Simulizi : Nini Maana Ya Mapenzi Sehemu Ya Pili
(2) “Haya, basi niambie sasa ilikuwaje juzi mpaka
kunirudia nyumbani jana?” “Mama, hata mimi sina
kumbukumbu” “Huna kumbukumbu kivipi? Erica ujue nimekuona na mwanaume
aliyekurudisha mkibusiana kwenye geti langu bila hata ya aibu? Kwakweli Erica
ningekuwa mzazi mwingine yani ningekufukuza kabisa. Yani wewe nakuona na
mwanaume halkafu unasema huna kumbukumbu kweli!” “Hivi mama hata
nikikwambia ukweli utaniamini?” “Niambie tu ukweli, kama huyo mwanaume
anakupenda sana basi akuoe uone jinsi ndoa vilivyo na uchakae hadi ukumbuke
chakula ulichokuwa unakula hapa nyumbani. Unataka kunificha nini kwa mfano?
Wakati shemeji yako aliona kila kitu ukiwa umelewa na kuondoka na mwanaume.
Erica naongea kwa uchungu hivi aaargh sitaki hata kuongelea tena, ni
kichefuchefu tu kukuangalia” Mama yake Erica aliinuka zake, Erica
aliwaza sana akaona ni vyema kumwambia mama yake ukweli ila alitaka tu kusikia
kuwa Bahati ameshatoka ndio amwambie ukweli mama yake kwani kauli ya kusema kuwa
alionekana amelewa na kuondoka na mwanaume ilimuumiza
sana. Erica aliingia chumbani kwake, na kukuta simu yake kuna
mtu alipiga kisha akakuta ujumbe, “Erica mpenzi wangu una nini lakini?
Hewani hupatikani, unafanya niwe na mawazo mwenzio jamani, unajua huku ni usiku
muda huu ila hadi sasa sijalala, usingizi hauji kabisa sababu yako, Erica basi
ingia fecebook kidogo tuongee mpenzi wangu” Ikabidi Erica aiwashe na ile
simu yake nyingine na kuingia kwenye mtandao, ni kweli alikuta jumbe kadhaa za
Rahim hadi zilimtia simanzi kwakweli na kuona ni jinsi gani Rahim alimpenda,
alijisikia fahari sana kupendwa na Rahim na kujiona ni msichana mwenye bahati
sana kati ya wenye bahati ulimwenguni. Aliwasiliana nae kwa bashasha
sana na kumwambia kuwa anakaribia kufungua chuo, basi Rahim akamuahidi kumtumia
pesa nyingine itakayokuwa ikimsaidia pindi atakapofungua chuo, Erica alifurahi
sana na kuona kweli mwanaume kapata, akawasiliana nae sana mpaka usiku ulifika
kwa upande wa Erica na kwa upande wa Rahim ilikuwa kumekucha,
alimwambia “Erica, kwa hakika leo nimekesha” “Pole Rahim, sasa
si utasinzia leo kwenye mambo yako” “Hapana siendi popote leo, ngoja
nilale tu. Nadhani ile hela nitakutumia kesho” “Asante mpenzi
wangu” Erica aliagana na Rahim huku akiwa na tabasamu kubwa sana usoni
mwake, alikaa akimuwaza sana Rahim kisha kuinuka na kwenda kufanya maandalizi ya
kula chakula cha usiku na kulala maana hakuwa na kazi nyingine ya ziada ya
kufanya kwa wakati huo, yani toka sakata la juzi basi mama yake amekuwa akifanya
kila kazi mwenyewe na wala hakupoteza muda wa kumuita ita mtoto wake kwani
aligundua ni mengi sana anamficha. Erica alienda jikoni na kuangalia
chakula ambapo alikuta mama yake ameshapika, ila akaona chakula cha siku hiyo
hataweza kukila mpaka apate soda maana ilikuwa ni ndizi nay eye alipenda kula
ndizi huku akinywa soda, kwahiyo akaenda kuchukua hela ili aende dukani kununua
soda. Wakati ametoka nje akitaka kwenda dukani, alishangaa kuona mtu
amejikunyata pale nje ya geti lao, akashtuka sana na kumshtua Yule mtu kuwa ni
nani, alishangaa sana kuona mtu huyo ni Bahati, “Kheee
Bahati!” Bahati aliinuka na kumkumbatia Erica, “Jamani Erica
wangu, nafurahi kukuona” “Unafanya nini hapa!” “Erica
nimeruhusiwa muda si mrefu kutoka selo, ila nikasema iendi nyumbani nitakuja
hapahapa nje ya nyumba yenu labda Mungu asikie kilio change nikuone. Nimeteseka
Erica, nimepigwa Erica bila ya kosa lolote, siwezi kukutenda chochote kibaya ila
nikashangaa nikipigwa eti nilitaka kukubaka kwakweli imeniuma
sana” “Sikuelewi Bahati” “Nielewe tu Erica, kwani hukujua kama
jana nilikuja hapa kwenu na mkasa huo wa kupelekwa selo kunikuta?” “Hebu
nieleze vizuri” Bahati akamueleza ilivyokuwa jana yake hadi yeye
kupelekwa selo, kwakweli Erica alishangaa sana kile kitendo cha kuambiwa kuwa
James alimpiga kwanza Bahati na kumpeleka polisi, “Jamani huyu James
ananitaka nini mimi jamani! Pole Bahati ila naomba uende
kwenu” “Nitaenda Erica, ila niambie kwanza ilikuwaje hadi simu zako
hazipatikani, na nyumbani kwenu kunihisi mimi vibaya ilikuwaje?” “Bahati
naomba uende kwenu, maana sitaki matatizo zaidi” “Matatizo
gani?” “Wewe nenda kwenu tu, na wakikuuliza ulikuwa wapi
utasemaje?” “Nitajua cha kusema” “Ila naomba usiseme kama ni
mimi ndiye nimesababisha umefungwa, kwenu wataniua” “Sikuelewi Erica,
una maana gani?” Erica hakuona umuhimu wa kumficha ilibidi amwambie
ukweli kuhusu nyumbani kwao walichomtenda siku ile aliyoenda kuangalia mabwawa
ya samaki, kwakweli Bahati aliumia zaidi baada ya kuambiwa vile kuwa kwao
walimshambulia Erica, kwa jinsi alivyochukia alitamani hata aruke kwenda kwao.
Ila alimsindikiza kwanza Erica dukani akanunue soda na kurudi kwao kisha yeye
akaondoka kwenda kwao. Erica alirudi ndani kwao na kula, kisha
alipomaliza alikaa na mama yake kumueleza maana muda huo aliamua kumueleza siku
hiyo kuhusu shemeji yake, “Mama, naomba saizi nikwambie ukweli
kilichotokea kwangu juzi” “Haya niambie” “Mama, shemeji alienda
na mimi hotelini kupata chakula cha jioni, nikaletewa kinywaji baada ya kunywa
nikahisi kizunguzungu na kutokujielewa kabisa, alikuja tu mtu kuninyanyua na
kuniondoa eneo lile kiukweli hata sikuelewa. Sasa nilipozinduka ndio Yule mtu
akaniambia ukweli, mama shemeji alitaka kunibaka” “Kheeee nilikaa kimya
nikisubiria hiyo kauli yako ya kusema alitaka kukubaka, hivi Erica huna aibu
kabisa! Yani James anavyotusaidia kwenye nyumba hii, ni kitu gani ambacho James
hatusaidii? Leo hii ndio atake kukubaka kweli? James amekujua wewe hata kujitoa
tongotongo huwezi halafu leo hii useme James alitaka kukubaka! Erica una
matatizo gani wewe mwanangu?” “Mama, kwani James kakupa nini wewe? Kama
ameweza kutembea na msichana wa kazi hadi kumpa mimba, ndio ashindwe kunibaka
mimi! Hebu mambo mengine uwe unafikiria mama yangu, nimeamua kukwambia ukweli,
ukiukubali haya na ukiukataa haya, ila Yule James sitaki tena msaada wake, sio
mtu mzuri kwangu Yule. Anataka kunibaka, hata kama unamuamini vipi ila ndio
hivyo alitaka kunibaka” Erica aliinuka na kwenda chumbani maana hakutaka
mama yake amuelewe au asimuelewa ila yeye alitaka kusema ukweli na ndivyo
alivyofanya. Alitaka kulala ila kabla hajalala alipigiwa simu na Babuu
akiulizwa hali yake na kumjibu kuwa yupo salama, “Vipi naweza kukuona
kesho” “Mmmh nitaangalia kama nitakuwa na muda” “Jamani Erica,
basi hata nije kwenu nikuone” “Nitakwambia basi, ila usipende kunipigia
pigia sana simu usiku mimi ni mchumba wa mtu” “Ila Erica kwani huyo mume
unaishi nae jamani! Najua upo kwenu ndiomana nimekupigia” Basi akaongea
ongea nae kidogo pale na kulala, ila ikiwa ni saa kumi alfajiri alisikia kama
mlio wa simu yake, akaangalia na kukuta ni Rahim alimtafuta, akajua lazima
atakuwepo facebook akaamua kuingia kwenye simu yake, “Tayari
nishakutumia Erica, nimekutumia milioni mbili” Yani Erica hadi usingizi
ulikata maana alijua hela ya matumizi angemtumia ndogo tu ila kuona kamtumia
hela nyingi alijikuta hadi akiamka vizuri na kuendelea kusoma jumbe zingine za
Rahim huku akimjibu na kumshukuru. Kwa upande mwingine alianza kupanga matumizi
kwa ile hela aliyotumiwa, alikuwa tu akijisemea “Ila mimi sinaga
matumizi ya hela nyingi hivi. Yani laity Rahim angejua kama maisha yangu ni ya
kawaida kabisa hata asingehangaika kunitumia hela nyingi hivi” Aliongea
ongea pale na Rahim kwa njia ya ujumbe huku akipanga kuwa kesho yake ndio aende
akatoe zile pesa. Kulipokucha aliamka saa nne asubuhi kwasababu
toka ile saa kumi alikuwa akitumia tu facebook mpaka saa moja asubuhi, sasa
alilala tena na kuamka saa nne. Alimkuta mama yake sebleni na kumsalimia kisha
mama yake akamwambia, “Mmmmh hii tabia ya kuamka saa nne hapana
mwanangu, haifai kwa mtoto wa kike” “Samahani mama, ni leo
tu” “Ni leo tu wapi wakati ndio tabia yako siku hizi hiyo, hata sijui
chuo unasomaje” Alimkanya kanya pale ila baada ya hapo tu Erica
alijiandaa na kutoka. Moja kwa moja alienda benki ambayo ingekuwa rahisi
kwake kutoa zile pesa, alipokuwa nje alipigiwa simu na Babuu akiulizwa mahali
alipo, sababu hakuwa na mashaka yoyote na Babuu alimtajia tu alipo kisha akakata
simu na kuingia benki ila muda kidogo Babuu alimtumia ujumbe, “Unajua
mimi muda huu hata sipo mbali na hapo uliposema, nakuja nitakusubiri nje nipo na
mamdogo” “Sasa mamako mdogo wa nini?” “Niliwahi kumwambia kuwa
kuna msichana mmoja niliwahi kumpenda sana, ndio leo nimekutana nae kanisikia
nikiongea nawe kwenye simu kapenda akuone” “Mmmh! Haya sawa, utanisubiri
basi” Erica alifanya zile harakati zake za kutoa pesa na kuweka katika
pochi yake kisha akatoka, na alishasahau wazo la kuonana na Babuu kabisa kwani
alipochukua zile hela akili yake ilikuwa ikiwaza hela tu. Akawa
anaondoka, mbele kidogo Babuu alimuita, “Erica, Erica,
Erica” Erica akageuka nyuma na kumuangalia Babuu akamuona kwa mbali kuna
mwanamke kasimama nae, alipomuangalia mwanamke Yule vizuri aligundua ni
Mrs.Peter yaani mama yake Rahim. Erica alifanya zile
harakati zake za kutoa pesa na kuweka katika pochi yake kisha akatoka, na
alishasahau wazo la kuonana na Babuu kabisa kwani alipochukua zile hela akili
yake ilikuwa ikiwaza hela tu. Akawa anaondoka, mbele kidogo Babuu
alimuita, “Erica, Erica, Erica” Erica akageuka nyuma na
kumuangalia Babuu akamuona kwa mbali kuna mwanamke kasimama nae, alipomuangalia
mwanamke Yule vizuri aligundua ni Mrs.Peter yaani mama yake Rahim. Erica
alishtuka kidogo na akili ya haraka haraka ikacheza kuwa Yule ndio mamake mdogo
na Babuu kwahiyo kuna undugu flani upo kati ya Babuu na Rahim, hakutaka kupoteza
muda kwakweli maana aliisikia bodaboda ikipitakaribu yake aligeuka na
kuisimamisha akapanda na kuondoka bila kujali Babuu alimuita kwa kiasi gani,
kwani hakutaka kuanza kuulizana tena maswali na Yule mama halafu alihisi Yule
mama hajamuona vizuri kwahiyo alishukuru ile bodaboda kupita karibu yake, yani
ni alimuelekeza tu kwao kisha Yule wa boda boda akampeleka. Erica
alifika kwao na kuingia ndani akamkuta mama yake akiendelea na ile kazi yake ya
kushona, akamsalimia mama yake kisha baada ya salamu alimuuliza mama
yake, “Mama unataka hela?” “Hivi kuna mtu asiyetaka hela
mwanangu? Katika dunia hii, kuna mtu asiyependa hela? Nataka ndio” Erica
akaingia kwanza chumbani kwake, halafu akamchomolea mama yake laki tano na
kumpelekea, mama yake alihamaki sana, “Erica, hela zote
hizi?” “Ndio mama, kwani kuna tatizo gani?” “Isije kuwa ndio
posa napewa kwa mtindo wa tofauti!” “Hapana mama sio posa, ila kuna
mwanaume ananitongoza ndio kanipa hela hizo” “Kheee mwanangu jamani, una
bahati sana. Huyo mwanaume mlete nyumbani haraka umtambulishe. Nitawapa baraka
zote” Erica akacheka na kusema, “Mama na wewe” “Sio mama
na wewe, mwanaume wa kukupa hela zote hizi ni wa kumshikilia tena umshikilie
haswaaa, ungemleta tu nyumbani nimtambue” “Nitamleta mama, ila kwasasa
hayupo nchini. Akirudi tu namleta” “Wow, Erica sikujua kama una akili
kiasi hiko, yani umetafuta mwanaume wa maana kiasi hiko! Erica mwanangu nakupa
Baraka zote kwa huyo mwanaume” Erica alitabasamu sana na kwenda chumbani
huku akimuwaza mama yake pia kuwa anaona pesa mbele tu na kama angemuonyesha
zote ambazo Rahim alikuwa anatuma ingekuwaje. Erica alitulia chumbani kwake
akiwaza vitu vingi sana, hakuwa na matumizi mengi ya pesa kama wanawake wengine
kwahiyo ile pesa kwake ilikuwa ni nyingi sana. Alichukua simu yake na
kukuta amepigiwa sana na Babuu, kisha akaamua kumpigia, “Erica mbona
umenikimbia? Umefanya nionekane mjinga kwa mamdogo” “Sikutaka tu
kukwambia ukweli ila sikutaka kuonana na ndugu yako yoyote” “Kwani kuna
tatizo gani Erica, maana hata Yule mamdogo ameuliza kuwa kwanini
ulikimbia” “Kwani aliniona wakati naondoka?” “Amekuona ndio
wakati ile bodaboda uliyopanda ikiondoka, akaniuliza kuwa wewe ni Erica
gani?” “Ukamjibuje?” “Sikumjibu chochote sababu
hakufahamu” “Babuu sikia, mimi hukuniandaa kabla zaidi ya kuniandikia
ujumbe tu kuwa upo na mamako mdogo, kiukweli sikujiandaa kukutana na mtu
mwingine yeyote asiyenizoea. Nisamehe kwa hilo” “Poa. Usijali
Erica” Alikata simu kwani alianza kuwaza namna ya kumkwepa Babuu kwani
aligundua kuwa Babuu ana undugu na Rahim yani ni mtoto wa mamkubwa na mdogo na
hawezi kumuacha Rahim kwasababu ya Babuu kwahiyo alitafuta njia tu za kumkwepa
Babuu. Alitulia ila jioni yake alisikia mtu akigonga geti lao, akatoka
na kukuta ni Bahati, akamuuliza kwa mshangao, “Bahati tena! Umekuja
kufanya nini sasa?” “Erica sikujua yote ambayo ndugu zangu wamekutendea,
Erica bora hata ndugu zangu wote wanitenge lakini sio wewe. Nakupenda
sana” “Ila mimi sikupendi” “Erica najua unasema kwa hasira tu,
nakupenda sana. Wewe ndio mke wangu, ndoto zangu zote ni kuwa na wewe. Nakupenda
Erica wangu” “Hivi Bahati nifanye kitu gani ili uamini kwamba sikutaki
tena? Sijawahi kukupenda Bahati na sitokupenda kamwe, yupo mwanaume mwingine
nimpendaye” “Ndiyo huyo Erick au?” “Sio Erick ila yupo mwingine
nimpendaye, tafadhali bahati endelea na mambo yako tu” “Kama hunitaki
Erica ujue nipo tayari nifie hapa mlangoni kwenu” Erica alimuacha pale
mlangoni na kuingia zake ndani. Erica alikaa ndani kwao kwa
muda sana ila akafikiria akili za Bahati akaona kuwa hawezi kuondoka pale, na
kiukweli hakupenda kuona Bahati akiteseka sababu yake, akaamua kutoka nje na
ilikuwa saa nne usiku lakini alimkuta Bahati pale pale nje, kwa bahati siku hiyo
mamake alikuwa ndani tu kwahiyo angetoka toka nje angemuona
Bahati. Alimkuta pale ikabidi aongee nae kwa utaratibu, “Bahati
jamani, unajua sipendi kuona ukipata shida au kuhangaika” “Ila mimi
nahangaika sababu yako Erica, nakupenda sana” “Sikia nikwambie kitu,
kama wanipenda sana naomba huu muda unaopoteza hapa utulie ufanye biashara zako.
Kwa hakika ukitoka kimaisha itakuwa rahisi kuwa na mimi” “Ila Erica,
mimi nahangaika kwenye shughuli zangu sababu yako ila wewe kama hunitaki tena
shughuli zangu zina maana gani! Sioni umuhimu wa shughuli zangu ikiwa hunitaki
tena” “Kwahiyo nikikutaka ndio utakuwa busy na shughuli
zako?” “Nitafanya shughuli zangu kwa raha sababu najua
upo” “Sasa Bahati jamani, fanya shughuli zako kwaajili ya watoto wako na
sio mimi” “Hao watoto nitapata nikiwa na wewe Erica, nakuomba Erica uwe
na mimi” “Sikia basi masharti yangu, ukifata haya masharti ndio nitakuwa
na wewe” “Niambie hayo masharti Erica” “Nataka uwe busy na
biashara, unanipigia simu hovyo hovyo ndiomana nilizima simu yangu. Sitaki
unipigie simu hovyo hovyo, nyumbani kwetu unapajua ila sio sababu yaw ewe kuja
kila unapojisikia. Nakuomba Bahati, tafuta maisha kwanza ndio iwe rahisi kwa
mimi kuwa na wewe, ukiendelea hivi kuhangaika hangaika kwa hakika hakuna kitu
utakachokuwa unafanya, yani utapoteza hela tu bila matunda yoyote. Tafuta maisha
kwanza” “Sawa Erica, ila basi naomba niwe naongea nawe hata kwenye simu
kidogo itakuwa afadhari kuliko hivi Erica. Usinione hivi ila nawaza maisha yetu
sana tu, hapa nataka nikiingiza faida ya kutosha kwenye ile biashara yetu,
nianzishe biashara nyingine ambapo ukimaliza chuo wakati unasubiria ajira
utakuwa unaendelea nayo” “Yani wewe una mawazo ya biashara
tu” “Ndio nina mawazo ya biashara ila hela tu ndio inakuwa shida kwangu
ila nina uhakika hizi biashara nikizikazania haswaaa yani maisha yatakuwa mazuri
tu. Maisha yetu yatabadilika Erica, siwezi chezea hela zile ulizonipa lazima
zizae matunda na ipo siku nitakufanyia kitu ambacho huwezi kukifikiria kuwa
naweza kufanya ila nitakufanyia kitu kikubwa sana Erica” Erica
alimwambia asubiri kidogo na kuingia ndani, Bahati hakujua ni kitru gani ambacho
Erica anaenda kufanya ila alimsubiria tu. Muda kidogo Erica alirudi na
kumwambia, “Sasa, nataka uwe busy na biashara, si umesema kuna biashara
unataka kunianzishia na mimi ili nikimaliza chuo nihangaike nayo. Sasa mimi
harakati za kuanzisha biashara kwasasa sina ila hela ninayo, nakupa hela hii
ukafanye hiyo biashara” “Lakini Erica sijasema kuwa nataka
pesa” “Nakuomba upokee hela hii Bahati, nina maana yangu halafu naomba
usiwe unanifatilia sana. Nahitaji kuwa huru sio kugandwa gandwa na mwanaume kila
ninapokuwa hadi nashindwa kupumua ndiomana sikutaki” “Ila hapana Erica
siitaki hiyo hela” “Kama hii hela huitaki basi, usinifatilie tena na
mimi na wewe basi” Ilibidi Bahati awe mpole na kupokea ile hela kwa
Erica huku akiahidi kufata masharti yake maana anaogopa kweli kuambiwa hatakwi
na Erica, kisha Erica alimwambia akodi bodaboda aondoke, “Ila bado kitu
kimoja Erica” “Kitu gani hicho?” “Naomba namba yako ya simu
nyingine” “Bahati, kwetu unapajua, kwa dadangu unapajua, chuo
ninachosoma unakijua unataka nini tena? Namba ya simu sikupi hadi ujirekebishe
tabia yako, sitaki unitafute mara kwa mara yani kuanzia leo hapa kwetu uwe
unakuja mara moja kwa mwezi” “Dah Erica kwanini lakini unanifanyia
hivyo?” “Siku ukiendelea na kununua gari ninalopenda mimi ndio
nitakuruhusu uje kwetu mara kwa mara, ila kwasasa kafanye kazi” “Dah!
Erica unanitesa lakini?” “Ukitaka kupatana na mimi fanya kile
ninachosema, fanya kazi kwa bidii maana sioni fahari niseme kuwa mpenzi wangu ni
mvuvi. Tafadhali jiimalishe na ubadilishe aina ya kazi. Kwaheri” Bahati
ilibidi akubali kila kitu maana alihisi pengine akiendelea kuongea labda Erica
atabadilisha mawazo tena na kumtimua kabisa, alipigia simu bodaboda kisha
ikafika akapanda na kuondoka zake. Erica alirudi ndani, yani
hata alikuwa hajutii kitendo cha kutoa hela kwa Bahati kwani yeye aliwaza kuwa
pengine baada ya Bahati kupata zile hela angemkimbia hata alishangaa kuona bado
Bahati akimng’ang’ania. Basi alienda kulala tu muda huo, ila kwa upande
wa Bahati alikuwa na hisia kubwa sana kuwa Erica anampenda sana sababu si rahisi
kwa mtu asiyekupenda kukupa pesa kama Erica anavyofanya kwa Bahati, aliiangalia
vizuri ile hela aliyopewa na Erica ilikuwa ni milioni moja na alipanga kufanya
kitu cha maana zaidi ili siku atakayoonana tena na Erica amuonyeshe kitu kizuri
alichokifanya, muda mwingi Bahati aliutumia akimfikiria Erica ila tofauti kwenye
kichwa cha Erica maana kwa kipindi hiko hakuweza kutumia hata sekunde tu
kumuwaza Bahati ila alifanya vitu ili Bahati aismfatilie tena wakati huo huo
hakutaka kumuumiza. Mawasiliano ya Erica na Rahim yalipamba moto na
hakutaka Babuu ajue chochote kwani aliwaza kama Babuu angejua basi
angemuharibia. Erica alifungua chuo na kwenda chuoni kama kawaida
akitokea kwao kwani toka yale maswala ya yeye kusifika kwa jina baya chuoni
hakutaka tena kuishi hosteli. Alikuwa akienda chuo na kurudi kwao huku
akiwasiliana na Rahim tu kwa kipindi hiko hata Babuu alipompigia simu alimwambia
kuwa yupo busy sana na masomo yake kiasi kwamba hawezi kuonana na mtu
yeyote. Siku hiyo Mage alienda nyumbani kwao kuzungumza na mama
yao, muda huo Erica alikuwa chumbani kwahiyo alisikia kila kitu ambacho dadake
aliongea na mama yao. Mama Erica alimsimulia Mage vile alivyoambiwa na Erica
kuwa James alitaka kumbaka, “Hivi unaamini hilo jambo
Mage?” “Mama, Erica ni ndugu yetu sisi tusimuamini halafu tumuamini
James inakuja kweli? Kumbuka James kampa mimba msichana wa kazi tena mama
sijakwambia lingine, kumbe kuna msichana pale mtaani kazaa na James nimezipata
hizo habari ila sijataka kumwambia mdogo wangu atachanganyikiwa” “Kheee
kumbe yule mwanaume ndio ana akili fupi kiasi hicho?” “Ndio hivyo mama
ila usipaniki wala nini, halafu hiyo habari ya James kutaka kumbaka Erica naomba
ibaki kuwa siri yetu na isifike kwa Bite, ana mtoto mdogo kwasasa
atachanganyikiwa” Mama yao alikubaliana nae na kumwita Erica ambapo
waliongea nae kuwa habari ile ifanywe kuwa ni siri kati yao. “Hakuna
shida, nimesema ukweli ili nisiendelee kusingiziwa kwenye mambo ambayo
sijayafanya” “Sawa, ila Erica nataka niongee mara moja na wewe
tu” Ilibidi muda wa kuondoka dada yake amsindikize na aweze kuongea
nae, “Nasikia Erica ulikuwa na mahusiano na Derick kabla ya kujua ni
ndugu yako” “Hapana dada, nani kakwambia?” “Usibishe Erica,
nataka nikusaidie unajua kutembea na ndugu ni laana tena laana kubwa sana tu,
nataka nikusaidie mdogo wangu” “Sijawahi kuwa na mahusiano
nae” “Basi ilimradi umekataa siwezi kukulazimisha” Basi Erica
aliagana na dada yake na kuondoka, aliwaza sana kuwa siri ya kutembea na Derick
nani kaitoa, akawaza tena kuwa pengine ni Derick mwenyewe ila amewezaje wakati
ni aibu kwa wote wawili, ila kwa upande wake aliona ni vyema kumkatalia dada
yake kuwa hajawahi kuwa na mahusiano na Derick kabla. Kipindi
hiki chuoni hakuwa na makubwa sana kwani wale waliokuwa wakimtisha wote
walishamaliza chuo yani Tumaini na Dora walishamaliza kwahiyo alibaki na watu
wachache tu, hata Derick alikuwa kashamaliza na walikuwa wakijiandaa kwaajili ya
kwenda kwenye mahafali. Ilikuwa kesho yake ndio siku ya mahafali na
Erica alipanga siku hiyo ya kesho asifike kabisa chuoni, ila akakutana na
Fetty, “Erica umepotea sana” “Fetty kumbe upo!! Nilijua ni mmoja
kati ya waliomaliza chuo” “Nipo ndio, ila pole nasikia kipindi cha
likizo ulipata matatizo” “Matatizo gani tena?” “Si nasikia
ulitekwa” Akakumbuka kuwa dada yake alimwambia kwamba kupotea kwake
aliulizwa na Derick kwahiyo kwa vyovyote vile ni Erick ndio kasema habari hiyo
ila aliamua kuikana pale kwa Fetty kwani alijua habari bila kuikana ndio inazidi
kutembea na kukuchafulia jina, kisha Fetty akamuuliza tena, “Vipi kesho
umeandaa zawadi gani za kuwapa watu wako wa karibu?” “Hapana kesho
siji” “Kwanini?” “Sina mtu yeyote wa karibu, sitakuja
kesho” “Ila ungekuja Erica, ungepata uzoefu wa mahafali yako
mwakani” “Fetty, mahafali yangu mwakani itakuwa ya kipekee kwahiyo sina
haja ya kupata ujuzi” Kisha akamuaga Fetty ila lile swala la kusema kuwa
mahafali yake mwakani yatakuwa ya kipekee lilimuingia vizuri sana Fetty kwenye
akili yake, ila alimuangalia tu Erica muda mwingine alimuona kama ni msichana
mwenye malingo sana. Erica aliondoka na kurudi kwao, usiku wa siku hiyo
aliwasiliana sana na Rahim, “Nataka kuja nchini Erica” “Wow,
nitafurahi sana” “Ila sitasema nyumbani kama nimekuja nataka iwe siri ya
mimi na wewe. Nyumbani nitaenda tu ila sitaki wajue kama narudi siku
ipi” “Karibu sana Rahim, itakuwa ni lini hiyo?” “Nahisi baada ya
miezi mitatu au mine” “Ukija kipindi nimefunga chuo itakuwa vizuri
sana” “Basi utaniambia tarehe za kufunga chuo, ila nitakutumia pesa
kidogo ya maandalizi ya kunipokea” “Nitakwambia” “Ila ungependa
nikuletee zawadi gani?” “Yoyote tu Rahim” “Sema
bhana” “Basi niletee cheni, heleni na saa” “Aaah sawa,
nitakuletea na nimefurahi umetaja zawadi uitakayo” Erica aliwasiliana
kwa furaha sana na Rahim na alijiwekea asilimia mia moja kuwa Rahim ndio mume
wake moja kwa moja kwani kitendo tu cha kutaka kurudi kwaajili yake ni kitendo
cha tofauti, alilala akiwa na furaha sana. Siku hiyo alitafutwa
sana kwenye simu na Babuu ikabidi apokee ili asikie kuwa anataka kuongea nae
nini, “Nahitaji kuonana na wewe Erica” “Njoo nyumbani
kwetu” Kwa kipindi hiko Erica hakutaka kuonana na mtu mbali na nyumbani
kwao kwa kuhofia usalama wake, pia alikuwa akijilinda kwaajili ya mpenzi wake
Rahim. Babuu alifika nyumbani kwao na kumpigia simu ambapo Erica alitoka
nje kwenda kuzungumza nae, “Erica jana nilienda chuoni kwenu kwenye
mahafali” “Ulienda kufanya nini?” “Na nilijua utakuwepo kumbe
wala haupo, kuna ndugu yangu amemaliza chuo ndio nilikuwa pale kwenye mahafali
yako. ILa nilikutana na Yule rafiki yako Dora dah habari aliyonipa
sikuielewa” Kwa muda huo Erica hakutaka kufahamu ni ndugu gani wa Babuu
alikuwa kwenye mahafali ila alitamani kujua kuhusu habari alizopewa ni zile zile
za siku zote au ni habari gani, akamuuliza na kumsikiliza kwa makini kuwa ni
habari gani, akashangaa babuu akimpa zile habari ambazo zilizagaa chuo kuhusu
yeye. “Hizo habari ni za uongo Babuu” “Hata mimi sijaziamini ila
Erica, ningependa usafishe jina lako” “Sasa nitalisafishaje na wenyewe
washaamini hivyo?” “Nilihusu nikusaidie kulisafisha” “Kivipi?
Hebu niambie utalisafishaje” “Subiri utaona ila nitasafisha jina lako na
hautokuwa tena na sifa mbaya” “Haya nashukuru” Aliongea ongea
nae pale na kuagana nae, kisha yeye kurudi ndani kwao. Hakutaka kujua Babuu
atatumia njia gani kusafisha jina lake kwani hata jina lake kuchafuliwa bado
haikuwa tatizo sana kwake kwani aliamini kwasasa yupo mwanaume ampendaye na
mwenye vigezo vyote. Kitendo cha Babuu kusema kuwa anataka
kusafisha jina la Erica kwenye kile chuo kilifanya Babuu awe karibu sana na
Erica huku akiwasiliana nae mara kwa mara bila kumwambia kuwa ni njia gani
atazitumia kulisafisha jina lake. Erica alipoona anakaribia kufunga
chuo, alimtaarifu Rahim nae alimwambia tarehe atakayoenda kisha akamtumia pesa,
alimtumia milioni moja kwaajili ya maandalizi ya kwenda kumpokea. “Erica
naomba unitafutie hoteli ya kufikia maana sitaki kufika nyumbani moja kwa moja,
shida yangu nikuone wewe kwanza” “Sawa Rahim nitafanya
hivyo” Siku ambayo Rahim alikuwa anafika, Erica aliaga kwao kuwa anaenda
chuo mara moja kumbe alikuwa na yake ya kumpokea Rahim. Aliondoka kwao
na kwenda kutafuta kabisa hoteli ambayo Rahim angefikia kwasababu alishaambiwa
kuwa atafute kabisa hoteli ya kufikia Rahim. Alipokodi mahali akaondoka na
kwenda uwanja wa ndege sasa kwa lengo la kumpokea Rahim, wakati yupo ametulia
akimsubiri Rahim akapigiwa simu na Babuu, “Erica kuna mahali nakuona
halafu nina shida na wewe” “Shida gani?” “Tuonane kwanza Erica,
nina shida na wewe” “Babuu jamani, tutaongea siku
nyingine” “Unajua nakuona, upo uwanja wa ndege” Erica akaona
ameonekana kweli, ikabidi tu amwambie amfate ili aongee nae, muda kidogo Babuu
alifika, kwahiyo hakuwa mbali na pale kwakweli Erica alihisi kama akili inamruka
vile kwani kabla hajaongea na Babuu, alipokea ujumbe toka kwa
Rahim, “Erica, hii ni namba yangu ya hapa, nishaingia nchini upo upande
gani mpenzi wangu?” Alihisi kuchanganyikiwa kabisa maana pale alisimama
na Babuu halafu Babuu ana undugu na Rahim. Erica akaona
ameonekana kweli, ikabidi tu amwambie amfate ili aongee nae, muda kidogo Babuu
alifika, kwahiyo hakuwa mbali na pale kwakweli Erica alihisi kama akili inamruka
vile kwani kabla hajaongea na Babuu, alipokea ujumbe toka kwa
Rahim, “Erica, hii ni namba yangu ya hapa, nishaingia nchini upo upande
gani mpenzi wangu?” Alihisi kuchanganyikiwa kabisa maana pale alisimama
na Babuu halafu Babuu ana undugu na Rahim. Akili ikamcheza pale na
kumwambia Babuu amsubirie pale kwani yeye anaenda uwani, Babuu alikubali na
Erica akaondoka. Simu yake ilikuwa ikiita sana na alikuwa akipigiwa simu
na Rahim, sababu alikuwa kachanganyikiwa hata kupokea hakuweza, alitafuta gari
ya kukodi na kupanda huku dereva akimuuliza kuwa anaenda wapi ila hata kumjibu
hakumjibu kwani akili yake ilishapotea kabisa. Muda kidogo akapokea
ujumbe mwingine toka kwa Rahim, “Mpenzi nimekutana na ndugu yangu ambaye
sikutegemea kukutana nae kabisa kwa muda huu, uko wapi nikutambulishe tu maana
nimemwambia asiseme popote nipo na shemeji yake” Erica alisoma ule
ujumbe na kuhisi akili kumruka kabisa. Akili ikamcheza tena muda ule ule
na kumwambia Yule dereva wa ile gari asogee yale mazingira ambayo Rahim na Babuu
wamesimama, alipokuwa anawaona vizuri alimwambia dereva asimamishe kwanza gari
kisha akachukua simu yake na kumpigia Babuu, “Hellow Babuu nina shida
huku uwani nakuomba mara moja” “Ila kuna ndugu yangu nimekutana nae
hapa, kuna mtu tunamsubiria au nije nae?” “Usitake kunikera Babuu,
nilishakwambia maswala ya kunijia na watu, wewe unajua nimekutwa na nini huku
hadi uje na ndugu yako? Njoo mara moja bhana” “Haya
nakuja” Babuu alionekana kumuaga Rahim na kuondoka, muda ule ule Erica
hakutaka kupoteza muda alimwambia dereva asogeze lile gari hadi alipo Rahim,
halafu akazima simu yake na kushuka ili kumshtua Rahim, kwakweli Rahim alifurahi
sana na Erica hakutaka kupoteza nae muda kwani alipanda nae kwenye lile gari na
kuondoka kuelekea hotelini ambako aliambiwa na Rahim kuwa amkodie hoteli. Muda
wote huo Erica alikuwa amezima simu yake kwani hakutaka Babuu ampate hewani
kabisa kwa muda huo. Walifika hotelini na kuingia kwenye chumba
ambacho Erica alimkodia Rahim, kisha kabla ya vyote Rahim alitaka kwenda kuoga
kwanza ila Erica alitoka mule ndani na kwenda kuagiza chakula, alipoenda kuagiza
chakula aliwasha tena simu yake na kukuta jumbe kama tatu za Babuu akilalamika
kuwa mbona simu haipokelewi, Erica aliamua kumtumia ujumbe, “Mwenzio
nimeshikwa na tumbo la kuhara, nimeona unachelewa nikaamua kukodi bajaji. Nipo
nyumbani saivi” “Sasa ile shida yangu ya maongezi na
wewe” “Tutaongea siku nyingine Babuu, mwenzio naugulia
tumbo” “Pole Erica” Basi aliposoma huo ujumbe, akazima tena simu
yake kwani hakutaka iwe wazi akihofia kupigiwa tena na Babuu. Alirudi
chumbani huku akisubiri kile chakula ambacho alimwagizia Rahim, na chakula
kilifika kisha yeye na Rahim wakala na kukaa wakifanya maongezi huku Rahim
akimtolea zile zawadi ambazo alimuagiza na Erica alizipenda sana kwani zilikuwa
za kuvutia, ilipoanza kuingia jioni Erica alimwambia Rahim kuwa anarudi
kwao, “Yani unamaanisha unataka uondoke Erica uniache peke
yangu!” “Sasa Rahim si nishafanya vyote ulivyosema?” “Ndio
umefanya ila leo huondoki hapa, yani tutalala wote kwakweli, huwezi ukaniacha
peke yangu niboreke basi haikuwa na maana ya mimi kutokufikia nyumbani
kwetu” “Ila sijaaga nyumbani Rahim!” “Sio tatizo, piga simu
nyumbani kwenu waambie kuna sehemu umeenda kufanya project ili wasiwe na mashaka
ila leo huondoki hapa” Ilibidi Erica awashe simu na kupiga simu kwa mama
yake kwani ndio anakuwaga wa kwanza kushikwa na uoga, akamwambia kuwa kuna
sehemu ya gafla wamesafiri kimasomo na wamechelewa kurudi kwahiyo kwao ataenda
kesho, mama yake aliitikia ila kwa shingo upande tu, ilibidi amuamini hivyo
hivyo ingawa ilikuwa ni ngumu sana kuamini kile alichoambiwa na
Erica. Erica hakuwa na namna nyingine zaidi ya kuwa pamoja na
Rahim tu kwani alishajitoa kuwa ndiye mpenzi wake, kwahiyo siku hiyo usiku mzima
alikuwa pamoja na Rahim. Palipokucha alikuwa amechoka kwakweli na
hakuweza tena kuendelea na chochote zaidi ya kumuomba Rahim arudi kwao
tu, “Nitakuruhusu Erica ila bado sijaridhika” “Basi naomba
nikapumzike kidogo tu nyumbani” “Mmmh mbona umeanza kunitisha mapema
hivyo? Hivi utaweza kweli kuishi kwenye ndoa?” “Nitaweza
ndio” “Sasa, mume mwenyewe si ndio mimi. Ndoa inahitaji uvumilivu Erica,
sasa kama vitu vidogo hivi kuvumilia huwezi vikubwa je?” “Sio hivyo ila
kumbuka nyumbani nimewaambia kuwa narudi leo sasa mama hawezi
kunielewa” “Sikia nikwambie kitu, tutakodi usafiri kwenda kwenu halafu
utamuaga mama yako kuwa mnasafiri kimasomo, utajiandaa halafu tutarudi tena hapa
hotelini. Hupendi kuwa na mimi Erica?” “Napenda” “Sasa kama
unapenda mbona unachoka mapema sana?” Erica hakuwa na jibu zaidi ya
kukubaliana na kile alichosema Rahim, kisha kujiandaa na kuondoka nae hadi kwao
ambapo Rahim alikaa mahali akimsubiri atoke kwao. Erica aliingia kwao
ila alikuwa na mawazo sana kwani katika maisha yake ya mapenzi yote, siku hiyo
alichoka na kuumia halafu mtu ndio anamsubiri bado ila kwavile alikuwa akiiota
ndoa ilibidi avumilie tu kwani aliona uvumilivu ndio
utamsaidia. Hakumkuta mama yake ndani, akajiandaa kisha akamuandikia
mama yake barua na kumuwekea laki mbili ndani yake kwani ugonjwa wa mama yake ni
hela na alishaujua kwahiyo alivyomuwekea hivyo alijua mama yake asingemsumbua
tena na angemuamini hiyo safari aliyoenda. Kisha akatoka na kumpigia
simu Rahim ambapo alikodi tena gari na kurudi nae tena hotelini. Walikaa
huko hotelini na Rahim ila baada ya siku tatu uzalendo ukamshinda Erica, ingawa
aliandika barua kwa mama yake kuwa ni safari ya wiki ila baada ya siku tatu
aliomba tu kurudi kwao, “Rahim, sidhani kama tunachofanya ni sawa. Maana
sie bado hatujaoana” “Ndio umetambua leo kwamba bado
hatujaoana?” Erica aliitikia tu ila alitamani apate nafasi ya kwenda
kupumzika, na kwa wakati huu Rahim alimruhusu kwani alisema kuwa ameridhika
kiasi, kisha akamwambia, “Swala langu linabaki pale pale, usiwe karibu
na mama yangu sawa!” “Sawa” Kisha ukafanyika mpango wa kurudi
nyumbani kwao. Kwakweli Erica kilanga cha kumuwaza Rahim
kilimuisha kabisa, akaanza kumkumbuka Bahati jinsi alivyokuwa mpole kwake,
akakumbuka siku alikutana na bahati kimwili ila alipomwambia amechoka tu Bahati
alimsikiliza na kumuacha apumzike ila kwa Rahim imekuwa tofauti maana hakujua
neno la nimechoka yani yeye ukisema nimechoka ni kamavile unasema endelea, Erica
aliwaza sana ila kwavile maji alishayavulia nguo akajisemea ni sharti ayaoge
maana bado kwenye akili yake alimuweka Rahim kama mume wake. “Kuna
wakati pesa ni mbaya sana, nimekuwa mtumwa wa penzi la Rahim sababu ya hele zake
ila isingekuwa hela zake wala nisingekuwa mtumwa kiasi hiki. Sijui kitu gani
nifanye nisipende hela, ila mimi sina matumizi makubwa ya hela tatizo lipo kwa
watu wanaonizunguka. Inabidi nivumilie tu kuhusu Rahim maana ndio mume
wangu” Alikuwa akijisemea tu mwenyewe, muda kidogo Mama yake alimuita na
kumuuliza vizuri mahali alipokuwa, “Erica, toka umeanza chuo sijawahi
kukusikia umesafiri kimasomo, eeeh kipindi hiki imekuwaje? Ulisafiri kimasomo
kweli?” “Ndio mama” “Erica mwanangu, kumbuka kuna mimba. Nahisi
sijawahi kukwambia swala hili, hebu kaa chini nikueleze” Erica alikaa
akimsikiliza mama yake sasa, “Erica, ukipata mimba na kuzaa kabla ya
ndoa halafu Yule mwanaume aliyekupa mimba asikuoe yani utayaona maisha kuwa
machungu sana mwanangu. Wanaume wengi hawapendi kuoa wanawake wenye watoto yani
utajikuta unaolewa na watu wazima sababu ndio wanakubali, kwenye vijana
wanaokubali ni wachache sana. Jichunge mwanangu, sitakuwa na furaha kukuozesha
kwa mzee pia sitakuwa na furaha kwa mwanangu wewe msomi kuzalia nyumbani. Naomba
ujichunge Erica” “Sawa mama nitajichunga” Alimuhasa sana maana
alitambua akili za vijana huwa zinabadilika kama kinyonga, baada ya hayo alienda
chumbani kwake na kulala, kiukweli alikuwa na uchovu sana maana alipokuwa na
Rahim hakupata muda wa kupumzika maana Rahim alikuwa kama mtu ambaye yupo
kazini. Kulipokucha alichukua simu yake na kuiwasha, na moja
kwa moja akampigia Rahim, kumuuliza kuhusu anavyojisikia na hali yake ikoje,
kisha akamuuliza kama ameshaenda nyumbani kwao, “Erica, mimi sikurudi
kwaajili ya kwenda nyumbani kukaa na mama, nilirudi nikiwa na maana yangu
kabisa” “Sasa utakaa hapo hapo hotelini?” “Ndio, nitakaa hapa
hapa, hakuna tatizo. Ukijisikia kuja niambie kwanza” Erica aliitikia ila
ile kauli ya niambie kwanza ilimpa mashaka maana aliwaza kuwa kwanini aambiwe
wakati ni jambo la kusema nipo nje, lakini kamwambia aambiwe kwanza, hakutaka
kuwa na mashaka nae sana na pia hakutaka kwenda kumtembelea wakati bado
anajiuguza maumivu yake ukizingatia hajawahi kuwa na mwanaume kwa kipindi kirefu
vile kwahiyo Rahim ni kama mwanaume wake wa kwanza kuwa nae kwa kipindi
kirefu. Kwahiyo kwa kipindi hiko alikuwa akiwasiliana na Rahim kwenye
simu tu. Erica alishukuru jinsi ambavyo Rahim hakumwambia tena kuwa
wakutane kwani alijua akikutana nae ni kwenda kuyazoa maumivu
mengine. Babuu nae hakuacha kumtafuta Erica kwani bado alikuwa
na ya kumueleza, ilipita kama mwezi mmoja ambapo Erica alimruhusu Babuu kwenda
kwao kuzungumza nae alichotaka kusema, hakumruhusu mapema kwa kuhofia kuwa Rahim
anaweza kufika kwao maana kwa mawazo ya Erica alihisi kuwa ni kwa kipindi
chochote kile Rahim angepeleka posa kwao, ila mwezi mzima ilikuwa kimya na wala
akiongea na Rahim kwenye simu haongelei maswala ya yeye kwenda kujitambulisha
kwao. Alihofia kuwa endapo Rahim angemkuta Babuu nyumbani kwa kina Erica
ingekuwa mtafaruku mkubwa, ila kwavile Rahim hakuonyesha lengo la kwenda kwakina
Erica ndipo Erica alipomruhusu Babuu kwenda kuzungumza nae. “Ila Erica
siku ile hukunifanyia vizuri kwakweli, yani kuniacha kwenye mataa
kweli!” “Nisamehe bure ni tumbo” “Sasa siku ile ulivyoondoka
alikuja ndugu yangu, yani sikutegemea kumuona pale na wala na yeye hakutegemea
kuniona. Tulisalimiana nikamuuliza vipi kumbe kama kawaida kwao hawajui kama
kaingia nchini, tena safari hii ameniambia anakomesha” “Anakomesha
nini?” “Yani huyo ndugu yangu ana wanawake wengi huyo ila mamake hajui
tu, anamuonaga mtakatifu balaa ila ana wanawake jamani dah! Siku ile yenyewe
kuna mwanamke wake mwingine alitaka kunitambulisha, Yule jamaa wanawake
wanampenda sababu ya ushombeshombe na wengine wanamuhonga sana pesa kiasi kwamba
hela zake anachezeaga tu hazina kazi” Erica alihisi kama kubanwa na
tumbo la kuendesha maana alijihisi vibaya na tumbo kuunguruma, aliomba kidogo
udhuru na kwenda chooni huku akiwaza kuwa anayoyasikia kuhusu Rahim ni kweli au
ni kitu gani, hakuelewa kwakweli ila alihisi kuchanganyikiwa
tu. Aliporudi alikaa tena na Babuu kumsikiliza hoja zake, ila
hakumuuliza alichokuwa akimuitia siku hiyo ila alimuuliza tu kuhusu huyo ndugu
yake, “Kwahiyo huyo ndugu yako ana wanawake wengi wapi? Hapa nchini
au?” “Yani ni hivi, Yule ni shombeshombe basi wanawake wengi wanavutiwa
nae, wengine huwa wanamtongoza wenyewe na kumpa pesa kiasi kwamba ana hela
nyingi sana Yule. Kwanza babake ana hela sana, kwahiyo babake tu anampaga hela
nyingi halafu na wanawake nao wanampa hela balaa, kwahiyo ana wanawake wengi
balaa ila ukimuona huwezi kumdhania anaonekana ni mpole balaa ila ni kicheche
hafai” “Babuu naomba uende, mama yangu atarudi muda sio
mrefu” “Ila swala langu bado sijakwambia” “Utaniambia tu siku
nyingine, ila kwasasa naomba uende” Babuu hakuwa na jinsi zaidi ya
kuondoka. Erica alihisi kuchanganyikiwa kabisa yani akili yake ilikuwa
haijisomi kwa muda huo tangu ameambiwa maneno yale na Babuu, alichukua simu na
kumpigia Rahim ila iliita sana hadi ilikatika, alikosa raha
kwakweli. Mama yake alirudi na kumkuta katika mazingira ya kutokuwa na
furaha, alimuuliza, “Nini tatizo mwanangu?” Leo Erica alijikuta
akimuuliza mama yake, “Mapenzi ni nini mama?” “Kheee swali gani
la kuniuliza hilo Erica?” “Samahani mama” Kisha akainuka na
kuelekea chumbani kwake, kwakweli akili yake haikuwa sawa kabisa kiasi kwwamba
hata siku hiyo hakuweza kupatwa na usingizi, alijikuta akishikwa na wivu
maradufu yani alitamani hata kufanya kitu asichokielewa ndipo alipotambua nguvu
ya wivu vizuri, “Yani Rahim, umetembea na mimi kumbe una wasichana
wengi. Kumbe unanipaga hela unayopewa na wasichana wako, kwanini Rahim umeamua
kunifanyia hivi?” Alilia sana, ila akawaza kitu kimoja je kama ana mimba
au ukimwi, maana ameshaambiwa kuwa Rahim ana wasichana wengi, alilia sana kisha
akasema kuwa kesho yake ataenda hospitali kupima mimba na
ukimwi. Aliwaza sana, kitendo hiko kilimfanya akose usingizi
kabisa. Kulipokucha Erica aliondoka kwao asubuhi na kwenda
hospitali ambapo alienda kupima mimba na ukimwi, majibu
yakaletwa, “Hongera, huna ukimwi ila una mimba” Alihisi akili
yake kuruka kabisa, akikumbuka ahadi yake ya mwisho alisema hatokuja kutoa tena
mimba katika maisha yake, ila sasa ana mimba ya mtu ambaye ni muhuni, aliwaza
sana na kulia kwa daktari hata daktari mwenyewe alimshangaa
akilia, “Sasa unalia nini wakati watoto ni Baraka kwa Mungu, hivi unajua
kuwa kuna watu wanatafuta watoto” “Tatizo sio mtoto, tatizo ni baba wa
mtoto” “Kwani kuna wanawake wangapi wanalea watoto wao bila baba? Hebu
ondoa mawazo mgando kwenye fikra zako. Kwa muda huu unatakiwa kuanza kuandaa
mazingira mazuri kwa mtoto ajaye.” Erica alitoka pale kwa daktari na
kuondoka bila hata ya kumuaga, akawaza kuwa mtu wa kwanza kumwambia ni Rahim,
kwa vyovyote vile alihisi pengine akimwambia Rahim kuwa ni mjamzito basi hilo
swala la kuwa na wanawake wengi litapotea kwa Rahim na ataanza kumfikiria yeye.
Akachukua simu yake na kumpigia Rahim ila iliita sana tu kama jana yake na bila
ya kupokelewa ila akakumbuka kuwa Rahim aliwahi kumwambia kuwa yupo hotelini kwa
mwezi mzima, ikabidi aende pale hotelini. Alifika chumba alichomkodiaga
Rahim na kugonga ila alifunguliwa na mwanamke, akawa anamshangaa Yule mdada
gafla akamuona Rahim akiwa amejifunga taulo yani ametoka
kuoga. Akachukua simu yake na kumpigia Rahim ila
iliita sana tu kama jana yake na bila ya kupokelewa ila akakumbuka kuwa Rahim
aliwahi kumwambia kuwa yupo hotelini kwa mwezi mzima, ikabidi aende pale
hotelini. Alifika chumba alichomkodiaga Rahim na kugonga ila
alifunguliwa na mwanamke, akawa anamshangaa Yule mdada gafla akamuona Rahim
akiwa amejifunga taulo yani ametoka kuoga. Akili ilimruka kabisa Erica
na kushindwa hata cha kufanya kwa muda huo huku akitamani hata kukimbia, wakati
amegeuka nyuma ili aondoke, alishikwa mkono na Rahim na kuingizwa chumbani,
kisha Yule mdada aliyekuwa mule chumbani kwa Rahim alitoka. Erica
alikuwa akilia sana, yani alilia hadi alihisi kuchanganyikiwa ila Rahim
alimkalisha chini, kisha kumuacha akilia halafu yeye akivaa nguo. Alipomaliza
alimsogelea na kumuangalia tu akilia hadi Erica aliona ni ujinga wa kuendelea
kulia, akanyamaza na kumuangalia Rahim kwa hasira sana, ila kabla hajaongea
chochote Rahim alimuuliza, “Sasa kinachokuliza ni nini?” Erica
alimuangalia Rahim na kuongea kwa gadhabu sana, “Yani bila hata aibu
unaniuliza kinachoniliza ni nini!” “Aibu gani sasa?” “Hivi Rahim
wewe ni mtu wa aina gani? Yani mimi nikutafutie hoteli halafu wewe ulale na
wanawake wengine?” “Kwahiyo hiyo hoteli uliyonitafutia unalipa wewe au
nalipa mimi?” Erica alizidi kupata hasira na kumwambia, “Hata
kama unalipa wewe ndio unifanyie mambo ya ajabu kweli? Ni haki
hiyo?” “Mambo ya ajabu yapi?” “Hivi unaona ulichofanya ni sawa?
Kulala na mwanamke mwingine unaona ni sawa?” “Erica hebu acha masikhara,
wewe ulichoka na nilikwambia kuwa nilirudi kwaajili yako ila ulidai umechoka
kwahiyo ulitaka nifanyeje?” “Yani Rahim ndio unaniambia hivyo kweli?
Asante sana” Erica akainuka, ila Rahim alimshika tena mkono na
kumkalisha chini kisha akamwambia, “Hebu acha mawazo ya kijinga,
nilikuwa napima uelewa wako na wivu kama unao. Hivi kweli Yule anagekuwa
mwanamke wangu angeondoka? Si angeanza kugombana na wewe? Halafu nianze tu
kutafuta wanawake na kulala nao kwenye chumba kile kile ulichonikodia? Si
nitakuwa sina akili, kwani hoteli hapa mjini zimeisha Erica? Kama ningekuwa na
tabia hiyo basi hata hii hoteli nisingekaa sana, lazima ningetafuta hoteli
nyingine ya kwenda kuwa na wanawake wengine” “Kwahiyo Yule mwanamke ni
nani?” “Hilo ndio swali ulilotakiwa kuniuliza toka mwanzo sio kuanza
kujiliza, Yule mwanamke nilimpa nguo zangu akanifulie na aliniletea leo, sasa
nikamwambia aniwekee kitandani sababu naoga, nashangaa ndio wakati anatoka sijui
wewe ndio umegonga na muda huo nimetoka bafuni. Yani una mawazo ya kijinga Erica
jamani! Huamini mama, amini nakupenda sana” Erica sasa akatabasamu kwani
hakuamini kama Rahim angeongea nae kwa uzuri kiasi kile, kisha akamuangalia na
kumuuliza, “Kwahiyo Rahim wewe sio muhuni?” “Hivi Erica,
ningekuwa muhuni ningehangaika nini kukutafuta wewe? Kwanza nani aliyekwambia
kama mimi ni muhuni? Sina hizo tabia mimi, nadhani hata mama yangu ashakwambia
mengi sana kuhusu mimi, sinaga mambo ya wanawake kabisa. Niambie kipenzi changu
maana naona umekuja kunishtukiza leo” Erica akafungua pochi yake na
kutoa yale majibu kuwa yeye ni mjamzito, kwakweli Rahim alonyesha kufurahi
sana, “Wow Erica jamani, umeamua kunibebea mimba! Nimefurahi sana Erica,
na mimi nitaitwa baba sasa” “Ndio, na mimi nitaitwa mama” “Sawa,
nakuomba Erica usitoe mimba yangu. Mwanangu nitamlea” “Siwezi kutoa, ila
uje nyumbani basi ujitambulishe na tufanye maswala ya harusi” “Sawa,
usijali kuhusu hilo, ila kwasasa nataka tena kusafiri. Yani nilitaka nikupigie
simu leo kuwa kesho narudi Marekani. Nitakuja safari nyingine na kuja kwenu
kujitambulisha na kukamilisha kila kitu” “Jamani Rahim, sasa itakuwaje?
Mama akijua?” “Usijali, mwambie mama, mume yupo yani sitakawia kurudi
Erica si unajua hata kwetu sijafika” “Sawa Rahim, ila mimba haina siri
mama akijua litakuwa balaa, unadhani mama yangu ataelewa nikimwambia kuwa mume
yupo? Hatonielewa kwakweli” “Usijali Erica, baada ya miezi miwili tu
narudi. Nitakuja kwenu kukamilisha kila kitu” Erica hakuwa na namna
zaidi ya kumkubalia Rahim tu kuwa kesho yake anasafiri na ataenda kujitambulisha
kwao akirudi baada ya miezi miwili ila alijipa moyo kuwa tumbo litakuwa bado
kujitokeza. Kisha Rahim akamwambia tena Erica, “Nakuomba leo tulale wote
mpenzi wangu ili kesho unisindikize” “Mmmh jamani hata nyumbani
sijaaga?” “Kwani na wewe huna njia ya kuaga nyumbani kwenu jamani Erica,
nahitaji kumuaga mwanangu, si unajua nasafiri naenda mbali. Naomba tulale wote
jamani Erica” Ilibidi Erica akubali na atafute namna ya kumwambia mamake
kwenye simu ili asiwe na wasiwasi. Kesho yake Erica aliamka na
Rahim kwenye ile hoteli kisha kujiandaa kwaajili ya kwenda uwanja wa ndege maana
Rahim alisema ndio safari yake imewadia, kisha Rahim alimpa hela Erica na
kumwambia, “Chukua hii milioni moja ikusaidie saidie maana mimba zina
mambo mengi sana, unaweza kutamani hiki mara hiki, hii pesa
itakusaidia” “Asante sana Rahim” Kisha Erica alichukua ile pesa
na kuiweka kwenye pochi yake, kisha Rahim alimwambia, “Erica napenda
kukwambia tena uwe mbali na mama yangu, sio saivi una mimba ndio unaenda
kumtafuta mama yangu sijui uwe nae karibu. Tafadhali kuwa mbali na mama yangu,
atakupa mawazo mama Yule. Mimba hazitaki mawazo Erica, mimba inataka pumziko la
moyo. Kuwa mbali na mama yangu, sitaki ndugu yangu yeyote awe karibu na
wewe” “Nimekuelewa Rahim ila kumbuka siku ile ulitaka kunitambulisha kwa
ndugu yako” “Yani Yule nilikutana nae kwa bahati mbaya, akaniuliza kuwa
mbona sijasema ujio wangu ndio nikamwambia yupo na shemeji yake yani
nikamgelesha tu ngoja nimtambulishe ila siku ile nilishukuru kweli alivyoitwa
maana hata mimi nilitaka kumfanyia mchezo pale wa bila kumtambulisha. Ndugu
zangu ni wambea wambea sana, ndiomana sipendi kuwa nao karibu. Ila nakusisitiza
tena kuwa mbali na mama yangu” “Nimekuelewa Rahim” Kisha
wakaondoka na kwenda uwanja wa ndege ambapo Erica alimuacha Rahim kaingia
uwanjani kisha yeye akarudi nyumbani kwao. Erica aliingia kwao ila kwa
muda huo mama yake hakuwepo kwahiyo alienda kuoga na kulala, alikuwa akishangaa
tu mimba ya kipindi hicho imeanza bila makeke ya kutapika au kujihisi
kichefuchefu. Erica aliamka usiku kwenye mida ya saa mbili na
kutoka chumbani kuelekea sebleni ambapo mama yake alikuwa amekaa,
akamsalimia, “Kheee kumbe ulirudi?” “Ndio nilirudi
mama” “Nilijua na leo utalala huko huko maana siku hizi unajiamulia
tu” “Ila mama si nilikwambia jamani!” “Erica mwanangu, Erica
binti yangu kila siku ninapokusema hapa unaona kama nakuonea ila ipo siku
utasema kweli mama alisema. Utanidanganya ila na mimi nilikuwa msichana kabla
yako, naelewa kila kitu. Nitakwambia ulikuwa kwa mwanaume ila utabisha, sawa
nidanganye tu ila mimi si ndio mama wa kudanganywa! Unasahau kama mama unatakiwa
umweke kama rafiki yako na umshirikishe mambo yako ili akushauri zuri na baya,
mwanangu hujaolewa bado, unawezaje kwenda kwa mwanaume na kulala nae hadi
asubuhi? Unajua wewe si mke, unawezaje kufanya hivyo? Mwanaume wa hivyo atakuoa
kweli? Hakuna mwanaume anayetaka kuoa mwanamke asiyetulia, atakuchekelea kuwa
ndio vizuri tulale wote hadi asubuhi ila kumbuka si mumeo huyo, ni mpenzi wako,
hata kama kakuahidi ndoa, basi subiri ndoa ndio ukakeshe nae kwenye kulala ila
sio mwanaume wakuitana sijui baby halafu unalala nae hadi asubuhi” “Ila
sikuwa kwa mwanaume mama” “Huwezi kukubali ila mimi ni mama naelewa kila
kitu na ipo siku utayakumbuka maneno yangu, napenda upate mwanaume mwenye pesa
aje kuwa mume wako ila sijasema ukipata mpenzi mwenye pesa basi ujiachie ukalale
nae. Sijasema hivyo, hata kama huyo mwanaume awe na pesa kiasi gani ila kitendo
cha wewe kwenda kulala kwake hadi asubuhi ni kujishushia heshima. Sio mke wewe,
usitake kujifanya unachukua majukumu ya mke kabla hujaingia kwenye ndoa. Yangu
ni hayo, utasema mama vipi anaongea sana ila maneno yangu
utayakumbuka” Erica alimtakia mama yake usiku mwema kwani alijua
akiendelea kuongea nae pale basi mama yake yatamtoka maneno mengi sana na
hakupendezewa nayo sababu yalikuwa yanamchoma. Alirudi chumbani kwake na
kutafakari maneno ya mama yake ila aliona hata akiyatafakari bado hayana
suluhisho kwake maana kama mwanaume kashalala nae kwa siku za kutosha tu, na kwa
kipindi hiki ana mimba kwahiyo maneno ya mama yake yalikuwa ni msumari wa moto
lakini usioweza kumchoma muhusika maana tayari ameshakosea. “Inabidi
mama nisimwambie kama nina mimba hadi pale Rahim atakaporudi na kujitambulisha
nyumbani. Natumaini tumbo halitakuwa kubwa” Alijipa moyo maana alijua
ikiwa mama yake atagundua kuwa ana mimba itakuwa ni balaa
hilo. Chuo kilifunguliwa na alianza tena kwenda chuo ila kwa
kipindi hiki alikuwa anachoka sana yani ile kwenda chuo na kurudi tena nyumbani
kwao ilikuwa ni swala la uchovu sana, ilibidi awasiliane na Rahim amwambie kuwa
anapata shida ya kutoka kwao kwenda chuo, “Kumbe hiko chuo ulichohamia
unakaa nyumbani?” “Ndio, nachoka sana” “Basi tafuta chumba cha
kupanga karibu hapo, nitakutumia hela ya kodi na nyingine ununue kitanda na
godoro upate sehemu ya kupumzika ukitoka chuo yani kwenu uende mara moja moja
sana” “Nashukuru sana kwakweli” Basi Erica alitumiwa hela na
Rahim kisha alitafuta chumba kwenye maeneo karibu na chuo na kuweka kitanda na
godoro na vitu kadhaa tu vya kumsadia akiwa kwenye chumba kile na kukaa, yani
akawa akitoka chuo anarudi kwenye kile chumba ila mama yake alimdanganya kuwa
anaishi hosteli, hakutaka kusema amepanga maana mama yake asingependezewa na
swala la kusikia kuwa amepanga. Kwa kipindi hiko alikuwa anaenda tu kwao
kwa kuchungulia yani siku hiyo hiyo anaondoka kiasi kwamba mama yake aliuliza
ila alidanganya kuwa masomo ya mwishoni yanasumbua sana akili kwahiyo muda
mwingi anatumia kusoma. Kwa kipindi hiko hakutaka kukutana na mtu yeyote
wala hakwenda kwa ndugu yake yeyote kiasi kwamba alikuwa akipigiwa simu na
shemeji yake James alikuwa akikata kwani hakutaka kabisa kuongea na shemeji yake
huyo. Siku hiyo akiwa anaelekea kwake alisimamishwa na Fetty
njiani, “Erica, mbona siku hizi umebadilika sana?” “Nimekuwaje
kwani?” “Umenenepa, wakati wewe sio mnene maana mwili wako huwa kawaida
tu ila kwasasa umenenepa” “Pengine sababu nakaribia kumaliza
chuo” “Vipi umewahi kuonana na Derick hivi karibuni?” “Hapana,
kwani imekuwaje?” “Mwenzangu Derick kumbe kuna wadada wawili hapa chuo
kawazalisha halafu hana mpango wa kuwaoa wala nini, hadi nikasema loh na rafiki
yangu Erica angeingia mkenge kumbe!” “Hivi inakuwaje mwanaume
anadanganya watu wawili kwa wakati mmoja?” “Kheee hujui eeeh! Sasa mbona
Derick alikuwa anakudanganya wewe wakati ana wanawake wengine? Yani mwanaume
akikwambia nakupenda msikilize palepale ila ndio usijiwekee moyoni ukaona
unapendwa balaa. Yani wanaume wenzako sijui wana mioyo mingapi maana mmoja
anaweza akapenda hata kumi” “Na wote akawaonyesha upendo
sawa?” “Ndio, mwanaume hashindwi ila nadhani anakuwepo mmoja anayependwa
sana. Ila mwenzio unafikiri wanaume nawaamini sana hata siwaamini, usiniona hivi
nishatoa mimba hadi sijui kama nitazaa tena, yani wanaume hawa loh! Kwahiyo
unaishi wapi siku hizi?” “Huko chini” “Basi siku moja nitakuja
kukutembelea unapoishi” “Sawa karibu” Fetty aliondoka na Erica
alienda anapoishi ila sio kwamba maneno aliyoambiwa hayakumuingia hapana,
yalimuingia vilivyo kuwa mwanaume mmoja anaweza kuwa na wanawake hata kumi,
alijihisi kuwa na wivu sana yani wivu aliokuwa nao kwa Rahim hajawahi kuwa na
wivu wa kiasi kile hadi alikuwa akijihisi vibaya, wivu wake kwa Rahim ulimfanya
hata akimtafuta hewani asipopatikana ajihisi vibaya sana na kugundua kuwa hisia
zake kwa kipindi hiko zinaendeshwa na wivu. Fetty alionekana
kumfatilia sana Erica na mwisho wa siku akapafahamu Erica alipokuwa akiishi, na
alikuwa akienda kumtembelea mara kwa mara ila Erica hakumwambia kama anaujauzito
ingawa tumbo liliendelea kuwa mbele, “Erica kama una
mimba!” “Jamani kwanini?” “Nikuonavyo tu” “Hapana sina
mimba” “Ila kuwa na mimba ni swala la kheri Erica, unajua mimba
zinatafutwa siku hizi! Mimi mwenyewe nikibeba mimba nazaa tu, umri ushaenda
nitajibana bana hadi lini, yani mimba ikijichomekea tu nazaa” Erica
alikuwa akicheka tu ila hakuthubutu kumwambia Fetty kuwa ni mjamzito ingawa
dalili zote alikuwa nazo halafu naye Fetty alishamuhisi kuwa Erica ni
mjamzito. Mara zote Erica alizokuwa akiwasiliana na Rahim alikuwa
akimuuliza tu kuwa atarudi lini ili aende kujitambulisha nyumbani kwao, ila
Rahim alimwambia swala moja tu kuwa ataenda karibuni, “Unajua Rahim
mimba hii inazidi kukua yani hata nyumbani wakijua sijui nitasema nini, utakuja
lini Rahim?” “Erica, usiwe na mashaka. Nitakuja tu yani hata usiwe na
wasiwasi” “Ila lini Rahim nijue siku niwe na uhakika” “Usijali
Erica, nitakuja tu” “Kumbuka uliniambia baada ya miezi miwili ila hadi
leo kweli ni miezi mingapi imepita Rahim? Hata huonekani jamani na husemi lini
utakuja” “Erica usijali mpenzi wangu, nitakuja tu” Yani jibu la
Rahim lilikuwa ni moja tu kuwa nitakuja usijali, wakati kwa upande wa Erica
aliona karibia siri itabumbuluka maana kama nyumbani kwao alikuwa akienda na
kuondoka ila alijisemea tumbo likizidi sana basi kwao hatokwenda
kabisa. Mimba ya Erica iliendelea kukua na kipindi hiki
walifanya mitihani ya mwisho chuoni kwahiyo wakafuna chuo ili wasubirie majibu
nyumbani na baada ya hapo yafanyike mahafali, akaona kwenda kuishi kwao na mimba
ishaanza kuwa kubwa ni swala la aibu kwahiyo aliendelea kuishi pale pale huku
akimdanganya mama yake kuwa bado chuo hajamaliza. Ulipita mwezi bila ya
Erica kwenda nyumbani kwao, mama yake akawa anamlazimisha kwenye simu kuwa arudi
nyumbani, “Erica mwanangu hebu rudi nyumbani” “Bado chuo
mama” “Bado nini? Mbona nasikia chuo mshamaliza muda
tu” “Tumeambiwa mpaka tusubiri matokeo” “Sasa kwanini hayo
matokeo usije kuyasubiria nyumbani jamani” “Hamna mama” “Hebu
niambie ukweli, nini kinakusibu mwanangu?” “Hamna kitu
mama” “Una mimba Erica?” Erica akashtuka na kushindwa hata
kumjibu mama yake, Yule mama alipoona kimya alimuuliza tena, “Una mimba
Erica?” Erica bado alikuwa kimya maana alishindwa kumjibu mama yake
ingawa ni kwenye simu. Mama yake aliendelea kuongea, “Erica, kumbuka
mimi ni mama yako na unapaswa kuniambia ukweli. Hivi ukinificha mimi utamwambia
nani?” “Sina mimba mama” “Sasa kwanini hutaki kurudi nyumbani?
Erica kama ni mjamzito halafu unanificha utakuwa umetenda kosa kubwa sana,
kwanza umenikosea mimi na umemkosea Mungu, unawezaje kupata mimba nje ya
ndoa?” “Sina mimba mama” “Rudia tu hayo maneno na iwe kweli huna
mimba maana ukiwa nayo sijui nitakufanya nini? Erica wewe ni binti yangu wa
mwisho, tunahitaji kucheza harusi yako, tusherekee kwa furaha sio uniletee
watoto nyumbani kabla ya ndoa. Narudia tena jichunge” “Nitajichunga
mama” “Sawa, na vipi kuhusu kurudi nyumbani?” “Nitarudi mama
usijali” Mama yake Erica alimsisitiza sana Erica kuhusu swala la kurudi
nyumbani, huku Erica akihofia kuonekana kwao akiwa mjamzito, na yale maneno ya
mama yake ndio yalimtisha maradufu hakujua mama yake angemwambia kitu gani pindi
akimkuta mjamzito. Siku hiyo alikuwa akiwasiliana na Rahim
kwenye mtandao wa facebook kama kawaida, alishangaa kukutana na ujumbe wa
Tumaini, “Erica, mambo vipi. Nimekumiss jamani, natamani nikuone. Erick
alirudi ila tulikutafuta hewani bila kukupata, na hajapenda kusikia nina ugomvi
na wewe. Anataka kuona tukicheka pamoja, alikuja na zawadi zako kaniachia
nikupatie, sasa je nije kwenu kukuletea” Erica alisoma mara mbili mbili
ila hakumjibu maana alijua kama akimruhusu atagundua kuhusu mimba yake maana kwa
kipindi hiko ndio tumbo lilikuwa limejitokeza haswaa, ila alijipa moyo kuwa
hawezi kuonana nae sababu haishi nyumbani kwao. Akiwa amekaa mule kwenye
chumba chake alisikia mlango wake ukigongwa, akainuka na kwenda kufungua,
akashtuka sana maana mlangoni alimuona Fetty akiwa ameambatana na mama yake
Erica. Akiwa amekaa mule kwenye chumba chake alisikia
mlango wake ukigongwa, akainuka na kwenda kufungua, akashtuka sana maana
mlangoni alimuona Fetty akiwa ameambatana na mama yake Erica. Erica
hakujielewa kwa muda huo, ila mama yake naye alipiga yowe kama kapatwa na habari
za msiba, “Yereeeee uwiiiii Mungu wangu, Erica mama umeniabisha. Uwiii
ndio msomi wangu wewe!” Huyu mama ilionyesha kachanganyikiwa kabisa,
ikabidi Fetty amuingize ndani kwa Erica kwa kuhofia kujaza watu pale
nje. Erica nae kwa upande wake hakujua ni kitu gani atafanya na mama
yake, ila wakati mama yake ndio kaingizwa ndani ili waweze kuzungumza wakiwa
ndani, Erica alipiga magoti na kutaka kuanza kumuomba msamaha mama yake ila
kabla ya kuongea alianza kulalamika tumbo kumuuma na alionekana kuwa na hali
mbaya gafla, ilibidi mama yake aache kulia sasa na kuanza kushughulika kumsaidia
mwanae, ambapo Fetty alienda kuchukua gari ya kukodi kisha wakaenda hospitali,
Erica aliingizwa kwa daktari. Mama yake alibaki nje akiwa na mawazo sana
juu ya mwanae, aliwaza vitu vingi maana mimba zina mambo mengi sana, akachukua
simu yake na kupigia dada zake Erica ambao walishangaa pia kwa lile waliloambiwa
na mama yao, kisha baada ya muda mfupi nao walifika hospitali alipopelekwa Erica
ila mpaka muda huo bado daktari hakutoa majibu yoyote na kufanya wamkute mama
yao kuwa na mawazo sana, “Mama jamani, punguza presha” “Yani
sielewi hapa watoto wangu, sielewi kabisa” “kwanza imekuwaje mama? Hebu
tueleweshe kwa ufupi, najua Mungu atamsaidia mdogo wetu na atakuwa
salama” “Sikilizeni, nadhani niliwapigia simu nikiwaambia kuhusu
mwenendo wa mdogo wenu kuwa nasikia washamaliza chuo ila yeye hataki kurudi
nyumbani, ila nyie mkapuuzia wakati haya mambo ilibidi yachukuliwe kwa umakini
sana, kwakweli nimeona kimya jamani wiki zinapita tu, miezi inapita tu kimya.
Leo nikaamua niende chuoni kwao, Mungu mwema nikakutana na huyu binti chuoni
sijui alikuwa anafanya nini ila nikamuuliza na kumwambia kuwa mimi ni mama yake
Erica, hakutaka kunipeleka anapoishi Erica ila alinihurumia kwani mimi ni mama
na pia napaswa kufahamu anapoishi mwanangu. Sasa tumeenda pale, ile kugonga
Erica katoka akiwa na mimba jamani, tena mimba kubwa tu, nyie Erica kanivua nguo
jamani” “Mama jamani, punguza presha. Cha muhimu ni uzima wa Erica sio
swala la kukuvua nguo. Kwani wangapi watoto wao wanapataga mimba mama? Ni wengi
tu, usiwe na presha kiasi hiko” “Nyie hamjui tu, hivi mjomba yenu
akisikia habari hizi itakuwaje? Yani alikuwa akitolea ada mbuzi jamani? Naomba
uzima kwa binti yangu ila kanitia aibu sana, na nitamsema sana” Wakati
wanazungumza akaja daktari na kuwaita ili kuzungumza nao, “Tumejitahidi
na kwasasa huyu mgonjwa wenu yuko sawa, kabakiza wiki chache tu kujifungua,
naona kuna mshtuko alipata ndiomana hali imekuwa hivi. Tunampa mapumziko hapa
hospitali kwa siku mbili tumuangalie hali yake ila tunaomba hata atakaporudi
nyumbani asifanye kazi yoyote kwasasa maana yupo kwenye hatari. Pia asipate kitu
chochote cha kumpa mawazo yani mkiwa mnaongea nae msiongee nae habari za kushtua
maana presha yake haipo vizuri” Daktari aliwaelekeza pale namna
watakavyoishi na Erica na wao wakaelewa. Basi daktari alivyoondoka
wakajadiliana, “Mama, kwasasa Erica asisemwe chochote mpaka ajifungue.
Bora umwngalie tu maana tutakosa vyote mama yangu tutamkosa Erica na mtoto wake,
tuwe wapole tu kwasasa” “Kheee jamani mimba hizi, kwahiyo siruhusiwi
kuuliza hata baba wa mtoto?” “Mama huwezi jua pengine ni jambo
litakalompa stress” “Jamani, mbona mimba zetu haikuwa
hivi!” “Hiyo ni zamani mama, siku hizi kuna mambo mengi
yanaingiliana” Wakaongea pale na kwenda kumuona Erica
sasa. Waliongea nae kwa ustaarabu sana kwani kila mmoja
alihofia kumpa matatizo Erica, kisha wakaongea nae kuwa akitoka hospitali
wamrudishe nyumbani kwahiyo vitu vya kule alikopanga vihamishwe, naye alikubali
kwahiyo dada zake walienda kwa lengo la kuhamisha vile vyombo vya Erica na
kuvipeleka nyumbani kwao. Walipelekwa na Yule Yule Fetty kwenye chumba
alichopanga Erica, walifika na kuingia ndani, kwakweli walishangaa vitu
vilivyokuwepo mule ndani kwa Erica, kisha wakamwambia Yule Fetty akawatafutie
usafiri wa kuhamisha vitu vile. Fetty aliondoka na kuwaacha wakishangaa
tu, “Hivi Bite unaelewa mdogo wangu?” “Hata sielewi
dada” “Yani huyu Erica kapanga lini jamani mpaka kununua vitu vyote
hivi!” “Tena vya gharama” “Mmmmh nahitaji kumjua huyo mwanaume
aliyempa Erica mimba” “Sio Yule Bahati kweli!” “Hapana, Yule
alikuwa amechoka sana. Sema hata hivyo tutajua mtoto
akizaliwa” Wakapanga panga vitu kisha Fetty akafika na usafiri,
wakasaidiana na vijana wa pale kupakia vitu kwenye gari kisha kuanza safari ya
kwenda kwao, kwenye safari zote hizo Fetty alikuwepo hadi nyumbani kwakina
Erica, usiku ulishaingia sana, ikabidi walivyofika tu asikae sana na kuaga kisha
akaondoka zake. Ndani walibaki mama yao, Bite na Mage, walikuwa
wakiongea tu kuhusu vitu alivyonunua mdogo wao, “Hivi mama, mwanao
kapata wapi hela ya kununua vitu vyote hivi?” “Hata mimi mwenyewe
nashangaa, yani sielewi kabisa” “Mmmh ngoja tumsubiri huyo mumewe lazima
atakuwa bonge la bwana” Ila mama yao leo katika siku zote hakuwa na
furaha hata kidogo yani ile misukosuko ya siku hiyo ilimkosesha amani na furaha
kabisa, alijikuta akiwaambia wanae, “Hao bonge la bwana unafikiri ni
waoaji? Hivi kuna muoaji kweli hapa? Mwanaume aweze kukununulia kila kitu cha
ndani ila ashindwe kuja kwenu kujitambulisha na kukuoa, kutembea na mwanaume
tajiri si ufahari ila ufahari pekee ni kupata heshima ya kuwa mke wa mtu
Fulani” Mage akamwambia mama yake, “Kheee mama kumbe kuna
heshima ya kuwa mume wa mtu hata kama huyo mume akiwa masikini!” “Hebu
nitoleeni mambo yenu kwanza leo nimechanganyikiwa” Wakaona wakiendelea
kuongea watamkera mama yao ikabidi wamuage na kupanga kukutana nae tena kesho
asubuhi hospitali kumuona Erica, na walifanya hivyo kwa siku zote ambazo Erica
alikuwa hospitali. Siku hiyo ilikuwa siku ya kutoka Erica
hospitali kwahiyo walienda kumchukua na kumrudisha nyumbani kisha alienda moja
kwa moja chumbani kwake huku wakimsisitiza asiwaze sana na apate muda wa kutosha
wa kupumzika, dada zake waliongea nae maneno mazuri tu kanakwamba hakuna kosa
alilolitenda kumbe wanaogopa kuhatarisha maisha ya mdogo wao, kwahiyo walikuwa
wanaombea tu ajifungue ili waweze kuongea ya moyoni. Siku hiyo usiku
ndio Erica alipata tena muda wa kushika simu yake maana toka ile siku ya
sekeseke hakushika simu kabisa, aliingia kwenye facebook na kukutana na jumbe za
Rahim, “Erica mpenzi, siku ya tatu leo haupo hewani. Tatizo ni nini
mama?” Erica alitabasamu kuona Rahim anaonekana kumjali sana, kile
kitendo kilimfanya ajipe matumaini kuwa Rahim anampenda sana na atakuja tu
kumuoa, “Rahim, nilipatwa na matatizo yani leo ndio nimetoka
hospitali” “Usiniambie mimba imetoka Erica!” “Hapana mimba
haijatoka ila nimeambiwa nisifanye kazi ngumu na nisiwe na stress, nimebakiza
wiki chache tu kujifungua” “Erica, tafadhali nakuomba fata ushauri wa
madaktari, mwanangu ni muhimu sana huyo. Nakuomba mwanangu asipate madhara
yoyote yale Erica, kuwa makini sana maana likitokea baya kwa mwanangu sijui
nitakutenda nini, kuwa makini sana na mwanangu” “Usijali Rahim, kumbuka
huyu ni mtoto wetu wa kwanza na tunampenda sana, nipo makini sitaki mawazo ya
ajabu ajabu yazingire kichwa changu, ila lini utakuja kunioa?” “Erica,
sidhani kama ni wakati muafaka wa kujadili hilo swala. Sikia, kesho nitakutumia
pesa za kufanya maandalizi yako wakati wa kujifungua, kuwa makini na mtoto
Erica. Usitembee tembee kwa miguu, uwe unakodi gari, zile hela nakutumia ili
unitunzie mwanangu” “Usijali Rahim” Erica aliongea kwa uzuri
sana na Rahim hata akalala kwa tabasamu na kusahau kabisa kama Rahim huwa anampa
ahadi za kuja kesho tu na wala hatokei. Aliamka asubuhi na kukuta kila
kitu akifanyiwa na mama yake tena bila ya kuulizwa chochote sijui kuhusu
mwanaume anayehusika sijui kuhusu mambo mambo gani yani hakuna kitu chochote
alichoulizwa na ile hali ilimfanya awe katika hali ya kawaida tu na asijione
kuwa amekosea sana kubeba ile mimba. Jumbe za Tumaini kwenye facebook
alikuwa akizipotezea tu kanakwamba hazioni kwani hakutaka afanye nae mawasiliano
ya kufika kwao maana aliogopa angemuona na ile mimba, halikadhalika hata simu za
Babuu alikuwa hazipokei kabisa. Siku ilifika ambapo alipatwa na
uchungu sana, kisha mama yake kumkimbiza hospitali yani hapo ndio akaelewa
kwanini mama kaitwa mama maana sio maumivu yale aliyokuwaga anayapata pindi
akienda kutoa mimba, yale yalikuwa cha mtoto maana hapo ndio alisikia yale
maumivu yenyewe yenye neno la uchungu wa mwana aujuaye mzazi. Alijikuta
akipiga kelele za maumivu bila ya machozi na aliyaugulia yale maumivu kwa muda
hadi akabahatika kujifungua, yani alionyeshwa tu mtoto wako huyu hapa halafu
hapo hapo akazimia ilibidi madaktari waanze harakati za kumsaidia
Erica. Mama yake alikuwa nje na alikuwa amechanganyikiwa sana, aliona
mwanae akitolewa leba na kupelekwa kwenye chumba cha wagonjwa wanaohitaji
uangalizi sana, jamani hapo huyu mama alichanganyikiwa zaidi, maana kwanza ndugu
zake wengine hakuwaambia kuhusu matatizo ya Erica halafu maswala kama hayo
yasiyoeleweka yalizidi kumpa kichaa yani hakujielewa kabisa, aliwapigia simu
wanae hovyo hovyo maana alishawaambia kuwa yupo hospitali nab ado walikuwa
hawajafika, na walipofika walimkuta mama yao akiwa na hali mbaya sana yani
amechanganyikiwa kabisa, “Mama sasa, usijage hospitali, bora tuwe
tunakuja wenyewe sasa unachanganyikiwa hivyo ndio nini? Si tuulize vizuri
madaktari kuliko kuchanganyikiwa hivyo” Wakaona Erica akitolewa kwenye
kile chumba cha wagonjwa wa uangalizi maalum na kupelekwa wodini, ikabidi
wamuite daktari ili awaeleze vizuri, “Mtamuona sasa, msijali ni mzima
kabisa. Alichoka sana kusukuma kwahiyo alizimia ila yupo vizuri kwasasa na mtoto
yupo vizuri” “Oooh asante Mungu, kajifungua mtoto
gani?” “Hongereni sana, kajifungua mtoto wa kike” Wakafurahi
pale na kumshukuru sana daktari, kisha wakaomba kwenda kumuona Erica na mtoto,
waliruhusiwa maana hospitali ile ilikuwa ni ya binafsi kwahiyo haikuwa na
masharti mengi. Walifurahi sana kumuona Erica na mtoto, waliambiwa kuwa
Erica ataruhusiwa kutoka kesho yake ili kuangalia vizuri
anavyoendelea. Walimpa mtori pale anywe ambao alibebewa na Mage, kisha
walivyomuaga walipanga kumpelekea chakula kingine badae ambapo walimuacha na
juisi na matunda kwanza. Waliondoka na kwenda moja kwa moja nyumbani ili
kujadiliana kwa ufupi tu, “Jamani tumeletewa mwarabu mama, yani Yule
kama sio mwarabu basi mpemba” “Jamani ni utoto tu akikua
atabadilika” “Wapi? Mtoto wa kiarabu Yule, watoto wa Kiswahili
wanajulikana bhana, Yule ni mwarabu kabisa. Hebu mama sema” “Sina usemi
mimi ila alipojidumbukiza mdogo wenu sijui nani atamuopoa, kwenda kuzaa na
waarabu kweli? Aaah huyu mtoto kanishinda tabia mimi jamani loh! Huyo baba wa
kiarabu atakuja kweli hapa nyumbani? Jamani sijui mimi ila mmenidhalilisha mama
yenu” “Usiseme hivyo mama, ngoja tuandae chakula cha mzazi sie, iwe
mtoto wa kiarabu au wa kipemba ndio mtoto wetu tuliyepewa na
Mungu” Kiukweli mama yao alikuwa akiwaza tu aibu atakayoipata kwa ndugu
zake maana hakujua hata ataweka wapi sura yake kuwakwepa. Erica
alitoka hospitali na kurudi nyumbani ambako aliendelea kupewa vyakula vya mzazi
na kuhudumiwa kama mzazi anavyohudumiwa, ni kweli ilikuwa inamuuma sana mama
yake ila alijikaza na kumuhudumia mwanae hadi alikuwa katika hali ya kawaida tu,
Erica alikuwa anafanya kazi ya kumpiga picha mtoto na kumtumia Rahim ambapo
Rahim alionyesha kufurahia sana ujio wa mtoto wao huyo, “Eeeeh tunamuita
nani mama?” “Kwani wewe unapenda tumuite nani?” “Chagua tu jina
wewe mwenyewe, nimekupa nafasi hiyo” “Napenda nimuite
Angel” “No, aitwe tu Malaika” “Ila Malaika na Angel si jina moja
jamani kasoro lugha tu” “Ndio, ila itapendeza zaidi akiitwa
Malaika” “Jamani, mi naona nitapendeza zaidi nikiitwa mama
Angel” “Erica, huoni kama akiitwa Malaika itapendeza
zaidi?” “Basi, mimi nitakuwa namuita kwa kingereza halafu wewe unamuita
kwa Kiswahili” “Jamani mama Malaika, unapenda mabishano eeh! Jina mtoto
si aitwe moja tu au nimpe jina la mama yangu” “Nani?” “Tumuite
Mwajuma maana mama yangu anaiitwa Mwajuma” “Mwajuma? Ndio jina gani
hilo? Mama yako si anaitwa Mrs.Peter jamani, hiyo Mwajuma imetoka
wapi?” “Ndio jina lake, Peter ni jina la mumewe” “Aaah hilo jina
silitaki mimi, mwanangu ataitwa Angel tu” “Sawa nimekubali hakuna
tatizo, ataitwa vile unavyopenda wewe” Erica aliwasiliana na Rahim ila
alikuwa na maswali mengi sana kwenye akili yake kuwa mama yake Rahim kumbe
anaitwa Mwajuma, yani akawaza vitu vingi sana ikiwa ni pamoja na jambo la dini
kuwa lazima yeye na Rahim kutakuwa na utofauti, “Mungu wangu sasa
atanioaje? Ooooh nimeruka mkojo nimekanyaga mavi, si bora na Bahati aliyeniambia
ukweli toka mwanzo jamani, mmmh ila hapana huenda Rahim ni mkristo nitamuuliza
tu” Aliwaza bila ya jibu. Erica alipomaliza miezi
miwili ya uzazi, mama na dada wa Erica walitoka kidogo na kuzungumza kuhusu
mtoto wa Erica, “Jamani wanangu nadhani sasa ni kipindi muafaka cha mimi
kumuuliza mdogo wenu kuhusu baba wa mtoto wake au mnasemaje?” “Ni kweli
mama muulize, na hivi mtoto mwenyewe mwarabu sijui baba yake
nani?” “Kanitia aibu mtoto huyu jamani loh! Kazaa mtoto mzuri kweli ila
raha ya mtoto awe na baba sio mtoto tunaishi nae hata baba hajulikani, mwezi wa
pili huu hatujawahi kumuona baba wa mtoto wala ndugu wa mwanaume. Inamaana huyo
mwanaume hana ndugu jamani? Mimi huyu mtoto kanishinda
tabia” “Usilalamike mama, muulize kwanza maana huwezi jua ni kwanini
mwanaume hajafika hadi leo” Wakakubaliana na mama yao pale ili amuulize
kisha walipoaga na kuondoka ndipo mama yao alipomuita Erica na kuanza kuongea
nae. “Haya Erica mwanangu, najua sijawahi kukuuliza wala hatujakaa
tuongee, niambie huyo baba wa mwanao yuko wapi na atakuja lini hapa
nyumbani?” “Yupo Marekani, na amesema atakuja tu” “Kwahiyo ni
Mmarekani?” “Hapana, yupo kule kimasomo tu ila ni wa
hapahapa” “Haya, anaitwa nani?” “Anaitwa Rahim” “Kheee
Rahim? Mwanangu jamani mwanangu wewe, akili yako ikoje jamani? Kumbe ni
Mwislamu” “Ni Mwislamu!” “Inamaana hujui au? Yani msomi mzima
unashindwa kutofautisha dini kwa majina? Wewe wa wapi wewe?” “Sikujua
kama ni Mwislamu mama” “Haya sasa, wewe na yeye mtafunga ndoa gani?
Usije ukaniletea uwehu wa kubadili dini, yani nyie watoto wa kike jamani mpo
kama mafungu ya nyanya, mtu akitaka kupika mchuzi haya, akitaka kukatakata
kachumbari haya, akitaka kutengeneza chachandu haya. Hivi ulishindwa kuchagua
maisha uyatakayo? Unajifanya kushangaa hapa, unashangaa nini
sasa?” Erica alikuwa kimya tu kwani kama hakuelewa elewa vile, mama yake
aliendelea kuongea, “Erica, narudia kukuita Erica, ukithubutu kubadili
dini sahau kuwa mimi ni mama yako. Yani utajua mwenyewe utakachofanya na huyo
mpemba wako ila ukithubutu kubadili dini Erica, nisahau kabisa. Umenitia aibu
wewe mtoto na wala sikutegemea jamani aaah!” Erica alikosa raha kabisa
kwani alizidi kupata picha kuwa amekosea sana kumuamini Rahim na kuacha
mahusiano yake yaliyopita, kwa muda huo alimuona Bahati kuwa ndiye mtu pekee
aliyekuwa anajieleza kwa ukweli kwake, sasa atafanyeje kuhusu Rahim, alihisi
kuchanganyikiwa. Usiku ulipofika aliwasiliana na Rahim na kuanza
kumdadisi kuhusu kuoana yeye na Rahim, “Halafu Rahim kumbe mimi na wewe
tumetofautiana dini?” “Ndio, kwani ulikuwa hujui” “Nilikuwa
sijui Rahim” “Kwahiyo ungejua ungenikataa? Mapenzi hayana dini
Erica” “Sawa nakubali mapenzi hayana dini, ila je utanioa kwa ndoa ya
aina gani?” “Upo tayari kubadili dini nikuoe?” Hilo lilikuwa ni
swali la utata kwa Erica na kumfanya achanganyikiwe
zaidi. Usiku ulipofika aliwasiliana na Rahim na kuanza
kumdadisi kuhusu kuoana yeye na Rahim, “Halafu Rahim kumbe mimi na wewe
tumetofautiana dini?” “Ndio, kwani ulikuwa hujui” “Nilikuwa
sijui Rahim” “Kwahiyo ungejua ungenikataa? Mapenzi hayana dini
Erica” “Sawa nakubali mapenzi hayana dini, ila je utanioa kwa ndoa ya
aina gani?” “Upo tayari kubadili dini nikuoe?” Hilo lilikuwa ni
swali la utata kwa Erica na kumfanya achanganyikiwe zaidi. Ila aliamua
kumuuliza tena Rahim, “Hivi hakuna njia nyingine ya mimi na wewe kuoana
zaidi ya kubadili dini?” “Unadhani tunaweza kuoana kwa njia
gani?” “Si kuna ndoa za bomani Rahim!” “Ndoa za bomani kwangu ni
haramu, Erica kubali kubadili dini nikuoe” “Ngoja nifikirie
basi” “Ila sio swala la kufikiria sana, ni swala tu la kutolea maamuzi.
Kama unahitaji kuishi na mimi basi kubali kubadili dini nikuoe” Kwakweli
Erica aliona wazi kabisa ndoto yake ya kuolewa na Rahim imekufa maana Rahim
kashasema hawezi kumuoa hadi abadili dini na mama yake kashasema kuwa akibadili
dini basi asahau kuwa yeye ni mama yake yani hapo akashikwa na mkanyiko wa
mawazo sana. Alimuangalia mwanae na kuamua kulala tu kwani kwa vyovyote
vile Yule atabaki kuwa mtoto wake, “Angel wangu, niolewe au nisiolewe
ila nitakupenda daima” Alimkumbatia mwanae na
kulala. Palipokucha kama kawaida alikuwa wa kwanza kuamka maana
kipindi hiko mtoto anaamka mapema sana kwahiyo kwa vyovyote vile aliamka na
kuanza kumnyonyesha mwanae na kumuweka katika hali ya usafi. Kama kawaida mama
yake alifika na kuanza kumuogesha mjukuu wake, alipomaliza alimvalisha kisha
Erica alimnyonyesha na mtoto kulala. Mama Erica alianza tena kuzungumza
na binti yake, “Vipi kuhusu huyo mwanaume wako
hujanijibu?” “Sielewi mama” “Huelewi nini
sasa?” “Sikujua kama Yule mwanaume ni Mwislamu mama” “Haya
umejua sasa, una mpango gani?” “Sijui mama, itakuwaje?” “Yani
wewe mtoto tumekusomesha bure tu, ndiomana serikali ilikunyima mkopo maana akili
zako walishaziona kuwa hazimo, masikini kaka yangu kajitahidi kwa uwezo wake
wote kuhakikisha unasoma halafu leo aje asikie umezaa na mwarabu sijui mpemba
halafu upo upo tu hata huelewi cha kufanya” “Ila mama unanilaumu bure
tu, wewe ndio uliyesababisha yote kwenye maisha yangu. Ulisema nichague mwanaume
mwenye hela” “Nilikutuma mimi ukapanue miguu yako kwa huyo mpemba wako?
Nilikutuma? Hebu Erica uwe na akili muda mwingine, ndio nilisema utafute
mwanaume mwenye hela, je nilisema ukimpata ukalale nae mzae watoto kabla ya
ndoa? Mambo mengine ni ya kujiongeza tu, maisha ni wewe mwenyewe unavyoyachagua
na sio watu wanavyosema, wewe msomi mzima hujui hili ni zuri au baya?
Nilikwambia utafute mwanaume mwenye hela ndio, ila sikuwa na maana mbaya,
sikutaka mwanangu upate shida kwenye ndoa yako sababu mimi nishapitia ila
sikukwambia ukabebe mimba kabla ya ndoa. Au uliambiwa ukizaa na mwanaume ndio
kigezo cha mwanaume huyo kukuoa? Unajua Erica bora hata ungekuwa mkubwa sana
ningesema mwanangu kaona umri umeenda kaamua kuzaa, mwanangu ndio kwanza una
miaka 23, dah umenitia aibu sana. Haya sasa huyo mpemba ana mpango
gani?” Erica aliona hata aibu kumjibu mama yake kuwa Rahim kamwambia
abadili dini maana aliwaza kuwa ataanza njia gani kumueleza hayo wakati
kashakatazwa yani alikuwa njiapanda haswaa, kwavile hakumjibu tena mama yake
aliamua kuondoka zake kuendelea na kazi zingine maana aliona ni kama kumpigia
mbuzi gitaa. Siku hiyo walifika dada zake na wao wakaongea nae
kuhusu swala lile lile la baba wa mtoto wake, walikaa chini na kuongea na mdogo
wao. “Erica tulijua baada ya kutenda kile kitendo cha kukutoa mimba
ungejifunza mdogo wetu, hivi huyu mtoto ulipanga au ni vipi?” “Ni bahati
mbaya dada” “Bahati mbaya? Yani tuseme Erica hukujua hata nji za uzazi
wa mpango jamani!” “Nilikuwa najua dada zangu, ila kwa maoni ya watu
wengi walisema kuwa ukitumia njia za uzazi wa mpango unaweza usizae maisha
yote” “Yani na wewe msomi unasikia na kuamini hizo stori za wadada wa
mitaani?” “Hapana dada, ila kuna watu kabisa nilikuwa na ushahidi nao
ndiomana sikuweza kutumia, walisema ni afadhali uzae kabisa ndio
utumie:” “Sasa utatumia kwasasa wakati
ushakosea?” “Msinikandamize dada zangu, nakubali kuwa nimekosea ana ila
msinikandamize kiasi hiko” “Hatukukandamizi ila unampa mawazo mama ujue,
raha ya mtoto ni awe na baba, sasa mtoto wako unabaki kusema tu baba yake yupo
yupo, yuko wapi?” Akadakia Bite na kusema, “Hatuwezi sema ni
Yule kijana wa watu maana mtoto hamfananii hata chembe, tuambie Erica baba wa
mtoto ni yupi na una mpango nae upi?” Yani Erica aliona ndugu zake
wakimpa kizunguzungu tu, na usiku ulipofika alijaribu kuwasiliana na Rahim ila
msimamo wa Rahim ulikuwa pale pale kuwa Erica abadili dini amuoe, yani swala la
kubadili dini kwa Erica lilikuwa kizunguzungu sana kwani hakutaka kumkosa Rahim
na muda huo huo hakutaka kumkosea mama yake. Na kila siku mama yake
alimwambia jambo moja kuwa amlete kijana aliyezaa nae amfahamu, “Hata
kama hamna ndoa, basi nimfahamu Erica, mlete huyo kijana
nimfahamu” “Nitamleta mama” “Yani wewe mtoto hujielewi kabisa,
hujielewi Erica, umeharibu maisha yako ukiwa na miaka 23 tu. Ijui unategemea
lini huko mbele ya safari” “Mama jamani” “Sio mama jamani,
umlete huyo mjinga mwenzio ambaye mlishindwa kufikiria hadi mkazaa sijui unataka
kumuweka mtoto kwenye kundi gani?” “Atakuja mama” Yani kichwa
cha Erica kilivurugwa haswaa kwani kila akimuuliza Rahim kuwa anarudi lini
alipewa jibu moja tu kuwa nitakuja usiwe na wasiwasi. Kadri
alivyoulizwa na mama yake kuhusu baba wa mtoto wake ndivyo alivyozidi kupatwa na
mawazo mbalimbali hadi kufikia hatua ya kuwa na mawazo yasiyofaa, “Yani
dunia nzima, mkosa ni mimi tu natamani hata kufa kwakweli” Alichukua
simu yake na kuingia kwenye mtandao wa kijamii, wakati anaperuzi tu akakutana na
makala yenye kichwa “HAKUNA SABABU YA KUJIUA, MAISHA NI MATAMU SANA. UKIANGUKA
INUKA NA USONGE MBELE” alivutiwa na makala ile na kuanza kuisoma, kwakweli
iliandikwa vitu vilivyogusa maisha yake, kuna mahali alisoma, “Unapoamua
kujiua, fikiria kwanza unaowaacha, unawaacha vipi? Unaweza kuamua kujiua sababu
ya mtu mmoja kakuudhi ila unaacha watu milioni moja wanaokupenda sana na
wanapenda uwepo wako. Unaweza kujiua sababu kuna jambo limekukera ila fikiria
maisha kuna mambo mangapi mazuri ambayo Mungu ametuzawadia? Jambo moja tu
likufanye ukose maisha na mbingu? Ukianguka usiwaze sana ila inuka na usonge
mbele, usikubali kilichokuangusha kikuangushe tena. Fikiria watoto unaowaacha,
wazazi, marafiki wanaokupenda, ndugu, majiraniwA wanaokupenda. Kwanini ujiue na
kuacha wote hawa na simanzi? Ni dhambi kubwa sana kufikiria kujiua, kumbuka
Mungu katupa uhai na pumzi bure tu, kwahiyo anatupenda sana na atakusaidia utoke
kwenye hiyo hali inayokupa wazo la kujiua” Erica hii makala ilimuingia
akilini sana, akamtazama mtoto wake Angel na kuona kweli ana sababu ya kuendelea
kuishi kuyapigania maisha ya Yule mtoto mdogo asiye na hatia. Leo
nyumbani kwao kulifikwa na ugeni, alifika mama Derick ambaye alipoelezwa na Mage
kuwa Erica ana mtoto alipenda kwenda kumsalimia, na kwa bahati muda aliofika
mama yake Erica hakuwepo alikuwa ameenda kwenye vikoba vyake, Erica
alimkaribisha na kumsalimia. “Kumbe kwetu
unapafahamu?” “Napafahamu ndio, nimewahi kuishi hapa
ujue” “Aaaah karibu sana” “Asante, niliwasiliana na Mage,
akasema una mtoto nikaona ni vyema kuja kukuona” “Mmmh inamaana na
Derick anajua kama nina mtoto?” “Hapana, unajua Derick alisafiri. Hajui
chochote, kwani hutaki Derick ajue?” Erica alicheka tu ila kiukweli
hakutaka Derick ajue kwani alijua kama habari ikifika kwa Derick basi yeyote
atakayekutana nae atamueleza kuhusu yeye, kwahiyo alitafuta kauli ya
kumdanganyishia mama yake Derick kuwa asimueleza Derick kuwa ana
mtoto, “Basi mama, usimwambie Derick” “Kwanini?” “Nataka
siku akikutana na mimi ashangae tu, yani iwe ni kitu cha kushangaza kwake.
Asijue kwasasa” Mama Derick aliitikia kisha akamuomba Erica akamlete
mtoto ili amsalimie, Erica alienda kumtoa mtoto ndani na kumpa mama Derick,
ambaye alimuangalia kwa muda na kusema, “Umezaa mtoto mzuri sana Erica,
hongera kwa hilo. Ila huyu mtoto sio mswahili eeh!” Erica akacheka na
kumuuliza, “Kwanini unasema hivyo?” “Namuona ni mtoto wa
kipemba” Erica akacheka, kisha mama Derick akaendelea, “Baba
yake yuko wapi?” Kiukweli swali la baba wa mtoto lilikuwa linamkera sana
Erica na kumkosesha raha kabisa, ila aliamua kuongea kikubwa kwa mama Derick
kwani anajua kuwa hata huyu mama ameshawahi kupitia changamoto za mapenzi,
kwahiyo alihisi pengine anaweza akampa mawazo mazuri, “Baba wa mtoto
yupo, ila nimetofautiana nae dini na ameniambia nibadili dini ndio
anioe” “Nilihisi tu mtakuwa tofauti dini, ila Erica ngoja nikwambie
kitu. Usibadili dini sababu ya mapenzi yani usithubutu kabisa kubadili dini
sababu ya mapenzi” “Kwanini?” “Sikia nikwambie, dini ni mambo ya
imani halafu ni kitu kikubwa tofauti na sisi tunavyokichukulia. Dini
inabadilishwa ikiwa moyo wako umeridhia yani umesikia mafundisho ya dini
nyingine, umeyaelewa ndio unabadilisha ila sio kubadilisha sababu ya mapenzi. Ni
kazi bure kubadili dini sababu ya mapenzi kwanza ukumbuke hiyo dini utaenda tu
ila kiukweli haipo kwako, kwahiyo utakuwa unajidanganya mwenyewe. Badili dini
kwa maamuzi yako binafsi ila sio mapenzi” “Sasa mwanaume anasema
nibadili dini ndio anioe” “Erica kama mwanaume hataki kukuoa huwa
wanatafuta sababu nyingi sana, kwamaana hiyo unaweza kubadili dini akakuoa kisha
akakufanyia mambo ya ajabu. Mimi nina mifano iliyo dhahiri na pia najiona
nilikosea sana. Mimi ni Mwislamu yani nimelelewa katika maadili ya dini tu ila
mwanaume wa kwanza kuzaa nae alikuwa Mkristo na aligoma kunioa kwa kigezo cha
dini ingawa kwa kipindi hiko nilikuwa tayari kugombana na wazazi wangu ili
nibadili dini niolewe na Yule mwanaume, nikaanza kufata mambo yote wakristo
wanayoyafanya, nilianza hadi kwenda kanisani mimi, nikabatizwa kisiri bila
familia yangu kujua kisha nikamwambia Yule mwanaume nimekuwa mkristo na tuoane
ili tulee mtoto pamoja ila mwisho wa siku mwanaume akazingua na kuoa mwanamke
mwingine. Niliumia sana na kuona kama dunia imenitenga, nikarudi kwa wazazi na
wakanisaidia kumlea Yule mtoto, ndipo nikapata mwanaume wa kuishi nae ambaye pia
alihitaji nimzalie mtoto. Nikazaa mtoto, nikamuomba tuoane. Yule mwanaume
alikuwa ni Mwislamu kama mimi ila alipodokezewa na watu kuwa mimi nimewahi
kubadili dini aliniacha na kusema hawezi kuoana na mwanamke kigeugeu, nikaumia
sana na hata hivyo hakumpenda kabisa mwanangu wa kwanza. Ndio kwenda nikampata
baba yenu Jose, akaahidi kunioa, nikamuuliza wewe ni mkristo utawezaje kunioa na
mimi wakati una mke? Akaniambia nisiwe na shaka kwani kuna wakristo wanaishi na
wake wawili, akanitaka nibadili dini, nikabadili tena yani kwa kifupi sikuwa na
msimamo ila naye ndio yakanitokea yale yaliyonitokea. Erica, msimamo ni kitu
chema sana katika maisha, usipende udhaifu ulikuangusha uendelee kukuangusha,
yani ule udhaifu chukulia kama changamoto katika maisha yako. Mimi nilifanya
makosa sana sababu sikuwa na msimamo, ukikosa msimamo maisha yanakuwa ni
machungu sana. Ushakosea ndio ila sio mwisho wa maisha yako, chagua maisha
uyatakayo sasa, usikubali kubadili dini sababu ya mapenzi” Gafla mama
yake Erica akaingia ndani, ila cha ajabu alikuwa akitabasamu sana, kisha alianza
kuongea, “Nilichungulia kwanza na kukuona ni wewe, nilishikwa na gadhabu
ya hali ya juu, ila niliposikia ulichokuwa ukimshauri mwanangu kwa hakika
kimenigusa sana. Nakushukuru mdogo wangu, umemshauri jambo jema
mwanangu” Kisha mama Derick akainuka na kukumbatiana na mama Erica, huku
wakiongea mambo mbalimbali kanakwamba hawajawahi kugombana katika maisha yao
yote, mama Erica alizidi kumshukuru mama Derick kisha akamuuliza, “Ila
kwanini umemshauri Erica asibadili dini ikiwa ni dini yako? Huoni kama utaongeza
muumini?” “Sikia dada, dini ni zaidi ya tunavyoitafakari, unatakiwa
kuhamia dini nyingine kwa kuamua kutoka moyoni sio sababu ya mapenzi. Kubadili
dini sababu ya mapenzi ni kumchezea Mwenyezi Mungu na kukosa msimamo, akija huyu
utamfata, akija huyu utabadili tena, dhana ya kusema mwanamke hana dini tuiache.
Inasemekana hivyo sababu inajulikana mwanamke hana msimamo, ila tungekuwa na
msimamo basi isingesemekana kuwa mwanamke hana dini. Mimi naamini kuwa kama mtu
anakupenda kweli basi ndoa mtafunga nae tu, mbona za bomani zipo? Mkiishi ndani
na kuiona dini ya mwenzio nzuri, umeielewa vizuri unaweza kuifuata ila sio
kufuata sababu ni lazima kufuata yani utajikuta hutendi vile inavyopaswa
kutenda. Tufikie hatua ya kubadili dini ikiwa tumeielewa vyema dini
tunayoiendea” “Kwahiyo kwasasa wewe ni dini gani?” Mama Derick
alicheka kisha akasema, “Nilirudi kwenye dini yangu, niliomba toba basi
nikarudi, najua nilikosea sana na ndiomana nasema ili mwingine asikosee kama
mimi. Maisha yanataka msimamo, ila ukikosa msimamo tu basi utasumbuliwa sana na
maisha, sikuwa na msimamo mimi jamani yani kipindi kile hata mpagani angetokea
basi ningemfata yani maisha niliona yamenibadilikia kabisa. Ila saivi nina
misimamo yangu yani sitaki kutetereshwa” “nashukuru kwa ushauri wako kwa
binti yangu, Erica umesikia ushauri huo sasa ole wako ubadili
dini” “Dada usimwambie hivyo, unatakiwa tu kumfundisha, unajua
unapomwambia ole wako usibadili dini bado hujafanya kitu. Ila mpe mafundisho ya
dini yako ilia pate ugumu kwenye nafsi yake mwenyewe akifikiria swala la
kubadili sio ole wako usibadili, bado hujafanya kitu hapo. Wanawake sie akili
zetu tunazijua wenyewe yani, unatakiwa tu uwe mpole dada
yangu” “Nimekuelewa” Wakaendelea na maongezi mengine hadi pale
mama Derick alipoaga, Erica aliamua kumsindikiza kidogo ambapo huyu mama
aliendelea kumshauri, “Erica kutenda kosa si kosa bali kurudia kosa,
usije ukasubiri kurudia makosa, umeshatenda kosa angalia mstakabali wa maisha
yako” “Sasa sitaolewa?” “Kama huyo mwanaume anakupenda basi
atakuoa tu bila kujali dini, na pia usijiwekee kuwa asipokuoa ndio mwisho, huyo
ni mmoja tu ila kuna wengi wanaotamani uwe mke kwahiyo usikate
tamaa” “Nashukuru kwa ushauri wako” Akaagana nae kisha Erica
akarudi ndani kwao. Erica akiwa amekaa nyumbani, leo kwa mara
ya kwanza aliamua kumpigia simu Bahati maana ni muda mrefu hakuwasiliana nae.
Yeye ndio mwenye namba za Bahati ila Bahati hana namba zake sababu alibadilisha,
kwakweli Bahati alihisi hata kuchanganyikiwa ile kuzungumza na
Erica, “Kwa hakika ningekuwa Dar, basi leo ningekuja nyumbani kwenu
kukusalimia yani nimefurahi sana Erica” “Uko wapi kwani?” “Nipo
Tanga, kuna mzigo nimeufata ila nikirudi tu Dar nakuja kwenu” “Sawa, ila
ngoja nikuulize jambo. Mimi mkristo na wewe Mwislamu hivi tukitaka kuoana
tutaoana kwa ndoa ipi?” “Erica jamani, hapo si ndoa ya bomani tu. Upo
tayari nije nikuoe Erica” “Hapana, nimekuuliza tu” “Jamani
Erica, unaumiza moyo wangu ila najua ipo siku tu utakubali niwe mume
wako” Basi Erica alikata simu huku akiwaza kuwa endapo Bahati akigundua
kuwa ana mtoto itakuwaje? Alijikuta na mawazo pia, ila akaendelea kujipa imani
kuwa kuna muda Rahim atafikiria pia kufunga nae ndoa bomani. Akiwa kule
chumbani, alimuona mama yake alifika na kumuita, “Erica, kuna mgeni
wako” Ikabidi ajiandae na kutoka nje ili kuangalia ni nani huyo
mgeni. Alifika na kushangaa kuwa mgeni mwenyewe ni
Babuu, “Nimeona kimya sana Erica, leo nimeamua kujitoa muhanga na kuja
kwenu” “Karibu” Muda kidogo mtoto wa Erica akaamka na kuanza
kulia, mama yake Erica alifika sebleni na kumwambia Erica, “Kanyonyeshe
mtoto kaamka huko” Ikabidi Erica aende ndani kumnyonyesha mwanae, Babuu
alikuwa akishangaa tu kuwa Erica ana mtoto. Baada ya muda Erica alirudi
na kumtoa Babuu nje kwani hakutaka Babuu amuone mtoto wake, “Erica
umenitoa nje ili nisijue kama una mtoto jamani! Ila mbona nimesikia mama akisema
ukamnyonyeshe, Erica unaficha hata mtoto. Kamlete basi
nimuone” “Kalala” “Haya, si ulisema utazaa ukiolewa, kikowapi
sasa? Erica si bora hata mimi ningekuoa kwanza ndio nikuzalishe, huyo mchumba
uliyesema unae ndio kakuzalisha kabla ya ndoa? Pole ila atakuoa tu, nilikupenda
sana Erica dah na bado nakupenda” “Sema kilichokuleta
uende” “Jamani Erica usiwe na hasira hivyo, nilipita kukusalimia tu. Leo
nilikuja mitaa ya huku kwenu kuna ukumbi wa harusi nilikuja kuuangalia maana
ndio tumeshauriwa tutumie ukumbi huo” “Harusi ya nani?
Unaoa?” “Hapana, mimi kuoa bado. Unakumbuka siku ile uwanja wa ndege
ulinikimbia, sasa nilikutana na ndugu yangu Yule niliyekusimulia ndio
anaoa” Erica alihisi kama tumbo la uzazi linamcheza na kuuliza kwa
makini, “Anamuoa nani sasa?” “Yani wanaume sisi dah! Yule jamaa
kachezea mabinti wengi sana, halafu anakuja kuoa msichana mwingine aliyetunziwa.
Binti mwenyewe anakaa kwa mama yake, anaitwa Salma” Yani hapo alihisi
kama tumbo la kuendesha limemshika gafla. Erica
alihisi kama tumbo la uzazi linamcheza na kuuliza kwa makini, “Anamuoa
nani sasa?” “Yani wanaume sisi dah! Yule jamaa kachezea mabinti wengi
sana, halafu anakuja kuoa msichana mwingine aliyetunziwa. Binti mwenyewe anakaa
kwa mama yake, anaitwa Salma” Yani hapo alihisi kama tumbo la kuendesha
limemshika gafla. Badiliko la Erica hata Babuu alilifahamu na kufanya
amuulize kwa makini zaidi, “Erica sikuelewi nini
tatizo?” “Sijisikii vizuri, kwaheri” Akamuacha Babuu pale nje
kisha yeye akaingia ndani kwao, moja kwa moja alienda uwani kwanza maana alihisi
tumbo lake si zuri. Na alipotoka aliingia chumbani kwake na kujifungia mlango
ambapo alilia sana, yani alilia kupita siku zote alizowahi kulia sababu ya
mapenzi, “Hivi wanaume kwanini mpo hivi jamani? Yani umeniharibia
maisha, umenizalisha mtoto halafu leo unaoa msichana mwingine kweli? Kwanini
mimi nina kasoro gani? Kwanini wanaume wote hawawi na moyo kama wa Bahati, mbona
Bahati ana upendo sana jamani?” Erica alikosa raha kabisa, na alikuwa
analia tu hata anamnyonyesha mwanae huku akilia kiasi kwamba mama yake alihisi
kitu na kwenda kumgongea mlango kwani alivyoufungua aligundua kuwa
umefungwa. Erica alifuta machozi na kwenda kumfungulia mama
yake, “Mwanangu, umejifungia mwenyewe chumbani. Ila kujifungia chumbani
sio vizuri, hebu njoo na sebleni kidogo na mtoto” “Sawa nakuja
mama” Kuna jambo mama Erica alilielewa kutokana na ile sauti ya Erica,
kisha alimuangalia mwanae kwa simanzi sana na kwenda kumbeba mjukuu wake kisha
kumwambia Erica amfate sebleni. Erica alienda sebleni alipo mama yake,
Yule mama alimshika vizuri mtoto wa Erica kwa mtindo wa kumrusha rusha
akisema, “Mjukuu wangu mzuri mwenyewe yani anastahili kuitwa Angel, huyu
mtoto ni mzuri mwanangu yani kazuri sana. Hivi Erica umeuona kweli uzuri wa
mwanao huyu?” “Ndio mama, ni mzuri ndio ila naikumbuka kauli yako bado
kuwa uzuri wa mtoto haujakamilika kama hana baba” “Ndio, mtoto anatakiwa
kuwa na baba na mama ila mtoto anapokosa baba inaashiria nini? Prngine mama
humjui baba wa mtoto au baba kamkana mtoto wake, ila kwa yote ni mtoto kulelewa
kwenye maadili yanayofaa ingawa akiwa na baba inapendeza zaidi. Kwani baba yake
kasemaje?” Erica alikuwa kimya tu hakumjibu mama yake, kisha mama yake
akaendelea kuongea, “Erica, inaonyesha ulikuwa unalia. Haya nini
kinachokuliza?” “Hapana mama silii” “Erica usinifiche nakujua
vizuri sana, mwanangu ni kweli umefanya makosa na umenitia aibu sana ila ni
wakati sasa wa kuongea na huyo mwenzio ili tujue mstakabali wake kuhusu huyu
mtoto. Sasa ukilia Erica inasaidia nini? Hapa tunaangalia maisha ya huyu Angel,
kuna leo na kesho mtoto anapaswa kumujua baba yake, usifikirie ninavyokuuliza
uliza sikupendi, tena nakupenda sana sana mwanangu hujui
tu” “Nimekuelewa mama” “Kama unanielewa basi usikazane kulia ila
kazana kumwambia huyu mwanaume afike hapa nyumbani, najua mwanangu wewe sio
malaya kiasi cha kutokumjua baba wa mtoto wako. Ni dhahiri unamtambua naye pia
anajua, basi tumia elimu yako kumfanya aje hapa nyumbani” “Sawa
mama” Erica aliitikia ila alijua yote anayotasema mama yake hayawezekani
maana mwanaume mwenyewe ndio amepata taarifa kuwa anataka
kuoa. Usiku ulipofika Erica aliingia kwenye mtandao wa kijamii
ili awasiliane na Rahim, aliamua kupiga moyo konde na kumuuliza muhusika, kwani
alipenda kufahamu mbichi na mbivu kutoka kwenye kinywa cha muhusika. Kwa kipindi
hicho haikuwa kama zamani kwani mawasiliano yake na Rahim yalipungua wakati kuna
muda hadi alikuwa akimtafuta kwenye simu ya kawaida ila sio kwa kipindi hiki
yani Erica ndio alikuwa akimvizia ili akimuona hewani kwenye facebook basi
awasiliane nae, na kwa bahati siku hiyo alimkuta hewani na kumsalimia kisha
kuanza kushusha makala yake ya malalamiko, “Hivi Rahim kipi
nilichokutenda kibaya mimi mpaka kunifanyia hivi? Ulishindwa kusema kuwa Erica
nipo na wewe tu ila sikuoi? Hivi kweli mimi ni wa kusikia kuwa Rahim unaoa? Tena
unamuoa Yule Yule Salma uliyesema umetafutiwa tu hata humtaki? Rahim, hukutaka
niwe karibu na mama yako sababu hukutaka nijue ukweli kuhusu mambo unayoyafanya.
Rahim wewe wa kunichezea mimi na kuniacha kweli jamani? Liko wapi neno ulilokuwa
unasema siku zote kuwa Erica nakupenda sana? Ulisema nibadili dini kama njia tu
ya kufanya kuwa imeshindikana kunioa sababu ya dini ila kiukweli ulishapanga
yote haya. Umeniumiza Rahim ila Mungu atanilipia” Alimtumia huo ujumbe
huku akisubiri jibu kutoka kwa Rahim, alitegemea atajibiwa makala pia, ila
alijibiwa kwa kifupi tu, “Erica, sikuelewi” Erica alishikwa na
hasira sana na kumuuliza huku akiwa na jazba, “Hunielewi nini Rahim
wakati unaoa?” “Namuoa nani?” “Si unamuoa Salma” “Hizo
habari nani amekupa?” “Unadhani duniani kuna siri? Hakuna siri duniani,
mambo yaote yako wazi, najua kama unaoa Rahim ila ulichonifanyia sio
sawa” “Erica, usipende kusikiliza maneno ya watu. Sasa mimi kama naoa
nikufiche ili iweje? Kipi naogopa kutoka kwako, usinikere bhana. Kwanza ni usiku
sana saa hizi huko hebu lala, unanitesea mwanangu na masimu simu
yako” Erica alisoma huu ujumbe mara mbili mbili na kuona kweli thamani
yake imeshuka maana Rahim hata hakujali kuhusu maumivu yake ya moyo zaidi ya
kumtaka alale, kiukweli Erica hakuweza kulala kabisa sababu ya mawazo kwani
aliwaza sana bila ya kuwa na majibu na alijiona kama kuna kitu kimepunguka
katika maisha yake. Aliendelea kuperuzi facebook ingawa Rahim
hakuonekana tena hewani toka muda aliomwambia alale, wakati anaperuzi akakutana
na mtu kaandika, “Yani mimi mwanaume akijifanya anafanya siri eti rafiki
zake wasinijue sijui ndugu wasinijue, yani siku nafika mbele yao namuaibisha
balaa, na siku hiyo ndio atajua kichaa changu vizuri. Anikatae mbele ya hao
asiotaka wanijue” Akakuta kuna watu wamesapoti wangine wakicheka,
wengine wakisema ndio kukomesha wanaume, yani aliona kila mmoja na wazo lake ila
mawazo ya wengi yalikuwa yakusapoti kile kilichoandikwa, nay eye alijikuta
akipata wazo jipya pale pale, “Hivi kwanini nisiende hiyo siku ya harusi
nikamuaibishe Rahim? Yani naenda na mtoto, hapo ndio watanijua vizuri, kila
mmoja kwao atajua kuwa nimezaa na Rahim” Ila akawaza pia kuwa atajuaje
ratiba za ndoa ya Rahim? Aliona ni vyema kama atauliza kwa ujanja ujanja kwa
kupitia Babuu ili ajue vizuri. Ila wakati ameafikiana na hilo wazo lake sasa,
aliweza kupata moyo wa kulala. Kulipokucha aliamua kumpigia simu Babuu
ili kumuuliza hiyo sherehe ya ndugu yake ni linin a inafanyika ukumbi
gani, “Erica, kwani vipi? Unataka kuhudhuria?” “Kwani vibaya
nikihuduria?” “Sio vibaya, ila niambie kwanini unataka
kuhudhuria?” “Babuu, mimi napenda sana vyakula vya kwenye sherehe halafu
pia napendaga kuona watu wakicheza kwenye sherehe. Sijapata tu nafasi ya
kuhudhuria sherehe mbali mbali ila napenda ndiomana nimekuuliza, hutaki nije
jamani?” “Basi hakuna tatizo, nitakuelekeza Erica. Na kama ukifika
ukazuiliwa nipigie simu nitakuingiza” Basi Babuu akamtajia sehemu hiyo
sherehe itakuwepo, tarehe na muda, na Erica alimshukuru sana ila tu hakujua kuwa
Erica ana mpango gani. Baada ya hapo, Erica aliona sasa mpango wake wa
kumuaibisha Rahim utatimia maana ataenda moja kwa moja kwenye harusi
yao. Ilikuwa siku ya kumpeleka mwanae kliniki, kiukweli kwa
siku zote za kumpeleka Yule mtoto wake kliniki alikodi gari kwani hakutaka mtu
yeyote amuone, na alienda hospitali ya mbali na kwao kwani hakutaka hata
kukutana na jirani yao na akagundulika kuwa ana mtoto kwani wengi watajiuliza
kuwa harusi vipi, na siku hiyo kama kawaida alimpigia simu dereva wa gari za
kukodi kisha kujiandaa na kusubiria afike ili ampeleke mtoto wake
kliniki. Wakati anatoka na lile gari, akamuona Tumaini akiwa amebeba
pochi na boksi na alionekana kama anaelekea nyumbani kwao, alijiuliza
sana “Yule Tumaini anaenda kwetu kufanya nini? Au ndio zile zawadi
alizosema ni Erick amenipa? Mungu wangu jamani, akijua kama nina mtoto
itakuwaje? Erica mimi dah!” Akachukua simu na kumpigia simu mama
yake, “Mama, kuna rafiki yangu nimemuona anakuja hapo nyumbani, nakuomba
usimwambie chochote kama nina mtoto. Tafadhali mama yangu” “Hadi kwa
rafiki zako unaficha?” “Nakuomba mama usimwambie” “Kwahiyo
nimwambie umekwenda wapi?” “Mwambie nimeenda kwa dada, nitarudi kesho
ili aondoke mapema. Akishaondoka unipigie simu nirudi nyumbani” “Hahaha
wewe mtoto loh! Unanifundisha mamako uongo kama wako” “Nisaidie mama,
nakuomba” “Haya sawa” Kisha Erica akakata ile simu na kuendelea
na safari yao ya kliniki, alifika na kushuka na mwanae kisha Yule dereva
kuondoka, yeye akampeleka mtoto kliniki na kumaliza mambo ya vipimo vya
mtoto. Wakati anatoka kliniki akiwa anataka kutafuta usafiri wa
kumrudisha nyumbani kwao, akashtuka akishikwa bega, alipogeuka alikuwa ni Rehema
rafiki wa dada yake, ambaye amewahi kumpa ushauri pindi anasoma kuwa asiendekeze
wanaume, “Kheee Erica kumbe una mtoto?” Erica alikuwa kimya tu
kwani kama alikumbwa na bumbuwazi na kushindwa hata kumjibu kuwa ana mtoto au
la, kwani atakataaje ikiwa mtoto yupo nae mwenyewe, ila aliendelea
kumwabia, “Mtoto wako mzuri sana Erica, hongera mdogo
wangu” “Asante” “Vipi sherehe za kimya kimya hata hatualikani
jamani mdogo wangu?Umeolewan lini? ” “Hamna dada sijaolewa, nimezaa
tu” Erica aliongea kwa aibu aibu flani hivi, Rehema alielewa na
kumwambia, “Ila usijali mdogo wangu, kuzaa kabla ya ndoa sio mwisho wa
maisha na kuolewa kupo tu. Unaniona dada yako, nikikusimulia jinsi nilivyoteseka
ni huyu mdudu anayeitwa mapenzi utanihurumia. Nilijua sitakuja kuolewa kamwe,
maana nina watoto watatu halafu kila mtoto na baba yake yani kwa kifupi hadi
nilishajikatia tamaa. Ila wiki ijayo ni harusi yangu, nitakuja kuwaletea kadi ya
mualiko na pale nyumbani” “Mmmh dada kwanini umeniambia yote
hayo?” “Nimekwambia haya mdogo wangu sababu nimeona sura yako wakati
nimekuuliza swali la je umeolewa? Ukainamisha sura chini na kunijibu, hata
usijisikie vibaya mdogo wangu, ngoja mambo yangu ya harusi yaishe nitakuja
kuzungumza na wewe” “Sawa dada nashukuru” “Ila hongera sana
mdogo wangu, umepata mtoto mzuri sana, mshikilie huyu yani mfanye kila kitu
katika maisha yako na wala hao wanaume hawatakuumiza akili mdogo
wangu” Kisha akaagana nae na kutoka nje ya ile hospitali, akampigia simu
mama yake akiulizia kama Yule mgeni ameshaondoka, alipoambiwa kuwa aliondoka
alifurahi na kupanda gari kisha kumwambia dereva ampeleke
kwao. Alifika nyumbani kwao na kumkuta mama yake, akamsalimia
ila kabla hajauliza kuhusu mgeni aliyefika mama yake akamwambia, “Mgeni
wako kakuachia huu mzigo wako, amesema nikupatie halafu anasema mbona hupatikani
hewani? Eti kakukumbuka sana” “Aaah asante” Erica akachukua lile
boksi na kuingia nalo chumbani kwake huku akishikwa na kimuhemuhe kujua kuna
nini kwenye lile boksi, kwavile mwanae alikuwa amelala akamlaza halafu akafunga
mlango wa chumbani kwake na kuanza kufungua lile boksi. Alipofungua, juu
kabisa alikutana na kadi halafu na karatasi ndogo yenye maandishi, akaichukua na
kuisoma, “Kwako Erica, nimetumia njia ya zamani kidogo sababu najua kama
tungeanza mapenzi yetu kipindi kile basi tungetumia njia hii pindi tungesoma
shule za mbali mbali, ila Erica ulikubali maneno ya watu yatenganishe mapenzi
yetu. Nakiri kukupenda toka siku ya kwanza kukuona darasani, wewe ni msichana wa
kwanza kwangu kumpenda nab ado nakupenda toka kipindi kile. Ni mengi nimeambiwa
na dada yangu kuhusu wewe, na picha nimetumiwa ila nikawaza sana kuwa kwanini
maneno yaendelee kuharibu mahusiano yetu? Moyo wangu unaniambia kuwa wewe ndiye
mama wa watoto wangu, inawezekana umepata habari kuwa nilikuwa na wasichana
wengi sana na wengi walitamani kuzaa na mimi ila kwavile nimeshaipanga akili
yangu kuwa nahitaji kuzaa na wewe basi siwezi kuzaa na yeyote Yule labda ukatae.
Nikawa na msichana huku ila sina furaha maana wewe ndio umebeba furaha yangu,
Erica nakupenda sana na pia najua kuwa unanipenda sana. Watu wengi husema ni
vigumu wapendanao kuwishia pamoja ila najua kwetu itawezekana ikiwa tu tutaamua
kuishi bila kusikiliza maneno ya watu. Upatapo ujumbe huu Erica tafadhali
nitafute hewani, usiponitafuta najua ujumbe wangu hujaupata na kama nimeambiwa
umeupata na hujanitafuta nitajua moyo wako haupo tena kwangu. Tunapendana Erica,
naomba tuwe pamoja. Zawadi niliyokuwekea ni kitu ambacho ulionekana kuvutiwa
nacho sana siku ile kwenye picha hotelini, hukujua ila kuna picha moja ulivutiwa
nayo sana na ilikaa akilini mwangu na leo nimeweka zawadi hiyo kwenye boksi
hili. Nakupenda Erica, ni mimi kipenzi chako Erick” Chozi lilimtoka
Erica kwani alijiona ni msichana mpumbavu kuliko wote maana alichoandikiwa na
Erick ndio kitu alichokuwa anakitamani maisha yote ila atafanyaje sasa na ana
mtoto na mwanaume mwingine? Je Erick atamuelewa kweli? Alihisi kama
kuchanganyikiwa vile, kwani ukweli upo wazi anampenda sana Erick na alitamani
siku moja aambiwe maneno aliyoambiwa na Erick kwenye barua, sasa bahati hiyo
imemjia ila ana mtoto tayari, akisoma barua ya Erick anaona ni jinsi gani
mwanaume huyo kajiuzuia asiwape wasichana mimba sababu anataka mtoto azae na
Erica, vipi yeye aliyejiachia na kupata mimba na kusahau kabisa kama kuna Erick
wakati anampenda sana? Alihisi kupagawa hata akashindwa kumtafuta Erick hewani
na wala hakuendelea kulifungua lile boksi kwani alijua ni atajiumiza zaidi kwani
anampenda sana Erick. Akainuka na kulibeba lile boksi kisha kuliweka kwenye
kabati lake na kulifungia, alirudi kitandani na kuinama huku akilia kwani moyo
wake uliumia kila alipofikiria kuhusu Erick maana ndiye mwanaume ampendaye ila
Rahim ndiye baba wa Angel yani hapo alihisi akili yake
inakengeuka. Kesho yake alitumiwa ujumbe na Babuu, “Ile
shughuli ni leo” Erica alishtuka sana na kisha kujiandaa ili awahi
ukumbini maana aliambiwa saa tisa mpaka saa kumi itakuwa imeanza. Basi ilipofika
saa kumi akamvalisha mwanae na kuita gari ili iwapeleke, wakati anataka kutoka
tu mama yake akamuwahi, “Haya haya, kiguu na njia. Miguu imeanza
kukuwasha eeh! Unaenda wapi na mjukuu wangu?” Kwavile hakujiandaa kusema
chochote alijikuta akijiuma uma tu, “Naenda kumsalimia Johari” “Usinichekeshe mie, si wewe mwenyewe ulisema kuwa hutaki watu
wajue kama una mtoto! Iweje utake kwenda kwa Johari na mtoto?” “Aaah
mama, sikuona mtu wa kumuachia hapa nyumbani, halafu Johari kaomba
niende” “Haya mlete” Erica alimkabidhi mtoto mama yake, kisha
mama yake akamwambia, “Nenda mwenyewe huko unapotaka kwenda, mjukuu
wangu niachie” Kwakweli pozi lilimuisha gafla Erica maana hakuelewa
kabisa, ila kwavile alishaita na gari ilibidi atoke tu ili aende. Wakati
anatoka getini ili apande gari, alimkuta Bahati nje ya geti ndio anataka
kugonga. Erica alimkabidhi mtoto mama yake, kisha mama
yake akamwambia, “Nenda mwenyewe huko unapotaka kwenda, mjukuu wangu
niachie” Kwakweli pozi lilimuisha gafla Erica maana hakuelew kabisa, ila
kwavile alishaita na gari ilibidi atoke tu ili aende. Wakati anatoka
getini ili apande gari, alimkuta Bahati nje ya geti ndio anataka
kugonga. Bahati alimsogelea Erica na kumkumbatia, ila gari nalo lilikuwa
nje likimsubiri Erica, alimuangalia Bahati hakujua kwa muda huo amwambie kitu
gani, Bahati alimuuliza Erica, “Vipi mbona uko hivyo?” “Kuna
mahali natakiwa kuwahi” “Basi twende wote” “Aaah wewe nisubiri
tu hapa” Erica akasogelea lile gari na kufungua mlango ili aingie, ila
Bahati akamshika mkono na kusema, “Erica, nimeacha kazi zangu zote na
nimekuja kwa lengo la kukuona wewe. Kumbuka hata ningekupigia simu yangu
usingepokea, ila unataka kuondoka na kuniacha una maana gani? Nimekwambia twende
wote hutaki” “Bahati, nielewe yani kuwa muelewa pale mtu anaposema
jamno. Niache niende, kuna mahali nawahi” “Kwahiyo mimi sio wa
muhimu?” “Sijui kama unanielewa” Ila kabla Bahati hajamuachia
mkono, mara alitoka mama Erica pale nje na kumwambia Erica, “Eeeeh
afadhali bado hujaondoka, mtoto kacharuka mwenzangu” Yani Erica ndio
aliona hapo pamechanganywa maji na mafuta maana mama yake nae kaja kuvuruga tu
kama kawaida. Ikabidi ampe Yule dereva pesa ya usumbufu, halafu aingie ndani
ambapo Bahati nae alimfata nyuma huku akijiuliza maswali kuhusu mtoto
aliyecharuka. Erica aliingia ndani na kumchukua mtoto kwa mama
yake kisha kwenda nae chumbani kumnyonyesha, kwahiyo sebleni alibaki mama Erica
na Bahati. Ambapo Bahati alimsalimia vizuri sasa huyu mama, kisha huyu mama
alianza kwa kumuomba msamaha, “Nisamehe mwanangu kwa yaliyopita, yani
sikujua nilijua ndio unaniharibia mwanangu hadi tukakupeleka polisi. Nisamehe
sana” “Usijali mama” “Yani kijana una moyo wewe, nilijua toka
siku ile hutokuja tena nyumbani kwangu, ila umekuja jamani una moyo sana. Haya
mwenzio huyo ana mtoto” “Ana mtoto?” “Ndio, kumbe
hujui?” “Sijui mama” “Mtoto angekuwa wa Kiswahili tungekuhisi ni
wewe ila mtoto ni wa kiarabu sijui kipemba na baba yake
hajulikani” Kiukweli Bahati alijihisi vibaya sana ila hakuweza
kujionyesha pale kuwa kajihisi vibaya na hakuweza kumjibu zaidi huyu mama kwani
maneno yale yaliujeruwi moyo wake, huku akitamani sana kusikia kutoka kwenye
kinywa cha Erica maana bado hakuamini amini kama Erica ana mtoto. Baada
ya kimya kuzidi mama Erica alimuuliza tena Bahati, “Utakunywa kinywaji
gani?” “Aaah usihangaike mama” “Hapana sio nisihangaike,
hujawahi kunywa chochote hapa nyumbani kwangu, leo nahitaji utie baraka kwa
kunywa kitu kwenye nyumba yangu” “Basi maji mama” Basi mama
Erica alienda kuleta maji na kumpa Bahati ambapo bahati alikunywa maji yale na
kuyamaliza kwa muda mfupi tu kwani alihisi kama kuna kitu kimekaa kooni halafu
Erica hakutoka chumbani wala nini, ikabidi wakati mama yake anarudisha kikombe
aende na kumuita Erica. Alimkuta kalala pembeni ya
mwanaye, “Yani Erica umeingia kumnyonyesha mtoto na kulala hapo hapo
wakati kuna mtu anakusubiri kweli!” Erica akashtuka na kukumbuka ni
kweli Bahati alikuwa akimsubiria ila usingizi ulimpitia alivyokwenda kumyonyesha
mtoto kitandani na kuwa na mawazo mengi kuhusu harusi aliyoambiwa ni ya Rahim.
Akainuka ili akamsikilize Bahati, alipotoka mama yao alitoka nje na kuwaacha
waendelee na maongezi. Erica hakuongea chochote ila Bahati ndio alianza
kuongea, “Erica kumbe una mtoto? Mbona hukuniambia?” Erica
alikuwa kimya tu, na Bahati aliendelea kuongea “Ungeniambia mapema
Erica, unajua ni jinsi gani nakupenda na sipo tayari kuona ukiaibika. Mamako
kaniambia kuwa baba wa mtoto hajulikani ila ungeniambia mapema ingekuwa rahisi
kuliweka sawa swala hili. Naweza kuwa baba wa mtoto, haijalishi mtoto huyo
anaonekanaje, mama kasema sijui ni mwarabu au mpemba, ninachojua mimi ni kuwa
kitanda hakizai haramu, naweza kuwa baba wa mtoto Erica sio sawa kuwa na mawazo
kiasi hiko. Yani unapatwa na tatizo unashindwa hata kunishirikisha jamani Erica?
Ulihisi nitakataa au?” Erica alikaa kimya tu ila alikuwa akijiuliza kuwa
Bahati ana upendo wa aina gani maana alikuwa ni tofauti na wanaume wote
ulimwenguni, alishangaa sana kwani hakujua kama kuna wanaume wenye moyo kama wa
Bahati, kwakweli alimshangaa sana na kubaki akimuangalia tu bila ya kumjibu.
Bahati aliendelea kuongea, “Sema neno lolote nielewe Erica, mimi nipo
kwaajili yako” “Nashukuru sana kusikia kuwa bado upo kwaajili yangu, ila
kuhusu mtoto haikuwa nafasi nzuri kwa leo kuliongelea hilo swala. Nilitaka
nikutafute kwa muda wangu nikueleze ila kwavile umejua sina budi kukwambia, ni
kweli nina mtoto na kuhusu swala la baba wa mtoto bado ni kitendawili kwangu.
Ila bado nina msimamo wangu ule ule wa tafuta pesa kwa bidii Bahati ili leo na
kesho mkeo na watoto wako wafurahie uwepo wako” “Mke wangu ni wewe na
mtoto wangu wa kwanza ni huyo uliyemzaa wewe Erica, nitafanya kazi kwa bidii
kweli ili mimi,wewe na mtoto wetu tuishi vizuri. Na kwa hakika kabisa Erica
huwezi amini ambayo Mungu katutendea, najua ulishakosea ila hujakosea bado maana
hujanikosa mimi. Biashara yetu imekuwa kubwa sana, yani huwezi amini samaki
wamekuwa na soko kubwa ambalo sikulitegemea, pia nilikuanzishia biashara ambayo
nilisema utaifanya ukimaliza chuo ila sababu unalea acha niendelee tu
kuifanya” “Ni biashara gani?” “Erica, siwezi kutoka nje ya
ufugaji kwahiyo biashara ambayo nilianzisha ni ya kuku wa kienjyeji. Uwiii
natamani uone jinsi biashara hiyo ilivyo na neema yani Erica jamani biashara
imekuwa kubwa naogopa, na juzi nilikuwa mkoani kuchukua kuku wengine niliagizwa.
Na leo nilikuwa nabahatisha tu, ila kwasasa nitakuletea kuku na samaki uwe
unakunywa na supu kwaajili ya afya yako na mtoto” Mara mtoto wa Erica
alianza kulia, na Erica akainuka ili akamchukue, Bahati
akamwambia, “Naomba uniletee mwanetu nimuone Erica” Basi Erica
alipotoka ndani alitoka na mtoto, ambapo Bahati alimshika mtoto Yule na
alionekana kumfurahia balaa kama mwanae vile. Bahati hakuondoka mapema
kwakina Erica na kuzidi kufanya Erica kukosa muda kabisa hata wa kwenda tena
ukumbini kama alivyopanga, basi kwenye mida ya saa mbili na nusu usiku ndipo
Bahati alipoaga kuwa anaenda, alimwambia Erica amuitie mama yake ili amuage
ambapo Erica alifanya hivyo, wakati mama yake anatoka Erica alienda kumlaza
mtoto ndani, kwahiyo mama Erica alivyofika sebleni alimkuta Bahati akijiandaa
kuondoka, Bahati akampa mkono wa kwaheri mama Erica ambapo alimwachia na
pesa, “Asante mama, kwaheri. Tutaonana tena” Mama yake Erica
alitabasamu sana na kuendelea kumkaribisha hadi Erica alipotoka na kumsindikiza
hadi getini na kumuaga. Erica alirudi ndani na kumkuta mama yake akiwa
ameshika hela mkononi, “Kheee mama, hela za nini unaenda
wapi?” “Naenda wapi? Nimepewa hela na baba Angel” “Baba Angel!
Sikuelewi mama” “Si Yule kijana kanipa hela, yani sikujua kama Yule
kijana ana moyo wa upendo kiasi hiki” “Kakupa shilingi ngapi? Mama
bhana, sasa Yule kijana kawa baba Angel toka lini?” “Yule ndio baba
Angel mwanangu, ona alivyokaa kumbembeleza mtoto hapa. Yale ile ndio aina ya
wanaume wanaotakiwa ulimwenguni. Kanipa elfu hamsini ya pole ya kulea mzazi,
nimefurahi sana hata kama mtoto mwarabu ila Yule ndio baba yake” Erica
alimuangalia mama yake ambaye alienda chumbani nay eye akaenda chumbani
pia. Erica alimfikiria sana mama yake na kumkosea jibu
kabisa, “Mama yangu anashangaza sana, siku zote anasema mwanaume mwenye
hela ndio mwanaume halafu mimi kuzaa lawama zote kanipa haya leo kapewa hela na
Bahati kaanza kumsifia kuwa ndio mwanaume. Dah jamani mama yangu ni
balaa” Kisha akainuka na kwenda kuoga, halafu kula na kurudi na mawazo
yake ila kiukweli swala la Bahati lilimchanganya sana yani alishindwa kuelewa
kuwa Bahati ni mwanaume wa aina gani ambaye huwa haoni maovu
kwake, “Yani yeye kila kitu kwangu ni sawa, jamani kwanini wanaume
wengine wasiwe kama Bahati? Laiti Erick angekuwa na moyo wa Bahati ningefurahi
sana, lakini akijua nina mtoto najua upendo wake kwangu utaishia hapohapo. Au
anaweza kuwa na moyo kama Bahati! Jamani Bahati mbona yupo tofauti sana na
wanaume wengine?” Hakupata jibu ila aliingia kwenye mtandao ilia one
kama Rahim yupo amuulize maswali yake ila cha kushangaza siku hiyo hakumkuta
kabisa Rahim hewani na kumfanya aamini kuwa ni kweli alikuwa ameoa, roho
ilimuuma sana na kumfanya ashindwe hata kupata usingizi tena kwa mawazo. Mwanae
alipokuwa akiamka alikuwa akiongea nae kama mtoto anayesikia, “Angel
mwanangu, wanawake tuna mitihani mingi sana ila nisingependa ukikua uwe kama
mimi. Napenda uwe ni mtoto wa kusikiliza ushauri na kuupima, ona mama yako
nilimuamini baba yako ila kaniacha na kwenda kuoa mwanamke mwingine. Baba yako
katuacha Angel, haoni thamani yetu” Machozi nayo yalikuwa yakimtoka na
kumkosesha raha kabisa yani siku hiyo hakulala kabisa na alikuwa akigalagala tu
kitandani, akainuka na kwenda kuchukua lile boksi alilotumiwa na Erick na kutoa
ile barua ya Erick akaisoma tena na kulia haswaaa kwani muda huu ni kama alikuwa
akitonesha kidonda chake kwani hawezi kupingana na ukweli kuwa Erick ndiye
mwanaume anayempenda sana ila tu maisha ndio yaliyomtenganisha naye. Bado hakuwa
na ujasiri wa kufungua zawadi alizoletewa na Erick, alirudisha lile boksi
kabatini ila safari hii hakulifunga kabati. Alirudi kitandani na ile barua
aliyoandikiwa na Erick, alikuwa akiibusu huku akilia sana kisha akafungua mkoba
wake na kuiweka kwani alitaka kila muda akiitaka aichukue tu na kuisoma imchome
moyo wake, kwani alijiona kuwa anastahili kuchomwa moyo. Siku hiyo
alijikuta yuko macho hadi alfajiri kabisa kwahiyo ile asubuhi ndio akalala, tena
alilala sana ule usingizi wa hoi kabisa. Ilikuwa kwenye mida ya
saa tano na nusu asubuhi ambapo Erica aliamshwa na dada yake Bite, “Loh!
Yani wewe unalala kama mzigo? Ndio kusema mtoto kakusumbua sana usiku au? Mama
kamchukua mtoto kamuogesha hadi mtoto kalala tena ila wewe bado
umelala” Erica aliinuka ila macho yalikuwa mazito sana ni kweli mamake
wakati anamchukua mtoto kumuogesha alimsikia ila alishindwa kumjibu sababu ya
usingizi, na hakukumbuka chochote zaidi ya kulala, basi akaamka pale na
kumsalimia dada yake ambapo dada yake alimwambia akaoge ilia pate nguvu kwahiyo
Erica aliinuka na kwenda kuoga ili kupata nguvu na kuondoa uchovu wa
usiku. Erica alipotoka kuoga alimshangaa dada yake akiwa kitandani na
lile boksi yani kashalipekua lote na alikuwa ameshika vitu vya kwenye lile
boksi, Erica alimshangaa dada yake, “Kheee dada!” “Unashangaa
nini Erica? Kwani ni dhambi mimi kuona zawadi ulizoletewa na baba
Angel?” “Nani kakuonyesha hilo boksi dada?” “Nilikuwa natafuta
mtandio ndio nikafungua kabati lako na kukutana na hili boksi, oooh kumbe baba
Angel anakupenda kiasi hiki!” Ilibidi tu Erica awe mpole maana kama
boksi dada yake alishalisaula na kila kitu kilikuwa juu kwahiyo hata kama
hakupenda kuviangalia ilibidi aangalie tu, na kumuuliza dada
yake, “Kwanini unasema ananipenda?” “Unajua ukiona mwanaume
anakuletea zawadi hadi ya nguo ya ndani ujue anakupenda sana, anakujali yani
huyo mwanaume usimuache” Kisha dada yake alizishika zile nguo za ndani
na kuzitathmini vizuri huku akisema, “Ooooh ni nzuri hizo, mdogo wangu
una bahati sana. Nimeishi na James kwa miaka mingi, hadi tumepata mtoto, amekuwa
na kuchangamka sasa, anaita hata baba ila James hajawahi kuniletea zawadi ya
nguo ya ndani hata ndotoni. Siku zote nimekuwa nikijisifia kuwa James ananipenda
sababu ananipa pesa lakini pesa sio kila kitu katika maisha. Kuna vitu vingi
zaidi ya pesa, kama mtu kukujali na kukuthamini. Baba Angel simfahamu ila kwa
zawadi hizi kwa hakika anakupenda” “Dada jamani, yani kwa zawadi tu ndio
kusema mwanaume ana upendo jamani!” “Ndio, hebu angalia huu mkoba
aliokuletea yani dah mtamu huo unavutia hata kuuangalia, mwanaume anajua
kuchagua jamani, sijapata kuona.” Erica alimuangalia dada yake
alivyokuwa akisifia vitu vilivyoletwa na Erick akijua ni baba yake Angel kumbe
ni mtu mwingine kabisa maana baba Angel yupo mahali akila raha
zake. “Ngoja nikuulize dada, mapenzi ni nini?” “Mapenzi ni
kupendana, yani ukipendana na mume wako utajiona kama upo dunia nyingine sababu
unaishi na mtu anayekupenda na wewe unampenda. Ila kuishi na mtu unayempenda
halafu yeye hakupendi ni mzigo na kuishi na mtu anayekupenda halafu wewe
humpendi ni mzigo. Ubaya wa mapenzi upo sehemu moja, kuna watu ni waigizaji
nalaa, yani anaweza kukuigizia anakupenda kufa na kupona hadi ukaweka moyo wako
kwa mtu wa aina hiyo na mwisho wa siku unaumia na kujiuliza kuwa huyu mtu si
alikuwa ananipenda! Imekuwaje tena! Kumbe alikuwa anakuigizia, yani kupenda
bhana kupo automatic kuna viashiria Fulani ukiviangalia kwa mtu unaelewa kuwa
huyu ananipenda haswaa na ukiangalia kwa mwingine unaona kuwa huyu hakuna lolote
ila na stress zake tu ndio anakuja kumalizia kwangu kwa kujifanya kuwa
ananipenda.” “Wewe na shemeji mpo kwenye kundi gani?
Mnapendana?” “Jamani mambo ya mimi na James aache tu, mwanaume ni
muigizaji Yule sijapata kuona. Niliamini napendwa balaa, nikajitoa kwa moyo
wangu wote na kumpenda pia, jamani hadi nimezaa huyu mtoto ndio nimekuja kujua
James hakuwa na mapenzi na mimi kama nilivyofikiria ila navumilia nitafanyaje
sasa. Nahitaji mwanangu apate malezi ya baba na mama, halafu siwezi kumkimbia
James niache nafasi kwa lile janamke lisilokuwa na akili kurudi pale kwangu.
Erica mdogo wangu, mapenzi yanaumiza kichwa sana, mshikilie huyu baba Angel,
anaonyesha anakupenda sana na inaonyesha na wewe mnampenda. Utaishi nae vizuri
mlee mtoto wenu” “Haya dada asante” Erica aliamua kuitikia ilia
amridhishe dada yake ila kiukweli alikuwa anaumizwa sana, alianza kuvaa kisha
dada yake akamwambia kuwa alimfata sababu alikuwa na shida nae amsindikize
mahali,kisha dada yake alitangulia sebleni ambapo Erica alijiandaa halafu
akabeba zile zawadi ambazo dada yake amezisasambua pale kitandani na kuzirudisha
kwenye boksi kisha kuweka kabatini kwake ila alikuwa na mawazo sana kiasi kwamba
hakujua mume yupi ni sahihi kwake, alitoka sebleni ikambidi akamue maziwa ya
kumuachia mtoto wake halafu wakamuacha na mama yao na wenyewe
kuondoka. Wakiwa kwenye gari ya Bite, Erica alimuuliza dada
yake, “Ni wapi huko tunaenda dada?” “Sikutaka tu kusema nyumbani
ili mama asijue, nimemdanganya kuwa kuna mkopo nataka kuchukua inabidi Erica
akanisainie. Ila kiukweli mdogo wangu, dada yako hapa nimechanganyikiwa kabisa,
yani mapenzi yananichanganya haswaaa.” “Kivipi dada?” “Si Yule
msichana mjinga nae ana mtoto, nasikia James kampangishia nyumba mahali na
anamuhudumia. Tatizo sio kumuhudumia, tatizo ni kuwa James anashinda huko jamani
yani James asikii wala haoni, huwezi kuamini siku hizi hadi nyumbani harudi yani
akili yangu imegoma kufanya kazi kabisa.” “Kheee makubwa, sasa tunaenda
wapi dada?” “Tunaenda huko anapoishi huyo mwanamke, tukifika nataka wewe
uingie ndani kwanza halafu mimi nitakuwa nje.” “Sasa mimi nitaingia
kufanya nini dada?” “Nataka James ajue kama familia yote tumejua upuuzi
anaoufanya, unajua sijamwambia dada Mage wala mama maana haya mambo ya aibu
jamani yani dah! Huyu mwanaume siamini mwenzenu, sina raha kabisa yani. Sijui
nitakuwaje nikihakikisha kuwa ni kweli James anakuwaga kwenye nyumba hiyo,
nataka uingie ndani wewe kwanza, nitakuwepo nje nikisikilizia kama ni yeye au la
kisha nitaingia na mimi” Erica aliweza kumuona dada yake alivyoonyesha
kuumizwa na swala hilo la shemeji yake, kwahiyo alikubali kwenda kumfumania
shemeji yake. Walifika na dada yake kwenda kupaki gari mahali, kisha
wakashuka na kuanza kuelekea kwenye nyumba ambayo James alimpangia mwanamke
wake, ila kwa bahati Yule mwanamke hakuwepo hapo ndani kwa muda huo alikuwa
ameenda dukani. Bite alikaa nje na kumtaka mdogo wake aingie ndani,
Erica alifungua mlango na kuingia alimkuta James akiwa amekaa tu tena hana
habari, Erica alimwambia kwa mshangao, “Shemeji!” “Kheee Erica!
Umekuja kufanya nini?” “Nikuulize wewe unafanya nini?” “Jamani
Erica kipenzi changu, yani anaacha kuwa na wivu dadako unakuwa na wivu wewe.
Kweli tunapendana” Bite alichukia sana kusikia maneno
hayo. Bite alikaa nje na kumtaka mdogo wake aingie
ndani, Erica alifungua mlango na kuingia alimkuta James akiwa amekaa tu tena
hana habari, Erica alimwambia kwa mshangao, “Shemeji!” “Kheee
Erica! Umekuja kufanya nini?” “Nikuulize wewe unafanya
nini?” “Jamani Erica kipenzi changu, yani anaacha kuwa na wivu dadako
unakuwa na wivu wewe. Kweli tunapendana” Bite alichukia sana kusikia
maneno hayo. Kwakweli Bite hakuweza kuvumilia zaidi yay eye kuingia
ndani pia, alimuangalia mumewe kwa gadhabu sana, “James, hivi ni dharau
kiasi gani unanionyesha? Umeona kuzaa na msichana wa kazi haitoshi, ukaamua
kumpangishia nyumba na wewe kuzamia hukuhuku. Halafu bila haya unamuita mdogo
wangu kipenzi chako eti mnapendana sana, hivi James una nini
lakini?” Bite alikuwa na hasira sana hata maneno hayo alikuwa akiongea
huku machozi yakimtoka, James alikuwa kama amepigwa na butwaa vile maana
hakufikiria kama Erica amefika na mkewe, kitendo cha James kukaa kimya
kilimchukiza zaidi Bite na hasira zake alienda kumalizia kwenye vyombo vya
nyumba ile, “Unaniacha nyumbani, unaniambia siku hizi hela ngumu kumbe
unakuja kutumbua kwa malaya wako huku” Bite akaifata Tv na kuibeba juu
kisha akaibwaga chini, James akashtuka akasema, “Bite hebu acha uchizi
huo” Muda huo Bite alienda katika kabati la vyombo na kubwaga vyombo
vyote vilivyokuwa kwenye lile kabati, “Wewe Bite, kuwa na heshima basi.
Nyumbani kwa watu hapa” “Nyumbani kwa watu? Kwani mimi nyani? Yani
mwanaume una roho mbaya wewe hata shetani anakuogopa, hivi ni wa kunifanyia
vitendo vya ajabu kiasi hiki wewe? Hata humfikirii mtoto? Nimevunja ndio, wewe
si tajiri, na ununue vingine” Muda huo alikuwa anaelekea kwenye friji,
ilibidi James atake kumfata, ila Bite aliwahi kisu mikononi
mwake, “Ukinifata tu wewe kenge nakuchoma, yani leo napelekwa jela na
wewe unakufa halafu sijui mtoto atalelewa na nani” James akamuangalia
Erica na kumwambia, “Erica nakuomba mtulize dada yako” Kisha
James aliruka nje na kutoka maana aliona pale ni balaa tupu kumbe hata mwanamke
wake alikuwa amerudi ila baada ya kuona lile balaa alikimbia. Erica
alimuangalia tu dada yake, ni kweli aliona anachofanya dada yake si sawa ila
alitambua kuwa dada yake anafanya yale kwa hasira tu na si vinginevyo. Sema
alipaswa kumzuia kwani dada yake mwenyewe alionyesha kutokwa na damu kwamaana
hiyo vile vyombo alivyopasua vingine vilimchoma, Erica alimuangalia dada
yake, “Dada, hasira haijengi. Hebu mfikirie Junior, hivi wewe ukienda
jela na shemeji akifa halafu Junior akawa yatima kwa wazazi kujitakia hasara ya
nani? Twende mahali dada yangu ukatulize hasira zako, achana na huyu
mwanaume.” “Erica, niache. Huyu mwanaume si hela inamuwasha, atanunua
vingine” “Ndio dada, ila ufanyacho sio suluhisho dada yangu,
tuondoke” Erica alijitahidi kumwambia dada yake maneno ya kumsihi hadi
akakubali kuondoka, waliondoka na kwenda moja kwa moja walipoacha gari. Yani
walipoingia tu Bite alianza kulia kamavile kafiwa kama sio aliyekuwa anaongea
akitabasamu mwanzoni, hapo Erica akatambua kuwa mwanzoni dada yake alikuwa na
hisia tu sababu kashaambiwa kila kitu sasa pale kathibitisha na macho yake kuwa
kweli mumewe ana nyumba ndogo ndiomana imemuuma sana. Alilia sana kisha kuanza
kuongea mwenyewe, “Wanaume ni mbwa kabisa, yani wanaume hawafai. Lijitu
unalipenda, unajitunza kwaajili yake jamani, kwani hakukuwa na vijana wengine
walionitaka zaidi ya james? Ni vijana wengi walinitongoza mimi nab ado wengine
wananitongoza ila nilijitunza kwaajili ya mume wangu, siku zote nilisema
nampenda mume wangu, ndio chaguo langu nimepewa na Mungu na nilijua hata yeye
ananipenda pia. Hata baada ya kuzaa na msichana wa kazi nikahisi kuwa ni bahati
mbaya sababu sikuwa nyumbani, kumbe janaume lenyewe ni mbwa tena mbwa koko
uuuwiii jamani mimi huyu mwanaume huyu” Bite alikuwa akilia kama mtoto,
mdogo wake alikuwa akimbembeleza na kumsihi kuwa waondoke mahali pale, ilibidi
Erica ndio aendeshe gari, kwa bahati alikuwa amejifunza kuendesha gari maana
bila ya hivyo wangebaki kubembelezana tu bila mwisho. Wakiwa
kwenye gari, Erica aliona ni vyema waende nyumbani kwanza ila dada yake
alimkataza na kumuomba ampeleke nyumbani kwake, “Twende kwanza nyumbani
kwangu nikamchukue Junior wangu” Basi walienda hadi nyumbani kwa Bite na
kumchukua mtoto tu, kisha akampa hela Yule mdada wa kazi na kumwambia aende kwao
na atamwambia akimuhitaji tena, Yule msichana alishangaa ila ikabidi ajiandae na
kuondoka kisha Bite akafuna milango na kupanda kwenye gari akiwa yeye, mtoto na
Erica. Ila bado aliongea kwa uchungu sana, “Nimejikuta nikimchukia na
huyu mdada wa kazi wakati huyu hajanifanyia lolote baya, hivi kumbe mdada wa
kazi anaweza kukuchukulia mume kabisa kabisa ukabaki umebung’aa tu. Ila
uliniambia mdogo wangu, sema sikusikia mimi, nilijiamini napendwa, nilijiona
nimepata kumbe nimepatikana.” Alikuwa akitoa machozi tu hadi wanafika
nyumbani kwao, aliingia ndani na hata mama yao akawashangaa kuwa tatizo ni
nini, “Bite, nini tatizo mwanangu imekuwaje tena? Si mlisema mnaenda
kusaini mkopo? Imekuwaje tena” “Mama, subiri nikueleze” Bite
hakuweza kumficha mama yake kwani hakuweza kukaa na lile jambo moyoni, alihisi
moyo kulipuka tu muda wowote. Akamueleza mama yake kila kitu na hadi alivyoenda
na Erica, jinsi alivyomsikia James akisema na Erica, “Yani anathubutu
hata kumuita mdogo wangu ni kipenzi cahake? Imeniuma sana” “Yani kumbe
Erica alituambia ukweli ila tuylimpuuzia” “Alisema nini
mama?” “Alisema kuwa James alitaka kumbaka” Yani hapo Bite ndio
akashtuka zaidi baada ya kusikia kuwa mumewe alishawahi kutaka hata kumbaka
mdogo wake, alimuita Erica ili amsikie Erica mwenyewe, na Erica hakuacha neno
alimueleza kila kitu dada yake toka ile siku ya kwanza alivyotaka
kumbaka, “Jamani mdogo wangu, mbona hukuniambia?” “Sikutaka
kuvunja ndoa yenu dada” “Hukutaka ila imevunjika sasa, mama simtaki tena
James simtaki” “Tulia mwanangu, ni hasira tu hizo. Tuliza hasira, Yule
ni mumeo” “Sitaki mama, James sio mume wangu kuanzia sasa” Mama
yao alijua tu ni hasira na hakuweza kumshauri kwa chochote kwa muda huo. Badala
yake alimuacha na kumwambia aende chumbani akapumzike, “Bite mwanangu
hapa ni nyumbani kwenu, jisikie huru kabisa wala usibabaishwe na mambo ha mumeo
ila ndio wanaume walivyo. Usijali mwanangu yatakwisha tu” Alimwambia
akapumzike huku Erica nae akienda chumbani kwake na
mwanae. Kuna muda Erica aliwaza sana kuhusu mambo ya wanaume na
kukosa jibu, “Mfano ningejitunza, kwahiyo George angenioa sababu
angenikuta bikra? Je angenipenda kweli au angekuwa kanipenda sababu ya bikra? Na
je George ni mwanaume wa kuishi vizuri na mwanamke, ikiwa tu mimi aliniwekea
kisasi cha kunibaka kwa kosa ambalo sio langu? Ningeolewa na aina hiyo ya
mwanaume, si ndio yangekuwa haya haya ya dada Bite. Ila wanaume hawa
wanawafikiria na kuwakosea jibu kabisa, hivi wote wangekuwa kama Bahati, hivi
kuna mwanamke ulimwenguni hapa angelia jamani? Kwanini hawana moyo wa Bahati,
hivi Bahati anaweza kumtenda mwanamke kweli? Hapana jamani” Alijikuta
akiwaza sana, na kujaribu kutmtafuta Rahim hata kwa muda huo ila bado hakumkuta
hewani, na kumfanya ajipe asilimia mia moja kuwa Rahim ameoa
kweli. Alipoona dada yake amepumzika vya kutosha, akaona akamuulize
maswali kadhaa ya kuhusu mapenzi maana alihisi lazima atakuwa na majibu maana
tayari ameshaumia, “Dada samahani, hivi katika maisha yako, mwanaume
wako wa kwanza kumpenda ni shemeji?:” “Sikia mdogo wangu, katika maisha
yangu niliamini kuwa mwanaume asipokukuta bikra ndio anakusaliti na niliamini
wanawake wote wanaosalitiwa ni kwavile hawakukutwa bikra, nilijua wanaume wengi
wanapenda wanawake mabikira ni kweli wanapenda ila wanapenda kwavile anajisikia
raha kusema wanawake kadhaa nimewatoa bikira zao ila sio kwa mapenzi.
Nilijitunza mdogo wangu, nilijitunza sana, kuna mkaka mmoja nakumbuka vizuri,
alikuwa anaitwa Deus, alinipenda sana na kuja kuja kunipa habari za kunitongoza
mara kwa mara, nilijikuta nikianza kuvutiwa nae ila nikaona nitatenda dhambi
bure, nikaamua kuwa nae mbali kabisa. Nilfata mafundisho ya mama, ni heri nikae
kanisani kuliko kuwaza wanaume. Ilinisaidia sana kwani mawazo ya wanaume
hayakuchukua nafasi katika akili yangu, ndipo akaja James, na tena huwezi amini
ila James alikuja kanisani sababu yangu na kujifanya kaokoka pia, kwakweli
niliona napendwa yani mwanaume anaacha vitu vyote vya anasa sababu tako,
nikamkubali na akatangaza ndoa. Tulioana na kukaa kwenye ndoa kwa mwezi mmoja tu
ndipo James akasafiri na kwenda nje, nilikuwa na furaha moyoni kwa kupata
mwanaume mwenye upendo wa dhati, na zaidi ya yote ni mcha Mungu. Hiyo ilikuwa
furaha yangu, ila kumbe sikumjua James vizuri, kipindi amerudi nchini ndio
nimemjua James jamani, mwanaume kumbe ni mlevi balaa ila aliniigizia mimi tu
kipindi cha uchumba kujifanya hanywi pombe ili niamini ni mlokole kweli. Sasa
bora hata angekuwa ni mlevi tupu, kumbe ni mzinzi pia jamani, si kuleteana
maradhi huku eeeh! Mi bora niishi mwenyewe tu” “Pole dada, ila mapenzi
yanaumiza sana. Hivi inakuwaje mtu upo hivi ila unapata mwanaume yuko hivi yani
haendani na wewe. Na kwanini kwenye ndoa wengi wanalia? Yani wengine tunatamani
kuolewa halafu wengine mmechoka kwanini?” “Wewe tamani tu kuolewa, baba
Angel anakupenda sana. Sio mimi niliyependwa kwa kupewa pesa tu na kununuliwa
kile kigari ila sina furaha ya ndoa” Erica alitamani amueleze dada yake
kuhusu mikasa yake ya mapenzi ila aliona aibu na pia hakujua dada yake
angemchukuliaje, kwahiyo alijikuta akiitikia tu kuwa kweli baba Angel ana upendo
sana. Wakaongea vitu mbali mbali na kushauriana mambo mbalimbali,
ilikuwa ni jioni ambapo mama yao alienda kuwaita, “Haya, mabosi wenye
mawazo njooni mnywe supu mtulize mawazo yenu” Walitoka na kwenda sebleni
ambapo mama yao aliwawekea supu ya kuku, Bite alimuuliza mama
yake, “Kheee supu ya kuku! Umeenda kununua muda gani mama au wakati sie
hatupo?” “Hata sijanunua, kaja baba Angel kaleta kuku wane na misamaki
kibao nimeweka kwenye friji. Mwaka huu hadi mtu fidenge amalize kunyonyesha na
mimi nitakuwa nimefutuka” Erica alielewa kuwa mama yake anamuongelea
Bahati ila Bite hakuelewa bado alijua ni baba Angel aliyeleta zile zawadi ndio
kaleta na hizo kuku na samaki, “Kheee baba Angel ana upendo jamani.
Mungu ambariki” Akamgeukia mdogo wake na kumwambia, “Mshikilie
baba Angel mdogo wangu, huyu ndio mwanaume” Erica alitabasamu tu na
alipomaliza kunywa ile supu aliingia chumbani kwake na kumpigia simu
Bahati, “Kumbe ulikuja kwetu?” “Ndio, ila sikukukuta nikaamua
kumuachia mama mzigo” “Ndio una kuku wengi sana nini hadi umeleta
wane!” “Erica, afya yako ni bora kuliko kitu chochote kile. Kuku wapo
mama, wewe jilie tu na kama na kesho mtahitaji utaniambia” “Hapana
bhana, labda wiki ijayo, usilete tena” “Basi nitakuja kumsalimia
mtoto” “Usije hadi nikwambie, sawa” “Ila Erica usinifanyie
hivyo. Unajua kama ndugu zangu wote nimewaambia kuwa nimezaa na
wewe” Kwakweli Erica alimshangaa Bahati kuwa akili yake ikoje hadi
afikie hatua ya kuwaambia ndugu zake kuhusu mtoto ambaye anajua fika si wa
kwake, alimshangaa sana. Aliongea nae na kukata simu. Erica aliendelea
na shughuli zingine ila barua ya Erick ilimkaa sana kichwani mwake, alitamani
hata kumtafuta ila kilichomzuia ni swala la mtoto kuwa Erick akigundua ana mtoto
itakuwaje? “Ila nisipomtafuta pia atahisi simpendi tena. Ni kweli Bahati
ananipenda sana na yupo tayari kuishi na mimi kwa hali yoyote ile lakini
simpendi na hilo limekuwa tatizo kwangu, najitahidi balaa ila upendo kwake haupo
hata kidogo. Nikiangalia upande wa Rahim, ni baba wa mwanangu pia nimejitolea
kuishi nae ila inaonyesha hanipendi na alikuwa akinitumia tu. Maana halisi ya
mapenzi kutokana na maneno ya dada nadhani nikiwa na Erick ndio nitakuwa
nimekamilisha neno mapenzi kwangu, ila nawezaje kuwa na Erick wakati nishazaa na
mwanaume mwingine? Oooh Erica mimi jamani yani sijielewi kabisa.” Ni
kweli hakujielewa, na alikuwa akijishughulisha na kazi za hapa na pale ili tu
kupisha siku. Kesho yake alifika dada yao Mage maana alipata
ile habari kwa mama yao kuhusu James, kwahiyo alifika ili azungumze na mdogo
wake. Muda ambao Mage alikaa kuzungumza na Bite ilikuwa ni chumbani kwa
Erica kwahiyo Erica naye alikuwepo ndani. Mage alisema ili wote wajifunze, ila
bado ilikuwa ngumu kwa Bite kukubaliana na jambo alilolisema mage, “Dada
sijui kama kuna jambo utasema nikaelewa, dada sirudi tena kwa James bora niishi
mwenyewe tu” “Bite, elewa jambo moja. Una mtoto sasa na mtoto anahitaji
malezi ya baba na mama, unajua kila ndoa zinachangamoto nyingi. Najua utasema ya
kwako imezidi ila ukisikia za wengine utaona ndio balaa, angalia maisha ya
Junior kwasasa sio unajali tu furaha yako, jail na furaha ya
mtoto” “Dada sikuelewi, kwahiyo unanishauri nirudi tena kwa
James!” “Sikushauri kwa ubaya ila ndoa inahitaji uvumilivu wa hali ya
juu na wala haiitahi usikilize maneno ya watu, najua si maneno ya kuambiwa ila
ni kitu cha kushuhudia ila ni wewe unayeweza kuitetea ndoa yako na kuifanya
isimame tena. Kuikimbia ndoa sio suluhisho katika ndoa yako” “Ila
suluhisho ni kuendelea kuishi mahali ambako unajua fika utapata
ukimwi!” “Bite, ukimwi si kuna kupima jamani? Mimi nakupa ushauri
kwaajili ya mtoto wako, hakuna malezi bora kama ya baba na mama yani mtoto bora
ni Yule anayelelewa na wazazi wawili. Kama mzazi mmoja amekufa basin a ijulikane
amekufa sio yupo hai halafu haiwezekani kuishi nae au haiwezekani kuwa karibu na
mtoto, jamani kumuweka mtoto mbali na baba yake ni kumsononesha
mtoto” Erica alikuwa ameinamia chini tu kwani kwa kiasi Fulani nae yale
maneno yalimgusa, kisha dada yake Mage akamwambia, “Na wewe, hakuna kitu
chema kama mtoto kuwa na wazazi. Sasa wewe toka umlete huyu mpemba kwenye
familia hii mbona baba yake hatumuoni? Tatizo nini?” “Sasa dada
nifanyeje?” “Ufanyeje nini? Akuoe sasa” “Kama
hanitaki?” “Hivi ulianzaje kuzaa na mtu asiyekutaka, yani Erica kuna
muda unaongea kama sio msomi vile. Wewe umesoma, napenda kukwambia heshima ya
mwanamke sio elimu yake tu bali kuwa kwenye ndoa sio kutangatanga na kuzaa
hovyo” Erica alikuwa kimya maana walipewa darasa ambalo hata hakujua kwa
yeye atalichukuliaje hilo darasa maana kwa vitu vinavyoendelea kwake, alihisi
kuchanganyikiwa tu na hilo darasa. Mage aliwafundisha pale, na badaye
kuongea zaidi na mdogo wake huku akimsihi kuwa amsamehe James na wakaishi walee
mtoto wao, ila bado msimamo wa Bite ulikuwa palepale kuwa hawezi kumsamehe
James. Siku hiyo Erica alihisi kila akifikiria kichwa chake
kinavurugika tu, kwani tangu habari za ndoa ya Rahim, zilipita kama wiki mbili
na Rahim hakupatikana hewani kabisa, kitu hicho kiliumiza sana moyo wa Erica
kwani kila akikumbuka maneno ya dada yake kuwa mtoto anahitaji malezi ya baba na
mama aliumia sana, kwani bado aliona itakuwa ngumu sana kumkubalia Bahati kuwa
mtoto awe mtoto wake. Akapata wazo moja kuwa aende nyumbani kwakina
Rahim na akaongee na mama yake, akaona vyema akienda na mtoto kwani atakuwa na
uthibitisho kwa mama yake Rahim kuwa amezaa na Rahim. Akajiandaa kila
kitu na kutaka kutoka ila kama kawaida mama yake alimzuia kutoka na
mtoto, “Jamani mama, sasa kama naenda nae kliniki!” “Erica, sio
mjinga mimi eeh! Tarehe zote za kliniki nazijua. Huwa machale yananicheza kuwa
una mipango yako isiyopendeza ndiomana nataka uende mwenyewe na mjukuu wangu
niachie” Erica akaona isiwe shida, na kumuacha mwanae nyumbani kisha
yeye kuondoka zake. Alifika kwa Mrs.Peter na kugonga geti, alifunguliwa
na Salma yani msichana Yule Yule aliyeambiwa kuwa kaolewa na
Rahim. Erica alijikuta akishikwa na hasira za hali ya juu hata kutamani
kumparamia Yule dada, kwa hasira alizokuwa nazo alijikuta akimsukuma na kuingia
ndani. Yule dada alikuwa na mshangao kuwa huyu ana maana gani, akamsogelea na
kumuuliza “Kwanini umenisukuma?” Kabla Erica hajaeleza gadhabu
aliyokuwa nayo, alimuona kijana anayemfahamu akitoka kwenye nyumba ya kina Rahim
na kumfanya abaki na mshangao. Alifika kwa Mrs.Peter
na kugonga geti, alifunguliwa na Salma yani msichana Yule Yule aliyeambiwa kuwa
kaolewa na Rahim. Erica alijikuta akishikwa na hasira za hali ya juu
hata kutamani kumparamia Yule dada, kwa hasira alizokuwa nazo alijikuta
akimsukuma na kuingia ndani. Yule dada alikuwa na mshangao kuwa huyu ana maana
gani, akamsogelea na kumuuliza “Kwanini umenisukuma?” Kabla
Erica hajaeleza gadhabu aliyokuwa nayo, alimuona kijana anayemfahamu akitoka
kwenye nyumba ya kina Rahim na kumfanya abaki na mshangao. Yani
alibakinkama dakika tano hivi akishangaa kiasi hata Yule Salma alibaki
akimuangalia, mara akatoka Mrs.Peter, na kama kawaida ya huyu mama akimuonaga
Erica anavyomfurahia kwahiyo alimfurahia kama siku zote na kumuita kwa
nguvu, “Wao Erica binti yangu jamani” Alimsogelea na kumkumbatia
huku akimkaribisha pale ndani kwake ila Erica alibaki nje tu akimuangalia Yule
kijana ambapo Mrs.Peter alianza kwa utambulisho, “Erica, si nilikwambia
kuwa nina watoto wawili. Basi wa pili ndio huyu anaitwa John” Kisha
akamgeukia Yule mwanae na kumwambia, “John, huyu ni binti yangu pia
anaitwa Erica” John akamuuliza mama yake kwa mshangao, “Binti
yako?” “Ndio, ni msichana niliyezoea kumuita binti yangu maana nilitokea
kumpenda” John alimsogelea Erica na kumkumbatia kwa furaha kisha
akamwambia, “Yani leo siamini kama huyu Erica nimemuona tena
jamani” Mama yake alimuuliza kwa mshangao, “Kwani mnafahamiana
John?” Muda huu Erica alikuwa kimya kabia maana hata yale makeke
aliyoenda nayo kwenye nyumba ile hakuwa nayo tena, John aliongea kwa tabasamu
zito, “Mama, huyu ndiye msichana niliyekueleza kuwa nilimpenda sana.
Nilimtafuta sana bila mafanikio na siku ile kama angekuwepo yeye basi ni yeye
ndiye ningemvalisha pete ya uchumba kwani katika maisha yangu nilishasema ya
kwamba sitokuja kuchezea hisia za msichana kamwe na nikimpenda msichana
nitampenda kweli na wala maneno yangu hayatakuwa ya uongo kwake maana
nitahakikisha kumuoa” “Kheee kumbe Erica nisingemfahamu kwa njia ile ya
kukutana nae njiani basi ningemfahamu kwa njia ya kuolewa na mwanangu! Ila mimi
nampendaga tu huyu binti, hata mwanaume aliyempata pia ni mpole kama wewe John
mwanangu” Erica alikuwa kimya kabisa kwani aliona kama anagongelewa
msumari wa mto, ndoto yake kwa muda huo ni ndoa halafu anasikia kuhusu John
kutaka kuoa kwakweli alijikuta akikosa raha sana, kile kitendo cha kutokujibu
kilimfanya Mrs.Peter kuendelea kuongea, “Nisamehe Erica kwa
kutokukualika kwenye shughuli ya mwanangu, ni kwavile simu yako haipatikani na
sijui nini tatizo, ila ningekualika ungeona jinsi ilivyofana” Erica
alimuangalia John ambaye bado alionyesha ana furaha sana ya kuonana nae, kisha
John akamvuta Erica kwa pembeni kuzungumza nae kwani alimuona Erica kama kapigwa
na bumbuwazi Fulani hivi ambalo binafsi hakulielewa. “Erica, una tatizo
gani mbona kama sikuelewi au umechukia niliposema kuwa kuna msichana
nimemvalisha pete ya uchumba!” “Hapana” “Sasa mbona unaonekana
huna raha” “Basi tu” “Kweli Erica, niliposema nakupenda nilikuwa
namaanisha kuwa nakupenda na ndiomana nikakupa simu ili tuwasiliane. Cha
kushangaza gafla sikukupata hewani, kwa muda nikahisi kwavile umerudi shuleni,
nilihamishiwa kimsaomo nje ya nchi ila baada ya miaka miwili nilirudi na lengo
langu lilikuwa kukutafuta wewe. Nilihisi kuna siku ningekupata klwenye ile namba
ila sikuweza kukupata hadi mwaka juzi naipiga ile namba naambiwa tafadhali
ichunguze namba ya mteja unayepiga na upige tena, niliumia sana maana kila
nilipokuangalia Erica sikukupata. Ndipo nilipoamua kutafuta msichana mwingine wa
kutimiza ndoto zangu za kumaliza masomo na kuoa, na hivi ninavyokwambia ni baada
ya miezi miwili ndoa” Erica alihisi kama akiumia kuendelea kusikiliza
yale maneno na kujikuta akimuga John, “Naomba niende, nitakuja siku
nyingine” “Ila Erica, yani wewe ndio ulikuwa msichana wa ndoto zangu
maana nilitamani uwe ni mama wa watoto wangu, sijui ni kitu gani kiliingilia
kati hadi hukutaka tena kunitafuta Erica, nilijiuliza maswali mengi sana,
pengine hukunipenda ndiomana ikawa vile ila mimi nilikupenda sana
Erica” “Sawa, nitakuja siku nyingine ila kwasasa naomba niende
tu” Erica alianza kuongoza kwa kutoka nje hata John alimshangaa kuwa
Erica amekumbwa na kitu gani maana alionekana kama yupo tofauti sana, alimfata
tena na kumwambia, “Usichukie Erica, kwani unanipenda na
wewe?” Erica alikaa kimya tu na kuendelea kutoka, na alipofika nje
alisimamisha bodaboda ili impeleke stendi ingawa stendi haikuwa mbali ila
alifanya hivyo ili tu kumuepuka John. Alifika stendi na kuingia
kwenye daladala, kwa hakika alikuwa na mawazo mengi sana kiasi cha kumkosesha
raha kabisa kabisa. Wakati anashuka kwenye daladala ili aingie kwenye
daladala lingine alishikwa bega, alipogeuka nyuma alishangaa kuona aliyemshika
bega ni Dora yani Yule rafiki yake wa kitambo chuoni, halafu Dora alionyesha
furaha sana kukutana na Erica maana alimkumbatia kwa furaha, na kuanza
kumsalimia ila Erica hakuwa na furaha kabisa kwanza alikuwa na mawazo yake
halafu pia hakufurahishwa na kumuona Dora, rafiki msaliti kwake. “Jamani
Erica, bado tu unanichukia hadi leo jamani!” “Hapana
sikuchukii” “Yani ungejua nilivyofurahi kuonana na wewe
jamani!” “Kilichokufurahisha?” “Kwanza nimefurahi kukutana na
rafiki yangu wa muda mrefu, pia nimefurahi maana tatizo langu wewe unaweza
kunisaidia” “Tatizo gani?” “Erica, naomba tuweke tofauti zetu
pembeni kwa muda. Twende pale tuongee kidogo, nina shida rafiki
yangu” Erica alimuangalia Dora, ila kwa jinsi alivyokuwa akiongea
ilionyesha kweli alikuwa na shida, ikabidi asogee nae mahali chini ya mti kwenye
kivuli ili amsikilize alikuwa na shida gani, “Erica, nilikuwa mkoani
mwenzio nikapata mchumba na ananipenda ile ile yani yule mkaka ananipenda
haswaaa. Sasa nikaja Dar, kwa bahati mbaya nikakutana na mpenzi wangu wa zamani,
kwa hakika nilishindwa kumkataa na kujikuta nikibeba mimba maana ilikuwa ni siku
za hatari halafu nilimshauri atumie kinga akasema atamwaga nje ila matokeo yake
kanisababishia matatizo” “Sasa kubeba mimba ni tatizo Dora? Si uzae
tu” “Erica, najua unatambua vizuri kuwa kuzaa kunataka malengo. Siku
zote huwa natumia uzazi wa mpango maana nilivyotoaga zile mimba tatu sikutaka
tena ujinga nikawa natumia uzazi wa mpango ila tangu nilipopata Yule mchumba wa
mkoani niliacha sababu Yule mkaka alionyesha ana lengo na mimi na
kashanitambulisha kwa ndugu zake wote kule mkoani, ila yani mimba nazo kama
zinatumwa jamani yani nimeacha kunasa kwa Yule kaka nimekuja kunasa kwa huyu
mjinga. Na kumbambikia Yule kaka haitawezekana maana Yule mjinga alivyo mtoto
ataniumbua tu. Nataka kutoa shoga yangu, yani nitoe tu hii mimba” “Sasa
dora jamani, kutoa mimba ni siri ya mtu ndio unanieleza kweli!” “Erica,
mimi najua kila kitu kuwa hata wewe ulishawahi kutoa mimba, shida yangu
nielekeze hospitali uliyoendaga kutolea maana nimeenda pale pa siku zote dokta
kanizingua eti anasema nizae tu na mimi sipo tayari kuzaa na Yule mwanaume
jamani. Naomba nielekeze Erica” “Yani Dora naona unanichanganya tu
kwakweli na wala sielewi kitu chochote unachonieleza, habari za kutoa mimba mimi
sina na nikuambiavyo nina mtoto kwasasa” “Khee hongera Erica jamani,
umeamua kuzaa, hongera sana. Ila mimi sitaki kuzaa kabla ya ndoa na Yule mchumba
wangu kaniambia anakuja Dar kunitambulisha kwa ndugu zake wengine halafu tuanze
harakati za ndoa. Erica sitaki kuikosa ndoa sababu ya uzembe wa mimba, nahitaji
kuitoa hii mimba” “Sawa, ila mimi sijui madokta wa kutoa
mimba” “Poa, Erica nibanie ila hii mimba nitatoa na kwenye harusi yangu
nitakualika. Nipe namba zako” “Sina haja ya kuja kwenye harusi yako,
kwaheri” Erica aliondoka zake na kwenda kupanda daladala ya kwenda kwao
sasa, akiwa ndani ya daladala alijikuta akiwaza mambo mengi sana, “Au
Dora ndio mchumba wa John? Mungu wangu jamani, yani Dora na uuhuni wake lakini
ndio anapata bahati ya kuolewa jamani! Kweli kuolewa sio kutulia
loh!” Aliwaza sana bila ya kupata jibu la aina yoyote, alikuwa akiondoka
kwao huku ana mawazo mengi sana na hakuwa na raha
kabisa. Alivyofika kwao alishangaa kuna ugeni, alishangaa
kumuona kaka yake ambaye kwa siku nyingi sana alikuwa akiishi kwa mjomba wao,
alimsogelea na kukumbatiana kwa nguvu na kaka yake, “Kheee Erica mdogo
wangu umekuwa mkubwa jamani hadi una mtoto! Wakati kaka yako wala
sina” Erica alikuwa akitabasamu tu, kisha kumkaribisha vizuri kaka yake
nyumbani, “Kaka Tony, karibu sana ndio ulizamia Arusha jamani utafikiri
ulikuwa nchi nyingine ambavyo hukutaka kurudi nyumbani. Karibu
sana” Walifurahiana nae na kuongea mambo mbalimbali kwa furaha kisha
Erica aliinuka na kwenda chumbani kwake, alifunga mlango wa chumba chake kwani
alikuwa na mawazo sana na alihitaji apate hata muda kidogo wa
kulia. Alivyojifungia mlango alianza kulia huku akijilaumu jinsi
alivyoyafanya maisha yake, maneno ya mama yake kuwa yeye ndiye aliyekuwa na
uwezo wa kuchagua maisha yake yalimrudia akilini na kuanza
kujisemea, “Kama mimi ndio nilikuwa na uwezo wa kuchagua maisha yangu,
mbona maisha yangu nimechaguliwa? Nilikuwa nawasiliana vizuri sana na John hadi
tukaahidiana mambo mbalimbali ila kitendo cha mimi kusahau simu mezani ikawa
ndio mwisho wa mawasiliano yangu na John kwani hata niliporudi bado majanga,
mama alisema simu kaitumbukiza kwenye maji na laini imevunjika. Sikuweza
kuwasiliana tena na John. Kumbe alinitafuta sana, huenda ndio angekuwa mume
wangu na wala yote haya ya kukutana na watu wa ajabu ajabu yasingetokea, mama
yangu kachangia pakubwa sana kuharibu maisha yangu ila hataki tu kukubali
ukweli. Asingeleta vurugu shuleni wala usikute hadi leo ningekuwa na Erick na
wala nisingetangatanga na wanaume, akaniharibia kwa Erick, akaniharibia kwa John
na pia akaniharibia kwa Bahati halafu bado anajitoa kuwa hakuna alichoharibu
kwangu eti nimejiharibia mwenyewe” Akainama tena na kulia sana, ila muda
huu alikuwa hajamchukua bado mtoto wake, kwahiyo mama yake alienda kumgongea ili
amchukue mtoto wake, Erica alifuta machozi na kwenda kufungua
mlango, “Kheee nimekusikia saa nyingi sana kuwa umerudi na ulikuwa
ukiongea na kaka yako, kumbe hujaoga hata kuoga! Hebu nenda kaoge huko
umnyonyeshe mjukuu wangu, sio umnyonyeshe na majashojasho yako ya huko
njiani” Erica alienda kuoga ila bado alikuwa na mawazo sana, kwani
kimsingi maisha yake mengi yameharibika na chanzo kikubwa ni mapenzi, na sasa
alikuwa akihitaji mtoto wake apate malezi ya baba na mama, ila atajielezeaje
kwenye familia ya John kuwa alikuwa na mahusiano na Rahim yani hapo ndio
palimshinda na kumfanya hata siku hiyo ashindwe kujieleza maana kilishatokea
kitu cha kumuwekea pingamizi. Usiku wake alijaribu tena kuingia
kwenye mtandao, ila leo alimkuta Rahim yuko hewani. Kabla hata ya salamu, Erica
alimuuliza Rahim swali kwani hakuona umuhimu wa salamu, “Kwahiyo ndio
umemaliza honeymoon leo umekuja hewani sio?” “Honemooy ipi Erica? Unajua
mara nyingine sikuelewi yani unatoaga lawama tu” “Si ulishaoa kwahiyo
ulikuwa kwenye mapumziko ndio leo umekuja hewani” “Sasa nimemuoa
nani?” “Si umemuoa Salma wewe” “Hivi Erica una tatizo gani
kwani? Huyo Salma hata kumuona kwa macho sijawahi zaidi ya kutumiwa picha zake,
sasa kumuoa nimemuoa saa ngapi? Au umeanza tena maongezi na mama yangu kwahiyo
kashakuchanganya akili!” Erica akaona atumie nafasi hiyo hiyo kumwambia
kuwa alikutana na mama yake na kamuhakikishia kuwa ameoa, “Mama yako
mwenyewe kanihakikishia kuwa umeoa” “Si ungemwambia akupe picha za
harusi uzione, unajua wanawake msiwe na tabia ya kukurupuka. Hujauliza kuwa
nilikuwa na tatizo gani, mbona sikupatikana siku zote hizo ila wewe unakuja tu
kuniparamia na lawama eti sijui nimeoa nimetoka honeymoon, Erica mke gani wewe
mwenye lawama kila kukicha?” “Haya basi ulikuwa wapi?” “Ungeanza
na swali hilo mwanzoni ndio ningekujibu ila kwasasa siwezi kukujibu wakati swali
nimekupa mwenyewe. Vipi mwanangu anaendeleaje?” “Hivi wewe Rahim unajua
ni kwajinsi gani unaumiza moyo wangu? Unajua unavyonitesa?” “Nakutesa
kwa lipi? Je nilikataa mimba? Hapana, je nimekataa mtoto? Hapana, sasa nakutesa
kwa lipi. Mbona hutumii akili Erica” “Kwahiyo unaona unachofanya ni swa?
Yani mimi sielewi hatma yangu, sijui kama nitaolewa na wewe au la, yani
umenifanya niwe njiapanda” “Kwani Erica jamani una miaka mingapi hadi
uwe na mawazo ya ndoa kiasi hiko? Si nilishakwambia kwenu nitakuja kwani wewe
tatizo ni nini jamani? Kwani sikutumii hela za kumtunza mtoto? Unataka nini
sasa? Unajua nilijua nimepata mwanamke mwanachuo atakuwa anajitambua sana ila
kitendo cha kuona bado hujitambui Napata shida ya kuelewa shahada
uliyochukua” yani majibu ya Rahim yalikuwa yakimtia hasira Erica hata
akatamani angekuwa karibu maana sio kwa kumtia hasira vile kwa majibu
yale, “mapenzi hayana usomi, unaniumiza Rahim” “Nilishakwambia
kaa mbali na mama yangu, Yule mama atakupa kichaa bure. Nimeambiwa kuwa mdogo
wangu John alikuwa anamvalisha mchumba wake pete ndio wakafanya sherehe, ila
wewe uliambiwa mimi naoa loh! Ni maswala ya ajabu hayo Erica, narudia tena kaa
mbali na mama yangu. Atakuchanganya akili Yule mama” “Kiukweli Rahim
sikuelewi yani sikuelewi kabisa” “Naomba ulale na ukiamka utanielewa kwa
urahisi zaidi ila hivyo unavyobisha tu itakuwa ngumu sana
kunielewa” Erica alituma ujumbe mwingine ila hakujibiwa na Rahim,
ilibidi tu alale huku akiwa amechukia vilivyo moyoni mwake maana aliona kama
Rahim anamfanyia vitu vya makusudi. Alilala huku akiwa na mawazo
mbalimbali kuwa pengine mambo yake katika maisha
yatabadilika. Kesho yake alifika James nyumbani kwakina Erica,
akiwa ameongozana na Mage, alikuwa na lengo la kuomba msamaha ila kiukweli Bite
aligoma kabisa kuongea nae, aliwakuta sebleni ila Bite hakuitikia hata salamu
yake. Ila James alishangazwa kumkuta Erica na mtoto akicheza nae
sebleni, aliuliza kwa mshangao, “Mtoto wa nani huyo Erica?” “Wa
kwangu” “Kheeee kumbe Erica una mtoto? Mbona mimi sijui” Hapo
ndio Bite alipomjibu mume wake, “Utajulia wapi na siku zote upo busy na
malaya wako” Ikabidi Mage aingilie maana alijua ni mzozo mwingine
utaibuka, “Mmmh Bite mdogo wangu jamani, hata kama mtu kakukosea vipi
ila usimwambie maneno makali hivyo” “Sasa neno kali nillolitamka ni
lipi? Kumwambia ukweli ndio neno kali?” “basi yaishe, ila pokea msamaha
wa mwenzio” “Sitaki, tena naongea mbele ya wote hapa. James kuanzia leo
mimi na wewe basi” “Bite, kumbuka tumefunga ndoa ya kanisani na tulikula
kiapo kuwa hatutaachana mpaka kifo kitakapotutenganisha” “Usinibabaishe
na hayo maneno, ambacho hutaachana nacho mpaka kifo ni mwili wako tu ila sio
mimi tena unikome” Ilibidi Mage amtoe kidogo James na kwenda kuongea nae
kuwa arudi siku nyingine maana inaonyesha Bite bado alikuwa na hasira
sana. Ila kabla James hajaondoka aliomba kidogo kuongea na Erica, na
aliongea nae jambo moja tu, “Erica nitakutafuta ili unisaidie swala la
kurudiana na mke wangu, najua wewe unajua kuwa mimi nifanye nini ili Bite
akubali” “Sijui mimi, hebu nipishe wasije hisi unanitongoza tena
bure” “Erica najua unajua, na nitakutafuta tu” Kisha James
aliondoka zake, na Erica kurudi ndani ila dada yake alimkata jicho hilo ambalo
lilimtisha na kumwambia dada yake, “Mbona unaniangalia hivyo
dada?” “Ngoja utakapoolewa halafu ufanyiwe ninayofanyiwa mimi na James
uweze kuona moyo wako unavyokuwa” Erica alikuwa kimya tu kwani bado
kuolewa ila moyo wake ulikuwa na maumivu ya hali ya juu maana hata hakujua kuwa
ni nani atakayemuoa. Baada ya wiki kaka yao aliwaita ndugu zake
wote na kuwaeleza dhumuni la kwenda nyumbani kwao kwa kipindi
hiko, “Jamani nimepata mchumba, nikaona ni vyema nije kumtambulisha
nyumbani” Walimpa hongera pale, na mama yake akamwambia kuwa ni uamuzi
wa busara kumtambulisha mchumba wake, kwahiyo aliwaambia kuwa Jumamosi ya wiki
hiyo ndio wajiandae kumpokea huyo mgeni ambaye ni mchumba wake, basi wakafurahi
na kusema kuwa watajiandaa. Siku ya Jumamosi, walikusanyika wote
nyumbani yani mama yao, Mage, Bite na Erica huku wakimsubiri kaka yao amlete
huyo mchumba aliyempata. Muda kidogo kaka yao alifika na mgeni na kuanza
kumkaribisha, muda huo Erica alienda chumbani kumlaza mtoto wake, ila aliposikia
mgeni amefika alimlaza haraka mwanae na kwenda kumuona mgeni. Alipofika
tu sebleni alishangaa akigongana macho kwa macho na Dora, kwahiyo Dora ndio
mchumba wa kaka yake. Muda kidogo kaka yao alifika na
mgeni na kuanza kumkaribisha, muda huo Erica alienda chumbani kumlaza mtoto
wake, ila aliposikia mgeni amefika alimlaza haraka mwanae na kwenda kumuona
mgeni. Alipofika tu sebleni alishangaa akigongana macho kwa macho na
Dora, kwahiyo Dora ndio mchumba wa kaka yake. Erica alimtazama Dora na
kuanza kucheka sana hadi ndugu zake wakamshangaa kuwa imekuwaje, mama yake
akamuuliza, “Vipi Erica, mbona unacheka hivyo baada ya kumuona
mgeni?” Muda huu Dora alikuwa akitazama chini tu, kisha Erica
akasema, “Ukisikia usiyempenda kaja ndio leo loh!” “Erica
hatukuelewi” Erica akamsogelea Dora, na kuinama alipo kisha akapitisha
mkono wake na kumshika tumbo halafu akamuuliza, “Vipi shoga yangu, ile
mimba ulishaitoa?” Familia nzima ilikuwa ikishangaa tu, hakuna
aliyeelewa haswa Tony na ilimbidi amuulize Erica kwa hasira, “Wewe
Erica, mbona unamfanya hivyo wifi yako jamani? Mbona unakosa heshima
wewe?” “Kaka sikia, huyu mwanamke sio mara ya kwanza kumuona huyu Dora
namjua vilivyo tena alikuwa rafiki yangu” Kisha akamuangalia mama yake
na kuwaangalia dada zake na kusema, “Jamani huyu ni mtu aliyefanya nione
chuo kichungu, huyu ndio alipanga na watu wanibake ila hawakufanikiwa nab ado
akatangaza chuo kizima kuwa nimebakwa. Kaka kama unaamua kuishi na huyu mwanamke
ni juu yako ila nakwambia ukweli huyu mwanamke ni shetani” Mama yao
akamuuliza swali Erica, “Na mimba uliyomuuliza ni ipi?” “Huyu
Dora nimekutana nae hivi karibuni tu, alikuwa anatafuta daktari wa kumtoa mimba
akidai kuwa kabeba mimba bila kutarajia na kapata mchumba sasa itakuwa so huyo
mchumba akijua, dah inaniuma sana kuona mchumba mwenyewe ni kaka yangu jamani!
Kaka hivi hujaona wanawake wengine kweli?” Dora alikuwa ameinama ila
aliinuka bila kuongea na yeyote na kutoka nje, yani ni Tony ndiye aliyeanza
kumfata nyuma Dora huku akimuita ila Dora hakuitika kwani kiukweli
alishaaibika. Ikabidi Tony aendelee tu kumfata Dora ili akazungumze
nae. Ndani walibaki wenyewe kwenye familia huku wakisikitika
yale mambo waliyoyasikia, “Jamani Erica, usingekuwa unamjua huyo
msichana si ndio kaka yako angekuwa anadumbukia kwenye mdomo wa
mamba?” “Kweli mama,yani Erica asingemjua wala tusingekuwa na wasiwasi
nae maana anaonyesha ni mpole kweli” “Hata mimi nilipoanza urafiki nae
chuoni nilijua ni mpole yani hata sikudhania kama ana mambo ya ajabu kiasi hiki,
ila jamani mama na dada zangu mambo ya mapenzi yalivyo utashangaa kaka anapewa
uongo na Yule mwanamke hadi sisi tunaonekana wabaya” Bite akacheka na
kumwambia Erica, “Kweli umekuwa mdogo wangu naona unaanza kuelewa maana
ya mapenzi, yani mapenzi bhana ni kweli usemayo yani inawezekana wote
tukaonekana maadui hapa sababu ya mtu mmoja tu. Ila bora umesema mdogo wangu ili
leo na kesho likibumbuluka tutamwambia si tulikwambia, ila usingesema ingekuwa
ni lawama tu kwanini hukusema” Walijadiliana pale ila hawakujua
kilichoendelea kwa kaka yao, ila mama yao alionekana kuwa na misimamo yake ya
kumkataa huyo msichana hata iweje, ili mradi tu kajua kuhusu huyo mwanamke
hamtaki tena. Jioni ilifika kisha Mage akaondoka na kuwaacha wakibaki
wenyewe pale nyumbani, wakaendelea na maongeze mengine na usiku kufika wakalala
ila Tony hakurudi. Kesho yake wakiwa wanajadiliana kuwa Tony
mbona hakurudi nyumbani ndio alifika, kwakweli mama yao alimsema sana maana
hakupendezewa na lile jambo kabisa. “Mama jamani, nampenda Dora na hana
tabia hizo, huyu mwanao Erica anamsingizia tu” Erica
akadakia, “Nilijua tu, ila kaka kama ukiamua kujiweka kwenye mdomo wa
mamba shauri yako ila mimi nishakwambia ukweli” Mama yao aliendelea
kuongea, “Tony, huyo mwanamke simtaki katika nyumba yangu yani simtaki
kabisa na kama unaamua kumuoa basi utajuana na mjimba wako ila huyo mwanamke
simtaki” “Mama jamani, kwanini mnanifanyia hivyo? Erica aliyekutia aibu
hapa kwa kuzaa nyumbani wala huna tatizo nae ila mimi ninayeweka heshima kwa
kumtambulisha wangu humtaki” “Hivi wewe mtoto uambiwe vipi jamani eeeh!
Tushakwambia Yule msichana hakufai, au mpaka siku akuletee mtoto wa kipemba kama
dada yako ndio akili ikukae sawa. Haya na jana ulilala wapi?” “Mmmh
nilijua tu, muulizeni dada Mage, nililala kwake” Kisha akainuka na
kwenda chumbani kwake, kwakweli mama yao aliona Erica na kaka yake ni watu
wanaomchanganya sana akili. Siku hiyo walimuita tena Tony
kuongea nae habari za kusema Dora hawamtaki, ila na yeye alionekana kuanza
kuelewa elewa, “Mama, jana sikuwaaga ila nilienda kwakina Dora dah
nimemkuta na mwanaume amesimama nae halafu mazingira sikulizika nayo kabisa, eti
kaniambia ni kaka yake mmmh Napata shida kwa huyu mwanamke ila
nampenda” “Sitaki hiyo habari ya kumpenda huyo mwanamke
asiyefaa” Tony akainuka na kuondoka, mama yao akamtazama Erica sasa,
ikawa zamu ya Erica, kama kawaida yake hakuacha kuongelea swala la mume wa
Erica, “Haya wewe mtoto, huyo mwanaume anakuja lini?” Hili swali
huwa linammaliza nguvu kabisa Erica, yani huwa anakosa raha akiulizwa swali la
namana hii, muda ule ule alinyong’onyea na kumfanya mama yake
aongee “Nilijua tu utanywea, hivi Erica unataka sura yangu hii niiweke
wapi? Tunafanya siri kila kukicha, hivi mtoto ana siri? Unafikiri watu hawajui
kama una mtoto? Shida sio kwa majirani ila ndugu wakijua, jamani nitaweka wapi
sura yangu mimi? Erica, fanya juu chini umlete huyo mwanaume, ni afadhali
wakigundua niseme mwanaume yupo kuliko hivi. Umenisikia” “Sawa
mama” “Yani sio unanijibu sawa tu, kinachotakiwa ni vitendo. Waje hapa
wajitambulishe na kumuona mtoto wao, waniambie hatma yako kwa huyo mwanaume.
Inamaana huyo mwanaume hana ndugu jamani, maana hatujawahi kuona ndugu yake wala
rangi ya ndugu yake” Muda kidogo mtoto wa Erica aliamka na leo alitoka
mwenyewe hadi sebleni, Bite alisema, “Kheee Angel mjanja jamani yani
katoka mwenyewe chumbani kuja sebleni” Mama yao akadakia, “Sio
ujanja tu, hiyo ni kuonyesha kama mtoto amekua. Huyu Angel amekua
sasa” Erica akamchukua mwanae na kumpakata, mama yake
akasema, “Erica, hivi huoni aibu? Mtoto anazaliwa, anakaa, anatambaa na
sasa anatembea na wiki ijayo anaenda kufunga mwaka ila hakuna mwanaume wala
rangi yake. Hapo ulipo hata mahafali ulishindwa kuhudhuria sababu ulikuwa
unanyonyesha, Hivi iko wapi elimu yako? Iko wapi sifa yangu ya kusema mtoto
anasoma? Umenitia aibu Erica, haya huyo mwanaume yupo nje, ndugu zake je? Huyo
mwanaume hana ndugu? Basi sio binadamu wa kawaida kama hana ndugu. Kiukweli
umenitia aibu Erica jamani yani umenitia aibu balaa, haya baba wa mtoto yuko
wapi? Yani sitaacha kuuliza swali hili hadi nitakapomuona. Nilikuuliza toka
mtoto mchanga ukanijibu atakuja, atakuja hadi leo kimya na wiki ijayo mtoto
anatimiza mwaka ila baba hola, aua ulidanganyika siku ile niliposema kuwa Yule
muuza samaki ndio baba Angel? Kama umekubaliana nae basi mlete ajitambulishe
rasmi na akuoe maana sina muda wa kukwambia mwanaume gani anafaa kukuoa kwasasa,
ukizingatia ushaharibu maisha yako. Fanya ufanyavyo ila nahitaji kumjua baba wa
huyu mtoto. Erica, mtoto anahitaji malezi ya baba na mama, hivi hutamani ukiona
baba na mama wameongozana wakiwa wamebeba kitoto chao hutamani? Erica nahitaji
jibu, huu mwezi usipite mwanangu, huyu mtoto amekua sasa sio muda wa
kucheleweshana huu. Nadhani umenielewa” “Nimekuelewa mama” Erica
alikuwa mpole sana na kuinuka na mwanae kisha kwenda nae ndani, ila alipoingia
chumbani kwake alijifungia na kulia kama kawaida ingawa alijua wazi kilio chake
hakimsaidii kitu. Alilia sana na kujikuta akilaumu sana kuhusu Rahim,
ingawa maneno ya mama yake yalimchoma ila kuna muda aliona kuwa mama yake
alikuwa na ulazima wa kuyasema maana asingeweza kuacha mwanae
ateketee. Usiku wake kama kawaida alianza kumtafuta Rahim
hewani maana akisemwa semwa ndio anapoteza raha kabisa, alimtafuta na kumkuta tu
hewani akamtumia ujumbe maana siku hizo ilikuwa tofauti na zamani kuwa Rahim
ndio alikuwa anamtafuta Erica, kwa siku hizo ni Erica ndio wa kumtafuta Rahim
tena anaweza kutuma jumbe hata nne ndio akajibiwa, ile kitu ilimuumiza sana
Erica. “Rahim kwanini lakini unanifanyia hivyo jamani! Lini utakuja
kumuona mtoto?” “Erica, kwani kitu gani unataka haswaa maana huwa
sikuelewi” “Rahim jamani, kumbuka sisi ni wazazi. Na mtoto anahitaji
mapenzi ya baba na mama” “Kwani niliwahi kukwambia simpendi huyo
mtoto?” “Hapana Rahim sio hivyo, ila mbona umebadilika sana jamani Rahim
yani sio Yule ambaye nilikujua jamani” “Erica, hebu zungumza unachotaka
kusema sio kuanza kueleza eleza vitu visivyokuwa na kichwa wala miguu. Sasa kitu
gani ambacho nimebadilika mimi, mbona unaeleza vitu visivyoeleweka, wewe sema
unataka nini kwangu. Maana kama pesa za kumtunza mwanangu huwa nakutumia haya
kitu gani unataka” “Rahim, kumbuka nimezaa nje ya ndoa na nyumbani
hawakufahamu” “Kwahiyo unataka nini?” “Nataka nyumbani
wakufahamu na unioe” “Hahahaha unanichekesha Erica, unataka ndoa? Hiyo
ndoa utaiweza wewe au unaitaja tu ilimradi umeitaja” “Jamani Rahim kweli
ndio maneno ya kuniambia hayo? Kuna mwanamke asiyeweza ndoa hapa duniani? Rahim,
kumbuka ahadi zako kwangu, kumbuka uliniambia nini” “Si nilikwambia
ubadili dini nikuoe” “Rahim, dini sio kigezo cha wewe kushindwa kunioa.
Kuna ndoa za bomani, watu wanafunga na dini tofauti” “Hahahah hivi
sharia zetu unazijua wewe? Hebu ulizia vizuri uelezwe kama ulishawahi kuona mtu
kama mimi kafunga ndoa ya bomani au kabadilisha dini. Hivi wewe ni mwanamke gani
usiyemuelewa? Hujui kama mwanamke hana dini? Ukitaka nikuoe badili dini nikuoe
mwisho. Kama hutaki jua kwamba hakuna kitu kinachoitwa ndoa baina yangu na
wewe” Erica aliona machozi yakitoka machoni mwake, alijisikia uchungu wa
hali ya juu, kisha akabadilisha ujumbe wa kumwambia Rahim, “Sawa,
nimekubali hakuna ndoa basi njoo nyumbani uonekane. Umuone mtoto na ndugu zangu
wakufahamu, mama ananiuliza sana maana hata ndugu zako hujawaambia kuhusu mimi
na mtoto una maana gani?” “Ila nilishakwambia mama yangu alivyo, yani
siwezi kumwambia mama aje kwenu maana namjua vizuri. Pili mimi nitakuja tu, sasa
usinipangie siku ya kuja, jua nitakuja tu. Huyo mtoto sijamkataa, ni wangu na
ninampenda kwahiyo nitakuja tu hata usiwe na mashaka kuhusu swala la mimi
kuja” “Kwahiyo ni lini?” “Nimekwambia Erica usinipangie,
nitakuja tu” Hapa Erica alipumua na kuweka simu pembeni maana alianza
kulia tena na alilia hadi alihisi kichwa kumuuma na kujiona kama ametupwa
duniani na hana uelekeo kabisa, alikosa raha. Akikumbuka maneno ya mama
yake, na akiwaza kile alichoambiwa na Rahim alihisi kupata kizunguzungu kabisa,
alilia sana na kulala huku akilia kwani hakuweza tena kuongea na Rahim alihisi
kuendelea kuumia tu. Asubuhi palivyokucha ni dada yake alienda
kumgongea mlango na kisha kuinuka na kufungua, Bite aliingia ndani na
kumuangalia mdogo wake akamuuliza, “Nini tatizo Erica, mbona macho
yamekuvimba hivyo?” “Hakuna tatizo dada” “Hakuna tatizo wapi,
ulikuwa unalia wewe” Erica alikuwa kimya tu na kukaa kitandani kisha
Bite nae akakaa kitandani na kuendelea kuongea na mdogo wake, “Erica
mdogo wangu, unalizwa na maneno ya mama kweli? Yani unakosa raha sababu ya
maneno ya mama jamani?” “Hapana si maneno ya mama” “Basi kipi
kinakuliza” Erica alijikuta akianza tena kulia maana alishindwa kujizuia
na kusema, “Dada, nakubali kuwa nimefanya makosa tena makosa makubwa
sana ila dada sikutegemea kama ingekuwa hivi katika maisha yangu. Yani mama
anahitaji niolewe ila mwanaume hataki kunioa, ina niuma dada tena inaniuma
sana” “Usiumie mdogo wangu, wala sijaona sababu yaw ewe kuumia. Bado
mdogo wewe, huyo mwanaume mwache aende zake na utapata mwingine wa kukuoa.
Halafu usikimbilie ndoa mdogo wangu, zina mambo mengi sana yani unaweza hadi
kuchanganyikiwa sababu ya ndoa. Niangalie dada yako, si niliolewa mimi na harusi
na vigelegele kabisa ila kiko wapi? Hata nikirudi bado nitakuwa na maumivu
moyoni, mdogo wangu wewe ni binti mdogo, angalia maisha yako. Ukikosea usikae
kwenye makosa ila inuka na usonge mbele” “Sasa nitasongaje mbele dada?
Mwanaume hataki hata kujionyesha nyumbani” “BHivi wewe si kuna Yule
muuza samaki, ongea nae aje yeye kujitambulisha kama unahisi kupungukiwa na kitu
ila ningekuwa ni wewe hata nisingeusumbua moyo wangu” Maneno ya dada
yake kidogo yalimtia moyo, na dada yake akamtaka akaoge ili awe na nguvu na
aweze kumuogesha mwanae na kumlisha, kwahiyo alifanya hivyo na kuwa na
nguvu. Mchana aliamua kuwasiliana na Bahati, ila kabla
hajaongea nae lengo lake Bahati akamwambia, “Erica, tena bora umenipigia
maana kuna jambo nataka kukwambia” “Jambo gani
hilo?” “Nimeshawaambia ndugu zangu kuwa nimezaa na wewe, na wanataka
kuja kumuona mtoto” Erica akafikiria kwa muda kuwa itakuwaje, kisha
akamuuliza Bahati “Kwanini umechukua uamuzi huo wakati unajua mtoto sio
wako Bahati?” “Mtoto wako wewe ndio wangu Erica, kumbuka mimi ni
mwanaume wako wa kwanza kwahiyo lazima nichukue jukumu hilo. Erica, nishawaambia
ndugu zangu naomba usiniaibishe mpenzi wangu. Ndugu zangu wote wanajua nimezaa
na wewe mtoto wa kike, mama amefurahi sana hata zile tofauti na wewe zimeondoka,
naomba waje kumuona mtoto” “Sasa ndugu zako hawatashtuka kama
tunawadanganya Bahati?” “Erica, kitanda hakizai haramu. Nahitaji kukuoa
tena swala la mtoto itakuwa ndio kigezo kikubwa sana maana nitasema nataka
kumuoa mama wa mtoto wangu. Erica, huyo mtoto ni wa mimi na wewe, haijalishi
yukoje ila ni mtoto wetu” “Sawa kama umeamua hivyo” “Nakupenda
Erica, tafadhali mwambie mama kuwa keshokutwa nakuja na ndugu zangu kumuona
mtoto na tutajitambulisha siku hiyo maana nitakuja na mshenga kabisa na barua ya
kuomba mke” “Sawa nitamwambia” “Nakupenda sana
Erica” Kisha wakamaliza yale maongezi, kwa upande wa Erica alijihisi
amani kidogo kwenye moyo wake kwani kwa wakati huo hakuangalia kupenda sana wala
nini, ilimradi mtu afike kwake na lengo la kumuoa basi huyo
alimfaa. Alipomaliza kuongea nae, alienda kumwambia mama yake kuhusu
ujio wa Bahati na barua ya uchumba, “Kwahiyo huyo ndio baba
Angel?” Erica alikuwa kimya, na mama yake akamuuliza tena, “Huyo
ndio baba Angel?” “Ndio mama” “Siri ya mtoto unayo wewe, ulisema
baba yake anaitwa Rahim, saivi Bahati unataka kutupiga changa la macho kwa Yule
muuza samaki eeeh! Au umemdanganya mtoto wake!” Erica alikuwa kimya tu,
mama yake akasema tena, “Sawa nimekubali, ila tutakuwepo familia tu
hapa. Nitawaambia dada zako basi, tutakusanyika hiyo keshokutwa
kuwapokea” Kitu ambacho hakumueleza mama yake kuwa wanakuja na kumuona
mtoto ila alimwambia tu wanakuja kujitambulisha. Usiku wake
aliamua tena kumtafuta Rahim hewani, akamsalimia leo na
kumuuliza, “Rahim, kwahiyo unaniruhusu niolewe na mwanaume
mwingine?” “Hahaha hebu usinichekeshe Erica, nikupe ruhusa au nisikupe
kwani nimekuoa? Mwenye maamuzi ni wewe mwenyewe ila mimi siwezi kutoa maamuzi
juu yako” “Rahim, hivi huna wivu hata kidogo na mimi?” “Erica,
hata nikiwa na wivu itasaidia nini? Niko mbali mie sasa unadhani kuna
ninachoweza kufanya? Wewe fanya unachoona ni kizuri kwako, ukiamua kuolewa haya,
ukiamua kutokuolewa haya, ukiamua kunisubiri mie haya ila sikupi ruhusa yoyote
maana mimi sio wa kukupa ruhusa wewe. Hiyo ruhusu ichukue kwenye moyo
wako” “Dah” Erica aliona akidharaulika balaa na kila siku
aliyoongea na Rahim alikosa raha kabisa, maana mawazo yalizidi maradufu
kwake. Alilala kwa shida sana usiku ule maana aligubikwa na mawazo, hata
kesho yake usiku hakuweza tena kumtafuta Rahim kwani alijua atamuongezea mawazo
maradufu. Wote leo walitulia wakisubiri ugeni walioambiwa na
Erica, na muda kidogo ugeni uliwasili, alikuwepo Bahati akiwa ameongozana na
mbaba wa makamo kisha na mama yake Bahati na dada zake waweli. Mama Erica
aliwakaribisha kwa vizuri kabisa, kisha kuanza kusalimiana nao na walionyesha
kuwa na furaha tu. Walikaa na Erica akaitwa, alitoka bila mtoto ila
alipofika tu sebleni mtoto wake nae alimfata nyuma, na alikuwa ndio ameanza anza
kuongea, Yule mtoto akawa anamuita Erica, “Mama, mama” Pale
sebleni wote walikuwa wakimuangalia Angel, muda huo Bahati alionyesha tabasamu
kubwa na kumwambia Angel “Njoo mama” Basi Angel akawa
anamsogelea Bahati na alipofika pale Bahati alimuinua na kumpakata, ila kabla
hawajafanya maongezi mengine alisikika mama Bahati akiuliza, “Kwahiyo
Bahati, mtoto wako mwenyewe ndio huyo?” “Ndio mama, ndio huyu anaitwa
Angel” Huyu mama alisimama na kung’aka, “Wewe mtoto hebu nitolee
uchizi mimi, hata kipofu hawezi kudanganywa kuwa huyu mtoto ni wake maana hata
akimpapasa nywele tu atajua si mtoto wake. Wewe mwenye macho mawili kabisa
unaanzaje kusema huyu mtoto wa kiarabu ni wako?” Wote walinyamaza kimya,
Erica alishindwa hata aseme nini maana mambo kama yale aliyahisi
tu. Huyu mama alisimama na kung’aka, “Wewe
mtoto hebu nitolee uchizi mimi, hata kipofu hawezi kudanganywa kuwa huyu mtoto
ni wake maana hata akimpapasa nywele tu atajua si mtoto wake. Wewe mwenye macho
mawili kabisa unaanzaje kusema huyu mtoto wa kiarabu ni wako?” Wote
walinyamaza kimya, Erica alishindwa hata aseme nini maana mambo kama yale
aliyahisi tu. Yule mama aliwaangalia ndugu zake na
kusema, “Tulihisi tu kuwa tunaenda kupigwa changa la macho maana huyu
binti hawezi kuwa mkweli kamwe. Tuondokeni” Kisha akamuangalia mwanae na
kusema, “Acha ubwege, weka mtoto chini twende” Kiukweli hili
swala hata Bahati hakulipenda kwani aliona kama amedhalilishwa, kwahiyo aliinuka
na kutoka na familia yake nje maana ilikuwa ni aibu kwake na wala hakufikiria
kama familia yake ingeweza kufanya kitu kama kile, haswa mama yake. Na wakati
wanatoka, mama na dada zake Bahati walimuangalia Erica na kumsonya yani kila
mmoja alikuwa akimsonya. Kitendo hiki kilimkera sana mama yake Erica, aliinuka
na kuwazuia kutoka nje, “Hivi nyie mmepata wapi ujasiri wa kuongea
shombo zenu kwenye nyumba yangu? Na ubaya zaidi kumsonya mtoto wangu, kuna
sababu gani nyie ya kumsonya mwanangu? Nawauliza? Kama mwenye matatizo hapa si
kijana wenu na sio mtoto wangu, tena sikieni leo ndio iwe mwanzo na mwisho kwa
nyie kukanyaga katika nyumba hii. Haya ondokeni” Muda huu wakati mama
Erica anaongea hakuna aliyethubutu kumjibisha maana hata ndugu wa Bahati
waliogopa kuanza varangati kwenye nyumba ya mtu, wataonekana wakorofi ila
kiukweli angekuwa kwenye eneo lao wangeanza kumchamba kama kawaida yao, mama
Erica akawapisha watoke nao walitoka ila Bahati alirudi nyuma na kwenda kupiga
magoti kwa mama yake Erica, “Mama, naomba nisamehe mimi. Sio wale
watakaoishi na Erica ila ni mim, nampenda sana Erica mama usinichukie
mimi” “Inuka na uende na nduguzo tafadhali” “Mama
nisamehe” Mama Erica hakujibu na kwenda kukaa ila hakujua tabia ya
Bahati kuwa anaweza akapiga magoti pale mpaka kesho yake asubuhi asipopewa jibu
kuwa amesamehewa, na kweli ndugu wote wa Bahati na Yule mshenga walikuwa
wameondoka ila Bahati alibaki amepiga magoti tu ndani kwakina
Erica. Bite alimfata mama yao na kumwambia kuwa Yule kijana bado kapiga
magoti, mama yao alishangaa sana, “Mpaka muda huu!” Erica
alikuwa akijiinamia tu ila swala la kusikia Bahati bado amepiga magoti ikabidi
amuombe mama yake akamwambie kuwa amemsamehe aende, “Kwahiyo wewe
umeridhika na kile walichofanya ndugu zake?” “Sijaridhika nacho mama,
ila Bahati namfahamu mama. Yani anaweza piga magoti hapo hadi
asubuhi” “Kheee mkubwa” Mama yao aliinuka na kumwambia Bahati
kuwa amemsamehe na aende, ndipo Bahati aliinuka na
kuondoka. Ndugu wa Bahati walichukizwa sana na kitendo cha
Bahati kubaki ndani akipiga magoti kwa kuomba msamaha, walipokuwa pale nje
kabisa na nyumba ya kina Erica maana walitoka nje kabisa, walijadiliana ambapo
alianza dada yake Bahati, “Hivi mama huyu kijana wako ana nini jamani,
kwanini anakuwa hivi?” “Hata mimi nashangaa dada, mama inabidi tufanye
kitu. Haiwezekani Bahati akawa bwege kiasi hiki, au huyu msichana kamapa dawa
ndugu yetu?” “Inawezekana maana sio hali ya kawaida, mtu unaona kabisa
mtoto sio damu yako ila unakazana kusema mwanangu. Hivi kwani Bahati ana shida
gani kwasasa? Kila kitu anacho, biashara nzuri hadi gari hii kanunua (akionyesha
gari aina ya Noah waliyoenda nayo kwa kina Erica), kanunua kwa pesa yake
mwenyewe. Sasa kitu gani kinamfanya amng’ang’anie huyu mwanamke? Saivi ameanza
ujenzi na nyumba karibia inaisha” “Sio karibia, ni imeisha ila mjinga
Yule kasema akimuoa huyu mwanamke wake ndio ataenda kuishi nae kule. Kwahiyo
bado anakaa kwenye chumba cha kupanga sio kwamba nyumba haijaisha, imesha ila
mjinga kasema mpaka akaishi na Erica, sijui Yule mtoto nimfanye nini
jamani” Mshenga alikuwa akiwasikiliza kwa makini sana na alikuwa kimya
muda wote, ila sasa ndio akaongea, ‘Unajua leo ndio nimeshangaa, kumbe
Bahati ana maendeleo kiasi hiki! Unajua tulivyokuwa tunakuja na gari hii nilijua
labda kaomba rafiki zake kama kipindi kile alivyokuwa anaomba bodaboda, kumbe ni
yake jamani huyu kijana loh! Kumbe na nyumba amejenga! Kweli ana kila sababu ya
kuoa, sasa tunaweza kulalamika bure hapa kuwa inakuwaje ila kwa mazingira
yalivyo ni wazi kuwa Bahati kapewa dawa na huyu msichana. Sasa mimi nina ushauri
kama mtaafiki” “Ushauri gani huo?” “Kumbuka nina binti yangu,
Yule Nasma ndio kamaliza kidato cha nne mwaka jana. Kwanini Bahati asimuoe
huyo?” Wakatazamana, kisha mama Bahati akasema, “Itakuwa vizuri,
ila itawezekanaje?” “Sikia niwaambie, sababu Bahati kapewa madawa
itakuwa ngumu sana kwa kumwambia hivi hivi ila inatakiwa tumuendee kwa mtaalamu
kisha apewe dawa. Najua kwenu ndio itakuwa rahisi kumfanyia dawa hiyo na
atajikuta akikubali kumuoa Nasma, na akikubali tu yani ndoa tunaifanya haraka
haraka tusipoteze muda kabla mambo hayajaharibika, nitampaka binti yangu
akiingia ndani tu abebe mimba maana hata dawa za Yule zikianza tena Bahati
hawezi kumrudia sababu Nasma atakuwa na mtoto nae. Au mnasemaje kuhusu
hilo?” “Dah! Hilo swala zuri sana, kwanini hatukupanga siku nyingi? Dah!
Asante Mungu maana mwanangu atapata pumziko la moyo sasa” Wakaendelea
kujadiliana pale, mpaka Bahati alipotoka ndani kisha kupanda nao kwenye gari na
kuondoka nao maana hakutaka hata kuongea nao jambo lolote ukizingatia
walishamdhalilisha. Nyumbani kwakina Erica walianza kumsema
Erica, haswa mama yake, “Hivi Erica, angalia aibu uliyonitia mama yako
jamani! Hivi ulishindwa kupanga na huyu muuza samaki wako, kwani hukuelewa kuwa
ndugu zake wangefika wangeshtushwa na mtoto? Wangapi wanaolewa wakiwa na watoto
tayari? Ni wengi tu lakini wanakuwa na makubaliano na wenza wao yani hilo
linajulikana wazi, bora hata mtoto angekuwa wa Kiswahili, tatizo mtoto ni wa
kiarabu Erica yani hapo ndio kuna shida mwanangu dah hata sijui
inakuwaje” Erica aliinuka na kwenda chumbani kwake maana yeye alipata
aibu kushinda ile aliyoipata Tony kwa kumleta Dora. Alifika chumbani na
kumuweka mwanae pembeni ila machozi yalimtoka, kitendo hiko kilionekana
kinamuumiza pia mtoto wake kiasi kwamba hata mtoto wake alianza kulia, ikabidi
Erica anyamaze na kuanza kumbembeleza mtoto. Alitulia kimya sasa ila
baada ya muda kidogo dada zake yani Bite na Mage walienda chumbani kwa Erica
kuzungumza nae, “Erica, usisononeke kwa hili lililotokea ila sisi
tunaelewa mdogo wetu ulikuwa tu ukitaka kutuliza haja ya moyo wa mama ila ukweli
upo wazi kuwa Yule mwanaume si muhusika wa huyu mtoto, si
ndio?” “Ndio” “Basi kama ni hivyo, inamaana yote haya
uliyategemea mdogo wetu. Sidhani kama ni jambo jema kwako kuendelea kuwa na
mawazo” “Sawa dada zangu nimewaelewa” “Ila hebu leo tuongee
kirafiki, baba wa Angel yuko wapi? Na huwa anasema nini kuhusu swala la ndoa
wewe na yeye? Na huwa anasemaje kuhusu kumuona mtoto? Kuwa muwazi mdogo
wetu” “Dada zangu ngojeni tu niongee, baba wa mwanangu nadhani nilifanya
makosa sana kumuamini mwanaume kiasi hiki ila kiukweli kanitamkia wazi kuwa hana
mpango wa kunioa mpaka nibadili dini” Erica akainama na kulia, ila dada
zake wakamtuliza, “Eeeh swala la kutokukuoa bado sio tatizo, unaweza
kuolewa na mtu mwingine. Vipi kuhusu kumuona mtoto?” “Yani siku zote
huwa ananiambia nitakuja na hataki kusema atakuja lini?” “Na vipi kuhusu
kumuhudumia mtoto?” “Huwa anamuhudumia” “Basi sio
tatizo” “Ni tatizo dada, yani kiukweli Rahim kabadilika sana siku hizi.
Zamani kabla sijawa na mtoto alikuwa akinitumia hela nyingi sana, hata wakati
naenda kujifungua alinitumia hela nyingi ila siku hizi kabadilika kwanza shida
ya hela hadi nimwambie halafu hanitumii kwa kiwango kile alichokuwa ananitumia
mwanzoni. Yani siku hizi naweza nisimpate hewani hata mwezi na nusu halafu
akiibuka nikimwambia nashida na hela basi anatuma laki mbili, na hapo nikimtumia
ujumbe mwingine wa kumuomba hela hajibu ujumbe wangu. Ndiomana namuuliza mara
kwa mara atanioa lini? Pengine nikiishi nae atamuhudumia vizuri mtoto
wake” “Mmmh ila Erica, hebu tuambie ukweli unajua wewe hata mtu
akikusikiliza kuhusu swala la mwanaume kutokukutumia pesa hatokuamini kabisa,
kwanza toka mtoto kazaliwa huyu hujawahi kupanda nae daladala, unaendaga kliniki
ya mbali kabisa na unaenda na tax na kurudi na tax. Hufanyi kazi wala biashara
Erica, nina uhakika hata mama hajawahi kukupa hela ya tax ila ni hela zako. Kama
huyo mwanaume kabadilika siku hizi basi mwanzoni alikuwa anakutumia hela nyingi
sana si ndio? (Erica akatingisha kichwa kumuitikia dada yake) Haya sasa, alikuwa
akikutumia kama kiasi gani?” “Mara nyingine milioni moja, mbili au tatu
na akituma laki tano basi ndio ametuma hela ndogo” “Mmmh kwa aina hiyo
ya mwanaume mdogo wetu ulikuwa na haki ya kubabaika ila ungetushirikisha dada
zako na tungekufundisha mbinu za kula na kipofu, haya sasa hizo hela nyingi
umefanyia nini?” “Nifanyie nini dada? Nilikuwa natumia
tu” “Unatumia milioni tatu, sijui mbili kwa matumizi gani hayo? Erica
mdogo wangu hata hukuwaza kuanzisha biashara!” “Dada, kipindi kile
nilikuwa nasoma wala wazo la biashara sikuwa nalo. Kwanza nilijua nikimaliza
chuo basi nitaanza kazi, kwahiyo sikuwa na wazo la biashara kabisa
kichwani” “Sasa hizo hela ziko wapi? Inamaana zote
umekula?” “Dada, hela niliweka benki ila kwa matumizi yangu na mtoto
zimebaki kidogo sana na nikimwambia yeye ananitumia hela za mawazo hadi kichwa
change kimevurugika na sijui cha kufanya” “Watu huwa wanafurahia mapenzi
kabla ya ndoa na kabla ya kuzaa, ungetuuliza kwanza dada zako. Yani kabla
hujachukua uamuzi wa kubeba mimba, ungetuuliza kwanza, huyo kaka inaonyesha ana
hela, mwanaume afikie hatua ya kukutumia milioni tatu ya matumizi tu! Huyo ni
tajiri, sasa mdogo wangu ungeuliza ila cha ajabu hizo hela hata dada zako
hatujawahi kuziona. Kumbe ndiomana ulikuwa huoni shida kukodi gari kutoka
nyumbani hadi chuoni, kumbe ulikuwa na hela!” “Nisameheni dada zangu,
ila mnanishauri nifanyeje kwasasa?” “Cha kukushauri maana ulishakosea
tena ulikosea kabisa ila unatakiwa tu kuwa mpole, yani huyo mwanaume wasiliana
nae kwa upole kabisa, ila kwavile kasema hatokuoa hadi ubadili dini ujue hapo
ndoa hakuna” Bite akatoa ushauri mwingine, “Sasa dada, mdogo
wetu akitaka apate tena hela za Yule mwanaume ajifanye anakubali kubadili dini
ndio atamchota vizuri” “Bite mdogo wangu, unafikiri kuna muowaji kweli
hapo? Yani kuhusu dini ni kisingizio tu, yani hapo hamna cha ndoa wala nini ila
Erica shukuru Mungu umeshaujua ukweli halafu usonge mbele. Saivi angalia jinsi
ya kutunza mtoto wako tu, usihofu kuhusu mume utapata tu” Erica alianza
kuwaelewa dada zake na kuishiwa maumivu kidogo yale aliyokuwa anayawaza
moyoni. Usiku wake Erica aliwaza sana kuhusu yale aliyokuwa
akizungumza na dada zake kwa siku hizo, ila neno la dada yake Bite lilimuingia
akilini kuwa amwambie Rahim kuwa anakubali kubadili dini kwani kiukweli bado
Erica alikuwa na wazo la ndoa licha ya kumwambia kuwa aachane na wazo
hilo. Aliingia kwenye mtandao na kumtumia ujumbe Rahim, ambapo kwa leo
alianza na salamu kisha Rahim alimuitikia halafu Erica akaandika tena ujumbe
mwingine, “Rahim, nipo tayari kubadili dini unioe” Akamtumia
huku akisubiri majibu, ila alikaa kama nusu saa bila ya kujibiwa na kujiuliza
kuwa imekuwaje maana hakuelewa sababu alijua lile jambo lazima lingemfurahisha
Rahim, alipoona kimya akatuma ujumbe mwingine, “Mbona kimya
Rahim” “Kimya nini?” “Si nimekutumia ujumbe, mbona
hujanijibu” “Ujumbe gani?” “Si nimekwambia nipo tayari kubadili
dini unioe” “Sasa hilo ni swali umeniuliza au ni nini maana sijaelewa
ndiomana sijakujibu” “Rahim jamani, mbona unakuwa hivyo. Yani nakwambia
kitu kingine unanijibu vingine. Kwanini
lakini?” “Sijakuelewa” “Si ulisema nibadili dini ndio unioe?
Nipo tayari kubadili dini sasa, lini utakuja kunioa?” “Ila wewe Erica
hebu muda mwingine uniache nipumue jamani, kila siku hakuna vitu vya msingi
tunavyozungumzia zaidi ya ujinga ujinga tu. Kwanza mwanangu
anaendeleaje?” “Yani wewe mwanaume laity ungeingia kwenye moyo wangu na
kujua jinsi gani naumia sijui kama ungekuwa unanifanyia hivyo, huyu mwanao
unataka kujua anaendeleaje unampenda kweli? Kama ungempenda si ungekuja kumuona?
Yani Rahim kuanzia leo sitakwambia tena habari za mtoto” “Sasa Erica
huko unafika kubaya, kumbuka wewe ndiye mwandani wangu, kumbuka tumezaa Erica,
huyo mtoto anatuhitaji wote wawili sasa ukisema hutoniambia tena kuhusu mtoto
wangu utakuwa hunifanyii vizuri” “Ungeujua umuhimu wa huyu mtoto basi
ungejua na umuhimu wa mama yake” “Erica, nielewe ninaposema nitakuja.
Tatizo lako unapenda nifanye vitu ambavyo sina uwezo navyo kwasasa, kuwa muelewa
basi Erica. Kesho nitakutumia pesa” Rahim alitumia swala la kumwambia
Erica kuwa atamtumia pesa ili kumpooza maana alimuona ameshapaniki, naye Erica
hakuweza kuendelea kuongea nae zaidi, kwahiyo aliamua kulala
tu. Alipoamka aliendelea na kazi zingine ila akatumiwa ujumbe
na Rahim kuwa ametumiwa pesa, “Nimekutumia laki moja na
nusu” Erica alisoma ule ujumbe na kuona kweli Rahim kabadilika maana
mwanzoni ilikuwa akimtumia hela kubwa kubwa ila kwa ile hali inamaana kuwa kuna
siku atatumiwa elfu tano, ila kwavile alikuwa na shida alishukuru hata hiyo
aliyoipata maana kwa siku hizo Rahim alikuwa akimtumia moja kwa moja kwenye
akaunti yake. Muda kidogo akaitwa na mama yake, kisha mama yake akaanza
kumwambia, “Haya Erica mwanangu, umeona jana ulivyoniaibisha mama yako?
Umeona?” Erica aliitikia kwa kichwa tu, kisha mama yake aliendelea
kuongea, “Una mpango gani sasa? Una mpango gani na maisha yako? Au
unasubiri huruma za kudhalilishwa kiasi hiki hadi lini? Hujishtukii
mwanangu?” “Mama, nakuomba mama yangu
usinikandamize” “Sikukandamizi mimi ila ujinga wako ndio
uliokukandamiza, sijakutuma ulete mwanaume mwingine halafu umsingizie mtoto.
Hapa usinione hivi, nimechanganyikiwa, wiki ijayo wajomba zakowanakuja sijui
hata nitaweka wapi sura yangu” Kiukweli Erica hakujua cha kumjibu mama
yake na kujikuta akiwa kimya tu na kumuacha mama yake aongee hadi
anyamaze. Mchana wa siku hiyo alifika James na kumkuta Erica na mama yao
maana Bite hakuwepo siku hiyo, alienda nyumbani kwa Mage kwahiyo James alipata
upenyo wa kwenda kuzungumza pale. James alikaa sebleni na Erica
akizungumza nae, ni wazi James alihitaji sana kusamehewa na mke
wake, “Erica, niambie nifanye nini ili dada yako
anisamehe” Erica akawaza kuwa dada zake waliposikia alikuwa anatumiwa
pesa nyingi na Rahim walionyesha kumpenda sana na hata kuona mdogo wao hajafanya
makosa kuzaa na Rahim kwahiyo dada zake bado walihusudu pesa. Pia akakumbuka
dada yake aliwahi kulalamika kuwa ameambulia kigari kisichoeleweka kwahiyo
inamaana akipata gari nzuri zaidi atamsamehe mume wake, “Shemeji, najua
hela unayo ila kwanini usimnunulie mkeo gari nyingine? Mshtukize kwa kumletea
gari nyingine hapa, najua atakusamehe tu” “Sasa gari
gani?” “Yoyote nzuri, yani gari utayoona imezidi ubora ile gari ya
mwanzo maana huwa anailalamikia sana ile gari.” “Una uhakika Erica,
nikifanya hivyo dadako atanisamehe?” “Fanya hivyo kwanza halafu uone
kama atakusamehe au la” James aliona aage mapema kabla mkewe hajarudi na
kumkuta hapo nyumbani, kwani hakutaka mkewe ajue kama alifika
kwao. Usiku kama kawaida, Erica alianza kwa kumtafuta Rahim na
leo alimuuliza, “Mbona siku hizi hunitumii hela kama
zamani?” “Hela nyingi wewe unataka za nini?” “Jamani, kuna vitu
vingi. Mtoto ana mahitaji mengi kwahiyo ndiomana nahitaji pesa” “Yani
wewe Erica ni bure kabisa, umesoma lakini ni bure yani ndio nyie ambao elimu
haijawakomboa. Nilijua utaniambia nitumie hela nyingi nifanye biashara ila wewe
umekazania kusema tu una mahitaji mengi. Ndio mke wewe? Loh!” “Rahim
acha kunisema vibaya, najua mimi sio mke kwako. Nitakuwaje mke na wewe
umeshaoa?” “Ushaanza kuota tena, aliyekwambia nimeoa nani? Erica acha
mawazo mgando, mke wangu ni wewe” Katika siku alizotabasamu tangu awe na
mtoto basin i leo toka alipoambiwa kuwa mke wangu ni wewe yani alijihisi kuwa na
furaha iliyopitiliza kiasi kwamba hakuendelea tena kumtumia ujumbe mwingine
Rahim zaidi ya kumtakia siku njema na kulala huku akitabasamu na kuwaza kuwa
yupo ndani ya nyumba akiishi yeye, Rahim na mtoto
wao. Kulipokucha, alifanya shughuli za nyumbani kwao. Siku hii
ilikuwa ni siku ya kumpeleka mwanae kliniki kwahiyo alimuandaa vizuri nay eye
kujiandaa kisha kuita gari kwaajili ya kwenda kliniki. Gari lilifika na
alipanda na kwenda kliniki, ambapo alihudumiwa vizuri tu, wakati anatoka
akakutana uso kwa uso na Mrs.Peter akiwa ameongozana na Yule Salma yani Erica
alishindwa hata kujificha ila kwa bahati muda huo mtoto wake alikuwa mgongoni
amelala. “Kheee Erica, mtoto wa nani huyo?” “Wa dada
yangu” “Aaah ndio umemleta kliniki! Mwenyewe yuko wapi?” “Kaenda
kazini” “Aaah! Mimi nimekuja na mkwe wangu hapa, ana mimba change basi
inamsumbua balaa, ndio nimemsindikiza aanze kliniki” Swala la kuambiwa
Salma ana mimba lilipasua moyo wa Erica. Gari
lilifika na alipanda na kwenda kliniki, ambapo alihudumiwa vizuri tu, wakati
anatoka akakutana uso kwa uso na Mrs.Peter akiwa ameongozana na Yule Salma yani
Erica alishindwa hata kujificha ila kwa bahati muda huo mtoto wake alikuwa
mgongoni amelala. “Kheee Erica, mtoto wa nani huyo?” “Wa dada
yangu” “Aaah ndio umemleta kliniki! Mwenyewe yuko wapi?” “Kaenda
kazini” “Aaah! Mimi nimekuja na mkwe wangu hapa, ana mimba changa basi
inamsumbua balaa, ndio nimemsindikiza aanze kliniki” Swala la kuambiwa
Salma ana mimba lilipasua moyo wa Erica. Muda huo ilikuwa kama Erica
kapigwa na bumbuwazi maana alisimama tu bila kwenda mbele wala kurudi nyuma, ila
Mrs.Peter alikuwa ametangulia mbele akijua Salma anamfata nyuma ila muda huo
Salma alikuwa akisimama palepale na alionekana akimuangalia Erica kwa chuki ya
waziwazi, kitu ambacho kilimshangaza hata Erica mwenyewe, na
kumuuliza, “Mbona unaniangalia hivyo?” “Utaacha lini uongo wewe
mwanamke? Eti mtoto wa dada yangu (Huku akibana pua, na kuendelea kusema). Mtoto
wako mwenyewe unasingizia wa dada yako, kwani ni kipi unachohitaji kwa huyu
mama?” Erica alimuangalia huyu Salma na kutamani hata kumpa tusi ila tu
swala la kutukana halikuwepo kwenye kinywa chake, muda kidogo mwanae akaamka na
kuanza kulia, ikabidi Erica amfunue na kumgeuzia kwa mbele, muda huo Salma
alikuwa akiondoka kumfata Mrs.Peter ila Erica akamshika vizuri mkono Salma na
kumrudisha nyuma kisha akamwambia, “Mwangalie vizuri huyu mtoto ndio
utaelewa ni kwanini sikusema wa kwangu.” Kisha Erica akaondoka ila
alimuacha Salma akiwa na maswali mengi sana, aliendelea kumfata Mrs.Peter ila
kiukweli alikosa raha. Erica alipotoka pale hospitali hata
hakutamani kuita gari ya kukodi, na moja kwa moja alielekea kupanda daladala
maana alijiona kama ni kudhalilika tayari ameshadhalilika vya kutosha, aliamua
kuacha tu jamii yake ijue kuwa ana mtoto, hakuwa na sababu tena ya kumficha
mtoto wake. Akiwa kwenye daladala, alikaa siti ya nyuma ambako kulikuwa
na wamama wawili wamekaa kwa pembeni yake wakiongea, yale maongezi yao
aliyasikia yote na yalionyesha kuvuta sana hisia zake, “Yani mwenzangu,
kipindi kile natoka na mume wa mtu halafu mkewe hata simjui ila cha kushangaza
nilikutana nae njiani si nikagombana nae, yani jamani mapenzi bhana yana wivu
ambao mwizi humjui ila unashangaa unagombana nae. Niligombana na Yule mkewe hadi
mumewe akaja kutuamulia ndio hapo nikajua kumbe Yule ndiye mkewe, na ubaya
hakuniambia kuwa ameoa weee balaa lilizuka ila nikaamua kuwa mpole na
kujitoa” “Ila mapenzi ndio yalivyo, yani mnaweza kuwa mnatoka na mtu
mmoja hamjuani ila unashangaa kuna mambo gafla tu mnachukiana jamani, sijui wale
wanaoishi wake wawili au watatu wanajisikiaje ndani” “Washazoea wale,
ila katika ujana wangu nimejifunza jambo. Hawa wanaume ni bora kuwachuna tu,
ukijiendekeza kuwapenda utalia jamani, ni waongo balaa” “Hahaha, ila
wakweli wapo bhana, sio wote waongo kumbuka hata na wao wanalalamika kuwa
wanawake ni waongo” “Ndio, ila wao wamezidi” Basi kituo
kilichofata wale wanawake walishuka na kumuacha Erica akitamani hata kuwauliza
baadhi ya maswali ila hakuweza maana hakuwazoea. Ila waliposhuka tu kule
nyuma alipanda mkaka na kukaa karibu na Erica, Yule mkaka alimtazama Erica na
kumtazama mtoto wa Erica kisha akamwambia, “Dada, hongera sana una mtoto
mzuri. Halafu ana tabasamu vizuri” “Asante” “Mmmmh sijaanza hata
kukusalimia maana nilivutiwa na uzuri wa huyu mtoto, hali yako
lakini” “Nzuri, ila usijali” “Ngoja nijitambulishe kidogo, dada
mimi naitwa Moses. Nina duka langu zuri sana la nguo za watoto wakike na wa
kiume. Naomba uje dukani kwetu hata mara moja uone huduma zetu, business card
yangu hii” Akamkabidhi Erica, naye Erica akapokea huku akisikiliza
maelekezo mengine toka kwa Yule kaka, “Tafadhali dada, naomba ufike.
Nimevutiwa sana na mwanao. Najua atapendeza sana akivaa nguo zetu zile. Ila
unaitwa nani, na mwanao anaitwa nani?” “Mimi naitwa Erica, na mwanangu
anaitwa Angel” “Wow, majina mazuri sana. Nakutegemea basi dada ufike
dukani kwetu. Ila ungenipa na namba zako” Basi Erica akataja na namba
zake kwa Yule kaka, kisha alivyofika kwenye kituo chake alishuka na kuelekea
nyumbani kwao. Alifika kwao na kukutana na mama yake ametoka
dukani kwahiyo waliingia wote getini, mama yake alimuuliza kwa
mshangao, “Kheee Erica, leo umekuja kwa mguu bila gari? Yani mtoto wako
umemuacha wazi kabisa” “Nimechoka mama, nitamficha mtoto huyu hadi
lini?” “Ukiwaza hayo, wazo na kuwa utawezaje kueleza watu kuwa mtoto
hana baba?” “Jamani mama, kwani kuna watoto wangapi baba zao wamekufa na
wanaishi?” “Weeee usitake kufananisha watoto ambao baba zao wamekufa na
mwanao, kumbuka wale baba zao wapo ila wamekufa ila mwanao hana baba kabisa yani
hiyo ndio tofauti yao” “Mama, kwakweli humu ndani mnanichanganya jamani.
Mimi nishajiamulia kuishi na aibu yangu, kama huyu mtoto simtaki basi nikamuuze
huko ila sio kumficha” “Yani Erica, unamjibu mamako majibu ya shombo
kiasi hiko jamani. Wewe mtoto loh! Utajibu mwenyewe wajomba zako wakija, na Yule
mjomba wako aliyekuwa akikulipia ada utamuonyesha shahada uliyoipata chuo
ulipomaliza walikutunuku mtoto” Erica akaona si vyema ajibishane na mama
yake, kwahiyo aliamua kwenda ndani tu. Alicheza cheza na mwanae na
kumlisha, kiukweli mwanae hakuwa mtoto msumbufu na alikuwa na afya nzuri tu
kwahiyo haikumpa shida sana kwenye kumlea. Usiku wake akawaza jambo
moja, akakumbuka jinsi Rahim alivyomwambia kuwa anaomba hela za matumizi badala
aombe hela za biashara, akafikiria kumuomba Rahim hela ya biashara ila
akafikiria ni biashara gani sasa atafanya, “Mmmh nitaenda kwa yule kaka
kuangalia biashara ya hivyo vitu vya watoto halafu niianze hiyo
biashara” Akamsikia dada yake amerudi maana dada yake alianza tena
kwenda kazini, kwahiyo alimfata kuongea nae ili kumuuliza kama ameshawahi
kusikia biashara ya vitu vya watoto, alimsalimia pale na kumpa pole ya kazi
kisha akamuuliza kuhusu hiyo biashara, “Ni biashara nzuri sana umewaza
mdogo wangu, ila hiyo biashara ukitaka ufanye vizuri na uheshimike, unatakiwa
uwe na mtaji wa kutosha” “Kama kiasi gani dada?” “Kwa kuanzia
sio mbaya ukiwa na milioni kumi na tano” “Mmmh dada, mbona hela nyingi
hivyo?” “Hahaha Erica, bado hujaijua hela wewe yani milioni kumi na tani
ni nyingi? Ukiwa na hela hata sio nyingi, sema ni kwavile hela hamna
ndiomana” “Nataka nimuombe baba wa mwanangu” “Ila kama huyo
mwanaume alikuwa nankupa hadi milioni tatu, nne sidhani kama milioni kumi na
tano itamshinda. Tena atafurahi sana ukiwa na wazo la kufanya
hivyo” “Sawa dada, kwahiyo nimuombe milioni kumi na tano eeeh! Si
utanisaidia dada kwenye hiyo biashara?” “Nitakusaidia ndio, mimi nina
rafiki zangu wengi tu wanajishughulisha na maswala ya bishara. Hata usijali
nitakusaidia maana kusubiri kazi ni ngumu kwa kipindi hiki” Erica
alimshukuru pale dada yake, kisha muda wa kwenda kulala alimtafuta Rahimhewani
na alimkuta ila leo hakutaka kabisa kumuanzishia mada sijui amekutana na mama
yake pamoja na Salma, sijui swala la kumdanganya kumbe Salma ni mjamzito.
Hakutaka kuzungumza nae swala hilo, na moja kwa moja alimueleza swala lake la
kutaka biashara, “Biashara gani utaiweza wewe?” “Nataka biashara
ya kuuza nguo za watoto na vitu vyao vya kuchezea” “Kwahiyo unataka
mzigo ukachukue China na Dubai?” “Aaah ikiwezekana kufanya hivyo
nitafanya, ila kwasasa nahitaji kuanza hiyo biashara” “Haya, mtaji kiasi
gani?” “Milioni kumi na tano” “Na wewe una kiasi
gani?” “Mimi sina hela ndiomana nimekwambia wewe Rahim, si unajua
nimemaliza chuo nikawa kwenye uzazi, sasa hela nitatoa wapi
mimi?” “Usinitanie Erica, hela zote nilizokuwa nakupa ulizipeleka
wapi?” “Rahim jamani, hakuna hela uliyonipa bila sababu. Hel azote
zilikuwa na sababu na zilienda kwenye matumizi ya hizo sababu, sasa ningekuwa
nazo ningekuomba kweli?” “Erica, kuna wanawake wangapi wanauza maandazi,
vitumbua, kachori, visheti? Kuna wanawake wangapi?” “Wengi
sana” “Na wewe kwanini usiwe katikati ya hao wanawake?” “Jamani
Rahim, kwanini lakini unanifanyia hivyo? Sijazoea kuuza vitumbua, sijui visheti,
hizo biashara zinataka mazoea” “Aliyekwambia wale wamezoea nani? Yani
Erica unataka mimi nitoe milioni moja, mbili, tatu, nne hadi kumi na tano kweli?
Wewe msichana una akili kichwani mwako? Kichwa chako kizima hiko? Yani nitoe
milioni kumi na tano kweli? Yani unaitamka kama sijui ni hela ndogo. Erica,
kweli kabisa milioni kumi na tano?” “Jamani Rahim, unajua mimi nikifanya
biashara sitakusumbua wewe kuhusu swala la mtoto maana nitakuwa najitosheleza
kuliko hivi. Kumbuka ni wewe ulinishauri nifanye biashara, kweli saizi
unanishangaa jamani?” “Kama unataka kusaidia kwenye malezi ya mtoto,
kwanini usitafute kazi? Au basi ungeniambia naomba hela nianze biashara ya
sambusa, najua mtaji wake hata elfu hamsini haifiki, unaniambia kitu cha mtaji
wa mamilioni ya pesa jamani Erica? Unahisi sina majukumu mengine ila nina
majukumu ya wewe tu?” “Rahim, sikuelewi yani sikuelewi kabisa. Kwani ni
kitu gani unachotaka mimi niwe? Kwakweli Rahim hapana jamani, mtandaoni kwenyewe
nikutafute mimi, kila kitu nikubembeleze kama mtoto mchanga. Na kutwa kunitoa
akili yani kama duniani nipo peke yangu nisiyekuwa na akili. Nashukuru Rahim kwa
hayo unayoniambia” “Ila kwani nakwambia uongo? Erica kiukweli akili
huna, hata mwanaume atakaye kuoa atajuta, wewe sio mwanamke wa kuolewa maana
huna akili hata kidogo. Huwezi kuja kuniomba hela yote hiyo mimi, kwa kazi gani
ninayofanya?” “Kweli nimeamini, mwanaume akishakutumia anakuona huna
thamani tena. Siku zote hukujua kama sina akili hadi umenizalisha? Na ulianzaje
kuzaa na mwanamke asiye na akili? Rahim, kwasasa nimefika mwisho maana
nishajibembeleza kwako hadi nimechoka” “Kwahiyo unamaanisha
nini?” “Rahim, kuanzia leo sitakutafuta tena hewani, sitakuomba tena
hela yoyote ya matumizi ya mtoto yani sitakusumbua kwa chochote kile. Mimi ni
mwanamke ndio ila nitapambana na nitaishinda hii hali, nimepata aibu,
nimedhalilika ila bado sijafika mwisho. Kwaheri” Alituma ujumbe ule
akitegemea kujibiwa kwa kuombwa msamaha na Rahim ila ule ujumbe haukujibiwa na
ilipita saa nzima bila ujumbe kujibiwa huku Rahim akionekana hewani tu, kitendo
hiko kilimuumiza sana Erica, alijikuta akimwaga machozi. Alilia sana
hadi alisikia jogoo zikiwika na kugundua kuwa kumekucha, akachukua simu yake
kuangalia mida akakuta ni saa kumi alfajiri, alihisi kichwa kikimuuma kwa kulia
sana ila muda huu alijifuta machozi na kusema, “Leo ndio mwisho wa
kulia, sitalia tena. Kwasasa natakiwa kuinuka na kuonyesha kuwa naweza, mtoto
wangu nitamlea mwenyewe” Erica alilala kwa muda huo huku kichwa
kikimuuma sana. Kesho yake aliamka na kujiandaa kisha akamuacha
mwanae na mama yake na kwavile nyumbani kwao kulikuwa na mdada wa kazi wa dada
yake Bite, ikawa rahisi zaidi. Erica akaenda mjingi akizunguka kwenye
maofisi kadhaa kuulizia kazi, alizunguka sana siku hiyo hadi jioni alirudi kwao
akiwa amechoka sana bila mafanikio yoyote. Alichoka sana, dada yake
alimuita na kumuuliza kuwa alienda wapi siku hiyo, Erica alimueleza kuwa alienda
kutafuta kazi, “Kwani huyo mwanaume alikwambiaje kuhusu hela ya
biashara?” Erica alimueleza dada yake kila kitu alichojibiwa na
Rahim, “Kwahiyo mdogo wangu umechukia sababu hajakupatia hiyo milioni
kumi na tano?” “Hapana dada, sijachukia sababu hiyo. Ila nimechukizwa na
majibu anayonipa, kwani kutoa hela ni lazima? Si unasema tu sina, sasa majibu
aliyonipa dada ndio yaliyoniumiza sana” Erica aliamua kumuonyesha dada
yake jumbe zote alizokuwa akijibiwa na Rahim, kiukweli hata Bite alianza kujiwa
na huruma na mdogo wake, alijaribu kuhisi ni wapi anakopitia ndiomana kakosa
hata uelekeo na kuamka tu kuanza kutafuta kazi kwa kuulizia tu maana alikuwa
hana muelekeo. “Sikia Erica, umeshawahi kufanya field kwa shemeji yako
James, kwanini usiende tena huko” “Mmmh dada, kwa shemeji
tena!” “Usiogope Erica, tumeshajua kila kitu kwahiyo hakuna tatizo
lolote. Mwanzoni tulikuwa hatujui, najua James hawezi kukataa wewe usifanye kazi
kwenye ofisi yake ila vilevile hawezi kukufanyia tena vitendo vya ajabu wakati
ukweli tunaujua kama kukulazimisha kuwa akurudishe nyumbani, hawezi tena maana
kipindi kile ni mimi nilikuwa namtetea. Ila sasa swala la kuongea nae akuweke
kazini mimi silifanyi kwakweli maana huyo James ananitia kichefuchefu
tu” Erica aliongea ongea na dada yake na kwenda kulala, ila
alishafikiria jambo kuwa shemeji yake akifika kumuomba msamaha dada yake basi
ndio siku hiyo aongee nae kuhusu swala la yeye kwenda kazini
kwake. Siku hiyo alikuwa nyumbani kwao hana hata habari,
alishangaa kumuona shemeji yake James akifika, na kujua lazima atakuwa anataka
kuomba msamaha vizuri, na ni kweli kabisa James alikuwa amekuja kwa lengo la
kumuomba mkewe msamaha, James akamwambia Erica, “Nenda nje kaone gari
niliyomnunulia dada yako, sijui ataipenda? Hebu kaiangalie kwanza” Erica
alitoka nje na kuiangalia ile gari, kwa hakika ilikuwa nzuri sana, “Mmmh
jamani, dada alikuwa akitamani sana kupata gari ya mtindo huu. Sasa kaipata,
mmmh kweli shemeji ana pesa, dada yangu amsamehe tu” Muda kidogo Bite
naye alifika nyumbani kwao, na kupaki gari yake, akashuka na kumuangalia mdogo
wake akishangaa ile gari kisha akamuuliza, “Gari mpya nzuri hii ya
nani?” “Umeipenda dada?” “Nimeipenda ndio, ila hata nikiipenda
kazi bure. Kwasasa natakiwa kuwa mpole tu, hizi gari nzuri nitabaki kuziangalia
kwa macho” Basi Erica akampokea dada yake mkoba na kwenda nae ndani, ila
Bite alipomuona James alionyesha kuchukizwa na hata hakumsalimia na kupitiliza
ndani ila Erica aliongea na shemeji yake kwa ishara kuwa dada yake amelipenda
sana lile gari. James akainuka na kumwambia Erica asubiri kisha
aliporudi alikuwa na boksi mkononi, akalishusha chini, ilikuwa ni
keki. Erica akamuita dada yake kwa furaha, Bite alienda tu pale sababu
mdogo wake kamuita, kisha Erica alifungua lile boksi, akashangaa kuona keki
imeandika ‘Happy birthday Angel’ kwakweli Erica alijihisi kutokwa na machozi
maana kweli ilikuwa ni siku ya kuzaliwa mwanae ila hakutaka kuikumbuka kwavile
hakuwa na chochote cha kufanya kwaajili ya mtoto wake ila shemeji yake alimpa
mshtukizo wa hali ya juu, Erica alimuangalia na kumuuliza, “Umejuaje
shemeji?” “Nilimuuliza dada mkubwa Mage kubwa ulijifungua lini na mwanao
anaitwa nani, nikaona leo siku ya kuzaliwa ya mtoto huyu iwe ni siku ya furaha
kwetu. Ndiomana nikamletea na mke wangu zawadi ya gari alilokuwa analitamani kwa
siku nyingi sana, (Akamuangalia mkewe na kumwambia) Najua mke wangu huwezi
kukataa zawadi yangu kwenye siku muhimu kama hii ya kuzaliwa kwa malaika kwenye
familia yenu. Naomba nikiri wazi nakupenda mke wangu Bite na familia yako ni
familia yangu. (Kisha akatoa kadi ya gari na funguo kimkabidhi
Bite)” Bite alijikuta akimsogelea mume wake na kumkumbatia huku akitoa
machozi maana hakutegemea kama kitu kile kingempa furaha kiasi kile mdogo wake
ukizingatia kwa siku za karibuni tu alionekana akiwa na masononeko
mkubwa. Walikata keki na kufurahi kwa pamoja, kisha James akawaomba kuwa
waende mahali wakapate chakula cha usiku, ila Erica alikataa kwavile alitaka
shemeji yake na dada yake wapate muda wa kuzungumza. Kisha Bite
akajiandaa na kutoka na mumewe na walitumia gari lile jipya ambalo mumewe
alifika nalo kama zawadi ya Bite. Erica alitulia mwenyewe na
watoto sebleni maana mama yake hakuwepo ila baada ya muda mfupi alirudi na
kuulizia kuwa Bite yuko wapi, “Ametoka” “Ametoka muda huu? Mbona
gari yake ipo nje?” Erica alimueleza mama yake kuhusu kilichotokea kuwa
Bite kapatana na mume wake, “Nilijua tu, yani mambo ya mapenzi sio ya
kuingilia kabisa. Unaweza kusema hadi koo likukauke ila unashangaa hao
washarudiana” “Ila mama kwani hukupenda warudiane?” “Nisipende
kwa lipi? Unafikiri nafurahi kuona watoto wangu ndoa zinawashinda? Ila nilitaka
ampe adabu kidogo Yule mwanaume maana hanta adabu jamani, ningekuwa mimi hata
nisingekubali kirahisi hivyo. Ila mapenzi mmmh!” Baada ya usiku kuingia
vizuri Bite na James walirudi na kujiandaa kwaajili ya kurudi kwao, mama yao
akamuuliza Bite, “Usiku huu?” “Ndio mama, kesho si
kazini” “Mmmh haya bhana, mapenzi siyaingilii” Basi Bite
alijiandaa kisha kumuaga mama yao na kuanza safari, na waliondoka na ile gari
mpya, kwahiyo gari ya mwanzo ya Bite iliachwa pale pale nyumbani. Erica
alikuwa chumbani kwake kwa lengo la kulala, ila akafikiria sana, akatamani apate
mwanaume ambaye hata akifanya makosa anajua jinsi ya kuomba msamaha ila sio aina
ya Rahim ambaye hata hajali chochote. Akawaza kuhusu Bahati kuwa ndiye
mwanaume pekee aliyeonekana kumpenda sana, ila alishangazwa na hali ya Bahati ya
kutokumtafuta toka siku ile wakati sio kawaida ya Bahati, lazima angeenda
kuendelea kumuomba msamaha au angempigia simu ila ni kimya
kabisa. Aliamua yeye kumpigia simu ila hakuipata namba ya Bahati hewani,
jmbo lile lilimfanya ajihisi vibaya sana kwani kwa muda huo alihisi kuhitaji
sana uwepo wa Bahati. Basi wiki nzima alikuwa akifanya kazi ya kumtafuta
Bahati hewani ila hakumpata na kumfanya azidi kukosa amani, akaona ni vyema
aende anapoishi Bahati ili ajue nini kimempata Bahati maana sio kawaida
kabisa. Siku hiyo akajiandaa vizuri kabisa, kisha kumuaga mama
yake kuwa kuna mahali anaenda ila hakumwambia ukweli kama anaenda nyumbani kwa
Bahati, alimuacha mtoto wake pale na kuondoka. Alifika hadi mahali
ambako Bahati alikuwa amepanga, alikuta baadhi ya majirani, akawasalimia na
kwenda kwenye chumba cha Bahati ila alikuta kufuri kwahiyo Bahati hakuwepo.
Aliamua kumuuliza jirani mmoja wa Bahati, huyo jirani alikuwa ni
mdada. “Dada, samahani eti Bahati yuko wapi?” “Kheee Bahati,
yupo kuoa. Ana shughuli leo” “Kuoa!” Erica alishtuka sana na
kuuliza kwa umakini ila Yule jirani alimuhakikishia Erica kuwa Bahati yupo
kuoa, “Kwani hujui?” “Sijui” “Ngoja nikupeleke
anapofungia ndoa” Basi Erica akaanza kuongozana na Yule mwanamke
kuelekea mahali ambako Bahati alikuwa anaoa, walifika kwenye nyumba ambako
kulikuwa na watu wengi na shamra shamra, kitu kilichodhihirisha kuwa kuna
shughuli. Muda kidogo maharusi walikuwa wanatoka ndani yani ndoa
ilishafungwa, bado Erica alikuwa haamini na kuangalia kwa makini hao maharusi
wanaotoka ndani. Alishangaa kuona Bahati akiwa ndiyo bwana harusi, akiwa
ameambatana na binti mmoja ambaye ndio bibi harusi, yani Erica alihisi
kizunguzungu muda huo. Basi Erica akaanza kuongozana
na Yule mwanamke kuelekea mahali ambako Bahati alikuwa anaoa, walifika kwenye
nyumba ambako kulikuwa na watu wengi na shamra shamra, kitu kilichodhihirisha
kuwa kuna shughuli. Muda kidogo maharusi walikuwa wanatoka ndani yani
ndoa ilishafungwa, bado Erica alikuwa haamini na kuangalia kwa makini hao
maharusi wanaotoka ndani. Alishangaa kuona Bahati akiwa ndiyo bwana
harusi, akiwa ameambatana na binti mmoja ambaye ndio bibi harusi, yani Erica
alihisi kizunguzungu muda huo. Yule mwanamke aliyempeleka Erica pale
alimuona alivyokuwa anapepesuka, ikabidi amdake na kwenda nae mahali chini ya
mti na kumkalisha, kisha kumuuliza “Nini tatizo dada, umechanganyikiwa
gafla” “Acha tu dada yangu” “Pole, au Bahati alikuwa ni mwanaume
wako?” “Hapana, ila sijapenda vile hajanipa taarifa” “Ila
usimlaumu dada, hii ndoa yenyewe imekuwa haraka haraka sana hata sisi
tumeshangaa ila kwavile hatukumjua msichana wake labda pengine alikuwa nae
kitambo ila ndoa ya gafla sana hii” Erica aliomba asaidiwe kuinuka
aondoke, kisha Yule mwanamke akamsaidia na kumuitia bodaboda ambayo Erica
alipanda na kuondoka. Yule mwanamke alionekana kusikitika sana ni kweli
Erica alimdanganya ila yeye alihisi jambo kuwa pengine Bahati alikuwa na
mahusiano na msichana Yule, alikuja jirani mwingine na kumuelezea jinsi Yule
msichana alivyoondoka pale, “Kheee kwani wewe humjui
Yule?” “Simjui, ni nani kwani?” “Yule msichana amewahi kuja mara
moja au mbili pale nyumbani, na ukiongea na Bahati mar azote alisema ni jinsi
gani alimpenda Yule msichana hata nashangaa imekuwaje kuoa msichana mwingine.
Mmmh mapenzi haya!” “Mmmh kwa mtindo huo hata usiyalaumu mapenzi,
sidhani kama Bahati alikuwa akimuongopea Yule msichana ila baba yake Nasma huyu
binti anayeolewa na Bahati jamani baba ni mchawi Yule hakuna
mfano” Walijikuta wakiongelea tukio lile lile la Erica kutaka kuzimia na
jinsi ndoa ya Bahati ilivyofanywa kwa haraka sana. Erica
alirudi nyumbani kwao, na hata hakuongea na mtu kwani mwanae muda huo alikuwa
chumbani na bibi yake, basi Erica aliingia chumbani kwake na kujifungia mlango
kisha kulia sana, yani alilia ila alikumbuka maneno yake kuwa hatolia tena ila
bado machozi yalimtoka, “Hivi Bahati kweli ndio ulikuwa unasema
unanipenda sana na hakuna mwanamke unayemuona zaidi yangu kweli? Umeamua kuoa
Bahati, ama kweli mimi ni fungu la kukosa jamani. Inamaana Yule msichana kaanza
nae muda mrefu sana, huwezi kuniambia ndani ya wiki mbili tu umfahamu mtu mpaka
mfikie kuoana, yani lazima Yule msichana anajuana nae kwa siku nyingi sana.
Siamini kama Bahati kanisaliti jamani” Erica aliumia sana moyo wake na
kukosa raha kabisa ila hakuwa na la kufanya kwa wakati huo, akakumbuka jinsi
alivyokuwa akipewa hela na Rahim na jinsi alivyokuwa akimpa hela Bahati ila leo
hii Rahim kamkosa na Bahati kamkosa pia, alikosa raha kabisa na kujiona hana
thamani. Mama yake alimuhisi kuwa Erica amerudi na kumuita, ilibidi
Erica ajifute machozi yote na kwenda kumsikiliza mama yake, “Kheee yani
unarudi kimya kimya husemi jamani, na utafute msichana wa kazi sasa maana mtoto
utakuwa unamuachia nani? Utafute msichana wa kazi” “Sawa
mama” “Na mbona macho yamekuvimba? Ulipotoka huko umepigwa au
nini?” “Hamna kitu mama” “Unajua wewe mtoto utachanganyikiwa
jamani, siku hizi huendi kanisani yani upo upo tu. Huwa kuna mahubiri kwenye
redio, basi mara moja moja hata uwe unawasha na kusikiliza
mahubiri” “Sina redio mimi” “Hata simu zina redio, ila ngoja
nitakupa maana mimi nina redio mbili. Uwe unasikiliza na mahubiri uweze kukaa
vizuri na moyo wako” Yale maneno ya mama yake hayakumuingia wala nini,
badala yake alimchukua mwanae na kuingia nae chumbani ila muda huu hakuweza
kuendelea kulia maana mtoto wake alipomuona akilia alilia pia, kwahiyo alijizuia
asilia mbele ya mtoto wake badala yake alicheza nae tu. Usiku ulipofika
alijaribu kutafuta usingizi ila kiukweli usingizi aliukosa kabisa huku akijihisi
ni msichana mwenye mkosi katika maisha yake, kwa muda ule alitamani sana kupata
hata mtu wa kumbembeleza kwenye simu, akawaza sana kuwa afanye nini, akafikiria
watu aliokuwa kwenye mahusiano nao, Rahim ndio huyo kageuka mbogo, Bahati ndio
huyo kaoa, kusema Babuu asingeweza tena kuweka ukaribu nae kwani kiukweli ni
shemeji ingawa hajamuweka wazi, hapo wazo likamjia kumtafuta Erick tu maana kwa
muda huo hakuona mwingine wa kumliwaza kwa kumwambia maneno
matamu. Akainuka na kuchukua ile barua ya Erick kisha kuangalia namba
zake na kumpigia, ila simu iliita na kukata, akapiga tena simu iliita na kukata,
akahisi kuwa huenda Erick amelala kwa muda huo. Akaiweka simu pembeni
huku akijaribu kutafuta usingizi ila aligalagala kitandani kwa muda wote na wala
hakupata usingizi kwani kiukweli alikuwa na mawazo sana na ndiyo yalimfanya
asiweze kupata usingizi. Kwenye mida ya saa kumi alfajiri, alisikia simu
yake ikiita, aliichukua na kuangalia mpigaji akaona ni Erick, alitabasamu sana
akaipokea na kuanza kuongea nae, ila akagundua Erick alikuwa amelewa na kufanya
awe na maneno mengi sana, “Erick, mbona umelewa hivyo?” “Wewe ni
Erica?” “Ndio, mimi ni Erica” “Wewe ndio unayenipa sababu za
kulewa Erica, hivi unajua ni jinsi gani nakupenda? Kweli Erica siku zote hizo
ndio umenitafuta leo? Nimeona namba hata sijajua ni wewe nimepiga tu kumbe ni
wewe kipenzi change, nakupenda sana Erica” “Ila umelewa
Erick” “Ndio nimelewa ila nimelewa kwaajili yako” Na ikawa kimya
ilionyesha kama mtu anakoroma kwamaana hiyo Erick alilala na simu kwavile
alikuwa amelewa, ilibidi Erica akate ile simu, ila alitabasamu kuona kumbe Erick
bado anamkumbuka, na muda huo akalala na tabasamu usoni huku akisahau yote
ambayo yametokea mbele yake. Palipokucha aliamka na kufanya
shughuli zake zingine ila kwenye mchana hivi akapigiwa simu, kuangalia ni Erick
alikuwa akimpigia, Erica alipokea ile simu huku akitabasamu, “Hivi jana
nilikuwa naongea na wewe kweli Erica au mtu gani?” “Ni mimi mwenyewe,
umenisahau?” “Siwezi kukusahau Erica, ila umejua kuniumiza wewe mwanamke
kwanini lakini? Umepata ujumbe wangu muda mrefu tu ila umenikaushia, kwanini
ulinichunia Erica?” “Nisamehe Erick?” “Hunipendi
tena?” “Hapana, bado nakupenda” “Kama wanipenda, kwanini
unafanya niumie moyo Erica? Nilirudi nchini ila sikuweza kukaa sana na kuamua
kuja tena Kusini maana nilihisi hutaki hata kuniona” Erica alijaribu
kuongea na Erick na walionekana kupatana sana ila katika maongezi yale Erica
hakuthubutu kumwambia Erick kuwa ana mtoto maana hakujua angechukulia vipi swala
hilo ukizingatia hakutaka kuumia kabisa. Kwahiyo siku ya leo ilikuwa ni
siku ya tabasamu zito kwa Erica hata mama yake aliweza kugundua ni jinsi gani
binti yake anavyoonyesha furaha. Jioni ilipofika alipigiwa simu na
shemeji yake James, “Erica, nimeambiwa na dada yako kuwa unahitaji kazi.
NImelifanyia kazi swala hilo, hivyobasi naomba ujiandae na wiki ijayo uje kuanza
kazi” “Shemeji unasema kweli?” “Ndio Erica, kuna muda
nimetaniana na wewe? Njoo kazini na utafurahi na moyo wako, ni mengi kanieleza
dada yako nimeingiwa na huruma sana ila najua utakapokuwa kazini itakuwa rahisi
kuendesha maisha yako. Naomba wiki ijayo uje kuanza” Erica alimshukuru
sana shemeji yake kwa uamuzi ule maana kwake ilikuwa ni faraja sana ukizingatia
katika maisha yake hiko kilikuwa ni kipindi kigumu sana. Alipomaliza
alienda kumueleza mama yake kuwa amepata kazi kwenye ofisi ya shemeji yake,
alijua mama yake angefurahi sana ila ilikuwa kinyuma. “Kheee mama, mbona
hujafurahi?” “Erica, unaweza ukahisi labda mama yako sikupendi au nini
na nini ila nakupenda sana, unajua nakupenda. Na yote ninayokwambia huwa
nakwambia kwa upendo, najua kwasasa una shida sana na kazi ila kazi ya kufanya
kwa shemeji yako sijaipenda” “Jamani mama, ila shemeji
kabadilika” “Wewe wasema hivyo, ila wanaume nawajua vizuri sana kushinda
hata wewe na ndugu zako mnavyowajua. Ulinipa habari kuwa James alimletea mwanao
keki, nilitabasamu tu eti anaonyesha kujali familia ya mke wake. Wapo wa kujali
familia ya mke ila sio kwa James, yani haaminiki hata kidogo. Gari ya mwanzo ya
dada yako imeachwa hapa nje, nina uhakika shemeji yako atakupa wewe. Na kazi
ndio hivyo kakupa, yani James ana akili kupita tunavyofikiria yani lazima
atakusumbua tu halafu sitaki ugombane na dada yako” “Jamani mama,
haiwezi kuwa hivyo” “Haya, ila mimi ni mkubwa nimetangulia kuliona jua.
Kwavile umeamua sawa, mimi nakutakia kila la kheri ila uwe makini
sana” “Usijali mama kuhusu umakini” “Uliniambia hivyo hivyo
mwanzo ila ukamaliza degree na degree ya mtoto, kuwa makini. Mwanaume sio ndugu
yako, yani muone kama samba na usipende kuwa nae karibu, sijui shemeji
itakutokea puani” Erica alimsikiliza mama yake ila alimuona mara
nyingine mama yake anaongea ongea tu ukizingatia ni yeye mwenyewe ndiye kafanya
hata atafute kazi sababu ya kumsema sana kuwa anakaa nyumbani hana shughuli
yoyote. Mama yake Erica aliinuka na kumletea Erica redio ambapo
alimwambia awe anasikiliza mara moja moja hata mahubiri maana akili yake
ilionekana kulala sana. Kiukweli Erica toka apewe na mama yake
redio hakuwahi kusikiliza mahubiri wala nini na mara nyingi alikuwa akiongea na
Erick tu. Siku ilifika ya Erica kwenda kazini kwahiyo akaenda kazini,
siku hizo alikuwa na tabasamu usoni ukizingatia mara kwa mara alikuwa
akiwasiliana na Erick, na mara nyingi aliwasiliana nae mtoto akiwa amelala
kwahiyo hakumweka wazi kuwa ana mtoto kwani hakujua Erick angechukulia vipi
swala la yeye kuwa na mtoto. Alifika ofisini na shemeji yake alimpokea
na kumuonyesha kazi ya kufanya ambapo alimuweka kwenye mapokezi ya kuingia
kwenye ofisi yake, “Yani mtu yeyote asije kuniona bila kupitia kwako
Erica, utafanya kazi zingine ila utahakikisha hilo. Sitaki watu wafanye mazoea
ya kuingia ofisini kwangu kama chooni” “Sawa bosi
nimeelewa” “Aaah usiniite bosi bhana” “Sasa nitakuita shemeji
wakati tupo kazini? Lazima nikupe heshima yako, wewe ni bosi
wangu” “Niite James itapendeza zaidi” Kisha James akaelekea
ofisini kwake na kumuacha Erica pale azoee mazingira. Alifanya kazi zake na muda
ulipofika tu alibeba mkoba wake na kuondoka kwani hakutaka ile tabia ya kuagana
na shemeji yake ukizingatia matendo ya shemeji yake tayari
alishayajua. Erica alienda kupanda daladala moja kwa moja, ila kabla
hajapanda alishikwa bega, kugeuka alikutana na Dora na alionyesha kuwa mpole
sana, “Erica, mambo” “Safi” “Erica, nihurumie mwenzio
angalia ninavyopata shida. Sikupenda iwe hivi ndiomana nakuomba msamaha, kwanza
kabisa napenda tuwe marafiki kama zamani hata kama sitaolewa tena na kaka yako
ila nahitaji tuwe marafiki.” “Dora, sitaki tena urafiki na
wewe” “Sikia Erica, hakuna binadamu aliyemkamilifu duniani, kila mtu
hajakamilika na kila mtu ana mapungufu sake. Nakubali kuwa nilikuwa malaya,
nishatoa mimba nyingi, ila nimebadilika sasa, hivi unadhani wewe ukihukumiwa kwa
makosa ambayo uliyafanya kipindi cha nyuma utajisikiaje? Erica, kuna mahali
nafanya kazi ili siku ziende tu ila kiukweli sina raha, toka lile songombingo la
nyumbani kwenu. Kakako kaniambia kuwa yeye hana matatizo ila anasema kwamba
uhuru wake umeubeba wewe yani wewe ndiye mwenye maamuzi ya mimi kuendelea na
kaka yako au la. Erica hata kama hutaki mimi niwe na kaka yako ila naomba basi
tuwe karibu, tuwe marafiki, nimejirekebisha Erica na ninakiri shoga
yangu” Erica alimuangalia Dora ambaye aliongea kama mtu kweli ila
kwavile Erica alishajiwekea kutokupatana tena na Dora, ikabidi aachane nae kisha
yeye kuondoka zake. Akaend kupanda daladala na
kuondoka. Alifika nyumbani kwao akiwa na uchovu sana ambapo
mama yake alimuuliza kuwa hiyo siku ya kwanza kazini aliionaje, “Aaah
mama ipo vizuri kabisa, yani pale ofisini wamenipokea vizuri ukizingatia
niliwahi kuwa pale kabla” “Hivi na mahubiri unasikiliza
kweli?” “Nasikiliza mama” “Haya kama unasikiliza” Erica
alimuitikia mama yake ili kiukweli hakuwahi kusikiliza toka mama yake ampe
redio, alienda kuoga na kula chakula cha usiku. Muda anaenda kulala siku
hiyo akaona ni vyema asikilize hayo mahubiri anayoyasema mama yake, akafungua
kituo alichoambiwa na mama yake na kukuta muhubiri akiendelea na
mahubiri, “Unajua mara nyingine ufanikiwi kumbe sababu ya kufanya mambo
mabaya kwa wenzio, hakuna kitu chema kama kusamehe ndiomana maandiko yanasema
samehe saba mara sabini, tunatakiwa kuwa watu wa misamaha. Tusamehe ili
kuachilia baraka zetu, swala la kukaa na kinyongo sio zuri” Erica
alihisi usingizi na kuzima redio ila yale mahubiri yalimuingia
vilivyo, “Kwa maana hiyo sina baraka sababu sijamsamehe Dora, labda
sababu namuwekea vikwazo Dora kuolewa na kaka yangu ndiomana na kwangu kumetokea
vikwazo. Inabidi nimsamehe tu, potelea mbali aliyonifanyia ila natakiwa
kumsamehe” Alijiambia na moyo wake kuwa atakapokutana tena na Dora
atamsamehe. Kesho yake alienda kazini, ila James alimuigta
kuzungumza naye, “Erica, kwanini jana hujaja kuniaga?” “Sikujua
kama napaswa kukuaga, nilipoona wengine wameondoka basi na mimi nikaunganisha
nao” “Erica, mimi ni shemeji yako na wakati huo huo mimi ni bosi wako.
Nimekuweka katika kitengo cha karibu na mimi kwa makusudi kabisa, kwanza
nakuamini halafu sitaki wafanyakazi wengine wakusumbue sumbue. Kitengo
ulichokuwepo hutakiwi kuondoka bila ya kuniaga, kwani kuna umuhimu mkubwa wa
kufanya hivyo ili hata muda huo najua kuwa umeondoka na nitakabiliana vipi na
watakaokuja kuniona. Usifanye tena hivyo Erica” “Sawa bosi
nimesikia” “Usiniite bosi Erica, niite tu James. Na vipi ulitumia
usafiri gani?” “Nimetumia daladala” “Sasa kwanini utumie
daladala wakati gari ya dada yako ipo tu pale kwenu imekaa, ngoja kesho
nikuletee funguo na uanze kuiendesha” Erica alimshukuru shemeji yake
pale kisha kuendelea na kazi zake za pale ofisini, kwenye mida ya mchana
walifika watu wawili wakiomba ruhusa ya kuongea na bosi wake, “Mnahitaji
kuongea nae nini?” “Kampuni yetu kuna bidhaa inajihusisha nazo, kwahiyo
tulihitaji kuongea nae ili atupe ruhusa tuweze kuzungumza na wafanyakazi
wake” Erica aliinuka na kwenda kuwaombea ruhusa kwa bosi wake ambapo
aliruhusu aingie mmoja wapo, kwahiyo Yule mwingine alibaki pale na Erica, mara
kidogo alifika na mwenzao mwingine, Yule akamsalimia Erica, Erica alimtazama na
kumuona ni Dora, kumbe alikuwa miongoni mwa wale watu kwenye ile kampuni, Dora
alipomuona Erica tu akaona sasa hapa itakuwa shida kupata nafasi maana alijua ni
jinsi gani Erica alimchukia. Dora kabla ya salamu alimfata Erica na
kumwambia, “Erica nakuomba jusitukatalie hili sababu na mimi nipo, Erica
ni kazi hii wenzio yani hapa ndio pananifanya niendelee kuishi, nakuomba
Erica” Dora akapiga na magoti na kumfanya Yule mwenzie aliyeambatana nae
amshangae, Erica alisimama na kumshika mkono Dora akimsimamisha kisha
akamkumbatia na kumwambia, “Nishakusamehe, huna sababu ya kupiga magoti
kwangu” Dora alionekana kufurahi sana, hata Yule mwenzao alipotoa kwa
bosi alishangaa kumuona Dora akifurahi sana ingawa yeye akutoka na furaha, Erica
akamuuliza imekuwaje, “Bosi kasema hakuna nafasi ya kuongea na watu
wake” “Aaah msijali, nitaongea nae na nitawapigia simu” Kwahiyo
wakamuachia Erica namba za simu na kuagana nae pale. Muda wa kuondoka,
Erica alienda kumuaga shemeji yake na kumwambia kuhusu wale watu kuja kuzungumza
nao, “Sasa Erica mimi nimeshindwa kupanga ratiba, labda upange
wewe” “Nitapanga basi bosi” “Aaah Erica jamani, sitaki unite
bosi. Acha hilo jina tafadhali” “Sawa” Kisha James akampa Erica
alfu ishirini kwaajili ya nauli ya siku hiyo, Erica alikataa ila James
alimsisitiza achukue kwahiyo alichukua na kuondoka
zake. Alirudi nyumbani kwao, akamkuta mama yake na
kumsalimia, “Ila leo umewahi kurudi?” “Nimerudi na bodaboda
mama” “Yani kuanza kazi tu ushaanza kukodi pikipiki za kukurudisha
nyumbani!” “Hapana mama, shemeji alinipa nauli ndio nikapanda
pikipiki” “Mmmh ameanza kukupa nauli? Sisemi kwa ubaya Erica, ila kuwa
makini sana na shemeji yako” “Nimekuelewa mama” Erica aliingia
chumbani kwake ila hakudhania kama kuna tatizo litatokea baina yake na shemeji
yake kwani kwa kipindi hiko hakutaka kujihusisha na maswala ya mapenzi kabisa,
aliona kuzungumza na Erick pekee inatosha, na siku hiyo kabla ya kulala
alimtafuta hewani na kuzungumza nae, “Tena Erica, kuna kitu nilikuwa
nawaza. Kwakweli natamani sana kuwa na mtoto, usingetoa ile mimba yangu saivi
mtoto wetu angekuwa mkubwa sana. Basi Erica naomba nitakaporudi tuzae, usitoe
tena mimba yangu” “Mmmh kabla ya ndoa hapana kwakweli” “Nitakuoa
Erica, nakupenda ujue ila tuzae kwanza. Nakuomba
tafadhali” “Tutajadiliana hilo, usijali” Walijadiliana mambo
mbalimbali kisha kuagana usiku mwema na Erica kulala, hakutaka kumwambia ukweli
Erick kuwa yeye tayari ana mtoto, swala hilo lilimuuma ila hakujua ni jinsi gani
angemwambia Erick. Kesho yake alienda kazini kama kawaida, na shemeji
yake kumkabidhi funguo za lile gari la dada yake kuwa awe anaenda na gari lile
ofisini, ila Erica alikuwa akienda bila gari kwani alijua angezua maswali mengi
sana kwa mama yake. Ile wiki yote aliimaliza kwa kutokwenda na gari kabisa, na
kila siku alimpa visingizio shemeji yake vya kwanini hakwenda na
gari. Ilikuwa ni Jumamosi asubuhi, Erica akapigiwa simu na
namba ngeni akapokea, Yule mpigaji alijitambulisha kuwa ni Moses na kuanza
kumkumbusha Erica walipokutana hadi Erica akakumbuka. “Naomba leo uje
ofisini kwetu” “Ila bado sina pesa ya kuja kununulia nguo au vifaa vya
kuchezea mtoto” “Hapana, sikuiti kwaajili ya kununua nguo au vifaa ila
kuna jambo lingine la muhimu sana nakuitia, naomba uje na mtoto
wako” Erica aliongea na Yule mtu na kukubaliana nae kuwa atakwenda,
baada ya kukata simu aliwaza kuwa atatokaje pale kwao na mtoto wake? Wakati
anawaza hayo, mama yake alimuita, “Erica, wiki nzima umefanya nishinde
nyumbani hapa na mtoto, ni wakati sasa wa kutafuta mdada wa kazi. Leo natoka,
naenda kukutana na wamama wenzangu maana wiki yote sijaonana nao” Erica
alimuitikia haraka mama yake kwani alijua akitoka tu, itakuwa rahisi kwake
kutoka pia. Na kweli mama yake alivyotoka tu, alijiandaa na kumuandaa
mtoto wake kisha akaita gari ya kukodi na kuondoka zake, alitamani aondoke na
gari ya dada yake ila aliwaza mtoto atamuwekaje kwenye gari ukizingatia hakuwa
na kiti cha kupanda na mtoto kwenye gari, halafu mtoto mwenyewe alikuwa na
utundu wa kimya kimya. Erica alifika kwenye duka la kina Moses na
kushangaa duka lilikuwa kubwa sana, na alipofika tu Moses alimsalimia na kumdaka
mtoto wa Erica huku akiita wenzie, “Njooni mmuone sasa mtoto huyu alivyo
mzuri” Wenzie wote walifika na kumbeba beba Angel huku wakimbusu na
kusifia kuwa ni mzuri sana, Moses alianza kuongea na Erica, “Kwanza
kabisa hongera kwa kupata mtoto mzuri hivi, yani ndoto zetu tulihitaji kupata
mtoto awe balozi wa bidhaa zetu na siku niliyokuona na mtoto wako nilivutiwa nae
sana, nimekuja kuwasilisha swala hilo kwa wenzangu waliafikiana na mimi na ndio
leo naona kila mmoja hana la kusema kwa uzuri wa mtoto huyu. Sasa upo tayari
tusaini mikataba mtoto wako awe balozi wetu?” Erica alikaa tu kimya
kwani kama alipigwa na bumbuwazi hivi kwa mwanae kupata ubalozi ikiwa si mtoto
wa mtu maarufu wala nini ila alipendwa tu, wakati amekaa kimya kwa muda akasikia
sauti ya mdada, “Kheee mtoto mzuri hivi, mamake yuko
wapi?” Erica akageuka kumuangalia mdada huyo, macho yake yakagongana na
Tumaini, ambaye ni dada wa Erick. Erica alikaa tu
kimya kwani kama alipigwa na bumbuwazi hivi kwa mwanae kupata ubalozi ikiwa si
mtoto wa mtu maarufu wala nini ila alipendwa tu, wakati amekaa kimya kwa muda
akasikia sauti ya mdada, “Kheee mtoto mzuri hivi, mamake yuko
wapi?” Erica akageuka kumuangalia mdada huyo, macho yake yakagongana na
Tumaini, ambaye ni dada wa Erick. Tumaini alipomuona Erica alimsogelea
kwa tabasamu zito na kumkumbatia, “Jamani Erica, za siku” Kabla
Erica hajajibu, Yule Moses akamwambia Tumaini, “Huyu sasa ndio mama wa
Yule Malaika mzuri unayemuona pale” Tumaini alimuangalia mara mbili
mbili Erica bila ya kummaliza maana alikuwa akishangaa na kupigwa na bumbuwazi
kidogo, ila Moses alikatisha ule mshangao wao na kumwambia Erica atoe maamuzi ya
kusaini mkataba kwao ili mtoto wake awe balozi, Tumaini akasema “Kabla
ya yote, naomba kwanza niongee na huyu mdada halafu atakuja kumalizana
nanyi” Tumaini akatoka nje na Erica, ambapo mtoto wa Erica
aling’ang’ania kubembwa kwahiyo ikabidi Erica amnyanyue mtoto wake na kuongozana
na Tumaini na kwenda kusimama mahali ili waongee. Tumaini alianza kumuuliza
Erica, “Umempata lini huyu mtoto Erica? Ina maana siku ile nilipokuja
kwenu ulikuwa tayari na mtoto?” “Ndio” “Mbona ni msiri kiasi
hiko Erica? Ndiomana hukutaka kunitafuta hewani kabisa, siku zote ukafanya
nipate lawama kwa Erick sababu yako kumbe tayari una mtoto!” Erica
alikaa kimya tu kwani alijihisi aibu na hata hakujua aseme kitu gani, Tumaini
aliendelea kuongea, “Je Erick anajua kuwa una
mtoto?” “Hapana” “Erica, unajua wewe ni muuwaji eeh! Hivi unajua
ni kiasi gani Erick anakupenda? Unashindwa kumwambia swala kama hili ili mwenzio
asonge mbele maana anakaa kukufikiria wewe kumbe tayari ulishazaa na mwanaume
mwingine” “Ni bahati mbaya Tumaini” “Bahati mbaya? Kwahiyo
ulibakwa? Kuna mapenzi huwa yanafanywa kwa bahati mbaya Erica? Ama kweli
unamuumiza kaka yangu, sasa Erica naomba swala hili la wewe kuwa na mtoto
umwambie mwenyewe, mimi sitasema ila umwambie mwenyewe” “Naogopa
nitamuumiza” “Kama unaogopa kumuumiza basi mwambie, maana unavyokaa
hivyo bila kumwambia ndio unamuumiza maradufu. Mwambie mapema ili ajue
anajipangaje, mimi sitasema huu ujinga wako ila wewe useme
mwenyewe” “Tumaini jamani nisamehe” “Nikusamehe nini sasa mimi?
Kuna ulichonikosea? Hakuna, ila umemkosea Erick, naomba umweleze ukweli wa mambo
ili mdogo wangu awe na maamuzi kama kusuka au kunyoa” “Sawa, basi
nitamwambia” “Nakujua vizuri Erica, binti cha uongo. Umesema hivyo
kuniridhisha tu, sasa naomba usikubali kusaini mkataba wa mwanao kuwa balozi
hadi pale utakapokuwa umemueleza ukweli Erick” “Sasa mimi nitaondokaje
hapa bila kusaini? Si itaonyesha nimekataa jamani?” “Erica, waambie kuwa
unaenda kufikiria kwanza. Sitaki usaini na ukiwa mbishi hata huo ubalozi mwanao
ataukosa kabisa, sijapendezewa na ulichofanya, sijapendezewa kabisa. Jitahidi
umwambie ukweli Erick” Erica alikubali kuwa atamwambia ukweli Erick,
kwahiyo aliingia tena dukani na kuwaomba mkataba asaini siku nyingine kisha
akaondoka zake. Hakuna aliyeelewa kuwa Tumaini alikuwa akiongea nini na
Erica ila walishangaa tu Erica akiwaambia kuwa mkataba atasaini siku nyingine,
mpaka akajifikirie kwanza wakati kiukweli kwa Erica wala halikuwa swala la
kujifikiria. Erica alirudi nyumbani na mwanae, tena kwa bahati
alikuta mama yake bado hajarudi maana angemkuta amerudi sijui angemueleza nini
amuelewe. Alitulia akitafakari kuwa ni namna gani atamueleza Eick, alitamani
sana ubalozi kwa mwanae ila je atatumia njia gani kumueleza Erick kuwa ana
mtoto? Alijikuta akiwaza sana bila ya jibu, hata hakujua aanzie wapi na aishie
wapi, aliwaza sana hadi kujikuta usingizi ukimpitia akiwa pale sebleni na
mwanae. Mama yake alifika na kumshtua, “Wewe Erica vipi? Kazi
ndio kwanza wiki ya kwanza, ndio unashikwa na uchovu kiasi hiko!” “Hamna
mama” “Halafu mbona inaonyesha kama mlitoka hivi!!” “Hamna mama,
tulikuwa hapa hapa nyumbani” “Haya, ila swala la kutafuta mdada wa kazi
ulifikirie na kulipa kipaumbele” Erica aliinuka muda huu na kwenda
chumbani kwake kumlaza mwanae nay eye kupumzika vizuri, aliwaza kuhusu maneno ya
mama yake, “Mama anaona sifai kufanya kazi kwa shemeji wakati huo huo
anahitaji nitafute msichana wa kazi, jamani nitamlipa nini sasa nisipokazana na
kazi?” Aliwaza ila alijua wazi kwa wakati huo hakuwa na uchaguzi wa aina
yoyot, aliamua tu kulala na mwanae. Aliamshwa na simu ya Erick na
kupokea kwa kuanza kumsalimia, “Erica, nimekumiss sana mpenzi
wangu:” “Hata mimi nimekumiss” “Sijui lini nirudi ili
tufanikishe swala letu la kuwa na mtoto” Hapo kidogo moyo wa Erica
ulisizi kwani alihisi kama akishindwa kuendelea kuongea zaidi na Erick kwani
hakujisikia kabisa kumueleza ukweli, aliamua kukatisha maongezi na kusema
anaenda kuoga atampigia akitoka. Alipokata alijitafakari
sana, “Hivi nitawezaje kumwambia Erick kuwa nina mtoto? Na je Erick
atalichukuliaje hilo swala? Sitaumiza moyo wa Erick kweli? Sitaki aumie kama
mimi nilivyoumia” Alishindwa kuongea nae kabisa na hakuweza tena
kumpigia simu. Siku ya kwenda kazini tena alijiandaa na
kuondoka ila aliogopa kuchukua lile gari la dada yake, alipofika tu ofisini
kwenye mida ya saa nne bosi wake alimuita, “Erica, unajua sikuelewi yani
gari nimekupa ila bado unakuja kwa daladala na kila siku unanipa visingizio
nisivyovielewa kabisa, mara leo nimechelewa nikaona nisije na gari sijui leo
imefanyaje. Kwani tatizo ni nini Erica?” “Ngoja nikwambie ukweli, sijui
kuendesha” “Kumbe ni hivyo tu jamani! Si ungeniambia mapema, basi
nitakupa pesa uende kusomea udereva. Kwahiyo utakuwa unawahi kutoka
ukasome” Erica aliitikia tu, kiukweli kuendesha alijua sema hakuwa na
leseni tu na hiyo haikuwa sababu sana ya yeye kutokwenda kazini na gari ila
alimuogopa mama yake, kwahiyo akaendelea na kazi zake zingine. Jioni
ilipofika, shemeji yake alimuita tena na kumkabidhi laki tatu kuwa akasomee
udereva, “Hapana shemeji usinipe pesa, nitasoma nikipata
mshahara” “Hapana Erica, nishakwambia usiniite shemeji. Naomba upokee
hii pesa na ukasome udereva, sikupangii pa kwenda kusoma ila wewe tafuta sehemu
yoyote ukasome, na pesa isipotosha njoo uchukue nyingine” Erica
alijijkuta yupo mtegoni tu, na kuchukua ile pesa kisha kuondoka
zake. “Kwahiyo nikatafute mahali pa kusomea udereva” “Kesho
usije ofisini, nenda katafute mahali kisha utakuwa unaenda ukitoka kazini.
Nitakuwa nakuruhusu mapema tu, najua ndani ya wiki mbili utakuwa tayari
umemaliza, na swala la leseni, kesho kutwa nitamuita mwenzangu wa TRA hapa na
atakupa mlolongo wote kisha ataenda kukutengenezea leseni” Erica hakuwa
na jibu la kumpa shemeji yake zaidi ya kukubaliana na kile alichokuwa akisema,
kisha James akaendelea kuongea, “Sina nia yoyote mbaya na wewe Erica,
nadhani bado huamini kama nimeachana nay ale mambo. Nafanya hivi kwa upendo kwa
mdogo wa mke wangu ambaye ni mdogo wangu pia, sitaki uteseke. Hujui tu ni jinsi
gani nimeumia alivyonieleza dadako kuhusu baba wa mtoto wako, nakuhurumia sana
Erica na sitaki ujione kama ni mwenye makosa sana duniani kwahiyo sifanyi vitu
kukuweka kwenye mitego yangu au nini, nafanya kwa upendo tu ndiomana nimekwambia
utafute mwenyewe sehemu ya kusomea udereva, hata usiniambie ni wapi ila nitakuwa
nakupa ruhusa uende kusoma” “Sawa nimekuelewa shemeji” “Jamani
Erica kila siku nakwambia usiniite shemeji” “Unadhani nitakuitaje?
Nakuheshimu na siwezi kukuita jina lako” “Hata kama ila hakuna tatizo,
usinifikirie vibaya Erica, hata sina nia mbaya na wewe” James aliongea
kama mtu aliyekuwa akijutia sana makosa yake, hivyo Erica alikubaliana nae na
kwenda kuendelea na kazi. Aliporudi kwenye kazi zake akakumbuka
kuwaandalia ratiba wale wakina Dora kuhusu kuja kuzungumzia bidhaa zao, kwahiyo
aliangalia namba zao na kupiga kuwa kashawaandalia barua ya ratiba waende
kuchukua. Baada kama ya lisaa limoja, Dora alikuwa mahali pale kuchukua
barua kutoka kwa Erica alisalimiana nae vizuri sana kisha Erica akampa ile barua
ila kiukweli Erica hakutaka ukaribu wa haswaa na Dora ila kwa Dora ilikuwa
tofauti maana alionyesha kutaka ukaribu zaidi na Erica. “Erica hongera
sana rafiki yangu, umepata kazi sehemu nzuri sana, nani
alikuunganishia?” “Kwanini umeniuliza hivyo?” “Na mimi Erica,
kama kuna aliyekuunganishia na mimi nahitaji” “Hakuna aliyeniunganishia,
mimi nilituma maombi ya kazi tu na kupata” “Basi na mimi nilete maombi
yangu ya kazi, na ukisikia kama kuna nafasi ya kazi uniambie Erica, tafadhali
maisha ni kusaidiana” “Leo ndio unalijua hilo?” “Erica, ulisema
tusahau yote yaliyopita na tuanze mapya” “Haya
yameisha” “Nashukuru Erica, kwaheri eeh!” Dora akaaga na
kuondoka, Erica alikuwa akiongea na Dora ilimradi tu maana alishamwambia kuwa
amemsamehe kwahiyo hakuona kama ni swala zuri kutokuongea vizuri na
Dora. Alipomaliza kazi zake kama kawaida, alienda kumuaga shemeji yake
na kukumbushwa swala la kesho yake kutafuta sehemu atakayo somea
udereva. Kwahiyo Erica aliondoka na kwenda kupanda daladala ili kuelekea
nyumbani kwao, alipokuwa kwenye daladala ile wakati akiwa na uchovu uchovu
sababu ya kukaa kwenye kompyuta kwa muda mwingi, alijikuta tu akisinzia kwenye
kiti cha daladala , mara akashtuliwa na mkaka mmoja aliyekuwa pembeni
yake, “Pole sana dada, inaonyesha umechoka
sana” “Asante” “Samahani dada yangu unaitwa
nani?” “Naitwa Erica” “Basi mimi naitwa Juma, nimefurahi
kukufahamu. Napenda tuwe marafiki, naomba namba zako” “Umesema unaitwa
nani?” “Naitwa Juma” “Namba zangu za nini?” “Nahitaji
tuwe tunawasiliana Erica” “Unikome tena unikome kabisa, sipendi mazoea
ya kijinga. Nikome, sihitaji kuzoeana na wewe” Huyu kaka alimshangaa
sana Erica kuwa ana tatizo gani maana kamjibu kwa hasira utafikiri kuna jambo
baya amemwambia, hadi mkaka wa watu akajihisi vibaya kuwa pale hajamtongoza je
akimtongoza itakuwaje? Alibaki akimshangaa kisha akamwambia, “Kwani dada
tatizo ni nini? Kufahamiana na mtu ni tatizo? Kama hutaki kunipa namba yako si
ungesema tu sitaki kuliko kuanza na mada za unikome sijui nini na nini
jamani?” “Tena usinizoee wala usiendelee kuniongelesha, kwenye daladala
yote hujaona wadada wa kuwasemesha zaidi yangu? Sitaki mazoea” Huyu kaka
alimshangaa sana Erica ila ilibidi awe mpole tu na kumwambia kwa
upole, “Binadamu hatwendi hivyo Erica, unaweza ukaanguka nikakuinua au
mimi nikaanguka ukaniinua. Binadamu hatujibishani vibaya” “Sikia wewe,
sijui Juma sikia nikwambie yani mimi hata ukiniona nakufa hapo niache nife ila
mazoea na wewe sitaki” “Kwanini umekuwa mkali hivyo dada?” “Nyie
wanaume ni watiu wabaya sana, yani hapo utakuwa unajiongelesha sijui namba yako
namba yako ila lengo lako ni kunitongoza. Nishakwambia naitwa Erica, na wewe
Juma umeona kabisa itikadi zetu hazifanani ila unakazana kutaka namba yangu.
Unanitakia nini mimi? Sitaki yani sitaki kabisa, mwisho wa siku ndio uniambie
badili dini nikuoe, nikisema nipo tayari ulete propaganda zingine, sitaki na
usiniongeleshe tena” Kituo kilichofuata Erica alishuka sio kwamba
alifika ila hakutaka kuendelea kuongea na huyu Juma ndiomana alishuka kituo
ambacho sio chake. Kisha alipanda daladala nyingine na kwenda hadi kituo
chake akashuka na kuelekea nyumbani. Alifika nyumbani, ila
alipokaa na kutafakari kuhusu alichomjibu Yule mkaka wa kwenye daladala aliona
yupo sawa kabisa, “Yani wanaume wana mazoea ya kijinga kabisa, sitaki
mazoea na mtu yeyote yule” Mama yake alimsikia na kumuuliza kuwa tatizo
ni nini, alimueleza mama yake kuhusu mkaka aliyemuongelesha kwenye daladala na
jinsi alivyomjibu, alijua mama yake angempongeza maana mama yake alikuwa akitaka
mwanae asiwe karibu na wanaume, ila mama yake hakumpongeza kabisa kwa kitendo
kile, “Erica mwanangu, sivyo nilivyokufundisha hivyo. Jifunze kuwa na
kauli nzuri kwa watu” “Sasa mama alitaka namba yangu ya nini kama sio
kunitongoza, anajijua kabisa yeye ni Mwislamu na mie ni Mkristo sasa alitaka
namba yangu ya nini?” “Dini sio tatizo, ila tatizo ni utu na ustaarabu.
Mtu unamjibu vibaya, hivi leo na kesho ukakutana nae mahali halafu ndio wa
kukusaidia unadhani atakusaidia?Huwezi jua mtu huyo utakutana nae wapi
tena” “Hahaha, hujamuona mtu mwenyewe mama. Kwa msaada gani alionao Yule
mtu? Hakuna lolote, hawezi kunisaidia chochote. Na siwezi kuhitaji msaada
wake” “Usimdharau usiyemjua Erica” “Hujamuona mtu mwenyewe mama,
anachekesha balaa” “Watu hatuendi hivyo Erica, huwezi kumuhukumu mtu kwa
kosa la mtu mwingine, si mkaka wa watu alikutuma uzae na huyo mwarabu wako.
Usipeleke hasira zako kwa watu wasikuwa na hatia, jifunze kauli mwanangu,
hatakama mtu humtaki hutakiwi kuongea nae kwa ukali. Mwambie kwa ustaarabu, nina
mume wangu siwezi kutoa namba yangu, basi ukiona huwezi kumpa namba yako na sio
kumjibu vibaya” “Sawa mama nimekuelewa” Alimuitikia mama yake na
kuinuka kwenda chumbani ila kuikweli yale maneno ya mama yake hayakumuingia
akilini hata kidogo maana yeye aliwaza kuwa njia pekee ya kuwakwepa wanaume ni
kuwajibu vibaya, kila alipofikiria mapito yake aliona ni vyema kuwajibu
vibaya. Kesho yake Erica alijiandaa kwaajili ya kwenda
kumtafutia mwanae nguo maana hakuona umuhimu wa kutafuta chuo cha udereva sababu
tayari alijua kuendesha kwahiyo zile hela aliona ni vyema akamnunulie mwanae
nguo, kwahiyo akajiandaa na kuondoka zake hata mama yake hakumwambia kama siku
hiyo haendi kazini maana alijua kuwa mama yake angekuwa na maswali mengi
sana. Alifika kwenye duka la nguo za watoto na kununua nguo baadhi
kwaajili ya mtoto wake, ila hakutaka kwenda kwenye lile duka la Moses maana
hakuwa tayari kumjibu maswali yoyote Tumaini. Wakati anatoka kwenye lile
duka, alishikwa bega kugeuka alimuona Fetty. Alikumbatiana nae kwa furaha maana
ni siku nyingi hakuonana nae, toka siku ya mimba. “Jamani Fetty, toka
siku ile ukapotea! Ulikuwa wapi?” “Nisamehe Erica, kwanza umejifungua
mtoto gani?” “Mtoto wa kike” “Hongera sana, anaitwa
nani?” “Anaitwa Angel, na wewe ulikuwa wapi kipindi chote hiko hata kuja
kuniona jamani! “Erica, acha tu maisha haya ni kizunguzungu haswaaa.
Yani mwenzio nilipatwa na majanga balaa, mapenzi haya yani acha
tu” “Yamekufanyaje tena?” “Ni historia ndefu ndugu
yangu” “Niambie hata kwa kifupi” “Nilipata mwanaume wa kuishi
nae, nikasafiri nae na kwenda Iringa. Ila yani alichonitenda Yule bwana sitakuja
kusahau kamwe, hebu fikiria nimezaa nae mtoto mmoja, eti gafla kasema ndugu zake
hawako tayari aoane na mimi kisa yeye Mkristo na mimi ni Mwislamu unajua
kanitimua kwake nikiwa sijielewi hata pa kwenda! Nashukuru Mungu nilikuwa
nafanya kazi ndio kitu kilichonisaidia, na nimeomba uhamisho na kurudi hapa Dar.
Sina hamu na wanaume” “Mmmh pole sana, sasa wanaume gani wazuri?
Wakristo au Waislamu?” “Wote wabaya ndugu yangu yani mwanaume huwa
anokoteza tu sababu na mimi nina mkosi kwakweli natongozwa na Wakristo tu,
nawachukia balaa” “Hata mimi nina mkosi sio peke yako, natongozwa na
Waislamu tu” “Mmmh hadi baba Angel sio Mkristo mwenzio?” “Sio
mwenzangu, nina mkosi tu” “Ila tusijiombee mikosi, sidhani kama dini ni
tatizo ila tunaokutana nao ndio tatizo ndugu yangu. Nitakuja kwenu tuongee
vizuri” Erica akafurahiana pale na Fetty kisha kuagana nae na kurudi
nyumbani kwao. Alirudi na zile nguo alizomnunulia mwanae, mama yake
akamuona na kuuliza, “Erica, hata mwisho wa mwezi haujafika, hizo hela
za kumnunulia mtoto nguo nzuri hivi umetoa wapi?” “Jamani mama, kwani
mimi sina hela?” “Kumbuka, ulikuwa ukilalamika umeishiwa hadi huruma.
Haya nguo hizi umezitoa wapi?” “Mama, kuna siku nilipata daladala na
walimpenda sana Angel, wamesema wanahitaji Angel awe balozi wa nguo za watoto
ndio leo wamenipigia simu nikachukue nguo hizi” Mama yake akafurahi sana
na kuona mtoto wake ana bahati, “Unaona sasa, mara nyingine ni vizuri
kupanda kwenye usafiri wa jumuiya maana unaonekana” Erica akacheka tu
maana tayari alishamdanganya mama yake. Kulipokucha alijiandaa
kwenda kazini, na kwenda kama kawaida kisha akaanza kufanya kazi zake, muda
kidogo James alitoka ofisini kwake na kwenda kumsalimia Erica, “Vipi
ulipata chuo?” “Nilipata ndio” “Basi vizuri, nishaongea na jamaa
wa TRA nadhani atafika muda sio mrefu na atakusaidia kuhusu swala la kupata
leseni” “Haya, asante” James alitoka nje huku Erica akiendelea
na kazi zake, muda kidogo Erica alipigiwa simu na James kuwa atoke nje
akatambulishwe huyo jamaa wa TRA ambaye ndio atamsaidia. Erica aliacha
shughuli zake na kutoka nje, kufika alipo James ndio akashtuka kuona jamaa
mwenyewe ni Yule Juma aliyekutana nae kwenye daladala juzi na akamjibu
vibaya. James alitoka nje huku Erica akiendelea na
kazi zake, muda kidogo Erica alipigiwa simu na James kuwa atoke nje
akatambulishwe huyo jamaa wa TRA ambaye ndio atamsaidia. Erica aliacha
shughuli zake na kutoka nje, kufika alipo James ndio akashtuka kuona jamaa
mwenyewe ni Yule Juma aliyekutana nae kwenye daladala juzi na akamjibu
vibaya. James alimuona Erica alivyosimama na kusita, kwahiyo
akamuita, “Erica, vipi mbona umeganda gafla?” Erica akasogea ila
alikuwa na hofu kupindukia, kisha James akaanza kutambulisha, “Erica,
huyu ni jamaa yangu wa TRA ambaye niliyesema nitaongea nae maswala ya leseni
anaitwa Juma. Ndugu yangu Juma, huyu anaitwa Erica, ni mfanyakazi wangu nan i
shemeji yangu ndiomana nahitaji umfanyie swala la leseni haraka
haraka” Juma alinyoosha mkono kama ishara ya kusalimiana na kufahamiana
na Erica, Erica nae alinyoosha mkono pia na kumpatia ila aligubikwa na aibu ya
hali ya juu kwani hakufikiria kama Yule Juma ndiye mtu wa kumsaidia, akakumbuka
hadi maneno ya mama yake kuwa huwezi jua utakutana wapi na mtu huyo na
atakusaidia nini, alibaki tu kumuangalia Juma kwa aibu na kushindwa hata kusema
nae chochote, basi James akamwambia, “Nenda pale ofisini kwako, kakae na
Juma akuelekeze vitu vinavyotakiwa, mimi natoka kidogo. (Kisha akamuangalia Juma
na kumwambia) Kwa swala lolote la hela, njoo kwangu.” Kisha James
akaondoka zke na kumuacha Erica akiongozana na yule Juma hadi
ofisini. Kwakweli Erica alikuwa akisikiliza tu kile Juma alichomwambia
na alichoagizwa na Juma ndio alichokifanya kwa wakati huo, kisha Juma
alivyomaliza alimwambia Erica aandike namba yake na aliandika bila pingamizi na
kumuga huku akimwambia, “Naomba tusahau yote yaliyopita,
nisamehe” “Usijali” Juma akaondoka zake, kwakweli hii haikuwa
siku ya furaha kwa Erica maana alihisi kudhalilika vibaya
mno. Kwenye mida ya saa kumi jioni, James alimuita Erica na
kumpa ruhusa ya kuondoka, “Yani hata hukumbuki kuwa unatakiwa kwenda
chuo?” “Nilisahau” “Hebu acha mawazo Erica, fikiria maendeleo
yako tu kwasasa, acha mawazo ya kijinga hayo mdogo wangu” Muda huu Erica
alijisikia vizuri sana kuitwa mdogo wangu na James, basi akamuaga pale na
kuondoka zake. Alienda kupanda daladala, ila leo kuna wakaka walikaa
pembeni yake na akasikia maongezi yao, “Yani mademu hawa vimeo vimeo,
kuna demu nimekutana nae, ukimuona ni staarabu kumbe ni mbwa tu” “Yule
wa siku ile? Nilikwambia lakini jomba hukunisikia, uliona kama nakuonea wivu
ndugu yangu, Yule demu jau yani kimeo cha mwisho” “Najuta hata
kutokufuata ushauri wako, ila mimi nikija kupata demu mwenye upendo wa dhati
hakika nitatulia” “Upendo wa mademu upo kwenye hela, yani ukiwa na pesa
utapendwa wewe balaa ila uwe kapuku sasa utajuta yani mademu kwa pesa huwawezi
ndiomana mimi sina demu wa kudumu huwa natembea nao na kuwaacha” Erica
aliwasikiliza mpaka alipofika kwenye kituo chake na kushuka ila kwa maongezi
yale aliyoyasikia aliona kuwa wanaume wanapenda kuchezea wanawake wakati hata
wao walikuwa wanalalamika kuwa wanawake wana matatizo. Alifika nyumbani
kwao na kumsimulia mama yake kuwa Yule mtu alifika ofisini kwao, ila hakumwambia
kilichomnfikisha pale Yule mtu, “Kumbe ni rafiki wa shemeji bhana Yule
mkaka” “Kheee mwanangu ila nilikwambia, kuwa makini na majibu sio kila
kitu ni kujibu vibaya” “Ila mama kama mtu anakutongoza na
humtaki?” “Si nishakwambia, mjibu kiustaarabu kwani ukisema hapana
sitaki kuna tatizo gani? Sio unaanza ooh wewe sijui dini nyingine, kimeenda
kimerudi sasa ndio nini hapo? Unatakiwa kuwa na jibu moja
linaloeleweka” “Sawa mama nimekuelewa na sitorudia tena mama
yangu” “Ndio usirudie, unanidhalilisha mimi ukifanya
ujinga” Erica aliinuka na kwenda chumbani haraka haraka maana alijua
pengine mama yake angemuuliza kuwa mbona kawahi kurudi. Alikaa chumbani
ila wazo la Erick lilimjia kichwani na wakati akimfikiria Erick alipigiwa simu
muda huo huo na Erick, kwakweli Erica akatabasamu na kuona ni jinsi gani upendo
kati yake na Erick ulivyo mkubwa kiasi kwamba hata Erick anamuwaza vile vile na
yeye anavyomuwaza, Erica akapokea ile simu “Mbona kimya mpenzi wangu
hukunitafuta tena?” “Siku hizi nimeanza kazi Erick, kwahiyo narudi
nyumbani nikiwa nimechoka balaa ila nakukumbuka sana tu, yani hata muda huu
nimetoka kukukumbuka” “Vipi facebook siku hizi
hutumii?” “Natumia” “Mbona huwa sikuoni?” Erica
akakumbuka kuwa alifuta urafiki na erick maana hakutaka kumkwaza Rahim,
alimwambia Erick, “Labda nilitoa urafiki kwa bahati mbaya, ngoja
nikuombe tena urafiki ili tuwe tunawasiliana” “Sawa” Erica
alikata simu na kwa mara hii akachukua ile simu yake na kuingia kwenye mtandao
ingawa kwa siku hizo hakupenda kuingia kwani kila alipomuona Rahim alihisi
kuumia sana, na leo alikuta Rahim yupo hewani vizuri kabisa ila hakutumiwa
ujumbe wowote na Rahim, akamtumia Erick ombi la urafiki na Erick alilikubali
muda ule ule na kuanza kuwasiliana nae kwenye mtandao sasa, “Ila Erick,
muda sio mrefu nitalala, maana nimechoka” “Sawa Erica, ila nakumiss sana
na ninatamani siku moja tuishi wote. Subiri tu nirudi kutoka Kusini, ila
usinisaliti Erica” Kidogo Erica alisita kujibu maana kama usaliti
kashaufanya sana tu mpaka na mtoto kapata, ila akamjibu kuwa asijali
hatomsaliti, bado hakuweza kumwambia Erick kuhusu mtoto aliyekuwa nae maana
alihisi kama upendo juu yake utapungua. Akamuaga Erick kuwa muda huo
analala, ila kabla hajatoka hewani alishangaa ujumbe kuingia kutoka kwa Rahim,
akaufungua na kuusoma, “Kweli mwenye asili haachi asili, kwahiyo
umemtafuta Erick hadi kuanza tena urafiki nae? Nashukuru Erica, hela zote
nilizokuwa nakupa ni kazi bure” Erica alisoma mara mbili mbili ujumbe wa
Rahim bila hata kuelewa kuwa Rahim amejuaje kuwa yeye na Erick wameanza urafiki
tena, ila akakumbuka kuwa facebook ina mtindo wa kuandika Fulani na Fulani
wamekuwa marafiki, kwahiyo inamaana labda Rahim kaona ujumbe huo ndio kajua kuwa
Erica na Erick wamekuwa marafiki tena. Erica hakujua ajibu nini kwahiyo
alipotezea huo ujumbe na kulala tu. Kulipokucha akajiandaa na
kwenda ofisini kama kawaida, leo akiwa ofisini akapigiwa simu na Yule Moses
mwenye duka la vitu vya watoto na nguo. “Erica, mbona unaniangusha
jamani, hujaipenda ofa yangu? Mpe mtoto nafasi hiyo huwezi jua atakuwa nani
ukubwani? Naomba ukubali Erica, mwanao awe balozi wa bidhaa zetu, inamaana bado
hujafanya maamuzi?” Erica akawaza kwa muda kuwa ajibuje kwani kiukweli
alikuwa akihitaji sana tu ila sharti alilopewa na Tumaini ndio lilikuwa gumu
sana kwake, ila Yule Moses alimuuliza tena, “Mbona kimya
Erica?” “Nimekubali” “Wow, lini sasa utakuja kusaini mkataba
wetu kisha mwanao aanze kuonekana kwenye matangazo yetu?” Erica
alitamani kuulizia kuwa Tumaini ni nani kwenye lile duka ila hakuweza kuulizia
na akawaahidi kwenda kesho yake na mtoto, aliona ni rahisi kwake sababu ni siku
yake ya kwenda kliniki. Alikubaliana nae hivyo na Moses alionyesha
kufurahishwa sana na swala hilo. Kisha Erica alipomaliza kazi zake, kama
kawaida akaenda kumuomba ruhusa bosi wake na kumwambia kuwa kesho atampeleka
mtoto kliniki kwahiyo hatoweza kufika kazini, “Hakuna tatizo Erica, yani
wewe ukiwa na swala lolote lile usisite kuniambia, sawa
eeh!” “Sawa” Kisha Erica akataka kuondoka ila James alimzuia
kidogo na kumpa laki moja ambayo Erica alikuwa akiikataa, “Hapana Erica,
pokea pesa hii itakusaidia kesho kumpeleka mtoto kliniki. Naelewa shida
unayopitia Erica, inaniumiza sana kuona kuna mwanaume mwenye miguu miwili kama
mimi na mwenye ufahamu kama mimi ila kaumiza moyo wako, inaniuma sana. Naomba
pokea hii pesa, si kwaajili yako ila ni kwaajili ya Angel” Erica
alipokea ile hela na kumshukuru pale kisha kuondoka zake na kurudi nyumbani
kwao. Leo mama yake alimuuliza kuwa mbona karudi mapema, “Kesho
nampeleka Angel kliniki kwahiyo nimeomba ruhusa mapema kwaajili ya
maandalizi” “Kheee makubwa, kuna maandalizi ya kumpeleka mtoto
kliniki!” “Si kama kutafuta kadi lake mama” “Haya nimekubali ila
kishingo upande” “Sasa mama unafikiria ni nini?” “Hakuna
kitu” Leo Erica alifanya mambo yake mengine yote ila hakuingia kwenye
mtandao kabisa, hadi saa ya kulala alimchukua tu mwanae na kumlaza pembeni
yake. Kesho yake alijiandaa na kutoka na mwanae, sababu hela
alikuwa nayo hakuona tatizo la kukodi gari la kumpeleka kliniki, wakati anatoka
kliniki na siku hiyo akagongana tena na Salma ila leo Salma alimpa Erica msonyo
huo uliomuacha mdomo wazi kisha akasema, “Najua umezaa na Rahim, hata
ufiche vipi mi naujua ukweli. Ila ngoja nikwambie kitu, kuzaa na Rahim
hakutakusaidia chochote maana umezaa mtoto wa kike, kama watoto wakike Rahim
anao wa kutosha tu, sio peke yako uliyezaa na Rahim mtoto wa kike. Ila humu
kwenye tumbo langu kuna kidume, mrithi wa Rahim” Erica alimuangalia
Salma ila akaona kujibishana nae ni kuweka mzozo tu, kwahiyo akaachana nae na
kuondoka zake. Kiukweli roho ilimuuma ila akaona hana sababu ya kuumia kwaajili
ya Rahim maana alishaamua kusonga mbele, kwahiyo alitoka pale kliniki na
kuelekea stendi kisha kupanda daladala na kwenda kwenye duka la
Moses. Alifika pale na kuonana na Moses kwakweli Moses alifurahi sana,
na kumpa ule mkataba ausome kisha asaini maana hakutaka kuchelewesha tena,
wakati Erica anasoma ule mkataba na wao walikuwa wakimjaribisha mtoto wa Erica
nguo huku wakimpiga picha, Moses alimpenda sana mtoto Yule maana hakuwa mlizi
kama watoto wengine na alikuwa na tabasamu muda mwingi, yani walimpiga picha
pale na kurudi kwa Erica, “Kweli huyu ni Angel jamani, mtoto anatabasamu
hadi raha. Una mtoto mzuri sana Erica, hongera tena na tena” Erica
alimjibu asante na kumkabidhi mkataba pale maana tayari
alishasaini. “Nimefurahi sana umekubali kusaini mkataba na sisi, huyu
mtoto wako atakuwa balozi wetu mzuri sana. Hakuna nguo anayovaa ikamchukiza,
angalia hizi picha tulizompiga” Moses akaanza kumuonyesha Erica zile
picha alizopigwa mwanae, kwakweli alipendeza sana hata yeye aliweza kuuona uzuri
wa mtoto wake kwenye picha, siku zote walimsifia mzuri mzuri ila yeye
alimchukulia kawaida ila kwenye zile picha aliona vizuri kuwa mwanae anastahili
kuitwa mzuri na mrembo. Lile swala la kusaini mkataba lilipoisha, Angel
alipewa baadhi ya nguo na kukabidhiwa Erica, “Sikia, ukimvalisha mpige
picha halafu tutumie. Sawa eeeh!” “Sawa hakuna tatizo” “Halafu
ukamfungulie mtoto akaunti benki ili hela zake tuwe tunaingiza huko, kwa kuanzia
tutakuingizia wewe kwenye akaunti yako ila mfungilia ili kila mwezi tuwe
tunamuingizia huko maana kila mwezi tutakuwa tunamlipa” “Oooh nashukuru
sana jamani” “Mshukuru mwanao, maana umepata bahati sana ya kupata mtoto
mzuri halafu anajua kutabasamu, mtoto ana pozi kama mtu mzima! Kwakweli kwa
mwaka huu huyu ndio mtoto bora kwangu” Erica akatabasamu na kuendelea
kushukuru kisha akahitaji kuondoka, hivyo Moses akamwambia, “Basi naomba
nikupeleke mwenyewe nyumbani kwenu maana ni vyema nikafahamu na kwenu hata leo
na kesho iwe rahisi kukupata, mfano tukishusha mzigo mpya tutahitaji mwanao
afike, sasa nikipajua kwenu itakuwa rahisi mimi mwenyewe kuja
kuwafata” “Sawa, hakuna tatizo” Kwahiyo Moses alipanda na Erica
kwenye gari yake kisha kuanza safari ya kwenda kwakina Erica huku akifata
maelekezo toka kwa Erica. “Ila kumbe una gari, mbona siku ile ulipanda
daladala” “Mfano nisingepanda daladala basi nisingekutana na wewe,
unajua kutembea na usafiri wako ni vizuri sana ila kutembea kwenye usafiri wa
jumuiya ni vizuri zaidi. Kwanza unaweza kufahamiana na watu usiowatarajia, pili
unaweza kupata fursa mbalimbali kwa kusikia mazungumzo ya watu kwenye daladala
na pia kuona vitu mbalimbali vinavyotendeka. Sio wote wanaopanda daladala hawana
usafiri binafsi, wengine wanao ila wapo kwenye daladala ili kujifunza changamoto
mbalimbali.” “Aaah hapo nimekuelewa” “Mimi huwa napanda gari
binafsi nikiwa na mambo ya haraka ila kama sina haraka basi daladala itanihusu
kwanza ni rahisi kujua mahitaji ya watu mbalimbali ukiwa nao
karibu” Erica alimuelewa sana Moses na kumuona ni mtu mwenye uelewa wa
hali ya juu. Walifika kwakina Erica ila Moses hakuingia ndani alimuaga
tu pale kisha kuondoka na kumuahidi kuwa ataingia ndani siku
nyingine. Mama yake Erica kama kawaida alishangaa mzigo wa nguo
aliorudi nao Erica ila bado Erica alimwambia swala lile lile kuwa mwanae
kachaguliwa balozi kwenye duka la nguo kwahiyo wanampa nguo kama
motisha. “Kheee una bahati sana mwanangu, hapa ndio mtu unaelewa ule
msemo wa watu kuwa usimtupe mtoto. Jamani Erica ulikuwa ukilia lia mwanangu na
kumuona kama mtoto wako huyu akiwa nuksi kumbe ana baraka zake kwa Mungu.
Hongera sana mwanangu” “Asante mama, ila hongera yetu sote maana ni wewe
uliyemlea mtoto huyu vizuri hadi kawa na afya ya kuonekana kupendeza machoni mwa
watu. Asante mama, yani Angel ana mwaka tu ila kila anayemuona anampenda yani
hadi najisikia raha” “Ila mwanangu kuwa makini na watu, maana sio wote
wanaomsifia mtoto ni watu wazuri. Hata usiwaachie mtoto bila sababu ya msingi
eti kwavile mtoto anatabasamu na kufurahi, achana nao yeni ukiwa mahali wewe
kuwa makini na mtoto tu, watu wanasifia mzuri mzuri gafla wanatoweka na mtoto,
utalia kilio cha mbwa mwanangu, mtoto anauma asikwambie mtu” “Sawa mama
nimekuelewa, naamini maneno yako uliyowahi kuniambia kuwa kila mtoto ni mzuri
ila ni vile tu mzazi anavyomuweka. Na umemfanya mwanangu aonekane kwenye
muonekano wa kuvutia maana umemuweka vizuri. Asante mama” Mama yake
alitabasamu kwa kuona kuwa Erica amethamini mchango wake kwa mjukuu wake, kisha
Erica alienda chumbani kwake ila alijiona kafanya jambo jema kwenda kusaini
mkataba mwanae awe balozi, “Jamani kuna watu wana roho mbaya, sasa
Tumaini mapenzi ya kaka yake yanamuhusu nini? Kama kaka yake namdanganya, yeye
anaumia na nini? Siwezi kumwambia Erick kwasasa maana nahitaji akili yangu ikae
sawa kwanza ndio nimwambie, maana sijui atachukulia vipi. Hapa nilipo ubongo
umejaa mawazo halafu nikaongeze na mawazo ya kukataliwa na Erick mwanaume
nimpendaye? Hapana kwakweli, siwezi kumwambia kwasasa, na swala la mwanangu kuwa
balozi nilikuwa nalihitaji sana kwani kwasasa sina sehemu yoyote ya kusaidiwa
kulea mtoto ila kwasaivi itanisaidia, hebu ona hela nilizopata hata itafanya
nisipokee tena hela za shemeji ambazo nina mashaka nazo kuwa zinaniingiza
matatizoni ingawa mwenyewe anajifanya hana tatizo. Halafu Yule Salma nae ana
nini jamani? Sijui kajuaje kama nimezaa na Rahim mmmh! Ila nimefanya vyema
kutokumjibu, asinibabaishe sijui mtoto wa kike sijui wa kiume, mtoto ni mtoto
asinibabaishe. Kwanza mwanangu kashakuwa balozi, aka mwenyewe naanza kujifaidia
matunda ya mtoto akiwa bado mdogo” Alikuwa akiongea mwenyewe tu huku
akitabasamu na kuendelea na shughuli zake zingine. Kisha muda wa kulala
ulivyofika alilala tu. Kesho yake alijiandaa na kwenda kazini
kama kawaida, ila alipofika tu James alimuita ofisini kwake, “Vipi jana,
ulimpeleka mtoto huku kliniki?” “Ndio nilimpeleka” “Vizuri sana,
Erica wewe ni mama bora unamjali mtoto wako” Erica akatabasamu tu, kisha
akakumbuka swala la kumfungilia akaunti mtoto wake na kumuomba ruhusa James kuwa
aende benki mara moja, “Unataka kwenda kufanya nini?” “Nahitaji
kumfungulia akaunti mwanangu ili niwe namuwekea pesa kidogo kidogo kwaajili ya
elimu yake” “Aaah nimekupenda bure Erica, wewe ni mama bora. Nakupa
ruhusa, tena naomba nikupe nah ii pesa iwe kama kianzio kwenye akaunti ya
mwanao” “Hapana bhana usinipe hela” “Erica, hii pesa si kwaajili
yako ila ni kwaajili ya mtoto wako. Vitu muhimu vya mtoto vyote
umebeba?” “Ndio nimebeba” “Naomba uchukue hii hela Erica, sio
yako hii ni ya mtoto. Ukishamuwekea uniletee na risiti” Erica akakubali
kwani aliona ni kweli James ana lengo la kumsaidia tu. Alipokea zile pesa toka
kwa James ambazo zilikuwa laki mbili. Kisha akaweka kazi zake sawa na
kwenda benki kwaajili ya kumfungulia mwanae akaunti. Alipofika benki
wakampa mlolongo mzima sema vitu vyote alikuwa navyo maana alijipanga tangia
nyumbani, kwahiyo walianza kufungua hiyo akaunti. Walipofika kwenye
picha za mtoto, mkaka aliyekuwa akishughulikia kumfungulia Yule mtoto akaunti
alichukua ile picha na kwenda kuwaonyesha wenzie kisha akarudi, “Dada,
naomba usijisikie vibaya, nimeshindwa kuangalia uzuri wa huyu mtoto peke yangu
ndiomana nikapeleka na wenzangu wamuone. Una mtoto mzuri
sana” “Asante” Alipomaliza, aliombwa kidogo kwa meneja wa benki,
kwahiyo akaenda na kuongea nae, “Dada, tutakuhitaji hivi karibuni kuna
mambo tunahitaji utusaidie” “Mambo gani hayo?” “Tutakwambia siku
hiyo ya kikao, ila tuachie namba yako ya simu hapa mezani. Najua ipo kwenye
mitambo yetu ila ni vizuri ukiniandikia kwenye hiki kitabu niwe na kumbukumbu
vizuri” Erica aliandika namba zake kwenye kitabu alichoonyeshwa kisha
kuondoka zake na kurudi ofisini ambapo alienda kumpelekea James risiti kuwa
ameweka zile pesa kwenye akaunti ya Angel. “Wow, Erica hata mwanaume
atakayekuoa atakuwa ni mwanaume mwenye bahati sana. Una akili sana, sikutegemea
kama ungeniletea risiti kweli! Wewe ni mwanamke makini” Erica
alitabasamu tu na kwenda kuendelea na kazi zake na muda ulipofika alienda kuaga
na kuondoka zake, bado aliondoka mapema ili kuonyesha kuwa anasoma ila hakuwa
akisoma wala nini bali alikuwa akienda nyumbani kwao. Siku hiyo
alienda kwenye duka la Moses moja kwa moja kumpelekea akaunti namba ambapo Moses
alifurahi sana kisha kuagana nae na kumuomba kuwa aende na mtoto Jumamosi
kwaajili ya kumpiga picha na nguo zingine. Erica alikubali na kuagana nae
pale. Alirudi nyumbani kwao na kuongea kidogo na mama yake kisha kuingia
chumbani kwake na kufanya mambo yake mengine. Siku hii usiku aliingia
kwenye mtandao maana alipokea ujumbe kutoka kwa Erick akimuomba aingie
mtandaoni, wakati akiwasiliana na Erick alishangaa Erick kumtumia picha ya mtoto
wake. Erica alishangaa kuwa Erick kaitoa wapi picha ya mtoto
wake. Siku hii usiku aliingia kwenye mtandao maana alipokea
ujumbe kutoka kwa Erick akimuomba aingie mtandaoni, wakati akiwasiliana na Erick
alishangaa Erick kumtumia picha ya mtoto wake. Erica alishangaa kuwa
Erick kaitoa wapi picha ya mtoto wake. Alikuwa kimya kwa muda,
akashangaa tena kuona Erick akimtumia picha kama tatu za mtoto wake, ikabidi
Erica ajibaraguze na kumuuliza Erick, “Kafanyaje huyo
mtoto?” “Nimekutumia uone uzuri wa huyo mtoto” “Kweli ni
mzuri” “Erica, nilipoona picha za huyu mtoto nimejikuta nikitamani kuwa
na mtoto balaa. Erica tafadhali naomba tuzae” “Tutazaa
tu” “Erica, usingetoa ile mimba mtoto wetu angekuwa mkubwa sana saivi,
natamani mtoto Erica, huwezi amini picha za huyu mtoto nimetumiwa jana basi
nimekaa nikiziangalia balaa yani muda wote najihisi nikitaka kumuangalia.
Natamani angekuwa mwanangu” Erica akawaza kuwa pengine Erick alikuwa
akimuweka mtegoni ila akajipa moyo kuwa ataukwepa mtego wa Erick, alikuwa kimya
tu akisoma jumbe za Erick. Kisha Erick alimuuliza tena, “Mbona kimya
Erica? Husemi chochote kuhusu huyo mtoto?” “Sasa niseme nini
Erick” “Nimekwambia mwenzako natamani tupate mtoto, wewe hata huchangii
kuwa unatamani pia” “Na mimi natamani, sema upo
mbali” “Nikutumie nauli uje South?” Erica akawa kimya kwa muda
maana aliona akiwa mtegoni zaidi, kisha akamjibu, “Hapana Erick, kuna
kazi ndio nimeanza kufanya, siwezi kuomba likizo mapema hivyo” “Kwani
huko kwenye kazi wanakulipa shilingi ngapi?” “Mmmh jamani
Erick!” “Niambie tu wanakulipa ngapi?” “Laki tisa kwa
mwezi” “Basi mimi nipo tayari nikupe mwenyewe kila mwezi hiyo hela,
nitakupa na hela nyingine ya matumizi. Erica, natamani tuwe na
mtoto” “Erick, ukirudi nchini tutapanga hayo mambo, hatutakiwi kufanya
kwa haraka hivyo” Erica aliamua kumpooza ila aliogopa kumuuliza kuwa
picha za mtoto Yule kazitoa wapi kwa maana alihofia angeanza maneno
mengine. Aliamua kuagana nae tu kwa muda huu na
kulala. Siku iliyofatia alienda kazini kama kawaida, alifika na
kufanya shughuli zake. Muda ulivyofika aliinuka na kwenda kumuaga shemeji yake
kwaajili ya kuondoka, “Kwa siku ulizo jifunza funza bado hauwezi
kuendesha hata kidogo Erica?” “Bado bado” “Aaaah haiwezekani au
wazembe hao!Basi siku za mwisho wa wiki nikufundishe mwenyewe” “Mmmh
nitaelewa tu shemeji usijali” “Mmmh Erica wewe” “Usijali
shemeji” Kisha Erica akamuomba kuondoka na kuondoka zake, ambapo moja
kwa moja alienda stendi ya daladala ila kabla hajapanda, alishikwa mkono na mtu,
kugeuka ni Fetty ambaye alimfurahia na kumkumbatia kisha Fetty akasema kwavile
wamekutana tena acha aende naye nyumbani kumuona mtoto, Erica hakukataa na
kuanza kwenda nae. Walifika nyumbani kwakina Erica na kumkuta mama yake
ambapo Erica alimsalimia kisha Yule Fetty nae akamsalimia, akaweza kumkumbuka
vizuri kutokana na siku ile waliyoondoka kwenda hospitali. “Karibu
sana” “Asante mama” Muda kidogo mtoto wa Erica alitoka chumbani
na kwenda sebleni, inamaana alikuwa ameamka maana alikuwa amelala, kwahiyo
alivyomuona mama yake alionyesha kufurahi sana, kisha Erica alimnyanyua mtoto
wake kama ishara ya kumsalimia, na kumpa Fetty amsalimia. Fetty
alimchukua mtoto Yule na kusema, “Hiiii jamani ni mzuri, uwiiii mzuri
sana” Mama Erica akasema, “Mmmh taratibu mtoto, huo uzuri mpaka
wa kushtuka wa huyo mtoto uko wapi? Mpaka ushangae kweli, kama kusifia si usifie
kawaida tu, kwanza ni wa kawaida. Mlete mjukuu wangu” Ilibidi Fetty ampe
mama Erica Yule mtoto ambapo alitoka nae nje, Erica alikuwa amesimama tu
akimshangaa mama yake na kushindwa hata kuongea jambo lolote. Alivyotoka
alianza kumuomba msamaha Fetty, “Fetty, naomba unisamehe mimi. Sijui
mama yangu vipi yani mambo yake daha nashindwa hata kuelewa, nisamehe
Fetty” “Hata usijali rafiki yangu, mimi ni muelewa na nimeelewa. Hata
hivyo nimeshangaa sana, ila sio kosa la mama ni kosa langu kushangaa
sana” “Jamani Fetty hadi najisikia vibaya” “Usijisikie vibaya
Erica, tena mama hajafanya chochote kibaya. Unajua watoto wengi sana wanazaliwa
wazuri, wanapendeza ila huharibika kutokana na maneno ya watu. Kila mtu na
mtazamo wake, mwingine anamsifia mtoto kumbe ana kinyongo moyoni, na usiombee
awe mchawi basi anaweza kumshika na kumsiriba kimavi” “Kimavi? Yani
anampaka kinyesi?” “Hapana, ila kimavi ninachosema hakionekani kwa macho
ya kawaida ila utashangaa mwanao ni mzuri anapendeza ila hakuna mtu anayetambua
uzuri wa mwanao, yani mtoto wako haonekani kabisa. Tena utashangaa vitu vingine
anapitwa kupewa, ujue mtoto kapakwa kimavi, yani kuna kipindi kinafika hadi kuna
jambo unafanya unashangaa wewe binafsi umemsahau mwanao kwenye jambo hilo na
kujiuliza kwanini kumbe mtoto kashapakwa kimavi” “Ooooh asante kwa
kunijulisha, sasa nitajuaje mwanangu anataka kupakwa
kimavi?” “Usimuachie mtoto mtu ambaye umeanza kuingia mashaka nae, na
ukiona mtoto ameshaanza kuwa na sifa za kutokuonekana, kutengwa yani unaweza
fika kliniki na mtoto, wenzio wakahudumiwa halafu wewe ukaachwa hadi ukamshtua
nesi kuwa mbona nipo, yani hapo kuwa na mashaka kuwa pengine ni wewe au mtoto
ana kimavi. Kama ni mtu wa jadi, mpeleke mtoto kwa mganga, na kama ni mtu wa
maombi basi mpeleke mtoto kwenye maombi” “Mmmh umenifungua macho Fetty,
sasa mama ana mashaka gani na wewe?” “Mama hajapenda vile
nilivyomshangaa mtoto ndiomana kainuka na mjukuu wake ila sio kosa lake
inaonyesha mamajo yupo makini sana yani hata mwanao wakimchafua basi mamako yupo
makini nae, usione mwanao anapendeza Erica unatakiwa kumshukuru mama
yako” Erica alimsikiliza Fetty maana alijua atakuwa amechukia sana ila
ni tofauti, ndio kwanza Fetty alikuwa akimuelekeza tu mambo asiyoyajua, kisha
Fetty akaaga kuwa anahitaji kuondoka, ikabidi Erica akaweke mkoba wake ndani na
kwenda kumwambia mama yake kuwa Fetty anaondoka. Mama yake Erica alitoka
kwa aibu kidogo maana alijua Fetty ameaga mapema vile sababu ya kumnyang’anya
mtoto, “Nisamehe mwanangu, najua sijafanya vyema” “Hapana mama,
nimekuelewa hata usijali” Mama Erica alimpa tena mtoto Fetty ili amuaga,
ambapo Fetty bila kinyongo alimchukua mtoto Yule na kumuaga kisha kumrudisha kwa
bibi yake na kuanza kutoka nje ambapo Erica
alimsindikiza. Fetty na Erica walikuwa wakisindikizana huku
wakiongea mambo mbalimbali, “Unajua Fetty, wewe ni mtu mzuri sana
nashangaa ni kwanini sikuwa na urafiki na wewe wa karibu chuoni” “Sio
kosa lako, kwa mtu ambaye hupendi umbea huwezi kuwa karibu na mimi sana. Mimi ni
mbea sana na ninajijua ndiomana wakati nilipokutana na mama yako na anaulizia
kwako unapoishi wala sikusita kumleta maana nina asili ya umbea” Erica
alicheka na kusema, “Yani wewe mbea na unajikubali?” “Ndio
mimini mbea yani najua hilo, kule nilipokuwa naishi na Yule mwanaume nimeachika
kwa mengi ndugu yangu. Mume ana mapungufu yake na mimi pia nina mapungufu yangu,
ila najua ananimiss sana maana nikishinda nyumbani mimi basi habari za mtaa
mzima ninazo. Bora nikienda kazini, ila kazini naenda siku zote halafu Jumamosi
na Jumapili napumzika, weee habari zote nazipata yani burudani kwahiyo nikianza
kumpa mlolongo wa habari Yule mume anabaki mdomo wazi. Ingawa kanitimua kwa
kusikiliza ndugu zake na kusingizia dini ila najua ananimiss
sana” “Hahahaha Fetty wewe, mawifi zako hawakupenda
umbea?” “Basi tu walikuwa na yao, halafu umbea wangu hata sikuwa nafanya
nao hata nawashangaa kunichukia. Ila ndugu yangu Erica, mwanaume anayekataa
majukumu ya mwanae huwa anaumbuka vibaya tena vibaya sana. Unajua watoto ni
baraka njema ambayo Mungu ametupatia, ila ikitokea mtu anakataa majukumu ya ile
baraka ambayo Mungu ameitoa basi ujue ipo siku mtu huyo ataumbuka balaa. Yani
aibu ya wale viumbe inanukia” Erica akacheka sana kisha gari likaja na
Fetty akapanda na kuondoka. Wakati Erica anarudi kwao, akakutana na
Johari na kushangaana kwa muda, “Erica kumbe upo kwenu
hatuambizani?” “Majukumu, nisamehee sana” “Vipi ulishamaliza
chuo?” “Mbona siku nyingi sana” “Mahafali umefanya kimya kimya
hata hatujaalikana” Erica akanyamaza kwa muda kwani kiukweli hata
mahafali yenyewe hajafanya kwahiyo swala la kuambiwa kafanya kimya kimya aliona
linamchanganya tu, ikabidi abadili mada, “Una watoto wangapi saivi
Johari?” “Wawili” “Kumbe wawili tu? Ulizaa na Yule Yule
au?” “Wawili tu kwani wachache? Wananitosha, natumia uzazi wa mpango
mwenzio unajua ukishaharibu maisha yako basi usipende kuendelea kuharibu. Yule
mwanaume achana nae, kumbe sikukwambia eeeh! Yule mwalimu bhana kumbe alikuwa na
mke wake, kipindi anakuja kuja kuniona mkewe hakuwepo alisafiri kikazi sasa ndio
akawa anamalizia shida zake kwangu. Mtoto wa pili sijazaa nae yeye, yupo mkaka
amenipenda na mwanangu ndio naishi nae ndiomana siku hizi huku sionekani sana
maana naishi huko sehemu nyingine na huyo mwanaume” “Pole na hongera kwa
kumpata huyo anayekujali” “Na wewe vipi, huna mpango wa kupata mtoto au
ndio hadi uolewe? Tupe basi kadi za harusi hiyo” “Mmmh Johari wewe,
nitakwambia tu hata usijali” Kisha Erica akajifanya anapitia dukani ndio
aende kwao, alifanya vile kwasababu hakutaka kwenda kwao na Johari. Kwahiyo
waliagana nae, halafu Johari aliendelea na safari yake nay eye kwenda dukani na
kununua kitu ambacho wala hakukihitaji kwa wakati huo. Baada ya hapo,
Erica alirudi kwao na jioni ilikuwa imeingia na kigiza nacho kuanza
kutanda. Alivyoingia tu ndani, leo mama yake alikumbuka kuhusu Bahati na
kuulizia yuko wapi, “Erica, hivi Yule muuza samaki aliishia wapi jamani
toka siku ile hadi leo kimya!” “Mmmh! Mama leo ndio unamkumbuka? Kweli
umuhimu wa kitu huonekana pale unapokikosa, yani Bahati hayupo tena ndio
unamkumbuka wakati siku zote huwa unajifanya humtaki” “Mmmh Erica jamani
ni lazima nimkumbuke, alikuwa anampenda Angel mwenyewe alikuwa anatuletea kuku,
samaki nimejifaidia haswaaa. Alikuwa ananiachia hela, jamani lazima nimkumbuke.
Akija anashinda na Angel, anacheza cheza nae na mtoto nae anafurahi anakuwa kama
watoto wengine wenye baba. Nimemkumbuka sana Yule kijana, yuko
wapi?” Erica akainama chini, hapo kumbukumbu zote za ndoa ya Bahati
zilimjia na kujikuta akiumia sana. Alikuwa kimya tu tangu mamake alipokumbushia mazuri ya Bahati, ilibidi mamake amuulize tena, “Kwani
kuna nini Erica? Kwani huyo Bahati yuko wapi?” “Mama, sielewi kabisa
yani sielewi, kweli mwanao mimi ni fungu la kukosa” “Kwanini unasema
hivyo mwanangu?” “Katika ulimwengu huu hakuna mwanaume niliyejua
ananipenda kufa kama Bahati, maana hata nikifanya baya ila kwake ataliona zuri
hadi nilijiona ni mwanamke mwenye bahati kama jina lake. Lakini huwezi amini,
Yule Bahati aliyenipenda kufa, aliyeonyesha kufanya vyote kwaajili yangu
ameoa” “Ameoa?” “Ndio ameoa” “Kwahiyo siku zote alikuwa
akija hapa tayari ana mke au?” “Hapana mama, ila wiki mbili tu baada ya
kutoka hapa huwezi amini mama nilimshuhudia Bahati kwa macho yangu akiwa
amefunga ndoa. Yani hili jambo sijaambiwa na mtu bali nimelishuhudia kwa macho
yangu, Bahati ameoa mama. Hadi nashangaa mama yani kwa wiki mbili tu Bahati
ameoa, sikuamini” “Mmmh yani kwa wiki mbili apate mwanamke mwingine
wapange maswala ya ndoa hadi kuoana! Mbona hainiingii akilini hiyo? Au
alishakuwa naye huyo mwanamke na walishapanga maswala ya ndoa ila walikuja kwetu
kujikosha ili mamake alete maneno ya shombo na tuseme ni mamake kumbe
wamejikosha” “Hata mimi nahisi hivyo mama, kwakweli watu wanajua kuigiza
yani Bahati alivyoniigizia ananipenda yani siamini, nashindwa kuamini kabisa.
Ndiomana inakuwa ngumu kwangu kuelewa maana ya mapenzi kama mtu anaweza
kukuigizia kama Bahati jamani mpaka unaamini unapendwa kumbe hakuna
kitu” “Ila usijali mwanangu, kama ridhiki yako ipo basi ipo tu hata
usijali, si unaona saivi sikupigii kelele kuhusu baba wa mtoto ingawa najua kaka
zangu wakija hapa ni balaa ila sitaki kuendelea kukuumiza kichwa mwanangu.
Usijali, hata mimi sikufikiria kama Bahati anaweza kufanya hivyo” Erica
aliinuka na kuelekea chumbani kwake kwani alijisikia kulia na hakupenda kulia
mbele ya mama yake kwahiyo aliingia chumbani na kulia, huko alijikuta akikumbuka
mambo mengi sana, “Hivi mapenzi ni nini? Siyaelewi kabisa, na kwanini
yalikuwepo? Niliamini Bahati ananipenda sana ndiomana hela nilizokuwa napewa na
Rahim nilimpa Bahati maana nilipenda awe na muonekano wa mwanaume ninayependa
kuwa nae, ila ni nini sasa kimenitokea? Bahati nimemkosa, Rahim nae
nimemkosa” Alilia sana hadi mama yake alienda kumgongea, “Wewe
Erica, hebu njoo umchukue mtoto umlaze chumbani” Erica alifuta machozi
na kwenda kumchukua mwanae kisha kuingia nae chumbani, hakutaka kuendelea kuwaza
sana badala yake aliamua kulala tu. Jumamosi ilipofika Erica
aliamka na kujiandaa kisha kumuandaa mtoto wake kwaajili ya kwenda dukani kwa
Moses maana alimwambia kuwa ampeleke mtoto Jumamosi hiyo, alikuwa anawaza kuwa
siku hiyo apande daladala na mwanae, “Mmmh kukodi tax kila leo
itaniumiza sana, nahitaji kumtunzia mwanangu hela za kumsaidia badae na masomo
yake. Mfano ningetunza zile pesa nilizokuwa napewa na Rahim labda ningefanya
kitu bora kuliko kumrundikia Bahati ambaye kaniacha na kwenda kuoa msuchana
mwingine. Inaniuma kila nikifikiria, namuomba Mungu tu anipe
ujasiri” Wakati analalamika hayo mamake alimsikia, na kutoka kumuuliza
kwa hamaki, “Wewe Erica, usiniambie kuwa ulikuwa unampa hela
Bahati?” Erica akakaa kimya, kisha mamake akaendelea
kuongea, “Yani unampa hela mwanaume? Umepata wapi akili ya kijinga hivyo
Erica? Badala mwanaume akupe wewe eti wewe ndio unampa hela mwanaume! Ulimpenda
sana eeeh! Nadhani Bahati alikuwa anakubembeleza sababu ya hela ulizokuwa unampa
na sio mapenzi. Wewe mtoto ni mjinga sana” “Ila mama, mbona wanawake
huwa tunapewa hela na wanaume? Kwanini iwe ngumu hivyo kwa wanawake kuwapa
wanaume?” “Hebu kuwa na akili kidogo wewe mtoto, tumesomesha kopo tu,
uwe unasoma hata maandiko basi, imeandikwa mwanamke atazaa kwa uchungu na
mwanaume atakula kwa jasho yani mwanaume anatakiwa kutafuta sio wewe utafute
umpe ili iweje? Si bora ungenipa mimi mama yako hata nisingekuwa nakusema sana
maana hela tumekula wote, ila hela umeenda kuzimwaga kwa tahira Yule, unaona
sasa kaona mwanamke mwingine! Mwanaume sio ndugu yako” “Sawa mama,
nimekuelewa” “Haya, unataka kwenda wapi na mjukuu wangu?” “Si
kule nilipokwambia mama kuwa mjukuu wako amekuwa balozi, sasa ndio leo wanaenda
kumpiga picha” “Mmmh mambo ya kizungu hayo hata siyaelewi, ila ita gari
ikupeleke hadi kituoni halafu upande daladala. Usimtembeze mjukuu wangu juani
kwa ujinga wako, jua kali hili” Ilibidi Erica achukue ushauri wa mama
yake na kwenda kupanda gari hadi kituoni halafu kupanda
daladala. Alifika dukani na kwenda moja kwa moja kwa Moses,
kama kawaida pale dukani walimfurahia sana mtoto wa Erica, kisha Erica akasogea
kuongea na Moses ambapo Moses alionyesha mzigo mpya ambao walitaka kumjaribisha
Angel na kumpiga picha, hilo zoezi halikuwa gumu maana mtoto wa Erica alipenda
picha sana kwahiyo ilikuwa rahisi sana kwake, kwani aliweka mapozi kama mtu
mzima, walipomaliza Moses akamwambia Erica, “Hiki ndio kitu kinachofanya
huyu mtoto awe tofauti na watoto wengine, kuna baadhi ya watoto kuwapiga picha
hadi uwavizie maana wakikuona na camera tu ni balaa ila huyu mtoto ana pozi na
kutabasamu kabisa. Nampenda sana huyu mtoto” Moses akamnyanyua Angel
huku akimuonyesha baadhi ya vitu vya kuchezea watoto, wakati Erica yupo
akitabasamu tu mara alitokea Tumaini na kumuita Erica pembeni, sura ya Tumaini
ilionyesha kuchukizwa sana, Erica alimfata nje na kuanza kuzungumza
nae, “Hivi wewe Erica una akili gani? Yani Erick hujamwambia ukweli
halafu umenizunguka na kuja kusaini mkataba. Kwanini umefanya
hivyo?” Erica alikuwa kimya na kumfanya Tumaini aendelee
kuongea, “Erica, ngoja nikwambie kitu. Kwa baba tumezaliwa wawili tu
yani mimi na Erick, kwa mama yangu tupo sita kwahiyo nina ndugu zangu wengine
kwa mama ila Erick kwa mama yake napo yupo peke yake kwahiyo ndugu pekee wa
Erick ni mimi tu, Erick anasikiliza ushauri wangu kupita ushauri wowote ule.
Sasa wewe umejifanya kiburi, hivi hujui kama naweza kukuharibia? Hujui? Nijibu
usinikalie kimya” Muda huu Erica aliona maneno yamemchosha kwahiyo
aliamua na yeye kutoa ya moyoni mwake, “Tumaini, sikia nikwambie.
Ulikuwa mtu mzuri sana kwangu, sikutegemea kama ungekuja kuwa mbogo kiasi hiko.
Haya ni maisha ya mwanangu, unaniambia nisisaini mkataba kweli?” “Maisha
ya mwanao? Unajua duka la nani hili?” “Si la Moses” Tumaini
akabana pua na kumgeza Erica yale maneno, “Si la Moses, unaongea kama
umetoka kufufuka. Si la Moses, unamjua sana Moses wewe? Nilikwambia umwambie
ukweli Erick nilikuwa na maana yangu kabisa” “Sasa hiyo maana yako
usiponiambia nitajuaje?” “Ni duka la Erick hili” Erica
alishangaa kusikia lile ni duka la Erick, kisha Tumaini akaendelea
kuongea, “Endelea kushangaa hivyo hivyo, unadhani Erick atakubali
kumuweka mtoto wa kambo balozi?” “Tumaini nakuomba usimwambie tafadhali,
usimwambie Erick” “Wewe si umejifanya kiburi, eti duka la Moses. Unamjua
sana huyo Moses eeeh! Subiri uone sasa kitakachotokea” Tumaini akaondoka
na kumfanya Erica abaki na mawazo, kisha akarudi dukani ili kumchukua mwanae.
Moses alimuona Erica alivyonyong’onyea gafla na kumuuliza, “Tatizo nini
Erica?” “Hakuna tatizo” “Yani kila ukiongea na Yule Tumaini huwa
unarudi umepooza sana, Yule nae sijui anatafutaga nini hapa. Kisa tu duka la
ndugu yake ndio kujifanya anakuja mara kwa mara” Erica alihamaki na
kumuuliza, “Kheee kumbe duka sio lako?” “Wengi wanajua duka ni
langu, ila humu dukani kuna bidhaa zangu pia. Duka hili ni la mtu mmoja anaitwa
Erick, ananiamini sana na ana duka lake lingine kubwa kama hili
South” Erica hakuwa na mengi ya kuongea ila alimwambia Moses kuwa
anaondoka, Moses akamkodia gari na kumpa baadhi ya nguo kwaajili ya Angel ila
hakuelewa ni kwanini Erica kaondoka akiwa amenyong’onyea
vile. Erica alifika nyumbani kwao akiwa hana raha kabisa,
mamake alimshangaa karudi na nguo za mtoto ila hana furaha wala nini. Alienda
chumbani kwake, muda huo alimuacha mwanae sebleni na bibi yake alikuwa
akitafakari sana, “Sasa jamani kama lile duka ni la Erick itakuwaje? Ila
bora nimeshasaini mkataba maana wakivunja mkataba itabidi wanilipe ila dah
inaniuma sana, kwani Tumaini hajawahi kukosea katika maisha
yake?” Wakati anawaza hayo, simu yake ilianza kuita, kuangalia ni Erick
alikuwa akipiga, Erica alijishauri kidogo na kupokea. Siku hiyo Erick hakuanza
na salamu, moja kwa moja alisema, “Erica, niambie kuwa sio kweli kwamba
una mtoto?” Erica alikuwa kimya, na kumfanya Erick aendelee
kuongea, “Niambie Erica kuwa nilichoambiwa ni uongo!” Mara Angel
aliingia chumbani kwa mamake huku akisema, “Mama, mama,
mama” Ile sauti ilisikiwa vilivyo na Erick na akauliza tena kwa
mshangao, “Kumbe ni kweli Erica una
mtoto!” Erica alikuwa kimya, na kumfanya Erick
aendelee kuongea, “Niambie Erica kuwa nilichoambiwa ni
uongo!” Mara Angel aliingia chumbani kwa mamake huku
akisema, “Mama, mama, mama” Ile sauti ilisikiwa vilivyo na Erick
na akauliza tena kwa mshangao, “Kumbe ni kweli Erica una
mtoto!” Erica alikaa kimya na kukata simu, kisha akamnyanyua mtoto wake
na kuanza kulia huku akimuangalia, na mtoto huyu kwasasa alikuwa ni Yule mtoto
anayejifunza maneno, “Mama aiya nini?” Angel alionekana kumfuta
mama yake machozi kwa mikono, Erica aliamua kunyamaza kwani aliona ni kumkosesha
mtoto furaha. Aliweka simu pembeni na hakutaka kuisikiliza tena. Jioni
mama yake alimuita na kuanza kuongea nae, “Hivi Erica redio niliyokupa
usikilizage unasikilizaga kweli?” “Huwa nasikiliza mama” “Haya
niambie, jana alikuwa akihubiri nani na mahubiri yalihusu nini?” “Ila
jana sijasikiliza” “Wewe mtoto wewe, unajijua kabisa akili yako haipo
sawa, kanisani huendi yani upo upo tu na mahubiri nayo kwenye redio usikilizi
kweli? Unadhani akili zako hizo mbovu zitaponaje?” “Nisamehe mama, leo
nitasikiliza” “Hebu acha ujinga, mama yako nakupenda. Waswahili husema
mtoto akiunyea mkono sio uukate bali uusafishe, sasa mimi nataka nikusafishe
wewe ila wewe ni mbishi balaa unajifanya huelewi ila Erica kuwa makini mwanangu
maisha haya, ushaharibu mwanzo usitake kuharibu hadi mwisho, kuwa makini
sana” “Nimekuelewa mama” Erica alimuitikia mama yake na kumpa
mwanae chakula, kisha muda alivyoenda chumbani kulala akaamua kufungua redio
kama mama yake alivyomshauri ili kusikiliza mahubiri, alishangaa kuona mahubiri
yakimlenga yeye tu. “Hakuna kitu kibaya katika maisha kama uongo, yani
jitahidi uikimbie dhambi ya uongo kumbuka uongo ndio ulifanya Adam na Eva wakala
lile tunda, maana walidanganywa na nyoka kwahiyo uongo umetumika hapo. Uongo
unatutenga na Mungu, halafu shetani ndio baba wa uongo kwahiyo ukiwa muongo ujue
baba yako ni shetani. Kwani ukisema ukweli utapungukiwa na nini? Hata kama
utaona kuwa kuna kitu utakipoteza kwa kusema ukweli bora upoteze kitu hiko na
Mungu atakusimamia kwenye ukweli unaosema ila uongo utakutesa siku zote za
maisha yako. Huwezi kukazana kumuomba Mungu akusaidie wakati katika maisha yako
hakuna jambo la kweli yani ni uongo mwanzo mwisho, na uongo hauwezi kukuokoa
kamwe. Ondoka sasa kwenye uongo na uwe mtu wa kusema ukweli, kumbuka ukweli
humuweka mtu huru” Erica alizima redio kwani aliona mahubiri yale
yanamgusa moyo wake kabisa maana tabia yake ilikuwa imehusishwa moja kwa moja
ila alifikiria sana kuwa anawezaje kuacha uongo, “Ila siku hizi
nimepunguza uongo, huwa sidanganyi ila sijibu. Nitawezaje kusema
ukweli?” Akawaza sana na kuamua kulala tu. Kesho yake
mamake alienda kanisani ila Erica alibaki nyumbani kama kawaida na mtoto wake
huku akifanya shughuli za hapa na pale, simu yake iliita tena akaiangalia ni
namba ya Erick, akaipokea, “Erica, leo nimeamua kwenda kanisani kwaajili
yako, jibu lako ndio litategemea uamuzi wangu. Niambie ukweli Erica, una
mtoto?” “Ndio nina mtoto” Simu ikakatika, Erica akajaribu kupiga
tena ile namba ya Erick ila hakuipata hewani kabisa, wasiwasi ulimshika Erica
maana hakujua ni nini kimempata Erick, alijikuta akijawa na mashaka kupita
maelezo, “Mungu wangu, ukweli humuweka mtu huru au ukweli humuongezea
mtu matatizo? Sasa Erick wangu kakumbwa na nini? Mungu wangu, sijui nani ataweza
nieleza habari za Erick” Siku hiyo hakuwa na raha kabisa siku nzima na
kila alipojaribisha namba ya Erick bado hakuipata hewani na kumfanya kuwa na
mashaka zaidi. Hata mama yake aliporudi aligundua hali ya
Erica, “Ndiomana nakwambiaga uwe unaenda na kwenye ibada, wewe ni mtu
gani kila siku mawazo?” “Hapana mama, ila ngoja nikuulize jambo. Ukweli
humuweka mtu huru au ukweli humuongezea mtu matatizo?” “Kwanini ukweli
ukuongezee matatizo? Ukweli ni mzuri sana na hukuweka huru, hebu fikiria
ungekuwa unakuja kwa mama yako na kuniambia ukweli, mama kuna mwanaume hivi na
hivi na vile, mimi kama mama ningekushauri kuhusu huyo mwanaume. Unafikiri
ingefikia hatua ya Angel kutokuwa na baba? Katika maisha tunatakiwa kujifunza
kusema ukweli maana unapokuwa mkweli ni rahisi kusimamia maneno yako ila njia ya
muongo ni fupi maana kuna muda utasahau hata ulikuwa unaongelea
nini?” “Sasa mama, kuna ukweli wa kuumiza, unawezaje kumwambia mtu
ukweli wa kuumiza wakati unajua unaumiza?” “Sasa hapo penye ukweli wa
kuumiza unatakiwa kupata ushauri kwa mtu anayeelewa kuongea na mtu mwingine
ambaye atatoa ukweli kwa ushauri. Ukijua ni kitu cha kuumiza, hutakiwi kutoa
ukweli kwa kukurupuka, unatakiwa kupata ushauri kwanza na ukishindwa hata mtumie
mtu mwenye busara kusema. Mfano madaktari wetu wamejifunza kuongea na mgonjwa na
endapo wakimpima mtu na kugundua kaathirika huwa hawakurupuki tu na kusema una
ukimwi maana wanajua ule ni ukweli ila unaumiza na ukikurupuka kumwambvia mtu
unaweza kumpoteza maana ile mara ya kwanza mtu kuambiwa una ukimwi huwa
inachangaya akili hatari mtu huwa anatamani hata kufa. Ila madaktari wetu
hutumia kauli za busara na upendo kiasi kwamba mtu Yule aliyeathirika
anapoambiwa ana ukimwi huwa tayari ameshaweza kukubaliana na hali yake na kuona
kuna watu wameathirika na bado wanaishi vizuri tu. Ukijua kabisa ukweli huu
unaumiza basi usiutoe kwa pupa” Erica akainama chini kidogo kwani jinsi
alivyomjibu Erick ni kwamba aliutoa ukweli kwa pupa na hakujua ni kipi kinaweza
kutokea kwa Erick, alimuuliza tena mama yake “Na kama hukujua hilo
ukajikuta umetoa ukweli kwa pupa itakuwaje?” “Kuna ukweli gani umeutoa
kwa pupa? Unajua unaposema ukweli inategemea na mtu unayemwambia huo ukweli,
mfano una mpenzi anakupenda sana na anakujali kwa kila kitu ila umejikuta
humpendi basi tafuta namna ya kumfikishia huo ujumbe sio unakurupuka na
kumwambia sikupendi, sikutaki yani hujui tu utasababisha nini kwa Yule mtu labda
kama hakuwa na upendo na wewe ila anayekupenda sana unaweza fanya akawa kichaa
wengine ndio huchukua hata jukumu la kujiua kama hajapata watu wazuri wa
kumshauri. Ukweli ni mzuri sana ila jifunze kutoa ukweli katika staili inayofaa,
na uangalie huo ni ukweli wa aina gani, kama wa kuumiza basi tafuta namna ya
utaratibu kufikisha ujumbe kwa muhusika” Erica alishajiona amekosea
alivyomueleza Erick, aliumia sana moyoni ila ndio alishamueleza na kumfanya
akose raha kabisa. Siku hiyo alikuwa na mawazo sana, hata usiku
hakushika simu wala chochote ila usingizi ulimpata kwenye mida ya saa
tisa. Kulipokucha mama yake alienda kumkurupua, “Wewe
Erica, huendi kazini?” Alikurupuka na kwenda kuoga kwaajili ya kwenda
kazini, alijiandaa na kwenda kazini kama kawaida ila alikuwa kazini na mawazo
sana. Alifika na kufanya kazi zake kama kawaida, ila hata James alijua
kuwa ana mawazo, alimuita ofisini kwake na kumuuliza kuwa mbona anaonekana
hayupo kawaida, ila Erica naye alimuuliza James, “Mfano bado hujaoa, na
kuna mwanamke unampenda sana ila unakuja kugundua huyo mwanamke ana mtoto na
mtoto kapata ndani ya mahusiano yenu na mwanaume mwingine,
utajisikiaje?” “Eeeh bhana eeeh! Hilo jambo limewahi kunitokea, inauma
asikwambie mtu yani inauma sana tena usikute ulimuomba mzae akagoma halafu
akaenda kuzaa na mjinga yani inauma sana.” “Sasa wewe ilivyokutokea
ilikuwaje?” “Unajua mara nyingi kwasababu ya Yule mwanamke mmoja nimeona
wanawake wote hawafai wakati Bite wangu yupo tofauti kabisa, yani ukimfanyia
hivyo jamaa yako unamchukiza sana tena anaweza kukuchukia milele. Ndio imetokea
kwako hiyo Erica nini? Maana nimeambiwa huyo uliyezaa nae hakujali, je ulikuwa
na mpenzi kabla yake ndio kakuchukia?” “Yani mwanaume ninayempenda ndio
kajua ukweli kuwa nina mtoto, na amechukia sana” “Ndio swala linakupa
mawazo hilo Erica?” “Naumia sana, sababu nampenda” “Hebu ondoa
hayo mawazo, tena ondoa mawazo hayo kabisa kichwani mwako. Huyo mwanaume hawezi
hata kukuoa maana tayari ushaingia doa, mwanaume atakayeweza kukuoa ni Yule
atakaye kukuta na mtoto kwasasa na akakupenda hivyo hivyo ila kwa huyo uliyetia
doa sahau. Ila usijali Erica, naomba leo usiondoke mapema nikupeleke mahali
ukarelax kidogo” Erica alimuitikia ila akajua kama kawaida shemeji yake
ameshaanza upuuzi wake, kwahiyo alimuitikia ili kumridhisha
tu. Alimaliza kazi zake leo ila hakwenda kumuaga James na kuondoka zake
kurudi nyumbani kwao. Akiwa njiani akakutana na Dora, ambapo alimsalimia
na kumkumbatia, “Erica unaenda wapi?” “Naenda
nyumbani” “Unakumbuka kuwa ni leo jioni ndio ulisema tuje ofisini kwenu?
Yani nipo na wenzangu wale pale ndio tunaelekea ofisini kwenu sasa wewe ndio
unaondoka tena jamani!” “Ila wapo wenzangu” “Ndio Erica, ila
uwepo wako ndio mzuri zaidi. Naomba tuongozane pamoja tafadhali” “Basi
ngoja na mimi nikuombe kitu” “Niombe tu” “Naomba mkimaliza useme
kuwa unataka kwenda na mimi nyumbani na usiondoke hadi tuondoke wote, hata
wenzio waondoke tu” Ilibidi Dora akubali maana kiukweli alihitaji sana
waweze kuongea na wafanyakazi wa ile ofisi, kisha wenzie Dora walifika pale na
safari ya kurudi kazini kwa James iliwadia. Walifika kisha
Erica alienda kumwambia James kuwa wale watu wa kuongea na wafanyakazi wake
wamefika, James alimwambia Erica aweze kuwaambia wafanyakazi wote ili wakutane
kwenye chumba cha mkutano maana tangazo alishabandika toka wiki iliyopita kuwa
karibia na muda wa kutoka kutakuwa na semina fupi, sema tu Erica mwenyewe
alisahau. Aliwaambia kisha wote wakajiandaa na muda ulipofika wakaenda
kwenye chumba cha mkutano ambapo wale wakina Dora walipewa muda wa nusu saa tu
ya kuzungumza mambo yao, na waliyazungumza walipomaliza waliwashukuru kila mtu
alirudi sehemu ya kazi yake kwaajili ya kufunga na kuondoka maana muda wa kazi
nao ulikuwa umeisha. Kwahiyo wale wengine waliondoka kisha kumuacha Dora pale
akimsubiria Erica. Kisha Erica akataka kwenda kumuaga shemeji yake maana
hakuweza kuondoka kama mwanzo sababu tayari alishaonekana kwenye kikao, ila
kabla hajaenda kumuaga shemeji yake alimwambia, “Erica nisubiri, kumbuka
kuna kitu nilikwambia kuwa kuna mahali tutaenda” “Aaaah shemeji, kuna
rafiki yangu ananisubiri niende nae nyumbani” “Rafiki yako yupi
huyo?” “Ni mmoja kati ya wale waliokuja kwenye semina” “Mwambie
atakufata siku nyingine” “Aaaah shemeji, leo kaacha shughuli zake zote
kwaajili yangu, itawezekanaje kumwambia hivyo? Sio vizuri eti” “Basi
nisubiri nae, nikamilishe kazi hapa mara moja” Erica hakumuelewa shemeji
yake kwakweli, ila ilibidi afate maagizo yake maana licha ya kuwa shemeji yake
wakati huo huo ni bosi wake. Kwahiyo Erica alienda kwa Dora na kumwambia
kuwa wasubiri mara moja, muda kidogo James alimaliza kazi zake na kumwambia
Erica amfuate pamoja na rafiki yake. Walipofika nje, James
alijitambulisha kwa Dora, “Hey, Dora mimi naitwa James nadhani
unanifahamu kama mmiliki wa hii kampuni ila pia mimi ni shemeji yake Erica. Jina
lako nimelisikia kwenye utambulisho wenu na Erica ameniambia kuwa wewe ni rafiki
yake wa dhati na kaniambia kuwa leo unataka kwenda nae kwao ila mimi nahitaji
kumpeleka mahali shemeji yangu akatulize akili yake kidogo maana imevurugika.
Kama hutojali basi tuungane” Dora hakujua kama akatae au akubali maana
kwenye makubaliano na Erica ni kuwa ajifanye kwamba anamsubiria Erica kwenda nae
nyumbani, ila kwa hoja ile hakujua kama akubali au akatae, Erica akaamua
kujibu, “Ila shemeji…” James akamkatisha Erica na
kusema, “Erica wewe nyamaza, mimi nimemuuliza Dora, je yupo tayari
kuungana na sisi au la” Dora alikubali ili kujua kuwa Erica na shemeji
yake wamepanga kwenda wapi. Basi wakapanda kwenye gari ili kuelekea ambako
anapajua James. Wakiwa kwenye gari James
akawaambia, “Sasa tutangulie sehemu moja hivi, wanapikaga kitimoto
kitamu hiko balaa. Twendeni tukale kitimoto” Erica akamwambia shemeji
yake, “Hapana mimi silagi kitimoto” “Kwanini huli
kitimoto?” “Basi tu imetokea huyo mdudu huwa sili” James
akamuuliza na Dora, “Wewe je?” “Mimi nakulaga” “Basi
tutapanga siku nyingine tukale mimi na wewe, yani Erica ana mambo ya kishamba
hadi yanakera. Basi twendeni tukale nyama ya mbuzi hadi tusahau
matatizo” Napo Erica akapinga, “Hapana huwa sili
mbuzi” “Una matatizo gani wewe Erica? Kwahiyo nyama gani
unapenda?” “Napenda kuku na samaki” “Basi twende mahali kuna
mishikaki ya kuku mitamu sana, yani wanajua kuchoma hao balaa huko tunakula huku
tunaangalia bendi” “Shemeji kumbuka nina mtoto mdogo bado ananyonya,
ananisubiri nyumbani, si vizuri nianze kuzurula zurula” “Erica usiwe
hivyo jamani, mimi nitakurudisha hadi kwenu. Nahitaji tu ukatulize mawazo yako,
tafadhali usiniuzi na mimi” Kwakweli Erica hakujisikia kabisa kwenda
mahali na shemeji yake ila kwavile shemeji alionekana kadhamiria siku hiyo
kutoka na Erica hakuwa na namna zaidi ya kumsikiliza mambo
mengine. Wakafika kwenye hiyo hoteli ambako walikuwa wanachoma kuku huku
kuna bendi inatumbuiza, walienda kukaa kwenye viti na kuagiza nyama kisha wa
vinywaji akaja, James akaagiza pombe yake, Dora nae akaagiza bia yake, Erica
akaagiza soda. James akamzuia muhudumu kwenda kumletea kwanza, “Erica
usituletee nzi hapa, utaagizaje soda?” “Shemeji, giza lishaingia sasa
hao nzi watoke wapi? Halafu niagize nini zaidi ya soda?” “Agiza bia,
yani usiagize juisi wala soda, sitaki kuchafuliwa meza” “Sinywagi
pombe” “Ila kuna pombe laini” “Hapana sinywi pombe, hata hivyo
nina mtoto mdogo bado ananyonya mwanangu siwezi kuchanganya maziwa yangu na
vilevi. Sinywi pombe nampenda mwanangu” James akamuangalia Erica na
kuruhusu muhudumu amletee kinywaji anachotaka, na alipoletewa tu na kumiminiwa
kwenye glasi, James akachukua na pombe yake kuimimina kwenye glasi ya
Erica, “Shemeji ndio unafanya nini?” “Erica, kunywa pombe sio
zambi hata hivyo pombe ukichanganya na soda haileweshi” Erica akakumbuka
mara ya kwanza kunywa pombe alishawishiwa na Derick na kuambiwa kuwa ile pombe
haileweshi, halafu akanywa na kulewa na kisha kufanya mapenzi na Derick hadi
kupata mimba na kuja kupata dhambi ya kutoa maana alibeba mimba ya ndugu yake,
halafu shemeji yake bila aibu anamshawishi anywe pombe, akaona ni
ujinga. Akawaza ni kwa jinsi gani atamkwepa shemeji yake, aliamua
kumuaga kuwa anaenda chooni na akirudi atakuja kunywa. Alienda
chooni Erica na kupita mlango wa nyuma halafu kuondoka zake, yani alimuacha
shemeji yake na Dora, kwa muda huo hakujali kuhusu Dora alimuacha mwenyewe
ajiokoe maana amekubali tu wito hata asioujua chanzo chake. Erica
alienda hadi nyumbani kwao na kumkuta mama yake ambaye alimfokea
sana, “Yani Erica mpaka muda huu kweli? Saa nne hii jamani? Hiyo kazi
kazi gani, mbona siku zote unawahi kurudi, huna uchungu na mtoto
wako?” “Namuhurumia mama ila leo tulikuwa na kikao ofisini, halafu
tulivyotoka foleni. Najua mara nyingine nawahi ila leo bahati mbaya mama.
Nisamehe mama” “Haya nenda ukaoge uje kumchukua mtoto
ukamlaze” Basi Erica alienda kuoga kisha akaenda kumchukua mtoto wake na
kwenda kumlaza, yeye hakuweza hata kula maana hakujisikia tena ila mama yake
alimwambia kuwa anatakiwa kula kwahiyo akala kidogo na kwenda
chumbani. Wakati yupo chumbani leo alijikuta gafla alijikuta akimkumbuka
Bahati hadi moyo ulimuuma maana ndiye mwanaume aliyekuwa tayari kumfanya mtoto
wake kuwa na baba, tofauti na Erick aliyemzimia simu maana aliamini kuwa Erick
alimzimia simu. Ingawa siku zote hakumpata Bahati hewani ila siku hiyo
alipiga na simu ya Bahati iliita, na muda kidogo ilipokelewa na ilipokea sauti
ya kike na kumfanya Erica kidogo ajiume ume, “Bahati
yupo?” “Anaoga, kwani una shida gani?” “Shida natakiwa niongee
nae yeye” “Mimi ni mke wake kwahiyo unaweza kunieleza shida
yako” “Mmmh! Nyie wanawake wengine ndiomana mnaachikaga nyie, kupokea
simu ya mume wako ndio nini?” “Wewe inakuhusu nini? Huyu ni mume wangu
mie, chochote chake nina uhuru nacho umesikia eeeh! Tena usinipandishe mashetani
yangu nikuangushie matusi saizi” Erica kusikia matusi akakata ile
simu, “Hivi kweli au naota? Yani muda mwingine nakuwa mgumu kuamini kuwa
Bahati kaoa ingawa nilimshuhudia kwa macho yangu. Kweli mwanaume sio ndugu yako,
yani Bahati alivyonigeuka gafla loh hadi nashindwa kuamini” Aliwaza ya
Bahati pale kisha akawaza ya shemeji yake na
kulala. Kulipokucha alijifanya kuwa anaumwa na hatoweza kwenda
kazini, ilibidi mama yake amuache kalala kisha akamtumia ujumbe shemeji
yake, “Jana nilishikwa na tumbo la kuhara, sikuweza tu kukwambia ila
nilikuwa na hali mbaya sana ndiomana nikaondoka, sasa leo ndio tumbo linaniuma
balaa” Akamtumia ujumbe huo na baada ya muda kidogo shemeji yake
alimjibu, “Pole sana” Erica alishukuru uongo wake umetenda kazi
muda huo na kuendelea kulala kujitoa kwenye uchovu. Kwenye mida ya
mchana, Erica alipokea ujumbe toka kwa Dora, “Siamini Erica kama umeamua
kunilipizia mambo yale ya zamani kwa stahili hii wakati ulisema umenisamehe dah!
Siamini kabisa” Kabla hajatafakari ule ujumbe alisikia mtu akigonga
mlango wao, akainuka na kwenda kumfungulia. Alipofungua tu ni Tumaini aliingia
ndani na baada ya kuingia alimnasa kibao Erica, na kabla Erica hajakaa sawa
alishtukia tu kibao cha pili kikiingia kwenye shavu
lake. Kwenye mida ya mchana, Erica alipokea ujumbe
toka kwa Dora, “Siamini Erica kama umeamua kunilipizia mambo yale ya
zamani kwa stahili hii wakati ulisema umenisamehe dah! Siamini
kabisa” Kabla hajatafakari ule ujumbe alisikia mtu akigonga mlango wao,
akainuka na kwenda kumfungulia. Alipofungua tu ni Tumaini aliingia ndani na
baada ya kuingia alimnasa kibao Erica, na kabla Erica hajakaa sawa alishtukia tu
kibao cha pili kikiingia kwenye shavu lake. Kwakweli Erica alikuwa
akiugulia vile vibao na kushangaa tu kuwa imekuwaje kupigwa kiasi kile, kumbe
mama Erica alikuwa ameenda dukani kwahiyo muda ule amerudi aliweza kushuhudia
mwanae akizabwa vibao. Tumaini akamzaba kibao kingine Erica kabla hata
hajajiweka sawa, muda kidogo alienda mbele ya Erica mamake na Erica kisha
akamkunja Tumaini na kumzaba vibao vinne mfululizo kisha akamuachia na
kumuuliza, “Wewe binti umezaa? Unaujua uchungu wa mtoto wewe? Utakuja
vipi nyumbani kwangu na kumnasa mwanangu vibao?” Kisha akamgeukia Erica
na kumwambia, “Hivi mwanangu Erica una akili wewe? Mtu anaweza vipi
kukupiga nyumbani kwenu?” Akamuangalia tena Tumaini aliyekuwa akiugulia
vile vibao alivyopigwa na mama yake Erica, kisha akamuuliza “Haya
niambie kilichokufanya umpige mwanangu ni nini? Sijali kuhusu urafiki wenu,
sijali kama mmechukuliana wanaume huko, ila hapa ni nhumbani kwangu na huyu ni
mwanangu, uchungu wa Erica naujua mimi na si mwingine. Haya sema
kilichokuleta” Tumaini alikaa chini na kuanza kulia ila mama Erica
alimuangalia tu na Erica alipotaka kuinama ili ambembeleze mamake alimzuia, na
kumwambia akae pembeni na wamuache Tumaini alien a atasema
kinachomsibu. Ila kabla hawajafanya lingine lolote, Tumaini alianza
kuongea “Umenipiga mama ila umenipiga kimakosa, ungejua kwanza binti
yako alichokifanya kwangu ndio ungenipiga. Mama kwa baba yangu nina kaka mmoja
tu ambaye nasaidiana nae kwa shida na raha, sasa mwanao huyu alichomfanya kaka
yangu ni Mungu anajua, asanteni sana Mungu atanilipia” Tumaini akainuka
na kuondoka, Erica alitaka kumfata nyuma ila mama yake alimrudisha ndani na
kuingia nae sebleni kisha akamkalisha chini na kuongea nae. “Haya
niambie hayo uliyomfanya kaka yake huyu ni yapi? Na je huyo kaka yake ndio baba
yake Angel?” “Hapana mama sio” “Haya ni yapi
umemfanyia?” “Mama, ngoja nikwambie ukweli maana nimejifunza kusema
ukweli hata kilichoniponza sasa ni kusema ukweli” “Niambie sasa sio
unazunguka zunguka” “Mama, kaka yake na Tumaini niliwahi kuwa na
mahusiano nae ila yupo Afrika kusini, sasa aliachana na mimi sababu ya huyu huyu
dada yake alimpa maneno ya unafki. Nikawa na baba Angel ambaye amenitenda, sasa
kipindi hiki kaka yake kanitafuta mwenyewe kwenye simu ila hakujua kama nina
mtoto, ndio juzi kaniuliza kuwa una mtoto? Nikamjibu ndio, basi akakata simu na
sikumpata tena hewani” “Yani hiyo ndio sababu ya huyu
kukupiga?” “Ndio hivyo hivyo mama” “Kwahiyo wewe kuwa na mtoto
ndio jambo la kusema umesababisha matatizo kwa kaka yake?” “Hata mimi
sielewi mama” “Ila mwanangu hebu uache ujinga mara nyingine, hivi
unaachaje mtu akuzabe vibao kwenye nyumba yenu? Huo si ujinga
huo?” “Lakini mama, si imeandikwa mtu akikupiga kofi upande wa kushoto
mgeuzie na wa kulia” “Mungu wangu, nina mtoto mjinga haijapata kutokea,
ndiomana nakwambiaga uwe unasikiliza mahubiri, usikie watumishi wa Mungu
wakifafanua neno. Hivi dunia ya leo ilivyo eti ukipigwa shavu la kushoto geuza
na la kulia, si utaonewa sana wewe! Nimekusomesha ili kufuta ujinga kwenye akili
yako hiyo, kama hadi umemaliza chuo na una ujinga wa namna hiyo inamaana akili
yako ilikuwa mbovu zaidi, pengine nisingekusomesha ningekuwa najuta tu. Kwa
stahili hiyo si utateswa sana mwanangu, hebu achaga ujinga, kwanza neno lolote
ukilisikia njoo uniambie mama yako nikuelekeze vizuri ila ukichukulia kwa pupa
na akili zako hizo si nitakukosa wewe. Ndio nyie mkianza kuokoka sababu hamjui
kuchambua maandiko unashangaa unakutana na wale manabii wa uongo wanaanza
kukufundisha lete pesa zote kwa Mungu, unashangaa unakufa masikini sababu tu
hukutumia akili. Tumepewa akili na utashi, kila jambo linaloingia kwetu lazima
tulitafakari ndiomana kuna watu wa kutafakari neno maana ukitumia kwa akili zako
yani utaona dini ni ngumu kuifuata ila ukijua kutafakari neno utaenenda sawa
sawa na mapenzi ya Mungu. Sitaki tena kuona ujinga wa namna hii, mtu anakupiga
nyumbani kwenu, sio kwao hapa pa kujichukulia sharia, hapa ni kwenu una uwezo wa
kumtimua ila sio kumuachia akupige” “Sawa mama
nimekuelewa” “Tena unielewe vizuri na habari zako za kutangatanga na
wanaume sitaki, ukipata mchumba mlete nyumbani, habari za kutanga tanga utamleta
mdogo wake Angel asiye na baba pia. Hivi hujisikii kuwa huna furaha kuona mtoto
hana baba, ni mama mama mama, jamani hakuna raha kama mtoto kuona mama na baba,
akijisikia anasema baba, akijisikia mama, ila mtoto ni mama mama mama, inauma
sana. Usirudie tena makosa, hurumia kizazi chako” Erica alimuitikia mama
yake kwani maneno ya mama yake yalimuingia vilivyo, kisha akaendelea na kazi
zingine hata akasahau tena habari ya Dora mpaka usiku
uliingia. Alipoenda kulala wakati anashika simu ndio akakutana
na ule ujumbe wa Dora, akawaza sana “Mmmmh shemeji kamfanya nini Dora
mpaka kalalamika hivi” Akaamua kumpigia simu Dora kumuuliza na kumpa
pole, Dora alivyopokea Erica alianza kuongea nae, “Dora, nisamehe rafiki
yangu. Nilikusamehe kwa moyo mmoja hata sijadhamiria kwa chochote, kwani shemeji
kakufanya nini?” “Njoo kesho nyumbani unione” “Nyumbani kwenu ni
wapi? Nitakuja asubuhi kabla ya kwenda kazini” Dora akamuelekeza Erica
nyumbani kwao kwa njia ya ujumbe kisha Erica alisema kuwa ataenda kesho yake
kabla ya kwenda kazini. Kisha aliamua kulala, ila alipigiwa simu
akashtuka na kuangalia simu yake, akaona ni namba ya Bahati akajua kuwa Bahati
amejirudi na kupokea ile simu ambapo alianza kuongea mwenyewe moja kwa
moja, “Kwakweli Bahati umeniudhi kupita kitu chochote maishani, kwanini
unifanyie hivi kwanza? Uko wapi ule upendo uliosema mpaka kufa kwako utanipenda
tu? Kwanini Bahati” Ila cha kushangaza akasikia sauti ya mwanamke ile ya
jana ambaye alijitambulisha kama mke wa Bahati, “Dada sikia nikwambie,
kama ulikuwa na mahusiano na Bahati ni huko mwanzoni ila sasa hivi Bahati ni
mume wa mtu. Jifunze kuwa na heshima na ndoa za watu, mimi na mume wangu
tunapendana na wala hajawahi kuniambia kama alipenda mdudu kama wewe. Naomba
umkome mume wangu” “Lakini mimi sijapiga simu, umenipigia simu
mwenyewe” “Ndio nimekupigia simu ili kukujua mwizi wangu usiyeheshimu
ndoa za watu. Jifunze kuelewa kuwa Bahati kaoa sasa, huo usumbufu wa kijinga
hatuutaki tuache na mume wangu tufurahi, ndoa yenyewe bado change hii unataka
uiwekeee kigundu! Utukome” Erica aliamua kukata ile simu maana aliona ni
itamfanya awe na hasira za bure tu na aache kuwaza mambo ya maana aweze ujinga
wa kugombana na mke wa Bahati. Kisha akasema, “Sijawahi kugombana na
mwanamke yeyote sababu ya mwanaume, hebu anitolee balaa mie” Kisha kabla
ya kulala akafungulia redio na kusikiliza mahubiri kidogo, “Jifunze
kuombea wengine, Mungu atafungua milango ya baraka kwako pale unapowaombea
wengine. Sio unajikumbuka wewe tu, ila kumbuka na wengine” Erica akazima
redio na kusema, “Hawa wahubiri nao kila leo wana jipya, kwahiyo
wanataka nimuombee mke wa Bahati? Nimuombee nini sasa? Wanaona kabisa nimemaliza
kuongea na adui yangu eti jifunze kuombea wengine. Jamani mambo mengine, ngoja
nilale zangu mie” Kisha akaamua kulala tu. Asubuhi na
mapema aliamka na kujiandaa kwenda kazini ila kama alivyopanga kuwa hatoenda
kazini kwanza hadi apitie kwakina Dora, kwahiyo alimtumia shemeji yake ujumbe
kuwa anapitia hospitali halafu ndio ataenda kazini, shemeji yake alimjibu
kawaida tu kuwa poa. Hakujiuliza sana akaona labda shemeji hataki kumuhoji hoji
sana. Erica alienda hadi kwakina Dora ambapo alipofika kituoni alipiga
simu halafu mdogo wa Dora alifika na kumpeleka hadi kwakina Dora, ambapo
aliingizwa hadi chumbani alikolala Dora kisha Yule mdogo wake alimuacha na Dora
na kutoka nje. Erica alikaa karibu na Dora na kumpa pole huku akimuuliza
kipi kimetokea, “Erica sikutegemea Yule shemeji yako ni mshenzi kiasi
hiki” “Mmmh Dora usitukane tafadhari” “Nisitukane kitu gani?
Unajua alichonitenda? Tena ngojea nikuonyeshe namna ya kumtusi” Dora
alianza kuporomosha matusi na kumfanya hadi Erica aogope, kisha
akamwambia, “Dora, ukiendelea na hayo matusi kwakweli sitaweza
kuvumilia, unajua kabisa mimi na matusi ni mbalimbali” “Mbona ukayafanya
hadi ukapata mimba na kuzaa” “Dora, Dora nakuhurumia ndiomana niko hapa,
sijaja unipe matusi au unionyeshe uwezo wako wa kutukana. Sijalelewa hivyo
tafadhari, kama hayo mengine niliyofanya yaache nilifanya ila siwezi hayo ya
kuongea. Wewe nishakupa pole, nimekuuliza nini kimekusibu unaanza kuporomosha
matusi hivi hata ukifika mahakamani ukaporomosha hivyo matusi ni nani ataonekana
mwenye makosa kati yako na shemeji yangu?” “Haya yaishe ila shemeji yako
kanifanyia kitu kibaya sana, hadi nikawaza kuwa labda umemtuma anifanyie vile
maana wewe ulikimbia na kuniacha nae” “Hapana, mimi tumbo lilinishika na
muda ule ningemuaga shemeji angekataa tu si unaona alikuwa akinibishia
nisiondoke” “Haya bhana, shemeji yako Yule nina haki ya kumuita mshenzi
maana alichonifanyia hakifai hata kidogo.Tulikunywa pombe na shemeji yako pale
balaa, na wewe hukutokea, nilikuwa nimelewa haswaa nikaamua kumuaga kuwa
naondoka ila shemeji yako akasema twende club, sababu nilikuwa nimelewa nikaenda
nae, huko nako tulikunywa sana na nilikuwa nimelewa sana. Shemeji yako
akanichukua sijui akanipeleka chumba cha hoteli kumbuka nilikuwa nimelewa,
shemeji yako akanibaka na kunifanyia mchezo mbaya maana alinifanya kinyume na
maumbile” Erica akashtuka na kushangaa sana, “Kheee shemeji ndio
ana tabia chafu kiasi hiko?” “Ndio hivyo, tena alivyo mshenzi sababu
nilikuwa sijitambui kanitoa pale hotelini na kaenda kunitupa karibu na mtaro,
watu ndio wameniokota na kunileta nyumbani. Kwakweli alichonifanyia shemeji yako
hapana, nimeenda kushtaki polisi ila shemeji yako kanikana kabisa kuwa hafahamu
chochote kuhusu mimi, yani Erica nimeumia sana, shahidi yangu ni wewe maana kesi
ipo mahakamani” Kwakweli Erica alisikitika sana maana alichofanyiwa
rafiki yake hakikuwa kitendo cha utu hata kidogo, ingawa rafiki yake huyo
amewahi kumtendea mambo mabaya ila yeye hakupanga vitu vibaya kwa huyo rafiki
yake. Erica alikuwa kimya tu kisha Dora aliendelea kuzungumza, “Eraca
tafadhari nakuomba uwe shahidi wangu maana ni wewe tuliyekuwa pamoja na ndio
unajua kuwa uliniacha na shemeji yako. Kanifanyia kitendo cha kikatili sana,
sina nguvu sasa nalala tu unadhani kubakwa ni jambo rahisi? Raha ya mapenzi
ufanye kwa utayari ila sio kwa kubakwa halafu kitu kinachoniuma zaidi ni kile
kitendo cha kuniingilia kinyume cha maumbile, Erica inauma asikwambie
mtu” “Pole sana rafiki yangu yani nawaza nakosa hata
jibu” “Nisaidie rafiki yangu, nahitaji kupata haki kwa kindendo
nilichotendewa, najua huyu mtu ni shemeji yako ila kumbuka kuwa mimi ni mwanamke
mwenzako” “Naelewa Dora, nitakusaidia. Pole sana” Kisha Erica
aliamua kumuaga Dora, na kumuachia hela kidogo kwaajili ya kumsaidia
saidia, “Sina pesa ndugu yangu, ila pokea hiki
kidogo” “Nashukuru Erica, ila usiache kuja mahakamani kutoa ushahidi
nakuomba” “Usijali nitafika” Kisha Erica akaondoka na kumuona
shemeji yake ni mtu asiyefaa kabisa kwenye jamii maana hakuelewa ni kwanini
katenda kitu kama kile kwa Dora. Alitembea njiani akielekea kituoni huku
akiongea mwenyewe, “Yani wanaume sijui wana akili gani jamani? Kweli
kabisa shemeji anafanya ujinga kiasi hiki! Nawachukia wanaume mie, siwataki
kabisa, bora niishi mwenyewe kwa stahili hii sio kwa haya jamani, dada yangu
namuhurumia maana sijui awe na moyo wa aina gani kuweza kupokea upuuzi huu
alioufanya mumewe” Wakati anaongea peke yake, kuna gari ilikuja na
kupaki mbele yake. Mwenye gari alishusha kioo na kumsalimia
Erica, “Habari yako binti” “Salama” “Si unaenda stendi,
twende nikusogeze” “Hapana, asante nafanya mazoezi ya
kutembea” “Aaah! By the way naitwa Jimmy, sijui wewe unaitwa
nani?” “Naitwa Erica” “Sawa Erica, basi naomba namba
zako” Akakumbuka maneno ya mama yake na kumwambia, “Hapana,
siwezi kukupa namba. Mimi ni mke wa mtu, na sipendi kuongea kwenye simu na mtu
mwingine zaidi ya mume wangu” “Hebu acha kunichekesha Erica, umesikia
wake za watu huwa hawatoi namba? Unajua namba yako naitaka ya nini? Pengine ni
maswala ya kazi? Sio kila mwanaume anayetaka namba zako ni ana lengo la
kukutongoza, hebu futa hiyo fikra kwanza. Utakosa bahati kwa kujifanya oooh mimi
mke wa mtu. Shauri yako, mimi nahitaji namba yako maana kuna kazi nataka
kukushirikisha” Erica akafikiria kidogo na kuamua kumtajia mtu Yule
namba yake sababu mtu Yule alionekana ni mtu wa makamo na mwenye heshima zake,
kisha akaagana na Erica. Erica alielekea ofisini, na alipofika
kwenye meza yake tu James alimuita, kiukweli Erica alienda ofisini kwa James ila
hakuwa na amani anayokuwaga nayo siku zote. James alimsalimia kisha
akamwambia, “Najua Yule mjinga kashakuelezea habari za kijinga ndiomana
umekuja bila amani” “Hapana shemeji ila kwanini umefanya
vile?” “Erica, wewe ni msomi ila nashangaa umeanza vipi urafiki na Yule
msichana asiye na akili hata kidogo” “Hata kama hana akili ndio umfanyie
vile kweli?” “Erica, unanifahamu vizuri shemeji yako na unamfahamu
vizuri mke wangu Bite, hivi nina mke mzuri kama Bite halafu nikafanye ujinga na
Yule rafiki yako mjinga mwenye sura nzito kama uji kweli? Nampenda sana mke
wangu, Bite wangu mzuri bhana, hawezi kufanana na ujinga ujinga
ule” “Mmmh shemeji, kumbuka nilikuacha nae” “Sikia Erica, labda
kama umepanga na Yule mjinga wako kunichafua jina langu ila kumbuka mimi ni
shemeji yako tena ni mume wa dada yako mzazi ambaye umezaliwa nae tumbo moja.
Ukisikiliza maneno ya kijinga unataka nini kwangu? Huwa nakusaidia kwa moyo
mmoja na hata sina lengo baya, nilikwambia mambo ya kijinga niliyoyafanya mwanzo
hayapo tena kwangu, nianze vipi kwa rafiki yako asiye na mvuto
Yule!” Erica alikuwa kimya tu akimsikiliza shemeji yake anavyojitetea,
kisha James akaendelea kuongea, “Sikia siku ile ilivyokuwa, baada yaw
ewe kuondoka na hukurudi tena nikakupigia simu hukupokea. Nikaenda kuangalia
chooni ila kuna mtu alikuona akasema kuwa uliondoka, nilirudi na kukaa na Yule
mjinga, nikamtaarifu kuwa umeondoka ila hakuwa hata na mashaka aliendelea kunywa
pombe na kula nyama. Msichana hajielewi hata robo Yule, anakunywa kila kilevi,
castle lite twende, dompo twende, valuer twende mpaka konyagi jamani Yule rafiki
yako kashindikana. Namwambia mimi naondoka anadai yeye anaendelea kupombeka
ikabidi kwa huruma yangu nimuachie hela hata akimaliza kulewa akodi tax arudi
kwao, nilimuachia elfu hamsini nikaondoka zangu. Nashangaa kuitwa polisi eti
nina kesi ya kubaka sijui kumuingilia mtu kinyume na maumbile na kumtupa, jamani
Yule binti sina hamu nae loh! Ataje aliokuwa nao kwenye ulevi wake, muda huo
nilikuwa na familia yangu mie nalala na mke na mwanangu halafu yeye ananiletea
habari za kijinga kiasi hiko” “Kheee kumbe ndio
ilivyokuwa?” “Ndio hivyo Erica, najua atakuwa amekulisha sumu ili
kuniona mimi mbaya. Hivi rafiki yako anachofanya si kunichafulia jina jamani!
Mimi nina kampuni yangu na nina pesa zangu halafu kijitu cha ajabu ajabu
kinataka kunichafulia jina jamani dah! Hivi nikitaka mwanamke mimi naweza
kukosa? Kama pesa ninayo, mgonjwa mkubwa wa mwanamke ni pesa, licha ya hivyo
machangudoa wamejaa tele si ningewachukua na kufanya nao ujinga huo kama
nahitaji kufanya ujinga ila mimi siwezi kufanya hivyo, naiheshimu familia yangu
Erica, nampenda dada yako naomba uelewe na uondoe dhana potofu kuwa mimi naweza
kufanya ujinga wa namna ile. Erica wewe ni binti uliyesoma, achana na marafiki
wasiojielewa” Erica alimsikiliza shemeji yake kisha akamuaga kuwa
anaenda kufanya kazi sasa, ila James aliendelea kuongea na
kumwambia, “Unapokuwa kwenye kazi zako hapo jaribu kufikiria kama mimi
naweza kufanya ujinga ulioambiwa na rafiki yako. Sipendi kusingiziwa mimi,
nampenda sana mke wangu” Erica alienda kukaa na kuendelea na kazi zake
ila kiukweli mpaka muda huo hakujua wa kumuamini ni nani kati ya Dora na shemeji
yake James maana wote walionekana kuwa wanaongea ukweli. Erica alifanya
kazi zake na alipomaliza alimuaga shemeji yake na kwenda zake
kwao. Alifika kwao akitafakari mambo ya Dora na shemeji yake
James ila hakupata jibu na hata hakujua kuwa akienda mahakamani atasema nini
maana hakujua ukweli, ukizingatia ukweli waliujua wenyewe wawili kwahiyo kwa
Erica ilikuwa kitendawili kikubwa sana. Basi akaoga na kula kisha kwenda
chumbani kwake na mwanae, muda kidogo akapigiwa simu, namba ilikuwa ni ngeni
akapokea na kuanza kuongea nayo, “Hallow, nani mwenzangu?” “Mimi
Jimmy, Yule umekutana naye mchana. Unaendeleaje muda huu?” “Salama
tu” “Mbona mimi huniulizi kuwa naendeleaje?” Erica akaona mitego
hiyo, ila akaamua kujigelesha na
kumuuliza, “Unaendeleaje?” “Kiukweli siendelei vizuri maana nina
mawazo haswaaa” “Aaah pole” “Asante, ila hujaniuliza ni mawazo
ya nini?” “Haya, ni mawazo ya nini?” “Erica, tangu nimekuona ile
asubuhi sina raha kabisa, nipo kazini nakuwaza tu wewe. Nakupenda
Erica” “Ila si nimekwambia mimi ni mke wa mtu?” “Kwani mke wa
mtu kitu gani Erica? Kwani ukinipa naondoka nayo jamani? Si inabaki kwako?
Niponye mtoto wa mwanamke mwenzio” Erica akakata ile simu na akaizima
kabisa kwani hakutaka gasia maana kwake zilikuwa gasia zile ukizingatia
alishaanza kukataa habari za wanaume, ingawa hakujua kati ya shemeji yake na
Dora ni nani mwenye makosa. Aliamua kulala, wakati amelala akajiwa na
njozi kuwa Erick yupo hospitali na ana hali mbaya sana, aliamka na kuhema sana
alijikuta tu akipiga magoti na kuomba, “Eeeh Mungu nakuomba mtetee Erick
na afya yake, sikukusudia mimi kumfanya aumwe au awe katika hali mbaya. Nakuomba
Mungu wangu nisamehe kwa yote niliyoyatenda, naomba itetee afya ya Erick.
Amen” Alirudi tena kitandani akachukua simu yake na kuiwasha, ila
alipoiwasha tu kuna ujumbe uliingia kuwa amepokea muda wa maongezi wa shilingi
elfu kumi, alipoangalia aliona umetokea kwa Yule mzee Jimmy, ila kwa muda huo
Erica hakutaka kufikiria kuhusu Yule mzee, kwahiyo alimpigi Tumaini ili kujaribu
kuulizia hali ya Erick ingawa hakujua kama Tumaini angepokea simu yake au la ila
kwa muda mfupi tu Tumaini alipokea ile simu na alivyopokea tu akamwambia
Erica, “Nakutumia namba za hospitali upige mwenyewe simu uongee na
Erick, sitaki kusema chochote mimi” Tumaini akakata simu halafu
akamtumia namba Erica, ambapo Erica alizipiga zile namba na kuomba kuongea na
Erick ambapo Erick alipewa ile simu, “Ni wewe Erica kweli ndio umepiga
muda huu?” “Ndio ni mimi Erick, nakuombea upone baba
yangu” “Erica umeniita baba?” “Ndio, wewe ni mwanaume na
unauwezo wa kunilea kwahiyo wewe ni kama baba kwangu” “Siamini Erica,
ila nitakutafuta kesho” Erick alionekana kuongea kwenye hali ya furaha
sana hapo mwishoni kwahiyo akaagana na Erica na kukata simu, kisha Erica akalala
sasa. Kulipokucha kama kawaida akajiandaa na kwenda kazini,
alifika na kufanya kazi zake, ila kwenye mida ya saa nne alipigiwa simu na Yule
meneja wa benki akimtaka Erica aende muda huo, kwahiyo Erica alienda kumuaga
bosi wake kisha kwenda huko benki. Alifika na kuingia ofisini kwa
meneja, “Nimekuita hapa, maana leo kuna kikao cha bodi na wakurugenzi
wote watakuwepo. Niliwasilisha kuhusu swala la mwanao na wamempenda sana,
tunahitaji mwanao awe balozi wa akaunti ya watoto hapa benki” Kwakweli
Erica alijihisi furaha sana moyoni mwake, na hata hakupinga kuhusu swala hilo
kisha baada ya lisaa limoja Yule meneja akamwambia Erica kuwa aende nae kwenye
kikao ili amtambulishe na kisha kesho yake amlete mtoto wake, Erica alikubali na
kuanza kufatana na Yule meneja. Kisha walipokarinia Yule meneja
akamwambia Erica, “Inabidi uwe na majibu mazuri maana leo na mkurugenzi
mkuu yupo” “Sawa” Wakaingia ndani, Erica akaona kuna wababa
watano, kisha kuna mmoja alikuwa amekaa kwenye kiti cha mbele ambapo Yule meneja
alimwambia Erica kwa taratibu, “Yule wa mbele ndio mkurugenzi
mkuu” Erica alipomuangalia vizuri, akagundua ndio Yule mzee
Jimmy. Wakaingia ndani, Erica akaona kuna wababa
watano, kisha kuna mmoja alikuwa amekaa kwenye kiti cha mbele ambapo Yule meneja
alimwambia Erica kwa taratibu, “Yule wa mbele ndio mkurugenzi
mkuu” Erica alipomuangalia vizuri, akagundua ndio Yule mzee
Jimmy. Alijikuta akiishiwa nguvu kabisa ila bado alisimama ili kujua
hatma yake, alimsikia Yule meneja akimtambulisha Erica kwa wale
wakurugenzi, “Huyu anaitwa Erica, ndio mama wa Yule mtoto” Kisha
meneja akatambulisha majina ya wale wakurugenzi kwa Erica, ila alishangaa kuona
mzee Jimmy hata hakushtuka wala hakujifanya kumfahamu zaidi zaidi walimuuliza
baadhi ya maswali kisha Mzee Jimmy akasema, “Binti, Jumamosi saa nne
asubuhi umlete huyo mtoto wako tuje tumuangalie vizuri na tukusainishe mikataba
yetu” Erica alikubali, kisha wakamruhusu kuondoka. Kwakweli alivyotoka
nje ya ile benki ndio aliweza kupumua sasa, huku akiliangalia lile jingo refu la
ile benki. Alikuwa amekubali tu ila hakujua kwakweli kama itakuwa rahisi maana
Yule mzee alishaonyesha kumtaka. Erica alirudi ofisini akiwa hana raha
kabisa, James alimuita na kumuuliza kuwa imekuwaje alipotoka maana alimdanganya
kuwa anaenda hospitali, “Mbona unaonekana huna furaha?” “Hamna
mbona nipo kawaida tu” “Erica, nakufahamu wewe pengine kupita hata
unavyojifahamu au umeanza tena kumuwaza Yule mwanaume
wako?” “Hapana” Kisha Erica akaenda kuendelea na kazi zake ila
muda huo ndio alianza kumfikiria Erick sasa, alitamani kujua Erick anaendeleaje,
aliinuka na kutoka nje kisha kupiga ile namba aliyopewa usiku, ila alipopiga
aliambiwa kuwa Erick aliruhusiwa kurudi nyumbani na aliendelea vizuri, muda huo
Erica aliamua kupiga namba ya Erick, na kweli iliita na kumfanya afurahi sana
kisha Erick akapokea simu, “Unaendeleaje Erick?” “Salama kabisa,
unanijali hadi kunijulia hali!” “Ndio nakujali Erick” “Hivi
kweli unanipenda Erica?” “Ndio nakupenda sana Erick” Muda huo
kumbe James alikuwa nyuma ya Erica kwahiyo lile neno la mwisho alilosema Erica
alilisikia vizuri sana, akamfokea Erica hadi akaangusha simu “Yani
unaacha kufanya kazi unaanza kuongea maswala ya mapenzi ofisini? Haya Erica,
nifate ofisini kwangu” Erica aliinama kuokota simu yake kisha akamfata
nyuma James kuelekea ofisini kwake ila kwa mara ya kwanza aliweza kuona sura ya
James ikichukia sana na kuonyesha hasira za waziwazi, Erica alipofika James
alianza kuongea, “Erica, kipi kimekufanya uwepo hapa
ofisini?” “Ni kazi bosi” “Sasa kazi ya kuongea na simu na
kumwambia mtu unampenda ndio iliyokuleta hapa ofisini?” “Nisamehe
bosi” “Aaah umenikera sana, mimi napenda kazi, muda wa kazi fanya kazi,
na muda wa madudu yako huko fanya madudu sikuzuii ila sio ofisini kwangu. Erica
katika wafanyakazi wangu umekuwa namba moja kuomba udhuru mara leo sijui
imekuwaje, mara nampeleka mtoto kliniki, mara naenda kumfungulia mtoto akaunti,
mara tumbo linaniuma siji, mara naenda hospitali yani umefanya kama ofisi hii ni
ofisi ya baba yako sasa yani unafanya unavyotaka wewe na sio anavyotaka mwenye
ofisi. Ushemeji wa mimi na wewe unaishia nyumbani lakini sio ofisini, ndiomana
watu huwa hawaajili ndugu zao sababu ya mambo kama haya yani kazi haziendi na
ndugu akitoa taarifa lazima umsikilize hata kama hiyo taarifa ni uongo.
Nimekuvumilia sana Erica, na sasa naomba nikwambie kuwa nimekusimamisha
kazi” “Jamani shemeji nihurumie” “Nishakwambia, ushemeji ni
nyumbani, ila nikiwa ofisini sina ushemeji na wewe. Yani uharibu kazi zangu kwa
dhana ya ushemeji? Kuna umuhimu gani wa kumuajiri mtu asiyejielewa kama wewe?
Yani huna akili hata kidogo, unabebwa ila hubebeki, unataka ufanyiwe nini
ubebeke? Erica, nishafanya upande wangu hata Mungu mwenyewe anaona ila kwasasa
nimechoka, na ninamaanisha kuwa nimekusimamisha kazi” Erica akapiga
magoti kwa shemeji yake huku akilia na kuzidi kuomba msamaha, “Naomba
unisamehe bosi, haitajirudia tena” “Mwambie huyo uliyekuwa unamwambia
kuwa unampenda sana akutafutie kazi ila kwangu umesimamishwa kwasasa, mpaka pale
nitakapoamua mimi kukurudisha tena kazini” Erica alikazana kuomba
msamaha ila shemeji yake alishaamua kwani alichukizwa sana na ile simu ya Erica
ya kusema ‘nakupenda sana Erick’ yani muda wote alijikuta hilo neno likiimba
kwenye kichwa chake kama mziki, kwahiyo hakuweza tena kuendelea kumuona Erica
hapo ofisini, kwahiyo Erica ilibidi ainuke na kwenda kuweka sawa kazi zake kisha
kudhikabidhi na kuondoka. Alikuwa na mawazo sana, alihisi kama kichwa
chake kitavurugika tena maana hakujua kuwa amekosa kazi atafanya nini tena,
maana lile swala la kwenda kazini tu lilikuwa likifariji moyo
wake. Akiwa kwenye daladala alichukua simu yake na kuiangalia, aliiona
kioo hakitamaniki kabisa maana aliiangusha sana na kumfanya akose raha zaidi ila
akaiwasha na ikawaka, akaona ni vyema imewaka ingawa imevunjika kioo ila swala
la kuwaka lilikuwa ni bora kwake maana hakutaka kutumia hela yoyote ya mtoto
wake kwaajili ya kununua simu ukizingatia kazi tena ndio ilikuwa basi, sasa
akianza kujiendekeza kutumia hela za mtoto itakuwaje? Alishukuru tu vile simu
inawaka. Alifika nyumbani kwao hata mama yake alishangaa jinsi
mwanae alivyowahi sana siku hiyo, “Mbona leo mapema
zaidi?” “Mama nimesimamishwa kazi” “Kheee James kakusimamisha
kazi au nini?” “Ndio” “Chanzo nini?” “Alinikuta naongea
na simu” “Wewe nae, unaongea na simu ofisini jamani! Hata hivyo simu tu
ndio usimamishwe kazi! Ni kawaida yako kuongea na simu au?” “Halafu mama
sikuongea ofisini, nilitoka nje kumbe na yeye alikuja nyuma yangu na akanisikia
kuwa naongea na simu ndio balaa” “Mmmh ngoja ninyamaze mie nisiongee
sana maana sizijui sharia za hiyo ofisi ila kuongea na simu mara moja tu jamani
loh! Tulia mwanangu, haikuwa ridhiki yako, kuna mahali Mungu kakuandikia, hata
usiwe na mawazo sana. Si unaniona mama yako eeeh! Nimekuwa mpole siku hizi,
sitaki tena kufanya makosa ya mwanzo kwako mwanangu, nahitaji ukae kwenye mstari
ulionyooka. Tulia mwanangu, kama ridhiki yako ipo basi ipo tu” “Asante
mama” Kisha Erica alienda chumbani kwake, kwavile alihisi kama kuvurugwa
vurugwa akaamua kulala. Ilikuwa jioni sana akastuliwa na mlio wa simu
yake, kuangalia mpigaji alikuwa ni Erick, akapokea na kuongea
nae, “Mbona muda ule ulikata simu gafla Erica?” “Aaah muda ule,
aaah simu iliniponyoka ikaanguka” “Aaah pole, haijaharibika
kweli!” “Imevunjika kioo tu, ila sio sana” “Pole sana Erica,
unafanya nini muda huu?” “Nimejilaza tu” “Mwanetu yuko
wapi?” Erica alijihisi fahari sana baada ya Erick kumuita mtoto wa Erica
mwanetu kwamaana hiyo Erick alikuwa amemkubali mtoto wa Erica, alijibu kwa
furaha sana, “Yupo kwa bibi yake” “Aaah sawa, haya pumzika mama.
Nitakutafuta tena. Msalimie sana mtoto wetu” Kisha Erick alikata simu
ila kwenye moyo wa Erica ilikuwa ni furaha sana maana hakutarajia kama ingekuwa
rahisi vile kwa Erick kumkubali Angel, alijikuta akisema, “Kweli kabisa
ukweli humuweka mtu huru, na ukisema ukweli Mungu nae atakusimamia. Kwakweli
Mungu kanisimamia ingawa nilitoa ukweli wa kuumiza ila mungu kanisimamia. Asante
Mungu” Erica aliinuka sasa na kwenda kumchukua mtoto kwa mama yake kisha
kuendelea na mambo mengine mpaka muda wa kulala. Kulipokucha
aliendelea na shughuli zake zingine, ila alipochukua simu yake alikuta kuna
ujumbe kutoka kwa Dora, “Erica, nakuomba mara moja. Njoo
nyumbani” Kwavile mwenzie alikuwa anaumwa, Erica aliamua kwenda kumuaga
mama yake kwanza ili apate ruhusa ya kwenda, “Haya, kazi umesimamishwa.
Unaenda wapi? Ndio kutafuta kazi nyingine?” “Hapana mama, kuna rafiki
yangu anaumwa ndio niende kumuona” “Na uwahi kurudi sio maswala ya
kunirudia usiku hapa wakati haupo kazini” “Sawa mama” Kisha
Erica akamaliza shughuli zake na kwenye mida ya saa sita alijiandaa na akaondoka
zake kwenda kwakina Dora. Alifika na kumkuta leo Dora kachangamka
tofauti na ile juzi aliyofika kumuona, akamuuliza kama anaendeleaje na Dora
alimwambia kuwa anaendelea vizuri kabisa. “Ila nilichokuitia hapa ni
yale yale, nakuomba msaada Erica, nahitaji kupata haki yangu. Wewe ndio shahidi
pekee uliyebaki, unajua nimeenda kwenye ile hoteli tuliyoenda kula kuku
wamenikana kabisa, hata Yule muhudumu aliyetuhudumia nikawa namkumbusha hadi
matukio yaw ewe kukataa pombe na kutaka soda ila amenikana kabisa na kusema
hajawahi kuniona na hawezi kutoa ushahidi kwenye kesi za uongo. Nimeenda kule
club ila napo wamenikana kabisa, hapa pale tulipoenda kulala na shemeji yako
wamenikana. Jamanai Erica najua watu hawa wamepewa pesa ndiomana hawawezi kuwa
upande wangu, sasa mtetezi wangu umebaki wewe tu” “Dora, samahani yani
mpaka hivi sasa kesi yenu bado inanipa maswali mengi maana wewe unavyonielezea
vingine na shemeji nae anavyonielezea vingine” “Anasemaje
kwani?” Erica akaanza kumuelezea vile ambavyo ameelezewa na James, ila
ambacho hakumwambia ni kuwa tu James amesema kuwa ana sura nzito, yani hilo ndio
hakumgusia ila yote aliyoelezewa na James alimwambia. “Khaaa Erica, Yule
shemeji yako ni muuwaji jamani, yani ametunga story kiasi hiko? Sikatai kweli
napenda kunywa ndio nibaki kunywa peke yangu? Na je ni nanai aliyekuwa
ananinunulia pombe? Erica nilikuwa na akili zangu timamu hadi tunaingia chumbani
naelewa ila ndio nikalala sababu ya pombe na shemeji yako akatumia mwanya huo
kunifanya vibaya na kwenda kunitupa. Au alijua nimekufa kwahiyo alinitupa ili
kuepuka ushahidi? Hapana kwakweli shemeji yako mtu mbaya sana.” Muda
kidogo Dora aliitwa nje kwahiyo alitoka na kumuacha Erica pale ndani, kwakweli
Erica bado alijiuliza maswali bila ya jibu, ukumbuke kashamuudhi shemeji yake
ofisini halafu asimame kwenye kesi amtetee Dora si atachukiwa zaidi tena sio na
shemeji yake tu bali hata dada yake atamchukia maana Yule ni mume
wake. Wakati akitafakari hayo, kuna ujumbe uliingi kwenye simu yake,
alipouangalia ulikuwa unatoka kwa mzee Jimmy, “Hujambo binti mzuri
Erica, naomba leo tuonane jioni saa kumi. Kuna mambo nahitaji kuongea na wewe
kabla ya kesho kusaini mkataba” Erica aliguna na kushindwa kujibu huo
ujumbe kabisa kwani alihisi kama unamuongezea mawazo tu. Alikaa kimya kwa muda,
ila akapokea ujumbe mwingine toka kwa mzee Jimmy, “Mbona hujanijibu
mtoto mzuri? Juwa bila mimi hakuna chochote kinachoweza kufanyika, nahitaji
kuongea nawe maswala ya biashara. Unajua kama hii ya mwanao kuwa balozi ni swala
la biashara? Basi kutana na mimi tujadiliane maswala haya, nijibu
tafadhari” Erica alikuwa kimya tu maana hakujua kuwa ni kitu gani amjibu
maana aliona akimchanganya tu, Dora akarudi ndani na kuanza kuongea na rafiki
yake “Yani kuna watu wana mambo ya ajabu sana, unajua mimi nilipopatwa
na matatizo juzi basi nilipelekwa kwanza kwa mamangu mdogo halafu ndio kuletwa
nyumbani kwahiyo mamdogo anajua kila kitu kilichonipata. Jamani mwanamke Yule
unajua kanitangazia kwa watu yani mpaka anawaambia msimuone hajaenda kazini ana
majanga ya kubakwa, jamani kweli kabisa huyo ni ndugu au muuwaji?” “Pole
mwaya, ila si mamako mdogo kabisa huyo?” “Ndio ila ni mbeya balaa hadi
kwenye ukoo wanamtengaga sababu ya umbea, sasa kunitangazia mimi nimebakwa ndio
anapata faida gani sasa? Kunichafulia jina tu mtaani hapa, halafu huyo shemeji
yako ajiangalie. Erica ngoja nikwambie kitu, nikishindwa kwenye kesi mimi, huyo
shemeji yako nitamuendea hata kwa mganga, kama amezoea kusumbua wengine basi sio
mimi” “Kheee Dora, bado una imani za waganga tu?” “Hebu na wewe
nitolee maswali ya kijinga huko, kuna mtu kwenye dunia hii haendi kwa mganga?
Wewe mwenyewe na familia yako mnaendaga ila mmefanya siri.” “Mmmmh
kwahiyo hata kaka yangu ungemroga wewe eeeh!” “Ningeamua hata
nisingeshindwa sema kwavile kaka yako mwenyewe ana hela za mawazo wala siwezi
kujisumbua, ila angekuwa dizaini ninayotaka mimi ningemroga ndio kwanini
nikufiche? Watu wanaroga huko na wanafanikiwa, maisha haya bila kujikinga kinga
ni ngumu kufanikiwa” “Mmmmh leo umeniambia makubwa Dora, hata
sikukufikiria. Ila kiukweli mimi sijawahi kwenda kwa waganga toka nizaliwe hata
sijui kukoje” “Basi siku nikupeleke” “Hapana shoga yangu, mimi
namuamini Mungu tu” “Ambaye hamuamini Mungu nani? Hao waganga wenyewe
wanamuamini Mungu, yani usijidanganye kuwa waganga hawana Mungu, hata wao
wanamuamini Mungu ndiomana wapo” “Mmmh haya rafiki yangu, ila kwa hilo
nimekushindwa tabia” “Hebu acha ujinga na wewe Erica
jamani” Muda huo simu ya Erick ilikuwa ikiita anaikata sababu mpigaji
alikuwa ni mzee Jimmy na hakuwa tayari kuongea nae ingawa hata hakujua hatma ya
mwanae na swala la kuwa nalozi wa benki. Kisha Erica aliamua kumuaga rafiki yake
ila bado Dora alimsisitizia kuwa akamtetee mahakamani siku ya kesi, Erica alimpa
moyo Dora kuwa ataenda ila kiukweli Erica alianza kukata tamaa ya kwenda kwenye
kesi kabisa, na vile mwenzie alivyosema maswala ya kwa mganga ndio yakamvuruga
kabisa. Basi Dora akaamua kujiandaa vizuri ili kumsindikiza Erica maana
leo alidai kuwa na nguvu kabisa tofauti na siku ile alikuwa na
maumivu. Basi wakawa wanatembea njiani wakielekea kituoni,
gafla kuna gari ilikuja na kusimama mbele yao, kioo kiliposhushwa ni mzee Jimmy
ambapo alimsalimia Erica, “Hellow Erica” Dora alimwambia Erica
kwa sauti ya chinichini, “Erica wewe matawi, hadi unafahamika na huyu
mzee” Erica alimuangalia Yule mzee na kuitikia salamu yake kisha
akamuamkia, Yule mzee akamuitikia na kumuuliza, “Mbona hupokei simu
zangu?” “Simu yangu imeharibika spika” “Aaah si ungeniandikia
hata ujumbe, twende basi kwenye mazungumzo” Erica hakushindwa kujitetea
hapo ila akamwambia Dora kuwa waende wote, yani Dora kwa Yule mzee alijikuta
akisahau kabisa mambo yaliyompata na kukubali kuongozana na Erica. “Nipo
na huyu sasa itakuwaje?” “Basi, twendeni wote” Basi wote
wakaingia kwenye gari ya mzee Jimmy na safari ikaanza, moja kwa moja walifika
mjini kwenye duka kubwa la simu kisha Erica akaambiwa achague simu anayoitaka,
Erica alisema yoyote, Yule mzee akachagua simu na kulipa pale milioni moja keshi
kisha Erica akakabidhiwa ile simu, alimshukuru Yule mzee na kuwataka warudi tena
kwenye gari kisha safari ikaendelea hadi kwenye hoteli Fulani ambapo walishuka
na kukaa mahali kisha Yule mzee aliwaambia waagize vinywaji halafu yeye aliinuka
kama kuna mtu anaenda kuongea nae. Waliagiza vinywaji, kisha Dora alimuangalia
Erica na kumwambia, “Unajua Erica una bahati sana, huyu mzee
umemjuaje?” “Tena nilimjua siku ileile niliyotoka kwenu alitaka kunipa
lifti kwa gari yake” “Aaah rafiki yangu una bahati, umeogea mpendwa
pendwa nini?” “Ndio nini?” “Aaah tuachane na hayo, ila rafiki
yangu una bahati. Jamani mzee tajiri huyu, ni ana hela uchafu halafu hana hata
familia ya kumuumiza kichwa maana watoto wake wote wakibwa, ni ana watoto wawili
tu. Mzee ana hela huyu Erica, uwiii yani huyu unamwambia akujengee nyumba tena
anakujengea ya kifahari, unamwambia akununulie gari, anakununulia gari la
kifahari, unamwambia nifungulie ofisi yani ukiwa na huyu mzee hata kazi kwa
shemeji yako unaacha” “Dora, umejuaje habari za huyu
mzee?” “Namfahamu huyu mzee ni tajari hapana” “Watoto wake wako
wapi?” “Sijui, sijawahi kuwaona nasikia wana malingo sana. Sitaki
kuwafahamu ila baba yao ni hatari, mzee tajiri huyu Erica. Kama anakutaka wala
usijifikirie mkubali upesi” “Mmmh kwakweli mimi nina mwanaume wangu
nampenda sana anaitwa Erick” “Na wewe Erica unaleta habari za vijana,
ulisikia wapi vijana wakawa na mapenzi ya kweli? Kitu wazee wanajua kupenda,
wanajua kuhonga yani hadi raha. Erica kweli rafiki yangu kama huyu mzee
anakutaka usimkatae” Muda kidogo mzee Jimmy akarudi na kuanza kuongea
nao, “Mbona mmeagiza juisi tu!” Dora akacheka na kutaka kuagiza
pombe ila Erica aliwahi na kumwambia mzee Jimmy, “Huwa hatutumii vileo
ndiomana tumeagiza juisi” “Aaah vizuri lakini” Kisha mzee Jimmy
alianza kuongea pale pale tena bila hata ya kumuhofia Dora, “Sasa Erica,
mwanao unahitaji awe balozi wa benki yetu. Mimi ndio mkurugenzi mkuu wa benki
ile, kama ukifanya ninavyotaka mimi basi mkataba wa mwanao dau lake litakuwa
mara tatu ya lilivyo sasa.” Erica alikuwa kimya huku akiinama chini na
kujiuliza kuwa Yule mzee anataka mambo gani tena, kisha Yule mzee akaendelea
kuongea, “Sijaona shida ya kuongea mbele ya rafiki yako, binti unaitwa
nani kwanza” Dora bila hiyana alitaja jina lake upesi
upesi, “Naitwa Dora” “Unanifahamu mimi?” “Nakufahamu
ndio hadi nyumbani kwako” “Sawa, basi vizuri. Sasa Dora, nadhani unajua
kuwa kila mwanadamu kaumbwa na kitu cha muhimu sana, kila mwanadamu kaumbwa na
hisia. Rafiki yako nampenda na sijaona shida yoyote ya kuongea hivi mbele
yako” Erica alihisi moyo wake ukienda mbio kwani alizidi kuona kama huyu
mzee hana nia njema kwake, kisha Yule mzee akamtazama tena Erica na
kumwambia. “Erica, huwa sinaga tabia ya kupindisha pindisha maneno
yangu. Mimi nakutaka, kama utakubali kuwa name siku zote sawa ila kama hutaki
kuwa name siku zote basi naomba kwa leo tu unipe hilo tunda lako hakika moyo
wangu utafarijika” “Hapana kwakweli, sipo tayari kwa
chochote” Dora akamkata jicho Erica na kumfinya kidogo, Erica
alimuangalia Dora na kusema tena, “Namaanisha nisemayo Dora, sipo
tayari” Yule mzee Jimmy alimuangalia Erica kisha akasema, “Erica
nakupa muda ujifikirire kuhusu swala hilo, naenda kuongea na muhudumu wa chumba,
hatuchukui muda mrefu ni dakika tano tu. Ilimradi roho yangu
isuuzike” Kisha Yule mzee akasimama na kuondoka, Dora akamuangalia Erica
na kumwambia, “Erica usiwe mjinga, kwa huyu mzee ni hela nje nje, hutaki
bahati wewe? Watu wengine mkoje? Yani unapewa bahati hutaki, ona mzee wa watu
alipita kukununulia hadi simu tena ya gharama ila bado unaleta ubishi wa kulala
nae mara moja tu! Kwani anaondoka nayo?” “Ingekuwa tatizo ni kuondoka
nayo nadhani hata wewe usingekuwa unalalamika kubakwa na shemeji, ila tatizo ni
utu na heshima. Yule mzee ni sawa na mzazi wangu, hata hivyo nina mpenzi wangu
nampenda sana. Siwezi tena kufanya makosa ya namna hii, kama shida ni simu hii
hapa akifika mpe” Erica alimpa Dora ile simu kisha yeye akainuka na
kuondoka zake, Dora alijaribu kumsihi asiondoke ila Erica hakusikiliza usia wa
Dora, alitoka nje ya ile hoteli na kusimamisha bodaboda kisha kuondoka
nayo. Erica aliondoka hadi stendi kisha kupanda daladala na
kuelekea kwao, ambapo alifika kwao na kumkuta mama yake amekaa na Angel kisha
akaanza kumlalamikia, “Erica kweli kwenda kumuangalia rafiki yako hadi
muda huu mwanangu? Unajua sipendi upatwe na matatizo?” “Nisamehe mama,
haitajirudia tena” “Kwenye kuomba msamaha ni mwepesi hatari ila mambo
unayoyafanya hayaendani na msamaha unaoomba. Ila nimekusamehe, usirudie tena
kuchelewa nyumbani” “Sawa mama” Erica alienda chumbani kwake ila
aliwaza sana kuwa Yule baba kwanini atake kumfanyia vile, “Jamani au
mzee kaathirika Yule anataka wa kwenda naye? Dora nae na ujinga wake hata
maumivu ya kubakwa hayajaisha vizuri ila Yule mzee akimtaka analala nae, jamani
nilikuwa mjinga nikisaka penzi la kweli ila sio kwa mzee mwenye umri wa mzazi
wangu, hapana kwakweli jana mama aliniambia, kama ridhiki yangu ipo ipo
tu” Aliamua kulala tu maana hakutaka hata kuwasiliana na mtu
yeyote. Kesho yake ilikuwa ni Jumamosi siku ambayo aliambiwa kuwa aende
kule benki ila alivunjika moyo jana na kusema kuwa hatoenda tena maana Yule mzee
asingekubali asaini mkataba ukizingatia alishakataa kutembea nae, kwahiyo
aliendelea na kazi zake tu. Kwenye mida ya saa nne, alipigiwa simu na
Yule meneja wa benki, “Erica habari, mbona hujafika mpaka saa hizi na
mtoto?” Erica akawa anajiuma uma tu maana alishajipa jibu mwenyewe,
kisha Yule meneja aliendelea kuongea, “Fanya haraka ufike na mtoto,
wakurugenzi wameshakaa kwenye kikao, ndio nimeitwa na nimeulizwa kuhusu
wewe” “Basi nakuja sasa hivi” Erica alijiandaa haraka haraka na
kumuandaa mwanae, akahisi kuwa labda Yule mzee hawezi kusababisha mwanae asipewe
mkataba ndiomana wamemuita tena. Alipomaliza kujiandaa, kwa bahati mama
yake alikuwa ametoka kwahiyo hata yeye ikawa rahisi kwake kujiandaa na kuondoka
haraka, aliita gari ya kukodi kisha aliondoka na usafiri huo hadi
benki. Alipofika alishuka na mwanae, ila kabla hajaingia benki alikutana
na Babuu akiwa ametoka kwenye ile ile benki, “Kheee Erica, kumbe huyu
ndio mwanao?” Erica aliitikia kwa aibu tu kuwa Yule ndio
mwanae, “Kheee mbona kafanana fanana na Rahim? Kwahiyo Erica umezaa na
Rahim?” Erica akawa kimya tu, muda huo huo alitoka John kumbe nae
alikuwa ndani kwenye benki hiyo, akamkuta pale Erica, Babuu na yule mtoto wa
Erica. Naye akashangaa na kusema, “Huyo mtoto mbona kafanana fanana na
Rahim?” Alipofika alishuka na mwanae, ila kabla
hajaingia benki alikutana na Babuu akiwa ametoka kwenye ile ile
benki, “Kheee Erica, kumbe huyu ndio mwanao?” Erica aliitikia
kwa aibu tu kuwa Yule ndio mwanae, “Kheee mbona kafanana fanana na
Rahim? Kwahiyo Erica umezaa na Rahim?” Erica akawa kimya tu, muda huo
huo alitoka John kumbe nae alikuwa ndani kwenye benki hiyo, akamkuta pale Erica,
Babuu na yule mtoto wa Erica. Naye akashangaa na kusema, “Huyo mtoto
mbona kafanana fanana na Rahim?” Erica alikuwa akiangalia chini tu, John
akamtazama Erica na kumsalimia “Mambo Erica” Erica
akajibu, “Poa” kisha John akauliza vizuri, “Kwani mtoto
wa nani huyu?” Babuu akamtazama John na kumuuliza, “Kumbe
unamfahamu Erica?” “Ndio namfahamu, alikuwa ni msichana wa kwanza
kumpenda. Nilimpenda sana msichana huyu” “Kheee Erica, ndugu wawili sasa
tumekutana kwenye mlolongo mmoja. Haya sasa, mtoto huyu kufanana na Rahim ni
wake?” John akamuuliza Babuu kwa mshangao, “Sijakuelewa Babuu,
unamaanisha nini?” Erica akaona hawa watu watamchanganya akili ni
watafanya achelewe kuingia ndani, akaachana nao pale nje akambeba mwanae na
kuingia zake ndani ya benki, hakutaka kujua nyuma walijadili vitu gani ila tu
alijua kama angeendelea kusikiliza hoja zao basi angechanganyikiwa kabisa.
Walijaribu kumuita ila kwavile Erica alishadhamiria kutokuendelea kusikiliza
hoja zao ikabidi aingie zake ndani ya benki. Alivyofika alienda
kwenye ofisi ya meneja moja kwa moja ambapo wafanyakazi wa pale walionyesha
kufurahi sana walipomuona mtoto wa Erica kwa macho yani mubashara na sio kwa
picha tena. Alifika ofisini kisha meneja akamkaribisha na Erica kukaa na
mtoto wake, Yule meneja alitabasamu na kumsifia mtoto wa Erica, “Kwa
hakika huyu mtoto anastahili kuitwa jina ulilomuita, yani una mtoto mzuri sana
hongera” “Asante” Erica alikuwa akitabasamu kisha Yule meneja
aliendelea kuongea, “Ila hata wewe ni mzuri, naona huyu mtoto kachukua
uzuri wako, sasa yeye na ushombeshombe ndio kazidi uzuri” Erica alikuwa
akitabasamu tu ila muda huo alikuwa akisubiri kupewa mkataba wa kusaini kwaajili
ya mtoto wake maana alihisi itakuwa rahisi kama kule dukani. Kisha meneja
akamwambia tena, “Erica, sijui umechelewa wapi wakati ntulipanga tangu
saa nne! Muda ule nakupigia simu, wakurugenzi walikuwa kwenye kikao yani sijui
unechelewea wapi ila hakijaharibika kitu, Mkurugenzi mkuu amenipa hii bahasha
amesema ukifika nikupatie maana ina maelekezo humo na kasema wiki ijayo ndio uje
na mtoto maana wenyewe kuna mahali wameenda.” Yule meneja akamkabidhi
Erica ile bahasha ambapo Erica alijiuliza kama apokee ile bahasha au afanyaje,
na akaona asipopokea lazima Yule meneja atajua kuwa kuna kitu hapo, ikabidi
apokee tu na kumuaga Yule meneja. Kisha akatoka na kuwaaga wale wengine,
alipofika nje alishukuru kuona John na Babuu walishaondoka kwahiyo ilikuwa
furaha kwake maana hakutaka tena mtu wa kumuumiza kichwa, kisha akapanda gari na
mwanae na kuondoka kurudi kwao. Alifika nyumbani ambapo mama
yake alikuwa bado hajarudi, Erica alikaa sebleni na kufungua ile bahasha, kwanza
kabisa ilitoka ile simu ya jana ambayo alinunuliwa na mzee Jimmy, “Uwiii
Mungu wangu yani ile simu kanipa tena!” Akaendelea kufungua na kukuta
kuna bahasha ndogo, akaichukua na kufungua hela zikaanguka kutoka kwenye ile
bahasha, mwanae alikuwa anacheza cheza ila kuona zile hela akaenda kuziokota na
kuanza kuzichezea, “Wewe Angel, acha hela hizo” Mtoto bado
alikuwa akichezea zile hela yani kwenye ile bahasha hapakuwa na kitu kingine
zaidi ya zile hela na simu, wakati akimwambia mwanae aache zile hela, mama yake
aliingia na kushangaa, “Kheee hela zote hizo Erica umezitoa
wapi?” Erica akamnyang’anya kwanza mtoto zile hela huku akijifikiria
namna ya kumjibu mama yake maana hata hakujua kama alitoka siku hiyo,
alipomaliza kuziokota mama yake akamuuliza tena, “Erica, hizo hela
umezitoa wapi?” “Mama, subiri nikwambie. Kuna mbaba mmoja huwa
ananitongoza ila nimemkataa ila leo nimeshangaa kamtuma kijana alete bahasha
kwangu, yani Yule kijana kaja kagonga geti na kunipa hii bahasha kisha akasema
imetoka kwa mzee Jimmy, ndio nimeichukua kufungua ndio nikaona hiyo simu halafu
kulikuwa na bahasha nyingine ndani ndio kulikuwa na hizo hela” “Kheee
huyo mzee ana maana gani? Hebu lete hiyo simu niione” Erica akampa mama
yake ile simu, mama yake akahamaki sana, “Hizi simu si ndio wanazisema
za gharama sana, jamani huyo mzee anataka nini kwako mwanangu?” “Sijui
mama” “Hebu hesabu na hizo hela” Erica akaanza kuhesabu zile
hela na kumwambia mama yake, “Ni milioni mbili mama” “Kheeee
mbona makubwa haya, yani mtu akupe simu ya gharama hivi na pesa zote hizo,
anataka nini huyo mzee jamani? Hao ndio wenye mpango mbaya na watoto wetu, huwa
sipendi ujinga wa namna hiyo kabisa, huo ni ujinga. Anatuona sisi tuna dhiki
sana eeeh kwahiyo anataka kukuteka kwa hela zake, umesema alimtuma kijana kuja
hapa?” “Ndio mama” “Dah! Hebu nipe hivyo vitu kwanza,
akikutafuta utaniambia amesemaje maana najua lazima akutafute” Erica
alirudisha zile hela kwenye bahasha na simu kwenye ile bahasha kubwa kisha
akampa mama yake, ambapo mama yake alionekana kuchanganywa nay ale mambo kabisa
kwani alienda chumbani kwake na ile bahasha bila kusema chochote. Erica
alienda chumbani na mwanae, akajilaumu sana kufungua ile bahasha
sebleni, “Zile hela si ningeenda kuweka kwenye akaunti ya mwanangu
jamani, mama naye loh! Kama hajasema turudishe sijui maana mama ana sheria huyu
balaa” Akawaza ila akaendelea na mambo mengine. Jioni
ilipofika, Erica akapokea ujumbe kutoka kwa mzee Jimmy, “Natumaini
zawadi zangu umezipata na umezipenda, sasa hiyo ni rasharasha tu, mvua yenyewe
itakuja. Naomba tukutane kwenye ile hoteli ya juzi, nina hamu sana na wewe binti
yangu. Njoo kwenye mida ya saa mbili usiku” Erica alifikiria sana
akasema, “Hivi huyu mzee ana akili kweli, si nimemwambia kuwa nimeolewa
sasa ataanzaje kusema kuwa tukutane kwenye hiyo hoteli? Mmmh mambo haya ni
makubwa, ngoja nikamwambie mama tu” Erica akaenda kumueleza mama yake na
kumuonyesha ule ujumbe, mama yake alisikitika sana, “Inamaana Erica,
ushawahi kulala na huyo mzee?” “Hapana mama” “Na kwanini aseme
tukutane kwenye hoteli ya juzi? Kumbe ndiomana juzi ulichelewa
nyumbani?” “Hapana mama, sijawahi kulala nae” “Hizi laana hapana
sizitaki katika maisha yangu umesikia eeeh! Huwa namuomba Mungu mwanangu upate
mume wa kukuoa, mume mwenye akili timamu na mapenzi ya dhati, mume mwenye hofu
ya Mungu. Sijamuomba Mungu upate mababa ya kukuingiza majaribuni, sasa jiandae
twende huko hotelini” “Jamani mama” “Hakuna cha jamani,
usiniletee ujinga kabisa mimi, sijakulea kijinga hivi.” Ikabidi Erica
aende kujiandaa na kumuandaa mtoto wake, kisha mama yake alimuita yani
alishajiandaa huyu mama na kumwambia Erica aite gari linalompelekaga
liwapeleke, “Sasa mama, mwenye gari atataka pesa” “Nitamlipa
bhana, sitaki ujinga ujue, mambo ya kijinga namna hii siyataki na siku nyingine
mizigo ya kijinga hivi usipokee” Kisha Erica akaita ile gari na kupanda
na mama yake hadi kwenye ile hoteli kisha mama yake akamwambia Erica apeleke
mzigo ule mapokezi na awaambie wampatie Yule mzee akifika, Erica alienda
kupeleka huku mama yake akimuangalia kwa makini akimkabidhi Yule wa mapokezi na
kusainishana kisha Erica kurudi kwa mama yake na kupanda tena gari kurudi
nyumbani. Walipofika mtoto wa Erica alikuwa kashalala, mama yake
akamwambia kuwa akamlaze mtoto halafu yeye aende aongee nae, alivyomlaza alirudi
sebleni na kumsikiliza mama yake, “Sikia Erica, kipindi nakuzaa kila mtu
alikupenda sana, yani ulikuwa mtoto wa pekee kwangu na wala sikutegemea kama
ingetokea ungezaa nje ya ndoa maana nilijua ungeolewa kwanza ndio ungezaa ila
haikuwa hivyo, basi nimekubaliana na matokeo lakini sio kwa stahili hii ambayo
inaendelea sasa, Erica sina hela ila nimetumia hela yangu kurudisha mizigo ya
huyo firauni maana najua wanaume wanaotumiaga hela hivi wana lengo gani, siku
zote hawana lengo jema. Kama mtu ana lengo jema, kwanini asiseme nipeleke kwa
wazazi wako nijitambulishe nikuoe, kwani tatizo liko wapi kama hela anazo! Ila
anazitumia hela hizo kukuchimbia kaburi, halafu licha ya hivyo, ushasema huyo ni
mtu mzima lazima ana familia yake, anaicha na nani familia yake hadi kuja kwako?
Huwa sipendagi ujinga wa namna hii kabisa, siku nyingine wakikuletea waambie
warudishe walipoutoa, maana pesa zina haribu sana fikra za watu najua hata huyo
aliyekupa mimba ulimvumilia sababu ya pesa, pengine hata ulijua kuwa matendo
yake hayafai ila pesa ikakuzugisha. Mwanangu jifunze kumsoma mtu kabla ya
matatizo hayajakutokea, huu ujinga siutaki tena katika nyumba
yangu” “Sawa mama nimekuelewa” “Sio kunielewa tu, fanyia kazi
nilichosema” “Sawa mama” Basi Erica akaagana na mama yake na
kwenda kulala, alisikia simu yake ikiita ila hakuipokea wala kuiangalia maana
alijua ni Yule mzee anapiga, na hakutaka kuongea nae kabisa maana kwa muda huo
alitaka kumuwaza Erick tu maana ndio alianza kumuamini kuwa ni mwanaume
anayempenda kweli. ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment