtoto wa yule mwanamke ana roho mbaya sana, nasikia baba alikuwa hampendi huyo mwanamke hatari. Baba hadi akataka kuoa mke wa pili, ila alipokuwa na mama wala wazo la kuoa mke wa pili hana”“Kumbe baba yako anampenda sana mama yako eeeh!”“Nilikuwa najua hilo mpaka sakata la jina la Erica lilipoanza, nilimuuliza bibi kuhusu huyo Erica, uzuri ni kuwa bibi yangu huwa hafichi kitu yani yeye anasema kila kitu unachotaka kukijua, kumbe kuna mwanamke alikuwa akiitwa Erica, nasikia huyo mwanamke ndio alikuwa roho ya baba, yani baba alimpenda sana ila huyo mwanamke alikuwa na tabia mbaya sana kwani alitembea na familia nzima ya baba”“Duh!!”“Habari ndio hiyo, kumbe majina yenu ya Erica yana mambo sana. Usiwe hivyo shoga yangu, unajua ukitembea na familia nzima unajiharibia sifa ya kuwa mwanamke, yani kama mimi ningetembea na Junior, halafu na Erick yani ningejiharibia sifa zaidi”“Mmmh ila huyo Erica alikuwa na tabia mbaya sana loh! Sijampenda hata kidogo”“Ndio hivyo ila nasikia baba anampenda sana huyo Erica, hapo ndio nimejua kumbe baba hampendi mama wala nini ila kuna mtu wake anayempenda, ila nitakueleza kwa upana zaidi”Mara kengele ya darasani ikapiga na wote kurudi darasani kwaajili ya kuendelea na masomo.Wakati wa kutoka shule, Erick alionekana kumkwepa Sarah ila Sarah alifanya kila jitihada za kuhakikisha anakaa na Erick siti moja ili amuulize,“Kwanini Erick unanikwepa hivyo?”“Sijapenda alichojibiwa mama yangu na mama yako”“Kivipi yani?”“Mama yangu kamfata mama yako kistaarabu tu kumuuliza kitu halafu yeye kamjibu vibaya mama na kumfanya ashindwe hata kulak wa raha”“Jamani dah! Kumbe ni hivyo, nitaongea na mama maana hata mimi sipendi kitu cha namna hiyo”Basi Erick alifika na kushuka, siku hii Erick na Erica walifika muda sawa nyumbani, kwahiyo waliingia kwa pamoja huku wakiongea ongea baadhi ya vitu vinavyoendelea,“Jamani Samia kaniambia kuwa majina ya wakina Erica hawajatulia, jamani mbona mama yetu ni mpole sana?”“Achana na maneno ya huyo Samia, kakwambia hivyo ili ujihisi vibaya ila achana nae, hawajatulia kivipi? Anaugua nini huyo, kutulia kwa mtu sio jina bali ni tabia tu, mbona yeye hajatulia, ndio aseme wakina Samia hawajatulia wakati wapo wakina Samia ambao ni wapole kabisa, mwehu sana huyo.”Kiukweli Erick hakutaka habari za Samia toka kipindi cha Junior basi alimtoa thamani Samia.Walifika nyumbani kwao na mama yao walimkuta kawapikia chakula kizuri sana leo, kwahiyo walienda tu kubadili sare za shule na kujumuika nae katika chakula.Kwakwlei kilikuwa ni chakula kizuri na wote walikula huku wakikisia kile chakula,“Leo nimeamua kuingia jikoni mwenyewe watoto wangu, mara moja moja nitakuwa nafanya hivi nifanyavyo, nahitaji watoto wangu mfurahi na muwe mara nyingine mnapata ladha ya chakula changu”Wote wakafurahi huku wakila na kuongea mambo mbalimbali.Leo Sarah aliporudi tu nyumbani kwao, alimsubiri mama yake arudi na aliporudi tu alianza kuongea nae,“Mama kwanini umemjibu vibaya mama Erick”“Kivipi?”“Erick kaniambia kuwa mama yake jana hata hakuwa na furaha sababu alikuja kuongea na wewe sijui ukamjibu vibaya”“Kheee huyu Erica sasa nahisi anataka kunipanda kichwani, nimemjibu vibaya muda gani? Kesho nitamfata ili niongee nae, mtu nina mawazo yangu kibao halafu anatokea mwingine wa kuniongezea mawazo, dah wanadamu bhana, wana mambo sana”Kisha mama Sarah akamuuliza kitu kingine mwanae,“Kuna jambo lingine ambalo amekwambia zaidi ya hilo?”“Hapana mama, hakuna lingine”“Sawa, nitaenda kuongea nae”“Ila mama, kiukweli mimi nampenda sana Erick, nataka awe mpenzi wangu”“Kheee kumbe ndio lengo lako hilo?”“Ndio mama, nampenda sana yani”“Sawa, unahitaji nikusaidie vipi mwanangu?”“Nisaidie kumpata mama”“Usijali na utampata tu, tena umeniambia kitu kizuri sana cha mimi kulipiza kisasi”“Kulipiza kisasi? Kivipi?”“Bado mdogo wewe, ila usijali nitakusaidia kumpata huyo Erick na atakuwa wako, usijali kitu ukiwa na mimi elewa kwamba kila kitu kinawezekana”Sarah alifurahi sana kusikia vile, yani aliona ni raha kwenye moyo wake sana.Leo jioni, Sia akiwa nyumbani kwake, alifatwa na Elly akiwa ametoka shuleni na barua mkononi na kumpa mama yake, ile barua ilimtaka Sia kumaliza ada ya mtoto, basi Sia akapumua na kusema,“Yani hapa ndio huwa mambo yananishinda jamani, nikiwa mpole kidogo tu mambo yataharibika, sitaki mwanangu ufukuzwe shule, niliahidi kukusomesha na kwa hakika nitakusomesha ili badae ujue umuhimu wa mimi mama yako. Ingia ndani tu ukale chakula”Basi Elly alienda ndani kwenda kula chakula kilichoandaliwa na mama yake. Sia alibaki kuwa na mawazo kiasi huku akifikiria ni kitu gani cha kufanya kwa muda huo,“Mmmh itabidi kesho nijitoe muhanga tu nikazungumze tena na Erica, ndio anasema Elly sio mwanae ila anipe msaada kidogo wa kumlea Elly, siwezi peke yangu kwakweli, mimi ni mwanamke, sina mwanaume nitaweza kweli kulea mtoto mwenyewe!! Siwezi kwakweli”Akapata na wazo jingine kuwa ampigie simu baba Angel ili ajaribu kumuomba msaada, na kweli alipopiga simu tu baba Angel alipokea ile simu na kuanza kuongea nae,“Samahani Erick, nakuomba nipo chini ya miguu yako msaidie mwanangu”“Kitu gani?”“Mwanangu anafukuzwa ada, nahitaji asome kama watoto wengine, nahitaji afike mbali naomba unisaidie”Muda huu baba Angel alikata tu ile simu yani hakumjibu kitu chochote kile kwa muda huo kwani hakutaka ukaribu sana na huyu mwanamke ukizingatia aliitambua akili yake kwahiyo alijia akijiingiza nae tu itakuwa ni tatizo kwake na familia yake.Basi Sia hakuwa na namna ya kufanya zaidi ya kwenda kulala tu, yani alilala akiwa na mawazo sana kwa siku hiyo.Kulipokucha tu, Sia alijiandaa na moja kwa moja kwenda nyumbani kwa mama Angel yani alipishana kidogo tu na muda ambao wakina Erica waliondoka na kwenda shuleni. Basi alifika na kumtaka mama Angel waongee pale nje yani kwenye kibaraza, ambapo mama Angel alitoka na kuanza kuongea nae,“Eeeeh unashida gani asubuhi asubuhi?”“Samahani Erica, najua kama mna uwezo na mnaweza kufanya chochote mnachojisikia sababu mnapesa. Watoto wenu wanaishi vizuri na kusoma shule nzuri bila ya mawazo yoyote, wanakuja kuchukuliwa kwa usafiri na wanarudishwa kwa usafiri. Tofauti na mimi sina uwezo wowowte, naishi maisha ya kawaida sana, ila napenda mwanangu nae apate elimu ile ambayo watoto wenu wanaipata, nikakwepa garama za usafiri kwa mwanangu kwenda shule kwa mguu na kurudi kw amguu, anasoma shule nzuri ndio ila hatumii usafiri wala nini, hilo sio tatizo kwangu wala sio tatizo kwake kwani anasoma vizuri tu na maendeleo yake ni mazuri. Kilichonileta hapa ni kumuombea msaada mwanangu kwaajili ya ada, kwani nahitaji nipate pesa nimlipie mwanangu ada na asiweze kufukuzwa shule wala nini”“Kheee huo ustaarabu umeutoa wapi? Na aliyekweambia mimi nina hela za kufanya chochote nikitakacho ni nani? Hata kwenye rekodi ya matajiri mia hapa nchini huwezi kukuta jina langu wala jina la mume wangu, haya huo utajiri wa kusifiwa hivyo ni utajiri gani? Hata sisi tunamaisha ya kawaida kabisa, unatakiwa ugangamale mwenyewe kama sisi tunavyogangamala na watoto wetu”“Dah sikutegemea kama utanipa jibu kama hilo”“Kwahiyo ulitegemea ukija kuniambia hizo habari basi nitaingia ndani na kutoa milioni mbili na kukukabidhi mjinga kama wewe. Mimi mwenyewe nipo kutafuta hela, kutwa kucha kiguu na njia hata mtoto wangu namuacha nyumbani ili nikatafute hela zingine kwaajili ya wanangu wasije kupata shida, ila wewe usiyekuwa na akili upo makini kuomba msaada, nitolee uchizi wako mie”Leo tena Sia hakuongea mengi ila alitoka tu moja kwa moja huku akiwaza mambo yake tu kichwani, alikuwa akiwaza cha kufanya huku akijisemea,“Nikiwa mpole hakuna ninachokipata, naambulia kejeli tu halafu nikiwa mkorofi oooh Sia wewe ni mkorofi sana, sasa wanataka nifanye nini na mwanangu ana shida!!”Aliwaza sana huku akiondoka eneo lile ila alikuwa kifikiria mambo mengi tu ya yeye kuweza kufanya katika eneo lile.Jioni ya siku hiyo, mama Sarah alijiandaa ili kwenda kuongea na mama Angel, yani yeye hakutaka yale maneno waliyoongea kuhusu baba yake mzazi na Sarah basi Sarah ayafahamu, hakutaka kabisa mwanae kufahamu kuhusu swala hilo. Basi moja kwa moja aliondoka na kwenda hadi kwa mama Angel, ila alipokuwa getini yani kabla hajagonga, kuna mtu alimshika bega, basi aligeuka na kumuangalia, ila ile sura ilikuwa ngeni kiasi ila yule mtu alimvuta pembeni na kuanza kujitambulisha kwake,“Naitwa Sia, umewahi kuniona mara moja tu. Nahitaji unifahamu zaidi maana mimi kwa kiasi Fulani nakufahamu wewe”“Mmmh!”“Ndio, tusogee kidogo tuzungumze”Basi mama Sarah alisogea pembeni na Sia kwenda kuzungumza nae,“Najua kama ulikuwa una mahusiano na Erick, je hapa umefata nini kw amkewe?”“Kwani wewe ni nani?”“Hata mimi nimewahi kuwa na mahusiano na Erick, ni mengi sana Erick aliyonitendea ila toka amekuwa na huyu mwanamke basi mimi ananiona kama kidudu mtu, ananijibu vibaya, nimezaa nae ila hataki kumjali mtoto wangu hata kidogo”“Kheee kumbe umezaa nae?”“Ndio, mtoto anaitwa Elly, yani Erick hataki kukubali hata kidogo kuwa huyo Elly ni damu yake, ananifanyia visa kila siku, nina shida hapa nilipo hadi kwenye makalio ila sio Erick wala sio mkewe wanaotaka kunisaidia”“Kheee pole sana, kwahiyo umelea mtoto mwenyewe siku zote?”“Ndio, yani nimehangaika na mtoto mwenyewe toka mchanga, mwanangu karudishwa ada, nimejaribu kuomba msaada kwa Erick ila nimeishia kukatiwa simu tu, nimejaribu kumfata mke wake ili nimuombe msaada ila alichonifanya yule mama ni Mungu tu anajua, kanitimua kama mwizi, kaita na mlinzi anitoe, kuna muda najuta mimi, najuta kumfahamu Erick, najuta kuzaa nae, ila maji yakimwagika hayazoleki”“Oooh pole sana jamani, yani umenitia imani sana ndugu yangu nimekuhurumia kwakweli, pole sana”“Asante, hapa hata sijui nitafanyeje”“Nahitaji kumuona mtoto wako halafu nitakwambia cha kufanya”“Twende nyumbani kwangu ukamuone”Basi Sia aliondoka na mama Sarah hadi nyumbani kwake, ni kweli Elly alikuwepo nyumbani kwa muda huo maana alikuwa ameshatoka shuleni, basi walifika pale na Elly aliwasalimia vizuri sana kiasi cha kumfanya mama Sarah ampende sana Elly yani alijikuta akivutiwa nae tu, basi alikaa pembeni na kuzungumza na Sia,“Mtoto wako anaonekana ana heshima sana!”“Ndio, kutokana na malezi niliyompa, yani mwanangu huyu kwakweli nampenda sana ndiomana nahangaika hivi kwaajili yake”“Sasa nikwambie kitu?”“Niambie”“Mimi nina shule, naomba unipe ruhusa ili Elly akasome katika shule yangu, bure kabisa hatolipa chochote na atakuwa akichukuliwa na gari la shule na kurudishwa na gari la shule”“Dah kama ndoto vile, mwanangu alikuwa akisoma shule nzuri ila alikuwa akienda kwa mguu na kurudi kwa mguu maana nilishindwa kulipa hela ya usafiri. Nashukuru sana”“Basi Kesho nitakuja kumchukua na kumpeleka kwenye shule yangu huku ukifatilia uhamisho wake”“Asante sana”“Usijali, tutaongea mengi zaidi, yani ikiwezekana hata siku nyingine awe anakuja kuishi nyumbani kwangu”“Kheee una moyo wa upendo sana, asante. Ila hata jina sijakuuliza jamani”“Mimi naitwa Manka, au mama Sarah”“Oooh nafurahi sana kukufahamu Manka, namshukuru sana Mungu kwa kunikutanisha na wewe”Basi wakapeana mawasiliano kisha mama Sarah akaagana na Sia na kuondoka zake.Mama Sarah hakwenda tena kuongea na mama Angel wala nini kwani moja kwa moja alirudi nyumbani kwake, na kukuta hata mwanae amesharudi ambaye alimuuliza mama yake kwama ameshaenda kuongea na aliyesema jana,“Umeenda kuonana na mama Erick mama?”“Mmmh nimeenda ndio, na tumeelewana, hata usiwe na tatizo mwanangu ila kuna kitu kikubwa sana nataka kukifanya kwako”“Kitu gani hiko?”“Ni siku nyingi sana umetamani kupata ndugu yako, nitakuletea ndugu yako natumai utampenda sana”“Mmmmh mama, ndugu yangu gani tena na anatokea wapi?”“Usijali, ni mtoto niliyeamua kumlea kwahiyo atakuwa ni ndugu yako”Mama Sarah aliongea mengi na mwane, kisha usiku ulipoingia kila mmoja alienda kulala, yani usiku wa leo mama Sarah alishangaa sana akimfikiria Elly, yani upole wa Elly ulimvutia sana, hadi alitamani Elly kuwa mtoto wake kabisa, basi akawa anajisemea,“Yani Erick anakataa mtoto kama Elly kweli!! Basi mimi nitamtunza Elly kwa niaba yake halafu ataona kuwa kati ya mimi na Erica ni nani mke mwema!”Yani alijikuta usiku wote akimfikiria Elly tu.Kulipokucha mama Sarah alijiandaa na kama alivyopanga, aliondoka nyumbani kwake na kwenda nyumbani kwa Sia kwa lengo la kumchukua Elly ili akamkabidhi kwenye shule yake.Kwakweli Elly alifurahi sana baada ya kuona yule mama kafanya kama alivyoambiwa na mama yake, kisha aliondoka nae kwenye gari lake kumpeleka shuleni, basi wakiwa kwenye gari Elly akauliza,“Itabidi sare za shule nipate zingine mama?”“Ooooh nimekupenda bure wewe mtoto, una heshima sana jamani. Ni kweli inatakiwa upate zingine ila usijali shuleni pale sare zipo yani unavaa na kuingia darasani. Oooh mtoto upo vizuri sana wewe”Mama Sarah alimfikisha Elly shuleni na kumkabidhi kwenye uongozi wa shule ile na kuongea nao ambapo moja kwa moja walimpeleka kumpatia sare kisha kumpeleka darasani ili akaendelee na utaratibu wa masomo kama wengine.Elly alipelekwa darasani na mwalimu na kutambulishwa pale kwa wanafunzi wengine, kwakweli muda huo Erick hakuwepo darasani ila aliporudi tu na kumuona Elly alishangaa sana kisha akauliza na watu wakamwambia kuwa ni mwanafunzi mpya, moja kwa moja alihisi ndio mambo yale yale ya yule mama aitwae Sia yanaendelea, basi Erick akasimama na kwenda uwani kwanza, huko alijiuliza,“Kwahiyo kile kimama kimeleta tena mtoto wake kwenye shule ninayosoma ili iweje? Ana mpango gani na mimi? Sikipendi kile kimama, nakichukia kabisa”Kisha Erick alirudi tena darasani, ila kadri alivyomuona Elly alikosa raha kabisa yani, hadi akawaza kuwa bora aende kiwandani tu ukizingatia hajaenda kwa siku nyingi sana.Akaona ni vyema aende kuomba ruhusa kuwa anaumwa, maana hapo shuleni toka Erick kazimia baada ya kuchapwa kiboko walianza kuwa na uoga nae sana kiasi kwamba kila kitu walimuhurumia mno, akisema anaumwa basi walitoa ruhusa kwake haraka sana kwani waliogopa watakayotokea, kimoyomoyo Erick alikuwa akijisemea,“Bora nikazane na kazi za kiwanda tu, naona shule naletewa maadui kila siku”Basi akamalizia kupata ruhusa yake na kuondoka zake.Kwavile Sia alishaelekezwa na mama Sarah kuhusu shule anayopelekwa Elly, aliona ni vyema siku hiyo akitoka kwenye mizunguko yake basi aende kuona tu ile shule ilivyo, basi asubuhi hiyo alianza kwenda kwenye mgahawa wake kwanza, halafu aliamua kwenda shule ambayo alikuwa anasoma Elly ili kumuombea uhamisho.Aliongea na walimu pale ili kupata utaratibu mzuri,“Tutamuandikia uhamisho ila unajua kuwa mwanao alikuwa anadaiwa? Bado anadaiwa laki tatu”“Duh walimu nitaitoa wapi mimi, nimekuja tu kuomba msaada ili muone jinsi gani mtanisaidia. Unajua sio kwamba nimemuhamisha ila mwanangu kapata tu msamalia ndio kampeleka kwenye shule yake, nawaomba walimu”“Ngoja tujadili ila mwanao anadaiwa hapa shuleni”Sia alijaribu kuwashawashi pale ila wale walimu walionekana kutokuelewa kabisa, basi moja kwa moja aliamua kuwaaga na kuondoka, kwa muda huu alienda moja kwa moja kwenye shule aliyoelekezwa na mama Sarah kuwa Elly kapelekwa hapo.Kufika pale shuleni alishangaa kumuona Erick akiwa anatoka shule, alitamani kujua kuwa Erick anaelekea wapi basi aliamua kumfatilia nyuma yake, Erick alivyopanda bodaboda naye akapanda bodaboda kumfatilia.Erick kufika kiwandani akashuka ila hakuwa ametembea na hela siku hii kwahiyo alienda ndani ya kiwanda ili kumuomba yule msimamizi wa pale kwenda kumlipa yule wa bodaboda, basi Yuda alimuacha Erick ofisini na yeye kutoka nje ili amlipe wa bodaboda ila alipofika tu nje ndio Sia nae alikuwa amefika na kushuka, ila Yuda alipomuona Sia alimshangaa sana na hata Sia alimshangaa Yuda yani hawakutegemea kuonana pale. Yuda alimuacha Erick ofisini na yeye kutoka nje ili amlipe wa bodaboda ila alipofika tu nje ndio Sia nae alikuwa amefika na kushuka, ila Yuda alipomuona Sia alimshangaa sana na hata Sia alimshangaa Yuda yani hawakutegemea kuonana pale.Basi Yuda alimfata karibu Sia na kumuuliza,“Sia, yuko wapi mtoto wangu?”“Mtoto wako? Unasemaje wewe!”“Unajifanya huelewi eeeh, si ulinifata wewe kipindi ulikuwa ukitaka mtoto wewe!”“Nitolee balaa mie, kwanza sikufahamu”“Unasemaje wewe? Hunifahamu mimi wakati unanifahamu fika mjinga wewe, tulikubaliana vizuri, unapafahamu hadi kwangu”“Usiniharibie siku, ungetaka ungenitafuta mapema sio unitafute kwasasa na kuniuliza kuhusu mtoto, mimi nifanye nini na wewe? Kwanza una uhakika gani kuwa huyo mwanamke ulivyokutana nae ulimpa mimba? Na nikufuate wewe ili unipe mimba, sikuwa na wanaume wengine? Hebu niache mie sikufahamu wala nini!”Yuda alionekana kukasirika, alitaka hata kumnasa vibao Sia, ila yule dereva wa bodaboda aliyemleta Erick alikuwa akitaka hela yake, kwahiyo ilibidi akamlipe kwanza, muda yeye anamlipa Sia nae alipanda tena ile bodaboda aliyoenda nayo na kumtaka aondoke muda huo, kwahiyo Yuda alishangaa tu kwa Sia kuondoka na ile bodaboda, akawaza pa kumpata tena yule Sia hakujua, na hakujua kama kuna mtu aliyekuwa akifahamiana na Sia pale kiwandani.Yuda alirudi tu kiwandani huku akiwa amenyong’onyea sana hata Erick alimuona na hiyo hali, alimuuliza kuwa tatizo ni kitu gani,“Yani acha tu, Erick wewe bado mdogo ila ngoja nikwambie hili. Kuwa makini sana na mwanamke unayekutana nae kimjini mjini wengi ni matapeli”“Kivipi?”“Katika ujana wangu huko, kuna mwanamke nilikutana nae, nikamtongoza sababu nilitokea kumpenda, ila siku niliyomtongoza alinikubali siku ile ile na nilipomwambia niende kulala nae alikubali na nilienda nae hadi nyumbani kwangu kwani ni kweli nilimpenda, ila tulipomaliza alisema kuwa alikuwa akihitaji sana kupata ujauzito na kwa muda huo ana uhakika kuwa atakuwa amepata ujauzito, tuliongea mengi sana ikiwa ni pamoja na mimi kwenda kujitambulisha kwao na kila kitu hata kumuoa. Ila alipoondoka pale kwangu hakutaka tena kupokea simu zangu na kunibadilishia namba kabisa baada ya kumsumbua sana, yani sijaonana nae tena hadi leo ndio nimemuona hapo nje ya kiwanda na anadai kuwa hanifahamu, ila sijui mtoto wangu yuko wapi jamani dah!”“Pole sana, ni kweli mimi bado mdogo na mengi siyajui, ila una uhakika kuwa kweli alipata mimba? Una uhakika kuwa kweli ana mtoto wako?”“Sina uhakika ila nahisi tu kuwa ni hivyo, maana kwa jisni alivyoondoka siku ile ilionyesha lile swala lake la kupata mimba limefanikiwa”“Unaweza kujuaje kama mwanamke kapata mimba yako?”“Aaaah wewe bado mtoto mdogo, mengine ni ya kikubwa zaidi, ukikua nitakuelekeza namna ya kugundua. Yani kuna namna Fulani mwanaume huwa unagundua kuwa huyu mwanamke nimempa mimba, na hata akikwambia nina mimba yako wala hushtuki”“Aaaah sawa, nikikua nitakuuliza tena hili swali. Kwahiyo nikiwa na umri gani ndio nitakuwa nimekua?”“Ukimaliza kidato cha nne, nitakwambia mengi sana hata usijali”Kisha muda huo kila mmoja alienda kuendelea na kazi za hapa na pale mule kiwandani.Leo Erick alipomaliza kazi za kiwandani aliwahi kuondoka sababu alitaka kupitia dukani pia ili akaangalie maendeleo ya lile duka lao.Ila akiwa njiani alikutana na Juma, ambaye alimsimamisha na kuanza kuongea nae, sababu Erick alitembea ili akapande daladala kwa muda huo, basi Juma alianza kumuuliza kisa cha yeye kutembea kwa muda ule, Erick alimuelezea tu kwa kifupi kuhusu kilichomkera hadi kuamua kwenda kuona biashara,“Erick, kila siku nakwambia ila hutaki kunielewa. Shule sio sehemu sahihi kwako, achana na shule fanya maisha”“Sasa wazazi wanataka nisome kwa bidii”“Nimekwambia ukisoma ndio utapata faida gani? Katika maisha ya sasa ukijua kujumlisha, kutoa, kuzidisha na kugawanya inatosha, ukijua kusoma na kuandika basi umemaliza mchezo, unataka kitu gani tena Erick? Hebu acha ujinga, sekondari kwenyewe ukifatilia masomo yake ni marudio tu ya kile ambacho umejifunza shule ya msingi ila wenyewe wanaongeza kidogo tu ili kuichanganya akili yako. Kuwa makini Erick, hebu amka achana na mambo ya shule hayotokusaidia kitu chochote”“Mmmmh huwa nahisi nikiacha shule, basi baba atachukia sana na anaweza hata kunifukuza nyumbani”Juma alicheka sana na kusema,“Erick usinichekeshe, sasa baba yako ana sauti gani pale nyumbani kwenu? Yani huwa unaona kitu akipanga baba yako bila mama yako kutia idhini kikafanikiwa? Nakwambia baba yako hana sauti yoyote juu ya mke wake, yani mama yenu kamuweka baba yenu katika kiganja chake. Kwahiyo baba yako hawezi kukufukuza hata iweje”“Mmmmh, mama akinifukuza je?”“Anawezaje kufanya hivyo ikiwa wewe ndio mtoto wa kiume pekee kwenye familia yenu. Hebu amka Erick, unatakiwa uushike uchumi wa familia kwenye kiganja chako, achana na mambo ya shule hayatakusaidia chochote kile. Na ukiona familia nzima imekuzingua utakuja kuishi na mimi kwanza kwani najua lazima watakuhitaji tena, achana na mambo ya shule, hayana msaada wowote katika maisha yako”“Mmmh nimekusikia, ila ngojea kwanza nifanyie kazi swala lako”“Sio ufanyie kazi, unatakiwa kuchukua hatua kuanzia sasa. Nitakununulia na simu ili tuwe tunawasiliana maana kwenu nako wana mambo ya kizamani sana”Basi Erick aliamua kuagana nae kuwa anaenda dukani, basi kwa muda ule aliachana nae halafu Erick aliendelea na safari yake ya kwenda dukani kwao.Alipofika dukani alimkuta Rama akiendelea kuuza kama kawaida, basi alimsalimia pale na kuanza kuulizana kuhusu kinachoendelea pale dukani, aliangalia bidhaa na kuongea kuhusu mambo mbalimbali, kisha walianza kuongea ya kawaida,“Vipi hali yako iko vipi kwasasa?”“Aaaah naendelea vizuri kwakweli”“Hujawatena na hasira?”“Unajua duniani kweli kuepeka vitu vya kukuudhi ni kazi sana, yani shule ninayosoma wamemleta adui yangu pale kwahiyo nitakuwa nasoma nae, sijapenda ile kitu hata kidogo ila tu sina cha kufanya wala nini”“Kheee pole sana, kwahiyo inakupa kero eeeh!”“Kwakweli sipendi hadi niliamua kuondoka na kuanza kuzungukia biashara za baba bila kupanga maana sikupanga kuja huku leo. Natamani hata kuhama shule”“Oooh usihame shule kama hiyo shule wanafundisha vizuri kazania tu, kwani tatizo ni nini? Kwanza huyo kwanini unamchukia? Usikute sio adui yako ila kuna mtu anayefanya mgombane”“Sijui kwanini namchukia, nimejikuta simpendi tu”“Sikia Erick, ukiwa shuleni jali masomo yako yani soma kwa bidii ila mengine achana nayo. Wewe soma tu kwani elimu inamsaada mkubwa sana katika maisha”“Ila mbona kuna mtu huwa ananishawishi kila siku niache shule na nifanye biashara?”Rama alishtuka kidogo na kumwambia Erick,“Ooooh Erick, wewe ni kama mwanangu au mdogo wangu, ngoja nikwambie kitu. Mtu anayekushauri uache shule mkimbie mtu huyo kama ukoma, hakufai kabisa, sio kila mtu anayeacha shule anapenda, hakuna wengi utakuta ni sababu hawana akili za darasani ndio wakaacha shule, au wengine ni sababu ya ada, ila shule ni ya muhimu sana. Ukiwa na elimu basi itakusaidia sana katika swala la utafutaji wa pesa, mimi mwenyewe huwa natamani ningesoma sana basi ingekuwa ni furaha sana kwangu. Nakushauri mdogo wangu usiache shule tafadhari, shule ni muhimu sana katika maisha. Naweza kukwambia kuwa shule ndio afya ya maisha”“Sawa nimekuelewa”“Weka kwenye akili yako kuwa shule ndio afya katika maisha, shule ni zaidi ya kazi utakayopata, ni zaidi ya biashara utakazofanya maana utakuwa umeongeza upeo katika kichwa chako. Mtu uache shule sababu imekubidi kufanya hivyo ila sio sababu ya mtu asiyekuwa na mawazo ya mbele kukwambia kuwa uache shule, usiache shule Erick”Erick aliongea mengi sana na Rama kwa siku hii, kisha waliagana na moja kwa moja yeye kuondoka zake na kurudi nyumbani kwao.Wakati Erick akielekea nyumbani kwao, alikutana njiani na mama Sarah ambaye alimsimamisha na kuanza kumsalimia, ila huyu mama leo alikuwa kawaida tofauti na siku zile ambazo alikuwa akilia akimuona tu, basi alianza kuongea nae pale,“Kheee umetoka wapi muda huu Erick? Nina uhakika hujatoka shuleni”“Ni kweli, nimetoka kuangalia duka letu”“Umemuona Elly, nimemleta leo kwenye shule yenu pale”Erick alikaa kimya kwa muda, kisha akamjibu kuwa kamuona, halafu mama Sarah aliendelea kuongea,“Unajua mimi ni mama wa tofauti sana, nina roho ya tofauti. Siwezi kuona nina mali halafu mwingine ateseke tu wakati uwezo wa kumsaidia ninao. Nimeamua kumsaidia Elly, kwasasa atasoma pale akiwa chini ya uangalizi wangu”“Oooh vizuri kwa hilo, hongera sana”“Kuna kitu amewahi kuniambia Sarah kuwa anakupenda sana wewe na ameshawahi kukwambia, je wewe unasemaje?”Kwanza Erick alimshangaa kwani hakuelewa kama Sarah na mama yake wana akili zinazofanana, basi akaanza kumwambia,“Ni kweli aliniambia ila nilimwambia kuwa sisi bado ni wadogo tunatakiwa kukazana na masomo, halafu vile vile mama aliniambia kuwa Sarah ni ndugu yangu, natakiwa kumuheshimu kama dada yangu”“Alikwambia undugu wako na Sarah upo vipi?”“Alisema kuwa Sarah ni mtoto wa babu yangu”“Aaaah kumbe mama yenu ndio ana akili mbovu kiasi hiko! Naomba twende pamoja”Erick hakumuelewa huyu mama ila aliondoka nae tu hadi nyumbani kwao, ambapo mama yake alikuwa ametulia tu ndani basi aliambiwa kuwa kuna mgeni anamsubiria nje, ikabidi atoke na alimkuta yupo kibarazani akimsubiria, basi alimsogelea ila mama Sarah akasogea pembeni zaidi na mama Angel na kuanza kumuuliza,“Kwahiyo ndio umewaambia wanao kuwa Sarah ni ndugu yao?”“Ndio, kwani si ndugu yao kweli?”“Sasa mbona umewaambia ni mtoto wa babu yao, kwanini usiwaambie kuwa ni mtoto wa baba yao? Si nilishakwambia kuwa Sarah ni mtoto wa Erick? Usipotaka kukubali ukweli basi Sraah na Erick watakuwa pamoja halafu wewe utajieleza mwenyewe kwa huyo mume wako, nimemaliza. Sarah ni mtoto wa Erick, hayo maswala mengine unayatafuta tu”“Sawa, hata kama ni mtoto wa Erick, bado undugu wao uko pale pale, hata awe mtoto wa Derrick, bado ni ndugu tu yani sijui unaongelea kitu gani. Na mimi sio wa kuwaambia hawa kuwa Sarah ni mtoto wa baba yao bali baba yao mwenyewe ndio atakuja kuwathibitishia hilo. Sina mengi ya kuongea pia, usitake tugombane bila sababu Manka”Mama Sarah akacheka na kusema,“Huyo mumeo akirudi niambie halafu utaona kitakachoendelea baina yangu na yake, sikia nikwambie Erica, mimi na wewe hatulingani wala hatufanani. Mimi ni mzuri tena ni mzuri sana, ukiangalia rangi tu lazima ukae chini ukubali kuwa mimi ni mzuri, na huyo Erick ningetaka kuolewa nae basi angenioa tu sema sikutaka kuoana nae ndiomana akakukazania wewe, ila Erick ananipenda hadi kesho”“Jamani Manka, unajua nilijua haya mambo umeacha. Sasa unajisifia uzuri kweli ndio utakusaidia kitu gani? Usiandikie mate wakati wino upo, huyo huyo mwanao Sarah nenda kamuulize leo kati yako na yangu nani mzuri halafu jibu lake kaa nalo moyoni na ujitafakari, uzuri unapimwa katika sehemu nyingi tu. Mwanao akishakujibu mwambie akupe na sababu za jibu lake. Nimemaliza pia, tumekuwa watu wazima sasa na sio kushindana kwa uzuri na ubaya ili itusaidie kitu gani? Hebu kua basi jamani, kwaheri”Mama Angel hakutaka hata kupoteza muda wake kwani aliamua kuingia ndani, hata mama Sarah aliamua kuondoka tu kwa muda huo.Mama Angel alipoingia ndani, moja kwa moja alienda chumbani kwa Erick ili amuulize maswali mawili matatu maana hata yeye hakuelewa kabisa mantiki ya yule mama kufika pale, basi alimuuliza na Erick alimwambia alivyokutana na yule mama na kile ambacho aliongea na yule mama, kwakweli mama Angel alisikitika sana na kumuona mama Sarah ni kama mtu aliyechanganyikiwa, ila Erick hakumwambia mama yake kuhusu Elly kusoma pale shuleni kwao.Kwakweli mama Sarah yale maneno ya mwishoni ya mama Angel yalimuingia vizuri tu, kiasi kwamba aliporudi tu nyumbani alimfata mwanae na kuanza kumuuliza, kwanza alimuuliza kama aliweza kumuona mgeni aliyempeleka,“Mmmh sijamuona mama”“Sawa, nitakutambulisha tu hakuna tatizo lolote lile”Kisha mama Sarah alimuuliza sasa maswali mengine,“Hivi Sarah unamuonaje mama Erick?”“Kivipi mama?”“Je ni mwanamke mzuri”“Ndio ni mzuri tena ni mzuri sana”“Mmmmh kivipi?”“Yule mama ana roho nzuri sana halafu ana upendo, yani mama yule ni mzuri wa sura na ni mzuri wa moyo”“Mmmh kushinda mimi mama yako?”“Jamani mama kwani kuna kushindana hapa? Mimi nimemuongelea yule mama, kwakweli sijaona ubaya wake na huwa ananifundisha mambo mazuri tu. Mama, mimi siwezi kupika ila unajua yule Erica anajua kupika kila aina ya chakula? Ni sababu ya malezi aliyoyapata kutoka kwa yule mama”“Jamani mwanangu, yale sio malezi ila ni kutesa mtoto. Kumbuka mimi nakupenda na sipendi uungue na moto huko jikoni ndiomana nikaweka mdada wa kazi mwanangu, nakupenda. Kwahiyo unataka kujifunza kupika?”“Hata sijui kama nahitaji kujifunza au la, ila naona kujua kupika ni raha sababu unapika kile unachokitaka”“Sawa mwanangu, usijali nitakufundisha kupika. Eeeeh kitu kingine cha kusema kuwa yule mama ni mzuri?”“Wakina Erick wana shangazi zao, wana bibi yao mzaa baba, wana wakina baba mkubwa na wadogo ila mimi hakuna ndugu wa baba ninayemfahamu hata mmoja, toka mama umesema baba yangu amekufa imekuwa ndio basi tena”Mama Sarah akaelewa hapo kuwa ile kitu pia inamsumbua mwanae, basi akamuahidi kuwa atamuonyesha ndugu wa baba yake, kisha aliondoka muda ule na kuelekea kufanya mambo mengine tu kwani aliona kichwa chake kikivurugika tu.Kulivyokucha, leo wakati Sarah akijiandaa kwenda shule, mama Sarah nae alijiandaa na kwenda nae pamoja huku akimwambia kuwa anataka kumtambulisha kwa huyo mwanafunzi mgeni aliyempeleka, ila alipofika shuleni tu alipigiwa simu na Sia kuwa waonane, ikabidi amuache Sarah aingie shuleni halafu yeye alienda kuonana na Sia ambapo alifika kwenye mgahawa wake, basi alianza kuongea nae,“Biashara yangu ndio hii ya mgahawa, ilikuwa inaenda vizuri sana ila hapa katikati ikasita kidogo kwani nilikuwa sifanyi vizuri kutokana na kipigo nilichopata”“Kipigo tena? Ulipigwa na nani?”“Yani siku hiyo nikiwa hapa mgahawani, alikuja Erick mdogo yani mtoto wa Erica, uwiiii sijui alisikia maneno gani kwa mama yake, yani alinipiga ngumi hizo balaa, nilianguka akanipiga mateke yasiyokuwa na idadi, baada ya hapo mwili wangu ukawa dhaifu sana maana nilikuwa naumwa mbavu na mwili wote”“Duh pole sana, yani Erick huyo ndio kakupiga kiasi hiko?”“Ndio, Erick huyo, kanipa kipigo sana. Kanidhalilisha mno hadi nikashangaa kwanini ameamua kunifanyia hivi alivyonifanyia jamani, kwakweli sina raha kabisa kwa hiki ambacho Erick kanifanyia”“Oooh pole sana”“Sasa, nimefatilia uhamisho kule shule aliyokuwa anasoma Elly, nimeambiwa ana deni la laki tatu, yani hata sielewi, na biashara bado haijakaa sawa.”“Oooh pole jamani, ila hiyo sio tatizo maana nitalipa. Nielekeze tu shule ambayo alikuwa akisoma Elly awali au twende wote ili nikamalize mambo yote”“Ngoja basi niache vizuri hapa”“Au nielekeze tu”Ilibidi Sia amuelekeze tu mama Sarah, ambapo alipoondoka muda huo moja kwa moja alienda hadi shule ambayo Elly alikuwa akisoma awali, na kumaliza kila kitu huko.Ila wakati anakaribia kuondoka alikutana na mwalimu wa nidhamu wa pale shuleni ambaye alikuwa ni mwalimu Haruni, ila walivyoonana tu waliweza kukumbukana,“Kumbe Haruni unafundisha siku hizi?”“Ndio, je wewe uliacha ualimu?”“Hapana sijaacha, ila mara nyingi huwa nafundisha mara moja moja kwa watoto wanaohitaji kufundishwa twisheni za binafsi yani mimi ndio huwa nafanya mambo hayo”“Kheee madam, yanalipa?”“Tena sana tu, kumbuka najitoa kwenda kumfundisha mtoto mmoja tu kwahiyo nalipwa hela ndefu, hata hivyo nina miradi yangu mingi tu. Na pia nina shule yangu”“Hongera sana, wengine bado tumegangamala na kazi za kuajiriwa ndugu yangu”“Ila vipi, hujaoa hadi sasa?”“Aaaah historia ndefu sana, ila na wewe yule mbaba wako nadhani atakuwa mbabu siku hizi bado upo naye?”“Acha zako hizo jamani”“Nipe mawasiliano yako basi, tuwe tunawasiliana Manka”Basi mama Sarah alimpa Haruni namba yake, kisha waliagana na muda huo mama Sarah kuondoka zake kuelekea shule aliyompeleka Elly yani aliamua tu kufata utaratibu ingawa angeweza kumuhamisha tu na utaratibu huo walimu wenyewe ndio wangefatilia.Alipofika shuleni aliomba kuitiwa Elly na pia aliomba kuitiwa Sarah, basi walipofika aliwatambulisha pale ili wafahamiane, kwakweli Sarah alionekana kufurahi sana kumfahamu Elly basi waliongea kidogo na kurudi kila mmoja kwenye darasa lake.Leo mama Angel alijiandaa kwenye mida ya saa nne ili aende kwenye ofisi yake, basi kama kawaida alimuachia mtoto Vaileth halafu yeye aliondoka zake kuelekea kwenye kazi yake. Alipoondoka tu ndipo Vaileth alipoweza kuwasiliana na Junior na kumwambia kuwa mama yao katoka, na kweli baada ya muda mfupi tu Junior alifika pale nyumbani,“Unajua nini Vai, yani nimepanda pikipiki ili niwahi hii nafasi, kasema anarudi muda gani?”“Nadhani ni jioni ndio atarudi, hata akiwahi tutamfanyia ujanja, cha muhimu uwe umemuelekeza vizuri mlinzi”“Nimemuelekeza ndio kuwa akiwa anakuja tu anitonye, yani hii nafasi sijataka kuiacha kabisa, huwezi amini nilivyotoroka shule leo sababu yako Vai, kwakweli nakupenda sana jamani”Basi kama kawaida mtoto aliachwa pale sebleni na wao walienda chumbani ili kukumbushiana mambo yao ambayo huwa wanayafanya.Muda wakiwa chumbani, alifika Tumaini pale na kukuta mtoto akilia, basi aliingia na kumchukua huku akiita Vaileth ila kimya kilitawala maana Vaileth alikuwa ndani, basi akawa anajiuliza,“Jamani, huyu binti kaenda wapi kwani na kuacha mtoto loh! Ndiomana watu huwa hawaamini mabinti kama hawa jamani”Muda kidogo Vaileth alifika na kumsalimia Tumaini,“Shikamoo shangazi”“Mjinga sana wewe, ulikuwa wapi na kuacha mtoto akilia hapa?”“Nilikuwa kuoga shangazi”“Haya, yuko wapi huyu mamake?”“Kaenda kazini”“Aaaah jamani, kashaanza tena mambo ya kwenda kazini kweli dah!! Yani huyu jamani”Basi muda ule ule Tumaini alimpigia simu kaka yake na kuanza kuongea nae,“Hivi mama Angel si ulishamwambia swala la yeye kukaa nyumbani na kulea watoto”“Ndio nilimwambia hivyo”“Basi na leo katoka na kuacha huyu mtoto mdogo akiwa na Vai tu hapa, nimekuta Vai kaenda kuoga na mtoto analia tu. Unajua kuna wakati unatakiwa kuwa mkali kwa Erica, bila hivyo utalia nakwambia”“Ngoja nikwambie kitu dada yangu, weka akilini hiki ninachokwambia. Hakuna kitu ambacho kinatendwa na Erica halafu mimi nisijue au hakuna kitu ambacho kinafanywa na mimi halafu yeye asijue, kwahiyo kama umekuta ameondoka hapo nyumbani ujue kuwa ameniambia hilo na mimi mwenyewe ndio nimemruhusu kufunya hivyo”“Ila nimekuta mtoto akilia jamani Erick”“Mimi na Erica tumefahamiana kabla ya huyo mtoto, kwahiyo usiwe na wasiwasi maana mke wangu ajua kile anachokifanya”“Kheee, haya sitakwambia tena kuhusu chochote. Yani Erick kuna mambo huwa sitaki kukwambia sababu hiyo hiyo, yani utafikiri mtu uliyerogwa jamani, huwa unaongea kama unatapika. Nishachefukwa hapa, kwaheri”Tumaini aliinuka kwa hasira na kumuaga Vaileth ambapo vaileth alimbembeleza mtoto na alipolala akarudi tena chumbani alipokuwa na Junior na kuanza kuongea nae,“Jamani huyu shangazi yenu nae ana visa sana, ila inavyoonekana baba anamjua vizuri”“Kafanyaje tena?”“Kampigia simu baba, halafu kaweka sauti kubwa kwahiyo nilikuwa nasikiliza kila kitu, kamlalamikia kuhusu mama jamani kashushuliwa balaa”Vaileth akawa anacheka huku akimsimulia yale maongezi,“Tatizo la shangazi yule sijui vipi. Wale wanapendana kwahiyo mambo mengi lazima waambizane, anafikiri mama anakurupuka tu kuondoka hapa bila ya kuongea chochote na mume wake? Yani shangazi yule nae loh! Ngoja tumalizie halafu nile niondoke asije akanikuta bure maana akianzaga na yeye balaa”vaileth alikuwa akifurahi tu kwani kwa kipindi hiko alijikuta akipenda sana kuwa karibu na Junior kuliko kitu chochote.Mama Angel alipomaliza kazi zake, alijiandaa vizuri kurudi zake nyumbani kwake kwani hakutaka agundulike kuwa aliondoka nyumbani kwake, basi alipokuwa akitoka ofisini kwake, kabla hajapanda kwenye gari yake akashikwa bega, kugeuka akamkuta Rahim ndio kamshika bega, akamuangalia kwa dharau sana kwani kwa kipindi hiko alijikuta akizidi kumchukia,“Una shida gani na wewe?”“Shida yangu ni wewe Erica, napenda utambue ni jinsi gani nakupenda Erica”“Sikia kwanza, naomba unisikilize kwa makini, sitaki huo ujinga wako wa kunipenda, niache kama nilivyo na maisha yangu. Nina mume wangu, na wewe una mke wako, hayo maswala ya kupendana yanatoka wapi? Sitaki huo ujinga Rahim, sitaki kabisa, achana na mimi”“Sawa, ila vipi kuhusu mtoto wetu Angel?”Mama Angel alimsonya Rahim na kuingia kwenye gari lake halafu akaondoka zake kwani hakutaka kuongea nae kabisa na aliona akimchefua tu kwa wakati huo.Wakati anatembea na gari yake, alipita karibu na mgahawa wa Sia, na kusimama kumsikia kwa muda huo ana jipya gani la kumueleza,“Oooh naona umesimama ili kuangalia naendeleaje? Unajua wewe huwa roho mbaya unaiigiza tu ila huiwezi hata kidogo Erica, huiwezi roho mbaya wewe yani unaiigiza tu”“Unaongelea nini?”“Ila usijali, sitakusumbua tena kuhusu Elly maana amepata mfadhili na atasomeshwa maisha yote, sema lingine”“Kheee bado una hayo hayo tu jamani, unaendeleaje lakini? Nimekuona ndiomana nimesimama ili nikusalimie”“Naendelea vizuri tu hata usiwe na wasiwasi juu yangu”“Haya, kwaheri”Mama Angel aliondoka na gari lake kwa muda huo na kurudi moja kwa moja nyumbani kwake tu, alimkuta Vaileth ametulia na mtoto sebleni maana muda huo Junior alikuwa ameshaondoka, basi alimsalimia pale na kuanza kuongea nae,“Vipi leo hajasumbua huyu?”“Aaaah hajasumbua mama, ila kuna muda nilienda kuoga akaamka na kuanza kulia, basi alifika shangazi Tumaini na kuchukia sana”“Kheee pole, najua lazima kakufokea sana”“Aaaah sio kunifokea ila alikuulizia, nilipomwambia haupo akachukia zaidi na kumpigia simu baba ila akaweka sauti kubwa”Kisha Vaileth alimueleza kile ambacho alisikia baba Angel akiongea na Tumaini yani hadi mama Angel alicheka na kumchukua mwanae kwenda nae chumbani, alikaa na kujitafakari kwa muda kidogo na kusema,“Ila mume wangu ananipenda sana jamani, yani hakutaka dada yake aniseme ingawa sikumuaga ila kanitetea kuwa nilimuaga, kwakweli Erick ananipenda sana”Muda huo huo akaamua kumpigia simu mume wake ili aombe msamaha kwanza,“Naomba unisamehe kwa kutoka bila kukuaga”“Usijali, kabla hujaomba huo msamaha tayari nimeshakusamehe”“Unarudi lini mume wangu”“Sikwambii ni lini maana nitakuja kukushtukiza tu mke wangu kwahiyo usijali kitu”“Jamani, nimekukumbuka sana”Wakaongea mengi mno kwenye simu, muda kidogo wakina Erica walirudi kutoka shule na moja kwa moja Erica alienda chumbani kwa mama yake na kuanza kuongea nae,“Yani mama, Samia jana kaniambia vitu vingi sana na leo karudia tena”“Vitu gani hivyo?”“Eti anasema majina ya wakina Erica hawajatulia, nimempinga ila leo karudia tena”Kisha Erica alimsimulia ambacho alisimuliwa Samia toka kwa bibi yake,“Achana na mambo ya Samia mwanangu atakuumiza kichwa tu, kwanza hiyo shule nitakuhamisha maana huyo Samia anakuchochea tu ili uwe mbea zaidi ya hapo ulipo kwasasa”“Kwahiyo niytahamia shule gani mama?”“Nitakwambia tu”Erica alitoka chumbani kwa mama yake na kuondoka zake kuelekea chumbani kwake.Usiku wa leo mama Sarah akafikiria jambo na kuongea na Sarah,“Hivi mwanangu, Ijumaa ya kesho nikimchukua Elly awe analala huku kwetu mwisho wa wiki utafurahi?”“Oooh mama nitafurahi sana kwakweli, hata mimi natamani sana Elly aje hapa kwetu, nimempenda bure”Mama Sarah alikubaliana na Sarah kuwa kesho yake ataenda kuongea na mama Elly ili Elly aende kulala hapo nyumbani kwake.Palipokucha tu wakati Sraah ameenda shuleni naye alijiandaa na moja kwa moja kwenda kwenye mgahawa wa Sia na kuongea nae kuhusu siku hiyo kumchukua Elly ili akalale nyumbani kwake,“Oooh hilo siwezi kupinga ingawa nitammisss sana Elly ila siwezi kupinga”“Basi badae nitakuja nyumbani kwako kwaajili ya kumchukua”Wakakubaliana hivyo na mama Sarah aliondoka zake, ila njiani alikutana na Johari ambapo alisimama na kuanza kuongea nae,“Kumbe upo? Hivi ulishaonana na Erick?”“Mmmh nionane nae wapi mwenzangu? Sijamuona halafu kasafiri ila nimeonana na Erica, mwanzoni unajua sikujua kama Erica na Erick ni mke na mum, kumbe walioana na watoto wanao wa kutosha tu”“Ndio, wale walikuwa wanapendana kweli. Nikikumbuka figisu tulizoweka juu yao ila hazikufua dafu kwani ndio kwanza walitafutana na kuoana. Ila unajua siku ile ulivyosema umezaa na Erick sikuelewa eti!”“Nimezaa nae ndio, nina mtoto wa kike ambaye baba yake mzazi ni Erick, kiukweli mambo ambayo Erick alinifanyia na nilivyokuwa nampenda nilijikuta kila nikisikia jina Erick najikuta nikilia tu jamani”“Pole sana maana na wewe ulipenda ndugu yangu, ila mapenzi haya loh! Ila bora ulizaa nae”“Sema sijui kama atakubali mtoto”“Mwambie akapime damu na mtoto”“Uwiiii huyo Erick umesikia kwanza alivyondondocha kwa huyo Erica! Kwani unafikiri ndio mimi tu aliyezaa nae! Kazaa na wanawake kibao ila watoto wote Erick amewakataa sababu tu hataki kumkera mke wake, yani Erick hataki hat kumsomesha mtoto wake mwenyewe kisa ni mtoto wa nje ya ndoa na anaogopa kumkera mke wake. Kwahiyo hiyo kupima damu hataki, yani hataki kitu chochote kile, anachokitaka yeye ni mke wake tu”“Duh! Jamani rafiki yangu Erica kampa nini mume wake anipe ushauri na mimi nimpe wa kwangu?”“Ila huyu Erick nimepanga kumkomesha, yani hatokuja kunisahau katika maisha yake yote. Lazima nimlize nakwambia”“Utamfanya nini?”“Wewe tulia, kuna mikakati nimeshaanza kuifanya, yani hakuna kitu ambacho kinashindikana kwangu ujue, nitamkomesha Erick najua hadi siku hiyo atakaa chini na kusema Manka umeniweza”“Mmmmh nidokezee basi”“Wewe tulia tu, nitakwambia vizuri mambo yalivyo”Waliongea mambo mengine tu na kuagana kwa muda huo kisha kila mmoja alienda sehemu yake.Mama Angel alikuwa akiongea na Vaileth kuhusu usafi wa mule ndani maana maua yalianza kunyauka sababu hayakumwagiliwa maji vizuri,“Jamani Vaileth maua yangu yanakufa ujue, kesho nikumbushe ili iwaambie Erick na Erica wakamwagilie maua”“Kweli mama, ila na pale nje ya geti kuna vile vimajani vimeota pembeni haviweki sura nzuri mahali pale”“Ni kweli, tena umenikumbusha kitu. Ngoja niende nikaving’oe maana baba yenu akniambia atarudi muda wowote, sitaki akute kuna taswira mbaya pale nje.”“Ila si ungeweka mtu tu mama wa kufanya hiyo kazi”“Aaaah mtu wa nini, naona mwenyewe naweza kufanya kile kitu acha tu nikafanye mwenyewe maana sehemu yenyewe hata sio kubwa wala nini”“Au basi niende mimi”“Hapana usijisumbue”Kisha mama Angel akamuachia pale mtoto na kumwambia akianza kulia amuite, halafu yeye akatoka zake hadi nje ya geti lake na kuanza kung’oang’oa yale majani yaliyojiotea hovyo pale nje.Muda huu Rahim alikutana njiani na mdam Oliva na kusimama akianza kuongea nae,“Oooh madam nimefurahi kukuona”“Aaaah wewe hufai kabisa, yani baada ya kunifatilia kwa muda mrefu nilijua lengo lako ni kutaka kunitongoza kumbe lengo lako ni kuwa karibu na Erica duh! Nilishangaa sana”Rahim alicheka kwa ile hoja ya madam Oliva, kisha alimwambia,“Aaaah ningetaka kukutongoza mbona ningekwambia siku ile ile, ila mimi nampenda sana Erica, na kwakweli leo umenikumbusha kitu, ngoja niende kwake hata nimuone tu moyo wangu uridhike”“Kheee makubwa hayo jamani”Basi waliachana pale na moja kwa moja Rahim alielekea nyumbani kwa mama Angel.Rahim alifika pale kwa mama Angel na alipomuona pale nje alifurahi sana, basi alimfata pale alipokuwa anang’oa nyasi na kusimama nyuma yake huku akimkumbatia yani mama Angel alishangaa sana na kuinuka ila bado Rahim alimsogeza karibu kwenye mwili wake na kumkumbatia, muda huo huo baba Angel alifika pale akiwa kwenye pikipiki kwahiyo aliona vizuri kilichotokea pale. Rahim alifika pale kwa mama Angel na alipomuona pale nje alifurahi sana, basi alimfata pale alipokuwa anang’oa nyasi na kusimama nyuma yake huku akimkumbatia yani mama Angel alishangaa sana na kuinuka ila bado Rahim alimsogeza karibu kwenye mwili wake na kumkumbatia, muda huo huo baba Angel alifika pale akiwa kwenye pikipiki kwahiyo aliona vizuri kilichotokea pale.Baba Angel alichukia sana, alifika pale karibu na kumpiga teke Rahim, alipogeuka alimpiga ngumi ya pua ambayo ilimpa kizunguzungu Rahim hadi akaanguka chini, kisha alimpiga mateke yasiyokuwa na idadi pale chini, kwa muda huo kulikuwa na Sia naye alikuwepo eneo lile kumbe, kwahiyo alisogea karibu ya Rahim na kumuomba baba Angel amsamehe,“Jamani Erick, kwanini lakini?”Baba Angel alionekana kuwa na hasira sana na yule mtu, ila muda ule Rahim nae akainuka na kusema,“Erick, nimekuachia sio kwamba siwezi kupambana na wewe ila muda haujafika wa mimi kupambana na wewe, kwakweli wewe ni mwanaume mpumbavu unaacha mambo yako na kuja kupigana na mwanaume mwenzio sababu ya mwanamke? Unashindwa kujiuliza mimi nimekuja kufanya nini hapa kama si yeye aliyeniambia nije? Unashindwa kujiuliza hilo? Mwanamke umemuoa, unampa kila kitu, unalea na mtoto wake wa nje ya ndoa, unamthamini na kumjali ila bado yupo kumkumbuka Rahim tu, ila hujiulizi hivyo zaidi ya kufika na kuanza kupambvana na Rahim, kuwa makini sana mimi nitakupoteza wewe kwa ujinga kama huu. Unadhani kukuchia Angel umtunze ndio nimeshindwa kumtoa kwako? Sijaamua tu, mtunze na ukimaliza nitakuja kumchukua rasmi na kamwe hatokumbuka uwepo wa baba chizi kama wewe”Baba Angel alimuangalia huyu Rahim na kupatwa na hasira zaidi hata kutaka kwenda kupambana nae tena ila mkewe alimshika mkono na kumkataza kufanya hivyo basi Rahim alicheka sana na kusema,“Si unaona mkeo anakukataza kuja kupambana na tamu yake, endelea kuwaza kuwa unapendwa sana na huyo mwanamke wakati ana sababu zake za kuwa karibu na wewe”Mama Angel hakumuachilia mume wake, alimsihi waingie ndani, alimuomba sana mumewe waingie ndani, basi baba Angel alikubali na waliingia ndani kwahiyo pale nje alibaki tu Rahim na Sia, basi Sia akamwambia Rahim,“Ila wewe kiboko, unaongea maneno ya kuchoma hayo”“Kwani unadhani nimeongea uongo? Yule mwanamke ananipenda kufa, yani pale hakuna anachoelewa kwa mumewe zaidi ya kunielewa mimi”“Duh! Ulimpa nini mpaka akakupenda kiasi hiko?”“Ni mapenzi tu, mimi nipo vizuri kimapenzi kushinda huyo Erick. Mimi najua kumuweka mwanamke katika mstari”“Sasa kwanini alikuacha?”“Ana ubavu huo wa kuniacha? Nilimzingua na kumuacha ndio akakimbilia kwa huyu bwege Erick, na kwenda kumpa hata yule mtoto Angel, na alivyomjinga, kamlea Angel, kamsomesha na kumuandikisha kwenye biashara zake akiamini kuwa Angel akija kusikia kuhusu baba yake mzazi basi hatomtaka huyo baba mzazi, kumbe anakosea sana. Mimi ni baba mzazi wa Angel, na ipo siku yule mtoto atarudi kwenye himaya yangu, muache tu na ujinga wake alee mtoto, amtunze na ampe haki yote halafu ataona picha ya badae”“Duh! Ila nimekupenda bure, unajua siku zote huwa nakuona tu ila sikufahamu kwa undani zaidi, yani nimekupenda bure, nipe mawasiliano yako ili tuwe tunawasiliana”Basi Rahim akampa Sia mawasiliano yake na muda huo kila mmoja aliondoka zake.Mama Angel na baba Angel wakiwa chumbani bado baba Angel alionekana na hasira sana dhidi ya Rahim kuwa pale nyumbani kwake,“Nani kamuita leo Rahim?”“Mimi sijui mume wangu hata mimi nimeshtuka tu kumuona pale nje”“Na wewe nini kilikupeleka pale nje?”“Nilienda kung’oa majani ambayo yameota pale karibu na geti letu”“Toka lini Erica umefanya hivyo? Ulishindwa hata kuweka kibaria wa kufanya hivyo jamani mke wangu, mbona kutaka kuniumiza moyo sababu ya huyu mtu jamani. Mpaka lini tutakaa na kupigania mapenzi mke wangu?”“Naomba unisamehe”“Kuniomba msamaha sio suluhisho, nimekuuliza lini tutaacha haya mambo eeeh! Nimeamua kuwa mume mwema kwako, usidhani sioni wanawake huko, ila najiuliza nifate nini kwao wakati mke wangu ana kila kitu! Halafu nakupenda sana, kwahiyo siwezi kwenda kutafuta magonjwa huko wakati wewe upo, ni kweli wapo wanaonishangaa sana ila mimi sioni aibu kuelezea kuwa nampenda sana mke wangu wakati wowote ule ila kwanini mtu kama huyu Rahim unamchekea? Bado unampenda?”Mama Angel alishtuka sana kwani hakutegemea kuulizwa swali kama hili na mume wake, alimuangalia na kumwambia,“Jamani Erick, kweli kabisa nimpende Rahim kwa lipi? Kwa yote aliyonitendea jamani! Tukiacha yote bado ukweli upo wazi kuwa wewe ndiye mwanaume nikupendaye kwa dhati, nakupenda mume wangu. Hata ukisema nizae watoto kumi kwaajili yako basi nitazaa tu, sipendi kuona ukikwazika jamani, na mimi sijapanga kitu na huyo Rahim”“Sasa kwanini afike muda tu ambao wewe upo nje hapo?”“Kwakweli sijui mume wangu, nahisi shetani anataka kutugombanisha tu”Mara simu ya mama Angel ilianza kuita na mpigaji alikuwa ni madam Oliva, basi mama Angel alipokea ile simu na kuweka sauti kubwa ili mumewe ajue ni nani anaongea nae maana alishaona mume wake kaanza kumuwekea mashaka,“Samahani mama Angel, mzima lakini”“Bila samahani, mimi ni mzima”“Leo njiani nilikutana na yule jamaa ambaye ulichukia sana nilipomleta kwako”“Nani huyo?”“Yule Rahim, ila muda nimekutana nae akasema amekukumbuka anakuja nyumbani kwako. Sasa muda huo sikuwa nyumbani halafu sikuweka vocha kwenye simu ndiomana saivi nimeamua nikupigie simu ili umzuie mlinzi wako asimkaribishe maana sidhani kama yule ana lengo zui na ndoa yako”“Asante kwa taarifa madam”“Haya asante pia, jioni njema”Basi alikata ile simu na kumuangalia mume wake, ambapo baba Angel moja kwa moja alimuuliza mama Angel,“Inamaana siku hizi huyu madam amaekuwa rafiki yako?”“Aaaah huwa nawasiliana nae mara moja moja tukiambizana mambo mbalimbali ya maisha”“Duh! Kweli maisha yanabadilika sana, ila ni vizuri kupunguza idadi ya maadui”Basi kwa muda huu walianza kuongea vizuri sasa na kuulizana kuhusu mambo mbalimbali ya huko alipotokea, halafu mama Angel alimuuliza mumewe kuwa amuandalie chakula gani kwa siku hiyo aliyofika,“Labda chapati na rosti ya maini”“Sawa mume wangu”Basi mama Angel alitoka na kumtuma Vaileth ili akanunue maini aweze kumuandalia mume wake, kwahiyo muda huo huo Vaileth alitoka ili akanunue hayo maini wakati huo mama Angel alibaki akianza kufanya maandalizi ya kumpikia mumewe kitu alichokihitaji.Vaileth alienda mpaka buchani na kununua alichokuwa ameagizwa, ila wakati anatoka buchani alikutana na Sia, na kusimama ili kumuuliza tena,“Vipi mwanao Erick umemfatilia tena?”“Mmmh yule mtoto unadhani ni mwanangu basi!! Leo nimemkataa kabisa yule mtoto simtaki tena jamani, ila sijui nini kilitokea ila yule mtoto si mwanangu”“Kwanini?”“Unajua alikuja kwenye mgahawa wangu na kunipiga sana, alinipiga ngumi na mateke, halafu leo nimemshuhudia baba yenu akimpiga mtu ngumi na mateke tena kampiga haswaaa kama Erick alivyonipiga mimi, yule ni damu yake, siwezi kuzaa toto lenye akili za kijinga kama lile jamani”“Kheee kumbe baba kapigana leo? Ndiomana alienda moja kwa moja chumbani hata kuongea nae sijaongea nae”“Basi kuna majanga aliyafanya balaa, ila…. Aaaah nenda tu ipo siku nitakupa siri hiyo hadi utakaa mdomo wazi”“Siri gani tena?”“Nenda tu”Vaileth alijitahidi kumshawishi pale ila hakumwambia lolote kwahiyo ilibidi aondoke tu, wakati anakaribia kwao, alikutana na kijana mmoja aliyemsimamisha, huyu kijana alionekana rika limepishana kidogo na wakina Erick ila hakumuamkia Vaileth wala nini ni sababu ya mwili mdogo aliokuwa nao ulifanya wengi waone huenda akawa ni mdogo, basi yule kijana akamwambia,“Samahani dada, eti Erica yupo ndani?”“Mmmh wewe ni nani kwani? Erica atakuwepo maana nahisi kasharudi shule, ila wewe ni nani?”“Mwambie Bahati, kwakweli dada ngoja nikwambie kitu. Yule Erica nampenda sana jamani, sijui nimwambiaje na nimpataje! Nimekuona nae mara nyingi maeneo ya Kanisa pale, nampenda sana Erica”“Kheee jamani, hiyo unaniambia ni ngumu kumeza hatari, yani unampenda Erica, uwiiii unatafuta balaa wewe”“Balaa gani sasa?”“Baba Erica hapendi kabisa ujinga na masikhara kwakweli, naomba tu uache kumfatilia Erica maana atakupoteza”Kisha Vaileth aliachana na yule kijana pale na moja kwa moja kuingia ndani na kupeleka kile alichoagizwa halafu kuendelea na mapishi ambapo alikuta Erica kweli alishafika nyumbani na alikuwa jikoni kusaidiana na mama yake katika kuchoma chapati,“Kheee kumbe Erica usharudi shule?”Mama Angel akajibu,“Kasharudi, hapa yupo kumtengenezea baba yake chapati yani alivyosikia karudi kafurahi sana”Basi wakawa wanacheka huku wakiendelea na yale mapishi.Usiku wa leo, Rahim alienda zake mahali na huko aliagiza pombe na kunywa maana alihisi kichwa chake hakipo sawa yani alijihisi kuwa na mawazo sana kwa muda huo.Wakati anakunywa, kuna mtu alifika na kukaa karibu yake, kumuangalia mtu huyo alikuwa ni Bahati mkubwa, basi mtu huyu alianza kuongea nae,“Tatizo nini Rahim, mbona unakunywa pombe kiasi hiko? Hujui kama pombe ni haramu?”“Naomba achana na mimi, yani mimi ukikuta nimeamua kuwa hivi ujue nachanganywa akili na mtu mmoja tu”“Nani huyo?”“Erica, ananichanganya sana akili huyu mwanamke”“Khaaaa jamani kumbe!! Ndugu yangu nakumbuka miaka mingi iliyopita tuligombana mimi na wewe sababu ya huyo mwanamke, ukapata bahati mwenzangu ya kuwa nae sababu ya pesa ulizokuwa nazo na kila kitu chako, ila mimi nilikosa hiyo bahati ingawa nilikuwa na mapenzi ya dhati. Bahati ile uliichezea ni kama ulikuwa ukichezea shilingi kwenye tundu la choo, ikadumbukia kwahiyo hukuwa tena na hiyo bahati, mwanamke akakukataa hakukutaka tena maisha yake yote. Laity ungejua yule binti kaaibika vipi sababu yako hata usingejifanya muda huu unalewa kwaajili yake, yule mwanamke kapigwa kwao yule, alikuwa anaficha mtoto ndani maana ni aibu kwani mtoto hakuwa na baba, aliogopa kuwaambia ndugu sababu ya aibu, kiukweli kateseka sana kutokana na familia aliyokuwa nayo. Sasa akatokea huyo waliyependana na kuwa pamoja, mimi pia nilimpenda sana na niliwasumbua sana mumewe ila namshukuru sana mke wangu ni mtu mwenye akili sana, ni mwanamke mcha Mungu, na mwenye akili ya dini, huwezi amini alihangaika sana na mimi ila akanifanyia dua na sasa wala siwezi kumsumbua tena Erica na mumewe. Wewe ndugu una nini lakini?”“Achana na mimi wewe, sisi hatufanani kabisa. Wewe hujawahi kupendwa na Erica, ila mimi nilipendwa na Erica hebu tofautisha hilo kwanza. Wewe ulitaka kubadili dini ili umuoe Erica ila Erica alitaka kubadili dini ili aolewe na mimi, hebu tofautisha mimi na wewe kabisa. Yule ni wangu, kumbuka kwanza nimezaa nae, mtoto wa kwanza kabisa kwa Erica ni mtoto wangu, sikumbaka Erica ila ni mapenzi yake akaamua kuwa na mimi na kuzaa na mimi kwa mapenzi yake, ukiona mwanamke hadi anaamua kuzaa na mwanaume jua anampenda sana. Siwezi sema Erica anampenda sana Erick sababu hakuna dalili yoyote ile. Erica kaamua kuolewa na Erick na kuzaa nae sababu Erick alionyesha upendo kwa mtoto wetu yani pale sio kumpenda Erick ila ni sababu ya Angel. Ukitaka jaribu kufatilia maisha anayopewa Angel na wale vikaragosi wengine ambao hawajulikani mwanzo wala mwisho wake ndio utajua kuwa Erick anapendwa sababu ya mtoto wangu”“Duh!”“Ndio hivyo, kwahiyo ukiwa unaongea usiongeee tu ilimradi, tena ngoja nikuhakikishie jambo moja kuna kipindi Erica atarudi kwangu na nitafunga nae ndoa. Na tutazaa mtoto mwingine”“Khaaaaa!”“Shangaa sana ila hivyo ndivyo ilivyo, yule mwanamke ananipenda sana mimi. Sina shida, acha ninywe pombe ili akili yangu izidi kuchangamka, hakuna kitu cha maana nitakachoambiwa na wewe kikaragosi”Bahati hakuwa na sababu ya kuendelea kuongea na huyu mtu kwani aliona ni kujisumbua tu ukizingatia hakuna alichokuwa anaambiwa akaelewa moja kwa moja. Basi akaondoka zake na kumuacha pale akiendelea kunywa pombe zake.Kulipokucha, Elly alikuwa nyumba ni kwakina Sarah, kwakweli ilikuwa ni ajabu sana kwake kulala kwenye nyumba nzuri vile, na alifurahia mandhari ya ile nyumba, basi waliamka wote na kwenda kunywa chai huku mama Sarah akimwambia Elly,“Yani Elly ujisikie amani kabisa kukaa hapa nyumbani kwangu, sina hiyana mimi na wala sina tatizo lolote mimi”“Sawa, nashukuru sana”“Najua pia unatamani kama hata tungeweza kutoka na kutembea kidogo”Sarah akadakia na kumwambia mama yake,“Mama, kwanini tusiende ufukweni leo?”“Umeniambia swala jema sana, ngoja twende ufukweni, basi mtajiandaa badae twendeni tukatembee”Ilikuwa ni furaha sana ile habari kwa upande wa Elly kwani yale maisha aliyafurahia sana, basi muda huo huo mama Sarah alisikia simu yake aliyoiacha kwenye kochi ikiita, basi akainuka na kwenda kuipokea, alikuta ni Sia ndio aliyekuwa anampigia, basi aka[pokea,“Jamani za huko, mmeamkaje?”“Salama kabisa, hofu kwako”“Salama, basi jana nilipita karibu kwenye nyumba ya Erica kumbe Erick ndio amerudi jana”“Weeee kumbe!! Ngoja nimpigie simu”Mama Sarah alikata ile simu ya mama Elly na kuanza kutafuta namba ya Erick ila akakumbuka kuwa hakuwa na ile namba kwenye simu, basi muda huo alienda chumbani kwake na kuchukua mkoba wake mmoja ambao anakumbuka kuna siku alikutana na Erick halafu alimpa namba zake za simu, akapekua na kukuta ile kadi basi akabonyeza zile namba na kupiga ambapo muda kidogo tu ile simu ilipokelewa,“Kheee Erick umerudi kimya kimya, nina shida ya kuonana na wewe”“Oooh unataka kuonana na mimi wapi?”“Kwanza unajua unayeongea nae?”“Sijajua, ni nani wewe?”“Mimi Manka, nina shida sana ya kuonana na wewe”“Sawa, tuonane wapi sasa?”“Badae naenda na watoto wangu ufukweni, basi tukutane huko”“Muda gani na ufukwe gani?”“Ngoja nikutumie ujumbe basi, maana mkeo asije akasikia”Basi mama Sarah alikata ile simu na moja kwa moja kutuma ujumbe kwenye ile namba kuhusu muda wa kukutana na ufukwe wa kukutana.Kisha mama Sarah aliwafata watoto wake na kuwaambia muda wa kwenda kutembea na ufukwe wa kwenda, na wote walifurahi bila ya kujua ni kwanini mama yao kapanga kile kitu.Leo baba Angel alitulia kidogo na kuona ana kila sababu ya kwenda kiwandani ili kuangalia maendeleo ya kiwanda,“Naona hadi Jumatatu nitakuwa nimepoteza vingi sana”“Basi nenda na Erick maana anatambua vingi sana pia”“Oooh sawa, nitaenda nae. Si ndio wanamwagilia maua? Basi nenda kamwambie kuwa nitatoka ne”Mama Angel alitoka na kwenda kuwafata watoto wake ambapo walikuwa wanamwagilia maua, aliwakuta wapo kumwagiana maji huku wakikimbizana na kucheza,“Ila nyie jamani loh! Ndio kumwagilia maua huko”“Mama Erick ndio mchokozi, ndio kaanza kunimwagia maji”“Hamna mama, ni Erica huyo”“Mmmeanza sasa, haya Erick utajiandaa kwenda na baba yako kiwandani”“Sawa mama”Basi Erica alimuangalia Erick na kumwambia,“Naomba niletee zawadi ukienda”Erick alicheka tu na mama yao akaondoka na kuwaacha hapo, kwahiyo Erick alimalizia pale kumwagilia maua na kwenda kujiandaa ili kuondoka na baba yake kwenda kiwandani.Na alipomaliza tu kujiandaa aliondoka na baba yake, basi baba Angel alikuwa akimuuliza maswali mbalimbali,“Eeeeh mwanangu, hebu niambie zile siku ulizokuwa unakuja kiwandani, nasikia upo vizuri sana kwenye maswala ya kiwanda”Mara kuna mbaba walimuona mbele kidogo na Erick alimwambia baba yake,“Yule mzee ni mteja wetu mzuri sana pale kiwandani, kwakweli anatuungisha sana”“Kheee upo vizuri mwanangu hadi wateja unawajua?”Basi baba Angel alisimamisha gari na kushuka kwenda kumsalimia huyo mteja ambaye ni mteja mkubwa sana, basi walisalimiana pale na kufurahi sana,“Nashukuru sana kwa kuwa mteja wetu mzuri”“Hata hivyo bidhaa zenu zipo vizuri sana na zinapendwa sana, ila hongera sana maana huyu kijana wako yupo vizuri sana”“Asante”Basi waliongea kidogo na kuagana ambapo walirudi kwenye gari na kuanza kuondoka, basi baba Angel alimuuliza mwanae kuwa yule mteja anaitwa nani,“Huwa wanamuita mwarabu, sema wakina Yuda ndio wanalijua jina lake halisi”“Anaonekana yupo vizuri sana”“Ni yupo vizuri kweli, halafu ana upendo sana. Yani mara nyingi akifika kiwandani lazima aulizie kuhusu mimi, nishafika hadi kwenye biashara zake, ana biashara kubwa sana inaonekana ana hela sana”“Inaonekana hivyo, ila ni vizuri mwanangu kuwafahamu wateja wetu, umekuwa vizuri sana”Basi moja kwa moja walienda zao kiwandani na kuanza kupeana maelekezo ya vitu vilivyopita.Mama Angel leo akiwa nyumbani kwake, alifatwa na rafiki yake Johari basi alimkaribisha vizuri sana na kuanza kuongea nae, ila alienda kuongea nae kwenye bustani yao ili wapate na upepo wa nje kidogo,“Kwanza kabisa asante sana kwa kule ulikonipeleka maana nafanya biashara kwasasa hadi najishangaa”“Hongera kwa hilo”“Unajua sikujaribu hapo kabla sababu moja, utakuta watu wanasema hawa wajasiriamali wanakufundiaha halafu ukitoka hapo huwezi lolote unakaa tu nyumbani, ila sasa nilivyofika pale alipita mama mmoja na kutufundisha kwakweli yale mafundisho yaliniingia akilini, alisema wengi hawafanikiwi sababu moja, akishatoka hapa anataka ajaribu kila kitu kwa wakati mmoja na mwisho wa siku anaona ni kujisumbua tu anaamua kuacha, utakuta anataka atengeneze mafuta, sabuni za aina zote, vikoi, tambi sijui mishumaa mara keki vyote kwa wakati mmoja halafu akija badae anajibu yale mambo hayalipi, hebu niwaambie wanawake wenzangu mjaribu kwanza kujikita sehemu moja mtafute soko na uhakika itakutoa tu, ndipo unapoongezea vingine, ila ukitaka vyote kwa wakati mmoja lazima uone hasara maana mtaka vyote hukosa vyote. Basi mafundisho yakaendelea, nilipotoka hapo nikasema ngoja nikomae na sabuni ya maji, uwiiii huwezi amini yani ndani ya muda mfupi nimekuwa na soko kubwa sana na ninaenda kusambaza sehemu mbalimbali. Kwakweli shoga yangu ubarikiwe sana kwa hili la kunitoa tongotongo mwenzio”“Nimefurahi kusikia hivyo, siku hizi wanawake ni kuinuana kwakweli maana uchumi wa sasa sio wa kutegemea kuletewa tu. Sema watu wengine huwa wanafikiria ni masikhara, ni kweli akisemacho utakuta mtu anahudhuria kila darasa la ujasiliamali ila kusema ngoja nifanye hiki nilichofundishwa sasa, nikomae nacho hakuna, ila utamkuta leo alienda hapa kesho yupo hapa. Na hata biashara zipo hivyo, mwingine akisikia vitunguu vinalipa basi kashahamia kwenye vitunguu, korosho zinalipa huyo kwenye korosho, akiambiwa kuna madini yanalipa sana, huyo kwenye madini mwisho wa siku kila biashara anaona ni mbaya kwake sababu hajui afanye nini, kitu jua kwanza faida na hasara zake basi utaweza kukabiliana nacho ila kuvamia vamia kila kitu utashangaa tu wenzio wamesonga mbele”Basi waliongea mengi sana na kuendelea kushawishiana mambo mengi, ndipo Johari alipoanza kumueleza na habari za Manka pia,“Nasikia Manka alikuja kukwambia kuwa kazaa na Erick!”“Jamani habari za Manka, hata sizitaki ila bado sijamuuliza mume wangu ili aniambie ukweli”“Mimi sijui na wala sitaki kuwa chanzo cha kukugombanisha tena na mume wako Erica, nakumbuka kipindi cha nyuma nilifanya mambo sio mazuri kabisa hata roho yangu ilinisuta tena sana. Siwezi sema kuwa mtoto kweli ni wa Erick au la maana yule Manka nae haaminiki kabisa”“Eti eeeh!!”“Sijui kwakweli, ila ngoja niende nitakuja tena siku nyingine”Basi Johari alimuaga mama Angel na kuondoka zake.Alipofika njiani Johari alikutana na Sia na kuanza kusalimiana nae,“Naona umetoka kwa rafiki yako”“Eeeeh nimetoka kwa rafiki yangu”“Ila nahitaji sana kukufahamisha kuhusu mwanaume aliyezaa na rafiki yako yule mtoto wake wa kwanza”“Mmmh unadhani nahitaji kumfahamu basi? Hata sihitaji kumfahamu kwakweli. Kwaheri”Johari aliondoka yani Sia alishangaa sana kujibiwa vile na Johari ila alijua kuna maneno tu atakuwa kaambiwa na mama Angel.Mama Sarah akiwa ufukweni na watoto wake, basi akapigiwa simu na ile namba ambayo alikuwa akimpigia Erick,“Na mimi nipo ufukweni, upo sehemu gani nije”“Niambie wewe ulipo nije maana nipo na watoto hapa, ngoja nije tuzungumze kwanza ndio tutakutana nao”Basi alielekezwa alipo na moja kwa moja aliwaaga watoto wake na kuondoka zake, muda huo Sarah na Elly walikuwa wakiongea kuhusu mambo mbalimbali,“Elly una mwanamke wewe?”“Mmmh mwanamke? Hapana, kwanza nasikia wanawake wanapenda sana hela sasa mimi nitampa hela gani mwanamke?”Basi Sarah alicheka sana, na kumuuliza tena,“Ushawahi kufanya mapenzi?”Elly akashtuka sana na kumuangalia vizuri Sarah kisha akamwambia,“Hapana, naogopa kabisa. Wewe je?”“Aaaah hapana sijawahi kabisa ila nasikia ni mchezo mzuri sana halafu raha”“Mmmmh umesikia wapi? Nani kakwambia?”“Kwenye simu yangu huwa naona watu wakifanya, kuna video nyingi huwa natumiwa. Tukifika nyumbani nitakuonyesha”“Mmmh nasikia huo ni mchezo mbaya sana, mtu mkubwa akikukuta hata unaangalia hizo video basi utapigwa sana”“Kwahiyo tukiangalia nani atatupiga huyo?”“Mama yako”Sarah akacheka na kusema,“Sijawahi kupigwa hata kibao na mama toka nimezaliwa, na hii simu wala mama yangu huwa haishiki kuangalia chochote kile ninachokiangalia yani mama yangu kaniacha huru kuangalia chochote na kuwasiliana na yoyote ninayetaka”“Kheee basi mama yako anakupenda sana, ila hata mimi mama ananipenda sana sema nikikosea lazima aniadhibu ili nisirudie tena”“Basi itakuwa mimi huwa sikosei maana mama huwa hanipigi, ananipenda sana”Wakaongea mengi na kukubaliana kuangalia hizo video pindi wakirudi nyumbani.Mama Sarah moja kwa moja alienda kukutana na yule mtu ambaye alifikiria kuwa ni Erick ila alivyofika pale hakukuta kuwa ni Erick alishangaa sana kuona ni mtu mwingine, basi yule mtu alimfata karibu na kujitambulisha kwake,“Habari, naitwa Rahim.”“Kheee mbona sio Erick?”“Kweli mimi sio Erick, utakuwa umekosea namba ila hiyo sauti yako ilinichanganya sana na kuhamisha kabisa ufahamu wangu nikajikuta nahitaji kukufahamu zaidi”Basi Rahim alitabasamu, kiukweli mama Sarah alihisi akipata raha sana kumuona, basi Rahim alisogea karibu yake na kushika kiganja cha mkono wa mama Sarah, yani hii kitu Rahim alikuwa akiijua vizuri sana kuwa tabasamu lake na mikono yake ilikuwa ikimaliza sana wanawake, kwani wengi walipenda kuona Rahim akitabasamu sababu ya mpangilio mzuri wa meno yake, ambayo yalivutia sana kuyaangalia na pia walipagawa mno alipowashika mikono kwani mikono ya Rahim ilikuwa ni milaini sana, kwahiyo mama Sarah nae alijihisi akisisimka sana huku akimuangalia tu Rahim bila ya kusema lolote, basi Rahim alimshtua tena kwa kumwambia,“Mbona umeduwaa?”“Hapana, basi tu”“Unajua sauti yako ilinichanganya sana, halafu nimekuona kuwa wewe ni mzuri sana. Unavutia kwakweli”Mama Sarah alitabasamu tu, kisha Rahim alimwambia tena,“Manka, naomba unipeleke nyumbani kwako nipafahamu”Kwakweli mama Sarah hakuwa na pingamizi kabisa juu ya hilo, basi akaondoka ili kwenda kuongea na watoto wake kuwa waende nyumbani.Ila walipofika pale, Elly alionyesha kumshangaa Rahim na kusema,“Kumbe mnafahamiana?”Mama Sarah alimuangalia Rahim, na Rahim alikuwa akimuangalia Elly maana hata hakumkumbuka. Kwakweli mama Sarah hakuwa na pingamizi kabisa juu ya hilo, basi akaondoka ili kwenda kuongea na watoto wake kuwa waende nyumbani.Ila walipofika pale, Elly alionyesha kumshangaa Rahim na kusema,“Kumbe mnafahamiana?”Mama Sarah alimuangalia Rahim, na Rahim alikuwa akimuangalia Elly maana hata hakumkumbuka.Rahim akamuuliza Elly,“Kwani na wewe unanifahamu?”“Ndio nakufahamu, nishawahi kukuona na mama”“Mama yako! Mama yako anaitwa nani?”“Anaitwa Sia”“Aaaah mbona simjui, utakuwa umenifananisha”“Hapana ni wewe mwenyewe”Mama Sarah akaingilia kati yale mazungumzo na kumwambia Elly,“Elly utakuwa umemfananisha, mkubwa akikataa ujue humfahamu usilazimishe kumfahamu”“Sawa mama, nisamehe”“Haya, jamani huyu ni rafiki yangu anaitwa Rahim kwahiyo mtamuita anko Rahim. Halafu hawa ni watoto wangu, huyu anaitwa sarah ndio maisha yangu yani ndio kila kitu kwangu, nampenda sana, nipo tayari kwa chochote kwaaajili yake. Halafu huyu anaitwa Elly, ni mtoto wa rafiki yangu kwahiyo Elly na Sarah ni kama mtu na kaka yake”“Oooh nimefurahi kuwafahamu”Basi Rahim akawapa mikono pale kama utambulisho, halafu mama Sarah akawaambia kuwa wanatakiwa kwenda nyumbani ili ampeleke yule mgeni nyumbani akatambue wanapoishi, basi Sarah akalalamika kidogo,“Jamani mama hata hatujafurahia sana huku ufukweni!”Basi Rahim alimuangalia tu mama Sarah, na kumwambia,“Waaache watoto wafurahi, twende kukaa kidogo tuzungumze halafu wakiridhika ndio tutaondoka nao”Basi mama Sarah alikubaliana na lile swala na hivyo aliondoka na Rahim na kwenda kukaa mahali wakiongea mambo mbambali.Ambapo Rahim alimuuliza mama Sarah,“Unafanya kazi gani? Umeolewa?”“Aaah mimi ni mwalimu wa kujitegemea ila pia nina miradi yangu ambayo huwa naisimamia. Sema sijaolewa”“Ooooh wow, hujaolewa kumbe!! Mwanaume je unaye?”“Hapana sina mwanaume, wewe je umeoa?”“Yani hata siamini kama nasikia vizuri hiki nilichokisikia, yani hujaolewa Manka na wala huna mwanaume! Imekuwaje mwanamke mzuri kama wewe kukosa mwanaume?”“Aaaaah kila kitu ni maamuzi tu katika misha, nilichoshwa na wanaume kwahiyo hata sikutaka mwanaume wa aina yoyote. Ila hujanijibu je wewe umeoa?”“Unajua kuna muda mtu unakawia kuoa kumbe unakawia sababu bado hujaona vyote duniani, sikujua ni kwanini nimekawia hivi kuoa kumbe ni sababu sikuona vyote vilivyopo. Mimi sina mke kabisa halafu katika maisha yangu sikutarajia kama nitakuja kuoa kabisa sababu wanawake wengi huwa nawaona ni wazinguaji na huwa wanapenda pesa tu. Ila sijui imekuawaje baada ya kusikia sauti yako kwenye simu, nilijikuta nikikosa muelekeo kabisa”Mama Sarah alitabasamu, kisha Rahim alimwambia mama Sarah,“Naomba nisivute vute maneno, kwakweli Manka nakupenda sana, sijawahi kuona mwanamke mzuri kama wewe Manka, kwakweli wewe ni wa gtofauti sana, ni mzuri na unavutia halafu upo vizuri kabisa. Naomba unielewe Manka, kwakweli nakupenda na ninahitaji uwe wangu na Mungu akipenda uwe mke wangu kabisa”Mama Sarah alikuwa akicheka tu na kusema,“Yani sijui nini kipo kwangu ila nilijisemea kuwa sitajiingiza tena kwenye mahusiano ya kimapenzi, hata sielewi nikujibu vipi yani, ila wanaume wamenichosha”“Mmmh usiseme hivyo tafadhari”Rahim alimsogelea karibu mama Sarah na kumshika bega huku akimuangalia kwa karibu, kisha mama Sarah akamwambia tena Rahim,“Katika maisha yangu kuna mwanaume mmoja ambaye nilimpenda sana halafu huwa sidhani kama kuna mwingine nitakayempenda kama huyo maana nilimpenda sana mwanaume huyu, ila kwasasa ana mke wake halafu siwezi kumpata, yani nilitulia hata sikutaka wanaume wengine kwaajili yake, nampenda sana”“Ndio huyo Erick?”“Ndio anaitwa Erick hata nashangaa ni kwanini hakunipa namba zake akanipa namba zako, sijui kwanini ila nampenda sana”“Ooooh halafu Erick mwenyewe simkumbuki, mimi ni mfanyabiashara kwahiyo huwa nakutana na watu wengi na huchukua kadi yangu ila huyo Erick hata simkumbuki kabisa. Ila nakuomba Manka ukubali kuwa na mimi tafadhari”“Utanipenda, utaniheshimu na utanithamini?”“Vyote nitafanya kwako, hakuna tatizo”“Nitakupata muda wote nitakaokuhitaji?”“Mimi nipo ndio, maana mimi ni mfanya biashara, halafu sio kwamba nafanya mwenyewe ila mimi ndio bosi yani nazisimamia tu. Kwahiyo utanipata ndio muda wowote unaonihitaji”“Hutonidanganya?”“Nikudanganye ili iweje Manka, kama upo tayari basi wiki ijayo nakuvisha pete ya uchumba”“Oooh kweli umeamua”“Ndio, sababu nakupenda Manka, tafadhari usikatae”Manka alicheka tu na kufanya waendelee na mazungumzo mengine pale na kukubaliana mambo mbalimbali.Sarah na Elly bado walikuwa wakizungumza kuhusu yule mwanaume ambaye mama yake alikuja nae,“Ila Elly yule baba ulimjuaje kwani?”“Niliwahi kumuona na mama yangu, nikajua labda anafahamiana na mama, nilipomuona na mama yako nikajua labda anafahamiana nae pia”“Ila kasema hamfahamu mama yako, ni rafiki wa mama yangu. Ila yule baba mzuri”“Kheee Sarah, hadi wanaume wazuri unawajua?”“Jamani, mtu akiwa mzuri anaonekana tu kuwa huyu ni mzuri bila hata kukupesa macho au maneno”“Na mimi je ni mzuri au mbaya?”“Oooh wewe Elly ni mzuri sababu una sura ya kike”“Nimefanana na mama eeeeh!!”“Simjui mama yako ila labda umefanana nae”Basi wakawa wanatembea tembea mule ufukweni, kuna mahali palikuwa pamejificha kidogo, wakaona watu wawili wamekaa walikuwa ni mwanamke na mwanaume, kwa pamoja walijikuta wakivutiwa kuwatazama watu wale, wale watu walikuwa wakishikana shikana na mwisho wa siku walionekana kufanya uzinzi sababu wapo mafichoni, basi Sarah akamuuliza Elly,“Unajua wanachofanya wale?”“Hata sijui”“Ndio wanafanya mapenzi vile”“Mmmh tuondoke Sarah, hapa hapatufai”“Kwani hufurahii kuwaangalia?”“MMmmh mimi naogopa kuwaangalia”“Ila Elly unachekesha ujue, kama sio mwanaume vile. Wanawake huwa tunaona aibu kuangalia mambo kama yale, ila kwa mwanaume hapana”“Mama lazima atakuwa anatutafuta”“Khaaaa Elly muoga sana wewe, haya twende”Basi wakaondoka mahali pale na muda kidogo mama yao alirudi na kuwataka waondoke, kwahiyo wakatoka hapo huku wakimuuliza,“Mama, mbona hatujaondoka tena na yule mgeni?”“Kapata dharula kidogo, kwahiyo kaondoka”Basi wakaenda moja kwa moja kupanda gari, ila wakiwa njiani mama Sarah akapata tena simu kutoka kwa yule mtu akimtajia hoteli wapiti waweze kula, basi mama Sarah alitabasamu tu na kupitia na watoto wake kwenye hiyo hoteli, ni kweli walimkuta Rahim yupo mahali pale na kuwataka waagize chakula wanachokitaka, kwahiyo waliagiza na kuanza kulak wa furaha.Usiku wa leo, mama Angel aliandaa tena chakula mwenyewe na alikaa mezani na familia yake huku wakila kile chakula kwa furaha tu kama zamani walivyokuwa wakila kwa furaha, mara simu ya baba Angel ilianza kuita, akataka kwenda kuipokea ila mke wake akamzuia na kumwambia,“Mume wangu, upo kula halafu uende kupokea simu ili iweje? Yani simu ikukatishie chakula kweli! Naomba umalize kula kwanza”“Sawa mama, hakuna tatizo”Basi waliendelea kula, na walipomaliza walielekea chumbani moja kwa moja, ambapo baba Angel aliichukua simu yake aliyoiacha mezani na kwenda nayo chumbani ila hakuangalia tena ni nani aliyekuwa akimpigia muda wa kula, zaidi zaidi alianza kuongea na mke wake,“Sasa leo kule kiwandani nimegundua mambo mengi sana yamebadilika, kwanza mke wangu asante sana kwa kujitoa kwako kiwizi wizi na kwenda kutembelea kiwanda ingawa nilikukataza”Mama Angel alitabasamu tu na kuitia asante ya mume wake,“Asante na wewe pia kwa kushukuru”“Kweli nilioa mke jamani, ndiomana kuna watu wananionea kijicho hata wakijaribu kila mbinu kuweza kusambaratisha penzi langu. Unajua Erica sisi tumetoka mbali sana, yani nikikumbuka penzi letu lilivyowekewa vikwazo najikuta kuzidi kukung’ang’ania mke wangu”“Ni kweli, na changamoto hazijatuacha kabisa, tunakutana mna masokomoko kila siku, mara Rahim, mara Bahati, mara Sia, mara Manka sijui na mwingine kaibuka hapa wa kuitwa Linah”“Aaaah mke wangu jamani, hao wasumbufu tu”“Tena nimekumbuka kitu, leo nieleze ukweli mume wangu, hivi ni kweli umezaa na Manka au?”“Yule mwanamke ni mwehu, sijazaa nae mie. Si ulisema kazaa na baba yangu sijui!”“Ndio, maana picha niliyomkuta nayo mwanao ni picha ya baba yako, ila yeye Manka kasema kuwa mtoto yule ni wako”“Ngoja nikwambie kitu mke wangu, ni kweli Manka nilikutana nae njiani na aliniambia kuwa amezaa na mimi ila ni kipindi gani kazaa na mimi? Yule mwanamke ni muongo, Manka alivyokuwa na sifa nadhani angeniambia mapema sana ila hajazaa na mimi, halafu kuhusu baba yangu labda alikuwa akitembea nae tu ila hajazaa nae sababu baba alikuwa na matatizo ya uzazi, ila sijui labda alimdanganya, ila kuna mwanaume ambaye ndio kazaa na Manka”“Ila ulikuwa na mahusiano nae?”“Tuache hizo habari mke wangu”“Aaaah tuziache vipi? Niambie ukweli Erick ulikuwa na mahusiano na Manka hapo kabla?”“Ni zamani sana ndio niliwahi kuwa na mahusiano nae, enzi zile za ujinga ila sijazaa nae”“Mara ya mwisho kuwa nae ni lini?”“Duh! Kwakweli sikumbuki ila ni zamani sana, mke wangu naomba uachane na mawazo hayo”“Na huyo Linah! Halafu ulikuwa ukitafuta wanawake wazuri tu”“Ni zamani mke wangu ila wote hawakufikii wewe kwa uzuri maana mke wangu umekamilika kila idara, naomba tuache mada hiyo tafadhari. Tujenge yetu na maisha yetu. Yani mimi huwa sipendi kukumbuka nilikopita kwani naona kama nikichafua sifa yangu, nina uhakika toka mwanzo ningekuwa na wewe basi nisingepita kwa hawa wote niliopita nao. Naomba tuache tu hiyo mada maana mimi inanitia kichefuchefu. Nakupenda mke wangu ni hivyo tu na weka akilini kuwa nakupenda sana”Mama Angel alitabasamu tu ila aliona kamavile hajajibiwa swali lake vizuri kuhusu Manka, kwani aliona kuwa anahitaji kufahamu vizuri kuhusu mke wake na Manka ili ajue kweli mtoto ni wa mume wake au la.Wakati mama Sarah akijiandaa kulala, alipigiwa simu na Rahim, basi alipokea na kuanza kuongea nae,“Kheee usiku huu?”“Uliniambia hujaolewa, na mimi sijaoa kwahiyo tushindwe kupigiana simu usiku kweli!”“Kheee haya basi, hivi hujaoa kweli?”“Ndio sijaoa mimi, sina mke wala nini ila nina watoto tu kama wawili tu”“Mama, yao yuko wapi?”“Ahhh hawa watoto nilizaa ujanani na mama zao ni tofauti, ila watoto nalea mwenyewe. Wanawake hawa walikuwa hawaeleweki ndiomana sijaoa hadi leo”“Ooooh haya pole kwa kupata wanawake wasioeleweka”“Ila Mungu kaniletea mke wangu ambaye ndio wewe Manka, yani nakupenda sana. Hapa nimeshindwa hata kulala hadi nisikie hiyo sauti yako tamu. Yani una sauti nzuri sana sijapata kuona jamani, Manka uliumbwa na ukaumbika jamani”“Haya, nashukuru. Usiku mwema”“Jumatatu watoto si wanenda shule, nije kukutembelea”“Njoo hata wakiwepo hawawezi kunipangia maisha”“Basi nitakuja Jumatatu”Waliagana pale na kila mmoja kulala, ila mama Sarah alijifikiria kwa muda kuhusu Rahim,“Hivi ni kweli mwanaume mzuri vile kakosa mke wa kuoa jamani! Mmmmh sijui, labda kweli aliwekwa kwaajili yangu. Hivi huyu anaweza kunifanya nimsahau Erick kweli? Maana mawazo ya Erick nayo yananichanganya sana”Akafikiria kwa muda na kuamua tu kulala kwa muda huo.Kulipokucha, mama Sarah alikaa na Sarah na Elly mezani wakinywa chai. Mama Sarah alimaliza kunywa na moja kwa moja kwenda chumbani kwake, basi Elly akamuuliza Sarah,“Baada ya kunywa chai ndio tutaenda Kanisani?”“Kanisani? Kufanya nini?”“Kusali, kwani hamuendagi kanisani?”“Aaaah hatuendagi, kwahiyo wewe huwa unaenda?”“Ndio, kila Jumapili mimi na mama lazima twende Kanisani. Kwani nyie dini gani?”“Sisi ni wakristo lakini huwa hatuendi Kanisani, ila hata dada Siku ni mwislamu lakini haendagi msikitini”“Kheee kwanini sasa?”“Sijui, labda tunaona hakuna umuhimu wa kufanya hivyo. Mimi sijui kwanini ila muulize na huyo dada kwanini huwa haendi Msikitini”Elly aliwashangaa sana hawa watu, muda huu Siku nae alifika kutoa vyombo kwahiyo Elly alimuulize lile swali kuwa kwanini huwa haendi Msikitini,“Sasa niende kufanya nini?”“Kumuomba Mungu”“Kwani mpaka niende? Hata nyumbani inatosha mbona, sio lazima kwenda”“Basi mimi nimefundishwa tofauti, mama yangu ni Mkristo basi kila Jumapili lazima niende nae Kanisani. Halafu kuna mtoto wa dadake mama anaitwa Amina ni mwislamu basi mama alikuwa akimsisitiza kila Ijumaa aende Msikitini na alikuwa akifanya hivyo hadi siku aliyoondoka kwenda kwa ndugu zake, yani mama yangu anapenda Ibada sana”“Kheee mama yako nae ni waajabu sana”Kisha Elly akamwambia Sarah,“Basi leo twende wote Kanisani Sarah tafadhari”Mara mama Sarah akatoka chumbani na kuwaambia,“Mjiandae sasa, kumbe kuna sherehe leo ya kuzaliwa kwa Manka mdogo, kwahiyo badae badae tutaenda huko, mmesikia wanangu eeeh!”Ilibidi na Elly aitikie maana hakujua aina ya maisha ambayo walikuwa wakiishi kwenye nyumba hiyo.Familia ya mama Angel leo wote walienda Kanisani kasoro Vaileth ambaye alisema kuwa anaumwa na tumbo, kwahiyo alibaki mwenyewe ila walipooondoka tu wote alifika Junior mahali pale na kuwa karibu na vaileth,“Yani leo nimesema naumwa na tumbo ili nisiende huko Kanisani”“Umefanya vizuri sana, uliponitumia ujumbe kuwa upo moyo wangu ulilipuka yani, kiukweli Vaileth nakupenda sana”Kisha Vaileth alienda na Junior kulala nae chumbani na walilala huko hadi baada ya kusikia mlango wa sebleni ukigongwa maana leo Vaileth alikumbuka kufunga mlango wa sebleni,“Jamani nani tena huyo?”“Sijui nani, ngoja nikamfungulie”“Wa nini bhana, muache agonge akichoka ataondoka mwenyewe”“Hebu mpigie simu mlinzi umuulize ni nani”basi Junior akachukua simu yake na kumpigia mlinzi wa pale na kuanza kuongea nae,“Eti ni nani huyo aliyekuja?”“Ni mama yako Junior, halafu nimejisahau nikamwambia kuwa Vaileth yupo ndani”“Aaaah unaharibu sasa jomba, sikia basi mfate mwambie ulisahau kumbe wote wameenda kanisani ili aondoke hapo. Huyo mama nae vipi, hajui kama leo ni Jumapili akasali huko jamani!”“Ngoja nikamwambie basi”Simu ilikatika halafu Junior akawa anaongea na Vaileth,“Huyu mama nae ana mambo ya ajabu sana, yeye baada akasali huko anajifanya kuja hapa ili iweje sasa jamani. Mambo mengine loh!”“Ila ni mama yako yule Junior, huwezi kuelewa kaja na jambo gani”“Atajijua mwenyewe, unadhani akiingia ndani humu itakuwaje? Atataka ukae nae tu sebleni halafu na mimi nitaondokaje? Mwache aende bhana”Basi muda kidogo mlinzi nae akampigia simu na kuanza kuongea nae,“Nimemwambia bhana ila kasema atasubiri mpaka warudi”“Aaaah huyo mama nae vipi jamani dah! Utanitonya basi kitakachoendelea maana hata kutoka haitowezekana hapa”“Sawa hakuna tatizo”Junior alimuangalia Vaileth na kulalamika,“Leo kazi ipo ujue, yani huyu mama kagoma kuondoka hadi warudi kwahiyo mimi leo siwezi kutoka hapa jamani dah! Ila poa tu nitajua cha kufanya, tuendelee na mambo yetu vai wangu”Basi waliendelea tu na mambo yao huku wakijipa moyo kuwa itakavyokuwa badae na iwe tu.Mama Angel na familia yake walitoka kanisani na kumkuta mama Junior pale nje hadi anasinzia, basi mama Angel akamkaribisha na kumpa pole,“Vipi lakini umeteseka hapa wakati vaileth yumo ndani!”“Jamani nimegonga sana, mlizni akaja na kuniambia kuwa wote mmeondoka”Basi walianza kugonga tena ila Vaileth hakutoka kufungua, ikabidi mama Angel ampigie simu, ndio baada ya muda kidogoVaileth alifika na kufungua mlango huku akidai kuwa alikuwa amelala sababu ya kuumwa na tumbo kwahiyo hakusikia mlango ulivyokuwa ukigongwa.Basi mama Junior alikuwa akilalamika tu kuwa hata mlinzi aliwaambia kuwa hamna mtu humo ndani, basi mama Angel akamuita na kumuuliza,“Halafu wewe Maneno, si nilikwambia mara mbilimbili wakati tunatoka kuwa Vaileth yupo huku ndani!”“Nilisahau mama, nilivyoona kagonga sana nikahisi wote mliondoka ndiomana nilimwambia kuwa hakuna mtu”“Haya, kaendelee na kazi zako”Kisha wakaingia ndani huku wakiongea mambo mbalimbali, basi mama Junior akamtaka mdogo wake wakazungumze nje kidogo ambapo alitoka nae hadi kwenye bustani,“Mwenzangu ndoa yangu huko inatikisika, na anayeitikisa ni Junior”“Mmmh! Kafanyaje tena wakati yupo shuleni”“Yupo shuleni ndio, ila yule binti kaletwa leo na mama yake na wamenibwagia hapo kwangu. Deo kachukia hatari, kasema nitafute pa kumpeleka yule binti au niondoke nae”“Duh mbona hatari hiyo ndugu yangu”“Naomba unisaidie mdogo wangu, naomba hata yule binti aje kuishi hapa kwako huku tukiangalia utaratibu mwingine”“Mmmh ila ngoja kwanza niongee na mume wangu kuhusu swala hilo maana siwezi kujichukulia maamuzi mwenyewe”“Basi kaongee nae”“Dada jamani, maamuzi mazuri ni yale ambayo mtu anatafakari, kwa leo nenda ukamuombe mumeo huyo binti alale hapo kwake halafu kesho ndio utamleta huku baada ya kukupa taarifa ya kuongea na mume wangu”“Mmmh wewe nawe, hivi huwa huna maamuzi mpaka mumeo?”“Hata wewe mwenyewe nina uhakika huwezi kufanya kitu bila mumeo ndiomana umekuja haihai hivyo, lazima nimuheshimu mume wangu maana ni sehemu ya maisha yangu au naweza sema ndio maisha yangu kwasasa”“Sawa, ni vizuri lakini. Ngoja niende kwasasa ili nikamuangalia yule binti maana kaachwa pale nyumbani kwangu”“Sawa, hakuna tatizo”Mama Junior aliondoka kwa muda huo na mama Angel alienda chumbani kwake.Mama Angel moja kwa moja alienda chumbani kwaajili ya kuongea na mume wake kuhusu hilo swala la kuishi na huyo binti,“Mmmh wewe umeamua nini mama yangu?”“Sijui nakusikiliza wewe tu”“Mimi sina tatizo, ila tu hakikisheni mnapafahamu vizuri anapotokea huyo binti tusijeleta matatizo bure hapa nyumbani”“Sawa hakuna tatizo, basi nitamwambia amlete kesho”“Hakuna tatizo”Mara kuna ujumbe uliingia kwenye simu ya mama Angel, alipoangalia ule ujumbe ulitoka kwa rafiki yake Johari, basi akausoma,“Leo, nimekutana na Manka, alikuwa kaongozana na watoto wake anaenda nao mahali. Ila nimeongea nae kidogo tu na bado akisisitiza kuwa yule mtoto ni wa Erick, cha kushangaza sasa, alikuwa kaongozana na mtoto mwingine wa kiume, akasema naye ni wa Erick pia, mmmh sijui labda Manka alizaa mapacha au ni kitu gani sikuelewa hapo!”Mama Angel alisoma ule ujumbe mara mbilimbili kisha alimuangalia sana mume wake bila ya kusema chochote kile, ila baba Angel alihisi tu kuna kitu hakipo sawa kwa mkewe, basi akamuuliza,“Tatizo nini mke wangu?”“Sijui ila najiona sipo sawa kabisa”“Kwanini wajiona hivyo?”“Baba Angel, unajua swala la Manka linaniumiza kichwa sana, yani kila nikifikiria naona kichwa changu kikizunguka mno”“Kwanini lakini?”“Nahitaji tu kujua ukweli, ni kweli Manka ulizaa nae au la”“Jamani, sijazaa na Manka huo ndio ukweli au unataka tukutane na huyo Manka tumuulize vizuri?”“Ndio, hiyo itakuwa nzuri zaidi”“Sina namba zake”“Mimi najua anapoishi”“Duh! Haya tutaenda basi mke wangu”Baba Angel anamjua mkewe vizuri kuwa akitaka jambo basi anataka lifanyike muda huo huo hata sio wa kusema nisubiri kwanza, maana inaonyesha alitaka sana kujua ukweli wa mtoto wa mama Sarah.Mama Sarah akiwa kwenye sherehe, muda ule ule akapigiwa simu na Rahim na kuanza kuongea nae,“Unajua natamani hata leo kuja nyumbani kwako”“Ila mimi sipo nyumbani, nimekuja huku na familia yangu kuna sherehe ya kuzaliwa ya wajina wangu”“Oooh sawa, kwanini basi tusikutane leo unipeleke huko kwako Manka? Naomba tukutane, waache watoto huko halafu tutawafata, niambie ulipo nije kukuchukua”Basi Manka hakuona tatizo lolote alikubaliana na Rahim na kumuelekeza mahali alipo, ambapo baada ya muda kidogo tu Rahim alimpigia simu kuwa kafika, basi alienda kuwaaga watoto wake kuwa atawafata badae.Akatoka na kuondoka na Rahim huku wakiongea mengi tu,“Huyo wajina wako umempelekea zawadi gani ya siku yake ya kuzaliwa?”“Unajua wamenishtukiza tu hata sijajua nimchukulie zawadi gani”“Kwahi huwa anapenda nini? Ana umri gani?”“Aaah bado mdogo ana miaka mitano”Wakati wanapita mahali waliona kuna duka la nguo na vifaa vya watoto, hivyo Rahim alienda kusimamisha gari maeneo yale na kumtaka mama Sarah wakachague zawadi, basi walishuka na kwenda dukani kuchagua zawadi ambapo zile zawadi zote zililipiwa na Rahim na kumfanya mama Sarah afurahi sana.Ila Rahim alipenda sana ukarimu wa yule muuzaji pale dukani, basi akamuachia kadi yake ya mawasiliano na kumtaka wawasiliane.Kisha mama Sarah na Rahim waliendelea na safari ya kwenda nyumbani kwa mama Sarah.Huku mama Angel na mumewe walijiandaa kwaajili ya kwenda nyumbani kwa mama Sarah ili wakaongee nae, na kweli waliondoka hapo na kuanza safari.Walipofika kwa mama Sarah walishangaa kumuona mama Sarah akiingia ndani kwake na Rahim. Walipofika kwa mama Sarah walishangaa kumuona mama Sarah akiingia ndani kwake na Rahim.Mama Angel na baba Angel waliangaliana kwa muda kisha baba Angel akamwambia mkewe,“Sasa mama watoto, kweli ndio mtu wa kwenda kumfatilia huyu atuambie ukweli kabisa!! Hebu mambo mengine tuache tu kama yalivyo, hebu tuondoke zetu”“Kwani ni kitu gani hiki? Umeelewa mume wangu?”“Sijaelewa na wala sina shida ya kuelewa, ila mke wangu nishakwambia mara nyingi kuwa maneno ya Manka usiyasikilize, ni sawa tu na maneno ya Sia, yani usiwasikilize kabisa. Mimi ndio nakwambia kuwa sijazaa na Manka, niamini mimi, kama nimezaa nae kwanini nikatae eeeh!! Siwezi kukataa kitu ambacho nimekifanya kweli, sijazaa na Manka, na kwa ujinga ule ambao ameanza wa kushirimiana na Rahim hata sina haja ya kufahamu zaidi kitu kinachoendelea, tuondoke tu hapa mke wangu”Basi wakaamua kuondoka, ila baba Angel hakwenda moja kwa moja nyumbani na mke wake bali alienda nae hotelini ili kupata chakula kidogo na kuongea mawili matatu maana ni siku nyingi alikuwa kasafiri, basi walifika pale na kuagiza chakula huku wakiongea mambo mbalimbali,“Nakumbuka kipindi hiko wakati nakufukuzia, hata hukutaka kunielewa kabisa, ulikazana na swala moja tu kuwa mimi ni muhuni sana wakati wala sikuwa muhuni wa kiasi hiko ila tatizo la kunikataa ndio likazaa swala la mimi kuwa muhuni, kwahiyo mara nyingine mke wangu unihurumie tu na tuendelee kuaminiana”“Nakuamini mume wangu, ila hawa wanawake wananipa presha hatari”“Wasikupe presha mke wangu maana mimi na wewe tunapendana kiukweli kabisa, kwahiyo hao vikaragosi wasikubabaishe”Wakati wanaongea pale, alifika eneo lile Fetty na kukaa karibu nao na kuwasalimia pale,“Nawaona wapendanao jamani, yani nyie mnapendana hadi shetani anawaogopa”Mama Angel na baba Angel wakatabasamu, na kusalimiana nae pale kisha mama Angel alimuuliza,“Umekuja mwenyewe huku?”“Hapana, nilikuja na mume wangu ila kuna mtu kamuita mara moja si unajua wafanyabiashara muda wote wanawaza biashara tu, kwahiyo ametoka kwenda kumpa mzigo mtu mzigo ndiomana kaniacha hapa sababu atarudi”“Ila nimefurahi leo kusikia kuwa ulikuja hapa na mumeo”“Ndio, mume wangu kabadilika sana siku hizi. Kwakweli namshukuru sana Mwenyezi Mungu maana tabia ya Bahati imekuwa mpya kabisa”“Hongera sana”Kisha Fetty alimuangalia baba Angel na kumwambia,“Shemeji kumbe ulisafiri?”“Ndio, umejuaje?”“Kheee jamani, mimi nisijue kweli! Hata kama Erica asingeniambia basi ningejua tu, na huu umbea nisijue kweli jamani! Haiwezekani”“Mmh yani wewe Fetty ni mbea hatari”“Mimi tena shoga yangu ni balaa, ila ngoja nigeukie kwako shemeji, unajua nini kuna mama alikuwa anakufanyia sana usafi huko ulipokuwa, alikuwa akifanya usafi mara kwa mara kwenye chumba chako, anaitwa Juli, yule mama ni rafiki yangu sana, kwahiyo alikuwa akiniambia mengi sana”“Eeeeh bhana eeeeh sikuwezi kwakweli, nyie wanawake ni noma sana jamani, yani yule mama kule unamfahamu kwahiyo mlikuwa mkiulizana kuhusu mimi!”“Ndio lazima nimuulize, ili nijue mwenendo mzima wa shemeji yangu kule ulipokuwa”Fetty aliongea huku akicheka na kuendelea na maongezi mengine, baada ya muda kidogo Bahati nae yani mume wa Fetty alifika na kuwasalimia pale ila alimtaka mkewe waondoke muda ule ule, kwahiyo ilibidi wawaage na kuondoka zao.Mama Angel na mumewe nao walikaa kwa muda kidogo na kuamua kuondoka kurudi nyumbani kwao kwani waliona pia muda umeenda.Usiku wa leo, Fetty alimuuliza mume wake kilichopelekea kutaka kuondoka mapema kiasi kile, basi mumewe alianza kumueleza,“Ni hivi mke wangu, kwanza huwa sipendi kukuficha kitu chochote, nina uhakika unanijua kushinda hata ninavyojijua, ni mwanamke wa pekee sana kwangu maana ulijitoa kunivumilia kwa kila hali ukiamini kuwa kuna siku nitakuwa sawa kabisa, ni hivi mke wangu, yule Erica ni mwanamke ambaye nilimpenda sana, huwa napenda kusema hili kuwa sehemu kubwa ya mabadiliko katika maisha yangu basi ni sababu ya Erica tu, mimi sikuwahi kupikia jiko la gesi bila Erica kuniletea, mimi sikuwaza kuwa na biashara kubwa kubwa hivi maana sikuwa na mtaji wa aina yoyote, mimi nilikuwa mvuvi tu, yani navua samaki na kupata shilingi mbili tatu ila ziliishia kwa matumizi ya nyumbani na matumizi yangu binafsi maana ingawa sikuwa na mbele wala nyuma ila bado nilitegemewa sana na familia yangu. Erica alikuja kwenye maisha yangu kwa lengo la kunibadili kabisa, maana alinipa mtaji na hapo niliweka mabwaya ya samaki, na kufungua bucha langu mwenyewe, na kweli biashara ilikuwa nzuri sana, akanipa tena mtaji, nikaweka kuku na kufanya biashara ya kuku ambayo ilinilipa sana. Nilijitajidi kufanya kwa bidii ili kumfurahisha Erica, kwani nilihitaji niwe kama aina ya wanaume anaopenda yeye. Na kweli nikapata kiwanja na kujenga nyumba, na kununua gari lengo kubwa ni kuishi na Erica kwa masiha ambayo najua alikuwa akiyatamani kwa kipindi hiko. Kwanza kwa hayo tu natakiwa nimpende Erica kufa na kupona, nampenda sana, huwa sikufichi juu ya hili, huwa nakwambia wazi”“Naelewa mume wangu”“Ujue chanzo cha mimi kuachana na Erica, ni madawa ya kishirikina waliyonifanyia hadi nikamuoa yule mke niliyemuacha Nasma, nasikia Erica ilimuuma sana, naweza kuhisi kidogo maumivu yake yalivyokuwa, kuna wakati hata huwa nalia”“Najua mume wangu, hayo mambo yanavyokuumiza, ila swali nimekuuliza lingine ila umeanza kunipa historia yako na Erica wakati swali langu hata halihusu historia yenu”“Hivi umeniulizaje?”“Nimekuuliza kwanini baada ya kukuta nimekaa na Erick na Erica pale ukadai tuondoke upesi upesi? Hilo ndio swali, nina uhakika hayo majibu yako hata hayapo katika swali”“Ngoja nikujibu, ni sababu bado nampenda, halafu sipendi kuona akiwa na Erick. Najizuia hisia zangu ndiomana kwasasa sipendi kuwa nao karibu wala kuwa karibu yake, najua baada ya miaka kupita itakuwa pia ni historia katika maisha yangu ila kwasasa acha niwe na amani mke wangu, ukikaa walipokaa wale usishangae naondoka. Nalinda ndoa yetu, na mke wangu huwa unanifanyia dua nzuri sana, kwanini nianze na tamaa na wanawake wengine mie? Kwakweli hapana, nitabaki na wewe tu”Hapa kidogo Fetty alikuwa na amani kwani alitumia muda wake wa kila siku kuweza kumrejesha mumewe katika mstari anaouhitaji.Leo kama kawaida, watoto walienda shuleni, kwahiyo Elly alivyotoka shule hakurudi kwakina Sarah kwani moja kwa moja alienda kwenye mgahawa wa mama yake na kuamua kurudi nae nyumbani,“Ila mama kuishi kule dah!”“Kwani kuna nini mwanangu?”“Hawana maadili mama, hawaendi Kanisani wala nini. Kwanini umekubali nikaishi kule mama yangu?”“Mwanangu kila kitu kinafanywa sababu ya shida tu, unadhani nafurahi basi kukuacha wewe uteseke? Natamani ningekuwa na pesa basi ningekulea mwenyewe bila kumtegemea mtu yoyote ila sina pesa mwanangu”“Basi jana, tulienda kwenye sherehe ila mama alituacha huko kwanza, jamani mama watu walivaa nguo za ajabu hizo balaa eti ndio uzungu, halafu sherehe yenyewe ya mtoto ila watu walivaa nguo za ajabu”“Kheee mwanangu, waswahili husema ukimchunguza bata sana huwezi kumla, kwahiyo mambo mengine acha kama yalivyo ila cha msingi ulelewe ili upate maisha mazuri”“Sawa mama nimekuelewa”Wakiwa wanakaribia nyumbani, walikutana na madam Oliva, ila Elly hakujua kama kuna tatizo kati ya madam Oliva na mama yake maana yeye alijua ni mwalimu wake tu,“Mama, huyu ni mwalimu wangu madam Oliva, madam na huyu ni mama yangu”Ila alishangaa bila kusalimiana, kisha Sia alimvuta pembeni madam Oliva na kuanza kuongea nae,“Hivi wewe ulishamwambia Steve kuwa mwanae anamkumbuka huku!!”“Unajua wewe kweli ni mwezi mchanga, yani kadri siku zinavyoenda napata kukufahamu zaidi. Sasa mtoto wa Steve au wa Erick?”Sia hakumwambia kitu, ila alirudi kwa mwanae na kumshika mkono kisha waliendelea kurudi nyumbani kwao.Siku ya leo Erick aliporudi nyumbani kwao alimpelekea hoja nyingine baba yake, na hiyo hoja ilikuwa ni kutaka kuhama shule,“Kwanini unataka kuhama Erick?”“Siipendi tena ile shule”“Aaaah basi ngoja nifikirie kuhusu hilo swala”Kisha baba Angel alienda kuongea na mke wake kuhusu swala la Erick kutaka kuhama shule,“Kwanini anataka kuhama sasa?”“Sijui anasema haipendi tu ile shule”“Unajua nini mume wangu, kuna mambo tunapokuwa na watoto tunatakiwa kuwa na kiasi chao, Erick anataka kuhama shule kwasababu gani? Au ni sababu ya huyo Elly aliyepelekwa pale, kwani huyo Elly anamsumbua kitu gani Erick?”“Oooh Elly mtoto wa Sia? Ndio kapelekwa kusoma hapo?”“Ndio si unamjua Sia ni mkorofi, huwa anatafuta sababu tu ya kutugombanisha”“Sasa nimeelewa kwanini Erick anataka kuhama, nitafanyia kazi hilo swala lake, ila ngoja nitaongea nae kwanza”Kisha Erica alifika kumuita mama yake maana mgeni alifika, mama Angel akatoka ndani na kukuta mgeni mwenyewe ni mama Junior akiwa ameambatana na yule msichana ambaye amedai kuwa ana mimba ya Junior, ilibidi tu amakaribishe na kuongea nae kidogo halafu alienda kumuonyesha chumba cha vaileth na kumwambia Vaileth kuwa atakuwa akilala nae, Vaileth aliguna ila alikubali tu ingawa alijua itakuwa ngumu sana kufanya mambo yake kwenye chumba hiko.Kisha mama Junior akamuaga ndugu yake, kwahiyo mama Angel alimtoa ndugu yake huku wakizungumza kidogo,“Yani nashukuru sana mdogo wangu kwa kunipokea huu mzigo, kwahiyo inabidi tutafute hela ya faini kwasasa”“Ila Junior hawezi kuoa, maana bado anasoma”“Ndio, hata hivyo huwezi kumlazimisha amuoe labda hampendi au vipi, ila huyu binto akae kae hapa hadi kujifungua maana kwao wameshamsusa hivyo”Basi waliongea kidogo na moja kwa moja waligana halafu mama Angel aliingia ndani na moja kwa moja kwenda cbumbani kwa vaileth ili kuongea na yule binti,“Unaitwa nani kwanza maana hata sijakuuliza”“Naitwa Daima”“Oooh Daima, sawasawa, karibu sana itaishi vizuri tu hapa. Nikikaa vizuri tutaenda wote kwenu ili niitambue familia yako”“Sawa hakuna tatizo”Basi mama Angel hakuwa na tatizo nae na alimuacha hapo na kwenda kuendelea na mambo mengine.Usiku wa leo wakati Vaileth ndio kaingia kulala na huyu Daima pembeni yake basi alianza kumuhoji maswali,“Kwahiyo hiyo mimba ya nani?”“Ya Junior”Vaileth alimeza mate kidogo na kuendelea kumuuliza,“Junior mwenyewe anajua?”“Ndio anajua ila mara zote huwa ananikatia simu, kwetu wamechukia ndiomana wamenipeleka kwao. Basi mama yake ndio kanileta huku, ila jana nililala kwakina Junior”“Duh! Ila kwenu nako watachukuaje maamuzi ya kukupeleka kwa mwanaume tu?”“Weee kwetu, hawataki mtu uzalie nyumbani, yani hawataki kabisa, mama yangu ni mkali sana, baba yangu nae ni makali sana, hawataki haya mambo kabisa, sina namna zaidi ya kukubaliana na hali halisi tu”“Ila umemaliza shule?”“Nimeishia kidato cha nne, ndio nimepata hii mimba ya Junior kwahiyo sijaweza tena kuendelea na shule”“Una miaka mingapi kwani?”“Aaaah mimi niliwahi shule tu, sababu nilikuwa na mwili mkubwa sana. Ikabidi tu niwahishwe shule. Wazazi wangu ni wakali sana, na mimi kwetu ni mtoto wa kwanza, hakuna aliyekubali jambo hili ndiomana imekuwa hivi”“Ila Junior unampenda? Anakupenda?”“Ninampenda kweli Junior, ila sina uhakika na yeye kama ananipenda kama mimi ninavyompenda. Nampenda sana Junior, yani sana, na hiki kitoto chetu kikiwa cha kiume nitakiita Junior”Vaileth alimuangalia ila kiukweli hakupenda kabisa, sema alikuwa anavumilia tu maana hakuwa na namna yoyote ya kufanya, sema moyo ulimuuma sana alijikuta siku hii akilala huku machozi tu yakimtililika, halafu akamtumia ujumbe Junior,“Hivi Junior unanipenda kweli?”Muda huo huo Junior alijibu ule ujumbe,“Aaaah Vai, mpenzi wangu jamani. Nisipokupenda wewe nimpende nani tena!!”“Na Daima je?”Ujumbe ule ulikawia kidogo kujibiwa na kumfanya Vaileth apate maumivu zaidi katika moyo wake, ila badae ujumbe ule ulijibiwa,“Jamani mambo gani tena hayo, huyo Daima simtambui maana ninayekutambua ni wewe tu Vai wangu na ninakupenda sana”Vaileth hakujibu huu ujumbe kwa muda huu na kuamua tu kulala kwani alikuwa na mawazo sana.Kilivyokucha, Vaileth alimuamsha Daima ili wakafanye kazi za mule ndani,“Kheee mimi nina mimba ujue, nitafanyaje kazi mimi?”“Kwani mimba ni ugonjwa? Ulisikia watu wakiwa na mimba hawafanyi kazi?”“Ndio, mama anasema mwanamke mjamzito anatakiwa kupumzika, kwahiyo mimi siwezi kufanya kazi sana mimba yangu isije ikatoka bure wakati mwanangu namuhitaji sana”Vaileth alimuangalia Daima bila ya kummaliza, kisha yeye akainuka na kwenda zake jikoni kuanza kazi za mule ndani.Leo shuleni, muda wa mapumziko kama kawaida ya Erica na rafiki yake Samia, walikaa pamoja na kuanza kuongea mambo ya nyumbani kwao, ambapo Samia alimuuliza kwanza Erica kama baba yake amerudi,“Hivi baba yako kasharudi Erica?”“Ndio karudi, ila mimi hiwa napenda sana baba akiwepo sababu ni mtu anayenisikiliza sana kuliko mama”“Oooh na mimi basi baba ndio hunisikiliza sana kuliko mama, unajua mama yangu ni daktari eeeh kwahiyo muda mwingi anakuwa kwenye kazi, mara shifti ya asubuhi, mara ya ya usiku yani mama yangu haeleweki. Ila nyie mnakuwa muda mwingi sana na mama yenu”“Ni kweli ila mama hapendi masikhara kabisa, kuna vitu unaogopa kabisa hata kumwambia mama ila baba akiwepo unamuambia tu. Eeeh niambie kuhusu baba yako na mama yako basi”“Basi bhana, unajua ile Jumapili baba aliondoka nyumbani, halafu alijua mama atakuwa shifti ya usiku, kumbe hakurudi hadi Jumatatu asubuhi yani jana, sijui ilikuwaje huko lakini dada yetu yule wa kazi kanieleza kidogo tu, inaonyesha baba kaanza na mwanamke mwingine”“Mmmmh mmejuaje?”“Si kwasababu alikuwa akimjibu mama vibaya, yani alikuwa akimjibu tu ilimradi, dada akaniambia inaonekana baba kaanza na mwanamke mwingine”“Ila baba yako ni noma sana”“Kweli ni noma sana baba yangu, ila baba yangu anapenda wanawake huyo balaa”“Umejuaje?”Kengele ya darasani iligonga, ikabidi waende darasani kuendelea na vipindi vya siku hiyo.Baba Angel aliamua kwenda na mkewe kiwandani baada ya mkewe kumwambia kuwa alikuwa akienda wakati yupo safarini, basi walimuacha pale nyumbani mtoto, Vaileth na yule Daima halafu wao waliondoka moja kwa moja na kwenda kiwandani.Walifika na kufanya kazi za kiwanda huku wakielekezana mambo mbalimbali,“Unajua kuna muda naelewa ni kwanini wanawake ni wasaidizi wa wanaume”“Kwanini?”“Sababu mpo kufanya pale tunapokwama, kwakweli wewe mke wangu umekuwa ni sehemu kubwa sana kwangu. Sikuamini wakati naelezwa vyote ulivyovifanya hapa kiwandani, kumbe nilikuacha msimamizi mzuri na hodari”Mama Angel alitabasamu tu kwa sifa alizopewa na mume wake.Basi wakati wakiendelea na kazi za hapa na pale, ndipo kuna mgeni alifika pale kiwandani, mgeni huyo alikuwa ni Juma, baba Angel alitoka na kuongea nae vizuri tu,“Unajua nini, nilikuwa napita hapo, sasa nikaona ni vyema nipitie hapa. Kumbe Erick umerudi kimya kimya jamani!!”Baba Angel alicheka tu, kisha Juma aliendelea kuongea,“Na vipi mkeo nae anaendeleaje?”“Nipo nae kiwandani”“Oooh haya, hongera zenu. Leo sina mengi ila ukirudi mpe salamu zangu Erick”Juma aliaga na kuondoka zake kisha baba Angel akarudi kuendelea na kazi zake na kawaida.Waliporidhika wakaona ni vyema kurudi nyumbani, ila wakati wanarudi baba Angel alianza kumwambia mke wake,“Hivi mke wangu, huyo Daima aliyekuja sijui mwenye mimba ya Junior, ushafanya utaratibu wa kufahamu wanapoishi wazazi wake? Au dada yako kashafanya hivyo?”“Mmmh hata sijui, ngoja nimpigie kwanza mama Junior nijue”Muda ule ule mama Angel alimpigia simu mama Junior, na alipokea simu na kuanza kuongea nae,“Samahani dada, unapajua wanapoishi wazazi wa huyu msichana uliyemleta kwangu, huyu Daima?”“mmmh hapana, hilo ni kosa nimefanya, yani alipokuja kumbwaga rasmi hata sijauliza wanapoishi wala nini”“Jamani dada jamani. Hivi tukipata matatizo je! Mtu mwenyewe ni mjamzito, kama unavyojua mimba zilivyo.”“Naelewa mdogo wangu, nisameheni bure”“Basi, ngoja nikamuulize ili ikiwezekana kesho anipeleke huko kwa wazazi wake”Mama Angel aliagana na dada yake na kukata ile simu kisha akamwambia mumewe,“Nitaongea na yule msichana ili anipeleke kesho kwa wazazi wake niwafahamu”“Ooooh sawa kama ni hivyo, maana si vizuri kuishi na mtoto wa mtu bila kujua kwao. Ila unajua kuna vitu sielewi”“Vitu gani?”“Hivi mtoto wako akipewa mimba na kijana, mfano kama binti yetu Erica au Angel, hivi mzazi unawezaje kuchukua hatua na kwenda kumsokomeza huyo binti yako kwenye familia ya huyo kijana ambayo huijui vizuri wala nini!”“Mmmh hapo pagumu, ila huwezi jua ni kwanini mzazi mpaka kafikia hatua hii, labda kashamkanya binti yake sana ila mtoto hajasikia”“Mfano hapafahamu nyumbani kwao huyo kijana ataenda wapi huyo binti yako? Au ukimpeleka huko napo akifukuzwa itakuwaje?”“Mmmmh sielewi”“Kwani sheria inasemaje?”“Hivi nikuulize wewe, mfano wale mabinti wote uliokuwa ukiwapa mimba wangeletwa kwenu ingekuwaje?”“Oooh tuachane na habari hizo mke wangu, tuongee mambo mengine. Unawaonaje watoto wetu?”“Nawaona wapo sawa tu”“Na Erica na ukuaji wake umemfatilia vizuri?”“Ngoja nikwambie kitu kuhusu Erica, yule mtoto tumempata ni mbea tu yani umbea kwake ni moto moto, ila Erica hana tabia chafu hata moja, halafu ninachompendea ni kimoja tu ukimkataza kitu harudiii tena”“Na Erick je!”“Yule nimempatia jina jipya, yani Erick ana kisirani sana, ila tukitoa hiko kisirani ni mtoto mzuri sana na mwerevu sana, kwakweli nampenda sababu hata yeye ukimkataza kitu hakai arudie tena hiko kitu”Baba Angel alifurahi kusikia wasifu wa watoto wake, wakaendelea na safari na kurudi nyumbani kwao.Walipoingia ndani, moja kwa moja mama Angel alienda jikoni na kumkuta Vaileth kambeba mtoto mgongoni huku akipika,“Kheee kwanini umefanya hivyo Vai?”“Alikuwa analia mama”“Sasa kwanini usingempa yule Daima ambembeleze?”“Mama, huyo Daima kasema kuwa yeye hawezi fanya kazi yoyote sababu ni mjamzito”“Kheee makubwa, kwahiyo yuko wapi?”“Aliamka tu kula, ila karudi tena kulala”“Ndio huwezi kufanya zile kazi ngumu, lakini hii ya kukaa na mtoto tu jamani, kuosha vyombo napo anashindwa? Au kapewa mapumziko? Khaaa huyu kanishinda tabia, haya mlete huyo mtoto”Basi mama Angel akamchukua mwanae na kwenda nae chumbani.Leo jioni Tumaini alikutana njiani na mama Sarah kwahiyo walianza kusalimiana maana ni muda mrefu sana hawakuonana,“Kheee jamani mama Leah, nyumbani kwangu sio mbali na hapa, naomba twende ukapafahamu”“Sawa, hakuna tatizo”Basi wakaongozana huku wakiongea mambo mbalimbali ikiwemo na lile swala la mama Angel,“Hivi Erica unafahamiana nae vipi maana sikufatilia”“Erica nimesoma nae kabisa, halafu unajua sikujua kitu kumbe na Erick ni ndugu yako kabisa”“Ndio ni mdogo wangu, unamfahamu pia?”“Ndio, nilisoma shule moja na Erica na Erick ila walifukuzwa sababu ya utovu wa nidhamu maana walileta mapenzi shuleni”“kheee ni Erica ndio mlikuwa mnasoma nae!”“Ndio, yani utovu wa nidhani ulifanya Erica na Erick wafukuzwe shule, ila nawafahamu vizuri sana na wao wananifahamu vizuri sana. Jina langu halisi ni Manka”“Oooh kumbe!! Nafurahi kukufahamu leo zaidi”Basi moja kwa moja walifika nyumbani kwa mama Sarah ambapo alimkarisha ndani na hapo walimkuta Sarah amekaa maana alishatoka shuleni, basi aliwasalimia pale nakuendelea na mambo yake, alikuwa akiangalia Tv huku akichezea simu na alikuwa makini nayo sana.Mama Sarah alimtambulisha Sarah pale kwa Tumaini,“Huyu ndio binti yangu mpendwa, mwanangu wa pekee ninampenda sana. Huyu ndio Sarah”“Oooh kumbe Sarah mwenyewe ndio huyu! Nafurahi sana kumfahamu”“Sarah, huyu ni rafiki yangu anaitwa mama Leah”“Sawa mama, nashukuru kumfahamu”Basi mama Sarah alimuaga kidogo Tumaini pale kuwa anaenda kuweka mkoba na kumwambia msichana wake wa kazi amletee juisi Tumaini, kisha akaondoka na kwenda kuweka mkoba wake.Tumaini alibaki akimuangalia Sarah pale, akamuuliza,“Upo busy na simu Sarah, kwani unafanyaje?”“Nipo instagram yani kuna vitu vingi vya kuchekesha sana”“Mmmh!! Unajua bado mdogo sana wewe! Kwahiyo huwa unaangalia hiyo instagram muda wote?”“Ndio, yani mimi facebook nipo, whatsapp na istagram, ila mara nyingine huwa naangalia video youtube”“Duh!! Wewe Sarah wewe bado mdogo sana kufanya vitu hivyo”Mama Sarah nae alitoka chumbani kwake na kukuta yale mazungumzo kati ya Sarah na Tumaini, basi akamuuliza Tumaini,“Unasema bado mdogo nani na kwanini?”“Nasema huyu Sarah bado mdogo katika kuchezea simu hivyo”“Mmmh na wewe kama mtu wa kale jamani, mimi mwanangu namlea kizungu, acha afahamu mambo mengi mapema wala haitamsumbua hapo badae, ni mtaalamu wa simu balaa”Tumaini hata hakutaka kukaa sana na kuamua kuaga, basi wakati mama Sarah akimsindikiza akarudia tena kumwambia,“Ila mama Sarah, yale sio malezi ya mtoto. Nimekaa muda mchache sana ila nimeweza kuona malezi ambayo Sarah amekuwa nayo, sio malezi mazuri”“Jamani kwanini?”“Mwnao kanywa juisi pale ila kashindwa kutoa kile kikombe wala nini, ndio kwanza anachezea simu tu hadi yule mdada wenu kuja kutoa”“Ila yule Siku ile ni kazi yake, namlipa mshahara kwasababu ya kazi ile, kwanini mwanangu ahangaike”“Haya, na kuhusu simu”“Kuhusu simu ni kuwa mwanangu anaishi kizungu, nimemlea hivyo toka mdogo. Huwezi amini ila yule mtoto hata kumpiga kibao sijawahi kumpiga”“Dah!! Hayo sio malezi kabisa mama Sarah haijalishi una pesa kiasi gani ila hayo sio malezi kwa mtoto. Siku nakuomba poteza muda wako uje kwangu nikufundishe jinsi ya kumlea mtoto, muwahi huyo Sarah, huko sio kumpenda bali ni kumuharibu tu”Tumaini aliagana nae na kuondoka zake muda huo.Usiku wa siku hiyo, mama Angel alimuita Daima na kuongea nae kuhusu wazazi wake na kumtaka kuwa kesho yake ampeleke kwa wazazi wake ili akawafahamu,“Sawa, hakuna tatizo, nitakupeleka”“Si mama yako na baba yako wapo?”“Wapo ndio, tena kesho hata baba atakuwepo nyumbani maana mara nyingi huwa anapumzika siku hiyo”“Sawa, kesho utajiandaa ili twende”Basi mama Angel alivyomaliza kuongea nae alienda tu kwa mume wake muda huo ili waweze kulala, ila mume wake akaongea nae jambo lingine,“Unajua nini, kuna mteja Fulani hivi Erick alinitambulisha nasikia anajulikana kwa jina moja la mwarabu, nimejaribu kufatilia nasikia ni mteja wetu mkubwa sana, nahitaji kuwa nae karibu zaidi ikiwezekana hata siku tumualike hapa kwetu kupata chakula cha jioni pamoja”“Ooooh hiyo ni zuri, tena tutamualika yeye na mke wake, kama ni mteja mkubwa basi inatakiwa tumkirimu zaidi ili kuendelea kuweka alama nzuri ya kuwa mteja kwetu”“Sawa mke wangu, kesho nitaenda kwanza ofisini kwangu kule halafu nitaenda kiwandani ambapo nitaondoka na Yuda ili tukapafahamu vizuri kenye biashara za yule mzee”Hapo sawa mume wangu”Wakaongea mengi sana na mwishowe waliamua tu kulala kwani muda nao ulikuwa umeenda.Kulipokucha, mama Angel alifanya tu shughuli zake kwanza na kumtaka Daima ajiandae ili waende nae huko kwao, na kweli baada ya muda mchache Daima alishajiandaa na kuanza safari ya kumpeleka mama Angel nyumbani kwao.Walipofika nyumbani kwakina Daima, mama Angel alipaki gari yake pembeni na kwenda sasa kuingia ndani ya hiyo nyumba, ambapo aliyewakaribisha alikuwa ni mama yake Daima, moja kwa moja waliingia sebleni ambapo palikuwa na baba yake Daima ila mama Angel alipomuangalia alishangaa maana ni mtu ambaye anamfahamu. Walipofika nyumbani kwakina Daima, mama Angel alipaki gari yake pembeni na kwenda sasa kuingia ndani ya hiyo nyumba, ambapo aliyewakaribisha alikuwa ni mama yake Daima, moja kwa moja waliingia sebleni ambapo palikuwa na baba yake Daima ila mama Angel alipomuangalia alishangaa maana ni mtu ambaye anamfahamu.Basi alimuangalia kwa makini, ila baba Daima alimuwahi na kumkaribisha nyumbani kwake,“Karibu sana, hapa ndio nyumbani kwangu, eti Daima umetoka wapi na mgeni huyu?”Daima alikuwa kimya tu, kisha mama Angel akamwambia baba Daima,“Kwanza sikujua kama huyu ni mtoto wako Babuu, kumbe una binti mkubwa kiasi hiki jamani!!”“Aaaah mkubwa wapi huyu mjinga, shule mmemshinda, ana ukubwa gani hapo alipo”“Si kamaliza kidato cha nne huyu!!”“Amalize wapi wakati mwaka jana kafanya mtihani wa kumaliza kidato cha pili amefeli, kwahiyo tulikuwa nae nyumbani nikifikiria kumrudisha tena shule akaanze kidato cha kwanza”“Mmmh ila hebu tuongee vizuri, kwanza sikujua kama ni binti yako huyu. Samahani sana, ila nilimwambia kuwa leo nahitaji kufahamu wazazi wako”“Kwani wewe umemfahamu vipi huyu Daima?”“Huyu, kaletwa tu nyumbani kwangu na dada yangu kuwa wazazi wake mmembwaga kwake na kusema kuwa ana mimba ya kijana wetu”Baba Daima akashtuka sana,“Kheee ana mimba!!”Akainuka na kusogea karibu na Daima na kumzaba vibao vitatu na kusema,“Wewe mjinga, shule umefeli halafu umeenda kubeba mimba!!”Mama Daima ilibidi aingilie kati maana wakati mumewe ameanza kuongea na mama Angel alitoka kidogo, ila aliposikia mumewe akimzaba vibao mtoto wao ikabidi atoke ili akamuamulie, basi akamtuliza pale mumewe na kumkalisha pembeni,“Kwani tatizo nini mume wangu?”“Tatizo nini? Yani kumbe huyu mjinga ana mimba na hujaniambia chochote”“Punguza jazba kwanza mume wangu nikueleze vizuri yaliyopo”Baba Daima alitulia huku akingoja maelezo,“Ni hivi, mtoto humu ndani alianza kuumwa, hataki kula chakula, anachagua chagua, nikaamua kwenda nae hospitali na ndio nikagundua kuwa ni mjamzito, kwakweli nilichanganyikiwa kwani nilijua ungegungua ingekuwa balaa, ila nilipanga kukwambia. Nilimbana mimba ya nani, ndio akanitajia huyo kijana wa kuitwa Junior, basi nikamtaka anipeleke kwao, yani nishaenda nae huko kwakina Junior mara kadhaa ila niliona huyo mama Junior haeleweki ndio nikaamua kumbwagia pale mtoto hadi atakapojifungua”“Khaaa hivi na wewe mke wangu una akili kweli eeeh!! Mambo mengine unatakiwa kunishirikisha mimi mwenyewe. Haya wewe Daima, hebu kaa vizuri hapo, una mpango gani na hiyo mimba?”“Nahitaji kuwa na mtoto baba”Baba Daima alisikitika sana na kusema,“Yani kumbe nilikuwa nakusomesha bure tu, huna maana hata moja, mjinga wewe”“Nisamehe baba”“Kwahiyo una mpango gani na huyo mjinga mwenzio?”“Nahitaji anioe baba, nahitaji awe mume wangu”“Kweli wewe mtoto ni tahira wa mwisho sijapata kuona, unajua kama unanichefua zaidi”Basi mama Angel aliamua kutuliza kidogo pale na kuelezea azma yake iliyompeleka mahali pale basi baba Daima akasema,“Kwa leo muache hapa huyu binti yangu, nishauriane na halmashauri ya kichwa changu kwanza halafu kesho tutamleta huko nyumbani kwako”Mama Angel hakuwa na maneno zaidi, basi aliaga tu na muda huo baba Daima aliinuka kwenda kumsindikiza mama Angel wakati huo Daima kabaki na mama yake ndani.Basi walipofikia gari ya mama Angel, baba Daima akamwambia,“Unajua mara nyingine ni bora kuoa yule uliyepanga toka mwanzo kumuoa katika misha kwani itasaidia na kujikuta mambo mengi sana mkifanana, ila haya maswala ya kuoa tu ili kutimiza sheria ndio madhara yake haya”“Kwanini?”“Kwakweli, wewe ndio ulikuwa mke wangu. Wewe ndio ulikuwa mwanamke wa maisha yangu”“Aaaah Babuu hayo yalishapita, tuyaacha bhana. Una maisha yako na mimi nina maisha yangu, namuheshimu mume ambaye Mungu amenipatia na wewe muheshimu mke ambaye Mungu amekupatia”“Namuheshimu mke wangu tena namuheshimu sana, tatizo lake ni moja tu tumeishi kipindi chote lakini huwa ananiogopa yani mambo mengi sana huwa haniambii ukweli kabisa hata sijui ana matatizo gani, tofauti na jinsi ulivyokuwa wewe”“Mwambie vile unavyopenda mbona atabadilika tu, yeye sio malaika kusema agundue ni kitu gani unapenda kutoka kwake. Mwambie ili naye afanye vile unavyotaka wewe”“Ila tuache masikhara Erica, unazidi kupendeza kwakweli, nakumbuka miaka hiyo wakati nakutana na wewe ukiwa binti mdogo sana, kwakweli mapenzi yaliniwehesha, wala sikusikia wala kuhema juu yako, kwakweli Erica nilikupenda sana na bado nakupenda ila namuheshimu mke wambaye Mwenyezi Mungu amenipatia kama ulivyosema kwani kila kitu kinachotokea katika maisha yetu basi ni Mungu ndiye anajua kwanini kimetokea”“Hapo sasa ni sawa, na tutaenda sambamba. Ila usimfokee sana na mtoto, tutajua tu cha kufanya kama wazazi tutaungana na kuwa letu moja”“Sawa sawa nimekuelewa”Basi wakaagana na moja kwa moja mama Angel alipanda kwenye gari na kuondoka zake.Mama Angel akiwa njiani alimuona rafiki yake Dorah, basi alisimamisha gari na kumpakia huku akiongea nae,“Kwani unaenda wapi muda huu?”“Naenda hapo mbele, kuna shule ndio anasoma binti yangu”“Aaaah sawa, ngoja nikupeleke basi”“Aaaah vizuri hivyo, utakuwa umenisaidia. Eeeeh nimekumbuka kitu Erica”“Kitu gani hiko?”“Jumapili nilimuona Rahim mahali akiwa ameongozana na mwanamke Fulani hivi ila namkumbuka mwanamke huyo”“Ni mwanamke gani?”“Mwanamke mmoja hivi, kipindi wakati nipo na mzee Jimmy alikuwa nae pia, nakumbuka wakati mzee Jimmy kajigundua kuwa ameathirika alikuwa akinilaumu sana mimi, alinisema sana kuwa nimemuambukiza. Ila kuna siku moja wakati nimeolewa niliwahi kumuuliza mzee Jimmy ni kwanini alikuwa akishutumu kuwa mimi ndio nimempa ukimwi wakati alikuwa na mwanamke mwingine? Huyo dada eeeh nimekumbuka jina lake anaitwa Manka, basi mzee Jimmy aliniambia katika wanawake wastaarabu aliowahi kukutana nao basi ni Manka, maana mara zote alizokutana nae kimwili basi Manka alikuwa akitoa kinga na kumvisha, kwahiyo 1alisema Manka hawezi kumuambukiza yeye ukimwi. Ila Jumapili nimemuona huyo Manka akiongozana kwa madaha na Rahim, laiti angejua kuwa ameenda kuuzoa ugonjwa hata asingetembea nae kwa madaha”“Kheee kumbe, ila Rahim nae anausambaza hatari”“Yule tabia yake kama ile yangu ya kipindi kile, ila ataacha tu”Basi mama Angel alimfikisha Dora kwenye shule aliyokuwa anasoma binti yake na kuagana nae.Baba Angel leo alienda ofisini kwake kwanza, halafu alitoka ili aende kiwandani, ila wakati yupo njiani kuna mtu alimuona na kumshangaa kidogo maana hakutegemea kama angemuona mitaa hiyo, basi akasimamisha gari ili kumsalimia maana alimuheshimu huyu mama, alikuwa ni bi. Aisha, basi akamsalimia pale na kuanza kuongea nae machache,“Nilimuona mkeo kaja kule kaburini kwa mzee wenu, tafadhari usimruhusu tena mkeo kwenda kule peke yake”Baba Angel aliona ni vyema kama akimuuliza vizuri kuhusu hilo, basi alisogea nae karibu na gari lake na kuanza kumuuliza,“Kwani mama tatizo ni kitu gani?”“Sikia nikwambie, ni kweli mzee Jimmy alikuwa ni baba yenu na aliwapenda sana watoto wake, yani ni kweli kabisa aliwapenda, ila huyu mzee naweza sema ni mzee ambaye alikuwa na tabia chafu ya kujaribu kufanya vitu ambavyo huwa vina matokeo mabaya badae ila tu huwa anajaribu kuona kama itakuwa anavyofikiria”“Kivipi, sikuelewi”“Ni kweli kunielewa itakuwa ngumu sana, mimi sikujua ni kipi kipo kati ya mkeo na baba yako mzazi, ila badae nikagundua kuwa baba yako alikuwa akimpenda sana mkeo, yani hata siku ya harusi yako alitamani yeye ndio amuoe mkeo, kile kitendo cha wewe kumpiku yeye kilimuuma sana. Ila hili sidhani kama lilikuwa tatizo sana, kwani mzee Jimmy umri ulienda na alikuwa na kila sababu ya kuacha wewe na mkeo mfurahie ndoa yenu. Ila sijui nini tena kilimuingia na kuanza kufikiria kufanya ujinga”“Ujinga gani?”“Erick, ukiwa na muda naomba ufike nyumbani kwangu na tuongee mengi sana. Nahitaji kuongea nawe kwa kirefu kuhusu baba yako, najua kuna mengine nayajua lakini wewe huyajui wala nini. Kwanza watoto wenu wale mapacha wanaendeleaje?”“Wanaendelea vizuri tu”“Basi nashukuru kwa hilo, maana katika vitu vyote ni wale watoto ndio huwa wananipa mashaka. Ila tutaongea vizuri tu”Kwakweli baba Angel alitamani siku hiyo hiyo asikie kila kitu, yani alijikuta akiwa tayari kuacha mambo yote ambayo alikuwa akiyafatilia siku hiyo ili akamsikilize huyu mama, basi alimuomba ampeleke huko kwake ili akamwambie ukweli,“Hapana Erick sio leo, nitagfute kwa siku yako”Basi yule mama alimpa tu baba Angel namba yake ya simu ili waweze kuwasiliana, baada ya hapo yule mama aliondoka zake.Kwakweli baba Angel alienda kiwandani ila mawazo yote ni kwa huyo mama kwani alitamani kuujua ukweli wa mambo yote ulivyo.Usiku wa leo, mama Angel anamueleza mumewe kuhusu kilichojiri wakati wa yeye kumpeleka Daima kwao,“Kumbe baba yake Daima ni mtu ambaye namfahamu”“Unamfahamu kivipi?”“Ni ndugu yake na Rahim, alinikumbuka basi tumeongea pale na wamesema kuwa watakuja kesho kwahiyo mtoto wao nimemuacha huko”“Dah! Kesho”“Ndio, kesho kwani kuna tatizo gani mume wangu?”Basi baba Angel alimueleza kuhusu bi.Aisha alivyokutana nae njiani, alimueleza yote ambayo aliongea na yule mama, kisha akamwambia mke wake,“Yani nilichokuwa nawaza ni kuwa kesho nifanye juu chini ili niende kwa yule mama na kumsikiliza kile anachokijua kuhusu baba yangu”“Dah! Kweli mume wangu, ila kesho kuna ugeni jamani, naomba twende wote keshokutwa, usiniache peke yangu kusikiliza hao wageni mume wangu”“Nimekuelewa mke wangu, basi sitaenda kesho, tutaenda wote keshokutwa maana nahisi hayo maneno hata wewe unatakiwa kuyasikiliza”Wakakubaliana kwenda wote kwa siku ya kesho kutwa, ila muda huo mama Angel aliona ni vyema kumwambia dada yake ili nae afike kesho yake wakati wazazi wa Daima wanafika ili waweze kuzungumza kuhusu Daima na Junior,“Sawa mdogo wangu nitakuja, nashukuru sana. Kwakweli umefanya jambo la akili sana, yani hata sikufikiria kabisa kuhusu swala hilo”“Tupo pamoja dada”Kisha kwa muda huo baba Angel na mama Angel waliamua kulala tu.Usiku huu Vaileth aliamua kumpigia simu Junior ili aongee nae vizuri kuhusu Daima maana leo Daima hakuwepo kwahiyo akaona kuwa ataongea nae vizuri,“Hebu nieleze ukweli Junior, huyu Daima ana mimba yako au sio yako?”“Kwani wewe Daima huyo umemfahamu vipi?”“Usiniulize Junior ila niambie ukweli, ninachotaka kujua ni ukweli tu”“Huyo Daima hana mimba yangu”“Kwahiyo mimba aliyokuwa nayo ni ya nani?”“Ngoja nikwambie ukweli Vai, ni kwamba niliwahi kuwa na mahusiano na huyo Daima ila ni zamani kidogo, nikaachana nae ila ndio akawa analazimisha tuendelee na mahusiano, kama unakumbuka kuna siku ulikuta ujumbe kwenye simu yangu wa mwanamke akisema kuwa katoa mimba na damu nyingi zimemtoka, basi ni huyo Daima, ila hakuwa na mimba bali aliongea tu. Kuna siku aliniambia kwavile simtaki basi atasingizia kuwa ana mimba yangu ili mimi nilazimishwe kuwa nae, kiukweli Daima hana mimba na wala hana mimba yangu, huyo binti ni malaya na nilishaachana nae zamani sana”“Mmmmh Junior”“Kweli hiki ninachokwambia, simpendi Daima wala nini, ninayekupenda ni wewe. Nasubiri nimalize shule ili mimi na wewe tuoane na tuwe mke na mume rasmi, usisikilize habari za watu wagombanishi Vai, nakupenda sana mpenzi wangu”“Mmmh!”“Usigune Vai, nakupenda sana mwenzio, tena sana. Ipo siku nitaongea mbele ya hao watu wote na mbele ya mama yangu kuwa nakupenda sana wewe, achana na maneno yasiyo na maana mpenzi wangu na tuendelee kupendana tu”Basi wakaongea pale na mwisho wa siku wakaagana na kila mmoja kulala tu.Kulipokucha tu, Vaileth aliamka na kuanza kazi za hapa na pale kama kawaida yake, ila siku hiyo mapema kabisa mama Junior alifika na kumkuta Vaileth ndio anamalizia usafi,“Kheee upo vizuri Vai, kumbe ndio unamalizia usafi muda huu!”“Ndio mama, shikamoo. Karibu”Basi mama Junior alimsubiria pale Vaileth amalize kudeki na kuingia nae ndani, ambapo mama Angel ndio alikuwa akipika chakula cha asubuhi,“Kheee dada, ndio umekuja asubuhi asubuhi!”“Ndio, yani hujui tu nimelala nikiwa na mawazo kiasi gani, jamani huyu Junior ataniua mimi. Mara nyingine ni bora hata uwe na watoto wawili na kuendelea kidogo kichwa kitatulia lakini akiwa mmoja tu dah”“Dada, unaweza ukawa na wengi ila nao wote wakakusumbua, cha muhimu ni kumuomba Mungu tu”Kisha walikaa pale na kuandaa chakula cha asubuhi na kuanza kula,“Yu wapi shemeji?”“Ametoka, ila atarudi tena maana nilimuomba na yeye awepo”“Oooh hapo sawa sawa”Basi wakaendelea na majukumu mengine ya siku hiyo.Baba Angel alijitahidi kumaliza majukumu yake mengine ili akawawahi hao wageni na kuwasikiliza maana mkewe alishaongea nao na walisema wataenda kwenye mida ya saa nane, kwahiyo kwenye saa saba baba Angel alitoka zake kwenye shughuli zake na kuanza kuelekea nyumbani kwake, ila njiani alimuona yule mteja muarabu ambaye alipanga kukutana nae rasmi ila hakuweza kuonana nae siku aliyoenda, basi akasimama na kuanza kumsalimia pale huku wakiongea mawili matatu,“Tulijaribu kukufata kwenye duka lile ulilotuelekeza ila ulikuwa umeondoka”“Kweli mimi ni mtu wa mihangaiko sana, si unajua sisi wafanya biashara tulivyo hatutulii sehemu moja”“Dah! Basi tukakukosa bhana”“Hakuna tatizo lakini, tuwe tunawasiliana ndio itakuwa rahisi zaidi kuonana”“Sawa, sawa”Baba Angel leo alichukua mawasiliano ya huyu mwarabu ili awe anawasiliana nae mwenyewe, basi akaagana nae na kwenda nyumbani kwake.Na alivyofika tu nyumbani, na wale wageni nao walifika, yani baba Daima, mama Daima pamoja na Daima mwenyewe.Basi waliwakaribisha pale na kuanza kuongea nao, wakati huo Vaileth alikuwa akiwaletea vinywaji pale ili washushie wakati wa maongezi, na maongezi hayo aliyaanza baba Daima,“Unajua kwanza nimeshtuka sana ile jana kugundua kuwa binti yangu ni mjamzito, yani kilichotuleta hapa ni kujua hatma ya hii mimba”Baba Angel aliongea nae,“Cha kwanza kabisa tujue, mimba hiyo ina umri gani?”Mama Daima akajibu,“Ina miezi mitatu kwasasa, ni mimi mwenyewe ndio nilienda hospitali na Daima na kugundua kuwa ni mjamzito”Basi baba Angel akaendelea kuongea,“Sawa, tuongee kama wazazi sasa, hatutaki baya litokee kwa mtoto wenu wala baya litokee kwa mtoto wetu. Hawa ni watoto wetu, inatakiwa sisi wazazi tujue jinsi ya kufanya”“Ila ni vizuri kama na huyo mwanaume angekuwepo hapa ili atujibu vizuri”“Baba Daima, wewe ni mwanaume mwenzangu nadhani unaelewa fika haya mambo yalivyo. Jamani mimi kwanza kabisa naomba msamaha kwaajili ya Junior, ila kwasasa yupo shuleni, na sisi kama wazazi tutakuwa bega kwa bega nanyi kwa jambo hili”“Kivipi? Kumbuka huyo Junior kaharibu maisha ya mwanangu maana mwanangu ana mimba sasa, je atamuoa? Tunahitaji hili jibu kutoka kwake”“Sawa, hakuna tatizo. Inabidi kikao kijacho awepo na Junior, mimi nitaenda kumfata Junior shuleni ili Jumapili awepo hapa na kikao hiko kifanyike akiwepo ila kwanza wazazi tupate muafaka”“Hakuna muafaka wa wazazi tupu hapa, nataka kauli ya kijana kwanza ndio niendelee kuongea kama baba. Yupo tayari kumuoa mwanangu? Nikijua ndio nitasema ninachotaka kusema”Baba Angel alipumua kidogo ila hakutaka kufanya marumbano pale, ikabidi wakubaliane kuwa Jumapili ataitwa Junior ili kusema pia kuhusu kumuoa Daima au la.Baada ya maongezi hayo, waliwakaribisha mezani ili waweze kula chakula, na kweli walikaa mezani na kula, huku wakinywa juisi, ila wakati wa kula baba Daima akasema,“Hii juisi nimekunywa tangu mwanzo nikashindwa kuongea, ila naomba niulize muda huu. Hii juisi imetengenezwa na mama mwenye nyumba eeeh!!”Baba Angel alimuangalia baba Daima na kumuangalia mke wake kisha akauliza,“Kwanini?”“Nishawahi kunywa juisi ilitotengenezwa naye”“Ni kweli nimetengeneza mimi”Mama Angel alisema ili kukatisha yale mazungumzo kidogo, kisha baba Daima akasema,“Ni nzuri sana kwakweli, hongera sana”“Asante”Basi walivyomaliza kula, waliongea ongea kidogo na kuamua kuondoka ila Daima waliamua kumuacha hadi hiyo Jumapili ambayo wataenda kufanya kikao kingine,“Ila huyu Daima abaki tu hadi hiyo Jumapili”“Hakuna tatizo, tutakuwa nae hapa tu”Kisha mama Daima na baba Daima wakaaga tena na kuondoka zao.Ila mama Daima na baba Daima walivyotoka tu nje ya geti, kuna mwanamke alikuwa karibu na pale, na kumuita baba Daima pembeni kwahiyo mama Daima alisimama tu kuwasubiri maana hakuelewa yule mwanamke kamuitia nini mume wake,“Samahani, najua hunijui”“Sikujui ndio”“Mimi naitwa Sia, ila kuna kitu nimekiona kwako”“Kitu gani?”“Wewe si umekuja kwaajili ya binti yako mwenye mimba ya Junior?”“Ndio, tatizo nini kwani?”“Huyu mama mwenye nyumba, ana mtoto anaitwa Angel, huyo mtoto baba yake anatamani sana kumuona ila huyu mama hataki kabisa mtoto amfahamu baba yake anamficha, kwahiyo ongea nae labda wewe atakuelewa”“Kwani wewe ni nani na huyo baba yake Angel”“Aaaah….. mimi aaaah…. Mimi ni msamalia mwema tu ambaye namuhurumia Angel na ninapenda amtambue baba yake wa halali”“Sikia nikwambie kitu, huyo baba Angel unayemsema ni ndugu yangu kabisa, anaitwa Rahim. Sasa sisi wenyewe wenye ndugu hatuna tatizo ila wewe jirani inakuuma nini? Angel kafanana sana na baba yake, kuna kipindi yeye mwenyewe atamtafuta baba yake halali”“Ndio, tatizo lenu wanaume hilo mpaka mnakosa haki yenu sababu ya mambo hayohayo, sijui mpoje. Hivi unajua kama mtoto akishajazwa ujinga na mama yake basi huwezi ukampata kamwe, yani wewe badala upigani haki ya ndugu yako unasema kuwa Angel atamtafuta mwenyewe baba yake. Umemuona huyo Angel au unaongea tu kujifurahisha?”“Kwanza nikuulize, wewe unamfahamu vizuri huyo Rahim? Amekwambia kuwa anashida na huyo mtoto kwasasa?”“Asingekuwa na shida basi asingekuja hapa na kupigwa na Erick”Baba Daima akacheka sana na kumwambia Sia,“Wee unachekesha sana, Erick ndio wa kumpiga Rahim? Hebu uwe unafikiria kwanza kabla ya kuongea huo utumbo”Halafu baba Daima alimfuta karibu mke wake na kuondoka nae.Leo walipofika nyumbani tu, mama Daima alishindwa kuvumilia na kujikuta akimuuliza mumewe kuhusu mama Angel maana aliona wana ukaribu zaidi,“Samahani mume wangu, kwani yule ni nani?”“Yupi huyo?”“Yule mama Angel?”“Oooh leo umeniuliza, ngoja nikwambie kwa kifupi. Yule anaitwa Erica, ni msichana mwenye bahati ya kupendwa sana”“Kivipi?”“Aaaah naona tutaweka mada ndefu bure, ila siku ukikutana na kaka yangu Rahim muulize Erica ndio nani katika maisha yake basi atakwambia mengi sana”“Sikuelewi, kwahiyo wewe uliwahi kunywa juisi ya kutengenezwa na yeye wakati yupo na kaka yako?”“Mengine nikiongea mke wangu utatafuta tu njia za kuumiza moyo wako ambazo hazina umuhimu wowote”“Aaaah niambie tu, kwani si yatakuwa ni mambo yaliyopita zamani, mimi wa nini tena? Nahitaji tu kujua na kumtambua vizuri huyo mwanamke”“Kwanza ulimuona yule mwanamama ambaye aliniita pale nje ya geti? Ngoja nikwambie alichokuwa anasema”Basi akamuelezea kile ambacho alikuwa akiongea na Sia, baada ya hapo akamwambia mke wake,“Tena nitampigia simu Erica kumweleza kuhusu hili, maana sijaelewa kama yule mwanamke ana maana gani kwake”“Kwahiyo Erica kazaa na Rahim? Au huyu Erica ndio yule niliyekuwa nasikia habari zake kipindi kile pale kwa mama yako mkubwa”“Habari gani?”“Si nilisikia huyo Erica katembea na nyie wote, yani hakujua kama nyie ni ndugu au ni yupi?”“Mmmh tuachane na hayo mke wangu, tuongee mambo mengine tu”Basi mama Daima hakuwa na maneno zaidi.Mama Junior nae aliaga na kuondoka zake, walikubaliana tu kuonana hiyo Jumapili,“Kwahiyo shemeji utamfata Junior huko shuleni”“Ndio, hata usijali shemeji yangu”Basi aliwaaga pale na kuondoka zake, muda ule ule baba Angel akakumbuka pia kuhusu bi.Aisha basi akamwambia mke wake,“Kwanini tusimuulize yule bi.Aisha muda huu alipo ili kama yupo nyumbani kwake tumfate na tuweze kuongea nae”“Mmmh tutaondoka muda huu? Ila kama muda umeenda?”“Sio sana mke wangu, kwanza wakina Erica karibia wanarudi kwahiyo watakuwepo tu hapa nyumbani. Ngoja nimpigie sasa hivi nimsikie”Baba Angel alichukua simu yake na kumpigia bi.Aisha ambapo baada ya muda mfupi tu alipokea,“Unaongea na Erick hapa mama, samahani uko wapi leo maana nilihitaji sana kuonana na wewe ili tuweze kuongea”“Oooh kwa leo haiwezekani, labda kesho”“Aaaah sawa mama, basi kesho nitakutafuta”“Jioni ndio itakuwa vizuri maana nitakuwa nimerudi nyumbani”“Sawa, mama yangu kwaheri”Basi baba Angel aliagana na huyu mama na kumpa ujumbe mkewe kuwa wataenda tu kesho,“Basi asubuhi nitaenda kwanza kwenye shughuli zangu halafu jioni nitakuja kukufata ili twende kwa huyo mama”“Sawa, hakuna tatizo”Kisha baba Angel aliamua kupumzika kidogo kwa siku hiyo ili kupumzisha mawazo yake kwanza.Usiku wa siku hiyo, simu ya mama Angel ilianza kuita, alipoiangalia alikuta ni baba Daima ndio anapiga, basi akaamua kupokea na kuanza kuongea nae, alimuelezea kuhusu mtu aliyekutana nae nje ya geti lao, na kumpa tahadhari kuhusu mtu huyo, basi alipomaliza kuongea mama Angel akamwambia mumewe,“Hii sasa imezidi jamani, huyu Sia amezidi mno”“Kafanyaje tena?”Mama Angel alianza kumuelezea kile ambacho alikuwa akiongea na baba Daima, kisha akamwambia mumewe,“Kwakweli hii tabia ya Sia inavuka mipaka sasa, yani tusipokuwa makini atafata hata wasiostahili kufatwa”“Sasa tufanyeje mke wangu”“Naona ni bora tukutane na huyu mtu tuongee nae ilia ache hii tabia, kwakweli ananikera sana mimi”“Sasa mke wangu tukakutane na yule chizi wa kazi gani?”“Hapana, inabidi tuonane nae tu. Kwakweli mimi ananichosha sana, tena inabidi tuwe pamoja”“Basi mke wangu tufanye hivi, kesho asubuhi twende wote tukaongee nae, halafu nikakurudisha nyumbani na kwenda kwenye shughuli zangu halafu jioni nitakufata tena kwaajili ya kukutana na yule bibi”“Sawa sawa, hapo nimeridhika sasa”Kwahiyo wakakubaliana asubuhi kwabisa kwenda nyumbani kwa Sia kwanza.Kulipokucha kama ambavyo walipanga kwenda kwa Sia, walijiandaa kwa kila kitu na kumuacha mtoto kwenye mikono ya Vaileth, halafu wao waliondoka.Basi walikuwa wakiongea mengi tu kwenye gari,“Ila mume wangu jamani, hadi ukapajua kwa Sia!”“Mtu anatusumbua kiasi hiki ndio nisijue nyumbani kwake kweli? NIliona ni lazima nipajue tu”Mama Angel alicheka tu na safari yao ikaendelea.Walifika nyumbani kwa Sia, na kushuka kwa pamoja ili waende kugonga, ila walipokuwa wanakaribia mlango walishangaa kuona Sia akiwa anatoka ndani kwake huku kaongozana na bi.Aisha. Walifika nyumbani kwa Sia, na kushuka kwa pamoja ili waende kugonga, ila walipokuwa wanakaribia mlango walishangaa kuona Sia akiwa anatoka ndani kwake huku kaongozana na bi.Aisha.Basi mama Angel ndio alianza kuongea,“Jamani bibi mwenyewe tunayesema tutamfata badae si ndio yule pale anatoka nje na Sia jamani?”“Ndio mwenyewe, swali ni kuwa anafanya nini nyumbani kwa Sia?”“Ndio hapo sasa?”Ila walipoangalia tena yule bi.Aisha ilikuwa kama kaingia ndani tena maana hakuonekana pale nje, ni Sia ndio alibaki peke yake, basi walimsogelea na bila ya salamu walianza kumuuliza, ni mama Angel ndio aliyeanza kumuuliza,“Yule bibi uliyeongozana nae muda mfupi uliopita yuko wapi?”“Yupi huyo?”“Yule uliyekuwa umeongozana nae”“Khaaaa unaugua macho au, nimeongozana na mtu saa ngapi jamani?”Baba Angel ilibidi aingilie kati na kuluuliza,“Yule bi.Aisha uliyekuwa umeongozana nae”“Jamani, ndio nani huyo?”“Halafu Sia, hebu acha huo uchizi wako, ni nani uliyekuwa umeongozana nae muda mfupi ulipita?”“Unajua mnaweza kusema mimi chizi ila na mimi nawaona nyie ndio machizi maana mnaniuliza kuhusu mtu nisiyemfahamu kabisa yani, sasa mimi nimeongozana na mtu gani kuja nje? Na nimetoka nae wapi?”“Umetoka nae ndani kwako humo?”“Kheeee niondoleeni balaa, humu ndani nilikuwa naishai mimi, mwanangu Elly na watoto watatu wa ndugu zangu ambao wote hao watatu nimewapeleka kwa mama zao, halafu Elly siku hizi huwa karibia na mwisho wa wiki analala kwa mamake mdogo huko, sasa nyie mnanieleza kuwa niliongozana na mtu ni mtu gani huyo?”“Unajua Sia achja kutuchezea akili, tukuone kabisa uongozane na mtu halafu ukatae kweli? Hebu kuwa mstaarabu basi”“Hivi mnachokifanya nyie ni ustaarabu? Mmefika hapa hakuna cha salamu wala nini zaidi ya kuniuliza mtu niliyetoka nae ndani, nitoke na mtu gani mimi? Ndiomana nawashangaa. Ila karibuni na sijui niwasaidie nini”“Haya hakuna tatizo, ngoja tu tuongee na wewe kitu kilichotuleta hapa”“Kitu gani?”“Tena ngoja nikwambie vizuri Sia, hili ni onyo la mwisho, sitorudia tena kukwambia chochote kile, sikia hatujakwambia utusaidie kumtafuta baba mzazi wa Angel, mimi ndio baba yake Angel na imeisha hiyo sitaki lingine lolote la ziada zaidi ya hilo, naomba kuanzia leo sitaki kusikia kwa mtu yoyote sijui umemsimamisha na kuanza kuongea nae kuhusu Angel najua unajua ni kitu naweza kukufanya, tafadhari kaa mbali na mtoto wangu, sitaki kukusikia tena ukisema lolote kwa mtu yoyote kuhusu Angel, nikisikia tu sitakuja kuongea na wewe kwa maneno bali nitaongea nawe kwa vitendo, mjinga sana wewe”Kisha baba Angel alimshika mkono mke wake na kurudi nae kwenye gari kwaajili ya kwenda nyumbani.Na kweli walianza safari ya kurudi nyumbani kisha baba Angel alimuuliza mkewe kuhusu kuonana na bi.Aisha,“Hivi tuendelee na wazo la kuonana na bi.Aisha?”“Mmmh sijui, yani sielewi, kwanza ameenda kufanya nini kwa Sia?”“Hilo sio tatizo sana, ila kwanini ajifiche? Inaonyesha katuona ndio kaenda kujificha, na hapo lazima tuwe na mashaka nae”“Kama kumsikiliza nenda tu halafu utaniambia”“Kwanza alisema jana haiwezekani kumbe ndio yupo kwa huyu chizi, naona ndio kalala huku huku, labda wana undugu sijui ila kwanini atukimbie?”“Na kwanini Sia agome kuwa hamfahamu?”“Yani hapo ndio penye utata, ila hata sijui kama nitaenda kumsikiliza”Basi walirudi nyumbani na mama Angel alishuka halafu baba Angel alienda kwenye shughuli zake.Mama Angel aliingia ndani kama kawaida alimkuta Vaileth kabeba mtoto mgongoni huku akiendelea na shughuli zingine, mama Angel hakuongea chochote na Vaileth kwani moja kwa moja alienda chumbani kwa Vaileth na kumfata Daima ambaye alikuwa yupo kuchezea simu, mama Angel alitikisa kichwa kidogo na kumuuliza,“Daima unaendeleaje?”“Sijambo, shikamoo”“Marahaba, hivi unadhani unachofanya ni sahihi? Mfano unaishi kwako, hutofanya chochote sababu ya mimba? Ni kweli mimba zinakuwaga na mtindo Fulani wa usumbufu ila kwako imezidi jamani, ndio hata kukaa na mtoto kidogo huwezi wakati mwenzio akiendelea na kazi zake?”“Samahani mama, naogopa mimba yangu itatoka”“Nani alikwambia mwanamke akifanya kazi mimba inatoka?”“Wanasema tusiiname, tusifanye kazi yoyote mpaka kujifungua”“Hizo ni mimba zenye matatizo, mfano wale wenye watoto wadogo na anaishi mwenyewe na ana mimba, unadhani wale watoto wake anawalea nani? Haya mimba inahitaji mazoezi, bora hata ungekuwa unatembea tembea ila unalala na simu tu muda wote ndio mimba gani hiyo wewe binti? Ndiomana mama yako hakutaki nyumbani, kumbe hujielewi kabisa wewe”Kisha mama Angel alimuacha na kwenda kumchukua mtoto kwa Vaileth na kwenda nae chumbani kwake.Baba Angel alipomaliza shughuli zake, aliamua kupita shuleni kwakina Erick na kumchukua Erick ili kwenda nae kiwandani, na kweli aliongozana nae hadi kiwandani na kuanza kufanya zile kazi za kiwanda huku wakiongea kuhusu mambo mbalimbali.Baada ya kumaliza mambo yote, wakati wapo ofisini, baba Angel aliuliza pia kuhusu duka,“Nilishampata muuzaji mpya, yupo vizuri sana baba, kwakweli ni mkarimu na ana upendo kwahiyo wateja wengi wanapenda kuhudumiwa nae”“Ooooh upo vizuri sana mwanangu, basi leo tukitoka hapa tutapitia huko”Walikubaliana na muda mfupi tu walivyotoka pale kiwandani walianza safari ya kwenda dukani.Ila walivyofika tu dukani, kuna mtu baba Angel alimuona akitoka dukani, ni mtu aliyemfahamu ila hakujua ni kitu gani ameenda kufanya pale dukani, basi moja kwa moja walipoingia dukani na kutambulishwa kuhusu Rama alianza kumuuliza,“Samahani, yule aliyetoka dukani muda mfupi uliopita unafahamiana nae?”“Hapana, ila aliwahi kuja kununua bidhaa mahali hapa, na alinunua nyingi tu. Basi tokea hapo kawa mteja mzuri kwani mara nyingi anakuja kununua bidhaa mahali hapa”“Sawa, kuna kitu huwa anaongea na wewe?”“Si mara zote, ni leo tu ndio kaniuliza kama naridhika kuwa hapa nilipokuwa, nami nilimjibu kuwa naridhika kwani kwakweli sehemu hii inanisaidia sana kwenye mambo yangu mengi tofauti na nilivyokuwa nimekaa bila ya kuwa na kazi ya aina yoyote ile”“Sawa nimekuelewa”Kisha baba Angel alifatilia mahesabu na kila kitu pale dukani, halafu yeye na Erick waliondoka zao kurudi nyumbani.Njiani, Erick alimuuliza baba yake,“Kwani yule aliyetoka ni nani?”“Aaaah sijui, nilikuwa namuulizia tu”“Kafanana na yule ambaye alikuwa anampa Erica hela?”“Kheeee kashawahi kumpa tena!!”“Ila Erica alikataa”Basi baba Angel alitulia tu na moja kwa moja kurudi nyumbani kwao.Leo Elly alipotoka shuleni, moja kwa moja alirudi akiwa na Sarah hadi nyumbani kwakina Sarah, basi walikuwa wakiongea mambo mengi sana ya kuhusu shule na kila kitu.Walimkuta mama yao nyumbani akiwa tu na shughuli zake,“Bora Elly umekubali kuja leo”“Ni mimi ndio nimemlazimisha mama, eti leo Ijumaa halafu anasema kuwa aje Jumamosi, nimemwambia weee tutaenda tu wote leo, ndio nimerudi nae”“Hivyo ni vizuri hata mimi nimefurahi ila leo sitakuwepo nyumbani maan akuna sherehe ya wenzangu inaanza saa mbili usiku kwahiyo kwenye saa moja moja nitaondoka hapa”“Sawa mama, hakuna tatizo”Basi moja kwa moja Elly nae alisalimiana vizuri na mamake Sarah na kwenda ndani.Muda ulipofika, mama Sarah alikuwa kashajiandaa na kuondoka zake kwenda kwenye hiyo sherehe, kwahiyo ndani alibaki Elly, Sarah na Siku.Muda kidogo Siku nae alimwambia Sarah,“Kuna mgeni wangu hapo barabarani tu, naenda kuongea nae na nitarudi badae”“Mmmh saa ngapi dada?”“Usijali, kwani unaogopa nini na Elly yupo humu ndani”Basi Siku nae akatoka zake kwahiyo ndani alibaki Elly na Sarah tu, walikuwa wakiangalia luninga muda huo, ila Sarah akamwambia Elly,“Eeeeh nimekumbuka, ngoja nije nikuonyeshe zile video, unajua hadi nina mikanda yake kabisa”“Mmmmh mikanda yake?”“Ndio”Sarah alisogea na kuweka mkanda kwenye video na ule mkanda ulianza kuonyesha muda ule ule,“Kheee Sarah! Ni vitu gani hivyo jamani?”“Si unaona mwenyewe wanavyofanya hapo? Ndio mapenzi hayo?”“Mimi naogopa kuangalia Sarah, watu hao wapo watupu kabisa”“Ndio yanavyofanywa, mapenzi hayafanywi na nguo”Elly alikuwa akiangalia kwa uoga, yani alikuwa anaangalia huku anaangalia kama kuna mtu anatokea kuwaona wakiangalia kitu cha namna hiyo, naye Sarah alielewa ile hali ya uoga ya Elly, basi alizima tv na kutoa ule mkanda, halafu akainuka na moja kwa moja kwenda chumbani kwake, na baada ya muda alirudi na kumuita Elly,“Twende chumbani kwangu”“Kufanya nini?”“Kuangalia ule mkanda maana nako nina video, halafu hujawahi kuingia chumbani kwangu eeeh!”Elly alikuwa na uoga ila aliinuka na kwenda moja kwa moja chumbani kwa Sarah ambapo ule mkanda ulikuwa ukiendelea, kisha Sarah akamwambia Elly,“Kwanini na sisi tusivue nguo ili tujaribu wanachokifanya?”Yani kwa muda huu Elly hata hakuweza kujibu kitu chochote ila alijikuta tu akivua nguo na mwisho wa siku alijikuta akiwa amelala na Sarah.Kilichokuja kuwashtua ni hodi iliyopigwa, ni hapo Sarah alipogundua kuwa Siku amerudi, basi Elly alikuwa na wasiwasi sana,“Usijali Elly, ni Siku huyo ngoja nikamfungulie”Sarah alijifunga taulo na kwenda kumfungulia Siku, ambaye aliingia na kufunga mlango wala hakuongea kitu kwani moja kwa moja alienda chumbani kwake, kisha Sarah alirudi alipokuwa Elly, kwakweli Elly alionekana kuona aibu kwani ni kitu ambacho alikiona kwa mara ya kwanza na ni kitu ambacho alikifanya kwa mara ya kwanza, ila muda kidogo alimuona Sarah kainama huku akilia, basi alimfata karibu na kumuuliza,“Unalia nini Sarah, nimekuumiza? Nisamehe tafadhari, nisamehe sana sikujielewa kwakweli naomba unisamehe”“Usijali, nalia sababu nimeharibu usichana wangu, unajua kufanya hivi ni kuharibu usichana, kwahiyo mimi sio msichana mdogo tena”“Nisamehe Sarah! Ila hizi video ni mbaya, naomba tusiangalie tena. Nisamehe Sarah”Elly aliinuka na kwenda chumbani kwake, na hapo hata Sarah alienda kuoga sasa.Kwakweli huu ulikuwa ni usiku wa mawazo sana kwa Elly kwani hakutegemea kutokea kwa kile kilichotokea, alibaki tu anakijutia katika moyo wake, alikumbuka pia mausia ya mama yake kuwa anatakiwa kuwa makini sana, basi alikuwa akijisemea,“Ila mama kanionya sana juu ya mambo haya, sijui kwanini nimefanya hivi jamani! Sarah kaniponza halafu atanichukia na kunifanya nianze kujilaumu mwenyewe”Yani hakuwa na raha hadi panakucha bado hakuwa na raha kabisa.Siku hii aliitwa tu kwenda kunywa chai maana hata hakutoka chumbani sababu roho yake ilikuwa ikimsuta sana, basi akatoka na kwenda kunywa chai ila hakuongea sana kwani alipomaliza tu kunywa chai alitoka nje na kwenda kukaa peke yake, huko Sarah alimfata na kuanza kuongea nae,“Mbona upo hivyo Elly?”“Nisamehe sana Sarah, najihisi vibaya, najihisi ni mkosaji”“Hujanikosea chochote, kumbuka ni mimi ndiye niliweka ule mkanda na sababu kubwa nilitaka kujaribu ile kitu ingawa nilijua kuwa itaharibu usichana wangu”“Ila nimekuumiza nisamehe”“Usijali, ni kweli nimeumia ila nasikia ndio inavyokuwaga kwa siku ya kwanza”“Naogopa mama akijua itakuwa ni tatizo kubwa sana”“Hata usijali, hii ni siri baina ya mimi na wewe, hatojua mama wala Siku, yani ni mimi na wewe tu. Hata usijali, sisi sio wa kwanza kufanya huu mchezo, dunia nzima wanafanya”“Ila dah nimeogopa”“Kwani haikuwa nzuri eeeh!! Hebu niambie na wewe ulivyojisikia, nilikuwa nakuona hadi ulibadilika yani”Elly hapa alicheka tu kwani hata maelezo hakuwa nayo kabisa, na baada ya hapo walianza kuongea kawaida tu kama walivyotambulishwa kuwa ni ndugu kwahiyo walianza kuongea kindugu na kirafiki hata mama Sarah alipowaona alifurahi sana na kusema kwa hakika Sarah kapata ndugu yake.Muda kidogo mama Sarah alijiandaa na kutoka kwahiyo aliwaacha wale watoto wakiwa na mambo yao pale nje, kwake ilikuwa ni furaha sana.Wakati alipokuwa njiani alipitia kwenye biashara ya Sia na kuanza kuongea nae mawili matatu,“Yani Elly ni mtoto mzuri sana, wanapendana na Sarah hadi raha jamani, yani Elly na Sarah wanapendana hadi raha”“Ooooh hiyo ni nzuri sana”“Halafu unajua ni ndugu wale eeeh!!”“Kivipi?”“Sarah ni mtoto wa Erick, halafu Elly pia ni mtoto wa Erick”“Kumbe ulizaa kweli na Erick?”“Ndio, ingawa hawataki kukubali huo ukweli, ila Erick anatambua wazi kuwa mtoto ni wake. Yani Elly na Sarah kama wanajuana vile ni ndugu kabisa maana wanapendana sana”“Oooh hiyo ni habari njema, nimefurahi sana kusikia habari hiyo”“Basi mimi nimepitia tu kukusalimia, kwaheri”Mama Sarah aliondoka zake.Muda kidogo pale alipokuwa Sia, alifika Tumaini na kumwambia,“Nimemuona mama Sarah kaondoka hapa, kumbe mnajuana?”“Ndio, yani mwanamke ana moyo wa upendo sana yule. Bora hata ingekuwa ni yeye ndio kaolewa na Erick”“Kivipi?”“Amezaa na Erick yule, yani kama unamfahamu huyo Sarah basi ni mtoto wa Erick”“Duh! Haiwezekani, sijawahi kumfahamu kabla. Sikia nikwambie kitu Sia, wanawake wa Erick karibia wote nilikuwa nawafahamu, yani kila mwanamke wake alikuwa akinitambulisha, huyo mama Sarah hapana kwakweli”“Na wewe kama umerogwa na huyo Erica, unavyomtetea kaka yako loh! Ila huyu mama Sarah ana roho nzuri sana”“Kakufanyia nini?”“Kamchukua mwanangu Elly anaishi nae na anamsomesha”“Kwahiyo Elly anaishi nyumbani kwa huyu mama na yule binti yake?”“Ndio, mbona kama umeshtuka vile”“Sijashtuka tu ila nasikitika sana, hata kama umechoka kulea mwanao ila sio kwenda kumpeleka akalelewe na yule mama, hajui kulea watoto yule, umemuona huyo mwanae Sarah! Ila sababu Elly ni wa kiume hakuna tatizo, ila mama Sarah hajui kulea watoto yule”“Naona nimekuambukiza tabia ya kufatilia maisha ya watu, pole utachukiw akama mimi bure”Tumaini akaona kuendelea kuongea na huyu mtu ni kujiumiza akili yake tu, basi akaamua kuondoka zake maana muda huo alikuwa akielekea nyumbani kwa baba Angel.Leo Erick na Erica walikuwa wakifanya usafi wa nje ya nyumba yao, kung’olea majani kwenye maua na kumwagilia maua, kwahiyo Tumaini alipofika aliwakuta ndio wanafanya hiyo kazi, aliwasalimia pale na kusema,“Hapa kweli kaka yangu amezaa watoto jamani, ninachowapendea nyie ni kujishughulisha, mpo vizuri sana kwenye kazi, sio kama dada yenu Angel ni mvivu hakuna mfano loh!”Akawaacha hapo nje na kuingia ndani, basi na wao wakaanza kuongea,“Ila kweli Erick, sisi ni wachapakazi ujue, na tutakuwa vizuri sana tukiwa wakubwa”“Sisi ni wakubwa tayari au wewe bado sio mkubwa”Erica alikaa kimya kidogo, na Erick aliendelea kuongea,“Kwani wewe Erica sio mkubwa? Kumbuka uliwahi kuniambia kuwa unaumwa ugonjwa wa kikubwa. Kama uliumwa ugonjwa wa kikubwa inamaana umeshakuwa mkubwa tayari, kwahiyo sisi ni wakubwa yani tunaendelea kukua tu”“Kwahiyo na wewe ushakuwa mkubwa?”“Ndio, si unaona sauti yangu imeanza kubadilika siku hizi”“Imekuwa mbaya, inataka kufanana na sauti ya baba”Walianza kucheka huku wakitaniana,“Mbona na wewe umekuwa na manyonyo kama mama”“Sitaki Erick, nitaenda kukusemea kwa mama sasa hivi”“Basi yaishe, halafu ujue huwa sipendi uchukie Erica! Najua nimekuudhi, nifanye nini ili ufurahi”“kaninunulie karata”“Sawa, nitafanya hivyo”Erick alimpa Erica ahadi ya kumnunulia karata kwani Erica alipenda sana kucheza karata.Tumaini aliingia ndani na kukutana na mama Angel yupo pale na mtoto wake, basi akamkaribisha vizuri kabisa, naye alifika na kukaa kisha akamuita Vaileth na kumuagiza juisi,“Kaniletee juisi Vai, maana najua humu ndani huwa hapakosi juisi”Mama Angel akacheka na Vaileth alienda kumletea na kumkabidhi, kisha mama Angel akamtuma Vaileth,“Halafu kamuite yule Daima, mwambie aje kunywa chai, jamani huyo mtu loh!”Vaileth aliondoka, na Tumaini alianza kuulizia,“Kwani Daima ndio nani?”“Mwenzangu kuna makubwa hapa, yani weee acha tu. Ni hivi kuna binti kapewa mimba na Junior, basi wazazi wa huyo binti walienda kumbwaga nyumbani kwa mamake Junior, ila kaka yako kawaka hatari imebidi mama Junior aje kuomba huyu binti aishi huku”“Kheee, huo ujinga mimi ndio siutaki, yani siwezi kukubali kabisa”Basi Daima alitoka na moja kwa moja alienda mezani kunywa chai, na alipomaliza alienda sebleni kumsalimia mgeni aliyefika, ila Tumaini alipomuona alimshangaa kidogo na kumuuliza,“Kheee kwani ulimaliza shule wewe?”“Amalize wapi? Nasikia kidato cha pili alifeli, na sasa ndio huyo mjamzito”“Nilijua tu, wewe mtoto unanikumbuka mimi?”Daima alitikisa kichwa kuwa hamkumbuki,“Ndio, ujinga wako ndio unafanya usinikumbuke. Mimi huwa sipendi ujinga, na nilijua tu utaishia njiani wewe mtoto”“Unamfahamu vipi huyu mtu wifi yangu?”“Unajua mimi, sijui nikoje yani ila nikiona watoto wanafanya mambo ya ajabu huwa naumia sana hata kama sio watoto wangu na wala sio watoto wa ndugu yangu, ila naumia kwani najua hata mzazi wa huyo mtoto akigundua ujinga anaoufanya mwanae lazima ataumia sana, sasa huyu binti nishawahi kukutana nae kama mara tatu hivi akiwa na rafiki zake wawili. Siku ya kwanza niliwakuta kwenye daladala, wamekaa siti ya nyuma na mimi ndio nikawa mtu wa nne kukaa kwenye ile siti ya nyuma, walitoa simu na kuanza kuonyeshana sijui video gani na muda huo huo walikuwa wakipiga stori za wanaume, sijui wewe mwanaume wako mzuri sijui nini na nini, kama mzazi niliumia sana, niliwaambia nakumbuka vizuri kabisa, nyie watoto elimu ni bora kuliko hayo mnayoyafanya, wanaume hawatawafikisha popote zaidi zaidi mtapata mimba na kuacha shule, niliwasema sana ila walikuwa tu wakinibinulia midomo yao michafu. Siku nyingine nilimuona na hao rafiki zake wawili, ni muda wa darasani ila wenyewe wamekaa chini ya mti eti wamechoka shule, kiukweli siku ile nilitamani kuwapiga kabisa, na niliwasema sana. Siku nyingine, haka katoto kalivaa nguo za nyumbani nikakakuta na mwanaume, nikamwambia si mwanafunzi wewe! Nikamwambia kwa mshangao, wewe ni mtoto mdogo sana. Akaniambii mtoto mdogo ulinizaa wewe? Una cheti changu cha kuzaliwa? Umeniona nimezaa sare za shule hapa? Achana na maisha yangu, nilijihisi vibaya sana siku ile. Ila haya ndio matokeo yake, haya hunikumbuki wewe mtoto?”Daima aliinama chini kwa aibu, kisha Tumaini aliendelea kuongea,“Huo ndio mshahara wa kiburi chako, kione vile sura ilivyokushuka kama umevaa sidiria ya mama nibebe vile”“Mmmh basi yanatosha wifi yangu, haya Daima rudi ulipokuwa huko chumbani”Daima akaondoka kwa aibu sana na kuelekea chumbani kwa Vaileth tu maana alipatwa na aibu muda ule.Kisha Tumaini akamwambia mama Angel,“Halafu msiwe mnakubali kirahisi rahisi hivyo kuwa ni mimba ya Junior, waambieni wazazi wake wakakae nae huko hadi mtoto azaliwe mkampime damu, maswala ya kutuchanganyia mada hatutaki, kwanza Junior amemsingizia tu. Ni kweli Junior ana tabia mbaya ila huyu binti kazidi sana”“Sawa sawa, ni bora na wewe uje kwenye kikao cha kesho”Ikabidi mama Angel amwambie kilichoongelewa mwanzo na hicho kikao cha kesho muda wake,“Ooooh nitakuja ndio, kama wameshindwa kumlea binti yao vizuri wasituletee matatizo bure sisi hatutaki ujinga kabisa maana huu ni ujinga. Mimi nitawaeleza wazazi wake ujinga wa huyu mtoto wake, na vile vyenzake sijui kama navyo shule haijawashinda”Wakaongea mengi sana kuhusu malezi ya watoto yani inaonyesha ile tabia ya Daima ilikuwa imemchukiza sana Tumaini.Leo wakati baba Angel anarudi kutoka kwenye kazi zake, njiani alimuona mama Sarah, ikabidi asimame na kumuita,“Manka”Aliitika na kusogea, na kutaka kumkumbatia baba Angel ila baba Angel alimkinga na mikono kwa maana kuwa hakutaka kukumbatiwa, mama Sarah akamwambia,“Yani Erick ndio hata kunikumbatia hutaki jamani”“Kwani tatizo ni nini? Kwani usiponikumbatia utauguwa?”“Kheee Erick, umepewa nini na huyo mwanamke jamani!”“Usiniulize kuhusu mke wangu, kwanza nashukuru sana nimekuona leo. Hivi kwanini ulimwambia mke wangu huo uzushi wako? Nimezaa na wewe muda gani?”“Erick na wewe hebu ongea kama mwanaume basi, kwani wewe sio mwanaume? Kwani wewe huwezi kumpa mwanamke mimba?”“Nisikie, mimi ni mwanaume niliyekamilika vizuri kabisa ila najua wazi kuwa sijazaa na wewe Manka”“Unakataa vipi wakati tumezaa mtoto Sarah pamoja jamani”“Tena ukome kabisa Manka, najua tulikuwa na mahusiano ndio ila sijazaa na wewe, na kama ungekuwa na mtoto wangu basi asingekuwa umri wa huyo Sarah, lazima angekuwa ni mkubwa sana kushinda hata watoto wangu, ila unaniletea mtoto rika la watoto wangu halafu unasema tumezaa? Hebu akili yako ifanye kazi basi, acha kunizushia ujinga”“Sawa, nilishaambiwa kabla kuwa ni tabia yako kukataa watoto wa nje kwahiyo hata Sarah unamkataa sababu unamuogopa mke wako”“Hayo mambo ya kumuogopa mke wangu hata hayakuhusu, ila sitaki unizushie, mwanamke mbaya sana wewe, ushamdanganya mwanao kuwa ni mtoto wa baba yangu”“Ila mimi sikujua kama mzee Jimmy ni baba yako”“Mjinga wewe, kwaheri”Baba Angel aliingia kwenye gari yake na kuondoka zake kwani hakutaka tena kumsikiliza mwanamke huyu.Jumapili ya leo ni Erica na Erick tu pamoja na baba yao ndio walienda Kanisani.Kisha walipotoka, baba yao aliwaacha karibia na nyumbani halafu yeye akaenda shuleni kwakina Junior ili kumfata Junior.Basi Erick na Erica muda huu walikuwa wakitembea kuelekea nyumbani kwao, ndio njiani walikutana na Abdi akiwa ameongozana na Bahati, pale Erica alishangaa sana na kuwauliza,“Kwani nyie ni ndugu?”Bahati alijibu,“Ndio, mimi ni kaka na huyu ni mdogo wangu”“Aaaaah kumbe!!"”Basi Abdi alianza kimsalimia Erica pale ila Erick alikuwa kimya tu kanakwamba hamfahamu Abdi wala huyu Bahati hajawahi kumuona.Basi Erica aliongea nao kidogo na kuondoka na kaka yake, ila leo Erick hakusema chochote hadi ilibidi Erica amuulize mwenyewe,“Mbona leo hujasema kitu?”“Sasa ulitaka niseme kitu gani?”“Mmmh haya basi, ila yanayoendelea nyumbani unayaelewa kuhusu yule msichana wa kuitwa Daima?”“Sijui”“Mmmh yani Erick mambo yako loh! Yule ana mimba ya Junior, ndiomana baba kamfata Junior leo shuleni. Sipati picha siku ikiwa wewe ndio umempa mwanamke mimba"“Erica unasemaje!!”“Aaaah hamna kitu, twende ndani”Erick hakusema kitu kingine zaidi ya kuingia ndani tu.Walipoingia walikuta kuna ugeni tayari pale kwao kwani mama Daima na Baba Daima walishafika, mama Junior nae alishafika kwahiyo muda huo walikuwa wakimsubiri baba Angel tu na Junior.Baba Angel aliondoka na Junior na kuanza safari ya kuelekea nae nyumbani, ila Junior alimuuliza,“Kwani kuna nini bamdogo?”“Utajua huko huko nyumbani, twende tu”Basi wakawa wanaendelea na safari tu.Ila walivyofika getini kuna mgeni nae aliwasili mahali pale, baba Angel alionekana kuchukia sana kumuona yule mgeni nyumbani kwake, alishuka kwa hasira toka kwenye gari. Ila walivyofika getini kuna mgeni nae aliwasili mahali pale, baba Angel alionekana kuchukia sana kumuona yule mgeni nyumbani kwake, alishuka kwa hasira toka kwenye gari yake.Moja kwa moja alimfata yule mgeni na kumuuliza,“Umefata nini hapa nyumbani kwangu Linah?”Linah nae alionekana kishtuka kwani ni kitu ambacho hakukitegemea pia, basi baba Angel akamwambia,“Naomba uondoke muda huu kwa amani tu, nilishakwambia wewe mwanamke sitaki unifatilie tena”Ambacho baba Angel hakuelewa vizuri ni kuwa yule mwanamama alimfata Junior mahali pale na wala hakumfata yeye, ila Linah hakujibu kitu zaidi zaidi aliondoka mahali pale.Baba Angel alirudi kwenye gari na kupiga honi, kisha kuingiza gari ndani na pale alishuka pamoja na Junior halafu wakaingia ndani.Kwakweli Junior alishtuka sana kumuona Daima mahali pale alitamani hata kukimbia ila hakuweza maana wote walikuwa wakimuangalia yeye, ilibidi awasalimie tu na kukaa pale kwenye kile kikao huku akiwa na hofu, kwanza baba Angel alimtambulisha Junior pale na kuruhusu kikao kiendelee, baba Daima alianza kwa kumuuliza swali Junior,“Wewe Junior kidume, unamtambua hutu Daima?”Junior aliitikia kwa kichwa tu hata mama yake akamfokea muda huo,“Huna mdomo Junior au ni kitu gani? Kwanini uitikie kwa kichwa?”“Samahani, namfahamu ndio”“Eeeeh unamfahamu kama nani?”Hapo Junior alinyamaza kimya kwa muda, hadi mama yake akamfokea tena ndio akasema,“Namfahamu kama rafiki yangu tu”“Unafahamu kama ana mimba?”“Hapana sifahamu”Baba Daima akamuangalia Daima na kumwambia aongee neno,“Junior leo unasema hufahamu kama nina mimba na wakati siku zote tupo pamoja”“Sifahamu kama una mimba Daima”“Hufahamu kivipi wakati mimba ni yako!”Ikawa kama kuna ubishano kidogo, ikabidi baba Angel aingilie kati na kumwambia Junior,“Junior usikatae wakati kitu kipo wazi kabisa, tumekuita hapa ili utuambie kama utamuoa Daima au utafanyeje kulea mtoto wenu”“Mimi siwezi kumuoa Daima”Wote wakamuangalia na jibu lile lilimfanya baba Daima awe na hasira zaidi,“Kwahiyo umeharibu maisha ya mwanangu halafu unakuja na jibu kama hilo! Huyu binti yangu ukitaka utamuoa usipotaka utamuoa maana ushamjaza mimba tayari”“Ngoja niongee ukweli ulivyo jamani, ni kweli jilikuwa na mahusiano na Daima, na alipata mimba kweli akaniomba hela aende kutoa hiyo mimba. Mimi nilimdanganya mama yangu na hiyo hela nikampa yeye akatoe mimba, ila baada ya kumpa hela nikamfumania na jamaa mmoja hivi, nilichukia sana nikamwambia Daima mimi na wewe basi. Toka siku ile sikufatilia habari zake, alinitumia ujumbe sijui katoa mimba na damu inamtoka sana, sikumjibu. Toka hapo nilikuwa simjibu ujumbe wake wowote. Halafu sasa kaibuka na kusema kuwa ana mimba yangu, hilo nakataa kabisa maana hiyo mimba sio yangu.”Baba Angel alipumua kidogo maana hawa ni watoto wadogo ila wanaongea mambo makubwa sana, akamuuliza tena Junior“Unakataa vipi kuwa sio yako? Labda hakutoa?”“Ingekuwa ndio ile mimba ya kipindi kile basi ingekuwa ni kubwa sana, sio kama hivyo. Mimi na Daima tuliachana siku nyingi sana, hiyo mimba naikataa na siwezi kumuoa Daima.”Muda huo huo Tumaini nae aliwasili na kukuta ndio Junior anamalizia kuongea, yani na yeye alidakia palepale bila hata ya salamu,“Jamani msimlazimishe Junior kuoa huyu mwanamke, hii ndio inaitwa asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu. Ndugu zangu kwa habari zenu”“Kheee jamani dada kwanini umeanza na maneno bila ya salamu?”“Salamu nimeitoa kama hivyo, ila huyu binti nyie msimtetee kabisa”Muda uleule alianza kueleza jinsi anavyomfahamu Daima, kwahiyo walibaki tu kushangaa na Daima aliendelea kuona aibu, kwakweli mama Daima alichukia sana na kumuuliza mwanae,“Daima, hebu tueleze ukweli hiyo mimba ni ya nani?”“Siwezi kudanganya, hii mimba ni ya Junior”“Mwanangu sema ukweli”“Huo ndio ukweli mama”Basi baba Angel akaamua kusema,“Sisi wote hatuujui ukweli, basi iwe hivi wazazi wa Daima nendeni tu na binti yenu halafu tutajitahidi kwa kila hali kusaidiana na ninyi, mtoto akizaliwa tutaangalia kama kafanana na Junior au la. Mnasemaje kwa hilo?”Baba Daima alijihisi aibu sana na kweli alikubaliana na hali ya kumchukua Daima mahali hapo ila Daima aligoma huku akilia sana, alidai kuwa wazazi wake wanaweza kumdhuru nyumbani maana kabeba mimba nje ya ndoa na vilevile kabeba mimba akiwa mdogo, alikuwa akilia sana hadi mama Angel aliingiwa na huruma na kusema waache akakae kae hapo kwanza kwani hakuna kitu alichomaliza mahali hapo ila tu walitaka kuwa na ushirikiano na wazazi wake, baba Daima aliafiki hilo swala.Kwahiyo walimaliza kikao na wale wengine kuanza kusambaratika wakati huo Junior akikazana kuwa alale hapo na kuondoka kesho kwenda shuleni, pia hawakuona kama ni wazo baya na wakaruhusu abakie pale nyumbani tu kwa siku hiyo.Baada ya wageni kuondoka, baba Angel alikaa na Junior na kumsema sana,“Ulianza lini hiyo tabia Junior?”“Naomba mnisamehe, ila sijui kwanini nimekuwa hivi, ni kwavile nilihisi kuwa sipendwi na mtu yoyote ndiomana nikaanza kuzunguka na wanawake ili wanipende”“Junior jamani, hadi mama yako uliona hakupendi?”“Mama siku zote anawapenda wale watoto wa baba, kitu kidogo tu alikuwa akitishia kunifukuza nyumbani”“Mmmh Junior, kwa stahili hiyo ungeweza kweli kumdanganya kitu mama yako ili upate pesa ya kwenda kumtoa mimba mwanamke?”“Badae niligundua kuwa mama yangu ananipenda sana na nilianza kujutia mambo yote niliyokuwa nikimtenda, nilijutia sana na kujiona mjinga maana mama ananipenda sana. Kuna mengi najutia katika maisha yangu kama swala la kutembea na wanawake wakubwa sana”“Kheeee ulifikia hatua hiyo?”“Ndio, yule tuliyemkuta getini nilikuwa natembea nae na alikuwa akinilea”Baba Angel alishtuka sana yani kama hakuelewa vile kilichokuwa kikiongelewa, alimuuliza kwa makini,“Inamaana umewahi kuwa na mahusiano na yule Linah?”“Ndio bamdogo, ila najutia kwasasa”“Jamani, yule si amemzidi hata mama yako yule! Tena ana watoto wakubea kushinda wewe, mbona mambo ya aibu haya Junior! Ulianzaje kwanza, yani sielewi ulianzaje?”“Nisamehe bamdogo, kuna binti fulani nilikuwa namfatilia ila hakunitaka, basi siku hiyo yule mama aliniambia kuwa anataka kunifundisha namna ya kutongoza, ndio siku hiyo hiyo ndani kwake nikaanza nae”Baba Angel alipumua na kusema,“Junior, unatakiwa kuwq makini sana, zingatia masomo yako na uache mambo ya kijinga. Fikiria maisha yako ya mbele, sitaki kusikia tena mambo kama haya yanatokea kwakweli sitaki.”Kisha baba Angel akamruhusu Junior kwenda, halafu yeye alienda ndani kwa mke wake ili amuage kidogo aweze kutoka,“Unataka kwenda wapi kwani baba Angel?”“Aaaah nikapunge upepo tu wa nje, nataka ninyooshe nyooshe miguu.”“Mambo ya leo yamekuchosha eeeh mume wangu, ila ndio ukubwa huu. Tunatakiwa kupambana tu, hakuna namna ila sitakuruhusu kwa muda huu kutoka mwenyewe, ukitaka tutoke wote twende tukatembee tembee”Baba Angel hakupinga hilo swala zaidi ya kukubali kutoka wote akiwa na mke wake.Mama Angel na baba Angel wakatoka na kuanza kutembea tembea, walikutana njiani na Sia, alionekana katoka kwenye shughuli zake na alisogea kuwasalimia,“Naona leo mmeamua kuangalia mazingira ila mbona muda umeenda sana?”“Tumeamua tu kwakweli kutembea tembea”“Ni vizuri kuliko kukaa tu ndani, ndiomana mengi yanayotendeka hamyaoni”Pale walipokuwa wamesimama kulikuwa na nyumba ya wageni jirani yake, walimuona mama mtu mzima akiingia na kijana mdogo mule ndani, basi wakati wakishangaa Sia akasema,“Sasa mnashangaa nini, mbona hiyo ni kawaida sana siku hizi. Mnaona kama mama na mtoto ila wale ni mtu na mpenzi wake”“Duh!”“Sasa na wewe Erick unashangaa nini jamani, mbona na wewe ulikuwa unatembea na dada zako na walikuwa wakorofi sana wakijua utawaoa. Umemsahau Linah!”Baba Angel akakumbuka kitu na kusema,“Nimekumbuka, kumbe Linah alikuwa akitembea na Junior!”Sia akadakia,“Na msipokuwa makini na huyo Junior humo ndani kwenu pia mtalia, mimi nikiongea huwa naonekana mzushi. Kwaherini”Baba Angel na mama Angel nao hata hawakutaka kuendelea na matembezi yao kwani muda huo huo walirudi nyumbani kwao tu.Usiku wa leo Vaileth hakuwa na raha kabisa kwa kitendo cha Daima kuachwa pale maana alikuwa akitaka yule Daima aondoke na wazazi wake, basi alikuwa akimuangalia tu yule Daima akijilaza kitandani, mara kuna ujumbe uliingia kwenye simu ya Vaileth, alipoangalia ujumbe ule ulikuwa ukitoka kwa Junior,“Mpenzi wangu Vai, najua unanipenda nami nakupenda sana, naomba uje chumbani kwangu tuongee kidogo japo kwa dakika tano tu, nakuomba sana mpenzi wangu. Sijaweza kuja huko chumbani kwako maana nimeambiwa ndio unalala na huyo kiberenge, nakuomba mpenzi wangu, nakuomba sana uje kunisikiliza”Kiukweli Vaileth hakutaka kuongea tena na Junior ila badae moyo ulimuuma sana kwani alihisi ni jinsi gani alimpenda Junior, ilibidi anyanyuke na aende chumbani kwa Junior.Alifika na kuingia, kisha Junior aliinuka na kufunga mlango, wala hakuongea kitu na Vaileth kama alivyomwambia kuwa anamuita kwaajili ya maongezi zaidi zaidi alimpapasa na mwishowe wakalala pamoja.Walipomaliza, Vaileth alinyanyuka na kuvaa upesi,“Junior siwezi kulala humu chumbani kwako, maana tunaweza kujisahau na kulala hadi asubuhi”“Nimekuelewa Vai wangu ila nimeridhika, najua bado kitambo kidogo tu mimi na wewe tutaishi pamoja kwa furaha”Basi Vaileth kabla hajatoka, Junior alimsogelea na kumbusu, kwakweli ile hali ilimfanya Vaileth aone kuwa anapendwa sana na Junior.Basi Vaileth alitoka na kurudi chumbani kwake, ila muda huu alimkuta Daima amekaa huku akilia tu, basi alimsogelea karibu na kumuuliza,“Unalia nini Daima?”“Najutia maisha yangu mimi, najutia sana. Niliamini zile kauli za nakupenda nakupenda. Niliamini Junior alinipenda kweli yani leo Junior wa kunikana mbele ya wazazi wangu? Imeniuma sana”“Kwani ni kweli ulitoa mimba ya Junior?”“Sijawahi kutoa mimba mimi na wala sijawahi kumuomba Junior hela ya kutolea mimba, na yeye ndio kanifanya mimi nianze umapepe”“Kivipi?”“Junior ndio mwanaume wangu wa kwanza, nilimkubali baada ya kuona wenzangu wote wana wanaume, niliacha kufata mambo ya dini mimi na kuendekeza ujinga. Nadhani hata mama yangu analia sana muda huu kwani hakutegemea kuwa angepata yale maelezo kuhusu mimi, nilikuwa nikiwa naenda shule najitanda juba mimi, ila nilipoanza na Junior alisema sipendezi nikijitanda basi nikaanza kuacha taratibu na mwishowe nikafanana na rafiki zangu wale wawili, tukawa hatuendi shule tunaenda tu huko kujirusha, Junior akinihitaji muda wowote ananipata na alisema kuwa ananipenda sana, katika maisha yake hakuna mwanamke atakayekuja kumuoa zaidi yangu yani aliniambia kuwa mimi ndio mwanamke wa maisha yake ndiomana nikaanza kiburi, ila alipokuwa akinizingua ndipo rafiki zangu walipokuwa wakiniunganisha na wanaume wengine ia bado moyo wangu ulimpenda sana Junior. Niliwahi kumuuliza nikibeba mimba itakuwaje? Akasema ni vizuri maana mama yake hana mtoto mwingine kwahiyo atafurahi kupata mjukuu, sikuwa na mashaka mimi, hata nilipofeli bado Junior alinitia moyo, nashangaa toka nilipomwambia nina mimba yake ndipo alipoanza kupiga chenga, ndiomana mama aliponibana nikaamua kumpeleka kwa mama Junior maana Junior aliwahi kunipeleka hadi pale, na mama yake alinipokea vizuri kabisa. Eti leo Junior amenikana na kunifanya nionekane kuwa mwanamke malaya sana, sawa Mungu atanilipia mimi, kama nimemsingizia Junior hii mimba basi naomba nife na mimba yangu, roho inaniuma sana”Daima alikuwa akilia kwa uchungu sana muda huu hata Vaileth alimuonea huruma ingawa na yeye alitoka kufanya uchafu na Junior ila kwa muda ule alichukua jukumu la kuanza kumbembeleza.Basi alimbembeleza pale na mwishoe alitulia na kulala, na Vaileth nae akalala.Ila palipokucha tu, Daima alikuwa wa kwanza kuamka leo na kumtaka Vaileth amuonyeshe kazi za mule ndani, na alipoonyeshwa moja kwa moja alienda kuosha vyombo wakati Vaileth akisafisha nyumba.Erick akiwa shuleni kwenye muda wa mapumziko alifatwa na Elly na kuanza kuongea nae,“Erick, naomba sehemu yoyote tuliyokosana tusameheane. Tuishi kwa upendo”“Sawa hakuna tatizo, tutaishi vizuri”“Kwanza Erica hajambo? Nimemkumbuka sana yule dada yangu”“Hajambo kabisa”Muda kidogo alifika Sarah pale walipokuwa wanaongea, basi alikaa karibu ya Elly, na kuanza kumsalimia Erick halafu akaongea na Elly,“Erick mambo? Jamani Elly kwanini uliondoka jana, mimi nilitaka leo tuje wote shuleni. Unaonaje ukianza kukaa kwetu moja kwa moja?”“Tatizo mama yangu atabaki mpweke sana”“Halafu Erick mbona nimekusalimia haujaitikia? Au umeona wivu mimi kuongea na Elly?"“Wivu? Sasa wivu wa nini? Tatizo Sarah unaongea sana, unanisalimia wakati huo huo unaongea na Elly sasa ulitaka nikujibu vipi?”“Haya basi, mambo vipi? Mama hajambo?”“Poa, hajambo kabisa”“Nampenda sana yule mama maana anaupendo wa kweli, nampenda sana. Ukirudi mwambie. Saivi nawapenda sana watu wanne”Erick na Elly walimuuliza kwa pamoja,“Wakina nani hao?”“Baba yangu, mama yangu, mama yake Erick, halafu nampenda sana na Elly”Elly alitabasamu ila Erick alikuwa kimya tu na kuinuka zake na kuondoka, basi Sarah akamuangalia Elly na kumwambia,“Usimjali yule, alifikiri nitasema kuwa nampenda na yeye, sasa nimpende kwa lipi jamani! Hata simpendi”Kengele ya kurudi darasani ililia na wote wakarudi zao darasani.Leo mama Angel pale nyumbani alishangaa sana jinsi Daima alivyokuwa akijibidiisha na kazi, yani alitaka afanye kila kazi hadi alikuwa akimzuia kazi zingine, aliamua kumuita na kumuuliza,“Mbona upo hivyo leo?”“Sitaki kuwa mzembe”“Kivipi?”“Naomba uniache nikae kae hapa, nakuomba mama”Halafu alianza tena kulia, kwakweli mama Angel hakumuelewa kabisa ilibidi aache tu kumuuliza kwa muda huo na kumuacha akiendelea na mambo mengine.Muda kidogo baba Angel alirudi kwakweli leo aliwahi kurudi kuliko siku zote na akapitiliza chumbani, ikabidi mama Angel amfate mume wake na kwenda kumuongea nae,“Tatizo ni nini baba Angel mbona unaonekana haupo sawa?”“Kwakweli mwili wangu haupo vizuri kabisa, najihisi kuchoka sana”“Au homa?”“Hapana ni uchovu tu, nahitaji kupumzika”Basi alipumzika, wakati huo mama Angel alienda kumuandalia mumewe kitu ambacho alihisi huenda mumewe akala.Elly alipotoka shule moja kwa moja alipita kwenye biashara ya mama yake na kumsalidia pale kisha kurudi wote nyumbani, njiani alikuwa akimuuliza mama yake,“Mama samahani, eti mapenzi ni nini?”Sia alishtuka kidogo na kumuangalia Elly kisha akamwambia,“Kwanza sikutegemea kama ungeniuliza swali kama hilo Elly, kweli mtoto wa nyoka ni nyoka pia. Jinsi ulivyokuwa unaonekana mtakatifu halafu leo unaniuliza mapenzi ni nini!”“Sijakuuliza kwa ubaya mama, nimekuuliza kwa wema tu”“Sawa, mapenzi ni kupendana. Watu wanapendana na kuwa pamoja katika mahusiano ya kimapenzi”“Na kufanya mapenzi ni nini?”Sia alishtuka tena na kumuuliza Elly,“Hebu niambie Elly ni nini unachotaka kujifunza? Usijiingize katika michezo michafu, sitaki kuwa kati ya wamama wenye malezi mabaya kwa watoto wao.”“Jamani mama, nimekuuliza sababu nataka kujua”“Kufanya mapenzi ni kitendo cha kuingiliana kimwili, mara nyingi ni kati ya mwanaume na mwanamke. Kitendo hiki huitwa tendo la ndoa, ni vyema likafanywa baada ya ndoa kwani kabla ya hapo kuna mambo yanaweza kuwa ni majuto kwako. Mfano msichana anaweza kupata mimba”Elly akashtuka sana na kumuuliza mama yake,“Kwahiyo ni lazima mwanamke apate mimba?”“Inawezekana ndio kama mtu amefanya mapenzi bila ya kutumia kinga halafu kama mwanamke yupo katika siku za hatari za kupata mimba huwa hivyo. Ila kwanini umeniuliza maswali hayo Elly?”“Hapana mama, nimekuuliza tu mama yangu sina maana nyingine yoyote”Basi wakaongozana na mama yake hadi nyumbani, muda kidogo simu ya mama Elly iliita na alipopokea, ilisikika sauti ya kike aliyejitambulisha ni Sarah na kuomba kuongea na Elly basi mama Elly alimpa Elly simu,“Niambie Sarah”“Huwezi amini, eti nimekaa tu nikakukumbuka hadi nimemuomba mama namba ya mama yako”“Aaaah kumbe!”“Ndio hivyo, wewe hujanikumbuka?”“Nimekukumbuka pia, tutaonana shule kesho”“Muombe mamako ruhusa ili kesho turudi wote nyumbani”“Sawa nitafanya hivyo, usiku mwema”Elly aliamua kukata simu na kumuaga Saraha, basi mama Elly alimsogelea mwanae na kumuuliza,“Vipi huyo Sarah ndio mpenzi wako?”“Hapana mama, ni dada yangu yule. Ni mtoto wa mama aliyejitolea kunisomesha”“Oooh kumbe ndio Sarah wa Manka?”“Ndio mama”“Oooh samahani kwa kukwambia hivyo mwanangu, alikuwa anasemaje?”“Unajua pale huwa hakuna mtu wa kuongea nae kwahiyo mimi kuwa pale alifurahi sana, ananiambia nikuombe ruhusa ili kesho nirudi nae kwao”“Sawa hakuna tatizo, mwanangu jitahidi usimuudhi huyo binti maana anapendwa na mama yake hatari, jitahidi uwe unamsikiliza, fanya kile anachokitaka, yani ukiona kitu kinamfurahisha basi mfanyie hata kama anapenda kuimbiwa jifunze kuimba mwanangu, ndio tunawategemea kwasasa, yani fanya kila kitu kumfurahisha. Ishi nae kama ndugu yako kabisa, usimkere wala kumuudhi”“Sawa mama nimekuelewa”Basi Sia aliampa mwanae mausia ya kutosha kuhusu kuishi na Sarah.Usiku huu, kila chakula ambacho mama Angel alimjaribisha mumewe alitapika chakula hicho, basi hakuwa na namna zaidi ya kutaka kumpeleka hospitali tu.Basi alijiandaa kisha yeye na Erick mdogo pamoja na baba Angel waliondoka pale nyumbani, wakati huo ni Erick mdogo ndio alikuwa akiendesha gari kuelekea hospitali.Walifika hospitali na kumshusha mgonjwa, sababu hakuwa na hali nzuri alitakiwa kupata matibabu ya haraka sana kwa wakati huo.Basi waliingia nae moja kwa moja kwenye chumba cha daktari na kumlaza kitandani huku mama Angel kasimama akimuangalia mumewe kwa huruma, muda huo nesi nae alikimbia kwenda kumuita daktari ili aende kumuhudumia yule mgonjwa maana daktari alitoka kidogo.Daktari alivyoingia tu, moja kwa moja macho yake yalimuangukia mgonjwa na kusema,“Khaaaaa kama mgonjwa mwenyewe ndio huyu, simuhudumii mimi”Ile kauli ilimshtua na kumchanganya sana mama Angel, ambaye aligeuka na kumuangalia yule dokta aliyetoa hiyo kauli ila macho yao yaligongana, dokta akasema kwa mshangao,“Kheeee mama Angel!!!” Basi waliingia nae moja kwa moja kwenye chumba cha daktari na kumlaza kitandani huku mama Angel kasimama akimuangalia mumewe kwa huruma, muda huo nesi nae alikimbia kwenda kumuita daktari ili aende kumuhudumia yule mgonjwa maana daktari alitoka kidogo.Daktari alivyoingia tu, moja kwa moja macho yake yalimuangukia mgonjwa na kusema,“Khaaaaa kama mgonjwa mwenyewe ndio huyu, simuhudumii mimi”Ile kauli ilimshtua na kumchanganya sana mama Angel, ambaye aligeuka na kumuangalia yule dokta aliyetoa hiyo kauli ila macho yao yaligongana, dokta akasema kwa mshangao,“Kheeee mama Angel!!!”Mama Angel alimuangalia kwa makini, ni mtu ambaye wanafahamiana nae sana, basi akamuuliza,“Kwanini dokta hutaki kumuhudumia mume wangu?”“Kumbe ndio mume wako huyo?”“Ndio ni mume wangu”“Samahani, ila nadani nikimuhudumia mimi naweza kumfanya kitu kibaya”Basi alimuangalia nesi na kumuomba akamuite dokta mwingine ili akamshughulikie, kwakweli mama Angel hakuelewa mantiki ya huyu dokta kugoma, basi nesi alienda kumuita dokta mwingine.Ni kweli baba Angel alikuwa akiugulia kwa maumivu sana ila huyu dokta wala hakuonyesha kushtuka kabisa, hadi pale alipoenda dokta mwingine kisha mama Angel alitoka nje pamoja na huyu dokta wakati yule mwingine akimuhudumia baba Angel.Ingawa hali ya baba Angel haikuwa nzuri ila bado mama Angel alihitaji kujua ni kwanini huyu dokta hataki kumuhudumia mumewe, basi alimsogelea na kumuuliza,“Dokta Maimuna, kwani unamfahamu mume wangu?”“Kwanza nisamehe kwa mimi kukataa kumuhudumia, ila sikutegemea kumuona yule kiumbe kabisa”“Niambie basi alikufanya nini?”“Sitakuficha sana, ni hivi nimewahi kuwa na mahusiano na mume wako”Mama Angel alishtuka sana, ila dokta aliendelea kuongea,“Kwasasa ningekuwa na mtoto mkubwa sana ambaye pengine angekuwa labda kaolewa tayari sababu alikuwa wa kike, huyu mjinga alikuwa akinitoa sana mimba. Nilipopata mimba ile nilikaa kimya ili nijizalie kimwanangu, hili jina lilikuja na madawa yake kayaweka kwenye juisi akanipa ninywe, mwishowe ile mimba ya miezi saba ilitoka na kitoto kilikuwa kimekufa. Nililia sana, huyu Erick ni muuwaji. Ningekusimulia mengi sana ila niache tu kwasasa.”Dokta Maimuna aliondoka zake na kumuacha mama Angel pale akiwa kaduwaa tu maana hakufikiria jambo lile hata kidogo.Basi yule dokta aliyekuwa akimuhudumia mumewe alitoka na kumpa taarifa mama Angel,“Kuna chakula mumeo alikula hakikuwa salama kwake, kilikuwa kama na sumu kiasi, nimemchoma sindano na kumtundikia dripu, atakuwa sawa tu”Basi mama Angel alienda kumuangalia ambapo muda huu alikuwa kapelekwa wodini, basi mama Angel alimtazama mumewe huku akijiuliza,“Kwanini kila mwanamke ana sifa mbaya juu ya mume wangu jamani!”Kidogo tu baba Angel alianza kutapika, tena alitapika sana, baada ya hapo mama Angel alimuita tena daktari ambapo baada ya kumuangalia alimwambia mama Angel,“Usijali kuhusu kutapika, kwanza ni bora ametapika kwani sumu ndio ilikuwa inatoka hivyo.”Basi dokta akamuelimisha pale, na kutoka kwenda kuendelea kuhudumia wagonjwa wengine.Usiku wa leo, mama Sarah aliwaaga watoto wake kuwa anaenda kwenye mkesha, kwakweli kipindi hiki hata Sarah alimshangaa mama yake maana haikuwa kawaida yake kabisa kwenda kwenye mikeha, basi kila mmoja alienda chumbani kwake kulala ila baada yamuda kidogo, Sarah alienda chumbani kwa Elly, na kuingia ndani, alimkuta Elly ndio anatafuta usingizi kwa muda huo basi alimuomba Elly aende nae chumbani kwake,“Mmmh hapana Sarah”“Jamani Elly utaniudhi ujue”Elly akakumbuka maneno ya mama yake, basi akamuangalia Sarah na kukubali kwenda nae chumbani kwake ambapo walipofika tu Sarah alifunga mlango na kuvua nguo zote halafu akamuwekea Elly zile video walizokuwa wakiangalia siku ile na kumwambia,“Elly angalia tena ili unifanyie kama siku ile”“Ila unajua kama sio vizuri kufanya hivyo?”“Kivipi?”“Vaa nguo Sarah, hiyo ni tabia mbaya tena ni dhambi”Muda huo Elly alikuwa akiangalia pembeni yani alikuwa akiona hata aibu kumuangalia Sarah ila Sarah hakujali, ndio kwanza aliweka zile video vizuri na kumtaka Elly aangalie zile video, na zilivyoanza Elly alijihisi hali yake kubadilika kwakweli kani alishikwa na hisia za hali ya juu kabisa, basi Sarah nae alikuwa akimsogelea huku akiwa mtupu kabisa na kuanza kuondoa nguo za Elly, yani Elly alijikuta akifanya tena na Sarah kile kitendo ambacho aliamini kuwa ni kitendo kibaya.Basi walipomaliza Elly akachukua nguo zake ili kuvaa ila Sarah alimzuia na kumwambia kuwa wakaoge pamoja,“Mmmh Sarah!!”“Ndio twende tukaoge wote, unaogopa nini kwani Elly jamani!!”Sarah alimshika mkono Elly hadi bafuni na wakaoga, kisha kurudi na kuvaa nguo, kwa muda huo Sarah alikataa Elly asiondoke kwanza kwani alitaka kuongea nae kidogo, basi alianza kumuuliza Elly,“Eeeeh una mpango gani na mimi?”Elly akashtuka na kuuliza,“Mpango gani kivipi?”“Kwani hujui kama mimi na wewe kwasasa ni wapenzi? Niambie utanioa au?”“Sarah naogopa mimi, mama yako kanichukua kama mtoto wake”“Unadhani mama yangu atakataa? Nikitakacho mimi haiwezekani mama yangu akakataa kwani ananipenda sana”“Muda umeenda sana Sarah! Tutaongea tena kesho”Elly alimuomba Sarah ili aweze kumruhusu akalale, ila mwishowe Sarah alimruhusu tu kwenda kulala, ila Sarah hakupata usingizi kwani alikuwa anawaza huenda Elly hampendi ndiomana hana jibu la moja kwa moja kwake, yani alijikuta akipitiwa na usingizi wakati pamekucha kabisa, ilikuwa hivyo hata kwa upande wa Elly ambaye alijihisi vibaya sana kwa kile kilichotokea na kumfanya akose usingizi kwa wakati, yani ile kunakaribia kukucha ndio akapitiwa na usingizi pia.Erick alikuwa amepitiwa na usingizi ndani ya gari, alikuja kushtuka pamekucha tayari, kwenye gari ndio kulikuwa na simu ya baba yake, ambayo ilianza kuita, basi Erick akaivuta na kuipokea ili amwambie kuwa baba yake amelazwa, ila kabla hajasema kitu yule mpigaji alianza kuongea,“Erick nimekukumbuka sana, ila wanawake wako wakiamua kukuroga utakuwa chizi wewe, kwataarifa yako mimi nishakuja kwa mganga huku jiandae tu.”Halafu simu ikakatika, kwakweli Erick alibaki akishangaa sana.Aliiangalia sana ile simu na bila ya kupata jibu lolote lile, aliamua kuchukua peni na karatasi na kuandika ile namba pembeni kwani alitamani sana kumfatilia yule mtu ili ajue tatizo ni kitu gani.Alipomaliza tu kuandika ile namba, alifika pale mama yake na kumsalimia kisha akamwambia,“Naona mwanangu leo tumekesha hospitali, pole sana hutoweza kwenda shule"“Cha muhimu ni hali ha afya ya baba, anaendeleaje?”“Mungu kasaidia kwakweli, anaendelea vizuri, asubuhi hii inawezekana tukaruhusiwa kwenda nyumbani”Yani muda huu mama Angel hata hakukumbuka kuhusu mtoto nyumbani maana alijikuta mawazo yote ni juu ya mumewe, na vile alivyoambiwa alipewa sumu ndio hakuwa na imani kabisa ya kumuacha mahali hapo, basi muda kidogo alimuona dokta Maimuna akitoka ambapo huyu dokta alipomuona mama Angel alimfata na kuongea nae,“Pole sana, nasikia mumeo alipewa chakula chenye sumu, pole sana”“Asante”“Kuwa makini sana, najua mumeo humjui vizuri ila kwa zile tabia zake nina uhakika ana maadui wengi sana, kwahiyo kuwa nae makini asile hovyo. Tena bora mmewahi kuja hospitali la sivyo tungekuwa tunaongea mengine sasa”“Dah sijui nani kamfanyia hivi”“Huwezi kumjua kwa kufikiria tu ila inatakiwa kuwa makini sana. Halafu kipindi kile si ulikuwa na mimba wewe!! Mtoto yuko wapi?”“Yupo nyumbani’“Haya, nenda kamchukue mumeo huko ataruhusiwa muda sio mrefu ukaangalie mtoto wako, mimi naenda nyumbani maana zamu yangu imeisha. Kwaheri”Dokta Maimuna aliondoka zake, na mama Angel nae alienda kumfata mume wake.Leo Erica hakwenda shule pia, kwani ndio alibaki kulea mdogo wake toka usiku na hadi asubuhi, yani alikuwa yupo vizuri na kulea hadi Vaileth alimshangaa na kumwambia,“Kwakweli Erica utakuwa mlezi mzuri, hadi nimekupenda bure. Maana toka usiku alipoondoka mama yako upo na mtoto tu, hongera sana”Erica alikuwa akitabasamu yani alifurahia kile alichokuwa anaambiwa na Vaileth, muda huu Daima alikuwa akishughulika tu na kazi za hapa na pale.Basi muda kidogo, mama Angel, Erick na baba Angel walirudi kutoka hospitali kwahiyo pale nyumbani walifurahi sana, mama Angel alienda kwanza kumshughulikia mume wake kisha alirudi kwaajili ya mwanae mdogo,“Masikini mwanangu jamani, ila kusingekuwa na watu nyumbani, hakuna namna ningeondoka nae tu”Vaileth akamwambia,“Ila mama, Erica yupo vizuri sana. Tangu umeondoka yeye ndio yupo na mtoto tu hadi muda huu”“Jamani, wanangu hadi kwenda shule leo imeshindikana jamani!!”Basi mama Angel alimchukua mwanae na kwenda nae chumbani.Kwakweli alikuwa akimuangalia mumewe sana huku akimuhurumia ila alimuacha apumzike kwanza.Leo Sarah na Elly hawakuenda shule maana walichelewa kuamka halafu walikuwa na uchovu, mama Sarah hakuelewa kitu kwani jana yake hakuwepo, alienda kwenye mkesha na kukawia sana kurudi kwahiyo aliporudi hata hakufatilia kama watoto walienda shule au la maana yeye alienda kulala moja kwa moja kutokana na uchovu aliokuwa nao.Kwenye mida ya saa tatu asubuhi ndipo Sarah na Elly walipokaa na kuweza kupata kifungua kinywa, ndio muda huo naye mama yao alitoka chumbani na kuwasalimia pale,“Kheee nyie vipi, mbona hamjaenda shule?”Sarah ndio akamjibu mama yake,“Jana tulijisahau mama, tuliangalia sana sinema tukachelewa kwenda kulala, kitendo hiko kimefanya tuchelewe kuamka leo”“Oooh sawa, ila msirudie tena kuangalia sinema hadi usiku sana, jamani leo nimechoka sana”“Kwani mama ulienda kwenye mkesha wapi?”“Aaaah huko mbali kidogo, ila nimechoka sana, ngoja ninywe chai ili nirudi kulala kwanza maana nimechoka sana”Na kweli alikunywa chai pale na kwenda zake chumbani.Basi walikaa kaa pale ila Sarah nae alijihisi uchovu na kuwa na usingizi kwahiyo aliamua kwenda kulala pia, ni Elly ndio alibaki pale sebleni huku akiwa na mawazo mengi sana, kwani alikuwa akijutia kile alichokifanya usiku.Muda huu wakati anaangalia sinema ila haelewi kitu sababu ya mawazo, alifika Siku na kumuuliza Elly kinachoendelea kwenye ile sinema ila Elly hakuelewa kitu,“Kheee unaonekana una mawazo sana Elly, unawaza nini kiasi hiko?”“Dah! Sijui kwakweli”“Wewe ni mtoto mdogo hata majukumu hujayaanza, halafu wewe ni mzuri mweeeh!”Elly alikaa kimya tu, kisha Siku aliendelea kumwambia,“Au hakuna mtu aliyewahi kukusifia kuhusu uzuri wako? Unajua pale wakati unafika sikuona uzuri wako ila umeishi hapa kidogo tu ndio nimekuona kuwa wewe kijana ni mzuri sana”“Ila wanawake ndio wanaosifiwa kwa uzuri na sio wanaume”“Khaaa jamani, kama mwanaume mzuri lazima apewe sifa zake, kwakweli wewe ni mzuri sana Elly, halafu jina lako ni zuri sana”Kwakweli Elly hakujibu kitu muda huu ila alimuaga Siku kuwa na yeye anaenda kulala kwa muda huo.Muda huu alifika Tumaini pia kuja kumuona kaka yake maana alipigiwa simu kuwa alikuwa anaumwa, basi alifika kumuona na kuongea nae kidogo, muda huu baba Angel alikuwa sebleni tu amejilaza kwenye kochi, basi alifika pale na kumsalimia na kumpa pole,“Pole sana mdogo wangu jamani, pole sana. Kwanini nini cha zaidi jamani?”“Yani hata sielewi”Basi mama Angel alimwambia wifi yake kuhusu daktari alichokisema, basi Tumaini alisikitika sana na kusema,“Kwasasa kuwa makini sana Erick, yani usile chochote kile. Kwanza ni kitu gani umekula hadi imekuwa hivyo?”“Hata sielewi, nakumbuka nilikula matunda yaliyokatwakatwa tu”“Nani alikuletea?”“Yani aliyeniletea huwa ananiletea siku zote hata sijui imekuwaje, ila sidhani kama ni matunda yale ndio yamesababisha hali kama hii, sielewi kwakweli”“Kuwa makini sana kwasasa”“Nitajitahidi kwa hilo dada yangu”Wakaongea mengi sana, na mwishowe Tumaini aliaga na kuondoka zake.Alipokuwa anaondoka kuelekea stendi, njiani akakutana na Sia na kusimama na kuanza kumsalimia,“Naona leo umetoka kumsalimia nduguyo”“Ndio, alikuwa anaumwa”Sia alishtuka kidogo na kuuliza,“Alikuwa anaumwa nini tena?”“Yani alikuwa hoi nakwambia, ndio Erica alimuwahisha hospitali jana, kumbe sijui wapi huko walimlisha sumu”“Jamani, nani huyo mwenye wazo la kumpa sumu Erick jamani, kwanini lakini?”“Sijui kwakweli, nadhani wanataka kummaliza kaka yangu”“Ila nitafatilia mwanzo mwisho hadi nijue ni nani, huwa sishindwi kitu mimi nikiamua, kwakweli nimeumia sana. Ila Tumaini zamani tulikuwa vizuri sana, ukiacha tofauti zetu najua ungeniambia mapema sana kuhusu hali ya Erick, yani hadi nikutane na wewe kweli!!”“Aaaah acha mambo ya zamani, wewe ndio umeharibu ukaribu wangu nawe kwa maneno yako yasiyokuwa na mwanzo wala mwisho”“Nisamehe kwa yote yaliyotokea ndugu yangu, ni mapenzi ndio yalinifanya niwe hivi nilivyokuwa. Tatizo langu nilimpenda sana kaka yako na nilijiaminisha kuwa ndiye atakuja kuwa mume wangu, ila kadri siku zinavyoenda naona haiwezekani. Ila bado siwezi kuwa na ubaya na Erick, kanisaidia vitu vingi sana wala siwezi kufurahia Erick apatwe na mabaya, niamini kuwa nitashughulikia hilo hadi nitajua ukweli wa nani alitaka kumdhuru Erick wangu”Basi Tumaini aliongea nae kidogo tu na kuondoka zake.Usiku wa leo, mama Angel alipokuwa chumbani na mumewe aliamua kumuuliza maswali kadhaa kuhusu uwepo wa dokta Maimuna, basi alimuuliza,“Mume wangu samahani, yule dokta Maimuna unamfahamu?”“Yule Maimuna namfahamu ndio, na sikujua kama ni dokta kwasasa”“Anasema kuwa ulimpa tunda ale na kusababisha mimba yake ya miezi saba kutoka, je ni kweli?”“Unajua mtu ukiwa na tabia Fulani basi kila kitu kikitokea katika maisha lazima utasingiziwa tu. Nilisema toka nakuoa kuwa nitajitahidi kuwa mkweli, na nitajitahidi kukueleza kila kitu kwa upana zaidi, ngoja nikueleze kwa kifupi”“Eeeeh nasikiliza”“Ni hivi, niliwahi kuwa na mahusiano na yule Maimuna kiukweli, tena kwa kipindi hiko nilimuona kuwa ana akili kwani alikuwa akiwaza sana ya mbeleni. Alikuwa anasoma, na yeye ndio alilalamika kupata mimba ya kwanza kabisa, basi mimi sikuwa na budi zaidi ya kumpeleka kwa rafiki yangu yule dokta ambaye anatoa sana mimba. Tena mimba ya Maimuna ndio ilikuwa mimba ya kwanza mimi kupeleka mwanamke kutoa mimba sababu ya yeye kusema haitaki mimba, ingawa kwa kiasi Fulani alinisaidia kwani hata mimi kwa kipindi hiko sikufikiria kufanya majukumu ya kutunza mtoto. Tumewahi kutoa mimba tatu na Maimuna, nikamshauri atumie dawa za uzazi wa mpango ila akakataa katakata, nakumbuka akapata mimba tena na hiyo hakuniambia hadi ilipokuwa kubwa kabisa, katika mambo yote nisingeweza kutoa mimba kubwa vile, akaniagiza matunda na nilikuwa namuhudumia vizuri tu. Nilienda kumchukulia matunda sehemu aliyoniagiza na nilipofika nayo tu alianza kuyala, ila muda ule ule tumbo lilianza kumuuma na kumuwahisha hospitali, alijifungua kabisa mtoto mfu. Basi toka hapo Maimuna akanichukia kupita kiasi, nilijaribu kumuomba msamaha na kumuelewesha ila hakutaka kunisikiliza, maelewano baina yangu na yake yalikatika hapo. Tukaachana kabisa, sasa itakuwaje nahusika kutoa hiyo mimba kubwa”Mama Angel akapumua kidogo na kusema,“Mmmh ila wewe ni noma jamani, wewe Erick hapana kwakweli. Hivi umesababisha mimba za wanawake wangapi zitoke? Au umewatoa mimba wanawake wangapi?”“Mimi mwenyewe huwa najutia kile kitendo tena huwa najutia sana, ila hawa wanawake walikuwa wakinitaka wenyewe, na mimi nilikuwa sipo vizuri kichwani yani nilikuwa na mawazo hadi basi, nikawa nawakubali tu. Lakini hakuna mwanamke hata mmoja ambaye sikuwahi kumwambia kuwa nampenda sana Erica, yani walikuwa na mimi ila waliamini siku akirudi Erica katika maisha yangu basi nitawageuka kabisa na kuwakataa, na huo ndio ulikuwa ukweli halisi maana moyo wangu upo kwa Erica tu. Nakupenda mke wangu, madhaifu yangu yaliyopita usifanye yanikandamize kwasasa, mimi nakupenda sana Erica wangu”“Mmmh, nimekusikia”Mama Angel hakuendelea tena kuhoji, ila alihisi tu kuna siku ataletewa watoto wa nje ingawa baba Angel alikuwa hakubali kuwa ana mtoto wa nje, sema mama Angel alihisi tu kuna siku ataletewa mtoto lazima.Kwa muda huo waliamua kulala tu, kwani ilikuwa ni usiku sana.Leo Elly na Sarah walienda shule kama kawaida ila Elly alikuwa na mawazo sana yani hakuwa na raha kama siku zote ambavyo huwa anakuwaga, ile hali hata Erick aliigundua na kwenda kumuuliza tatizo ni nini,“Kwani unaumwa Elly?”“Hapana, ila sijihisi vizuri natamani nirudi nyumbani”“Nenda kaombe ruhusa sasa, ili upate amnai ya moyo”“Wataniruhusu eeeh!”“Ndio”Basi Elly aliondoka na kwenda kuomba ruhusa, ni kweli walimruhusu muda huo huo kwenda nyumbani kwao.Elly alipoondoka, moja kwa moja alienda kwenye biashara ya mama yake na kumkuta pale kisha alimsalimia na kuanza kuongea nae,“Mbona mapema sana leo mwanangu Elly?”“Yani sijihisi vizuri sijui kwanini, moyo unaniuma sana ndiomana nimeamua kurudi”“Kheeee unahisi homa?”“Hapana mama, ila natamani kukutana na watu mbalimbali sijui kwanini ila moyo wangu unaniuma sana”“Haya, nisaidie kwa wateja maana naona umeamua”Basi Elly alikuwa akimsaidia mama yake kuhudumia wateja wao pale kwenye mgahawa.Leo Erica akiwa shuleni, kama kawaida alianza kuongea na rafiki yake Samia akiambiwa kuhusu kilichotokea nyumbani kwakina Samia,“Yani siku hizi nyumbani kwetu jamani, sijui baba kawaje”“Kwani vipi?”“Ni hivi, mara mama alipoondoka juzi kwenda kazini ule usiku, kuna simu nilimsikia baba akiwasiliana nayo, halafu akatoka pia na kurudi jana asubuhi. Basi unaambiwa acha asemwe na mama jamani maana alirudi muda ambao mama amesharudi, yani mama alichukia sana, tabia ya baba imeanza kumkera sana mama”“Duh! Poleni sana, huyo baba yenu kaanza tabia mbaya kwakweli”“Asante, yani hafai hata kidogo, namuonea huruma sana mama yangu jamani”Wakaongea pale mambo mengi sana, hadi muda wa kurudi darasani.Ulivyofika muda wa kutoka darasani kama kawaida wanafunzi wote walielekea kwenye gari za kurudi nyumbani kwao.Gari walilopanda wakina Erica, kuna mahali lilipata pancha, kwahiyo dreva alishuka kubadili tairi ila Erica aliamua kuondoka tu kwani ilikuwa ni mitaa ya nyumbani kwao.Ndipo alipopita karibu na mgahawa wa Sia, ila leo Elly alipomuona Erica alimkimbilia na kumkumbatia sana hata Erica alimshangaa sana Elly kufanya vile, alijitoa kwake na kumuuliza,“Tatizo ni nini Elly?”“Nimefurahi sana kukuona Erica, moyo ulikuwa unaniuma ila nilipokuona nimefurahi sana hata maumivu ya moyo wangu yamepungua”Basi Erica akamsalimia kidogo mama Elly na kutaka kuondoka, ambapo Elly aliamua kumsindikiza huku akimuuliza baadhi ya mambo,“Erica samahani, hivi unajua kupika?”“Najua ndio, umesahau huwa nakuja kumuuliza mama yako kuhusu mapishi ili nami nikapike?”“Nakumbuka ndio, kufua je na kuosha vyombo?”“Najua ndio, kwanini unaniuliza hivyo?”“Nimekuuliza tu, una simu wewe?”“Uwiiii mama yangu hataki kabisa nimiliki simu, yani huwa akinikuta na simu ni balaa. Kasema hadi nikue, mimi najiona nimekua ila kwa mama bado ananiona kuwa ni mdogo sana”“Je unaangaliaga sinema gani ukiwa nyumbani?”“Mmmh leo Elly unaniuliza maswali gani? Mimi nikiwa nyumbani mara nyingi mama anapenda kuangalia sinema za Kiswahili sijui kwanini huwa anapenda hivyo basi na mimi naangalia, halafu kaka anapenda za ngumi, basi nazo huwa naangalia, akija dada Angel anapenda zile tamthilia za wazungu basi huwa nazo naangalia, kwahiyo mimi sina ninachopenda zaidi ya kufanya wanachopenda wao. Kitu pekee ninachofurahia kufanya muda wote ni kupika tu”“Sawa, ila mama yenu kawalea vizuri sana, hongera zake kwakweli”“Hata wewe mama yako kakulea vizuri”Elly akatabasamu tu na Erica alikuwa amefika kwao, basi aliagana na Elly na moja kwa moja yeye akaingia nyumbani kwao.Muda Erick nae kafika kwao ndio akamuona Elly na Erica wakiagana, basi alipofika alimuita Elly muda huo Erica alishaingia ndani, Elly alisogea kisha Erick alimuuliza,“Wewe si ulisema unajihisi vibaya wewe!”“Ni kweli, ila kwasasa nipo vizuri”“Baada ya kumuona Erica sio!!”“Mmmh inawezekana, unajua Erica ana maneno yenye busara sana”“Kushinda Sarah”“Sijawashindanisha ila ni kwavile Erica nimemzoea zaidi kushinda Sarah”Kisha Elly aliamua kumuaga Erick kwani alihisi kuwa huenda wakagombana bure muda huo.Erick aliingia ndani na kusalimia wazazi wao kisha moja kwa moja alienda chumbani kwa Erica ambaye alikuwa akibadili sare za shule kwa muda huo, kwahiyo alipomuona Erick alishtuka kidogo nankumwambia,“Uwe unagonga mlango mara nyingine Erick, utakuja kuona visivyoonekana bure”“Kama vinini?”Erica akacheka tu na kumuuliza Erica,“Haya leo ni kitu gani kimefanya uje moja kwa moja chumbani kwangu”“Nataka kujua ulikuwa unaongea nini na Elly”“Khaaa kumbe ulituona, alikuwa ananiuliza tu kama najua kupika, kufua na kuosha vyombo”“Ili iweje? Yani alijua iwe nini sasa?”“Sijui ila kamsifia sana mama yetu kuwa ana malezi mazuri”Basi Erick akaondoka kuelekea chumbani kwake, yani Erica alimuangalia tu bila ya kusema kitu zaidi ya moja kwa moja kwenda kuoga.Elly alikuwa anarudi kwenye mgahawa wa mama yake huku akiwa na furaha kwa kuongea na Erica kwa siku hiyo.Basi alifika tu pale kwenye mgahawa, muda kidogo wakafunga mgahawa na mama yake na kuondoka kurudi nyumbani, basi walipofika wakaanza kuongea ongea,“Kwanza mwanangu niambie nini tatizo leo?”“Hakuna tatizo ila nilikukumbuka tu”“Mmmh jamani mwanangu”“Kweli mama, unadhani siwezi kukukumbuka?”“Unaweza mwanangu ila kama kuna tatizo naomba uniambie, usinifiche mimi ni mama yako”Muda kidogo walifikiwa na wageni mahali pale, wageni wale ilikuwa ni mama Sarah na mwanae Sarah, basi na siku ile ndio Sia alitambulishwa vizuri kwa Sarah kisha wakasema kilichowapeleka pale ni sababu Elly aliondoka shule kwa kuaga kuwa anaumwa, kwahiyo mama Sarah aliposikia akaamua kwenda na mwanae kumuona Elly. Basi alimuuliza pale kuwa hali yake ikoje kwa muda huo,“Naendelea vizuri kabisa”Basi Sia akadakia na kuwaambia,“Huyu nae mtoto wa mama hana looote, alinikumbuka tu”Basi wakaongea ongea kidogo pale na kuaga ila muda huu hawakumlazimisha Elly kuondoka nae.Usiku wa leo wakati madam Oliva katulia ndani na Steve, alipigiwa simu na ndugu yake,“Jamani, Paul kakukumbuka ujue, yani anaumwa”“Khaaaa jamani, Paul mkubwa hivyo aumwe sababu ya kunikumbuka mimi kweli!”“Ndio, hivyo kasema kesho anakuja”“Haya, mwache aje tu sina pingamizi mie”Basi simu ilipokatika alianza kumwambia Steve,“Nasikia mwanangu kanikumbuka sana, nimewaambia wamuache tu aje.”“Bora ili na mimi nikamfahamu”Madam Oliva akatabasamu kidogo na kusema,“Usijali utamuona Paul wangu, mtoto mpole sana. Huwa nampenda sana mwenyewe”Basi Steve alikuwa na hamu sana ya kumuona Paul maana siku zote anaambiwa sifa za Paul tu.Kulipokucha kwenye mida ya saa mbili, mtoto wa madam Oliva alifika kwa mama yake akiwa kaongozana na mamake mdogo.Cha kushangaza wakati madam Oliva kawafungulia mlango na kuwakaribisha pale, alishangaa kuona Steve na Paul wakikimbiliana na kukumbatiana kama watu wanaofahamiana. Kulipokucha kwenye mida ya saa mbili, mtoto wa madam Oliva alifika kwa mama yake akiwa kaongozana na mamake mdogo.Cha kushangaza wakati madam Oliva kawafungulia mlango na kuwakaribisha pale, alishangaa kuona Steve na Paul wakikimbiliana na kukumbatiana kama watu wanaofahamiana.Kwakweli madam Oliva alishangaa sana basi aliwaangalia kwa muda kisha, aliwasogelea halafu Paul alienda kumkumbatia na yeye na kumsalimia kisha alimuuliza,“Yani Paul ulimpita mama hapa ukaenda kumkimbilia mwingine! Kwanini?”“Sababu ni baba yangu”“Baba yako? Nani kakutambulisha?”Wakakaa kwenye kochi sasa ili kusikiliza maelezo, yani madam Oliva alitaka kuelewa imekuwaje, ingawa ni kweli Steve ni baba mlezi sababu yeye yupo naye ila kajuana vipi na Paul? Madam Oliva alihitaji kujua,“Kwani mmefahamiana vipi?”Basi Steve alianza kuelezea,“Unajua sikutegemea kama kuna siku nitakutana tena na huyu kijana, kuna mahali alikuwa akiishi nami nilikuwa nikiishi huko, basi mara kwa mara huyu kijana nilikuwa namuona akipita, nilijikuta nikimpenda sana kwani kila nikimuangalia naona karibia kila kitu naendana nae, nilimpenda sana, ni mpole na nilikuwa naongea nae mara nyingi. Aliniambia yeye ana mama lakini hana baba, nikamwambia basi mimi ndio nitakuwa baba yako. Kwahiyo siku zote alikuwa akiniita baba na tulikuwa tukipendana sana mpaka sikumuona tena, niliumia sana lakini sikuwa na namna yoyote ile. Siku zote ulipomuongelea Paul sikujua kama unamuongelea Paul huyu, jamani yani huyu ni mwanangu kabisa haijalishi chochote ila ni mwanangu”Madam Oliva alitabasamu kwani alijihisi vyema kuona mumewe mtarajiwa kawa na mapenzi ya hali ya juu na mtoto wake Paul, basi akamuuliza na Paul“Umejihisije mwanangu baada ya kumuona huyu?”“Yani nimejihisi furaha sana mama, nimefurahi sana. Mimi hapa siondoki, nitakuwa nasoma huku huku nikae na baba yangu"Yani kile kitendo wote kiliwashangaza sana jinsi upendo kati ya Paul na Steve ulivyokuwa hadi mama mdogo wa Paul yani mdogo wake na madam Oliva alikuwa akishangaa, kisha madam Oliva alitumia muda huu kumtambulisha Steve kwa mdogo wake,“Huyu ni mdogo wetu wa mwisho, anaitwa Mary. Na huyu ni shemeji yako anaitwa Steve”Basi Mary na Steve wakasalimiana pale na kuanza kuongea mambo mengine yaliyopo.Leo ilikuwa ni siku ya sikukuu ya kiserikali kwahiyo hawakwenda shule, Erick na Erica walibaki nyumbani tu na kufanya zile shughuli mbalimbali ila baba Angel alimtaka Erick aende kiwandani ila leo alimtaka aende na Erica maana aliona bora wawe wawili huku akiwasisitiza wasile chakula hovyo, kwahiyo walijiandaa na kuondoka zao.Mama Angel aliongea na mumewe,“Mmmh saivi unahofia chakula cha hovyo eeeh!”“Yani hata sielewi, unajua mimi kumuwekea mashaka mtu ni mara chache sana. Nakumbuka hata madam Oliva alikuwa akiniletea chakula kipindi kile nakula, angeamua kunidhuru basi naye lazima angenidhuru tu maana nilikuwa nakula bila ya wasiwasi wowote ule.”“Kweli angeamua angekupata kiurahisi, ila baba Angel huyu mtoto kakua sasa na mimi nahitaji kurudi kwenye shughuli zangu nifanye kama zamani, unajua kuna mambo mengine hayaendi eeeh sababu mwenyewe sipo”“Naelewa mke wangu, basi uwe unafanyaje! Yani uwe unaenda halafu saa ngapingapi unarudi sio unazamia hukohuko hadi jioni au usiku, yani hapo ndio kwenye tatizo na kufanya nione huyu mtoto hapati malezi mazuri. Kipindi cha hawa mapacha wetu, kwakweli mke wangu ulilea hawa watoto tena uliwalea sana, ila kwanini kuwe na tatizo katika kumlea huyu mmoja? Jitahidi mke wangu, kama pesa mbona na mimi natafuta sana! Haya hadi watoto nao wapo vizuri, inatakiwa mambo mengine tupunguze”“Sawa nimekuelewa, ngoja nikakuandalie chakula”Basi mama Angel alienda jikoni, na kumkuta Daima akiwa anajaribu kupika pale,“Kheee Daima jamani mbona kujichosha hivi?”“Mimba sio ugonjwa”“Kheeee sio hivyo, nadhani umeninukuu vibaya siku ile nilipokwambia mimba sio ugonjwa, ni kweli mimba sio ugonjwa ila mimba inahitaji uangalifu wa hali ya juu maana ukikosea kidogo unaweza kupoteza mtoto au wote kwa pamoja, ndiomana mama mjamzoito anaopaswa kutazamwa kwa jicho la tatu. Yani kuna kazi za kufanya ukiwa mjamzito ila zingine unaachana nazo. Kama kazi za kuinama sio nzuri kwa afya yako na mimba yako”“Sawa lakini mimi nahitaji kufanya kazi, sitaki kujibweteka tu”“Usifanye kazi ngumu, ukiwa mjamzito kuna mambo inatakiwa uyaepuke hata kama unayapenda sana. Ni kweli kusema huwezi fanya chochote sababu ya mimba inakuwa ni tatizo lingine ila vilevile ukiwa mjamzito huwezi kufanya kila kitu kama ambavyo mtu ambaye si mjamzito hufanya. Unatakiwa kujilinda wewe na kumlinda mtoto ajaye. Haya acha hapo niendelee mwenyewe”Daima aliacha pale ila alienda sehemu nyingine kutafuta kazi nyingine ya kufanya ni kwavile tu hakutaka tena kukaaa kaa na kulala lala bila kazi yoyote wakati hata hapo anaishi kwa bahatinasibu maana anawaza akirudishwa kwao itakuwaje tena na ile mimba yake.Erick na Erica wakiwa kiwandani, kama kawaida Erick aliendelea na kazi za kiwanda ila Erica alikuwa akizunguka zunguka tu.Siku hiyo alifika yule mteja wao mkubwa, yule mwarabu na kukutana nje na Erica, basi alianza kuongea nae,“Natamani sana kumfahamu mama yako?”“Kwanini?”“Una heshima sana halafu inaonekana umefanana nae”“Asante sana, ni kweli nimefanana na mama. Kwetu tupo wa nne ila mimi nimefanana sana na mama. Yupo dada yangu anaitwa Angel, nina kaka yangu Erick, na mimi ni Erica halafu kuna mdogo wetu wa mwisho ambaye bado ananyonya anaitwa Ester”“Ooooh natamani sana kuwaona kwakweli, ila nyie wengine mbona majina yenu yameanzia na E halafu huyo dada yenu peke yake jina limeanzia na A, kwanini?”“Sijui, naona pengine wazazi walitaka majina yetu yaanzie na A ila walivyotuzaa sisi walitupa majina yao maana baba na mama wanaitwa Erick na Erica, halafu sisi walituzaa mapacha, naona ndio herufi E ilipoanza”“Aaaah nimekupenda bure wewe mtoto, nitakuwa babu yako yani ukiniona uwe unaniita babu. Halafu uwe jnanitambulisha kwa ndugu zako kama huyo dada yako Angel nae nimejikuta nikitamani sana kumfahamu, naamini utanitambulisha”“Ndio, sema dada Angel yupo shule anasoma ya kulala huko huko”“Akirudi utamwambia babu anataka kukusalimia, halafu mtanipigia simi hapa nitakuja hapa hapa kiwandani. Ukienda tu kwa meneja mwambie mpigie babu mwarabu atanipigie”“Sawa hakuna tatizo”“Ngoja niingie kwanza, yani nimekupenda bure”Basi yule mwarabu alienda moja kwa moja ofisini kwaajili ya kuagiza bidhaa zake.Elly nae alikuwa muda mwingi na mama yake, na alipata muda pia wa kuzungumza nae na kwa siku hii alizungumza nae vitu vingi sana,“Kwani mama mwanamke anajigundua vipi kuwa mjamzito?”“Mmmh Elly, mbona unanitisha na maswali yako?”“Nahitaji tu kujua mama, nipo kujifunza.”“Sawa, kwanza kabisa mwanamke anakuwa hapati siku zake yani zinakata hadi atakapojifungua, hiyo ni nia ya kwanza kabisa mwanamke kujihisi kuwa ni mjamzito. Ila kwa njia ya haraka ni kupima mkojo”“Kivipi?”“Mwanamke anaweza kwenda hospitali kupima, ila vile vile kuna vipimo vya kupima mimba nyumbani, yani mtu anaweza akanunua kipimo hiko kwenye duka la madawa na kwenda kupima nyumbani”“Aaaah, kwahiyo akifika anasema nataka kipimo cha kupimia mimba?”“Kheee wewe Elly, mbona unataka kujua vingi sana. Niweke wazi mwanangu kuna nini kinaendelea ili nijiandae, kama umeshamjaza mtu huko mimba nijue mapema. Ila nishakukataza habari za uzinzi mwanangu, au umeanza uzinzi?”“Hapana mama, sina mambo hayo kabisa”“Unauliza sana kuhusu mimba, napata wasiwasi”“Jamani mama, nimeuliza tu nataka kujua, maana hapo badae natarajia kuwa daktari wa wanawake”“Oooh vizuri mwanangu utatusaidia mengi maana wanawake tuna magonjwa mengi sana”“Naelewa mama, na je mimba inazuiliwaje?”“Mmmmh!! Kwa kutumia kinga na kwa mwanamke kutumia uzazi wa mpango. Ila Elly niambie ukweli tu kama umeanza uzinzi”“Hapana mama, nilisema hadi nikiwa mkubwa”“Mmmh unanipa mashaka na haya maswali yako”“Sikuulizi tena mama”Basi Elly aliinuka na kwenda ndani ila alikuwa akiwaza kitu kuwa lazima akamshawishi Sarah ili wanunue kipimo cha mimba na wajaribu kupima, ila alikuwa akiogopa sana moyoni mwake.Wakati wa kurudi nyumbani, Erick na Erica waliamua kupitia kwanza dukani ili kuangalia mambo yanavyoendelea kwenye duka lao.Basi walimkuta Rama akiendelea na kazi zake kama kawaida, Erick alifatilia baadhi ya mambo na kuona kuwa yapo sawa, ila kabla hawajaondoka kuna mtu alifika pale na kuanza kuongea na Rama, mtu huyo walipomuangalia vizuri alikuwa ni Rahim ila hawakuonyesha kama wamemuona kwani waliendelea na mambo mengine tu, alipoondoka ndipo Erica alipomfata Rama na kumuuliza,“Unamfahamu yule uliyekuwa unaongea nae?”“Aaaah yule ni mteja, tena ni mteja mzuri sana halafu inaonyesha ana mtoto mdogo sana kwasasa maana siku ya kwanza kuja alichukua nguo za mtoto mkubwa ila siku hizi huwa anachukua nguo za watoto wadogo inaonyesha ana watoto wadogo sana kwasasa”“Aaaah kumbe, namjua yule ila sikujua kama ana watoto wadogo”Basi Erick na Erica wakamuga Rama na kuondoka zao, ila kabla hawajafika mbali walimuona Juma akielekea hapo dukani, ikabidi Erick asimamishe gari na ashuke kwenda kumsalimia maana ni kitambo sana hajaongea nae, ingawa wazazi wake walikuwa wakimkataza kuongea na Juma ila Erick hakuona tatizo lolote kufanya hivyo. Alimsogelea na kumsalimia,“Ooh Erick, nimefurahi sana kukuona. Naamini ni pacha wako Erica ndio kakushawishi kuja kunisalimia”“Hapana ni mimi mwenyewe, kwanini unasema hivyo?”“Naelewa moyo wa Erica ulivyo, ana upendo sana huyo binti ndiomana nasema kuwa ni yeye aliyekushawishi kuja kunisalimia”Erick alicheka tu ila leo hakuongea nae sana, muda kidogo alimuaga na kurudi kwenye gari lao na kuendelea na safari huku akimwambia Erica,“Ni kwanini watu wengi hukuona wewe kuwa na roho nzuri sana?”“Ndio ukweli huo mimi nina roho nzuri”“Na mbona ulitumwagia maji kitandani mimi na Sarah wakati ulijua wazi kuwa Sarah anaumwa?”“Sikumuamini Sarah ndiomana, namuona macho juu juu sana”“Kivipi?”Erica aliamua kubadilisha mada hadi pale walipofika nyumbani kwao.Usiku wa leo, Daima alikuwa amekaa huku akilia tu Yani ilionekana kwa kiasi kikubwa sana anajutia mambo ambayo aliyafanya, basi Vaileth akawa anambembeleza, akakumbuka kipindi yeye alipobeba mimba na shule kumshinda, alikumbuka hilo na kujihisi vibaya sana,“Pole sana Daima kiukweli nakuhurumia maana nimewahi kupitia hiyo kama yako”“Mimi imezidi kwakweli, hakuna hata wa kunibembeleza, Junior hanipigii simu, mama na baba nao wala hawana habari na mimi, nimekuwa kama kifaranga aliyeachwa kwenye mvua, nateseka mimi”“Pole sana, ila wewe na Junior si ilikuwa mnapendana sana!”“Tena sana hata sijaamini kuwa kuna siku itakuwa hivi, yani Junior atanikana kabisa hata kuongea maneno ya uongo juu yangu. Sikufikiria kabisa kama kuna siku kama hii katika maisha yangu”“Unachotakiwa kufanya ni kuamini kuwa hayo mambo yamepita na uangalie mambo mengine ya kufanya, kama kumlea mwanao”“Kumlea bila ya baba, wakati baba yake yupo”“Kwani wasiwasi wako nini? Mtoto akizaliwa walazimishe wakampime damu”“Mmmh hawajataka kupima kipindi hiki ndio watakubali mtoto akizaliwa?”“Watakubali tu hata usijali”Basi siku walijikuta wakiongea sana hadi wakachelewa muda wa kulala.Kulipokucha tu, Daima alikuwa wa kwanza kuinuia bila kujali kama usiku hakulala wala nini kwani moja kwa moja alienda kufanya usafi na kutaka kudeki ila mama Angel alimkuta na kumkataza kufanya hivyo, kisha akaongea nae,“Unajua Daima kwakweli mimi nashangaa sana kuwa imekuwaje hadi umekuwa hivyo, sikuelewi ujue”“Hunielewi nini mama?”“Kwanini unajipa kazi zenye uwezo wa kutoa mimba yako, narudia leo sitaki kuona ukifanya kazi ngumu”Basi mama Angel alienda kumtayarishia mumewe chakula ambaye alikula na kumuaga mke wake maana alitaka kidogo kwenda ofisini kwake.Baba Angel alipofika ofisini tu, muda mfupi alifikiwa na mgeni na kumkaribisha maana mgeni huyo alikuwa ni Sia, basi alimuuliza kitu kilichompeleka pale ofisini kwake,“Umefata nini Sia?”“Nataka kufanya utafiti juu ya aliyekupa sumu”Baba Angel alicheka sana na kumuangalia kwa makini,“Hayo maswala ya utafiti umeyaanza lini? Na nani aliyekwambia kuwa nilipewa sumu?”“Nilikutana na Tumaini akaniambia hivyo, nilikuwa natamani kuja kukuona nyumbani kweko ila kuna muda huwa namuhofia sana mkeo maana na yeye huwa anabadilika kama kinyonga yani mambo yake huwa hayaeleweki kabisa”“Haya mambo ya uchunguzi umesomea wapi?”“Hivi nikiamua kuchunguza langu naanzahe kushindwa kwa mfano? Sikujua kipaji changu toka utotoni, yani sikujua kama nina kipaji cha upelelezi ila ni kipaji changu hiki. Nimekigundua ukubwani, ni kweli sijasomea ila naweza kufanya kwa njia za kawaida na nikagundua chanzo cha tatizo kama wachunguzi wengine”“Ni kipi ulichowahi kukigundua wewe?”“Hivi mimi ningemjua vipi Rahim aliyezaa na Erica yule mtoto wenu Angel? Ningemjua vipi Bahati aliyempenda sana Erica na sasa anaishi na rafiki kipenzi wa Erica? Ningejua vipi maovu ya Dora na ulokole wake fake?”“Kheee umenishinda tabia, haya chunguza basi nani kanipa sumu”“Niambie kwanza sehemu unazokumbuka kula chakula kabla ya kuanza kuumwa? Au kwa urahisi niambie ulipokula siku kabla hujaanza kuumwa”“Aaaah nilikunywa maji tu na matunda”“Maji uliyatoa wapi na matunda hayo uliyatoa wapi?”“Maji ni hapa hapa ofisini, yale ambayo wote hapa huwa wanakunywa. Matunda kuna mama mmoja yuko hapo nje ya ofisi yetu huwa anatuletea matunda wote hapa na hata kwenye ofisi zingine halafu namuamini hawezi kunifanyia kitu chochote kile kibaya kwani ni mama mtu mzima kabisa”“Inawezekana sio yeye ndio ila yote hayo nitayapata baada ya kuchunguza”“Mmmh yani Sia akili zako huwa unazielewa mwenyewe”Basi muda ule Sia alimuaga baba Angel na kuondoka zake, kwakweli baba Angel alicheka tu na kuendelea na kazi zake kama kawaida.Sia alitoka nje na kujaribu kunywa maji pale ofisini kwa baba Angel kisha akatoka nje na kumfata mama mtengeneza matunda na kuanza kuzungumza nae kirafiki,“Vipi biashara inalipa hii eeeh!”“Kiasi chake inalipa, sema haiwezi kutosheleza mahitaji yote sema inasaidia”“Ila hata sijajitambulisha dah! Naitwa Sia au mama Elly, na wewe mwenzangu unaitwa nani?”“Nimezoeleka kwa jina moja la mama Juli”“Unajua mimi najishughulisha na shughuli za mama lishe, nina mgahawa wangu, kwakweli kwa kiasi chake napata pata vifaida jamani”“Hongera na wewe”“Aaah niambie ukweli basi, biashara inalipa hii?”“Kiasi chake tu sio sana”“Mmmh hutaki kuniambia ukweli sababu unahisi na mimi nitakuja kufanya hii biashara nini!"Huyu mama akacheka kidogo na kumwambia Sia,“Hamna ningekwambia ukweli, siwezi kukuficha. Ningepata faida sana kama ningekuwa na vitendea kazi vya kutosha ila sababu bado sijawa vizuri sana ndiomana”“Pole, kuna mahali wanakopesha wafanyabiashara wadogo wadogo, kwanini tusiende huko ili upanue biashara yako?”“Ningeenda ila kuna mama mmoja alikuja hapa na ameniahidi kuniongezea mtaji na amenihakikishia kabisa”“Una bahati sana wewe, hongera. Ilikuwaje hadi aseme atakupa mtaji unajua sio kitu cha kawaida hiko?”“Kweli hata mimi sikuamini kabisa, yule mama aliniletea matunda ya aina mbili alisema niyaoshe vizuri nimpelekee bosi Erick na yeye atanilipa, nilifanya vile na bosi aliyasifia sana”Sia alishtuka kidogo ila hakutaka huyu mama agundue mshtuko wake, akamuuliza tena“Baada ya hivyo tu ndio akakuahidi kukuongezea mtaji?”“Ndio alisema yeye husaidia wasiojiweza, ila nakumbuka mara ya mwisho alisema atakuja tena Ijumaa”“Yani kesho?”“Ndio kesho atakuja, alisema kwenye mida ya saa saba au saa nane atakuja”“Kwakweli hiyo ni bahati, hongera sana”Basi waliongea pale, Sia alimueleza vizuri mambo yake ya chakula na alikuwa muwazi kwa huyu mama ili naye awe muwazi kwake,“Yani kuna wanawake tuna shida sana jamani, mfano mimi mwanaume aliniacha basi mtoto nahangaika nae mwenyewe tu dah!! Tunashida sana wanawake, bora na nyie ambao kidogo mliolewa zamani”“Tuolewe wapi? Tena mimi ndio nina mkosi wa kutosha tu, historia yangu utakaa chini kabisa kuisikiliza”“Inasikitisha eeeh!”“Sio kusikitisha tu, yani hata haieleweki, kuna mambo nikikusimulia unaweza sema ni makusudi ila ndio hali halisi ya maisha yangu, nina mtoto mmoja tu na mtoto mwenyewe ni majanga”“Duh!!”“Nitakusimulia siku nyingine maana naona tushakuwa ndugu”“Haya, ngoja niende”Basi Sia aliagana na huyu mama na kuondoka zake ila kimoyomoyo alipanga kwenda tena kesho yake ili amuone huyo mtu wa kumpa mtaji huyu mama.Baba Angel alipomaliza kazi zake maana siku hii hakukaa sana kwenye kazi yake, aliamua kuondoka mapema, moja kwa moja alikuwa akielekea nyumbani kwake maana alikuwa ana uchovu kiasi, ila alipigiwa simu na mke wake,“Upo wapi muda huu?”“Nipo njiani narudi nyumbani”“Samahani, nimepata taarifa kuwa Derrick hali yake imebadilika, kama utaweza pitia nyumbani kwao basi”“Sawa, hakuna tatizo”Baba Angel aliamua kwa muda ule ule kugeuza gari na kuanza kuelekea kwakina Derrick, ni kweli alipofika alimkuta mama Derrick akilia tu kiasi kwamba hata yeye aliingiwa na wasiwasi, alienda kwa haraka kuangalia tatizo, alimkuta Derrick kalala tu yani hata hatingishiki, alimuuliza mama Derrick tatizo ni nini,“Sijui mwanangu ndio anakufa, sijui ni kitu gani sijui ni nini”“Kwani imekuwaje?”“Sijui, nimekuja kumuamsha Derrick haamki wala nini, mwanangu Derrick jamani”Baba Angel aliomba usaidizi pale na walimbeba Derrick na kumpakia kwenye gari kisha ikafanyika safari ya kumpeleka hospitali.Kufika kule, kweli hali yake haikuwa nzuri kiasi kwamba alikimbizwa moja kwa moja kwa wagonjwa mahututi.Basi walikaa pale nje ila mama Derrick alikuwa akilia muda wote, basi baba Angel alimpigia simu mkewe ili kumpa taarifa kuwa Derrick kapelekwa hapo hospitali,“Kwakweli hali yake si njema ila madaktari wanamuhudumia”“Tatizo ni nini kwani?”“Sijui maana hata mama yake nae hana maelezo mazuri kabisa yani, ngoja nisikilizie atakachokisema daktari”Basi baba Angel alipokata simu aliitwa na daktari na kuagizwa baadhi ya dawa zingine za kumpatia Derrick, kwahiyo alitoka na kwenda kununua hizo dawa, wakati anatoka kwenye duka lile la madawa, alikutana na vijana wawili yani Elly na Sarah ambao walimsimamisha na kumsalimia,“Kheee nyie mmetoka wapi?”“Aaaah tumetoka na sisi hapo duka la madawa”“Kwani mnafahamiana?”“Ndio mama zetu ni marafiki”Baba Angel aliwaaga ila alijiuliza kidogo kwani alimtambua Elly kuwa ni mtoto wa Sia, na aliambiwa Sarah kuwa ni mtoto wa Manka, basi alijiuliza,“Kheee urafiki wa Sia na Manka umetokea wapi? Mmmh hawa wanawake hawa, usikute wanapanga ujinga wao”Basi akaondoka zake kuelekea hospitali kwaajili ya kumuwahishia yule mgonjwa dawa.Usiku wa siku hiyo wakati baba Angel amerudi, mkewe alimuuliza hali ya mgonjwa na alisema kuwa anaendelea vizuri,“Kwani tatizo ni nini?”“Unajua mama yake mwanzoni hakuwa na majibu mazuri ila sasa badae baada ya kumuuliza vizuri zaidi ndio akaweza kuniambia kidogo maana hali ya mgonjwa ilikuwa afadhari”“Alisema tatizo ni nini?”“Alisema kuwa, chanzo ni jana Derrick alikuwa akilia sana, alipomuuliza tatizo ni nini alisema kuwa roho inamuuma sana sababu anajua wazi ana watoto ila hajawahi kuwatia machoni watoto hao hata mara moja. Kwahiyo yeye alikuwa akiumia sana moyo wake”“Kheee kumbe ndio sababu?”“Inawezekana maana unaambiwa alikuwa akilia sana, na ndio leo alipolala akalala, maana kila walipomuasha hakuamka wala kuitikia ndio mpaka tumemkimbiza hospitali tena dokta alisema tungechelewa tu ingekuwa balaa”“Duh!”Mama Angel alisikitika sana ila aliamua kulala tu kwa muda huo.Kulipokucha, baba Angel hata hakutaka kwenda popote kwa siku hiyo kwani kuna karatasi alirudi nazo nyumbani aliona bora azifanyie kazi akiwa nyumbani.Sia kama ambavyo alipanga siku hii kwenda ofisini kwa baba Angel ili kumchungulia yule mama ataonana na mtu gani wa maana maana alihisi huyo mtu ndio atakuwa aliyemuwekea sumu baba Angel.Basi alijibanza mbali kidogo ili aangalie kwa makini zaidi, kwenye mida ya saa nane kasoro kuna gari aliona ikisimama pale karibu na biashara ya yule mama halafu alishuka mwanamke Fulani na kuanza kuongea na yule mama, basi Sia alisogea karibu kidogo ili aweze kumuangalia yule mwanamke vizuri ila alishangaa sana kuona yule mwanamke alikuwa ni mama Sarah.Kulipokucha kwenye mida ya saa mbili, mtoto wa madam Oliva alifika kwa mama yake akiwa kaongozana na mamake mdogo.Cha kushangaza wakati madam Oliva kawafungulia mlango na kuwakaribisha pale, alishangaa kuona Steve na Paul wakikimbiliana na kukumbatiana kama watu wanaofahamiana.Kwakweli madam Oliva alishangaa sana basi aliwaangalia kwa muda kisha, aliwasogelea halafu Paul alienda kumkumbatia na yeye na kumsalimia kisha alimuuliza,“Yani Paul ulimpita mama hapa ukaenda kumkimbilia mwingine! Kwanini?”“Sababu ni baba yangu”“Baba yako? Nani kakutambulisha?”Wakakaa kwenye kochi sasa ili kusikiliza maelezo, yani madam Oliva alitaka kuelewa imekuwaje, ingawa ni kweli Steve ni baba mlezi sababu yeye yupo naye ila kajuana vipi na Paul? Madam Oliva alihitaji kujua,“Kwani mmefahamiana vipi?”Basi Steve alianza kuelezea,“Unajua sikutegemea kama kuna siku nitakutana tena na huyu kijana, kuna mahali alikuwa akiishi nami nilikuwa nikiishi huko, basi mara kwa mara huyu kijana nilikuwa namuona akipita, nilijikuta nikimpenda sana kwani kila nikimuangalia naona karibia kila kitu naendana nae, nilimpenda sana, ni mpole na nilikuwa naongea nae mara nyingi. Aliniambia yeye ana mama lakini hana baba, nikamwambia basi mimi ndio nitakuwa baba yako. Kwahiyo siku zote alikuwa akiniita baba na tulikuwa tukipendana sana mpaka sikumuona tena, niliumia sana lakini sikuwa na namna yoyote ile. Siku zote ulipomuongelea Paul sikujua kama unamuongelea Paul huyu, jamani yani huyu ni mwanangu kabisa haijalishi chochote ila ni mwanangu”Madam Oliva alitabasamu kwani alijihisi vyema kuona mumewe mtarajiwa kawa na mapenzi ya hali ya juu na mtoto wake Paul, basi akamuuliza na Paul“Umejihisije mwanangu baada ya kumuona huyu?”“Yani nimejihisi furaha sana mama, nimefurahi sana. Mimi hapa siondoki, nitakuwa nasoma huku huku nikae na baba yangu"Yani kile kitendo wote kiliwashangaza sana jinsi upendo kati ya Paul na Steve ulivyokuwa hadi mama mdogo wa Paul yani mdogo wake na madam Oliva alikuwa akishangaa, kisha madam Oliva alitumia muda huu kumtambulisha Steve kwa mdogo wake,“Huyu ni mdogo wetu wa mwisho, anaitwa Mary. Na huyu ni shemeji yako anaitwa Steve”Basi Mary na Steve wakasalimiana pale na kuanza kuongea mambo mengine yaliyopo.Leo ilikuwa ni siku ya sikukuu ya kiserikali kwahiyo hawakwenda shule, Erick na Erica walibaki nyumbani tu na kufanya zile shughuli mbalimbali ila baba Angel alimtaka Erick aende kiwandani ila leo alimtaka aende na Erica maana aliona bora wawe wawili huku akiwasisitiza wasile chakula hovyo, kwahiyo walijiandaa na kuondoka zao.Mama Angel aliongea na mumewe,“Mmmh saivi unahofia chakula cha hovyo eeeh!”“Yani hata sielewi, unajua mimi kumuwekea mashaka mtu ni mara chache sana. Nakumbuka hata madam Oliva alikuwa akiniletea chakula kipindi kile nakula, angeamua kunidhuru basi naye lazima angenidhuru tu maana nilikuwa nakula bila ya wasiwasi wowote ule.”“Kweli angeamua angekupata kiurahisi, ila baba Angel huyu mtoto kakua sasa na mimi nahitaji kurudi kwenye shughuli zangu nifanye kama zamani, unajua kuna mambo mengine hayaendi eeeh sababu mwenyewe sipo”“Naelewa mke wangu, basi uwe unafanyaje! Yani uwe unaenda halafu saa ngapingapi unarudi sio unazamia hukohuko hadi jioni au usiku, yani hapo ndio kwenye tatizo na kufanya nione huyu mtoto hapati malezi mazuri. Kipindi cha hawa mapacha wetu, kwakweli mke wangu ulilea hawa watoto tena uliwalea sana, ila kwanini kuwe na tatizo katika kumlea huyu mmoja? Jitahidi mke wangu, kama pesa mbona na mimi natafuta sana! Haya hadi watoto nao wapo vizuri, inatakiwa mambo mengine tupunguze”“Sawa nimekuelewa, ngoja nikakuandalie chakula”Basi mama Angel alienda jikoni, na kumkuta Daima akiwa anajaribu kupika pale,“Kheee Daima jamani mbona kujichosha hivi?”“Mimba sio ugonjwa”“Kheeee sio hivyo, nadhani umeninukuu vibaya siku ile nilipokwambia mimba sio ugonjwa, ni kweli mimba sio ugonjwa ila mimba inahitaji uangalifu wa hali ya juu maana ukikosea kidogo unaweza kupoteza mtoto au wote kwa pamoja, ndiomana mama mjamzoito anaopaswa kutazamwa kwa jicho la tatu. Yani kuna kazi za kufanya ukiwa mjamzito ila zingine unaachana nazo. Kama kazi za kuinama sio nzuri kwa afya yako na mimba yako”“Sawa lakini mimi nahitaji kufanya kazi, sitaki kujibweteka tu”“Usifanye kazi ngumu, ukiwa mjamzito kuna mambo inatakiwa uyaepuke hata kama unayapenda sana. Ni kweli kusema huwezi fanya chochote sababu ya mimba inakuwa ni tatizo lingine ila vilevile ukiwa mjamzito huwezi kufanya kila kitu kama ambavyo mtu ambaye si mjamzito hufanya. Unatakiwa kujilinda wewe na kumlinda mtoto ajaye. Haya acha hapo niendelee mwenyewe”Daima aliacha pale ila alienda sehemu nyingine kutafuta kazi nyingine ya kufanya ni kwavile tu hakutaka tena kukaaa kaa na kulala lala bila kazi yoyote wakati hata hapo anaishi kwa bahatinasibu maana anawaza akirudishwa kwao itakuwaje tena na ile mimba yake.Erick na Erica wakiwa kiwandani, kama kawaida Erick aliendelea na kazi za kiwanda ila Erica alikuwa akizunguka zunguka tu.Siku hiyo alifika yule mteja wao mkubwa, yule mwarabu na kukutana nje na Erica, basi alianza kuongea nae,“Natamani sana kumfahamu mama yako?”“Kwanini?”“Una heshima sana halafu inaonekana umefanana nae”“Asante sana, ni kweli nimefanana na mama. Kwetu tupo wa nne ila mimi nimefanana sana na mama. Yupo dada yangu anaitwa Angel, nina kaka yangu Erick, na mimi ni Erica halafu kuna mdogo wetu wa mwisho ambaye bado ananyonya anaitwa Ester”“Ooooh natamani sana kuwaona kwakweli, ila nyie wengine mbona majina yenu yameanzia na E halafu huyo dada yenu peke yake jina limeanzia na A, kwanini?”“Sijui, naona pengine wazazi walitaka majina yetu yaanzie na A ila walivyotuzaa sisi walitupa majina yao maana baba na mama wanaitwa Erick na Erica, halafu sisi walituzaa mapacha, naona ndio herufi E ilipoanza”“Aaaah nimekupenda bure wewe mtoto, nitakuwa babu yako yani ukiniona uwe unaniita babu. Halafu uwe jnanitambulisha kwa ndugu zako kama huyo dada yako Angel nae nimejikuta nikitamani sana kumfahamu, naamini utanitambulisha”“Ndio, sema dada Angel yupo shule anasoma ya kulala huko huko”“Akirudi utamwambia babu anataka kukusalimia, halafu mtanipigia simi hapa nitakuja hapa hapa kiwandani. Ukienda tu kwa meneja mwambie mpigie babu mwarabu atanipigie”“Sawa hakuna tatizo”“Ngoja niingie kwanza, yani nimekupenda bure”Basi yule mwarabu alienda moja kwa moja ofisini kwaajili ya kuagiza bidhaa zake.Elly nae alikuwa muda mwingi na mama yake, na alipata muda pia wa kuzungumza nae na kwa siku hii alizungumza nae vitu vingi sana,“Kwani mama mwanamke anajigundua vipi kuwa mjamzito?”“Mmmh Elly, mbona unanitisha na maswali yako?”“Nahitaji tu kujua mama, nipo kujifunza.”“Sawa, kwanza kabisa mwanamke anakuwa hapati siku zake yani zinakata hadi atakapojifungua, hiyo ni nia ya kwanza kabisa mwanamke kujihisi kuwa ni mjamzito. Ila kwa njia ya haraka ni kupima mkojo”“Kivipi?”“Mwanamke anaweza kwenda hospitali kupima, ila vile vile kuna vipimo vya kupima mimba nyumbani, yani mtu anaweza akanunua kipimo hiko kwenye duka la madawa na kwenda kupima nyumbani”“Aaaah, kwahiyo akifika anasema nataka kipimo cha kupimia mimba?”“Kheee wewe Elly, mbona unataka kujua vingi sana. Niweke wazi mwanangu kuna nini kinaendelea ili nijiandae, kama umeshamjaza mtu huko mimba nijue mapema. Ila nishakukataza habari za uzinzi mwanangu, au umeanza uzinzi?”“Hapana mama, sina mambo hayo kabisa”“Unauliza sana kuhusu mimba, napata wasiwasi”“Jamani mama, nimeuliza tu nataka kujua, maana hapo badae natarajia kuwa daktari wa wanawake”“Oooh vizuri mwanangu utatusaidia mengi maana wanawake tuna magonjwa mengi sana”“Naelewa mama, na je mimba inazuiliwaje?”“Mmmmh!! Kwa kutumia kinga na kwa mwanamke kutumia uzazi wa mpango. Ila Elly niambie ukweli tu kama umeanza uzinzi”“Hapana mama, nilisema hadi nikiwa mkubwa”“Mmmh unanipa mashaka na haya maswali yako”“Sikuulizi tena mama”Basi Elly aliinuka na kwenda ndani ila alikuwa akiwaza kitu kuwa lazima akamshawishi Sarah ili wanunue kipimo cha mimba na wajaribu kupima, ila alikuwa akiogopa sana moyoni mwake.Wakati wa kurudi nyumbani, Erick na Erica waliamua kupitia kwanza dukani ili kuangalia mambo yanavyoendelea kwenye duka lao.Basi walimkuta Rama akiendelea na kazi zake kama kawaida, Erick alifatilia baadhi ya mambo na kuona kuwa yapo sawa, ila kabla hawajaondoka kuna mtu alifika pale na kuanza kuongea na Rama, mtu huyo walipomuangalia vizuri alikuwa ni Rahim ila hawakuonyesha kama wamemuona kwani waliendelea na mambo mengine tu, alipoondoka ndipo Erica alipomfata Rama na kumuuliza,“Unamfahamu yule uliyekuwa unaongea nae?”“Aaaah yule ni mteja, tena ni mteja mzuri sana halafu inaonyesha ana mtoto mdogo sana kwasasa maana siku ya kwanza kuja alichukua nguo za mtoto mkubwa ila siku hizi huwa anachukua nguo za watoto wadogo inaonyesha ana watoto wadogo sana kwasasa”“Aaaah kumbe, namjua yule ila sikujua kama ana watoto wadogo”Basi Erick na Erica wakamuga Rama na kuondoka zao, ila kabla hawajafika mbali walimuona Juma akielekea hapo dukani, ikabidi Erick asimamishe gari na ashuke kwenda kumsalimia maana ni kitambo sana hajaongea nae, ingawa wazazi wake walikuwa wakimkataza kuongea na Juma ila Erick hakuona tatizo lolote kufanya hivyo. Alimsogelea na kumsalimia,“Ooh Erick, nimefurahi sana kukuona. Naamini ni pacha wako Erica ndio kakushawishi kuja kunisalimia”“Hapana ni mimi mwenyewe, kwanini unasema hivyo?”“Naelewa moyo wa Erica ulivyo, ana upendo sana huyo binti ndiomana nasema kuwa ni yeye aliyekushawishi kuja kunisalimia”Erick alicheka tu ila leo hakuongea nae sana, muda kidogo alimuaga na kurudi kwenye gari lao na kuendelea na safari huku akimwambia Erica,“Ni kwanini watu wengi hukuona wewe kuwa na roho nzuri sana?”“Ndio ukweli huo mimi nina roho nzuri”“Na mbona ulitumwagia maji kitandani mimi na Sarah wakati ulijua wazi kuwa Sarah anaumwa?”“Sikumuamini Sarah ndiomana, namuona macho juu juu sana”“Kivipi?”Erica aliamua kubadilisha mada hadi pale walipofika nyumbani kwao.Usiku wa leo, Daima alikuwa amekaa huku akilia tu Yani ilionekana kwa kiasi kikubwa sana anajutia mambo ambayo aliyafanya, basi Vaileth akawa anambembeleza, akakumbuka kipindi yeye alipobeba mimba na shule kumshinda, alikumbuka hilo na kujihisi vibaya sana,“Pole sana Daima kiukweli nakuhurumia maana nimewahi kupitia hiyo kama yako”“Mimi imezidi kwakweli, hakuna hata wa kunibembeleza, Junior hanipigii simu, mama na baba nao wala hawana habari na mimi, nimekuwa kama kifaranga aliyeachwa kwenye mvua, nateseka mimi”“Pole sana, ila wewe na Junior si ilikuwa mnapendana sana!”“Tena sana hata sijaamini kuwa kuna siku itakuwa hivi, yani Junior atanikana kabisa hata kuongea maneno ya uongo juu yangu. Sikufikiria kabisa kama kuna siku kama hii katika maisha yangu”“Unachotakiwa kufanya ni kuamini kuwa hayo mambo yamepita na uangalie mambo mengine ya kufanya, kama kumlea mwanao”“Kumlea bila ya baba, wakati baba yake yupo”“Kwani wasiwasi wako nini? Mtoto akizaliwa walazimishe wakampime damu”“Mmmh hawajataka kupima kipindi hiki ndio watakubali mtoto akizaliwa?”“Watakubali tu hata usijali”Basi siku walijikuta wakiongea sana hadi wakachelewa muda wa kulala.Kulipokucha tu, Daima alikuwa wa kwanza kuinuia bila kujali kama usiku hakulala wala nini kwani moja kwa moja alienda kufanya usafi na kutaka kudeki ila mama Angel alimkuta na kumkataza kufanya hivyo, kisha akaongea nae,“Unajua Daima kwakweli mimi nashangaa sana kuwa imekuwaje hadi umekuwa hivyo, sikuelewi ujue”“Hunielewi nini mama?”“Kwanini unajipa kazi zenye uwezo wa kutoa mimba yako, narudia leo sitaki kuona ukifanya kazi ngumu”Basi mama Angel alienda kumtayarishia mumewe chakula ambaye alikula na kumuaga mke wake maana alitaka kidogo kwenda ofisini kwake.Baba Angel alipofika ofisini tu, muda mfupi alifikiwa na mgeni na kumkaribisha maana mgeni huyo alikuwa ni Sia, basi alimuuliza kitu kilichompeleka pale ofisini kwake,“Umefata nini Sia?”“Nataka kufanya utafiti juu ya aliyekupa sumu”Baba Angel alicheka sana na kumuangalia kwa makini,“Hayo maswala ya utafiti umeyaanza lini? Na nani aliyekwambia kuwa nilipewa sumu?”“Nilikutana na Tumaini akaniambia hivyo, nilikuwa natamani kuja kukuona nyumbani kweko ila kuna muda huwa namuhofia sana mkeo maana na yeye huwa anabadilika kama kinyonga yani mambo yake huwa hayaeleweki kabisa”“Haya mambo ya uchunguzi umesomea wapi?”“Hivi nikiamua kuchunguza langu naanzahe kushindwa kwa mfano? Sikujua kipaji changu toka utotoni, yani sikujua kama nina kipaji cha upelelezi ila ni kipaji changu hiki. Nimekigundua ukubwani, ni kweli sijasomea ila naweza kufanya kwa njia za kawaida na nikagundua chanzo cha tatizo kama wachunguzi wengine”“Ni kipi ulichowahi kukigundua wewe?”“Hivi mimi ningemjua vipi Rahim aliyezaa na Erica yule mtoto wenu Angel? Ningemjua vipi Bahati aliyempenda sana Erica na sasa anaishi na rafiki kipenzi wa Erica? Ningejua vipi maovu ya Dora na ulokole wake fake?”“Kheee umenishinda tabia, haya chunguza basi nani kanipa sumu”“Niambie kwanza sehemu unazokumbuka kula chakula kabla ya kuanza kuumwa? Au kwa urahisi niambie ulipokula siku kabla hujaanza kuumwa”“Aaaah nilikunywa maji tu na matunda”“Maji uliyatoa wapi na matunda hayo uliyatoa wapi?”“Maji ni hapa hapa ofisini, yale ambayo wote hapa huwa wanakunywa. Matunda kuna mama mmoja yuko hapo nje ya ofisi yetu huwa anatuletea matunda wote hapa na hata kwenye ofisi zingine halafu namuamini hawezi kunifanyia kitu chochote kile kibaya kwani ni mama mtu mzima kabisa”“Inawezekana sio yeye ndio ila yote hayo nitayapata baada ya kuchunguza”“Mmmh yani Sia akili zako huwa unazielewa mwenyewe”Basi muda ule Sia alimuaga baba Angel na kuondoka zake, kwakweli baba Angel alicheka tu na kuendelea na kazi zake kama kawaida.Sia alitoka nje na kujaribu kunywa maji pale ofisini kwa baba Angel kisha akatoka nje na kumfata mama mtengeneza matunda na kuanza kuzungumza nae kirafiki,“Vipi biashara inalipa hii eeeh!”“Kiasi chake inalipa, sema haiwezi kutosheleza mahitaji yote sema inasaidia”“Ila hata sijajitambulisha dah! Naitwa Sia au mama Elly, na wewe mwenzangu unaitwa nani?”“Nimezoeleka kwa jina moja la mama Juli”“Unajua mimi najishughulisha na shughuli za mama lishe, nina mgahawa wangu, kwakweli kwa kiasi chake napata pata vifaida jamani”“Hongera na wewe”“Aaah niambie ukweli basi, biashara inalipa hii?”“Kiasi chake tu sio sana”“Mmmh hutaki kuniambia ukweli sababu unahisi na mimi nitakuja kufanya hii biashara nini!"Huyu mama akacheka kidogo na kumwambia Sia,“Hamna ningekwambia ukweli, siwezi kukuficha. Ningepata faida sana kama ningekuwa na vitendea kazi vya kutosha ila sababu bado sijawa vizuri sana ndiomana”“Pole, kuna mahali wanakopesha wafanyabiashara wadogo wadogo, kwanini tusiende huko ili upanue biashara yako?”“Ningeenda ila kuna mama mmoja alikuja hapa na ameniahidi kuniongezea mtaji na amenihakikishia kabisa”“Una bahati sana wewe, hongera. Ilikuwaje hadi aseme atakupa mtaji unajua sio kitu cha kawaida hiko?”“Kweli hata mimi sikuamini kabisa, yule mama aliniletea matunda ya aina mbili alisema niyaoshe vizuri nimpelekee bosi Erick na yeye atanilipa, nilifanya vile na bosi aliyasifia sana”Sia alishtuka kidogo ila hakutaka huyu mama agundue mshtuko wake, akamuuliza tena“Baada ya hivyo tu ndio akakuahidi kukuongezea mtaji?”“Ndio alisema yeye husaidia wasiojiweza, ila nakumbuka mara ya mwisho alisema atakuja tena Ijumaa”“Yani kesho?”“Ndio kesho atakuja, alisema kwenye mida ya saa saba au saa nane atakuja”“Kwakweli hiyo ni bahati, hongera sana”Basi waliongea pale, Sia alimueleza vizuri mambo yake ya chakula na alikuwa muwazi kwa huyu mama ili naye awe muwazi kwake,“Yani kuna wanawake tuna shida sana jamani, mfano mimi mwanaume aliniacha basi mtoto nahangaika nae mwenyewe tu dah!! Tunashida sana wanawake, bora na nyie ambao kidogo mliolewa zamani”“Tuolewe wapi? Tena mimi ndio nina mkosi wa kutosha tu, historia yangu utakaa chini kabisa kuisikiliza”“Inasikitisha eeeh!”“Sio kusikitisha tu, yani hata haieleweki, kuna mambo nikikusimulia unaweza sema ni makusudi ila ndio hali halisi ya maisha yangu, nina mtoto mmoja tu na mtoto mwenyewe ni majanga”“Duh!!”“Nitakusimulia siku nyingine maana naona tushakuwa ndugu”“Haya, ngoja niende”Basi Sia aliagana na huyu mama na kuondoka zake ila kimoyomoyo alipanga kwenda tena kesho yake ili amuone huyo mtu wa kumpa mtaji huyu mama.Baba Angel alipomaliza kazi zake maana siku hii hakukaa sana kwenye kazi yake, aliamua kuondoka mapema, moja kwa moja alikuwa akielekea nyumbani kwake maana alikuwa ana uchovu kiasi, ila alipigiwa simu na mke wake,“Upo wapi muda huu?”“Nipo njiani narudi nyumbani”“Samahani, nimepata taarifa kuwa Derrick hali yake imebadilika, kama utaweza pitia nyumbani kwao basi”“Sawa, hakuna tatizo”Baba Angel aliamua kwa muda ule ule kugeuza gari na kuanza kuelekea kwakina Derrick, ni kweli alipofika alimkuta mama Derrick akilia tu kiasi kwamba hata yeye aliingiwa na wasiwasi, alienda kwa haraka kuangalia tatizo, alimkuta Derrick kalala tu yani hata hatingishiki, alimuuliza mama Derrick tatizo ni nini,“Sijui mwanangu ndio anakufa, sijui ni kitu gani sijui ni nini”“Kwani imekuwaje?”“Sijui, nimekuja kumuamsha Derrick haamki wala nini, mwanangu Derrick jamani”Baba Angel aliomba usaidizi pale na walimbeba Derrick na kumpakia kwenye gari kisha ikafanyika safari ya kumpeleka hospitali.Kufika kule, kweli hali yake haikuwa nzuri kiasi kwamba alikimbizwa moja kwa moja kwa wagonjwa mahututi.Basi walikaa pale nje ila mama Derrick alikuwa akilia muda wote, basi baba Angel alimpigia simu mkewe ili kumpa taarifa kuwa Derrick kapelekwa hapo hospitali,“Kwakweli hali yake si njema ila madaktari wanamuhudumia”“Tatizo ni nini kwani?”“Sijui maana hata mama yake nae hana maelezo mazuri kabisa yani, ngoja nisikilizie atakachokisema daktari”Basi baba Angel alipokata simu aliitwa na daktari na kuagizwa baadhi ya dawa zingine za kumpatia Derrick, kwahiyo alitoka na kwenda kununua hizo dawa, wakati anatoka kwenye duka lile la madawa, alikutana na vijana wawili yani Elly na Sarah ambao walimsimamisha na kumsalimia,“Kheee nyie mmetoka wapi?”“Aaaah tumetoka na sisi hapo duka la madawa”“Kwani mnafahamiana?”“Ndio mama zetu ni marafiki”Baba Angel aliwaaga ila alijiuliza kidogo kwani alimtambua Elly kuwa ni mtoto wa Sia, na aliambiwa Sarah kuwa ni mtoto wa Manka, basi alijiuliza,“Kheee urafiki wa Sia na Manka umetokea wapi? Mmmh hawa wanawake hawa, usikute wanapanga ujinga wao”Basi akaondoka zake kuelekea hospitali kwaajili ya kumuwahishia yule mgonjwa dawa.Usiku wa siku hiyo wakati baba Angel amerudi, mkewe alimuuliza hali ya mgonjwa na alisema kuwa anaendelea vizuri,“Kwani tatizo ni nini?”“Unajua mama yake mwanzoni hakuwa na majibu mazuri ila sasa badae baada ya kumuuliza vizuri zaidi ndio akaweza kuniambia kidogo maana hali ya mgonjwa ilikuwa afadhari”“Alisema tatizo ni nini?”“Alisema kuwa, chanzo ni jana Derrick alikuwa akilia sana, alipomuuliza tatizo ni nini alisema kuwa roho inamuuma sana sababu anajua wazi ana watoto ila hajawahi kuwatia machoni watoto hao hata mara moja. Kwahiyo yeye alikuwa akiumia sana moyo wake”“Kheee kumbe ndio sababu?”“Inawezekana maana unaambiwa alikuwa akilia sana, na ndio leo alipolala akalala, maana kila walipomuasha hakuamka wala kuitikia ndio mpaka tumemkimbiza hospitali tena dokta alisema tungechelewa tu ingekuwa balaa”“Duh!”Mama Angel alisikitika sana ila aliamua kulala tu kwa muda huo.Kulipokucha, baba Angel hata hakutaka kwenda popote kwa siku hiyo kwani kuna karatasi alirudi nazo nyumbani aliona bora azifanyie kazi akiwa nyumbani.Sia kama ambavyo alipanga siku hii kwenda ofisini kwa baba Angel ili kumchungulia yule mama ataonana na mtu gani wa maana maana alihisi huyo mtu ndio atakuwa aliyemuwekea sumu baba Angel.Basi alijibanza mbali kidogo ili aangalie kwa makini zaidi, kwenye mida ya saa nane kasoro kuna gari aliona ikisimama pale karibu na biashara ya yule mama halafu alishuka mwanamke Fulani na kuanza kuongea na yule mama, basi Sia alisogea karibu kidogo ili aweze kumuangalia yule mwanamke vizuri ila alishangaa sana kuona yule mwanamke alikuwa ni mama Sarah. Basi alijibanza mbali kidogo ili aangalie kwa makini zaidi, kwenye mida ya saa nane kasoro kuna gari aliona ikisimama pale karibu na biashara ya yule mama halafu alishuka mwanamke Fulani na kuanza kuongea na yule mama, basi Sia alisogea karibu kidogo ili aweze kumuangalia yule mwanamke vizuri ila alishangaa sana kuona yule mwanamke alikuwa ni mama Sarah.Sia alishangaa kidogo na kujiuliza kama kweli mama Sarah anaweza kufanya kitu cha kumdhuru baba Angel, alijiuliza sana bila ya jibu lolote.Alitulia pale hadi mama Sarah alipoondoka ndipo alipoenda tena pale kwa mama Juli na kumsalimia kisha alianza kuongea nae,“Nikaona gari inaondoka hapa wakati nipo kwa mbali, ndio huyo tajiri wako nini?”“Ndio ni yeye, yani mama ana roho nzuri sana yule”“Kwahiyo kakwambia atakupa huo mtaji?”“Ndio kaniambia hivyo, kwakweli nafurahi sana kukutana nae”“Hajamuulizia bosi Erick?”“Aaaah hajamuulizia leo sijui kwanini ila hajamuulizia, hata hivyo anasema kuwa ni rafiki yake sana”“Kwahiyo huo mtaji ameshakupa?”“Kaniambia atakuja tena Jumatatu kwenye mida ya saa nane au saa tisa”Sia alijaribu kupeleleza zaidi ila hakupata jibu la moja kwa moja, basi aliagana na yule mama na kuondoka zake, ila bado alijiuliza sana kuwa ni kweli mama Sarah ndiye aliyetaka kumdhuru baba Angel? Alikisa jibu kabisa, alijiuliza zaidi kila muda“Amdhuru kwasababu gani? Sababu alizaa nae na amekataa mtoto au ni kitu gani? Lazima kuna kikubwa kati ya huyu Manka na Erick”Muda huu aliona ni vyema kurudi kwenye biashara yake tu, na aliporudi aliendelea na kazi zake kama kawaida ila muda kidogo alifika pale mama Sarah na alimkaribisha na kuongea nae vizuri tu kama hakuna kitu,“Unajua nilikuja mwanzoni nikakukosa, ndio nimekuja tena. Unadhurula sana wee mwanamke”“Si unajua tena nipo kwenye kutafuta ndiomana”“Huko kutafuta kwenye uzurulaji ni kutafuta kupi?”“Aaaah ni kuhangaika tu na maisha”“Haya sawa ni vizuri kuhangaika”“Ni kweli, mna raha nyie wenzetu ambao maisha mmeyapatia”Mama Sarah alicheka na kusema,“Katika ujana unatakiwa kuwa makini sana na kupanga maisha yako kwa mpango kamili, kuna vitu ukikosa kuvifanya ujanani basi uzeeni utaona kila mtu mbaya kwako. Maisha yakikuendea kinyume katika njia uliyopo unatafuta njia nyingine ili kujiinua. Nikwambie siri ya mafanikio yangu”“Eeeh niambie”“Mimi nilimpenda sana Erick na nilikuwa na mahusiano nae, maana mimi ni mwanamke mzuri tena ninajfuraha, ila Erick alikuwa na mambo mengi sana na alijua wazi hawezi kudumu na mwanamke mzuri kama mimi tena ninajiamini na uzuri wangu. Kuachana na Erick kuliniumiza sana ila hakukuwa sababu ya mimi kutokusonga na kuanzisha maisha mengine. Nilianza mahusiano na mwanaume mmoja hivi, yeye hakuwa akihonga hela wanawake ila mimi alikuwa akinihonga tena sana tu, ila wakati huo sio kwamba niliachana moja kwa moja na Erick hapana, nikikutana nae tunamalizana kama kawaida na ilikuwa ni furaha kwangu ila badae nikaona ni ujinga kwani natakiwa kupanga maisha yangu. Ndipo nilipopata baba mmoja hivi, alinipenda, alinijali na kunihudumia nilifanya chochote alichotaka na ndio chanzo cha utajiri wangu”“Kheee hongera, baba gani huyo?”“Aliitwa mzee Jimmy”Sia akashtuka hata mama Sarah aliona mshtuko wake na kumuuliza,“Mbona umeshtuka hivyo?”“Aaaah sio kitu, kwahiyo Sarah baba yake ni nani?”“Yoyote kati ya hao ni baba yake maana nilikuwa nao wote”“Kheee”“Badae nitakuja kumfata Elly nyumbani kwako, kwaheri”Muda huo mama Sarah aliondoka zake.Kwenye mida ya saa moja kasoro, Sia alikuwa amekaa nje na mwanae Elly huku akiongea nae,“Halafu mama Sarah alisema kuwa atakuja kukuchukua wewe, nashangaa mpaka muda huu hajaja”“Ila mama mbona napafahamu vizuri wanapoishi, naweza kwenda mwenyewe sio mpaka nije kuchukuliwa”“Ila mwanangu huoni ufahari eeeh! Unakuja kuchukuliwa na gari, hapa mtaani watu walikuwa wakituona tupotupo tu, wengine wakisema nawezaje kukusomesha shule za gharama ila kwasasa naona wameshindwa kusema zaidi maana kila mara magari yanakuja hapa. Ila mwanangu toka juzi nakuona kama una mawazo sana”“Aaaah mama, usijali kuhusu mimi mbona nipo kawaida tu”“Haya mwanangu yani mimi nilikuwa nakuona kama haupo sawa vile ila kama una tatizo lolote usisite kuniambia maana mimi ndio mama yako hakuna mtu mwenye mama wawili duniani, ni mama mmoja tu”“Nimekuelewa mama lakini....”Mama Sarah alifika muda ule ule na kusalimiana nao pale, kisha akamtaka Elly waondoke wote,“Yani leo Sarah kaniambia nisipomshawishi Elly kwenda nae nyumbani basi na mimi sitotoka kwenda popote, halafu nataka nitoke sasa”Elly akawaza kidogo ila mama yake akamshawishi ajiandae na aende, kiukweli Elly alikuwa akiogopa sana.Basi alijiandaa na kuondoka na mama Sarah na moja kwa moja mama huyu alianza safari huku akiongea mambo mbalimbali na Elly,“Hivi unamjua baba yako mzazi?”“Simjui na hata sitaki kumjua, mama aliniambia kuwa baba alinikataa toka siku nazaliwa, alisema kuwa sijafanana nae”“Oooh pole mtoto mzuri, hivi ukija kugundua kuwa ni mpango wa mama yako ili usimjue baba yako utafanyaje?”“Sidhani kama mama anaweza fanya kitu kama hiko juu yangu, naamini mama ananipenda sana na sidhani kama ana mpango huo wa kufanya mimi nisimjue baba yangu”“Je wewe una mpango wowote wa kukataa mtoto wako?”Elly akashtuka kiasi na kukaa kimya kwa muda kisha akajibu,“Aaah mimi siwezi, aaah siwezi kumkana mtoto wangu”“Hivi unajua kuwa unaweza kupata mtoto kwa umri huo?”Elly akatetemeka na kuogopa, alihisi labda Sarah kapima mimba, alijikuta tu jasho likimtoka na kukosa hata majibu, muda kidogo simu ya mama Sarah ilianza kuita na akaipokea, ilionekana aliyempigia alikuwa akimsubiria, basi aliongeza mwendo na walipofika nyumbani tu alienda kujiandaa na kuwaaga halafu akaondoka zake.Leo Elly alishindwa hata kula vizuri kwani alikuwa na mawazo sana, alipomaliza moja kwa moja alienda chumbani kwake huku akiwaza sana yani aliogopa mno.Akiwa chumbani kwake mida ule alienda Sarah mule chumbani na kumfanya Elly aogope zaidi na kitu cha kwanza alimuuliza Sarah,“Umepima mimba Sarah?”“Unaonekana unaogopa sana Elly, kwani mimba ni kitu gani? Usiwe muoga kiasi hiko Elly”“Niambie kwanza Sarah”“Hivi tulienda wote hadi duka la madawa kununua kipimo pamoja, ukaniacha nirudi nacho mwenyeww nyumbani unadhani naweza pima peke yangu? Hapana siwezi, nilikuwa nataka nawe uwepo ndio nipime, jana umeahidi kuja kulala kwetu ila hukuja ndiomana leo nilimuomba mama aje akulazimishe mwenyewe uje. Haya niambie tupime mimba au tusipime?”“Mmmh Sarah naogopa sana, natamani kujua ila naogopa sana kwani hata nikiujua ukweli bado sitaweza kuuchukulia maana naogopa sana, moyo wangu unatetemeka kwa mawazo”“Basi tusipime kwanza hadi tuanze kuwa na wasiwasi, ila hata hivyo kuna kitu shuleni walisema wataongea na watoto wa kike kuhusu afya na uzazi kwa mwanamke, kwahiyo nikisikiliza nitapata cha muhimu zaidi ya kupima. Naomba ushushe presha"Elly akapumua kidogo, na afadhari akawa sawa, ndipo Sarah alipomvuta mkono na kumtaka aende nae chumbani kwake, kwakweli hili swala lilikuwa ni mtihani mkubwa kwa Elly na aligoma kukataa kwani familia hii ndio ilimpa kila kitu kwa wakati huo, hata mama yake alimfundisha kuwa asimkasirishe Sarah kabisa.Akaenda nae chumbani kwa Sarah, na kama siku zote Sarah alihitaji kwahiyo ilibidi Elly afanye vile Sarah alivyotaka, baada ya hapo aliamua kurudi chumbani kwake, ila katika mambo yote tatizo lake lilikuwa sehemu moja tu, alijikuta akiwaza sana kuhusu mimba yani hakujua kama Sarah akiwa na mimba itakuwaje juu yake.Aluporudi chumbani tu kabla ya kujilaza alishangaa kusikia mlango ukigongwa, moja kwa moja alihisi ni Sarah tena basi aliinuka na kwenda kufungua ila hakuwa Sarah kwani aliyeingia alikuwa ni Siku ambaye moja kwa moja alimziba mdomo Elly na kuingia nae chumbani kwa Elly na kufunga mlango kisha akamwambia,“Elly najua kama wewe ni mwanaume rijali, najua kama wewe ni mwanaume uliyekamilika. Mimi ni siki nyingi sana sijafanya chochote, nakutamani siku zote hizi, nitakufundisha mapenzi. Kwangu utajua mapenzi ni nini na utazidi kuwa mwanaume wa ukweli”Elly akaogopa ila Siku alianza kumpapasa Elly, kwakweli wazo la Elly muda huo lilimwambia kuwa yote yale ni umasikini wa nyumbani kwao na hakuwa tayari kufanya chochote na huyu dada yao ila alijua yule mdada akiendelea kumpapasa basi atajikuta akifanya makosa tena, hivyo basi alionekana kukubali halafu akamwambia Siku,“Kuna kitu nahitaji muda huu halafu tutafanya kwa raha”“Kitu gani?”“Nahitaji kunywa maji”“Ngoja nikakuletee”“Hapana nisubiri hapa hapa nikanywe”Elly alitoka mule chumbani kama anaenda jikoni kunywa maji ila moja kwa moja alienda chumbani kwa Sarah, na kwa uzuri Sarah hakufunga na funguo mlango wake basi Elly akaingia na kufunga kisha moja kwa moja alienda kulala pembeni ya Sarah maana Sarah nae muda huo alikuwa amelala hoi kabisa.Kulipokucha, Sarah anashtuka na kumkuta Elly kalala pembeni yake, basi anamuamsha na kumuuliza,“Kheee Elly ulirudi kulala humu?”“Ndio, nilijikuta siwezi kulala mwenyewe”“Oooh umeanza kunipenda eeeh”Elly alikaa kimya kwa muda ila badae aliitikia na kumfanya Sarah afurahi sana, basi Elly akatoka kinyemela na kurudi chumbani kwake kwani muda huo hata Siku hakuwepo humo tena.Basi leo Erica anakumbuka kuwaeleza wazazi wake kuhusu yule mwarabu, baba Angel aliposikia vile aliona ni vyema kama siku hiyo waendw wote kwa pamoja kwenye biashara ya huyo mwarabu na waweze kumualika kwao kwa chakula cha jioni kwa siku nyingine. Basi mama Angel akauliza,“Jamani na mimi?”“Ndio na wewe mke wangu”“Hapana, huyo baba si ana hamu ya kunifahamu itakuwa vyema kama hatonifahamu kwa wakati ili mkimualika kwwnye chakula cha jioni aweze kufika na atanifahamia huku nyumbani”“Ila mke wangu una akili sana wewe jamani, ndiomana nikakuoa kwakweli, haya Erick na Erica mjiandae tuweze kwenda huko”Walijiandaa na kisha kuondoka hapo nyumbani kwahiyo pale alibaki mama Angel, Daima, Vaileth na Ester.Kama kawaida Daima alikuwa akijishughulisha na kazi mbalimbali kwakweli ile hali ilikuwa ikimkera sana mama Angel hadi alianza kujiuliza kuwa huyu binti ana lengo gani,“Daima unataka hiyo mimba itoke?”“Hapana mama”“Sasa kwanini unafanya vitu nilivyokukataza? Nani kakutuma upinde mgongo hapo kwenye kibaraza na udeki, nani kakutuma?”Daima alikuwa kimya kwa muda, kisha mama Angel akaendelea,“Nina madekio ya kusimama, ila wewe umeenda kuchukua tambala na kusafishia ili tukueleweje?”“Tambala linafuta vizuri mama”“Unajua usinichefue, nitakurudisha kwenu wewe, sitaki ufanye ujinga hapa kwangu”Daima alianza kulia tena alilia sana hata mama Angel alimshangaa na kushindwa hata kumbembeleza zaidi zaidi alimuita Vaileth na kumwambia kuwa ambembeleze,“Vai, mbembeleze mwenzio huyo, mimi siwezi jamani”Kisha mama Angel alienda zake ndani na kuendelea na mambo mengine.Ile habari ya kuhusu mzee Jimmy ilikuwa imeshtua kwa kiasi fulani Sia, na siku ya leo aliamua kwenda kwa Tumaini ili kumueleza habari hiyo kwani alijua ndio pekee anaweza kumsikiliza.Moja kwa moja alienda kwa Tumaini na alimkuta na kuanza kuongea nae,“Nina habari ndugu yangu na inaniwasha hatari”“Habari gani? Na wewe kwa umbea hujambo ndugu yangu”“Mmh sio umbea tu, natumai unamfahamu mama Sarah?”“Yule mwalimu?”“Ndio huyo huyo, alikuwa mwalimu wa kujitegemea ila yule hajasomea ualimu”“Kheee wewe jamani unafahamu mambo mengi sana ya watu”“Aliniambia yeye mwenyewe”“Mmmh ila wewe, haya kaja kukwambia tena kuwa mtoto wake ni wa Erick?”“Hapana, ila nimepata mapya”“Yapi hayo?”“Kumbe mama Sarah alikuwa akitembea na baba yenu mzee Jimmy, jana kaniambia vizuri na ile mali aliyokuwa nayo ni mambo ya mzee Jimmy”“Mmmh ila wewe hukawii kuniambia hata mtoto wake ni mdogo wetu”“Hajaniambia kuhusu mtoto ila habari ndio hiyo, usinifikirie vibaya, nimekuletea ujumbe tu”Basi muda kidogo aliaga na kuondoka zake, moja kwa moja alielekea kwenye biashara zake sasa.Alipofika tu alimkuta mama Sarah yuko hapo akimsubiria, basi akamwambia,“Ila na wewe unahangaika umeacha biashara hapa sijui ukaenda wapi?”“Sikuwa mbali sana nilikuwepo tu kufata madeni yangu”“Wamekulipa sasa?”“Ahadi kibao, ndiomana huwa sipendi kukopesha chakula, mtu akishakula, akienda chooni anasahau kila kitu loh”Mama Sarah akacheka tu na kumwambia Sia,“Unahangaika sababu hukupanga misingi imara ya maisha yako”“Aaaah maisha mara nyingine inatokea tu”“Hapana inatakiwa kupanga, mfano kabla ya kupata mtoto inatakiwa kupanga nazaa na nani? Mwanangu ataishi vipi? Atasomaje na atakula nini? Mavazi je, unataka mwanao awe vipi, maisha ni kupanga”“Kwahiyo wewe ulipanga?”“Ndio, mimi nilipanga na niliyezaa nae niliona ni sahihi, nilizaa na mzee Jimmy, ona maisha yalivyoninyookea, nina nyumba tatu na zote nimeachiwa na mzee Jimmy, nina shule mbili, nina viwanja na mashamba. Mwanangu Sarah hawezi kupata shida sababu baba yake kamuachia mali za kutosha”“Kheee hongera sana”“Asante, nilipita tu kukusalimia. Kwaheri”Mama Sarah aliondoka zake, yale maneno yalimpa mchecheto Sia yani alijikuta akiamani kuyapeleka kwa Tumaini, na muda huo huo aliondoka na kwenda tena hadi kwa Tumaini na hata Tumaini alimshangaa kwani giza lilishaanza kuingia kwa muda huo,“Mmmh Tumaini, kuna mambo duniani. Baba yenu aliwaachia vitu gani vya kurithi?”“Kivipi?”“Mama Sarah sasa, kaachiwa nyumba tatu na mzee Jimmy, shule kubwa kubwa mbili, viwanja vya kutosha na mashamba kibao. Mzee Jimmy alikuwa tajiri sana, halafu kumbe Sarah ni mdogo wenu halali”“Mmmh Sia nani kakwambia hayo maneno?”“Yeye mwenyewe mama Sarah”“Duh!! Haya, asante kwa taarifa”Sia aliamuaga Tumaini na kuondoka zake kwa muda huo kuelekea nyumbani kwake.Usiku wa leo Tumaini alijiuliza sana juu ya habari alizopewa na Sia, na kujiuliza kwanini baba yao alifanya siti hadi anakufa bila kuwaambia ukweli wowote ule, alijiuliza sana bila ya jibu, akaamua kulala tu siku hii.Jumapili ile kama kawaida Tumaini alienda kwenye Ibada, ila alipotoka akakutana na mama Sarah na kusalimiana nae pale, ila hakuweza kubaki na jambo lile moyoni, aliamua kumuuliza tu,“Mama Sarah, kwanini usituambie mapema kuwa Sarah ni damu yetu?”“Kivipi?”“Mzee Jimmy ni baba yetu mzazi mimi na Erick”Mama Sarah alijifanya kushtuka kamavile ni kitu ambacho hakukijua kabla, alimuuliza Tumaini“Kwani nani kakwambia hayo maneno?”“Siwezi kumtaja ila kwanini hutuambii ukweli kama Sarah ni mtoto wa mzee Jimmy!”“Yani hata mimi nashangaa maana huyo mzee hata aimfahamu jamani, yuko wapi kwani?”“Baba yetu alishakufa”“Oooh poleni sana, simjui huyo mzee”“Humjui wapi wakati kakuachia nyumba tatu sijui, shule mbili, na viwanja na mashamba, humjui wapi? Hilo la kukuachia mali sio tatizo ila tatizo kwanini umfiche ndugu yetu!”“Unajua nashangaa tu hapa, mimi sijui chochote jamani mama Leah. Nani kakwambia hayo maneno jamani!”“Kwaheri”Tumaini hakumtajia mama Sarah kuwa Sia ndio kamwambia hayo maneno, na akaagana nae muda huo na kuondoka zake.Jumatatu ya leo, baba Angel anaamua kumuaga mkewe na kwenda zake ofisini, ila mama Angel nae anamuahidi kuwa badae na yeye ataenda huko huko ofisini,“Sawa mke wangu”Basi baba Angel akaondoka muda huo na kwenda ofisini.Mama Angel akafanya majukumu mengine, ila pia alikumbuka kuhusu ndugu yake aliyekuwa hospitali basi alijiandaa pia na kwenda kumuona. Ila siku hii alitoka nyumbani kwake bila usafiri kwani hakujihisi kuendesha gari siku hii na pia hakutaka kumuita dereva wao, kwahiyo aliondoka hapo kwake mpaka stendi na kuchukua daladala kwenda mpaka hospitali.Akiwa njiani kwenda kumuona Derrick, alikutana na Rahim basi Rahim alianza kumsemesha,“Erica, bado una kisirani na mimi hutaki hata kunisalimia?”“Achana na mimi”“Nimeachana na wewe na wala sitokuwa nikikusumbua kama zamani kwani nimepata mchepuko wa Erick”“Mchepuko wa Erick!”“Nilijua kama hilo jambo lazima likushangaze sana, ndio mchepuko wa Erick alijisahau na kunipigia mimi simu basi ndio nipo nae”Mama Angel alielewa vizuri kuwa huyu Rahim anazungumzia nini maana walimuona siku akiwa na mama Sarah, ila hakutaka kuongea nae sana zaidi zaidi alimuaga tu,“Mimi nina haraka bhana, namuwahi mgonjwa wangu”“Au wivu umekujaa?”Mama Angel hakumjibu kitu zaidi zaidi alienda kuingia kwenye hospitali aliyokuwa akienda kumuona Derrick.Mama Angel aliingia moja kwa moja kwenye wodi aliyoelekezwa, ni kweli Derrick alikuwa na hali mbaya kwani hata kuongea hakuweza, basi aliongea kidogo na mama Derrick pale“Ila saivi hali yake unaionaje?”“Mbona afadhari, alikuwa na hali mbaya sana. Bila mumeo kwa hakika tulikiwa tunampoteza huyu mtu”Basi mama Angel aliongea kidogo na kuondoka zake, ila aliona ni vyema kwa muda huo kupitia ofisini kwa mume wake. Kwahiyo alichukua tu usafiri wa pikipiki kwa muda huo maana hakutaka tena kukutana na Rahim njiani.Basi alivyofika ofisini hata mumewe alishtuka kidogo kwani hakujua kama ataenda muda huo,“Unajua sikujua kama ungekuja muda huu?”“Nilipita hospitali kumuona Derrick nikaona ni vyema nipitie kukuona mume wangu. Au nimefanya vibaya?”“Hapana hujafanya vibaya mke wangu, hii ni ofisi yako na ukumbuke uliniambia kuwa utakuja”“Ndio mume wangu, ila nakuomba kwasasa uwe makini na chakula huku usile hovyo”“Sili tena mke wangu”“Nahitaji nirudi nyumbani halafu nikuletee chakula”“Hapana, hata leo nitawahi kutoka. Nenda kaniandalie chakula kizuri tu nikirudi nitakuja kula maana najua mke wangu kwa mapochopocho ni hatari”Mama Angel alitabasamu na kumuaga mumewe, ila wakati yupo njiani alikutana na mama Sarah, yani mama Sarah ndio alimuona mama Angel na kusimama nae njiani akimsalimia ila mama Angel alikuwa na hofu kiasi na mtu huyu, kiasi kwamba mama Sarah alicheka na kumwambia mama Angel,“Acha uoga wewe, una wasiwasi sana unahisi nitamuiba mumeo? Jiamini”“Mbona najiamini sana tu”“Hapana hujiamini, muda wote unahisi kuibiwa mumeo, kwanza pole sana. Ila kumbuka kunguru hafugiki, yule Erick ni kama kunguru tu”Mama Angel aliamua tu kuondoka kwani hakutaka kuongea zaidi na mtu huyu.Sia alijibanza pembeni kama kawaida, kwenye mida ya saa tisa kasoro alionekana tena mama Sarah akienda kwa yule mama na walionekana wakiongea kwa kirefu sana.Mama Sarah alipoondoka tu, Sia alienda kwa yule mwanamke ili kumuuliza vizuri,“Naona na leo bosi wako alikuja!”“Mbona unamfatilia sana, na wewe unataka msaada wake nini nimwambie?”“Hapana, mimi nilikuwa napita tu hapa ndio nikakuona naye”Sia akaona leo hakuna ushirikiano sana kwa huyu mama, akaamua tu kumuaga na kuondoka zake.Moja kwa moja alirudi kwenye biashara zake ila alishangaa sana kumkuta mama Sarah pale alisalimiana nae kisha mama Sarah alimuuliza,“Umetoka wapi?”“Kwenye mihangaiko yangu tu”“Mihangaiko ya kutafuta umbea”Sia alishtuka kidogo na kujibu kwa kujibalaguza,“Hapana bhana”Mama Sarah alicheka kwa kejeli kisha akamnasa kibao Sia na kumwambia,“Unanifatilia ili iweje?”Sia alikuwa akishangaa tu kwani hakutegemea kama mama Sarah angemgundua. Sia alishtuka kidogo na kujibu kwa kujibalaguza,“Hapana bhana”Mama Sarah alicheka kwa kejeli kisha akamnasa kibao Sia na kumwambia,“Unanifatilia ili iweje?”Sia alikuwa akishangaa tu kwani hakutegemea kama mama Sarah angemgundua.Mama Sarah akamuangalia tena na kumzaba Sia kibao kingene kisha akamwambia,“Kumbe ndiomana biashara yako haikui sababu kutwa kucha kufatilia maisha ya watu, haya ulikuwa unanifatilia ili iweje?”Sia aliona aibu kiasi na kuamua kumuomba mama Sarah ili wakazungumze pembeni ambapo mama Sarah alikubali hilo ingawa alikuwa na hasira sana, basi Sia alianza kumuomba msamaha,“Kwanza naomba unisamehe sana kwa kukufatilia, sijui ni vipi umenigundua ila naomba unisamehe sana”“Mimi ni mtu makini sana na hufanya vitu kwa umakini zaidi, nilikugundua toka siku nimekuona unachungulia pale karibu na ofisi ya Erick”Sia akapumua kidogo maana kumbe alionekana akichungulia, akaendelea kumuomba msamaha,“Nisamehe sana”“Na ulivyokuwa mjinga sasa, kila ninachokuambia unapeleka makatambuga yako kwa mama Leah kumwambia nilichosema, mimi ni mtu makini sana na kila kitu huwa nafanya kwa akili. Usidhani kila nilichokwambia ni cha kweli, bali nilitaka kupima kiwango chango cha umbea. Niambie sasa kilichokufanya uanze kunifatilia ni kitu gani?”Sia hakuwa na namna nyingine hivyobasi akaona ni vyema tu amwambie ukweli,“Ni hivi, nilipewa taarifa na Tumaini kuwa Erick ameumwa gafla, na hospitali walisema kuwa alinyweshwa sumu, ni hapo nilipoanza kufatilia kuwa hiyo sumu kapewa na nani? Nilipofatilia alichokula ndio nikagundua kuwa amekula matunda ya yule mama, ndipo nilipoanza kumfatilia na kukukuta wewe”“Kwahiyo unahisi kuwa mimi ndio nilimuwekea Erick hiyo sumu?”“Hapana, ila bado nilikuwa nachunguza”“Lazima ulinihisi na ndiomana ulikuwa ukifika pale muda ninaoenda mimi tu. Haya ulipogundua kuwa ni mimi ulichukua uamuzi gani?”“Mimi nilikuwa bado nachunguza kwani sikuamini kuwa wewe unaweza kufanya hivyo”Mama Sarah akacheka kidogo na kumuuliza tena Sia,“Sasa kwanini hukuja kuniuliza mwenyewe? Usijiumeume kuwa bado ulikuwa ukichunguza, ile siku ya kwanza wakati una mashaka nami, ungekuja kuniuliza, ila kwanini hukufanya hivyo? Hakika wewe sio rafiki, wewe ni mnafki sana”“Nisamehe ndugu yangu”“Haya, huyo Erick anakulipa nini kwa kumsaidia uchunguzi?”“Hanilipi chochote ila nimefanya tu sababu nampenda Erick”“Wewe nawe hebu nitolee balaa mimi, unampenda Erick huko kumpenda vipi? Unadhani unaweza kuwa nae? Ni bora mimi, kwanza Erick kuzaa na wewe nahisi huwa anajutia sana, hueleweki hapo ulipo, yani hueleweki kitu chochote”“Sieleweki lakini Erick alikuwa mpenzi wangu na tulipendana sana”“Jidanganye, hivi wanawake wa Erick unaweza kujifananisha nao? Umeniona mimi vizuri, huyo Erica mwenyewe haingii ndani kwangu kwa uzuri, yani hata shule alikuwa anaogopa balaa akisikia mwanaume ananifatilia mimi basi yeye anajiweka kando, akawa anajifanya binti mlokole maana hakuna wa kumchagua. Watu tupo na uzuri wetu”Sia hakumjibu hapa kwani hakutaka kubishana na huyu ukizingatia bado anahitaji msaada wake, kwahiyo alichokifanya yeye ni kuzidi tu kumuomba msamaha.“Nisamehe sana naomba yaishe”“Sasa sikia nikwambie na uweke akilini, hakuna kitu sipendi katika maisha yangu kama kufatiliwa, hata mimi na ndugu zangu huwa hatufatiliani yani kila mtu na mambo yake. Iwe nimemuwekea sumu kweli au sijamuwekea sitaki unifatilie kabisa, nadhani umenielewa!”“Nimekuelewa ndio, sitorudia”“Haya, mjinga wewe. Nenda kaendelee kuuza biashara yako ya kijinga, biashara haikui sababu ya umbea, unaacha kutafuta masoko huko upo makini kwenye kufatilia yasiyokuhusu”Sia alimuangalia tu mama Sarah ambaye kwa muda huo aliondoka zake na kuendelea na mambo yake mengine.Yani leo Sia alirudi nyumbani huku akijiuliza vitu vingi sana,“Hivi yule ana maanisha nini? Kwahiyo mimi mbaya jamani, mbona huyu mwanamke ana ringa sana dah!!”Muda kidogo Elly nae alirudi toka shuleni, basi Elly alivyopumzika tu kidogo, Sia akamuuliza mwanae,“Eti Elly mwanangu, mimi mama yako sio mzuri?”“Aaaah mama, wewe ni mzuri sana. Nani anakusema vibaya mama yangu?”“Hakuna, nimekuuliza tu”Basi Sia akaweka vitu vyake vizuri, ila siku hiyo umeme ulikatika na wakaamua kuwasha tochi ya kwenye simu, ilibidi Sia aende dukani kununua mshumaa kwa muda huo.Basi alifika dukani na kununua mshumaa, ila wakati anarudi kuna mbaba mmoja alimsimamisha na kuanza kuongea nae,“Samahani, unaishi wapi?”“Hapo juu kidogo”“Sijawahi kukuona mitaa hii, naomba nikusindikize kidogo”Sia hakuona tatizo na alianza kusindikizwa na huyu mbaba basi yule baba alianza kumsifia Sia,“Sijapata kuona mwanamke mzuri kama wewe”Sia alianza kucheka, tena alicheka sana na kumwambia huyu baba,“Hivi nyie wanaume mna matatizo gani? Huwa mnasifia hata vitu visivyokuwepo, Nitolee balaa mie:”Sia aliachana na yule mbaba na kutembea haraka haraka kurudi nyumbani kwake, ila alipofika tu na umeme nao ukarudi kwahiyo mshumaa wao ulipona kutumika kwa siku hiyo.Siku ya leo walivyoenda shule, muda wa mapumziko, Sarah alimfata Elly na kumuita pembeni kisha kuongea nae,“Kuna mahali nataka kwenda kesho itabidi unisindikize”“Tukitoka shule?”“Hapana, tutaomba ruhusa kabla hata ya kutoka shule kuna vitu vingine ni muhimu kuwahi zaidi”“Mmmh ni wapi huko?”“Utapajua tu hiyo kesho, kwani una tatizo gani?”“Hapana kitu”Basi Sarah akaondoka zake, kipindi hiki Sarah hata hakuwa karibu na Erick kama ilivyokuwa hapo mwanzo, basi Elly alivyorudi Erick alianza kumuuliza maana kwa kipindi hiki walikuwa wakiongea vizuri tu na sio ugomvi kama zamani,“Kwani ni kitu gani ambacho huwa unaongea na Sarah?”“Unajua nini, Sarah kawa dada yangu yani mimi nipo chini ya malezi ya mama yake”“Aaaah hapo nimeelewa sasa”Wakaendelea na vipindi kama kawaida, muda wa kutoka shule ulivyofika Erick alitoka leo ila hakutaka kupanda gari la shule, kwahiyo alitoka na wale wanafunzi ambao huwa wanapanda daldala.Moja kwa moja alipanda daladala la kurudi kwao, wakati anashuka kwenye ile daladala alikutana na Sia, ila Erick alitaka kumpita tu, sema Sia alimsimamisha na kuanza kuongea nae,“Erick unataka kunipita tu bila ya salamu, sio vizuri hivyo. Mimi sio mbaya wako ujue”Basi Erick akamsalimia na kutaka kuondoka ila Sia alimzuia na kumwambia,“Utaondoka tu Erick, ila ngoja nikwambie. Majina ya Erick ni watu wakarimu sana halafu hawana hasira kama wewe ufanyavyo”“Kwahiyo unataka kusema nini leo? Kuwa Erick sio jina langu au ni kitu gani?”“Hapana, sina maana hiyo. Sikia Erick, kuna vitu vingi sana vipo nyuma ya pazia na wewe huvijui ila siku ukivijua utaona kuwa mimi nilikuwa naongea nawe mambo ya maana. Ila nilisema kuwa naacha umbea, ngoja ninyamaze”Wala Erick hakutaka kuongea nae zaidi kwani muda huo huo na yeye aliondoka zake kwaajili ya kurudi nyumbani kwao.Kwenye mida ya mchana, wakati baba Angel yupo ofisini, mke wake alienda kumpelekea chakula cha mchana, kwakweli alifurahi sana kwani alitamani sana kwa mkewe kuanza kumfanyia hivyo,“Leo nimefurahi sana mke wangu, naona jinsi gani unanijali mume wako”“Ndio nakujali sababu nakupenda sana”“Kula mume wangu, leo nipo kwaajili yako. Nikitoka hapa nitapitia kidogo kwenye ofisi yangu”“Ila usikawie sana, sio ndio urudi nyumbani usiku sana”“Hapana nitageuza mapema tu”Wakaongea pale kisha baba Angel alipomaliza kula, mama Angel alibeba vyombo na kumuaga mumewe kisha akaondoka zake.Muda kidogop tu, kuna mgeni alifika kwenye ofisi ya baba Angel alimshangaa kidogo ila mgeni huyo alikuwa ni mama Sarah,“Kheee Manka, umejuaje hapa ninapofanyia kazi?”“Hakuna kitu ambacho mtu uamue kukigundua halafu usikigundue, hakuna hiyo kitu kabisa”“Haya lipi limekuleta? Ni kuhusu mtoto tena?”“Siwezi kukwambia kuhusu mtoto maana wewe kama umerogezewa na mkeo kuwa ukatae watoto wa nje wakati pia wewe ni mwanaume rijali”“Haya, kipi kimekuleta? Mambo ya mimi na mke wangu yaache kama yalivyo”Mama Sarah alitoa kontena dogo na kufunua, lile kontena lilikuwa na nyama ya kuchoma, pilipili pembeni na ndimu, kisha akamwambia,“Nimekuletea nyama, najua uchu wako ulivyo kwenye nyama. Najua sijawahi fika hapa ila leo nikasema nije na kitu cha tofauti kwako kama siku yangu ya kwanza kuingia kwenye ofisi yako, karibu sana”“Asante, mke wangu katoka hapa muda si mrefu na aliniletea chakula kizuri sana nimekula na nimetosheka, asante sana”“Ila hajakuletea nyama ya kuchoma, una wasiwasi gani kwani? Hii ni nyama tu, unaweza ukawa unatafuna huku unaendelea na kazi zako yani unaweza fanya kama unatafuna karanga”“Huo utakuwa ni uroho maana mimi nishashiba, ila kawape wengine wenye uhitaji”Kisha baba Angel akachukua ule mfuniko wa pembeni na kufunika kile chakula, mama Sarah alimuangalia na kutabasamu tu kisha akamwambia,“Ngoja nikwambie kitu Erick, kwa manufaa yako na yangu, ila sanasana manufaa yako. Mimi ni kweli kabisa niliwahi kuwa na mahusiano na mzee Jimmy, sikujua kama ni baba yako hadi pale Erica aliponiambia ukweli, roho iliniuma si utani kitendo cha kumchanganya baba na mtoto kwakweli niliumia sana, ila nilijikaza tu. Sikutaka iwe hivi ila ni katika mpangilio wa maisha tu. Ni hivi Sarah ni damu yenu haijalishi ni wako au wa baba yako ila ni damu yenu, halafu Sarah anampenda sana mwanao Erick mdogo huoni kama ni tatizo hilo? Ni laana kwa mtu kutembea na ndugu yake. Kuwa makini sana, hii ni kwa manufaa yako”“Sawa, je Erick anampenda Sarah? Yani huyo Sarah ndio kakwambia wewe kuwa anampenda Erick?”“Ndio, Sarah mwenyewe kaniambia jinsi anavyompenda Erick, ila Erick anamkwepa Sarah, sema huwezi jua watakapokutana vizuri”“Hivi una akili wewe?”“Kwanini?”“Mtoto mdogo kama Sarah kapata wapi ujasiri wa kuja kukueleza mama yake kuwa mimi nampenda Fulani?”“Hebu nitolee balaa hapa na wewe, Sarah ana udogo gani yule? Yupo kidato cha tatu ana udogo gani? Hata kama nilimuwahisha shule ila bado sio mdogo wa kuelewa chochote, kuna makabila huko binti akimaliza darasa la saba tu unakuta kashaolewa. Haya tuache mambo ya makabila, wewe hadi ulifukuzwa shule sababu ya mapenzi na ulikiri wazi kwa walimu kuwa unampenda sana Erica, ulikuwa na umri gani? Si ulikuwa kidato cha pili wewe? Kupenda kuna umri unadhani?”“Sina maana kuwa hawezi kupenda, ila nakuuliza kapata wapi ujasiri wa kukwambia hayo?”“Kwanini asiniambie, mimi ni mama yake, ni mshauri wake, ananiambia ili nimwambie kama huyo mtu anamfaa au hamfai. Nyie watu vipi lakini, hamjui kulea watoto eeeh! Unatakiwa kuweka wazi mtoto aelewe kila kitu na awe wazi kwako kwa kila kitu, unamficha ficha mtoto kila kitu unadhani hayo ndio maisha? Kwa mtoto kama Erick kutokujua chochote kuhusu uanaume wake hayo sio maisha, hebu fundisheni watoto wawe wazi kwa kila kitu. Halafu muwape watoto wenu uhuru”“Aiseee hongera sana kwa hilo, mimi ni mwafrika na nitalea watoto wangu hivyo, nitawakataza mabaya na kuwafunza mema tu. Maswala ya kuanza kuwafundisha waniambie wanaowapenda hapana kwakweli, siwezi na sitoweza”“Shauri yako, ila ndio nimeshakwambia hivyo akili kichwani mwako, kusuka au kunyoa. Nyama zangu umekataa. Ila nitaziacha hapa, utampa yoyote utakayejisikia”Mama Sarah alimuaga baba Angel na kuondoka zake kwa muda huo.Baba Angel alipotoka kazini, moja kwa moja alielekea nyumbani kwake, alifika getini na kuingiza gari yake ndani, ila akakumbuka ule mzigo wa mama Sarah aliomuachia ofisini, basi kwavile alifika nao nyumbani, akaona kuingia nao ndani kwake itakuwa balaa kwa mkewe, basi moja kwa moja alienda kumpa mlizi wao ambae alishukuru sana. Kisha baba Angel akaenda zake ndani, na kumkuta mkewe akiongea na dada yake Tumaini, basi alimkaribisha na kuongea nae mawili matatu,“Tena bora umenikuta maana shida yangu ni wewe”“Ipi tena hiyo?”“Sijui tukaongee wenyewe! Au na mama Angel awepo?”“Kwani ni kuhusu nini?”“Ni kuhusu mama Sarah”Baba Angel alifikiria kidogo na kuona ni vyema wakaongee na mkewe asikie kwani hapo alishasikia ni kuhusu nani, halafu asiposhirikishwa ataona kuna kitu anafichwa.Basi wakaondoka wote watatu na kwenda kwenye bustani ambapo Tumaini aliongea kile alichoambiwa na Sia, na vile alivyokutana na mama Sarah na jinsi mama Sarah alivyosema, kwakweli baba Angel alishangaa sana na yeye ilibidi aseme tu ukweli kuhusu mama Sarah alivyofika siku hiyo ofisini kwake na kile alichokisema, yani mama Angel alishangaa sana,“Kwahiyo Sarah anamtaka Erick? Malezi gani hayo?”“Ndio anasema yupo kwenye malezi ya kumuweka wazi mtoto kwa kila kitu na watoto wapate uhuru”Tumaini akasema,“Kumuweka mtoto wazi kwa kila kitu ni vizuri ila sio wazi kwa kila kitu jamani, yani kuna wazazi hawajui uwazi unaopaswa kumueleza mtoto. Na huo uhuru kwa mtoto unapaswa kuwe na miopaka, huyo Sarah muda wote yupo na simu ndio uhuru gani ule zaidi zaidi kumfundisha mtoto tabia mbaya, mitandao yote ya kijamii Sarah yupo, anaangalia vitu vya ajabu sana, nilimkuta siku ile nilisikitika sana kwa mtoto mdogo kama Sarah kuwa makini vile na simu sikupenda kwakweli. Kama kweli Sarah ni damu yetu atupe wenyewe tumlee asituharibie mtoto wetu jamani”Walikaa kimya kwa muda, kisha Tumaini akaongea tena,“Yani yule mtoto Sarah anaonekana kuwa muelewa, inatakiwa tumuwahi mapema hivi maana tukichelewa itakula kwetu jamani, tunatakiwa kuwa makini sana. Ikiwezekana tumfate huyo mama Sarah tufanye nae kikao na atueleze ukweli kuhusu Sarah, nipo tayari kumlea”Yani Tumaini alionekana kuchukizwa sana ila baba Angel na mama Angel walikuwa kimya kabisa, kisha mama Angel aliwaza kitu na kumuuliza baba Angel,“Ulisema Manka alikuletea nyama ofisini, umeziweka wapi? Sijui ni kwanini nimewaza hili?”“Kwakweli nimekuja nazo hadi hapa nyumbani na nimempa mlinzi wetu”“Aaaah kwanini lakini?”“Sasa ningeingia nazo ndani ungenielewa?”“Sio hivyo, kuna mambo tunatakiwa kuyaepuka. Hebu kumbuka vile viatu ambavyo uliletewa na madam Oliva ofisini kwako, mimi nikavichukua na kumpelekea Steve, nini kimetokea kwa Steve sasa? Hasikii haelewi kitu ingawa anadai sio madawa yaliyomfanya ampende madam Oliva. Haya leo umeenda kumpa nyama mlinzi, kama na yeye aliweka madawa je? Ni bora ungetupa tu”“Nilijihisi vibaya kutupa chakula”Mama Angel akamuacha pale Tumaini na kaka yake, halafu yeye moja kwa moja alienda kwa mlinzi wao ili kumwambia kama zile nyama anazo basi ampatoe, yani alipofika pale getini ndio kwanza alimkuta mlizni akimalizia zile nyama,“Kheee umezimaliza zote!”“Sijui bosi kazitoa wapi, ni nzuri hizo sijapata kuona”Mama Angel alishindwa la kuongea zaidi zaidi ya kupeleka jibu kuwa vimeshaliwa, na muda huo huo Tumaini nae aliaga na kuondoka zake huku akisisitiza swala la kufanya kikao kwaajili ya kujua hatma ya Sarah.Usiku wa leo wakati Vaileth na Daima wamelala, simu ya Vaileth ilianza kuita na alipoiangalia akaona kuwa ni Junior ndio anapiga ile simu, akapokea na kumwambia,“Tuma meseji nitakujibu”Halafu akakata ile simu, muda kidogo uliingia ujumbe toka kwa Junior,“Nimekukumbuka sana Vai wangu, nashindwa kufanya chochote sababu yako. Halafu siku hizi hapo sio pazuri tena kama zamani maana nikija tu huyo mjinga nae ananiona.”“Pole sana, ndio maisha yalivyo”“Wewe hujanikumbuka Vai?”“Nimekukumbuka pia”“Sikia, naongea na mlinzi nakuja mara moja”“Usiku huu Junior!!”“Ndio, nimekukumbuka sana”Kisha ujumbe mwingine toka kwa Junior ukaingia,“Sikia Vai, nakuja muda huu nitaongea na mlinzi na utanikuta kwenye bustani”Vaileth aliwaza kidogo na kukosa jibu kabisa, ila vile vile alishindwa kulala mpaka pale aliposikia kuitwa na mama Angel, basi Vaileth akaiweka simu kwenye meza ya pale chumbani na kwenda alipoitwa na mama Angel.Moja kwa moja mama Angel alienda nae kwenye chumba kile cha kumbembelezea Ester na kumwambia amshikie Ester wakati akimkorogea maziwa,“Yani leo maziwa yangu yamekuwa machache sana, Ester hashibi kabisa, nishikie kwanza maana anapiga kelel tu chumbani halafu baba kalala”Kwahiyo Vaileth alimshika mtoto na kuanza kumbembeleza huku mama Angel akimuandalia Ester maziwa mengine ya kopo, huku akiongea ongea na Vaileth, kwakweli Vaileth alikuwa akiitikia tu ila hata hakupenda kabisa.Daima akiwa anajigeuza geuza tu kitandani, akasikia simu ya Vaileth ikiita pale mezani, aliinuka kuiangalia kwani muda mrefu sana alitamani kujua ni mtu gani anayewasiliana na Vaileth kila mara, alipoitazama simu aliona jina lililotokea ‘Junior’ akashtuka sana na kujiuliza,“Kwahiyo Junior ndio anampigia huyu dada? Ili iweje?”Akaamua kupokea bila ya kuongea chochote, alaimsikia Junior akisema,“Njoo hapa kwenye bustani nishafika tayari”Daima alikata ile simu na kuirudisha pale mezani, kisha alinyata na kutoka chumbani hadi kwenda kutoka mlango wa nje, hawakumgundua sababu walikuwa vyumbani pia, basi moja kwa moja Daima alienda nyuma kwenye bustani ni kweli alimkuta Junior amekaa akimsubiri Vaileth, na alipofika mwanzoni kabla Junior hajaangalia vizuri alimwambia,“Nimekutumia meseji muuuda kuwa utoke ila mpaka nimekupigia simu ndio umekuja”Kwakweli Daima alimtazama Junior na kuanza kulia, Junior alipomuangalia vizuri aliona ni Daima, kwakweli Junior alishtuka kwani hakutegemea, basi akamkwepa ila Daima alikuwa akimfata kwa kilio,“Wewe Daima, hebu nyamaza huko, mambo gani haya unataka kufanya?”Daima akamdaka Junior kwa nguvu na hakutaka kumuachia, alitaka Junior amwambie ukweli kuwa kamuita Vaileth wa kazi gani,“Niambie ukweli Junior, una mahusiano na yule dada wewe, muda wote unawasiliana nae”“Hamna mimi huwa nawasiliana nae kuhusu wewe”“Hamna usinidanganye Junior ni mpenzi wako”“Niachie bhana Daima”“Sikuachii Junior, nataka watu wote humu ndani wajue sababu ya wewe kunikataa mimi. Kumbe ni sababu ya huyo mdada!”Akamshika kwa nguvu, Junior akajitahifi kutoka ila wapi, ndipo Junior alipoamua kumnasa kofi mbili za nguvu Daima hadi mwenyewe alimuachia na kuanza kupiga kelele kwa nguvu sasa, Junior alikimbia na kutoka nje ya geti kisha akamwambia mlinzi kuwa amfichie siri.Kelele zile za Daima ziliwashtua wote mule ndani, kaisi kwamba wote waliamka, na kukimbilia bustanini ila Vaileth hakukimbilia bustanini moja kwa moja kwani alikimbilia chumbani kwake, na kuchukua simu yake akakutana na ujumbe toka kwa Junior,“Futa meseji zetu zote, futa namba yangu ya simu, futa kila kitu. Sitaki jambo hili lijulikane kwa muda huu”Yani Vaileth alikuwa akitetemeka na kufuta kila kitu kisha akaiacha simu pale mezani na yeye kutoka nje kujua kuna nini, alimkuta baba Angel na mama Angel ndio wamemzunguka Daima, ila Erick na Erica nao hata hawakutoka, basi Daima alikuwa akiulizwa kilichomtoa nje na kumpigisha kelele,“Ni Junior alikuwa mahali hapa”“Junior!! Alikuja kufanya nini?”“Mama na baba, naomba mjue kuna kitu kinaendelea kati ya Junior na huyu dada humu ndani”“Kivipi?”Daima alianza kuelezea ilivyukuwa hadi simu ya Junior aliyopokea toka kwenye simu ya Vaileth, walishangaa na kumuangalia Vaileth, muda huo huo mama Angel alimshika mkono Vaileth na kumwambia,“Twende ukanipe simu yako niangalie”Vaileth alienda nae hadi ndani na mama Angel alichukua simu ya Vaileth ila hakuona hata namba ya Junior, basi alimuangalia Vaileth na kumuuliza,“Umefuta?”“Muda gani mama?”“Mbona ulichelewa kutoka wakati kuna kelele?”“Nilikuwa namlaza vizuri mtoto mama, sijafuta chochote hata nashangaa tu”Mama Angel alitoka tena nje na moja kwa moja kwenda kwa mlinzi na kumuuliza,“Eti Junior alikuja leo?”“Junior? Hapana, hajaja Junior leo”Moja kwa moja mama Angel alihisi kuwa Daima atakuwa na matatizo, alirudi na kumwambia mumewe amuache tu yeye na Daima,basi mumewe alienda zake chumbani kuendelea na usingizi, mama Angel alikaa kidogo na Daima na kumwambia,“Unampenda sana Junior eeeh!!”“Ndio nampenda sana”“Haya nenda kalale kwanza, halafuy kesho tutawasiliana vizuri”Basi mama Angel aliingia ndani na Daima na kufunga mlango vizuri maana alihisi kuwa Daima hayupo sawa kwenye kichwa chake.Kulipokucha, wakina Erick walijiandaa na kwenda shuleni yani wao hata hawakuelewa chochote kile ambacho kiliendelea usiku, basi mama Angel na baba Angel waliongea kidogo kuhusu Daima,“Naona tumrudishe kwa wazazi wake”“Hata mimi naona hivyo, tutawaita tu tuongee nao vizuri maana huyu ameanza kuchanganyikiwa jamani”“Ni kweli mke wangu, ngoja nijiandae niende kazini”“Badae nitakuja huko, leo nitakuletea chakula pia. Tafadhari usile popote pale nakuomba”“Naelewa mke wangu, siwezi kula sehemu yoyote ile”Baba Angel alijiandaa na kuondoka zake kuelekea kwenye kazi yake, muda huu mama Angel aliendelea na mambo mengine ila alichogundua siku hii ni kuwa Daima hakuweza hata kula alikuwa akilia tu kwa muda mwingi, basi alimfata kuongea nae,“Daima, tatizo ni nini jamani?”“Inaniuma sana, kuona Junior amenikana sababu ya huyu dada humu ndani na hakuna mtu anayenielewa. Huyu dada anatembea na Junior”“Unajua nini Daima, mara nyingine uwe na ushahidi na unachokiongea, tupo hapa na Vaileth toka mwaka jana, na tumeishi nae vizuri kabisa, hawezi kufanya ujinga kama huo. Hebu shusha presha au unataka tukurudishe kwenu?”“Hapana, msinirudishe nyumbani”“Haya, kula chakula basi”Yani Daima alienda kulak wa kujivuta vuta tu sababu hata hakutaka, mama Angel aliendelea na mambo mengine.Ila kuna simu ikaingia kwake, na alipopokea alikuwa ni mama yake na Derrick akimwambia kuwa hali ya afya ya Derrick imebadilika kwa muda huo,“Naomba mwanangu uje, hata sijui cha kufanya”“Ila madaktari si wapo kumuhudumia mama?”“Wapo ndio ila hali ya Derrick ni mbaya sana”“Sawa nakuja huko”Mama Angel ilibidi aweke mambo yake sawa na muda huo huo akajiandaa na kuondoka zake kuelekea hospitali.Kama ambavyo walipanga, Sarah na Elly walitoka shule muda huo ambapo Sarah ndio aliomba ruhusa na hawakuweza kumkatalia kwahiyo waliondoka na moja kwa moja Sarah alimtaka Elly waende nyumbani kwao na wakina Elly kwanza ili wakabadilishe nguo, basi walienda na Sarah alivaa nguo zingine alizozibeba kwenye begi, halafu Elly nae ikabidi abadilishe nguo na kuondoka na Sarah.Elly alikuwa akimuuliza Sarah,“Tunaenda wapi lakini?”“Ni mahali Fulani hivi, nataka nikachome sindano ya uzazi wa mpango, nahitaji waone kuwa mimi ni mkubwa maana nitawaambia kuwa wewe ni mdogo wangu. Halafu wewe useme umemaliza kidato cha nne sio kuniletea mambo yako ya kitoto toto”“Mmmh, sindano ya uzazi wa mpa ngo Sarah! Ili iweje?”“Ili iweje? Si ili nisipate mimba? Au unataka nipate mimba?”Elly alitulia na kuendelea na ile safari, na kweli walifika kwenye duka moja kubwa la madawa ambapo kwa upande wa duka hilo walikuwa wakitoa huduma hiyo, Sarah alijiandikisha kuwa ana miaka kumi na nane, na alimdanganya vitu vingi yule nesi,“Mara ya mwisho kuona siku zako ilikuwa lini?”“Aaaah ni juzi tu hapo”“Aaaah basi, hapo sawa”Basi yule nesi alimchoma sindano Sarah bila kuzingatia vitu vingine.Muda huu Elly alikuwa nje akihofia kiasi yani hakuelewa cha kufanya na kujikuta akiinuka na kuanza kuondoka.Mama Angel alifika hospitali na kuangalia hali ya Derrick kweli ilionekana kubadilika, na alikuta mama Derrick kuna dawa kaandikiwa kuwa akamnunulie Derrick, kwahiyo muda huo huo mama Derrick alimkabidhi mama Angel lile karatasi la dawa, basi mama Angel aliondoka na kwenda kununua hizo dawa.Alipotoka kununua dawa, alishangaa kumuona Elly, basi alimsimamisha na kumtaka aondoke nae, ambapo Elly alipanda kwenye gari ya mama Angel basi akaanza kumuuliza,“Muda huu wa masomo, wewe unafanya nini huku?”“Aaaah kuna rafiki yangu nilimsindikiza kununua dawa?”“Yuko wapi na anaumwa nini?”“Aaah….aaaah….hapana, ni mimi ndiop naumwa”“Mbona unajiuma uma sana”Elly alishindwa kumjibu mama Angel, walifika hospitali na mama Angel alisimamisha gari, ila alishuka na Elly kwani alijikuta kuwa na maswali mengi ya kumuhoji huyu kijana, alikumbuka alichokifanya Tumaini kwa Daima, kwahiyo aliona ni vyema na yeye kuuliza vizuri kuhusu elimu ya huyu kijana.Moja kwa moja aliingia nae kwenye wodi aliyolazwa Derrick na kusogea kwenye kitanda cha Derrick, ila Elly kwa ile hali ya Derrick aliyoiona ilimfanya asikitike sana na kujikuta akitoa machozi huku akimsogelea Derrick kitandani. Machozi ya Elly yalianguka kwenye kiganja cha mkono cha Derrick cha kushangaza Derrick alifumbua macho na kutabasamu. Moja kwa moja aliingia nae kwenye wodi aliyolazwa Derrick na kusogea kwenye kitanda cha Derrick, ila Elly kwa ile hali ya Derrick aliyoiona ilimfanya asikitike sana na kujikuta akitoa machozi huku akimsogelea Derrick kitandani. Machozi ya Elly yalianguka kwenye kiganja cha mkono cha Derrick cha kushangaza Derrick alifumbua macho na kutabasamu.Na muda huo huo Derrick aliyekuwa akihangaika mwanzoni pale kitandani aliweza kukaa halafu akamkumbatia Elly, yani kila mtu alikuwa akishangaa pale kuwa ni kitu gani, Derrick alimkumbatia Elly huku machozi yakionekana kumtoka tena yalikuwa ni machozi ya furaha maana yalimtoka huku akicheka, mama Derrick pamoja na mama Angel walikuwa pembeni tu wakishangaa kile ambacho kimetokea.Kisha Derrick alikaa vizuri pale kitandani sasa yani kwa kuishusha miguu yake chini huku akimtaka Elly akae pembeni yake ambapo Elly alifanya hivyo.Mama Derrick aliamua kumuuliza Derrick,“Nini kimekutokea mwanangu?”“Mama, kwa hakika nimepona kabisa”“Inaonekana kweli umepona ila nini kimekutokea?”Muda huo alifika daktari pia aliyekuwa akishangaa kuona hali ya Derrick ikiwa imetengemaa vile, na Derrick aliomba aandikiwe ruhusa aende nyumbani, basi daktari alijaribu kumuangalia kidogo pale hakuona kama ana tatizo lolote, kwahiyo alimuandikia tu ruhusa, na muda huo Derrick aliomba waondoke wakiwa wameongozana na Elly.Basi mama Angel ikabidi ndio awarudishe nyumbani kwakina Derrick sababu bado alikuwa akijiuliza sana ni kitu gani kimetokea baina ya Derrick na yule mtoto Elly? Hakuelewa kabisa.Waliondoka hadi nyumbani, ila muda wote Derrick alionekana akimuangalia sana Elly, mpaka wanaingia ndani hakuna aliyekuwa anamuelewa Derrick, ila kabla ya yote walipoingia tu mama Derrick alihitahi kujua kilichokuwa kimetokea, ni kweli kafurahi kwa mwanae kupona, ila alitaka kujua ni kitu gani kimetokea, basi Derrick aliakaa na kuanza kuwaambia,“Nilikuwa naumwa sana, nilikuwa na hali mbaya sana ila muda wote niliokuwa kitandani nilikuwa naletewa picha ya huyu mtoto, yani ndio picha halisi iliyokuwa ikinijia, kuna muda nilipata ndoto kuwa atafika na kuangusha machozi yake kwenye kiganja changu. Sijawahi kumuona huyu mtoto, ila nazungumza kwa uhakika kabisa, huyu ni mwanangu, sijui mama yake kama ni Oliva au Manka ila huyu ni mwanangu”Mama Derrick na mama Angel waliangaliana bila ya majibu, kisha mama Derrick alimuuliza mama Angel,“Kwani wewe umemtoa wapi huyu mtoto?”“Namfahamu huyu, tena namfahamu vizuri sana, sasa leo nilikuta mahali na ni muda wa shule ndiomana nikamchukua kuongozana nae ili nimuulize kwanini hayupo shule na ni muda wa shule? Maana nilijifunza kitu mtoto wa mwenzio ni mtoto wako pia, kwahiyo nilitaka nimuhoji vizuri sababu namfahamu”Kisha mama Angel alimuangalia Derrick na kumwambia,“Ila mbona huyu mtoto sio wa Oliva wala wa Manka, ni wa mtu mwingine kabisa”“Sijali, ila ninachojua ni kuwa huyu ni mwanangu”Derrick alimuangalia Elly na kumuuliza,“Kwani baba yako mzazi yuko wapi? Na kwanini ulitoa machozi kwangu pengine hiyo itasaidia hawa kuamini kuwa wewe ni mwanangu”Yani Elly alikuwa kama kapigwa na butwaa vile, basi akasema,“Mimi sina baba, mama aliniambia kuwa baba alikimbia kipindi nimezaliwa tu. Halafu mimi nilipokuona sijui hata imekuwaje ila nilijikuta tu nikitokwa na machozi na kukusogelea karibu”“Unaona? Wewe ni mwanangu, hata mama yako anatakiwa atambue kuwa wewe ni mwanangu, mwambie mama yako kuwa nimemuona baba yangu”Mama Angel akapumua kidogo na kumuuliza Derrick,“Unamjua mama wa huyu mtoto lakini?”“Hata awe nani lakini huyu ni mwanangu, na nimefurahi kumuona kabla ya kifo changu. Naomba mtoto kwa leo au kesho uniletee mama yako hapa nimfahamu”Mama Angel alishindwa kabisa kuongea na muda huo akamwambia Elly kuwa aondoke nae tu waende kwa huyo mama yake ili kumueleza yaliyojiri, yani Derrick hakutamani hata yule mtoto aondoke, na alimuomba mama Angel amletee tena yule mtoto kwani ni mtoto wake, kwakweli mama Angel hakuwa na usemi zaidi kwani alihisi huenda Derrick ameanza kuchanganyikiwa.Basi mama Angel aliondoka na Elly na moja kwa moja walienda nae kwenye biashara ya Sia, kwakweli Sia alishangaa kumuona mama Angel yupo pamoja na Elly basi aliwafata na kumwambia mama Angel,“Naona sasa umekubali kuwa Elly ni damu yenu?”“Dah! Wewe jamani, kumbe huyu Elly ni mtoto wa Derrick”“Wa Derrick kivipi? Kwanza Derrick gani?”“Yule ndugu yangu”“Yule tapeli? Mimi nikazae na tapeli nina kichaa au ni kitu gani?”Mama Angel akamueleza vile ilivyokuwa hadi kusema kuwa Elly ni mtoto wa Derrick, hata ile habari Sia nae ilimchanganya kidogo ila akasema,“Haiwezekani hiyo, tena haiwezekani kabisa, huyu mtoto sio wa huyo tapeli ila ngoja nifanye uchunguzi wangu”Mama Angel alimuangalia kisha akamuangalia Elly na kumwambia,“Natumai unatufahamu ndugu zako sasa, unafahamu wazi baba yako alipo”Halafu mama Angel aliondoka zake na kumuacha Sia akiwa na mawazo mengi sana.Muda huu nyumbani kwa mama Angel kulikuwa na mzozo kati ya Vaileth na Daima maana Daima hakutaka kukubali kwakweli, aliona ni wazi kuwa Vaileth anatembea na Junior halafu anajigelesha, basi alimfata alipokuwa na kuanza kumwambia kwa shari kamavile anataka kupambana nae,“Mwanamke mtu mzima kama wewe huoni haya kutembea na mtoto mdogo kama Junior”“Kutembea nae kwenda wapi?”“Unajifanya huelewi au? Unaweza kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Junior? Wadanganye wengine humu ndani ila sio mimi niliyeona simu yako”Daima aliongea sana kama kumkujeli Vaileth, ndipo Vaileth alipomwambia,“Unajua Daima, wewe ni mdogo sana kwangu halafu ukizingatia na hiyo mimba unatakiwa utulie na ulee mimba usubirie kuzaa. Halafu kuhusu mimi kuwa na mahusiano na Junior kwani wewe inakusumbua nini ikiwa Junior alitamka mbele ya watu wote hapa kuwa hakutaki tena!! Halafu mimi na mwanamke, na Junior ni mwanaume kwahiyo tukiwa pamoja tatizo ni kitu gani?”“Hivi una akili timamu wewe mdada au umepagawa, yani unajisifia kabisa na uanaona sawa kwa wewe kutembea na Junior?”“Sioni tatizo ndio”Daima akachukia sana na kumvamia Vaileth mwilini maana alitaka kupigana nae, kwa bahati nzuri mama Angel nae alikuwa karidi muda huo na kuwaamulia huku akimsema Vaileth,“Jamani Vai, wewe ni mkubwa wa kutosha tu. Hivi ukapigana na mtu kama Daima kweli?”“Mama, mimi sikuwa nikipigana nae ila ni yeye ndio alikuja kunivaa mimi.”“Tatizo ni nini kwani?”Mama Angel akawakalisha chini ili wamuelezee tatizo ni nini hadi kupelekea wao kupigana namna ile, Daima alianza kuelezea,“Mama, nadhani ile usiku hamkunielewa. Nampenda sana Junior, ni kweli hii mimba ni ya Junior ila Junior kanikataa mimi sababu ya huyo mdada huyo, huyu Vai ana mahusiano na Junior na kwangu kakubali wazi kabisa”Mama Angel akamuangalia Vaileth na kumuuliza,“Eti Vai ni ya kweli haya?”“Mama, hata mimi nabaki kushangaa tu hapa, sijui huyu msichana ana matatizo gani jamani yani sielewi kabisa, Junior alikuwepo hapa siku zote kama kuwa nae si ningekuwa nae jamani! Mimi sina mahusiano na Junior”Daima akadakia,“Sema ulichokuwa ukiniambia mimi kuwa Junior ni mwanaume na wewe ni mwanamke kwahiyo lazima muwe pamoja”Basi mama Angel akawaambia,“Sitaki mzozo jamani, sitaki mzozo kabisa. Muda umeenda sasa ila nadhani kabla ya muda wa kulala kufika tutakuwa tumepata suluhisho, ila sitaki mzozo wowote kuendelea”Basi moja kwa moja, mama Angel aliinuka na kwenda chumbani kwake tu kwa muda huo.Mama Angel aliingia chumbani kwake yani kwa matukio ya siku hiyo alijikuta kichwa chake kikiwa kimejawa mawazo tu yasiyokuwa na majibu mwanzo hadi mwisho, kwanza alifikiria kuhusu mtoto Elly, akafikiria kuhusu Sia akidai kuwa Erick ni mwanae, pia akafikiria yaliyotokea kwa Derrick siku hii,“Mmmh hivi Sia hakuwa na mahusiano na Derrick kweli, nina mashaka nae maana hata haeleweki”Muda kidogo baba Angel nae alirudi kutoka kazini na kumkuta mke wake pale nyumbani, basi alimuuliza ni kwanini hakwenda kazini kwake siku hiyo, mama Angel alimsimulia yote ambayo yametokea siku hii, yani baba Angel alibaki akistaajabu na kushangaa sana,“Kwahiyo Derrick amepona baada ya kumuona Elly”“Ndio hivyo”“Halafu Derrick anadai kuwa Elly ni mtoto wake?”“Yani hapo ndio kwenye utata maana Sia anakataa katakata kuwa kwenye mahusiano na Derrick, sasa ni kivipi Derrick adai kuwa Elly ni mtoto wake?”“Ila mke wangu nawe umesahau akili za Sia zilivyo? Anaweza kukataa kumbe kweli, na ukweli wote utakuta anaujua kuwa alikuwa na mahusiano na Derrick hadi kumzaa Elly, hivi unasahau alivyokuwa anazusha hapa kuwa Erick ni mwanae! Tena anakomaa kabisa na kukazana hadi mtoto akakosa imani na raha, akamaliza hayo akaanza kukazana kuwa Elly ni mtoto wangu hadi kwa mama habari ilifika, yule Sia ni mgonjwa wa akili kwahiyo usimuamini moja kwa moja, kuna uwezekano mkubwa kabisa kuwa alizaa na Derrick”“Je Steve ni vipi?”“Mke wangu, yule Sia haeleweki ujue, ukimuwaza sana utapata kichaa bure, cha muhimu siku tumshikilie na atuambie ukweli. Ila kama Derrick anasema yule ni mtoto wake huenda ikawa kweli, ujue damu ni nzito kuliko maji eeeh! Ndiomana huyo Elly na Derrick wamejikuta tu wameweza kuungana, hizo habari tuziache kwanza ila tutajua tu ukweli wa mambo”“Sawa, mume wangu sasa kuhusu Daima ndio kuna balaa”“Kafanyaje tena”Mama Angel akamsimulia jinsi ambavyo alikuwa akitaka kupigana na Vaileth,“Khaaa huo ni ujinga, tena ni ujinga sana hebu wapigie simu wazazi wake waje wachukue mzoga wao, anataka mimba imtoke hapa halafu iweje kwetu!”“Ndio hapo sasa”Basi mama Angel alichukua simu na moja kwa moja alimpigia baba Daima ila aliyepokea simu alikuwa ni mama Daima, alisalimiana nae na kuongea nae,“Samahani, huyu mtoto wenu mje mumchukue maana hapa anataka kuleta balaa, au kama hamuwezi kuja basi mimi nimlete”“Aaaah usimlete kwanza, ngoja baba yake atawapigia simu akirudi. Siwezi sema chochote, baba yake ndio ataamua kitu gani kiendelee”“Mmmh haya”Mama Angel alikata ile simu na kuongea kidogo na mume wake, kisha kumwambia kuwa anaenda kumuandalia chakula kwa muda huo.“Unajua nataka chakula gani leo?”“Eeeh nikuandalie nini?”“Usisumbuke sana mke wangu, niandalie tu ugali na samaki, nitafurahi sana kwani sijala siku nyingi chakula hiki”Basi mama Angel alienda kuandaa kile chakula, na kilivyoiva walikaa wote mezani na kula kile chakula, kasoro Daima hakutaka chakula kile kwahiyo alipika anachokipenda na kukaa pale kuanza kula, hawakuwa na tatizo nae sana kwani wanaelewa jinsi gani mimba zinavyosumbua, ila yeye mwenyewe alianza kusema,“Nikiwa mzima tu huwa sipendi kula ugali na huwa siupendi kabisa ugali, halafu na hali hii ndio nikale ugali kweli!! Hapana aisee hiko chakula sikipendi kabisa”“Kwanini hupendi ugali?”“Huwa nakiona kama ni chakula cha kimasikini, yani mimi hakinipi ladha kabisa”Mama Angel hakumuhoji zaidi kwani yale majibu yalimtosha kabisa na kumfanya asiendelee kumuhoji.Walimaliza kula, na kila mmoja kwenda moja kwa moja kwenye vymba vyao vya kulala tu.Usiku ule kwakweli Vaileth alishindwa hata kulala mule chumbani kwani kidogo tu alikuwa akitupiwa maneno na Daima, yani aliona kama ule usiku ni mbaya sana kwake, na hakuweza kubishana na Daima kwavile alihofia ile hali ya mimba aliyokuwa nayo.Basi Vaileth kwa kuepusha shari, kwa muda huo aliamua kwenda tu sebleni na alilala sebleni kwa siku hiyo. Aliamka mapema sana na kuanza usafi kwani hakutaka wajue kuwa alilala sebleni kwa siku hiyo, yani kwakweli uwepo wa Daima ulikuwa ukimkosesha raha kabisa na alijikuta hana furaha hata kidogo.Wakina Erica walitoka pale na kwenda shule kama kawaida, baba Angel nae alitoka ila siku hii alimwambia mkewe kuwa asimpelekee chakula sababu atawahi kurudi nyumbani tu.Kwahiyo mama Angel alikaa tu nyumbani, ila akakumbuka kitu kuwa mama Daima alisema kuwa baba Daima angepiga simu usiku wa jana ila hakupiga simu kabisa, basi aliamua tena kuchukua simu asubuhi ile na kuwapigia,“Inamaana hukunielewa au kitu gani? Huyu mtoto wenu inatakiwa arudi kwenu kama mimba tutalea huko huko akiwa kwenu”“Si nilikwambia baba yake atakupigia simu!”“Hakupiga sasa”“Basi subiri tu atakupigia tu, kwani unaharaka na kitu gani jamani!”Mama Daima alikata simu, kwakweli mama Angel alichukia sana kwa majibu ya mama Daima kwani walionekana ni watu wasiojali kabisa.Leo baba Angel alitoka mapema kazini kwake kama alivyopanga ila kabla ya kwenda nyumbani aliamua kwenda kupitia mahali kumchukulia mke wake zawadi, basi aliamua moja kwa moja kwenda katika lile duka ambalo huwa anamnunulia zawadi mama Angel ila leo alikuwepo mama Emma tu, kwani mumewe hakluwepo,“Kheee jamani, ukatukimbia kabisa”“Aaah nilisafiri ndiomana sikuonekana, na mumeo yuko wapi?”“Nae kasafiri, hata hayupo wala nini”“Aaaah kumbe!!”“Nimekuja kumchukulia mke wangu zawadi tena leo”“Nitamchagulia zawadi nzuri kabisa, na hakika ataipenda sana”Basi mama Emma alimchagulia viatu, na baba Angel alipoviangalia aliona kweli ni vzuri na vitamfaa mke wake, moja kwa moja akakubali kufungiwa viatu vile na kurudi navyo nyumbani.Alifika pale na kula kwanza, halafu alipoingia chumbani akamwambia mke wake,“Leo nataka usiku tutoke, tutaenda kula pamoja chakula cha usiku hotelini”“Familia nzima?”“Familia nzima ya kazi gani? Hii ni mimi na wewe tu mke wangu, hii ni kwaajili yetu tu. Natamani sana tuwe tunakumbuka mapenzi yetu siku zote za maisha yetu”Mama Angel alifurahi sana, ilivyofika jioni wakati watoto wamerudi, alienda kuongea na Erica kwaajili ya kumuachioa mtoto na baada ya hapo alimuandalia mtoto maziwa na kila kitu kisha alienda kujiandaa, ila alipomaliza kujiandaa ndipo mumewe akamtolea vile viatu, basi mama Angel alifurahi na kumshukuru mumewe pale halafu akavijaribisha na kutembea navyo kidogo tu, mumewe akamwambia,“Hivyo viatu ndio utavivaa tunapotoka leo”“Mmmh mume wangu, naomba unisamehe ila viatu hivi vinanibana”“Vinakubana? Mbona ni namba yako kabisa hii!”“Hata mimi nashangaa mume wangu, ila vinanibana”Basi baba Angel hakutaka kumlazimisha mkewe kuvaa viatu vinavyombana, zaidi zaidi alimchagulia viatu vingine na akavivaa viatu hivyo na kufurahi kwa pamoja tu.Kwenye mida ya saa moja usiku, mama Angel na baba Angel walitoka zao na kuwaacha pale nyumbani, wenyewe moja kwa moja walienda kwenye hoteli na kuanza kuongea kidogo kisha waliagiza chakula na kuanza kula huku wakiongea,“Huoni raha mke wangu, tukipata muda kidogo na kutoka kuja sehemu kama hii tukiongea na kukumbuka mapenzi yetu yalivyokuwa”“Huwa nafurahi sana, sababu sisi tunapendana kila siku, tunaletewa chokochoko, maneno mbalimbali ila bado tunapendana kwakweli Mungu ni mwema sana katika maisha yetu na anatufanya tuzdidi kupendana sana”“Ndio, sio sababu tuna watoto basi muda wote ni kukaa nyumbani na watoto, muda mwingine tunakuwa peke yetu kama hivi, tunazidi kuweka mapenzi yetu kwenye viwango vingine”Basi wakati wanaendelea na maongezi, simu ya mama Angel iliita na kuangalia mpigaji alikuwa ni baba Daima, basi alipokea na kuanza kuongea nae,“Nimepata habari mnasema kuwa tuje kumchukua mtoto wetu?”“Ndio mje mumchukue Daima, kwakweli siwezi kuendelea kuishi nae nyumbani”“Hilo haliwezekani kabisa, yule mtoto kapewa mimba na kijana wenu. Tumejadiliana hapa kama familia tunasema kuwa hilo haliwezekani yani tunachongoja hapa ni nyie kuleta posa na kumchukua jumla”“Hivi una akili kweli?”“Ndio nina akili kwani unadhani mimi ni chizi”“Unajua kama unaongea kama unatapika, huyu ni mtoto wenu”“Kuongea kama kutapika ndio kuongea vipi? Ni mtoto wetu ndio ila kapewa mimba na kijana wenu, au tufungue kesi na kijana wenu aende miaka thelathini jela”“Kwa uanafunzi gani aliokuwa nao Daima? Yani ajineng’eneshe huko halafu useme utamfunga kijana wetu miaka thelathini jela, fungua hiyo kesi ila uje kuchukua mtoto wako huku”“Siji kumchukua, na tunasubiri posa tu. Huyu kijana wenu atake atamuoa Daima, asitake atamuoa Daima, mimi sio kama wazazi wengine ambao watoto wao wanazalishwa na vidume halafu wao wanatulia tu. Huyo mtoto mtaoa mtake msitake”“Ndiomana nikakuuliza una akili kweli wewe?”“Nisingekuwa na akili ungeweza kukubali niwe mwanaume wako wa kwanza”Hii kauli ilimshtua baba Angel maana simu ilikuwa kwa sauti kubwa, baba Angel alichukua ile simu na kumwambia baba Daima,“Naona unataka kunipanda kichwani sasa, kwaheri”Akakata ile simu na kumwambia mkewe,“Ujinga wa namna hii huwa siupendi kabisa, haya ni matztizo kabisa ujue, ukoo hausogei yani unazunguka hapo hapo, inakuwaje huyu Junior akatembee na mdada ambaye ni mtoto wa mtu wako wa zamani! Yani ukoo hausogei mwisho wa siku tunapata matatizo tu”“Nisamehe kwa hilo, ila ukoo wetu hausogei toka mwanzo, fikiria mimi nimeoana na wewe, Tumaini kaolewa na Tonyo wakati huo Tumaini ni dada yako upande wa baba halafu Tony ni kaka yangu, tunakuja upande wa Dada Bite, kaolewa na Deo. Wakati Deo ni kaka wa Tumaini kwa mama yake halafu Dada Bite ni dada yangu, yani ukoo hausogei kweli hata ukienda kushtaki unaenda kushtaki wapi ikiwa kila mmoja atajifanya anakufahamu sana”“Ni muda wa kusogeza ukoo wetu, huyu Daima tunamfuta kwani kubeba mimba ni kitu gani? Wangapi wanazalia kwao huko? Kama kweli mtoto wetu tutalea kama si kweli watalea wenyewe, ila Daima wao tunamrudishia”“Ila weka akilini kuwa inasemekana Junior ana mahusiano na Vaileth, kama ni kweli je inakuwaje? Utawabariki waoane?”“Aaaah watajijua wenyewe, ila hata hivyo Vaileth si wa ukoo wetu. Yani habari za huyo baba Daima zimenichanganya kidogo, kwani si ndio ndugu wa Rahim huyo? Nakumbuka vizuri sana”Mama Angel aliangalia chini na kuamua kubadilisha mada ingawa baba Angel alikazana na msimamo wake kuwa atakaporudi nyumbani kwake basi atamrudisha Daima kwao.

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog