Simulizi : Penzi Ama Kaburi
Sehemu Ya Tano (5)
“Mh! Kama ni kweli, moyo wangu utaniuma sana,” aliendelea kujisemea.
Hawakuchukua muda mwingi wakafika nyumbani, wakateremka na kuingia ndani. Ngwali hakutaka kusubiri, moyo wake ulikuwa na shauku ya kutaka kujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, hivyo akatafuta nafasi ya kuwa na Shadya na kuanza kuzungumza naye.
“Mbona umebadilika hivyo?” aliuliza Ngwali.
“Nimekuwaje?”
“Umeonana na mimi ila huna furaha kabisa, yaani ni kama hukupenda kuniona, tatizo nini? Umempata mtu mwingine zaidi yangu?” aliuliza Ngwali, macho yake yalianza kuwa mekundu, yaani hakuwa na mwanamke aliyetegemea kulala naye zaidi ya huyo Shadya.
“Hapana! Nimechoka tu!”
“Ila unanipenda?”
“Ndiyo! Mbona leo unauliza mambo yanayonichanganya? Yaani hata kuuliza za masomo, imekuwaje huko, wewe unaulizia mapenzi tu, sijui unanipenda, sijui nimebadilika, hivi unajali kuhusu masomo yangu?’ aliuliza Shadya.
“Nisamehe mpenzi!”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Unajali?”
“Ndiyo maana nimesema nisamehe!” alisema Ngwali, hapohapo Shadya akarudi ndani huku akijifanya kukasirika.
Hakumtaka tena Ngwali, mwanaume huyo hakuwa na kitu, alikuwa kapuku tu, mwalimu wa madrasa ambaye pesa zake alitegemea mpaka michango ya wanafunzi wa madrasa ama pale ambapo wangepata shughuli ya kichuo kwenda sehemu
Kila alipomwangalia hakuona kama kungekuwa na maisha naye hapo baadaye na ndiyo maana muda mwingi alitafuta nafasi ya kuachana naye.
Huyo Ngwali hakuwa mwanaume sahihi kwake, hakusoma, alikuwa ustaadhi tu, ila kila alipomfikiria Alex, moyo wake ulikuwa na shauku ya kutamani kuendelea kuishi naye maisha yake yote kwa kuwa tu walifanana.
“Hii mijanaume mingine...” alijisemea kwa hasira na kuelekea chumbani kwake.
Ngwali alibaki akiwa amesimama tu, moyo wake ulichoma kama pasi, hakuamini kilichokuwa kimetokea. Ni kweli Shadya alibadilika lakini yeye kama mpenzi wake alitakiwa kumuonyesha mapenzi na si kumuuliza maswali yaliyoonekana kumtia hofu nzito.
“Ila nilitaka kujua! Mungu wangu! Hivi huyu Shadya akiniacha nitampata nani mie? Ngoja nimuombe msamaha!” alijisemea.
Hilo ndilo alilolifanya siku hiyo, siku nzima alimwandikia meseji za kumuomba msamaha na kumwambia asingerudia tena kufanya ujinga wa namna hiyo.
Alituma meseji ndefu zaidi ya hamsini lakini hapakuwa na meseji yoyote ile iliyojibiwa. Hilo lilimuumiza, mapenzi yakaanza kuonekana kuwa machungu kwake.
Usiku wa siku hiyo akabaki akilia kitandani mwake, moyo wake ukatokea kulichukia Jiji la Dar es Salaam kuliko sehemu yoyote ile duniani kwa sababu iliyaiba mapenzi yake ndani ya moyo wa mpenzi wake.
Wakati akilia chumbani, moyo wake ukisononeka, upande wa pili Shadya alikuwa akiwasiliana na Alex kwenye simu, mapenzi yalimteka na hakufikiria kitu chochote kile zaidi ya kuwa na mwanaume huyo maisha yake yote.
Siku ziliendelea kukatika, Ngwali alitamani sana kuonana na Shadya lakini hakuweza kuonana naye tena kwani simu hazikupokelewa wala meseji kujibiwa mpaka kipindi cha likizo kilipokwisha na kurudi chuoni huku akiwa amefaulu masomo yote vizuri.
“Nilikukumbuka sana,” alisema Alex huku akimwangalia Shadya.
“Nilikukumbuka pia! Leo nataka nije kulala kwako!” alisema msichana huyo.
“Haina shida. Karibu!” alisema.
***
“Nisikiliza Bhoke,” alisema mwanaume mmoja, alikuwa daktari, alivalia koti kubwa jeupe huku uso wake ukiwa na miwani ya macho.
“Moyo wangu unaniuma!”
“Kuathirika si mwisho wa matatizo, wengi wameathirika na bado maisha yanaendelea. Kuna dawa zitakazokufanya kuishi kwa kipindi kirefu,” alisema daktari huku akimwangalia msichana aliyekuwa akiongea naye.
Kwa jina aliitwa Bhoke Ahmed, alikuwa miongoni mwa wanawake warembo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kila alipokuwa akipita wanaume walimwangalia kwa macho ya matamanio, walimpenda kwa kuwa alikuwa na sura nzuri na walimtamani kwa kuwa alikuwa na wowowo kubwa.
Alifanya mapenzi na wanaume wengi chuoni hapo, hakuamini kutumia mpira, siku zote aliwaambia wanaume kwamba utamu wa pipi ni kuila bila ganda hivyo kufanya nao kwa kuamini angekuwa salama.
Baada ya kuhisi kama alikuwa na tatizo ndipo akaenda kupima na kugundulika alikuwa na virusi vya ugonjwa wa UKIMWI.
Hilo lilimuumiza mno, hakujua ni mwanaume gani ambaye alimwambukiza kwani alifanya na wengi, idadi yake ilikuwa kubwa kupita kawaida. Wanaume wote aliofanya nao mapenzi tangu aingie hapo chuoni wakaanza kujirundika kichwani mwake, walikuwa kama ishirini na mbili, na hakukumbuka hasa ni yupi alikuwa na tatizo hilo.
“Kenny, Maliki, John, Godwin, Alex, Jafari, Omar na wengine wengi,” alijisemea.
Hakuwa na nguvu za kubadilisha ukweli, alikubaliana na vipimo hivyo kwamba aliathirika na muda huo ulikuwa ni wa kutumia vidonge vya ARV kwa ajili ya kuongeza maisha yake na kuonekana kuwa na afya tele.
Hakutaka hilo lijulikane na mtu yeyote, aliwafikiria watu aliotembea nao, marafiki zake na hata maadui, kulikuwa na watu wengi ambao wangefurahia yeye kupata virusi hivyo na wachache mno wangehuzunishwa na hicho.
“Kuathirika kwangu kutakuwa siri yangu milele,” alijisemea wakati akiondoka ndani ya hospitali aliyokwenda kupima.
.
.
Maisha yalikuwa matamu mno, kwa Shadya hakutaka kusikia kitu chochote kuhusu Alex, alimpenda kutoka moyoni mwake, hapakuwa na mwanaume aliyekuwa na uwezo wa kuuchukua moyo wake zaidi ya huyo.
Penzi lake kwa Gibson lilipotea kabisa, na hakumkumbuka mwanaume huyo kwa lolote lile. Kwa kuwa penzi lake kwa Alex lilikuwa kama upofu fulani hakuweza kugundu kitu chochote kile, hata zile ishara ambazo zilionyesha kuwa na walakini kwa mwanaume huyo kwake ziligonga mwamba.
Alijitahidi kumuonyesha mapenzi yote ambayo hakuwahi kumuonyesha mwanaume yeyote yule, akili yake ilihama kabisa na muda huo alichanganyikiwa na penzi hilo jipya.
“Nitakupenda mpaka kifo changu,” alisema Shadya huku akimwangalia Alex machoni mwake.
Kila wikiendi wakawa watu wa kutoka kwenda sehemu mbalimbali kwa ajili ya kula raha tu, hawakuwa watu wa kukaa chuoni, mara nyingi nyakati za usiku walichukuana na kwenda kula raha.
Huko ndipo taratibu Shadya akajifunza kunywa pombe. Zilikuwa chungu siku ya kwanza, alizitema lakini kadiri alivyokuwa akiendelea kunywa zikazoeleka mdomoni mwake, sasa akawa na uwezo wa kunywa hata chupa hata tatu bila tatizo lolote lile.
Maisha ya starehe yalimchukua, yule Shadya aliyetoka Zanzibar hakuwa huyu wa sasa, alizoea kuvaa hijabu na mavazi yote ya heshima lakini cha kushangaza naye akaanza kuvaa suruali za kubana na kuyaacha mapaja yake wazi.
Hapakuwa na mtu aliyemshangaa, wanafunzi wa chuo walizoeana, mwaka wa kwanza watu huwa kama washamba fulani hivi, wana adabu, begi kubwa la kubebea madaftari lakini wanapoingia mwaka wa pili, kila kitu hubadilika kabisa, ndivyo ilivyokuwa kwa Shadya.
Alex alimpeleka mbio, alichanganyikiwa. Wakati mwingine alinogewa na pombe, alikunywa mpaka kuzima kabisa, alibebwa na Alex na kuingizwa ndani ya gari na kuondoka naye, alipokuwa akiamka asubuhi, alijishangaa akiwa chumbani.
Wakati hayo yote yakiendelea Rahim alikuwa akiyaona tu, moyo wake ulikuwa na ucungu mno, alimuona dada yake akibadilika lakini hakuwa na cha kufanya.
Kitu kilichokuwa kikimnyima furaha kabisa ni hali aliyokuwanayo ya kufanya mapenzi ya jinsia moja, aliona kabisa endapo angemwambia kuhusu tabia zile, mabadiliko yake basi naye angemwambia kuhusu mchezo wake mchafu.
Akaogopa kufanya hivyo, moyo wake uliumia ndani kwa ndani, alivumilia, alisononeka lakini hakuthubutu kumwambia hata mara moja.
“Leo kuna muziki babu kubwa klabu! Ungependa twende?” aliuliza Alex.
“Mh! Nitaweza kweli?”
“Kwa nini usiweze! Utaweza tu! Twende mpenzi,” alisema Alex.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku iliyokuwa ikifuata alikuwa na mambo mengi ya kufanya kwenye masomo yake, hakutaka kwenda huko lakini kwa kuwa aliombwa na mpenzi wake, hakuwa na jinsi, akakubaliana naye na kwenda huko.
Usiku wa saa tano ndiyo walikuwa wakiingia klabu. Kulikuwa na watu wengi, ila wanachuo ndiyo walikuwa wengi zaidi.
Kila mmoja alikuwa na mpenzi wake, watu walicheza muziki na wanaume wengine walikuwa peke yao, yaani walifika hapo kwa ajili ya kuwinda, mwanamke yeyote ambaye angejipendekeza, basi wangeondoka naye.
“Alex! Sikusomi ujue!” alisema jamaa mmoja, alimvuta Alex pembeni.
“Kwani wasiwasi wako nini?” “Naona kama unataka kunigeuka!”
“Hapana! Naomi yupo wapi?” aliuliza.
“Nishamseti! Leo anakwenda kulala na wewe. Na huyo Shadya inakuwaje sasa?” aliuliza jamaa huyo, aliitwa Christian.
“Huyu demu kama unamtaka ni lazima umnyweshe pombe, zinamchanganyaga sana, halafu zinahamiaga chini. Akilewa, jibebee mzigo wake, kapige mambo halafu jikatae! Yaani asijue kama aliondoka na wewe, asubuhi nitakuja!” alisema Alex.
“Poa! Haina shida.”
Ulikuwa ni mpango kabambe, Alex alimchukulia Shadya kuwa msichana wa kawaida, mapenzi kwake yalipotea kabisa na kitu pekee alichokuwa akikifikiria ni kutembea na wanawake wengine.
Mwanake ambaye alitamani kuwa naye kwa kipindi hicho alikuwa Naomi, msichana mrefu, macho ya goroli aliyekuwa na muonekano kama msichana wa Kinyarwanda.
Alimtaka, alimtumia rafiki yake, Christian kumuonganisha naye, halikuwa tatizo, naye kijana huyo akahitaji kuwa na Shadya, usiku mmoja tu, ampe raha usiku kucha.
Wakakubaliana wawapeleke wanawake hao klabu na ndivyo ilivyokuwa. Shadya hakujua kilichokuwa kikiendelea ila Naomi alisetiwa kabisa. Msichana huyo akapewa pombe nyingi, akanywa, alijiamini kwa kuwa alikuwa na Alex, alikunywa na aliposhikwa huku na kule, alilegea, yaani ni kama mwili ukakosa mawasiliano.
“Ngoja nikaruke naye,” alisema Christian.
Akamchukua Shadya ambaye alikuwa hajiwezi na kwenda naye katika loji moja iliyokuwa Sinza, akaingia naye ndani, kilichofuata ni kufanya naye mapenzi, alingoneka usiku kucha huku msichana huyo muda wote akijua alikuwa akifanya mapenzi na Alex kumbe siyo.
Wakati hayo yakiendelea, naye Alex alikuwa na Naomi chumba kingine, kwenye loji hiyohiyo. Alifanya naye ngono usiku kucha na muda wa saa moja asubuhi, alikuwa tayari kutoka kwenda katika chumba alichokuwa Shadya na Christian.
Shadya aliamka majira ya saa mbili asubuhi. Kichwa chake kilikuwa na pombe, akakaa kitanda, akajipekua chini, alikuwa ameingiliwa, tena ilionyesha siku hiyo aliingiliwa kwa muda mrefu isivyo kawaida.
Akaanza kukumbuka usiku uliopita alikuwa wapi. Akapata jibu kwamba alikuwa klabu, alipelekwa na Alex, alikunywa mpaka akazidiwa, akahisi waliondoka na kuingia ndani ya hiyo loji.
Wakati akijiuliza hivyo, mara mlango ukafunguliwa na Alex kuingia, uso wake ulikuwa na tabasamu pana, akamsogelea kitandani.
“Unajisikiaje mpenzi?” alimuuliza.
“Nimechoka sana!” alijibu kwa uchovu.
“Unataka tena?”
“Mh! Leo inaelekea ulifanya kwa kunikamia mno!”
“Kwa nini?”
“Hebu paangalie palivyo! Leo umenikomesha!” alisema msichana huyo huku akimuonyesha Alex katikati ya mapaja yake.
“Nilikuwa na hamu! Nataka tena mpenzi,” alisema Alex, akamlaza msichana huyo na kufanya naye mapenzi, kwani kwa jinsi alivyomuona asubuhi hiyo, akamtamani sana.
Huo ndiyo ulikuwa mchezo wake, kila mwanaume ambaye alimtaka Shadya, haraka sana Alex hakutaka kuremba, kazi yake kubwa ilikuwa ni kupewa pesa na yeye ndiye alifanya mchakato wa wanaume hao kufanya mapenzi na msichana huyo kwa staili ileile.
Shadya alitumika kingono bila kujua, wanaume wakaambiana na hivyo kuonana na Alex ambaye alifanya kama alivyomfanyia Christian na wanaume wengine.
“Ila mtoto mtamu sana! Aisee jamani Wazanzibar watamu!” alisema jamaa mmoja, alikuwa akiwaambia wenzake, alifanya ngono na Shadya zaidi ya mara tatu, hakumchoka, kila alipokuwa akimuona, alimtamani zaidi.
“Na mimi namtaka!” alisema jamaa mmoja, aliitwa Kizota.
“Haina noma. Kazungumze na Alex, andaa alefu thelathini yake, pombe za elfu ishirini za kumnywesha yule malaya, hela ya gesti anakuachia mzigo!” alisema Omary, mwanaume ambaye naye kama kawaida alifanya mapenzi na msichana huyo.
Kizota akaondoka na kumfuata Alex, alimwambia dhamira yake, kwa kuwa alitanguliwa dau, Alex hakuwa na ujanja, alikuwa akiingiza pesa kupitia msichana huyo, hivyo akakubaliana naye na hivyo kwenda klabu ambapo huko Shadya alinyweshwa pombe kali, alipolewa na kutokujitambua, Kizota akamchukua na kwenda naye loji.
Akafanya naye mapenzi mno, usiku mzima, asubuhi ilipofika, haraka sana akachukua kamera, akamuweka mtupu kitandani pale na kuanza kumpiga picha mfululizo.
Alipiga picha chafu, za kila aina, hakujipiga yeye, ila alimpiga msichana huyo, akachukua kiungo chake na kumuwekea mdomoni kuonekana alikuwa akiongea na maiki, akachukua na kumuwekea katikati ya mapaja yake, yaani alipiga picha za kila aina huku sura ya msichana huyo ikionekana waziwazi, alipomaliza, akamuita Alex ambaye alikuja chumbani ili ionekane yeye ndiye aliyempeleka mule na kufanya naye mapenzi kumbe mwanaume mwingine.
.
.
.
Shadya, msichana aliyekuwa na sura ya kipole, mrembo, mwenye moyo uliokuwa na upendo mwingi hakujua kilichokuwa kikiendelea nyuma ya pazia chuoni hapo.
Alimpenda sana Alex, alikuwa mwanaume wake aliyehisi ni wa kufa na kuzikana kumbe upande wa pili mwanaume huyo alikuwa akifanya mambo ya ajabu, ya kumdhalilisha na kumfanya kuonekana mtu asiyekuwa na thamani yoyote ile.
Alimpenda kijana huyo, alifanya kila kitu alichokitaka, hakuwa mnywaji wa pombe, ila kwa sababu yake akajikuta akiingia kwenye unywaji.
Dunia ilimchukua, ikaanza kumpoteza pasipo kugundua hilo. Alijiona msichana wa kawaida aliyewahi kufanya mapenzi na wanaume watatu tu kumbe haikuwa hivyo, zaidi ya wanaume kumi walikuwa wamelala naye, walimfaidi, waliujua utamu wake, sauti yake ya kimahaba kitandani waliijua vilivyo.
Baada ya manyanyaso ya kingono aliyofanyiwa bila kugundua akaanza kuyaona mabadiliko chuoni hapo, alishangaa, kila alipokuwa akipita watu walikuwa wakimwangalia kwa kumnyali, ni kama walishangaa ni kwa namna gani alifanya kitendo fulani cha aibu kwa mtu kama yeye.
Alitamani kujua hilo lakini hakuligundua kwa sababu tu alikuwa msichana mkimya ambaye hakuwa na mazoea na watu wengi.
Wale wachache ambao aliwazoea, waliogopa kumwambia, hawakujua angejisikiaje, waliumia mioyoni mwao, walimuonea huruma mno lakini bado midomo yao ilikuwa kimya, kama ilipigwa kufuli.
“Shadya!” alisikia akiitwa na mwanaume mmoja, alikuwa amekaa pembeni ya uwanja wa mpira wa kikapu chuoni hapo.
Shadya alimwangalia mwanaume huyo, alihisi alikuwa akitakwa kama wasichana wengine walivyokuwa wakihisi kila walipoitwa na wanaume fulani.
Alimwangalia mara moja halafu akampuuzia.
“Shadya!” mwanaume huyo akaita tena, mara hii akasimama na kuanza kumsogelea.
Shadya hakutaka usumbufu wala kuonekana malaya, kwa akili zake alizotoka nazo Zanzibar zilimwambia kuongea na wanaume wengi ni umalaya, mwanamke anayejiheshimu hatakiwi kuzungumza na mwanaume yeyote yule zaidi ya ndugu zake na watu wa karibu.
“Nimekuita lakini!” alisema mwanaume huyo kwa sauti ya upole, Shadya akasimama, alisubiri kusikia akiambiwa nini, japokuwa hakupenda sana kusimama kama alivyofanya.
“Unasemaje?” aliuliza huku akiangalia huku na kule, aliwaogopa watu ila mtu aliyemuogopa zaidi alikuwa Alex kwani alidhani angehisi jamaa huyo alikuwa mtu wake.
“U msichana mzuri sana!” alisema jamaa huyo kwa sauti ya chini, sauti ambayo ilibeba ujumbe mzito ndani yake.
“Ndilo unalotaka kuniambia?” aliuliza huku akionekana kubadilika.
“Ninakupenda sana na ndiyo maana ninataka kukwambia ninalokwambia, upendo wangu kwako ni wa matendo na si maneno. Kama hao unaodhani wanakupenda ingekuwa kweli, basi wangekwambia mapema hili ninalotaka kukwambia,” alisema, Shadya akaanza kupiga hatua, jamaa akamshika mkono.
“Nisikilize kwanza!” alisema kwa upole huku akijaribu kumvuta.
“Nimesema niache! Nitapiga kelele!” alisema msichana huyo kwa hasira.
“Shadya! Si kila mwanaume anayekusimamisha anataka kukutongoza, jaribu kunisikiliza,” alisema, kidogo maneno hayo yakamfanya msichana huyo atulie na kuanza kumwangalia.
“Unataka kuniambia nini?”
“Unajua kitu gani kinaendelea chuoni kuhusu wewe?” aliuliza jamaa huyo.
“Kitu gani?”
“Unahisi umezungukwa na watu sahihi?” aliuliza swali lililomfanya Shadya kumkazia macho.
“Unamaanisha nini?”
“Pole sana!”
“Pole ya nini?”
Kabla jamaa hajajibu, simu ya Shadya ikaanza kuita, akashukuru Mungu, haraka haraka akaitoa na kuangalia jina, alikuwa Alex.
Akasogea pembeni na kuanza kuongea naye, hakuridhika, akatumia njia hiyo kama kumkimbia mwanaume yule, akaanza kupiga hatua kukatiza uwanjani kuelekea katika mabweni ya Magufuli.
“Shadyaaaa...” aliita jamaa, msichana huyo akawa anapiga hatua kusonga mbele.
Hiyo ilikuwa nafasi yake, hakutaka kumuacha msichana huyo, alikuwa na mengi ya kumwambia, akaanza kumfuata lakini naye baada ya kuona anafuatwa, akaanza kupiga hatua zaidi.
“Shadya! Alex anakuharibu!” alisema jamaa huyo baada ya kumfikia, kusikia hivyo, Shadya akasimama.
“Hebu subiri baby nitakupigia,” alisema Shadya kwa sauti nyororo kabisa, akakata simu na kumwangalia mwanaume huyo.
“Shadya! Kitu nitakachokwambia kisikushtue, usichukue uamuzi wowote ule mbaya,” alisema
“Kitu gani?”
“Nitakalokwambia na kukuonyesha ni kwa sababu nakupenda, sikupendi kimapenzi bali nakupenda kama ndugu yangu, dada yangu wa damu,” alisema huku akimwangalia Shadya.
“Unanichelewesha, niambie unataka kusema nini! Mara Alex, mara ndugu yako wa damu, hebu niambie!” alisema Shadya, sasa akabadilika, alitamani kuondoka lakini alishangaa kuona akiendelea kusimama.
“Picha zako zimesambaa!” alisema mwanaume huyo.
“Picha zangu! Picha gani?”
“Za utupu, ukiwa na mwanaume chumbani! Shadya hivi unajua unaonekana kama malaya chuoni hapa?” alisema jamaa huyo.
Shadya alimsikiliza, kwanza akapuuzia, alihisi kama jamaa huyo alikuwa akitumia njia hiyo kumpata kimapenzi, badala ya kuuliza zaidi, ndiyo kwanza akatoa tabasamu.
“Hii njia yako ya kumtongoza mwanamke nimeipenda...eti picha zangu...” alisema Shadya kwani alikuwa na uhakika hapakuwa na picha zake zozote zile za utupu.
Alichokifanya jamaa huyo ni kutoa simu yake, akafungua sehemu ya picha na kumuonyesha msichana huyo. Shadya akachukua simu ile na kuanza kuangalia.
Macho yake yalipotua kwenye picha zile, alishtuka, hakuamini alichokuwa akikiangalia. Moyo wake ukapiga paaa! Akahisi kama waya uliokuwa na umeme ukipita mwilini mwake.
Pale aliposimama alihisi kupigwa ganzi, kulikuwa na upepo uliokuwa ukivuma kutoka kwenye miti lakini cha ajabu, ni ndani ya sekunde chache tu, kijasho chembamba kikaanza kumtoka.
Mara ya kwanza alihisi ni picha zilizoeditiwa, akaanza kuangalia sura, ilikuwa yake, akaja kifuani, alikuwa yeye na alipoangalia pajani, aliliona doa lake, alikuwa yeye kabisa, hazikuwa picha za kueditiwa.
“Ma...ma...ma...ma...ma...” alitaka kuzungumza maneno fulani lakini alishindwa, mdomo wake ukawa mzito kufunguka, alihisi kama kulikuwa na mtu aliyekuwa akimzuia kusema kitu fulani.
Machozi yakaanza kutoka machoni mwake na kutiririka mashavuni, hakuamini alichokiona na wakati mwingine alitamani kile kilichokuwa kikionekana kwenye simu ile kiwe ndoto fulani.
Miguu ikaanza kulegea na kujikuta akikaa chini na kuanza kulia kwa sauti ndogo. Haikuwa picha moja, zilikuwa nyingi, zilizokuwa na aibu mpaka mwenyewe akaanza kuogopa.
“Alex...”
Hilo ndilo jina lililomjia kichwani mwake. Alichanganyikiwa, alimpenda mwanaume huyo lakini kitu cha ajabu alimfanyia jambo la kinyama sana.
Hakujua kwa sababu gani mwanaume huyo alifanya uamuzi wa kupiga picha hizo na kuzisambaza, alikumbuka kila kitu kwamba alikuwa akilewa mara kwa mara kumbe mwanaume huyo alichukua nafasi hiyo kupiga picha hizo.
“Shadya! Huyu si Alex...” alisema mwanaume huyo, hapo Shadya akashtuka tena, akasimama.
“Ni mwanaume mwingine. Umekuwa ukifanya ngono na wanaume tofautitofauti bila kujua.
Alex aliamua kukutumia kingono, kuna wanaume zaidi ya kumi umefanya nao mapenzi! Pole sana Shadya, hakuna mtu anayetaka ulijue hili na ndiyo maana nimekwambia marafiki uliokuwanao si sahihi katika maisha yako!” alisema jamaa huyo.
“Alex amenifanyia hivi mimi?” aliuliza Shadya huku akilia.
“Pole sana! Pombe zilikufanya kutokug...” alisema jamaa huyo, hata kabla hajamaliza sentensi yake Shadya akatoka mahali hapo, akaanza kukimbia.
Hakutaka kubaki chuoni, ilikuwa ni aibu kubwa, alikimbia kama mtu aliyechanganyikiwa, moyo wake ulichoma, uliuma kupita kawaida.
Jamaa alijaribu kumuita ila hakuitikia zaidi ya kuendelea kukimbia kwa kasi kubwa. Alipofika getini, akatoka mpaka nje, mguuni alikuwa na kiatu kimoja, na hakulijua hilo.
Wakati akikimbia akaanza kumkumbuka Alex, chuki dhidi ya mwanaume huyo ikaanza kujijenga moyoni mwake, hakuamini kilichokuwa kimetokea.
Alipomaliza kwa Alex akaja kwa Gibson kisha Ngwali. Alijiona mjinga mno, aliikumbuka siku ambayo aliondoka Zanzibar na kuelekea Dar es Salaam, aliyakumbuka maneno ya mpenzi wake huyo aliyomwambia kuhusu jiji hilo.
Kulikuwa na wanawake wapole, washamba waliokuwa wakiingia humo kutoka sehemu mbalimbali, wanawake ambao hawakujua kitu chochote kile ila baada ya kuishi humo, wakajikuta wakianza kubadilika.
Wengine wakafakamia pombe, starehe zikawapata, wakaanza kufanya ngono na wanaume wengi na mwisho wa siku kupata mimba, na kama walichoma sindano za kuzuia mimba, wakajikuta wakipata UKIMWI.
Hilo likamtisha mno, na mbio zake hizo alikuwa akikimbia kuelekea hospitalini, na hospitali ya karibu kutoka hapo alipokuwa ilikuwa ni Megra.
Huku akiwa amechoka, akafika hospitalini hapo na kuingia ndani. Ilikuwa ni majira ya saa 12:49 jioni, hapakuwa na watu wengi, hivyo akaunganisha mpaka mapokezi.
“Karibu dada...” alimkaribisha nesi aliyekuwa ampokeze.
“Nimek....uja kump...ima...” alisema huku akihema, jasho lilikuwa likimtoka, kila mtu aliyekuwa akimwangalia, alimshangaa.
“Kupima malaria?” aliuliza nesi huyo.
“UKI..MWI...” alijibu.
Japokuwa kilikuwa kitu cha kushangaza sana kutokana na muonekano wake lakini nesi hakushangaa, akamwambia chumba alichotakiwa kwenda hivyo kufanya hivyo.
Alipofika huko, akaelezea shida yake na kufanya kila alichotakiwa kufanya na kuelekea katika chumba husika na kutolewa damu yake.
Alikuwa na mambo mengi ya kufanya lakini hilo lilikuwa muhimu kwake. Maneno ya mwanaume aliyekutana naye na zile picha alizomuonyesha zilimtisha mno, moyo wake haukuweza kumsahau Alex, alionekana kuwa mwanaume mwenye moyo wa kinyama kupita kawaida.
“Alikuwa akiniuza kila nilipolewa?” alijiuliza huku akianza kulia pale kwenye benchi.
Mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kwa nguvu, hofu ikamtanda, moyo wake ukagawanyika, upande mmoja ulimtia nguvu kwa kumwambia asihofu yupo salama lakini upande mwingine ulimwambia asijisumbue kwani tayari aliathirika.
“Allah naomba unisaidie!” aliomba kimya kimya.
Baada ya dakika arobaini na tano akaitwa, akainuka na kuanza kuelekea kwenye chumba alichohitajika. Akafuta machozi yake lakini macho hayakuacha kuwa mekundu kwa sababu ya kulia sana.
Alipofika, akakaa, alikuwa akitetemeka. Mbele yake alikuwa mwanamke mtu mzima, alionekana kuwa na hekima kuliko watu wote ndani ya dunia hii.
Alivalia miwani na mikononi mwake alishika karatasi iliyokuwa na majibu ya damu ya msichana huyo. Kabla ya kumwambia kuhusu majibu hayo akaanza kumuuliza maswali mengi na kumshauri pia.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mara yako ya mwisho kufanya mapenzi ilikuwa lini?” alimuuliza mwanamke yule.
“Wiki mbili zilizopita!” akadanganya.
“Ulitumia kondomu?”
Akakaa kimya kwa sekunde chache.
“Ndiyo nilitumia.
“Una wapenzi wangapi?”
“Mmoja!”
“Ulishawahi kuja kupima naye?” “Hapana!”
“Kwa sababu gani?”
“Anaogopa!”
“Na wewe ni mara ya ngapi umekuja kupima?”
“Mara ya tatu!”
“Mara ya mwisho ilikuwa lini?”
“Miezi mitatu iliyopita!”
“Ukikuta hujaathirika, utachukua uamuzi gani?” aliuliza mwanamke huyo.
“Nitawalinda watu wote wanaonizunguka!” alijibu, alikuwa akitetemeka mno.
“Na ukikuta umeathirika?” Napo akakaa kimya kwa sekunde chache.
“Nitawalinda wote kwa kutumia kondomu, kula vizuri na kudumisha afya yangu,” alijibu.
Muda wote huo alikuwa na hofu, hakujiamini hata kidogo, aliona kabisa mwanamama huyo alikuwa akijichelewsha na matokeo yalikuwa wazi kwamba aliathirika. Lawama zote zikawa kwa Alex.
“Hivi Alex alishawahi kupima?” alijiuliza.
Baada ya maongezi ya nusu saa huku akifarijiwa kwa maneno matamu na ushauri wa hali ya juu, akapatiwa majibu ya damu yake, na kitu alichokiona zaidi ni neno HIV/ POSITIVE.
Hapohapo akajikuta akinyong’onyea, akaanguka chini kama mzigo.
Puuuu!
.
.
Shadya alirudiwa na fahamu akiwa juu ya kitanda, alifumbua macho yake na kuangalia huku na kule, hakuwa na kumbukumbu juu ya mahali alipokuwa muda huo.
Dripu ilikuwa ikining’inia kwa juu ambayo ilikuwa ikipeleka maji katika mshipa wake, akaangalia huku na kule, akagundua alikuwa hospitalini hapo.
Akaanza kuvuta kumbukumbu zake, akaanza kukumbuka kilichokuwa kimetokea.
Majibu ya vipimo vya Ukimwi yakaanza kujirudia kichwani mwake, palepale kitandani akaanza kulia.
Hakuamini, Shadya yeye, msichana mrembo, aliyekuwa na uzuri wa kila aina, leo hii alikuwa ameathirika kwa virusi vya Ukimwi.
Hapo ndipo alipoanza kumtupia lawama Alex, alijua mwanaume huyo ndiye aliyesababisha hayo yote. Hakujua michezo yake kwamba alikuwa akitumika kingono, aliumia, alitamani muda urudi nyuma akarekebishe alipokosea lakini ilishindikana kabisa.
Baada ya dakika kadhaa yule mama aliyempa majibu akaingia, alipomuona, sura yake ikavikwa na simanzi nzito, Shadya alikuwa binti mdogo, aliyekuwa na ndoto kubwa maishani mwake lakini alihisi kila kitu kingeharibika baada ya kuathirika.
“Shadya...” aliita mwanamke huyo kwa sauti ya chini.
“Nimeathirika! Alex ameniua...” alisema huku akiendelea kulia.
“Nisikilize mwanangu! Kuathirika si mwisho wa maisha! Bado una nafasi ya kuendelea kuishi! Kuna watu wengi wanaishi na virusi vya Ukimwi, usikate tamaa, utatakiwa kufuata ushauri wa vyakula nilivyokwambia,” alisema mwanamke huyo.
“Alex ameniua mama....kwa nini Alex ameamua kuniua?” aliuliza Shadya, muda wote alikuwa akilia tu.
Mwanamke huyo alipata kazi ya ziada kumbembeleza kitandani pale na kuendelea kumwambia kuwa na virusi vya Ukimwi haikumaanisha ndiyo ulikuwa mwisho wake.
Alilia lakini hakubembelezeka ila ilivyofika majira ya jioni akaruhusiwa kuondoka na kuambiwa alitakiwa kufika hospitalini hapo mara kwa mara.
Akaondoka, kichwa chake kilikuwa na mawazo tele, hakujua ni kwa namna gani angeendelea kuishi na virusi vya Ukimwi. Moyo wake ulikuwa na maumivu makali na lawama zote zilikuwa kwa Alex.
Huku akimlaumu mwanaume huyo kwa kumtumikisha kingono lakini upande mwingine wa moyo wake ukaanza kumlaumu yeye mwenyewe.
Alikuwa na mpenzi wake, Ngwali huko Zanzibar, alimpenda na kumthamini lakini baada ya kwenda jijini Dar es salaam kila kitu kikabadilika, starehe zimampata, akakutana na wanaume waliokuwa wakijua kuongea sana na mwisho wa siku kufanikiwa kulala naye.
Akafika bwenini, moyo wake ulikuwa na maumivu makali mno, alishindwa kujua ni kwa namna gani angeweza kuishi na virusi vile.
Huku akiwa akifikiria mambo yote hayo, kitu pekee kilichokuja mbele yake ni kujimaliza tu kwani aliona giza na hakuwa tayari kuona akiusambaza ugonjwa huo kwa watu wengine.
“Siwezi kuishi na virusi vya Ukimwi,” alijisemea.
Kabla ya kufanya kitu chochote kile akampigia simu mdogo wake, Rahim na kuomba kuonana naye, hilo halikuwa tatizo, kijana huyo akafika mahali alipoambiwa kwenda na kuonana na dada yake huyo.
Kwa jinsi alivyomuona tu, alibadilika, hakuwa Shadya yule aliyezoea kumuona, alikuwa na huzuni na macho yake yalikuwa mekundu yaliyoonyesha alitoka kulia sana dakika kadhaa zilizopita.
“Kuna nini Shadya?” aliuliza Rahim huku akimwangalia dada yake huyo.
Shadya alitamani kuzungumza kitu lakini alishindwa kabisa, hakujua ni kwa namna gani ndugu yake angemuelewa kile kilichokuwa kimetokea.
“Niambie kuna nini! Naona unalia tu!” alisema Rahim.
“Nimeathirika!” alimwambia.
Rahim ni kama hakusikia vizuri, alimwangalia ndugu yake huyo kwa macho yaliyomtaka kurudia tena kile alichokuwa amemwambia muda huo.
“Unasemaje?” aliuliza.
“Nimeathirika! Alex ameniua!” alijibu kwa huzuni.
“Yaani sijaelewa, unamaanisha nini?”
Hakuzungumza tena, moyo wake ulimchoma mno, hakutaka kubaki mahali hapo, akasimama na kuondoka zake. Rahim alijaribu kumuita lakini hakuitikia wala kugeuka.
Akamkimbilia na kumshika mkono, Shadya akajitoa, akaanza kuelekea bwenini. Kitu pekee kilichokuja kichwani mwake ni kujiua tu, hakutaka kuendelea kuishi.
Aliyachezea maisha yake, alikuwa na ndoto nyingi mbele yake lakini alihisi zote hizo zisingeweza kutimia kwa sababu tu aliathirika.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Moyo wake kwa wakati huo uligawanyika mara mbili, kuna upande ulimwambia hakutakiwa kujiua kwa sababu bado angeweza kuishi miaka mingi lakini upande mwingine ulimwambia ni lazima ajiue kwa sababu tu kusingekuwa na maisha zaidi, mbaya kuliko yote, watu wangekuwa wanamcheka tu.
“Yaani watu wakijua umeathirika, hutokaa kwa amani, utachekwa, utanyapaliwa, yaani hutokuwa na maisha ya raha hata kidogo,” aliisikia sauti moyoni mwake.
Hiyo ndiyo ilimtia hofu na kuwa na msimamo wa kutaka kujimaliza tu. Hapo bweni hakukaa sana, akaondoka na kuelekea mtaani ambapo akanunua sumu ya panya na kurudi tena na kukaa kitandani mwake.
“Allah naomba unisamehe!” Hakutaka kusubiri, moyo wake ulikuwa na maumivu makali mno, kila alichokuwa amekipanga alihisi kama kingevurugika kwa kuwa tu aliathirika alipokuwa chuoni.
Akachukua glasi ya maji na sumu ile, akachanganya na kunywa, akajifunika na shuka lake, tumbo likaanza kumkata na hakuchukua dakika nyingi, akatulia, mapovu yakamtoka mdomoni na kufariki dunia.
Hakuna mtu aliyejua kama msichana huyo alifariki dunia, alionekana kama amelala, baada ya masaa matatu ndipo watu walipokuja kugundua.
Kila mmoja alishangaa, taarifa zikaanza kusambaa kwamba Shadya amejiua kwa kunywa sumu akiwa bwenini. Taarifa zilipofika kwa Rahim, hakuamini, alilia mno, hapakuwa na mtu aliyejua sababu zaidi yake, na hakutaka kumwambia mtu yeyote zaidi ya ndugu zake tu.
Mwili wake ukachukuliwa na kupelekwa hospitalini, ukahifadhiwa mochwali baada ya kugundulika alikuwa amefariki dunia.
Wazazi, ndugu, jamaa na marafiki walilia kwa ajili yake, kila mmoja alijaribu kujiuliza sababu ya msichana huyo kuuchukua uamuzi mkubwa namna hiyo lakini hakuna aliyejua lolote lile zaidi ya Rahim ambaye aliamua kuwa kimya kwa sababu maalumu.
Siku iliyofuata mwili ukasafirishwa mpaka Zanzibar. Wazazi wake walihuzunika mno, walijitahidi kutafuta pesa kwa ajili ya binti yao, waliishi maisha ya shida kwa sababu yake na kaka yake, ili wasome tu.
Watu waliwacheka walipoona wakimsomesha mtoto wa kike kwa kuwa wasichana wengi wa Zanzibar hawakuwa wakipelekwa shule, wao waliamua kuwa tofauti nao, walimsomesha kwa nguvu zote lakini mwisho wa siku Shadya akaja kujimaliza akiwa chuoni, tena alibakiza mwaka mmoja kabla ya kuchukua Diploma yake ya kwanza.
“Kwa nini amejiua?” lilikuwa swali walilojiuliza wazazi wake kila siku, Rahim hakuwajibu kwa kipindi hicho mpaka baada ya mwezi mmoja ndipo akaamua kuwaambia ukweli kile alichoambiwa na Shadya.
“Alikuwa ameathirika!” alisema Rahim kwa unyonge kabisa.
“Aliathirika? Kivipi yaani?”
“Aliniambia hivyo! Akaondoka, baada ya saa kadhaa ndipo nikapata taarifa kwamba alijiua,” alijibu Rahim.
Huo ukawa mwisho wa Shadya, watu walihuzunika kwa sababu ya kifo chake. Alex aliendelea kuishi vizuri japokuwa aliathirika, hakujua kwa kuwa aliogopa kupima.
Kupitia sura yake ya kipole, bado aliendelea kutembea na wanawake wengi chuoni hapo, kila msichana mzuri aliyekuwa akimuona, alijitahidi kumfuata kwa upole na kujifanya mshauri na mwisho wa siku kulala naye na kumwambukiza Ukimwi.
Wanaume kama Alex bado wapo, wana nguvu, wanatembea na wanawake mavyuoni na mitaani. Hawajali kuhusu afya zao, wanaendelea kusambaza virusi vya Ukimwi kwa kila mwanamke watakayelala naye.
Wasichana kama Shadya nao wapo, wanamaliza shule na kujiunga na masomo ya chuo. Wanapofika mwaka wa kwanza, hawajui lolote lile, kila mwanaume anayewafuata na kuwasaidia anaonekana mwema mbele ya macho yao.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hawafikirii kuhusu ndoto zao, ni kwa jinsi gani wazazi wao wamejinyima kwa ajili yao, wapate elimu bora na kuwaondoka katika giza la umasikini, wanapofika chuoni, maisha ya starehe yanawavamia na kuingia mitegoni na mwisho wa siku kuharibu ndoto zao.
Kumbuka kwamba UKIMWI UPO MAVYUONI, MITAANI NA MAOFISINI. Ikibidi acha ngono, ukishindwa, tumia kondomu.
Ujumbe huu uwafikie vijana wote ambao wanapambana kwa ajili ya maisha yao ya badaye.
MWISHO
-
0 comments:
Post a Comment