Simulizi : Nauza Bikira Yangu
Sehemu Ya Nne (4)
Ni saa nne zilikua zimekwisha pita pasipo kupokea simu ya aina yeyote, Hali hiyo ilimfanya kuwa na wasiwasi, Udogo wa kazi aliyofanya ndio ulimfanya kujiamini kupita kiasi ila muda wa majibu ya
kazi ndio ulimfanya kuwa na hofu. Kila baada ya sekunde alikua akitizama simu yake huku ikiwa haina hata dalili ya simu kuita. Mawazo ya tukio lililopita huku akifikiri ni wapi alipokosea hakupata jibu na kuishia kujipa tumaini la kuendelea kusubiri. Chupa ya Wine aina ya Apple tin ilikuwa juu ya meza, Akiwa mwenye mawazo alinyanyua Glass na kupeleka taratibu kinywani huku akiwa na huzuni ghafla uso wake ukapambwa na tabasamu,
Tabasamu kama ameona kitu cha kufurahisha mbele ya macho yake. alishusha glass ya wine na kuweka juu ya meza kisha akachukua simu yake harakaharaka na kuanza kubonyeza namba fulani baada ya sekunde chache ujumbe zikaanza kuingia kama mashindano katika simu yake, Alitabasamu huku akijiuliza kwa kitendo cha kuwa msahaulifuanapokuwa katka kazi. Ni kitendo cha kuweka namba za kuzuia simu kuingia katia simu yake wakati naingia kukutana na Taylor Kurt.
Alianza kupita ujumbe mmoja mmoja katika simu yake huku sura yake ikionyesha hakuna ujumbe ambao ulimvuta Mara sura yake ikachanua wakati anasoma ujumbe,
"Samahani najaribu kukupigia haupatikani mimi Taylor Kurt"
Ni ujumbe kutoka kwa Taylor Kurt ndio uliomfanya kufurahi. Tayari kitufe cha kupiga simu kilikua kimebonyezwa kwa kidole gumba huku akitegemea kukutana na sauti pande wa pili. Simu iliia kwa muda mrefu kisha ikakatika akajaribu kwa mara ya pili bado hali ilikua ni ile ile akaweka simu chini kwa unyonge na kuchukua chupa ya wine akanywa pasipo kutumia glass.
**** ****
Mdaktari walikua busy katika chumba cha wagonjwa mahututi ndani ya hospitali ya Agha Khan, Ni sauti za mikasi ndizo zilikua zikisikika huku madaktari wakipishana katika kuokoa uhai wa mtu muhimu kwa familia fulani. Mashine ya hewa safi ilikua ikisaidia kumpa uhai mgonjwa aliyekuwa kalala kitandani pasipo kujitambua.
Nje ya chumba cha wagonjwa mahututi Neelam alikua kakaa kwenye benchi kamlalia mama yke mapajani huku akilia. Mama yake Neelam alikuwa kachoka kwa kulia huku pembeni yake wamekaa wazee wawili wa kihindi huku wakiwa na mawazo macho yao yakiwa yanatazama mlango wa chumba cha wagonjwa mahututi. Kitendo cha mlango wa kufunguliwa kilifanya Neelam na mama yake kusimama na kukimbilia mlango wa chumba kile.
"Doctor nini inaendelea humo chumbani"
Mama yake na Neelam alimuuliza swali Doctor swali ambalo lilipokewa kwa tabasamu na Doctor tabasamu ambalo liliamsha tumaini katika sura za Familia ya Mzee Pandya.
"Anaendelea vyema baada ya muda kidogo mtaweza muona"
"Doctor i need to see my dad" (Dokta nataka kumuona Baba yangu)
Neelam aliongea kwa huku akitokwa machozi.
"Calm down my girl you will see him soon" (Tulia binti yangu utamuona muda si mrefu"
Dokta alijibu huku akimshika kichwa Neelam, Ghafla Sauti ikatoka chumba cha Wagonjwa mahututi, Sauti ya Nesi aliyekuwa akimuita yule Dokta. Dokta akakimbia kurudi ndani ya kile chumba akakutana na hali tofauti na aliyoiacha muda mfupi. Mashine ya hewa safi likuwa imesimama huku mgonjwa akia ametulia kimya. Kipimo cha mapigo ya moyo kilikuwa kinafanya kazi na matokeo yalimfanya Dokta kuinamisha kichwa chini na kumfunika shuka mpaka usoni.
"He is Dead"
**** ****
Hali ya jiji la Mwanza ilikuwa tulivu pilika pilika za wakazi wa jiji hilo zilikuwa kama kawaida, Wafanya biashara ndogondogo waliojipanga pembezoni mwa barabra walikwa wakitizama kila mpita njia kwa ajili ya kuwauzia bidhaa. Vijana waliojiajiri kupitia mitandao ya simu nao walikuwa na miamvuli yao pembezoni mwa barabara wakisajili line za simu, wakirudisha namba zilzopotea na hata kuuza vocha za simu. Rajiv akiwa na Tusmo alikua akishangaa Jiji hilo huku akifananisha na jiji la Dar es Salaam,
“Samahani nataka namba yangu imepotea”
Rajiv alimwambi kijana aliyekaa kwenye meza iliyo na mwamvuli wa Air tel.
“Ndio utapata ni shilingi elfu mbili tu”
Yule kijana alijibu huku akifungua laini mpya iliyo katika lailoni. Rajiv akatoa noti ya shilingi elfu Tano na kumpa yule kijana.
“Nitajie namba yako iliyopote na namba tano ulizokuwa unapiga mara kwa mara”
Yule kijana allimwambia Rajiv, Rajiv akachukua kalamu iliyo katika meza na kuandika juu ya kitabu cha kuandikia pale mezani.
“Unaitwa nani?”
“ Naitwa Rajiv Roshan”
“sawa Line yako iko tayari ila utaiweka katika simu baada ya nusu saa kuanzia sasa”
Rajiv akapokea ile line pamoja na kiasi cha fedha kilichobaki kutoka kwa yule kijana na kuaga kisha wakaondoka.
**** ****http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Taarifa ya Msiba iliwachanganya sana Familia ya kina Neelam, Kifo cha Ghafla cha Mzee Pandya kilisambaa jiji zima kama Moto katika nyasi kavu. Neelam akiwa mwenye mawazo akifikiri ni kitu gani baba yake alitaka kumwambia bila kupata jibu. Wazo la kuangalia mkoba aliokuja nao baba yake mara ya mwisho ndilo lilifuata na kukimbilia chumbni kwake akiwa kakumbatia mkoba wa baba yake. Kelele ndiyo ilimshtua mama yake na Neela na kukimbilia chumbani kwa Neelam, Macho yake yakatua juu ya picha nne zilizo juu ya kitanda cha Neelam, Picha zilizomuonyesha Rajiv akiwa na mwanamke wa kiafrika tena akiwa uchi. Jasho likamtoka na kumsogelea binti yake.
“Umepata wapi picha”
“Kutoka kwa mkoba wa baba, Rajiv ndio source ya kifo cha dad”
Neelam akavuta Droo ya Dressing table iliyo pale chumani na kuchukua simu yake akabonyeza sehemu ya majina akakutana na jina Honey na kubonyeza kitufe cha kupigia simu. Simu iligana sikioni kwa muda huku akiwa haamini jibu lililokuwa likitoka katika simu ile. Ni kweli namba ya Rajiv ilikuwa haipatikani.
**** ****
Mvua kubwa ilikua ikinyesha ikiambatana na upepo mkali, Baridi ilikua imelishika jiji la nmwanza huku kila mtu akiwa ndani kajifunik kwa blanketi kubwa ili kuzuia baridi. Hali ilikuwa tofauti kwa Rajiv na Tusmo. Wepesi wa bei uliendana na wepesi wa shuka lao la kujifunikia. Baridi ile haikupata shida kupenya katika miili yao na kugonga mpaka ndani ya mifupa ya miili yao. Mlio wa simu kuita ndio ulimtoa Rajiv katikatiy shuka na kupokea.
“Hellow Rajiv”
Ni saut ya Neelam ndiyo ilimshtua Rajiv
“Neelam”
“Rajiv Tumar vaada yaad hai kya?” (Rajiv unakumbuka ahadi yako?)
“Ha muje yaad hi” (Ndio nakumbuka)
“Kya vaada kiya tha?” (Uliniahidi nini?)
“Jindagi bar tume pyarkarti hoo” (Kukupenda milele)
“Phir kya kiya tumne?” (Kwahiyo umefanya nini?)
“Muje maaf karna” (Nisamehe)
“Mai tume kabhi nahi bulunga aur tumse nafrat kartahoo” (Siwezi kukusahau na nakuchukia sana)
“Neelam Suno..” (Neelam sikiliza)
“Mere mere bareme sochna band karo” (Nyamaza tena sitaki kukusikia katika maisha yangu)
Simu ikakatwa Rajiv akiwa kapigwa na butwaa bila kujua la kufanya, Akajaribu kupiga namba ikawa haipatikani. Mvua iliendelea kunyesha huku baridi ikizidi na kusababisha Rajiv kuanza kutetemeka. Kwa mwendo wa taratibu akahamia katika kitanda alicholala Tusmo na kumkumbatia kwa nguvu, Kitendo ambacho Kilimshtua Tusmo kutoka usingizini, Joto alilopata kutoka katika mwili wa Rajiv wenye vinyweleo vingi lilimfanya ashindwe kuongea na kutoa ushirikiano wa kutosha na kuzidi kumkumbatia Rajiv. Shetani wa ngono alizidi kuchukua nafasi katika ubongo wa Rajiv, Imani ya umalaya na dhambi walionayo wanawake wa kiafrika aliyojengewa toka akiwa mtoto ilizidiwa nguvu na pepo wa ngono, Kama wafanyavyo wacheza filamu za ngono Rajiv alianza kuchezea maziwa madogo ya Tusmo huku Tusmo akihema kwa haraka haraka kitendo kilichosababisha Rajiv kushusha suruali yake na kuimalizia kwa miguu huku akitumia mkono mwingine kushusha nguo yake ya ndani ndani ya sekunde chache alikua kama alivyozaliwa ma mama yake miaka ishirini na sita iliyopita huko Doha india. Sauti za kuishiwa na nguvu huku nguvu za mahaba zikiwa zimemtawala zilikuwa zikisikika kupitia matundu ya pua ya Rajiv, Kwa harak mkono wake ulipita katika kanga aliyojifunga Tusmo na kukutana na kaptula aliyovaa ndani kama chupi mpira wa kaptula ile ulikuwa unatanuliwa na mkono ili kuruhusu mkono kuingi ndani na kukutana na kilichozibwa na kaptula hiyo. Kama umeme Tusmo aliruka pembeni huku akijiziba matiti yake yaliyokuwa wazi baada ya ile kanga kuondolewa na Rajiv.
"Rajiv unataka kufanya nini?"
"Let me love you Tusmo, Your body is so hot" (Wacha nikupende Tusmo, Mwili wako ni Moto sana"
Rajiv aliongea huku akitetemeka akiwa anamuangalia Tusmo kwa Woga.
"Rajiv sitaki kuhuharibu usichana wangu nipo kwa ajili ya mwanaume wangu wa ndoa"
Tusmo aliongea kwa msisitizo huku akijiziba matiti kwa mikono yake miwili.
"Ni nnni huyo mwanaume wako? Ni nini hicho hutaki haribu"
Rajiv aliuliza huku sura yake ikiwa na uhitaji wa Tusmo kuwa karibu yake.
"Mimi ni bikira Rajiv"
Rajiv kwa mshangao huku akimuangalia Tusmo kwa macho ya Kustaajabu
"Wewe ni Bikiraaaaaaaaaaaa"
**** ****
Ujumbe ulioingia kwenye simu yake ulioashiria kuna simu ilikuwa ikipigwaa katika simu yakee bila mafanikio ulimpeleke kufungua ujumbe ule na kukutana na namba ambayo alishawahi kuiona mahali ila hakumbuki ni wapi. kwa haraka akafungua ujumbe ule na kupiga ile namba iliita kwa muda kisha ikakatika. wakati anajaribu tena mara smu ikaingia kuangalia namba inayopiga ni ileile akakata na kupiga huku akisubiri kwa shahuku simu ikapokelewa na sauti ya kike toka upande wa pili.
"Naweza kukusaidia tafdhali"
"Taylor Kurt hapa anaongea h"
Taylor kurt alijibu kwa haraka
"Ndiyo nafahamu nilitegemea simu kutoka kwako"
Sauti upande wa pili ilimjibu
"sawa, Jana nimekutafuta sana hukupatikana hewani"
Taylor Kurt aliongea huku akiskiliza kwa makini jibu kutoka upande wa pili.
"pole ila kawaida madini ni ghali sababu yanapatikana kwa shida sana, Na faida kubwa haipatikani kirahisi, Pole kwa kusumbuka kunitafuta hewani"
Karma alimjibu Taylor kurt.
"Naomba tuonane leo kama hutojali"
"Oh pole Taylor nipo ufaransa nina mkutano na kampuni ya persey Perfum soko lao limeyumba wanahitaji msaada wangu"
"oh mungu wangu sasa unarudi lini"
"Ukiweza kukodi ndege naweza rudi leo leo namaliza mkutano baada ya saa moja"
"hiyo si shida shida ni ndege gani nayoweza pata kwa sasa"
"Usijali hiyo kazi niachie we andaa Dola laki mbili baada y a robo saa utafanya malipo ya ndege hiyo"
Karma alijibu kwa sauti ya ukakamavu isiyohitaji mzaha kwa wakati huo.
"Sawa hakuna shaka utanifahamisha"
"sawa"
simu ikakatwa, Taylor kurt Akashusha pumzi kwa uchovu.
**** ****
**** ****
Kikao kizito kilichokuwa kikiendelea ndani ya Jengo la ofisi ya agha khan, Ni wakuu wa umoja wa wahindi waishio Tanzania walikuwa wakijadili kuhusiana na Kifo cha pandya na sababu ya kifo chake. Jina rajiv rosha likitawala katn ndilo lilikuwa likitawala katika midomo yao kama pilipili iliyo katika Tambuu. ghadhabu zao dhidi ya Rajiv zilionekana waziwazi huku wakilaani kwa kwa kitendo cha Rajiv kutia doa umoja huo kwa kutembea na Mwanamke wa kiafrika ambao kwao ni dhambi kubwa huku wakifananisha na kutembea na mnyama. Maamuzi ya kutengwa kwa Rajiv na kuondolewa katika umoja huo na kutotambulika kama muhindi, Amri ilitolewa na waraka ukasambazwa kwa wahindi wote Tanzania kutomsaidia chochote Rajiv na picha yake ikasambazwa sehemu mbalimbali katika ukanda wa afrika mashariki huku kukiwa na taarifa ya kutengwa kwake.
**** ****
Rajiv akiwa amekaa katika kitanda chake anavaa viatu tayari kwa kutoka, Tusmo akiwa kasimama karibu na dirisha akitizama nje.
"Rajiv nisamehe kwa tukio la jana"
Tusmo aliongea huku akiangalia kule nje kupitia dirishani.
"Tusmo mimi ndio wa kuomba radhi, Kwa kitendo nilichotaka kukifanya usiku wa jana, Nisamehe sana"
Tusmo alimuangalia Rajiv wakati anaongea na kutabasamu.
"Usijali Rajiv hali ya hewa ilichangia kupelekea sisi kufikia hali ile"
"Nashukuru kwa kunisamehe, ila naweza kukuuliza swalikama hutojali?"
Rajiv aliongea huku akimkazia Tusmo macho kwa makini kama anataka kujua kitu kutoka kwake.
"Usihofu we uliza tu"
"Ni kweli wewe ni Bikira?"
tusmo aliachia Tabasamu pana baada kusikia swali kutoka kwa Rajiv.
"Ndio ni kweli, Simjui mwanume tokea nimezalia na sikumbuki kama kuna tukio lolote lililosababisha mimi kupoteza bikira yangu"
Rajiv hakuridhika na jibu kutoka kwa tusmo alitikisa kichwa kuashiria hajakubaliana na jibu lililotoka kwa Tusmo.
"Inawezekaje mwanamke wa kiafrika akawa na bikira"
"Mh usijali Rajiv najua huamini ila nikipata mume wa kunioa ndio atajua nini namaanisha, Tuzungumze mambo mengine tafadhali"
Tusmo alimjbu rajiv huku kionekana kutokupendezwa na maswali y Rajiv.
"Oh Iam sorry" (oh nisamehe)
"Usijali, Samahani Rajiv hivi tutaishi maisha haya katika nyumba ya wageni mpaka lini?"
Rajiv alishusha pumzi kwa swali lile na kumuangalia Tusmo kama anataka kusema kitu kisha akasimama.
"Pia mimi huwa nafikiri, Now nenda tafuta kazi na nyumba ya kupanga tutoke hapa nyumba ya wageni"
Tusmo alitabasamu ishara ya kukubaliana na wazo la Rajiv.
"Nimefurahi kusikia hivyo na mimi itabidi nitafute kazi pia ili tusaidiane katika mahitaji ya kila siku si vyema kuwa tegemezi"
Rajiv alizidi kushangazwa na mawazo ya tusmo tayari akili yake ilikuwa imetekwa na Tusmo, Aliaga na kuondoka huku kichwa chake kikifikiri kuhusu tusmo pekee.
**** ****
Macho yakiwa yamemtoka kumyazama binti mrembo aliye mbele yake, Maneno liyokuwa anaongea kwenye simu ndiyo yalimchanganya zaidi. Hakutaraji majibu yale kujibiwa kwa wakati ule na yule binti. Bastola yenye rangi ya dhahabu aina ya Swift swiss c56 ilikua mbele ya binti yule. Sauti isiyo na mzaha ilikuwa ikitoa Amri kwa wakati huo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hatuna muda wa mchezo piga simu kwa Taylor mwambie unataka onana nae sasa”
Ni Martine Cruez alikua akitoa Amri kali kwa Karma, Karma kwa Tabasamu akitoa simu sikioni bila woga na kuirudisha katika pochi huku kila sekunde inayoongezeka iliongeza tabasamu katika sura yake.
“Martin Cruez Hauwezi kushinda kwa risasi sita pekee zilizo katika bastola yako, Bila kujua adui yako silaha yake ina risasi ngapi na amevaa bullet proof ama la ”
Karma alitoa jibu kuku akijiangalia katika kioo kidogo cha mkononi na kutumia muda huo kujipodoa. Martin Cruez aliishiwa na ujanja akajikuta anashusha silaha yake chini na kuketi katika kiti taratibu.
“Martin unapamba na mtu hatari sana pia yeye ana watu wanamlinda kama wewe, Siwezi sema nipo America nikamatwe kizembe, Je kama amejua mpango wetu, Nipe muda nifanye kazi yako”
Karma akiwa kachukia aliongea kisha akaamka na kumuacha Martin Cruez kakaa peke yake pale ndani.
*** ***
Akiwa kachoka kwa kuzunguka katikati ya jiji la Mwanza, Kila ofisi aliyoingia kutafuta kazi aliambulia patupu. Taaluma yake katika mambo ya mawasiliano na Intaneti haikuweza kumpatia ajira ndani ya jiji la mwanza. Kila kampuni aliyoingia iliogopeshwa na vyeti vyake na kujikuta wakishindwa kumuajiri kwa kuhofia mshahara watakaomlipa. Rajiv akipanda ngazi za jengo la Gopar Govinda co. Ltd kwa uchovu macho yake yakatua katika picha kubwa iliyobandikwa katika ubao wa matangazo huku ikiwa imewekwa alama ya njano katika paji la uso. Ni Picha yake yenye alama ya kutengwa alaama watumiayo wahindi kufahamishana muasi wa dini yao na maagano yao. Miguu ikishindwa kusonga mbele huku harufu ya jasho kumtiririsha ikikutana na pua zake mwili kukosa nguvu huku mguu wa mbele ukijitahidi kunyanyunyuka na kuupita mguu wa nyuma, Ni hatua za kurudi kinyumenyume na kutokomea alipotokea. Ugumu wa maisha na uchungu wa jiji la mwanza ndio uliomuandama. Mngao wa ngozi yake ulianza kufifia na kufanana na muhindi aliyechoka sana. Wakiwa wanaishi katika chumba kimoja cha kupanga katika eneo la Mabatini eneo wanaloishi watu wa hali ya chini. Tusmo akiwa anajishughulisha na biashara ya kuuza samaki wa kukaanga. Tayari alikua na umaarufu mkubwa eneo hilo kama mke wa muhinndi huku Rajiv akijishughulisha na kazi za kutengeneza simu kazi aliyokua anafanya nje ya nyumba anayoishi. Kipato kidogo walichopata kiliwatosha kusogeza maisha katika jiji la Mwanza.
“Tusmo sasa tumeishi muda mrefu kwanini tusioane?”
RaJiv alijikuta akiongea na Tusmo bila woga wakati wa usiku.
“Mmh Rajiv kweli tutaweza kuwa mke na mume kwa jinsi nilivyokuzoea kama kaka yangu”
Tusmo alimjibu Rajiv huku akimuangalia usoni jibu ambalo lilimfanya Rajiv kupepesa macho kwa woga na aibu.
“Lakini mwisho wa maisha haya mpaka lini”
Rajiv alijitetea kwa swali ambalo aliamini Tusmo hakuwa na jibu lake.
“Ok Nikisema tufunge ndoa tuna Fedha gani za kufunga ndoa,na tutafunga ndoa ya kihindi au?”
“Hapana hatutofunga ndoa ya kihindi, Kwani wewe ni dini gani?”
Rajiv Alimuuliza Tusmo swali ambalo lilimgusa sana Tusmo na kujikuta akijibu kwa upole.
“mimi ni muislam”
Kwani dini yenu inasemaje kuhusu ndoa.
“Inapasa Mwanamke akubali kuolewa na kisha mahari itolewe kulingana na msichana alivyotaka na kisha baada ya hapo ndoa inaweza kuhalalishwa”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Je mimi nikikupatia mahari siwezi kukuoa sasa”
Tusmo alitabasamu na kumuangalia Rajiv machoni na kuona kila anachoongea anamaanisha.
“Unapaswa kusilimu na kuwa muislam, Na kufahamu taratibu za dini ya kiislam, Kukiri ya kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa Haki ila Mungu mmoja na Muhammadi ni mjumbe wake”
Rajiv alitikisa kichwa kuridhika kwa kile alichoambiwa na kukaa kimya kwa sekunde kadhaa.
“Kesho nitaenda katika msikiti wa pale chini na kuzungumza na Shekh juu ya dhamira yangu ikiwezekana nianze mafunzo mapema”
Rajiv aliongea kwa kumaanisha kuku akimuangalia Tumbbo na kuunganisha na Tabasamu lililomkosha Tusmo, Tayari msisimko wa mahaba juu ya Rajiv ulianza kuonekana.
“Hakika nitakua tayari kukupa ile zawadi ya mwanaume wangu wa ndoa”
“Zawadi ipi hiyo Tusmo?”
Rajiv alijikuta akiuliza kwa shauku.
“Bikira Yangu”
***
Kila alichokigusa katika ofisi yake hakikumfaa, alizunguka zunguka ndani ya ofisi yake kama anatafuta kitu.Mzimu wa Jambo fulani lililokua likimchanganya ndio uliokua ukimuandama. Saa kubwa iliyo ukutani ilikua ikigongana na macho yake mara kwa mara na kuzua mikunjo katika sura yake. Mshale wa Sekunde ulikua ukienda Taratbu kama umelazimishwa huku mshale wa Dakika ukiwa unajikongoja kwa mwendo wa kinyonga na kusababisha mshale wa saa uonekane kama umesimama kabisa na usio na dalili ya kusonga mbele, Saa ile kusoma ni saa tisa na nusu haukumshawisi kabisa kuamini muda ule. Macho yakihama na kutua kaitka kompyuta iliy mezani kwake na kukutana na muda unaoshahabiana na ule wa kwenye saa. Akishusha pumzi kwa ishara ya kuchoshwa na muda ule na kujiegemeza juu ya viganja vya mikono huku akitafakari kiitu Sura yake ikitazama juu ya mezkuba ya ofisi yake. Mshtuko alioupata baada ya mlango kufunguliwa bila tarifa ni mshtuko ambao kidog ungesababisha msukumo wa damu katika moyo ungebadilika na kuwa wa kasi ambao ungesbabisha tatizokwake, kwa macho yenye Ghadhabu na maneno yaliyojaa ukali yakatua kwa Katibu Muhtasi wa ofisi yake aliyesimama mbele yake kwa unyenyekevu.
“Monica mbonaumeingia bila taarifa?”
“Samahi boss nimepiga simu zaidi ya maramoja haikupokelewa”
Tay lor Kurk akifikir kitu na kutafakari kelele ya kitualiyokua akiisikia muda mchache ndani ya ofisi yake na kuipuuza kelele hiyo zaidi ya mara mbilina kugundua ilikua ni simutoka kwa katibu muhtasi wake.
“Nakusikiliza sasa”
“Holand Czevelote inc wametuma nukushi wanauliza kuhusu oda yao ya simu maana bidhaa imeisha na wana uhitaji mkubwa sana”
“Oh! Sawa wajibu muda si mwingi oda yao itakua njiani inakuja”
“Sawa”
Monika akiwa anatoka na kuufikia mlango anafungua mlango anashtshwa na sauti ya Taylor Kurt.
“Sihitaji mgeni yeyote kwa sasa”
“Sawa Boss”
**** ****
Moyo ukiwa unakwenda kasi huku akisogelea msikiti wa Mabatini woga wa kuingiandani ya msikiti ule ulimtanda sana, Akiwaangalia waumini wakiwa wanatawadha (Udhu) na kujikuta akisogea mpaka pale na kuchukua kopo kisha akachota maji na kuanza kunawa miguu.
“Asalaam Aleykum”
Sauti ya salamu toka kwa mzee wa makamo aliyefika pale na kuchukua kopohuku akichota maji, Hakuweza kumjibu kwa kuwa hakujua ni jibu lipi anapaswa kulitoa kwa mzee yule. Huku akimuangalia mzee yule akitawadha Rajiv alisimama wima akiwa kashika kopo lake la maji bila kuua baada ya miguuanapaswa kunawa nini. Kengele ya woga ilizidi kugonga kichwani mwake baada ya kugundua kakosea hatua za awalii za kujiswafisha kabla ya kuingia msikitini.
“Samahani Dugu yangu”
Rajiv alijikuta akianza maongezi na yule mzee
“Bila sanmahani”
“Nahitaji onana na Shekh kwa maongezi naye”
“aah ngoja nikuitie maana muda wa sala bado”
Yule mzee akaingia nadani na kutoka na mzee wa umri wake akiwa na ndevu nyingi sana kidevuni, Wakasogea mpaka alipo Rajiv.
“A Salaam aleykum Mwarahma tullah, Taala wabarakatu”
Yule Shekh alitoa salamu ambayo kwa Rajiv ilikua ni utata zaidi maana ilikua na urefu zaidi ya salamu ya awali ya yule mzee.
“Salama”
Rajiv alijibu kwa mkato huku akipooza maneno kwa kutabasamu na kupeleka mkono kushika mkono wa Shekh aliokua kaunyoosha ili wapeane mikono. Wakaenda kukaa katika kibarazakilicho nje ya msikiti ule.
“Eh nakusikiliza”
Shekh alianza mazungumzo na Rajiv
Mimi naitwa Rajiv Roshan, ni Indian na ni dini ya Hindu.Nimekua katika imani ya Hindi kwa miaka mingi sana ila kwa sasa nahitaji kuwa Islam kwa kuwa naamini ndani ya Islam kuna amani na upendo”
“Ishallah ni kheri kuweza kuifuata dini ya hakhi na kweli na Allah anatufundisha ya kuwa Hakuna apaswaye kuabudiwa kwa Hakhi ila Mungu mmoja na Muhammadi ni Mtume wake, kama unataka kukiri kwa kushahadia basi wewe u mmoja kati ya waja watakayoiona pepo ya Allah siku ya kiama iwapo tu utafuata maagizo yake”
“Kwani kaagiza tufanye nini”
“Kwanza ni SHAHADA ambayo ni shahidi wa Imani ni kusema kwa kusadikisha, “La ilaaha illAllaah, Muhammadur Rasulullah.” Maana ya matamshi haya ni, “Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu (Allaah), na kwamba Muhammad ni Mjumbe (Mtume) wa Mwenyezi Mungu.” Sehemu ya kwanza, “Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki, isipokuwa Mwenyezi Mungu,” inamaanisha kwamba hapana mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu peke Yake, na kwamba Yeye hana mshirika wala mwana. Ushahidi huu wa Imani unaitwa Shahada, ambayo ni kanuni nyepesi ambayo inapaswa itamkwepa moja na kusadiki ili mtu aweze kuingia katika Uislamu, Pili ni SALA Waislamu huswali Swalah tano kila siku. Kila Swalah huchukuwa muda mfupi wa dakika chache tu. Swalah katika Uislamu ni mawasiliano ya moja kwa moja kati ya mja na Mwenyezi Mungu. Hakuna kishenga baina ya Mwenyezi Mungu na mfanyaji ibada. Na tatu ni KUTOA ZAKA Kila kitu ni cha Mwenyezi Mungu, na hata mali zinazohifadhiwa na wanaadamu kama dhamana. Maana khalisi ya neno Zakaah ni zote mbili ‘kutwaharisha’ na ‘kukua.’ Maana ya kutoa Zakaah ni kutoa asilimia iliyotajwa bayana kutokana na mali fulani kwa kuwapatia makundi fulani ya watu wenye dhiki. Asilimia inayopaswa kulipwa kutokana na dhahabu, fedha na pesa taslimu zenye kufikia kiasi kinacholingana na gramu 85 za dhahabu na kubaki katika miliki ya mtu kwa mwaka mmoja wa Kiislamu ni asilimia mbili unusu. Tunavyovimiliki hutakasika kwa kutenga pembeni sehemu ndogo tu kwa ajili ya wenyedhiki, na kama vile kupogoa matawi ya mimea, huku kupunguza salio na kunatia moyo wa ukuaji mpya. Mtu anaweza kutoa zaidi kadiri atakavyo kama Sadaka. Nne ni KUFUNGA RAMADHANI, Kufunga katika Mwezi wa Ramadhaan Kila mwaka katika mwezi wa Ramadhaan Waislamu hufunga tangu Alfajiri hadi kuchwa kwa jua, kwa kujizuia kula, kunywa na tendo la ndoa.
Ingawa Swaum ni yenye faida za kiafya, huchukuliwa kimsingi kuwa ni namna ya kuisafisha nafsi kiroho. Kwa mmojawapo kujizuia dhidi ya starehe za kidunia, japo kwa muda mfupi, mfungaji hupata huruma ya kweli kwa wanaopatwa na njaa, kadhalika na kuongezeka kwa maisha yake ya kiroho. Na tano ni HIJJAH, Hija ya kila mwaka Makkah ni faradhi ya kufanywa mara moja tu maishani kwa wenye uwezo wa kimwili na mali katika kuitekeleza. Kadiri ya watu milioni mbili huenda Makkah kila mwaka kutoka kila sehemu duniani.na hii ni kwa wenye uwezo tu.Hivi ndivyo vitu uislam unataka”
Maelezo yale kutoka kwa Shekh yalitosha kabisa kupooza kiu cha Rajiv na kuwa na Shauku ya kutaka kubadili dini na kutekeleza maaizo ya Uislam.
“Je na uislam unasemaje kuhusu Kuoa”
“Katika Qur’an 30:21 Inasema
“Na katika lama zake amewaumbieni wake kutokana na nyinyi wenyewe ili muishi kwa utulivu nao, na akawatia upendo na rehema kati ya nyoyo zenu. Kwa hakika katika haya ni ishara kwa wenye kufikiri”.
“Je naweza badili dini na nikaoa?”
Shekh akamuangalia Rajiv kwa tabasamu na kufurahishwa na maswali yake yenye Tija ya kufahamu jambo kabla ya kufanya.
Quraan na hadithi vimetoa maelekezo ya kila kitu cha kufuata muumini wa Kiislam na pia suala na kuoa pia. Katika hadithi ya Mtume S.A.W inasema Enyi vijana, aliye na uwezo wa kuoa aoe, kufanya hivyo kutamsaidia kuinamisha macho yake chini na kuwa mtii. Na utii ni sehemu ya imani”
Rajiv alitabasam na kujikuta akiwa na amani kuwa mahali pale.
“Samahani tena Je naweza kubadili dini leo kasha nikaruhusiwa kuoa siku hiyo hiyo”
Yule shekh alitabasamu tena na kuzidi kuvutiwa na Rajiv,Alimshika kichwa ishara ya kufurahishwa nae.
“Mimi nashauri ujifunze kwanza dini inasema nini juu ya ndoa ili uweze kufanya vyema katika ndoa ndipo uoe, Maana katika uislamu ndoa ni nusu ya dini”
Rajiv alishusha pumzi na kumuangalia Shekh kwa sekunde kadhaa na kutaka kuuliza kitu, Kabla hajasema kitu mara sauti ya Muadhini kuwaita waumini wakasali ikasikika.
“Karibu katika Darasa la dini ifikapo saa kumi hapa tuna madrasa utafahamu mengi sana juu ya dini hii, Muda wa kuswali umefika Shahadia basi tutaungana katika swala”
Shekh aliamka na kuingia msikitini huku Rajiv akimuangalia kwa tabasamu.
**** ****
Sauti za kubishana kati ya wasichana wawili zilisababisha muingiliano wa sauti uliozalisha kelele katika masikio yao. Nindani ya ofisi moja huku mmoja akitaka kuingia na mwingine akikataa asiingie.
“Nina jambo muhimu sana na Boss wako”
“Sawa hiyo haijalishi ila kasema haitaji kuonana na mtu yeyote siku ya leo”
Katibu Muhtasi alikua akimjibu Yule msichana huku akiendelea kusoma kitu kutoka katika kompyuta yake.
Yule msichana alichukizwa na kauli za Yule katibu muhtasi na kuamua kuingia kwa nguvu huku akivuta mlango wa kuingilia katika ile ofisi kitendo kilichosababisha askari kuitwa na kuanza kumvuta nje Yule msichana. Kitendo cha mlango kuguswa kilimshtua Taylor Kurt na kutka nje na macho yake kukutana na tukio ambalo hakutegemea. Msichana aliyekua anamsubiri Takribani Saa mbili alikua akivutwa nje na mlinzi wa kampuni ya Jobson Security kampuni yenye dhamana ya kulinda usalama wa kampuni yake. Kwa sauti ya juu alitoa amri Yule msichana aachwe kitendo kilichotekelezwa kwa haraka sana. Karma akijifuta huku akinyoosha nguo yake iliyokua imeshikwa na mlinzi na kutengeneza mikunjo.
“Samahani sana kwa Lililotokea Karma”
Taylor Kurt aliomba Radhi kwa Karma wakati wanaingia ndani katika ofisi yake.
“Usijali chochote kizuri hakiji kirahisi rahisi, Hata faida kubwa unayoenda kuipata inahitaji ujasiri kuifikia”
Taylor Kurt alizidi kushangazwa na majbu ya Karma huku akimuona ni msichana wa ajabu sana.
“Habari za Ufaransa”
“Ni Baridi sana, Matajiri wanajitahidi kuongeza fedha na masikini wanatazam pale alipo tajiri ili wafike, Hii ndiyo dunia ya sasa kama ukiwa tajiri unahitaji mbinu za ziada kuweza kubaki hapohapo bila hivyo wakina Martin Cruez watakutoa katka nafasi hiyo”
Taylor kurt alitabasamu huku akifikiri mtu sahihi amekuja wakati sahihi katka kampuni yake.
“Mimi sina Tatizo nahitaji kuipatia kampuni yenu Tenda ya kufanya Parking ya bidhaa zangu”
“Mmh ni wazo zuri sana kama umeafiki kufanya kazi na sisi”
“Ndio sasa sijui tunweza sign lini mkataba”
Karma akitoa karatasi katika mkoba wake na kuliweka mezani
“Mkataba wa mafanikio hufnyiwa makubaliano katika wakati wa uhitaji wa mafanikio, Muda ndio njia ya mafanikio hatupaswi kusubiri sherehe waati tunahitaji kuongeza fedha katika fedha zetu”
Karma alitoa jibu huku akitoa kalamu katika ule mkoba na kumpatia Taylor Kurt.
“Unamaanisha nini?”
“Mkataba ninao, kama unaamini naweza kupandisha kiwango cha utajiri wako kupitia bidhaa yako iweje ushindwe kuamini kuwa nitaulinda na kuuheshimu mkataba huu”
Taylor Kurt alitabasamu na kukamata kalamu, Akaupitia mkataba kisha akatikisa kichwa kuridhika nao na kuanguka sahihi juu ya karatasi ile.
“Sasa sisi na nyie ni marafiki wa kibiashara nahitaji msichana atakayekua anasindikiza mizigoyenu kutoka katika kampuni yenu”
“Kwanini msichana na si mvulana”
“Daima msichana hutongozwa na mvulana”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwani msichana hatongozi”
Ni tofauti sana na mvulana mara chache wao hutongoza na huwa na ujasiri ndani ya siku kumi kabla ya kuingia Hedhi na wakati huo ndio utakua ni wakati wake wa kupumzika ili asiharibu kazi”
“Hapo nimekuelewa sasa”
“Vizuri kazi tunaanzia wapi”
“Mzigo unapaswa kwenda Holand na sasa ni ruksa ninyi kuandaa mzigokwa kupelekwa katika kampuni ya Holand Czevelote Inc”
“Sawa, Tegemea faida mara mbili”
Karma alita jibu lililozidi kumchnganya Tayor Kurt na kusababisha kushusha pumzi ya furaha huku akiwa na mategemeo ya kufanya biashara zaidi.
**** *****
Sasa Endelea...,
Hakuna kitu kimlifurahisha Martin Cruez ama Karma kufanikiwa kupata Tenda ya kufanya Parking Katika kampuni ya Taylor Curt, Ukubwa wa kampuni ile na urahisi kupata tenda wa Karma ulimshangaza sana na kujikuta akimpatia pesa mara dufu na kumshirikisha zaidi katika mipango inayoendelea. Alihitaji mawazo yake sana katika kuendesha kampuni feki waliyoifungua yenye lengo la kummaliza mfanyabiashara mwenzake. Tenda ya kazi za ? Dharura zilitangazwa kwa ajili ya kupata vijana watakaofanya kazi ya kufanya Parkin ya mzigo. Kazi ya kufanya Parkin ya simu ilikua imekwishaanza huku batery zikiwekwa katika kontena lake na simu zikiwa katika kontena lake. Kila simu moja iliwekwa kalamu ya kuandikia yenye maandishi I’ma superstar huku kukiwa na sahihi ya Taylor Kurt. Hyio ilikua ni zawadi ya kila mteja atakaye nunua aina hiyo ya simu. Mzigo wa kwanza katika Parkimg tofauti ulikua ukielekea katika kampuni ya Holand Czevelote Inc, Baada ya wiki moja katika nchi ya Holand hali ilibadilika kila mwanafunzi wa chuo alikua akigombania aina hiyo ya simu huku wakiwa na kalamu mfuko wa shati kila mmoja aone pia yeye ni superstar anatumia Micphone. Mzigo uliisha kwa haraka sana tofauti na awali na kupelekea mzigo mwingine kuagizwa kuelekea nchini Holand, Taylor kurt alichanganyikiwa na mafanikio yale nakujikutaakimpatia Karma Bonuszaidi kwa biashara aliyofanya ndani ya mwezi mmoja tena katika nchi moja pekee. Tayari kontena zaidi ya Elfu kumi zilikuwa zikisafiri kuelekea Afrika zikiwa na simu. Afrika nako simu ilipokelewa kwa aina tofauti. Kila kijana na mfanya kazi alinunua aina hiyo ya simu huku wanafunzi wa sekondari mpaka chuo wakihakikisha wanatumia simu hiyo ghali. Furaha ilizidi kuongezeka mara Dufu baaya ya Utajiri wa Taylor Kurt kuongezeka kwa asilimia ishirini zaidi na kushika nafasi ya juu kwa utajiri duniani ambapo baada yua kutangazwa katika jarida maarufu nchini Marekani liitwalo Forb na kumfanya Taylor Kurt kumualika Karma kwa chakula cha Jioni katika mgahawa maarufu nchini marekani uitwao Macdonald.
Siku hiyo ilikua siku ya Furah kwa Karma kwani ndiyo siku ambayyo Karma alipanga kuweza kumaliza utata, Kuweza kuhakikisha anamuingiza Taylor kurt katika mtego hatari. Akiwa ndani ya chumba chake mbele ya meza yenye kioo maalumu ya kujiremba akiwa anajaribu kila nguo na kujitazama kisha anavua, Tayari rundo kubwa la nguo lilikua pembeni maana kila nguo aliyovaa aliona haimfai. Gauni la rangi nyeupe lililoukamata vyema mwili wake. Akiwa katengeneza nywele zake vizuri katika mtindo wa African Beauty, Macho yake yaliyozungukwa na nyusi ndefu huku nyusi zikilnda macho makubwa yenye ushawishi kwa mwanaume yeyote yule. Viatu vya Italian Tone high Heels vya rangi ya dhahabuiliyoendana na mkoba aliobeba pamoja na hereni alizovaa. Glass ya Mvinyo aina ya Love Tempted Mvinyo ambayo kazi yake ni kulegeza macho na kuongeza mvuto wa kimapenzikwa mwanamke ilikua ikipita katika koo lakena baada ya dakika chache tayari alikua anarembua macho yake makubwa. Gari aina ya Porcheslikiwa limepaki nje ya nyumba yake Dereve Howd akiwa anamtazama Karma kwa tamaa alijikuta akiachia Tabasamu na kumfananisha Karma na mmmalaika. Akiwa kakaa katika kiti cha nyuma safari ilianza kwa mwendo wa Taratibu kuelekea katika mgahawa wa Macdonald kwa ajilli ya kupata chakula cha jiono na Tajiri Taylor Kurt.
**** ****
Urahisi wa kufunga ndoa aliokutana nao hakuutegemea kwa mahariya shilingi elfu kumi iliyotamkwa na Tusmo wakiwa watu wanne tu ambao walikua wamekaa katika Msikiti wa Mabatini, Rajiv na Tusmo walikua wakifunga ndoa baada ya Rajiv kubadili dini huku jinalake likiwa ni lilelile Rajiv. Furaha iliongezeka zaidi baada ya kusikia Tusmoalikuamaekubali kuolewa nae baada ya taarifa kuletwa na shagidi wake katika ile ndoa na kitendo kilichopelekea kuungana na Tusmona kujikuta akimbusu kwa mara ya kwanza. Ni ndoa ambayo ilihusisha mioyo wa watu wawili huku ikiwa na mashahdi wawili tu n mahalalishaji mmoja mabaye ni Shekh wa msikiti wa mabatini na kupokewa na Mungu huku malaika wake wakiwa wamezunguka tendo lile. Safari ya kurudi nyumbani wakitembea kwa furaha huku wameshikana mikono ilikua imeanza huku hakuna mtu aliyekua akigundua kama wawili hao wametoka kufunga ndoa dakika chache zilizopita. Kabla ya kuelekea nyumbani Tusmo na tajiv ambao kwa wakti huo walikua ni mume na mke waliohalalishwa kwa mujibu wa dini wanayoiamini walikubaliana wapite sokoni na kununua chakula cha kupikasiku hiyo kwani ilikua ni siku ya furaha sana katika maisha yao. Wakiwa wameshikama mkono wakizunguka katikati ya soko huku wakinunua mahitaji yao walibeba kapu kubwa lililoshehena vyakula na kuamua kutembea wakiwa wamelibeba kwa mikono yao kulelekea nyumbani. Wingi wa watu waliokuwanje ya nyumba wnayoishi uliwaanya kupatwa na mshtuko, mshtuko ambao uliyeyusha furaha yao na kukumbwa na kihoro kihoro cha kujua ni kitu gani kilichojiri katika nyumba ile. Hatua zao zikiwa zinaongezeka urefu kukaribia nyumba ile macho yao yakakutana na Gari ya polisi ikiwa na polisi kadhaa. Macho ya watu wale yakageuka kuwatazama kwa wasiwasi huku mmoja wa watu waliokua pale akinyoosha kidole kuwaashiria wao. Polisi wawili waliwafuata na kumshika Tsmo na kumuweka chini ya ulinzi.
“Nimefanya nini jamani”
Ni swali lililotoka kwa Tusmo na kukupokelewa na kibao kikal kilichoamsh hasira toka kwa Rajiv na kujikuta akimpiga kibao askari polisi aliyempiga Tusmo. Polisi walimshambulia Rajiv kwa virungu kitendo ambacho kiliingiliwa na raia wenye hasira na kupelekea polisi kuacha kumpiga Rajiv na kumchukua Tusmo wakaelekea kituo kikuu cha polisi. Rajiv akijikokota kutoka pale chini na kuelekea kulelilipoelekea lile gari huku akilia kwa uchungu, Hakuna mtu aliyemsaidia wala kuongea chochote zaidi ya kumuangalia kwa huruma.
Wakati tukio lile likiendelea kijana mmoja maarufu jijini hapo aliyeamua kuacha kufuatilia mambo ya watu baada ya kukumbwana mkasa mzito, Ni mkasa wa Kizuizi uliompelekeakuishi maisha ya Taabu huku akiuguza mguu wake uliobadilisha mwendo wake wa kutembea kwa madaha na kujikuta akitembea kwakuvuta mguu. Yule pepo wa kufuatilia mambo ya watu aliibuka ghafla na kujikuta akitamani kujua kilichotokea juu ya watu wale. Akitumia ujanja wake wa kudadisi lakini hakuambulia chochotekinachoweza kumsaidia kuweza kujua na angalau kupata pesa ya kula kutokana na mkasa ule, Silaaha moja aliyoiona inaweza kumsaidia ni wenyeji wake ndani ya jiji hilo na kujuana na polisi wengi na furaha iliikumba nafsi yake baada ya kujua walioapatwa na tatizo ni wageni katika jiji lile. Maisha ya kifahari aliyokua anaishi jijini Dar es Salaam huku akiwa anaishi katika nyumba kubwa aliyopangishiwa na Bibiana na akiwa mmiliki wa banda kubwa la kutoa huduma ya Mpesa. Alijikuta akifuta jasho kwa kiganja cha mkono wake na kuamua kijivuta kumfuatilia Rajiv ili aweze kujua ni nini kinachomsibu na aweze kumsaidia ili apate kitu kidogo cha kumaliza siku hiyo. Akiwa ameachana na Rajiv hatua chach kabla hajamfikia Rajiv aligundua kuna mtu anamfuata nyuma alipogeuka macho yake yakagongana na kijana mdogo aliyekua akitembea kwa kuchechemea wazo la uadui likamvaa na kujikuta akifikiri mtu anayemfuata anaweza kuwa kibaka mwenye lengo la kumkaba akajiandaa kwa ajili ya shambulizi tena shambulizi la kushtukiza dhidi ya adui aliyekua anakuja kwa mwendo wa kuchechemea.
*** ***
Pamoja na kuwa Jambauyzi mkubwa nchini marekani lakini bado alkua ni mdhaifu mkubwa sana katika suala la mapenzi. Akiwa anaishi katika nmba ya vyumba viwili hakuna kitu alichokua akifanya zaidi ya kujidunga dawa za kulevya na kunywa pombe. Mtu pekee aliyekua akimchanganya akili yake kama Michel. Michel ni msichana pekee ambaye anachanganya akili yake. Hakuna alichokua akitaka akakakosa. Ni usiku wa saa tano wakiwa watupu juu ya kitanda ndipo Don alipomuelezea mkutano wake na Martin Cruez na mpango wa kummaliza Taylor Kurt.Habari hiyo kutoka kwa Mpenzi wake Don ilizunguka katika ubongo wake na kuamua kufuatilia mpango mzima na akiweza aweze kumuokoa Taylor Kurt huku akitegemea ujira mkubwa toka kwa tajiri huyo. Kila kilichokua kikiendelea Michele alipata taarifa toka kwa Don na Don hakufikiri kama Michel anazichukulia zile taarifa kwa ukubwa zaidi. Akiwa nje ya mgahawa wa Macdonald macho yake yalikua yakitazama kila mtu aliyekua anaingia katika mgahawa ule. Moyo ulimuenda mbio baada ya kumuona Taylor Kurt akiwa anaingia ndani ya mgahawa ule. Shauku ya kumfuata ilimshika ila tatizo ni eneo aliloelekea kukaa halikumruhusu yeye kukaa maana ni eneo la watu wenye fedha. Akiangalia namba fulani katika simu yake na kukutana na jina lililoandikwa Taylor Kurt hapo ndipo alipoenda uwanja wa sms na kuanza kuandika ujumbe.
Taylor Kurt akiwa kakaa peke yake huku kahawasafi toka Meru Coffee kahawa inayolimwa katika viunga vya jiji la Arusha nchini Tanzania na kusambazwa na kampuni ya Meru Coffee mpaka nchini Marekani. Watu wengi hupenda kahawa ya Meru Coffee pindi wanapofika katika mgahawa wa Macdolald. Mlio wa simu yake kuashiria ujumbe umeingia. Akishusha kikombe cha kahawa na kuruhusu kidole chake kufungua ujumbe na kukutana na ujumbe.
“Mwanamke unayekutana nae ni hatari sana atakuangamiza tafadhali ondoka hapo”
Taylor Kurt alishtushwa na ujumbe ule na kugeuka nyuma kuangalia kama atakutana na mtumaji wa ujumbe lakini alijikuta yupo peke yake katika eneo lile. Aliporudisha macho katika mlango wa kuingilia macho yake yakagongana na Karma akiwa anakuja kwa mwendo wa madaha huku Kiatu cha Italian tone high Heels kikilalamika katika sakafu ya eneo hilo. Taylor Kurt bila kujua nini cha kufanya alijikuta akipigwa na bumbuwazi huku Karma akizidi kusogea eneo alilokaa.
*** ***
Hakuna kazi iliyokuwa ikimpa woga kama kazi ya Martin Cruez, Hakutaka kabisa kuingia katika kashfa ya kushirikiana katika mpango wowote ulio kinyume na maadili ya kazi yake. Alitamani kutunukiwa shahada ya Utumishi bora pindi atakapostaafu kazi yake na kubaki na heshima katika nchi ya Marekani. Kutokana ni lazima kufanya kazi ya Martin Cruezkwa mujibu wa maagizo aliyopokea kutoka kwa wakuu wake wa kazi ilimfanya kuchukua tahadhari kwa kila anachokifanya. Hakumuamini hata kidogo Don, Muda wote alikua akimtazama huku akiwa haamini kama yule ndiye Don aliyekuwa akimsikia kila mara na kuona picha zake katika maeneo mbalimbali kama Gaidi anayetafutwa na serikali ya Marekani. Muonekano wake haukufanana hata kidogo na ukatili wake anaoufanya. Utekaji wa Gari la wanafunzi wa shule ya awali na kuwachinja mmoja mmoja ili kuishinikiza serikali ya Marekani kumuachia Lowedre aliyefungwa katika Gereza la gwantanam kwa tuhuma za kuhusika katika kifo cha mtoto wa Seneta wa jimbo la Texas miaka minne iliyopita. Don alionekana ni kijana mpole na mwenye upendo wa hali juu. Duke afisa usalama wa taifa alijikuta akianza kumfuatilia Don kwa kila anachofanya.
Ni siku ya tano tokea aanze kumfuatilia Don hakuweza kuona chochote kibaya kutoka kwa kijana huyo huku akiwa anafanya kazi katika kampuni ya Home Cleaner ambapo Don alikuakatika kitengo cha kufua Mazulia. Mshahara mdogo aliopokea ndio alikuwa akitumia kwa matumizi yake ya kila siku. Kila jioni aalikua akipata chakula katika mgahawa wa watu wa hali ya chini sana ukilinganisha na jinsi Jina la Don lilivyo kubwa Duke alizidi kuamini kuwa yule siye Don halisi. Akiwa anaishi katika nyumba ya kawaida hakuna mtu hata mmoja aliyewahi kuonekana akimtembelea Don. Kupitia kitabu cha wateja wa simu za majumbani Duke aligundua nyumba haina simu ya ndani kwa miezi sita hapo ndipo alizidi kuchanganyikiwa kwa jinsi maisha aliyokuwa akiishi Don. Ikiwa ni jumamosi jioni baada ya Duke kukaa muda mrefu akiangalia nyumba ya Don Mara Gari aina ya Bugate ya rangi nyekundu ikapaki nje ya nyumba ya Don. Kwa kutumia miwani yenye kamera zenye uwezo wa kuvuta kitu kilicho mbali alijikuta akifuatilia tukio lile kwa ukaribu zaidi. Msichanamrembo alishuka akinekana ni mmsichana anayeishi maisha ya hali ya juu sana. Mara Don akatoka akiwa kavaa singlend na kumkumbatia yule msichana na kuanza kunyonyana ndimi kitendo kilichomaanisha ni wapenzi. Kwauzoefu aliokuwa nao Duke aliweza kuwafuatilia bilakugundulika mpakaalipoweza kutegesha kinasa sauti katika chumba cha kulala cha Don na kuondoka huku akiamini atapata chochote kutoka kwao. Ni baada ya siku mbili siku ambayo Michel alikua katika mgahawa wa Macdonald kuweza kumwambia ukweli Taylor kurt kuhusiana na mpango mchafu unaoendelea. Muda huo0 ndio muda ambao Duke alikua akisikiliza mazungumzoya Michel na Don katika kinasa sauti. Akili ya duke ilitaharuki na kuona mpango unaharibika kwa haraka akakimbilia kituo cha zimamoto na kuonyesha kitambulisho kisha akapewa Gari ya zimamoto ili kuepusha msongamano wa magari. Kwa kasi ndani ya dakika kumi alikua ndani ya Mgahawa wa Macdonald na haikuwa kazi kumtambua Michel. Kosa kubwala Michel ni kwenda Chooni hapo ndipo alipokutana na pigo. Pigo kali lililomdondosha chini na kusafirisha fahamu zake nje ya dunia hii kwa muda kidogo.Simu ya Michel ikiwa katika kiganja cha Mkono wa Duke tayari alikua akipitia simu na ujumbe akakutana na ujumbe uliotumwa na Michel dakika chache kwenda kwa Taylor Kurt. Kama mashine akaandika ujumbe na kutuma kisha akatoa simu yake akaandika ujumbe mwigine na kutuma huku akishusha pumzi kwa nguvu.
****
Gari la Polisi lililombeba Tusmo lilisimama nje ya kituo kikuu cha Mwanza na Polisi wawili wakiwa na bunduki wakamshusha kama jambazi mkubwa aliyekua akitafutwa kwa muda mrefu. Tusmo akilia huku akiugulia maumivu aliyoyapata kutokana na kipigo cha polisi. Akiongoza mpaka mbele ya kaunta ya polisi na kusukumwa nyuma ya kaunta huku akiamriwa akae chini. Askari mmoja wa makamo aliyekula chumvi nyingi akiwa amekamata file la rangi ya khaki alimuangalia Tusmo kwa dharau huku akionekana asiye na huruma.
“we malaya unaitwa nani”
Lilikua ni swali lenye kukera kutoka kwa askari yule lililojaa udhalilishaji likatua katika kifua cha tusmo na kuzalisha machozi yaliyotokana na maumivu yaliyotokea ndani ya kifua chake na maumivu yale kusafirishwa kupitia mishipa ya fahamu na kuibua simanzi ndani ya nafsi yake. Kimya cha Tusmo kilimkera yule askari kwa kutumia mguu wake wa kulia ulioonekana wenye nguvu alimpiga teke mgongoni na kupelekea tusmo kutoa jibu la swali lile haraka.
“Naitwa Tusmo Raheem”
“Kumbe unajua kuongea kwanini unajifanya bubu kenge wewe”
Yule askari aliongea kwa ukali huku akimkata jicho la hasira Tusmo aliyekua kakaa pale chini kwa unyonge.
“Umezaliwa wapi?”
Swali lingine lenye utata lilimkabili Tusmo na kujikuta akilijibu kwa haraka huku akiogopa kipigo kutoka kwa yule askari aliyekuwa amejiandaa kwa kumshushia pigo jingine.
“Nimezaliwa jamuhuri ya watu wa kolo”
Jibu lile liliamsha vita tena vita kubwa sana kati ya polisi na Tusmo Sauti kali ya polisi yule kuwaita wenzake walio nje ilimtetemesha Tusmo na kusababisha kuzidi kutetemeka na kukumbwa na hofu zaidi. Askari wanne walifika na kusikiliza walichoitwa na mwenzao.
“Kweli Huyu ni muhamiaji Haramu”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kauli ya askari yule ilihamsha hali tofauti pale kituoni nihali ya kelele za kitu kupigwa kwa kushambuliwa huku sautiza maneno ya kashfa zikimshukia anayepigwa. Tuhuma za uhalifu kufanywa na wahamiaji haramu zilimshukia huku polisi wakishusha lawama wao ndio wanafanya kazi yao inakua ngumu. Kimya kimya kiltwala jasho likiwa linawatoka kila mmoja akiwa kashika kichwa na asijue ni kitu gani afanye, Harufu ya kesi ya jinaiilikua ikitanda eneo lile. Picha yaowakivua magwanda na kuwekwa katika sero inayotoa harufu kali ya mkojo na yenye chawa ambayo hutumia kuwaweka wahalifuka iliwajia katika eneo la taswira ndani ya ubongo wao. Kwa taharuki polisi aliyekua akichukua maelezo alijikuta akizunguka zunguka kulia na kushoto huku akiwashia wenzake lawama kwa kipigo kikali walichomshushia mtuhumiwa yule. Macho yake yakiwa juu ya mwili wa Tusmo uliokuwa umelala kimya pale chini bila kujigusa.
“Tusilaumiane hapa tushauriane nini tufanye”
Askari mmoja alijikuta akitoa ushauri uliowatoa wenzake katika mawazo ya nifanye nini.
“Jamani hichi ni kifungo mnaonaje tukaenda mtupa ziwani Tupoteze ushahidi bila hivyo tutafia gerezani”
Kabla wenzake hawajaongea chochote macho yao yakatua juu ya gari aina ya Suzuki kuu kuu iliyopaki nje ya kituo hicho kwa fujo.
“Tumekwisha..”
Askari aliyekuwa anachukua maelezo ya Tusmo alijikuta akitamka neno hilo kwa kukata tamaa.
****
Rajiv akiwa anajiandaa kukabiliana na mtu ambaye anamjia mbele yake huku akiamini ni kibaka, Sura ya upole iliyopambwa na Tabasamu pana ilimrudisha katika faraja na kujikuta akisubiri kijana huyo afike karibu na kukabiliana nae kwa chochote kitakachotokea.
“Rafiki usiwe na hofu mimi ni mwema kwako”
Jose B aliongea huku akijikongoa mpaka alipo Rajiv.
“Pole kwa matatzo yaliyokupata hao ndio polisi wa mwanza kama hujuani na mtu katika mji huu utateseka sana”Jose B alirusha kombora lake la kwanza lililomlegeza Rajiv na kumfanya akili yake kukimbilia kwa Jose B na kumuona kama malaika ambaye Mungu kamleta kaika kipindi muhimu.
“Sasa nitafanyaje Rafiki”
Jose B alifurahishwa na Swali la Rajiv.
“Usijali kwani una kitu kidogo hapo maana hao watuni wa kutlizwa na kitu kidogo tu tna mbele yangu mimi alwatan hata kama ana kesi ya mauaji lazima atoke tu”
Jose B alijitapa mbele ya Rajiv na kumfanya Rajiv kuvutiwa nae na kuhitji msaada wake kwa gharama yeyote.
“Pesa si shida ndugu yangu”
Sawa kama una pesa usijali mimi ndiye Jose B binadamu pekee niliyeshinda kifo katika mikono hatari ya wauaji”
Jose B aliendelea kujitapa mbele ya Rajiv.
“Inabidi Tuchukue Gari na sio Tax maana tukienda na Tax watatuona sisi ni Matajiri”
Jose B aliongea haraka haraka huku akiangalia huku na kule.
“Sasa gari tutapata wapi”
“Usijali uko na Jose B wa ukweli hapa kuna rafiki yangu ana suzuki ngoja nimpigie tupite huku”
Jose B alita jibu lililoleta faraja kwa Rajiv huku wakipita njia ya mkato na kutokea barabarani na tayari simu ilikua imekwishapigwa. Ndani ya dakika tano Gari iaina ya suzuki kuu kuu ilikua imepaki kwa mwendo wa haraka Jose B akafungua mlango na kuingia kisha Rajiv akafuatia na Gari kuondolewa kwa kasi.
****
Tabasamu alilotoa Karma lilitosha kabisa kurudisha amani ya Taylor Kurt, Ujumbe aliosoma Taylor kurt ulioingia punde kutoka kwenye namba ileile aliyopokea ujumbe wa tahadhari ulimkunjua sura yake kutoka katika woga na kumrudisha katika furaha ya awali.Akimpokea Karma kwa kumpa mkono na kumuwekea kiti vizuri tayari kwa maongezi. Karma akirekebisha Koo lake vizuri huku akimuangalia Taylor Kurt kwa furaha.
“Pole sana kwa ujumbe niliokutumia”
Karma alianza maongezi kwa taratibu
“Kwanini umenitisha vile”
“Nilitaka kujua kama unaweza kuniamini au la, Na pia nilitaka kujua kiasi gani cha woga ulichonacho”
Karma alitoa jibu lililozalisha kicheko kikubwa kutoka kwa Taylor Kurt huku akimnyoshea kidole Karma na kuchombeza maneno ya kumsifia kwa jinsi alivyo na akili.
“Laiti ningelikufahamu miaka miwili iliyopita ningekuwa na mafanikio makubwa sana katika Kampuni yangu”
Taylor Kurt alijikuta akisema maneno ambayo yalimuongezea ushindi Karma na kumfanya apange mashambulizi kwa mteja wake ambaye amepewa ahakikishe anaharibu mfumo wa biashara zake na maisha yake kwa ujumla.
“Vipi hali ya biashara kwa sasa?”
Karma aliuliza swali la kichokozi lililopokewa na Taylor Kurt kwa furaha na kujibiwa kwa usahihi kabisa
“Kweli Mafanikio hupangwa katika lugha ya mafanikio, Nimepata faida kubwa sana katika kipindi kichache, Nimepokea Oda nyingi sana mpaka kampuni inalemewa, Kiwango cha uzalishaji ni kidogo kulingana na Mahitaji mpaka nimeamua kuingia mkataba na kampuni ya China Agent ili waweze kutengeneza mzigo kwa wingi zaidi”
Karma alivuta pumzi na kushusha kisha akato bahasha nyeupe katika pochi yake na kuiweka mezani huku akimuangalia Taylor Kurt
“Ni eneo gani ambalo Umepokea Oda kubwa kwa wakati huu na bado hujalifikia”
“Nimepokea Oda kutka Afrika tena huko ndipo kwenye uhitaji zaidi mpaka kichwa kinanioma kwa fedha nitakazoingiza kutoka huko”
“Vizuri sana, Unafahamu kampuni ya CAM 2025”
“Ndio naifahamu si ile ya Camillah Hosein inayosaidia nchi za kiafrika?”
“Ndio, Je unajua mpaka sasa ina muda gani tokea ianze kusaidia Afrika na maana ya jina la kampuni hiyo”
“Ndio, Mpaka sasa ina miaka kumi na mbili na Maana ya jina hilo ni Camillah African Mother”
Karma alicheka sana mpaka machozi yakamtoka, Taylor Kurt alipatwa na mshangao kwa jinsi Karma alivyokuwa akicheka kupita kiasi.
“Mbona unacheka?”
“Kumbe na wewe ni kati ya watu wengi duniani wasiojua ukweli kuhusu Mama yule”
“Ukweli upi?”
“Hosian ni mume wa Camillah alikua akiishi Zimbabwe huko afrika na alikua akimiliki hekari nyingi za mashamba katika nchi hiyo. Shida ilitokea kupishana kwa maelewano kati yake na wafanyakazi wake ambao ni wazawa wa Kiafrika. Ugomvi huo ukasababisha kisasi ambacho kilipelekea kuteketezwa kwa nyumba yake akafia ndani akiwa na mtoto wake mdogo Cliff na wakati huo Camillah alikua Supermarket. Alipokua kairudi akakuta Watu wengi mbele ya nyumba yake huku Moto mkubwa ukiangamiza nyumba yao. Ndani kukiwa na mume wake mpendwa na Mtoto wake kipenzi Cliff.”
Taylor Kurt alijikuta akiingiwa na simanzi kubwa sana.
“Je unadhani kwa tukio hilo Camillah anaweza kuipenda Afrika”
“Hapana haiwezekani”
“Unahisi kwanini anasaidia Afrika na nchi ya kwanza kuanza kuisaidia ni Zimbabwe”
“Nafikir hapo kuna siri kubwa”
“Vizuri sana, Maana ya CMA 2025 ni Change African to Mental 2025”
“Sijakuelewa”
Taylor Kurt alivutiwa na mazungumzo yale na kujikuta akitaka kujua zaidi.
Karma akafungua ile bahasha akatoa kidonge kidogo kama tembe ya Piriton na kumuonyesha Taylor Kurt.
“Unajua hichi ni nini?”
“Hapana sijui ni kitu gani”
“Hichi ni kidonge kinaitwa HD yaani Heroid Deseas, Nii Dawa ya kulevya inayopandikiza ugonjwa wa uchizi katika ubongo wa Binadamu baada ya siku 365 baada ya matumizi”
“Mmh”
Taylor Kurt alijikuta akiguna na kupigwa na mshngao zaidi kwa yale anayoasikia”
“sasa Camillah anasambaza Vidonge hivi katka nchi za Afrika na vijana wengi wanavipenda sana kuvitumia na nia yake mpaka kufika mwaka 2025 Afrika nzima wawe Vichaa na anatumia fedha nyingi sana kukamilisha mpango wake”
“Lakini hiyo ni hatari sana akigundulika”
Taylor Kurt alijikuta akizungumza kwa wasiwasi huku akimuangalia Karma Machoni.
“Camillah ni mwanamke Tajiri sana na Marekani inamtegemea kama inavyokutegemea wewe hakuna nchiinaweza kubali Tegemezi lake likapotea analindwa kila mahali, Hakuna mzigo wake unakaguliwa ni sawa na wewe mzigo wako haukaguliwi sehemu yeyote Duniani.”
“Ooh ni kweli lakini”
“Je uko tayari kupat faida mara nne?”
Karma alimuuliza swali Taylor Kurt swali lililomzindua kutoka katika mawazo, Mawazo dhidi ya mwana mama Camillah.
“Faida mara nne? Hakuna mfanyabiashar yeyote duniani anaweza kataa hata muuza bagger hawezi kataa ofa hiyo”
“Sawa katka Parking yetu ya simu tunatenganisha batter na simu, Na kuna eneo ambalo hukaa Batter katika simu. Tunaweza tumia Eneo hilo kuhifadhi HD kwenda Afrika utalipwa Fedha nyingi mara dufu na Kampuni ya CAM 2025”
Taylor kurt alitaharuki na kusogea pembeni huku akitetemeka.
“Hapana bint siwezi fanya hiyo biashara kabisa, Sitaki kuingia katika matatizo katika maisha yangu TSiwezi kufanya hivyo”
Wakati Taylor Kurt akizungumza kwa jazba Karma alikua akitabasamu na sura yake kuongezeka uchangamfu zaidi.
“Taylor hii si vita ni mazungumzo t, Sababu wewe umekua Rafiki kwangu niliona nikushirikishe katka biashara hii ili usije sikia biashara anafanya Martin Cruez ukasema kwanini sikukwambia wewe ok Sahau tulichozungumza .”
Karma akarudisha kidonge katika bahasha huku Taylor kurt akiwa ametulia akimuangalia Karma, Karma akaoa simu yake na kubonyeza namba fulani kisha akapeleka sikioni na kusikiliza kwa sekunde kadhaa.
“Hellow Naitwa Karma natumai nazungumza na Martine Cruez”
Taylor Kurt alichukizwa na kitendo cha Karma kumpigia simu Martin Cruez mbele yake, Neno faida mara nne lilizunugka katika ubongo wake na kuona kasi ya Martine Cruez ya kumpita kwa utajiri itakavyokuwa. Uwezo wa Karma katika biashara ulimuogopesha zaidi na kupima mafanikio aliyoyapata kwa kipindi kifupi tokea aanze kufanya kazi na kampuni ya Karma. Alijikuta akikunja ngumi na kugonga meza kwa nguvu.
“Samahani kata simu ya huyo mpuuzi tuzungumze”
Taylor Kurt alijikuta akitamka kwa hasira.
****
Macho ya Afande aliokuwa mapokezi yaligongana na Macho ya Jose B wa Ukweli, Kumbukumbu za haraka wapi alimuona kiumbe yule zilisonga akili yake huku askari wengine wakipigwa na bumbuwazi wasijue nini cha kufanya. Askari mmoja aliyekuwa katika tukio la kumkamata Tusmo alichanganyikiwa zaidibaada ya kumuona Rajiv akitoka ndani ya lile gari huku akielekea katika kile kituo. Ujasiri aliofundishwa miaka kadhaa katika chuo cha polisi ccp huko Moshi ulimtoka na kujikuta akiruhusu mkojo kutoka pasipo kuvua nguo. Jose B kama kawaida yake aliingia kituoni kwa mbwembwe na kusalimia kwa uchangamfu huku akimuomba yule askari aliyesimama kaunta wakaongee pembeni. Hiyo ilikua nafuukwa askari yule pasipo kupinga alitoka kwa haraka na kumdaka Jose B mkono na kumvuta pembeni kabla kajafika karibu ili asione mwili wa Tusmo uliolala chini kimya.
“Afande nina shida si kubwa sana”
Jose B alianza kwa mbwembwe huku yule askari akimuangalia kwa makini.
“Subiri kwanza wewe niliwahi kukuona wapi?”
Yule askari aliuliza swali lililompa hofu Jose B wa ukweli na kujikuta akiishiwa na maneno huku akifikiri kuna tatizo litafuata kumkabili.
“Aah itakua hapahapa Mwanza”
“Oh nimekumbuka wewe si ulikufa tulikupakia kwenye Gari kule Dar ulichomwa na kisu?”
“Dah afande ni kweli ni story ndefu kidogo, unajua siku ile nilipochomwa kisu nilipoteza damu nyingi na mliponipeleka muhimbili nilipelekwa moja kwa moja chumbacha kuhifadhia maiti sasa wakati naandaliwa kuingizwa muhudumu wa chumba kile aligundua bado nipo hai ndipo akamuita Dokta na wakanitoa na kunipatia huduma ya kwanza, Kule Dar hakuna anayejua kama mimi ni mzima ila Mungu ndiye anayejua hata familia yangu hawajui chochote kuhusiana na tukio la mimi kusadikiwa kufa dar”
Jose B alitoa Maelezo yaliyomshangaza yule askari huku Akionyesha kovu la kisu.
“Pole sana”
“Ah ndio maisha, Sasa afande kuna mwanamke yupo hapo kituoni kaletwa muda huu naomba msaada aachiwe nitakutoa”
Kabla yue askari hajajibu mara akasikia sauti akiitwa na wenzake akamuacha Jose Bna kukimbilia kule kituoni. Alipofika alikuta Tusmo kaamka akipepesa macho huku na huko. Jose B akafika huku akiendelea kuomba msaaa kwa yule askari.
“Kijana hii ni kesi ya uhamiaji huyu ni muhamiaji haramu”
Rajiv alisikia ile kaulina kusogea kisha akaongea kwa sauti iliyojaa uchungu.
“Huyo ni mke wangu na mimi ni mtanzania”
“Mkeo mmefunga ndoa”
Askari mmoja aliuliza swaliambalo lilijibiwa na Rajiv kishujaaa
“Ndionacheti cha ndoa hichi hapa”
Rajiv alitoa cheti cha ndoa alichokihifadhi katika mfuko wakewa suruali alichopewa muda mchache baada ya kufunga ndoa msikitini. Yule askari alikiangalia akaguna.
“Mh muachieni tu huyo mwanamke kwa mujibu wa sheria ni mke halali wa huyu bwana na kwa kuwa bwana ni mtanzania na yeye nimtanzania pia”
Yule askari alitoa jibu lililozalisha tabasamu katika sura za watu wawili, Jose B wa ukweli na Rajiv Roshan.
Tusmo akisimama kwa taabu na kumkimbilia mume wake wakakumbatiana,Joto la mahaba likamchoma Rajiv na kusahau kama wako nje ya kituo cha Polisi.
****
Maghala yalikua yakinunuliwa katika nchi mbalimbali za afrika, Yakiwa yamezungushwa ukuta mrefu na waya zenye umeme kwa ajili ya usalama huku katika ukuta kukiwa na maandishi makubwa American Bussiness Solution. Magari yenye kontena kubwa yakiwa yanapishan akuingika katika kila ghala kwenye nchi mbalimbali za Afrika. Vijana waliovalia Ovaroli za rangi ya kijani yakiwa na maandishi meupe yaliyoandikwa Neno STAFF mgongoni walikua na kazi moja tu kupakua mzigo wa mabox makubwa yenye simu na kuingiza ndani ya Ghala. Wasichana wazuri waliokuwa wamekaa katika mabenchi marefu huku wakiwa wamevaa magauni marefu yasiyo na mifuko mkononi wamevaa Gloves za rangi nueupe. Kaz yao ilikua ni kutoa Vidonge vya HD katika eneo la kuhifadhia batter na kuziweka katika mabox maalum. Kampuni ya American Bills Security ilikua ikihakikisha inaweka ulinzi wa kutosha eneo hilo huku kamera zikiwa kila mahali na chumba maalumu chenye kompyuta na tv nyingi kukiwa na wazee wanne wa makamo wakifuatilia kila kinachofanyika. Ni mwanamama Camillah ndiye aliyewezesha kazi hiyo kufanyika kwa makini zaidi na kwa usahihi huku akihakikisha analipa mshahara mzuri kwa watendaji wa kazi hiyo ili kwenda sawa. Hasira aliyokuwa nayo dhidi ya waafrika akikumbuka kifo cha mume wake Hosain hasira ilimpanda zaidi.
Serikali za nchi zilizopata nafasi ya kujengwa kwa maghala ya American Bussiness solution ikiwemo nchi ya Tanzania zilijivunia sana kwa kampuni hiyo kupendekeza maghala hayo kujengwa katika nchi zao, Ukiondoa kodi inayoingia katik nchi hizo suala lililowafurahisha ni ajira kwa vijana zilizotolewa nakampuni hiyo huku wakilipwa mshahara kwa kiwango cha mshahara wa Marekani. Vidongevya HD vilianza kusambazwa nchini Afrika huku vijana wengi wakiwa wanachangamkia. Pombe aina ya Spirite ambay ilifungwa katika paketi na kuuzwa kwa bei nafuu ilikuwa ni pombe maarufu sana nchini tanzania. Viana wengi waliifurahia na kununua kila dakika. Ni pombe hiyo ndiyo iliyotumika kuwekwa vidonge vya HD na kuwa ni moja ya njia Rahisi kuwanasa vijana japokuwa hata wazee n kina mama walichangamkia pombe hiyo bila kujua nini kilichopo ndani yake. Mauzo makubwa ndiyo yaliyomfurahisha Camillah kuku akifurahia lengo lake kutimia kwa muda mfupi ndani ya nchi ya Tanzania.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“KONTENA LA POMBE KALI ZA PAKETI ZENYE DAWA LAKAMATWA TANZANIA”
Ni kichwa cha h bari katika Gazeti la Kanjanja gazeti maarufu nchini Tanzania, Watu wengi walikua wakiangalia Gazeti hilo nyakati za asubuhi katika vibanda mbalimballi vya wauza magazeti. Wakati hayo yakiendelea ndani ya Ofisi iliyo ndani ya Ghala la American Bussiness Solution kulikua na kikao kizito wazee wawili walikua wakiongea na mwanamama Camillah kupitia mtandao wa Skype. Hasira za mama huyo juu ya kukamatwa kwa kontena hilo zilionekana dhahiri. Maamuzi ya Camillah kusafiri haraka na kuja nchini Tanzania kuweza kuhakikisha habari hiyo inakanushwa ikiwezekana na Waziri wa Afya wa Tanania. Hakutaka kuona kiumbe yeyote anakwamisha mpango wake wa kuiteketeza Afrika. Ndege yake kubwa aina ya Boeng C 456DD ilikua ngani tayari kuitafut Tanzania kwa ajili ya kuzima habari inayozidi kusambaa kama Moto wa kifuu.
****
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment