Search This Blog

Tuesday, 1 November 2022

THE WORST VALENTINE’S DAY - 4

 








Simulizi : The Worst Valentine's Day

Sehemu Ya Nne (4)







“itabidi tukufanyie upasuaji Faith kama uko tayari kupona,,ingekuwa toka mwanzo tumelifahamu hili tungeweza kukupa vidonge vinaitwa Salazopyrin ambavyo uneanza dozi na baada ya miezi mitatu tungekuangalia inakuwaje,,lakini kwasasa inabidi upasuaji” aliongea huku akinitazama usoni. Sikujua cha kusema lakini upasuaji wa tumboni tena wa kuondoa utumbo mkubwa ungeweza kusababisha kifo changu,,sikuwa tayari kufa bila kumuona Jamshid lakini kwa hali ya mateso yangu niliona sasa ndiyo ulikuwa mwisho wanguna nilikuwa tayari kwa lolote.

“nini madhara ya kufanya huo upasuaji dokta” nilimuuliza nikitaka kujua ni nini kitanikabili kwa siku za usoni.

“madhara yake si makubwa sana ila unachotakiwa kukijua ni kwamba itakuepusha kupata saratani ya utumbo”

“na hiyo mnanifanyia hapa au?”

“ndio atakuja mtaalamu hapa mda si mrefu, atakuambia kila kitu” aliongea daktari na kabla hajamaliza nilimuona daktari wa kike akiingia pale wodini.

“habari zenu jamani” alisalimia na wote waliitika.

“nipe habari dokta” alimgeukia yule daktari

“habari ni nzuri tumefanya vipimo vizuri kama ulivyoshauri na anaonekana vidonda ni vikubwa na tayari hali imeanza kuwa mbaya” aliongea yule daktari. Baada ya hapo yule daktari alinigeukia.

“habari mpendwa” alinisalimia huku akitabasamu.

“salama dokta” niliitika kwa sauti ya unyonge.

“mimi naitwa dokta Mourine,,napenda sana kuitwa Mourine yani bila dokta, sawa ee?” aliniuliza tena huku akitabasamu..tabasamu la dokta Mourine lilinifanya nimkumbuke sana mama yangu,,machozi yalianza kunitoka lakini nilijikaza ili wasijue nilikuwa nalia moyoni,,kila nilipomuwaza mama yangu nilikuwa nikijiwa na picha ya siku aliyobakwa na wale watu nane wasiokuwa na huruma,, kilikuwa kitendo cha kumzalilisha sana na tena mbele ya baba yangu mzazi lakini si mimi wala baba tulioweza kumsaidia zaidi tu ya kumuonea huruma na kulia pamoja nae.

“anatakiwa afanyiwe upasuaji mwezi mmoja mbele ilia pate mda wa maandalizi ya dawa zile za kusafisha utumbo na zile dawa nyingine zote apewe, mumuandikie na mlo anaotakiwa kula ili wasije wakampa chakula kitakacholeta madhari kwenye upasuaji” aliongea dokta Morine na yule dokta mwingine na kisha kunigeukia.

“You will be fine my dear”(utakuwa sana mpendwa) alinishika shavuni na machozi hayakuweza kuweza tena kuzuilika kusambaa kwenye mashavu yangu.

“nateseka sana Mourine,,nateseka kwa kosa ambalo si langu,,nimetengwa na watu niwapendao na kila mtu anayeonyesha dalili ya kunisaidia anakufa katika mazingira ya kutatanisha,,please Mourine, you have shown me the heart of help but don’t help me they will come after you as they came after every one who wanted to rescue me”(tafadhali Mourine, umenionyesha moyo wa kunisaidia lakini usinisaidie watakufata kama walivyowafata wengine waliotaka kuniokoa) nilizidi kulia na wala sikujua nilichokuwa nikikiongea kwa sasa.

“nani hao unawaongelea” aliniuliza Mourine kwa mshituko na hapo aliwaambia wale maaskari waliokuwa pale ndani pamoja na wale madaktari wengine watupishe kidogo.

“nieleze nini kinakusumbua binti”,,alinieleza huku akiwa amenishika mkono.

“there are people who want to see me suffer and finaly dead”(kuna watu wanataka kuniona nikiteseka na mwishowe nife) nilimueleza huku bado machozi yakinitoka, nilijua kabisa pengine na Mourine angekufa kama angejeribu kwa namna yoyote kunifanya nisiteseke na sasa sikuwa tayari mtu mwingine afe kwaajili yangu.

“hao watu ni kinanani” aliniuliza Mourine na sasa sikujua nimjibu nini,,kilichokuwa kikiendelea kwenye maisha yangu ni vigumu sana kuaminika na mtu wa kawaida asiye na imani za tofauti na mimi au asiyenifahamu.

“hutanielewa ila jua tu, hutakiwi kuhakikisha napona bali hakikisha nateseka ili maisha yako yawe salama na kama utaweza jitoe kabisa kwenye kunihudumia”. Nilimueleza kwa umakini kabisa na kwa sauti iliyojaa msisitizo. Baada ya kumwambia hivyo Mourine alinyanyuka na kuondoka wakati anaondoka alifika mlangoni na kuongea na wale maaskari na madaktari manesi waliokuwa pale kisha waliingia ndani na kuanza kufungua zile drip na vifaa vingine na hapo nilianza kushangaa.

“mbona mnanifungua hapa” ailiuliza huku nikitaka kunyanyuka.

“tunakuhamisha wodi, dokta Mourine ameenda kuchukua kibali cha kukuhamisha ili ukawekwe sehemu yenye usalama zaidi ya hapa” nilishtushwa na iyo kauli na kisha sikuweza kuuliza chochote kwani Mourine alikuwa tayari amesharudi pale na watu wengine kisha aliwapa wale maaskari karatasi nao wakaweka sahihi zao na kumrudishia kishwa walinihamishia kwenye kitanda kingine na kuondoka kuelekea sehemu ya chini kabisa ya hospitali ile upande wa wodi za watoto na huko kulikuwa na chumba ambacho hata mimi nilikubali kuwa kilikuwa salama kwa pale, lakini ukweli ni kwamba kama wakihitaji kunifata haitashindikana hata ingekuwa ni kule gerezani, maisha mapya ya hospitali yalianza na kila mara nilijifanya kuwa niko hoi ili nisirudishwe tena mahabusu,, niliongea na dokta Mourine kuwa aniandikie nienelee kubaki pale hospital nae alikubali.

WIKI MBILI MBELEhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Ilikuwa imebaki wiki mbili ili niweze kuanyiwa upasuaji na muda wote huu nilikuwa nikiishi pale wodini chini ya ulinzi mkali na uangalizi wa dokta Mourine. Nilikuwa naishi na pingu mikononi kama vile nilikuwa jambazi sugu lililoshindikana na sikuwa nafahamu ni lini kwenye maisha yangu nilikuja kukosea na kujiingiza kwenye mkondo huu wa mateso,, sikutaka hata kidogo kujilaumu kwa kujuana na Jamshid,,hata kama ingekuwa ndio chanzao cha matatizo haya nisingekuwa tayari kujilaumu kwa kuwa na Jamshidi kwakuwa yeye ndiye mwanaume pekee aliyejua nitakacho pale nitakapo na ndiye pekee aliyefanikiwa kuukamata moyo na hisia zangu,,kwangu Jamshid alikuwa ndiyo kila kitu haijalishi kilichotokea baina yetu,,kama ningefanikiwa kujifungua vyema basi yeye leo hii ndiye angekuwa baba wa mtoto wangu, yeye na Magret na Clara leo hii ndiyo wangekuwa familia yangu,,japo Magret hakustahili kufa lakini hata yeye angejisikia fahari kama angekufa kwaajili yangu na Jamshid, tayari kwa muda mfupi ambao tulimuingiza Jamshid kwenye familia yetu alikuwa ameshakuwa sababu ya furaha yangu na Magret na siku zote ningetamani kila aliyekufa kwaajili yangu afufuke.

“ndio mimi ni mwanasheria wake na karatasi ya utambulisho toka mahakamani hii hapa nimekuja kuongea nae ili niandae utetezi wake” nilishtuka kutoka kwenye dimbwi la mawazo baada ya kusikia kwa mbali sauti ya mwanamke ikijitambulisha nje ya kile chumba na kisha nilimshuhudia Samah akiingia ndani akiwa na file na makaratasi mengine kisha kwa tabasamu lake la kinafiki lililojaa unyama na usaliti alinisalimia na mimi niliamua kukaa kimya.

“ni bora ukaitikia salamu yangu kwakuwa ukimya wako hautakusaidia kitu Faith,,uhuru wako uko mikononi mwangu,,ni mimi nitakayeamua ushinde kesi au ukanyongwe,,ni sisi tuliohakikisha kuwa hujifungui na kweli mtoto wako amenywewa damu,,tuliamua utoe sadaka ukakataa na ukasababisha kifo,,Clara alikuwa akusaidie lakini tukamdhibiti na mengine mengi,,,unajua dhahiri kuwa tuna nguvu ambayo haitazimwa kwa wewe kukaa kimya bali kwa wewe kufanya kile ambacho tunakuelekeza” aliongea na mda wote huo nilikuwa nikilia hasa baada ya kugundua kuwa mtoto wangu alikuwa amenywewa damu na hawa mashetani.

“lakini kwanini mnanifanyia haya yote,,kwanini mnaua kila anayenihusu” niliuliza huku machozi yakiendelea kuniandama.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“tutaongea kuhusu hilo siku moja lakini sio sasa”,,kilichoniudhi kuhusu Samah ni kitendo chake cha kutoa tabasamu lililowaonyesha watu kuwa tulikuwa watu wenye maelewano sana na kumbe haikuwa kweli,,nilimchukia Samah kuliko kifo na wala sikutaka kabisa kujuana nae katika siku zote za maisha yangu.

“I came here for only one big reason”(nimekuja hapa kwasababu kuu moja tu) aliongea Samah huku akiendelea kutabasamu na hapo alifungua yale makaratasi yake na kuanza kuongea.

“we want everthing back”(tunataka kila kitu kirudi) nilishtuka na masikio yangu sasa yalikaa sawa kama antenna nikisubiri sentensi moja zaidi ya Samah itakayokuwa ni kuniambia kuwa nirudi tena kama mwanachama hai wa kundi lile,,sikuwa tayari tena kurudi kwenye kundi la freemason na nilikuwa tayari kufa lakini sikuwa tayari tena kwenda kuhudumia malaika wa nuru ambao hata ivyo baada ya kwenda nao kinyume niliteseka siku zote hizi.

“what things”(vitu gani) nilimuuliza kwa sauti ya hamaki.

“tunahitaji mali na kila kitu ulichonacho kwakuwa tulikusaidia lakini ukatudharau” kauli hii pengine aliona itanishtua sana lakini kwangu haikuwa kitu,,mali na utajiri wote niliokuwa nao haukuwa na maana kwangu kwakuwa katikati ya shida nilizokuwa nazo pesa haikuwa na nafasi,,kipindi hiki kigumu kwangu kilinifunza kuwa ni bora uwe na furaha na Amani tu bila pesa kuliko kuwa na pesa bila furaha.

“chukueni kila kitu, sihitaji chochote kwakuwa tayari nimeshakufa” nilimwambia kwa sauti iliyojaa ujasiri.

“kwenye akaunti yako ya CRDB ukiasi cha shilingi milioni 165,,EXIM una milioni 56 na CITI bank ya South Afrika ya kusini tumeangalia una randi 535081.64 sawa na shilingi millioni 95, jumla kwenye akaunti zako zote kuna fedha kiasi cha shilingi milioni 316,,ni sawa? Aliniuliza huku akinitazama usoni na mimi nilimtazama kwa macho yaliyoonyesha kuwa hayo yote si kitu kwangu.

“mmesahau akaunti moja ya Barclays tawi na Helinsik ina Euro laki tano, mmesahau pia saluni kubwa ninazomiliki kwenye majiji ya Mwanza, Dar na Arusha ambazo huingiza zaidi ya milioni 15 kwa mwezi,,mmesahau nyumba ninayo miliki mbezi beach yanye thamani ya milioni mia tano,,hati zote nenda nyumbani kwangu chumba cha pembeni ya pale ulipomuulia Magret, kasogeze kitanda kisha vuta lile kapeti utakuta kapeti nyingine ya plastiki ifunue kisha utakuta shemu ya kuingiza namba hapo kwenye sakafu nenda pale ingiza namba 6699 ikifunguka iyo sehemu utakuta sanduku kisha ingiza namba 9966 litafunguka, beba makabrasha yote uje nayo hapa ndiyo utakuwa umekamilisha vitu vyote” wakati huu wote Samah alikuwa akinisikiliza kwa makini kabisa na baada ya mimi kumueleza hayo alinyanyuka na kuondoka. Sikujua kuwa alikuwa akienda wapi lakini hiyo haikunipa shida nilibaki pale nikisubiri kuona ni nini kitatokea na baada ya muda mfupi dokta Mourine aliingia na huku akionekana akiwa na sura ya huzuni, na hapo nilijua kabisa mambo hayakuwa sawa.

“Mourine whats wrong”(Mourine nini tatizo) nilimuuliza kwa shauku.

“my kid is dead,,my only kid”(mtoto wangu amefariki,,mtoto wangu pekee), niliinamisha kichwa chini na kumshika Mourine mkono,,sikujua kuwa mwanae alifariki kwaajili ya nani lakini hii ilikuwa njia ya kumfanya asinihudumie, nilifikiri hivyo.

“alikuwa anaumwa au” niliuliza kwa majonzi

“hapana, aliondoka asubuhi ya leo akielekea shule na wakati wanarudi akiwa kwenye gari na dereva waligongwa na gari ndogo na wote wawili walifariki palepale”,,akili yangu bado ilinituma kuendelea kuuliza maswali japo kwa kujishtukia

“namba ya gari iliyomgonga waliipata” nilizidi kuuliza wakati huo Mourine akizidi kulia

“yes wamesema ni T666XXX” moyo wangu ulikufa ganzi kwakuwa gari hii niliifahamu,, gari yenye namba hiyo ilikuwa ni gari ndogo aina ya GX100 inayomilikiwa na mzee Rorbahcho, nlikuwa nikitoa machozi lakini bado sikuwa pale kiakili.

“nimekuja kukutaarifu hilo na file lako nimelikabidhi kwa dokta yule wa mwanzo ili akuangalie wakati unajiandaa kwaajili ya upasuaji”.. aliongea hayo na mimi nilimkatisha kwa maswali zaidi.

“hakuna mtu yoyote aliyekufata leo mda wowote?” nilimuuliza kwa sauti ya msisitizo

“hapana hakuna aliyenifata” alinijibu na hapo alinyanyuka na kuanza kuondoka lakini alipofika mlangoni aligeuka na kurudi.

“yupo mtu nilipishana nae asubuhi wakati naingia ofisini, akaniambia nizingatie sana uliyoniambia, nijiweke mbali, hata hivyo nilikuwa kwenye haraka na sikuweza kumsikiliza vizuri au kuyatilia maanani maneno yake” aliongea huku akionekana kutaka kujua nini kilikuwa kinaendelea.

“huyo mtu yukoje” nilimuuliza

“ni mwanamke aliyekuwa amevaa hijabu nyeusi iliyofunika uso, mnene kiasi na mrefu”,,sikutaka maelezo zaidi nilijua dhahiri kuwa yule alikuwa Maysa.

“kuna nini kinaendelea hapa” aliniuliza na sikuwa na cha kumjibu nikaamua kukaa kimya huku nikilia.

“ndo wamenifata si ndio??ndo wale waliomuua mtoto wangu??mh nambie Faith,,ndo wale??” aliniuliza huku akilia na mimi nilishindwa lakufanya zaidi ya kulia sana,,Mourine alilia mpaka akakaa chini na baada ya muda alinyanyuka na kuniambia nimueleze kila kitu,,nilimueleza yote bila kumficha chochote katika maisha yangu na katika hali ya kushangaza alinikumbatia na kunifuta machozi.

“nimempoteza mtoto wangu ambaye ndio zawadi pekee aliyoniachia marehemu mume wangu,,yeye ndiye alikuwa ndugu yangu na wazazi wangu,,mimi ni yatima sikuwahi kumjua baba wala mama yangu,,sikuwa na ndugu nililelewa na wasamaria wema amabo nao hawapo,,,niko tayari kukusaidia kwakuwa sasa sina tena cha kupoteza,,,usiogopa na kwenda kumzika mwanangu na nitarudi” aliongea na kuondoka,,nilibaki nikilia pale na muda mfupi mbele Samah aliingia pale na muda huu alionekana mwenye haraka.

“kila kitu kiko sawa,,naomba uweke sahihi yako kwenye karatasi zote hizi hapa ikiwa ni pamoja na mali nyingine, tunahamisha kiasi chote cha pesa kwenye akaunti zako na tutakuachia shilingi milioni 20 tu,,,nyumba zote tunaziuza,,saluni nazo zitakuwa si mali yako pamoja na magari yote na kila kitu,,hivyo utabakiwa na pesa kwenye akaunti yako ili ikitokea hujafa basi ikusaidie kujiua au kuanzisha maisha mapya ukiwa nje ya kundi” alimaliza na kunipa zile karatasi kisha nilizisaini na kumkabidhi,,ilikuwa ni zaidi ya shilingi za kitanzania milioni 300 zilizokuwa zinahamishwa kwenda kwenye Masonry Fund na pia mali zisizohamishika zenye thani ya milioni 900 yani nyumba zangu mbili na saluni zangu,,pia magari yangu yote yalikuwa yanataifishwa,,hii haikuwa shida kwangu,,baada ya kumaliza kuweka sahihi nilikaa kimya nikimsikiliza Samah aliyekuwa akiongea pumba tu mbele yangu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“nashukuru kwa ushirikiano wako,,pia kuna barua hapa nitakuachia” alinikabidhi ile barua na kuondoka ila kabla hajafika mlangoni nilimuita.

“naombeni mnisaidie” nilimuongelesha kwa sauti ya upole

“tukusaidie nini?” aliuliza na kuonyesha lile tabasamu

“I want to see Jamshid”(nataka kumuona Jamshid) niliongea huku machozi yakinitoka.

“don’t cry sweetheart,,you are going to see him this evening and this time don’t messup”(usijali mpenzi,,utamuona leo jioni na wakati huu usifanye makosa),aliniambia vile na kuondoka,,hapo waliingia wale walinzi na kutaka kunifunga zile pingu lakini nilijaribu kuwaomba waniache walau kwa muda mfupi kwani zile pingu zilikuwa zinaniumiza mikono na wao walikubali na kuniacha mikono bila pingu,,nilikuwa na furaha sana baada ya kuambiwa nitamuona Jamshid pale ndani..niliwaza Jamshid alikuwa akitokea wapi na angejisikiaje kuniona nikiwa pale hospitalini na pingu mkononi,,nilijiuliza angejisikiaji kusikia nilikuwa naenda kufanyiwa upasuaji ambao pengine ungehatarisha maisha yangu.



SAA MOJA JIONI LEO



Ilikuwa ni saa moja jioni ndipo niliposhtuka toka kwenye taharuki, furaha na majonzi ya kumuona Jamshid, nilikumbuka kuwa Samah aliniachia barua ambayo sikuisoma, nilinyanyua mto na kuitoa, mikono yangu haikuwa na nguvu sana kutokana na zile pingu nilizokuwa nikifungwa lakini kwa leo nilijisikia nafuu baada ya kufungulia,,niliinyanyua ile barua na kuanza kuiangalia, ilikuwa ni barua ya kingereza iliyosomeka hivi kwa Kiswahili;http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Umoja wa kundi la Freemasons, tawi la Tanzania limepokea barua ya kukuondoa kwenye ushirika kufuatia barua yako uliyowahi kuituma kwa katika wa tawi la serel la huko Uingereza. Hivyo tunakuarifu kuwa kwasasa uko huru na hautahusika na mambo ya kundi hili na pia uko tayari kuurudia uanachama wako saa yoyote. Ikumbukwe kwamba kama mwanachama aliwahi kupewa sharti la kutoa sadaka na hakufanya hivyo kwa hiari yake basi hatakubaliwa kuondoka kabisa bila sadaka hiyo.

Hivyo ndivyo ilivyosomeka sehemu ya barua hiyo,,niliikunja na kuiweka kwenye mto na kisha nilikaa pale nikitizama pale mlangoni, lakini cha kushangaza hakukuwa na askari nilisikia mlango ukifunguliwa na Samah aliingia na watu wa nne waliovaa kidaktari na bila kuongea na mimi walinivisha kitambaa cheusi usoni na kunibeba kwenye kitanda cha wagonjwa,,kisha nilimsikia Samah akiniambia.

“you better keep quite and you will be safe”(ni vizuri ukakaa kimya na utakuwa salama),,nilikuwa na hofu lakini sikujali tena na nilikuwa tayari kwa lolote,,,tulifika mpaka chini bila kuonekana na hapo nilihisi kupakizwa kwenye gari na gari liliondoka kwa kari na baada ya lisaa limoja nilifikishwa nisipopajua na kile kitambaa kilitolewa,,nilipotazama mbele yangu kulikuwa na wazungu wanne na wahindi wa tatu na hapo walivuta pazia kubwa na sikuamini nilichokiona,,alikuwa ni Jamshid hakuwa amefungwa popote na alionekana kuwa na afya nzuri,,nilimkimbilia na wote tulikumbatiana huku akilia kwa uchungu;

“ulikuwa wapi Jamshid,,where were you my love”(ulikuwa wapi mpenzi wangu) nilimuuliza huku nikilia kama mtu niliyekuwa nimefiwa,,Jamshid alilia mpaka ikabidi nimbembeleze.

“najua unateseka mpenzi wangu nimejaribu kukupigania ila wamenifungia ndani siku zote,,nakupenda Faith,,nakupenda mpenzi wangu,,wewe ndio maisha yangu,,wewe ni kila kitu kwangu” alizidi kuongea kitu kilichonifanya nizidi kulia bado tukiwa pale tumekumbatiana.

“Jamani achaneni tunataka tufanye haya mambo haraka kidogo”,,ilikuwa sauti ya Samah na hapo wale wazungu walikuwa bado wanatuangalia,,walifungua tena pazia jingine na hapo ndipo nilipotamani kuzimia lakini haikutokea.

“Faith” aliniita yule niliyemuona,,nilimkumbatia na kulia nae kwa uchungu sana,,,alikuwa ni Clara,.

“I heard u died”(nilisikia umekufa) nilimuuliza huku nikizidi kulia, kilichoniliza ni hali niliyomkuta nayo Clara ambaye ndiye mwanasheria aliyekaribia kunitoa hatiani, alikuwa amekatika mkono mmoja na hali yake ya kiafya ilikuwa si nzuri sana.

“sikufa walinichukua muda mfupi baada ya kupata ile ajali” aliniambia hivyo na hapo niliona meza ikitengwa pale na visu vikali vililetwa pale na vifaa vingine,,kisha Jamshid aliwekwa mbele yangu na kufungwa mikono na pia Clara vivyo hivyo…mambo yalitokea haraka sana na sikujua nini kilifata.

“tulikupatia barua ya kukuondoa kama ulivyoomba lakini bado una deni na huu ndiyo muda wa kulipa deni au sisi tukusaidie kulipa,, utachagua katia ya hawa wawili ni yupi auwawe na utamtoboa kisu kwenye moyo na kuchana iyo sehemu ili uutoe moyo wake na kutukabidhi hapa,,ukishindwa tutawaua wote…………….”

“Nooooo,,,siwezi,,,noooo”





Huu ulikuwa mtihani mwingine mkubwa katika maisha yangu, nilizidi kulia ili hata wale watu wanionee huruma lakini hakuna aliyejali,,nilikuwa nimepewa dakika kumi za kufanya zoezi lile la sivyo,, niliendelea kujishauri nisijue cha kufanya,,sikuwa tayari kufanya kosa tena wakati huu nikasababisha vifo vya watu wawili lakini pia sikuwa tayari kushiriki kuoa uhai wa mtu,,nilimtazama Clara aliyekuwa akilia mda wote pale nikamwonea huruma, Clara alinisaidia sana, alijitolea maisha yake kuhakikisha kuwa naachiwa huru kwenye kesi inayonikabili,,alikuwa amekatwa mkono kwasababu yangu, ni mimi ndiye niliyemuingiza Clara kwenye tabu zote anazozipata.

***

Niliitazama ile saa ya ukutani ilikuwa ikinionyesha kuwa zilikuwa zimebaki dakika sita, akili yangu ilifanya kazi haraka na kupata jibu kuwa nijitoe sadaka mwenyewe kwa kujichoma kisu ili nife mimi kuliko kumuua mwanaume wa maisha yangu au Clara, sikuwa tayari kabisa kufanya hivyo na kuwafaidisha maadui zangu,,nilisali pale huku nikilia na kumuomba mungu anionyeshe njia lakini bado mbele yangu ilikuwa ni giza kuu, mshale wa sekunde ulikuwa ukikimbia kuliko kawaida huku ule wa dakika nao ulikuwa ukizikimbilia dakika kumi nilizopewa,,pamoja na maumivu niliyokuwa bado ninayo ya ule ugonjwa uliokuwa ukinikabili lakini sasa niliitajika kuwa imara na kufanya walichoniagiza.

“usijaribu kujichoma wewe mwenyewe” ilikuwa sauti ya mzee wa kizungu aliyekuwa pale mbele yangu, nilimtazama kwa makini na wakati huo jasho, machozi na kamasi viliujaza uso wangu, hofu ilinikabili na kutetemeka kulifunga ndoa na mwili wangu,,saa ilikuwa ikionyesha kuwa zilibaki dakika tatu na mimi taratibu huku nikitetemeka niliisogelea ile meza yenye visu na kuchukua kisu kidogo na kisha nilimsogelea Jamshid ambaye naye alikuwa akilia.

“Clara amekusaidia sana Faith, usimuue,,niue mimi na sio yeye, niko tayari kufa na siko tayari kuona ukimuua Clara,,niue mimi,,fanya hivyo sasa muda una kwenda” aliongea Jamshid huku akilia kwa uchungu hali iliyonifanya nishindwe kujizuia na kuanza kulia kwa nguvu. Iweje nimuue Jamshid hata kama alikuwa tayari? Nitaanzania wapi kumuua mtu aliyemaanisha maisha kwangu, mtu pekee katika hii dunia aliyenipa sababu ya kuyaingia mapenzi, Jamshid sio tu alikuwa mpenzi wangu lakini yeye ndiye pacha wangu kwa sasa,,nilimpoteza Magret lakini siko tayari kumpoteza tena Jamshid katika hali ya kawaida. Nilimkumbatia na taratibu huku nikijifanya nalia niliongea nae namna ya yeye kutoka pale alipokuwa na niliingiza mkono kwenye ile nguo yangu na kutoa kisu kidogo nilichochukua bila wao kuniona nikakiingiza kwenye suruali yake mfuko wa nyuma,,Jamshid alikuwa amefungwa mikono nyuma na kifua chake kilikuwa tayari kwa kutolewa ule moyo walioutaka lakini hakikuwa kitu rahisi cha mimi kufanya. Nilimuachia Jamshid na taratibu nilimsogelea Clara huku macho yangu yakiwa makavu na yaliyojaa ujasiri,,nguvu zilianza kunijia na nilipomuangalia Clara alianza kulia;

“Usiniue Faith,,nipe muda wa kuishi Faith,,sitaki kufa kwa sasa niache kwanza na muda ukifika utaniua lakini niache kwasasa tafadhali,,utaua watu wawili na damu itatembea na wewe siku zote,,sistahili kuuwawa iwe ni kwasababu yoyote,,kataa kuwatumikia hawa wauaji kwakuwa na wewe utakuwa kama wao” aliongea Clara maneno hayo huku akizidi kulia kwa uchungu, sikumuelewa vizuri na hapo ilibidi nimsogelee huku na mimi machozi yakinitoka nikamsikiliza vizuri.

“unamaana gani unaposema kuwa nitaua wawili” nilimuuliza.

“nina ujauzito” alinijibu na hapo ndipo machozi yalipoanza kufurika tena kwenye uso wangu.

“we are going to get out of here, right now,just be brave”(kuwa jasiri tutanatoka hapa muda huu). Nilimwambia hivyo na kutazama ile saa nikagundua ilibaki dakika moja nikawageukia tena wale watu pale na kuwaambia;

“ I cant use a knife, I want a pistol, I have a courage of giving what you want but not by this fucking knife”(nina ujasiri wa kuwapa mtakacho lakini si kwa kutumia hiki kisu, nataka bastola, siwezi kutumia kisu) niliongea kwa ujasiri na kurudisha kile kisu pale mezani.

“you don’t give terms here, you are executing our orders not yours”(hautoi masharti wewe, unatekeleza maagizo yetu na si yako) aliongea mmoja wa wale wazungu waliokuwa mbele yangu.. nilipotazama kwa makini kulikuwa na bastola moja tu pale ndani aliyokuwa ameishika yule mzungu aliyenijibu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“then I wont kill them, and if they die I have nothing to loose, they died already to me and I too I am already dead”(basi sitawaua na hata wakifa sitakuwa na cha kupoteza kwakuwa kwangu walishakufa na mimi pia nimeshakufa) niliongea hayo na kuamua kurudi mpka pale alipokuwa Samah nakumtazama usoni kisha nilimuambia kwa dharau.

“hey bitch, handcuff me and get me out of here either dead or alive that will be your fucking choice”(we kahaba nifunge pingu na unitoe hapa ndani nikiwa mzima au mfu iyo itakuwa maamuzi yako) nilimtazama Samah usoni kwa ukaribu na yeye alionekana kuwa na woga na wakati huo nilisikia wale wazungu wakiongea;

“she wont kill them by knife, seems she mean it”(hatawaua kwa kisu na inaonekana anamaanisha) aliongea yule aliyekuwa ameshikilia ile bastola,,baada ya wale walinzi kunileta pale wao waliondoka na hesabu ya pale ndani kwa sasa ilikuwa ni wazungu wale wanne kwakuwa wale wahindi watatu waliondoka kabla ya mimi kuambiwa cha kufanya.

“give her the pistol”(mpe bastola) aliongea yule mzungu aliyekuwa ameketi na ambaye ndiye alionekana kuwa ni mkuu kwa pale.

“no sir, she have to do it by knife”(hapana mzee anatakiwa afanye kwa kisu)

“I say give her a damn pistol”(nimesema mpe bastola), yule mzungu alinisogelea na kunipa ile bastola,,niliifungua na kuangalia ndani ilikuwa na risasi 9 kisha niliifunga na kuikoki, hapo nilimsogelea Clara na kumnyooshea mdomo wa ile bastola kwa nyuma,,nilishuhudia mkojo ukipenya kwenye ile nguo aliyokuwa amevaa,na mshale wa ile saa ulionyesha bado sekunde tano,, niliwatazama wale wazungu walikuwa wamejiweka shemu moja na hapohapo bila kupoteza muda nilifyatua risasi kuelekea kwa yule mkuu wao na ilipenya kifuani kama vile mtu alikuwa akigongelea msumari kwenye mgomba,,sikupoteza muda nilifyatua risasi nyingine iliyomlenga begani yule mzungu mwingine na hapo wengine walianza kutimka na ndipo nilipomfungua Jamshid na kumuacha pale na mimi kuanza kuwatafuta wale waliokimbia na hapo nilifanikiwa kuwaona kwa mbali na kuwafyatulia risasi zilizowamaliza wote na kuiacha bastola ikiwa haina kitu kwasasa,,,nilirudi mpaka ndani na kumkuta Jamshid akiwa na damu mkononi huku ameshikilia kisu na ndipo nilipogundua alikuwa amemalizia yule niliyempiga risasi ya bega,,cha kushangaza Samah bado alikuwa pale akitetemeka na kulia na Jamshid alikuwa akimwendea na kisu ili amuue;

“hapana Jamshid usimuue,,bado ninakazi naye” nilimsihi Jamshid ambaye kwasasa alikuwa ameshamkaribia Samah amuachie na Jamshid hakunisikia,,alimfata na kumkaba shingoni huku akikipenyeza kile kisu kwenye koromeo la Samah;

“Jamshid naomba umuache tafadhali,,hatutafanikiwa kwenye lolote kama hatutakuwa na maelezo ya kutosha ya namna ya kumaliza haya mambo yote kwa wakati,,nakuomba,,fanya hivyo kwaajili yangu tafadhali” nilimuomba Jamshid na taratibu alimuachia Samah,,damu zilikuwa zimeanza kumtoka Samah na hapo ilibidi kumuwekea chumvi iliyokuwa pale kwenye meza yenye visu,,alilia sana kwani iliuma na bila kupoteza muda tulitoka nje ya lile jengo na kukuta gari waliloacha wale wazungu lakini hakukuwa na funguo pale ikabidi Jamshid arudi ndani na kwenda kuwapekua mifukoni na aliporudi alikuwa na funguo na pesa mkononi,,,tuliingia kwenye gari na safari ya kuelekea tusipopajua ilianza,tulitembea kwa mwendo mrefu na mshale wa mafuta kwenye gari ulionyesha kuwa mafuta yalikuwa chini ya kawaida na hapo tulisimamisha gari kituo cha mafuta na kujaza mafuta lita kumi kisha safari ilianza,,baada ya mwendo wa kilomita moja tulikuja kujikuta tumetokeza mlandizi na hapo ndipo nilipogundua kuwa tulikuwa tumepelekwa Bagamoyo au maeneo ya bunju, hapo hatukuwa na sehemu ya kwenda zaidi ya kuondoka kabisa na karibu na maeneo ya jiji la Dar.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“twendeni mikumi, baba yangu alijenga huko,kuna nyumba yetu huko na hakuna anayeishi huko” ilikuwa sauti ya Clara aliyekuwa akituelekeza pa kuelekea.

“una uhakika hakutakuwa na tatizo huko” nilimuuliza tena.

“ndio hakutakuwa na tatizo na Faith”. Baada ya Faith kusema hivyo wote kwa pamoja tulikubaliana kuondoka mpaka ubena na tulipofika pale Jamshid alishuka na kwenda duka la dawa kwaajili ya kununua dawa za kumsafisha Samah kidonda na dawa nyingine kwaajili ya wote. Aliporudi alikuwa na madawa mengine na hapo safari ya kuelekea mikumi ilianza, tukiwa tunakaribia Bwawani na wakati huo nikiendelea kumfunga Samah kile kidonda niliona begi nyuma ya siti ya ile gari na nilipolifungua nilikuta vitu mbalimbali na pesa taslim shilingi milioni nne,,hiyo ilikuwa furaha kwakuwa hatukujua ni namna gani tungeweza kufika mikumi bila mafuta ya kutosha kwenye gari,,lile begi tulilitupa njiani,,gari ilikuwa ikikimbizwa sana na tulipofika morogoro tuliingia kwenye mgahawa kwaajili ya kupata chai lakini Jamshid yeye aliondoka kwenda kujaza gari mafuta na upepo, Samah alikuwa ndani ya gari pia kwakuwa kwa hali yake tusingeweza kumshusha pale,,baada ya kunywa chai na kumaliza tulinunua nguo kwenye duka lililokuwa karibu na ule mgahawa na muda si mrefu Jamshid aliingia pale na kwa haraka alituambia tuondoke,,baada ya kupanda kwenye gari alinirushia gazeti la Mwananchi lililokuwa na maandishi makubwa yaliyosomeka MTUHUMIWA WA MAUAJI ATOROKA HOSPITALI; Dokta wake mbaroni kwa kumsaidia kutoroka,,,mapigo ya moyo yalishuka hasa baada ya kuona picha ya sura yangu ikiwa juu ya lile gazeti,,nilijua kuwa huu ndio ulikuwa mwanzo wa mimi kuishi mafichoni lakini sikujali kitu,,tuliondoka Morogoro na kilomita ishirini mbele tulifika njia panda ya Mzumbe na kwa mbali tuliona maaskari wakiwa wameweka kizuizi barabarani huku wakikagua magari yaliyopita palejamshidi alituambia tuiname chini siti na wote tulifanya ivyo, hofu ilizidi kutanda moyoni kwangu na hii ni kwakuwa sikutaka kurudi tena kwenye mikono ya binadamu, baada ya ukaguzi ambao hata hivyo haukuchukua muda sana tuliruhusiwa na kuondoka na hapo roho yangu ilitulia,,tuliendelea na safari na baada ya muda Clara alilala na Samah pia alilala na hapo nilipata wasaa wa kuongea na Jamshid, nilikuwa na furaha sana japo mashaka na woga viliujaza moyo wangu lakini sikujali tena,,tuliongea sana na baada ya nusu saa tulikuwa tumeshamalzia geti la pili la mbuga ya wanyama ya mikumi na muda mfupi mbele tulikuwa tumeshafika mizani ya mikumi ndipo nilipomuamsha Clara na akatuelekeza kuwa tufate njia ya kuelekea Udzungwa,,tulitembea kwa mwendo wa kilomita 45 ndipo tulipofika kwenye nyumba iliyokuwa imejitenga kabisa na mji na sehemu ya makazi ya watu na muda huo ilikuwa imeshafika saa kumi na nusu jioni tulipofika pale Clara alishuka na kwenda getini ambapo alikuwapo kijana mmoja wa kiluguru na baada ya mazungumzo ya muda mfupi niliona wakicheka na geti lilifunguliwa,,baada ya kuingia ndipo nilipokuja kugundua kuwa yule ndiye aliyekuwa akiishi pale kwa wakati huo akilinda nyumba hiyo. Tuliingia mpaka ndani na baada ya kuonyeshwa pa kulala kila mtu Jamshid aliamua kuondoka kwenda kununua chakula kwenye soko lililokuwa kilomita mbili toka pale tulipokuwa. Aliporudi alikuwa na vyakula vyakutosha na mabomba mengine ambayo sikuyaelewa ni ya kazi gani na dawa nyingine na sindano.

“Jamshid hayo mabomba ya nini?” nilimuuliza na hakunijibu chochote zaidi ya kucheka tu na kunipa ishara ya kuwa nimfuate,,nilimfuata mpaka chumba ambacho tulikuwa tumemlaza Samah ambaye hata hivyo alikuwa hajapata fahamu.

“hii ni mirija ya kumlishia siunaona hapo iyo sehemu mpaka iunge ndio ataweza kula kwaiyo we shika hii nikuonyeshe kitu” alinipa mirija ile nishike na aliweka kwenye ile chupa chakula laini na kuichomeka ile mirija kisha alianza kuiingiza puani kwa Samah,,sikuweza kuangalia lile zoezi lilivyokuwa likiendelea pale nilifunga macho na nilipokuja kufungua nilikuta amemaliza na sasa alifungua kile kidonda na kuanza kukisafisha vizuri na kisha alichukua sindano na uzi akaanza kushona ile sehemu taratibu na alipomaliza alimchoma sindano ya tetenasi na sindano nyingine aliyonitaarifu kuwa ni sindano ya diclofenac ya kumfanya asijisikie maumivu akiamka. Sikuataka kuuliza yeye alijuaje yote yale, baada ya kumalizana na Samah alimuita Clara na hapo alimfungua ule mkono wake uliokatwa na kuanza kumsafisha na pia alimpiga sindano ya tetenasi na kukifunga tena kile kidonda vizuri.

*****

Baada ya chakula cha jioni kila mtu alielekea chumbani kwake na mimi nilienda na Jamshid kwenye chumba chetu, nilimkosa sana Jamshid kitandani siku nyingi lakini hata hivyo sikuwa na nguvu za kufanya chochote hasa ukizingatia bado nilikuwa mgonjwa nanilikuwa nina msongo wa mawazo.

“baby can I ask u a question?”(mpenzi naweza kukuuliza swali) ilikuwa sauti ya Jamshid.

“yes ofcourse” (ndio, hakika) nilimjibu huku nikiwa nimelalia kifua chake kilichonikumbusha mara ya mwisho nafanya mapenzi na Jamshid.

“ule ugonjwa niliousoma kwenye ile habari kwenye gazeti la mwananchi ni kweli unaumwa?” aliniuliza na kuniondoa tena kwenye hali nzuri niliyokuwa nayo.

“ndio ni kweli na niliambiwa nisipofanyiwa upasuaji basi nitaweza kupata saratani ya utumbo” nilimueleza kwa sauti ya upole iliyojaa mchoko.

“hapana hutapata saratani nitahakikisha hupati,,huo ugonjwa tunaweza kuuwahi kwa wewe kunywa vidonge vya ‘ant-biotics’ ambavyo vitakwenda kuondoa ile athari taratibu na baada ya mda mfupi utaanza kutumia Salazopyrin, hivi ni vidonge ambavyo vinativu ivyo vidonda vya utumbo mkubwa na kuna dawa nyingine tutanunua mpenzi wangu” aliniambia na hapo nilinyanyuka na kukaa vizuri.

“wewe umejuaje yote hayo Jamshid” nilimuuliza huku nikimtazama usoni.

“mimi ni daktari” alinijibu huku akitabasamu na kuruhusu vishimo vidogo vilivyovutia nijitengeneze kwenye mashavu yake.

“kweli?” nilimuuliza tena kwa shauku.

“ndio ni kweli, nilisoma shahada yangu ya udaktari nchini India na baadaye shahada ya pili ya udaktari wa magonjwa ya tumbo na mfumo wa chakula huko Havard na baada ya hapo nilirudi Tanzania na kufanya kazi pale Ocean road na baadaye nilifanya kazi Regency,,baada ya muda mfupi ndipo mambo yalipobadilika na kufikia pale uliponikuta” alieleza na kwa muda huu hakuwa na furaha sana kueleza alivyoanza na kumalizia taaluma yake, nilihisi haikuwa imemfurahisha yeye kuelezea sehemu ya furaha yake iliyoharibiwa na wingu la ushenzi na ulafi wa utajiri wa wazazi wake,,nilielewa dhahiri kuwa Jamshid alifanywa kuwa mtu ambaye hakuwa vile, lakini mimi ndiye mtu niliyetakiwa kumfanya asahau machungu na majuto ya nyuma yaliyomkuta na kumbadilisha roho yake ya asili.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“usijali mpenzi, sasa ndio mwisho wa kila jambo,,tuko pamoja mpenzi wangu” nilijua pengine sio mwisho wa kila jambo kwakuwa polisi walikuwa wakinitafuta lakini sikuwa na namna ya kumfariji Jamshid zaidi ya kumwambia hivyo.

*****

Siku iliyofuata nilichelewa kuamka na nilikuja kustuka baada ya mionzi iliyokuwa ikipenyeza kutoka katika jua lililoonekana vyema kutoka katika milima ya udzungwa na tayari saa ya ukutani ilikuwa ikisema ni saa tatu asubuhi,,nilitazama huku na huku sikumuona Jamshid na ndipo nilipoamua kwenda kumtafuta sebuleni,,,nilikuta akitenga chai mezani na baada ya Clara kuamka na kuingia bafuni wote tulikaa mezani na kuanza kupata kifungua kinywa.

“jamani kuna kitu nataka kuwaambia” ilikuwa sauti ya Clara.

“mmh we are listerning”(tunakusikiliza) nilimjibu na kisha aliweka koo sawa na kuanza kuongea.

“Jana usiku niliongea na Gerald, anakuja Tanzania kunichukua, najua pengine huu ndo muda wa sisi kukaa pamoja lakini kwa yote yaliyotokea sina budi kurudi Uingereza ili nikalee ujauzito nilionao, hivyo Gerald ameondoka jana usiku nchini Afrika ya kusini ambako alikuwa kikazi na ataingia hapa Tanzania kesho kisha atakodi chopa hadi huku” niliishiwa nguvu kwa taarifa hii lakini ilikuwa ni taarifa njema kwa Clara na sikuwa na pingamizi juu ya hilo.

“Gerald ni nani” aliuliza Jamshid na mimi nilidakia.

“ni mchumba wake ambaye alikuwa nae toka tukiwa chuoni kule Finland” nilimjibu Jamshid na kumgeukia Clara kwa huzuni kubwa huku machozi yakinitoka nilianza kumsemesha.

“Clara umekuwa msaada mkubwa sana kwenye maisha yangu, najua hatukuwa marafiki wakubwa sana lakini umekuja kuwa msaada mkubwa sana kwangu,,nashukuru kwa yote,,sina lolote la kukulipa zaidi ya kusema asante sana, nashukuru sana na pia mungu atakulipa kwa yote,,atakujaza nguvu utajifungua salama mtoto mzuri mwenye afya” niliongea huku machozi yakinitoka na wote kwa pamoja tulikumbatiana,,siku ya leo ilikuwa ya huzuni kwa kila mmoja wetu,,hali ya manyunyu ya mvua na kaubaridi kalitufanya tukae ndani tu mda wote, na mchana Jamshid aliondoka kwenda kununua baadhi ya mahitaji na kuniletea zile dawa alizosema ili niweze kuanza dozi yangu kama alivyopendekeza.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“koh koh” ilikuwa sauti ya mtu akikohoa na wote kwa pamoja tuliacha kucheza karata pale tulipokuwa na kusikiliza ni wapi sauti hiyo ilitokea, baada ya wote kukaa kimya tuligundua ilikuwa kwenye chumba kile alichokuwapo Samah, tulinyanyuka wote na kuelekea kwenye kile chumba na kumkuta Samah akijaribu kunyanyuka, tulimnyanyua taratibu na Jamshid bila ya kusubiri akae sawa alianza kumuuliza maswali ya papo kwa hapo ambayo hata hivyo hakuyajibu zaidi ya kumtazama tu;

“Jamshid hana nguvu ya kujibu,,tumuache kwanza apumzike” nilimuomba Jamshid ambaye hata hivyo alionekana hakupenda kabisa Samah kuwepo pale, aliniagiza nikachukue kopo la glucose na nilienda niliporudi alimkorogea na kumnywesha kisha tulimbeba mpaka pale sebuleni kisha nilianza kuongea nae japo alionekana kuongea kwa shida ila nilimuelewa;

“Samah mimi ndo sababu ya wewe kuwa hai mpaka sasa hivi, haitakusaidia kama utanyamaza kimya na kuendelea kuona watu wakiteseka, niambie nawezaje kujiepusha na hao watu” nilimbembeleza ili aniambie na wakati huo Jamshid na Clara walikuwa kimya.

“Faith, kundi ulilojiunga halikuwa Freemason” ALIONGEA SAMAH.







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog