Simulizi : Penzi Ama Kaburi
Sehemu Ya Pili (2)
Alipomaliza kusoma, akatoka na kuelekea bwenini, alipofika huko, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kuchaji simu yake, halafu kuanza kuitafuta namba ya Gibson, kitu cha ajabu, hakuweza kuiona.
“Ilikuwa humu! Eeh! Imefutika?” alijiuliza.
Hakutaka kukubali, akampigia simu Diana na kumuomba namba ya Gibson kwani alikuwa na uhitaji nayo sana.
“Wewe ya nini tena?” aliuliza Diana.
“Nataka nizungumze naye!”
“Are you guys in love?” (mpo kwenye mapenzi?)
“Nope! I wanna talk to him, pleaseeee...” (Tafadhali...nataka kuzungumza naye)
“What is it about?” (kuhusu nini?)
“About something...” (kitu fulani)
“Is it love?” (ni mapenzi?)
“I said no! Something else...” Nilisema hapana! Kitu kingine)
“Sawa mama! Ila kuwa makini na moyo wa Gibson, nilichokisikia juu yake, kinasikitisha mno,” alisema Diana, wakati Shadya alipotaka kuuliza kuhusu hicho alichokisikia rafiki yake kuhusu huyo Gibson, simu ikakatwa na baada ya sekunde chache meseji iliyokuwa na namba ya Gibson ikaingia kwenye simu yake.
Sasa kukawa na vitu viwili alivyokuwa navyo, na alitamani sana kuvisikia. Kitu cha kwanza kilikuwa ni kuhusu yale maneno aliyomwambia kule kwenye ukumbi lakini kitu cha pili kilikuwa ni kutaka kufahamu kwa undani kile alichoambiwa na Diana.
Akabaki katikati, hakujua ni kitu gani hasa alitakiwa kuuliza.
“Labda nianze na hili la Gibson kuhusu ule msemo wake, halafu nitamuuliza Diana kuhusu huyu kijana! Kuna mambo gani hapo?” alijisema huku akionekana kuingia kwenye dimbwi la mawazo kwa vitu ambavyo havikumuhusu kabisa, na hapakuwa na ulazima wa kuyajua.
Hapo akaanza kukaribishwa jijini Dar es Salaam, kwa watu waliokuwa na mbinu za kila namna pale walipokuwa wakihakikisha msichana fulani ilikuwa ni lazima walale nae.
“Gibson! Upo wapi?” aliuliza Diana.
“Nyumbani!”
“Kwani unaishi kwenu?”
“Ndiyo! Si unajua nafanya kazi!” alisikika mwanaume huyo.
“Unafanya kazi?”
“Ndiyo! Huku nasoma!”
“Mwaka wa kwanza?”
“Ndiyo! Kwani ni ajabu Shadya?”
“Hapana! Si ajabu.”
“Kwanza namba yangu umeitoa wapi?”
“Nilikuwa nayo!”
“Haiwezekani hata kidogo!”
“Kwa sababu gani?”
“Namba yangu huwa haichukuliwi na watu wanaotumia simu zenu,” alisikika mwanaume huyo.
“Jamaniiii! Yaani bado unatuponda tu!”
“Ndiyo! Nitafanya hivyo mpaka nitakapokuona unabadilika na kununua simu nyingine!” alisema mwanaume huyo.
“Sasa wewe unataka nitumie simu gani?”
“iPhone!”
“Mh! Nitaweza kuwa nayo?”
“Kwa nini ushindwe! Umeingia chuo kumbuka, kuna mikopo kama yote!”
“Najua! Ila si natakiwa nifanyie mambo mengine!”
“Kama yapi?”
“Tuachane na hayo! Niambie kuhusu kile ulichokuwa umeniambia darasani....”
“Kipi?”
“Ule mfano wa gari na matairi, ulikuwa unamaanisha nini?” aliuliza Shadya huku akitoa tabasamu.
“Halooooo...” alisikika Gibson akiita.
“Halo! Nasema niambie sasa...”
“Halooo...Shadya...halooo...”
“Gibson....”
“Haloooo...”
Mara simu ikakatwa, alipojaribu kumpigia, haikuwa ikipatikana.
“Shiiiiiiiit....” alijikuta akisema Shadya kwa hasira, akagundua kwamba Gibson alimfanyia makusudi, alimsikia ila akajifanya kama hakuwa akimsikia vile.
***
“Diana, niambie kitu kimoja!”
“Kitu gani?”
“Kuhusu rafiki yako!”
“Yupi? Ninao wengi!”
“Namaanisha yule kipenzi kabisa!”
“Shadya?”
“Ndiyo!”
“Amefanya nini?”
“Hivi unauonaje ule uzuri wake?”
“Kwani upoje?”
“Yaani nyie wanawake hamuwaonagi wenzenu walivyokuwa wazuri ama kiburi cha uzima tu? Hahaha!”
“Mtoto wa Kipemba yule!”
“Ni mashallah! Nataka nipite!”
“Unamaanisha nini?”
Yalikuwa ni mazungumzo ya watu wawili, Gibson aliyekuwa akizungumza na Diana, rafiki yake na Shadya.
Walikuwa wamekaa sehemu fulani na kuanza kumzungumzia msichana huyo mrembo, alikuwa na mvuto wa aina yake, kila wanaume walipokuwa wakimwangalia, walimpenda na kumuona kuwa msichana wa aina yake kabisa.
Wanaume walimfuatilia, na miongoni mwa wanaume hao alikuwa Gibson. Alimpenda, alivutiwa naye lakini aliona kuna ugumu mkubwa wa kumpata kwani endapo angemuingia kichwa kichwa, asingefanikiwa kumpata hata kidogo.
Alitakiwa kuwa na akili ya aina yake, kumfuatilia kwa mtindo ambao kusingekuwa na mtu yeyote ambaye angegundua, si hao tu bali hata Shadya mwenyewe asingegundua kama alikuwa na lengo hilo.
Kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kuuteka umakini wake. Kumtia hamu na kumfanya kuwa na hamu ya kuonana naye.
Huo ndiyo mtihani wa kwanza ambao wanaume wengi walifeli, waliwafuatilia wanawake kihovyohovyo na mwisho wa siku kuambuliwa kukataliwa, kama mwanaume unayejitambua, unapomtaka msichana fulani ni lazima uwe na mipango yako madhubuti na kufanikiwa kukaa naye chumbani, tena kitandani.
Silaha ya kwanza ilikuwa ni kulijua jina la mwanamke, kumuonyesha kwamba alikuwa maarufu, alijulikana kila kona, ni njia nzuri ambayo kama akifuatwa msichana yeyote yule na mwanaume asiyemjua, ilikuwa ni lazima ampate hata kama ni mgumu kama chuma.
Alimfahamu Shadya, walikuwa wakijuana, hivyo njia hiyo haikuwa sababu ya kumfanya kuwa wake, kulikuwa na plan B ambayo alitakiwa kuifanya kuhakikisha anampata, na hiyo ilikuwa ni kumuwekea umakini, hamu ya kuonana naye kutokana na maswali aliyokuwanayo juu yake.
“Hii ni njia nzuri sana,” alijisemea huku akimwangalia Diana.
“Njia gani?”
“Kumpata Shadya!”
“Sasa kuna ugumu gani kwani?”
“Wewe uliniambiaje mwanzo?”
“Kwamba ana mtu wake!”
“Yaap! Kuna njia za kuwafuata wasichana waliokuwa na watu wao, wale waliokuwa singo, walioolewa, wanaofanya kazi benki na sehemu nyingine, na pia kuna njia za kuwafuata hata wale wanaofanya kazi ya mama ntilie!” alisema Gibson maneno yaliyomfanya Diana kunyamaza kwanza.
“Mh!” akaguna.
“Unaguna nini?”
“Hayo unayoyasema! Kwa maana hiyo kuna njia mpaka ya kunipata mimi?” aliuliza Diana.
“Ndiyo! Tena wewe ni kesho tu tungekuwa gheto tunafanya yetu...Hahaha...” alisema Gibson na kuanza kuchak.
“Hebu nitolee ujinga wako!”
“Diana! Ninamtaka Shadya! Ninataka kuiteka akili yake kwa kitu kimoja tu!”
“Kipi?”
“Kuipa maswali ya jambo fulani, awe na hamu ya kunitafuta kila siku,” alisema Gibson.
“Ipi?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hebu naomba namba yake,” alisema Gibson, Shadya akashangaa kwani walikuwa kundi moja chuoni, sasa kwa nini hakuwa na namba yake.
“Kwani wewe huna?”
“Acha uswahili! Unadhani ningekuwa nayo ningekuomba?” aliuliza Gibson, Shadya akampa namba hiyo.
Gibson akaichukua na kuondoka zake, kichwa chake kilikuwa na jambo moja, ilikuwa ni lazima amtafute Shadya na kuanza kumfuatilia kwa njia ambayo alikuwa ameipanga.
Hakuona ugumu kabisa, alimtafuta na alipompata ndipo akampa suala la gari la Range kuwa na tairi la Vitz.
Hilo likaanza kumsumba Shadya kichwani, akahisi kabisa kijana huyo kulikuwa na kitu cha umuhimu alichokimaanisha hivyo kuanza kumtafuta ili amwambie alimaanisha nini.
Huo ulikuwa mtego namba moja, ilikuwa ni lazima atafutwe kwanza, kwa kipindi fulani, aanze kuleta mapozi, amringie lakini mwisho wa siku amuite sehemu ambayo hata kwa dawa asingeweza kuchomoka.
“Gibson! Hivi unaniona mimi bibi yako!” alisema Shadya, alijifanya kukasirika, walikuwa wakiongea kwenye simu.
“Kwa sababu gani?”
“Kwa nini hutaki kuniambia!”
“Siwezi kwa sababu kila mwanaume chuoni atanishangaa wakijua nimekwambia!” alisema Gibson, maneno hayo yakazidi kumpagawisha Shadya.
“Wanaume wa chuo?”
“Ndiyo! Wote wanajua, na wanakushangaa sana! Aiseee! Hivi ni kweli Shadya?” aliuliza Gibson, ili kumtia presha, akakata simu.
Moyo wa msichana huyo ukawa na presha kubwa zaidi, alihisi kulikuwa na jambo kubwa lililokuwa likiendelea ambalo Gibson hakutaka kumwambia hata kidogo, akaanza kuogopa na kuanzia siku hiyo akaanza kukosa amani, kila alipomuona mwanaume hapo chuo, akahisi naye huyu alikuwa akijua.
Hilo likamfanya kila siku alipokuwa akitoka darasani tu, alikimbilia bwenini na kujifungia, hakutaka kutoka, hakutaka kuonekana kwani tayari moyo wake ulionekana kuwa na hofu.
Alikaa chuo, alimsubiri Gibson ili aje kumwambia ukweli lakini kijana huyo hakutokea. Kichwa kikawa na mawazo, sasa akawa hamfikirii sana Ngwali, mtu aliyekuwa akimfikiria alikuwa Gibson, na mbaya zaidi alitamani sana kupokea simu ya kijana huyo kuliko hata ya yule mpenzi wake.
“Gibson! Why?” alijiuliza kila siku.
Baada ya siku tatu, Gibson akatokea hapo chuo, Shadya alipomuona tu, akamkimbilia, siku hakutaka kabisa kumuacha kijana huyo, ilikuwa ni lazima aambatane naye na kumwambia alichokuwa akikimaanisha ambacho kilimpa maswali mengi.
“Niambie!”
“Sina muda. Nimekuja mara moja tu, ni jambo kubwa, si la kuzungumza kwa dakika moja ama kumi,” alijibu Gibson, tena alijifanya kuwa bize mno.
“Mbona unaonekana una haraka?”
“Nataka kuondoka! Nimekuja mara moja tu!”
“Sasa ndiyo hutaki kuniambia?”
“Nitakwambia hata kesho!”
“Hapana! Ninataka leo!”
“Basi ngoja niende sinema kuna muvi mpya imetoka, nitakwambia!”
“Hapana! Twende wote, ninataka mpaka uniambie,” alisema Shadya.
Gibson akabaki kimya, hicho ndicho alichokuwa na hamu ya kukisikia, hapakuwa na tatizo, akamchukua na kwenda naye Mlimani City ambapo hapo akakata tiketi ya muvi ya saa kumi na mbili na kungia.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa msichana huyo kuingia humo, alishangaa, hakuzoea kuona mambo hayo alipotoka, aliburudika, aliona kama ameonyeshwa ulimwengu mwingine wa maisha ya binadamu.
Waliangalia mpaka saa mbili na nusu, Gibson akaongezea na kuangalia nyingine mpaka mishale ya saa nne, walipomaliza, wakatoka.
Shadya akamzoea Gibson, na hata mpenzi wake alipokuwa akipiga simu, hakutaka kupokea, alihitaji kuambiwa kile alichohitaji kuambiwa na kijana huyo lakini pia la zaidi lilikuwa ni kutamani sana kuendelea kuwa naye kwani alimuonyesha ulimwengu mwingine kabisa.
“Twende Sinza!” alisema Gibson.
“Kufanya nini?”
“Kula! Au umekula?”
“Bado!”
“Basi twende!”
Wakaondoka na kuelekea huko, walikuwa wakizungumza mambo mengi. Kwenye maneno yote hayo Gibson hakutaka kumficha Shadya, alimwambia jinsi alivyokuwa mzuri, alivyovutia na kuonekana kuwa mwanamke mwingine wa tofauti kabisa.
“Shadya! Nimeona wanawake wengi, ila wewe ni wa tofauti kabisa,” alisema Gibson huku akitembea na msichana huyo.
“Kwani mimi nipoje?”
“U mzuri, mtanashati, unajua kuvaa, unapendeza sana,” alijibu Gibson maneno ambayo yalimfanya Shadya kujisikia mtu wa tofauti.
“Hebu toka huko!”
“Shadya! Ninakwambia ukweli! Hebu jiangalia ulivyo! Kila mwanaume anajisikia raha kuwa na mwanamke kama wewe. U mrembo sana, unaongea vizuri, lipsi zako zinavyochezacheza, hakika hakuna mwanaume ambaye anaweza kuthubutu kutoa macho yake kuangalia pembeni!” alisema, alizidi kuongeza sifa.
“Ndivyo unavyojidanganya!”
“Shadya! Unajua kwa nini nimekuomba tukaangalie muvi?” aliuliza.
“Sikukuomba! Nilitaka mwenyewe!”
“Sawa! Kwa nini kwako nimekuwa mwepesi sana kukubali?” aliuliza.
“Mh! Sijajua!”
“Ni kwa sababu ya jinsi ulivyo!”
“Nipoje?”
“Nimekwishakwambia kwamba u mzuri sana. Uliona watu walivyokuwa wakikuangalia pale tulipokuwa kwenye viti kusubiri kuingia ndani?” aliuliza, kiukweli hapakuwa na watu waliokuwa wakimwangalia, ila aliongeza chumvi kwa kuwa alijua msichana huyo hakuwa makini.
“Walikuwa wakiniangalia?”
“Ndiyo! Sikufanya makosa kwenda na wewe. Shadya! Unajua kuvaa, sura nzuri, hutumii make up, unajijali, una mvuto wa aina yake, hata siku nikiambia niwe na msichana mrembo, hakika nitakuchagua wewe,” alisema Gibson.
“Shindwa!”
“Shadya! U mzuri mno mno mno....” alisema Gibson.
Japokuwa alijifanya kukaza lakini moyo wake ulijisikia tofauti kabisa. Alimzoea Ngwali, alikuwa mpenzi wake lakini hakuwahi kumsifia kama alivyokuwa akimsifia Gibson muda huo.
Maneno ya mwanaume huyo yalibadilisha kila kitu na kujiona mtu mpya, aliyezaliwa kwa mara ya pili na kuhisi katika dunia hii hapakuwa na msichana aliyekuwa mzuri kama yeye, hapakuwa na msichana aliyekuwa akijua kuvaa kama alivyokuwa akivaa.
Gibson alikuwa akimsikilizia pumzi zake tu, alitamani kusikia ni kitu gani angesema msichana huyo, alipoona maneno hayo yamemuingia, sasa ukawa muda wa kutaka kufanya jambo moja kuona kama angemkatalia, akaupeleka mkono wake na kuushika mkono wa msichana huyo, hakugoma.
“Una mikono lakini sana, laini mno!” alisema Gibson.
“Mbona kawaida!”
“Na inanukia mno! Unatumia mafuta gani?”
“Ya nazi!”
“Oh! Ni mazuri sana! Sijawahi kumshika mwanamke mwenye mikono laini kama yako!” alisema Gibson, Shadya akajikuta akichekacheka tu.
Wakafika mpaka Sinza, kila mmoja aliona kama wamewahi kufika, wakaingia kwenye mgawa mmoja na kuanza kula chakula. Muda wote huo kazi ya Gibson ilikuwa ni kumsifia Shadya tu, jinsi alivyokuwa mrembo, alivyokuwa na mvuto wa aina yake.
Msichana huyo alijisikia furaha mno moyoni mwake, hakuamini kama sifa zote hizo alikuwa akisifiwa yeye, wakati mwingine alijiona mrembo zaidi ya Alicia Keys ama muigizaji Mila Kunis.
“Gibson! Unaniangalia sana mpaka naona aibu!” alisema Shadya wakati alipogundua kijana huyo alikuwa akimwangalia kwa zaidi ya dakika tatu nzima.
“Najaribu kuuangalia utaalamu wa Mungu! Alikuumba akiwa kwenye utulivu wa hali ya juu,” alisema kijana huyo.
“Unajua unanifanya nisikie aibu!”
“Shadya!”
“Abeee...”
“Nakupenda!” alisema Gibson! Msichana huyo akabaki kimya.
“Umenisikia?”
“Ndiyo! Ila nina mtu wangu!”
“Sijakwambia umuache, ni mwanaume mwenye bahati sana, endelea naye tu! Ila jua kuna mtu anakupenda!” alisema.
Hiyo ilikuwa njia ya pili aliyokuwa ameitumia. Kwa mwanaume hakutakiwa kuonyesha chuki kwa mwanaume aliyekuwa na mwanamke uliyekuwa ukimpenda, bali alitakiwa kumpongeza kwa kumuona mtu aliyekuwa na bahati sana.
Hilo likamfanya Shadya kuona kama mtu huyo hakuwa na lengo lolote kwake, yaani alikuwa innocent kabisa. Sasa moyo wake ukaanza kuwa tayari kwa lolote kwa kijana huyo.
“Kila mwanaume anapenda kuwa na mwanamke mzuri, kama jinsi ulivyokuwa,” alisema Gibson, akajiona kule alipokaa kuwa mbali, akamsogelea karibu, miguu yao ikaanza kugusana.
“Unamaanisha nini?”
“Jiangalie jinsi ulivyo, ulivyokuwa na ngozi laini,” alisema Gibson, akauchukua mkono wake na kuupeleka kwenye upaja wa Shadya, alivalia baibui kubwa jeusi.
“Oh! Unafika mbali sasa!”
“Hapana! Ninatamani kukugusa kila kona, una ngozi laini sana, unanukia vizuri mno! Shadya! Ninakupenda mno! Sijajua ni kwa namna gani natakiwa kukwambia hili,” alisema Gibson, akaanza kuupeleka mkono huku na kule kwenye paja lile, halafu akamuachia.
“Unanipa majaribu sana! Hebu niambie kuhusu mfano wa gari!”
“Nitakwambia tu! Shadya! Wewe ni msichana mzuri! Jua hilo!”
“Umeniambia tayari!”
“Wewe ni gari la kifahari, wakati mwingine unatakiwa kutumia vitu ambavyo vinadhihirisha uzuri wako!” alisema Gibson.
“Kama vipi?”
“Simu na vitu vingine!”
“Gibson!”
“Simaanishi kwa ubaya! Shadya! Unapendwa na wengi sana chuoni, yote ni kwa sababu ya uzuri wako! Naomba umalize haraka nikurudishe!” alisema Gibson.
“Chuo?”
“Ndiyo!”
“Nimechelewa sana!”
“Unataka kwenda wapi?”
“Popote ila si chuo!”
Gibson akakaa kimya kwa sekunde kadhaa. Hapo kukaja kitu kingine kichwani mwake, ulikuwa ni muda wa kumuonyesha Shadya kwamba alikuwa Gentleman, hakutakiwa kuwa na haraka.
Alikuwa na uwezo wa kumchukua na kumpeleka nyumbani kwao, lakini akajiuliza kama lingekuwa jambo jepesi ama la, kwani kwa mwanaume kuvumilia usiku mzima ilikuwa ni kazi kubwa.
“Au nifanye naye? Ila akikataa? Nitaanza kuona noma na mwisho wa siku nitaomba nisionane naye! Ngoja nivumilie,” alijisemea.
“Basi twende nyumbani!”
“Kwenu?”
“Yaap!”
“Kuna chumba cha wageni?”
“Hapana!”
“Sasa nitalala wapi? Sebuleni?”
“Hapana! Chumbani kwangu!”
“Na wewe?”
“Humohumo!”
“Hapana!”
“Shadya! Kuna mengi huwa yanatokea, ila naomba uchukue saa ishirini na nne tu katika maisha yako uniamini,” alisema Gibson.
“Mh!”
“Pleaseeee...”
“Nimwamini mwanaume?”
“Ikiwezekana! Hata kama wote huwaamini! Mwamini Gibson basi!” alisema.
Shadya akajifikiria kwa dakika kadhaa, akakubali na hivyo kuondoka mpaka alipokuwa akiishi kijana huyo, wakaingia ndani, akaandaliwa maji ya kuoga, akaoga, akakaribishwa kitandani na kulala.
Hakupata usingizi, muda wote mawazo yake yalikuwa yakimfikiria huyo mwanaume, ni kwa namna gani angeweza kuvumilia kulala naye mpaka asubuhi pasipo kumgusa, lakini hakuamini mpaka asubihi ilipofika, hakuguswa, akaamshwa, akaelekea bafuni, akaoga na baadaye kurudi chuoni, kila alipomfikiria Gibson, hakumpatia majibu, hakujua kama mwanaume huyo alikuwa na hesabu zake, na kwa kifupi, kabla ya kumuonyeshea madhara, alitakiwa kumwamini.
Hiyo ilikuwa njia ya tatu kumnasa msichana. Ufanye moyo wake uingie na imani kubwa juu yako ili iwe rahisi kuvuliwa nguo.
***http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Rahim alikuwa mpweke chuoni, alikosa furaha kabisa kwa sababu kwa hapo chuo alipokuwa akisoma, hapakuwa na mwanaume yeyote yule ambaye angemwambia anampenda na hata kulala naye.
Mwili wake ulikuwa na hamu kubwa, hakujua ni kwa namna gani angeweza kumwambia mwanaume yeyote kuwa alitamani kulala naye usiku kucha.
Kichwa chake kilikuwa na mambo mengi, kila siku usiku alipokuwa akilala, alikuwa mtu wa kufikiria mambo lukuki, kwenye chumba alichokuwa akikaa, kulikuwa na wanaume watatu, Hamisi, Alfonce na Maliki.
Kati ya watu hao wote, Hamisi ndiye alikuwa mtu wake wa karibu, rafiki waliyeshibana lakini hakuweza kugundua kama alikuwa akiendekeza mapenzi ya jinsia moja.
Kila siku kijana huyo alipokuwa akivua fulana yake na kubaki wazi, Rahim alichanganyikiwa, akili ilimruka, alipagawa kupita kawaida.
Alitamani kumwambia jinsi alivyomtamani lakini alishindwa kufanya hivyo kwa kuwa aliogopa.
Wakati yeye akifikiria hayo yote, Hamisi naye alikuwa na mambo yake kichwani mwake. Alimfikiria rafiki yake huyo. Kilichomuumiza ni kwamba hakuwahi kumuona na mwanamke yeyote yule.
Kwa kipindi chote hicho alichoishi naye kilimfanya kujiuliza maswali mengi. Alitamani kumwambia tatizo lilikuwa nini, kulikuwa na wanawake wengi waliokuwa wakimtaka lakini hakutaka kuwachukua, hakutaka kuwa nao kabisa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwani kuna nini Rahim?” aliamua kuuliza Hamisi huku akimwangalia rafiki yake huyo kwa macho ya mshangao.
“Ninamtumikia Allah!” alijibu.
“Allah?”
“Ndiyo!”
“Ndiye anakufanya usiwe na mwanamke yeyote?”
“Ndiyo! Ni dhambi kubwa sana!”
Hamisi akabaki akimwangalia Rahim, hakujua mwanaume huyo alimaanisha alichokuwa akikisema ama la. Kile alichokizungumza Rahim kiliwezekana kabisa lakini kwa umri aliokuwanao, tena kwa jinsi alivyokuwa akipendwa na wanawake kulimfanya kuhisi kabisa alikuwa akikosea kufanya hivyo.
Hakutaka kuzungumza naye sana, alichokifanya ni kuondoka na kwenda kuonana na msichana mmoja aliyejulikana kwa jina la Hawa.
Alihitaji kumtumia msichana huyo kwa lengo la kwenda kumtega Rahim. Alihitaji kufahamu kama alikuwa na tatizo ama kulikuwa na sababu nyingine iliyomfanya kutokutamani kuwa na mwanamke yeyote yule.
“Hawa!” aliita Hamisi.
“Niambie!”
“Poa! Naomba kuzungumza nawe kidogo,” alisema Hamisi huku akimvuta Hawa pembeni, msichana huyo akakubali na hivyo kusogea pembeni.
Kwa kumwangalia tu, Hawa alikuwa msichana mrembo, aliyevutia, nywele ndefu, suruali ya jinzi na macho yake alibandika kope, midomo iliyopakwa lip stick, alionekana kuvutia.
“Kuna nini?”
“Kuna kitu nahitaji unisaidie,” alisema Hamisi.
“Kitu gani?”
“Unamfahamu yule rafiki yangu, Rahim?”
“Yule Mzanzibar?”
“Yeah!”
“Kafanyaje?”
“Ninataka umtege, uende naye chumbani, yaani umtege kwa staili hiyo!” alisema Hamisi, Hawa akashtuka.
“Nimtege?”
“Ndiyo!”
“Halafu!”
“Nitakulipa pesa! Kama laki moja hivi kama ukifanikiwa kulala naye,” alisema Hamisi, alijiahidi hata kulipia pesa lakini alihitaji kujua mengi kuhusu rafiki yake huyo.
“Mzanzibar?”
“Ndiyo!”
“Hivi wewe hujui michezo ya Wazanzibar?” aliuliza.
“Ipi?”
“Hahaha! Haloooo...”
“Mbona unacheka! Si uniambie!”
“Hivi unahisi siuthamini?”
“Huuthamini nini?”
“Nauthamini sana! Siwezi kudate na Mzanzibar! Naanzaje kudate naye! Eti natoka niende kwa Mzanzibar! Haiwezekani! Nauthamini sana! Wana michezo ya kifirauni sana wale,” alisema Hawa huku akionekana kugoma kabisa kumfuata mwanaume huyo.
Hamisi hakutaka kushindwa, alijitahidi kumbembeleza kijana huyo kukubaliana naye lakini ilishindikana kabisa. Hakutaka kuachana naye kwani aliamini mwisho wa siku angekubali na hivyo kufanya kama alivyokuwa akitaka kufanya.
Siku ziliendelea kukatika huku Hamisi akiendelea kumwambia Hawa kwamba lingekuwa jambo jema kama tu angekubaliana naye kumfuata rafiki yake huyo na kufanya naye mapenzi kama alivyokuwa amezungumza naye.
“Ila pesa ipo?” aliuliza Hawa kabla ya yote.
“Ipo!”
“Ila zungumza naye, yale mambo yao sitaki mie!” alisema Hawa, aliipenda pesa lakini wakati mwingine alikuwa na wasiwasi tele.
“Hahah! Hawa bhana! Sawa nitamwambia!” alisema Hamisi na hivyo kuondoka huku akimuacha msichana huyo afanye kile alichomwambia.
Hawa hakuwa na presha, alijiamini, alikuwa na umbo matata sana, kwa nyuma alijaa na kifua chake kilikuwa kidogo kabisa, sura yake iliita na mapaja yake manene yaliwachanganya wanaume wengi waliokuwa wakimwangalia.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kila alipojiangalia, hakuona kama kungekuwa na mwanaume yeyote angetoka mikononi mwake endapo tu angeamua kwa roho moja kulala naye. Kwake, huyo Rahim hakuwa tatizo lolote ila kilichomuogopesha ni michezo ambayo alisikia ikichezwa sana kisiwani humo.
Aliogopa ila alipiga moyo konde na hivyo kuanza harakati zake za kumnasa mwanaume huyo. Siku hiyo ya kwanza kabisa alimuona akiwa darasani, amejikalia zake akiangalia muvi kwenye laptop yake.
Hawa akaingia na kumfuata Rahim pale alipokuwa. Alitembea kwa mwendo wa maringo, alivalia sketi fupi iliyobana kiasi kwamba kila alipokuwa akitembea darasani humo nyakati za jioni, watu waliokuwa wakipiga stori walinyamaza na kumwangalia yeye.
“Jamani sasa ni muda wa matangazo...” alisikika kijana mmoja, alikuwa mzungumzaji mzuri kwa wenzake, ila baada ya Hawa kupita, akatangaza muda wa matangazo, yaani watulie na kumwangalia msichana huyo.
“Koo...koo..koo..koo...” sauti ya viatu vyake vilisikika.
Alikwenda mpaka mahali alipokaa Rahim, hakuongea, kwanza akamwangalia mwanaume huyo, alihitaji kujua ni kwa namna gani angeanza kumtega kwa kumuonyesha alikuwa akimuhitaji sana.
Wakati akiwa amekaa, Rahim alitulia tu, ni kama hakumuona mtu aliyeingia hapo na kukaa karibu naye. Japokuwa kwa mwanaume yeyote rijali angeshtuka lakini kwake hata kumuangalia hakumwangalia.
Hawa akaona kama angeshindwa, alichokifanya ni kujiweka vizuri kitini na kukunja nne, mapaja yake yakaanza kuonekana vilivyo. Mlengwa wa kutegwa alikuwa Rahim lakini cha ajabu wanaume waliokuwa pembeni ndiyo walianza kutegeka lakini kwa mhusika hakusisimka hata kidogo, yaani ni kama mwanaume alikuwa akimwangalia mwanaume mwenzake.
“Rahim....” aliita Hawa baada ya kuona amepotezewa, Rahim akawa bize na muvi, alichokifanya ni kuvipitisha vidole vyake katika mkono wa Rahim, hapohapo akashtuka, akatoa earphones na kumwangalia msichana huyo.
“Mambo...” alisalimia kwa sauti ya kubembeleza kabisa.
“Poa!” alisema Rahim na kuendelea kuangalia muvi.
“Unaangalia nini?”
“Muvi...”
“Naomba tuangalie wote!” alisema Hawa, alijitahidi sana kuweka mapozi ya kike kumtega jamaa huyo lakini ilikuwa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa acheze.
“Lete flashi nikuwekee...” alisema.
Hawa akaishiwa pozi, alimwangalia vizuri Rahim machoni, hakuamini alichokuwa amemwambia, yaani yeye alitamani kuangalia naye muvi lakini kitu cha ajabu kabisa mwanaume huyo alimwambia ampe flashi ili akaangalia kwa wakati wake.
Hakutaka kukubali, ilikuwa ni lazima aonyeshe umwamba na kuhakikisha anafanikiwa katika suala hilo. Aliendelea kuzungumza naye kwa dakika kadhaa, hapo ndipo alipobaini mambo machache kuhusu mwanaume huy.
Wakati mwingine alikuwa akijisahau, alileta mapozi ya kike, alizungumza kikikekike lakini hata kwa jinsi vidole vyake alivyokuwa akiviweka wakati alipokuwa akibonyeza keyboard ya kompyuta ilimshtua Hawa.
“Mh!” alijikuta akiguna.
“Nini tena?” aliuliza Rahim huku akimwangalia msichana huyo.
Hawa hakutaka kubaki mahali hapo, haraka sana akasimama na kuanza kuondoka. Ni kama Rahim alijua kilichokuwa kikiendelea, hapohapo akasimama na kuanza kumfuata msichana huyo.
Katika mambo yote yaliyokuwa yakiendelea, hakutaka kabisa kuona mtu yeyote akifahamu kama alikuwa akijihusisha na mapenzi ya jinsia moja, ilikuwa ni lazima ailinde heshima yake kwa vyovyote vile.
Alijisahau mbele ya Hawa na kujikuta akifanya mambo kama mwanamke, aliamini kama angemuacha msichana huyo aondoke, kitu ambacho kingefuata mahali hapo ni kutangazwa kwamba alikuwa na chembechembe za umama, hivyo ilikuwa ni lazima alizuie hilo.
“Unakwenda wapi?” aliuliza Rahim huku akiwa amemuwahi msichana huyo na kumshika mkono.
“Nakwenda kupumzika!” alijibu Hawa huku akionekana kuwa na wasiwasi.
“Kwa hiyo unataka kuniacha hivihivi?” aliuliza.
“Hivihivi kivipi?”
“Umekuja pale, umenionyesha mapaja, halafu kweli rijali mimi unaniacha hivi? Haiwezekani!” alisema Rahim kama mwanaume kweli.
“Kwa hiyo sasa unataka kuniambiaje?”
“Na mimi nataka!”
“Unataka nini?”
“Kilichomfanya Samson anyolewe nywele.”
Hawa akabaki kimya. Alishangaa, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea. Aliamini hapo kabla kwamba jamaa alikuwa na umama lakini kitu cha ajabu kabisa, alimuwahi na kumwambia anataka.
Kusudi lilikuwa ni kumpa, ndivyo alivyopanga lakini pia akaanza kujiuliza kama kweli alikuwa na uwezo au alitaka kujishembendua tu. Wakaendelea kuzungumza na kukubaliana kwamba siku inayofuata usiku waende kutafuta chumba sehemu na kumpa kama alivyotaka, ila alitakiwa kumlipa.
“Pesa si tatizo!”
“Basi haina shida.”
Kazi ikabaki kwa Rahim! Hakujiamini, alijua kabisa hakuwa na uwezo wa kulala na mwanamke lakini kwa sababu alihitajika sana kuonyesha ubavu wake ilikuwa ni lazima ajilazimishe.
Hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya. Hapo akakumbuka kwamba kulikuwa na dawa za kuongeza nguvu za kiume zilizokuwa zikijulikana kama mkongo ama mputululu, ilikuwa ni lazima azitumie hizo kwa siku moja kumalizana na msichana huyo.
Hakujua angezipata wapi hivyo kitu alichokifanya ni kuwasiliana na dada yake, Shadya kwa lengo la kuzungumza naye kuhusu dawa hizo, angezipata vipi kwani alikuwa akienda kuaibika.
“Yaani siamini!” alisema Shadya alipoambiwa kuhusu dawa hizo.
“Naomba unisaidie! Nitakuja kuaibika! Naomba unisaidie kuzungumza na watu kuhusu dawa hizo,” alisema Rahim.
“Yaani umenichanganya sana!”
“Shadya! Usiponisaidia katika hili! Chuo kizima kitajua kwamba mimi nafanya michezo hiyo. Naomba unisaidie kutafuta,” alisema Rahim huku akionekana kuomba sana.
“Sasa wewe ni mwanaume, waambie wenzako naamini watakusaidia!” alisema Shadya.
“Siwezi!”
“Kwa nini?”
“Naona aibu!”
“Rahim! Wewe ni mwanaume!”
“Najua! Ila naona aibu! Naomba unisaidie!”
Shadya akashusha pumzi ndefu, hakujua ni kitu gani hasa alitakiwa kufanya. Ni kweli alihitaji sana kumsaidia kaka yake lakini hakujua ni kwa namna gani angeweza kupata dawa hizo na kumpatia kwani hakuwa na marafiki wengi.
“Gibson....” hilo lilikuwa jina la kwanza lililokuja kichwani mwake, ilikuwa ni lazima amtafute, amwambie amsaidie kwenye suala hilo.
“Nitakusaidia! Tuonane baadaye!”
Wakaagana na Shadya kuondoka. Kichwa chake kilivurugika, ilikuwa ni lazima amsaidie kaka yake huyo hivyo haraka sana akawasiliana na Gibson na kuomba kuonana naye.
“Nipo nyumbani! Kuna nini kwani?”
“Basi nakuja! Nina shida. Ila naomba usiniulize maswali! Nitahitaji unisaidie, nakuomba,” alisema Shadya.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sawa! Ila si uniambie kiasi gani kabisa nikatoe benki!”
“Sihitaji pesa.”
“Unahitaji nini?”
“Msaada wako ila si wa kifedha!”
“Sawa. Njoo home!”
“Kuna nani?”
“Leo nipo peke yangu!”
“Sawa nakuja!” alisema na kukata simu, akaanza kuelekea nyumbani kwa kijana huyo huku kichwa chake kikiwa kimechanganyikiwa kupita kawaida.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment