Simulizi : Kichaa Wa Mtaa
Sehemu Ya
Tano (5)
Siku zilisonga, miezi nayo ikajongea kijana Nyogoso akiendelea kuhaha mtaani na uchizi wake ilihali Mazoea naye akiwaza ni vipi atafanikisha kumpata kichaa huyo wakati huo huo Suzani akizidi kusongwa na mawazo, Nyogoso akionekana kumvuruga hisia zake.
Naam! Hatimaye ile siku ya hukumu iliwadia, Dokta Luanda alipandishwa kizimbani, ukosaji wa dhamana ukaharalisha kifungo chake. Luanda alilia sana mbele ya mbele ya hakimu, hakuwa na lakujitetea kwani ushahidi wote uliwekwa wazi. Alilaani roho ya tamaa iliyomuingia, alijilaumu kwa nini hakuridhika na mshahara wake lakini yote kwa yote hakuwa na budi kukubaliana na hukumu hiyo. Baada ya hukumu ya Dokta Luanda, nje maisha yaliendelea. Alionekana Suzani na Loi wakitembea kunyoosha miguu baada kuketi sehemu moja kwa muda mrefu.
"Suzani, unajua Lidai anakupenda sana ila anashindwa kukwambia", aliongea Loi akimwambia Suzani. Suzani alicheka baada kuyasikia maneno aliyoyasema rafiki yake. Alipokatisha kicheko chake akasema "Loi, hivi unavyoniona Lidai ni mwanaume wa kutembea na mimi?.. Au umetumwa?. *
" Kwanini Suzani, kwani yeye sio mwanaume?. ", akianza kwa taharuki, aliuliza Loi. Suzani akashusha pumzi kisha akajibu" Hapana sina maana hiyo, lakini upande wangu naona hanifai. Halafu naona amekutuma, unaonaje ukienda wewe?, " alijibu huku akionekana kukasirika. Loi alitambua hilo, alibidi awe mpole ambapo alimtuliza kwa kumwambia" Ok, samahani best kama nimekukwaza ila mimi nimefikisha kile nilicho ambiwa ", Suzani alikaa kimya wakati huo huo honi ya gari ilisikika nyuma yao. Walipisha kando. Gari hilo lililowapigia honi liliwapita kisha likasimama mbele yao, punde si punde ndani ya gari hilo alishuka kijana Lidai akiwa katika mavazi mazuri ya kupendeza, alivaa suruali ya kitambaa cheusi iliyonyooka vizuri, shati alivaa nyeupe ya mikono mirefu iliyotundikwa na tai nyekundu, bila kusahau viatu vyeusi vilivyoonekana kung'aa kwa mkolezo wa kiwi. Lidai siku hiyo alionekana kuwa nadhifu, alijaribu kuufanyia kazi ushauri aliopewa na marafiki zake, ambapo aliambiwa kuwa ili ampate mrembo Suzani basi inambidi awe mtanashati, walimuaminisha kuwa wasichana walio wengi hasa hasa wale wa geti kali hupenda wanaume waliokuwa safi. Kwa mbwembwe zote Lidai alivua miwani yake usoni, akaachia tabasamu pana kisha akatupia macho yake kutazama kule wanapotokea Suzani na Loi. Punde si punde wawili hao walimpita Lidai pasipo hata kumsalimia. "Ahahaha hahahaha", aliangua kicheko Lidai huku akijitazama vizuri namna alivyotupia kisha akwatazama warembo hao ambao tayari walikuwa wamempita hatua kadhaa. Alishusha pumzi ndefu halafu akajisemea "Loh! Sijui hata sijui nimuenzeje, japo nimetupia kuliko siku zote", aliwaza Lidai. Lakini punde alipiga moyo konde, akapasa sauti kumuita Suzani, ila Suzani licha ya kuisikia sauti hiyo kamwe hakugeuka nyuma wala kusimama. Loi hakufurahishwa na kitendo hicho alichofanya Suzani, alikemea kwa kusema "Sio vizuri Suzani, siku zote kataa maneno na sio wito. Simama umsikilize shida yake", Suzani alisimama, Lidai aliachia tabasamu baada kuona Suzani amesimama, alinyoosha mikono juu kumshukuru Mungu kisha akajongea kumkaribia. Alipomfikia, Loi alikaa kando kuwaachia nafasi wawili hao ili wazungumze kwa uhuru pasipo buguzi yoyote. Lidai alikohoa kidogo, akamsalimu Suzani ambapo naye aliitikia kisha akakaa kimya kumsikiliza. Woga ulimjaa kijana huyo, alishindwa kujua namna ya kumuanza Suzani, na hatimaye Suzani alikereka akamwambia "Ongea shida yako, wewe si umeniita?.."http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Eeeh ndi..ndio.. Ndio Suzani nimekuita nao..", alijibu Lidai huku akitetemeka, alishindwa kujiamini akajikuta aking'ata ulimi wakati huo huo pembeni yao alionekana kichaa Nyogoso akipita. Suzani alipomuona alistuka, haraka sana alimkimbilia ilihali huku nyuma yake akimuacha Lidai akiwa amepigwa na butwaa. Macho ya yake hayakuweza kuamini kile alichokuwa akikiona, na kilicho mshangaza zaidi ni baada Suzani kumkumbatia kichaa Nyogoso pasipo woga.
"Loi, huyu Suzani yupo sawa kweli?..", alihoji Lidai kwa hamaki kubwa.
"Hata mimi namshangaa sana",alijibu Loi huku naye akionekana kupigwa na bumbuwazi wakati huo huo kichaa Nyogoso alimsukuma Suzani kwa nguvu kisha akasema "Achana na mimi, unajua? Hapa mjini chunga sana utakumbatia mjini Ebo", kichaa Nyogoso alipokwisha kusema hivyo aliangua kicheko kwa sauti. Suzani alinyanyuka kutoka chini, alimsogelea kwa mara nyingine tena akamwambia "Ndio nqkufahamu, naomba unipe dakika chache nikukumbushe."
"Jambo gani utaniambia wewe?..", alihoji kichaa Nyogoso, muda huo huo sauti ya Loi ilisikika ikisema "Suzani huyo ni kichaa, achana naye bwana", Maneno ya Loi aliyasikia kichaa Nyogoso, alicheka kwa mara nyingine tena kisha akasema "Hivi kati ya mimi na wewe nani kichaa? Ukitathimini kwa umakini utagundua kuwa mabinti kama nyinyi wenye nyodo, huishiwa kuchezewa na kuachwa. Sababu ya dharau. Labda nikwambie kitu kimoja ambacho akili yako haiwezi kujua, mwanamke kuwa bikira haimanishi kwamba eti ndio msafi sana, kwani hata baadhi ya ardhi hazipandwi mazao kwa sababu hazina mbole... "
" Unamana gani we kichaa ", alihoji kwa hamaki Loi.
" Utakuwa unajua nilicho manisha kwa sababu unaaakili timamu, ila kama umeshindwa kujua maana basi wewe ndio chizi mjinga. Wanja kama wepa ya fuso, ukome kudharau watu ", alisema kwa hasira kichaa Nyogoso huku akimnyooshea kidole Loi. Loi aliogopa sana wakati huo huo Nyogoso alimgeukia Suzani akamwambia." Kama unamazungumzo na mimi, njoo nyumbani kwangu ", kwa hofu Suzani akamuuliza.
" Wapi?.. "
" Sinza makaburini", alijibu Nyogoso kwa sauti ya mbali kabisa.
"Makaburini?..", alijiuliza Suzani huku akimsindikiza kwa macho Kichaa Nyogoso.. Punde si punde kijana Lidai alikasirika sana, alilaani kitendo alicho kifanya Suzani kwani siku hiyo alivunja kabati akiamini njia hiyo ya kupendeza ingeliweza kumshawishi Suzani, lakini hatimaye alichokumbana nacho hata hakuweza kuamini.
"Kichaa? Suzani wa kumpenda mwendawazimu?..",akiwa na wingi wa ghadhabu alijiuliza Lidai kisha akaingia kwenye gari lake akaondoka zake. Akiwa ndani ya gari aliwaza sana, hasa hasa akimfikiria mara mbili mbili Suzani dhidi ya kichaa Nyogoso. "Huu ni upuuzi, inawezekana vipi Suzani ampende kichaa anikatae mimi? Hapana kuna jambo hapa si bure. Sasa lazima nile sahani moja na yule kichaa, nikishamalizana naye, nutahimia kwa kwa Suzi. Nina imani atanielewa tu,ngoja niwastue wana ili tukamnyooshe yule mjinga anayetaka kupindua meza kibabe. Kichaa?.. Ahahahah Hahaha hii ngumu kuamini ", alijigamba Lidai.
Lidai akaishia zake huku Suzani naye alionekana kupigwa na butwaa kwa muda wa dakika moja ingawa mwishowe alikaa sawa hapo wakiendelea na safari akiwa sambamba na rafiki yake kipenzi aitwaye Loi.
"Suzi,hivi kumkumbatia namna ile yule kichaa ulikuwa na maana gani?.." alihoji Loi akimuuliza Suzani kitendo kile alichofanya kwa kichaa Nyogoso. Suzani alikaa kimya kwanza kabla ya kujibu swali la Loi, lakini baadaye alifungua kinywa chake kusema"Loi rafiki yangu,ugua vyote ila sio mapenzi. Hebu tazama,utajiri wote walionao wazazi wangu pia uzuri nilio nao mimi..najikuta nampenda sana yule mkaka mpaka sijielewi"
"Suzani unasemaje? .." Loi alistaajabu jibu la Suzani. Na hapo Suzani akaongeza kusema " kipi kinacho kushangaza hasa Loi? .."
"Kinacho nishangaza ni wewe kumpenda mwenda wazimu" alijibu Loi.
"Je, unauhakika kuwa yule ni kichaa?.."
"Ndio uhakika ninao"
"Haya ukowapi?.."
"Suzani best yangu,mtu mwenye akili timamu hawezi kuishi makaburini"
"Alaah kwahiyo hiyo ndio point yako?.."
"Ndio "
Suzani alicheka kwa kebehi baada Loi kumjibu hivyo,na mara baada kumaliza kicheko chake alisema "Loi kwa taarifa yako,yule mkaka awe kichaa asiwe kichaa,mimi nitampenda milele"
"Shauri yako mimi simo ", alisema Loi wakati huo wakikaribia kufika nyumbani kwao Suzani. Siku hiyo Loi aliamua kulala na Suzani, walizungumza mambo mengi sana siku hiyo.
Kesho yake asubuhi,kijana Lidai aliamka akiwa na hasira kali za hapa na pale moyoni mwake. Ukweli kitendo cha yeye kukataliwa na Suzani kilimuuma sana, hasa pale Suzani alipo kwenda kumkumbatia kichaa na kumbusu mbele ya macho yake akidiriki kumuacha yeye ambaye alionekana kuwa nadhafu kila kona ya mwili wake. "Kudadeki siwezi kukubali mimi,huyu kichaa ana nini hasa mpaka apendwe na demu kama Suzani?..hakyamungu lazima nimhamishe mtaa" alijisemea Lidai. "Ama sivyo nitamcharaza fimbo ili hata siku nyingine amwogope Suzani,pumbafu zake" aliongeza Lidai. Kisha akatoka nje. Akaelekea bafuni kuoga, muda mfupi baadaye aliamliza ambapo alikwenda kijiweni kukutana na marafiki zake.
Washkaji zake walipo muona Lidai akitembea kuja kijiweni,mmoja alisema "Oya wadau,hivi kwa mtoko ule wa jana jamaa alimkosa kweli yule mrembo?.."
"Mmh moyo nao unamambo bwana,ngoja afike tumuulize ", alidakia mwingine wote wakimzungumzia kijana Lidai aliyevunja kabati kwa kununua nguo nzuri ilimradi amnase Suzani.
Hatimaye Lidai alifika kijiweni,marafiki zake wote walimtazama yeye wakingojea jambo kutoka kwake kuhusu mrembo Suzani,naye baada kuketi kwenye benchi,aliwasalimu washkaji kwa kuwapa tano kisha akanza kuzungumzia masuala ya mpira. Lakini kauli hiyo ilikatishwa na jamaa, jamaa huyo aliitwa Mikidadi.
Mikidadi ni moja ya vijana wa kijiji waliotoroka wakidhania kuwa wamemuuwa kichaa Nyogoso baada kumpiga kipigo cha mbwa mwizi akituhumiwa kutaka kubaka wanawake aliowakuta kisimani, ni kipigo ambacho kilimpelekea Nyogoso kupoteza fahamu,kitendo kilicho mstua Mikidadi, aliogopa sana alihisi ataishia jela akidhania kuwa tayari wameuwa. Na hivyo alikimbilia jiji Dar es salaam ambapo napo maisha yake yalikuwa ya kuunga unga. Magumu sana kiasi kwamba hata familia yake aliyo iacha kijijini kwao aliisahau akawa mtu wa kuishi vijiweni akigongea shilingi mia kwa mia mbili.
Mikidadi alikatisha mada hiyo ya Lidai kwa kusema "Mada za mipira sisi hapa hatutaki,ratiba zote za ligi kuu England tunazo. Nani asiyejua kama leo Manchester utd anampiga tena mtu goli nne? Acha mambo yako bwana,we tuambie mrembo umempata?..", alisema Mikidadi huku akiungwa mkono na vijana wengine waliokuwepo mahali hapo. Lidai alikosa la kujitetea, zaidi alisema "Tulieni mambo mazuri hayataki haraka"
"Sawa kabisa..haya tupe mambo hayo" alidakia mwingine wakati huo Lidai akifikiria ajieleze vipi mbele ya vijana wenzake ili apate kueleweka na sio kudharauliwa. "Nikiwadanganya kwamba nimekula tunda?! Nitasifiwa lakini moyoni nitabaki naumia, pia nikisema sijafanya chochote!! Nitaonekana domo zege...mmh nifanyeje mimi?.."alijishauri Lidai kwa muda wa nusu dakika. Lakini mwishowe aliamua kusema ukweli kilichotokea ambapo marafiki zake wote walistaajabu huku wengine wakionekana kutokukubaliana na kile asemacho Lidai.
"Huyo kichaa mwenyewe unamfahamu?..",alihoji Mikidadi.
"Kwa mara yangu ya kwanza kumuona mtaa huu,lakini nikikutana naye tena nitamiumbuka tu", alijibu Lidai.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ok cha msingi inabidi tuungane pamoja ikiwezekana tumpoteze kabisa huyo kichaa", jamaa mwingine aliyefahamika kwa jina Tino alidakia kwa kusema hivyo..
"Enhee tukishamalizana na huyo kichaa,kazi itabaki kwa mshkaji wetu hapa ajinafasi,akishindwa basi akose cha kusinginzia"
"Kweli kabisa" Wote kijiweni hapo walikubaliana hilo suala. Na sasa wakabaki kusubiri siku watakayo muona kichaa Nyogoso wamfanyie kitendo kibaya ilimradi tu Nyogoso aachane na Suzani, wasijue kuwa Sizani ndiye aliyependa wala Nyogoso hana mpango naye.
Upande mwingine baada Suzani kunywa chai alijiandaa haraka haraka, alipo jihakikishia kuwa yupo safi alizipiga hatua mpaka kwenye gari lao,akiwa sambamba na Loi walipanda wakaelekea makaburi ya Sinza ambapo huko ndipo yalipo makazi ya kichaa Nyogoso.
Walipofika walizama ndani kwenye wigo ulio tengenezwa kwa sinyenge kisha wakaanza kumtafuta kichaa mahali alipo ilihali upande wa pili alionekana mama Mazoea akiwa ndani ya gari akielekea kwa rafiki yake kipenzi,siku huyo alikwenda kumtembelea rafiki yake ili wazungumze mambo kadha wa kadha ikiwezekana ampe ushauri juu ya binti yake aliyezama kwenye penzi la kichaa Nyogoso.
Baada ya safari ya kitambo kirefu hatimaye lifika,alikaribishwa kwa furaha sana ambapo alipo ulizwa kinywaji anacho tumia. Alihitaji maji tu. Aliletewa akanywa bunda moja la maji kisha akashusha pumzi kwa nguvu halafu akasema yote yale yaliyotokea nyuma mpaka sasa juu ya binti yake.
"Pole sana shoga yangu,lakini kwa ushauri wangu mimi. Nasema usithubutu kukatisha penzi la mwanao kwa kijana huyo mzoa takataka. Shoga kumbuka penzi upovu,na endapo ukiweka pingamizi basi jiandae kumpoteza mwanao", alisema rafiki yake mama Mazoea. Alifahamika kwa jina mama Yoranda.
"Kwahiyo Shoga unadhani Dar yote hii ilivyokuwa kubwa nitamuona wapi huyo kijana? Maana kila siku Mazoea ananibana..kila siku yani mpaka nakosa amani kabisa"
"Mmh" aliguna mama Yoranda.
"Ok hapo inabidi upige ramli,utajua tu alipo kwa sasa", aliongeza kwa kusema mama Yoranda.
"Ramli ndio nini?..", alihoji mama Mazoea.
"Unakwenda mganga wa kienyeji anakutazamia kwenye TV yake asilia " alijibu.
"Anhaa..sawa. Ingawa mimi sipendi ushirikina ila kwenye hili jambo nimekubali tu",alisema mama Mazoea Kisha akahoji "kwahiyo tutakwenda lini?.."
"Ikiwezekana hata leo,kwani saa ngapi muda huu?.."
"Saa nne.."
"Sawa ngoja nikajiandae tuondoke "
Kwisha kusema hivyo, mama Yoranda alizama chumbani kwake, akavaa taulo. Akazipiga hatua bafuni kuoga ambapo napo hakuchukuwa muda mrefu alitoka akavaa nguo safi akajipulizia marashi ya kunukia vizuri,hapo alitoka chumbani akiwa safi kapendeza,naye mama Mazoea hakuficha husia zake alimsifu. "Ahsante ", alijibu huku wakielekea kwenye gari.
Safari ya kwenda kwa mganga ilianza, alifahamika kwa jina Ndikumana. Ni mganga ambaye mama Yoranda alimuamini sana, hivyo alitambua fika tatizo hilo kwake si kitu. Makazi ya mganga huyo wa jadi yalikuwa Kimbiji polini kabisa. Lakini wakati wawili hao wakiwa walipokuwa wakielekea kwa mganga wa kienyeji ili awasaidie kutambua mahali alipo Nyogoso,upande wa pili Suzani alifanikiwa kumuona kichaa Nyogoso akiwa amelala juu ya kaburi lililojengewa na kupigwa lipu kwa chokaa ya kutosha.
Suzani alitaharuki kumuona Nyogoso juu ya kaburi hilo, akiwa na wingi wa furaha alipasa sauti ya kumuita. Kichaa Nyogoso alipo sikia sauti ya Suzani aligeuka kutazama kule ilipo tokea sauti, alipo waona warembo hao Suzani na Loi,alishuka kutoka kwenye kaburi huku akicheka,alisema " Mmeona hawa walio lala humu kwenye nyumba zao wanafaidi,ndio maana na nyinyi mmekuja na pumzi zenu,vipi mnataka kuwafuata hawa ndugu zenu ama?..", aliongea kichaa Nyogoso huku akiendelea kucheka.
Suzani alitazamana na Loi mara baada kusikia maneno hayo ya Nyogoso,Suzani alishangazwa na maneno hayo, akajisemea ndani ya nafsi yake "Kweli yawezekana huyu akawa kichaa",wkati Suzani anajiaminisha suala hilo, kichaa Nyogoso alionekana akizipiga hatua za pole pole kuelekea mahali walipo simama mabinti hao. Loi aliogopa sana,alimugopa Nyogoso. Alijikuta akimeza mabunda ya mate kila mara yote ikiwa dalili ya woga. "Suzani tuondoke bwana,huyu kichaa atatudhuru" ,alisema Loi, akimuasa Suzani. Suzani alijibu "Huyu ni kichaa anaejielewa,hivyo hupaswi kuogopa Suzi"
"Anajielewa? Hebu acha ujinga wa mapenzi Suzani,kichaa anayejielewa asingesema kwamba tunataka kuwafuata ndugu zetu walio kufa" ,akiwa amekasirika Loi alimjibu Suzani.
"Kawaida,sasa unadhani angesemaje wakati tumekuja hapa makaburini" ,alisema Suzani. Na muda huo tayari kichaa Nyogoso alikuwa amewakaribia,punde Nyogoso alilalama njaa kwa maana usiku wa siku uliopita hakupata kitoweo.
"Ama kweli kuvuja kwa pakacha, nafuu kwa mchukuzi",alijigamba Suzani baada kusikia Nyogoso akilalama njaa. Aliamini kuwa shida hiyo ya Nyogoso, itampa nafasi ya kutoka nae pale makaburini, aende naye akampe chakula. "Twende nikakupe chakula", alisema Suzani huku tabasamu bashasha likitamaraki usoni mwake.
"Ahahahah Hahaha", kichaa Nyogoso aliangua kicheko aliposikia maneno hayo ya Suzani. Alipokatisha kicheko chake akasema. "Kweli nikipata hicho chakula,naamini Mungu atakubariki milele. Pia nitamuomba akupe mume mwenye roho nzuri kama wewe. Sura yako yaendana na matendo yako", maneno hayo ya kichaa Nyogoso yalimfanya azidi kutabasamu. Moyo wake ulijaa furaha, ukahisi baridi mithili ya kumwagiwa chenga za barafu. Lakini wakati Suzani akiwa katika hali hiyo, Loi yeye alionekana kukasirika.Hasa akikasirishwa na harufu mbaya aliyokuwa akitoa Nyogoso.
Kwengineko,kule kwa mganga Ndikumana. Mama Mazoea akiwa na rafiki yake walibisha hodi ingali mganga huyo alikuwa nyuma ya nyumba yake akichimba mihogo ili achemshe apate kifungua kinywa. Jua tayari lilikuwa limshaanza kuwa kali, utumbo wake sasa ulihisi njaa.
"Karibuni sana", alisema mganga Ndikumana huku akitua chini jembe lake na mihogo aliyokuwa ameifumba kwa mkono mbafuni kwake. "Ahsante,tumeshakaribia bwana mtaalamu" aliitikia mama Yoranda. Mzee Ndikumana alizama ndani kuvaa nguo zake za kazi,na punde si punde aliwaita wateja wake mama Mazoea na mama Yoranda waingie ndani. Walitii wito ambapo baada wawili hao kuketi kwenye jamvi la la mtaalamu Ndikumana, alianza kupiga manyanga yake huku akiimba nyimbo zake za asiri. Aliimba kwa muda wa nusu saa,alipo maliza alimgeukia mama Mazoea na kisha kusema. "Mama umefanya vizuri sana kuwahi mapema kufika hapa"
"Eeeh" ,aliitikia mama Mazoea wakati huo akionekana kukaa sawa kumsikiliza mganga anachotaka kumueleza. Lakini punde mganga Ndikumana aling'aka akasema "Usisime hivyo,itikia tawile..sawaaaa"
"Tawile" aliitikia mama Mazoea.. akifauta agizo la mganga.
"Mama,nimeshajua shida yako ni huyu kijana. Tazama ukutani kwenye Tv yangu asiria", alisisitiza mganga huyo mzee, upesi macho ya mama Mazoea na rafiki yake yalitazama ukutani mahali ambapo palikuwa na kitambaa cheupe ilihali mganga Ndikumana alirudia kuimba nyimbo zake huku akipandisha mizimu yake. Takribani dakika tano, pale ukutani mahali kilipo kitambaa alionekana kichaa Nyogoso. Kwenye Tv hiyo asiria alionekana kichaa Nyogoso akiambulia kichapo kutoka kwa vijana wa vijiweni, kundi hilo likiongozwa na Lidai. Mama Mazoea alistuka sana, hakuamini macho yake wakati huo huo mganga Ndikumana akaizima Tv yake kisha akaangua kicheko, alipokatisha kicheko chake akamgeukia mama Mazoea na kumuuliza
"Si ndio huyo?.."
"Haswaa., mtaalamu hakika upo sahihi kabisa" alijibu mama Mazoea.
"Sawa sawa, haya lengo lako ni nini hasa", aliongeza Ndikumana.
"Nataka nitambue mahali alipo, ikiwezekana nipajue anapoishi",alijibu mama Mazoea huku akiwa na shauku ya kutaka kujua. Mganga huyo alimuelekeza mahali alipo kwa muda huo lakini pia mahali anapoishi. Ila alitaharuki kusikia Nyogoso anaishia makaburini, ni suala ambalo lilimjaza maswali mengi kichwani mwake. Na hivyo alihitaji kujua kipi hasa kinacho mfanya kijana huyo kipenzi cha binti yake kuishi makaburini, kwani si rahisi kufanya jambo hilo hasa kwa mtu mwenye akili timamu
"Kwa sababu ni kichaa.." alijibu mganga. Na kabla mama Mazoea hajasema chochote,mganga huyo aliendelea kusema "Uchizi wake umetokana na mama yake,kijana yule alikaidi maneno ya mama yake ambaye alikuwa mjane. Mama yake hakupenda kijana wake aondoke mbali naye kwa sababu umri wake ulikuwa tayari umekula chumvi nyingi. Kwa maana hiyo basi asingeweza kumudu kazi zote hasa zile za shambani. Lakini licha ya mama yake kumtaka mwanaye asiondoke, ila bado kijana alikataa nasaha hiyo,ambapo aliondoka zake kuelekea jiji Dar es salaam kutafuta maisha. Huko alikumbana na mikasa mbali mbali,na moja ya mikasa hiyo ni kutumikia jela, msamaha wa raisi ndio ikawa ponea yake. Aliachiwa huru, alipo pata nauli alirejea nyumbani kwao kijijini kwa lengo la kumeomba msamaha mama yake kwa yale aliyomtendea. Dunia ilimfunza. Ila tumaini lake lilipotea,alikuta mama yake ameshafariki,kitendo ambacho kilimdatisha mpaka kupelekea kutwa na wazimu" Mizimu ya mganga Ndikumana ilieleza kisa kifupi cha kijana Nyogoso. Ni kisa ambacho kilimuacha mdomo wazi mama Mazoea, na hapo alipatakumbuka kuwa mara ya mwisho alimfumania Nyogoso akitaka kutoroka katika nyumba yake baada kumaliza kufanya mapenzi na binti yake ambaye ni Mazoea. Mwisho wa tukio hilo Nyogoso akawa amefunguliwa shtaka la kumtuhumu kuwa amemuibia mali zake, pasipo ushahidi ila nguvu ya pesa ikawa imeharalisha kifungo chake. Miaka sita alifungwa. Mama Mazoea alikumbuka tukio hilo la mwisho,alisikitika sana alipigwa na butwaa kwa muda wa sekunde kadhaa,lakini mwisho alizinduka kutoka kwenye dimbwi la mawazo alishusha pumzi kisha akasema " Mtaalamu, huwezi kutusaidia kijana huyu aweze kupona? ..",alihoji Mama Mazoea akitamani sasa kichaa Nyogoso arudi katika hali yake ili binti afurahi pindi atakapo mtia machoni. Lakini kabla mganga hajamjibu mama Mazoea kuhusu suala la kichaa Nyogoso kuponywa, upande wa pili kichaa huyo alikuwa akiambulia kichapo kutoka kwa kundi la Lidai,yote hiyo ni kumkomesha na kumpa onyo juu ya mrembo Suzani. Kitendo hicho Suzani hakufurahishwa nacho, alitamani kuingilia kati ila aliogopa na hivyo aliamua kupasa alipasa sauti kuita watu ili wamsaidie kichaa Nyogoso, ajabu kila mtu aliyejitokeza eneo hilo la tukio, alipoona watendaji wa tukio ni vijana wa hapo hapo mtaani walikaa kando. Nyogoso alipigwa kipigo cha mbwa koko. Roho ilimuuma sana Suzani, na hapo aliona hero lawama kuliko fedhea, alijitoa muhanga alijaribu kuingilia kati kumtetea lakini alisukumwa. Kitendo hicho kilimfanya kuchukuwa uamuzi mgumu, alikumbuka mahali mama yake anapo ficha bastora. Haraka sana alitimua mbio kuifuata huku nyuma akiacha Nyogoso akiendelea kupigwa, na hatimaye aliishiwa nguvu akaanguka chini wakati huo aliyafumba macho yake,sasa akawa hajiwezi huku akipumua kwa mbali sana, damu nayo ikimtiririka mithili ya maji. Ila pindi kichaa Nyogoso alipokuwa yupo katika hali hiyo,kwa mbaali alihisi kumuona marehemu mama yake akizipiga hatua kuja mahali alipoangukia. Punde mama alimkaribia kisha akamwambia "Mwanangu sikubali kushindwa hata siku moja,ukianguka inuka uendelee na safari. Wewe ni mwanangu pekee wa kiume, jembe nakutegemea sana kwahiyo hupaswi kuwa lege lege kaza msuri ufanikishe malengo yako",alisema mama Nyogoso. Hayo yalikuwa ni mawazo,Nyogoso akikumbuka miaka kadhaa ya nyuma pindi alipokuwa amekaa na mama yake usiku wa mbalamwezi wakipiga zogo. Marehemu mama yake aliwahi kumtia moyo kwa kumpa maneno hayo ya kishujaa. Maneno ambayo yalimfanya Nyogoso enzi hizo kujiona kidume, hata usiku wa saa sita alitembea kijijini pasipo kuogopa. Maneno hayo hayo yalimtia nguvu Nyogoso alisimama kama mzimu kutoka mahali alipo angukia,aliukunja mkono wake ambao ulionyesha kukunja ngumi nzito huku akiwa amesimama kikakamavu damu zikimtoka mapuani na maskioni. "Usikubali kushindwa" Maneno hayo ya marehemu mama yake bado yalijirudia kichwani mwake..
Jasho la damu likimtiririka kichaa Nyogoso,alipasa sauti akasema "Kama nyie vidume,njooni sasa". Watu waliokuwa kando wakishuhudia namna kichaa Nyogoso alivyokuwa akiambulia kichapo, sasa kila mmoja alitulia kuangalia jinsi ugomvi huo utakavyokuwa. Na katika watu hao alikuwepo mrembo Mazoea, Mazoea alistuka kumona mzoa takataka wake akiwa katika hali hiyo,ghafla alidondosha chozi na hata asiamini kama kweli ni yeye ama macho yake yanadanganya wakati huo upande wa pili mganga Ndikumana alisema "Uwezekano wa kumtibu huyu kichaa upo mama shaka ondoa, mimi ndio kisiki cha mpingo.."
"Sawa mtaalamu tufanyie tiba tafadhali" alisema mama Mazoea. Mganga akajibu"Si mimi ni nitakaye mponya,bali maombi ya kijana huyu kutembelea kaburi la mama yake nakisha kupasa sauti ya kuomba msamaha juu ya kile alicho mfanyia mama yake enzi za uhai wake.." ,mama Mazoea alikaa kimya kwa muda wa dakika kadha akionekana kutafakari jambo fulani lakini mwishowe alifungua kinywa chake na kisha kusema "Mtaalamu,tambua kuwa kijana huyu ni kichaa. Istoshe nimemjulia mjini tu..kijijini kwao sijawahi kufika hata mara moja, huoni kama huo ni mtihani? Kichaa atapakumbukaje nyumbani kwao?.." alisema mama Mazoea. Ndikumana alicheka sana kusikia maneno hayo ya mama Mazoea. Alipokatisha kicheko chake,alisema "Mama hapa umefika kwa mganga nisiyeshindwa jambo. Labda kubadilisha mbalamwezi kuwa jua hivyo basi..shika hii dawa. ", aliongea mganga huyo huku akimkabidhi dawa ilyokuwa imefungwa fundo kwenye kitambaa cheusi. Mama Mazoea alipokea. "Hiyo dawa utakapo muona huyu kijana. Mmwagie kisha litaje jina lake la zamani alilokuwa anatumia kijijini kwao,utakapo fanya hivyo,kumbumbu zitamrudi kwa masaa yasiyo pungua arobaini na nane. Nafasi hiyo itumie kuondoka naye hadi kijijini kwao moja kwa moja ufike kwenye kaburi la mama yake kisha muhimize apase sauti ya kuomba msamaha kwenye kaburi hilo la mama yake. Jina la utoto la kijana huyo anaitwa Yadunia" ,alisema mtaalam Ndikumana kwa sauti kali akimuasa mama Mazoea .
"Msamaha huo utakao tolewa na huyo kijana, kamwe hatoenda bure lazima asemehewe" aliongeza Ndikumana.
"Enhe na hilo kaburi tutalijuaje?.." alihoji mama Yoranda aliyemleta,lakini swali hilo Ndikumana hakulijibu bali aliwaambia watazame kwa mara nyingine tena kwenye Tv yake asiria. Haraka sana wawili hao walitupia macho yao kwenye Tv hiyo asiria,nayo ikaonyesha mazingira halisi ya kijijini kwao Nyogoso,picha hiyo ilijongea mpaka kwenye makaburi ya kijiji. Yalionekana makaburi mengi sana,mkaburi hayo yalikuwa ya dini mbili tofauti yalijengewa na mengine hayakujengewa. Katika kaburi la marehemu mama Nyogoso,palikuwa na mti umemea,si mrefu wala mfupi,mti huo ulikuwa tofauti na miti mingine ya makaburini hayo.
" Halama harisi ndiyo hiyo", alisema mtaalamu Ndikumana. Na hapo sasa mama Mazoea akawa amekamilisha maelezo, kilicho baki ni vitendo alinyanyuka kutoka kwenye jamvi akatoa sadaka kisha akaondoka zake na rafiki yake huku wakimuacha mganga akiimba nyimbo zake za asiri. "Mganga zake nyimbo " alijisemea mama Mazoea wakati huo wakielekea kwenye gari ili warejee mjini.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Upande wa pili,kichaa Nyogoso alikuwa amesimama kidete akisubiri mtu atakaye wmsogelea ili akabiliane naye. Umauti wa watu uliokusanyika mahali hapo kwenye tukio ulitulia wakisubiri kuona ngumi zikitembezwa,na kila mmoja alimkodolea macho kichaa Nyogoso ambaye alionekana akivuja jasho la damu huku mikono yake yote miwili ikiwa nimekuja ngumi nzito.
Lidai na kundi lake walitazamana wakijishauri kipi cha kufanya kwa Nyogoso, ingawa woga uliwatawala mioyoni mwao lakini walijitahidi kupiga moyo konde. "Vipi tutamuweza lakini?.." jamaa mmoja alihoji.
"Ndio,lazima tupigane naye,watu watano kwa mtu mmoja atushindeje sasa!.." ,alidakia mwingine.
"Ok hakuna kuogopa,woga hauna maana washkaji. Mnadhani endapo tukiogopa tutazificha wapi sura zetu? Hebu angalieni kulia kwenu,kushoto kwenu pia mbele na nyuma yenu. Kuna watu wengi mno wanatushangaa,kibaya zaidi kuna mademu wakali. Kwahiyo hatustahili kuogopa washkaji. Namfahamu vema huyu kichaa, si lolote wala si chochote", huyo ni Mikidadi alikuwa akiyasema hayo.
"Kama vipi tunzunguke haraka sana tumchakaze" Lidai naye alidakia,mara moja wakafanya hivyo. Wakamuweka mtu kati kichaa Nyogoso. Akijiamini kabisa alisimama wima huku akijifanya kama haoni kinachotaka kutokea.
Kwa pamoja vijana hao watano walimvagaa kichaa Nyogoso, na hapo Nyogoso aliachia ngumi yake moja nzito iliyokwenda kumpata Lidai. Ghafla Lidai akajikuta akiona giza mchana,akahisi kapigwa jiwe na sio ngumi. "Mamaa nakufaaa" alilalama Lidai. Watu waliokuwepo mahali hapo waliangua vicheko,wakati huo Nyogoso akiendelea kutembeza mateke kwa wale vijana wanne waliogangamala.
Lakini katika vijana hao,mmoja alikimbia. Punde si punde akarudi na nondo fupi,mkono wa kulia akiwa na panga. Jamaa huyo alizipiga hatua za haraka haraka huku akijiapiza kummliza kichaa Nyogoso,watazamaji walimkataza jamaa kufanya kitendo kile lakini huyo jamaa hakutaka kuelewa maelezo ya mtu,alizidi kukazana na panga mkononi bila kusahau nondo,alipania kumuua kichaa huyo kwa hasira alivuwa shati kisha akaingia mzima mzima kwenye ugomvi uliokuwa ukiendelea. Mazoea alishika kichwa aliogopa akidhania kuwa endapo nondo hiyo itampata Nyogoso, huwenda ikampelekea umauti. Akiwa na hofu juu ya suala hilo, Mazoea alifungua kinywa chake akapasa sauti huku akiwa amenyoosha kidole kule anakotokea jamaa aliyeshika nondo na panga. "Nyogoso, geukaaaaaa..", kichaa Nyogoso aliposikia sauti hiyo alitazama kwanza kule ilipotokea. Macho na mawazo yalimkumbuka kwa mbali sana binti huyo ambaye ni Mazoea. Alijikuta akiachia tabasamu pana ambalo mrembo Mazoea naye alijibu wakati huo huo aliinamana,kitendo ambacho kilimfanya yule jamaa kumpiga nondo mwenzake. Taharuki inazuka mahali hapo, mtu huyo aliyepigwa nondo alianguka chini mapovu yalimtoka, punde akapoteza maisha. Lakini bado jamaa huyo aliyempiga nondo mwenzake hakutaka kulidhika,kwani baada kumkosa Nyogoso kwa nondo alichika panga kikamlifu akalizungusha zungusha jinsi awezavyo. Nyogoso aliishiay kumtazama wakati huo Mikidadi alipoona yale mauaji ya mtu aliyepigwa nondo, alijua tayari muda wowote polisi wanaweza kuwasili mahali hapo. Aliogopa na hivyo alitazama upenyo wa kutokea,haraka sana akatimua mbio. Watu waliokuwa wakitazama huo ugomvi,waliangua kicheko huku vijana nao wakipiga mirunzi ya kila aina ingawa kuna baadhi waliamua kuondoka baada kuona mauwaji yametokea.
Hatimae sasa kundi la Lidai walibaki wawili,yule mwenye panga na mwingine mmoja ambaye hakuwa na siraha yoyote huku kijana Lidai akishindwa kuendelea na pambano. Uzito wa ngumi ya kichaa Nyogoso ulimfanya apoteze kumbukumbu,alijikuta hajitambui,ngumi ya Nyogoso aliyompiga kwenye taya ilivuruga mipangilio mzima wa ubongo. Awali ilionekana kama mas'ihara lakini baadaye watu walijua kweli Lidai amekuwa kichaa,kichaa yule asiyejitambua. Umati wa watu wachache waliokuwa waliendelea kushuhudia pambano la kichaa Nyogoso na vijana hao walistaajabu kumuona Lidai akivua nguo na kuanza kuongea maneno yasiyoeleweka.
Mambo si mambo, ndipo jamaa yule aliyekuwa na panga mkononi alipoona balaa lililomkumba rafiki yake. Alitupa panga chini haraka sana akatimua mbio,alibaki mmoja ambapo naye alionekana kumeza mabunda ya mate kila mara akimuogopa Nyogoso wakati huo huo jeshi la polisi lilifika eneo hilo ilihali Suzani naye alifika huku mkononi akiwa na bastora huku upande mwingine mama alionekana mama yake akitoka ofsini ,akaingia kwenye gari lake moyoni akijisemea "Bado sijaimaliza vita,nimemshindwa kwa mikono yangu, sasa nitamuawa kwa nguvu za giza. Bado sikubaliani na suala la mwanangu kutoka kimapenzi na kichaa ", maneno hayo alijisemea mama Suzani wakati tayari yumo ndani ya gari ambapo alichukuwa simu yake ya mkononi,akabonyeza haraka haraka kisha akapiga. Akaweka Simu sikioni,punde ikasikika sauti ikisema "Upo?"
"Mh shoga yangu nipo bwana, vipi wewe upo nyumbani?.." alihoji mama Suzani.
"Hapana,muda huu nipo kariakoo kuna vitu nanunua" sauti hiyo ilijibu. Sauti ya rafiki yake mama Suzani ambyae anaitwa Sauda.
"Ok nataka nikuulize,hivi yule mganga Buheli yupo?.."
"Buheliiiii!! Yeah yupo..vipi unashida naye?.."
"Sana shoga yangu,kama nilivyo wahi kukwambia. Mwanangu ndio kabisa kadata kwa kichaa. Tena kibaya zaidi kichaa huyo kwa sasa haishi mbali na mtaani kwetu" alijibu mama Suzani.
"Kwahiyo?.." Sauda alihoji.
"Kwahiyo nini?..nimemshindwa kwa bastora,nimeharibu pesa zangu kumhonga daktari amuuwe. Lakini bado sjafanikiwa. Kwahiyo nataka nimuendee kwa mganga mzee Buheli" ,mama Suzani alijibu. Sauda alimuunga mkono kwa kusema "Hapo utaweza maana hawa vijana kutoka mikoa ya bara wanandagu sio mchezo,huwenda mwanao kashapewa ndumba" alisema Sauda.
"Haya shoga yangu kama haupo mbali jivute utanikuta hapa Jangwani nakusubiri ili twenda leo leo nikamalize kazi"
"Sawa nakuja,pia nakuhakikishia mzee Buheli hashindwi kitu. Yani lazima kichaa azame chini mwanahidhaya mkubwa yule " alidakia Sauda. Na pindi wawili hao walipokuwa wakijiandaa kwenda kwa mganga kufuata hitimisho la kummaliza kichaa Nyogoso, muda huo huo mama Mazoea nate aliwasili eneo la tukio kwani alishaambiwa na mganga mahali alipo Nyogoso,ghafla alistaajabu kuona umati wa watu ila hakutaka kuishi kutazama akiwa ndani ya gari, zaidi alishuka kwenye gari lake huku akiwa na dawa mkononi, dawa ambayo amepewa na mganga Ndikumana kwa niaba ya kumponya kichaa Nyogoso.
Kwa muda wa nusu saa, Sauda alifika mahali ambapo mama Suzani alikuwa akimngojea. Walisalimiana kwa furaha na tabasamu bashasha kisha Sauda akaingia ndani ya gari, safari ya kuelekea kwa mganga Buheri ikaawa imeanza. Mama Suzani aliliendesha gari lake kwa kasi ya ajabu, safari sio kifo hatimaye walifika, mganga huyo amakazi yake yalikuwa yapo Mbezi maramba mawili. Wawili hao iliwalazimu kuacha gari na kisha kutembea kwa miguu shauri ya barabara kuwa mbovu kiasi kwamba gari lisingiliweza kupita, walitembea kwa muda wa dakika kumi na tano kutoka nyuma walipoacha gari. Nyimbo za asiri zilisikika, hapo ndipo mama Suzani alipotambua kuwa safari yao imefika ukiongoni "Afadhali tumemkuta", alisema mama Suzani.
"Haswaa! Maana naye siku nyingine anaboa sana. Mara umkute mara usimkute. Yani ni shida", alidakia Sauda wakati huo tayari wamekikaribia kibanda cha mganga Buheri.
"Karibuni sana", mganga Buheri aliwakaribisha wawili hao huku akitoka nyumba kubwa akielekea nyumba ndogo ambayo ilionekana kibanda kilicho jengwa mjengo wa suti, kuta ya nyasi kama lilivyo paa.
"Tumekaribia bwana habari za siku nyingi", alisema Sauda.
"Ni nzuri, karibuni ndani msiogope", alijibu mganga. Mama Suzani na Sauda waliingia ndani ya kibanda hicho. Walipoketi, mganga Buheri akasema "Tatizo lako ni ndogo sana kwangu", maneno hayo yalimstua mama Suzani akiwa na taharuki kubwa akajiuliza "Mtaalamu amejuaje shida iliyonileta pasipo kumwambia?.."
"Hahahah.. Hahahahah!", Buheri aliangua kicheko kisha akaongeza kusema "Mama, usiwe na shaka. Mimi ndio mganga kati ya waganga hapa ulimwenguni, mimi ni mganga ila hao wengine ni waganga njaa. Sasa ngoja nifanye kazi yangu", kwisha kusema hayo, alinyanyuka akatoka ndani akapasa sauti kumuita mjukuu wake. Aliitwa Samingo.
"Samingo.. Samingo"
"Naam babu"
"Njoo hapa mara moja", punde Samingo alitii wito wa babu yake.
"Sasa mjukuu wangu unatikiwa kwenda kuchimba viazi kwa niaba ya chai kesho au unasemaje?..", mganga Buheri aliongea akimwambia mjukuu wake ikiwa nia na dhumuni lake ni kumuondoa mazingira ya hapo nyumbani ili afanye kazi kwa nafasi pasipo mjukuu wake kujua.
" Sasa hivi au baadaye?.. ", aliuliza Samingo mvulana mwenye umri wapata miaka saba. Samingo alikuja kumtembelea babu yake muda wa rikizo fupi.
Ndio sasa hivi!.. ", alisisitiza mganga Buheri wakati huo upande mwingine, polisi walipofika kwenye tukio walipiga risasi kadhaa angani ili kuwatawanya watu waliokuwa wamekusanyika mahali hapo. Punde si punde nao waliogopa, mkubwa hakuweza kumkumbuka mdogo na wala kijana hakuweza kumkumbuka mzee kila mmoja alikimbia kivyake kuogopa jeshi la polisi lililotinga mtaani hapo. Jeshi hilo la polisi lilipohakikisha watu wote wametawanyika, haraka sana kwa puta walimfunga pingu kichaa Nyogoso kisha wakauchukuwa mwili wa kijana yule aliyepigwa nondo kichwani wakaupakia kwenye gari lao wakaondoka. Mama Mazoea alishuhudia tukio hilo, alitaharuki kuona jambo hilo limetokea. Baada kuona Nyogoso amebebwa na polisi hima alirejea ndani ya gari lake, aliwasha akarudi nyuma kisha akaenda mbele kwa kuzipangilia gea ipasavyo. Hapo gari likawa sawa, sasa kazi ilibaki kuifuatilia gari lile la polisi ambalo limembeba kichaa Nyogoso. Lakini kabla mama Mazoea hajaondoka, alisikia sauti ikimuita punde Mazoea akaonekana akirikbia gari "Panda panda haraka", alisisitiza mama Mazoea. Mazoea aliharakisha alifungua mlango akaketi "Funga mkanda pandisha kioo", aliongeza kusema mama Mazoea,naye alifanya hivo. Uwezo wa kuendesha gari mama Mazoea ulidhihirika baada kuanza safari ya kuifuata gari ile ya polisi, siku hiyo ilikuwa tofauti sana. Ni siku ambayo jiji la Dar es salaam hasa barabara kuu zilionekana kutokuwa na foleni. Hali ilikuwa shwari kabisa kiasi kwamba mama Mazoea hatimaye alilikaribia gari lile la polisi mpaka wanafika kituoni ambapo walifika kwa pamoja.
"Teremka haraka haraka", alisema kamanda mmoja ambaye kabira lake mjita. Maneno hayo akimwambia Nyogoso huku akimpiga mateke, lakini pia alimdhihaki wakati tayari kichaa Nyogoso alikuwa ameshashuka chini akiwa na pingu mkononi. Hapo napo kamanda huyo hakuweza kumuacha, alimvuta kwa nguvu kumpelekea kwenye chumba maulumu cha mateso huku akasema "Wewe si kichaa? Sasa utapona uchizi wako. Watu kama nyinyi hamfai kukaa jela, mtamaliza ugali wa bure", mlango wa chumba hicho ulifunguliwa lakini kabla kichaa Nyogoso hajaingizwa katiika chumba hicho, ilisikika sauti ya mama Mazoea ikisema "Afande subiri kwanza tafadhali", afande huyo aliyekuwa akimnyanyasa Nyogoso pasipo huruma aligeuka ilipotokea sauti hiyo kisha akasema "Unasemaje?."
"Nipe dakika mbili tu kamanda, nina jambo muhimu nataka kuzungumza na wewe"
"Jambo gani?..", alihoji kamanda ilihali gari hilo lililo mfikisha Nyogoso kituoni iligeuka ikaelekea muhimbili kuipeleka maiti. Pumzi alishusha mama Mazoea kisha akazipiga hatua kumfuata kamanda ili aseme naye jambo kabla hajamuingiza Nyogoso kwenye chumba cha mateso. Punde si punde Mazoea naye alishuka kwenye gari, akaliegemea huku macho yake yakitazama kule aliposimama mama yake ambaye alikuwa akizipiga hatua kumfuata kamanda.
"Mungu wangu saidia", Mazoea aliomba dua,ikiwa wakati huo huo tayari mama yake alimkaribia kamanda, na hapo alikumbuka maneno ya mtaalamu Ndikumana ""Hiyo dawa utakapo muona huyu kijana. Mmwagie kisha litaje jina lake la zamani alilokuwa anatumia kijijini kwao,utakapo fanya hivyo,kumbumbu zitamrudi kwa masaa yasiyo pungua arobaini na nane. Nafasi hiyo itumie kuondoka naye hadi kijijini kwao moja kwa moja ufike kwenye kaburi la mama yake kisha muhimize apase sauti ya kuomba msamaha kwenye kaburi hilo la mama yake. Jina la utoto la kijana huyo anaitwa Yadunia", maneno hayo aliyamumbuka mama Mazoea na ndipo alipomtazama kamanda kisha akasema "Afande tambua huyu ni kichaa, kwahiyo kumtesa namna hii ni dhambi kubwa kwa Mungu", kamanda hiyo mwenye sura mbaya kama ndala ya nyumba za wageni (Guest) alimuangalia mama Mazoea kwa jicho pembe akajibu "Kwahiyo umenisimamisha ili unifundishe kazi?..", kwisha kusema hivyo alimsukuma Nyogoso ndani kisha akafunga mlango. Akiwa na mkong'oto wake mkononi afande huyo aliongeza kusema "Haya ongea tena sasa", mama Mazoea hakusema neno lolote, alikaa kimya ingawaje alitambua kuwa vitisho vyote hivyo dawa yake ni pesa. Hivyo alinyoosha vidole viwili shahada na kidole gumba akavikutanisha kwa kuvisugua akionyesha ishara ya pesa. Ghafla afande huyo aliachia tabasamu wakati huo akitazama kulia na kushoto kana kwamba amefumaniwa ugoni, ikiwa upande wa pili ilibaki gumzo. Kila raia aliyeshuhudia ugomvi ule wa kichaa Nyogoso na kundi la Lidai alisimulia ambaye hakushuhudia. Wengi hawakuamini kama kweli ngumi ya Nyogoso ingeliweza kumvuruga mtu mapaka kufikia hatua ya kuwa kichaa, na hapo ndipo baadhi ya walipoamua kumbatiza Nyogoso kwa kumuita KICHAA WA MTAA kwa sababu siku hiyo alithubutu kufunga mtaa. Hiyo hali ikiwa imepamba moto mtaani, kwingeneko alionekana Suzani akihaha kumpigia simu mama yake ili amsaidie kumfuatilia Nyogoso kituo cha polisi lakini simu haikupatikana. Hakika Suzani alikasirika sana wakati huo huo kule kwa mganga, baada mganga kuimba nyimbo zake hatimaye kazi rasmi ilianza. Mtaalamu Buheri alichukuwa chungu chake kilichokuwa na maji, alinyunyuzia dawa huku akiendelea kuimba japo si kama alivyokuwa akiimba awali. Zoezi hilo lilpokamrika aliita mizimu yake, punde katika chungu hicho chenye maji alionekana mama Mazoea akiwa sambamba na Nyogoso.
"Ahahahahah.. Hahahahah", aliangua kicheko mganga Buheri kisha akasema "Mama, kazi imekwisha", kwisha kusema maneno hayo alimkabidhi mama Suzani sindano maalumu.
"Nadhani mbaya wako umemuona, kamata sindano hii. Usiogope mchome kwenye utosi na hapo kazi itakuwa imekwisha rasmi",alisisitiza mganga Buheri, mama Suzani kwa kujiamini kabisa aliipokea sindano hiyo tayari kwa dhumuni la kummaliza kichaa Nyogoso. Lakini kabla mama Suzani hajaigusisha sindano hiyo kwenye utosi wa Nyogoso ambaye alikuwa akionekana kwenye maji yaliyomo kwenye chungu, ghafla Nyogoso alitoweka akatokea mume wake. Alistuka sana,haraka akaurudisha mkono wake nyuma akiwa na taharuki akasema "Mbona namuona mume wangu?.."
"Anaonekana mume wako?..", aliuliza mganga Buheri.
"Hebu nyanyuka", aliongeza kusema, akimtaka mama Suzani anyanyuke mahali hapo alipokaa. Naye alifanya hivyo. "Naona hizi dawa zinataka kuvuruga akili yangu sasa", aliendelea kusema wakati huo akitafuta dawa nyingine kwenye ungo uliokuwa pembeni yake, ungo huo ulionekana kujaza mazagazaga mengi ya dawa za kienyeji.
"Ahahaah", aliangua kicheko mara baada kuipata, aliifungua ikiwa kwenye fundo la kitambaa cheusi. Dawa hiyo akaimimina kwenye chungu chake chenye maji, kisha akasema "Haya mama, bila shaka sasa kazi imekwisha", mganga Buheri alipokwisha kusema hayo kwa mara nyingine tena alimkabidhi sindano mama Suzani, aliipokea akaishika vizuri mkononi mwake,pole pole akaushusha mkono wake kwenye chungu hicho akaamini kabisa kazi inakwenda kuisha. Lakini ghafla tumaini lake lilipotea baada sura ya Nyogoso kutoweka kwa mara nyingine tena, na safari hiyo ilionekana sura yake. Hima akarudisha mkono nyuma huku akiwa ameyatumbua macho kama mjusi aliyebanwa na mlango, mapigo ya moyo yalimuenda mbio wakati huo huo mganga Buheri akamuuliza "Mbona huchomi?."
"Nitajichoma mwenyewe?..", alijibu mama Suzani na hata asiamini kile akionacho.
"Unamaana gani?.."
"Nina maana, sura ya mbaya wangu imepotea tena. Najiona mwenyewe", alijibu mama Suzani, akionekana kukasirika mno.
"Acha utani wewe mama", aliong'aka Buheri wakati huo akinyanyuka na kusogea mahali alipokaa mama Suzani kwa dhumuni la kushuhudua kile alichokuwa akikiona mama huyo. Alipotazama, alikunja uso wake kisha akamtazama mama Suzani kisha akasema "We mama, kwanini unanijaribu?.."
"Kukujaribu? Mbona sikuelewi mtaalamu. Unamaana gani?.", akiwa na taharuki juu ya kile alichokisema mganga Buheri, mama Suzani alihoji "Mbaya ni wewe,kwanini mwanzo imekuja sura ya mumeo halafu mara hii imekuja sura yako? Mpaka hapo mjadala hakuna! Sitaki unishushie heshima yangu. Nasema hivi nenda kwa mwingine, mimi siwezi kazi yako", alisema kwa jazba mganga Buheri. Mama Suzani na Sauda walitaharuki, akiwa katika hali hiyo aliuliza "Kwanini lakini mtaalamu"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nimesema ondokeni, tafadhali msinipande kichwani. Nitawageuza vifuu vya nazi sasa", alisisitiza Buheri. Haraka sana wawili hao walinyanyuka, wakatoka ndani ya kibanda hicho lakini kabla hawajatoka mlangoni, mganga Buheri akasema "Mnaondokaje bila kutoa sadaka!.."
"Sadaka? We mzee vipi yani nitoe sadaka kwa kazi gani uliyofanya?..", aligoma mama Suzani huku Sauda akimuunga mkono. Maneno hayo yalimchefua sana mganga Buheri ambapo aliangua kicheko kwa sauti kali kisha akasema "Mimi ndio Buheri, nasema hivi endapo mkifika huko muendako basi nitajizika mzima", kwisha kusema hivyo alirudia kucheka ilihali muda huo huo mama Suzani alionekana kurudi nyuma, akatoa sadaka shilingi Elfu tano, safari ya kurudi nyumbani kutafakari plan B ikaanza baada plan A kuota mbawa.
Upande wa pili mama Mazoea alifanikiwa kuongea na kamanda yule aliyekuwa akimuingiza Nyogoso kwenye chumba cha mateso, pesa ilimfanya kamanda huyo kumuachia huru jambo ambalo lilimfurahisha sana mrembo Mazoea, hima alimkimbilia na kisha kumkumbatia kwa mahaba kem kem. Alimshika mkono akaingia naye kwenye gari, akakaa naye siti ya nyuma ingawa nguo zake zilikuwa zikitoa harufu mbaya lakini Mazoea hakujali suala hilo.
"Nyogoso unanikumbuka?..", wakiwa ndani ya gari, Mazoea alimuuliza Nyogoso lakini kichaa Nyogoso hakujibu ambapo Mazoea alirudia tena kumuuliza ila bado mambo yalikuwa yale yale na hatimaye aliamua kumuacha kitendo ambacho kilizua ukimya ndani ya gari,baadaye kimya hicho kilitoweka baada kichaa Nyogoso kuanguka kicheko. Kicheko ambacho Mazoea hakujua sababu iliyopelekea acheke. Alimtazama kwa tabasamu bashasha kisha akaguna wakati huo akili mwake akitilia shaka hali aliyonayo, alihisi kuwa Nyogoso ni kichaa ila alivuta subira mpaka pindi atakapofika nyumbani ndipo amuulize mama yake ukweli wa kile anachokihisi.
Hatimaye walifika nyumbani, waliposhuka kwenye gari Mazoea alimsogelea mama yake, kwa sauti ya kunong'ona alimuuliza "Mama wataka kuniambia mpenzi wangu kichaa?..", mama Mazoea aliposikia swali hilo alilomuuliza binti yake kwa sauti ya chini iliyojaa simanzi akajimjibu "Ndio ila usijali mwanangu, kila kitu kipo sawa. Hebu subiri uone", kwisha kusema hivyo, alifungua mkoba wake, akatoka na kitambaa cheusi chenye fundo. Alimtazama kichaa Nyogoso ambaye alionekana kusimama hatua kadhaa pembeni ya gari huku akitazama kulia na kushoto. Punde si punde mama Mazoea alichotaka dawa kidogo iliyokuwa kwenye fundo la kitambaa hicho cheusi kisha akaipuliza kuelekea kule aliposimama kichaa Nyogoso wakati huo huo akasema "Yadunia", sauti hiyo ilikwenda sambamba na dawa hiyo, nayo ilipompata ghafla Nyogoso kumbukumbu zikamrejea baada kupotea kwa muda mrefu. Akiwa na taharuki, alijitazama nguo zake alizovaa, alijishika kichwani akajikuta ananywere nyingi zilizo chakaa kama zilivyo nguo zake. Hakika alistaajabu sana, ilihali Mazoea naye akionekana kutokwa na machozi ya furaha. Hakuamini kama kweli mama yake amepambania furaha ya moyo wake,kwa furaha binti huyo alimkumbatia mama yake kisha akasema "Mama, sina cha kukupa mama yangu, ila nakuomba Mungu akupe maisha marefu na yenye baraka tele"
"Usijali mwanangu, nakupenda sana. Lakini bado kazi haijaisha", alijibu mama Mazoea.
"Kazi gani tena mama?..", kwa taharuki Mazoea alimuuliza mama yake. Mama huyo naye hakusita kumwambia kile alichoambiwa na mganga Ndikumana pindi atakapo mmbwagia dawa ya kumrejeshea kumbukumbu. Alipokwisha kumueleza hayo, alimtaka akajiandae kwa safari ya kuelekea kijijini alikozaliwa kichaa Nyogoso.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nimefikaje hapa?..", ilisikika sauti ya Nyogoso akiuliza huku macho yake yakitazama kila pande katika nyumba hiyo, ilihali kumbukumbu zikimkumbusha kuwa mara ya mwisho kukanyaga katika nyumba hiyo ni siku ile aliyofanya mapenzi na Mazoea, kitendo ambacho mwishowe kilimpelekea kufungwa jela. Swali hilo lilimfanya mama Mazoea kuingiwa na woga, ila alipiga moyo konde akamsogelea Nyogoso kisha akasema "Kwanza sahau yote yaliyopita, nisamehe sana. Lakini pia muda huu tunakwenda na wewe kijijini kwenu"
"Kufanya nini na wewe ni kama nani? ..", kwa sauti kali alirudia kuhoji Nyogoso.
"Mimi ndio mama yako mkwe, na mimi ndio nanaye jua mahali lilipo kaburi la mama yako" mama Suzani alijibu.
"Yadunia, tunakwenda kijijini kwenu", aliongeza kusema mama Mazoea,ni maneno ambayo yalimfurahisha Nyogoso. Aliachia tabasamu huku akitazama huku na kule, ghafla macho yake yakagonga kwenye dirisha la chumba cha Mazoea, alikumbuka utundu aliofanya na Mazoea kisha aliyarudisha macho yake kumtazama mama Mazoea. Alitikisa kichwa ikiwa kama ishara ya kukataa jambo fulani. Pindi Nyogoso yupo kwenye hali hiyo, Mazoea alitoka ndani akiwa amependeza, Nyogoso alitazama kule anakotokea Mazoea, paji la uso wake likafongana na paji la uso wa Mazoea wakati huo huo Mazoea alimfinyia jicho moja huku akitabasamu, ajabu Nyogoso hakujali mbwembwe ya Mazoea zaidi alijiuliza kitu gani kilicho mfikisha mahali hapo ikiwa hapo awali alirudi kijijini kwako baada kupata msamaha wa Raisi.
"Haya tuondoke", alitoa amri mama Mazoea. Mazoea alimfungulia mlango Nyogoso. Nyogoso akiwa na wingi wa maswali kichwani mwake aliingia kwenye gari kisha Mazoea naye akafuatia, safari ikaanza, ni safari ambayo ilichukuwa masaa kumi na mbili, masaa mawili baadaye waliyatumia kufika kijijini alikozaliwa Nyogoso. Kwa kuwa Nyogoso kumbu kumbu tayari alikuwa nazo,hivyo mama Mazoea alimwambia waende makaburini. Nyogoso akaambatana nao mpaka kwenye makaburi ya kijiji. Na hapo mama Mazoea alikumbuka maelekezo ya mganga Ndikumana kuhusu kaburi la mama Nyogoso wakati huo Nyogoso alisimama tu hakujua afanye nini wakati tangu awali baada kurejea kijijini alilitafuta na hakuliona.
Mama Mazoea alizunguka huku na kule,bila mafanikio wa kuliona kaburi muda nao ukizidi kutaradadi. Hofu ilimjia pindi alipoona muda inazidi kukuletea kwenda mafanikio ikiwa mganga alishamwambia kuwa kumbu kumbu za Nyogoso zitakaa kwa muda wa masaa Arobaini na nane. Muda huo ukipita kabla Nyogoso hajapasa sauti ya kuomba msamaha kwenye kaburi la mama yake, basi hatopona tena. Pumzi alishusha mama Mazoea alipagawa sana huku akiruka kaburi hili likifuata lile na lile na lile, yote akihaha kulisaka kaburi la marehemu mama Nyogoso kipenzi cha binti yake.
Upande wa pili,mama Suzani baada kuona mganga Buheri kashindwa matakwa yake,alipo fika nyumbani aliita baadhi ya vijana nyumbani kwake. Ni baada kumkuta Suzani amelala usingizi fo fo fo baada kulia kwa muda mrefu pindi alipoona simu ya mama yake haipatikani ikiwa yeye anahitaji msaada wa kumkomboa mpenzi wake aliyeshikiliwa na jeshi la polisi.
Vijana hao wasio pungua sita,vijana walioonekana ngangali,walikaa kwenye sofa kumsikiliza tajiri mama Suzani. Mama akasema "Najua nyie ni wanaume, achana na hao waliopigwa jana na kichaa. nyinyi ndio wanaume wa shoka. Hivyo basi kuna kiasi kikubwa mno cha pesa nimewaandalia endapo mkifanikisha kumuua huyu kichaa wa mtaa kama wasemavyo watu wa mtaa huu. Hakika nitawapatia pesa hiyo yote kiasi kisicho pungua million kumi.."
"Sitaki mniletee taarifa,nataka mniletee kichwa chake"
Aliongeza mama Suzani, vijana wao walitazama kisha mmoja akasema "Mama kwa hilo wewe ondoa shaka, KICHAA WA MTAA lazima azimishwe kama mshumaa"
"Na hiyo ndiyo plan B yangu, chungeni isiende kombo", alisisitiza mama Suzani huku akimimina bia kwenye grasi.
"Pasipo na shaka mama, kazi yako itafanyika upesi", walijigamba vijana hao,wakimuhakikishia mama Suzani kutekeleza kile alichowatuma.
Baada kufikia muafaka vijana hao waliondoka,mara moja walianza kumsaka kichaa Nyogoso huku wakijiapiza kummaliza popote pale watakapo muona.
"Jamani,pesa aliyotoa huyu mama ni Nyingi mno. Kwa maana hiyo basi kazi lazima ifanyike bila kinyongo chochote,wahenga walisema ukitaka kuruka agana na nyonga nadhani mmenielewa hakuna kulembe mwandiko", alisisitiza moja ya kijana kati ya wale waliotumwa na mama Suzani. Huyo alifahamika kwa jina Victa.
"Sawa victa tumekuelewa,lakini kumbukeni yule kichaa sio wa mchezo mchezo,tusipokuwa makini ukweli jehanamu itatuhusu" alidakia mwingine naye akitoa maoni yake,hapo Victa kama kiongozi wa kundi. Alimtazama huyo jamaa aliyesema maneno hayo kisha akajibu "Acha mambo ya kike boya wewe. Kama huwezi kaa pembeni. Wanaume tufanye kazi". Victa aliungwa mkono na wenzake. Naye huyo aliyeonyesha hofu ya kumkabili kichaa Nyogoso, alijikuta akiwa mdogo mithili ya plitoni. Na hapo alijirudi kwa kusema "Sawa jamani nilisema tu kama maoni lakini msinielewe tofauti. Tufanye kazi".
Amri ikatoka kwa Victa,"Haya kila mmoja apite mtaa wake. Mmoja wetu endapo akimuona kichaa tunayemtafuta,mara moja apige simu ili tuje kummaliza. Vile vile msiogope kuulizia kwa watu kuhusu huyu kichaa maana huwenda ikawa rahisi sana kumpata. Sawa?.."
"Sawa sawa", waliitikia.
Baada makubalino kwenda sawa kila mmoja alipita mtaa ,vijana hao sita wakimuwinda kichaa Nyogoso ili wamfyeke kichwa kutimiza hazma ya mama Suzani. Mama ambaye kwa muda mrefu anamtafuta Nyogoso ili amuuwe akiepuka mwanaye kutojenga mahusiano na kijana huyo ambaye hapo awali kabla ya kuwa kichaa alikuwa mzoa takataka. Suzani alitokea kumpenda Nyogoso tangu mara ya kwanza alipomuokotea pochi yake ambayo ilikuwa na vitu vya thamani. Lakini mama Suzani hafurahiii na maisha hayo ya binti yake aliyojiamulia. Maisha ya kutoka kimapenzi na kijana hohe hahe masikini asiye na mbele wala nyuma. Na hapo ndipo anaamua kufanya kila njia kumpoteza Nyogoso ili kukata mzizi wa penzi hilo linalo taraji kuja kwa kasi ya ajabu,licha ya kujaribu kila njia ila bado alishindwa kufanikisha lengo lake lakini hachoki, bado anapambana bila kukata tamaa huku akiamini atafanikiwa tu.
Wakati hayo yakaendelea ndani ya jiji la Dar es salaam. Upande wa pili kule kijijini kwao Nyogoso, mama Mazoea aliendelea kulisaka kaburi la mama Nyogoso. Alizunguka huku na kule bila mafanikio ya kuliona,lakini baada kulisaka kwa kipindi kirefu, hatimaye aliliona likiwa limependwa mti ule ule alio ambiwa na mganga Ndikumana.
Pumzi ndefu shusha mama Mazoea asiamini kama kweli kaliona kaburi hilo ambalo kimuonekano tuta lake lilikuwa limesha sambaa kiasi kwamba laiti usingelikuwa mti huo uliopandwa kwenye hilo kaburi basi mama Mazoea asingiliona. Kwa hakika mama Mazoea alijikuta akidondosha machozi. Si machozi ya maumivu la hasha, machozi hayo yalikuwa ya furaha. Na papo hapo alipasa sauti ya kumuita binti yake ili aje na NYOGOSO walisogelee kaburi. Mazoea alimshika mkono Nyogoso kisha wakazipiga hatua kumfuata mama yake alipo simamakando ya kaburi. Walipofika mama Mazoea alitazama mwanaye kisha akasema "Mazoea, anaitwa nani huyu mchumba wako"
"Anaitwa..Nyogoso ", alimjibu Mazoea huku akiachia tabasamu. "Anhaaa! Nyogoso,hili ndilo kaburi la mama yako. Hivyo muda huu unatakiwa upase sauti hapa juu ya kaburi hili la mama yako umuombe radhi kwa yale uliyomkosea ili maisha yako yawe na amani hapa duniani. Tafadhali fanya hivyo upesi" alisema mama Mazoea akimwambia Nyogoso.
"Mazoea nenda kwenye gari kalete mataji yale matatu tuliyokuja nayo", aliongeza kusema mama Mazoea. Haraka sana Mazoea alikwenda kuyafuata hayo mataji,ihali huku nyuma baada Nyogoso kuyasikia maneno hayo ya mama Mazoea,alimtazama kwanza usoni kisha akalitazama kaburi la mama yake.
Machozi yalimtoka,Nyogoso alilia sana huku akipiga magoti pembeni ya kaburi wakati huo huo akipasa sauti ya kuomba msamaha. Alikumbuka alipo hangaika kulitafuta kaburi la mama yake mara baada kutoka jela ili amuombe msamaha akawa hajaliona hali iliyopelekea kuwehuka. Alikumbuka tabu alizo zipata pindi alipofika Dar es salaam kwa mara ya kwanza nyuma akiwa amekaidi maneno ya mama yake aliyekuwa mjane.
Kiukweli Nyogoso alikumbuka mengi mno, yoote hayo alikuwa akiyakumbuka huku akilia na kuomba msamaha juu ya kaburi la mama yake ilihali mama Mazoea alikuwa kando akiyafuta machozi kwa kitambaa chake naye aliguswa na kilio hicho cha kijana Nyogoso.
Mwishowe Mazoea alirejea akiwa na mataji kwa mikono yake. Na hapo alimkabidhi mama yake kisha akamnyanyua mpenzi wake huku akimfuta machozi. Nyogoso alipo simama alikabidhiwa mataji ili ayaweke kwenye kaburi la mama yake huku moja akilivisha kwenye msalaba.
"Pole sana mpenzi", alisema Mazoea. Shughuli ikawa imemalizika namna hiyo. Hata ule muda uliokuwa ukimtia hofu mama Mazoea ulipo wadia, Nyogoso alibaki na hali yake. Hatimaye akawa mzima. Furaha ilimjaa mama Mazoea na mwanaye, Mama Mazoea akasema "Kijana samahani sana tena sana kwa mambo mabaya niliyo kufanyia. Hakika nimeamini mapenzi hayana mwenyewe,nilikosea sana kuyaingilia kati mapenzi yenu. Ila kwa sasa nasema Mungu awabariki sana katika mapenzi yenu. Nakuheshimu kama mkwe wangu..pia Mazoea mchunge mumeo,kumbuka ulitaka kujiuwa kisa yeye" Alisema mama Mazoea. Nyogoso alitabasamu kidogo kisha akajibu "Mama nimeshakusamehe, msaada wako huu unatosha sana nawe Mungu akubariki akupe maisha marefu" Alijibu Nyogoso..huku Mazoea akiachia tabasamu akifurahia sauti ya kijana Nyogoso.
"Amina..enhe vipi utatutembeza kijijini kwenu ili tukione vizuri?..", aliongeza kusema mama Mazoea. "Ndio inawezekana.." Nyogoso alijibu.
"Ok,ingia kwenye gari,kuna mfuko chukuwa nguo na viatu pia kuna kofia vaa tuanze kuzunguka" Mama Mazoea alimwambia Nyogoso.Nyogoso aliingia ndani alivaa haraka haraka kisha akatoka akiwa kapendeza. "Mmh umetokelezea mpenzi wangu? Ila uko kama mtu wa Jamaica! .." Alisena Mazoea kima'sihara. Wote kwa pamoja walicheka kisha Nyogoso akasema "Haya twendeni mkione kijiji chetu "
Nyogoso akiwa na mpenzi wake pia na mama mkwe wake walitembea kila kona ya kijiji, watu walio mfahamu walistaajabu kumuona Nyogoso akiwa mzima. Hata wale wakina mama waliomzushia kesi kipindi cha chuma kwamba Nyogoso kawabaka, walijikuta wakimshangaa huku vijana baadhi wa kijijini hapo walio shiriki kumpiga Nyogoso walistaajabu. Na baadhi yao walipinga kuwa yule ndio kichaa Nyogoso wingine wakisema ndiye. Ubishi mtindo mmoja.
Lakini yote Kwa yote walirudi kwenye gari yao aiana ya Hulux,safari ya kurejea Dar es salaam ikaanza.
"Kijiji chenu kizuri? .." alisema Mazoea akimwambia Nyogoso. Nyogoso alicheka kisha akajibu.."Ndio hapo nilipo zaliwa vipi upo tayari tukaishi hapo? .."
"Wee siwezi kiukweli,kwanza kuchochea kuni jikoni pia kubeba ndoo ya maji kichwani bado kuchanja kuni. Mmmh mimi siwezi bwana", alisema Mazoea wakati huo wakiwa safarini kurudi Dar, furaha isiyokifani ikitamaraki mioyoni mwao.
***BAADA YA SIKU MOJA***
Hatimaye walifika Dar es salaam. Mama Mazoea alimkabidhi chumba Nyogoso huku akiwata wawili hao kutokufanya mapenzi kwa huku akiwaahidi anataka awafungishe ndoa ya kifahari. Lakini licha ya kusema hivyo mama Mazoea, ila jambo hilo lilikuwa ngumu sana kwa Mazoea. Kwani alitoroka usiku kutoka chumbani kwake nakwenda kwa Nyogoso kumkatikia viuno feni. Nyogoso, mchezo huo aliupenda sana, utamu wa Nyogoso ulimpagawisha mno. Tabia hiyo ilikuwa enderevu wakati huo kila siku jamaa wale waliopewa jukumu la kumuua Nyogoso waliendelea kumsaka kila kona bila kufanikiwa. Nyogoso alifichwa ndani akisubiri ndoa.
Siku ile iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu iliwadia, siku ya ndoa watu maarufu wenye pesa zao walihudhuria sherehe hiyo ya Nyogoso na Mazoea. Hadi mama Suzani na Suzani wake walifika wakiwa hawajui nani anaoa ila walifika kama wageni waalikwa katika sherehe hiyo . Lakini cha ajabu mama Mazoea alifika kwenye sherehe akiwa na bastola yake ndani ya mkoba. Popote pale atakapo mwona Nyogoso basi halali yake.
Naam! Siku hiyo alimuona, alishtuka sana. Si yeye tu bali hata mwanaye naye alishtuka kumuona Nyogoso ndani ya suti huku kando yake akiwa na binti mrembo wa kuitwa Mazoea. Mapigo ya moyo yalimuenda mbio, mama huyo alitamani amalize mchezo pale pale lakini alihofia ulizi mkali uliokuwepo eneo hilo. Mama Suzani na jeuri yake aliogopa lakini Suzani alipata mstuko alidondoka chini h akapoteza fahamu. Hima masaada wa kumuwahisha hospital Suzani ulifanyika lakini alipofikishwa hospital, wakati alifumbua macho mara moja punde akafumba, Suzani akawa amepoteza maisha.
Mama Suzani alilia sana kumpoteza mwanaye,alijikuta akijilaumu kwanini alimbania mwanae juu ya kijana Nyogoso. Ila yote Kwa yote akajikuta akiwa mpweke maana mtoto pekee alikuwa ni Suzani. Na uwezekano wa yeye kuzaa mtoto mwingine hiyo ilibaki kama ndoto ya abunuasi. Umri wake tayari ulikuwa umsesonga. Huzuni kilio na majonzi kwa mama Suzani,hakuwa na pakuegemea ilihali mumewe aliamua kuachana naye baada kupata mwanamke mdogo aliyemuona anafaa kuishi naye na kujenga familia mpya. Maisha ya mama Suzani ghafla yalibadirika sana, usongo wa mawazo ulimfanya kushindwa kwenda kazini. Kila siku alikuwa mtu wa kulewa na kulala tu, maisha yake yalienda kombo hali iliyopelekea kufukuzwa kazi kwenye kampuni kwa uzembe wa kazi.
Hapo sasa ilimlazimu mama Suzani kuuza nyumba,akauza magari. Pesa iliyokuwa kwenye akaunti yake ilifidia mahali alipo acha pengo kazini aliko kuwa ameajiliwa,wakati huo vijana waliopewa jukumu la kumtafuta Nyogoso walipoona matumaini ya kumnasa kichaa hayapo waliachana na dili hilo wakaendelea na shughuli zao.
**BAAADA YA MIEZI MIWILI.**
Mama huyo mwenye roho mbaya alijikuta akiuza machungwa barabarani ili apate mkate wa kila siku. Maisha yale ya kuponda pesa kwa dhumuni la kuupoteza uhai wa mtu asie na hatia, ghafla yanayeyuka mithili ya mawingu yayeyukapo angani.
Siku moja Nyogoso akiwa ndani ya gari lake,gari aina ya Land Rover,alijikuta akiwa na kiu kama sio hamu ya kula chungwa. Hamu hiyo ilimjia pindi alipoyaona kando ya barabara yakiuzwa. Alisimamisha gari akashusha kioo kuhitaji chungwa, muuzaji alikuwa ni mama Suzani ambapo alistuka kumuona Nyogoso, alimtazama huku akakumbuka jinsi kijana huyo alipokuwa akihaso mtaani na uchizi wake,akakumbuka jinsi alivyo muendea kwa mganga ili amuuwe. Pumzi ndefu alishusha mama Suzani, alisikitika sana huku akililia rohoni.
"Niwekee machungwa saba mama", alisema Nyogoso. Haraka sana mama Suzani alifanya hivyo akataja bei. Nyogoso aliposikia bei hiyo alizama mfukoni alichomoa noti ya shilingi elfu kumi akampa kisha akasema "Chenji utakunywa maji mama yangu", alisema na wala asijue kuwa mama huyo alikuwa akimuwinda kwa udi na uvumba ili amuuwe.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ahsante sana baba", alijibu mama Suzani kwa sauti ya chini iliyojaa huzuni ndani yake. Nyogoso aliwaaha gari akaondoka zake akimuacha mama huyo akiisindikiza gari hilo kwa macho.
Dunia ikiwa adaa kwa mama Suzani, alitumia pesa zake kumtesa mnyonge naye sasa mwishowe anajikuta akiishi maisha ya kinyonge,kila siku heri ya jana. Na wakati hayo yakiwa ndio maisha ya mama Suzani, upande wa pili baba Mazoea aliitaka familia yake Africa kusini ili aishi nayo huko, Mama Mazoea aliondoka na mwanaye bila kumsahau Nyogoso. Huko baba Mazoea alizidi kutia baraka kwa Nyogoso na binti yake akiwatakia maisha mema. Miradi ya biashara baadhi alikabidhiwa Nyogoso. Maisha kwa kijana huyo na mkewe yakawa safi. Tanzania alirudi mara moja kwa mwaka kuja kulisafisha kaburi la mama yake ambapo alilijengea ili lisipotee. .?
PENZI LA MZOA TAKATAKA 2...KICHAA WA MTAA
MWISHO
0 comments:
Post a Comment