Search This Blog

Tuesday, 1 November 2022

UMENIFUNGULIA DUNIA - 5

 







    Simulizi : Umenifungulia Dunia

    Sehemu Ya Tano (5)





    Jumamosi asubuhi japo ni mwisho wa wiki, lakini katikati ya Jiji la Mwanza watu walikuwa wakiendelea kuhangaika kule na huku kila mmoja akifanya yake. Mgasi tayari alikuwa amewasiliana na Mwinyi

    na kumwambia kuwa wazazi wa Anisa walimfuata asubuhi sana ya

    siku hiyo.

    Walikua wakitaka kujua ni wapi alipo Mwinyi, tena leo wamekuja kiupole hasa, nimeongea nao

    “Nimewaambia upo Dodoma, wakaniomba niwaambie ukweli, maana Anisa ameonekana Mwanza, sasa kama upo nae wanasema wamekusamehe, rudi myaongee ama muachie Anisa arudi, hawatomuadhibu. Nikawauliza sasa mtakuwa mmemsamehe kwa kosa gani?

    Wakatazamana na kujibu mama Anisa kuwa Wewe unajua ulicho wakosea, hivyo mimi nikajua hawa ni wasanii, nikawaambia kwamba wewe suala la kurejea kwa kipindi hiki ni gumu sana, maana unatarajia kusonga mbele zaidi hadi Arusha, nilishikilia msimamo wangu huohuo, ama nimekosea?”

    “Safi sana, msimamo wako ndio msimamo wangu kaka, wewe ndio nahodha, liongoze jahazi hii lisizame.., hawajakwambia ni nani kamuona Anisa huku Mwanza?”

    “Hapana hawajaniambia, mpo wapi kwa sasa?”

    “Tunatoka hotelini kwenda Pasiasi kuangalia nyumba kisha tutaelekea salon na kurejea hotelini,”

    “Sawa kuweni makini sana, mchunge sana Anisa, huenda kuna watu wanaomfahamu wanamfuatilia kila wakati na kutoa habari huku,epukeni kutembea umbali mrefu kwa miguu, wala msitumie sana daladala na mjiepushe kuwa pamoja kwenye makundi, sawa kamanda?”

    “Nimekusioma mkuu, umekuwa ni kila kitu kwangu, shikamoo Mzee!”

    “Acha utani wewe, tayari umejisahau kama una matatizo eenh? Kama vipi baadae dogo,”

    “Powwa” Mwinyi akamuhadithia Anisa juu ya yale aliyoongea na Mgasi wakaanza kufikiria na kujiuliza, ni nani aiewajuisha juu ya uwepo wa Anisa Mwanza? Iikuwa ni swali lenye jibu jepesi tu..Firdos! na hapohapo ndio waiposhikilia.

    Wazo liilofuatia ni kuhama hotel ile haraka iwezekanavyo, walikuwa na uhakika kuwa ni lazima wazai wake watafika pale iwapo tu kama Fardos ndie aliesema kuwa wapo kule. Wakatoka na mizigo yao

    wakiacha mshangao kwa muhudumu.

    Wakaondoka hadi Salma Cone wakitumia gari ya Sammer, wakafika pale na kufungua kinywa kisha wakaendelea kutafuta hotel nyingine kwa ajili ya malazi. Walipata na kuilipia kwa siku 1 tu kwani hivyo ndivyo walivyoamua safari hii.

    Saa 6 mchana wakaingia Salon moja iliokuwa na salon pacha, Mwinyi akaingia sehemu ya Wanaume na Anisa akaingia sehemu ya wanawake.wakati Anisa akiingia akamuona Bi harusi mmoja akitoka, akasikia akimuita jina lake.

    Aliitika japo hakuwa amemtambua lakini ile sauti aliitambua japo pia muitaji hakumkumbuka. Alipomuuliza yeye ni nani, akajibiwa kwa sauti ya kejeli kwa kuuliza

    “Mwinyi hajambo?” Anisa alishtuka lakini akajikaza

    “Simtambui, wewe ni nani?” safari hii bibi harusi Yule hakujibu, bali alifanya ishara ya kumuita mmoja wa wapambe wake na kumueleza kitu Fulani sikioni.

    Anisa akiwa bado kasimama haelewi kinachoendelea, mpambe akafungua mkoba na kutoa bahasha nyeupe na kalamu, kisha akamkabidhi bibi harusi. Akatoa kadi na kuiandika andika kisha akairejesha na kumpa Anisa kwa nyodo.

    Alikataa kuipokea Anisa, hadi pale Bibi harusi Yule alipomwambia

    “Chukua Anisa, utampa Mwinyi, nae atakwambia mimi ni nani, siku njema!” wakatoka wakimuacha Anisa kapigwa na butwaa, wakaingia kwenye magari yao kadhaa na msafara wake ukaondoka Anisa akiushuhudia.

    *** Looh!!





    Nae akafungua pochi yake na kudumbukiza bahasha na kuendeea na ile liliompeleka pale, alipomaliza na kutoka, aliwakuta Mwinyi na Sammer wameketi garini wakimsubiri. Walimsifu kuwa amependeza sana, aliwashukuru na msafara ukaanza kuelekea wanapo pajua wao.

    Safari ilikuwa ikielekea Tunza beach kwa ushauri wa Sammer ambae alikuwa amekaa nyuma kwenye gari ile na mbele walikuwa wamekaa wapendanao, kushoto Mwinyi na usukani ulishikwa na Anisa ambae alikuwa akiendesha kwa kufuata maelekezo toka kwa Sammer hadi huko TUNZA beach.

    Jioni kabisa wakiwa wamekaa ufukweni, wanapata vinywaji, ndio

    akashtuka na kutoa bahasha ndani ya mkoba wake na kumpa Mwinyi, alishangaa huku akipokea

    “Mh! Ya nani hii?” aliuliza Mwinyi sasa akiwa ameishika akiigeuza geuza.

    “Ya kwako hiyo,” nae Anisa akamjibu huku akitabasamu.

    “Imetoka wapi? Ama ni bomu nini?”

    “We si nimekwambia kuwa ni ya kwako? Fungua usome utajua ilipotoka,”

    “Mi mwenzio naiogopa kweli, inaweza kuwa ni talaka,”

    “Na haswa” alitania Anisa huku akimuegamia begani

    “Ah basi mi sisomi, chukua mwenyewe,”

    “Nakutania wewe, fungua tuione bwana,” Mwinyi akaifungua na kukuta ni kadi ya mwaliko wa harusi.

    Alipojaribu kuyasoma majina ya wahusika, wala hakuweza kuyatambua, akamgeukia Anisa na kumuuliza ni wapi alipoitoa kadi ile?

    “Majina yetu yameandikwa vizuri sana, lakini majina ya wahusika wa ndoa yenyewe mbona siwafahamu? Ama ni ndugu zako?”

    “Aka! Mi nimepewa na mtu nisiemfahamu,” hapo akawahadithia tangu alivyokutana nae

    “Ah mtego huo, mbona hawa watajwa hapa mie siwajui?” Sammer akaichukua na kuyasoma majina kwa sauti, yakiwa yameandikwa Glory na Victor kisha akamalizia

    “Kama hamuwatambui, achaneni nao,” alimaizia na kumpa Mwinyi kadi ile.

    Wakati akiwa anairudisha kadi ndani ya bahasha, akaona maandishi nyuma ya kadi, maandishi ambayo Anisa hakuwa ameyaona, yaisomeka ‘Sipendi nikuone kwenye harusi yangu, ila usikose kwenye sherehe yangu’ sasa aihisi huyu mtu anamjua vizuri sana

    Kichwa kikaanza kumuuma, alikuwa akijiuliza huyu ni nani? Maana hata mwandiko hakuutambua pia. Anisa nae akaichukua na kuusoma ujumbe ule, aliishia kuguna tu, hakuambulia chochote, wakaamua wasiende kwenye sherehe hiyo walio alikwa.

    Sammer aifanikiwa kuwashawishi na kukubali kwenda kwa ahadi

    kuwa wachelewe kidogo ii wakute watu wengi wakiwa tayari

    wameingia ukumbini, lengo likiwa ni kujua ni nani alie waalika kwenye harusi hiyo.

    Waliingia ukumbini saa 3 usiku, walikuta tayari waalikwa karibu wote wameisha ingia na hata wahusika pia walikuwa wapo ndani.kutokana na umbali waliokuwepo, bado hawakuweza kuwatambua maharusi, wakatafuta nafasi nzuri na kuketi.

    Mwinyi hakuwa ni mtu wa kukaa sana mahala pamoja akatulia, mara kwa mara alikuwa akitoka nje kwenda kupunga upepo na wakati mwingine kuangalia hali ya usalama ambao ulikuwa ukimtia shaka pasina kujua ni kwa nini.

    Akiwa kwa nje akijitayarisha kuingia ndani, akaweza kumuona Anisa akiongea na Fardos, nafsi ikapiga mshindo... akahisi kitu! Fardos hakukaa sana pale akanyanyuka kuelekea nje kule alipo Mwinyi. Mwinyi akajificha hadi Fardos alipompita.

    Kukawa kuna maswai mawlii yanamzunguka kichwani, aongee na Far ili ajue wazo lake ama aende ndani kwa Anisa akamuulize walichokuwa wakiongea na Far? Kabla hajapata ufumbuzi akaona Far anatoa simu, pale pale akajua tayari...

    Akamsogelea na kumkumbatia kwa nyuma kisha kumbusu shingoni. Fardos alishtuka kwa kitendo kile, lakini alipojua kuwa ni Mwinyi, nae akambusu usoni na kuendelea kupiga simu hiyo, kuonesha kuwa amedhamiria.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwinyi aikuwa akijaribu kumzuia Fardos kupiga simu, maana tayari alikuwa ameisha hisi ni nini kinafuatia. lakini Fardos kama vile alikuwa nae alijua, akawa anamfanyia ishara ya kutulia, ikamlazimu Mwinyi kuwa mpole, akasubiri

    “As salaamu alaykum”

    “Ammi nimemuona, tupo nae hapa ukumbini mliponileta, nyie mpo wapi sasa hivi?”

    “Ahaa, sawa, msichelewe basi,” kisha akakata simu na kumgeukia Mwinyi.

    “Mambo?”

    “Poa!” Mwinyi aijibu kifupi

    “Sasa jana ndio ukanifanyia kitu gani?”

    “Si nilikununuia kinywaji lakini mpenzi wangu?”

    “Kwani nilikwambia nina kiu ya kinywaji?”

    “Oh Samahani basi, ila nilikuambia awali kuwa nina ahadi na mtu Fulani hapa. Ila hilo sio tatizo, leo tupo pamoja au vipi?”

    “Nami leo sikuachi, ila kwanza ngoja niingie ndani, wewe vipi... upo kwenye hii sherehe pia?” Mwinyi akaruka kimanga

    “Hapana mimi nilimlea jamaa tu hapa,”

    “Poa sasa usiondoke, ukanifanyia kama jana.”

    “Unaingia ndani kufanyeje? kama vipi si tuondoke tu?” Tayari Mwinyi alikuwa ameisha usoma mchezo, hivyo alichokuwa akikifanya ni kuridhisha tu hisia zake kama ni za kweli ama lah. Fardos akamjibu

    “Kuna ndugu yangu nilie kwambia jana kuwa tulikuwa nae Vila tulipotezana nae, lakini hapa nimekutana nae, hivyo ngoja nikamtoe kisha mengine yatafuatia baadae,”

    Hakuwa tena na haja ya kutafuta ushahidi mwingine, akawa pia amejua ni nini kinafuatia. Akachukua simu yake na kumpigiaAnisa, akawa hapatikani, akaingia ndani ili kumtafuta, pale alipomuacha kwenye kiti hakumuona. Baada ya kumtafuta kwa umakini, ndio akamuona mbele kabisa akiwa na bibi harusi.

    Watu wakiwa wanagonga glasi zao na maharusi, Mwinyi bila ajizi akaamua kumfuata Anisa kulekule, aliemuona kule mbele, akaishiwa nguvu na kusahau kiichompeleka kule mbele, bai akaropoka

    “Salama... ni wewe? Hata siamini!”

    Sauti yake ilimezwa, haikusikika kutokana na sauti kubwa ya muziki mnene uiokuwa ukirindima pale ukumbini. Kama aliekumbushwa kilichompeeka kula mbele, akamsogelea Anisa aliekuwa anaonekana akiongea na bi harusi na kumvuta mkono.

    Watu karibu wote waliona tukio lile pale ukumbini, akiwemo hata Fardos, maana ilikuwa ni mbele kabisa. Ikalazimu Bi harusi amuachie mkono Anisa na kumtazama Mwinyi aliekuwa anaonekana kumkokota Anisa na kumtoa ukumbini mbiombio.

    Walifanikiwa kutoka hadi nje, lakini kabla hawajaifikia gari, Far alikuja kasi na kusimama mbele yao, kwa mshangao Mwinyi akasema

    “Shit!” Far akauliza huku akiwaangaia kwa zamu.

    “Anisa unamjua huyu? Eti Mwinyi unamfahamu huyu?”

    Mwinyi hakujibu wala Anisa hakufungua mdomo, ila aliendelea

    kuisogelea gari na kufungua mlango wa dereva, Anisa sasa akajitutumua na kumjibu Fardos

    “Ndio ninamfahamu, kwani na wewe unamjua huyu?” hata kabla jibu

    halijatoka mdomoni kwa Far, simu yake ikaita. Akamuelekeza mtu alieekuwa akiongea nae mahala pale walipo.

    Kama upepo, Mwinyi akateremka garini na kumfuata Anisa

    “Ingia garini, baba yako anakuja huyo, atatukuta hapa, Far ametuchoma tayari,” Anisa hakuweza kuelewa kwa haraka, maana tukio lile kwake lilikuwa ni la ghafla mno. Aliposhtuka na kukimbilia garini alikuta tayari Mwinyi ameishaliweka njiani.

    Fardos alipohisi kuwa atakimbiwa na hawa watu na wakati huo yeye tayari ameisha waambia kuwa yupo nae, itakuwa ni aibu kwake, akasogea na kusimama mbele ya gari, watu kibao walitoka ukumbini kuja kutazama filamu ile iliyozinduliwa bila kiingilio.

    Mwinyi akateremka chini kwa ghadhabu na kumtandika Far kibao cha hatari, Far akachachamaa na kumuuliza Mwinyi

    “Yaani Mwinyi unanipiga kwa sababu ya Anisa?” akamvuta hadi pembeni na kumuacha Far akilia, lakini hakufanikiwa kurudi garini, bali aliweza kuiona gari ya Poisi ikiwasili pale ikiwa na askari wanne nyuma wenye silaha na kusimama palepale kwenye kundi la watu.

    Wakati huo Anisa nae alikuwa ameshuka garini kusogea eneo lile ililokuwa na ugomvi, hivyo aiweza kuonekana vizuri na watu wote.

    “Huyu ndio Anisa, sijui Mwinyi yupo wapi,” Anisa aliisikia sauti ya baba yake na kuishiwa nguvu palepae, lakini aliweza kupasa sauti ya juu sana na kusema

    “Mwinyi ondokaaa Kimbiaa,” hakujiuliza tena mara mbili, bali alisogea kwenye kundi la watu na kujichanganya, hawakuweza kumuona. Isingewezekana kuondoka na gari katika mazingira yale.

    Kitendo kile cha Anisa kutamka vile kilimkera Far aliekuwa pembeni na kuwasogeea askari kisha akawaambia huku akiwaonyesha ile Rav 4 nyekundu.

    “Hiyo hapo ndio gari yake ameikimbia,” Anisa akamtazama Far kwa jicho la chuki na kuropoka

    “Muongo wewe, hilo sio gari lake,” akajaribu kutetea

    “Binti unasema hiro ndio rigari rake hiro rituhumiwa?” aliongea askari kwa lafdhi ya kikurya

    “Ndio amekuja nayo yeye hapa ukumbini,” Anisa akageuka na kumtemea mate Far usoni, baba Anisa akamchapa kelb Anisa usoni, askari wa kike akamuingiza Anisa garini na wale askari wengine wawili wakaingia garini na kuondoka.

    Rav 4 aliokuja nayo Mwinyi pale ukumbini ilikuwa ipo Silencer hadi wakati anaikimbia, hivyo askari mmoja akaingia na kumtaka Far nae aingie, na askari akaanza kuiendesha wakiondoka nayo. Watu pale nje wakabaki wamepigwa na butwaa.

    Yalisemwa mengi sana, lakini waliokuwa wakiujua ukweli tayari walikuwa hawapo, waliobakia wote walibaki na labda safari ikaelekea kwanza kituo cha Polisi kati ambapo Rav 4 ilibaki pale.

    Mwinyi nae akachukua Taxi na kuelekea moja kwa moja hadi Guest aliopo,hakukumbuka kuhusu gari hadi aipofika nje ya guest ndio akampigia simu Sammer na kumueleza hali halisi juu ya yaliyotokea

    Sammer akatoka usiku uleule na kuelekea kule ukumbini, hakuona gari na hata idadi ya watu waliokuwepo pale ukumbini ilikuwa ni ya kuhesabu, wengi walikuwa tayari wameisha ondoka. Akawauliza wachache ilipowekwa gari ile, wakamwambia kuwa gari ile imechukuliwa na Polisi tangu muda uleule.

    Jumapili asubuhi. Wakati Mwinyi akiamka, akakuta kuna sms iliyotumwa usiku uliopita ikimuuliza alipo. Alifyonza na kuitupia simu kitandani yeye akaelekea bafuni kuoga. Wakati akioga simu yake ikaita, aliidharau tu kwani laijua aliepiga ni Fardos.

    Aipomaliza kuoga akiwa anajifuta maji mwilini kwa taulo lake, akakumbuka kuangalia namba ipi iliompigia wakati akiwa anaoga. Hamadi.. kumbe hakuwa Fardos..

    “Ah! Anisa..” akapiga yeye haikupatikana, akajaribu tena na tena, bado haikuwa hewani, kwa hasira aakaitupia kitandani.

    Ghafla nayo bila kuchelewa ikaanza kuita tena, safari hii akaikimbilia, kukuta mpigaji ni Fardos akasonya na kuikata, ikaita tena akaikata, sasa akaazimia kuizima kabisa, lakini akajiuliza je Anisa akimtafuta itakuwaje? Hakuwa tayari kupoteza mawasiliano na Anisa, akaamua kuiacha wazi tu.

    Far hakukata tamaa, akaendeea tu kupiga. Baada ya kuwa ni kero, akapanga kama atapiga tena, basi ataipokea na kumtukana kiasi kikubwa na atamwambia kuwa asimsumbue. Lakini kabla haijaita, ikaingia sms, hakujua imetoka kwa nani, akaifungua

    ‘Mambo Mwinyi? Bado ninakupenda sana, nipo Airport narejea Tabora, sijapenda iwe hivi ila nafanya hivi kwa ajili ya usalama wako, nimeambiwa kila kitu kuhusu uhusiano wako na Fardos, sijali amini nimekusamehe kwa kuonyesha mapenzi makubwa sana mbele yake pale ukumbini. Popote ukimuona Far.. mwambie sitamsamehe hadi siku nakufa, nimekuachia pesa nyingine kwenye begi langu, maelezo zaidi, tunza mawasiiano hasa usiku, nakupenda Mwinyi, Mwaaah!’ hivyo ndivyo alivyomaliza Anisa kwa kiss laini.

    Hata kama ungekuwa wewe na moyo wako huo wa chuma, ungelainika tu, sasa ndio Mwinyi alijua thamani ya penzi, naam.. utamu wa penzi. Chozi lilimdondoka, hasira ikampanda, hakutaka tena kusubiri simu ya Far, sasa akampigia yeye.

    Far akaipokea katika hali ya kawaida kabisa kama hakuna tatizo na kusalimia

    “Sitaki salamu yako wala nini Malaya mkubwa we, haya nieleze sasa, umepata faida gani? Umeona raha gani? Kazi ya wivu wa kijinga tu...” Alitukana Mwinyi kadri ya hamu yake na kiu yake ilipoisha ndio akakata simu.

    Ama kwa hakika simu yake ilikuwa busy sana, alipoiweka chini ikaita tena, akaitazama Display, ile namba ikamfanya aipokee

    “Sasa Mwinyi jana usiku sikutaka kukusumbua wainiambia nirudi leo asubuhi na sasa ndio nipo hapa na mdada Fulani anaitwa Far ambae anaiwakilisha Famiia ya kina Anisa”

    “Sawa Sammer,kwa hiyo wamesemaje?”

    “Wanataka wakuone hapandio waliachie gari”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nani asema maneno hayo? Askari ama familia ya kina Anisa?”

    “Askar.. maana familia yenyewe ya hao kina Anisa ndio huyo Far mwenyewe”

    “Nipe huyo Far niongee nae”

    “Sawa huyu hapa” Sammer akampelekea simu Far na kumpa.

    “Mambo vipi Mwinyi?” salamu ya Far Mwinyi hakuiitikia

    “Kama uivyotaka wewe yawe na sasa yamekuwa, nashangaa kuona hujaridhika na kesi hii umeamua kuifuatiia, sijui una lengo gani?”

    “Mwinyi nisameh,sikujua kama ni hivi ambavyo najua sasa, nataka kuonana na kuongea nawe, njoo hapa kituoni”

    “Wewe umechanganyikiwa nini? Mie nije kituoni? Kwanza unajua niipo?”

    “Sijui uipo ila njoo tulimalize hili tatizo,”

    “Siji, wewe si umetumwa unikamatishe nami pia?”

    “Si hivyo Mwinyi, hutakamatwa tena,nimeisha yamaiza, njoo kituoni ili gari ya Sammer itoke”

    “Nipo mbali kwani sina uhakika waa usalama wa maisha yangu,”

    “Upo wapi?”

    “Hupaswi kujua nilipo, kwani wewe nani hadi ujue yasiyokuhusu?”

    “Napaswa kujua kama mtetezi wako,”

    “Toka hapa, mtetezi utakuwa wewe?”

    “Sawa, nina haki Mwinyi ya kujua ulipo kwa ajili ya amani kwako na kwa Anisa pia,” linapotajwa jina la Anisa, Mwinyi huwa mpole

    “Nini? Unasemaje wewe?” ilikuwa sauti ndogo ya upole.

    “Niambie moja unakuja ama hauji?” Far sasa nae akabadilika na kuwa mkali, Mwinyi akashusha pumzi kwa nguvu na kufikiri kwa sekunde kadhaa kisha akasema

    “Umenisikia we Malaya, mimi ninakuja kwa sababu kuu mbili, kwanza ni kwa ajili ya amani ya Anisa na pili ni kwa ajili ya gari y a Sammer iliyo kamatwa ikiwa mikononi Mwangu, ila tambua siji kwa amri yako,”

    “Mimi sijali sababu gani inayokuleta hapa, jambo la muhimu ni wewe kufika hapa basi,” kila mmoja akakata simu kwa jazba.

    Mwinyi akalisogelea begi la Anisa na kuifungua, akakuta pesa taslimu kiasi cha shilingi 2,675,000= milioni mbili laki sita na sabini na tano elfu za kitanzania. Hakuamini, akachomoa laki moja na sabini na tano na kutoka nazo kuelekea kituoni

    Alikuwa akiamini pale kituoni ukiwa na nguvu kidogo, unaweza kuipindisha sheria, iwe kwa hiari ama kwa lazima. Akiwa njiani akampigia simu Anisa akawa bado hapatikani, akamtumia sms akimtaarifu kuwa anakwenda kituoni kujisalimisha.

    Kisha akampigia simu Mgasi na kumuelezea mkanda mzima. Mgasi aliishiwa pozi na kumtaka Mwinyi apambane kulimaiza tu ile tatizo, hadi anamaliza maongezi nae, akawa amefika kituoni.

    Aliwakuta Sammer na Far wamekaa pamoja wakipiga story, akaungana nao na kuwauliza ni kipi kinachoendelea.Far ndio aliekuwa akiongea.

    “Mwinyi kwanza ninaomba unisamehe kwa yote yaliyotokea awali, nimekuita hapa tuyamalize, twende kwanza kwa mkuu kwani tayari nimeongea nae kilichobaki ni yeye kukuona tu, yatakayoendelea baada ya hapo niachie mie,”

    Kauli yake haikuwa na yoyote wa kuipinga, ila Mwinyi akamsisitizia Sammer kumuwekea dhamana, Sammer akakubali, Mwinyi akatoa laki moja na kumkabidhi, Far akamtoa woga kuwa hakuna kitu kama hicho. Wakaelekea ofisi ya mkuu wa Kituo

    “Wewe ndio unatorosha watoto wa watu si ndio?”

    “Hapana Mkuu, mimi sijamtorosha,” alijibu Mwinyi akiwa hajiamini.

    “Unakataa hujamtorosha?”

    “Sio kama nakataa, bali mimi sijamtorosha,”

    “Yeye amefikaje huku?”

    “Hata nami sifahamu, maana nimeonana nae huku huku Mwanza,” kwa msaada wa Far mambo yalinyooka na wakaruhusiwa kuondoka na gari yao bila kutoa hata senti nyekundu.

    Tangu awali ilionekana kuwa shida ya wazazi wa Anisa ni mtoto wao tu basi, walikamilisha kila kitu na kutoka na gari yao, Sammer akiendesha na Mwinyi akiwa pembeni yake nyuma alikaa Far peke yake wakiwa kimya kabisa.

    Sammer ndio alivunja ukimya kwa kuuliza

    “Mwinyi vipi mbona doro?” akamgeukia Far na kumuhoji hivyo hivyo

    “Oyaa Far, kimya hicho kinanitisha wangu...” Far akapata nguvu ya kuongea maana alikuwa na hamu sana ya kuongea, lakini hakuwa anajua ni wapi aanzie, akasogea kidogo kwa mbele na kusema

    “Sammer, nina hamu sana ya kuongea na Mwinyi ila tu nahisi ana hasira sana,”

    “Hapana Far, huo ni wasiwasi wako tu,”

    “Upo sahihi kabisa, natamani hata humu garini nikushushe, sema una

    bahati kwa kuwa hii gari si yangu, maana sitamani hata kukusikia licha ya kukuona,”

    “Si nilikwambia Sammer? Umeamini?” aliongea Far kwa sauti ya upole.

    “Mwinyi mshikaji wangu hapo sasa unafanya sio, unapaswa kusamehe hata kama umekosewa,”

    “Kwa kosa lake huyu Malaya hapaswi kusamehewa, hata Anisa ameniasa hivyo,”

    “Mwinyi kumbuka mimi ni mpenzi wako...”

    “We we wee! Ishia hapo hapo, nani mpenzi wako? Hukohuko kenge wee,” akasonya na kutazama mbele, maana aligeuka kumtazama

    “Sawa tu ila ukweli utabaki hivyo hata kama leo utanikana. Natambua Anisa ni ndugu yangu na alitoroka nyumbani kwenye maandaizi ya harusi yake aliokua akitajia kuolewa siku chache zijazo, tena na ndugu yangu, nami sikutambua kama una uhusiano nae wewe na ndio

    uliemtorosha...” Mwinyi akamkatisha na kumsemesha Sammer

    “Sam unaona? Unamuona huyu mwanamke alivyokuwa na maneno ya kejeli? Nani kakuhakikishia kuwa ni mimi ndio nilimtorosha? Na kama ungejua ni mpenzi wangu ungefanyeje?” Mwinyi akafyonza tena na kutazama pembeni.

    “Huenda yasinge fika huko yalipo fikia,”

    “kwani nani kayaleta huku kama sio wewe? Unafiki tu, mwanamke mbeya ona minywele hiyo, kama mbuyu mkavu, nasikia kukuchukia,” wakati akisema maneno hayo alikuwa akimtazama, alipomaliza akawa anatazama mbele barabarani.

    “Najua hilo Mwinyi, kwa sasa hunipendi, lakini unapaswa ujue kuwa, kama hutaki kuelewana nami, Anisa hutamuona tena...” Aliongea Far na kumwambia Sam amuache palepale.





    Wote walishtuka garini na kumtazama Far ambae sasa alipata kiburi, Mwinyi alitamani kujua zaidi, akamuuliza Fardos anamaanisha nini. Far hakujibu bali alishika kitasa cha mlango ili afungue na kutokomea, Mwinyi akauzuia.

    Lakini Far aifanikiwa kuufungua na kutoka nje, Mwinyi akatoka pia na kuanza kumbembeleza Far amueleze kinachoendelea

    “Nitafute kwa muda wako leo hiihii kabla ya saa 11 jioni, ukichelewa

    baada ya hapo, itakula kwako, wewe si ni kiburi? Kwa heri,” akawa sasa Far anajibu kijeuri huku akiondoka

    Mwinyi hakumruhusu kiurahisi tu aondoke, hadi Sammer alipofika na kuwatenganisha. Far akaingia kichochoro Fulani hivi na Mwinyi akaingia garini kwa nguvu ya Sam. Mawazo yakaanza kukitawala kichwa cha Mwinyi.

    “Hivi ni nini kina endelea kutokea huko mbele? Far anasema sitamuona tena Anisa, ni kwa sababu gani? Ama ndio anakwenda kuolewa? Lakini kuolewa kunaweza kusababisha nisimuone tena? Hapana... sasa napaswa kuwa mpole na kumtafuta Far ili kujua undani…” akashtuliwa na sauti ya Sam

    “Oyaa vipi? Tumefika Guest, nenda kapumzike.”

    “Kweli mwanangu, Far tayari kanichanganya.”

    “Huyu achana nae kwa sasa, tumtafute baadae, muda huu kapumzike, lakini ule kwanza, au vipi?”

    “Poa Mwana, tuwasiliane baadae angalau sa 10 jioni,” wakaagana na kila mmoja akashika njia yake, Mwinyi akaingia ndani kupumzika na

    Sam akaelekea katikati ya jiji kwenye mishemishe zake.

    Saa 9 alasiri Far akampikia simu Mwinyi na kumuuliza alipo, Mwinyi akamuelekeza na baada ya dakika chache Far akawa amefika kwa kutumia usafiri wa bodaboda. Lengo la Far lilikuwa ni kulimaliza suala lile kimaongezi na wala sio kiugomvi na ndio maana alikubali kuwa mpole kwa Mwinyi ili mambo yaishe.

    Aliingia Far hadi chumbani na kumkuta Mwinyi kakaa upande mmoja wa kitanda lakini kaegamia ukuta, Far alikaa upande mwingine wa kitanda upande wa kichwani akiwa amekumbatia mto miguu ikining’inia chini.

    “Mwinyi samahani, najua nimekukosea na ndio sababu nipo hapa ili kusawazisha, kwani kesho nina safari, ninapenda niondoke nikiwa nipo safi kati yangu mie nawe, ni mengi mema ulinifanyia...” Mwinyi akamkatisha kauli kwa kumuuliza

    “Unaelekea wapi?”

    “Naelekea Dar Es Salaam kwenye harusi ya Anisa,”

    “Eti? Kufanya nini?” mwinyi alipatwa na mshtuko na kunyanyuka alipokuwa ameegamia.

    “Kesho Maghribi ni ndoa ya Anisa, ndio nataka kwenda,”

    “Mama yangu, mama yangu.. unasema? Hata siamini... hebu rudia... kesho?”

    “Mwinyi sio hilo lililonileta hapa...”

    “Anisa nisikilize, aah samahani Fardos, unachosema ni kweli kabisa ama?”

    “Ndio, kwanini nikudanganye Mwinyi lakini?” aliongea Far kwa sauti ya dhati.

    Kauli ile ikazidi kumchanganya Mwinyi, muda huo alikuwa amesimama, akaketi na kusimama tena, hakujielewa.. alichanganyikiwa masikini

    “Unasema harusi wapi?”

    “Harusi ni Dar.”

    “Sasa mbona Anisa yupo Tabora?”

    “Hapana tangu ametoka hapa ameelekea Dar moja kwa moja, ila kabla hawajaondoka walimwambia kuwa wanarudi Tabora,”

    “Ah! Anisa... kwanini imetokea hali hii? Kwanini niiruhusu hali hii itokee mikononi mwangu?” aliongea kwa kuhisi ananong’ona kumbe alikuwa akisema kwa sauti ya juu ambayo hata Far aliisikia.

    Fardos akamsogelea na kutaka kumshika begani, aliponyanyua tu mkono kutaka kumshika, Mwinyi akamzuia na kumbwatukia

    “Niache Fardos, wewe ndio umesababisha yote haya,”

    “Unanilaumu bure Mwinyi, mimi ningefanyaje sasa? Sikujua lolote naomba unisamehe...” Mwinyi akamkatisha kauli kwa kumpa mtihani

    “Naweza tu kufikiria suala la kukusamehe iwapo tu utaniambia kila kitu tangu kuonana kwako na Anisa hadi kumkamatisha kwa baba yake,”

    “Ni hivi Mwinyi, mimi nilikutana nae Villa, sikujua yupo na nani, baadae wewe ukanipigia simu, mimi nikaondoka na kumuacha pale mezani nilipomkuta bila hata kuchukua namba ya simu, japo tayari alikua amenielekeza sehemu aliyofikia,” akapumua na kuendelea

    “Baada ya wewe kuninunuia kinywaji na kupotea, nikarudi kule alipokuwa amekaa Anisa, nae pia nikamkosa. Basi nikaanza kumtafuta ukumbi mzima na bado sikufanikiwa kumuona. Nikaamua kuachana nae kwa kuamini kuwa nitamfuata siku ifuatayo kule guest midhali ninapafahamu,” Far akamtazama Mwinyi akakuta anamtazama yeye, akaendelea

    “Lakini wakati natoka pale kwenye lango la Villa Park, nikakutana na rafiki yangu mmoja hivi anaitwa Victor, ambae alikuwa akifunga ndoa siku ifuatayo, akanipa kadi ya mwaiko wa sherehe ambayo ilipangwa kufanyika siku hiyo hiyo ya ndoa , nikaipokea. Niipoitazama nikakuta ni ya Double nami nilikuwa Single, nadhani tupo pamoja Mwinyi?”

    “Wewe endelea tu mimi nakusikiliza,”

    “Hapo ndio nikapata wazo la kutmtafuta Anisa usiku uleule, nikahisi kwenda guest bila ahadi ni uzushi, ndio nikampigia simu anti yangu ambae ni mama yake Anisa kumuomba namba ya Anisa, sasa ndio taabu ikaanzia hapo,”

    “Ilikuwaje?” aliuliza Mwinyi kwa shauku huku akiwa anauweka mto vizuri kifuani

    “Mwanzo sikumuelewa anti, ila baadae akaniambia kuwa Anisa hayupo na simu yake haipatikani, mimi bwana bila kujua kinachoendelea, nikasema nilikuwa nae dakika chache zilizopita, hapo sasa pakawa ni patamu zaidi...”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nini kiliendelea?” Mwinyi alikuwa akitamani Far asinyamaze, aendelee tu kuhadithia bila kuacha hata kidogo.

    “Nikasikia Anti akimuamsha Ammy, nahisi akampa simu na utangulizi

    kidogo, maana Ammy baada ya salamu tu akaniuliza kama ni kweli nimemuona Anisa huku Mwanza, nikakiri na kujiuliza mwenyewe kulikoni? Lakini kama mtu aliekuwa anajua kuna kitu kinaendelea kichwani mwangu, Ammy akaniambia kwamba, Anisa ametoroshwa na kijana mmoja hivi wa Kiswahili,”

    “Hawakukutajia jina lake?”

    “Hapana hawakunitajia na wala mimi pia sikuuliza. Ila Ammy tu akasema, asubuhi ya siku ifuatayo atakuja hapa Mwanza, chochote kitakachotokea mi nimjulishe, hiyo ndio ilikuwa awamu ya kwanza ya mazungumzo baina yangu na wazazi wa Anisa usiku ule kupitia simu,”

    Fardos akanyamaza na Mwinyi akashusha pumzi kwa nguvu akiushusha mto alilokuwa ameukumbatia na sasa akauweka ukutani na kuuegamia. Far nae akanyanyuka pale alipokuwa amekaa na

    kwenda dirishani.

    Pale dirishani alifungua pazia kidogo na kutazama nje kisha akageuka na kumuangalia Mwinyi, akaendelea kuongea.

    “Kwa sababu tayari Ammy alikuwa ameniambia kuwa Anisa amekimbia ndoa, tena ya ndugu yetu sote, mie nikaamua nimtafute ili niongee nae juu ya tukio lile, nikatota asubuhi ya jana na kuelekea Smart House ambapo aliniambia anapatikana, sikumkuta bali nikaambiwa ameondoka na mpenzi wake. Sikuwa na jinsi nikarejea nyumbani hadi Ammy alipofika saa 11 ya jioni,” Far akarejea kitandani na kukaa pale pale alipokaa awali.

    “Ammy alipofika, jambo la kwanza kuniuliza ni wapi nilipomuona Anisa? Nikamjulisha na akataka nimpeleke eneo lenyewe, kisha nikampitisha Smart akachukua chumba pale akiamini Anisa anaweza kurudi na mpenzi wake ambae hadi muda huo mimi sikuwa najua kama ni wewe, basi tukatoka na kuanza kuzunguka Mjini hapa na pale, huku na kule,”

    “Kwa hiyo mlikuwa mnazunguka kututafuta?”

    “Ndio, Yule Mzee aikuwa anafikiri jiji ni kama kijiji, kwamba utamtafuta mtu kwa macho na kumuona. Basi tulizungukaje.. kama unavyojua maisha ya mjini, huwezi kumuona mtu unae mtafuta kibahati bahati tu, hadi saa 1 usiku tunarejea nyumbani, hatukufanikiwa kumpata Anisa popote,”

    “Subiri kwanza, kwa maana hiyo muda wote huo mlikuwa pamoja na

    wazazi wako ndani ya garini mkizunguka kutusaka?”

    “Ndio tuikuwa pamoja hadi baada ya chakua cha usiku waliponileta ukumbini kisha wao wakarudi nyumbani na kuahidi kunifuata shughuli ikiisha ili tuendelee kuwatafuta kwenye kumbi za starehe, huenda mkawa huko,”

    “Ok! Sasa unaweza kuendelea.”

    “Sikutegea wala sikudhani kama naweza kumuona Anisa ukumbini, hivyo nilimsogelea na kuongea nae kwa dakika kadhaa,akanieleza kuwa yupo pale ukumbini na mpenzi wake ambae hadi muda ule sikuwa ninamtambua ni nani, ndio akaniambia wapo mle kwa ofa ya bibi harusi ambae anajuana na mpenzi wake” Mwinyi akamuuliza swali ili apate kujua

    “Vipi alikuwa tayari ameisha kutajia huyo mpenzi wake ni nani?”

    “Bado hakuwa ameniambia na ajabu wala hilo halikunishughulisha kabisa. Basi ndio nikatoka nje na kumpigia simu Ammy ambae muda huo kumbe alikuwa bado yupo mitaani akiendelea kumsaka mwanae, na ndio maana hakuchelewa kufika pale nilipomuita nikiwa pamoja nawe, ile ilitokea vile kwa sababu hakuwa mbali” akanyamaza na kumeza mate

    “Nafikiri picha yote umeipata sasa Mwinyi na utakuwa umejua kwamba mie sina kosa na sipaswi kulaumiwa kwa chochote, au wewe unaonaje?”

    “Fardos huwezi kuibadili rangi nyeusi kuwa nyeupe, wewe bado ni mkosaji tu hata ujitetee vipi. Sawa kwa lile la awali unaweza kujitetea kuwa ulikuwa huelewi, lakini mbona hata baada ya kujua uliendeea kuzuia gari wakati nilipotaka kuondoka na Anisa?”





    “Sawasawa Mwinyi niliitegemea sana swali hio, na jibu lake ni hili, baada ya kugundua kuwa mtu alie nae Anisa pale ukumbini ni wewe, roho iliniuma sana na palepale nikasikia hasira na kuhisi chuki ya ajabu kwa Anisa, hasa baada ya kukumbuka ulivyoniacha kule Villa, niliumia sana na ndio maana nikaamua niwakomeshe, tendo ambalo kwa sasa nalijutia, maana ishara zilikuwa zikijionyesha dhahiri shahir kuwa, mimi sina nafasi tena kwako”

    “Nami hicho ndio kinachonishangaza, yawezekana masikio ni mabovu, lakini je hata ishara tu huzioni?”

    “Haa! Mwinyi unaniambia hivyo kweli?” aliuliza Far huku akijionyesha kidole kifuani kwake. Lakini kabla Mwinyi hajajibu, simu yake iliokuwa

    kitandani ikaita

    “Yeah! Nambie…” alipokea na kujibu kisha akajibu tena

    “Poaa, we njoo tu chumbani si unapajua?” kisha akakata simu.

    “Mwinyi hutaki kunisamehe kosa nililotenda bila kukusudia japo uliniahidi kunisamehe iwapo nitakueleza, nimekuelezea na sasa umejua, hatimae unaniruka”

    “Wewe nani alikupa ahadi ya kukusamehe? Mimi siwezi kukuahidi hivyo, nikikusamehe itakuwa ni sawa na kumsaliti Anisa ambae amesema wewe hufai kusamehewa hadi kufa.”

    Mlango ukagongwa, lakini kabla haijaitikiwa Sam akawa tayari

    ameingia ndan

    “Haa! Samahani jamani nimeingia bila rukhsa, nilikuwa nikijua kuwa yupo mtu mmoja,”

    “Usijali Sam, karibu uketi kitandani hapa,” Mwinyi alimtoa hofu

    “Poa kaka mkuu” Sam alijibu kisha akamgeukia Far na kumsalimia huku akimpa mkono.

    “Shwari tu Sam, mzima?” hakuwa mtu mwenye furaha.

    “Hofu kwako tu mrembo, mbona upo hivyo?”

    “kawaida tu mwenzangu, haya ndio maisha,” Sam akahisi hapa si salama, kuna kitu kinaendelea kati yao

    Akamgeukia Mwinyi na kumuuliza kulikoni, akabetua midomo na mikono akitoa ishara ya kutokujua. Akamsogelea Far na kumbembeleza amueleze tatizo ni nini

    “Unasikia Sam, wewe unajua kila kitu, nimejaribu kumuomba msamaha Mwinyi lakini hataki kunielewa japo aliniahidi msamaha,”

    “We mimi sijakuahidi msamaha, nilikuambia nitafikiria kukusamehe, sasa usibadili maneno hapa,” alimkaripia Far

    “Sawa mimi ninachokitaka ni kauli yako tu kuwa umenisamehe basi, sitaki kingine chochote,” alisema Far huku mikono yake ikiwa dirishani

    “Na hata ungekuwa unataka usingepata, maana huo tu msamaha ulio uomba ni mtihani kuupata, hicho chochote ndio itakuwaje?” Sam akaigilia kati ili kutatua tatizo lililopo.

    “Aah bhana ee, acheni taarabu, tulimaize tatizo kwanza, Mwinyi tatizo ni nini?”

    Mwinyi akamueleza kifupi tu tangu mwanzo wa maelezo ya Far hadi walipofikia sasa. Kwa hekima zake Sam, akamshauri Mwinyi amsamehe tu Far, kwani hadi sasa pande zote wameisha muweka Far kwenye wakati mgumu sana

    Mwinyi alitafakari na kukubaliana na ushauri wa Sam ambao aliona una mashiko kwa kiasi kikubwa.

    “Sawa Far nimekusamehe kwa dhati kabisa, ila ninaomba unisaidie kitu kimoja tu, tena kipo ndani ya uwezo wako, utanisaidia?” alimuuliza kimtego huku akimtazama

    “Sijui, niambie ni nini?”

    “Nataka kujua alipo Anisa,”

    “Si nimekwambia kuwa Anisa yupo Dar?”

    “Sawa Dar kubwa, Dar sehemu gani?”

    “Unataka kwenda tena kumtorosha?” kulikuwa ni maswali matupu, hakukuwa na jibu

    “Hapana nataka kumuona mara ya mwisho,”

    “Sikuamini tena Mwinyi, hadi sasa familia zote mbii zimeisha ingia gharama kubwa sana kuifanikisha shughuli hii ya ghafla, sasa wewe unaweza kwenda na kuharibu kila kitu, hapana sintokueleza,” alikataa Far huku akitikizsa kichwa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Tafadhali ninakuahidi sitafanya chochote Far naomba unielekeze niende,”

    “Hapana hapana! Nahofia kuharibu sherehe ya watu, hadi viza tayari imeisha tumwa,”

    “Fardos nawe nielewe basi, haitotokea jambo hilo,” alibembeleza hasa Mwinyi, sasa ilikuwa ni zamu yake yeye kubembeleza

    Baada ya maombi ya muda mrefu, Far akalegea na kukubali kutoa maelekezo, lakini akagoma kumuelekeza ni wapi alipo Anisa, bali alitoa namba ya simu kwa Mwinyi na kumwambia yeye mwenyewe sasa atajua cha kufanya.

    Sama alijaribu kuipiga muda ule ule ikawa haipo hewani, wakaachana nayo na kuamua watapiga baadae. Far akaaga na kutoka pale guest ikiwa ni saa mbili usiku na kuahidi kuwasiliana nao siku ifuatayo kuwapa utaratibu wa yatakayofuatia.

    Sama nae alikaa hadi saa 5 usiku ndio akatoka na kuelekea kwake Mabatini. Sasa ndio akapata muda wa kukaa peke yake na kutafakari. Kilichomchanganya Mwinyi ni kitu kimoja, hakuwa amemuamini Far kwa asilimia mia moja.

    Ni wapi alipo Anisa? Yupo Dar ama Tabora? Far amesema kaelekea Dar, mbona yeye mwenyewe Anisa laimwambia anaelekea Tabora? Nani mkweli? Akajijibu mwenyewe kuwa ni lazima mmoja atakuwa amesema uongo.

    Maswali yakaendelea, kama Anisa ni muongo, kwa nini amdanganye wakati anajua kabisa kuwa wanapendana? Hapana Anisa ndio atakuwa anasema kweli, huyu Far ndio atakuwa ni muongo.

    Lakini pia kwa nini Far anidanganye? Au Far ametumwa na wazee wake kuja kunilaghai hapa ili kuna jambio ifanyike? Mbona maisha yamekwenda mbio kiasi hiki kwa ghafla mno? Hapa si bure kuna kitu.

    Akachukua simu na kuipiga tena namba ile aliyopewa na Far, bado ilikuwa haipatikani, akajaribu na ile anayoijua yeye, zote zikawa hazipatikani, akajivuta kitandani alipokua amekaa na sasa akajilaza chali akitizama juu ilipo feni iliyokuwa ikizunguka taratibu

    Wazo jipya ikamuijia, akachukua simu na kumpigia Mgasi, akamueleza mkasa mzima bila kuacha hata kidogo, mwisho akampa kazi ya kwenda kwa kina Anisa siku ifuatayo ili kufuatilia kama karudi ama bado.

    Haikuwa ni vigumu kwa Mgasi kukubali, alimuhakikishia kulifanya zoezi lile mapema tu na kumjulisha. Wakamaliza maongezi yao kwa makubaliano hayo na wakaahidiana kuwasiliana asubuhi.

    Hivyo ndivo ilivyoisha siku ya Jumapili na ikimaanisha siku ifuatayo kwa mujibu wa Far, ndio harusi ya Anisa. Juma3 ambayo huenda ikabadili matarajio ya watu waliopendana. Mwinyi akatikisa kichwa na kulala akisubiri matokeo.

    **********



    Saa 2 asubuhi siku ya Juma3 Mgasi akampigia simu Mwinyi na kumueleza juu ya kazi aliyompa, maelezo aliyompatia ni sawa kabisa na yaleyale aiyopewa na Far, hayakuwa na tofauti hata kidogo, akachoka kabisa.

    Sasa nae akatamani kufunga safari kuelekea Dar, akampigia simu Anisa kwa namba zote mbili alizo nazo, lakini kama ilivyokuwa usiku uiopita, hazikupatikana pia. Hakuwa na cha kufanya zaidi ya kumpigia simu Far

    Cha kwanza kukifanya aimuuliza alipo, Far akamjibu yupo nyumbani muda ule ila baada ya muda atatoka kueekea Airport kwa ajili ya safari ya kuelekea jijini Dar. Akamwambia hampati Anisa hata kwa namba ile aiyompa, inakuwaje.

    Far akamuambia kuwa Anisa amezuiliwa kutumia simu na mama yake

    “Sasa utanisaidiaje ili niweze kuongea nae?” alihoji Mwinyi kwa sauti

    ya upole

    “Hata nami sijui, labda wewe una ushauri gani?”

    “Hauna hata namba ya mtu wake wa karibu?” alitoa ushauri

    “Namba ninayo ila ni ya anti yangu ambae ni mama yake, unafikiri inaweza kukusaidia hiyo?”

    “Sana tu, nitumie hiyo hiyo,” alijibu kwa haraka akiwa hajiamini kabisa.

    “Nakutumia Mwinyi, lakini angalia sana, mimi mwenzio sipendi matatizo, ohoo!”

    “Usihofu Far, sintokuangusha,” wakakubadiliana kumtumia baada ya muda mchache.

    Mwinyi akajitupia kitandani, miguu ikiwa chini huku akitazama darini, simu yake ikaingia sms, akajua tu lie itakuwa ni kutoka kwa Far ambae atakuwa katuma namba ya Anisa, na hivyo ndivyo iivyo kuwa.





    Likabaki swali moja namba ile ni ya mama yake Anisa, akipiga ataanzaje kuongea nae? Akaishiwa mapozi, akanyanyuka na kuzunguka zunguka chumbani hadi alipopata wazo jipya akatoka haraka hadi nje na kumuita muhudumu.

    “Samahani dada yangu uliniambia unaitwa nani vile?”

    “Grace, naitwa Grace…”

    “Ahsante dada Grace, nina shida ninaomba unisaidie tafadhali,”

    “Sawa kaka yangu, sijui nikusaidie nini?” huku akimsogelea na kujifuta maji kwenye viganja vya mikono.

    Mwinyi akamueezea kifupi tu kwani nae aikuwa amemuona Anisa wakati wakija pale, kisha akamwambia anachotaka Grace akifanye ni kupiga simu kwa namba ile na kujidai anaitwa Salama. Ajidai anamchangamkia saana mama Anisa kama vile anamjua.

    Pia ajidai kwamba anawakumbuka sana hasa kwa wema wake wakati alipokaa kwake kule Tabora na mwisho amuulizie Anisa. Grace alitabasamu na kutikisa kichwa ishara kwamba ameielewa somo.

    Haikuwa kazi kubwa sana kwa mtoto wa mjini japo alikuwa ni muhudumu wa Guest lakini alikuwa yupo makini sana, lengo

    lilifanikiwa, mama Anisa akajaa mwenyewe

    “Naam Salama, za siku nyingi? Namba yangu umeitolea wapi jamani?”

    Swali lilikuwa tete

    “Kipindi kile nimekuja pamoja na namba yake, Anisa alinipa na hii ya kwako, akasema ikiwa haipatikani ya kwake, wewe utakuwa na jibu kwanini hayupo hewani, sasa mimi nilikuwa Rwanda na sasa nimerejea sijampata hewani nilipojaribu kumtafuta, lakini vipi hajambo?” ulikuwa ni uongo uliojitosheleza kabisa, ukatoa jibu la ukweli

    “Mh! Hajambo, tupo kwenye maandalizi hapa, shoga yako anaolewa”

    “Haa! Kweli mama? Naomba kuongea nae kama upo karibu nae” hapo Mwinyi aliekuwepo pale jirani akifuatilia mazungumzo kwa umakini, akatoa alama ya dole kwa Grace na kumtaka aendeleze maongezi.

    “Kwa sasa yupo bafuni anaoga, akitoka nitamwambia na atakupigia, sawa Salama mwanangu?”

    “Sawa mama!” wakaagana na kukata simu.

    Muda si mrefu Mwinyi na Grace wakiwa wanaongea kuhusu ubora wa juu wa kuongea alio nao Grace, simu ya Mwinyi ikaita Grace akaipokea

    “Helow mambo?” sauti ilikuwa ni ngeni kwa wote Grace akahisi huyo sasa ndio Anisa

    “Nadhani ninaongea na Anisa.”

    “Ndio yeye, nani mwenzangu?” Mwinyi alitamani ampokonye Grace simu, lakini akamzuia

    “Mimi naitwa Grace, nataka kuongea nawe faragha, inawezekana?”

    “Yap! Kwani nipo chumbani peke yangu ninavaa,”

    “Sawa, haya ongea na huyu...” hapa sasa ndio Grace akampa simu Mwinyi.

    “Anisa, Mwinyi hapa,” yaani Mwinyi alionekana anataka kuongea kila kitu kwa wakati mmoja

    “Aah! Mwinyi mpenzi wangu jamani” haraka Anisa akaenda na kujifungia mlango kwa ndani ili awe huru zaidi

    “Nimekukumbuka sana Mwinyi, bado upo Mwanza?”

    “Ndio Anisa, ni kweli upo Dar?”

    “Ndio na samahani mpenzi wangu, ninafunga ndoa leo usiku, na kesho ninaondoka kwenda Muscat Oman, sijapenda kabisa Mwinyi kitu hiki

    nimelazimishwa tu na wazazi”

    “Mungu wangu... Mungu wangu! Anisa unasema?”

    “Mwinyi mpenzi wametishia kunilaani iwapo nitakataa, naogopa mimi, nisamehe Mwinyi wangu.” alisema Anisa akilia

    “Nakupenda Anisa, sipendi kukupoteza, kwanini unitoke kiurahisi hivyo,” lilikuwa ni swali kutoka chini kabisa ya uvungu wa moyo

    “Najua Mwinyi hata nami nakupenda pia, sijui nifanyeje? Niambie nifanye nini mpenzi wangu,” wote sasa walikuwa wakilia

    Wangefanyeje? Hawakuwa na chochote cha kufanya... Grace alikuwa mbali lakini ilimlazimu kusogea pale alipo Mwinyi kujua ni nini kinaendelea, Mwinyi sasa alikuwa amekaa chini kabisa akiomboleza, alitia huruma sana.

    “Anisa siwezi kuzuia hilo lisitokee, bali natamani kukuona kwa mara ya mwisho kabla huja ondoka, nitakupataje pataje?”

    “Mwinyi mpenzi wangu njoo Dar leo hii mapema kabla ya saa 10 jioni kwani baada ya hapo sidhani kama tutaonana tena, wamenibana sana,”

    “sasa ni saa 4 asubuhi, acha niende Airport sasa hivi, tutawasiliana vipi?”

    “Kama hivi ulivyofanya, nakupenda Mwinyi.”

    “Nakupenda pia Anisa,” akakata simu na kusimama akiegemea ukuta na kuwa kama teja

    Grace alimsemesha Mwinyi aliekuwa mpole, lakini hakuweza kumsikia hadi alipomfikia na kumgusa, Mwinyi alishtuka na ajabu yeye ndio akaomba msamaha. Grace alisikitika na kumpa pole

    “Pole sana kaka yangu, nimeguswa sana na tatizo lako, inaonekana mlikuwa mkipendana sana, lakini jua kuwa binadamu huwa hawapendi kuona watu wawili wakipendana,” Mwinyi aliona Grace anampigia kelele tu

    “Ni kweli dada yangu, hebu ngoja nije...” akamuacha anashangaa yeye akaelekea chumbani kwake.

    Hakuchelewa akatoka na begi lake dogo pia na pochi ya Anisa iliokuwa ni ya wastani, akamsogelea Grace na kumpa pesa kiasi kidogo, nae aliuliza za nini?

    “Nashukuru sana kwa msaaada ulionipatia japo unaona ni mdogo, ila

    kwangu mie ni mkubwa sana, shika hiki kiasi kidogo cha pesa,

    ninakwenda Dar, siku nitakayo rudi nitakutafuta,” akaondoka na kutotaka kumpa nafasi Grace ya kuhoji chochote.

    Wakati anatoka akampigia simu Sam na kumuuliza alipo, akamwambia kuwa muda ule yupo garage anafanya Service ya gari lake kwani

    amepata safari ya dharula kuelekea Arusha

    “Kama vipi twende zetu tukang’aze macho.”

    “Hapana Sam, muda huu naelekea Airport kutafuta usafiri kuelekea Dar haraka iwezekanavyo,”

    “Ndugu yangu, muda huu bila booking utapata usafiri kweli? Lakini nenda kajaribu,”

    Akachoka kuelekea Airport akiwa kwenye bodaboda. akiwa njiani akapigiwa simu na Mgasi akimwambia kuwa anae yupo safarini kuelekea Nzega kwa shughuli za kiofisi lakini atarejea Tabora siku ileile.

    Mwinyi nae akatumia fursa ile kumueleza mpango wake wa safari ya kuelekea Dar ambao umekuwa ni wa haraka na kumpa ratiba nzima iliopo kule Dar kisha wakaagana wakitakiana mafanikio katika safari na mipango yao

    Aliwasili Airport na kuelekea kwenye dirisha la maulizo ili kupata utaratibu

    “Kaka yangu ndege ya mchana tayari imejaa na ile ya jioni kwa leo haipo kwani imefutwa. Hivyo basi tumebaki na ndege moja tu ya usiku ambayo itaondoka hapa Mwanza saa 2 usiku na kutua jijini Dar saa 6 usiku, lakini itasimama Kilimanjaro, vipi nikupe Ticket?” Jibu lile lilimvunja nguvu lakini hakuwa na jinsi, akalazimika kukata ticket na kuondoka.

    Alielekea hadi mabatini kule kwenye garage alipo Sam na kukaa kule hadi jioni. Hakuwa tena na mawasiliano kati yake na Anisa, aipopiga simu ya mama Anisa iliita, alie ipokea alikuwa ni Mama Anisa mwenyewe, Mwinyi akashindwa kuongea.

    Hakuongea wala pia hakukata ile simu, aliacha tu hewani vilevile, akasikia

    “Sijui nani kapiga simu halafu haongei? Ama sijui simu imejipiga?” ilikuwa ni sauti ya Mama Anisa ilio tamka maneno hayo na kuikata simu ile ambayo haikupatikana tena kwa muda ule hadi anafika Dar

    usiku, sio ile tu hadi na zile zingine zote hazikupatikana.

    Usiku uleule Mwinyi akampigia simu Far na kumjulisha kuwa amemtafuta Anisa kwa muda mrefu na hajampata, ila alimwambia ukweli kuwa aliongeea nae mchana wa siku ile. Far akamwambia kuwa yeye yupo nao na kesho wanaondoka saa 12 jioni

    “Wewe utaonana nae saa ngapi?”

    “Kuanzia saa 5 asubuhi nitakuwa nae, maana wapo hotel,”

    “Poa, naomba ukiwa nae uniwezeshe kuongea nae,”

    “Haina shida!” Mwinyi akachukua Taxi ilio mpeleka nyumbani kwao Mwananyala.

    “Samahani Mwinyi, muda wakuondoka Anisa sio saa 12 jioni, bali ni saa 6 mchana, hivyo muda huu wapo kwenye msafara wakielekea Airport, nami naelekea huko sasa, kama itawezekana nikifika huko nitakuwezesha, wala usijali wangu,”

    “Haa! Fardos unasema kweli?”

    “Ndio Mwinyi, acha mie niwahi,” Fardos akakata simu ilhali Mwinyi akiwa bado anataka kuongea.

    Bila kuoga wala kufanya chochote, shati mkononi, hadi nje ya nyumba yao akasimamisha Bajaj na kumtaka dereva amuwahishe Airport haraka iwezekanavyo

    “Ndugu niwahishe Airport nina saa 1 tu kabla ndege haijaondoka, hivyo ni nusu saa inapaswa tuwe tumefika pale, nisaidie ndugu yangu,” alibembeleza Mwinyi

    “Usiwe na shaka ndugu yangu,” sauti ya kichagga ilimtoa hofu.

    Na kweli, mwendo haukuwa wa taratibu, iikuwa ni kasi ya ndege, waliondoka Mwananyamala saa nne na madakika, lakini saa 5 kasoro dakika kadhaa iiwakuta wapo JKNIA. Alimlipa haraka haraka dereva wa Bajaji kiasi walichokubaliana na kukimbilia sehemu ya kusubiria wageni.

    Aikuta tayari wasafiri wameisha ingia kwenye vyumba vya ukaguzi kama dakika chache zilizopita, alikata tama ya kumuona tena Anisa.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mtu wa kwanza kumuona alikuwa ni baba yake na Anisa, akajificha hadi alipompita.

    Ndio hapo sasa akaanza kumfuatilia kule anapoelekea, lakini ghafla

    kama muujiza, akamuona mtu aliekuwa akimtafuta. Pasina kujiuliza

    wala kujishauri, bila kuhofia askari wala wazazi, tena bila kujua waliopo pale ni kina nani, akamkimbilia Anisa na kumkumbatia.

    Kabla ya kumfikia Anisa, tayari nae alikuwa amemuona nakushangaa, hivyo alipomkaribia, akamuita na kujisogeza kwake na kutoa ushirikiano wa kutosha. Hawakupata nafasi ya kukumbatiana kwa dakika moja nzima isipokuwa walitenganishwa.

    Pamoja na kuwa waliwatenganisha, lakini sio siri, watu wote waliokuwepo eneo lile waligubikwa na huzuni na kusikitika kutokana

    na muonekano wa vijana wale ambao muda ule walikuwa wakilia.

    Huku akiburutwa, Anisa alimuaga Mwinyi ambae wakati huo alikuwa ameshikiliwa na askari wawili. Baba na mama Anisa walikuwa pembeni pamoja na Far walikuwa wakishangaa Mwinyi kafikaje

    Wakaona Mwinyi anaingizwa kwenye kichumba Fulani, wao wakaachana nae na kupanda ngazi kuelekea juu ili waweze kuwaona wasafiri wakiwa wanaingia ndani ya ndege, nae kule ndani ya kile chumba kidogo aliweza kushuhudia kila kilichoendelea uwanjani kupitia kioo kikubwa sana kilichopo upande wa uwanja.

    Aliweza kumuona Anisa akiingia kwenye ndege, machozi yalimtoka, hakujua cha kufanya, na wala tu hakikuwepo. Alilia huku akijisemea moyoni ni kwa nini alimpenda mtoto Yule wa Kimanga. Mawazo yake yalishtuliwa na mkono uliomshika begani.

    Alipogeuka alikuta ni Fardos akiwa amemshika bega la kushoto kwa mkono wa kulia, aliona aibu kumtazama kwa vile kulikuwa machoni mwake kuna machozi yakimtoka, akageuka upande mwingine na kujifuta machozi yaliyokuwa bado yakibubujika.

    “Twende tuondoke, ndege tayari imeisha ondoka” alimsemesha Far na kabla hata Mwinyi hajajibu lolote, baba Anisa akamsemesha kwa kejeli huku akitabasamu

    “Kijana vipi, hujambo?” Mwinyi hakumjibu bali alimtazama kwa jicho la chuki, jicho lililomtisha hata Fardos aliekuwa amemshika Mwinyi mkono wa kushoto

    Alichokifanya Mwinyi ni kuitoa mikono yake kwenye mikono ya Fardos na kuondoka kwa kasi eneo lile akiwaacha na kicheko wazazi wa Anisa lakini huzuni kwa Far kwani sasa alikuwa yupo pamoja nae



    Sura ya 6



    KUKUBALI MATOKEO.



    Ilipita miezi 6 pasina mawasiliano yoyote baina ya Anisa na Mwinyi wala Fardos na Mwinyi. Polepole Mwinyi alianza kusahau maumivu ya Anisa japo si kwa asilimia mia, lakini aliukubali ukweli, hali halisi ilikuwa imeisha jitokeza, kuwa Anisa ni mke wa mtu kwa sasa japo aliamini hicho sio kigezo cha kumsahau.

    Aliamua muda wake mwingi kujituma katika biashara zake za kutoa samaki wa maji chumvi huko Pemba na kuwauza kwa wafanyabiashara wakubwa wenye viwanda vya kusindika samaki, biashara iliyomlipa kwa kiasi kikubwa.

    Moja ya sababu kubwa iliyokuwa ikisababisha kutokumsahau Anisa moja kwa moja ni biashara ile ambayo mtaji wake ni ile pesa aliyo muachia, hivyo muda mwingi sana alikuwa akikaa anamkumbuka, lakini pia hakutaka kabisa kuwasiliana nae japo alitamani siku moja aongee nae na kumpa shukran kwa kumfungulia maisha.

    Kwa sasa Mwinyi anaishi Dar Es Salaam, akiwa amejipanga vema kimaisha, hana nyumba, ila ndio ujenzi unaendelea na yeye amepanga eneo la Ilala, ana gari ndogo ya matembezi na ana pikipiki 3 aina ya Bajaj zinzomletea pesa ya kula.

    Kifupi maisha kwake si taabu tena, lakini bado hadi muda ule, hakuwa na mchumba wala mke achilia mbali mpenzi, kila alipoulizwa swala la kuoa, alijibu muda bado, kwani wakati utakapofika, hata jamii haitoamini, akawaasa wavute tu subira.

    Siku moja akiwa katikati ya jiji maeneo ya soko kuu la Kariakoo akihemea matunda akamuona msichana aliemtambua. Msichana Yule alikuwa na mabadiliko kiasi Fulani, lakini yeye aliweza kumtambua hivyo hivyo na kumsogelea.

    “Samahani bi... Oh! Nimesahau jina, bi nani vile?”

    “Haa! Mwinyii... mambo vipi?” Huku wakikumbatiana.

    “Poa Salama, aha nitajie jina Lako la kanisa nimelisahau,”

    “Glory bwana, wewe ita lolote tu. Mh, za masiku tele?”

    “Ni shwari tu Glory” alisema Mwinyi huku akicheka na kufurahi

    “Acha mambo zako wewe, upo wapi kimaisha? Tabora, Mwanza ama Dar?”

    “Mimi nipo hapa Dar” walioongea ongea kidogo, wakapeana namba za simu na kuahidi kuonana siku nyingine.

    Waliogopana bado, maana kila mmoja alionekana mambo safi, hakuna alie onekana kachoka kipesa, hata gari zao zilijionesha hivyo, Mwinyi alishangaa sana kwa hali aliyonayo Salama kwa sasa. Lakini Salama ndio alimshangaa zaidi Mwinyi.

    Wiki mbili zikapita bila mawasiliano kati yao, Mwinyi katika kutafuta tafuta namba ya rafiki yake Fulani, akakutana na namba ya Salama, akampigia. Alimuuliza alipo na kumuambia yeye yupo Mwanza na siku chache zijazo yeye atakuwa Dar wakapanga wawasiliane mara tu yeye akifika ndani ya jiji.

    Siku 3 mbele saa 12 asubuhi, Salama akampigia simu Mwinyi na kumwambia siku ileile atakuwa safarini kuelekea Dar na anategemea kuwasili Dar saa 5 asubuhi kuja kumpokea mumewe anaetarajiwa kuwasili siku ile jioni kutokea China. Mwinyi akamuomba kwenda kumpokea Salama.

    “Sawa kama hutajali, mie hufikia Bondeni Hotel, huoni kuwa nitakupotezea muda?”

    “Usijali” Mwinyi akaingia kuoga na kutinga viwalo vya ukweli na kusubiri muda wa kuelekea Airport kumpokea Salama ama Glory.

    Saa 5 asubuhi Salama alitua na kupokelewa na Mwinyi na safari ya kuelekea katikati ya jiji ikaanza. Njiani Mwinyi alimuuliza kwanini alibadili jina, Salama akamwambia kuwa ni kwa sababu ya ndoa yake na Victor ndio ilimfanya abadili dini na jina pia. Akatikisa kichwa Mwinyi kuonesha amemuelewa.

    “Umeoa?” lilikuwa ni swali la ghafla sana kwa Mwinyi, hakuwa akitarajia

    “Bado Salama.”

    “Unasubiri nini hadi leo?” aliuliza tena akiwa na shauku

    “Natafuta wa kumuoa Salama” alimjibu akiwa anaangalia mbele kwa

    umakini mkubwa

    “Anisa yupo wapi?” Swali likamfanya Mwinyi atabasamu na kumuangalia Salama

    “Aliolewa siku mbili tu baada ya wewe kuolewa,” Salama akishangaa na kukanusha

    “Nini? Acha utani bwana,” hapo gari inatembea taratibu kutokana na Jam za barabarani jijini Dar, Mwinyi akamuhadithia kifupi tu.

    Huruma ilimuingia sana Salama na kumpa pole Mwinyi alieonesha bado alikuwa na mapenzi na Anisa. Tatizo Salama alikuwa na maswali ya papo kwa hapo, akamuuliza tena

    “Ramlat nae yupo wapi?” moyo wa Mwinyi ukapiga mshindo… Pah! Aliisha msahau kiumbe Yule kitambo

    “Dah Salama niliisha msahau na hata sijui ni wapi alipo,”

    “He wewe, Yule si ana mtoto wako jamani?”

    “Sijakataa, lakini sifahamu ni wapi alipo nakwambia, mimi niliachana nae akiwa na mimba, na hadi sasa sijui yupo wapi katika hii Dunia ya Mungu,”

    “Ok tuyaache hayo, tumeisha fika, kwa hiyo sasa?”

    “Nitakuijia kwa chakula cha mchana, saa ngapi nikufuate?” aliuliza Mwinyi akimtazama

    “kuanzia saa 9 alasiri, nitakupigia,” wakaagana.

    Masaa mawili baadae, Mwinyi akapokea simu ikimtaarifu ofa ya chakula cha mchana huko pande za Kigamboni ambayo Salama alimwambia amemuandalia. Mwinyi alikuwa yupo maeneo ya kivukoni, akaomba nusu saa kwamba atakuwa amefika kule.

    Alifika na kumkuta Salama walikula huku wakibadilishana mawazo na walipomaliza Mwinyi alimshukuru Salama na kumuomba amshindikize Airport, Salama akakubali, lakini akamwambia kuwa anyanyuke waende kumuona rafiki yake. Hakuuliza ni wapi, bali alinyanyuka na kumfuata Salama ambae alitangulia.

    Walifika kwenye jingo la ofisi na kumkuta Secretary aliewakaribisha tena alionekana kumfahamu Salama, wakaelekea moja kwa moja kwenye mlango wa ofisi mojawapo ilioandikwa CEO, wakaingia.

    “Ha! Ramlat...” Mwinyi hakuamini macho yake, akamgeukia Salama ambae alikuwa ametabasamu, Ramlat akateremsha miwani kidogo na kuacha kuandika, akamtazama aliemuita jina lake, akamtambua… akanyanyuka kwa furaha na kasi na kumfuata akiwa ametanua mikono

    “Oh! Mwinyi tumekutana tena jamani” Mwinyi nae alikuwa ametanua mikono yake na kumpokea Ramlat, walikumbatiana na kufurahi hasa.

    Salama alihisi ni nini kitafuatia baadae, akaaga kwa kisingizio cha kwenda Airport kumpokea mumewe, wakamruhusu huku wao wakiwa wameshikana mikono kama watu wanaocheza ukuti ukuti. Alipotoka Salama, Ramlat akamketisha Mwinyi kwenye sofa la wageni na kumuagizia kinywaji kupitia simu yake ya mezani.

    Walisalimiana tena na kuulizana habari za kitambo, walitawaliwa na furaha

    “Ama leo ni siku ya bahati sana kwangu, kukuona mtu ambae sikutegemea kukuona tena..”

    “Hata nami pia hebu niambie, tayari umeishaoa?”

    “Ramlat acha tu, mie bado sijaoa, labda nikuulize wewe, mumeo hajambo?” ajabu Ramlat hakujibu





    “Mh Mwinyi nashindwa kukubaliana na macho yangu, hivi kweli ni wewe?”

    “Ndio mimi Ramlat, amini upo sahihi” sura zao zilikuwa na tabasamu muda wote wa maongezi

    “Hapa hapatufai, twende kwangu tukaongee zaidi,” Ramlat alianza kunyanyuka na kumpa mikono Mwinyi, akaipokea na kunyanyuka kwa kuivuta kwake.

    Muonekano wa Ramlat ulimfanya Mwinyi kuungua nafsi yake na kutamani sasa kuwa nae kwa mara nyingine, maana sasa alikuwa ni Ramlat kweli. Alitangulia na kutaka kuingia garini

    “Sasa mbona nami nimekuja na gari pia?” aliuliza akiwa ameshika mlango wa abiria

    “Dah kumbe mambo safi best, basi wewe nifuate na gari lako kwa nyuma yangu,”

    Hawakwenda Mbali sana, wakaingia kwenye kasri moja la ukweli hasa, palikuwa na gari nyingine moja, nao wakapaki na zile zingine kisha wakashuka na Ramlat akamfuata Mwinyi aliekuwa akishangaa ule mjengo. Alipomkaribia, uzalendo ukamshinda na kuuliza

    “Nyumba hii ni ya nani Ramlat?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ni yangu Mwinyi, karibu ndani,” hakusema lolote ila aliongozana na Ramlat kuingia ndani.

    Walipoingia ndani wakakuta msaidizi na baada ya salamu, Ramlat akauliza alipo Moo, akaambiwa Moo kalala, wakapitiliza hadi Sitting room. Alimkaribisha na kukaa nae kwa dakika moja wakiongea mawili ma3, Ramlat akaenda ndani kwake kubadili mavazi.

    Mwinyi alibaki akitazama mandhari ya nyumba ile na kuvutiwa nayo sana, alisimama na kusogea dirishani kuangalia nje, hadi aliporudi Ramlat na kumfuata Mwinyi hadi pale aliposimama na kumshika kiunoni

    “Mwinyi mpenzi wangu siamini kama leo tumekutana, nimekutafuta sana, lakini sikufanikiwa kabisa, lengo ni...” Mwinyi akamkatisha huku akigeuka kumtazama

    “Ngoja kwanza Ramlat, ni mengi sana yametokea hapa katikati, kabla ya kuendelea na maongezi yetu mengime, ninaomba unisamehe kwa yote,”

    “Nilishasahau kitambo hayo, sasa nina mapya kichwani, achana na habari ile,”

    “Sawa, nilikuacha kitambo sana ukiwa ni mjamzito, vipi ilikuwaje?” alidadisi Mwinyi kwa aibu.

    “Nilifanikiwa kujifungua salama mtoto wa kiume anaitwa Mohammed, ambae ndio Yule niliemuulizia kwa jina la Moo, ambalo ndio kalizoea, dada akajibu amelala,”

    Aibu ilimtawala sana Mwinyi na kumuomba msamaha Ramlat kwa mara nyingine huu moyoni kiwa na furaha kwa kuona ana mtoto, Ramlat akamwambia amemsamehe wala asijali.

    “Poa. Pale nilipokukuta na Salama ndio ofisini kwako?”

    “Ndio, nami ndio mmiliki wa hoteli ile,”

    Wakarejea na kukaa sofani huku Ramlat akimpa baadhi ya story zake

    “Hata hii nyumba ni yangu, mali yangu, pia gari zote zile mbili ninamiliki mwenyewe,”

    “Ramlat umepata wapi pesa ya kumiliki vitu vyote hivi?”

    “Ni story ndefu Mwinyi, ila mimi nitakupa kifupi tu mpenzi wangu,”

    Ramlat alinyanyuka na kutoa juice na kuleta glass kisha akamimina na

    kumkarimu Mwinyi, akaketi na kuanza kumuhadithia jinsi alivyopata mali ile.

    “Mara baada ya kifo cha mama mie nilitoroka nyumbani na kwenda kuishi kwa rafiki yangu huko Shinyanga, hadi nilipojifungua ndio nikarejea nyumbani Tabora na kukuta wapangaji tu nyumbani, Side nae hakujulikana ni wapi alipo, nilimtafuta kwa takriban miezi mi3 ndio nikampata, akaniambia yeye kwa sasa anaishi Senegal na hana tena mpango wa kurudi Bongo, akaniambia kila kilichopo Bongo ni changu, yeye kule tayari ni mambo safi. Mimi nikaamua kuuza kila kitu kilichopo Tabora na kuamua kuja kuishi huku Dar”

    Akanyamaza na kunywa juisi yake, kisha akamnyanyua Mwinyi na kutoka nae nje huku akisimulia

    “Hili eneo ni letu tuliachiwa na baba yetu, ndio nikaamua kupaboresha. Na kwa vile sikuwa na pesa ya kutosha nami nilikuwa tayari nina malengo yangu kichwani, ikabidi nikate sehemu na kuikodisha kwa miaka 25 nikalipwa pesa yangu na kuwekeza kwenye lile jingo alilokuleta Salama, niliamua nianzie kule kwa sababu lile ni eneo la biashara, nilijua kule patanibeba tu hata iweje, na kweli kule pakaninyanyua. Nilipofikia hatua Fulani wakatokea wafanya biashara Fulani wakapapenda, wakataka kupamalizia, nikaingia nao mikataba na kuwakabidhi jengo”

    “Ulitumia akili sana Ramlat, enhe.. na hili kasri ulilopo sasa?”

    “Mwinyi kashfa hizo sasa, hapa kasri lipo wapi?” wakataniana kidogo kisha Ramlat akajibu swali la Mwinyi

    “Pesa zote walizonipa wale watu, nikaanza kuzielekeza kwenye jengo hili”

    “Hongera sana Ramlat...” kabla hata hajamaliza kuongea alichotaka ukisema, akaja mtoto wa kiume ambae hata Mwinyi hakuuliza, ilikuwa ni sura yake kabisa.

    Mtoto akasogea kwa mama yake na kumnyooshea mikono ambebe, Ramlat akachuchumaa na kumwambia Moo

    “Mwamkie baba” Moo akagoma kuamkia hadi alipo bembelezwa sana ndio akaamkia.

    Mwinyi aliona aibu sana hata akatamani asingemuona Ramlat siku ileila Ramlat kama vile alitambua, akamtoa hofu na kumwambia asihuzunike kwani ameisha msamehe kitambo tena hata kabla hajaomba radhi kwa sababu anampenda sana.

    “Ni usiku sasa, na kwa hiyo leo ninafikiri tutakuwa pamoja leo”

    “Hapana Ramlat, nitakuja hapa kesho, leo niache niende mpenzi wangu”

    “Hilo haliwezekani, leo hutoki humu, siwezi kukuacha utoke, halafu baadae niteseke, ni heri nisingekuona kabisa, hakika hutoki baba Moo”

    Baada ya majadiliano marefu, Ramlat akashinda na Mwinyi akalala pale. walipeana penzi moto hasa ukizingatia walikuwa na muda mrefu hawajakutana. Walipopata muda wa kupumzika, Ramlat alimuuliza Mwinyi kama anaweza kumuoa, Mwinyi akamwambia tena suala hilo anatarajia kulifanya kwa haraka mno.

    Siku iliyofuata Ramlat aliamka mapema sana na akiwa ni mwenye furaha tele hata mfanyakazi wake wa ndani alishangaa, maana zile kazi ambazo alikuwa hazifanyi, sasa alizifanya yeye mwenyewe kama

    kupika na kufua nguo za Mwinyi

    Alipofika ofisini hata wasaidizi wake nao walishangaa kuona siku ile bosi wao hakai ofisini na alikuwa mchangamfu mno wakati wote, hawakujua kilichomchangamsha vile hadi alipowaletea mtu na kuwaambia kuwa ndio baba wa mtoto wake, walikuwa hawajaonana kwa muda mrefu hadi jana ndio wameonana.

    Kila mtu aliekutana nae alimtambulisha Mwinyi, hadi Mwinyi sasa akaanza kuona aibu kumbe mwenzie furaha ndio inamuongoza kufanya vile.

    Haukutimia mwezi, wakawa wamemuita Sheikh na kuwafungisha ndoa iliyoudhuriwa na watu wengi, hakika walikuwa ni wengi akiwepo Mgasi na Sammer, ila sherehe iliyofanyika jioni ndio ilihudhuriwa na watu wachache. Walihudumia wageni kwa siku 3 kisha wakawaruhusu warudi makwao.

    Waliunganisha nguvu zao na kuboresha biashara zao na kumalizia sehemu za lile jingo wanaloishi ambalo kwa wakati huo lilikuwa limemilikishwa kwa kijana wao Mohamed Mwinyi.

    Mwaka uliofuatia Familia nzima ikafunga safari wakiwa na gari yao hadi Tabora kusalimia ndugu na jamaa, walionana nao karibu wote, lakini walipofika kwa kina Anisa wakaambiwa kwamba mama Anisa alifariki kitambo na baba Anisa kwa sasa anaishi Oman kwa mwanaehttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walizuru kaburi la mama Ramlat kwa mara nyingine na kurudi zao Dar kuendelea na maisha yao, njiani wakati wanarejea, Ramlat akamwambia Mwinyi kuwa maisha ni zawadi, japo wengine hawajazifungua zawadi zao hadi sasa. Alimuuliza anamaanisha nini?

    “Mwinyi, bila kutokea hayo yaliyotokea, amini hadi leo familia yetu ingeendelea kuwa ni masikini wa kutupwa na ninaamini hata lile eneo kule Kigamboni tungeliuza na kutolionea faida yake” Mwinyi alitikisa tu kichwa kukubali, Ramlat akafunga mjadala kwa kusema



    “UMENIFUNGULIA DUNIA…

    Kuwa ninayotaka!”



    ***MWISHO***


0 comments:

Post a Comment

Blog