Simulizi : Kurudi Kwa Moza Sehemu Ya Tatu
(3) Rose alikuwa kwenye maua akifanya dawa kwaajili ya
mzimu wa Moza usifike kwenye nyumba yake maana alianza kupata hisia kuwa huenda
mzimu wa Moza ndio unaosumbua akili yake, basi alipiga magoti kwenye lile ua
ambalo moza aliwahi kulifukua na kutoa kile kimpira kilichopelekea mpaka kifo
chake, kwa upande wa Rose hili ua lilikuwa na maana kubwa sana kwake na lilikuwa
likimsaidia vitu vingi sana kwahiyo alipiga magoti na kuanza kusema maneno
ambayo hayatakiwi yakatishwe akianza kuyasema mpaka ayamalize, akiwa katikati
yay ale maneno alishikwa bega na Sara, “Mama, mama” Rose
hakumjibu chochote Sara na aliendelea na kusema maneno yake ila Sara nae
hakuacha kumuita mama yake hadi akawa anamtingisha, “Mama, mama jamani
mama ndio uchawi gani huu sasa mpaka umeanza kufanya peupe ili tujue kama mama
yetu ni mchawi jamani!” “Mama, namuhitaji Ommy wangu, nirudishie Ommy
mama. Nipo tayari kuachana nae ila nirudishie Ommy mama” Alipoona mama
yake hamjibu chochote zaidi ya kuendelea na kitu anachofanya, akapata wazo la
kuchukua maji na kumwagia hivyo akafanya kama wazo lake lilivyomtuma. Akafungua
bomba na kukinga maji kwenye ndoo kisha akaenda kummwagia mama
yake. Kwakweli hakuna siku ambayo Rose aliwahi kuchukia kama siku ya leo
maana aliinuka kwa hasira halafu alimpiga mwanae hadi alizimia yani kipigo
alichompiga haikuwahi kutokea, mlinzi alisikia kelele tu na kumfanya azunguke
nyuma ambako kelele zilitokea ila akaona Sara akipigwa na mama yake hadi kuzimia
kisha mama yake alimuacha Sara hapo na kwenda ndani, yani Rose hakujali kama
mwanae amezimia au nini alikuwa na hasira zilizopindukia. Mlinzi
alijaribu kumuinua Sara pale, sema sababu alikuwa na nguvu kwahiyo aliweza
kumuinua na kumuweka pembeni kwenye kivuli kisha akaanza kumpepea ila
hakuzinduka kwa muda huo. Salome nae alitoka ndani na kukuta yale
yaliyopo kisha akachukua maji na kummwagia Sara, yale maji yalimfanya Sara
azinduke ila alikuwa na maumivu makali sana ya kupigwa na mama yake, kisha
Salome na mlinzi wakasaidiana kumshika Sara na kumtembeza hadi chumbani ambako
walimuweka kitandani apumzike. Mlinzi alitoka na kumuacha Salome akiwa na Sara
chumbani, kwakweli Sara alikuwa na maumivu mwili mzima kiasi kwamba hata
alivyopigwa pigwa na mama yake hakukumbuka vizuri huku akijiuliza
mwenyewe, “Hivi kilichonipeleka nyuma kule na kuanza kumfanyia fujo mama
ni nini? Hivi kilichofanya nichungulie mama anachofanya ni
nini?” “Usijilaumu kwa chochote Sara, katika maisha kila kitu huwa
kinapangwa na kinakuwa na maana yake kwahiyo usijipe lawama za
bure” “Hapana Salome, nimejitakia mwenyewe. Mwili wote unaniuma yani
wote unaniuma. Mama yangu hajawahi kunipiga kiasi kile, mama yangu hajawahi kuwa
na hasira na mimi kiasi kile. Hata kama mama yangu ni mchawi ila sikutakiwa
kumfanyia fujo kiasi kile” Salome alimuangalia Sara kisha akaondoka na
kumuacha Sara mwenyewe chumbani akijilaumu tu kwanini amemfanyia fujo mama yake
maana mwili wote ulikuwa unamuuma, “Eti nampigia kelele mama amrudishe
Ommy wa kazi gani sasa Ommy, janaume Malaya vile la nini? Kama limewekwa msukule
na liwe tu msukule, ona nilivyopigwa na mama, huyu Salome nae sio wa kumsikiliza
ushauri wake. Hivi yeye anaweza kufanya kwa mama yake ujinga kama huu! Mama ni
mama hata akiwa mchawi, natakiwa kwenda kumuomba msamaha mama” Sara
aliinuka kwa kujikongoja akajivuta hadi chumbani kwa mama yake ambapo aligonga
bila kufunguliwa, ikabidi afungue mwenyewe. Alishtuka na kushangaa mama yake
akiwa mtupu kabisa ila Rose alizidi kupatwa na hasira kwa mwanae na kuongea kwa
hasira, “Hivi wewe mtoto una nini wewe? Unataka upate laana yangu
au?” sara aliondoka kwa aibu hata hakuweza kuzungumza na mama yake kwani
hakutegemea kama angemkuta mama yake akiwa mtupu kabisa, Sara alirudi chumbani
kwake huku akijiongezea makosa aliyomkosea mama yake kwa siku hiyo na kujiona ni
mtoto mpumbavu asiye na maadili halafu ndio mtoto wa kwanza wa mama yake halafu
maadili hana anafanya mambo ya ajabu kama yale. “Nimemdhalilisha mama
yangu, sifai mimi yani sifai kabisa” Alikuwa akijilaumu tu kwa wakati
huo. Kwa upande wa Neema aliamini kuwa mwanae angeenda nyumbani
kwa siku hiyo na angechukua ushauri aliopewa na mama Pendo wa kumpeleka Salome
kwenye maombi, “Ila mwanangu atachukia akijua nimewaambia watu kuhusu
yaliyomkuta, ila sikuwa na jinsi maana Yule mtu alituona” Akawaza ila
uhakika wa Salome kufika siku hiyo hakuwa nao, wanae wale wadogo nao walikuwa
wamerudi na wametulia sebleni kwao wakimuangalia mama yao akiwa na mawazo sana,
mmoja akamuuliza “Mama mbona una mawazo hivyo?” “Nawaza kuhusu
dada yenu Salome sijui leo atakuja” “Si umpigie simu
mama” “Salome hana simu” “Mbona anayo, huwa tunamuona nayo
akiongea na watu na akiitumia” Neema akashangaa kusikia kuwa mtoto wake
ana simu maana yeye aliamini kuwa mwanae hana simu, aliwauliza wanae kwa
mshangao. “Hebu achene maneno yenu, lini mmemuona dada yenu na
simu?” “Kila siku tunamuona nayo mama, tena muda mwingine anakuwaga
anaitumia sana. Toka tumehamia huku anayo” “Mmh sijui alinunuliwa na
nani? Au Ashura?” “Sijui ila mamdogo Ashura toka siku ameanguka wakati
tunakula ndio hatujamuona tena” Neema akazidi kushangaa na kuwauliza
vizuri watoto wake, “Mbona siwaelewi?” “Dada alituambia
tukacheze eti yeye na mamdogo wanacheza michezo ya kutaniana, na tulipoondoka
badae akatuita na kutupakiza kwenye gari halafu tukahamia
hapa” “Inamaana hapa hamkuja na Ashura?” “Hatukuja nae, dada
Salome alisema mamdogo kaondokea kule kule. Ila mimi nilifurahi maana ona huku
tunaishi kwa amani sana” Wakatoka nje na kucheza huku wakimuacha Neema
kwenye maswali mengi sana, akajiuliza na kama Ashura aliondokea kule kule ni
kwanini Salome alimdanganya kuwa aliondokea kwenye nyumba mpya waliyohamia? Na
michezo gani hiyo ya kuanguka wakati wa kula? Alijiuliza maswali mengi sana bila
ya majibu, na kubwa zaidi ni kuhusu kumiliki simu kwa Salome. Alijiuliza sana na
mwishowe akaamua kuchukua simu yake na kumpigia Ashura ila namba haikupatikana,
alipiga na kupiga lakini aliambiwa haipatikani. Sara bado
hakuwa na raha kwani alijiona ni mkosaji sana kwa mama yake akawaza namna ya
kumuomba msamaha mama yake, muda huu akatoka chumbani ila alimkuta Salome kwenye
korido yao halafu Salome akamwambia Sara nifate, Sara hakujiuliza mara mbili
zaidi ya kwenda kumfata Salome. Alimfata taratibu hadi kwenye chumba
ambacho Salome alichukua ufunguo juu na kufungua kisha akaingia nae ndani na
kufunga mlango kwahiyo ndani wakawa wawili tu, halafu akamwambia Sara huku
akimuonyeshea mlango mdogo wa kwenye chumba kingine ndani ya chumba
hiko, “Fungua ule mlango” Sara alikuwa akishangaa maana hajawahi
kuingia kwenye chumba kile na wala hakuelewa kama kuna chumba kidogo ndani yake
kama choo. Ila kwa muda huu aliamriwa na Salome kuwa afungue kile kimlango, Sara
akakataa, “Hapana Salome, unataka nifunguie ili iweje? Sijawahi kuingia
humu ndani, sijawahi kujua kama chumba hiki kina chumba ndani yake halafu leo
unaniambia nifungue hapana sifungui” “Kama hutaki basi, ila mimi lengo
langu ilikuwa ni kukusaidia” “Kunisaidia kivipi?” “Wewe kafungue
tu halafu utaona nitakusaidiaje” Sara akaanza kusogea akitaka kufungua,
ila gafla akashtuliwa na sauti iliyotokea nyuma yake ilikuwa ni sauti ya mama
yake. “Unafanya nini hapo?” Sara aligeuka na kumtazama mama yake
ambaye alikuwa amemkazia sura vilivyo, ila cha kushangaza alivyoangaza huku na
huku hakumuona Salome. Itaendelea kesho
usiku……!!!!!! Jumapili huwa situmi sababu huwa natingwa sana, yani siku
yangu hii inakuwa na mambo mengi. Ila leo afadhali kidogo nimeweza hata kujivuta
vuta nakutuma. Asanteni kwa maombi yenu. Sara akaanza
kusogea akitaka kufungua, ila gafla akashtuliwa na sauti iliyotokea nyuma yake
ilikuwa ni sauti ya mama yake. “Unafanya nini hapo?” Sara
aligeuka na kumtazama mama yake ambaye alikuwa amemkazia sura vilivyo, ila cha
kushangaza alivyoangaza huku na huku hakumuona Salome. Sara alishangaa
sana kwa kutokumuona Salome hadi mama yake akamuuliza, “Mbona unashangaa
hivyo?” Akataka kumwambia mama yake kuwa alikuwa na Salome ila
akashangaa mdomo unakuwa mzito kupita maelezo, akabaki tu kimya na mara
akamuuliza mama yake, “umeingiaje humu?” “Badala nikuulize wewe
umeingiaje humu eti unaniuliza mimi! Badala uniulize utatokaje humu unauliza
nimeingiaje? Hujui kama humu ni ndani kwangu, popote nina uhuru wa kuingia. Haya
umeingiaje humu? Na umefuata nini” Sara alikuwa kimya tu akimuangalia
mama yake kwani kiukweli hata yeye mwenyewe hajui humo amefuata nini maana
alikuwa akimfuata tu Salome ndiye aliyempeleka humo ingawa hakumuona tena, mama
yake alimuangalia tena kwa hasira na kumuuliza, “Ulikuwa unafata nini
humu? Unashida gani humu wewe mtoto lakini? Yani yote uliyonitendea leo unaona
hayatoshi zaidi ya kuendelea kunichokonoa chokonoa? Ngoja nisiongee kwanza humu
tutoke kwanza” Rose alimvuta mwanae mkono kisha akafungua mlango tu
kawaida kanakwamba haukufungwa na funguo halafu akatoka nae ila Sara
alimchoropoka mama yake kwani bado alikuwa akijiuliza kuwa Salome yuko wapi,
alienda moja kwa moja kwenye chumba ambacho huwa analala Moza na kufungua mlango
ilia one kama Salome yupo ila alifungua mlango na hakumuona yoyote, mama yake
alikuwa nyuma yake na kumuuliza, “Sasa unatafuta nini?” Sara
alitamani kumwambia mama yake kuwa kwenye chumba kile aliingia na Salome na
hakumuona tena kwahiyo alitaka kumuangalia kama chumbani kwake yupo, ila mdomo
ulikuwa mzito kusema hayo na alishindwa. Mama yake alipoona mwanae anabung’aa
bung’aaa akamvuta tena mkono na kupita nae sebleni, halafu akaenda nae kwenye
sebule nyingine ambayo wale mapacha hupenda kuitumia. Akakaa nae na
kumuuliza, “Sara, mimi ni mama yako au sio mama yako?” “Wewe ni
mama yangu” “Kwanini huniheshimu sasa?” “Mama sio kwamba
sikuheshimu ila linapokuja kwa wewe kuhusishwa na habari za kichawi ndio
huogopa” “Una uhakika kama mimi ni mchawi?” “Mbona Ana ni mchawi
mama” “Kwahiyo kama Ana ni mchawi huo uchawi nimempa
mimi?” “Hapana mama sijamaanisha hivyo” “Na kama nimempa Ana
uchawi basi nyie wote kwenye nyumba hii ni wachawi, unaponaje kuwa mchawi wakati
mama yako mzazi ni mchawi? Uchawi unaujua wewe? Kwanza nani aliyekuambia kama
mimi ni mchawi?” “Sijui mama” “Sara mwanangu, acha fikra mbaya.
Wewe ni mwanangu wa kwanza na mambo mengi nafanya kwaajili ya maisha yenu,
kumbuka baba yako alikukataa wewe toka upo tumboni mwangu. Je alikukataa kwavile
nilikuwa mchawi? Nimehangaika mimi nimeteseka, nikawapata kaka zako nao
wakakataliwa na baba yao. Sasa mimi kumpata mtu na kumdhibiti asifurukute kwenye
himaya yangu na awajali nyie na kuwapenda na kuwapa chochote mtakacho ni uchawi
huo? Kumtafuta mtoto kama Ana ili kuongeza upendo kwa mwanaume niliyempata, ni
uchawi huo? Unaacha kujiuliza kwanini huolewi na umri umeenda umekazana kutafuta
uchawi wa mama yako. Sitaki yakukute yaliyonikuta mimi, usiamini maneno au
vitendo vya kusema mimi ni mchawi ila nafanya vitu kwaajili na maisha yenu yani
wewe na wadogo zako. Sina tatizo na Ana, ni wa tofauti na nyie Yule. Sahau
katika maisha yako kama utakuja kuolewa, na kaka zako wasahau maishani mwao kama
watakuja kuoa, ila Ana ataolewa na ataolewa sababu nataka amtese mume wake. Mimi
sio mchawi mwanangu, na sitaki unifatilie tena. Nadhani
tumeelewana!” “Nimekuelewa mama na ninakuahidi sitakufatilia tena, ila
kwanini unasema kuwa mimi sitaolewa wala kaka zangu
hawataoa?” “Nitakwambia sababu ila sio leo, nyie mtaishi name miaka
yote” Rose aliondoka na kumuacha mwanae kwenye dimbwi la mawazo, alikosa
jibu kuwa kwanini hatoolewa ila aliweza kuolewa kuwa ni kwanini kila mwanaume
anayemleta mama yake anampinga mwanaume huyo, yani hapo ndio akaelewa kuwa mama
yake hataki yeye aolewe, akasema lazima awataarifu kaka zake kuhusiana na hicho
alichoambiwa na mama yao. Kisha Sara aliinuka pale na
kutoka. Wakati Sara anatoka kwenye ile sebule aliamua kupitia
jikoni, alishangaa kumuona Salome anapika na kumuuliza kwa
mshangao, “Kheee Salome unapika?” “Ndio napika, unafikiri sijui
kupika? Mamangu amenifundisha kupika” “Sio kwamba nashangaa unapika ila
nashangaa ulivyotoweka kwenye kile chumba” “Nimetoweka!” “Ndio
umetoweka, wewe Salome ndio mchawi na sio mama yangu” Salome akacheka
kisha akamuuliza Sara, “Lini nimekwambia kuwa mama yako ni
mchawi?” Sara akajaribu kuvuta kumbukumbu lakini hakupata siku ambayo
Salome alimwambia kuwa mama yake ni mchawi, akajiuliza tena kuwa kuhusu mama
yake ni mchawi ni nani amemwambia, lakini hakupata jibu. “Mbona
umenyamaza? Ni kuwa huna jibu ya kuwa lini nimekwambia kuwa mama yako ni mchawi,
wewe mwenyewe umekuwa ukisema kuwa mama yako na mdogo wako ni
wachawi” “Ni kweli nilisema mwenyewe” “Haya sasa, mimi nitajulia
wapi uchawi wa mama yako? Kumbuka kuwa mimi ni mtoto wa mama mwingine na
ninatokea mbali, sijawahi kuishi na mama yako ila wewe uliyeishi nae ndio
ulisema hivyo. Jibu ni kuwa sijawahi kukwambia hivyo ila kuwa makini sana na
maamuzi yako” Sara akaondoka na kuacha kumuuliza tena Salome kuwa ni
kivipi alitoweka na vipi anapika, je ameambiwa afanye hivyo. Ila Sara siku ya
leo alikuwa akisubiria kwa hamu kaka zake warudi na awape ujumbe wa mama
yao. Muda kidogo alimsikia Ana akirudi nyumbani ila Salome alimfata Ana
chumbani kwake. Kitendo hiko Sara alikiona na kufanya aende taratibu kwenye
mlango ili asikilize maongezi ya salome na Ana. Kwa upande wa Ana kitendo cha
kumuona Salome chumbani kwake kilimchukiza sana na kumfanya aulize kwa
hasira, “Kwanini umenifata tena bila ya hodi?” “Nahitaji
kuzungumza na wewe” “Ila mimi sihitaji kuzungumza na wewe” “Na
ujue kwamba sikulazimishi na ukigoma jua nitazungumza na wewe kwa lazima kwa
muda wangu” “Unaniambia hivyo wewe kama nani?” “Ninakwambia hivi
nikiwa kama mtu niliyekushuhudia kitendo ulichofanya leo, Ana muachilie Yule
mwalimu lasivyo nitakuumbua mbele ya wanafunzi wenzio na walimu
wote” “Hivi unanitishia mimi unanijua vizuri au Kitendo nilichofanya
mimi unakijua wewe? Najiamini na hakuna chochote utakachoweza kunifanya wewe.
Tena utoke chumbani kwangu kabla sijachukia” Salome akacheka sana, kisha
akamwambia Ana, “Subiri sasa utakachokiona” Kisha Salome akatoka
na kumkuta Sara mlangoni ambaye alikuwa amepigwa na butwaa tu kwa maneno ambayo
Salome alimwambia mdogo wake, kisha yeye akaingia ndani kwa mdogo wake ili
kumuona vizuri na kujaribu kumuuliza mawili matatu, “Ana
vipi?” “Vipi nini, nani amekwambia na wewe uingie chumbani kwangu bila
ruhusa?” “Jamani Ana” “Jamani nini? Naona na wewe unanitafuta
kama huyo mtoto wa kuokota uliyemleta humu ndani eti aje atupe vitisho, sikiliza
wewe mdada usiyejielewa na akili zako mbovu hizo. Usitake na leo nikufanyie kitu
kibaya” “Kwani wewe Ana ni mchawi?” “Ndio mimi ni mchawi ulikuwa
hujui eeeh! Mimi ni mchawi wa wachawi na huwa sibabaishwi na vikaragosi kama
wewe na huyo mwehu mwenzio” “Kheee kumbe kweli wewe ni mchawi sasa
umepata wapi uchawi?” “Nimepata wapi? Usinichekeshe na wewe, uliona wapi
mtoto wa paka akawa mbwa?” “Inamaana mama naye ni
mchawi?” “Usiniulize maswali mwehu nini wewe, tena usinikere sasa hivi.
Nina uwezo wa kukugeuza hata mende namuonea huruma tu mama yako. Ondoka chumbani
kwangu upesi” Sara aliondoka ila ndio akapata maswali mengi zaidi kuwa
ni kweli mdogo wake na mama yake ni wachawi. Mr.Patrick
hakuonekana kabisa lakini Salome alielewa kitu gani kimempata Mr.Patrick na
alihitaji kumsaidia bila yaw engine kuwa na mashaka, akajifanya kumuita mama yao
sebleni maana alijua muda huu ni karibia wale mapacha walikuwa wanarudi, ni
kweli baada ya kumuita tu wale mapacha nao walikuwa wamerudi, Salome alianza kwa
kumuuliza, “Yuko wapi baba
yangu?” “Sijui” “Hujui!” “Ndio nimekwambia sijui, halafu
wewe mtoto sitaki maswala ya kunipanda kichwani kwenye nyumba yangu mwenyewe
sitaki unipande kichwani” “Sawa sitakupanda kichwani ila kila mmoja humu
ndani ataona baba alipo leo” “Unamaanisha nini?” “Si hujataka
kusema baba yuko wapi, basi nitamuonyesha kila mmoja alipo baba” “Hivi
wewe msichana una nini na kwanini unajiamini hivyo?” “Unaogopa kujiamini
kwangu eeh! Najiamini sababu najua hakuna wa kunishinda, baba yangu yuko wapi?
Nimekuwa mpole sana kwa siku zote hizi ila hujiongezi wala nini. Subiri tena
nakwambia kila mmoja nitamuonyesha baba alipo leo” kisha Salome
akaondoka zake na kwenda chumbani kwake, kwakweli Rose alimshangaa sana Salome
kuwa anajiamini na nini mpaka anafikia kumwambia yeye maneno yale wakati watu
wengi sana wanamuogopaga yeye, ikabidi aonoke aende chumbani kwa binti yake Ana
kuzungumza nae basi na yeye akamueleza mama yake vitisho alivyopewa na
Salome, “Hivi anajiamini nini Yule?” “Hata mimi mwenyewe
namshangaa mama sijui anajiamini nini?” “Tunatakiwa kufanya jambo mapema
iwezekanavyo” “Ndio mama” “Sasa tutafanya
nini?” “Tumuingize kwenye kile chumba” “Sawa sawa
mwanangu” Wakaanza kukubaliana pale namna watakavyomtokomeza Salome,
bila ya kujua kuwa mbinu nyingi Salome anazijua. Muda huu Sara
alienda kuwafata kaka zake na akaongea nao namna ambavyo mama yake alimwambia
mchana, ila wale mapacha wakapinga vikali kauli ya mama
yao, “Haiwezekani, kwakweli haiwezekani kabisa. Mimi nitaoa labda wewe
Doto ndio hutooa” “Mimi pia nitaoa, labda wewe mwanae wa kwanza ndio
hutaolewa. Sisis tusioe kwa misingi gani? Kwanza mchumba wangu yupo tayari, ni
kitendo tu cha kumleta nimtambulishe” “Mmmh msiwe wabishi, mwenzenu
mchumba wangu amepotelea humu kwenye nyumba” “Kivipi?” Sara
aliwaeleza jinsi Ommy alivyopotea kiajabu ajabu, na kuwaambia kuwa kitu hiko
amekiona kwenye ndoto. “Mmh kwa staili hii simleti tena Yule mchumba
wangu” “Mimi nitamleta tu bila kujali chochote, Yule ni mama yetu lakini
hatakiwi kuingilia kwenye mahusiano yetu. Kwanza tusioe kwanini? Au wewe
usiolewe kwanini? Hebu acha hizo bhana.” Mmoja akajikuta akikumbushia
ishu ya Salome, “Jamani huyu dogo Salome mnamuelewa
kweli?” “Jamani Yule mtoto kaka zangu ni ana mambo ya ajabu yani ya
ajabu sana, nimejaribu hata kulala nae nimchunguze ila cha kushangaza nikilala
nae nakuwa kama mzigo yani nikilala sishtuki hadi kunakucha yani hata chooni
siendi. Yule dogo mi mwenyewe simuelewi” “Ila wewe Sara una moyo, hata
kulala na mtu asiyeeleweka vile unaweza mmmh! Mtoto haeleweki Yule, sijawahi
kumuelewa toka siku ya kwanza amekuja humu ndani” “Ila kuna kitu nahisi
kuhusu huyu dogo” “Kipi hicho doto?” Gafla wakasikia sauti ya
mama yao akimuita Salome kwa ukali sana, ikabidi nao waende kushuhuia kuwa kuna
nini mbona ameitwa hivyo. Kufika sebleni walimkuta mama yao akiwa na Ana
halafu muda kidogo Salome nae alifika ila kabla hakijaongelewa chochote
walishangaa kumuona mama yao akimsogelea Salome na kumsukuma kwa nguvu. Rose
alijua Salome ataanguka chini ila ilikuwa kinyume maana Salome hakuanguka chini,
Rose akamsukuma tena ila Salome alisimama kamavile mlingoti. Muda huu Rose
alipotaka kumsukuma tena Salome alishangaa mkono wake ukianza
kutetemeka. Rose alijua Salome ataanguka chini ila
ilikuwa kinyume maana Salome hakuanguka chini, Rose akamsukuma tena ila Salome
alisimama kamavile mlingoti. Muda huu Rose alipotaka kumsukuma tena Salome
alishangaa mkono wake ukianza kutetemeka. Kila mmoja ndani ya nyumba yake
alimshuhudia Rose akitetemeka mkono, Ana akainuka kwani aliona mama yake asije
akaumbuka yeye kisha Ana akamsukuma yeye Salome ila kwake ndio ikawa kinyume
kabisa kwani mkono wake uliganda kwenye mwili wa Salome, kila mmoja alikuwa
akishangaa na kati ya wale mapacha na Sara hakuna aliyeweza kuongea neno
lolote. Mara Salome alianza kuelekea vyumbani ila Ana ambaye mkono wake
uliganda kwa Salome alikuwa akimfata nyuma, halafu Rose naye ambaye mkono wake
ulikuwa ukitetemeka alikuwa akimfata nyuma pia, kitendo hiko kiliwafanya wale
mapacha na Sara wafate nyuma kwani walitaka kujua ni nini kinaendelea au ni kitu
gani huyo Salome anataka kufanya. Salome aliongoza moja kwa moja mpaka
chumbani kwa Rose na kufungua mlango, kila mmoja alikuwa akimfata nyuma huku
wengine hawaelewi elewi, alikutwa Patrick akiwa amelala chini sakafuni, Salome
akamuangalia Rose na kumuamuru, “Muamshe” Rose akiwa
anatetemeka, alisogea kwa Patrick na kujaribu kumuamsha. Alimuamsha kwa muda
akashindwa, akainua kichwa chake na kumtazama Salome kwa uoga kisha
akamwambia, “Nakuomba basi wanangu watoke humu chumbani
nimuamshe” “Unashindwa nini kumuamsha hivyo hivyo?” “Tafadhali
usinidhalilishe, nakuomba watoke kwanza ndio nimuamshe. Nipeni dakika chache tu
nitakuwa nimemuamsha” Salome akatoka nje na wengine wote walimfata nyuma
hadi sebleni kwahiyo walimuacha mama yao akiwa chumbani na Patrick. Kila
mmoja alikuwa akimshangaa tu Salome na wala Ana hakuweza kuutoa mkono wake
kwenye mwili wa Salome maana uligandia alipotaka kumsukuma, kwahiyo walikuwa
wamesimama tu na hakuna yeyote aliyethubutu kukaa wala kusema neno lolote kwa
wakati ule kwani wote walijikuta wakimtazama tu Salome. Baada
ya muda kidogo, mama yao alirudi na Patrick sebleni na muda huu hata Ana akaweza
kuutoa mwili wake kwenye mwili wa Salome, basi Salome alienda kumfata Patrick na
kumkalisha kwenye kiti kisha akapitisha mkono wake machoni pake na
kusema, “Nataka uone yote na zaidi ya yote amabayo mkeo amekuwa
akikutendea kwa miaka yote hii” Ikawa kama akili ya Patrick imefunguka
kiasi hivi kwani alianza kujishangaa na kuhoji kuwa yuko wapi, “Nikowapi
hapa?” Ni Salome pekee aliyekuwa na ujasiri wa
kumjibu, “Unatakiwa kutulia kwanza maana ndio umetoka kifungoni ni ngumu
kujua kwa mara moja ulipo. Tulia kwanza tuliza akili halafu utajua ulipo na kila
kitu ingawa kuna baadhi ya vitu utavitambua badae sana” Patrick alikaa
kimya kwani alikuwa kama haelewi elewi vile. Walitamani kumuhoji Salome
lakini hakuna aliyekuwa na ujasiri wa kufanya hivyo, kisha Salome akainuka na
kwenda zake ndani kisha akawaacha wote pale sebleni. Yani kama kuna siku ambayo
Rose aliwaonea wanae aibu basi ilikuwa ni siku ya leo maana nae hakuweza tena
kukaa pale sebleni bali aliondoka na kwenda chumbani kisha Ana nae akafata na
kwenda chumbani kwake. Kwahiyo sebleni walibaki wale mapacha, Sara na Patrick.
Muda kidogo Patrick alimuangalia Sara na kumuomba jambo, “Naomba
kaniletee simu yangu na funguo za gari chumbani” Sara hakubisha wala
nini, alifanya hivyo na kwenda chumbani kwa mama yake ambapo aligonga na mama
yake alimkaribisha kwani alijua ni Ana, akashangaa kumuona ni Sara. Akamuuliza
kwa mshangao, “Vipi tena?” “Baba kanituma funguo za gari na simu
yake” “Chukua hivyo hapo mezani mpelekee” Yani siku ya leo hata
kuhoji hakuhoji zaidi ya kusema funguo zilipo na simu ya mumewe, simu ambayo
mume wake ana kitambo sana hajaishika wala kuwasiliana na watu. Sara alichukua
na kwenda kumpelekea baba yake huyo wa kambo. Alipompa tu Patrick alitoka nje na
kuondoka zake, tena hakuna aliyemuaga kuwa anaenda wapi. Wale mapacha
waliangaliana na dada yao Sara, halafu Sara akawaambia, “Yani kwa
matukio haya naogopa hata kulala peke yangu” “Sasa utalala na
nani?” “Sijui yani” “Basi kalale na Ana au Salome” “Mmmh
hao watu ni bora uniambie nikalale getini na mlinzi, nawaogopa hao watu kama
kitu gani” Mara Salome akatokea, Sara akajikuta tu
akimwambia “Baba kaondoka tena bila kuaga, halafu leo kachukua na simu
yake” “Ungekuwa ni wewe ungeweza
kuaga?” “Kivipi?” “Unajifanya hujui ambayo baba yangu alikuwa
akitendewa kwenye nyumba hii? Sasa anatambua kila kitu, maswala ya kumfanya
mwenzenu kama ndondocha mwisho” Sara aliwaangalia wenzie, halafu Salome
alitoka nje kabisa na alionekana akielekea getini ambako alitoka na
kuondoka. Sara aliwauliza wenzie, “Jamani mnamuelewa huyu
mtoto?” “Simuelewi na sitaki kuongea sana” “Hata mimi pia
simuelewi na naogopa kuongea sana” Kisha wale mapacha wakaondoka zao na
Sara akaondoka zake. Rose alipoona mwanae Ana hajaenda chumbani
kwake ikabidi yeye mwenyewe ndio aende chumbani kwa Ana, aliingia na kumuuliza
mwanae, “Hivi wewe umeweza kumuelewa huyu Salome?” “Mama naomba
tuzungumze usiku kwenye muda wetu sio muda huu” “Hata tukisema
tuzungumze usiku hatatusikia kweli?” “Mama, mimi ndio nimekwambia na
bado natafakari maana sipo sawa kabisa. Amewezaje Yule kugandisha mkono wangu
mama? Yule msichana ana majini sio bure” “Ndiomana nakwambia tujadili
sasa hivi, unajua ile majuzi nilienda kwa mganga mwingine halafu ndani kwa
mganga nilimkuta Moza” “Moza!” “Ndio nilimkuta Moza” “Si
amekufa huyo mama” “Mwanangu hatuna uhakika na kifo cha Moza, kumbuka
maiti yake ilitoweka kaburini” “Ndio ilitoweka ila nikajua utafanya
jambo, na imekuwaje hadi Moza awe hajafa kweli?” “Sijui mwanangu, ila
kama ile dawa iliyomuua Moza ilichomwa moto basi tumeisha” “Unamaana
gani mama?” “Ile dawa mwanangu nilipewa na ilikuwa hairuhusiwi kuonekana
na mtu yeyote halafu sitakiwi kuiweka mbali na nyumba yangu ndiomana nikaifukia
kwenye ua ili nijue ni ua gani nimeifukia. Ni ya muda mrefu sana ile dawa na
ilikuwa hairuhusiwi kuonekana na mtu yeyote wala kuungua na moto ndiomana hata
kuunguza mboga humu kwenye nyumba yangu huwa sitaki. Sasa kama imechomwa moto
sijui itakuwaje, ndiomana tulitakiwa kumzika nayo Moza” “Sasa mama kama
imechomwa moto imechomwa na nani wakati Moza alikuwa amekufa nayo
mkononi” “Kwamaana hiyo inawezekana ipo mahali eeh! Lakini mbona
tuliitafuta bila kuiona popote” “Mi nadhani mama tufanyie usafi kile
chumba cha Moza tuitafute kabla hayajawa majanga” “Sasa lile shetani
linalolala kwenye chumba kile tutalifanya nini?” “Yani huyo mtu
ananiumiza kichwa balaa, ila mama na wewe kwanini dawa ya maana hivyo ukaenda
kuifukia kwenye ua? Mbona mimi dawa yangu ile ipo chini ya godoro” “Ni
masharti ya ile dawa, kwanza haikutakiwa kuwekwa ndani ya nyumba ila inatakiwa
iwe karibu na nyumba halafu haitakiwi mtu aione.” “Basi mama nitatumia
dawa yangu kufanya kitu ili tuweze kupekua kile chumba cha Moza” “Sawa
mwanangu, ndiomana nilikuwa nakufata tujadili. Sasa wewe unataka tufanye kwenye
muda wetu, unadhani mambo yalivyotinga hivi tutakumbuka kujadiliana kweli! Ni
ngumu mwanangu” “Kweli mama ila chanzo cha mambo yote haya ni mwanao
Sara, yani simpendi Yule mdada simpendi kabisa” “Kweli mwanangu ni
chanzo cha yote lakini ni mwanangu, kumbuka hilo. Yule ni dada yako mpende
tu” Rose akajiribu pale kumshawishi mwanae ili ajende upendo kwa ndugu
yake maana alikuwa anapenda watoto wake wapendane. Salome
alienda nyumbani kwa mama yake na kumkuta kama kawaida akiwa na wale wadogo zake
John na Joseph. Aliwasalimia kisha mama yake akamuomba chumbani kwake ili
wakazungumze “Kwanza imefurahi umerudi nyumbani maana mambo yako siku
hizi siyaelewi kabisa. Halafu ngoja nikuulize, hivi una simu” Salome
akacheka, “Sio unacheka Salome, nijibu una simu?” “Ndio nina
simu” “Umeitoa wapi?” “Baba yangu kaninunulia ili niweze kuongea
nae” “Haya, wadogo zako wameniambia Ashura hakuja huku kwenye nyumba
mpya, halafu wewe na Ashura kuna mchezo mlikuwa mnacheza kisha Ashura akaanguka.
Unajua sijaelewa naomba nieleweshe maana huyo Ashura hata nikimpigia simu zangu
hapokei zaidi ya kunitumia ujumbe tu” “Hivi hat nikikueleza unaweza
ukanielewa!” “Nieleze tu, kwanini nisikuelewe?” “Acha tu ufahamu
unavyofahamu, Yule Ashura si ndugu yako? Uliza kwa ndugu zenu
alipo” “Hivi wewe mtoto unaongelea nini mbona sikuelewi?” “Huyo
mamdogo Ashura yupo kwenye kijiji cha baba yenu amesema anaenda kuangalia kaburi
la baba yenu kwahiyo ungeenda na wewe kijijini ili uulize vizuri kuhusu
Ashura” “Tutaenda na wewe?” “Hapana, mimi nitabaki ila utaenda
na wadogo zangu. Mimi nabaki na baba yangu.” “Haya nitafikiria
kwenda” Salome akainuka, na kumfanya Neema amuulize tena, “Sasa
mbona unaondoka kabla hata sijamaliza maongezi na wewe” “Subiri nakuja
sasa hivi” Salome aliondoka zake, Neema nae alitoka ila kiukweli
hakumuelewa kabisa mwanae na mambo aliyokuwa anayafanya. Alipokaa muda
kidogo mwanae alirudi kisha akampa mama yake tiketi, “Nimeshakukatia
tiketi, wewe na wadogo zangu ya kwenda kutembelea kaburi la babu” “Kheee
kwahiyo ndio unataka tusafiri!” “Ndio, si mnaenda kukaa wiki tu
mnarudi” “Kwahiyo tiketi umekata ya kuondoka lini?” “Kuondoka
kesho” “Kheee Salome hebu acha masikhara, tutaondokaje kesho wakati
hatujajipanga!” “Unataka mjipangaje?” “Sijapanga nguo za watoto,
sijawanunulia mama zangu vitenge” “Ni hayo tu au kuna
mengine?” “Ni hayo ndio” “Basi nitakusaidia, yani wewe tulia tu
nitakusaidia kupanga ila tiketi ni ya kesho” Neema alimshangaa sana
Salome kuwa mtoto wake amebadilika sana na amekuwa na maamuzi ya haraka haraka,
akawa anaziangalia tu zile tiketi ambazo alikuwa amekatiwa na
Salome. Usiku kwenye mida ya saa tatu, Neema akiwa
amejipumzisha kidogo akamsikia Salome akiingia ndani kwake na
kumwambia, “Mama kila kitu nimekupangia kwahiyo kesho
safari” “Na nguo zangu, na za wadogo zako umepanga?” “Ndio
tayari” “Ila vitenge bado sijanunua” “Nilishaenda
kununua” “Kheeee hebu tuvione” Salome alimtolea Neema vitenge
ambavyo aliviangalia na kushangaa tu kuwa Salome amewezaje kwenda mjini kwa muda
mfupi vile na kuchagua vitenge bvizuri vile, akainuka na kuangalia mabegi ni
kweli yalikuwa yamepangwa vizuri kabisa kwahiyo hakuwa na cha kubisha kuhusu
safari ya kesho, swala hilo hata likamsahaulisha kuwa alishauriwa mwanae
ampeleke kwenye maombi. “Nishaongea na dereva tax, kwahiyo atakuja
kuwachukua kesho asubuhi” “Kwahiyo nyumba nani atafunga?” “Mimi
nitafunga, na mkiwa mnarudi mtanikuta maana nitakuwa narudi mara kwa
mara” Neema alimuangalia mwanae Salome hakummaliza maana kwa kawaida
Salome wake ni muoga ila leo hii anakubali kuachwa mwenyewe nyumbani na anasema
atakuwa anaenda mara kwa mara hata wakirudi watamkuta, alimshangaa kwakweli ila
akajisemea labda ndio kukua kumemfanya abadilike. Usiku wa
manane, Rose alichukuana na mwanae kwenda kufanya msako kwenye chumba cha Moza
kutafuta ile dawa iliyomuua Moza maana walihisi bado ipo ndani. Basi walipekua
na kupekua lakini hawakufanikiwa kuiona, ndipo walipoanza kupekua nguo moja moja
ya Moza ila Ana akamwambia mama yake, “Mama, tutajichosha bure. Ngoja
twende chumbani kwangu nikachukue ile dawa yangu ituonyeshe” Rose
aliafikiana na mwanae na kujilaumu kuwa kwanini walikuwa wakijichelewesha wakati
kuna njia rahisi ya kufanya, basi wakatoka mule chumbani kwa Moza na kuelekea
chumbani kwa Ana walipofika walishangaa kumuona mtu amekaa kitandani kwa Ana
halafu mtu huyo akawaangalia na kuwafanya wagundue kuwa ni
Moza. Rose aliafikiana na mwanae na kujilaumu kuwa kwanini
walikuwa wakijichelewesha wakati kuna njia rahisi ya kufanya, basi wakatoka mule
chumbani kwa Moza na kuelekea chumbani kwa Ana walipofika walishangaa kumuona
mtu amekaa kitandani kwa Ana halafu mtu huyo akawaangalia na kuwafanya wagundue
kuwa ni Moza. Kwa mara ya kwanza Ana alishikwa na uoga ambao hajawahi
kuupata kabla, wakafunga mlango haraka haraka na huku wakihema juu juu, hakuna
aliyeelewa kwa wakati ule ila wakajikuta tu wanaenda tena chumbani kwa Moza, ila
kwa wakati huu napo walimkuta amekaa kitandani, katika siku zote leo mkojo
ulimtoka Ana kwa uoga walifunga tena mlango na kukimbilia sebleni huku wakihema
juu juu na wakikumbatiana mama na mtoto, kwa wakati huo hakuna uchawi walioweza
kuufanya maana uwepo wa Moza uliwachanganya kuwa ni mzimu au ni kitu gani. Hata
sebleni hawakuweza kukaa sana kwa uoga wakafungua mlango na kukimbilia nje.
Kitendo hiki kilimshtua pia mlinzi aliyekuwa kalala, aliamka na kwenda kuwauliza
kuwa tatizo ni nini, Ana alijikuta akiropoka, “Kuna mzimu
ndani” “Mzimu!” “Ndio, kuna mzimu wa Moza” Gafla
wakahisi kama eneo hilo linatingishwa yani kama mtu anatingisha ardhi, kisha
wote wakazimia. Rose, Ana na mlinzi wao. Kulipokucha, wale
mapacha waliamka na kujiandaa kutoka kama kawaida na wazo lao walihisi kumkuta
mama yao sebleni ila hawakumkuta, muda kidogo Sara nae akatoka na kuwauliza kaka
zake, “Eti mama ameshaondoka?” “Sijui, sisi wenyewe hatujamkuta
hapa sebleni” “Nimeenda kumuangalia chumbani kwake nimemkosa, sijui
atakuwa wapi” “Sie tunaondoka bhana” “Nisubirini, yani jumba
lote hili mniache peke yangu” “Mbona zamani ulikuwa unaweza kubaki peke
yako!” “Ushasema zamani, siku hizi mambo yamebadilika. Nisubirini
bhana” Wakamsubiri dada yao ajiandae, alipomaliza akatoka kisha wakatoka
nje ili kuondoka ila wakashangaa walipotoka kumuona mama yao, mdogo wao na
mlinzi wakiwa chini wamelala maana walipowaamsha waliamka na kushangaa sana,
Sara alimuuliza mama yake, “Imekuwaje mama?” “Sina jibu
kwasasa” Yule mlinzi aliinuka na kwenda kwenye lindo lake, kisha Rose na
Ana waliinuka na kwenda ndani. Ila muda huo Rose aliwaomba wanae wasiondoke
wamsubiri kwanza, ikabidi wamsubiri kwani hakuna aliyekuwa anajua kuwa mama yao
amepatwa na nini. Wakati ameenda kujiandaa walienda kumuuliza mlinzi
kuwa ni kitu gani kimetokea, “Hata mimi sielewi” “Huelewi
kivipi?” “Yani sielewi sijui hata imekuwaje mpaka nimelala
pale” “Kwahiyo hujui ni kitu gani kilitokea?” “Sijui kweli yani
sijui kabisa” Wakamuacha na kurudi ndani wakimsubiri mama yao na Ana.
Baada ya muda kidogo mama yao akatoka, na swali la kwanza alimuuliza
Sara, “Salome mbona sijamuona kaenda wapi?” “Aliondoka jana na
hakurudi tena” “Aaah sawa, jamani leo mkitoka nawaomba muda wa kurudi
msubiri hadi niwapigie simu, asirudi yeyote hapa ndani hadi niwapigie simu. Mimi
na Ana kuna mahali tunaenda” Watoto wake wakatazamana maana hawakuona
kama lile jambo lilikuwa na umuhimu kiasi cha wao kurudishwa wasiondoke kwa muda
huo na wasubirie maana angeweza hata kuwapigia simu na kuwapa ujumbe huo, baada
ya maongezi hayo nyumba nzima wakatoka, kwakweli Rose hakuwa hata na muda wa
kuulizia kuhusu Patrick kwani kadri siku zilivyoenda mbele ndivyo akili yake
ilivyozidi kuchanganyikiwa. Rose alikuwa na mwanae kwenye gari
na safari ilikuwa ni kwenda kwa mganga, “Kwahiyo mama tunaenda kwa
mganga yupi?” “Kuna mganga alikuwa ananisaidia sana, ila yupo mbali yani
gari haifiki kule anapoishi. Hapa itabidi tuache gari mahali halafu tuanze
kukanyaga kwenda, huyo ni kiboko najua atatusaidia na hili jinamizi la
Moza” “Kwahiyo mama kwa huyo mganga ni mbali hivyo, bora ungeenda
mwenyewe tu mi nitachoka kutembea” “Mwanangu usichoke, nitawaomba hata
watu wakubebe maana ukiwa na pesa kila kitu kinawezekana” “Sawa mama,
ila una uhakika atatusaidia huyo? Hivi mama hukuwahi kufikiria mambo kama
haya?” “Kwanza sijawahi kufikiria kama kuna mtu angeiona ile dawa
niliyoichimbia chini kwenye lile ua ukizingatia nilikuwa nataka kila siku
limwagiliwe maji ili palowane na pasiunguzwe na jua. Yani Yule mwehu Yule dah
sijui nafanyaje kumuepuka, ila twende huko mwanangu” Wakaenda hadi
wakafika mahali pa kuacha gari na kuanza kutembea kwa miguu, “Kheee
mama, lile daraja nitawezaje kuvuka?” Wakati anafikiria namna ya mwanae
kuvuka hapo darajani, akamuona kijana na kumuomba ili amvushe mwanae ila Ana
machale yakamcheza na kukataa kuvushwa na yule kijana kisha akamwambia mama yake
ambebe tu mgongoni, “Jamani mwanangu, unajua umekua sasa” “Ndio
nimekua mama ila kuvushwa na huyo kijana hapana, nibebe tu mwenyewe univushe.
Nitakwambia kwanini nimegoma kuvushwa na Yule kijana” Basi Rose akaamua
kumbeba mwanae mgongoni na kuvuka nae, lile daraja lilikuwa na mwendo kidogo ila
walimaliza kuvuka na kufika ng’ambo ya pili. Rose alimuuliza mwanae kuwa
kwanini amegoma kuvushwa na Yule kijana, “Hakuwa mtu wa kawaida Yule
mama” “Kivipi?” “Mama, kumbuka ulivyonielezea kuhusu kule kwa
mganga ulipoenda unajua kwanini yalikukumba
maswahibu?” “Kwanini?” “Kwasababu uliliokota lile begin a
kuliweka kwenye gari lako halafu ukatembea nalo kila mahali, yani Yule kijana
angenivusha pale darajani asingekubali anishushe na tungeenda nae mpaka kwa huyo
mganga halafu yangetupata maswahibu” “Mmmh mwanangu!” “Ndio
hivyo mama” Wakaendelea na safari yao, mahali ambako Ana alichoka
alimwambia mama yake ambebe na alitembea nae, walitembea kwa takribani lisaa
limoja, kwakweli Ana alichoka sana ila alivumilia sababu yeye na mama yake
walihitaji tiba haswaa kwa muda huo. Hatimaye walifika kwa mganga
waliyemtaka na walikuta foleni ya watu kama watatu hivi, nao wakaunga foleni.
Huyu mama akamuuliza wa mbele yake “Hivi hakuna njia rahisi ya kutuleta
huku?” “Njia ipo ila ni mbali sana, unazunguka sana mpaka kufika huku
yani unaweza kutumia siku nzima” “Kheee lakini gari si
linapita?” “Gari linapita ndio, ila inatakiwa kuwa makini sana huko. Ila
hata huku sio mbali kivile ni daraja tu ndio linaharibu njia lakini boaboda
zipo” “Mbona hatukuziona?” “Hamkuziona? Labda zilikodiwa zote
ila huwa zipo” Kidogo Rose alishukuru alivyosikia bodaboda zipo maana
kwa huyo mganga alikujaga muda mrefu sana, kwahiyo hakujua kama kuna maendeleo
ya kuwepo bodaboda ingawa hawakuziona na mwanae muda walipokuwa wanaenda hata
njiani hawakukutana na bodaboda ya aina yoyote. Siku ya leo
wale mapacha na dada yao walienda sehemu moja ila njiani wakakutana na Salome
akidai kuwa anaenda nyumbani, “Ila hakuna mtu nyumbani” “Kuna
nguo yangu naenda kuichukua” “Unawezaje kwenda kwenye nyumba ya watu
bila ya wenyewe kuwepo?” “Leo unaniuliza hivyo Sara, hivi siku ile
ningeogopa kuja ungepona macho yao hayo?” “Ila mama amekataza kwenda
nyumbani amesema hadi apige simu?” “Amewakataza ninyi sio
mimi” “Mmmh kasema mtu yeyote” “Jamani nina uhakika hata
nikiwauliza sababu ya kukataza mtashindwa kunijibu, Ngoja niende zangu
tu.” Sara akawa kimya kwa muda basi Salome akawaaga na kuondoka, wakati
Salome anaondoka tu kabla hawajaongea chochote alitokea rafiki yake na Sara,
kisha aliwasalimia na kuwauliza kuwa Salome ni nani yao, “Yule
aliyeondoka ni nani yenu?” “Ni ndugu yetu” “Aaah kumbe siku zile
alipona?” “Siku gani?” “Siku ile aliyoangukia
kaburini” Wote wakamshangaa kwani hakuna aliyekuwa na wazo kuwa ni
Salome ndio aliangukia kaburini, “Mbona hatukuelewi?” “Siku ile
wakati anazikwa Yule mdada wenu wa kazi basi huyu msichana ndio aliangukia
kaburini na akawa kama amepigwa shoti” “Mmmh au
umemfananisha?” “Hapana sijamfananisha, zile nguo ndio zile zile alikuwa
amezivaa siku ile. Halafu nilimshuhudia hadi anapakizwa kwenye gari ili apelekwe
hospitali. Nikataka kwenda na mimi ila wakanikatalia. Tena nakumbuka hata dereva
aliyembeba ni mtu ambaye anafahamiana na mtu ninayemfahamu, ngoja tukamuulize
vizuri ila ni yeye” “Mmh wewe rafiki yangu wewe Jesca, acha maneno
yako” “Jamani mimi ule umbea mlinifukuzaga kwenu pale nisikanyage
nimeshaacha na wala huu ninaoongea sio umbea ni ukweli kabisa. Yule msichana
alitumbukia kaburini na akakauka kama amepigwa shoti ya umeme” Wale
mapacha hawakuyaamini maneno ya rafiki wa Sara na kuomba wapelekwe kwa huyo
dereva kwa uthibitisho kwani lazima dereva aliyembeba alikuwa anajua, na Yule
msichana aliamua kuacha mambo yake aliyokuwa anafanya kwa muda huo na kwenda
kumtafuta huyo dereva. Zamu yao ilifika ya kuingia kwa Yule
mganga, waliingia na kumkuta ambapo kabla hawajamueleza matatizo yao Yule mganga
aliwaambia, “Najua kila kitu, yani kitu pekee kinachowasumbua ni
Moza” Walishtuka na kuangaliana sababu huyu mganga amejua kabla hata
hawajamueleza, Rose akamuitikia Yule mganga, “Tawile baba, yani hata
hatujui tufanye nini” “Hapa ndio mwisho wa matatizo, yani mimi ndio kila
kitu. Mimi ni tishio la vitu vyote vya ajabu, Yule Moza amerudi kwa lengo moja
la kukukomesha wewe. Yule msichana alijua siri zako mapema sana kabla hata
hujajua kuwa anafatilia siri zako, na kitendo chake cha kupata ile dawa ndio
kila kitu kimekuwa wazi kwake” “Kwahiyo inamaana Moza ni
mzimu?” “Moza ni zaidi ya mzimu ambao unajua wewe, Moza ana nguvu za
ziada kwani ana nguvu za kutoka kwenye mzimu wa bibi yake na ana nguvu za ile
dawa yako maana ilichomwa” Rose alishtuka sana kusikia kuwa dawa yake
ilichomwa kwani hapo alihisi kila kitu kimeharibika, kwakweli alihisi nguvu
kumuisha akauliza kwa upole, “Sasa kama ile dawa yangu ilichomwa,
aliichoma nani na je nifanye nini?” “Ile dawa ilichomwa na mume
wako” Rose na Ana walishangaa sana kuwa ile dawa imechomwa na
aliyeichoma ni Patrick, kwahiyo walijiuliza kuwa Patrick alipata wapi ujasiri wa
kuchoma ile dawa na kwanini alifikia uamuzi wa kuchoma ile dawa, “Kama
nilivyowaambia, Moza anaongozwa na mzimu wa bibi yake na mzimu huo ndio ulimtuma
Patrick akachome ile dawa halafu Moza aliongezeka nguvu mara mbili. Nyie mnahisi
Moza amekufa ila kiuhalisia Moza hajafa na amerudi kwaajili yenu” “Sasa
tufanyaje?” “Cha kufanya hapa ni kimoja tu” “Kipi
hiko?” Akamuangalia Rose na kumwambia, “Unatakiwa ulale na
mlinzi wako” “Nilale na mlinzi wangu?” “Ndio, unatakiwa ulale
nae” “Kheee nitawezaje kulala na mlinzi wangu?” “Nitakupa dawa
ya kukusaidia, na ukilala nae kwa hakika kila kitu utaona
kimebadilika” “Jamani mganga sikuelewi, kwanini mlinzi wangu nilale
nae?” “Yule mlinzi alikuwa anampenda sana Moza yani alikuwa na mapenzi
ya dhati na Moza. Unatakiwa kulala nae ili kutimiza ile azma ya mapenzi yake kwa
Moza kisha ndio tutamuweza Moza. Tena unatakiwa ulale nae kwenye chumba
alichokuwa analala Moza” “Mmh mbona umenipa mtihani mkubwa sana, je
litawezekana hilo?” “Nitakupa dawa na itawezekana” Rose
alijifikiria sana namna ya kulala na mlinzi wake maana siku zote amekuwa
akimdharau sasa leo anatakiwa alale nae, kwakweli aliona ni mtihani mkubwa sana
ila kwavile alichoshwa na vimbwanga vya hapa na pale akajisemea ni lazima afanye
hivyo ili aepukane na vimbwanga vile. Kwahiyo akakubali kuchukua dawa
aliyopewa na mganga, kisha kuuliza kuwa baada ya kulala nae
afanyaje. “Baada ya kulala nae tu, yani kwanza mumeo atarudi na kuwa
chini yako halafu Moza atakufa kweli. Nitakupa tu maelekezo ya hii dawa, ukifika
getini iweke mdomoni usiongee chochote na mlinzi wako, yani wewe mshike mkono tu
hadi chumbani kwa Moza halafu lala nae” “Hawezi kuniletea
shida?” “Usiongee kitu chochote, na kukataa hawezi hata
usijali” Basi Moza akachukua ile dawa na kuanza safari ya kuondoka akiwa
na binti yake Ana, ila muda huu walipata usafiri wa boaboda hadi
darajani. Salome alifika na kumkuta mlinzi akiwa getini, basi
Salome akamuomba kitu Yule mlinzi, “Kuna mahali nataka
nikuagize” “Mmmh yani niondoke niache lindo langu? Hapana
kwakweli” “Katika maisha yako, umewahi kupewa hela ipi nyingi kwa
mkupuo” “Nimewahi kupewa laki tano” “Basi mimi nataka nikupe
milioni mbili ila tu ukiniahidi kwenda ninapotaka kukuagiza” Yule mlinzi
aliposikia milioni mbili, kwakweli akili yake iliruka kidogo na kusikiliza
anapotaka kuagizwa, “Sio sehemu mbaya, nakuagiza hotelini alipo mzee
Patrick uende ukamshawishi hadi urudi nae hapa. Jitahidi kwa ujui wako wote
umshawishi arudi” Yule mlinzi hakuona kama ile ni kazi ngumu, ila
alihitaji kupewa hizo hela kabisa na kuuliza tena, “Na hapa getini
atakaa nani?” “Mimi nitakaa hapa getini kwa siku ya leo na siendi
popote, unajua Yule ni baba yangu. Nahitaji aje nyumbani” Kisha Salome
akamkabidhi pesa Yule mlinzi na kumuelekeza mahali alipo mzee Patrick halafu
Yule mlinzi akaondoka zake, ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Yule mlinzi kuondoka
kwenye lindo lake hilo wakati mama mwenye nyumba hayupo. Muda kidogo
alirudi Rose na binti yake Ana, ila walimkuta mlinzi yupo getini amesinzia. Rose
alikunywa dawa yake na kuanza kumvuta mlinzi mkono ili waelekee nae ndani, ila
mlangoni akakutana na Salome. Rose akashtuka kwani hakutegemea kukutana na
Salome mlangoni, halafu Salome akamuuliza, “Vipi huyo mlinzi unampeleka
wapi?” Rose alitamani kumjibu Salome ila akakumbuka masharti aliyopewa
na mganga kuwa asiongee kabisa akimeza ile dawa, hakujibu ila akataka kuingia
ndani ila Salome akamzuia mlangoni na kumfanya Rose achukie sana akatamani hata
mwanae Ana angekuwa karibu apambane na Salome kwani muda huu Ana alikuwa
ameachwa getini akisubiria mama yake amalize kwanza shughuli na
mlinzi. Rose akawa anang’ang’aniza aingie ndani, “Sikupishi hadi
uniambie huyo mlinzi unampeleka wapi?” Rose alipambana na Salome pale
mlangoni hadi akajikuta akimwambia, “Nipishe bwana weee” Salome
alimpisha huku akicheka sana, Rose alikuwa na hasira sana na alijiuliza kama
dawa itafanya kazi kama alivyoambiwa na mganga maana kashakosea masharti na
kuongea wakati aliambiwa asiongee chochote. Aliingia na Yule mlinzi
kwenye chumba cha Moza na kumuweka kitandani, kisha yeye akainuka na kuanza
kuvua nguo zake ila alipomaliza tu kutazama kitandani hakumuona mtu
yeyote. Salome alimpisha huku akicheka sana, Rose
alikuwa na hasira sana na alijiuliza kama dawa itafanya kazi kama alivyoambiwa
na mganga maana kashakosea masharti na kuongea wakati aliambiwa asiongee
chochote. Aliingia na Yule mlinzi kwenye chumba cha Moza na kumuweka
kitandani, kisha yeye akainuka na kuanza kuvua nguo zake ila alipomaliza tu
kutazama kitandani hakumuona mtu yeyote. Mlinzi alikuwa ametoweka,
kitendo hiki kilimshtua sana Rose na kumfanya achukue nguo zake haraka haraka na
kuvaa kisha kukimbia kutoka kwenye kile chumba cha Moza, ila kwenye korido
akakutana na Salome yani muda huu hakuweza hata kuongea na Salome zaidi ya
kukimbilia nje alipo mtoto wake, Salomealicheka sana kisha akaenda kukaa sebleni
na kuwaangoja Rose na mwanae watakavyorudi tena ndani. Basi Rose alifika
alipo mwanae Ana kwenye kile kijumba cha mlinzi, Ana alimuuliza mama
yake, “Tayari mama?” “Tayari nini mwanangu? Mambo
yameharibika” “Kivipi?” Mara geti lilifunguliwa halafu wakamuona
mlinzi ambaye aliingia na kwenda kufungua geti kubwa na liliingia gari la
Patrick. Rose alishtuka sana na kufikicha macho yake kwani alihisi ni kiini
macho. Alimshika mwanae mkono na kumpakiza kwenye gari kisha akaondoa gari nje
hata mlinzi na Patrick walikuwa wakishangaa ila Patrick alihisi kuwa Rose
anamkimbia kwani anajua kuwa anaujua ukweli wa mambo yote
sasa. Patrick na mlinzi waliingia ndani na kumuta Salome,
kwakweli Salome alimpongeza sana Patrick kwani aliona jinsi alivyomfanyia kazi
yake kuwa rahisi kwa siku hiyo, kisha akamkaribisha Patrick pale
ndani, “Karibu tena kwenye nyumba yako” “Ni kweli hii ni nyumba
yangu mwanangu, ila sina hamu nayo na siwezi kuishi humu
tena” “Kwanini?” “Sijisikii tena kuishi na mwanamke shetani kama
Rose, nilimuacha mke wangu mpole, mzuri na mcha Mungu Neema, aliyenipenda kwa
dhati. Lakini nilimuhisi vibaya kwa makosa ya kusingiziwa, kumbe alisingiziwa
kila kitu juu yake. Ashura ni ndugu wa mama yako ila ni mtu mbaya
sana” “Hapana Ashura hakuwa ndugu wa mama” “Kivipi hakuwa ndugu
yake na wakati alikuwa akiishi nae?” “Niambie kwanza Ashura ni mtu mbaya
kivipi na nitakueleza ni namana gani hakuwa na undugu na mama” Patrick
alianza kumueleza kwa kifupi jinsi ilivyofikia hadi kuachana na mama
yake, “Sikia, sikuwa namjua Ashura ila nilikutana nae nyumbani kwa Rose
na alitambulishwa kwangu kama msichana wa kazi wa Rose, wakati tunamuongelea mke
wangu basi Yule Ashura alidai ya kwamba anamfahamu yani yeye na Neema
wamechangia baba. Na akaanza kunieleza kuhusu historia ya Neema, anasema Neema
alianza uhuni mapema sana toka yupo darasa la tano na ametoa mimba nyingi sana,
ingawa mimi nilimuoa mapema pia ila hakuweza kunizalia sababu kizazi chake
hakikuwa na uwezo wa kuzaa maana katoa mimba sana. Ndiomana sikuona umuhimu tena
wa kuendelea na Neema wakati ukweli nimeujua. Niliporudi kwa Neema nilikuwa na
lengo moja tu la kumuacha kwani mawazo yangu kwa muda huo yalikuwa ni kuanzisha
maisha na Rose. Ila Neema aliweza kunishawishi hadi tukashiriki nae tendo la
ndoa, na baada ya hapo nikaondoka ila nikapata shinikizo la kumfukuza kwani
niliambiwa Neema alikuwa na mahusiano na kijana Fulani pale mtaani, na
nikambamba akiongea nae kwakweli nilikuwa na hasira sana nikamfukuza kabisa.
Nikashangaa baada ya mwaka mama ananiambia eti kuna mtoto nimezaa na Neema,
sikuamini. Kuna moyo mwingine ulikubali lakini niliendelea kujazwa ujinga kuwa
haiwezekani lazima mimba ile ilikuwa ya mtu mwingine kwahiyo nisijihusishe na
huyo mtoto. Sikutaka kujihusisha kweli, ila niliamini zaidi baada ya kuona Neema
akiishi na Ashura, hapo ndio nikajua ni ndugu yake.” “Pole sana, hizo
zote ni mbinu za Rose. Neema hakuwa na undugu wowote na Ashura ila kuna mipango
ilipangwa ndiomana ikawa hivyo na utaelewa tu” “Ila wewe nae
unanishangaza, mara nyingine unamuongelea Neema kamavile sio mama yako nan i mtu
uliyekuwa nae labda sawa” “Usijali kuhusu kuongea kwangu, huwa naongea
ili mtu anielewe, ila huyu mlinzi amefanya kazi nzuri sana” Salome
akamuita Yule mlinzi na kuwaandalia chakula mezani. Kisha akawakaribisha mezani
Patrick na mlinzi wale chakula, ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mlinzi kula ndani
ya ile nyumba. Wakina Sara walifikishwa na Jesca kwa mkaka
ambaye anasadikika kuwa alimbeba Salome wakati ameanguka kaburini, waliweza
kufika baada ya Yule Jesca kuwaunganisha na Yule ambaye alikuwa akimjua vizuri
Yule dereva. Walifika na kusalimiana kisha wakaanza maongezi ya hapa na
pale na haswa ni kuulizia kuhusu Salome, “Jamani hata mimi mwenyewe
sielewi, Yule mtoto alikuwa na mama yake kwenye gari na mama yake alikuwa akilia
sana, gafla nilisikia akiongea na mama yake na muda kidogo mama yake akaniambia
kuwa tusiende tena hospitali bali twende nyumbani kwao. Basi nilifanya hivyo kwa
kuwapeleka nyumbani kwao” “Mmmh kwahiyo hujui alizindukaje zindukaje.
Wewe si ulimbeba na uliiona hali yake?” “Ni kweli nilimbeba na alikuwa
kama mtu aliyepigwa na shoti ya umeme tena nilijua amekufa yani nilikuwa naenda
nao tu hospitali ila nilikuwa najua lazima tutaambiwa kuwa amekufa. Hata mimi
nilipomsikia anaongea tena akiwa mzima kabisa nilishtuka sana” “Mmmh
inabidi tukaongee na mama yake, lazima kuna kitu anakijua. Unapajua
kwao?” “Napakumbuka vizuri sana, kwa tukio kama lile lazima nikumbuke
kwao ni wapi” Basi wale kaka wa Sara wakamuomba huyu dereva awapeleke
kwao na Salome ili wakaongee na mama yake kwani kuna kitu walianza kuhisi kuwa
hakipo sawa na Salome na walihisi kuwa wakiongea na mama yake wataujua ukweli wa
mambo yote. Basi safari ikaanza ya kuelekea kwakina Salome, na kweli
walifika ila kwa bahati mbaya ilikuwa ni kwakina Salome kwa zamani na hakuna
hata mmoja pale mtaani aliyejua nyumba mpya waliohamia wakina Salome, na
waliambiwa ni kitambo sana wamehama. Ikabidi waachane pale na kila mmoja
kuelekea sehemu yake, ambapo wale mapacha na dada yao waliamua kurudi tu
nyumbani kwani siku ya leo hakuna walichofanya zaidi ya kufatilia mambo
hayo. “Ila mnakumbuka kuwa mama alisema tusirudi mpaka atupigie
simu” “Sasa mpaka saa hizi jamani, saa mbili hii labda mama kasahau.
Tumpigie tu simu sisi wenyewe” Wakaamua kumpigia simu mama yao ila simu
ya mama yao iliita bila ya kupokelewa ikabidi wakubaliane tu kurudi
nyumbani. Rose na Ana waliamua kwenda hotelini kwanza kutuliza
akili, Rose alianza kuongea na mtoto wake jinsi ndani ya nyumba alivyopatwa na
mauzauza, “Ila mama si ungejitahii usiongee!” “Mwanangu,
ningewezaje kujitahidi kufanya hivyo? Ilihali nishakwambia hali halisi
ilivyokuwa. Yule mwehu alikuwa ananizuia mlangoni, yani Yule mtoto sijui katumwa
Yule loh!” “Sasa mama tutafanyaje? Ni kurui kwa Yule mganga
au?” “Ndio, hakuna jinsi zaidi ya kurudi kwa Yule mganga
tu” “Kwahiyo mama usiku wetu wa leo tutamalizia humu
hotelini?” “Ndio, hakuna namna mwanangu” “Hapana mama turudi
nyumbani, hatutakiwi kuwa waoga kiasi hicho kwenye nyumba yetu wenyewe. Turudi
nyumbani mama, yani ni nyumbani tu ndiko tunakoweza kufanya hata dawa zetu
zikafanyika, ila huku hotelini tutachukua muda mrefu sana kufanya mambo
yetu” Ana akatumia muda mrefu sana kumshawishi mama yake ili aweze
kukubali warudi nyumbani na hatimaye akakubaliana na Ana, kisha wakaagiza
chakula kwanza na kula halafu ndio safari ya kurudi nyumbani ikafatia ingawa
ilikuwa ni usiku tayari. Salome alikuwa nyumbani ila Leo
aliongea sana na Patrick pamoja na yule mlinzi, kisha Patrick akataka kuondoka
tena ila muda huu Salome alimruhusu kuondoka kiasi cha mlinzi kushangaa kuwa
imekuwaje tena wakati alimpa hadi hela kuwa amlazimishe mzee huyo warudi nae
nyumbani, sasa iweje amruhusu kuondoka tena ila hakutaka kuhoji zaidi. Kisha
yule mlinzi alirudi getini halafu nae Patrick alienda kupanda gari yake na
kuondoka zake. Basi mlinzi akiwa amekaa pale karibu na geti, Salome
alienda na kumuuliza maswali, "Hivi kifo cha Moza, wewe umekionaje onaje
au unahisi kama ni kitu gani?" "Mimi nahisi kamavile ni kifo cha
kimazingara maana sukuelewa mwanzo wala mwisho" "Na Moza mwenyewe
ulikuwa unamuonaje?" "Sijui niseme nini ila nakiri wazi kuwa
nilimpenda" "Mbona hukumwambia?" "Ningemwambiaje vile alivyokuwa
anafanya mambo anayopenda yeye, ila nilitaka kumwambia hivyo hivyo sema umauti
tu ndio umeharibu mambo" "Je unaamini kama Moza amekufa
kweli?" "Hata Sijui niamini au, ila kama hajafa kweli basi atakuwa wapi
yani najiuliza bila jibu" "Mbona mimi unanijibu kila ninachokuuliza
tofauti na Moza ulimwambia hupendi umbea" Mlinzi akacheka kidogo na
kujibu, "Hela hii yani hela inafanya mtu hadi aongee ya ndani, mbona na
wewe unaniuliza bila kujali kuwa ni usiku sasa?" Kabla hajajibu,
waliwasili wale mapacha pamoja na dada yao Sara. Ila baada ya salamu tu, Salome
aliwakaribisha nao ndani hata wakashangaa kuwa Leo inakuwaje wanakaribishwa
kwenye nyumba yao wenyewe, wakaingia ndani na kumuuliza Salome kama mama yao
alirudi, “Bado hajarui, kwani mmeshawasiliana nae?” “Hapana,
hapokei simu” “Basi, na mimi sijamuona kurudi” Kila mmoja
aliendelea na shughuli zake nyingine pale nyumbani kwao kama kula halafu kwenda
chumbani kila mmoja, ila Salome alikuwepo pale pale sebleni siku hiyo maana
hakwenda kabisa chumbani kwake kule. Kwenye mida ya saa tano usiku, Rose
na mwanae Ana walirudi na kumkuta Salome pale sebleni ila hawakuongea nae kitu
chochote kile zaidi ya kupitiliza na kwenda vyumbani mwao. Rose
aliingia chumbani kwake akihisi kwamba Patrick atamkuta maana alimuona akirudi
ila alijiuliza kitu, “Inawezekana akawa Patrick wa mazingaombwe Yule.
Mlinzi mwenyewe hata kumsalimia namuogopa maana sina hakika kama ni yeye
kweli” Akaenda kuoga kisha akarudi, ila leo akakumbuka dawa zake ambazo
huwa zinamsaiia kumtoa uoga kabisa, na mara nyingi huzitumia kama anataka
kufanya tukio la tofauti ili asipatwe na uoga. Sasa kutokana na matukio ya siku
hiyo na yale ya siku za karibuni akaona ni vyema kuchukua hiyo dawa yake na
kuanza kuichoma, kwahiyo akachukua kiberiti na kuanza kuwasha dawa zake hizo
ambapo harufu ya dawa zile ilienea nyumba nzima. Mara akasikia mlango wake
ukigongwa, akainuka na kwenda kufungua, akamkuta Salome mlangoni akionyesha
kujawa na hasira halafu akamwambia, “Zima hizo dawa
zako” “Nizime ili iweje? Kwani wewe zinakusumbua
nini?” “Sizitaki zinaniumiza kichwa, nimekwambia zima” “Wewe
mtoto usinitishie maisha, kwanza umeharibu sana mfumo mzima wa maisha yangu
halafu saivi unajifanya unajua kila kitu. Dawa hizi sizimi na utanitambua baada
ya kumaliza kuchoma hizi dawa” “Unasema huzimi?” “Ndio
sizimi” “Unajiamini kabisa?” “Najiamini ndio na sizimi,
usinibabaishe” Rose akafunga mlango wake kwa nguvu kwani aliona kamavile
Salome anampigia makelele tu, kisha akarui na kuendelea kuchoma dawa zake ambazo
kwa yeye zilikuwa zinmburudisha sana na alikuwa anajisikia vyema moyoni ila ile
dawa ilikuwa inawaumiza sana watu aliowafungia kwenye chumba chake na ndiomana
Salome hakuitaka maana aliweza kuyahisi maumivu waliyoyapata watu
wale. Rose akiwa amestarehe kabisa na dawa zake, huku amezishika
akizichoma gafla alihisi kama kuna mtu amekuja na kuzizima, alipoangalia vizuri
alimuona Salome. Rose akashtuka kidogo kisha alimuuliza Salome, “Hivi
wewe ni mchawi? Umeingiaje humu?” “Dawa imeanza kukupa ujasiri
eeh!” “Nijibu umeingiaje?” “Kama ambavyo wewe huingiaga kwenye
vyumba vya watu vikiwa vimefungwa” “Wewe ni mchawi” “Hapana mimi
si mchawi” Gafla Rose akainuliwa na nguvu ya ajabu yani alikuwa kama
yupo juu akimtazama Salome kwa chini na mara akaona kama macho ya Salome
yakiwaka waka taa, kwa mara ya kwanza Rose alishikwa na uoga kiasi na kutaka
kupiga kelele ila alihisi kama akizibwa mdomo na hapo hapo akapata jibu kuwa mtu
pekee anayewasumbua kwenye nyumba ile si Moza bali ni Salome, yeye alihisi kuwa
Moza ameshakufa ila Salome ana nguvu za kichawi ndio anawasumbua. Kitu
kilichomshangaza kuhusu Salome kuwa ni mchawi wa aina gani ambaye hatambuliki na
wachawi wengine. Mdomo wa Rose ulikuwa umezibwa na akaamua awe mpole, alimuomba
jambo moja tu Salome, “Niruhusu hata nikalale sebleni kwa siku ya
leo” “Kwani unaogopa? Wewe ni jasiri, unatoa wapi uoga wa namna hiyo?
Kama umeweza kufuga watu na hawafurukuti kwako unawezaje kumuogopa mtu kama
mimi?” Rose alikuwa kimya tu akitetemeka kwani ukweli ni kuwa uoga
ulimshika vilivyo. “Muda wa kufanya uwanga wako unafika? Unajua matatizo
ya uchawi wa kununua? Utakudhuru mwenyewe tu. Haya toka ukalale
sebleni” Akajikuta tu ameachiwa na kuanguka kisha akainuka upesi na
kuanza kutoka chumbani kwake kwa uoga na kufanya haraka haraka, kufika sebleni
akamkuta Salome amekaa kwenye kochi, hapo ndipo akili yake ikapoteza dira
kabisa. Akajikuta tu ameachiwa na kuanguka kisha
akainuka upesi na kuanza kutoka chumbani kwake kwa uoga na kufanya haraka
haraka, kufika sebleni akamkuta Salome amekaa kwenye kochi, hapo ndipo akili
yake ikapoteza dira kabisa. Akashtuka ila Salome akacheka na
kumuuliza, “Unashtuka nini sasa?” Rose alikuwa kimya kabisa na
kushindwa kujibu kwani kadri alivyomuona Salome ndivyo uoga ulivyokuwa
ukimshika, kisha Salome akamwambia tena, “Wewe si ulikuwa unataka mimi
niuwawe wewe, eti unamwambia Ashura aniwekee sumu kwenye chakula, sasa unashtuka
saivi umeona mzimu au nsyuka? Si kila siku unaniona hapa, sasa unashtuka nini?
Pona yako wewe ni kuachana na mambo unayoyafanya, kwanza kabisa uwafungulie wale
uliowafungia” Rose alikuwa akitetemeka tu, ila Salome aliendelea
kuongea, “Nipe ahadi utawafungua lini?” “Nisamehe kwa hilo
sitaweza kufanya, naogopa kufa” “Kama wewe unaogopa kufa mbona unaua
wenzio bila huruma? Kwani Moza alikukosea nini hadi ufurahie kifo
chake?” “Sikufurahia na wala sikutaka afe ila Moza alikuwa mbea ndio
kitu ambacho sikukipenda” “Mbea wa kuchunguza mambo yako mabaya
unatyoyafanya, uliona nini kuacha baada ya kugundua ni mbea? Na hata hivyo,
sababu mbea ndio utake afe? Angekuwa muongo je? Unajua tofauti ya mbea na
muongo? Muongo huongea vitu vya uongo, ingawa kuna uongo wa aina mbili wa
kubomoa na kujenga. Ila mbea anaongea vitu vya ukweli, tofauti ya ukweli na
uongo ni moja tu, ukweli unauma ndiomana mtu mbea anaonekaga kuwa mbaya kuliko
muongo. Ila siku ukikutana na mtu muongo na mnafki ndio utasema bora ya
mbea.” “Unanichanganya Salome, sipo hapa kuulizia tofauti ya mbea na
muongo ila nipo hapa ili nipumzike kidogo, uwepo wako unanifanya nisiweze
kupumzika” “Toka lini wewe ukapumzika usiku? Huu si ndio muda wa kufanya
mambo yako yasiyofaa? Halafu unataka mimi niende wapi nikapumzike
pia?” “Si kule chumbani kwa Moza” “Chumba ambacho ulitaka
kufanyia uchafu! Mimi niko makini kuliko wewe, niingie kwenye chumba ulichotaka
kuzini na mlinzi wako!” Kumbe Sara aliposikia mabishano sebleni alitoka,
na muda huo ndio akasikia kuwa chumba cha Moza, mama yake alitaka kuzini na
mlinzi wao. Alijikuta akisema kwa nguvu, “Mama azini na
mlinzi!” Salome alijibu kanakwamba alitambua kuwa Sara angekuja na
kuuliza hilo swali, “Ndio, mama yenu alitaka kuzini na mlinzi kwenye
chumba cha Moza. Muoneeni huruma mama yenu, kaeni nae chini muongee nae
anapoelekea atazini hadi na maiti ili arekebishe nyumba yake. Rose nyumba
imebadilika hii kama kitumbua tayari kimeingia mchanga, swala ni wewe tu
kuachana na hayo unayoyafanya” Rose aliinama chini kwani hapo ataliweza
kudhihilika wazi kuwa anafanyaga mambo ya ajabu yani hata kujitetea hakuweza
kabisa, alimuangalia mwanae kwa macho ya kuibia ila cha kushukia Salome
alinyoosha mkono wake juu kisha Rose na Sara walijikuta wakilala pale
sebleni. Ilikuwa ni siku nyingine, siku hii Neema alikuwepo
kwenye kijiji cha mama yake na kuamua kwenda kutembelea kaburi la baba yake
kisha kwenda kumsalimia aliyekuwa mama yake wa kambo, na hapo akakumbuka kuhusu
Ashura na kuamua kuuliza. “Eti mama, nilikuwa na ndugu yangu mwingine
kwa baba?” “Mmmh atoke wapi?” “Eti alizaliwa na mama
mwingine” “Neema, baba yako alikuwa na mtoto mmoja tu ambaye ndiye wewe
ila hakuwahi kuzaa tena mtoto mwingine” Ikabidi Neema amueleze mama yake
huyu jinsi alivyokutana na Ashura na jinsi alivyojitambulisha kwake kuwa ni
ndugu yake, ila huyu mama alionekana kushangaa sana na kumwambia
Neema, “Sikia Neema, wewe ni mtoto wa pekee wa marehemu baba yako.
Hajawahi kuwa na mtoto mwingine sehemu yoyote, alipatwa na ugonjwa wa ajabu baaa
tu ya kuzaliwa wewe na hakuweza kuzalisha tena, hata mimi sijazaa nae sababu ya
matatizo hayo. Sasa hizo habari za huyo ndugu yako wa kuitwa Ashura sizijui,
ningekuwa simjui vizuri mume wangu sawa, ila nilimjua vizuri sana na alipenda
watoto balaa kwahiyo ingekuwa huyo mtoto wake lazima ningejua. Labda huyo Ashura
ni ndugu yako kwa mama yako huko ila baba yako hajawahi kuwa na mtoto mwingine
zaidi yako” Neema alishangazwa sana na ile habari na kukumbuka jinsi
Ashura alivyoonyesha kumfahamu, na jinsi alivyoishi nae kama ndugu yake hadi
ilifikia hatua ya kumpa hadi siri zake, alishangaa kusikia baba yake hakuwa na
mtoto mwingine kwahiyo Ashura hakuwa ndugu yake ila akajiuliza kama ni kweli
hakuwa ndugu yake sasa kwanini kamdanganya? Hakupata jibu ila huyu mama yake wa
kambo alimsisitizia kabisa kuwa hakuwa na ndugu wa dizaini
hiyo. Ana ndiye aliyemuamsha mama yake baada ya kumkuta
anakoroma sebleni, "Mama, mama imekuwaje tena?" Rose aliamka ila
alikuwa akishangaa shangaa tu, mara wale mapacha nao walikuja na kumuamsha Sara
maana waliona mama yao akiamshwa na Ana. Walimuuliza dada yao kuwa kapatwa na
nini hadi kalala sebleni, hakukumbuka kwa wakati huo, wakamsogelea na mama yao
ila mama yao akawaambia wamuache na alitaka kwenda chumbani kwake ila aongozane
na Ana, basi akaondoka na Ana na kuwaacha wale wengine pale
sebleni. Walibaki wakiendelea kumuuliza tu Sara kuwa ni kitu gani ila
bado Sara hakuweza kuwajibu kwani hakuwa na jibu la imekuwaje kwa wakati huo,
akili yake ilikuwa kama imesizi hivi kwa kiasi fulani, basi kaka zake
wakamshauri kuwa akajiandae ili waondoke pamoja, nae Sara akainuka ili akafanye
hivyo alivyoshauriwa na kaka zake. alipofungua mlango wa chumbani kwake
alishtuka sana kwani alimkuta Salome akiwa kitandani kwake
amejilaza, "Kheeee Salome!" "Ndio ni mimi, mbona umeshtuka
sana?" "Sikutegemea kukukuta chumbani kwangu, umeingiaje bila ruhusa
yangu!" "Na wewe kwako kunataka ruhusa? kwani mama yenu kabla ya kufanya
yote aliyoyafanya aliomba ruhusa?" Ndio hapa Sara akajikuta akikumbuka
mambo ya usiku na kujikuta akiuliza kwa makini, "Ni kweli mama yangu
alitaka kuzini na mlinzi?" "Nadhani itakuwa vyema kama ukimuuliza
mwenyewe" Sara hakuendelea tena kuuliza chochote bali alitoka na moja
kwa moja akaenda chumbani kwa mamake, na kugonga mlango ila alimkuta mama yake
ndio alikuwa anatoka na Ana, "Kheeee mama unaenda wapi?" "Ndio
salamu hiyo?" "Hapana mama, shikamoo" "Sina haja, Ana twende
mwanangu" Wakatoka na kumuacha Sara akiwa palepale mlangoni, ila
alijaribu kuwafata nyuma ambapo aliwashuhudia tu wakiondoka bila hata kuwaaga
wale mapacha waliokuwepo pale sebleni. Sara aliwasogelea kaka zake, ila na wao
wakamshangaa kuwa hajajiandaa toka muda ule, "Vipi bado hujajiandaa
tu!" "Jamani, si muda huu huu jamani!" "Muda huu huu!
Tumekusubiri hapa karibia lisaa limoja, unasema muda huu huu, kwakweli
tunaondoka Sara" "Jamani acheni masikhara, lisaa limoja limepita saa
ngapi wakati ni muda huu huu!" "Utatukuta ukija" Na wao wakatoka
na kuondoka kwahiyo wakamuacha Sara pale sebleni. Muda kidogo Salome
alitoka na kumwambia Sara, "Ulitaka kuniacha peke yangu, hapana leo
utashinda na mimi hapa" Sara alimuangalia Salome na kuona kama mtu
anayefanya mambo ya ajabu kwenye nyumba yao, ila hakumuuliza chochote zaidi ya
kwenda chumbani kwake ili ajiandae na atoke hivyo hivyo. Basi Sara
akajiandaa na alipomaliza alitoka sebleni ilia toke nje na aondoke zake ila pale
sebleni alikuwepo Salome ambaye alimwambia Sara, “Si nimekwambia leo
tunabaki wote!” “Tunabaki wote kivipi? Mimi nina safari zangu
bhana” “Usiwe mbishi Sara, leo tunabaki wote humu ndani. Mimi leo siendi
popote na wewe leo huendi popote. Tunabaki wote” “Na wewe Salome aaah
usinibabaishe bhana” Sara akafungua mlango na kutoka nje, ila gafla
akajikuta yupo chumbani kwake, “Jamani si nimefungua mlango wa kutoka
nje, iweje nimerudi tena chumbani?” Hakuelewa aliona kamavile ni mchezo
wa kuigiza, akatoka mule chumbani kwake na kwenda tena sebleni ambako alimkuta
Salome amekaa kama kawaida na kuwaza kuwa mwanzoni laba ilikuwa ni mawazo yake
ila si kweli kuwa alifungua mlango na kutoka nje, basi akajikuta akimuuliza
Salome, “Hivi tumeongea mimi na wewe muda si mrefu?” “Ndio
tumeongea, kwanini umeuliza?” “Ulinikataza kutoka nje na ukasema
tutabaki wote leo?” “Ndio, leo tutabaki wote. Mimi siendi popote na wewe
utabaki hapa na mimi” Sara akamuangalia Salome bila ya kummaliza, kisha
akaenda tena kufungua mlango wa nje na kujikuta yupo chumbani kwake tena. Akili
yake sasa ikaanza kuchanganyikiwa kwani aliona kamavile ni mazingaombwe kabisa
ukizingatia mambo hayo yalikuwa ni ya ajabu sana kwake, alijiuliza kuwa ule
mchezo anafanyiwa na nani, kama ni Salome basi Salome ni mtu wa aina gani mwenye
uwezo wa kukurudisha chumbani wakati ulikuwa ukitoka nje? Alifanya hivyo kama
mara tano, na mar azote alijikuta akirudi chumbani. Uoga ukamshika na kuamua
kukaa chini pale chumbani, akachukua simu yake na kumpigia mama
yake. “Mama, nipo ndani nataka kutoka ila nashindwa, eti kila nikitoka
najikuta nimerudishwa chumbani” “Mbona sikuelewi Sara, hebu
nieleweshe” “Sijui nikueleze vipi ila kutoka ndani ya nyumba
siwezi” Sara aliamua kama kumuelekeza mama yake kwenye simu ila bado
ilikuwa ngumu kwa Rose kumuelewa mwanae, ikabidi Sara akate tu simu ya mama yake
na kujibaza kwenye kitanda chake. Rose muda huu alikuwa
mwenyewe akielekea kwa Yule mganga, siku ya leo alimuacha Ana aende shule kama
kawaida halafu yeye ndio alienda tena kwa Yule mganga, na njiani nio alipigiwa
simu na mwanae Sara akimueleza jinsi hawezi kutoka ndani ya nyumba. Hiki kitu
kilimstaajabisha sana Rose ila alijisemea kuwa atamwambia na swala hilo mganga
kwani bado hakukata tamaa kuwa ameshindwa kupambana na alioamini kuwa ni mzimu
ndio unasumbua ingawa mganga alimuhakikishia kuwa sio mzimu. Alifika kwa
mganga na kama bahati leo hakukuta foleni kubwa kama alivyoena mara ya mwisho.
Yule mganga kama kawaida alianza kwa kumuelezea yeye matatizo
yake, “Najua kuwa umekosea masharti, tatizo lako mdomo, yani huwezi
kunyamaza kimya” “Nisaidie mganga nifanyeje?” “Sasa inatakiwa
nitume kombora la kushambaratisha nyumba nzima, yani kila kilichopo ndani
kombora langu litaenda kusambaratisha” “Ndani ya nyumba
yangu?” “Ndio nyumbani kwako, natakiwa kutuma kombora yani kila kitu
kinasambaratika mule nani. Nyumba inakuwa nyeupe kabisa” “Sasa mwanangu
Sara yupo ndani” “Yeye hajatoka? Mpigie simu na umshawishi
atoke” “Ametoka kunipigia simu na amesema kuwa kila akijaribu kutoka
anashindwa” Yule mganga akaanza kuangalia kibuyu chake, kisha akatikisa
kichwa na kumwambia Rose, “Ndani kwako kuna mtu yani yeye anajua mipango
yetu kabla hata hatujapanga, kwamaana hiyo amefanya makusudi mwanao asitoke ili
kombora likitumwa basin a mwanao adhurike” “Huyo mtu ni
nani?” “Namuona binti mdogo, mwenye sura ya kipole ila ana roho ya
kikatili” “Anaitwa Salome huyo mganga, sijui ni
mchawi” “Najaribu kuangalia nguvu alizonazo huyu binti
nashindwa” “Mwanzoni huyo binti niliweza kumdhibiti lakini saivi siwezi,
nilikuwa najua tunasumbuliwa na Moza kumbe ni Yule Yule Salome. Je Moza yuko
wapi?” “Naona kuna nguvu za Moza zikifanya kazi kwenye nyumba yako ila
alipo simuoni, sema sijajua huyu binti ana nguvu za aina gani. Nadhani ni vyema
kama nitakuja kwako” “Dah utakuwa umenisaidia sana, huyo mtoto Salome
sikumpenda toka mdogo ila kila nikijaribu kumuua nashindwa” “Basi
tutafanya kitu, nitakuja nyumbani kwako” Rose alifarijika sana kusikia
kuwa huyu mganga atafika nyumbani kwake, na aliamua kumuomba kuwa waende nae
siku hiyo hiyo. Alimuomba sana na hatimaye Yule mganga
akakubali. Rose na mganga walijiandaa kisha wakaianza safari ya
kwena nyumbani kwa Rose, walienda vizuri njia nzima hadi walifika getini kwa
Rose na kufungua mlango na kuingiza gari ndani. Rose alimuonyesha Yule mganga
alipo mlinzi wake, Yule mganga alitikisa kichwa tu. “Basi jana alitoweka
ndani huyo” “Ni mazingaombwe tu hayo, ila usijali maana sasa kila kitu
kinaenda kufika mwisho” Basi wakashuka kwenye gari na kwenda kufungua
mlango wa sebleni ili waingie nani, ila walipofungua tu walishangaa kujikuta
wapo kibandani kule kule kwa mganga walipotoka. Basi
wakashuka kwenye gari na kwenda kufungua mlango wa sebleni ili waingie nani, ila
walipofungua tu walishangaa kujikuta wapo kibandani kule kule kwa mganga
walipotoka. Yani kila mmoja alimuangalia mwenzie kwa mshangao, tena Rose
akawa wa kwanza kumuuliza mganga, “Mbona tumerudi tena huku huku wakati
tulishafika mpaka nyumbani?” “Hata mimi mwenyewe sielewi imekuwaje, ila
ngoja nifanye dawa zangu kwanza. Naomba nisubiri nje” Rose alitoka nje
ya kibanda cha mganga huku akiangalia huku na kule, kwani mazingira ni hay ohayo
na waliondoka kabisa hadi akakumbuka kuwa alimuonyesha mganga mlinzi na
wakaongea halafu wameruishwa tena kule kule, kwakweli ilikuwa ngumu sana kwa
Rose kuelewa. “Kama ni uchawi basi huu ni wa viwango vingine, inamaana
ni Moza au Salome! Yule mtoto atapata wapi nguvu za hivi? Anapata wapi uwezo wa
kufanya makubwa haya? Ila sidhani kama ni yeye, ila na huyo Moza kwa staili hii
ya kurudishwa na mganga tutaweza kupambana nae kweli? Kuna uwezekano wa
kupambana na huyu kiumbe kweli?” Alijiuliza sana huku akingoja mganga
wake afanye dawa, na baada ya muda mganga alimuita tena Rose na kuanza kuongea
nae, “Unajua nguvu aliyokuwa nayo Yule binti nyumbani kwako ni kubwa
mno, yani kiasi kwamba tunaweza siku nzima ya leo hadi usiku wa manane tukawa
tunaenda kwako na kurudishwa hapa hapa” “Sasa
tutafanyaje?” “Inabidi tutoe kafara” “Kafara
ipi?” “Kafara ya damu, damu ya mtu unayempenda” “Mmmh labda
Patrick” “Huyo ndio umpendae?” “Ndio” “Si kweli, mtu
umpendae huwezi kukubali kwa haraka haraka hivyo atolewe kafara, huyo
humpendi” “Ya watoto wangu hapana, nimefikia hatua hii sababu yao.
Nawapenda sana wanangu, tafadhari kafara isiwe ya wanangu, bora Patrick nipo
tayari kumtoa” “Upo tayari, ila kumtoa huyo mtu ni ngumu
sana” “Kwanini ni ngumu?” “Huyo mtu analindwa sana, naona
amezingirwa na ulinzi wa hali ya juu. Kumtoa kafara haiwezekani” “Basi
nimtoe mlinzi wangu” “Hausiani na wewe huyo, bora siku ile ungekuwa
umefanikisha zoezi la kulala nae ningekuruhusu kumtoa ila kwasasa haiwezekani.
Inatakiwa ni mwanao tu” “Tafadhari mganga bora tutafute mbinu nyingine,
wanangu ndio maisha yangu. Tafadhari nisiwatoe kafara wanangu, nawapenda sana.
Sijaweza kujiunga makundi ya wachawi wazoefu sababu ya kuogopa kutolewa wanangu,
nawapenda sana” “Unawapenda wanao ila unaishi na hatari ndani ya nyumba
yako” “Tujaribu tena kwenda mganga” “Hata tukijaribu ni kazi
bure, tutarudishwa tena hapa hapa, labda uende kwanza wewe halafu mie nije leo
leo au hata kesho” “Leo leo mganga, pale kwangu hapalaliki mganga, njoo
leo leo” “Ila ngoja nikupe onyo kabla hujaondoka” “Onyo
gani?” “Msifanye sherehe yoyote pale kwako mpaka nije kufanya dawa, yani
msifanye tukio lolote la sherehe sijui ya kuzaliwa, sijui kipaimara
msifanye” “Sinaga tabia ya kufanya sherehe nyumbani kwangu, hata
birthday za wanangu huwa nikiamua basi naenda nao hotelini ila huwa hatufanyi
sherehe nyumbani” “Sawa sawa, nimekutahadhalisha kabisa kwani pale kwako
hapatakiwi kusikika vigelegele vya shangwe kwa kipindi hiki mpaka nitakapofika
na kufanya dawa, kuna nguvu kubwa sana pale kwenye nyumba
yako” “Nimekuelewa ila naomba ufike mapema
iwezekanavyo” “Usijali kwa hilo, ngoja tu nifanye dawa
kwanza” Bas Rose akamuachia mganga nauli ya kutosha kisha yeye akaanza
safari ya kurudi nyumbani kwake kwa mara nyingine. Rose alifika
kwake wakati usiku ulikuwa umeshaingia hadi akajishangaa kuwa ametumiaje muda
hadi usiku umeingia vile, aliangalia saa yake aliona ni saa tatu ya usiku.
Aliingia ndani na kukuta familia yake yote ikiwepo sebleni, halafu wakionekana
kama walikuwa wanamngoja kwa shauku kwani alipoingia tu, wote wakapiga
kelele, “Surprise” Rose akawashangaa sana kuwa ni surprise ya
kitu gani, ila wote walianza kumuimba mama yao, “Happy birthday to you,
happy birthday to you, happy birthday dear mommy, happy birthday to
you” Na vigelegele vikasikika, yani Rose alichoka kabisa na kukaa chini
kwani aliona wanae wakiharibu kila kitu. Alipokaa chini walidhani mama yao
amevutiwa na walichokuwa wanafanya basi wakamuagiza Ana alete keki ambapo Ana
alileta keki na kuanza kuimba, “Kata keki tule……” Ila mama yao
alitahamaki sana na kusema, “Hadi wewe Ana!” Akaanguka chini na
kuzimia kidogo, wote wakashtuka “Jamani surprise gani hii kwa mama yetu
mpaka amezimia!” Wakaanza kumpepea, ila Salome akaenda kuchukua maji
kidogo na kuja kumwagia kwahiyo Rose akazinduka na alivyozinduka tu watoto wake
wakapiga kelele za shangwe kisha Sara akaanza kumwambia mama yao, “Mama
jamani usistaajabu kiasi hiko, watoto wako tunakupenda na hatujawahi kukufanyia
kitu cha namna hii hata mara moja. Nashukurun leo Salome katukumbusha kitu hiki,
kumbe alikuwa ananikataza kutoka sababu leo ni siku yako ya kuzaliwa. Natumai
mama yetu umefurahi! Tumeandaa keki na vyakula tofauti tofauti vya kujipongeza
kama familia” “Naomba niacheni kidogo niende chumbani” Kisha
Rose akainukana kwenda chumbani kwake,watoto wake wakashangaa sana kwani mama
yao hakuonyesha kufurahia lile jambo hata kidogo, na keki yao hakukata wala
nini. “Jamani, mama tumemfanyia kitu kikubwa hivi ila haonyeshi
kufurahishwa nacho kabisa. Hebu Ana kaongee na mama” Ana akaondoka na
kuwaacha pale sebleni wakijadiliana kwanini mama yao hajapendezwa na kile kitu
walichomfanyia, ila Salome akawapooza, “Mnajua mambo ya kumshtukiza mtu
huwa yanachanganya sana, itakuwa leo hakujipanga kabisa kuhusu sherehe labda
ndiomana amestaajabu sana ila natumai kafurahia” “Natumai pia
kafurahia” Kuhusu swala la kuandaa sherehe fupi ya kuzaliwa kwa Rose ni
Salome aliipanga na wote walimsifia kwani hawakuwahi kumfanyia mama yao
sherehe. Ana alimfata mama yake chumbani na kuanza kuzungumza
nae, alimuuliza mama yake kwanini hajafurahishwa na ile surprise
yao, “Ana nilikuwa nakuamini sana, sikutegemea kama na wewe ungeweza
kuingia kwenye mtego kiasi hiko jamani! Toka lini birthday yangu ikawa mwezi
huu? Hivi kwanini kupena kuharibiana dawa? Nani ametoa wazo
hilo?” “Mama, mimi sijui. Kama kawaida nimerui kutoka shule na kuwakuta
hapa nyumbani wamejipanga vilivyo kuwa kuna sherehe ya kuzaliwa wewe, mwanzoni
nilibisha ila Sara alileta vitambulisho vyako na vilionyesha tarehe ya leo na
mwezi wa leo, kwakweli hata mimi niliona ni wazo jema kukufanyia wewe sherehe
ukizingatia hatujawahi kukufanyia hivyo. Siku zote huwa sishirikiani nao ila leo
niliona ni jambo jema” “Ana mwanangu, ni mtego huo unajua umeharibu dawa
zangu na hivyo vigeregere vyenu! Yani mganga amenisisitiza sana kutofanya
sherehe ya aina yoyote ile na kutokupiga vigeregere ila nimerudi nyumbani ndio
kilichotokea” Rose alianza kumueleza Ana kuhusu siku hiyo na jinsi
walivyofika hadi hapo nyumbani na kurudishwa tena kwenye kibanda cha mganga,
hadi mua huo kuamua kuja mwenyewe. “Mama, kwamaana hiyo huyu Salome ni
mchawi eeh!” “Angekuwa mchawi tungemtambua, ni zaiddi ya mchawi halafu
mganga amesema kuwa Salome ana nguvu nyingi sana, ambapo amejaribu kuziangalia
ila hajaweza kuzichanganua” “Mmmh sasa mama tutafanyaje?” “Hata
sijui maana masharti nishayaharibu tena, hapa hata sielewi nianzie wapi na
niishie wapi” “Ngoja nikatafakari mama” Ana alitoka mule
chumbani kwa mama yake na kwenda chumbani kwake kutafakari ambapo alijaribu
kufanya dawa zake halafu kitu kikamuonyesha kuwa kama hawatokata ile keki
waliyomuandalia mama yao basi wanaweza kidogo wakapona kwenye mtego, kwahiyo
akainuka ili aende akaitupe ile keki, kufika sebleni alishangaa kuona dada yake
Sara na wale mapacha walishaikata ile keki kitambo na walikuwa wanakula huku
wakimuita walipomuona, “Ana, keki tamu hiyo yani tamu
sana” “Sasa kwanini mmekata kabla mama mwenyewe hajakata? Nani katoa
wazo la kuikata kabla ya muhusika kuja?” “Salome katushauri tukate labda
mama amechoka sana, ndiomana tumeamua kuikata na jinsi ilivyokuwa inatamanisha
ndio kabisa yani” Ana alisikitika sana kwani ndugu zake ndio wamekuwa
rahisi kabisa kutekwa akili zao tofauti na mtu mwingine. Akaamua
kuichukua ile iliyobaki na kuibwaga chini, ila kabla haijafika chini alishangaa
kuiona bado ikiwa kwenye sahani yake, kitendo hiko kilimchanganya sana ingawa
ndugu zake walihisi kama Ana amewafanyia mazingaombwe hapo maana walishamjua kwa
uchawi, ila hawakujua kama kitendo hiki kilimshangaza sana Ana na akajikuta
akikimbilia chumbani kwa mama yake na kumueleza kuhusu dawa aliyokuwa akifanya
na jinsi alivyopata ushauri wa kuhusu keki, na alichokiona
sebleni. “Mama, sasa nimeanza kuelewa kuwa ilikuwaje mkajikuta
mnarudishwa kwa mganga wakati mlifika hapa nyumbani. Yani ile keki niliona
kabisa nimeibwaga chini ila mara gafla naiona tena kwenye sahani, hapa naelewa
kabisa kuwa inawezekana leo sio siku yako ya kuzaliwa ila hizi tarehe
zimechanganywa changanywa ndani kwetu. Hivi mama hakuna kingine cha kufanya
kweli kudhibiti hili maana naona mbona kama hao waganga wako
wanashindwa” “Hapana mwanangu, basi leo tulale wote tufanye vitu wenyewe
tuone inakuwaje kuwaje” “Mmmh mama sijawahi kufikiria kama kuna kiumbe
kitakuja kunisumbua sumbua mimi” “Usijali mwanangu, cha kuhakikisha ni
kuwa kila mmoja akalale chumbani kwake halafu mimi na wewe tulale pamoja
tushughulike na majanga ya humu ndani” “Usijali juu ya hilo, yani wale
wakimaliza tu kula najua kila mmoja ataena kulala chumbani kwake” Basi
Ana na mama yake wakakubaliana siku hiyo walale pamoja, kisha Ana akaenda
chumbani kwake kujipanga kwaajili ya mashambulizi ya usiku
huo. Pale sebleni wale mapacha na Sara, walikula ile keki,
walikula chakula na kunywa kwa furaha sana yani siku hiyo walikuwa kama watu
waliolewa vile. Kisha walienda kukaa kwenye kochi na kuendelea na maongezi,
ilikuwa ni mara ya kwanza kwa wao kufanya maongezi usiku huo sebleni maana muda
kama huo kila mmoja kati yao huwa chumbani kwake anajiandaa na kulala ila siku
hiyo walikuwa sebleni wakipiga stori, Salome nae alikuwepo sebleni ila alikuwa
kimya kabisa kamavile hayupo. Muda kidogo, wote pale sebleni walipitiwa
na usingizi na wakalala pale pale kwenye makochi. Ana alikuja kuwaangalia kama
washaondoka, alishangaa sana kuwaona bado wapo sebleni na ubaya wamelala kabisa,
Ana aliwashangaa na kumsogelea Sara kisha kuanza kumtikisa, “Sara,
Sara” “Niache bhana nina usingizi” “Inuka ukalale
ndani” “Niache bhana” Alienda kuwatingizha nao kaka zake
walimjibu vile vile ila aliposogea ili amtingishe Salome alijikuta mkono wake
ukishindwa kumshika Salome, kisha akainuka na kwenda kumwambia mama
yake, “Mwanangu hakuna namna hapo, ila Yule mganga nitaongea nae aje tu
hivyo hivyo maana kila tunachokifanya hatuwezi” “Sawa basi mama tusubiri
usiku wa saa nane kasoro ndio mzuri ili na sisi tujaribu ya kwetu” “Sawa
mwanangu” Walikazana kufanya mambo mengine huku wakisubiria usiku wa saa
nane kasoro ufike, ila kila walipoangalia saa iliwaonyesha kuwa ni saa sita yani
kila walipoangalia iliwaonyesha ni saa sita. Kuja kutahamaki walisikia jogoo
akiwika na walipoangalia saa muda huo ilionyesha ni saa kumi na moja
alfajiri, “Mama tumepitiliza wapi?” “Kivipi? Muda si bado
haujafika” Ana akamuonyesha saa mama yake, ambaye alishangaa pia kwahiyo
siku hiyo wamefanya mkesha usiokuwa na faida yoyote ile. Ila mama yake
akamuahidi Ana kuwa siku hiyo watahakikisha kila kitu
kitafanikiwa, “Asubuhi ya leo naenda kuongea na dereva tax amlete Yule
mganga hapa kwa gharama zangu, najua akiletwa na mtu mwingine haitotokea zengwe
kabisa. Atafika na mambo haya yatafika mwisho” “Itakuwa vizuri mama,
kwahiyo leo nisiende shule eeh!” “Ndio usiende shule” Rose
alikubaliana pale na mwanae Ana jinsi atakavyofanya siku
hiyo. Kulipokucha kabisa, pale sebleni kila mmoja aliamka na
kujinyoosha huku wakiwa na uchovu wa hali ya juu na kila mmoja kusema kuwa
hatotoka kwa siku hiyo, watabaki tu nyumbani. Pacha mmoja alimwambia dada
yake, “Leo nitamwita na wifi yako aje umfahamu” “Sawa ila mama
asijue kama ni wifi” “Mama atajulia wapi? Hakuna kumwambia, atajua siku
ya ndoa” Wakawa wanacheka pale, mama yao nae alitoka sebleni
wakamsalimia akaitikia na kutaka kwenda nje. Ila Salome
alimuuliza, “Mama, unataka kwenda wapi?” “Safari zangu
hazikuhusu” Rose akataka kufungua mlango, ila kabla hajafungua Salome
alimwambia, “Usihangaike, mgeni wako nimekuletea” Kisha Salome
ndio akaenda kufungua mlango na mara akaingia Yule
mganga. Wakawa wanacheka pale, mama yao nae alitoka
sebleni wakamsalimia akaitikia na kutaka kwenda nje. Ila Salome
alimuuliza, “Mama, unataka kwenda wapi?” “Safari zangu
hazikuhusu” Rose akataka kufungua mlango, ila kabla hajafungua Salome
alimwambia, “Usihangaike, mgeni wako nimekuletea” Kisha Salome
ndio akaenda kufungua mlango na mara akaingia Yule mganga. Kwakweli Rose
alishangaa sana alijikuta akikaa chini kabisa kwani hakuelewa kabisa
kinachoendelea na aliona kiini macho kikifanya kazi vilivyo, ila Salome
akamwambia Rose, “Sasa umeshtuka nini? Unakosa raha kwanini? Si nio
ulikuwa ukimuhitaji huyu! Ulitaka hadi kwenda kutuma dereva wa kumfata, mimi
nimekuletea eti unaishiwa nguvu kabisa” Rose hakujibu chochote ila Yule
mganga aliingia na kukaa pia, halafu akamuangalia Rose na
kumsalimia, “Habari za tangu jana” Rose
akajibu, “Mbaya” Salome aliwaambia watoto wengine wa Rose
wamuache mama yao aongee na mgeni, “Kwetu nilifundishwa kuwa mama
anapopata mgeni natakiwa kuondoka na kumuacha mama anazungumza na mgeni, kwahiyo
kitendo cha kukaa hapa wakati mama kapata mgeni sio picha nzuri” Basi
nao wakasikiliza ushauri wa Salome kisha kila mmoja kuinuka na kwenda zake
chumbani ila Salome alienda kwenye sebule ambayo wale mapacha walipenda kuitumia
kwa sana. Rose alibaki sebleni na Yule mganga, kisha akamuangalia kwa
makini kwani alihisi kama ni kiini macho, akamuuliza “Hivi ni wewe au ni
nini?” “Ni mimi ndio” “Umefikaje hapa?” “Niliona
yaliyokutokea usiku wa jana, kwahiyo leo mapema nikaanza safari ya kuja huku. Ni
sababu tulishakuja mwanzo kwahiyo nilishika njia” “Ulishika njia vile
tumekuja na kurudishwa kimaajabu?” “Ndio nilishika njia, kwahiyo
huniamini kuwa ni mimi!” “Nakuamini ila mambo yamenichanganya sana,
unajua umekuja kiajabu ajabu mpaka nimeshangaa. Kwahiyo tutafanya dawa siku ya
leo?” “Ndio tutafanya dawa, ila kwanza ukanionyeshe kila kitu ambacho
huwa unatumia kwenye mambo yako” Rose akafikilia kidogo kisha akakubali
kwenda kumuonyesha kwahiyo yeye na Yule mganga wakahamia ndani na baada ya muda
walitoka na kuondoka kabisa pale nyumbani, na Rose alimuaga mwanae Ana tu kuhusu
anapoenda na Yule mganga. Baada ya muda watoto wa Rose walirudi
sebleni na siku hii Salome aliwaandalia chakula cha kuwafurahisha sana, hadi
wakawa wanamsifia haswa wale mapacha, “Yani wewe Salome ni binti mdogo
ila unajua kupika kila chakula jamani halafu unapika vizuri balaa” Kisha
Doto akamuangalia dada yake Sara na kumwambia, “Dada na wewe ujifunze
kupika jamani, kwa staili yako utaolewa kweli wewe!” “Aliyekwambia
anataka kuolewa nani, hebu nitoleeni balaa” “Basi dada usichukie kiasi
hiko jamani, leo wifi yako anakuja. Nishampigia simu kumuelekeza kwahiyo akafika
tu nitaenda kumchukua nje na utamuona na hakika utamfurahia” “Bora
uongelee mada za hivyo sio kuniletea mada za upishi upishi kama sijui kupika ni
mimi msinilazimishe” Sara alionekana kuchukizwa kabisa na swala la
kuambiwa kuwa atakosa mume sababu hajui kupika, na kujikuta akimkumbuka Ommy
ambaye alijua wazi kuwa Sara hajui kupika ila alionyesha kumpenda hivyo hivyo,
ila akakumbuka kuwa Ommy kafichwa na uchawi wa mama yake na kujikuta akikumbuka
kuwa Ommy alimsaliti na mtu mwingine, kila alipokumbuka Ommy ni msaliti basi
huruma yake kwa Ommy ilipotea muda huo huo. Alikuwa kimya kwa muda hadi
Salome akamshtua, “Unawaza nini dada Sara?” “Niache
tu” “Pole sana, mapenzi yanaumiza eeh! Ila bado, utaona yanavyoumiza
zaidi” “Kivipi Salome mbona sikuelewi” “Utanielewa tu, mapenzi
yanaumiza sana ila kuna jambo linaweza kutokea ukajihisi labda utapata unafuu wa
moyo ila ukashangaa unafuu hupati zaiddi ya maumivu” Wale mapacha nao
wakaingilia hizo stori, “Jamani achene hizo habari za kuumizwa na
mapenzi, wengine hatutaki kusikia kabisa. Ziacheni bhana, kila mtu ashughulike
na penzi lake” Salome alitabasamu tu kisha akaenda tena kwenye ile
sebule ambayo mapacha wa Rose huwa wanapenda kukaa. Kwa upande wa Ana
alikuwa chumbani kwake tu toka mama yake katoka na Yule mganga kwani yeye
alijikuta akiwaza kuwa ni mtego tu mama yake kawekewa maana hakuwa na wazo kuwa
Yule ni mganga waliyoendaga kabisa, “Na kama ni yeye amewezaje kuja
mapema hivi ukizingatia kule anakotoka ni ndani ndani sana? Nina
mashaka” Akajaribu nae kukaa akifanya fanya dawa zake huku akiwa
amejifungia kabisa kwenye chumba chake, hakutaka kabisa kuongea na mtu yeyote
kwa muda huo. Wakiwa pale sebleni Sara na kaka zake, basi kaka
yake akasema kuwa mchumba wake amefika kwahiyo akaenda kumpokea kwahiyo Sara na
kaka yake mwingine wakabaki wenyewe wanamsubiri huyo wifi kwa Sara na shemeji
kwa Kulwa. Ila Sara alimuuliza kaka yake, “Vipi unamjua huyo mchumba wa
Doto?” “Hata simjui kabisa, Doto msiri sana hajawahi kunionyesha hata
mara moja huyo msichana wake” “Wewe je umeshawahi kumuonyesha wa
kwako?” “Hapana, mimi mwenyewe sijawahi kumuonyesha hata mara moja ila
nimepanga siku nimtambulishe hapa nyumbani. Hata leo nilitamani aje pia ila
kaniambia amepata udhuru” “Sawa” “Na wewe wako? Najua ni Ommy
ila sijamuona siku zote hizi” “Achana na huyo mtu, kwanza ananiumiza
kichwa tu. Yani mapenzi yameniumiza kweli mimi, kumbe Ommy alikuwa ananisaliti,
kunionyesha kote upendo kule kumbe amepata kasichana kengine ananisaliti nako.
Siku niliyogundua niliumia sana” “Kwahiyo Ommy yuko
wapi?” “Achana nae bhana, atajijua mwenyewe alipo” “Mmh dada
jamani, unajua mtu akikusaliti unatakiwa kuwa mpole kwanza, ujue ni kwanini
amekusaliti sio kuweka hasira mbele” Sara alianza kukohoa na kumuomba
kaka yake huyu akamchukulie maji ya kunywa, “Mmmh maneno yangu
yamekufanya upaliwe, basi pole. Ngoja nikakuchukulie hayo maji” Basi
Kulwa akainuka na kwenda kumchukulia maji ya kunywa Sara, ila muda huu huu Doto
nae alikuja na kuingia ndani kisha akamwambia dadake asimame kumkaribisha mgeni
maana ameshafika, “Mmmh kama tunamkaribisha raisi jamani! Kumbe utamu wa
mtu” “Acha maneno yako Sara bhana” Basi akamkaribisha Yule
msichana ndani, ila Sara alipoangusha macho yake kwa Yule msichana alishtuka
sana kwani alikuwa ni Mishi, alijikuta akimuuliza kaka yake kwa umakini huku
akifikicha fikicha macho, “Kaka, mwanamke mwenyewe ndio
huyo?” “Ndio, kwani vipi mzuri eeh!” Sara alifikicha tena macho
yake, ila kabla hajasema chochote Kulwa nae alikuwa ametoka jikoni akiwa na
glasi ya maji ila alipomuona shemeji yake huyo, alihamaki na kumuita kwa
mshangao, “Mishi!!!” Mishi aliangalia kwa aibu sana, na
hakuongea lolote zaidi ya kufungua mlango wan je na kuondoka kuelekea getini,
alifika getini na kutoka ila alivyotoka tu alijishangaa akijikuta tena yupo pale
pale sebleni halafu mara Salome nae alitoka kwenye ile sebule nyingine akicheka,
na kuwakuta pale sebleni huku Mishi akiwa anashangaa shangaa, kisha Salome
akasema, “Sasa Mishi unashangaa shangaa nini? Unaona kama maajabu eeh!
Wakati unatenda vitu vya namna hii hukujua kama ni maajabu ya namna hii
yangetokea mbele yako? Unataka kukimbia uende wapi na ukimbie kwasababu ya nini?
Kaa hapo ujieleze, ni kwanini umechanganya ndugu hawa” Doto alikuwa na
hamaki tu na kujikuta akimuuliza Kulwa, “Kwani huyu msichana
unamfahamu?” “Nio huyu nilisemaga mchumba wangu mwenyewe, leo nilitaka
anitembelee pia akasema ana kazi kumbe ananichanganya na pacha
mwenzangu!” Sara nae akadakia na kutoa dukuduku lake la
moyoni, “Yote tisa, kumi ni kuwa huyu dada ndio kidudu mtu aliyekuwa
anatembea na Ommy hadi moyo umeniuma sababu yake” Wote wakashangaa kuwa
Mishi amewachanganya kiasi kile, Doto akajikuta akimwambia, “Yani
kukuhudumia kote kule Mishi bado ulikuwa unanichanganya na ndugu
yangu!” Mishi alikuwa kimya kabisa kwani aibu aliyoipata leo
hakuitegemea kabisa, Salome nae akaongea, “Yani sio kwamba wewe Doto
ulikuwa ukimuhudumia peke yako, ni hivi huyu binti wote mmeshiriki kumuhudumia.
Kulwa pia umemuhudumia sana huyu binti, halafu hata Sara umemuhudia sana maana
hela zote ulizokuwa unampa Ommy alikuwa anapeleka kwa huyu binti. Haya sasa
nirudi kwako wewe fundi wa kuumiza mioyo ya watu, hivi hukuwahi kuwaza kuwa
mambo unayoyafanya ipo siku utaumbuka? Hivi ni bahati za watu wangapi
umezifunika wewe mmoja? Yani wewe utembee na Kulwa, wewe utembee na Doto na wewe
utembee na mwanaume wa dada yao, kwahiyo umechanganya familia
vilivyo” “Nisameheni sikujua kama ni ndugu” MIshi alipiga
magoti, na kumfanya Salome acheke sana na kusema, “Kwahiyo kama si ndugu
ni sawa kuwafanyia hivyo? Mwanzoni nilijua ni Ommy anakudanganya kumbe ni wewe
unaewadanganya wenzio, hivi ungefanyiwa wewe hivi
ungejisikiaje?” “Nisamehe jamani, nisameheni” Sara alikuwa na
hasira sana na huyu Mishi, hata wale mapacha nao walikuwa na hasira nao vilivyo
wakatamani wote wamvamie na wampige ila Salome aliwakataza na kwenda kumkinga
Mishi ili wasimpige. “Tafadhalini jamani msimpige wala msimuumize,
mwacheni jamani nataka huyu atembee na laana yangu” Doto alikuwa na
hasira sana, ila Salome alimzuia kabisa kumpiga mishi yani alijikuta akiganda tu
bila kumpiga. Salome alifungua mlango na kumruhusu Mishi aondoke ila
akamwambia, “Kumbuka utatembea na laana yangu siku zote, leo utafurahi
sana kuwa umewachanganya ndugu lakini hujafanywa lolote ila utatembea na laana
yangu siku zote. Laiti kama ningekuwa wewe nisingeondoka leo ila ningekesha
nikiomba msamaha” Mishi hakutaka kusikiliza sana kwani alitoka muda huo
huo na hakutaka tena kubakia kwenye nyumba hiyo kwani alijiona kama anamkosi kwa
siku hiyo. Kwakweli si Sara wala wale mapacha waliofurahishwa na kitendo
kile kwani kila mmoja alienda njia yake mule ndani akiwa na mawazo yake, haswa
Doto alihisi kudhalilishwa sana na Yule mwanamke, kwahiyo sebleni alibaki Salome
peke yake. Mishi alitumia muda mrefu sana kufika kwao, hata
akashangaa kuwa imekuwaje tena wakati ametoka kule muda mrefu. Wakati akitembea
aliona usiku umeingia, mara alikatisha kwenye njia hiyo na kujiona yupo mwenyewe
hadi akaogopa na kujiuliza, “Hii njia leo vipi jamani? Imekuwaje yani
sioni watu!” Mara akashikwa bega, kugeuka ni chizi alikuwa amemshika
bega, alishtuka sana na kuanza kukimbia ila Yule chizi alimzidi nguvu na
kuanguka chini halafu akapiga kelele lakini hakuna mtu yeyote aliyeonekana
kumsaidia hadi Yule chizi akambaka halafu akamwambia, “Asante sana kwa
penzi lako” Yule chizi akaondoka zake na kumuacha Mishi akilia sana,
muda kidogo walitokea vijana wawili ambapo Mishi alipowaona aliwaita na kuwaomba
msaada kwahiyo wakamuinua Mishi pale chini huku wakimpa pole “Pole sana
dada, ila saizi saa saba usiku mtoto wa kike unatafuta nini
njiani?” Mishi alishangaa sana kuwa ni usiku wa saa saba wakati
aliondoka mapema sana kwakina Doto, “Jamani nisaidieni jamani, sikujua
kama ni usiku sana saa hizi” Wale vijana waliondoka na Mishi ila njiani
nao wakamgeuka na kumbaka, kwakweli siku ya leo ilimfanya Mishi achanganyikiwe
kabisa kwani walimbaka kwa nguvu hadi akazimia pale pale. Rose
alirudi nyumbani kwake usiku, na kwenda chumbani kwa Ana moja kwa moja ili ampe
habari ya kitu alichofanya na Yule mganga. Ila cha kushangaza kabla hajamueleza
chochote, Ana alianza kusema, “Mama ila sina imani na Yule mganga
uliyeondoka nae. Naogopa hata usiniambie ambacho umefanya na Yule mganga maana
sina imani nae kabisa. Simuamini Yule mganga mama” “Usiseme hivyo
mwanangu, nimefanya nae vitu vingi sana” “Ndio mama ila sina imani nae,
kwanza ujio wake wa kiajabu ajabu sina imani nae kabisa” “Mwanangu
lakini kanirekebishia vitu vingi sana, utaona mabadiliko kuanzia
kesho” “Kabla ya hayo mabadiliko, naomba kesho asubuhi twende kwa huyo
mganga tujue mbivu na mbichi mama manake sina imani kabisa
hapa” “Kwahiyo hutaki nikueleze chochote ambacho kimetendeka
leo” “Hata usinieleze na wala usiniambie ulipokuwa siku ya leo, sina
furaha kabisa na sidhani kama ulipokuwa palikuwa ni pema” Ikabidi Rose
akubaliane na mwanae kuwa ataenda nae kesho yake kwa Yule mganga, ingawa yeye
binafsi alikuwa ameridhika kwa huduma ambazo alifanyiwa siku hiyo na Yule
mganga, kwahiyo akaenda chumbani kwake baada ya kumaliza maongezi na
Ana. Ila siku hiyo Ana hakuweza kulala kabisa kwani alikuwa na mauzauza
yaliyopitiliza, hakuweza kufanya chochote na wala hakuweza kulala alitamani tu
pakuche ili aende na mama yake kwa huyo mganga, alihisi kwa siku hiyo mamake
badala ya kuyajenga yani ndio kayabomoa kabisa. Basi kulivyokucha tu ni yeye
ndiye alienda kumuamsha mama yake ambaye alimkuta amelala hoi kabisa, yani siku
hiyo Rose alilala hadi alijisahau basi mwanae alivyomkurupua ndio akaenda
kujiandaa kisha wakatoka na mwanae na kuanza safari ya kwenda nyumbani kwa
mganga. Walivyofika walishangaa kuona watu wengi sana wamejaa kwa mganga
Yule na walipoulizia kwa umakini zaidi, walipewa taarafa ya kuwashangaza
sana, “Eti kuna nini?” “Kwani huna taarifa?” “Taarifa
gani?” “Mganga amekufa” “Kheee amekufa? Lini tena jamani wakati
jana nilikuwa nae” “Ulikuwa nae wapi na muda gani wakati kafa usiku wa
kuamkia jana!” Rose alimuangalia mwanae Ana akiwa anashangaa
sana. Walivyofika walishangaa kuona watu wengi sana
wamejaa kwa mganga Yule na walipoulizia kwa umakini zaidi, walipewa taarafa ya
kuwashangaza sana, “Eti kuna nini?” “Kwani huna
taarifa?” “Taarifa gani?” “Mganga amekufa” “Kheee
amekufa? Lini tena jamani wakati jana nilikuwa nae” “Ulikuwa nae wapi na
muda gani wakati kafa usiku wa kuamkia jana!” Rose alimuangalia mwanae
Ana akiwa anashangaa sana. Alishindwa kujibu kuwa alikuwa nae muda gani na wapi
kwani kila akikumbuka matukio ambayo kafanya na huyo mganga halafu anaambiwa
kuwa amekufa alihisi kuchanganyikiwa kabisa, Yule mwanamke akamuuliza
tena, “Ulikuwa nae kivipi ndugu wakati amekufa jana alfajiri na amezikwa
jioni” “Kheeee na kuzika tayari?” “Ndio, ila bado nakushangaa
ulikuwa nae wapi” “Ni juzi, nimechanganya siku. Yani kifo
kimenichanganya hiko” Ilibidi ajigeleshe lakini ukweli ni kuwa kifo cha
huyu mganga kilimchanganya vilivyo ukizingatia na yaliyotokea baina yake na
mganga huyo siku ya jana, kumbe mganga alikuwa ameshakufa na jioni aliyomuaga
ndio alikuwa anazikwa kwakweli Rose alijihisi kudata kabisa. Akaamua asogee kwa
mke wa mganga ili apate tetesi kuwa hata ilikuwaje maana bado alikuwa gizani.
Alimkuta mke wa mganga akiwa kajiinamia kwa majonzi, na kumpa pole pale kisha
kumuuliza kuwa imekuwaje, “Eti imekuwaje tena maana ni gafla
sana” “Kweli ni gafla sana, kazi aliyokuwa anafanya mume wangu ni kazi
ya hatari sana yani nilijua tu ipo siku nitamkosa kama leo jamani” Huyu
mama aliinama tena akilia, basi Rose akawa anambembelea huku akiendelea
kumsikiliza kuwa ni kitu gani kilitokea, “Mume wangu aliniambia amepata
kazi ya hatari sana, nilimwambia aachane na kazi hiyo ya hatari ila hakunisikia
alisema lazima ataifanya. Sasa juzi jioni aliniambia kuwa mteja wake huyo mwenye
kazi ya hatari kamzuia asifanye sherehe yoyote maana akifanya hivyo atadhurika
yeye kwani nyumba ya huyo mteja alianza kuizungushia dawa huku huku. Usiku wake
akaniambia mteja amekiuka masharti kwani amefanya sherehe na kupiga vigelegele,
yani alikuwa anaumia sana na kujishika tumbo huku akisema wanamuumiza kwa kupiga
vigelegele, nilikuwa naogopa sana. Mara akasema wanamuua kwa kukata keki,
sikuelewa kabisa ila gafla niliona kimya na nilianza kupiga makelele ya kuomba
msaada. Ila walipokuja kumuangalia waliona ameshakufa” Yule mwanamke
akaangua tena kilio, basi Rose akawa anambembeleza huku akijlaumu moyoni kwani
alijiona kuwa yeye ndio chanzo cha mambo yote hayo maana kama watoto wake
wasingefanya ile sherehe basi yale yote yasingetokea. Ila hakusema hapo kuwa
mteja mwenyewe mwenye majanga ndio yeye kwani aliogopa kusema na kuona kuwa
atamuweka hasira huyu mama ukizingatia anaonekana alimuonya sana mume wake
kuachana na kazi ya hatari kama yake. Rose alimfariji fariji pale mfiwa
kisha akaaga na kuondoka na mwanae ila siku hiyo hata nguvu ya kusubiri pikipiki
hawakuipata waliamua kutembea tu mpaka kwenye gari yao, na kwavile walikuwa na
mawazo basi hata hawakuona kama ni mbali kutoka kule kwa mganga hadi walipoacha
gari. Waliingia kwenye gari huku akili ya Rose ikiwa haifanyi kazi
kabisa, “Lakini mama nilikwambia kuwa nina mashaka” “Mwanangu
usiongee sana, hapa nimechanganyikiwa kabisa yani kabisa kabisa, unajua nimezini
na marehemu!” “Kheeee umezini na marehemu?” “Tuache hizo habari,
twende nyumbani tu. Nishachanyikiwa hapa” Rose alikuwa amechanganyikiwa
kweli yani akili yake haikufanya kazi kabisa kwa muda huo, Ana alikuwa
akimuhurumia tu mama ingawa alimuonya kabla ya yote. Rose alikuwa akiendesha
gari kurudi nyumbani ila aligubikwa na mawazo mengi sana. Kwa
upande wa Mishi, alishtuka akiwa nyumbani kwao wanampepea na aliposhtuka wote
walimpa pole akauliza, “Nimefikaje hapa?” “Umeokotwa tu mwanangu
na wasamalia wema ndio umeletwa muda sio mrefu, hivi ndio tulikuwa tunakupa
huduma ya kwanza halafu tukuwaishe hospitali.” Mishi alijitahidi kuinuka
na kumwambia mamake asiangaike na swala la hospitali, ingawa alikuwa na maumivu
makali sana ila alijua ni maumivu ya kubakwa kwani tukio zima la usiku wake
lilimjia kichwani mwake. Alijitahidi kwenda kuoga na kwenda kupumzika chumbani
kwake ila mama yake alionekana kumuhurumia sana binti yake, ila Mishi
alijiinamia tu chumbani kwake huku akikumbuka maneno ya Salome kuwa bora
angekesha siku nzima pale akiomba msamaha kuliko kuondoka, “Kwani
msichana anayechanganya wanaume nip eke yangu jamani! Kwanini kunipa laana ya
hivi! Kwahiyo nimebakwa ndio furaha yao? Yani kama nimepata ukimwi nahakikisha
nausambaza kwao, haiwezekani nikafanyiwa hivi. Kwanza Yule ni mtu wa aina gani
wa kutoa laana kwangu? Ila dah nimekoma jana, sijui kama nitarudia. Najipa moyo
tu” Aliwaza sana, hakutaka waende hospitali wala hakutaka kuwaeleza
nyumbani kwao kilichompata, kwanza alishukuru Mungu kuzinduka kabla ya kupelekwa
hospitali kwani kwa yeye ni aibu kubwa mno kusema kuwa alibakwa. Alitulia kidogo
na kumuaga mama yake kuwa anaenda duka la madawa, “Kwanini usimuagize
mtu mwanangu Mishi?” “Mama, mimi ni mzima, acha tu niende
mwenyewe” Hakutaka kuagiza mtu kwani bado alihisi huenda mtu ambaye
angemuagiza angejua tatizo lake, alifika duka la madawa na kununua dawa
azitakazo ila wakati anarudi kwao, njiani akakutana na Salome na kumfanya
ashtuke sana, “Mbona unashtuka hivyo Mishi? Umeona mzuka, mzimu au kitu
gani?” “Aaaah hapana kitu” “Hukutegemea kuniona hapa
eeeh!” Mishi alikuwa kimya tu kwani alianza kumuona Salome kama kidudu
mtu kutokana na ile laana aliyompa jana yake, “Mishi, nimekuja kukupa
ujumbe mmoja tu. Acha tabia yako hiyo, kama unahitaji mwanaume basi upate
mwanaume akuoe na uwe mke wa mtu na utulie kwenye ndoa yako sio kutwa kucha
kiguu na njia. Unawazibia wenzio liziki zao, wadada wenzio wapo wengi tu
wakitaka wachumba halafu wewe bila aibu una miliki wote. Aibu umeipata kwa
wachache tu wale, ila ukiendelea ipo siku nitakukutanisha na wanaume wote
unaowachanganya, tulia upate mume” Mishi alimuangalia Salome kisha
alijiuliza kimoyo moyo kuwa huyu binti mdogo hivi anajiamini nini mpaka kusema
yale ila hakujua Salome anajiamini nini, hakumjibu kitu na kuanza kuondoka ila
Salome akamwambia, “Ningekuwa ni wewe ningeuliza kuwa baada ya kubakwa
kitanipata nini ili nikijua nianze kuchukua hatua ila kwavile wewe ni kiburi na
mjuaji basi utakula jeuri yako” Salome akaondoka na kumfanya Mishi
ajiulize sana, na moja kwa moja akahisi labda ni ukimwi. “Itabidi
nikapime ukimwi, jamani katokea wapi binti Yule? Hata sijui kanijulia
wapi” Mishi alirudi kwao ila akiwa na wazo la kwenda kupima ukimwi
tu. Rose na mwanae Ana walifika nyumbani, kiukweli Rose alikuwa
na mawazo sana. Walipoingia sebleni tu walimkuta Salome akiwa peke yake
pale sebleni, na Walipoingia tu aliwapa pole ya msiba, Rose alimwangalia na
kujiuliza kuwa amejuaje, ikabidi amuulize, "Pole ya msiba wa
nani?" "Si wa mganga wako" "Halafu wewe Salome, nakuangalia tu
muda mrefu. Siku zote nakuangalia tu, na utahama humu ndani
mwangu" Kisha Rose akaondoka na Kwenda zake chumbani ila Salome alikuwa
akicheka tu kiasi kwamba alimfanya Ana amuangalie kwa hasira sana, ila Salome
alimuangalia pia Ana na kumwambia, "Na bado, mpaka mtaacha" Ana
aliondoka na kuelekea chumbani kwake pia ila alijiuliza sana kuwa huyu Salome
anajiamini kitu gani mpaka awe anacheka kwa dharau vile, kumbe mama yake nae
alikuwa alijiuliza swala hilo hilo maana Ana aligundua baada ya kwenda kwa mama
yake ili wakajadili vizuri na kumkuta mama yake akiongea, "Hivi huyu
Salome anajiamini nini?" Ana aliingia na kumwambia mama yake kuwa hata
yeye kitu hiko kinampa sana mawazo, na kumuuliza mama yake, "Tutamuweza
kweli!" "Kwanini tusiweze wakati ni binadamu wa kawaida tu
yule" "Kwahiyo tutafanyaje mama?" "itabidi tutumie nguvu, yani
yule Salome tumtoe kwa nguvu maana bila hivyo atatushinda" "Sawa mama,
ila je umeshajua kinachowamaliza waganga tunaowatafuta! Sio huyu huyu Salome
kweli!" "Atatoa wapi nguvu za kufanya vitu vikubwa
hivyo?" "Mama, hebu jaribu kufikiria kwanza. Unakumbuka jana asubuhi
yule mganga alifika hapa kabla hujaenda kumfata halafu Salome akakuambia kuwa ni
yeye ndio amemleta mganga yule, ukawa huru na kumuonyesha kila kitu, tumeenda
kwake na kugundua alikufa juzi kwahiyo yule wa jana labda alikuwa mzimu au
uliletewa marehemu bila kujijua" "Ana tafadhali mwanangu usiendelee
kuongea, unanikumbusha machungu. Unajua yule mganga nimefanya nae vitu vingi
sana, hadi nimeenda kumuonyesha ile nyumba yangu ya juu ambayo haikaliwi na mtu.
Samahani kwa kukwambia haya mwanangu ila yule mganga nimezini nae" "Yani
mama kwa swala hilo tambua kwamba umezini na marehemu, kuanzia leo hata sitaki
tena mazoea na yule Salome, na amesema na bado mpaka tuache. Mama bado nina
maswali mengi sana, Salome si mtu wa kawaida. Nitaendelea na dawa zangu mwenyewe
nikishindwa basi ila kwa waganga wako siendi tena. Inaonyesha nao
hawamuwezi" "Hutakiwi kukata tamaa mapema hivyo mwanangu, ngoja tutumie
nguvu kwanza halafu kuna mganga wangu mwingine ndio kiboko
kabisa" "Mama, siku ile yenyewe tulijaribu mikono ikaganda. Kwakweli
sitaki tena" "Mwanangu naomba tujaribu mara ya mwisho tafadhali na
sitokusumbua tena tikishindwa kwasasa" Rose alitumia muda wa ziada
kumshawishi mwanae mpaka akakubali mipango ya mama yake. Wale
mapacha pamoja na dada yao Sara hawakuwa na raha kabisa yani hata siku ile
hawakutoka nyumbani kabisa, walikaa ndani tu kwahiyo hata muda ambao mama yao
amerudi hawakumsikia sababu walikuwa na mawazo sana. Walikaa wote kwenye sebule
ile nyingine huku wakijaribu kujadiliana. “Jamani mimi sijapendezewa
kabisa na Yule Mishi kuondoka bila kumpiga kidogo” “Nyie ni wanaume ila
wote mmemuogopa Salome alivyo mkingia kifua Yule Mishi, yani msichana simpendi
Yule loh alifanya nione mapenzi machungu na nilie siku nzima ila ni Salome huyo
huyo aliyenizuia kumpiga” “Ila hatuwezi jua jamani, labda tujipange
namna ya kumshambulia Yule binti ila nitawaachia nyie, sina hamu nae mimi yani
ananiambia kuna mahali anaenda kumbe analetwa kwetu kutambulishwa na ndugu
yangu! Sina hamu nae Yule msichana kabisa” “Jamani nyie achene tu,
nishapoteza hela zangu nyingi sana kwa Yule msichana na lazima nitamkomesha
siwezi kukubali” Doto alionekana kuwa na hasira zaidi na Mishi sababu
amejiona kama mjinga na alipata aibu jana ukizingatia ni yeye aliwaambia wenzie
kuwa mchumba wake anakuja kumbe mchumba mwenyewe anajulikana na wote maana
kashawaharibia mahusiano yao wote, Doto alikuwa na mpango kabambe kwa Mishi na
hakutaka kushirikisha wenzie kwani hakutaka kuzuiwa kufanya anavyotaka yeye,
kwahiyo walivyoongea ongea pale akawaaga wenzie kuwa anatoka kidogo nao
hawakutaka kumuhoji zaidi. Doto aliondoka zake na safari yake ilikuwa ya
kwenda kwakina Mishi, ambapo alifika na kuambiwa kuwa Mishi kalala ila aliomba
kuongea nae, Mishi bila ya kujua kuwa ni nani alitoka ila alipomuona kuwa ni
Doto akatamani kurudi ndani ila kwavile hakutaka kupata aibu pale kwao kuwa
amegonganisha ndugu ikabidi atoke nae, aliposogea nae tu Doto hakuweza
kuzungumza na Mishi kwanza kwani alijikuta akinyanyua mkono wake na kutaka
kumzaba kofi ila cha kushangaza kabla ule mkono haujaangukia kwenye shavu la
Mishi, Doto alijikuta yupo sebleni kwao halafu Salome akiwa mbele yake. Doto
alishangaa sana, akajikuta akiuliza “Imekuwaje?” “Imekuwa hivyo
hivyo ilivyokuwa, si nishawakataza kumpiga Mishi nyie! Kwanza na nyie mmeyataka
wenyewe, wewe unakuwaje na mwanamke halafu pacha mwenzio humuonyeshi? Mnataka
nini kama sio kutembeleana? NImesema Yule msichana asipigwe ila atapigwa na
laana yangu, na nina maana kubwa sana kufanya hivi” Doto alimuangalia
Salome kwa hasira sana kwani alionekana ni msichana mdogo ila aliyekuwa na amri
zaidi, ila bado alikuwa hajielewi elewi hata alivyorudishwa nyumbani na
kumuuliza swali Salome bado hakuelewa kabisa, akataka kutoka tena nje ila kabla
hajatoka akamuona mama yake akiwa na Ana wakija kwa kasi sana na wameshika
sufuria la maji ya moto na kummwagia Salome, ila muda huo huo alishangaa kuona
kuwa yale maji kumbe alikuwa anamwagiwa yeye na sio Salome, alijikuta akipiga
kelele za maumivu. ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment