Search This Blog

Sunday 20 November 2022

KASRI YA MWINYI FUAD - 2

 

    Simulizi : Kasri Ya Mwinyi Fuad

    Sehemu Ya Pili (2)





    Watu walikuwa wakiingla na kutoka ndani ya kijumba hicho na wengi kwa namna walivyovalia walionyesha ni watu waliotoka sehemu za mashamba kama yeye Vuai.



    “Ati Bwana, mtu anaweza kuonana na nani hapa akiwa na tatizo lo lote?” Vuai alimwuliza mtu mmoja aliyetoka ndani ya kijumba kile.



    “Una shida? Je, ushafukuzwa shambani nini?” aliuliza yule mtu.



    “Si hayo, ni mengine kabisa,” Vuai alijibu.



    Hakutaka kumwambia mtu ye yote yale aliyokuwa nayo moyoni ila tu kwa yule aliyehusika.



    “Ingia hapo ndani mkono wa kulia utaona mlango. Ing’’a humo na utamkuta mtu na huyo utaweza kumwelezea shida zako,” alisema yule mtu.



    “Ahsante Bwana.”



    Yule mtu alikwenda zake na Vuai aliingia ndani ya kile kijumba. Aligonga mlango na alipata amri ya kuingia ndani. Alifungua mlango na mbele yake alimkabili kijana mmoja aliyekuwa amekaa juu ya kiti na meza mbelc yake. Alikuwa anashughulika na kuandika hata hakumtazama yule aliyeingia ndani.



    Baadaye yule kijana aliinua uso wake akamwona Vuai amesimama miangoni.



    “Karibu ndugu,” alisema yule kijana.



    Alimkaribisha kukaa juu ya kiti kimoja katika viti vilivyozungushwa chumbani mle na mara yule kijana alianza kumsaili Vuai.



    “Je, naweza kukusaidia ndugu?” aliuliza yule kijana.



    “Bwana shida yangu niliyo nayo ni ndogo tu,” alianza. Vuai.



    “Kwanza ndugu napenda uelewe hapa hapana ‘Bwana’. Sisi sote ni ndugu; ndugu tulioungana kuwapiga vita mabcpari na mabwana shamba,” yule kijana alimwambia Vuai.



    “Ahsante Bwana nimesikia, “alijibu Vuai.



    Alikwisha zoea kumwita ‘Bwana’ kila aliyemhisi amemzidi, kwani alikuwa ameishi kwa mamwinyi siku nyingi na alikwisha zoea kumtetemekea kila mtu. Yule kijana aliyaelewa haya na alimwacha aendelee kumwita Bwana ijapokuwa yule kijanamwenyewe hakupenda.



    “Mimi Bwana natokea Koani, nafanya kazi katika shamba la Bwana Fuad. Mara nyingi nahudhuria mikutano inayofanywa hapa mjini na mimi na wenzangu wa huko Koani tuna mambo fulani hatuyafahamu.”



    “Umefanya uzuri kuja,” alianza yule kijana. “Sisi tunawatafuta hasa watu kama nyinyi ambao wana mambo hawayafahamu na wanataka kufahamishwa; kusema kweli hukukosea kuja hapa kwani hayo ndiyo madhumuni ya ofisi hii...” yule kijana alimwelezea Vua.



    “Umesema uko shambani kwa nani vile?”



    “Kwa Bwana Fuad.”



    “Fuad! Fuad! Fuad!” yule kijana aliendelea kulitamka jina la Fuad kama kwamba linamkumbusha kitu. “Aha” Fuad! Tunazo habari. zake hapa. Hebu ngoja kidogo.”



    Yule kijana aliondoka pale juu ya kiti alipokuwa amekaa na kwenda kwenye kabati kubwa lililokuwa hapo penye pembe ya meza. Alitoa bunda la makaratasi na kuanza kuyapekua.



    “Aha, Fuad, ndiyo! Tunazo habari zake hapa. Bwana shamba huyu aliwahi kutaka kumkamata kwa nguvu msichana mmoja aliyekuwa akifanya kazi shambani mwake.” alielezea yule kijana. “Huko shambani mnakofanya kazi hapakuwa na msicbana mmoja aitwaye Mariam?”



    “Mariam? Yeye alikimbia siku moja, nafikiri alitaka kupigwa na Fuad, mana’ake siku hiyo alipokimbia alianza kutolewa maneno na kutukanwa na Fuad,” alieleza Vuai.



    “Basi ukweli wa mambo ni kwamba alitaka kumkamata na kumnajisi ndiyo maana akakimbia.”



    “Hivyo?” aliuliza Vuai akistaajabu sana.



    “Sasa sikiliza. Wenzako ulio pamoja nao huko shambani kwa Fuad ni watu madhubuti au ndio hivyo tu?” aliuliza yule kijana.



    “Wako waliokuwa madhubuti na wako ambao si barabara.” alijibu Vuai.



    “Sasa mambo gani hasa mnataka kuyajua, wewe na weozako?”



    “Sisi tunataka kuyajua mambo yote ambayo tunayasikia kuhusu maisha yetu sisi wakulima,” Vuai alisema.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    “Sikiliza, nenda ukaonane na wenzako uwaambie kuwa maisha ya wakulima yatabadilika Fuad akitaka asitake. Vile vile ilawa mnaweza kufanya mipango minu naweza kuja huko huko Koani ili kuzungumza na watu wa huko kwa jumla. PeDgine hilo litakuwa jambo la maana zaidi.”



    “Anasema Fuad akitaka asitake maisha yetu yatabadilika,” Vuai aliwaeleza wenzake waliokuwa wakimsikiliza kwa makini walipokuwa wamekaa pale barabarani, usiku, wakizungumza.



    “Akitaka asitake namna gani: kwa nguvu?” aliuliza mkulima mmoja.



    “Sijui kama kwa nguvu au kwa hiari, mimi kaniambia Fuad akitaka asitake maisha yetu yatabadilika.”



    “Ah, mambo ya ajabu hayo,” alisema yule mkulima.



    “Hata mimi naona ajabu!” alitilia mkazo mkulima mwingine.



    Mazungumzo ya akina Vuai na wenzake yalikuwa yamebadilika kabisa. Hawakuwa tena wakizungumza habari za ngoma na wanawake wazuri. bali kila walipokutana walikuwa wanazungumza matatizo muhimu kuhusu maisha yao.



    Fikra za Vuai zilibadilika kabisa. Aligeuka kuwa ni mwalimu wa kuwasomesha wenzake juu ya maisha na wapi ulimwengu unakoeodea. Kuna waliokubaliana naye na kuna wale ambao hawakuamini aliyokuwa akiyasema. Hata hivyo, hakukasirika hata kidogo na wale wasiokubaliana naye. Aliamini kuwa kila mmoja katika wao alitaka mabadiliko katika hali ya maisha yake. Kila mtu alikuwa amekwisha choka na mateso ya mabwana shamba.



    Huko mjini mambo yalikuwa ya moto kwani habari za vishindo walivyokuwa wakivifanya wafanyakazi ziliwafika akina Vuai na wakulima wengineo wa sebemu mbali mbali za Unguja.



    “Sasa lazima tufanye mpango yule kijana aweze kuja hapa ili aweze kuzungumza nasi,” alisema Vuai katika mazungumzo yao hapo barabarani.



    “Vipi ataweza kuja huku na kuonana nasi? Bwana Fuad siku hizi kawa mkali zaidi kuliko zamani.” Alisema mkulima mmoja.



    “Tutafanya mipango. Hivyo Fuad mmoja ndiyo anaweza kutushinda sisi aote kwa akili?” Vuai aliuliza.



    “Mipango gani? Hapana hata mmoja kati yetu mwenye pahala penye nafasi ambapo tutaweza kukutana na huyo kijana.



    “Nafasi ni kitu cha kutengenezwa. Muhimu tukubaliane tu. Na nafikiri haina haja ya kujificha kwani Fuad mwisho atayajua tu haya, na sidhani kama kuna haja ya kumwogopa.” Vuai aliwaelezea wenzake.



    “Si suala la kumwogopa lakini sharti tuchukue hadhari mana’ake tukifukuzwa hapa...”



    Kabla yule mkulima mwinginc aliyekuwa akisema kumaliza maneno yake Vuai aliyakatiza kati kati.



    “Sikiliza Umari. wenzetu kadha wa kadha kutoka sehemu mbali mbali washafukuzwa na mpaka leo wanaishi. Mimi nafikiri madhalitumedhamiria kulifanya jambo natulifanye haidhuru kitokee cho chote. Tahadhari ni lazima kuchukua kwani haina haja ya kufanya mambo kiendawazimu; lakini kikitokea kitu hatuna budi kukikabili.



    “Basi tumwite huyo kijana. Tutafanya kila njia ili tuweze kukutana naye ijapokuwa mwituni,” alisema Umari. “Sasa lini utakwwenda tena mjini?” aliuliza.



    “Kama kawaida, akitoka tu Fuad kwenda kuuza karafuu na mimi nitaondoka....”



    Siku ile Fuad alirejea kutoka mjini saa sita za usiku amelewa chopi. Aliliendesha gari mbio na alipofika hapo kwake aliiliza honi ya motokaa yake kwa makelele na kila mmoja aliamka lakini hapana aliyemjali.



    Huko mjini wakati alipokuwa bar akilewa, alisikia mazungumzo mengi kuhusu kikundi cha walu waliodhamiria kuwapia mabwana shamba. Maneno haya yalimkera sana na alikula yamini kwamba yuko tayari hata kumwua ye yote atakayelota habari kama hizo shambani kwake.



    Makelele ya honi ya gari lake hayakumshughulisha mtu isipokuwa Kijakazi aliyekatiza usingizi wake na kuja mbio kumsikiliza Bwana wake mpenzi. Alikwenda mpaka lilipo lile gari na kumkuta Fuad yumo ndani amekaa humo mlango ameufungua. Aliinyemelea ile gari kidogo kidogo lakini mara aliisikia sauti ya kilevi ya Fuad ikiuliza,



    “Unataka nini hapa saa hizi?”



    “Ah! Bwana, nimekuja kukusikiliza; nikifikiri umefikwa na jambo!” alijibu Kijakazi kwa sauti ya hofu.http://pseudepigraphas.blogspot.com/



    “Ha! ha!” alicheka Fuad kwa sauti kubwa na kusema.



    “Hata nikifikwa na jambo utafanya nini kizee kama wewe. Toka hapa nenda zako, mpumbavu mkubwa we!”



    Kijakazi aligeuka upesi upesi na kurejea alikotokea lakini mara aliisikia sauti ya Faud ikiita tena.



    “Lakini hebu njoo!”



    Kijakazi alirejea tena kwa Fuad na mara Fuad alianza kumwuliza.



    “Mkongwe yuko wapi.”



    “Nafikiri amekwisha lala Bwanal” alijibu Kijakazi.



    “Mmm! Basi nenda zako.”



    Fuad alitoka garini akafunga milango yote halafu akakaa hapo kwa muda kidogo ak’liegemea, Siku ile ulevi wake ulimwelekeza kwa Mkongwe na kutoka hapo alikwenda mpaka lilipokuwa banda lake.



    Hakubisha hata hodi alipofika hapo. Aliusukuma mlango wa kumbesa uliokuwa umezuiliwa kwa kisiki cha mti. Mkongwe alishituka na kuruka kutoka pale kitandani alipokuwa amelala akipiga makelele.



    “Mwizi! Mwizi! Mwizi!”



    Usiku ulikuwa mkubwa na kelele za Mkongwe ziliweza kusikilizana mbali.



    Watu walitoka vibandani mwao kila mtu na silaha yake mkononi, mwenye panga. mwenye mngu, mwenye mtalimbo au silaha yo yote aliyoweza kuipata. Wote waliloka nje na kuelekea kule yalikotokea yale makelele.



    “Yuko wapi huyo mwizi!” walianza watu kuulizana.



    Mara walisikia sauti ya Fuad ikijibu, “hakuna mwizi! Mwizi gani atakayethubutu kuja shambani kwangu. Huyu Mkongwe anataka kukuhangaisheni tu.”



    “Ala, Bwana Fuad! Mbona saa hizi uko huku?” aliuliza Vuai aliyekuwamo katika kundi lililokwenda kumkamata mwizi.



    “Haya nendeni mkalale, upesi!” Fuad aliamuru.



    Fuad hakuwahi kulifanya alilotaka kulifanya na aliona bora arejee nyumbani kwake akalale kwani nishai za ulevi zilikuwa zinamzidi.



    Mkongwe hakulala kucha usiku ule. Alidhani Fuad angerudi tena saa yo yote ile lakini kwa bahati hakuja tena.



    Ilipofika asubuhi kila mtu aliendelea na kazi yake kama kawaida na minong’ono ya hadithi ya Fuad ilitapakaa kote. Kwa Vuai hayakuwa mapya kwani alikwisha kuambiwa yale aliyotaka kumfanyia Mariam. Wafanyakazi wa shambani kwa Fuad hawakuonyesha kama walishughulishwa na mambo ya Fuad lakini kila mtu alikuwa na lake moyoni.



    Fuad hakutahayari wala kuona vibaya kwa yale aliyoyafanya kwani hakuwajali bata kidogo wote wale waliokuwa wakiishi shambani kwake Alihisi anaweza kufanya jambo lo lote bila ya kujali cho chote. Bali, hakuhisi tu alifanya hasa mambo mengi ya utovu wa adabu.



    Vuai na wcnzake walitayarisha mipango madhubuti ya kumwita yule kijana kutoka mjini ili aje kuzungumza nao. Walijaribu kutafuta pahala lakini mwisho waliona wakutane pale pale barabarani wanapofanyia baraza lao la kawaida nyakati za usiku. Waliamini kwamba hapana ye yote ambaye angewatilia shaka akiwakuta pale.



    Kiasi cha saa mbili za usiku yu’e kijana alifika Koani, Baada ya kupatafuta kidogo tu pale alipoelekezwa na Vuai, aliwakuta watu kiasi ya kumi wamekusanyika barabarani wanamngojea. Hawakuonyesha kama wanamngojea mtu, na adui ambaye angetokea ghafla angelifikiri walikuwa katika mazungumzo ya kawaida tu kama ilivyo desturi ya washamba kukaa barabarani na kuzungumza.



    Yule kijana alifika hapo kwa baskeli yake na baada ya kufika tu aliiweka pembeni. Alivalia kama wanavyovalia wakulima wengine ili asijulikane kama yu mgeni.



    Vuai alikuwa wa kwanza kumtambua yule kijana. Alirakaribisha na wote wakakaa kwenye pembe ya barabara.



    “Je, ndugu habari ya hapa?” aliuliza yule kijana.



    “Habari za hapa nd’o kama tulivyokwisha kuzungumza Bwana,” alijibu Vuai.



    “Kama mnavyojua, mimi m mjumbe kutoka huko mjini. Nimeletwa kwenu na ndugu zenu baada ya huyu ndugu kuja kuonana na sisi,” alisema yule kijana huku akimwonyesha kidole Vuai.



    “Mimi jina langu Vuai.”



    “Ala! Mimi naitwa Marijani,” alisema yule kijana.



    “Basi Bwana Marijani nd’o kama tulivyokwisha zungumza huko ofisini kwako. Sisi tunakusubiri hapa kwa hamu kubwa na siku ya leo ni siku ambayo tumeisubiri siku nyingi. Wenzangu wana mengi wanayotaka kujua, kwa hiyo, baada ya kuwazungumza nafikiri bado watakuwa na maswala mengt ya kukuuliza.”



    “Sikilizeni,” alianza Marijani, amezungukwa, amewekwa kati kati kila mtu ana hamu ya kumsikiliza atasema nini. “Shida mlizo nazo nyinyi nd’zo shida walizo nazo wakulima wote nchini. Kuna wengine, shida zao zimezidi zenu kwani wao washafukuzwa mashambani. Mimi mwenyewe kwetu ni shamba, kule Donge, na ijapokuwa sasa naishi mjini wazec wangu bado wako huko huko na nawatembelea kila wiki. Kwa hiyo, matatizo yenu nayaelewa vizuri.”



    “Lakini Bwana...” alisema mkulima mmoja lakini mara Marijani alimkatiza maneno yake.



    “Sikilizeni tafadhali msiniite Bwana, Mimi ningelipendelea mniite ndugu, man’ake naona fahari zaidi kuitwa hivyo.”



    Marijani aliendelea na maneno yake. “Sisi tuna mipango madhubuti kuhusu maisha ya wakulima kwa jumla Si kama tunataka kukudaeni kwa mabwana shamba halafu wao wakuoneeni huruma, hasha. Wao hawana huruma, na haina maana kuzitaka huruma pahali zisipokuwa. Tuna mipango mizuri zaidi ya hapo baadaye, lakini habari hii tutazungumza tukisha fahamiana vizuri. Jambo muhimu ambaio napenda mlijue ni kwamba wakulima wote waliofukuzwa mashambani washapata ardhi na wanaendesha maisha huko na kila atakaye fukuzwa kutoka kwa bwana shamba atapatiwa ardhi ya kumtosha.”



    Wote walikuwa wakisikiliza kwa hamu, wamemfumbul’a macho ili wamwone katika giza lililokuwa limetawala usiku huo. Kimya; mara moja moja tu ilisikika sauti ya bundi au ya komba, wakiimba baada ya kunyvva tembo. Marijani pekee ndiye aliyekuwa akisema. Kila alipopita mtu kwenye mkutano wao wa siri Marijani aiikatisha mazungumzo yake mpaka mtu huyo atoe salam, ajibiwe na aende zake.



    “Mnajua ndugu; sasa sina budi niondoke nirejee mjini mana’ke wakin.’ona napita usiku huu pale polisi Mwera wataanza matala yao,” Marijani aliwaambia wenzake.



    “Nani hao walakaokufanyia matata?” aliuliza Vuai.



    “Askari wanatutabisha sana, lak’ni haidhuru!”



    “Basi ye yote katika nyinyi akipata nafasi anaweza kupenya na kuja mjini siku yo yotc ile,” alisema Marijani huku akiwashika mikono na kuaga.



    Marijani na Vuai walikutana tena na tena hapo Kijangwani na walipanga mipango mingi. Kila alilozungumza na Marijani, Vuai aliwaarifu wenzake na mahusiano kati ya ofisi kuu ya wakombozi wa wananchi yalikuwa mazuri.



    Haya yote yalifanyika kwa siri bila ya Fuad kujua. Si kama kwamba hakuielewa ile chuki iliyokuwapo kati ya wakulima na mabwana shamba katika nchi kwa jumla. Aliloshindwa kufikiria tu ni kwamba lingekuwapo vuguvugu la mwamko wa wakulima na zaidi ya hivyo kwamba hilo vuguvugu lingewakumba hata watwana wale shamban’ kwake.



    Baada ya mwezi tu tokea Marijani kuonana na kikundi cha wakulima wa huko Koani, wakombozi wa wananchi walitangaza kuwapo kwa mkutano mkubwa hapo hapo Kijangwani mbele ya ofisi yao. Siku hiyo Fuad naye alikuwa na safari ya kwenda mjini, sio kwa sababu ya kuhudhuria mkutano huo, bali kwa sababu ya kufuatia starehe zake.



    Vuai hakutaka fursa hiyo impite na alifanya kila jambo ili afike. Baada ya Fuad kuondoka alijitahidi kutafuta gari lakini hakufanikiwa.



    Kwa kawa’da Magari mengi yalikuwa yakipita nj’a hiyo ya Koani lakini siku hiyo bahati ilikuwa mbaya haikutokea gari yo yote kwa muda mrefu. Vuai aliupiga mguu na hakupata gari mpaka baada ya kutembea maili nne na kufika pale Ms’kit’makufuli. Alipofika Kijangwani alikuta watu washaanza kukusanyika. Wengi wao walikuwa wamevaa nguo chafu; dalili ya kuwa walitokea makazini na hawakuwahi kufika majumbani kwao.



    Mkutano ulikuwa wa kusisimua na wakati ulipita b la ya Vuai kutanabahi kwamba anatarajiwa kurudi Koani kwa haraka. Mkutano ulimalizika saa kumi na mbili magharibi na hata baada ya kumalizika Vuai alibaki hapo hapo na kuzungumza na watu aliokwisha kujuana nao kwa kuja kwake sana hapo Kijangwani.



    Hata alipotanabahi, ilikuwa saa moja na nusu usiku na hapo Vuai alianza tena kuutwanga mguu kurejea shamba. Mara hii alikwenda kwa mguu kitambo kirefu na usiku ulimkuta njiani. Alipofika hapo karibu ya Mweia, kwa mbali aliziona taa za motokaa zilizomulika mwanga mkali. Alikata shauri kuisimamisha tu hata ikiwa gari ya nani.



    “Ho! Ho! Ho!” Vuai alilipigia kelele lile gari lilipofika karibu yake.



    Ama siku hiyo kweli ilikuwa ni siku ya bahati mbaya kwa Vuai. Gari lile lilikuwa la Fuad! Kwa bahati mbaya zaidi Fuad alisimama kwa jeuri akitaka kujua ni “mbvva” gani yule aliyethubutu kumsimamisha. Alikuwa amelewa lakini si sana na aliweza kuzungumza na mtu bila ya ulevi wake kutambuliwa ila labda kwa yule anayeijua harufu ya ulevi.



    “We nani wewe?” aliuliza Fuad baada ya kusimamisha gari yake.



    Ilikuwa kiza. Fuad hakumwona vizuri Vuai. Dimbidi atoe kichwa nje ya gari kumwangalia aliyemsimamisha.



    Vuai alikwishaitambua gari ya Fuad. Lo, hakuwa na hila yo yote ya kufanya ili asitambuliwc.



    “Wewe unafanya nini huku saa hizi?” aliuiiza Fuad kwa hamaki.



    Vuai aliduwaa kimya. Hakuwa na la kujibu wala bakuweza kuzua uwongo wo wote ule ambao ungelimnusuru.



    “Ala, kumbe ndiyo desturi yenu hiyo; tutaonana.”



    Fuad aliliondoa gari lake ambalo alikuwa hakulizima moto alipokuwa akizungumza na Vuai na kumwacba pale pale.



    Vuai hakusitushwa na maneno ya Fuad na baada ya hapo aliamua kutembea taratibu tayari kulikabili lo lote litakalomtokea. Haukupita muda baada ya Fuad kupita alitokea mwenye baiskeli na Vuai akamwomba amsaidie. Huyu bwana mwenye baiskeli alikubali akampakia kwenye kibao cha nyuma na kumchukua mpaka Koani ambako alimkuta Fuad amekwisha kwenda zake kulala.



    Usiku ule Vuai alirejea nyumbani amechoka. Hakwenda barazani ijapokuwa wenzake walikuwa wakimngojea kwa hamu kubwa. Hakusimama po pote ila alifululiza bandani kwake kwenda kupumzika.



    Fuad alikuwa si mpumbavu wa kuelewa basira za wakulima zilivyo dhidi ya mamwinyi na alikuwa na hakika kwamba ile haikuwa mara ya kwanza kwa Vuai kutoroka shambani kwenda mjini.



    Kitendo cha Vuai kilimkasirisha sana na alikichukulia kuwa ni utovu wa adabu mkubwa kwa Vuai kutoroka. Joto la moyo lilimpanda na usiku kucha hakulala kila alipofikiri kwamba hata wapagazi wake sasa hawana woga na wanathubutu bata kutoroka. Baada ya kupambazuka Fuad alitoka na gari lake mpaka mjini. Aliranda mjini na kuangalia mandhari ya asubuhi na alipofika kiasi cha saa tatu alifika Darajani.



    Alilisimamisha gari lake mbele ya jumba kubwa la kizamani lililotengenezwa vizuh.



    Chini ya jumba hilo walionekana watu wakiingia na kutoka. Pembeni ya mlango wa jumba hilo palikuwa na meza na kijanaaliyekuwa amekaa nyuma ya meza hiyo alikuwa amezongwa na watu kadha wakimpa pesa na yeye akiwaandikia hati za stakabadhi.



    Alipofika tu mlangoni Fuad alikabiliana na mtu mmoja aliyevalia vizuri. Alikuwa amevaa kofia ya mkono, iliyokaa vizuri juu ya kichwa chake, koti zuri la lasi na kanzu ya dorya.



    “Salam alaikum,” Fuad alimsalimu yule mtu.



    “Alaiku musalam, khabari za asubuhi?”



    “Nzuri,” alijibu Fuad huku akionyesha mwenye haraka.



    “Je, Bwana Marejebi nimemkuta?”



    “Sasa hivi nilimwona hapa,” alisema yule mtu huku akiangaza huku na huku kama kumtafuta yule aliyeulizwa. “Hebu mtazame juu; labda amepanda huko,” aliendelea.



    Fuad pale pale alipanda juu na kwa haraka aliyokuwa nayo alipanda ngazi mbili mbili. Alipofika juu alimwuliza mtu wa kwanza aliyekutana naye na mtu huyo alimpeleka mpaka ofisini kwa Bwana Marjebi. Fuad aligonga mlango, akakaribishwa, na kuingia ndani.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Alimkuta Bwana Marjebi ameuziba uso wake gubi gubi kwa gazeti alilokuwa akilisoma. Alikuwa amekaa juu ya kiti cha kuzunguka, akijizungusha huku na huku. na huku akisoma gazeti lile.



    “Salam alaikum,” Fuad alimsalimu Bwana Marjebi aliyekuwa bado amejigubika kwenye gazeti kama kwamba hakusikia mtu akiingia ofisini mle. Bwana Marjebi alijifunua lile gazcti na alipomwona Fuad alisema kwa Furaha, “Ah, ya Bin Malik!”



    Aliliweka lile gazeti juu ya mcza kubwa iliyokuwa mbele yake na kujitandaza zaidi juu ya kiti chake cha kuzunguka.



    Meza iliyokuwa mbele yake ilikuwa inang’ara na imepambwa kwa mabuku makubwa yaliyopangwa vizuri katika kila pembe ya meza ile. Katikati ya mabuku yale palikuwa na kidau kizuri cha wino na kalamu ndcfu iliyotoswa ndani ya kidau kile.



    “Unasemaje Bin Malik? Leo naona umetamani kuja kututembelea ofisini kwetu; karibu kaa kitako.” Bwana Marjebi alimkaribisha Fuad kukaa juu ya kiti k’moja ya viti viwili vilivyokuwa mbele ya meza ile.



    “Ahsante Bwana, ahsante.”



    “Je, nini khabari Bin Malik? Sikupata kukuona hata siku moja ofisini kwetu; je, kumezidi nini tena leo?



    “Khabari Bwana Marjebi, nimekuja, nataka unieleze khassa, mana’ake hawa ...” Fuad alisita kidogo na kumtazama Bwana Marjebi huku akitafuta neno la kusema, “ng’ombe hawa, nisameh Bwana Marjebi sijakusudia kutukana mbele yako, lakini sina vingine vyo vyote vya kuwaita ila hivyo - hawa siku hizi wamekuwa hata hawaogopi”



    “Nani tena hao wanaokushughulisha akili yako,” aliuliza Bwana Marjebi huku akiichezeachezea tai iliyomkaba vizuri rohoni.



    “Si hawa wanaojidai, sijui, wakombozi. Jana nimemkuta mpagazi wangu mmoja anatoka mjini kwa miguu. Nafikiri alikuwa anatoka huko huko kwa hao wakombozi. Sasa naona Bwana Marjebi mambo yamezidi hata hawaogopi tena. Alla - izza, hata vile vitwana vya shambani kwangu vimekuwa haviogopi. Zamani ilikuwa hathubutu kuondoka mtu kwenda hata hatua mbili bila ya amri yangu. Ati nasikia wanadai usawa - usawa gani wanataka hawa? Hata Mungu hakuumba vidole sawa. Hawa, Wallahi...”



    “Sikiliza Bin Malik,” Bwana Marjebi alianza kumtuliza Fuad aliyekuwa kahamaki. “Hawa watwana wasikushughulishe akili yako; wamoja havai mbili. Wao washajaaliwa kuwa nyuma, watakuwa nyuma maisha yao. Wakombozi, wakombozi, wakikomboe nini hawa. Hawana lao jambo. Ati wanataka wapewe nchi waongoze! Unafikiri wana wanaloliweza hawa; hawawezi cho chote,” Bwana Marjebi alisema kwa hasira. “Wewe Bin Mal’k unafikiri Mwingereza mpumbavu awape nchi wale wapumbavu waiongoze. Uchaguzi tushawashinda; uhuru tunautia mkononi tarehe tisa Disemba; usitie wasi wasi wo wote - Chama cha Raiat-el-Sultani kiko imara hapana khof,” Bwana Marjebi alisema na kumtia moyo Fuad, lakini pale pale aligeuza sauti yake na kuuliza huku akitabasamu



    “Kwanza mchango wa sherehe za uhuru ushatoa?”



    “Bado Bwana, lakini azma n’nayo.”



    “Basi. la-takhaf bin Malik, nenda zako kafanye kazi zako. Ukimwona yo yote katika hao wapagazi wako anajidai kutaka kuwa mkombozi, naye mfukuzilie mbali tu.”



    “Ahsante, ahsante, Bwana Marjebi; na kesho nikijaaliwa nitaleta mchango wa sherehe za uhuru.”



    “Tena usiwache kuleta, babu-el-hadid peke yake kaleta shilingi alf.”



    “Stoacha Bwana. Haya fi-amani-llah”



    Fuad aliondoka pale akiwa mwingi wa furaha. Angelionekana mwendawazimu tu kama si hivyo, angelipiga chereko pale pale. Alishuka chini mbio moja kwa moja mpaka ndani ya gari yake akaitia moto na kuirejesha nyuma mbio, na baada ya kuigeuza, hakusimama mpaka Koni.



    Siku ile hakutaka kuzungumza na mtu, kwani aliona akifanya hivyo ataichafua furaha yote aliyokuwa nayo moyoni.



    Asubuhi ya siku ya pili Fuad aliamka mkali kuliko kawaida yake. Alip’ga makclele na kutukana ovyo. Haya yalikuwa matayarisho ili atakapokutana na Vuai awe ameshakuwa mkali kama anavyotaka yeye mwenyewe.



    Alikuwa akifuata kij’a kimoja kinachotokea nyuma kwake na kuelekea kule iliko kambi ya wachumaji karafuu alipokutana na Mkongwo ambaye hakuweza kumpita bila ya kumsemesha kwa namna anavyomwashiki.



    Mkongwe alikuwa amechukua furushi la majani kwapani amekazana kwenda kuwalisha ng’ombe. Alikuwa amejifunga kanga mbili zilizo kongwe, moja kichwani na moja amejiandaa. Mzuri wa kimaumbile, Fuad alipomtupia macho hakujizuia kumsemesha.



    “Unakwenda wapi?” Fuad alimwuliza Mkongwe kwa hamaki.



    “Si unaniona nimechukua majani? Basi mwenyewe huwezi kukisia kama natoka kuchuma majani?” Mkongwe alimjibu huku woga na hasira vimemjaa kila akifikiri siku ile Fuad alipotaka kumwingilia ndani ya kibanda chake kwa nguvu.



    “Ebo! Wewe unathubutu kunijibu mimi namna hivyo?” Fuad alipiga kelele huku akitaka kumkamata.



    Mkongwe alimkwepa na kukimbilia mbio bandani mwa ng’ombe, furushi lake la majani kwapani.



    “Yuko wapi mbwa yule?” Fuad aliuliza bila ya hata kujua anamwuliza nani.



    Alikuwa akipiga makelele peke yake na hasa aliomba akutane na Vuai apate kummiminia hamaki zote zilizokuwa moyoni mwake.



    Vuai ambaye alikuwa akipiga majalbe kwenye miche michanga ya mikarafuu alikuwa amekwisha zisikia kelele za Fuad lakini aliendelea na kazi yake kama kawaida. Alikwisha kata shauri Ia kumjibu Fuad kweli tupu na amtazame atafanya nini.



    Mara Fuad alimwona Vuai anashughulika, jembe mkononi, ameinamia pale pale palipo na kazi yake. Vuai naye alikwisha baini kwamba Fuad yupo pale lakini hata hakutaka kujipa taabu ya kumtazama.



    “Wewe! Wcwe! Mimi nakutafuta wewe tokea saa ile!” alianza Fuad huku akimwelekezea kidole chake cha shahada. Fuad aliendelea na makelele aliyoyaanza tokea alipotoka kwake.



    Vuai alisita na kazi yake na kumtazama Fuad bila kuonyesha kustuka wala kutaharaki. Alikuwa amesimama, moyo wake tanda kabisa. akingojea nini Fuad atasema.



    Mara Fuad aliendelea na makelele yake. “Juzi ulikuwa unatokea wapi?”



    “Mkutano” alijibu Vuai bila ya kumwita Fuad Bwana’ kama ilivyo kawaida yao.



    “Mkutano? Mkutano gani?” alizidi kuuliza Fuad.



    “Mkutanoni pale Kijangwani,” alijibu Vuai.



    Kijangwani palikuwa pashakuwa pahala maarufu sana na ni watu wachache tu wasiopata kusikia habari zakc. Si wakulima tu waliopaelewa Kijangwani bali hata mabwana shamba na mabepari walikuwa wanapaelewa vizuri. Mara nyingi Fuad alikwishazisikia hadithi za Kijangwani lakini aliwaona wote waliofika pahala pale kwa haja yo yote kama watu wajinga wasioweza kufanya jambo lo lote.



    Fuad alianza kumvaa Vuai kwa maneno, “Ala, na wewe pia,! Na wewe p’a ushakuwa mkombozi wa wananchi? Wacheni upumbavu wenu huo Nyie mnafikiri mnaweza kufanya n’ni?”



    Chuki ilikuwa imemjaa. Alikwishazisikia hadithi nyingi za wakuiima waliohudhuria mikutano ya hapo Kijangwani kutoka kwa mabwana shamba wenzake wakati wanapokuwa katika starehe zao huko mjini au hata mashamba wanapotembeleana. Pale pale aliamua kumfukuza Vuai shambani mwake.



    “Hilo jembe liwache hapo hapo na uondoke shambani mwangu sasa hivi. Usichukue kitu cho chote, uondoke wewe tu!”



    Haya hayakumshitua Vuai kwani hata mwenyewe alikuwa akitumainia kwamba iko siku moja atafukuzwa kutoka shambani kwa Fuad. Alifanya kama alivyoambiwa. Bila ya kumwambia Fuad kitu cho chote alifuata njia na kuja zake mjini.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Vuai alizidisha idadi ya wakulima wallofukuzwa mashambani. Na si yeye peke yake. Haya yaliwafika wakulima wengi kutoka kila pembe ya kis’wa cha Unguja. Wote waliishia hapo Kijangwani. Vuai alikuwa mwenyeji hapo na alipofika tu alijua akaonanc na nani.



    Alimkuta Marijani chumba kile kile alichomkuta siku ile katika hali ile ilekainamia makaratasi, kalamu mkononi; mara aitazame karatasi hii mara aitazame karatasi ile. Alisimama mlangoni na kugonga.



    “Je, ndugu nini khabari?”



    Marijani alisimama pale alipokuwa amekaa na kuja kumsalimu Vuai.



    “Jamaa wote hawajambo huko?” Marijani alimwuliza Vuai huku akimvuta mkono na kumwongoza kukaa juu ya kiti.



    Wote wawili walikaa bega kwa bega na kabla Marijani hajasema kitu cho chote Vuai alianza kusema bila ya kujibu yale aliyoulizwa.



    “Ndugu, mimi nimekwisha fukuzwa kutoka huko shambani kwa Fuad. Alinikuta njiani nikirejea kutoka ule mkutano uliokuwepo juzi. Tena siku hizi mambo yake yamefurutu ada, manaake amezidi kuwa hana adabu. Siku ile uliniambia kwamba alitaka kumkamata Mariam kwa nguvu, basi hivi majuzi alitaka kumwingilia Mkongwe kibandani mwake usiku. Mkongwe alipiga kelele na sote tulitoka na silaha zetu.”



    Vuai alisita kusema kidogo na kutikisa kichwa, mara aliendelea na hadithi yake.



    “Ah, ama kijana yule bado zake zipo. Ingelikuwa hakujitambulisha kwetu kama ni yeye, basi nafikiri tungelimvaa kwa mapanga.”



    Vuai alikuwa anazungumza kwa hasira kubwa, kipovu kinamtoka mdomoni. Jasho jombamba lilimiminika kutoka usoni kwake na mara kwa mara alikuwa akilipangusa kwa mikono yake iliyojaa vumbi la udongo. Jasho hilo liliteremka mpaka kifuani na kulowanisha shati la mardufu bovu lisilokuwa na kifungo hata kimoja alilolivaa.



    Marijani alikaa kimya akimsikiliza Vuai na hata mara moja hakumwingilia katika mazungumzo yake. Alitaka aseme mpaka amalize yote aliyotaka kusema. Lakini mara Vuai alisita na kuonyesha kama amekwisha maliza kusema maneno yake.



    “Enhe!” Marijani aliingilia kati kama kumtaka Vuai aendelee na maelezo yake.



    “Basi alinijia na kuniuliza nilikuwa nikitoka wapi pale aliponikuta nik’rejea kutoka mjini kwa miguu. Mimi sikutaka kumficha na nilimwambia wazi wazi kwamba nilikuwa nikitoka kwenye mkutano wa wakombozi wa wananchi.



    “Alisema nini ulipomwambia hivyo?” mara Marijani aliingilia kati kuonyesha hamu ya kutaka kujua.



    “Kwa hakika sikumwambia kuwa ulikuwa mkutano wa wakombozi wa wananchi. Nilimwambia tu kuwa nilikuwa mkutanoni Kijangwani.”



    “Ah, wewe ulipomtajia Kijangwani tu lazima mwenyewe alifahamu ulikuwa mkutano gani,” Marijani alisema.



    “Sikiliza ndugu,” Marijani aliendelea, “wewe una mke na watoto?”



    Vuai aliukunjua kidogo uso wake uliokuwa umejaa hamaki na kutabasamu. “Mimi mjane bado. Wazee wangu walitaka kunipa mke mwaka jana lakini niliikataa na ulikuwa ugomvi mkubwa baina yangu na wao lakini...”



    Marijani hakutaka kujua zaidi juu ya ugomvi wa Vuai na wazee wake kwa kukataa kupewa mke. Aliingilia kati ya maelezo hayo na kusema, “Kama huna mke na watoto ni vizuri zaidi. Leo kiasi cha saa hedashara itakuja gari hapa, na mimi na wewe tutakwenda pahala, na hapo utawakuta wenzako wengi ambao naamini utapenda kuishi nao. Utajifunza mambo mengi buko. Sasa kama una kazi zako za kufanya hapa mjini unaweza kwenda kuzifanya na tukutane hapo saa hizo nilizokwambia.”



    “Mimi sina kazi yo yote ya kufanya. Nitasubiri pale nje chini ya miti mpaka zitakapotimia hizo saa.”



    “Sawa sawa,” Marijani alijibu.



    Vuai alitembea temboa na kufanya mambo madogo madogo aliyotaka kuyafanya na ilipofika saa nane alifika Kijangwani.



    Uwanja wa Kijangwani ulikuwa umezungukwa na miti mirefu ya mikungu, miembe na mizambarau. Ijapokuwa joto lilikuwa kali, uwanjani hapo palivuma upepo wa kuburudisha na miti yote hiyo kwa umoja ilitupa vivuli vyake uwanjani hapo. Kwa mtu aliyechoka na hata kwa asiyechoka, palikuwa ni pahala pazuri pa kupumzikia na kupunga upepo. Watu wengi walikuwa wakipita hapo.



    Vuai alikaa chini ya mti na mara usingizi ulimchukua.



    Haikuwa saa kumi na moja kama walivyoagana. Marijani alichelewa kiasi cha nusu saa. Alipofika alimkuta Vuai amekaa chini ya mti bado anapunga hewa nzuri ya Kijangwani. Marijani alifika na mwenzake aliyekuwa akiendesha hilo gari. Lilikuwa gari dogo, kongwe, lililokuwa wazi nyuma, lcnyc nafasi ya kuchukua kama watu wanane. Wote watatu walikaa sehemu ya mbele na bila ya kupoteza vvakati walianza safari yao.



    Vuai alikaa katikati na roara kwa mara alikuwa akijibenua huku na huku kwa nafasi ndogo ya hapo mbele iliyosababishwa na unene wa yule dereva. Wote walikaa kimya, ukisikika mlio wa gari tu.



    Mara Marijani alikivunja kile kimya na kuanza kuzungumza na Vuai. “Huko tunakokwenda tunakuita ‘Dambwe’. Tunakuita hivyo kwa sababu ni pahala pa siri, hendi mtu ila aliyehusika tu, yaani, kama wewe. Unajua Vuai, serikali hii haitaki kutuona sisi wakulima tuldfanya jambo lo lote la kutunufaisha sisi. Wao wanataka daima tuwe watumwa wa mabwana shamba tu. Pindi wakibaini kwamba tunapo pahala ambapo tunaweza kujipatia maisha basi watafanya kila njia ili watuharibie. Ukifika huko utakutana na wenzako ambao watakuelekeza la kufanya. Watakuonyesha eneo la kuweza kuishi wewe na watakusaidia kujenga banda lako la kujisetiri.”



    Vuai alinyamaza kimya ak’fikiri hayo maisha mapya anayokwenda kuishi huko Dambwe.



    “Unajua,” Vuai alisema kwa ghafla kama mtu aliyekumbuka kitu alichokisahau.” zana zangu zote nimeziacha kule kwa Fuad, n’na jembe langu zuri na miundu miwili yote nimeinunua hivi karibuni, n’na koade nzuri ya muhogo na nilikuwa karibu nivune viazi vyangu. Vyote hivyo hakuniruhusu niondoke navyo.



    “Sikiliza Vuai, hayo yote huna haja ya kufikiri. Hao utakaowakuta huko tunakokwenda yamewafika kama hayo au zaidi yake,” Marijani alimwambia Vuai.



    Yule dereva alikuwa hasemi cho chote ameshughulika na usukani wa gari. Mara moja moja tu alikuwa akiguna wakati gia inapofanya matata kuingia.



    “Lakini unajua Vuai, ijapokuwa utakuwa unaishi mbali na wale wenzako lazima ufanye kila njia uwe unakutana nao. Lazima, japo iwe kwa mwezi mara moja. uende Koani na uonane na wale ndugu zako. Fuad hataweza kukufanya cho chote hata akikuona huko,” Marijani aliongezea.



    Walifuata barabara itokayo mjini kuelekea kaskazini ya kisiwa cha Unguja kwa muda mrefu na baadaye waliacha barabara kubwa na kufuata njia ndogo na baada ya mwendo wa kiasi cha nusu saa walifika huko Dambwe. Kwa muda hawakumwona mtu ye yote, labda kwa sababu kila mmoja alikuwa kondeni kwake. Jua lilikuwa limekwisha kutua na si desturi ya wakulima kukaa kondeni mpaka saa kama zile. Palikuwa na vibanda vidogo vidogo vya udongo vilivyoezekwa makuti na havikuwa pamoja. Vilitawanyika kimoja huku na kimoja kule. Konde za mpunga zilizostawi zilionekana kwa mbali na sehemu nyingine zilikuwa zimelimwa mazao mbali mbali.



    Gari liliposimama Marijani alitoka nje akamwacha Vuai na yule dereva ndani ya gari. Baada ya kuingia kichakani na kupotea humo kwa muda mfupi alirejea amefuatana na mtu, mrefu, mwembamba, aliyejifunga shuka chafu. Tumbo lake lilikuwa wazi na miguu haikuwa na viatu. Alikuwa amcchomeka kisu kikubwa kiunoni kikiwa ndani ya ala iliyotengenezwa kwa bango la mpopoo. Marijani na yule mtu aliyefuatana naye walisimama mbali kidogo na lilipokuwa lile gari na baada ya mazungumzo mafupi Marijani alirejea peke yake.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    “Sasa Vuai sisi tutakuacha hapa na tutarejea mjini. Unamwona yule kijana niliyekuwa nikizungumza naye. Nenda pale na yeye atatengeneza kila kitu,” Marijani alimwambia Vuai huku akimfungulia mlango wa gari ili apate kutoka.



    “Basi kwa heri, tutaonana na tutazungumza zaidi”.



    Marijani aliingia ndam ya gari na hapo hapo gari liligeuzwa na kuanza safari ya kurejea mjini.



    Vuai alifuatana na mwenyeji wake wakapita njia za ndani kwa ndani vichakani. Mara walitokea pahala paliposafishwa vizuri ambapo palikuwa na kibanda kama vile alivyoviona akiwa garini. Karibu na kibanda hicho palikuwa na mwembe mdogo na walipofika chini ya mwembe huo yule mwenyeji wa Vuai alimwomba mgeni wake amsubiri hapo. Aliingia ndani ya kibanda hicho na mara alitoka na mkeka akautandika na kumkaribisha Vuai akae.



    Vuai alipokuwa amekaa chini ya mwembe zilimjia fikra mbali mbali nyingi. Alijiona hajui alipo wala hawaoni hao watu alioambiwa atawakuta pale. Hakujua maisha yangekuwaje pale lakini hata hivyo alikuwa na matumaini mazuri. Kwa vyo vyote yasingekuwa kama yalivyokuwa kwa Fuad.



    Kiza kilikuwa kimeingia na bado mwenyeji wake hakutokea. Hata hivyo. hilo halikumtia wasiwasi. Alixuwa ana hakika kuwa atakuja tu bila ya shaka yo yote. Mara alisikia parakacha parakacha na mwenyeji wake alijitokeza kutoka kichakani na kuja pale alipokuwa.



    “Umenisubiri muda mrefu enh?”



    “Hapana kitu ndugu, mimi nahisi niko nyumbani tu,” Vuai alijibu.



    Mwenyeji wa Vuai aliingia ndani ya kile kibanda chake akatoka na taa ya kibatari mkononi. Aliiweka pembeni na kuja kukaa juu ya mkeka pamoja na Vuai.



    “Unaitwaje mwonzangu?” aliuliza yule mtu.



    “Mimi naitwa Vuai; na wewe je?”



    “Mimi naitwa Kondo.” Palikuwa na kimya kidogo na mara Kondo akaanza mazungumzo.



    “Basi karibu ndugu. Hapa ndipo tunapoishi na maisha yanakwenda kama kawaida. Usione kimya hapa, tupo wengi na pole pole utawajua wote. Wewe rafiki yangu ni mwanamapinduzi?” aliuliza Kondo.



    Vuai hakuwahi kusikia kitu kama hicho na mara aliuliza, “Mwanamapinduzi wa kitu gani?”



    “Ala, kwani yule kijana uliyekuja naye hakukueleza” Kondo aliuliza.



    “Amenieleza mengi lakini hayo ya mapinduzi hakunieleza,” Vuai alijibu.



    “Ikiwa yeye hakukueleza basi mimi nitakueleza,” Kondo alisema huku akincha mikono yake. “Sisi tuliopo hapa sote m wakulima tuliotukuzwa mashambani na mabwana shamba wenye kumiliki ardhi. Kabla ya kutufukuza walitutesa na kutuletea unyonge mkubwa na hivi sasa tupo hapa soto tumejikusanya pamoja, tunaishi kama ndugu, na azma yetu hasa ni kuipindua serikali ya kimwinyi ili tuwe na serikali itakayoleta maslahi na mabadiliko katika maisha ya wakulima na masikini wote katika nchi. Kuhusu jambo hili sisi tunaoishi bapa tumejitolea kufa na kupona; je, unasemaje Vuai?”



    “Unafikiri jambo hilo linayumkinika?” aliuliza Vuai.



    “Kwa nini lisiyumkinike; linayumkinika sana tena wala...”



    Kabla hakumaliza mara mazungumzo yao yalikatwa na sauti ya kike iliyoita kutoka kule kibandani kwa Kondo:



    “Bwana! Tayari.”



    “Ala! Tayari siyo? Lete basi!” alisema Kondo.



    Hapo tena alitoka mwanamke aliyejifunga shuka ya kaniki kifuani akiwa amebeba sinia iliyoonyesha nzito kwa vile alivyoichukua. Aliiweka ile sinia juu ya mkeka waliokalia Vuai na Kondo na ndani ya sinia hiyo mlikuwamo sahani ya ugali wa muhogo na bakuli la mchuzi wa nazi.



    “Tuletee maji ya kunawa mikono basi!” aliamuru Kondo.



    “Ntaleta.”



    Yule bibi alirejea kule alikotoka. Kondo akamwambia Vuai, “Yule ni mama watoto wangu.”



    Mara alitoka na sufuria ya maji na kumpa Kondo na wote wawili wakakosha mikono yao na kula. Kwa hakika Vuai alikuwa na njaa sana na alikula bila ya kutaka kuzungumza tena.



    Walipomaliza kula walibaki pale pale juu ya mkeka wakaendelea na mazungumzo waliyoyakatiza.



    “Basi ndio hivyo ndugu; Lazima tupindue na kama hatukufanya hivyo basi tutaendelea kuteswa maisha yetu. Sisi sote tuliopo hapa ni wapinduzi na tuna mipango kamili iliyo madhubuti, si kama tutajifanyia mambo kijiendawazimu.”



    “Mimi nimefukuzwa kutoka shambani kwa Fuad na huko nimewaacha wenzangu wengi na wote hawana uhakika wa maisha yao ya siku za mbele,” alisema Vuai.



    “Najua, kwani hapa haletwi mtu isipokuwa amekwishafukuzwa shambani kwa bwana shamba. Tena waliokuwa hawana hakika ya maisha yao ya siku za mbele siyo hao waliokuweko huko ulikotoka wewe tu; wakulima wote nchini hawana hakika ya maisha yao ya siku za mbele na kwa sababu hii ndiyo tukaamua kupindua,” alisema Kondo.



    “Mimi niko pamoja na nyinyi, kufa au kupona,” Vuai alisema.



    “Barabara! Lete mkono ndugu,” alisema Kondo huku akiwa amefurahi kupata mwana mapinduzi mwenzao.



    Usiku ule Vuai alikuwa mgeni wa Kondo. Alitengenezewa nafasi kibandani mwake na ilipatikana nafasi ndogo ya kuweza kujinyesha na saa zilipokuwa nyingi waliingia ndani na kulala.



    Kama alivyoahidiwa, Vuai alisaidiwa kujenga banda lake la kuishi. Siku zilivyoendelea ndivyo alivyozoea maisha yake mapya. Alipata wenyeji. akajuana na jamaa wengine wanaoishi huko Dambwe. Alifahamishwa mipango zaidi kuhusu mapinduzi na mara kwa mara aliwaona wajumbe kutoka mjini wakija na miongoni mwao akiwa Marijani. Ycye alikuwa akija kutoa nasaha na kufahamisha yaliyokubaliwa na wakuu wa wakombozi wa wananchi.



    Kama alivyonasihiwa na Marijani Vuai hakuwatupa wale wenzake huko Koani. Kila alipopata nafasi aliwatembelea na kuwajulisha wale aliowaamini mipango ya mapinduzi na jinsi ilivyokuwa ikiendelea.



    Nchi ilikuwa imeharibika. Serikali ya kisultani ilizidi kuwakandamiza wafanyakazi na wakulima. Kila wakombozi wa wananchi walipofanya mikutano yao basi mikutano hiyo ilimalizika kwa wananchi kupigwa marungu na askari wa serikali ya Sultani, Magari yote yaliyotoka sehemu zote za mashamba kuja mjini ilibidi yapekuliwe katika vituo maalum vya polisi kabla hayajafika mjini.



    Lakini wapi! Kila serikali ya Sultani ilivyozidi kukandamiza wakulima na wafanyakazi ndivyo nao walivyojiandaa na kutayarisha mipango ya kuipindua.



    Huko Dambwe, akina Kondo walikuwa wakijiandaa kwa kukusanya kila silaha waliyoweza kipata. Hawakupata silaha za kisasa lakini bado waliamini kwamba kufanikiwa au kutofanikiwa kulitegemea watu zaidi kuliko silaha. Silaha walizokusanya zilikuwa ni mapanga, mashoka na zana nyinginezo wanazotumia wakulima katika kazi zao za kila siku.

    ILIPITA miezi miwili hivi. Hata usiku romoja kama saa tano Vuai aliyekuwa amelala kibandani kwake alizindushwa na mlio wa gari kwa mbali. Kwa namna alivyousikia mlio ule alikuwa na hakika kwamba gari lile lilisimama; tena kwa muda mrefu. Hakulala tena. Baada ya saa mbili hivi alilisikia gari lile likitia moto tena na kuondoka. Alikuwa na hamu kubwa ya kutaka kujua ilikuwa m gari la nani. Kuja kule usiku ule ni jambo lisilokuwa la kawaida.



    Alfajiri watu wote waliamka na wakati ulipofika kila mtu aliteremkia kondeni kwake. Kumbe wageni waliokuja na gari jana usiku walimjia Kondo. Walikuja kumpa habari muhimu kuhusu matayarisho ya mapinduzi na ilimbidi ampitie kila mmoja kondeni kwake na kumwarifu jun ya ‘ngoma’ kesho yake usiku nyumbani kwake. ‘Ngoma’ m msemo wao kwa siku kama hiyo wanapoarifiana juu ya mambo muhimu.



    Usiku ulipofika wote walikusanyika chini ya ule mwembe mdogo mbele ya nyumba ya Kondo katika kiza.



    “Salamu zenu nyingi kutoka Kijangwani,” Kondo alianza kusema, “Wanasema, wakati umekaribia na siku haiko mbali. Mamao yote madhubuti na maboma yote mawili tutayakamata siku moja. Tutaanzia kwa silaha hizi hizi tulizonazo na tutamalizia kwa silaha tutakazonyakua toka kwao.”



    Wote walimsikiliza Kondo kwa makini; hapana aliyesema kitu.



    “Itakapofika siku yenyewe hasa, tutapata taarifa mapema ili tuweze kujitayarisha. Mimi sina zaidi. Nafikiri haina haja ya kukaa hapa kwa muda mrefu. Lakini, Vuai, n’na salamu zako kutoka kwa Marijani. Anasema ufanye kila njia ufike Koani ukawaarifu wale unaokutana nao na anasema hala hala usiache kwenda. Wenzetu wa sehemu nyinginezo pia watapelekewa habari kama tulivyoletewa sisi na siku ya siku itakapowadia sote tutakuwa pamoja.”



    Kondo alimaliza hotuba yake na wote wakatawanyika kila mmoja akaenda kibandani kwake.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Vuai alielewa vizuri umuhimu wa jukumu alilopewa. Kwake yeye haikuwa shida kubwa kufanya safari ya kwenda Koani. Hakulazimika tena kungoja Fuad aende mjini kuuza karafuu kama alivyofanya alipokuwa akimfanyia kazi. Huku aliko aliweza kwenda atakako bila ya kuingiliwa na mtu ye yote. Kwa hiyo, siku ya pili asubuhi alianza safari ya kwenda Koani.



    Alipanda gari ya kwanza ilotokea Mchangani na aliona bora kwanza apitie Kijangwani kuonana na Marijani kabla ya kuendelea pale na safari yake.



    Alipofika pale hakukuta ghasia kama zile alizozoea kuzikuta kila alipokwenda. Palikuwa pamepooza kidogo ila kila baada ya muda aliingia mtu mmoja halafu akatoka hapo hapo kama kwamba alisahau kitu halafu akarudi kukichukua baada ya kukumbuka na kisha akaenda zake.



    Vuai aliingia ndani ya ofisi ya Kijangwani akaufungua mlango wa ofisi ya Marijani kwa utaratibu bila ya kugonga. Alipochungulia alimkuta Marijani amekaa juu ya kiti, mikono yake miwili ameisimamisha juu ya meza na amekilaza kichwa chake katika viganja vya mikono yake. Alionekana kama mtu aliyetaka mapumziko mafupi baada ya kufanya kazi iliyomchokesha sana.



    Mlio wa mlango uliokuwa ukifunguliwa taratibu ulimzindua na alipoinua kichwa alimwona Vuai amesimama mlangoni.



    “Umeshakwenda Koani?” Marijani alimuuliza Vuai bila ya hata kumsalimu kama kawaida yake.



    Marijani alikuwa amebadilika na hakutaka mzaha hata kidogo. Nguo zake zilikuwa zimechafuka na kidevu chake kilichozoea kunyolewa kila siku kilikuwa na ndevu changa za kiasi ya siku sita nivi.



    “Nimeona bora nije kuonana na wewe kabla sijaenda huko Koani,” Vuai alijibu.



    “Kwani Kondo hakukueleza kila kitu?” Marijani aliuliza tena akionekana kama hakupendezekewa na hatua aliyoichukua Vuai. “Lakini si vibaya,” Marijani aliukunjua uso wake kidogo na kuanza kuzungumza na Vuai kama kawaida yake ya siku zote. “Sasa wewe nenda Koani, wale ndugu unaoonana nao kila siku wambie kama alivyokwambia Kondo. Jambo moja tu zaidi, waulize kama washakusanya silaba. Tena fanya haraka mana’ake katika mipango yote tukikosea pamoja tu basi ujue tumeharibikiwa. Mambo yote lazima yafanyike kama yalivyopangwa. Sasa bora uende bila ya kupoteza wakati.”



    Vuai alitoka. Alipofika Mikunguni tu alipata gari lililoendea Koani.



    Alipofika ilikuwa taabu kumpata mtu ye yote katika wenzake. Wote walikuwa wamo katika kumtumikia Fuad. Alijaribu kila rai akijichunga sana asionekane na Fuad akatia shaka fulani.



    Vuai alikuwa mwenyeji shambani kwa Fuad kutokana na miaka mingi ya utumishi wake shambani mle. Alikijua kila kichaka. Alikwenda kila sehemu aliyojua angemwona mmoja wa wafanyakazi lakini hakufanikiwa. Alipokuwa amekwisha kata tamaa, na kidogo aketi chini apumzike kabla ya kuendelea zaidi, alimwona Mkongwe akitoka kisimani.



    “Hebu ningojc nikuulize!” Vuai alimwambia.



    Mkongwe alisituka, akinkiri Fuad anataka kumfanyia unyama wake. Lakini sauti iliyomwita haikufanana na yake. Alipogeuka kwa ghafla alimwona Vuai.



    “He, Vuai masikini! Ulikuwa wapi?” Mkongwe aliuliza. Aliutua mtungi wa maji aliokuwa nao kichwani na kwenda kule aliko Vuai. “Ulikuwa wapi sikn zote hizi?” Mkongwe alimwuliza tena Vuai huku akimwonea huruma kubwa. Alimkaribia na kutaka kumkumbatia kwani hakufikiria kama angemwona tena.



    “Samahani ndugu, huu si wakati wakuulizana maswala mengi. N’na haraka sana na tafadhali fanya kila njia uniitie Umari, na mwambie n’na haja naye muhimu sana. Mwambie namngojea hapo kibandani pake atanikuta ndani.”



    Bila ya kutaka kuzungumza zaidi na Mkongwe, Vuai alikwenda zake.



    Mkongwe alipigwa na mshangao kidogo lakini pale pale alijitwisha mtungi wake wa maji na alipokwisha kuutua mtungi ule alitoka akaenda kumtafuta Umari.



    Alipomkuta tu, Mkongwe hakutaka kuzungumza naye kitu cho chote bali alimsogelea na kumnong’oneza, ‘Vuai anakwita; utamkuta kwako ndani,” huku akiangaza huku na huku asije Fuad akatokea na kuwakuta nale wanazungumza.



    “Kaja? Lo!”



    Umari ambaye alikuwa akipalilia migomba aliliweka jembe lake chini na bila ya kupoteza wakati alikimbilia kwake. Alipofika aliukuta mlango umesindikwa kidogo na Vuai amekaa juu ya kitanda cha mayowe kilichokuwa mle ndani.



    “Je. kumezidi nini?” Umari aliuliza.



    “Kwanza silaha mshakusanya.”



    “Tayari lakini si nyingi; mambo unayajua tena.”



    “Basi mambo yanakaribia. Jitayarisheni kwa wakati wo wote ule ingawa siku ikifika atakuja mtu kukwambieni mapema. Wape habari jamaa wote; siwezi kukaa tena. Kwa heri. Nisalimie wote.”



    Pale pale Vuai alitoka na kuanza safari yake ya kurejea Dambwe. AIipitia Kijangwani kutaka kuonana na Marijani amwarifu yote lakini hakumkuta. Alirejea Dambwe na alipofika huko ilikuwa jioni.



    Mapinduzi yalikuwa yananukia. Huko mjini watu walikuwa hawazungumzi kitu tena - wakitazamana tu wanafahamiana. Huko Dambwe wote walikuwa wanajiandaa; wakingojea ujumbe tu kutoka mjini.



    Ulipita mwezi mzima hakuwapitia mtu ye yote kutoka mjini lakini hata hivyo wakati wote walikuwa katika hali ya kuwa tayari.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Baada ya mwezi kupita, Idasi ya saa saba mcbana siku moja, liliingia gari kubwa la mizigo. Gari hili halikupata kuja pale na Vuai ambaye alikuwa karibu alikwenda kuona ni wageni gani waliokuja nalo. Gari lenyewe lilikuwa la serikali la kupakilia mizigo. Lilikuwa na rangi ya kijani na nyuma li wazi. Vuai alipokaribia alimwona Marijani akishuka kutoka mle garini na akionyesha kuwa ana haraka.



    “Imekuwa kheri umetokeza! Yuko wapi Kondo?” Marijani aliuliza.



    “Kondeni kwake.”



    “Twende!”





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog