Simulizi : The Worst Valentine's Day
Sehemu Ya Tatu (3)
MWEZI MMOJA MBELE
Ilikuwa ni siku ya jumanne asubuhi na mapema nililetewa nguo nzuri zenye marashi mazuri,,ilikuwa ni suti mpya na niliivaa na leo tofauti na siku nyingine nilionekana kuwa mrembo japo nilikonda kupita maelezo lakini bado nilionekana mrembo. Leo ilikuwa ni siku ambayo Clara aliniambia ndo kuanza kusikilizwa kwa kesi yangu na leo upande wa mashitaka ndio ulikuwa unaenda kuanza kesi,,Clara alinieleza kuwa sehemu hii ya kwanza ya kesi ndiyo sehemu itakayotabiri muelekeo wa kesi kwakuwa upande wa mashitaka unatakiwa kuthibitisha kuwepo kwa kesi ya kujibu na ndipo hapo ambapo wao huleta ushahidi ili kuithibitishia mahakama kuwa nilikuwa na kesi ya kujibu,,na ikitokea wakathibitisha pasipo shaka yoyote kuwa kuna ushahidi unaonyesha kuwa nina kesi ya kujibu basi mahakama itaingia kwenye sehemu ya pili ya kesi ambapo itakuwa ni zamu ya utetezi kuleta hoja zake na ushahidi wake,,na iwapo ikitokea wameshindwa kuthibitisha pasipo shaka basi kesi inaweza kufutwa au kubadilishwa kutoka mauaji ya kukusudia mpaka mauaji ya bila kukusudia au kufutwa kabisa kwa kesi..
“Ikupendeze muheshimiwa, naitwa Clara Mshasa ni wakili wa utetezi” ilikuwa sauti ya Clara ikijitambulisha pale mahakamani.
“Ikupendeze muheshimiwa Jaji, naitwa Revocatus Mnyata ni wakili wa serikali katika kesi hii. Baada ya hapo kesi ilianza,,mwenendo wa kesi haukunipa matumaini hata kidogo ya kushinda hii kesi japo Clara alijitahidi sana lakini mazingira ya kesi hii yalikuwa ni magumu kuyatolea ushahidi wake,,hata nilipomueleza Clara ukweli wa kila jambo lililotokea alionekana kutokuamini lakini kikubwa alionekana kama vile hana matumaini ya kushinda kesi hii ila alichoniambia ni kuwa tutaangalia aina ya ushahidi ambao upande wa mashtaka utauleta na sisi tutaweka walakini kwenye ushahidi huo ili kuithibitishia mahakama kuwa kesi ile haieleweki. Pale mahakamani niliwaza mamabo mengi sana lakini kikubwa nilikuwa nikiwaza juu ya usalama wa afya yangu na motto wangu kwa sasa na zaidi juu ya hatima ya uhai wangu.
“mheshimiwa napenda kuielekeza mahakama yako tukufu kwenye kielelezo na 7 ambacho ni ushahidi wa kielekroniki na ambao ningependa mahakama yako tukufu iupokee kama ushahidi”,,aliongea yule wakili wa serikali na hapo macho yalinitoka ili nione huo ushahidi wanaousema.
“muheshimiwa tutatumia projector ili kila mmoja humu ndani aweze kuona,,hii ni nakala halisi ya kanda ambayo ilitolewa chumba ambacho kipo ndani ya nyumba ya mtuhumiwa na ni katika chumba hicho ndipo mitambo ya kamera zote zilizofungwa kwenye ile nyumba umewekwa,,,polisi walipoingia kupekua walikuta katika chumba hicho kompyuta zikiendelea kurekodi matukio yote kwenye kamera za nje na za ndani ya ile nyumba,,hivyo tuliichukua kanda iliyokuwa na tukio la siku hiyo ambapo vifo vya vya marehemu vilitokea na ndiyo kanda ambayo inamuonyesha moja kwa moja mtuhumiwa akitenda mauaji yale” yalikuwa maelezo ya wakili wa serikali na wakati huo mahakama ilikuwa kimya kabisa huku jaji akionekana kutokwa na kijasho chembamba kilichoonyesha shauku ya kutaka kujua nini kilikuwa ndani ya ule ushahidi,,nilihisi kufa hasa ukizingatia nilikuwa naenda kuona jinsi mpenzi wangu na ndugu yangu alivyouawa na watu waliotaka nichague mmoja wao ili wanywe damu yao. Ilikuwa kama filamu ya kimarekani kwa yale mambo yaliyoonekana pale kwenye ile projector,,alionekana msichana aliyekuwa amevaa hijabu nyeusi na kufunika uso wake akiingia pale sebuleni na moja kwa moja aliingia mpaka kwenye korido ambapo inaonekana kama vile Magret alikuwa ameinama na hapo ndipo alipomshtua na mage alipogeuka alikutana na kisu kilichopenya kwenye ziwa lake la kushoto na hapo yule mtu alionekana akiwa ameinama pale chini na kisha alinyanyuka akiwa amebeba kitu cheusi kama chupa,,na hapo aliinama na kuchora alama ya bikari chini kisha aliondoka pale bila kusema chochote na sasa alionekana tena kwenye korido akielekea jikoni na hapo alikutana na mtu mwingine na kumchoma tena kisu kwenye sehemu ya moyo na ilionekana kuwa mtu huyu wa sasa alionekana kuwa ni mwanaume,,kama mara ya kwanza na sasa pia aliinama na kuchora alama ya bikari kisha na ile chupa alinyanyuka nayo kisha akaingiza mkono ndani ya hijab na kutoa kitambaa chekundu kisha alijifuta uso bila kuvua kile kitambaa usoni na kisha alirudisha kile kitambaa chekundu mfukoni na hapo ndipo alipovua kile kitambaa na kisha kuitazama kamera.
“ooh god,,it’s not me,,I didn’t kill them,,”(ooh mungu,,sio mimi sijawaua mimi),,haya ndio yalikuwa maneno niliyoyatoa kwa nguvu huku nikilia baada ya kuona ile video ikionyesha sura yangu pale yule dada alipoonyesha sura yake kwenye kamera,,hapohapo Clara alinigeukia huku akishangaa,,mahakama nzima ilishtuka na sauti za watu wakinong’ona zilitanda,,,nililia kwa nguvu huku nikisema kuwa sihusiki mpaka jaji alishindwa kuendelea kusikiliza kesi ile na ndipo walipoiahirisha kwa muda ili jaji akapitie ule ushahidi vizuri na baada ya lisaa limoja mahakama ingerudi tena.
“najua huusiki kwenye mauaji,,lakini swali la msingi ni kwavipi sura yako iwe ndo sura ya yule msichana?,,yule ni nani? Ulishawahi kumuona popote?” aliniuliza Clara kama mtu aliyetaka kujua ukweli wa mambo ambayo tayari anajua ukweli,,alinyanyuka na kutembea huku na kule lakini sikuwa nimejibu lolote mpaka mda huo.
“Faith we are running out of time,,please tell me what the hell are you hiding”(Faith muda unaisha, tafadhali niambie ni kitu gani unaficha) aliuliza Clara.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“yule msichana sio mimi,,ile sura inayoonekana pale ni yangu lakini sio mimi,,yule ni Samah Bigumar, alikuwa ni mwanasheria wa familia yetu kabla ya baba yangu kufariki lakini pia alikuwa mmoja kati ya wale majini waliokuja nyumbani kwangu usiku wa valentine,,,baada ya lile tukio la siku ile niliambiwa kuwa Samah aliacha maswala ya nguvu alizokuwa anazitumikia na sasa alijiunga na freemasons na kwamba yuko karibuni kupewa kazi yake ya kwanza,,lakini sikujua kama hii ndiyo kazi niliyoambiwa atapewa” niliongea huku nikimtolea Clara macho ili aweze kunisoma vizuri na kuelewa nisemacho.
“kwahiyo sura yako imefikaje pale kwenye kamera?” lilikuwa swali lililofata baada ya kueleweka majibu ya swali la kwanza.
“wao wananguvu na uwezo mkubwa wa kutengeneza au kuharibu chochote wanapoamua,,ikiwa ni pamoja na kutengeneza sura ya mtu mwingine na kumuwekea mtu mwingine.” Nilimjibu na sasa Clara alionekana kuridhika,, alitoka nje na kuniacha pake ndani ya kile chumba kisha alirejea mda mfupi akiwa na chupa ya maji na mtu mwingine ambaye alionekana kuwa alikuwa ni mchungaji,,nilipomtazama vizuri yule mtu alikuwa ni mchungani Patrick Mponda wa Assemblies of God,,ambaye alikuja na kunishika kichwani na ndani ya dakika tano alikuwa amemaliza kuniombea.
“sawa upande wa mashtaka endeleeni kuleta mashahidi wenu na pia niwakumbushe watu wote ndani ya hii mahakama kuwa hakuna anayeruhusiwa kufanya chochote kitakachoharibu utaratibu au kuchelewesha ustaarabu wa humu ndani” aliongea jaji na mashahidi waliitwa, muda wote sikuwa nawaza kitu zaidi ya kujutia kuingia kwenye hili kundi ambalo hata ivyo sijaona faida yake zaidi ya kuniletea matatizo.
“defense, you can cross examine the witness”(upande wa utetezi mnaweza kumhoji shahidi) ilikuwa sauti ya jaji na hapo ndipo nilipotoka tena kwenye dimbwi la majuto na kurudi tena mahakamani.
“shahidi wewe umesema ni askari polisi na pia ni mpelelezi kwa miaka mitano sasa” ilikuwa sauti ya Clara.
“ndio” alijibu yule askari.
“na umefundishwa vyema kufanya upelelezi na kuchunguza ushahidi vyema”
“ndio”,,baada ya yule askari kujibu niliona Clara akirudi mpaka pale kwenye meza na kuchukua karatasi mbili na kisha alienda tena pale mbele.
“unaweza kuiambi mahakama kilichoandikwa kwenye karatasi hii?” alimkabidhi yule shahidi ile karatasi na kisha kukaa pembeni.
“ni barua ya kupewa onyo” alisema askari.
“nani anapewa onyo?anapewa onyo na nani na kwanini?”
“ni mimi nilikuwa napewa onyo na mkuu wa upelelezi kwa kuwa baada ya kuupata ushahidi yaani ile kanda ambayo imeonyeshwa hapa niisahau bar na nilipogundua nilirudi kuitafuta na kisha niliiona” alijibu yule askari kwa sauti ya kutetemeka.
“kwaiyo unaihakikishiaje mahakama hii kuwa kanda hiyo ndiyo ile mlioikuta pale ndani na sio nyingine ambayo ilibadilishwa na kuwekwa picha ya mteja wangu pindi ulipoiacha pale bar?”,,yule askari alishindwa kujibu na Clara aliamia kwenye swali lililofata..
“sasa nikuelekeze kwenye ushahidi ambao wewe kama mpelelezi umeuleta kwa mwanasheria wa serikali,,kwenye picha za kaseti ambayo mmeiwasilisha hapa inaonyesha nani na nani waliuawa?”
“inaonyesha Jamshid Jabir na Magret” alijibu askari
“umejuaje kuwa ni Jamshid na Magret? Je umewahi kuwaona watu hao kabla ya kifo chao?”
“Hapana ilabaada ya uchunguzi kufanyika ndio tuliweza kutambua majina ya marehemu”
“muheshimiwa nimeupitia ushahidi ambao umewasilishwa na upande wa mashtaka na kuna kasoro ambazo ningependa afisa wa polisi ambaye pia ni shahidi aweze kuutolea majibu”,,nilimuona Clara akisogea mpaka ilipokuwa laptop ya wakili wa serikali na kisha alirudisha nyumba ile video na kuisimamisha kisha aliivuta na kuikuza lakini bado sikumuelewa bado kwakuwa nilikuwa ninatatizo la kuona mbali na sikuwa na miwani kwa pale kwahiyo nilisubiri kusikia ni nini Clara alikuwa akijaribu kuelezea, alirudi tena hadi pale mezani nakufungua begi lake na kisha kutoa albamu ya picha ambayo niliweza kuitambua na aliomba nimuelekeze kila kitu changu kilipo ili aweze kukusanya ushahidi,,baada ya kutoa albamu ile ambayo ilikuwa na picha za mimi na Jamshid na picha nyingine za Magret na mfanyakazi wa getini na watu wengine, alichomoa picha moja na kumsogelea yule askari kisha akamuonyesha;
“huyo kwenye hiyo picha ni Faith ambaye ni mteja wangu na mvulana unayemuona hapo kwenye picha wakifurahi na kutabasamu ni mpenzi wake,,ni kila kitu kwake,,ni mwanaume pekee kwenye maisha yake ambaye ameweza kuzishika hisia zake na ndiye moja kati ya watu ambao hata iweje yeye hawezi kuwaua kwa mkono wake au kwa kumtuma mtu,,swali ni JE HUYO MWANAUME NDIO YULE PALE KWENYE HUO USHAHIDI ULIOULETA?” nilishtuka na Clara alikuja hadi pale nilipo na kuniambia nitulie kimya kisha alichukua picha nyingne kubwa kama zilezile na kumpa mheshimiwa jaji na yule wakili wa serikali.
“shahidi unapoteza muda wa mahakama,,jibu swali langu ndio huyo”aliuliza Clara aliyeonekana kuchoshwa na ukimya wa yule askari.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“sio yeye” alijibu na hapo moyo wangu nilisikia ukipasuka kwa mshangao,,,nilisikia kama kutapika lakini nilijizuia na hapo nikaanza kutokwa na machozi tena.
“je nyie kama ofisi ya upelelezi mnawezaji kuleta ushahidi wa uwongo kama huu” kabla hajajibu mahakama ilifurika tena kelele na jaji alisimama na kuomba askari kutuliza kelele pale mahakamani na kisha Clara aliendele kuongea.
“muheshimiwa, naomba kuitambulisha mahakama yako tukufu kuwa huyo marehemu aliyeonyeshwa kwenye iyo video na ushahidi mwingine wa upande wa mashtaka sio Jamshid Jabir ni Juma Ismail ambaye ni mlinzi wa geti wa nyumbani kwa Magret”…nilishtuka kwa mara nyingine na nguvu ziliniishia,, sikutokwa na machozi bali sasa kichwa changu kilijiuliza mara mbili na sasa niliona kama ni ndoto,, nilisubiri kusikia kuwa na mwanamke kwenye ile video hakuwa Magret lakini haikuwa hivyo.
“Lakini kwenye ushahidi huo huo muheshimiwa,, picha inayoonyesha sura ya mteja wangu na inayomuhusisha mteja wangu na tukio hilo la mauaji imetengenezwa, muheshimiwa nielekeze sasa kwenye huohuo ushahidi ambao upande wa mashtaka umeuleta,,”,,nilimuona tena Clara akiisogelea ile kompyuta na sasa alipeleka mpaka pale ambapo yule mtu alionyesha sura yake na kisha kuisimamisha,,
“muheshimiwa sasa naomba kwa pamoja tuangalie jinsi ambavyo picha hii imetengenezwa kwa teknolojia iliyongumu kuitambua,,,shahidi ikitokea umejiangalia kwenye kioo na ukasogeza uso je, ni wakati gani taswira yako iliyondani ya kioo nayo itasogea?” aliuliza Clara.
“sijaelewa swali”alijibu yule askari
“ukiwa unajitazama kwenye kioo na ikatokea umesogeza uso kidogo,je ni muda gani ile taswira yako kwenye kioo nayo itasogea?” alirudia swali kwa taratibu ili yule askari aweze kumsikia vizuri.
“mda uleule unaposogea” alijibu yule askari
“na je mlipoichunguza picha iliyoonyesha kuwa mteja wangu ndiye alikuwa muuaji hamkuona utofauti wowote wa kati ya sura na mwili?”
“hapana picha na sura viliendana” alijibu na hapo kwa umakini wa hali ya juu Clara aliicheza tena ile video.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“mheshimiwa Jaji,,picha ya hii ya kuonyesha sura ya mteja wangu ilionyesha katika dakika ya 8 na sekunde kumi kwenye mzunguko wa video nzima,,lakini dakika ya nane sekunde ya kumi na moja kama inavyoonyesha hapo mwili huyo muuaji ulisogea kidogo ila sura ikasogea sekunde ya kumi na mbili,,hii sio video ya mnato kwa maana ya slow motion useme pengine picha ilichelewa,,hii inaonyesha kuwa sura ya mteja wangu ilipachikwa,,istoshe wakati mtu huyo anaonekana akitoa kitambaa chekundu hijab yake ilionyesha sehemu ya mkono ikiwa imechorwa,,lakini mteja wangu sio tu hajawahi kuchora ua lolote au alama yeyote siku zote za maisha yake bali hana pia rangi nyeupe kiasi kile kilichoonyeshwa kwenye mkono wa yule muuaji,,lakini zaidi ni je kwanini basi shahidi asiieleze mahakama kuwa kama kanda ya kurekodi matukio ya kwenye kamera waliikuta kule je ni kwanini haionyeshi matukio ya mchana kutwa badala yake inaonyesha matukio ya usiku tu tena hili tu la mauaji? Kama ilikuwa edited how can this honourable court admit such kind of evidence?”(kama ilihaririwa iweje mahakama hii tukufu ikubali ushahidi wa aina hiyo?).. ni hayo tu muheshimiwa” alimaliza Clara nakukaa chini.
Clara alifaa sana kuwa mwanasheria alifumbua macho yangu juu yamengi ambayo sikuweza kuyafahamu ila sasa swali kubwa ni je Jamshid yuko wapi na kwanini hakuuliwa?...mashahidi waliitwa wote watano wakaisha na sasa ilikuwa muda wa pande zote kufanya majumuisho ili mahakama ije kuamua kama nilikuwa na kesi ya kujibu au la! Baada ya upande wa mashtaka kufanya majumuisho yake Clara alinyanyuka na kuanza kufanya majumuisho kulingana na mahojiano aliyofanya na wale mashahidi.
“Mheshimiwa napenda kuikumbusha mahakama yako tukufu kuwa kosa la mauaji ni kosa kubwa Tanzania na duniani na ambalo adhabu yake ni kunyongwa mpaka kufa kama sheria inavyoeleza,,na kwa ushahidi ulioletwa na upande wa mashtaka ni wazi kwamba haukidhi vigezo vya kiushahidi vya kumfanya mteja wangu awe na kesi ya kujibu,,ushahidi wa kutengeneza sio tu unakwenda kinyume na maadili ya kisheria lakini ni kuidanganya mahakama na kupoteza muda na rasilimali za mahakama,,lakini pia kama mahakama siku zote katika utoaji wa haki itajielekeza kwenye fabricated evidence (ushahidi wa uongo) kwa kujua au kutokujua at the end the court will not be the home of justice but of injustice(mwishoni mahakama haitakuwa nyumba ya haki bali nyumba dhalimu)..ili mshtakiwa awe na kesi ya kujibu lazima upande wa mashtaka utoe ushahidi wa kutosha na wa kuridhisha,,katika kesi ya R V. MAKUZI ZAIDI AND ANOTHER (1969) HCD 249,, Jaji mkuu George kama alivyokuwa kipindi hicho alinukuu sehemu ya Hukumu ya kesi ya BAMAULAL PRAMBAKALL BHAT V. R (1957) EA. 332 akisema,,ili iitwe kesi ya kujibu lazima iwe baraza au mahakama makini ikijikita katika sheria na ushahidi inaweza kutoa Hukumu kama hakutakuwa na maelezo mengine kutoka kwa upande wa utetezi,,nukuu hii pia imewahi kutumiwa kwenye kesi za MURIM V. R(1957) EA 542 CA (T), SUNDERJI V. R (1971) HCD 316 na WILLIAM HANNING V. R (1970) HCD 1971..Swali la kujiuliza hapa ni JE kama upande wa utetezi hautajitetea na kuacha ushahidi huo ambao umejaa mashaka na usanii wa hali yajuu mtamuhukumu mteja wangu kifo?? Au kwakuwa ni mjamzito basi mtamuhukumu kifungo cha maisha ili alelee motto wake akiwa magereza? Je mahakama itakuwa ni nyumba ya haki? ASANTE.
Baada ya maelezo hayo kesi iliahirishwa mpaka siku ya pili yake,,lakini siku hii nilikuwa nafuraha sana kwakuwa nilijua ushahidi utanitoa nje ya kuta za magereza.
KESHO YAKE:
Ilikuwa ni siku nzuri sana nikitarajia kesi yangu leo ilikuwa ikifika mwisho au hata kubadilishiwa kosa na sasa nilitegemea kupata dhamana na kwenda kumtafuta Jamshidi huko aliko lakini zaidi kwenda kulea kiumbe changu. Tulifika mahakamani mapema ila Clara alikuwa hajafika,,nilikaa kwenye chumba cha kuhifadhia mahabusu na muda ulipofika nilipelekwa mahakamani na hapo Jaji aliingia kisha alianza kuita mawakili wapande zote lakini Clara hakuwa amefika.
“Mtuhumiwa wakili wako yuko wapi” aliniuliza Jaji
“sina taarifa lakini nadhani ni foleni tu za jijini” aliongea na kisha niliona askari mmoja akiingia na Jaji alimuita akaenda pale mbele na kumnong’oneza kisha alimpa karatasi Fulani na kuondoka.
“nina habari sio nzuri hapa toka polisi,,wakili wa upande wa utetezi,,ndugu yetu Advocate Clara amefariki dunia wakati akiwa anakuja hapa mahakamani asubuhi hii,,amepata ajali mbaya ya gari na amefariki pale pale” nilisikia homa na moto ukipanda tumboni kwangu lakini hakuna nilichosema zaidi ya kusema nimekwisha.,mahakama ilisimama kwa muda na wakat bado nikilia nilimsikia Jaji akisema.
“Nadhani kwakuwa huna wakili sasa siwezi kutoa ruling(maamuzi) mpaka tukutafutie wakili mwingine” aliongea jaji na hapo nilisikia mlango ukifunguliwa.
“Mheshimiwa tuendelee tu,,naitwawakili SAMAH BIGUMAR niko hapa badala ya marehem wakili Clara na barua ya replacement of the deceased advocate (barua ya kuchukua nafasi ya wakili aliyefariki) hii hapa” . Woga ulinipata lakini kabla sijapiga kelele Samah alikuwa ameshafika pale akampa Jaji ile barua na kunifata na kwasauti ya chini nilimsikia akiniambia;
“Tunae Jamshid,,na iwe unataka au hutaki nitakuwa wakili wako,,ukiendelea kuonyesha wasiwasi atakufa na hicho kiumbe tumboni utapoteza”
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sikuwa na cha kusema tena zaidi ya kukubaliana na Samah,,katika maisha yangu nilijiona nina gundu sana lakini sikuwa na namna ya kufanya zaidi ya kukaa na kumuomba mungu pale mahakamani kesi isiende vibaya,,muda wote nilikaa na kuwaza watu ambao wamefariki dunia kwa ajili yangu,,nilimuwaza sana Clara na sikujua kama ajali yake ilikuwa ni ya kupangwa au ya bahati mbaya.
“baada ya kupitia ushahidi ulioletwa na upande wa mashtaka na pia mahojiano na submission(majumuisho) yaliyofanywa na pande zote pamoja na kujielekeza katika sheria na taratibu za kisheria, mahakama imeweza kuja na yafuatayo.
1. Ushahidi uliotolewa na upande wa utetezi ni ushahidi usio na mashiko na kwanamna moja au nyingine unashindwa kumuhusisha moja kwa moja mtuhumiwa na kosa lililotendwa,, kama mtuhumiwa aliua lazima ionyeshwe sit u kuwa alikuwa ni mtu pekee ambaye alikuwa na uwezo wa kuwaua marehemu bali ionyeshwe pia kuwa mtuhumiwa ndiye aliyetenda kosa hilo,,ushahidi huo uliosheheni walakini na kuacha maswali mengi kama alivyoelezea wakili wa upande wa utetezi ambaye ni marehemu kwasasa,,ushahidi huo pamoja na mambo mengine umeonyesha jinsi upande wa jamuhuri usivyokuwa makini na namna ya kufanya upelelezi wake.
2. Kwamba ushahidi huo haujaweza kuthibitisha chochote kuwa mtuhumiwa alihusika kwenye mauaji ya watu wawili ambao hata hivyo mmoja alikuwa sio yule waliosema amefariki.
Kabla yule jaji hajamaliza kuongea kila mtu alishtuka alipoona ghafla kuwa yule jaji alikuwa ameanguka chini,,maaskari walikimbia pale juu na watu walianza kutolewa nje harakaharaka kisha maaskari wengine walikuja pale na kunifunga pingu wakiniweka chini ya uangalizi,,nilitamani kutoroka pale lakini sikuweza,,maaskari waliokuwa pale juu wakimnyanyua yule jaji walishtuka na kuanza,,kupiga kelele wakimtaka yule muhudumu wa mahakamani aite gari la huduma ya kwanza na ndipo walipoanza kupiga simu na muda si mrefu timu ya madaktari iliingia pale na walimsongeza pembeni yule na kumgeuza,,,nilichokiona kilinifanya nitapike palepale,,shingo ya yule jaji ilikuwa imekatwa na koromeo lilikuwa nje ila hakukuwa na damu hata kidogo.
“Toa watu madirishani huko na waambie hao maaskari magereza wafanye mchakato wa kumrudisha huyu mtuhumiwa mahabusu” ilikuwa sauti ya askari aliyekuwa na cheo cha nyota tatu,,na hapo chini ya uangalizi mkali nilitolewa nje ya mahakama,,na kabla sijapanda kwenye gari lile kwa ajili ya kurudishwa mahabusu,,Samah alinifata na kwa sauti ya utaratibu aliniambia.
“this is just the beginning sweetheart”(huu ni mwanzo tu mpenzi),,alinitazama kwa tabasamu zito na kisha aliongea na yule askari magereza na kisha kuondoka.
***
Nilichukuliwa na kupelekwa tena mahabusu,,nililia sana lakini haikusaidia, akili yangu bado ilikuwa ikitafakari haya yaliyotekea siku ya leo,,nilikumbuka jinsi Clara alivyonisaidia pale mahakamani nikachoka zaidi nilipokumbuka kuwa Clara alifariki siku hii ya leo kwa ajali japo sikujua ni nini tatizo,,nakumbuka siku ya kwanza namjua Clara ilikuwa siku niliyokuwa nimefika chuoni Helinsik na kupangiwa chumba kimoja na yeye,,sikuwa nampenda sana kwani alionekana ni mtu wa maringo hasa ukizingatia ukweli kwamba Clara alikuwa ni mrembo kushinda mimi na kila mwanaume alionekana kumtamani ingawaje si kila mmoja alifanikiwa kumpata,,Gerald Hutson motto wa jaji mkuu wa Mexico City ndiye aliyebahatika kuvinjari na Clara katika viwanja vya Helinsik na maeneo mengi ya nchini Finland,,Clara alikuwa ni mwanasheria bora toka kipindi anasoma,,nakumbuka alikuwa anasoma muda mwingi sana na muda uliobaki aliutumia na Gerald au kulala.
****
BAADA YA MWEZI MMOJA
Ilikuwa majira ya saa nane usiku ndipo niliposhtuka na kukuta mwanga mkali ndani ya chumba kile cha mahabusu,,mpaka sasa nilikuwa sijajua ni ipi ilikuwa hatima ya kesi yangu hasa kwa vile mpaka sasa nilikuwa sijabahatika kupata taarifa yoyote juu ya kesi yangu… nilipotazama vizuri ilikuwa ni mwanga wa tochi na mimi niliinuka kwa hofu na kuketi.
“Habari yako Faith” ilikuwa sauti ya afande Evelyn iliyokuwa na upole ndani yake.
“usiogope Faith, nimekuja kuongea na wewe leo kama rafiki” aliongea vile na kuketi, sikuamini kama Evelyn alikuwa na sauti ya upole vile muda mwingine.
“Faith najua sikukutendea haki katika mambo yote niliyokufanyia,,najua hayo niliyokutendea hayakunipasa kuyafanya na yasingenifurahisha mimi kufanyiwa,,nimegundua makosa yangu na leo nimekuja kukuomba msamaha kwa dhati ya moyo wangu” aliongea huku machozi yakimdondoka
“kwanini ulinifanyia vile na kwanini ulimfanyia bibi Eunice vile” nilimuuliza kwa utaratibu
“mengi yametokea kwenye maisha yangu Faith yaliyonifanya nimchukie kila mtu,,mama yangu alikuwa ni muuzaji wa pombe za kienyeji huko butimba mkoani mwanza,,tuliishi kwa biashara ya mama kuuza pombe za kienyeji na yeye kujiuza mwenyewe,,lakini kuna kipindi nikiwa mdogo nilikuja kugundua mama yangu alikuwa na virusi vya ukimwi na ndio maana aliamua kuuacha mwili wake uingiliwe na kila mtu,,sikuipenda tabia ya mama yangu lakini sikuwa na la kufanya,,kuna siku baada ya mama yangu kulewa sana aliamua kuniuza kwa mwanaume mmoja,,sikuwa tayari lakini nilinyweshwa pombe na kubakwa,,kesho yake nilirudi nyumbani nikiwa nimepania kumuua mama yangu lakini nilipofika nilikuta mama yangu amefariki,,kuanzia pale sikuwa na la kufanya niliendeleza biashara ya mama huku nikiwa naendelea na shule ya msingi na pia huo ulikuwa mwanzo wa biashara ya kujiuza,,nilikuwa nikiuza mwili wangu ili kupata fedha ya kutunza wadogo zangu ambao hata ivyo baadaye walikuja kufariki siku nyumba yetu ilipoungua kwa moto baada ya mlevi mmoja kuacha kipisi cha sigara kitandani”
“pole sana na nini kilifuata”,,nilimuuliza Evelyn na wakati huu nilikuwa nikimuonea huruma kwa yote yaliyotokea.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“nilianza maisha mapya na sasa nilikutana na mzee mmoja ambaye alijitolea kunipeleka kidato cha nne,,sikujua nia yake lakini nilikubali na nilipofika kidato cha pili alisema hayuko tayari kunisomesha tena mpaka nijitolee kufanya mapenzi na yeye,,hiyo kwangu haikuwa shida nilijitoa muhanga na kumpa penzi yule mzee lakini alikuja kunikatisha tamaa alipoanza kusema kuwa hana tena ela za kuniendeleza lakini angenisaidia kupata wateja wa kununua mwili wangu ili nipate ela ya kujisomesha,,nilimkatalia lakini kila mara alikuwa akija chumba kile alichonipangia na kunitishia kuwa angenifukuza pale kama sikuwa tayari kufanya mapenzi na wanaume aliowaleta,,sikuwa na namna zaidi ya kukubali na hapo nilianza kuingiliwa kimwili hata na wanaume watatu kwa siku,,nilipofika kidato cha nne nilimaliza na kupata daraja la tatu na sasa nilishindwa kwenda kidato cha tano kwakuwa yule mzee alinipa ujauzito mara ya mwisho nilipofanya nae mapenzi na alipogundua alikimbilia visiwa vya ukerewe,,hivyo nilivumilia na kujifungua lakini baada ya uchunguzi wa muda mrefu nilikuja kugundua yule mzee alikuwa baba yangu mzazi na huyu motto niliyenae nilizaa na baba yangu mzazi,,toka pale niliwachukia wanadamu,,na baada ya miaka miwili ilitangazwa nafasi ya kazi katika jeshi la magereza na nilijiunga,,baada ya kumaliza mafunzo na kuajiriwa nilipata nafasi ya kwenda kusoma Russia na huko ndipo hatima ya maisha yangu ilipoandikwa,,katika mafunzo yale nilitoroka kambini na kwenda kunywa pombe kwakuwa nilikuwa na msongo wa mawazo huko nilijuana na wasichana Fulani na waliniingiza kwenye biashara ya madawa ya kulevya na kwa siri kubwa nilijiunga nao lakini nilikamatwa siku moja na sikupelekwa popote ila nilichomwa sindano ya sumu ambayo itaniua kesho saa 3 asubuhi,,hii ni miaka kumi baada ya kuchomwa ile sumu,,nimekaa miaka yote hii nikijua kuwa kesho saa 3 asubuhi nitakata roho,,hivyo nimekuja kuomba msamaha kwakuwa nilikuwa mkatili kwako,,naomba msamaha wako ili nipate kibali kwa mungu” alinieleza haya huku akilia hali iliyonifanya na mimi nilie kwa uchungu,,hakika nilimuonea huruma na niliamua kumsamehe,,aliniachia rozari na kuondoka. Kesho yake asubuhimajira ya saa nne taarifa zilizokuwepo ni juu ya kifo cha Evelyn,,nililia sana niliposikia Evelyn amefariki na ingawaje alikuwa mkatili kwangu lakini kifo chake kilinihuzunisha kwakuwa sasa nilijua kwanini alikuwa katika hali ile.
***
Maisha yaliendelea sawia na sasa nilikuwa nimetimiza miezi saba toka niingie pale mahabusu na hakukuwa na dalili yoyote ya kesi yangu kuitwa tena kwa ajili ya kusikilizwa. Ilikuwa ni miezi takribani nane sasa ya ujauzito wangu na maandalizi ya kujifungua nilishaanza kuyafanya nikiwa kule mahabusu,,nilikuwa nikiisubiri sana siku ya kujifungua mtoto wangu ambaye baba yake sikujua alipo.
Majira ya saa nne asubuhi nilikuja kufatwa na kuchukuliwa mpaka mahakamani, sikuwa nimepewa taarifa kuwa ningepelekwa mahakamani leo lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida nilifikishwa mahakamani na na nilipofika tuliingia moja kwa moja mpaka chumba cha mahakama na jaji aliingia.
“Leo tutasoma maamuzi ya mwisho yaliyotakiwa kusomwa siku ile kabla ya mauti ile ya kushangaza iliyomkuta Jaji wetu,,na pia utaratibu mwingine utafahamika lakini kabla ya hapo ningependa tena kuwajua mawakili wa pande zote mbili” alimalizia Jaji na hapo hapo Samah alinyanyuka na kwa sauti iliyojaa nguvu alianza kujitambulisha.
“ikupendeze muheshimiwa naitwa Samah Birghum ni wakili wa upande wa utetezi” alijitambulisha na mimi muda wote huo nilikuwa nimeinama nikimuomba mungu atende miujiza pale ili niweze kupatiwa dhamana nikajifungulie nyumbani,,wakati bado nikisali nilishituliwa na sauti ya mwanamke iliyonifanya nikatishe ile sala na kumtazama.
“Ikupendeze muheshimiwa naitwa wakili Maysa Alfaruq ni wakili wa serikali na niko hapa kwa niaba ya Jamuhuri,,na ninaiomba mahakama yako ilipokee jina langu na kuingiza kwenye court records(kumbukumbu za maharama) kama replacement(mbadala) ya wakili wa serikali aliyefariki mwezi mmoja uliopita”,,niliishiwa nguvu na maini yalianza kupata joto baada ya kuona kuwa wabaya wangu wote sasa walikuwa kwenye kesi yangu,,kilichonishangaza ni yale maamuzi yaliyotolewa pale ambayo yalikuwa tofauti kabisa na yale ya mara ya kwanza,,nilisikiliza kwa makini na machozi yalizidi kunitoka pale alipohitimisha.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Na hivyo baada ya kupitia ushahidi wote kama ulivyoletwa na upande wa mashtaka na pamoja na mabadiliko yake ya jina,, mahakama kuu imemkuta mtuhumiwa na kesi ya kujibu kufuatia kumuua mfanyakazi wake wa ndani na ndugu yake anayefahamika kama Magret..dhamana kwa mtuhumiwa imefungwa kwakuwa kosa lake linanyimwa dhamani chini ya sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai,,na upande wa utetezi unatakiwa kuanza kesi yake hapo kesho” alimaliza na bila yeyote kuuliza aligonga ile nyundo mezani na kuondoka,,kisha mahakama iliahirishwa,,nilimuona Samah akimfata Maysa na wote walikaa pale mahakamani wakati mimi naondoka.
Tumbo lilianza kuniuma wakati nipo kwenye gari nikipelekwa mahabusu na tulipofika maeneo ya tazara hali ilizidi kuwa mbaya na mwendo wa gari ulipunguzwa huku maaskari wakiendelea kuwasiliana na wenzao na tulipofika banana gari ilisimamishwa na ambulance ililetwa na hapo sikujua tena nilipopelekwa lakini nilikuja kushtuka kama masaa nane baadae nikiwa kitandani na nilikuwa nina pingu mikononi,,sikuweza kuongea kwani mdomo ulikuwa mzito,,nilitazama tumbo langu na kuona kuwa lilikuwa limepungua ukubwa na hapo ndipo furaha ilipoujaza moyo wangu kwakuwa pamoja na kwamba miezi ilikuwa bado muda mchache lakini nilijua lile lilikuwa tumbo la uchungu,,nililala nikifurahi pale na machozi yaliendelea kutembea kwenye mashavu yangu.
“ooh god, am a mother now, show me the way that I deserve”(ooh mungu,mimi ni mama sasa,,nionyeshe njia ninayostahili),,nililia sana hasa nilipotazama huku na huku na kuona niko mwenyewe tu,,nilitamani niwaone Magret na Jamshid pamoja na Clara wakiwa pembeni yangu wakinipa moyo lakini hawakuwepo,, kuwa mama ndio ndoto pekee niliyokuwa nikiiota na ikinifurahisha toka siku ya kwanza nilipomuona Jamshid,,nilitamani sana kuzaa nae lakini pia nilitamani sana kuzaa na kulea watoto wangu katika mazingira salama,,nilikaa macho nikisubiri daktari aingie lakini mpaka nilipitiwa na usingizi hakuna aliyekuwa ameingia na sasa nilishtuka ilikuwa asubuhi na nilipoamka nilikuta daktari akinifanyia vipimo kisha aliniambia nipumzike kidogo atakuja dokta mkuu kuongea na mimi,,nilitazama vizuri tena lile shuka lililokuwa limeandikwa MNH na hapo niligundua kuwa nilikuwa katika hospitali.
“Faith unatatizo na inabidi unisikilize kwa makini ili tuelewane” ilikuwa sauti ya daktari iliyokuwa sasa ikinipa maelekezo.
“nakusikiliza dokta”
“mimba yako imeharibika na imetushangaza sana” aliongea dokta kwa lugha rahisi sana bila kujua ni kiasi gani taarifa ile imenichoma.
“hapana dokta usiseme ivyo” nilianza kulia pale na wale maaskari waliokuwa wakinilinda waliingia na kuanza kunilazimisha kunyamaza.
“baada ya tumbo lako kusumbua tulilazimika kukupa maji ya uchungu na ndipo uliposukuma na kutoa bonge kubwa la damu,,hali hii inaweza kuwa imesababishwa na shuruba au msongo wa mawazo au kama uliwahi kujigonga sehemu,,”aliongea na kutoka kidogo kisha alirudi na kibeseni kidogo cha chuma na baada ya kukifunua ilitoka harufu kali na bonge kubwa la damu iliyoonekana kuanza kuharibika na iliyokuwa imejitengeneza kwa umbo la mtoto ndilo lilikuwa pale,,nililia kwa uchungu huku nikitazama kwa makini na ndipo nilipogundua kuwa katika ile damu kulikuwa na alama ya bikari ambayo ni alama inayotumika na kundi la freemason,,nilinyanyua macho kwa hofu kubwa na hapo daktari aliendelea..http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“zaidi ya hilo una ugonjwa ambao si hata ri lakini siugonjwa salama sana” aliendelea dokta kuongea na hapo alifunua tena yale makaratasi
“nimeathirika?” niliuliza kwa mshangao huku jasho na kamasi vikinitoka
“hapana,,unaugonjwa unaoitwa Ulcerative colitis,,huu ni ugonjwa unaoshambulia utumbo mkubwa,,ni ugonjwa mpya na uko kwenye uchunguzi bado haijulikani ni nini kisababishi cha huu ugonjwa japo kunasababu zinazotajwa ambazo hatahivyo bado hazijathibitika,,tumejaribu kuchunguza kwa makini unavidonda vikubwa sana kwenye utumbo wako mkubwa ambavyo kiukweli sasa vimefikia sehemu mbaya sana na hii sio tena sehemu ya sisi kukupa dawa kwakuwa inaonekana ugonjwa wako umefikia mahala pa juu kabisa ambapo kama hatua za haraka hazitachukuliwa basi utapata kansa ya utumbo hivi karibuni.
“kwaiyo tiba ninini”nilimuuliza dokta huku bado nikiwa nalia
“Lazima tukufanyie upasuaji na tuondoe utumbo mkubwa”
“WHAT”
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment