Simulizi : Kurudi Kwa Moza Sehemu Ya Nne
(4) Doto alimuangalia Salome kwa hasira sana kwani
alionekana ni msichana mdogo ila aliyekuwa na amri zaidi, ila bado alikuwa
hajielewi elewi hata alivyorudishwa nyumbani na kumuuliza swali Salome bado
hakuelewa kabisa, akataka kutoka tena nje ila kabla hajatoka akamuona mama yake
akiwa na Ana wakija kwa kasi sana na wameshika sufuria la maji ya moto na
kummwagia Salome, ila muda huo huo alishangaa kuona kuwa yale maji kumbe alikuwa
anamwagiwa yeye na sio Salome, alijikuta akipiga kelele za maumivu. Rose
na Ana walistaajabu pia kwani hakuna aliyedhania kuwa yale maji yangemmwagikia
Doto, kitendo cha Doto kupiga kelele kiliwafanya watupe sufuria na kwenda
kumshikilia hata Sara na ndugu yake Kulwa walikuja kwa kasi ya ajabu kwani
kelele za Doto ziliwashtua hadi mlinzi getini aliingia ndani kuona kuna nini
tena maana zile kelele hazikuwa za kawaida. Sara alimkuta mama yake amemshikilia
Doto huku nae analia pia, Sara akauliza “Kuna nini?” “Nenda
kachukue funguo ya gari tumpeleke Doto hospitali” Sara akaenda chumbani
kwa mama yake kuchukua funguo kisha kurudi nazo, ambapo mama yake aliwaomba
wasaidiane kumkokota Doto mpaka kwenye gari ili wampeleke hospitali. Wakati huo
Salome alikuwa pembeni tu kanakwamba haoni tukio linalotokea ila alikuwepo na
alikuwa akiwaangalia tu, walimpakiza Doto kwenye gari kisha nyumba nzima
wakaenda kumpeleka hospitali kasoro Salome na mlinzi ambaye anabaki kulinda
nyumba. Walipoondoka, huyu mlinzi alimshangaa sana Salome na kumfata
kumuuliza, “Mbona unaonekana hujali kabisa! Utafikiri kitu hakijatokea
ndani, yani kama mtu ambaye hujui kinachoendelea” “Ulitaka
nifanyeje” “Yani huonyeshi kujali kabisa, wenzio wote wameenda hospitali
kasoro wewe” “Mbona na wewe hujaenda?” “Mimi ni
mlinzi” “Ila unajua kwamba mimi naweza kufika hospitali kabla yao? Ila
wale hawaendi hospitali kwasasa” “Wanaenda wapi?” “Wakirudi
watakwambia walipoenda” “Unajua wewe sikuelewi toka siku umefika
hapa” “Na kamwe hutokaa unielewe” Kisha mlinzi akaamua kwenda
kuendelea na kazi yake kwani kiukweli hakumuelewa kabisa Salome na muda wote
alimuona kama mtu wa ajabu. Wakiwa ndani ya gari kwenda
hospitali, walienda mwendo mrefu sana na kuona hospitali kisha wakashuka ila
wakashangaa tena hapakuwa hospitali ila ni kwa mganga. Rose alikumbuka kuwa huyo
ndiye mganga aliyekuwa akizungumza na Ana kuwa ataenda kwa huyo, watoto wake
walimuuliza kwa mshangao, “Mama vipi tena, mbona hapa sio hospitali?
Panaonyesha ni kwa mganga” “Hata mimi mwenyewe sielewi tumefikaje hapa,
ila nadhani ni Mungu katuleta kwani mganga huyu nilikuwa namuhitaji sana bora
tuingie tu” Ana alimuangalia mama yake na kumtahadhalisha, “Mama
tulisema tunampeleka kaka hospitali, ila hatukukubaliana kumleta kwa mganga.
Sidhani kama tupo sehemu sahihi” “Mwanangu Ana, usiwe na mashaka. Acheni
mimi niingie kwa mganga maana huu ni uchawi aliofanyiwa Doto” “Ila mama
kumbuka kuwa yale maji tuliyopanga kuyamwaga hayakuwa ya kichawi, tunamuumiza
Doto ujue, bora tumpeleke hospitali” Hapa ndio wengine wote wakaelewa
kuwa mama yao na Ana wanafanyaga uchawi ndiomana wamesema maji waliyoyamwaga
hayakuwa ya uchawi. Rose alikuwa mbishi sana, kwavile tayari alishafika kwa
mganga kwahiyo aliona ni vyema kuingia kwa mganga na kuzungumza
nae. Rose alivyoingia kwa mganga, Ana akawapa ushauri ndugu zake kuwa
wampeleke Doto hospitali kwakweli hata wao walishangaa sana kuwa moyo wa Ana
umebadilika kiasi kile, Kulwa aliingia kwenye gari kisha wote kupanda kwenye
gari na kuanza kuulizia kwa watu waliowaona pale njia ya kuelekea barabara kuu
na kuulizia hospitali. Rose hakujua kama amebaki mwenyewe kwa Yule
mganga, kisha akaanza kumueleza matatizo yake, “Yani hapa nilipo,
mwanangu kaungua na maji mwili mzima. Naomba unisaidie, ni kweli maji
nimemmwagia mwenyewe ila lengo langu ilikuwa ni kummwagia mtu mwingine ila eti
akamwagikiwa yeye, si nifanyiwa mambo yasiyofaa hayo babu” “Sikia Rose,
unajua kwamba wewe ndio chanzo cha wale waganga wawili waliokufa, yani wote
walitaka kukusaidia wewe wakafa. Sasa umekuja na kwangu unataka kunimaliza na
mimi!” “Hapana, ila nahitaji maisha yangu yarudi kama zamani. Nahitaji
kufurahia tena maisha, ona mume wangu hataki hata kuniona na hata sijui akija
siku na hasira zake atanifanya nini, dawa zangu hazifanyiki. Nyumba yangu ila
siwezi kufanya chochote utafikiri sio nyumba yangu” “Kwanza niambie
umefikaje leo hapa” Rose akamuelezea kwa kifupi kuwa walikuwa
wakimpeleka mwanae hospitali ila wakashangaa wamefika hapo, “Hata
hukugundua kuwa umebadilishiwa njia, badala ya kwenda hospitali ukaja huku! Na
kama ameweza kukubadilishia njia huyo mtu basi ujue kuwa anauwezo wa kuzunguka
na wewe kila mahali, kwahiyo tunaweza tukapanga dawa mimi na wewe ila akawa
ameshatusikiliza yote. Huyo mtu lazima anajua kuwa unapenda sana waganga
ndiomana amekuleta kwangu kwa makusudi kabisa” “Babu, nahitaji kujua ni
mtu gani huyo anayenifanyia vitu hivi?” “Mfano ukishamjua,
utafanyaje?” “Tumshughulikie” Basi Yule babu akaanza kupiga
ramli zake kwa muda kidogo kisha akatulia na kumwambia, “Siwezi
kukwambia nimekatazwa” “Jamani babu, umekatazwa na nani?” “Sikia
Rose nikwambie kwa usalama wako, rudi nyumbani kwako na ukiona kuna mtu nyumbani
kwako anakuelekeza sana basi fatilia anachokiataka mtu huyo” “Mtu
anayependa kunifatilia nyumbani siku hizi ni mmoja tu, na tangu amefika nyumbani
kwangu ndio mambo yamebadilika simpendi hata kidogo ila sidhani kama ana nguvu
za kichawi kiasi kwamba aniumize mimi” “Kwanza unajua kama muda umeenda
sana, na usiku umeingia. Huwa sifanyi kazi usiku ila alfajiri ndio muda mzuri
kwangu” “Kwahiyo unanishauri nije kesho” “Ndio njoo
kesho” “Bora nilale hapa hapa na wanagu ili niwahi kesho” Rose
hakuwa na wazo la haraka haraka kuwa Doto anahitajika hospitali kwani alichowaza
yeye ni kutibiwa na mganga tu. Basi akatoka nje ili akawaambie watoto
wake ujumbe wa mganga ila hakuwakuta, alishtuka sana kwani hata gari hakuikuta
na vitu vyake vyote aliviacha kwenye gari. Akarudi tena kwa mganga, ila mganga
alimshauri alale hapo hadi asubuhi ili waangalie watoto wako wapi, Rose hakuwa
na namna zaidi ya kukubali tu. Neema nae alifika usiku na
familia yake yani wale watoto wake mapacha, akiwa amechoka sana ila alikuta
ndani kwake kama kuna mtu na kuhisi ni Salome, kisha akagonga mlango na kweli
Salome alienda kuwafungulia na kuwapokea huku akionyesha tabasamu zito sana.
Neema alikaa na kuzungumza na mwanae, “Hukuondoka kabisa nini toka siku
ile?” “Niliondoka mama” “Sasa umejuaje kama leo ndio
narudi?” “Sikujua ila huwa narudi kila jioni, halafu nikahisi kama
mnarudi vile ndiomana nikapika kabisa” Neema alitulia tu ila huyu Salome
wake wa kipindi hiki alikuwa akimshangaza sana, kwanza Salome wake ni muoga ila
kaweza kulala hapo nyumbani kwa siku zote alizokuwa safarini, halafu Salome wake
alikuwa mvivu ila huyu kazi zote anafanya, kama hapo kawapikia kabisa kwahiyo
walienda kujimwagia maji tu na kula huku akimpa salamu Salome za kutoka kwa bibi
zake na ndugu zake wengine, “Ila wamekukumbuka, haswaaa bibi yako
anaomba uende ukamsalimie” “Nitaenda tu hata wasijali” “Ila
mwanangu umebadilika sana” “Kwanini mama?” “Ulikuwa mvivu sana
zamani, yani kama leo ningekuta hujafanya chochote. Halafu ulikuwa muoga sana
yani ningekuta umeenda kuishi kwa marafiki huko” “Nimekuwa
mama” “Amakweli umekuwa sasa” Aliongea ongea nae kisha akamuaga
na kwenda kupumzika huku wadogo zake Salome wakiwa wamelala muda tu walipomaliza
kula kutokana na uchovu wa siku hiyo. Basi Salome nae akaenda chumbani kwake,
kwahiyo ilijulikana kuwa nae amelala. Kwenye mida ya saa tano
usiku ndio Sara, Ana na Kulwa walirudi nyumbani na kumuacha Doto akiwa amelazwa
hospitali, kwahiyo walifika wakiwa wamechoka sana. Mlinzi aliwauliza kuwa
imekuwaje huko hospitali, “Amelazwa, ni ameumia sana” “Eti
Salome alisema hamuendi hospitali” Ana akauliza, “Yeye Salome
yuko wapi yani huyo msichana ni nuksi tena nuksi kabisa. Ni kweli hospitali
tumeenda badae maana mwanzoni tulijikuta kwa mganga. Hivi wewe unamuonaje huyu
Salome, kwanza yupo?” “Hayupo, ametoka” “Basi nitakuja tuongee
vizuri” Mlinzi alishangaa sana kwa Ana kuongea vizuri vile na yeye
kitendo hicho kilimshangaza sana ingawa mambo ya Salome ndio yalikuwa
yanamshangaza zaidi. Waliingia ndani huku wakiamini kwa
vyovyote vile mama yao amebaki kwa Yule mganga, walitamani kumuuliza Ana ila
walimuogopa maana ana muda wake wa kubadilikia watu. Ana aliwaacha ndugu
zake ndani na kutoka tena kwenda kuongea na mlinzi wao. “Hebu niambie,
kwanza wewe unamuonaje huyu Salome!” “Kwakweli sijui nisemaje ila
simuelewi yani huwa simuelewi kabisa kabisa” “Unahisi anaweza akawa ni
mchawi?” “Inawezekana maana haeleweki kabisa. Na mama mmemuacha
wapi?” “Yani habari ya mama sijui tukuelezeje ila kwa kifupi amebaki kwa
mganga. Hivi mtu akitaka kuacha uchawi anafanyaje? Anaenda kwa mganga kutolewa
au anafanyaje?” “Kwa mganga ni kuuzidisha uchawi sijui sasa mtu
anawezaje kuacha uchawi, unataka kumpeleka Salome?” “Hapana, kuna jambo
nataka kulifanya. Utalijua tu” Kisha Ana akarudi tena ndani na kuwaona
dada yake na kaka yake pale wakijadiliana na kukubaliana kesho wawahi hospitali
kisha waende kumchukua mama yao maana hakuna aliyejua kuwa mama yao atarudije
ila kitu pekee walichojua ni kuwa yupo kwa mganga wa kienyeji. “Sasa
basi tuchemshe chai tunywe tu na ile mikate tuliyonunua” “Ndio tufanye
hivyo hakuna namna” Kwahiyo Sara akaenda kuandaa chai ili waweze
kunywa. Mishi akiwa ndani kwao, mara alijiwa na rafiki yake ule
usiku, ikabidi atoke kumsikiliza, “Mmmh mbona usiku sana, saa sita
kasoro hii!” “Ni usiku kweli ila sijaweza kulala na habari
hii” “Habari gani?” “Leo nilikuwa hospitali kumuona ndugu yangu,
gafla nikaona kuna mgonjwa analetwa na ameungua vibaya vibaya ndio wametoka
kumfunga funga mabandeji na kumpaka dawa, kila mtu kashikwa na huruma pale,
ikabidi nimsogelee kumpa pole. Jamani ni Doto Yule mpenzi wako” Mishi
akashangaa sana na kumuuliza rafiki yake, “Una uhakika ni
Doto?” “Ndio ni Doto maana nilisikia ndugu zake wakimuita
Doto” Mishi alikaa kimya kwa muda kwanza kwani tukio la Doto
lilimshangaza toka muda alikuja kuongea nae, akakumbuka kuwa alienda pale
kuongea nae ila alitaka kumpiga kibao na mara hakumuona huyo Doto mwenyewe
halafu muda huu anapata habari kuwa Doto ameungua na maji ya moto haikumuingia
akilini kabisa. “Au Doto amekufa, aliyekuja kwangu huku ni
mzimu!” “Hapana hajafa bhana, ni mzima ila ameungua
sana” “Unajua watu kufa huwa wanachelewa chelewa kidogo, usikute amekufa
anangoja tu muda wa kufa kabisa hapo” “Kwanini unasema atakuwa
amekufa?” “Sababu Doto alikuja kuongea na mimi jioni jioni hivi na
akataka kunipiga mara gafla akatoweka hata
nikaogopa” “Alitoweka?” “Ndio
alitoweka” “Alitowekaje?” “Hata sijui nikuelezee kwa namna gani
ila alitoweka” “Inawezekanaje mtu atoweke jamani? Mbona haiwezekani au
ulikuwa unaota Mishi! Na kwanini alitaka kukupiga?” “Hakuna kitu bhana,
ila endelea kushangaa kutoweka kwake” Mishi akainuka pale ila cha
kushangaza alitokea kwenye sebule ya kina Doto, na pale sebleni alikuwepo Kulwa,
Sara na Ana wakinywa chai kwahiyo nao wakapatwa na mshtuko kumuona ndani
kwao. Mishi akainuka pale ila cha kushangaza alitokea
kwenye sebule ya kina Doto, na pale sebleni alikuwepo Kulwa, Sara na Ana
wakinywa chai kwahiyo nao wakapatwa na mshtuko kumuona ndani
kwao. Wakainuka wote kwa mshangao na kutaka kumfata ila Mishi akaanza
kutafuta sehemu ya kutokea na bahati akauona mlango wa kutoka nje na kufungua
akakimbia, wakataka wamfate maana hakuna aliyekuwa anaelewa kuwa imekuwaje vile
yani kila mmoja alishikwa na uoga wa hali ya juu huku akishangaa mara gafla
kabla hawajatoka nje akatokea Salome huku akicheka sana, wakajikuta wakisema kwa
pamoja tena kwa mshangao, “Salome!!” “Ndio ni mimi, mnadhani
mnaota?” “Umekujaje kimiujiza?” “Mbona huyo aliyeondoka
hamkumuuliza kuwa amekujaje?” Wakamuangalia Salome, kisha wakamuacha na
kwenda getini ambako walimkuta Mishi ndio akiishia getini kutoka, Ana alimfata
mlinzi na kumuuliza, “Mbona umemuachia atoke?” “Sikumuelewa na
yeye pia anaonyesha hajielewi, sijamuona kuingia ila nimemuona kutoka kwakweli
sikumuelewa” “Na Salome yupo ndani” Mlinzi alishtuka sana
kusikia kuwa na Salome yupo ndani wakati hakumuona akiingia, “Mbona
sijamuona akiingia?” “Ndio ushangao hapo, Yule msichana ni mchawi hata
naogopa kulala ndani ya nyumba” Muda kidogo Kulwa na Sara nao walitoka
wakidai kuwa hawawezi kulala ndani ya nyumba yao maana Salome hakuwa mtu wa
kawaida, basi wakakubaliana kuwa watoke nje hata waende wakakodi hoteli ya
karibu na kulala huko, mlinzi alitamani pia kuondoka ila alihofia kazi yake huku
akiwa na mashaka sana, aliwashuhudia tu wakipanda kwenye gari na kutoa gari nje
kisha kuondoka zao. Mlinzi alikuwa na mashaka sana ila Salome alimfata
Yule mlinzi pale getini na kumwambia, “Umefanya jambo jema sana
kutokufatana nao” “Ila naogopa pia, hivi wewe Salome ni mtu wa kawaida
kweli?” “Kwanini mimi nisiwe mtu wa kawaida?” “Sijakuona
ukiingia ila gafla nakuona ukitokea ndani” “Yani hiyo tu ndio inafanya
mimi nisionekane mtu wa kawaida? Mbona Yule msichana pia hukumuona akiingia na
umemuona akitoka, je nae ni mchawi? Ila usiogope sana, hata mimi natoka siwezi
kuendelea kulala humu ndani peke yangu” “Unaogopa?” “Ndio
naogopa pia, mimi ni mtu wa kawaida kwahiyo kitu cha ajabu kama hivi kikitokea
lazima niogope” Salome alitoka na kumuacha Yule mlinzi pale getini,
kwakweli aliogopa sana huku akiangalia ile nyumba kwa uoga ila alijipa moyo
sababu yuko nje kwahiyo alihisi lolote baya likitokea basi
atakimbia. Mishi alikuwa na uoga wa hali ya juu maana
hakudhania kama ingetokea muda angerudishwa kimaajabu kwakina Doto, kwakweli
alichanganyikiwa sana. Njiani aliona vijana watatu alianza kukimbia huku akipiga
kelele kwani alijua ni lazima angebakwa tu, ila wakati anakaribia nyumbani kwao
walitokea vijana wengine na kumpiga teke kisha kuanza kumbaka, Mishi alipiga
kelele sana na watu walijitokeza kumsaidia kisha wale vijana wakakimbia, wale
waliomsaidia Mishi walikuwa ni ndugu zake, na walimrudisha nyumbani huku wakimpa
pole na kumuonea huruma sana, mama yake alikaa karibu na binti yake chumbani
kumpa moyo, “Yani mwanangu tulikumbwa na uoga wa hali ya juu ndiomana
wote tulikuwa macho tukikutafuta, maana mwenzio alivyosema umetoweka kila mmoja
alishikwa na mashaka hapa. Ilikuwaje mwanangu?” “Hata sielewi
mama” “Ulitowekaje?” “Hata sielewi mama” “Haya ni
maajabu sana mwanangu, sijui hata tufanye nini yani hadi naogopa. Hapa naogopa
hata kulala” “Sio wewe tu mama, hata mimi mwenyewe naogopa hata
kulala” “Ndugu zako wote hapo nje wapo kwaajili wamepata habari ya
kutoweka kwako, wale mafirauni waliokuwa wanakufanyia kitendo cha kikatili
hatujawapata mwanangu, yani tutawatafuta popote pale” “Mnadhani
mtawapata mama? Hata msijisumbnue, kesho nitakupeleka mahali nilipopewa hii
laana” “Laana! Umepewa laana kivipio mwanangu?” “Mama, ni aibu
hata kusema ila nimepewa laana na binti mdogo kabisa yani nadhani yote haya
yanatokea kwa laana yake. Mama nipo tayari kuolewa na mzee Juma” “Kheeee
upo tayari kuolewa tena?” “Ndio, bora niwe mke wa mtu labda itapotea hii
laana. Naomba niolewe mama” “Sasa mwanangu mbona gafla sana, na kwa huyo
mtu tutaenda saa ngapi?” “Tutaenda kesho, lakini baada ya mimi kuolewa.
Naomba ukaongee na mzee Juma kesho asubuhi mwambie nipo tayari kuolewa nae, iwe
kesho, tufunge ndoa hata ya fasta ila niolewe tu mama” Mamake Mishi
alimshangaa sana binti yake kwa maamuzi hayo ila kwavile hakujua ni kitu gani
kilimsumbua binti yake huyo, ikabidi tu akubaliane nae kwani hata yeye tukio la
binti yake kutoweka lilimshtua sana. Sara, Kulwa na Ana
walifika kwenye hoteli moja ndogo kisha kulipia vyumba vitatu vya kulala kwani
Ana na Sara bado ilikuwa haiivi kulala kwenye chumba kimoja, kwahiyo kila mmoja
aliingia kwenye chumba chake kisha wakakubaliana kuwa asubuhi waamshane mapema
ili wawahi kurudi nyumbani na waandae chakula cha kumpelekea
mgonjwa. Cha kushangaza walipoamka kila mmoja alijikuta kwenye chumba
chake nyumbani kwao, kwahiyo kila mmoja alikuwa na mshangao peke yake kuwa
imekuwaje tena. Sara aliinuka na kuangalia vizuri, alikumbuka fika kuwa mara ya
mwisho alilala kwenye chumba cah hoteli sasa imekuwaje kujikuta wamelala ndani
kwao? Alikuwa na mashaka sana, akaamua kutoka nje na kwenda sebleni, ni kweli
ilikuwa ni ndani kwao, muda kidogo alimuona Kulwa akitoka na Ana akitoka na wote
wakiwa na mshangao huku wakiulizana, “Jamani imekuwaje?” “Labda
tukuulize Ana imekuwaje!” Sara alisema hivyo ila hiyo kauli ilimkera Ana
kwani ilionyesha wazi kuwa yeye ana nguvu za ajabu na ndio amefanya hivyo kwao,
ila Ana aliwajibu kawaida tu “Jamani, mimi na nyie tulikuwa eneo moja
kwahiyo swala la kuniuliza kuwa imekuwaje hata mimi sijui. Cha muhimu
tumesharudi nyumbani basi tukamuandalie chakula kaka na tumpelekee
hospitali” Ikabidi wakubaliane kufanya hivyo ingawa hawakujua kuwa ni
chakula gani wataenda kumpelekea hospitali kwa wakati huo, na wakaona kuandaa
itawachukua muda mrefu kwahiyo wakajadiliana kuwa waende tu hospiatali kisha
wataenda kumnunulia chakula huko huko. Ikabidi waende kujiandaa tu muda huo,
kila mtu alijiandaa upesi upesi kwani kila mtu alikuwa na mashaka kupita maelezo
ya kawaida, na walipomaliza walitoka nje, walipofika getini mlinzi alishtuka
sana na kuwauliza “Mmeingiaje humu ndani?” Hawakumjibu kitu
kwani hata cha kumjibu kingekuwa ni kitu gani, ila mlinzi aliendelea
kusema “Kwa stahili hii sidhani kama kuna umuhimu wa mimi kuendelea
kulinda hapa, ikiwa watu wanavyoingia ndani siwaoni ila nawaona wakati wa kutoka
tu” Wakina Sara hawakumjibu zaidi ya kumsalimia tu, kisha wakatoa gari
na kuondoka zao. Walivyofika hospitali walimkuta ndugu yao akiwa
anaendelea afadhali kidogo kisha wakamuuliza chakula cha
kumletea, “Hapana msihangaike, Salome alikuja hapa saa kumi na mbili na
kaniletea mtori. Kaninywesha hadi nimeshiba kabisa, Yule binti ana moyo wa
huruma sana” Ana akadakia, “Ana moyo wa huruma wakati ndio
chanzo cha kuungua kwako” “Ana nyamaza usitake niongee sana, yeye ni
chanzo wakati chanzo ni wewe na mama, si wewe na mama ndio mmenimwagia maji ya
moto! Unafikiri sikumbuki eeh! Nakumbuka vizuri, ni nyie ndio mmefanya niteseke
hivi” “Mmmh basi yaishe, cha muhimu upone tu na uendelee
salama” Wakaongea ongea nae pale na kumuaga kuwa wataenda tena mchana
kumuona, naye aliwaitikia kisha wakaondoka na kuanza safari ya kumfata mama yao
ambaye walimuacha kule kwa mganga. Nyumbani kwa Neema, siku
hiyo alishangaa asubuhi asubuhi binti yake amepika na kuondoka halafu muda
kidogo akarudi, “Kheee ulienda wapi Salome?” “Kaka yangu
amelazwa” “Kaka yako!” “Ndio, mtoto wa Yule mama wa kule mke wa
baba” “Kheee anaumwa nini tena” “Eti aliungua na maji ya
moto” “Basin a mimi tutaenda wote kumuona mchana” Salome
alimkubalia mama yake kuwa mchana wa siku hiyo ataenda nae kumuona hospitali,
huku akionekana kushughulikia chakula cha mgonjwa. Yani Salome alikuwa akifanya
vitu ambavyo alijua badae vitaleta majibu gani. Wakina Sara
walienda hadi kwa Yule mganga ambaye walimuacha mama yao na walikuta bado mama
yao akiwa ndani ya kile kibanda cha mganga kumbe kulipokucha bado mganga aligoma
kumuhudumia kwahiyo alikuwa akimbembeleza, ilibidi watoto wake wamsubiri
tu. Rose aliendelea kumuomba Yule mganga amsaidie, “Sasa wewe
mganga unavyokataa hivyo, mimi atanisaidia nani? Maji yamenifika shingoni
sasa” “Sijui nani atakusaidia kwakweli ila mimi siwezi, maisha yangu
nayapenda sana. Watoto wangu bado wadogo, wengine wananitegemea kwakila kitu,
sipo tayari kuwaacha. Nilikuwa nakupa moyo tu jana ila kukusaidia
siwezi” “Inamaana na wewe unamuogopa huyo anayetutisha kwenye nyumba
yetu!” “Wewe Rose una dawa nyingi sana, fanya dawa zako na wewe kuweza
kutokomeza hali hiyo” “Ni kweli nina dawa nyingi lakini sijui jinsi ya
kuzitumia” “Na mimi siwezi kukwambia namna ya kufanya na siwezi
kukusaidia kwakweli, labda uende kwa waganga wengine” Rose alitumia muda
mrefu sana kumshawishi huyu mganga ila jitihada zake ziligonga mwamba, ikabidi
aanze kumfikiria mganga mwingine wakati akili yake imepata jibu juu ya mganga
mwingine wa kwenda akaamua kufanya hivyo, ndipo alipotaka kutoka kwa mganga Yule
ila alishangaa Yule mganga akimzuia na kumwambia kuwa atamsaidia, Rose alifurahi
na kukaa chini ili kusikiliza Yule mganga atamsaidiaje, kisha Yule mganga
akaanza kupiga tunguli zake, na alipomaliza akaanza kuongea nae, “Kwanza
kabisa, Yule mtoto wako ambaye kaungua na maji ya moto hamtakiwi kumpeleka
hospitali” “Mmmh mganga sijui kama watoto wangu watarudi tena hapa,
kumbuka usiku sikuwaona au bado wapo nje?” “Sijui ila hutakiwi kumpeleka
hospitali” “Basi ngoja nijaribu tena kuwatafuta” Rose alitoka
mule kwa mganga huku akiwa na mawazo sana kuwa watoto wake walielekea wapi ila
alishangaa kufika nje, kuona gari yake na watoto wake ndani ya gari na
ilionyesha wazi walikuja kumfata mama yao. Alijiuliza kuwa mbona usiku wa jana
hakuwaona, kwamaana hiyo waliondoka au imekuwaje hapo, hakupata jibu kabisa.
Aliwafata na kuwauliza kulikoni mbona usiku wa jana hakuwaona alipotoka kwa
mganga, Sara alikuwa wa kwanza kumjibu mama yao, “Mama tumekuja kukufata
wewe, Doto kalazwa hospitali twende ukamuone” “Kwahiyo Doto mmempeleka
hospiatali?” “Ndio mama” “Nyie watoto jamani mbona mnanitafutia
ubaya!” “Ubaya upi mama? Doto yupo hospitali na tungemchelewesha tu
tungemkosa, naomba twende mama” Rose alikuwa ameduwaa tu nje huku akiwa
hajielewi kuwa afanye kitu gani, Kulwa alishuka kwenye gari na kumpakia mama yao
kinguvu kisha akapanda kwenye gari na kuondoa gari hiyo. Rose alikuwa kimya tu
kwani bado alikuwa akitafakari bila ya jibu, mganga kamwambia kuwa mtoto wake
asipelekwe hospitali na huku washampeleka hospitali kwahiyo hata akienda
kumbembeleza tena mganga ni kazi bure kwa wakati huo. Ikabidi atulie tu kwenye
lile gari, na alijiuliza tena kuwa mganga alikuwa na maana gani kuwa mtoto wake
asipelekwe hospitali! Bado hakuwa na jibu, hadi wanafika hospitali ilikuwa ni
mchana tayari, ila walipofika walizuiliwa na kuambiwa kuwa muda wa kuona
wagonjwa umeisha, ikabidi Sara aulize “Jamani mbona asubuhi mlituruhusu
wakati muda ulikuwa umeisha?” “Asubuhi aliyewaruhusu aliwaruhusu
kimakosa, njooni jioni ndio muda uko wazi” “Sasa mgonjwa wetu
hajala” “Ameshakula, kuna ndugu yenu kashampa chakula. Atatoka muda sio
mrefu” Yule nesi alisogea kidogo, na muda sio mrefu wakamuona Salome
akiwa ameongozana na mwanamke mmoja, Rose alipomuangalia vizuri Yule mwanamke
aligundua ni Neema ambaye ni mama yake na Salome. Salome na mama yake
hata hawakuangalia upande, walikuwa wanaondoka tu ila Rose alimuita
Neema, “Neema” Neema akageuka na kumuona kuwa ni Rose, uoga
ukamshika kwani bado alikuwa anamuogopa Rose vilivyo, ila Rose alimsogelea Neema
na leo kwa mara ya kwanza alimsalimia vizuri kabisa, “Hujambo
Neema” “Sijambo shikamoo” “Mbona unaniogopa
hivyo!” Salome akadakia, “Anakuogopa sababu umezoea
kumtishia” Neema alimkatisha mwanae kuwa asiendelee kuongea maneno hayo,
Rose alimwambia Neema “Sina ugomvi na wewe na nimefurahi kukuona.
Natumai umetoka kumuona mwanangu, mwanao pia nimempokea vizuri kwenye nyumba
yangu ila mwanao ni mshirikina” Neema
akashtuka “Mshirikina!” Salome akacheka sana, kisha akamshika
mama yake mkono na kumlazimisha kuwa waondoke eneo hilo, ila Neema alikuwa
mbishi kufanya hivyo. Salome alimwambia mama yake, “Mama, sijakuleta
hapa kuja kubishana na huyu mtu. Halafu nina mambo mengi ya kufanya siku ya leo,
tafadhali tuondoke nyumbani” Neema alikuwa mbishi mbishi kwani bado
alitaka kusikia kuwa kwanini mwanae kaitwa mshirikina ila ikabidi akubaliane tu
na mwanae kuwa waondoke, ambapo salome alikodi bajaji iwapeleke nyumbani kwao
ila kitendo cha Salome na mama yake kuondoka na ile bajaji, Rose alienda
kuwaomba watoto zake kuwa waifate hiyo bajaji hadi wajue wanapoishi Salome na
mama yake, kwahiyo walifanya hivyo na kuanza kuifatilia ile
bajaji. Nyumbani kwakina Mishi mamake alipoenda tu kumwambia
mzee Juma kuhusu maamuzi ya Mishi wala hakubisha Yule mzee kwani siku zote
alitamani Mishi akubali amuoe ukizingatia kashakula hela zake nyingi sana,
kwahiyo hakutaka hata kupoteza muda ni siku hiyo hiyo akaita watu na kumuoa
msichana huyo, ilifungwa tu ndoa ya kawaida yani haikuwa na shamra shamra zozote
kwani ni ndoa ya haraka halafu haikupangwa ila Mishi alifurahi kuolewa na mzee
huyu na hakumwambia kama alibakwa au alikutwa na matukio yaliyomfanya akubali
kuolewa nae, ingawa alikuwa akijiuliza sana kuwa inakuwaje kuwaje mambo
hayaeleweki kabisa. Alipomaliza kufunga ndoa, akatembelewa na mgeni na
kuambiwa kuwa kuna mgeni wake, alitoka kwa mashaka sana kwani bado hakuwa na
imani na jambo lolote na uoga ulikuwa umemtawala. Alipoenda kuzungumza nae
alishangaa kuwa ni Salome, akataka hata kurudi kwa ndugu zake ila alishangaa
miguu yake ikigoma kufanya hivyo, kisha Salome akaanza kuongea
nae, “Usiniogope mimi sio mla watu, wala sio mchanganya wanaume kama
wewe” Mishi alikuwa kimya tu akimsikiliza, “Umefanya uamuzi wa
haraka sana kuolewa, hivi unajijua kama hapo ulipo una mimba? Au unataka hiyo
mimba umsingizia Yule mzee wa watu?” “Nina mimba ya nani?” “Mi
nitajuaje na umebakwa na watu wengi. Unajua wakati wa kubakwa ni vigumu kujizuia
tofauti na ukitaka mwenyewe, sasa vipi unataka kumsingizia mzee wa
watu!” “Hapana sikuwa na nia hiyo ila nimeamua tu kutoka moyoni
kuolewa” “Kama umeamua kutoka moyoni mwambie ukweli, Yule mzee
anakupenda na atakuelewa tu. Halafu kama umeamua kweli kwa moyo wako, tulia na
mumeo. Ni mwanaume gani anaweza kukubali kufunga ndoa ya haraka haraka kiasi
hiko? Anakupenda mwenzio, ni wa kawaida tu Yule hata sio mtu mzima kihivyo,
mpende sababu umeamua mwenyewe uache tabia ya kuumiza moyo
wake” “Nimekuelewa na ninakuahidi nitampenda sana na nitamwambia ukweli
wa kila kitu” “Usiniogope, mimi ni binadamu wa kawaida tu kama wewe.
Kwavile umesema utatulia kwa mumeo, naifuta laana yangu kwako” Salome
aliondoka, na Mishi alikuwa anamuangalia hadi alipoishia, hata alipoulizwa na
mama yake kuwa mtu huyo alikuwa anaongea nae nini bado hakuweza kumjibu kwani
kwake bado lilikuwa ni swala la aibu. Wakiwa ndani ya bajaji,
Neema alimshangaa mwanae amelala mpaka wanafika nyumbani ndio anamshtua kuwa
washuke na waingie ndani, walipoingia ndani mara na wao wakina Rose walikuwa
wamefika ila Salome alifanya jambo na kumfanya mama yake kuingia chumbani ili
wakigonga mlango wa sebleni wasimkute mama yake na wamkute yeye. Basi kweli
wakagonga mlango wa sebleni na kusikia sauti ya Salome
ikiwakaribisha, “Fungua mlango ingia” Basi wakafungua na
kuingia, Rose alikuwa wa kwanza kuingia mule ndani ila alishtuka sana kwani
alijiona yupo nyumbani kwake na aliyewakaribisha alikuwa ni Patrick na sio
Salome. Basi wakafungua na kuingia, Rose alikuwa wa
kwanza kuingia mule ndani ila alishtuka sana kwani alijiona yupo nyumbani kwake
na aliyewakaribisha alikuwa ni Patrick na sio Salome. Kila mmoja
alipoingia alishtuka, kisha Patrick akawauliza kwa kejeli, “Mnashtuka
nini sasa? Mnashtuka kuniona kwenye nyumba yangu mwenyewe? Hapa si nyumbani
kwangu, kwahiyo siruhusiwi kuja?” Wote walikaa kimya kwani kila mmoja
alikuwa akijiuliza kuwa imekuwaje tena wamerudi nyumbani kwao wakati walikuwa
wakiingia kwakina Salome na aliwakaribisha, Patrick aliwashangaa kuwa hawasemi
chochote akajua wanamfanyia kiburi bila ya kujua kilichowasibu. “Nyie
jifanyeji kiburi tu, mmenikuta kwenye nyumba yangu, hata salamu kutoa hamjatoa
eti mnashangaa shangaa. Haya endeleeni kushangaa tu mkimalia
mtaniambia” Patrick akakaa chini akiwaacha wao wamesimama huku bado
wakishangaa tu, Rose nae alikaa chini huku akitikisa kichwa chake na
kusema, “Hivi ni kweli au naota?” Alidakia Ana na kumjibu mama
yake, “Ni kweli mama, tumerudishwa nyumbani tena bila ridhaa yetu.
Anayetufatilia kwa hakika ana nguvu zaidi yetu” Wote walikuwa kimya tu,
Rose alipumua kwa nguvu maana mambo yalikuwa yakimchanganya zaidi na kuanza
kuhisi huenda swala la kumpeleka Doto hospitali ndio limeendelea kuzua hayo
wanayoyaona. Alipojitafakari vilivyo akamuangalia Patrick sasa na kuanza
kumuomba msamaha maana kwa hakika Patrick alihisi
wamemdharau, “Tafadhali tusamehe bure ila yaliyotupata kwa siku ya leo
hapana kwakweli” “Yaliyowapata yapi hayo?” “Mume wangu
unanichukia bure tu ila familia yetu inafatiliwa na wachawi” “Wachawi
kushinda wewe uliyemuua mama yangu!! Yani mimi naongea na wewe bure tu ila wewe
Rose ni mwanamke mbaya sana, umeniulia mama yangu, umefanya niiache familia
yangu iteseke, nimeacha ndugu zangu wakiteseka huku mimi nikila raha ya maisha.
Nimeacha mwanangu akiteseka huku wanao nikiwalea maisha ya kifahari, wewe ni
mwanamke mbaya sana Rose” “Naomba unisamehe kwanza, halafu hayo si
maneno ya kuongelea mbele ya watoto” “Unataka nikaongelee wapi?
Umenitesa sana wewe mwanamke, na kwa taarifa yako ndugu zangu wanakuja hapa sio
siku nyingi” “Patrick! Ndugu zako wanakuja!” “Ndio ndugu zangu
wanakuja hapa na watakuwa wanakaa hapa” “Haiwezekani Patrick, huwezi
kufanya jambo bila kunishirikisha mimi. Humu ndani mimi ndio mama mwenye
nyumba” “Mke wangu ni Neema na ndio mama mwenye nyumba” “Neema
kivipi? Kumbuka Patrick, ulimuacha Neema na kunioa mimi, iweje leo useme mke
wako ni Neema! Umechanganyikiwa wewe sio bure” Kisha Rose akawaangalia
watoto wake na kuwaambia, “Hivi na nyie hamuwezi kwenda kufanya mambo
mengine hadi make msikilize mazungumzo ya mimi na baba yenu!” Patrick
akadakia, “Waonyeshe baba zao watoto wako, mimi sio baba yao. Na kibaya
zaidi hata huyo mtoto wako wa mwisho nae sio wangu, nilijivunia nimepata
mwanamke kumbe ananiacha ndani anaenda kuzaa na mwanaume mwingine
nje” Wakina Sara baada ya kuona jicho kali la mama yao ikabidi watoke
nje na kuwaacha sebleni kwani Patrick aligoma kwenda kuongelea popote pale zaidi
zaidi ya hapo sebleni. “Jamani Patrick twende tukaongelee chumbani mambo
hayo” “Twende chumbani ili ukaniroge? Rose umeniroga kwa miaka mingi
sana, akili yangu imefunguka sasa na huwezi kunishawishi juu ya kuniroga tena,
mwanamke mbaya wewe” Rose alijaribu kila njia ya kumtuliza Patrick ila
leo alikuwa hatuliziki kabisa, inaonyesha wazi aliamua na
alidhamilia. Kule nje walienda moja kwa moja kwa mlinzi wao na
kumuhoji kuwa Yule baba yao alienda saa ngapi pale nyumbani, ila mlinzi
alivyowaona alishtuka sana badala ya kumuuliza yeye aliwauliza
wao, “Mmeingia muda gani humu ndani?” “Tunataka kukuuliza baba
amekuja muda gani?” “Humu ndani mbona mmekuwa na mambo ya ajabu sana
sijapata kuona, yani siwaoni kuingia ila gafla nawaona ndani” Basi
akafikicha fikicha macho yake na kuiona gari ambayo walitoka nayo ikiwa imepaki
uwani, yani hapo ndio akashangaa kabisa kuwa hata gari ilivyoingia hakuiona yani
aliona mambo ya ajabu na kuhisi nyumba yote hiyo ni wachawi. “Mama
akirudi namuomba mshahara wangu naacha kazi” “Usiache kazi bhana, uache
kwasababu gani? Hata hivyo mama yuko ndani” Mlinzi akashtuka
tena, “Yuko ndani? Ameingiaje?” “Tulikuja nae” “Hii
nyumba hapana, imenishinda kwakweli yani imenishinda kabisa siwezi kuendelea
kuishi humu” “Usiondoke, haya mambo yatarekebishwa tu hata usiende
popote” “Hapana siwezi, yani watu unawaona wakati wa kutoka tu ila
wakati wa kuingia huwaoni!” “Inamaana nae baba hujamuona wakati wa
kuingia?” Ana aliuliza kwa makini swali hilo kwani alitaka kujua kama ni
kiini macho wamefanyiwa au ni kitu gani, “Mzee yeye kafika vizuri,
tumesalimiana nae hapa na kuuliza mko wapi na akaingia ndani kuwangoja. Yani
nyie ndio mmenifanyia maajabu, na toka mzee aje sijatoka kabisa hapa getini leo,
haya niambieni mmeingiaje” “Yani hata sisi wenyewe hatujui kwahiyo
utakuwa unatushutumu bure tu” Ila huyu mlinzi alishikilia wazo lake tu
kuwa yeye ataomba mshahara wake aondoke kwenye nyumba hiyo, wakati wanaongea na
Yule mlinzi alifika mtu na kugonga geti alipomfungulia alikuwa ni Salome,
walibaki wanamtazama kama dakika kadhaa ndio kumkaribisha ila Salome alitabasamu
tu na kuingia ambapo moja kwa moja alienda ndani na kuwakuta Rose na Patrick
wakiwa kwenye majibizano makubwa sana. Alipoingia tu kama kawaida yake
aliingilia yale mazungumzo, “Wewe mama ushaambiwa usamehewi, sasa ya
nini kulazimisha msamaha!” “Hata maandiko yanasema samehe saba mara
sabini” Salome alicheka sana ten asana kisha akamwambia, “Hivi
leo ndio unatambua maandiko yamesema hivyo, je ulipokuwa unamuua bibi wa watu
asiyekuwa na hatia ulikumbuka maandiko? Ulipomtumia Ashura ajifanye anaundugu na
Neema ili tu azidi kumkandamiza ulitumia maandiko? Wakati Salome anateseka na
maisha wakati baba yake anakula raha ulitumia maandiko? Na zaidi ya yote,
uliowafuga ndani kwenye chumba chako cha siri unatumia
maandiko?” Patrick akashtuka sana kusikia kuwa mkewe kuna watu anawafuga
pia kwenye chumba cha siri, “Kheee wewe mwanamke kweli ni shetani yani
wewe una matendo hata shetani anayaogopa. Kwahiyo kuna watu umewafuga ndani
kwako?” “Salome jamani usizidi kunikandamiza jamani,
nisameheni” “Nani akusamehe mwanamke shetani kama wewe? Yani umefanya
maovu mengi napo umeona hayatoshi ila ukaongezea na kuwafungia watu kwenye
chumba cha siri!” “Anafuga watu ndio huyu, hujui tu baba ila ndio hivyo
anafuga watu huyu. Siku ukinijua vizuri utaelewa nimejuaje siri zako na njia
zako, sipendi unavyowatesa wale watu, waachie waendelee na maisha yao
mengine” Kisha Salome akamgeukia Patrick na
kumwambia, “Wasichana wa kazi wote wanaopotea kwenye nyumba yako halafu
anasema kawafukuza ni muongo, anawafungia kwenye chumba cha siri, ikitokea mtu
kaumia kwenye nyumba hii damu ikamtoka basi asitoke mlangoni maana akitoka tu
anajikuta kwenye chumba cha siri, huyu mama ni mpumbavu sana, anafanya mambo ya
kijinga. Watu wa watu wamekonda sababu ya kufungiwa, ni bora ujue ndugu yako
amekufa kuliko kujua ni msukule, huyu mama ni mbaya sana” Sara na Kulwa
walikuwepo mlangoni na walisikia yote ambayo mama yao alikuwa akishutumiwa, muda
huu Ana alikuwa getini na mlinzi ila wao wakati Salome ameenda ndani walienda
kukaa mlangoni, kwahiyo kila kitu kilikuwa wazi kwenye masikio yao na kuelewa
kirahisi kuwa wote wanaohisi wamepotea kumbe mama yao amewafungia kwenye chumba
cha siri, ndipo Sara nae alipojiwa na swala la Ommy, akaweza kufikiria ni jinsi
gani Ommy alikuwa akiteseka kwenye hiko chumba cha siri, alijikuta akiingia
ndani na kumwambia mama yake, “Mama tafadhali mfungulie Ommy
wangu” Sara machozi yalimlengalenga kwani leo alielewa mchezo vizuri
kabisa kuwa mama yao ni mchawi tena mchawi haswaa wala sio wa kusingiziwa kama
wengine. Rose hakuweza kuvumilia hizi shutuma akaamua kukimbilia chumbani,
kwahiyo sebleni alibaki Salome, Patrick na Sara. Hizi habari za mkewe
kuwa na chumba cha siri zilimshtua sana Patrick kwani aliweza kupata kumbukumbu
kuwa kuna rafiki yake aliwahi kupotea kwenye nyumba yake hiyo na hakujulikana
alipoenda hadi leo hajui ila hapo kapata jibu kuwa huenda nay eye amefungiwa
kwenye chumba cha siri, akamuangalia mwanae Salome na kumuuliza, “Wewe
umejuaje hizi habari za huyu mwanamke kufungia watu kwenye chumba cha
siri” “Nilijua toka siku ya kwanza nilipokuja kufanya kazi
humu” Sara na Patrick walishangaa na kujikuta wakimuuliza kwa
pamoja, “Ulipokuja kufanya kazi humu!!” “Ndio, ila msinihoji
zaidi yani nyie mjue tu kwamba nilijua.” “Sasa tutafanyaje ili
awatoe” “Najua cha kufanya ila njia yangu ni hatari sana, hatari kwake
na kwa familia yake ndiomana nataka awatoe mwenyewe kwa hiyari
yake” Wakajikuta wakimuangalia Salome na ilionyesha wazi hawamuelewi
elewi maana vitu vingine aliongea kamavile ni mtu wa aina nyingine na sio wa
kawaida, Kulwa nae aliingia ndani na kuwaambia kuwa kasikia kila kitu na
anashangazwa na habari hizo za mama yake kuwa kuna watu amewaeka msukule, basi
akawa anajadiliana pale na dada yeka kisha Salome aliomba kutoka na baba yake
ambapo alikubali na kuondoka na Salome halafu wakawaaga
pale. Neema alikuwa bado yupo chumbani kwake tangu muda ule
walipotoka hospitali hadi anaiona jioni ikikaribia, akapigiwa simu na rafiki
yake mama Pendo na kuanza kuzungumza nae ambapo mama Pendo alimkumbusha Neema
swala la kumpeleka mwanae salome kwenye maombi, “Usipuuzie Neema, mwanao
anatakiwa aombewe” “Sijapuuzia, nilisafiri ndiomana uliona
kimya” “Sasa lini utakuwa tayari ili nimwambie mchungaji
wetu” “Nitakwambia tu, siwezi kusema siku wakati Salome mwenyewe
sijaongea nae chochote. Nikiongea nae nitakwambia ni lini” Basi
akakubaliana nae hivyo na kukata simu, kisha akatoka na kuanza kumuita Salome
ila akaona kimya na kugundua kuwa Salome ameondoka, aliwakuta tu wanae wale
mapacha wakiandika andika, “Nyie dada yenu kaenda wapi?” “Sijui
ila ametoka” “Yani huyu mtoto ameanza tabia ya kutoka bila kuniaga!
Kweli wa kufanyiwa maombi huyu” Ikabidi Neema aanze kufanya kazi zake za
hapa na pale, ila hadi anamaliza kupika kisha watoto wake wale mapacha kwenda
kulala ila Salome alikuwa hajarudi na kushangaa kuwa Salome kama alikuwa anaenda
kulala huko huko si angalau angemuga basi, wakati analalamika hivyo akasikia
hodi, alipoenda kufungua alikuwa ni Salome na Patrick ambapo aliwakaribisha
vizuri tu kisha Salome akawaambia, “Mi naenda chumbani kwangu, kwahiyo
nyie endeleeni na mazungumzo tu” Salome aliondoka, ila Patrick na Neema
waliganda tu wakiangaliana na hakuna aliyemsemesha mwenzie kwani kwa muda huo
kila mmoja alijiuliza kuwa nani anastahili kuanza kuongea kati yao. Muda nao
ulizidi kwenda ikabidi Neema ajitoe muhanga, “Nakusikiliza
Patrick” Wazo la haraka haraka la Neema alihisi kuwa Patrick ameenda
kudai zile pesa zake alizomleteaga ndiomana alishindwa kuanza kuongea nae, ila
Patrick leo alikuwa kama mtu aliyeshikwa na ganzi, “Sijui hata nisemaje,
ila nisamehe Neema” “Mi nishakusamehe siku nyingi
mbona” “Nifanye nini unisamehe?” “Wewe mbona mimi nishakusamehe
jamani!” Patrick alikuwa kimya tena kwani kadri alivyomuangalia Neema
aliona anazidi kuwa mzuri, alimuona Neema akiwa mrembo zaidi kupita Yule Neema
aliyemuoa akiwa na miaka kumi na sita, alijikuta akitamani kumuuliza kuwa mbona
urembo ulizidi ila mdomo ulikuwa mzito, Neema nae alimuona Patrick akiwa zaidi
ya vile alivyomuoa kipindi cha nyuma, alimuona Patrick amekuwa na sura ya
kuvutia hatari, akajikuta anamwambia, “Naenda kulala
bhana” Neema hakutaka tena kumuangalia Patrick kwani alihisi kumtamani
ila ile alivyoinuka baada ya kumwambia naenda kulala, Patrick nae aliinuka na
kufatana na Neema hadi chumbani, kwahakika Neema hakuweza kumfukuza Patrick
ukizingatia alishakuwaga mume wake. Kulipokucha, Patrick
alikuwa amelala pembezoni mwa Neema na alijisikia vizuri sana, walijiona
kamavile mapenzi yao ndio wametoka kutongozana. Waliamka wakitabasamu, na
walipotoka chumbani walikuta Salome ameshawaandalia kifungua kinywa, kisha
akawakaribisha mezani na kusema, “Baba, kuanzia leo naomba uhamie
hapa” Patrick alicheka tu ila kicheko cha furaha kwani alijihisi kama
amekuwa mtu mpya kabisa kwa siku hii na alikubaliana na kila jambo aliloambiwa
na Salome. Rose aliamshwa na sauti ya mlinzi wake aliyemuomba
kwaajili ya maongezi, alipotoka alimsalimia kisha Yule mlinzi akamwambia hoja
yay eye kutaka kuondoka kwenye nyumba hiyo. “Jamani kwanini unataka
kufanya hivyo?” “Mama siwezi, sijawahi kukukosea heshima hata mara moja
mama yangu ila kwa hili naomba tu nirudi nyumbani, siwezi kuendelea kuishi humu
ndani” “Jamani nimekuzoea ujue Lazaro, sipendi unavyosema unaondoka.
Nitakuongezea mshahara ila usiondoke hapa nyumbani kwangu” “Mama, hapana
acha tu nirudi kwetu” “Tumetoka mbali Lazaro, kumbuka wewe ni mtu pekee
unayefahamu vitu vingi kuhusu mimi, nakuomba Lazaro usiondoke. Kumbuka umeanza
kukaa kwangu ukiwa kijana mdogo sana, tafadhali Lazaro usiondoke
jamani” “Basi, naomba niruhusu niende nikasalimie tu halafu baada ya
wiki nitarudi” Kuhusu hilo ikabidi Rose akubali ila wazo la Yule mlinzi
ilikuwa akiondoka tu basi harudi tena, basi Rose akampa mlinzi wake hela baadhi
na kuagana nae. Mlinzi alibeba kila kilicho chake kwani lengo lake
lilikuwa ni kuondoka na kutokurudi tena kwenye nyumba hiyo, na kweli aliondoka
eneo hilo na kwenda kupanda basi la kwenda kwao, ila alipofika tu stendi ya kwao
na kushuka kwenye lile basi alijikuta yupo ndani kwenye nyumba ya Rose huku
mizigo yake ikiwa pembeni. Mlinzi alibeba kila kilicho chake
kwani lengo lake lilikuwa ni kuondoka na kutokurudi tena kwenye nyumba hiyo, na
kweli aliondoka eneo hilo na kwenda kupanda basi la kwenda kwao, ila alipofika
tu stendi ya kwao na kushuka kwenye lile basi alijikuta yupo ndani kwenye nyumba
ya Rose huku mizigo yake ikiwa pembeni. Alishangaa sana na kupatwa kama
na sintofahamu maana ilikuwa ni kitu cha ajabu kwake ukizingatia alipanda gari
la kwenda kwao na gafla anajikuta tena nyumbani kwa Rose, kwahiyo alikuwa
akishangaa shangaa tu pale huku mizigo yake ikiwa pembeni. Salome alienda pale
getini na kumshangaa pia halafu akamuuliza, “Vipi na
mizigo?” “Yani sielewi, sielewi kabisa. Nilikuwa nishaondoka kwenye
nyumba hii, nilishafika hadi stendi kwetu cha ajabu nimerudishwa tena
hapa” “Nani kakurudisha sasa?” “Sijui ni nani, ila mimi mwenyewe
nakumbuka kuwa mara ya mwisho nilikuwa stendi ya kwetu nashangaa nimerudi tena
hapa. Kwanza saa hizi saa ngapi?” “Saa tisa, kwani vipi?” “Haya
ni mambo ya ajabu sana, kutoka hapa hadi kufika kwetu ni masaa saba, ni kweli
hapa nimetoka saa mbili asubuhi ila nimerudishwa kwa sekunde jamani, hii si haki
yani hata kijijini kwetu sikufika, nilifika tu mkoani. Hili swala sio haki
kabisa” “Sasa nani kakufanyia hivyo?” “Sijui ila natamani nifike
kwetu jamani, nimechoka mimi na maajabu ya nyumba hii” “Unatakiwa tu uwe
mvumilivu, utapoteza nauli bure tu. Wewe tulia na usifikirie kila anayerudishwa
hapa ni mchawi, je wewe ni mchawi?” Akakumbuka jana yake aliwaambia watu
wa humo ndani wote wachawi kwasababu alikuwa anawaona kutoka halafu hawaoni
kuingia ila leo jambo hilo lilikuwa limempata yeye, akaona kwa staili ile ni
ngumu kwake kuondoka ila hapo hapo alipata wazo la kuwasiliana na kwao ili
awaeleze kuhusu tatizo hilo maana limekuwa kubwa sana kwa upande
wake. Rose baada ya mlinzi wake kuondoka asubuhi ya siku hiyo,
na yeye alifanya safari ya kumtafuta mganga wake aliyemfikiria kichwani,
alimtafuta sana bila ya mafanikio ila njiani akakutana na rafiki yake wa muda
mrefu sana ambaye aliwahi kumshauri kuhusu swala la waganga kwahiyo alivyokutana
nae alifurahia sana, na kuanza kumshirikisha kuhusu swala lake linalomsumbua
kichwa. “Basi mwezi uliopita mwenzio nilipatwa majanga hayo balaa, yani
kuna mavitu yalichanganya kichwa change kama nini ila kuna kijana huyo ni
matata, kwanza kijana haogopi kitu yani hakuna takataka yoyote inayomshinda.
Huyo kijana ni kimbilio la watu wengi sana, wanaotafuta watoto, wanaotafuta mali
yani kila kitu. Nina uhakika huyo kijana hawezi kushindwa, hao waganga wako
wamechoka halafu waoga” “Huyo atakuwa mzuri kweli, nilijaribu kumtafuta
hata Yule wa mwanzo aliyewahi kunipa dawa ya kufukia ndani kwangu ila
sijampata” “Unadhani Yule unampata kirahisi hivyo? Yule hakuwa mganga ni
jinni lile, na anapatikana kwa waganga wanaojiweza tu, Yule mganga tuliyeenda
kipindi kile alikuwa anajiweza ndiomana ikawa rahisi kukutana na Yule wa dawa.
Ingawa masharti mengi umeyavuruga ila kwa Yule ndio kiboko” “Naomba
nipeleke ndugu yangu, nipo tayari kutoa kitu chochote kile ila niepukane na aibu
hii maana kwangu ni aibu na fedheha” Basi huyu rafiki wa Rose akajitolea
kumpeleka Rose, na kwavile alimuomba ampeleke siku hiyo hiyo akajitolea kufanya
hivyo ingawa ni mbali sana hiyo sehemu. Patrick hakujisikia
kuondoka kabisa nyumbani kwa Neema, na alichofanya Salome ni kwenda kumchukulia
Patrick nguo zake zote na kumfanya afurahi zaidi kurudi kwa Neema, alimuomba
Neema asimfukuze eneo hilo kwani alizidi kufunguka mawazo ya kuhusu mali zake na
nyumba zake ambazo zingine alikuwa hata haendi kuzitembelea kwavile
alishazisahau ila Neema akawa kama amemkumbusha kwahiyo alifurahi sana kumalizia
muda wake kwa Neema, na pia watoto wale mapacha wa Neema aliwaona ila aliogopa
kuuliza kuwa wale watoto ni wa nani, ila alijikaza na kuuliza, “Samahani
Neema, na hawa watoto wako wengine baba yao yuko wapi?” Neema akacheka
kisha akamwambia, “Baba yao ni wewe” “Ni mimi?
Kivipi?” “Najua huwezi kukumbuka au kujua, hii kitu niliiweka siri siku
zote za maisha yangu” “Niambie kivipi?” Basi Neema ilibidi
amueleze Patrick ilivyokuwa, “Kuna kipindi nilikuwa nauza baa, na
ulikuja kunywa sijui ulikuwa na mawazo gani ila ulikunywa sana hadi ulilewa.
Ikawa kila mwanamke anayepita mbele yako unamshika, ilibidi nidanganye kuwa
umenihitaji mimi na kwenda na wewe chumbani, ila kwa nguvu ya pombe
uling’ang’aniza kulala na mimi, kwavile nilikuwa bado nakupenda sikuweza
kukataa, nililala na wewe ila usiku wake niliondoka na kukuacha umelala fofofo.
Kulipokucha uliondoka halafu na mimi niliacha kazi pale kwenye ile baa, sikuwahi
kumwambia mtu yeyote kilichotokea baina yangu na yako, na baada ya mwezi
nilijigundua kuwa nina ujauzito hapo ndipo nilipoamua kufanya siri hadi
nimejifungua. Ilikuwa ni siri yangu hata ndugu yangu Yule Ashura sikuwahi
kumwambia chochote, ingawa sasa nimegundua hakuwa ndugu yangu, yani kama hakuwa
ndugu yangu alikuwa na mipango gani kwangu? Ni siri yake kwakweli, ila hakuwahi
kujua kuwa watoto wangu ni wa nani sababu mar azote alizoniuliza nilimwambia
kuwa nilibakwa” Patrick alishangaa sana hii habari, na kujaribu kuvuta
kumbukumbu ya siku aliyolewa sana, alikumbuka tu kuna siku alilewa sana ila
hakukumbuka ni kitu gani alikifanya, “Na hiyo siku niliyolewa sana ndio
siku iliyobadilisha maisha yangu kabisa, maana tangu siku hiyo niliporudi
nyumbani ndio nikafanywa kama ndondocha yani sikuwa na uwezo wa kwenda sehemu
yoyote ile bila ruhusa ya Rose, yani kipindi hiko ndio mateso yalizidi kwangu
maradufu” “Pole sana, basi hivyo ndivyo ilivyokuwa kuhusu hawa watoto.
Yani ni wanao kabisa” “Kwakweli nimeteseka sana mimi, siku ile
ilipelekea kunywa sana pombe baada ya kumuona mke wangu akiniwekea dawa kwa
macho yangu, mimi sio mlevi kiasi kile ila siku ile nililewa sababu ya mawazo.
Ila kitendo cha kurudi nyumbani ndio nikawa ndondocha kabisa, yani hakuna kitu
nilichokuwa nafanya kwa akili yangu.” Patrick aliomba aitiwe watoto wale
ili awaangalie kwa karibu maana hakuamini amini kuwa alikuwa na watoto, maana
alijua kuhusu Salome ila hakujua kama ana watoto wengine. Neema aliwaita
watoto wake, nae Patrick aliwakumbatia kwa furaha hata wale watoto walibaki
kushangaa tu kwani hawakutegemea huyo mtu kuwafurahia kiasi kile tena huku
akiwaita wanangu, walikuwa wakishangaa shangaa tu ikabidi Neema
awaambie, “Baba yenu huyo” Na wao wakashangaa na kufurahi maana
hawakufikiria kutambulishwa baba, kwani siku zote walipokuwa wakiulizia kuhusu
baba yao Neema alikuwa akiwafokea sana. Patrick akazidi kupata uchungu
dhidi ya Rose na mali zake, ilimuuma sana na kumfanya sasa awaze namna ya
kurudisha mali zake kwenye mikono yake ili watoto wake
wafaidi. Ana alishaamua kujitoa kabisa kwenye maswala ya
waganga na kumkataza mama yake kwa kadri awezavyo lakini mama yake alikuwa
mbishi sana, yeye Ana alikuwa na uwezo wa kupata hisia za mama yake alipoenda
kwahiyo siku hiyo akapata hisia kuwa mama yake kaenda tena kwa mganga ila
inaonyesha wazi alishindwa kumuaga sababu alijua angemzuia. Ana alikuwa
chumbani kwake, alifunua godoro lake na kutoa dawa yake, kwa mara ya kwanza
aliamua kutumia dawa yake ili avuruge akili ya mama yake na kumfanya arudi
nyumbani na ili aweze kubaini ni nani anaewaumiza kwenye nyumba yao. Aliamua
kwanza abaini ane waumiza katika nyumba yao, “Jitokeze nikuone wewe
unayetusumbua humu ndani” Alisema maneno hayo kama mara tatu na gafla
alihisi kuna mtu kasimama mbele yake, aliinua kichwa chake huku amejawa hofu ila
alijitia ujasiri na kumtazama mtu huyo, alikuwa ni Moza kwakweli Ana alishtuka
sana na kumfanya ashindwe hata kumuuliza chochote zaidi ya kutetemeka tu. Moza
alimuangalia Ana na kucheka ila Ana hakuweza kumtazama zaidi Moza, na badala
yake alijikuta akizimia tu pale ndani kwake. Muda huu Sara alikuwa nje
ya chumba cha Ana akigonga na aligonga kwa muda mrefu sana bila ya kufunguliwa
hadi ikabidi afungue mwenyewe, alishtuka sana alipoingia ndani kwani alimuona
Ana akiwa kajifunika makhanga halafu kuna kitu pembeni yake ambacho alikishangaa
sana Sara kwani hajawahi kuona kitu cha namna ile tangia azaliwe, alipiga kelele
na kumfanya kaka yao Kulwa aje ndani pia ila alishangaa alichokiona pembezoni
mwa Ana muda huo Ana akiwa kazimia, alimshika mkono Sara na kumtoa nje haraka
haraka kisha kumwambia, “Yule mdogo wetu ni mchawi, yani bila ubishi
Yule ni mchawi, sasa ndugu yangu maswala ya kumfatilia mchawi ni maswala mazito
sana. Pale tunamuona kama kaanguka ila huwezi jua labda ameenda kwenye uchawi
wake utashtukia anashtuka na kuanza na wewe, tukae mbali dada yangu tunaishi na
nyoka humu ndani” Sara hakuweza hata kuchangia hoja kwani kiukweli mambo
ya nyumbani kwao yalimchosha tena sana tu ila hakuwa na jinsi na hakuwa na
pakukimbilia, muda kidogo Salome nae alitokea nje na kuwafata sebleni Sara na
kaka yake kisha kuwauliza kuwa kuna nini, ila Sara nae alimuuliza, “Hili
hujalijua au?” “Ningelijua ningeuliza?” “Na sisi hatujui kuna
nini” Salome alicheka kisha akaelekea njia ya vyumbani, ila Sara
alimuangalia sana Salome kwani siku hizi alianza kuwa na mashaka nae
pia. Rose kule alipopelekwa kwa mganga walifika jioni kabisa
karibia na usiku hata hivyo mganga mwenyewe hawakumkuta, ni baadae ambapo giza
lilikuwa limeingia kabisa ndio alirudi na kukuta kuwa anangojwa kwa hamu zote.
Rose alitaka kuhudumiwa usiku huo huo ingawa Yule mganga pia alikataa
kumuhudumia kwa usiku huo kutokana na mlolongo wa matatizo yake. “Labda
tuanze tiba saa nane usiku” “Nipo tayari hata saa ngapi ila hili jambo
liishe, nateseka sana” “Litaisha tu, hapa ndio mwisho wa matatizo
yote” Rose alisubiri kwa hamu zote hata kulala kidogo hakutaka, rafiki
yake aliyempeleka aliamua kuondoka na kumuacha Rose muda uleule, kwahiyo Rose
alibaki peke yake kwa Yule mganga huku akisubiri tiba, hakujali kukoje kukoje
kule ila alichojali yeye ni kupata tiba tu. Rafiki wa Rose alijulikana
kwa jina la mama Jack, muda aliokuwa anarudi kwake ni usiku tayari ulishaingia
kutokana na kwake kuwa mbali kidogo na kwa mganga huyo, ingawa alitumia usafiri
wa kukodi ila alichelewa sana kufika nyumbani kwake. Alipofika tu
alimuona mtu yupo pembezoni mwa nyumba yake akilia kanakwamba ni mtu aliyekuwa
na shida, alipomuangalia alimuona ni binti mdogo tu, alimfata na kumuuliza
tatizo, “Vipi binti?” “Nimefukuzwa na mama wa
kambo” Huku Yule binti akiendelea kulia, mpaka mama Jack alimuonea
huruma kwani alijua wazi kuwa ikiwa atamuacha hapo nje binti huyo anaweza
kubakwa na vijana wasio na huruma kwahiyo alimwambia aingie nae ndani kisha
kuzungumza nae na kumuahidi kuwa kesho atamsaidia afike kwa mama yake. Yule
binti alikubali na kumshukuru sana huyu mama, kisha Yule mama akamuandalia
sehemu ya kulala binti Yule. Hakuwahi kumuona, hakuwahi kumfahamu ila ni huruma
tu ndio iliyomfanya amsaidie. Yule binti alionyesha kumshukuru sana Yule mama
kiasi cha kumfanya Yule mama ajisikie vizuri na ajione kuwa katenda jambo jema
sana kumsaidia Yule binti. Ilipofika saa nane usiku Yule mganga
alianza kufanya dawa zake, Rose alikuwa macho kabisa kwani alitaka kwanza
kushuhudia anavyofanyiwa dawa. Yule mganga alijifungia kwa mud, kisha akatoka na
kumwambia Rose, “Unahisi ni nani anayekufanyia mambo ya
ajabu?” “Ni Yule binti Salome, sijui kapata wapi
uchawi” “Hapana, anayekuchezea wewe ni Moza” Rose alishtuka na
kumuuliza mganga kwa mshangao, “Moza” “Ndio Moza, amerudi kwa
lengo moja tu la kukutesa wewe” “Kwahiyo Moza alikufa na
kurudi?” “Hapana, Moza hakufa kama unavyofikiria ila Yule unayemsema
Salome si Salome ni Moza Yule. Nimekwambia amerudi kwa kasi ya
ajabu” “Kheee, kwahiyo Salome yuko wapi?” “Salome yupo mahali na
amelala usingizi mzito sana, si mimi wala si wewe tunaoweza kumuamsha labda Moza
mwenyewe apende kumuamsha na atamuamsha endapo azma yake
ikikamilika” “Mmmh ana azma gani kwangu?” “Anataka uwaachie wale
watu uliowafungia kwenye kichumba” “Mmmh siwezi mganga, itanigharimu
maisha yangu yote, siwezi” “Anatambua hilo kuwa itakugharimu maisha yako
yote ndiomana anataka wewe mwenyewe uwatoe, huyu Moza ni amejipanga yani
amejipanga haswaaaa” “Sasa nitafanyaje?” “Inahitajika
kafara” “Nipo tayari kuwatoa kafara wale niliowafuga” “Hapana
hawatakiwi hao, kafara inayohitajika ni kafara ya mtoto wako” Rose
alipata hofu kusikia habari ya kutoa mtoto wake kafara tena, uoga ulimshika
kwani hakutaka kuona mtoto wake yeyote anakufa kwaajili yake. “Hakuna
njia nyingine?” “Hakuna, zaidi ya kutoa kafara. Ikiwa unahitaji
kuendelea kubaki kwenye nafasi yako, toa mtoto wako kafara” “Mmmh sasa
nitamtoa mtoto wangu gani?” “Mtoe mwanao wa hospitali, kwani itakuwa
rahisi sana kusema kuwa kafia hospitali sababu ya kuungua maji
moto” Kidogo maneno ya huyu mganga yalikuwa yakimuingia vilivyo Rose na
kuanza kuhisi kuwa huyu mganga ni mkweli, akafikiria kuhusu mwanae Doto ila
badae akaona ni vyema kumtoa kafara mwanae Yule mmoja na kuokoa maisha yake na
maisha ya watoto wake wengine, akamkubalia mganga na kusubiria maelekezo
atakayompa. Ila mganga alikubaliana nae kumpa masharti asubuhi ya siku
inayofuata. Asubuhi yake, mganga alimtaka Rose kwenda mtoni na
kumwambia kuwa huko ndiko ambako ataenda kutoa kafara, kuna dawa alimpa na
kumwambia kuwa ataenda kuinyunyiza mtoni halafu kingetokea kitanda cha hospitali
ambacho kalazwa Doto kisha kitanda hicho akisukumie mtoni hapo atakuwa
amefanikiwa na kumtoa kafara mtoto wake, Rose aliona hilo swala ni jepesi kwake
kwani halikuwa sharti gumu kumfanya shindwe kulitekeleza, kwahiyo alichukua hiyo
dawa na kuanza safari ya kwenda mtoni. Alivyofika mtoni alimwaga dawa
ile kwenye mto, ni kweli kikatokea kitanda pembeni na alipoangalia aliyelala
kwenye kitanda hicho hakuwa Doto bali alikuwa ni
Moza. Alivyofika mtoni alimwaga dawa ile kwenye mto,
ni kweli kikatokea kitanda pembeni na alipoangalia aliyelala kwenye kitanda
hicho hakuwa Doto bali alikuwa ni Moza. Rose aliogopa na mkono wake
kuanza kutetemeka hata akashindwa kukisukuma kile kitanda mtoni badala yake
alikimbia haraka haraka kurudi nyumbani kwa Yule mganga. Alifika anahema
sana, ila alimkuta mganga amechukia vilivyo, “Umefanya nini
wewe?” “Nimemwaga dawa ila hakutokea Doto, bali alitokea
Moza” “Hata kama ungemsukuma mtoni hivyo hivyo, yani ushaharibu kila
kitu” “Nisamehe” “Nikusamehe nini na ushaharibu” “Sasa
hutotoa kafara mtoto wako mmoja, itabidi utoe wawili” Rose alishtuka
sana kusikia atoe kafara ya watoto wake wawili ukizingatia huyo mmoja tu alikuwa
anafikiria sasa kuhusu wawili ataweza kweli, ikabidi amwombe mganga akafikirie
kwanza. “Hili si jambo la kufikiria ila ni jambo la kufanya
maamuzi” “Mganga nina watoto wane tu, watoto wangu wote ni wa muhimu
kwangu” “Kwahiyo wanao ni wa muhimu kuliko maisha yako?” “Sikia
ndugu yangu, yani watoto hawa ndio wamefanya siku zote hizi nihangaike sababu
yao. Yani yote haya ninayoyafanya kwenye maisha ni sababu yao, yani leo
nikawatoe kafara kweli?” “Chagua moja, kuwatoa watoto wako kafara au
wewe kuumbuka” Yule mganga akainuka na kumuacha Rose akiendelea kuwaza
kuhusu kuwatoa kafara watoto wake, aliwaza sana bila ya kupata jibu na kufanya
kama akili yake kukosa uelekeo. Yule mganga alirudi tena na kumuuliza
Rose kuwa amechagua jambo gani sasa, “Hapana kwakweli, siwezi kuwatoa
kafara watoto wangu” “Yani hapo watoto wawili tu unasema huwezi, je
ukiambiwa wote?” “Hapana siwezi” “Basi wewe ndio utolewe
kafara” Rose akashtuka na kuuliza kwa makini, “Nitolewe kafara
kwanini?” “Umekiuka masharti yangu, na mimi sipo tayari kufa kwaajili ya
ujinga wako kwahiyo nitakutoa kafara wewe” Katika vitu ambavyo Rose
alikuwa anaviogopa katika maisha yake basin i kifo, yani kwake ilikuwa ni rah
asana kusikia wengine wamekufa ila yeye hata akianza kuumwa tu basi hofu ya kifo
humkaa kichwani, kwahiyo swala la kuambiwa kuwa atolewe kafara yeye
lilimchanganya akili vilivyo hadi akajikuta anakubali kuwatoa kafara watoto
wake. “Nitawatoa hao wanangu wawili kafara” “Kwahiyo utamtoa
yupi na yupi?” “Wale mapacha” “Mapacha hata ukiwatoa wote bado
utaonekana umemtoa mmoja sababu wale wamezaliwa siku moja, kafara yao inabidi
iwe ya siku tofauti ili iwe na nguvu ila kwa siku moja itakuwa haina nguvu na
kafara ninayoitaka mimi ni ya siku moja. Mweke mwingine wa kumtoa kafara
hapo” “Ana najua haiwezekani ila Sara, jamani yani nimtoe mwanangu Sara
kifungua mimba wangu! Nampenda Sara jamani, tafadhari nisimtoe
Sara” “Unatakiwa kumtoa, ndiomana nimekwambia kama huwezi basi kafara
tukutoe wewe” Kwa kuhofia kifo akajikuta anakubali kuhusu kuwatoa watoto
wake kafara, kwahiyo kilichofatia ni mganga kumpa masharti ya kafara anavyoitaka
iwe, kwahiyo Rose alikuwa makini kabisa kusikiliza mlolongo wa
kafara. Mr.Patrick alimuaga Neema kuwa anaenda kumchukulia kitu
Fulani ila hakutaka kumtajia, ukweli ni kuwa alijiona mwenye bahati sana
kupokelewa tena na Neema na alimuona Neema ni mwanamke mwenye upendo sana juu
yake. Aliondoka nyumbani hapo kwa Neema na alienda kwenye nyumba
nyingine aliyowahi kujenga ili aiangalie kama inafaa kumuhamishia Neema hapo,
ila wakati yupo kwenye ile nyumba mara wakaja vijana watatu na kumsalimia kisha
wakajitambulisha kuwa wao ni wafanyakazi wa Rose, kwahiyo Patrick alitulia
akiwasikiliza kwa makini kuwa wana jambo gani wanalotaka kuongea
nae, “Sikia tukwambie, kuna kazi mama alitupa ila kazi yenyewe sijui
alipanga yale mazingira tumekuta mambo hayaeleweki kabisa, halafu tunamtafuta
hewani hatumpati” “Hata siwaelewi mjue” “Hutuelewi kivipi kwani
kazi za mkeo huzijui?” “Bado siwaelewi” “Sisi tunamtafuta hewani
tumpe habari kuwa ile maiti tuliyoendaga kuitupa tumeenda kuifukunyua tumekuta
imeoza na ananuka vibaya ila sura ni ya Yule ndugu yake aliyetupa
kazi” “Maiti? Bado siwaelewi” “Huyu mzee vipi jamani, hatuelewi
nini? Hebu toa simu yako umuonyeshe picha za ile maiti
tulivyoikuta” Mmoja akatoa simu na kumfungulia picha Patrick aione,
kwakweli Patrick alitamani kuruka, picha ilionyesha maiti kaoza oza ila sura
yake inatambulika bado na ilikuwa ni sura ya Ashura. Kwakweli Patrick hakuweza
hata kuitazama mara mbili na kuamua kuwauliza tena, “Inamaana mmemuua
Ashura?” “Hapana ila sisis tulipewa kazi tu ya kutupa ile maiti na
tuliambiwa ni maiti ya mtu mwingine halafu tulikuwa tunawasiliana na huyo huyo
Ashura nahisi kuna mtu katuzunguka kamuua Ashura halafu kataka sisi tubebea
maiti tukijua ni yeye kumbe ni Ashura” “Mtu gani huyo?” “Sisi
tulitumwa kubebe maiti ya binti mmoja anaitwa Salome, na tulivyobeba tulijua ni
Salome kumbe ni Ashura” Yani hapo ndio walizidi kumchanganya kabisa
Patrick kwani hakuelewa kitu chochote kile, halafu wale vijana wakaanza
kumueleza kwa utaratibu sasa jinsi ilivyokuwa ambapo kwa mujibu wa maelezo ya
wale vijana inaonyesha wazi mtu aliyemuua Ashura atakuwa ni
Salome. “Hapana, hapana kabisa haiwezekani, mwanangu Salome hawezi kuwa
muuwaji” “Kumbe ni mwanao!” “Ndio ni mwanangu” “Kama ni
mwanao kwanini mkeo alitaka tumuue?” Patrick hakuwa na jibu kwani muda
huu akili yake kama ilipoteza majira hivi, alikuwa haelewi kitu chochote kile
hakuendelea hata kuangalia nyumba aliamua tu kuondoka zake eneo
lile. Rafiki wa Rose, leo aliamka na kumkuta Yule binti
aliyemkaribisha kwake akiwa ameamka pia huku akifanya shughuli za mule ndani
hadi mama Jack akashangaa kuwa huyu mgeni ni wa wapi kiasi cha kufanya shughuli
za nyumbani kwake, kwahiyo alisalimiana nae na kumsikiliza kuwa anataka
amsaidiaje, “Mimi naomba unipeleke kwa mama yangu” “Lakini kwa
mama yako si unakujua, kwahiyo nitakupakiza tu gari uende” “Nakuomba
twende wote, napenda mama asikie mtu aliyeniokoa alinikuta kwenye mazingira
gani. Naomba unipeleke, mama yangu ana hela na atakulipa kwa shukrani
ulizomfanyia” Mama Jack akasikiliza maneno ya Yule binti ila muda
mwingine kama moyo wa imani ulimshika kwahiyo akamuomba waende mchana mchana na
Yule binti alionyesha kufurahishwa sana, “Asante sana mama yangu,
nitakumbuka ukarimu wako siku zote za maisha yangu” “Usijali binti
mzuri” Kwahiyo mama Jack alijikuta akisaidiana na Yule binti kwenye kila
kitu hadi muda ulipofikia wa kwenda nyumbani kwa binti, ila wakiwa njiani binti
alimuomba mama Jack amsindikize hospitali kumuona ndugu yake nae alifanya hivyo
bila hiyana yoyote, walifika hospitali na kumuomba mama Jack amsubiri nje ya
wodi, huyu mama alikubali ila hakuelewa kitu chochote wala hakumuelewa huyu
binti sababu hakumjua ila alimsaidia, baada ya muda kidogo Yule binti alitoka
huku akimsaidia mgonjwa wake kujikokota na kusema kuwa karuhusiwa, sababu mama
Jack alikuwa na usafiri hakuona hiyana ya kumsaidia Yule binti kumrudisha na
huyo anaedai ni kaka yake nyumbani. Rose alitulia akisikiliza
dawa anazopewa na Yule mganga, ambapo alianza kwa masharti, “Hakikisha
siku ya leo hakanyagi rafiki yako yoyote nyumbani kwako” “Hata hivyo
hakuna rafiki yangu anayepajua nyumbani kwangu” “Sawa, ukifika tu getini
utapuliza dawa hii” “Sawa, baada ya hapo” “Utaingia ndani bila
kuongea na yeyote ila cha kwanza kabisa, utaanza kumuita jina mwanao aliyeko
hospitali maana ukifanya hivyo tu mwanao kule atakufa. Kisha unajifanya ulikosea
unaanza kumuita mwanao mwingine wa Kafara, ataanguka alipo na kufa. Hakikisha
unaita majina wakati ushaingia ndani kabisa na kwenye kochi umekaa, yani ita
kamavile huna wasiwasi na kilichopo au kitakachotokea. Ukipata habari ya msiba
wa watoto wako, jifanye umechanganyikiwa na upotee nyumbani kwako yani uje huku
mpaka watakapozika. Utakaporudi watakuonyesha tu makaburi ya watoto wako ila
baada ya hapo, kila mtu mjini atakujua wewe ni nani maana mali zako zitaongezeka
maradufu na utazidi kuheshimika” “Nimeipenda hiyo ingawa wanangu
wananiuma ila hiyo ya mali zangu kuongezeka nimeipenda sana” “Ila
hakikisha nyumbani kwako asifike mgeni wa aina yoyote” “Haiwezekani
mganga, kwanza saivi watoto wote wanapaogopa pale nyumbani kwahiyo hata kualika
rafiki zao ni ngumu” “Sawa, na rafiki zako pia
wasifike” “Hawatofika, yani hakuna anayepafahamu pale” Rose
alijiaminisha vilivyo kuwa hakuna anayepajua nyumbani kwake, mganga alimpaka
dawa nyingine ya kumkinga akimwambia kuwa hiyo itamsaidia zidi ya Moza kwani
hatomuona tena kwenye macho yake na hatoweza tena
kumsumbua. Mama Jack alifika nyumbani kwakina Yule binti na
kukaribishwa vizuri sana, mama Jack hakuelewa kuwa alikuwa mtegoni maana Yule
binti alikuwa ni Salome ambapo alipitia hospitali kumchukua Doto kwahiyo mama
Jack alifika kwenye nyumba ya Rose bila kujua kuwa pale ni nyumbani kwa Rose, na
kwavile mama Jack hakuwazoea watoto wa Rose kwahiyo ilikuwa vigumu sana kwa yeye
kugundua kuwa wale ni watoto wa Rose, mtoto pekee wa Rose aliyemfahamu alikuwa
ni Ana na muda huo aliofika Ana alikuwa bado yupo
shuleni. Walimkaribisha vizuri sana huku Salome akiwaambia kuwa Yule
mama kamsaidia sana bila ya kusema kuwa kamsaidia vitu gani, ila Salome
alimuomba huyu mama asubiri mama yao atarudi nyumbani muda sio mrefu, Sara
alimuuliza Salome, “Una uhakika mama atarudi leo?” Salome
alimuangalia kwa jicho kali Sara na kumfanya Sara ainuke tu pale alipokuwa
amekaa kanakwamba alimwambia kuwa aondoke, kisha Salome akabadilisha mada na
kuanza kuongea na Doto habari za hospitali na jinsi anavyojisikia, kwavile
habari ilibadilika kidogo, Sara alijikuta akirudi tena sebleni huku akiwa
ameongozana na Kulwa ambaye alifurahi kusikia kuwa Doto ametoka
hospitali. Patrick alirudi moja kwa moja kwa Neema na kujikuta
akimueleza Neema kile ambacho kaelezwa na vijana aliokutana nao, kwakweli Neema
alishangaa sana na kuuliza kwa makini “Kwahiyo Ashura
amekufa?” “Ndio, nimeona hivi picha akiwa ameanza kuoza kwakweli sijui
kama ile picha itatoka akilini mwangu ila siamini kama Salome anaweza kutenda
kitu cha namna hiyo” “Nimeumia sana, ingawa kuna mengi nimeyagundua
kijijini lakini Ashura niliishi nae kama ndugu yangu kabisa, alikuwa kama mdogo
wangu na aliwapenda wanangu. Ila siamini kama Salome anaweza kutenda kitu cha
namna hiyo, hapana kwakweli. Salome ni mwanangu, namjua vyema sana, hawezi
kufanya jambo la namna hiyo. Salome hawezi kuua” “Hata mimi nimekataa
kuwa Salome hawezi kuua” “Naomba hao vijana watupeleke huko nikaone
jambo alipotupiwa ndugu yangu Ashura jamani nimeumia sana, sasa mbona nilikuwa
nawasiliana nae jamani aaah haiwezekani” Akajikuta akikumbuka kuwa wanae
hawa wadogo wamewahi kumwambia kuwa mama yao mdogo Ashura alianguka na povu
kumtoka halafu Salome akawaambia ni mchezo wanacheza, akajikuta
anasema, “Ina maana……” “Ina maana nini?” “Aaah tuachane
na habari hizo, jamani Ashura ndugu yangu hapana jamani. Hata kama hakuwa ndugu
yangu, hakustahili kuzikwa kinyama hivyo” Alichukua simu yake na
kujaribisha ile namba aliyokuwa anawasiliana na Ashura ila hakuipata hewani na
kumfanya hadi tumbo limuume na kuzidi kuamini kuwa itakuwa kweli ashura kauwawa
ila bado moyo wake ulikataa kuwa kauliwa na Salome kwani hakutegemea kama mwanae
anauwezo wa kuua. Rose aliondoka kwa mganga na kwenda nyumbani
kwake, alifika getini na kumwaga ile dawa kisha kuingia ndani, kwanza alishangaa
kumuona mlinzi getini kwake wakati alimshuhudia akiwa anaondoka ila hakuweza
kuongea nae kwa kuhofia kuharibu masharti ya dawa, alisalimiwa lakini hakuitikia
kiasi kwamba Yule mlinzi alifikiria kuwa Rose hajapenda kumuona
tena. Rose aliongoza hadi ndani kwake na kuingia sebleni, alishangaa
kumuona rafiki yake akiwa amekaa sebleni, halafu pembeni yake yupo Doto, Sara,
Kulwa na Salome ila kabla hajaita hata jina moja alishangaa kuona rafiki yake
akianguka chini na kuanza kujipigiza kama mtu mwenye kifafa huku mapovu
yakimtoka. Rose aliongoza hadi ndani kwake na kuingia
sebleni, alishangaa kumuona rafiki yake akiwa amekaa sebleni, halafu pembeni
yake yupo Doto, Sara, Kulwa na Salome ila kabla hajaita hata jina moja
alishangaa kuona rafiki yake akianguka chini na kuanza kujipigiza kama mtu
mwenye kifafa huku mapovu yakimtoka. Alijikuta anainama kumpa rafiki
yake huduma ya kwanza huku akimuita, “Mama Jack, jamani mama
Jack” Kile kitendo cha kumuita tu kilimfanya awe kimya gafla hata kule
kujipigiza aache, kwakweli Rose alichanganyikiwa yani kama kuchanganyikiwa sasa
hapa alichanganyikiwa tena sio kwa kujifanyisha ila ni kuchanganyikiwa
kweli. Alijikuta akikazana kumita ila kadri alivyomuita ndivyo
alivyozidi kukauka, yani watoto wake wote walikuwa wakishangaa lile tukio huku
wakitaka kwenda kumsaidia mama yao ila Salome
aliwazuia, “Muacheni” Sara alimuangalia kwa gadhabu Salome na
kumwambia, “Hivi una nini wewe? Yani mama yetu yupo kwenye matatizo
unasema muacheni, unataka tukusikilize au?” Sara akataka kwenda, ila
Salome aliwazuia na kuanza kuwaambia, “Hivi nyie hata hamjui mtu ameanza
kutapatapa sababu ya nini halafu manataka mkamsaidie, mkipata kesi ya kujibu
je?” Walitamani kwenda kumsaidia mama yao ila kuna uzito uliingia ndani
kwao na kujikuta wakiishia kuongea tu bila ya kwenda kumsaidia. Rose
alilia sana huku akimuita rafiki yake, yani kwa muda huu hata hakukumbuka kama
kakosea masharti au vipi maana alishachanganyikiwa kuwa rafiki yake kaanguka
ndani ya nyumba yake, ila kwavile yeye alikuwa na mwili na rafiki yake alikuwa
mwembamba, alijikuta akimbeba bila hata msaada wa watoto wake, alimbeba na
kumtoa nje kisha akampakiza kwenye gari na yeye kupanda kwenye gari na
kuondoka. Njiani alikuwa akiendesha kwa kasi sana kwani alikuwa
anamuwaisha rafiki yake kwa mganga kwani alijua akichelewa tu ataharibu kila
kitu na rafiki yake anaweza akapoteza maisha kweli. Ila leo ilimchukua
muda mrefu sana kufika kwa mganga kiasi kwamba aliendesha gari hadi alichoka
huku ana machungu kuhusu rafiki yake ila mara kidogo alipofika mbele ya safari
yake alijikuta akishindwa kuendesha gari tena halafu akapitiwa na usingizi mzito
sana. Pale ndani walibaki watoto wa Rose wakiwa na Yule Salome
huku wakimlaumu Salome kwanini kawakataza kumsaidia mama yao, “Hivi nyie
hamuwezi kujiongeza au? Mama yenu anajua kilichompata rafiki yake ndiomana
kambeba hapa bila msaada wa mtu yeyote sababu anajua ni kipi kimempata nan i
wapi atampeleka” “Kwani wewe Salome kuna chochote
unatambua?” “Mngekuwa misukule leo ndio mngeniuliza kuna kuna chochote
natambua, mama yenu alitaka kuwatoa kafara” Wote wakashangaa, kuwa mama
yao awatoe kafara kwa misingi ipi na kumbishia Salome kuwa mama yao hawezi
kuwatoa kafara, “Aaah ningemuacha awatoe eeh!” “Mama anatupenda
sana, hawezi kufikia hatua hiyo. Kwanza atutoe kafara kwa lipi!” “Sasa
nitamuacha awatoe kafara halafu hayo maneno yenu mkayazungumzie kuzimu
huko” “Sidhani kama umetuelewa Salome, tunauliza mama atutoe kafara
kwasababu ipi!” “Tulieni tu tena mnishukuru mie, la sivyo mngekuwa
marehemu nyie. Mnafikiri Yule mama anaenda kupona? Yule ndio basi tena, mama
yenu akirudi hapa muulizeni kuhusu Yule mama atawaambia” Walikaa kimya,
baada ya muda mfupi Ana nae alirudi ila leo ndio hakuongea na mtu yeyote kwani
alipitiliza chumbani kwake hata ndugu zake wakamshangaa kwani walijipaga moyo
kuwa Ana amebadilika ila kitendo cha kupitiliza bila kuwasalimia kiliwafanya
waanze kuhisi kuwa amesharudi kwenye matendo yake. Ana hakuwaongelesha
sababu alikuwa akienda kwenye dawa zake, na aliweza kutazama na kuona mama yake
alipewa masharti ya aina gani na alitaka kufanya nini na kitu gani kimetokea,
Ana kwa kutumia dawa yake mara nyingine alikuwa na uwezo wa kuona matendo
yaliyotokea ila tu hakuweza kuona matendo yatakayotokea, kwahiyo aliweza kuona
masharti ambayo mama yake alipewa na alichokifanya hadi ameondoka. Ana
akahisi kuwa mama yake amerudi tena kwa Yule yule mganga, aliweza kuangalia njia
vizuri kwa dawa zake na kuiona, kisha akabalisha nguo za shule na kuondoka tena
bila ya kuongea chochote maana alitaka akakutane na mama yake na amzuie
kutokwenda tena kwa Yule mganga kwamaana kunapoendelea aliona mama yao anaweza
kumtoa kafara hata yeye ukizingatia anaogopa kufa. Kwahiyo aliwaacha
wote wakiwa wanamshangaa anatoka hadi anaishia zake, walimuangalia tu na
hawakuelewa kuwa alikuwa anaenda wapi. Usiku ulimkuta Ana akiwa
njiani na kuamua kwenda kulala hotelini, ingawa alikuwa anajiamini sana ila
hakutaka kutembea usiku ule peke yake. Alijiaminisha kuwa asubuhi ya siku hiyo
angeondoka zake, pale hotelini alienda kula kwanza na kusikia watu wakipiga
stori huku wakisema kuhusu wachawi, “Yani wachawi bhana hakuna
kinachowashinda, natamani kuwa mchawi” “Mimi ningekuwa mchawi ningekuwa
naingia benki kuchukua hela si mchawi bhana hawanioni” “Mimi ningekuwa
mchawi wangenikoma mtaani kwangu, yani ukiwa mchawi hakuna kitu
kinachokushinda” Ana alitabasamu na kuinuka kisha kuingia kwenye chumba
alichokodi huku akijaribu kuzitafakari akili za wale watu kuwa wana akili mbovu
na wanaona kuwa mchawi hakuna kinachoweza kukushinda wakati wao Salome tu
anawatoa jasho. Ila kadri alivyokaa mule ndani alijisikia kwenda kuwafundisha
adabu wale wote waliokuwa wanazungumzia mada za kichawi, na usiku wake alienda
kuwatembelea kwa uchawi na kwa bahati mbaya alimuua mmoja wao na kurudi kwenye
chumba chake huku akijiambia kuwa hakutaka kuua ila Yule mmoja kiherehere chake
kimemponza ila yeye binafsi hakutaka kuua, toka muda huo hakuweza kulala hata
alivyorudi kwani muda mwingine roho ya kibinadamu inamjia na anaona huruma ila
muda mwingine anaona ni sawa kwa Yule mtu kufa. Kulipokucha alisikia kelele za
vilio sehemu ile na kuamua kuondoka zake kwani hakutaka kusikiliza kelele za
vilio vya msiba aliosababisha mwenyewe. Kwahiyo aliendelea na safari
yake ya kwenda alipoenda mama yake. Salome alirudi nyumbani
kwao siku ya leo na kumkuta mama yake na baba yake wanataka wajiandae kwenda
kuwatafuta wale vijana ili wawaonyeshe ile maiti ya Ashura na waifanyie
utaratibu wa maziko, aliwauliza kuwa wanajiandaa kwenda wapi, “Mwanangu,
kumbe mamako mdogo Ashura amekufa” “Kwani nyie
mmejuaje?” Wakamshangaa vile ambavyo hajaonyesha kushtushwa hata kidogo,
kisha Patrick aliamua kumueleza vile ambavyo alikutana na wale vijana na jinsi
walivyomueleza na kushutumu kuwa atakuwa ni Salome ndio kahusika na kumuua
Ashura, ila cha kushangaza Salome akacheka na kuwafanya waangaliane kwa zamu
maana hawakumuelewa anachochekea kisha akamuuliza Patrick, “Ni ushahidi
gani wamekuonyesha kuwa Ashura amekufa?” “Wamenionyesha picha ya maiti
yake ikiwa imeharibika sana” “Matapeli hao” “Matapeli!
Kivipi?” “Msiwafatilie hao ni matapeli, watawatapeli na kuwafanya muumie
tu. Hakuna cha mwili wa Ashura wala nini, amekufa wakati tunawasiliana nae kila
siku! Achana na hao” Kisha Salome akaenda chumbani kwake na kufanya
Patrick na Neema wazidi kupatwa na maswali, ila bado hawakutaka kubadili wazo
lao la kuwatafuta hao vijana ili kama ni kweli basi wamzike Ashura sehemu
stahiki, kwahiyo wakaondoka hivyo hivyo. Walifanya ile safari yao, ila
wakiwa njiani wakashangaa gari yao ikisimamishwa kisha kijana mmoja wapo kati ya
wale vijana ambao Patrick aliwaona jana aliwasimamisha halafu akawasalimia na
kuwaambia kuwa ataenda kuwaonyesha ulipo mwili wa Ashura kwahiyo walipanda nae
kwenye gari na kuanza safari ila walivyofika mbele ya safari, walishangaa
wakishikwa na usingizi na kulala kwenye gari tena fofofo kamavile wapo
kitandani. Nyumbani nako ambapo walikuwepo Kulwa, Doto na Sara
walikuwa wakizungumzia kuhusu tukio la jana yake, kuhusu Yule mtu ambaye alienda
na Salome nyumbani kisha kurudi mama yao na Yule mtu kuanguka akitapatapa kisha
mama yao kumbeba na kuondoka nae, walikuwa wakijiuliza sana kuhusu lile tukio na
jinsi mdogo wao alivyorudi kutoka shuleni na kuondoka ambapo mpaka siku hiyo
hakuwa amerudi nyumbani, “Ila jamani mara nyingine kwenye hii nyumba
tunafanya vitu kama tumerogwa vile, hivi kweli sisi tunalala kabisa wakati mdogo
wetu hatujui alipo! Bora mama ni mtu mzima ila Ana bado mdogo
sana” “Weee Kulwa nawe umeanza kuugua kichaaa nini, si ulimuona mwenyewe
akitoka hapa jana mbona hukumuuliza mdogo wangu unatoka unaenda
wapi?” “Yani wewe Sara badala umuhurumie mtoto wa kike mwenzio eti na
wewe unamkandamiza na kuona ni sawa kabisa Yule mtoto kutokurudi
nyumbani” “Mimi dada ila nyie ni kaka zake, mmeshindwa kuwa na sauti
kweli kwa mdogo wenu wa kike? Kumbukeni nishawahi fanywa kipofu, nishawahi
fanywa bubu na huyo mnaemuita ni mtoto, Ana ni mtoto kwa nje ila ndani ni
mkubwa” “Mmmh jamani Sara, sasa unashauri nini?” “Mimi mwenyewe
roho inaniuma sana kuhusu mama na Ana, mama yetu amekuwa mtu wa kutojielewa
kabisa siku hizi kwakweli roho inaniuma sana ila nashindwa cha kusema. Kuna kitu
nikiwaonyesha kaka zangu na nyie pia mtashangaa sana” “Kitu gani
hicho?” “Ndani ya nyumba hii, kuna chumba cha siri cha mama ambacho
hatukijui ila cha kushangaza Salome alikijua” Wote walishangaa kusikia
habari za chumba cha siri na wakatamani kwenda kukishuhudia hiko chumba cha siri
walichoambiwa. Patrick na Neema walikuwa kwenye usingizi mzito
sana, ila aliyekuwa wa kwanza kushtuka alikuwa ni Neema ambaye alimuamsha
Patrick walishangaa wakiwa nyumbani tena wakiwa wamechoka sana hata vichwa
vilikuwa vinawauma na kuwafanya kutokukumbuka kwa muda huo huo kuwa walikuwa
wapi mara ya mwisho, muda kidogo Patrick akakumbuka tena akiwa na macho ya
usingizi bado na kumwambia Neema, “Si tulikuwa kwenye gari
sisi?” Neema nae akakumbuka vilivyo ila nay eye macho yalikuwa mazito
hatari, yani yalizingirwa na usingizi, “Ndio tulikuwa kwenye gari
tunaenda kufata mwili wa Ashura. Yuko wapi Yule kijana wa kutupeleka? Halafu
mbona tuko nyumbani?” “Hata mimi sielewi kabisa, tumerudije hapa? Gari
yangu imepona kweli” Patrick akataka kuinuka ili akaangalie kama gari
yake ipo lakini usingizi ukamzidia na kumfanya ashindwe hata kuinuka zaidi ya
kulala vizuri, Neema nae alipomuangalia Patrick amelala akajikuta nay eye
akilala usingizi wa nguvu tena usingizi wa safari hii haukuwa sawa na ule
usingizi wa kwanza kwani huu ulikuwa mzito zaidi. Kwahiyo wenyewe
walilala chumbani kisha Salome akawaandalia wadogo zake chakula ambapo walikula
bila kuhoji zaidi kuhusu wazazi wao, halafu akawapeleka nao kulala huku yeye
akiondoka kabisa hapo nyumbani kwao. Ana ilikuwa inamchukua mud
asana kufika kwa Yule mganga sababu alitumia usafiri wa jumuiya tofauti na mama
yake alitumia gari lake, Ana alikuwa anapanda kwenye gari hii na kushuka mbele
sababu safari yenyewe kwa kutumia madaladala ilikuwa ni ya kuunganisha
unganisha, ila Ana alikuwa akisumbuliwa sana kichwa na Yule mtu aliyemmaliza
kichawi usiku uliopita, ilikuwa ni kwenye hasira tu akajikuta akimmalizia ila
hakupanga kummalizia. Ila damu ya huyu mtu ilimuumiza sana kichwa Ana, ikabidi
atafute mto kwanza kwahiyo alivyofika kwenye maeneo ya karibu na kwa mganga
alitafuta mto kwanza na kwenda kuoga mtoni kwani yeye aliamini kuwa unapooga
kuna vitu vinaondoka kwenye mawazo yako haswa kumfikiria huyo mtu ambaye alimuua
bila ya hatia. Alichukua muda mrefu sana kuoga huko mtoni kisha
alipomaliza akavaa nguo zake vizuri tu, ila kuangalia pembeni akaona kitu
kinang’aa sana na kuhisi kuwa huenda ikawa dhahabu na kwavile kule kulikuwa
sehemu ya ndani ndani kwahiyo uwezekano wa kitu hicho kuwa dhahabu ulikuwa
mkubwa sana, ingawa Ana ni mtu mwenye machale sana ila kitendo cha kuona dhahabu
kilimaliza machale yake, akainama na kuiokota kisha kuiweka vizuri kwenye mifuko
yake kuwa ataenda nayo kila mahali na atarudi nayo mjini kwaajili ya kuiuza,
baada ya kuiweka vizuri ndipo akaendelea na safari yake ya kufika kwa
mganga. Sara aliwachukua wenzie mpaka ile sehemu aliyochukua
funguo na Salome kisha kufungua hiko chumba na kuingia ndani, wote
wakashangaa, “Inamaana siku zote hizi tulikuwa hatujui kama hiki chumba
kinaingilika au ni nini jamani mbona sielewi yani hatujawahi kukihisi hata mara
moja!” “Sasa nasikia kuna watu mama kawafungia kwenye hiki chumba,
unaambiwa ukisukuma lile kabati utaona mlango mwingine na hapo kuna chumba
kingine” Ikabidi Kulwa asukume kabati kwani hawakutaka kuandikia mate
wakati wino upo, na kweli alivyosukuma kabati aliona mlango wa chumba kingine
kinachoonekana kama choo cha ndani, Kulwa alitaka kuwa shahidi bado na
kukisogelea kile chumba kisha akashika ule mlango ila aliganda pale pale, akawa
anajaribu kuutoa mkono wake ila haikuwezekana na mara chumba kile kikaanza
kutingishika na kuwafanya wengine yaani Sara na Doto waanguke chini huku Kulwa
akiwa kaganda pale pale mlangoni na mara akaanza kukauka kama anapigwa na shoti
ya umeme. Ikabidi Kulwa asukume kabati kwani
hawakutaka kuandikia mate wakati wino upo, na kweli alivyosukuma kabati aliona
mlango wa chumba kingine kinachoonekana kama choo cha ndani, Kulwa alitaka kuwa
shahidi bado na kukisogelea kile chumba kisha akashika ule mlango ila aliganda
pale pale, akawa anajaribu kuutoa mkono wake ila haikuwezekana na mara chumba
kile kikaanza kutingishika na kuwafanya wengine yaani Sara na Doto waanguke
chini huku Kulwa akiwa kaganda pale pale mlangoni na mara akaanza kukauka kama
anapigwa na shoti ya umeme. Sara na Doto walitamani wakamsaidie ndugu
yao lakini hawakuweza kwani chumba kilikuwa kinatingishika na wao wapo chini,
ile hali ilizidi kuwa mbaya kwa upande wao na gafla ikakatika mara tu ya mlango
wa kuingilia chumba kile ulipofunguliwa na aliyeingia alikuwa ni Salome,
walibaki wakimtazama tu kasoro Kulwa kwani hata kilichoendelea hakujua na
alikuwa amekauka kama kapigwa na shoti ya umeme, alionekana Salome akipuliza
upepo kutoka mdomoni kwenda kwenye mkono ambao Kulwa alishika kitasa cha ule
mlango mwingine, na gafla alijikuta kakiachia na kuanguka chini ila akiwa vile
vile hajitambui, Salome akamwamuru Sara amkongoje Kulwa kutoka kwenye kile
chumba kwani Doto alikuwa bado na maumivu ya kuungua. Kwahiyo Sara
aliinuka na kuanza kumburuza Kulwa nje huku hofu ikiwa mmemtanda moyoni kuwa
huenda Kulwa amekufa maana alikuwa kimya kabisa kama kabigwa shoti ya umeme na
alikuwa amekauka kabisa, ila Salome alimwamuru Sara amvutie hadi nje kabisa
ambapo Sara alimburuza Kulwa hadi nje kabisa, kwa hakika alichoka maana Kulwa
alikuwa mzito sana, alimuhurumia kumburuza ila ilibidi afanye vile kwani hakuwa
na jinsi zaidi ya kumburuza tu, ukizingatia alishapewa amri na Salome kuwa
afanye hivyo kisha akarudi sebleni ambako Salome alikuwa amekaa na Doto, hapo
Sara akauliza, “Hivi Kulwa atapona kweli?” “Angekuwa haponi wala
nisingekusumbua kuwa umbebe. Na ulianzaje na wewe kuwapeleka wenzio kwenye kile
chumba?” “Hata sijui kwakweli, ila nilitaka kuwaonyesha kuwa kuna chumba
ambacho hatukifahamu humu ndani” “Haya sasa, faida yake umeiona? Kaka
yako atapona ila itamchukua muda sana kurudi kwenye hali ya kawaida, familia
mnazidi kuugua magonjwa yasiyoeleweka” “Sikuelewi” “Si huwa
mnabisha nyie siku zote kuwa mama yenu ni mchawi! Haya sasa kama mama yenu si
mchawi, kile chumba kwanini kipo kisiri? Na kwanini mtake kuumia sababu ya
kukichunguza kile chumba?” “Unajua ni vigumu sana mtu kuamini kuwa mama
yako mzazi ni mchawi” “Basi ndio hivyo, wakati nafanya kazi hapa kwenu.
Siku niliyoamua kukichunguza kile chumba nilizimia muda mrefu
sana” “Wakati unafanya kazi hapa kwetu!!!” Sara na Doto
walijikuta wakishangaa kwani waliona Salome anaongea maajabu ukizingatia kwenye
nyumba hiyo wamemjua badae sana ila yeye anawaambia wakati anafanya kazi pale
kwao, ila Salome hawakuwajibu chochote ila aliwaambia wasitoke nje mpaka Kulwa
atakapozinduka. Rose alikuja kushtuka na kugundua kuwa alilala
pale usiku mzima na kazinduka kesho yake huku mwili wa mama jack ukiwa kwenye
siti ya nyuma ya gari lake kama alivyouweka, alishangaa sana kisha kuanza tena
kuendesha gari kwa haraka haraka hadi akafika nyumbani kwa mganga ila alimkuta
akiwa amechukia sana, kwani aliposhuka tu kwenye gari lake na kukutana uso kwa
uso na Yule mganga alishangaa akifokewa na Yule mganga, “Ndio umefanya
nini sasa Rose?” “Sielewi” “Huelewi nini na umemtoa kafara
rafiki yako? Nenda kamzike sasa” Rose alihisi kuishiwa nguvu kabisa
kwani hakutegemea kama rafiki yake atakuwa amekufa, “Nisamehe
mganga” “Na bora ungewahi jana ile ile, sasa mwili umeshapoa kabisa ndio
unamleta kwangu? Nenda kazike tu” “Nisamehe tafadhari sijui cha
kufanya” “Hujui nini? Nenda kazike” “Sijapanga kumtoa kafara
rafiki yangu hata sijui imekuwaje” “Hivi wewe mwanamke una akili gani?
Mwanzo si nilikutuma na dawa mtoni wewe nikakwambia ukimwaga utamuona mwanao
kitandani halafu msukume mtoni, ila wewe ukamuona sijui Moza wako ukakimbia na
hukuweza kumsukuma, sasa nimekupa dawa umwage mlangoni kwako, usiongee na mtu
yeyote zaidi ukifika ndani uanze kutaja majina ya unaowatoa kafara. Ni kweli
hujaongea chochote ila umeanza kumtaja rafiki yako huyu, ulikuwa na mpango gani
nay eye zaidi ya kumtoa kafara tu. Na hiyo kafara haikusaidii chochote ni kama
umetoa sadaka tu, haya nenda kazike mzoga wako” Rose alijikuta akikosa
nguvu kabisa kwani haya mambo yalivyoenda ndivyo sivyo yalizidi kumchanganya
akili na akaona kunapoelekea sasa hata yeye binafsi atajikuta amejiua kwa presha
au kwa namna nyingine yoyote maana hakuelewa chochote, hakujua aanzie wapi
kuzika au aishie wapi. “Sasa mimi nitamzikaje?” “Kwani hujui
watu wanazikaje? Wewe mwanamke ni mjinga sana, rafiki yako kakusaidia kakuleta
kwangu halafu umemtoa sadaka, yani wewe mwanamke ni mpumbavu” “Nakuomba
mganga tumsaidie rafiki yangu kwa namna yoyote ile” “Tumsaidie nini na
mwili umepoa huo? Labda utoe kafara ya watoto wako wote” Rose
alichanganyikiwa kabisa, ila Yule mganga aliondoka na kwenda kwenye chumba chake
cha uganga na kumuacha Rose akiwa na mawazo yasiyo na kifani. Aliwaza
kuhusu watoto wake na kuona kuwa vyote alivyovifanya kwa kipindi chote ni kazi
bure, “Hivi mimi si ndio nilimtesa yule mwanaume yani Patrick na
kumfanya kama ndondocha sababu ya watoto wangu! Nilitaka waishi vizuri, wale
raha ya maisha, yani leo nikawatoe wote kafara kweli! Hao wawili wenyewe
nilikubali kwa shingo upande, naweza kuwatoa kafara watoto wangu kweli! Kuna
sababu gani ya mimi kuendelea kuishi na kutafuta mali kwa haj azote ikiwa watoto
angu nimewatoa kafara, kuna faida gani ya kuishi vizuri huku nikinyooshewa
vidole na watu kuwa niliwatoa kafara watoto wangu! Nawapenda sana, niishi bila
Sara, Kulwa, Doto na Ana kweli! Hapana kwakweli, na huu mwili wa rafiki yangu
sijui nitafanya nao nini” Aliwaza sana bila ya jibu la mawazo yake na
alijihisi ni mkosanji kila alipofikiria kwani aliona anapoelekea sasa sio
kuzuri, yani awatoe watoto wake wote. Yule mganga akamtuma mtu ambaye
alienda kumuita Rose na kuingia kwenye chumba cha mganga, na baada ya kuingia tu
aliulizwa alichokiamua, “Utaenda kumzika rafiki yako au utawatoa watoto
wako kafara?” “Nitaenda kumzika rafiki yangu” “Yani wewe naelewa
sasa kwanini wachawi wenzio hawashirikiani na wewe, yani wewe uchawi wako mkubwa
ni kutegemea nguvu za waganga wa kienyeji, hakuna mchawi ambaye hatoi kafara,
wewe ni mchawi gani wewe? Nakuuliza mara ya mwisho, utaenda kumzika rafiki yako
au utawatoa watoto wkao kafara?” “Nitaenda kumzika rafiki
yangu” Mganga ilibidi acheke huku akisikitika, alimuangalia kwa makini
sana Rose halafu akamwambia tena, “Nakupa machaguzi ya mwisho, nenda
kafikirie kati ya kumzika rafiki yako na kuwatoa kafara watoto
wako” Rose alitoka tena na kukaa chini ya mti huku kichwa chake kikiwa
kimejawa na msongo wa mawazo. Kulwa alishtuka kama mtu
aliyeshtuka usingizini halafu moja kwa moja akakimbilia ndani huku akihema sana,
ni Sara aliyeenda kumdaka maana haikujulikana kuwa alitaka kukimbilia chumba
gani ukizingatia Salome alishawaambia kuwa akili yake itakuwa kidogo inasumbua
kufanya kazi kwa kipindi hiko kutokana na kuanguka kwenye kile
chumba. Kwahiyo Sara alimshikilia kaka yake huku akimsihi kuwa akae
kwanza akili itulie, ila Kulwa alipokaa tu alianza kuropoka kuwa kuna vitu
aliviona wakati amelala, “Vitu gani hivyo?” “Kwanza mama yuko
wapi?” “Hayupo, unajua fika mama tangu jana aliporudi na rafiki yake
kuanguka akaondoka nae ndio hajarudi hadi leo” “Basi nilichokiona ni cha
kweli” “Kitu gani hicho?” “Nimeona mama yupo kwa mganga, yani
Yule rafiki wa mama wa jana eti amekufa” Wenzie wakashangaa na
kuuliza, “Amekufa!!” “Ndio nilivyoona, na mama kapewa achague
chaguo moja na Yule mganga, yani aende akamzike rafiki yake au atutoe sisi wanae
kafara. Kwenye kumuona kwangu yani bado mama anafikiria kuhusu hilo swala kuwa
atutoe kafara au akamzike rafiki yake” “Yani mama yetu atutoe kafara
sisi!” Doto aliuliza kwa mshangao, na Kulwa akamjibu “Ndio,
kapewa chaguo hizo kuwa atutoe kafara au akamzike rafiki
yake” “Haiwezekani, haiwezekani mama kututoa kafara sisi. Hayo ni mawazo
yako tu yasiyokuwa na maana yoyote Kulwa” Salome aliyekuwa akiwasikiliza
tu akacheka sana kisha kumuangalia Doto na kumwambia, “Tena wewe ndio
usiseme kabisa, nadhani leo ndio ingekuwa mazishi yako. Mama yako alishakubali
muda mrefu sana kukutoa kafara wewe, na badae akakubali kukutoa wewe na Sara,
ila kwa ninavyomjua angekutoa wewe kwanza” Wote walikaa kimya kwanza
baada ya kusikia kuwa walikuwa kwenye orodha ya kutolewa kafara, na lile swala
aliloongea Kulwa kuwa mama yao yupo kwenye machaguzi ya kuwatoa kafara wao au
kumzika rafiki yake. Doto alijikuta akiuliza, “Jamani sasa tutafanyaje
ikiwa mama atapanga kututoa kafara wote?” Kulwa akawaambia wenzie kwa
msisitizo, “Jamani sikilizeni, kama mama alipanga kuwatoa kafara nyie
mwanzoni ila Salome alipokuja na Yule mgeni wote tulimshangaa ila kumbe ndio
ametolewa sadaka kwaajili yenu. Hapa hatuna budi zaidi ya kumwambia Salome
atusaidie” Kisha akamgeukia Salome na kumwambia, “Salome
tusaidie maana kwajinsi nilivyomuona mama anasuasua kwenye ndoto kwa hakika
atachagua kututoa kafara tu, naomba utusaidie” Sara nae
akachangia, “Kweli Salome tusaidie” Sasa nyie mnaniombaje hivyo
binadamu mwenzenu badala mmuombe Mungu awasaidie, ombeni Mungu awasaidie na
muelewe kuwa mama yenu sio mtu mzuri, kila siku nawaambia kuwa mama yenu sio mtu
mzuri ila hamtaki kuelewa ila muelewe sasa, na mkitaka niwasaidie tushirikiane
kwa pamoja ili mama yenu aachane na uchawi na arudi kwenye maisha wanayoishi
binadamu wa kawaida” “Kwahiyo ni kweli mama kahifadhi watu kwenye kile
chumba kidogo?” “Yani siku wakitoka mtashangaa sana, kwanza ni wamekonda
mno halafu watu wengine hata hamuwezi kuwadhania kama wapo humo” “Mmmh
hivi wewe Salome ni mtu wa kawaida kweli?” Salome akacheka na
kuwaambia, “Mimi ni mtu wa kawaida ila ipo siku mtanijua mimi halisia
kuwa ni nani na kwanini nilikuwa nafanya yote haya” Walijikuta wote
wakitamani kumjua Salome halisia ni nani ila Salome aliwabadilishia mada na
kuwataka kuwa wakapate chakula ila alimtaka Sara akamuite mlinzi ili siku hiyo
ale chakula pamoja na mlinzi. Sara alifanya hivyo kwenda kumita mlinzi
ila mlinzi aligoma na kusema kuwa hawezi kwenda kula ndani kwenye nyumba
hiyo. “Kwanini?” “Sitakli tu, na siwezi kuja” Sara
alirudi na kumpa huo ujumbe Salome ambaye alisema, sawa hakuna tatizo ila muda
mfupi tu mlinzi alikuwa mezani akishangaa shangaa kuwa ameingiaje ndani ya
nyumba wakati alikataa. Patrick na Neema muda huu waliamka tena
na kujiona kuwa sasa wapo sawa kiasi yani ule uchovu umepungua pungua ila muda
nao ulikuwa umeenda sana yani giza lilishaanza kutanda, waliamka na uchovu na
kutoka sebleni ambapo Neema alianza kwa kumuita Salome ila ilikuwa kimya na
kuhisi kuwa Salome hakuwepo, “Unajua huyu mtoto kipindi cha nyuma
alisema kuwa anakuja kukaa nyumbani kwako ili akae karibu na baba yake, sasa
kipindi hiki uko hapa ila mbona haonekani nyumbani?” “Labda kaenda
kujisomea na wenzie” “Aende kujisomea wapi? Yule mtoto amekataa kwenda
shule kama hujui, na ndio kwanza yupo kidato cha tatu ila kwenda shule amegoma
sijui ataingiaje hiyo kidato cha nne mwakani maana miezi inazidi kukatika
tu” “Kumbe hasomi? Kwanini umeacha mtoto hasomi?” “Sassa kakataa
shule mwenyewe unadhani mimi ningefanyaje? Hivi unakumbuka kwanza mara ya mwisho
kabla hatujarudi nyumbani tulikuwa wapi?” “Hata safari ya kurudi
nyumbani sijui imefanyajwe fanyajwe. Ila Neema mchunguze mtoto, haiwezekani
mtoto akatae tu gafla kwenda shuleni halafu wewe ukae unamchekelea tu, labda
kaanza wanaume usikute wanamuongopea” “Mmmh kama nakumbuka kitu hivi,
Salome aliniambiaga ana simu umemnunulia wewe” “Mmmh sijawahi kumnunulia
Salome simu” Neema machale yakamcheza na kuanza kuhisi vile alivyoambiwa
na Patrick kuwa usikute mwanae ana mwanaume ndiomana hataki shule, akaamua
kwenda kupekua chumbani kwa Salome kuwa pengine anaweza kukuta hata barua ya
mapenzi na ajuwe ni wapi aanzie na mtoto wake huyu. Wakati ameenda
kupekua chumbani kwa salome, aliona begi dogo na kulifungua, alikuta simu ila
alishtuka sana kwani ilikuwa ni simu ya Ashura. Rose aliitwa
tena na mganga ili atoe chaguo lake alilolifikiria, “Muda unakwenda
Rose, na usiku huo unaingia, chagua moja kumzika rafiki yako au kutoa kafara
wanao” “Hapana kwakweli, kuwatoa kafara wanangu hapana, nipo tayari
kumzika rafiki yangu” “Kumbuka utaenda kumzika peke yako na giza hili,
hakuna wa kukusaidia. Chagua tena” Rose hakuwa na jibu la zaidi ya
kumzika rafiki yake, “Kama umeamua hivyo sawa, inabidi azikwe leoleo
yani maiti yake isilale tena maana yatatokea majanga bure” “Majanga
gani?” “Usiniulize majanga gani, jua kuwa yatatokea majanga. Yani
unatakiwa uizike maiti leoleo, ila kwa usalama wako ukiwa unatoka hapo mlangoni
kwenda kuizika hiyo maiti usiongee na mtu yeyote Yule ila nenda moja kwa moja
kuna mahali utakuta shimo halafu utamdumbukiza rafiki yako huku ukitaja majina
yote ya watoto wako baada ya hapo utarudi na kulala hapa. Nadhani
tumeelewana” “Ndio tumeelewana” “Haya lamba dawa hii na usiseme
chochote” Rose akalamba ile dawa na kutoka nje, ila kabla hajalisogelea
gari lake akashangaa kumuona mwanae Ana akiwa amemfata kule kwa mganga,
alishangaa sana na kujikuta akisema, “Ana!” “Ndio ni mimi mama,
nimekufata nata……” Ila kabla Ana hajamaliza sentensi yake, Rose
alianguka chini na kuanza kutapatapa. Rose akalamba ile dawa na
kutoka nje, ila kabla hajalisogelea gari lake akashangaa kumuona mwanae Ana
akiwa amemfata kule kwa mganga, alishangaa sana na kujikuta
akisema, “Ana!” “Ndio ni mimi mama, nimekufata
nata……” Ila kabla Ana hajamaliza sentensi yake, Rose alianguka chini na
kuanza kutapatapa. Ana alipatwa na hofu sana baada ya kumuona mama yake
katika hali ile ila gafla alijikuta akipata wazo la kutoa lile jiwe la dhahabu
ila hakujua kuwa afanye nalo kitu gani. Akalitoa lile jiwe la dhahabu na
kujikuta akilishika na kuliweka kwenye kifua cha mama yake na gafla wakatoweka
mahali pale. Mganga alikuwa pembeni akiwaangalia na akiangalia
kinachoendelea kwahiyo alishangazwa sana na kuona kuwa gafla watu wale
hawaonekani ila gari ya Rose ilibaki pale pale na mwili wa mama Jack ulibaki
mule mule kwenye gari, mganga alishangaa sana na kumwambia msaidizi
wake, “Mwanamke mshenzi sana Yule, ananiletea uchawi wake kwenye nyumba
yangu pia! Kaacha maiti yake hapa, akimaanisha nini? Na nitamkomesha kwakweli
yani nitamkomesha haswaa” Msaidizi wa mganga alikaa kimya kwani hata
yeye hakuelewa kitu chochote kile kinachoendelea, na pia hakuelewa kuwa yeye na
mganga watafanya nini na maiti ambayo imeachwa ndani ya
gari. Nyumbani kwa mama Jack napo hawakuelewa kabisa kuhusu
mama yao, walijaribu kuulizia sehemu mbali mbali ila hakuna mahali walipopata
jibu la kueleweka, ila wakakumbuka tu kuwa mara ya mwisho mama yao alimsindikiza
Yule binti aliyemuokota na kuamua kumpeleka kwao, watoto wake walijiuliza kuwa
bora hata wangeenda na mama yao kumsindikiza ila kwavile waliona ni mtu mzima
basi wakamuacha aende mwenyewe ila kitendo cha kutokupata mawasiliano yake na
kitendo cha kutokurudi nyumbani kiliwapa hofu kubwa sana, walijiuliza maswali
mengi bila majibu na mwisho wa siku walipanga kuwa wakatoe taarifa polisi maana
walihisi kuwa huenda mama yao ametekwa na watu wenye lengo la kumuibia gari
sababu aliondoka na gari, basi wakakubaliana kufanya hivyo ila walipotoka nje
walishangaa kuona gari ya mama yao iko pembeni kama vile alirudi na kuondoka
tena bila ya gari, “Jamani gari imerudije?” “Lazima alirudi
jamani, inawezekana vipi gari lirudi lenyewe?” Wakalisogelea gari lake
na kulichunguza, funguo za gari zilikuwa mlangoni na kila kitu kwenye gari
kilikuwepo kasoro tu mama Jack ndio hakuwepo, ila kwavile waliona gari wakajipa
matumaini kuwa atarudi tu na kuacha kwenda kutoa ripoti polisi, “Maana
kama karudisha gari basi yupo hapa hapa mtaani atakuja tu, na akiona tumeenda
kutoa taarifa polisi atatuona sisi ni wajinga sana. Bora tumeona gari kidogo
mioyo imetulia” “Hivi lakini mama arudishe gari halafu asiingie hata
ndani?” “Labda sehemu aliyokuwa anaenda ni ya muhimu sana, atakuwa kwa
majirani tu huko sidhani kama kaenda sehemu ya mbali aache
gari” Wakakubaliana kuwa atakuwa mazingira hay ohayo na kuwafanya hofu
iondoke kwenye mioyo yao kuwa mama yao yupo. Wakina Rose
waliamua kwenda kulala sababu usiku ulishafika, ila Salome aliwaaga kuwa
anaondoka muda huo. “Kheee mbona usiku tayari?” “Aaah kuna
umuhimu wa mimi kuondoka muda huu, natakiwa niwahi nyumbani” “Kwanini
usingelala hapa ukaondoka kesho asubuhi?” “Hivi mmeshaniona nikilala
hapa toka siku mama yenu alipotaka kufanya mambo ya ajabu kwenye chumba change?
Mi naenda kulala nyumbani kwetu” Wakatazamana ila hakuna aliyemjibu la
zaidi, kisha Salome akaondoka zake na kuwaacha wakijadiliana, huku Doto akiuliza
kuwa ni mambo gani ya ajabu ambayo mama yao alitaka kuyafanya chumbani kwa
Salome. “Jamani mimi kama nilisikia sikia tu kuwa eti mama alitaka
kuzini na mlinzi wetu” Wote wakashangaa na kuuliza kwa makini huku
wakimfikiria mama yao na Yule mlinzi wao, “Hivi kweli mama anaweza
kufikia hatua hiyo ya kutaka kuzini na mlinzi wetu? Yule mlinzi si yupo sawa na
sisi tu?” “Hivi kama mama ameweza kutaka kututoa kafara sisi
atashindwaje kutaka kuzini na mlinzi? Mama yetu kawa na mambo ya ajabu,
tutakataa hilo ila ndio ukweli huo, mama amekuwa na mambo ya
ajabu” “Mimi naona tusiendelee kujadili tena mambo hayo, jamani tunataka
kwenda kulala na mkumbuke kuwa mimi nalala peke yangu” “Hivi unaweza
kwenda kulala chumbani kweli leo?” “Basi nawaomba jambo moja, tulale
wote sebleni jamani” Wakakubaliana na Sara kuwa wote walale sebleni kwa
usiku wa siku hiyo. Swala la Neema kukuta simu ya Ashura kwenye
begi la Neema ni swala lililompa wasiwasi zaidi, akajikuta akitoka nayo kwa
Patrick na kumueleza kuwa ile ni simu ya Ashura na ameikuta chumbani kwa
Salome. “Hivi umesema kuwa tangia Ashura aondoke umekuwa ukiwasiliana
nae kwa njia ya ujumbe” “Ndio, hata nikashangaa kusema kuwa eti umeona
picha ya maiti yake ikiwa imeoza ila nimeshangaa zaidi kukuta simu ya Ashura
kwenye pochi ya Salome na kunitia uwoga zaidi kuwa huenda Salome anajua kuhusu
kifo cha Ashura au huenda ndio yeye mwenyewe aliyekuwa akiniandikia ujumbe mimi.
Tuseme….” Akafikiria kidogo kuwa Salome ndio kamuua Ashura, akajikuta
akitikisa kichwa chake na kusema, “Hapana, mwanangu sio mkatili kiasi
hicho. Mwanangu hawezi kuwa amemuua Ashura, kwanza kwa lipi baya alilofanyiwa na
Ashura hadi amuue? Hapana kwakweli, haiwezekani yani haiwezekani
kabisa” Patrick akamshauri Neema kuwa awashe ile simu ya Ashura ili
wajaribu kuangalia kuwa ni namba gani zimewahi kupigwa na ujumbe mingapi
iliyowahi kujibiwa kwenye simu hiyo. Basi Neema akajaribu kuwasha simu ile ila
haikuwaka na kugundua kuwa haikuwa na chaji kwahiyo ikabidi aiweke kwenye chaji
huku wakiwa na hamu ya kujua kuwa ni watu gani wamekuwa wakiwasiliana nae kwenye
simu ile. Muda kidogo alijaribu tena kuiwasha ila iliwaka na ilipowaka
tu kuna ujumbe ambao inaonyesha ulikuwa unasubiri kuingia kwahiyo uliingia muda
huo huo, ilionekana ni namba mpya ambayo haijatunzwa kwenye simu hiyo ndio
imemtumia huo ujumbe, ujumbe ule ulisema, “Umeona mambo uliyoyafanya
sasa Ashura yani umenivurugia kila kitu, huyu Salome amekuwa mtihani mkubwa sana
katika maisha yangu. Nilikutuma umamalize ila ukakimbia bila ya kummaliza, sasa
huyu mtoto amekuwa na nguvu za ajabu na anataka kunimaliza mimi. Je utafurahi
ukisikia ndugu yako nimemalizwa na huyu mtoto wa laana? Sijapendezewa kabisa na
ulichofanya” Neema na Patrick walitazamana kwani kuelewa huo ujumbe moja
kwa moja ilikuwa ngumu kabisa ukizingatia mtumaji wa ujumbe ule hawakumfahamu,
hivyo wakaamua kufatia mazungumzo kwa namba hiyo na jumbe zilizotumwa, mwishowe
waligundua kuwa mtuma ujumbe alikuwa ni Rose na walishangaa sana kwani waliona
hadi jinsi Rose alivyopanga mipango ya kummaliza Salome kwa kushirikiana na
Ashura yani hadi walijikuta wakishindwa kuangalia jumbe zingine zaidi ya zile
kwani ziliwatisha kwakweli, “Yani kumbe Ashura nilikuwa naishi nae
halafu anajuana na Rose! Kumbe alipanga mipango ya kumuua mwanangu! Sielewi
kabisa sielewi” Patrick alikuwa kimya tu kwani yeye ndio hakuelewa
zaidi, muda kidogo walisikia mlango wa sebleni ukigongwa kisha Neema kwenda
kufungua, alikuwa ni Salome ila Neema alishindwa hata kumfokea Salome kwa kurudi
usiku huo nyumbani kwani jumbe za kwenye simu ya Ashura zilikuwa zimemtisha
sana, badala yake alijikuta akimkaribisha ndani na kumuuliza kuhusu Ashura kama
ana mpango wa kumuua yeye alijuaje na je imekuwaje hadi simu ya Ashura ipo
kwake, “Mama na Baba naomba niwaeleze kwa ufasaha kabisa, kama mmesoma
hizo jumbe mtakuwa mmapata maana kuwa Ashura alikuwa ni mtu wa aina gani katika
maisha yetu. Mama ulimchukulia Ashura kama mdogo wako ila kiukweli kuna kazi
alipewa ndiomana alikuja kukaa hapa, Ashura na Rose hawakumuweza Salome sababu
alikuwa na kinga thabiti kutoka kwa marehemu mama yake na
Patrick” Walimshangaa kuwataja majina yao ila kwavile walitaka kujua
zaidi ndiomana walikuwa wakimuuliza tu maswali kuhusu Ashura, “Eeh
mwanangu hebu nieleze vizuri, ilikuwaje tena yani ilikuwaje hadi kutaka kukuua
wewe na ilikuwaje hadi simu yake ipo kwako?” “Mama, nilimsikia kwa
masikio yangu akiongea na simu kuhusu dawa ya kuweka ili wanimalize, ndipo
akaandaa chakula na kuniwekea hiyo dawa kwenye chakula ila mimi nilifanya mchezo
wa kumbadilishia sahani ya chakula na ndipo alipokula alianza kutoka povu na
kutapatapa na akawa kimya hapo hapo kumbe ilikuwa ni sumu kali sana ya kuua kwa
muda mfupi. Nikachukua simu yake na kugundua kuwa kuna vijana alizungumza nao
kuja kubeba mwili wangu, kwahiyo nikampakia yeye kwenye viroba na kuwatumia wale
vijana ujumbe kuwa waje wabebe tayari ila mimi niliondoka kwani nilipata pesa
kwenye begi la Ashura na kuja kutafuta nyumba. Kwahiyo wale vijana walijua
wameenda kunitupa mimi. Nilifanya hivyo kwasababu ni kesi kukutwa na maiti tena
imeuwawa kwa sumu, nilifanya hivyo kuficha ushahidi kwani hata yeye alipanga
kufanya hivyo” Neema alishindwa kuwa alie au acheke kwani hakujielewa
kabisa, siku zote alimchukulia Ashura kama mdogo wake ila hakuelewa kama Ashura
alikuwa akimzunguka, ndipo akaelewa jinsi alivyoulizia habari za Ashura kwa
mamake wa kambo na kuambiwa kuwa huyo mtu hawamtambui kabisa, alijaribu
kuunganisha picha ya jinsi alivyokutana na Ashura na kupata jibu ya maswali
aliyokuwa akimuuliza na kujua kuwa Ashura alitumwa katika maisha
yake. Salome akawaeleza vingi sana kuhusu Ashura na kuwafanya wabaki
wameduwaa tu na hawakuelewa chochote kile, yani Neeema hakujua alie kwa kupata
uhakika wa kifo cha Ashura au acheke sababu mwanae kanusurika na kifo,
walijikuta wakikaa kimya tu wakitafakari kuhusu Ashura na kutumwa na Rose, yani
Patrick alijikuta akijutia maisha yake, “Najuta kumfahamu Rose, najuta
kuanza kufanya biashara na mwanamke huyu. Alinifanya niifukuze familia yangu,
amefanya nisiwathamini wanangu, amefanya mamangu auwawe kikatili, amenifanya
niwasahau ndugu zangu, amefanya niwe kama ndondocha kwenye mali zangu mwenyewe.
Najuta, amefanya niamini maneno ya Ashura kuwa ni ya ukweli sababu ni ndugu yako
kumbe ni mtu ambaye amempanga kuja kuharibu maisha yetu, huyu mwanamke sijui
nimfanye nini? Yeye ni mchawi ila mimi nitamfanyia kitu cha kawaida tu ambacho
hatokisahau maishani mwake” Patrick alionyesha kutokufurahishwa kabisa
na mambo ya Rose, waliinuka na kwenda kulala ila si Patrick wala si Neema
waliopata usingizi, kwani usingizi haukuwajia hata kidogo, muda wote Neema
aliwaza alivyokuwa akiishi na Ashura jinsi alivyokuwa akishauriana nae halafu
kumbe alikuwa na mipango ya kuuwa mtoto wake, ila tu alijiuliza kuwa kama
alikuwa na mpango huo kwanini hakuweza kumuua mtoto wake wakati akiwa mdogo
kabisa ndio kutaka kumuua mkubwa vile, aliwaza sana bila ya jibu la aina yoyote
ile. Kwa upande wa Patrick nae alikuwa akiwaza tu toka siku ya kwanza
alivyomfahamu Rose na jinsi alivyotelekeza familia
yake. Asubuhi ilipofika walikuwa palepale sebleni yaani Sara,
Doto na Kulwa. Waliamka na kusalimiana, mara wakashangaa kumuona mama yao
akitoka chumbani, wakajikuta kwa pamoja wakisema, “Mama!” Muda
kidogo wakashangaa kumuona na Ana nae akitoka chumbani, na kujikuta wakisema
tena kwa pamoja, “Ana!” Ila Ana na mama yao walikuwa wakishangaa
pia kwani ilionyesha kuwa nao hata hawakujijua kama wapo hapoa nyumbani, ikabidi
Rose atoke nje ili akaangalie kama gari yake ipo, alipotoka hakuiona ile gari
ambayo alienda nayo ikamfanya ajiulize sana kuwa imekuwaje yeye amerudi ila gari
yake haijarudi? Halafu akakumbuka kuhusu rafiki yake aliyetakiwa kumzika wakati
mwili ulikuwa ndani ya lile gari, hapo bado hakuelewa, akarudi ndani na
kumtazama Ana kisha akamwambia, “Mara ya mwisho nakumbuka nilikuona wewe
ila kilichoendelea sikumbuki, imekuwaje mwanangu nimerudi
nyumbani?” “Hata mimi sielewi mama, nakumbuka ulianguka na kuanza
kutapatapa. Kuna jiwe la dhahabu nililiokota mtoni, nikachukua na kukuwekea
kifuani ila kilichoendelea sijui, ninachojua ni kuwa nimeamka asubuhi hii nipo
chumbani mwangu” “Unasema jiwe la dhahabu? Liko wapi
hilo?” “Sijui lilipo, yani mara ya mwisho ni kulitoa na kuliweka kwenye
kifua chako ila sikumbuki limekwenda wapi” “Unasema uliliweka kifuani
mwangu?” “Ndio mama” Rose alikaa chini na kuanza kulia, watoto
wake wote wakamshangaa kuwa anacholilia ni kitu gani maana wao hakwakuona cha
kushangaza na kumfanya mama yao hata alie, walimuuliza kuwa analia
nini, “Ana mwanangu umenimaliza, yani umenimaliza kila
kitu” “Kivipi mama?” Mara akaanza kuulizia kuhusu Salome na
kuacha mada ya kuwa anamalizwa, “Salome yuko wapi?” “Yupo
kwao” “Sio Salome Yule, wanangu Yule ni
Moza” “Moza!!!” Waliuliza wote kwa mshangao wa hali ya
juu, “Ndio ni Moza” “Kivipi mama?” “Nyie nieleweni tu,
Yule sio Salome ni Moza” “Mmmh kwahiyo Salome yuko wapi?” “Sijui
ila Yule ni Moza anatumia tu mwili wa Salome” Wote walikuwa wanashangaa
ila gafla wakasikia mtu akicheka na mara kidogo akatoka sebleni, na kusikia
sauti ya Moza ikisema sasa, “Unasemaje Rose?” Kila mmoja alikuwa
anatetemeka na hakuna aliyeweza kumtazama Moza
machoni. Wote walikuwa wanashangaa ila gafla wakasikia
mtu akicheka na mara kidogo akatoka sebleni, na kusikia sauti ya Moza ikisema
sasa, “Unasemaje Rose?” Kila mmoja alikuwa anatetemeka na hakuna
aliyeweza kumtazama Moza machoni. Ila sauti ya Moza iliendelea
kusema, “Waambie yote watoto wako sio unawaambia tu kuwa Yule si Salome
ni Moza, sasa Moza nimekuja mwenyewe na uzungumze yote mbele yao” Hakuna
aliyeweza kuinua uso wake wala hakuna aliyeweza kusema kitu chochote na kumfanya
Moza aendelee kuongea, “Najua hapa nitakapoondoka kila mmoja atatafuta
pa kwenda na kuogopa kurudi tena kwenye nyumba hii, ila niwaambie kuwa hakuna
mtakapoenda nisiwarudishe. Yani mkienda popote pale mtajisumbua tu kwani mimi
nitawarudisha ndani ya sekunde. Mnashindwa kuuliza kitu au kuongea chochote
sababu mnaniogopa eeh! Naondoka ila kuanzia sasa, mkinitaja tu
nakuja” Kimya kikatanda na wote walikuwa kimya kila mmoja akiogopa
kunyanyua kichwa chake na kutazama kwani hofu ilishatanda kwenye mioyo yao. Sara
aliuliza wenzie huku bado kainamisha sura yak echini, “Jamani,
ameshaondoka?” Hakuna aliyejibu ila ikabidi Sara ainue kichwa chake na
kutazama, akaona kweli ameondoka na kuwahakikishia wenzie kuwa ameondoka, hakuna
aliyeweza kucheka wala kusema neno lolote kwa muda huo kwani kila mmoja alikuwa
na mashaka na nafsi yake. Kisha aliinuka mmoja mmoja na kuelekea
chumbani kwake na kuwaacha Rose pamoja na Ana kwani walikuwa kama ni watu
waliopigwa na shoti vile maana ni kitu ambacho hakikutarajiwa kabisa kwa siku
hiyo. Walikaa kaa pale sebleni kisha Rose aliinuka na kwenda
ndani kwake, kisha akachukua simu yake na kuiwasha yani ziliingia jumbe mbali
mbali kwenye simu ile kanakwamba zilikuwa zikimsaubiri awashe tu simukwahiyo
ziliingia jumbe nyingi hata akashindwa aanze na ujumbe upi na kumalizia na
ujumbe upi, wakati anataka ajiweke sawa sasa asome akashangaa simu yake inaita,
ilikuwa ni namba ngeni ila alipopokea ndio akagundua kuwa ni wale vijana wake wa
kai ndio walikuwa wanapiga, “Mama mbona hujibu ujumbe tunakutumia,
hupatikani tatizo ni nini?” “Yani nisameheni bure vijana wangu, simu
ndio naiwasha leo. Nilikuwa na majanga mengi sana” “Basi mama, ule mzoga
tulioenda kutupa tumejaribu kuufukunyua ili tuone ni nini, mama ni maiti ya
Ashura, yani aliyeuwawa na tuliyemtupa ni Ashura” “Nini?” “Ndio
hivyo mama ni maiti ya Ashura, nadhani tulifanyiwa mchezo ndiomana namba ya
Ashura tukipiga alikuwa haongei anatuma tu meseji” Rose alihisi kushikwa
na tumbo kabisa na kumwambia Yule kijana kuwa atampigia tena, aliinuka na kwenda
chooni kuendesha yani tumbo lilimvurugika kabisa kwani alipewa habari ambazo
hakuzifikiria kabisa, yani alihisi kuwa ni vitu vingine vimetupwa ila
hakufikiria kama ni Ashura ndio alikuwa amekufa. Alitulia chooni kwa muda kadhaa
kwani tumbo lilimvurugika vilivyo ingawa hakuna chakula kinachoeleweka
alichokula ila tumbo lake lilivurugika, alirudi tena chumbani kwake na kujitupa
kitandani huku akiwaza bila ya kupata jibu, “Yani Ashura ndio
amekufa!” Hakujua kuwa aanze kupiga kelele za msiba au afanye kitu gani,
alichukua tena simu yake na kupigia wale vijana kisha akaomba wakutane nae ili
akaonyeshwe hapo ambapo walimtupa Ashura, nao wakakubaliana nao. Kwakweli leo
Rose alichanganyikiwa kabisa, kwani aliona kama likitoka hili basi linaingia
lile na kuzidi kumchanganya. Alijiandaa na kutoka sebleni ambako
aliwakuta tena wanae muda huu wamekaa sebleni kasoro Ana ndio alikuwa bado
chumbani, kisha akawaaga na kuwaambia, “Jamani natoka, nadhani badae
tutaongea vizuri” Alikuwa ni mtu mwenye hofu na mashaka halafu machozi
yalionekana kumlengalenga, kitu hicho kilifanya wanae wamuulize kuwa mama yao
anaenda wapi na kulikoni yani ni kitu gani kilichomsibu, “Wanangu,
Ashura amekufa” “Ashura amekufa?” “Ndio amekufa” Machozi
yalikuwa yakimtililika na kuondoka huku akiwaacha wanae wakijadiliana
pale. Walijiuliza kuwa huyo Ashura amekufa kivipi yani taarifa
zimeletwaje maana mama yao alionekana kuchanganyikiwa kabisa na taarifa hiyo,
Kulwa alijikuta akiwauliza wenzie, “Sasa kama mama ni muoga hivi wa kifo
hadi amechanganyikiwa kwa kifo cha Ashura, mbona alitaka kututoa kafara sisi?
Angeweza kweli kuvumilia wakati watoto wake tumekufa kwa kutolewa kafara nay
eye?” “Unajua hata mimi mwenyewe namshangaa sana mama, kama anashtuka
hivi na kifo cha Ashura je kifo chetu sisi angefanyaje!” “Mi nadhani
kwasababu kifo chetu alikuwa anakitarajia kwahiyo kisingemshtua sana, ila kifo
cha huyo Ashura hakukitarajia. Sijui kafa vipi nay eye
mmmh!” Walijadiliana sana bila ya majibu yoyote yale ya moja kwa
moja. Patrick siku ya leo aliomba asafiri kwani aliona ana
ulazima wa kufanya hivyo ili aende kwa ndugu zake, Neema hakumpinga hata kidogo
zaidi zaidi akamsaidia kujiandaa na kisha kumsindikiza kwenda kupanda magari ya
kusafiri kwenda mkoa mwingine. Patrick hakuondoka na gari badala yake aliliacha
gari lake nyumbani kwa Neema kwahiyo waliagana kisha Neema wakati wa kurudi
akapitia tena kwa rafiki yake mama Pendo ambaye baada ya maongezi mafupi bado
alimsisitizia kuwa mtoto wake ampeleke kwenye maombi, “Sasa ndugu yangu
Yule si mtoto mdogo kusema nitambeba mgongoni kwenda nae huko kwenye
maombi” “Ushawahi kuongea nae lakini kuhusu maombi?” “Sijawahi
yani kila nikitaka kuongea nae yanatokea mambo mengine najikuta sijaweza kuongea
nae, yani usinione hivi nina makubwa ndugu yangu hata siju nianzie wapi na
niishie wapi” “Inatakiwa na wewe uende kwenye maombi” “Nitakuja
unipeleke, yani akili yangu haipo sawa kabisa” Akaongea ongea nae pale
kisha akaagana nae na kwenda kupanda daladala ili aweze kurudi nyumbani kwake,
alipokuwa kwenye lile daladala kuna vijana pembeni akawasikia
wakiongea, “Yani muvi zingine za ajabu kweli yani, eti mtu anakufa mara
mtu huyo anarudi kwenye mwili wa mtu mwingine sasa huyu mtu mwingine
wanamshangaa kuwa anafanya mambo ya ajabu ambayo hajawahi kufanya kabla,
unashangaa mtu alikuwa hanywi mara gafla anakuwa mlevi kupitiliza. Yale mambo
ingekuwa kweli sijui ingekuwaje!” “Lakini kuna baadhi ya vitu ni kweli
sema tu tunapuuziaga vitu hivi” “Mmmh hivi inawezekana kweli mtu akarudi
kwenye mwili wa mtu mwingine? Hapo ikitokea itakuwaje?” “Kwani hiyo
picha iliishia wapi?” Mara wale vijna kituo chao kikatangazwa na
kushuka, kwa jinsi Neema alivyovutiwa na maongezi yao ni hakika kama ingekuwa ni
kituo cha kushuka yeye basi angepitilizwa ili aendelee kusikiliza walichokuwa
wakizungumzia. Akajiuliza mara mbili mbili kuwa inawezekana vipi kwa mtu
mwingine kuingia kwenye mwili wa mtu mwingine, kisha akaanza kuwaza jinsi mtoto
wake Salome alivyobadilika yani anatenda mambo ya tofauti kabisa na aliyokuwa
anayafanya awali, na mara nyingine anapika chakula kinachoendana na alichokuwa
akipika Moza, akaanza kujiuliza, “Inamaana Moza… Hapana haiwezekani, ile
walikuwa wanasimuliana ni muvi tu. Haiwezekani mwanangu Salome akawa Moza, Yule
ni Salome na wala sio Moza, halafu Moza alishakufa” Akawa anawaza huku
akikataa majibu yake mwenyewe anayoyawaza kwani aliona akichanganyikiwa tu, kuja
kushtukia kapitilizwa kituo chake sababu ya mawazo, kwahiyo akashuka na kupanda
gari nyingine ili aende nyumbani kwake. Alipokuwa kwenye gari nyingine
alisikia sauti ya mtu ikimwambia, “Pole kwa mawazo mama” Sauti
hiyo ilimchanganya vilivyo kwani ilikuwa ni moja kwa moja sauti ya Moza, kwahiyo
akashindwa hata kugeuka kumtazama mtu huyo kwani hofu tayari ilikuwa imeanza
kuingia kwenye moyo wake, alifika kituo chake na kushuka ila alihisi Yule mtu
ameshuka nae, na kila alipotembea kwenda nyumbani kwake alihisi kuwa Yule mtu
yupo nyuma. Alipatwa na uoga kadri alivyoongoza mwendo mpaka anafika kwenye geti
la nyumbani kwake, bado alihisi Yule mtu yupo nyuma yake, akagonga geti kwa
nguvu huku akijaribu kugeuka nyuma ili kama akikutana na maajabu basi apige
kelele, ila alipogeuka nyuma hakuona mtu yeyote, kidogo moyo wake ukatulia na
kujiona kuwa ni muoga sana ambapo alikuwa anaogopa kitu cha
mawazoni. Akajiona ni mjinga zaidi kugonga geti lake wakati linakuwaga
wazi muda wote, akalifungua na kuingia ndani, aliwakuta wale wanae mapacha
wakiwa sebleni na kuwauliza, “Dada yenu yuko wapi?” “Amerudi
muda sio mrefu yani nadhani mliongozana mama, maana muda huu huu kaingia ndani.
Yupo jikoni” Neema bado aliganda kwani alikuwa kama haelewi elewi kitu
vile, alikaa kwenye kochi huku akihema kwa nguvu ili kujitoa hofu
kwanza. Rose alikutana na wale vijana wake na moja kwa moja
wakampeleka kule wakikotupa ule mwili, nay eye aligundua tu nguo za
Ashura, “Jamani ni kweli Ashura wangu” “Ndio mama, ni Ashura
kumbe ndio tulimtupa na tukajua ni kile kitoto” “Jamani nani kamuua
Ashura wangu?” “Mama itakuwa ni kile kitoto tu ndio kimetuchezea mchezo
mchafu, labda ndio kamuua Ashura halafu akatuma ujumbe kuwa tukambebe na
kumtupa” Yani Rose hakujua cha kufanya kwa muda huo kwani vitu hivyo
vilikuwa vikimchanganya sana, hawa vijana walimuuliza kuwa ni kitu gani
kifanyike kwa mwili wa Ashura ulioharibika na kuwaomba kuwa wachimbe hata shimo
na kumzika kwani hakuelewa kuwa hata wafanyeje, “Sisi tutachimba mama
ila mshiko ndio tunaouhitaji” “Nitawapa jamani, naomba tu mchimbe bora
kidogo niwe na amani kuwa ndugu yangu hata alizikwa, yani roho inaniuma sana
kumuona Ashura katiaka hali hiyo.” Wale vijana hawakupoteza muda na
kuanza kuchimba shimo, ila wakati wanataka kumzika Ashura lile shimo lilijaa
maji na kumfanya Rose ashangae kuwa shimo limechimbwa vizuri halafu lijae maji
tena, akawaomba wale vijana wachimbe tena. Walichimba mashimo kama matatu na
yote yalijaa maji wakamwambia, “Nadhani tuzike hivyo hivyo tukisema
tuchimbe chimbe tutabambwa hapa, ujue vitu vya magendo hivi tunafanya? Na
tukikamatwa ni kifungo cha maisha hakuna atakayetuelewa, tutaonekana tuliua na
ndio tumeamua kuja kuzika mtu tuliyemmaliza” Rose hakuwa na jinsi
ikabidi wazike hivyo hivyo kwenye mimaji na kufukia, roho ilimuuma sana kuona
ndugu yake amezikwa kama mnyama, ndugu yake kazikwa kikatili na ameuwawa ingawa
bado hakuelewa kuwa dawa aliyoweka ili auwawe Salome ndio dawa hiyo hiyo
iliyomuua Ashura. Walimaliza, akawalipa wale vijana na kuondoka, alikuwa
anarudi nyumbani kwake huku ana mawazo mengi sana haswaa akiwaza kuwa afanyaje
na huyu mtu wa kuitwa Salome ilihali kashaujua ukweli kuwa huyo Salome ndio Moza
ila huyo Moza akija kwenye umbile lake la Moza asilia anatisha sana bora akija
kama Salome, na hapo akajiona mapambano ya kupambana na Salome yakimshinda
kabisa. “Natakiwa nimtafute Patrick nimwambie ukweli kuwa mwanae Salome
ni mtu mwingine” Alipanga kumtafuta Patrick ila alijaribu kupiga simu za
Patrick kwa wakati huo hakuzipata hewani zilikuwa
hazipatikani. Neema alikuwa pale sebleni ila ndani ya muda ule
ule, Salome alikuja kumwambia kuwa chakula ni tayari na kumfanya uoga umshike
zaidi kuwa amekipika saa ngapi ikiwa watoto wale wamemwambia kuwa karudi muda
sio mrefu, ila kabla hajamuuliza chochote Salome akamwambia, “Mama
unajiuliza kuwa chakula nimepika muda gani, unafikiri nimekipika sasa hivi basi?
Nilikiacha jikoni, na mimi nilienda dukani” Kidogo alivyosema hivyo hofu
ilimuisha Neema na kujikuta akiinuka kwenda kula, ila macho yake hayakuisha
kumuangalia Salome, alikuwa akimuangalia kwa jicho la wizi lakini alikuwa
akimuangalia haswa wakati anakula alimuangalia sana, kwa kawaida Salome hakuwa
na utaratibu wa kula ila alishangaa Salome wa sasa hivi alikuwa na utaratibu wa
hali ya juu hata wakati anakula hakuwa akiongea wakati Salome hadi alikuwa
akipaliwa kwa mtindo wake wa kula na kuongea. Walipomaliza kula aliamua
kuzungumza na Salome kuhusu swala aliloambiwa na mama Pendo la
maombi, “Sawa nitaenda, ila nipe sababu ya kunipeleka mimi kwenye
maombi?” “Salome umekataa kusoma, sasa unafikiri nisikupeleke kwenye
maombi kweli!” “Kusoma sijakataa ila nimekwambia nimechoka kwa kipindi
hiki na nitasoma mwakani, kwani mbali jamani mwakani si hapo tu. Halafu kitu
kingine kwani mtu asiposoma ndio ana matatizo hadi aombewe? Wangapi hawajasoma
na maisha yao ni mazuri tu” “Hatakama Salome, ila mimi ni mama yako
naomba twende kwenye maombi” “Sawa mama tutaenda” “Kesho jiandae
nikupeleke kwenye maombi” Salome alimuitikia Neema bila ya pingamizi
lolote ila muda wote Neema alikuwa akijiuliza maswali bila ya majibu huku
akijaribu kuhusisha stori za wale vijana na jinsi alivyo Salome wake, ila
alijikuta akipinga kuwa Salome wake hawezi kuwa amevamiwa na mzimu ila ni Salome
Yule Yule sema kabadilisha matendo yake. Kwa Yule mganga ambapo
Rose aliacha lile gari likiwa na mwili wa mama Jack, mganga akataka afanye jambo
la kichawi ili mwili ule urudi kwa Rose kisha Rose angejijua mwenyewe, mganga
alimchukua msaidizi wake na ule mwili kisha wakauweka kwenye kile chumba cha
mganga na kuanza kufanya dawa zake ili ule mwili uende nyumbani kwa Rose, basi
alifanya dawa zake kwa muda kama wa nusu saa na ule mwili ukatoweka machoni
mwao, mganga alijisifia, “Mimi ndio kiboko wa kila kitu” Mara
gafla ule mwili ulirudi kibandani kwake na kumfanya mganga na msaidizi wake
wabaki wanashangaa, “Imekuwaje tena?” “Nadhani kuna mtu anacheza
na akili yangu, ila sikubali” Akafanya tena dawa zake kama kwa nusu saa
hivi, na mwili ukatoweka kweli. Sasa muda huu alitaka kujua kuwa ulipo mwili ni
kitu gani kinatokea, akachukua kioo chake na kuangalia alishangaa sana kuwa muda
huo mwili wa mama Jack ulionekana nyumbani kwa mama Jack na watu kwenye nyumba
hiyo walikuwa wakishangaa tu. Akafanya tena dawa zake
kama kwa nusu saa hivi, na mwili ukatoweka kweli. Sasa muda huu alitaka kujua
kuwa ulipo mwili ni kitu gani kinatokea, akachukua kioo chake na kuangalia
alishangaa sana kuwa muda huo mwili wa mama Jack ulionekana nyumbani kwa mama
Jack na watu kwenye nyumba hiyo walikuwa wakishangaa tu. Mganga
alishtuka sana na kumuangalia msaidizi wake, “Sijui ni wapi nimekosea
yani sijui, badala mwili uende nyumbani kwa Rose eti umerudi kwa familia
yake” “Sasa tutafanyeje?” “Sijui ila kuurudisha huku siwezi,
hata mwanzo nimeshangaa ulirudi huku sasa sijui ndio ulienda nyumbani kwa Rose
au ni kitu gani halafu saivi umeenda nyumbani kwa mama jack. Sina jinsi itabidi
tu nikubali kuwa anaenda kuzikwa nyumbani kwake ingawa ni mbaya sana ila sina
cha kufanya” Msaidizi wa mganga alikuwa kimya tu huku akishangaa matukio
ya siku hiyo. Nyumbani kwa mama Jack, walishtushwa sana na
kitendo cha kukuta mwili wa mama yao upo ndani tena inaonyesha alikufa siku
mbili au tatu zilizopita, kwakweli walilia sana na kufanya wakose hata la
kufanya na mwili huo, wengine wakawaambia wakazike tu maana utakuwa na harufu,
ila walikataa kuwa haiwezekani kuzikwa bila ya kuchunguzwa kwanza, kwahiyo
wakakubaliana kuwa mwili ule ukafanyiwe uchunguzi maana hata ulivyofika pale
nyumbani ilikuwa ni kiajabu ajabu kwahiyo wakaita watu na kusaidiana kupakia
kwenye gari ili kuupeleka hospitali kwaajili ya uchunguzi, kila mmoja alikuwa
haelewi na watoto wa mama Jack walilia tu kuwa mama yao umekuja mwili amekufa
wakati walijipa moyo kuwa yupo, na kama mama yao kauwawa hao waliomuuwa walikuwa
na lengo gani maana gari halikuibiwa lilikutwa tu nyumbani ila mwili wa mama yao
umekutwa ndani, hakuna aliyeelewa moja kwa moja kuwa yale ni mambo ya
kishirikina. Basi walipanda kwenye gari na ule mwili wa mama yao ila
wakati wanakaribia hospitali ule mwili ulitoweka kwahiyo walifika hospitali bila
ya ule mwili kuwepo kwenye gari, kila mmoja alimtazama mwenzie na kufanya waanze
kuogopa sasa, huku wakirudi na gari upesi upesi nyumbani n hakuna aliyeweza
kubaki nyumbani hapo kwani wote walikuwa na mashaka muda wote, ndipo kuna ndugu
yao mmoja aliyetoa wazo kuwa waende kwa mganga wa kienyeji ili wakaangalie maana
yake hayakuwa mambo ya kawaida. Upande wa Yule mganga,
walitulia kwa muda na kuhisi kuwa ule mwili wa mama jack utakuwa tayari
umeshazikwa kwake ila walishangaa gafla mwili ukirudi kwenye kibanda chao,
kwakweli mganga hakutaka tena kushindana na zile nguvu zaidi ya kumuomba kijana
wake watafute vijana wawasaidie kuchimba kaburi kisha auzike huo
mwili, “Nitamkomesha huyu mwanamke aitwaye Rose, anadhani ni rahisi
rahisi hivi kunitesa mimi! Nitamkomesha” Yule msaidizi akaenda kutafuta
vijana nao wakachimba kisha kwenda kwaajili ya kuzika ila kaburi lilijaa maji,
mganga hakutaka kujisumbua zaidi kuwa wachimbe kaburi lingine badala yake
aliwaambia wazike hivyo hivyo kaburi likiwa na maji, nao wakafanya hivyo ili
wakimbizane na muda kwani giza lilikuwa linaanza kuingia, na walipomaliza
waliondoka zao. Rose alifika nyumbani kwake na kukutana na
watoto wake getini wanataka kuondoka, ikabidi awaulize kulikoni, “Mama
kuna vioja huko ndani, unajua tulikuwa tumekaa pale sebleni mara ikaletwa maiti
ya Yule rafiki yako na kuwekwa pale kati kati yetu yani kila mmoja hapa
alichanganyikiwa na gafla ikapotea tena” “Mmmh jamani, sio mawazo yenu
tu!” “Mawazo yetu! Mawazo wapi? Kila mmoja ameona kwakweli ni mambo ya
ajabu, hakuna anayeweza kuishi tena humo ndani” “Kwahiyo na Ana yuko
wapi?” “Yupo chumbani kwake, yeye hajatoka kabisa tangia muda
ule” “Wanangu tafadhari msiondoke, maana hata mkiondoka hamtatui tatizo
kabisa, hili ni tatizo ila halimalizwi kwa kuondoka” “Mama
tunaondoka” Mlinzi akawaambia, “Hata msijisumbue kuondoka,
mtashtukia mmerudishwa hapa hapa” Ndipo wakakumbuka na maneno ya Moza
kuwa wasikimbie nyumba hiyo kwani hata wakikimbia watarudi, pia wakakumbuka siku
ambayo walikimbia na kwenda kulala hotelini ila wote walirudishwa nyumbani
kwenye vyumba vyao, mwisho wa siku wakaona hata kukimbia ni kazi bure na kuamua
kurudi na mama yao ndani, ila walipoingia tu ndani wakamwambia mama
yao, “Mama tafadhali toa ile misukule yako kwenye kile chumba cha siri
maana ndio vitu vinavyotumika kututesa sisi” Rose aliwashangaa wanae
kuwa wamejuaje kuhusu kile chumba chake cha siri, ila Kulwa aliendelea
kujua, “Usishangae tu kuwa tumejuaje kuhusu kile chumba cha siri ila
ujue kwamba tumejua kuwa ulitaka kututoa kafara watoto wako. Mama umeugua sana
na kifo cha Ashura, hivi watoto wako sisi sio zaidi ya huyo Ashura? Sisi si ndio
uliotutolea uchungu mama, ila ukataka kututoa kafara mama ili upate faida gani?
Na kama kupata mali, utumie na nani wakati watoto wako umetutoa
kafara” Rose alikaa chini kwanza kwani hakufikiria kuwa watoto wake
wamejua habari zake za kutaka kuwatoa kafara pia, yani habari za chumba
hazijaisha zimekuja habari zingine za kutaka kuwatoa kafara. Akajikuta tu
akiongea kwa unyonge, “Nani amewaambia habari hizo wangu?” Kulwa
ndiye aliyemjibu mama yao maana leo alijitoa muhanga haswaa kwa hakika
alichoshwa na kilichokuwa kinaendelea kwenye nyumba yao. “Mama sekeseke
lilianzia kwenye chumba chako cha siri ambako mtoto wako nilipigwa na shoti,
sijui umeweka nini kwenye kile chumba. Nilizimia ila nililetwa ulipo kwa mganga
na alikupa machaguo mawili kuwa umzike rafiki yako au uwatoe kafara watoto
wako” “Lakini sikuchagua kuwatoa kafara wanangu” “Mama
hukuchagua ndio ila kumbuka kuwa ulishataka kuwatoa kafara Doto na Sara, hivi
wewe ni mama wa aina gani ambaye huna upendo na watoto wako? Siku zote umekuwa
ukihangaika kwaajili ya maisha yetu, kuhangaika kwako huku ili tule vizuri na
tulale vizuri, leo hii uliowahangaikia uwatoe kafara kweli?” “Nisameheni
wanangu” Rose alijikuta akitoa machozi tu, muda ule ule Ana nae alitoka
chumbani na kusema, “Tena nisingekuwahi mama, ungeenda tu kumzika Yule
rafiki yako basi ungetutoa kafara na sisi maana uliambiwa utaje majina wakati
unamzika, yani ungemtaja mwanao mmoja mmoja na huku ingekuwa
kwaheri” “Umejuaje Ana?” “Mama, tambua kuwa mimi nina utambuzi
mkubwa sana. Nashukuru lile jiwe la dhahabu nililoliokota maana lilikuwa na
nguvu za ajabu, mwanzoni tulipotoweka nilijilaumu kuliokota lile jiwe ila baada
ya kujua ukweli nashukuru kwa kuliokota lile jiwe. Mama hata mimi uchawi
umenichosha sasa, jamani ndugu zangu msiniogope ila nisaidieni natamani kuacha
uchawi” Wote walimshangaa Ana kuwa amebadilika hivyo kwa muda mfupi tu,
na amekubali kuacha uchawi, Sara alijikuta akimsogelea mdogo wake ingawa kwa
uoga uoga ila alimkumbatia na kumpongeza kutaka kuachana na uchawi, ila alikuwa
anampongeza huku ana mashaka bado, sema Kulwa hakuacha hoja yake kumwambia mama
yao kuwa atoe misukule aliyoiweka kwenye chumba chake cha siri, mama yao
akawaomba kuwa wampe muda kidogo ajifikirie kwanza, akainuka na kwenda chumbani
kwake. ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment