Simulizi : Nini Maana Ya Mapenzi Sehemu Ya Tatu
(3) Kulipokucha akachukua simu yake na kuangalia,
akakuta aliyekuwa anapiga ni Erick, akajisikia vibaya sana, na kuamua kwenda
kutafuta vocha ili ampigie. Akajiandaa kwaajili ya kutoka, ila mama yake
akamuuliza, “Erica, asubuhi yote hii? Unaenda wapi?” “Naenda
dukanini mama kununua vocha” “Aaah chukua chupa basi, na mimi
ukaninunulie soda” Basi Erica akachukua na chupa kisha kuondoka, alifika
dukani na kununua vocha ila lile duka hakupata soda ambayo mama yake alikuwa
amemuagiza ikabidi aende kwenye duka lingine la barabarani. Wakati yupo
pale dukani akinunua soda aliyoagizwa, alifika mama wa makamo kwenye gari,
alisimamisha gari yake na kuomba achukuliwe maji dukani, ikabidi Erica
amchukulie na kumpatia, Yule mama akamshukuru sana Erica na
kumuuliza, “Unaitwa nani binti?” “Naitwa Erica” “Wow,
jina zuri sana. Nimekupenda bure, una moyo wa kipekee maana nilikuwa naona uvivu
haswaa kushuka kwenye gari na kuagiza maji, halafu mwenye duka nae ana wateja
wengi ila wewe na huruma yako umenichukulia maji dukani na kuniletea, asante
sana” “Usijali” “Basi kama hutojali binti, naomba namba
yako” Erica akampa Yule mama namba yake kisha kuagana nae, halafu Yule
mama akaondoa gari yake na kuondoka zake, Erica akachukua soda dukani na kurudi
kwao. Mama yake alimuuliza kwanini kachelewa, “Sikukuta soda
uliyoniagiza duka la karibu ilibidi niende maduka yale ya barabarani
mama” “Nikajua umeanza tena mambo yako ya kukutana na
wazee” Basi Erica aliingia chumbani kwake na kuweka vocha kisha kutaka
kumpigia Erick, ila kabla hajapiga kwa Erick, simu yake ikaita na mpigaji
alikuwa Erick kwahiyo alivyokuwa anawaza kumpigia Erick ndivyo Erick nae
alivyokuwa anampigia, kwahiyo hilo swala lilifanya moyo wa Erica kujawa
tabasamu, “Erica, mbona jana usiku hukupokea simu
yangu?” “Nilikuwa nimelala ndiomana” “Basi badae nitakupigia,
kuna mambo nahitaji tuongee” “Sawa, hakuna tatizo” Kisha Erick
akakata simu na kumuacha Erica akibaki na tabasamu tu, gafla akapokea ujumbe
kutoka kwa mzee Jimmy, “Erica, sijapenda kurudisha zawadi ambazo
nimekupatia yani sijapenda kabisa” Erica hakujisumbua kujibu huo ujumbe
wala nini, kisha mamake akamuita na kumuaga kuwa anaenda kanisani, kama kawaida
Erica alibaki nyumbani na mwanae maana bado hakupata muhamko wa kwenda kanisani
kwani bado hakuwa huru kueleza kuhusu mtoto aliyenaye na ukizingatia kule
kanisani kwao walimjua vilivyo. Wakati yupo nyumbani kwao akapokea
ujumbe toka kwa Dora, “Nakuja kwenu Erica” Akajua lazima kuna
jambo ndiomana Dora anakuja, basi alitulia akimsubiria. Muda kidogo
akapigiwa simu na dada yake Bite, na baada ya salamu dada yake
alimuuliza, “Wewe Erica, umemfanya nini shemeji yako?” “Jamani
dada, sijamfanya kitu chochote, kwani kasemaje?” “Erica mdogo wangu
mbona umekuwa na tabia mbaya kiasi hiki jamani! Kesho nitakuja kuongea na
mama” “Ila dada unanionea hakuna nilichofanya kweli
tena” “Unabebwa hubebeki, unataka mtu afanyaje? Nasikia umeanza urafiki
na watu wa ajabu ajabu na kuna mambo umemfanyia shemeji yako, sikutegemea kweli
mdogo wangu ungefanya hivi tena kwa shemeji yako mume wa dada yako! Sikutegemea
kwakweli” Bite akakata simu na kufanya Erica abaki na maswali kweli
maana hakuna kibaya alichofanya kwa shemeji yake zaidi yay eye kusimamishwa
kazi, alishangaa kusikia kibao kinamgeukia, alijiuliza kuwa ni kitu gani
hakupata jibu kabisa. Baada ya muda Dora alifika kweli, kisha
Erica akamkaribisha vizuri tu ndani kwao. Akamsalimia pale na kuanza
kumuuliza maswali mawili matatu kwa kilichotokea juzi, “Eeeh Dora,
uliondoka pale?” “Erica, naanzaje kuondoka kwa mfano? Ila Erica shoga
yangu una bahati jamani sijapata kuona, mwenzio natamani nipate bahati kama zile
ila sibahatiki ila wewqe bahati kama ile unaichezea, kweli upele humuota asiye
na kucha” “Sasa Dora, kutakwa na mtu mzima Yule ndio
bahati” “Kwani utu uzima wake unakuathiri nini? Ng’ombe hazeeki maini
upo! Halafu watu siku hizi hawaangalii utu uzima wanaangalia
pochi” “Kwahiyo wewe ulitulia tu kumsubiri” “Sikia Erica,
kwavile uliondoka mimi ilibidi nimsubiri mzee wa watu maana nilimuhurumia
ukizingatia alisema kuwa ana ugumu, halafu masikini mzee wa watu alishakodi
chumba, Erica una dhambi wewe loh! Kwani ungelala nae mara moja tu kingeharibika
kitu gani?” “Hivi Dora unafikiri mimi naweza kusikiliza ushauri wako
tena! Labda niwe chizi, wewe ndio ulifanya nikaachana na mpenzi wangu Babuu,
wewe ndiye uliyechochea mapenzi ya mimi na George na wewe ndio ukafanya nilale
na George wakati unajua wazi anataka mabikira. Unadhani nasahau? Ni kweli
nimekusamehe ila kusahau siwezi” “Mmmh Erica jamani! Basi tuachane na
hayo, juzi bhana Yule mzee alinyong’onyea sana nilipomwambia kuwa umeondoka na
simu aliyokununulia umeiacha, alipooza hadi nikamuonea huruma, basi nikamwambia
nipo mimi nitakuliwaza, akafurahi basi nikaenda nae kwenye chumba alichokodi.
Ile hoteli ni nzuri Erica dah nzuri sana, basi bhana jamani Yule mzee nikampa
mambo hayo sio ya nchi hii, yani nilitumia ufundi wangu wote kwa kujua kuwa
angenipa ile simu aliyokununulia wewe. Ila tulipomaliza cha kushangaza hakunipa
ile simu akasema ile simu ni yako na lazima ikufikie, niliumia sana. Basi akatoa
pesa, burungutu la fedha, nikajua nimelamba bhana, loh mzee Yule sijaamini
amenipa laki tu halafu hela zote karudisha, niliumia halafu akaniambia angekuwa
Erica, hizi hela zote ningempa. Jamani Erica una nini mwenzangu na mimi unigawie
eeeh! Mbona bahati kama hizi sizipatagi mimi? Ila hata hiyo laki nashukuru maana
wanaume wangu akikuhonga laki sijui umfanyie nini ila Yule baba dakika chache tu
kanipa laki, ila mihela ile nilikuwa na hamu nayo dah!” Erica
alimuangalia Dora na kumsikitikia kwakweli maana alimuona anaongea kama mtu
asiyejitambua, Dora alipoona Erica asemi chochote akamuuliza tena, “Vipi
ile simu alikuletea?” “Aliniachia bahasha kwenye benki yao, nilipofika
nyumbani nilikuta kaweka simu na milioni mbili” Dora akawaka kwa
mshangao, “Milioni mbili!!” “Ndio milioni mbili” “Jamani
shoga yangu, naomba kidogo basi” “Mama aliniona wakati nafungua kwahiyo
hela na simu tulirudisha mapokezi kwenye hoteli aliyosema
tukutane” “Yani Erica na mamako mmerudisha hela milioni mbili! Mtakufa
masikini nyie, tangu lini hela ikarudishwa?” “Mama yangu hataki kabisa
huo ujinga” “Uwiii angekuwa mama yangu anavyopenda hela yani
ningeozeshwa kwa huyo mzee hata mke wa mbali tu inatosha. Sasa Erica tufanye
kitu” “Kitu gani?” “Basi kubali kulala na Yule mzee mara moja tu
tuuage umasikini” “Hivi unaakili wewe Dora? Yani unaongea kama uliishia
la saba, yani mwanaume umelala nae wewe halafu na mimi nikalale naye inakuja
kweli hiyo?” “Kwani tatizo liko wapi? Mbona George aliwahi kuwa mpenzi
wangu na wewe ukalala nae” “Kuhusu George sikujua maana ulinificha ila
sio kuhusu Yule mzee, hata hivyo simtaki kama hela zake akae nazo
tu” “Hivi Erica unajihakikishia nini maisha haya? Kwani Yule mzee
akilala na wewe itakuwaje? Ataondoka nayo? Si itabaki kwako kama kawaida?
Ningekuwa mimi ndio wewe, ningetumia hii fursa hatari, swala la kusoma nimesoma
ndio nikijua nitapata kazi nzuri ila wapi, kazi zenyewe manyanyaso tu halafu
mshahara mdogo ila mzee kama Yule anatoa tu hela, jamani Erica tafadhali mkubali
Yule mzee” Mamake Erica aliingia ndani na kuwaka, “Amkubali
nani?” Kisha akamuangalia vizuri Dora na kusema, “Khaaa kumbe
wewe changudoa ndio umekuja tena kwangu! Haya toka, ondoka upesi sitaki
kukuona” Ikabidi Dora ainuke na kuanza kutoka, Erica akataka
kumsindikiza ila mama yake akamkataza, “Na wewe unataka kwenda wapi?
Kalisha makalio yako chini mjinga wewe” Ilibidi Erica akae kwa
kusikiliza maneno ya mama yake, alianza kusema, “Ndiomana dadako
kanipigia simu, jamani Erica umeanza na urafiki na huyu firauni kweli? Ikiwa
kweli maneno aliyoniambia dada yako tutaonana wabaya kwakweli” “Maneno
gani hayo mama” “Umeniudhi sana, ngoja nikapumzike, labda badae
nitasema” Kisha mamake Erica alifunga mlango wa kutoka nje na funguo
halafu funguo kwenda nazo chumbani kwake akimaanisha kuwa hataki Erica
atoke. Erica naye aliingia chumbani kwake huku akitafakari
jinsi mama yake alivyomtimua Dora, ila hakumlaumu sana maana maneno ya Dora kama
mama yake kayasikia vizuri basi ana haki ya kumtimua maana sio maneno ya busara
kabisa. Ilikuwa ni jioni na wakasikia mlango wao ukigongwa, kwa maana
hiyo kulikuwa na ugeni, mama Erica alitoka na funguo ili akafungue mlango muda
huo Erica naye alikuwa nyuma ya mama yake ili kuchungulia ni nani aliyekuwa
anagonga. Baada ya kufungua mlango, akamsikia mama yake
akisema, “Kheee Mwajuma hadi kwangu kweli!” Erica alisogea
kumuona huyo Mwajuma, alishangaa kumuona Mrs.Peter yani mama yake na Rahim akiwa
ameongozana na Babuu. Baada ya kufungua mlango,
akamsikia mama yake akisema, “Kheee Mwajuma hadi kwangu
kweli!” Erica alisogea kumuona huyo Mwajuma, alishangaa kumuona
Mrs.Peter yani mama yake na Rahim akiwa ameongozana na Babuu. Alishangaa
vile ambavyo mama yake alionekana kumfahamu Mrs.Peter, kisha mama yake
aliendelea kuongea pale pale mlangoni kabla hata hajawakaribisha
vizuri, “Eeeeh kilichokuleta nyumbani kwangu ni nini?” “Kheee
tulia mama weee, hata kilichonileta si wewe , nimekuja sababu ya binti yako huyo
anayechungulia. Tusiondoleane ladha mapema hivi” Mamake akageuka na
kumuangalia Erica ambaye alisimama tu akiwaangalia na
kumuuliza, “Unawajua hawa?” “Ndio mama” Kisha mamake
Erica akaachia mlango waingie ndani ila hakuwakaribisha wala nini na ile
ilionyesha kwamba hawa watu wana ugomvi wa siku nyingi. Mrs.Peter
alipita na kukaa kwenye kochi, Babuu alimsalimia mama yake Erica na kukaa pia,
ila mama yake Erica alikuwa na chuki bado za wazi wazi kabisa, walipokaa
alimuuliza tena mrs.Peter, “Kilichokuleta?” “Usiniulize mimi,
muulize huyo binti yako. Erica mbona unasimama tu, njoo umwambie mama yako
kilichotuleta” Erica akasogea na kusema, “Karibuni ila hata mimi
sijui kilichowaleta” Mrs.Peter aliwaka kwa msahangao, “Hujui
kilichotuleta? Mtoto mbaya wewe sikutegemea” Mama Erica
akamwambia, “Weee hakuna mtoto mbaya duniani, usiniitie mwanangu mbaya,
uishie hapo hapo na useme kilichokuleta” “Kwanza usinifikirie vibaya,
sijasema mbaya kwa kumaanisha ni mbaya, kila mmoja anajua kuwa Erica ni mzuri
hata kichaa akimuona Erica atasema kuwa dada huyu ni mzuri na si kwamba ni
msichana wa kujiremba ndio uone uzuri wake hapana ila Erica ni mzuri asilia.
Sasa niliposema mbaya sikumaanisha ubaya unaoufikiria wewe, ila alichofanya
kwangu ndio kimefanya nimuite mbaya” “Haya kafanyaje?” “Erica
namfahamu, na sijamfahamu juzi wala jana ni kipindi kirefu sana namfahamu ila
mwanao anatumia uzuri wake vibaya, kwanza mtoto muongo huyu yani kazaa na
mwanangu halafu kashindwa kuniambia kuwa kazaa na mwanangu kweli? Tena
nilikutana nae hadi kliniki akanidanganya kuwa mtoto aliyembeba ni wa dadake
kumbe ni mjukuu wangu ila hakutaka nimuone jamani Erica kweli wewe wa kunifanyia
hivyo!” Erica alitazama chini tu kwa aibu kisha Mrs.Peter aliendelea
kuongea, “Yote tisa kumi, yani Erica kumbe umekuwa na mahusiano na
wanangu wote kweli? Rahim na John, na licha ya hivyo hata huyu ndugu yao Babuu
umekuwa na mahusiano nae, kweli hiyo? Yani uzuri wako ndio unafanya uchanganye
ndugu jamani” Erica alibaki kimya, kisha mamake alimuangalia na
kumfokea, “Hebu njoo ukae hapa, usitusimamie kama mlingoti na useme kama
yasemwayo ni ya kweli?” Erica alienda kukaa kwa aibu ila hakusema
chochote, kisha mamake akaendelea, “Kweli umezaa na mtoto wa huyu
mwanamke? Na kweli ulikuwa na mahusiano na watoto wake wote?” Erica
alikuwa kimya tu, kisha Mrs.Peter akaongea, “Anaona aibu kusema ukweli,
ila kaumiza sana mioyo ya watoto wangu, na kama anabisha basi niwalete wote na
akatae mbele yao kuwa sikuwa na mahusiano nao. Haya mfano tosha ni huyu Babuu
yupo hapa akatae kama hajawahi kuwa na mahusiano nae, na mtoto aliyenaye kazaa
na mwanangu Rahim” Kwakweli Erica aliona amepewa aibu iliyopitiliza
maana hakufikiria kama mama yake hata amewaza kuwa mwanae amewahi kuwa na
mahusiano na wanaume wengi vile zaidi ya Yule aliyemoa mimba, ila anajielezaje
hapo, aliona aibu sana na kushindwa kuongea kabisa ila mama yake alimfokea sana
ikabidi aongee, “Jamani vitu vingine mtanilaumu bure tu, nisameheni
bure. Sipendi kuongelea maswala ya hao wanaume labda tuongelee kuhusu mtoto
tu” Mrs.Peter akadakia, “Kwanza mtoto mwenyewe yuko wapi? Maana
kwa mtindo huu usikute hata mwanangu anabambikiwa, familia moja ushatembea na
watatu je huko nje? Wewe mtoto ni shimo la taka, usikute wanangu hawa wameona
mwarabu mwarabu wakamfananisha na Rahim labda hata sio wa Rahim, kama wanaume
ulikuwa nao wengi. Mlete kwanza huyo mtoto nimchunguze kama ni wa mwanangu
kweli” Erica akataka kuinuka akamchukue mtoto maana alikuwa kalala, ila
mama yake alimzuia na kusema, “Weee Erica, kalisha mbaliga zako chini
huwa sitaki ujinga mie, mtoto hapa hali, havai, halali au kitu gani mwanao
hapati?” “Anapata kila kitu mama” “Sikieni, huwa sipendi dharau.
Halafu wewe Mwajuma umekuja na kufoka mwanangu muongo sijui hakukwambia kama ana
mtoto wa mwanao, ngoja nikuulize swali. Kwanini usimuulize huyo mwanao kama
kweli kazaa na Erica? Si ungemuuliza kwanza mwanao upate uhakika, eti mlete
mtoto nimchunguze, mjukuu wangu hachunguzwi umesikia eeeh! Tena naomba muondoke
kwa amani kabisa, mkiwa na uhakika kuwa ni wa kwenu karibuni ila sio leo ya
kumchunguza mwanangu sawa! Mtoto hachunguzwi huyu, Erica tulia hapo mwanangu,
hata mimi wanangu hamkuchunguzwa iweje mjukuu wangu achunguzwe? Mwanangu wewe
sio changudoa wa kusema humjui baba wa mtoto sijui hadi achunguzwe, leo
utachunguza kwa macho, kesho utaomba kupima DNA na mtoto, sio kwa mjukuu wangu
tafadhali, ondokeni” “Sasa mama Mage unakuwa mkali hivyo kwa lipi? Hivi
wewe ukiambiwa mwanao wa kiume ana mtoto sehemu hutotaka kumchunguza huyo
mtoto?” “Nitamuuliza mwanangu kwanza, akikubali basi mtoto nitamkubali.
Kwahiyo wewe nenda ukamuulize mwanao, maswala ya kuchunguzwa kwa mwanangu sio
kazi yako. Nora hata baba mtoto ndio angesema nakuja kumchunguza mtoto ila wewe
unikome. Nimesema tokeni kwenye nyumba yangu” Wakati huo aliongea kwa
ukali sana ilibidi Mrs.Peter na Babuu wainuke na kutoka maana mwenye nyumba
alishaonyesha kuchukizwa vilivyo. Sasa walibaki ndani wawili
kama kawaida, Erica na mama yake, kisha Erica akamuuliza mama yake, “Ila
mama kwanini umegoma wasimuone mtoto?” “Sijagoma wasimuone mtoto ila
kauli zao ndio zimefanya nigome, Erica nimewazaa, nimewalea, niwatunza hadi
mmekuwa wakubwa, haiwezekani mtu aniletee fadheha kwenye nyumba yangu mwenyewe,
eti anataka amchunguze mtoto, yeye kama nani? Sijui bibi, si akamuulize mwanae
huko kama ana mtoto huku au la! Wenzie hawasemagi wamchunguze, angeomba kuona
mjukuu wake, angeletewa na ndio hapo angemchunguza yani kashamkubali hata moyo
wa kumletea unakuwa nao, ila mtu kashaweka mashaka umletee amchunguze ili iweje?
Na wewe Erica, kweli kabisa ulikosa watu wote hadi kwenda kuzaa na mtoto wa Yule
mwanamke? Jamani simpendi dah!” “Kwani kakufanya nini
mama?” “Unajua Yule Mwajuma ndio dada wa mama yake Derick” Erica
alishangaa hapo na kukumbuka alipoambiwa na Babuu kuwa alienda kwenye mahafali
maana kulikuwa na ndugu yake, ndio akakumbuka kuwa ni Derick ndio ndugu wa
Babuu, alibaki tu kushangaa kwa mama yake na kumuuliza kuwa
alimfanyeje, “Kheee kumbe ni ndugu na wakina Derick, sasa alikufanya
nini mama?” “Yule mwanamke hana akili kabisa, kipindi nagombana na mdogo
wake hadi nikamfukuza hapa, jamani jamani mwanamke alinitukana huyu sijapata
kuona, nadhani kipindi kile kungekuwa na simu ndio ningeyaoga matusi kabisa.
Kuna kikundi Fulani cha wanawake, tulikuwa vizuri kweli kwenye kukopeshana na
kwenye michango nilikuwa vizuri si ndio aliponifahamia. Kile kikundi tulikuwa
tunakutana kwa wiki mara nne, na kilikuwa imara kweli jamani kila nikikutana nae
mwanamke Yule ni matusi tu, Yule mama hana hata simile, yeye ni kutukana tu.
Mdogo wake alifikia mahali akakubaliana na matokeo ila Yule mwanamke ni kutukana
tu, kuna kipindi hadi tulipigana hadi nikamshangaa kuwa mapenzi ya mdogo wake
yeye anayaingilia nini. Halafu ubaya zaidi, uwiii Yule Mwajuma ni mbea jamani
haijapata kutokea, ni mbea na mnafki, alinitangazia maneno ya uongo hadi
wanawake wote kwenye kikundi wakanichukia, nikaona kikundi kichungu ila sababu
nilikuwa natetea kuhusu mume wangu, sikuachana na mume wangu ila niliachana na
kile kikundi maana lengo lake lilikuwa niachane na mume wangu ili mdogo wake
achukue nafasi yangu” “Kheee makubwa hayo mama” “Yani Yule
Mwajuma sina hamu nae kabisa, halafu watu huwa wanamuamini maneno yake sijui
kwanini, ila Yule mwanamke hafai, alifanya niache na hela zangu kwenye kile
kikundi maana mama yako nina hasira sana, mwenyekiti ilibidi aniletee walipokuwa
wakivunja kikundi huku akisema kuwa mwajuma anahitaji kupafahamu kwangu maana
inaonyesha mdogo wake hakutaka kumleta maana hapendi shari ila huyu mwanamke
sidhani kama kajirekebisha si unamuona hata leo kaja kishari shari na
kimbeambea, simpendi hasirani sijui umeanzaje na wewe kuzaa na mtoto wake
aaah!” Kisha mama Erica akainuka na kwenda chumbani kwake, kwavile jioni
iliingia ikabidi Erica aanze kufanya kazi za pale kwao za jioni kama kuandaa
chakula cha usiku na vitu vingine huku akiwaza sana. Usiku
wakati wa kulala, Erica aliamua kusikiliza redio kwani alijiona hayupo sawa
kabisa, akahisi pengine akisikiliza mahubiri kama mama yake anavyomshauri
ataweza kupata amani kiasi, alipowasha tu akamsikia Yule muhubiri
akisema, “Hakuna kitu chema kama kuomba toba mbele za Mungu, toba
inatuweka karibu na Mungu. Hakuna mwanadamu aliyekamilika, sote tuna mapungufu,
tunatakiwa kuomba toba mbele za Mungu. Toba inafuta makosa yetu na tunakuwa
wapya baada ya toba, kumbuka kutubu mbele za Mungu wetu” Mara simu ya
Erica ikaanza kuita, ikabidi azime redio ili apokee ile simu, alipoiangalia
alikuta ni Babuu ndio anapiga, akapokea ile simu na kuongea
nayo, “Erica, unajua sikukutegemea kabisa kama unaweza kufanya hivyo,
kweli umezaa na Rahim?” “Sasa wewe mpaka umefikia hatua ya kumleta mama
yake Rahim ulikuwa huna uhakika au ni nini?” “Nakuuliza kwa upendo tu,
yani Erica umenichanganya na ndugu zangu wote? Unajua nimemuuliza mamdogo kuwa
kamjuaje mama yako ndio kaniambia kuwa Derick ni ndugu yako, nikashangaa sana
ikabidi nimpigie Derick simu kumuuliza akasema kuwa naye aliwahi kulala na wewe.
Khee Erica, ulilala hadi na ndugu yako? Kaka yako wa damu? Umeshindikana
Erica” Erica aliamua kukata ile simu maana aliona inamletea kizunguzungu
tu, alivyokata tu akapokea ujumbe toka kwa Derick, ilikuwa ni mara ya kwanza leo
maana hakuwasiliana nae kwa muda mrefu sana. Akafungua ule ujumbe na
kuusoma, “Haya sasa kiko wapi, Derick malaya malaya, kumbe wewe ndio
malaya, kweli Erica wa kutembea na ukoo mzima kweli? Nasikia umezaa na Rahim,
hivi huoni aibu? Utasingizia kwangu nilikunywesha pombe, haya na hao wengine
walikunywesha pombe? Mbona mwanamke hujiheshimu wewe? Heshima ya mwanamke iko
wapi kwako? Kweli mwanamke mzuri asiye na akili zitakazoumia ni sehemu zake za
siri, kumbe Erica wewe ni malaya kiasi hiko? Tena ni malaya koko, najuta kuwa na
ndugu wa dizaini yako.” Huu ujumbe uliumiza sana moyo wa Erica na hisia
zake na hata hakujua kosa lake lipi maana kwa kipindi chote alikuwa akitafuta
penzi la dhati kumbe alitembea na ndugu kwakweli aliumia sana roho, alilia sana
alipomaliza kusoma ule ujumbe, alijikuta akisema, “Ooooh Mungu wangu,
hivi ni mimi tu ndiye mkosaji dunia nzima? Hivi ni mimi tu mwanamke nisiye na
akili dunia nzima? Kwanini lawama zote napewa mimi, hawa wanaume mbona na
wenyewe hawajilaumu jamani” Alilia sana, akasikia ujumbe mwingine
unaingia kwenye simu yake, kuangalia umetoka kwa Babuu, akausoma, “Erica
una laana wewe, kutembea na kaka yako ni laana hiyo, na kuniacha mimi ni laana
pia. Ujue mimi ndio nilikuwa mwanaume wako wa kwanza, hukutakiwa kuniacha ila
swala la kuniacha mimi ukajipatia laana ya milele, na itakutafuna hadi unaingia
kaburini” Erica alizima simu yake na kujikuta akilia sana, akakumbuka
mahubiri aliyotoka kuyasikia kwenye simu kuwa ni vizuri kufanya toba, alipiga
magoti chini na kuanza kutubu akisema, “Eeeeh Mwenyezi Mungu, najua
nimekutenda mengi mabaya, nimefanya makosa mengi sana ila yote sababu sikuona
anayenipenda kwa dhati. Naumia moyoni, nilipenda siku moja na mimi niwe na mume
wangu, na maisha yangu na watoto wangu tukifurahi pamoja ila sikupenda maisha
yangu yawe ya majuto kiasi hiki. Naomba Mungu wangu nisamehe kwa yote
niliyoyatenda, naomba laana ninazopewa zisinipate. Amen” Akalia sana
maana mambo yale yalichanganya akili yake, alipomaliza kulia alipanda kitandani
na kulala. Palipokucha aliendelea na shughuli zake za hapa na
pale, mama yake nae alimuangalia na kumuuliza, “Weee mbona macho
yamekuvimba hivyo?” “Hamna kitu mama” “Umevimba sababu ya jana
kuitwa malaya? Kwani ni kweli ulitembea na ndugu wote? Najua bado una mawazo ila
ukitulia njoo uniambie kila kitu mama yako, unieleze kila kitu usinifiche
chochote hata kama kibaya mimi kukijua nieleze tu na nitakwambia cha kufanya,
usiwe na mawazo sana mwanangu” Erica alimuitikia mama yake pale kisha
kuendelea na kazi zake zingine, mchana wa siku hiyo alifika dada yake Bite na
kukaribishwa na mama yao, akakaa sebleni, kisha Erica akafika na kumsalimia dada
yake, alipomuitikia tu alimtupia leseni ya udereva, “Haya, leseni yako
hiyo hapo” Erica alipokea bila kusema chochote kwani bado alikuwa na
mshangao kuwa leseni si alitakiwa akachukue mwenyewe, sasa imekuwaje kuletewa na
dada yake? Kisha dada yake akamwambia, “Haya, kalete funguo za gari
langu” Erica akainuka na kwenda kuleta funguo za gari, kisha akaja nazo
na kumkabidhi dada yake, ambapo dada yake alimuangalia mama yao na
kumwambia, “Unaona mama, unaona” “Nimeona
mwanangu” “Maana tungesema tu ingekuwa kama tunamsingizia, labda
tungemuona James muongo ila unaona uthibitisho
huu!” “Naona” “Haya Erica, shemeji yako alikupa shilingi ngapi
ukasome udereva?” “Laki tatu” “Na alikupa shilingi ngapi
umpeleke mtoto kliniki?” “Laki moja” “Haya, na alikupa pesa
ngapi ya kwenda kumfungulia mtoto akaunti?” “Laki mbili” “Unaona
mama, yani huyu Erica huyu loh!” “Naona mwanangu, yani hata sijui niseme
kwa lugha ipi Erica apate kunielewa” Kwakweli Erica alikuwa kwenye
mshangao tu maana hakuelewa kuwa mambo yote yale yametoka wapi, akaendelea
kumsikiliza dada yake akiongea, “Erica si wewe mwenyewe uliniambia kuwa
James alitaka kukubaka ila ukatumia ujanja kumtoroka? Wewe mwenyewe uliniambia
kuwa shemeji yako alikuwa anakwambia anakupenda, sasa kiko wapi leo? Unaenda
kutangaza shida za nyumbani kwetu kwa shemeji yako kweli? Nilikuonea huruma
mdogo wangu kukaa nyumbani bila kazi, nikakuombea kazi kwa shemeji yako halafu
umeenda kufanya ujinga kwenye kazi jamani! James aliniuliza kuwa uliyezaa nae
yuko wapi? Nikamueleza ukweli na akakuhurumia haswaaa ndio hadi kukupa kazi,
kumbe wewe umetumia swala hilo kama nafasi ya kujiachia kwako, kazini unaenda
kwa kupenda, mara uende mara usiende, ukifika kazini unaanza kueleza shida za
nyumbani sijui mama ana matatizo, sijui hatuna pesa yani umenitia aibu haswaaa
Erica. Umeenda kumuomba hela ya kumpeleka mtoto kliniki, kweli jamani Erica wa
kuomba hela ya kliniki kwa James? Kwani ndio baba wa mtoto wako huyo? Halafu
unaenda kuomba hela ukasomee udereva, kweli Erica hujui kuendesha gari wewe?
Yani sababu Yule ni shemeji yako ndio amekuwa kitega uchumi kwako? Haya leseni
shemeji yako alipie, mara hela ya kumfungulia mtoto akaunti, Erica hivi James ni
mume wako au mume wangu mimi? Mbona sikuelewi wewe mtoto jamani eeeh! Yote tisa
kumi, kumbe gari nimeliacha hapa imekuuma roho hatari hadi kumuomba shemeji yako
funguo ili uendeshe wewe, jamani si ungeniomba hata mimi mwenyewe! Nadhani una
yako kwa shemeji yako Erica. Haya sasa shemeji yako kakufuma unaongea na simu ya
mapenzi ofisini kakusimamisha kazi halafu umemuenezea maneno kwa wafanyakazi
pale eti shemeji yakokambaka rafiki yako ndiomana umeacha kwenda ofisini, Erica
wa kumpakazia shemeji yako vitu kama hivyo kweli? Tena nasikia umejipanga kwenda
mahakamani kutoa ushahidi kuwa shemeji yako kambaka rafiki yako maana tayari
mshafungua na kesi, hivi kumchafulia huko jina mume wangu kwanini Erica?
Sijapenda kwakweli, sijapenda kabisa, haya kata sasa maana ushahidi wote upon a
vithibitisho vipo” Kwakweli Erica hakujua aanzie wapi na aishie wapi
maana hakuelewa jinsi shemeji yake alivyoweza kuyatunga maneno kiasi kile, yani
kwa jinsi dada yako alivyoongea akaona hata aseme vipo bado ataonekana muongo,
alikaa kimya, mama yake akamfokea “Wewe Erica wewe, si unajua sana
kunitia aibu haya kata na haya sasa. Na huyo rafiki yako aliyebakwa na shemeji
yako ni nani?” “Ni Yule Dora mama” “Hivi una akili wewe, (Kisha
akamuangalia Bite na kumwambia) Huyo Dora ndio lile changudoa lililoletwa na
kaka yenu hapa, hivi ukae na Yule kiumbe upange nae jinsi ya kumtafutia kesi
shemeji yako!” “Ila mama, ni kweli alimbaka” “Nyamaza kenge
wewe, hivi Yule Dora ni wa kubakwa Yule? Wapo wa kubakwa ila sio Yule dora, hata
aseme amebakwa na wanaume kumi ni wazi ametaka mwenyewe. Na hata angetaka
mwenyewe, shemeji yako si mchafu kiasi hiko. Haya sasa, hizo hela ulizokuwa
unachukua kwa shemeji yako sijui nyumbani kuna shida ziko wapi?” “Sina
mama” “Yani nimezaa kopo kopo jamani, Erica nilijua wewe ni msomi mahali
wa kuikomboa familia yako kumbe nililipa ada ya bure tu. Kwanza mahafali
hukusherekea, halafu nyumbani umeniletea shahada ya mtoto, umeenda kuzaa na
mtoto wa adui yangu, na sasa unaanza kufanya mambo ya ajabu kwa shemeji yako.
Nilikuuliza mimi kwanini umesimamishwa kazi, ukasema ooh simu sijui shemeji
kanionea kumbe unaongea mambo ya mapenzi ofisini” “Sio hivyo
mama” Mama yake akawa mkali sasa na kuinuka, kisha
akamuuliza, “Sio hivyo nini?” “Amenisingizia” “Wewe
mwenyewe umeleta funguo hapa, na umekubali kupokea pesa saivi unasema ana
kusingizia? Una akili kweli wewe?” “Akili ninazo mama” Mama yake
akamzaba kofi lililompelekea Erica ajihisi kama kizunguzungu maana lilishuka kwa
nguvu sana kwenye uso wake, alijikuta akisema kwa uchungu
sana, “Unanionea mama” “Nakuonea nini na nilishakuonya toka siku
ya kwanza umesema unaenda kuanza kazi kwa shemeji yako!” Mama yake
akamzaba kofi lingine, Erica akainuka na kukimbilia chumbani kwake akajifungia
mlango na kulia sana, alijiona kama mtu asiyekuwa na bahati katika maisha,
alilia kwa muda mrefu hata mtoto wake alipoamka alimkuta mama yake akilia na
kumfanya Yule mtoto nae kuanza kulia. Bite alibaki na mama yake
sebleni ila Bite akamuaga mama yake, “Mama, ngoja niende kuangalia
familia yangu mie mambo hya hapa nyumbani siyawezi. Ila kaa sana na huyu Erica,
aache mambo ya kumsingizia shemeji yake na kutuweka ubaya kwenye
familia” “Usijali mwanangu” Bite aliondoka zake, mama yao
alipoona Erica hatoki chumbani na muda ulienda alishikwa na huruma kwa binti
yake ikabidi aende kumgongea, “Erica mwanangu, toka chumbani tuongee
vizuri. Unajua mama yako nilikupiga sababu ya hasira” Basi Erica alitoka
ila macho yake yalivimba kwa kulia maana hakuwa na furaha hata kidogo, mama yake
alimuhurumia sana, hakupenda tabia ya mwanae aliyoambiwa ila alimuonea huruma
maana hakuna mtoto kati ya watoto wake aliyekuwa na sura ya upole kama Erica,
kwahiyo muda wote ukiambiwa kafanya chochote lazima uhisi kasingiziwa ndiomana
mama yake alijua anajitetea tu sababu anajua ana sura ya upole, akamuita na
kumuuliza tena, “Yaliyosemwa na dada yako ni kweli?” “Mama, si
kweli hakuna ukweli hata mmoja” “Sasa funguo za gari la dada yako
ulikuwa wafanya nazo nini? Na hizo hela ulizokubali kupewa alikupa za
nini?” Ingawa Erica alikuwa na hasira ila alijaribu kumueleza mama yake
kwa kifupi ilivyokuwa hadi akapewa zile hela na funguo za gari, ila hakumueleza
tu kuhusu kubakwa kwa Dora na simu aliyokuwa akiongea nayo. “Ila Erica
mwanangu si nilikukataza wewe, nilikwambia bora kazi utafute sehemu nyingine ila
sio kwa shemeji yako Yule. Umeyaona leo? Na nisingekupiga hapa dadako angeona
nakuendekeza, ila muache afurahi na wakafurahi na mumewe. Nisamehe mwanangu,
siku hizi nitakuwa nachunguza habari zote nitakazo zisikia kuhusu wewe, kuanzia
leo hata shemeji yako aseme kuwa urudi ofisini kwake kufanya kazi hakuna kurudi?
Kama hujapata kazi kaa hapa hapa nyumbani tutakula kama kawaida
kitakachopatikana, sawa? Ila hakuna tena kwenda kufanyakazi kwa
James” “Sawa mama, nimekuelewa” “Basi usilie tena mwanangu,
nisamehe mama yako. Sawa mama eeeh! Unataka kula nini leo usiku nikuandalie
mwanangu” “Chochote tu” “Basi usilie tena mwanangu jamani, sawa
eeeh!” “Sawa” Kisha Erica akarudi tena chumbani ila mtoto
alimuacha na mama yake maana mama yake alisema abakie na mjukuu wake muda huo
acheze cheze nae. Usiku ulipoingia aliamua kuwasha simu yake
maana ni tangu alipoizima jana yake na ndio aliiwasha muda huo ila ilipowaka tu
kuna jumbe ziliingia mfululiza, jumbe moja wapo ilitoka kwa Erick
ikisema, “Nakutafuta mpenzi wangu Erica mbona hupatikani? Nini tatizo?
Basi naomba kesho uwe hewani, nitakupigia simu mchana” Alifurahi sana
kuona jumbe ya Erick, akachukua simu ili ampigie muda huo ila akashangaa kuwa
salio halitoshi na kukumbuka kuwa salio aliloliweka alilimaliza, akaona ujumbe
toka kwa mzee Jimmy, “Erica, umenizimia simu sio vizuri ujue. Katika
maisha yangu hakuna binti niliyetokea kumpenda kama wewe, ila kwa mara ya kwanza
nimetoa zawadi kubwa lakini imerudishwa unataka nikufanyie nini Erica ili unipe
angalau mara moja tu! Ila mimi sio mtu wa kukata tamaa na nitakutafuta
tu” Huu ujumbe ulimkera sana, na muda tu alipomaliza kuusoma mzee Jimmy
alianza kumpigia simu, Erica akaona afanye jambo moja tu la kuzima simu tena na
kujisemea kuwa angeiwasha kesho yake mchana muda ambao Erick angempigia
simu. Aliamua kulala ila kulipokucha tu aliamua kuwasha simu yake kwa
kuhisi kuwa pengine Erick angemtafuta kuanzia asubuhi, ila alipowasha tu
alipokea ujumbe kutoka kwa Rahim na kushangaa sana maana ni siku
nyingi, “Erica ingia kwenye mtandao kuna mambo nataka kujadili na
wewe” Erica akafikiria na kuhisi pengine ni mambo ya msingi, akaamua
kuwasha ile simu yake nyingine kisha kuingia kwenye mtandao na alipoingia tu
alipokea ujumbe kutoka kwa Rahim, “Erica sijapenda, si nilikwambia kuwa
usimueleze chochote mama yangu? Nini kimekufanya ukamueleza mama
yangu?” “Sijamueleza mbona” “Mama yangu sio mjinga Erica, na
kajuaje kama mimi na wewe tuna mtoto eeeh! Erica, kwanini umemueleza mama
yangu?” Kwakweli Erica bado hakumuelewa kabisa Rahim kuwa ni kwanini
hapendi mama yake ajue ukweli, na akaona kuendelea kubishana nae ni kupoteza
wakati akaamua kutoka kwenye mtandao na kuzima simu ile ila baada kama ya nusu
saa alipokea ujumbe wa kawaida toka kwa Rahim, “Erica unajifanya una
kiburi, sasa subiri kiburi chako kitakuponza” Kwakweli bado hakuelewa
maana alihisi tu kuchanganywa na mambo, ikiwa asubuhi bado akiwa anatafakari ule
ujumbe aliotumiwa na Rahim akapigiwa simu na Dora, “Erica, nakuomba hapa
nje kwenu mara moja” Erica alijua tu ni kuwa Dora amekuja kumfata maana
ile ndio ilikuwa siku ya kesi, akaamua kwenda nje ili kumwambia kuwa hatoweza
kwenda nae. Akatoka nje, alivyofungua geti tu akamuona Dora ambaye
alimvutia kwa nje na gafla akamuona mzee Jimmy akija yani kumbe Dora alimpeleka
mzee Jimmy kwakina Erica. Erica alijua tu ni kuwa Dora
amekuja kumfata maana ile ndio ilikuwa siku ya kesi, akaamua kwenda nje ili
kumwambia kuwa hatoweza kwenda nae. Akatoka nje, alivyofungua geti tu
akamuona Dora ambaye alimvutia kwa nje na gafla akamuona mzee Jimmy akija yani
kumbe Dora alimpeleka mzee Jimmy kwakina Erica. Erica akapigwa na
butwaa, halafu Dora akamvutia mkono hadi kwa mzee Jimmy ambapo mzee Jimmy
alitaka amuinguze Erica kwenye gari kinguvu, ila bila kutegemea Erica alianza
kupiga kelele za kuita mama yake kama anakabwa vile, “Mama, mama, mama
nakufa huku mama” Mzee Jimmy akaogopa sana na kumuacha Erica kisha
akaingia kwenye gari yake na kuondoa gari, mama Erica alitoka na kukuta gari ya
mzee Jimmy ikiishia huku pale yupo Dora na Erica, sababu kitendo cha mzee Jimmy
kuondoka kilikuwa cha gafla kwahiyo bado walikuwa wamesimama
palepale. Mama Erica alipotoka alijua labda Dora alimkaba mwanae,
akamfata Dora na kumpiga vibao vya kutosha kisha akamshika Erica mkono na
kumuingiza ndani. Alikaa nae na kumuuliza, “Wewe mtoto umefata
nini nje asubuhi yote hii? Na Yule malaya kakufanya nini?” “Mama, Yule
Dora kweli kama ulivyoniambia ni rafiki mbaya, ngoja nikueleze kwanza chanzo cha
Dora na mimi kuwa karibu.” Erica akamueleza mama yake alivyomsamehe
Dora, na akamueleza jinsi walivyofika ofisini pia akamueleza kisa cha shemeji
yake kutaka kwenda nae kutembea mpaka alivyomualika Dora na kuwakimbia na hadi
Dora alivyomuelezea kuwa amebakwa, “Sasa leo ndio siku ya kesi ya Dora,
alivyosema nitoke yupo nje kwetu nikajua anataka nimsindikize kwenye kesi,
nikatoka ili nimwambie kuwa sitoenda tena, ndio nikashangaa kuwa alikuja na mzee
Jimmy, sijui walikuwa na lengo gani ila Yule mzee alitaka kunipakia kwenye gari
lake ndio nikapiga zile kelele, na zile kelele ndio zilimfanya Yule mzee apande
gari na kukimbiza gari yake” “Khaaa kumbe! Huyo mzee anakutakia nini
mwanangu jamani? Yani hana hata haya jamani, na huyo Dora mwanangu sio rafiki
yani sio rafiki kabisa, ningemuona kipindi mnasoma ningekwambia mapema mwanangu
kuwa huyo sio rafiki, hakufai mwanangu. James nae kweli kabisa alimbaka Dora?
Mweeeh ila wanaume nao sio wa kuwakatalia sana kuwa hawajafanya maana akili zao
wanazijua wenyewe. Erica mwanangu, kuanzia sasa mimi ndio rafiki yako yani
usifanye chochote bila kunishirikisha mimi maana mimi ndio mama yako na mimi
ndio najua ni vitu gani nilipitia hadi kukupata wewe, najua hata wewe hutopenda
kuona Angel akiumia au akipotea, ndio hivyo hivyo na kwangu, sipendi kukuona
ukiumia au ukipotea.” “Sawa mama nimekuelewa ila yote haya ni sababu
nilimsamehe Dora ndio nikawa nae karibu tena, ila nisingemsamehe yote haya
yasingetokea, nilisikiliza yale mahubiri kuwa ni vizuri
kusamehe” “Erica, ni kweli kusamehe ni vizuri sana ten asana kwani hata
kwa Mungu ni mengi tunayatenda ila Mungu ni mwaminifu huwa anatusamehe. Ila
kiubinadamu swala la kusema huyu ni binadamu ana akili za kibinadamu liko pale
pale, kusamehe ni vizuri ila usirudi nyuma tena kusema kwamba huyu mtu
kabadilika maana huwezi jua ya mbele, kusamehe ni kuzuri maana kama kuna cha
kumsaidia utamsaidia tofauti na mtu ambaye hujamsamehe huwezi kumsaidia. Sasa
wewe kumsamehe Dora si kosa ila kosa lako ni kumfanya Dora kuwa rafiki yako tena
wakati unajua fika Dora ni mtu wa aina gani? Na licha ya hivyo, umeweza
kujionea, bado ana tamaa na anaweza kukuingiza kwenye mdomo wa mamba Yule, kuwa
makini mwanangu, mamako nakupenda ndiomana naongea haya” “Asante
mama” Erica alitabasamu na kumuitikia mama yake maana aliona siku hiyo
mama yake amempa maneno ya faraja kuliko siku zote. Akaendelea
na kazi zake za hapa na pale, kisha badae alipomlisha mwanae na kumuacha
akicheza na bibi yake, akaingia chumbani na kuchukua simu yake ambayo kwa
kipindi hiko ilikuwa kama hakimu maana alitumiwa ujumbe wa lawama na kuhukumiwa
tu, alichukua ili kuangalia kama Erick amemtafuta, ila alikutana na ujumbe toka
kwa mzee Jimmy. “Siamini Erica umenidhalilisha kiasi hiki, Erica
umenidhalilisha kweli kwa kosa lipi? Unajua nilitaka kufanya nini kwako? Unajua
nilitaka kuongea nini na wewe? Unajua mimi nina wadhifa gani hadi
umenidhalilisha kiasi hiki? Sitasahau kamwe ulichokifanya leo wewe binti maana
hata sikufikiria kama unaweza kutenda kama hivi.” Erica hakujua hata
ajibu vipi huo ujumbe wa mzee Jimmy na kubaki kimya tu, muda kidogo sasa ndio
akapigiwa simu na erick, pale alijawa na tabasamu zito sana na kuanza kuongea
nae, “Upo sehemu nzuri Erica, kiasi kwamba tunaweza kujadili ishu za
mimi na wewe?” “Ndio nipo sehemu nzuri tu, tunaweza
kuongea” “Sawa, najua sijawahi kukuuliza maana kidogo akili yangu
ilishikwa na sintofahamu ila naomba nikuulize sasa” “Niulize
tu” “Naomba unieleze kwa kifupi kuhusu Angel, yani mwanaume uliyezaa nae
yuko wapi? Ana mpango gani? Anasemaje kuhusu mtoto ili nijue tunaanzia wapi na
tunaishia wapi” Erica akapumua kidogo maana hakuelewa kuwa aanzie
kumueleza Erick sehemu gani ila aliamua kuanza popote tu ilimradi ujumbe ufike
kwa Erick, “Mwanaume niliyezaa nae Angel, alinilaghai na nikahisi kuwa
ananipenda ila nilipozaa tu aligeuka kuwa mbogo na hakutaka mtoto ajulikane na
familia yake hata yeye tangu nizae huyu mtoto sijawahi kumtia tena machoni pangu
yani kwa kifupi hata mtoto hajawahi kumuona tangu azaliwe. Nina mengi sana ya
kuongea Erick ila nasikia uchungu kila nikifikiria” “Aaaah pole sana
Erica, pole sana huyo mwanaume hana akili kabisa yani kuumiza moyo wa malkia
wangu kiasi hiko! Sijapenda, na ulipomuuliza kuhusu swala la kuja kumuona mtoto
alisemaje?” “Mwanzoni alikuwa ananiambia nitakuja nitakuja, ila saivi
inaonyesha hiyo kuja ni ndoto tu maana hata huduma za mtoto kasitisha. Erick,
naomba unisamehe ila sijui hata nisemaje uelewe ninavyojutia” Erick
alimsikia Erica akilia na kweli alijisikia huruma sana na
kumwambia, “Tafadhali Erica acha kulia na futa hayo machozi yako maana
mfariji wako nipo. Kwahiyo kwa kifupi Angel hana baba?” “Naweza sema
hivyo Erick maana baba yake hamjali tena” Erica akawa analia tena, Erick
akamwambia, “Nimesema Erica acha kulia mpenzi wangu. Kumbuka mara ya
mwisho shuleni nilikubusu kuonyesha ishara ya mapenzi yangu kwako, ni kweli
nilikupenda Erica, nakupenda na nitaendelea kukupenda. Hivyobasi swala la Angel
kutokuwa na baba hata lisikuumize kichwa, naomba kuwa baba yake” Erica
alikaa kimya kwani yale maneno kama yaliingia kwenye moyo wake na kuugusa
vilivyo kwani hakuamini kabisa, mpaka Erick aliongea tena, “Erica,
unanisikia kweli? Naomba kuwa baba wa Angel.” “Erick sijui niseme nini,
nadhani ungepasua moyo wangu na kuona furaha niliyonayo moyoni mwangu hata
ungeshangaa, Erick nakubali uwe baba wa mwanangu kwa asilimia zote” “Wow
Erica, sikia nikwambie kitu kingine.” “Niambie tu” “Naomba huyo
Angel umuandikishe majina yangu, namaanisha maana hata kwenye mali zangu nay eye
atakuwa mmoja wapo kama mwanangu, na hata nikifa basi atakuwa mrithi wa mali
zangu” Kwakweli hili swala lilichanganya akili ya Erica, yani hakuelewa
kama Erick anaongea kwa kumaanisha au ni kitu gani na kujikuta hata akishindwa
kumjibu, Erick akasema tena, “Nadhani nimekupa swali gumu, ila nakupa
muda ufikirie na fikiria maisha ya badae ya mtoto wetu. Waswahili husema
ukipenda boga penda na uwa lake, mimi napenda uwa la boga kama ndio boga
lenyewe, nakupenda wewe Erica na ninampenda Angel, pengine hao waliopita kwako
hawakujua thamani yako ni nini ila mimi naijua na sitajivunia kuwa wa kwanza
kwako ila nitajivunia kuwa wa mwisho kwako. Nakupenda Erica” “Nakupenda
pia Erick” “Sikia Erica nikwambie kitu, ni mengi sana tumepitia mimi na
wewe, kutokuwa karibu kumesababishwa sana na maneno ya watu. Sitaki kukubali
kauli ya kusema kuwa watu wanaopendana hawadumu na hawaishii pamoja, najua
inawezekana kama tukiamua kuwa na jambo moja. Erica najua ushafanya yako machafu
mengi tu ila kwavile moyo wako haukuwa na msimamo, na mimi nishafanya yangu
machafu mengi tu sababu moyo wangu haukuwa na msimamo pia. Usikae kusikiliza ya
watu sijui Erick alikuwa malaya, sijui Erick alikuwa anabadilisha wasichana kama
nguo, hayo yaache yalipita ila sasa tuangalie ukurasa mpya wa maisha
yetu” “Sawa Erick nimekuelewa, sitasikiliza ya watu
tena” “Napenda kurudia hili, najivunia kuwa wa mwisho kwako Erica, mimi
ndio najua thamani yako. Nakupenda sana” “Nakupenda sana pia
Erick” Kisha Erick akakata ile simu yani Erica alijikuta akijilaza
kidogo kitandani huku akimfikiria Erick, alijikuta akifikiria kuwa yeye, Erick
na Angel wameongozana wakifurahi na kucheza pamoja, alijilaza kitandani akiwaza
kwa furaha hata hakutaka kuinuka kwani Erick alitawala tu kwenye kichwa chake
kwa muda huo. Mama yake alifanya kumuita tu ila Erica alienda
kwa mama yake akiwa amejawa na tabasamu, huku mama yake akimuuliza kuwa
amefurahi nini ila bado alikuwa na tabasamu tu hadi usiku ulipoingia alikuwa
akitabasamu muda wote. Basi usiku akashika simu yake ili atume ujumbe
kwa Erick, akashangaa akikuta ujumbe mwingine toka kwa Dora, “Yani Erica
ndio umefurahi sasa kwa shemeji yako kukutwa hana hatia juu yangu wakati unajua
fika kuwa shemeji yako alinibaka. Ndio msamaha gani ulionipa huo Erica? Msamaha
wa visasi?” Erica aliamua kumjibu Dora maana aliona sasa anataka
amuwekee mazoea yasiyo na maana, “Dora sikia, niliposema nimekusamehe
sikusema kuwa tuendelee kuwa kama zamani, tena nilikwambia wazi kuwa
nimekusamehe ila hutokuwa rafiki yangu tena. Naona unataka kunipanda kichwani,
sikukutuma ukanywe pombe na shemeji yangu, sikukutuma ulewe hadi usahau kwenda
kwenu. Inawezekana shemeji alikubaka kweli au hakukubaka maana mtu mwenyewe
ulikuwa umelewa, mtoto wa kike unakunywa pombe kama kichaa, utafikiri hukusoma,
tena unikome sitaki mazoea ya kijinga, ukaribu na wewe ni mwisho sitaki unizoee
tena” Akatuma ujumbe huo kwa Dora kisha akamtumia ujumbe Erick kuwa
amekubali mtoto wake atumie majina ya Erick, basi Erick akampigia simu kwani
alikuwa na furaha sana ya jibu lile, “Ni swala la haraka Erica ili mtoto
apate na kadi ya bima ya afya, yani ukishakamilisha tu, nitakuelekeza mahali
upeleke cheti cha kuzaliwa na picha za mtoto ili washughulikie” “Sawa
Erick, kesho tu nitaanza kushughulikia” “Sawa ila naomba nikuombe swala
lingine” “Niombe tu Erick” “Erica, ukiangalia mapenzi yetu
mwanzoni kabisa yalivunjwa na rafiki yako, naomba usiwe na marafiki wa aina
hiyo. Ukiwa na swala linakutatiza bora uniambie mimi, naomba niwe rafiki
yako” “Erick, nishaachana na habari ya marafiki kwasasa, kwahiyo swala
unalosema kuwa wewe uwe rafiki yangu sio ombi maana wewe ni rafiki yangu
tayari” “Kumbuka nakupenda Erica” Kisha Erick akakata simu,
kwakweli Erica alijihisi kama yupo ndotoni, maswala hayo aliogopa kumshirikisha
mama yake maana alihisi kuwa huenda angemkataza wakati yeye moyo wake umeridhia
kumbadilisha mwanae majina, kwani alipenda sana mwanae apate kuthaminiwa kama
watoto wengine. Wakati anatabasamu akapokea ujumbe toka kwa
Dora, “Erica kumbuka ni mambo mangapi nimefanya na wewe, ni mambo
mangapi nimekushirikisha ila leo hii unaongea kama mtu anayetapika? Asante sana
Erica, ila kumbuka unachomtendea mtu nawe utatendewa vilevile tena na
zaidi” “Usinitishe na ujinga wako, tena ukome kuniletea mababu nyumbani
kwetu. Huyo mzee Jimmy tembea nae mwenyewe, simtaki na wala benki kwake siendi
tena” Erica aliona anamzingua tu huyu, akaamua kuweka simu pembeni na
kulala. Kesho yake tu alimuaga mama yake kuwa anatoka kidogo na
kwenda kushughulikia cheti cha kuzaliwa cha mtoto wake ambapo aliambiwa kuwa
kitatoka baada ya wiki moja. Yani wakati huo hata aliacha kufatilia
mambo ya mkataba wa benki kabisa kwani hakutaka kuwa karibu na mzee Jimmy,
ingawa mzee huyo alimtumia ujumbe mara kwa mara kuwa aende benki wakamalizie
hatua za mkataba ila Erica hakutaka tena hata alipopigiwa na Yule meneja napo
hakutaka kabisa maana alijiona anatosha kwa aliyoyapitia. Ilimradi Erick
kajitolea kumtunza mtoto ilikuwa inamtosha kwakweli. Siku aliyoenda
kufata cheti cha mtoto wake, wakati anarudi alikutana na Yule mama ambaye
walikutana dukani akamsaidia kuchukua maji, Yule mama alisimamisha gari yake na
kumuita, “Erica” Erica alienda kwa Yule mama ambaye alijawa na
tabasamu tu, akamsalimia kisha Yule mama akasema, “Yani nilipoteza namba
yako, moyo ukaniuma kweli ila Mungu ni mwema nimekuona tena, ngoja nikuulize
swali, una kazi? Yani unafanya kazi?” “Hapana, nipo nyumbani
tu” “Umesoma mpaka wapi?” “Chuo, nina shahada ya
biashara” “Jamani, ndio huna kazi kweli binti mzuri kama wewe dah!
Sikia, chukua hii kadi yangu ya biashara, wiki ijayo njoo ofisini kwangu na
vyeti vyako” “Asante” Erica alimshukuru sana Yule mama kwani
aliona kama ni kitu cha ajabu ametunukiwa kwa muda huo, kisha akaagana nae na
kurudi nyumbani. Alifika na kujisemea, “Kweli Mungu ana njia
zake za kubariki, nadhani Erick ni baraka tosha katika maisha yangu. Nikijaribu
kuunganisha matukio naona wazi kuwa Erick ni baraka tosha kwangu, kwanza Erick
alinipigia simu nikawa na kimuhemuhe cha kumpigia na kuamua nikanunue vocha,
mama akaamua aniagize na soda ndipo nikakutana na Yule mama mwenye roho nzuri.
Haya Erick kasema nifatilie cheti cha kuzaliwa cha mtoto, natoka kukifata
nakutana na huyu mama na ananiahidi kazi, wow nadhani Erick ni baraka
kwangu” Alitabasamu maana ilikuwa ni furaha kwake. Alirudi kwao,
kwa kipindi hiko mwanae alikuwa ameanza utundu wa kimya kimya kiasi kwamba
alikuwa akirudi tu basi mwanae alichukua mkoba na kuangalia kuwa mama yake
kamletea zawadi gani, bibi yake alikuwa akicheka sana na kusema, “Yani
Angel ananikumbusha kipindi kile wakati wewe mdogo, mtu akikuangalia anakuona
mtoto mpole kumbe una utundu wa kimya kimya ninaoujua mimi tu, sasa mtu hawezi
kudhania kama Angel anaweza fungua mkoba na kupekua ila ona hapo. Hahaha mpaka
apate anachotaka” Kwahiyo Erica alikuwa akinunua matunda mara nyingi
ambapo akifika tu anampa mwanae ili mwanae asimpekue mkoba. Alichukua
mkoba wake na kuingia chumbani ambapo aliweka vizuri CV yake na vyeti vyake,
aliweka kwenye bahasha nzuri kwaajili ya kuvipeleka kesho kwa Yule
mama. Alipomaliza alimpigia simu Erick kuwa kashapata cheti cha mtoto na
picha anazo, basi Erick akamuelekeza mahali pa kupeleka ili mtoto atengenezewe
kadi ya bima ya afya, kwahiyo Erica aliona ni vyema afanye vyote kwa
pamoja. Siku hiyo aliondoka asubuhi kwao na kuanza kwenda
kwenye ofisi ya Yule mama akifata maelekezo ya kwenye ile kadi aliyopewa na
kufika, kisha akaenda mapokezi na kumuulizia, “Una miadi
nae?” “Ndio” “Ngoja nimpigie simu, nimwambie unaitwa
nani?” “Erica” Basi Yule wa mapokezi akapiga simu, Yule mama
alipokea ila alionyesha alikuwa na kikao na kuomba kuongea na Erica, ambapo Yule
wa mapokezi akamkabidhi simu Erica kisha Yule mama akamwambia aache nakala ya
vyeti vyake kwa Yule mtu wa mapokezi, Erica alimshukuru kisha wakakata ile simu
na kumuachia Yule wa mapokezi bahasha ya vyeti vyake halafu yeye
kuondoka. Moja kwa moja alienda mahali ambako Erick alimuelekeza kuwa
apelike vile vitu kwaajili ya mtoto kupata kadi ya bima ya afya. Basi
alifika kama alivyoelekezwa na moja kwa moja alienda mapokezi na kukutana na
mdada ambaye alimsalimia kisha kumuachia vile vitu vya mtoto ambavyo vilikuwa
kwenye bahasha iliyoandikwa jina la Erick nje maana ndio maelekezo aliyopewa na
Erick, “Aaaah sawa, basi kikiwa tayari tutakupigia simu uju
uchukue” “Sawa nashukuru” Basi Erica akaondoka zake, wakati yupo
kwenye stendi ya daladala, kuna mdada alifika mbele yake na huyo mdada
alionyesha kumfahamu Erica ila Erica alishamsahau, ikabidi Yule mdada aanze
kumkumbusha, “Unakumbuka siku ile umefika kwa Bahati nikakupeleka
alipokuwa anaoa Yule Nasma hadi ukaanguka, unakumbuka” Erica alimtazama
huyu mdada na kumjibu, “Nakumbuka ndio” “Vipi, uliweza kuacha
maisha yaendelee? Mapenzi ndivyo yalivyo mdogo wangu, muda mwingine unaumia hata
usipotarajia” “Nishasahau mie” “Basi Yule Nasma saivi ni
mjamzito, yani Bahati hajachelewesha yupo vizuri huyo” Erica aliona huyu
nae yupo kumchanganya tu wakati yeye ameshaanza kusahau mambo hayo, aliamua
kumuaga na kuondoka zake kuelekea kwao, kwani hakutaka kuumiuza kichwa kabisa
kwa muda huo kumfikiria tena bahati aliyemshuhudia akifunga ndoa, kwahiyo
alipanda basin a kurudi kwao ambapo alimkuta mama yake kama kawaida ila leo mama
yake alimwambia, “Mwenendo wako kwa hivi karibuni umenifurhisha sana,
ukienda mahali unawahi kurudi, sijasikia ujinga wa kuleta marafiki wa ajabu
ajabu kama Dora. Mwanangu bora umeachana na aina ile ya marafiki, narudia tena,
mimi ndio rafiki yako wa kweli. Kama una shida yoyote au una jambo lolote
usisite kuniambia mimi rafiki yako wa ukweli” “Sawa mama” Basi
akafurahi sana maana kwa siku hizo alikuwa akiongea kwa upendo tu na mama
yake. Siku hiyo akiwa ametulia tu kwao akapigiwa simu kuwa kadi
ya mwanae tayari hivyo aende kuichukua, aliahidi kuifata kesho yake, kwakweli
Erica alifurahi sana kwani ndio kitu alichokuwa anahitaji kuona mwanae akiishi
maisha yasiyompa mawazo kabisa. Basi kesho yake akajiandaa na kumuaga
mama yake kuwa anatoka kidogo kama kawaida, ila alienda moja kwa moja kwenye ile
ofisi kwaajili ya kuchukua kadi ya mwanae. Alimkuta Yule dada wa siku
ile ambapo alimsalimia kisha akamwambia asubiri, muda kidogo walikuja wadada
wawili na kukaa karibu yake wakati Yule wa mapokezi ameenda kumchukulia kadi ya
mtoto. Mmoja wa wale wadada alimuuliza, “Samahani dada, erti
Erick ni nani yako?” “Kwanini umeniuliza hivyo?” “Nimekuuliza
kwa maana yangu, nijibu kwanza ni nani yako?” Huyu mdada alionekana
akiuliza kwa shari sana, ila Erica akawa mpole na kumjibu ukweli, “Erick
ni mpenzi wangu” “Mungu wangu, haiwezekani yani Erick mimi nimsubiri
kipindi chote hiki anifanye kama mtoto kweli! Unasema Erick ni mpenzi
wako?” “Ndio ni mpenzi wangu” “Hapana sikubali” Yule
dada aliinuka na kumkunja Erica, kwakweli Erica alikuwa kwenye mshangao tu kuwa
imekuwaje leo akunjwe bila sababu, Yule mwenzie akawa anamzuia kuwa asifanye
chochote kibaya, “Hebu tulia na wewe, hujui inavyouma kuibiwa mpenzi,
mimi niibiwe nitulie tu siwezi” Alikuwa akiongea kwa jazba, Erica
hakuweza hata kujitetea toka kwa Yule mdada kwani alionekana ni mkubwa sana
halafu alionekana kuwa na nguvu. Kisha Yule dada alimsukuma Erica ambapo Erica
alitaka kuanguka chini, sema kuna mdada alitokea nyuma yake akawa kama kamkinga,
Erica alipogeuka akamuona Yule mdada kuwa ni Sia yani msichana aliyewahi
kuambiwa kuwa ana mahusiano na Erick ila ndio alimsaidia siku hiyo
asianguke. Alikuwa akiongea kwa jazba, Erica hakuweza
hata kujitetea toka kwa Yule mdada kwani alionekana ni mkubwa sana halafu
alionekana kuwa na nguvu. Kisha Yule dada alimsukuma Erica ambapo Erica alitaka
kuanguka chini, sema kuna mdada alitokea nyuma yake akawa kama kamkinga, Erica
alipogeuka akamuona Yule mdada kuwa ni Sia yani msichana aliyewahi kuambiwa kuwa
ana mahusiano na Erick ila ndio alimsaidia siku hiyo asianguke. Wakati
Erica alikuwa akimshangaa huyu Sia, basi huyu Sia alimvutia Erica nje ya ile
ofisi na kumuuliza, “Kwani umefata nini hapa?” Kabla hajajibu,
Yule msichana aliyekuwa akipambana na erica alitoka nje pia ila Sia alimkingia
kifua Erica na kumwambia Yule msichana, “Ukithubutu kumgusa nitaenda
kusema kwa mkurugenzi, najua unajua siogopi” “Wewe unamtetea huyo kama
nani? Unajua nini kuhusu huyo msichana? Kwa kifupi tu, wewe humpati Erick, wala
mimi simpati wala yeyote humu ofisini aliyewahi kuwa na Erick maana sasa yupo na
huyo msichana” “Hata kama Linah, bado hutakiwi kumpiga huyu
msichana” Basi Yule dada akachukia sana na kurudi ofisini kisha Yule
mwenzie akamfata, halafu Sia akamuomba Erica wasogee mbali kidogo, Erica hakuwa
na ubishi ila alimwambia kuwa hapo alienda kufata kadi, na Sia akamuuliza kuwa
hiyo kadi nani anampatia, “Yule secretary ameenda
kunichukulia” “Jiongeze Erica, huyo mtu kafata kadi mbinguni hadi wewe
utake kupigwa? Kwanza ilikuwaje maana bado nashindwa kupata
muunganiko” “Nilikuja wiki iliyopita kushughulikia kadi ya bima ya afya
ya mtoto, nilielekezwa na Erick kuwa nilete cheti cha kuzaliwa cha mtoto na
picha. Nikafanya hivyo, na jana Yule dada alinipigia simu kuwa nije nichukue,
nikamwambia nitaenda leo na ndio nilipofika ameenda kunichukulia” “Pole
sana, yani nakupa pole sana. Huyo aliyekushughulikia wiki iliyopita lazima ndio
aliyemwambia Yule Linah maana anajua kwa ofisini humu hakuna mwanamke wa Erick
mkorofi kama Linah, pia leo hakuwa na sababu ya kwenda kukuchukulia mbali, ni
wazi alienda kuwaita wale wakorofi. Sasa swala la kuipata hiyo kadi niachie
mimi, ndio nitaifatilia na utakuja kuichukua kwangu, Yule secretary anakuuzisha
sura tu” “Kwahiyo siipati leo?” “Hebu subiri
kidogo” Erica alisubiri pale nje kisha Sia aliingia kwenye ile ofisi,
kwakweli Erica alikuwa akiwaza vitu vingi sana, akakumbuka maneno ya Erick kuwa
asimsikilize mtu yeyote Yule zaidi yay eye, na je asisikilize yeyote kweli kwa
hali kama hiyo iliyompata siku hiyo? Alikuwa na maswali mengi sana, muda kidogo
Sia alirudi na kumwambia, “Itabidi uje keshokutwa na hiyo kadi
nitakukabidhi mimi, ila usimwambie Erick. Nipe namba zako” Basi Erica
akampa Sia namba zake, ila Sia alimwambia kuwa anahitaji kuongea nae haswaa ili
amwambie la moyoni mwake, Erica alitulia akimsikiliza, Sia
alianza “Nakumbuka mara ya mwisho ilikuwa ni kunisaidia mimi niweze kuwa
na Erick, imekuwaje tena Erick yupo na wewe?” Erica alikuwa anajiuma uma
tu, ila Sia akaongea tena, “Mimi sio mpambanaji kama Yule aliyepambana
na wewe, ila tu nilishtuka kusikia kuwa na wewe ni mpenzi wa Erick. Sijui
mlianzaje, najua nilikosea mwenyewe kusema upewe namba za Erick wakati namjua
mpenzi wangu vizuri alivyo kuwa kisimpitie mbele. Na ubaya zaidi ni macho ya
Erick, najua yanawachanganya wasichana wengi sana maana huwezi kuchomoa
akikutazama usoni, sijui wewe na Erick mlianzaje ila Erick bado ni mpenzi
wangu.” Bado Erica alikaa kimya tu, kisha Sia akaendelea
kuongea, “Kwa kifupi, hakuna rangi ambayo Erick hajaiona, hakuna umbile
ambalo Erick hajapitia, mnene, mwembamba, saizi ya kati, mrefu, mfupi, mweupe,
mweusi, maji ya kunde yani kila aina ya mwanamke unayoijua wewe duniani Erick
amepitia. Mimi kuwa na Erick hadi leo nimejitoa muhanga hata wote wanalijua
hilo, nishagombana na wengi sana, ila niliwaambia jambo moja tu kuwa mimi siwezi
kuachana na Erick hata wafanye nini na wao wajijue kuwa ni wapitaji tu kwa Erick
maana mimi ndio wake. Upo? Je upo tayari na wewe kupitiwa tu?” Erica
bado alikuwa kimya huku moyo unamuuma balaa, kisha Sia aliendelea
kuongea, “Usifikirie Erick anagombewa na wanawake sababu ana hela
nyingi. Ni kweli wakina Erick kwao ni matajiri, hata yeye ana hela haswaaa ila
kinachofanya Erick agombewe na wanawake sio hela ila Erick ni mwanaume wa
tofauti sana, ni mwanaume ambaye kila mwanamke atatamani kuwa na aina yake ya
mwanaume, Erick anajua kubembeleza jamani kupita mwanaume yeyote uliyewahi
kumuona ulimwenguni. Yani kubembeleza kwa Erick ndio mwisho wa matatizo, Erick
anabembeleza haswaa na akilitaka lake ni lazima alitimize, anajua kujali Yule
mwanaume na anajua kupenda. Mimi nishawahi kumfumania Erick mara nyingi tu tena
hivi kwa macho sio kwa kuambiwa, tena muda unamfumania anaweza hata kukutimua
ila mkikutana wawili uwiii utaona kama dunia ni mali yako peke yako maana
mwanaume atakubembeleza Yule yani utasahau machungu yote ya kumfumania na utaona
Yule mwanamke aliyekuwa na Erick ndio mbaya, najua hata ukimueleza haya Erick
atakubembeleza wewe hata utasahau kama nishakutana na watu kibao ambao ni
wanawake wa Erick” Muda huu Erica aliamua kuongea kidogo, na kumuuliza
Sia, “Sasa nifanyeje?” “Cha kukushauri kama hupendi kuumia
achana na Erick, mimi nishazoea maudhi ya Erick na kila kitu kwani hadi marehemu
baba yangu wakati anakufa aliniambia mwanaume wa kukuoa ni Erick tu maana
alimfahamu. Mama yangu nae huwa anamuulizia Erick tu, siwezi kumuacha Erick
kwani mara zote mama huulizia kama nawasiliana na Erick, mama yangu uzima wake
unategemea furaha iliyopo kati yangu na Erick. Sikia nikwambie Erica, hii ofisi
unayoiona ni mali ya baba yake Erick, na Erick ndio kila kitu kwenye hii ofisi
japo aliteua wakurugenzi wa kusimamia hii ofisi maana yeye anashughulikia mambo
yake mengine South, sikia nikwambie karibia asilimia kubwa ya wadada wanaofanya
kazi humu basi wamewahi kutembea na Erick maana ukiona kamtafutia mtu kazi humu
ujue ni wake. Narudia tena, cha kukushauri achana na Erick” Kwakweli hii
habari ya leo ilikuwa mbaya sana kwa Erica maana alihisi kama kapigwa ganzi vile
mwilini, alijihisi vibaya mno, aliamua kumuaga Sia na kuondoka
zake. Erica alienda taratibu kama mtu aliyechanganyikiwa,
kwanza hakuelewa kuwa huyu Erick amemtakia nini yeye ikiwa ana sifa mbaya kiasi
kile, alijiuliza sana moyoni kuwa Erick anafaa kuwa mume wake? Na kama hafai,
jina la mtoto kambadilisha ili iweje? Alihisi kizunguzungu haswaaa, aliingia
kwenye daladala huku akiwa na mawazo sana. Alijilaza kwenye siti ya daladala,
pembeni yake walikuwa wamekaa wakaka wawili wakizungumza ingawa alikuwa na
mawazo sana ila aliweza kusikia mazungumzo ya wale wakaka, “Sisi wanaume
bhana, unaweza ukahangaika na wasichana wa kila aina ila kuna mmoja tu
anayekukosha yani kwa huyo hupumui jamani, unajikuta tu huna usemi ila wengine
wote hawa huwa unawaambia nakupenda nakupenda, ila kuna mmoja tu kipenda
roho” Mwenzie akawa anacheka sana na kuongezea, “Ndiomana
unaweza kukuta mtu ana wake hata wanne ila kama kipenda roho hayupo kati ya wale
wanne bado hawezi kutulia maana bado hajampata Yule anayemuhitaji” “Na
akiwepo lazima wenzie waone wivu maana yeye ndio atasikilizwa sana haijalishi ni
mkubwa au mdogo” Wakawa wanacheka ila yale maneno yao yalimuingia sana
Erica, wakashuka, alitamani kujua kuwa unajuaje kama mwanaume huyu kipenda roho
wake ni huyu ila akashindwa kuwauliza hadi wameshuka. Na yeye alivyofika
alishuka huku akijiuliza kama kati ya wanawake wa Erick basi ni yeye tu
anayependwa au kuna mwingine? Maana kama kubembeleza imekuwa ni sifa ya Erick,
je atajua kuwa anapendwa kwa kubembelezwa wakati mwanaume Yule ni kawaida yake
kubembeleza? Huo ulikuwa mtihani mkubwa sana kwake, akafika nyumbani kwao
amechoka kimawazo na kifikra hata mama yake alimuona hali aliyoingia nayo mwanae
na kumuuliza, “Tatizo ni nini Erica?” Hakutaka kumwambia ukweli
mama yake maana alijua kuwa mama yake kama angejua ukweli basi angemsema sana,
kwahiyo akamdanganya tu, “Nilienda kufanya usahili leo, tumepewa
mtihani, maswali yalikuwa magumu sijui kama kazi yenyewe
nitapata” “Mbona hukuniambia mwanangu? Kumbe ulienda kufanya usahili wa
kazi! Ila muamini Mungu kuwa anaweza yote hata usijali, kama ridhiki yako ipo
basi ipo tu” Erica alimuitikia mama yake pale kisha akaenda chumbani
kwake ambapo mtoto wake naye alikuwa amelala basin a yeye akajilaza pembeni ya
mtoto wake huku ana mawazo mengi sana. Jioni ya siku hiyo
aliamka na kufanya kazi za hapa na pale ila ilimradi tu muda uende, na usiku
ulipoingia alienda kulala, ila kabla hajalala alipigiwa simu na Erick,
aliitazama na kutamani hata kutokuipokea ila aliipokea tu kishingo
upande, “Erica, mbona unaongea kwa kupooza kiasi hiko? Tatizo ni nini
mpenzi?” “Hakuna tatizo” “Hapana najua tatizo lipo tu, Erica
nimekuzoea haupo hivyo niambie tatizo ni nini eeh! Mimi ndio mpenzi wako na mimi
ndio rafiki yako, unaponificha mimi utamwambia nani mwingine?” Erica
alijihisi kama machozi yanamlengalenga na kujikuta akishindwa kukaa na lile
swala moyoni, akamwambia, “Erick, kila siku unasema nakupenda Erica nami
naamini hilo. Umeniambia nimbadilishe mwanangu majina niweke yako nami nimefanya
hivyo, kweli leo Erick naenda kukutana na msululu wa wasichana zako
jamani!” Erica alikuwa akilia hata Erick alimsikia kwenye simu, kisha
Erick akamwambia, “Kwanza futa machozi yako Erica, hayo machozi yana
thamani kubwa sana kwangu, sipendi kuona malkia wangu akilia sababu ya
wapumbavu. Sikia Erica, wewe ni msichana pekee nikupendaye hakuna mwingine, ni
wewe tu katika maisha yangu. Erica nilikwambia toka siku ile kuwa utasikia stori
zisizofaa kuhusu mimi sijui Erick malaya sijui nini na nini ila yote ni sababu
ya kutafuta penzi la dhati ambalo lipo kwako Erica. Wewe ndiye uliyefanya mimi
niwe malaya, ndiomana hata swala la wewe kuwa na mtoto nimesamehe maana mimi
ndiye nimefanya wewe uzae na mwanaume mwingine, Erica sikia nakuomba tufute yote
ya nyuma na tuonane wapya, nione Erick wako ni mpya kabisa kwako, na mimi
nakuona wewe ni mpya kabisa kwangu, umenisikia Erica mama yangu
eeh!” Erica alinyamaza ila akauliza tena, “Lakini Erick unajua
inaumiza sana, ni kweli sitamani kujua ya nyuma ila inaumiza sana kuona mlolongo
wa wanawake zako, na inasemekana hujaachana nao” “Erica, niamini mimi
sina mwanamke mwingine zaidi yako. Wewe ndio maisha yangu, wewe ndio pumzi
yangu, wewe ndio kila kitu kwangu, bila wewe siwezi Erica? Unataka nitangetange
hadi lini wakati furaha yangu ni wewe? Wewe ndio mwanamke wa maisha yangu, ni
wewe tu Erica, hakuna mwingine zaidi yako” Erica alitabasamu kwa maneno
matamu aliyopewa na Erick na kujikuta akiongea nae kwa furaha sana kwani aliweza
kuamini kuwa kweli yeye ni chaguo la Erick, kisha Erick aliendelea
kuongea, “Tafadhali Erica, usisikilize maneno ya watu nisikilize tu mimi
mumeo. Na siku nitakayo kuoa wewe hao wanaokupa maneno ya uongo watabaki midomo
wazi na hawataamini maana nitamuoa mwanamke nimpendaye, Erica nakupenda sana,
usisikilize maneno ya watu” “Nimekuelewa Erick” Kwakweli furaha
ya Erica iliweza kurejea tena, hadi muda wanatakiana usiku mwema na Erick
alikuwa akitabasamu tu. Baada ya hapo aliona kuwa huo muda atalala kwa furaha
sana, akapokea na ujumbe toka kwa Erick, “Mpenzi wangu Erica, lala
ukijua kwamba nakupenda sana. Wewe ni wa thamani sana katika maisha yangu,
hakuna kama wewe. Mimi ndio rafiki yako, nieleze kila kinachokutatiza, usisite
kuniambia, usiondoe furaha yako sababu ya maneno ya watu. Wewe ndio chaguo
langu, nakupenda sana” Erica alitabasamu na kuibusu simu yake huku
akiikumbatia na kulala akimuwaza tu Erick kwenye kichwa chake hadi ndoto yake
alitamani itawaliwe na Erick tu. Asubuhi na mapema aliamka na
kufanya shughuli zake za hapa na pale hata mama yake alimshangaa kuwa ndio huyu
jana aliyerudi bila furaha ila leo ni anatabasamu muda wote kumbe alikuwa
akifurahishwa na maneno ya Erick tu. Siku hiyo mchana alifika dada yake
Mage, alienda kuongea na mama yao kwahiyo alimuacha dada yake aongee na mama yao
kisha yeye alienda chumbani akicheza cheza na mwanae maana alikuwa na furaha
sana siku hiyo. Wakati yupo chumbani Erick alipiga simu na kumwambia
Erica, “Upo na Angel hapo karibu, mpee simu niongee na mwanangu. Mwambie
babake anataka kumsalimia” Erica alitabasamu na kumpa Angel simu ambaye
alionekana kuchekelea pia, basi Erick aliongea nae vile vile kitoto maana Angel
hakujua maneno yote, bado alikuwa kwenye kujifunza kuongea. Alipomaliza
Erica alichukua simu na kutabasamu kisha Erick akamwambia, “Siku hizi,
kila siku jioni nitakuwa napiga simu umpe mwanangu niongee nae,
sawa” “Sawa nafurahi sana” “Furaha yako ndio furaha yangu,
nawapenda sana familia yangu” Yani Erick alikata simu ila bado Erica
alijawa na tabasamu lisiloisha kwani kuna muda mwingine alijiona ni mwanamke
mwenye bahati sana ulimwenguni kwa kumpata Erick anayejua kupenda, kwa wakati
huo hakutaka tena kukumbuka swala la kuambiwa kuwa Erick kubembeleza ni kawaida
yake, alitaka tu kuamini kuwa Erick anampenda basi na si
vinginevyo. Jioni dada yake aliaga, kisha Erica alienda kuongea na mama
yake, “Dada yako kasema mumewe anataka kuja kulipa faini, nimewakubalia
maana hata baba yenu alisema wakijifunza basi atakubali. Nimeshamwambia
utaratibu wa kumuelekeza mumewe kwahiyo hivi karibuni watakuja, siku hiyo
tutakuwa wote hapa kama familia na tutafurahi pamoja. Nitampigia na kaka yenu
simu, aache wazimu wake wa kupenda matatizo” “Ndiomana alisafiri bila
kuaga sababu ya kumkatalia kumuoa Dora eeeh!” “Yani Yule akili zake loh!
Alisafiri bila kusema, eti kafika kule ndio ananiambia mama nilisafiri, ila mimi
ni mzazi siwezi kumuwekea kinyongo mtoto. Unajua kumuwekea kinyongo mtoto ni
kumfungia milango ya baraka eeeh! Nakufundisha wewe sababu ni mzazi pia, usije
ukathubutu kumuwekea kinyongo Angel, mpende, msamehe na umthamini” “Sawa
mama” Basi akapanga pale na mama yake, na namna jinsi watakavyofanya
kuwapokea wageni wa dada yake, ila ilikuwa ni furaha tu maana Erica alijawa na
tabasamu. Siku iliyofuata wakati anafanya shughuli zake za hapa
na pale alipigiwa simu na Yule mama aliyekutana nae dukani, akapokea na
kumsalimia kisha Yule mama akamwambia, “Unaweza kuja ofisini muda
huu?” “Ndio naweza mama” Basi alivyokata simu, Erica alijiandaa
haraka haraka maana hakutaka kuchelewa kwenda ofisini kwa Yule mama ukizingatia
anauhitaji mkubwa sana wa kazi, akatoka na kumuaga mama yake, “Wapi tena
Erica?” “Kule nilipofanya usahili ndio wameniita mama” “Mungu
akutangulie mwanangu” “Asante mama” Basi Erica aliondoka pale
kwao na moja kwa moja kuelekea kwenye ofisi ya Yule mwanamama. Alifika
pale mapokezi na kama kawaida mtu wa mapokezi alimzuia hadi awasiliane na
muhusika, ndipo alipoambiwa kuwa amruhusu aende. Erica alikuwa na
kimuhemuhe haswaaa maana swala la kupata tena kazi kwa urahisi vile lilikuwa ni
furaha kwake, akafika na kugonga mlango wa ofisi ambapo Yule mwanamama
alimkaribisha. Aliingia akiwa amejawa na tabasamu na kumsalimia tena
Yule mama ambaye alimkaribisha kukaa kwenye kiti cha mbele yake, “Karibu
sana Erica, nakupenda, navutiwa na ucheshi wako” Erica alikuwa
akitabasamu tu na kujibu, “Asante mama” “Kwakweli inaonyesha
kwenu wana furaha sana kwa uwepo wako, sijui kama huwa unachukia. Nimekupenda
toka siku ya kwanza, nilikuomba unichukulie maji dukani, ulinichukulia kwa
tabasamu, uliniletea kwa tabasamu. Nilipokutana na wewe tena ulikuwa ukitabasamu
hata nikiongea na wewe kwenye simu unatabasamu, leo umekuja umejawa na tabasamu.
Nitakuita binti tabasamu” Erica aliendelea tu kutabasamu na tena amepata
na sifa basi ndio tabasamu lilionekana vilivyo hadi Yule mama alifurahi zaidi.
Kisha akamwambia, “Nimekuita leo ili tu nikuone, maana ningeweza
kukwambia kwenye simu ila nilitaka tu nikuone tena. Sina haja ya kukufanyia
usahili wowote, labda nikuulize swali dogo, ungependa mshahara tukulipe kiasi
gani?” Kwakweli hili lilikuwa swali la mtego sana kwa Erica, na
alijikuta akishikwa na uoga kujibu ila alijikaza kujibu, “Mmmh mshahara,
mnilipe tu kiasi kile kitakachoendana na kazi yangu” “Kama kiasi
gani?” “Kiasi mnachoona kinafaa mimi kupatiwa, kulingana na maisha na
kazi ninayofanya” Huyu mama akacheka kiasi na kusema, “Umeogopa
kusema kiasi eeeh! Ila ungekuwa huru tu, basi usijali utalipwa kulingana na kazi
kama ulivyosema. Basi wiki ijayo njoo uanze kazi” “Wow, asante mama
yangu” “Jisikie vizuri tu, wiki ijayo njoo. Ukifika njoo ofisini kwangu
moja kwa moja, nikuonyeshe eneo la kazi” “Asante
sana” “Usijali” Kisha Erica aliagana na huyu mama halafu yeye
akaondoka kurudi kwao. Moja kwa moja alienda kwenye stendi ya daladala
ili apande basi la kurudi kwao, ila akakutana tena na Yule mdada wa siku ile
ambaye alikuwa akimueleza habari za Bahati, “Mambo Erica!
Mzima” “Mi mzima tu” “Erica, sikia nikwambie kuhusu
Bahati” “Nilishakwambia kuwa hayo mambo nishaachana nayo” “Hata
kama ila ngoja nikwambie hili, unajua nini Yule Bahati inavyoonyesha si mapenzi
yake kumuoa Nasma, inavyoonyesha bahati hata hakumpenda Nasma ila kuna uchawi
umetumika” “Uchawi?” “Ndio uchawi, yani Yule Bahati wamemfanyia
madawa inaonyesha ni ndugu wa Bahati wakishirikiana na baba yake Nasma maana
hatukuwahi kumuona Bahati akiwa karibu na Yule binti, halafu Yule baba kwa
ushirikina ni noma, anasifika sana kwa ushirikina, yani Bahati ile sio akili
yake, ile ni limbwata ndiomana ukimuona Bahati tu utajua maana hana furaha na
ndoa yake, kwanza amekonda yani badala ya kupendeza sababu kaoa ila Bahati
kaisha na kuchukiza. Ana hela ila kama hana hela yani yupo yupo tu mpaka
tunamuonea huruma” “Asante kwa maelezo yako dada, ila kwasasa inatosha
sihitaji tena kujua kilichotokea kwa Bahati” “Sikia nikwambie, ni wewe
tu wa kumsaidia Bahati, wewe ndio unaweza kumtoa Bahati kwenye madawa
aliyofungwa” “Nawezaje sasa?” “Hapo ndio sawa, sasa mimi huwa
nipo maeneo haya ya stendi sababu napika chakula. Siku tupange uje mapema
nikuelekeze cha kufanya ili kumkomboa Bahati” Erica akamuitikia tu huyu
mwanamke, kisha huyu mwanamke akamuomba Erica namba ya simu ambapo Erica
alimpatia na kuondoka zake akielekea kwao. Alifika na kumkuta mama yake,
ambapo baada ya salamu alimuuliza, “Eti mama, kuna dawa ya
mapenzi?” “Mapenzi hayana dawa mwanangu, kwanini umeuliza?” “Si
watu husema kuna limbwata, na mtu anafanya maamuzi sababu ya
limbwata” “Ni kweli limbwata lipo ila huchukua muda mfupi tu kuisha na
likiisha utaomba ardhi ipasuke, penzi la dawa si penzi zuri, penzi zuri ni lile
penzi la dhati. Kuna mtu unataka kumfanyia limbwata?” “Hapana mama
siwezi fanya hivyo, nimesikia tu kwa watu ndiomana nikaamua
kuuliza” Basi Erica aliongea na mama yake pale, kisha kufanya shughuli
zake zingine. Muda wa kulala ulipofika, Erick alipiga simu na
Erica alipokea, muda huo mtoto Angel alikuwa macho maana siku hiyo alichelewa
kulala, na Erick aliposikia mtoto anaongea ongea akamwambia Erica, “Mpe
simu mwanangu nimsalimie” Lile neno lilikuwa linamfurahisha sana Erica,
akampa simu Angel na Angel nae alikuwa na tabasamu tu maana kila aliposikia
sauti ya Erick mtoto alionekana na furaha sana. Kisha Erica akachukua
simu, “Huwa unaongea vinini na mtoto mbona huwa anacheka muda
wote!” “Jamani huwa namwambia mwanangu jinsi ninavyompenda na kumjali,
vipi bima ya afya ya mtoto ushachukua?” “Bado” “Kwanini bado
wakati waliniambia ni tayari?” “Sijui ila nilienda wakaniambia
bado” “Au ndio ulienda siku ile uliyoanza kuniuliza yale maswali na
kuweka mashaka kwa upendo wangu kwako? Erica, jiamini mama nakupenda sana. Uwe
unaniambia kama kuna yeyote kakutenda chochote nitashughulika nae, narudia
usisikilize maneno ya watu. Nisikilize mimi tu, nenda kesho ukachukue kadi ya
mtoto” “Sawa” Erica alikubaliana nae, hata hivyo akakumbuka kuwa
siku ile Sia alimwambia aende kesho kutwa ambayo ndio itakuwa kesho, kwahiyo
alimuitikia tu Erick na kulala huku akitabasamu kama
kawaida. Palipokucha, alijiandaa kama kawaida na kumuaga mama yake, ila
leo mama yake hakumuuliza kuwa anaenda wapi na ile ikawa faraja kwake maana
hakujua hata siku hiyo angemwambia uongo gani. Aliondoka kwao akielekea
kwenye ile ofisi ya wakina Erick. Alifika ofisini ila kabla
hajaingia alikutana na Sia mlangoni ambaye alimsalimia kisha
akamwambia, “Kheee una kumbukumbu wewe, yani mi nilishasahau ila subiri
hapo nje nikuletee” Basi Erica alisubiria, baada ya muda mfupi Sia
alirudi na kadi ya mtoto ila sura yake haikuwa ya furaha kama mwanzo, kisha
akamwambia, “Tuseme Erica umezaa na Erick? Yani umekuwa na mahusiano nae
hadi umezaa nae?” Erica aliitikia kwa kichwa akimaanisha kuwa amezaa
nae, kwakweli Sia hakupendezewa kabisa, alimpa Erica ile kadi huku
akilalamika, “Yani Erick kanitoa mimba ngapi? Na sio mimi tu, ni
wasichana wengi kawatoa mimba maana ana daktari wake kwaajili ya hiyo kazi,
halafu leo hii kaenda kuzaa na wewe aliyekujua juzi? Aaah hii sio sawa kabisa,
Erick sio binadamu, hii sio sawa naumia sana, nadhani unaweza kuelewa jinsi gani
naumia. Napenda kukwambia, kuzaa kwako na Erick sio kusema umempata Erick moja
kwa moja, ngoja nikukumbushe tu kwamba mimi binafsi siwezi kumuacha Erick,
nampenda sana” Erica aliweka ile kadi kwenye mkoba na aliamua kuondoka
tu kwani alijua kukaa pale zaidi ni kuzua mengine, aliondoka na kuelekea
kwao. Kufika kwao kama kawaida, mtoto wake alichukua mkoba na kufungua
akabwaga vitu vyote chini, bibi yake alikuwa akicheka tu kama kawaida ila wakati
Erica kainama aokote vitu vyake, mama yake aliiona ile kadi ya bima ya afya na
kuichukua, akaisoma na kushangaa kisha akamuukliza Erica, “Wewe si
ulisema Angel baba yake ni Rahim! Mbona huku inasomeka Angel
Erick?” Erica aliweka ile kadi kwenye mkoba na aliamua
kuondoka tu kwani alijua kukaa pale zaidi ni kuzua mengine, aliondoka na
kuelekea kwao. Kufika kwao kama kawaida, mtoto wake alichukua mkoba na
kufungua akabwaga vitu vyote chini, bibi yake alikuwa akicheka tu kama kawaida
ila wakati Erica kainama aokote vitu vyake, mama yake aliiona ile kadi ya bima
ya afya na kuichukua, akaisoma na kushangaa kisha akamuukliza
Erica, “Wewe si ulisema Angel baba yake ni Rahim! Mbona huku inasomeka
Angel Erick?” Erica alikaa kimya kwanza kwani hakujipanga kumjibu mama
yake kwa wakati huo, mama yake akamuhoji tena kwa ukali, “Wewe Erica,
hebu nijibu hii ina maana gani? Ungeandika jina la marehemu baba yako
nisingeshangaa ila umeandika jina la mtu mwingine, hebu nieleze
nikuelewe” “Nisamehe mama” “Yani wewe Erica ni mwepesi sana wa
kuomba msamaha, unajua fika jambo unalofanya si sahihi ila unajua silaha pekee
unayotembea nayo ni kuomba msamaha. Sasa siwezi kukusamehe mpaka unipe ukweli wa
hili jambo, imekuwaje huyu badala ya kuwa Angel Rahim amekuwa Angel
Erick?” “Kwahiyo mama ningemuandikisha Angel Rahim?” “Hebu
niondolee ujinga wako hapa, huyo Rahim si amegoma kuja hapa nyumbani. Sijakutuma
kwenda kumuandikisha jina lolote mtoto, nilikwambia nitamtambua huyo Rahim
endapo atafika hapa nyumbani na si vinginevyo, ila nieleze kwanza hii ya Erick
imetoka wapi?” Erica alikaa kimya na kufanya mama yake aongee
zaidi, “Unajua wewe Erica muda mwingine huwa najiuliza kuwa akili zako
hizo umezitoa wapi maana huwa unazijua mwenyewe tu. Unafanya kitu unachotaka
wewe, nilikwambia kuwa kitu chochote kabla hakijatokea nishirikishe, ila umeamua
kwenda kubadilisha jina la mtoto hata bila ya kunishirikisha mama yako. Haya
niambie ukweli huyu Erick ni nani na kwanini mtoto aitwe Angel
Erick?” Erica alijifikiria na kutambua kuwa ingawa atapewa lawama na
mama yake ila ni lazima amwambie ukweli, aliamua kujitoa muhanga kwa muda huo
kuwa liwalo na liwe. “Mama, ni kweli Angel baba yake ni Rahim na wala
sikuongopa kusema baba wa Angel ni Rahim ila kama unavyojua mama huyo Rahim
hanijali, wala hajaonyesha uwepo wake toka nina mimba hadi mtoto kakua sasa
sijaona tumaini lake lolote ndio kwanza hata kuongea na mimi siku hizi hataki.
Kuhusu Erick sasa, ni kijana anayedai ananipenda sana na kaahidi kuja kunioa,
aliposikia nina mtoto akamkubali kuwa mwanae pia na kasema atamtunza ndio
akaniambia nikamuandikishe mtoto majina yake.” “Kwanini
hukunishirikisha?” “Nisamehe kwa hilo mama” “Unajua kama
umemuuza mtoto wewe kwa mambo yako ya kijinga, una uhakika gani kuwa huyo Erick
atakuoa? Una uhakika gani? Wangapi wamekudanganya? Una uhakika gani anakupenda?
Mpaka leo unashindwa kujua uongo wa wanaume Erica? Yani wanaume walivyo halafu
kirahisi rahisi tu akubali mtoto, akwambie mbadilishe na jina labda kama kuna
kitu cha ziada anachotaka kutoka kwako ila sio mapenzi tu
nakataa” “Nisamehe mama, sasa nitafanyaje?” “Usiniulize mimi
utafanyaje mjinga wewe ila muulize huyo mwanaume uliyemuuzia mtoto kuwa
utafanyaje? Mwambie mama yangu kaona kadi ya mtoto kwahiyo itakuwaje? Erica,
huwa sipendi ujinga yani sipendi ujinga kabisa ndiomana hukunishirikisha huu
ujunga wako maana ulijua wazi ningeukataa na kweli nisingeweza kukubali, ushauza
mjukuu wangu sasa mwambie huyo shababi wako aje nyumbani hapa afanye harakati za
harusi sio kujimilikisha mtoto wakati hana kitu, shamba walime wengine mazao
avune yeye, huo ujinga sitaki kabisa kuusikia.” “Sawa
mama” “Niitikie tu na ujinga wako huo, kuna muda huwa unaniudhi hadi
sijui natamani nini, yani Erica wewe dah!” Erica aliendelea kumuomba
msamaha mama yake kisha kwenda chumbani kwake. Jioni kama
ambavyo Erick aliahidi kuwa atakuwa akipiga simu kila jioni aongee na Angel
ndivyo alivyofanya na kwa jioni hiyo. Alipoongea tu na Angel, Erica
alishika simu na kuanza kuongea nae, “Erick, leo nilenda ofisini
kuchukua kadi ya mtoto” “Aaah umefanya vizuri, tena nilitaka nikuulize
kuwa hujachukua tu!” “Ila sio hiko kilichofanya nikwambie kuwa nimeenda,
kuna lingine” “Lipi tena hilo Erica?” “Kwanza napenda utambue
kuwa na mimi ni binadamu nina moyo, nina wivu na kila kitu kwahiyo naumia sana.
Ni kweli umesema nisisikilize ya watu ila kuna vitu vinaniumiza sana, Erick
nasikia wewe hakuna mwanamke ambaye atakupitia usimuache? Kweli hiyo ndio sifa
bora ya mwanaume?” “Erica, sijakuficha kitu chochote, nilikueleza kila
kitu kuwa utasikia mengi kuhusu mimi sijui Erick malaya na mengine kibao ila
yote haya ni sababu sikuwa na penzi la dhati. Nilihitaji penzi la dhati,
nilihitaji kumpata Yule ninayempenda ambaye ni wewe, kote huku nilikuwa
nazunguka kuwa pengine nitapata pumziko la moyo, ila pumziko la moyo wangu lipo
kwako Erica. Sikupenda kuwa muhuni, sikupenda kuwa na wasichana wengi ila sababu
nilikuwa na stress za mapenzi huku nikiwaza kuwa nitapata pumziko la moyo. Erica
ni wewe ndiye nikupendaye, wewe ni mwanamke wa maisha yangu” “Swala la
kunipenda mimi sio mwisho, ila swala ni kuwa hawa wanawake zako utaachana nao
lini?” “Erica, kitendo cha kusema nimekubali kuwa mtoto wako awe mtoto
wangu ujue kwamba hao wanawake wote hawana nafasi kwangu. Ni wanawake wangapi
wazuri nimekutana nao? Ni wanawake wangapi wenye watoto nimekutana nao? Ni
wangapi hawana watoto ila bado moyo wangu upo kwako. Hao wote hawana nafasi
kwangu, wewe ndio maisha yangu, nielewe Erica, hivi naanzaje kusema mwanao
umuandikishe majina yangu wakati sikutaki? Kumbuka leo na kesho, Angel ana haki
kwenye mali zangu maana nimemuhesabia kama mwanangu, na katika vitu vyangu
nimeanza kuweka uwepo wake, kwa mfano ningekuwa sikuhitaji hivi nijitoe kwaajili
ya mtoto kwa lipi? Erica elewa nakupenda, na nampenda Angel kama mwanangu,
kuanzia siku niliyokwambia umuweke Angel jina langu, kwenye moyo wangu
kulishabadilika kuwa na mimi ni baba kwasasa, nina mtoto anaitwa Angel. Kitu
gani kingine kinakusumbua mama?” “Kitu kingine, mama yangu ameoana kadi
ya mtoto na amesema kama wewe ndio baba wa mtoto basi uje nyumbani ujitambulishe
na unioe” “Wow, hilo ni swala jema sana kwenye masikio yangu, Erica
usiwe na mashaka na mimi, maana mimi ndio mume wako. Unatakiwa kuniamini mimi,
kuna mambo nayaweka sawa na nitakaporudi utanitambulisha kwa familia yako name
nitakutambulisha kwa familia yangu, kisha tutaoana yani hakuna tatizo juu ya
hilo kabisa. Mwambie bimkubwa aondoe mashaka, mimi nakupenda nay eye ni kama
mama yangu vilevile nampenda” Maneno ya Erick yalimpa faraja Erica na
kujikuta akifurahi na kusahau yote aliyoulizwa na mama yake, kisha akaagana na
Erick. Kesho yake mapema kabisa, alipigiwa simu na Dora, kisha
Erica alipokea na kumsikiliza, “Erica, kumbe ulisimamishwa kazi pale kwa
shemeji yako!” “Ndio, nani kakwambia?” “Dunia haina siri Erica,
nasikia ulifumaniwa unafanya mapenzi ofisini na mfanyakazi mmoja. Kweli Erica
ndio unajifanya mtakatifu wakati unafanya mapenzi hadi ofisini!” “Wewe
Dora wewe, umetoa wapi hizo habari jamani? Mambo ya uongo kama hayo huwa mnaenda
kuyatunga wapi nyie watu?” “Erica, mimi siijui ofisi yenu na wala
siwajui watu wa pale ofisini ila kuna mtu kaniambia tu kuwa wewe na huyo kaka
mmesimamishwa kazi maana mlikutwa mnafanya mapenzi ofisini” “Basi
makubwa” “Sijakwambia kwa ubaya ila nimekwambia kwa wema tu, Erica
unakataa kuwa na watu wenye pesa zao uwe tajiri ila unaenda kuharibu maisha yako
na msaka tonge kama wewe. Kweli kabisa hukuona guest au, kwenda kufanya mapenzi
ofisini? Tamaa gani hiyo?” “Inatosha Dora, kwaheri” Kisha Erica
akakata simu maana alihisi inampa tu hasira, alijiuliza sana kuwa ni nani
kamuenezea taarifa hiyo ya kufanya mapenzi ofisini, katika mambo yote aliyowahi
kuyafanya hajawahi kufikiria kufanya mapenzi ofisini kwahiyo swala la
kusambaziwa habari hiyo lilimchanganya kiasi, ila badae alifikiria akaona
pengine Dora anatafuta namna ya kuwa nae karibu kwa kutunga habari za uongo
maana hakufikiria kwa ofisi ile ya shemeji yake kama kuna mtu wa kusambaza
habari za namna ile, kwahiyo aliachana na mambo ya kuambiwa na
Dora. Aliendelea na kazi zake tu, mchana wa siku hiyo mama yake alimuita
na kuanza kuongea nae, “Kuna habari nimepata Erica, kwakweli kama mama
yako zimenishtua sana na sitaki ziwe za kweli. Niliahidi kukuamini basi naomba
nikuamini kuhusu hili na uniambie ukweli” “Kitu gani hiko
mama?” “Bite kanipigia simu, amesema mume wake alikuwa akimficha siku
zote kisa cha kukusimamisha wewe kazi, ila jana baada ya kumbana bana kaamua
kusema ukweli. Hivi kweli kabisa Erica unaweza kufanya hivyo?” “kufanya
nini mama?” “Nasikia shemeji yako alikufuma kumbe, alikufuma wewe na
mfanyakazi mwingine mkifanya mapenzi ofisini, kwakweli sitaki kuamini Erica
unanifanyia vitu vya aina hii, unataka niweke wapi sura mama
yako?” Erica alifikiria na kuweza kuoanisha maneno aliyoambiwa na Dora
pia, kiukweli ilimchukiza sana ila ilibidi aongee kwa busara na mama
yake, “Mama, napenda nikwambie mimi mwanao siwezi kufanya kitu kama
hiko. Sijafikia hatua hiyo maana si kukudhalilisha wewe bali nitakuwa
najidhalilisha na mimi pia, ila najiuliza sana hivi huyu James ananitakia nini
mimi? Au kwavile ananisingizia vitu na mimi nanyamaza kimya? Huyu mtu nadhani
anaelekea pabaya na hashindwi kuniharibia mambo yangu mengi maana ameamua, na
mimi nitafanya jambo” “Unataka kufanya nini Erica? Usiniletee ujinga,
Yule ni shemeji yako, unapaswa umuheshimu” “Hata mimi nahitaji heshima
mama, kwanini kila siku anisingizie maneno mabaya? Kwanini anifanyie hivi?
Kwakweli sipendi yani sipendi kabisa” “Hata kama hupendi, mshtakie Mungu
tu, ila kama hayo mambo hutendi nashukuru sana. Usitake kuweka ligi na shemeji
yako, umenisikia?” “Sawa mama” Erica alirudi chumbani kwake huku
akifikiria mambo mengi sana, “Huyu shemeji anataka kunipanda kichwani,
ushemeji gani huu kunidhalilisha kila siku maana kila inayoitwa leo
ananidhalilisha sasa na mimi nitamdhalilisha tu na atakoma na tabia yake hiyo,
kwakweli na mimi nina moyo kama wengine siwezi kukubali kudhalilishwa na uonevu
huu siutaki kwakweli” Akawa anawaza cha kumfanya shemeji yake
adhalilike. Ulipofika usiku mama yake alimwambia
tena, “Erica usisahau ni Jumamosi hii ndio dada yako Mage na mumewe
wanakuja kulipa faini na kukamilisha mambo mengine kwahiyo familia yote
itakuwepo. Nishamwambia Tony atakuja Ijumaa yani sijui mambo ya kupika
itakuwaje? Maana siku zishaenda, unajua leo ni Alhamisi eeeh! Kwahiyo kesho ni
Ijumaa kaka yako atakuja, halafu kesho kutwa Jumamosi yani hata sijui mambo ya
chakula nifanyeje?” “Kwani umealika watu gani mama?” “Mmmh
siwezi kualika watu wengi mwanangu, ni mimi, Mage na mumewe na ndugu wa mumewe
watatu kisha watoto wa Mage wote. Bite na mume wake, na Yule mdogo wangu ambaye
hajagi kunisalimia ila Jumamosi atakuja, na Yule shangazi yenu maana hao
niliwaeleza yote wanajua” “Aaaah sawa, wajomba je?” “Tena ukae
kimya, niite wajomba zako nizue mapya hapa eeeh! Niliyonayo yananitosha,
ukibahatika kuolewa basi wajomba zako watakuja kwenye harusi yako, kwanza hii ni
upatanisho tu kwahiyo sio swala la kutaka watu wengi, hao hao
wanatosha” “Sawa mama” “Sasa nawaza kuhusu
chakula” “Usijali mama, tutapika tu mbona watu sio wengi hao, kwa haraka
haraka watu hao hawazidi ishirini, mbona chakula kinapikika tu” “Utapika
wewe eeeh!” “Hahahah usijali mama” Basi Erica alitabasamu tu na
mama yake ila kichwa chake kilikuwa na mipango mingi sana. Akaingia
chumbani kwake kwa lengo la kulala ila akajiwa na wazo na kuona kuwa asilale
bila kufanyia kazi wazo lake, akachukua simu yake na kumpigia shemeji yake
James, “Hallow shemeji nina mazungumzo na wewe ila napenda dada
asisikie, sijui upo nyumbani?” “Ndio nipo nyumbani ila dada yako kalala,
ngoja nitoke chumbani nikupigie tuongee vizuri” Kisha akakata ile simu,
Erica akajiandaa maneno ya kuongea na shemeji yake, kisha shemeji yake akampigia
simu na Erica akapokea, “Habari James” “Wow umeniita James muda
huu Erica, nimefurahi sana. Sipendi unavyoniita shemeji” “Huwa nakuita
hivyo ili dada asisikie. Ila kuna jambo nataka kuongea na wewe” “Jambo
gani hilo Erica kipenzi changu?” “James unanionea sana, unanisingizia
vitu vingi sana ambavyo hata sijafikiria kufanya, kweli mimi wa kusema umekuta
nafanya mapenzi ofisini jamani! Mbona unataka kunichafulia jina? Lini utaacha
kunichafulia jina kama hivi jamani, au unataka nifanye nini?” “Mbona
kitu kidogo erica, nataka kufanya mapenzi na wewe, hivyo tu basi. Nipe tunda
uone kama nitakuchafulia jina tena” “Lakini mimi si mdogo wa mkeo
jamani! Mimi ni shemeji yako” “Ya shemeji ndio tamu, hujui hilo Erica?
Kila siku nakuimbia wimbo mmoja kuwa nakupenda sana Erica, yani upendo
ninaokupenda wewe hata dada yako hafikii, yani Erica nipe tunda tu nitatulia na
hutosikia tena nikikuchafulia popote pale” “Sawa, nipo tayari kukupa
hilo tunda” “Erica unasema kweli? Hata siamini, kweli
Erica?” “Ndio kweli nipo tayari ila kuna jambo nataka unifanyie
kwanza” “Jambo gani?” “Jumamosi kuna wageni nyumbani, nimepewa
kazi ya kupika na mama ila naona uvivu kwakweli halafu hiyo Jumamosi ndio
nitakupa tunda kwahiyo nikipika nitachoka sana. Kwahiyo naomba uandae watu
wapike na watuletee chakula tu nyumbani” “Erica, hilo ni swala rahisi
sana kwangu, sema lingine. Walete chakula cha watu wangapi, na vinywaji je? Yani
mwambie mama asiwe na wasiwasi kwa swala la chakula na vinywaji, sitaki uchoke
kabisa mrembo wangu” “Sawa, chakula cha watu ishirini. Halfu ombi
lingine, nilikuwa naomba uniletee funguo za gari ya dada unajua alininyang’anya
eeeh! Wakati ulinipa mwenyewe, tena ukiniletea nikabidhi mbele yake kuwa
umejisikia kunipa tu gari maana dada nahisi ameanza kunionea
wivu” “Erica, hilo ni swala dogo sana kwangu, hata gari mpya ungetaka
ningekununulia. Niambie kingine unachotaka” “Nataka uniletee na pesa,
unajua pesa hujanipa siku nyingi sana. Nilikuwa sikuombi unanipa mwenyewe ila
leo nimekuomba niletee, laki tano uniwekee vizuri kwenye bahasha” “Erica
unanisisimua sana, malizia kingine unachotaka mama” “Halafu tunda unajua
nitakupea wapi?” “Eeeeh wapi?” “Sijui, panga
wewe” “Hotelini” “Tatizo nyumbani nitaaga vipi?” “Sikia
Erica, mimi nitamwambia Bite kuwa nahitaji kwenda na wewe mahali tukachukue
mzigo kisha tutaenda zetu hotelini kujilia raha” “Sasa nyumbani
tutawaonyesha mzigo gani tukirudi?” “Vya kuchukua vipo vingi Erica? Yani
wewe niachie mimi, dah natamani hata hiyo Jumamosi ingekuwa kesho, nina hamu na
wewe dah!” “Usijali James umenipata” “Nakupenda
Erica” Basi Erica akakata ile simu na kufurahi na roho yake pia
akafurahi alivyoweza kujikaza kuongea na James maana alichoshwa kutungiwa habari
za uongo na kutokusikilizwa kila anapoeleza kuwa anasingiziwa. Baada ya
hapo ndio akaamua kulala sasa maana moyo wake ulikuwa na
furaha. Kesho yake aliamka na kufanya kazi zake kama kawaida,
kisha akamfata mama yake na kumwambia, “Mama tusihangaike tena kuhusu
chakula cha wageni maana shemeji James amesema kuna wapishi wa hotelini wataleta
chakula na vinywaji” “Jamani James, ana moyo wa upendo huyu kijana
jamani dah! Mungu amzidishie, si unaona shemeji yako alivyo halafu wewe ulitaka
kumuwashia moto jana, kama anakusingizia si yeye mwache akusingizie cha msingi
na muhimu anafanya vitu vinavyofaa kwenye familia yetu” “Sawa
mama” Basi Erica akafanya mambo yake ya siku hiyo hadi kaka yake
alipokuja na kumpokea huku wakijiandaa kuhusu kesho kwaajili ya wageni na
kufurahi nyumbani Jioni Tony alimuita mdogo wake ili kuongea nae
kidogo, “Erica, bado una chuki na Dora mdogo wangu
jamani?” “Kaka huyo msichana hafai, unajua hafai yani hafai kabisa.
Najua mapenzi hayaingiliwi ila huyo msichana hafai, kama huamini
subiri” Erica alimpigia Dora simu na kuweka sauti kubwa kisha akaanza
kuongea nae kiurafiki ili kaka yake aweze kusikia kuwa Dora ni mtu wa aina
gani, “Unajua Dora sina ugomvi na wewe ila swala la kutaka mimi nilale
na Yule babu uliyelala nae ndio silipendi” “Erica kwani tatizo liko
wapi? Kwani ukilala na Yule babu anaondoka nayo? Mbona mimi nimelala nae na nipo
vilevile? Tena kwa taarifa yako hata jana nimtafuta hadi nimelala nae
tena” “Mmmh Dora jamani, hujionei huruma ujue yani ulibakwa nab ado
umemtafuta huyo babu mara mbili kulala nae, akikufanyia kitendo kibovu
je?” “Nikifanyiwa kitendo kibaya na huyu babu haitaniuma sababu mzee ana
pesa, sio Yule shemeji yako kanibaka, kaniingilia kimwili hata hela hajanipa nab
ado kesi karuka yani Yule shemeji yako amenikera sana. Ila Erica subiri uone
mchezo Yule shemeji yako si anajifanya mjanja, nitampata tu mimi na atakaa
kwenye kumi na nane zangu na atajuta” “Unampango wa kufanya nae
nini?” “Subiri Erica, nitakwambia tu. Kanidhalilisha sana, kwani
angeniomba kistaarabu ningemnyima? Nisingemnyima nap engine hata ningekuwa
nyumba ndogo yake” “Mmmh Dora, inamaana kaka yangu humtaki
tena?” “Atafute hela kwanza, kipindi kile nilimtaka sababu nilitaka ndoa
ila nyie mlivyozingua nikaona bora niwe vilevile kama zamani tu” Tony
akamuomba Erica akate ile simu, ilibidi Erica akate simu kwakweli ilionyesha
kumchanganya sana Tony kiasi kwamba hakuongea kitu ila aliamua kwenda kulala tu.
Ila kwa upande wa Erica alishukuru kufunguka kwa Dora kwani kumesaidia kaka yake
kujua ni mwanamke wa aina gani alikuwa akimng’ang’ania. Kisha baada ya
kukata tu akapigiwa simu na Erick kuwa aongee na Angel kiasi kwamba Angel
alizoea kuongea na Erick na alikuwa akifurahi sana anapoongea nae. Mama
yake Erica hakujua kuwa Erica anawaza nini sana ila kumbe Erica bado alikuwa
anawaza swala la kumdhalilisha shemeji yake kama ambavyo humdhalilisha yeye kwa
kusema maneno ya uongo. Muda wa kulala ulifika na walienda kulala huku
Erica akiwa bado na mawazo ya mambo ya kesho
yatakavyokuwa. Jumamosi ilifika na Erica aliamka mapema kabisa
kufanya usafi na kila kitu, kisha wageni wao kuanza kufika ambapo katika wageni
wa shemeji yake wa dada yake Mage yani wale watatu alishangaa kuona mmoja wapo
ni mfanyakazi wa James, akamsalimia alikuwa ni mdada na aliitwa
Linda. Baada ya kukaribisha wageni sebleni, Erica alitoka kidogo nje na
Yule Linda ili ajaribu kuulizia kuhusu habari juu yake. “Samahani Linda,
samahani kwa kukuuliza hili. Eti kuna habari gani ofisini imeenea kuhusu mimi?
Sikujua kama una undugu na shemeji yangu kwa dada Mage, karibu sana, ila naomba
niambie ukweli kuhusu hili. Yani kipi kinasikika kuhusu mimi kusimamishwa
kazi?” “samahani Erica, najua mimi na wewe hatujazoeana ila kuna habari
pale ofisini hadi kila mtu ameshangaa kuwa wewe umefanya vile ilihali hunaga
hata mazoea na mtu” “Ni habari gani?” “Tumesikia kuwa, wewe na
mlinzi mlifumwa ofisini mkifanya mapenzi. Mmmh kila mtu ameshtuka, ila samahani
kukwambia hivi” “Aaah usijali” Kisha wakarudi ndani na harakati
zingine zikaendelea, ambapo Bite alifika na mumewe na walikuwa na furaha pia
wakajumuika na wale wengine huku mambo ya kulipa faini yakiendelea na kila kitu
kisha wakaja wale wa chakula na vinywaji, kwakweli watu walikula na kunywa na
kusifia sana kwani ilikuwa ni furaha haswaa. Kisha wale wa vyakula na vinywaji
wakaondoka na kuacha pale vinywaji na nyama ambazo nazo zilikuwa kwenye bajeti
ya kile chakula, kwahiyo waliondoka na vyombo vyao tu maana shughuli zao
ziliisha. Walipomaliza James alimuita Erica na Bite na kumkabidhi Erica
funguo za gari huku akisema kuwa ameona vyema Erica kumiliki lile gari, Bite
hakupinga hata kidogo maana Yule ni mdogo wake. Ila Erica akasema na
mama yake aitwe ili naye aone mwanae akikabidhiwa hizo funguo, kwahiyo mama yao
aliitwa na hakupinga pia kwani kwa siku hiyo alikuwa na furaha
sana. Wakarudi ndani huku wakiendelea kunywa na kula nyama, James
alikuwa akimtumia ujumbe Erica kuwa wanachelewa kufanya mambo yao ila Erica
akamwambia kuwa wasubiri subiri watu wapungue pungue kwakweli ilikuwa ngumu sana
kwa James kwani alikuwa na uchu uliopitiliza, ikabidi amwambie mkewe kuwa kuna
mzigo inabidi akachukue na Erica, mama yao alisikia na kuuliza, “Kwanini
asiende na Tony?” James akasema, “Hapana mama, inabidi
nikachukue na Erica” Erica alikubali, kisha akainama kama kumnong’oneza
James ambapo James kuna bahasha aliitoa mfukoni kwake na kumkabidhi Erica,
halafu Erica aliinuka na kwenda chumbani kwake aliporudi aliwaomba watoto wote
watoke nje maana kuna jambo la muhimu anataka kuongea na wakubwa mule ndani,
kwahiyo watoto wote walitoka nje. Erica aliwaomba wale wakubwa watulie
na wamsikilize, kisha akasogea kwenye redio yao na kuunganisha simu yake na
redio halafu akaanza kusikilizisha sauti ambapo ilikuwa ni sauti yake na ya
James, kumbe maongezi ya siku ile yote Erica aliyarekodi kwenye simu
yake. Kwakweli Bite alihisi kama kuzimia kwa yale
maongezi. Kila mmoja ndani alibaki mdomo wazi, huku
James akiinamisha kichwa chini maana alikuwa kadhalilishwa haswaa, akataka
kuinuka ili aondoke ila Erica akamshika mkono na kusema, “Sasa leo, sema
ule uongo wako unaotungaga kwaajili yangu kwenye familia yangu. Waambie yale
yote unayosemaga kuhusu mimi, sijui niliwahi kukutaka sijui nilikutega yani
hakuna cha kukwepa” James hakujiandaa kwa chochote kwa muda huo kwahiyo
hakuweza kujibu chochote alishangaa sana kuwa Erica katoa wapi ujasiri wa
kufanya vitu vya namna hiyo maana hakumfikiria kama kuna siku angeweza
kumdhalilisha namna hiyo. Kisha Erica akaendelea kuongea, “Sikuwa na
haja na funguo za gari na wala sikuwa na haja na pesa ila nimetaka yote haya ili
wajue kuwa wewe una jambo lako kwangu ndiomana huishi kunisingizia mambo
mbalimbali” Wakati Erica anataka kuongea, mama yake akainuka na kumvutia
Erica chumbani maana hali ya mwanae Bite ilikuwa inabadilika kila muda toka
asikilize yale mazungumzo, kwa wakati huo ni Mage ndio alikaa karibu na Bite
huku James akiondoka kwa aibu. Erica alipelekwa na mama yake chumbani,
akaanza kuongea nae, “Mwanangu, yameisha. Mbona kumdhalilisha hivyo
shemeji yako?” “Mama, hata mimi kazoea kunidhalilisha kila siku
kunizulia mapya kwanini? Leo zamu yake, tena nimemuhurumia nilitaka
nimdhalilishie chumbani kabisa mmuone ujinga wake, ila nimemuheshimu sana
kuwasikilizisha redio tu, aache ujinga wake” Kisha mama yao alitoka tena
na kumchukua Bite kwenda nae chumbani maana Bite alionekana kukosa raha na
kutokujitambua kabisa, alipoingizwa chumbani tu alijikuta akianza kulia na
alilia kama amefiwa kwahiyo mama yake ndio akafanya kazi ya
kumbembeleza. Kwakweli ilikuwa ni aibu sana ambayo imefanywa na Erica,
hakuna aliyefikiria kama Erica angeweza kufanya kitu cha fedheha kiasi hiko tena
kwa wageni. Ilibidi mama Erica aende kusema shughuli imeisha
ili kila mmoja aondoke, “Haya ni mambo ya kifamilia kwahiyo msijali
tutayasuluhisha kama familia” Kwahiyo ilibidi waondoke na wawache pale
kama familia tu ambapo hata mume wa Mage ilibidi amuache Mage tu kisha yeye
kuondoka na watoto zao. Kwakweli mama yake Erica aliona aibu sana kwa
siku hiyo, wageni walipoondoka walimuita Erica sebleni na kuanza kuongea nae kwa
karibu maana Bite alikuwa kachanganyikiwa kabisa huku akibembelezwa tu na mama
yao. Alianza mama yao kumsema Erica, “Unajua Erica ulichofanya
si kitendo cha kiungwana, hata kama shemeji yako mbaya ila sio kumdhalilisha
hivi mbele za watu kweli mwanangu!” “Mama, na mimi ni binadamu unafikiri
siku ile umenipiga bila kosa nilifurahi? Nikaacha yapite, khee mtu hakomi
anakuja kunizushia na mengine, mtu huyu nimeona sio wa kumchekea maana hashindwi
kuharibu hata siku nataka kuolewa, bora ijulikane moja tu. Yeye si alimwaga
mboga, basi mimi nimemwaga ugali” “Sasa hali ya dada yako Bite
umeiona?” “Nimeiona mama, ila Dada Bite anatakiwa kujua anaishi na mtu
wa aina gani, tulimfuma siku ile na msichana wa kazi nikamwambia dada kila kitu
kuwa shemeji alitaka kunibaka ila dada akaenda kulishwa sumu na shemeji
kanichukia hadi mimi, kwakweli kleo sijakubali kabisa. Tena ngoja niwamalizie
lingine, Yule Dora alibakwa na James na tena alimuingilia kinyume na maumbile,
huyo ndio mume anayeishi na dada” Walishika vichwa maana hata mama yake
aliyembishia siku ile lakini kwa mambo ya siku hiyo hakuwa na jinsi zaidi ya
kushangaa na tena kusikia alimuingilia kinyume na maumbile ndio akashangaa
zaidi, Mage alisema, “Kwakweli huyu James hafai, mama hakuna sababu ya
kumlaumu Erica tena kafanya vizuri sana maana hata mimi Bite alinipigia simu
kuwa Erica kakutwa akifanya mapenzi ofisini, nikasikitika sana na kujiuliza kuwa
mdogo wetu kawaje kumbe ni James ndio anamuenezea Erica sifa mbaya, na amemuonea
sana sababu Erica nae alikuwa msiri mno kwahiyo James hakufikiria kama ujinga
wake tungeujua na uthibitisho kabisa.” Cha kushangaza wakati wote
wanaongea maneno tofauti tofauti, Tony alianza kucheka ikabidi mama yao
amuulize, “Sasa na wewe Tony unacheka nini? Kuna kinachochekesha
hapa?” “Hapana mama, ila nimecheka kwasababu zangu. Kwanza kuanzia leo
Erica nitamuita foma kiboko ya uchafu, jamani Erica eeeh mdogo wangu
sikutegemea, umemaliza kuniumiza moyo jana, halafu leo umehamia kwa Bite.
Natumai mage mumeo yupo vizuri maana kama mchafu wa tabia mtahadhalishe kabisa
maana Erica atamsafisha” “Kwahiyo wewe umefurahi kwa shemeji yako
kudhalilishwa na Erica?” “Mama, Yule hajadhalilishwa wala nini ila tabia
yake imejulikana. Ila mdogo wangu Erica nakupongeza sana, jamaa kakupa gari kwa
hiyari yake, kakupa laki tano keshi, na leo katulisha tumekula hadi kujimwagia
na bado kaumbuliwa. Khaaa niacheni nicheke kabisa, kweli mwanamke hatabiriki,
kumbe ulikuwa unamrekosi kaka wa watu Erica jamani! Ngoja nikanyooshe miguu
kidogo” Akainuka na kutoka kwahiyo pale alimuacha mama yao, Erica, Bite
na Mage. Na muda kidogo Erica nae akaenda chumbani kwake ambapo mwanae alikuwa
amelala tayari kwahiyo alimuacha pale mama yake amalizane na watoto
wake. Kwa muda huo Erica hakutaka kujiona kama amekosea maana
shemeji yake ameshamdhalilisha sana, kwahiyo aliona kafanya sawa kabisa,
akachukua simu yake akakuta Erick kashampigia kama mara tatu hivi, na kukumbuka
ile ahadi yake ya jioni kutaka kuongea na Angel, ikabidi ampigie simu mwenyewe
kwani kwa bahati nzuri alikuwa na salio. Aliongea nae na kumwambia kuwa
Jumatatu anaanza kazi kwahiyo simu awe anampigia usiku kuanzia saa
moja, “Jamani Erica, utakuwa unanikatili mno” “Sasa nitafanyeje
Erick na ndio kazi za watu. Uwe unanitumia meseji kwa sana” “Utajibu
meseji zangu” “Nitajitahidi niwe najibu” Kisha Erick aliendelea
kumsisitiza Erica kuwa atarudi tu na kufika kwao kujitambulisha, kisha akaagana
nae ili alale. Lla alivyokata simu tu akapokea ujumbe toka kwa Rahim na
kushangaa sana kuwa bado Rahim anamkumbuka, “Erica, ingia facebook nina
shida na wewe, ni muhimu sana” Kwakweli Erica hakutaka kuchanganya akili
yake kabisa, zaidi zaidi akaweka ile simu pembeni na kujilaza tu kwani hakutaka
hata kujua kuwa Rahim anataka amuandikie ujumbe gani, kwa kifupi alishatumbukiwa
nyongo na majibu ya Rahim kiasi kwamba hakutaka kumsikia
tena. Kulipokucha, Erica alitoka chumbani kwake na kumkuta mama
yake yupo mwenyewe maana hakutoka nje tena toka ule muda alioenda chumbani,
akamsalimia na kuanza kuongea nae, “Mama, kwahiyo wakina dada waliondoka
kumbe!” “Ndio waliondoka” “Dada Bite je?” “Alikuwa
anakataa ila nikamwambia ndoa ni uvumilivu, si alichagua mwenyewe kuishi na aina
ile ya mwanaume, akamvumilie tu yakimshinda atarudi ila hana furaha
kwakweli” “Mama samahani kwa kilichotokea jana, ila mama nilichoka
kudhalilishwa na shemeji, na kwa hakika asingeacha kunidhalilisha maana ndio
tabia yake, na hapa nyumbani mnamnyenyekea kwahiyo kila anachosema ni ndio.
Kwakweli mama sikuweza kuvumilia ule uonevu maana ni uonevu kwangu, mtu kila leo
anidhalilishe kwa mantiki gani? Na mimi nimemdhalilisha aone uchungu wa mtu
kudhalilishwa, tena bora mimi nimemdhalilisha kwa ukweli wa tabia yake. Ila dah
mama mmenisema sana jana kiasi kwamba sikuweza kuvumilia kuwasikiliza na kwenda
zangu chumbani, naomba unisamehe tu” “Erica nawe hujanizoea tu mama yako
jamani! Jana nilikuwa nakusema ili Bite aone na mimi nimeumia ila kwa upande
wangu nimefurahi sana maana hata mimi sikupenda ile tabia ya kijinga jinga
anayoifanya mara akusingizie hiki mara kile mwisho wa siku angeweka uhasama kati
yako na dada yako ila kwavile tumejua ukweli wa mambo ni rahisi na nimemfundisha
hapa Bite jinsi ya kuishi na mwanaume wa aina ile, walee mtoto bado mdogo
Yule” “Sawa mama, kwahiyo tutamuita Dada Bite ili nimkabidhi zile pesa
za mumewe?” “Weweee tumpe za nini, kitakachorudishwa hapo ni funguo tu,
napo hakuna kurudisha mpaka aje kuomba msamaha tena kwangu ndio nitakwambia
umrudishie hiyo funguo. Ujinga ujinga sitaki kabisa. Ila pesa iliyotoka hiyo ni
malipo ya kukutangazia vibaya mwanangu, hairudishwi hiyo maana kashakutangazia
sana vibaya. Haya kachukue laki mbili unipe mama yako” Erica alicheka
sana maana alijua na leo ni kama zile hela za Mzee Jimmy ambazo mama yake
alisema warudishe ila za leo kagoma kuwa hazirudishwi, Erica alienda chumbani
kwake na kutoa laki mbili kumpa mama yake, huku akimwambia “Mama mbona
za mzee Jimmy ulisema turudishe na hizi umegoma?” “Mwanangu, Yule mzee
humfahamu halafu unataka kula pesa zake si zitakutokea puani. Ila huyu shemeji
yako kashakudhalilisha vya kutosha, na umefanya vizuri sana kusema akuletee pesa
maana ndio malipo kwa kukusingizia uongo wake. Hiyo ni yako mwanangu, jilie
tu” Erica alicheka tu kisha akaendelea na mambo yake mengine ambapo mama
yake alijiandaa na kwenda kanisani. Erica alibaki nyumbani, na kaka yake
Tony nae alirudi na kumkuta dada yake, alikaa nae na kuanza kuzungumza
nae, “Erica, siku uliyoniletea chokochoko kuhusu Dora nilijua mdogo
wangu una roho mbaya sana ila sikujua kama ulikuwa unaniponya kaka yako,
nashukuru sana mdogo wangu. Dora ananiona nimechoka eti sina hela, angejua vitu
nilivyonavyo ni vikubwa mno, hakuna ajuaye ila kwasasa nitamwambia mama
yangu” “Vitu gani hivyo kaka?” “Hivi unajua kama mimi nina
nyumba? Maisha ni nyumba kwanza kabla ya kitu chochote” “Una nyumba
kaka?” “Ndio nina nyumba, ningemuoa Dora nisingeenda nae kupanga bali
ningeenda nae kwenye nyumba yangu, ila yeye kanidharau. Angeonyesha tabia njema
hata baada ya kumuacha ningemfikiria ila kumuacha ndio nimempa tiketi ya kufanya
uhuni! Bora ameondoka kwangu, angeniua Yule mwanamke. Tatizo wanawake wengi
wakiona mtu ana gari ndio wanaona maisha yamekamilika, mimi gari sina ila nina
nyumba na mke nitakayempata nitampenda na atafurahi kuwa na mimi” Basi
Erica aliongea ongea pale na kaka yake huku wakishauriana, ila kaka yake
aliendelea kumsisitiza kuwa kitendo alichofanya jana hakikuwa kibaya wala nini
maana itamsaidia kubadilisha tabia ya shemeji yao na hawezi kumsumbua
tena. Usiku ulifika na kwenda kulala tu na kuacha yaliyopita yawe
yamepita. Palipokucha, Erica aliamka mapema kabisa na kujiandaa
kisha kumuaga mama yake kuwa anaenda kwenye ile kazi, “Erica, kumbuka na
swala la kupata msichana wa kazi hapa nyumbani maana itakuwa ndio yale yale ya
kipindi kile. Mtu wa kubaki na mtoto hakuna” “Sawa mama” Erica
akaenda kazini, alipofika tu alienda ofisini kwa Yule mama ambaye alifurahi
kumuona kisha kumuonyesha kazi ya kufanya huku akimpa maelekezo baadhi ya namna
ya kufanya, na kumwambia, “Kuna mtu inabidi ndio awe anakuelekeza maana
ndio mtakuwa mnasaidiana nae, ila leo hajaja ofisini, atakuja kesho na
utaendelea nae kwenye kazi” “Sawa asante” “Kwa leo, fanya hizo
chache tu na uwahi tu kutoka maana hakutakuwa na kazi ya ziada mpaka kesho Yule
afike kukuelekeza vizuri” Basi Erica akafanya kazi aliyopewa hadi ule
muda wa kuondoka ulivyofika akaondoka zake na kwenda kwao. Alivyofika
alimkuta mama yake na kumsalimia ila leo mama yake alimkalisha chini ili
kuzungumza nae tena, “Unajua Erica bado najiuliza kuhusu huyo
uliyemuuzia mtoto, najiuliza sana, huyo kijana ni wa aina gani?” “Ni
kijana mzuri tu mama” “Uzuri wake hausaidii Erica, hivi ushawahi kuwaza
maisha ya badae ya mwanao? Huyo kijana umempa mtoto atampa nini mwanao leo na
kesho, yani mtoto wako atakuwa na nini cha kujivunia kuwa na baba kama huyo?
Unatakiwa kufikiria Erica, huyu ni mtoto na maisha yake ni muhimu sana kupita
unavyofikiria.” Erica alikuwa kimya tu, kisha mama yake akaendelea
kuongea, “Erica mwanangu sikia nikwambie, mambo ya kuendekeza mapenzi
yalipitwa na wakati sijui ananipenda sana sijui nampenda sana, hayo mambo
yamepitwa na wakati mwanangu. Umekuwa mtu mzima sasa, baba wa mtoto haeleweki
umeamua kutoa mtoto zawadi kwa baba mwingine, je mtoto atafaidika na nini na
huyo baba mwingine? Jamani mimi nafikiriaga mbali sana ujue, natamani wote
mngekuwa na fikra kama zangu, sipendi watoto wangu mkosee kabisa, maana maisha
haya ukishakosea moja ujue mbili itakupiga chenga haswaa, sema mapema ili
tufanye kitu. Usimkuze mtoto na jina lisilokuwa na faida kwake, huyo mwanaume
ana nini cha maana hadi umemzawadia mtoto?” “Mama, Erick ananipenda sana
na mimi nampenda sana” “Nishakwambia sitaki kusikia habari za kupendana,
niambie ana kipi cha maana kama hana chochote kwakweli nitagharamia tu ukamuweke
mjukuu wangu jina la baba yake, najua Yule Mwajuma nitakabana nae koo ingawa
sitaki ahisi nina shida nae ila nitamkaba koo tu maana huyu ni mjukuu wake, leo
na kesho watamtafuta. Niambie huyo Erick ana kipi cha maana?” “Mama,
kwanza kabisa huyu Erick ndiyo mmiliki wa lile duka la vitu vya watoto ambapo
Angel kawa balozi huko na kupatiwa zawadi za nguo na kulipwa kila mwezi, yani
unavyomuona angel hapo analipwa kila mwezi sababu ya kuwa balozi kwenye hilo
duka. Pia huyu mwanaume ndio kamuandikishia kadi ya bima ya afya mwanangu kiasi
kwamba sitahangaika wala nini mwanangu akiumwa, hata nisipokuwa na pesa najua
mwanangu atatibiwa. Na kashaniambia kuna vitu amemuandikisha mwanangu kwenye
mali zake” “Erica, unasema kweli!” “Ndio ni kweli
mama?” “Mmmh hivi inawezekana kweli? Yani kirahisi rahisi tu hivyo,
unajua mimi siamini kabisa kama kitu hiko kinawezekana, wanaume wa hivyo wapo
kwenye dunia hii kweli? Ikiwa tu mwanaume mwingine hata kununua nguo ya mtoto
ambaye si wake ni ngumu halafu unaniambia huyo mwanaume ndio kafanya hivyo! Sikujua, kumbe hata bima ya afya kafanya mpango yeye, aaah sina pingamizi
tena mwanangu, acha tu Angel aitwe Angel Erick” Erica akacheka sana
maana mama yake kuna muda anakuwa kigeugeu sana, ila mama yake akasema
tena, “Ila nitachunguza maana bado hainiingii akilini yani mwanaume
amthamini hivyo mtoto ambaye si wake mmmh! Nahisi kama kuna kitu nyuma ya pazia,
nitachunguza, nitakuwa nakuuliza maswali kila mara maana nataka kujua
ukweli” Erica alimuitikia tu mama yake maana alijua hata akichunguza
bado atapata ukweli kuwa Erick na Erica wanapendana. Usiku
alijiandaa kwaajili ya kulala ila akapigiwa simu na Erick akimsalimia na
kumuuliza kuhusu kazini alipoenda amepaonaje kwa siku ile ya
kwanza, “Aaaah ni pazuri tu” “Kama ni sehemu itakayokuboa
niambie Erica, unajua mwanzo sikufikiria kama unauhitaji wa kazi, ila kwavile
ushapata sio mbaya, sema kama ni sehemu inayoboa niambie ili nikuunganishie
sehemu nyingine” “Sawa, ila pako sawa kabisa na nimepapenda. Mazingira
mazuri, pametulia na panavutia” Basi wakaongea mengi mengi hadi muda
wakaagana na kulala, kwakweli moyo wa Erica ulikuwa umepumzika kwa kipindi hiko
maana hakukuwa na kitu cha kuumiza akili yake tena kama mwanzo, ukizingatia kama
kazi kapata, na yupo mpenzi anayemjali na kumsikiliza kwahiyo alikuwa na furaha
sana. Kesho yake kama kawaida alijiandaa na kwenda kazini ila napo
hakumkuta Yule wa kumuelekeza, na siku hiyo Yule mama alimruhusu mapema zaidi na
kumuhakikishia kuwa Yule wa kumuelekeza atafika kesho. “Unajua nini,
lazima Yule awepo maana ndio anajua mlolongo mzima hapa. Hata wiki iliyopita
nilikwambia wiki hii ni sababu yake, ila jana nilipompigia alisema kuwa kesho
kutwa yani kesho ndio atakuwa hapa ofisini, ni kijana mzuri tu, mstaarabu na
utafanya nae kazi vizuri” “Asante mama” Kisha aliruhusiwa
kuondoka, wakati yupo stendi akisubiri daladala ndipo akakutana tena na Yule
jirani wa Bahati ambaye alimuita na kumwambia, “Tena afadhali nimekuona
Erica, twende” “Wapi?” “Twende mara moja, kuna mahali
nilionyeshwa twende” Kwakweli Erica alimshangaa huyu dada kuweka mazoea
ya karibu hivyo na yeye ila hakupenda kumfanyia dharau kwa kukumbuka kuwa watu
wote ni sawa, na usipende kumdharau mtu maana hujui anataka kusema
nini. Akaondoka na huyo dada, kuelekea sehemu anayomwambia waende,
kufika mbele walipanda bajaji na kufanya kidogo Erica awe na mashaka na kuhisi
pengine huyu dada anampeleka nyumbani kwa Bahati, “Ila dada si
nilishakwambia, mambo ya Bahati sitaki tena” “Ni kweli hutaki mambo ya
Bahati Erica, ila Bahati ile sio akili yake halafu kuna kitu kingine nimeambiwa
juu yako ndiomana nimeamua kufanya hivi” “Kitu gani?” “Erica,
nimeambiwa kuwa wewe kuna kitu umepakwa, tunaita kimavi yani hapo utatanga
tanga, utahangaika hangaika ila hutokuja uolewe kamwe. Yani aliyechafua kuhusu
Bahati alimalizia tu kuchafua kuhusu wewe, hebu jiulize binti mzuri kama wewe
una kasoro gani ya kutokuolewa? Kwanini usiolewe, sikujui Erica ila
nilichoambiwa kuhusu wewe kimeniuma kama mzazi pia, utakuwa unajiona huna
bahati, mikosi imekuandama kumbe wamekuchafua.” “Ila mimi nina mchumba
wangu” “Sikatai unae ila unaweza shangaa huyo mchumba anawiwa vigumu
sana kutaka kukuoa wewe maana kuna vitu umefungiwa” “Kwahiyo unataka
kunipeleka wapi?” “Kwa mtaalamu Erica” Erica alimwambia Yule
dereva wa bajaji asimamishe, kisha Yule dereva akasimama halafu Erica
akamuuliza, “Unatudia pesa ngapi?” “Ya pale hadi
hapa?” “Ndio” “Elfu mbili” Erica akatoa elfu mbili na
kumpa Yule dereva, kisha akatoa elfu tano na kumpa Yule dada kisha
akamwambia, “Nashukuru kwa kunihurumia, kwaheri” Erica akaondoka
zake, akavuka barabara na kupanda daladala. Alifika kwao ila
hakutaka kufikiria kabisa kuhusu swala la kuambiwa yeye sijui kapakwa kimavi
sijui nini na nini hakutaka kabisa kujua maswala hayo hata hakuona kama ni ya
msingi kumueleza mama yake, aliingia ndani na kumsalimia na moja kwa moja kwenda
chumbani kwake. Ila mama yake alimuita na kumueleza yaliyojiri kuhusu
shemeji yake, “Basi nasikia shemeji yako hadi leo hajakanyaga nyumbani
kwake, ndio mapya hayo” “Kheee makubwa, vipi kazini kwake
mmeulizia?” “Bite kasema kauliza kaambiwa kazini ameenda, jana, leo ila
nyumbani hajaenda” “Huyo anatafuta sababu tu, ila atarudi kwake
mwenyewe” Kisha Erica akainuka na kurudi tena chumbani kwake maana
tayari alikuwa na mawazo yake ya kumtosha tu. Mpaka muda analala alikuwa
hataki kuweka mawazo ya Yule dada kwenye akili yake ila maneno ya Yule dada
yalikuwa yakisikika tu kwenye kichwa chake hadi alipopitiwa na
usingizi. Kesho yake kama kawaida alijiandaa na kwenda kazini, alifika
na kwenda kwa Yule mama ambapo Yule mama alimwambia, “Leo Yule ambaye
utafanya nae kazi pamoja amefika, ngoja nimuite nikutambulishe
akufahamu” Kisha Yule mama alipiga simu na kusema neno moja
tu, “Njoo ofisini kwangu” Baada ya muda kidogo muhusika alifika,
Yule mama akamwambia “Karibu ukae nikutambulishe” Erica
akamuangalia huyu aliyeingia ofisini kwa huyu mama alikuwa ni George Yule
aliyewahi kuwa mpenzi wake chuoni, hadi akawa na visasi
nae. Kisha Yule mama alipiga simu na kusema neno moja
tu, “Njoo ofisini kwangu” Baada ya muda kidogo muhusika alifika,
Yule mama akamwambia “Karibu ukae nikutambulishe” Erica
akamuangalia huyu aliyeingia ofisini kwa huyu mama alikuwa ni George Yule
aliyewahi kuwa mpenzi wake chuoni, hadi akawa na visasi nae. George
alionekana kumuangalia Erica, nae alimuangalia George huku moyoni akiwaza kuwa
kwanini wa kufanya nae kazi awe George na si mwingine, basi Yule mama akaendelea
kumtambulisha, “Erica, huyu anaitwa George ndio kijana mtakayekuwa
mkisaidiana nae na atakuelekeza kazi za kufanya. George, huyu anaitwa Erica,
ndio Yule msaidizi tuliyekuwa tunamuhitaji” George alimpa mkono Erica wa
kumkaribisha, naye Erica alimpa mkono pia, hawakutaka kuonyesha tofauti zao
mbele ya bosi wao. Kisha George akamkaribisha Erica kuwa amfuate eneo la
kazi, Erica aliinuka na kufatana nae. Walipofika kwenye ofisi ambayo
wapo wenyewe wawili tu, George akaanza kumuelekeza Erica kazi ambapo kabla ya
yote alimuhoji, “Erica, umemuhonga nini huyu mama hadi kakupa
kazi?” “Kwani hapa kazi watu hupata kwa kuhonga? Na wewe ulihonga
nini?” “Umeanza kuwa na majibu ya shombo hivyo loh! Kumbuka ni mimi ndio
wa kukuelekeza kazi hapa, na vilevile mimi nipo juu yako, sasa kuniletea majibu
ya shombo hivyo nitaenda kukushtaki?” “Sikia George, sijaja kufanya kazi
nilumbane na mtu, wewe utaniulizaje mimi kuwa nimehonga nini? Kuna cha kuhonga
nilichokuwa nacho? Sikia, hayo maswali kamuulize bosi maana ni yeye aliyeniajiri
hapa” “Mmmh sawa, ila ngoja nikwambie. Bosi alisema anatakiwa mtu wa
kunisaidia kazi, na tukatangaza kazi na kuchukua watu ishirini kwaajili ya
usahili, nilisimamia mwenyewe ule usahili na sikukuona kabisa ila iweje wale
wote wamepigwa chini uwekwe wewe! Hainiingii akilini kabisa” “George,
nishakwambia nenda kamuulize muhusika sio mimi” “Umekuwa na majibu Erica
eeh!” “Tufanye kazi George, maswali ya kijinga jinga hapana
kwakweli” George akamuangalia Erica na kuanza tu kumuelekeza kazi
ilimradi siku iende, maana ingekuwa ni ofisi yake kwa majibu yale ya Erica basi
angemsimamisha kazi kwa hasira zake maana huwa anapenda
anyenyekewe. Muda wa kazi ulivyoisha, Erica aliondoka zake na kurudi
kwao. Leo hakukutana na Yule dada stendi kwahiyo alishukuru tu kwavile hakuonana
nae, alipanda daladala na kwenda kwao. Alifika kwao ila kitendo
cha kufanya kazi ofisi moja na mtu aliyewahi kumfanyia vitu vya ajabu maishani
mwake alichukia sana, hakupenda kwakweli. Siku hiyo hata mama yake alimuona kama
mwanae hakuwa na raha, akamshangaa maana hata jana yake alirudi bila raha. Baada
ya salamu akamuuliza, “Erica unajua tangu jana sijakuelewa kabisa, jana
umekuja bila raha na leo tena umerudi bila raha tatizo ni nini na kazi ndio
umeanza?” “Hakuna tatizo mama” “Lipo, mimi naliona, Erica hata
kama unahisi tatizo hilo ni la kijinga niambie mama yake na nitakusaidia kwa
vitu vingi tu, kwa ushauri au kwa lolote, niambie mwanangu hata kama unahisi ni
la kijinga” “Sijui nianzie wapi mama” “Anzia popote tu ila
niambie” “Ila usinifikirie vibaya mama yangu” “Erica niambie tu
tatizo ni nini, mimi ni mama yako lazima tatizo lako liwe kwangu pia,
nisipokusaidia mimi atakusaidia nani tena?” “Mama, kuna mwanamke
nilikutana nae jana akasema kuwa mimi nimepakwa kimavi ndiomana siolewi, eti
naweza kuona muda bado ila nitatanga tanga ila sitaolewa kamwe maana nimepakwa
kimavi” “Kumbe ndio jambo linalokupa mawazo hilo
mwanangu!” “Ndio mama ila niliona sio la muhimu ndiomana
sikukwambia” “Sikia, lisingekuwa la muhimu basi lisingesumbua akili
yako, halafu waswahili husema lisemwalo lipo na kama halipo linakuja, unajua
mambo kama hayo sio ya kuyafumbia macho! Tena nashukuru mwanangu kwa kuniambia
maana nitaanza kuombea jambo hilo na kuwaomba watumishi wa Mungu wanisaidie,
sikia usipuuze mambo ya muhimu kama hayo ukiambiwa ila unatakiwa uchukue
tahadhari mapema sana, hicho kitu sio cha kukikalia kimya, halafu miaka iende
ndio tushtuke kuwa kuna tu analisema hivi, kwanini hatukufanyia kazi
tulivyoambiwa? Wakati ni huu na wakati ni sasa” “Ila mama kwani ni
muhimu sana mtu aolewe” “Wewe mtoto usiniletee laana hizo, kuolewa ni
muhimu hata maandiko yamesema utawaacha wazazi wako utaambatana na mwenzako na
mtakuwa mwili mmoja, mambo ya kusema sijui kwani lazima kuolewa sitaki kuyasikia
kabisa, Mungu aliumba mwanaume na mwanamke kwa makusudi kabisa, kungekuwa hakuna
umuhimu wa kuoana basi Mungu asingeumba mwanamke maana mwanaume angetosha ila
alisema si vizuri mtu huyu awe peke yake, kwahiyo mashetani ya kuniambia sio
lazima kuolewa sitaki kuyasikia kabisa. Sema tumuombe Mungu uolewe na mtu
anayefaa ila sio swala la kuniambia kwani kuolewa ni lazima, tena nyamaza
kabisa” “Sawa mama nimekuelewa” “Ila nashukuru kwa kunihabarisha
kuhusu hayo uliyoambiwa maana ni ya muhimu sana kwangu, sisi ni wanadamu huwezi
jua ni kitu gani kimefunga huko, huyo mtu namshukuru” “Ila alisema
niende nae kwa mtaalamu kutibiwa” “Sitaki kusikia na huo ujinga, toka
nimekuzaa lini nimekupeleka kwa mtaalamu wewe? Lini? Sitaki hayo mauza uza
kabisa, nichanganye maji na mafuta ya nini? Kwani Mungu hasikii? Tumuombe Mungu
tu atatusikia ila maswala ya waganga siyataki kwenye nyumba yangu” “Sawa
mama” Erica alimuitikia mama yake na kwenda chumbani kwake ambapo
alifanya shughuli zake zingine, alienda kula na kujiandaa kulala, alipotaka
kujilaza tu mwanae aliamka maana alimkuta kalala. Basi Erica alianza
kujigelesha kwa kila hali huku akimbembeleza mtoto ili alale tena nay eye aweze
kulala ila mtoto hakulala, hadi saa sita usiku mtoto alikuwa macho, kila Erica
alipojaribu kulala mwanae alimfanyia fujo hadi hakuweza kulala, Erica
alijitahidi kumbembeleza ila mtoto hakulala, ikabidi aanze kumuuliza kwa
taratibu, “Kwani mwanangu unataka nini leo jamani? Unajua sio kawaida,
kweli hadi muda huu hujalala jamani? Unataka nini, eti Angel unataka nini
mwanangu?” Mwanae alimjibu kitu ambacho kilimshangaza sana kwa muda
huo, “Ataka ongea ababa” “Kheee makubwa, Erick kashaniharibia
mtoto” Ikabidi achukue simu yake ili ampigie Erick, ila simu haikuwa na
salio, uwiii Erica aliona sasa atakesha na huyu mtoto, akainuka ili amuombe mama
yake simu ampigie Erick. Akamgongea mama yake na kumuomba
simu, “Erica, simu yangu usiku huu unataka ya nini?” “Nina shida
nayo mama, naomba tafadhali” “Kuna kivocha change, ukikimaliza kesho
ujue kununua” “Sawa mama” Erica akachukua simu kwa mama yake na
kurudi chumbani, kisha akampigia Erica ambapo kwa muda mfupi tu
alipokea, “Naomba nipigie Erick, mimi Erica” Kisha akakata simu
na baada ya muda kidogo tu Erick alipiga na kusalimiana na
Erica, “Unajua kabisa kitu ulichomzoesha mwanangu jamani Erick halafu
humpigii simu!” “Erica useme mwanao tu, sema mwanetu, huyo ni mtoto wetu
sote. Kashalala?” Muda huo Erica alishang’anywa simu na mtoto wake,
kwakweli alicheka tu maana mtoto anavyoonyesha kupenda kuongea na Erick ni
balaa. Baada ya kuongea nae ndio alimpa simu mama yake kisha akasogea
akajilaza tena kitandani, Erica akamuuliza Erick, “Unampaga maneno gani
mwanangu wewe hadi leo anigomee hadi aongee na wewe?” “Usiseme mwanao
sema mwanetu, nahitaji anizoee maana mimi ndio baba yake, vipi namba
uliyonipigia mwanzo ya nani” “Ya mama ile” “Kwahiyo niitunze
eeeh!” “Ifute weee” “Naitunza, maana siku nisipokupata tu basi
nampigia mama” “Yani wewe loh! Tutaongea kesho basi, saivi ngoja
nilale” Basi wakaagana pale na Erica akalala sasa maana hata mtoto wake
alilala. Kulipokucha alijiandaa na kwenda ofisini, alifika na
kukuta George kashafika alimsalimia na kuanza zile kazi alizomuelekeza jana, ila
George akaanza kusema, “Unachukua muda mwingi sana kujiremba hadi
unachelewa ofisini” Erica hakumjibu na kuendelea na zile
kazi, “Ila unapendeza sana, umekuwa mrembo Erica hadi natamani tena kuwa
na wewe” Bado Erica hakumjibu na kuendelea na kazi, na alipomaliza
alimuomba amuelekeze zaidi ili aendelee kufanya kazi, “Sasa kazi
itafanyika vipi kama tunafanya kibubu?” “Kibubu
kivipi?” “Nakuuliza kitu hunijibu ila ukiwa na shida wewe tu ndio
unaniuliza” “Sikia George, tuulizane mambo ya kazi uone kama sitokujibu.
Unaniuliza mambo binafsi kwenye kazi kweli! Nakujibu vipi” “Kukwambia
umependeza ni vibaya? Usinifanyie hivyo Erica, unajua nimekuwa na maisha yangu
sasa, na ninaishi mwenyewe nahitaji mwenzangu” Erica hakumjibu kitu, na
kuendelea na kazi hadi muda wa kuondoka ulipofika, alichofanya Erica ni kumuaga
tu kuwa wataonana kesho, “Hapana Erica, subiri nikupeleke kwenu unajua
nina usafiri siku hizi eeh!” “Asante kwa lifti ila napenda zaidi kupanda
daladala” “Erica umekuwaje kwani? Hunitaki tena?” “Unajua
usinichekeshe George, tangu lini nimekutaka? Naomba tufanye kazi” Erica
akaondoka zake na kuelekea stendi, kwakweli George alishangazwa sana na majibu
ya Erica, alihisi kuna kitu Erica anajivunia nacho maana hakuona kama ni kawaida
kwa Erica kuwa na majibu ya aina ile. Erica alisimama stendi ili kupanda
daladala, ila kabla hajapanda akavutwa na Yule dada, ila kiukweli Erica
hakupenda namna ambavyo Yule mdada alimvuta maana ndio alitaka kupanda kwenye
gari. Erica alimuuliza Yule mdada, “Lipi jipya
leo?” “Erica, usione nakufatilia, napenda maisha yako. Nilienda mwenyewe
nikaambiwa kuna mtu unamfahamu utakutana nae, na huyo atahusika sana kuzidi
kuvuruga maisha yako ila ninachokwambia kuwa makini, sikulazimishi tena kwenda
kwa mtaalamu ila kuwa makini kwa yeyote unayekutana nae. Ni kweli Bahati karogwa
yani hasikii wala nini ila dawa zitakapoisha atateseka sana kwani Yule mtaalamu
kaniambia kuwa Bahati anakupenda wewe. Erica natamani kukusaidia ila sijui wewe
unanifikiriaje, ni hayo tu kwaheri” Huyu dada aliondoka ni kwavile
alijiona tu akitiririka kuelezea wakati hata Erica hakuwa na muda wa kumjibu,
kisha Erica alipanda basin a kurudi kwao. Alipofika kama kawaida
alimsalimia mama yake ambapo mama yake alikaa nae na kuanza kuzungumza
nae, “Unajua Erica maneno ya huyo mtu kama yanaanza kuniingia akilini
ila najua Mungu ni mwaminifu atatusaidia tu. Sijui ni wapi walikupaka huo ujinga
mwanangu ila najua Mungu ni mwema” Erica alimuitikia tu mama yake na
kuingia ndani, leo alipigiwa simu na Erick muda ule ule na alianza kumuuliza
kuhusu kazini ila Angel alikuja na kupokonya simu ambapo akaongea kidogo na
Erick na alipolizika alirudisha simu kwa mama yake, “Yani huyu mtoto
jamani” “Muache mtoto Erica, kwani si vibaya kuchukua simu na kuongea na
baba yake. Kuna mzigo mpya natuma dukani kwahiyo Jumamosi umpeleke mtoto
akajaribishe” “Sawa hakuna shida” “Halafu, vipi kazini kwako
kupo salama?” “Ndio kupo salama” “Umepapenda?” “Mapema
sana Erick kuniuliza hivyo, kumbuka ni wiki ya kwanza hii” “Sawa ila
bado nasisitiza kama unapaona hapako sawa basi acha, mimi nitakutafutia
pengine” “Sawa, nimekuelewa Erick” Basi akaagana nae na
kumalizia mambo yake mengine na kulala tu. Kulipokucha
alijiandaa na kwenda kazini kama kawaida, siku hiyo aliwahi kushinda George na
kuanza kazi zake, muda kidogo George nae alifika na kuendelea na kazi za hapa na
pale. Kisha Erica aliitwa ofisini na Yule mama na kuamua kwenda, alipofika
alimsalimia kisha Yule mama alimuuliza, “Unaionaje kazi
Erica?” “Ni nzuri tu mama” “Ila jitahidi uongeze ubunifu katika
kazi, umefikia. Jaribu kuangalia kwa makini anavyofanya George nawe ufanye,
najua ni mara yako ya kwanza kufanya kazi hii ndiomana inakuwa sio kwenye ubora
ule ninaotaka mimi. Ila kuwa huru, lolote linalokutatiza uje kuuliza,
sawa” “Sawa mama, asante” “Haya kaendelee na kazi” Erica
alirudi kuendelea na kazi ila kuna kitu alielewa maana alihisi George amfundishi
kwa ufanisi, aliendelea na kazi kwa muda kisha akamfata na
kumuuliza, “George, kwanini unaniweke kinyongo mimi hadi leo? Kumbuka
mimi ndio natakiwa kuwa na kinyongo na wewe ila sio wewe kuwa na kinyongo na
mimi, kumbuka umenifanyia mambo ambayo hayastahili kabisa ila mimi nimenyamaza,
kwanini usinielekeze kwa ufanisi sasa” “Kwani nimekuelekeza
vibaya?” “Ndio, kwanini bosi aniulize kuwa sifanyi kiufanisi wakati wewe
unasema umenielekeza vizuri. George haya ni maisha tu, nipo hapa nikitafuta
maisha kama wewe ambavyo unatafuta maisha” “Usijali, ila nikuombe
kitu” “Kitu gani?” “Naomba unipe mapenzi tena, kwa hakika
nitakufurahisha na utapendwa sana” “George sikia, huwa sili matapishi
nikishatapika. Nione kawaida kabisa tena kama dada yako wa tumbo moja, maana
hicho ulichosema hakiwezekani na hakitawezekana kamwe” “Kwanini
kisiwezekane Erica, kunipa mara moja tu!” “Hivi wewe George una matatizo
gani? Sitaki” “Mbona kipindi kile ulinipa?” “Kipindi kile
ulikuwa mpenzi wangu ila sio kwasasa, naomba uachane na habari hiyo kwangu
kabisa, sipo hivyo unavyonifikiria” “Unajifanya mstaarabu sio, wakati
masela wengi washakupitia” “Hivi si wewe ndio ulisema unataka wanawake
bikra, sasa bikra imerudi kwangu? Sitaki” “Wewe Erica, unajifanya keki
wakati kipindi kile ulitoa tu” “George sikia, Erica wa kipindi hiko sio
Erica wa kipindi hiki. Nilikuwa natafuta penzi la dhati na sasa nimelipata, sina
sababu ya kusaliti penzi langu, unikome na ukiendelea kuniondolea furaha katika
kazi sitakaa kimya, nitasema tu kwa bosi” Ila George alicheka sana, na
Erica alienda kuendelea na kazi zake, na alipomaliza alienda kwa bosi wake
kumuomba ruhusa ya kutokufika kesho yake kazini, “Usijali, hata hivyo
Jumamosi ni siku fupi hakuna shida.” Erica alishukuru kisha akajiandaa
na kurudi kwao. Wakati yupo stendi, akamuona Yule mwanamke anayempaga
habari za Bahati, kwa muonekano wa Yule mwanamke ni wazi alikuwa akimtafuta
Erica, kwavile Erica alikuwa akimkwepa basi gari lililokuwa limekuja ingawa
lilijaa ila alipanda hivyo hivyo ili kwa siku hiyo asiongee tu na Yule
mwanamke. Alifika kwao ila hakumkuta mama yake inamaana alikuwa ametoka,
akawaza kuhusu mtoto ila naye hakusikika ndani kwamaana hiyo mama yake alitoka
nae, baada ya muda kidogo mama yake na mtoto walirudi, akamsalimia na
kumuuliza, “Kheee mama leo ulitoka na Angel?” “Wee nitamficha
mjukuu wangu hadi lini? Kwanza amesifiwa njia nzima, na anavyojua kupokea sifa
mwanao yani anatabasamu tu yeye, mtoto huyu kwakweli ana haki ya kupendwa.
Halafu leo nimemfananisha na wewe wakati mdogo, hukujua kununa Erica, labda
ukubwani ndio unanuna mara nyingine ila udogoni ulikuwa ni mtu wa tabasamu
tu” Erica alitabasamu kwa kufurahia ile sifa aliyopewa na mama yake,
kisha akamchukua mtoto kwenda nae chumbani, alipofika tu simu ikaita, kuiangalia
ni Erick alikuwa anapiga, Erica akaipokea, ile kusema tu, “Hallow
Erick” Mwanae alimpokonya simu na kuiweka sikioni kwake, kwakweli Erica
alikuwa akicheka na kusema kuna siku ataweka sauti kubwa ili asikie ni maneno
gani Erick anaongeaga na mtoto wake kiasi cha kumfanya Yule mtoto kupenda
kuongea nae ingawa bado hajui kuongea vizuri. Kisha Angel alimkabidhi
mama yake simu huku akitabasamu tu na Erica akaongea na Erick pale huku
akiendelea kumsisitiza kuhusu kesho kwenda dukani, “Nitamtuma mtu aje
awachukue mapema” “Sawa hakuna tatizo” Kisha akaagana nae na
kuamua kufanya mambo mengine hadi kulala. Jumamosi kulipokucha
alijiandaa mapema kabisa na mwanae, na gafla alipigiwa simu na Moses
akapokea, “Erica, nipo hapa nje ya nyumba yenu
nikikusubiri” Kwakweli alitabasamu, alijua kuwa Moses kapewa oda tu ya
kumfata, kisha akamuaga mama yake na kuondoka ambapo walienda kupanda gari na
kuelekea dukani. Walifika na moja kwa moja Angel alianza kujaribishwa
nguo na kupigwa picha maana nyuma ya duka palikuwa na bustani nzuri sana,
kwahiyo walitumia eneo hilo kumpiga picha Angel. Wakati Angel akiendelea
kupigwa picha, Erica akaitwa na kutoka nje ili kuona nani anamuita alishangaa
kumuona Tumaini siku hiyo akimuita kwa nje, akamfata na
kumsalimia, “Sihitaji salamu yako, msichana ni mbaya sana wewe tena ni
mchawi” “Uchawi wangu nini sasa?” “Yani uzae na mwanaume
mwingine halafu mtoto umbambikizie kaka yangu kweli? Erica unaona ulichofanya ni
kizuri? Mwanamke wa kaka yangu umegombana nae na umeharibu mimba yake ambayo
ndio ya mtoto halali wa Erick” “Kwani Tumaini tatizo lako ni nini?
Unajua huwa sikuelewi?” “Tatizo langu ni wewe kumkandamiza kaka yangu
kwa uchawi wako, ona sasa ulichofanya kwa wifi yangu? Umeenda kupambana nae ili
tum toe mimba aliyobeba ambayo ina mtoto halali wa Erick, wewe ni
muuwaji” “Bado sikuelewi” “Hunielewi nini, muangalie Yule
humtambui?” Tumaini akanyoosha mkono ambapo Erica aligeuka na kuangalia,
alishangaa kuona Yule mwanamke aliyemsukuma ofisini mpaka akadakwa na Sia ndio
anakuja. “Bado sikuelewi” “Hunielewi nini,
muangalie Yule humtambui?” Tumaini akanyoosha mkono ambapo Erica
aligeuka na kuangalia, alishangaa kuona Yule mwanamke aliyemsukuma ofisini mpaka
akadakwa na Sia ndio anakuja. Erica akaona hapo ni balaa kwa upande
wake, kwani akikumbuka huyu mdada alivyomsukuma hadi akataka kuanguka ilionyesha
kuwa ana nguvu sana, akahofia isije huyu mdada akamchangia na Tumaini na
kumfanya awe mboga yao bure kwa muda huo. Kwakweli hata Tumaini
hakuelewa jinsi Erica alivyomtoroka ila alimshangaa tu akiwa mlangoni wa duka
akiingia ndani. Erica alienda kwa Moses moja kwa moja na
kumuomba, “Moses, tafadhali naomba niondoke na mwanangu” “Ila
bado hatujamaliza, tena nilikuwa naanza kukutafuta hapa maana ulitoweka
gafla” “Sipo salama hapa, naomba niende” “Haupo salama kivipi?
Kipi kinakutisha kwani?” “Tumaini hataki kuniona hapa
dukani” “Kwani Erica wewe na Tumaini kuna nini kinaendelea kati yenu?
Unajua huwa sielewi” “Hamna chochote ila hapendi tu kuniona
hapa” “Erica, Tumaini sio mwenye hili duka hata asikubabaishe. Hebu
twende kwanza huko bustanini maana mtoto wako amenuna kwa
kutokukuona” Basi Erica akaongozana na Moses hadi bustanini ambapo Angel
kweli alikuwa amekaa pembeni tu hacheki wala nini kumbe tatizo ni hakumuona mama
yake, ila alipomuona alifurahi sana na kumkimbilia akamkumbatia huku akimtaka
waende nyumbani, “Bado hatujamaliza mwanangu” Ila alionyesha
aking’ang’ania kwenda nyumbani, Erica akaona dawa ya mtoto wake huyo ni kumpigia
Erick ili aongee nae kwani alijua atatulia tu, basi Erica alimpigia simu Erick
kisha kumwambia kuwa aongee na Angel, ambapo Erick aliongea nae kidogo na baada
ya muda alikubali tena kubadilishwa nguo na kupigwa picha, kile kitendo cha
Angel kuongea kwanza na Erick kilimshangaza sana Moses, na baada ya zoezi la
picha aliamua kumuuliza Erica, “Inamaana mwanao kamzoea sana Erick
eeeh!” Erica akacheka tu kisha Moses akaamua kuwabeba kwenye gari yake
na kuwarudisha kwao, ambapo Angel alishafungiwa nguo za kurudi nazo
nyumbani. Walifika na kushuka kisha Moses akawaaga na kuondoka
zake, Erica aliingia ndani na mwanae na kumkuta mama yake ambapo alianza
kumuonyesha zile nguo alizopewa Angel. “Kweli siku hizi kuna rah asana,
yani mtoto anapata nguo za bure tu. Ndiomana umemshikilia huyo mwanaume, aje
nyumbani sasa” Erica akacheka tu kisha akamuuliza mama yake kuhusu dada
yake Bite kuwa anaendeleaje, “Anaendelea vizuri tu, ila unajua shemeji
yako ni aibu tele imemshika hataki kurudi kwake” “Kutokutaka kurudi sio
tatizo, ila tatizo ni kuwa analala wapi? Dada aende kazini kwa shemeji jumatatu,
na amtishie jambo moja tu kuwa ataondoka na amtishie kuwa akiulizwa atasema
ukweli wa kilichomfanya aondoke, mama shemeji atarudi tu nyumbani sidhani kama
atataka aumbuke mara mbili” Mama yake alikubali swala hilo maana aliona
ni jambo jema sana, kisha Erica alienda kufanya kazi zake zingine na kumpa
mwanae chakula. Muda wa kulala ulipofika, Erica alienda kulala na mwanae
ila kabla hajalala alipigiwa simu na Erick, “Erica, si nilikwambia uwe
unanieleza kila kitu kinachotokea kwako?” “Ila hakuna
kilichotokea” “Mbona nimesikia leo hadi ulitaka kuondoka dukani sijui
sababu ya Tumaini, kwani tatizo ni nini?” “Hamna tatizo ila sijui ni
kwanini hadi leo dada yako hanipendi” “Erica swala hilo lisikupe shida
hata kidogo, yule ni dada yangu na wewe ni mpenzi wangu, nyie wawili mnacheza
nafasi tofauti katika maisha yangu sidhani kama kuna sababu ya nyie kuchukiana.
Erica, mimi ndio nakupenda wewe, si lazima dada yangu akupende, cha muhimu ni
mimi kukupenda wewe. Halafu kingine lile ni duka langu, sio duka la Tumaini
lile, naomba uwe huru kabisa unapoenda pale, sawa” “Sawa
nimekuelewa” “Sitaki tena uwe na simanzi kipenzi changu, nakupenda
Erica, sitanii namaanisha nisemayo, nakupenda” “Asante, nakupenda
sana” Basi akaagana nae na kulala ila alikuwa na furaha sana kwa siku
hizo Erica, alihisi kama kaibeba dunia. Kama kawaida ya siku
hii mama yake alijiandaa na kwenda kwenye ibada na kumuacha Erica akiwa
mwenyewe, ila leo alipigiwa simu na dada yake Mage na
kumsalimia, “Erica, mdogo wangu kuna habari nimepata nahisi ni ya kweli
ila ulinificha kwasababu zako binafsi” “Habari gani
dada?” “Nasikia umewahi kulala na Derick” Erica alishtuka kuona
ile habari imefika kwa dada yake, akamuuliza kwa uoga, “Nani amekwambia
maneno hayo dada?” “Dunia haina siri Erica, usidhani ukificha wewe kila
mtu ataficha tena habari yote nimeipata” “Si kweli
dada” “Usitake kupinga wala kukataa Erica, ni Derick mwenyewe kanieleza
mambo haya. Erica nilikuuliza kwa kukupenda kabisa maana hiyo ni laana ambayo
wewe na Derick mmeifanya” “Ila Dada, sijui niseme vipi naomba nisamehewe
sikujua kama Derick ni ndugu yangu hata hivyo alininywesha pombe. Naomba hii
habari isifike kwa mama” “Kwa mama labda uifikishe mwenyewe, sina huo
mpango wa kufikisha habari hii kwa mama, ni aibu na fedheha kwakweli ila mimi
kama dada natakiwa nisimamie swala hili maana ni laana kwenye
ukoo” “Sasa tutafanyaje dada?” “Natakiwa nikawashirikishe kwanza
wakina bamdogo na wao wataniambia cha kufanya ila lazima wewe na Derick muwepo,
kwakweli mlifanya kitendo cha ajabu sana, ndugu jamani mmmh!” “Sikujua
dada” “Basi ngojea nitakupigia simu nikishajua cha kufanya, ndiomana
nilikuwa nakuuliza mapema kuwa kuna lolote mmefanya mkawa mananikatalia wakati
mnajua fika mshaharibu” Kisha Mage akakata simu, kwakweli Erica
alichukia sana kwa Derick kutoa ile siri maana hakutaka ile siri ifichuke maana
aliona inamuoinyesha yeye kama mtu mchafu sana wa kutembea hadi na kaka
yake. “Nakuchukia Derick, na wewe George nakuchukia maana ndio chanzo
cha kufanya Derick na mimi tuwe karibu maana kunibaka kwako ndio nikapata msaada
kwa Derick, jamani sijui hata nifiche wapi aibu hii, kama hadi wakina bamdogo
wanaenda kuambiwa ni lazima mama nae atajua tu” Kiukweli alikosa raha
kabisa, hadi mama yake anarudi kanisani bado hakuwa na raha ila alijaribu
kujigelesha kwenye macho ya mama yake asionekane kuwa na
matatizo. Usiku wa siku hiyo alilala tu hata hakutaka
kusikiliza simu wala kitu gani, asubuhi alikurupuka na kujiandaa kisha kwenda
kazini. Alipofika na kuanza kazi zake ndipo alipokumbuka kuwa alisahau
simu yake nyumbani ila halikuwa tatizo sana kwake hilo alijua akifika tu
nyumbani basi ataikuta sema alikuwa tu anawaza kama mwanae ataiona simu hiyo
itakuwaje? Akaamua kutoa mawazo hayo na kuendelea na kazi. Wakati
anaendelea na kazi zake, George alimfata leo na kumuomba namba yake ya simu
maana ile ya awali haikupatikana, “George tunafanya kazi sehemu moja ila
haina maana kuwa wewe uwe na namba yangu, ni bora tusiwasiliane
tu” “Hivi Erica wewe unawazaga nini? Yani muda wote unawaza kuwa mtu
anataka kukutongoza jamani kweli! Nakuomba namba ya simu sio maswala ya mapenzi
ila hapa tupo kikazi kuna kuhabarishana mambo mbalimbali ila unagoma kutoa namba
yako ya simu. Sikulazimishi ila kuna siku utaona umuhimu wake” Kisha
George aliondoka kuendelea na kazi zake zingine ila ilionyesha kuwa alichukizwa
na jibu la Erica kiasi kwamba toka muda huo hadi wanafunga kazi hakumuongelesha
tena. Muda ulifika na Erica akaenda nyumbani kwao, alipofika tu mama
yake alianza kumwambia, “Leo kumbe ulisahau simu, basi mjukuu wangu
akaileta. Nimeiweka hapo juu, ikapigwa na kupigwa ila sikuipokea ila kuna mtu
alipiga kwenye simu yangu, nikapokea na kumuuliza nani akaniambia ni Erick, sasa
mimi nikasema Erick wa wapi? Jamani mwanao alivyonipora ile simu hata
sikutarajia” Erica akacheka sana, mama yake akamuuliza kuwa anacheka
nini, “Yani Angel bhana, akisikia tu Erick anapiga basi
anachanganyikiwa” “Mtoto wako hafai yani kashikilia ile simu kisha
akanipa mwenyewe halafu Yule kijana kaniaga tu bila kujieleza, nikahisi ndio
yule uliyemuokota na kumpa Angel. Haya mtoto kaanza vipi kumzoea
hivyo?” Erica akamueleza mama yake jinsi Erick anavyopiga simu kila siku
akitaka kuongea na Angel na mwisho wa siku kamzoesha, “Aaah kumbe, huyo
Erick ni hatari, ukiona mkaka anavutiwa hivi na mtoto huyo ni mlezi mwema na
atafanya mtoto kujisikia furaha kuwa nae. Ila ni tatizo pia maana mwanao hata
ukija kumuonyesha baba yake wa ukweli atamkubali tu ila hatompenda kama
huyo” Erica akatabasamu tu na kwenda ndani kwake ila kwa yeye ndio kitu
alichokuwa akikitaka, hakutaka Angel awaze tena kuhusu Rahim hata akimtambulisha
amuone kawaida tu maana tayari alishaingiwa chuki na
Rahim. Kesho yake alijiandaa na kwenda kazini ila ilikuwa kama
kuna chuki ipo kati yake na George maana hapakuwa na mawasiliano mazuri kabisa
kati yao, hata hawakuongea tena yani walikuwa wakifanya tu kazi hata Erica
akiuliza kitu kwa George hajibiwi vile inavyotakiwa hadi kumfanya asijisikie
vizuri kabisa. Ilikuwa Ijumaa ambapo Erica hata akatamani kwenda kuongea
na Yule bosi wao kuhusu tabia ya George maana hakuielewa kabisa, ila kabla
hajajipanga kwenda kuongea nae, bosi wake alipiga simu na kumuita ofisini kwake
ikabidi Erica aende, akamsalimia na kukaa. “Erica, nimekuita hapa
kukuuliza kuhusu maendeleo ya kazi. Vipi kazi unaionaje?” “Ni nzuri
mama” “Na George unamuonaje?” Erica akatamani kusema kuhusu
George ila moyo mwongine akaona si jambo jema kumchongea, kwahiyo akajibu kwa
upole tu, “Yupo vizuri, tunashirikiana nae vizuri sana” “Nilijua
tu kuwa lazima mtashirikiana vizuri, kwakweli George ni kijana aliyetulia, mpole
na mwerevu yani toka nimeanza kufanya nae kazi hapa najivunia sana uwepo wake.
Erica umeolewa?” Erica akasita kidogo, na kujibu huyu
mama, “Sijaolewa ila nina mchumba” “Yuko wapi huyo
mchumba?” “Anaishi nje ya nchi” “Unamuamini?” “Ndio
namuamini” “Waswahili husema fimbo ya mbali haiui nyoka, sitaki
kukuvunja moyo ila huwa sina imani na penzi la mbali. Ningekuwa ni wewe
ningeangalia mwanaume mwenye malengo na mimi, na mwanaume mwenye malengo na wewe
ni Yule aliyekaribu nawe kwamaana mtaweza kupanga nae chochote
kile” Erica hakuelewa ni kwanini huyu mama ameamua kumueleza haya yote
ila hakuweza kumpinga kwa chochote kwani ndio mwenye ofisi kwahiyo akamsikiliza
tu. Kisha Yule mama akaendelea kuongea, “Oooh nimeshasahau kama ni
ofisini, sikia Erica naomba kesho tule wote chakula cha mchana muda wa kuondoka
tafadhali” Erica alimuitikia huyu bosi wake kisha akamruhusu kuendelea
na kazi, Erica alirudi kwenye kazi zake na kufanya zile kazi. Muda wa kuondoka
ulivyofika aliondoka zake na kwena nyumbani. Kwa siku hizo zote
hakukutana tena na Yule dada ambaye alikuwa jirani wa Bahati kwahiyo kwa namna
nyingine aliona ni afadhali hakutani nae. Alifika kwao na
kumsalimia mama yake kisha kwenda chumbani, na baada ya muda tu mama yake
alimuita, “Erica, nasikia shemeji yako alitishiwa kama ulivyosema basi
karudi kwake na aibu hatari halafu Bite alichomwambia ni kuja kuomba msamaha,
nahisi kesho au keshokutwa watakuja” “Sawa hakuna shida” Erica
aliitikia na kutaka kurudi tena chumbani kwake ila mama yake akamzuia na
kusema, “Mbona una haraka hivyo wee mtoto, sijamaliza yangu ujue. Haya,
huyo Erick anakuja lini? Nataka kujua maana ushauza mtoto” “Atakuja tu
mama” “Kwa Rahim ulisema hivyo hivyo, atakuja atakuja na siku zikaenda
unajua mara nyingine nawaza Yule aliyesema una kimavi usikute kweli mwanangu.
Hebu leo muulize huyo Erick wako atakuja lini na unipe jibu, yani leo na kesho
nakupa hiyo kazi halafu keshokutwa nitakuuliza tena swala la kuniambia atakuja
tu sitaki kulisikia” “Sawa mama” Erica alimuitikia mama yake ila
alihisi naye anataka kumchanganya tu kwani bado alikuwa na maswali mengi sana
kichwani kuwa kwanini Yule mama amsifie George na badae kumuuliza kuhusu
mahusiano yake, alijaribu kuwaza bila hata ya jibu ila hakutaka kile
anachofikiria kiwe kweli maana alihisi huenda George na Yule mama ni watu wa
karibu mno kwahiyo George amemueleza Yule mama kuhusu yeye na Yule mama
anatafuta namna ya kumuweka karibu na George, “Mmmmh ashindwe, simtaki
George na sitamtaka kamwe bora nikose kazi ila sio kuwa tena na shetani kama
George” Aliwaza sana na mwishowe akapigiwa simu na Erick kama kawaida
ila akaona hapo ni muda mzuri kumuuliza kuhusu alichoulizwa na mama
yake, “Erick, mama anahitaji kujua ni lini utakuja
kwetu?” “Nitakuja tu Erica” “Ndio utakuja, ila ni
lini?” “Basi ngoja niandae mazingira kwanza, halafu kesho jioni nitakupa
jibu kuwa ni lini” “Halfu kitu kingine Erick, kama umeamua kweli kuwa na
mimi naomba hao wanawake zako wote uachane nao.” “Mbona nishaachana nao
Erica” “Bado hujaachana nao bhana, ukiachana nao nitajua. Waambie wazi
watambue ya kwamba kuna unayempenda, nahitaji uachane nao kweli ili niwe na
furaha kuwa napendwa na wewe” “Sawa nitafanya hivyo Erica, nakupenda
sana ujue” “Nakupenda pia ila fanya hivyo nitafurahi
sana” “Furaha yako ndio furaha yangu, vipi mwanetu
kalala?” “Hahaha kalala ndio, si angenipora simu hapa” “Basi
akishtuka akitaka kuongea nami nibipu tu nitapiga” “Sawa” Basi
Erica akaagana na Erick na kuamua kulala kwa muda huo. Kesho
yake kama kawaida, alijiandaa na kwenda kazini, ila siku hiyo ilikuwa ni siku
fupi tofauti na siku zingine. Alifika na kufanya shughuli zake, muda wa
mchana ulivyofika yani karibu na kuondoka Yule mama alimuita Erica na
kumkumbushia swala lake la kwenda kula nae chakula cha mchana, kwahiyo
alimwambia amsubirie kidogo ambapo Erica alifanya hivyo. Basi Yule mama
alipomaliza alitoka na Erica na kupanda nae kwenye gari yake kisha wakaenda
kwenye mgahawa mmoja mzuri sana na kumwambia Erica aagize anachotaka na yeye
akaagiza. Wakiwa wanasubiri chakula Yule mama alianza kuongea kwa
kumuuliza Erica, “Ulisema mchumba wako yupo mbali?” “Ndio yupo
mbali” “Napenda kukushauri Erica, kuwa na mwanaume anayejielewa.
Kwakweli George ni kijana anayejielewa” Erica akatabasamu tu, kisha huyu
mama aliendelea kuongea, “Nakumbuka nilipokuwa binti kama wewe mapenzi
yalinitesa sana sababu tu nilijifanya nachagua wachumba, uwiii yakanitokea puani
yani mwanaume niliyezaa nae huwa najuta tu kuwa nilianzaje kuchukua maamuzi ya
kuzaa nae. Ipo siku nitakueleza kwa undani zaidi, mimi nilibeba mimba nilikuwa
nalia kila siku, nilijisemea nikizaa wa kike nitamfundisha kuwa wanaume ni
viumbe wabaya na wenye roho mbaya. Nikasema nikizaa wa kiume basi nitamfundisha
mwanangu awe na upendo wa kweli, asimuache mwanamke kulia, ajue kumbembeleza
mwanamke maana lile shetani langu hata kubembeleza halijui” Chakula
kililetwa na kabla hawajaanza kula, yule mama alipigiwa simu kwahiyo aliinuka na
kwenda kuongea na simu yake, alivyorudi alianza kuongea na Erica kuhusu simu
aliyopokea na kusahau mada za nyuma, “Kumbe mwanangu alikuwa akinipigia
simu, jamani mimi nina mtoto mmoja tu kama jicho langu ila mtoto huyu ni pasua
kichwa jamani mpaka huwa nahisi kizunguzungu sijui nilikosea wapi kwenye mimba
yake” “Kwanini mama?” “Unajua alichoniambia? Eti kapata mchumba
anataka kuja kumtambulisha kwangu, unajua nimechoka eeeh! Wasichana wengi
wanakuja kwangu wakilia kuhusu mwanangu, nasikia uchungu sana kwangu na mimi
nimepitia katika hali kama yao, huwa namuuliza mwanangu kwanini yupo vile?
Hanijibu na mimi nakosa jibu kwakweli, nilishindwa kukaa nae hadi ilibidi akakae
na babake tu labda karithi kutoka kwa babake huo uhuni. Kwakweli sitaki aniletee
mwanamke mwingine kunitambulisha, kuna mmoja tu ndio namkubali, akishindwa kuoa
huyo basi” Erica alimuangalia tu huyu mama, kwani bado hakuelewa ni
kwanini anamueleza yote hayo. Wakati Yule mama akiendelea kulalamika
kuhusu mwanae, simu yake ikaita tena na kuinuka kwenda kuongea nayo, baada ya
kurudi akamwambia Erica, “Mkwe wangu nimpendaye kanipigia simu, ila
analia huyo balaa yani kashalizwa na mwanangu, nimemwambia aje hapa tuongee.
Jamani mwanangu sijui kwanini anamliza mtoto huyu wa watu wakati nishamfundisha
asimlize mwanamke, sijui amekuwaje jamani” Kwakweli Erica hakujua kama
aongee kitu gani maana alihisi kama ni mada zisizomuhusu vile, alipomaliza kula
aliamua kumuaga huyu mama, “Aaah jamani Erica, hutaki kumuona mkwe
wangu?” “Nitamuona siku nyingine mama” Basi Yule mama akampa
ruhusa ya kuondoka tu bila kinyongo, wakati Erica anatoka kwenye ile hoteli
alimuona Sia mlangoni, alishtuka sana akaamua kujibanza ili Sia asimuone basi
Sia akapita pale na Erica akaanza kumfatilia nyuma kuwa Sia anaenda wapi,
akamuona akienda alipo Yule mama na alipofika alikumbatiana na Yule mama, ndipo
akili ikamjia kuwa Yule ni mama Erick. Basi Yule mama
akampa ruhusa ya kuondoka tu bila kinyongo, wakati Erica anatoka kwenye ile
hoteli alimuona Sia mlangoni, alishtuka sana akaamua kujibanza ili Sia asimuone
basi Sia akapita pale na Erica akaanza kumfatilia nyuma kuwa Sia anaenda wapi,
akamuona akienda alipo Yule mama na alipofika alikumbatiana na Yule mama, ndipo
akili ikamjia kuwa Yule ni mama Erick. Kwakweli Erica aliishiwa raha
muda ule, hata furaha hakuwa nayo tena, akaondoka na kuelekea nyumbani
kwao. Alipotoka tu nje ya ile hoteli wakati anatembea akielekea kituoni,
hakuangalia mbele, kuna mmama aligongana nae na kujikuta akiangusha vitabu vya
Yule mama ambavyo alikuwa amevibeba, aliinama kuviokota huku akimuomba msamaha
sana Yule mama, ila Yule mama alimwambia, “Usijali binti, ila unaonyesha
una mawazo sana” Erica alicheka tu ili kujigelesha swala la kuwa na
mawazo, basi Yule mama alimuomba Erica namba ya simu na kusema, “Mimi ni
mwanamaombi, nimeomba namba yako ili niwe nakualika kwenye maombi kanisani
kwetu. Hivi nawahi kanisani” Kwavile Yule mama alijitambulisha kuwa
mwanamaombi basi Erica hakusita kutoa namba yake kwa Yule mama kisha alimuaga na
kuendelea na safari ya kuelekea kituoni. Wakati yupo njiani akielekea
kupanda daladala, alikutana na Moses njiani ambaye alisimamisha gari na kutaka
kumpa lifti, “Hapana usijali, naenda tu mwenyewe” “Hapana Erica,
yani nikuone hapa njiani nikuache kweli! Unataka nionekanaje mimi, naomba
nikupeleke tu, si unaenda kwenu?” “Ndio” “Basi, naomba
nikupeleke” Basi Erica hakuona kama ni vyema kuendelea kubishana na
Moses pale kwahiyo alipanda ile gari ya Moses na safari ya kuelekea kwao
ikaanza. Ila Moses alimuona Erica kama anainesha hana furaha ilibidi
amuulize, “Mbona unaonekana huna furaha?” “Hamna nipo kawaida
tu” “Ni muda mfupi nimekuzoea Erica, hapana hivi ulivyo sio kawaida,
inaonyesha una tatizo. Haya bhana kama hutaki nilijue” Erica aliamua
kubadilisha mada na kumuuliza, “Kwani ulikuwa unaenda
wapi?” “Aaah leo niliwahi kutoka ili nimuwahi mke wangu, nimemmiss sana,
wiki yote hii nipo busy sina siku ya kupumzika yani kila siku nipo kazini,
kwakweli leo nimewahi kutoka na kesho nimemuomba udhuru Erick maana sitafungua
duka nahitaji kuwa karibu na mke wangu” “Sasa kumbe unawahi kwa mkeo,
mbona umejitolea kunipeleka mimi nyumbani?” “Erica, hivi naanzaje
kumwambia Erick nilikutana na Erica njiani akielekea nyumbani ila sikumpeleka,
naanzaje kusema? Unajua sielewi kipi kipo katikati yenu wewe na Erick ila nahisi
mnajuana, mi nikikupeleka ndio nitaenda kwa mke wangu najua hata Erick
nikimwambia hivyo atafurahi sana” Erica akatabasamu tu na kumuuliza tena
Moses, “Inaonyesha unampenda sana mke wako” “Yani nahisi
nampenda kuliko hilo neno na sana, yani nampenda balaa” “Hukuwahi kuwaza
kumsaliti?” Moses akacheka, “Erica, huwa nakutana na wasichana
warembo kama wewe hivyo ila kwakweli sababu mke wangu nimempa nafasi ya kwanza
basi anakuwa ni mrembo kuwazidi wote. Na kwanini umeniuliza hilo
swali?” “Nasikia wanaume hawajatulia na mwanaume hawezi kutulia na
mwanamke mmoja yani lazima atatafuta wa pembeni” “Tatizo watu hutoa jibu
kwa mfano wa mtu mmoja tu. Mimi toka nimuoe mke wangu sijawahi kumsaliti hata
mara moja na wala sifikirii kumsaliti nampenda sana. Sisi wanaume pia tunapenda,
ukiona mwanaume anahangaika na huyu mara Yule ujue hajapata bado Yule wa kwenye
roho yake ndiomana anashika huyu mara huyu ili kuangalia je anaweza akamteka
akili yake, ila akishampata wa kwake lazima atatulia. Yani mara nyingine sio
mambo ya kulaumu sana sijui wanaume hawajatulia sijui nini na nini, watu
hawaelewi tu mtu anakuwa hajapata hitaji lake au anayempenda kwa dhati anazingua
ndio utakuta anahangaika hangaika ila akimpata wake hadi utashangaa ndio huyu
kweli wa kuruka ruka na wanawake” Erica alitabasamu tu kwani hapo
aliweza kuelewa kuwa kwa Erick basi ni yeye ndiye mwenye nafasi kubwa sana,
Moses alimuona Erica akitabasamu tu na kumuuliza, “Vipi mbona furaha
tu” “Nimefurahi, nimependa vile ulivyosema unampenda sana mkeo. Hakika
ulimwengu ungekuwa kama unavyosema basi hata magonjwa ya zinaa yasingekuwepo.
Tatizo ni moja tu huyo mwenye upendo wa dhati utamjuaje?” “Inamaana wewe
humjui unayempenda kwa dhati? Yani mtu ukimpenda jamani, hata ukisikia jina lake
tu unajisikia furaha, unaweza ukakaa halafu labda likatokea jambo unajikuta
ukiwaza angekuwepo Fulani hapa yani unajikuta unapenda tu uwepo wake. Ila kama
mtu upon aye tu kupeleka siku mbele vyovyote vile unaona sawa, awepo asiwepo
unaona sawa, apige simu, asipige unaona sawa yani hata hujali uwepo wake ila
unaweza kujigelesha na kujifanya kuwa unamkumbukaga kumbe kiukweli hakuna
kitu” Walifika nyumbani kwakina Erica, kwakweli Erica alimshukuru Moses
na alishukuru pia kwa mazungumzo aliyozungumza nae kwa siku hiyo, kisha akamuaga
na kuingia ndani. Aliingia ndani kwao na kumkuta dada yake Bite
pamoja na James, inaonyesha walifika kama mama yao alivyosema kuomba msamaha,
pia ilionyesha ni muda huo huo ndio wametoka kufika. Baada ya salamu Erica
aliambiwa na mama yake akae pale kwani walihitaji wasikie wote msamaha anaouomba
James kwa Erica, basi james alianza, “Erica shemeji yangu, mdogo wangu
naomba unisamehe maana nilichokuwa nafanya kwako sio sawa. Ni shetani tu huyu
anataka kuharibu undugu wetu, naomba unisamehe sana. Mimi bado ni shemeji yako
na mimi bado ni mwanafamilia wenu. Naomba unisamehe Erica” “Hakuna
tatizo, nishakusamehe ilimradi umegundua kosa lako basi
nimekusamehe” “Nashukuru sana, mama naomba nawe unisamehe sana mtoto
wako. Nisamehe kwa yote niliyokuwa nasema kuhusu Erica, nisamehe kwa tukio lile,
ni shetani tu alinipitia” “Nilikuwa nakusikiliza kwa makini sana habari
za kusema shetani kakupitia, James usisingizie shetani ila ni akili zako mbovu
ndio zimekutuma kufanya vile. Mimi sina tatizo, kaa chini na mkeo mlee mtoto
wenu, ujinga ujinga wa kuendekeza ngono utakuponza. Mbona mwanangu Bite mzuri tu
jamani kwanini unashindwa kuridhika James? Hebu tulia na mwenzio, na kipindi
ukimchoka niletee mwenyewe nikae nae.” “Usifike mbali mama yangu,
nisamehe mtoto wako” “Nishakusamehe na sina tatizo tena. Ila naomba
nikuombe jambo moja” “Jambo gani mama?” “James, ingawa
tumekusamehe na hatuna tatizo na wewe ila tafadhali sana sitaki ukaribu wako
tena na Erica maana huyo shetani wako akakupitia tena ukasababisha matatizo kwa
wanangu bure. Sitaki tena ukaribu wako na Erica, una shida yoyote kwa Erica
niambie mimi nitafikisha ujumbe” “Sawa mama nimekuelewa” “Sawa,
najua na mkeo mlishaombana msamaha huko mpaka mmefika hapa” Bite
akajibu, “Ndio mama, nimeshamsamehe” “Ila sio unasema
umeshamsamehe huku bado una kinyongo moyoni, mumeo kakiri mwenyewe hapa ana
urafiki na shetani hadi huwa wanapitiana, kwahiyo elewa kabisa sio unaitikia
halafu kesho na keshokutwa unaanza sijui mama kimeenda kimerudi
sitaki” “Sawa mama” Kisha wakainuka na kushikana mikono, na muda
ule ule Bite na mumewe waliaga kwani bado James aliona aibu kuendelea kuwa
mahali hapo akizingatia mama yao na wakina Bite hajambakisha na kitu, amemwambia
ukweli tu. Walipoondoka, Erica nae alienda chumbani
kwake. Kwakweli Erica hakuwa na raha kabisa, kuna mambo mengi
sana alikuwa akijiuliza bila jibu hata kidogo, “Hivi hii maana yake nini
katika maisha yangu? Nilikuwa na shida haswaa baada ya kuachwa kwenye mataa na
George, akatokea msamalia mwema kunisaidia, akaonyesha kunipenda na kunijali
huku akitamani hata ningekuwa mtoto wake, msamalia mwema huyo ndio mama wa
Rahim, hakutaka hata kusikia kuwa nina mahusiano na mtoto wake kiasi kwamba hata
mjukuu wake hana imani naye, kwamaana hiyo mama huyu imani na mimi imemuondoka
gafla, haya sasa katokea mama mwingine na kunifuta machozi ya kutokuwa na kazi
kwani kanipa kazi ila ndio mama yake Erick, kuna nini katikati yangu jamani!
Sidhani kama ni baraka hii ila ni mkosi tu hata sijui nifanyeje, sitamani hata
Jumatatu ifike maana akiambiwa kuhusu mimi hivi atanionaje?” Aliwaza
bila ya jibu, ila kwa upande mwingine akakumbuka kuwa kuna mama alikuwa
akimuombea msamaha Erick, ila mbona hakuwa huyu bosi kama ndio mama wa Erick?
Kwakweli hakuwa na raha kabisa ila alihitaji kuujua ukweli, akaamua kujilaza
kidogo. Mwanae ndio alimuamsha na giza lilishaingia tayari kwahiyo
aliamka na kwenda kumuogesha mwanae kisha kumpa chakula, kwakweli yeye
hakujihisi hata hamu ya kula kwangu alikuwa anahisi kila kitu ni kibaya kwa
upande wake, akatamani kumueleza ukweli Erick ila akawaza kuwa ataanzia wapi,
kuna moyo mwingine ukamuambia kuwa lazima aseme ukweli ili Erick ajue kuwa
itakuwaje, muda kidogo wakati anatafakari Erick alipiga simu na kama kawaida
mwanae alichukua na kuongea nayo kisha kuirudisha kwake, halafu Erica akaanza
kuongea na Erick ila alitaka kujua ukweli kwanza kama Yule mwanamke wa ofisini
ni mama yake Erick, alianza kumuuliza kwa mitego, “Hivi Erick, Yule mama
aliyekuwa akikuombea msamaha ofisini kipindi kile unafukuzwa shule ndio mama
yako mzazi?” “Hapana, Yule alikuwa mama mdogo, maana mama yangu kuna
kipindi aliniacha nalelewa na mamdogo” Kisha akaona bora amuulize kwanza
kuhusu alichomwambia jana ili asikie Erick ana jibu gani hapo, “Erick,
niambie sasa utakuja lini kwetu na utanioa lini?” “Erica, unaweza kuhisi
nakuongopea au ukahisi sina lengo jema na wewe ila si kweli Erica, nakupenda
sana na lazima utakuwa mke wangu ila kuna mazingira tu lazima niyaweke sawa
kwanza” “Mazingira gani? Niambie” “Ngoja nikueleze ukweli Erica,
nimemwambia mzee wangu kuhusu swala la mimi kutaka kuoa jamani huyu mzee
kanipinga vikali sana akidai kuwa mimi bado ni mtoto mdogo, sasa mimi nina udogo
gani jamani? Wanaoa vijana wa miaka ishirini sembuse mimi kweli! Nadhani ni
sababu baba yangu hajawahi kuoa maishani mwake, ila akaniambia kitu cha
kunishangaza sana, kuwa hivi karibuni na yeye ataoa kwahiyo nimsubirie yeye aoe
ndipo na mie nianze na wazo la kuoa. Ilibidi niachane na huyu mzee, nikampigia
mama, yani na yeye ni shida tupu. Kuna msichana mmoja anaitwa Sia, huyu msichana
anampaga maneno ya sumu sana mama yangu hadi mama kajikuta anampenda huyu
msichana na kunichagulia mimi kuwa nimuoe ila mimi simtaki Sia, yani mama
nimerumbana nae sana, na jioni katoka kunipigia simu sijui yupo na huyo Sia yani
tumegombana tu. Sasa, kwa baba na mama kote sijafika nao muafaka ndiomana nakuwa
mgumu sana kusema kuwa ndoa ya mimi na wewe ni lini? Erica, tunaweza kuoana tu
ila baraka za wazazi nazo ni muhimu. Naomba nipe muda niliweke sawa jambo
hili” “Mfano wazazi wako wakikazana kuwa hawataki tuoane
utafanyaje?” “Erica nipe muda tafadhali. Nishakwambia kwasasa hakuna
kitu cha kunifanya mimi nikuache wewe, nakupenda sana. Wazazi wangu watanielewa
tu maana hata wafanyeje bado mimi ni mtoto wao. Nipe muda Erica
nakuomba” Erica alikubali na kuagana nae, baada ya kukata simu aliwaza
swala la mama yake Erick, jinsi alivyokuwa akiongea nae na jinsi Sia alivyofika,
yani pale picha halisi inakuja ya mama yake Erick ila akawaza kama akimwambia
Erick kuwa mama yake ndio bosi wake kazini inaweza ikawa tatizo kubwa maana Yule
mama atamjua mapema na pengine kumletea longolongo, akaona bora kama yakimshinda
kabisa basi ndio amwambie Erick kuwa huyo mama ndio bosi wake. Kwa muda
huo aliamua kulala ila kabla hajalala kuna ujumbe uliingia kwenye simu yake,
akafungua na kusoma akakuta umetumwa na Yule mwanamama aliyesema kuwa ni
mwanamaombi, ujumbe ulisema kuwa “Mkumbuke muumba wako siku za ujana
wako” Akawaza ni kwanini Yule mama amemtumia ujumbe huo kwa muda huo ila
hakutaka kufikiria sana akaamua kulala tu. Palivyokucha wakati
mama yake akijiandaa kwenda kanisani, Erica nae alijiandaa na kumwambia mama
yake kuwa siku hiyo ataenda nae kanisani, “Kheee kwakweli Mungu mkubwa
yani leo kwa hiyari yako Erica umekubali kwenda kanisani?” “Ndio
nimekubali mama” Basi akajiandaa na kumuandaa na mwanae na kwenda
kanisani. Wakati wanatoka kanisani, kuna wamama walisogea wakimuuliza
Erica kuwa mtoto wa nani, aliposema ni wake walikuwa wanakataa kabisa maana
hawakuwahi kumuona akiwa na mimba, “Kheee mtoto una siri wewe, kumbe
ulibeba mimba hadi ukazaa?” Mwingine akasema, “Hata mama yake ni
msiri, hata kutudokeza hamna jamani!” Erica alicheka tu, wakamuangalia
mtoto pale hadi kuondoka ana kwenda nyumbani, walipofika nyumbani mama yake
alianza kuongea, “Yani wale wanawake ulisimama nao ni waongo hao hatari,
ndiomana nilivyoona wamesimama na wewe tu nikajificha” “Kheee mama, watu
wameokoka halafu wanakuwa waongo?” “Sikia Erica, uongo ni tabia ya mtu
halafu mwingine anasema ameokoka si kweli mbona hata maandiko yamesema sio wote
wasemao Bwana Bwana watauona ufalme wa mbingu. Cha msingi ni wewe kushikilia
kile unachokiamini, usimuamini mtu sababu kasema ameokoka yani usiamini kabisa,
kuwa na imani yako moyoni itakayokuongoza” “Sawa mama, ila leo
nimejisikia afadhali. Sema kuna jambo nataka nikushirikishe mama
yangu” “Jambo gani hilo?” Erica akawaza sana, na kutokuelewa
anaanzaje kuelezea kuhusu mama yake Erick, ila akajaribu kumuuliza swali mama
yake, “Hivi mama mfano unataka kuolewa ila wakwe zako hawakupendi
inakuwaje?” “Mwanangu, hakuna ndoa inayoumiza moyo kama ndoa ya
kuchukiwa na wakwe sijui mawifi sijui mashemeji, tena ndoa ya hivyo bora uombee
mumeo awe upande wako, ila akiwa upande wa ndugu zake utahisi dunia ikipasuka.
Kwanini umeniuliza hivyo?” “Mama, wakwe zangu
hawanipendi?” “Unawajua? Ushatambulishwa?” “Bado, ila hawataki
hata kunifahamu” “Mmmh ndio wazazi wa Erick hao?” “Ndio
mama” “Kheee na mtoto ushauza kwenye ukoo wa watu wasiojielewa kama hao,
mmmh ila usipaniki ngoja mwanangu nitaliombea swala hilo” “Nashukuru
mama” Erica alienda chumbani kwake sasa, alitulia kidogo kuwa kamueleza
mama yake ingawa hakumwambia ukweli wote. Aliamua kulala ila kabla
hajalala alisikia simu yake inaita, akaichukua na kuiangalia akakuta ni Dora
anampigia, akaamua kuipokea kwani hakujua ni jambo gani limemfanya apige simu
usiku huo ukizingatia ni muda tangu aongee nae, alipokea ambapo Dora alianza kwa
kumsalimia kisha akamwambia, “Erica, una mpango gani na Yule
baba?” “Hivi Dora kwanini huelewi? Nishakwambia Yule mzee simtaki tena
simtaki kabisa” “Sikia Erica, Yule mzee anakupenda kweli. Aliniuliza
kuwa rafiki yako nimfanyie nini akubali, nikamwambia labda umuoe maana rafiki
yangu ni muda mrefu sana anahitaji ndoa. Yule mzee kanihakikishia kuwa hataki
kukuchezea, anataka kukuweka ndani kabisa uwe mke wake, na kasema ataifanya
familia yako ifurahie utajiri wake. Erica Yule mzee anakupenda” “Dora
usione nimenyamaza nakusikiliza ukadhani nafurahia huo ujinga wako unaozungumza,
yani ungejua unanichefua tu. Dora, mimi na wewe urafiki ulishaishha na licha ya
hivyo huyo mzee Jimmy mfikishie ujumbe kwamba Erica hata umuhonge dunia
hakutaki. Kwaheri” Erica alikata simu ya Dora, ila hakutaka kufikiria
alichokuwa akiongea na Dora badala yake alikuwa akiwaza tu kuhusu Jumatatu kwani
aliiona ni mbaya kwake ukizingatia hakujua ni maneno gani Sia kamwambia Yule
mama, alikosa raha kabisa kiasi kwamba alilala kwa
mang’amung’amu. Kulivyokucha, mapema kabisa aliamka na
kujiandaa na kwenda kazini, alifika na kuanza kazi zake na kama kawaida alimkuta
George ila hakupewa salamu wala nini, ilibidi leo aamue kumsalimia mwenyewe ila
George aliitikia kwa sauti ya chini kabisa na kumfanya Erica ajiulize sana kuwa
kwanini George anamfanyia vile ila bado halikuwa tatizo hilo kwake kwani hakuwa
hata na wazo la kurudiana na George. Wakati anaendelea na kazi zake,
muda kidogo aliitwa na Yule bosi wake ambaye alianza tena kuongea nae kuhusu
habari za George, “Erica, binti yangu sikia, nimekuita hapa ili
kukwambia jambo moja. Tangu nimeanza kufanya kazi na George hapa ni miaka
imepita na hakuna siku aliyowahi kuniambia kuwa kuna mtu kampenda, kwakweli ni
mara ya kwanza George kaniambia kuna mtu kampenda na anataka kumuoa. Erica,
kwakweli George anakupenda sana ila kukueleza anashindwa ndiomana kaniambia
mimi” Erica akamjibu huyu mama, “Mama, ila mimi nina mchumba
wangu na ninampenda sana” “Ila si nishakueleza madhara ya kuwa na
mchumba wa mbali Erica!” Kabla Erica hajampa maelezo mengine, simu ya
Yule mama ikaita na akaipokea na kuongea nayo. Alipomaliza akamuangalia Erica na
kusema, “Kwakweli wanawake tunashida jamani ndiomana huwa wanasema
tuombee matumbo yetu kabla ya kubeba mimba na kuzaa, jamani mimi sijui nimezaa
kituko cha aina gani, hivi mwanangu ni wa kunifanyia hivi
kweli?” Ilibidi Erica aulize, “Kafanyaje?” “Jamani, eti
kapata mwanamke ila huyo mwanamke ana mtoto kumbe halafu yeye kajimilikisha huyo
mtoto na kuchukua majukumu ya mtoto kama yeye ndio baba, yani hapa ndio dadake
kanipigia simu alikuwa ananieleza, nimemwambia aje hapa ofisini ili niongee nae
vizuri, nahiotaji kumjua huyo shetani aliyevuruga akili ya
mwanangu” Erica akaona hapa ni balaa juu yake hadi alihisi akishikwa na
tumbo la kuhara, na kuomba ruhusa mara moja. Alienda chooni ila hata
hakuweza kujisaidia, alihisi tu tumbo likimsokota, alitulia kwa muda hadi tumbo
lilipotulia. Akarudi kwenye ofisi yake ila hakuweza kufanya kazi ya aina
yoyote kwani aliona kila anachoshika hakishikiki, wasiwasi wake ni pale Tumaini
atakapofika na kumkuta, ikabidi atumie kigezo cha kuumwa na tumbo ili kuomba
ruhusa ya kwenda nyumbani. Alienda kwa bosi wake na kumueleza jinsi
tumbo linavyomsumbua, “Mbona gafla jamani, kwani tangu asubuhi lilikuwa
likikusumbua?” “Hapana, limeanza gafla tu. Huwa nina vidonda vya tumbo,
nahisi ndio vimecharuka” “Aaah pole sana, nenda nyumbani kapumzike ila
kuwa makini sana na vyakula unavyokula kuepuka hivyo vidonda” Erica
alimuitikia huyu mama, kisha akainuka na kwenda kuchukua mkoba wake na
kutoka. Wakati anatoka mlango wa nje, sababu alikuwa na harakati
akajikuta akigongana kikumbo na mtu, kumuangalia vizuri alikuta ni Tumaini naye
akimuangalia pia. Wakati anatoka mlango wa nje, sababu
alikuwa na harakati akajikuta akigongana kikumbo na mtu, kumuangalia vizuri
alikuta ni Tumaini naye akimuangalia pia. Erica alishtuka na kuwa kama
amesizi kwa muda maana ndio huyo huyo alikuwa akikimbia ili asimkute halafu ndio
kagongana nae kikumbo, Tumaini alitingisha kichwa na kusema, “Ama kweli
wewe binti ni mchawi, yani hadi ofisini kwa mama yake Erick! Ulikuwa unafata
nini huku?” Kwavile Erica alishavurugwa, aliamua kumjibu tu kwani kwa
muda huo alijisemea kuwa liwalo na liwe, “Hivi wewe Tumaini kwani
unanitakia nini mimi? Sio kwa kunifatilia huko” “Nakutakia nini? Achana
na mdogo wangu” “Unajua wewe una mambo ya Kiswahili sana halafu ndio
unasema baba yenu tajiri umelelewa maisha ya kitajiri, na umesoma ila una
uswahili mwanzo mwisho. Kufatilia yangu, kwanini muda huo usikae kufatilia ya
mumeo atakayekuoa? Kwani wewe huna mchumba? Huna mpenzi? Yani unaacha kupanga
mambo na mchumba wako huko, unakazana kila leo kumfatilia Erica, unapata faida
gani unapofanya hivyo? Na unasema niachane na mdogo wako, huyo mdogo wako
unamtaka wewe au nini?” Alipoongea hayo alikuwa mbali kabisa anaishia
maana alijua kama angekuwa karibu basi Tumaini angemdunda, maana pale Tumaini
alionyesha amechukizwa sana kiasi kwamba Erica angekuwa karibu basi
angemkomesha. Erica aliliona jicho la Tumaini linavyomuangalia kwa
hasira, hivyo akaamua kusimamisha bodaboda na kupanda kuelekea nayo
stendi. Wakati amepanda daladala, leo alikutana tena na Fetty
na kumfurahia sana, ambapo waliongea mengi mengi, Fetty akamuomba wakae mahali
waongee na kushauriana mambo mbalimbali, kwavile ilikuwa mapema Erica hakuona
tatizo la kukaa na kuongea na Fetty. Kwahiyo walishuka mahali na kwenda
kukaa kwenye mgahawa Fulani wakiongea huku wakipeana ushauri
mbalimbali, “Erica nimefurahi sana kukutana na wewe, kuna mambo
yananitatiza akili yangu ila najua nimekutana na wewe utanishauri” “Yapi
hayo?” “Bhana mwenzio kuna kitu nimefanya, kwakweli sijapenda ila
niliamua kufanya maana maji yalinifika shingoni” “Kitu gani
hiko?” “Nishawahi kukwambia kuhusu baba wa mwanangu, sasa baada ya
kunitimua kule na kurudi nyumbani. Watu wakaniambia nisikubali nizunguke zunguke
maana sio hali ya kawaida, na mimi nimeangalia kweli sio hali ya kawaida
ukizingatia mwanzoni alikuwa akinipenda tu. Nikaamua kwenda kwa
mtaalamu” Erica akaamua asikilize kwa makini
sasa, “Eeeeh!” “Sasa bhana, mtalaamu Yule kiboko yani anaonyesha
kila kitu unaangalia kwenye kioo kama sinema vile. Ni kweli ndugu wa baba wa
mwanangu hawakutaka awe na mimi, sasa kuna mwanamke walimtafutia ndugu yao,
walichofanya ili ndugu yao aachane na mimi ni kwenda kwa mganga wakachukua dawa.
Ila dawa zenye nguvu bhana huwa zinataka muhusika mwenyewe atende kile kitendo
kwahiyo Yule mwanamke alipika chakula na kuweka dawa aliyopewa kisha yeye
mwenyewe akamtengea Yule bwana chakula kisha Yule bwana akala si ilikuwa kwao
bhana, hata kujiuliza kwanini chakula nitengewe na huyu hakuna, kala kile
chakula ndio akaanza varangati kwangu hadi kunifukuza. Kwakweli nimesikitika
sana Erica, sasa Yule mtaalamu kasema kazi anaiweza, eti nishirikiane nae
tutengeneze makombora ya kumrushia Yule mwanaume ili arudi kwangu. Nimemuitikia
tu kuwa nitaenda tena, ila nikajifikiria, Yule mwanaume kapewa dawa, na mimi
nimpe dawa zingine si ndio mwanzo wa kuwa chizi Yule!” “Dah! Rafiki
yangu Fetty, kwanza nakupongeza kwa kuwa na moyo wa huruma kama huo maana mwisho
wa siku mtamchanganya tu huyo mwanaume, mi naamini kuwa dawa huwa zinaisha
nguvu, yani kuna siku tu atarudi kuwa na akili zake timamu.” “Ni kweli
Erica, ila ndugu jamani sijui akili zao zikoje yani wanaacha kufatilia mambo yao
wanaanza kufatilia mambo ya watu wengine. Yani wanashangaza sana” Erica
akaamua kumueleza pia kuhusu yeye na Bahati, na jinsi alivyoambiwa kuwa Bahati
karogwa, “Tusiandikie mate wakati wino upo, una elfu kumi
hapo?” “Ya nini?” “Nataka twende kwa huyo mtaalamu na wewe
ukaone kila kitu kilichotokea kwa huyo mwanume. Majina yake yote si
unayajua?” “Ndio nayajua, ila Fetty mimi sijawahi kwenda kwa mganga
yeyote toka nizaliwe” “Erica, kwani tunaenda kuua? Tunaenda kupata
ukweli tu, twende acha uoga” “Kwanza mganga mwenyewe yuko
wapi?” “Yupo Kigamboni” “Mmmmh jamani Fetty, toka kigamboni si
nitachelewa sana nyumbani” “Hivi Erica mbona unachekesha, kuna watu
wanakaa chamanzi na wanafanya kazi kigamboni, wanaenda na kurudi kila siku
sembuse wewe wa karibu hapo” “Kigamboni yenyewe sehemu
gani?” “Kigamboni kwa huyo mtaalamu sio pale ni kigamboni kule unaweza
hadi kukutana na Mbagala. Kwahiyo tukubaliane tu tuwahi kwenda ili tuwahi
kurudi” “Jamani Fetty” “Usijali, kutoka nitakusindikiza hadi
kwenu” Basi Fetty akamshawishi shawishi pale mwisho wa siku akakubali na
kwenda na Fetty kwa mganga. Walifika kwa huyo mganga na kukuta
kuna watu wachache tu, kisha walipoisha waliingia wao ili kuangaliziwa matatizo
yao, Erica aliamriwa aweke elfu kumi kwenye kimtungi kidogo kisha aliambiwa
ataje jina la huyo mtu anayehisi amefanyiwa limbwata ili waone imeanzia wapi.
Baada ya hapo, Yule mganga alipaka unga kwenye kioo chake na kuanza kuwaonyesha
Erica na Fetty, kwakweli Erica alishangaa sana kwani ilikuwa kama anaangalia
sinema. Aliwaona ndugu wa Bahati na Yule mshenga wakienda kwa mganga
kuchukua dawa, na baada ya hapo walimkabidhi dawa Yule binti ila Yule binti
kisha alienda nyumbani kwakina Bahati na kumuandalia Bahati chakula ambapo
alimtayarishia na kula, kisha Bahati akaonekana amepatwa na usingizi baada ya
kile chakula. Ikaonyesha tena Yule dada alipelekwa tena kwa mganga na
baba yake, safari hii akapewa dawa nyingine, ile dawa Yule dada alionekana
akiiweka sehemu za siri baada ya hapo akaandaa chakula na kumpelekea Bahati na
alionekana anakula kisha alimpa kinywaji ambacho kiliwekwa pia dawa hiyo,
alikunywa pia na baada ya hapo ilionekana harusi kisha Yule mganga akafuta ule
unga kwenye kile kioo na kikawa tu kioo cha kawaida, kwakweli Erica alishangaa
sana kwani hakuwahi kushuhudia mambo kama yale, aliamua kumuuliza Yule
mtaalamu, “Sasa kwanini dawa nyingine ile aliweka sehemu za
siri?” “Sehemu za siri zina nguvu sana, na ukifanyiwa limbwata la sehemu
za siri huwa nguvu yake si ya mchezo yani unajikuta ukisahau kila
jambo” “Mmmmh makubwa” “Inatakiwa tuanze tiba mapema, si unataka
arudi kwako” “Aaah muache tu mpaka dawa zitakapoisha” Yule
mganga akamuangalia Fetty na kumuangalia Erica kisha akasema, “Wewe
Fetty, ya kwako hatujamalizana, huyu rafiki yako naye hatumalizi tunaacha viporo
tu kwanini?” Fetty akajitetea pale, “Yani sisi babu tulitaka tu
kujua ukweli” “Haya sawa, ukweli mmeshaujua. Ngoja nikuombe kitu kimoja
Fetty, kamsubiri nje huyu rafiki yako Erica, halafu wewe Erica ubaki hapa na
mimi kuna mambo nataka nikuonyeshe” Basi fetty akatoka, Erica alibaki
mwenyewe na Yule mganga ila alikuwa na wasiwasi sana, Yule mganga alikoroga dawa
na kumpa Erica ili anywe, pale pale Erica akakumbuka jinsi limbwata linavyofanya
kazi nay eye ana damu ya kupendwa pendwa akaogopa maana inawezekana hata mganga
akawa amempenda, hakutaka kumuwekea mashaka ila hakutaka kunywa ile dawa,
aligoma kuinywa na kumfanya Yule mganga amuulize kwanini anagoma
kunywa, “Sijaja kwa ugonjwa hapa, kwahiyo sioni sababu ya kunywa
dawa” Yule mganga alimuangalia Erica, na kumpulizia kitu ambapo kwa muda
mchache macho ya Erica yalikuwa kama yamepuliziwa pilipili na kumfanya
ajifikiche sana, basi Yule mganga akawa anampa ile dawa anywe kuwa ndio pona
yake ila bado Erica aligoma, na muda ule ule aliinuka na kutazama kwa shida hadi
kutoka nje kwani macho yalikuwa yakimuwasha ila alivyofika nje muwasho uliisha
pale pale, hakutaka hata kukaa alimwambia tu Fetty waondoke ikabidi Fetty amfate
kwa nyuma, kwakweli Erica alitembea kwa haraka haraka sana, mpaka ilibidi Fetty
atembee kwa mwendo kama wa kukimbia, walivyofika stendi Fetty alimuuliza Erica
kuwa imekuwaje, “Unajua Yule mganga alikuwa akinilazimisha ninywe dawa
yake, kumbuka Fetty sijaja huku kwa ugonjwa” “Ila kwanini umegoma
kunywa?” “Fetty, tumetoka kuangalia pale pale limbwata linavyofanya kazi
je kama Yule mganga kanitamani je!” “Hahaha Erica jamani, sasa kwanini
Yule mganga akutamani?” “Hujui tu Fetty, kwakweli niende nyumbani
kwasasa, nimechelewa hivi sijui mama nitamueleza vipi?” Walipopata
usafiri basi safari ikaendelea. Kwenye mida ya saa tano usiku
ndipo Erica aliingia nyumbani kwao, kwakweli mama yake alifoka sana maana
hakupendezewa kabisa kuona mwanae kachelewa kufika nyumbani kiasi
kile. “Erica, kweli mpaka muda huu mwanangu” “Nisamehe
mama” “Sijapenda, yani sijapenda kabisa” Akataka kumchukua mtoto
ili akamlaze chumbani, “Hebu nenda kaoge huko usinipakie mjukuu wangu
unajisi, najua umetoka wapi hadi muda huu kweli? Nenda kaoge huko” Basi
Erica alienda kuoga kisha kumchukua mwanae kwenda nae chumbani, kiuwekili hata
hamu ya kula hakuwa nayo kabisa. Aliamua tu kulala, akiwa katikati ya
usingizi, akamuona Yule mganga ndotoni akimwambia, “Nakupenda sana
Erica, nitakufanyia kila kitu utakacho. Nakupenda sana” Kisha akamuona
Yule mganga akimsogelea kama anataka kumbusu hivi, Erica akashtuka huku jasho
likimtoka, akaogopa sana hata kulala tena aliogopa na kuanza kukumbuka story za
watu kuwa kuna majini mahaba, kwahiyo alijikuta akijawa na mashaka sana kuwa
pengine akute majini mahaba. Alikaa kaa kisha akaamua kulala tena, muda
huu aliona kama yupo ka Yule mganga halafu anataka kunywa kile kinywaji, Erica
alishtuka na kuita mama yake kwa nguvu, mama yake alifika na kumkuta Erica
akihema sana ikabidi amuulize kuwa tatizo ni nini, “Kuna mtu wa ajabu
nikilala ananijia mama yani nakosa hadi usingizi” Ikabidi mama yake
aingie kwenye maombi, na baada ya yale maombi ndipo Erica akalala
sasa. Kulivyokucha, mama yake alienda kumshtua saa mbili
asubuhi, “Kheee wewe huendi kazini? Wewe mwenyewe urudi saa tano za
usiku halafu hadi saa hizi hujaenda kazini tatizo ni nini?” “Nilisahau
kuamka mama” “Haya amka ujiandae” “Ila mama
nishachelewa” “Aaah sitaki kusikia hizo mada, jiandae uwende kazini
utatafuta jinsi ya kumueleza bosi wako ila uende kazini, na kama huendi utoe
taarifa sio kama mambo ya shemeji yako James kuwa kila siku ulikuwa unamuomba
ruhusa, kumbuka huko ni ofisi mpya” Basi Erica aliinuka kitandani na
kwenda kuoga halafu kujiandaa ili aende kazini, sema kiukweli hakutaka kwenda
tena kazini ila akaenda tu sababu ya mama yake. Basi alifika ofisini
kwenye mida ya saa nne kasoro, akaona ni vyema aende kwanza kwa bosi wake
kuripoti ili ajue mbivu na mbichi ila cha kushangaza alivyofika kwa bosi wake
hakumkuta ofisini, kwahiyo akaamua kwenda kwenye ofisi yao na kumkuta George
akiendelea na kazi, akamsalimia kisha George akamuuliza, “Mbona leo
umechelewa sana?” “Nilishikwa na tumbo la asubuhi yani limeniendesha
sana” “Aaah pole ila mbona upo hivyo?” “Nipoje?” “Aaah
hamna kitu” “Na bosi yuko wapi maana nilikuwa nataka nimwambie kuwa
kwanini nimechelewa” “Hivi unadhani huyu mama huwa anafatilia kiasi
hiko? Kama kitengo hiki ninayefatilia ni mimi, sema na uzuri ni kuwa leo
hajafika ofisini na sijui kwanini hajafika” “Aaah kumbe” Basi
Erica akaanza kufanya kazi za pale ila alikuwa na mawazo sana kiasi kwamba
hakuwa na raha kabisa. Muda wa kutoka, leo George alimwambia tena swala
la kumpa lift Erica ila Erica aligoma kwani bado alikuwa na kumbukumbu ya
kitendo cha kipindi kile cha George kutaka kumbaka, sasa akimgeukia humo kwenye
gari itakuwaje? Kwahiyo akaona ni vyema akapande daladala tu kama
kawaida. Basi akaondoka na kwenda stendi ya daladala kama kawaida, ila
leo kabla hajapanda alihisi kama kuna uwepo wa mtu nyuma yake, akageuka ila
hakumuona mtu yeyote, akaamua kusogea eneo lingine bado alijihisi kuna mtu
kasimama nyuma yake, ila alipogeuka hakuona mtu tena. Hofu ikamshika na kutamani
daladala ifike tu apande maana hakuelewa ni mtu gani anamfatilia, gafla
akapigiwa simu na kupokea, Yule aliyempigia alijitambulisha kuwa Yule jirani wa
Bahati, kwa hapo akahisi kuwa ni huyo ndio anamfanyia mchezo wa kukaa nyuma yake
ila akamsikiliza’ “Erica, ikija daladala hata kama imejaa ingia upande,
ukifika nyumbani nipigie nikwambie maana mtu aliyekuwa nyuma yako si mtu mzuri.
Usinijibu ila panda daladala iliyojaa akose nafasi” Erica aliogopa hata
kumjibu Yule dada, na kweli daladala ilikuja imejaa maana muda wote alikuwa
akisubiri daladala tupu ili akae kwenye siti, ila toka ameambiwa hivyo alipanda
daladala iliyojaa na kuondoka zake. Alivyofika kwao,
alimsalimia mama yake kisha aliingia chumbani kwake kwani alikuwa na hamu sana
ya kujua kuwa ni kitu gani Yule mdada anataka kumwambia, akampigia simu na
kumsikiliza, “Ushafika nyumbani?” “Ndio
nimefika” “Erica, kuna mtu alikuwa akikufatilia ila si mtu mzuri Yule
maana alikuwa akitokea na kutoweka” Erica alishtuka na kumuuliza Yule
mwanamke kuwa huyo mtu yukoje, kwa jinsi Yule mwanamke alivyomueleza moja kwa
moja Erica alijua ni Yule mganga maana sifa zote za Yule mganga ndio
alizoambiwa, kwakweli Erica aliogopa na hakuweza kukaa kimya zaidi akaamua
kumueleza ukweli huyu dada jinsi alivyoenda na rafiki yake kwa mganga na jinsi
Yule mganga alivyotaka kumpa dawa na yote yaliyomtokea usiku, Yule dada
alishtuka sana na kumuuliza vizuri Erica, “Eeeeh huyo mganga ni wa
wapi?” Ikabidi Erica aanze kumuelekeza vile alivyokwenda na rafiki
yake, “Uwiii Erica umepotea yani umepotea kabisa, bora hata ungeniomba
ushauri kwanza. Huyo mganga ni mzuri sana ila ana majini makali sana, yani kama
hivyo kashakupenda tayari na ili kumuepuka labda tupate mganga wa zaidi yake.
Namfahamu stori zake huyo mganga, kashalala na wadada wengi waliokwenda kwake
ilimradi awapende tu, yani yeye hakutongozi usoni ila atakuvutia kwa dawa na
ndotoni” “Naogopa dada, sasa nifanyeje” “Inatakiwa twende kwa
mganga zaidi yake, ila leo ngoja nikufundishe cha kufanya maana atakufata usiku
utajikuta tu umelala nae hata ndotoni” Kwakweli Erica aliogopa sana na
kuanza kusikiliza maelezo anayopewa na Yule mdada, kisha alipokata simu akatoka
na kumuaga mama yake kuwa anaenda dukani ila alienda kutafuta vitu alivyoambiwa
na Yule mwanamke. Kwakweli mama yake hakumuelewa kabisa na
kujiuliza kuwa mwanae ana matatizo gani, maana toka amerudi kazini hakuekeweka
kabisa, akajipanga kumuuliza kuwa tatizo ni nini akitoka dukani ila Erica
alikawia sana kurudi mwisho wake wakati anarudi alimkuta mama yake amesinzia
sebleni na mjukuu wake mikononi. Erica aliingia chumbani akawasha dawa
aliyoambiwa kisha akaenda kuoga, ile harufu ya ile dawa ndio ilimshtua mama yake
usingizini na hadi akaanza kutafuta harufu inatokea wapi, wakati huo Erica
alitoka kuoga na kurudi chumbani kwake ila aliona kama kuna ujumbe umeingia
kwenye simu yake, akachukua na kuuangalia, akaona umetoka kwa Yule mwanamke
aliyesema ni mwanamaombi ulisema, “Watu wangu wanaangamia kwa kukosa
maarifa” Akashangaa kwanini katumia ujumbe huo na Yule mama, kisha mama
yake akamgongea kwa nguvu, Erica akafungua na mama yake akaanza
kufoka, “Umewasha mavitu gani kwenye nyumba yangu?” Erica
alimuangalia tu mama yake, kisha mama yake alichukua maji na kwenda kuzima,
ndipo Erica sasa akamwambia mama yake, “Aaah mama umezima wakati nataka
kujifukiza” “Hivi wewe mtoto una akili kweli? Mambo ya kiganga haya,
nieleze sasa umeanza lini kwenda kwa waganga?” “Mama
nisamehe” “Mjinga wewe, nisamehe ndio nini? Hebu fungua madirisha huko
harufu yako itoke hii, kuniletea ujinga kila kukicha kwenye nyumba yangu, hivi
una nini lakini Erica jamani? Kwanini unakuwa hivyo, iko wapi elimu yako? Na
usomi huo bado unaamini waganga? Wewe mtoto una matatizo gani? Fungua madirisha
hayo na uje sebleni unieleze ujinga wa hizo dawa umeutoa wapi uchome kwenye
nyumba yangu” Basi Erica alifungua madirisha ya chumbani kwake na kwend
akuzungumza na mama yake, alipofika sebleni alimuona mama yake amechukia sana
akitamani hata kumnasa vibao Erica, ila akamuangalia tu na kumtaka aeleze ukweli
wote asimfiche jambo lolote. Ilibidi Erica amueleze kila kitu mama yake
kwani akaona hata akificha hatopata faida na ile hali itazidi kumtesa,
akamueleza hata jana yake kuwa ndio chanzo cha yeye kushtuka usiku wa manane
maana huyo mganga alikuwa akimfatilia kwenye ndoto. Kitu pekee ambacho
hakumwambia mama yake ni kuhusu kazini kwake tu, kwakweli yale maelezo mama
Erica alionekana kuchukizwa sana na kuanza kusema, “Unajua nimechukia
sana ila sitaki kuongea kwa hasira maana hutonielewa, unajua mara nyingine mtu
unafanya vitu ambavyo badae unakuja kujutia. Ujinga wako ungefanya uwe mke wa
mganga wewe, badala uje kusema mama kuna hili na lile na lile, nisaidie maombi
mama ila wewe miguu inakuwasha moja kwa moja kwa mganga haya unayachukua na
kuyachukua, nakwambia utamsahau huyo Erick na yeye atakusahau kwa ujinga wako.
Kijana wa watu ana moyo balaa, yani hupatikani kwenye simu sijui upokei ila
anapiga na kuongea na Angel yani wewe Erica wewe usipojiangalia utakosa mwana na
maji ya moto” “Nisamehe mama, naomba unisaidie mama yangu yani
sielewi” “Sitaki kuongea sana ila tutasali pamoja na kama usiku ukiona
chochote hukielewi basi uniamshe mama yako tuombe sio kesho tena miguu ikuwashe
uwende kwa mganga mwingine.” “Sirudii mama kufanya hivi” Basi
mama yake alienda nae chumbani kwake na kufanya maombi kwa muda kidogo kisha
akamwambia akale ndio alale maana hata kula alikuwa hajala, basi Erica alienda
kula na kurudi chumbani kwake ili alale. Tangia jana hakuwasiliana
kabisa na Erick sababu hakupata muda wa kumtafuta kutokana na muda aliofika na
kulala, jana kumaliza shughuli zote alilala saa sita, na siku hiyo baada ya
mambo yote alijiona saa sita ikimgongea na muda huo akataka kulala ila alipigiwa
simu, kuangalia ni namba ya Yule mwanamaombi, akapokea na kuanza kuongea nae
baada ya salamu, “Erica, najikuta Napata mzigo juu yako kuwa nikuombee
sana. Napata picha kuwa unapitia kwenye magumu sana” “Kweli kabisa
napitia kwenye magumu” “Basi usiache kuomba, kilichonifanya nikupigie
simu usiku huu ni kitu kimoja” “Kitu gani hiko?” “Kuna kitu
nakiona kipo siku ya kesho, sijui ni kitu gani ila naona kipo kwako. Kama
utaweza basi kesho tulia kwenu tu ukifanya ibada na usiende popote” Basi
Erica alimshukuru na kukata simu ila alijifikiria na kusema, “Mmmmh ndio
hawa hawa anaanza nakuombea nakuombea, sijui kesho usitoke kuna kitu kibaya
kwako. Yeye kajuaje? Halafu kesho atanitafuta na kutaka sadaka na kusema
nimekuzuia sijui nini na nini. Ngoja nilale zangu mie” Basi akataka
kujilaza ila aliamua kufanya maombi kwanza kwa muda mfupi ingawa aliomba na mama
yake ila alijiona ana sababu za kufanya maombi, “Eeeh Mungu nisaidie,
mimi ni mwenye dhambi nakukosea sana nisamehe Mungu wangu. Naomba nisianguke
kwenye mikono ya wote wanaonihitaji kwa mabaya, Yule mganga asinipate wala
yeyote Yule asinipate, naomba nitunze kwaajili ya Erick tu.
Amen” Alimaliza maombi yake ila akajiuliza, “Hivi maombi ndio
yanatakiwa yawe hivi kweli? Lakini sijui kuomba, Mungu atanisaidia tu maana
ananijua” Muda huo aliamua kulala na alilala vizuri tu kwani hakujiwa na
ndoto yoyote kama iliyomjia jana yake. Kulipokucha ni mama yake
alimuamsha kuwa aende kazini maana mama yake hakujua chochote kinachoendelea
kwenye kazi juu ya mwanae, kwa upande mwingine Erica alihisi kwamba huenda Yule
bosi wake hajaelezwa ukweli na Tumaini maana kama angeelezwa ukweli basi jana
yake angemkuta, ila kwavile hakumkuta alihisi ni amani tu kwake na ataendelea
kufanya kazi huku kujizuia kuwa Yule mama asimjue. Alijiandaa vizuri na
kwenda kazini, alifika na kwenda ofisini kwao moja kwa moja ila hakumkuta George
akashangaa kuwa siku hiyo George kachelewa au vipi ila kuna upande mwingine
aliamua kwenda kwa bosi wao yani Yule mama yake Erick, alivyofika mlangoni kabla
ya kugonga alitegesha sikio na kusikiliza Yule mama anaongea na nani maana
alisikia kama anaongea na mtu, ndipo akagundua kuwa anaongea na George,
akategesha vizuri sikio kusikiliza, “Yani George, kumbe Yule Erica hafai
hafai kabisa huwezi amini, nimemuajiri hapa kumbe nimeajiri nyoka wa kumtafuna
mwanangu.” “Kuna lipi kafanya tena” “Yule msichana kazaa huko,
halafu mtoto kamsingizia mwanangu” “Kumbe ana mtoto Erica” “Ndio
ana mtoto, jana nilienda na Tumaini mahali kwakweli alivyonionyesha
vimenisikitisha sana. Sikutegemea kama binti niliyemuona mpole, mtulivu na mcha
Mungu kumbe ni shetani wa mashetani, hivi kashafika uniitie? Usimwambie lolote,
nitaongea nae mwenyewe” Erica akaona msala, aliingia kwenye ofisi yao na
kuchukua mkoba wake na kutoka, alipita pale mapokezi kama kishada vile yani
hakutaka hata kusimama. Alipotoka nje ya ofisi wakati anatembea
akielekea stendi, alishangaa kuna gari ilipaki pembeni yake milango ikafunguliwa
na muda huo huo akaingizwa kwenye lile gari yani kilikuwa kitendo cha muda mfupi
na kumfanya ashindwe hata kupiga kelele, wakati ameinua sura yake apige kelele
alishangaa kumuona Mzee Jimmy ndio yupo ndani ya gari
lile. Alipotoka nje ya ofisi wakati anatembea
akielekea stendi, alishangaa kuna gari ilipaki pembeni yake milango ikafunguliwa
na muda huo huo akaingizwa kwenye lile gari yani kilikuwa kitendo cha muda mfupi
na kumfanya ashindwe hata kupiga kelele, wakati ameinua sura yake apige kelele
alishangaa kumuona Mzee Jimmy ndio yupo ndani ya gari lile. Erica akaona
hapo asipotumia akili basi atabakwa, kwahiyo aliamua kuwa mpole ili kuona kama
anaweza kuiteka akili yam zee Jimmy, kwakweli hata yeye alimshangaa Erica maana
mwanzoni alionyesha kama kutaka kupiga kelele ila gafla alivyomuona mzee Jimmy
alitulia tuli, ilibidi mzee Jimmy amuulize, “Mbona hujafanya purukushani
sasa ili nikushushe?” “Nifanye purukushani za nini sasa? Nitakuwa sina
akili, Dora kaniambia kila kitu jinsi unavyonipenda halafu nianze purukushani
kweli?” “Aaaah kwahiyo nawe umeridhia? Mbona Dora alisema
umegoma?” “Niligoma ili nione Dora nae ana lengo gani maana Yule rafiki
yangu ana tamaa sana, ila nilipofikia unataka kunioa nilifurahi sana maana hiyo
ndio ndoto ya maisha yangu” “Erica nitakuoa kweli, basi chagua eneo
tukafurahi pamoja” Erica alifikiria kisha akachagua mahali ambapo alijua
ni rahisi kwa yeye kuweza kurudi kwao, kisha Yule mzee akaenda nae
alipopachagua, kiukweli Erica hakutaka kufanya fujo yoyote maana hakujua huyu
mzee kajipanga vipi ukizingatia, nyuma ya lile gari la mzee Jimmy kulikuwa na
gari nyingine ndogo ambayo nayo ilienda pale pale kwenye hoteli ambayo Erica
aliichagua na walikaa meza ya pembeni kidogo na ile aliyokaa Erica na mzee
Jimmy. Kisha Erica na mzee Jimmy wakaagiza vinywaji huku Erica
akiendelea kumuhoji mzee Jimmy ili kuweka uaminifu kwake, “Kwahiyo
utanioa lini?” “Yani mwaka huu haupiti Erica, utakuwa mke wangu. Ila
nina hamu mwenzio, basi twende ukanipe” “Sawa usijali, tunywe kidogo
tupate nguvu na nikakupe kwa staili yoyote unayotaka” Alikuwa akisema
hayo huku akiwaza sana maana hakujua hata afanye kitu gani, muda kidogo
akapigiwa simu alipoiangalia aliona ni Yule mwana maombi, ikabidi Erica apokee
kwani aliona kama mkosi wa siku hiyo ndio umejengeka, “Hallow Erica,
sehemu uliyokuwepo si salama, ondoka upesi” Erica akakata ile simu na
kumuangalia mzee Jimmy huku sura yake ikionyesha machozi, ikabidi mzee Jimmy
amuulize kuwa imekuwaje, “Mama kanipigia simu eti mwanangu kazidiwa
sana, Mungu wangu sijui nitafanyaje mimi!” “Sasa itabidi apelekwe
hospitali, basi twende wote kwenu” “Tukienda wote mama yangu hatotuelewa
kabisa, masikini mwanangu sijui nafanyaje” “Sikia basi, twende nje pale
nikuchukulie tax halafu uende nayo hadi kwenu mchukue mtoto muwaishe hospitali,
halafu utanijulisha ni hospitali gani usijali kila kitu nitalipa
mimi” Basi Erica alionekana kuchanganyikiwa kabisa hadi mzee Jimmy
alimuhurumia, wakatoka nje na kumchukulia gari ya kukodi ambapo akampa pesa
Erica za kumlipa Yule dereva ili kama pesa aliyompa haikutosha maana kuna pesa
nyingine alimpa Yule dereva wa gari ya kukodi. Kisha Erica alipanda
kwenye ile gari na dereva alianza safari ya kumpeleka
kwao. Walivyofika Erica aliingia ndani kwa muda na kuweka mkoba
wake, kisha akatoka na kusimama mlangoni akimwambia Yule dereva aondoke tu
akamwambia kama mzee Jimmy atamuuliza amwambie kuwa ulikuta gari nyingine
inasubiri kunipeleka hospitali, kwavile dereva alishalipwa chake kwahiyo hakuona
tatizo kujiondokea tu. Erica akarudi ndani kwao, hakutaka hata kuongea
chochote na mama yake zaidi ya salamu na kwenda chumbani kwake, kakweli
hakuamini kama karudi nyumbani akiwa mzima kabisa, ila kwa tukio lile kuna jambo
kubwa sana alikuwa kajifunza. Kwanza alijiuliza, Yule mzee Jimmy
ilikuwaje akapita pale nje ya ofisi ya mama Erick? Na alijuaje kama yeye yupo
pale? Alijiuliza na kukosa jibu ila alimshukuru Mungu tu kwa kumuokoa maana
mpaka muda huo hakuamini kabisa kama alikuwa amepona toka mikononi mwa mzee
Jimmy, aliamua kujilaza sasa. Jioni ndio mama yake akaenda kumuamsha na
kumfanya aamke na kwenda kuoga ili kuondoa uchovu, kisha mama yake alimuita na
kuongea nae, “Unajua Erica sijakuelewa tangu umerudi, maana umenisalimia
tu ukapitiliza kulala. Tatizo ni nini maana leo umerudi mapema kutoka kazini
halafu hukuwa kwenye hali ya kawaida, tatizo ni nini?” “Ngoja nikwambie
ukweli mama yangu” “Niambie” Akaanza kumueleza mama yake
alivyokutana na Yule mwanamaombi na zile jumbe alizokuwa akimtumia na tangu jana
alivyomwambia kuwa asitoke, “Sasa mimi leo uliponiambia niende kazini
nikaamua kwenda tu, sikutaka kusikia yale maswala ya usitoke wala nini maana
nilihisi nae pengine ana mambo kama ya waganga wa kienyeji. Ila nilipokuwa
kazini, nikatoka nje mara moja gafla nilikamatwa na mtu na kuingizwa kwenye
gari, kuangalia mama alikuwa mzee Jimmy yani ilikuwa hatari leo” “Eeeeh
kwahiyo huyo mzee akakubaka?” “Hapana mama hakunibaka” “Ila
ikawaje?” Ikabidi amueleze ilivyokuwa hadi akaweza kuondoka mikononi mwa
Yule mzee, “Kwakweli mama leo ingekuwa habari nyingi, maana ningebakwa
hivi najiona” “Wewe mtoto una kilanga, tena una kilanga haswaa, mtu wa
watu kaonyeshwa kuwa kuna baya mbele yako na kakwambia usitoke ila wewe mjuaji
basi kiguu na njia Yule ukatoka. Ulishindwa nini kuniambia leo mama siendi
kazini sababu ya moja mbili na tatu, ningekataa? Yani na ungebakwa ungekuwa
umejitakia mwenyewe kwa kilanga chako? Mtoto hujielewi kabisa wewe, kila siku
nasema wewe ni bure kabisa, sikukuzaa hivyo Erica hata huwa sielewi hiyo akili
mbovu unaitoa wapi” “Mama jamani” “Sio mama jamani, tena nahisi
huyo mzee ameathirika yani leo ungepata mimba na ukimwi juu. Mshukuru sana huyo
aliyekuwa akikuombea maana ulimpa mzigo mzito wa kufanya maombi juu yako, hata
hiyo akili ya kumkwepa leo mzee Jimmy ni Mungu tu kakusaidia mjinga wewe.
Ulishindwa nini kunieleza jana mama yako? Unahisi ni mazuri maswala
haya?” “Hapana mama ila sijui hata ilikuwaje sikukwambia” “Hivi
na huyo mzee anataka nini kwako mwanangu? Naomba akikutafuta mwambie aje
nyumbani, nataka nizungumze nae kama mzazi, hivi anakutakia nini mwanangu
jamani? Ujanani ale na nani na uzee aje amfie nani? Kuna watu wengine
hawajiheshimu kabisa, anatakiwa kuheshimu hisia zako kuwa humtaki sio
kukulazimisha lazimisha” “Nishamwambia simtaki mama ila namshangaa
kwakweli, ila leo dah sijui ingekuwaje jamani hata sielewi” “Sikia
Erica, siku zote nakwambia ila hunielewi nazungumzia nini. Nimekwambia kuwa
lisemwalo lipo na kama halipo linakuja, hayo ni maneno ya waswahili ila yana
maana sana. Unapopata ujumbe wowote usiupuuzie na kusema kuwa haiwezi kutokea,
haitotokea kama utasimama kweli kumuomba Mungu kuwa hilo jambo baya unalikataa
lisitokee katika maisha yako. Sio kuomba hujui halafu unajifanya eti hakuna kitu
wakati mtu kashakuzuia usitoke” “Mama sikujua, nilihisi anajisemea
tu” “Hata mtu akiwa anjisemea tu unatakiwa kukemea sio kujifanya hamna
kitu. Maneno yanajenga, maneno yanaumba. Mwisho wa siku unaanza kujilaumu kuwa
ningejua ningejua, na kumbuka kuwa majuto ni mjukuu, wewe mtoto usinitafutie
makubwa ujue, kila kitu uwe unaniambia maana nishaanza kuona kama akili zako
mbovu. Umenisikia, kila kitu uwe unaniambia” “Sawa mama nitakuwa
nitakwambia” “Mficha maradhi kifo humuumbua, na kumbuka kusali tu kwani
maombi ndio silaha tosha, mambo yako ya kushawishiwa kwenda kwa mganga sitaki
kuyasikia sawa” “Sawa mama” Erica alimuitikia mama yake na
kwenda kufanya mambo mengine, kisha kumchukua mwanae na kwenda nae
chumbani. Kabla ya kulala leo alipigiwa simu na Erick, kisha akapokea na
kumsalimia, “Kweli Erica jamani mpenzi wangu, siku mbili nzima hakuna
kuwasiliana kweli?” “Nisamehe bure” “Namba yako kila nikiitafuta
siipati jamani, nimekuwa nikimtafuta bibi yake Angel tu ili niongee na Angel, ni
haki kweli hiyo unayonifanyia Erica?” “Nisamehe Erick
jamani” “Au kwavile nimesema hadi nifikirie cha kufanya kuhusu swala la
ndoa mimi na wewe ndio ukaamua kunifanyia visa hivi!” “Erick, ngoja
nikwambie ukweli. Kazi ninayofanya inanibana sana kiasi kwamba nakosa muda
kabisa hata sielewi labda simu inakuwa imejizima au nini ila narudi nimechoka
sana” “Kama ni hivyo basi hiyo sio kazi inayokufaa, bora ukae nyumbani
tutafute kazi nyingine Erica kuliko kazi ya kukufanya hadi usahau majukumu yako.
Unafikiri itakuwaje hata tukiishi pamoja yani upon a kazi tu hakuna muda wa
familia unafikiri inakuwaje? Naomba tukubaliane Erica, hiyo kazi
uache” Kwavile Erica alihitaji kuacha kazi kutokana na kujua ukweli
kuhusu bosi wake, kwahiyo hakuona tatizo la kusema kuwa anaacha hiyo kazi, ila
tu hakutaka kumwambia ukweli Erick kama bosi ni mama yake kwani alihisi ni
kumchanganya zaidi, “Erick nimesikia, nakuahidi naacha hiyo
kazi” “Unaacha lini?” “yani kuanzia leo ndio nimeacha hivyo,
kesho sitaenda tena maana nisijenikaenda wakanilazimisha nisiache, bora nisiende
tu na kisha waniachishe wenyewe moja kwa moja” “Sawa sawa, nimefurahi
kuona una masikio ya kunisikiliza mumeo ninachotaka. Tutatafuta kazi nyingine na
kama nikiona kazi zinakubana sana basi nitakutafutia biashara ya kufanya kwani
najua kukaa nyumbani kunabore sana, kuhusu swala la pesa nitakuagizia pale
dukani ukachukue, sawa” “Sawa, asante” Erica alitabasamu zaidi
aliposikia kuhusu swala la pesa kwani kwa yeye pesa ndio inayomfanya atafute
kazi na kuhangaika na mambo mbalimbali ila akiwa na uhakika wa kupata pesa basi
atajishughulisha na mambo madogo madogo tu, yani hadi anaagana nae kulala
alikuwa na furaha sana. Usiku wa manane kwenye ndoto akajiwa tena na
Yule mganga, safari hii alimwambia, “Haijalishi ni jinsi gani unanikwepa
ila lazima nitakupata Erica” Akawa kawa anamsogelea ili ambusu, Erica
alianza kupiga makelele na mama yake alienda chumbani, kisha akamsimulia mama
yake kuhusu aliyoyaota, ikabidi mama yake aingie kwenye maombi na baada ya hapo
ndipo alilala tena hadi panakucha hakujiwa na ndoto ya Yule mganga
kabisa. Kulipokucha Erica akaamshwa na mlio wa simu, kuangalia
ni Yule mama muombaji, akapokea na kumsalimia kisha aliamua kumueleza
kilichomtokea jana, “Kwakweli simu yako ndio ilinisaidia” “Ni
Mungu ndio kakusaidia Erica, ila unatakiwa kuomba sana. Na jana usiku ni kitu
gani kilikupata? Maana nilishangaa nikipata mguso wa kuomba kwaajili
yako” Basi Erica aliamua kumueleza huyu mwanamke kuhusu swala la yeye na
rafiki yake kwenda kwa mganga na jinsi huyo mganga anavyomsumbua katika ndoto na
jinsi anavyomuamshaga mama yake na kisha kufanya maombi. “Erica,
mshukuru Mungu sana una mama anayemjua Mungu maana kwa mapito yako ungejikuta
upo sehemu mbaya sana” “Kwakweli namshukuru Mungu kwa
hili” “Sasa ngoja tuendelee kumsihi Mungu tujue tatizo ni nini mpaka
huyo mganga anaweza kuendelea kuja ndotoni, Mungu ni mwaminifu Erica na
atatujulisha tu. Unajua tukijua chanzo inakuwa rahisi sana kuifunga ile namna
anayopitia kuja katika ndoto zako. Nitaendelea kukuombea ila na wewe uendelee
kujiombea” “Asante, nashukuru” Basi akakata simu na kuamua
kuamka tu kama kawaida ila siku hii wala mama yake hakumuimiza tena kwenda
kazini, ila ile asubuhi alimuuliza tu kuwa inakuwaje na maswala ya
kazi, “Mama nimeona Yule mzee kashapajua pale ninapofanyia kazi
atanisumbua sana, nimeamua kuacha kazi tu” “Aaah mwanangu, unaacha kazi
kirahisi kama hivyo sababu ya mjinga mmoja anayekusumbua akili yako. Sikia
mwanangu naomba huyo mzee akikutafuta tena mwambie aje nyumbani, nahitaji
kuzungumza nae maana sio kitu kizuri huwezi fanya kazi sehemu yoyote ile maana
akiijua tu unaanza kuwa na mashaka na maisha yako, nahitaji afike hapa
nizungumze nae maana sijapendezewa na tabia yake kabisa. Vipi
hajakutafuta?” “Hajanitafuta mama” “Sawa, halafu inabidi
tuendelee na maombi na wewe usiache kuomba maana ni makubwa sana umeenda kutazoa
kwa yule mganga” “Sawa mama nimekuelewa” Akaelewana na mama yake
pale kisha akaendelea kufanya mambo mengine. Kwenye mida ya mchana akiwa
chumbani kwake alipigiwa simu na dada yake Mage ikabidi apokee na asikie kuwa
ana kipi cha kumwambia, baada ya salamu dada yake alianza kumueleza kuhusu
alipofikia kwenye swala la yeye kutembea na ndugu yake, “Erica,
tumeongea na baba wadogo nimewaeleza ukweli, wamesema inabidi tukafanye
tambiko” “Tambiko?” “Ndio tambiko Erica, unajua ili jambo sio la
kawaida yani bila tambiko hiyo laana haitofutika” “Ila dada kwanini
tusiende kwenye maombi tu” “Wewe Erica hebu niondolee kichaa mie, wakati
unaenda kulala na Derick mlikumbuka maombi? Hayo unayoyaita maombi, ulikumbuka
kuyafanya wakati unaenda kulala na ndugu yako?” “Jamani
dada” “Sio jamani dada, ujinga wa namna hiyo siwezi kuukubali hata
kidogo umesikia? Tunatakiwa tukafanye tambiko, nimejitoa kwaajili ya maisha yako
wewe na Erick, kumbuka sihusiki kwa lolote ila ni nyie wawili ndio mmefanya hadi
inabidi tukafanye tambiko” “Lakini dada” “Hakuna cha lakini,
mwenzio nishamwambia na amekubali, ni Jumamosi tutasafiri kwenda kufanya hilo,
kwahiyo na wewe ujiandae” “Ila dada mama amekataza mambo hayo ya
waganga” “Aliyekwambia tambiko ni mambo ya waganga nani? Inamaana kusoma
kote huko hujui maswala ya tambiko? Umefanya mambo ya ajabu lazima tufanye
tambiko” “Kwanini tusifanye maombi tu badala ya tambiko?” “Hivi
wewe Erica unajua maombi wewe? Tangu lini ukajua maombi? Ungeyajua maombi
ungezaa nje ya ndoa? Ungeyajua maombi ungetembea na ndugu yako? Ungeyajua maombi
ungezaa na mtu unayotofautiana nae dini? Maombi huyajui wewe, hebu nitolee balaa
na ukizidi kubisha nitamweleza mama kila kitu halafu uone mama atasemaje baada
ya kusikia kuwa ulilala na kaka yako” “Jamani dada usimwambie mama
tafadhali” “Basi jiandae Jumamosi tusafiri tukaivunje hii
laana” “Sasa mama nitamwaga vipi?” “Ni siku nyingi hatujaenda
kuwasalimia baba wadogo, unatakiwa umuage mama kuwa unaenda kuwasalimia baba
wadogo ila mmmh hapana mama atagoma maana anaugomvi wake na wale watu. Basi
mwambie mama kuwa kuna mahali unaenda na mimi, ili aniulize mimi na nitajua cha
kumwambia yani wewe mwambia kuwa hufahamu chochote kuhusu sehemu unayoenda.
Jiandae mapema kabisa, tukutane stendi kuu asubuhi na mapema, Jumatatu utakuwa
umerudi nyumbani” “Mtoto je?” “Mtoto utaenda nae
wapi?” “Ila bado ananyonya dada” “Huyo mtoto unamnyonyesha
uchafu tu, sikia tutakavyoondoka ndio itakuwa njia pekee ya kumuachisha mwanao
ziwa maana utakavyorudi atakuwa ashazoea” “Dada jamani, nilitaka
mwanangu afike miaka miwili kwanza ndio nimuachishe” “Kwani miaka miwili
ndio nini?” “Kliniki wanashauri kuwa ni vizuri kwani mtoto anakuwa na
afya” “Achana na habari za kliniki, mtoto akitembea tu anaachishwa ziwa
sembuse huyo Angel anayemaliza maneno. Haya sisemi lingine tena ila jiandae tu
Jumamosi kwaajili ya hiyo safari” “Sawa dada” Kisha dada yake
akakata simu, kwakweli hakuwa na namna ya kufanya zaidi ya kukubali tu kwani
hakuwa na namna zaidi ingawa kila akifikiria kuwa baada ya hapo itakuwa mwisho
kumnyonyesha mwanae aliumia zaidi maana alipenda aendelee kumnyonyesha mpaka
afunge miaka miwili. Alitoka chumbani na kwenda sebleni ambako alikuwepo
mama yake ila kumwambia chochote hakuweza, wakati akiongea nae mengine simu yake
iliita na alipoiangalia ilikuwa ni namba ya mzee Jimmy, akasita kidogo na mama
yake akamuuliza, “Mbona unasita wakati simu inaita?” “Ni mzee
Jimmy mama” “Sikia, pokea na umwambie kuwa aje nyumbani nahitaji kuonana
nae, yani mwambie lolote ila aje hapa nionane nae haiwezekani animalizie furaha
ya mwanangu kiasi hiki” Basi Erica alipokea ile simu na kuongea nayo
ambapo akamwambia kuhusu swala la kufika nyumbani kwao kwanza kwani mama yake
anataka kumuona, “Aaah mama mkwe anataka kuonana
nami?” “Ndio” “Anataka tusemezane kitu gani?” “Sijui,
ila anataka kuonana nawe” “Basi mwambie nitakuja kesho
jioni” “Sawa nitamwambia” Basi alivyokata simu akampa huo ujumbe
mama yake, na kumuuliza, “Sasa mama, utaongea nae nini?” “Erica,
mimi ni mzazi na ninaumia sana tofauti na wewe unavyodhani. Nahitaji kuongea nae
kwani najua kuwa hata yeye ni mzazi, hapa ni nyumbani kwangu nimemuita hapa kwa
makusudi kabisa na akili zangu zinachemka” “Sasa mama kama akifanya
kitendo kibaya hapa nyumbani?” “Hapa ni nyumbani na hata hivyo naamini
Mungu atatusimamia katika hili, nahitaji kuongea nae ukweli sio kukukosesha raha
na furaha kiasi hiko, kwanini akufanyie hivyo? Mapenzi huwa
hayalazimishwi” “Sawa mama nashukuru kwa upendo wako maana
nilishachanganyikiwa juu ya hili swala” Wakajadiliana pale kuhusu mambo
mbalimbali ila hakuthubutu kugusia kuhusu swala la yeye na dada yake kwenda
kufanya tambiko kwani alijua akimwambia tu mama yake basi habari yake kuwa
alilala na Derick itajulikana na yeye hakutaka ijulikane. Usiku
ulipofika kama kawaida hakutaka tena kupoteza muda bila kuwasiliana na Erick,
aliongea nae na kumpa mtoto aongee nae kisha yeye kuendelea kuongea nae ambapo
Erick alimuuliza, “Kwahiyo leo hukwenda kazini kama tulivyokubaliana
jana usiku si eti eeh!” “Ndio, sikwenda si nilikwambia naacha kwahiyo
nimeacha” “Sawa, sasa unapenda kufanya kazi gani
nyingine?” “Kazi yoyote tu” “Sawa, kuna mtu nimeongea nae kuhusu
maswala ya kazi nadhani atakutafuta Jumamosi ili uongee nae vizuri, najua atakaa
na wewe vizuri kazini maana nishamwambia kuwa asikupe kazi za kukuchosha mwili
wala akili yako” “Sawa Erick, nashukuru sana” “Unajua Erica wewe
ndio mke wangu, mimi nakupenda sana wewe yani wewe si sehemu tu ya maisha yangu
bali wewe ni maisha yangu” Kwakweli Erica alikuwa akijihisi rah asana
kila alipoongea na Erick kwani Erick alikuwa na maneno matamu sana ya kumvutia,
kisha akaagana nae na kulala. Kama kawaida ya kipindi hiko, alijiwa na
Yule mganga kwenye ndoto na akaanza kumwambia, “Erica, siwezi kukuacha
na nitaanza na huyo unayehisi unampenda sana. Kesho usiku ukithubutu tu kuongea
nae kwenye simu nammaliza” Erica akashtuka na kupiga kelele tena, ambapo
mama yake alitoka na Erica alimsimulia mama yake alichokiota, “Mmmmh
Napata mashaka sana, unajua tunafanya maombi ya kumtuliza huyo mtu maana baada
ya maombi haji tena kwenye ndoto zako ila inabidi tufanye maombi ya kumuondoa
kabisa yani asikuone. Kuna kipi chake unacho?” “Sina chochote chake
mama” “Lazima kipo, haiwezekani akufatilie kiasi hiki Erica, ngoja
tuingie kwenye maombi” Basi mama yake aliomba sana kuhusu swala lile
kisha alimwambia mwanae, “Erica, haya ni mapambano makubwa umeenda kuzoa
mambo mwanangu. Habari za waganga nilishakukataza mwanangu, ona sasa. Itabidi
nishirikishe na watu wengine wa maombi wanisaidie swala hili maana anachosema
huyo mtu unaweza ukahisi ni ndoto ila ndio hali halisi, na wewe unatakiwa ujue
kujiombea Erica” “Sawa mama” Kisha Erica akalala tena, muda huu
alilala vizuri tu hadi panakucha. Ila alikuwa na mawazo sana
kwa siku hii yani hakuwa na raha kabisa kila akikumbuka maneno ya Yule mganga
kuwa asithubutu kuongea na simu usiku, yani hakuwa na raha kabisa, aliwaza
kwanini Fetty alimpeleka kwa mganga kama Yule? Kwakweli ile siku hakuwa na
raha. Ilikuwa inakaribia jioni, sikmu yake ikaita akaangalia mpigaji
akaona ni Fetty, akapokea na kuanza kumueleza kuhusu yale yote anayoyaona kwenye
ndoto kuhusu Yule mganga, “Pole rafiki yangu, mimi pia sikujua tabia ya
Yule mganga, ndio nimeambiwa na watu nikaamua nikupigie simu rafiki yangu kama
umepona. Nasikia Yule mganga kashalala na wateja wake wengi sana kwa kutumia
madawa, kwakweli niliposikia imeniuma nikasema ngoja nikuulize rafiki yangu
maana nakumbuka siku ile wakati umetoka haraka kwa mganga uliangusha leso, sasa
watu wanasema Yule mganga akipata kitu chako kimoja basin i rahisi sana
kukuteka. Nimekumbuka hilo nikaamua kukupigia simu” “Mmmh sasa
tutafanyeje maana ananitishia kwenye ndoto” “Sikia cha kufanya, kuna
mganga mwingine nimeambiwa nasikia wengi waliotendwa na Yule mganga wanaenda kwa
huyo mwingine, ni kiboko yeye ana nguvu zaidi” “Hapana Fetty, sitaki
tena kwenda kwa mganga” “Erica, uliangusha leso unadhani kama aliichukua
utapona kweli? Ataendelea kukufatilia kila siku, ujue” “Ngoja
nikamwambie mama, ila swala la kwenda tena kwa mganga hapana
aisee” Erica akakata simu na kwenda kufungua mkoba wake ili kuhakikisha
kama kweli aliangusha leso, alifungua mkoba wake na kukuta leso yake ipo,
akajiuliza kuwa kama kaangusha leso mbona bado ipo kwenye mkoba? Akaichukua
kuiangalia vizuri, akashtuka sana kwani leso ile ilikuwa kipande, yani hapo ndio
akapata maswali zaidi kuwa kipande kilichobaki kikuwapi? Akawa anatoka
ili akamueleze mama yake, alivyofika sebleni tu alisikia mtu akigonga, na mama
yake aliinuka kwenda kumfungulia kwahiyo yeye alisimama pembeni kuangalia kuwa
ni nani, mama yake alivyofungua alishangaa kumuona mzee Jimmy ila hakushangaa
zaidi kwavile alimwambia jana kwamba anaitwa na mama yake, ila kilichomshangaza
ni kuwa mama yake alinyanyua mkono na kumnasa kibao mzee Jimmy kamavile ni mtu
anayemfahamu. Akawa anatoka ili akamueleze
mama yake, alivyofika sebleni tu alisikia mtu akigonga, na mama yake aliinuka
kwenda kumfungulia kwahiyo yeye alisimama pembeni kuangalia kuwa ni nani, mama
yake alivyofungua alishangaa kumuona mzee Jimmy ila hakushangaa zaidi kwavile
alimwambia jana kwamba anaitwa na mama yake, ila kilichomshangaza ni kuwa mama
yake alinyanyua mkono na kumnasa kibao mzee Jimmy kamavile ni mtu
anayemfahamu. Kisha mama Erica aliwaka na kusema, “Haya
kilichokuleta kwangu ni nini wewe firauni mkubwa? Unataka nini nyumbani kwangu,
shetani kama wewe?” Erica akasogea kwa mama yake na kumwambia mama yake
kuwa Yule ndiye mzee Jimmy ila mama yake ndio alizidi kuongea, “Kheee
kumbe ndiomana umekazana kutaka watoto maana watu wazima wote ushamaliza, hivi
wewe mwanaume unataka nini kwa walimwengu wewe? Unadhani nasahau ujinga uliotaka
kunifanyia, nikiwa na mtoto mdogo huyu huyu ambaye leo unamtaka, shetani mkubwa
wewe. Tena umkome mwanangu, ondoka hapa shetani wewe, sikujua jina lako kumbe
unaitwa Jimmy, ondoka kwangu upesi shetani wewe na mwanangu umkome, ukiendelea
nasema mambo yako yote unayofanyiaga watu, tamaa tu. Hivi watu wazima wameisha?
Utaacha lini umalaya wewe? Si ufate watu wazima wenzio, mwanangu mkome mzee
wewe, na uondoke kwangu sitaki hata kuongea nawe” Mzee Jimmy hakusema
neno zaidi kwani alionyesha kushikwa na aibu sana kwahiyo alitoka moja kwa moja
hadi nje ya geti na kupanda gari lake na kuondoka zake, ila mama Erica
aliendelea kuongea hadi Yule mzee alipokuwa ametoka nje bado mama Erica alikuwa
akiongea, “Huna akili hata kidogo wewe mzee, yani maisha yako uhangaike
huko balaa halafu uje kuhangaisha na watoto wetu tena, muone vile. Muache
mwanangu kama alivyo” Kisha Yule mama aliingia tena sebleni na kufunga
mlango huku akiongea kwa hasira sana na kulaani vikali kitendo cha Yule mzee
kuonekana mahali pale. Ikabidi Erica asogee kwa mama yake na kumuuliza
kwa makini kuwa vipi anafahamiana na huyo mzee, “Mama, kumbe
unafahamiana na Mzee Jimmy? Umemfahamu vipi?” “Yule mzee ni mbwa tena
mbwa koko, yani mzee yule hafai ni malaya hatari, kumbe bado anaendelea na tabia
yake loh! Unajua sikumjua kuwa ni yeye ulipokuwa unasema mzee Jimmy mzee Jimmy
wala sikuwa na wazo kuwa ni yeye maana sikumjua jina lake ila tulimuita kiwembe
tu kipindi hiko maana anakata huku na huku” “Eeeeh mama” “Yani
mzee huyu ni malaya tena malaya koko yani hafai kabisa, ngoja nikueleze
nilivyomfahamu huyu mbwa huyu, si uniona mama yako huwa natembea kama
nachechemea eeh!” “Ndio mama” “Basi chanzo ni huyu
mbwa” “Kheee kumbe! Ilikuwaje?” “Kipindi cha nyuma kama
unavyonijua mama yako napenda kujishughulisha basi ndio hivyo tulikuwa na chama
chetu tunakopa huko benki halafu msimamizi alikuwa huyu mzee, jina la kiwembe
lilianza pale ambapo alitembea na dada mtu na mdogo mtu ndio watu wakamuita
kiwembe kuwa anakata kata tu, sasa kumbe ukitaka mkopo haraka lazima ulale nae
ndio upate yani hiyo ndio ilikuwa tabia yako. Sikutaka hata kukutana nae yani
nilikuwa namuona ona tu hata sikutaka mazoea nae, kipindi hiko wewe mdogo
nakubeba mgongoni, siku hiyo zamu yangu ya kupata mkopo ilifika nimeenda akaanza
kuniletea habari zake kuwa lazima nilale nae ndio anipe mkopo, nikamwambia ila
mimi nimefata taratibu zinavyosema wala sitaki kwa njia za panya ndiomana
sijaharakisha kupata, ila akasisitiza kuwa lazima nilale nae ndio nipewe mkopo
nikamgomea kwakweli. Sasa siku hiyo akaniambia kuwa niende ofisini kwake
nikasaini makaratasi ya mkopo, basi nikajibeba na mwanangu hadi ofisini kwa
bahati nzuri mwanangu nilikuwa nimekubeba kwa mbele maana ingekuwa mgongoni basi
saivi nadhani usingekuwepo kwenye macho yangu, nikaingia mule ofisini ili
nisaini namsikia mshushe mtoto nikagoma, akasema leo lazima ulale na mimi ndio
usaini hizi karatasi, nikagoma kuwa kama ndio hivyo basi, weee Yule mbaba
hakukubali akaanza kunilazimisha kuwa nishushe mtoto, nikawa nimegoma tukaanza
kupambana yani alinisukuma vibaya nikaanguka chini kwa mgongo hivi dah nilihisi
viungo vyangu vimekatika, namshukuru Mungu ulikuwa mbele kwahiyo nilianguka ila
nilichokumbuka ni kukushikilia mwanangu bila kujali maumivu ninayopata pale
chini, baba asiye na huruma Yule akaainama na kutaka kuanza kunivua nguo,
nikapiga kelele ila wapi kelele zangu hazikugonga mwamba, ila ikawa bahati tu
kwani muda ule ule kuna watu walikuja na kugonga kwenye ofisi yake, ndipo
aliponiachia na kuruhusu wale watu waingie huku akijifanya kuwa ananipa huduma
ya kwanza eti nilianguka, yani sina hamu nae, nilitoka nachechemea na kurudi
kwangu kumbe kulikuwa na maumivu ya ndani kwa ndani juu yangu, kumbuka hatukuwa
vizuri kipesa kipindi hiko. Nilitaka nikafungue kesi kuhusu huyu kiwembe ila
watu wakanishauri kuwa itanishinda maana huyu pesa anayo na mimi sina hela
kwahiyo kesi itanishinda tu, nilikuja kwenda hospitali wakati tatizo limeshakuwa
kubwa na mpka leo nachechemea mwanangu sababu yake. Toka hapo nikaona kuwa sisi
wanyonge hatuna mtetezi maana kama nikifungua kesi basi mwenye pesa atanishinda,
mtetezi pekee wa wanyonge ni Mungu tu, ndipo nilipoamua kuokoka ili niwe
nashtaki kwa Mungu” Erica alikuwa akilengwa lengwa na machozi kwa
maelezo hayo ya mama yake, na akaona kweli ana haki ya kumzaba kibao mzee Jimmy,
kwa stahili hiyo hafai kabisa, alimuhurumia mama yake kwani ni kweli alikuwaga
akichechemea kwenye kutembea, siku zote hakujua chanzo cha mama yake kuchechemea
kumbe ilikuwa ni yeye mwenyewe, “Pole mama, Mungu atakusaidia mama
yangu” “Mungu ameshanisaidia mwanangu na anaendelea kunisaidia, si jambo
jema kuona Yule Yule mtu aliyetaka kunibaka mimi ndio atake kumbaka na mwanangu
kweli?? Mara nyingine huwa nahisi yeye alitia kama mkosi kwako mwanangu hata
unapata maswahibu mbalimbali katika maisha yako, yani namchukia Yule halafu leo
nimuone nimchekee, weee haipo hiyo kwakweli” Erica alizidi kumpa pole
mama yake kwani aliweza kujua kwa undani zaidi ubaya wa mzee Jimmy na kumfanya
hata asishangae kuona katembea na Dora nab ado anahitaji kutembea na yeye,
kwakweli alikuwa akishangaa sana huku akiendelea kuongea mambo mbalimbali na
mama yake. Kisha Erica aliinuka na kwenda chumbani kwake, na
giza lilishaanza kuingia, akaona simu yake inaita kuangalia akakuta Erick
anapiga, kwakweli akaogopa kupokea maana alikumbuka maneno yale aliyoambiwa
kwenye ndoto na Yule mganga, ndipo akakumbuka hata ile leso ambayo ipo nusu
kwahiyo alitoka tena ili kumueleza mama yake. Akamwambia alivyozungumza
na Fetty na jinsi alivyoenda kuangalia pochi yake na kukuta leso
nusu, “Mmmh mwanangu, hatujamaliza hili linazuka lingine jamani tutapona
kweli?” “Sijui mama” “Hebu mpigie Yule mwanamaombi umueleze hayo
na mimi ngoja niwapigie watumishi wengien niwaeleze maana sio kitu cha kawaida
hiko” Basi Erica alichukua simu yake na kumpigia Yule mwanamaombi, kisha
baada ya salamu alimueleza Yule mganga alivyomtokea usiku na akamueleza jinsi
alivyoongea na rafiki yake na jinsi alivyoona leso yake, “Erica, kwanza
tunatakiwa kumshukuru Mungu sana kwa hilo. Kwakweli Mungu wetu ni muaminifu
sana, tulihitaji kujua ni kwanini bado anakufatilia? Ila Mungu katuonyesha kwa
wazi kabisa kumbe Yule mganga ana kipande cha leso yako, sasa naomba niingie
kwenye maombi ili nijue cha kufanya na hiyo leso. Na wewe uombe
tafadhali” “Sawa, na mimi naomba” Erica alivyokata simu
akamueleza mama yake aliyokuwa akiongea na Yule mwanamaombi, “Hata mimi
watumishiwamesema waombee kwanza swala hilo na kunitaka na mimi kuingia kwenye
maombi. Njoo tuombe kwa pamoja mwanangu” Basi Erica alisogea kwa mama
yake na kushikana mikono kisha kuanza maombi ya kwa pamoja ambapo yalifanyika
kwa muda kama wa nusu saa, kwakweli Erica alijihisi kuchoka maana hakuyaweza
maombi ya vile ila ni mama yake tu ndio alikuwa akiomba. Basi baada ya
maombi wakati wametulia tulia, simu ya Erica iliita tena na alikuwa ni mwanamaombi anapiga, basi Erica alipokea na kuanza kuongea nae, “Sasa
Erica, chukua hicho kitambaa na mtoke nje kabisa ya nyumba yenu kimwagie mafuta
ya taa na ukichome moto huku ukiendelea kuomba, maana huyo tayari ni adui kwako
hafai” Basi Erica alipokata simu alimfahamisha mama yake kisha walibeba
kile kitambaa mpaka nje na kukitupa kisha kumwaga mafuta ya taa na kukichoma
yani kilikuwa kinatoa harufi kama kuna damu inaungulia, hadi mama Erica
akasema, “Mmmmh mara nyingine tunakaa ndani kiajabu jamani, sasa kukaa
na kitambaa kinachomwa kinakuna kama damu mmmh! Makubwa
haya” Walihakikisha kitambaa chote kimeungua kisha walirudi ndani na
kujiandaa kwaajili ya kulala kwani ilikuwa ni usiku tayari, walifanya tu maombi
ya kulala na kwenda kulala. Kwakweli kwa siku ya leo Erica alilala tu
kwani hakutaka hata kuongea na Erick kwenye simu kwani bado alikuwa na uoga nay
ale maneno ya Yule mganga. Kulipokucha, Erica aliamka na kuanza
kufanya mambo yake mengine kisha alienda kumsalimia mama yake ambapo alimuuliza
kuhusu usiku wa jana kuwa ulikuwaje kwake, “Vipi lile shetani lilikujia
tena ndotoni?” “Hapana mama, sikumuona ndotoni” “Basi itakuwa ni
kile kitambaa ndio kilikuwa kinamfanya aje kwa urahisi kwenye ndoto zako,
mwanangu hilo liwe fundisho sasa mambo ya waganga hapana, yani utahisi una nia
njema ya kwenda kwa mganga ila atakachokufanya utajuta maisha yote. Waganga
hawana tiba yoyote zaidi ya kukuongezea majini tu ambayo yakicharuka yatafanya
ufanye vitu vya ajabu” “Ila mama nilienda ili kujua ukweli kuhusu
Bahati” “Eeeh ukishajua ukweli?” “Nijue tu basi” “Yani
wewe nae una mambo ujue, yani Yule Bahati kafanyiwa michezo na ndugu zake, acha
kama ilivyo, kwani wewe ndio una uchungu zaidi na Bahati kushinda ndugu zake?
Kwanini kujitakia matatizo yasiyo na lazima? Ukiujua ukweli ufanye nini sasa?
Kama kachezewa na ndugu zake acha, Yule sio mumeo kusema uhangaike nae mpaka
utake kuingia matatizoni, angekuwa mumeo sawa ila sio mumeo Yule, usitake
kujiletea tena matatizo. Maana utaambiwa kuna mganga wa kumrudisha Bahati kwako
utaenda, huku mtoto ushamuuza kwahiyo atakuwa na baba watatu au?” Erica
alikaa kimya tu na mama yake aliendelea kumuasa kuwa aachane na hayo mambo ya
kwenda kwa mganga wa kienyeji maana hayatamsaidia chochote. Basi
akaendelea kufanya mambo mengine, muda kidogo akapigiwa simu alipoangalia ni ile
namba ya Yule bosi wake ambaye ni mama yake Erick, kwa hakika alishindwa kupokea
kwani aliogopa na kuacha iite hadi ikatike hata ilipopigwa tena napo hakupokea
wala nini. Jioni ya siku hiyo, akapigiwa simu na namba ngeni, alikuwa na
mashaka nayo ila aliamua kuipokea, sauti ilikuwa ni ya Yule bosi wake ambaye ni
mama yake Erick, alimsalimia kwa uoga kisha Yule mama akamuuliza, “Mbona
hujaonekana kazini kwa siku ya tatu sasa?” Alikuwa akijiuma uma tu kwani
hakuwa na cha kujieleza, kisha Yule mama aliendelea kuongea, “Hata kama
ulihitaji kuacha kazi, hukujua kama kuna utaratibu wa kuacha kazi? Ungekuja na
kuniuliza, kwani kuna siku nimegombana na wewe Erica hadi uache kazi gafla
hivyo?” “Hapana sijaacha kazi” “Sasa kwanini huji
kazini?” “Aaah naumwa” “Hujui taratibu za kazi? Huwa watu
wakiumwa hawaji tu kazini? Kuna taratibu zake,na hata kuacha kazi kuna taratibu
zake” “Naomba nisamehe” “Sawa, Jumatatu nakuhitaji hapa kazini
na ulete na uthibitisho wa daktari kuwa ulikuwa unaumwa, nimekupa siku nyingi za
kushghulikia swala hilo. Kuumwa au kuacha kazi kuna taratibu zake, sio
kujiamulia tu, hii kazi sio ya baba yako au ya mama yako. Nakuhitaji kazini
Jumatatu, kwaheri” Yule mama akakata simu, kwakweli Erica alibaki na
mawazo kwani hakuelewa kuwa ataanzaje kwenda kazini ikiwa Yule mama anaujua
ukweli wote ila akasema atajua hiyo hiyo Jumatatu kuwa ataenda au
la. Usiku uliingia na alifanya mambo yake kama kawaida ila
akapigiwa tena simu na Erick, bado alikuwa anaogopa kupokea kutokana na maneno
ya Yule mganga, kwahiyo hakupokea ingawa iliita na kuita ila hakupokea. Alijua
kama anafanya makosa na anaumiza moyo wa Erick ila hakutaka kupokea kwani alijua
kama Erick angepata matatizo basi kwake ndio ingekuwa kuzidi. Aliiacha
tu ile simu kuita hadi kukatika, muda wa kulala ulifika na akalala. Saa
kumi alfajiri akapigiwa na dada yake Mage na kupokea, “Amka Erica
ujiandae, saa kumi na moja utoke hapo uje stendi” “Dada jamani, mama
ushamwambia?” “Ukiwa unajiandaa, ukimaliza kujiandaa nibipu halafu mimi
nitapiga kumwambia mama ni wapi tunaenda?” “Sawa dada” Basi simu
ikakatika na Erica akaanza kujiandaa hadi alipomaliza kupakia na nguo zake
kwenye begi la mgongoni akambipu dada yake kisha ilionyesha kama mama yao
kapigiwa maana alimsikia akiongea na simu huku akitoka chumbani kwake inaonyesha
alikuwa anakuja kwenye chumba cha Erica. Alimuangalia mwanae sana aliona
atamkumbuka sana kwa hizo siku mbili atakazokuwa huko mkoani. Kisha mama
yake alifika chumbani kwake na kumwambia, “Kumbe Erica una safari na
dada yako? Kwanini hukuniambia?” “Nilisahau mama, yani dada ndio
kanikumbusha asubuhi hii. Nisamehe mama” “Haya mfanye haraka, leo uwahi
kurudi sitaki ujinga wa kuchelewa” “Sawa mama” Hakujua ni wapi
ambapo mama yake ameambiwa na dada yake, ila alimshika mwanae na kumbusu kisha
kumuaga mama yake na kuondoka, kitu pekee ambacho mama yake hakukielewa ni
kumuona akibeba begi la mgongoni na pochi ila hakuuliza sana kutokana nay ale
aliyoelezwa na Mage, Erica hakuelewa ni kitu gani mamake alichoambiwa na dada
yake ila yeye alishukur tu kupata ruhusa na kuondoka. Alifika
stendi na kukutana na dada yake kisha wakaingia kwenye basi, na muda kidogo
safari ilianza na alikuwa kimya tu safari nzima, ila walipokaribia kufika
alimuuliza dada yake, “Dada, umemuaga vipi mama?” “Nimemwambia
kuna kuna project nafanya, kwahiyo namuhitaji Erica maana zinatakiwa zipigwe
picha alfajiri, akakubali ndiomana hata umetoka na begi mgongoni hajakuuliza
maana nimemwambia kuwa utabeba nguo kadhaa” “Kheee na tusiporudi
leo?” “Wewe tulia tu, jioni nitampigia simu mama. Najua jinsi ya
kumpanga na atanielewa tu” Erica alimuitikia dada yake, na hatimaye
karibia na jioni ya siku hiyo walifika kwenye kijiji cha baba zao wadogo na
kupokelewa vizuri sana. Baada ya muda kidogo Derick nae alifika, na
kwenda kupokelewa ambapo nae alifikia hapo kwa baba zao wadogo., na walikaa
nyumbani kwa baba yao mdogo ambaye ndio mkubwa kwenye eneo hilo Baba zao
wadogo watatu walifika na walikaa nao ili kuzungumza nao, ambapo kwanza
waliambiwa kuwa kesho asubuhi wataenda kwenye kaburi la baba yao na kuweza
kuanza kufanya hayo matambiko, Erica alitulia kimya
akisikiliza. “Kwakweli mimi kama baba yenu mdogo ambaye ndio mkubwa
kwasasa nimesikitishwa sana na haya mambo nilipoyasikia. Unajua baba yenu ndio
alikuwa wa kwanza kwenye familia yetu, kwahiyo kitendo kama hiki ni laana kubwa
sana na hakitakiwi kabisa kwa jamii. Ni bora mmeamua kukiri ili tuvunje laana
hii, kwanza kabisa Erica na Derick mshikane mikono na kukubaliana kuwa nyie ni
ndugu maana mmetenda vitendo vya aibu sana” Erica alifanya hivyo ila
hakuwa na tatizo kabisa, kwani hakuwahi kuwa na matamanio na Derick hata kulala
nae ni Derick ndio alifanya njama ila kwa yeye mwenye hakutaka kitu cha namna
hiyo kitokee. Kisha baba zao wadogo walitaka kujua chanzo cha wao
kujikuta wakifanya laanza hiyo, ila walijitetea kuwa walikuwa hawafahamiani kama
ni ndugu, basi baba zao walisema kuwa wamewasamehe na kuwa tayari kufanya
tambiko la kuvunja hiyo laana kwao. Walipomaliza pale, baba yao mdogo
aliwapeleka mtoni ili wapate kuona mandhari ya mto hata wakipenda kuoga waoge
huko, kwakweli mandhari ile ilikuwa nzuri sana ila hapakuwa na watu kabisa,
Erica akauliza, “Mbona mandhari inavutia lakini hakuna watu
baba?” “Unajua siku hizi, asilimia kubwa wana mabomba nyumbani kwahiyo
huku mtoni watu huja mara moja moja kutembea tu. Ila panavutia sana na maji yake
ni mazuri kushinda hata yanayotoka nyumbani, mara nyingine huwa tunakuja kuoga
huku kama kuondoa mikosi katika maisha yetu” Erica alipenda wazo la maji
kutoa mikosi, hivyo akaamua kuchota ili akaoge nyumbani maana walienda nan doo,
na baba yao mdogo aliwaambia wabebe ndoo kwavile maji yale hupendwa na watu
wengi sana, kwahiyo alijua watayapenda tu. Usiku walikula na kuonyeshwa
sehemu za kulala, kweli Mage alimpigia mama yao simu na kutafuta namna ya
kumdanganya kuwa siku hiyo haitawezekana kurudi, “Hivi Mage unajua kuwa
Erica ana mtoto mdogo nab ado ananyonya?” “Mama nawe jamani! Huu ndio
wasaa mzuri kwa huyo mtoto kuacha ziwa” “Ila bado hajafikisha miaka
miwili” “Mama, siku hizi nani ananyonyesha mtoto miaka miwili? Hiyo
ilikuwa zamani bhana, ila tusamehe mama mambo yameingiliana” Basi
alikubali tu ili kishingo upande. Kesho yake waliamka na kwenda
mtoni kuchota maji kwani tayari Erica aliyapenda maji yale, kisha walirudi na
kuoga na kujaribu kujishughulisha kidogo pale, wakisaidiana na mama yao mdogo
huku wakisubiri muda wa tambiko, ila Yule baba yao mdogo alikuja na
kusema, “Jamani, mzee wa mila kaniambia kuwa hii sio siku nzuri kwa
tambiko kwahiyo itabidi tufanye kesho” Erica akashtuka
kidogo, “Jamani hadi kesho!” “Ndio, hadi kesho nadhani hamjui
vizuri mambo ya tambiko. Mambo mengine sio ya kulazimisha, siku nzuri kwa
tambiko ni Jumanne na Alhamisi yani hata kesho Jumatatu tutafanya tu ila Jumanne
ilikuwa nzuri zaidi. Ila leo Jumapili ni mbaya haifai” Ilibidi tu
wakubali kwani wao hawakujua mambo ya tambiko, kisha wakaendelea na mambo
mengine ya pale nyumbani kwa baba yao mdogo huku wakitembelea mashamba
mbalimbali na kuangalia vitu mbalimbali. Mchana wa siku hiyo, Erica
alipigiwa simu na mama yake, akapokea na kumsalimia, ila mama yake alianza kwa
kumpa lawama, “Wewe mtoto una nini lakini? Umeondoka hata mwenzio
hujamuaga ni haki hiyo Erica? Halafu simu zake hupokei kwanini? Unajua una mambo
ya ajabu wewe, hebu pokea simu ya mwenzio sio vizuri ujue” “Sawa mama
nimekuelewa” “Tena kijana wa watu anaonekana ana upendo sana ila
namuhurumia kwakweli maana wewe huwa hueleweki kabisa, kwanza huko ulipoenda na
dada yako sipaelewi kabisa. Vipi mnarudi saa ngapi leo?” Erica hakuwa na
jibu bali alimkimbizia dada yake simu ili aongee na mama yao, kama kawaida Mage
alitafuta Kiswahili cha kumlainisha mama yao kisha akakata simu, muda huo Erica
alikuwa nje, kisha dada yake aliweka simu kabatini. Erica akiwa hana
habari nje, simu yake ilianza kuita na ni Derick ndio aliiona na kuifata
kuiangalia, akaona mpigaji ameandikwa ‘My love Erick’ Kiukweli alijihisi
kutokuwa na furaha gafla na kupokea ile simu, hata Erica hakujua kuwa ni kitu
gani Derick aliongea na Erick. Jioni ya siku hiyo Erica alitaka
tena kwenda mtoni kuteka maji kwavile alijikuta akipenda sana maji ya kutoka
mtoni, akamuomba dada yake amsindikize, “Dada, nisindikize nikachote
maji” “Aaah jamani Erica, asubuhi si tumeenda jamani, unataka maji yam
to kila muda loh! Hata hivyo sio mbali sana unaweza kwenda tu” “Ila
naogopa mwenyewe, sijazoea halafu bamdogo alisema watu hawaendi endi
kule” Akatokea Derick na kusema kuwa yeye atamsindikiza maana hana cha
kufanya na alitaka kuendelea kuangalia mto, na Mage akadakia, “Bora
umsindikize maana Erica kwa uoga ni balaa” Kwahiyo Erica aliondoka na
Derick kuelekea mtoni kuchota maji. Kufika mtoni Derick alianza
kumchombeza Erica, “Hivi Erica, huwa ukikaa
hunikumbuki?” “Nikukumbuke kivipi?” “Yani huwa hukumbuki kabisa
kama umewahi kuwa na mahusiano na mimi?” “Aaah hayo yashapita Derick,
sisi ni ndugu ujue” “Ndugu wa kweli Erica ni Yule uliyezaliwa naye mama
mmoja kwani mama ndio anajua ukweli wa mtoto kuwa baba yake
nani” “Kwahiyo una maana mimi si ndugu yako?” “Hapana, ila
mwenzio nakukumbuka sana Erica” “Hebu acha habari hizo Derick, sisi ni
ndugu nione dada yako kama mimi ninavyokuona kuwa u kaka yangu” “Ila
Erica, yani kesho laana itakuwa imevunjwa ila leo tumeachiwa kwa makusudi
kabisa” “Sikuelewi” “Tumeachiwa siku ya leo kufunga ukurasa
wetu, tafadhali Erica, nipe mara moja tu” “Hivi una akili wewe, huko
kichwani ni mzima? Yani huna hata aibu kweli kabisa mimi nikatembee tena na
wewe? Kwanza wewe si mpenzi wangu, ninaye wangu tayari, pili wewe ni ndugu yangu
yani wewe ndiye umefanya tufike huku kuvunja laana halafu bila aibu unaniambia
ushetani huo” “Erica sio ushetani, kiukweli nakutamani sana yani kadri
tunavyoenda mie nazidi kupatwa na hisia, sina raha kabisa Erica, naomba mara
moja tu. Nimeamua kukwambia ukweli, sina raha tangu nimekuona Erica, naomba mara
moja tu” “Nitolee ujinga wako mie” Erica alichota maji na kubeba
ndoo yake kisha kuanza safari ya kurudi kwani alijua kuendelea kuongea na Derick
hapo ni kutafuta matatizo tu. Erica aliongoza mbele sana, ila akasikia
kishindo kuwa Derick kaanguka kwakweli hapo alishikwa na huruma ukizingatia ni
ndugu yake, akatua ndoo yake na kurudi nyuma kumuangalia, wakati anamuangalia
Derick alimvutia kwa chini ambapo Erica alianguka chali sababu hakujipanga,
kisha Derick akaenda juu ya Erica ilionyesha wazi alikuwa na lengo la
kumbaka. Erica alichota maji na kubeba ndoo yake kisha
kuanza safari ya kurudi kwani alijua kuendelea kuongea na Derick hapo ni
kutafuta matatizo tu. Erica aliongoza mbele sana, ila akasikia kishindo
kuwa Derick kaanguka kwakweli hapo alishikwa na huruma ukizingatia ni ndugu
yake, akatua ndoo yake na kurudi nyuma kumuangalia, wakati anamuangalia Derick
alimvutia kwa chini ambapo Erica alianguka chali sababu hakujipanga, kisha
Derick akaenda juu ya Erica ilionyesha wazi alikuwa na lengo la
kumbaka. Kwakweli Erica aliona hafanyiwi jambo jema, kama kawaida
hakutaka kupambana sana na Derick sababu alijijua nguvu hana kwahiyo kama
kupambana Derick atamshinda tu na hakika atambaka, yani kumuumiza atamuumiza na
kumbaka atambaka, kwahiyo akawa mpole gafla na kuongea sauti kama ya
kubembeleza, “Derick kwanini unifanyie hivi jamani wakati haya mambo
yanahitaji starehe eeh!” “Erica nakutamani na wewe unakuwa mbishi, sasa
mimi nifanyeje unadhani?” “Hebu angalia mazingira haya yalivyo eeh! Hivi
watu wakitukuta watatufikiriaje, uandhani wakina bamdogo wakija huku watasemaje
eeh! Sikia mimi na wewe tupange twende mahali tukafanye yetu kwa
uhuru” “Leo leo?” “Ndio leo leo, yani hujui tu ulivyokuwa
unaongea hata mimi umenipa hamasa balaa, nakumbuka siku ya kwanza tumefanya
nikiwa nimelewa halafu leo unibake jamani ni haki hiyo? Nisisikie hata utamu
wako jamani Derick” Kwakweli Derick alianza kulegea na kuingia laini kwa
kinachosemwa na Erica maana alikuwa akiongea kwa kubembeleza sana, ilibidi
Derick akubaliane na Erica kuwa wakirudi nyumbani watatoka mara
moja, “Sawa hakuna tatizo, ngoja tufike nioge halafu twende huko
tukajifaidie. Ila mazingira ya huku unayajua vizuri Derick?” “Nitauliza
tu, hakuna mahali ambako hakuna nyumba za wageni, Erica mwenzio nina hamu na
wewe? Ikishindikana basi twende hata bafuni kwa bamdogo unipe” “Sawa
hakuna tatizo Derick” Kisha Erica akaambusu Derick na kumfanya Derick
aweze kuinuka pale juu ya kifua cha Erica, wakati wanainuka pale chini
waligundua kuwa kulikuwa na mtu anawaangalia, waliposhtuka Yule mtu aliondoka
kwahiyo walimuona kisogo tu yani alikuwa ni mtu wa makamo, ila Derick hakujali
kitu ingawa Erica ilimpa mashaka kidogo, “Mmmh Mungu wangu, kumbe
tulikuwa tunaonwa!” “Aaah usijali Erica, kwani wakituona tatizo ni nini?
Hawajui mapenzi wao? Yule mzee mzima badala atulie kwake na familia anafanya
kazi ya kuangalia vijana. Mwehu Yule, sikia Erica, twende haraka nyumbani ili
tuwahi mahali tukafanye yetu, hapa kila nikikuangalia nakutamani tu bora
tukafanye” “Sawa hakuna tatizo” Kisha walisogea alipoacha Erica
ndoo ya maji na Derick akamsaidia kumtwisha ndoo ya maji kisha wakaelekea kwa
baba yao mdogo. Njia nzima Derick alikuwa akiongea tu mada za mapenzi na Erica
hadi wanaingia kwa baba yao mdogo. Walipofika, Erica alienda
kuoga, kisha akaenda chumba walichotengewa, akapokea ujumbe tu toka kwa
Derick, “Naenda kuulizia vyumba Erica, nikishapata tu nakuja kukuchukua
ili twende pamoja, kwahiyo nitakushtua nje hapo utoke” Erica alisoma ule
ujumbe huku akitafuta namna tu ya kumkatalia, alitamani dadake awe karibu nae
zaidi ili wazo la Derick lisiwepo tena maana Derick alimsumbua ilihali akijua ni
nduguye. Kwenye mida ya saa moja moja, Derick alionekana kurudi ila
alipiga simu ya Erica ambayo haikupokelewa kwahiyo ilibidi amuagize dada yao
Mage kuwa anamuita Erica, dada yao alivyofika ndani alimwambia
Erica, “Wewe, kakako anakutafuta huko nje” “Dada, naomba
nikwambie kitu” “Kitu gani? Unataka kuanza tena habari za mama,
nilishakwambia niachie kuhusu mama najua jinsi ya kuongea nae.” “Hapana
dada, sio kuhusu mama” “Ila kuhusu nini?” “Ni kuhusu huyu
Derick” Mara simu ya Erica ilikuwa inaita na mpigaji alikuwa Derick,
dadako akamkazania kuwa apokee simu au atoke akaongee na Derick kisha wao
wataongea badae, “Hapana dada sio badae, ni muda huu inabidi
tuongee” “Ni kuhusu nini?” “Dada, huyu Derick
ananitaka” “Aaaah Erica hebu acha zako mdogo wangu, Derick mwenyewe ndio
kaniomba tuivunje hii laana halafu mwenyewe akutake inawezekana kweli
hiyo?” “Ila Dada, mimi ni mdogo wako nisikilize” “Hata Derick
nae ni mdogo wangu” “Dada, siendi kuongea na Derick hadi kesho kwenye
tambiko, na hata hapo nje sitoki leo” “Erica,
sikuelewi” “Nielewe tu” Basi dada yake alitoka, na Derick
alipiga tena ikabidi Erica apokee ili amkatalie ajue msimamo
wake, “Derick, sitaki tena sitaki ujinga wako huo” “Unajua
nataka kukwambia nini lakini?” “Nini?” “Toka
nje” “Sitoki” “Ni hivi vyumba nimekosa Erica, kwahiyo nilikuwa
nakwambia basi twendo bafuni kama tulivyopanga” “Nikome Derick, mimi ni
dada yako. Kwaheri” Erica akakata simu ila kiukweli alikuwa na hofu hata
ya kwenda nje kwa siku hiyo kwani alihisi pengine Derick anaweza kumvizia hata
chooni, kitendo hiko kilimfanya Erica asitoke nje kabisa, hata chakula cha usiku
hakula na kusema kuwa ameshiba ila si kweli kwamba alishiba ila hakutaka kula
sababu hakutaka kutoka nje kwenda uwani kujisaidia hata haja ndogo maana alihisi
vibaya kuhusu Derick kuwa huenda akamvizia uwani na kumbaka sababu Derick
alionekana hana hata habari ya undugu wao. Wakati anataka kulala,
akapigiwa simu na mama yake, ikabidi apokee na kumsalimia, “Hivi Erica
una akili gani wewe? Yani huna uchungu hata na mwanao? Hupati wasiwasi hivyo
hujamuona mwanao hadi leo?” “Nisamehe mama” “Nikusamehe kitu
gani na umemfanyia roho mbaya mwanao, siku ya pili hii inakatika ukiwa mbali na
mtoto, unamsononesha mtoto kwakweli. Halafu kitu kingine ni kwanini unamtesa
kijana wa watu?” “Nani mama?” “Wewe mwenyewe uliniambia ooh mama
nampenda sana Erick, hivi mtu unayempenda sana unaweza kumfanyia huo ujinga?
Yani unaenda mahali hata humuagi? Kuwa mbali sio kigezo ila swala la kumuaga
lipo palepale, ulitakiwa kumpigia simu mpenzi wako na umuage, ushauza mtoto
halafu unafanya ujinga kweli? Kijana wa watu anakupigia simu unampa mwanaume
apokee kweli Erica?” Hapo Erica alishangaa kuwa ni mwanaume gani kampa
aongee na Erick, ila akashindwa namna ya kumuuliza mama yake vizuri na kuishia
tu kumuomba msamaha, “Sasa kesho uwe hapa nyumbani, sitaki kusikia hizo
habari sijui tunaenda kupiga picha, sijui ujinga ujinga gani sitaki kusikia.
Mmekazana kupiga piga picha mmekuwa waigizaji nyie, mnatengeneza filamu? Hebu
tuwekane wazi basi, huo ujinga sitaki, kesho muwe hapa nyumbani.
Sawa!” “Sawa mama nimekuelewa” Basi Erica akakata simu ya mama
yake ila alijiuliza maswali mengi sana kuhusu na aliyepokea simu ya Erick, muda
huo huo akapokea ujumbe toka kwa Erick, “Erica, nakupigia simu mpenzi
wangu hupokei ila leo ukaamua kumpa mwanaume apokee simu kweli Erica jamani!
Mbona mimi nakupenda sana, kwanini unifanyie hivyo? Halafu mwanangu umemuacha
wakati bado alikuwa ananyonya, mmemkosesha haki mwanangu, nimeumia
sana” Yani Erick aliandika kamavile ni baba mzazi wa Yule mtoto kiasi
kwamba yale maneno Erica yalimuingia, akatamani kumpigia simu Erick ili ajaribu
kumuelewesha ila simu yake haikuwa na salio, na muda huo huo dada yake na watoto
wengine wa baba yake mdogo waliingia kulala kiasi kwamba hakuweza tena
kumsimulia vizuri dada yake kuhusu sakata la
Derick. Kulivyokucha, waliamka na kufanya shughuli ndogo ndogo
kisha baba yao mdogo ambaye ndio alikuwa mkubwa alifika na wale wengine watatu
na kuwataka Erica, Derick na Mage waongozane nao kwenda
makaburini. Waliondoka na walivyofika kwenye kaburi la mzee wao alifika
mzee wa kimila na kuanza kusema mambo ya kimila wanayotakiwa kufanya, kwanza
kuna mashuka walitakiwa wavae kisha wakae kwenye lile kaburi sababu baba yao
alikufa, kwa maana hiyo angekuwa hai basi angewapakata wakati Yule mzee
anawasomea mila. Basi kimya kilitanda wakati Yule mzee akifanya mambo
yake ya mila za kuvunja laana ya kutembeleana ndugu, alipokaribia kumaliza
aliweka mikono yake juu ya vichwa vya wale watoto yani Derick na Erica na
kusema, “Hawa watoto nawaleta kwenu mizimu muwaangalie, watoleeni laana
iliyokuwa mbele yao. Huyu wa kike apate mume wa kuolewa nae na huyu wa kiume
apate mke wa kumuoa. Laana yote juu yao imevunjika muda huu.Hawakutambua makosa
yao, wahurumieni” Kisha aliendelea na maneno ya kilugha kwa muda na
kuwataka wainuke kisha kuna mahali walitakiwa wakanyage na kulikuwa na kitu kama
mbao laini ambapo kila alipokanyaga mmoja ile mbao ilivunjika kisha Yule mzee
akachukua vile vipande na kuchimba pembeni ya kaburi la baba yao na kuvifukia,
hapo wakaambiwa ndio mwisho wa tambiko lao ila wanatakiwa waende kwanza mtoni
wakaoge. Kwahiyo walianza safari ya kwenda mtoni muda ule, kisha wakaoga
kwa maelekezo ya Yule mzee na walioga na nguo, kisha walitakiwa kukaa pembeni
kukauka yani wanakauka na nguo zao huku Yule mzee akiendelea na mambo mengine ya
mila zao. Baada ya hapo waliambiwa ni muda wa kurudi kule walipofikia
ila ilikuwa mchana tayari na jua lilikuwa ni kali sana, kiasi kwamba walikuwa
wakitembea na kupumzika yani hadi wanafika nyumbani walikuwa wamechoka choka kwa
mizunguko ya siku hiyo na mambo yaliyokuwa yakifanywa. Kufika
nyumbani, Erica alimwambia dada yake kuwa wajiandae na waondoke siku hiyo hiyo,
baba yao mdogo alikuwa akiwapinga kuondoka siku hiyo, “Jamani si bora
mngeondoka asubuhi!” “Natakiwa kazini bamdogo, kwahiyo bora tuondoke leo
na tutaingia usiku wa manane nyumbani” “Jamani Erica, ila wewe mtoto
mbishi sana na ukiamua lako huwa hutaki kupingwa haya, ila sidhani kama ni vyema
kufanya hivyo” Mage hakumbishia sana mdogo wake kwani tayari
alishamdanganya sana mama yao kwahiyo hata yeye aliona ni vyema waondoke tu
wafike kwao usiku, ila kabla ya kwenda kujiandaa Yule mzee wa kimila alisema
kuna kitu kimoja alikisahau na anatakiwa kukifanya juu yao, walimsikiliza vizuri
na kuwaambia kuwa inatakiwa wachanjwe, kwakweli Erica alishtuka na
kuuliza, “Kuchanjwa tena!” “Ndio, hii itawasaidia kuwapa kinga
kwani hata watu wabaya hawataweza kuwapata” Erica hakuweza kukataa kwani
dada yake alimkazia macho kwahiyo akakubali kisha mzee wa mila akaanza na mmoja
mmoja na kuwachanja, ila zamu ya Erica ilipofika ilikuwa kazi sana maana Erica
alikuwa muoga kiasi kwamba hakumchanja vizuri inavyotakiwa, ila akampaka dawa
hivyo hivyo. Baada ya hapo aliwaambia kuwa wanatakiwa wasioge hadi
kesho, baba yao mdogo akasema, “Basi inabidi waondoke kesho maana huyu
mtoto mbishi leo anaweza kwenda kuoga huko kwao” Baba yao mdogo alisema
kuhusu Erica, na baba zao wadogo wote wakaafiki kuwa waondoke kesho yake,
kwahiyo hawakuwa na namna zaidi ya kukubali kuondoka kesho yake
tu. Wakati bado wamesimama pale wakiongea ongea, alifika mzee mmoja na
kusalimiana na Yule mzee wa kimila kisha na wale baba zao wadogo, ambapo baba
yao mdogo mmoja alianza kumtambulisha Yule mzee kwa wale watoto wa ndugu yake,
Yule mzee alihamaki huku akiwaonyeshea kidole Erica na Derick, “Kwahiyo
hawa watoto ni ndugu?” Baba yao mdogo akamjibu, “Ndio ni ndugu,
watoto wa kaka” “Kwakweli kuna tatizo kubwa hapa, tena tatizo
kubwa” “Tatizo lipi hilo?” “Hawa watoto nimewakuta jana kule
kichakani karibu na mtoni wakifanya mapenzi” Kila mmoja alishangaa na
kuwaangalia Erica na Derick, huku baba yao mdogo akiuliza kwa
hamaki, “Eti nini?” “Nimewakuta hawa wakifanya mapenzi,
nimewaona kwa macho yangu haya mawili, mliposema ni ndugu nimeshangaa sana
amakweli dunia imeisha” Baba yao mdogo aliwauliza, ila Erica akakaa
kimya maana hakujua kama mada ya jana ingeibuka hapo kwa namna hiyo, baba yao
alipoona Erica kanyamaza alijua ni kiburi tu kinamsumbu, ikabidi amuulize
Derick, ambaye aliamua kujibu, “Tusameheni baba wadogo, naomba mtusamehe
sana. Kwavile tuliona tunaenda kuvunja laana, Erica aliniomba tufanye mapenzi
mara ya mwisho, jamani mimi ni mwanaume sikuweza kukataa, naomba
mtusamehe” Wale baba wadogo walimuangalia Erica kwa ukali sana, na
kumuamuru kuwa apige magoti chini kwa hasira huku baba mdogo wake akiongea kwa
gadhabu, “Wewe mtoto una matatizo gani eeeh! Kumbuka wewe mezaliwa na
mama halali wa ndoa yani mke halali wa baba yenu, yani leo mnakuja kusuluhishwa
kwa ujinga mlioufanya halafu unaenda kumshawishi ndugu yako kufanya tena kile
kitendo kweli!” Ikabidi Mage aingilie kati, “Ila wewe Derick
hebu kuwa mkweli, unajua jana Erica aliniambia kuwa unamtaka nikamwambia
haiwezekani, hebu kuwa mkweli Erica amekushawishi wewe kufanya hivyo jamani! Ni
kweli Erica ana kiburi, mbishi lakini hawezi kufanya hivyo, hana tamaa ya
mapenzi kiasi hiko” Erica nae alijaribu kujitetea na kuonyesha ule
ujumbe wa Derick kuwa hata alitaka kutafuta chumba ili wakalale, ila Derick
alijitetea, “Erica, hebu kuwa mkweli si ni wewe mwenyewe ndio uliniambia
hujaridhika pale polini, unataka nikatafute chumba twende huko tukamalizane
kabla ya leo, na jana nilienda tu kujigelesha ili kukuridhisha na muda ule
nimekuita nje nilitaka kukwambia kuwa chumba sijapata ili wewe uweze kuachana na
wazo hilo” “Jamani Derick unanisingizia hivyo kweli!” Alikuwepo
na mama yao mdogo, mke wa baba yao mdogo akasema, “Lakini hapa kuna
namna, kwanini Erica alikuwa anang’ang’ania jana kwenda mtoni, hata dada yake
alimkatalia ila aling’ang’ania, lazima maneno ya Derick yaaminike maana kwanini
ulitaka kwenda mtoni jioni ile?” Yule mzee nae akaongezea na
kusema, “Kwa mimi naweza kumuamini huyu kijana kwani kwa macho yangu
nilimshuhudia huyu binti akimshika huyu kijana na kumbusu” Lile swala
lilifanya wote wazidi kumuangalia kwa mshangao Erica, kiasi kwamba Erica
alijilaumu kwa kutokurekodi mazungumzo ya yeye na Derick maana ingemsaidia kwa
kiasi Fulani kulalamika, hakuweza kujitetea zaidi kwani huwa hawezagi kujitetea
kwahiyo alijikuta akiinama na kuanza kulia. Ikabidi dada yake ainame
akimbembeleza mdogo wake maana alimfahamu vizuri sana, kwakweli hadi wazee
walijikuta wakikosa maamuzi kwa muda huo, wakasema wasubiri kesho wafanye
maamuzi ila Erica aligoma, alilia sana akimwambia dada yake kuwa anataka aende
nyumbani tu. Dada yake akamwambia, “Erica kulia hakusaidii kitu, simamia
ukweli wako ila ukilia utajiumiza bure tu” Kisha Mage aliinua macho yake
na kumtazama Derick kisha akamwambia, “Yani sikujua kama wewe ni mbaya
kiasi hiki, huna vitu vingine vya kufanya zaidi ya kumsingizia Erica
eeh!” “Sasa mimi nimsingizie kwa lipi jamani, muulize kama hakuwahi
kutoa mimba yangu, muulize hapo” Wale baba wadogo walimuangalia Erica
kwa masikitiko sana, mmoja akamuuliza, “Kumbe hadi mimba ulipata na
kutoa? Kheee jamani mbona makubwa haya!” “Tena huyu Erica asitake
kuniweka mimi ubaya, hapo alipo ana mtoto ambaye hata hajui baba wa mtoto ni
nani sababu alitembea na familia nzima” Baba wadogo wakashangaa zaidi
kwani habari za mtoto walifichwa kwahiyo kubumbuluka huko kuliwashangaza sana,
ilibidi wamuangalie Mage ili awaambie ukweli, “Yani hadi wewe Mage
wakutuficha sie kweli!!” “Tusameheni jamani, tulitaka kutafuta siku
maalumu ndio tuwashirikishe kuhusu hili, hata mashangazi
wanajua” “Kwahiyo nao wametuficha? Kweli wanawake mnajuana, ila mficha
maradhi kifo humuumbua. Kumbe Erica una tabia chafu kiasi hiki
kweli” Kwakweli Erica alichoka kusikia yale maneno na akaamua kutoa ya
kwake ingawa huwa akiongea kama ana hasira hivyo ndio huwa anaonekana hana adabu
kabisa, “Nashukuru sana, mimi ni mwanamke ndiomana nimeonekana malaya
sababu nimezaa, sijui unasema nimetoa mimba nashukuru sana. Ila huyo Derick kama
wanaume wangekuwa wanapata mimba basi angekuwa na mimba hadi ya pua, sitaki
kuongea sana kwaherini” Erica aliinuka pale alipopigishwa magoti na
kuingia ndani kuchukua begi lake, kwakweli baba zake walisikitika sana maana
waliona kama kawadharau kitendo cha kuinuka walikompigisha magoti. Ila
Erica alitoka ndani na begi lake tayari kwa kuondoka, ilibidi Mage nae akachukue
begi ili waondoke, kisha wakaenda pale kwa baba zao kuwaaga maana Mage
asingeweza kumuacha mdogo wake aondoke mwenyewe ikiwa ni yeye aliyemshawishi
mdogo wake kwenda kule, ila Yule mzee wa mila aliwaomba wasiondoke
kwanza, “Erica, naomba nikufanyie dawa kwanza. Unaonekana una matatizo
sana wewe binti” “Hapana, sitaki tena dawa yoyote” Erica aligoma
ila dada yake alimbembeleza akubali kufanyiwa hiyo dawa waondoke, kwavile Erica
alitaka kuondoka, akakubali kufanyiwa hiyo dawa ambapo Yule mzee wa mila
alimpaka paka madawa usoni na shingoni na kumsomea somea maneno pale kisha
kuwaruhusu waondoke. Muda ulikuwa umeenda sana, kwahiyo ilibidi
wakapande zile gari zinazofanya safari za usiku kwa usiku yani Erica alitaka
afike kwao tu. Wakawasindikiza hivyo hivyo kishingo upande,
wakafika stendi na kupata basi, kisha Erica na dada yake wakapanda, kwakweli
Erica alijihisi gasia sana na zile dawa alizopakwa kiasi kwamba hakutaka
kukutana na yeyote anayemfahamu hadi aingie kwao, maana alijihisi kunuka midawa
ya kienyeji mwili mzima, ile hali ilikuwa inamkera sana, “Dada,
tukishuka tu itabidi nichukue tax hadi nyumbani” “Ndio tutachukua gari
ila hiyo hali mama akikuona nayo itakuwa balaa, me nadhani tuchukue gari twende
kwangu kwanza ukaoge halafu ndio uende nyumbani” “Ila bora ningepata
sehemu hata huku huku ningeoga” “Haitakiwi kuoga Erica, maana kuna dawa
umepakwa kwahiyo hadi kesho” Kwakweli Erica alikuwa amekereka sana ila
kwavile alihitaji kufika nyumbani tu aliona ni afadhali. Basi gari ile
ilitembea usiku kwa usiku, ilivyofika saa saba usiku kuna mahali ilibidi isimame
kwa muda kisha kwenye mida ya saa kumi iliendelea na safari mpaka wakafika
stendi kuu, ilikuwa pamekucha kabisa tayari maana ilikuwa kwenye mida ya saa
moja asubuhi. Walishuka na moja kwa moja walisogea kwa dereza wa gari za
kukodi ili kuongea nae awapeleke wanapohitaji kwenda, wakati wanaongea nae
alifika mama kwa Yule dereva akimwambia, “Kijana nimekuja kukushukuru,
umenipa ushauri mzuri sana wa kumpeleka ndugu yangu apande bodaboda awahi basi,
na kweli ameliwahi kashanipigia simu kuwa kapanda tayari” “Aaah usijali
mama” Kisha Yule mama alionekana kama anatoa hela ya kumpa Yule dereva
kama asante, wakati huo Yule mama alimuangalia Erica na kusema maana Erica
alimpa mgongo kwahiyo hakumuona usoni, “Mbona umbo la huyu binti kama
nalifahamu” Yule mama akazunguka kwa mbele kumuangalia, akashtuka na
kusema, “Kheee Erica!” Erica naye alimuangalia huyu mama,
alimtambua kwa sauti ila alipomuangalia ndio akamtambua vizuri, alikuwa ni Yule
bosi wake yani mama yake na Erick. Yule mama
alimuangalia Erica na kusema maana Erica alimpa mgongo kwahiyo hakumuona
usoni, “Mbona umbo la huyu binti kama nalifahamu” Yule mama
akazunguka kwa mbele kumuangalia, akashtuka na kusema, “Kheee
Erica!” Erica naye alimuangalia huyu mama, alimtambua kwa sauti ila
alipomuangalia ndio akamtambua vizuri, alikuwa ni Yule bosi wake yani mama yake
na Erick. Erica alikaa kimya tu, kisha Yule mama aliendelea
kuongea, “Unanuka madawa ya kienyeji mwili mzima, mmh mtoto mshirikina
wewe. Nilijishangaa kukuingiza kazini bila hata usahili kumbe mtoto mshirikina
loh!” Erica akaona ni tatizo pale, akaanza kumwambia dada yake kuwa
wafate gari nyingine, ila wakati wanaondoka Yule mama alimvuta
Erica, “Umeshindwa hata kunisalimia
kweli!” “Shikamoo” “Mpaka niombe Erica! Au mganga wako kakwambia
kuwa usiongee na mimi? Ila namshukuru sana Mungu kwa kunionyesha rangi yako
halisi, hata nilitaka nikufikirie kidogo ila siwezi kukufikiria tena Erica, wewe
ni mchafu sana” Erica akaona hata akijitetea kwa hali ile hawezi
kusikilizwa na Yule mama, hivyo aliondoka tu na kuingia kwenye gari nyingine
kisha Mage alipanda pia na kumtaka dereva awapeleke waendapo. Safari
ilikuwa moja kwa moja kwa Mage, ila ambacho hawakujua ni kuwa Mama Erick alikuwa
akiwafatilia nyuma na walipofika ndipo aliondoka kwani alijia pale ndio kwakina
Erica, basi waliingia ndani na moja kwa moja Erica akajiandaa ili akaoge, dada
yake akamwambia kuwa akimaliza kuoga anywe chai kwanza ndipo aende kwao maana
hata usiku wa jana hakula, alikubaliana nae na alienda kuoga kwanza ili kwenda
kwao akiwa safi na hata mama yake asimshtukie, alipomaliza kuoga, alikwenda
kuvaa, wakati anatoa nguo zake kwenye begi aliona kuna kitu kama dawa
imeviringishwa kwenye karatasi, alishtuka sana ila hakuelewa imefika fika vipi
kwenye begi lake na hakuelewa ni kwanini imewekwa kwenye begi lake ila alivaa na
kurudisha vitu kwenye begi lake kisha akataka kwenda kumuuliza dada yake kuhusu
hiyo dawa, muda huo aliweka mizigo yake sebleni. Sasa wakati anatoka nje
alimsikia dada yake akiongea na shemeji yake na kugundua kuwa shemeji yake
ameambiwa kuwa yeye yupo hapo kwake, akamsikia akimwambia mkewe, “Huyo
mdogo wako unadhani namuamini tena! Hata kuja kwangu hapa sitaki, yani mtoto
kamuumbua James Yule balaa, ndiomana kazaa mtoto asiye na baba” “Usiseme
hivyo jamani mume wangu, Yule ni mdogo wangu” “Hata kama, hafai kabisa,
hafai kuigwa na jamii. Sasa dada yake akiachana na mume wake yeye atapata faida
gani? Na usikute ni yeye katengeneza kila kitu ili James aonekane mbaya,
nilikutana na James dah aliongea kwa masikitiko sana, na kilichomuumiza zaidi ni
kuambiwa aombe msamaha kwa Yule mdogo wako eti ampigie magoti, kwakweli mimi
simtaki hapa kwangu” Kwakwele Erica akajihisi vibaya sana, kisha akatoka
mule ndani na kumsalimia shemeji yake ambaye alionekana kumuitikia ilimradi tu,
kisha akamwambia dada yake kuwa anahitaji kuondoka, “Aaaah subiria mdogo
wangu unywe chai” “Nitaenda kunywa nyumbani, kwaheri
dada” Aliingia sebleni na kuchukua begi lake kisha kuanza kuondoka, hata
dada yake alipomsimamisha ili amsindikize hakusimama na muda huo alipofika
njiani akasimamisha pikipiki na kupanda kisha akamuelekeza Yule bodaboda
ampeleke hadi kwao maana alitaka tu kuwahi nyumbani, sababu moyo wake alihisi
kama una fundo vile. Kwakweli dada yake hakumuelewa kabisa kuwa kwanini
kafanya vile, hakujua kama maongezi aliyokuwa akiongea na mumewe yote Erica
kayasikia. Erica alifika nyumbani kwao akiwa na hasira sana,
kwanza sehemu aliyoenda na dada yake na maneno aliyoyasikia toka kwa shemeji
yake, aliingia ndani na kumkuta mama yake ambaye alisikitika sana baada ya
kumuona, akamsalimia kisha akataka kwenda chumbani ila mama yake alimrudisha
nyuma, “Weee weee rudi hapa, rudi hapa upesi yani huna hata aibu unataka
kwenda chumbani? Leta hilo begi lako hapa” “Kwanini
mama?” “Nimekwambia lete” Ikabidi Erica ashushe lile begi la
mgongoni ampe mama yake, kisha mama yake akamwaga nguo zote za kwenye lile begi,
kisha na kile kifurushi cha dawa kilianguka na kumshtua zaidi mama yake ambapo
alianza kukishika kile kifurushi, Erica alijaribu kumsihi mama yake aachane
nacho ila mama yake hakukubali, alikifungua kile kifurushi na kukuta dawa mbali
mbali za kienyeji zikiwa zimeandikwa vitu mbali mbali, nyingine iliandikwa ‘dawa
ya mvuto kazini - ya kuweka kwenye mkoba’ ‘dawa ya kumvuta mpenzi aliye mbali -
ya kuchoma na kunuiza’ ‘dawa ya mapenzi – ya kujifukiza’ Kwakweli mama
yake alimuangalia kwa mshangao Erica, “Kheee Erica mwanangu kumbe
ulienda tena kwa mganga?” “Hapana mama” “Hapana kitu gani na
uthibitisho huu hapa? Yani umeenda kutafuta dawa ya mvuto kazini? Dawa ya kuvuta
mpenzi aliye mbali? Unataka nini wewe ikiwa kijana wa watu anakupenda jamani
Erica? Umeenda kutafuta dawa ya mapenzi? Nani amekudanganya kuwa mapenzi yana
dawa jamani Erica!” Mama yake alimpa lawama zote, na kisha kumtaka akae
ili aongee nae vizuri, “Kwanza niambie vizuri ulipoenda na dada yako
hadi kupata kilanga cha kumuachisha mtoto ziwa, kupata kilanga cha kulala mbali
na mtoto wako, kupata kilanga kushindwa kupokea simu ya mwanaume unayeimba wimbo
kuwa unampenda sana, kupata kilanga cha kutafuta dawa zisizoeleweka. Kwanza
kabla ya yote ni kwanini ulikuwa hupokei simu ya kijana wa watu?” “Mama,
kuhusu simu niliogopa kutokana na yale maneno niliyoambiwa na Yule mganga kwenye
simu, kwahiyo niliogopa asije kupatwa na madhara kweli” “Akili mbovu
kabisa wewe, sasa apatwe na madhara gani?” “Mama, uliniambia lisemwalo
lipo na kama halipo linakuja kwahiyo mimi nikaogopa kitu kibaya kumpata
Erick” “Ila kwanini Erica unapenda kuharibu maana ya maneno, hivi iku
ile tumeingia kwenye maombi hadi kuchoma ile leso chanzo ni nini? Chanzo ni
maneno mabaya na jinsi alivyokuwa akikufatilia Yule mganga ila tulivunja maneno
yake kwa kuchoma kile kitambaa na kukemea, halafu wewe hupokei simu ya kijana wa
watu sababu ya ujinga?” “Nisamehe mama” “Haya niambie ukweli
ulienda wapi na dada yako? Sitaki ujiume ume nataka uniambie ukweli na ukweli
mtupu ndio nauhitaji” “Mama nisamehe ila kiukweli tulienda kwakina baba
wadogo” “Hivi una akili wewe? Kwanini mnifiche mimi na kwanini muende
kule? Ni miaka mingapi sijaenda kwa hao baba zenu wadogo? Hivi Erica una akili
kweli?” “Dada alisema twende” “Aaaah yani huyu Mage huyu. Ya
kwake hajamaliza halafu anaanza na mengine, kwahiyo hao baba zenu wadogo ndio
wamekupa na hii dawa eeeh!” “Hapana mama, hata mimi sielewi hiyo dawa
imetokea wapi?” “Punguani wewe, nenda ukaoge huko na hili begi niachie
mwenyewe, umeniudhi sana mimi” Erica alimuitikia mama yake maana
alishamuona kuwa kacharuka, kisha akainuka na kwenda chumbani kwake ambapo
alienda kuoga tena kama ambavyo mama yake alimwambia, kisha akabadilisha nguo,
na kwenda tena sebleni kumuuliza mama yake kuwa mwanae yuko wapi, “Sasa
unadani yuko wapi?” “Sijui mama” “Amelala chumbani
kwangu” Basi akaenda kuchukua chakula na kula, gafla mama yake akapigiwa
simu na kuanza kuongea nayo, kwa jinsi mama yake alivyokuwa akiongea alihisi tu
aliyempigia ni baba yake mdogo na ilionyesha alikuwa akilalamika swala la Erica
kuwa na mtoto na wenyewe kutokuambiwa, mama yake alivyomaliza kuongea na simu tu
akasema, “Ujinga mlioufanya na dada yako kwakweli sijaupenda kabisa,
ngoja nimpigie simu huyo dada yako” Mama yake alionekana kumpigia simu
Mage na kumwambia kuwa aende nyumbani kwao, ilibidi Mage nae akubali maana
alijua tayari ana mashtaka kwa mama yake. Baada ya kumaliza
kula, Erica alienda chumbani kwake kupumzika na kuamua kulala kidogo kwani
alikuwa na uchovu sana, ingawa alijua wazi kuwa mama yao kanpigia simu dada yake
ila alitaka dada yake akifika ndio aamke na hadi akiitwa ndio ataenda kusikiliza
mamake anachoongea na dada yake, wakati usingizi umempitia vizuri leo akapigiwa
simu, akashtuka na kuangalia akaona ni namba ngeni, kupokea ni Mzee
Jimmy, “Kweli kabisa Erica wa kunidanganya mimi mtu mzima na ndevu
zangu?” “Nimekudanganya nini tena?” “Ulinidanganya kuwa mwanao
anaumwa kumbe unanikimbia, sikia Erica sijawahi kupenda mwanamke hivi katika
maisha yangu. Ingawa huyo mwanamke ni mama yako kiasi cha kutotaka mimi niwe na
wewe ila Erica nakupenda sana, sitaki kukuchezea nahitaji kukuoa. Yani wewe
kubali tu nitangaze ndoa na utachagua tufungie wapi” “Nashukuru sana kwa
wazo lako la kutaka kunioa ila mimi nina mchumba wangu nampenda sana, hata bila
ya mama na wewe kujuana ila nampenda sana mchumba wangu, ni yeye ndio atakuwa
mume wangu, hujui tu siku ile ilikuwaje ila mimi nishamuomba Mungu kuwa mwili
wangu huu uwe ni mali ya mume wangu tu, sitaki mwingine wa kuchezea mwili wangu,
samahani sana sikutaki, sikuhitaji, nisamehe bure. Nampenda sana mume wangu
mtarajiwa” “Mmmh wewe binti wewe labda nisijue kama unaolewa maana
nitahakikisha huolewi” Erica akaamua kukata ile simu kwani hakutaka
kusikia mtu yeyote akimpa vitisho tena kuhusu Erick, kwa muda huo alikuwa
akisubiri usiku aongee vizuri na Erick kwenye utulivu maana alijua lazima Erick
amechukia kwahiyo alitaka aongee nae vizuri zaidi ili Erick apunguze hasira
zake, akaangalia simu yake na kukumbuka kuwa hakuwa na vocha kwahiyo akaamua
kwenda dukani kununua vocha. Aliponunua vocha tu, akashikwa began a mtu
akashtuka na kugeuka, akashangaa kumuona Sia, alishangaa sana kwani hakutegemea
kumuona mtaani kwao, “Mbona unashtuka sana, umeona mzimu au
nini?” “Hapana, nashangaa mitaa ya kwetu huku umefuata
nini?” “Kumbe unaishi mitaa ya huku eeh! Huku ni kwetu pia, ila
nimefurahi kukuona kuna kitu nataka nikuulize” “Kitu
gani?” “Hujaongea na Erick kwa siku
ngapi?” “Kwanini?” “Nilimpigia simu, anaonyesha ana jazba sana.
Nikamuuliza tatizo nini anasema ni kwavile hajaongea na wewe, Erica umempa nini
Erick na mimi nimpe?” “Sijampa chochote” “Erica, nilishakwambia
kuwa erick ndio moyo wangu, erick ndio maisha yangu, umempa nini Erick mpaka
kuchanganya akili yake kiasi hiki! Mama yangu ni mgonjwa, alihitaji kuongea na
Erick ila Erick ananijibu kuwa hawezi kuongea na mama yangu sababu akili yake
imevurugika hajaongea na wewe. Limbwata gani Erica umempa
Erick?” “Sijampa chochote ila mimi na erick tunapendana
sana” “Humpendi Erick wewe, ungempenda usingezaa na mwanaume mwingine.
Erica kwanini usiende kuwa na mwanaume uliyezaa nae jamani hadi kuwa na Erick
kweli? Unanikosesha raha Erica, unaikosesha familia yangu raha, unadhani mama
yangu akifa leo lawama nitampa nani kama sio wewe?” “Utakuwa unanionea
Sia, mwenye maamuzi ni Erick sio mimi. Najua nampenda Erick ila bado Erick ana
maamuzi kama awe na mimi au la, najua Erick kawa na mimi sababu ananipenda,
kwahiyo usinifikirie vibaya” “Erica, tafadhari naomba uachane na Erick
kwa usalama wa maisha ya mama yangu, nakuomba uachane na Erick kabisa, sitaki
shida mimi. Nahangaika na mama yangu, hataki kula toka juzi sababu ya
kutokuongea na Erick, nadhani unaelewa jinsi gani mama anauma, naomba uachane na
Erick” Erica akaona akiendelea kuongea na Sia hapo wanaweza kugombana
bure maana aliona sura ya Sia inavyobadilika na kuwa na gadhabu zaidi, basi
aliamua kuondoka tu ila hakujua kuwa alipokuwa akirudi kwao Sia nae alikuwa
akimfata nyuma nyuma, hadi anaingia nyumbani kwao hakujua kama Sia alimfatilia
hadi kwao ila Erica aliingia tu kwao. Alipoingia tu ndani
akasikia dada yake akizungumza na mama yake na kujua kuwa dada yake alifika,
tena dada yake alionyesha kumwambia habari yote mama yao na hapo alijihisi aibu
sana, alipoingia tu mama yake alimuita na kumwambia akae ili asikilize ile
habari. Kwakweli dada yake alikuwa akiongea hadi Erica alikuwa akijihisi
aibu, alipomaliza dada yake kueleza akamwambia mama yao, “Muulize mwanao
huyo kama kuna uongo hapo?” “Eeeh Erica, kuna uongo
hapo?” “Hakuna” “Ila nilikwambia uniambie ukweli wote wewe mtoto
jamani, jioni hii umeumbuka ona sasa!” “Nisamehe
mama” “Ulivyohodari kuomba msamaha sasa huwa hukumbuki hata ujinga
unaoufanya” Kisha mama yao akamgeukia Mage na kuanza kuongea nae kwa
kumfokea, “Ila na wewe Mage huna akili yani huna akili kabisa,
sikutegemea kama unaweza kufanya ujinga wa aina hii. Haya mdogo wako angebakwa
na huyo Derick ungepata faida gani? Halafu una uhakika gani Derick ni mtoto wa
baba yenu? Mtoto gani haendani tabia na baba yenu hata kidogo eeeh! Huyo Derick
ndio alimfanya mdogo wako kuona chuo kichungu halafu mnakaa na kumsikiliza, na
wewe unasikiliza na kufanya maamuzi yako. Erica ni mwanangu, kafanya makosa
mlete kwangu niambie sijui katembea na kaka yake, ulishawahi kusikia katembea na
Tony? Huyo hamjui ndiomana imekuwa hivyo, na hiyo laana ndio ya kuvunja kwa
matambiko jamani! Yani na wewe Mage kama sijakulea kwenye dini vile, ulishindwa
kuja kuniambia mama hivi na hivi ili niombe halafu unampeleka mdogo wako kwenye
matambiko kweli! Sijapenda yani sijapenda kabisa” “Mama unanilaumu bure,
badala umkanye huyo Erica unanilaumu mimi mama jamani. Na huyo mtoto wako wakina
bamdogo wamenipigia simu kuwa jana alivyoondoka kwa kisirani vile wamechukizwa
sana” “Kheee usinitibue, wewe na hao baba zenu wadogo kwanza wamenipigia
simu hapa nimekorofishana nao tu na wewe usinitibue, ulitaka aendelee
kukandamizwa kuwa amemtaka Derick kimapenzi au! Hata kama Derick sio ndugu yake
bado sana Erica kumtaka kijana kama Derick, aisee umenitibua leo Mage, ondoka tu
nenda kwa mume wako” Ilibidi Mage ainuke na umuaga mama yake ila mama
yake alionyesha kuchukizwa sana, muda huo Erica hakuamini macho yake kuwa mama
yake ameamua kuwa upande wake na kumtetea kwakweli alijihisi furaha
kiasi. Basi wakati dada yake ameondoka na yeye akainuka ili
kwenda chumbani, ila mama yake aliongea kwa ukali, “Wewe mjinga, hebu
kuja ukae hapa” Erica alirudi kukaa na kumuangalia mama yake
aliyeonyesha kubadilika kabisa sura, kisha akaanza kusema, “Wewe mjina
ulianzaje kutembea na mjinga kama Derick? Kuwa muwazi kwangu, niambie ukweli
nikusaidie, usinifiche chochote” Sababu dada yake alishaelezea mambo
mengi ikabidi Erica awe mkweli tu akaanza kumueleza mama yake toka siku
aliyotaka kubakwa na wakina George na jinsi Derick alivyomsaidia, akaeleza pia
jinsi Derick alivyomuwekea kilevi na kujikuta akilala nae, alimueleza kila kitu
hadi walivyokutwa na Mage, yani alimueleza mama yake kila kitu kasoro swala la
kutoa mimba tu kwani alihisi lingemchukiza zaidi mama yake. “Kheee Erica
mwanangu kumbe huko chuo ndio ulifikia hali hiyo ya kwenda hadi disco mwanangu
kweli!! Ila mimi nilijua siku nyingi sana kuwa huyu Derick ni shetani, ila
mwanangu kwanini hupendi kusema unakaa na siri moyoni? Hebu ona vitu walivyoenda
kukufanya nab ado amekusingizia ujinga, naomba uniruhusu nikachome zile dawa na
zile nguo zako zote zinazonuka madawa” “Jamani mama” “Usitake
kunifanya nipate kichaa, tena unyamaze kimya, ungetaka kusema jamani mama basi
ungeniambia kabla ya kwenda huko kwenye tambiko. Haya njoo unionyeshe nguo zote
walizokuwa wakifanya tambiko” Basi walitoka na lile begin je huku giza
likiwa limeingia tayari, Erica alimuonyesha mamake nguo ambazo alimwagia mafuta
ya taa na kuzichoma pamoja na ile dawa huku akimtaka Erica amsimulie kilichokuwa
kikifanywa kwenye tambiko, “Ila tuliambiwa ni siri” “Wewe hakuna
siri kwa mama yako, tena uniambie kila kitu usinifiche chochote” Ilibidi
Erica aanze kumsimulia mama yake kutoka mwanzo hadi mwisho, hadi muda aliposikia
mwanae anaita bibi kuwa kaamka, basi Erica alienda ili kumpokea mwanae maana ni
siku nyingi sana, ila mwanae akampita na kwenda kwa bibi yake ambaye alimnyanyua
na kuingia ndani, “Jamani mama, Angel hanitaki” “Atakutaka vipi
ulimkimbia, hata simu ya uongo na ukweli kuwa nimpigie mwanangu hakuna,
atakutaka vipi?” Erica alijiona kweli ana makosa, hivyo akaamua kuanza
kumbembeleza mwanae hadi badae akamkubalia na kukaa nae kwa muda. Muda
wa kulala ulipofika alienda nae chumbani kulala, ila aligoma na kutaka kulala na
bibi yake kwahiyo Erica hakuwa na jinsi zaidi ya kumruhusu mtoto wake akalale na
bibi yake, kisha yeye kurudi chumbani kwake ambapo aliweka ile vocha na kumpigia
Erick na baada ya muda tu Erick alipokea ile simu, kwahiyo Erica alianza kwa
kumuomba msamaha kwa kuondoka bila kumuaga huku akimbembeleza na kuongea nae
vitu vingi, “Ila Erica sijapenda kwa simu yako kupokelewa na mwanaume,
kwakweli sijapend kabisa, Erica hujawahi piga simu yangu ikapokelewa na mwanamke
na kwanini mimi unifanyie hivi?” “Nisamehe Erick” “Na mwanaume
anajitapa kabisa kuwa ni mtu wako, Erica kwanini unifanyie hivi? Au ni sababu
nimekwambia swala la ndoa mimi na wewe mpaka niweke mambo sawa” “Hapana
Erick sio hivyo, nakupenda sana hata sielewi huyo mtu aliyepokea simu alikuwa na
maana gani.” Erica alitumia njia ya kumbembeleza sana Erick na mwisho wa
siku Erick alimuelewa kisha akamuuliza jambo lingine, “Je kuna siku
ambayo dada yangu amekusumbua tena? Au kipi kingine
kilichokusumbua?” “Kinachonisumbua ni mwanamke wako Sia, kila akikutana
na mimi ananitaka mimi niachane na wewe na kusema kuwa yeye hawezi kuachana
nawe, nahisi utatuoa wawili yani moyo unaniuma sana ila huwa siwezi kubishana
nae. Erick, wewe ndiye mwenye maamuzi ya mwisho, nakumbuka ulisema kuwa
unaachana na wanawake zako wote, hivi kama huyu Sia ungekuwa umeachana nae, hivi
angewezaje kunitishia mimi niachane na wewe” “Erica, huyo mwanamke hana
akili tu yani anajua ukweli kuwa nakupenda wewe ila yeye anajifanya ni
king’ang’anizi, ila simtaki” “Kama humtaki mbona huwa unawasiliana
nae?” “Huwa ananitafuta mwenyewe sasa” “Mwambie huwezi
kuwasiliana nae tena, sitaki anipe vitisho najua mimi na wewe
tunapendana” “Sawa malkia wangu” Basi Erica aliongea kwa furaha
sana na Erick na kisha kuagana na kulala. Kesho yake Erica
aliamka na kufanya mambo yake ya hapa na pale, kisha kwenda kumchukua mwanae,
ila muda huo wa asubuhi akapigiwa simu na Erick tena, kwahiyo akapokea na
kuongea nae, “Erica, Yule mtu wa kazi alikutafuta ila ndio ulikuwa
hupokei, alitaka akutafute leo ila nimemuomba akutafute Jumamosi ili Jumatatu
ukaanze kazi, sawa” “Ila hata leo angenitafuta kusingekuwa na tatizo,
niko tayari kuanza kazi” “Aaah pumzika kwanza, kaa kidogo na mtoto na
utaenda tu kufanya kazi, usiwe na haraka” Basi akaongea nae na kukata
simu, kisha muda huo huo akaona ujumbe toka kwa Rahim akaufungua na
kuusoma, “Erica, hutaki kuingia kwenye mtandao, hutaki kuongea na mimi
ila unachokifanya kitakutokea puani. Mwezi ujao narudi nakuja kumchukua mtoto
wangu” Kwakweli bado kidogo akili imruke baada ya kusoma ujumbe huo ila
kwavile alikumbuka mama yake alimwambia kila kitu awe anasema ikabidi aende kwa
mama yake kumueleza kuhusu ujumbe aliopokea kutoka kwa Rahim, akamsikiliza mama
yake atakachosema, “Erica mwanangu usiwe na mashaka, ila lazima uwaze
maana mtoto ushamuuza kwa mwanaume mwingine, yani hayo ndio makosa uliyoyafanya
bila kunishirikisha. Ni kweli wanaume huwa wanakera sana ila si vizuri kuuza
mtoto kwa baba mwingine, labda kama baba wa mtoto alimkataa” “Ila mama
hata Rahim alimkataa Angel” “Ila alikuwa akimuhudumia mwanzoni, kuna
wanawake huko amebeba mimba tu anamwambia mwanaume ila mwanaume anasema sitaki
uniambie habari hizo, hiyo mimba siijui, kwahiyo wewe ulipata bahati sana. Hata
alibadilika labda kuna kitu alifanyiwa maana wanaume ni wahuni sana na uhuni wao
wakikutana na wanawake waliojichokea akili huwa wanawakorogea dawa basi hapo
ndio anakuwa mbogo na wala haelewi kitu. Kosa lako wewe ni kuuza mtoto
tu” “Sasa mama nitafanyaje?” “Hebu tulia kwanza, yani usiwe na
presha wala nini, anaanzaje kufika tu na kuchukua mtoto? Kuna taratibu, na hata
hivyo mtoto hachukuliwi kwa mama hadi afike miaka saba, ila una uwezo wa
kukataa, wanasema mtoto ni wa baba ila kiukweli mtoto ni wa mama yani mama
anaouwezo wa kufanya chochote kwa mtoto, usiwe na mashaka mwanangu. Kesho
nitakwambia cha kufanya ila kwasasa kuwa na amani kwanza” Basi Erica
alisikiliza ushauri wa mama yake na kuendelea na mambo mengine kwa siku
hiyo. Usiku kama kawaida aliwasiliana na Erick, ila leo alimpa
habari iliyomfurahisha kidogo, “Erica, Yule Sia hatokusumbua tena,
nishamalizana nae, nahitaji kuwa nawe Erica” “Nimefurahi sana kusikia
hivyo” “Halafu mwezi ujao narudi, Erica lazima nikuoe kwahiyo usijali
kitu yani lazima tuishi wote” Kwakweli Erica alifurahi sana kwani jambo
hili lilimpa raha vilivyo. Akalala huku akitabasamu, kulipokucha
alisikia kelele nje ya nyumba yao na kumfanya ashtuke na kutaka kutoka,
akakutana na mama yake ambaye pia alikuwa akitoka maana zile kelele alizisikia,
walishangaa kuona kuna binti akijigalagaza na kulala kwenye uwanja wao, ikabidi
mama Erica na Erica wamsogelee binti Yule ili kumuuliza kuna nini,
walipomsogelea na kumuinua na kumuuliza, binti aliinua kichwa na Erica alishtuka
sana kwani alikuwa ni Sia halafu alisema kwa uchungu, “Erica umeniulia
mama yangu” Hata mama Erica alishangaa kusikia
vile. kulipokucha alisikia kelele nje ya nyumba yao na
kumfanya ashtuke na kutaka kutoka, akakutana na mama yake ambaye pia alikuwa
akitoka maana zile kelele alizisikia, walishangaa kuona kuna binti akijigalagaza
na kulala kwenye uwanja wao, ikabidi mama Erica na Erica wamsogelee binti Yule
ili kumuuliza kuna nini, walipomsogelea na kumuinua na kumuuliza, binti aliinua
kichwa na Erica alishtuka sana kwani alikuwa ni Sia halafu alisema kwa
uchungu, “Erica umeniulia mama yangu” Hata mama Erica alishangaa
kusikia vile. Ilibidi mama Erica amuinamie vizuri Sian a kuongea
nae, “Hebu ongea taratibu binti nikuelewe” “Erica kaniulia mama
yangu” “Sasa usipayuke hivyo nyumbani kwangu, utanijazia watu, Erica
kamnyonga huyo mama yangu, kamtilia sumu au kamfanya kitu gani hadi useme
kamuua?” Sia alikuwa akilia tu, ilibidi mama Erica amuinue na kumuingiza
ndani maana pale aliona angemjazia watu, na angemjazia watu kweli jinsi
alivyokuwa akilia kwa kisirani, alipomuingiza ndani ndipo alipoanza kumuuliza
tena, “Hebu ongea taratibu binti nikuelewe, mimi ndio mama wa huyu Erica
unayesema kakuulia mama yako, nataka kujua kamuua vipi? Maana nipo na Erica
usiku wote, sasa katoka muda gani kuja kumuua mama yako?” Sia alikuwa
akilia tu, kisha mama Erica akamwambia tena, “Lia, ukimaliza utanieleza
vizuri maana sikuelewi (Halafu akamuangalia Erica na kumuuliza) Au wewe
unamuelewa?” “Simuelewi pia mama” Hapo ndipo Sia alipoibuka na
hasira, akasogea karibu na Erica na kumzaba kofi, mamz Erica akamrudisha nyuma
na kumpa onyo, “Wewe binti usitake kunipandisha kichaa change, na mimi
ni kichaa kama wewe. Nishakwambia mimi ndio mama wa Erica, huyo Erica kakuulia
mama yako vipi? Unainuka na kumpiga mwanangu kofi, sasa mimi sitajali umefiwa
wala nini, nitakusambulia hapa uione dunia chungu, haya sema sasa Erica kamuua
vipi mama yako” “Anajua mwenyewe, ila Mungu atanilipia nashukuru
sana” Akainuka na kutaka kutoka pale kwakina Erica, ila mama Erica
akamzuia na kusema, “Wewe ungekuwa na haja ya kuacha Mungu akulipie
sidhani kama ungefika hapa kwangu na kupiga yowe, nahitaji kujua tatizo ni nini?
Nahitaji kujua mwanangu huyu kaanza lini uuwaji? Huondoki hapa bila ya kunieleza
kwakweli” “Unanionea tu wakati mimi nina uchungu, ni hivi mama yangu ni
mgonjwa sana na Erica anajua hilo, mama yangu huwa nafuu yake ni kuongea na
Erick, nampenda sana Erick ni mpenzi wangu na tumekubaliana kuoana, mama
anatambua hilo hata marehemu baba yangu anatambua hilo na kabla ya kifo chake
alinipa baraka zote za kuolewa na Erica, sasa huyu Erica kamwambia Erick
asiongee na mimi wala mama yangu wakati anajua ni mgonjwa sana, hivi
tunavyoongea mama yangu yupo kwenye hali mbaya sana, toka jana Erick amegoma
kuongea na mama, na mama yangu anakufa ila chanzo ni Erica” “Kwahiyo
huyo mama yako bado hajafa ila yupo kwenye hali mbaya?” “Ndio mama yangu
yupo kwenye hali mbaya sana, hakuna matumaini ya kupona” “Kwahiyo mamako
akiongea na Erick ndio atapona?” “Ndio” Huku akiendelea kulia,
ila mama Erica alimtuliza na kumwambia, “Sasa hukutakiwa kuja na kupiga
kelele mlangoni kwangu, mambo kama hayo ulitakiwa kuongea kuwa ni hivi na hivi
na hivi unaeleweka sio kupiga kelele sijui Erica kaniulia mama yangu sijui nini
na nini haipendezi, hivi watu wangejaa unadhani ingekuwaje na wangemfikiriaje
Erica? Haya nenda kwa mamako na Erick atampigia simu muda sio mrefu,
kwaheri” basi Sia alitoka na kuondoka zake, mama Erica hakuongea
chochote na Erica ila alienda humbani kwake na kuchukua simu yake kisha kumpigia
simu Erick, kwakweli hata Erick alishangaa siku hiyo kupigiwa simu na mama yake
Erica, basi alipokea na kumsalimia ila kabla Yule mama hajaitikia salamu
akamwambia Erick, “Wewe kijana fanya majukumu yako, unajua kuna mama
anayetegemea simu yako kwa maisha yake, mpigie simu mama huyo, usimtafutie
mwanangu matatizo, kwaheri” Mama Erica akakata simu kisha akarudi
sebleni. Muda amerudi sebleni Erica alikuwa ameenda chumbani,
akamuita kwa ukali sana, ikabidi Erica aende kumsikiliza mama
yake, “Hivi Erica, hukuona wanaume wengine au nini? Ni raha gani ya
kugombea mwanaume? Sipendi kitu kinaitwa kugombea mapenzi jamani, sipendi
kabisa. Kwanini mapenzi yapo hivi lakini? Erica umeshindwa kabisa kupata mpenzi
wako peke yako hadi mpenzi wa kugombea hadi uambiwe umeua mama wa watu sababu ya
kugombea mapenzi Erica?” “Mama, kiukweli nampenda Erick, nampenda
sana” “Hivi unajua kupenda wewe, nakuuliza unajua kupenda? Huyu Erica
sio ndio Yule kijana aliyekusababishia matatizo wakati upo shuleni
kweli?” “Ndio yeye mama” Mama yake akamnasa kibao pia na
kumwambia, “Nimekupiga kwa uzembe, yani mwanaume aliyekusababishia
matatizo shuleni umeamua kumkubali hadi mtoto kumuuzia, hivi wewe Erica ni
mjinga kiasi gani? Huyo Erick ana nini cha zaidi huyo hadi mtu afike na
kugalagala hapa ooh Erica ananiulia mama yangu, sijui nishaahidiwa Erick ndio
mume wangu, haya na wewe uliahidiwa na majengo ya shule yenu ile kuwa Erick ndio
mume wako?” “Hapana mama” “Kuanzia leo sitaki kusikia habari za
huo uchafu wa kuitwa Erick, tulia wewe mtoto upate wako, mbona mwanangu wewe ni
mzuri tu unahangaika na nini jamani? Erick, Erick ndio nani yeye, ni mwanaume
pekee duniani? Mbona kuna wanaume wengi sana” “Ila mama nampenda
Erick” “Unampenda ila yeye hakupendi, kashamuahidi msichana wa watu
atamuoa, sasa wewe atakuweka wapi? Mbona hujiongezi jamani!” “Ila mama
Erick ananipenda pia” “Nimekwambia sitaki kusikia habari za Erick kwenye
nyumba yangu, sijui habari za Bahati sitaki kusikia, maana kasikia raha
kuendeshwa na madawa huko, sitaki kusikia habari zake” “Sasa mama niwe
na nani?” “Usiniulize mie, unataka nikufanyie chaguo la wa kuwa nae?
Kwanza tushughulike swala la Angel maana tayari ushamuuza kwa huyo Erick kumbe
ana mwanamke kashaahidiana nae huko hadi kuoana, sitaki kumsikia huyo Erick,
maana kashanitibua tayari” Kwakweli leo ilikuwa siku mbaya kwa Erica,
yani hakuamini kama mama yake mwishoni angefikia maamuzi ya kutokumtaka Erick,
aliinuka na kwenda chumbani kwake, akawaza sana na kufikiria kuhusu Erick,
hakika alimpenda sana yani moyo wake aliona ukijaa kuhusu Erick tu kwahiyo swala
la kuambiwa kuwa Erick asisikike mule ndani kwao lilimpa ukakasi
sana. Aliingia ndani na kulala tena yani hata kuoga hakwenda kuoga,
ilimbidi mamake ndio amuogeshe mtoto amlishe na abaki akicheza cheza
nae. Jioni ya siku hiyo, mama yake Erica aliamua kumuita mwanae
maana hakumuelewa kwani hakula kabisa siku hiyo na alipomuita alijibu kuwa
hajisikii kula, mama yake akasema, “Yani sababu ya Erick ndio hadi kula
umesamehe, masikini mwanangu, huyo Erick kakupa nini eeeh! Huyo Erick ana nini
ambacho wanaume wengine hawana” “Mama hujui tu, nampenda Erick, nampenda
sana” “Katika maisha yako hujawahi kupenda mwingine zaidi ya
Erick?” “Sijawahi mama” “Kwahiyo ulikuwa unatembea nao tu,
ukamaliza familia nzima kutembea nayo bila kuwapenda, ukatembea na mtu hadi
ukazaa nae bila kumpenda, hivi inaingia akilini hiyo? Erica eeeh! Hebu niambie
labda mimi sijui, Erick ana nini ambacho wanaume wenzie hawana?” “Mama,
nampenda tu naomba niruhusu niwe na Erick” “Haya kuwa nae ila baada ya
wiki mbili unijibu kuwa Erick ana nini ambacho wenzie hawana” Kitendo tu
cha mama yake kumruhusu kuwa na Erick kilikuwa ni kitendo cha furaha sana kwake
maana alihisi kama kadhulumiwa nafsi kwa kuambiwa kuwa aachane na Erick wakati
anampenda sana. Kwahiyo muda huo alifanya shughuli zake zingine na kula,
hadi muda wa kulala ulipofika. Leo mwanae alikubali kwenda kulala nae, kumbe
alikuwa na nia zake, alitaka kuongea na Erick, kwahiyo ikabidi Erica apige simu
na kumpa Angel aongee nae, alipomaliza akaichukua yeye sasa na kuanza kuongea
nae, “Erica, niambie ni nini kimetokea leo?” Ikabidi Erica
amsimulie jinsi Sia alivyofika nyumbani kwao na jinsi alivyokuwa akilia
lia, “Poleni Erica, najua ni kosa langu ila naomba mnisamehe sana.
Erica, kipindi umeniacha sikujielewa yani sikujielewa kabisa, nimeanza kunywa
pombe sababu yako Erica, nikawa na wanawake wengi sababu yako ndio mwisho wa
siku hadi nikaangukia kwa Sia, ila yote nilikuwa natafuta penzi la dhati kuwa
labda kuan mahali nitapenda kama ninavyokupenda wewe, ila sijaweza Erica, na
watu hawa wamekuwa wagumu kuelewa kama siwapendi maana zamani nilikuwa
nawaigizia kuwa nawapenda, Erica nilifanya yote haya kupata unafuu wa moyo,
Erica nimeanza kukupenda muda mrefu sana, siku ya kwanza kukuona tu nilikupenda
na wala sio kwamba nilikutamani, hapana ila nilikupenda. Erica, nakuomba vumilia
tu kwa yote yanayotendeka ila upendo wetu ubakie vilevile, tuendelee kupendana
siku zote za maisha yetu” “Erick nakupenda, sitamani chochote
kitenganishe mapenzi yetu, ni kweli naumia sana kuhusu wanawake zako wa nyuma
ila ongea nao vizuri wasinifanyie fujo, Sia anadai uhai wa mama yake unategemea
simu yako wewe” “Yule nae aniondolee wazimu mie, nitashika uhai wa mama
yake mimi nimekuwa Mungu? Wale wajinga sana, badala wampeleke mama yao hospitali
eti wanasema akiongea na mimi ndio atapoan, balaa likiwashika ndio atakumbuka
maneno yangu niliyokuwwa nikimwambia kuwa tatizo sio mimi ila mpelekeni
hospitali huyo mama, oooh ukiongea nae ndio anapona, jamani mimi nimekuwa
malaika hadi nisaidie watu kupona? Nimekuwa dakari? Huwa siwaelewi
kabisa” Basi Erica alikuwa akifarijiana tu na Erick na kujisikia amani
sana kwa kufanya hivyo kwani aliona kupata amani ya moyo, hadi wanaagana alikuwa
na furaha sana. Zilipita siku tatu, ilikuwa ni jioni wakati
mama Erica akifagia uwanja wake, akashangaa kumuona tena Sia, na leo alivalia
nguo nyeusi huku macho yakiwa mekundu kweli kweli, kwakweli mama Erica alihisi
kuna jipya linazuka tena muda sio mrefu, ikabidi amuulize kulikoni, ila Sia
alimsogelea mama Erica akamkumbatia na kulia sana, Yule mama akamuuliza kuwa
imekuwaje, “Mama yangu amekufa kweli, sina mama mimi. Liwazo langu
kaondoka” Akaendelea tena kumkumbatia mama Erica akilia, ikabidi mama
Erica amuulize, “Tatizo ndio lile lile la Erick kutokuongea na mama yako
ndio kasababisha kifo au nini?” “Hapana mama, Erick alikuwa akiongea
vizuri kabisa na mama yangu hata leo asubuhi kaongea nae ila hali ya mama
imebadilika jioni hii wakati tunatafuta usafiri tumuwaishe hospitali mama
alikuwa ameshakufa” Akaendelea kulia, ikabidi mama Erica aanze biashara
ya kumbembeleza, kisha akaenda ndani kwake na kujivika kanga vizuri na kumuaga
Erica, “kuna msiba wa gafla umetokea ndio naenda” Hakumpa Erica
maelezo ya kutosha ila aliyoka nje na kuongozana na Sia kwenda
msibani. Alifika pale msibani kisha sia kwenda kuungana na ndugu zake
wengine wakiendeleza vilio, Mama Erica aliingia nae ndani na kutoa pole kisha
akatoka nje ili kuungana na wanawake wengine katika shughuli za pale kama
kuandaa chakula na kuweka sawa mazingira ya msiba maana msiba hauna ugeni,
aliwakuta wanapika chakula cha watu kwa usiku wa siku hiyo, sema hapakuwa na
wamama wengi sana sababu msiba ndio umetokea siku hiyo hiyo, hadi mama Erica
akaauliza, “Mbona watu si wengi?” “Aaah kwani na wenyewe
walikuwa na tabia ya kushtuka msiba ukitokea basi? Baba yao ndio alikuwa hodari
na alipokufa basi tena ila wat wengi watakuja siku ya mazishi” wakati
wanapika pika na wanawake wa pale wakaanza kuongea wakiongea, “Yani hawa
watoto akili zao jamani ni mbovu tu, mama yao anaumwa siku nyingi badala
wampeleke hospitali eti atapona tu” Mwingine akadakia, “Mimi
nilikuwa nikimkuta kazidiwa, nikiwaambia habari za hospiatali wanasema wana dawa
zao” “Kwanza cahanzo cha ugonjwa wa mama yao ni nini?” “Huyu
mama tangu mumewe amekufa basi na yeye akaanza kuumwa, ila kipindi hiki ndio
vikachachamaa ila watoto wanadai wana dawa zao” “Dawa gani hizo? Mbona
mama yao kafa sasa kama wana dawa zao?” “Yani watoto wajinga wale, sijui
dawa gani wenyewe. Nakumbuka miaka miwili iliyopita kulikuwa na kijana mmoja
anabadilishaga magari Yule mvulana, kazuri zuri hivi, ndio alikuwa anakuja na
kumpeleka Yule mama hospitali hadi akawa anaendelea vizuri ila nimeshangaa mwaka
huu toka uanze ukimkuta kazidiwa unajibiwa kuwa kuna dawa zake” “Unajua
hospitali ni muhimu sana, hata kama unatumia dawa za kienyeji ila nenda
hospitali kwanza ujue unaumwa na nini, hata waombeaji wenyewe huwa wanasema
kapime kwanza, maana ugonjwa ukijulikana ni rahisi zaidi tofauti na ugonjwa
usipojulikana” Mama Erica alisikiliza kwa makini sana na kugundua kuwa
pale kulikuwa na tatizo licha ya Yule mama kuugua hadi kufa ila kulikuwa na
tatizo. Basi mama Erica alishughulika pale kisha alipoona usiku umeingia
sana akaamua kuondoka kidogo kurudi nyumbani kwake maana asingeweza kulala hapo
msibani kwani hata kwake hakutoa maelezo ya kutosha. Alimkuta
Erica akiwa sebleni tu maana ilikuwa ni usiku tayari. Erica alimsalimia mama
yake kisha kumuuliza kuwa alikuwa akiwahi kwenye msiba wa nani maana alimwambia
tu kuwa anaenda msibani, “Nilienda kwenye msiba wa mama wa mke
mwenzio” “Mama wa mke wmenzangu? Kivipi?” “Mama yake na Sia
amekufa” “Kheee mamake amekufa, masikini jamani” “Hiyo
kusikitika ya leo mbona haikuwepo siku ile Erica eeeh!!” “Jamani mama!
Lazima nisikitike maana si kitu nilichokitarajia, mbona niliongea vizuri na
Erick kuwa awe anampigia simu mara kwa mara mama yake Sia, jamani mama wa watu
amekufa! Inamaana Erick alikuwa apigi simu?” “Hebu wewe nawe nitolee
ujinga mie, huyo Erick ni daktari kusema akipiga simu anasema watumie dawa
Fulani au nini? Erick ndio malaika mtoa roho kusema huyu nimchukue sasa au nini,
hebu nitoleeni balaa, sema uzuri hujawa chanzo tena cha kifo cha huyu mama.
Nadhani kifo chake kilifika ila kama kawaida wanadamu hutafuta sababu tu,
mwishowe wakuchukie bure.” Erica alibaki kusikitika tu, kisha akaenda
chumbani kwake na kumpigia simu Erick ila simu yake haikuwa na salio, yani pale
alipata mawazo sana kwani alihitaji haswa kuongea na Erick, akawaza akaona ni
vyema akanunue vocha ili ampigie na kuongea nae, akatoka chumbani kwake na
kujifunika kanga, ila mama yake alikuwa sebleni na kumuuliza, “Haya saa
hizi unataka kwenda wapi?” “Nataka kwenda dukani mama kununua
vocha” “Hapana, siwezi kukuruhusu uende dukani muda huu, Erica mwanangu
kumekuwa na matukio kwako yasiyoeleweka kabisa, hivi naanzaje kukuruhusu kwenda
dukani eeeh! Ngoja kesho utaenda” “Jamani mama” “Nimesema leo
hutoki, umenisikia? Wewe jione ni mtu mzima ila mimi nakuona bado ni mdogo sana,
leo hutoki kwenda popote muda huu” kisha mamake akaenda kufunga mlango
na kwenda na funguo chumbani kwake, kwahiyo Erica hakuwa na namna yoyote ile
zaidi ya kurudi chumbani kwake, ila alikuwa na mawazo sana hadi hakuwa na raha
sababu alitamani sana muda huo aongee na Erick na hakujua ni kwanini Erick
hakumpigia simu siku hiyo. Alipokuwa amekaa na mawazo chambani kwake
muda kidogo akapigiwa simu na namba ngeni, Erica alipokea simu hiyo kwani
alikuwa na mawazo sana na Erick, kwani alikuwa akidhani mtu akimpigia simu ni
Erick ingawa alikuwa akiona kabisa ile namba si namba ya nchi aliyokuwepo Erick,
alipokea na kuongea nayo na kugunduwa kuwa mpigaji ni mzee Jimmy, “Kheee
bado unanifatilia wee mzee?” “Naachaje kukufatilia Erica eeeeh! Katika
maisha yangu sijawahi kumpenda mwanamke yoyote kama ninavyokupenda wewe,
usisikilize maneno ya mama yako, nikubali mimi na huyo mwanao ataishi maisha
mazuri kama jina lake” “Asante kwa hayo maisha mazuri ila mimi
nimeridhika” “Erica, nishaiambia familia yangu yote kuwa nataka kuoa na
wote wamenikubalia, niruhusu nikuoe Erica” “Unajua unanichosha yani
unanichosha sana, huwa sipendi hata kukusikia ukiongea kwenye simu unanichosha
balaa” “Erica, pole kwa kukuchosha. Naomba unisamehe, nifanye nini ili
unisamehe?” Erica akakumbuka kuwa anahitaji vocha, alijikuta tu
akimuambia, “Nitumia vocha” “Hilo tu Erica? Niambie kitu gani
tena?” “Nitumie vocha nina shida nayo” “Nikutumie ya shilingi
ngapi?” “Ya elfu tatu” “Sawa nakutumia Erica, nakupenda sana
umechanganya akili za mtu mzima mimi” Basi Erica akakata ile simu na
baada ya muda mfupi vocha iliingia kwenye simu yake, kuangalia ilikuwa ni vocha
ya elfu hamsini, akatabasamu kisha akabonyeza namba za Erick na kumpigia, ambapo
simu iliita bila kupokelewa, alipiga kama mara tatu na sim haikupokelewa,
alikuwa na mawazo sana maana sio kawaida kabisa, hakuwa na ugomvi mkubwa na
Erick wa kusema ashindwe kupokea simu, akashangaa sana, alikaa kama lisaa
lizima, yupo macho tu akajaribu tena kupiga simu muda huu Erick alipokea simu ya
Erica, ila Erick aliongea katika hali ya ulevi sana, mpaka Erica
akamshangaa, “Erick umeanza tena kunywa pombe kiasi hiko kweli? Si
ulisema ulevi ulianza sababu yangu, leo vipi upo na mimi na unakuwa
mlevi?” “Erica huelewi tu” “Sielewi nini sasa” Erick
alikuwa hata kujibu hajibu vizuri sababu ya kulewa hadi Erica aliamua kukata
simu kwa hasira, huku akichukia sana moyoni, alihisi Erick kuna mwanamke
mwingine anamsumbua ndiomana kaamua kunywa pombe, alijikuta akiumia sana yani
siku hiyo hakuweza kulala kabisa. Kwa kukosa usingizi hadi aliamua
kuingia tena kwenye mtandao wa kijamii baada ya kipindi kirefu sana tangu
alipogombana na Rahim, na alivyoingia tu alikutana na jumbe kadhaa za Rahim
zikimpa lawama tu, kisha muda huo huo Rahim alituma tena ujumbe, “Erica,
leo umeingia mtandaoni siamini” “Nipo” “Habari Erica, mtoto
anaendeleaje?” “Leo ndio umejua kuwa una mtoto na mimi? Wewe si
ulijifanya kunijibu shombo wewe?” “Erica, una matatizo wewe sio bure,
kwani hujui kosa lako la mimi kuwa vile? Hivi unawezaje kumuomba mwanaume
milioni kumi na tano? Kuna mwanaume kichaa anayeweza kufanya hivyo? Hakuna
mwanaume wa kukupa hela hiyo hata awe na hela kiasi gani” “Si kweli
Rahim, ungekuwa na malengo na mimi ungenipa. Najua hiyo hela uwezo nayo unao, na
hata kama ungekuwa huna ungeniambia kiustaarabu ila sio kwa majibu yal
uliyonipa, sikufurahishwa nayo kwakweli” “Sawa, hukufurahishwa nayo ila
namtaka mwanangu Erica” “Usinichanganye, unamtaka mwanao kivipi? Mama
yako mwenyewe alikuja hapa na hata kurudi tena hajataka, na mtoto mwenyewe
alikuwa na mashaka nae kuwa si wa kwako halafu wewe unamuhijtaji mwanao kwa
kigezo kipi haswa?” “Unajua fika Yule ni mwanangu, yani hata uongee vipi
ila ukweli unaujua kuwa Yule ni mwanangu, sikukutuma uje kwangu ila umalaya wako
ndio uliokuleta kwangu, hadi ukadanganya kwenu kuwa unasafiri wakati unakuja
kulala na mimi sababu ya umalaya wako na mimba ukabeba ukijua nitakuoa, ulibugi
kwakweli kwani siwezi kuoa mwanamke kama wewe” “Yani leo hii Rahim ndio
unaniita malaya? Kwahiyo mtoto umezaa na malaya?” “Erica, unajua sipendi
kuongea sana, namtaka mwanangu. Ndio wewe ni malaya, kwani nani hajui hilo? Wewe
mwanamke hufai ndiomana hata wazo la kukuoa halikuwepo katika akili
yangu” “Ulivyokuwa unaniambia unanipenda?” “Nilikuwa nawe ili
kupoteza muda tu, nilikwambia vile ili uniamini ila kiukweli wala sikukupenda.
Mwanamke gani wewe, nasikia ulitembea na familia yangu nzima, na atakayekuoa
wewe atakuwa chizi, hakuna mwenye akili timamu atakayemuoa mwanamke wa dizaini
yako, na hata huyo mtoto namtaka tu ila sijui kama naye hajanitia aibu maana
mtoto wa nyoka ni nyoka” “Kwahiyo ndicho ulichotaka kuongea na mimi
hicho mtandaoni kuwa kila siku ingia mtandaoni kumbe ndio ujinga huo unataka
kuniambia?” “Sio ujinga ila nakwambia ukweli, kawaida wanaume kuwa na
wanawake wengi ila mwanamke kuwa na wanaume wengi kwa hakika huyo mwanamke hafai
kwenye jamii, Erica huwezi kuolewa wewe kamwe, maana mtu akijua tu tabia yako
atakuacha” Erica alichukia sana na kutoka kwenye mtandao wa kijamii huku
akianza kutokwa na machozi na kuitathmini tabia yake, ila alihangaika kote
kutafuta penzi la kweli, alijiona mjinga sana kuhangaika na wanaume waliomwambia
kuwa wanampenda kwa kumsanifu tu. “Hivi mtu unawezaje kujifanya
unampenda mtu wakati humpendi? Kweli kabisa leo hii huyu Rahim ndio ananiambia
maneno haya jamani? Kuna uwezekano mkubwa sana wa wote waliosema wananipenda
kumbe hawanipendi wala nini? Ni nani anayenipenda kweli? Hivoi Erick ananipenda
kweli au na yeye atanigeuka siku moja kama leo alivyolewa? Lakini hapana Erick
ananipenda bhana, nayachukia mapenzi, sijui kwanini yapo.” Kiukweli siku
hiyo hakulala kabisa kwani alijikuta akiwa na mawazo mengi sana mpaka
asubuhi. Mama yake alijiandaa mapema kwenda msibani na kumuaga
Erica pale kwani kulikuwa na hati hati kuwa wanaweza kuzika siku hiyo, basi
akaondoka zake na Erica kurudi chumbani kwake. Alifika msibani na kweli
alikuta kuna mipango ya mazishi siku hiyo wakashugulika na kazi za pale kisha
kwenye mida ya saa sita walienda kuzika na kurudi tena pale nyumbani, alimuona
Sia ameongozana na binti mwingine ambaye sura ilimjia jia kuwa anamfahamu,
walipofika karibu yake ndio akagundua kuwa Yule binti ni Tumaini ambaye alikuwa
akijua ni rafiki wa Erica, muda huu Sia alimsogelea tena mama yake Erica na
kumkumbatia kwa kilio, “Mama yangu hayupo tena, nimebakiwa na Erick
tu” Basi mama Erica alikuwa akimbembeleza lakini hakuelewa ni kwanini
alikuwa akiyasema yale aliyokuwa akiyasema, basi Tumaini nae akasogea karibu na
Yule mama ili kumsalimia, na alipomaliza kumsalimia tu
akamwambia, “Familia tunamtambua Sia, familia tunamtaka Sia kuwa mke wa
Erick, nakuomba mama mwambie Erica akae mbali na Erick maana
hatumtambui” Kwakweli mama Erica alikuwa akiwashangaa sana wale mabinti,
hakufikiria kama wangeleta habari hizo msibani, muda huo huo Tumaini akamwambia
mama Erica kuwa anaenda kumuita na mama Erick ili amwambie jinsi Erica
wasivyomtaka kwenye familia yao, ila muda ule ule Sia alifatwa na mama yake
mdogo ila alipofika pale alianza kumshangaa mama yake Erica na
kusema, “Kumbe ni wewe!” Walitazamana kwa muda na kujikuta
wakikumbatiana kwa furaha. Kwakweli mama Erica alikuwa
akiwashangaa sana wale mabinti, hakufikiria kama wangeleta habari hizo msibani,
muda huo huo Tumaini akamwambia mama Erica kuwa anaenda kumuita na mama Erick
ili amwambie jinsi Erica wasivyomtaka kwenye familia yao, ila muda ule ule Sia
alifatwa na mama yake mdogo ila alipofika pale alianza kumshangaa mama yake
Erica na kusema, “Kumbe ni wewe!” Walitazamana kwa muda na
kujikuta wakikumbatiana kwa furaha. Kisha wakaenda pembeni kuzungumza,
kwahiyo Sia alibaki mwenyewe pale akishangaa tu kuwa watu wale wamejuana vipi,
wakati huo Tumaini nae alifika na mama yake Erick ila hawakumkuta mama Erica,
Tumaini akamuuliza Sia kuwa mama Erica ameenda wapi, “Muda ule ule
alifika mama yangu mdogo, sasa sijui wanafahamiana vipi, wakachukuzana na
kuondoka” Ikabidi Tumaini aombe radhi kidogo kwa kumsumbua mama Erick,
kisha akamwambia, “Ila mama usijali, napafahamu kwakina Erica, au
nikupeleke muda huu?” “Hapana, saivi kuna mahali nataka kwenda, nilikuja
kuzika tu” Basi akaondoka na kumuacha Tumaini na Sia pale huku Tumaini
akimpa mpa moyo Sia kuwa aijali yeye ndio mke halali wa
Erick. Sababu ya kutokulala usiku, basi muda huo Erica alikuwa
hoi na usingizi hadi maam yake anarudi na kugonga mlango kwakweli Erica alikuwa
amelala sana hadi ilibidi akamgongee dirishani ndipo Erica alipotoka na
kuwafungulia kisha mama yake akaingia na Yule mgeni huku akimkaribisha
sana, “Karibu, karibu. Hapa ndio nyumbani kwangu” “Jamani ni
siku nyingi sana” “Ten asana” Basi Erica akawasalimia na kurudi
kulala chumbani kwake kwani kiukweli alikuwa na usingizi sana, basi mama yake na
Yule mwenzio walijikuta wakiongelea mambo mbalimbali ya zamani hadi kuanza
kuongelea na msiba uliotokea, “Hivi aliyekufa pale ni nani
yako?” “Ni dada yangu” “Aaah pole sana, dada yako tumbo
moja?” “Ni dada wa bamkubwa na bamdogo yani tumbo moja” “Kwani
alikuwa akisumbuliwa na nini?” “Mwenzangu hata hatuelewi maana ugonjwa
aliokuwa akiumwa nadhani ni siri ya watoto wake, nilikuwa naenda kumuona yani
kuna kipindi unakuta kazidiwa haswaa naanza kufokea wale watoto kuwa kwanini
hawampeleki dada yangu hospitali, basi wanasema Sia ndio anajua dawa ya mama
yao, Sia ndio Yule binti nilikukuta nae. Ni mtoto wa dada yangu Yule, ndio
mwanae wa mwisho. Nikimuuliza Sia dawa ya dada ni nini, ananiambia subiri basi
sijui anapiga simu wapi na kumpa mama yake aongee nayo baada ya hapo utakuta
dada kaamka na kuanza kula tena, nilikuwa nashangaa sana, na sijui kwanini
walikuwa hawampeleki hospitali” “Ila ndugu mnatakiwa kujua sababu, sio
watoto kuwaficha ficha” “Na hakika wanatuficha ficha sana, ila Yule Sia
ndio huwa simuelewi kabisa, msiba umetokea muda kidogo na yeye akapndoka, ila
asilimia kubwa ya watu waliofika msibani wanasema habari wamepewa na Sia,
nadhani alienda kusambaa habari si mbaya ila yule mtoto wa dada yani hata sijui
kapagawa na nini? Wewe umemfahamia wapi maana ndio nilikukuta
nae” Ikabidi mama Erica amwambie kwa kifupi tu jinsi alivyo mfahamu
Sia, “Kheee mtoto ana wazimu Yule, yani aje kulia mlangoni kwake jamani!
Mtoto mjinga Yule, ila kiukweli nimefurahi sana kuonana na wewe, tuachane na
hizo habari za huyo mtu ila nataka kujua kwani huyo kijana na mwano wana mpango
gani?” “Wamepanga kuoana, wana mtoto tayari” “Oooh hongera sana,
jamani binti yangu kazaa na mwanaume huyo hajielewi wala nini, mtoto anaenda
miaka minne sasa ila baba haeleweki na hajawahi kuja kumuona mtoto
wake” “Pole ndugu, ndio uzazi huo” Basi wakawa wanaongea mambo
mbali mbali na kukumbushana vitu vingi ila Yule mama aliaga na kusema kuwa
angerudi siku nyingine ili waongee vizuri, “Ngoja nikamalize mambo ya
msiba kwanza, nitakuja kukuaga na tutaongea vizuri, ila habari za watoto
zisikuumize kichwa hizi, nitaenda kuongea na Sia tu nijue muafaka ni nini. Sawa
ndugu yangu!” “Sawa, utakuwa umenisaidia sana” Basi
akamsindikiza na kuagana nae, alivyorudi ndani sasa alimkuta Erica ametoka
sebleni na mtoto wake, “Yani wewe pindi mgeni yupo ndani hapa ndio
ukajifanya hutoki chumbani, umeona kaondoka ndio umetoka” “Nisamehe
mama, kwani ni nani Yule?” “Ungekuja kumsalimia ningekutambulisha, ni
rafiki yangu wa siku nyingi sana. Nilikuwa nasoma nae. Ila una tabia mbaya,
umesubiri kaondoka ndio umetoka” “Hapana mama, nilikuwa na
usingizi” “Kwahiyo saivi umeisha?” “Angel ananisumbua
mama” “Mpe chakula, mtoto njaa huyo” Basi Erica akamuacha pale
mtoto na mama yake na yeye kwenda jikoni kumuandalia mwanae
chakula. Muda huo huo simu yake ilianza kuita, ila ilikuwa na mtetemeko
tu maana alitoa sauti ila muda huo simu ilikuwa kwenye kochi basi Angel akashuka
kwa bibi yake na kwenda kuichukua, bibi yake akaidaka ili kuangalia mpigaji,
akakuta ni Erick, akacheka na kumuita Erica aliyekuwa jikoni, “Haya
mpenzi wako anapiga simu maana hadi kaandikwa my love mmmh!! Wewe mtoto wewe
mapenzi yanaumiza sana, sijui hujawahi kuumia na mapenzi?” “Nimewahi
mama na nimeumia mara nyingi tu” “Ungekuwa umewahi usingethubutu
kuandika hata mpenzi, yani ungeweka jina lake tu bila vikorombwezo vingine, mtu
pekee wa kujidai nae na kumpa majina uyatakayo ni mume wako ila hawa
wasioeleweka utajiumiza moyo bure” “Jamani mama!” “Sio cha
jamani, pokea simu hiyo, ona ishakatika” Na kweli simu ilikatika muda
ule wakati Erica akiongea na mama yake, ila Erica alikaa chini na kuongea na
mama yake, “Mama, mapenzi ni nini? Sielewi yani sielewi kabisa, kichwa
changu kinavurugika kila kukicha” “Maliza kuandaa chakula cha mtoto,
mlishe kisha njoo ukae sasa uniulize nikuelekeze kidogo” Basi Erica
alienda kumalizia kuandaa chakula cha mtoto na alipomaliza alimlisha kama mama
yake alivyomwambia. Muda huu sasa alimfata mama yake kwani
alihitaji kujua mapenzi ni nini ikiwa kila anachofanya kinamuumiza tu katika
mapenzi, “Mama, nimemaliza sasa nahitaji kujua mapenzi ni
nini?” “Kwanza kwanini unataka kujua mapenzi ni nini? Tuanzie hapo ndio
nitaweza kukuelewesha kidogo” “Mama, mwanao nimekuwa nikipata changamoto
mbalimbali za mapenzi, nimekuwa nikikutana na watu mbalimbali wakidai
wananipenda ila kumbe si kweli walikuwa na lengo lao tu, yani mpaka
nachanganyikiwa hapa kuwa mapenzi haya ni kitu gani na kwanini mimi yananiumiza
hivi” “Mwanangu pole sana, ila mara nyingine ni kosa langu kutokukaa na
wewe na kukuelimisha kuhusu swala zima la mapenzi kwani sikufikiria kuwa
mwanangu umekuwa sasa, ila mwanangu mapenzi yamejaa unafki sana, kwanini nasema
hivi sababu mtu anaweza kukuonyesha anakupenda hadi unaweza hisi nikimuacha huyu
atakufa, kumbe kuna kitu anahitaji toka kwako ndiomana anaonyesha anakupenda,
haya yuko wapi baba Angel? Si ulisema alikuwa hadi anakutumia pesa? Ziko wapi
hizo pesa sasa? Angekuwa mwingine si ndio angekujali sana hivi una mtoto wake?
Yani mapenzi kila mtu anayatafsiri kwa namna yake ila yakikupitia ndio unajua
haswaa mapenzi ni nini, ndiomana nimekuuliza hujawahi kuumizwa na mapenzi? Kama
umewahi, unawezaje kumuamini mtu asiye mume wako? Ingawa hata kwenye swala la
ndoa kuna watu wanaingia kwenye ndoa sio sababu ya mapenzi ila kuna kitu
anahitaji, yani mapenzi ni swala pana kidogo” “Mama, jana nimetukanwa
sana mwanao na huyo unayemsema baba Angel, ndiomana nashindwa hata kuelewa
mapenzi ni nini. Huyu mwanaume aliniambia kuwa ananipenda kuliko msichana yeyote
humu ulimwenguni, ila jana alivyonitukana kama si yeye aliyesema maneno yale
kipindi kile” Mama yake alicheka kama anamcheka mwanae vile, kisha
akamwambia amuonyeshe alivyomwambia, kwavile Erica alishaamua kuwa mkweli kwa
mama yake hakuona kama ni tatizo kumuonyesha alichoandikiwa na Rahim, alienda
kuchukua ile simu yake na kufungua mtandao wa kijamii kisha kumuonyesha mama
yake zile jumbe ambazo Rahim alikuwa akimtumia jana, “Yani kaniita
malaya kweli!” “Hajakosea, wewe ni malaya ndio ndiomana ukamkubali
shetani kama yeye bila hata kujiuliza, kumbe ulikuwa ukiniongopea nasafiri
halafu unaenda kukutana na shetani kama hili! Watu wanagombana ila sio kufikia
hatua ya kutukanana na kuhisi mmoja hafai, Erica mwanangu nilikufundisha kama
naimba nyimbo, mwanangu jitunze hadi ndoa ila wapi ukaona natwanga maji kwenye
kinu, umeona asante ya mwanaume eeeh! Yani mwanaume anakupa na mbinu ya kutoroka
kwenu ila mwisho wa siku anakuona malaya kwa starehe yake mwenyewe, ila mwanangu
usijali wala usiumizwe na maneno ya huyu Rahim, mi ninachokuombea ni uolewe tu
mwanangu na huyu Rahim na familia yake yote tutawaalika kwenye harusi yako, wala
maneno yake yasikukatishe tamaa, yani kuna mijitu haina akili hata kidogo,
mwanamke kajitoa kubeba mimba kwaajili yako, kazaa kwa uchungu na analea mtoto
wako kwenye mazingira ya kusemwa kila siku kuwa kazaa nje ya ndoa halafu
unashindwa hata kufikiria mazingira anayopitia Yule mwanamke unafurahi tu
kumuita malaya! Nimechukia sana, simpendi huyo Rahim yani simpendi kabisa,
nimechukia sana. Acha tu mwanangu uendelee kujifariji kwa huyo Erick, natumaini
atakuwa wako kweli” Kwahiyo alijikuta na mama yake mada yako ya
kuelezana mapenzi ni nini imeishia hapo kusikitishwa na majibu ya Rahim tu,
maana hata mama yake Erica hakufikiria kama Erica angepata tabia za kuweza
kuitwa kwa jina baya vile, alimuangalia mwanae na kusema tena, “Unajua
nakuangalia Erica sikumalizi, hivi ni kweli ni wewe niliyekulea katika maadili
yote? Mtu anafikia kusema hakuna mwanaume atakayekuoa mwanamke kama wewe, kwaini
aseme hivyo? Najiuliza sana, hivi ulianzaje kutembea na familia nzima? Najiuliza
bado, ulianzaje kutembea na shetani kama Derick? Unajua ninavyokuangalia na haya
mambo yanayokuhusu hakika huendani nayo, hivi ilikuwaje Erica! Aaah kama
sikukulea mimi vile dah! Najaribu kukufikiria nakosa jibu, si utakuwa umemaliza
kijiji mwanangu wewe, na sijui kama huyo Mzee Jimmy hukutembea nae kweli! Wewe
uliweza hata kutembea na Yule Bahati kipindi kile anavua samaki hukuona hata
kinyaa mmmh! Ila mwanangu ni mchafu wewe loh! Bora nikalale mie, nisije kuongea
na mengine” Erica nae alijisikia vibaya sana, ilikuwa ni usiku tayari
alienda chumbani kwake. Alipofika chumbani kwake aliinama na
kutoa machozi kwa hakika alitamani siku zirudi nyuma na awe Erica mpya,
alijikuta akijuta sana kwa yale matendo yaliyopita nyuma, “Najuta
kumfahamu Babuu maana ndio kanifanya niyajue mapenzi, najuta kumfahamu pengine
nisingemfahamu ningeweza kujitunza hadi ndoa ila kwavile nilishaharibu sikuweza
tena kujitunza. Najuta mimi Erica, ila nimebadilika sema natazamwa kwa yale
matendo ya nyuma tu” Alijikuta akilia sana, simu yake iliita tena
alipoitazama ni Erick alikuwa akipiga tena, akapokea huku akiendelea kulia na
kumfanya Erick ajue pengine Erica analia kwa kitendo chake cha kulewa jana
yake, “Erica nisamehe mpenzi wangu, nilikwambia nitakuwa nakunywa
kistaarabu, naomba unisamehe Erica tafadhari, sitarudia tena” “Silii
hicho Erick ila nalia sababu mimi nimekuwa mwanamke asiyefaa” “Nani
kasema wewe ni mwanamke usiyefaa?” “Erick, wanawake wanaofaa wote
wanaolewa wakiwa bikra ila sio kama mimi” “Erica, hebu achana na hizo
desturi potofu, kwani ukiwa na bikra au usipokuwa nayo ndio nini katika maisha
eeeh! Tunachoangalia ni upendo, Erica kuna wasichana wengi wadogo wanatamani
kuwa na mimi, kuna wasichana wengi waliobikra na hawana watoto wanatamani kuwa
na mimi ila mimi siwataki nakutaka wewe, unajua kwanini? Sababu moyo wangu upo
kwako, wewe ndiye mwanamke wa maisha yangu, wewe ndiye nikupendaye kwahiyo hata
utokee mlolongo wa wasichana ujipange kwaajili yangu siwezi kuchagua yeyote
maana kwangu upo wewe tu. Erica usilie wala usiwe na mawazo, kuzaa nje ya ndoa
si kusema kwamba ni malaya, hapana, tena mimi naweza kukuita wewe ni mwanamke
shujaa maana najua ni vikwazo vingapi umekumbana navyo wakati wa mimba ya Angel,
Erica mama yangu usilie ila furahi kuwa na Angel na ufurahi kuwa na mimi, kwa
pamoja tutamlea Angel na kumuweka katika maadili yanayofaa” Kwakweli
maneno ya Erick yaliupa faraja moyo wa Erica kwani alijikuta akitabasamu tu na
kusema, “Erick nakupenda” “Hunifikii mimi malkia wangu,
nakupenda sana” Yani Erica kila akiongea na Erick alikuwa akijihisi raha
sana, basi akaagana nae na kuweza kulala, kwakweli alilala kwa tabasamu zito
sana, yani hata hakumuuliza Erick kuwa kwanini jana yake alilewa ila alilidhika
tu na kubembelezwa na Erick. Kulivyokucha, mama Erica alijua
kama kawaida kuwa angemkuta Erica amevimba macho kwa kulia kwa yale maneno
aliyomwambia jana ila alishangaa sana kuona Erica ameamka na tabasamu huku
akifanya kazi za hapa na pale, alimsalimia mwanae na kumuuliza, “Nipe
siri ya tabasamu lako” “Hamna mama, nimefurahi tu” “Mmmh Erica,
najua tu kipo kilichokufurahisha” Simu ya Erica ilikuwa mezani na
ikaanza kuita, mama yake akachungulia na kuona mpigaji ni Erick kisha akona
Erica akichukua simu na kwenda kupokelea chumbani huku akiwa amejawa na
tabasamu, kwakweli hapo ndio akaelewa furaha ya mwanae imekuwa
Erick, “Ila huyu Erick anagombewa na Sia, mmmh sijui itakuwaje? Ngoja
nitulie mie” Ilibidi tu aka echini akimsubiri huyo mwanae amalize
kuongea na simu, basi Erica nae alikuwa akiongea na simu, “Jana
nilisahau kukwambia Erica, kuna mzigo mpya umeingia, kwahiyo Jumamosi uwende na
Angel” “Mmmh umesahau kuniambia au ulitaka kuongea na mimi
tu!” “Nilisahau kukwambia kweli, kwani jana
nilikwambia?” “Hapana hujaniambia, ila si Moses yupo
angeniambia” “Erica bhana, ila kiukweli nilimiss tu kusikia sauti yako
kipenzi change, ngoja nifanye kazi zangu huku nahitaji tuishi maisha ya furaha
sana. Nakupenda Erica” “Nami nakupenda pia” Kisha akakata simu
na kwenda sebleni kwa mama yake ambaye alisema, “Nimesikia nakupenda
pia, hahaha penzi likiwa change unajihisi kama una miliki dunia” “Jamani
mama, usiseme hivyo. Niombee tu mwanao nifike mbali na Erick” “Unafikiri
sikuombei mwanangu, mafanikio yako ndio mafanikio yangu” Wakasikia mtu
akibisha hodi, ikabidi mama Erica ainuke kwenda kufungua kwani muda huo huo
Angel alikuwa akilia kwahiyo Erica alienda kumbeba mtoto wake, alipofungua
mlango alishangaa kumuona Sian a Tumaini, hakutaka kuongea nao vibaya mlangoni
kwahiyo aliwakaribisha ndani na kuanza kusikiliza kilichowaleta, baada ya salamu
Tumaini alianza kuongea, “Mama, samahani sana usione kama tunakusumbua
ila huyu wifi yangu kwasasa yupo kwenye hali mbaya sana, tafadhali mwambie Erica
amuache kidogo Erick aweze kuwasiliana na familia yake.” Sian aye
akaongea, “Mama, nipo chini ya miguu yako, Erick ndio kila kitu kwangu,
Erick ndio pumzi yangu, siwezi kitu mimi bila Erick nampenda sana, nisaidie mama
yangu, ongea na Erica ni mwanamke mwenzangu anielewe ninakopitia
mwenzie” Mama Erica baada ya kuwasilikiliza kwa makini akaanza kuwajibu,
muda huo Erica alipogundua ni wao alijibanza chumbani hakutaka kwenda sebleni
kuonana nao, Yule mama alianza kuwaeleza, “Nimewasikia yote, toka jana
nimewasikia ila kuna swali nataka nikuulize wewe Sia” “Niulize tu
mama” “Kati ya mama yako mzazi na huyo Erick nani ni muhimu
kwako?” “Mama jamani, mama yangu mzazi ameshakufa kwahiyo Erick ndio
amebaki katika maisha yangu kwasasa” “Tuchukulie mfano mama yako bado
yupo, je kati yake aliyeingia leba kukuleta wewe mtoto mpumbavu na huyo Erick
nani wa muhimu kwako?” “Sasa mbona unanitusi mama?” “Sikutusi
ila nakwambia ukweli, ungekuwa mjinga wewe ungeelimika ila wewe ni mpumbavu,
yani hujui umuhimu wa aliyeingia leba kupigana na maisha yake sababu yako, ila
unajua umuhimu wa mwanaume unayekutana nae kwaajili ya atarehe za kimwili tu.
Wewe mama yako kafariki juzi, jana hapo tumezika, leo kiguu na njia kuja
kugombania mwanaume, hivi una akili wewe? Ndio nyie wazazi wanawazaa kutoa
change tumboni tu maana ungebaki kwenye tumbo la mama yako basi ungemuua kwa
uvimbe” “Jamani mama” “Hakuna cha jamani hapa, wewe Sia huna
akili hata robo, unakuja kwangu kwa sura ya huruma sijui Erick ndio uhai wangu,
sijui ndio pumzi yangu, siwezi ishi bila yeye, Erick ni nani katika maisha yako?
Unakuja kunieleza mimi kuhusu Erick kukuchanganya ili nikusaidiaje? Unajua nyie
watoto wa siku hizi hamna akili kabisa, unaendekeza mapenzi, unaacha kumthamini
mama yako aliyehangaika na mimba yako miezi tisa, bado akaenda kuteseka leba kwa
uchungu na kukulea kwa shida, leo bila aibu unakuja kuniambia ujinga kuwa Erick
ndio wa muhimu kwako? Saivi ulitakiwa kutulia huko ukiomboleza kifo cha mama
yako, ukikumbuka mazuri ya mama yako na kuyaenzi ila wewe kiguu na njia kuja
kutafuta penzi, jana nimekustai tu pale nilijua utajirekebisha kumbe hamna kitu.
Haya nigeukia upande wako wewe Tumaini, huna mama
wewe?” “Ninae” “Huna mpenzi?” “Ninae” “Mpenzi
wako na mama yako nani muhimu zaidi?” “Mama ni muhimu
zaidi” “Sasa kama unatambua hilo kwanini unamfundisha ujinga huyu
mwenzio, ulitakiwa umwambie rafiki yangu, sijui wifi yangu, huu ni muda wa
kuomboleza kifo cha mama, mapenzi yapo tu jamani, nyie watoto wa siku hizi
mkoje? Mbona mnatupa simanzi wazazi wenu, naombeni muondoke sasa hivi, Sia rudi
katafakari mambo mema ya mama yako uyafate, ujinga ujinga
muache” Hawakuwa na neno la ziada zaidi ya kuaga na kuondoka zao, na
walivyoondoka tu Erica ndipo akatoka chumbani na kwenda kwa sebleni kwa mama
yake kwani hakuamini kama mama yake angewatimua hao watu. “Kheee mama
umewafundisha vizuri” “Ndio ujinga sitaki, hivi nyie watoto hamjui
uchungu ambao mama anapitia au? Hivi Angel huyo awe mkubwa halafu aseme
aliyekutana nae ukubwani ndio muhimu zaidi kushinda wewe, atakuwa anawaza kwa
kutumia nini jamani? Yani hawa nimewaangalia sana na ujinga wao toka
jana” Erica akacheka tu kwani alijua akiendelea kumwambia chochote kwa
muda huo mama yake basi mada itamgeukia yeye. Basi akaendelea na
shughuli zingine hadi muda wa kulala, na kuchukua simu yake kumpigia Erick,
alimuuliza pia swala la kazi ambayo alisema angemtafutia, “Vipi kuhusu
yule mtu wa kazi?” “Kuna jambo lingine nimelifikiria
Erica” “Jambo gani hilo?” “Nimewaza kuhusu kazi, nimeona
itakufanya ukose muda wa kuwa karibu na mtoto ila nilikuwa nafikiria namna ya
kukusaidia, unaweza kufanya biashara?” “Mmmh sijawahi, ila kila kitu ni
kujaribu, sidhani kama nitashindwa” “Sawa basi kesho utaniambia ni
biashara gani unafikiria kujaribu kuifanya” Kisha wakaongea mada mbali
mbali na kuagana. Kesho yake Erica alijifikiria sana, maana
mwanzo alifikiria kuhusu biashara ya vifaa vya watoto ila akajifikiria tena kuwa
mbona ndio biashara kwenye duka la Erick, akawaza tena na kukumbuka maneno ya
Rahim kuwa hakuna mwanaume anayeweza kumpa kiasi cha pesa alichowahi kuomba,
aliwaza hilo jambo, hakuwa na wazo la biashara yoyote ila akajisemea kuwa Erick
akimpigia atajaribu kumuomba hela hiyo asikie kuwa naye
atasemaje. Mchana wa siku hiyo Erick alipiga na kuongea nae vizuri sana
kisha akamuuliza, “Umeshafikiria biashara ya kufanya?” “Hapana,
ila nimefikiria mtaji wa kuanza nao” “Unataka kuanza na kiasi
gani?” “Ningependa nianze na milioni kumi na tano” “Biashara
gani hiyo Erica ya milioni kumi na tano?” Akafikiria na kuamua kujibu
kama wazo lake la mwanzo, “Nilifikiria kufanya biashara ya kama lile
duka lako la vitu vya watoto na nguo” “Mmmh mbona mtaji uliofikiria ni
mdogo sana?” “Nilikwambia lakini sina ujuzi vizuri wa
biashara” “Basi ngoja, kuna kitu nitafanya, tulia tu” “Mmmh nini
hiko Erick?” “Sikwambii ila hiyo siku utakijua, subiri tu ila nadhani
kuhusu kazi ungevumilia kidogo tuangalie na michakato mingine hii
inasemaje” “Sawa, nimekubali” Basi aliongea nae kwa tabasamu
zito sana, kisha kukata simu. Alipokata ile simu tu ikaingia simu
nyingine, kuangalia ni Tumaini alikuwa akipiga, Erica akapokea na kuongea
nae, “Erica unajua ulichosababisha kwa Sia?” “Nimesababisha nini
kwani?” “Huna huruma na msichana mwenzio, wewe binti hufai hata
kidogo” “Sikuelewi Tumaini” “Utanielewa tu,
subiri” Kwakweli Erica hakumuelewa Tumaini kuwa ana maana gani, muda huo
alimsikia mama yake akimkaribisha mgeni, akatoka na mwanae kwenda kumuona huyo
mgeni, alikuwa ni Yule mama ambaye mama yake alikuja nae kutoka msibani kwa mama
Sia, Erica akamsalimia huyu mama ila Yule mama alionekana kumshangaa sana mtoto
wa Erica, hadi mama Erica akamuuliza, “Vipi mbona umemshangaa
hivyo?” “Jamani, duniani wawili wawili yani huyu mtoto kafanana na
mjukuu wangu balaa” “Aaah! Mjukuu wako, baba yake ni
nani?” “Usingeniambia kuwa mwanao ana mchumba ningefikiria ndiyo Yule
mjinga kazaa nae pia” “Nani huyo?” “Mjinga mmoja hivi anaitwa
Rahim” Kwakweli mama Erick alishtuka kidogo na kutambua tabia ya
Rahim. Erica akamsalimia huyu mama ila Yule mama alionekana
kumshangaa sana mtoto wa Erica, hadi mama Erica akamuuliza, “Vipi mbona
umemshangaa hivyo?” “Jamani, duniani wawili wawili yani huyu mtoto
kafanana na mjukuu wangu balaa” “Aaah! Mjukuu wako, baba yake ni
nani?” “Usingeniambia kuwa mwanao ana mchumba ningefikiria ndiyo Yule
mjinga kazaa nae pia” “Nani huyo?” “Mjinga mmoja hivi anaitwa
Rahim” Kwakweli mama Erick alishtuka kidogo na kutambua tabia ya
Rahim. Mama Erica akauliza tena kwa makini, “Unasema
Rahim?” “Ndio mjinga mmoja hivi anaitwa Rahim, hebu fikiria mtoto
anatimiza miaka minne sasa, Yule Rahim hajawahi kufika nyumbani” “Kheee
pole mwenzangu” “Asante” “Ila wewe ushawahi
kumuona?” “Nimewahi ndio, kipindi hicho anamdanganya danganya mwanangu
na vihela vyake, kumbe Yule mjinga anapewaga hela na wanawake wengine, ila
tuachane na hizo habari, nimekuja kukuaga tu” “Karibu ukae basi, ndio
wima wima jamani!” Mama Erica alikuwa akiongea ila moyoni mwake alikuwa
anajisikia vibaya sana kutokana na kusikia habari za Rahim, basi Yule mama
akakaa kidogo na kufanya maongezi ya hapa na pale na mwenzie maana ni kipindi
kirefu ila hakuweza kuongea nae sana sababu alikuwa na haraka zake, basi muda
huo huo aliamua kuaga ila wakati anaaga gafla akapigiwa simu, na kuipokea ila
ilionekana kama hiyo simu imemchanganya kidogo, kwahiyo alivyokata ilibidi mama
Erica amuulize kuwa kulikoni, “Mwenzangu, eti mtoto wa marehemu
kalazwa” “Kalazwa? Anaumwa nini tena?” “Eti alitaka kujinyonga,
jamani huyu mtoto mbona anatutafutia makubwa sisi! Ngoja niende huko hospitali,
nishachanganyikiwa sasa hivi” Ilibidi mama Erica nae avae mara moja na
kuondoka na Yule mwenzie wakielekea hospitali. Erica alibaki
nyumbani na mwanae ila alijisikia vibaya sana kwani yale maongezi ya Yule mama
na mamake aliyasikia yote, akajiuliza sana kuwa au ndio ile simu aliyopigiwa na
Tumaini kuwa kuna kibaya kimetokea kwa Sia, “Yani Sia alitaka kujinyonga
sababu ya mapenzi kweli? Inamaana Sia anampenda zaidi Erick kuliko mimi
ninavyompenda? Hapana haiwezekani, mbona mimi nampenda sana Erick ila hata
nilipoachana nae sikuthubutu kujidhuru, siamini kama Sia anampenda Erick kuliko
mimi. Ila lawama naletewa mimi, kweli mimi nimsababishie kifo jamani? Mbona
naonewa sana?” Erica aliwaza sanahuku machozi yakimklenga lenga ila
alipokumbuka mambo ya Rahim, hakutaka kuwaza tena maana mambo ya Rahim
yalimchefua sana, yani kijana aliyekuwa akiifiwa na mama yake kuwa ni kijana
mtulivu kumbe ndio kijana mchafu hafai, ingawa siku ile alimtusi ila alijipanga
kuwa siku hiyo usiku amtafute hewani amsikie sera zake za kukimbia
watoto. Jioni alijifikiria akaona ni vyema awasiliane na Erick ili ajue
kama anajua kuwa Sia alitaka kujinyonga, basi akampigia simu Erick kama kawaida
Erica alivyoanza kuongea tu mwanae alimpora ile simu kwahiyo Erica alimuangalia
tu mwanae aongee na Erick, alipomaliza ndio alimpa mama yake, Erica alicheka na
kumuuliza Erick, “Hivi huwa unaongea nini na huyu mtoto hadi
anachanganyikiwa hivi?” “Mambo ya baba na mtoto yaache tu, wenyewe
tunajua tunachoongeaga, hivi hujui? Mtoto wa kike ni wa baba na wa kiume ni wa
mama kwahiyo huyu lazima anipende baba yake” “Yani wewe loh! Tuachane na
hizo habari, ila umesikia?” “Kusikia nini?” “Majanga
yaliyotokea?” “Yapi hayo?” “Nasikia Sia alitaka kujinyonga
eti” “Nani kakwambia?” “Tumaini alinipigia simu” “Kwanza
Erica, huyo dada yangu mblock kwenye simu yako wala usiwasiliane nae tena,
nadhani hana jema na penzi langu, Erica nakupenda, tafadhali usisikilize maneno
ya watu, ajinyonge sababu yangu ni mumewe mimi? Lini nimeoa labda ndio
kanifumania na kuchukua uamuzi mbaya, yani mtu kama huyo wala asikuchanganye
Erica wangu akili, achana nao kabisa. Mimi nakupenda wewe yani hadi dunia nzima
iwe kinyume na mapenzi yangu kwako bado nitasimama na kusema nakupenda wewe,
kwanini Erica unashindwa kusimama kwaajili ya penzi langu? Huyo dada yangu labda
akikutafuta na namba nyingine mwambie malalamiko aniletee mimi maana mimi ndiyo
nimependa ila wasisumbue akili yako kabisa” “Ama kweli Erick unanipenda
sana, hadi najihisi raha” “Erica, wewe nenepa tu upo na mimi. Yani
katika akili yako tambua kwamba hakuna mwanaume anayekupenda kama anavyokupenda
Erick” “Asante sana nami nakupenda” Kiukweli Erica alipata
ahueni ya moyo kwani hakutegemea kama Erick angempa moyo kiasi kile, ila
alifurahi sana kuzungumza na Erick. Hadi muda wa kulala ulifika
ila mama Erica alikuwa hajarudi kiasi kwamba Erica alikuwa na mashaka na
kusinzia sebleni akimsubiri mama yake, muda kidogo alirudi ila alionekana
kuchoka sana kiasi kwamba hakutaka kuhojiana maswali na kwenda kuoga, kula na
kulala. Erica nae aliamua kwenda chumbani kwake, ila muda huu usingizi ulikata
maana alikumbuka ahadi yake ya kuingia kwenye mtandao ili amseme Rahim, na kweli
alipoingia tu alimkuta Rahim yupo hewani kama kawaida, akamsalimia na
kumuuliza, “Hivi wewe Rahim, watoto wangapi
umetelekeza?” “Niondolee balaa mimi huwa sitelekezi
mtoto” “Unajua wewe mamako anakuona msafi sana, kumbe ni mchafu mchafu
hufai, sikukujua vizuri, nasema tena sikukujua vizuri, kumbe kutelekeza watoto
ndio kawaida yako loh! Mwanaume hufai wewe” “Erica, usitake niongee
maneno machafu, sasa wewe unafaa kwa lipi? Umetembea na familia yangu nzima,
ndio unafaa wewe? Kumbe umetembea hadi na kaka yako, ndio unafaa wewe? Ushatoa
mimba ya Derick, ndio unafaa wewe? Hapo ya Derick tu ndio tunaifahamu, ila
nahisi ushatoa mimba zaidi ya kumi hata huyo mtoto umezaa kwa kuhurumiwa tu,
Erica nikija kumchukua huyo mwanangu itabidi nikapime DNA” Yani Erica
ingawa ni yeye alianzisha mada ili amseme Rahim ila ilimshinda maana hakuweza
kuendelea kuongea nae ukizingatia kila alichosemwa na Rahim kilimshika vilivyo,
alijihisi vibaya sana moyoni mwake, alijikuta tu akimuandikia, “Usiku
mwema” “Unalala? Kweli siku hizi huna soko Erica, hivi wapo
wanaobabaishwa na wewe tena kweli? Nakwambia hata ndotoni huwezi kuwa mke wangu
Erica, maana nitakuwa naoa uchafu tu, mwanamke umepitiwa na kila aina ya
mwanaume, hapana kwakweli” Erica akazima mtandao na kuamua kulala tu
kwani alijihisi maumivu haswa kwenye moyo wake, kuna muda alitamani kuyachukia
mapenzi ila alipofikiria kuhusu Erick alitabasamu tu na kuamua kuendelea
kuyapenda mapenzi. Kulivyokucha Erica aliamka na kufanya
shughuli zake za hapa na pale ila muda kidogo mama yake alimuita na kuanza
kuongea nae, “Erica, sikuwahi kuwaza kuwa kuna watu wanasumbuliwa na
mapenzi kiasi hiki, Sia ametaka hata kujiua sababu ya Erick! Tena unaambiwa mama
Erick ndio aliyemuokoa, ila hatukumkuta hospital alishaondoka, Erica mwanangu
kama mzazi nimejihisi vibaya sana. Ngoja nikuulize kitu” “Niulize
mama” “Ni kiasi gani unampenda Erick?” “Nampenda Erick mama,
sijui ni kiasi gani ila nampenda sana” “Kwanini
unampenda?” “Sina sababu mama ila nampenda tu yani Erick amekaa kwenye
moyo wangu mama” “Na je huyo Erick anakupenda kama wewe
unavyompenda?” “Ndio mama Erick ananipenda sana” “Ila mwanangu
Erica mapenzi unayajua vizuri kweli? Wanaume wanabadilika kama kinyonga, hata
Sia aliamini kuwa Erick anampenda sana na hawezi kumuacha mwisho wa siku
kamuacha, Erica mimi ni mama yako na ndio naujua uchungu wako, mimi ndiye
nikupendaye kwa dhati mwanangu. Unanielewa Erica?” “Nakuelewa
mama” “Naomba uachane na Erick” “Hapana mama,nampenda sana
Erick” “Kumbuka kuna mtu alijaribu kujiua sababu ya Erick, je moyo wako
utakuwa na amani iwapo Sia akifa?” “Hapana mama, ila je wewe utakuwa na
amani iwapo mimi nikifa?” “Kwanini unasema hivyo sasa?” “Mama,
mkiniachanisha na Erick basi sina sababu ya kuishi pia” “Wewe mtoto ni
punguani sana, hebu nitokee mbele ya macho yangu hapa tafadhali. Erick, Erick ni
nani kwenye nyumba yangu? Aah watoto wa siku hizi, tuzaa basi tu” Erica
aliondoka na kwenda kuendelea na shughuli zingine ila alishukuru vile
alivyomwambia mama yake ukweli kuwa hawezi kuachana na Erick. Jioni ya
siku hiyo kuna simu ilimpigia Erica, alipoiangalia kwa makini akaona ni namba ya
mzee Jimmy, hakutaka kupokea ila aliipokea tu, “Erica, hupendi kuishi
kwenye nyumba ya kifahari nay a kisasa?” “Unazungumzia nini
kwani?” “Aaah nilikuwa nakusalimia tu, binti chaurembo” “Haya
asante, kwaheri” Erica akakata simu kwani hakutaka kutumia muda wake
mwingi kuongea na Mzee Jimmy wakati hamtaki. Siku moja jioni,
wakati Erica akifanya shughuli zake, alishangaa kupata ugeni na mgeni huyo
alikuwa ni Dora, ila Erica alimkaribisha tu sababu hakuwa na ugomvi nae kwa
kipindi hiko, kwao alimkaribisha ila mialiko ya Dora hakuitaka. Dora
alianza kuzungumza na Erica, “Erica nimeamua kuja kukwambia jambo hili
sio unicheke au unione kuwa sina akili hapana, nimekuja kukwambia tu ili na wewe
ujilinde” “Jambo gani hilo Dora, siwezi kukucheka” “Erica
nimetangatanga sana, yani mimi nadhani nimetembea na wanaume wa kila rangi ila
siku zote nilikuwa naenda kupima na kujikuta niko mzima tu, kiasi kwamba
nilihisi ukimwi haupo duniani, niliona watu wanaosema tuna ukimwi hajajifikiria
vizuri, ila kipindi hiki yamenitokea puani, huwezi amini, nimeenda kupima wiki
iliyopita nimekutwa nimeathirika, Erica Yule mzee jimmy
ameathirika” Kiukweli Dora alikuwa akiongea kama mtu anayejutia sana na
alitia huruma, hata Erica akamuonea huruma sana, Dora aliendelea
kuongea, “Erica, Yule mzee si mtu mzuri, anaambukiza mabinti wengi sana,
Yule mtu mzima kumbe ana lengo lake la kuua vijana, hadi huwa najuta vile
nilivyokuwa nakulazimisha utembee na Yule babu, Erica nisamehe rafiki
yangu” “Usijali nishakusamehe” “Jambo lingine Erica, tena ngoja
nikwambie kabla sijasahau” “Jambo gani hilo?” “Kama una mpenzi
Erica, usitaje jina la mpenzi wako kwa huyu mzee, yani alichomfanya mpenzi wangu
dah!” “Kamfanyeje?” “Nitakwambia tu siku moja ila kwa leo
yanatosha hayo niliyokwambia” “Mmmh Dora ungeniambi kidogo” Dora
aliamua kubadilisha mada kwani hakutaka kujadili kile ambacho mpenzi wake
alifanywa na mzee Jimmy. “Ila uwe unakuja kunitembele, mwenzio sina raha
kabisa kabisa Erica” “Sawa usijali, pole sana” Kisha Dora
hakukaa sana aliondoka zake, kwakweli Erica alitafakari sana na akatafakari kama
ingetokea siku hiyo Yule mzee angembaka ingekuwaje, “Kwakweli Mungu
alinisaidia sana jamani, Mungu nilinde hadi niolewe na Erick” Alikuwa
akijisemea tu, giza lilipoingia alienda chumbani kwake na kusikia simu inaita,
kuangalia ni namba ngeni, akapokea na kukuta ni mzee Jimmy, Yule mzee baada ya
salamu tu akaanza kumwambia Erica, “Usisikilize maneno ya Dora, Yule
binti ni mjinga sana sijapata kuona” “Mbona
sikuelewi?” “Kaniambia kuwa anakuja kukwamabia kwamba mimi nimeathirika,
Yule binti ni mpumbavu na wivu tu unamsumbua, kisa kaona kuna nyumba nzuri
nimenunua na nimesema nataka nikupe wewe zawadi kwenye siku yako ya kuzaliwa
basi yeye kasikia wivu akaniambia ooh siku zote unakuwa na mimi halafu ukampe
zawadi Erica kweli? Akasema anakuja kukwambia kuwa mimi nina ukimwi ili
unichukie ila si kweli Erica” “Iwe kweli au si kweli, bado sina mpango
na wewe nampenda sana mpenzi wangu” “Anaitwa nani huyo mpenzi
wako?” Erica akakumbuka maneno ya Dora kuwa huyu mzee hata akikuuliza
jina la mpenzi wako usimwambia sababu ana hela, anaweza akamfanyia jambo lolote
baya, basi Erica akamwambia, “Hapana, sikwambii na sio muhimu wewe
kumfahamu” “Ila Erica, kumbuka nakupenda sana hata ukisema vipi ila
upendo wangu kwako uko pale pale” Erica aliamua kukata simu tu kwani
alihisi ni kizunguzungu. Muda kidogo aliitwa na mama yake maana na siku
hiyo alitoka pia, Erica alienda kuongea na mama yake, “Nilienda tena
kumuona Sia, mwanangu Sia anatia huruma sana, ila kuna kitu sielewi
kabisa” “Kitu gani mama?” “Yule binti ni mjinga sana, hivi
kupendaje huko hadi utake kudhuru maisha yako sababu ya mwanaume loh! Watoto
wetu mmepotea kwakweli, ila ngoja nikuulize tena na wewe” “Niulize
mama” “Utawezaje kuishi na mwanaume ambaye ndugu zake wote
hawakutaki?” “Mama, ngoja niseme mambo ambayo huwa yananitokea, sijawahi
kupata mwanaume yoyote ambaye ndugu zake wakanipenda, je sitaolewa? Nashukuru
Mungu ingawa ndugu wa Erick hawanitaki ila Erick ananipenda” “Ushawahi
kujiuliza kwanini ndugu huwa hawakutaki?” “Huwa sielewi mama ila hakuna
ndugu wa mwanaume amewahi kunipenda mimi, anaweza kunipenda ila akisikia tu nina
mahusiano na ndugu yake basi upendo wake unaishia hapo” “Je mama yake
Erick umewahi kuonana nae?” “Ndio nimewahi mama, yani Yule mama alikuwa
akinipenda sana mwanzoni ndio kazini kwake nilikuwa nafanya kazi ila gafla Yule
mama aliposikia kuwa nina mahusiano na mtoto wake akanichukia tena kanichukia
haswaa bila hata sababu, je wewe umeonana nae?” “Hapana sijaonana nae
ila kwa inavyoonyesha Yule mama hakutaki kabisa kutokana na maelezo niliyopata
kwa Tumaini, tena anasema kuwa umemroga mtoto wake. Ila Erica ningekuwa mimi ni
wewe nisingeendelea na huyo mtu” “Mama samahani kwa hili
nitakalokuuliza, umewahi kusema hata uliiba ng’ombe kwenu ili uolewe na baba, si
inamaana ulimpenda sana kiasi kwamba hukujali lolote lile, mbona mimi
unanikataza kumpenda Erick mama? Nampenda sana Erick, labda aniache yeye ila
mimi sina mpango wa kumuacha” “Kweli hapa mtoto sina jamani, haya
nimechoka hayo maneno yako ya nampenda nampenda nampenda, mwambie aje hapa
nyumbani na tufanye harusi, maswala ya kupendana siyataki” “Atakuja
mwezi ujao” “Ndio alivyokudanganya hivyo! Haya bhana, nenda kalale tu
maana kila nikiongea nawe nachefuka” Basi Erica aliondoka ila alikuwa na
imani kuwa ipo siku Erick atamuoa, kipindi hiko aliamua kujitoa kwa hali zote
kuwa amsubirie Erick tu bila kujali kama Erick akibadilisha maamuzi atamuumiza
kwa kiasi gani, kichwani mwake aliona bora amuwaze Erick tu. Aliingia
chumbani kwake na kujisemea, “Kwa kipindi hiki nitakomaa na Erick hadi
kieleweke, hata akiniacha najua na Mungu naye atanipigania ila siwezi
kutangatanga tena na mapenzi, imetosha kuitwa majina ya ajabu, nimekuwa Erica
mpya. Dunia haina usawa kabisa hii, mtu anakutongoza na kukuonyesha dalili zote
za kukupenda, unaamua kumkubali na kuwa naye, unamuheshimu na kumpenda, eti
kesho na keshokutwa anakuita malaya kweli? Malaya sababu ulimpenda, malaya
sababu ulijitoa kwaajili yake? Rahim nimemvumilia, nilikuwa naumia ila nakazana
kwani niliamini ndiye mume wangu, ila leo ananiita malaya kweli? Ananiita
mwanamke nisiyefaa kwenye jamii sababu nilitunza mimba aliyonipa na kuzaa?
Wanaume hawa, ila nampenda Erick hata iweje nampenda Erick” Aliwaza sana
na kutaka kulala, ila kabla hajalala akapigiwa simu na Erick na kutabasamu
vilivyo, alipopokea simu ya Erick akamsalimia, “Mambo
Erick” “Mmmh unatakiwa uanze kujifunza sasa Erica” “Kujifunza
nini?” “Uwe unaniambia uhali gani mume wangu, unajua mimi ndio mumeo
eeh!” Erica akatabasamu tu yani kiukweli alikuwa akisikia raha sana
kuongea na erick. “Kuna kitu nataka kukuuliza Erica” “Niulize
tu” “Hivi umezaliwa tarehe ngapi na mwezi gani? Nataka kujua siku yako
ya kuzaliwa” Erica akatabasamu na kumjibu Erick maana kipindi chote
amekuwa akiwasiliana na Erick ila hawajawahi kuulizana kuhusu tarehe zao za
kuzaliwa, leo ilikuwa ni mara ya kwanza yani Erica alihisi labda kuna kitu Erick
anataka kufanya kwaajili ya siku yake ya kuzaliwa, alimjibu kwa bashasha kubwa
sana, “Nimezaliwa tarehe nne mwezi wa nne” “Kheee Erica, hapana
kwakweli” “Hapana nini?” “Unajua na mimi nimezaliwa tarehe
ngapi?” “Ni ngapi ndio” “Tarehe nne mwezi wa nne yani tarehe
hiyo hiyo na mwezi huo huo uliozaliwa wewe, kwakweli tunahaki ya kupendana
Erica, sisi ni wa tofauti ujue” Erica alitabasamu tu ila kiukweli
hakupendezewa kuwa na tarehe moja ya kuzaliwa na Erick maana alianza kuhisi vitu
vingi sana. Ila aliongea tu kama kawaida na kuagana na Erick. Alipokuwa
analala akajiwa na wazo, “Mungu wangu isije kuwa Erick nae ni ndugu
yangu, kwanza nafanana nae majina, halafu nimezaliwa nae tarehe moja mmh! Jamani
nina mashaka na hivi watu wanaibaga watoto uwiii, naomba asiwe na undugu na mimi
jamani nampenda sana” Alisubiri pakikucha amuulize kwa mitego mama
yake. Palivyokucha, alifanya shughuli zake na alipomaliza
alitaka kuongea na mama yake ila hakuwepo kumbe alidamkia tena hospitali
kumuangalia Sia, kwenye mida ya mchana mchana ndio akarudi ndipo Erica aliongea
na mama yake, “Hivi mama hujawahi kuzaa mapacha wewe?” “Mmmh
sijawahi, hata kwetu hakuna historia ya pacha. Kwanini umeuliza
hivyo?” “Napenda sana mapacha, natamani siku moja nizae
mapacha” “Ili uwaite Erick na Erica sio, maana umeona mwanaume mnafanana
kidogo majina basi ndio umekufa umeoza” Erica akacheka tu na kumuuliza
tena mama yake, “Hujawahi kuzaa mtoto mwingine wa kiume zaidi ya kaka
Tony?” “Kwakweli Tony, ndio mwanangu pekee wa kiume. Nilipokuwa na mimba
yako nilijua labda atakuwa wa kiume ila wapi, nikajifungua wa kike ila
nawakubali watoto wangu ambao Mungu amenipa” “Mama hujawahi kuwaza kuwa
pengine mimi niibadilishwa hospitali!” “Nibadilishiwe kwa lipi? Wewe ni
change langu na nimekukubali, mimi nimezaa kawaida kabisa, na mtoto nimempokea
mwenyewe, nabadilishiwaje sasa, halafu wewe badala uniulize habari za hospitali
unakazana kuniuliza maswali ya kijinga” “Jamani mama” “Sio,
jamani mama badala uulize Sia anaendeleaje wala hujishughulishi kujua wala
nini?” “Nilisahau mama, anaendeleaje?” “Mpaka nikuseme loh! Roho
mbaya hiyo, Sia anaendelea vizuri ila nashangaa kwakweli huwa wanasema mama
Erick anampenda sana Yule binti ila tangia nianze kwenda hospitali sijawahi
kukutana na huyo mama Erick hata kidogo, ndio upendo ule hapana. Sasa mwanangu
ile sio familia kama mtu wanatempenda ndio wanamfanyia hivyo, je wewe
wasiyekupenda itakuwaje, tafakari chukua hatua mapema, sina mengi ya kusema ila
kuwa makini” Erica alimsikiliza mama yake ila kwa muda huo alishakata
shauri la kumpenda tu Erick hata iweje. Jioni ya siku hiyo Erica
alipigiwa simu na Dora, akapokea na kuanza kuongea nae, “Erica sina nia
mbaya na wala si wivu unaofanya nikwambie haya, Yule mzee kanunua nyumba ya
kukupa wewe ila kuna siri nzito sana katika hiyo nyumba” “Ila Dora si
nilikwambia kuwa simtaki huyo mzee wala chochote chake, au hukunielewa jamani!
Huyo mzee hata anipe dunia simtaki” “Erica, Yule mzee ana akili sana
usifikiri hajui kuwa utaikataa ila mpango alioweka kwako ni kabambe, utajikuta
ukikubali mwenyewe” “Kheee Dora ushindwe na ulegee” “Yani wewe
badala ya kusema ni nini eti unasema nishindwe, nilitaka nikusaidie ila sababu
hutaki kusaidiwa basi kwaheri” Dora akakata ile simu ila Erica alibaki
na maswali mengi sana, sema aliamua kupotezea kwani hakuhisi kuwa kuna lolote
baya juu yake ukizingatia Yule mzee hakumtaka. Basi wkati wa kulala
aliamua kumpigia simu Erick ili kuongea nae tu kwani baada ya kuwa na uhakika si
ndugu yake alijikuta akiwa na upendo nae maradufu, “Eeeh Erick kwanini
jana uliuliza kuhusu tarehe yangu ya kuzaliwa?” “Subiri uone kuna kitu
nitafanya siku hiyo, na hivi ni tarehe moja na yangu nataka iwe siku ya
kumbukumbu kwenye maisha yetu:” “Kitu gani hiko?” “Hapana
sikwambii Erica ila ni kitu cha kukushtukiza tu” Erica alimbembeleza
sana amwambie ila hakumwambia, kwahiyo alibaki tu kungoja kuwa ni kitu gani
kitatokea siku hiyo, aliagana nae na kulala. Ilikuwa siku ya
Erica kumpeleka mwanae kliniki, kwahiyo alijiandaa kisha akampeleka mtoto wake
kliniki, wakati anatoka akakutana na mwanamke akiwa na mimba kubwa tu
ameongozana na mumewe, basi akajikuta akigongana macho na Yule mwanaume,
akashangaa sana kuona kuwa yule mwanaume ni Bahati ila kile kitendo cha Erica
kugongana macho na Bahati kilikuwa kama kimewehusha akili ya Bahati, kwani
alionekana kama mtu aliyeshtuka toka usingizini na
kusema, “Erica” Ilikuwa siku ya Erica
kumpeleka mwanae kliniki, kwahiyo alijiandaa kisha akampeleka mtoto wake
kliniki, wakati anatoka akakutana na mwanamke akiwa na mimba kubwa tu
ameongozana na mumewe, basi akajikuta akigongana macho na Yule mwanaume,
akashangaa sana kuona kuwa yule mwanaume ni Bahati ila kile kitendo cha Erica
kugongana macho na Bahati kilikuwa kama kimewehusha akili ya Bahati, kwani
alionekana kama mtu aliyeshtuka toka usingizini na
kusema, “Erica” Erica alimuangalia tu bila kusema chochote, ila
Bahati alimsogelea Erica na kumshika yani kama mtu anayechunguza jambo Fulani,
kisha akasema “Erica, kumbe ni wewe” Akamkumbatia, mkewe alikuwa
pembeni tu akimuangalia ila alikuwa amechukizwa sana, na Erica aliweza kuiona
chuki ya Yule msichana, ikabidi ajigeleshe na kumwambia Bahati, “Wewe
Bahati kwani vipi?” Ile sauti ya Erica ni kama iliongezea kumshtua
Bahati kiasi kwamba Bahati akumbuke hadi Yule mtoto wa Erica aliahidi kuwa
atakuwa wa kwake, “Erica, mwanetu hajambo? Nipe Angel
nimbebe” Mke wa Bahati akasogea karibu na kuingia kati yale maongezi ya
Bahati na Erica, akamwambia Bahati, “Mme wangu tumekuja kliniki au
umekuja kuongea na wanawake zako jamani?’ Bahati aliongea kitu cha
kumjibu Yule mkewe hadi Erica alishangaa kwakweli, “Hivi mimi nimekuoaje
wewe Nasma, naanzaje kukuoa wewe na kumuacha Erica? Sikutambui” Erica
akaona kutakuwa na mgogoro hapo kwahiyo akaamua kuondoka ila Bahati alimuacha
mke wake pale na kumfatilia Erica hadi nje ya ile hospitali, Erica alitaka
kupanda bajaji ila akamzuia na kusema, “Kwanini upande Bajaji wakati
mimi nipo nina gari?” “Bahati, nenda kwa mkeo kule
anakusubiri” Erica akasimamisha bajaji na kupanda kisha akaondoka na
kumuacha Bahati akiwa ameduwaa pale. Bahati alionekana kama
kuchanganyikiwa hivi kwani alikuwa hata haelewi imekuwaje amuoe Nasma wakati
anayempenda ni Erica? Akaamua kwenda kwenye gari yake ili aende kwakina Erica
maana alikuwa anakufahamu ila hajaelewa tu imekuwaje mpaka kipindi chote hiko
hajawahi kwenda kwakina Erica. Wakati Erica yupo kwenye bajaji,
Moses alimpigia simu na kumwambia kuwa afike dukani mara moja, kwahiyo Erica
alimuelekeza Yule wa bajaji ampeleke dukani ili aonane na Moses ajue anamuitia
nini. Alipofika alimkuta Moses akimsubiria nje, Erica alishuka na
mwanae, Moses akamsalimia na kumuuliza, “Imekuwaje upande
bajaji?” “Hahaha, tunapanda kile ambacho tunaweza
kugharamia” “Erick anajua hilo?” “Kwanini umeniuliza
hivyo?” “Nimeuliza tu, karibu” Basi Erica aliongozana na Moses
hadi kwenye ofisi ya duka, kisha alianza kumsikiliza kuwa ni kitu gani
alichomuitia, “Kuna faili unatakiwa usaini” “Linahusu
nini?” “Kwani Erick hajakueleza?” “Hapana, hajaniambia
chochote” “Kuna event ipo tarehe nne mwezi wan ne, unatakiwa usaini ili
niipeleke kwa wahusika” “Wahusika ndio wakina nani hao?” “Wewe
isaini halafu muulize hayo maswali Erick atakujibu” Basi Erica alichukua
kweli na kusoma, akaona muhusika wa hilo jambo ni yeye na Erick, hakuelewa ni
jambo gani sema sababu alimuamini Erick aliamua kusaini bila mashaka yoyote,
kisha akataka kuondoka ila Moses alimwambia kabla hajaondoka anataka ampeleke
kwenye duka lingine la Erick, kwakweli Erica alishangaa kidogo na kukubali,
kisha walitoka pale na Moses na kupanda gari ya Moses wakielekea
huko. ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment