Karibu Katika Maktaba ya Simulizi, Riwaya, Chombezo na Hadithi Afrika Mashariki. %% Welcome to the Library of Stories, Novels, Comedy and Stories in East Africa.
BURE SERIES: https://bure0.blogspot.com/
kumfahamu”“James, na huyu ni rafiki yangu anaitwa Angel”“Oooh nafurahi kukufahamu Angel”Kisha James akampa mkono wake Angel, ila moja kwa moja James alijikuta akimpenda Angel yani alijikuta akimpenda gafla tena kimapenzi, basi mpaka muda Hanifa anamsindikiza Angel basi James alikuwa akimuangalia tu Angel hadi alipoishia yani alishindwa kutoa jicho lake kwa Angel.Hanifa alivyorudi dukani, James alianza kumuuliza vizuri kuhusu Angel,“Samahani dada, yule Angel ana mpenzi?”“Mmmh unataka nini? Binti mrembo vile utamuweza? Yani yule Angel kwao hawana dhiki ujue, sasa utaweza kumuhudumia unamuulizia, basi ushamtamani hivyo”“Yani sio kumtamani, nampenda sana, jamani nimempenda haswaaa nadhani usiku nikilala nitaota Angel tu”“Sasa unadhani Angel anaweza kukukubali mtu kama wewe? Aaanze tu, ila Angel hana mchumba yani huyu binti licha ya urembo wake na uzuri wake, hana mchumba wala mpenzi halafu mama yake ni mtu wa dini sana, halafu ni mkali sana yani anambana binti yake kiasi sidhani kama anaweza kuwa na mwanaume mama yake asigundue”“Aaaah usinifanyie hivyo bhana Anifa, mimi nampenda Angel yani nimempenda sana hapa naona kama yeye ndio pumzi yangu”Hanifa akacheka sana na kumwambia James sasa,“Kwa taaarifa yako huyu Angel nimemuita leo hapa sio kwasababu yako ila ni kwasababu ya mjomba, yani mjomba ni anampenda Angel kufa kabisa, sasa tuone kama una uwezo wa kushindana na mjomba anayekulisha, kukuvisha na kukusaidia uende chooni mjinga wewe, yani mimi Angel ni rafiki yangu haswaaa ila nimemuita sababu ya mnjomba, sema tu mjomba mwenyewe katingwa leo, kwahiyo ndugu yangu tafuta lingine, kuhusu Angel umekosea namba”“Sawa nakubaliana na wewe ila nipe hata namba yake tu yani utakuwa umefanya kitu kikubwa sana kwangu”“Hahaha, namba utamuomba mwenyewe ukimkuta mahali ila sikupi namba yake kabisa, andika maumivu tu”“Ila roho mbaya hiyo Hanifa”“Roho mbaya unayo wewe unayetamani mwanamke ambaye ameshatamaniwa na mjomba wako”Basi James aliumia tu kwani alijiona wazi kuwa amempenda Angel tena amempenda sana.Angel alirudi nyumbani kwao na moja kwa moja alienda kupika kwani alijua wadogo zake karibu watarudi, nyumba yao ilikuwa kubwa na nzuri lakini mama yao hakuweza msaidizi wa kazi pale nyumbani kwahiyo kazi zote walikuwa wakizifanha wenyewe kasoro za nje tu ambazo zilikuwa zikifanywa na mlinzi wa nyumba ile.Wakati Angel anapika, simu yake ikaita alipoichukua na kuangalia alikuwa ni mama yake basi alipokea kwa shauku sana na kuanza kuongea nayo,“Kwanini hujaenda shule leo?”“Jamani mama, si nimewapeleka wadogo zangu”“Hivi Angel mwanangu kwanini lakini eeeh! Nahitaji usome na ufike mbali, ndoto yangu ni kuwa wewe utakuwa daktari mkubwa sana na mashuhuri hapa nchini, ila kwanini unakuwa mzembe hivyo!”“Jamani mama, shule tunafungua wiki ijayo”“Mjinga wewe, wiki ijayo ya wapi? Mwalimu wako Harun katoka kunipigia simu muda sio mrefu kuwa kidato cha nne wenzio walianza kwenda toka wiki iliyopita, sitaki ujinga Angel, kesho shule, sio kwavile sipo basi ndio utegee, kesho nimesema shule”“Sawa mama, nimekusikia”Angel alikata simu ya mama yake ila alichukia sana kwani alijua ni mwalimu wake Haruni ndio kamsemea kwa mama yake,“Yani mwalimu mbea yule, mwanaume mzima mbea, sijui anamtaka mama yangu!! Ngoja, nitamwambia baba halafu atakoma”Basi akamalizia kupika na kwenda kuangalia tv tu maana aliona mama yake kashamletea habari za shule ambapo alitaka kutegea mpaka wiki nyingine, baada ya muda kidogo wadogo zake nao walirudi kutoka shule basi alianza kuongea nao kuhusu siku ya kwanza shuleni,“Haya wadogo zangu wapendwa, shule ile mmeionaje? Mazingira yakoje? Mmeipenda au?”“Kama hatujaipenda mtatuhamisha?”“Ushaanza Erick na ujinga wako, muhamishwe muende wapi? Pale mpende msipende mtasoma pale pale”“Sasa ulikuwa unatuuliza ili iweje? Kwanza njaa inaniuma?”“Kheee yani hili toto, sijui mama kaliokota wapi. Nenda jikoni huko ukajipakulie, niambie Erica, umeionaje shule mdogo wangu”“Shule ni nzuri sana na nimeipenda ila dada leo Erick kapigana”“Kheee siku ya kwanza shuleni na kupigana jamani! Picha gani mmeonyesha? Amepelekwa kwa mwalimu?”“Hapana, ila kampiga mtoto wa watu ngumi”“Ndiomana umerudi tu na kulalamika njaa, ngoja nimpigie simu mama yako nimwambie ujinga wako wa kupigana”Hakuna mtu ambaye huwa wanamuogopa kama mama yao basi Erick alirudi kumuomba msamaha dada yake ili asipige simu kwa mama yao,“Dada nisamehe tafadhari, naomba nisamehe dada. Usimwambie mama”“Ukipigana tena je!”“Sirudii tena kupigana dada yangu, naomba unisamehe”“Msamaha wangu kwako, nakuletea sare zangu za shule uzipige pasi maana na mimi kesho naenda”“Sawa dada nitafanya hivyo”Basi Angel alicheka na kwenda kuchukua sare zake ili mdogo wake ampigie pasi halafu yeye alirudi kukaa huku akiangalia vizuri vipindi vya kwenye Tv.Muda kidogo Angel aliona uvivu na kuinuka kwenda chumbani kulala, basi Erica alipomuona kaka yake akihangaika na zile nguo za Angel kuzipiga pasi tena kabla ya kula wakati alilalamika kuwa njaa inamsumbua, basi akamsogelea na kuhitaji kumsaidia,“Erick, acha nizipige mimi. Nenda kale tu”“Oooh ndiomana Mungu alifanya uwe pacha wangu, muda mwingi unanihurumia, asante Erica”Basi Erica alinyoosha zile nguo vizuri kabisa kisha kumpelekea dada yake kuchumbani na kuziweka vizuri ila Angel hakuwa amelala kabisa maana alikuwa akichezea tu simu basi zile nguo zilivyoletwa na Erica akauliza,“Mbona umeleta wewe na sio Erick ambaye nimempa hiyo adhabu”“Erick anakula dada”“Kwa kuteteana nyie mapecha siwawezi, haya niwekee vizuri hapo”Erica aliweka na kutoka mule chumbani.Kesho yake asubuhi na mapema walijiandaa wote na kwenda shuleni, na walipofika Angel aliwaacha wadogo zake kwenda kwenye madarasa yao halafu yeye kwenda kwenye madarasa ya wenzie wa kidato cha nne, ila alipoingia tu darasani kuna mkaka aligongana nae macho na kugundua kuwa yule mkaka alikuwa ni mgeni katika darasa lao, yani Angel alikuwa akimuangalia huyu mkaka na huyu mkaka pia alionekana akimuangalia Angel hadi alipokaa walikuwa wakiangaliana na kila mmoja alionekana kuogopa kumfata mwenzie labda kumsalimia, kwani huyu mkaka alijiona kuwa ni mgeni kufanya hivyo haipendezi, naye Angel aliona kuwa akimfata yule mkaka itakuwa kama anajipendekeza kwa mgeni.Basi yule mkaka akameza mate tu mpaka mwenzie wa pembeni akamstua na kumwambia,“Wewe naona unamuangalia mrembo wa darasa kiasi hiko utamuweza!! Yule binti ni matawi ya juu, kwanza umeona alivyo mrembo?”“Nimeona yani ni mrembo haswaaa”“Basi fata masomo yako, usimuone hivyo, walimu wenyewe ofisini wanagongana vikumbo kwaajili yake, wanafunzi hapa shuleni ndio balaa yani, kwakweli mtoto kaumbika yule”“Anaitwa nani?”“Anaitwa Angel au Malaika, yani yule ni Angel kweli, hata ukimuangalia lazima uvutiwe nae, pole sana ila najua kumpata huwezi”“Siwezi kweli, ila nitajaribu”“Ila kwenu mna uwezo nyie”“Ni kweli ila mimi kutongoza sijui kabisa, sema nimempenda sana”Mwenzie akacheka na kumwambia,“Wengi wanampenda ila kumpata hawawezi, kwanza mama yake ni mkali huyo balaa. Akiongozana nae huwezi hata kumsalimia”Yule mkaka akaguna tu na kuendelea na mambo mengine wakati huo Angel nae akiendelea na mambo mengine ila rafiki yake aligundua kitu toka kwa Angel sababu alimuona akimuangalia sana yule mkaka,“Mmmh Angel mbona umemuangalia sana yule mkaka?”“Naona sura yake ni ngeni, ndiomana nimemuangalia sana ulihisi nini?”“Nilihisi unampenda eti? Nikawaza huyu Angel si huwa anajifanya hapendi wanaume, imekuwaje tena kwa huyu?”Angel akacheka tu na rafiki yake akaendelea kuongea,“Yule mkaka anaitwa Samir”“Aaaah Samir!! Yani ushaenda kudaka jina la mgeni jamani Yusra”“Sasa mgeni anapendeza vile nisidake jina lake kweli jamani, inawezekana hiyo eeeh!”“Umempenda?”“Sijasema hivyo jamani Angel”Basi wakaongea na kuendelea na mambo ya masomo maana muda huo na mwalimu aliingia kufundisha.Muda wa kutoka shule ulipofika, Angel alitoka na alikuwa akisubiriwa na wadogo zake na kuwauliza kwa makini,“Erica, vipi leo Erick hajapigana?”“Jamani dada, sijapigana”“Haya sasa, tunarudi nyumbani kwa amani”Walirudi nyumbani wakiwa wamechoka na njaa ziliwasumbua, wakaanza kulalamika,“Jamani kuna umuhimu wa kuwa na mdada wa kazi, hivi kwanini mama anatufanyia hivi jamani!”“Ila siku zote baba huwa anasema kuwa mdada wa kazi ni wa muhimu sana ila mama hataki hata kusikia, hebu ona tulivyochoka, hivi nani anaweza kupika kwasasa? Hebu kamuagizeni huyo mlinzi mkate, tule mkate na chai tupumzike”Basi wakamuagiza mlinzi mkate ambapo baada ya muda mfupi aliwaletea na wakanywa chai baada ya hapo Angel aliwaambia wadogo zake,“Haya leo ofa, nendeni kavueni sare zenu za shule nikazifue”Basi waliharakisha na kumpatia dada yao kisha kila mmoja kwenda kuoga wakati dada yao ameenda kufua zile nguo na kuoga.Muda huu Erick na Erica walikaa sebleni ila Erick alikuwa akipiga miayo sana ikabidi Erica amuulize,“Ulishiba kweli Erick?”“Nitashiba wapi? Mkate wenyewe mdogo ule, mimi ni mtoto wa kiume yani kula vitu vyepesi vile nateseka”“Pole jamani, nikakusongee ugali?”“Kheee Erica ndio unajitoa kiasi hiko!! Asante sana kwa kunijali, wewe ni mtu muhimu sana katika maisha yangu”Basi Erica aliinuka na kwenda kumsongea ugali kaka yake ambapo ulipokuwa tayari, Erick alikula ule ugali kwa maziwa mtindi, basi Angel alikuja ndani na kushangaa,“Kheee Erick umesonga ugali?”“Angel huyo kanisongea”“Kumbe Angel unajua kusonga ugali? Ndiomana mama hataki kuweka msaidizi wa kazi maana anajua kazi zote wanae tunaweza”Basi Angel akasogea na kuubonya bonya ule ugali na kuona kuwa umeiva kisha alienda chumbani kwake.Angel akiwa chumbani kwake alishangaa sana kwani kila muda alikuwa akikumbuka tukio la kukutanisha macho na Samir, halafu kwenye akili yake alihisi kama jina la Samir limeanza kutawala, kiasi kwamba Erica alienda chumbani kwake na kumshtua naye akageuka na kusema,“Samir”Erica alicheka na kumuuliza dada yake,“Mmmh dada, Samir ndio nani?”“Mmmh umbea huo, haya ulikuwa unasemaje?”“Mama amepiga simu ya mezani pale, kasema Ijumaa wanarudi”“Jamani hadi Ijumaa dah! Mimi nitakuwa nimeshachoka na kazi za nyumbani kwakweli, arudi aje afanye mwenyewe”Erica alicheka na kuondoka chumbani kwa dada yake maana hata yeye alikuwa na chumba chake.Basi Angel akakumbuka alichoongea na Hanifa kuhusu Ijumaa ikabidi ampigie simu kwani hakujua atafanyaje wakati wazazi wake ndio wanarudi,“Hanifa mwenzangu nitashindwa kuja hiyo Ijumaa”“Jamani Angel ni kitu cha muhimu sana tafadhali, nakuomba usikose na wala haitochukua muda mrefu”“Ni kitu gani jamani eeeh!”“Sikia rafiki yangu, kwani unaogopa nini kuja?”“Mama na baba wanarudi Ijumaa, sasa mimi nitakuja vipi?”“Sikia Angel, Ijumaa huwa watu wanawahi kutoka shule kwahiyo wewe ukitoka pitia hapa dukani mara moja tu halafu unaondoka”“Halafu wewe unanichuza ujue maana hata shule huji ila umekazana tu kuuza duka halafu mimi unataka kunichuza”“Hapana, nadhani unanielewa Angel, naanzaje kufanya kitu kinyume sasa jamani eeeh!”“Haya nitaangalia uwezekano”Basi akakata ile simu na kuendelea na mambo mengine ila usingizi ukampata pale pale.Angel aliamka kwenye mida ya saa tatu na alikuta wadogo zake ndio wanakula, basi na yeye alikaa na kuanza kula, ila aliguna,“Mmmh hiki chakula kapika nani tena?”“Erick huyo kapika”Angel akacheka na kusema,“Kweli nyumba inavituko hii jamani, yani Erick ndio kapika leo dah! Sio kwa michumvi hii uliyoitia kwenye hizi tambi mdogo wangu jamani! Ngoja kesho nitapika tambi za sukari na mtajiramba haswaaa, haya hebu nipeni hiyo juisi nionje nayo”Basi wakammiminia ile juisi na kuinywa huku akisema,“Hii lazima imetengenezwa na Erica”Basi Erica akatabasamu na kuitikia kuwa ni yeye ameitengeneza, basi Angel akasifia na kusema,“Kwa hakika mume atakayekuoa mdogo wangu atafaidi sana”Erick alionekana kuchukia, akadhira chakula na kuinuka,“Kuleni wenyewe sasa”Angel alicheka na kusema,“Kheee ulitaka na wewe nikusifia na michumvi hii! Susa baba, wenzio tunakula kama kawa, umetujazia michumvi hadi tuumwe safura halafu unataka nikusifie”Basi Angel alikula kula pale ila aliona ambavyo Erica hakuwa na raha na kumwambia,“Wewe achana na yule aliyesusa, sisi tujilie zetu tukalale, achana na wehu wa kususa”“Ila dada ungembembeleza kidogo”“Biashara hiyo sifanyi, mama yake angekuwepo labda ndio angeenda kumbembeleza, sikia inuka kambembeleza pacha wako huko maana naona nawe umeishiwa na amani, ndio shida ya kuzaliwa mapacha hii”Basi Erica aliinuka na kwenda chumbani kwa Erick, na Angel aliendelea kula huku akilalamika kuhusu chumvi na hatimaye kuinuka kwenda kulala tena.Basi Erica akaanza kuongea na Erick,“Jamani twende ukale ndio uje kulala Erick”“Kwakweli wewe Erica una moyo wa mama kabisa na roho ya baba, ila dada Angel jamani dah! Yani anajijua mwenyewe na anajijali mwenyewe tu”Basi akainuka na kwenda mezani na kuendelea kula ambapo Erica alimuuliza kaka yake,“Ila wewe ni kitu gani kilikukera kwa alivyoongea Angel hadi ukagoma kula?”“Tuachane na habari hizo Erica, ngoja ninywe juisi nikalale. Ni kweli hii juisi uliyoitengeneza ni tamu sana”“Kwahiyo ni kweli mume atakayenioa atapata raha”“Hivi Erica wewe na udogo huo unaanza kuongelea habari za mume wa kukuoa? Ngoja mama aje nimwambie”“Hapana jamani, mimi nilikuwa nafata maneno ya dada tu”Basi walimaliza kula na kila mmoja alienda kwenye chumba chake kulala.Siku hiyo walichelewa kuamka na kufanya wajiandae haraka sana, na kugundua kuwa hata gari la shule limewaacha,“Sasa dada tutafanyaje?”“Ngoja nimpigie dereva simu aje atupeleke shuleni”Basi Angel akampigia dereva wao ambaye baada ya muda mfupi tu alifika kuwachukua ili waende shule, basi pale mbele alikaa na Angel na kuanza kuongea nae,“Ila mbona siku hizi Angel hutaki niwapeleke safari zenu?”“Aaaah wewe unakera bhana”Yule dereva aliendelea kuongea ila hakuna jambo ambalo Angel alimjibu, basi walifika shuleni na kushuka ambapo dereva alimuuliza Angel,“Vipi wakati wa kutoka nije kuwachukua?”“Aaaah tutarudi na gari la shule”Basi wakaachana nae halafu wao wakaelekea kwenye madarasa yao.Leo wakati Angel anaingia darasani akagongana kikumbo na Samir na kujikuta wakitazamana sana, na wote kusema kwa pamoja,“Samahani”Basi wakajikuta tena wakiangaliana, Samir akampa mkono Angel na kumwambia,“Naitwa Samir, sijui nawe waitwa nani?”Naye Angel alimpa mkono na kumwambia,“Naitwa Angel”Cha kushangaza walisikia kelele darasani na kugeuka darasani ili kuangalia kuna nini, wakagundua kuwa wanafunzi kwenye darasa lao wanawashangilia huku wakipiga na makofi, yani kwa mara ya kwanza Angel alijihisi aibu sana kiasi kwamba hakuweza kuingia darasani na kutoka nje kabisa ambapo Samir nae alitoka na kuelekea alikokuwa akienda.Baada ya muda kidogo ndio Angel akaingia darasani, alipokaa tu rafiki yake Yusra alianza kumcheka na kumwambia,“Naona shoga yangu umepatikana, sio kutazamana kule na Samir jamani mmmh!! Unampenda eeeh!”“Aaaah mambo gani hayo Yusra?”“Sio mambo gani, unajua saivi sisi ni wakibwa, kidato cha nne sio mchezo yani, unamtaka?”“Mimi nataka kusoma”“Huna lolote, unamuogopa mama yako tu ila unamtaka”Angel alitabasamu tu bila ya kusema chochote kile.Muda wa kutoka ulipofika, Samir alijikaza na kumsogelea Angel ambapo alimuomba namba yake ya simu nae Angel hakusita kwani muda huo huo alimpa Samir namba yake huku akiagana nae na kwenda kuwafuata wadogo zake ambapo aliondoka nao hadi nyumbani kwao.Walipofika nyumbani basi Angel akafanya kama kawaida kwani aliwaambia wadogo zake kuwa wapike chai na wale tena mkate ila Erick aligoma,“Jamani dada kwanini lakini unafanya hivi? Tupikie chakula tule, kumbuka ahadi yako ya jana”“Kheee nyie watoto jamani, basi ngoja niende chumbani kubadili nguo ndio nianze kupika”Basi Angel akaelekea chumbani kwake, ila alichukua simu yake na kuiwasha, muda huo huo ukaingia ujumbe ukisema,“Angel, ni Samir hapa. Vipi ushafika kwenu? Nimekumiss teyari”Angel akatabasamu na kumjibu Samir, muda huo akajikuta ameanza kuwasiliana na Samir na kusahau ahadi yake kwa wadogo zake kuwa anaenda kuwapikia chakula.Alikaa chumbani hadi wadogo zake wakamfata dada yao,“Jamani dada Angel mbona unatufanyia hivi!! Njaa zinauma”“Ila na nyie mmezidi jamani, kumbukeni mimi sio msichana wa kazi humu ndani eeeh! Ngoja nimpigie mama”Basi Angel alimpigia mama yao ambapo muda huo huo alipokea, basi Angel alimsalimia na kuanza kuongea nae,“Kwakweli mama kuna umuhimu wa kuwa na mdada wa kazi humu ndani, wanao tunateseka sana, hebu ona tumetoka shuleni tumechoka na chakula hamna”“Ushaanza uvivu wako Angel”“Sio uvivu mama ila nimesema ukweli, tunachoka sana na masomo”“Haya, hilo swala la mdada wa kazi nalifanyia kazi. Nipe Erica niongee nae kwanza”Basi Angel alimpa Erica simu ambapo aliongea na mama yake ila Angel alimyang’anya simu na kusema imeisha chaji, basi akakata ile simu. Si kweli kwamba iliisha chaji ila alitaka kuwasiliana na Samir tu kwa njia ya ujumbe, hadi wadogo zake wakaamua tena kwenda kujipikia wenyewe.Yani Angel kwa muda huo alikuwa na simu tu basi Samir akamuuliza,“Simu huwa unaiweka wapi ukija shule?”“Huwa naiacha nyumbani”“Naomba njoo nayo?”“Mmmh, nitaitumiaje shule sasa?”“Njoo nayo ili tuwe tunawasiliana hata darasani, kesho njoo nayo”Yani Angel alijikuta akishindwa kukataa kabisa, kwani alihisi asilimia kubwa ya mawazo kwa muda huo yalikuwa juu ya Samir tu.Hata kuamka kula hakujishughulisha kula chakula kilichopikwa na wadogo zake, bali alikunywa chai na mkate na kwenda kulala ila aliwasiliana na Samir hadi analala.Kulipokucha walijiandaa na kwenda shule, ila siku hiyo darasani alikuwa na simu tu chini ya dawati na alikuwa akijibu jumbe za Samir halafu waliangaliana na kutabasamu.Kuna muda mwalimu alikuwepo darasani ila Angel aliinama na kutuma ujumbe kwa Samir, mwalimu akamsogelea Angel na kumuuliza,“Nini unafanya chini ya dawati huko?”“Hamna kitu mwalimu”Basi mwalimu akapenyeza mkono wake chini ya dawati la Angel na kukuta ile simu ambayo Angel aliitumia kutuma jumbe kwa Samir.Kuna muda mwalimu alikuwepo darasani ila Angel aliinama na kutuma ujumbe kwa Samir, mwalimu akamsogelea Angel na kumuuliza,“Nini unafanya chini ya dawati huko?”“Hamna kitu mwalimu”Basi mwalimu akapenyeza mkono wake chini ya dawati la Angel na kukuta ile simu ambayo Angel aliitumia kutuma jumbe kwa Samir.Mwalimu aliichukua ile simu na kumwambia Angel,“Baada ya kipindi uje ofisini kwangu”Kwakweli Angel hakuwa na raha kabisa kiasi kwamba alichofundish mwalimu kwa muda huo hakukielewa kabisa, basi mwalimu alifundisha na kumaliza kisha alimuangalia Angel na kumwambia kuwa afatane nae, yani Angel aliinuka huku akiwa hana amani katika moyo wake.Moja kwa moja walienda kwa yule mwalimu, alikuwa ni mwalimu Harun ambaye alihusika pia na mambo ya nidhamu pale shuleni, walivyofika ofisini alimwambia Angel apige magoti ambapo Angel alifanya hivyo kisha akamwambia,“Umeanza lini tabia ya kuja na simu shuleni Angel? Mama yako anatambua hili?”“Nisamehe mwalimu”“Hivi unatambua kuwa hii ni kesi kubwa sana? Nikiipeleka kwenye uongozi wa shule, jua kabisa huna shule na upo kidato cha nne sasa utakimbilia wapi? Na nikipeleka kwa mama yako, nadhani siku hiyo utataja jina lako la kuzaliwa, kwanini umefanya hivi Angel? Kwanza ulikuwa ukiwasiliana na nani muda wa kipindi?”“Nisamehe mwalimu”“Msamaha wangu ni wewe kumtaja uliyekuwa ukiwasiliana nae darasani muda wa kipindi”“Hakuna mtu mwalimu”“Kwahiyo unadhani nimegundua vipi kama ulikuwa na simu? Wewe mtoto ni mjinga sana, yani unafanya ujinga kama huu shuleni halafu unasemaje? Hivi hujihurumii Angel, upo kidato cha nne na unatakiwa kuwa makini sana, kuzingatia masomo yako ili ufanye vizuri kwenye mtihani wa taifa, ila wewe bila aibu unawasiliana na watu darasani. Ila kwavile umekataa kumtaja uliyekuwa ukiwasiliana nae, basi utapiga magoti hapo hadi kesho”Angel hakuona tatizo la yeye kupiga magoti ila hakuona vyema kumtaja Samir ambaye alikuwa ni mgeni katika shule hiyo, alimuhurumia iwapo angefukuzwa shule, ingekuwaje? Alijikuta akipiga magoti kwa muda mrefu sana hadi akaanza kulia ili mwalimu amsamehe ila mwalimu alikataa na kumtaka ataje aliyekuwa akiwasiliana nae, mara alishangaa kuona mlango wa ofisi ile ukifunguliwa na aliyeingia alikuwa Samir, kwakweli Angel alishtuka na kumuangalia Samir kuwa alitaka kufanya nini, ila alimuona Samir akimfata mwalimu na kumwambia,“Ni mimi ndiye nilikuwa nikiwasiliana na Angel muda wa kipindi darasani”“Hivi una akili wewe kijana? Nadhani ndiomana huna shule unayodumu wewe mjinga, haya Angel inuka hapo na uondoke, mimi nitashughulika na huyu mjinga”Angel akawa akishangaa shangaa tu, yule mwalimu akasema kwa ukali,“Inuka Angel, toka hapa ofisini ila hii simu nitabaki nayo, mimi nitashughulika na huyu kidume sasa”Angel aliinuka na kutoka ila alijihisi vibaya sana, nje ya ofisi kulikuwa na wadogo zake, ndio akagundua kuwa muda wa kutoka ulifika na wadogo zake walienda kumuulizia na kuambiwa kuwa yupo huko kwahiyo walimfata basi alitoka nao na kuondoka nao.Walivyofika nyumbani cha kwanza kabisa walimuuliza,“Kwani dada ilikuwaje leo?”“Aaaah achaneni na habari hizo”“Halafu mbona macho yako yamevimba?”“Nimewaambia achaneni na hizo habari, ngoja nikapumzike”Erick na Erica walitazamana maana dada yao alionekana kuwa alilia na ilionyesha kuwa hana raha maana hata habari ya kupika ili wale hakuwa nayo, ikabidi tu wenyewe wajipangie majukumu na kwenda kubadilisha nguo kwanza halafu kuanza kupika,“Kwahiyo Erick tupike kwanza ndio tukafue nguo, eti eeeh!!”“Tutafua hata kesho bhana, kumbuka kesho ndio Ijumaa”Sawa hakuna tatizo”Basi wakaenda kupika pamoja huku wakielekezana cha kupika na kufurahi tu wakati wanapika, mara simu ya mezani ilikuwa ikiita, moja kwa moja Erica alihisi ni mama yao tu kwahiyo aliikimbilia ile simu na kuipokea kisha akaanza kuongea nayo,“Mama shikamoo, tumekumiss”“Marahaba mwanangu kipenzi, nimewamiss pia. Mnaendeleaje hapo nyumbani lakini?”“Salama kabisa mama, ila dada Angel hayupo salama maana leo tulivyotoka darasani tukaenda kumuangalia kwenye darasa lao ili tuondoke pamoja ila hatukumkuta wala nini, na ndio mkaka mmoja akatuambia kuwa dada yupo ofisini kwa mwalimu wa nidhamu, basi tuliongozana nae na yeye aliingia baada ya muda dada alitoka ila macho yake yalikuwa mekundu sana”“Jamani Angel, kafanyaje tena? Mmemuuliza dada yenu?”“Tumemuuliza ila kakataa kutujibu na kasema anaenda kulala, hapa tunahangaika na kupika, kwakweli mama kuna kila sababu ya kupata msaidizi hapa nyumbani”“Mmmh Erica unaongea sana wewe, kama redio jamani! Huyo msichana wa kazi nitakuja nae, ila nahitaji kuongea na Angel, nimejaribu kupiga simu yake haipatikanbi, hebu kaniitie”“Sawa mama”Erica aliweka simu pembeni na kwenda chumbani kwa Angel kumuita,“Dada Angel, mama amepiga simu anataka kuongea na wewe”“Basi ushamwambia hivyo!!”“Ndio, nimemwambia kuwa hatukukukuta darasani bali ofisini na macho yako yanaonyesha kuwa umelia sana”“Kione vile, umbea tu”Angel aliinuka na kumsukuma mdogo wake kichwa, kisha akatoka nje kuelekea kwenye simu ambayo mama yake alipiga, akamsalimia na kuanza kuongea nae,“Kwanini hupatikani hewani?”“Sijawasha simu mama”“Kwanini wamekukuta ofisini? Na kwanini macho yako yalionyesha kama ulilia?”“Mama, macho yananiuma leo na nilienda ofisini kuchukua dawa, yani mama unamsikiliza Erica? Huyu mtoto ni muongo”“Nitajua tu ukweli wote, bado nasisitiza kuwa kesho narudi. Sasa amka ule chakula, kama mnaona uvivu kupika, basi muagize dereva akawanunulie chakula ila sio kuwaacha wadogo zako na njaa”“Sawa mama”Angel alimaliza kuongea na mama yake na kukata simu kisha akamuita Erica na kuanza kumsema,“Hivi wewe katoto ukoje? Mbona mmbea hivyo? Haya umepata faida gani sasa kumwambia mama? Ipo siku nitakupiga hadi ushangae”Erick akatokea mbele yao na kusema,“Kwenye swala la kumpiga Erica hapo usahau dada, sababu siwezi kuacha umpige Erica nakuangalia”Basi Angel akawasonya na kuondoka zake, maana Angel hakupenda kubishana sana na Erick maana alikuwa ni mrefu kushinda wao kwahiyo mtu pekee aliyemuweza ni Erica tu sababu hakuwa mrefu sana.Basi Erick na Erica walienda kuendelea na kupika.Ijumaa hiyo waliamka asubuhi na kujiandaa kwenda shuleni ila Angel alikuwa na mawazo sana kwani hakujua ni adhabu gani ambayo Samir amepewa baada ya kusema ukweli kuwa ni yeye ndio aliongea nae.Basi walifika shuleni na moja kwa moja Angel alienda darasani, ila alishangaa muda mfupi badae Samir nae aliingia darasani na kwenda kukaa tu akiendelea na masomo kanakwamba hakuna kitu kilichotokea, kwakweli Angel alitamani sana kujua kuwa imekuwaje ila hakujua wala nini.Basi masomo yaliendelea hadi muda wa kutoka darasani wala Samir hakuonekana kujali kitu chochote, basi Angel alitoka ila muda huu aliitwa na mwalimu yule wa nidhamu na kwenda nae ofisini kisha mwalimu akamwambia,“Angel, hili ni onyo la mwisho kwako, kwakweli hii kitu ikijirudia utaona shule ni chungu hii, najua na mama yako angejua basi hata nyumbani kwenu ungepaona pachungu, nakurudishia hii simu ila sitaki kusikia ukiwasiliana tena na Samir, zingatia masomo yako. Tumeelewana?”“Ndio nimekuelewa mwalimu, asante kwa kunisamehe”Kisha mwalimu yule alimkabidhi Angel ile simu ambapo Angel alitoka na kuwafuata wadogo zake ambao walikuwa wakimsubiri na kurudi nao nyumbani.Walipofika kwao siku hii ilikuwa ni ya tofauti sana kwani walikuta mama yao na baba yao wamerudi, walifurahi sana na kuna mdada walitambulishwa pale kuwa ndio atakuwa msaidizi wao wa kazi pale nyumbani,“Wanangu wapenzi, huyu dada anaitwa Vaileth, atakuwa akitusaidia kazi za hapa na pale hapa ndani, naamini atawalea katika maadili niyatakayo”Angel alifurahi sana kusikia hili kwani ndio jambo ambalo alikuwa akililia kwa muda mrefu sana,basi alimwambia mama yake,“Asante sana mama”“Ndio nimeamua kuwafurahisha wanangu”Basi wakainuka ili waende kubadilisha sare zao za shule, ila mama yao alimuita Angel na kumwambia“Angel, lete simu yako”Angel akaitikia na moja kwa moja kwenda chumbani kwake, kisha akaitoa ile simu toka kwenye begi lake la shule na alijua moja kwa moja mama yake anataka akaikague, basi akafuta kila kitu ambacho kiliendelea kwenye simu yake halafu akampelekea mama yake ile simu akitumai baada ya muda mchache angemrudishia ila mama yake hakufanya hivyo wala nini.Muda wa kula chakula cha jioni ulipofika, wote walikaa pamoja na kula huku wakifurahi ila baba yao alisema amechoka sana hivyo akawahi kwenda kulala kwahiyo sebleni alibaki mama na watoto wake akaanza kuongea nao,“Eeeeh niambieni kwanza maisha ya kuishi wenyewe? Najua haijawahi kutokea ila kipindi hiki ilibidi tu wanangu kutokana na majukumu ya hapa na pale, eeeh niambieni”Walikaa kimya kidogo basi mama yao akaanza,“Niambie mwanangu Erica, maisha ya kuishi wenyewe uliyaonaje?”“Mmmh yalikuwa magumu mama”Erick nae akadakia,“Yani mama, usiku tunalala kwa kunywa chai na mikate jamani!”“Kheee Angel, kweli ulikuwa unawalaza wadogo zako kwa chai na mikate!”“Mmmh mama jamani, mimi ni dada yao ndio ila sio kusema kuwa kila jukumu nitaweza maana mimi pia bado mdogo, hebu angalia niende shule, nirudi kupika, niwafulie, nilikuwa nachoka mama”“Mmmh dada jamani, umetufulia mara moja tu”“Na wewe Erick, kwani kufua hamjui hadi mummpe hilo jukumu dada yenu?”“Hapana mama, alisema mwenyewe”Mara simu ya Angel ilianza kuita pale, basi mama yake akaangalia na kukuta jina la mpigaji limetokea Hanifa, akampa Angel na kumwambia aongee nayo, basi Angel akaipokea na kutaka kuondoka pale ili akaongee nayo ila mama yake alimshika mkono na kumwambia,“Kaa hapo uongee nayo”Basi Angel hakuwa na namna zaidi ya kuongea na ile simu mbele ya mama yake,“Jamani Angel, nimekusubiri leo hujatokea kwanini jamani!”“Tulichelewa kutoka shule”“Basi naomba kesho uje, nipo chini ya miguu yako”“Sawa”Angel akakata ile simu kisha mama yake akamuuliza,“Ulikuwa ukiongea nae nini?”“Hanifa hakuja shule leo, alikuwa anauliza tu kama tuliwahi kutoka au la!”“Mbona mwishoni umemjibu sawa!”“Kaniambia Jumatatu nisisahau madaftari nyumbani ili apitie tulichosoma”“Kwahiyo kuna kipindi huwa unasahau daftari au kitu gani?”“Hapana mama, ila kuna masomo huwa sitembei na daftari zake mara kwa mara”“Angel, utaona mama yako nakufatilia sana ila nina maana kubwa sana, badae utashukuru na kuona ni vyema nilikuwa nakufatilia, naielewa dunia hii ilivyoharibika, yani wanaume wakiona mtoto mzuri kama wewe lazima mate yawadondoke, sitaki mjinga yoyote aharibu maisha yako”Angel akawa anamuangalia tu mama yake ingawa kiukweli hakupenda vile ambavyo mama yake alikuwa akimchunga, basi mama yao aliwaangalia Erick na Erica na kuwaambia,“Ninavyomchunga dada yanu ni sawa na nyie, kwanza nadhani sharia za nyumbani kwangu mnazifahamu, sitaki marafiki wa ajabu hapa nyumbani kwangu, yani kabla hujawa na rafiki ni lazima apitie kwangu nimkague kwanza na nimuhoji maswali, kama nitaridhika nae basi atakuwa rafiki yako, vinginevyo sitaki marafiki hapa kwangu. Nahitaji nyie ndio muwe marafiki, jambo likikutaziza, mwambie mwanafamilia hapa akusaidie, mpo watatu mnatosha kabisa”Erica akauliza,“Kwahiyo mama na wakina Junior je?”“Sasa wale ni marafiki? Hebu kuweni na akili, wale ni ndugu zenu, yani hapa ni ndugu tu ujinga ujinga wa kuharibu wanangu siutaki, Erica sitaki marafiki wa ajabu ajabu, halafu sitaki kusikia kuna wanaume huko wanakuchanganya akili, Erick uwe mlinzi wa dada yako, nawe Erick sitaki marafiki wa ajabu, na maswala ya wanawake sitaki kuyasikia, kwahiyo Erica utakuwa mlinzi wa kaka yako. Halafu nyie wawili mtamlinda dada yenu Angel, yani sitaki kusikia ujinga wa aina yoyote ile. Nadhani mnanielewa!”“Tumekuelewa mama”Walijibu kwa pamoja kisha mama yao akawaruhusu kwenda kulala.Kiukweli Angel alienda kulala akiwa na mawazo sana, alijikuta akimfikiria sana Samir na akijiuliza maswali mengi sana,“Hivi mfano Samir akapiga na simu yupo nayo mama itakuwaje? Mmmh hivi mama nae alikuwa anafanywa hivi kama anavyotufanyia sisi jamani!”Basi akajibembeleza pale kitandani na kulala, ila siku hiyo aliota yupo na Samir na wapo sehemu nzuri sana wakifurahi huku Samir akimwambia kuwa anampenda sana, yani ile ilikuwa ni ndoto ya furaha sana kwa Angel na kumfanya akiamka huku akitabasamu na kujiuliza,“Hivi ni kweli Samir ananipenda? Mbona nimewasiliana nae siku zote hajaniambia kuwa ananipenda? Au alitaka tu kuwa rafiki yangu! Na mbona toka lile sekeseke la mimi kukamatwa na simu hajaniongelesha tena? Mmmh hebu mawazo ya kupendwa na Samir yatoke kwenye kichwa change”Kisha akaendelea kulala mpaka kulipokucha.Ilikuwa ni siku ya Jumamosi, na siku hii baba yao aliwaambia wajiandae ili waende kwenye matembezi kwani alitamani sana kwenda kwenye matembezi na watoto wake ukizingatia yeye na mkewe walikuwa safarini, kwahiyo walijiandaa na kutoka pale kwao, mtu pekee waliyemuacha nyumbani alikuwa ni Vaileth, na walimuacha sababu hakuonekana kupenda kutembea.Basi wakiwa kwenye gari, Angel akauliza,“Baba, unatupeleka wapi kwani?”“Tunaenda ufukweni, yani huku mama yenu huwa anapapenda sana ila ni muda mrefu sijawahi kuja nae”Mama yao akauliza,“Kheee kumbe tunaenda ufukweni?”“Ndio, tena ufukwe ule ambao wewe huwa unaupenda sana”Mama yao alionekana kutabasamu kiasi, halafu gari lilienda hadi ufukweni ambapo walishuka na kuchagua sehemu moja na kukaa kama familia, basi Angel akawaomba wazazi wake,“Naomba niende nikachezee chezee maji baba”Na wadogo zake nao wakaomba hivyo hivyo basi baba yao akawaruhusu ila mama yao alitaka kukataa swala lile mpaka baba yao akamwambia,“Acha bhana mke wangu watoto wafurahi leo, ujue tumetaka kuwafurahisha”“Sawa, hakuna shida”Basi Angel na wadogo zake wakainuka na kwenda kuanza kucheza cheza karibu na maji, mule kwenye maji aliona watu walioonyesha wapo karibu yani ni wapenzi wakimwagiana maji na kutoka nje mara wakirushiana mchanga, basi Angel alijikuta akiwaangalia kwa muda mrefu sana hadi mdogo wake Erick alimshtua,“Mmmh dada, mbona unawaangalia sana wale?”“Nawaangalia wanavyopendana, inaonekana wanapendana sana”“Kama baba na mama”Basi Erica akasema,“Weee baba na mama wanapendana zaidi jamani, sijui enzi za ujana wao walikuwaje, na mimi nikija kuolewa basi natamani nimpate mume mwenye upendo kama baba”Basi Erick akamuuliza,“Kwahiyo unataka mumeo aitwe Erick? Maana Erick ni jina la baba!”“Mmmh wewe nawe, sina maana hiyo ila nimesema mwenye upendo”“Na mimi nikioa nataka nipate mke mwenye upendo kama mama”“Sasa ulinipinga nini mimi mwanzoni? Kwahiyo unataka mkeo aitwe Erica? Maana Erica ni jina la mama”Basi Angel akacheka na kusema,“Nyie watoto msinichekeshe jamani, ila twendeni tuwaulize baba na mama kwanini mimi waliniita Angel halafu nyie mkawa Erick na Erica ambayo ni majina yao? Kwanini?”Basi wakatoka eneo lile na kurudi tena kwa wazazi wao ambapo Angel ndio alianza maswali kwa wazazi wao,“Eti mama kwanini mimi mliniita Angel halafu hawa mkawapa majina yenu?”Mama yao alicheka na kumuuliza,“Kwahiyo nawe ulitaka majina yetu?”“Ndio, maana mimi ndio mtoto wa kwanza, nilitakiwa niitwe Erica”Baba yao akacheka sana na kuanza kumjibu Angel.“Wewe umeitwa Angel sababu ulikuja kwenye maisha yetu na kubadili kabisa mfumo mzima wa maisha yetu yani ulikuwa kama malaika kwetu ndiomana tukakuita Angel, sawa mama yangu eeeh!”Angel alitabasamu kusikia vile na alifurahi sana kwani aliona kuwa kapewa heshima kubwa sana, kisha Erica nae akamuuliza baba yao,“Na sisi je baba?”“Kwani na nyie hamjihisi furaha kupata majina ya wazazi wenu? Kipindi tunakuwa watu wengi walidhani mimi na mama yenu ni mapacha, ndiomana tulipowapata ninyi tukaona tuwaite majina yetu, kwahiyo na nyie mnathamani kubwa sana kwetu ndiomana tumewapa majina yetu”Erick na Erica walitazamana huku wakitabasamu na kumuangalia dada yao ambapo nae alitabasamu tu ila kwa muda huo mama yao hata hakuongea chochote kile, kisha baba yao akawaambia warudi kwenye gari ili waende mahali kula chakula cha jioni, nao walifanya hivyo ambapo waliingia kwenye gari na moja kwa moja baba yao alienda hadi hotelini na kila mmoja kuagiza chakula anachokitaka na kuanza kula ila muda kidogo Angel akaomba aende maliwatoni ambapo mama yake alimruhusu.Angel akiwa anataka kuingia maliwatoni akashangaa akishikwa bega, kugeuka akashangaa kumuona James yule ndugu wa Hanifa na kuanza kusalimiana nae,“Umenikumbuka Angel?”“Mmmh nakukumbuka ndio ila jina lako limenitoka”“Mimi ni James, yule ndugu wa Hanifa, nimefurahi sana kukuona. Tafadhari naomba namba yako ya simu”Angel akafikiria kidogo na kushindwa kujibu kwani simu ilishachukuliwa na mama yake, basi akamwambia,“Mimi sina simu”“Mmmh mbona Hanifa uliwasiliana nae kwenye simu?”“Ndio ila imeharibika”“Usinifanyie hivyo Angel”Basi James akamshika Angel mkono, kwakweli Angel alishtuka kidogo kwani hakuwa na mazoea ya kushikana mikono na mwanaume ambaye si ndugu yake kama hivyo, mara mama yake akatokea na Angel kuutoa mkono wake kwa James huku akiwa na wasiwasi, kisha mama yake akamuuliza,“Wewe Angel, ndio chooni hapo?”Basi James akataka kuondoka ila mama Angel alimzuia na kumuuliza Angel,“Niambie huyu ni nani?”“Huyu ni ndugu wa Hanifa”“Aaaah kumbe mnapigiana simu na Hanifa sababu ya huyu!!”“Hapana mama”Kisha mama Angel alimuangalia James na kumuuliza,“Unaitwa nani na ulikuwa na agenda gani na Angel?”“Naitwa James, nilikuwa namsalimia tu”Huyu mama alitema mate pembeni na kumwambia James,“Ondoka mbele ya macho yangu, unanichefua. Hivi wewe Angel akili yako ikoje hiyo, mbona kuwaza ujinga kiasi hiko! Huyu James atakupa nini ambacho mimi na baba yako tumeshindwa kukupatia? Kwakweli sijapenda, haya nenda chooni nakungoja mlangoni”Basi Angel akaingia chooni na baada ya muda alitoka na kuondoka na mama yake ambapo mama yake alikuwa akimlalamikia njia yote,“Sasa nisikilize kwa makini, sitaki kusikia habari za James, sitaki kusikia kuhusu Hanifa sitaki kitu chochote. Mbona unataka kunitia aibu jamani Angel loh!”Walirudi mezani na mama yao aliwataka kufunga chakula na kwenda kula nyumbani, sema sababu mumewe alikuwa akimsikiliza sana kwahiyo alikubali na muda huo huo kuamua kuondoka pale hotelini.Siku hiyo usiku watoto wa familia hii waliambiwa kuwa wawahi kulala ili kesho yake wawahi ibadani, basi mama yao akawaambia kuwa kesho wawahi kuamka kwaajili ya kwenda Kanisani basi kila mmoja alienda kulala ambapo Angel alilala hoi kabisa ila Erica alijihisi kutokuwa na usingizi kabisa kwa wakati huo basi alikaa tu chumbani kwake mara Erick nae akaenda chumbani kwa dadake na kuanza kuongea nae,“Yani mama katufukuza mapema sana kulala, mimi sina hata usingizi”“Hata mimi sina usingizi jamani”“Sasa tufanye nini?”“Tucheze karata”“Kheee karata umezipata wapi?”“Usiulize, ngoja nizitoe tucheze”Basi Erica akatoa karata kisha yeye na kaka yake wakaanza kucheza karata yani walicheza karata hadi usiku sana bila kugundua ni usiku sana, mara mama yao alienda chumbani na kuwashtua,“Yani nimepita hapa na kushangaa taa inawaka, nikajiuliza huyu Erica hajalala au kasahau kuzima taa au anaogopa, kumbe mnacheza karata nyie wajinga, mnajua saa ngapi saa hizi?”“Tusamehe mama”“Tusamehe mama ndio nini, haya Erick inuka nenda chumbani kwako na ulale nakuja kukuangalia muda sio mrefu na wewe Erica lala muda huu sitaki ujinga wa kucheza karata usiku’Wote walifanya vile ambavyo mama yao alisema kisha mama yao akazima taa na yeye kwenda chumbani kwake kulala huku akilalamika tu.Kulipokucha, mama yao aliamka mapema kabisa na kwenda kuwaamsha watoto wake, kiukweli Erick na Erica walikuwa na usingizi sana ila mama yao aliwaambia wajiandae na kwenda ibadani, basi Erick akasema,“Mama, naomba mimi niende mchana”“Mjinga wewe, niliwatuma kucheza karata usiku eeeh!”Pale Angel akasikia habari za wadogo zake kucheza karata ila hakusema neno lolote zaidi zaidi alienda kujiandaa kisha wote watatu wakaondoka na dereva wao sababu wazazi wao walienda na usafiri mwingine.Walipotoka Kanisani, Erick na Erica walikaa siti ya nyuma na walikuwa wamesinzia huku siti ya mbele akiwa amekaa dereva na Angel, basi dereva akamwambia Angel,“Yani umependeza leo Angel balaa, kama malaika vile. Asubuhi nilishindwa kukusifia ila kiukweli Angel wewe ni mzuri sana”“Ushaanza maneno yako, mimi ni mzuri ndio na najitambua kwahiyo sitaki porojo zako”“Porojo zangu kivipi? Kwakweli Angel unaonyesha mtamu kama jina lako”“Ila nahisi wewe huipendi hii kazi, unajua siku nikimwambia baba au mama yani wewe ndio basi tena kwenye hii kazi! Sitaki ujinga”“Basi Angel, ila kiukweli nakupenda sana. Katika maisha yangu sijawahi kuona mwanamke mrembo kama wewe”Angel alikaa kimya ila muda huo Erica alishtuka na kusema,“Kheee dada huko si ndio kutongoza, yani anko Ayubu anakutongoza naenda kusema kwa mama”“Hivi wewe Erica una nini lakini? Unajua kutongoza wewe?”“Mama alisema mtu akikutongoza basi umwambie, ila mbona wewe hutaki kusema kuhusu anko Ayubu? Mimi nitasema”Yule dereva aliona aibu kiasi kwamba hakutaka hata kuongea ila alijua ni namna gani Angel anaweza kuongea na wadogo zake.Walivyofika nyumbani, Angel akatoka na kumvuta pembeni Erica na kuanza kuongea nae,“Wewe mtoto, huo mdomo wako uufunge. Ni kweli kanitongoza ila kumbuka yule anko ana familia yake, tukimsemea tu kwa wazazi wetu lazima atafukuzwa kazi, tunatakiwa kuwa na huruma, yule anajisemea tu ila usiende kusema kwa mama”“Mmmh ila sijui”“Halafu wewe unataka kusema ya watu tu, haya na karata mlizokuwa mnacheza mlizitoa wapi? Nimwambie mama akuulize, unafikiri sikuona wakati ukipewa hizo karata?”“Basi dada yaishe”Basi wakaingia ndani na mama yao akaingia na muda huo huo alimuita Angel na kuanza kuongea nae,“Wewe Angel una ajenda gani na huyo Hanifa? Maana amepiga sana simu, una ajenda gani?”“Hakuna kitu mama, labda alitaka kuniambia kuhusu kesho shuleni”“Aaaah eeeh! Ngoja tumpigie na niweke sauti kubwa ili nisikie mazungumzo yenu”Mara simu ya Angel ilianza kuita pale pale basi mama yake akaichukua na kuiangalia akakuta mpigaji ni Samir, yani mama Angel alipoona hili jina alichukia na kukunja sura kabisa.Mara simu ya Angel ilianza kuita pale pale basi mama yake akaichukua na kuiangalia akakuta mpigaji ni Samir, yani mama Angel alipoona hili jina alichukia na kukunja sura kabisa.Kisha akamuangalia angel na kumuuliza kwa ukali,“Samir ndio nani? Unamahusiano nae yapi na kwanini amekupigia simu?”kisha mama Angel aliipokea ile simu na kuweka sauti kubwa kisha kumpa Angel kuongea nayo ile simu, kwakweli Angel aliongea nayo kwa uoga sana,“Hallow”“Mbona sauti yako inatetemeka hivyo Angel?”Angel alikuwa kimya tu kwani alishindwa kusema lolote sababu ya mama yake kisha Samir aliendelea kuongea,“Au umechukia sababu sikukuongelesha tena! Nilifanya vile sababu ya yule mwalimu, halafu nahisi anakutaka yule, sikutaka aone tukiwasiliana tena, ila nikwambie kitu Angel?”Angel akakata ile simu kwani alijua mada itakayoendelea pale haitomfurahisha mama yake hata kidogo, ila mama yake alikuwa makini sana kumuangalia kisha akamwambia,“Mbona umekata? Angel naomba uniambie kila kitu kinachoendelea juu ya huyo Samir kabla sijaenda shuleni kwenu, nieleze kila jambo”Angel alikaa kimya tu bila ya kusema chochote kisha mama yake akamwambia tena kwa ukali,“Unanyamaza kimya una maana gani? Umeanza kiburi Angel eeeh! Yani unaongea na mwanaume hapo mbele ya macho yangu halafu unanikalia kimya? Najua unanijua nilivyo, sijali umekuwa kwasasa, naweza kukubutua hapo hadi ukasahau njia ya chumbani kwako”Mara Erick akatokea na kumwambia mama yao,“Mama, unaitwa na baba”Basi akainuka na kumuacha Angel pale sebleni kisha yeye akaenda kuongea na mume wake.Mama Angel alifika chumbani na kumkuta mumewe ameshika kitabu tu na kuanza kuongea nae,“Nimeitikia wito”“Nimekuita ili tukae wote kidogo, mke wangu hayo malezi yako kwa watoto kwakweli sio malezi”“Kivipi?”“Nimekuangalia pale wakati ukiongea na Angel, yani mtoto hadi kakosa amani kabisa, hivi unafikiri kwa hali ile utawezaje kuongea na mtoto?”“Sikia baba Angel nikwambie, yani mimi sitaki watoto wapiti njia mbaya, au wapiti maisha niliyopitia mimi”“Kwahiyo wewe umepitia maisha mabaya? Hebu mkumbuke mama yako, alikuwa mkali sana ila je alikuwa mkali kama wewe kwa watoto? Umezidisha mke wangu jamani kwakweli sijapenda”“Najua umeumia moyo sababu namsema Angel”“Hata kama, yani hata ungemsema Erick au Erica kwa stahili hiyo lazima ningeumia, hebu kaa vizuri na mtoto umsikilize anasumbuliwa na kitu gani sio kumfokea kiasi kile, unamtisha mtoto kwakweli”“Ila mume wangu mtoto akiharibikiwa yule, aibu kwa nani?”“Sasa ukifanya ukali ndio utamuokoa asiharibikiwe? Hebu kuwa kama rafiki yake na umuulize kwa utaratibu akujibu”“Sawa nimekuelewa mume wangu, ngoja nifanye hivyo ingawa nina hasira sana”Basi mama Angel alitoka na kurudi tena sebleni ambapo Angel alikuwa amekaa pale pale kwani hata kuinuka alishindwa sababu ya uoga wa maneno ya mama yake, basi mama yake akaanza kumwambia,“Angel mwanangu, mama anatakiwa kuwa mzazi, mlezi na rafiki wa milele. Usimfiche mama kitu chochote kile kinachokusibu katika maisha, usimdanganye mama jambo lolote lile, sema ukweli ili upone mwanangu. Samir ni nani? Na kwanini anakupigia simu? Na huyo mwalimu imekuwaje?”Angel hakuwa na namna nyingine zaidi ya kumueleza mama yake ukweli kwani alijua hata angeficha basi mama yake angefukunyua hadi ukweli aujue maana mama yake alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo, basi akaanza kumueleza,“Mama naomba unisamehe, Samir ni mwanafunzi mwenzangu nasoma nae, nilimpa namba ya simu na nilikuwa nikiwasiliana nae, kuna siku nilijisahau nikaenda na simu shuleni ndio mwalimu Harun akanikamata nayo ila kanirudishia ndio hiyo hapo, naomba unisamehe mama”“Kwahiyo Samir kakutongoza eeeh!”“Hapana mama, hajawahi kunitongoza wala kuniambia habari za mapenzi”“Una uhakika huyo Samir hajawahi kukutongoza?”Mara Erica akaenda pale na kusema,“Dada mwambie ukweli mama kuwa anko Ayubu kakutongoza”Mama yao akashtuka na kuuliza kwa makini,“Inamaana na Ayubu kakutongoza?”Kwakweli Angel hakuweza kuficha zaidi na kuamua kusema ukweli tu kisha mama yake akamwambia kuwa akabadili nguo na aweze kula maana alianza kumbana hata kabla hajapumzika kwa siku hiyo.Kisha mama yake aliinuka moja kwa moja kwenda kwa mumewe na kumueleza kile alichogundua,“Unaona mume wangu, kumbe na Ayubu nae yupo katika harakati za kutaka kutuharibia mtoto”“Kivipi?”Basi akamueleza aliyoambiwa na watoto wake na pale pale mumewe akachukua hatua nae maana hakupenda kusikia kuna ujinga unataka kutendeka kwa watoto wake ingawa hakuwa mkali kwa wanae, akachukua simu yake na kumpigia Ayubu,“Uje nyumbani uandike ni kiasi gani unatudai kisha uache gari yetu maana kazi tena basi”“Kwani nimefanyaje mzee?”“Ukija utatambua hilo”Kisha ile simu na kumwambia mkewe,“Hili la Ayubu nitashughulikia, usijali mke wangu”Basi mkewe alifurahi sana kwani alikuwa akipenda vile ambavyo alishirikiana na mumewe kwa kila kitu.Erica aligundua kuwa dada yake amechukia kwa kitendo chake cha kusema kuhusu dereva wao, akaamua kwenda kumuomba msamaha,“Nisamehe dada, nilipitiwa tu kusema vile”“Ulipitiwa wapi? Umbea tu, kione vile, toka zako hapa”Erica akatoka ila alinyong’onyea sana kwani hakupenda kumkwaza dada yake, basi Erick akamfata na kumuuliza kilichomfanya apooze,“Si nilimwambia mama ukweli kuwa anko Ayubu alikuwa akimtongoza dada Angel”“Eeeh Erica, hebu niambie kutongoza unaanzaje?”“Mimi sijui”“Kama hujui umejuaje kama anko Ayubu alikuwa akimtongoza dada Angel?”“Sijui, mimi nilikuwa namsikia tu anamsifia basi”“Kumbe kusifia ndio kutongoza, na ukishatongoza ndio inakuwaje?”“Sitaki hayo maswali Erick, kamuulize mama”“Basi, nilikuwa nakuchangamsha akili tu. Twende tukacheze tena karata”Basi wakaenda chumbani kwa Erica na kuanza kucheza tena karata, walicheza sana karata hata jioni iliwakutia mule mule chumbani wakicheza karata ila Erick alijihisi kuchoka na kuanza kusinzia basi akajiegesha kwenye kitanda cha dada yake na kujilaza pale, naye Erica kuona Erick amelala basi akajikuta nae akilala hoi kabisa.Mama yao ndio alienda kuwakurupua wakati wa chakula cha usiku, alikuta wamelala hoi kabisa, alitikisa kichwa na kuziona zile karata pembeni, na kusema,“Yani walikuwa wakicheza karata tena, jamani hawa watoto aah”Akaanza kuwatingisha ambapo waliamka na kuanza kujinyoosha, kisha mama yao alianza kuwasema,“Hivi nyie hizi karata ndio kila kitu kwenu, mnajisahau mnacheza karata na kulala hapahapa, kwakweli sijapenda na kuwahakikishia kuwa sijapenda naenda kuchoma hizi karata”Erica akakurupuka vizuri sasa na kumsihi mama yake asiende kuchoma zile karata,“Tena msinikere, nendeni mkale, hizi karata naenda kuzichoma”Kisha mama yao akatoka na zile karata, kiukweli Erica alitoka chumbani ila toka mama yao azichukue zile karata alikosa raha kabisa na kujikuta akiwa na mawazo sana hadi wanamaliza kula na kwenda kulala tena bado alikuwa na mawazo.Leo kama kawaida Angel na wadogo zake walikuwa wameenda shule, basi Erica akiwa darasani pamoja na kaka yake Erick, alifatwa pembeni na mwanafunzi mwenzao na kuanza kuongea nae,“Erica, ziwapi karata zangu?”“Mmmh nimezisahau nyumbani”“Ila kumbuka ulisema leo utazileta?”“Ndio, ila nimezisahau. Samahani”Erick aliingilia yale mazungumzo kwani hakupenda yule aongee na dada yake, na vile alipojua kuwa dada yake alipewa karata na huyo akajikuta akichukia sana, alimwambia“Erica asikuongopee, hajasahau karata wala nini bali mama amezichoma moto”Erica alimuangalia kwa hasira kaka yake kwani hakupenda wala nini ila yule mwanafunzi alimuangalia Erica na kumwambia,“Usijali kuhusu hilo Erica, nitakuletea karata zingine”Erick akachukia na kumuangalia kwa hasira yule mwanafunzi na kumwambia,“Hivi wewe una nini lakini? Yani ndio kwanza shule tumeanza, ila una mambo ya ajabu kichizi”“Sijasema kwa ubaya, usitake kuniletea kama mambo ya siku ile ya kupigana, hapana mimi nilikuwa naongea na Erica tu”Kisha yule mwanafunzi akainuka na kwenda kukaa sehemu nyingine, basi Erica akamwambia kaka yake,“Na nitaenda kuongea na mwalimu atuhamishe madarasa yani wewe sijui ukoje”“Ndio kamwambie, na nikirudi nyumbani leo na mimi namwambia mama kuwa zile karata ulizitoa kwa Abdi”Erica alikaa kimya na kumuangalia kaka yake, muda wa mapumziko Erica alienda kumtafuta dada yake na kumueleza ambayo huwa yanatokea darasani,“Kweli wewe na Erick inatakiwa msome madarasa tofauti, yule nae sijui vipi! Hataki mashemeji au?”“Mashemeji? Wa nini dada?”“Aaaah na wewe nawe, ngoja nikaongee na mwalimu awaweke madarasa tofauti’Basi Angel akamuaga Erica pale na moja kwa moja alienda kuongea na mwalimu wa taaluma sababu ndiye aliyekuwa akipatana nae sana kuliko walimu wote katika shule yao.Basi alienda kuongea nae kisha mwalimu akamwambia,“Ni jambo jema ulilosema ila nadhani kama na kidato cha nne tungekuwa na madarasa mawili basi wewe na Samir tungewatenganisha”“Ila mwalimu Samir sio ndugu yangu”“Ni kweli, sasa madhara ya mdogo wako Erick na Erica hayawezi fikia madhara ambayo wewe utakumbana nayo kwa Samir, unajua mara nyingine walimu tunaonekana kama tunapiga kelele ila huwa tunaona mbali sana, Angel natamani siku moja nikuone katika maisha mazuri, yani umesoma kwa bidii, umepata kazi nzuri na unaishi vizuri, na mwisho wa siku uolewe na kufurahia maisha ya ndoa ili uheshimike ila sio kuruka ruka na wakina Samir, kwanza huyo Samir atakudanganya tu na kuichanganya akili yako maana hatokuja kukuoa wala nini, watu wazima tunapoongea inapaswa tusikilizwe, natumaini umenielewa”“Nimekuelewa mwalimu”“Sikutaka maisha ya shule yawe magumu kwako, sikutaka kukufanyia jambo baya hata uchukie shule ndiomana sikuita mzazi wako kwaajili ya swala la wewe kuja na simu shuleni. Angel hujawahi kuja na simu shule ila nina uhakika ni yule Samir ndio kakushawishi, sasa kwa usalama wako Angel kaa mbali na Samir na utaweza muendelea mbele na kuona mafanikio ya maisha yako kwa ujumla.”Angel alimuitikia mwalimu kisha akaamua kurudi darasani ili kumalizia vipindi na muda wa kutoka ufike arudi zake nyumbani.Leo walipotoka shule, wadogo zake walimfata kuondoka ila ilionekana kuwa wamenuniana maana hakuna aliyeonekana kumuongelesha mwenzie, basi aliongozana nao hadi nyumbani kwao na kumuuliza Erica,“Mbona inaonekana huongei na Erick?”“Kachukia eti mimi na yeye kutengwa madarasa”“Aaaah achana nae, mwache avimbe apasuke, kwani kutengwa madarasa ndio nini? Mwache achukie”Basi wakaingia ndani ambapo Erick alishaingia mud asana, basi walipoingia walimkuta yule dada yao wa kazi na kuuliza kuhusu mama yao alipo,“Kaniaga kasema anaenda kwa dada yake, ila na nyie kwani mama yenu ni mtu wa kushinda nyumbani?”“Yani mama akiwa ametoka ujue kuna mambo muhimu anafatilia, na huwa tusipomkuta ni mlinzi anakuwa ameachiwa maagizo ila leo hajatuambia kitu ndiomana tukakuuliza”“Kwahiyo mama yenu huwa anashinda nyumbani?”“Hapana, ila kazi anayoifanya sio ya kufanya tusiwe nae kwa muda mrefu”“Aaaah sawa, chakula kipo tayari”“Asante”Walienda kubadilisha nguo na kwenda kula ila Erick hakuonekana kwenda kula kabisa, basi Angel alianza kusema,“Yani Erick kasusa hadi kula, jamani hii tabia sijui kaitoa wapi huyu kiumbe?”Erica alijihisi vibaya na kutaka kuinuka kwenda kuongea nae ila dada yake alimshika nguo na kumkalisha kisha akamwambia,“Sasa unataka kwenda wapi na wewe? Si ni yeye ndio kagoma kula? Achana nae, mtu mwenyewe ana njaa ya kufa yule, atakuja mwenyewe, hebu tujilie sie, mamake akirudi ataenda kumbembeleza”Angel aliendelea kula ila Erica hakuonekana na furaha tena, akavizia dadake akiwa makini na chakula akainuka na kuelekea moja kwa moja chumbani kwa Erick.Erica alifungua mlango na kukuta Erick kajilaza tu, basi akaenda karibu yake na kumuamsha,“Erick twende ukale”Erick aliinuka na kumuangalia Erica kisha akamwambia,“Kwanini umenifanyia vile?”“Kwani nimefanyaje? Nisamehe Erick”“Yani kweli Erica unaonekana kufurahi mpaka jino la mwisho kisa nimehamishwa darasa?”“Nisamehe jamani”“Ngoja baba arudi, kwakweli na shule ile nitahama maana naona hupendi kuona nikisoma pale”“Jamani Erick usiwe hivyo kaka yangu, nisamehe tafadhali, naomba twende ukale”Basi Erica akatumia muda mrefu sana kumbembeleza Erick ili ainuke na aweze kwenda kula, mwishowe Erick alikubali ila kishingo upande kwani bado alikuwa na kinyongo sana ukizingatia hakupenda jinsi dadake alivyomcheka wakati anahamishwa darasa.Basi Erick alienda kula ila alipomaliza tu alirudi chumbani kwake yani hata hakutaka kufanya mazungumzo kama siku zote anavyofanyagaBasi kila mmoja mule ndani kwao aliendelea na mambo yake ila siku hiyo baba yao aliwahi kurudi nyumbani na Erick alienda kuongea na baba yao,“Baba, naomba unihamishe shule”“Kwanini unataka kuhama shule? Mbona ile shule ni nzuri sana mwanangu?”“Baba, ili mtu usome ni lazima uridhike na mazingira ya shule, wanafunzi na kila kitu kinachokuzunguka. Kwa mimi kama nitaendelea kusoma pale lazima nitafeli baba, nakuomba unihamishe”“Kwahiyo Erica nae nimuhamishe?”“Hapana, mimi nimejisemea mimi kama mimi, naona Eria amepapenda pale”“Sawa mwanangu usijali, ngoja tu wiki hii ipite na nitakupa jibu”Kwakweli Erick alifurahi sana kwani alijua kama ataendelea kusoma shule moja na dada yake basi itakuwa ni tatizo kwake maana atagombana na kila mtu.Mama yao alirudi usiku na kukuta wanae wapo sebleni wakiangalia Tv basi akawasalimia pale na kuanza kuongea nao,“Jamani Junior atakuja kusoma nanyi pale shuleni, kwahiyo Angel unapata nduguyo darasani”“Khee mama, Junior si yupo kidato cha nne, atapataje uhamisho?”“Atapata tu, mamake ashaongea na mwalimu wenu kwahiyo subiri tu utamuona shuleni Angel”“Haya mama”Basi mama yao akainuka na kwenda chumbani kuongea na mume wake, ambapo alimpa taarifa ya Junior ambaye ni mtoto wa dada yake kwenda kusoma shule moja na Angel, basi mumewe alimuuliza,“Na kwanini anamuhamisha shule aliyokuwa akisoma?”“Mmmh yule mtoto ni pasua kichwa mume wangu, yani sijui kachukua tabia za babake, pale kashahamishwa shule hadi dada yangu anahisi kuumia kichwa sababu ya yule mtoto”“Ila yule mtoto nae balaa, kumbe hajabadilika tu!!”“Hajabadilika ndio, yani ndio kwanza amepamba moto, kwakweli dada yangu pale ana kazi. Ndiomana nimemwambia ampeleke shule anayosoma Angel ili Angel amuangaliage”“Mmmh nawe mke wangu mambo mengine unayataka, yani huyo junior ndio aangaliwe na Angel kweli? Katoto kenyewe kale kameanza tabia chafu siku nyingi jamani, huoni kama ukikaweka karibu na Angel kataanza kumnyemelea?”“Mmmh jamani mume wangu, ndugu yetu yule ujue, mimi na mama yake tumezaliwa tumbo moja jamani! Inawezekana vipi hiyo?”“Hapana ila Junior ana tabia chafu bhana, labda umkanye kwanza na huyo Angel umkanye pia maana mmh!”“Unataka kusema nini sasa? Inamaana Angel nae muhuni?”“Sina maana hiyo mke wangu, hata usipaniki”Basi wakaongea ongea pale na kuendelea na mambo mengine ila mumewe hakumueleza habari za Erick kutaka kuhama shule kwani alijua ni lazima mke wake angepinga tu.Usiku wa leo Erica alienda chumbani kwa dada yake na kumueleza kuhusu maamuzi ya Erick baada ya kwenda kumbembeleza kula mchana,“Achana nae huyo, unafikiri mama anaweza kumuhamisha shule? Yani asahau kabisa hilo swala”“Anasema eti sisi hatupendi kusoma nae shule moja”“Muache aahame mdogo wangu kwanza hatupunguzii kitu, kumbuka Junior nae anahamia pale shuleni kwahiyo kuhama kwake wala hakuleti tatizo. Ila pia kumbuka mama hawezi kumkubalia upuuzi wake huo”Basi erica aliongea na dada yake siku hiyo na kuamua kulala pamoja nae hadi kulipokucha ambapo waliamka na kwenda kujiandaa kwaajili ya kwenda shuleni.Njiani Erick alimwambia Erica,“Kwahiyo ukaamua kuhama na chumba chako kwasababu nimekwambia nahama shule!”“Kheee mimi sijahama chumba changu, ila jana nililala kwa dada”Wakaachana na kila mmoja kuingia kwenye darasa lake.Leo Angel alifurahi sana kwani alimkuta Hanifa akiwa amefika shule, kwahiyo alimkumbatia na kumkaribisha ambapo Hanifa alianza kumpa lawama,“Tabia mbaya hiyo Angel, yani mimi nimekusubiria hujatokea jamani”“Oooh nisamehe, halafu simu kaichukua mama yani siwezi kuwasiliana na yeyote”“Mmmh mama yako nae anakuchunga utafikiri kitu gani jamani, nina uhakika hata hufurahii maisha Angel, kwenu kuzuri, wazazi wako wana pesa ila hauna uhuru, katika maisha hakuna kitu bora kama uhuru yani yote hayana maana ila uhuru ndio una maana kubwa katika maisha”“Sasa nitafanyaje na mama hataki?”“Sikia, Ijumaa tukitoka naomba twende pale dukani kwenu”“Kwani naenda kufanya nini jamani!”“Kun jambo la muhimu sana huko, hata leo tungeenda ila ni vizuri twende Ijumaa. Tuwahi kutoka shule halafu twende yani utafurahi nakwambia”“Sawa, hakuna shida”“Halafu Angel, kuna sura ngeni nimeiona humu darasani, yule kaka ni mgeni?”“Ndio, anaitwa Samir”“Oooh basi atakuwa wangu”“Mmmh na wewe Hanifa jamani”“Ndio, unataka awe wako jamani! Angel kuwa na huruma na wenzio, kila mkaka anakupenda wewe, je sisi tupendwe na nani jamani? Kisa wewe ni mzuri? Hivi unadhani wanakupenda kweli? Hamna lolote, wakaka kama hao huwa wanapenda wadada kama sisi”Angel akaguna tu, kisha akaingia mwalimu wa kipindi na baada ya muda aliwaachia kazi na kutoka, ambapo alimuita Hanifa ofisini sababu hakuonekana shule kwa siku zote, basi Hanifa alivyoondoka ndipo Yusra aliposogea kwa Angel na kumwambia,“Mimi huyu Hanifa simpendi jamani yani simpendi kabisa”“Kwanini?”“Anajishauwa sana”“Wakati kuna watu humu darasani hawanipendi hata mimi jamani! Ndiomana nikaanza kuwa na urafiki na Hanifa maana humu darasani wadada hawataki kuongea na mimi zaidi yako na Hanifa halafu wewe na Hanifa hampatani jamani!”“Humu darasani ni wivu tu, wanakuonea wivu sana Angel, na vile wengi wana kusifia basi wao wanaumia sana kwenye roho zao ila usijali mimi nipo, sema huyu Hanifa simpendi”“Ila kwanini humpendi?”“Anajishauwa, inaonyesha sio rafiki mzuri wala nini”Angel akacheka tu ila alijua ugomvi wa hanifa na Yusra ulisababishwa na nini na aliwahi kuelezewa na hanifa kwahiyo alibaki kucheka tu.Basi wakaendelea na ile kazi ya mwalimu waliyopewa.Wakati Angel amekaa darasani alishangaa kuona hanifa akitoka ofisini na moja kwa moja kwenda kwenye dawati alilokaa Samir, kwa mara ya kwanza Angel alijihisi kuwa na wivu juu ya Samir na moyo ulimuuma sana, basi akamngoja Hanifa amalize mazungumzo yake halafu Hanifa alirudi kukaa na Angel na muda ule ule Angel alimuuliza Hanifa,“Ulikuwa unaongea nini na yule mkaka?”“Nilikuwa namwambia ukweli kuwa yeye ni mzuri sana na nimemuomba namba yake ya simu, amenipa kwahiyo nitakuwa nikiwasiliana nae. Ila nimemkuta yupo busy sana sijui hata anaandika vitu gani jamani!”“Kwanini umefanya hivyo Hanifa?”“Kivipi?”“Sikia Hanifa, sijawahi kujihisi hivi kabla juu ya mwanaume yoyote ila ulivyokaa na Samir roho imeniuma sana”Hanifa alianza kucheka yani alicheka sana kisha akamwambia Angel,“Na ushamba huo wa mapenzi ulionao unataka kujitwika gunia la kumpenda huyo Samir wakati anaonekana macho juu juu kweli, Angel rafiki yangu tulia kuna watu wenye wadhifa wao wanaokupenda na watakufanya ufurahie maisha sio hao wakina Samir, ingia kichwa kichwa kwenye mapenzi na urudi kwenu na mimba ya Samir sijui utamueleza nini mama yako na alivyo makali vile, kwa hakika atakufanya supu wewe na kitoto chako. Kuwa makini Angel”“Mmmh!”“Usigune, hao wakina Samir tuachie sisi tulioshindikana ndio tunawaweza, unaweza kuona kama najipigia debe ila nakuonea huruma, ungekuwa ni binti machepele ningekwambia sawa Samir anakufaa ila Angel umetulia jamani hadi vibaya kupata mtu wa kukusumbua akili, mimi nahitaji upate mwanaume mwenye hadhi yake yani ambaye akikupata tu basi tunakula pilau la harusi yenu sio huyo Samir”Angel akamuangalia Hanifa kw amuda huo bila ya kumjibu chochote kisha wakaendelea na masomo hadi muda wa kutoka.Wakati wa kutoka ulipofika, basi Angel akabeba begi lake kwaajili ya kuondoka ila alivyofika nje akavutwa kidogo kwa nyuma, kuangalia akaona ni Samir amemvuta huku akitabasamu. Basi Angel alisimama na kumuangalia, basi Samir akamwambia,“Najua hatuwezi kuongea vizuri hapa kwani kila jicho lipo juu yako, ila nina ujumbe wako”Samir alitoa karatasi iliyokunjwa vizuri na kumkabidhi Angel, kisha Angel alichukua karatasi ile na kuiweka kwenye mfuko wa sketi yake ya shule basi akaondoka na kurudi nyumbani kwao akiwa na wadogo zake.Walipofika tu nyumbani mama yao akawaambia,“Haya nendeni kavueni sare zenu mlete niwafulie”Nao wakafanya hivyo kisha mama yao akazikusanya na kwenda kuzifua, sasa Angel akakumbuka kitu, yani akakumbuka ujumbe ambao alipewa na Samir akaona ni tatizo basi akaenda haraka haraka ambapo mama yake alikuwa akifua, akashtuka kwani alimkuta mama yake ndio kashika lile karatasi akilisoma.Kwakweli Angel alishtuka sana na akatamani kurudi nyuma ila mama yake alimuona na kumuita,“Angel hebu njoo haraka, kwakweli huyu Samir hapana jamani nahitaji kumfahamu”Angel akamuangalia tu mama yake bila kusema chochote kwani hata kilichoandikwa kwenye karatasi hakujua ni kitu gani.Kwakweli Angel alishtuka sana na akatamani kurudi nyuma ila mama yake alimuona na kumuita,“Angel hebu njoo haraka, kwakweli huyu Samir hapana jamani nahitaji kumfahamu”Angel akamuangalia tu mama yake bila kusema chochote kwani hata kilichoandikwa kwenye karatasi hakujua ni kitu gani.Mama yake akamwambia tena,“Njoo Angel nimekuita”Basi Angel akamsogelea mama yake huku akitetemeka kisha mama yake akamuuliza,“Umeisoma hii karatasi uliyopewa na Samir? Niambie ukweli mwanangu”“Hapana mama sijaisoma”“Haya nenda kaendelee na mambo yako”Angel alishindwa hata kumwambia mama yake ampe ile karatasi ili na yeye aweze kusoma zaidi zaidi aliondoka huku akiwa kanyong’onyea.Mama Angel alifua nguo za wanae huku akisikitika sana kuhusu Samir na ile karatasi aliitunza vizuri sana.Usiku baada ya kula chakula mama Angel alienda kuongea na mumewe ambapo kwanza alimpa lile karatasi lenye ujumbe aweze kusoma, kwakweli mume wake nae alitikisa kichwa na kuuliza,“Huyu kijana ndio nani?”“Ndio huyo Samir ambaye Jumapili ile ndio alimpigia simu Angel na nikaanza kumfokea Angel”“kwahiyo hii karatasi umekuta ndio Angel anaisoma?”“Kwa bahati hajaisoma yani nimeikuta kwenye sketi yake ya shule, yani kama Mungu tu nikawaambia leteni sare zenu nifue ndio nakutana na ujumbe wa namna hii”“Sasa mke wangu unajua cha kufanya?”“Nifanye nini hapo unadhani?”“Unafikiri kwa maneno ya huyu kijana Angel anaweza kuchomoka? Hapa Angel hachomoki yani kujana anajua kutongoza hatari, ana maneno yaliyoenda shule, nimemvulia kofia”“Mmmh kama wewe kipindi kile unanifatilia”Baba Angel akacheka na kuendelea kusema,“Sasa cha kufanya kaa chini na Angel, zungumza nae, mueleze kuhusu mambo ya vijana na mbinu zao, mimi nikipata muda nitazungumza nae pia, mueleze Angel ajue maana bila kujua kwa maneno ya huyu kijana Angel hachomoki yani hatumpati tena Angel, muda wote atakuwa akimuwaza huyu”“Sasa, mume wangu jamani unanitisha ujue. Sitaki mtoto wetu aharibike, nahitaji Angel asome na afike mbali na elimu yake”“Kama unahitaji hilo basi jua jinsi ya kumfundisha, natambua jinsi wanaume tulivyo ila mfundishe Angel vizuri”“Yani niliposoma huu ujumbe hadi nimehisi ukucha unanicheza, namuhurumia mwanangu Angel jamani, ndio kuna wakware hivi sheleni kwao? Isingekuwa kidato cha nne ningemuhamisha kwakweli”Basi mama Angel aliongea kwa kulalamika sana na mwishowe waliamua kulala tu.Siku ya leo walienda shuleni, basi Angel aliingia darasani na Samir alipomuona Angel alikuwa akimchekea tu na kumpa kama ishara ambayo Angel hakuielewa wala nini ila alipomuangalia vizuri midomo yake aliona akisema “I love you” Angel akainama chini na kuogopa kumuangalia Samir vizuri ila Hanifa aliona na kuguna kisha akainuka na kumfata Samir,“Mmmmh wewe muhuni, yani ni mgeni ila umemuanza Angel jamani”“Mimi sio muhuni ila Angel nampenda tena nampenda sana”“Mimi je hujanipenda?”“Hapana”“Inamaana mimi sio mzuri?”“Sijasema wewe sio mzuri ila upendo wa kweli hauangalii uzuri wala sura ila upo moyoni, kwakweli Angel nampenda na nitasema hivi siku zote hata mbele ya wazazi wake”“Mmmh unajiamini eeeh! Ila yule Angel ni binti mlokole, mama yake ni mkali hatari”“Simba ni mkali ila anazaa, mimi siogopi ukali wa wazazi wake, ila naangalia moyo wangu, ni kweli nampenda Angel”“Kheee una ujasiri wewe kijana!”“Mbele ya Angel lazima nipate ujasiri, nampenda sana”“Mmmh!”Hanifa akainuka na kwenda alipokuwa Angel baada ya muda kidogo walipata mgeni mpya kwenye darasa lao, kwakweli Angel alifurahi sana kumuona kwani alikuwa ni Junior mtoto wa mama yake mkubwa, basi mwalimu alimtambulisha pale kisha aliwaacha wamkaribishe darasani na yeye akatoka, kwakweli Angel alifurahi sana na kumkaribisha nduguye ila kile kitendo cha Angel kumfurahia Junior kiliumiza sana moyo wa Samir na kujikuta akikosa raha kabisa hadi aliamua kutoka nje ya darasa.Basi Angel alikuwa akiongea na Junior pale mpaka mwalimu alipoingia na kuanza kipindi.Muda wa kutoka Angel aliongozana na Junior ambapo Junior alikuwa akimuuliza Angel kuhusu mazingira ya ile shule yao, basi Yusra nae akasogea kwa Angel na kumuaga kuwa wataonana kesho, muda huo huo ambapo Yusra kaondoka tu basi Junior aliacha kuuliza habari za shule bali alianza kuuliza kuhusu Yusra,“Angel, yule rafiki yako anaishi wapi?”“Mmmh Junior, nini sasa kaka yangu jamani! Siku ya kwanza hii”“Kwani siku ya kwanza kitu gani? Hupendi yule awe wifi yako?”“Mmmh sikuwezi, muulize mwenyewe kesho atakujibu anapoishi”Basi Erick na Erica nao walifika pale na kumsalimia Junior huku wakifurahia uwepo wake halafu wakaondoka zao kurudi nyumbani.Walimkuta Vaileth akiendelea na kazi za pale ndani, wakamsalimia na kwenda kubadili nguo kisha Vaileth alienda chumbani kwa Angel na kuongea nae,“Samahani Angel, kwani dereva wenu alikuwa anakufanya nini?”“Mmmh alikuwa akinisifia tu, kwani vipi?”“Yani nimemuonea hadi huruma leo, anasema alikuwa akikusifia tu na asingeweza kufanya chochote na wewe. Yani mama yako kamfukuza kazi hadi huruma”“Ila sio kosa langu, sikutaka kusema kwa mama ila ni kosa la Erica yani katoto kambea kale balaa”“Mmmh ila wewe ndio ulitakiwa umuombee msamaha kwa wazazi wako”“Weee wale wazee wakiamua lao unadhani naweza kupinga? Haswaa mama yani mama yetu ni mkali sana”Basi Vaileth akamuacha pale Angel na kuondoka zake kwenda kuendelea na kazi zake.Muda kidogo mama yao alirudi na wote walienda kumpokea na kumsalimia maana walikuwa na utaratibu huo, basi mama yao akawauliza pale baadhi ya maswali kisha akawaambia,“Kesho kuna anko mpya nitawatambulisha”“Sawa mama”Basi wote wakainuka na kwenda kuendelea na kazi zao ila muda kidogo mama yao alitoka nje na kuwaita watoto wake,“Jamani wanangu kwa bahati anko mpya kafika leo, huyu anaitwa anko Maiko”“Shikamoo anko”Wote walimsalimia na Maiko aliitikia ile salamu kisha mama yao aliwaruhusu kwenda ndani tu kuendelea na mambo mengine.Kwakweli Erica hakupenda mwenendo wa Erick maana toka siku aliyonuna basi hadi leo alionekana hana furaha kama siku zote, basi aliaenda tena chumbani kwake kuongea nae,“Kwani Erick una tatizo gani?”“Sina tatizo wala nini?”“Sasa mbona unakuwa hivyo jamani?”“Kwani wewe nikiwa hivi unaumia nini/ Si unaongea vyema na Abdi eeeh! Basi mthamini Abdi”“Sio hivyo Erick jamani, haya niambie nikupe zawadi gani ili ufurahi kama zamani”“Zawadi yangu mimi ni moja tu, sitaki kukuona ukizungumza na Abdi”“Kama ni hivyo tu sawa, nakuahidi sitazungumza na Abdi tena kaka yangu, sawa eeeh! Basi furahi kidogo, twende nje tukacheze”“Oooh tutakuwa kama mitoto, unajua tumekuwa kwasasa, lazima tuenende kikubwa”Mara dada yao Angel akafika na kusema,“Eeeh Erica, nimekufata chumbani kwako sijakukuta, nikajua tu upo huku kwa kisirani wako. Nataka nikutume kitu mdogo wangu”“Kitu gani dada”“Njoo nikwambie”Basi Erica alitoka nje na dada yake ili kumsikiliza ni kitu gani anataka kumtuma,“Sikia, nenda chumbani kwa mama halafu nichukulie ile simu ambayo mimi nilikuwa naitumia, naomba fanya hivyo mdogo wangu halafu nitakupatia kitu kizuri sana”“Mama, akinibamba je?”“Hakubambi, kwanza bado yupo nje anaongea na yule dereva”Basi Erica akatoka pale na kwenda chumbani kwa wazazi wao, na kweli simu aliikuta mezani tu, basi akaichukua na kutoka nayo ila alipotoka tu njiani akakutana na mama yao nae akiwa anaelekea chumbani ila simu ilianza kuita na kumshtuka mama yao, Erica alishtuka pia na kutamani hata kukimbia, basi mama yake alimuangalia kwa hasira na kumwambia,“Lete hiyo simu mjinga wewe”Basi Erica akamkabidhi mama yake ile simu ambapo alinaswa kofi na kuambiwa,“Kaniitie huyo Angel sasa maana najua ndiye aliyekutuma”Erica aliondoka akiwa kanyong’onyea sana hadi chumbani kwa dada yake, ambapo Angel alimpokea kwa bashasha,“Eeeeh hiyo simu iko wapi?”“Mama, kanibamba nayo anakuita”“Nilijua tu, bora hata ningemtuma Erick”Angel aliinuka kwa hasira na kumsukuma kichwa mdogo wake.Erica alimuangalia dada yake na kutoka kule chumbani kwa dada yake ila aligongana kikumbo na Erick ambaye alimuhurumia pia kisha akamwambia,“Mama kakupiga halafu aliyekutuma nae kakutia sinki, pole mdogo wangu jamani”Halafu Erick akamkumbatia na kuondoka nae kuelekea sebleni ili wakaangalie Tv na aweze kupunguza machungu ya kutumwa kitu kisichoruhusiwa.Angel alienda chumbani kwa mamake sasa ila alishangaa sana siku hiyo wala mama yake hakumfokea wala hakumwambia kiukali zaidi zaidi alimwambia akae ili wazungumze, basi Angel alikaa na kuanza kuongea na mama yake,“Eeeh niambie mwanangu Angel ulikuwa unataka simu umpigie nani?”“Nilitaka nimpigie Hanifa mama”“Niambie ukweli, kumbuka mimi ni mama yako Angel”“Naelewa mama ila huo ndio ukweli”“Haya, simu hii hapa mpigie huyo Hanifa hapa nisikie unachotaka kuongea nae”Muda huo huo akakumbuka kile alichoahidiana na Hanifa kuwa watoroke Ijumaa, akaona akimpigia simu itakuwa ni msala kwake kwahiyo akajigelesha kupiga ile simu.“Ila mama jamani, naomba tuache tu hata sikutaka kupiga simu”“Kwahiyo unanidanganya mimi Angel eeeh!”“Hapana mama”“Haya, piga ulipotaka kupiga, au ulitaka kumpigia Samir”“Jamani mama mbona hivyo, yani mama mambo yako kama askari hadi tunakosa uhuru humu ndani”Basi Angel akainuka ili aondoke, mama yake akamvuta nyuma na kumnasa kofi kisha akamfokea,“Mjinga wewe, umeona leo nimeongea nawe kwa upole basi unajifanya kuleta kiburi, mimi sio shangazi yako wa kumfanyia jeuri”Muda huo simu ya mama Angel ikaanza kuita kwahiyo mama Angel alimwambia Angel atoke mule chumbani kwake na kupokea ile simu, ila mpigaji alikuwa ni dada yake na kuanza kuongea nae,“Mbona unaongea hivyo mdogo wangu jamani”“Si huyu Angel jamani, ataniua kwa presha huyu mtoto dah!”“Kafanyaje tena?”“sheleni kwao kuna kivulana kinaitwa Samir sijui sasa ndio kinamsumbua akili, kweli leo hii naongea halafu Angel ananiambia naongea kama askari, eti nawanyima uhuru kweli Angel wa kunijibu hivi!”“Ila mdogo wangu mambo mengine umeyataka mwenyewe, huyo mtoto toka mdogo kazi kumsifia tu, oooh mwanangu mzuri sana, mwanangu mzuri kama malaika, haya sasa ndio anakuonyesha mambo ya uzuri wake, nilikwambia mdogo wangu ni kweli mwanao ni mzuri ila usimsifie kupitiliza, umeona sasa ameanza kukujeuria hadi wewe. Pole mdogo wangu, nisingekuwa na majanga ningesema huyo Angel aje kukaa kwangu kidogo ila na mimi mwanangu tu huyu ananitoa pumu, dawa ya Angel mpeleke kwa mama yani akikaa na bibi yake huyo atashika heshima na adabu”“Sawa dada, nashukuru kwa ushauri wako nitaufanyia kazi. Eeeeh niambie”“Sasa mwenzangu ni kuhusu huyu wifi yetu maana sio wifi yangu tu ila ni wifi yetu, kwakweli kuolewa ukoo mmoja ni vibaya jamani, miukoo mingine ni shida tupu jamani”“Unamaanisha Tumaini? Kafanyaje?”“Ndio huyo huyo, kwani mimi na wewe tunashea wifi yupi? Si ndio huyo mdogo wangu, yani ananipasua kichwa kwakweli”“Anafanyaje dada”“Yani kaleta mitoto yake kwangu, mwezi umepita sasa halafu yeye nasikia yupo Arusha anakula bata na mumewe”“Khee wote wanne?”“Ndio, watoto wenyewe kawazaa kama ngazi halafu wote kawaleta kwangu jamani, kisa nyumba zetu zipo karibu, najuta kuwafahamu, wakati huo ana dadake nae katuma wanae wawili waje kwangu jana, kwakweli Napata mawazo mimi jamani. Junior anisumbue kichwa na mawifi nao wanisumbue kichwa kwanini lakini!”“Pole sana dada yangu jamani”“Ongea na mumeo jamani, aongee na dada yake”“Ila kumbuka na mumeo nae ni dada yake”“Hamsikilizi ila mumeo atamsikiliza, kuna vitu Tumaini anamuheshimu sana kaka yake huyo, naomba umwambie jamani nimechoka, yani nimechoka la sivyo nawaleta hawa watoto na kwenu ili tusaidiane majukumu ya kulea, aliona raha kuzaa kila siku halafu kulea kunamshinda jamani loh!”Dada wa mama Angel alionekana kuongea kwa hasira sana kuhusu wifi yao huyo ambaye wamechangia undugu yani mume wa mama Angel ni kaka wa Tumaini ambaye wamechangia baba na mume wa mama Junior ni kaka wa Tumaini kwa upande wa mama yani amechangia nae mama halafu huyo Tumaini kaolewa na kaka yao.Basi waliongea pale na kuagana ila mama Junior alionekana kuwa na hasira sana na huyo wifi yao.Basi wakati mumewe amerudi aliamua kuongea nae pia na habari ya Angel na jinsi alivyoongea na dada yake,“Dada kanishauri kuwa Angel tumpeleke kwa mama yani akalelewe na bibi yake”“Hebu acha ujinga huo Erica, hayo ni mawazo ya kijinga. Mama aliwalea ninyi na kuwahudumia, kila kitu alifanya juu yenu, huu ni wakati wa yeye kupumzika sio kuanza tena kusumbuana na wajukuu kama alivyokuwa akisumbuana na nyie, ni wakati wa kumuonea huruma mama yenu, huyu Angel shughulika nae mwenyewe maana wewe ndiyo mama wa Angel, sasa unataka nani akabebe mzigo wa mwanao? Usitake kumtesa bibi wa watu, waende kumsalimia tu sio kumsumbua”“Mmmh na wewe mume wangu jamani, haya dadako nae ni mwezi sasa katupia watoto wake wote kwa dada yangu”“Haya ndio mambo ya familia kuoana jamani, hebu ona sasa, yani dada pale anahisi kuwa ana uhuru na haki ya kufanya hivyo akiangalia pale kuna wifi yake ambaye ni dada wa mumewe na kuna kaka yake pale, yani ana uhuru wa kufanya chochote kile”“Mmmh mbona huku hawaleti?”“Tumaini hawezi kufanya hivyo nyumbani kwangu sababu anajua mimi sipendi ujinga, ila haya ndio madhara ya kutambua starehe ukubwani jamani, yani Tumaini katambua starehe ukubwani basi ndio anajifanya anatumia muda wake, na usinge mshauri vizuri nadhani kwasasa angekuwa na watoto hata kumi”Mama Angel alicheka sana na kusema,“Ila Tumaini jamani anafanya mambo kama sio msomi”“Kusoma sio ndio njia ya kukufanya uelewe kila kitu, kuna mambo mengine ni elimu jamii yani ukiwa mtu wa jamii ndio utaelewa zaidi, sasa yule dada yangu alikuwa mshamba wa mwisho kabisa, kaolewa ndio kafanya kazi ya kuzaa double double”“Wewe una utani na dadako, haya mama Junior kasema ataleta watoto wa Tumaini hapa kwahiyo ongea na dadako vizuri”“Weee huo ujinga nani atautaka? Napenda sana watoto ila sio kwa stahili hiyo kwakweli, awapeleke kwa bibi yao kama alivyotaka Angel aende kwa bibi yake”Kisha baba Angel akaamua kulala ikabidi na mama Angel nae alale tu.Kulipokucha walienda shule kama kawaida na kila mmoja alienda kwenye darasa lake, basi leo Angel alivyoingia darasani tu akapambana macho na Samir ambaye alimuangalia sana ila Angel alikwepesha macho yake kwani aliogopa kumuangalia Samir usoni, basi aliondoka na kwenda kukaa kwenye dawati lake, Hanifa akamfinya kidogo na kumwambia,“Nimekuona hapo ulivyogongana macho na Samir, mmmh kweli unampenda ila hakufai mwali wangu jamani”“Mmmh na wewe Hanifa, mbona sijamuangalia wala nini jamani! Nimeangalia sehemu nyingine tu”“Mmmh nimeona jamani, unampenda yule ndiomana umemuangalia vile”Basi Angel akacheka tu na kuendelea na mambo mengine pale darasani.Mwalimu akaingia na kufundisha ila siku hiyo Angel alijihisi kabisa mawazo hayapo darasani kabisa hadi mwalimu akamshtua kwa kumpiga na chaki,“Wewe Angel, unawaza nini? Niambie unawaza kitu gani Angel? Baada ya kipindi unifate ofisini”Basi kipindi kilipoisha ilibidi Angel aende ofisini alikoitwa na mwalimu ambapo alianza kuongea nae,“Unawaza nini Angel? Kwanini huzingatii masomo? Bado Samir anakuumiza kichwa”Angel akashtuka kidogo na kukaa kimya, kisha mwalimu akamwambia,“Niambie Angel, yule Samir niliongea nae siku ile ya simu. Je anakuumiza kichwa? Unahisi kumpenda Samir? Angel, wewe ni kama mwanangu naomba nikwambie kuwa Samir hakufai, yule ni mwanaume tu mchezaji yani kazi yake ni kuchezea mabinti kama wewe, usiumize kichwa chako kumfikiria Samir, zingatia masomo ndio ya muhimu kwako”“Ila mwalimu mimi simfikirii Samir, kwanza sina mahusiano nae na wala hajawahi kunitongoza”“Ila alikiri wazi kwangu kuwa anakupenda sana”Angel alinyamaza kimya na kuangalia chini, kisha mwalimu alimuuliza Angel,“Kwani na wewe unampenda?”“Hapana mwalimu, mimi napenda masomo”“Ooooh usiwaze nilikuwa nakutania tu nione utasemaje, Samir hajawahi kuniambia kuwa anakupenda ila nilitaka kujua kama kuna chochote kati yako kinaendelea. Ila bado nasisitiza hata akikwambia jua kuwa Samir sio mwanaume sahihi kwako, soma umalize shule salama nami nitakuonyesha mwanaume sahihi katika maisha yako. Haya kaaendelee na masomo”Basi Angel akatoka na kurudi darasani ambapo Hanifa alianza kumwambia,“Mmmh Angel huyu nduguyo Junior ana matatizo gani?”“Kwanini?”“Ni mgeni ila kashamtongoza Yusra na kashanitongoza na mimi”Angel akacheka sana maana tabia aliyokuwa analalamikiwa Junior ni tayari alishaionyesha kwenye shule nyingine.Muda wa kutoka ulivyofika, leo wakiwa katika harakati za kuondoka wakati tu wamepanda kwenye gari, akasogea Abdi na kwenda kumnong’oneza kitu Erica ambapo Erica alionekana akicheka baada ya kuambiwa na Abdi ila kile kitendo kilimchukiza sana Erick na siku hiyo walirudi nyumbani akiwa na kinyongo sana kwani aliona Erica amevunja ahadi yake ya kutokuzungumza na Abdi maana yeye hakupenda Abdi awe karibu na dada yake.Walipofika nyumbani dada yao wa kazi alitambua tofauti aliyokuwa nayo Erick maana alionekana kuchukia zaidi siku hiyo, basi alimuuliza tatizo ni nini,“Kwani Erick una tatizo gani?”“Hapana dada, sina tatizo”“Unaonekana haupo sawa yani, pole sana”Kisha akawakaribisha chakula ambapo kwa siku hiyo kila mmoja alikula kivyake tu, na hata Erica hakwenda kumbembeleza Erick kama ambavyo huwa anafanya.Mama yao alirudi mapema siku hiyo na aliwaita kuwaambia jambo,“Jamani watoto zangu, kesho alfajiri yani nitaondoka saa kumi kabisa kuna mahali inabidi niende ila baba yenu ameenda leo”Angel akauliza,“Halafu mnarudi lini mama?”“Nadhani kesho hiyo hiyo au keshokutwa”Basi wakamtakia mama yao safari njema na kila mmoja kuendelea na shughuli zake za hapa na pale.Alfajiri na mapema mama Angel aliondoka kama ambavyo aliwaaga watoto wake, na wenyewe palipokucha walijiandaa kwa lengo la kwenda shule kama kawaida ila mpaka wanahitaji kutoka Erick hakujiandaa wala nini ilibidi Angel amuite na kumwambia kuwa inakuwaje haendei shule maana hata kujiandaa hakujiandaa,“Leo siendi”“Kwanini huendi?”“Nimejisikia tu kutokwenda”“Kheee hivi wewe Erick una wazimu au kitu gani eeeh!”“Nimesema siendi”“Aaaah umeona mama katoka mapema ndio na wewe kusema huendi shule, sasa subiri uone mama akirudi yani nitamwambia mambo yako yote. Yale ya kupigana shuleni, kuchukia bila sababu na leo kutokutaka kwenda shule”“Kwani lazima kwenda shule jamani? Kwanza leo Ijumaa, nitaenda Jumatatu. Tusipangiane maisha”Halafu akaondoka zake na kurudi chumbani, ila kiukweli Angel alichukia na kutamani hata kumzaba makofi ingawa walilingana nae urefu ila alijivunia kwakuwa yeye ni dada.Ikabidi tu aongozane na Erica kwenda shuleni na kuachana na Erick pale nyumbani.Vaileth alijihisi vibaya kwakweli na kuona yule mtoto lazima kuna tatizo linamsumbua ndiomana yupo vile basi alimuita ili kuongea nae,“Kwani Erick una matatizo gani?”“Sina matatizo yoyote”“Sikia, naomba mimi na wewe tuongee kama marafiki na wala sitamwambia yoyote, nieleze una matatizo gani ila niweze kukusaidia rafiki yangu jamani”“Kwakweli hata mimi sielewi nina matatizo gani, Erica ni pacha wangu yani najikuta muda wote nikitamani kuwa karibu yake tu, natamani mimi tu ndio niwe rafiki yake wa kiume, ila Erica sijui vipi anaanza kuongea na wanaume shuleni kwakweli moyo unaniuma sana hata nimemwambia baba anihamishe shule ingawa sijamwambia sababu, yani mimi sipendi kabisa. Sasa kuna mmoja anaitwa Abdi kwakweli simpendi yani simpendi kabisa, sasa tulikubaliana na Erica kuwa hatoongea tena na Abdi halafu jana wananong’onezana na kucheka, kwakweli nimekasirika na kuona bora nisiende shule kabisa”“Sasa kwanini unakuwa hivyo eeeh! Yule Erica si dada yako wewe!”“Ndio ni dada yangu ila najikuta namjali sana, naona kama hawa vijana watamuharibia maisha yake”“Kwakweli mimi naafiki swala la wewe kuhama shule ila hutakiwi kuchukulia hasira kiasi hiko hadi leo kugoma kwenda shule jamani. Kama kweli unahitaji kumlinda Erica basi unahitaji kuwa nae karibu sana ili aweze kupita njia sahihi. Usichukie Erick, mpende dada yako, wapende dada zako usiwanunie”“Sawa nimekuelewa”Basi Erick alikubaliana na huyu mdada wao wa kazi na kufanya mambo mengine.Leo kama ambavyo hanifa alipanga na Angel, basi walipokaribia mapumziko tu wakajiandaa ili waweze kutoroka, sasa wakati wanatoka nje ya eneo la shule, Hanifa alitangulia ila wakati Angel anatoka akadakwa na mwalimu na kuulizwa kuwa anaenda wapi, kwakweli Angel alikosa maelezo basi mwalimu aliamua kumpa adhabu.“Sasa leo, muda wenzio wanatoka darasani wewe nataka ubaki na utafanya haya maswali, hakikisha unayaleta nayasahisha ndio unaenda nyumbani”Sasa mwalimu kuangalia pembeni akamuona Samir nae kabeba begin a kutaka kupita njia ile ile aliyopita Angel, basi mwalimu alimuita pia na kumpa adhabu ile ile aliyompa Angel,“Mmenielewa nyie”“Sawa madam”Waliamua kurudi darasani huku wakisubiri muda wa kutoka waweze kuianza adhabu yao.Erick aliona ni vyema yeye ndio aende kuwachukua dada zake shuleni na kwavile alijifunza kuendesha gari hakuona tatizo, basi akawasha gari na kwenda hadi shuleni kwao, kwakweli Erica alifurahi sana kuona kaka yao ndio amewafata pale shuleni. Basi Erick alimuuliza Erica,“Angel yuko wapi?”“Sijui, labda darasani kwao”Basi wakamsubiria kwa muda ila walipoona haendi wakaamua kwenda darasani kumuangalia dada yao.Ni kweli leo Angel alichelewa kutoka kutokana na adhabu ambayo alipewa na mwalimu ila alipoona muda umeenda na wengine wote wameondoka akaona ni vyema nae aondoke tu ukizingatia mule darasani walibaki wawili tu yani yeye na Samir basi Angel akainuka ili atoke ila Samir alimvuta mkono hadi nyuma ya darasa na kuanza kumbusu mdomoni, Erica aliingia na kushangaa huku akisema,“Dada”Angel alishtuka na kuogopa maana alijua kila kitu kitafika kwa mama yao ukizingatia mdogo wake ni mbea sana.Ni kweli leo Angel alichelewa kutoka kutokana na adhabu ambayo alipewa na mwalimu ila alipoona muda umeenda na wengine wote wameondoka akaona ni vyema nae aondoke tu ukizingatia mule darasani walibaki wawili tu yani yeye na Samir basi Angel akainuka ili atoke ila Samir alimvuta mkono hadi nyuma ya darasa na kuanza kumbusu mdomoni, Erica aliingia na kushangaa huku akisema,“Dada”Angel alishtuka na kuogopa maana alijua kila kitu kitafika kwa mama yao ukizingatia mdogo wake ni mbea sana.Basi Angel alijiengua toka kwa Samir na kuanza kutoka nje ila bado Samir alimvuta na kumwambia,“Nakupenda sana Angel”Kisha akamuachia aende, kwakweli Angel alihisi kama mapigo ya moyo wake yakienda kwa kasi na kuwakimbilia wadogo zake kisha, akaona gari ya nyumbani kwao akaogopa sana ila hofu ikapungua alipomuona Erick akimuita kuwa akapande na waende nyumbani, basi Angel alipanda huku akiona aibu hata kuwatazama wadogo zake na safari ya kwenda nyumbani ikaanza.Walipofika nyumbani basi Erick alimuuliza kwanza dada yake,“Angel, utanisemea kwa mama kuwa sijaenda shule leo?”Angel Akaka kimya tu na kushuka huku akielekea ndani, basi Erica nae akashuka ila Erick alivyoshuka akamvuta Erica kwa nyuma na kumwambia,“Kilichotokea kwa dada leo ndio kitu kinachofanya nihofie pia kuhusu wewe Erica, kiukweli nakupenda na sipendi upotee jamani”Erica alimuangalia tu kaka yake na kuingia ndani bila ya kusema chochote kile kwani taswira ya alivyomkuta dada yake ilikuwa ikimjia kwenye kichwa chake.Angel alienda kujilaza tu kitandani hata sare za shule hakuvua wala nini kwani kile alichofanyiwa na Samir kilikuwa kikitembea katika akili yake, na lile neno la mwisho aliloambiwa na Samir kuwa anapendwa sana lilikuwa linatembea vizuri sana katika akili yake yani hadi akimfikiria anajikuta akisisimka tu mwili mzima na kujisemea,“Oooh Samir, kwanini najihisi hivi? Yani ndio nakupenda? Sitaki Samir, niache nisome. Oooh hata masomo yenyewe hayapandi tena maana kichwa change kimezungukwa na Samir”Yani hakuwa na amani kwani muda wote alikuwa akimuwaza Samir, hata dada yao alipowaita kwaajili ya chakula alilihisi hilo sema hakuwa na uhakika kama Angel anaweza kumwambia ukweli.Basi Vaileth alimuita Erica ili kumdadisi tu kama anafahamu kinachoendelea kwa Angel,“Dadako anaonekana kuwa na mawazo sana, nini kinamsumbua”“Labda sababu nimemfuma leo anahisi nitamwambia mama”“Umemfuma kivipi?”“Nimemkuta ananyonyana midomo na mwanaume darasani kwao”Mama yao nae alikuwa akiingia kwahiyo alisikia hilo vizuri sana na kushindwa kuanza hata na salamu zaidi ya kumuuliza Erica vizuri,“Erica unaongelea nini?”Erica nae alishtuka kwani hakujua kama mama yao angerudi kwa muda huo kutokana na jinsi alivyoongea nao jana yake, basi mama yake akamuuliza tena,“Hebu nieleze Erica, ni kitu gani kimetokea kwa Angel?”“Mama, kiukweli leo dada Angel alichelewa kutoka darasani basi nikaamua kwenda kumuangalia ndio tukamkuta akifanya kama wazungu wanavyofanyaga kwenye video”“Alikuwa na nani?”“Simjui ila ni mkaka wa kwenye darasa lao”Basi mama yao akamuacha pale sebleni na kisha kuondoka zake ambapo moja kwa moja Erica alijua tu mama yao anaenda kumuhoji Angel. Basi alimuhurumia dada yake na kumwambia Vaileth,“Dada, eti mama atampiga Angel eeeh!”“Sijui ila mama yenu amechukia sana”Basi nae Erica akainuka na kuondoka pale sebleni.Moja kwa moja mama Angel alienda chumbani kwa Angel na kumkuta kajilaza tu, yani alikula na sare zake na alienda tena kujilaza na sare zake, hakujishughulisha kuzivua kabisa, basi mama Angel akamshtua Angel na kumuuliza,“Hivi Angel mara ya mwisho kukupiga ulikuwa na umri gani?”Angel alikaa kimya tu, kisha mama yake akaongea,“Ni mvulana gani uliyekuwa ukifanya nae tabia mbaya shuleni?”“Mama, haikuwa dhamira yangu”“Haikuwa dhamira yako nini, hivi unayajua madhara ya mapenzi wewe? Unajua mapenzi yanaweza kukutenda kitu gani? Unaelewa mapenzi ni shetani gani? Unajua mapenzi wewe?”Angel alikaa kimya tu, na mama yake akamuuliza tena,“Niambie, ni Samir eeeh!”Angel aliitikia kwa kichwa, kwakweli mama Angel alisikitika sana na kujikuta akimnasa vibao vitatu Angel halafu akatoka chumbani kwa Angel na kwenda chumbani kwake ambapo alikaa na kujikuta akilia tu huku akisema,“Ni wapi nimekosea kwenye malezi ya huyu mtoto jamani! Mbona nimejitahidi kila kitu kama mama bora, kwanini mwanangu anaharibikiwa? Kitu gani Angel sijampatia, nimempa maisha mazuri, nimempeleka shule nzuri, kila kitu nawapa humu ndani, kila hitaji lao wanapata na kwanini inakuwa hivi jamani. Huyu Angel anataka kunitenda nini mimi?”Muda huo huo mumewe nae aliingia ndani na kumkuta akilia basi alimbembeleza na kumuuliza kinachomliza,“Sikia nikwambie, nimejitahidi kwa kila hali ila Angel asipitie maisha ambvayo mimi nimeyapitia, sitaki Angel azae nje ya ndoa kwani naelewa maumivu ya kuzaa nje ya ndoa, mtu unadharaulika, thamani yako inapungua na utu wako unapungua, kila mtu anakuona kuwa mkosaji, kwa hakika mimi bila wewe nadhani ningechanganyikiwa maana kila siku akili yangu ilikuwa haisongi, sasa kwanini Angel anataka kurudia maishayale niliyopitia mimi jamani!”“Kwani kafanyaje?”Basi akamuelezea kile ambacho ameelezewa kuhusu Angel, mumewe alimpooza pale na kumwambia,“Usilie mke wangu, wewe ni mama bora, haya mambo mengine ni kawaida tu hata yasikuumize kichwa. Jumatatu nitaenda shuleni kwakina Angel, na nitaonana na huyo kijana, kwa hakika nitamuonya kwani sitaki masikhara na binti yangu kabisa.”Mama Angel alifarijika kusikia vile na kumkumbatia mumewe, ila kiukweli alihisi kupatwa na mawazo sana juu ya mtoto wake.Usiku wa siku hiyo, Angel alijihisi kujiwa na ndoto juu ya Samir tu na alijihisi kumpenda Samir haswaaa hadi alikuwa akishtuka na kumtaja,“Samir”Alikaa kitandani na kulaumu sana kichwa chake kuwa na mawazo ya Samir kiasi kile yani hata kibao alichopigwa na mama yake hakikumuingia kwenye akili yake kabisa.Kulipokucha, mama yake akaenda chumbani kwake na kuongea nae,“Mwanangu Angel naomba niambie mwanangu huyo Samir kakupa nini?”“Kwanini mama?”“Unajua hadi usiku unaita Samir jamani, kwanini lakini jamani! Angel mwanangu naomba usome, nahitaji uwe mtu unayejitambua kwenye maisha, soma mwanangu jamani”Angel alimuangalia tu mama yake kisha mama yake alimtaka ajiandae ili atoke nae kwani aliona ni vyema kufanya hivyo ili kuichangamsha akili ya mwanae kidogo.Basi Angel alijiandaa na kutoka na mama yake.Nyumbani wakina Erick na Erica nao waliamua kutulia na kuangalia Tv, kwenye luninga ile kulikuwa na tamthilia inaendelea ambayo ilihusu mapenzi na kufanya waiangalie kwa makini sana, basi vaileth nae alienda na kuongea nao kuwa ile tamthilia ni muendelezo,“Yani kila siku huwa inaonyeshwa sema mnakuwa shule”“Inahusu nini dada?”“Yani humu kuna mdada na mkaka wanapendana ila wanashindwa kuambiana basi wanavyofanyiana hadi raha kuwaangalia”“Mmm jamani kwanini wanashindwa?”“Kutongoza kipaji Erica, yani sio wote wanaweza kusema ni kiasi gani wanapenda, utakuta mtu anaumia tu moyoni mwake lakini kusema ukweli anaogopa”Mara Erick aliinuka na kuondoka, ambapo vaileth alimuuliza,“Erick rafiki yangu hujaipenda au?”“Aaaah basi tu kichwa change hakipo sawa”“Basi tutaongea vizuri rafiki yangu”Basi Erick akaondoka na Erica alimuuliza Vaileth,“Kwahiyo dada Erick pekee ndio rafiki yako eeeh!”“Hamna wote nyie ni marafiki zangu ila huwa napenda sana kuongea na Erick, kwanza sio muongo, sio muigizaji, yani akikwambia kitu basi lazima anyooshe maelezo yake na kama kitu hakipendi lazima utajua tu kuwa hakipendi”“Mmmh dada, nani muongo sasa humu ndani?”“Sijasema kuwa nyie ni waongo hapana ila namaanisha kuwa Erick yupo tofauti sana”Basi Erica alimuangalia tu huyu dada yake kisha akaendelea kuangalia ile tamthilia.Angel na mama yake wakati wanarudi nyumbani, basi mama yake akaguswa bega, kugeuka nyuma alifurahi sana kwani alimuona mtu ambaye walifahamiana ila ni muda mrefu umepita tangu kuonana kwao,“Khee jamani Dora upo!!”“Nipo, za siku. Yani tumepotezana kabisa”“Ni kweli tumepotezana ten asana tu, nipe habari. Mumeo hajambo!”Dora aliinama chini kidogo na kumfanya mama Angel amuulize kwa makini kuwa imekuwaje,“Vipi Dora jamani?”“Mume wangu alifariki”“Jamani, pole sana ndugu yangu jamani. Kwahiyo sasa hivi unaishi wapi?”“Nilikuwa naishi nae mkoani na ndiko alikofia, yani nimerudi siku sio nyingi ila kuna nyumba tulijenga na ndio ninayoishi, kaniachia mtoto mmoja, kwahiyo kwasasa naitwa mama Jesca”“Oooh hongera kwa kupata mtoto, hivi kumbe James alikufa! Hata nyumbani hatujapata taarifa”“Ndugu yangu ndugu yangu mngepatia wapi taarifa? Mume wangu kafa kifo cha aibu, nitakusimulia vizuri ila nina mengi sana ya kuzungumza na wewe rafiki yangu, halafu kwenu nimepasahau nilitaka hata kwenda kumsalimia mama yako, halafu dada yako nina ujumbe wake ambao niliachiwa na mume wangu, kwakweli nina mengi sana”“Karibu nyumbani basi”Ilibidi mama Angel amshawishi ili rafiki yake huyo afike kwake mara moja na aweze kupafahamu ili siku nyingine aweze kufika, basi alikubali na kuondoka nae huku wakiongea mambo mbalimbali ambapo walianza kucheka na kukumbushana mambo ya usichana wao.Mama Angel alikuwa akiendesha gari huku rafiki yake akiwa amekaa pembeni basi akamwambia,“Ila Erica una bahati sana wewe, yani una bahati sijapata kuona jamani, kwahiyo hadi leo unaishi vizuri tu na Erick?”“Ndio, tumezoeana mno kwasasa, tofauti na kipindi kile cha uoga uoga”Wakacheka na akamkumbushia tena,“Hivi na wale waliokuwa wanakufukuzia kipindi kile waliacha? Kwanza vipi Bahati jamani natamani nijue kaishiaje”Mama Angel alicheka na kumwambia rafiki yake,“Kuna mtoto kumbuka”“Halafu hujanitambulisha, ndio Angel huyu”“Eeeeh ndio mwenyewe”“Kheee kakuwa huyo, halafu saivi kidogo anafanana fanana na wewe, hizo nywele za Rahim hizo”“Mmmmh naomba acha hizo stori rafiki yangu”Mama Angel hakutaka kuongea chochote kuhusu mambo ya zamani ya Angel kwani hakutaka Angel amjue baba yake halisia ni nani kwani hakuwa yule ambaye Angel alizoea kumuita baba, basi waliondoka hadi kufika nyumbani kwa mama Angel na kushuka huku akimkaribisha sana pale nyumbani kwake.Dora aliingia na kusifia uzuri wa ile nyumba,“Jamani hongera shoga yangu, kwakweli maisha umeyapatia jamani”Mama Angel alicheka tu na kuingia ndani ambapo alimkuta Erica na kumtambulisha kwa yule mgeni, ambaye alishangaa,“Kheee anaitwa Erica? Si jina lako hili?”“Ndio jina langu ila nimeona nimpe mwanangu, unajua nilizaa mapacha, basi kuna huyu Erica na kaka yake Erick, wewe Erica hebu kamuite Erick”“Kumbe ile mimba ndio ulizaa mapacha, nakumbuka nilikuacha na mimba”“Basi ndio hao watoto”Basi Erica alinyanyuka na kwenda kumuita kaka yake ndani, na muda kidogo tu Erick alifika na kumsalimia yule mgeni kisha mama yake alimtambulisha ila mgeni yule aliguna sana baada ya kumuona Erick mpaka mama Angel alimuuliza,“Mbona umeguna hivyo?”“Hamna kitu, nimefurahi tu kuwafahamu watoto wako, nami nitakuletea mwanangu umfahamu. Ila kwasasa naondoka kwani natakiwa kuna mahali niwahi halafu nitakuja tena tuongee vizuri”Wakabadilishana namba pale na mama Angel alitoka kumsindikiza ila bado alimuuliza kwanini aliguna baada ya kumuona Erick,“Mbona umeguna sana dora, tatizo ni nini?”“Hakuna tatizo ila kwanini mmewapa watoto majina yenu?”“Kani kuna ubaya? Nataka watoto hawa wapendane kama ambavyo wazazi wao tulipendana”“Hebu acha masikhara yak ohayo, nyie mlipendana ila mlikuwa wapenzi, ila watoto hawa ni ndugu halafu unataka wapendane kama nyie, una maana gani?”“Hapana sio hivyo unavyomaanisha wewe, nataka wanangu wawe na upendo tu, halafu sababu mimi na baba yao wengi walituhisi ni mapacha”“Mmmh hata kama, unajua unavyotoa majina uwe unaangalia na nyuma ikoje”“Kivipi jamani, kwani watoto huwa hawachukui majina ya mama zao? Huwa hawachukui majina ya baba zao?”“Ni wengi tu huchukua hivyo ila na nyie mna historia gani? Sina ubaya kusema hivi ila nimewapenda wanao wana heshima hadi raha, vipi Angel hujampeleka kwa babake nini?”“Ni historia ndefu, ila kwa kifupi babake Angel yani Rahim alikuwa na lengo baya la kunivunjia ndoa yangu, niliruhusu awe anakuja kumuona mtoto ila akawa anafanya mambo ya ajabu sana, tukipata muda nitakueleza vizuri zaidi, kwahiyo mimi na mume wangu tuliamua kuhama tulipojenga na kujenga pale na kuanzisha maisha mapya yap eke yetu yani sisi na watoto wetu, basi tokea hapo Angel hajui kama alishawahi kuwa na baba wa kuitwa Rahim”“Oooh haya, akija Erick msalimie sana”Kisha mama Jesca akaondoka zake.Angel aliingia chumbani kwake na kukumbuka maneno ya yule mama kuwa huyu mtoto nywele zake kama Rahim, basi akaanza kujiuliza,“Rahim ni nani? Kwanini mimi nywele zangu ni kama za Rahim?”Alikosa jibu na kuvizia mama yake akiingia ndani basi alimfata chumbani na kumuuliza,“Mama, kwani Rahim ni nani?”“Mwanangu kuna siku nitakaa na wewe na nitakueleza vizuri juu ya huyo mtu na utaelewa tu”“Unajua mama sielewi, kwani baba sio baba yangu?”“Nyamaza wewe mtoto, funga mdomo wako huo, asingekuwa babako angekupenda kiasi hiki? Angekusomesha, angekulisha na kukujali?”“Ndiomana nikawa nashangaa mama, sijauliza kwa maana mbaya kwani mimi najua baba ndio baba yangu na ananipenda sana”Na muda huo baba yao nae alirudi kwahiyo alimsalimia na kumpisha mule chumbani kwa mama yake, kisha baba Angel alimuuliza mama Angel maana alisikia kidogo,“Kuna nini kwani? Umemwambia ukweli Angel?”“Hapana mume wangu siwezi kufanya hivyo, tutamuharibu Angel kisaikolojia maana siku zote anakufahamu wewe kama baba yake halafu leo uje umwambie kuna mjinga mmoja ndio baba yake, kwakweli tutamuharibu kisaikolijia”“Aaaah nikajua umemwambia ukweli, ila mazungumzo hayo yalianzia wapi?”Basi mkewe alimueleza jinsi walivyoenda mjini na kukutana na rafiki yake ambaye alifika nae nyumbani kwake,“Kheee bado tu una urafiki na yule mtu na umemleta hadi nyumbani, ila mke wangu yule ni mropokaji sana, yani usishangae siku akiropoka kwa Angel”“Hapana bhana, saivi amekuwa, ni mama ujue, ana mtoto mmoja wa kike”“Hata kama, ile ni tabia yake ya kuropoka na hawezi kuiacha, ila sijui labda kabadilika siku hizi. Haya nilikoenda yote nimeyafanikisha na jumatatu nitaenda shuleni kwakina Angel halafu Erick nitamuhamisha shule tayari nafasi nimeshapata”“Kheee Erick unamuhamisha shule?”“Ndio, kaniomba sana kuwa ile shule haitaki na mimi nimemsikiliza, nataka watoto wangu wasome na sio waishie kati kama mimi baba yao, kwahiyo kama kasema mahali Fulani hapataki na ana sababu zake nikaona ya nini kumlazimisha? Basi nimemtafutia sehemu nyingine na Jumatatu nitaenda kumchukulia baraua shuleni kwao”“Ila ungefanya jambo la muhimu zaidi kumuhamisha Angel shule maana yule ndio yupo kwenye wakati mbaya.”“Mke wangu, Angel kabakiza mwaka tena sio mwaka ni miezi tu kumaliza kidato cha nne kwanini tuanze kumsumbua hivyo?”“Mbona kuna wengine wanahamisha watoto wao”“Naweza sema kuwa hawajielewi, yani ni muda mchache tu umebaki, tutaichanganya akili ya mtoto.”Mama Angel alitulia tu kwani kwenye kundi la wasiojielewa inamaana hadi dada yake yupo humo kuwa nae hajielewi kwani kahamisha mwanae wa kidato cha nne.Jumapili ya leo walijiandaa vizuri kwenda kanisani ila Angel alidai kuwa anaumwa kwahiyo hakwenda na kubaki nyumbani tu, hakuwa akiumwa ila alikuwa na mawazo sana kuhusu Samir.Basi walipoondoka wote, Vaileth alimuita na kuongea nae,“Angel, hebu niambie mdogo wangu tatizo ni nini? Eti wakati huyo mwanaume anakubusu ulijihisi vipi”Angel alimuangalia huyu dada na kumwambia,“Yani sijui nielezaje jamani, ila siku ile hata sijui nilijihisi vipi”“Ila Angel mdogo wangu, masomo ni muhimu zaidi, usichanganye mapenzi na shule utakuja kujutia, mapenzi yapo na daima yataendelea kuwepo yani hayaishi wala hayatoisha kwahiyo muda muafaka ukifika utayapata tu mapenzi na utakuwa nayo hadi utayachoka”“Mmmh!”“Usigune Angel, sikia nikwambie ni kweli wewe ni binti mrembo sana una kila sifa ya kufanya kila mwanaume avutiwe na wewe ila sio kila mwanaume atakupenda kweli, maana wengine watakutamani tu kuwa nawe kwa muda mfupi na kisha kuachana na wewe, kwakweli unatakiwa kuwa makini sana mdogo wangu, mapenzi yapo na yataendelea kuwepo kwahiyo shule kwanza, soma mdogo wangu kwani elimu ni ya muhimu sana”“Ila kwanini mimi najihisi hivi sasa?”“Hiyo ni kawaida tu wala usione ni tofauti sema cha kufanya jiweke mbali na huyo mtu na umuone kuwa ni mbaya na anataka kuharibu maisha yako, hebu fikiria ukipata mimba sasa utaendelea na shule? Unadhani ataendelea kukupenda na kukujali? Nione hivi mimi, nilipata mimba nikiwa kidato cha pili, kwakweli niliacha shule na ndoto ya kusoma ilikatika pale, mwanaume alinikimbia na maisha yakawa magumu sana kwa upande wangu”“Kwahiyo mwanao yuko wapi kwasasa?”“Yupo kwa wazazi wangu na mimi nimeamua kuja kufanya kazi za ndani, kwakweli huwa najutia sana, nilijitoa ufahamu na kujiingiza katika mapenzi wakati nikiwa bado mwanafunzi na sasa najutia mdogo wangu tena najutia sana”“Pole dada Vai”“Hiyo pole yako itatenda kazi kwangu vizuri endapo utaamua kuendelea na masomo yako na kuachana na mambo ya mapenzi kabisa, fikiria masomo Angel’Basi Angel alimsikiliza Vaileth na kiasi Fulani kuwa kama mtu aliyeelewa alichokuwa akiambiwa, kisha akamuuliza tena,“Ila nitafanyaje sasa ili nisimuwaze sana”“Unatakiwa ufanye kwa makini unachofanya, yani kuwa makini sana. Fikiria maisha yako ya mbeleni, panga maisha yako sasa, ukiona unamuwaza sana basi njoo unisaidie kazi za hapa na pale maana ukijishughulisha utashangaa tu huna mawazo nae wala nini”“Sawa dada nimekuelewa”“Kuwa makini sana Angel, dunia ina mambo sana hii, zingatia masomo”Basi Angel akiendelea kuongea na Vaileth pale alishangaa kuona Hanifa akifa pale kwao ilibidi amkaribishe vizuri tu.“Mmmh shoga yangu za tangu Ijumaa? Nimeona bora leo nikufate”“Ila kitu chenyewe mpaka niende kwenu jamani hanifa?”“Ndio, ni muhimu sana tena sana shoga yangu”“Ila hatuchukui muda mrefu?”“Yani wala hakuna kuchukua muda wala nini, muda huu huu tunarudi”“Basi twende haraka haraka maana mama na baba wameenda kanisani na leo sidhani kama watawahi kurudi, twende muda huu”Basi Angel alienda kujiandaa haraka haraka na kutoka ila vaileth akamwambia,“Angel unaenda vipi mahali bila kumuaga mama yako?”“Sikia dada, yani hata hatuchukui muda mrefu, ni jambo la muhimu halafu ni siku nyingi acha leo nikaone mara moja”Basi yeye na Hanifa wakaondoka zao hapo nyumbani.Vaileth alibaki na muda ulienda ila Angel hakurejea nyumbani wala nini, akawaza mama yao wale watoto akirudi itakuwaje yani lazima atamfokea tu, na kweli muda kidogo walirudi kutoka kanisani na kama kawaida mama Angel aliamua kwenda kumuangalia Angel chumbani ili kujua anaendeleaje maana alisema kuwa anaumwa asubuhi, alishangaa kwenda chumbani kutokumkuta mtoto wake, basi akarudi kwa Vaileth na kumuuliza,“Angel yuko wapi?”“Alikuja rafiki yake mmoja hapa wa kuitwa Hanifa ndio kaondoka nae”“Kheee jamani huyu mtoto loh! Sijui huyo Hanifa anakaa wapi jamani”Kwakweli alihisi hata chakula kichungu kwa muda huo kwani alikuwa akimuwaza mtoto wake tu, basi akawaita Erick na Erica na kuwauliza kama wanapafahamu kwakina Hanifa,“Eti jamani kuna anaepafahamu kwakina Hanifa?”Wote waligoma ila Erick alikumbuka jambo na kusema,“Nadhani huyo nafahamu dukani kwao, maana kuna siku za nyuma niliwahi kwenda na dada mara moja”“Oooh naomba nipeleke mwanangu, jamani huyu Angel ataniua kwa presha dah!”Basi Erick alitoka nje na mama yake na kuingia kwenye gari na kuanza safari ya kumpeleka dukani kwakina Hanifa.Angel na Hanifa waliongozana hadi dukani ila wakamkuta James ambapo hanifa alimuuliza,“Mjomba kaenda wapi?”“Mmm katoka kidogo ila kasema mumsubirie”“Aaaah tuna haraka jamani, ngoja nikamuangalie nyumbani”Basi Hanifa akaondoka na kumuacha James pale akiwa na Angel ambapo James alianza kuongea na Angel,“Katika maisha yangu sijawahi kuona msichana mrembo kama wewe, hakika nakupenda sana Angel”Basi Angel alikaa kimya tu, ambapo James aliendelea kumuelezea jinsi alivyo mrembo,“Kwakweli nakupenda sana, na nikikupata hakika utajihisi unamiliki dunia maana nitakupenda, nitakujali, nitakuthamini na kukuheshimu”Halafu James akasogea ili ambusu Angel, ila Angel alimsukuma pembeni na kusema,“Sitaki, sijafata hayo mimi”“Ila umefata nini?”Angel akakaa kimya ambapo James aliendelea kumwambia,“Ni heri unipe mimi mtoto mwenzio kuliko huyo mtu mzima unayetaka kumpa”“Kumpa nini?”“Tunda”“Tunda lipi?”“Kumbe hujui kama una tunda? Twende ndani nikakuonyeshe”Angel alichukia na kumsonya james, yani katika vitu ambavyo James hakuvipenda ni kusonywa na mwanamke, basi akamwambia“Angel umenisonya, ila ungejua nilivyo hata usingethubutu kunisonya”Muda huo huo alifika Hanifa na mjomba wake ambapo Hanifa alimtambulisha Angel pale na Angel alimsalimia kwa heshima zote yule mjomba,“Shikamoo mjomba”Ila huyu mjomba hakuitikia wala nini na akatangulia ndani ya chumba ambacho kilikuwepo dukani, halafu Hanifa nae alimshika Angel mkono na kuingia nae kwenye chumba hiko halafu alimuacha humo kisha yeye alitoka na wala hakuongea chochote na James zaidi ya kuondoka tu.Erick alifika na mama yake kwenye lile duka na wakashuka kwenye gari ambapo nje ya lile duka walimkuta James, yani huyu mama alichukia sana ukizingatia ashawahi kumuona huyo James akimnyemelea mtoto wake, basi alimfata na kumkukunja huku akimwambia,“Wewe mjinga, nionyeshe mtoto wangu alipo”James akawa anajiuma uma basi mama Angel akamnasa kibao na kumwambia,“Nitakufunga wewe mtoto ujue, yuko wapi mwanangu Angel?”James hakuongea neno zaidi ya kuongozana na yule mama hadi kwenye chumba cha lile duka. Basi walipofika akaanza kugonga ila mama Angel alimsukuma pembeni na kufungua ule mlango, alishtuka sana kumkuta mwanae akiwa chini hana fahamu halafu yule mwanaume ndio anataka kumuingilia kimwili, yani mama Angel alipatwa na hasira sana na kwenda kumsukuma yule mwanaume pembeni ambapo alianguka chini kwani kilikuwa ni kitendo cha gafla sana kutokea.Yule mwanaume alipoanguka ndipo alipotazamana vizuri na mamake Angel, yule mama alisikia akisema kwa jazba,“Kumbe ni wewe!!”Yule mjomba alitazama macho chini kwa aibu maana alikuwa akifahamiana na huyu mama.James hakuongea neno zaidi ya kuongozana na yule mama hadi kwenye chumba cha lile duka. Basi walipofika akaanza kugonga ila mama Angel alimsukuma pembeni na kufungua ule mlango, alishtuka sana kumkuta mwanae akiwa chini hana fahamu halafu yule mwanaume ndio anataka kumuingilia kimwili, yani mama Angel alipatwa na hasira sana na kwenda kumsukuma yule mwanaume pembeni ambapo alianguka chini kwani kilikuwa ni kitendo cha gafla sana kutokea.Yule mwanaume alipoanguka ndipo alipotazamana vizuri na mamake Angel, yule mama alisikia akisema kwa jazba,“Kumbe ni wewe!!”Yule mjomba alitazama macho chini kwa aibu maana alikuwa akifahamiana na huyu mama.Kwakweli mama Angel alikuwa na hasira sana na kwenda kumuinua mwanae ambaye alikuwa hajitambui kwa wakati huo kisha akambeba na kutoka nae nje ambapo walimpandisha kwenye gari na kumtaka Erick awahishe hospitali ili akamuangalie Angel kazimia na nini ila walipofika karibu na hospitali Angel alizinduka huku akishangaa shangaa kwakweli mama yake alifurahi kumuona mwanae kazinduka yani akajikuta akishindwa hata kumfokea kabisa.Basi alitaka waende hivyo hivyo kwa daktari ila Angel akagoma ikabidi warudi nyumbani tu yani kwakweli huyu mama hata hakujua aanzie wapi kumsema Angel kwani akikumbuka ni machozi yalimtoka tu.Walifika nyumbani na kumtaka Angel aende chumbani halafu yeye hakuongea kitu zaidi ya kwenda chumbani kwake na kuanza kulia kama ambavyo alilia siku aliyoambiwa mwanae amefumwa akiwa na Samir,“Jamani kwanini lakini? Kwanini Angel ananifanyia hivi? Huyu mtoto ananitaka kitu gani jamani!”Alilia sana mpaka pale Erica alipoenda chumbani na kumgongea maana kuna mgeni alikuwa amekuja,“Mama, mamkubwa kaja”Basi mama Angel akajifuta machozi na kutoka kwenda kuongea na dada yake.Alifika sebleni na kumkuta dada yake nae akionyesha sura ya hasira ila alimpokea na kumkaribisha vizuri, sema dada yake nae aligundua kuwa mdogo wake ana matatizo basi aliomba kuongea nae kwanza ili kujua kakumbwa na matatizo gani, ikabidi watoke pale ndani ya nyumba na kuelekea kwenye bustani ili kuweza kuongea maana hata yeye aliona vyema akimwambia dada yake atapumua,“Nini kinakusumbua mdogo wangu? Una maisha mazuri, mumeo anakupenda sana, huna mawazo kama hela ipo, tatizo ni kitu gani yani nini kinakusumbua?”“Ni Angel dada”“Kafanyaje Angel/ niambie mdogo wangu, usikae na kitu moyoni maana kitakuumiza zaidi natumai unaelewa nikisema hivyo”“Naelewa dada”“Haya, niambie”Basi akamsimulia kwa kifupi jinsi ambavyo amemkuta Angel,“Kheeee hatari, kwahiyo kambaka?”“hapana hajambaka ila ningechelewa kidogo tu basi angembaka jamani mwanangu”“Pole sana mdogo wangu, huyu Angel nae kwanini amekuwa hasikii kiasi hiko jamani? Huyo mwanaume nae amekuchanganya kwanini?”“Nadhani dada sijawahi kukwambia kuhusu hili, kuna mwanaume alikuwa akiitwa George, nilikutana nae kipindi nasoma chuo, mwanzoni niliamini ananipenda kumbe anahitaji msichana bikra, yani alipotembea na mimi na kukuta si bikra aliniacha peke yangu nikiwa sina hata nauli, nakumbuka siku hiyo nililia sana na kulaumu kwanini nilimuamini kiasi kile nilichomuamini. Nikaja kujua ukweli kuwa huyo mwanaume ni muhuni balaa, na pale alipo ameathirika yani kaathirika kitambo sana, yule rafiki yangu Dora alitembea pia na huyu George, halafu leo nimemkuta anataka kunibakia mwanangu kwakweli nimeumia sana, kwanini mimi jamani? Kwanini mimi nafanyiwa hivi!! Yani watu wananifatilia na utu uzima huu jamani, sio wakati wangu wa kulia kwasasa, ila kwanini Angel ananitesa kiasi hiki, kwanini huyu mtoto ananieleleza sana mimi!”“Nadhani ni vyema sasa ukamwambia Angel asili yake, anatakiwa amfahamu babake wa ukweli”“Mmmh si ndio itakuwa balaa”“Hapana, unatakiwa kumueleza Angel kuhusu ukweli wa maisha yake, mueleze jinsi ulivyohangaika nae, mueleze jinsi babake alivyokutenda, ili kama akiamua kuyafanya maisha yake hovyo ajue ukweli kabisa kuwa anakuumiza kwa kiasi gani, mwambie Angel ukweli”“Nasubiri hata afike chuo ndio nimwambie ukweli maana kwasasa nitaichanganya akili yake, unajua siku zote Angel anajua huyu ndio baba yake mzazi! Kwakweli nimepata mume mwenye upendo sana, yani anampenda mwanangu hadi nafurahia kwakweli, sijui ningefanyeje mimi kama huyu asingekuwa mume wangu ila kwanini Angel ananifanyia hivi jamani!”“Mwambie ukweli, nakwambia mdogo wangu ukweli utakuweka huru, mwambie ukweli. Si unaona kama Junior anaelewa fika kama baba yake alikuwaje”“Eeeeh tena bora umenikumbusha dada, nilikutana na Dora, nasikia James amekufa”“Ndio amekufa”“Kumbe unajua dada?”“Najua vizuri ila sikuwaambia wala nini, kwanza ni kujichoresha, kwa yule mwanaume niliondoka mwenyewe, sasa niseme kitu gani? Alikufa ndio”“Eeeeh aliumwa nini?”“Na wewe nawe, aliumwa nini kivipi? Si alikuwa na ukimwi yule? Ila hapa mwishoni nasikia alianza tena uhuni yani uhuni ndio ulipamba moto na amefia guest akiwa na mwanamke, sasa sijui kitu gani ila kafia guest”“Kheee shemeji nae, hakuacha uhuni jamani loh!”“Basi ndio naimba wimbo mmoja na Junior kila siku, baba yake kafia guest sijui nay eye anataka hivyo jamani! Katoto kale kanahitaji maombi kwakweli, peke yangu siwezi, nishamkanya hadi nimechoka jamani ila mtoto hasikii hahambiliki jamani”“Kheee pole dada”“Ila sio kilichonileta huku, bali kilichonileta ni watoto wa wifi yako jamani mimi nimechoka, huyu tumaini anaweza fanya tuharibu undugu kwakweli”“Eeeeh wamefanyaje tena dada”“Watoto ni wavivu wale sijapata kuona, ila ni malezi ambayo mama yao kawalea yani tumaini kawaendekeza sana watoto wake jamani, yule mdogo yupo darasa la pili ila hawezi kufua hata nguo yake ya ndani jamani! Malezi gani haya sasa? Kwakweli Tumaini anakera, yani watoto wake wananikera jamani, nilijua nitamkuta mumeo nilitaka niongee nae ili aongee na dada yake, mimi nimechoka jamani”“Pole, tulipotoka kanisani kuna mahali alipitia”“Ila jamani Mungu huyu kweli mkali, hadi mumeo nae anaenda Kanisani mmmh! Yani kabadilika kabisa kama sio yeye, ila wanaume hawaaminikagi ujue”“Kivipi dada? Unamaanisha atakuwa ananisaliti?”“Sina maana hiyo”Mara simu ya mama Junior ikaita na kumfanya aipokee ila alipata habari ya kumshtua kidogo na kumuaga mdogo wake,“Vipi tena dada?”“Nasikia Junior huko kapiga mtu, sasa kashikiliwa polisi. Ngoja niende”“Kheee watoto hawa jamani, tuzaage tu kutoa machango tumboni, hawa wangebaki kwenye viuno vyetu basi tungetolewa uvimbe kama kichwa cha mtu. Pole dada, utaniambia yatakayojiri”Basi mama Junior akaondoka na mama Angel alirudi ndani.Muda huu mama Angel alienda tena chumbani kwa Angel na kuongea nae kwa ukaribu zaidi,“Mwanangu unajua hatujaongea kabisa, hebu niambie imekuwaje kwanza?”“Mama, kwakweli sikujua kabisa, siku zote Hanifa kaniambia kuna kitu anataka kunionyesha na sikujua ni kitu gani kwakweli”Basi Angel akaanza kumueleza mama yake toka siku ile alipoenda pale dukani kwakina Hanifa na jinsi walivyotaka kutoroka shule na kupewa adhabu na vile alivyoondoka nae siku hiyo,“Sasa tumefika pale, kumbe ndio kaenda kumuita mjomba wake, tumeingia pamoja kwenye kile chumba na mwenzangu akaondoka mara yule mjomba wake akasogea na kusema kuwa ananipenda sana, pale pale niliinuka na kutaka kuondoka ila yule mjomba alinivuta na kunipulizia sijui nini usoni basi nikapata usingizi na kuanguka chini”“Kheee mwanangu, ila kila siku naongea kuhusu marafiki jamani, kuna wengine katika maisha sio marafiki wazuri, wapo kwa lengo la kukuharibia maisha tu, sasa Hanifa kwako sio rafiki mwema kabisa, ona alichotaka kukutenda sasa jamani! Yani mjomba wake angekubaka, halafu unajua kama ameathirika!”“Ameathirika!!”“Ndio, ana ukimwi yule alitaka kukuambukiza mwanangu, jamani Angel hebu tulia basi, hutaki uwe kama mama yako? Muda muafaka utapata mume sahihi katika maisha yako na atakujali na kukuheshimu ila sio hawa wa kutaka kukuharibia masomo yako, kuwa makini mwangu. Nadhani unanielewa”“Nakuelewa mama”“Leo sitakupiga kabisa, maana hata nikikupiga ni kazi bure tu ila nakwambia kuwa jipende mwanangu, maisha yako ni ya thamani sana kuliko kitu chochote kile”Angel alimuitikia mama yake pale na kumuomba msamaha kwani alijua wazi kuwa ameshamkosea mama yake, basi mama yake akainuka na kuondoka.Alibaki Angel mwenyewe akijisemea,“Kwakweli nimemkosea mama, ila kaacha mambo yake yote na kuja kuniokoa mimi, hivi kwanini sisiskii jamani!! Kwani Angel una matatizo gani??”Akawa akijiuliza mwenyewe tu kwani alijishangaa pia kwa kutokusikia anachoambiwa.Baba yao aliporudi, mama yao alienda kuongea nae na kumwambia jambo lililotokea siku hiyo,“Unajua huyo mwanaume aliyetaka kumbaka Angel ni nani?”“Nani?”“Ni George, yule mwenye undugu na mamako”“Khaaa yule jamaa kakumbwa na nini lakini, mbona anatenda mambo ya ajabu sana? Yani nashangaa jamani, maukoo mengine yana watu wa ajabu hatari, utanipeleka huko nikazungumze nae, kwakweli sijapenda kabisa hilo jambo jamani”“Ndio hivyo mume wangu”Basi wakongea na mwishowe wakalala ila kulipokucha mapema kabisa baba Angel alijiandaa na watoto wake ili aende nao shuleni kama alivyoamuahidi mke wake kwani alitaka pia kuonana na huyo Samir.Basi alipanda nao kwenye gari yake na kuondoka pale nyumbani wakielekea shuleni, walifika na alishughulikia maswala ya uhamisho wa Erick kisha akamuulizia Samir ili apate kumuona na kuzungumza nae,“Samahani mwalimu, namuhitaji huyu kijana wa kuitwa Samir, yupo kidato cha nne. Nahitaji kuzungumza nae”Basi mwalimu alienda kumuangalia na kurudi na jibu,“Oooh kumbe hajaja shule leo”Mwalimu mwingine akasikia na kusema,“Huyu Samir, mama yake amepiga simu na kusema mwanae anaumwa”Basi baba Angel alishindwa kuonana na Samir, zaidi ya kumalizia uhamisho wa Erick na kuondoka nae ili waelekee kwenye shule ambayo alipata nafasi.Leo Angel anaangalia darasani kwa makini sana na anatamani kumuona Samir ila hakumuona maana Samir hakwenda shule siku hiyo, basi Yusra alisogea karibu na kumuuliza,“Angel muda wote unaangaza macho kwani unamtafuta nani?”“Nilikuwa namuangalia Samir naona leo hayupo”“Hata Hanifa pia hayupo”“Dah usiniambie habari za Hanifa, yani yule sio rafiki bali ni nyoka”“Umeona eeeh! Nilikwambia mimi ukawa unakataa kuhusu Hanifa, ila hata kaka yako Junior pia hayupo”“Ooooh, jamani watu kidato cha nne halafu hawaji shule”“Inategemea na mapenzi yao na shule, watu wengine hawapendi shule kabisa, yani wanakuja shule tu kwasababu ila shule hawaipendi, wa kwanza wao ni Hanifa”Kwakweli leo Angel hata hakutaka kuzungumzia habari za Hanifa kwani alihisi kumchefua kila akikumbuka ambacho alitaka kufanyiwa na mjomba wa Hanifa, basi Yusra akamwambia tena,“Ila nahisi Samir yupo na Hanifa leo ndiomana wote hawajaja shule”Angel aliinama chini, na Yusra alielewa kuwa ile mada imemuumiza Angel basi aliamua kumbadilishia mada na kuzungumza nae kuhusu vitu vingine.Leo Erica akiwa darasani kuna mgeni aliletwa pia, na yule mgeni alitambulishwa kwa jina la Elly, yani alivyoingia darasani tu moja kwa moja alienda kukaa kwenye dawati moja alilokaa Erica na wote darasani wakacheka na kupiga makofi, alivyofika pale alimwambia Erica,“Naitwa Elly, na wewe je?”“Naitwa Erica”“Nafurahi kukufahamu”“Asante”Basi wakaendelea na masomo yao ila Elly alionekana kumuangalia sana Erica kiasi cha kumfanya Erica amuangalie kwa macho ya wizi, yani hadi wanamaliza masomo na kuondoka nyumbani bado Elly alimfata Erica na kumuaga,“Kwaheri Erica, leo nitaenda kumwambia mama yangu kuwa kuna rafiki nimempata na nimependa sana kuwa nae karibu, najua mama yangu atafurahi sana. Yani mama yangu ana upendo sana, akikuona atakufurahia na atakuzawadia. Kwaheri Erica”Bado Erica alimuangalia sana Elly aliyeonekana kumzoea ndani ya siku moja tu, basi Angel alifika kumchukua mdogo wake ambapo nae alimkuta bado Elly yupo, yani alimuaga Erica ila alikuwepo tu yani hata hakujishughulisha kuondoka, na alipomuona Angel alimsalimia vizuri sana,“Kumbe Erica una dada yako, ooh dada wewe ni mzuri sana nimefurahi kukufahamu, mimi naitwa Elly”“Na mimi naitwa Angel, ila mbona unaongea sana?”“Ni kweli naongea sana ila mimi ni mstaarabu sana, mama huwa ananiambia kuwa nimerithi ustaarabu toka kwa baba yangu, ila mimi sijawahi kumuona baba maana alimkimbia mama kitambo sana. Nataka kupambana na maisha nije kumsaidia mama yangu, na niwe baba bora sio kama baba yangu”“Ila si umesema baba yako ni mstaarabu sana?”“Ndio baba yangu ni mstaarabu sana na amenirithisha mimi ustaarabu wake”“Kheee wewe Elly unaachwa na basi la shule shauri yako, wenzio tukiachwa kuna dereva huwa anatufata”“Mimi sipandi basi la shule, ila naenda kwetu kwa mguu tu hata sio mbali wala nini, karibuni sana nyumbani kwetu”Basi Angel na Erica wakaondoka na kumuacha Elly ambaye aliondoka pia kurudi nyumbani kwao.Walivyofika nyumbani, Erick nae alikuwa amefika nyumbani basi walianza kuongea habari za Elly,“Kwani Erica umemtoa wapi yule?”“Dada, yule ni mgeni yani kaja leo ujue, ila namshangaa kanizoea vile”Erick aliwapita pale kama hawaoni vile na kuelekea ndani basi Angel alicheka sana na kusema,“Jamani mtu fidenge kahama shule lakini bado roho inamuuma loh!”Erica hakuchangia neno kabisa, kwani alipoingia tu ndani moja kwa moja alienda chumbani kwa Erick na kuanza kuongea nae,“Eeeeh niambie shule mpya ikoje Erick”“Ni nzuri tu”“Kwahiyo umeona ni vyema kuwa mbali nami jamani Erick!”“Sijapenda kuwa mbali nawe, hujui jinsi gani naumia kukuona unaongea na wale vichaa wakina Abdi, kwakweli roho inaniuma sana”“Kwani huwa unafikiria ni nini kaka yangu jamani!”“Nahisi lazima watakutaka tu”“Hapana kaka yangu, nipo makini sana”“Una uhakika Erica hakuna atakayekuwa anakurubuni huko shuleni? Unajua mimi sipendi kuona nakukataza jambo halafu bado unalifanya, ila hivi tunacyokuwa mbali mbali inajenga kitu katika mioyo yetu yani lazima utakuwa unanikumbuka tu uwepo wangu kwako nami nitakuwa nakumbuka uwepo wako, hivyo kufanya kila mmoja wetu kujua thamani ya mwenzake”“Ila sio vizuri kwakweli, wewe ndio ulikuwa mtetezi wangu”“Mimi bado ni mtetezi wako, nitakuwa nakuja kukuona Erica hata usijali ila nisingeweza kwakweli kusoma shule moja na wewe na kuendelea kuona ule upuuzi wako na Abdi maana ipo siku ningepigana nae zaidi na kutoana hata ngeu. Ila kwasasa naomba uwe mkweli kwangu,chochote kitakachotokea shuleni naomba uniambie. Upo tayari kwa hilo?”“Nipo tayari”“Haya, nieleze leo huyo Elly ni nani na alikuwa akisema nini?”Basi Erica alimueleza kuhusu Elly, jinsi alivyofika kwenye shule yao na jinsi alivyokuwa akiongea nae, ilionyesha kidogo Erick karidhika nay ale maelezo kwani alitabasamu na kuendelea kuwa na furaha kama siku zingine, basi Erica akaamua kwenda kuendelea na mambo mengine maana kiukweli hakupenda kumkera Erick kabisa.Mama Angel siku ya leo aliwasiliana na mumewe na kwenda nae pamoja kwenye duka la wakina Hanifa ambapo ndio Angel alitaka kubakwa kwenye duka hilo, basi walifika ila walikuta lile duka limefungwa inaonyesha kuwa aliogopa kuwa huenda anafunguliwa kesi na ndiomana akafunga duka.Basi wakasikitika pale kisha baba Angel akasema,“Ngoja nimpigie mama yangu ili nijue huyu George ni kitu gani kimemsibu”Basi akapiga simu na muda huo huo mama yake alipokea ile simu kisha akamsalimia na kuanza kuongea nae,“Naona leo umenikumbuka”“Mbona mimi huwa nakukumbuka kila siku mama jamani!”“Unikumbuke wapi? Simu mpaka nipige mimi ndio kunikumbuka huko na leo sijui umelala ubavu gani hadi kuamua kunipigia”“Aaah mama jamani, achana na hizo habari ila nilikuwa nakuuliza kuhusu George, yuko wapi siku hizi nan i kitu gani kimempata?”“George sijui ana matatizo gani ila siku hizi ana hela si haba, halafu kuna watoto wawili na ndugu zake anawalea, ila nasikia siku hizi kawa mshirikina”“Kheee mshirikina? Kivipi mama jamani?”“Ndio hivyo hivyo usishangae wala nini, George ni mshirikina na anafanya vitu vya ajabu balaa halafu nasikia hataki kuoa kabisa, kwakweli simuelewi jamani”Basi baba Angel akaagana tu na mama yake na kumtaka mkewe kuwa waondoke mahali hapa,“Nitakuja mwenyewe ipo siku, sina hofu na ushirikina wake wala nini”Basi wakaongozana na kurudi nyumbani tu.Leo wakina Angel walijiandaa na kwenda shuleni kama kawaida ila baba yaao hakwenda tena bali alienda kwenye shughuli zake tu.Walivyofika shule yani Angel kabla hajaingia darasani alishangaa Samir kumsogelea na kumkumbatia kwa nguvu, Angel akabaki kusema tu,“Samir niachie, watu wanatuangalia”Samir akamuachia na kucheka kisha akwambia,“Kwani watu kitu gani wakati nakupenda sana, natamani dunia yote ijue ni jinsi gani nakupenda Angel”Kwakweli Angel alibaki kimya tu kwani hakutegemea kwa muda huo kama angesikia maneno hayo toka kwa Samir, kisha Samir akaongea tena,“Nimeumwa jana tu ila nimeona kama mwaka jamani, nakuwaza sana Angel, natamani muda wote nikuangalie kisura wangu”Angel aliamua kukimbilia darasani kwani yale maneno ya Samir yalikuwa yanasisimua moyo wake na mwili wake.Angel alikaa darasani ila aliwaza sana kuhusu Samir kwa muda huo, kiasi kwamba akisikia Samir anaitwa basi anashtuka yeye, naye Samir alikuwa akimuangalia sana Angel basi aliposhtuka kila aliposikia jina la Samir ilikuwa ni furaha sana kwa Samir kwani aliona ni jinsi Angel nae anampenda yeye.Muda wa mapumziko, Samir alimfata Angel karibu na kumwambia,“Angel, najua unanipenda pia usivunge”“Samir tafadhali niache”“Kwani nimekufanyaje Angel jamani? Unajua bado nakumbuka siku ile tulivyokiss”Angel akainuka na kutoka kabisa mule darasani kwani alihisi kuingiwa na ushawishi.Muda wa kutoka darasani ulivyofika basi Angel alitoka ila nyuma alifuatwa na Samir ila hakujua kama Samir anamfata kwa nyuma, alipofika nje alimkuta mdogo wake anamsubiria ila Samir alisogea pia pale pale mbeleya mdogo wake Angel akambusu Angel na kumwambia,“Nakupenda sana Angel”Kwakweli Angel alijihisi kusisimka sana, hadi mdogo wake akamvuta mkono kuwa waondoke ndipo Angel aliondoka pale shuleni kwao.Walifika nyumbani ila kuna muda Erica alikuwa akimuona dada yake anatabasamu mwenyewe, na alipofika kwao ni moja kwa moja akaenda chumbani kwake, basi Erica nae akaenda chumbani kwa mama yao kwani hakupenda kabisa kumuona yule Samir akimbusu tena Angel mbele ya macho yake.Alimkuta mama yake akiwa amejilaza maana siku hiyo hakutoka kwenda popote, basi alimuamsha na kumsalimia kisha alianza kuongea nae,“Mama, kuna jambo limetokea shuleni kwakweli sijalipenda hata kidogo”“Jambo gani mwanangu?”“Mama, yule mkaka leo kambusu tena dada halafu mbele ya macho yangu”Mama Angel alikurupuka kutoka kitandani utafikiri kapewa habari gani maana alihisi kuchanganyikiwa baada ya kuisikia ile habari, alimuuliza tena Erica,“Hebu nieleze vizuri mwanangu”“Yani tulikuwa tunatoka shule, dada akaja nilipo ili tuondoke,na nyuma yake alikuja yule mkaka na kumsogelea dada halafu akambusu na kumwambia kuwa anampenda sana”Mama Angel alipumua kwanza kwani aliona mwanae Erica anajionea mengi sana ambayo asingepaswa kuyaona kutokana na kuwa bado mdogo, akajiuliza cha kufanya ila alimshukuru mwanae kwanza na kukaa chini maana hata jibu la kufanya na Angel dhidi ya yule kijana hakuwa nalo wala nini, alijihisi kuumwa na tumbo kwakweli maana kila alipomfikiria huyo kijana alikosa jibu kabisa ila hata akashindwa kwenda kumuuliza Angel kwani alihisi kupata mawazo ya hali ya juu.Muda huo Erica alitoka na kwenda chumbani kwa Erick ambaye naye alikuwa amerudi kutoka shule basi alimueleza jinsi dadake alivyokuwa akipewa busu na Samir,“Eeeeh Erica, hebu nionyeshe alimbusu vipi?”“Alimbusu mdomoni”“Kama vipi?”Basi Erica alimsogelea kaka yake kumuonyesha mfano wa Angel alivyofanywa na Samir, ila alijishtukia baada ya kufanya vile na haraka haraka akatoka chumbani kwa kaka yake, alimuacha Erick akiwa anacheka tu.Angel alikaa akiwa na mawazo sana juu ya Samir, muda wote alikuwa akiwaza jinsi Samir anavyomwambiaga na jinsi alivyofanya siku hiyo, akaanza kujiambia,“Huyu Samir itakuwa kweli ananipenda jamani, wengine wote walikuwa wakinidanganya ila huyu Samir atakuwa anamaanisha kweli”Mara mama yake aliingia chumbani kwa Angel maana baada ya kujishauri sana aliamua kufanya hivyo, alimkuta Angel akiwa kajiinamia tu basi akamwambia,“Mawazo juu ya Samir hayo mwanangu eeeh!”Angel alimuangalia mama yake kwa aibu na kumsalimia pale, kisha mama yake akamwambia,“Angel mwanangu, katika dunia hii ni mimi na baba yako ndio tunakupenda kweli na tupo tayari kwa chochote kwaajili yako ila sio huyo Samir mwanangu, atakuharibia masomo yako. Mbona umekuwa huelewi kiasi hiko lakini jamani! Unataka niongee kwa lugha gani labda ndio utaelewa? Niweke tarumbeka ndio uelewe mwanangu! Huyo Samir hakufai, kwakweli ukiendelea hivi itabidi tu nikuhamishe shule, sijali upo kidato cha ngapi ila nitakuhamisha shule”Kisha mama Angel alitoka mule chumbani kwa Angel ila maneno yake hayakumzuia Angel kuendelea kumuwaza Samir.Kesho yake kulipokucha kama kawaida waliondoka na kenda shuleni ila leo baba yao hakuwepo kwahiyo mama yao alibakia mwenyewe huku akiendelea kuwa na mawazo kuhusu Angel,baada ya watoto wake kuondoka sasa aliamua kuongea na Vaileth ili amwambie vile anavyojihisi kuhusu Angel,“Unajua huyu mwanangu simuelewi kabisa kiasi kwamba hata cha kufanya sijui yani”“Nakushauri dada uende shuleni kwakina Angel, muite huyo kijana na Angel na umuulize mbele ya mwalimu wao wa nidhamu”“Eti eeeh! Ngoja nijiandae sasa hivi niende”Basi mama Angel alienda kujiandaa huku akiwa na mawazo sana juu ya binti yake, baada ya hapo aliondoka na kuelekea shuleni kwakina Angel.Alifika shuleni na kuongea na mwalimu wa taaluma maana wa nidhamu hakumkuta ambapo aliomba aitiwe Angel na Samir, naye mwalimu hakusita bali alifanya hivyo.Angel na Samir walipofika, basi mama Angel alianza kumfokea Samir na kumuuliza,“Hivi kwanini unamsumbua mwanangu wewe kijana?”Samir alimjibu huyu mama kwa ujasiri kabisa tena bila hata na uoga,“Nampenda sana Angel”Huyu mama alimuangalia na kumnasa kibao kwa hasira.Alifika shuleni na kuongea na mwalimu wa taaluma maana wa nidhamu hakumkuta ambapo aliomba aitiwe Angel na Samir, naye mwalimu hakusita bali alifanya hivyo.Angel na Samir walipofika, basi mama Angel alianza kumfokea Samir na kumuuliza,“Hivi kwanini unamsumbua mwanangu wewe kijana?”Samir alimjibu huyu mama kwa ujasiri kabisa tena bila hata na uoga,“Nampenda sana Angel”Huyu mama alimuangalia na kumnasa kibao kwa hasira.Muda ule mwalimu wa nidhamu nae akafika kwahiyo alimkuta mama Angel akiwa na Angel pamoja na Samir, kwahiyo na yeye alishuhudia kile kibao ambacho mama Angel alimnasa Samir ikabidi asogee karibu na kuuliza,“Kulikoni mama?”“Kulikoni nini? Yani mnashindwa kuthibiti wanafunzi wenu? Si mapenzi shule yamekatazwa? Mnawezaje kuruhusu mambo kama haya yatokee kwenye shule yenu? Yani mtoto huyu anajibu kwa ujasiri na kujiamini kabisa kuwa nampenda sana Angel, ujinga ujinga tu”“Basi mama, tulia tuzungumze”“Sina cha kutulia, wewe Angel nenda kabebe begi lako tunaenda nyumbani sasa”Angel aliondoka na kwenda kuchukua begi lake, na mama yake alibaki pale akiwa na jazba sana yani hakutaka kusikia hili wala lile kwa wakati huo.Angel aliporudi na begi lake alimshika mkono na kutoka nae hapo shuleni na moja kwa moja alielekea nae nyumbani kwao.Walipofika akaanza kuongea na bintiyake,“Angel tafadhali mwanangu, najua upo kwenye darasa baya ila naomba nikuhamishe shule, yule kijana hakutakii mema mwanangu, anataka kukuharibia masomo yako tu”“Sawa mama”“Haya,nenda chumbani”Halafu muda huo huo mama Angel alijiandaa na kutoka kwani kuna shule tayari alishaifikiria kwenye akili yake akaona ndio itamfaa mwanae kwa kipindi hiko.Angel alitulia chumbani kwake kisha Vaileth alimfata na kuanza kuongea nae,“Kwani Angel wewe unajihisi vipi kuhusu huyo mkaka?”“Hata sijui dada, yani sijui kwakeli ila akinisogelea nasisimka sana”“Ila Angel majuto ni mjukuu, mzazi huwa anaona mengi sana. Huwezi jua ni kwanini anakukataza kuwa karibu na huyo kijana. Je upo tayari kuhama shule? Yani upo tayari kwenda shule atakayokutafutia mama yako?”“Nipo tayari dada, nahitaji kusoma kwakweli, ila huyu Samir anaichanganya akili yangu kweli yani, sema nahitaji kusoma kama mama. Halafu ile shule walinizoea sana, yani shule yetu kuna mambo yanayaachia mno, ikiwezekana hata Erica wamuhamishe pale, yani shule ile wanafunzi kuwa na mahusiano darasani ni kawaida, na wakaka wote wamekuwa wakinifatilia ila wamenikosa, sasa namshangaa huyu Samir jamani yani nashindwa hata kumwambia sitaki”“Sasa hapo umepata picha kamili, itakuwa Samir anapata ushawishi toka kwa wanafunzi wengine wa darasani kwenu,kuwa makini sana, anapokutafutia mama yako ukasome na ukamilishe masomo yako vizuri, usimtese mama yako na kumfanya aimbe wimbo mmoja kila siku, hebu muhurumie jamani”“Nimekuelewa dada”“Nashukuru kwa kunielewa, nikupe chakula ule?”“Hapana, kwasasa sina njaa”Basi muda huo huo alifika mama yake mkubwa yani mama Junior na kumshangaa Angel kwa kutokuwa shule,“Vipi wewe?Muda huu ulitakiwa kuwa shuleni!”“Ni kweli mamkubwa ila kuna mambo machache tu yamekwamisha”“Mambo gani?”“Kwanzambona Junior toka Jumatatu haji shuleni?”“Kwakweli Junior kawa donda sugu, jamani nyie watoto tunawazaa tu ili tusionekane wagumba ila mnachotufanya wazazi wenu, anajua Mungu tu”“Vipi tena mamkubwa?”“Yani junior atanitoa pumzi huyu mtoto, nilikuwa hapa nikaondoka juu juu eti Junior kapiga mtoto wa mtu na yupo polisi, yani nimechanganyikiwa, kufika nyumbani ili niulize vizuri hicho kituo cha polisi nikapigiwa simu kuwa nitume laki moja ili junior aachiwe halafu Junior nae anaongea kama yupo kwenye wakati mgumu, jamani angalia kulia kushoto nikatuma hiyo hela mbele ya mtoto yena. Khaaa leo ndio nakuja kujua ukweli kumbe Junior alimpachika mimba mtoto wa watu huko ndio alikuwa akihangaika kupata hela za kutoa hiyo mimba, yani nimechoka”“Kheee pole mamkubwa, yani Junior ndio kafikia huko jamani!!”“Ndio hivyo, kwa kifupi Junior hafai tena hafai kabisa, ni muongo hakuna mfano wake”Kwa upande mwingine Angel alimuonea huruma mama yake mkubwa kwani alionekana kuongea kama mtu aliyechoka kabisa kwenye kumlea Junior.Mama Junior alisinzia pale pale, hata Angel alimsikitikia sana na kuona kweli mamake mkubwa ana matatizo, muda kidogo mama Angel alirudi na kumkuta dada yake pale nyumbani kwahiyo yeye ndio alimuamsha,“Kheee dada,vipi tena?”Dada yake akaamka huku akianza kulalamika,“Jamani mtoto huyu atania mdogo wangu, mbona mimi sikumbuki katika kumsumbua mama yetu jamani?”“Hivi dada nae watoto wake wanamsumbua kama wa kwetu?”“Kheee hujui kwani? Yule mtoto wa kwanza wa dada, si aliolewa yule? Basi kaachika kisa kaenda kumzalia mumewe mtoto na mwanaume mwingine akiwa ndani ya ndoa”“Kheee ile mimba kumbe haikuwa ya mumewe?”“Ndio hivyo, hata sijui kuna laana gani kwetu jamani loh!”“Eeeeh na wewe vipi Junior na huko polisi”“Sina hamu na yule mtoto, kakomba laki moja yangu kumbe alienda kumtoa mdada wa watu mimba”“Kheee kivipi dada?”Basi dada yake akampa maelezo ambayo aliwapa wakina Angel, kwakweli mama Angel alisikitika sana na kumpa pole dada yake,“Kheee pole dada jamani!”“Asante, kabinti kawatu kalizimia wakati kakitolewa mimba, yani jasho la meno limenitoka jamani! Sijalala jana yote,nimesema leo nije tu kwako nipumzishe mawazo kidogo”“Kheee pole dada jamani, kwanini Junior anafanya hivi!! Na hako kabinti kanaendeleaje sasa?”“Kanaendelea vizuri namshukuru Mungu, ila sina hamu kwakweli yani, sina hamu kabisa. Na wewe vipi huyu Angel? Naona leo hayupo shule?”Basi alianza kumsimulia dadake mkasa mzima na jinsi alivyoenda shuleni kwao,“Ila dada, nimepata bahati ya kupata shule karibu na kule unapoishi, nilishindwa tu kupita sababu akili yangu haikuwa sawa”“Mmmmh umeogopa kuwakuta watoto wa wifi yako, ni wavivu hao hatari yani hadi kichefuchefu jamani. Yakila yanaacha vyombo hapo ila nimewanyoosha yani, nadhani hadi mama yao akirudi watakuwa wamenyooka”“Ila vipi maadili yao?”“Kheee watoto wana heshima wale sijapata kuona, unajua hawawezi kwenda popote bila kukwambia? Na hawawezi kuchelewa kurudi, hawana marafiki wa ajabu yani urafiki wao ni wenyewe na ndugu zao, wanasikitika sana tabia ya Junior na kumsihi asinitese, watoto nawapenda sababu ya heshima tu wale”“Nilijua tu kwenye heshima hapo ni mia ya mia, maana mama yao ni mtu wa maadili sana. Unajua alipanga chumba chuo ila kwenye chumba chake huwezi kuta mwanaume waaina yoyote, kwkweli alikuwa akijiheshimu sana, na alikuwa akichagua marafiki wa kuwa nae karibu, nakumbuka ni yeye aliniambia kuhusu Dora kuwa hafai kuwa rafiki yangu, kwakweli Tumaini kwenye mambo ya maadili nampa mia ya mia”“Sasa ndugu yangu kwanini tusimpe watoto wetu hawa atusaidie kidogo kuwalea”Hapa mama Angel akapunguza sauti kidogo na kusema,“Watoto wetu hata hawamuhusu hawa, tunampelekeaje? Kumbuka hatujazaa na kaka zake”“Lakini anaishi na kaka yetu”“Hata kama, ila ngoja akirudi nitajaribu kuongea nae, sijui yeye anawezaje kuwafundisha watoto maadili kiasi hiki halafu kashindwa kuwafundisha kazi jamani!!”“Tatizo la yule anapenda sana kuwa na wasichana wa kazi ndiomana, hivi umesema shule uliyomtafutia Angel ipo karibu na kwangu?”“Ndio, ile shule kubwa kule”“Oooh sasa huyu Angel nimuone anafanya ujinga ajue ni halali yangu, yani nikimkuta hata kasimama na mwanaume, uwiiii atanikoma”Mama Angel alicheka sana na kumwambia,“Kakushinda Junior unayeishi nae ndani utamuweza Angel anayeenda kusoma tu”Basi wakacheka tu na kuendelea kutiana moyo juu ya watoto wao.Leo Erica alitoka shule akiwa mwenyewe, basi Elly alimfata na kuona jinsi alivyopooza,“Mbona upo hivyo?”“Dada yangu nasikia kaondoka na mama kwa hasira sana nahisi anaenda kumuhamisha shule, na kaka yangu nae amehamishwa shule, mimi nabaki mpweke jamani kwenye shule hii”“Usijali Erica, kuanzia sasa jua kuwa una kaka anayeitwa Elly maana nitakulinda, nitakusaidia na nitakuwa nawe bega kwa bega, usijali vchochote kile Erica, tuko pamoja dada yangu”Erica akatabasamu na kufurahi sana kisha aliagana na Ellyn a kuelekea zake nyumbani.Alipofika nyumbani alimkuta mama yake na mama yake mkubwa, aliwasalimia pale na akawaambia kuhusu Elly,“Mama, nimepata kaka shuleni. Anaitwa Elly, kasema kuanzia sasa yeye ndio atakuwa kaka yangu na atanilinda na kunisaidia, kwahiyo mama usiwe na wasiwasi tena kuhusu mimi”Halafu akaondoka na kuelekea chumbani kwake, ila mama yake mkubwa alicheka na kusema,“Mmmh hawa watoto jamani, kitoto cha kidato cha kwanza hiki kinatuletea habari kuwa kimepata kaka shuleni, yasije kuwa mambo ya Samir badae”“Dada jamani usimuongelee huyo kiumbe, kabisa maana hadi nahisi kichefuchefu nikimfikiria”Basi dada yake alicheka tu na kuaga maana aliona kashapumzika vya kutosha sasa, kwahiyo mama Angel alitoka na kwenda kumsindikiza dada yake.Wakati wapo kwenye kituo cha daladala, mama Angel alishangaa kushikwa bega na kugeuka ila akamuona mtu aliyehisi kumfahamu ambaye hakuonana nae kwa muda mrefu sana ila yule mtu alionekana kubadilika sana kiasi kwamba mama Angel hakukumbuka vizuri kuwa alionana wapi na huyo mtu, basi alianza kusalimiana na mtu huyo,“Jamani za siku nyingi Erica? Naona unashangaa sana, unanikumbuka?”“Nimekusahau ila sura yako sio ngeni kwenye macho yangu”“Mimi John, ndugu wa Rahim”Mama Angel alishtuka kidogo ila alijigeresha,“Oooh John, za siku nyingi?”“Salama tu, vipi mtoto wetu hajambo? Jamani ni siku nyingi sana, tunamuhitaji mtoto wetu ili atutambue baba zake”“Oooh nipe mawasiliano yako, nitakutafuta tu”Basi yule john alimpa namba zake ila mama Angel alijifanya amezishika kichwani huku akidai kuwa simu yake kaisahau nyumbani halafu namba zake hajazishika,“Basi usijali nikifika nyumbani tu nitakupigia”“Ila kama sio mbali na hapa, twende wote ili nipafahamu pia”“Oooh ni mbali na hapa, tutawasiliana tu”Kisha mama Angel akapanda daladala moja na dada yake ili yule mtu asielewe chochote.Walipokuwa ndani ya daladala ikabidi dada yake amuulize vizuri,“Vipi kwani kuhusu yule?”“Ni historia ndefu ila yule ni ndugu wa Rahim, sitaki wamfahamu Angel kwasasa kwani akili ya mwanangu wataivuruga sana kama kaka yao alivyotaka kuvuruga ndoa yangu”“Kheee pole sana”Basi kufika mbele alishuka na kukodi bajaji ambayo ilimrudisha hadi nyumbani kwake, ila muda anashuka nyumbani kwake mumewe alimuona maana nae ndio alikuwa kafika na gari lake na kuingia nae ndani.Walivyofika ndani alimuuliza vizuri ili amueleze kuwa alitoka wapi na bajaji kwa muda huo, basi mama Angel alimueleza kila kitu na mtu waliyekutana nae hadi akapanda bajaji,“Ila mke wangu, Angel ana haki ya kufahamu ndugu zake ujue? Maana kuna leo na kesho, je Angel akitembea na kaka yake itakuwaje? Maana huyo Rahim nadhani alikuwa na watoto kila kona”“Nitakuwa makini kuhusu hilo, sitaruhusu Angel atembee na ndugu zake ila siwezi kuruhusu Angel awe karibu nao kwasasa, nasubiri afike chuo ndio nimwambie maana nitakuwa naichanganya akili yake kwasasa”“Ila fikiria pia kuhusu hilo kuwa kuna muda ukweli utajulikana tu, ni kweli Angel namlea kama mwanangu na kamwe haitakuja kubadilika hilo, nitampenda Angel siku zote za maisha yangu, kabeba jina langu na ukooo wangu ila bado anahitaji kujua ukweli wa ndugu zake, hata kama walimtelekeza mwanzo ila kuna umuhimu way eye kutambua ukweli wote. Halafu itapendeza zaidi kama ukiamua kunizalia mtoto mwingine mke wangu”“Mmmh jamani kwa umri huu kweli nianze kubeba mimba jamani? Wakina Erick wana miaka kumi na tatu ndio wapate mdogo wao kweli?”“Ndio, kwani tatizo liko wapi, nizalie mtoto mwingine, nimetamani sana kuwa na mtoto mdogo ndani ya nyumba, nakumbuka kipindi kile wakati Angel mdogo nilikuwa nacheza nae na kufurahi nae, kipindi mapecha wangu wadogo nilikuwa nacheza nao na kufurahi nao ila kwasasa hata na wao wanaona aibu kuja kuongea nami mambo ya kijinga waliyokuwa wakiongea muda wote, nizalie mke wangu jamani”“Kwa umri huu!”“Kwani umri kitu gani jamani? Tutamlea mtoto wetu huyo, na uzuri wakina Angel wapo basi nao watatusaidia kumlea, ila natamani sana tuwe na katoto kadogo humu ndani”“Ngoja, nitafikiria hilo swala. Nilijua nimemaliza kuzaa jamani, ila ngoja nitafikiria mume wangu”“Sawa mke wangu fikiria kuhusu hilo, yani tambua nina uhitaji sana wa katoto kadogo mke wangu”“Sawa, nimekuelewa”Mama Angel aliona mumewe akimpa mawazo mengine sasa, akajifikiria jinsi atakavyokuwa na mimba tena, je ataweza kukimbizana na wakina Angel maana ndio kama masikio yao yaliwekwa pamba kwa kipindi hiko, ila kwa upande mwingine alifikiria na kuona ana haki ya kumfurahisha mume wake, ila akaona ni vyema akaongee na mama yake kwanza kuhusu hilo.Kesho yake watoto walijiandaa kwenda shule, na mama Angel alitoka na Angel na kumpeleka kwenye shule mpya aliyomtafutia, aliweza kupata nafasi kwa haraka maana alifahamiana na mwenye shule ambaye alikuwa ni rafiki wa mume wake, basi alimkabidhi Angel hapo huku yeye kuendelea na taratibu zingine, ambapo alirudi tena katika shule ya awali aliyokuwa akisoma Angel ili kufanya taratibu vizuri za uhamisho, nao walimu hawakukataa sababu hali halisi na wao waliiona kwa Angel pale shuleni.Alipomaliza hayo, sasa aliamua kwenda kwa mama yake ili akamsalimie na akaongee nae kuhusu jambo aliloambiwa na mumewe. Alifika kwao na kumkuta mama yake na kumfurahia sana, mama yake hakuishi na yeyote kwa kipindi hiko zaidi ya msichana wa kazi tu ambaye alikuwa akimsaidia kazi za hapa na pale kwani yeye kidogo umri ulienda enda,basi alianza kuongea nae,“Nilijua utaniletea wajukuu zangu jamani Erica, sasa mbona umekuja mwenyewe?”“Nitawaleta tu mama, hata usijali”“Juzi nilikuwa kwenye kile chumba ulichokuwa unalala, jamani miaka inaenda sana hii, nikajikuta namkumbuka Angel kipindi kile alipokuwa mtoto na vile vituko vyake, hivi Angel alikuwa anaongeaga nini na babake kwenye simu kipindi kile? Nimekumbuka na kucheka sana, maana alikuwa akianza mpaka utamtafuta ili aongee nae”Mama Angel nae alicheka na kumwambia mama yake,“Tena umenikumbusha, ngoja nitamuuliza mume wangu kuwa alikuwa anaongea nini na Angel wakati mdogo maana si kwa mtoto kung’ang’ania kule kuongea na babake kama anaelewa vile”“Yani ila nimewakumbuka sana wanangu, tulikuwa tukiishi vizuri sana, kidogo tu ushanikorofisha na kuniumiza kichwa”“Mmmh jamani mama unayo hadi leo hayo mambo jamani, itakuwa ndiomana Angel ameanza kunisumbua pia, yani hapa nimeshamuhamisha shule ndio nilikuwa nashughulikia hayo mambo, mtoto ananiumiza kichwa yule balaa”“Kafanyaje tena?”Mama Angel akacheka na kumwambia mama yake,“Mambo yale yale ya mapenzi ambayo yalinifanya mama yake akili iniruke”“Ooooh maji hufata mkondo, yani kuna mambo huwa tunayatenda katika maisha lakini yakitugeukia tunaanza kulaumu, ila mimi sikuwa hivyo kwahiyo usifikiri kuwa wewe ulirithi kwangu hapana, ila huyo Angel karithi kwako kuwa makini sana mwanangu, mambo ya kuletewa mimba mapema hivyo hapana jamani. Bora mimi nilishakuwa na ujukuu tayari, ila wewe wa kuwa na mtoto mdogo mwingine halafu mwanao akuletee ujukuu jamani! Pole mwanangu”“Asante mama, eeeh tena umeongea jambo lingine nililotaka kukwambia, eti baba Angel anataka nizae mtoto mwingine”“Ndio zaa, mtu kizazi unacho kwanini unakibania kwa mumeo? Zaa jamani, mumeo anakupa kila hitaji utakalo, kwanini usimzawadie watoto? Eeeh! Kumbuka Angel sio wake, yani watoto wake ndio wale mapacha tu kama jicho vile, hebu mpatie watoto wengine”“Mama nawe”“Sio mama nawe, usiwe kama dada yako, yani anaona Junior anamtosha, ukimwambia zaa na mumeo utasikia oooh yule mwanaume ana watoto watatu tayari, ndio ana watoto watatu ila ni vizuri akipata nae mtoto pia, mngekuwa hamna vizazi sawa, ila vizazi vipo sema kuzaa hamtaki, hebu mzalie mumeo nae afurahi jamani! Sasa anateseka na kazi kiasi hiko ili iweje? Mtafutie mtoto apate sababu ya kuendelea kuchakarika”“Ila watoto si wapo wale mama?”“Hawatoshi, muongezee mmoja mumeo afurahi”“Kwa umri huu mama”“Hebu nenda huko, una miaka mingapi ya kushindwa kuzaa? Hebu nenda kamzalie mumeo jamani”“Sawa mama nimekuelewa”“Sio kunielewa tu ila fanyia kazi nilichosema hapa, maana kunielewa tu haitoshi”“Sawa mama, nasikia mtoto wa dada kafukuzwa na mumewe kisa amemzaa na mwanaume mwingine?”“Unadhani mume afanyeje sasa hapo? Mara nyingine tunaweza kulaumu bure tu, ila hakuna kitu kinauma kama kusalitiwa ndani ya ndoa, muache akae kwao labda akili imkae sawa”“Mmmh sawa mama”Basi aliongea pale na mama yake na mwisho wa siku akamuaga na kuondoka zake kwani alishakipata alichokuwa akikitaka, yani alitaka tu kusikia mama yake akimwambia kuwa ni sahihi kwa yeye kuzaa tena au si sahihi kwa yeye kufanya hivyo.Angel kwenye ile shule mpya, alijitahidi sana kuzoea yale mazingira na kweli alikuta wanafunzi wapo makini sana, na alitambulishwa na kukaribishwa vizuri sana darasani. Haikuwa kama shule aliyotoka maana ile ilikuwa muda wote walimu wanafundisha na wakitoka basi wanakuwa wameacha maswali ya kujadili darasani yani jioni kabisa ndio walitoka shuleni na mama yake ndio alipita kumchukua ili kurudi nae nyumbani.Basi akiwa kwenye gari alimuuliza kuwa anaionaje shule mpya aliyoenda,“Eeeh vipi shule, umependa mazingira yake, wanafunzi, walimu vipi unaionaje?”“Hii shule inaonekana wapo makini sana mama, yani wanafunzi ni kujadiliana tu darasani, sijaona mambo mengine sijui kwa siku za usoni huko ila ipo vizuri”“Hujakumbuka marafiki zako?”“Marafiki wenyewe ndio wale wakina Hanifa, hata siwataki tena. Rafiki yangu ninayemkumbuka ni Yusra tu basi maana alikuwa akinipenda na akinielekeza yaliyo sahihi”“Sawa mwanangu, nahitaji usome kwa bidii, kuanzia kesho utakuwa ukiletwa na yule dereva na ndio atakuwa akija kukuchukua. Angel mwanangu nahitaji usome na ufike mbali, unataka kuwa nani badae?”“Nataka kuwa Mwanasheria”“Basi zingatia masomo ili ndoto zako zitimie”Walifika nyumbani na moja kwa moja Angel alienda chumbani kubadilisha nguo na kwenda kufanya maswali ambayo alipewa na mwalimu wake, ila muda huo Erica na Erick nao walikuwa wamesharudi.Basi Erica alimfata mama yake na kuanza kumwambia kuhusu Elly,“Jamani mama huyo Elly anachekesha huyo yani ana vituko”“Kafanyeje kwani?”“Kuna mwanafunzi mmoja huwa anapenda sana kuongea na mimi anaitwa Abdi, basi leo wakati akiongea na mimi akaja Ellyn a kumwambia Abdi, ole wako umtongoze dada yangu nitakuvimbisha makalio”Basi Erica akaanza kucheka tena na kumwambia mama yake,“Halafu akamchora mtu kwenye karatasi ana makalio makubwa na kusema eti ndio Adbi yule akijaribu kunitongoza”Alicheka tena na kumpa ile karatasi mama yake, ambaye nae alicheka baada ya kuiona ile karatasi na kusema,“Inaonyesha huyu Elly ana vituko sana”“Yani ana vituko huyo balaa, ukimuona mama siku hiyo utacheka sana”“Haya mwanangu, nitafurahi kumfahamu Elly”Kisha Erica ndio akaondoka sasa, yani mama yake akacheka sana kwani mtoto wake huyo ilionyesha kuwa hawezi kufanya kitu bila kusema.Siku hiyo usiku wakati wanajiandaa kulala, simu ya mama Angel ilianza kuita alipoangalia aliona kuwa ni wifi yake ndio anampigia basi alianza kuongea nae,“Wifi za siku?”“Nzuri tu, jamani kwani vibaya kwa watoto wangu kukaa kwa shangazi yao jamani! Mbona dadako ananifanyia hivi jamani!”“Sio vibaya, ila na wewe umezidi yani tangu uondoke hadi leo hujarudi unategemea nini? Na tunasikia kuwa upo kula bata tu, ulikuwa wapi kula bata hapo nyuma jamani! Haya mambo ya kugundua stepu wakati mziki ushaisha ni mabaya sana”“Umeanza maneno yako ya karaha, hivi kwani huwezi kuongea vizuri bila maneno ya karaha, kwahiyo ulitaka nami kaka yako anikute na mtoto kama ambavyo kaka yangu alikukuta wewe na mtoto?”“Kheee nimeshindwa”Kisha mama Angel akamkabidhi mumewe simu na kumwambia kuwa aongee na huyo wifi yake,“Ongea mwenyewe na dada yako”Mumewe akachukua ile simu na kuanza kuongea nayo,“Na bora umepiga, yani nilitaka nikupigie mwenyewe, kwanini dada yangu unafanya mambo ya ajabu kiasi hiko? Kwanini lakini? Wale si watoto wako, wewe ndio unajua uchungu wake, kwanini kutaka kumsumbua mwenzio kisa ni shangazi yao”“Ila yeye hana mtoto mdogo pale, kwahiyo nimempelekea ili wamchangamshe”“Mjinga wewe, angewataka si angewaomba mwenyewe? Hana mtoto mdogo sababu hajaamua kuwa nae sio kwamba anataka watoto wako wakachangamshe nyumba yake, yani Tumaini nakwambia hivi dada yangu mpaka kuisha kwa wiki hii nikikuta hujaenda kuwachukua watoto wako basi nitawabeba na kuwapeleka kwa mama yako, huwa sipendi ujinga kabisa mimi. Huo ujinga usifanye”“Jamani Erick”“Hakuna cha jamani wala nini, jitahidi urudi ukachukue watoto wako, yani mimi nitauliza hadi Jumamosi nikiona hujaenda kuwachukua basi nawabeba wote na kuwapeleka kwa mama yako, huo ujinga sitaki kuusikia kabisa, wewe ni dada yangu ila wakati mwingine hebu jiongeze basi, unatesa wenzio kwakweli”“Sawa nimekuelewa”Kisha Tumaini akakata simu na kumfanya baba Angel kumkabidhi mkewe ile simu huku akisema,“Yani huyu dada yangu asinitanie kwakweli, atashangaa tu nikipeleka watoto wake kwa mama yake”Mama Angel hakuongeza neno kwani alitaka mumewe abaki na maamuzi anayoyataka.Siku hiyo kama kawaida watoto walijiandaa na kwenda kwenye shule ambazo walikuwa wanasoma, ilikuwa ni siku ya Ijumaa kwahiyo kila mmoja alijua wazi kuwa siku ile huwa ni fupi sana na Angel nae alikuwa shuleni kama siku ya kwanza kwa Ijumaa kuwepo katika shule ile.Basi aliendelea na masomo yake kama kawaida, ila hawakuwahi kutoka na kupewa tena maswali na kazi mbalimbali za kufanya hapo shuleni.Hadi jioni kama kawaida ndio walitoka na dereva wao alifika kumchukua na kuondoka nae.Walipofika getini Angel alishtuka sana, kwani alimkuta Hanifa akiwa na Samir pale nje kwao inaonyesha Samir aliamua kumfata kwao.Walipofika getini Angel alishtuka sana, kwani alimkuta Hanifa akiwa na Samir pale nje kwao inaonyesha Samir aliamua kumfata kwao.Angel alimuomba dereva amshushe, basi yule dereva alimshusha Angel halafu Angel akawa anawafata Samir na Hanifa ili kuwaambia waondoke maana anaelewa kama mama yake akiwakuta hapo itakuwa balaa tupu, ila wakati anawasogelea, Samir alimuona na kuinuka pale nje ya geti na kumfata Angel kisha akamkumbatia kwa nguvu sana na kumwambia kuwa,“Angel nakupenda, siwezi mimi kuishi bila ya wewe”Huku akimbusu kila sehemu katika mwili wake, muda huo huo mamake Angel nae alikuwa akirudi kwahiyo aliona jinsi Angel alivyokumbatiwa na Samir pale nje ya geti, kwakweli alichukia sana na kushuka kwenye gari kwa hasira.Akawafata karibu na kuwaachanisha kwa hasira kisha alimkunja Samir na kumwambia,“Sasa wewe mtoto nadhani unataka kunitibua uzazi, haya naomba upambane na mimi!”Samir nae akamjibu,“Kwani mama nimekuja kupambana na mtu hapa!! Nimekuja kumuona Angel sababu nampenda sana”Mama Angel alizidi kupata hasira na kumsukuma Samir ambaye alianguka chini, halafu alimsogelea Hanifa na kumnasa kibao, kisha akamshika mkono Angel na kuingia nae ndani yani gari yake alimtuma tu dereva aende kuiingiza, yani siku hiyo alikuwa na hasira sana alijikuta akimsukuma tu mwanae kuingia nae ndani, moja kwa moja alienda kujifungia nae chumbani na kuanza kumwambia,“Siku zote huwa nakwambia nitakupiga nitakupiga ila huwa sikupigi, yani leo ndio nitakupiga Angel, unaniletea ufedhuli ndani ya nyumba yangu!!”Mama Angel alichukua mkanda wa suruali wa mume wake na kuanza kumtandika nao Angel, yani Angel alikuwa akipiga makelele tu ya kuomba msaada.“Mama nisamehe, mama utaniua”Ila mama yake alikuwa akimpiga kwa hasira alizokuwa nazo maana yeye alihisi kuwa Angel ndio kawaita Hanifa na Samir, wala hakuwaza vingine zaidi ya hivyo, basi Vaileth alienda mlangoni huku akigongea mama Angel mlango na kumsihi amsamehe Angel,“Mama nakuomba msamehe Angel, nakuomba mama”Erick na Erica nao walienda mlangoni kwa mama yao huku wakionyesha kulia na kuomba mama yao amsamehe dada yao kutokana na makelele ambayo Angel alikuwa akiyapiga, kwa bahati Erick alikumbuka jambo na moja kwa moja alienda kwenye chumba ambacho baba yao huwa anahifadhi funguo za ziada, kisha alisogea pale mlangoni na kufungua mlango, moja kwa moja alimkimbilia dada yake chini ambapo alikuwa akipigwa na mama yao, kiasi kwamba zile fimbo za mikanda zilikuwa zikishuka katika mwili wake ila hakujali zaidi ya kumtoa Angel kutoka kwenye mikono ya mama yao, yani ilionyesha kuwa mama yao alikuwa na hasira sana kwani walipomtoa Angel nae alifunga mlango na komeo la ndani kabisa, alikaa chini na kuanza kulia sana yani alijikuta akilia mno huku akisema,“Hivi kosa langu ni nini jamani! Kwanini mimi inanitokea hivi, tuseme siwezi kulea au ni kitu gani jamani! Mbona wazazi wengine wanatulia na watoto wao, haya maswala ya kuzaa na wababa wasiojielewa ndio yameenda kuibuka kwa mwanangu Angel, kwanini anisumbue hivi,? Nimeacha hela ngapi katika shule niliyomtoa? Nimetoa hela ngapi katika shule niliyomuhamisha? Kwanini jamani, kwanini mimi?”Alilia sana hadi alizimia pale pale sababu ya kulia kwa hasira.Hanifa akiwa bado nje na Samir, alimshika mkono Samir ili waondoke ambapo bado Samir alikuwa akigoma, basi Hanifa alimwambia,“Samir, sitaki kesi ujue, babake Angel akitukuta hapa kuna mawili yatatokea, either tupelekwe monchwari au tupelekwe ICU, mimi sipo tayari kwa lolote kati ya hayo”Basi alimshika mkono na kumlazimisha kuondoka, mwisho wa siku aliondoka ila kishingo upande kwani bado alikuwa akitamani kukaa hapo hapo kwakina Angel.Wakina Erick walimpeleka Angel chumbani kwake huku akilia na akiwa na alama za mikanda ambayo mama yake alikuwa akimtandika nayo,basi Vaileth ndio alibaki nae chumbani huku akijaribu kumuweka sawa kisaikolojia na kumpooza na vile viboko alivyochapwa na mama yake,“Angel usimchukie mama yako, kafanya kwa hasira hakujua. Msamehe bure”“Ila mimi hakuna kibaya nilichofanya jamani, mimi nimetoka shule na wale nimewakuta nje ya geti yani najilaumu kushuka kwenye gari kwani nilikuwa nawaambia waondoke wasije kutwa na mama, ona sasa kilichonipata mimi”Angel alikuwa akilia na Vaileth alikuwa akimbembeleza huku akijaribu kumtia moyo kwa kile kilichotokea.Wakina Erick walivyoona kimya chumbani kwa mama yao wakapatwa na wasiwasi, yani muda huo huo walienda kwenye simu yao ya mezani na kumpigia baba yao na kumueleza kilichotokea, ndani ya muda mfupi tu baba yao alikuwa nyumbani ila mlango haukufunguka maana mama Angel aliufunga ndani kwa komoe, ilibidi mumewe ajitwike ufundi na kuvunja ule mlango wao, kwakweli alimkuta mkewe chini amezimia, na yeye alihisi kiwewe, moja kwa moja alienda kumuamsha mkewe ambaye hakuamka wala nini,kwakweli alipatwa na mashaka pia ila alipomuangalia vizuri aligundua kuwa kazimia basi akamwagia maji na kumfanya azinduke, alikuwa akishangaa shangaa tu basi mumewe akawaambia wote watoke na kuongea na mkewe,“Naomba ujiandae muda huu tunatoka”“Tunaenda wapi mume wangu?”“Jiandae tu utajua tunapoenda”Basi mama Angel aliinuka ila alijaribu kukumbuka vizuri aliona hakumbuki zaidi ya kichwa kumuuma tu,aliamua kwenda kuoga na muda huo wakati anaoga mumewe alienda kuzungumza na Angel ili kujua kuwa ilikuwaje, ambapo Angel alimueleza huku akilia, basi alimkumbatia mwanae na kumwambia kuwa yataisha tu na kila kitu kitakuwa sawa,“Mwanangu usijali, nakuomba umsamehe mama yako ana hasira sana. Unajua tumemkuta kazimia eeeh!”Angel alishtuka kusikia kuwa mamake alizimia basi mamake akamtoa uoga,“Ila usiogope wala usijali kwani anaendelea vizuri kwasasa, mimi na yeye tunatoka kwahiyo mtabaki na dada yenu hapa naomba mmuheshimu na mumsikilize. Pole mwanangu”“Asante baba”Basi baba yao alitoka mule chumbani kwa Angel na kurudi chumbani kwao huku akijaribu kurekebisha mlango ambao aliuvunja kidogo ila mama Angel alipotoka bafuni alimuuliza mumewe“Vipi huo mlango umefanyaje?”“Aaaah achana nao, nitamuita fundi aje aurekebishe, basi malizia kujiandaa mke wangu tutoke”Na kweli alijiandaa na wakatoka huku akimuachia maagizo Vaileth kuwa awaangalie vizuri watoto wake.Wakati gari ikitoka nje ya geti lao alijikuta akikumbuka kila kitu huku akiangalia mara mbili mbili, aliuliza.,“Angel yuko wapi?”“Tukirudi nyumbani utamkuta”“Unajua huyu mtoto kanikera sana leo, hujui tu”“Wewe ndio hujui tu, hivi mama yako angekuwa anakupiga kiasi ambacho umempiga Angel ingekuwaje? Mama yako alikuwa anakupiga ila kwa kiasi sio kwa stahili hii mke wangu, utaua mtoto nakwambia, hasira ni hasara, twende tu ukapunguze mawazo kwanza"“Hivi nimempiga sana eeeh!”“Tena sio ya kuongea maana hadi umemtoa alama mtoto, unataka kumuharibu sura halafu utamuoa wewe? Mbona sura yako haikuharibiwa jamani!”“Kwahiyo wewe ulinipendea sura?”“Mapenzi hayachagui kitu kikoje, huo upendo wa dhati unatoka moyoni, kama sura ni wanawake wangapi wenye sura nzuri ambao nilikutana nao ila sikuwataka nikakutaka wewe!”“Kwahiyo mimi sio mzuri eeeh!”Mama Angel alionekana kuchukia na mumewe akamwambia,“Yani tatizo lenu ndio hilo wanawake, mtu akisema hivi basi wewe unasema vile, nimesemea uzuri umeanza kusema kwahiyo mimi umenipendea sura, nakwambia kupenda kunatoka moyoni unasema kwahiyo mimi sio mzuri, jamani mama Angel sisi ni watu wazima sasa, hebu tuachane na hayo mambo ya kijinga”“Kumbe unaniona mimi mjinga!”Muda huu ndio alinuna kabisa ikabidi mumewe aanze kumbembeleza,“Sijasema wewe ni mjinga mke wangu, hivi ningeanzaje kuoa mwanamke mjinga jamani!! Mke wangu wewe ni mwanamke wa kipekee una akili sana ndiomana sikutaka kukuacha kwakweli, nimepigani penzi langu mno na wewe ni shahidi wa hilo, na kuhusu uzuri, kwakweli mke wangu wewe ni mzuri kuliko wote ulimwenguni, umerandisha hadi watoto wamekuwa visura wanavutia ndiomana wameanza kufatiliwa wakiwa wadogo, kwakweli kama kuchagua mimi ni namba moja maana nimeona kisura, mrembo, mzuri na mwenye akili yani sifa zote nzuri unazo mke wangu”Kisha baba Angel alisimamisha gari kidogo na kumbusu mke wake, yani ile kitu ilimfanya mama Angel ajihisi ufahari sana, kwakweli alifurahi sana na alikuwa akitabasamu tu huku baba Angel alkiendelea na safari sasa.Basi walifika kwenye hoteli na kushuka kisha wakakaa na kuagiza chakula ambapo walikuwa wakila na kuongea mambo mbalimbali,“Sasa mke wangu, nikuombe kitu kimoja”“Kitu gani hiko?”“Unaonaje Angel akimaliza kidato cha nne tumpeleke Africa kusini”“Mmmh hapana jamani, inamaana hutaki kumuona Angel nyumbani eeh!”“Sina maana hiyo mke wangu, ila nilitaka kumtenganisha na hawa wanaume wakware”“Kwani huko Afrika kusini hakuna wakware? Ningekuwa naenda kuishi nae sawa, ila kwenda kuishi peke yake hapana jamani, nataka nione watoto wangu wote pamoja, ila ninapokosea kwenye malezi nijue mume wangu”“Sawa, nimekuelewa mke wangu. Ila nilikuwa natoa wazo tu hilo”“Huko tuendage sisi wenyewe, ila watoto wangu hapana jamani”Mara mama Angel alishangaa kushikwa bega, kugeuka hivi ni mtu ambaye alikuwa akifahamiana nae vizuri sana, ambaye alimwambia kwa mshangao,“Kheee Erica!”“Jamani Fetty kumbe upo!”Basi walikumbatiana kwa furaha kisha Fetty alikaa na kumsalimia baba Angel pia huku akisema,“Kweli nimeamini katika dunia kuna mapenzi ya dhati, kwa hakika nyie mlipendana yani hadi leo mpo pamoja?”Mama Angel na baba Angel walitabasamu huku baba Angel akimwambia,“Ndio, penzi la kweli lipo ila cha muhimu ni kumpata mtu ambaye atakupenda kweli na utampenda kweli. Katika mapenzi si vizuri kukurupuka, yani ukikurupuka lazima ukutane na mauzauza na mbeleni yakakushinda”“Kweli kabisa uyasemayo, kama mimi najuta kukurupuka kuolewa”Mama Angel alimuuliza,“Kivipi? Si uliolewa na Bahati wewe?”“Ndio, nilijua atanipenda na kunijali vile alivyokuwa akikupenda wewe na kukusumbua kumbe hakuna kitu wala nini?”“Kheee jamani, tena nimekumbuka kuhusu Bahati (Kisha akimuangalia mumewe na kumuuliza) Hivi yule Samir sio mtoto wa Bahati kweli? (Alimuangalia Fetty na kumuuliza) Bahati hana mtoto wa kuitwa Samir?”“Kafanyeje huyo Samir?”“Ni anamsumbua mwanangu balaa, yani hadi kichwa kinaniuma sababu ya huyo mtoto, haogopi kitu na haogopi mtu yeyote, yani anachojua yeye ni usumbufu tu basi”“Duh! Pole, huyo Samir simfahamu labda kama alizaaga na kumficha ila kuna mambo ya Bahati yanatia hadi kichefuchefu”“Mambo gani hayo?”“Yani huwezi amini, Bahati alizaa na yule mkewe aliyemuacha na kunioa mimi, kumbe alizaa pia na mdogo wa mke wake, halafu kumbe Bahati alimbaka mama mkwe wake na yule mama akapata ujauzito na kwenda kuutoa ila kumbe iligoma kutoka, kwahiyo Bahati kazaa na familia nzima, yani ninavyokwambia hadi kichefuchefu kuanza kufikiria hayo”“Mmmh mbona mtihani huo pole”Baba Angel aliwaaga kidogo kuwa anakwenda maliwatoni kwani aliona hao wanawake hawakawii hata kuzungumzia na yeye, basi aliondoka na kuwaacha pale ambapo Fetty aliendelea kuongea,“Asante shoga yangu, kikweli nimechoka yani nimechoka kabisa, maana hao watoto wote wamebwagwa pale nyumbani, halafu kumbuka mimi nina mtoto pia nilizaa na yule kichwa rungu, kwahiyo jumla wanne, halafu Bahati nimezaa nae watoto wawili jumla watoto sita, na sijui huko nje kama hana watoto wengine, umenipa habari zakina Samir tena kichwa kinanipasuka hapa”“Kwahiyo wewe umekuja hapa hotelini mwenyewe?”“Ndio, nimekuja kupumzisha mawazo jamani, ile sio ndoa bali ni ndoano, yani kukurupuka huku kubaya sana. Leo alikuja yule mama mkwe wake, uwiii katukana jamani, katukana mkoo wangu mzima, kiukweli najuta kumfahamu Bahati, najuta kuolewa nae”“Ila wewe ulikuwa huyajui hayo wakati unaolewa nae?”“Mimi nilijua tu kazaa na yule mke wake, na vile mkewe alikuwa mshirikina basi niliona ana sababu madhubuti kabisa ya kuachana na mkewe. Kuna kipindi alikuwa akinisumbua hatari wakati nina mimba ya huyu mtoto wa mwisho, si ndio wakanibwagia watoto wote, nimepata shida shoga yangu balaa. Ila wanaume hawa sio wa kuwaamini jamani, mwanaume sio mama yako wala sio baba yako”“Ila mimi mume wangu namuamini”“Usimuamini kivile, siku ukiletewa mtoto aliyezaa huko wapi sijui nadhani utapata ugonjwa wa kupooza, jamani usimuamini mwanaume, ni kweli anakupenda ila usimuamini kupitiliza. Hebu ona toka ameenda chooni hadi sasa hajarudi mmmh!”“Mmmh na wewe Fetty jamani, hadi shemeji yako unamnanga mmmh!!”“Hivi kwanza Bahati hajakusumbua? Kuna kipindi wimbo wake ulikuwa ni wewe, oooh mke wangu alikuwa ni Erica, sijui Erica ndio aliumbwa kwaajili yangu, jamani mwanaume ana wazimu yule sijapata kuona”“Mmmh makubwa”Muda huo huo baba Angel alitoka maliwatoni na kwenda pale kwenye meza ambapo alimtaka mkewe waondoke, kwahiyo mkewe na Fetty walibadilishana namba, kisha wakamuaga pale,“Ila na mimi ndio narudi kwangu”Basi wakaagana nae na kuondoka eneo lile.Fetty alirudi kwa mume wake ambaye alianza kumfokea kwa kitendo cha kuchelewa kurudi,“Kweli kabisa mke wa mtu ndio unarudi nyumbani kwako muda huu!”“Kumbe ulikuwa ukifurahia yale matusi ambayo mama mkwe wako alikuwa akinitukana mchana? Ulikuwa ukifurahia eeeh!”“Kheee mke wangu jamani! Nina haki ya kukuhoji”“Haya na mimi nina haki ya kukuhoji, niambie Samir umezaa na mwanamke gani?”“Samir??”“Ndio, usijifanye humjui mtoto wako, yani ningekujua toka mwanzo wewe mwanaume sidhani kama ningekubali kuolewa na wewe, sijui ndio unataka kuanzisha timu ya mpira jamani! Haya Samir umezaa na nani na yuko wapi?”“Jamani, watoto wangu wote wapo hapa nyumbani, sina mtoto wa kuitwa Samir”“Hivi wewe kumbuka siku watoto wameletwa hapa nyumbani ulisemaje? Ulisema kuwa ulipewa madawa na ukawa unatembea tu na wanawake, sasa unashangaa vipi kuhusu mtoto wako Samir? Yani najua kuolewa na wewe jamani, natamani nirudishe miaka nyuma ili nisikubali hata ndotoni kuolewa na wewe. Nakiri wazi sikupendi”“Jamani mke wangu, toka nakuoa unaelewa kabisa hali halisi inayoendelea kwangu, ni wewe ndio ulikuwa ukinieleza mambo ya kufanya, na hata wakati nataka kuteleza tena ulikaa chini na kunionya huku ukinielekeza mambo sahihi ya kufanya, sasa ni nini cha kufanya mimi na wewe tugombane? Ni hao watoto? Kwani historia yake sijakwambia? Bora ningekuwa sijakwambia ila nimekueleza kila kitu mke wangu yani hakuna kitu katika maisha yangu ambacho hukifahamu mke wangu. Nakupenda na ninapenda tuishi kwa upendo, hivi ningekuwa na mtoto wa kuitwa Samir si ningekwambia mke wangu jamani! Kwanini nikufiche sasa kitu kama hiko!”Fetty hakutaka kumsikiliza mumewe kwani alijua kuwa anaongopewa tu na mumewe ila huyo Samir ni mtoto wake, ingawa hakumuona ila aliamini kuwa Samir ni mtoto wa Bahati baada ya kuambiwa na mama Angel.Kulipokucha, baba Angel alimwambia mke wake,“Hivi leo si ndio Jumamosi?”“Ndio leo ni Jumamosi, kwani kuna nini?”Subiri, baba Angel alienda kujiandaa na baada ya hapo alimuaga mke wake kuwa anatoka ila alimwambia jambo moja,“Jitahidi leo uzungumze vizuri na mtoto maana umemuweka katika mazingira ya uoga, mwambie ni jinsi gani unaumia kuona yeye akitaka kuharibikiwa, ila usimfanyie ukali tafadhali’“Sawa nimekuelewa”Basi baba Angel akaondoka ila hakumwambia mkewe anapoelekea kwani alijua fika lazima angemkatalia tu.Basi mama Angel nae aliinuka na moja kwa moja kwenda chumbani kwa Angel ambaye alikuwa akilalamika kuwa viungo vinamuuma kutokana na zile fimbo alizochapwa na mama yake,“Pole sana mwanangu, yani mama yako nilikuwa na hasira sana kwa muda ule. Fikiria ni hela ngapi nimepoteza kwaajili ya elimu yako, halafu nikukute katika hali ile kwakweli nilichukia”“Lakini mama ungeniuliza kwanza ili nikuelezee”“Sasa ningekuuliza nini pale? Ningekuuliza kama na wewe unampenda Samir au kitu gani?”“Hapana mama sio hivyo, ila ungeniuliza kama nami nimekubaliana na wale kuja, kwani hata mimi pia nilishangaa kuwaona nyumbani kwetu mama, kwakweli sikutegemea”“Labda nikuulize hivi, je na wewe unampenda Samir?”“Mama jamani!”“Sio mama jamani, nijibu”“Hapana mama, mimi bado mwanafunzi. Nahitaji kutimaza malengo yangu na ndoto zangu”“Sawa, ngoja nikuuliza kitu kingine. Je kuna chochote ambacho huwa unahitaji nakunyima?”“Hapana mama, kila kitu unanipa”“Unaweza sema mbona simu nimekunyang’anya ila nimekunyang’anya simu baada ya kukuta ukiwasiliana na hao wajinga wakina Samir na wakina Hanifa, mwanangu nakupenda sana jamani, yani sitaki nikupoteze kwa mambo ya kijinga, hebu thamini upendo wangu japo kidogo kwa kuniheshimu. Nakupenda mwanangu naomba ujithamini pia na ujiheshimu. Sina mengi ya kukwambia ila nakupenda sana mwanangu”Angel alifurahia maneno ya mama yake na kumkumbatia kwa furaha.Baba Angel moja kwa moja alienda kwa mama Junior yani dada yake na mama Angel, basi alifika pale na kumkuta nyumbani kwake amekaa huku akionyana na mtoto wake, basi akawasalimia pale na kuuliza nini tatizo,“Jamani shemeji, tatizo ni huyu Junior, ananiumiza kichwa kwakweli hata sijui nifanyeje nae. Maana mtoto ana mambo ya ajabu sijapata kuona, hapa mtaani hakuna mtu asiyemjua Junior jamani”“Wewe Junior, kwanini unafanya mambo ya ajabu kiasi hiko?”Junior aliangalia chini kwa aibu kwani kwa upande mwingine alikuwa akimuogopa baba yake mdogo huyu, kisha baba Angel alimwambia,“Haya muombe msamaha mama yako kwa yote uliyomfanyia na useme mbele yangu hapa kuwa hutorudia tena kufanya ujinga wa namna hiyo”Basi Junior alimwambia mama yake,“Mama nisamehe, sitarudia tena”Ila baba Angel alimwambia kwa ukali tena,“Msamaha gani unaomba hivyo? Hebu piga magoti huko”Basi Junior alipiga magoti kwa mama yake na kumuomba msamaha mama yake, yani mama yake alishukuru sana kwa ujio wa shemeji yake huyu. Junior hakuweza kufanya kiburi kwa bamdogo wake huyu kwani mara nyingi huwa anamfata akiwa na shida ya hela halafu huyu baba yake mdogo anamsaidia.Basi mama yake alimwambia kuwa amemsamehe pale na kisha baba Angel alimtaka kwenda kujisomea, nae Junior alifanya hivyo basi mama yake alianza kuongea pale,“Nashukuru sana umekuja yani huyu Junior ni wawili tu ndio huwa mnamuweza, wewe na mjomba wake Tony, kwakweli nashukuru sana”“Aaah usijali dada yangu, shemeji yangu usijali tupo pamoja. Eeeeh hawa watoto wa Tumaini wako wapi?”“Wapo, wamelala muda huu. Watoto wavivu hawa hatari”“Naomba kaniitie”Basi mama Junior alienda kuwaamsha na kuwaambia kuwa mjomba wao anawaita, ambapo walitoka wote na kwenda kumsalimia, kisha akawaambia,“Naomba mjiandae na mbebe mabegi yenu maana tunaenda kwa bibi”Wale watoto hawakubisha kwani muda huo huo walienda kujiandaa, kisha mama Junior alimuuliza baba Angel,“Shemeji, unawapeleka kwa bibi? Kivipi?”“Nawapeleka kwa bibi yao ndio, mama yake mzazi na mama yao”“Kheee mwenyewe hataki watoto wake waende kule”“Sikia shemeji nikwambie, yule ni bibi yao haijalishi chochote ila yule ni bibi yao. Halafu kama baba Junior kashindwa kuwapeleka hawa watoto kwao, ngoja mimi nifanye hilo jambo. Naomba usinikatalie maana hawa watoto ni watoto wa dada yangu, mimi ni mjomba wao. Kwahiyo acha tu nifanye hili shemeji”“Mmmh sawa, mimi sina neno”Basi baada ya muda watoto walikuwa wamejiandaa kisha baba Angel aliaga pale na wao wakaaga halafu akaondoka nao.Baba Angel aliwapeleka wale watoto kwa bibi yao na kuwafikisha huku akimwambia,“Mama, Tumaini kanipigia simu kuwa hawa watoto wake niwalete huku”“Jamani, Tumaini anajua fika watoto wake walivyowavivu hawa, si kutaka kunitesa tu jamani!”“Sina jinsi mama, ndio kanituma hivyo, mimi naenda”Basi alimuaga pale na kuondoka zake, na kuona sasa katua mzigo wa dada yake maana akijua kuwa watoto wake wamepelekwa kwa bibi yao basi atafanya hima kurudi kwani anaufahamu uvivu wa watoto wake na hakupenda kumtesa mama yake.Basi baba Angel wakati anarudi nyumbani kuna kijana alimuona njiani,alijikuta akishtuka sana ilikuwa bado kidogo tu amgonge, yani alisimamisha gari kwa haraka sana na kumuuliza yule kijana,“Una matatizo gani wewe? Hebu ona jamani mpaka nimetaka kukugonga, si kesi hizi mnataka kutuwekea?“Samahani baba yangu, ni mawazo tu”“Kijana mdogo kama wewe unakuwa na mawazo ya nini? Ni kitu gani unawaza hadi unakuwa hivyo?”“Nisamehe sana”“Unaitwa nani?”“Naitwa Samir”Baba Angel alishtuka na kumuangalia vizuri yule kijana akamwambia,“Au ndio wewe Samir unayemsumbua mwanangu Angel?”Samir kusikia vile aliamua kukimbia kwani alikumbuka maneno ya hanifa kuwa baba Angel sio wa mchezo mchezo, kama hujapelekwa monchwari basi ICU, yani alikimbia bila kuangalia nyuma.Kwakweli baba Angel alimuangalia yule Samir huku akisikitika sana na kurudi nyumbani kwake.Alipofika kwake alimsimulia mke wake tukio zima,“Kheee lazima ndio huyo Samir ndiomana amekimbia, mtoto mwehu sana yule”“Ndio, ila nimeshtuka sana kumuona”“kwanini?”“Kuna mtu namfananisha nae, yani vile vile alivyo yule mtoto, nahitaji kujua wazazi wake, nahitaji kujua ukoo wake”“Kheee mtu gani? Kafanana na nani?”“Ngoja tu nitakuletea picha za mtu niliyemfananisha nae, yani ni vile vile nahisi ni mwanae”“Mtu gani huyo? Si uniambie, kwahiyo Samir ni ndugu yetu tumkaribishe? Si ndio atatubakia watoto hadi tuzimie”“Sijasema ni ndugu yetu na wala sijasema tumkaribishe jamani! Sijasema kafanana na ndugu yetu ila nimesema kuna mtu kafanana nae, nikikuletea picha zake utasema kweli duniani wawili wawili”“Huyo mtu simfahamu? Mbona mimi sijamfananisha Samir na yoyote?”“Wewe nae una mambo mengi sana mke wangu, ila unamfahamu vizuri kabisa, sema una mambo mengi sana”“Anaitwa nani?”“Nitakukumbusha mambo ya kale bure, naomba tuachane na hayo mke wangu. Vipi Angel anaendeleaje?”“Salama kabisa mume wangu”“Sawa, nimechokaje hapa”“Kwani ulikuwa wapi?”“Kwenye mizunguko yangu tu”Kisha baba Angel aliamua kwenda kulala ili akapumzike kidogo tu.Kulipokucha wakati wakijiandaa kwenda Kanisani, walishangaa asubuhi asubuhi mtu akiita kwa nguvu nje,“Erica, wewe Erica weee”Basi mama Angel alitoka ndani ili kuangalia anayeita, alishangaa kuona ni wifi yake, ambapo walipokutana tu, yule wifi yake alimsogelea mama Angel na kumnasa kibao cha nguvu ambacho kilimpeleka hadi chini.Kulipokucha wakati wakijiandaa kwenda Kanisani, walishangaa asubuhi asubuhi mtu akiita kwa nguvu nje,“Erica, wewe Erica weee”Basi mama Angel alitoka ndani ili kuangalia anayeita, alishangaa kuona ni wifi yake, ambapo walipokutana tu, yule wifi yake alimsogelea mama Angel na kumnasa kibao cha nguvu ambacho kilimpeleka hadi chini.Kwakweli mama Angel alisikitika sana, halafu akainuka na kumuuliza wifi yake,“Kwani kosa langu nini Tumaini?”“Hivi wewe una akili kweli? Utapelekaje watoto kwa mama yangu wakati unajua anaishi mwenyewe? Sawa ni bibi yao ila kwanini usiwapeleke kwa mama yako ambaye ni bibi yao pia”“Jamani sio mimi niliyefanya hivyo, kwanza nashangaa tu maana unanipa lawama nisizozielewa”“Najua ni wewe tu maana akili zako huwa unazijua mwenyewe, hivi unajua kwanini niliwaweka wale watoto kwa mama Junior? Mbona sikuwaleta kwako? Kwanini usijiulize hilo, na kwanini mama Junior asiniambie mwenyewe zaidi ya wewe kamavile ni watoto wako? Unajichukulia maamuzi tu kama kichaa”Tumaini akanyua tena mkono wake ili amzabe kibao tena mama Angel, ila muda huu baba Angel alitoka ndani na kuudaka ule mkono wa dada yake kabla hata haujashuka tena kwenye shavu la mke wake, kisha yeye ndio akamzaba kibao dada yake na kumwambia“Hivi ndio ustaarabu wa wapi huo? Yani unafika kwa watu huna hata salamu unaanza ubondia wako, hivi lini utaacha hayo mambo yako dada yangu! Haya nipige mimi sasa”“Jamani Erick ndio unanipiga mimi dadako!”“Nilishawahi kukwambia na sasa nakwambia tena, huyu mwanamke akiumia ni mimi nimeumia, kwahiyo ukimpiga huyu mwanamke jua kwamba umenipiga mimi. Na sasa nimekuruhusu upigane nami”Basi Tumaini akawa mpole na kuanza kuomba msamaha,“Nisamehe tafadhali ila ilikuwa ni hasira”“Hasira gani hiyo? Huo ni ujinga na sio hasira, halafu unamuonea sana wifi yako, sijui una nini wewe lakini”Kisha baba Angel alimsogelea mke wake na kuwa kama akimpukuta vile kutokana na alivyoanguka, basi yule wifi wa mama Angel aliendelea kuomba msamaha tu,“Nisameheni tafadhari”Basi baba Angel alimuangalia mkewe na kumuuliza,“Je tumsamehe!”“Ndio, mimi sina tatizo nae lolote lile”“Haya sasa, tuambie hiyo hasira yako uliyokuja nayo ilikuwa inahusu nini?”“Samahani tena jamani, yani mimi nilichukia kuhusu watoto wangu, kwanini wapelekwe kwa mama”“Sasa wewe umeuliza ni nani kafanya hivyo? Ila licha ya hivyo si nilikwambia jamani kuwa ukichelewa basi napeleka watoto kwa mamako, najua kule ndio unauchungu nako, hivi kweli wewe unakaa miezi miwili unakula bata huna hata habari na watoto jamani!”“Ila kabla ya yote mngeniuliza kwanza kwanini nimewapeleka kwa mama Junior, mbona sikuwaleta hapa jamani! Haya yaishe maana nimesharudi”“Ila cha muhimu kweli umerudi, na wewe dada yangu kuzamia Arusha kiasi hiko ndio nini jamani!”“Yani mama alivyonipigia simu jana nilihisi kiwewe, ila Erick hufai jamani loh!”Tumaini akawa anacheka mwenyewe, mara wakina Angel wakawa wanatoka ndani maana walishajiandaa kwa kwenda kazini, basi Tumaini alipomuona Angel akasema,“Jamani huyu mtoto kadri anavyokua ndio anavyozidi kuwa mrembo jamani, mfuge mbwa sasa”Baba Angel na mama Angel wakacheka na kumtaka waende nae tu kanisani,“Sawa tutaenda ila tukitoka nahitaji kwenda na wifi yangu mahali”“Kheee mshapatana tayari!”Tumaini akamuangalia mama Angel na kusema,“Eti wifi yangu kwani bado una kinyongo? Wifi yangu mzungu bhana wala hana mambo ya Kiswahili”Mama Angel alitabasamu tu kisha wote wakaondoka na kuelekea Kanisani.Walipotoka kama ambavyo Tumaini alimtaka wifi yake waende pamoja basi alimsindikiza maana hakujua hata anaenda nae wapi, ila alishangaa tu wakienda nyumbani kwa wifi yake ambapo walipofika alimkaribisha vizuri sana kisha akamwambia,“Karibu wifi yangu, kwanza kabisa naomba unisamehe kwa nilichofanya leo kwako sikutegemea kufanya vile yani hasira hizi kweli hazifai, nisamehe wifi yangu. Najua niliapa kutokupiga tena kibao hata sijui leo kimefanyika kitu gani kwangu”“Hamna shida nimekusamehe nakumbuka kuna kipindi zamani uliwahi kuninasa kibao tena nikiwa kwetu”Tumaini akacheka na kusema,“Halafu sikomi tu sijui kwanini, kipindi kile nilidundwa na mama yako na leo Erick kanidunda, jamani hii tabia ya kunasa vibao naiacha rasmi yani wifi yangu hata usijali. Naomba unisamehe tu”“Usijali pia nimekusamehe”“Sasa nimekuita hapa kwangu unisaidie jambo moja tu, ndugu yangu leo kaka yao kuna wageni anakuja nao halafu wale watu wanataka chakula cha tofauti ambacho hawajawahi kula, nakumbuka kuna kipindi ulipika biryani pale nyumbani kwako, naomba na mie unipikie biryani leo yani kila kitu kipo ila ni pishi lako tu ndio ninalihitaji, mimi huwa napika ila najua kwako ndio mwisho, najua watajiramba humu. Nakuomba wifi yangu tafadhari”“Hakuna shida, na watoto wako wapo wapi?”“Oooh nadhani wamelala”“Kwani uliwachukua muda gani?”“Yani jana nilivyopigiwa simu, ni muda ule ule nilienda kukata tiketi ya ndege, kwahiyo nimeenda usiku kuwachukua kwa mama, sasa leo asubuhi ndio nimepigiwa simu na mume wangu kuambiwa hiyo kitu kwahiyo nikanunua mahitaji yote na kuja huko kwenu sasa”“Mmmh ila wewe mshari sana”“Tuachane na hayo bhana, twende ukakaangize mambo yako yanayomchanganya kaka yangu”Basi Tumaini akamletea wifi yake nguo ya kubadilisha ili waanze mapishi kwanza nae mama Angel alifanya hivyo na kuanza yale mapishi aliyoombwa na wifi yake, muda huo Tumaini alikuwa akitengeneza juisi ya kunywa hao wageni.Baada ya kumaliza, basi mama Angel alichukua ile juisi na kuionja kisha akamwambia wifi yake,“Sasa kwenye hii juisi ongeza na passion kidogo kuleta ladha nzuri zaidi”“Oooh ndiomana nakupenda wifi yangu, ngoja nikanunue pale gengeni”Basi aliondoka na kwenda kununua passion kisha akarudi na kuzisaga vizuri na kuongeza kwenye ile juisi ambapo wifi yake alikunywa tena na kuisifia kuwa ni nzuri.Kisha walikaa kidogo kuongea wakati wifi yake ameanza kujiandaa kuondoka, ila alimuuliza,“Wifi unajua sijaelewa, watoto wako wapi?”“Wapo kujisomea, halafu hawajajua kama umekuja, ngoja nikawaite”Basi alienda kuwaita watoto wake ambao walifika na kumsalimia shangazi yao kisha kurudi zao chumbani,“Unajua kuna kitu sijaelewa”“Kitu gani?”“Mwanzoni ulisema wamelala, na sasa ukasema wapo kujisomea yani nashindwa kuelewa kwakweli, hwakai kuangalia Tv? Au inakuwaje?”“Humu ndani mimi na watoto wangu kuna ratiba kabisa, kwahiyo kuna masaa ya kufanya chochote kitakachofanyika, kuna muda wa kulala, kuna muda wa kusoma, kuna muda wa kucheza na kuna muda wa kuangalia Tv, huwezi kuwakuta muda wa kulala wanaangalia Tv au muda wa kusoma wanacheza, haipo hiyo kitu nyumbani kwangu”“Umewezaje kufanya wawe hivo?”“Ni mazoea tu, unajua nimewajengea mazoea toka wadogo, mimi wakati naishi na baba, kuna mdada wa kazi kwakweli huwa namsifu sana mdada yule kwakweli kanilea katika maadili yanayofaa, hata mama huwa anamsifu ila kitu kimoja tu ambacho hakunifundisha vizuri ni kufanya kazi na kujitegemea ila vingine vyote alikuwa vizuri”“Kwahiyo na wewe watoto wako umeacha wawe wavivu au?”“Hapana, ila watafanya kazi gani? Bado wadogo”“Wadogo? Huyo wa kwanza ana miaka kumi na mbili jamani angekuwa anaosha hata vyombo”“Kheee kwahiyo wakina Erica wanafanyaga kazi kwani?”“Kheee wanangu wameanza kufanya kazi muda tu, hata nikiwaacha peke yao hawalali njaa wale, wanajua kupika, kuosha vyombo, kufua yani kazi zote wanafanya, nani awafanyie? Mimi nimewafundisha kila kazi”“Khee hongera sana, basi nitaanza kumfundisha Leah kufanya kazi”“Ila nakupa nawe hongera sana kwa kuwalea watoto wako katika maadili, jamani mimi ni mkali sana ila hao wakina Erica tu wananivizia na kukaa kuangalia Tv, halafu kitu kingine ni Angel ananiumiza kichwa jamani”“Anafanyeje kwani?”“Kuna kijana anaitwa Samir, uwiii ananiumiza kichwa balaa, sijui nifanyeje mimi”“Kwani huyo kijana anafanyeje?”“Anamtongoza Angel, yani anamfatilia balaa hadi sina raha”“Oooh halafu Angel si ndio yupo kidato cha nne!!”Ilibidi mama Angel amueleze kila kitu wifi yake kuhusu Angel na huyo Samir, basi Tumaini akamwambia,“Naomba unipe Angel niishi nae kwa kipindi hiki tu, mimi sisafiri tena kwasasa”“Oooh utakuwa umenisaidia kwakweli”“Basi Jumatano nitakuja kumchukua, anatoka shule muda gani?”“Jioni kabisa”“Mmmh atakuwa kajiandaa kweli kuja huku jamani!! Sijui ila tutawasiliana basi, au nije Ijumaa?”“Yani hadi Ijumaa nitakuwa nimetokwa na pumu kabisa”“Basi Jumatano nitakuja”Basi wakaongea ongea pale na kuagana kisha mama Angel akaondoka zake.Mama Angel alipanda bajaji kuelekea nyumbani kwake kwani hakutaka kupelekwa na wifi yake, na alimwambia kuwa asubirie tu wageni.Basi wakati anakatisha na ile bajaji akamuona Samir na kumwambia yule kijana wa bajaji asimamishe ambapo alisimamisha na mama Angel alimwambia Samir,“Wewe kijana!”Samir akasogea alipo mama Angel na kumsalimia ila mama Angel alimnasa kibao Samir na kumwambia,“Nadhani siku ile sikukwambia ila ukome kumfatilia binti yangu”“Ila mama unanionea bure tu, sio kosa langu wala sio kosa la mwili wangu”“Sasa ni kosa la nani?”“Ni kosa la moyo wangu”Kisha Samir alikimbia baada ya kusema vile, basi mama Angel alirudi kwenye bajaji huku akisonya tu, basi yule dereva wa bajaji akamwambia,“Inaonekana huyu kijana anampenda sana binti yako”“Kwanini umesema hivyo?”“Macho yake yanaonyesha tu wakati akisema sio kosa lake, yani nadhani alitamani hata kulia mbele yako kuwa anampenda sana mwanao”Mama Angel hakumjibu kitu huyu kijana, basi alifika nyumbani kwake na kushuka ila alipoangalia kwenye mkoba hakuwa na hela ya kutosha, ilibidi apige simu ndani na simu yake ilipokelewa na Angel,“Angel naomba niletee elfu kumi na tano hapo kabatini”Basi akakata simu na muda kidogo Angel alitoka na kumkabidhi mama yake ile hela, yani yule kijana alikuwa akichukua ile hela huku macho yote yakimuangalia Angel huku akisema,“Naitwa Ally”Mama Angel alichukia na kusema,“Mjinga wewe, sasa mwenye haja ya kufahamu jina lako hapa ni nani? Muone vile, chukua hela yako na uondoke. Halafu wewe Angel hebu rudi ndani huko”Basi yule kijana alichukua zile hela na kusema,“Ila mama kwakweli umezaa jamani, naomba nikuite mama mkwe”“Una kichaa nini wewe! Nani mama mkwe wako? Hebu ondoka huko”Mama Angel akaingia getini na kumkuta Angel akiwa kasimama tu ndani ya geti na kumuuliza nay eye kilichomsimamisha hapo ni kitu gani,“Na wewe nini kimekusimamisha hapo?”“Hamna kitu mama ila nilitaka kukuuliza”“Haya niulize”“Siku zote huwa unasema tusitumie hela vibaya ila mbona leo umetoa elfu kumi na tano na kumlipa yule dereva wa bajaji?”“Kheee na wewe mtoto kwani kumlipa dereva wa bajaji ni kutumia hela vibaya? Yule kanifanyia huduma kwahiyo lazima nimlipe. Haya twende ndani”Basi wakaingia ndani ambapo Erick na Erica walikuwa sebleni wakiangalia video tena walikuwa hawana hata habari, basi alivyoingia wakamsalimia, ndipo alipowauliza“Mmeshajisomea?”Walikaa kimya tu wakimuangalia, basi akawaambia tena“Hebu nendeni mkajisomee huko”Akatokea Vaileth na kumwambia,“Mmmh mama jamani, watoto hawafanywi hivyo, saivi jioni ni muda wao wa kupumzika na kujifunza mambo mbalimbali si kama unavyowaona hapo wanajifunza kipindi cha mapishi, halafu twende jikoni nikakuonyeshe”Basi mama Angel alienda na Vaileth jikoni halafu Vaileth akamuonjesha kitu mama Angel, ambaye alikula na kusifia sana huku akimwambia Vaileth,“Aiseee, unajua sana kupika”“Unadhani ni mimi nimepika basi!!”“Ni nani sasa?”“Ni Erica huyo, yani yeye mwenyewe kaja jikoni leo nakusema dada kuna kitu nataka nijaribu kupika, basi nikamuacha akachukua unga wa ngano na kukanda na mwisho akapika hivi, hadi nimemuuliza vinaitwaje hivi kasema visheti, yani Erica ni mtaalamu haswaaa”“Oooh huyu mtoto nahisi nimejizaaa mweeeh! Yani kapika vizuri hivi!”Basi alisahau hata kama alikuwa akiwafukuza wakajisomee, zaidi zaidi wakati anaelekea chumbani kwake akamuita Erica ili amsifie vizuri zaidi,“Kwakweli mwanangu hongera, kumbe upo vizuri eeeh!”“Asante mama”“Ila umejifunza wapi kupika visheti? Nani kakufundisha?”“Ni Elly ndio kanifundisha mama”“Elly? Jamani Elly si mtoto wa kiume?”“Ndio ila mama yake ni mtaalamu mzuri sana wa kupika visheti, sasa Elly aliniletea shuleni na nikapenda ladha yake basi nikamwambia anielekeze namna ya kuvipika ndio akanielekeza”“Oooh vizuri sana mwanangu, nadhani huyo Elly ni rafiki mwema, ipo siku nitamfahamu”Basi mama yake aliingia chumbani halafu Erica akarudi sebleni na kumkuta Erick akila vile visheti huku akisema,“Yani leo sitaki kula chakula chochote kingine, nadhani hivi visheti vinanitosha”Erica alitabasamu na kumwambia Erick,“Nimejitahidi eeeh!”“Sio umejitahidi, ni umeweza kabisa mdogo wangu. Yani ladha ya hivi vidude nimeipenda sana”Angel nae alikuwa amekaa pale sebleni ila aliinuka na kuelekea chumbani kwake.Usiku wa siku hiyo Angel alijikuta akiwa na mawazo sana juu ya Samir hata alihisi usingizi hamchukui, yani alikuwa akikumbuka matukio yote ambayo Samir amemtendea na jinsi Samir alivyokuwa akimueleza kuwa anampenda sana, basi alikuwa akikumbuka kila kitu na kujisemea,“Natamani hata ningekuwa na simu basi ningempigia Samir”Sasa aliamua kujisomea ili aweze kuacha mawazo juu ya Samir, akachukua madaftari yake na kuanza kujisomea, wakati anapekua vizuri alishangaa kuona karatasi imeandikwa namba na akakumbuka kuwa hiyo ni namba ya Samir ambayo alipewa kwa mara ya kwanza kabisa ila hakutilia maanani siku aliyopewa, basi akashika kile kikaratasi huku akitamani sana kuwasiliana na Samir kwa muda huo, alipoona ndani ni kimya sana yani wote wamelala, akaangalia muda kwenye saa ya ukutani na kubaini kuwa ilikuwa saa nane usiku, basi akatoka chumbani kwake kwa kutembea taratibu hadi sebleni ambapo kulikuwa na simu ya mezani halafu akapiga ile namba ambayo kwa muda mfupi iliita na muda huo huo ilipokelewa na Samir, na alivyopokea tu alisema,“Kipenzi changu Angel, kumbe unanifikiria kama mimi ninavyokufikiria!”Angel akashtuka na kumuuliza,“Umejuaje?”“Yani huwezi amini nilikuwa na mawazo sana juu yako, basi nikamuomba Mungu hata muujiza utokee ili angalau nisikie sauti yako na kweli Mungu kajibu maombi yangu, ulipopiga tu nikajua lazima utakuwa wewe. Nakupenda sana Angel, nadhani hii ndio kauli yangu pekee utakayoisikia hadi siku naingia kaburini, sitoacha kukwambia ni jinsi gani nakupenda, kwakweli Angel wewe nakuona ndio kila kitu katika maisha yangu, nakupenda sana”Angel akapumua kiasi na kushindwa hata kujibu kwani midomo yake ilikuwa ikitetemeka, basi Samir aliaendelea kuongea,“Angel, huongei jamani kipenzi changu! Najua hata wewe unanipenda pia, kwakweli Angel katika maisha yako jua kuwa wanaume wote wanaokwambia wanakupenda basi hawakupendi kweli kasoro mimi tu, yani wewe umeumbwa kwaajili yangu na mimi nimeumbwa kwaajili yako. Nakupenda sana Angel”Angel akajikaza na kusema jambo moja tu kwani alihofia kuja kubambwa hapo akiongea na ile simu,“Usiku mwema Samir”“Oooh unataka kulala kipenzi, lala ukijua kuwa nakupenda sana, mawazo yangu ni juu yako. Mimi na wewe tutajenga familia moja yenye nguvu iliyofunikwa na mapenzi ya dhati”Kisha Samir akambusu Angel kwa njia ya simu yani Angel alifumba hadi maco kwa kupatwa na hisia na lile busu kisha akakata ile simu na kurudi chumbani kwake.Alilala huku akitabasamu tu kwani aliona ni ufahari sana kwa yeye kupendwa na Samir.Kulipokucha kama kawaida walijiandaa wote na kwenda shuleni, basi Erica akiwa darasani kwao kama kawaida alikaa dawati moja na Ellyn a kuanza kumuhadithia kuhusu mapishi ya jana aliyoyafanya nyumbani kwao,“Jamani Erica, sasa mbona hujaniletea nami nionje?”“Aaah nimesahau jamani, yani nimesahau kabisa, nisamehe”“Sawa nimekusamehe ila siku nyingine ukipika basi niletee nami nionje”“Sawa, halafu mama yangu anataka kukufahamu”“Hata mama yangu pia anataka kukufahamu, huwa namueleza kuhusu wewe basi anasema nahitaji kumfahamu huyo Erica”“Hakuna tatizo, ipo siku atanifahamu tu”Akasogea Abdi na kumnong’oneza kitu Erica ambapo Erica alionekana kuduwaa kwa muda basi Elly akauliza,“Nini tena? Halafu wewe Abdi si nimekukataza maswala ya kumfata fata dada yangu!”“Ameshindwa Erick ndio utaweza wewe!!”“Sasa Erick ni Erick na mimi ni Elly, nione tu hivi hivi ila sitaki masikhara”Elly alikuwa akiongea kama mtu aliyechukia sana, ilibidi Abdi aondoke tu hapo na masomo yakaendelea kama kawaida.Wakati wa kutoka, Erica alishangaa akitafutwa na mtu ambaye alipofika alimgundua kwani ni mara kadhaa alimuona na dada yake, mtu huyo alikuwa ni Samir basi alimwambia Erica,“Natumai unanifahamu?”“Ndio nakufahamu, wewe ni Samir”“Sio Samir tu bali mimi ni shemeji yako”Erica akawa kimya basi Samir akamwambia,“Naomba chukua huu ujumbe wangu na ukampe dada yako, tafadhali umpe dada yako tu wala asione mwingine”Kisha Samir alimpa Erica karatasi ambayo ilibanwa na pini za kubania karatasi na kumuaga pale ambapo Erica alipanda kwenye basi la shule kurudi nyumbani kwao huku akijiuliza kuwa ile barua imeandikwa vitu gani.Erica alifika nyumbani kwao na moja kwa moja alienda chumbani kwake kuvua sare zake za shule kisha alifungua ule ujumbe aliopewa na Samir kuwa ni wa dada yake, basi alianza kuusoma yeye, muda anamaliza kuusoma nae Erick aliingia chumbani kwa Erica na kumkuta yuko makini sana kwahiyo kama alimshtua na kumfanya Erica afiche lile karatasi, basi Erick alimuuliza,“Unaficha nini sasa?”Erica hakusema kitu, basi Erick akasema tena,“Umeanza kunificha na mimi Erica?”“Hapana kaka, ila kuna ujumbe nimesoma”“Ujumbe gani?”Basi Erica akamuelezea alivyokutana na Samir na jinsi alivyompa ujumbe wa kupeleka kwa dada yao, kisha alimpa Erick ausome huku akimwambia,“Jamani dada Angel anapendwa, yani nimesoma hadi nimetamani niwe mimi ndio naambiwa hayo maneno”“Mmmh Erica na wewe, umeanza mambo”“Hamna, hebu soma huo ujumbe loh! Samir anampenda sana dada”Erick nae aliusoma ule ujumbe na kuguna sababu kweli ulikuwa unamaneno mazito sana, basi Erick alimtazama Erica na kumuuliza,“Je unaweza kupenda kama huyu anavyopenda?”“Kwanini nisiweze? Ila nasubiri nikue maana kwa umri huu siwezi kufanya chochote kinyume na mama ila dada anapendwa jamani”“Ila kwa kumuokoa dada yetu tafadhali tusimpelee huu ujumbe”Kisha Erick akaondoka na ule ujumbe na kwenda nao chumbani kwake.Mama Angel akiwa katulia alipigiwa simu na wifi yake na kuanza kuongea nae,“Kwakweli wifi asante sana, yani jana wale wageni wmaekula na kusifia balaa yani nimepata sifa hizo mke wangu hadi balaa”Muda huu mumewe nae alirudi kwahiyo aliongozana nae chumbani huku akiongea na ile simu,“Kwakweli kaka muache tu achanganyikiwe juu yako”Basi mama Angel alikuwa akicheka hadi mumewe kutaka kujua akizungumza na nani, basi mama Angel alimpa mumewe ile simu kuwa nay eye aongee nae, basi mumewe alianza kuongea nae,“Yani Erick jana bhana, niliondoka hapo na mkeo ili anisaidie kupika, uwiii vitu alivyopika huku jamani ni Mungu pekee anajua yani wageni wangu wamejilamba haswaa”“Oooh huyo ndio mke wangu bhana”“Ndiomana unampenda”“Nampenda ndio ila sio sababu ya kupika tu hapana, hiyo kupika ni ziada ila ninampenda mke wangu kwasababu zangu mwenyewe”Basi waliongea pale na kukata ile simu kisha baba Angel alimuangalia mkewe na kumwambia,“Na mimi nataka unipikie hiko chakula ulichopika kwa Tumaini, sio nje huko mnaenda kuwapikia mapochopocho halafu ndani unasahau maana naona toka tuje na Vaileth basi kila siku kula chakula cha Vaileth tu, nimekumbuka chakula chako mke wangu”“Basi kesho nitapika”Wakaongea ongea na kuamua kulala pale.Kesho yake wakati wakina Angel wameenda shuleni, basi mama yao aliamua kubaki nyumbani na muda huo alitaka kusaga juisi.Akaenda jikoni na kukuta kidude cha kuchomeka kwenye soketi hakipo basi alimuuliza Vaileth nae akamjibu,“Oooh hiko nilimuona nacho Erick, nadhani alienda nacho chumbani kwake”“Aaaah huyu mtoto nae na vidude vya umeme jamani ni hatari’Basi alitoka pale na moja kwa moja kuelekea chumbani kwa Erick, wakati akiangaza macho yake akaona barua mezani kwa Erick basi akaenda kuichukua na kuisoma, yani alishtuka sana kuona ni barua kutoa kwa Samir kwenda kwa Angel,“Mmmh sasa inafanya nini humu chumbani kwa Erick jamani!!”Basi akaisoma mara mbilimbili akakuta ujumbe wa chini ukisema,“Kesho nitakuja kwenu Angel, nitasimama pembezoni mwa ukuta wenu naomba uje tu unikumbatie yani hiyo itakuwa ni furaha yangu, nakupenda sana Angel mpenzi wangu”Huyu mama akapumua kidogo na kusema,“Yani hiyo kesho si ndio leo? Jamani hawa watu wanataka kunifanyeje mimi? Kwanini wananifanyia hivi!!”Basi mama Angel alitoka nje na kukaa mitaa ile ile ya nje ya nyumba yao huku akisubiri kwa hamu kama gari itapiga honi basi atajua kuwa Angel amefika na atakimbilia nje kabisa ili Angel asiende huop upande uliotajwa na Samir, na kweli alitoka pale nje mara kadhaa bila kumuona huyo Samir kwahiyo aliamua tu kungoja pale ndani ya geti, yani hakufanya chochote tena zaidi ya kungoja Angel arudi. Ila alipoona Erica na Erick wamerudi akaona ni vyema nay eye akitoka nje kabisa.Wakati Angel anarudi, basi karibu na kufika kwao gari yao ilipata pancha, basi dereva akamwambia asubiri abadili tairi lingine,“Khaa jamani huu ni ujinga sasa, nyumbani ni pale napaona halafu nisubirie uweke tairi lingine kweli!! Subiri nishuke niende nyumbani tu, wewe tengenezaga”Basi yule dereva alibaki kupachika tairi lingine wakati Angel akishuka na kutembea kuelekea kwao, ila kabla hajasogea vizuri alishangaa akivutwa mkono na aliposhtuka aliona mkono ule kavutwa na Samir basi alimuangalia tu bila ya kusema chochote, Samir alimvuta Angel hadi pembezoni mwa ukuta wao na kumkumbatia huku akimbusu na kumwambia ni jinsi gani anampenda, muda ule ule mama Angel nae alionekana eneo lile akiwashangaa yani alijikuta akiishiwa hadi nguvu.Basi yule dereva alibaki kupachika tairi lingine wakati Angel akishuka na kutembea kuelekea kwao, ila kabla hajasogea vizuri alishangaa akivutwa mkono na aliposhtuka aliona mkono ule kavutwa na Samir basi alimuangalia tu bila ya kusema chochote, Samir alimvuta Angel hadi pembezoni mwa ukuta wao na kumkumbatia huku akimbusu na kumwambia ni jinsi gani anampenda, muda ule ule mama Angel nae alionekana eneo lile akiwashangaa yani alijikuta akiishiwa hadi nguvu.Ila muda ule ule anapatwa na hasira ya gafla na kujikuta akipiga kelele, ila kile kitendo kinafanya Angel na Samir wamshangae yani Samir hakukimbia wala nini hadi mlinzi wa wakina Angel alipotoka na kumkamata Samir kwani alihisi ndio tatizo, kisha mama Angel alinyamaza kupiga kelele na kumtaka mlinzi ampeleke Samir ndani, ambapo yule mlinzi alifanya kama alivyoambiwa na bosi wake.Basi mama Angel alimvuta Angel na kuingia nae ndani kisha alimwambia,“Yani leo utaona ambacho huwa namaanisha ni kitu gani?”Kisha mama Angel alichukua simu na kupiga mahali, na baada ya muda walikuja askari na kumkamata Samir, kwakweli Angel aliumia sana moyo, yani kwa mara ya kwanza alijikuta moyo wake ukiwa kama na vidonda vile, alitamani kumuhoji mama yake kuwa kwanini amefanya vile ila mama yake alimfokea na kumfukuzia ndani, Angel aliingia ndani huku akilia kwakweli hadi Vaileth alimuonea huruma.Muda huu mama Angel aliondoka na wale askari ili akamuandikie mashtaka Samir na awekwe rumande.Basi Angel alikuwa amejifungia ndani huku akilia, Vaileth aliamua kumfata ili amnyamazishe na kuanza kuongea nae,“Mdogo wangu, kulia hakutokusaidia kitu chochote”“Ila Samir hana kosa jamani”“Natambua hilo mdogo wangu, ila kuna kitu nataka nikushauri”“Kitu gani dada?”“Kwanini usiwasiliane na baba yako? Huwa naona ni muelewa sana, hebu mtafute hewani, nenda kampigie simu atakuelewa”Angel nae aliona ni jambo jema kama akimwambia baba yake maana baba yake ni mtu muelewa sana, basi akatoka chumbani na kwenda kumpigia baba yake simu sebleni kwenye simu ya mezani, na kwa muda kidogo tu baba yake alipokea,“Baba, mimi ni Angel, samahani kwa hili baba”“Lipi hilo?”“Baba, leo wakati natoka shule gari yetu iliharibika karibu na nyumbani basi nikashuka ila kumbe pale kwetu alikuja Samir na kunivuta mkono basi mama alikuja muda huo huo na kutuona kisha akaita askari basi Samir kakamatwa na kupelekwa polisi”“Sasa wewe Angel unatakaje? Yani unataka mimi nifanye nini?”“Baba, Samir hana kosa lolote”“Ila mwenye kosa ni wewe?”“Hata mimi sina kosa baba”“Usinichanganye na hayo mambo yasiyoeleweka, nina kazi zangu muda huu”Kisha baba yake alikata ile simu na kumfanya Angel alie zaidi, basi Vaileth alienda tena kumbembeleza,“Angel jamani usilie sana”“Baba nae hataki kunielewa, baba na mama lao moja wale, sasa kosa la Samir ni nini?”“Kosa lake ni kuja hapa kwenu, ila wazazi wako wapo sahihi Angel, kwahiyo tuwaachie wenyewe tu wanajua cha kufanya ambacho ni sahihi zaidi”Basi Angel alienda tena chumbani akilia, na baada ya muda Erick na Erica nao waliamka maana walikuwa wamelala kwa muda wote kwahiyo hata hawakuelewa kilichoendelea hapo kwao.Mama Angel akiwa anakaribia kuondoka pale polisi baada ya kuandikisha maelezo, alishangaa akipigiwa simu na mumewe na kutoka nje ili aongee nayo,“Uko wapi muda huu mke wangu?”“Niko hapa kituo cha polisi”“Kipi hicho?”“Hapa karibu na kwetu”“Nisubirie hapo hapo nakuja”Basi baba Angel alikata simu kwakweli mama Angel alimshangaa sana mume wake kuwa anaenda kituoni kufanya kitu gani? Basi ilibidi tu amsubirie kama alivyosema.Baada ya muda kidogo baba Angel aliwasili na kumsogelea mke wake huku akimuuliza ni kitu gani kimempeleka polisi,“Mume wangu, yani leo Angel na huyo Samir wake wamenishinda tabia kabisa, huwezi amini leo Samir alikuja tena nyumbani na kumkumbatia Angel, yani nilitoka na kuwaona hadi nguvu ziliniisha nikatamani hata niwameze”“Kwahiyo uamuzi wako wa mwisho mke wangu ni kumfunga Samir?”“Ndio ili adabu imshike”“Basi mimi naomba mke wangu tukafute hiyo kesi na kumuachia Samir ila tutapa onyo”“Kheee unasemaje mume wangu, yani nilipe tena hela za kufuta kesi?”“Nitalipa mimi kwani tatizo liko wapi?”Mama Angel alichukia sana ila hakuwa na namna zaidi ya kwenda kufuta kesi, na mumewe akalipa kila kitu halafu Samir akaachiwa, kisha baba Angel alimchukua Samir na kwenda nae pembeni kisha akamuuliza,“Hivi kwanini umekuwa msumbufu hivyo!”“Nisamehe mzee”“Nisamehe yako unafikiri itasaidia kitu gani? Hivi hujihurumii kuwa bado ni mwanafunzi tena upo kwenye darasa gumu, unadhani ukifeli huyo Angel atakukubali? Sisi wenyewe hatuhitaji wanaume waliofeli katika maisha yetu, sawa kufeli kupo ila mfeli kwa bahati mbaya hata wazazi tuseme kweli juhudi zilikuwepo ila haikuwa ridhiki sio mfeli kwa makusudi, muda kama huu inatakiwa kuwa makini sana na masomo ila na ujinga wao unawaza mapenzi, unadhani huyo Angel atakusaidia nini wewe katika maisha yako? Unatakiwa upambane kama mwanaume, kwanza pambana na utafute pesa za kutosha kisha uje kwetu kumfata Angel uone kama tutakukatalia mjinga wewe, nimekuhurumia tu kuwa utaozea huko jela bila kupata msaada wowote kwa ujinga wako wa mapenzi. Haya ondoka, ila safari ijayo ukifumwa nitashughulika na wewe mimi mwenyewe na hapo ndio utanijua vizuri”“Asante mzee wangu”Kisha Samir akaondoka mahali pale na baba Angel alisogea kwa mama Angel na kumtaka waondoke ila mama Angel alikuwa amenuna sana, yani aliondoka na mumewe ilimradi tu ila alikuwa kanuna.Basi wakiwa ndani ya gari akamuulza,“Ila kwanini umeamua kumtoa Samir? Unafurahia jinsi anavyomsumbua Angel? Kwa mfano Angel angekuwa Erica ungejihisi vipi?”“Kheee wee mwanamke hebu acha gubu, toka lini katika maisha yetu nimemtenga Angel? Toka niliposema kuwa mimi ndiye nitakuwa baba yake, lini umesikia nimemtenga? Ulipowazaa Erica na Erick je nlimtenga Angel? Alibaki kuwa ni mwanangu wa thamani sana, nampenda kuliko unavyofikiria, nampenda kuliko hata huyo babake mzazi angefanya, hebu wanawake muda mwingine muelewe mnaongea kuhusu nini sio mnavyojisikia kuropoka basi mnaropoka. Unajua ni kwanini wanawake wengi wanaachwa walee watoto wenyewe? Sababu ya midomo, yani hakuna mwanaume anayeweza kuvumilia kila siku unamsema jambo moja wakati yeye anajitahidi kulifanya sahihi, nadhani katika ulimwengu huu ni mimi tu ninayeweza kuvumilia”Kisha akacheka ila mama Angel akamwambia,“Naomba nisamehe kwa maneo yangu”“Nakuelewa mke wangu, yani huwa nakuelewa kuliko unavyofikiria, nakuelewa sana tena sana, ila mke wangu jaribu kuangalia ninachokifanya, hivi mfano Erick awekwe rumande sababu ya kumfatilia mwanamke utajisikiaje?”“Aaah Erick hawezi kufanya hivyo”“Sawa, mfano mimi kipindi kile nakufatilia wewe ningewekwa ndani sababu ya kukufatilia unajua ningeumia sana, nilifukuzwa shule bado niliumia sana”“Ila hawa ni wadogo sana kuanza kupendana”“Hakuna cha udogo wala nini, nakumbuka mimi nilikupenda kwa mara ya kwanza kukuona tukiwa kidato cha pili, mbona tulikuwa wadogo sana ila nakupenda hadi leo. Ila hii sio point yangu wala nini, unachofabnya si kibaya ila jaribu kukifanya kwa nja sahihi. Kumfunga Samir hakutasaidia chochote kile, ila ni Angel kuijua thamani yake na kuithamini, unatakiwa kukaa na Angel na kumfundisha ajijue kuwa yeye ni mtu wa aina gani”“Inamaana mimi nimeshindwa kumfundisha Angel?“Sijasema umeshindwa, ila sidhani kama tunaelewana mke wangu naomba tuache huumjadala”“Ila Tumaini alisema Jumatano atakuja kumchukua Angel na kwenda kuishi nae kwake hadi atakapomaliza kidato cha nne”“Sawa hakuna tatizo”Basi walirudi hadi nyumbani ambapo Angel alikuwa kajifungia ndani tu muda wote.Usiku wa siku hiyo baba na mama Angel wanaamua tu kulala bila ya kuzungumza na watoto wao maana walihisi kuwa huenda wamechoka.Basi kulivyokucha, Erica na Erick walijiandaa na kwenda shule ila Angel siku hii hakujiandaa wala nini, ilibidi mama yake aende kumuuliza kuwa kwanini hajaenda shule, alishangaa kumkuta binti yake macho yamemvimba kwa kulia, yani mama Angel alisikitika sana na kumwambia Angel,“Ama kwa hakika nimepata binti mjinga sana na asiyejielewa hata kidogo halafu wewe ndio mtoto wangu wa kwanza, hivi Angel unafundisha nini wadogo zako? Unataka nao wawe wasumbufu kama wewe? Kwanini Angel kunitenda hivi mama yako jamani? Mbona mtoto huna huruma wewe loh!!”“Mama, wewe ndio huna huruma sasa mimi nina raha gani hapa nilipo ikiwa Samir amelala ndani”“Jamani Angel kalala ndani kivipi? Mbona baba yako alimtoa tayari, hata kama angelala ndani ndio sababu ya wewe kulia hadi kuvimba macho, kwahiyo unampenda Samir kuliko sisi wazazi wako?”Angel alikaa kimya, kisha mama yake akaenda kuchukua ile simu aliyokuwa anatumia na kumwambia,“Haya mpigie Samir hapo akwambie kama yupo rumande au yuko wapi”Basi Angel alichukua ile simu na kumpigia kweli Samir ambapo baada ya muda mfupi Samir alipokea ile simu,“Oooh siamini, leo Angel umenipigia”“Uko wapi Samir?”“Nipo shule”Muda huo huo Angel alisikia sauti upande wa pili ikisema,“Yani Samir, wenzio wapo darasani na wewe upon je unaongea na simu!! Leo ni mara ya tatu nakufuma, twende ofisini sasa”Kisha ile simu ilikatika, inaonyesha ni mwalimu alimbamba Samir akiongea na simu, basi Angel pia alishusha ile simu na kumkabidhi mama yake kisha mama yake akamwambia,“Umeamini sasa kuwa Samir alitolewa? Basi jiandae maana kesho shangazi yako mama Leah anakuja kukuchukua, kwahiyo jiandae ila nitaongea nae aje akuchukue leo tu ili kesho utokee kule kwenda shuleni”“Nimeamini mama, ila huko kwa shangazi naenda kutembea tu au?”“Unaenda kuishi huko hadi umalize kidato cha nne yani ni mimi na nduguzo ndio tutakuwa tunakuja kuwaona, ila mara kwa mara nitakuwa nawasiliana na shangazi yako”Halafu mama yake alitoka kule chumbani, basi Angel akawa akijitafakari haswaaa maneno ya mwalimu kuwa ile ilikuwa ni mara ya tatu kumbamba Samir akiongea na simu, basi akajiuliza,“Je mara zote hizo huwa anaongea na nani?”Akakosa jibu na kuamua kwenda kuoga ili kupata nguvu ya kupanga nguo zake kama alivyoambiwa na mama yake.Samir alipelekwa ofisini na mwalimu wa nidhamu na kuanza kuongea nae kwanza,“Unajua Samir kutenda kosa si kosa bali kurudia kosa, nilikuhurumia sana mwanzoni kuwa mtoto huyu itakuwa kakosea, Samir nilimfuma Angel akiwa anatumiana na mtu ujumbe darasani, na ukaja mwenyewe kusema kuwa anawasiliana na wewe, nikakupa onyo, ile ilikuwa mara ya kwanza, mara ya pili nilikukuta ukiongea na simu na nilipokubana ulisema ulikuwa unawasiliana na mamako ana matatizo, nikakusamehe ila nikwambia isijirudie tena na nikakwambia kuwa simu haziruhusiwi shuleni, acha simu yako nyumbani kwenu. Ulinikubalia na uliandika barua ya maelezo, haya na leo tena na kufuma na kosa lile lile, kwakweli sitasikiliza mjadala, sijali kuwa hili ni darasa gumu wala nini bali nakuandikia barua ya kusimamishwa shule”“Jamani mwalimu!!”“Hakuna cha jamani, unatakiwa kuzingatia masomo sio kuleta mambo ya kijinga shuleni, yani kaa ukijua muda huu ndio siku yako ya mwisho kuonekana hapa shuleni”Basi Samir alijitahidi kumbembeleza mwalimu ila alishindwa kwani yule mwalimu hakukubali wala nini kwahiyo ilibidi Samir akachukue begi lake na aende kuchukua barua yake na kurudi nyumbani tu.Muda Samir anaondoka, Erica nae alikuwa akienda chooni kwahiyo Samir alikutana nae na kumwambia Erica,“Mwambie Angel kuwa nimefukuzwa shule, ila siku zote nitampenda hadi mwisho wa maisha yangu, hata nisipomuona nitaendelea kumpenda tu. Mwambie kuwa nampenda sana”Basi Erica alimuangalia huyu Samir na kumuitikia tu bila ya kusema kitu kingine chochote kile, basi Samir akamuaga na kuondoka zake.Mama Angel anawasiliana na wifi yake kuwa aende kumchukua Angel siku hiyo hiyo kwani hakutaka aendelee kukaa hapo nyumbani, ukizingatia alishaona jinsi binti yake alivyoathiriwa na mawazo juu ya Samir.“Wifi naomba uje leo kumchukua Angel, nishamwambia ajiandae”“Oooh sawa, halafu nilikuwa na safari ya kuja huko huko, ila siji na gari”“Hakuna shida, dereva atawapeleka maana ndio atakuwa anakuja kumchukua Angel na kumpeleka shuleni”“Sawa, hakuna tatizo”Basi mama Angel aliona ni afadhari iwe vile maana hakutaka matatizo tena na Angel, na alijua kwamba Angel akienda kwa shangazi yake basi ataepuka vitu vingi sana vya kuhusu Samir.Baada ya muda kidogo wifi wa mama Angel aliwasili na kuanza kuzumza nae,“Eeeeh huyo Angel kashajiandaa lakini?”“Kashajiandaa ndio”“Basi hakuna tatizo, leo kuna mahali nilikuwa naenda jioni ndiomana nikakwambia nimpitia kabisa saa hizi, vipi mbona hajaenda shule”“Mmmh alichelewa kuamka”“Jamani Angel nae loh! Kwangu atakuwa anwahi huyu vizuri tu”Hakutaka kumueleza wifi yake kuhusu yaliyotukia jana, ila aliacha kama kujishuhudia basi akajishuhudie mwenyewe huko huko.Basi mama Angel alienda tu kumshtua Angel ilia toke ndani na aondoke na shangazi yake ambapo alifanya hivyo na kutoka na begi lake la madaftari pamoja na begi lake dogo la nguo zake. Kisha akamsalimia shangazi yake pale na kumwambia mama yake,“Mama, mimi nabeba hizi nguo kidogo tu zibebi nyingi”Shangazi yake akasema,“Ubebe nyingi za nini? Hizo hizo kidogo zinakutosha maana zitafanya uwe makini zaidi”Basi mama yake alipiga simu kwa dereva wao ambaye alifika kuwachukua, pia alimpa maagizo kuwa toka siku hiyo atakuwa akimfata Angel huko kwenda shuleni na atakuwa akimrudisha huko huko, basi yule dereva alikubali na kuondoka nao.Wakina Erica walirudi shuleni, basi kwavile Erica alikuwa na ujumbe kwa dada yake akamsubiri arudi ndio amwambie maana yeye alijua kuwa dada yao kaanda shuleni, ila alishangaa kuona hadi giza linaingia bila dada yao kurudi nyumbani, ikabidi akamuulize dada yao wa kazi vaileth,“Eti dada samahani, dada Angel mbona leo kachelewa kurudi shule?”“Sio kachelewa ila hayupo”“Khee hayupo? Kivipi?”“Kaja hapa shangazi yenu kumchukua, kwahiyo ameenda kuishi kwa shangazi yenu!”“Jamani!!”Erica akasononeka, basi Vaileth akawahadithia kisa cha jana yake na hapo kumfanya Erica aelewe kuwa ile barua ilibambwa na mama yao, ila moja kwa moja alihisi mtu mbaya ni Erick tu kwenda kupeleka barua kwa mama yao, basi akamfata Erick chumbani, alipofika alifungua tu mlango na kumkuta Erick ametoka kuoga yani ndio kalifungua taulo ili avae nguo, basi Erica alishtuka sana ambapo Erick nae alijifunga na taulo kisha akamkaribisha dadake ambaye alikuwa ameduwaa pale mlangoni,“Kilichokufanya ushangae hivyo ni nini?”“Kumbe Erick ndio upo hivyo!!!”“Wewe nawe, si nimekuwa unadhani nitaendelea kuwa vile vile kama zamani! Hujioni wewe umetokwa na maziwa kifuani mbona mimi sisemi kitu!”“kheee nisamehe basi”“Mi nilishakusamehe ila sidhani kama ni vibaya kwa pacha wako kukuona ulivyo, angeniona mtu mwingine ingekuwa vibaya ila kwa pacha wangu sio vibaya”“Haya, tuachane na hayo. Eeeh ile barua ya da Angel aliyoandikiwa na Samir ulisema utaificha imekuwaje imemfikia mama?”Ndipo Erick akakumbuka sasa sehemu aliyoweka hiyo barua, basi akaanza kuangalia bila kuikuta na kusema,“Oooh kumbe niliiacha mezani, mmmh inamaana mama aliingia humu chumbani!”“Yani na wewe ukaweka mezani kweli! Unasahau kama mama huwa naingia kwenye vyumba vyetu kama chumbani kwake, na anapekua atakacho, basi ndio mama imemfikia hivyo”“Wewe umejuaje?”Akamsimulia jinsi ambavyo alisimuliwa na Vaileth kuhusu yaliyotokea jana,“Khee tulikuwa wapi kwani? Mbona hatujasikia hayo?”“Nadhani ni muda ambao tulikuwa tumelala, mfano mimi jana nilichoka sana jamani”“Hata mimi jana nilichoka sana, ila ndio inavyokuwaga Jumatatu. Pole kwa dada Angel jamani maana nahisi aliambulia kipigo tena”“Hapana, angepigwa basi tungesikia tu. Ila mama kachukia hadi leo da Angel kapelekwa kwa shangazi ujue”Erick akashangaa na kutaka kuelezwa zaidi basi Erica alimueleza vile ambavyo alielezwa na Vaileth, kwakweli Erick alisikitika sana kwa dada yake kuondolewa sabau ya uzembe wao.Kisha alimuuliza jambo Erica,‘Vipi Elly hajambo?”Erica alicheka na kumwambia kaka yake,“Maajabu, leo umemkumbuka Elly?”“Nimemkumbuka ndio, sababu leo hujaleta swaga zako za kusema Elly kafanya hiki mara kafanya kile ndiomana nimekuuliza”“Mmmh leo hajaja shule ujue”“Khee anaumwa?”“Sijui, ila kesho nitajua”“Basi utampa pole”Erica alitoka chumbani kwa kaka yake ila alishangaa sana kwa kaka yake kumuulizia Elly wakati huwa hathubutu kabisa kumuulizia Abdi, ila Elly alimuulizia na kusema mpe pole kama anaumwa, kwakweli Erica alishangaa sana ila aliondoka tu kuelekea chumbani kwake.Tumaini akiwa na Angel nyumbani kwake, anaanza kumpa Angel masharti ya nyumba yake hiyo, na kipi hataki kitokee au kitendeke kwenye nyumba yake,“Angel mwanangu, karibu kwenye himaya yangu, nyumba hii mwanangu ina masharti yake. Upo tayari uyasikiliza”“Nipo tayari shangazi”“Haya, humu ndani kila siku ina kitu chake cha kufanya, kwanza kuna muda wa kuamka, kuna muda wa kulala, kuna muda wa kujisomea, kuna muda wa kuangalia Tv, kuna muda wa kucheza na kuna muda wa kula. Kwa kifupi kila kitu kinafanywa kutokana na ratiba ya humu ndani, ila kutoka Jumatatu hadi Ijumaa hakuna mtoto au mwanafunzi yoyote anayeruhusiwa kuangalia Tv kwa muda wowote, yani muda wa kuangalia Tv upo Jumamosi na Jumapili ingawa hapo kuna muda wake pia kwani sio siku nzima unatumbulia macho Tv. Hiyo ni sheria namba moja, huwa sina kawaida ya kutuma watoto dukani ila huwa ikitokea nataka uende moja kwa moja ninapokutuma na kurudi nyumbani ni hivyo hivyo kama una kitu unahitaji kununua, hata hivyo huwa napenda niandikiwe mahitaji yote ili niyanunue na yawepo nyumbani. Hapa kutoka haitakiwi izidi saa kumi na mbili yani saa kumi na mbili jioni inavyogonga basi hairuhusiwi kutoka hata nje ya geti langu lile, naonekana mkali sana ila nalinda uzao wangu maana watoto wangu wote ni wakike, nikicheza basi nimewapoteza. Umenielewa Angel”“Nimekuelewa shangazi”“Ukitoka shule ni nyumbani na ukifika nyumbani hakuna kutoka tena, utafata ratiba tu inasemaje kwa muda huo hadi pale unapoenda kulala, ujinga nyumbani kwangu sitaki, sijui kusikia mambo uliyokuwa ukiyafanya kwenu kuyaleta hapa sitaki. Mimi ni shangazi yako kwahiyo kuwa makini sana na mimi na uniheshimu”“Sawa shangazi”“Haya, twende nikakuonyeshe chumbani”Basi Angel alipelekwa hadi chumbani na kuweka begi lake na muda huo huo aliambiwa asome ratiba ya siku hiyo inasemaje, yani ratiba ilikuwa imebandikwa nyuma ya mlango wa kile chumba, kwakweli Angel alihisi kama yupo kwenye kifungo vile ila ilibidi tu akubaliane na hali halisi na kufanya vile ambavyo ratiba ya kile chumba ilisema.Watoto wa shangazi yake waliporudi kutoka shule wala hawakuonekana kuwa na hofu na ile ratiba kwani waliizoea tu, basi walimsalimia dada yao pale na kuanza kuvua sare zao za shule, basi Angel akaenda kwa shangazi yake na kumwambia,“Sasa shangazi, mimi nitalaleje na watoto ndani?”“Ndio ujinga ambao mama yako kakufundisha, ndiomana unafanya vitu kinyemela. Sawa sio taizo, nakuhamisha chumba ila kuwa makini sana”Basi Tumaini akaenda kumuonyesha Angel chumba kingine cha kulala ambacho katika nyumba yake huwa ni chumba cha kulala wageni, ila aliona kwa kipindi hiko kitamfaa Angel, kisha akamwambia Angel,“Ila nilikuwa nakujaribisha u mule kuwa utasemaje, haa hukujiuliza kuwa kule ungelalaje? Na ungelala wapi? Nilikuwa nakujaribu tu mule, ila chumba chako kitakuwa ni hiki ila napo nitakuja kukubandikia ratiba nzima ya kuishi humu ndani”“Sawa shangazi”Basi Angel akaweka tena vitu vyake vizuri huku akitaakari yale yaliyopo.Kulipokucha Angel alijiandaa kwenda shuleni na alienda shuleni kama kawaida na kukua mama yake kumbe alishaoa maelezo ya kwanini jana yake hakufika shuleni basi wote walibaki kumpa pole maana alisema kuwa anaumwa.Basi alishiriki vizuri kabisa kwenye masomo na alipenda wanafunzi wa shule ile jinsi walivyokuwa na ushirikiano kwani waliweza kumuelekeza kila kitu ambacho kilifundishwa siku ya jana ambayo hakufika shuleni. Kuna mdada alimzoea kidogo kwahiyo akawa kama rafiki yake hapo shuleni, aliiwa Husna, aliipenda sana tabia yake kwani alionekana kupenda kusema ukweli muda wote, basi siku hiyo muda wa mapumziko akawa anaongea nae,“Kwakweli Angel wewe ni mzuri sijui kama unatambua hilo!”Angel alikuwa akicheka tu, kisha Husna alimwambia jambo lingine,“Ila uzuri unakamilika ukiwa na akili timamu, wazungu wansema beut with brain, kwahiyo unatakiwa uwe mzuri na uwe na akili ili uzuri wako uthaminike”“Akili ya kufanyeje?”“Aili ya kuitambua thamani yako, mama yangu huwa ananifundisha jambo moja sana kuwa mimi ni wa thamani sana, natakiwa muda wote nitambue thamani yangu, nisikubali kitu chochote kuvuruga thamani niliyokuwa nayo. Siku tukipata muda vizuri nitakuelekeza mambo mengi Angel, ia kiukweli nimekupenda bure, maana wewe ni mzuri halafu muelewa, halafu una akili, nimekupenda bure kwakweli”Basi Angel alifurahi sana kusikia vile na kumfanya aishie kutabasamu tu.Muda wa masomo uliisha na kurudi nyumbani kwa shangazi yake bila tatizo lolote, na alikuwa akienda shuleni kwa muda na kurudi muda unaotakiwa hadi shangazi alihisi kuna mambo Angel alikuwa akisingiziwa.Ilikuwa siku ya Ijumaa ambapo kama kawaida, Angel alienda shule na kama kawaida ile asubuhi kabisa waliwahi darasani na kufanya jaribio la siku maana katika ile shulle ilikuwa kila siku kuna jaribio asubuhi, kwahiyo aliwahi na kufanya vizuri kabisa.Kwenye mida ya saa mbili na nusu asubuhi wakiwa wametulia darasani wakijisomea, mara aliingia mwalimu na mwanafunzi mgeni ila hakutaka wainuke kumsalimia ili asiharibu umakini wao na muda huo Angel ndio alikuwa makini na kitabu chake akisoma tu, basi mwalimu alitangaza,“Jamani tumepata mwanafunzi mgeni, kwahiyo nahitaji ushirikiano wenu mwema kwake. Anaitwa Samir”Angel alihisi moyo wake ukifanya paaa, na kuinua sura yake, kwakweli hakuamini kwani macho yake yaligongana na macho ya Samir kwa muda huo.Walijikuta wakiangaliana kwa muda kidogo kisha kila mmoja kuendelea na mambo yake ambapo Samir alikaribishwa vizuri na kiongozi wa darasa na kuonyeshwa sehemu ya kukaa na kuendelea na masomo.Ila leo Samir hakumfata Angel wala nini yani ilikuwa kama vile yeye na Angel ni watu wasiofahamiana kabisa, muda kidogo Samir alikuja kuitwa na mwalimu ambapo mama yake mzazi alikuwa amekuja tena pale shuleni, ingawa ni yeye alimtafutia Samir hiyo shule ila aliamua kurudi tena kuongea nae, basi wakaingia ofisini na kuanza kuongea na Samir ambapo mama yake alianza kumwambia,“Naona nyumbani nimeshasema sana hadi pumu imenishika, leo nimekuleta hapa shuleni, huwezi amini nimeenda hadi stendi ya daladala ila sijapata hamu ya kupanda gari nimeamua kuja tu kuongea na wewe, si unajua mume wangu ana usafiri lakini leo alifungia magari yote maana hataki kusikia huu ujinga wako. Jamani Samir, leo naongea na wewe kwenye hii ofisi kwa mara ya mwisho, naongea kama mama mwenye uchungu na mtoto wake, Samir tafadhari sitaki ujinga, yani sitaki ujinga kabisa yani kile leo nakuhamisha shule sababu ya ujinga wako, ile shule ya kwanza ulimshika mwalimu makalio ukafukuzwa, shule ya pili ulimpiga mwanafunzi mwenzio ukafukuzwa, sasa shule ile ya tatu umeanza kuongea na simu shuleni jamani na skendo za mapenzi zimekufukuzisha, hivi Samir akili yako ikoje? Nani aliyekuroga? Hebu soma mwanangu, upate kazi nzuri uone kama kuna mwanamke yoyote wa kukukataa wewe Kwakweli Samir ukifanya ujinga wako na shule hii ujue sina dhamana na wewe, yani ufukuzwe shule basi tutabaki nyumbani tukiangaliana, ujinga sitaki jamani!”“Sawa mama, nimekuelewa na haita jirudia tena”“Haya nipe simu yako, yani umefanya kila mtu anitukane kuwa sina malezi bora kwako hata mume wangu kanitukana mjinga wewe umeniletea balaa tu katika maisha yangu”Basi Samir akaitoa simu aliyokuwa ameiweka kwenye mfuko wa suruali yake, kisha kumkabidhi mama yake ambaye aliichukua na kuiweka kwenye mkoba wake kisha Samir akaambiwa arudi darasani, kisha walimu wakaanza kumsema mama Samir,“Ila na wewe una makosa, utamuachaje mtoto anakuja shuleni na simu? Yani sisi tungemkamata nayo u basi tusingejari ni hela ngapi umetoa zaidi zaidi tungemfukuza shule, inaonyesha kijana wako ni kiburi sana”“Jamani walimu naomba mnisaidie tafadhari, naomba mnisaidie, natambua kuwa nyie pia ni walezi naomba mnisaidie yani huyu mtoto anafanya niumwe kichwa kila kukicha jamani, naomba mnisaidie walimu. Muwe nae karibu tafadhari”Akajitokeza mwalimu mmoja na kusema,“Usijali mama Samir, mimi nitakuwa na huyu bega kwa bega”“Asante sana mwanamke mwenzangu, Napata shida mimi”“Basi usijali, yani mimi ndiye mwalimu ninayeogopewa na wanafunzi wote hapa shuleni, kwahiyo usijali wala nini”“Asante sana”Basi mama Samir aliaga wale walimu na kuondoka zake.Muda wa kukaribia kutoka, mwalimu ambaye alijulikana shuleni kwa jina la madam Hawa, alimuita Samir na kuanza kuongea nae,“Sasa Samir, mimi ndio nimeachiwa wewe hapa shuleni nikuangalie na kukulea, nasikia kichwa chako hiko ni kitupu basi mimi nitakijaza maji na mchanga ili upande uwa kichwani. Sikia nikwambie kitu, unapokuja shuleni unatakiwa uje kuniona mimi na unapoondoka shuleni unatakiwa kuja kuniona mimi pia. Hilo sio ombi bali ni amri, sijui tumeelewana”“Nimekuelewa ndio”“Haya unaweza kwenda sasa”Katika shule hii hapakuwa na usafiri kama shule zingine, kwahiyo wanafunzi waliondoka na kwenda kupanda madaladdala kurudi nyumbani kwao niomana hata Angel alikuwa akipelekwa na dereva na kufatwa na dereva, mama Angel hakupata nafasi ya kumpeleka Angel kwenye shule atakazo kwahiyo ilibii ampeleke kwenye hiyo shule kwani alisikia nayo inafundisha vizuri.Basi Samir aliondoka ili kurudi kwao ila aliongozana na yule kiranja wa darasa ambaye alimkaribisha na alikuwa akiitwa Adam basi alianza kuongea nae,“Naona madam Hawa alikuita?”“Ndio, alikuwa akinipiga mikwara yake”“Ana mikwara yule madam hatari sababu anajua wanafunzi wengi tuna muogopa, ila yule madam tatizo lake hana mume”“Kheee kwanini?”“Sijui alitendwa huko anajua mwenyewe, yani madam ana hasira yule sijapata kuona, ukimsogelea tu utashangaa umenaswa kofi, sasa kama kashakupiga mikwara basi ujipange ndugu yangu”“Aaaah sawa, nimekuelewa”Basi waliongozana na kuongea hadi stendi ya daladala na kila mmoja alipanda daladala ya kuelekea nyumbani kwao.Leo baba Angel alirudi mapema nyumbani kwake na alimuita mkewe chumbani ili kuzungumza nae mawili matatu,“Mke wangu jamani nataka watoto”“Kheee bado una mambo hay ohayo jamani!”“Ndio, furaha ya ndoa ni watoto. Kwa mama yangu nimezaliwa peke yangu, na kwa baba yangu tumezaliwa waaili tu kama jicho, kwakweli nahitaji kupata watoto ili tufurahi pamoja na familia iwe kubwa mahali hapa”“Sawa, mfano je nikiwa sina uwezo tena wa kushika mimba?”“Ukiwa huna uwezo wa kushika mimba hiyo inajulikana mke wangu na wala sio sababu ya mimi kuchukia ila mke wangu najua uwezo huo unao sema unatumia zile njia zenu za uzazi wa mpango, mke wangu ulipozaa tu watoto wetu mapacha ukaweka kitanzi, nikatulia tuli miaka kumi na mbili ikapita na wala huna mashaka wala wasiwasi wowote kuwa nimzalie tena mume wangu, zaidi zaidi kumsema dada yangu kuwa kazaa kama panya, sawa kazaa kama panya ila ni furaha kubwa kwa mumewe ambaye ni kaka yako, tunawasema sasa ila badae tutawafurahia. Mke wangu mambo ya kitanzi sijui ndio ukayachoka, umeenda kuweka kijiti kweli jamani ni haki hiyo? Halafu unasema kama huna uwezo wa kushika mimba je wakati uwezo huo unao jamani mke wangu, mimi nataka watoto”“Jamani Erick, mimi nimechoka kulea mimba”“Kwani hiyo mimba utailea mwenyewe? Si tutakuwa sote katika kulea? Na safari hii nakwambia nitakuwa nawe bega kwa bega, nakupenda sana mke wangu kwakweli nahitaji mtoto. Kama kuna kitu nilikukosea kwenye mimba ile ya mapacha naomba unisamehe”“Unadhani nasahau uliyoyafanya kipindi nakaribia kujifungua? Ndiomana sina hamu hata ya kubeba mimba”“Naomba unisamehe mke wangu na hayo yapite, haitojirudia tena”Baba Angel alipiga na magoti kabisa, ilionyesha ni kwa jinsi gani alikuwa na uhitaji wa watoto wengine toka kwa mke wake, basi mama Angel alimjibu kuwa amaemuelewa.“Sawa nimekuelewa”“Eeeh na ile ahadi ya kunipikia kile chakula kizuri imekuwaje? Maana tatizo lako mke wangu muda wote kuchunga watoto hata unasahau kuhusu mumeo”“Nisamehe kwa hilo mume wangu, ngoja nikakuandalie leo”Basi aliinuka na kumuacha mumewe chumbani kisha alienda kumuandalia chakula anachokitaka.Angel alirudi kwa shangazi yake, na aliporudi tu shangazi yake alimuita na kumuuliza,“Ni kitu gani kimetokea leo shuleni?”“Jamani shangazi hata salamu!! Shikamoo”“Marahaba, nasikia kuna mkaka aliingia darasani kwenu mkaangaliana sana”Angel alishangaa kuwa shangazi yake amejuaje tukio lile, basi alinyamaza kimya tu kisha shangazi yake akaendelea,“Angel, kuwa makini na masomo yako, mama na baba yako sio wajinga kuhangaika na wewe kila siku yani kila siku wimbo ni Angel tu kwakweli tumechoka, kuwa makini na masomo na sitaki kusikia habari za wewe kumuangalia tena kijana hivyo”Basi Angel alienda chumbani ila alikuwa na maswali mengi sana kuwa kwanini shangazi yake ameelewa kile kilichotokea shuleni kwa siku hiyo? Ila hakuwa na jibu wala nini zaidi ya kuamua kwenda ndani na kufanya mambo kama ratiba inavyosema.Kulipokucha alijiandaa na kwenda shuleni kama kawaida ila leo Husna alimwambia jambo lingine,“Unajua Angel unapitwa na vitu vingi kwa unavyoletwa na gari na kufatwa na gari? Utajifunza lini jinsi jamii ilivyo?”“Sasa mimi nifanyeje unadhani?”“Ongea na kwenu wapunguze gharama za wewe kufatwa na gari kila siku, bora kuletwa tu ili usichelewe shule ila kufatwa na gari jamani mambo mengi sana unayakosa Angel”“Mmmh nitafikiria uyasemayo”Basi waliendelea na masomo ila Angel alijikuta akimuangalia Samir kwa macho ya wizi ila hata Samir nae alionekana akimuangalia Angel kwa macho ya wizi kiasi kwamba kila muda walijikuta wakigongana macho yao na kushusha sura zao chini.Muda kidogo aliingia madam Hawa na kumuita Samir ambaye aliinuka na kumfata madam Hawa.Kiukweli Angel hakupenda ile hali ila ilibidi atulie tu kwani alikumbuka maneno ya shangazi yake kuhusu kutulia na kuangalia maisha yake. Ila muda ule ule Husna alimuuliza tena Angel,“Mbona kama umeshtuka kwa mwalimu Hawa kumuita Samir? Unafahamiana na Samir”“Mmmh hapana, sifahamiani nae. Halafu sijashtuka hicho bali nilikuwa na mawazo yang utu”“Aaah nilijua labda unafahamiana nae”“Hapana simfahamu”Angel aliona ni vyema kwake kukataa kuhusu kufahamiana na Samir ili abaki kuwa huru katika fikra zake.Muda wa kutoka kama kawaida, dereva alifika kumchukua na kumrudisha kwa shangazi yake na alivyofika tu kama kawaida shangazi nae alianza kumuuliza za shule, naye alimjibu vyema tu kisha shangazi yake akamwambia,“Leo nimefurahi maana sijasikia chochote kibaya kuhusu wewe, ila ngoja nikwambie jambo moja kwenye nyumba hii kufaulu ni lazima na sio hiyari, yani lazima ufaulu mitihani yako”“Nakuhakikishia nitafaulu shangazi, si unaona hata mitihani ya kawaida ninavyofanya!”“Nimeona ndio”Basi Angel alienda ndani ila kiukweli ratiba ya hapa kwa shangazi yake ilikuwa ikimchosha, maana hakuna ratiba kusema atapika, kufua au kuosha vyombo, ila tu huwa anakuta sare zimefuliwa na msichana wa kazi, chakula kimepikwa na vyombo vimeoshwa. Kwavile hakupenda aina ile ya maisha aliamua kwenda kuongea na shangazi yake,“Shangazi nina ombi moja”“Niambie ni ombi gani?”“Shangazi, unajua mimi na wakina Leah tupo tofauti sana, mimi ni mkubwa na wakina Leah ni wadogo kwahiyo si vizuri ratiba yangu iwe sawa na wakina Leah. Shangazi, kwenye ratiba yangu hakuna kupika, kufua wala kuosha vyombo na hizo ndio kazi za kike shangazi, sasa mimi nitakuwa nakaa tu kila siku bila kufanya kazi yoyote?”“Ndiomaana nina wafanyakazi wawili, mwingine anakuja kila siku na mwingine analala hapa hapa”“Hata kama shangazi, ila kuna ulazima wa mimi kuwasaidia kazi au la punguza mfanyakazi mmoja. Jamani pale kwetu mama kaweka mfanyakazi hivi karibuni ila tumekuwa pale bila mfanyakazi yoyote yule, shangazi tafadhari naomba hata kwa Jumamosi tu raiba yangu isome kupika au kuosha vyombo au kufua tafadhari”“Sawa nitafikiria na hilo, kuna lingine?”“Ndio shangazi, ningeomba huyu dereva anayenipeleka, mpunguze gharama kidogo yani asiwe anakuja kunichukua shuleni”“Kheee wee mtoto una wazimu eeeh! Hakuna kitu kama hiko, hebu sahau kuhusu hilo”Basi Angel akainuka tu na kuondoka wala hakuongea kingine chochote na shangazi yake.Erica akiwa getini kutoka shuleni, alishtuka kuona mtu kamziba macho kwa nyuma, basi akaanza kukisia,“Nani wewe jamani, ila vidole vyako ni vya Erick”Alikuwa akimpapasa mikono ili akisie ni nani, basi Erick alimuachia huku akicheka sana na kusema,“Kweli unanijua, hadi vidole Erica wangu jamani”Erica nae akacheka na kusema,“Yani mchezo huo anao Elly shuleni, sasa kumbe na wewe unao”“Hivi Elly nani? Mbona vitu vingi vyangu unasema ni kama vya Elly?”“Elly nae ni kaka yangu, wewe si uliondoka kunilinda hukutaka tena, basi akapatikana Elly”Wakaingia ndani huku wakiongea ongea, ila Vaileth aliwauliza,“Jamani nyie mnasoma shule tofauti ila kila siku mnarudi pamoja, huwa mnaambizana au inakuwaje?”Erick akajibu,“Hii inatokea tu wala huwa hatuambizani”“Oooh ni sababu nyie ni mapacha eeeh!”Wote wakacheka na kila mmoja kwenda chumbani kwake kwaajili ya kubadili sare za shule.Leo walipotoka kubadili sare zao walirudi sebleni na kuanza kuangalia Tv, yani hadi muda mama yao anarudi aliwakuta sebleni wakiangalia Tv, basi alikaa chini na kusema,“Haya ndio malezi ambayo wifi yangu hayataki kwakweli, hivi Erica na Erick huwa hamna homework? Huwa hamna vitu vya kujisomea kweli? Kile chumba cha kujisomea niliweka cha nini jamani! Haya sitaki kuwaona hapa, muende mkajisomee”Basi Erica na Erick waliondoka zao na kuelekea kwenye vymba vyao, hata hawakuelekea kwenye chumba cha kujisomea.Muda kidogo baba Angel nae alirudi ikabidi mama Angel aende na mumewe chumbani basi walisalimiana pale na kuanza kuongea ya hapa na pale ambapo baba Angel alimuuliza,“Leo usiku tunakula chakula gani?”“Mmmh hata sijaangalia, ngoja nikamuulize dada”“Oooh huyu sio mke wangu jamani”“Kwanini?”“Unajua sijakuzoea hivi kabisa! Chakula ukamuulize dada kweli jamani! Nahitaji uniandalie wewe chakula”“Umeanza sasa, ndio unataka nibebe na mimba jamani, hiyo mimba nitaibeba mgongoni au? Ili nibebe na niwe nakuandalia chakula”“Mbona kipindi una mimba tulikuwa tunapika wote na kula wote, itakuwaje kwasasa nishindwe!”“Halafu mambo ya biashara kule yananitinga mume wangu, kwahiyo narudi nimechoka”“Jamani, jamani kwani huwa nasemaje mimi!! Sawa tuache hayo, ila kwa leo sili chakula kilichoandaliwa na Vaileth, nataka uniandalie wewe”Mama Angel alitoka chumbani akiwa amechukia kiasi ila hakuwa na namna zaidi ya kwenda kumuandalia mumewe chakula, aliona kama anampa adhabu vile, akajiuliza kuwa labda kwavile hajabeba mimba maana alishindwa kumuelewa mumewe kuwa analengo gani naye mpaka amwambie kwenda kumpikia kwa muda huo.Basi alipomaliza alimuandalia mumewe na kumkaribisha chakula, basi mumewe alifurahi sana na kusema,“Huyu sasa ndio mke niliyemuoa”Akatabasamu na kukaa pamoja na mumewe wakila kile chakula, kwakweli hata Vaileth alijikuta akitamani sana maisha ambayo baba Angel na mama Angel walikuwa wakiyaishi, hata alijiuliza kama huwa wanagombana kwa jinsi walivyokuwa wakila kwa pamoja na kutabasamu pale mezani.Muda huo Erica na Erick pamoja na dada yao walikuwa wameshakula kwahiyo walikaa sebleni huku wakiongea kwa chini chini ambapo Vaileth ndio aliyaanzisha maongezi yale,“Wazazi wenu wanaonyesha kupendana sana, hivi wamewahi kugombana?”“Mmmh hapana, hatujawahi kusikia wakigombana”Kisha Erica na Erick waliinuka na kwenda chumbani ambapo nao wazazi wao walimaliza kula na waliinuka na kwenda chumbani pia.Muda wa kulala, Erica alienda chumbani kwa Erick na kuanza kuongea nae kuhusu wazazi wao,“Mama na baba wanapenda sana kama dada Angel na Samir vile”“Ila wewe Erica kuna muda una wazimu ujue, yani mama na baba ukawafananishe na Angel na Samir kweli?”“Aaaah basi nimesemea tu”“Haya niambie, huu ni muda wa kulala kwani unakuja kulala chumbani kwangu leo?”“Kheee jamani Erick loh!! Mimi niliona nimeboreka na usingizi sina ndiomana nikaja huku, nitalalaje chumbani kwako sasa?”“Unadhani kuna ubaya wowote? Hakuna ubaya wala nini, vipi Abdi hajakupa tena karata tucheze? Ila hata hivyo kesho ni shule ujue”“Sawa, ngoja nikalale tu”Erica aliondoka na kwenda chumbani kwake kulala, basi Erick alibaki akijiuliza,“Huyu dada yangu ana nini lakini? Muda huu alikuja kufanya nini? Nakumbuka hapo nyuma ni mimi nilikuwa msumbufu kwake ila kwanini kwasasa yeye ndio kawa msumbufu?”Akaachana na mawazo na kuamua kulala tu.Kulipokucha kama kawaida walijiandaa na kwenda shuleni ila Erica alipofika leo alizibwa macho na Elly yani kama jana yake alivyofanyiwa na Erick basi akacheka na kusema,“Nimekugundua ni Elly wewe”Basi Elly alimuachia na kucheka pia huku akimwambia,“Mwanzoni nilikuwa nikikugusa lazima ukosee ila leo umesema upesi upesi kuwa ni Elly”“Ndio maana shuleni ni wewe ndio mwenye mtindo wa kuniziba macho na nyumbani ni Erick ndio mwenye mchezo huo”Basi walicheka kwa pamoja na kuingia kwenye kipindi vizuri.Kitendo cha Erica kuwa karibu na Elly kilikuwa kinamkera sana Abdi, na kuona kamavile Elly kaja kumzibia nafasi yake kwa Erica, basi akasogea alipo Erica ingawa kashapewa onyo mara nyingi tu na Elly ila alisogea na moja kwa moja alimpa Erica karata maana alitambua ndio ugonjwa wake,“Erica, nimekuletea karata leo”“Oooh Abdi jamani, asante sana. Nashukuru kwa hili”Elly alimuangalia Abdi na kumwambia,“Nilikwambiaje?”Erica akasema,“Jamani Elly achana na hayo mambo, Abdi ni rafiki yangu mkubwa kama ulivyokuwa wewe, kwahiyo hata usiwe na mashaka na Abdi.”Kisha akamuangalia Abdi na kumwambia,“Nashukuru sana kwa karata Abdi”Basi Abdi akasogea na kumnong’oneza kitu Erica ambapo Erica alicheka tu.Angel nae akiwa shuleni bado Husna alimwambia umuhimu wa kurudi na kuongozana na wenzie yani asiwe anatumia usafiri kila leo,“Angel, unapitwa na kuona mengi na kujifunza mengi pia. Unajua mimi napenda utambue dunia imezungukwa na vitu gani? Na watu gani? Watoto wengi wa matajiri huwa hampati nafasi ya kujifunza mambo mengi yanayoizunguka jamii, jaribu kuongea na dereva wenu ili upate nafasi na wewe nya kutembea na wenzio, kuongea mambo mbalimbali”“Sawa nimekuelewa, ila sijui kama nyumbani watanielewa”“Wewe ongea na dereva tu, naamini atakuelewa. Tena kesho ni Ijumaa Angel, jitahidi tuondoke pamoja hadi stendi”“Sawa, hakuna tatizo”Basi muda huo huo alifika tena madam Hawa na kumuita Samir, yani ilikuwa ni kawaida kwa huyu madam kufika na kumuita Samir.Muda wa kutoka ulipofika kama kawaida dereva alifika kumchukua Angel na kuondoka nae, walipokuwa njiani Angel akamwambia dereva,“Sikia anko, kesho nipeleke tu shule ila usije kunichukua”“Mmmh unadhani mama yako atanielewa?”“Atakuelewa ndio, ila usimwambie nakuomba. Na mimi nahitaji kupanda daladala, yani kipindi mama na baba wamesafiri nilikuwa nafaidi sana na kupanda daladala ila kwasasa kila sehemu dereva jamani nimechoka, naomba kesho usije kunifata bhana”“Ila usimwambie mama yako ukweli”“Sitomwambia, na leo usinifikishe nyumbani kwa shangazi kabisa ila nishushe karibu na pale nitembee kidogo”Yule dereva alikubali na kweli walipofika karibu alimshusha Angel ambapo alianza kutembea kuelekea kwa shangazi yake, wakati anakaribia getini, ilipita bajaji mbele yake kisha yule mwenye bajaji alisimamisha na kumwambia Angel,“Oooh siamini kama leo nimekuona tena Malaika”Kwakweli Angel hakuwa na kumbukumbu yoyote ya kuonana na huyu dereva bajaji kabla, kwahiyo alibaki akimuangalia tu, kisha yule dereva akamwambia,“Mimi naitwa Ally, niliwahi kumleta mama yako nyumbani kwenu kisha wewe ukaniletea hela. Uminikumbuka?”Angel akajaribu kuvuta kumbukumbu, na kukumbuka lile tukio ila sura ya huyu dereva wa bajaji ilikuwa imemtoka na kumwambia,“Nimekumbuka ndio, kumbe ni wewe?”“Ndio ni mimi, naomba namba yako mrembo”“Sina simu”“Mmmmh mtoto mrembo kama wewe huna simu! Basi hakuna tatizo maana nitakuletea simu”“Mmmmh hapana usiniletee maana nitaiweka wapi? Siruhusiwi kumiliki simu maana mimi ni mwanafunzi bado”“Kheee maisha gani unayoishi hayo mrembo jamani, siku hizi mtoto wa miaka kumi anamiliki simu sembuse wewe jamani”“Hapana, mimi siruhusiwi”“Oooh basi nitakuwa nakuvizia mida kama hii ili angalau nikuone tu mrembo, mmmh watu wengine jamani kama hamjisaidii vile”Angel aliondoka zake na kwenda kuingia ndani kwao ila leo shangazi yake hakuwepo nyumbani kwahiyo aliingia tu bila kuulizwa chochote kile.Kama kawaida, Erick na Erica nao walirudi nyumbani kwao ambapo kila mmoja alienda chumbani kwake kuvua sare za shule, ila baada ya muda kidogo tu Erica alienda chumbani kwa Erick na kumuonyesha zile karata, basi Erick alichukia na kumwambia,“Ni Abdi kakupa eeeh!”Alipoona kaka yake kachukia ilibidi abadili ukweli na kumwambia,“Hapana, nimepewa na Elly”“Oooh sawa, basi tutacheza hizo karata”“Ila kaka mbona Elly huchukii ila Abdi unachukia?”“Sijui ni kwanini ila Abdi simuamini hata kidogo nadhani imetokea tu hivyo”“Basi naziweka kwako halafu kesho tuatacheza”Erica aliziacha pale kwa kaka yake kisha yeye alienda chumbani kwake.Siku hiyo hawakuweza kucheza karata kwani kila mmoja alikuwa kachoka kwahiyo usiku walilala tu ndiomana walisema kuwa karata wangecheza kesho yake usiku.Kulipokucha kama kawaida walijiandaa na kwenda shuleni basi wakiwa shuleni, Erica alifatwa na Abdi leo ambapo alimuuliza,“Ujumbe wangu kwenye zile karata umeuona?”“Ujumbe? Ujumbe gani kwani?”“Kuna ujumbe wako nimeuweka katikati ya zile karata”“Ni mzuri au mbaya?”“Kwani vipi?”“Zile karata nimempa kaka yangu Erick aziweke kwanza”“Oooh kwanini umefanya hiyo Erica jamani!! Naomba ukirudi tu kwenu ukazichukue zile karata na kuzichambua ili utoe ule ujumbe”Erica alimuangalia Abdi aliyeonyesha kachukizwa kabisa kuhusu karata kuachiwa Erick wakati zina ujumbe wake.Leo Angel akiwa shuleni basi hakuwa na mashaka sana kwani alishamwambia dereva kuwa asimfate na alikuwa na uhakika wa kuondoka na Husna kama walivyopanga.Ila muda kidogo Husna alianza kulalamika tmbo, yani tumbo likawa linamsumbua sana ikabidi hadi mwalimu ampe ruhusa ya kwenda nyumbani kwahiyo Husna aliondoka na kwenda kwao na hivyo Angel kubaki mwenyewe.Muda wa kutoka ilibidi Angel aondoke mwenyewe huku akifatiliza tu wanafunzi wenzie wanapoelekea, gafla akaitwa“Angel”Akageuka na kukuta ni Samir ndio alimuita ila alikuwa akihema, basi Angel alimuuliza,“Mbona unahema hivyo?”“Nilipokuona unaondoka mwenyewe nikaanza kukukimbilia, yani yule madam nae ananitesa balaa”“Kwani anakuitiaga nini?”“Yani acha tu, nikija shule lazima niripoti kwake na nikitoka lazima niripoti kwake pia”“Pole sana”“Asante kipenzi changu”“Umeanza hivyo, mimi sitaki bhana, usiniite hivyo”“Ila Angel, mimi na wewe inatakiwa tupate sehemu tuongee vizuri. Hata macho yako yanaonyesha kuwa unanipenda pia”Angel akaona atembee tu bila kumjibu chochote Samir kwani alihisi kuwa anaanza tena kumshawishi.Mama Angel kwasasa aliona nafuu kidogo kwani hakupata malalamiko yoyote kuhusu Angel yani hakusikia chochote kinachoendelea juu ya Angel, ila aliona ni vyema kama atapita shuleni kwao ili akamchukue mwenyewe na ajaribu kuongea nae mawili matatu na mwanae kwahiyo alimtumia tu ujumbe dereva,“Leo usiende kumchukua Angel, naenda mwenyewe”Basi alikuwa kwenye gari yake na moja kwa moja alielekea shuleni kwakina Angel.Alipofika alishangaa kukuta ndio muda huo wanafunzi wakiwa wanatoka shuleni, alishangaa mbele kuona Angel ameongozana na Samir wakitembea kuelekea kwenye stendi ya daladala.Alipofika alishangaa kukuta ndio muda huo wanafunzi wakiwa wanatoka shuleni, alishangaa mbele kuona Angel ameongozana na Samir wakitembea kuelekea kwenye stendi ya daladala.Kwakweli mama Angel alichukia sana na kutamani hata kushuka ili awafuate maana njia waliyopita huwa hayapiti magari, kwakweli alichukia sana na kuwasha gari yake ili awakute stendi.Ila alivyofika stendi tu na wao ndio walikuwa wakipanda daladala, yani alichukia mno na kupigia honi ile daladala ila wala haikusimama yani alijikuta akijawa na hasira katika moyo wake balaa huku akisema,“Huyu Samir ananitakia nini tena jamani, yani nimemuamisha Angel shule ila kamfata jamani!”Wakati akiwaza hayo kumbe alikuwa kasimamisha gari barabarani na kusababisha foleni basi honi nyingi zikawa zinapiga kwake, akashtuka na kuogopa ila alipoangalia hakuiona tena ile daladala kwani zilipita nyingi nyingi, basi hasira zilimzidi yani alikuwa akiendesha gari huku ana mawazo na hasira aliamua kulipaki pembeni kwani kwa hali aliyokuwa nayo angeweza hata kupata ajali, akampigia simu tu dereva wao ili apande bodaboda na aende mahali alipo ili waweze kuondoka.Angel akiwa kwenye daladala na Samir, basi konda alipokuja kudai nauli Samir alilipa nauli ya watu wawili yani yeye na Angel, basi Angel akamuangalia na kumwambia,“Ila mimi nauli ninayo”“Sijasema kuwa huna ila mimi ni mwanaume na lazima nikuhudumie”“Kheeee makubwa”“Usishangae Angel, mtu unapopenda kuna mambo unayafanya kama umechanganyikiwa vile”“Pole”“Sio pole tu, unatakiwa uonyeshe ushirikiano”“Sasa ushirikiano gani?”“Uwe unaniambia kuwa unanipenda pia ili nami nifurahie, najua unanipenda ila niambie”Basi Angel alikaa kimya, na alipofika kituo anachoshuka alishuka ila Samir nae alishuka na kuongozana na Angel ambapo Angel alimuuliza,“Kwani na wewe unaishi huku?”“Hapana”“Sasa mbona umeshuka?”“Lazima nihakikishe kuwa unafika salama ndio nami niondoke”“Mmmh hapana, usifike nami kwa shangazi, unataka kuniletea balaa wewe”Basi Angel aliita bajaji ambapo alipanda na kumtaka dereva aondoke, kilikuwa ni kitendo cha haraka kwahiyo Samir hakuweza kupanda pia.Basi Angel akiwa kwenye ile najaji alishangaa kukuta ni yule Ally ndio kambeba kwenye bajaji,“Kheee kumbe ni wewe?”“Ndio ni mimi, yani leo nahisi nitalala huku nikitabasamu kwa kumbeba mrembo kwenye bajaji yangu”“Mmmh wewe nawe loh!!”“Sio hivyo ila wewe ni mrembo sana”Angel aliamua kukaa kimya tu mpaka walipofika getini kwa shangazi yake na kushuka huku akimuuliza yule dereva,“Unanidai pesa ngapi?”“Hapana sikudai mrembo, nimekubeba tu”“Mmmh!”Basi Angel aliingia kwenye geti lao na moja kwa moja alienda chumbani kwake maana hakumkuta shangazi yake pale sebleni.Leo Erick aliwahi kurudi nyumbani tofauti na siku zote ambazo huwa anarudi na Erica, basi akabadili sare zake na kwavile alijihisi kuchoka aliamua kuchukua zile karata zilizoletwa na Erica ili acheze kidogo.Basi alikaa kitandani na kuzichukua ambapo alizichanga ila kuna kikaratasi kilianguka ikabidi akiokote na kukisoma,“Nakupenda sana Erica”Erick alishtuka mno na kujiuliza,“Inamaana Elly ndio kamuandikia Erica huu ujumbe? Mmmh nae ameanza huu ujinga kweli!”Erick alishangaa sana ila alimngoja Erica arudi na aliposikia tu kuwa amerudi basi aliinuka na kwenda chumbani kwake, naye alifika chumbani kwa Erica na kufungua tu mlango yani hakugonga wala nini na kumfanya Erica apige kelele maana kifuani alikuwa wazi, ila alipoona ni Erick alinyamaza na kujifunga na khanga kisha akamsema,“Erick tabia mbaya hiyo, unaingia chumbani kwangu bila hodi!”“Mbona na wewe huwa unaingia chumbani kwangu bila hodi?”“Kwahiyo ndio umenilipizia? Muone vile”“Ila kifua chako kimekuwa kizuri”“Sitaki ujinga Erick, muone vile haya sema kilichokuleta”“Chukua ujumbe wako wa kwenye karata”Basi akampa ile karatasi na kumuuliza,“Inamaana Elly ndio kakuandikia hivyo!! Elly si huwa unasema ni kaka yako?”“Mmmmh aaaah karata hajanipa Elly”“Ila alikupa Abdi eeeh!”“Ndio”“Nilijua tu, yani Erica unataka kuruhusu ujinga wa huyu mapema ukuharibie masomo!! Bora nilihama hiyo shule, sitaki kujiumiza kichwa, sasa endelea na ujinga wako halafu utaona nitakacho kifanya”Halafu Erick aliondoka zake, huku Erica akisoma kile kiujumbe kifupi na kwenda kukitupia chooni.Mama Angel alifika kwa wifi yake akiwa na hasira sana, aliingia sebleni na kuita kwa hasira,“Angel, Angel, Angel”Wifi yake alitoka na kumuuliza,“Kuna nini kwani?”Angel nae alitoka, basi mama yake alimvuta na kumzaba kofi mbili mbili huku akimsema,“Hivi wewe mtoto unataka hadi usikie mamako amekufa ndio utafurahi”Shangazi yake akauliza,“Kafanyaje tena?”“Yani huwezi amini wifi, leo nikasema ngoja nikamuangalie Angel shule na nimchukue mwenyewe hadi dereva nikamtumia ujumbe kuwa asiende kumchukua Angel, nilichokikuta sasa? Eti Angel yupo na yule mjinga mwenzie Samir wakielekea kwenye kituo cha daladala, mjinga huyu kafanya leo bado kidogo tu nipate ajali jamani”“Kheee pole wifi yangu jamani”Kisha Shangazi akamuangalia Angel na kumuuliza,“Inamaana Samir nae anasoma hapo shuleni kwenu?”“Ndio shangazi, hata mimi sikujua kumbe aliahamia pale”“Haya niambie imekuwaje mpaka ukaongozana nae kurudi nyumbani”“Shangazi ni hivi, mimi na Husna tulipanga leo kurudi pamoja tu, ila Husna akaumwa gafla na kurudi kwao basi wakati wa kutoka ikabidi tu niondoke mwenyewe, ila dereva hahusiki kwa hili maana nilimdanganya kuwa asije kunichukua, ila wakati naondoka gafla alikuja Samir ila kweli kabisa shangazi sikutaka kuongozana nae”“Haya, nenda chumbani kaendelee na ratiba yako ya leo”Mama Angel alimshangaa wifi yake kujibu kirahisi hivyo, pia alishangaa mwanae kwa mpangilio wa lile jibu na kumuuliza wifi yake,“Una uhakika alichokujibu ni cha ukweli?”“Mimi sitaki kumjengea mtoto mazingira ya uoga ila namjengea mazingira ya kuniheshimu, na nikisema nitakupiga basi ujue nishampiga maana sina msemo wa nitakupiga, atazoea na kujua ni uongo tu. Halafu huwa nawafundisha kuwa wakweli maana mimi ni mchunguzi kupita unavyoelewa, kwahiyo swala la Angel niachie mimi mwenyewe tu kwani huyu Angel nitamnyoosha, kama alikuwa akikudanganya ni wewe maana mimi sidanganywi kirahisi namna hiyo”“Kheee saa wifi tufanyeje? Tumuhamishe shule au?”“Hapana wala usiingie gharama nyingine wifi yangu ila mimi nitakula nae sahani moja huyu hata usiwe na mashaka wifi yangu”Mama Angel alikaa sasa akapumua kisha wifi yake aliamua kumletea juisi ili ashushie na zile hasira alizokuwa nazo.Aliongea kidogo tu na kuaga maana dereva alimuacha ndani ya gari.Mama Angel alipofika na dereva nyumbani kwake aliamua kumwambia sharti lake kuu,“Ni lazima kumpeleka Angel shule na kwenda kumchukua hata akisemaje ni lazima kufanya hivyo”“Sawa mama nimekuelewa”Basi mama Angel aliingia ndani na kumkuta Vaileth akipika, basi alimuuliza,“Dada, unapika nini leo?”“Wali dada, njegere na nyama. Si shemeji atakula?”“Atakula ndio maana huwa anapenda”Kisha mama Angel aliondoka ila Vaileth alimuita na kuongea nae kidogo,“Mama samahani, kuna ndugu yangu anataka kuja kunitembelea?”“Anataka kuja lini?”“Jumapili mama”“Sawa hakuna tatizo, anakaribishwa”“Asante mama, ila ataondoka Jumatatu”“Sawa hakuna tatizo”Kisha mama Angel akaenda zake chumbani kupumzika kwani alikuwa na mawazo yake ya kutosha tu ukizingatia kilichotokea siku hiyo.Baada ya muda kidogo tu mumewe alirudi na kugundua kuwa mke wake amechoka ila alimuamsha na kuanza kuongea nae ambapo mama Angel alimueleza yaliyotokea siku hiyo,“Duh mke wangu hadi nakuonea huruma jamani, huyu Angel atakutoa kizazi mweeeh!! Hebu nizalie mie wadogo zake, acha habari za kumfatilia Angel”“Ila una nini mume wangu jamani! Kwahiyo Angel akileta mimba hapa nyumbani itakuwaje?”“Nitaelea”“Kheeee!!”Mama Angel alichukia na kuinuka kisha moja kwa moja alienda chumbani kwa Angel kwahiyo alimuacha mumewe chumbani akiwa mwenyewe.Ilibidi mume wake amfate kwani kitu ambacho huwa hapendi katika maisha yake ni kugombana na huyu mwanamke,“Sasa mke wangu unataka kuweka picha gani kwa watoto jamani eeeh! Hebu turudi chumbani”Basi mama Angel aliinuka na kurudi chumbani, kisha mumewe alianza kumuomba msamaha ambapo mama Angel alikuwa kajinunisha tu kisha mumewe akamwambia,“Mama Angel, nilishakwambia na bado nakwambia kuwa wanaume kama mimi katika dunia hii tupo wachache sana na labda nimebaki mwenyewe, mwingine labda atakuwa na masalia yang utu, mke wangu sipendi kukukera, sipendi uchukie, sipendi unune kwani tabasamu lako ndio afya kwangu. Nakupenda sana mke wangu, ila nilikuwa naongea tu ili hawa watoto tusiwafatilie kivile, tuwafatilie ndio ila sio kwa stahili hiyo ambayo unaifanya, kwakweli itakutesa mwenyewe mke wangu, nakupenda sana. Naomba unisamehe”Kisha baba Angel alimbusu mama Angel, naye mama Angel alitabasamu kuonyesha kwamba ule msamaha kaupokea vizuri kabisa, kisha walianza kushirikiana kwenye mambo mbalimbali.Muda wa kula walitoka na kwenda kula pamoja na familia ila leo walikula chakula ambacho kiliandaliwa na Vaileth, kwakweli Vaileth nae alifurahi sana kwani alipenda mno kumuona baba mwenye nyumba akila kile chakula chake huku akitabasamu.Basi Erica na Erick nao walipomaliza kula waliinuka ili kuondoka zao ila mama Angel alimuita Erick na kumwambia,“Mwanangu naomba kesho uamke mapema unioshee gari yangu, sawa baba eeeh!!”“Sawa mama hakuna tatizo”Basi waliawaaga wazazi wao pale na kila mmoja aliondoka zake na kuelekea vyumbani kwao ila Erick alivyofika chumbani kwake tu alichukua zile karata ili ampelekee Erica.Alivyofika tu akamwambia Erica,“Chukua karata zako hizi urudishe kwa huyo kichaa wako”“Jamani Erick, usiseme hivyo, njoo tucheze pamoja”“Hapana, siwezi cheza karata za huyo mpuuzi”“Basi tusicheze karata, ila njoo tusimuliane mambo mbalimbali”Basi Erick alitulia na kwenda kukaa kitandani kwa Erica kisha walianza kuongea mambo mbalimbali yanayoendelea, ambapo Erica alianza kwa kumuuliza Erick,“Hivi mama na baba leo walienda kwa dada Angel kufanya nini?”“Mmmmh jamani, mimi nitajuaje hayo? Niliwaona tu wakienda ila sijui walienda kufanya nini”“Ila baba na mama wanapendana eeeh!!”“Ndio wanapendana, hivi Erica unajaribu kuniambia nini? Hebu tucheze karata tu”“Basi, twende tukacheze karata chumbani kwa dada Angel”Erick alikubali na moja kwa moja waliondoka nakuelekea chumbani kwa Angel, walikaa kitandani na kuanza kucheza zile karata. Walicheza sana hadi mwisho wa siku wakachoka na ilikuwa ni usiku sana yani kila mmoja alijikuta akilala palepale huku karata zipo pembeni yao, kwahiyo kwa siku hiyo walilala chumbani kwa Angel.Kulipokucha asubuhi na mapema, basi baba Angel alijiandaa na kuonoka zake kuelekea kwenye shughuli zake, mama Angel nae aliamka na kutoka ambapo alimkuta Vaileth tayari kashafanya usafi wa ndani na moja kwa moja alienda nje kisha akarudi ndani na kuanza kuongea nae,“Hivi Erick bado hajaamka eeeh!”“Bado mama”“Nilimwambia jana kuwa leo aamke mapema na aoshe gari yangu halafu kumbe kalala mpaka muda huuj”“Si unajua mama leo ni mapumziko, nadhani analipiza siku alizoenda shule”“Wakati jana waliwahi kulala, na Erica nae!”“Hajaamka pia”“Mitoto mijinga sana hii”Kisha mama Angel alienda zake moja kwa moja chumbani kwa Erick ila alishangaa kutokumuona wala nini, akashangaa kuwa kaenda wapi na kujiuliza kuwa pengine kaamka, basi moja kwa moja alienda chumbani kwa Erica ila napo hakuwakuta yani akawaza na kujiuliza sana,“Hawa watoto wameenda wapi jamani!!”Hakupata jibu na kuamua kurudi tena kwa Vaileth na kumuuliza kama kawaona,“Kwani hujawaona Erick na Erica?”“Sijawaona mama, kwani vyumbani mwao hawapo?”“Hawapo ujue, watoto wehu hawa jamani”Ilibidi mama yao atoke na kwenda kumuuliza mlinzi wa getini kama amewaona labda wakitoka.Erica ndio aliyeanza kushtuka na kumshtua Erick ambapo alimwambia,“Erick amka, Erick amka”Erick akaamka na kushangaa na kugundua kuwa walilala chumbani kwa Angel, kisha alimwambia,“Kheee kumbe tumelala chumbani kwa Angel? Hivi ni saa ngapi saa hizi?”Erica aliangalia saa ya ukutani kwa pale chumbani na kumwambia Erick,“Kheee ni saa tatu”Basi Erick alikurupuka pale kitandani na moja kwa moja alitoka kuelekea chumbani kwake ambapo Erica nae alitoka kuelekea chumbani kwake pia na kwenda kuoga moja kwa moja.Erick alitoka chumbani na kumkuta mama yake sebleni akionekana kuwa na mawazo sana, akamsalimia kisha mama yake akamfokea na kumuuliza,“Mjinga wewe, mbona nimekuja chumbani kwako sijakukuta?”“Mbona nilikuwa chooni mama”“haya, nenda kaoshe gari yangu mjinga wewe”Basi Erick alitoka na kwenda nje moja kwa moja kuosha gari ya mama yao ambayo aliambiwa kuwa aende kuiosha.Ericanae alimkuta mama yake sebleni ambapo alijibu kamaErick utafikiri waliambizana kujibu vile, basi mama yao alikuwa amechukia sana na kuwafokea,“Mmeniudhi sana leo, huko chooni ni choo gani hiko kinachofanya niite na msinisikie? Haya nenda kaoshe vyombo maana nilimwambia kuwa daa asioshe, leo ni zamu yako”Basi Erica alienda zake kuosha vyombo ambapo mama yao sasa ndio aliweza kwenda kujiandaa kwaajili ya kutoka yani ambavyo hakuwaona watoto wake alianza kujihisi vibaya katika moyo wake.Basi alipomaliza kujiandaa naye Erick alikuwa amemaliza kusafisha gari ambapo mama yake alipanda na kuondoka nalo kwani kuna mahali alikuwa anawahi kwa siku hiyo.Basi pale nyumbani walibaki Erick na Erica pamoja na Vaileth kwahiyo siku hiyo wakaitumia kama siku yao ya kuangalia video mbalimbali maana mama yao anayewakataza hakuwepo kwa siku hiyo.Basi mama Angel alifika kwenye shughuli zake na kushughulikia vizuri tu ambapo kwa kipindi hiko kulikuwa na mazao ambayo aliyafatilia, wakati anamaliza zile shughuli zake alishangaa mtu kumuita,“Erica”Basi alisimama na kumuangalia ila hakuwa na kumbukumbu kama amewahi kuonana na mtu huyu, basi alisalimiana nae na kuanza kuulizana nae,“Samahani sijui tulionana wapi?”“Mmmh najua huwezi kunikumbuka, siku zote mala ndizi hakumbuki ila mtupa maganda ndio huwa anakumbuka.”“Kwani nani wewe, samahani jamani?”“Kuna kipindi zamani kabisa ulikuwa na matatizo, mwanaume wako alioa na ukaja mtaani hadi ukazimia, ni mimi niliyekupeleka na tukawa tukikutana stendi ulipokuwa ukifanyia kazi”“Ooooh nimekukumbuka sasa”Mama Angel alimkumbuka mwanamke huyu kama aliwahi kuonana nae, basi yule mwanamke alianza kumueleza mambo ya kale ambayo kwa mama Angel yalibaki kama historia.“Basi yule mwanamke aliachwa, na Bahati akaoa mwanamke mwingine ila amezaa watoto wengi huyo balaa na wanawake tofauti tofauti”“Mmmmh!”“Ndio hivyo, yani Bahati ana watoto wengi tena wa kila rangi na asipokuwa makini basi watoto wake wanaoana”Mama Angel alizidi tu kumshangaa mwanamke huyu ambapo aliendelea kuongea,“Basi ana mtoto anaitwa Abdi, ni katoto kadogo ka kidato cha kwanza ila mtoto huyu ni hatari, yani mtoto mdogo ila anatembea na wanawake wakubwa kwa wadogo”Mama Angel akashtuka kidogo kwani jina la Abdi amewahi kulisikia kabla, kwahiyo alijikuta akiogopa kwakweli na muda huo huo aliagana na yule mwanamke ambapo alihitaji mawasiliano nae na alimpatia basi akaondoka zake ila alijikuta akitafakari sana kuhusu Abdi.Mama Angel alivyorudi nyumbani kwake ilikuwa tayari ni usiku kwahiyo alishindwa kuongea na watoto wake kwani aliwakuta tayari wamelala, ukizingatia walichoka sana na usiku wa jana walichelewa sana kulala.Muda kidogo mumewe nae alirudi na kwenda nae chumbani ambapo alimuuliza,“Mbona siku hizi Jumamosi unachelewa sana kurudi?”“Hata wewe umechelewa leo mke wangu, kumbuka nilikupigia simu ukasema bado hujarudi nyumbani, sasa niwahi kurudi halafu niwe na nani?”“Si unacheza hata na watoto”“Ooooh umeniambia jambo jema sana, Jumatatu asubuhi kuna sehemu tutaenda”“Sehemu gani tena?”“Nitakwabia tu hata usijali mke wangu”Kisha siku hiyo baba Angel alimtaka mkewe wajiandae tu na wakale nje na nyumbani kwao kwahiyo walifanya vile na kuondoka zao.Vaileth alibaki nyumbani kama kawaida ila kiukweli alitamani sana maisha aliyoyaona kwa baba Angel na mama Angel basi alikaa na kuanza kukumbuka maisha yake ya nyumba,“Hivi watu wengine tukoje jamani! Huwa tunakosa bahati kama hizi kwanini? Nakumbuka mimi mwanaume aliyenizalisha, yani siku niliyomwambia nina mimba yako basi ndio ukawa mwisho wa mawasiliano yetu, nimeishi kwa shida mwanzo mwisho, nikiomba kazi za ndani wananikatalia sababu ya kuwa na mtoto mdogo. Nikaamua kumuacha nyumbani ila bado nilikuwa sipati kazi za ndani, ila huyu mama Angel katokea kama bahati kwangu, ila kawezaje kupata familia yenye upendo kiasi hiki!! Hadi raha jamani, natamani na mimi ningekuwa na maisha haya. Ila nadhani mama Angel ni kati ya wanawake waliojitunza na mwisho wa siku wamekuja kufurahia maisha, ila na mimi mbona nilijitunza sana? Ila niliyempata ndio akaniharibia maisha mazima kabisa, sijui wengine tuna gundu jamani loh!!”Alikuwa akiongea huku akiumia sana moyoni mwake, kwakweli aliyapenda sana maisha ambayo mama Angel na mumewe waliishi na jindi ambavyo walipendana na kusikilizana.Mama Angel na baba Angel waliporudi tu ni moja kwa moja walienda kulala maana walishashiba tayari, basi asubuhi waliamka na kuamsha watoto wao kisha kujiandaa na kwenda nao Kanisani.Vaileth alitulia huku akiwasiliana na ndugu yake namna ya kufika mahali hapo sababu ndugu yake huyo alihitaji kuja kumtembelea, na jinsi alivyomuelekeza haikuwa ngumu sana kwani yule ndugu wa Vaileth alifika pale vizuri kabisa na alimkuta Vaileth getini akimsubiri.Basi Vaileth alimkaribisha vizuri kabisa, na yule ndugu alikuwa akishangaa tu uzuri wa ile nyumba,“Kheee jamani Nyanda ndio unaishi kwenye nyumba nzuri kiasi hiki!!”“Weee halafu nilisahau kukwambia, mwenzio mjini nimezoeleka kwa jina la Vaileth. Hilo jina lenye gundu nililiacha kijijini”“Kheee nitazoea hilo jina lako jipya kweli?”“Mbona rahisi tu, sema Vai”“Oooh sawa, ila bora mimi nilipewa jina zuri toka zamani”“Ndio jina lako ni zuri lakini umesahau bibi anavyokuitaga? Yani bibi haiwezi hiyo Prisca anaita Purisika”Basi wote walianza kucheka na kuongea mawili matatu huku akimuuliza alipofikia,“Si nimefikia kwa Shangazi, ndio nikasema nahitaji kumsalimia Nyanda ndio akanipa namba zako. Ulipataje bahati ya kupata kazi kwenye nyumba nzuri hivi ndugu yangu?”“Yani hii bahati acha tu, halafu nyumba hii usifikiri ni uzuri wan je tu, jamani hadi watu wa humu ni wazuri na wana roho nzuri sana, yani kazi za humu unadhani nafanya peke yangu basi!! Mama akiwepo tunasaidiana, watoto wa humu ndani wanaweza kazi zote, si wa kiume, si wa kike yani hakuna kazi inayowashinda, tofauti na nyumba zingine za matajiri ila hii ni mwisho”“Ooooh hongera sana, na mimi nahitaji kazi za ndani ila kwenye nyumba kama hii”“Si mpaka upate hiyo bahati!! Ni mimi tu nimejaaliwa, yani nyumba hii kwakweli imebarikiwa na Mungu, hapa unavyoona ni wote wameenda kusali, wanapenda ibada hao balaa”Basi Prisca nae alijikuta akiyapenda maisha yanayoendelea kwenye ile nyumba kwa kuhadithiwa tu na Vaileth.Siku hii Tumaini nae na familia yake, walienda Kanisani na kurudi kwa pamoja, ila kama ambavyo Angel aliomba kuwa abadilishiwe ratiba basi Tumaini alimwambia kuwa awapikie chakula siku hiyo maana Angel alionekana kuwa na hamu ya kupika. Angel aliwapikia chakula kile na kukiandaa mezani ila walifika wageni wawili ambao walikuwa ni rafiki wa mume wa Tumaini na kula kile chakula kwa hakika wote walikisifia kuwa ni kizuri sana, jambo lile lilimfanya Tumaini ampende Angel maradufu, basi wakati wameenda jikoni akamwambia Angel,“Angel mwanangu ukiendelea hivi kwa hakika utaolewa na mwanaume mzuri kama baba yako Erick”Angel alitabasamu tu, kisha shangazi yake akaendelea kumwambia,“Ila mwanangu unatakiwa kuwa mpole na mtulivu ili kumpata mume mwema”Angel akaitikia na kwenda kutoa vyombo ambavyo walikuwa wanatumia wale wageni, ila katika wale wageni kuna mmoja wapo alikuwa akimuangalia sana Angel yani alikuwa akimuangalia kila kitu alichokifanya.Na baada ya muda waliaga kuwa wanaondoka sababu muhusika hawakumkuta, basi waliwapa mikono ambapo yule mgeni aliposhika mkono wa Angel alimtekenya huku akitabasamu, ila Angel alibaki tu kumshangaa, kisha Tumaini aliwasindikiza wale wageniWalipotoka Kanisani, familia ya mama Angel waliamua kwenda kidogo ufukweni kupata upepo na badae kidogo walirudi nyumbani kwaajili ya maandalizi ya kesho yake, Vaileth aliwatambulisha kwa yule mgeni wake na wao walimkaribisha vizuri tu kwa upendo kisha wote kwenda kulala tu.Kulipokucha kama walivyopanga basi waliamka tu kwenye saa mbili asubuhi na kujiandaa kisha kuondoka pamoja, ila gari ya baba Angel ilielekea hospitali moja kwa moja na kumfanya mkewe aulize,“Mbona tunaenda hospitali sasa?’“Ndio tunaenda hospitali, hapa kuna dokta mzuri sana wa wanawake, nahitaji akakuangalie wewe kama una tatizo lolote maana nilishaongea nae, na leo hiko kijiti chako akitoe ili unibebee mimba”Basi mama Angel hakusema neno lingine lolote zaidi zaidi ya kukubali atakavyo mume wake.Basi waliingia pale hospitali na moja kwa moja walienda kwa dokta, kwakweli mama Angel alishtuka sana kumuona huyu dokta kwani ni mtu aliyekuwa akimfahamu vizuri tu.Basi mama Angel hakusema neno lingine lolote zaidi zaidi ya kukubali atakavyo mume wake.Basi waliingia pale hospitali na moja kwa moja walienda kwa dokta, kwakweli mama Angel alishtuka sana kumuona huyu dokta kwani ni mtu aliyekuwa akimfahamu vizuri tu.Basi yule dokta akampa mkono mama Angel ila mama Angel alisita kutoa mkono wake na kumtaka mumewe waondoke, mume wake alimshangaa pia,“Kwani kuna nini mke wangu jamani!!”“Siwezi kuongea chochote na huyu dokta maana atafanya nibebe mimba ya utosi”“Kwani kuna nini? Mnafahamiana?”“Ndio”Kisha mama Angel akatoka nje, ikabidi baba Angel amuombe msamaha daktari halafu akamfata mkewe nje, kwakweli mama Angel wala hakutaka kubaki tena kwenye ile hospitali hivyobasi ilibidi mumewe nae aondoke nae, waende mahali ili akamueleze ni kwanini hataki kutibiwa na yule dokta.Walivyofika tu, walikaa na muda huo huo baba angel akamuuliza mke wake,“Kwani tatizo ni nini?”“Nadhani wewe, umesahau ila nitakukumbusha. Yule dokta anaitwa dokta Doroth, katika maswahibu yangu ya kipindi kile cha ujana nilishawahi kuongopa kuwa tumbo linaniuma wakati ametokea Rahim, nakumbuka ulinikimbizia hospitali ila haikuwa hospitali ile nadhani kahamia pale. Basi nilimkuta yule dokta na kumuomba akuongopee na kusema ninavidonda vya tumbo ila alitaka hela nyingi sana kwa mimi kusema uongo, kwakweli aliniumiza mno, naweza sema kuwa yeye ndio chanzo hadi niliosha vyombo vya hoteli mimi”Mumewe nae alionekana kuanza kukumbuka,“Ooooh sasa nimekumbuka vizuri kabisa, pole mke wangu kwa kukukumbusha matukio ambayo yalipita”“Asante”“Basi nikupeleke kwa yule dokta rafiki yangu”“Naona umenichoka sasa baba Angel jamani, mimi naomba jambo moja tu. Kesho nitaenda mwenyewe hospitali na kutoa hiki kijiti, naomba wala usihangaike kutafuta madokta mume wangu tafadhari”Basi baba Angel alimuangalia tu bila ya kusema chochote kile.Basi leo Prisca alianza kuongea na Vaileth kuhusu ile nyumba ya mama Angel kwani kwa muda huo hakukuwa na mwingine kwenye ile nyumba zaidi yao tu,“Ndugu yangu Nyanda usiwe mjinga, hebu angalia mjengo huu jamani!! Inafaa kabisa wewe kuwa mmiliki wa mahali hapa”“Loh Prisca hebu niondolee dhambi hizo za lazima jamani! Yani unamaana nimpindue mama mwenye nyumba?”“Ndio mpindue ili wewe ubaki kuwa mama mwenye nyumba”“Jamani Prisca unaongelea vitu gani jamani, hebu achana na huo ujinga”“Wewe ndio mjinga Nyanda, unaacha kujipatia mali hizi!! Umeweza kubadili jina ila kwanini huwezi kufanya vitu vya msingi kama hivi!!”“Sikia nikwambie jambo Prisca, watu kama nyie ndio huwa mnafanya wenye nyumba waseme kuwa wadada wa kazi wana nia mbaya na nyumba zao kwa kuchukua waume zao. Sikia jambo, huwa mama mwenye nyumba namuheshimu sana na ninampenda, hata yeye ananiheshimu na kunipenda ndiomana ananiamini kuniacha na nyumba yake, kingine watoto wake wananiheshimu sana na kunipenda, ni kweli naonea wivu familia hii jinsi walivyo na upendo ila hiyo sio sababu ya mimi kumpindua mama mwenye nyumba. Nataka hizi mali, najua wamechumaje? Najua wameanzia wapi? Hata msingi wa nyumba najua ulivyowekwa? Sawa, tufanye mfano nilikuwepo au nilishiriki kwenye ujenzi, je hiyo inamaana kuwa nyumba ni yangu? Unajua mara nyingine utu ni bora kuliko mali, nawapenda hii familia ni kama familia yangu naamini na mimi ipo siku nitapata mume mwema atakayenijali na kunithamini”Prisca akacheka sana na kumwambia,“Huyo mume mwema utampata vipi na ushazalishwa? Hakuna mwanaume anayependa mwanamke mwenye mtoto, hakuna nikwambie, yani hayupo mwanaume anayeweza kulea damu isiyo yake, hapo ni kufanya ndumba tu ili umpate”“Kama ni hivyo basi jamii nzima itakuwa imejaa ushirikina maana kwasasa ni asilimia kubwa ya wanawake wamezalishwa na wanaume wamewakimbia. Ila mimi siamini kuhusu hilo, naamini mtu akipenda boga basi anapenda na ua lake, najua akinipenda basi atampenda na mwanangu”“Naona hilo jina la vaileth limekuharibu, unanikera mimi”“Pole sana ila huo ujinga sahau, siwezi kufanya kabisa, humu ndani nawaheshimu na kuwathamini najua nami Mungu atanisaidia nitapata mume mwema na kuanzisha nae familia ila kwasasa nipo mafunzoni. Nipo kujifunza maisha ila sio kuiba waume za watu”Basi Prisca alichukia sana, na Vaileth alienda kumalizia kazi zake ili aweze kumsindikiza.Erica alikaa darasani akiendelea na masomo yake, Abdi akasogea kumnong’oneza,“Ujumbe wangu uliuona”Erica alimwambia jambo moja tu,“Sitaki huo ujinga Abdi, naomba niache na kesho nakuletea karata zako”Maana alikumbuka jinsi kaka yake alivyochukia kuhusu ule ujumbe, basi Erica aliendelea na masomo kama kawaida, kuna muda alihisi haja ndogo basi akainuka na kwenda maliwatoni.Alipomaliza kujisaidia alishangaa wakati akitoka akakumbana na Abdi mlangoni ni kama alikuwa akimaliza ajisaidie, basi alimuuliza,“Unafanya nini kwenye vyoo vya kike?”Abdi hakujibu bali aliingia na Erica kwenye kile choo na kufunga mlango huku akimwambia,“Nakupenda sana Erica, niamini nakupenda sana”“Kheee wewe una wazimu au? Niache bhana, nitapiga kelele”“Piga tu hizo kelele, si hunitakii mema utakuwa, pengine hutaki kuniona hapa shuleni ila nakupenda sana”Halafu Abdi akamsogelea Erica mdomoni na kuanza kumbusu, muda huo Erica alikuwa akipambana na Abdi mule chooni ilia toke na mtindo wa vyoo vya shule ile hata ukipiga kelele chooni ni sawa na bure tu yani hakuna aliye nje ambaye atasikia zaidi ya mtu ambaye yupo kwenye korido ya choo, na kwa muda huo wanafunzi wote walikuwa darasani.Erica alianza kupiga kelele ili Abdi amuachie basi Abdi alicheka na kumwambia,“Kumbe hujui eeeh!! Humu chooni hakuna sauti inayotoka nje, yani sauti zote zinaishia humu humu ndani, cha kufanya nikubalie tu, onyesha ushirikiano ili wote twende darasani”“Sasa ushirikiano gani unaousemea Abdi jamani!”“Naomba nione kifua chako tu nitaridhika”Erica alikuwa akimshangaa sana Abdi ila bado hakuweza kufunua kifua chake, na kujaribu kuendelea kupiga kelele ingawa alijua hazifiki popote ila Abdi alikuwa na nguvu kidogo na kumshinda nguvu Erica kwani alifanikiwa kumfunua sketi yake ila gafla mlango wa kile choo uligongwa na pale Erica kuona kuwa usalama wake umefika, mlango uligongwa sana na Abdi akamziba mdomo Erica ila alishangaa kusikia sauti ya Elly,“Fungua mlango Erica, nimesikia sauti yako”Erica alipambana ili wafungue mlango ila Abdi alimshinda nguvu na kutokufungua mlango basi Elly akamwambia,“Naenda kuita mwalimu ilia je avunje huu mlango”Ila muda huo huo Elly alitumia nguvu zake za ziada na kusukuma ule mlango hadi kitasa kilijiachia na ulifungua, cha kwanza alimvuta Abdi na kumpiga ngumi ya pua ambayo ilipoteza mawasiliano kabisa kwenye pua ya Abdi na kumfanya Abdi aanze kutokwa na damu puani, ila hilo halikuwa tatizo kwa Elly kwani yeye cha muhimu kwake ilikuwa ni kumuokoa Erica tu.Kulikuwa na mwalimu anapita karibu na kile choo cha wasichana kwahiyo alisikia ule ugomvi na kuingia ila alikuta Abdi akitokwa na damu mfululizo basi ilibidi awachukue wote kwenda ofisini ambapo alimpigisha Elly magoti na Erica nae alitakiw akujieleza huku Abdi akipewa huduma ya kwanza.“Kwanza, wewe Elly choo cha wasichana ulikuwa unatafuta nini?”“Sikia mwalimu, mimi toka siku ya kwanza nilimumwambia Erica kuwa nitakuwa nikimlinda na kumtetea kwani mimi ni kaka yake na tulikubaliana hivyo, ila leo sikuelewa huyu Abdi alikuwa ananyemelea nini kwa Erica, basi kuna muda Erica alitoka darasani nikahisi lazima ameenda chooni, muda kidogo Abdi nae akatoka nikawa nahisi kitu, basi nilivyoona Erica anakawia kurudi nikaamua kwenda chooni kwao kuangalia imekuwaje ndio nikakuta Erica akipiga kelele, niliwasihi wafungue mlango ila Abdi aligomea usifunguliwe basi nikaamua kuuvunja, nisamehewe kwa hilo tu naye Abdi alipotoka nilimpiga ngumi moja ya pua”“Hivi una akili wewe? Umeshindwa kuja kushtaki? Kati yaw ewe na Abdi unadhani ni nani mwenye makosa? Kwanza umeingia choo cha kike, pili umevunja mlango, tatu umempiga mwenzio”“Ila mwalimu Abdi alitaka kumbaka Erica”“Una uhakika gani juu ya hilo? Hebu kuwa na huruma, unatakiwa uje na mzazi wako mjinga wewe”Kisha mwalimu alimchapa Elly kwa fimbo za kutosha tu, na kumwambia kuwa aondoke nyumbani hadi aje na mzazi wake, muda huo Erica alikuwa akitetemeka sana na kusema kuwa hawezi pia kuendelea kubaki shuleni kwani hana amani, mwalimu yule naye akamfokea sana,“Ujinga ujinga tu, huna amani kitu gani? Huyu Abdi angeota kuwa unaenda chooni? Na wewe ondoka zako na ukamuite mzazi wako, waje waseme ni malezi gani amekupa wewe mtoto wake”Mwalimu mwingine akadakia pembeni,“Uwiii mzazi wa Erica usimuite tafadhari kwa kesi za kijinga hivi, mama mtata yule, akifika hapa yani walimu wote tutaipata unajua Angel alimuahamisha kivungu pia”Ndipo pale yule mwalimu alipoelewa kuwa mzazi wa Erica ndio mzazi wa Angel basi akamwambia tu aende akapumzike nyumbani siku hiyo.Erica aliondoka na Ellyna kutaka aende nae kwao ili akaongee na mamake Elly ila Elly akamwambia,“Usijali Erica, kwanza mama yangu hayupo”“Jamani, roho inaniuma sana. Pole Elly jamani, yani umepata matatizo sababu yangu”“Usijali, labda nikusindikize tu kwenu”“Hamna usijali, mimi nachukua bajaji inipeleke nyumbani halafu ataenda kulipwa kule kule, usijali”Basi Elly alimsindikiza tu Erica hadi kwenye bajaji halafu yeye akaondoka zake kurudi nyumbani kwao.Erica alienda na bajaji hadi kwao, basi alivyofika alimuuliza tu dereva ni kiasi gani cha pesa kisha akaingia ndani na kwenda kumwambia Vaileth ambapo alimpatia hiyo pesa na akaenda kulipa ile bajaji na kuingia ndani. Muda huu vaileth ndio alimuuliza,“Kwani tatizo ni nini Erica?”“Dada, nitakusimulia ila bado natetemeka yani sina amani kabisa, leo yangesikika mengine”“Kivipi mdogo wangu?”“Naomba nikapumzike dada”Halafu alienda zake chumbani, basi Prisca akaanza tena kumuhoji Vaileth,“Kwahiyo hadi unaweka hela za akiba?”“Ndio”“Sasa huyu mtoto katoka wapi na bajaji hadi kalipa elfu saba?”“Katoka nayo shuleni kwao”“Kheee kwahiyo ni kawaida hiyo?”“Hapana ni dharula kama leo, huwa anarudi na gari la shule mbona”“Kwahiyo huyo bosi wako akija utamwambiaje?”“Huyu mama mwenye nyumba ni mwelewa sana, hujui tu unamuongelea mtu gani. Inuka nikusindikize sasa”Basi Prisca aliinuka ila hadi anatoka nje ya ile nyumba alikuwa akiishangaa tu jinsi ilivyokuwa, kwakweli ilimvutia mno kwa uzuri wake kwani ilikuwa ni nzuri na ya kuvutia.Yani muda wote wanatembea barabarani bado aliendelea kuisifia ile nyumba na kumtaka Vaileth afanye jambo kwajili ya kumdaka baba mwenye nyumba,“Yani Prisca naomba uachane na hizo habari”“Nitaachana nazo ndio ila hata shangazi nitamwambia kuhusu hili, yani sisi tunakufa na umasikini wakati wewe unauwezo wa kuchota utajiri tu hapa”“Ni bora niwe masikini maisha yote ila sio kuiba mume wa mtu, haswaaa mume wa mama Angel, kamwe sitafanya huo ujinga”Basi aliachana na ndugu yake akipanda daladala la kurudi kwao huku yeye akirudi anapofanyia kazi.Angel leo alitulia darasani kwani hakutaka tena makubwa yamkute kwa siku hiyo ukizingatia shangazi yake kashampa onyo hadi basi, alikaa darasani na kuendelea na masomo ya hapa na pale, hata Samir nae aliendelea na masomo yake ila muda wa kutoka kuna ujumbe Samir alimuandikia Angel na kumuwekea Angel kwenye daftari.Sababu walikuwa wakitoka basi Angel akaona kuwa ni vyema asome ule ujumbe akiwa nyumbani kwao, basi dereva alivyoenda kumchukua aliondoka nae tu na kurudi kwa shangazi yake.Kufika kwa shangazi yake, aliingia sebleni na kumkuta shangazi yake basi akamsalimia na kutaka kwenda chumbani ila shangazi yake alimuita,“Angel, naomba begi lako hilo”Ilibidi Angel avue begi lake na kumpa shangazi yake ambaye alifungua na kutoa lile daftari ambalo Samir alimuwekea ujumbe Angel, akalifunua lile daftari na kutoa ule ujumbe kisha akarudisha lile daftari na kumwambia Angel aende chumbani tu.Kwakweli Angel alienda chumbani huku akijiuliza mno inakuwaje shangazi yake kajua kuhusu hiyo barua? Au mtu aliyesema ameangaliana sana na Samir ndiye aliyemwambia kuhusu ile barua? Alijikuta akijiuliza bila jibu lolote, na je huyo mtu anayemfatilia ni nani? Hakuelewa kwakweli.Muda kidogo shangazi yake alienda chumbani na kuanza kuongea nae,“Angel mwanangu, wewe ni binti mzuri na unavutia sana unaweza sema wazazi wananifatilia sana hapana, tunataka kukutengenezea maisha bora binti yangu. Mwanaume anayekupenda kweli atasubiri umalize shule ndio aanze propaganda zake za kukupenda ila anayekusumbua wakati wa masomo ujue huyo hakupendi wala nini. Kuwa makini sana binti yangu, sipendi kuona ukiishia kati eti sababu ya mimba sijui sababu ya mapenzi, napenda usome kama sisi tulivyosoma. Angel upo vizuri mwanangu na tena umeanza kupendwa toka utotoni, yani wewe una akiba zako benki za kutosha tu ila bila akili ni sawa na bure mwanangu, vitu vyote hivi vinataka akili, jitahidi sana ujue jinsi ya kutunza maisha yako. Jitunze na maisha nayo yakutunze, usipokuwa na akili, huo uzuri wako ni sawa na bure, yani kila mtu atakuona kinyago. Tulia mwanangu, mapenzi yalikuwepo, yapo na yataendelea kuwepo, tuliza akili hizo na ukae mbali na Samir, jicho langu ni kali sana nilikwambia ukiwa tena karibu na Samir nitakufanyaje?”“Ulisema utanifanya unachojua wewe”“Eeeeh ndio, nitakufanya ninachojua mimi. Nataka uishi vizuri, uwe mtoto mzuri na uzuri wako wa asili usipotee. Haya endelea na ratiba ya leo”Shangazi yake aliondoka, kwahiyo Angel hata hakujua kuwa ile barua ilisema vitu gani sababu hakuisoma wala nini.Mama Angel alirudi mwenyewe kwani kuna mahali aliachana na mumewe, kwahiyo yeye moja kwa moja alienda zake nyumbani kwake, basi alimkuta Vaileth ambapo baada ya salamu Vaileth alimuelezea jinsi Erica alivyorudi siku hiyo, basi aliamua kumuita mwanaeili amueleze imekuwaje siku hiyo.Alivyofika, moja kwa moja Erica alienda kumkumbatia mama yake na alimsimulia kila kitu ambacho kilitokea shuleni siku hiyo, kwakweli mama Angel alisikitika sana na kukumbuka jinsi alivyokutana na yule mwanamke ambaye alimwelezea kuhusu mtoto wa Bahati aliyeitwa Abdi, moja kwa moja alitambua kuwa yule Abdi ndio huyo mtoto wa Bahati, alisikitika sana kusikia alitaka kumbaka mwanae, ila alimshukuru sana Elly kwa kumuokoa mwanae.Erick aliingia ndani na alisikia kila kitu wakati Erica akielezea, basi akasema“Nilijua tu, sikuwa na imani na yule Abdi toka siku ya kwanza jamani. Mama fanya kitu”Kisha alienda kumkumbatia Erica na kumsema,“Namshukuru Elly aliyekusaidia mdogo wangu”Ila Erick alikuwa na kisasi na Abdi hatari, hata mama yake alimuona jinsi alivyokuwa akichukia anavyomtaja huyo Abdi basi mama yao akasema,“Hivyo ndio inavyotakiwa, naona Erick umeumia sana mwanangu, pole baba”Basi Erick aliinuka na kwenda chumbani kwake.Leo baba Angel alichelewa kurudi hivyo alivyofika ilikuwa tu ni maongezi mengine hata mama Angel alisahau kumueleza habari za Abdi, ila tu baba Angel alikumbuka jambo moja tu na kumwambia,“Mke wangu naomba kesho usisahau kwenda kutoa hiko kijiti”“Sawa mume wangu, hata usijali”Na kulivyokucha, baba Angel aliondoka zake na mama Angel aliondoka pia ili kutimiza ahadi aliyomuahidi mumewe ya kwenda kutoa kijiti.Kwahiyo moja kwa moja alienda hospitali.Basi mama Angel anafika kwenye hospitali aliyoichagua yeye, na kuonana na daktari wake ambaye alimfanyia tiba vizuri tu, alimpenda huyu daktari sababu mara kwa mara alikuwa akihudumiwa naye kwa kipindi hiko, alimfurahia sana, daktari huyu alijulikana kwa jina moja haswaaa la dokta Maimuna, basi leo aliongea nae mawili matatu na kuagana.“Ila mama Angel mimi na wewe tumefahamiana muda ila hatujawahi kutembeleana, karibu kwangu siku moja jamani”“Nitakaribia dokta Maimuna hata usijali wala nini”“Au siku tupate mahali tuongee mawili matatu”Mama Angel akaitikia tu huku akitabasamu na kuendelea kuagana na yule dokta halafu akaondoka zake, ila wakati anataka kuelekea kwenye gari yake alikutana na mtu aliyemfahamu ambaye nae alikuwa akielekea hospitali, yule ndio aliyemshtua mama Angel,“Erica, Erica, wewe Erica”Mama Angel alisimama na kumuangalia, mtu huyu alishawahi kuwa kwenye mahusiano nae ya kimapenzi, alikuwa ni mwanaume wake wa kwanza kabisa, ila kwa kipindi hiko walikuwa wakiheshimiana.“Za siku nyingi Erica?”“Nzuri tu Babuu, wewe na mkeo hamjambo?”“Hatujambo kabisa, yani sisi ni wazima wa afya. Vipi wewe na familia yako?”“Nasi ni wazima wa afya, naona umekuja hospitali”“Ndio ila hapa kuna shemeji yangu”“Shemeji yako! Kivipi!”“Hapa kuna mke wa Rahim”Mama Angel alishangaa kwani Rahim alimfahamu fika ila mke wa Rahim hakujua kama yuko hapo hospitali, sema siku nyingi tu huwa hataki kukutana na mwanamke huyo, hivyobasi aliamuwa kumuaga Babuu kuwa anaondoka, basi Babuu akamwambia,“Kheee unamuogopa yule mwanamke? Yule alikuwa na wazimu ujue, hata hivyo Rahim ana mke mwingine”“Kheeee jamani!! Kumbe alioa tena?”“Aaah yule kaka yetu tunamjua wenyewe, unaishi wapi kwani siku hizi?”Hili swali hakulitaka hivyobasi alijifanya ana haraka na kuagana nae halafu akaondoka zake.Erica alivyofika shuleni, Elly nae alifika ila moja kwa moja alienda darasani na kumpa kifuko kidogo Erica na kumwambia,“Erica, hivyo ni visheti mama yangu alivitengeneza, nikaona bora nikuletee. Mimi itakuwa ndio mara ya mwisho leo kuja hapa shuleni”“Kwanini Elly? Umefukuzwa?”“Hapana ila mama yangu kwasasa yupo busy sana, hawezi kuja huku shuleni, usijali Erica nilitamani kuendelea kuwa karibu nawe ili nikulinde ila ndio hivyo haitawezekana. Kwaheri Erica”Kwakweli Erica alijihisi vibaya sana na kumfanya ashindwe hata kubaki darasani kwani nay eye alifatana tu na Elly kutoka nje ya shule kwani hakuona sababu ya kuendelea kuwepo mahali hapo ikiwa kuna mtu hawezi tena kuendelea na shule sababu yake.Basi walivyofika nje ya shule alimwambia,“Elly, nakuahidi kesho mama yangu atakuja nawe utarudi shuleni”“Kwahiyo, kesho nije shule?”“Ndio njoo, yani mama yangu ndio atakuja kusimamia swala hili. Najua sijaaga shuleni ni kesi pia ila mpaka pale watakapoonyesha kukuelewa wewe.”“Asante Erica kwa kunijali”“Asante na wewe”Basi wakaagana ambapo Erica alipanda tena bajaji na kurudi kwao.Leo Angel alikaa mbali kabisa na Samir, yani hataki hata ukaribu nae ila kitendo kile kilimfanya Samir aone kamavile Angel kamdharau maana kuna ujumbe alimwambia kwenye barua ila Angel hajautelekeza, kumbe Angel hata barua yenyewe hakuisoma, ila kitendo kile kilimkosesha raha kabisa Samir, muda kidogo aliingia madam Hawa na kumuita Samir ambapo aliondoka nae na kuelekea nae ofisini kwake halafu alianza kuongea nae,“Unajua nilitoka kufundisha darasa lingine, nikapita pale darasani kwenu na kuchungulia ila nikakuona umeshika tama na sura yako inaonyesha kuwa na mawazo sana, tatizo ni nini kijana wangu?”“Hapana sina tatizo madam”“Mimi najua saikolojia ya mwanafunzi ilivyo, najua kama una matatizo Samir, niambie. Mimi ni kama mlezi wako, kuwa huru niambie chochote kile”Samir akaona bora amueleze tu huyu mwalimu jinsi anavyompenda Angel kuwa labda mwalimu anaweza kumsaidia kisaikolojia,“Madam ipo hivi, sijui hata niseme imetokeaje ila shule niliyotoka nilipohamia tu nilikutana na mdada wa kuitwa Angel kwakweli madam nilijikuta nikimpenda sana na bado nampenda, halafu hapa shuleni nimemkuta pia yani nakosa raha nikimtazama sababu hataki kusema kuwa ananipenda pia. Naumia sana madam, sina raha jinsi ninavyompenda”“Ooooh kumbe ni mapenzi yanakusumbua, sasa Samir hebu hayo mawazo ya mapenzi yatoe kabisa kwenye akili yako. Halafu Jumamosi njoo nyumbani kwangu ili tuongee vizuri, sawa Samir”“Asante madam Hawa”“Yani rudi darasani na umuone Angel kama dada yako wala usihisi kuwa wampenda kimapenzi, jitahidi kwa hilo halafu kesho nitakuuliza pia kuwa imekuwaje ila kesho kuna jambo nitalifanya ila nataka ujiandae kisaikolojia. Samir wewe ni mvulana mzuri, unatakiwa utulie na usome ili ufike mbali, usianze kuchanganywa na habari za wanawake mapema kiasi hiko”“Nashukuru mwalimu, nimekuelewa”Kisha Samir alitoka mule ofisini na kuelekea darasani ila alipofika darasani alimuona Angel akiongea na Husna tena akionyesha kuwa hana wasiwasi na jambo lolote lile, kitu hiko kilimuumiza moyo zaidi.Erica anarudi nyumbani mapema na kumtaka tena Vaileth ampatie pesa ambayo anenda kuilipa bajaji, baada ya kulipa Vaileth anaamua kumuhoji,“Erica, na leo imekuwaje tena?”Erica anaelezea ilivyokuwa, basi Vaileth anamuuliza tena,“Inamaana Elly akiacha shule na wewe utaacha?”“Dada sio hivyo, hebu fikiria jana nimemueleza mama jambo hili nilijua atachukua hatua ya kwenda na mimi shuleni ili akamtetee Elly, cha kushangaza mama hajaenda shule wala nini sasa Elly atatetewa na nani? Wakati kaondolewa shule sababu yangu!”“Hilo nalo neno”“Sasa leo nangoja wote warudi hapa baba na mama ndio nianze kuongea nao”“Mmmh nakuona Erica, unatumia nafasi yako kudeka vizuri”“Ndio lazima nideke maana mimi ndio mtoto wa mwisho”“Kheee kwa uzee gani aliokuwa nao mama yako!! Akiamua kuzaa mtoto mwingine je? Halafi kwani wa mwisho peke yako, na Erick je?”“Erick ni Kulwa na mimi ni Doto kwahiyo mimi ni wa mwisho, na kuhusu mama kuzaa watoto wengine basi angekuwa kawazaa siku nyingi sana ila hadi leo hakuna basi mimi ndio wa mwisho. Mamangu kwao yeye ndio wa mwisho na anaitwa Erica yanbi jina langu ndiomana na mimi kaniita Erica, na baba nae kwao ndio wa mwisho na anaitwa Erick ndiomana kaka anaitwa Erick. Kwahiyo mimi ndio wa mwisho tu, na mama hupenda kuniita mziwanda”“Haya bhana, kitoto cha mwisho, furahia maisha mwaya”Erica alitabasamu kwani hii hali ya kuwa mtoto wa mwisho ilikuwa inamfurahisha sana kwani alikuwa akisikilizwa sana na wazazi wake.Leo mama Angel moja kwa moja alipitia ofisini kwa mume wake kwani alitaka kumpa habari ya kutoa vile kijiti, ila alipofika kuna mtu alitoka kwenye ofisi ya mume wake nakupishana malngoni ambapo walisalimiana tu ila hakutaka kumjali mtu huyo wala nini.Aliingia ofisini kwa mumewe, kwakweli hata baba Angel alifurahi sana kumuona yani akawa na furaha na kusema,“Kwa jinsi nilivyofurahi naomba nifunge ofisi twende nyumbani mke wangu”Basi mama Angel alikubali na kumfanya wafunge ofisi na kuondoka kwa pamoja kuelekea nyumbani.Walivyofika tu nyumbani walishangaa kumkuta Erica akiwa sebleni na sare zake na begi lake yani hata kwenda kuvua nguo hakwenda, basi aliwasalimia ilibidi wakae ili wamsikilize kuwa kwanini muda huo yupo nyumbani na sio shuleni, basi Erica akawaambia,“Kabla ya yote naomba muonje hivi visheti ambavyo mama yake Elly kaviandaa”Basi Erica akatoa na kuwapa wazazi wake, ambapo baba Angel hata bila kuuliza alimega kisheti na kuanza kukila, ila alishtuka sana na kufanya wote wamuangalie.Basi Erica akatoa na kuwapa wazazi wake, ambapo baba Angel hata bila kuuliza alimega kisheti na kuanza kukila, ila alishtuka sana na kufanya wote wamuangalie.Mama Angel alimuuliza mumewe kuwa imekuwaje,“Mpenzi, nini tatizo tena?”Baba Angel hakusema kitu ila alinyanyuka, na kufanya mama Angel amfate nyuma, kuelekea nae chumbani, ila walivyofika chumbani baba Angel alimwambia mama Angel,“Naomba nipumzike kidogo”Basi mama Angel ilibidi amuache apumzike kidogo kitandani, kisha akarudi sebleni kuongea na Erica, alimuuliza swali,“Kwani visheti hivi kakupa nani?”“Kanipa Elly, mama yake ndio amevipika”“Nahitaji kumuona mamake Elly”“Kheee mama unafikiri utamuonea wapi? Huyo mama hata mimi sijawahi kumuona, leo tu kagoma kuja shule kwaajili ya mwanao, yani yupo tayari afukuzwe shule kuliko yeye aje kumtetea, eti yupo busy sana”“Kwani Elly kafanya nini?”Ikabidi Erica amsimulie tena mama yake, yani mama yake ndio kama akakumbuka na kuuliza vizuri,“Yani walimu wenu wana wazimu kweli, ngoja niwapigie simu”Basi mama Angel alichukua simu yake na kupiga ambapo mwalimu Harun ndiye aliyepokea halafu alianza kuongea nae,“Yani nyie, mtoto wangu atake kubakwa, halafu mtu aliyemsaidia mwanangu asibakwe ndio mnamfukuza shule, hivi nyie walimu mpoje? Mmeshindwa kumdhibiti huyo bakabaka!”“Samahani mama, kwani imekuwaje?”“Ngoja, Erica akueleze labda utaelewa”Kisha mama Erica akampa Erica simu ambapo alianza kumueleza mwalimu jinsi ilivyokuwa, ndio mwalimu kidogo kuelewa na moja kwa moja alimuita mwalimu mwenye kesi hiyo aweze kuongea na mama Angel,“Mama Angel jamani usipaniki kiasi hiko”“Nisipaniki ndio nini? Yani mtoto aliyemuokoa mwanangu mmemfukuza shule halafu bakabaka mmemuacha”“Hapana mama hatujafanya hivyo, ila tumemwambia Elly aite mzazi wake sababu kavunja kitasa cha mlango wa chooni”“Na asingevunja hiko kitasa si ndio mwanangu angebakwa? Hivi hamjafikiria hilo? Kwanini huyo mzazi wa Abdi asiitwe mpaka mzazi wa Elly? Jamani hebu achene bangi walimu, muacheni Elly arudi kuendelea na masomo yake”“Sawa mama Angel hakuna tatizo, samahani kwa hilo. Kesho Erica aje shuleni tu kama kawaida”“Na Elly je?”“Naye aje shuleni tu”Basi mama Angel alikata ile simu kisha aliinuka zake na kurudi chumbani ila leo kwa mara ya kwanza alimuona mumewe akikoroma sana, kwakweli mama Angel aliogopa kiasi kwani haikuwa kawaida kwa mumewe kukoroma hata achoke vipi, basi akachukua simu yake tena na kumpigia mama yake, ambapo alimueleza toka walivyorudi na mumewe kula vile visheti,“Na wewe mama Angel jamani, kila siku nasema ni vizuri kuombea chakula kabla ya kukila. Sio mara zote chakula kinakuwa na sumu, ila vyakula vingine vina manuizo mabaya, huwezi jua kuhusu hilo. Haya usichelewe, sasa hivi ingia kwenye maombi maana hiyo hali sio ya kawaida, ingia kwenye maombi sasa hivi”Mama Angel alipata hofu kidogo ila akajitia ujasiri na kuchukua biblia ambapo alisoma na kisha kuanza maombi ya kumuombea mumewe.Baada yay ale maombi baba Angel aliamka na kuanza kujinyoosha nyoosha, basi mkewe alifurahi sana kisha alikaa karibu na muemewe na kumsikiliza kuwa anajisikiaje,“Vipi hali yako lakini mume wangu?”“Yani sijui vipi, huwezi amini hapa nililala halafu nilikuwa nikiota ndoto za zamani kabisa, eti nilikuwa nikiota mambo ya zamani kuwa yalikuwaje jamani, yani jinsi nilivyokuwa zamani ndio nilichokiota”“Pole sana mume wangu, nikakuandalie chakula gani?”“Labda chapati tu”Basi mama Angel alitoka na kwenda kumuandalia mumewe chapati.Angel aliporudi kwa shangazi yake leo, alimkuta yupo na kumsalimia ambapo shangazi nae alimuuliza habari za shule,“Ni nzuri tu shangazi”“Vipi leo hujaongea na Samir?”“Sijaongea nae shangazi”“Vizuri sana, zingatia masomo yako yani masomo ndio yawe kila kitu kwako”Basi Angel alienda chumbani ila kwa upande mwingine wa moyo alikuwa akiumia sana kuishi maisha ya bila kuongea na Samir ingawa wanaonana.Usiku wa siku hiyo wakati amelala, akaota kuwa Samir ana mahusiano ya kimapenzi na madam Hawa, akawaona wameongozana pamoja huku wakikumbatiana, kwakweli Angel alishtuka sana toka kwenye ule usingizi, alikaa kitandani huku akijiuliza,“Inamaana Samir kweli anaweza kuwa na mahusiano na yule mama mtu mzima inawezekana kweli? Hapana jamani, halafu yule mwalimu si ana mume wake yule, hawezi nadhani ni ndoto tu hii”Basi aliendelea kulala ila hii ndoto ilikuwa ikifanya kazi katika akili yake.Kulipokucha alijiandaa na kwenda shuleni, basi akiwa amefika shule alimuona Samir akiwa kaongozana na madam Hawa, aliumia moyo na kuamua kwenda kukaa kisha akamuuliza Husna,“Hivi mume wa madam Hawa yuko wapi?”“Ooooh yule madam hana mume ujue ndiomana mkali vile, sijui wanaume walimfanya nini, kwa kifupi yule madam anawachukia zaidi wanaume.”“Oooh, hapo nimekuelewa”Muda kidogo Samir aliingia darasani, halafu baada ya muda kidogo madam Hawa alienda kumuita Samir na kuelekea nae ofisini, kwakweli ile kitu ilikuwa ikimuuma sana Angel ila alijifanya kuwa hajali kitu chochote wala nini.Mama Angel alibaki nyumbani siku ya leo ila alijikuta akitafakari sana kuhusu mama Elly, yani aliona kuwa ni kitu cha ajabu sana kisha alimuuliza Vaileth,“Eti Vaileth, hivi jana umeona ni kitu cha kawaida kwa baba kula vile visheti na kushtuka halafu kwenda kulala?”“Mmmmh sio kawaida mama, hata mimi nilishangaa tu. Ila mbona vile visheti nilikula mimi na Erica na hatukuona tatizo lolote”“Yani mimi niliogopa hata kuvionja jamani, tatizo lilikuwa nini sijui”“Sijui kwakweli ila ni vyema ukamfahamu mama wa Elly kwani itasaidia sana na umshirikishe jambo hilo”“Eti eeeh! Basi ngoja nitafanya hivyo tena leo leo”“Ni vizuri uende muda ule ambao wanatoka shuleni kisha umwambie huyo Elly akupeleke kwao”“Oooh umesema jambo la maana sana Vaileth, ndiomana nakupenda jamani. Itabidi tu leo niende mwenyewe shuleni kwakina Erica”“Sawa mama, fanya hivyo”Basi mama Angel alijiandaa na kumuaga Vaileth,“Kuna mahali nitapitia halafu ndio nitaenda huko shuleni kwakina Erica”“Sawa mama, badae”Basi mama Angel akaondoka zake kuelekea kwenye shughuli zake.Muda kidogo simu ya Vaileth iliita, kuangalia mpigaji ni shangazi yake, basi akapokea na kuanza kuongea nae,“Shikamoo shangazi”“Shikamoo mwenyewe kama ni mali, shikamoo tena na tena. Yani wewe ni mjinga sana kumbe unaishi kwenye jumba la kifahari halafu ndugu zako tunapata shida jamani!! Unashindwaje kuwaonea huruma ndugu zako?”“Jamani shangazi”“Sio jamani, unatakiwa ufanye kitu na umiliki nyumba hiyo, Jumamosi ninakuhitaji huku kwangu, uje ili tuzungumze”“Mmmh kuhusu hayo shangazi au kuna mengine?”“Kama kuna mengine si utayajua huku huku, ila nahitaji kukuona Jumamosi’“Sawa shangazi nitakuja”Basi Vaileth alikata ile simu na kuanza kuwaza sana kuhusu ndugu zake,“Kwani ndugu zangu wana nini jamani, yani mimi nikawe na mahusiano na baba Angel kweli? Nimsaliti mama Angel jamani! Kwa jinsi wanavyopendana halafu mimi nikavuruge upendo wao? Hapana kwakweli, nipo tayari kufa na umasikini wangu ila sio kuharibu furaha ya watu”Kisha akaamua kuendelea na kufanya kwake usafi.Mama Angel alifika sehemu ambayo alikuwa amepitia kwanza ili aweze kwenda huko shuleni alikopanga, ila mama yake alimpigia simu hivyobasi aliamua kwenda kwanza kwa mama yake na sio kwenda shuleni kwakina Erica tena.Moja kwa moja alienda kwa mama yake, ambapo alimkuta na kumsalimia pale,“Oooh mama nimeitikia wito”“Mwanangu, yani leo nimekukumbuka sana, nimekaa hapa nimekuwaza hatari na hivi jana uliponipigia simu ndio kabisa”Mama Angel alifurahi sana kusikia mama yake alimkumbuka, halafu mama yake alianza kumuuliza kuhusu jana yake,“Eeeeh mwanangu jana uliomba eeeh!”“Ndio mama, niliomba ila ninahitaji kuonana na yule mama Elly”“Na itakuwa vizuri sana, ili umfahamu”“Ndio, nilitaka kwenda leo. Ila ndio nimeshakuja huku tena”“Oooh na hapa huondoki muda huu mwanangu, nina hamu yakula chakula chako, yani nahitaji leo unipikie n anile chakula chako. Nimekimiss sana mwanangu, nakumbuka kipindi ukiwa mdogo tukisumbuana tu akili hapa, leo nimekukumbuka sana jamani mwanangu”“Haya mama, unataka nikupikie nini tena?”“Nisongee ugali tu, ila nimekumbuka na samaki. Hivi yule mwanaume wako wa samaki aliishiaga wapi yule?”Mama Angel alicheka sana na kumwambia mama yake,“Kumbe hujui mama, yule alimuoa rafiki yangu Fetty”“Kheee Fetty aliyaweza yale maradhi kweli? Nakumbuka kipindi kile akilala nje ya geti pale. Hahaha alikuwa na wazimu sana yule jamani”“Ila mama nawe, loh ulimfunga kijana wa watu”“Ndio nilimfunga, ila ni ujinga wake ndio ulisababisha yale, yule hakuwa na upendo ila ni uchizi ule. Ila si mimi niliyemfunga jamani, alikuwa ni marehemu James, kumbe na yeye anakunyemelea loh!”“Ila maisha mama jamani, yapitage tu tuingie kwenye kipindi kingine. Yani kipindi kile, nilikuwa kama chizi, sikuwa na raha hata kidogo jamani. Basi ngoja nikakuandalie upendacho mama”Kisha mama Angel alienda kumuandalia mama yake chakula akitakacho.Erica leo aliingia darasani akiwa na Elly kwahiyo kwa kiasi walifurahi, na Abdi nae alikuwa darasani ila hawakuongea nae chochote kile na walitulia tu kuendelea na masomo, kisha Abdi aliitwa na mwalimu ambapo aliambiwa akamuite mzazi wake, kutokana na mlango wa choo ambao ulivunjwa na Elly basi Abdi aliondoka moja kwa moja na kwenda kwao kwaajili ya kumuita mzazi wake.Basi muda wa mapumziko, Elly alianza kuongea na Erica ambapo kitu cha kwanza alimuuliza,“Vipi vile visheti mlikula?”“Ndio, ila kwani mama yako aliweka nini kwenye vile visheti?”“Kwanini?”“Baba yangu alivyokula alishtuka halafu alienda kulala, yani mama alikuwa na mashaka sana”“Jamani mbona mama yangu hajaweka kitu chochote, na alinipa kwa upendo tu, akasema kampe rafiki yako Erica awapelekee kwao nao waonje mapishi yangu, hajaweka kitu mama”“Aaaah ila kuja shule ndio kagoma?”“Yani mama yangu yupo busy sana, si nilikwambia kuwa baba alimkimbia mama wakati nipo mdogo kabisa kwahiyo mama ndio wa kuhudumia familia nzima, kwahiyo mama ndio wa kutafuta kila kitu”“Kwani kwenu mpo wangapi?”“Nimezaliwa peke yangu, ila kuna watoto wa mama mkubwa tunaishi nao, ni yatima kwahiyo wanahudumiwa kila kitu na mama, yani mama yangu hana muda kwakweli, ndiomana kaniambia nisifanye kitu kibaya kwani yeye hana muda wa kuja shule na nikifanya mabaya basi nitakaa nyumbani kumsaidia kusambaza visheti”“Kheee kumbe!! Sasa na wewe ada unalipiwa na nani huku?”“Yani mama yangu yupo radhi alale njaa kuliko mimi nisome shule mbaya, anataka nisome shule nzuri yani hadi majirani wanamshangaa kwakweli, kupanda basi la shule nilikataa mwenyewe ila ningekubali basi mama angetafuta hela kivyovyote viel nipande basi la shule, ila nilimuhurumia”“Kwakweli mama yako anakupenda sana Elly”“Ndio ananipenda sana, ndiomana na mimi nampenda”Basi waliongea ongea pale na kisha kurudi darasani.Abdi alirudi kwao ili kumuita mzazi wake kama alivyokuwa ametumwa na mwalimu, ila Abdi alikuwa akiishi na mama yake wa kambo, sababu baba yake hakuishi na mama yake mzazi, basi alifika na kumsalimia mama yake huyu kisha mama yake alimuuliza,“Vipi tena mbona mapema?”“Wanakuita shuleni mama”“Oooh huo ujinga sifanyi jamani, ulipokuwa shule ya msingi kila leo naenda mimi kwenye makosa yako ya shuleni, sasa leo ataenda baba yako, kwakweli mimi siwezi hiyo biashara jamani. Mbona mwenzio Bahati hayupo hivyo?? Kila siku wewe tu, likitoka hili linaingia lile, kwakweli siwezi jamani siwezi kabisa”“Jamani mama”“Msubiri baba yako hapo arudi ndio uende nae huko shuleni, tena mng’ang’anie uende nae leoleo maana kesho haitawezekana, babako anasafiri”“Sawa mama”Basi Abdi akatulia kwao ambapo alimsubiria baba yake ili aje na waondoke pamoja kwenda shuleni.Baba yake alivyorudi basi alimuelezea kuwa anaitwa na mwalimu, baba yake alianza kufoka,“Mambo gani tena hayo jamani!! Yani walimu hawa huwa wananikera mno jamani, sasa wananiitia nini?”Mkewe akadakia na kumwambia,“Usilalamikie tu walimu, uliza kwanza mwanao kafanya nini hadi uitwe”“Kweli, haya Abdi umefanya nini mwanangu?”“Twende tu ukashuhudie mwenyewe baba, kosa sio langu ila walimu wanataka kunisingizia tu. Twende baba”Mama yake akadakia,“Wakusingizie kwa lipi? Kwani walimu hawana akili hadi wakusingizie? Nendeni huko shule jamani”Basi baba yake alijiandaa na kuondoka na mwanae kuelekea shuleni, huku baba yake akimuuliza Abdi kama amefanya kitu gani hadi aitwe shuleni ila Abdi hakumwambia baba yake wala nini kwani angemwambia swala la yeye kuvunja kitasa cha mlango wa chooni basi baba yake angegoma kwenda kabisa.Ila walipofika njiani, baba yake alisimamisha gari na kushuka maana kuna mtoto alimuona njiani na kumfanya mwanae amuulize,“Baba vipi?”“Aaaah hapana, huyu mtoto kafanana sana na mama yangu”Kisha alimfata yule mtoto aliyekuwa wa kike na rika kama la Abdi, alimuuliza maswali na kumuomba ampeleke kwa mama yake kwahiyo safari ya kwenda shuleni kwakina Abdi ilihairishwa na muda huo huo walielekea nyumbani kwa yule mtoto aliyejitambulisha kwa jina la Rukia.Walipofika kwa mama Rukia, ndipo baba Abdi alipogundua kuwa huyo Rukia pia ni mtoto wake, basi muda huo huo aliomba kuondoka na mwanae kuliko mwanae kuhangaika mitaani kama alivyomkuta,“Naomba tu nikakae nae mwenyewe”“Oooh afadhali, maana hata mimi nimechoka kulea mtoto peke yangu”Basi Rukia aliandaliwa na moja kwa moja baba Abdi alipanda nae kwenye gari na kumrudisha nyumbani kwa mke wake, ambapo mkewe alichukia sana na kuanza kulalamika pale pale,“Mtoto mwingine tena!! Kwakweli nimechoka jamani, yani wewe baba ipo siku isiyo na jina mimi nitaondoka mahali hapa, siwezi hii kitu kwakweli”Hakuwa na la kufanya kwakweli basi aliongea na Abdi kuwa kesho yake hatosafiri tena, kwani atampeleka Rukia kwa mama yake na badae ndio ataenda nae shuleni kama alivyoitwa na walimu.Mpaka muda wa kutoka hakuonekana Abdi wala mzazi wake, kwahiyo walimu walijua kuwa ataenda kesho yake, basi wakina Erica nao walitoka na kama kawaida waliondoka na kila mmoja kuelekea nyumbani kwao.Erica alivyofika Vaileth alimuuliza kama mama yake hakufika shuleni kwao,“Hakuja, labda kuna mahali ameenda”“Anataka kuja kumuona mamake Elly”“Sidhani kama ni rahisi, mama nimemwambia kuwa yule mama haonekani kirahisi ila mama mbishi, haya aje kumuona tu”Kisha Erica akaenda zake chumbani kwake, ila alishangaa sana kukuta Erick yupo chumbani kwake eti kajilaza, alimshtua na kumuuliza,“Kheee Erick, umerudi muda gani na mbona upo huku chumbani kwangu?”“Nimerudi muda sio mrefu, ila leo nilikukumbuka sana, yani nilijikuta natamani sana kukuona jamani. Sasa nimekuona moyo wangu umeridhika”Basi Erica alitabasamu na kufurahi sana, kisha alimsogelea kaka yake na kumkumbatia ambapo naye Erick alijihisi vyema na muda huo akaondoka kuelekea chumbani kwake.Mama Angel alivyorudi jioni ya siku hiyo alimuita Angel na kumwambia kuwa kesho yake ataenda shuleni kwao.“Nahitaji kuonana na mamake Elly”“Ila mama ni ngumu nimekwambia”“Ni ngumu ndio ila nahitaji sana kuonana nae, kwahiyo kesho nitakuja shuleni kwenu kukuchukua wewe na huyo Elly kwahiyo mimi ndio nitamrudisha nyumbani kwao”“Mmmh labda itawezekana ukamuona”“Sio labda, nitamuona tu. Nahitaji sana kumfahamu”Kisha akaachana na mwanae na kuondoka zake kwenda kuongea na Vaileth ambapo Vaileth alimwambia kuhusu dhumuni lake la Jumamosi kwenda kumtembelea shangazi yake,“Halafu mama, nilikuwa naomba Jumamosi unipe ruhusa ili niende kumtembelea shangazi”“Hakuna tatizo, ila tu uwahi kurudi”“Asante sana mama”Basi mama Angel aliamua kwenda kuendelea na majukumu yake ya siku hiyo.Angel alirudi kwao ila alikuwa na mawazo sana, sema akakumbuka maneno ya shangazi yake kuwa ajiweke makini na masomo ili aweze kuyakwepa yale mawazo aliyokuwa nayo.Siku hiyo hadi wakati analala usiku ni kama alikuwa akihisi kuwa madam Hawa ana mahusiano na Samir,ila alijiuliza sana,“Sasa kama kweli, kwanini naumia?”Aliwaza na kukosa jibu, basi aliamua kujilazimisha tu kulala.Kulipokucha alienda shuleni kama kawaida, ila na siku hiyo pia alimuona madam Hawa akifika na Samir halafu muda kidogo baada ya Samir kuingia darasani yule madam alifika na kumuita Samir, basi alimuangalia na watu darasani walionekana kuguna kwa siku hiyo.Basi Husna akaanza kumwambia Angel,“Unajua kwasasa kila mtu kaanza kupatwa na mashaka yani sio ukaribu huu wa mwalimu na mwanafunzi, huyu madam Hawa anatushangaza kwakweli”“Kumbe na nyie mmemuona eeeh!”“Ndio, kwanini kila siku asubuhi afike nae? Na kwanini baada ya kufika tu aje kumuita? Huwa anaenda kuongea nae nini ofisini?”“Ila huyu madam mbona ni mtu mzima?”“Ni mtu mzima ndio, ila kumbuka kuwa hana mume halafu huyu ni madam anayeogopewa shule nzima hii, ni kwanini aweze kuwa karibu hivyo na Samir? Hivi hujajiuliza swali hilo Angel?”“Nimejiuliza ila nikakosa jibu”“Basi jibu ni kuwa anatoka nae”Wakaongea ongea pale ila Husna hakujua tu ni kwa jinsi gani jambo lile lilimuuumiza Angel.Ilikuwa ni karibu na muda wa kutoka, walimu wakiwa ofisini waliona kwa mbali Abdi akishuka na baba yake kwenye gari kuelekea ofisini, basi walianza wenyewe kuongea,“Uwiii jamani huyu Abdi kaamua kuja na baba yake mweeeh!”“Ila hukumwambia kuwa aje na mama yake?”“Nilimwambia, hata sijui kwanini anakuja na baba yake jamani!”“Yule mama ni muelewa ila huyu baba ni mtata balaa, yani sijui itakuwaje mweeeh!”“Hivi na siku ile aliyotoka na damu puani ilikuwaje?”“Tulimwambia asiseme, alivyopona basi, tulimpa huduma ya kwanza ila tulimwambia kuwa asiseme, yani ugomvi huu una wazazi wasumbusu jamani hadi kero”Baba Abdi aliingia ofisini, huku Abdi akikaa nje ya ofisi kusubiria baba yake aongee na walimu.“Eeeeh nimeitikia wito, niambieni tatizo”“Samahani mzee, ni hivi huyu Abdi kuna kitu kafanya shuleni hapa. Tulisikia sauti chooni, kwenda ndio tukamkuta Abdi, pamoja na binti mmoja na mvulana mwingine, Abdi alitaka kumbaka yule binti, sasa….”Baba Abdi akawakatisha kwanza na kuwauliza tena,“Mnasema Abdi alitaka kubaka? Jamani mnataka kuchekesha wasionuna, sasa Abdi abake kitu gani wakati hata kubalehe hajabalehe jamani, hivi walimu mna akili nyie kweli eeeh! Sasa Abdi abake vipi?”“Tusikilize mzee kwanza, halafu mlango wa chooni umevunjwa, kwahiyo inabidi ulipe gharama za kutengeneza kitasa”“Kwahiyo Abdi ndio kavunja huo mlango katika harakati za kubaka?”“Hapana, ila mlango alivunja kijana aliyeenda kumuokoa yule binti”“Hivi mnajua siwaelewi kabisa, yani siwaelewi. Mlango avunje nani na alipe nani? Hebu niitieni kwanza huyo aliyetaka kubakwa na huyo muokoaji”Ikabidi mwalimu akamuite Ellyn a Erica kwani ulikuwa ndio muda wa kutoka, kwahiyo moja kwa moja walienda ofisini na kumkuta baba Abdi, ambapo walitambulishwa na walimu pale, kisha mwalimu akamwambia baba Abdi,“Binti huyo hapo ambaye mwanao alitaka kumbaka, anaitwa Erica”Baba Abdi akashangaa sana na kusema tena,“Erica!!!”“Ndio, anaitwa Erica, halafu huyu mvulana anaitwa Elly ndio ambaye alienda kumsaidia Erica”“Hebu muiteni Abdi kwanza”Walimu walimuita Abdi ambaye alikuwa nje ya ile ofisi ambaye aliingia na baba yake alimuuliza,“Eti mwanangu, ulitaka kumbaka Erica?”“Hapana baba, sijataka kumbaka”Kisha baba Abdi akamuangalia Erica na kumuuliza,“Eti ni kweli Abdi alitaka kukubaka wewe?”“Ndio”“Ulijuaje kama anataka kukubaka? Ulishawahi kubakwa?”Yani walimu walichukia sana, walitamani hata kumwambia huyu mzee amuhamishe mtoto wao ili waepuke ule usumbufu wake, wakati kabla Erica hajajibu alifika mwalimu wa taalumu na kusema kuwa mzazi wa Erica yupo nje anamsubiri mtoto wake, basi mwalimu mmoja akasema,“Eeeeh vizuri sana, mwambie aje”Basi yule mzazi wa Erica akaitwa, alipoingia tu ofisini, macho yake yaligongana na macho ya baba Abdi kwani ni watu waliofahamiana.Basi yule mzazi wa Erica akaitwa, alipoingia tu ofisini, macho yake yaligongana na macho ya baba Abdi kwani ni watu waliofahamiana.Kimya cha muda mfupi kikatawala mahali pale, kisha mwalimu akavunja ule ukimya kwa kusema,“Tena sfadhari mzazi wa Erica umefika, maana hapa kuna ubishano kidogo juu ya mtu anayepaswa kutengeneza mlango wa choo”Basi baba Abdi akasema,“Ubishano upi tena mwalimu?”“Si umekataa kuwa mwanao hahusiki? Na anayetakiwa kulipa ni Elly ambaye alimsaidia Erica? Bora amefika mzazi wa Erica maana ndio alitupigia simu na kutusema sana, na tukaona sio vizuri kweli sababu chanzo cha tatizo anajulikana”Baba Abdi akasema tena,“Kwani Abdi kavunja nini na nini?”“Abdi hajavunja ila inasemekana kuwa alitaka kumbaka Erica, ndio huyu Elly akaenda kumsaidia kwahiyo ilibidi avunje mlango wa choo yani mwanao ilibidi ashtakiwe ujue”“Jamani walimu ndio mnataka kukuza mambo kiasi hiki, haya mambo si ya kuyamaliza tu. Hebu niandikieni hapo gharama za huo mlango na nitazilipa ili mtengeneze”Walimu wote walishangaa maana huyu baba alivyokuwa mpole muda huu utafikiri sio huyu ambaye alikuwa akiwabishia humo ofisini na kukataa kabisa kulipa ila muda huu anataka kupewa gharama na kuahidi kuwa atalipa za utengenezaji, walimu walidhani ni masikhara, basi wakasema pale,“Ule mlangi inatakiwa laki mbili ndio utengenezwe”“Aaaah kumbe!! Sasa si mngesema toka mwanzo tu jamani”Kisha baba Abdi akatoa wallet yake na kutoa laki mbili taslimu pale na kumkabidhi mwalimu yani wote walikuwa wakishangaa tu ila walishangaa zaidi kwa mama Erica maana hakuongea jambo lolote zaidi ya kumvuta Erica na kutoka nae nje ambapo Elly nae alimfata nyuma.Baba Abdi alipomaliza kulipa alitoka pia ambapo mwanae nae alimfata nyuma, halafu baba Erica alikuwa akimuita mama Erica,“Erica, Erica, Erica”Ambapo mtoto Erica ndio alikuwa akigeuka nyuma na kumwambia mama yake,“Mama, baba Abdi ananiita”“Twende nyumbani wewe, acha ujinga”Basi wakaingia ndani ya gari ila kabla mama Erica hajaondoa ile gari yake alishangaa baba Abdi kukaa mbele ya ile gari kwa maana kuwa alikuwa radhi amgonge au amsikilize, kwahiyo ilibidi mama Erica ashuke kumsikiliza, kwanza alimuuliza,“Una tatizo gani kwani?”“Inamaana umenisahau Bahati wako?”Mama Erica alicheka na kusema,“Hivi unajua sisi ni watu wazima sasa, tuna familia zetu hebu acha mambo ya kijinga jamani”“Nipe kwanza mawasiliano yako ndio nitaacha, kwakweli sijui nikwambiaje ila nilipokuona leo akili yangu yote imeruka na kupoteza uelekeo kabisa”Mama Erica akaona isiwe tabu maana alimpa namba yake kisha kuagana nae ambapo kila mmoja alipanda gari lake na kuondoka zake.Moja mwa moja mama yake Erica alitaka Elly ampeleke kwao ambapo Elly alifika nae hadi nyumbani kwao ila mama yake Elly hakuwepo basi mama Erica alimuuliza Elly,“Kwani mama hako huwa anarudi muda gani?”“Mama, hana muda maalum wa kurudi, kwahiyo sijui”“Ooooh sawa, akija basi mwambie kuwa mama yake na Erica anahitaji sana kumuona”“Sawa, nitamwambia”Basi mama Erica alipanda kwenye gari na binti yake na kuanza kurudi kwao huku Erica akimwambia mama yake,“Si nilikwambia mama, huwezi kuonana na yule mama yupo busy sana”“Nimekuelewa mwanangu, ila huwezi jua ni kwanini nahitaji kumuona”“Kwanini mama?”“Bado mdogo kujua haya”“Sawa, hivi na yule baba Abdi unafahamiana nae?”“Achana na maswali hayo”Basi waliendelea na safari ambapo Erica alikuwa akijiuliza mambo mengi sana kuhusi baba yake Abdi na mama yake, kwahiyo alipanga baba yake akirudi nyumbani amuhadithie yani yeye hata hakufikiria kama sio vizuri wala nini.Baba Abdi nae alikuwa akielekea kwake huku akitabasamu tu, mwanae alikuwa akimuuliza,“Baba, mbona umelipa hela kubwa ya mlango wakati ule mlango matengenezo yake haifiki hata elfu hamsini”“Nyamaza kimya kenge wewe, unafanya makosa halafu unajifanya kujieleza ujinga hapa”Walipoingia tu nyumbani kwao, siku hiyo baba yake alipitiliza kulala tu, ilibidi mama aliyeishi nao kuanza kumuuliza Abdi,“Leo hamjaokota mtoto mwingine wa kuja nae nyumbani?”“Hapana mama, ila kuna jambo lingine limetokea”“Jambo gani?”“Wakati tupo shuleni, alifika mama yake na Erica”“Mama yake nani?”Baba yake nae alitoka chumbani na kumuita Abdi ambapo Abdi alienda kumsikiliza baba yake, alimfunga mlango na kumwambia,“Yani wewe umefanya makosa, umefanya nilipe pesa isiyokuwa na sababu halafu saa hizi upo nyumbani kuchonga mdomo kwa mama yako. Unamweleza hayo ili iweje? Unataka aondoke halafu hapa atawalea nani wajinga nyie”Kisha akachukua mkanda wake wa suruali na kumtandika nao sana yani hadi mama yake alienda kumuombea msamaha ndio akamuachia.Basi mkewe akamuuliza,“Nini sababu ya kumpiga hivyo mtoto jamani!”“Huyu mtoto ni mjinga sana, unajua alichofanya shuleni?”“Eeeeh kafanyaje?”Baba Abdi alianza kumueleza mkewe kile alichoambiwa na walimu, yani kile alichokuwa anakibishia ndio alichomueleza mkewe, basi mkewe alikuwa akishangaa tu na kuona kuwa mumewe alikuwa sahihi kumuadhibu mtoto huyo ila kwa muda huo alikuwa ameshaachana na mada ya mtoto wake kuwa alipofika mama Erica ilikuwaje.Erica akiwa nyumbani alimuhadithia Erick kuhusu kilichotokea shuleni halafu akamwambia jinsi alivyomuuliza mama yake na jinsi alivyomshushua, kisha akamwambia Erick,“Sasa mimi nitaenda kumuuliza baba”“Ukisikia umbea ndio huo, dada Angel alikuwa akigombana nawe kila siku hapa sababu ya huo umbea kwani Erica huwa huwezi kupotezea kitu? Hata kama wakifahamiana, wewe mtoto inakuhusu nini au itakusaidia nini? Je utayafahamu maisha ya wazazi wetu kipindi hiko? Maisha yao yalivyokuwa ni siri yao pekee, sisi watoto hayatuhusu, kama mama kasema achana na habari hizo basi achana nazo”“Mmmh jamani!”“Ndio, mimi nakupenda ndiomana nakwambia ukweli Erica, sio jambo jema kufatilia mambo yanayofanywa na wazazi”“Basi sifatilii tena, nitakuwa nafatilia mambo yako”“Ndio, yangu ukifatilia ni sawa kabisa. Tena anza muda huu huu kufatilia, ila sio mambo ya wazazi kwanza hawatapenda wakigundua hilo, pili sio tabia nzuri”Basi ile ikawa kama dawa, maana alivyoambiwa tu vile, hakutaka tena kujihusisha na mambo yasiyomuhusu. Basi kaka yake alimwambia tena,“Kesho ni Ijumaa mdogo wangu una mpango gani?”“Mpango gani kivipi?”Mara Vaileth alienda kuwaita maana walikuwa kwenye kile chumba cha kusomea,“Nyie mnaitwa na wazazi wenu kwenda kula huko”Basi wakainuka na kuelekea sebleni ambapo baba na mama yao walikuwa mezani wakila, kwahiyo waliulizia kama na wao wamekula ndiomana waliwaita, basi waliwasalimia pale na kuchukua chakula na kuanza kukila.Wakati wa kula simu ya mama Angel ambayo alikuwa ameiacha kwenye kochi iliita sana basi akamwambia Erica akamchukulie ili aangalie nani anapiga ila Erick akamwambia mama yake,“Mama, siku zote huwa unatufundisha kuwa si vizuri kuongea wakati wa kula. Pia sidhani kama ni vizuri kupokea simu wakati wa kula”Baba Angel nae akasapoti na kusema,“Kweli kabisa alichosema mtoto”Basi wote waliendelea kula, ila yule mpigaji inaonyesha aliamua kupiga maana simu ilikuwa ikiita tu, yani ikikatika inaanza tena kuita hadi kero.Ikabidi tu mama Angel ainuke na kuizima ile simu kisha alirudi kula na walipomaliza waliagana pale ambapo moja kwa moja walienda vyumbani.Baba Angel alimuuliza mke wake kuhusu ile simu iliyokuwa ikipigwa muda wote,“Ni nani aliyekuwa akipiga vile?”“Sijui, ni namba mpya”“Labda ni mtu wa maana au labda kuna tatizo maana kapiga sana mke wangu, hebu jaribu kumtafuta usikie, huwezi jua”Basi mama Angel aliwasha tena ile simu na kuipiga ile namba ambayo muda ule ule ilipokelewa na sauti ya kika,“Nani mwenzangu”“Nikuuliza wewe uliyepiga ni nani?”“Oooh niliona umenipigia sana, ndiomana nikakupigia ili kujua ni nani?”“Hebu niambie kuwa ni nani wewe maana hii ni simu ya mume wangu”“Oooh samahani”“Samahani ya nini? Wewe ndio kimada chake eeh!”Mama Angel alikata ile simu na mumewe alimuangalia na kumuuliza,“Nani sasa?”“Nadhani alikosea namba maana namuuliza nani na yeye ananiuliza nani”“Oooh achana nae, tufanye yet utu mke wangu. Kesho kuna mahali nataka twende pamoja”“Wapi huko mume wangu?”“Mmmh ila tutarudi Jumapili”“Inabidi tuwaage watoto basi”“Tutawaaga kesho asubuhi, hakuna tatizo”“Sawa, na hiyo Jumapili tutarudi asubuhi au jioni?”“Jioni mke wangu”“Sawa, hakuna tatizo”Kisha wakaamua kulala tu kwa muda huo.Kulipokucha, mama Angel na baba Angel walishajiandaa kwahiyo wakati wanatoka walikuta watoto wao nao wamejiandaa basi waliwaaga kuwa wanasafiri na wangerudi Jumapili jioni, Vaileth nae alikuwepo pale basi alimkumbusha mama Angel safari yake ya kesho kwa ndugu zake,“Mama, je mimi naweza kesho kwenda kwa shangazi yangu kumsalimia?”“Hakuna tatizo ilimradi jioni utakuwa umerudi dada”Basi Vaileth alishukuru na kuwatakia safari njema, basi waliondoka zao na watoto wao walienda shuleni kama kawaida yao.Erica akiwa shuleni leo alishangaa mno kuona Elly akiwa kama kavimba mkono vile, basi muda wa mapumziko aliamua kumuuliza kuwa imekuwaje,“Elly, tatizo nini jamani? Mbona mkono umevimba?”“Toka udogo wangu sijawahi hata mara moja kupigwa na mama yangu ila jana amenipiga hadi nilijihisi kizunguzungu”“Kheee kwanini sasa mamako alikupiga jamani Elly?”“Sijui kwanini ila mama kachukia sana nilipomwambia kuwa nilienda na mama yako nyumbani, na nilipomwambia kuwa mama yako anataka kufahamiana nae, nilishangaa mama akichukia na kunipiga sana, sasa wakati nakimbia ndio kuna kitu alinitupia kikanipata hapa mkononi hadi mkono ukavimba hivi. Kwakweli nimeshangaa sana, sijui kwanini mama kachukia kiasi hiki jamani! Tena kasema nisirudie tena na pale tunapoishi tutahama”“Mmmh, kwahiyo mama yako hataki kuonana na mama yangu jamani!”“Sio mama yako tu ila mama huwa hataki kuonana na mtu yeyote asiye ndugu yetu, naomba Erica usimwambia haya mama yako tafadhari, nakuomba sana”“Usijali Elly, ila dah nakuhurumia sana. Sasa dawa gani umetumia?”“Dada alinikanda”“Dada yako yupi?”“Ni mtoto wa makubwa, basi ndio kanikanda mkono, kiukweli mama alikuwa na hasira sana, hadi muda analala alikuwa amenuna na leo asuhubi hata sijaongea nae. Roho inaniuma sana, mama yangu ni kila kitu katika maisha yangu hata sijui ni kwanini amechukia kiasi hiki”“Pole sana Elly, nakuahidi sitomwambia mama na wala sitotaka tena kuja nae kwenu kuonana na mama yako. Pole Elly jamani”Basi waliingia darasani ila Erica alikuwa akijiuliza vitu vingi sana kwani hakuona mantiki ya Elly kupigwa na mama yake.Angel leo akiwa shuleni, basi Husna alikaa nae karibu wakijisomea, ila muda wa mapumziko siku hiyo walishangaa sana Samir kuelekea ofisini, na aliweza kumuona maana yeye na Husna walikaa karibu na ofisi kwahiyo waliona kila kitu, na baada ya muda mwalimu aliwaita basi Husna na Angel walienda, akawaambia watoe vile vyombo na kupeleka kwenye jiko la shule.Basi waliingia na kutoa vile vyombo, ila Samir nae alikuwepo mule ofisini na alikaa meza moja na madam Hawa, kwahiyo walitoa vile vyombo na kupeleka jikoni. Ila roho ya Angel iliumia sana, basi alimuuliza Husna,“Inamaana madam Hawa ana mahusiano na Samir?”“Mmmh sijui, lakini inawezekana maana madam Hawa hajawahi kuwa karibu kiasi hiki na mwanafunzi yoyote yule”“Kwahiyo inamaana yupo nae?”“Mbona unaulizia hivyo Angel? Unamtaka Samir?”“Hapana, nimeuliza tu”“Hawa wavulana shuleni ukitaka kusoma kwa raha waone wote kama kaka zako, inamaana hata akifanya nini haitakuumiza moyo maana unaona kama kaka yako ndio amefanya. Una kaka nyumbani Angel?”“Ndio, yupo mdogo wangu wa kiume anaitwa Erick”“Basi ukitaka kufaulu vizuri muone kila mvulana shuleni kama mdogo wako Erick”“Ila sijasema kuwa namtaka Samir”“Hata mimi sijasema kuwa unamtaka ila nimeongelea tu rafiki yangu”Basi walirudi darasani na baada ya muda Samir nae alirudi darasani na kuendelea na masomo.Muda wa kutoka ulivyofika, leo madam Hawa alifika mwenyewe darasani kwakina Angel na kumuita Samir, ambapo alimwambia,“Samir, jiandae tuondoke”Basi Samir alibeba begi lake na kuondoka na yule madam, yani kitu hiko kiliumiza sana moyo wa Angel, aliumia na fikra zake zote.Angel aliporudi nyumbani alikuwa na mawazo sana, shangazi yake alipomuona alielewa tu kuwa Angel hayupo sawa basi alimuita kabla ya kwenda chumbani na kuanza kuongea nae,“Angel, ni kitu gani kinakukosesha raha malaika wangu?”“Shangazi sijui nisemeje, ila swala la kumuona Samir akiwa karibu na madam Hawa, naumia sana moyo”“Ngoja nikuulize swali mwanangu, umeenda shule kwaajili ya kusoma au kwaajili ya Samir?”“Kwaajili ya kusoma shangazi”“Basi soma, unamfatilia Samir ni nani katika maisha yako? Na atakusaidia kitu gani? Je Samir ndio atasaidia kuongoza maisha yako? Bila Samir huwezi kuishi?”“Hapana shangazi”“Basi achana na mawazo ya Samir kabisa, kwanza hakufai mtoto mdogo anatembea na wamama watu wazima, yani hakufai kabisa mwanangu. Zingatia masomo yako”“Asante shangazi”Basi Angel muda huu alienda chumbani kwake tu na kuanza kufanya mambo mengine yaliyokuwa kwenye ratiba yake, ila kwavile hakumaliza vizuri mawazo yake basi muda huo alitoka tena nje, na siku hiyo kwa mara ya kwanza alikaa nje ya geti na muda kidogo ni kamavile aliambizana na yule dereva wa bajaji kwani alifika muda ule ule pale getini kwakina Angel na kuanza kumsalimia,“Mrembo uhali gani?”“Mmmh wewe nawe loh!!”“Wewe nawe nini, yani sijui ni kitu gani kimenipitisha hapa, nadhani ni moyo wangu ndio umenipitisha hapa. Nakupenda sana Angel”Mara shangazi wa Angel alitoka nje na kushangaa sana,“Kheee kumbe wewe upon je badala ya kukaa chumbani kwako”Kisha akamvuta mkono na kuingia nae ndani, kisha akamchapa makofi ya kutosha na kumwambia,“Angel huwa sipendi kupiga ni mpaka mtu anipe sababu ya kupiga, na kwa unachofanya Jumatatu nitaenda shuleni kwenu nikaseme kinachoendelea juu yako. Usinitie uchizi mie”Angel alinyong’onyea na kumwambia shangazi yake,“Nisamehe shangazi tafadhari, usiende shule”“Unaniahidi kitu gani?”“Nakuahidi shangazi hii kitu haitajirudia tena, nisamehe shangazi”“Haya rudi chumbani kenge wewe”Basi Angel alitia huruma sana na moja kwa moja alielekea chumbani kwake.Erica leo alivyorudi nyumbani kwao tu, wakati amekaa sebleni na Erick alimuhadithia juu ya Elly kupigwa na mama yake, kwakweli hata Erick alishangaa sana,“Jamani, kwanini sasa? Kisa kutokufahamiana na mama yetu?”“Ndio, Elly kasema kuwa mama yake hataki kuonana na mtu yeyote mgeni kwake zaidi ya ndugu zake”Vaileth nae aliyasikia hayo na kumuuliza Erica,“Kama huyo mama hataki kuonana na mama yenu, kwanini alimpa Elly visheti akuletee ili ulete nyumbani?”“Mmmh sijui”“Kuwa makini sana Erica, sio kila unachopewa basin i cha kuleta nyumbani, kuwa makini sana utaangamiza wazazi wako”“Inamaana mama yake Elly ni mbaya?”“Sina maana hiyo, ila tu nimekwambia kuwa makini basi”“Sawa dada, nimekuelewa”Basi Erica aliendelea kuongea na kaka yake ambaye kwa muda huo waliinuka na kwenda ndani kucheza zile karata za Abdi, basi wakati wanacheza ndipo Erick akamtania Erica,“Hizi karata ndio zingesababisha ubakwe Erica”“Toka zako huko, halafu baba yake Abdi sijui yukoje, eti akaniuliza umewahi kubakwa?”Erick alicheka sana na kumuuliza,“Ulimjibuje?”“Nilikaa kimya tu”“Siku nyingine wakikuuliza hivyo waambie nimewahi ndio kubakwa na kaka yangu”“Kheee Erick unaongelea nini kwani?”“Kwani hapa tunaongelea nini?”“Kheee basi, tucheze tu karata”Basi waliendelea na kucheza zile karata huku wakiendelea kuambizana mambo mbalimbali, muda wa kulala ulifika na kujikuta wote wakiwa wamelala sehemu moja yani chumbani kwa Erica maana ndipo walipokuwa wakicheza karata humo.Erica alishtuka usiku wa maneno na kuhisi njaa sana ila Erick alikuwa amelala hoi, ilibidi amuamshe maana alijua pia lazima na yeye ana njaa.Na kweli alivyoamka pia alikuwa na njaa na siku hiyo waliona umuhimu wa mama yao kuwa nyumbani kwani yeye huwa anawakumbusha kila siku muda wa kula ila leo dada yao aliwaacha waendelee kulala tu, basi waliamka na kwenda jikoni ambapo walipakua chakula na kula, ila waliposhiba hawakuwa na usingizi kabisa, hivyo waliamua kuwasha Tv na kuanza kuangalia ambapo walilala pale pale sebleni.Vaileth alipoamka asubuhi kwakweli alicheka sana kukuta wamelala sebleni, aliwashtua na kuwauliza kuwa imekuwaje, Erica alianza kusema,“Ila dada una tabia mbaya jamani, yani umeacha kutuamsha jana tuweze kula”“Jamani, nilijua labda hamna njaa ndiomana mlienda kulala mapema. Kwahiyo ndio mliamka usiku na kuja kula”“Ndio, na usingizi ulikata na tulipokaa sebleni ndio tukajikuta tukilala tena”“Ila nyie jamani, hivi mama yenu angekuwepo mngefanya ujinga wa namna hii eeeh!”Basi Erick akaondoka zake kuelekea chumbani kwake, kwahiyo ilibidi vaileth amuage Erica kuwa siku hiyo atatoka ila badae atarudi.Baada ya hapo Vaileth alifanya usafi wote wa ile nyumba na kisha kujiandaa na kuondoka, muda huo Erica na Erick wamelala maana baada ya pale kila mmoja alienda chumbani kwake kulala tena.Basi Erick alipoamka aligundua kuwa yule dada yao hakupika hata chai wala nini, ikabidi akapike mwenyewe maana hakikuwa kitu kigumu kwake, tena siku hiyo alipika chai, alichemsha mayai na kwenda kununua mkate wa kula yeye na Erica, yani Erica alipoamka alikuta kaka yake ameshaaandaa kila kitu akatabasamu na kumwambia,“Kwa hakika mke utakayemuoa atakuwa na raha sana”“Sidhani kama nitakuja kuoa mimi”“Kwanini?”“Sababu ninayempenda hawezi kuwa mke wangu”“Mmmh kumbe kaka yangu ushapenda tayari, nidokezee basi nimjue wifi yangu ni nani na kwanini hutoweza kumuoa?”“Hebu njoo tu tunywe chai, maswali mengine hayana msingi hayo”Basi walikaa na kuendelea kunywa chai.Vaileth alifika kwa shangazi yake na kupokelewa kwa kofi kwanza, yani alibaki tu kushangaa na kumwambia shangazi yake,“Jamani shangazi, hilo kofi ndio salamu?”“Ndio, mjinga sana wewe yani unaishi kwenye nyumba ya kifahari halafu wazazi wako tunaishi kwenye nyumba ya shida hivi ndio unaona vizuri? Bora hata wifi asingekuzaa toto jinga kama wewe”Prisca alienda na kusema,“Bora shangazi useme wewe, yani mimi kwakweli kwa jinsi nilivyoiona ile nyumba hadi nilisisimka na kujiuliza hivi Nyanda anafanya kitu gani?”Basi shangazi yake akasema tena,“Mwanangu Vaileth kama ulivyojiita jina zuri la kizungu ila mbona unakosa akili kwenye bichwa lako hilo?”“Sasa shangazi, mimi nitafanya kitu gani?”“Kumbe hujui eeeh! Mbona swala ni jepesi sana, ni kumtega yule baba mwenye nyumba na kumuweka kwenye kumi na nane zako”“Mmmmh yule baba mwenye nyumba hana mambo hayo kabisa”“Basi hata kwa ndumba mwanangu, kuna mtaalamu huyo yuko vizuri yani ni swala tu la wewe kuweka dawa mara moja kwenye chakula cha huyo baba halafu kwisha habari yake”“Mmmh!”“Sio mmmh ndiomana nilikupigia simu ile asubuhi kuwa uwahi kuja ili twende huko. Haya tuondoke”Yani Vaileth alikuwa akishangaa tu kwakweli, kisha yule shangazi aliondoka nae na kwenda kupanda daladala ambapo walienda mbali kidogo na pale na kulikuwa na bibi wa makamo ambaye ndio alikuwa mganga, basi alianza kuongea nao,“Kwanza huyu mwenye nyumba mnayemtaka kafatiliwa na wadada wengi sana, nikikupa idadi ya wanawake ambao wamemfatilia huyo baba basi utabaki tu na mshangao, na hajaanza kufatiliwa leo bali siku nyingi sana ila huyo baba anampenda sana mkewe”Shangazi wa Vaileth akachukia na kusema,“Jamani jamani, kwahiyo haiwezekani kwa Nyanda kumpata?”“Imefika kwangu jua kwamba inawezekana, kwanza wenye nyumba hao wamesafiri, si ndio”Vaileth akajibu,“Ndio”“Basin i vizuri kwani nakupa dawa kwanza ambayo utatakiwa kuiweka getini yani inatakiwa ikae masaa kumi na nane ndio ianze kufanya kazi, kwamaana hiyo ni kwamba, watakaporudi kesho na kukanyaga hiyo dawa basi itakuwa ndio njia ya kwanza kumteka, halafu nitakupa dawa nyingine ya kuweka kwenye chakula”“Sawa”“Ila fanya kama nitakavyokuelekeza, kwanza wakati unaiweka usiruhusu mtu yoyote kuiona”Basi yule bibi alifanya dawa zake na kumkabidhi Vaileth zile dawa ambapo shangazi yake alimpa onyo kuwa asipuuze kufanya hizo dawa,“Yani ukipuuza Vai ujue huna ndugu katika maisha yako”Basi na muda huo huo walimtaka Vaileth aondoke aelekee kwa bosi wake, yani Vaileth aliondoka huku akiwa na mawazo sana, kwani kile kitu hakuwahi kukifikiria na wala hakutaka kukifanya kabisa ila kila akikumbuka maneno ya shangazi yake aliogopa sana, maana hadi anaondoka aliambiwa ole wake asifanye hiyo dawa.Erica na Erick muda huu walitulia sebleni wakiangalia Tv, mara kwenye Tv kulikuwa na tamthilia ambayo ilionyesha mwanamke akimuwekea limbwata mume wake, basi Erick akasema,“Yani wanawake akili zenu ni mbovu sana, sasa huyu akimloga mume wake ndio anapata faida gani?”“Mmmh sio wanawake wote, mbona mama hayupo hivyo?”“Haya badili kipindi basi, mimi mavitu ya ushirikina hayo sitaki kuyaangalia”“Sibadili”Basi walianza kugombana sababu Erica ndio alishika ile rimoti ya Tv, na wakati wanagombana Erica aliinuka na kuanza kukimbia ambapo Erick alikuwa akimkimbiza, cha kushangaza erica alikimbia kwa kuelekea nje wakati sio kawaida yao kutoka nje ya geti ila wakati kafungua geti alijikuta akimsukuma Vaileth na kumfanya aangukie huko hadi vitu vya kwenye mkoba wake kuanguka, ni pale walipoanza kushangaa wakati wanaviokota, Erica alivishika na kumuangalia dada yao kisha akamwambia,“Dada, kumbe wewe ni mshirikina!!”Vaileth alishtuka na kuogopa sana, kile kitendo cha mshtuko kilifanya aanguke na kuzimia.Basi walianza kugombana sababu Erica ndio alishika ile rimoti ya Tv, na wakati wanagombana Erica aliinuka na kuanza kukimbia ambapo Erick alikuwa akimkimbiza, cha kushangaza erica alikimbia kwa kuelekea nje wakati sio kawaida yao kutoka nje ya geti ila wakati kafungua geti alijikuta akimsukuma Vaileth na kumfanya aangukie huko hadi vitu vya kwenye mkoba wake kuanguka, ni pale walipoanza kushangaa wakati wanaviokota, Erica alivishika na kumuangalia dada yao kisha akamwambia,“Dada, kumbe wewe ni mshirikina!!”Vaileth alishtuka na kuogopa sana, kile kitendo cha mshtuko kilifanya aanguke na kuzimia.Basi Erick na Erica walimuita mlinzi wao ambaye alimuinua Vaileth na kumuingiza ndani, ila Erick alikusanya zile dawa za Vaileth na kwenda kuzitupa kwenye mtaro halafu akarudi tena nyumbani kwao ambapo Vaileth alikuwa amezinduka ila walipomuuliza alikuwa akilia tu.Basi walimpeleka ndani kabisa ambapo Erick na Erica walikaa nae na kumuhoji, kwani Erica bado alikazania lile lile swala,“Dada, tuambie ukweli, wewe ni mshirikina?”Vaileth alikuwa akilia tu, kisha aliwajibu,“Jamani mimi sio mshirikina ila zile dawa nimepewa na shangazi yangu amesema za kunikinga”“Kwani dada huamini kuwa Mungu pekee ndio kinga ya kweli?”“Naamini wadogo zangu, haikuwa nia yangu kuwa na zile dawa, ni shangazi kanipa”“Sawa dada, basi kesho twende wote Kanisani”“Sawa tutaenda, naomba mnisamehe sana wadogo zangu”Kisha Vaileth alienda chumbani, kiukweli alikuwa akijutia mno kile kitendo, alijikuta akilaani mno kuhusu shangazi yake kumpeleka kwa mganga na kupewa zile dawa, yani alikuwa kajifungia tu chumbani akilia.Basi Erick na Erica walikuwa sebleni ambapo Erica alimwambia Erick,“Lazima nimueleze mama kuhusu swala hili”“Wewe nawe, kashatuomba msamaha, sasa mama umueleze kitu gani?”“Yani wewe Erick unapinga kila kitu, una uhakika gani kuwa zile dawa ni zake mwenyewe? Unajua tutadhurika humu ndani? Dalili ya mvua ni mawangu”“Hata kama ila subiri kwanza mdogo wangu, tusiwe hivyo jamani, mtu kaomba msamaha halafu tumfanyie hivyo kweli!!”“Mmmh haya, maana wewe kila kitu unapinga jamani”Basi na wao waliendelea na mambo mengine.Mama Angel na baba Angel walikuwa mahali ambapo baba Angel alichagua ili yeye na mkewe wakae kwa karibu zaidi na kusahau yale yanayowafanya muda wote wasifikirie mambo yao zaidi ya biashara tu wanazofanya,“Jamani mume wangu si ungeniambia sasa!”“Aaaah kumbe hujui eeeh! Safari za kushtukizana ndio nzuri mpenzi. Mimi na wewe tunapendana, kwahiyo naweza panga safari yoyote kwa muda wowote kwani najua huwezi kukataa. Je hujafurahia huku mke wangu?”“Nimefurahi sana yani, mara nyingine watoto nao wanachanganya sana akili, mtu ukipata sehemu kama hii unashukuru sana kwakweli”Mara simu ya mama Angel ilianza kuita, kuangalia ni ile namba ya siku ile, wasiwasi wake ni kuwa huenda mpigaji wa ile simu ni baba Abdi sababu siku ile ni mkewe aliongea na kwa haraka haraka alihisi ile sauti kama ni sauti ya Fetty vile, basi mumewe akamwambia kuwa apokee,“Pokea mke wangu, huwezi jua ingawa sikupenda tukiwa huku tusumbuliwe na simu”Basi mama Angel alipokea, na kama alivyohisi ni kweli baba Abdi ndiye aliyekuwa akimpigia ile simu,“Oooh asante sana kwa kupokea simu yangu, ujue nimekumiss sana wewe mwanamke”“Kwani wewe una matatizo gani jamani!!”“Sina matatizo yoyote, wewe ndio chanzo cha mimi kuoa mwanamke asiyeeleweka, na wewe ndio chanzo cha yule mwanamke kunifanyia dawa mimi hadi nikazaa hovyo, na wewe ndio chanzo cha mpaka sasa siishi kwa amani na mke wangu maana muda wote nakukumbuka na kukutaja sana kwani ungeishi nami najua watoto wangu wangepata malezi mazuri sana”“Una wazimu wewe”Kisha mama Angel alikata ile simu na mumewe alimuuliza, ambapo hakutaka kumficha kwani alimwambia ukweli wote,“Kheee jamani, hivi huyu si ndio kwenye harusi yetu aliongea sana nikajua yameisha mke wangu, bado tu anakufatilia!! Nahitaji kuongea nae kiume”“Hata mimi namshangaa, eti analalamika maisha yake yameharibika sababu yangu”“Huyu ni mjinga, maana mtu unaharibu maisha mwenyewe na sio mtu mwingine, kwani wewe umeharibu vipi maisha yake?”Mama Angel alimwambia mumewe waachane tu na habari hizo na waendelee kufurahia kilichowapeleka kule kwani hakutaka kuongea yaliyopita.Leo ndio ilikuwa Jumamosi ambayo Samir alienda nyumbani kwa madam Hawa, ambaye alisema kuwa siku hiyo ndio aende akaongee nae vizuri, kiukweli hata yeye huwa haelewi mantiki ya kinachofanywa na yule madam kwahiyo anachukulia kawaida tu, basi alienda kumsikiliza,“Madam, nimeitikia wito”“Maisha unayoishi sasa yani mimi nikionekana kama mzazi wako unayaonaje?”Samir alinyamaza kimya kidogo, kumbe kile alichokuwa akifanyiwa ni kama mtoto wa mwalimu, basi alipumua kidogo na kujibu,“Nimeyapenda”“Mbona umewaza sana? Ulikuwa ukifikiria ni kitu gani? Au ulifikiria kuwa nakutaka?”“Hapana madam”Kisha madam hawa akacheka na kusema,“Siwezi katika maisha yangu yote kuwa na mahusiano na kujana mdogo kama wewe, yani maisha ninayokupa shuleni nahitaji ujione kama mtoto wa mwalimu na usome kwa bidii na uache kumfatilia Angel yani ukitaka kufanya ujinga ujue kuwa mama yangu yupo hapa shuleni ananiona. Mimi sikuhitaji kwakweli, na walimu wote wanaelewa kuwa kwanini nafanya hivi, nakuweka vizuri kisaikolojia. Haya niambie kwasasa, unasumbuliwa sana na mawazo ya Angel?”“Hapana”“Sawa, mara nyingi huwa unafanya nini?”“Mara nyingi umekuwa ukinipa zoezi na maswali ya kufanya, kwahiyo nikirudi nyumbani nakosa muda wa kukaa na kuwaza maana asubuhi huwa unahitaji nikupatie hayo maswali, na moja kwa moja huwa unakuja na kuniita darasani kwahiyo nimejikuta nikiwa busy sana”“Na hiko ndio nilichokuwa nakitaka toka mwanzo, nilitaka wewe ukazanie masomo na sio kitu kingine chochote. Kama ulikuwa unawazo kuwa madam Hawa anakutaka kimapenzi naomba usahau kabisa kabisa, maana mimi nakupenda kama mtoto wangu ndiomana niliongea na mama yako aniruhusu nianze kukulea mwenyewe shuleni ili kukurudisha kwenye mstari, si vizuri kufanya mzazi atupe hela kila siku sababu ya kukuhamisha wewe shule, si vizuri kwakweli mnatuumiza wazazi, niliumia sana wakati mama yako akiongea ndiomana nikabeba jukumu la kuwa nawe bega kwa bega”“Asante sana madam”“Sasa nadhani utakuwa huru zaidi maana mwanzoni ulikuwa na mashaka kuwa sijui huyu madam ananitaka sijui nini na nini, ondoka kabisa hayo mawazo maana mimi ni kama mama yako tu”Basi Samir aliitikia ambapo yule madam alimpa maswali mengine na kuagana nae kuwa arudi kwao.“Moja kwa moja nyumbani Samir, nitawasiliana na mama yako maana anajua kama ulikuja kwangu”“Sawa madam”Basi Samir aliondoka muda ule na kuelekea kwao.Samir alipofika kwao alimuona mama yake akimsindikiza mwanaume, kwahiyo alisimama akimuangalia hadi pale mama yake aliporudi na kumuuliza,“Mama, na yule ni baba yangu?”“Hebu kuwa na adabu wewe mtoto, kila mtu baba yako jamani eeh! Nisiongozane na mwanaume basi ndio kashakuwa baba yako, kwani baba yako ninayeishi nae hakutoshi?”“Mama, yule baba ana kisirani sana”“Hata awe na kisirani ndio kashakuwa baba yako, usinipangie maisha”“Sawa mama, sikupangii maisha ila ni vizuri mimi kumjua baba yangu wa ukweli”“Aliyekwambia kuwa huyu sio baba yako wa ukweli nani? Mimi ndio mama yako na mimi ndio niliyekuonyesha huyu, kwahiyo heshima na adabu ifate mkondo wake”“Ila mama hujui tu ni kwanini simtaki huyu baba”“Kwanini?”“Jamani baba ana watoto kila sehemu, mwisho wa siku ndio mambo ya kujikuta nimeoana na dada yangu, baba gani huyu, kila kina ana mtoto. Nina uhakika watoto wake wengine hata hafahamu wako wapi na wanaishije, mimi ningeweza ningejibadilishia baba”“Punguani mmoja wewe, usumbue, uhangaishe ila mimi na baba yako bado tupo pamoja na wewe. Tena kuna muda huwa nimekata tamaa kabisa ila baba yako utasikia tusimuache mtoto nyumbani, aende shule, halafu mjinga kama wewe unadai unamtaka baba mwingine. Kama umejizaa tafuta baba mwingine, ungejua hadi kuzaliwa kwako ni nini kilifanyika hata usingejiongelesha hapo”Huyu mama ilionyesha amechukizwa na kumsonya mwanae kisha akaenda ndani kujiandaa na kumuaga kuwa anaenda kazini, muda huu Samir alikuwa na dada yake aliyeitwa Samia basi akamwambia,“Kwakweli mimi nikiwa mkubwa siji kuoa mke dizaini ya mama kabisa”“Kwanini?”“Muda wote kazini, yani yeye hana cha usiku wa manane, asubuhi, mchana wala jioni. Haya saizi kashaondoka eti anaenda zamu, jamani si jioni hii basi atarudi kesho asubuhi, kwakweli siji kuoa mke dizaini ya mama kabisa”Kisha akaingia zake ndani na kuanza kufanya kazi ambayo alipewa na madam Hawa.Leo Jumapili baada ya kutoka Kanisani, shangazi wa Angel alifika na mama mmoja nyumbani kwake na kumuita Angel kisha akamtambulisha kwa mama yule,“Huyu anaitwa mama Sarah, ni mwalimu mzuri sana. Nimemuomba awe anakufundisha hesabu maana nimejaribu kupitia madaftari yako nimeona kidogo inakupiga chenga, kwahiyo nakubadilishia ratiba maana ukitoka tu shule huyu mama atafika hapa nyumbani na kukufundisha, tumeelewana?”“Ndio shangazi, asante”Kisha Angel akarudi chumbani huku shangazi yake akiendelea kuongea na yule mama Sarah, kisha aliamua kumsindikiza, ila wakati ametoka kumsindikiza alikutana na mtu ambaye hakutarajia kabisa kukutana nae, yule mtu alimuita,“Tumaini”Basi aligeuka na kumuangalia, alishangaa sana na kusema,“Kheee Derrick, siamini kama nimekuona tena”“Kwahiyo ulijua nimekufa?”“Niliposikia umeathirika moja kwa moja nilijua kifo kinakunyemelea, kwahiyo mtu angesema umekufa wala nisingeshangaa”“Acha fikra potofu dada yangu, ukimwi sio mwisho wa maisha cha muhimu ni kujikubali na hali halisi na kula vizuri na kutumia dawa vizuri. Je ukiniona hivi unaweza kusema nimeathirika?”“Ndio nakushangaa hapa maana unaonekana kuwa na afya nzuri kabisa”“Basi kuathirika sio mwisho wa maisha, mtu anakufa kwa maradhi mbalimbali kwanza ukimwi hauuwi mtu ila magonjwa nyemelezi ndio yanaua, ndio utasikia mara kafa na presha, sijui malaria, sijui kisukari ila ukimwi tunauandama tu. Mimi nadundika bado”“Eeeeh vipi, mkeo na watoto hawajambo”“Basi nilioa nikakaa na huyo mke dada yangu!! Sijui nina gundu gani, kamke kenyewe kalikuwa kashirikina hatari, nilikaoa na nikakaambia wazi kuwa mimi nimeathirika na alikubali vile vile na hali yangu, cha kushangaza eti ananifanyia limbwata nimpende sana, jamani mtu nishapigwa na ukimwi halafu atake tena kunipiga na malimbwata loh! Nikakapa talaka na kalisepa bhana”“Kwahiyo watoto je?”“Sikuzaa nae, ila bhana kumbe nina mtoto mkubwa hatari, kuna mwanamke alibeba mimba yangu wakati nipo chuo ila niliikataa basi ndio mtoto nimemuona sasa yani kafanana na mimi mweeeh ila nimegomewa kuishi nae kisa nilimkataa. Unaishi wapi Tumaini?”“Twende, karibu kwangu, sio mbali kutoka hapa”Basi wakaongozana hadi nyumbani kwa Tumaini ambapo waliongea ongea kisha Tumaini akamuita Angel amtambulishe mjomba wake huyo maana huyu Derrick alikuwa na undugu na mama Angel ila Tumaini alisoma nae ndiomana wakafahamiana.Basi Angel alitoka na kutambulishwa kwa mjomba wake huyu, ila huyu mjomba alionekana kumuangalia sana Angel hadi alikuwa akijiramba midomo, basi Tumaini akamshtua hivi,“Kheee wewe Derrick huachi tamaa zako jamani, mwanao huyu ujue!!”Mara Derrick alianza kulia na kumfanya Tumaini amwambie Angel arudi ndani kisha kumuuliza Derrick kwanini analia,“Erica alitoa mimba yangu, mtoto wetu angekuwa mkubwa kuliko huyu”“Hivi wewe Derrick una kichaa au kitu gani jamani!! Erica si dada yako wewe? Inamaana ulitembea na dada yako hadi kupeana mimba?”“Alikuwa ni mpenzi wangu kabla hatujajua ni ndugu”“Kheee mbona umeniambia mapya leo, kwahiyo kipindi kile chuo ni hadi ulitembea na Erica?”“Ndio, muulize Dora anaelewa kila kitu”“Duh!! Naomba uende Derrick, kwanza tutakuja kuongea siku nyingine”Basi Derrick aliinuka na kuondoka ila kiukweli lile jambo lilimuacha Tumaini akiwa na maswali sana.Erica toka tukio la jana alikosa imani kabisa na dada yao vaileth kiasi kwamba akiwa anapika jikoni basi anakuwa nae kwenye mapishi, yani yeye haamini kabisa kuwa zile dawa ni za kumsaidia yeye, anahisi kuwa lazima dada yao huyo ana dawa zingine.Basi hioni ya siku hiyo alikuwa akipika nae jikoni, kuna muda alimuagiza chumvi ambayo waliisahau kwenye meza ya chakula basi na yeye alimuita Erick ili alete ile chumvi maana hakutaka hata kidogo kumuacha dada yao apike mwenyewe jikoni, basi Erick alipeleka ile chumvi huku akicheka kwani alijua ni kwanini Erica anafanya vile.Ila Vaileth alimuuliza Erics,“Mbona na wewe umemuagiza Erick?”Erica huwa hawezi kuficha jambo milele maana muda ule ule alimwambia,“Unafikiri yale madawa yako ya jana nakuamini? Yani sikuamini hata kidogo, ni kwavile tu Erick kasema nisiseme kwa mama ila lazima ningesema tu, yani sikuamini dada”Vaileth alikaa kimya kwani aliona aibu sana, muda kidogo walifika wazazi wao basi Erick na Erica walienda kuwapokea huku Vaileth nae akiwa nyuma yao na kuwakaribisha, sema roho yake ilimsuta sana.Basi mama Angel na baba Angel walikuwa wamekuja na zawadi na kuwapatia watoto wao, ilikuwa ni saa zinazofanana, basi Erica na Erick walifurahi sana na kwenda kuweka zile zawadi zao chumbani, mama Angel hakumsahau Vaileth kwani alimletea zawadi ya heleni na mkufu pamoja na kitenge, basi nae aliwashukuru na kufurahi sana kisha akapeleka chumbani kwake.Yani vaileth kila alipokuwa akitembea mule ndani basi roho yake ilimsuta sana na kujilaumu sana kusikiliza matakwa ya shangazi yake, maana kama hivyo uaminifu tena umefutika kabisa, ukizingatia wakina Erica hawakumuamini tena.Basi muda wa kula chakula cha usiku uliwadia na chakula kiliwekwa mezani kwanza na wote walienda mezani ila kabla ya kuanza kula kile chakula Erica akaongee,“Jamani dada Vai ndio apakue chakula kwanza kuonja halafu ndio tuendelee na chakula”Mama yake alimshangaa na kumuuliza,“Kwanini Erica?”“Kwani mama hujui? Mfalme na Malikia hawapaswi kula chakula kabla hakijaonjwa na mpishi kwahiyo mpishi anatakiwa kuwa wa kwanza kuonja halafu ndio mfalme na malkia wafatie”“Kheee kwahiyo humu ndani nani ndio mfalme na nani ndio malkia?”“Baba na mama nyie ndio mfalme na malkia halafu mimi na Erick ni Prince na Princes kwahiyo wote hatutakiwi kula chukula kama hakijaonjwa ili tusipate madhara”Basi mama yake alicheka na kutikisa kichwa tu kisha akamwambia Vaileth,“Haya, hebu onja mpishi”Ilibidi Vaileth apakue kidogo na kula kile chukula halafu wao ndio wakapakua na kula kile chakula na baada ya hapo waliongea ongea kidogo na kuinuka kwaajili ya kujiandaa na kulala.Basi Erica akiwa chumbani alifatwa na Erick ambaye alimuuliza na kumlaumu,“Kwanini unafanya hivyo sasa Erica jamani! Unajua unamkosesha raha yule dada Vai!”“Hata yeye alitakiwa kukosa raha kwanza wakati kabeba kifurushi cha zile dawa”“Si alishasema ni za kwake?”“Hatakama kasema ni za kwake yani mimi bado haijaniingia akilini kwakweli, najua lazima zile dawa alikuwa akileta kwaajili yetu humu ndani”“Kwanini unasema hivyo?”“Hebu angalia baada ya kumbamba nini kilitokea? Alilia mwanzo mwisho, yani anajuta kwanini tumembamba, halafu pili yupo na wasiwasi muda wote, halafu tena akituona tu anashtuka si anataka kufanya kitu huyo”“Haya leo umemsimamia jikoni na bado hujamuamini kwani hadi umeomba aonje kwanza chakula yeye, kwanza nikuulize je siku zote utakuwa ukimsimamia? Je wakati tupo shuleni ni nani atamsimamia?”“Nilichofanya leo ni kumuweka wazi kuwa kuanzia sasa nimeanza rasmi kumfatilia kwahiyo asishangae kuwa siku nimemmwagia chakula usoni yani nikiwa na mashaka nae tu ajue ameisha. Nawapenda wazazi wetu ujue, hivi wakifa kizembe unadhani nani wa kulaumiwa?”“Unamaana anataka kuua wazazi wetu? Mbona sura yake ya upole sana?”“Usimuamini mtu kwa kumuangalia usoni”Basi Erick aliona watabishana sana, badala yake aliagana na Erica na moja kwa moja kwenda kulala.Ila Erica alibaki na msimamo wake tu wa kumfatilia Vaileth kwani hakumuamini tena toka simu wambambe na zile dawa, aliona kamavile zile dawa alileta ili awaangamize mule ndani haswaa akikumba maandishi ya kwenye zile dawa, kuwa weka kwenye chakula, mwaga mlangoni basi hakuwa na imani kama zile dawa zilikuwa kweli za kumkinga yule dada tu.Kulipokucha kama kawaida walijiandaa kwenda shuleni huku baba Angel na mama Angel wakitoka pamoja pia kwani nao waliaenda kwenye kazi zao.Vaileth alibaki nyumbani ila alikuwa na mawazo sana na kujisemea,“Ona sasa hata siaminiki tena kama zamani, kwakweli shangazi na Prisca wameniponza. Ningejua bora hata Prisca asingefika hapa au bora nisingeenda”Mara simu yake ilianza kuita, alipoangalia aliona ni namba ya shangazi yake basi ilibidi aipokee na kuanza kuongea nayo,“Shangazi shikamoo”“Haina haja, ushafanya hiyo dawa?”“Mmmh shangazi, kwanza nimepata aibu sana yani kwasasa naishi kwa fedheha kubwa”“Khaaa unasemaje wewe”Ilibidi Vaileth amueleze shangazi yake kuhusu yote yaliyotokea, jinsi yeye alivyobambwa na zile dawa, yani shangazi yake alichukia sana,“Mjinga sana wewe, yani kumbe zile dawa uliweka kwenye mkoba?”“Ndio shangazi, ningeweka wapi sasa?”“Si nilikwambia uweke kwenye maziwa mjinga wewe? Kwani hujui ni wapi ambapo wanawake huwa wanaficha vitu vyao muhimu? Yani umenikera sana, kwahiyo umechukua uamuzi gani?”“Wale watoto walienda kumwaga zile dawa, kwakweli nimelia sana kwa kuwasihi wasinisemee kwa wazazi wao, yani nina mawazo hatari”“Hebu niondolee ujinga ujue, kesho nitamuagiza Prisca aje huko na atakuletea dawa yani atakuja mara moja na kuondoka na ole wako ufanye ujinga tena”“Jamani shangazi, sitaki hayo mambo”“Mjinga wewe, hutaki nini? Yani jua kuwa usipofanya hivyo undugu na wewe umeisha, na katika maisha usiombee kabisa kutengwa na shangazi maana ukoo mzima utakutenga, yani wewe unataka kuniletea ujinga muda wote? Umenikera sana mjinga wewe. Sasa Priscaatakuletea kesho hizo dawa”“Mmmmh shangazi”“Sitaki miguno wala nini, nimemaliza. Kesho Prisca atakuja na lazima uifanye hiyo dawa, utake au usitake”Halafu shangazi yake alikata simu ile na kumfanya Vaileth apate maswali zaidi.Erica kama kawaida mda wa mapumziko alikaa na Elly na kuanza kuongea nae mambo mbalimbali, basi Erica aliamua kumueleza kuhusu yaliyotokea Jumamosi nyumbani kwao, yani kuhusu yule mdada wao wa kazi, kwakweli Elly alishangaa sana na kusema,“Kheee huyo mdada hawafai ujue, kumbe ni mshirikina”“Ndio, nimechukia sana kwakweli”“Anaitwa nani?”“Anaitwa Vaileth, jamani kwakweli nimebaki tu kumshangaa kuwa mchawi halafu anajifanya kutuchekea chekea”“Muwe nae makini sana huyo jamani. Kwenu sipajui ila nahisi huyo kawaonea wivu tu”“Halafu Erick anasema eti tusiwaambie wazazi”“Mmmh sijui, ila nitamuhadithia na mama yangu najua atanipa ushauri uliobora”“Sawa sawa Elly”Basi walirudi darasani na kuendelea na masomo.Muda wa kutoka ulipowadia, Erica moja kwa moja alielekea kwenye gari ya kurudi kwao ila Abdi alimsogelea na kumwambia kwa sauti ndogo,“Kuna jambo kati ya mama yako na baba yangu”Halafu Abdi akaondoka, kwakweli Erica hakumuelewa ila alimuangalia tu.Erica alivyofika kwao, moja kwa moja alienda jikoni ambapo Vaileth alikuwa akipika na kuanza kumwambia aonje, yani Vaileth alifanya tu vile sababu Erica alionekana kutokuwa na masikhara ila alipomaliza kuonja alimuuliza Erica,“Kwanini unanifanyia hivi?”“Sikuamini kwakweli, yani sikuamini kabisa. Imani yangu kwako imekufa”“Duh! Haya bhana”Basi Erica alienda chumbani na muda wa kula ulivyofika alirudia kile kile alichokifanya jana kuwa kile chakula aanze kukionja, kwakweli wazazi wao hawakuelewa kwahiyo walibaki tu wakishangaa ila hawakuhoji sana ambapo Vaileth alifanya vile na kisha waliendelea kula kama kawaida na kuongea kidogo na kwenda kulala.Leo baba Angel aliamua kumwambia mama Angel,“Hivi kwanini tusimuulize mtoto kuwa kwanini anafanya hivi?”“Mmmh mimi naona anafanya kwa kujifurahisha”“Kweli kujifurahisha ndio kila siku? Kesho tumuulize mtoto mama Angel wala tusichukulie kawaida hili swala mke wangu”“Sawa mume wangu nimekuelewa, basi kesho tutamuuliza maana hata mimi nimeanza kujiuliza maswali kadhaa kuwa kwanini afanye hivi anavyofanya? Unajua imekuwa tofauti kabisa”Basi wakaongea na kuamua kulala.Kulipokucha kama kawaida walienda kwenye shughuli zao tu.Leo Vaileth alikuwa na mawazo zaidi kwani kadri Erica alivyokuwa akimfatilia ndio ambavyo alizidi kukosa raha kabisa mule ndani, basi wakati akiendelea na kazi za hapa na pale muda ule ule alifika Prisca, kwahiyo alimkaribisha huku akiwa na mawazo sana, basi Prisca alianza kumwambia,“Acha ujinga shoga yangu, hii nyumba ni mali yako lazima tuimiliki sisi kwasasa. Hivi huoni raha kuishi kwenye nyumba kubwa kama hii! Nyumba ambayo imejaa kila kitu, yani ina mali na utajiri, hebu angalia kwanza hiyo Tv ilivyokubwa, angalia Friji jamani, halafu ukifungua friji unakuta kuna kila kitu hivi mtu utakuwa mjinga hadi lini eti uteseke wakati kuna maisha mazuri unayachezea tu. Hebu acha ujinga huo Nyanda, hii nyumba tunatakiwa tuiweke kwenye kumi na nane zetu na huyu baba mwenye nyumba aporomoshe magorofa na kwetu pia, na sisi tupate magari ya kutembelea, tumechoka kutembea kwa miguu ujue, yani mimi nimechoka kabisa kila siku kupuyanga na miguu, hakikisha huyu baba hapindui”“Jamani, mimi sitaki hayo mambo”“Utake au usitake ni lazima ufanye”Basi Prisca alimshika mkono Vaileth mpaka kile chumba alichokuwa akilala Vaileth na kisha kutoa zile dawa na kuziweka mezani kisha akamwambia,“Hii dawa unatakiwa uifanye leo, yani tunapotoka pale getini umwage kidogo ila nyingine uende ukamwage kidogo kwenye mlango wa chumba cha mabosi zako. Ni kikuwapi chumba chao?”Vaileth alikaa kimya, basi Prisca alimtishia kumsemea kwa shangazi yao, ikabidi amuonyeshe ambapo Prisca aliimwaga ile dawa kidogo na kusema watakapopita asubuhi ndio itaanza kufanya kazi vizuri, kisha akamgeukia Vaileth na kumwambia,“Yani ujue ndio kazi imeanza hivi yani lazima huyu baba aingie kwetu”Kisha akamshika tena mkono Vaileth na kurudi nae chumbani halafu akamwambia,“Sasa hii dawa utaiweka kwenye chakula usiku wa leo, yani usiache”“Je hiko chakula hakitanidhuru mimi?”“Yani iko hivi, hii dawa ni kwaajili ya muhusika tu sema muhusika anatakiwa ale zaidi ya wote kwahiyo unapoweka kwenye chakula hakikisha upande ule anaochukua baba ndio unaweka nyingi zaidi, yani utaona matokeo yake kwakweli ni kesho tu huyu baba mwenye nyumba atakutaka, halafu kuna hii unanawia chini yani akikutaka tu hata usirembeshe yani unampa muda huo huo wakati ushanawia hii dawa basi kwisha habari yao”“Mmmmh naogopa”“Acha ujinga wewe”Basi Prisca alimpa Vaileth zile dawa ambazo aliziweka mezani kwake huku Prisca akimwambia kuwa asisahau kumwaga getini maana Vaileth alishindwa kumsindikiza kwa kusema kuwa ana kazi nyingi, kiukweli hakupenda kabisa mpango wa ile dawa na kwa haraka haraka alitamani kwenda hata kuimwaga ila alipigiwa simu na shangazi yake muda huo huo na kupewa onyo kali.Erica akiwa shuleni na Elly, leo Elly ndio aliyeanza kumwambia Erica kutokana na ushauri aliopewa na mama yake,“Erica, mama yangu kaniambia kuwa huyo dada yenu wa kazi itakuwa anamtaka baba yenu yani anataka baba yenu amuache mama yenu na awe na yeye”“Kheee kwahiyo yeye ndio achukue nafasi ya mama?”“Ndio hivyo”“Kheee, lazima nimwambie mama kwa mtindo huo yani amtoe mama yetu halafu akae yeye jamani? Kwakweli huo ni ujinga kabisa, yani mimi naenda kumwambia mama leo siwezi kukubaliana na hiyo hali”Yani Erica muda wote siku hiyo alikuwa na wazo la dawa aliloambiwa na Elly, basi muda wa kutoka shule ulipofika waliondoka kama kawaida kwenda nyumbani.Siku hiyo Erica alivyofika nyumbani alikutana na Erick nae ndio amefika na hata wazazi wao nao waliwahi sana siku hiyo.Basi walivyoingia tu pale pale sebleni, Erica hakutaka hata kupoteza muda kwa wakati huo kwani alianza kuongea pale pale wakati wazazi wake hata hawajaenda chumbani,“Baba na mama jamani nimekaa na hili swala ila nimeshindwa kuvumilia kabisa, naomba twendeni tukamchunguze dada Vaileth”“Kivipi Erica”“Nifateni”Erica aliongoza hadi chumbani kwa Vaileth wakati huo Vaileth akiwa jikoni, basi walipofungua mlango tu hata hapakuwa na haja ya kupekua kwani walikuta dawa zile zipo mezani.Basi walivyoingia tu pale pale sebleni, Erica hakutaka hata kupoteza muda kwa wakati huo kwani alianza kuongea pale pale wakati wazazi wake hata hawajaenda chumbani,“Baba na mama jamani nimekaa na hili swala ila nimeshindwa kuvumilia kabisa, naomba twendeni tukamchunguze dada Vaileth”“Kivipi Erica”“Nifateni”Erica aliongoza hadi chumbani kwa Vaileth wakati huo Vaileth akiwa jikoni, basi walipofungua mlango tu hata hapakuwa na haja ya kupekua kwani walikuta dawa zile zipo mezani.Kwakweli walishangaa sana na aliyeshangaa zaidi alikuwa ni mama Angel na kufanya amuite Vaileth kwa nguvu sana,“Wewe Vaileth weee, hebu njoo upesi”Basi Vaileth alienda hadi mule chumbani kwake huku akitetemeka, kisha mama Angel alimuuliza kwa ukali,“Unamaana gani na hizi dawa?”Vaileth alianza kulia huku akiomba msamaha, yani mama Angel alizidi tu kuchukizwa na kumuulia vizuri,“Kuwa wazi mjinga wewe, una mpango gani na hizi dawa? Yani lengo lako ni kitu gani?”“Sijui mama kama mtanielewa”Kwakweli walisikitika sana, kisha mama Angel alimuangalia mume wake na kumwambia,“Haya ndio mambo niliyokuwa nayachukia kuhusu wasichana wa kazi, yani nimekuwa nikiwachukia sababu ya mambo kama haya”Kisha akamuangalia tena Vaileth na kumuuliza,“Haya niambie, ulikuwa na maana gani na hizo dawa?”Bado Vaileth alikuwa akilia, basi Erica akasema vile ambavyo aliambiwa na Elly,“Mama, leo shuleni nilivyomuhadithia Elly kaniambia kuwa dada atakuwa anamtaka baba yetu kwahiyo anataka akupindue wewe, ndio ambavyo kaambiwa na mama yake”Mama Angel alichukia zaidi na kutaka kujua kuwa yale mambo yemeanzia lini, ilibidi Erica aeleze mlolongo mzima na aseme kuwa ni kwanini hawakusema mapema,“Ila Elly alivyoniambia hivi nimeogopa sana, na ile sinema tuliyoangalia Jumamosi yani nimeogopa zaidi na kuamua kuwa tuje tumchunguze dada”Kwakweli mama Angel alimuangalia Vaileth kwa hasira sana, na muda ule ule hata hakutaka maelewano nae kwani alimwambia kuwa afungashe kila kitu na aondoke zake, basi wakatoka mule chumbani na kumuacha Vaileth akiwa analia.Baba Angel na mama Angel wakaelekea chumbani kwao ila kabla hawajaingia ndani, gafla walisikia sauti kutoka kwa Vaileth ikisema,“Msiingie kwanza”Wakageuka na kumuangalia ambapo Vaileth alienda na tambala bichi na kuanza kufuta pale mlangoni huku machozi yakimtoka kwani alikuwa akiifuta ile dawa ambayo ilimwagwa na Prisca, basi mama Angel alimuangalia kwa ukali sana mpaka alipomaliza kupadeki pale mlangoni kisha waliingia ndani ila hawakuongea nae chochote kile na Vaileth aliondoka kuendelea kujiandaa kuondoka kwenye nyumba hiyo.Baba Angel na mama Angel walikuwa chumbani ila walikuwa wakiongelea lile tukio ambalo limetokea kwa siku hiyo, yani mama Angel bado alikuwa na malalamiko yako ya kuhusu wasichana wa kazi,“Ndiomana sipendi wasichana wa kazi mimi”“Ila mke wangu mbona huyu binti alionekana kuwa mastaarabu sana”“Kwahiyo unataka tumuache ili akuibe wewe!!”“Sina maana hiyo, ila nahitaji ukae nae na uongee nae nap engine ukaelewa kuwa tatizo hilo chanzo chake ni nini, yani mimi sidhani tu kama aliamua kujichukulia hayo maamuzi lazima kuna chanzo. Hebu kaa nae uzungumze nae, unajua hawa wadada wa kazi hatuwahitaji ila kuna muda wana umuhimu wao katika maisha yetu mfano tuna watoto wanasma, huoni kama ni kuwachosha yani watoke shule na waanze kupambana na kazi za nyumbani! Mimi nakuomba mke wangu uongee nae kwanza kabla ya kuondoka hata pindi tutakapotafuta mdada mwingine tujue tumchunguze wapi na kitu gani tufanye ili kuishi nae na kama haeleweki pia basi tumfukuze”“Nimekuelewa mume wangu ila kusema ukweli yani huyu Vaileth amunikera sana, hapa nilipo simtamani hata kidogo. Kweli kutaka kuniibia mume wangu jamani!! Anajua ni wapi mimi na wewe tumetoka? Anajua ni njia gani tumepita hadi sasa tuko pamoja? Kwakweli nimechukia sana”“Naelewa mke wangu, ila fanya hivyo. Nakupenda sana mke wangu”Basi mama Angel alikubali kwenda kumuuliza kwanza Vaileth kabla ya kumtimua kabisa aondoke.Vaileth alikuwa akipanga vitu vyake huku machozi yakimbubujika na kujiona kuwa ni mjinga sana kati ya wajinga na wala hakuelewa kuwa kwa muda huo ataenda wapi,“Hivi mimi Vai kwanini nimekuwa mjinga kiasi hiki!! Kwanini niliogopa vitisho vya shangazi, kwani wao ndio maisha yangu? Kwakweli nimekuwa mjinga sana”Alijilaumua mno kwa jambo lile lililotokea, kwani angekataa mapema basi lile jambo hata lisingemkuta.Muda kidogo mama Angel aliingia chumbani kwa Vaileth na kumkuta akimalizia kujiandaa basi alimkalisha chini na kuanza kuongea nae,“Hivi Vai unajua kuwa nilikuamini sana, kiasi cha kukuachia nyumba yangu, watoto wangu na pesa zangu, yani huoni ni imani gani niliyokuwa nayo juu yako! Hivi kwanini ukataka kunifanyia hivi! Ni kwanini umtake mume wangu? Je unajua ni wapi tulipotokea, unajua ni kwanini tuko pamoja hadi leo?”“Nisamehe sana mama, kwakweli halikuwa lengo langu kufanya hivi na hata sikutaka na wala nisingefanya hivi”“Kwahiyo ulikuwa na lengo gani? Na kwanini kutuletea dawa ndani?”“Mama, nitakueleza kila kitu cha kweli kabisa wala sitakuficha chochote kile, na sijui kama utanielewa”“Haya nieleze”Basi Vaileth ni kweli aliamua kumueleza kila kitu tangu siku ambayo Prisca alifika pale na alivyomwambia na jinsi alivyoitwa na shangazi yake na kupelekwa kwa mganga wa kienyeji na jinsi alivyofika na dawa na kukamatwa na wakina Erica, na jinsi Prisca alivyofika tena na kuleta hizo dawa nyingine na dawa nyingine kumwaga kwenye mlango wao wa kuingilia chumbani huku akimsisitiza kuwa nyingine akamwage kwenye geti lao la kuingilia,“Kiukweli mama sikuzitaka hizi dawa, na niliweka mezani ili niweze kwenda kuzimwaga, ila sijui nimejisahau na nini. Nisamehe sana mama yangu, naomba msamaha, sitorudia mimi. Naomba msamaha”Mama Angel alipumua kwanza wala hakuwa na jibu kwa muda huo kisha alimwambia Vaileth,“Subiri basi, tutaongea badae”Ila kabla mama Angel hajainuka, simu ya Vaileth iliita na aliamua kupokea basi mama Angel aliamua kukaa ili asikilizie vizuri, na vaileth alipokea ile simu na aliweka sauti kubwa kabisa kwani mpigaji alikuwa ni shangazi yake,“Wewe mjinga, vipi ushafanya hizo dawa?”“Hapana shangazi, nilishakataa kwa Prisca haya mambo sitaki”“Hebu mtoto acha ujinga wewe, hivi akili zako zikoje kwani? Unafikiria kwa kutumia makalio au nini? Mara ya kwanza umetupa hizo dawa kwa makusudi kabisa, na sasa Prisca kakuletea unasema hutaki kuzifanya, hivi mtoto una laana gani wewe?”“Shangazi, mimi ni heri nife na umasikini wangu ila kama nilivyokwambia siwezi kufanya haya mambo na hizo dawa zenu nimeenda kuzimwaga. Sitaki kabisa hayo mambo yenu”“Wewe mtoto wewe loh! Nilikwambia usipofanya hizo dawa sahau kuhusu undugu wetu yani hata ukiumwa usitushirikishe”“Sawa shangazi ila mimi siwezi kufanya hizo dawa”“Hivi una nini lakini wewe mtoto? Hivi unaona raha kwa ndugu zako kua na umasikini eeeh! Naomba uje huku Jumamosi”“Kwa jambo kama hilo shangazi siji”“Wewe mtoto usinitanie ujue, kesho nakuja huko na Prisca”Kisha shangazi akakata simu kwa hasira yani ilionekana amechukizwa sana na majibu ya Vaileth, basi mama Angel alimuangalia kwa muda Vaileth kisha akamuomba simu yake ambapo Vaileth alimpatia halafu mama Angel aliondoka nayo.Basi Erica alimfata Erick na kuongea nae kuhusu jambo lile ambalo limetokea siku ile, basi alianza kuongea nae,“Kaka, je nimefanya vibaya nilivyofanya vile?”“Hapana hujafanya vibaya”“Kwahiyo umenielewa? Sipendi kukukera kaka yangu ujue”“Naelewa hilo dada yangu, kwahiyo hata usijali”Basi Erica alifurahi na kuondoka zake kuelekea chumbani kwake, ila alipokuwa chumbani kwake akakumbuka jambo toka kwa kaka yake hivyo basi akaenda tena na kufungua mlango wa chumbani kwa kaka yake, kwakweli alipofungua mlango alikuta kaka yake akiwa kajilaza kitandani yani alikuwa mtupu kabisa kwamaana hiyo Erick alivua nguo zote na kujilaza, kwakweli Erica alishtuka sana na leo alitoka nje kwa uoga kabisa kwani hata aliogopa tena kuingia chumbani kwa kaka yake, kisha akarudi zake haraka haraka chumbani kwake huku akijiuliza kwanini alienda kwa kaka yake bila hodi, basi baada ya muda mfupi Erick nae alienda chumbani kwa Erica huku akicheka na kumwambia Erica,“Usijali dada yangu, usijali kitu. Fanya kama hujaona chochote kile”“Mmmh nimeogopa”“Sasa umeogopa nini jamani!!”“Aaaah hamna kitu”“Fanya kama hujaona chochote dada yangu, usiku mwema”Halafu Erick alitoka mule chumbani na kurudi zake chumbani kwake.Yani Erica alikuwa akiwaza sana na kujiuliza kuwa kwanini aliingia kwa kaka yake siku hiyo bila hodi kwani maumbile ya kaka yake yalianza kutembea kichwani mwake, wakati alishawahi kumuona akitoka kuoga ila siku hiyo ikawa tofauti sana kwani aliona maumbile ya kaka yake yakitembea tu muda wote kwenye akili yake.Yani siku ile mama Angel alilala akiwa na mawazo sana, yani hakuelewa kuwa ni kitu gani afanye kwa Vaileth yani hakuelewa kabisa.Basi palivyokucha, baba Angel aliongea kidogo na mke wake kabla ya kuondoka ambapo mkewe alimuuliza,“Sasa mume wangu tutafanya nini na hili swala la Vaileth? Je tumfukuze au?”“Mke wangu kwakweli nakuachia wewe mwenyewe, yani wewe ndio utaamua kuwa ni kitu gani kifanyike”“Sawa mume wangu”“Najua una busara sana mke wangu na utajua ni kitu gani kifanyike”Basi baba Angel alijiandaa vizuri kabisa kisha alimuaga mke wake na kuondoka maana mama Angel siku hiyo alisema kuwa atabaki nyumbani tu.Basi kabla mama Angel hjaenda kufanya shughuli nyingine au kuongea na Vaileth alisikia kuna ujumbe umeingia kwenye simu ya Vaileth basi aliichukua na kusoma ule ujumbe aliona jina ni Prisca, kwahiyo ulitoka kwa Prisca,“Yani Nyanda umefanya shangazi apatwe na presha kabisa sababu ya ujinga wako, na badae nakuja na shangazi hapo nyumbani kwenu. Tutafanya dawa kwa nusu saa tu, halafu tutaondoka. Kwahiyo wewe usishughulike tena na chochote kile, mambo yote tutayanya wenyewe”Basi mama Angel aliandika ujumbe kumjibu Prisca,“Haya karibuni”Halafu aliondoka kwenda kuongea na Vaileth ambapo alipofika tu kule alimwambia Vaileth ajiandae ili aende nae sehemu basi Vaileth hakukataa kufanya vile kwani muda ule ule alienda kujiandaa na baada ya hapo aliondoka akiwa ameongozana na mama Angel.Angel akiwa shuleni, kwasasa aliweza kwa kiasi kikubwa sana kuzuia hisia zake kwa Samir kwani muda mwingi aliutumia kwaajili ya masomo yake na alikuwa wala hahangaiki kumsalimia Samir ukizingatia alihisi kuwa Samir ana mahusiano na madam Hawa kutokana na ile tabia ya madam Hawa aliyokuwa akiifanya ya kumuita Samir kila muda.Basi alikaa akijisomea siku hiyo ila alishangaa sana alipoitwa na madam Hawa, kwakweli aliinuka kwa uoga flani ila alienda na kumfata yule madam mpaka ofisini ambapo yule madam alimuuliza,“Angel, unayaonaje maisha ya hii shule?”“Yapo vizuri tu, nishazoea kwasasa”“Na vipi wanafunzi unawaonaje?”“Nawaona wapo vizuri tu madam”“Na vipi kuhusu Samir?”Angel alishtuka kidogo na kukaa kimya bila ya kujibu hilo swali ambapo madam Hawa alimuuliza tena,“Mbona hunijibu Angel? Vipi kuhusu Samir?”“Sijakuelewa madam, kuhusu Samir kivipi?”“Aaaah yani unamuonaje Samir darasani?”“Namuona kama mwanafunzi mwenzangu na kama kaka yangu”“Vizuri sana, hivyo ndio maisha ya shule yanavyotakiwa yawe, unatakiwa kumuona hivyo Samir na si vinginevyo ila nikisikia kuwa kuna hata chembe za mapenzi kati yako na Samir yani nitakushulikia mwenyewe yani sitasubiri mzazi wako wala nini, umenielewa”“Nimekuelewa madam”“Nahitaji usome kwa bidii na mwisho wa siku ufaulu vizuri, si unajua mnakaribia kufanya mitihani ya taifa?”“Naelewa hilo madam”“Sawa, na usome kwa bidii sasa”Angel alimuitikia madam kisha aliruhusiwa kurudi darasani na kuendelea na masomo yake.Mama Angel na Vaileth walikuwa mahali ambapo hata Vaileth hakuelewa ni kwanini wapo mahali hapo na wala hapakuwa mbali na nyumbani kwao, baada ya muda ujumbe uliingia kwenye simu ya Vaileth,“Tumeshafika, tupo hapa getini”Basi nae akajibu,“Nisubirini hapohapo”Na muda kidogo akamwambia Vaileth kuwa warudi nyumbani, kiukweli Vaileth hakuwa akielewa chochote kila, na muda ule ule waliondoka hadi pale kwake ambapo nje ya geti waliwakuta shangazi wa Vaileth pamoja na Prisca, basi mama Angel pamoja na vaileth walisogea pale ambapo mama Angel aliwasalimia kwanza ila Vaileth alikaa kimya tu kwani hakuelewa kuwa ni kitu gani ambacho mama Angel alitaka kukitenda kisha mama Angel alimwambia mlinzi afungue geti halafu waliingia ambapo aliwakaribisha wale wageni yani nao walikuwa wakiingia kwa uoga uoga sana, alifika nao kwenye kibaraza na kukaa nao kisha alianza kuwauliza,“Samahanini jamani, kwani mimi nina kasoro gani kukaa ndani ya nyumba hii?”Walikaa kimya tu kwani hata hawakuelewa, halafu akawauliza tena,“Kwani Vai akishampata mume wangu basi nyie mtafaidika na nini? Mnajua mimi na mume wangu tumetoka wapi? Mnajua hii nyumba tumeijenga vipi? Unajua kuna kipindi nilikuwa nawaona wasichana wa kazi ni wabaya sana ila nimegundua kuwa kuna wengine sio wabaya ila wanapata ushawishi toka kwa ndugu zao, hivi mkishavunja undugu na Vaileth ndio mnapata faida gani?”Walikaa kimya na kuona aibu sana, basi Prisca aliona jambo jema ni kuomba msamaha tu kwa wakati huo kwani alihisi kuwa wameshaumbuka,“Naomba dada utusamehe”Ila shangazi alidakia na kujifanya hajui kosa lao,“Kwani msamaha Prisca unaomba kwa kosa gani?”Prisca alikaa kimya kisha mama Angel alisema tena,“Yani wewe shangazi mtu ndio huna hata aibu wakati wewe ndio kuongoza wenzio kiguu na njia kwenda kwa waganga wa kienyeji, kama ulikosea maisha ni wewe ujue! Yani kama ulikosea na kuolewa na mwanaume asiyejielewa ni wewe, usitake kwenye maisha wote tufanane, ndiomana kuna wasichana wa kazi, kuna wakulima, kuna manesi, kuna madereva, kuna makonda, kuna wabeba zage yani kila mtu na karama zake katika haya maisha yani unatakiwa kuwa makini sana kwa unayoyafikiria kuyafanya. Je ulidhani utapata faida gani ikiwa mimi nimemkamata Vaileth akiweka dawa? Na nikimfukuza huyu Vaileth utakuwa umeupata huo utajiri? Yani ni mtu mzima lakini huna akili hata moja”Kiukweli shangazi aliona aibu sana kiasi kwamba aliinuka na kuanza kuondoka ila mama Angel alimvuta kwa nyuma na kumwambia,“Mbona una kiburi sana wewe shangazi, hivi unajua kama hapa ni nyumbani kwangu?”Basi yule shangazi kwa aibu kubwa alisema,“Naomba nisamehe, naomba pia uniruhusu niende”Basi mama Angel alimuangalia ambapo yule shangazi alitoka halafu Prisca alimfata nyumba, kisha yeye na Vaileth walirudi ndani kwao.Erica leo shuleni alimuhadithia Elly kuhusu kila kitu kilichotokea jana yake nyumbani kwao kuhusu yule dada yao wa kazi, basi Elly akamuuliza,“Kwahiyo wazazi wako wamechukua uamuzi gani?”“Mmmh hata sijui kuwa wameamuaje ila chochote watakachoamua ni sawa tu kwani mimi nishawaambia ukweli wa mambo yote ulivyo”“Sawa, umefanya vizuri sana, ila leo mama yangu kaniuliza kuhusu dada yako Angel na kaka yako Erick, eti wanaendeleaje?”“Wanaendelea vizuri tu, kwani mama yako anamfahamu dada Angel na Erick?”“Sijui ila aliniuliza hivyo ila nadhani anawafahamu”“Sasa anawafahamu vipi?”“Mbona hata wewe anakufahamu!”Yani Erica alishangaa sana na kusema,“Mimi atakuwa ananifahamu kwa jina”“Hadi kwa sura, mama yangu anakufahamu”“Kwakweli Erica alishangaa mno kusikia mama yake Elly anamfahamu vizuri sana yeye, ila aliacha kuendelea kuuliza maswali zaidi na moja kwa moja walirudi darasani.Muda wa kutoka ulipofika, kila mmoja aliondoka zake ila na laeo Abdi alimfata Erica na kumwambia,“Jana nimeongea kidogo na baba na kaniambia kuwa katika maisha yake hakuna mwanamke aliyewahi kumpenda kama mama yako, hebu mwambie mama yako amuhurumie baba yangu hata aongee nae kidogo kwani atakuwa amemfariji”“Hivi Abdi huwa unaongelea vitu gani?”“Naongelea kuhusu mapenzi, baba yangu hajawahi kupenda kama alivyompenda mama yako kwa maana hiyo hata mama yetu wa sasa baba hampendi wala nini kwani upendo wake wote upo kwa mama yako”Kwakweli Erica alimuangalia tu na kuondoka zake, kwani alienda kupanda gari na walielekea nyumbani kama kawaida.Ila leo Erica alivyofika nyumbani kwao tu moja kwa moja aliamua kwenda chumbani kwa mama yake, aligonga na kumkuta ndani ambapo mama yake alimkaribisha yani hakuvua hata sare za shule, baada ya kumsalimia mama yake alianza kumuuliza,“Eti mama, wewe na baba Abdi kuna nini kiliendelea kati yenu?”“Unauliza nini wewe? Umeanza kukosa adabu eeeh!”Basi Erica alimuomba msamaha mama yake na kuanza kumuelezea vile alivyokuwa akiambiwa na Abdi,“Kheee na wewe unakosa adabu kama huyo Abdi? Mtu alitaka kukubaka, unawezaje tena kukaa chini na kuongea nae?”“Huwa sikai nae mama, ila huwa ananifata muda wa kutoka”“Hebu niondolee ujinga wako, na siku nyingine ukija kuniuliza maswali ya kijinga namna hiyo basi nitachukua jukumu la kukutandika, mjinga wewe. Si bora uongee na Elly tu ingawa mama yake hataki kufahamika nasi”Basi Erica alimuomba msamaha mama yake na kuanza kumueleza habari za Elly yani jinsi mama yake alivyowasalimia Angel na Erick,“Kheee amewajuaje?”“Hata mimi nashangaa, tena Elly anasema sio kwa majina tu bali anawafahamu hadi kwa sura”“Kheee jamani, inamaana huyo mamake Elly anatufahamu vizuri sana?”“Nasikia hadi mimi ananifahamu vizuri mama na sijawahi kumuona kwakweli”“Mmmh mbona Napata mshangao hapa”“Ndio hivyo mama, hata mimi nimeshangaa pia”“Haya, nenda kavue hizo sare za shule ule chakula na ukajisomee”Basi Erica alitoka mule chumbani kwa mama yake ila mama yake alibaki na maswali mengi sana akijiuliza kuhusu mama Elly maana inaonyesha ni mtu ambaye anaifahamu familia yake vilivyo, akajiuliza sana kuwa je mama Elly ni nani? Hakupata jibu kwakweli.Baba Angel aliporudi leo usiku aliamua kwanza kumueleza kile kilichotokea siku hiyo kuhusu ndugu wa Vaileth na kile alichokifanya, mumewe akamuuliza,“Kwahiyo Vaileth humfukuzi tena?”“Simfukuzi kwanza ila nipo kwenye kumchunguza kwa karibu sana, kuna mambo nahitaji kujifunza”“Sasa, utamchunguzaje?”“Mume wangu, wewe usijali niachie kuhusu hili”Kisha alianza kumueleza jinsi Erica alivyomsimulia kuhusu mama yake Elly, kwakweli baba Angel alishangaa pia ila mkewe alimuuliza,“Au mama Elly aliwahi kuwa mwanamke wako? Elly sio mwanao kweli?”“Jamani mke wangu umeanzaje kunihisi hivyo jamani! Yule Elly si rika moja na wakina Erica, mimi sikuwa tena na mambo ya wanawake toka kipindi nimeanza kumlea Angel jamani, kwahiyo Elly hawezi kuwa mwanangu”“Sasa kwanini inakuwa hivi! Kumbuka mamake Elly hataki nimfahamu halafu familia yangu yote anaifahamu si ndio mwanzo wa kuripuliwa njiani bila kujua maana bora adui ujue kuliko adui akujue wewe halafu wewe humjui”“Unamaanisha kuwa mamake Elly ni adui yetu?”“Ndio, kwanza hebu kumbuka vile visheti. Kwanini ulipokula ilikuwa vile ni mpaka nilipoingia kwenye maombi! Kwakweli sina imani na mama yake Elly, nahisi ni adui yangu na familia yangu”“Basi mke wangu ngoja tuukate mzizi wa fitina, ile shule tulimuhamisha Erick, tukamuhamisha Angel na kwanini tusimuhamishe Erica? Ukizingatia kwanza kuna wanafunzi wabaya ambao walitaka kumbaka Erica wetu halafu sisi kama wazazi tumetulia tu yani hatujachukua hatua yoyote ile, hivi mfano Erica angebakwa ingekuwaje? Pili kuna mwanafunzi ambaye mzazi wake anafatilia maisha yetu na kama unavyomjua Erica ni mropokaji, basi mambo ya nyumba yetu yote anayamwaga kwa Elly, kwahiyo inakuwa rahisi kwa huyo mamake Elly kutufahamu kiundani zaidi. Naona ni vyema tukimuhamisha shule Erica”“Sasa tutampeleka shule gani?”“Ngoja, nitaongea na Erick na tutajua shule ya kumpeleka Erica, wala usiumie kichwa mke wangu sababu ya mambo madogo kama hayo, hapo ni kumuhamisha mtoto shule tu”“Sawa mume wangu nimekuelewa”Basi mama Angel alikubaliana na mume wake kuhusu kumuhamisha Angel shule aliyokuwa akisoma ili kumuepuka huyo Elly.Leo Samir akiwa nyumbani alimuona mama yake akiwa nyumbani pia basi alimuuliza,“Vipi mama, leo huendi kazini?”“Zamu yangu ni kesho asubuhi”“Mmmmh!”“Sasa mbona umeguna?”“Na baba nae yuko wapi?”“Hivi wewe mtoto kwani maisha yangu mimi na ya baba yako yanakuhusu nini? Mbona unakilanga wewe?”“Mmmh msms, leo wakati nimetoka shule nilikutana na mtu njiani alikuwa akiongea ongea na kusema anamtafuta sana baba yake, baada ya kumpeleleza niligundua kuwa baba yake ndio huyu huyu baba yetu wa hapa nyumbani. Jamani mama kwa huyu baba tupo wengi sana yani ingekuwa ni uwezo wangu basi ningejibadilishia baba”“Una laana wewe, unakula bure, unalala bure, unaenda chooni bure, hulipii maji wala umeme nab ado unafanya madudu shuleni ila tunatumia gharama zetu kukuhamisha shule, sasa badala ukazanie masomo umebaki tu kusema humtaki baba huyu. Yani umtake au usimtake ndio tayari mume wangu mimi, ndio tayari ni baba yenu hata awe na watoto kila mtaa ila ndio baba yenu, umeona watoto wake wanaishi hapa? Ukimkuta tena mtoto wake mwambie aende kwa bibi yao maana bibi yao bado mzima na mwenye afya na nguvu kwahiyo analeaga tu wajukuu. Ujinga sitaki Samir”Mama yake alionekana kachukia sanakwani muda huo huo aliondoka zake na kwenda kulala na kumuacha Samir akiendelea kuongea swala lake la kubadilishiwa baba.Siku hiyo, mama Angel aliamua kwenda hospitali ili kuangalia kama tayari amenasa au bado na kama bado ajue kuwa atumie chakula gani kwani alitamani amfurahishe mume wake kwa kupata mimba tena na kumzalia watoto.Basi alifika hospitali na kwenda moja kwa moja kwa dokta Maimuna ambaye alimuandikia vipimo na kwenda kupima kisha alifika na kusomewa majibu,“Oooh hongera sana mama Angel, tayari wewe ni mjamzito”Mama Angel alifurahi sana na kujua mumewe lazima atafurahi zaidi, kisha akamwambia daktari,“Basi niandikie vyakula vya kula kuanzia kipindi hiki, nataka mimba yangu hii niwe nayo katika hali salama kabisa”daktari alitabasamu na mara simu ya daktari iliita basi aliomba samahani kidogo kwa mama Angel na kuanza kuongea na ile simu, alipomaliza alimwambia mama Angel,“Oooh leo mume wangu kaamua kunitembelea hospitali, ni vyema sana ukamfahamu”“Sawa, itakuwa ni vizuri sana”Basi dokta Maimuna akampigia simu mumewe na kumtaka moja kwa moja aingie ofisini kwake ili amtambulishe pia kwa rafiki yake mama Angel.Baada ya muda kidogo mlango wa ofisi ya dokta Maimuna ulifunguliwa na aliingia mume wa dokta Maimuna, kwakweli mama Angel alishangaa sana na kutoa macho kwa yule mume wa dokta Maimuna kwani ni mtu aliyemfahamu sana.Baada ya muda kidogo mlango wa ofisi ya dokta Maimuna ulifunguliwa na aliingia mume wa dokta Maimuna, kwakweli mama Angel alishangaa sana na kutoa macho kwa yule mume wa dokta Maimuna kwani ni mtu aliyemfahamu sana.Ila dokta Maimuna wala hakuangalia mshangao wa mama Angel zaidi zaidi alimtambulisha mumewe kwa mama Angel,“Oooh mama Angel, huyu ni mume wangu anaitwa Rahim. Mume wangu, huyu ni mteja wangu nan i rafiki yangu anaitwa mama Angel”Kwakweli mume wa dokta Maimuna alitumia kama dakika tano kujibu na vile vile kwa mama Angel alishindwa hata kusema neno, basi yule mume wa dokta Maimuna akanyoosha mkono wake ili kumsalimia mama Angel huku akisema,“Nafurahi kukufahamu”Ila mama Angel hakunyoosha mkono wake wala nini, badala yake aliinuka na kutoka pale ofisini na kuondoka, kwakweli dokta maimuna alikuwa akishangaa tu ile hali maana hakuielewa.Basi mama Angel moja kwa moja alienda kwenye gari yake na kuondoa gari huku akiwaza vitu vingi sana, akakumbuka kuwa hapo hospitali alishawahi kukutana na mtu mwingine aliyefahamiana nae, na mtu huyo alisema kuwa kuna shemeji yake pale hospitali kwahiyo alipata picha kamili, basi alianza kujiuliza,“Inamaana dokta Maimuna kaolewa na Rahim? Vipi kuhusu mke wa Rahim imekuwaje? Mmmh mwanaume msumbufu yule, sidhani kama nitarudi tena kwenye hii hospitali hata kama dokta Maimuna amekuwa dokta wangu wa kipindi kirefu sana”Basi mama Angel aliamua muda huo kurudi nyumbani kwake tu huku akiwa na mawazo mengi sana.Ilikuwa ni jioni wakati baba Angel ametoka kazini ila alimchukua mwanae Erick na kutoka nae, kuna duka lake alihitaji kumuonyesha, yani hakuingia hata ndani ila alivyomuona Erick tu aliondoka nae.Walifika mpaka kwenye hilo duka na kumuonyesha mwanae,“Eeeeh mwanangu, unasemaje kuhusu hili duka?”“Lipo vizuri sana baba”“Nataka Jumatatu lianze kufanya kazi, si unajua maisha yangu mimi ni biashara yani sina maisha mengine zaidi ya biashara”“Naelewa baba”“Naamini biashara zangu utazifanya vyema, Angel anafahamu biashara zangu nyingi sana”“Ila baba, naomba nikuulize swali?”“Niulize”“Mbona dada Angel ana nywele kama za kiarabu?”“Mmmh wewe mtoto wewe, yule Angel kafata nywele za marehemu bibi yangu”“Aaaah sawa”Kisha baba Angel alienda mahali na Erick kisha alimuuliza,“Nataka kumuhamisha Erica shule, nimuhamishie shule gani?”“Oooh baba, mimi naona ni vyema ukimpeleka shule ya wasichana tupu”“Ooooh kwanini?”“Sababu huko hatokutana tena na wakina Abdi”Yani mtu pekee ambaye Erick hakumpenda katika maisha ya dada yake ni Abdi tu, basi baba yake aliafiki swala la kumpeleka Erica shule ya wasichana, kisha baada ya maongezi hayo waliamua kuondoka pale na ilikuwa ni usiku tayari.Wakati wanaondoka, wakiwa njiani baba Angel alimuona mtu ambaye alikuwa akimfahamu basi alimpigia honi na mtu huyo akageuka, basi baba Angel alishusha kioo ila yule mtu baada ya kumuona baba Angel alikimbia sana hata yeye mwenyewe hakuelewa ni kwanini alikimbia basi ilibidi tu arudi nyumbani kwake.Walipokuwa nyumbani, mama Angel aliamua kumuuliza mumewe kuwa alienda wapi na Erick,“Ulienda wapi na Erick?”“Nilienda kumuonyesha duka letu jipya”“Umeanza ubaguzi eeeh!”“Kivipi jamani mke wangu?”“Kumbuka ahadi yako, kila biashara utaanza kumuonyesha kwanza Angel? Na kwanini uende na Erick tu na kumuacha Erica?”“Unajua mke wangu kuna muda huwa sikuelewa kabisa kuwa unataka kitu gani, yani huwa sikuelewi mke wangu, sasa hapo kosa langu ni nini? Yani kipi nimekosea, kuonyesha biashara kwa Erick? Kwani Erick sio mtoto wetu? Hebu niambie kwanza maana wewe ndio mama”“Sasa ndio maneno gani hayo? Unamaana mimi nilichepuka?”“Sina maana hiyo mke wangu, hebu jaribu kunielewesha, kuwa katika nyumba hii na katika watoto wetu natakiwa kufanya nini na nini? Na kitu gani sitakiwi kufanya kwa watoto wetu? Au nikifanya kitu gani kwa mtoto huyu basi kwa mtoto huyu nisifanye?”“Hapana sijasema hivyo ila umeanza kumpendelea Erick sababu ndio mwanaume mwenzio”“Sasa nilivyokuwa nampendelea Angel kuna sababu gani katikati? Unajua mama Angel mara nyingine uwe unafikiria kabla ya kuongea”“Kwahiyo mimi ni mjinga eeeh!”“Oooh usikuze mambo mama, nakupenda sana”Basi mama Angel alitabasamu kwani alipoambiwa nakupenda sana na mumewe alikuwa akijihisi rah asana kwenye moyo wake, na hapo alianza kumwelize swala la kwamba yeye ni mjamzito, kwakweli baba Angel alifurahi sana baada ya kusikia mkewe ni mjamzito kwani kitu kile alikuwa akikitamani kwa muda mrefu sana, basi alimwambia,“Najua na hapo utanipatia mapacha tu”Mama Angel alitabasamu na kusema,“Eeeeh tutawaita wakina nani?”“Mke wangu, tutatoa tu majina hakuna wasiwasi wowote ule, ila hao ni mapacha lazima”Basi mama Angel muda huo alikuwa na furaha sana.Erick moja kwa moja alienda kwa Erica na alimueleza sehemu ambayo walienda na baba yao, kiukweli Erica hakuwa hata na haja ya kuzungukia biashara za baba yake kiasi cha kumfanya asione wivu wanapomwambia kuwa walienda kwenye biashara ndiomana hata baba yake alikuwa hamchukui mara nyingi kumpeleka kwenye biashara zake, basi Erica alibaki tu kumpongeza kaka yake,“Hongera sana kaka, naamini biashara za baba utazisimamia vizuri”“Ila leo nimemuuliza baba, kuwa mbona dada Angel ana nywele za kiarabu wakati mimi na wewe tuna nywele za kawaida?”“Eeeeh akasemaje?”“Akasema kuwa dada Angel kafanana na marehemu bibi yake”“Jamani huyo bibi na mimi si angenirithisha zile nywele, nazitamani ujue, ona nywele zangu zilivyo kama nywele za mama”Basi Erick alicheka na kumwambia,“Ila hivyo hivyo na nywele zako unapendeza, unajua wewe unafanana sana na mama. Yani nahisi mama kakulandisha kila kitu”“Hapana sio kila kitu maana mimi sina kisirani kama mama”Walianza kucheka ila mama yao aliingia kule chumbani na kuwafokea,“Mnasemaje nyie, mimi nina kisirani?”Erica na Erick walikaa kimya tu, kisha mama yao akawaambia,“Haya, twendeni mkale nyie wajinga, waone vile”Basi wakainuka na kufatana na mama yao kwenda kula kwanza.Angel leo baada ya kula chakula cha usiku, alimfata shangazi yake na kuanza kuongea nae,“Asante sana shangazi, nakupenda sana”“Nakupenda pia mwanangu, ila hiyo asante ya nini?”“Umenisaidia sana shangazi, yani kwasasa nimejikuta napenda kusoma kuliko kitu chochote”“Ooooh hiko ndio nilichokuwa nakitaka, haya mwanangu nenda ukapumzike eeh!”Basi Angel aliondoka zke, leo na mjombawake alikuwepo yani mume wa Tumaini ambaye alifurahi sana kuona vile basi alimfata mke wake na kumkumbatia kisha akambusu na kumwambia,“Nakupenda sana, kwa hakika watu wangekuwa na moyo kama wako basi kusingekuwa na unyanyasaji”“Kwanini?”“Unajua siku narudi na kukuta Angel yuko hapa nilijiuliza sana kuwa anaishije na wewe, ila kila siku naangalia maisha ambayo Angel anaishi na wewe, kwakweli mke wangu unastahili pongezi na unastahili sifa”“Sasa jamani mimi nimchukie Angel nipate faida gani?”“Najua unaelewa kuwa ni kitu gani ninachoongelea mke wangu, basi twende tukalale tu”Tumaini akatabasamu na moja kwa moja kwenda na mume wake kulala.Leo ilikuwa ni siku ya Jumamosi, mume wa Tumaini alimwambia mke wake kuwa anahitaji kwenda nae katika matembezi, basi Tumaini alijiandaa kisha jioni ya siku hiyo alitoka na mume wake.Ambapo mume wake moja kwa moja alimpeleka ufukweni, kwakweli katika maisha yao ya ndoa basi hawakuwa na harakati hata mara moja za kwenda ufukweni kwahiyo ilikuwa ni mara ya kwanza, basi Tumaini akamuuliza mumewe,“Umenileta huku kufanya nini?”“Kwahiyo ulivyosikia tunaenda kutembea ulijua ni wapi?”“Yani mimi nilijua kuwa labda tutaenda hotelini sijui wapi wapi yani sikuwa na wazo kuwa tutakuja huku”“Kwahiyo huku hujapapenda mke wangu?”Kabla Tumaini hajajibu swali hilo, alikuja mtu na kumziba macho huku akimwambia,“Otea mimi ni nani?”Mume wa Tumaini alikuwa akicheka tu kwani alijua itakuwa huyo mtu anafahamiana na mke wake, na hakuwa na mashaka nae kwani alikuwa ni mwanamke, basi Tumaini akajaribu kufikiria na kukosajibu kabisa, kisha akamwambia,“Dah! Nimeshindwa kuotea”basi yule mtu alimuachilia Tumaini mikono huku akicheka sana, kwakweli Tumaini alifurahi kumuona kwani alikuwa ni rafiki yake wa muda mreu ila alitengana nae kwa kipindi sababu walikuwa na matatizo nae kidogo,“Oooh jamani Sia, hata siamini kuwa ni wewe!”“Ni mimi Tumaini, umeanza kupenda lini kuja ufukweni?”“Aaaah ni shemeji yak oleo ndio kaamua anitoe ushamba kidogo”Basi Sia alimuangalia mume wa Tumaini na kumsalimia pale kisha akamwambia,“Unajua toka kipindi cha harusi yenu sijaonana nanyi tena!”“Eeeeh vipi na wewe upo ufukweni na nani?”“Niwe na nani mwenzangu? Nipo mwenyewe”“Kheee mumeo yule yuko wapi?”“Mmmmh yule mwenzangu aliota mapembe, yani nilijuta kumfahamu kitu alichonifanyia yule ni Mungu pekee anajua, sitaki hata kumuona”“Na kipindi kile ulikuwa una mimba, mtoto je upo nae au yupo nae?”“Oooh mtoto ninae mwenyewe, ila tuachane na habari za mtoto ila tuongelee mambo ya maana. Vipi kaka yako na mkewe?”“Mmmh sijui, sijawasiliana nao muda sana”“Basi naomba mawasiliano yako”Kisha Tumaini akabadilishana mawasiliano na Sia halafu Sia alimuaga Tumaini na kuondoka zake, basi mume wa Tumaini akasema,“Hivi huyu si ndio alikuwa akimtaka mdogo wako huyu kipindi kile? Hadi alitaka kuharibu ndoa yao si ndio huyu!”“Ndio ni yeye, ila alibadilika”“Mmmmh sijui mke wangu, ila ukweli anaujua yeye mwenyewe”Basi walikaa kaa kidogo ambapo Tumaini alidai kuwa warudi nyumbani tu, basi wakarudi nyumbani.Leo baba Angel alikuwa nyumbani kwake, muda huo alikuwa kwenye kile chumba cha kujisomea huku akisoma magazeti yake, mara akapigiwa simu na dada yake,“Mmmh otea leo nimeonana na nani?”“Jamani mimi nitajuaje sasa mtu uliyeonana nae wewe?”“Aaaah na wewe hata hutaki kujaribu kuotea, nimeonana na Sia”“Kheee Sia?”“Ndio, na nimeongea nae mengi sana”“Ooooh alikuwa anasemaje sasa? Unajua jana pia nikiwa njiani nilimuona mtu kama yeye, halafu nina uhakika alikuwa ni yeye ila nilipompigia honi akageuka nami nikashusha kioo cha gari jamani toka hapo alitembea haraka na kunipotea, sijui bado ana kisirani na mimi?”“Hapana bhana, sidhani kasema tu nikusalimie wewe na mkeo”“Oooh sawa”Basi wakaongea pia kuhusu maendelea ya Angel na kuagana, ambapo baba Angel alikata ile simu na muda huo huo mama Angel aliingia mule kwenye kile chumba na kumuuliza mumewe,“Ulikuwa unaongea na nani?”“Na Tumaini, alikuwa akinipa habari za Angel”“Oooh nishamkumbuka mwanangu, sijui lini niende nikamuone jamani?”“Unaonaje tukienda kesho baada ya kutoka Kanisani?”“Oooh jambo zuri sana hilo, sawa mume wangu basi tutaenda kesho”Basi wakakubaliana kufanya hivyo.Muda wa kulala ulifika na wote walienda kulala ila Erica alienda chumbani kwa kaka yake na kumtaka wacheze karata, basi Erick alikubali kwani anamtindo wa kukubali kila kitu anachoambiwa na Erica, walianza kucheza zile karata huku wakicheka na kufurahi basi erica akamuuliza kaka yake,“Hivi inamaana ukioa ndio mwisho wa mimi na wewe kucheza pamoja?”“Jamani Erica mbona unakuwa huelewi, mimi nilikwambia sitokuja kuoa maishani mwangu”“Kwanini sasa?”“Sababu ninayempenda siwezi kumuoa kamwe”“Nani huyo?”“Unataka kumjua?”“Ndio, nataka sana nimfahamu?”“Basi kesho nitakuonyesha picha yake”“Duh! Hadi picha yake unayo? Kweli unampenda jamani, sikufikiria hilo. Ila kama wewe hutooa basi na mimi sitoolewa wala nini?”“Kwanini sasa?”“Sijui ila nadhani sitaolewa sababu na wewe hutaki kuoa, siku ukioa basi na mimi nitaolewa siku hiyo”Erick alicheka na kumtaka dada yake waendelee kucheza karata na kama kawaida yao walicheza karata sana na kujikuta wamelala hapo hapo.Kulipokucha mama Angel aliamka na kujiandaa yeye pamoja na mumewe kwaajili ya kwenda kanisani ila alishangaa kuona watoto wake bado hawajaamka, basi aliamua kwanza kwenda chumbani kwa Erick ili akamuamshe halafu aende chumbani kwa Erica.Basi alishangaa sana alipoingia chumbani kwa Erick kukuta wamelala pamoja na Erica yani hawana hata habari na zile karata zipo pembeni, kwakweli alisikitika sana na kujisemea,“Ooooh karata tena jamani!”Basi alisogea karibu na kuwashtua ili kuwaamsha,“Nyie wajinga hebu amkeni huko”Erick na Erica walishtuka huku wakijinyoosha na kuwa kama wakishangaa, basi mama yao akaanza kuwasema,“Hivi nyie mmeanza lini ujinga wa kulala pamoja? Hivi unajua kuwa mshakuwa wakubwa nyie?”Baba tyao alisikia mama Angel akiwasema watoto wake na kuamua kwenda ili kuwatetea, ambapo aliuliza kwanza na mkewe alikuwa akimueleza kwa jazba sana basi akamwambia,“Mke wangu, hebu punguza presha, hao ni ndugu sasa ubaya uko wapi wakilala pamoja? Mbona huku uswahili utakuta wazazi wanachumba na sebule tu na watoto wa kutosha na watoto wao wote wanalala chumba kimoja bila kujali jinsia, sembuse hawa? Hebu acha kuwatisha watoto, wamekuwa wakubwa ndio ila acha kuwawekea sababu ya kufanya mengine. Watoto hawa toka wana miaka mitano umekuwa ukiwatenga, je mke wangu unataka kuwajengea nini hawa watoto?”“Baba Angel tafadhali, usinifundishe kulea”“Sikufundishi, ila hata mimi na dada yangu Tumaini mbona tunaishi kawaida tu sababu tumeshazoeana na tunajuana kama ni ndugu”“Usinifundishe kulea tafadhali”“Haya yameisha, haya nyie jiandaeni twende kanisani na leo tukitoka Kanisani basi tunaenda kumuona dada yenu Angel”Erick na Erica walifurahi sana na moja kwa moja walianza kujiandaa kisha wazazi wao nao wakatoka mule chumbani kwa Erick.Wakati Erica akimalizia kujiandaa alishangaa Erick akienda chumbani kwake, basi Erica alimwambia,“Eeeeh Erick, umekuja kuniangalia kama nimemaliza?”“Ndio, maana wewe nawe ukianza hata humalizi. Halafu nimekuletea picha yako”“Picha yangu?”“Ndio”Basi Erick alitoa picha na kumkabidhi Erica, kwakweli Erica alishangaa sana kwani ile picha yake ya muda kidogo, walipiga kwenye mahafali ya darasa la saba, basi akamwambia Erick,“Kumbe picha yangu hii ulikuwa nayo eeeh! Tabia mbaya hiyo, kila siku naitafuta”“Aaaah na mimi nimeiona leo wakati natoa nguo hizi kabatini”“Ila asante sana”Basi Erick aliondoka zake, naye Erica aliendelea kujiandaa na badae alitoka pamoja na wazazi wake kuelekea Kanisani kama ambavyo walikuwa wamepanga.Leo Vaileth akiwa mwenyewe nyumbani, alishangaa tu kumuona Prisca akiwa amefika pale nyumbani kwa mama Angel,“Jamani Prisca, umekuja kufanya nini tena? Mbona hamnitakii mema na kazi yangu hii jamani!”“Sio kwamba hatukutakii mema, ungejua ni muda gani nimekaa hapo nje ya geti lenu nikkisubiri hao mabosi wako waondoke hujui tu, yani walivyoondoka tu na mimi nimekuja, kwakweli Nyanda hatuhitaji kufa kwa umasikini wakati utajiri tunauona”“Mimi nipo tayari kufa masikini ila kuharibu kazi yangu sipo tayari, yani kwa dawa yoyote unayotaka kuifanya sipo tayari. Na leo ningeenda pia Kanisani ila sijisikii vizuri ndiomana wameniacha, kwakweli Prisca naomba uende”“Hapana, mimi siondoki hadi tufanye hizi dawa”“Prisca, nitamuita mlinzi akuondoe yani sina masikhara kabisa kuhusu hilo ndugu yangu. Usinitanie ujue”“Kheee yamekuwa hayo Nyanda?”“Ndio, sitaki ujinga. Nawe katafute kazi halafu ufanye huo ujinga wako”“Yani Nyanda unanijibu hivyo, ujue naweza nikakuharibia hata hii kazi ukaiona chungu!”“Niharibie tu hakuna tatizo”Kisha Vaileth akaenda kumuita mlinzi ili amuondoe Prisca, yani kile kitendo kilimuuma moyo sana Prisca na alisema kuwa ni lazima atalipiza kisasi.Leo wakati Tumaini na familia yake wametoka kanisani wakapata ugeni na mgeni huyo alikuwa ni Derrick, basi Tumaini akamwambia,“Kwanini umekuja bila taarifa?”“Hapa ni kwa ndugu yangu ujue, sasa unataka nitoe taarifa, taarifa gani?”Wakati wakiongea hayo mara mama Angel na familia yake nayo wakafika nyumbani kwa Tumaini, ila Derrick alipomuona mama Angel alionekana kufurahi sana kwani alimkimbilia na kumkumbatia kwa furaha.Wakati wakiongea hayo mara mama Angel na familia yake nayo wakafika nyumbani kwa Tumaini, ila Derrick alipomuona mama Angel alionekana kufurahi sana kwani alimkimbilia na kumkumbatia kwa furaha.Kiukweli mama Angel hakuipenda ile kitu hata kidogo na kujikuta tu akijitoa mikononi mwa Derrick ila Derrick alionekana kutaka kuendelea kumkumbatia ndipo baba Angel alipoamua kumuachanisha Derrick na mkewe huku akisema,“Inatosha sasa”Ila Derrick akasema,“Dah shemeji, una wivu hadi kwa ndugu? Au umesahau kama huyu Erica ni ndugu yangu? Ni dada yangu huyu, baba yetu ni mmoja”Baba Angel hakujibu kitu, basi mama Angel alisogea moja kwa moja kwa wifi yake Tumaini na kumuuliza,“Umeanzaje kumkaribisha huyu?”“Aaah mimi sikuelewa, ila ninachojua ni kuwa ni ndugu yako na sijui kama kuna mengine kati yenu na hata hivyo sijamkaribisha bali amekuja mwenyewe”Muda huo Angel nae alikuja na kuwakumbatia ndugu zake kwa furaha sana kwani ni muda mrefu hajaonana nao.Basi alimfata baba yake sasa na kuanza kuongea nae kwani Angel alimpenda sana baba yake, ni mara nyingi aliongea na baba yake na alijionea vizuri sana kwani baba yake pia alimpenda sana,“Baba nafurahi sana kwani shangazi anakaa vizuri sana na mimi”“Oooh nafurahi kusikia hivyo, ukimaliza shule utaniambia ni wapi unataka kwenda kutembea”“Asante sana baba, nakupenda sana”Basi Angel alikuwa akimkumbatia baba yake kwa furaha hadi Tumaini akasema,“Haya sasa wapendanao wamekutana, maana nahisi Angel ndio roho ya mdogo wangu jamani”Wote walikuwa wakicheka kasoro Derrick aliyeonekana yupo kimya toka muda ule baba Angel amtoe toka mikononi mwa mke wake.Ila alikaa kimya kidogo na kuanza kumwambia Tumaini,“Hey, Tumaini ulimuuliza Erica kuhusu lile swala”“Swala gani?”“Swala la mimba yangu”Mama Angel akaona huyu anataka kumuharibia siku basi akainuka na kumshika mkono halafu akaenda nae nje na kuanza kuongea nae,“Hivi Derrick una nini lakini? Hivi unajua kama ni muda mrefu sana umepita jamani, kwanini upo hivyo hadi leo eeeh!”“Nisamehe ila najua mtoto wangu angekuwa ni mkubwa kushinda huyo Angel”“Hivi wewe umesahau yote yaliyotokea kati yangu na yako? Kwani tulienda kufanya tambiko ili iweje jamani eeeh! Hivi wewe si kaka yangu jamani! Yani natamani marehemu baba angekuwepo na angerekebisha makosa yake, nina uhakika asingeruhusu uzaliwe mjinga wewe, hivi unaacha kufatilia maisha mengine ila unawaza ujinga tu muda wote jamani!!”“Sikia Erica, kipindi naanza na wewe si kwamba nilitaka kukujaribu hapana bali nilikupenda kwa dhati sema ilitokea tu mimi na wewe tukawa ndugu, kweli huwa naumia hadi leo kwani leo hii ni mimi ambaye ningekuwa naishi na wewe na sio huyo kichaa Erick”Mara mume wa mama Angel alitoka nje na kumwambia Derrick na mama Angel,“Jamani, hivi kwanini sieleweki Kiswahili!! Derrick nakuomba umuache mke wangu tafadhali, ni ndugu yako ndio ila sikuamini ndiomana nakwambia uwe mbali na mke wangu”Tumaini nae alitoka na kumshika mkono Derrick ambapo moja kwa moja alitoka nae nje ya geti na kumwambia,“Derrick kwaheri, siwezi Kurusu uharibu amani ya nyumba yangu”Kisha akaingia ndani na kufunga geti halafu akamfata mama Angel na baba Angel na kuwataka warudi tu ndani na waendelee na maongezi kama kawaida.Nyumbani kwa dokta Maimuna, leo alimuuliza mumewe kwa makini kuwa ni kwanini mama Angel alishtuka baada ya kumuona na aliamua kuondoka,“Aaaah yule mwanamke ana kichaa ujue, nafahamiana nae yule”“Unafahamiana nae kivipi?”“Enzi hizo za ujana, niliteleza na kuwa na mahusiano nae, na nikabahatika kuzaa nae mtoto mmoja, yani huyo Angel ni mwanangu mimi”“Kheee kumbe!! Una mtoto mwingine wa kuitwa Angel!! Sasa yeye yuko wapi?”“Yuko nae huko, unajua yule mwanamke ni kichaa yani yeye na mumewe wamejimilikisha mwanangu na kufanya ni mtoto wao, hawataki hata mwanangu anifahamu yani sijui hata wanapoishi”“Kheee hukuwafatilia?”“Sikuwafatilia wapi? Nilijitahidi kwa kadri ya uwezo wangu, na walipokuwa wakiishi mwanzo nilikuwa napafahamu vizuri tu hata nilikuwa naenda kumuangalia mwanangu tena kafanana na mimi balaa, ila sijui vipi wakaamua kuhama pale na kuuza nyumba kabisa ili mimi tu nisijue wanapoishi”“Kwao kabisa na huyo mama Angel unapafahamu? Toka walipohama uliwahi kwenda kwao?”“Kiukweli, kwao kabisa nilikuwa napafahamu ila kwasasa nimepasahau kabisa. Ila naamini kuwa kuna siku yule mtoto atahitaji kunifahamu baba yake wa ukweli na mama yake hatokuwa na jinsi zaidi ya kumleta tu kwangu”“Yani hiyo ndio shida yenu wanaume, huwa mnakimbia majukumu yenu kwa kuamini kuwa mtoto akikua atakutafuta baba yake, unajua mtoto kwa kadri anavyolelewa na mama ndivyo anavyozidi kupandikizwa chuki kuhusu baba yake aliyemtelekeza? Kiasi kwamba hata kukuona tena hatamani! Hivi unajua hilo?”“Aaaah najua mwanangu atanitafuta tu, unajua nimefanana nae!”“Ila kumbuka ni mtoto wa kike, ambavyo amekuwa na kuanza urembo huko kufanana nae kutatokea wapi? Hebu kuwa makini bhana mfatilie mwanao”“Kheee una nini leo Maimuna? Katika maisha ya kufahamu watoto wangu hata mara moja hujawahi kuniambia kuwa nimfatilie mwanangu, na siku zote nikikwambia kuwa akikuwa atanitafuta huwa unakubalianana kauli yangu, mpaka wenyewe wanapelekwaga tu kwa mama yangu kule. Ila huyu Angel imekuwaje? Unamfahamu kwani?”“Simfahamu ila nahitaji umfatilie”“Haya, nimekuelewa mke wangu”Kwakweli dokta Maimuna alishangaa mno akihitaji kufahamu zaidi kuhusu Angel, yani alitamani sana kumuona huyo Angel na kujua kuwa kwa kipindi hiko anafanya nini na anafanana vipi.Leo mama Junior alimkumbuka sana mdogo wake na alihitaji kwenda kumuona ila hakutaka kumtaarifu wala nini, hivyobasi moja kwa moja aliondoka kwake na kuelekea kwa mama Angel bila kujua kuwa mama Angel hayupo wala nini.Basi alivyofika karibu na getini kwa mama Angel alishangaa kumuona mtu kama akimwaga kitu halafu alianza kusota yani kama mtu anayefanya uchawi, kwakweli mama Junior alichukia sana na kumfata yule mtu pale getini kisha alimuinua na kumkunja halafu alimnasa vibao vya kutosha huku akimuuliza,“Nani kakutuma wewe mbwa? Unafanya nini hapa? Unafanya uchawi kwenye nyumba ya mdogo wangu? Haya mambo huwa nayasikia tu, kumbe ni kweli!”Basi mama Junior alimuita mlinzi wa nyumba ile ambapo alitoka nje na yeye alishangaa sana baada ya kuambiwa kile ambacho huyo msichana alichokuwa akifanya, basi akasema,“Hivi wewe si nimetoka kukutimua ndani!! Kumbe umekuja kufanya maovu yako huku nje”Mama Junior nae alishangaa sana na kuuliza,“Kumbe alianzia ndani?”“Ndio, ni ndugu yake na Vaileth huyu”“Khaaa kumbe!! Vaileth, wee Vaileth”Basi Vaileth alienda haraka haraka na kushangaa kukuta Prisca ameshikwa na mama Junior kisha mama Junior alimwambia alichokuwa akifanya ndugu yake huyo, kwakweli Vaileth alishindwa kabisa cha kusema, na muda huo huo mama Junior alimuamuru mlinzi kuwa amfunge kamba yule Prisca mpaka muda ambao wakina mama Angel watakaporudi ili na wao wajionee hayo.Ilipofika jioni,familia ya baba Angel waliaga pale kwa shangazi wa Angel na kuondoka zao, wakiwa kwenye gari Erica aliwauliza wazazi wake,“Mama, kwani yule mbaba tuliyomkuta kwa shangazi ni nani?”“Aaaah yule ni mjomba wenu”“Aaaah sasa mbona inaonekana kama hamumtaki kabisa, maana naona mlikuwa kama mkimfukuza hivi”“Mmmh na wewe, hebu mara nyingine uwe una nyamaza kimya maana kuna mambo hata huwa hayakuhusu”Basi ilibidi Erica akae kimya tu.Walipofika nyumbani walishangaa sana kumkuta Prisca akiwa kibarazani huku kafungwa mikono na miguu, kwakweli mama Angel alishangaa sana na mara dada yake alitoka na kuanza kumueleza mlolongo mzima, kwakweli muda huu baba Angel alichukia pia, na moja kwa moja alienda kumshika Prisca na kuanza kumzaba makofi,“Kwanini unanifanyia ujinga hivi kwenye nyumba yangu? Nadhani hunijui vuzuri wewe”Na muda huo huo baba Angel alipiga simu polisi na muda kidogo walifika maaskari na kumkamata Prisca halafu wakampeleka rumande, yani muda huo Vaileth alikuwa ndani tu, yani pale ndio mtu unaelewa kuwa damu ni nzito, yani alikuwa akimuhurumia sana ndugu yake.Basi mama Junior akasema,“Tena huko rumande wamuweke mwezi mzima, yani nilichomkuta anafanya kwakweli huyu msichana hafai kabisa”“Aaaah wiki tu inamtosha dada”“Kheee unamuonea huruma wakati alitaka kuharibu nyumba yako mwenyewe? Na hata sijajua ni dawa gani ameweka mlangoni jamani!”“Hamna shida, inabidi ndugu yake akafagie”Kisha mama Angel alimuita Vaileth ambaye alitoka chumbani na kumwambia kuwa akafagie eneo lile, basi Vaileth alienda kufagia ila huku akiwa na mawazo sana yani alikuwa akifagia huku machozi yakimtoka.Muda wa kulala, siku hiyo Vaileth alikaa kitandani kwa muda kwanza akitafakari na kujiuliza,“Hivi kwanini umasikini unafanya tudhalilike kiasi hiki!! Yani tunadhalilika sababu ya umasikini, tunahitaji utajiri wa lazima, ndugu yangu Prisca hajataka kabisa kukubaliana na hali halisi kuwa hata mimi nilibambwa, na hata tulibambwa wote pamoja na shangazi ila leo bado kapata ujasiri wa kuja tena kufanya dawa? Hivi kwanini mambo haya lakini, ndugu yangu anateseka rumande jamani sababu ya umasikini”Alijikuta akiinama huku akitokwa na machozi, yani hakuwa na raha kabisa, alijihisi kuumia moyo sana, akakumbuka kipindi wapo kijijini akiwa ameongozana na Prisca huku wakiongea mambo mbalimbali, akakumbuka jinsi walivyoahidiana kufanya kazi kwa bidii ili kupata pesa na kufanya maendeleo ikiwa na kuwasaidia wazazi wao. Kwakweli aliumia sana, ila atafanyaje sasa ikiwa na yeye ile kazi anaihitaji sana kwani hakuwa na msaada wowote ukizingatia hata mwanaume aliyezaa nae alimkimbia kwahiyo alikuwa na uchungu sana moyoni huku akilaumu umasikini wao.Basi siku hiyo alilala kwa mbinde sana kwani alihisi pia yeye ataishia vibaya sana kwani yakiisha mambo ya Prisca aliona pia kuwa yeye hawatamuacha salama kwani nae ataonekana kuwa ni mtu mbaya na asiyefaa.Kulipokucha, Vaileth alishangaa akiitwa na leo aliyemuita alikuwa ni baba Angel basi alitoka moja kwa moja na kwenda sebleni na kuanza kuongea nae,“Najua una uchungu sana kwa kile tulichofanya kwa ndugu yako, ila hata wewe ungekuwa ni sisi basi ungefanya kitu hiko hiko, unajua haiwezekani kabisa mtu tumeongea nae swala moja mar azote ila anajifanya kama hasikii zaidi zaidi anaenda kuleta dawa zingine na kuanza kuzisambaza getini kwetu, kwakweli nimechukia sana. Tusamehe bure kwa hilo, ila nduguyo tumempeleka polisi ili tu kumshikisha adabu”“Naelewa shemeji, hakuna tatizo”“Ila muda huu nimekuita ili nikuulize jambo moja, ni kitu gani wewe kama wewe ulitamani kukifanya baadaa ya kupata hela?”“Kitu pekee nilichokuwa natamani ni kuboresha nyumba wanayoishi wazazi wangu kani bati lake limeoza na huwa wanaingiliwa na mvua kipindi cha masika. Kwahiyo nikipata pesa basi kitu cha kwanza nitakachofanya ni hiko”“Oooh sawa, hakuna tatizo. Basi tutaongea vizuri, ila acha kuwa na mawazo Vaileth”Kisha baba Angel alienda chumbani na kumuaga mke wake maana siku hiyo mke wake alisema kuwa hatoenda popote halafu yeye aliondoka zake kwani shida yake ilikuwa ni kwenda kumtafutia Erica shule nyingine ukizingatia ile shule aliyokuwa akisoma Erica walishaikataa kabisa.Leo Erica alikaa na Abdi na kuanza kuongea nae mambo mbalimbali, ambapo Elly alianza kumwambia Erica,“Basi mama yangu anasema kuwa anamfahamu hadi shangazi yenu”“Shangazi yetu? Anamfahamu kivipi?”“Nyie shangazi yenu si anaitwa Tumaini? Halafu nasikia ukoo wenu umeingiliana sana, mamangu anasema lazima mtakuwa na laana”“Kivipi? Unajua sikuelewi?”“Ni hivi, mama yako na baba yako, halafu shangazi yenu Tumaini na mjomba wenu Tony yani baba yenu ni ndugu wa shangazi yenu yani kaka na dada hafu mama yenu na mjombaTony ni ndugu pia yani kaka na dada, halafu kuna mama yenu mkubwa na mumewe wote kuna undugu katikati, basi mama yangu anasema hiyo ni laana maana hairuhusiwi”“Jamani, mbona sisi tunaishi kawaida tu!”“Ndio ila kuna laana katikati yenu, maana ukoo wenu umeingiliana ingiliana”“Kheee makubwa, sikujua kama ni hivi ila mama huwa nikimuuliza hata hanijibu vizuri. Jana tulienda kwa shangazi na kukutana na mbaba mmoja anaitwa Derrick, kiukweli huyu sijamwelewa kabisa yani na mama hataki kusema ukweli”“Basi usijali, sababu mama yangu anafahamu mengi sana ya ukoo wenu, nitamuuliza kuhusu hilo pia halafu kesho nitakuletea majibu”“Oooh asante sana Elly, nashukuru kwa kuniambia mambo ambayo hata mimi binafsi nilikuwa siyafahamu kama yanahusu familia yetu”Basi baada ya maongezi hayo walirudi tena darasani.Muda wa kutoka ulipofika, kila mmoja aliondoka zake na kwenda kwao.Ila Erica alivyofika kwao alijihisi kuwashwa sana na ile habari aliyoipata basi moja kwa moja alienda chumbani kwa kaka yake na kuanza kumsimulia ila muda huo bila kujua kumbe mama yao alikuwa mlangoni akiwasikiliza maana nay eye kuna kitu alikuwa anaenda kufata chumbani kwa Erick, basi akamsikia Erica akimwambia Erick,“Yani Elly kaniambia kuwa kesho atanieleza kila kitu kuhusu huyo mjomba Derrick maana mama yake anajua kila mtu kwenye ukoo wetu”“Duh! Huyo mamake Ellyn i noma, ila ni nani jamani! Kwanini anajificha sasa? Kama ni mtu mwenye lengo zuri ni kwanini ajifiche jamani!”“Hata mimi namshangaa ila nahisi ni mtu ambaye mama na baba wanamfahamu vizuri sana”“Ila mimi simuamini maana lazima atakuwa ni adui wa familia yetu ndiomana anafahamu mambo mengi yanayoendelea kwenye familia hii”“Aaaah sio kweli, sio adui yetu wala nini. Mimi nina uhakika tukija kumfahamu tutamfurahia”“Binafsi sitaki hata kumfahamu huyo mama maana naona hana lengo jema na familia yetu”“basi kesho ataniambia kila kitu kuhusu huyo mjomba Derrick, mama si amenificha? Ngoja kesho nije nikueleze”Kwakweli mama Angel alichukia sana na kujikuta akimchukia Elly na mama yake kwani alijua kuwa hana lengo jema na familia yake, kwa upande mwingine aliona mwanae Erick ana akili zaidi ya Erica kwani ameweza kutambua kwa haraka kuwa huyo mama hafai ila Erica anaona huyo mama ni mtu mzuri tu kwake.Basi usiku wa siku hiyo mama Angel alimsimulia mumewe kila kitu kuhusu kile ambacho Erica na Erick walikuwa wakiongea, kwakweli hata baba Angel alishangaa sana na kujiuliza,“Huyo mwanamke ni nani sasa?”“Yani hapo ndio pabaya, adui usipomjua utapata shida sana”“Ni kweli mke wangu, yani tungemjua huyo mwanamke ingekuwa rahisi sana kwetu, ila kuna shule tayari nimeshamtafutia Erica”“Bora, sitaki tena kesho Erica aende kwenye ile shule”“Kesho, nitaenda nae kwenye shule mpya ili akafanye usahili kwanza maana hizi shule zingine wana sharia sana”“Shule yenye sheria ni nzuri mume wangu, yani ni kumpeleka tu huko huko maana huyu mtoto naye anataka kuanza vituko tu”Basi mama Angel na baba Angel walikubaliana kuhusu swala la Erica kuhamishwa shule ile anayosoma.Kulipokucha baba Angel alijiandaa na kutoka ambapo alimkuta Erica nae amejiandaa basi alimuita na kuongea nae,“Mwanangu, leo kuna shule nakupeleka ukafanye usahili maana nataka kukuhamisha ile shule”Erica alinyong’onyea sana na kulalamika kwa baba yake,“Jamani baba, kwanini unihamishe shule jamani! Mimi nimeizoea ile shule”“Ila shule ninayotaka kukuhamishia ni bora zaidi”kwakweli Erica alichukia sana ila hakuwa na namna zaidi ya kupanda kwenye gari na baba yake huku wakianza safari ya kuelekea huko shuleni.Baba Angel alimuona mwanae jinsi alivyochukia kutokana na lile swala la kutaka kumuhamisha shule, basi aliona njia ya pekee ili mwanae afanye usahili vizuri ni kumwambia maneno mazuri ili aweze kufanya usahili vizuri zaidi, basi alimwambia,“Mwanangu sikia, leo ukifanya usahili vizuri basi ukimaliza nakupeleka shuleni kwenu ili ukaongee na wanafunzi wenzio na upate kuwaaga ila ukifanya usahili vibaya sahau kabisa kama utarudi tena kule shuleni kwenu maana nipo radhi niwaombe walimu wakuchukue hivyo hivyo”“Baba nakuahidi kuwa nitafanya usahili vizuri sana, yani baba yangu hata usiwe na mashaka na mimi maana nitafanya usahili kwa umakini wote”Basi baba yake alitabasamu na kuendelea na safari.Walipofika shuleni, moja kwa moja Erica alipelekwa kwenye usahili na kupewa mitihani ambayo aliifanya kwa umakini mkubwa sana kiasi kwamba walimu walipoichukua ile mitihani walifurahi sana na kumwambia baba Angel kuwa mtoto wake apelekwe tu kesho akaanze shule maana anaonekana yupo vizuri sana.Basi wakapanda kwenye gari na kuanza safari ya kurudi nyumbani, wakiwa njiani Erica aliuliza,“Sasa baba mbona hatuendi tena kule shuleni ili nikawaage rafiki zangu?”“Tutaenda kesho, ngoja leo turudi tu nyumbani kwani nina mambo mengi sana ya kufanya”Yani Erica kilichokuwa kikimuumiza moyo ni kuhusu habari ambayo Elly alimwambia kuwa atamwambia, basi alichukia sana ila hakutaka tu kumuonyesha baba yake kuwa amechukia.Kuna mahali walikuwa wakikatisha na gari mara Erica alimuona mtu na kumshtua baba yake,“Kheee baba, yule sio kaka Junior?”Baba Angel alisimamisha gari na kuangalia vizuri ni kweli kabisa alimuona Junior akiingia kwenye nyumba ya kulala wageni tena akiwa ameongozana na mwanamke aliyemzidi sana kwa umri, kwakweli baba Angel alichukia sana hivyo alipaki gari lake vizuri na kushuka hadi kwenye ile nyumba ya kulala wageni.Alifika pale na kumuulizia Junior, ila pale alikuwa ameandikisha jina lingine,“Hakuna Junior hapa mzee wangu”“Aaaah namtaka yule mtoto aliyeingia hapa muda huu, hivi mnajua kama yule ni mwanafunzi? Nitawafunga nyie”Wale wahudumu wakaogopa hivyobasi wakamuonyesha baba Angel chumba ambacho Junior ameelekea na yule mwanamke, basi baba Angel akiwa na hasira sana alienda hadi kwenye kile chumba na kujaribu kufungua ila kilikuwa kimefungwa kwa ndani hivyo na kuamua kugonga ambapo mlango ulifunguliwa na Junior mwenyewe akijua ni muhudumu wa ile guest, kwakweli baba Angel alichukia sana na kumvuta kisha alimzaba vibao vya kutosha na kuondoka nae ambapo alimpakia kwenye gari lake na moja kwa moja kwenda nao nyumbani kwake.Kwakweli mama Angel pia alisikitika sana baada ya kusikia habari za Junior, basi baba Angel alikaa nae chini na kujaribu kuzungumza nae,“Hivi wewe Junior una tatizo gani lakini?”“Sina tatizo mimi baba mdogo ila sina raha kabisa”“Kwanini?”“hakuna mtu anayenipenda”“Hivi wewe mtoto una kichaa au nini? Familia yako yote tunakupenda, mama yako na sisi wote tunakupenda tena sana tu. Sasa kwanini useme hakuna anayekupenda?”“Sijawahi kuishi na baba yangu mimi, muda wote mama hunitukana na kuniambia kuwa tabia zangu ni kama za baba yangu, hata akinituma nikimwambia nimechoka basi huwa anasema tabia zangu ni kama za baba yangu na mara nyingi huwa anasema anajuta kunizaa anasema angejua angetoa hata mimba yangu. Haya na baba ninayeishi nae pia, hataki hata kuniona ingawa mama analea watoto wa baba vizuri tu ila yule baba hanitaki mimi kabisa na hata hanipendi. Kwahiyo mimi sina furaha yoyote ya maisha zaidi ya hii, yani kuzunguka na wanawake ndio furaha yangu”“Sasa Junior, hayi sio maisha ujue mwanangu, yani sio maisha kabisa. Naomba kwasasa uishi hapa nyumbani kwangu, nitaenda kukuchukulia nguo zako na kukuletea hapa, kwahiyo utakuwa ukienda shule na kurudi hapa, ila Junior sitaki ujinga hapa nyumbani kwangu, achana na habari kusema kuwa watu wote hawakupendi wakati tupo tunaokupenda sana tu, sawa!”“Sawa, bamdogo nimekuelewa”Basi baba Angel alipanga kwenda kesho yake kumchukulia Junior nguo zake ila kwa siku hiyo alimtaka ake hapo hapo na asiende popote pale.Siku hii asubuhi kabisa, baba Angel alimuita Vaileth kwanza na kuanza kuongea nae tena,“Vaileth, mimi nitakupatia pesa ili uwatumie wazazi wako waweze kukarabati nyumba yenu”“Oooh asante sana jamani, mungu akubariki baba. Nashukuru sana”“Ila naona kama bado haupo sawa, najua kinachokuumiza akili ni ndugu yako ambayo bado yupo rumande, ila nilimpeleka kule aweze kupata adabu kidogo”Vaileth alinyamaza kimya tu, kisha baba Angel akamwambia,“Ila usijali kitu kwani leo kabla sijaenda kwenye shughuli zangu basi nitapita kwanza polisi na kumtoa ndugu yako”Vaileth alionyesha tabasamu na kumfanya baba Angel aelewe wazi kuwa jambo lile lilikuwa likimuumiza sana kichwa Vaileth.Basi aliondoka na kama alivyoahidi ni moja kwa moja alienda polisi kumtoa Prisca, kisha alienda kwenye shughuli zake za kila siku, maana Erica alipelekwa leo na mama yake kwenye ile shule mpya sababu baba yake alisema kuwa kuna mambo anayafatilia kwanza, ikiwa na kwenda kuchukua nguo za Junior.Alipomaliza shughuli zake ni moja kwa moja alienda kuchukua nguo za Junior kwa shemeji yake, ambapo alimueleza tu kwa kifupi na shemeji yake alisikitika sana juu ya mtoto wake ila alimwambia,“Shemeji, kuna siku nitakuja ili tuzungumze vizuri juu ya hili swala la Junior, naimani utanielewa”“Sawa, shemeji hakuna tatizo. Msalimie sana mdogo wangu na watoto”Basi baba Angel aliagananae na kuaondoka zake.Wakati anakaribia nyumbani kwake alishangaa sana kuona watu watatu nje ya geti lake na wote walikuwa ni wanawake na katika watu hao mmoja alikuwa mtupu kabisa na walionekana wanafanya mambo kama ya kishirikina.Wakati anakaribia nyumbani kwake alishangaa sana kuona watu watatu nje ya geti lake na wote walikuwa ni wanawake na katika watu hao mmoja alikuwa mtupu kabisa na walionekana wanafanya mambo kama ya kishirikina.Baba Angel alishtuka sana hadi alitamani kushuka kwenye gari yake ili aende kuwauliza vizuri pale getini, ila alisita kushuka, hivyobasi akaanza tu kupiga honi ambapo mlinzi alifungua geti na moja kwa moja baba Angel aliingiza gari ndani na yule mlinzi alifunga geti lao yani wale watu nao walisogea pembeni na walijifanya kama hawaoni ile gari ingawa walisogea pembeni.Basi baba Angel alishuka na moja kwa moja alienda sebleni na kumuita mke wake ambapo alimueleza kile alichokiona getini kwao basi mama Angel nae aliamua kutoka ili akashuhudie, muda huo Vaileth nae alisikia na Junior pia alisikia kwahiyo wote waliongozana na kwenda nje ili kushuhudia kitu ambacho kinaendelea nje ya nyumba hiyo, na walipotoka tena kweli waliwakuta pale wakiendelea na walichokuwa wanafanya, kwakweli Vaileth alikuwa wa kwanza kushangaa na kuona aibu sana kwani wale watu walikuwa ni Prisca, shangazi yake na yule mganga yani yule mganga ndio alikuwa mtupu kabisa.Junior nae alichukia sana na pale pale alienda kumkaba yule mama aliyekuwa mtupu kabisa na kuanza kumpiga yani kile kitendo kilikuwa kama kimewazindua wale watu kwani walikuwa kama wamepigwa na bumbuwazi hivi, kisha mlinzi nae aliwakamata na kuwaingiza ndani ambapo waliwakalisha chini, kwakweli baba Angel alisikitika sana kumuona tena Prisca,“Hivi wewe si nimetoka kukutoa tu asubuhi ya leo jamani!! Sasa unapata faida gani kufanya haya?”Prisca aliishia tu kusema nisamehe yani hata hawakujua wanaongelea kitu gani, inaonyesha walichanganyikiwa, basi shangazi akaanza kumlaumu yule mganga,“Si ulisema hatutaonekana?”“Hata mimi nashangaa imekuwaje tumeonekana”Mama Angel aliwaambia,“Nyumba ya maombi hii, mlidhani mtafanya ujinga wenu tusiwakamate/ nyumba yangu daima naifunika kwa damu ya Yesu, hakuna mtakalofanya kwangu likafanikiwa. Hivi siku zote tunawakamata, hata hamjishtukii kuwa hiki tunachokifanya hakifai?”Kisha mama Angel alimuangalia Vaileth ambaye alikuwa kajiinamia akilia kwani ni aibu kubwa sana ndugu zake wamemletea,“Vai, hebu waulize ndugu zako vizuri ni lini wataacha kufanya huu ujinga? Au wanataka tukufukuze kazi?”Junior akadakia,“Sasa mamdogo umfukuze kazi sababu ya hawa wanga? Yani hawa ni wakuwashughulikia tu, mimi mkiniachia hawa lazima maji wataita mma na siku hiyo sijui kama wataendelea tena na uchawi maana kipigo nitakachowapatia wakizinduka watakuwa hoi na watakufa kabisa”“Mmmmh Junior jamani, hayo mambo sio kabisa. Ngoja niongee na nyie watatu, jamani hili ni onyo la mwisho, nawaambia hamnijui mimi nilivyo, mimi ni katili sana kupita mnavyoniona, nasema kuwa hili ni onyo la mwisho, nimemaliza”Kisha mama Angel akasema kuwa waachiwe tu, ila Vaileth akaomba jambo moja,“Naomba jambo moja toka kwako mama, naomba hawa ndugu zangu wapelekwe tu kanisani, muwaache huko wafanyiwe maombi”Mama Angel na baba Angel waliona hilo ni wazo zuri basi waliwapandisha wale watu kwenye gari lao huku yule aliyekuwa mtupu akipewa kanga na shangazi mtu ili ajistiri kisha wakaondoka nao kuelekea kanisani ili wakawaache kwenye maombi.Ndani ya nyumba alibaki Vaileth na Junior, ila muda huu Vaileth alikaa sebleni huku kajiinamia akilia yani alikuwa akiona aibu sana kwa kitendo kile hata hakujua ni kwanini ndugu zake waliamua kufanya vile, basi Junior alienda kumbembeleza,“Pole sana, usilie wala nini ni mapito tu”“Kwakweli sielewi kabisa, ndugu zangu wananitakia nini mimi? Wanataka mimi nifukuzwe kazi jamani! Nitaenda wapi mimi wakati hapa nilipo sina lolote mimi”“Hamna usiseme hivyo Vai, wewe ni mtu wa maana sana, achana na hao ndugu zako vichaa. Kuwa na amani Vaileth, nyamaza”Basi Vaileth aliinua kichwa chake na Junior alikuwa akimfuta machozi yake, muda huo Erick na Erica walirudi kutoka shuleni kwahiyo walivyoingia ndani walimkuta Junior akimfuta machozi Vaileth, basi waliwasalimia tu na moja kwa moja Vaileth nae aliinuka na kwenda jikoni kufanya mapishi ya jioni.Basi Junior nae alimfata kule jikoni na kumwambia,“Kama kuna kitu cha kukusaidia niambie maana mimi naweza kupika vyakula vya aina zote”Vaileth akatabasamu tu na kusema,“Basi nisaidie kukuna nazi”“Oooh hiko tu, nipe nikune”“Aaaah mimi natania bhana”“Ila si kweli unataka kupika chakula cha nazi?”“Ndio ni kweli ila nitakuna mwenyewe”“Kwani hizo nazi ziko wapi?”Junior aliuliza hivyo huku akiangaza jikoni na alivyoziona tu zikiwa tayari zimeshavunjwa kwahiyo Vaileth alishaziandaa kwaajili ya kukuna, basi Junior alivuta kibao cha kukunia nazi na kuanza kukuna ile nazi, kwakweli Vaileth alimuangalia tu na kumshangaa sana maana yeye alikuwa akimfanyia masikhara tu ila alishangaa kuona Junior alimaanisha na alianza kukuna nazi hiyo.Basi muda huo Erica na Erick kila mmoja alikuwa chumbani kwake, ila Erica alipomaliza tu ni moja kwa moja alienda jikoni ili kuangalia chakula ila alivyomkuta Junior akikuna nazi alishangaa sana hadi Junior alimuuliza,“Unashangaa nini Erica? Kwani hujawahi kumuona mwanaume akikuna nazi?”“Hamna kitu”Kisha Vaileth akamwambia,“Chakula kipo cha mchana kwenye hotpot ya pale juu”“Hamna hata sitaki chakula ila nilikuja kuangalia tu chakula cha usiku unapika chakula gani?”“Napika wali na njegere, walindio huu namalizia na njegere naziunga muda sio mrefu”“Sawa, mimi nitakula hiko”Kisha Erica aliondoka na moja kwa moja alienda chumbani kwa kaka yake na kuanza kumwambia,“Erick, hivi tulivyoingia ndani uliwaelewa dada Vaileth na Junior?”“Sikuwaelewa ila nahisi kama Junior alikuwa akimbembeleza Vaileth”“Sasa muda huu nimeenda jikoni na nimemkuta Junior akikuna nazi”“Mmmh!”“Ndio hivyo kaka, unahisi nini kinaendelea?”“Jamani, huyo Junior kaja jana tu halafu leo ndio kaanza kumnyemelea na huyo dada!”“Ila akimkubali ni ujinga wake, maana kila siku humu ndani inaongelewa tabia mbaya ya Junior halafu yeye amkubali kweli mmh!”Kisha Erica akaenda kitandani kwa Erick na kujilaza ambapo usingizi ulimpata pale pale.Basi baba Angel na mama Angel walirudi usiku na kuita pale na kuanza kuwasimulia kilichotokea kwenye maombi, ila muda huu Erica hakuwepo maana bado alikuwa amelala chumbani kwa Erick, basi mama Angel alipomaliza kuelezea aliuliza,“Erica yuko wapi?”Erick alijibu,“Amelala, ngoja nikamuite”Basi Erick aliinuka na mama Angel nae aliinuka na kumfata kwa nyuma, alishangaa kuona Erick akielekea chumbani kwake, basi alimuuliza,“Kwani Erica kalala huko kwako?”“Ndio mama”“Jamani, si nimeshawakataza hiyo tabia lakini!”“Ila mama jamani, Erica si dada yangu! Kwanini unanitenga nae kiasi hiki!”“Sitaki kusikia hayo”Basi moja kwa moja mama Angel alienda hadi kule chumbani kwa Erick na kuanza kumuamsha Erica kwa kumpiga vibao ambapo Erica alishtuka kisha mama yake alianza kumsema,“Hivi wewe mtoto unanitaka nini lakini? Siku zote nakukataza kuingiliana vyumba na kaka yako, mmekuwa wakubwa sasa, nimewatengea kila mtu chumba chake nikiwa na maana nzuri kabisa, niondolee balaa hilo mimi, haya inuka upesi hapo”Basi Erica aliinuka na kuelekea chumbani kwake, yani muda huo mama Angel nae alielekea chumbani kwake huku akilalamika ila mumewe nae alikuwa huko na kumsikiliza mkewe akilalamika kisha kumuuliza vizuri ambapo malalamiko ya mkewe yalikuwa ni yale yale ya siku zote kuhusu Erica na Erick,“Ila mke wangu utafatilia hao watoto hadi lini jamani! Hebu kuwa na imani maana hao ni ndugu ujue, acha kuwawazia mabaya watoto”“Mimi siwawazii mabaya ila sipendi tabia ambayo wanaifanya wakati kila mmoja ana chumba chake, haswaaa Erica jamani ameanza tabia mbaya sana”Basi waliongea kidogo pale na kuamua tu kulala kwani walikuwa wamechoka sana kutokana na shuruba za siku hiyo.Tangu Junior aanze kuishi hapa nyumbani kwa mamake mdogo alibadilika sana kitabia, kwani alikuwa akitoka shuleni ni moja kwa moja anarudi nyumbani na alionekana kusoma kwa bidii sana tofauti na siku zote, mpaka shuleni alifatwa na Husna ili kuulizwa vizuri,“Junior mtoro mwenzangu, siku hizi nini kimekukumba? Maana sikuelewi ujue, yani siku hizi kila siku upo shuleni na hata hukosi hata siku moja”“Nimegundua kuwa elimu ni kila kitu katika maisha, unaweza kuwa na mali nyingi na pesa nyingi ila bila elimu ni ngumu sana kuendesha hizo mali, utajikuta tu utazitapanya na mwisho wa siku unarudi tena kwenye ufukara. Acha nisome kwa bidii, naelewa ninachokifanya”“Na lile ombi lako la kunitaka, nimekubali”Junior alicheka na kumwambia Husna,“Hiyo ni sawa na mtu aliyekuwa kwenye mfungo wa Ramadhani halafu wewe uje kumwambia kuwa umekubali awe mpenzi wako, unataka afanye nini sasa? Atende dhambi au kitu gani?”“Sina maana hiyo Junior, kwani wewe upo kwenye mfungo?”“Hapana ila kwasasa nimeamua kuwa makini na masomo kwanza, kama umeamua kunikubali basi na wewe uamue tu kuwa busy na masomo yani hapo tutaenda sambamba”“Jamani Junior, unanikatili ujue! Mimi masomo hayapandi wala nini na ubaya ni kuwa kila muda nakuwaza ndiomana nimeamua kukwambia haya”“Husna, mimi ni kijana nisiyefaa kabisa, unionavyo hapa ni kijana mdogo ila nishatembea na watu wa kila dizaini unayoijua wewe, yani hata wewe hutokuwa na jipya kwangu”“Sasa kwanini ulinitongoza?”“Mimi kutongoza ni kawaida yangu tu ndiomana hata hapa shuleni ukifatilia unaweza kuta karibia kila msichana nilimtongoza, atakayenikubalia ndio huyo huyo, ila kwasasa nimestaafu kwanza”Husna alichukia sana kusikia vile, aliona kumbe Junior siku zote alizokuwa anamfatilia alikuwa akimjaribisha tu, basi alichukia mno na moja kwa moja akaondoka zake.Muda wa kutoka, Junior kama kawaida ni moja kwa moja alirudi nyumbani kwa mamake mdogo na Vaileth alikuwa sebleni, kumbe kwa siku hizo Junior alikuwa akikaguliwa daftali zake na Vaileth,“Umeona, nipo makini sana kwasasa”“Hivi ndio inavyotakiwa, usijali kuhusu mimi ila ninachohitaji ni kuona kuwa umesoma na umefika mbali kimaendeleo na kimaisha”“Asante sana Vai ndiomana upo kwaajili yangu”Leo Erica aliwahi kurudi kushinda Erick kwahiyo alimkuta Junior akiongea lile neno la mwisho na kumfanya agune sana, kisha aliwasalimia na kuondoka zake, ila Vaileth na Junior walimuangalia tu, ndipo Junior alipomwambia Vaileth,“Usijali matendo ya huyu dogo ndio zake, anapenda umbea umbea tu”“Namjua mambo yake”Basi Junior aliinuka na Moja kwa moja alienda chumbani kwake yani kwa kipindi hiko ilikuwa ni masomo tu masomo na yeye.Leo Elly wakati katoka shuleni alionekana kumkumbuka sana Erica, yani alitamani mno uwepo wake, kwa siku hizo alikuwa ni mpweke sana ukizingatia Erica hata kuaga hakuaga wala nini basi roho ilimuuma sana.Siku hiyo wakati wanatoka shule, Abdi alimfata na kumuuliza,“Vipi dada yako Erica yuko wapi?”“Aaaah usiniulize bhana”Basi Abdi alicheka sana na kusema,“Dada, dada halafu dada mwenyewe hujui chochote kinachoendelea juu yake. Kaka wa Erica ni Erick tu, wewe sijui ulitokea wapi, ungemuona Erick alichokuwa akifanya kwa dada yake ndio ungeelewa maneno yangu kuwa kaka wa Erica ni Erick tu lakini sio wewe wa kujipendekeza kama mimi, ukanivizia chooni na kunipiga juu ila mbona hujui dada yako alipo!!”Abdi aliondoka huku akimcheka, yani maneno yale yaliumiza sana moyo wa Ellyn a siku hiyo alivyorudi kwao alimsimulia mama yake jinsi alivyomkumbuka Erica na jinsi Abdi alivyomshushua, basi mama yake akamwambia,“Usijali mwanangu, nitahakikisha napafahamu wanapoishi wakina Erica na nitakupeleka tu”“Uuuh asante mama kwa kunijali”“Usijali mwanangu, mimi mama yako niko tayari kufanya chochote kwaajili yako hii yote ni sababu ya upendo nilionao juu yako”Elly alitabasamu na kufurahi sana kwani aliona kuwa mama yake anamjali sana.Mama Angel kwasasa kidogo mimba yake ilianza kumchosha ingawa bado ilikuwa ni ngumu kuonekana, mumewe alikuwa akifanya jambo moja kwake kila siku yani ilikuwa kama siku hiyo mkewe alitoka basi muda wa kurudi lazima aende kumchukua yani kile kitendo kilikuwa kikiwatia wivu watu wengi sana.Basi siku hiyo baba Angel aliamua kwenda kumfata mke wake kama kawaida yake, basi alivyotoka tu walishangaa kukutana na mtu ambaye walikuwa wakimfahamu kwa muda mrefu sana, mtu huyo alikuwa ni Dora yani yule rafiki wa mama Angel, basi aliwasimamisha na kuanza kuongea nae,“Kheee jamani wapendanao, yani nyie mnafanya kila mtu atamani maisha ya mahusiano huku akifikiria kuwa maisha yote ya mahusiano yapo hivi kumbe ni bahati tu”“Hapana jamani, sio bahati ili ni kufanya maamuzi tu, wote wawili mkiamua kwa nia ya dhati basi inawezekana”“Ila nashukuru kuwaona jamani, shemeji najua una miradi mbalimbali naomba umsaidie mdogo wangu”“Mdogo wako!!”“Ndio, yule mdogo wangu Steve yani yupo tu hana kazi yoyote ya kufanya, naomba mumsaidie jamani”“Kwani huyo Steve yuko wapi?”“Yupo nyumbani”“Kheee huyo Steve si alioana na Sia! Inamaana yupo nyumbani kwenu na mke wake!”Mama Angel aliuliza kwa mshangao sana na Dora alimjibu,“Kwa kifupi ni hivi, Steve haishi tena na yule mwanamke, waligombana na kutalikiana, si unajua mapenzi ya dawa huwa hayadumu! Sasa Steve na udogo ule wa kipindi kile akaishi na mwanamke mkubwa kama Sia ili iweje jamani! Kwahiyo Steve yupo nyumbani tu”“Na mtoto wao je?”“Mmmh jamani, maswali mengine mtamuuliza mwenyewe, ila naomba tu mnipe kibali ili nimwambie aje kwenye ofisi zenu na mumpatie hiyo kazi”Mama Angel na baba Angel waliangaliana kwa muda kisha baba Angel alitoa kadi yake yenye namba za simu na kumkabidhi Dora kisha akamwambia kuwa huyo Steve amtafute halafu atawasiliana nae, na baada ya hapo walimuaga na kuingia kwenye gari lao kisha safari ya kwenda nyumbani kwao ikaanza.Wakati Dora nae akitaka kuondoka eneo lile alishangaa mtu akimsimamisha na kumuuliza,“Unawafahamu vizuri wale?”“Ndio nawafahamu”“Yule mama anajishauwa sana, yani anaona kamavile kaibeba dunia”“Mmmh, kwanini unasema hayo?”Yule mwanamke aliondoka zake, ila Dora aliona ni vyema akipata muda amtahadharishe rafiki yake kwani aliona kuwa kuna watu hawana lengo zuri na rafiki yake.Leo wakati Tumaini kaamka akifanya usafi kidogo wa nyumba yake, alipigiwa simu basi aliamua kuipokea na kuanza kuongea nayo,“Tumaini, ni mimi Sia”“Oooh jamani kumbe, halafu sijui namba yako sikuaiandika jamani!”“Hamna bhana ila sikukupa, ila leo nimekukumbuka sana nahitaji kukutembelea ili niongee kidogo tu na wewe”“Oooh karibu nyumbani kwangu basi, karibu sana”“Nielekeze basi ili nije, maana nataka kuja le oleo”Basi Tumaini alimuelekeza Sia mahali ambapo anaishi kisha akaagana nae na yeye aliendelea na kazi zake kama kawaida.Basi alivyorudi kupumzika, alikaa kidogo na Sia alimpigia tena simu maana tayari alishafika nje ya geti lake, basi Tumaini alienda kumfata nje na kumkaribisha vizuri sana, ambapo Sia nae alikaribia ndani na moja kwa moja walianza kuongea mambo mbalimbali ya zamani,“Nikikumbuka kipindi kile nacheka sana, yani Tumaini tulikuwa tukienda nyumbani kwakina Erica na kufanya vurugu zetu ila leo hii umenisahau kabisa, kweli nimeamini maneno ya watu yani mawifi sio wa kuwaamini kabisa maana ufata upande ule wa kaka zao”“Mmmh na wewe Sia bado una hay ohayo tu jamani!!”“Sikia nikwambia Tumaini yani kamwe siwezi kusahau, ujue Erick nilimpenda sana yani nilimpenda kiasi kwamba hadi kesho bado nampenda”“Duh! Ila ni mume wa mtu tayari”“Najua hilo na ninaheshimu ndoa yake ten asana tu, ila natamani kuonana nao ili angalau hata niwaombe msamaha maana hata sikumbuki kama walinisamehe”“Mbona walikusamehe kitambo sana, tena Erick aliniambia kuwa kuna siku alikuona akasimamisha gari na kukupigia honi ila ukaondoka kwa haraka haraka”“Mmmh jamani, sijamuona mbona, ila unaonaje tukienda kwao muda huu!!”“Dah! Sijajipanga kabisa kwenda huko jamani, yani leo hata sijajipanga”“Mimi nakuomba shoga yangu, nikawasalimie tu”Mara simu ya Tumaini ilianza kuita na mpigaji alikuwa ni kaka yake basi aliinuka na kutoka nje ili aongee nayo, na alipoipokea tu alianza kusema,“Mwenzangu leo Sia kaja nyumbani kwangu na amekazana nimlete kwenu”Kumbe kwenye ile simu alikuwa ni mama Angel ambaye alishtuka sana na kusema,“Aaaah Tumaini, kumbe bado una ushirika na huyo mtu!! Simtaki nyumbani kwangu kabisa”“Oooh samahani wifi”“Haya niambie ni ajenda gani ambayo huwa unapanga na kaka yako dhidi ya huyo mwanamke?”“Hakuna lolote ndugu yangu, nisamehe bure tu”Ilionekana mama Angel kachukia sana hata Tumaini aligundua hilo basi alivyorudi ndani ilibidi amdanganye maneno mengine Sia,“Yani nimepigiwa simu na mume wangu hapa, kasema nimfate sasa hizi kazini kwake, samahani shoga yangu sitaweza”“Basi nielekeze, niende mwenyewe”“Hapana Sia, yani hata kukuelekeza sijui naanzia wapi yani sehemu yenyewe haielekezeki ujue”“Mmmmh Tumaini, unanifanyia kusudi, haya bhana kajiandae tuondoke wote”Yani Tumaini hakuwa na namna zaidi ya kwenda kujiandaa ili kuondoka tu na moja kwa moja alielekea ofisini kwa mume wake ingawa hakutaka kufanya hivyo.Tumaini alipofika ofisini kwa mume wake hakuwa na wasiwasi wowote ule kwani moja kwa moja aliamua kwenda ndani ya ofisi, alishangaa mumewe kaka halafu kuna mwanamke amekaa mbele ya mumewe na huyo mwanamke alikuwa amevaa nguo za mitego sana.Tumaini akapatwa na hasira kwani alimsogelea yule mwanamke na kumkunja halafu alimzaba vibao kama vitano ila alipomuachilia yule mwanamke alianguka chiniTumaini akapatwa na hasira kwani alimsogelea yule mwanamke na kumkunja halafu alimzaba vibao kama vitano ila alipomuachilia yule mwanamke alianguka chini kabisa.Ilibidi mumewe asogee karibu na alipo mkewe ila Tumaini wala hakushtuka kitendo cha yule dada kuanguka wala nini, mumewe alianza kumfokea,“Ndio mambo gani haya umefanya mke wangu jamani! Ona sasa”“Ulitaka nifanyeje sasa? Kumbe unakawia kurudi nyumbani sababu ya malaya kama hawa!”Mumewe aliinama chini na kujaribu kumuamsha yule dada, kumbe alikuwa amezimia kwahiyo ilibidi ampatie huduma ya kwanza kwa kummwagia maji ambayo yalikuwepo mule ofisini na mdada alizinduka na yule mume wa Tumaini akawa anafanya kazi ya kumuinua pale chini ila kile kitendo ndio kwanza kilizidi kumuumiza Tumaini na muda huo huo Tumaini aliinuka na kuondoka zake bila ya kusema chochote kile.Alirudi kwenye gari lake na kukaa kwa muda kisha alijikuta akianza kulia yani alitokwa sana na machozi na kwa muda huo hakujua ni wapi aende ilia pate faraja ya kile kilichomtokea, akaona ni vyema aende kwa wifi yake mama Angel ili akaongee nae kidogo kwani alihisi pengine atamfariji.Muda ule ule aliwasha gari yake na kuondoka mahali pale, moja kwa moja alienda hadi kwa mama Angel ambapo mlinzi alimfungulia geti na alipoingia ndani tu alimuomba mama Angel ili akaongee nae kwenye bustani kwani hakutaka kuongea nae ndani, kwa haraka haraka mama Angel alijua kuwa wifi yake anataka kuongelea habari za huyo Sia, basi aliondoka nae huku kajipanga ya kumjibu ila alishangaa alichoanza kumueleza,“Sikia Erica ni hivi, nilipomkatalia Sia kumleta huku basi nikamdanganya kuwa mume wangu kanipigia simu na anataka niende ofisini kwake, basi akasema hakuna shida nakusubiri twende wote, sikuwa na jinsi kweli zaidi ya kwenda nae tu ambapo nilimshusha pale ofisini na tuliagana halafu mimi nikaingia ofisini kwa mume wangu, nilichokutana nacho sasa!!”Tumaini aliangusha machozi kwa mara ya kwanza na kumfanya mama Angel amuulize kwa makini,“Kwani kitu gani ulichokutana nacho?”Tumaini akaanza kumsimulia wifi yake jinsi alivyomkuta mumewe na yule mwanamke ofisini, kisha akasema,“Yani mimi ndiomana katika maisha yangu nilikuwa sipendi kuolewa, sipendi kuwa na mahusiano, wanaume hawaaminiki kabisa. Nampenda mume wangu, namuheshimu namjali na sijawahi kufikiria kumsaliti hata mara moja, wala kuongea na wanaume wengine sitaki kwani mimi hawanitongozi? Nina ubaya gani wa kushindwa kufatwa na wanaume wengine? Kwanini yeye nimkute ofisini kaka na yule mwanamke kwa mikao ya kihara namna ile halafu anajifanya kumjali zaidi yule mwanamke kuliko mimi!! Najuta kwanini hata nilikubali kuolewa”“Jamani wifi yangu ndio umepaniki hivyo jamani!! Ila sidhani kama kaka yangu ana mahusiano na huyo mwanamke jamani!”“Najua unamtetea tu”“Kweli Tumaini, kaka yangu hawezi kufanya hivyo jamani”“Hebu kaniitie Erick, labda anaweza akanielewa”Basi mama Angel aliinuka na kwenda kumuita mume wake ambaye baada ya muda mfupi alifika nae kwenye ile bustani, basi Tumaini alianza kumueleza kaka yake kuhusu kile kilichotokea ambapo nae kaka yake alimtia moyo na kumwambia kuwa haiwezekani kwa shemeji yake kuwa na mahusiano na huyo mtu,“Hapana, nyie mnamtetea tu, natamani niondoke nyumbani kwangu”“Jamani mama Leah, sasa uondoke nyumbani kwako kwasababu hiyo kweli! Hebu kumbuka ni miaka mingapi mmeoana na kaka yangu je kuna lolote baya amewahi kukutendea? Ni wazi kuwa kaka yangu anakupenda sana ila nadhani hujaelewa kilichotokea kabisa wifi yangu, ila najua akirudi nyumbani mtayasuluhisha tu”Basi walijaribu pale kumshauri na kumpa moyo ambapo kidogo alifurahi na mwisho wa siku aliaga na kuaondoka zake.Usiku wa leo Elly akiwa nyumbani na mama yake, alipewa ujumbe ambao ulimfurahisha sana kwani mama yake alimwambia,“Mwanangu Elly, tayari nimeshapafahamu anapoishi Erica”“Jamani mama, ni kweli!”“Ndio mwanangu, si nilikwambia kuwa, kwako wewe nipo radhi kufanya chochote kile sababu nakupenda sana”“Asante sana mama”Elly aliinuka na kumkumbatia mama yake kwa furaha kwani alijihisi rah asana kwa mama yake kumtimizia hitaji lake, kisha akamuuliza tena,“Eeeeh mama, na lini nitaenda kumuona baba yangu au ndugu zake baba?”“Sasa utaendaje kumuona baba yako wakati alikukataa ukiwa mdogo kabisa mwanangu! Yani ulipozaliwa, sijui baada ya miezi miwili, baba yako akaanza oooh huyu mtoto mbona sifanani nae, mara hii miguu mikubwa sio yangu, mara haya macho sio yangu yani alikuwa akitoa kila kasoro, huyo bibi yako na shangazi yako walipofika ndio kabisa yani walikataa katakata kuwa wewe ni damu yao, hivyobasi waliondoka na baba yako na toka kipindi hiko hakurudi tena kabisa, kwahiyo mwanangu ningefanya nini tena mimi? Niliamua tu kukulea kwa nguvu zangu zote ili ukue na uwe mtoto mzuri na badae uweze kunisaidia, kwakweli nashukuru sana kwa hilo kwani nimekulea kwa kipindi chote hiki hadi leo”“Ila mama, je ni kweli huyo hakuwa baba yangu?”“Mmmh sasa swali gani unaniuliza hilo mwanangu jamani! Utaniumiza kichwa change bure, ila amini kuwa nakupenda sana mwanangu, hakuna ninayempenda maishani mwangu kama wewe, nakupenda sana”“Asante sana mama ila lini tutaenda kwakina Erica mama?”“Subiri mwanangu, tutaenda tu”“Nashukuru mama”Elly alifurahi sana na kumkumbatia mama yake kwa furaha.Mume wa Tumaini aliporudi nyumbani na kumkosa mke wake, moja kwa moja aliamua kwenda nyumbani kwa baba Angel kwani alihisi kuwa lazima mke wake amekimbilia huko, kumbe wakati kaondoka ndio wakati huo huo mkewe nae alikuwa kaondoka kwa mama Angel.Basi alivyofika nyumbani kwa mama Angel moja kwa moja dada yake alimkaribisha vizuri sana na kuanza kuongea nae,“Oooh yani wifi yako sijamuelewa ujue, yani kilichomfanya achukie hivyo ni nini?”“Kwani huyo msichana alikuwa ni nani kaka yangu?”“Yani unafikiri naelewa basi, yule msichana alifika ofisini kwangu, yani hata dakika mbili hazijapita yani hata kuongea nae sijaongea nae ila mke wangu aliingia muda huo huo na kuanza kufanya varangati lake, kwakweli mimi sielewi na yule msichana hadi nimemmwagia maji ndio kazinduka basi nikamuinua na kumuweka kwenye kiti ndio mke wangu kachukia na kuondoka, ila yule msichana nae aliondoka baada ya muda mfupi tu yani hata mimi mwenyewe binafsi sijaelewa chochote. Yule msichana alifata nini ofisini kwangu? Unajua hata kama nataka kufanya ujinga basi siwezi kufanya huo ujinga kwenye ofisi yangu jamani!”“Duh! Pole sana kaka, ila kaa vizuri na mkeo tu umueleweshe unajua mara nyingine kuna mambo mengine yanatendeka bila kujua ni kwanini yametendeka kumbe lengo kubwa ni kusambaratisha ndoa yenu, mueleweshe vizuri mkeo”“Asante dada yangu, ngoja niondoke kwanza”Basi mume waTumaini aliaga na kuondoka zake na wala hakuonana na baba Angel kwa muda huo maana baba Angel alikuwa kalala.Basi mama Angel moja kwa moja alienda chumbani kwake na kuamua kupumzika tu.Kwakweli Erica kwenye hii shule mpya alikuwa kapooza sana kwani alijikuta akipenda sana shule zenye mchanganyiko wa jinsia kuliko shule za jinsia moja, basi siku hiyo alipokuwa darasani kuna msichana mmoja alikaa nae karibu na kuanza kuongea nae,“Erica mbona unaonekana hupendi kukaa karibu na wengine? Yani wewe hujishughulishi na maongezi ya aina yoyote ile”“Aaaaah mimi ni msikilizaji tu na sio muongeaji”“Ila mimi nakupenda sana, yani natamani uwe rafiki yangu”“Usijali basi, tumekuwa marafiki. Si unaitwa Samia eeeh!”“Ndio, ndio jina langu hilo”“Basi, kuanzia leo sisi nimarafiki”“Oooh nimefurahi sana, nitamuhadithia mama yangu kuhusu wewe na kwa hakika atafurahi sana, ujue nini eeeh! Mama yangu lazima atataka kukufahamu si hautakuwa na tatizo kwa hilo eeeh!”“Aaaah sina tatizo juu ya hilo, hata mama yangu atapenda kukugfahamu pia na kufahamu kwenu pamoja na kumfahamu mama yako”“Basi tunakuwa marafiki wazuri”Erica na Samia walikumbatiana na kufurahi juu ya hilo kuwa wamekuwa marafiki sasa.Mpaka muda wanaenda nyumbani waliagana vizuri sana na kila mmoja kupanda kwenye basi la shule linaloelekea mitaa ya kwao.Erica alivyofika nyumbani kwao, jambo la kwanza alianza kumsimulia mama yake kuhusu rafiki yake mpya aitwaye Samia,“Oooh ushapata rafiki eeeh! Naimani mwanangu hautopooza tena”“Ndio mama, nimefurahi sana ila naimani mara moja moja utaniruhusu nikamtembelee kwao”“Hakuna hiyo kitu labda yeye ndio aje hapa”“Sawa mama, napo hakuna tatizo”Basi Erica aliingia chumbani kwake na alipomaliza kubadili nguo tu alienda kumwambia Erick kuhusu rafiki mpya aliyempata maana kwake ilikuwa ni kawaida kwa jambo lolote likitokea kwake basi ni lazima aje kuhadithia,“Ooooh hongera sana mdogo wangu, nimefurahi kusikia hivyo kwani najua sasa utaanza kuwa na furaha, tatizo lako hupendi kuwa na urafiki na wasichana wenzio ila leo Mungu ni mwema maana umeweza kuwa na urafiki na msichana mwenzio kwakweli nimefurahi sana mdogo wangu”Basi wakaongea ongea pale na kisha wote kwa pamoja kutoka na kwenda kula.Muda wanakula, ni muda ambapo Junior na Vaileth nao walikuwa wanakula kwahiyo mezani walikuwa wanne ila macho ya Erica yalikuwa yakigonga kwa Junior na Vaileth ila aliwaona kama wakikonyezana vile, basi alikuwa akiwaangalia sana na wao hata hawakuwa na habari kuhusu lile swala na walipomaliza kula, Vaileth alitoa vyombo vyake pamoja na vyombo vya Junior huku Erica akitoa vyombo vyake na vya kaka yake.Waliporudi chumbani, Erica alienda tena kuongea na kaka yake,“Mmmmh leo sasa, ndio dada Vaileth na Junior nimewaona kabisa wakiwa wanakonyezana”“Ila usishangae sana Erica, yule ndio shemeji yangu kwa Junior ujue na wewe ndio wifi yako”“Ila mbona dada Vain i mkubwa kwa Junior?”“Mapenzi hayana umri Erica!”“Mmmmh!”“Ndio hivyo, mapenzi hayachagui umri, hayachagui kabila wala rangi, mapenzi ni kama nyasi yani huota popote”“Aaaah kumbe! Basi nimekuelewa”Siku hiyo Erica alirudi tu chumbani kwake na kwenda moja kwa moja kulala tu.Leo mama Angel alienda kwenye biashara yake, ila alipofika na kukaa kaka kidogo alipigiwa simu na rafiki yake Dora,“Nipo mitaa ya ofisi yako hapa, uko wapi?”“Mbona nipo ofisini”“Basi nakuja”Baada ya muda kidogo Dora aliwasilia kwenye ofisi ya mama Angel na kuanza kuongea nae mambo mengi ikiwa ni pamoja na kusifia ile ofisi yake,“Unajua sikuwahi kuingia humu jamani, kwakweli hongera sana rafiki yangu”“Asante”“Kwasasa naamini kuwa mara nyingine maisha ni jinsi wewe binafsi unavyochagua, yani Mungu ni mwema kwetu ila sisi wanadamu tuna mtindo wa kulazimisha mambo na mwisho wa siku tunaharibu kusudi la Mungu katika maisha yetu. Nakumbuka mimi nilikuwa muhuni sana, na uhuni ulikuwa kama sehemu ya maisha yangu, sikutaka mtu aniambie chochote kile, yani mtu akisema swala la Dora acha uhuni basi mtu huyo nilimuona ni mbaya na sikutaka hata kumuona tena, ila kwasasa sitamani hata kidogo mwanangu Jesca kuwa na tabia kama zangu, mimi nikawa kama sijasoma vile yani kama nimesomea uhuni sasa maana kila aina ya umalaya niliifanya, kwakweli kuna muda mwingine nastahili kukupongeza sana tu”“Mmmh ila shoga yangu nami nimepitia makubwa sana, yani dah huwa nikikumbuka hadi huwa siamini kama niliwezaje kukwepa ile misumari, loh! Nimeandamwa mimi jamani, nimeandamwa hatari, kila niliposhika palikuwa hapashikiki na kote naambulia machungu tu, ila kwa Erick nashukuru sana Mungu maana alinisimamia”“Nakumbuka shoga yangu, na yule mjinga Sia ndio angekuvuruga kabisa nay ale madawa aliyotaka kumpa Erick, uwiii ule ndio ulikuwa muda ambapo Erick angekusahau nadhani sijui ungeenda kuolewa mke wa pili kwa Bahati maana ulikuwa na mawazo wewe”Mama Angel alicheka kisha akamwambia,“Tena umenikumbusha kuhusu huyo Sia”“Eeeeh kafanyaje tena?”Basi mama Angel alianza kumsimulia mlolongo mzima wa jinsi alivyompigia simu Tumaini na jinsi ilivyokuwa hadi muda ambao Tumaini alienda kwake akilia, kwahiyo yote alimsimulia basi Dora akamwambia,“Mmmmh shoga yangu, unajua mimi hadi leo simuamini Sia kabisa, yani simuamini yule mwanamke kama kweli aliamua kwa moyo safi kuachana na nyie!! Sijui kwakweli ila sina imani nae”“Ila kwanini unasema hivyo?”“Hebu angalia hata hilo tukio la Tumaini, alimgomea kuja nae kwako, Tumaini akadanganya anaenda ofisini kwa mumewe ila hajakubali hadi kamsindikiza, haya sasa nini kimetokea baada ya kumshusha? Tumaini kamkuta mumewe na mwanamke ofisini hivyo Tumaini akapaniki na moja kwa moja akaja kwako, yani hapo jua kuwa Tumaini alivyokuja kwako basi nae alikuwa nyuma yake yani hapo tambua kuwa nyumbani kwako panajulikana na Sia tayari”“Mmmmh!”“Usigune, angalia tena hilo tukio huyo mwanamke kaingia dakika mbili kwenye ofisi ya kaka yako na muda kidogo Tumaini nae kaingia, kamzaba vibao kidogo kazimia, haya kazinduka Tumaini kaondoka kwa hasira na huyo mwanamke nae kaondoka, je kwanini asieleze shida yake kama ni kweli alikuwa na shida?”“Inamaana ni ushirikina?”“Mambo mengine sio hata ushirikina ila watu wana mbinu zao za kijasusi”Dora alicheka kidogo kisha akasema tena,“Yani ni hivi, yule Sia mimi simuamini ujue yani simuamini kabisa, kwa alichokifanya kwa Steve hapana kwakweli”“Alifanyaje kwani?”“Kwanza, alienda kujifungua kimya kimya tena kwa operesheni, hivi jamani mtu unajifungua kwa kisu kimya kimya kweli! Haya sasa, karudi kwa mumewe baada ya mwezi mmoja, hivi nani atamuamini yule mwanamke kama hajatoka kwa mwanaume wake mwingine kulelewa huko? Steve nae akachekelea tu mtoto wangu, mtoto wangu loh siku hiyo tumeenda na mama kumuona mtoto Mungu wangu yani mtoto hafanani na sisi hata ukucha, tukamuomba kwenda kupima kagoma, sasa tufanyeje jamani! Unajua Sia hajatulia kabisa, yani yule ana wanaume wengi hadi mwisho wa siku hajui baba wa mtoto ni nani, ila baada ya hayo ikawa kama akili ya Steve imerudi hivi basi tukaondoka na mdogo wetu tena kutugelesha mwanzoni alianza kumuita mtoto Steve, mwanamke shetani kabisa yule”“Kheee kumbe ndio alifanya hivyo jamani!”“Ndio, kuna siku nilikutana nae wakati mtoto sijui ana miezi saba nikakuta mtoto anasura nyingine yani sio ile ya udogoni, kwakweli ndio hafanani na sisi hata kidogo, kama hajazaa na wavua samaki huko ilia pate samaki wa bure sijui, nikamuuliza, ndio huyu Steve? Akasema ooh nyie si mlimkataa, nimembadilisha jina, anaitwa John, nikasema huyu mwanamke hajielewi yani anatanga tanga tu, sasa nadhani anampelekea baba yoyote na kumwambia mtoto wake na kumpa jina la huyo baba ila mtu aamini kuwa ni mwanae. Nikakumbuka hadi kipindi kile alichodai kuwa ana mimba ya Erick”“Yani yule msichana ana wazimu ujue, sikapendi kweli. Kalinichanganya sana akili kipindi kile, ila ushanitisha tayari, inamaana amepafahamu kwangu?”“Usichanganyikiwe ila kuwa makini tu shoga yangu yani mimi nimefanya kukutahadharisha tu na si vinginevyo”“Sawa, nashukuru”Kisha Dora akamkumbusha swala la kumtafutia mdogo wake kazi, kisha alimwambia kuwa atamkumbusha mumewe juu ya swala hilo.Kwa muda huo waliongea sana hadi muda ulipofika ambapo mama Angel alienda kufatwa na mumewe ili waende nyumbani kwani mama Angel alikuwa anaenda hapo ofisini kwake ili asilale sana nyumbani.Baba Angel na mama Angel muda huu waliona ni bora kupitia hotelini ili wapate chakula cha hoteli kwa siku hiyo na wakirudi nyumbani wawe wameshiba tayari.Basi walienda hotelini, wakati wameanza tu kula walishangaa kuna mtu alienda kukaa kwenye meza yao na kuwasalimia, mama Angel alishtuka sana ila kumuangalia mtu huyo alimuona ni baba Abdi, basi akamwambia,“Bahati!!”“Ndio ni mimi, mbona umeshangaa hivyo kwani umeona miujiza?”Ila siku ya leo baba Angel alikaa kimya kabisa akiangalia tu kinachoendelea kanakwamba hakimuhusu vile, basi baba Abdi akaanza kusema,“Nasikia umemuhamisha mwanao shule?”“Ndio, ulitaka asome pale ili iweje? Abakwe na mtoto wako?”“Jamani, mwanangu sio mbakaji. Samahani Erick, naongea haya ila kiukweli huyu mwanamke ni mwanamke ambaye nilimpenda sana nab ado ninampenda yani nusu na robo ya maisha yangu ipo kwenye mikono ya huyo mwanamke, unionavyo mimi nimebakiwa na robo tu ya maisha hapa nilipo”Baba Angel hakujibu lolote lile, ila gafla pale walipokaa alienda mwanamke mmoja na kumkunja baba Abdi kisha akamwambi,“Bahati! Bora leo nimekuona, wewe mwanaume ni mbaya sana, uliniacha na mimba, nimehangaika nayo peke yangu na nimekutafuta sana ila sikukupata kabisa, nimelea mtoto kwa shida sana tena peke yangu kwahiyo leo mguu wako mguu wangu twende nyumbani ukamuone mtoto wako na ikiwezekana tutaondoka wote kwenda kwako ili mwanangu nae apate maisha mazuri, yani unatanua tu wakati mtoto anapata shida”“Duh utaniumiza jamani, hebu niachie kwanza”Yule mwanamke akamuachia kisha baba Abdi akamwambia mama Angel,“Haya ndio madhara uliyonisababishia baada ya kuniacha, sijui sasa huyu ni mtoto wangu wa ngapi!”Kisha akainuka na kuondoka na yule mwanamke, kwa upande mwingine mama Angel alimsikitikia sana Bahati kwani kwa tabia alikuwa akimfahamu vizuri sana, hakuwa na tabia mbaya kusema labda kachukua mwanamke huyu mara yule ila kuna madawa alipewa ndio yamesababisha awe katika hali ile na kumsababishia kuwa na watoto wengi sana mpaka anahisi kuchanganyikiwa kabisa.Basi walipomaliza kula ni moja kwa moja waliinuka na kuelekea nyumbani ambapo moja kwa moja waliamua kwenda kuoga tu na kupitiliza kulala.Kilikuwa ni kipindi cha kujiandaa na mitihani ya taifa, kwahiyo kwa kipindi hiko Junior alikuwa anakaa macho mpaka usiku sana akijisomea, na siku hiyo alikaa sana usiku akijisomea mwisho wake kesho yake alichelewa kuamka, kwahiyo alipitiliza.Vaileth alishangaa sana kwa siku hiyo kutokumuona Junior akienda shuleni asubuhi, basi aliamua kwenda moja kwa moja chumbani kwa Junior ili kumuamsha,“Junior, wewe Junior, muda umeenda sana huendi shule?”Junior alikurupuka sana na moja kwa moja kwenda kuoga, sasa wakati Vaileth akitoka chumbani kwa Junior mama Angel nae alikuwa akipita pale na kugongana macho na Vaileth, kwakweli mama Angel alimshangaa sana Vaileth kwani tabia za Junior zilikuwa zinajulikana.Junior alikurupuka sana na moja kwa moja kwenda kuoga, sasa wakati Vaileth akitoka chumbani kwa Junior mama Angel nae alikuwa akipita pale na kugongana macho na Vaileth, kwakweli mama Angel alimshangaa sana Vaileth kwani tabia za Junior zilikuwa zinajulikana.Basi akamshtua pale Vaileth ambaye alishtuka utafikiri kashtuliwa na nini, kisha mama Angel akamuuliza,“Wewe umeenda kufanya nini chumbani kwa mtoto wa kiume?”“Aaaah mmmh mama….”“Acha kujiuma uma, hebu eleza maelezo kamili”“Mama ni hivi, leo sikumuona Junior kwenda shule, siku hizi huwa anasoma sana nikahisi labda kapitiliza kulala basi ndio nikaja kumuangalia na kweli nimemkuta alipitiliza kulala”“Ni hivyo tu na hakuna lingine?”“Kweli mama, ni hivyo tu mama”“Mmmmh! Sema kama kuna mengine!”“Sasa mama, mengine yapi na Junior ni mtoto mdogo”“Mtoto mdogo! Anatembea na wakubwa kushinda hata umri wangu huyo mtoto hata haaminiki”Mara Junior nae alitoka chumbani akiwa kavaa sare za shule sasa huku ana haraka kweli kiasi kwamba hata hakuangalia kama mamake mdogo pamoja na Vaileth walisimama kwani aliwapita pale pale na kuondoka, ilibidi mama Angel amkimbilie nje na kumsimamisha,“Wewe Junior vipi?”“Nimechelewa kweli leo mamdogo”“Ngoja nikuwaishe shule basi”Ilibidi mama Angel akachukue funguo haraka haraka na moja kwa moja kutoka nje halafu kupanda na Junior kwenye gari na kumpeleka moja kwa moja shule.Ila njiani mama Angel alikuwa akimuuliza baadhi ya maswali Junior,“Nasikia unasoma sana Junior?”“Ndio mamdogo, sitaki kufeli”“Hongera sana kwa hilo”“Asante sana, yani namshukuru bamdogo sana kwa kuniokoa toka kwenye njia mbaya, pia nakushukuru nawe mamdogo ila shukrani zangu za pekee nitakujakumwambia mtu huyu wa kuitwa Vaileth yani huyu amekuwa msaada mkubwa sana kwangu na kunifanya nisome kwa bidii, amekuwa akiniambia vitu vyenye uhalisia sana, naona niliyokuwa nayafanya yote hayana maana tena kwenye maisha yangu”“Oooh nafurahi kusikia hivyo”Basi safari iliendelea hadi shuleni kwakina Junior.Walipofika shule, Junior alimshukuru sana mamake mdogo basi alimshusha, na wakati amemshusha tu mwalimu wa nidhamu katika shule hiyo ambaye ni mwalimu Harun alimfata mama Angel na kusalimiana nae kisha alimuuliza,“Kumbe ni wewe ndio unakaa na Junior siku hizi?”“Ndio ni mimi”“Oooh hongera sana, kwakweli unastahili pongezi yani umeweza kuibadili tabia ya Junior kiasi hiki!! Hongera sana, siku hizi yupo vizuri kwa maudhurio shuleni, siku hizi anasoma kwa bidii na anafanya mitihani vizuri naamini Mungu atamsaidia hata mtihani wa mwisho atafanya vizuri sana”“Asante sana mwalimu”Basi mama Angel aliongea ongea kidogo pale na mwalimu na kuagana nae halafu akaondoka zake, ila wakati anakatisha gari lake kuna mtu alimuona na kuamua kulisimamisha gari lake mahali kisha akashuka na kumfata yule mtu ambapo alimshika bega yani yule mtu alishtuka sana kwani hakutarajia kukutana na mama Angel, basi mama Angel alimuangalia na kumsalimia,“Za siku nyingi Sia”Sia alijibu kwa kujiumauma,“Nzuri tu”“Nasikia ulitaka kupafahamu kwangu, haya twende basi ukapafahamu”“Aaaah hapana, leo nina kazi nyingi sana”“Maana niliposikia nikasema sio vizuri wakati muhusika nipo, leo nimekutana na wewe nimefurahi sana na kukuomba twende ukapafahamu kwangu”“Hapana Erica”Kisha Sia akaondoka zake, basi mama Angel alimuangalia sana kisha akarudi kwenye gari lake na kuelekea nyumbani kwake.Mama Angel alivyofika kwake alijiandaa tena na kutoka kwani alijikuta akimkumbuka sana mama yake, basi aliamua kwenda kwa mama yake siku hiyo ili akamsalimie.Alipofika kwa mama yake alishangaa sana kukutana na rafiki yake wa muda mrefu sana Fetty, basi walikumbatiana pale na kusalimiana, kisha alikumbatiana na mama yake na kusalimiana nae, basi walianza kuongea mawili matatu,“Kwanza kabisa Fetty sikutegemea kama ningekukuta huku ujue!”“Ni kweli, ila leo jamani nimesema acha nije kwa mama kupumzisha mawazo na akili kidogo, yani mimi ndoa imenifikia kooni jamani! Maji ya shingo kabisa yamenifika”“Vipi tena?”“Unajua karibu tunaanzisha timu ya mpira pale nyumbani maana sio kwa watoto wale jamani! Kweli nilijitoa muhanga kuishi na Bahati, niliamua kuolewa nae maana alipokuwa anaelekea kipindi kile ni kuwa kichaa, basi nikasema isiwe kesi ngoja nijitoe niolewe nae, na kweli tulioana na mwanzoni tukaishi vizuri tu. Kivumbi kilipoanza ni pale mtoto mmoja baada ya mwingine kuja kubwagwa kwangu yani naletewa watoto wa kila sampuli, sasa majuzi nimeletewa tena mtoto mwingine, kwakweli nachoka ujue yani nachoka sana”“Eeeeh pole jamani Fetty”“Asante, ndiomana nipo hapa ili mama anipe busara zake”“Mwanangu, sijui kama nitakupa busara nzuri sana mimi sababu mimi nina hasira mno ten asana. Baba yao hawa alizaa mtoto huko na mama wa mtoto pamoja na mtoto wakaja hapa, hakika niliwatimua kama mbwa, najua unamfahamu Derrick, yule usishangae undugu wake na Erica ukoje, yani ni baba mmoja hawa ila mimi niliwatimua, jamani mimi nina hasira sana. Ila sikushauri mwanangu kuwatimua ila ongea na mumeo ajenge nyumba kwaajili yako na watoto wako kwani leo na kesho ni ugomvi mkubwa utatokea hapo”“Mama, hata akijenga nyumba kwaajili yangu na watoto wangu kumbuka ile moja haiwezi kuwatosha watoto wote wale, yani lazima watanifanyia fujo tu”“Basi mwambie akupe hela hata za mtaji ili ufanyie kitu cha maana, ila Fetty si ulikuwa unafanya kazi wewe lakini?”“Ni kweli nilikuwa nafanya kazi mama, ila kuolewa huku nako ni balaa, yule mume wangu alinishauri jambo na kwa muda huo niliona ni jambo la msingi sana kuwa tushirikiane nae kwani alisema ni vyema tushirikiane na biashara alizokuwa akifanya, na kweli tumeshirikiana vizuri tu na ile biashara inaingiza hela kw asana tu ila kwasasa nilipumzika kidogo kwani aliniaomba nikae nyumbani kuangalia viumbe vyake yani ndio kila leo vinaongezeka, kwakweli nimechoka”Basi mama Angel alimuuliza,“Kwahiyo kuna watoto wangapi kwasasa?”“Yani, kwasasa nyumbani kwangu kuna watoto kumi, ndiomana nimechanganyikiwa kwasasa. Halafu rika lao sasa linafanana mwanzo mwisho”“Kheee pole sana”“Asante yani hata sijui cha kufanya”Basi mama Angel akamshauri jamabo,“Kama utaweza Fetty, naomba siku umshauri mumeo mje nae hapa ili niongee nae kidogo”“Sawa mama, hakuna tatizo”Kiukweli hata mama Angel aliumia moyo, ingawa yeye hakuwahi kuletewa mtoto wan je ya ndoa ila aliweza kuona ni kwa jinsi gani ile hali ya kuletewa watoto inavyoumiza moyo wa mwanamke mwenzie.Basi mama Angel aliamua kuaga kwa mama yake na hivyo kuondoka akiwa ameongozana na Fetty ambaye aliomba aachwe njiani kwanza maana kuna mahali alikuwa akipitia, basi alifika njiani na kumshusha halafu mama Angel akaondoka na kurudi nyumbani kwake.Junior alipotoka shuleni leo, moja kwa moja alipitiliza jikoni ambapo Vaileth alikuwa akipika, basi alikuwa akimuangalia sana anavyopika huku akitabasamu yani kwa muda huo hata Vaileth hakujua kama kuna mtu anamuangalia wala nini, kisha Junior alisogea karibu yake na kumkumbatia kwa nyuma, yani Vaileth alishtuka sana ila alipogeuka alimkuta ni Junior,“Jamani Junior, umenishtua ujue”“Ulijua ni nani?”“Aaaah mimi sikujua bhana, sijui umeninyatia, muone vile”“Usishtuke jamani Vaileth ila nashukuru sana kwa kunijali, yani leo umefanya kitu kikubwa sana kwangu. Asante sana Vaileth”Vaileth alitabasamu tu, kisha Junior aliondoka na kwenda chumbani kwake ambapo nae Vaileth alimaliza kupika na kueleka chumbani.Muda wa kula ulipofika ni wote walifika mezani na kula kile chakula halafu kila mmoja alielekea chumbani kwake ikiwa ni pamoja na Vaileth.Ila usiku wa leo ulikuwa ni wa tofauti sana kwa Vaileth kwani alijikuta kichwa chake kikiwa kimezongwa na lile tukio ambalo lilitokea jikoni la Junior kumkumbatia kwa nyuma, alijikuta kila akikaa anapatwa na wazo hilo, akajisemea,“Jamani! Nini sasa, kwanini Junior lakini. Mmmmh mtoto mdogo huyu jamani, kwanini namuwaza hivi!!”Alijitahidi mno asimuwaze Junior ila kwa siku hiyo hilo wazo liligoma kutoka katika akili yake zaidi zaidi lile wazo likaanza kukumbusha na matukio ya nyuma, kamavile ambavyo anakaa karibu na Junior akimpa ushauri, jinsi Junior alivyokuwa akimfuta machozi na kummbembeleza, na jinsi alivyomsaidia kukuna nazi, alijikuta akimuwaza sana Junior yani hadi alikosa amani katika moyo wake.Basi palivyokucha aliamka na kufanya shughuli zake ila alijikuta kwa siku hiyo akiwa na hamu sana ya kumuona Junior kwanza.Wakati anaosha vyombo huku akiwa na mawazo hayo, nyuma yake alitokea Junior na kumkumbatia tena kwa nyuma halafu akambusu na kumwambia,“Naenda shule Vaileth, badae”Halafu Junior akaondoka na kumuacha Vaileth akiwa kama amesizi kwa muda kidogo na kupumua kwani kile kitendo ndio kwanza kinamzidishia mawazo maradufu.Leo baba Angel ndio aliamua kumuita Steve ambaye ni mdogo wake Dora kwenye ofisi yake, basi Steve nae alifika kwa muda muafaka kabisa na kuanza kuongea nae,“Karibu sana, sasa nilishaongea na Dora tayari na nilikuwa na biashara yangu mpya ni vyema nikakuweka ili uisimamie”“Oooh asante sana”“Sawa, ila kwasasa unaishi wapi?”“Kwasasa naishi nyumbani kwetu”“Ila wewe ni kijana mkubwa ujue!”“Ni kweli, ila sikuwa na uelekeo sahihi ndiomana ikatokea hivi”Basi baba Angel akainuka na kutoka nae ambapo aliondoka nae hadi kwenye biashara yake mpya na kumuonyesha huko, ambapo walikubaliana kuwa kesho yake aende kusaini mikataba yake halafu aweze kuanza ile kazi ambapo waliagana na baba Angel kisha Steve akaondoka zake.Steve akiwa njiani, alishikwa began a mtu kugeuka akamuona Sia, basi alishangaa sana,“Kheee Sia!”“Kama umeona mzuka eeeh! Ndio ni mimi”“Za siku? Mtoto hajambo?”“Kheee leo hata unakumbuka kuhusu mtoto kweli! Si ni wewe uliyemkataa yule mtoto na kusema sio wako? Leo unamkumbuka wa nini? Poa tuachane na hayo ila ngoja nikwambie kilichonileta”“Kwanza umejuaje kama nipo mitaa hii?”“Hujui tu Steve ila huwa nakufatilia kupita maelezo ya kawaida, huwezi kunikimbia mimi, sikukufata sio sababu sijui pa kukupatia ila sikuwa na sababu ya kukufata ndiomana niliacha uende”“Mmmh!”“Haya, tuachane na hayo kwanza, ngoja tuongee ya maana. Kuna kitu nataka tufanye mimi na wewe”“Kitu gani hiko?”“Nitakwambia, ila najua siku moja utakaa chini na kusema katika maisha yako yote hujawahi kuona mwanamke mwenye akili kama Sia, mimi nina akili wewe usinione hivi!! Kuwa na akili sana sio mpaka usome sana, wengine tuna akili zetu tu za kuzaliwa. Kwakweli mimi nina akili na nina haki ya kujisifia. Kwanza kitu nilichokuwa nakitaka kwako kwa muda mrefu ni kuona ukifanya kazi kwenye kampuni ya Erick na ili limeenda kutimia, kwakweli hiyo ni moja ya furaha yangu. Ila naomba chondechonde usimwambia dada yako kuwa umeonana na mimi. Achana na habari za ndugu zako, mimi na wewe ni wazazi, achana na mambo yao, hawakuwepo wakati wa kupeana mimba na wala hawakuwepo leba na mimi kwahiyo achana nao. Mimi ndio mama wa mtoto na wewe ndio baba wa mtoto, kwahiyo achana na maneno ya ndugu zako. Nitakufata tena ili tuongee vizuri, kwaheri”Halafu Sia aliondoka na kumuacha Steve akimuangalia pale bila hata ya kummaliza, ila tu na yeye aliamua kuondoka tu.Mama Angel alikuwepo tu nyumbani kwake, basi muda huu alikaa sebleni na Vaileth ila alishangaa kumuona Vaileth kila muda akionyesha tabasamu, yani alitabasamu peke yake basi akamuuliza,“Vipi wewe? Kitu gani hiko kinachokufanya utabasamu mwenyewe?”“Hamna kitu mama”“Mmmmh jamani! Hamna kitu kweli!! Yani kwa jinsi unavyotabasamu basi ni lazima kuna kitu kinakufurahisha tu”“Hamna mama, kuna kitu cha zamani sana nimekumbuka ndio kilikuwa kinanichekesha”“Jamani tuwe tunashirikishana ili tucheke wote basi!!”Vaileth akatabasamu tu na kuendelea na mambo mengine kwani aliinuka na kwenda jikoni, baada ya muda kidogo Erick na Erica walirudi na moja kwa moja walipomsalimia mama yao tu Erica alibaki pale na kuongea na mama yao,“Mama, kesho kutwa yani Jumamosi Samia anakuja hapa nyumbani kwetu”“Hamna tatizo, mwambie anakaribishwa”“Oooh mama, asante sana”“Mimi nilikwambia sina tatizo lolote na huyo Samia, hata akitaka kuja kulala mwambie ni ruksa tu”“Jamani mama, asante sana”Basi Erica aliondoka zake na moja kwa moja kwenda kumpa habari kaka yake kuwa mama yao amemkubalia kwa ujio wa Samia, maana kwa kipindi hiko ndio ilikuwa habari yake kuu yani kila alichozungumzia ni kuhusu Samia.Basi moja kwa moja alienda chumbani kwa Erick, na kama kawaida yake alifungua tu mlango bila hata kubisha hodi ambapo alimkuta Erick akiwa anavaa,“Oooh samahani Erick”“Unajua wewe, siku hizi unafanya makusudi maana hii bahati mbaya mmmh! Ndio kila siku jamani!”“Si unisamehe!”“Yani nahisi mwili wangu unaujua kama wako vile, itabidi na mimi siku nikuvizie ili nikuchungulie vizuri”Basi Erica alicheka tu halafu akaondoka mule chumbani kwa kaka yake na kurudi chumbani kwake.Basi Erica alifika chumbani kwake na kujiandaa kuoga, na alipotoka kuoga alijiuliza sana kwanini kila akienda chumbani kwa Erick basi alimkuta akiwa ametoka kuoga, anavaa au amejilaza mtupu kabisa,“Mmmmh kwanini sasa inakuwa hivi jamani!! Yule Erick anaweza kuona kweli nafanya makusudi ila mimi sifanyi makusudi bali inatokea tu hata mimi sielewi ni kwanini inatokea”Aliwaza ila akaona haina maana kuwaza kitu kama hiko kwakuwa kimeshatokea tayari.Usiku a leo baba Angel alimueleza mama Angel namna alivyozungumza na Steve na kazi ambayo alimpatia kwenye duka lao jipya,“Duka lipi hilo?”“Lile duka ambalo nilimpeleka hata Erick”“Aaaah kumbe duka lile!! Kumbe hakukuwa na msimamizi pale?”“Ndio, sababu sikupata mtu ninayemuamini, ila kwasasa imekuwa afadhari sababu msimamizi huwa napenda nimfahamu ndugu zake na wazazi wake”“Aaaah nimekuelewa mume wangu, umefanya vizuri kwa hilo”Muda wa kulala ulifika wakalala tu.Kulipokucha siku hiyo mama Angel alitoka nyumbani kwake mapema kabisa akienda hospitali, kwani kwa kipindi hiko alikuwa ameanza kliniki.Basi moja kwa moja alienda kwenye hospitali ambayo alikuwa akitibiwa kwa kipindi hiko maana kwa yule dokta Maimuna alishaacha kabisa kwenda, basi alifika hospitali na kufanyiwa huduma zote alizozitaka na baada ya hapo akaanza kuondoka ila wakati anatoka akakutana na dokta Maimuna, ambaye alimfurahia kumuona na kumsalimia vizuri sana,“Jamani mama Angel, za siku nyingi jamani!”“Nzuri tu, za wewe!”“Salama, ndio umenikimbia jamani toka siku ile. Yale mambo ya kawaida tu ndugu yangu hakukuwa hata na haja ya kunikimbia wala nini, mimi na wewe tungeongea kiuanamke na kuyamaliza, asiyeyajua matatizo ya hawa wanaume nani? Tunawaelewa vizuri sana, hawa wanaume wana matatizo balaa, yani unaweza ukaona kama wewe ndio ulitendewa jambo baya ila ukisikia la mwenzio utasema kumbe wewe hakuna baya ulilotendewa”“Oooh nimekuelewa”“Tupate siku tuzungumze kuhusu hili, wala sikulazimishi sijui umuonyeshe mtoto Rahim au umpeleke Rahim kwa mtoto, huo ni uamuzi wako, wewe ni mama na ndiye mwenye maamuzi na mtoto wako, mimi naongea tu kwa upande kama dokta na kwa upande mwingine kama mwanamke mwenzio, mimi mwenyewe nishawahi kupitia matukio mbalimbali ya kukataliwa ila kwasasa niliruhusu maisha yaendelee mbele na wala sioni kama nina kasoro yoyote zaidi ya kuishi kwa amani na furaha”“Nimekuelewa”“Usiseme umenielewa tu, inatakiwa tuzungumze jambo hili kwa upana sana ndugu yangu, basi naomba nikikutafuta upokee simu yangu”“Sawa hakuna tatizo, nitapokea simu yako na tutawasiliana vizuri sana”Basi dokta Maimuna aliagana nae na moja kwa moja mama Angel alienda kupanda kwenye gari yake na kuondoka ila siku hiyo hakwenda nyumbani kwake kwani moja kwa moja alikwenda ofisini kwa mume wake, yani kwenye ile ofisi hata walivyokuwa wakimuona amefika basi wote walitulia kimya kwani wengi wao walionekana hawapendi mama Angel kufika ofisini kwa mume wake.Leo ilikuwa siku ya Ijumaa na wanafunzi wa kidato cha nne walikuwa kwenye maandalizi ya mwisho kwaajili ya mtihani wa taifa unaoanza Jumatatu, kwahiyo wengi walionekana wapo makini sana na masomo yao.Siku hiyo darasani kwakina Angel kila mmoja alikaa kwenye kona yake akijisomea, yani kwa siku hiyo kila mtu aliona kuwa ajikumbushie yale waliyoyasoma kwa kipindi kirefu.Muda wa kutoka darasani ulifika na darasa lilikuwa kimya sana, basi Angel alifunga daftari zake na kuzirudisha kwenye begi lake ili aondoke, ila alipoangalia vizuri darasani aliona hakuna mwanafunzi zaidi ya mmoja tu ambaye nae alikuwa makini na kujisomea kwa muda huo ila walijikuta wakitazamana macho na mwanafunzi huyo, huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni Samir, yani walipotazamana hivi moyo wa Angel ulilia pa yani alijikuta kwa muda huo akitamani sana hata akimbatiane tu na Samir halafu moyo wake utaridhika yani alijiona akifanya hivyo basi Jumatatu ataingia kwenye chumba cha mtihani akiwa na furaha moyoni.Wakati Angel akitafakari hayo alishangaa tu kuona Samir akiinuka na kwenda karibu yake halafu alimkumbatia kwa nguvu sana inaonyesha hata yeye alikuwa na wazo kama la Angel.Wakati Angel akitafakari hayo alishangaa tu kuona Samir akiinuka na kwenda karibu yake halafu alimkumbatia kwa nguvu sana inaonyesha hata yeye alikuwa na wazo kama la Angel.Yani ilipita kama dakika tano kila mmoja kushtuka na kugundua kuwa wanachofanya pale si sahihi, basi waliachiana halafu kila mmoja akatoka darasani ila walipofika nje waliona kumbe wenzao kuna mahali wamekutanishwa kwa muda huo ndiomana mule darasani walibaki wenyewe tu, basi walisogea walipo wenzao yani wote waligeuka nyuma kuwaangalia wao wawili, basi mwalimu aliwauliza,“Angel na Samir, nyie ndio mlikuwa wapi?”Wote wawili walitazama chini tu, basi mwalimu aliendelea na mada ambayo alikuwa akizungumza pale na wanafunzi wote,“Yani kama nilivyowaambia umakini unahitajika kwa kiasi kikubwa sana, yani jitahidi kusoma maelekezo vizuri kabisa kabla ya yote yale, halafu kumbuka kuandika namba yako ya mtihani, sio jina ni namba jamani maana kuna watu kwenye moko mlitufanyia ujinga, sasa mkirudia tena kwenye taifa mjue imekula kwenu na zero itawahusu”Wanafunzi walikuwa kimya kabisa wakisikiliza maelekezo ya mwalimu, na pale mwalimu alipomaliza kutoa maelekezo ndipo alipowaruhusu kwenye nyumbani.Muda huo dereva wa kumfata Angel tayari alishafika na kumfanya Angel aende kupanda lile gari na kuanza safari ya kwenda nyumbani kwa shangazi yake.Samir nae leo alienda moja kwa moja kwao kama kawaida, na aliona ni vyema apumzike kwanza halafu ndio aamke na kuendelea kujikumbushia masomo yaliyopita kwani aliona kama kila kitu ameshasoma ila tu ni kujikumbushia kwaajili ya mtihani.Basi muda alipoanza kujisomea alifika dada yake na kumwambia,“Kaka, kesho kuna mahali nitaenda kwa rafiki yangu”“Kheee haya, sina pingamizi mimi”“Asante kaka”Basi dada wa Samir alifurahi sana baada ya kuruhusiwa na kaka yake, hivyobasi aliondoka na kwenda kufanya maandalizi ya siku ya kesho ambayo ameapanga kwenda kwa rafiki yake.Samir alitulia na mama yake aliporudi siku hiyo alimuita mwanae na kuongea ongea nae kidogo,“Mwanangu, nakutakia mitihani mema jamani, maana mimi kesho asubuhi nasafiri”“Ooooh kumbe hutokuwepo mama!”“Ndio sitakuwepo, kuna mahali inabidi niende nadhani nitarudi baada ya miezi miwili au mitatu”“Jamani mama, inamaana hata kwenye mahafali yangu hutokuwepo?”“Sitakuwepo ila tutakuwa pamoja mwanangu jamani, hata usijisikie vibaya wala nini”“Ila ile shule nayo, sijui kwanini mahafali wameyapanga baada ya mitihani!”“Sio, vibaya lakini kwani mnakuwa huruzaidi tena ni vizuri zaidi. Ila mwanangu usijali”Basi mama Samir alimpa Samir ushauri idogo pale kisha akaondoka zake kwani alitakiwa kupata muda wa kutosha kujiandaa kwaajili ya safari ya kesho yake.Mama Angel akiwa bado ofisini kwa mume wake, aliamua kuongea nae jambo ambapo mumewe aliamua kuondoka nae kwa muda huo ili kwenda nae anapopataka mkewe.Basi muda huu baba Angel aliwaaga wafanyakazi wake na kuondoka zake na mkewe ila kiukweli waliumia sana kwenye mioyo yao kwani hawakupenda hata kidogo kabisa kuona mama Angel akiongozana vile na mumewe.Basi walitoka pale na moja kwa moja walienda sehemu ambapo mama Angel alihitaji kupelekwa na mume wake ambapo palikuwa ni kwenye biashara mpya ya mumewe ambapo kamuweka Steve kuwa msimamizi wa biashara hiyo, na kweli walivyofika pale Steve alikuwa tayari yupo mahali pale basi walimuita na kusalimiana pale, kisha mama Angel alianza kuhojiana nae,“VIpi Steve, umepaonaje hapa?”“Pako vizuri tu, hata wateja wapo”“Ila unadhani ni kipi kifanyike ili tuweze kutengeneza wateja wengi zaidi eneo hili?”“Aaaah mama, kwanza bado nipo kuangalia mazingira ya hapa ila nikishafanikisha basi nitawaambia cha kufanya, ila kwasasa ngoja niangalie kwanza mambo yalivyo”“Basi sawa, ila nakuomba jambo moja kubwa”“Jambo gani?”“Hapa kwenye biashara sitaki umkaribishe Sia”Kisha mama Angel akamtazama mumewe na kumwambia,“Baba Angel, hii biashara ya hapa nitakuwa nakuja mwenyewe mara kwa mara kuiangalia”“Sawa, hakuna tatizo mke wangu”Basi baada ya hapo waliizungukia zungukia ilebiashara halafu wakaondoka zao.Steve na alikaa kaa kidogo na kuamua kufunga ili kuondoka ila wakati anaondoka tu, njiani akakutana tena na Sia ambaye alimsimamisha na kuanza kuongea nae tena,“Steve, naona leo mabosi wako walikuja na walikuwa wakitembelea biashara yao”“Unajua kuna mara nyingine huwa sikuelewi kabisa Sia, yani mimi hata huwa sielewi kuwa ni wewe ndiye mwanamke niliyekuwa naishi nae”“Na kamwe huwezi kunielewa hadi ile siku itakapofika na wewe kukaa chini na kugundua ni akili za kiasi gani zilizokuwa katika kichwa changu”“Mmmmh!!”“Haya, acha kuguna kwanza. Nataka kuongea nawe mambo ya maana”“Mambo gani hayo?”“Kwanza, wote ambao huwa wanaachiwa duka na Erick basi huwa anawaachia vibali vyote vya duka lake dukani, vipi na hapo?”“Mmmh ndio, hivyo hivyo”“Sasa tulia mimi nikufundishe jambo wewe, tena jamabo la akili mno. Kesho nitakuja hapo dukani yani nitaingia ndani ya duka”“Kufanya nini?”“Utaona hiyo kesho ninachokuja kufanya”“Unajua mwenyewe kasema nisikualike kabisa wewe kwenye duka lake? Unajua tayari kapatwa na mashaka kuhusu wewe! Yani limekuwa ni onyo lake namba moja kuwa nisikualike pale dukani”“Hebu na wewe muda mwingine kuwa kama mwanaume, sasa wewe unatishiwa na mwanamke? Kwani mwanamke yule ndio nani? Nilijua Erick kakuambia hivyo!! Kumbe ni yeye ndio kasema hivyo, hebu acha ujinga huko. Mimi kesho nafika hapa. Kwaheri”Basi Sia akamuaga na kuondoka zake.Kiukweli kwa muda huo Steve akaona hata asiende kwao kwanza, kwani moja kwa moja aliondoka na kwenda nyumbani kwa dada yake, ingawa muda ulikuwa umeenda ila aliona kuwa ni vyema kwenda kwa dada yake kwanza ili kujaribu kuongea nae kuhusu hilo na aone ni kitu gani atamshauri.Na alipofika tu kwa dada yake alimkuta akiendelea na mambo yake mengine, basi alianza kuongea nae pale na kumuelezea kuanzia siku ya kwanza ilivyokuwa na mpaka siku hiyo,“Mmmmh mimi ndiomana huwa nasema yule Sian i jasusi, maana ana mipango hiyo sijawahi kuona, yani hapo anachokipanga anajua yeye na roho yake ila mdogo wangu unatakiwa kuwa mwanaume kweli, hebu simama katika nafasi yako usiruhusu mwanamke akakuharibika sababu ya raha zake. Unajua yule Sia hata wa kumgananisha nae sijaona kwakweli, yani iko hivi Sia alimpenda sana Erick tena alitamani mno mali za Erick na alipenda yeye ndio awe mmiliki na sio Erica kama ilivyokuwa. Ila kwasasa roho inamuuma sana kila anapoona kuwa wanapendana, yani mdogo wangu huyo Sia atakudanganya tu ila anachokitaka hapo lazima mwisho wa siku atakuliza tu na kukufanya ukose kazi kabisa”“Sasa dada nifanyeje?”“Usikubali aingie kwenye ofisi ya duka, kwanza anafata nini? Erick sio mjinga kiasi hiko, ni kweli huwa anaweka vibali dukani ila hainamaana kwamba, hivyo ndio vibali pekee vya biashara yake, jamani yule kafanya biashara toka siku nyingi sana, yani hiyo sio biashara yake ya kwanza wala nini ila hiyo ni kati ya biashara nyingi alizonazo, hebu acha kusikiliza ujinga wa Sia kabisa, yani usitake kufata anachokisema, kwanza ni mwanamke gani huyo? Anajishughulisha na nini? Anapata wapi pesa za kukufatilia? Mmmmh!”Dora akawaza kitu na kusema tena,“Unajua kuna jambo nimewaza hapa, usikuite Sia kuna watu anashirikiana nao halafu hao watu wanaugomvi na Erick, itakuwa hao watu wana lengo la kumshusha Erick kwahiyo wanamtumia huyo mjinga kutekeleza mambo yao, ila bado nabaki na msimamo wangu ule ule usimkubalie Sia kabisa, na ikishindikana, mwambie ukweli bosi wako”“Sawa dada, nimekuelewa vizuri sana”Basi waliagana na dada yake pale na kuondoka kwani muda ulikuwa umeenda kwakweli na aliona kuwa ni vyema kama akiwahi na kupata muda wa kupumzika kidogo ili kesho yake aweze kuwahi kwenye kazi yake.Mama Angel na baba Angel muda huu walikuwa nyumbani kwao, na walikaa pamoja mezani na watoto wakila, na walipomaliza walikaa kidogo sebleni huku wakiongea ongea ambapo wakakumbuka kuwa Jumatatu kidato cha nne wanaenda kuanza mtihani wa taifa, basi mama Angel alamwambia baba Angel,“Itabidi Kesho twende kumuona Angel kidogo na kumtakia mtihani mwema”“Kweli kabisa, umeamua vyema”Waliongea pale na moja kwa moja kila mmoja alienda kulala tu.Kulipokucha, baba na mama Angel walifanya kwanza mambo mengine waliyotakiwa kufanya asubuhi hiyo maana siku hiyo hawakwenda kwenye biashara zao wala nini.Walipomaliza mambo yao walijiandaa na kutoka.Walipoondoka tu, pale nyumbani walibaki Vaileth na watoto kama kawaida ila Junior na leo ndio alikuwa chumbani kwake kabisa kajifungia mwenyewe akiendelea na masomo yake kama kawaida.Sebleni walikaa Erica na Erick, muda kidogo rafiki wa Erica aitwaye Samia alifika kwakweli Erica alifurahi sana na kumkaribisha vizuri sana rafiki yake, ila siku hiyo ndio ilikuwa mara ya kwanza kwa Samia kumuona Erick maana siku zote alikuwa akihadithiwa tu na Erica kwamba ana pacha wake wa kuitwa Erick, basi alifika pale na kumuangalia sana huku akiongea ongea, ambapo aligundua kuwa Erick alipenda sana mikanda ya ngumi yani ile mikanda yenye muvi za mapigano, basi akasema pale,“Wiki ijayo Erica nitakuja tena na nitawaletea mkanda mmoja hivi wa ngumi, ni mzuri huo”Erick aliposikia hivyo basi alianza kusapoti na yeye huku akiulizia vizuri kuhusu huo mkanda, alipenda uletwe hata Jumatatu,“Kama utaweza, basi Jumatatu mletee ilia je nao nyumbani niuone”“Oooh sawa, hakuna tatizo. Unapenda mikanda ya ngumi eeeh!”“Napenda sana yani”“Basi usijali, kwetu zipo muvi nyingi sana za ngumi maana hata kaka yangu pia huwa anapenda kuangalia”“Nitafurahi sana ukizileta”Basi Erick alianza kumfurahia Samia sababu ya hizo muvi alizosema kuwa angezileta kesho yake.Leo Steve akiwa dukani, kama ambavyo Sia alipanga, ni muda alifika pale dukani na kukutana na Steve na kumtaka kuwa waende ofisini,“Hapana haitawezekana, maana ofisi bado ipo kwenye matengenezo kwahiyo kuna mafundi”“Ila mimi nahitaji kuiona tu”“Kwani ukishaiona utapata faida gani wakati bado haijaisha?”“Hivi mbona Steve umekuwa na tabia kama za kike jamani! Ndiomana unashikiliwa akili na ndugu zako, hivi wewe huwezi kujisimamia mwenyewe jamani! Hujui kama wewe ni mwanaume unatakiwa usimame mwenyewe jamani! Hebu ifike wakati uwe mwanaume Steve”“Mimi ni mwanaume ndio na siwezi kukuruhusu leo kuingia kwenye ofisi hii”“Huo sio uanaume Steve, yani endelea kujidanganya ila huo sio uanaume wala nini”Kisha Sia akaondoka zake, ila alionyesha kwa kiasi Fulani amechukia sana ingawa alionekana kuwa amekubaliana na hali halisi.Basi Steve alikaa na kujiuliza kuwa kitu ambacho yule mwanamke alikuwa akikitaka ni kitu gani, yani kwanini ang’ang’anie ofisini kwa Erick kiasi kile? Ila ukweli wote alikuwa nao mwenyewe Sia kwani hata yeye awaze vipi bado asingeweza kupata jibu la aina yoyote ile.Mama Angel na baba Angel kama ambavyo walikuwa wamepanga, basi leo walienda moja kwa moja kwa Tumaini ili kumuona mtoto wao na kumtakia mtihani mwema, na walipofika tu kweli walimkuta yupo ndani anajisomea, basi walimuita na kumsalimia kisha wakamtaka kuendelea na masomo yake kama kawaida, basi na wao walikaa wakiongea pale na Tumaini kuhusu mambo mbalimbali, na muda kidogo mume wa Tumaini nae aliwasili na kusalimiana nao pale halafu alianza kuongea nao,“Jamani eeeh! Leo niliamua kufatilia lile tukio mjue, yani nimefatilia nijue yule mdada ofisini kwangu alikuja kufanya ninina kwanini ikawa vile”“Mmmh kaka, kwahiyo umemgundua sasa?”“Yani ni hivi, yule binti alikuwa ni mgeni machoni mwa wote pale ofisini, ila nilivyouliza kwa watu wengine walidai kuwa wanamfahamu yule dada, kuwa yule dada ni mpiga madili, watu wakasema kwamaana hiyo kuna mtu atakuwa kampa kazi ya kuja ofisini kwangu ila mpaka muda huu sijajua ni mtu gani na alikuwa na lengo gani”Pale ndio maneno ya Dora yalianza kufanya kazi vizuri katika akili ya mama Angel na moja kwa moja, na kumfanya azidi kumchukia Sia kwani jibu alilokuwa nalo kwenye akili yake ni kuwa Sia hakuwa mtu mzuri tena, basi alimuuliza tena kaka yake,“Kaka Tony, hivi hakuna hata mtu mmoja aliyesema kuwa huyo dada huwa anatumiwa na nani?”“Nasikia huwa anatumiwa na watu mbalimbali, kwa maana hiyo hata kuanguka hakuanguka wala nini, yule alikuwa kwenye maigizo tu”“Ooooh sema kwa mtindo huo basi inatakiwa kuwa makini sana”“Ni kweli, haswaaa kwasisi wafanyabiashara maana utakuta mara nyingine unafatiliwa na mtu bila hata kujua kuwa unafatiliwa, ila inatakiwa kuwa makini sana. Nataka kufunga kamera kwenye ofisi yangu”“Oooh utakuwa umefanya jambo la maana sana”Kisha mama Angel alimuuliza baba Angel,“Hivi na ile ofisi mpya mume wangu umefunga kamera kweli!”“Mmmmh bado sijafunga kule”“Mi naona ni vyema nako ufunge kamera”“Sawa sawa, nitafanya hivyo tu”Basi wakaongea pale na kuamua kuaga, ambapo baba Angel na mama Angel waliondoka kwani waliona muda wao umeisha wa kuendelea kukaa mahali hapo.Mama Angel na baba Angel walipofika nyumbani waliwakuta watoto wao wakiwa makini sana na kuangalia Tv, kama kawaida mama Angel aliwatimua maana hakupenda wakae pale sebleni kwa muda mrefu ila kitendo cha kuwatimua wale watoto wake muda huo walienda tu chumba kimoja ambapo walienda chumbani kwa Erick na kuanza kuongea mambo mbalimbali, Erica alimuuliza kaka yake,“Sasa hizo muvi za ngumi Samia akizileta tutakuwa tunaangalia wapi ikiwa mama anatufukuza sebleni?”“Ooooh mbona jambo dogo hilo, sikia nikwambie mimi na wewe inatakiwa letu liwe moja. Mbona kwenye ile sebule ya juu ina Tv pia, si huwa wanasema hadi wageni waje? Mimi ndio ninafungua za vyumba vyote humu ndani kwahiyo hata usijali tutakuwa tunaenda na kuangalia kule”“Jamani, ndiomana nakupenda Erick, ila mimi picha za ngumi naogopa sana”“Sasa unaogopa nini wakati utakuwa unaangalia na mimi? Usiogope maana tutaangalia wote”“Sawa kaka yangu, basi tucheze karata na leo”Erick alikubali na kuanza kucheza karata ambapo kama kawaida walicheza sana hadi usiku na wakajikuta wameshikwa na usingizi mule mule chumbani kwa Erick.Kulipokucha, Erick alikuwa wa kwanza kuamka leo na kumshtua dada yake ambaye nae alikurupuka, kwahiyo ile tabia ilikuwa kawaida kabisa kwao maana haikuwa mara ya kwanza ukizingatia mara nyingi walijikuta wakiwa pamoja.Basi asubuhi ile nyumba nzima leo walienda kwenye ibada hadi Junior, ingawa huwa ni mbishi kwenda ibadani ila leo alienda, kwahiyo nyumba nzima waliondoka.Wakiwa ibadani, Erica alitoka mara moja maana kuna kitu alikiona nje ya Kanisa wakati wanataka kuingia, kwahiyo walipokuwa Ibadani tu aliwavizia na kutoka zake nje ili kuangalia kile alichokiona, basi aliondoka hadi lile eneo ila kuna kijana aligongana nae kikumbo na kuanza kuombana nae msamaha,“Nisamehe tafadhari”“Nisamehe mimi kwa kutoangalia mbele”“Aaaah usijali chochote, by the way naitwa Bahati, vipi wewe unaitwa nani?”“Naitwa Erica”“Ooooh jina zuri sana, hongera”“Asante”Erica macho yote yalikuwa pale alipoona alichokuwa anakitaka ila kuangalia vizuri alikuta kimeshanunuliwa, na kujikuta akisema,“Aaaargh washachukua tayari”Yule Bahati alimuuliza,“Wamechukua kitu gani?”“Kuna kiatu nilikiona pale, nikakipenda sana, yani nilitaka kukinunua jamani, wamekichukua tayari”Basi Bahati alisogea pale na Erica na kujua ambaye alichukua kile kiatu kisha kwenda kumuomba ili waweze kununua kile kiatu, yule mtu aliwaambia labda wampe hela mara mbili ya bei ya kawaida ya kile kiatu. Kilikuwa ni kiatu cha kawaida kabisa ila Erica alionekana kukipenda sana, kiliuzwa elfu tano kwahiyo yule mtu alisema labda apewe elfu kumi, Bahati akamuangalia Erica na kumuuliza,“Je utakinunua kwa bei hiyo?”Erica aliitikia tu na kufanya Bahati amuulize tena ila Erica alikaa kimya, kwani kiukweli hakuwa na hela yoyote pale ila alikuwa akijitutumua tu kuwa anataka kununua kile kiatu, badae akamwambia Bahati,“Mwache tu aende, nilikuwa nakiangalia tu”“Mmmh jamani, hadi tumemrudisha ujue!”“Aaaaah kumbe hela yenyewe sina”Basi Bahati alitoa hela yake na kununua kile kiatu kwa yule mtu kisha alimkabidhi Erica kile kiatu, kwakweli Erica alitabasamu na kufurahi sana huku akimwambia,“Asante sana”“Usijali, natumaini tutaonana tena”Basi Erica moja kwa moja alirudi tena kanisani lakini hakuna mwanafamilia wa Erica aliyegundua kuwa Erica alitoka nje ya kanisa ule muda wa ibada.Ibada ilipoisha wote wanarudi nyumbani na moja kwa moja Erica anaenda kuweka vile viatu chumbani kwake, kwakweli alivipenda sana vile viatu ingawa vilikuwa ni vya kawaida sana ila alijikuta akivipenda sana, basi alikuwa akiviangalia na kukumbuka tukio lote la kugongana na yule mtu wa kuitwa Bahati, pia alikumbuka sura ya mtu yule ilivyoonekana kwani yule mtu alikuwa na sura ya upole sana, basi alikuwa akitabasamu tu na kusema,“Anaitwa Bahati, kweli nimepata bahati ya kukutana nae, mvulana mwenye sura ya upole kiasi kile”Basi siku hiyo alikuwa na furaha sana kupita maelezo ya kawaida.Mambo mengine yaliendelea pale nyumbani kama kawaida, walipomaliza kula chakula cha usiku kwa siku hiyo, mama Angel alimuuliza mwanae,“Vipi leo ndio upako umekushukia au?”Erica alicheka na kusema,“Ndio mama”“Naona maana sio kwa tabasamu hilo ulilokuwa nalo, nimebaki najiuliza hapa, kuwa mwanangu umefurahishwa na kitu gani. Ila kama upako umekushukia basi nafurahi kusikia hivyo ila leo jamnai muwahi kulala maana kesho shule”“Sawa mama”Na muda huo huo waliondoka na kila mmoja kwenda chumbani kwake kulala kama kawaida.Ila leo mama Angel alimwambia mumewe kuwa kesho yake angeenda tena kutembelea lile duka ambalo walimuweka Steve asimamie, na mumewe hakuona kama ni tatizo kufanya hivyo kwani aliona ni jambo jema.Kesho yake wanafunzi wa kidato cha nne walikuwa wameshaanza mtihani wao wa mwisho, kwahiyo kulikuwa na ukimya sana mashuleni, na madarasa ya vidato vingine walikuwa kimya pia kwani hawakutakiwa kuonekana hata kukatisha maeneo ambayo kidato cha nne walikuwa wakifanya mtihani.Sehemu ambayo alikaa Angel ilikuwa ni kiti cha kwanza kabisa, ila mtihani wa kwanza ulipoisha na kukusanya ile mitihani, wakati wamesimama aligundua kuwa alipokaa ilikuwa ni sehemu ambayo moja kwa moja alionana na Samir ambaye alikaa mwishoni kabisa.Ila walipotazamana walijikuta wakitabasamu tu, kisha kutoka kwenye chumba cha mtihani na moja kwa moja kwenda kujipanga kwaajili ya mtihani mwingine ulikuwa ukifatia kwa siku hiyo.Leo Sia aliamua kwenda tena sehemu ambako Steve anafanya kazi, basi alifika na kuingia ingawa Steve alimkatalia, basi alivyoingia akacheka na kusema,“Hivi wewe unaweza kunikatalia mimi kweli? Wewe ni nani? Hivi unajua mimi ni nani kwa huyo Erick?”Steve alikaa kimya tu kwani alikuwa na hasira sana ila muda kidogo mara mama Angel nae aliingia mule ofisini na wakagongana macho na Sia, kiukweli mama Angel alichukia sana.Steve alikaa kimya tu kwani alikuwa na hasira sana ila muda kidogo mara mama Angel nae aliingia mule ofisini na wakagongana macho na Sia, kiukweli mama Angel alichukia sana.Akajikuta akianza kumfokea Steve,“Nilikwambia nini wewe lakini? Kufanya hii kazi hutaki au”Sia alikuwa pembeni akicheka tu utadhani aliyoyafanya yalikuwa ni mazuri, il kitendo kile cha kucheka ndio kilizidi kumchukiza mama Angel, na kujikuta akimuuliza kwa hasira,“Na wewe ni kitugani kinachokuchekesha?”“Unayenichekesha ni wewe, badala ya kuniuliza mimi kuwa imekuwaje nipo hapa unafanya kazi ya kumfokea huyo Steve, kwanza unajua kama Steve ni mume wangu? Je wewe unaweza kumtimua mume wako? Kama ilivyokuwa vigumu kwako ujue hata kwa Steve kunitimua mimi mke wake ni vigumu sana, na ukumbuke kuwa mimi na Steve tuna mtoto kwahiyo nina haki ya kujua kuwa mtoto wetu atalelewaje na ataishije”“Hivi unaongea au unaropoka?”“Kwani wewe unahisi kitu gani? Unahisi naongea au naropoka? Wewe Erica, usijifanye kuwa unajua kila kitu, kuna mengine huyajui na huwezi kuyajua maana kuna werevu na wajuaji zaidi yako”Halafu Sia aliondoka zake na kumuacha pale mama Angel akiwa na Steve.Basi mama Angel alimuangalia tena Steve kwa muda kidogo ila hakuongea jambo lolote kwa muda huu zaidi zaidi alitoka nje pia na kupanda gari lake ambapo moja kwa moja alienda ofisini kwa mume wake.Mama Angel alifika ofisini kwa mume wake,ila pale pale mapokezi alimuona binti mmoja naye akionekana kutaka kwenda kumuona mume wake ofisini, muda huo kengele ya hatari ikalia kichwani mwake, akamsogelea yule binti na kumuuliza,“Una shida gani binti?”“Nahitaji kuonana na bosi”“Karibu basi”Mama Angel alimshika mkono na kwenda nae hadi ofisini kwa mume wake kisha akamwambia akae kwenye kiti, halafu yeye akakaa kwenye kiti kingine na kuanza kumsikiliza shida yake, kwakweli yule binti inaonyesha hakujua kama mama Angel ndio angekuwepo kumsikiliza, muda huo baba Angel hakuwepo ofisini wala nini alikuwa ametoka, kwahiyo mama Angel alimuangalia tena yule msichana na kumwambia,“Nielezee shida yako”“Samahani, nilikuwa naomba kazi”“Mbona unajiuma uma hivyo? Kazi gani unataka kwa kujing’atang’ata hivyo?”“Nisamehe ila kilichonileta hapa ni kuomba kazi tu”“Una shida ya kazi wewe? Umekuja kutafuta kazi kwa hivyo ulivyo? Umevaa kope za bandia, kucha za bandia, yani upo kama jini hivi kuna kazi gani utafanya wewe? Au kuna mwenye ofisi yake ya kumkaribisha mtu kama wewe! Kwanza huna maadili hata kidogo, umevaa nguo fupi hivyo, ndio walivyokudanganya kuwa ukienda kuomba kazi uende umevaa nguo fupi ili kumvutia bosi wa kiume? Haya umenikuta bosi mwanamke ambaye vyombe ulivyoviweka sina haja navyo na hakuna hata kimoja kilichonivutia juu yako, kwasasa inuka tu, jikung’ute na utoke nje”Na kweli yule binti aliinuka pale kwenye kiti na kutoka nje kwa aibu kubwa sana ambapo nje alikutana na baba Angel ambaye kwa muda huo alikuwa akielekea ofisini kwake, basi alimuangalia na kutikisa kichwa, na moja kwa moja alipoingia ofisini alimkuta mkewe ambaye alianza kumsimulia kuhusu yule mwanamke.“Kwakweli mume wangu pole sana, yani kumbe huwa mnakutana na vituko vya kiasi hiki!! Pole sana, ila mimi naomba nikuombe kitu kimoja”“Kitu gani?”“Nitaenda kuongea na mtu wa mapokezi ili watu wa ajabu ajabu wote wasiweze kuingia humu ofisini kwako, kama mtu anakuja ofisini kwako ajiheshimu basi! Sio kukaa kama shetani sijui la wapi, mtu kajibandika mikucha mirefu kama jini, kope nazo hadi zinataka kugusa nywele, halafu bila aibu anakuja kuomba kazi, tafadhari watu wa namna hii sitowataka katika ofisi yako”“Sawa mke wangu”Ni muda huo huo mama Angel alienda kuongea na yule mtu wa mapokezi na kumueleza kuwa ni aina gani ya watu ambao hawataki kwenye ofisi ya mume wake wala nini.Na baada ya hapo alirudi ofisini ambapo na mume wake walijiandaa kwaajili ya kutoka tu.Iliuwa ni nyumbani kwa baba Abdi, ambapo kwa siku hii hakwenda kwenye shughuli zake kwani aliamua kupumzika tu kwa muda huo, mara alikuja mama wa mwanae na mwanae, huyo mwanamke kipindi cha nyumba aliwahi kuwa mke wake na aliitwa Nasma ila kwa kipindi hiki alijulikana kwa jina la mama Bahati kutokana na jina la mtoto wake.Basi alifika hapo tena bila hata salamu alianza kuongea,“Jamani, hivi hawa watoto wengine wakoje eeeh! Najua ni kwa kipindi kifupi tu nikasema basi na mimi nikae kidogo na mtoto wangu huyu, ila mnajua alichonitenda?”Fetty aliuliza,“Kwani kakufanyeje tena? Yani katika watoto wote humu ndani kidogo huyu Bahati ana afadhari, kwanza ni mtoto muelewa na asiye na makuu yoyote”“Kheee mtoto muelewa! Jamani, huyu mtoto kuna mahali nilimtuma jana nikampa elfu kumi ila cha kushangaza, karudi nyumbani hana shilingi kumi kwa kifupi hakuwa na hela yoyote, halafu namuuliza ananijibu kirahisi tu kuwa kapoteza, jamani hiyo ni sahihi?”Bahati akaangalia na baba yake ambaye alimuuliza,“Eti Bahati, hiyo hela umeipeleka wapi?”“Imepotea baba”Basi huyu baba alitoa elfu kumi nyingine mfukoni mwake na kumkabidhi mama Bahati ambaye kwa kiasi flani alichukia zaidi na kusema,“Sijapata kuona mwanaume anayeharibu watoto kama wewe, sasa ndio nini hivi! Yani huwezi kumsema mtoto jamani, hivi unajua kuwa elefu kumi ni kubwa sana yani kirahisi rahisi tu kama hivi unatoa nyingine”“Kwani ulikuwa unataka nini mama Bahati?”“Unatakiwa kumuadhubu huyu mtoto, hayo sio malezi nikwambie”Fetty nae akachangia,“Bora useme wewe, yani mimi humu ndani nishaongea hadi basi, hawa watoto hakuna kosa wanalofanya wakaadhibiwa yani hakuna kabisa, huyu baba muone tu hivi hivi ila yeye ndio anawahonga hawa watoto yani hawa watoto wanafanya wakitakacho kwani baba yao ana wachekea sana”Basi baba Bahati akawaambia,“Jamani mnajua mara nyingine hata mnacholalamika sikijui jamani, kwani hawa watoto tatizo ni nini? Kama leo huyo Bahati tatizo ni nini, kasema kuwa kapoteza hiyo hela, nianze kumuhadhibu kweli nitakuwa sijatumia utu kabisa. Halafu Nasma si nishakurudishia hiyo hela yako! Chukua nah ii ya usumbufu”Alitoa elfu kumi nyingine na kumkabidhi, yani mama Bahati aliinuka na kusonya halafu kuondoka zake, yani hakuondoka na mtoto wala nini ilibidi Bahati amfate nyuma mama yake ili ajue kama bado ataendelea kuishi nae au ataanza tena kuishi pale kwa baba yake.Fetty alimuangalia mume wake na kumwambia,“Tena umenikumbusha, nilienda kwa mama yake Erica, kaniambia kuwa anaomba kuongea na wewe, kwahiyo tupange siku twende tukaongee”“Basi huko ulienda kumuelezea kuwa mume wangu ana watoto kumi nje ya ndoa, tena utakuwa umeeleza kamavile hujui chanzo cha mimi kuwa na watoto wote hawa. Je niwatupe? Niwakatae au niwatenge? Wewe ni mwanamke wa pekee sana kwangu, huwa siwezi kusahau upendo wako kwangu, kunijali kwako kote huko huwa sisahau maana bila wewe sijui mpaka leo ningekuwaje Fetty, sema tatizo lako hutaki kuijua nafasi yako kwangu. Hebu fikiria ni kiasi gani umeweza kubadilisha maisha yangu na umeweza kubadilisha fikra zangu, fikiria kuwa ni kiasi gani huwa unasimama kunitukana na kuniambia maneno machafu, je kuna siku yoyote nimewabhi kusema kuwa nimechoka kwa matusi yako na kejeli zako kuwa kila mmoja aishi maisha yake? Kuna siku yoyote nimefungua mdomo wangu kusema hivyo! Unapataga hasira na kuaondoka nyumbani, kuna siku hurudi hata saa saba za usiku, je nimewahi kukulalamikia? Yote sababu nakujali sana na kukupenda ila sijui kwanini hutambui hilo mke wangu”“Hujanijibu nilichokwambia, je tutaenda?”“Hakuna tatizo tutaenda ila nilikuwa najaribu tu kukuelewa kuwa ni kwa jinsi gani ninavyokuthamini na kukujali katika maisha yangu, wewe ni mtu wa maana sana kwangu Fetty”Fetty alimuangalia tu mume wake ila kwa kiasi Fulani alikuwa akiyafurahia yale maneno ambayo mume wake alikuwa akimwambia.Wakati wakina Erica wanatoka darasani, ilibidi Samia ampe Erica mikanda ambayo aliamuahidi kuwa atampelekea,“Ile mikanda ya ngumi nimekuja nayo”“Basi Erick atafurahi sana”“Ila hongera sana Erica, una kaka mpole huyo, halafu mzuri mwenyewe”“Mmmmh na wewe Samia jamani! Ila ni kweli kaka yangu ni mzuri”“Yani hilo nakupa hongera sana, yani ana mwili wa kiume kaka yako ujue, kwanza mrefu yani anapendeza”Erica alicheka ila kwa kiasi Fulani alimshangaa sana Samia kwa kumsifia kaka yake wakati alikuwa akimuona Samia kuwa ni mdogo pia, kwahiyo kitendo cha kumsifia kaka yake kilimshangaza kidogo.Basi Erica alifika na nyumbani kwao na kuingia muda mmoja alioingia Erick na moja kwa moja alimuonyesha ule mkanda ambapo aliletewa na Samia, na baada tu ya kubadilisha nguo kwa muda huo walienda sebleni na kuuweka na kuanza kuangalia, muda huu walikaa sebleni pamoja na Vaileth.Ilivyofika jioni, Junior nae alitoka shuleni, ni alikuwa ametoka kwenye mtihani, basi alivyoingia ndani wote walimpa pole kwa mitihani ambayo alikuwa ameifanya siku hiyo ambayo ndio ilikuwa inaishia.Basi Vaileth aliinuka na kuelekea jikoni ili kumuandalia chakula Junior ambaye alitoka kufanya mitihani, ila Junior nae alienda jikoni na kumkumbatia Vaileth, ambapo Vaileth leo alimuuliza kuwa ni kwanini anapenda kufanya vile,“Nilkimaliza mitihani kabisa nitakwambia sababu ya mimi kufanya hivi!”Basi Vaileth aliandaa chakula na wote walifika na kukaa na kula kile chakula ila baada ya kula hata wakina Erica waliondoka kwamaana hiyo hata wazazi wao waliporudi siku hiyo hawakujua kuwa watoto wao walikaa kuangalia video kwa siku hiyo.Steve, siku ya leo alivyoondoka pale kazini alifatwa tena na Sian a kuanza kuongea nae,“Kwani wewe Sia una nini?”“Sina tatizo lolote, ila kesho nitamleta mtoto wetu hapo dukani”“Kivipi na anakuja kufanya nini?”“Yule ndio mrithi wa hilo duka kama hujui, kama una ujasiri basi muulize huyo Erick hilo duka amelitengeneza kwasababu gani? Na ilikuwaje hadi akalianzisha? Nani aliyempa wazo la yeye kuwa na duka kama hilo? Ukiweza kumuuliza hayo na akakujibu kwa hakika utaelewa ni kwanini nafanya hivi mimi kwahiyo kesho nitamleta mwanangu hapo dukani, yeye ndiye mrithi wa halali wa hilo duka”Yani Steve bado alikuwa akimshangaa sana Sia, yani alimtafakari bila kumpatia jibu la moja kwa moja, basi aliachana nae pale na kuondoka huku akitafakari sana yale maneno ya Sia huku akisubiri kwa hamu siku ya kseho yake ambayo Sia atamleta mtoto wake.Siku hiyo moja kwa moja alirudi tu nyumbani kwao na kuamua kupumzika huku akitafakari mambo mbalimbali.Kesho yake Steve alifika dukani na kuanza kufanya mambo mbali mbali huku akijua kuwa ujio wa Sian a mtoto itakuwa muda sio mrefu, ila haikuwa hivyo kwani pale dukani kwa muda huo alifika baba Angel na mafundi wa kufunga kamera kwenye lile duka kale, basi alisalimiana nae na kuanza kuongea nae mambo mbalimbali, ila baba Angel hakumuuliza chochote cha kuhusu ujio wa Sia wala nini, basi Steve aliamua kumuuliza kwa utani tu,“Eti kaka samahani, hivi ni nani aliyekupa hii idea ya kuanzisha duka hili au eneo hili?”“Unajua kuna siku moja nilikuwa mahali kwenye hili eneo, nakumbuka nilikutana na mvulana mmoja hivi ila sijawahi kumuona hadi leo mtoto yule, basi yule mvulana nilijikuta nikiongea nae mambo mengi sana, moja wapo la jambo ambalo nilikuwa nimeongea nae ni kuwa watu wa eneo hili wana uhitaji sana na huduma hizi ambazo nimeweka kwenye hii biashara yangu, yule mtoto aliniambia kuwa angekuwa na uwezo basi angefanya yeye hicho kitu, kwakweli niliumia kumsikiliza na pale niliamua kumpa pesa kidogo na tangia hapo ndio nikaanza kupafanyia kazi eneo hili. Na ndiomana hili duka nilipolimaliza basi mtu wa kwanza kumleta hapa ni mtoto wangu wa kiume aitwaye Erick, kwani hili ni duka lake yani ni mali ya mtoto wangu Erick”“Ooooh! Hapo nimekuelewa tayari bosi wangu”Basin a yule mtu aliyekuwa akifunga kamera, alizifunga kwenye duka lile na baada ya hapo baba Angel alimuaga Steve kwa kumwambia,“Nitamleta tena mwanangu Erick ili umfahamu nan a nimfahamishe pia kuwa hili duka ni lake”“Sawa, hakuna tatizo”Mwisho wa siku baba Angel akaondoka zake, ila Steve alikuwa na maswali mengi sana akijiuliza bila majibu ya aina yoyote ile ila pia Sia hakufika kabisa siku hiyo hadi siku ikaisha wala hakuonekana Sia kabisa.Siku hiyo Erick akiwa shuleni wala karibia na muda wa kutoka, alishangaa tu kuona baba yake akiwa ameenda kumfata pale shuleni, kwa upande mwingine alifurahi sana kwa kitendo cha kufatwa na baba yake kwani aliweza kuona ni kwa jinsi gani baba yake alimpenda sana.Basi baba yake aliongea nae kuwa anataka apitie nae kwanza kwenye ile biashara yake, waliingia kwenye gari huku wakiongea mawili matatu,“Najua wewe ni mtoto wa kiume, sio mropokaji kama dada yako Erica, sasa nataka twende tena huku kwenye duka maana hili ni duka lako”Erick alitabasamu, kisha baba yake akaendelea kuongea,“Nitakuonyesha vitu vyote vya muhimu kwenye duka hilo mwanangu, nataka hata muda mwingine kama zile siku za mwisho wa wiki uwe unaenda dukani kuangalia maendeleo ya duka”“Mama atakubali kweli niwe natoka?”“Nitaongea nae, lazima mama yenu aelewe kuwa wewe ni mtoto wa kiume, tunavyomlea Angel na Erica ni tofauti kabisa na tunavyotakiwa kukulea wewe, leo na kesho mimi nisipokuwepo ni nani atasimama kwaajili ya dada zake? Yani wewe kaka mtu ukishindwa kusimama unajua nini kitatokea? Ndiomana nataka kufanya haya mapema sana, hii ni biashara ya kwanza, hata biashara ya Erica nitakupeleka wewe kwanza ili ukaone vizuri ilivyo nataka mwisho wa siku niwe nimewafundisha watoto wangu kuwa wafanyabiashara wazuri zaidi yangu, sio mimi ni mfanyabiashara mzuri halafu watoto wangu hawajui chochote kuhusu biashara, yani hii kitu inaniumiza sana kichwa mjue. Kwahiyo mwanangu ujue nina maana kubwa sana kufanya hiki ninachofanya”“Sawa baba, nimekuelewa na ninakuahidi kuwa sitakuangusha kabisa, yani usiwe na mashaka yoyote juu yangu”Basi walifika hadi dukani ambapo Baba Angel alimtambulisha Erick kwa Steve pale, na pia kumuonyesha mambo yote ya muhimu Erick, kisha akamwambia Steve,“Naomba huyu mtoto anapokuja umpe ushirikiano unaotakiwa maana huyu ndio wa kuwaongoza dada zake, kwahiyo hakuna chochote kwasasa kitakachofanywa kwenye duka hili bila kumshirikisha huyu. Kwa kifupi huyu ndio bosi wako”“Sawa sawa nimekuelewa”Erick alifurahi sana kwani aliona baba yake kampa heshima kubwa sana na aliona kuwa ile kazi ndio iliyokuwa inamfaa yeye kwani siku zote alitamani sana kukaa dukani na kufanya biashara ya duka kuliko kukaa darasani muda wote.Walipomaliza pale, walimuaga Steve na moja kwa moja baba Angel na mtoto wake waliondoka na kuelekea nyumbani, yani siku hiyo walionekana tu wamerudi pamoja ila hawakuwaelewa tu kuwa wamepitia sehemu gani hadi kufika pale wakiwa pamoja kama vile.Ilikuwa siku ya kumaliza mtihani wa mwisho na siku hiyo walimaliza mapema sana, na ilikuwa ni furaha kubwa kwa wanafunzi wote wa kidato cha nne, basi kwa shule ya wakina Angel walipanga kesho yake ndio iwe siku ya mahafali kwa wanafunzi wale waliomaliza kidato cha nne.Kwanza kabisa wote walikutanika sehemu moja ambapo walimu waliwapa soda kila mmoja na vitu vya kutafuna tafuna kama kujipongeza kwanza kwa kumaliza mtihani, basi kila mmoja alikuwa na furaha sana, basin i siku hiyo ambayo Husna alimkumbusha Angel kwa kumuuliza,“Hivi Angel, siku ile wakati wote tumeitwa pale kuungumza ni kitu gani kilitokea hadi wewe na Samir mlichelewa kuja?”“Sijui, ila bora umenikumbusha, tabia mbaya hiyo Husna yani uliniacha darasani ukitegemea nini?”“Hivi unajua kuwa mimi sikuwepo darasani wala nini? Hata mimi mwenyewe nilishanga tulipoenda pale wakati mwalimu akizungumza mara watu wakageuka nyuma, kuangalia ni wewe na Samir mlikuwa mkitokea, hata sijui ni kitu gani kilitokea katikati”Mara Samir akawafata katika maongei yao na hapo akasema mbele ya Husna,“Husna, naomba wewe uwe shahidi wa haya maneno yangu nitakayotamka leo. Angel, sijasema unikubali au usinikubali ila mimi nasema kile kilichopo moyoni mwangu, kiukweli nakupenda sana Angel, yani hilo haliwezi kubadilika na kitu chochote kile, hata iweje ni siku zote nitaimba wimbo huu mmoja kuwa nakupenda sana”Husna alicheka na kuguna ila Angel alishindwa kujibu kabisa. Muda kidogo alifika mwalimu na kumuita Angel kwaaana aliitwa na mzazi wake, kwahiyo Angel ilibidi aachane nao na moja kwa moja kwenda alipoitwa na mama yake.Mama yake alimkumbatia kwa furaha sana huku akimpongeza kwa kumaliza mitihani yao, na kumwambia,“Haya panda kwenye gari tukamchukue na Junior, yani leo nimefurahi sana jamani. Twendeni mahali kwanza mkale mnachotaka halafu ndio tutarudi nyumbani kwaajili ya maandalizi ya hayo mahafali yenu”Angel hakuwa na sababu ya kukataa kwani moja kwa moja alipanda kwenye gari ya mama yake na kuondoka eneo lile la shule yao na moja kwa moja walienda shuleni kwakina Junior ambapo walimchukua naye Junior na kuondoka nae, kisha mama Angel aliwapeleka wanae kwenye duka lao kubwa la nguo na kuwataka wachague nguo ya kuvaa kwa muda huo ambapo walichagua na kubadilisha zile sare za shule halafu moja kwa moja alienda nao mahali ambapo alisema kuwa wataenda kupata chakula wakitakacho kwa muda huo.Wakati wametulia wakila chakula hoteli yani mama Angel, Angel pamoja na Junior, mara muda huo alionekana Husna akiwa ameongozana na James ambao walienda pale kuwasalimia.Ila leo mama Angel aliamua kumuuliza swali huyu James,“Samahani, kwani wewe baba yako ni nani na yuko wapi?”Junior alimuuliza mamake mdogo,“Mbona umemuuliza hivyo mamdogo?”“Aaaah Junior, unajua huyu kafanana sana na baba yako”“Mmmh tuseme huyu ni ndugu yangu!!”James akajibu,“Kwakweli mimi sijui baba yangu alipo, nimeishi na mama kwa kipindi chote hiki na kwasasa tunaishi na mjomba wetu na ndiye anayetulea. Hata hapa tulikuja nae ila alipoona tu meza hii basi mjomba aliondoka”Mama Angel akatingisha kichwa kidogo na kusema,“Mjomba wenu ndio huyo George?”“Eeeeh ndio”Basi mama Angel akatoa kadi yake yenye namba na kumkabidhi James kisha akamwambia,“Mpe huyo mjomba wako, mwambie kuwa nahitaji kuzungumza na yeye maana nahitaji sana kufahamu kuhusu wewe, ni vyema kwa ndugu kufahamiana. Unaitwa James, na kiukweli ni kuwa unafanana sana na James, kwahiyo kuna uwezekano mkubwa sana kwa James kuwa baba yako halafu huyu Junior ni ndugu yako”Basi kwavile walimaliza kula, hivyobasi waliinuka na kuwaaaga Husna na James pale na kuondoka zao kurudi nyumbani.Kesho yake walijiandaa kwaajili ya kwenda kwenye mahafali ya siku hiyo ambayo shule ya wakina Angel ilikuwa imepanga kufanya vile, basi ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wazazi wa wanafunzi wale walikuwa wamekutanika pale shuleni ili kufatilia shughuli nzima ya mahafali inavyoenda.Wakati wameshakabidhiwa vyeti vyao vya kawaida pale shuleni ilikuwa ni furaha ambapo walipiga picha na mambo mengine yaliendelea, basi wakati wa kula chakula, Angel alishangaa akivutwa mkono na Samir nae alijikuta akimfata tu Samir alipompeleka ambapo Samir alimpeleka hadi eneo ambalo hapakuwa na watu kwa wakati ule na kuanza kumwambia tena,“Angel, nakupenda sana ten asana. Wewe ni mwanamke wa maisha yangu, bila wewe siwezi kitu”Angel alikuwa akimuangalia tu Samir kwani alijikuta kuwa Samir akimuongelesha kitu na yeye kushindwa kumjibu kabisa zaidi zaidi kuishia akimuangalia tu.Basi Samir alimvuta karibu yake na muda huo huo alianza kumbusu Angel mdomoni, ila muda huo mama Angel nae aliinuka kuongea na simu ila kutokana na makelele ya pale aliamua kuzunguka kidogo ili aweze kusikilizana na aliyempigia, kwahiyo kitendo cha kumkuta Samir na Angel kilimshtua sana kwa wakati huo.Basi Samir alimvuta karibu yake na muda huo huo alianza kumbusu Angel mdomoni, ila muda huo mama Angel nae aliinuka kuongea na simu ila kutokana na makelele ya pale aliamua kuzunguka kidogo ili aweze kusikilizana na aliyempigia, kwahiyo kitendo cha kumkuta Samir na Angel kilimshtua sana kwa wakati huo.Yani hadi simu aliiweka pembeni na kwa hasira alisogea na kumchukua Angel, na muda huo huo alienda kuwaita ndugu baadhi waliokuwa pale shuleni na kuondoka nao, kwahiyo aliondoka na Angel akiwa wala hajamaliza mambo ya mahafali wala nini.Moja kwa moja walienda nyumbani yani mama Angel alikuwa na hasira sana kwa wakati huo, basi baba Angel ne muda huo alirudi nyumbani kwani alikuwa akitaka kupumzika kidogo halafu aunganishe shuleni kwa mwanae ambako ndio kulikuwa na mahafali, ila alishangaa kumkuta mkewe nyumbani tena akiwa na hasira sana, basi moja kwa moja alienda nae chumbani kuzungumza nae,“Kwani vipi? Mbona unaonekana ukiwa umejawa na jazba kiasi hiko mke wangu? Na je mahafali yameisha kweli?”“Yaishe wapi? Huyu mtoto ni punbguani sijapata kuona jamani, yani Angel ni punguani, punguani namba moja. Kweli wa kumkuta kasimama na huyo Samir wake kweli wamekumbatiana!”Ila mke wangu jamani, unajua kuna kitu nafikiria hapa kuhusu huyo Angel na Samir inaonyesha wanapendana sana yani mimi na wewe tutajitahidi kwa kila hali ila bado itashindikana kuwatenganisha”“Inamaana umeshindwa tena kumlinda Angel?”“Sijasema kuwa nimeshindwa”“Sasa unawezaje kumuachia huyo Samir kuwa na Angel? Huyo sio mwanaume bora katika maisha ya mtoto wetu, ila leo nimeona ule uamuzi wako wa kumpeleka Angel Africa kusini basi ufanye kazi, maana nadhani akiishi mbali ndio itakuwa vizuri zaidi”“Hakuna tatizo juu ya hilo, ila tu nilikuwa nakwambia mke wangu tunatakiwa kuwa makini sana. Unajua huyo Angel na Samir bado hawajawa pamoja kwahiyo wanaona kila tunachofanya ni kuwazuia tu, ila tungejaribu kuwaacha pamoja japo kwa mwezi mmoja tu, watachokana wenyewe nakwambia na kila mmoja ataona bora aendelee na mambo yake kuliko kuendekeza mambo ya mapenzi”“Hapana mume wangu, sipo tayari kwa hilo. Ni heri Angel aende sehemu ya mbali”“Sawa, ila mimi naona basin i vyema kama akienda kuishi na mama yangu maana nae anaishi peke yake halafu yupo mbali kule na anatamani sana kuishi na mtoto”“Ooooh napo ni wazo zuri tu”Mama Angel hakuwa na tatizo juu ya Angel kwenda kuishi na mamake na baba Angel maana mama huyo mara nyingi alikuwa yupo na mambo yake tu kwahiyo hakuweza kumnyanyasa au kumtesa mtoto.Basi wakakubaliana kuwa Angel watampeleka huko sababu ni mbali pia kwahiyo waliona itasaidia sana, ila baba Angel aliona ni vyema kwa swala hilo kulifanya mapema, hivyo siku hiyo hiyo aliwasiliana na mama yake na kukubaliana kuwa kesho yake aweze kumpeleka Angel huko kwani mama yao nae alisema kuwa kwa siku ya kesho ndio atakuwa na muda mzuri zaidi wa kupokea wageni.Usiku wa siku hiyo, Samir alikuwa nyumbani kwao baada ya uchovu wa siku nzima hiyo, kwahiyo alitulia kwao kwa muda huo akiwa amechoka haswaaa ila alishukuru sana kwa ile siku kuisha.Mdogo wake Samia alimfata kaka yake na kuongea nae kidogo,“Hivi umejisikiaje kuwepo kwenye mahafali bila ya wazazi? Yani mama hayupo wala baba hayupo?”“Nilikuwa kawaida tu, kwani wazazi wetu ni kawaida kwa wao kutokuwepo katika matukio muhimu hivi kwahiyo hakuna kitu ambacho nimeshangaa wala nini”“Ila kaka, hivi unamuelewaga baba?”“Mimi sijawahi kumuelewa huyu baba hata mara moja, yani hakuna hata siku moja ambayo nimewahi kumuelewa huyu baba, kwanza sina uhakika kama ni baba yetu mzazi”“Kwahiyo sisi tuna baba mwingine eeeh!”“Ndio, hebu wewe jiulize kitu kimoja. Watoto wengi wa huyu baba huwa wanapelekwa kwa bibi yani kwa mama yake, ila sisi tukitaka kwenda kwa bibi tunapelekwa kwa bibi mzaa mama, yani hakuna siku hata moja tumeenda kwa mzaa baba, na yote tisa kumi ni kuwa hajawahi kuja hapa hata mara moja.hivi bado unaamini kuwa huyu ni baba yetu?”“kweli kabisa kaka, huyu sio baba yetu ila baba yetu ni nani sasa?”“Hilo swali, jibu lake analo mama tu. Ila ipo siku ambayo mama itabidi tu atueleze ukweli halisi kuhusu baba yetu mzazi”Samia alikubaliana na maneno ya kaka yake, na baada ya hayo walienda kufanya tu mambo mengine na moja kwa moja kwenda kulala.Ila usiku wa siku ile Samir alipigiwa simu na mama yake na kuanza kuongea nae,“Mwanangu Samir, wakati unasubiri majibu kuna kazi nimekutafutia huku. Kwahiyo kesho au keshokutwa utatakiwa kusafiri kuja huku, nadhani tunaelewana”Hakuna tatizo mama, ila je ni kazi gani?”Utaijua huku huku”Samir hakutaka kubishana chochote na mama yake zaidi ya kukubaliana nae tu kuwa ataenda kufanya kazi ambayo mama yake alikuwa amemtafutia kwa kipindi hiko.Kulipokucha ilibidi Samir ajiandae maana mama yake alimtafuta tena na kumtaka aweze kusafiri kwa lengo la kwenda hiyo sehemu, kwahiyo Samir alijiandaa na kuondoka kwahiyo alimuaga tu mdogo wake na kuondoka zake yani alisafiri kwa muda huo.Leo Baba Angel alifika na Angel kwa bibi yake yani kwa mama yake mzazi, yule mama aliwakaribisha vizuri kabisa na kuongea mawili matatu na mtoto wake,“Kwahiyo mmeona ni vyema aje apumzike kidogo huku kwangu?”“Ndio mama, ukizingatia huna mtoto mwingine yoyote yule hapa nyumbani!”“Ni kweli, hata mimi nimefurahi kwa kumleta hapa”Basi Angel alionyeshwa tu chumba ambacho atakuwa analala kwa kipindi hiko kisha baba Angel aliaga kwa mama yake kuwa anaondoka, basi walipotoka nje mama yake alimuuliza tena,“Hivi kuhusu swala la kumleta huyu mtoto kwangu umekubaliana vizuri na mama yake kweli?”“Ndio mama, na mama yake ndio kaona kuwa ni vyema kama akija huku kupumzika kidogo maana ndio kashamaliza mitihani”“Yani sina tatizo, ila mwanangu. Hivi na mke wako mlizungumza vizuri kuhusu huyu mtoto kweli?”“Kivipi mama?”“Usinifikirie kwa ubaya, ila toka huyu mtoto akiwa mdogo kabisa nilikwambia mwanangu kuwa mtoto hafanani na sisi huyu ila nakumbuka ulinijibu kuwa kitanda hakizai haramu, siwezi kukataa kwani mimi na mama wa mkeo ni marafiki wakubwa sana, ila kuna ulazima wa kufatilia uhalisia wa huyu mtoto ingawa najua unapingana na ukweli kwani vitu vingi sana ushawekeza kwa kutumia huyu mtoto. Usichukie mwanangu, ni kawaida tu hii, nilikuwa nakupa changamoto tu”Baba Angel alimuangalia mama yake kisha alimuaga na kuondoka zake, ila pia aliona kuwa ile sio sehemu sahihi kwa mwanae, sema kwa kipindi hiko hakutaka mtoto huyo aende Afika kusini kwani alitaka kama akimpeleka huko basi mtoto asiwe peke yake, ndiomana kwa kipindi hiko aliona ni vyema kumleta Angel huku alipomleta.Baba Angel alipotoka tu kwa mama yake, moja kwa moja alienda kwa dada yake, na alimkuta na kuanza kuongea nae, ambapo dada yake alimuulizia kuhusu habari za Angel nae alimuelezea,“Ila nyie ni mna vilanga sijapata kuona katika maisha haya jamani, mbona mmekuwa na vilanga hivyo na mke wako. Angel nimeishi nae vizuri kabisa hapa hadi kamaliza mitihani, ila huyo mkeo kumkuta kidogo tu Angel sijui na mwanaume basi mshipa wa fahamu ushamtoka kabisa, jamani Angel ni mtoto wa kike hivi mnaweza kumbana hadi lini? Halafu malezi mnayompa Angel sio malezi wala nini, mfundishe mtoto atambue baya na jema yani atambue yote na ikitokea amefanya kitu yani ajue kama hiki ni kibaya au hiki ni kizuri, hivi kwa staili hii inayofanyika mtaweza kweli kumuweka Angel katika mstali unaotakiwa jamani!! Anazidi kukua yule, utamshikilia hadi atakapoolewa utaweza?”“Sio kosa langu lakini”“Sio kosa lako nini, halafu mmekubaliana kumpeleka mtoto kwa mama yako, hivi yule mama toka lini kalea mtoto? Wewe mwenyewe hakukulea wala nini, sema tu ukweli si umelelewa na mamako mdogo wewe! Je alikulea mama yako? Aaache kuwaza mambo yake akaanze kumuwaza Angel jamani, yani mara nyingine hadi mnakera, huyo Erica kabeba mtoto bila hata ya kunishirikisha halafu saivi unaniambia kuwa mmempeleka kwa mama yenu, jamani na msinishirikishe kwa lolote lingine lile. Mtu unaweza ukawa na pesa ila usiweze kulea watoto katika misingi inayotakiwa, sasa unachofanya kwa huyo Angel sio kujenga bali kubomoa”Tumaini alionekana kuchukia haswaa kwa kitendo cha kumuondoa mtoto bila ya kushirikishwa kitu chochote kile.Baba Angel hakutaka kumaliza maneno pale kwani muda ule ule aliaga na kuondoka zake tu.Kesho yake Steve akiwa dukani siku hiyo, ndipo Sia alipoenda na binti mmoja na kumtambusha pale kwa Steve, kwakweli Steve alimshangaa na kumuuliza,“Ni nani huyu mtoto?”“Huyu ndio mwanetu”“Hebu acha masikhara, kwani sijui kama mtoto alikuwa ni wa kiume au? Huyu mtoto ni nani?”“Huyu mtoto anaitwa Samia”“Kheeee Samia! Ni mtoto wa nani na umemtoa wapi?”Sia alimuangalia Samia na kumwambia,“Chagua chochote unachokitaka kwenye duka hili kama ambavyo nilikuahidi”Basi Samia alianza kuchagua ila Steve alimzuia na kufoka pale, kwanza alimfokea Sia,“Unamaanisha nini lakini? Kwani wewe mwanamke una nini eeeh! Sia sijawahi kukupiga ila ukiendelea na huu upuuzi kwakweli nitakupiga”“Thubutu, mimi ndiye niliyekufundisha maisha wewe, unipige thubutu”“Unajua huna akili wewe, unawezaje kwenda kuchukua watoto wa watu huko na kuwaambia sijui waje wachague wanachokitaka jamani kutoka kwenye hili duka? Hili duka ni lako”“Kumbe hujui eeeh! Hili duka ni langu ndio, maana hili duka ni la mtoto wangu”Steve alitikisa kichwa na kucheka,“Unajua mara nyingine, hebu tuwe na akili basi, usifanye umasikini ukakudhalilisha kiasi hiko unachotaka, hiyo ni aibu unayofanya. Kila siku kubadili watoto, hata kama mwanao ndio ametoa wazo hili la kuwa na duka eneo hili ila bado huwezi sema kuwa duka hili ni la mtoto wako. Kwakweli hii sasa umezidisha”Steve akaona bora tu atumie uanaume wake, kwani alimvuta Sian a kumtoa nje ya duka lile kisha aliongea na mlinzi kuwa mwanamke yule asimruhusu tena kusogelea duka lile, halafu alirudi dukani na kumwambia Samia,“Wewe mtoto ondoka na huyo mama yako sijui nani yako”“Hapana sio mama yangu halafu mimi na yeye hata hatufahamiani”“Duh! Kwahiyo kakutoa wapi?”“Aliniuliza kama namfahamu Erica na Erick nami nilimjibu kuwa nawafahamu, basi akasema ananipeleka kwenye duka lao na nikachague kitu chochote ninachokitaka kwenye hili duka ila mimi sifahamiani na huyu mama wala nini”Steve alimuangalia huyu mtoto na kumtaka tu na yeye aondoke ila kiukweli hakuelewa ni kwanini Sia anafanya vitu vya namna ile.Muda wa kutoka Steve alijiandaa kwaajili ya kwenda nyumbani kwao, kwahiyo alifunga vizuri duka ila wakati anaondoka aliona kuna kijana mdogo ambaye alikuwepo karibu na lile duka, basi alijikuta akipatwa na shauku ya kuongea na yule kijana,“Habari yako kijana”“Salama, shikamoo”“Marahaba, samahani unaitwa nani?”“Naitwa Elly”“Mbona upo hapa kwa muda huu?”“Ni hivi, leo kuna jambo nimeambiw ana mama yangu kuhusu hili duka”“Jambo gani?”“Mama yangu kaniambia kuwa hili duka ni mali yangu, kwahiyo kwa siku ya leo nikae hapa kumsubiria mmiliki ili anikabidhi duka langu”Steve alimuangalia sana huyu kijana kisha akamwambia,“Huyo mama yako anaitwa Sia eeeh!”“Kwanini umeniuliza hivyo?”“Naomba ongozana na mimi”Kisha Steve alisimamisha bajaji na kupanda na yule kijana halafu akaondoka nae hadi nyumbani kwao.Moja kwa moja alienda nae chumbani kwake na kuanza kuongea nae,“Hivi unajua ya kuwa huyo mama yako Sia ni mtu ambaye hana akili timamu? Iko hivi, unionaye hapa, nimewahi kuwa mume wa mama yako”“Kheee inamaana wewe ndiye baba yangu!”“Inawezekana ikawa hivyo ila mama yako si mkweli katika maisha yake, na ndiomana anakufanya uwe unatangatanga tu bila kujua uelekeo wako wa aina yoyote ile. Kwasasa naomba ukae hapa na mimi, najua ni kitu gani kitafanya ili kuweza kukusaidia maana yale unayoishi sio maisha hata kidogo”Basi kwa siku hiyo Elly alilala hapo nyumbani kwao na wakina Steve, yani hata Steve hakutaka kujua kama huyu ni mtoto wake au la sema alichoona yeye kuwa ni sawa kwa wakati huo ni kumuokoa huyu mtoto toka mikononi mwa Sia kwani alimuona kama mtu asiyekuwa na akili timamu.Kulipokucha, Steve alijiandaa na kwenda kazini na aliondoka na yule mtoto ila walipofika tu pale nje ya duka, walimkuta Sia yupo pia, kiuweli Sia alipomuona Steve na yule mtoto alimfata na kumzaba vibao viwili vya nguvu kisha alimchukua yule mtoto na kuondoka nae, yani Steve hakumuelewa kabisa ni kwanini anafanya kile alichokuwa anakifanya, zaidi zaidi aliamua tu kwenda dukani na kuanza biashara kama kawaida ya siku zote.Leo kwenye duka alifika Erick kama ambavyo aliambiwa na baba yake kuwa awe anakuja kutembelea duka hilo mara kwa mara, ila leo Steve aliweza kuongea mambo mengi sana na huyu Erick,“Unajisikiaje kuwa mmiliki wa hili duka?”“Ila sidhani kama hilo ni swali maana baba yangu ana miliki maduka mengi sana, kaniweka hapa ili niweze kuzoea biashara na si vinginevyo kwahiyo hii kwangu sio ajabu wala sio miujiza wala nini”Steve aliamua tu kuongea nae mambo mengine huyu Erick kwani alionekana kuwa na majibu sana, basi Erick alitembelea tembelea lile duka kiasi kisha aliondoka zake na kurudi kwao.Erick alipofika kwao tu, alifatwa na dada yake ambaye alimuuliza,“Haya, leo ni mwisho wa wiki ila uliondoka ukaenda wapi?”“Nilienda kuangalia biashara ya baba, je unataka siku twende wote?”“Ndio, tena itakuwa vizuri sana”Wakati wanaongea pale nje alifika Samia na kuanza kusalimiana nao kisha aliwaeleza yaliyotokea yote kwa yeye kupelekwa kwenye duka lao na kuambiwa kuwa achague anachokitaka,“Unamfahamu huyo mama?”“Hata simfahamu jamani, yani yule baba wa dukani nae aliniuliza swali kama hilo”“Haya, ulikuwa ukifanya nini muda huo hadi kuchukuliwa na huyo mama?”“Mimi nyumbani kwetu naishi kwa uhuru sana kwanza huwa nafanya ninachotaka mimi kwa muda ninaotaka mii, kwasasa mama na kaka yangu wote hawapo kwahiyo nyumbani huwa nabaki mimi na msichana wa kazi tu, nilitoka kidogo na kukutana na yule mama”“Kwahiyo unapoishi sio mbali na lile duka?”“Ni kweli sio mbali, leo twendeni kwetu mkapafahamu”Waliona kuwa ni jambo zuri tu, hivyo moja kwa moja walienda ndani na kumuaga Vaileth halafu wote watatu yani Erick, Erica na Samia waliondoka, wakati huo Erick ndio alikuwa akiendesha lile gari.Nyumbani Alibaki Vaileth akiwa na Junior maana kwa kipindi hiko Junior aligoma kabisa kurudi nyumbani kwao, kwahiyo yeye aliona kuwa ni vyema kuendelea kuishi kule kule kwa mamake mdogo kuliko nyumbani kwao, basi Vaileth alienda jikoni kuandaa chakula, ila Junior pia alienda jikoni, ila leo Vaileth aliamua kumuuliza Junior ni kwanini anapenda kumfata fata vile,“Junior, kwanini lakini? Unajua kipindi kile unasoma hadi unaingia kwenye mitihani nilikuwa najiuliza sana kuwa ni kitu gani kinachopelekea wewe kuwa karibu na mimi kiasi hiki!”“Unataka kukijua Vaileth?”“Ndio, niambie ni kitu gani?”“Usiwe na haraka sababu nitakwambia kitu kinachonipelekea mimi kuwa hivi kwako”“Mmmmh!”“Usigune, ila nitakwambia tu”Basin a siku hiyo Junior alimsaidia Vaileth katika mapishi yote na walipomaliza walitulia na wote waliporudi pale nyumbani walikula na kwenda kupumzika, yani wazazi wakina Erica hata hawakujua kama siku hiyo watoto wao walitoka nyumbani wala nini yani hawakujua chochote kile.Wakati wa kulala, Vaileth alishangaa muda huo Junior akiingia chumbani kwake, basi alimuuliza kwa mshangao,“Junior, unafanya nini chumbani kwangu?”“Nyamaza Vaileth, kuna kitu nataka kukwambia”“Kitu gani?”Junior alimsogelea Vaileth na kuanza kumbusu, yani Vaileth hakuweza kumsukuma Junior wala hakuweza kumfukuza, zaidi zaidi alijikuta akishirikiana nae na mwisho wa siku walilala pamoja chumbani kwa Vaileth.Siku hiyo asubuhi, mama Angel aliongea na baba Angel kuhusu Junior,“Unajua nini, mama Junior jana kanipigia simu kuwa anamtaka mtoto wake”“Na yeye aache kutusumbua akili, kwanza huyu mtoto sio mtoto mdogo, tumuache Junior aamue mwenyewe ni lini ataenda kwa mama yake ila sio mtu ambaye tutampeleka kama mzigo au kitu gani?”“Unayoyasema ni kweli, ila pia tunaweza kumshauri Junior aende tu akamsalimie mama yake”Basi wakaona kuwa jambo hilo lipo sawa, na moja kwa moja walipotoka waliamua kumshauri Junior jambo hilo ila na yeye aliwaomba jambo moja,“Mnajua siku hizi nimebadilika sana kiasi kwamba sipendi kutembea mwenywe, kwahiyo mimi nawaomba kama hamtojali basi niende kumsalimia mama nikiwa nimeongozana na Vaileth”“Ooooh, hilo sio tatizo hata kidogo, unataka kwenda lini ili tumwambie Vaileth afanye kazi zake mapema siku hiyo?”“Nadhani kesho au kesho kutwa”“Basi tutaongea nae, hakuna tatizo”Mama Angel alikubaliana na Junior ila hakujua kuwa ni kitu gani kilichopo baina ya Junior na Vaileth.Basi siku hii ya leo walijiandaa na kwenda Kanisani kama kawaida, na walienda wote kwa pamoja na walipomaliza ibada walirudi nyumbani wote kwa pamoja.Muda huu Erick alienda moja kwa moja chumbani kwa Erica na kumuuliza,“Nasikia kuna viatu ulinunuliwa na mwanaume, viko wapi?”“Viatu nilinunuliwa na mwanaume? Nani amekwambia?”“Nionyeshe kwanza viko wapi?”“Jamani, ni siku nyingi mambo hayo, nani kakwambia Erick?”“Mimi ni kaka yako na ninapaswa kujua mambo yote yanayoendelea juu yako. Viko wapi hivyo viatu Erica?”Ilibidi Erica atoe hivyo viatu na kumuonyesha kaka yake ambaye aliviangalia na kusema,“Kuanzia leo Erica nakuomba, unapohitaji jambo lolote lile niambie mimi, nakuomba sana isije ikatokea tena ukanunuliwa kitu na mwanaume”“Ila mbona hakuna ubaya!”“Erica, elewa kaka yako naongelea kitu gani. Nimesema sitaki hiki kitu kijirudie kabisa”Kisha Erick alionekana kutoka kwa hasira, ila Erica hakuelewa kuwa kaka yake alipewa ile habari na nani mpaka kachukia kiasi kile.Angel akiwa nyumbani kwa bibi yake huyu, ilionekana kuwa huyu bibi hakuwa na muda kabisa wa kufatilia mtoto sijui kafanya nini au atafanya nini, zaidi zaidi alimpatia simu ili aweze kuwasiliana na marafiki zake na kutokujisikia mpweke.Angel kule aliweza kupata marafiki mbalimbali kiasi kwamba aliona kuwa yale ndio maisha ambayo alikuwa ameyakosa kwa kipindi kirefu sana tangia anaishi kwa mama yake.Siku hiyo akiwa ametulia nyumbani kwa bibi yake, alipigiwa simu na namba ngeni ila akagundua kuwa mpigaji amekosea namba nakumwambia,“Utakuwa umekosea namba maana unayemuulizia sio mimi”“Samahani,kwani wewe unaitwa nani?”“Mimi naitwa Angel”“Basi itakuwa ni jambo la busara kama tukifahamiana, mimi naitwa Mussa”“Oooh sawa, kwaheri”“Aaaah usikate simu Angel, nitafurahi sana kama nikikuona”Angel alimkubalia huyo Mussa kuonana nae, na alichokifanya ni kumuelekeza nyumbani kwa bibi yake ili huyo Mussa afike hapo kwa bibi yake waonane.“Basi nitakuja kesho”“Sawa, karibu”Angel hakuwa na tatizo lolote kwani bibi yake huyo alikuwa akiishi nae kama marafiki na walijikuta wakiongea vitu vingi sana.Siku hiyo ndio ambayo Angel alipanga kukutana na Mussa, na huyo Mussa alipanga kufika hapo nyumbani kwakina Angel yani kwa bibi yake Angel, basi muda ulifika na Mussa alifika na moja kwa moja alimpigia Angel simu kuwa yupo nje ya pale kwao, basi Angel aliinuka na kumwambia bibi yake kuwa kuna mgeni wake,“Mwambie akaribie tu ndani”Basi Angel akatoka nje ili kumkaribisha Mussa, ila alipoonana na Mussa alishangaa sana yani yeye alikuwa akimshangaa Mussa na Mussa nae alikuwa akimshangaa Angel. Basi Angel akatoka nje ili kumkaribisha Mussa, ila alipoonana na Mussa alishangaa sana yani yeye alikuwa akimshangaa Mussa na Mussa nae alikuwa akimshangaa Angel.Baada ya muda kupita wakishangaana, yule Mussa alimuuliza Angel,“Kwani wewe unaitwa Angel nani?”“Mimi naitwa Angel Erick, na hapa nilipo ni nyumbani kwa bibi yangu mzaa baba”“Aaaah sawa, basi duniani wawili wawili, ila dah tunafanana sana kama ndugu vile”“Hata mimi ndio nakushangaa, mbona tumefanana hivi jamani!! Tena sio ndugu tu ila ni kama mapacha vile”“Ila cha muhimu, mimi na wewe sio ndugu hilo ndio la msingi. Duniani wawili wawili, kwanza nisingefurahi tuwe ndugu, dah wewe ni mrembo sana Angel”Angel alimuangalia tu huku akitabasamu na kumkaribisha ndani ila muda huo huo simu ya Mussa iliita na kufanya amuage Angel huku akimwambia kuwa,Ilimradi nimepafahamu hakuna tatizo, nitakuja tena kukuona”Basi Mussa aliondoka, halafu Angel alirudi ndani alipo bibi yake ambaye alimuuliza,“Huyo mgeni yuko wapi?”“Aaaah kapata dharula bibi, kwahiyo kaondoka ila imechukua kama dakika tano mimi na huyo mgeni tukiangaliana”“Kwanini?”“Jamani bibi, ninafanana nae balaa. Yani kama ndugu yangu vile ila ukoo wetu ni tofauti”Bibi alimuangalia Angel kwa muda kidogo, kwani alipatwa na hisia moja kwa moja kuwa huyo mtu ni ndugu wa Angel ila Angel anaona ukoo tofauti sababu hafahamu ukweli wa ukoo wake, sema bibi yake hakuongeza neno lolote lile kuhusu ukoo wa Angel.Leo Junior aliondoka na Vaileth kuelekea kwa mama yake, na walifika na kumkuta mama yao akiendelea na mambo yake ya siku hiyo, mama Junior aliwakaribisha na kusema,“Eeeeh leo na wewe Vaileth umetaka kupafahamu kwangu!”Vaileth akatabasamu tu kisha mama Junior alimwambia mwanae,“Kwanza hongera sana kwa kumaliza kidato cha nne mwanangu, halafu pili bora umekuja kwani nataka wiki ijayo twende pamoja kwa bibi yako”“Aaaah mama, nitaenda mwenyewe tu”“Kheee kwanini wakati mimi nipo?”“Usijali mama, nitaenda mwenyewe kwa bibi”Mama Junior hakutaka kuongea zaidi ila pia hakujua ni kwanini mtoto wake ameenda na Vaileth kwa siku hiyo kwani hakujua kazi ya Vaileth ni kitu gani.Jioni ilipofika, Junior aliaga kuwa anaondoka na Vaileth kuelekea kwa mamake mdogo, mama yake alimsihi sana alale ila Junior alikataa kabisa na hivyobasi akaondoka akiwa ameongozana na Vaileth.Wakiwa njiani, Junior alimwambia Vaileth,“Nitakutambulisha kwa ndugu zangu wote, nataka wote wajue ni jinsi gani nakupenda”“Mmmh Junior, unajua ni tatizo kubwa hilo?”“Tatizo lipi sasa? Kwani kupenda ni dhambi? Kupenda sio dhambi wala nini, ni kweli nakupenda kweli kwahiyo sioni kama kuna sababu ya kunizuia mimi kufanya kile nitakacho, siwezi kwenda kuishi tena nyumbani kwani nahitaji muda mwingi niwe nakuona wewe”Vaileth hakuongeza neno lolote zaidi ya kutabasamu tu, kwa upande mwingine alijiona kuwa yupo sawa ila kwa upande mwingine aliona kuwa anafanya makosa makubwa sana.Mama Angel, leo alirudi mapema tu nyumbani kwake, ila baada ya muda mfupi tu Junior na Vaileth nao walirudi na kumpa salamu za kule walipotoka, basi aliongea nao kidogo na moja kwa moja akainuka na kuelekea chumbani kwake.Ila alipofika tu chumbani kwake, alipigiwa simu na mama Junior na kuanza kuongea nae,“Weee mama Angel, hivi huyo Junior na Vaileth nini kinaendelea kati yao?”“Kwanini dada?”“Mmmh nahisi kama kuna mahusiano ya kimapenzi kati yao!”“Mmmh sidhani dada, Vaileth anatambua wazi tabia za Junior, kweli kabisa aanze tu kuwa na mahusiano na Junior jamani! Basi atakuwa hana akili kabisa, ila naona wakiishi tu kama kaka na dada”“Hebu kuwa makini mdogo wangu, kwa siku hii moja tu nimeweza kuelewa kuwa kuna kitu hakipo sawa kati yao, unajua kama mzazi basi jambo kama hilo lazima liniumize, halafu huyu Vaileth ni mkubwa, halafu si ana mtoto huyu!”“Ndio ana mtoto, tena mkubwa tu, nadhani kwasasa mwanae ana miaka mitano”“Haya sasa, mwanamke mwenye mtoto mkubwa wa miaka mitano ndio akawe na mahusiano na mwanangu kweli!! Hapana jamani, sijapenda, hebu fatilia hilo swala kwakweli, unajua sio kawaida eeeh! Ni kweli Junior ana mapungufu yake, ila haijawahi kutokea kwa Junior kugoma kulala hapa nyumbani kwangu na vile vile kugoma kuongozana na mimi kwenda kwa bibi yake na badala yake anadai kuwa ataenda mwenyewe, nahisi kuna kitu kipo juu ya huyu msichana”“Sawa nimekusikia dada, nakuahidi kuwa nitafanyia kazi hilo swala na nitajua imekuwaje, yani nitaelewa tu mbivu na mbichi”Mama Angel aliongea na dada yake na kumpa moyo pale, ila baada ya kukata ile simu alijiona wazi kuanza kuhangaika na kazi mpya sasa ya kumfatilia Junior na Vaileth wakati amepumzika kumfatilia Angel.Ila wakati akiongea na simu ile kumbe mwanae Erica alikuwepo mlangoni, na kwavile alikuwa akiongea kwa nguvu basi mwanae Erica alisikia kila kitu ambacho mama yake alizungumzia kwenye ile simu.Usiku wakati wa kulala, Erica alimfata Vaileth chumbani na kuanza kuongea nae,“Basi leo nimemsikia mama akiongea na simu na mama mkubwa, na walikuwa wakiongelea kuhusu wewe na Junior”Vaileth akashtuka kidogo na kuuliza kuwa alikuwa akiwaongelea kitu gani,“Inasemekana wewe na Junior mna mahusiano ya kimapenzi, sasa mama kasema kuwa atawachunguza”“Mmmmh ila Erica, kuna muda huwa unakera ila kuna muda huwa unafaaa sana kwa matumizi mbalimbali. Asante sana kwa ujumbe wako”“Ila je ni kweli kuna mahusiano yanaendelea kati yako na Junior?”“Mmmh jamani Erica, kama ni kweli kuna siku nitakwambia mwenyewe”“Kwahiyo sio kweli?”“Naomba tuachane na habari hizo, kwani nahitaji kupata muda wa kupumzika kwasasa”Erica aliagana nae na moja kwa moja alienda chumbani kwa kaka yake ili kumpa huo ujumbe, ila muda ameingia chumbani kwa kaka yake basi kaka yake nae alikuwa ametoka bafuni kuoga, kwahiyo Erick alimkuta moja kwa moja Erica yupo chumbani kwake na kumuuliza,“Vipi una mpya gani?”“Ni hivi, nimemkuta mama akiongea na mamkubwa na walikuwa wakiongelea swala la Vaileth na Junior. Je wewe unahisi kuwa Vaileth na Junior wana mahusiano?”“Kwani wakiwa na mahusiano tatizo ni nini? Vaileth na mwanamke na Junior ni mwanaume”“Mmmh jamani, ila kumbuka Vaileth ni dada yetu. Kwahiyo Junior ana mahusiano na dada!”“Kwani wewe unatakaje? Unataka Abdi aletwe hapa ili nae uishi nae nyumba moja”Erica aliinuka huku akicheka kicheko cha kimbea na kusema,“Sio Abdi bhana, saivi ni mambo ya Bahati”Halafu Erica akaondoka zake, ile kitu ilimfanya Erick ajiulize maswali mengi sana, kuwa huyo Bahati ni nani? Anajua tu kuwa Erica alipewa viatu na mwanaume ila hakumjua huyo Bahati, kwahiyo alijikuta akitamani sana kumfahamu huyo Bahati ambaye kwa muda huo ametajwa na Erica, basi alitafakari kwa muda kidogo ila hakupata jibu wala nini.Moja kwa moja aliamua zake kulala tu.Kulipokucha, walijiandaa kwaajili ya kwenda shuleni kama kawaida, basi Erick alienda shuleni ila siku hiyo gari lao la shule lilipata hitilafu kidogo kwahiyo dereva alisimamisha na kuanza kutengeneza gari lile, wakati dereva akitengeneza gari lile, baadhi ya wanafunzi walikuwa wameshuka na wapo pembeni ya gari wakiangalia kinachoendelea ndipo alifika binti mmoja ambaye walikuwa wakisoma nae ila Erick hakuwa na mazoea na binti huyo kwani yeye hakuwa na ukaribu kabisa na watoto wa kike, basi yule binti alimfata Erick karibu na kuanza kuongea nae,“Naitwa sarah! Nipo kidato cha pili”“Oooh, mimi nipo kidato cha kwanza”“Unajua nimekuangalia sana, mbona unaonekana umekaa peke yako peke yako kwani una tatizo gani?”“Hapana, sina tatizo lolote”“Hupendi kuongea na watu? Ila unaonekana unatokea kwenye familia nzuri sana, unajua katika maisha niliwahi kusikia stori moja hivi kuwa mahusiano mazuri ya kimapenzi huanzia shuleni”“Unazungumzia nini kwani?”Lile gari lilitengemaa na wanafunzi wote walirudi kwenye gari halafu safari ya kwenda shuleni ikaendelea.Ila walipofika shuleni, yule binti alimpa Erick ujumbe halafu yeye aliondoka zake na kuelekea darasani kwao, kwakweli Erick alimshangaa sana na hakuelewa kuwa yule binti alikuwa na maana gani.Nyumbani siku hii walibaki Junior na Vaileth tu, ambapo Vaileth alimueleza Junior kile ambacho aliambiwa na Erica,“Nilijua tu, yani mama yangu huwa anaacha kufatilia mambo ya maana ila yeye huwa anakazana na kufatilia ujinga tu ambao huwa haumsaidii chochote kile.”“Ujinga upi?”“Sasa aanze kunifatilia mimi kweli ataweza? Mbona kipindi kile hakuweza, kiukweli Vaileth umebadilisha sana maisha yangu, tena umeyabadilisha kwa kiasi kikubwa sana kwahiyo hata waseme kitu gani kwangu ni sawa ma bure tu”“Ila tunatakiwa kuwa makini sana, kwani tukigundulika kuwa tupo pamoja ni hatari kubwa sana. Ni hatari kwangu na ni hatari kwako pia”Muda kidogo alifika mgeni, na mgeni huyo alikuwa ni mama Junior, hakwenda kwa taarifa kwavile alitaka ajaribu kuona kuwa ni kitu gani kinaendelea.Basi Junior alikaa na mama yake na kuanza kuzungumza nae,“Mama, hivi bamdogo alikueleza kuwa ni mazingira gani ambayo alinikuta nayo mimi kabla ya kuchukua uamuzi wa kuja kuishi nae hapa kwake?”“Kivipi?”“Bamdogo alinikuta mimi nikiwa guest, na nilikuwa na mwanamke mkubwa sana. Kiukweli maisha yangu yaliharibika sana na kila kitu mlichokuwa mnanisema niliona kama ni kumpigia mbuzi gitaaa. Ila nakuuliza sasa, je maisha yale na haya ninayoishi sasa yapi ni bora?”“Sikuelewi Junior, kwani unazungumza kuhusu nini?”“Mama, jana nimekuja kwako kukuona nikiwa nimeongozana na Vaileth ila umeanza kunihisi vibaya, hata kitendo chako cha kufika leo hapa ni kwamba unataka kunichunguza. Hivi mama umeshindwa kunichunguza siku zote hizo ndio unichunguze leo kweli? Unajua wazi kuwa sipendagi unafki, niambie mimi wazi ni kitu gani unanihisi sio kuanza kunichunguza chunguza. Haya nikiwa na mahusiano na Vaileth, je wewe nakupunguzia kitu gani mama yangu? Kwani Vaileth sio mwanamke wa kufaaa kuwa na mimi? Watoto wa kike ndio huwa wanachungwa kwani wanaweza leta mimba nyumbani, ila mtoto wa kiume sio wa kuchungwa, nikileta watoto kwako ni baraka kuwa mtoto wako ni rijali”Mama Junior alimuangalia mwanae na kutikisa kichwa, kwakweli hakuona kabisa umuhimu wa yeye kuendelea kuwepo kwenye eneo lile, kwani muda huo huo aliamua kuondoka tu.Kwakweli mama Junior alitembea njiani huku akitafakari mambo mengi sana na kusema,“Kweli mtoto wa nyoka ni nyoka, yani huyu Junior ni tabia za baba yake mtupu, kupenda wanawake, na muda wote kuona kuwa anachofanya yeye sio kosa yani anaona kuwa anachofanya yeye kipo sahihi. Yani hapa kwakweli sijazaa kabisa bali nimeingia kwenye matatizo”Wakati akitembea mara akashikwa bega, kugeuka alimuona mtu ambaye alimfahamu vizuri sana, na kumshangaa,“Kheee wewe kumbe upo?”“Nipo dada, kwanza kabisa naomba unisamehe kabisa kwa yote ambayo nilikukosea”“Kumbe bado unayo hayo?”“Unajua, kuna muda huwa nafikiria sana kuhusu wewe na kuona kuwa kiburi nilichokufanyia basi leo kimekuja katika maisha yangu”“Kivipi?”“Mimi nilikuwa msichana wako wa kazi na ulinilea vizuri kabisa, ulinifanya kama mdogo wako ila sikuwa na huruma kwani niliamua kutembea na mume wako hadi kupata ujauzito, mumeo alinipangishia nyumba na kuanza kuishi na mimi kwa siri siri hadi siku ambayo wewe na mdogo wako mlikuja na kufanya fujo katika nyumba ile. Dada nikianza kukuelezea niliyopitia kwa hakika utanihurumia sana, ila kwa kifupi na mimi nilipata bahati ya kuolewa, ila unajua kilichotokea kwangu? Mume wangu pia alienda kuzaa na msichana wa kazi, yani dada huwa nalia mno kwani maisha kumbe ni duara, yanazunguka pale pale”“Usijali, kwangu yalishaisha kitambo sana. Hajambo mwanao?”“Hajambo, ila ninao na wengine. Mwanangu yule nilimuita James, jina moja na baba yake, yule mtoto alikataa shule, yani kanisumbua sana, kwasasa anaishi na mjomba wake, ila ana matukio mengi ambayo hayafurahishi hata kidogo. Kuna muda huwa najutia sana, na kujilaumu sana, ila ndio hivyo maji yakimwagika hayazoleki wala nini. Nimefurahi kukuona tena, kama hutojali basi naomba mawasiliano yako”Mama Junior hakuwa na pingamizi la aina yoyote ile zaidi zaidi ya kubadilishana namba na yule mwanamke, wala hakutaka kumfikiria sana kwani kwa muda huo hata yeye alikuwa na mawazo yake ya kutosha tu.Muda wa kutoka shule ulipofika, Erick alitoka na kwenda kupanda kwenye gari ili kurudi nyumbani kwao, ila siti aliyokaa basi pembeni yake alienda kukaa binti ambaye walionana asubuhi ya siku hiyo, binti aliyeitwa Sarah.Basi yule binti alianza kumuongelesha,“Unajua muda huu wa kutoka nimefurahi sana kukaa na wewe. Sikia usinifikirie vibaya wala nini, wakaka wengi huwa wanafikiria kuwa mwanaume ndio anayetakiwa kumtongoza mwanamke, ila kuna muda mwingine inatokea tu kwa mwanamke kumtongoza mwanaume”“Kwahiyo wewe unanitongoza?”“Na unajua kuwa haipendezi kwa mwanaume kumkatalia mwanamke, yani siku zote hizi huwezi amini huwa nakuangalia sana na leo nimeamua kujitoa muhanga tu na kukwambia ukweli, nadhani ni kusudi la Mungu kwa gari letu la shule kuharibika siku ya leo. Kwa kifupi, Erick nakupenda sana, katika maisha yangu nimetamani sana nianze mahusiano nikiwa shuleni, na nilipokuona wewe niliona kuwa hii ndio nafasi yangu ya pekee kabisa. Nakupenda sana, nahitaji uwe wangu”Yani Erick alimuangalia sana huyu Sarah kwani hakuwahi kufikiria kama kuna binti mdogo kamaSarah mwenye ujasiri wa kusema yale aliyoyasema, kwahiyo alibaki akimuangalia tu huku akimshangaa, kisha Sarah akamwambia tena,“Sio lazima uniambie kwa muda huu, hata Jumatatu hakuna tatizo, nitasubiri jibu langu”Erick alifika nyumbani kwao na kushuka, moja kwa moja aliingia ndani ila leo alimkuta Junior akiangalia video ya ngumi, basi alipobadilisha nguo nae alirudi pale sebleni na kuungana na Junior kuangalia ile video, kisha Junior alimuuliza,“Hivi mikanda mizuri hii ya ngumi kaileta nani? Najua mamdogo hawezi kufanya kitu cha namna hii”“Kuna yule rafiki yake na Erick, wa kuitwa Samia, basi ndio mletaji wa mikanda hii”“Oooh halafu yule Samia anaonekana anakupenda”Erick alicheka tu halafu Junior alimuuliza tena,“Hivi Erick, huwa huna mwanamke eeeh! Hata siku moja hujawahi kuja kuniuliza chochote kile”Mara mlango ulifunguliwa na Erica aliingia ndani na kujibu lile swali,“Yani wewe Junior, tabia zako basi unataka kila mtu awe nazo, hivi huoni kama Erick ni kijana mdogo! Sasa awe na wanawake wa kazi gani?”“Ila wewe nawe, wanaume ndio tunaongea hapa. Sijakuuliza wewe, yani wewe tukisikia hata kuna mwanaume anakunyemelea basi huyo mwanaume ataipata, maana nyie watoto wakike mnatakiwa kulindwa, ila Erick ni mtoto wa kiume kwahiyo ni haki yake kuwa na wanawake”Erica alichukia na moja kwa moja kuelekea chumbani kwake.Mama yao aliporudi siku hiyo, moja kwa moja Erica alienda kumueleza mama yao kile ambacho Junior alikuwa akiongea na Erick, kwakweli mama Angel alichukia sana na kumfanya ahisi kuwa Junior anataka kuanza kumfundisha mtoto wake tabia mbaya.“Haya mwanangu, asante kwa taarifa”Basi Erica aliondoka zake, na baba Angel aliporudi mama Angel alimueleza lile jambo zima kwa vile alivyoelezewa na Erica,“Aaaah mke wangu jamani, hebu wasikuchanganye kitu hao watoto jamani, yani wasikuchanganye mke wangu. Saivi tulee mtoto wetu huyo, tukianza kufikiria mara Junior hivi, mara Erick vile kwakweli tutashindwa kufanya mambo ya maana”“Kwahiyo umeanza kutetea ujinga eeeh!”“Mimi sitetei chochote kile ila naongea ukweli mke wangu, hebu tufikirie mambo ya maana basi. Mwanetu huyo tutamuita nani? Na vitu kama hivyo”“Kheeee yani wewe, haya umewasiliana na Angel?”“Oooh sijawasiliana nae, ngoja nimpigie simu mama”Basi baba Angel alimpigia simu mama yake na kuomba kuongea na Angel ambapo waliongea nae Angel huku wakimuulizia kuwa maisha ya kule anayaonaje,“Ni kuzuri baba, nishazoea tayari”“Ni vizuri kusikia hivyo, ongea na mama yako”Basi alimpa simu mama Angel ambaye aliongea na mwanae na kisha kuagana nae, kikweli mama Angel alikuwa ameridhika sana kuongea na mtoto wake kwahiyo kwa muda huo aliweza kulala tu kwa amani na kusahau yote aliyokuwa akiyasema.Angel na bibi yake walianza kuongea, ambapo bibi yake alimuuliza,“Mbona hujawaambia wazazi wako kuwa na wewe una simu yako ili wawe wanakupigia humo?”“Mmmmh bibi, usiwaambie, yani mama hataki kabisa nimiliki simu ujue”“Kwanini sasa jamani?”“Hata sijui, ila mama hapendi niwe na simu”“Aaaah na mama yako nae ana mambo ya kizamani utafikiri ni mmama wa enzi zetu jamani, wakati ni mmama wa kipindi hiki, anatakiwa kulea watoto wake kisasa, kwani mkimiliki simu ndio nini sasa? Hebu anitolee ushamba mie. Mjukuu wangu, kesho tutaenda mahali, ni pa muhimu sana maana kuna wafanyabiashara wa maana naenda kuonana nao”“Sawa bibi”“Basi mapema kabisa ujiandae, sawa”“Sawa, hakuna tatizo”Basi Angel alienda zake kulala, kwakweli Angel alipenda sana maisha ya kuishi na bibi yake huyo kwani alikuwa akimfanya ajiachie sana na kumfanya ajihisi vizuri sana kuishi na bibi yake.Wakati analala alipigiwa simu na Mussa na kuanza kuongea nae,“Kesho nitakuja tena kwenu Angel, nina shida sana ya kuonana na wewe”“Aaaah ni ngumi maana kesho kuna mahali naenda na bibi yangu, kwahiyo sitaweza kuonana na wewe”“Sawa, hakuna tatizo lolote. Itabidi tuonane kw awakati mwingine”Basi Angel alikubaliana na Mussa kuonana na wakati mwingine na moja kwa moja kwa muda huo aliamua kulala tu.Kulipokucha, ni kama ambavyo alipanga na wifi yake, kwani alijiandaa halafu bibi yake alimuita na kuondoka nae pamoja mpaka kwenye kikao cha wafanyabiashara ambapo bibi yake alikuwa ameenda kuonana nao.Basi bibi yake alikuwa akimtambulisha Angel karibu kwa kila mtu aliyekuwepo eneo hilo, kuna rafiki yake mmoja alimuita pembeni na kuongea nae,“Huyu mtoto unayemtambulisha hivi ni nani yako?”“Mjukuu wangu huyu, mtoto wa Erick”“Oooh, ndio wamekupa wewe umlee?”“Ndio, mimi si bibi yake”“Mmmh! Hao wazazi nao wamechoka kulea mtoto au? Yani wamekuletea wewe, hivi unakuwaga na muda kweli wa kuangalia watoto wewe! Yule wako mwenyewe umshukuru mdogo wako, hivi wewe ni wa kulea mtoto kweli!”“Wewe nawe umetumwa au kitu gani? Hebu achana na mimi na mjukuu wangu”Kisha bibi Angel akaenda kumfata mjukuu wake na moja kwa moja alienda kukaa nae kwenye meza ambapo wageni mbalimbali walikuwa wakifika kwenye kikao kile.Siku ya leo Samia alipeleka tena mikanda mingine nyumbani kwakina Erica, na alivyofika baada ya kuwakabidhi ile mikanda aliwaambia jambo ambalo Erick lilimchanganya kidogo,“Basi leo kabla sijaja huku, nilipitia pale kwenye duka lenu, nikakutana na yule mama ambaye alisema kuwa niende pale nikachukue ninachokitaka, ila nimemkuta yule mama akigombana na yule mkaka wa kwenye lile duka”“Mmmmh! Akigombana nae kivipi?”“Yule mama alikuwa akimwambia yule kaka kuwa lile duka ni la mtoto wake”Erick alishangaa sana kwani ugomvi wa duka lile hakuwahi kuushuhudia wala hakujua kama kuna kitu cha namna hiyo, basi hakutaka hata kupoteza muda kwani muda huo akatoka zake nje na kupanda kwenye gari lao kwahiyo hakuondoka na Samia wala na mtu mwingine yoyote yule.Erick alifika dukani, na kweli alimkuta Steve akibishana na mwanamke mmoja ambaye yeye hakumfahamu, basi alisogea karibu na kuuliza,“Kwani tatizo ni nini hapa?”“Tatizo la hapa ni huyu mama, yani huyu mama binafsi huwa simuelewi kabisa”Basi Erick alimuangalia yule mama na kumuuliza,“Kwani tatizo ni nini dada?”“Usiniite dada mie, niite mama, hebu kuwa na heshima kwa wakubwa wako”“Haya mama, unalalamika kitu gani hapa dukani?”“Nenda kamuulize baba yako vizuri, kuwa lile duka ni la nani na yeye atakueleza vizuri”“Una kichaa wewe mama au? Nimuulize vizuri wakati duka ni la kwangu”“Kwani wewe ni nani?”“Kumbe hata unayeongea nae humjui! Mimi ndio mmiliki halali wa hili duka”“Hili duka ni la mtoto wangu”Erick alimuangalia huyu mama na kumwambia,“Huwa sipendi kubishana katika maisha yangu, naomba uondoke sasa hivi”“Kheee inawezekanaje mtoto kama wewe kunitishia maisha mimi? Hivi unanijua vizuri mimi? Yani laiti ungejua mimi ni nani basi usingethubutu kufungua mdomo wako na kusema chochote kile”Erick hakuwa muongeaji sana, hivyobasi hakutaka kubishana zaidi na huyu mama zaidi zaidi aliamua kumsukuma ila kitendo kile kilimfanya yule mama atoe kilio cha ajabu utafikiri kafanywa kitu gani,.Kilio kile kilifanya watu wengi sana wajae katika duka lile, halafu yule mama alianza kusema,“Yani mtoto niliyemzaa mwenyewe, leo hii ananisukuma kama mwizi”Steve na Erick walibaki wakishangaa tu. Erick hakuwa muongeaji sana, hivyobasi hakutaka kubishana zaidi na huyu mama zaidi zaidi aliamua kumsukuma ila kitendo kile kilimfanya yule mama atoe kilio cha ajabu utafikiri kafanywa kitu gani,.Kilio kile kilifanya watu wengi sana wajae katika duka lile, halafu yule mama alianza kusema,“Yani mtoto niliyemzaa mwenyewe, leo hii ananisukuma kama mwizi”Steve na Erick walibaki wakishangaa tu.Erick alimuuliza Steve,“Kwani huyu mwanamke anazungumzia kitu gani?”kwakweli hata Steve hakumuelewa yule mwanamke, na sababu alizidi kufanya watu wajae pale dukani ikabidi Steve apige simu moja kwa moja kwa baba Angel ili afike mahali pale kwani alihisi labda baba Angel ndio anaweza kuelewana na yule mwanamke.Watu walijaa pale huku wakimsikiliza ambapo alikuwa akiwaambiwa stori ambayo walikuwa wakishangaa tu,“Kwahiyo mtoto wako mwenyewe aliyekusukuma ni yupi?”Alikuwa akimnyooshea Erick ila Erick alisema,“Sio mama yangu huyo jamani!”Steve nae alikuwa akisema pale,“Jamani jamani, msimsikilize huyu mwanamke ana wazimu tena wazimu uliopitiliza, huyu sio mwanae”Kisha Steve alimfata karibu yule mwanamke na kumwambia,“Nimemuita baba mwenyewe mwenye hili duka, endeleza uchizi wako nadhani utajuana nae vizuri tu”Wakati akiongea nae hayo, mara gari la baba Angel nao liliwasili eneo lile, ila baada ya yule mwanamke kuona lile gari tu aliinuka haraka na kukimbia toka eneo lile.Kwakweli baba Angel hakupenda kabisa jinsi watu walivyojaa nje ya duka lake na kuanza kuwatimua ambapo wengi walisambaratika, halafu aliingia dukani na kumuuliza Steve kuwa kuna nini huku akimuangalia Erick aliyekuwa kainama chini tu,“Kwakweli sijui nikwambiaje bosi, ila nisamehe kwakweli. Toka nianze kazi hapa amekuwa akifika Sia, nadhani unamfahamu vizuri sana hata mama alishawahi kumkuta”Basi baba Angel alimchukua Steve pembeni na kuanza kuongea nae kwa undani zaidi,“Huyo Sia huwa anakuja kufanya nini na huwa anafanya kitu gani na leo kafanya nini hadi kujaza watu namna ambayo nimekuta? Yani haya ndio matatizo ya kuweka duka uswahilini jamani, hadi najuta hapa. Niambie kwanza imekuwaje?”Steve alianza kumueleza kuanzia mara ya kwanza ambapo Sia aliasema kuwa duka lile ni mali ya mtoto wake na jinsi alivyosema wazo la kujenga duka hapo amelitoa wapi, na jinsi leo alichokifanya hadi kujaza watu kiasi kile, baba Angel aliweza kuelewa ni kwanini hata Erick amepooza basi alimfata na kuanza kuongea nae,“Mwanangu, kwanza kabisa na wewe niambie leo kitu gani kimekuleta huku?”“Baba, ulisema kuwa niwe nakuja kuangalia hili duka mara kwa mara, sasa leo alikuja rafiki yake na Erica na amesema kuwa kuna mwanamke yupo dukani akigombana na huyu anko basi ndio nikaamua kuja”“Sawa, kwa kifupi nimeelewa mwanangu”Kisha baba Angel alimuangalia Steve na kumwambia,“Nahitaji kupata muda wa kutosha niweze kuongea na huyo Sia, najua kuwa ipo siku au kuna muda atarudi tu. Na usimwambie chochote kile ila kuna askari watakuwepo na akija tu basi watamkamata na kunipigia simu”Kisha baba Angel alimtaka Erick waweze kuondoka, na moja kwa moja alienda nae hotelini kwani mwanae huyu alimuona kuwa ni mkubwa na anapaswa kufahamu vitu vingi sana.Basi baba Angel alifika na Erick hotelini na kuanza kuongea nae,“Kwanza kabisa Erick nakupongeza sana kwa kuwa kijana mzuri kwa kipindi chote hiki, inaonyesha mtoto wangu wewe hupendi makuu. Mimi baba yako nilianza mahusiano ya kimapenzi nikiwa mdogo sana, yani wakati nipo darasa la nne tayari kuna wanawake nilianza kuwatamani na kuna wengine waliokuwa wakinitaka kimapenzi, ila nilipofika kidato cha pili ndio nilimuona yule mama yenu kwa hakika nilijikuta nikimpenda sana ila sikuweza kumpata sababu tulikuwa tunasoma. Kwanini nimekwambia yote haya? Sababu nahitaji mwanangu uwe makini sana, haya maisha bila umakini hakuna utakachoweza kufanya, kama ukipenda kitu basi kishikilie hiko hiko, mimi nilipomkosa mama yenu ndio nikazidi kuwa muhuni kiasi kwamba nilikuwa na kila aina ya mwanamke na mwishowe nikaangukia kwa yule chizi ambaye umemuona amefanya vurugu dukani, unajua kuna watu mbalimbali unaweza kukutana nao katika maisha na wengine wakapita tu bila ya tatizo lolote katika maisha yako ila kuna watu ni ruba yani wenyewe huwa hawapiti bila kukusababishia matatizo katika maisha yako. Yule mwanamke hana lengo jema katika maisha yangu, naona bado ana kinyongo kikubwa sana na mimi sababu tu sikumuoa yeye ila nikamuoa mama yenu, mengine nitakusimulia zaidi mwanangu. Ila kwasasa, nakuomba kitu kimoja, usimsimulie mama yako chochote kile kilichotokea pale dukani halafu yale yote ambayo yule mwanamke kaongea kwako ona kama hakuna cha maana alichozungumza yani wewe achana nayo tu hata usiyajali wala nini. Mimi naelewa ni kwanini kasema vile, kwahiyo mwanangu hata usichukulie maneno ya yule mwanamke kuwa na maana, mimi ni baba yako na mama yako ndiye mama yako yani sisi ni wazazi pekee ambao tupo katika maisha yako. Achana na maneno ya yule mwanamke mwanangu. Natumaini umenielewa, mimi najua ni kwanini yule mwanamke kakwambia vile ila wewe achana na maneno yake”“Nimekuelewa baba, hakuna tatizo”Halafu mwanangu, nitaenda kukuonyesha duka lingine. Sipendi ukae kwenye duka ambalo lina migogoro, kwanza lile duka nitalifunga tu, dah yule mwanamke kanikera sana”Erick alimuitikia baba yake ila maswali aliyokuwa akijiuliza kichwani ni mengi mno, kwanza kwanini asimueleze mama yao kuhusu lile swala, halafu kwanini baba yake anaonekana kuona lile jambo kuwa la kawaida kabisa, ila hakusema chochote kile zaidi zaidi walimaliza maongezi yao na kurudi tu nyumbani kwao.Angel akiwa na bibi yake kwenye kile kikao, muda huu Angel aliomba ruhusa kwa bibi yake kuwa anaenda uwani mara moja, ila wakati ameondoka kuna mbaba mmoja ambaye alikuwa ni mfanya biashara mkubwa sana alimfata Angel kwa nyuma na kuwa kama akimvizia atoke chooni, na kweli Angel alipotoka alianza kuongea nae,“Binti, sijafanya vibaya kuja kukusubiri huku ila ningefurahi zaidi kama ningepata mawasiliano yako”Kwavile bibi yake alishamtambulisha kwa mfanyabiashara huyo basi yeye hakuona tatizo kabisa basi akatoa simu yake ili aangalie namba na amtajie ila simu ile alivyoishika tu ilizimika, ni simu ambayo alikuwa akiwasiliana nayo ila ilikuwa ikimsumbua sana katika swala la chaji, basi Angel alimuangalia yule mbabu na kumwambia kuwa simu imezimika, halafu akarudi nae kwenye kikao ambapo kikao kile walikuwa wakimaliza kwa muda ule, ila yule baba alimfata bibi yake Angel na kumwambia,“Julieth, kweli simu gani hiyo ya kumpa mjukuu wako atumie jamani!”“Aaaah unajua hiko kimeo kilikuwa ndani, sasa mjukuu wangu hakuwa na simu kwahiyo nikaona ni vyema atumie tumie tu”“Aaaah sijapenda kabisa, yani mfanyabiashara mkubwa kama wewe mjukuu wako anaanza kutumia vimeo kweli jamani!”“Oooh wewe nawe, ushaanza mambo yako, haya mnunulie mjukuu wangu simu”Bibi yake Angel aliongea kwa lengo la kujifurahisha tu, ila yule babu aliahidi kuwa kesho yake angemletea simu Angel, basi wakaongea pale na kuagana na wale wafanya biashara wengine halafu kila mmoja kuondoka ambapo Angel aliondoka na yule bibi yake.Njiani, Angel alimuuliza bibi yake,“Sasa, bibi yule ataniletea simu gani?”“Ngoja tu utaiona kesho, halafu yule hanaga masikhara jamani mimi nilikuwa namtania tu. Ila sio kosa langu kwa wewe kutumia kimeo, ni kosa la wazazi wako. Yani wanafanya mambo kama hawana hela vile, hivi kweli kabisa baba yako na mama yako wameshindwa kukununulia simu jamani! Ila sio mbaya, yule babu atakununulia”“Kwani anafanya biashara gani yule?”“Ilimradi nimeanza kuja nawe kwenye vikao vua biashara basin i wengi utawafahamu ila yule babu ni mfanyabiashara mkubwa sana, yani ana biashara nyingi nyingi halafu zote ni kubwa, anatambulika kwa jina moja kubwa la Mr.Peter”“Oooh sawa bibi”Basi walifika hadi nyumbani ambapo kwa siku hiyo Angel aliamua kulala tu kutokana na uchovu na mizunguko ya hapa na pale na bibi yake.Muda ambao Erick na baba yake walirudi nyumbani, walimkuta mama Angel alisharudi nyumbani muda mrefu tu, basi mama Angel aliwauliza,“Kheee wenzetu mmetoka wapi muda huu?”Baba Angel alicheka tu na moja kwa moja kutangulia chumbani ambapo mama Angel nae alimfata nyuma na kuanza kuongea nae,“Leo hata kunifata umeona ni shida halafu saizi ndio mmeingia nyumbani, umetoka wapi na mwanao?”“Ila na wewe mke wangu mara nyungine jamani, unajua kuna vitu vingine ni lazima kwa baba kuzungumza na mtoto wake wa kiume kama ilivyokuwa mama kuzungumza na mtoto wake wa kike”“Sasa unadhani mimi nitazungumza nini na Erica jamani! Bora hata Angel, maana huyu Erica ni kitu gani mtu unaweza kuzungumza nae akakuelewa”“Kwanini sasa?”“Mtoto ni mbea na hakuna anachokuelewa hata umwambie nini!”“Sasa unadhani Erica katoa wapi tabia ya umbea? Ukiona hivyo ujue wazi kuwa hata wewe ulikuwa mbea ndiomana Erica nae yupo hivyo”“Hapana jamani, mimi sikuwa na tabia hiyo kabisa, yani siwezi kuongea chochote na Erica sababu ya tabia yake ya umbea”“Subiri akikua ataacha”“Ila katika yote, huyu Erick ndio huwa ananishangaza sana. Kwa jinsi tabia yako ilivyokuwa nilijua nitapata shida sana kwa Erick kama angefata tabia yako, yani hakuna pa kupona kwake, wewe tabia moto, baba yako alikuwa moto yani kwakweli nafurahi sana kuona Erick yupo na tabia tofauti kabisa. Na hivi tuna pesa si ndio ingekuwa balaa, maana mtoto wetu ni mzuri jamani, yani angekuwa muhuni basi kwa hakika ingekuwa balaa yani tabia yake ingekuwa ya Junior ikasome”“Erick hawezi kufanya ujinga, halafu katika watu wenye tabia mbaya, naomba usiniweke mimi kabisa. Inamaana basi hata Angel unamuonea tu maana kachukua tabia yako”Hilo lilimkera mama Angel kwani binafsi yake hakuipenda tabia ya Angel haswaa kuhusu Samir, ila alichukia kwa muda na kusema,“Natumaini mwanangu alipo atarudi akiwa amenyooka vya kutosha”“Ndio, atarudi kanyooka”Baba Angel hakutaka kuongea mengi kwa muda huo kwani hakutaka hata kuelezea yale ambayo yalitokea kwa siku hiyo kuhusu Sia.Angel leo akiwa ametulia na bibi yake, walipata ugeni ambapo mgeni alikuwa ni yule baba Mr. Peter, basi walimkaribisha vizuri sana ambapo alikuwa katimiza ile ahadi yake ya kumletea Angel simu ambapo alimkabidhi pale, bibi yake alishangaa kidogo na kusema,“Kheee mbona umemchukulia simu ya gharama sana jamani! Yani simu ambayo hata bibi yake tu situmii!”“Na wewe Julieth hebu acha mambo yako, kwani hiyo simu ina ugharama gani jamani! Simu ya milioni mbili tu ndio inakutoa roho kiasi hiko jamani! Mwache mtoto atumie simu inayoendana na hadhi yake”“Haya, Angel chukua hiyo simu babu yako kakuletea”Angel aliichukua pale na kumshukuru yule mzee ambaye alimsaidia pale kuweka laini kwenye ile simu huku akimwambia,“Mjukuu wangu, tena wewe sababu ni kijana basi utajua matumizi mengi sana kwenye hiyo simu yani sio kupiga na kutuma ujumbe tu ila hiyo simu ina mambo mbalimbali, kuna mitandao ya kijamii humo yani mambo mengi mengi, utajifunza na kujiunga”“Sawa, nashukuru sana”Angel alimuacha bibi yake pale na yule mzee kisha yeye alienda zake chumbani ambapo alianza kutumia ile simu.Muda ule ule alipigiwa simu na Mussa, kwahiyo alipokea na kuanza kuongea nayo,“Jana nilitaka kuja Angel, ila umenikatili ujue”“Aaaah pole”“Unatumia simu ya aina gani?”“Ni mpya, kwani unatakaje?”“Aaaah, nilikuwa nataka kukununulia simu nyingine, kesho nakuja Angel”“Haya, karibu”Angel alimaliza maongezi na Mussa na kukata ile simu, kisha aliamua kuanza kuibonyeza bonyeza ile simu na kuingia katika mtandao wa facebook ambao alijiunga kwa siku hiyo hiyo, ila alishangaa kwa muda ule ule kutumiwa ombi la urafiki na mtu ambaye alikuwa akimfahamu kwa jina ila mtu huyo hakuweka picha yoyote kwenye mtandao, aliona jina Samir, kwanza alipoona moyo wake ulishtuka halafu alijiuliza,“Je huyu ni Samir yule niliyekuwa nasoma nae au ni kitu gani?”Ila alikubali ombi la urafiki wa Samir ambapo muda huo huo Samir alianza kuwasiliana nae,“Hivi ni wewe Angel tuliyosoma wote au?”“Hata mimi najiuliza, hivi ni wewe Samir au?”“Kama ndio hivyo basi tumekutana kweli, dah nimefurahi sana. Kuna mambo yanaweza kutokea katika maisha ila hujui maana yake wala nini?”“Kwanini? Na umejuaje kuwa ni mimi? Maana ndio kwanza nimejiunga leo kwenye huu mtandao”“Ni hivi Angel, mimi nipo na mama yangu kwaajili ya kazi Fulani huku. Sasa leo, aliniambia kuwa nijiunge na facebook kwani kuna kundi sijui anataka awe anaangalia picha za mishono ya nguo, kwahiyo nilijiunga kwasababu ya mama. Yani nikashangaa nimemaliza tu kujiunga, naona jina lako kuwa naweza tuma ombi la urafiki kwako basi ndio nikatuma”“Mmmh Samir, kuna nini kati yetu?”“Sidhani kama kuna kingine zaidi ya upendo, yani upendo baina yangu na yako ni mkubwa sana kiasi kwamba hauwezi kuzuiwa na chochote kile, ndiomana kila kinachofanyika baina yetu basi lazima tujikute tukiwa pamoja, halafu nitumie na namba yako ya simu”Angel aliitwa na bibi yake, kwahiyo aliacha ile simu na moja kwa moja kwenda kuongea na bibi yake,“Kheee Angel umejifungia chumbani, mgeni anataka kuondoka. Ndio nimekuita akuage”“Oooh, karibu sana”“Asante mjukuu wangu, nashukuru”Kisha mr.Peter alimuangalia bibi yake Angel na kumwambia,“Julieth, nadhani nitatafuta siku ili twende kufurahi na mjukuu wetu. Unajua nimempenda sana huyu mtoto, anaonekana yupo vizuri, kwanza hana kiburi na hana majivuno yani ni maringo tu kidogo”“Aaaah mtoto wa kike huyu kwahiyo kuringa ni lazima, ila ukimzoea utamuona kawaida tu”Basi Angel alimuaga yule babu na moja kwa moja kutaka kurudi chumbani kwake ila bibi yake alimwambia,“Angel, nilipenda sana chakula ulichokipika juzi, pika tena kama kile mjukuu wangu ili tule”Basi Angel alipitiliza jikoni na kuanza kupika chakula ambacho bibi yake naye alikihitaji.Usiku wa siku hiyo, Angel aliingia tena kwenye mtandao na kuanza kumtafuta Samir, yani kwenye ule mtandao alikuwa akiwasiliana na Samir tu na hata marafiki alikuwa na rafiki mmoja tu ambaye ni Samir halikadharika na kwa Samir pia, alikuwa na rafiki mmoja tu na muda ule Samir nae alikuwa hewani akisubiri ujumbe toka kwa Angel, basi Angel alimtumia Samir namba yake ya simu halafu akamuuliza,“Halafu Samir, ni kitu gani kilikuwa kinaendelea kati yako wewe na madam Hawa?”“Hakuna chochote, yule madam alinichukulia kama mwanae, na aliataka nisome basi. Unajua yule madam nilimueleza ukweli kuhusu wewe”“Mmmh kwahiyo ulimwambia nini?”“Nilimwambia kuwa nakupenda sana, yani katika vitu vyote sikuweza kumficha kuhusu wewe, ni kweli nakupenda sana Angel. Mimi sina nia sijui ya kukuharibia masomo yako, sijui kukuharibia usichana wako hapana, ila mimi nakupenda, yani wazazi wako hawakuelewa tu kuhusu mimi, yani mimi ile ukaribu tu na wewe nasikia kuridhika katika moyo wangu yani hakuna kingine zaidi ya hiki”“Mmmh! Kwahiyo mimi na wewe tuwe wapenzi?”“Jamani Angel unauliza majibu kweli! Mimi na wewe tuwe wapenzi ndio, wala tusitumie papara wala nini kwani ni wazi kuwa mimi na wewe tunapendana sana, ila pia tusikubali kutenganishwa mapenzi yetu. Siku moja nitakuhadithia historia ya mama yangu katika mlolongo wa mapenzi maana mimi huwa naongea na mama kiurafiki kabisa. Kwahiyo Angel, mimi nina maana kubwa sana kukufata wewe sababu nakupenda kweli na sitaki kutengwa na wewe, siwachukii wazazi wako kwani najua walikuwa wakifanya jitihada zote za kuhakikisha kuwa huwi na mimi ila tu hawakujua nguvu ya mapenzi ambayo ipo kwangu juu yako”Yani Angel alikuwa akisoma huu ujumbe mara mbili mbhili huku akitabasamu, yani aliwaza vitu vingi sana vya tangia anafahamiana na Samir, na jinsi walivyokuwa wakitenganishwa basi alikuwa akitabasamu tu na kuaendelea kuwasiliana nae.Mwisho wa siku walijikuta wakilala usiku sana, yani kwenye saa tisa usiku ndio walilala sababu ya kuwasiliana sana.Leo mama Angel aliamua kwenda kumtembelea mama yake mzazi kwani na tumbo lake lilikuwa kubwa sana kwa kipindi hiko ila aliona ni vyema kama akienda kumsalimia mama yake,“Oooh mama kijacho, karibu sana. Ila katika mimba zako zote basi hii mimba umeibeba kwa uhuru sana”Mama Angel alicheka kidogo, kisha akamwambia mama yake,“Ila hata mimba zingine nazo sikupata shida, kama mimba ya Angel ndio kabisa”“Usitake kujisifia hapa. Mimba ya Angel si ndio ulikuwa ukijificha nayo mwanzo mwisho, hata mtoto ulikuwa ukimficha asionekane na watu. Halafu leo hii unasemaje? Eeeeh na Angel yuko wapi? Maana ajiandae kupokea mdogo wake huyo”“Mmmh mama, mbona Angel yupo kwa bibi yake yani mama yake na Erick”“Kheee kweli Erica umechoka mwanangu, kwa wingi gani wa watoto hadi umempeleka Angel huko?”“Mama jamani, Angel alikuwa hajatulia kwahiyo niliona ni vyema kama nikimpeleka kwa bibi yake huko”“Yani Erica, kila kitu unaelewa yani hakuna usichoelewa, yule mama toka lini akalea watoto? Huyo Angel unamtakia nini? Kwahiyo umemkimbiza Angel ili asikimbizane na wanaume, unafikiri huko ndio umemuokoa? Yani yule Julieth namfahamu vizuri sana, jamani hajui kulea watoto yule ni hajui kabisa, tabia atakazorudi nazo Angel huko kwa hakika utaimba haleluya na hutoweza kumrekebisha tena yani kila ukitaka kumrekebisha ndio utakuwa unamuharibu zaidi”“Jamani mama unanitisha”“Sikutishi ila nakwambia ukweli mtupu, yani huko mwanangu umemtumbukiza mwanao nakwambia. Yule mama hajui kulea watoto kabisa, na hivi huwa anajifanya anaishi kizungu sababu kaishi sana nchi za nje, subiri tu picha kamili ya ulichokipeleka huko”“Jamani mama, unajua hadi umenikosesha raha”“Na ukose vizuri tu hiyo raha, hivi raha iko wapi kwa kulelewa mtoto? Tumaini ndio alikuwa yupo vizuri kwani hata watoto wake unaona jinsi anavyowalea, ila yule mama uliyempelekea mtoto kuna mtoto gani hata wa ndugu yake aliyemlea vizuri? Unataka nikupe historia ya yule mwanamke katika kulea watoto? Huyo mumeo aliharibika wakati anaishi na mama yake, na ikawa kidogo afadhari alivyoishi na mamake mdogo yani hata ukikutana na Julieth mwenyewe anakuelezea. Yani yeye huwa naangalii kama hiki ni kizuri kwa mtoto na hiki ni kibaya, yule huwa anahisi watoto wote ni kama watoto wa kizungu, kuna tofauti kubwa sana ya kulea watoto wa Kiswahili na watoto wa kizungu, haijalishi una pesa kiasi gani ila mtoto wa Kiswahili ni wa Kiswahili tu. Akili kichwani mwako, sikujua huo ujinga ambao umeufanya jamani, bora hata mngeniletea mimi mjukuu wangu nikae nae mwenyewe”“Basi mama, nitaenda kumchukua”“Yani katika siku ambazo umeongea na mimi, leo umeongea na mimi kitu cha kunichefua Erica. Yule mtoto kweli!!! Jamani utaniambia mimi, yani wewe huwa unamsifia kila leo ooh mwanangu mzuri mzuri basi kwa yule bibi yake hizo sifa zako ni mara mia yani Angel atakuwa anajiona kama malaika katika ulimwengu huu. Fanya kitu mapema kabla mtoto hajaharibika zaidi”“Sawa mama, nimekuelewa mama yangu”Basi siku hiyo mama Angel hakuwa na amani tena kiasi kwamba hadi muda anaondoka kwa mama yake bado alikuwa na wazo moja tu juu ya Angel.Usiku wa siku hiyo mama Angel aliamua kuongea na mume wake kuhusu kwenda kumchukua Angel,“Naona umemkumbuka mtoto wako tayari!”“Ndio nimemkumbuka, tena sana tu”“Je huogopi kuwa wakina Samir watamfata tena?”“Aaaah hata wakimfata, nitajua jinsi ya kuwathibiti ila kiukweli nimemkumbuka sana”“Sawa basi tutaenda wote kumfata, siwezi kukuacha umfate peke yako katika hali hiyo uliyokuwa nayo mke wangu”Mama Angel alikubaliana na mume wake kuwa kesho yake ataenda nae pamoja kwenda kumfata Angel.Leo usiku Angel nae alikuwa akiwasiliana vizuri sana na Samir, yani kwa siku hizi chache, mawasiliano yake na Samir yalikuwa ya hali ya juu.Muda anawasiliana na Samir, basi Mussa alimpigia simu na kuanza kuongea nae,“Mbona siku hizi Angel hupokei simu zangu?”“Jamani, mbona nimepokea, unataka nipokeaje?”“Unanipotezea siku hizi, sijui hata kwanini. Ila kesho nitakuja”“Hakuna shida karibu”Kwa upande wa Angel, hakumuona Mussa kama mtu baki bali alikuwa akimuona kama ndugu yake, tofauti na Mussa ambaye alikuwa akimuhitaji Angel kimapenzi. Yani Angel na hivi aliona kuwa kafanana na Mussa ndio kabisa yani, alimuona kama ndugu yake kwahiyo alikuwa akiongea nae kawaida tu.Baada ya hapo aliendelea kuongea na Samir, na kama kawaida hadi alichelewa kulala kwa siku hiyo pia sababu ya kuongea na Samir.Kilipokucha, Angel aliitwa na bibi yake ambapo siku hiyo mapema kabisa, yule bibi alimuaga Angel kuwa anatoka kidogo maana kuna biashara alikuwa akiishughulikia.Jioni ya siku hiyo, Angel alipigiwa simu na Mr.Peter ambaye alimwambia Angel,“Toka hapa nje ya geti nina shida na wewe”Basi Angel moja kwa moja alitoka nje, ila alipofika tu yule Mr.Peter alimsogelea Angel na kumkumbatia, muda huu mama Angel na baba Angel nao walikuwa wamewasili pale kwa bibi yake Angel, ila mama Angel alishtuka sana kwa kumuona huyu mzee na kusema,“Mr.Peter!!!”Huyu mzee nae alikuwa kama kapigwa na bumbuwazi kwani alikuwa akimshangaa pia mama Angel. Jioni ya siku hiyo, Angel alipigiwa simu na Mr.Peter ambaye alimwambia Angel,“Toka hapa nje ya geti nina shida na wewe”Basi Angel moja kwa moja alitoka nje, ila alipofika tu yule Mr.Peter alimsogelea Angel na kumkumbatia, muda huu mama Angel na baba Angel nao walikuwa wamewasili pale kwa bibi yake Angel, ila mama Angel alishtuka sana kwa kumuona huyu mzee na kusema,“Mr.Peter!!!”Huyu mzee nae alikuwa kama kapigwa na bumbuwazi kwani alikuwa akimshangaa pia mama Angel.Baba Angel nae alikuwa akishangaa na kumuuliza mke wake,“Mnafahamiana kumbe!”Angel aliwakimbilia wazazi wake, kanakwamba hakuna kitu ambacho kimetokea pale, kwakweli mama Angel hakuongea jambo lolote zaidi ya kumtaka Angel aingie ndani tu halafu yeye alimfata kwa nyuma yani hakuna kingine cha zaidi alichozungumza kwa muda ule.Alifatana na Angel hadi ndani na kumwambia,“Haya fungasha kila kilicho chako tuondoke”“Jamani mama, ujue bibi hayupo”“Sitaki kusikia, awepo au asiwepo ila leo tunaenda nyumbani”Kwakweli Angel hakumuelewa mama yake wala nini na muda huo mama yake alienda kukaa sebleni huku akiwa na mawazo sana haswaa kitendo cha kumkuta Mr.Peter akimkumbatia mwanae.Muda kidogo, baba Angel nae aliingia sebleni na kukaa karibu na mke wake ila alijifikiria kidogo kumuongelesha kwani huwa anamfahamu mkewe kama ni mkali sana, na muda ule mama Angel alimuita Angel,“Wewe Angel bado tu!”Ikabidi mumewe amuulize,“Kwani bado nini?”“Kwani hapa tumekuja kufanya nini? Si tumekuja kumchukua Angel?”“Ushamuulizia mama yuko wapi?”“Mimi hayanihusu, nimemfata mwanangu”“Yani mke wangu unajua mambo mengine unayoyafanya kwa hasira huendi kwa utaratibu maana huo sio utaratibu ujue”“Sitaki habari za kusikia ni utaratibu au sio utaratibu, huyu Angel ni mwanangu. Ni damu yangu mimi yani mimi ndiye mwenye uchungu na mtoto huyu”“Aiseeee ningekuwa ni aina nyingine ya mwanaume sijui yani”Baba Angel aliinuka na kutoka nje kwani hakutaka hata kubishana na mke wake.Moja kwa moja baba Angel aliamua kumpigia simu mama yake ili kumpa taarifa tu kuwa wanaondoka na Angel kwa muda huo,“Mama samahani, mama Angel kamkumbuka sana mwanae kwahiyo tumekuja kumchukua”“Kheee mbona gafla hivyo!! Hebu nisubirini kwanza nifike”“Mama, kwakweli hapa itashindikana kukusubiri”“Kwanini sasa? Nimesema nisubirini”Yule bibi Angel alikata ile simu ila wakati baba Angel akirudi ndani ili kumpa mkewe ile taarifa alishangaa kukuta mke wake tayari kashainuka na kuanza kutoka na Angel kwaajili ya kuondoka, basi akamwambia mke wake,“Mama Angel, tumsubirie kwanza mama basi”Mama Angel hakusikiliza swala hilo hata kidogo kwani muda huo huo alimvuta mtoto wake mkono na kutoka nje, kwahiyo baba Angel hakuwa na namna ya kufanya jambo lolote lile zaidi zaidi ya kufatana na mke wake tu.Basi walienda kupanda kwenye gari na safari ya kurudi nyumbani kwao iliwadia, yani mama Angel alionekana kuwa na hasira sana.Walifika nyumbani usiku sana kwani kidogo kule kwa bibi yake Angel kulikuwa na mwendo, moja kwa moja Angel alienda chumbani kwake na wazazi nao walienda chumbani kwao.Ila baba Angel alikuwa amechukia sana siku hiyo kwa kile kilichofanywa na mkewe, kiasi kwamba hakuweza kusema chochote kile na moja kwa moja alienda kulala tu.Mama Angel alitulia tuli akifikiria jambo, kwanza alianza kuwaza,“Hivi yule mr.Peter ni kitu gani alikuwa akifanya na mwanangu? Ndiomana mama aliniambia kuwa yule mama hajui kulea mtoto wala nini hata sijui nilianzaje kumwambia mume wangu apelike mtoto kule jamani!”Ingawa walirudi na Angel ila alikuwa na mawazo sana.Usiku wa leo Angel alikuwa akifikiria vitu vingi sana pale kwao, kwanza aliwaza ni kwanini mama yake alichukia sana baada ya kukuta kakumbatiwa na yule mzee,“Ila mama nae jamani sijui ana matatizo gani, yule mzee si sawa na babu yangu tu!! Sasa yeye kachukia nini yani kitu gani kilichomchukiza kwa yule mzee kunikumbatia jamani wakati alikuwa akinisalimia tu! Na hii simu itabidi niwe naificha maana akigundua basin i balaa, lazima atanipokonya tu”Kwahiyo Angel aliona ni vyema kwa simu yake kufanya nayo mawasiliano ndani tu na kweli alipoiwasha tu muda huo alikutana na ujumbe toka kwa Samir,“Yani nilikukumbuka sana Angel mpenzi wangu?”“Mmmh wewe nawe jamani! Hata mimi nimekukumbuka”“Kwasasa upo wapi?”“Nilikuwa kwa bibi ila mama yangu kaja leo na tumeondoka nae hai hai kwahiyo nipo nyumbani kwasasa”“Kheee mama yako nae naona huwa hana kazi za kufanya yani kazi yake ni kukufatilia wewe tu, hebu mwambie baba yako afanye kazi ya ziada”“Kazi gani?”“Ampe mimba, hahaha”“Tayari anayo, yani yupo kuhangaika na mimba yake”Basi Samir alikuwa akicheka sana huku akiendelea kuwasiliana na Angel, na siku hiyo pia waliwasiliana sana kiasi kwamba Angel alilala saa nane za usiku.Kulipokucha, Angel aliamka na kutoka sebleni kisha kuanza kuongea na Vaileth ambaye alimkuta yupo karibu sana na Junior,“Mmmh makubwa, kwahiyo siku hizi Junior ndio unapika pamoja na Vaileth?”“Kwani kuna ubaya gani? Maisha kusaidiana”“Mmmmh! Mama anayajua haya kuwa mnasaidiana?”“Achana na habari za mama, maana yeye huwa anajielewa mwenyewe tu. Yani mama huwa anapinga kila kitu, kiwe kibaya au kizuri basi yeye anapinga tu”“Kheee kumbe na nyie mmeshamjua?”“Ndio, yani yeye kazi yake ni kupinga jamani! Yani hana jambo lolote zuri hata mara moja”Basi walicheka pale kisha Junior akasema tena,“Hapa cha msingi kila mtu kufanya jambo analoliona yeye ni zuri maana ukifatilia anayoyataka mama basi utachina maana huyu mama anajijua mwenyewe, tunatakiwa kufanya kitu ambacho roho inapenda”Angel nae alicheka kisha alirudi chumbani kwake kujaribu kumtafuta Samir kwani kwa muda huo alihisi kuwa ameshamkumbuka.Ila alipochukua simu yake tu, alishangaa kukutana na ujumbe toka kwa Mussa,“Ulichonifanyia Angel sio kizuri, nimekuja hapa kwenu ila sijakukuta, ujue nakupenda sana”Angel alishtuka kidogo kwani hakufikiria kama kuna muda ambao Mussa atamueleza habari za kumpenda sana ila hakumjibu wala nini na kuendelea na mambo yake.Baba Angel leo akiwa kazini alipigiwa simu na mama yake ambaye alianza kumlaumu moja kwa moja kwa kitendo chake cha kuondoka na Angel,“Hivi wewe Erick una akili kweli? Kwanini sasa umefanya ulichokifanya? Mimi nilikwambia kuwa kuhusu Angel nisubirini nirudi ila mmemchukua mtoto bila kunishirikisha, halafu kilichowafanya mumjibu vizuri yule baba wa watu ni kitu gani?”“Tumemjibu vibaya nani jamani mama?”Yule mr.Peter, hivi mnaelewa yule ni nani? Yule baba ni mfanyabiashara mkubwa sana, mmeanza kumuwazia vibaya kuhusu Angel, jamani yule baba aanze kumtamani Angel kwa lipi? Yule baba ana familia yake, ana mke, watoto na wajukuu tena wakubwa kushinda Angel halafu kweli mmmeanza kumdhania mabaya kwa Angel jamani!”“Mama jamani sijui hata kama naweza kukueleza jambo lolote lile ukanielewa, ila nitakuja tuzungumze vizuri. Unajua mke wangu alivyo na kisirani”“Yule mwanamke jamani! Yani asingekuwa mtoto wa mtu niliyemfahamu kwa hakika nisingeruhusu uoane nae, maana mambo yake anajijua mwenyewe yule mwanamke. Nipeni jibu linaloeleweka kuwa kwanini mmemchukua mtoto bila ridhaa yangu”Bibi Angel alikata ile simu, kwakweli baba Angel aliona mke wake kamsababishia matatizo tu sababu ya tatizo lake la kuchunga mtoto. Basi siku hiyo alipomaliza shughuli zake, moja kwa moja alienda ofisini kwa mke wake ili kuongea nae kwa ufupi.Alimkuta akiwa anaendelea na kazi zake, basi alikaa nae na kuanza kuongea nae,“Hivi mke wangu kile kitendo cha jana unaona ni sawa?”“Ngoja na wewe nikuuliza, hivi yule mbabu kumkumbatia mtoto wetu unaona ni sawa?”“Hivi unamjua yule mbaba kwani? Nasikia ni mfanyabiashara maarufu sana”“Dah! Sijui kama unaweza kunielewa, mama mzazi wa Rahim anajulikana kwa jina la Mrs.Peter na yule Mr.Peter ndio mume wake, najua umenielewa sasa kwanini nilipaniki jana”“Ila sio tatizo mke wangu, kumbe ni babu yake!!”“Hivi unaongelea kitu gani Erick? Hebu niambie agenda yako ni nini?”“basi yameisha, hata hivyo kilichonileta hapa sio hiko ila tu nahitaji kwenda na wewe mahali tukapumzike kidogo kwa siku ya leo”Yani baba Angel wala hakumueleza tena malalamiko ya mama yake, kwani hakupenda pia kwa swala zima la kumkera mke wake hata kidogo.Leo, wakati Erick akitoka shuleni akiwa hana wazo lolote lile ingawa kwenye gari alisumbuliwa na Sarah ambaye alikuwa na kawaida hiyo ya kumsumbua Erick, kwanza kabisa alimwambia jambo,“Erick, unatakiwa kuwa na simu ili mimi na wewe tuwe tunawasiliana”“Sijafikiria kabisa swala la kumiliki simu”“Kheee mtoto wa kiume huna wazo la kumiliki simu kwanini? Erick nakuomba uwe na simu ili tuwe tunawasiliana maana nina mambo mengi sana ya kuzungumza na wewe”Kuna muda Erick hakumjibu huyu binti kwani alimuona ni kama mtu aliyetrumwa vile.Ila leo aliposhuka tu kwenye gari, alishangaa akiitwa jina,“Erick!!”Basi alisimama na kuangalia kuwa ni nani aliyekuwa akimuita kwa muda huo, basi aliposimama pale ndipo aliposogea mwanamke mmoja hivi ambaye alimkumbuka sura yake kuwa ni mwanamke wa dukani ambaye alidai kuwa ni mwanae na kujaza watu wengi, basi Erick alimuangalia huyu mwanamke kwa muda ila yule mwanamke alimsogelea Erick na kumwambia,“Erick mwanangu, hujambo?”“Kwani wewe mwanamke una matatizo gani lakini? Mimi sio mtoto wako”“Hebu acha kujiongopea huko, mimi ni mama yako na hilo haliwezi kubadilika kamwe, mimi ndiye ambaye nilikubeba miezi tisa”“Unazungumzia kitu gani?”“Kuna siku utanielewa tu vizuri sana ila kwasasa utaona kama mwanamke kichaa ndio anaongea mbele yako, iko hivi. Erick wewe ni mtoto wangu na hilo wala halibadiliki, kwanza jiangalie jinsi ilivyokuwa kati yako wewe na huyo mama unayeishi nae humo ndani, je huyo mama anakupenda kweli? Huyo mama anakujali kama mtoto wake wa kumzaa? Hebu fikiria swala la baba yako kukupatia lile duka, hebu fatilia, ni hivi huyo mama yako ni anapinga vikali sana swala hilo yani hataki kabisa wewe umiliki chochote katika nyumba hii. Usifikiri hajui kama wewe sio mwanae! Anajua wazi kuwa wewe sio mtoto wake na hana uchungu wowote ule na wewe, nakwambia ukweli wewe ni mwanangu, wewe ni damu yangu, unatakiwa kuwa karibu na mimi ili ufahamiane na ndugu yako”“Sikuelewi”“Huwezi kunielewa, ila wewe ni mwanangu. Baba yako analijua hilo na mama yako analijua hilo, hii familia itaendelea kukutenga hadi mwisho na siku zote hutokuwa na amani wala raha, ila ukishirikiana na mimi basi utairudisha furaha yako kwani umepata bahati sana kumpata mama mwenye akili kama mimi. Katika maisha yangu niliomba sana Mungu anipatie mtoto wa kiume, na kweli akanipatia wewe yani wewe una kazi kubwa sana kwangu, wewe ndio wa kubadilisha maisha yangu na ndiye pekee wa kubadilisha historia yangu na kunifanya nionekane mtu mpya yani hiyo kazi ipo juu yako wewe. Sikukuzaa kwa bahati mbaya ila nilikuzaa kwa lengo maalumu kabisa. Nimejionyesha kwako ili utambue kuwa mimi ndiye mama yako mzazi, fanya yote ila mimi ndiye mama yako mzazi na sasa naenda tena kupigania mali yako”Halafu yule mwanamke akaondoka zake, kwakweli lile jambo lilikuwa ni la ajabu sana machoni na masikioni mwa Erick, hakuelewa na alizidi kuona akili yake ikichanganyika na kumfanya azidi kukosa raha.Basi aliingia ndani na kuwaza vitu vingi na moja kwa moja alianza kujiona tofauti na watu wengine kwenye familia hiyo, kwanza alikumbuka jinsi baba yake alivyomwambia kuhusu dukani kuwa asimueleze mama yake, na pia aliwaza jinsi ukaribu wa mama yao na Angel pamoja na Erica halafu ukaribu wake na mama yake, aliona kweli kuna kasoro, kwakweli lile jambo lilimfanya aumie sana moyo wake na moja kwa moja alikaa chumbani tu akiwa na mawazo sana kwa siku hiyo.Baba Angel na mama Angel walitoka pale ofisini na moja kwa moja walienda hotelini ambapo huko waliagiza chakula na vinywaji, kwahiyo wakaanza kula huku wakiambizana mambo mbalimbali yanayoendelea,“Hivi ushaenda kuangalia mtoto wetu huyu ni jinsia gani?”“Mmmmh yani kwasasa nadhani huyu mtoto anataka kutushtukiza tu, maana kila nikienda kupima basi Napata jibu kuwa mtoto kajificha, kwahiyo jinsia yake haijulikani”“Ila nadhani atakuwa wa kiume”“Kwanini sasa awe wa kiume?”“Ili mke wangu upumzike kidogo maana naona Angel na Erica wanafanya akili yako iruke kabisa”Mara simu ya baba Angel ilianza kuita, na aliyekuwa akipiga ni Steve, basi aliipokea na kuanza kuongea nayo,“Bosi, yule mwanamke kaja na leo, na uzuri ni kuwa huyu askari kamshikilia kwahiyo unaweza kuja kuonana nae”“Sawa”Baba Angel alimuangalia mke wake kwa muda pale kwani aliona si vizuri kama akienda kule na mke wake, kwahiyo aliona ni vyema kama atatumia njia nyingine ili tu asiende na mke wake kule, basi akamwambia,“Mama Angel, unajua kwa hali yako ilivyo kwasasa sio vizuri kukaa hotelini kwa muda mrefu!! Inatakiwa upate muda wa kutosha ili upumzike mke wangu”“Oooh nashukuru sana kwani inaonekana kuwa unanijali sana”Basi baba Angel alimuomba muhudumu kumfungia kumfungia kile chakula chao kilichobaki halafu ni moja kwa moja walirudi nyumbani tu.Muda huu familia ilikuwa imejiachia kabisa, yani waliendelea na vipindi vyao kwenye Tv bila ya tatizo lolote, sababu tu waliamini kuwa wazazi wao hawapo ila katika watu wote ni Erick pekee ndio hakuwa na raha kabisa na kwa muda huo alikuwa amekaa tu chumbani kwake. Erica kama kawaida alienda kwa kaka yake ila alimuona pia kuwa hakuwa na furaha kabisa, ila hata yeye aliumia kwani hakumzoea kumuona Erick katika hali kama hiyo.Basi muda kidogo mama Angel na baba Angel walirudi ila muda ule ule baba Angel alitoka tena, ila kwa muda huo huo Erica alienda chumbani kwa mama yao kuongea nae kuhusu Erick kama ilivyokawaida yake kwa jambo lolote linalotokea ndani ya nyumba yao basi kulisema kwa mama yao,“Mama, yani leo toka Erick atoke shuleni sijui ana matatizo gani, yani hana furaha hata kidogo hata chakula amekataa”“Jamani, mwanangu kapatwa na nini tena?”“Sijui mama, ila leo hata mimi hataki kuongea nami vizuri kwani kila nilichokuwa namuongelesha hakunijibu halafu inaonekana ana majonzi sana mama.”“Mmmh! Ngoja nikaonhee nae basi”Muda huo huo mama Angel aliinuka na moja kwa moja alienda chumbani kwa Erick ila hata yeye alimuona mwanae kuwa hana raha kabisa halafu alionekana kila alipojaribu kujiweka katika furaha hakuwa na furaha kabisa, basi mama Angel alianza kuongea na mwanae,“Mwanangu Erick, tatizo ni nini baba? Mbona unaonekana huna furaha kabisa?”“Samahani mama, kuna jambo nataka nikuulize”“Jambo gani hilo? Niulize tu”“Kwanza mama, ni kwanini hunipendi?”Mama Angel alishtuka sana kwa swali lile maana hakutegemea kama swali kama lile lingetoka kwenye kinywa cha mtoto wake, basi nae alimuuliza,“Sikupendi? Kivipi Erick? Yani mimi niache kumpenda mtoto pekee wa kiume niliyenaye?”“Sikia mama, kuna mambo huwa nafanya na baba na mara nyingi huwa anasema nisikushirikishe, kama swala la mimi kupelekwa kwenye lile duka jipya la baba. Swali langu mama ni kuwa, ni kweli mimi ni mtoto wako?”“Jamani jamani Erick, mbona unataka kuniumiza tumbo la uzazi wewe mtoto jamani! Katika uzao wangu, nimezaa mapacha kwa mara moja tu yani wewe na Erica na ndiomana tuliwapa majina yani tukimaanisha kuwa ni mimi na baba yenu. Erica kachukua badala yangu na wewe umechukua badili ya baba yenu. Sasa kama wewe sio mwanangu basi na Erica sio mwanangu pia maana ni watoto ambao niliwazaa pamoja. Halafu dhana ya kusema kuwa mimi nakuchukia unaitoa wapi Erick?”“Sijui mama, ila kuna mama nimekutana nae na ameniambia kuwa yeye ndio mama yangu mzazi, na wewe na baba mnalitambua hilo. Mama niambie ukweli, kama mimi ni mtoto wa kuokotwa nijue moja halafu ni vyema kama nikiwajua wazazi wangu halisi, hata kama ni masikini hakuna tatizo mimi nitaishi nao tu”“Jamani Erick mbona unataka kuniliza wewe mtoto eeeh! Nani kasema kuwa wewe sio mtoto wangu? Nikubebe mwenyewe tumboni, nikusae kwa uchungu, nikunyonyeshe kwa matiti yangu haya, leo hii anaibuka mtu na kusema kuwa wewe sio mtoto wangu kweli! Erick hayo maneno yametokea wapi jamani! Umeyatoa wapi hayo maneno Erick mwanangu!”Mama Angel pia machozi yalimtoka kwani maneno ya mtoto wake yalikuwa yakimuumiza sana, kiukweli alikosa raha gafla pia na hakuelewa kuwa mwanae hayo maneno kayatoa wapi, basi alimsogelea mwanae na kumkumbatia huku akilia na kusema,“Mwanangu hebu niambie ni wapi umeyatoa hayo maneno jamani, yani nani amekueleza vitu vya namna hiyo? Mimi sikukatazi dukani sijui sababu sio mwanangu hapana jamani, hata baba yako anajua ni kwanini nakukataza, mimi mwanangu nataka usome na ufike mbali, ukianza kuwaza biashara kwasasa ni wazi kuwa utaona elimu haina maana yoyote katika maisha yako ila hiko sio kigezo kuwa sikupendi mwanangu. Kwanza nani kakwambia hayo maneno jamani! Mtoto nimzae mwenyewe halafu leo asiwe mwanangu! Toka nizaliwe sijawahi fikiria jambo la namna hiyo. Nani kakwambia mwanangu?”“Mama kuna mwanamke ambaye huwa anagombana na yule anko pale dukani, na yule mwanamke ameyasema maneho hayo siku nimeenda pale dukani na watu wengi walijaa ila baba alikuja na kusema kuwa nipuuzie maneno ya yule mwanamke. Leo wakati nimetoka shule, nimekutana na yule mwanamke nje ya geti letu na ameniambia tena kuwa mimi sio mtoto wa familia hii bali ni mtoto wake na nyie mnalitambua hilo ndiomana hamnipendi”“Oooh jamani kuna watu wanaweza kukukumbusha hadi siku uliyoingia leba, kwakweli sijawahi kufikiria kitu cha namna hii kwa mtoto wangu pekee wa kiume, hivi mimi nisikupende Erick jamani, nimpende nani sasa? Subiri kwanza”Mama Angel aliinuka na kwenda chumbani kwake ambapo alibadilisha nguo kisha akamfata Erick na kumtaka waondoke ili waende dukani kwani lengo lake lilikuwa ni kuongea na Steve kwani alihisi lazima Steve anafahamu vizuri kuhusu huyo mwanamke, kwahiyo mama Angel na Erick waliondoka muda huo.Mama angel alipoondoka tena, huku nyuma familia ilifurahi kidogo ila kama kawaida ya Erica, muda mama yake anaongea na Erick basi alikuwa mlangoni akisikiliza kila kitu.Kwahiyo walipoondoka, moja kwa moja alienda chumbani kwa Angel ili akamuelezee mambo yake, alipoingia chumbani kwa Angel alimkuta na ile simu ila Angel alishtuka sana yani ilibakia bado kidogo tu aangushe ile simu na kuanza kumsema mdogo wake,“Jamani wewe Erica, hebu jifunze kuheshimu vyumba vya watu wengine, ukiwa unaingia basi ujue jinsi ya kugonga hodi”“Kheee samahani dada, ila nimeona hiyo simu nzuri sana. Ndio haya mambo anayoyalalamikia Erick, humu ndani kuna upendeleo, hebu ona wewe una miliki simu kubwa na nzuri halafu inaonekana ya gharama wakati sisi hata kupiga ile simu ya mezani ukigundulika ni balaa”“Halafu wewe nawe mambo mengine yatakushinda, hebu uachage vitu vingine vikupite. Halafu nikusikie fyokofyoko kwa mama kuwa nimemuona Angel na simu ndio utanielewa vizuri. Mimi ni mkubwa na sio kila ninachokuwa nacho mimi basi na nyie muwe nacho, hebu kuwa mpole tu. Haya kilichokuleta muda huu”Erica akaanza kumuelezea toka Erick alivyorudi amepooza hadi jinsi alivyokuwa akiongea na mama yao na jinsi mama yao alivyoondoka nae,“Kheee mambo mengine yanachekesha, sasa Erick nae anafatiliza maneno ya watu mbona atapata shida sana? Sasa bora hata yeye, mie mwenzie nasemwa kila leo kuwa nafanana na waarabu na wala sina tatizo lolote lile kwani najua huyu ndio mama yangu na baba ndio baba yangu, hata mtu atokee wapi na kusema hawa sio wazazi wangu basi nitambishia. Yani mtu akisema sifanani na wazazi wangu basi nitasema nimefanana nao hata kucha, unajua maisha haya ni kawaida kabisa kutokufanana na wazazi hata mama amewahi kuniambia hivyo. Sasa Erick anataka nini lakini jamani!!”Simu ya Angel ilianza kuita na muda huo huo Angel alimwambia Erica,“Haya chaumbea nipishe niongee na simu maana wewe najua nitakayoongea nayo kwenye simu basi utayabeba kama yalivyo na kwenda kutabwaga unapopajua wewe”Basi Erica aliinuka ila hakupenda vile dada yake alivyomuita chaumbea.Mama Angel na mwanae walifika dukani, na moja kwa moja walipoingia ofisini walimkuta baba Angel, Steve na yule mwanamke ambaye ni Sia, na yule mwanamke alipomuona mama Angel alipiga makofi na kusema,“Sasa ukweli utajulikana, nimefurahi sana wote mmekuja”Mama Angel alimuangalia Sia kwa gadhabu sana, na kujikuta akipatwa na hasira juu yake na kwenda moja kwa moja kumzaba kibao ila cha kushangaza mama Angel alianguka chini na kuanza kugalagala. Mama Angel alimuangalia Sia kwa gadhabu sana, na kujikuta akipatwa na hasira juu yake na kwenda moja kwa moja kumzaba kibao ila cha kushangaza mama Angel alianguka chini na kuanza kugalagala.Kitendo kile kilifanya wote waanze kumshughulikia mama Angel ambapo walimbeba na kumtoa nje na kumpakiza kwenye gari, halafu baba Angel pamoja na Erick wakaondoka nae kuelekea hospitali.Kwahiyo pale dukani alibaki Steve na Sia, ila kiukweli Steve pia alichukizwa na ile tabia ya Sia, nay eye mwenyewe kuamua kumsogelea Sia huku akitaka kumzaba kibao ila Sia alikamata ule mkono wa Steve na kumuuliza,“Kinachokufanya utake kinipiga ni kitu gani?”“Hivi unajua wewe mwanamke huna akili!”“Ni kweli mimi sina akili tena sina akili kabisa, nadhani akili zangu hujawahi kuzijua ila mimi ni chizi kushinda unavyofikiria wewe. Halafu wewe unawezaje kutaka kunipiga mimi kibao? Mwanamke niliyekufundisha mapenzi, niliyekuonyesha mapenzi ni kitu gani wewe halafu unajitia ushujaa kutaka kunipiga mimi! Hebu jiheshimu dogo”Halafu Sia alitoka na kuondoka zake, yani Steve alimuangalia yule mwanamke bila ya kummaliza, alikaa chini na kutafakari baadhi ya mambo. Alianza kukumbuka mambo ya zamani ambayo yaliwahi kutokea katika maisha yake, kwanza kabisa alimkumbuka mwanamke ambaye aliwahi kumpenda katika maisha yake ila kwa kipindi hiko hakujua kuwa yule mwanamke yuko wapi, akakumbuka pia jinsi alivyoanza mahusiano na Sian a kusema,“Isingekuwa lile tunda lake lenye dawa basi mimi nisingekuwa nae, ila kitu kingine isingekuwa uroho wangu basi nisingekuwa na huyu mwanamke, ni aina gani ya mwanamke hii jamani! Eeeh Mungu ninusuru”Alibaki tu analalamika, ila aliona ni vyema kufunga duka tu kwa muda huo kwani tayari ilikuwa ni usiku.Basi wakati mama Angel amepelekwa hospitali ni moja kwa moja daktari alimchukua na kwenda kumuhudumia, muda huu Erick alikuwa nje na baba yake kwahiyo hawakuweza kuongelea chochote kile maana mawazo muda huo yalikuwa ni juu ya mama Angel tu. Basi Erick alimwambia baba yake,“Baba, huwa mnasema kila kitu tunapaswa kuomba. Kwanini tusimuombee mama!”“Oooh umenikumbusha jambo jema sana, kuna mama mmoja hivi tulikuwa tukimtumia sana kwenye maswala ya maombi, ngoja leo nimpigie simu”Basi baba Angel alimpigia simu huyo mama na kuongea nae kwa muda kidogo kisha kufanya nae maombi na kukaa pale na mtoto wake huku wakisubiri majibu kuwa ni kitu gani kilimsibu mama Angel muda kidogo Daktari alifika na kumwambia baba Angel,“Hongera sana, mkeo kajifungua”“Oooh! Mungu ni mwema kwakweli, huyo mwanangu ataitwa Ester”“Kheee umejuaje kama ni wa kike au mlipima?”“Halafu nimejikuta tu nikiropoka hilo jina sababu muda sio mrefu nilikuwa nikiongea na mama mmoja wa maombi anayeitwa Ester”“Basi hongera sana, mkeo kakupatia huyo Ester”Baada ya muda kidogo ndipo baba Angel pamoja na Erick waliruhusiwa kwendfa kumuona mama Angel pamoja na mtoto, kwakweli walifurahi sana, hata mama Angel alifurahi yani kwa muda huo walisahau kila kitu kilichotokea mwanzo sababu ya ile furaha.Ingawa ilikuwa ni usiku ila walikuwa na furaha sana kiasi kwamba waliona kuwa ni mapema kabisa kabisa.Basi walikazana kuongea nae pale, huku baba Angel akipigia simu baadhi ya ndugu zao na kuwapa ile taarifa ya kuhusu kujifungua kwa mama Angel, na kila alipopiga simu alisema kuwa mwanangu Ester amezaliwa.Baba Angel na Erick waliporudi nyumbani walitoa taarifa kwa wote kuwa mama yao kajifungua mtoto wa kike, basin a wao walifurahi sana.Muda Erick akiwa chumbani kujiandaa kulala kutokana na uchovu wa siku hiyo, akafatwa na Erica ambaye alianza kuongea nae,“Haya sasa Erick, mama kaongeza jinsia yetu tena. Kwahiyo wewe unabaki kuwa mtoto wake wa pekee”“Mmmh sisi wote ni watoto wake wa pekee, haijalishi ni jinsia gani?”“Shauri yako, mimi nakwambia ukweli yani mama atazidi kukupenda wewe maana umebaki kuwa mtoto wake wa pekee wa kiume maana wote sisi ni wanawake. Dada Angel, mimi na sasa tuna Ester, mmmh sijui atakuwa mbea kama mimi!”“Kheee kumbe unajijua! Niache nipumzike kwanza Erica kwa muda huu maana najua ukianza kuongea hapo hata hutomaliza wakati wewe ulishalala, mwenzio sijalala hata kidogo halafu kesho tunaenda tena shuleni”Basi Erica alimuacha kaka yake na moja kwa moja kwenda chumbani kwake kulala.Kulipokucha kama kawaida, walijiandaa na kwenda shuleni, ila leo Erick alipokaa kwenye kiti cha basi la shule, basi Sarah nae alifika na kukaa hapo halafu akaanza kumuuliza,“Mbona unaonekana umechoka hivyo Erick?”“Aaaah jana nimechelewa sana kulala, kwani tulikuwa hospitali na mama”“Kheee kafanyaje tena?”“Amejifungua mtoto wa kike, kumbe ilikuwa ni uchungu”“Oooh jamani, wifi yangu mwingine kazaliwa jamani! Nitakuja kumuona Erick”Basi Erick alimuangalia tu Sarah, kwani huyu binti alikuwa na vituko ambavyo ilikuwa ngumu sana kwa Erick kuvielewa.Leo mama Angel aliruhusiwa kurudi nyumbani, kwahiyo alirudi nyumbani na mtoto akiwa ameambatana na mumewe pamoja na mama yake ambaye kwa kipindi hiko ilibidi aje akae hapo ili kumsaidia mwanae kwaajili ya uzazi ule.Kwahiyo walirudi pale nyumbani na kuanza kufanya mambo mengine ya familia ikiwa ni pamoja na yule mama kuelekeza chakula cha kupika kinachomfaa mama mzazi, ilibidi wakina Angel wawe wapole sana kwani Angel alimtambua bibi yake huyo.Basi muda huu Angel na Junior walitoka nje na kwenda kukaa kwenye bustani huku wakiongea mambo mbalimbali,“Angel, swala la huyu bibi kuwepo hapa unalionaje?”“Mmmh majanga ujue, yani huyu bibi nahisi atatufatilia hadi muda wa kulala, na usipokula utaulizwa kwanini hujala, na ukichelewa kulala basi ujiandae maswali kwanini umechelewa kulala”“Kumbe unamjua eeeh!”“Namjua ndio, niliishi kwake siku tatu tu ila nilijiona kama naishi miaka, jamani bibi anafatilia huyu balaa, hapa nawaza akianza mambo yake ni balaa”“Ila usijali Angel, kwasasa tumekuwa wakubwa, huyu bibi tutamnyoosha”Yani wakajikuta wakipanga mambo mbalimbali kuhusu bibi yao ambaye kwa kipindi hiko ndio alifika kwaajili ya uzazi wa mama Angel.Muda wa kutoka shule siku hiyo, Erick na Erica waliingia pamoja nyumbani kwao, kwahiyo walipofika tu moja kwa moja walienda kumuangalia mtoto mpya ambaye mama yao alikuwa kamleta nyumbani.Ila mama Angel alimuuliza Erick,“Mwanangu unaendeleaje?”“Salama mama”Mama Angel aliona bora aanze hiyo tabia ili Erick asijisikie vibaya tena kama ambavyo alijisikia mwanzoni.Baada ya hapo, Erick aliondoka kuelekea chumbani kwake naye Erica alienda chumbani kwake pia.Baada ya muda kidogo, Erica alienda chumbani kwa Erick na kuanza kuongea nae,“Erick, nikwambie kitu”“Niambie”“Yani leo, nilipoenda jikoni nimemkuta dada Vaileth na Junior wanabusiana”“Mmmmh Erica na wewe jamani! Eeeeh walifanyaje?”Basi Erica akainuka na kwenda kumuonyesha kaka yake ambavyo amewakuta Vaileth na Junior ndani ila kile kitendo kilijenga hisia kali sana kwa Erick, hata Erica mwenyewe alijishtukia na kuondoka mule chumbani kwa kaka yake, basi Erick alikaa chini na kuanza kujiuliza,“Kwanini nimejihisi hivi baada ya Erica kunibusu? Au ndiomana yule mama anasema kuwa mimi sio mtoto wa familia hii? Hapana haiwezekani, mimi ni mtoto wa familia hii na Erica ni pacha wangu ila tu sijui inakuwaje, nayeErica ananifanyia kama makusudi hivi!”Basi aliamua kufanya mambo mengine tu kwa muda huo.Siku hii ilikuwa ni siku ya Jumamosi, kwahiyo hawakwenda shuleni walikaa tu nyumbani huku wakiendelea na kazi mbalimbali za nyumbani.Kwenye mida ya mchana, Junior alikuwa amekaa bustanini yani kwa siku hizo Junior alijikuta akipenda sana kukaa bustanini zaidi kuliko kukaa ndani, basi Erick alimfata Junior na kuanza kuongea nae, ambapo Junior alimwambia,“Eeeh sasa huo ndio uanaume, sio muda wote kukaa karibu na wanawake tu. Yani wewe sababu pacha wako ni mwanamke basi huna rafiki mwingine zaidi ya Erica tu, hivi kuna hata rafiki zako ambao unabadilisha nao mawazo Erick!”“Hapana, hata marafiki kiukweli kabisa sina. Kwanza mama anawatunza sana watoto wake wa kike, na alishawahi kuniambia kuwa hataki marafiki wa kiume kwani wataharibu watoto wake, kwahiyo mimi sinaga marafiki kabisa, ndiomana hapa utaona wanakuja rafiki wa Erica kw asana maana hata Angel alikatazwa kuhusu swala zima la marafiki”“Ila mamdogo jamani, hata sijui alizaliwa kipindi gani yani ana mambo ya kishamba sijapata kuona. Na hivyo kazaliwa mjini na kukulia mjini, hivi angezaliwa kijijini hata sijui ingekuwaje? Sasa anawakataza msiwe na marafiki ili muishi maisha gani? Maisha bila marafiki hayaendi kabisa, mimi muda mwingi utanikuta nipo na simu kwani rafiki zangu wengi sana nawasiliana nao na licha ya kuwasiliana nao huwa natoka kwenda kuwatembelea na kuongea nao mambo mbali mbali. Sasa wewe Erick ukijifungia muda wote, ni lini utachangamsha hiyo akili yako? Lini utatambua jambo la kutenda kwa muda huu au ule? Unajua kuna mambo tukiyakwepa maishani basi tutakuja kuyafanya kwenye utu uzima na kuonekana ni kituko, binafsi huwa sipendi kufatiliwa kwenye mambo yangu. Nilishawahi kukuuliza, hivi una rafiki wa kike ila hukuwahi kunijibu”“Dah! Unaongea sana Junior. Ngoja nikuulize kitu, hivi ukimpenda mwanamke unajisikiaje katika moyo wako?”“Kwanza unajihisi kutamani kumuona mwanamke huyo muda wote, ila kuna siri moja katika mwili wa mwanaume mdogo wangu, yani mwanamke unamtamani kwanza halafu unampenda, yani cha kwanza unachoona kwa mwanamke uliyevutiwa nae basin i wazo kuwa upo nae kitandani yani ukivunja nae amri”“Unasemaje!”“Ona unavyoshangaa jamani! Hivi wewe ni mzima kweli? Hivi umekamilika wewe! Katika maisha ya mwanaume hiko ndio kitu kikubwa sana, hebu acha uzoba. Basi kwa akili zako nadhani unawaza yale maneno kuwa tendo lile ni mpaka uoe, hivi utaoa lini ili ufaidi? Hizo ni akili za kimama, ndiomana nakwambia jichanganye na wanaume wenzio ili upanue akili hiyo”“Kumbuka nipo kidato cha kwanza”“Kwani kidato cha kwanza ndio nini? Watu walianza toka darasa la kwanza huko, sembuse kidato cha kwanza! Yani wakati unaanza unajaribu jaribu hadi mwishowe unakuwa mtaalamu kabisa”“Mmmmh! Haya, na kama umempenda mwanamke ila huyo mwanamke hakutaki ni kitu gani unaweza kufanya ili kumsahau?”“Jamani wewe jamani hadi unatia huruma, hivi mwanamke umpende asikutake kwasababu gani? Akikutaa dawa ni moja tu, unatakiwa kuwa na mwanamke mwingine wa kuweza kumtia wivu yule mwanamke umpendaye.”“Kwahiyo wewe una wanawake wangapi?”Muda huo Vaileth alikuwa akienda kuwaita kwaajili ya chakula, kwahiyo alijikuta maongezi yao mengi sana ameyasikia, ila kiukweli aliumia sana moyo wake kwa yale maneno ya Junior ila hakusema chochote zaidi ya kuwaita tu kwaajili ya chakula basi nao waliinuka na kwenda kupata chakula tu kama kawaida.Maneno ya Junior yalianza kukaa kwenye kichwa cha Erick, aliona ni vyema kwake kama atakubali kuwa na Sarah, alihisi huenda akikubali kuwa na Sarah basi wazo la hisia juu ya dada yake litapotea kabisa,“Mmmh ila mama akigundua itakuwa balaa. Ila mimi ni mtoto wa kiume niogope nini sasa? Wapo watoto wa darasa la kwanza na wameanza hayo mambo sembuse mimi wa kidato cha kwanza!”Aliona kuwa ni sahihi kwa yeye kufikiria hivyo, ila muda huo Erica alienda tena chumbani kwake kama kawaida kumpelekea habari ambazo alizichota huko.“Erick basi nikwambie leo jamani, nilienda tena jikoni yani nimetoka jikoni muda sio mrefu. Vaileth alikuwa akipika, halafu Junior akaenda nyuma ya Vaileth na kumkumbatia halafu alitaka kumbusu kama ile jana, kheee maaajabu ya leo sasa, dada Vaileth akamtoa Junior halafu akamnyooshea kidole na kumwambia kuwa usinizoee”“Kheee una uhakika na unachokisema Erica?”“Ndio, yani nimeshuhudia mwenyewe, itakuwa wamegombana tu. Ila yule dada nilikuwa namuhurumia sana, jamani Junior hafai kabisa, Junior sio mwanaume wa maana”“Sasa mwanaume wa maana kwako ni yupi?”“Mwanaume wa maana kwangu awe kama baba, yani anipende mimi tu. Katika maisha yake kusiwe na aina yoyote nyingine ya mwanamke zaidi yangu mimi. Anijali, aniheshimu na anithamini. Mwanaume wa hivyo basi nipo radhi kumpa nusu na robo ya maisha yangu”“Mmmh kumbe! Wanawake mnapenda kupendwa eeeh!”“Nenda kamuulize mama, yani muulize hitaji kubwa la mwanamke ni kitu gani? Basi mama atakujibu kuwa hitaji la kwanza la mwanamke ni kupendwa, ila nahisi katika dunia hii mama yetu ana rah asana jamani! Unajua baba haendi popote toka mama ajifungue, akitoka basi muda mfupi tu anarudi kumuona mama na Ester, kwakweli baba ana upendo sana”“Kama mimi, nina uhakika watoto wangu watasema kama wewe unavyosema sasa”“Mmmh kujisifia tu, huna lolote na wewe”Halafu Erica aliondoka zake, ila kaka yake alimuangalia tu bila ya kusema kitu chochote kile.Muda wa kulala ulipofika, Vaileth alienda chumbani kwake ila kiukweli maneno ambayo Junior alikuwa akiongea na Erick kwa siku hiyo hayakumfurahisha hata kidogo,“Jamani, yani mimi Vaileth nimejidumbukiza kabisa. Mara nyingine ni heri tu kuwa na mtu mzima maana ana mawazo ya kikubwa ila kuwa na mtoto kama Junior ni kazi kubwa, yeye anawaza kubadili wanawake tu, yani hanifai kabisa. Najuta hata kwanini nilimkubali”Junior alienda kugonga mlango wa Vaileth ambapo alienda kumfungulia, ila Junior alivyoingia akafanya kama kawaida ambapo alimfata karibu Vaileth na kumkumbatia ila leo Vaileth alimsukuma kwa pembeni na kumfanya Junior amuulize kuwa tatizo ni kitu gani,“Kwani una shida gani Vaileth? Tumekuwa wote vizuri sana kwa kipindi chote hiki au huyu bibi kakusema vibaya?”“Hivi wewe Junior unaona mimi ni mtoto mwenzio eeeh! Kiasi cha kunifanya utakavyo?”“Sikia nikwambie, mapenzi hayana ukubwa wala udogo. Kwani mimi na wewe tumepishana miaka mingapi? Si miaka mitano tu! Siku zote huwa nakwambia katika miaka hiyo ona kuwa mimi ndio nimekupita wewe na wala usifikirie kuwa wewe umenipita mimi, tatizo lako ni nini sasa? Umri au kitu gani? Unaweza kunizidi ila kwenye swala la mapenzi nimekuzidi na mengine nakufundisha”“Unajua usinizoee wewe, tena usinizoee kabisa, wewe mtu gani wewe. Upo na mimi kumbe unawaza wanawake wengine?”“Jamani jamani, aliyesema nawaza wanawake wengine ni nani? Mbona unataka kunizulia tum engine Vaileth wangu jamani!”“Hivi unafikiri sikukusikia wakati unazungumza na Erick leo? Nimesikia kila kitu”“Kheee kumbe kwasababu hiyo tu! Yale mimi nilikuwa naongea tu kufurahisha mdomo, kwanza Vaileth umebadilisha sehemu kubwa sana ya maisha yangu. Ujinga niliokuwa namwambia Erick, mimi siwezi kuufanya kabisa. Nakupenda sana, usinifikirie vibaya”Junior akamsogelea karibu tena Vaileth ila kwa muda huu Vaileth alijikuta akiwa mpole kabisa, yani kwa Vaileth ilikuwa kamavile Junior anamfata na sumaku maana hata malalamiko yake aliyakuta yanayeyuka kwa muda mfupi, kisha wakaamua kulala pamoja kwa muda huo.Kulipokucha siku hiyo Vaileth alichelewa sana kuamka, yani tofauti na siku zingine na hii ilitokana na sababu ya yeye na Junior kutumia muda mwingi sana katika kubembelezana usiku wa siku hiyo, basi bibi wa Angel alienda moja kwa moja chumbani kwa Vaileth na kufungua mlango ila leo Vaileth hakukumbuka kufunga mlango kwani Junior alivyoingia usiku alikuwa na kisirani nae kwahiyo walijikuta tu wakiongea huku mlango umefungwa kawaida na hata hivyo familia hii haikuwa sana na utaratibu wa kufunga milango ndiomana watu walijikuta wakiingia tu ndani.Ila kwa muda huu Junior alikuwa ameenda chooni, kwahiyo huyu bibi alimkuta Vaileth amelala mwenyewe na kumshtua,“Wewe Vaileth, mpaka muda huu kweli! Unalala vipi hadi saa hizi!”Vaileth alishtuka na kumsalimia huyu bibi huku akimuomba samahani, basi bibi nae katika kupepesa macho yake mule chumbani akaiona suruali ya Junior, sema kwavile hakuijua suruali ile kama ni ya Junior akauliza,“Wewe Vaileth, ile nguo ya kiume inafanya nini chumbani kwako?”Vaileth nae akaiangalia ile suruali na kupumua kidogo kwani hakuwa hata na jibu la kusema, basi yule bibi akaguna na kutoka ila kumbe hakwenda mbali kwani alikuwa pale pale mlangoni.Basi Junior nae alitoka chooni ila Vaileth alimuwahi kule kule chooni na kumwambia,“Mmmh bibi aliingia huku muda sio mrefu ujue, sijui umemsikia?”“Dah! Hata sijamsikia maana nilikuwa na mawenge ya usingizi”“Halafu kaona suruali yako, kaniuliza nimekosa jibu la kumjibu. Kwahiyo ni vyema kama ukiondoka muda huu”“Weee huyu bibi tunamjua wenyewe, wewe toka tu, halafu mimi nitatoka kwa muda wangu au ukiona kaenda chumbani kumuogesha mtoto ndio uje unitonye nitoke, bibi ni mchunguzi huyu balaa”Mara mlango wa chumbani ulifunguliwa tena halafu bibi akasema,“Wewe Vaileth, unajikanyaga kitu gani sasa?”Basi Vaileth alitoka kule chooni na kufunga ule mlango vizuri ila huyu bibi aliguna tena yani mawazo ya huyu bibi alihisi kuwa Vaileth alikuwa na mlinzi wa nyumba hiyo tu yani hakuwaza kuwa ni Junior ndio alikuwepo chumbani kwa Vaileth.Baada ya muda kidogo ndio Vaileth alikuja na kumwambia Junior kuwa atoke maana yule bibi tayari alienda kumuogesha mtoto.Muda Junior anatoka kama mwizi, alikutana na Angel ambaye alimuangalia kwa muda na kucheka ila muda huo Junior alikuwa kashaondoka na kuelekea chumbani kwake, yani Angel alicheka na kujisemea,“Jamani mapenzi haya loh! Sasa huyu Vaileth wa kuwa na Junior kweli jamani! Yani mapenzi ni upofu”Halafu akaondoka zake na kuelekea jikoni kwani ilitakiwa siku hiyo wajiandae kwaajili ya kwenda kanisani kwani ilikuwa ni siku ya Jumapili.Baba Angel na mke wake walikuwa nyumbani tu siku hii pamoja na mama yao, na Vaileth. Basi bibi Angel alianza kuongea na mwanae kuhusu alichokiona siku hiyo,“Hivi mwanangu hapa nyumbani kwako umeshawahi kuchunguza?”“Kitu gani mama?”“Yule mlinzi wako unajua kuwa ana mahusiano na Vaileth?”“Kheee kumbe! Mama hata sikujui kabisa, kumbe Vaileth ana mahusiano na yule mlinzi! Jamani, ujue mama yule mlinzi ana mke?”“Kheee kumbe ana mke wake! Basi msichana wako ndio anadanganywa hapo, ukiona mambo hayaeleweki humu ndani jua ni mlinzi wako na msichana wako wa kazi”“Ngoja niwe vizuri mama ndio nitaweza kushughulika na hawa watu, ila nitafanyeje sasa?”“Waambie kama wanapendana waoane, oooh ila ndio hivyo kumbe mlinzi ni mume wa mtu. Sikia mwanangu ongea nae Vaileth vizuri, mwelezee kuhusu maisha yalivyo unajua sio vizuri aharibikie nyumbani kwako”Mama Angel hata hakutaka kupoteza muda kwani muda huo huo alimuita Vaileth ambaye moja kwa moja alienda chumbani, kwa kipindi hiki yani mchana basi mama Angel alikuwa akishinda kwenye chumba maalum ambacho kiliwekwa kwaajili ya mtoto, kwahiyo moja kwa moja Vaileth alienda kwenye chumba hiko kusikiliza, ila muda huu bibi Angel nae aliitwa mara moja na baba Angel kwahiyo aliinuka hapo na kwenda kumsikiliza mkwe wake, kwahiyo mule ndani alibaki Vaileth na mama Angel.“Hebu kaa chini Vai”Basi Vaileth alikaa na kuanza kumsikiliza,“Eti una mahusiano na mlinzi?”Vaileth alibaki akishangaa bila kujibu chochote, mara simu ya mama Angel iliingia ujumbe kwahiyo alichukua na kusoma kwanza ule ujumbe,“Hongera sana kwa kupata mtoto wa kike, yani wewe uzao wako ni wanawake tupu. Ni mimi Sia”Kwakweli mama Angel alichukia sana kusoma ujumbe huu na kujikuta akimwambia Vaileth akaendelee tu na kazi zake hata hakuweza kuongea nae tena.Leo ni Angel pamoja na wadogo zake na Junior tu ndio walioenda Kanisani, kwakweli ilikuwa ni siku nzuri sana kwa upande wa Angel na ilikuwa siku nzuri sana kwa upande wa Erica kwani walijiona kuwa watakuwa huru sana katika mambo yote ya siku hiyo na hawatafatiliwa sana.Wakati Erica akiwa Kanisani siku hiyo alijikuta kila muda akiinuka na kutoka nje kidogo, muda ulipokaribia kutoka na yeye aliinuka na kutoka nje kabisa na alipofika nje alionana na Bahati kanakwamba Bahati nae alikuwa mitaa hiyo akimuangalia Erica, basi alisogea karibu na kuanza kumsalimia,“Kwani wewe unakaa karibu na hili Kanisa au na wewe unasali hapa?”“Hapana, mimi nilipita tu ili nikuangalie kama wewe umekuja leo. Huwa napita mara kwa mara ila leo nimebahatika kukuona tena”“Unaonekana ni mstaarabu sana wewe”Bahati akawa anatabasamu tu, ila muda kidogo alisogea pale Erick na alionekana kuchukizwa sana kwani muda huo huo alianza kumsema mdogo wake,“Yani wewe Erica kweli unatoka Kanisani na kuja nje kufanya upuuzi?”Basi akamzaba kibao maana Erick kwa kawaida yake alikuwa ni mtu wa hasira sana, alishangaa baada ya kumzaba kibao alitokea Elly kumbe naye alikuwepo kwenye ibada kwahiyo muda huo walitoka, Elly alimuuliza Erick,“Sasa Erick ndio unapata faida gani kumpiga kibao Erica?”“Usiingilie mambo ya undugu wetu hayakuhusu”“Jiheshimu wewe, hayakuhusu ndio nini?”Erick alichukia na kutaka kumzaba kibao na Elly, ila gafla mkono wa Erick ulishikwa na muda huo huo Elly alisikika akiwaambia wenzie huku akitabasamu,“Jamani, huyo ndio mama yangu”Alikuwa ni mwanamke ambaye alimshika mkono Erick ili asimnase kibao Elly, basi Erick alimuangalia mwanamke yule na kuona kuwa ni yule yule mwanamke ambaye anadai kuwa ndiye mama yake. Erick alichukia na kutaka kumzaba kibao na Elly, ila gafla mkono wa Erick ulishikwa na muda huo huo Elly alisikika akiwaambia wenzie huku akitabasamu,“Jamani, huyo ndio mama yangu”Alikuwa ni mwanamke ambaye alimshika mkono Erick ili asimnase kibao Elly, basi Erick alimuangalia mwanamke yule na kuona kuwa ni yule yule mwanamke ambaye anadai kuwa ndiye mama yake.Kwakweli Erick alichukia zaidi muda huu kwa kitendo cha kumuona huyu mama tena kwani kila alipomuona huyu mama alihisi kuharibiwa siku kabisa, basi muda huo huo alimsjika mkono Erica na kuanza kuondoka nae, ila Angel na Junior walimuona kwahiyo walimfata kwa nyuma na moja kwa moja alienda kuingia nae kwenye gari na kuanza kuendesha akielekea nyumbani kwao yani akili yake ilikuwa haisomi kabisa kwa muda huo, basi Angel alimuuliza,“Erick, unajua sijakuelewa leo, mbona imekuwa hivi!”Erica akajibu,“Unajua hata mimi nimemshangaa Erick, kwanza kanipiga kibao bila hata kuniuliza chochote kile, halafu katokea Elly na mama yake pale ndio Erick kachukia hatari na kunishika mkono huku akinikokota tuondoke”“Kheee Erick jamani mdogo wangu, unakuwaje wewe?”Junior akawasema wale waliokuwa wakimsema Erick,“Jamani, hebu mambo mengine subirini tufike nyumbani, yani anayeendesha gari ni Erick halafu ndio mnamshambulia kwa maneno mnataka nini? Subirini tufike nyumbani”Basi walinyamaza kimya ila Erica alichukia sana kwa kitendo ambacho kimefanywa na kaka yake ingawa yeye hakujua ukweli kuhusu mama yake Elly ndio anayemwambia Erick kuwa ni mtoto wake.Mama Angel muda huu alikuwa na hasira sana halafu akili yake ilikosa muelekeo kabisa, moja kwa moja mama yake alivyorudi chumbani mule hata hakumuuliza kuwa alikuwa akiongea nini na mumewe wala nini kwani muda huo huo alitoka na kumkimbilia baba Angel ambapo alimuita na kwenda nae chumbani kuzungumza, na kabla ya kusema nae chochote alimpa ule ukumbe ambao alitumiwa na Sia,“Chukua usome”Basi baba Angel alisoma na kukunja sura pia huku akisema,“Jamani, huyu Sia ananitakia nini na familia yangu lakini?”Kisha mama Angel alianza kumsimulia kisa cha siku ile ambapo walienda na Erick kule dukani hadi akapatwa na uchungu,“Yani chanzo ni huyo mwanamke, kamlisha sumu mwanangu kuwa mimi sio mama yake. Unajua mwanzoni wakati Erick akinielezea sikumuelewa kabisa maana hata Erick hakumfahamu Sia, ila tulivyofika pale dukani ndio nikafahamu. Jamani Sia ana nini na mimi lakini? Eti anasema uzazo wangu ni wanawake tu, kwahiyo Erick sio mwanangu? Inamaana sikuzaa mapacha au ni nini mbona sielewi?”Baba Angel akapumua kidogo na kumwambia mke wake,“Unajua ndiomana siku hizi huwa wanataka hadi baba ande akashuhudie watoto wanavyozaliwa, ila mimi nitashuhudiaje wakati unajifungua na mar azote inakuwaga kama gafla? Ila mke wangu usiwe na mawazo, kuna mambo ya kujiuliza”“Mambo gani sasa? Kama Erick sio mwanangu inamaana mwanangu yuko wapi? Sitaki kukubaliana na hilo jamabo kabisa, Erick ni mtoto wangu, inamaana nilizaa mapacha wakike tupu? Je mwenzie na Erica yuko wapi? Hapana, hawa ni watoto wangu”“Mke wangu naomba uondoe hayo mawazo kabisa, hebu kumbuka siku ile mimba yako tulipoamua kwenda kupiga ultrasound, tulikuta kuna mapacha wakike na wakiume na hiyo ikawa ni furaha kubwa sana kwangu na kwako mke wangu. Na siku umejifungua, ingawa ulijifungua kwa operesheni ila ulikuwa peke yako, na nilifanya yote kuhakikisha unapata huduma inayotakiwa, kisha tulikabidhiwa watoto wetu wawili yani wale wale tulioambiwa kabla, na hapo kwa furaha tuliyonayo tuliamua kuwapa hawa watoto majina yetu japo wengi sana walipinga ila sababu ya upendo wetu tuliamua kufanya hivyo na hawa watoto tuliona kuwa ni kiunganisho chema zaidi kwetu kwani watafanya tuzidi kudumisha upendo wetu. Leo hii atokee mjinga mmoja, mwendawazimu mmoja, asiye na akili mmoja aje kuchanganya akili zetu sijui mtoto sio wa kwetu, sijui huwa unazaa watoto wa kike tupu. Kwanini akili iharibiwe na chizi? Watu husema chizi akikwapua nguo zako kisha ukaanza kumkumbiza basi utaonekana chizi maana utakuwa mtupu halafu unakimbiza mwenye nguo. Yule mwanamke ni chizi, hata siku ukipata muda wa kuonana nae na kuongea nae utaona kuwa ni chizi na zaidi ya chizi, nakuomba mke wangu uwe na amani katika moyo wako. Mimi ndio baba wa Angel, na mimi ndio baba wa Erick na Erica na tena ni baba wa Ester, hata jamii nzima itokee na kusema hawa watoto wote sio wangu sioni tatizo lolote kwani hawa ni watoto wangu, nakupenda mke wangu na ninakuamini kwa vyovyote vile. Achana na chizi asiharibu mawazo yako, na hata ungezaa wa kiume tupu au wakike tupu basi bado ningekupenda. Naomba mke wangu kuwa na amani katika moyo wako, watoto wangu wote nawapenda, haijalishi chochote. Huyo Angel washaongea hadi basi na mimi ukweli naujua ila hata siku moja hujawahi kunisikia wala hutowahi kunisikia nikisema kuwa sio mwanangu, hawa ni watoto wangu na wote nawapenda”Maneno ya baba Angel yalisuuza moyo wa mama Angel na kujikuta faraja na amani ya moyo wake ikirudi upya kabisa, alijikuta akimkumbatia mume wake kwa furaha kwani alimuona kuwa ni mwanaume wa pekee sana katika maisha yake, basi baba Angel nae alimkumbatia kisha akamuuliza,“Mke wangu, unataka nikuletee zawadi gani leo maana nitatoka kidogo!”“Mmmh, yoyote tu utakayoichagua wewe na utakayoipenda wewe”“Haya mke wangu, nakupenda sana”Basi wakakumbatiana tena pale halafu baba Angel alitoka zake na kuondoka kisha mama Angel alirudi kule chumbani alipo mama yake na mtoto.Basi mama yake alimuuliza,“Kheee mwanangu, ndio ulienda kumuuliza mumeo kitu alichokuwa akizungumza na mimi?”“Hapana mama sio hivyo, nilienda kuongea nae kuhusu mambo mengine kabisa, wala sio hayo mama yangu”“Haya sawa, ila huyu mtoto anaonekana atakuwa mtu wa dini sana”“Kwanini mama?”“Hata mimi namuona, anaonekana atakuwa vizuri mwanangu. Nilikuwa naongea na mumeo mambo ya maana tu ni kuhusu mkwe wako ila usijali tutazungumza mwanangu na kuyaweka sawa”Mama Angel alijua tu yatakuwa yanaendelea yale yay eye kumchukua mtoto kinguvu ila kwavile mama yake alisema kuwa atamwambia basi hakuwa na papara kuhusu hilo.Wakati baba Angel anatoka ndipo alipokutana na watoto wake wakiwa wametoka Kanisani, ila aliona kuwa Erick kama hayupo sawa, ilibidi amuite mwanae kwenye gari lake ambapo Erick alienda moja kwa moja kwenye gari ya baba yake halafu baba Angel hakuongea nae jambo lolote kwa muda huo zaidi ya kuondoka nae na kwenda nae mahali ambapo palikuwa na mgahawa halafu akaagiza chakula na kumtaka Erick nae aagize chakula ambapo alifanya hivyo halafu alianza kuongea nae,“Eeeeh mwanangu Erick unajua nimewaangalia pale mlivyoingia ndani nimeona kuwa haupo sawa kabisa, kwani tatizo ni nini mwanangu?”“Unajua baba sielewi kabisa, kwa kifupi simuelewi yule anayedai ni mama yangu”“Kwani kakufata tena?”“Ni hivi baba, ile shule niliyohama ambapo nilimuacha Erica, alikuja kijana mmoja kusoma pale na alikuwa akiitwa Elly, yani stori za Erica kwa kipindi hiko ni Elly Elly tu”“Oooh nimemkumbuka mwanangu, nakumbuka kuna siku Erica alileta visheti nyumbani na vikanidhuru, alisema kapewa na Elly sijui”“Ndio, kumbe yule mwanamke ndiye mama yake Elly, na leo tumesali nao Kanisani”“Kumbe!! Sasa kwanini anaifatilia familia yangu kiasi hiki jamani! Mwanangu niskilize, mimi ni baba yako naomba unisikilize kwa makini sana. Upo tayari kunisikiliza?”“Nipo tayari baba”“Nakumbuka nishawahi kukwambia jambo hili, katika maisha inatakiwa mtu uwe makini sana usijaribu kuharibu maisha yako au kuyachanganya kwa chochote kile. Mimi nilichanganya maisha yangu mwanangu na mwisho wa siku nikakutana na watu wasiokuwa na akili timamu kama huyo mwanamke, hata namshangaa kuifatilia familia yangu, hakuna nilichomkosea hata kimoja ila namshangaa sana. Mwanangu ninachotaka kukwambia sasa ni wewe uwe makini sana na huyo mwanamke, yani ni chizi asije siku akakudhuru mwanangu, kama aliweza kumpa visheti huyo Ellyn a akaniletea mimi vikanidhuru je hawezi kutenda jambo baya? Halafu anadai kuwa ni mama yako, toka lini mtu unakuwa na mama asiyekupenda? Yani mama gani ambaye hakupendi? Kwa mujibu wa Steve pale dukani ni kuwa yule mama anang’ang’ania duka lile kwaajili ya mwanae na sasa nimepata picha, kumbe mwanae ni huyo Elly. Jamani mwanangu acha kuumia kichwa kabisa, huyo mama ni chizi najua ataendelea kufatilia familia yetu ila wewe ni mtoto wa kiume nan i wajibu yako kuilinda hii familia ili isisambaratike. Je mwanangu unahitaji nikupatie nini ili kuboresha mawasiliano baina yetu maana huyu mwanamke sitaki tena awe anakutia ujinga, popote utakapokutana nae na chochote atakachokuambia nataka unitaarifu”“Sijui baba, labda simu”“Umejibu vyema kwani ndicho nilichokuwa namaanisha mwanangu, uwe na simu ili tuwe tunawasiliana na hiyo ni muhimu sana kwa baba na mtoto”Kuna mtu alisogea pale na kuvuta kiti kisha kuwasalimia baba Angel na Erick, mtu huyu Erick alimfahamu maana alikuwa ni mwalimu wake basi Erick alimtambulisha yule mwalimu kwa baba yake,“Baba, huyu ni mwalimu wangu, tumemzoea kwa jina la madam Oliva, madam huyu ndio baba yangu”“Oooh nafurahi sana kukufahamu baba Erick jamani, kwanza hongera sana. Nilipowaona hapa nikaamua nisogee ili niwasalimie, na nimefurahi sana kugundua kuwa wewe ndiye baba Erick”“Na mimi nimefurahi pia kukufahamu madam”Ila baba Angel alikuwa akijiuliza kuwa huyu mwalimu alimpa hongera ya nini, ila aliwaza kuwa pengine ni sababu ya kupata mtoto ila huyu mwalimu anatambua swala hilo? Basi alimuuliza,“Hey, ila sijakuuliza umenipa hongera ya nini?”“Ooooh! Nimekupa hongera juu ya kijana wako Erick, kwakweli hapa mtoto umepata jamani. Hongera sana, huyu mtoto sio namsifia tu sababu yupo ila hata kama asingekuwepo basi ningekwambia hili. Umepata mtoto mwerevu, na mtoto asikivu na siye na makuu kabisa. Hongera sana”“Asante sana madam”“Ni vyema kama nikipata mawasiliano yako ili niwe nakwambia maendeleo ya mtoto darasani”Baba Angel hakuona kama hilo ni tatizo kabisa, basi alimpa yule madam kadi yake ya namba za simu ili kuweza kuwasiliana nae kwa kipindi kingine.Basi yule madam hakuondoka pale kwani alikaa nao hadi mwisho yani muda baba Angel na Erick waliaga ndipo yule madam pia alipoondoka.Basi baba Angel alienda na Erick moja kwa moja dukani ili achukue simu ya kutumia, na alipoichagua alimnunulia na kwenda kununua laini kwaajili ya mwanae huyo kisha akamuuliza,“Mama yako nimpelekee zawadi gani maana nilimuuliza na akasema yoyote, sasa nimpelekee nini?”“Mmmh baba, huo mtihani mgumu ila mpelekee zawadi rahisi kabisa ambayo hawezi kuifikiria kuwa utampelekea halafu utaona atasemaje?”“Zawadi gani sasa?”“Twende dukani baba, ukaone ni zawadi rahisi kabisa ambayo hata mtoto anaweza kuinunua”Basi Erick alienda dukani na baba yake kisha akachukua zawadi na kusema kuwa ni zawadi ya mama yake, kwakweli hata baba Angel alishangaa sana ila aliichukua tu na kumwambia mwanae,“Ila dah! Yani sijafikiria ujue kama zawadi yenyewe ndio hii!”“Safari ijayo atakutajia zawadi anayoitaka baba, ila ukiona kasema tena yoyote basi atakuwa ameipenda hata hii”Baba yake alicheka tu kisha wakaingia kwenye gari na kurudi nyumbani moja kwa moja.Ilikuwa ni usiku tayari wakati baba Angel na Erick wamerudi nyumbani, kisha baba Angel alienda kumsalimia mke wake ambaye kwa muda huo alikuwa ameenda kulala kwahiyo alikuwa chumbani, mkewe alimuuliza cha kwanza,“Nasikia ulipotoka tu ukaongozana na Erick, ulienda nae wapi?”“Aaah nilienda kuongea nae, unajua huyu mtoto amechanganywa sana akili na Sia. Nilimuona kama hayupo sawa, kumbe ni kweli walikutana na Sia”“Kheee alikutana nae wapi tena?”“Kumbe leo Sia alienda kusali Kanisa lile lile ambalo huwa tunasali, basi ndio wameonana nae, halafu kumbe yule Elly ndio mtoto wa Sia maana walikutana nae na akawatambulisha mama yake”“Kheee kumbe Sia ndio aliyetoa vile visheti jamani, ana nini yule mwanamke lakini!”“Ndiomana nilikwambia mke wangu kuwa yule mwanamke ni chizi, hata asiumize akili yako”“Ila licha ya uchizi wake, kuna mambo lazima tuwe makini nayo. Kwanza hakupenda tufahamu kuwa yeye ni mama yake Elly kumbuka, nimeenda pale kwake kama mara mbili ila siku mkuta. Kama angekuwa mtu mzuri tungemfahamu kitambo kuwa ni yeye, halafu jambo lingine kamtuma Elly ampe Erica visheti ambavyo vilikudhuru ulipokula. Mume wangu inatakiwa kuwa makini sana na huyo mtu, kwamaana hiyo watoto wasiende tena kusali pale Kanisani”“Kheee watoto wasisali sababu ya huyo chizi?”“Ndio, bora wakasali Kanisa la mjini”“Jamani mke wangu, unaweza kwenda na huko akatufata pia. Kumbuka chizi huwa hachoki”’“Kwahiyo unafurahia anachokifanya?”“Hapana sifurahii ila nimejaribu tu kusema mke wangu”Kisha baba Angel akamtolea ile zawadi mke wake na kumwambia,“Haya, zawadi hii hapa!”“Kheee yani ndio umeniletea pipi ya kijiti jamani! Zawadi ya kumpa Ester ndio umeniletea mimi!”“Aaaah mke wangu, nimekuuliza nikuletee zawadi gani ukanijibu yoyote. Sasa mimi ningekuletea nini jamani!”“Mbona siku zote huwa nakwambia yoyote ila hujawahi kuniletea pipi?”“Ila hii ni idea ya Erick, nilipomwambia akuchagulie zawadi basi ndio akakuchagulia hii”“Mwambie nimeipenda sana”Kisha mama Angel akaifungua ile pipi na kuanza kuila huku akitoka sebleni, nia yake ilikuwa ni Erick kumuona akiila ile pipi, ni kweli aliwakuta watoto wake sebleni wakila chakula cha usiku na moja kwa moja Erica alianza kucheka na kusema,“Mama jamani, unakula pipi kama mtoto!”Erick akajibu,“Ni wapi pipi imeandikwa kuwa ni ya mtoto tu!!”Mama Angel nae akasema,“Nyie watoto ni washamba sana, hii ni zawadi yangu nimepewa na mtu muhimu sana katika maisha yangu ndiomana naila kwa madaha. Kwakweli aliyemshauri baba yenu aniletee zawadi hii nimemfurahia sana, nilikumbuka pipi jamani mimi! Nilikumbuka sana”Kitendo kile kilimfanya Erick ajihisi raha sana kwenye moyo wake, alifurahi mno kuona kuwa zawadi yake imependwa na mama yake.Erick alienda kulala baada ya kula tu kwani alikuwa amechoka kwa siku hiyo kutokana na ile mizunguko ya kutoka Kanisani na moja kwa moja kwenda kuzunguka na baba yake, basi alipoingia chumbani, dada yake alimfata na kuanza kuongea nae,“Eeeeh na mimi zawadi yangu?”“Kheee zawadi ya nini sasa wewe?”“Mbona mama kaletewa zawadi na baba?”“Sasa mama akiletewa zawadi na baba ndio lazima mimi nikuletee wewe zawadi?”“Mama si Erica, kaletewa zawadi na baba ambaye ni Erick. Sasa wewe ni Erick gani ambaye huna upendo wa baba? Ndiomana mama yako ni mwingine?”Halafu akaondoka na kuelekea chumbani kwake, ile kauli ilimchukiza sana Erick, hivyobasi na yeye kwa hasira alienda chumbani kwa Erica ili akamseme, alifika na kufungua mlango na kumkuta Erica akivua nguo, yani Erica alipiga kelele zilizofanya hadi mama yao akimbilie chumbani ajue kuna nini,“Nyie watoto vipi jamani! Mtatuumiza kwa presha!”Alimkuta Erica kajifunga khanga, huku Erick akiwa amesimama pembeni kwani nae alikuwa akishangaa jinsi dada yake alivypoga kelele, wakati yeye ni mara nyingi tu anamkuta akivua nguo ila hajawahi kupiga kelele, akamshangaa sana ila Erica alimjibu mama yake,“Niliona mende mama, nadhani hata Erick kakimbia kuangalia tatizo gani”“Mende kwenye nyumba yangu! Nyie watoto hebu achene masikhara, kesho itabidi nimuite yule mtu wa dawa, yani mende anafanya nini sasa?”“Ila nahisi ni mawenge yang utu”“Muone vile, yani wewe utaniumiza kichwa kwa kelele zisizokuwa na maana”Basi mama yao akatoka, na yeye Erick alitoka zake na kumuacha Erica mwenyewe mule chumbani.Muda Erica anapiga kelele, ni muda ambao Junior alikuwa chumbani kwa Vaileth na zile kelele walizisikia ila walizipuuzia sababu ile sauti ni ya Erica na wanaifahamu, basi Vaileth akamwambia Junior,“Kheee hutaki hata kwenda kuangalia mdogo wako ana tatizo gani?”“Aaaah yule mtoto mwenyewe mbea balaa, nikamuangalie ana tatizo gani ili iweje? Atajijua mwenyewe na wazazi wake huko, kwasasa ni wewe unayeshughulisha moyo wangu”Vaileth alitabasamu tu kwani aliona ni fahari na raha kupendwa na Junior ila muda kidogo mlango wa Vaileth uligongwa kwani leo alifunga mlango, basi Vaileth alishtuka na moja kwa moja Junior alienda kujificha chooni ila kwa muda huu alikimbia na nguo zake.Vaileth akafungua, na mgongaji alikuwa ni bibi yake Angel ambaye alimuuliza Vaileth,“Mbona leo umelala mapema sana?”“Bibi, nimeona nimemaliza kazi halafu nilikuwa na uchovu ndiomana nimelala mapema”“Sawa”Kisha bibi aliingia chumbani kwa Vaileth na kukaa kitandani halafu akaanza kuongea nae,“Vaileth usifikirie kuwa nakuingilia maamuzi yako au uhuru wako, unajua kwa nguo niliyoiona asubuhi nimejitafakari sana na kama sitokwambia sasa basi ni nani atakwambia haya! Hivi wewe si una mtoto?”“Ndio, nina mtoto bibi”“Baba wa mtoto wako yuko wapi?”Vaileth aliinama chini na kujibu,“Hata sijui bibi, alinikimbia”“Je unataka kuzaa mtoto wa pili na kukimbiwa na huyo mwanaume? Najua jibu litakuwa hapana, starehe zipo na zinafanywa kila leo, zilikuwepo, zipo na zitaendelea kuwepo kwahiyo akili kichwani mwako. Wanaume ni waongo sana, kama wanaume anakupenda kweli mwambie aende kwenu akutambulishe na muoane ila mwanaume wa kukutumia tu mwili wako huyo hakupendi mjukuu wangu. Nimeona nije kukupa hili angalizo kabisa, huyo mwanaume ambaye unamahusiano nae, achana nae maana atakupeleka pabaya. Anayekupenda kweli mwambie akuoe, maisha ya ndoa ni matamu sana na sio maisha haya ya kuruka tuka na kuszalishwa watoto halafu unaachwa. Yangu kwa leo ni hayo tu, saa hizi ni usiku ndio nimekuja kukwambia haya ili uyatafakari muda wote unaolala. Usiku mwema”Bibi alitoka na kumuacha Vaileth akifunga tena mlango wake kisha Junior alitoka kule chooni alikokuwa amejificha na kurudi kitandani, basi Vaileth akamwambia,“Umesikia maneno ya bibi? Unatakiwa unioe Junior”“Ila na wewe Vaileth jamani, huyu ushasema ni bibi sababu mambo yake yamepita ndiomana kaitwa bibi. Sikia nikwambie, mimi nitakuoa tu, ndoa sio kitu cha kukurupuka. Hivi kwasasa nikuoe twende tukaishi wapi? Tule nini? Mimi nilishakwambia sitakuongopea kitu chochote, kwasasa sitaweza kukuoa maana bado sijajipanga kimaisha, hivi huoni raha, tunaishi hapa vizuri tu kama mke na mume, tunakula, tunashiba na tuna sehemu nzuri ya kulala, hakuna tunacholipia, si bili ya umeme, ya maji wala hatununui chakula ila tunakula tunachotaka na mambo yetu tunafanya. Unajua huyu bibi anapokwambia kitu kuna vingine unaweza hata kumshushua maana havina mantiki yoyote, hebu achana na maneno yake. Mimi nitakuoa tu, ila sio kwasasa. Tukijipanga nitakuoa. Achana na maneno ya bibi na tuendelee kula raha tu, kila kitu kipo hapa unataka tuhofie nini jamani Vai? Achana na maneno ya bibi”Vaileth akapumua kidogo huku Junior akianza kumpapasa na kujikuta hata akisahau yale maneno ya bibi kabisa.Muda huu bibi alienda pia chumbani kwa Angel, ila naye Angel alikuwa amefunga mlango kwani kwa muda huo alikuwa akitumia ile simu yake ya magendo ambayo wazazi wake hawaijui, kwahiyo bibi aligonga mlango na Angel alienda kumfungulia.Kama kawaida bibi alimpa maidha yake pale Angel ila kwa muda huo ilikuwa ni kazi kwani Angel mawazo yake yalikuwa kwenye simu tu, hata hakuwa na wazo la kusema kuwa bibi yake kuna kitu cha muhimu anamwambia,“Angel mjukuu wangu, kuwa makini sana. Ni wengi watakwambia kuwa wewe ni mzuri ila hawana upendo wa aina yoyote na wewe, unatakiwa kuwa makini na kuyajali maisha yako”“Sawa bibi nimekusikia ila muda huu nina usingizi sana, nahitaji kulala”“Basi tutaongea kesho maana nina mengi sana ya kuzungumza na wewe”“Sawa bibi, usiku mwema”Yani Angel alimuaga haraka haraka bibi yake ilia pate muda wa kuwasiliana na ile simu yake, basi bibi yake aliondoka na kufanya Angel akafunge mlango kwanza na kuendelea kuwasiliana na simu yake,“Oooh Samir, bibi yangu alikuja humu chumbani kwangu mara moja”“Ila Angel nimekumiss sana, yani natamani hata kukuoana. Sikia nikwambie kitu, kesho asubuhi kabisa nitapita hapo kwenu, naomba utoke ili angalau nikupungie mkono tu”“Sawa hakuna shida, basi nitatoka ule muda ambao wadogo zangu wanaenda shule, kwa kesho nitajifanya nawasindikiza nje ya geti kidogo”“Nitafurahi sana Angel, yani nimerudi leo mara moja na kesho natakiwa kuondoka tena, kwahiyo nakuomba hiyo asubuhi nikuone hata kwa mbali”“Usijali utaniona”Angel aliwasiliana na Samir kisha kuagana na kulala tu moja kwa moja.Kulipokucha, wakati wakina Erica wakitoka ndani, Angel nae alitoka nao kama alivyopanga na Samir, yani wakati wanatoka hata Erick alimuuliza,“Dada, leo vipi?”“Jamani nawasindikiza, kwani vibaya?”“Sio vibaya dada”Basi wakatoka wote hadi nje ya geti ambapo Erick alikuwa akisubiri gari la shule akiwa pamoja na Erica, ila ilitangulia gari ya shuleni kwakina Erica na kufanya Erica aondoke ila muda ule ule alifika yule mwanamke ambaye huwa anadai Erick ni mtoto wake, yani Sia ila wakati wanamshangaa pale mara alifika na Samir, ila ni tofauti na jinsi Samir alivyopanga na Angel kuwa atampungia mkono tu kwani cha kushangaza Samir alisogea pale karibu na kumzaba yule mama kibao. Basi wakatoka wote hadi nje ya geti ambapo Erick alikuwa akisubiri gari la shule akiwa pamoja na Erica, ila ilitangulia gari ya shuleni kwakina Erica na kufanya Erica aondoke ila muda ule ule alifika yule mwanamke ambaye huwa anadai Erick ni mtoto wake, yani Sia ila wakati wanamshangaa pale mara alifika na Samir, ila ni tofauti na jinsi Samir alivyopanga na Angel kuwa atampungia mkono tu kwani cha kushangaza Samir alisogea pale karibu na kumzaba yule mama kibao.Kitendo kile kiliwashangaza wote pale haswaa Angel ambaye alishangaa zaidi na kumfata Samir,“Hey mbona unampiga mama wa watu hivyo? Huoni kama huyo ni sawa na mzazi wako!”Mara gari ya shule yakina Erick lilifika kwahiyo Erick alienda kupanda na kuondoka, basi Samir alionekana kuwa na hasira sana na yule mwanamke na kumwambia Angel,“Laiti siku ukimfahamu huyu mwanamke vizuri basi utamchukia maisha yako yote”Yule mwanamke nae akamuangalia Samir na kumwambia,“Nakushangaa huna adabu kiasi hiki!! Ila baba yako hayupo hivi, na wewe laitti ukijua baba yako wa kweli ni nani basi hata huyu Angel hutomfatilia tena”Halafu Sia akaondoka zake, na kufanya Samir na Angel watazamane pale, kisha Samir akamwambia Angel,“Umeona huyu mwanamke alivyo! Yani huyu mama huwa anajifanya anaifahamu sana familia yangu, akitokea yeye basi nyumbani hakuna amani, hata mama yangu hapatani nae. Yani huyu mama huyu hapana”“Ila sawa na mama yako huyo”“Weee siwezi kuwa na mama wa dizaini ya huyu mama, hawezi kuwa mama yangu kamwe. Labda niwe kaburini, nakwambia ukimfahamu huyu mama vizuri basi utamchukia maisha yako yako, na ukijua sababu ya mimi kumnasa kibao muda huu basi utaelewa kwanini nimekuwa na hasira hivi!! Kwanza kashaniharibia siku kabisa, Angel ngoja niondoke”Basi Samir akaondoka zake, yani inaonyesha Samir kachukizwa sana na yule mama hata Angel hakuelewa ni kwanini maana kwa muonekano wa haraka haraka basi Sia alionekana ni mama mmoja mstaarabu sana na asiye na makuu, kwahiyo Angel alibaki akishangaa tu na kuamua kurudi ndani kwao yani ile furaha ambayo alijua ataipata kwa kumuona Samir alishangaa tu kutokuwa nayo kabisa.Moja kwa moja na yeye alijikuta akimchukia yule mama kwani aliona amekatisha furaha yake, ila wakati anaingia ndani tu mama yake alimuuliza,“Angel, umetoka wapi hii asubuhi?”“Mama, nilienda kuwasindikiza wakina Erick, kwahiyo nilikuwa nao hapo nje ya geti wamepanda gari basin a mimi nimerudi ndani”“Umeanza lini hiyo tabia?”“Mama jamani, yani nimekaa na kujikuta nakumbuka shule, nakumbuka kuamka asubuhi kwahiyo nikaona ni vyema kama nikianza kuwasindikiza wakina Erick mama, kwani vibaya?”“Si vibaya, ila kabla hujafanya hivyo uwe unakuja kuniambia”Angel aliondoka kuelekea chumbani kwake huku akiilalamikia tabia ya mama yake ya kumfatilia sana hadi kumkosesha uhuru.Erick nae akiwa kwenye gari alikuwa na mawazo sana, yani moyoni mwake alichukia mno kwa kitendo cha kufatwa na yule mwanamke nyumbani kwao, basi alipokuwa amekaa muda ule ule alisogea Sarah karibu yake yani Sarah alipishana na mtu ili akae karibu na Erick, basi Sarah alimuuliza Erick,“Yule mama ambaye alikuwa amesimama nanyi getini ni ndugu yenu?”“Kwanini umeuliza hivyo? Yani hujaulizia wote pale zaidi ya yule mama?”“Nimeuliza tu Erick nina maana yangu, nijibu kwanza ni ndugu yenu?”“Hapana, ni mpita njia tu”“Jamani yule mama simpendi, unajua simpendi balaa”“Kwanini humpendi sasa, kafanyaje kwani?”“Yule mama ni mshirikina, hata mama yangu kagombana nae tayari. Ila ugomvi wa huyu mama na mama yangu hata huwa siuelewi mwanzo wala mwisho maana huwa wakikutana ni wanarushiana maneno tu. Kwa kifupi huyu mama ni mkorofi halafu anajifanya anajua maisha ya kila mtu, hebu fikiria mimi mwenyewe huwa ananiambia kuwa anamfahamu baba yangu ni nani!”“Kheeee! Kwahiyo kakwambia ni nani?”“Hapana, ila kasema nikitaka kujua ukweli basi niende nyumbani kwake ila mimi siwezi kwenda kwani yule mama ni mshirikina sana”“Kwani wewe humjui baba yako?”“Simjui ila kwa mujibu wa mama ni kuwa baba alikufa wakati nipo mdogo sana, aliniacha nikiwa na miaka miwili na huwa mara kwa mara tunaenda na mama kupalilia kaburi la baba, kwahiyo huyu mama huwa namshangaa sana kwa kusema aliyekufa si baba yangu ila baba yangu yupo na yeye ndio anayemfahamu. Yani mama aliyenizaa amfahamu mwingine halafu yeye amfahamu mwingine! Mama hafai yule, nahisi ni mchonganishi wa familia za watu, msimkaribishe kwenu yani familia yenu nzima mtajikuta mnagombana sababu yake”“Kumbe!! Nashukuru kwa kunipa huo ujumbe, halafu kwasasa nina simu Sarah”“Ooooh katika habari njema ulizowahi kunipa, ya kwanza ni hiyo, naomba namba zako”Basi Erick alimtajia namba zake, yani Erick kwa muda huo alikuwa na furaha kidogo baada ya kujua tabia ya yule mwanamke na kuona kuwa sio peke yake anayemfatilia bali ni wengi anawafatilia.Siku hiyo Erick aliongea vizuri sana na Sarah kiasi kwamba hata Sarah alifurahia yale mazungumzo yake na Erick hadi walipofika shuleni ambapo kila mmoja alienda kwenye darasa lake kwani Sarah alikuwa kidato cha pili, wakati huo Erick akiwa kidato cha kwanza.Basi siku ya leo Steve akiwa dukani akiendelea na kazi yake, alipigiwa simu na dada yake na kumuelekeza ambapo lile duka lilipo kisha dada yake alienda kumtembelea kwa siku hiyo hiyo, Steve alifurahi kuonana na dada yake maana kwa kipindi hiko walikuwa hawaishi pamoja wala nini, basi alianza kuongea nae,“Unajua kwanini nimekutafuta leo?”“Kheee kwanini dada?”“Basi leo nimekutana na kale kasichana ambako ulikuwa unakapenda sana, kumbe ana mtoto”“Kheee dada ulikuwa hujui jamani! Toka kipindi hiko asiwe na mtoto kweli! Kwanza sio kasichana bali atakuwa ni mmama. Ila nilimpenda sana yule, isingekuwa kuingiliwa na huyu jini basi ndio angekuwa mke wangu yule”“Jini mkata kamba alikuvuruga akili mdogo wangu, ila unajua huwa najilaumu sana, yani mimi tabia zangu za awali ndio zimeniathiri na familia yangu kwa kiasi kikubwa sana. Nakumbuka yule Sia hakuwa na mambo ya waganga kabisa yani yeye alikuwa na upendo wake anaouamini katika moyo wake, yani mimi sijui kilanga gani kikanituma kumueleza kuhusu babu wa Bagamoyo na kumpeleka kule, mwisho wa siku dawa zikaja kukuathiri mdogo wangu. Halafu mpaka leo maisha yako hayapo vizuri sababu ya kuchanganywa akili na yule mwanamke. Pole mdogo wangu”“Asante sana, yani kiukweli hata nikifikiria kuishi na mwanamke basi moyo wangu huwa naona tu umesizi, hakika alichonifanya Sian i Mungu tu anajua”Muda kidogo Sia nae alifika pale dukani na kumfanya Dora amshangae na kusema,“Hutajwi?”“Ndio sitajwi, kwanza kwanini mnanitaja? Ndio kusema mnanipenda sana? Halafu wewe Steve mara nyingine hebu kuwa mwanaume, achana na maneno ya hawa ndugu zako yatakuharibu. Huyo dada yako amedanga weee, nani ambaye hakujui Dora kama ulikuwa ni mdangaji maarufu hadi umelizoa la kulizoa ndio umejifanya umeokoka na kusema wenzio vibaya. Hii Mbingu kama inapokeaga watu wa aina yako basi kwa hakika kila mtu ataenda Mbinguni. Hivi Dora ni kipi unaweza kunisema mimi? Yule James alikuoa wewe na amekufa na kukuachia mali zake zote si kwasababu yay ale madawa uliyompindua pindua nayo! Mali zote unazo wewe, unatumia wewe na kile kitoto chako tu, kwani James hakuwa na watoto wengine! James nae ana watoto tu wa kutosha, kama umeokoka kweli kwanini usikae chini na kusema watoto wote wa James waje niwape urithi wao? Ila mali zote za James unatumia wewe, hakuna kazi unayoifanya ila kutwa kucha kutembea na biblia na vitabu vya nyimbo, sababu uanjua unakula hela za James muda wote unaoutaka. Kama kuna mtoto mwenye haki zaidi na mali za James basi ni mtoto wa Bite, ila kwasasa eti kachukuliwa na Erica ndio anaishi nyumbani kwake wakati yule mtoto hata angeamua kuwa na mjengo wake angeweza. Kuwa na huruma wewe mwanamke, sio kila muda Sia kafanya hivi, Sia kafanya vile, ushawahi kufikiria dhambi zako au unaziona dhambi za Sia tu ndio kubwa sana! Na hii tabia wala sijaitoa mbali bali nimeitoa kwako mwenyewe, tulichotofautiana na wewe, ni kwamba mimi nampenda mwanaume mmoja maisha yangu yote na nitampenda hadi naingia kaburini ila wewe unampenda kila mwanaume unayemuona mbele ya macho yako. Tutaona na hiko kitoto chako Leah kitakuwaje? Nahisi kitatembea na kaka zake wote”Dora alichukia sana kwa maneno ya Sian a kumsogelea karibu ili amnase kibao ila Sia alidaka ule mkono wa Dora na kumwambia,“Hujawahi kunipiga na hutowahi kunipiga, mimi ndio Sian i namba nyingine mimi. Huwa naongea kile ninachojisikia, na huwezi kunipangia cha kuongea, na maneno yangu haya siku moja yataokoa familia nyingi sana. Umechukua pesa za James na kwenda kujengea familia yako, siku zote ulipenda wanaume sababu ya pesa, wewe hata shemeji yako huyo Erick ulimtaka sababu ya pesa zake ila leo hii unaona Sia ndio anafanya mambo ya ajabu kupita wote duniani, na wewe utajiacha na nani! Ptuuu! Endelea na ulokole wako feki kwa kudanganya watu, yani na wewe umeokoka! Nicheke mie, dunia simama nishuke labda njiani kuna mti wa mapera, nichume pera moja nitafune halafu nikateseke chooni, wewe mwanamke loh!”Halafu Sia akaondoka zake na kumuacha pale Steve na Dora wakiwa kimya tu, yani kimya kilitawala kwa muda kidogo halafu Dora alikaa chini na kuinama, alijikuta machozi yakimtoka tu na kukumbuka maisha yake ya nyumba, jinsi alivyosababisha wengi wapate ukimwi sababu yake, ila atawezaje kwasasakugawa mali za James ikiwa hafanyi kazi yoyote na anategemea mali hizo zimlishe na kila kitu katika maisha yake? Aliwaza sana, basi mdogo wake alimwambia,“Dada, yani ndio kitu cha kuumia hiko jamani, yule Sia achana nae, hata bosi hapa husema kuwa Sian i chizi na ukimfatiliza utapata tabu sana dada yangu, achana na maneno yake. Wewe umeokoka basi amini hivyo”“Mmmh mdogo wangu ila ulokole mgumu jamani, sasa mimi nikitoa kila kitu nitaishije? Nitaenda wapi? Si ndio nitakuwa kama yule mwanamke wa kuitwa Ester jamani ambaye waumini ndio wamemuonea huruma na kumjengea nyumba, dah sijui katumwa huyu!!”“Achana nae dada, angalia maisha yako ila ukifatilia maneno ya Sia utaumia sana, yani huyu kafanya hadi Erica apatwe na uchungu hapa na kwenda kujifungua”“Kheee kumbe Erica ana mtoto mwingine?”“Ndio, tena wa kike”“Oooh ngoja nikamuone rafiki yangu, kwaheri mdogo wangu”Basi Dora aliondoka pale dukani na muda huo alielekea moja kwa moja nyumbani kwa mama Angel.Mama Angel akiwa na mama yake ndani huku wakiongea habari mbalimbali ikiwa na namna ya kuishi na kufundisha watoto wake,“Ila hawa watoto wako unatakiwa kuwa nao makini sana mwanangu na ikiwezekana basi kila siku uwe na utaratibu wa kuongea nao”“Mama, unajua kuna muda hadi nahisi kuchanganyikiwa sababu ya hawa watoto haswaa Angel na Erica, ni bora ya Erica mambo yake mengi yapo wazi, sababu anapenda umbea na hilo linajulikana, yani Erica kama akiwepo anaweza hata kunyata na kusimama mlangoni wa chumba change ili tu kusikia mimi na baba yake tunazungumza kitu gani hadi sijui hiyo tabia niidhibiti vipi. Halafu huyu Angel ndio ananiumiza kichwa kabisa, maana huyu mtoto ana mchezo wa kufanya mambo kimya kimya, yani kuna mambo yake mengine huwezi kuyatambua kabisa”“Ila usishangae, huyu Angel kabeba tabia zako ujue, ulikuwa ukinipa shida sana. Mtoto unajifanya una siri yani kila kitu unaficha, hadi mambo ya muhimu yanakusibu ila huwezi kukaa chini na kunieleza mama yako, sasa huyu Angel kafata tabia zako yani na yeye namuona ana mtindo wa kufanya mambo ya kimya kimya, kiasi kwamba hataki kuweka wazi mambo anayoyafanya na ukienda kuongea nae anakujibu juu juu”“Sasa mama nifanyeje na hao watoto?”“Nadhani njia pekee ni kuwa uongee nao mara kwa mara na kama utaweza basi hata kila siku hebu wafundishe maisha ni nini, huyo mbea mfundishe vizuri kuna mahari atapata shida sababu ya umbea wako, na huyo msiri hebu ongea nae vizuri maana kuna vitu sio vya kuficha kabisa”“Sawa mama, nitaongea nae”Basi Dora nae alifika muda huu na moja kwa moja alipelekwa na Vaileth kwenye kile chumba cha mtoto maana alienda kumuona mtoto, basi aliingia huku akifurahi sana.Basi bibi Angel nae alimkaribisha vizuri tu Dora, halafu akainuka kwenda kumuelekeza Vaileth kitu cha kupika kwa muda huo, basi ndani mule alibaki mama Angel pamoja na Dora na mtoto tu ambaye kwa muda alikuwa amelala, basi Dora alianza kuongea na rafiki yake huyo,“Mmmh unajua habari hii nimeenda kuipata dukani nilipoenda kumtembelea Steve, ndio akaniambia. Ila unajua maajabu niliyoyakuta dukani kwako?”“Maajabu gani kwani?”“Mwenzangu, nimekaa kidogo pale nazungumza na mdogo wangu si akaja yule jini mkata kamba jamani! Yani yule mwanamke simpendi tena simpendi kabisa”“Yupi huyo?”“Sia huyo”“Nahisi unapoishia wewe kutokumpenda ndio mimi ninapoanzia, yani kanitoka huyo mwanamke namshangaa hadi leo hataki kuiacha familia yangu kwa amani”“Anaiacha vipi? Kaniambia kuwa katika ameisha yake amempenda mwanaume mmoja tu na atampenda mpaka kufa kwake, yani huyo sio mwingine ni mume wako, kwakweli unakazi ya ziada kwa yule mwanamke”“Ila nifanyeje sasa?”“Yani Sia ashukuru Mungu kwasasa sina mambo ya ajabu ila ingekuwa enzi zangu, mbona Sia angenielewa vizuri yule. Ila nahisi huyu Sia kuna kipindi ataniangusha tena tu kwa maneno yake”“Aaaah usiseme hivyo Dora, kumbuka ulipotoka na uliposasa, maisha ni safari na kuna siku utafika sehemu ile unayoitaka wewe. Usikatishwe tamaa na maneno ya mtu”Basi Dora aliongea ongea pale kidogo kisha akaaga kwani alipitia tu mara moja ukizingatia hakujipanga kabisa kufanya hivyo kwa siku hiyo.Dora alipoondoka tu, ndipo bibi Angel nae alienda na kuanza kuongea na mtoto wake,“Kheee kumbe bado una urafiki na huyu mtu!”“Mama, Dora amebadilika ujue”“Hata kama ila yeye ndio chanzo cha dada yako kuachana na mumewe”“Mmmh mama jamani hayo si yalishapita lakini, dada mwenyewe kwa kushauriana na wewe alienda mahakamani kudai talaka, haya si akapata mtu mwingine wa kumuoa, sasa utasema nini mama”“Unajua siku zote ndio ya kwanza ndio tamu, si unaona hiyo ndoa ya pili ya dada yako haikuwa na shamra shamra zozote, yani wale kama wamevutana tu kwenda kuishi pamoja. Ni kama dada yako Mage na mume wake, yani ndoa iliyofanyika ni wewe na Erick, na Tumaini na Tony, hizi ndio ndoa ila ya huyu dada yako na huyo mwanasheria wake sio ndoa wala nini ni kuvutana tu. Hebu kumbuka kipindi dada yako alipokuwa akiolewa na James! Ingawa ulikuwa mdogo ila najua ile ndoa ilikuvutia na wewe ndiomana ulikuwa ukililia mapenzi ya kweli, mwanangu huyu rafiki yako hata ajisafishe vipi ila bado ni mbaya kwani aliiba mume wa dada yako”“Ila mama hayo mambo yaliisha ujue, hata dada Bite hana tatizo kabisa”“Hana tatizo wapi, anaumia moyoni sana tu. Unafikiri huwa hamkumbuki mume wake? Mwanaume kachuma nae mali mbalimbali ila kuna mwanamke mwingine ndio anazifaidi, hata Junior hajaambulia kitu, unafikiri haumii! Huyo Deo unadhani kuna kitu atampa Junior, mtu mwenyewe wala hakai kama baba wa Junior wala nini, unafikiri huyo Junior bila kujiendeleza mwenyewe atafika popote!”“Halafu ndio muhuni balaa”“Hapana, Junior kwasasa katulia sana. Kumbuka Junior huwa hatoki kabisa, unajua Junior kabadilika, nishamkuta hadi anamsaidia Vaileth kuosha vyombo, kwakweli Junior kabadilika na kawa mtoto mzuri, ila simshangai kwanini hataki kurudi kwa baba yake yule ni sababu yule baba hana upendo na mtoto kwahiyo Junior anaona ni vyema akae huku tu”“Ila baba Angel alisema ataongea na mama Junior, na pia ataongea na Deo kwani Junior bado anahitaji upendo wa wazazi kwa ukaribu zaidi”“Ila kaukosa sababu ya huyo rafiki yako Dora, na ushukuru tu wewe baba Angel alikuwa na msimamo ila isingekuwa hivyo basi huyu rafiki yako lazima angempitia tu”“Jamani mama!”“Ndio hivyo”Bibi Angel alionekana kutokumpenda kabisa Dora ingawa ni rafiki wa mwanae wa muda mrefu sana ila hakuwa na upendo nae.Vaileth alifika na kumletea chakula mama Angel ambaye alianza kukila huku akikisifia,“Jamani, mbona chakula cha leo kitamu sana”“Umesahau kuwa nilikuwa jikoni kumuelekeza”“Oooh nimekumbuka mama, yani hizi ndizi za leo balaa, zimekolea nazi hadi nimezipenda”Vaileth alicheka tu na kurudi zake jikoni, ambapo Junior alikuwa sebleni nae akila zile ndizi huku akisifia,“Kheee ndizi tamu hizo, kukaa nyumba moja na mama aliyejifungua raha sana”Vaileth akacheka tu ila kwa muda huo Angel alienda kubeba chakula na moja kwa moja kwenda nacho chumbani, alikuwa anataka ale huku akitumia simu kwahiyo kwa pale sebleni asingeweza kabisa kwani ile simu kwake ilikuwa ni simu ya magendo.Na kweli Angel alikuwa kila huku akiwasiliana na simu kwa njia ya ujumbe, na muda huo alikuwa akiwasiliana na Samir pamoja na Mussa, na wote walimuuliza kuwa anakula nini, kwahiyo alipiga picha zile ndizi na kuwatumia, basi alianza Samir kumwambia,“Hizo ndizi zinaonekana ni tamu sana, ama kwa hakika mke wangu wewe ni mpishi hodari”Mussa nae alimtumia ujumbe,“Nina hakika hizo ndizi umepika wewe Angel, chakula chako kitamu kama jina lako”Basi Angel alikuwa akijihisi raha sana yani alikuwa akisoma zile jumbe huku akitabasamu na kufurahi, ila Mussa akatuma ujumbe tena kwa Angel,“Kwani Angel unaishi wapi? Nielekeze ili nije nikusalimie maana pale kwa bibi yako haupo tena”“Mmmh kwetu ni geti kali balaa, yani sina sehemu ninayotoka nisiulizwe, sasa nitawezaje kuonana na wewe”“Aaaah Angel jamani, unajua wewe ni mdada mkubwa, je huwa huendagi dukani?”“Nitaenda dukani kufanya nini sasa?”“Kheee kwenu, hakuna mahitaji ya kwenda kununua dukani?”“Vitu vingi unakuta vipo ndani na ukitaka kitu, basi mama yupo radhi amtume dereva akanunue”“Duh! Hebu aga unaenda kununua pedi”“Humu ndani kwetu, huwa mama anamtindo wa kununua dazani ya pedi yani sijui ni kitu gani, huoni hata vocha mara nyingi huwa nakuomba, yani kwetu kutoka ndio balaa”“Jamani Angel sasa itakuwaje? Nahitaji sana kukuona kwakweli!”“Sijui sasa”“Hebu nielekeze kwenu kwanza”Basi Angel alimuelekeza kwao na Mussa akamwambia,“Nitakuja, yani nitakutumia tu ujumbe kuwa nipo nje kwenu hata utoke mara moja tu, kiukweli Angel natamani sana kukuona”Angel akajifikiria kidogo na kumwambia tu karibu maana aliona kuzidi kumkatalia ni kama kumfanya ajihisi vibaya ukizingatia mara kwa mara huwa anamuomba Mussa amtumie vocha.Basi ujumbe mwingine uliingia toka kwa Samir,“Angel, unajua leo yule mbibi kaniharibia siku sana ila nitakuja tena tuonane hata nikukumbatie kidogo tu kipenzi changu”“Ila si unajua kama kwetu geti kali jamani Samir?”“Naelewa, ila utafanya kama leo Angel, siku nikija nitakutumia ujumbe hata utoke kidogo tu nikukumbatie jamani Angel”Basi Angel alihisi rah asana kuambiwa vile na Samir, wala hakuwaza jinsi kwao walivyowakali ila alichowaza ni kuonana na Samir tu.Kisha alipomaliza kula aliinuka na sahani yake kuirudisha jikoni ila njiani alikutana na bibi yake ambaye alianza kumsema,“Kheee Angel, ndio tabia gani hiyo ya kwenda kula chumbani? Meza ya chakula imewekwa ya kazi gani? Na huko chumbani kuna nini hadi uende kula huko”“Samahani bibi”“Oooon naona umeanza tabia ya mama yako, kufanya kosa makusudi na kukimbilia samahani, sijaipenda hiyo tabisa, siku nyingine ule mezani pale sio kukimbilia na chakula chumbani”“Sawa bibi”Yani Angel hakuwa muongeaji sana, mara nyingi yeye mtu akimsema basi atamsikiliza tu na sio kuanza kujibishana nae.Muda wa kulala ulipofika, kama kawaida Junior alienda chumbani kwa Vaileth maana kwa kipindi hiko Junior alifanya kwa Vaileth kama ndio chumbani kwake maana muda wa kulala ulipofika tu alikimbilia huko, basi walianza kuongea na Vaileth,“Eeeeh Junior, kama bibi siku akienda chumbani kwako halafu asikukute itakuwaje?”“Weee yani ambacho huwa nafanya pale ni kuzima taa ya chumbani halafu huwa nafunga na funguo nahisi huyo bibi atagonga hadi vidole viingie tumboni”Basi Vaileth akawa anacheka huku wakiendelea kuongea na kutaniana, ila muda kidogo mlango wa Vaileth uligongwa na kumfanya Junior akimbilie chooni kama kawaida, ikabidi Vaileth ainuke na kwenda kufungua, na kweli alikuwa ni bibi yao ambaye aliingia chumbani kwa Vaileth na kuanza kuongea nae,“Mbona nimesikia kama ukiongea na mtu Vai?”“Hapana bibi, sikuwa naongea na yeyote”“Bado nakusisitiza, maisha ni tofauti na unavyofikiria, unaweza kupoteza maisha yako ndani ya siku moja tu. Kuwa makini, wanaume ni waongo sana. Upo ndani ya nyumba hii kwasasa na atakwambia nakupenda kwasana ila siku utakapoondoka hapa na hauna kazi tena basi hayo maneno yake ya nakupenda sana hutoyasikia kabisa, kuwa makini sana. Usiku mwema”Kisha bibi aliinuka na kuondoka zake, halafu Vaileth akafunga tena mlango na Junior alitoka chooni na kusema,“Jamani mtoto akue tu ili huyu bibi arudi kwake, yani ananiumiza kichwa huyu bibi hadi nakosa raha jamani!”Vaileth alikuwa akicheka, kisha yeye na Junior walilala kama kawaida yani maneno ya yule bibi yalikuwa ni kama kumpigia mbuzi gitaa tu.Kulipokucha kila mmoja aliendelea na mambo yake siku hiyo, na wanafunzi walienda shuleni kama kawaida yao, ila siku hii Angel alishikiliwa na mama yake kuwa aoshe vyombo kwahiyo alikuwa akiosha vyombo halafu mama yake alienda karibu na kuongea nae,“Unajua Angel siku hizi umebadilika sana mwanangu, yani humu ndani hufanyi kazi yoyote muda wote unalala kwani huko kulala kunakusaidia nini mwanangu?”“Mama, huwa najihisi uchovu tu ndiomana naamua kulala”“Haya hapo kuosha vyombo tu ila umejinunisha utafikiri unafanya kazi gani”Kisha mama yake akaondoka na kumuacha Angel akiosha vile vyombo na baada ya kumaliza alirudi chumbani kwake na kuchukua simu yake ila alikutana na ujumbe toka kwa Mussa,“Angel, nipo hapa nje ya geti lenu”Akakuta ujumbe mwingine toka kwa Mussa tena,“Mbona Angel unanifanyia hivyo jamani, toka kidogo tu nikuone”Basi Angel aliweka simu pembeni na kuamua kutoka nje, na moja kwa moja alienda getini na kutoka nje ya geti ila alipofika nje alimkuta Mussa kasimama na kijana mwingine ila alipomuangalia vizuri aligundua kuwa kijana huyo ni Samir tena ilionekana wanaongea kama watu wanaofahamiana sana. Basi Angel aliweka simu pembeni na kuamua kutoka nje, na moja kwa moja alienda getini na kutoka nje ya geti ila alipofika nje alimkuta Mussa kasimama na kijana mwingine ila alipomuangalia vizuri aligundua kuwa kijana huyo ni Samir tena ilionekana wanaongea kama watu wanaofahamiana sana.Angel alisimama kwa muda kidogo akiwashangaa, kisha aliwafata kuwauliza,“Tuseme mnafahamiana?”Halafu na wao wakaulizana kwa pamoja,“Tuseme tulikuwa tunamfata msichana mmoja?”Angel akatabasamu, kisha Samir akamwambia Angel,“Sisi tunafahamiana ndio ni ndugu huyo kwenye ukoo ukoo”“Aaaah kumbe!!”Mara Angel alisikia sauti ya mama yake ikiita, ikabidi Angel awaache pale nje na akimbilie ndani alipokuwa akiitwa na mama yake, yani aliposogea karibu tu na mama yake alinaswa kibao na mama yake halafu ndio swali likafatia,“Kule nje ya geti ulienda kutafuta nini? Una nini wewe mtoto lakini eeeh!”Angel alikaa kimya tu na kumfanya mama Angel azidi kuchukia kwakweli, kisha akamwambia,“Sasa ole wako nikuone umetoka tena mjinga wewe!”Halafu mama yake akaelekea chumbani ila Angel alielekea bustanini ambako alimkuta Junior amekaa naye Angel alienda kukaa pembeni yake huku kainama chini, basi Junior alimuuliza tatizo ni nini,“Mbona hivyo Angel, tatizo ni nini?”“Unajua mama yangu huwa simuelewi kabisa, watoto wengine wapo huru majumbani mwao ila mimi nachungwa utafikiri kitu gani, yani sipumui jamani, nikitoka hata nje ya geti ni tatizo sijui mama anafikiria nini kuhusu mimi?”“Mimi nadhani mama yako kuna kitu anaogopa kuhusu wewe, hebu jaribu kumuuliza kwa ukaribu kuwa mama unataka mimi niweje? Kwanini hutaki nitembee tembee, yani unakaa ndani kama mfungwa jamani, umekuwa kuku wewe! Ndio nyie mkipata siku upenyo lazima wanaowachunga wajute maana huwa mnaota mapembe”“Unamaanisha nini?”“Unadhani siku ukiachiwa wewe si utaenda hadi kukutana na wasiopaswa kukutana nao jamani! Ila mama inabidi aangalie kila kitu, atakuchunga hadi lini? Wewe unakua kila siku, na mwisho wa siku utaanza chuo, je huko atakuchunga? Si ndio akili itakuwa imekuruka kabisa”“Mmmmh wewe nawe, mie akili iniruke kwa mtindo upi? Najitambua mimi na siwezi kurukwa na akili, sikia nikwambie, mama anadhani nitakuwa na wanaume, ila mimi wanaume wa kazi gani? Yupo mmoja tu nimpendaye”“Na huyo mmoja umpendaye ndio mwenye uwezo wa kuchanganya akili yako wewe au kukuacha ubaki na akili timamu, Angel mapenzi ni matamu sana ila mapenzi usipotumia akili utaumia mno”“Aaaaargh na wewe sijui unazungumzia nini, unadhani mimi ni kama wewe mwenye wanawake kila kona!”“Sasa unafikiri nilikuwa napenda kuwa na wanawake kila kona? Unakuwa na huyu, mnakuwa vizuri kabisa, siku mnafumaniwa na jamaa yake, kumbe ana mtu wake, basi unaachwa kwenye mataa, unadhani nitafanya nini zaidi ya kutafuta mwingine? Unampata na anajua kabisa kuwa mimi ni mwanafunzi yani sina pesa sababu sifanyi kazi nasoma tu, ila unamkuta anakuorodheshea mahitaji hayo hadi kichwa kinapasuka, kuna demu jamani hadi nilihisi kizunguzungu, mwanzoni nilikuwa najikakamua ila badae nilivyoshindwa ikabidi niachane nae na niwe na mwingine”“Sasa alikuwa akitaka umnunulie nini?”“Yani yeye matatizo yote ya nyumbani kwao basi niyatatue mimi, sijui mara mama yake anaumwa, mara baba yake anaumwa, mara anataka sijui hela ya saluni, mara dawa za mama yake zinahitajika, hivyo sio shilingi mbili utakuta ananiambia laki mbili au laki tatu, jamani nikashindwa, mwingine kila atakachokiona wakati tumeongozana anakitaka, yani mapenzi yanaumiza kichwa hatari ndiomana ukipata sehemu ya kutulia unaona bora utilize moyo wako. Namuonea huruma Erick ambaye hajui hata mapenzi ni kitu gani yani akianza kupenda uwiii atafilisi biashara za baba yake”“Wewe nawe, hivi unajua kama Erick yupo tofauti sana yani hata baba huwa anamsifia, yani Erick huo ujinga labda aanze badae ila wewe nadhani ulipoanza kutembea tu”Wote wakacheka kwa muda huo na kuanza kuongea habari za kuwafurahisha ili kupoteza mawazo na malengo ya kitu ambacho kimetokea kwa siku hizo.Muda wa kutoka shule ulipofika, Sarah kama kawaida alienda kupanda kwenye gari ya shule na kukaa karibu na Erick kwani alikuwa anahisi furaha sana kukaa na Erick, basi alianza kuongea nae,“Lini nije kumuona wifi yangu mdogo Erick?”“Kheeee kashakuwa wifi yako?”“Ndio”“Hivi Sarah huna aibu kabisa, maana kila siku upo kuniambia habari za kuwa wapenzi”“Sasa aibu ya nini Erick, nakwambia kweli wewe ni mtanashati na kama mabinti hawakuwa wakikufata labda sababu ya ulivyo maana una hasira sana na hupendi kucheka, ila wadada wengi wangekufata na wengi wanaumia juu yako Erick, ila nadhani mimi ndio zaidi yani mpaka nimejitoa muhanga kuongea ujue sio kawaida”Erick alitabasamu tu na kuamuangalia Sarah, basi waliendelea kuongea mambo mbalimbali kisha Erick alipofika kwao alishuka na kuingia ndani kama kawaida, ila leo alipoingia tu alikutana na mama yake ambaye alimuuliza,“Vipi leo yule shetani hujakutana nae tena?”“Sijakutana nae mama”“Aaaah sawa, ila ukikutana nae niambie mwanangu yani usiache kusema”“Sawa mama, nimekuelewa”Basi Erick akaenda zake chumbani kwake na kubadili sare za shule, kisha alienda moja kwa moja kula chakula ambapo alimkuta Junior na Angel wakila pia huku wakiongea ongea mambo ya utani utani, basi Angel akamtania pale mdogo wake,“Eti Erick, nani wifi yangu?”Muda huo Erica nae alisogea kula na kusema,“Kheee dada na wewe umeanza mambo kama ya Junior jamani!! Sasa Erick wifi wa kazi gani? Huoni kama Erick bado mdogo?”Junior akadakia,“Ana udogo gani sasa Erick jamani!! Kidato cha kwanza ni mdogo, nani kasema”Mama Angel nae alikuwa akipita pale na kuwafokea,“Halafu Junior ujinga kwenye nyumba yangu sitaki, na kesho nina kikao na nyie watoto naona mmezidisha ujinga kwenye nyumba hii”Wote wakanyamaza kimya na kuendelea kula maana huyu mama yao walimfahamu vizuri sana.Usiku wa siku hiyo, mama Angel alikaa na baba Angel na kuanza kuzungumza kuhusu mtoto maana ile tabia ya Angel ya kutoka nje ya geti kidogo ilimkosesha raha na amani mama Angel,“Unajua siku hizi Angel kaanza tabia ya kutoka nje ya geti sijui hata huwa anafanya nini, jamani mtoto ananichanganya huyu hata sijui cha kufanya kwakweli!”“Ila mke wangu, nadhani umuulize Angel kitu gani anataka, unajua kwasasa wamemaliza shule na wapo tu nyumbani inawezekana anachoka sana kukaa nyumbani. Nadhani itakuwa ni vyema sana kama ukimuuliza kitu anachotaka kufanya”“Sasa kitu gani jamani mume wangu? Unajua huyu mtoto tusipokuwa makini nae basi ataleta mabalaa hapa nyumbani!!”“Naelewa mke wangu, ila ndio tuwe makini ila mtoto kumbana sana nako sio umakini ila ni kumfundisha mtoto atambue jema na baya, unajua akili ya Angel ishaanza kuchanganywa na mapenzi kwasasa, kwahiyo tusipokaa chini kumfundisha basi tunampoteza”“Na tumfundishaje sasa?”“Wewe ni mama, lazima utajua namna ya kumfundisha. Hebu angalia njia ulizopita wewe kwanza halafu ujue jinsi gani uweze kukaa na huyu mtoto na kumuelekeza cha kufanya ili asitende makosa ambayo ulishayapitia”“Umeanza sasa, kwani mimi nilipenda kutenda makosa”“Hilo ndio tatizo lako, mtu akiongea basi huhisi anataka kukusema. Mimi nimemaliza kwa upande wangu, tusigombane mke wangu kwa vitu vidogo vya watoto, sisi tulianza kabla ya hawa watoto, tushikamane tu na tuwalee vizuri”Kisha baba Angel aliamua kulala kwani hakutaka kufanya mabishano na mke wake.Angel nae wakati amelala, alitafutwa kwenye simu na Samir ambaye alianza kuongea nae,“Angel kipenzi, kumbe huwa unaongea na Mussa mara kwa mara?”“Nitumie ujumbe Samir, kuongea na simu hapa nyumbani ni tatizo kidogo”Basi Samir akamtumia ujumbe na kumuuliza kuhusu yeye na Mussa,“Eeeh naomba nieleze mahusiano yako na Mussa”“Sina mahusiano yoyote na Mussa, ni vile alikosea namba ya simu na tukaanza kuwasiliana na huwa tunawasiliana kawaida tu”“Mussa hajawahi kukutongoza?”“Hapana, sijawahi kutongozwa na Mussa kabisa huo ndio ukweli, yani huwa tunawasiliana tu kama marafiki”“Naona kabisa wazi kuwa penzi langu litaibiwa, Mussa ni ndugu yangu ila simuamini hata kidogo. Naomba Angel uache tabia ya kuwasiliana na Mussa”“Ila sina mahusiano na Mussa jamani”“Ila Angel kuna jambo ngoja nikushauri”“Jambo gani?”“Kwanini usimwambie mama yako kuwa akupeleke kwenye chuo cha kujifunza kompyuta ili ujifunze funze wakati unasubiria matokeo ya kidato cha nne? Najua huko itakuwa rahisi sana kwa mimi na wewe kuonana mara kwa mara”“Mmmh wazo zuri, sasa chuo gani?”“Usijichagulie, mwache mamako akuchagulie mwenyewe, maana ukijichagulia utamfanya akuhisi vibaya, mwache akuchagulie halafu tutajua cha kufanya”“Sawa, nitaongea nae kuhusu hilo”“Ila Angel nakuomba acha kuwasiliana na Mussa jamani, mimi ndio namjua Mussa ni ndugu yangu na sio mtu mzuri kwako”“Nimekuelewa Samir, hakuna tatizo na hata sitawasiliana nae tena”“Nakupenda sana Angel, yani kumbuka hilo. Muache Mussa kabisa”Basi Angel na Samir waliongea sana kiasi kwamba Angel alichelewa kulala, kwahiyo alilala saa kumi alfajiri.Kesho yake kama ambavyo mama Angel alipanga na mumewe, kwanza alimuita Angel na kuanza kuongea nae,“Angel mwanangu kitu gani unataka kufanya, ni nini kipo katika akili yako kwa muda huu?”“Mama, kwakweli nimechoka kukaa nyumbani. Mimi nilikuwa napenda labda hata nikasome kozi ya kompyuta”“Oooh sawa, itabidi basi uende kusoma na Junior”Hapo kidogo Angel alikaa kimya kwa muda kwani hakufikiria kama mama yake anaweza kutoa wazo la yeye kwenda kusoma na Junior, ila hakuwa na budi zaidi ya kukubali tu,“Sawa mama,hakuna tatizo”Basi mama Angel akawaita wote yani watoto wote kwenye nyumba yake maana siku hiyo ilikuwa Ijumaa na wakina Erica waliwahi kutoka shule, akaanza kuongea nao,“Jamani, nyie watoto nimewaita hapa ili niongee nanyi mambo ya msingi yanayoendelea, kwakweli tabia mbaya kwenye familia yangu sitaki, mambo ya ajabu ajabu kwenye familia yangu sitaki. Junior, mambo ya kumwambia mwanangu Erick aanze kuwa na wanawake sitaki kuyasikia, Angel na Erica kama ambavyo huwa naongea na sasa naongea tena sitaki kusikia wala kuona marafiki zenu wa kiume hapa nyumbani, nilipiga marufuku hata marafiki wa Erick sababu yenu halafu nyie ndio mniletee maajabu ya dunia sitaki huo upuuzi kabisa. Na wewe Erick, fanya kile unachoona sahihi katika maisha sio kile unachoshauriwa na mtu, kwa kifupi stori za ajabu ajabu kwenye nyumba yangu sitaki. Halafu wazo la Angel nalifanyia kazi, kwahiyo Junior jiandae utakuwa ukienda na Angel kwenye chuo cha kompyuta mkajifunze huko. Sasa Junior wewe ndio utakuwa kama mlinzi wa Angel, akipatwa na tatizo lolote ni wewe ndiye utakaye nijibu, nadhani nimemaliza sasa, mmenielewa lakini?”Wote waliitikia,“Tumekuelewa mama”“Haya mwenye swali aniulize, au kama hamna maswali sasa basi muda wote mtakapokuwa na maswali yenu njooni mniulize nami nitawajibu”Kisha mama yao akainuka na kuondoka zake, basi watoto wakabaki wanaangaliana na Angel ndio akaanza kusema,“Ila jamani, mbona siku hizi kama mama kawa mkali zaidi? Yani kila kitu anasema hapendi, tatizo ni nini?”Junior akajibu,“Itakuwa mumewe hampi utamu vizuri”Wote waliinuka na kumuacha Junior peke yake kwani ujinga ujinga walioambiwa kuwa wasizungumze basi ndio Junior alikuwa kama anataka kuuanzisha tena.Ila kama kawaida ya Erica alipoinuka pale alikuwa na yake kichwani tayari na moja kwa moja alienda kwa mama yao na kumueleza swali alilouliza Angel na jinsi Junior alivyosema, kiukweli mama Angel alichukia sana na kuuliza,“Kwahiyo mkasemaje wengine?”“Tuliondoka mama”“Mnaujua utamu nyie? Hivi Junior ana akili gani lakini jamani! Aaaargh mitoto mingine sijui imelelewajwe”Kisha mama Angel alimuita Junior kwa nguvu sana na Junior akaenda kisha akamnasa vibao vya kutosha na kumuuliza,“Unaujua utamu wewe? Unazungumzia nini? Mbona una tabia mbaya sana?”“Nisamehe mamdogo, nisamehe sana nilichokuwa nazungumzia ni kingine kabisa ila sijui wamefikiria nini”“Haya ulikuwa ukizungumzia nini, yani bila aibu sababu hapewi utamu wa kutosha na mume wake, hivi una nini wewe mtoto? Nitakurudisha kwa mama yako!”“Nisamehe mamdogo jamani, sikumaanisha hivyo unavyomaanisha. Yani nilikuwa nasema bamdogo hajawahi kukuletea vitu vitamu kama keki”Mama Angel akamnasa kibao kingine na kumfanya Junior apige na magoti kuomba msamaha, kwani hapo wazo lilikuwa la kurudishwa kwao tu ambapo alikuwa hataki iwe hivyo, basi alipiga magoti na kuendelea kumuomba mamake mdogo msamaha,“Sasa nenda ukawaambie hao ulikuwa unawaambia huo upuuzi na ukarekebishe hiyo kauli yako, mjinga wewe. Toka hapa”Basi Junior aliinuka lakini moja kwa moja alihisi mpeleka maneno ni Erica tu, ila ilibidi afanye kama alivyotumwa na kuwaita wote yani Angel, Erick na Erica kisha kuanza kuongea nao,“Jamani, mmenifikiria vibaya, mimi sikumaanisha utamu wowote zaidi ya utamu wa keki na pipi na juisi, haya Erica mpeleka maneno umemaanisha utamu gani? Unaujua utamu wewe? Jamani katika maisha yangu sijawahi kuona mtu mbea kama wewe Erica, yani hufai hata kidogo, nimetengua kauli yangu jamani, sijamaanisha hivyo, mistake nifukuzwe kwenye nyumba hii, mimi nimependa kuishi hapa, niacheni niishi kwa furaha”Angel alimuangalia Junior alivyokuwa akiongea halafu alimuangalia Erica kwani mdogo wake kweli alikuwa mbea tena wa kutosha tu, ila walikubaliana pale na kila mmoja kuelekea tena chumbani kwake. Ila kiukweli Junior nae alimchukia Erica, yani katika ile nyumba ni Erick pekee ambaye kidogo alikuwa akikaa kaaa na kuongea mengi na Erica kwani hata Angel alikuwa hapendi kuongea na mdogo wake huyo tena kwa kipindi hiko ambacho ana simu ya magendo ndio kabisa, akaona akiwa anaongea nae mara kwa mara basi atapeleka maneno kwa mama yao.Leo usiku wakati Erica kaka zake chumbani huku kajiinamia tu, Erick alienda kuongea nae kwani alikuwa akimfahamu vizuri na alijua lazima Erica atakuwa kachukia vile kusemwa na Junior,“Erica, vipi mdogo wangu umejiinamia tu”“Unajua humu ndani hawanipendi yani hakuna anayenipenda hata mmoja”“Usijali mimi nakupenda mdogo wangu”“Kila mtu ananisema mimi mbea, ila umbea wangu ni nini wakati nasema ukweli?”“Hata kama unasema ukweli ila huo ndio umbea, yani umbea ni kutoa maneno sehemu moja na kuyapeleka sehemu nyingine, mfano umesikia mtu anasemwa, halafu wewe kuchukua yale maneno na kuyapeleka kwa muhusika basi huo ndio unaitwa umbea na uongo ni kusema maneno ambayo hayapo yani unajitungia tu”“Ila mimi nasema ukweli”“Ndio unasema ukweli ila unausema katika sehemu ambao hauhitajiki, mdogo wangu hiyo ndio sababu ila usiwe na mawazo sana”“Kwahiyo na wewe hupendi?”“Aaaah mimi nishawahi kusema kuwa sipendi? Wala sina tatizo juu ya hilo, ila tu nikuulize mdogo wangu kwani utamu ambao uliuelewa wewe ni upi?”“Aaaah jamani achana na mambo hayo, yameshapita jamani Erick”“Nilikuwa nakutania tu, ila nimemiss ile tabia yako ya kuja chumbani kwangu bila hodi ila mimi siku ile kuja kidogo tu umepiga kelele hadi mama akaja jamani!”Erica alicheka na kusema,“Unajua siku ile sikutarajia kama unakuja, halafu nilikuwa sijavaa”“Ila hujawahi kushtuka kiasi kile, ulikuwa na mambo yako wewe ndiomana kama sio ulikuwa ukimuwaza yule jamaa wa Kanisani sijui”“Jamani Erick sio hivyo jamani!”Basi siku hii waliongea vizuri tu na kuamua kuanza kucheza karata zilizowapelekea kulala mule mule chumbani kwa Erica.Usiku wa leo Junior alimwambia Vaileth kuwa itanidi autumie kupunguza machungu yake ya kupigwa na mama yake mdogo,“Unajua sijapenda kabisa jinsi mamdogo alivyonipiga ila yote ni sababu ya umbea wa Erica”“Pole Junior jamani!”“Sio pole tu, unatakiwa leo unipe vitu adimu hadi nisahau haya maneno ya mamdogo”“Vitu gani Junior, yani wewe umenifanya mimi kama mke wako jamani!”“Ndio wewe ni mke wangu yani mimi na wewe ni mke na mume ila tu hatujaenda kuhalalisha ila mimi na wewe ni wanandoa, neno la Mungu linasema kilichofunguliwa duniani na Mbinguni kimefunguliwa kwahiyo mimi na wewe tumeshakubalika na Mungu, achana na watu kutushuhudia”“Ila Junior una vituko jamani wewe, hadi umeanza kuongea na neno la Mungu jamani!”“Ndio, kwani neno halisemi hivyo!! Mimi na wewe Vaileth ni wanandoa tayari, ukisikiliza maneno ya yule bibi utapata shida sana, unatakiwa kunisikiliza mimi mumeo kama mama mdogo anavyomsikiliza bamdogo”Basi Vaileth alikuwa akitabasamu tu kwani maneno ya Junior yalikuwa yakimfurahisha, kwa kipindi hiko Junior alimfanya Vaileth kama mke wake kwahiyo alikuwa akimtumia kwa muda wowote anaoutaka yeye ila usiku wa leo walitumia muda mrefu sana kuwa pamoja kiasi kwamba walichelewa sana kulala yani nao walilala kwenye saa kumi alifajiri sababu ya uchovu na kila kitu.Kulipokucha bibi Angel na mama Angel walikuwa macho ila leo humu ndani palikuwa kimya sana yani inaonekana watoto wote walikuwa wamelala, basi bibi Angel alimuuliza mwanae,“Inamaana leo hadi Vai bado kalala?”“Hata mimi nashangaa mama, sijui jana wamelala muda gani watoto wa nyumba hii jamani!”“Ila unajua kuw awatoto wako siku hizi wana mtindo wa kwenda ile sebule ya juu kuangalia mikanda ya ngumi, usikute jana wameangalia sana na ndiomana wamelala hadi muda huu, ngoja nikamuite Vai kwanza”Bibi aliondoka na kwenda kugonga chumba cha Vaileth, yani kwakweli alikurupuka pia kwani hata hakutegemea kwa muda kuwa umeenda kwa kiasi hiko, basi alimshtua Junior pale,“Uwiiii nahisi bibi anagonga, tumechelewa sana kuamka leo”Junior nae alikurupuka kama kawaida na kwenda kujifungia chooni, basi Vaileth akafungua mlango huku akiwa amechoka sana,“Kheee wewe Vai una nini leo? Mbona umechelewa kuamka hivi!!”“Nisamehe bibi”“Hebu nenda ukaanze usafi huko”Kisha bibi alitoka kwa Vaileth na moja kwa moja kwenda chumbani kwa Angel ambapo aligonga mlango na kufunguliwa na Angel ambaye nae alichoka na usingizi, kwakweli bibi alitingisha kichwa sana,“Yani nyie watoto jamani, hivi mnajua ni muda gani huu? Mbona mna mambo ya ajabu sana! Hebu amka na leo ndio umuandalie mama yako chakula cha asubuhi”Basi Angel alijivuta vuta na kutoka chumbani kwake, kisha moja kwa moja bibi alielekea chumbani kwa Erica, ila alikutana na Erick akiwa anatokea chumbani kwa Erica akamuuliza,“Na wewe vipi asubuhi asubuhi kwenye chumba cha dada yako?”“Nilienda kumuamsha bibi maana leo kachelewa sana kuamka”“Ooooh umefanya vizuri sana, kwani jana usiku mlikuwa mnafanya nini watoto wa nyumba hii? Mlikuwa mnaangalia mikanda eeeh!”“Hapana bibi”“Hiyo tabia nitaikomesha, watoto gani nyie”Kisha bibi Angel akarudi tena kwa mama Angel na kuongea nae,“Inatakiwa uwe makini sana na hawa watoto, ujue wanakesha kuangalia mikanda ndiomana wanachelewa kuamka”“Mama, umemuamsha na Junior?”“Ngoja niende”Bibi wakati anaenda kwa Junior ndio alimkuta Junior mlangoni kwake akifungua mlango kwa funguo, kwakweli bibi alishangaa sana na kumuuliza,“Wewe Junior, inamaana hukulala chumbani kwako au kitu gani?”“Kwanini bibi?”“Mbona muda huu ndio unafungua na funguo?”“Hapana bibi, nilitoka kidogo bustanini na nikajisahau na kufunga mlango”Basi bibi aliamuangalia kwa muda kidogo ila hakuwa na uhakika na mashaka yake, ikabidi tu arudi kuendelea kuwahimiza wakina Vaileth katika kufanya kazi za siku hiyo.Siku hiyo mchana alifika rafiki wa Erica, yani Samia na alikuwa ameleta tena mikanda ya ngumi yani hiyo mikanda ambayo bibi yao alihisi kuwa walikuwa wakiangalia ndio kwanza Samia aliileta siku ya leo na alipokelewa na rafiki yake na kukaribishwa vizuri tu, basi Samia alikuwa akiongea mambo mengi sana na Erica moja wapo alimuuliza kuhusu Erica,“Huyu kaka yako ni vipi lakini Erica? Mbona hapendi kuongea na watu?”“Mmmh huyo mzoee tu ndio zake hizo”Basi aliongea mambo mengi sana na siku hii Erica aliitumia kumtambulisha Samia kwa mama yake ambaye nae alionekana kumfurahia ila tu hakujua kama Samia ndio huwa anawaletea watoto wake mikanda ya ngumi, basi Samia wakati anaaga akamwambia mama Angel,“Mama, siku moja naomba umruhusu Erica aje na kwetu”“Hakuna shida, atakuja na kaka zake”“Ni vizuri hata hivyo, nitafurahi sana. Mimi naenda”“Haya, karibu tena”Ila wakati Samia anatoka basi Junior leo alijitolea kwenda kumsindikiza Samia, wakati Erica kaishia getini ni moja kwa moja Junior alimsindikiza Samia kituoni kwenda kupanda gari la kurudi kwao kwani Samia alikuwa yupo huru sana nyumbani kwao na hakufungiwa kama ambavyo Erica alikuwa akifungiwa.Basi Junior alikuwa akimsindikiza huku akiongea nae mambo mbalimbali,“Kwenu mpo wangapi Samia?”“Wawili tu, mimi na kaka yangu”“Oooh! Ila unaonekana wewe ni binti mpole sana, mkarimu na muongeaji mzuri”“Asante sana”“Sema ningependa tuwe tunawasiliana zaidi, una simu?”“Hapana, labda simu ya kaka”“Sawa hakuna tatizo Samia, usijali nimekuelewa”Basi alimsindikiza hadi Samia alipopanda gari na yeye kurudi nyumbani kwao pale, ila lile tukio la Junior kumsindikiza Samia lilimchukiza sana Vaileth ukizingatia Junior alikuwa kijana ambaye haaminiki kabisa.Siku hiyo usiku wakati wa kulala, kawaida ya Junior alienda chumbani kwa Vaileth kulala ila alimuona kuwa Vaileth amechukia na kumuuliza ambacho kimemchukiza,“Mbona unaonekana huna furaha leo”“Unaona ulichofanya kipo sawa, mbona siku zote huwa humsindikizi yule mtoto lakini leo umemsindikiza”“Jamani Vai, ushasema yule ni mtoto sasa mimi wa nini jamani!”Basi Junior alianza kumpapasa papasa Vaileth ili aweze kumsahaulisha lile wazo la yeye kumsindikiza Samia.Mara wakasikia mlango ukigongwa na moja kwa moja walihisi ni bibi yao tu, basi kama kawaida Junior alikimbilia chooni kujificha, na Vaileth alienda kufungua mlango ila aliyeingia alikuwa Erica ila cha kushangaza moja kwa moja Erica alikimbilia chooni kwa Vaileth na huko alibambana na Junior na kumfanya Erica apige kelele kama kawaida yake. Mara wakasikia mlango ukigongwa na moja kwa moja walihisi ni bibi yao tu, basi kama kawaida Junior alikimbilia chooni kujificha, na Vaileth alienda kufungua mlango ila aliyeingia alikuwa Erica ila cha kushangaza moja kwa moja Erica alikimbilia chooni kwa Vaileth na huko alibambana na Junior na kumfanya Erica apige kelele kama kawaida yake.Yani Junior muda ule ule alimkimbilia Erica na kumziba mdomo kisha kutoka nae kwenye chumba cha Vaileth ambapo Erick alivyokuwa anakuja na mama Angel walikutana na Junior akiwa kamshikilia Erica, basi mama Angel akauliza,“Kwani tatizo nini jamani?”“Nadhani bahati mbaya, tumekutana hapo njiani na Erica tukagongana”“Jamani na nyie usiku huu mnaenda wapi jamani!”Basi mama Angel akamchukua Erica toka mikononi mwa Junior na kumpeleka chumbani kwake yani chumbani kwa Erica, ila muda huo Junior alikuwa na wasiwasi sana kuwa Erica anaweza kusema ukweli ukizingatia ni mbeya yani alihisi kila kitu kinaenda kuharibika, basi wakati Erica yupo na mama yake muda ule ule Junior alienda kuzima umeme wa nyumba nzima ili wote washughulikie umeme na washindwe kuongea na Erica, na kweli umeme wa nyumba nzima ulipokatika yani mama Angel alihisi kiwewe kwa mtoto wake mchanga kuwa giza, hivyobasi alimuacha Erica pale na kwenda kukimbilia chumbani kwa mtoto wake mdogoila muda huo huo Junior nae aliingia chumbani kwa Erica na kumwambia,“Ole wako uropoke ulichokiona leo”Kisha akatoka na kurudi tena kwenye soketi kubwa na kurudisha umeme kwahiyo hawakujua kuwa tatizo ni kitu gani mpaka umeme kukatika gafla vile kwa nyumba nzima.Mama Angel alikuwa akilalamika tu kwa mume wake,“Ni kitu gani kimetokea leo jamani, kwanini umeme ukatike gafla hivi! Yule fundi wako hakutengeneza vizuri”“Nitamuita kesho aje kuangalia ila sidhani kama kuna tatizo mke wangu maana alitengeneza vizuri tu”“Sasa kama hakuna tatizo ni kwanini ukatike gafla hivi! Si kuna jenereta jamani tena ametuunganishia la moja kwa moja kuwa ukikatika wa kawaida basi jenereta liwake, kwakweli mimi binafsi sielewi hii hali jamani! Sio kawaida”“Basi mke wangu usijali, kesho nitamuita fundi atengeneze, usiwe na wasiwasi”“Sawa, na lile swala la Junior na Angel kwenda kusoma kompyuta umelishughulikia?”“Ooooh umenikumbusha kitu, ngoja niwasiliane na huyu mtu”Basi baba Angel alichukua simu yake na kumpigia mtu aliyekuwa akimsema, mtu huyo alikuwa ni madam Oliva, alishawahi kuongea nae na huyu madam alishawahi kumueleza kuwa ana sehemu yake ambapo anawafundisha watu kozi ya kompyuta, yani baba Angel hakujali ule ni usiku wala nini ila nia yake ilikuwa ni kumpa jibu linaloeleweka mke wake,“Hallow baba Erick, mbona usiku!!”“Samahani mwalimu, nilikuwa naulizia kile kituo chako cha kufundishia kompyuta, nina vijana wangu nataka kuwaleta”“Ooooh hakuna tatizo, walete tu Jumatatu nitakuwepo na kuwaonyesha mazingira, walete tu”“Sawa, asante. Usiku mwema”Basi baba Angel aliagana na huyu madam na kumpa mkewe jibu kuwa Jumatatu atawapeleka Junior na Angel, basi mama Angel nae akamzogodoa pale mumewe kidogo,“Ndio usiku huu na wewe, si ungempigia kesho tu!!”“Mmmh mke wangu wewe nakujua mwenyewe, ningesema sijafatilia lazima ungeongea yako muda huu, uanze kusema ingekuwa sina mtoto mdogo ningeenda mwenyewe, haya mama nimefatilia sema sikuulizia vizuri tu na mwalimu ndio huyo niliyekuwa naongea nae”“Haya nimekuelewa mume wangu hakuna tatizo”Basi waliamua tu kulala kwa muda huo.Jumapili hii kama kawaida walijiandaa kwa kwenda Kanisani, na kama ilivyokuwa kwa wiki iliyopita basi leo waliondoka vile vile Junior, Angel, Erick na Erica ila leo Erick aliwapeleka wenzie kwenye kanisa lingine kabisa kwani yeye ndio aliyekuwa akiendesha gari, ila Erica alichukia sana,“Yani wewe ukiamua kitu ndio hicho hicho”Junior akasema,“Muache, huyo ndio baba mwenye nyumba, kwahiyo ndio mwenye maamuzi, huwezi kwenda kinyume nay eye la sivyo uhame nyumba”“Aaaargghh”Basi walishuka na kwenda kwenye hilo Kanisa ambalo Erick aliwapeleka wenzie, kwahiyo kwa siku hiyo waliabudu kwenye hilo Kanisa.Baada ya ibada walitoka na moja kwa moja kuingia kwenye gari na safari ya nyumbani ikaanza, ila njiani Erica aliona watu anaowafahamu na kushangaa kuona wameongozana,“Jamani, yule si Bahati na Abdi wale!!”Erick akadakia,“Ndio wenyewe”“Kheee au ni ndugu!”“Itakuwa, ndio uone kuwa naona mbali”Basi Erica hakuendelea tena kuongea ila mbele kidogo walimuona Elly na mama yake, ila Erick akataka kuongeza mwendo sema gari likazimika gafla na kumfanya Erick kuchukia sana basi Junior alimuuliza,“Kwani tatizo ni nini Erick?”“Hata sielewi, limezimika gafla tu”“Basi tushuke, tuliangalie kidogo”Ikabidi washuke ili waangalie tatizo ni nini, ila wakati wanashuka basi Elly na mama yake nao walifika eneo lile, naye mama yake Elly akamwambia Erick,“Yani huwezi kunikimbia mimi, ona ulitaka kuongeza mwendo ila gari imesimama kwaajili yangu. Nilitaka tu kukusalimia, na hiyo gari haijaharibika wala nini ni nzima kabisa ila iligoma tusalimiane”Angel nae alimua kushuka kwenye gari na kumuuliza mama Elly,“Kwani mama una tatizo gani? Nakumbuka mara ya kwanza nilikuona kwetu ambapo Samir alikunasa kibao”Elly akauliza kwa mama yake,“Yani mama kuna mtu alikunasa kibao?”“Achana na hayo mambo mwanangu, tufikirie vitu vya muhimu. Ukiwaona hawa uwaone kama ndugu zako”“Kivipi mama?”“Kuna siku nitakaa chini na kuzungumza na wewe mambo ambayo huyajui kabisa wala huyafikirii kabisa ila jua kwamba hawa ni ndugu zako”Yani Erick ndio alizidi kuchukia huku akitamani hata kumtukana yule mama ila alimuangalia tu na kurudi kwenye gari na alipojaribu kuwasha ni kweli liliwaka yani hakuna sehemu ambayo ilikuwa inamatatizo kwenye gari wala nini. Basi wote wakaingia kwenye gari na Junior aliuliza wakati Erick akiendesha lile gari tena,“Kwani yule mama alikuwa akiongelea vitu gani maana sijamuelewa hata kidogo”“Ni bora usimuelewe hivyo hivyo maana ukimuelewa utaharibu siku yako”Junior alimuangalia tu Erick kwa lile jibu ila pia alijiuliza ni kwanini Erick ameonekana kuchukia zaidi baada ya kumuona yule mama na hakupata jibu ila waliendelea tu kwenda nyumbani.Muda huu mama Elly aliongozana na mwanae hadi kwenye duka ambalo Steve alikuwa akiuza, kwanza kabisa alimuuliza mwanae,“Katika maisha yako, mfano ukawa tajiri na mali nyingi ni nani wa kwanza utakayemfikiria?”“Ni wewe mama yangu, hakuna mtu mwingine yoyote zaidi yako”“Mfano watu wakinibeza na kunichukia na kunitenga, je wewe utanichukuliaje?”“Mama, nilishakwambia nab ado nakwambia hata dunia nzima ikukatae, hata dunia nzima ikikutenga bado mimi nitakuwa sambamba na wewe, nakupenda sana mama yangu yani wewe ndio maisha yangu”“Nakupenda pia mwanangu”Basi mama Elly alimkumbatia mwanae na kuingia nae kwenye lile duka, kiukweli Steve alipowaona hata alikumbuka ushauri wa bosi wake tu kuwa Jumapili awe anapumzika, yani kilichomfanya leo kufungua duka ndio kitakachompambanisha na huyu mwanamke, kisha alimuuliza,“Na wewe umefuata nini tena?”“Hivi huwa huelewi nilichofuata hapa? Hapa nimefuata mali za mwanangu”“Mali za mwanao kivipi? Unajua sikuelewi, mwanao huyo mwenye hizi mali ni mwanao gani? Huwa unamsema Erick au huyu Elly?”“Kwani wewe unahisi ni mwanangu gani?”“Sijui, wewe ndiye unayejua maana ulinitambulisha kuwa huyu ndio mtoto wako na mara ukasema Erick ni mtoto wako, vipi mwenzetu ulizaa mapacha?”Elly naye alimuuliza mama yake,“Kwani mama una mtoto mwingine zaidi yangu?”“Achana na huyu mwanangu, ila hili duka ni lako. Hii ni mali yako”“Kivipi mama?”“Mwanangu si nilikwambia kuwa mimi ni mama yako na nitafanya kila kitu kukufurahisha katika maisha yako, na katika jitihada zangu basi kuna hili duka. Natumaini umelipenda, hili duka ni mali yako mwanangu, nishakuja hapa na wewe mara nyingi tu hata nashangaa kwanini unashangaa jambo hili, nataka ujue kuwa hili duka ni mali yako na baada ya mwezi huu nitakukabidhi kila kitu kinachohusiana na hili duka, yani hadi huyu mfanyakazi atakuwa chini yako”Kisha Sia alimshika mkono Elly na kuondoka naye, huku Steve akibaki anamuangalia tu na kumshangaa.Leo wakina Erick walivyofika nyumbani tu, kuna mgeni alienda kumtembelea Erick kama ambavyo alimuahidi na mgeni huyu alikuwa ni Sarah ambapo Vaileth alimkaribisha vizuri tu na moja kwa moja alisema kuwa anamuhitaji Erick, naye Erick alifika kusalimiana nae ila hata Erick hakuamini kama Sarah angeenda kweli kumtembelea kama ambavyo alikuwa akisema,“Kheee umekuja kweli Sarah”“Ndio, ulidhani nadanganya? Haya ahadi yangu iko pale pale, nimekuja kunuona mtoto na nimebeba zawadi za mtoto”“Haya karibu”Basi moja kwa moja Erick alienda kumuita mama yake na kumueleza juu ya ujio wa rafiki yake ambaye ameenda kumuona mtoto,“Kheee mwanangu, rafiki yako yupi huyo?”“Anaitwa Sarah!”“Kumbe ni msichana! Haya mwambie aje”Basi Erick akaenda kumkaribisha Sarah, ila kiukweli mama Angel alipomuona Sarah alijikuta akimpenda sana kwani Sarah alionekana ni binti mchangamfu, muongeaji na mcheshi sana, basi akamkaribisha vizuri sana na moja kwa moja Sarah alimkabidhi zawadi za mtoto,“Ooooh wow, nimefurahi sana unaonekana ni mcheshi sana”Sarah alikuwa akitabasamu tu kwani ndio kitu alichokipenda zaidi na kuongea kwahiyo alisema,“Napenda sana watoto, wakati Erick kaniambia amepata mdogo wake nikatamani sana kuja kumuona maana mimi kwa mama yangu nimezaliwa peke yangu, napenda sana watoto. Anaitwa nani?”“Anaitwa Ester”“Oooh jina zuri sana jamani, na mtoto mwenyewe ni mzuri kwakweli nimempenda”“Hata mimi nimekupenda sana”Basi mama Angel alitumia muda mrefu sana kuzungumza na Sarah maana alijikuta kampenda binti huyu, yani alikuwa akihisi raha tu kuongea nae kwa muda wote.Jioni ilipofika Sarah aliaga, na Erick nae aliomba ruhusa ili aweze kumsindikiza Sarah ambapo mama yake alikubali Erick amsindikize.Mama Angel alibaki mwenyewe huku akitabasamu tu kwa maongezi ya Sarah, alikuja bibi na kuanza kuongea na mwanae,“Katika wageni wote wanaokujaga hapa nyumbani nahisi huyu amekukosha”“Yani mama, huyu Sarah yani huwezi amini nimetamani hata angekuwa mwanangu pia, mtoto anaongea vizuri huyu, yani maneno yake yana kituo na yanaeleweka halafu nio mcheshi sana”“Haya usijali lakini maana ndio mkwe wako”“Kheee mkwe kivipi?”“Unadhani huo ukaribu na Erick ni wa kawaida?”“Hamna mama, Erick hana mambo hayo ujue, ila hata hivyo hapo badae nikipata mkwe kama Sarah nitafurahi sana nimempenda sana, mama hebu nivutie huo mfuko nione kamletea mtoto zawadi gani!”Basi mama yake alimvutia mfuko ambao alienda nao Sarah, yani mama Angel alifungua ule mfuko na kujaa tabasamu katika sura yake baada ya kuona zawadi ya Sarah kwa mtoto kisha akamwambia mama yake,“Mama, ona alichokileta huyu Sarah”“Kheee kaleta mdoli jamani!”“Tena mdoli wa pinki na nyeupe, hivi huyu mtoto kajuaje kama napenda wadoli na ninaipenda hii rangi!”“Si nimekwambia mkwe wako huyo! Ila mdori mzuri na unavyopendaga wadori nahisi umefurahi sana. Ila siku hizi naona hupendi kama zamani”“Ni kweli ila huyu Sarah atakuwa amerudisha upendo wangu kwa wadori unajua watoto wangu wote hakuna anayependa wadori hata mmoja, huyo Erica ndio kwanza yeye ni karata basi karata na yeye, huyo Angel anachopenda naye anajua mwenyewe. Kwakweli huyu Sarah karudisha tabasamu usoni mwangu”Mama Angel alionekana kumfurahia sana Sarah hata mama yake alimuelewa kwa ile hali aliyokuwa nayo ya kumfurahia Sarah, yani katoa hadi ruhusa kwa Erick kuwa ampeleke Sarah sababu kampenda sana.Basi Erick akiwa kwenye gari wakati anampeleka Sarah kituoni ila akamwambia kuwa atampeleka hadi kwao na kumfanya Sarah afurahi zaidi kwani aliona sasa safari yake itakuwa vizuri zaidi,“Oooh Erick jamani, leo nitaota kwakweli. Ila kwenu mna upendo sana haswaa mama yako yani nimempenda bure, oooh sijawahi kufikiria kama ningemkuta mama mwenye upendo kiasi hiki yani mama ambaye nimetumia muda mrefu sana kuzungumza nae, kwakweli Erick nimempenda sana mama yako”“Hata yeye anaonekana amekupenda sana, huwa sio kawaida ya mama kuongea na rafiki zetu kwa kiasi kile, kwahiyo wewe utakuwa umeugusa moyo wake”Basi Sarah alifurahi sana kwani kile ndio kitu alichokuwa anakitaka, alitaka kupendwa na familia ya Erick maana alishampenda Erick kwahiyo alitaka familia ya Erick imkubali pia, basi alimuuliza swali lingine,“Ila mbona dada zako sikuwaona?”“Aaaah wanapenda sana kulala ndiomana hujawaona, ila usijali kuna siku ukija utawaona tu”“Ila najua watakuwa na upendo kama mama yenu, kuna yule mmoja nilimuona kwa mbali siku ile niliyowakuta na yule mama pale getini kwenu ila kwenu inaonekana mna upendo sana, sema natamani pia kumfahamu huyo pacha wako”“Usijali utamfahamu tu”“Halafu nataka awe rafiki yangu, safari ijayo nikija nitamletea zawadi yeye kwani nataka niwe nae karibu zaidi”“Mmmh yani wewe Sarah, sikuwezi kwakweli unajitambua mwenyewe tu”Basi mpaka walifika nyumbani kwakina Sarah ambapo naye Sarah alimuomba Erick hata akamsalimie mama yake tu kwani alijua na mama yake atafurahi sana kwa salamu ya Erick, ilibidi Erick nae ashuke na kwenda kumsalimia mama yake Sarah, basi walimkuta tu akiendelea na mambo yake mengine ndani ya nyumba yake, ila Sarah alipofika na kumtambulisha Erick kwa mama yake alishangaa kuona mama yake akifurahi sana ila alitoa machozi kwenye macho yake kitu ambacho hata Sarah hakuelewa ni kwanini mama yake alionekana kufurahi ila alilia, basi yule mama moja kwa moja alienda kumkumbatia Erick na alimkumbatia kwa muda mrefu sana huku akitoa machozi, baada ya hapo ndio alimkaribisha,“Karibu sana Erick, karibu nyumbani kwangu”Sarah alimuuliza mama yake,“Mama, mbona inaonekana una furaha halafu unalia?”“Sarah! Huwezi jua mwanangu, ila hili jina limenikumbusha mbali sana, yani mbali sana kuna siku nitakueleza vizuri. Karibu sana Erick nyumbani kwangu, karibu sana mwanangu. Muda wowote utakaojisikia kufika basi unakaribishwa”Yani Sarah alimshangaa sana mama yake, yani jina tu ndio limtoe machozi, kwakweli Sarah hakumuelewa kabisa mama yake kwa hilo.Basi Erick alipomaliza kusalimia alikuwa akiaga ila yule mama hakukubali Erick aondoke bila ya kula chochote kwenye nyumba yake na kumwambia,“Naomba, ule japo kidogo tu ili utie baraka kwenye nyumba yangu. Nimekupenda bure kijana”Muda ule yule mama alishandaa chakula na kumfanya hata Sarah aanze kumlazimisha Erick kula kidogo ambapo Erick alikaa na kula kidogo tu kisha aliaga tena na kuondoka, basi Sarah na mama yake walimsindikiza hadi nje kwenye gari yake huku wakimuaga mara mbili mbili basi Erick alipanda zake kwenye gari na kuondoka zake ila hata yeye hakuelewa ni kwanini yule mama alionekana kafurahi ila alikuwa akitoa machozi kwa wakati mmoja, na kwanini alimkumbatia kwa muda mrefu sana, kwakweli Erick hakuelewa kabisa.Siku hii Erick alifika nyumbani kwao akiwa ameshiba tayari kwahiyo hakuweza kula tena na mama yake alimuuliza swali moja tu,“Umemfikisha Saraha salama”“Ndio mama, na mama yake amefurahi sana”“Ooooh sawa mwanangu”Basi Erick alienda chumbani kwake ila Erica alijiuliza sana kuhusu huyo Sarah ni nani hadi mama yake amuulizie vile, muda wa kulala ni moja kwa moja Erica alienda chumbani kwa Erick na kumuuliza,“Huyo Sarah ndio nani?”“Ni rafiki yang utu wa shule, leo alikuja kumuona mama na mtoto”“Mmmh! Jamani mbona haya mambo sijawahi kuyasikia kabla, kwani nini kinaendelea kati yako na huyo Sarah?”“Hakuna kitu, yule ni rafiki yang utu yani mimi na yeye tumezoeana kawaida kabisa yani ile kirafiki, usinifikirie vibaya”“Halafu inakuwaje mama aseme ulimfikisha salama? Kwahiyo ulimpeleka hadi kwao? Jamani huyo Sarah ni nani? Natamani sana kumfahamu”“Usijali utamfahamu tu”Basi Erica alitoka zake chumbani kwa kaka yake, na kumfanya Erick achukue simu yake ambayo alikuta namba za Sarah zimempigia sana, ikabidi nay eye ampigie,“Nilikuwa nauliza Erick umefika?”“Ndio nishafika, ila na mimi nilikuwa na swali”“Niulize tu”“Mbona mama yako alikuwa akilia?”“Hata mimi najiuliza sijui kwanini, ila usijali nitampeleleza na ataniambia ukweli tu.”“Sawa, ila mama yako ni mtu mzuri sana hata mimi nimekupenda”“Kama yeye alivyokupenda ujue, yani mama kakupenda sana Erick. Basi kesho kama kawaida kwenye siti yetu ile”“Sawa, usiku mwema”Erick aliagana na Sarah kwani hakuwa na maongezi naye sana wala nini.Kulipokucha kama kawaida waliondoka wote na kwenda kwenye shughuli zao hata baba Angel aliondoka pia ila baada ya muda kidogo alirudi kwa lengo la kuwachukua Angel na Junior kwenda nao huko kwenye chuo cha yule madam.Basi aliondoka nao na kuwasiliana na yule madam hadi kwenye kile chuo, ambapo Angel na Junior walipelekwa kwanza kuzoea mazingira, huku madam akiongea na baba Angel,“Kwanza madam samahani sana kwa kukupigia simu usiku”“Unadhani kuna tatizo basi! Mimi mwenyewe bachela, sijaolewa wala nini”“Kheee hujaolewa madam! Nilijua wewe ni mke wa mtu?”“Hapana sijaolewa, wanaume wenyewe nyie hamueleweki”“Aaaah jamani, wengine tunaeleweka”“Sema wewe unaeleweka sio wengine, usione hadi leo nipo hivi nishapitia milima na mabonde ya mahusiano hadi nilikuwa chizi mimi ila kwasasa nimechoka nikasema acha niishi mwenyewe, hata usijali wewe nitafute muda wowote tu mimi napatikana. Ukiona nipo hotelini au kwenye mgahawa basi ujue nimeenda mwenyewe tu kushangaa shangaa na kupoteza muda maana sina hata wa kunitoa matembezi”Kuna muda baba Angel alimuangalia huyu madam na kumuhurumia kwani alikuwa ni mzuri tu hata alishangaa jinsi anavyolalamika kuwa mapenzi yamemtenda sana, ila bado alimpa moyo,“Ila usikate tamaa madam maana mume wako yupo mahali anaandaliwa kwahiyo usijali”“Jamani huyo mume anaandaliwa hadi lini? Na mimi mwanadamu ujue na nina mahitaji yangu muhimu ya kimwili, sasa huyo mume wanaandaliwa tu, watu hadi tutakufa na utamu wetu”Baba Angel alicheka ila aliamua kubadili stori kwani aliona stori zile zinaweza kupelekea katika mambo mengine, kwahiyo aliona ni vyema kwa muda huo kubadili stori tu,“Madam, hapa nimeleta hao vijana wangu wawili ila nahitaji uangalifu wako mkubwa sana kwa hao watoto si unajua dunia imeharibika hii”“Usijali kitu, walimu hapa wapo vizuri sana, muda mwingi mimi nashinda kule shuleni kwakina Erick maana ndio ninakofundisha halafu mimi ndio mwalimu wa taaluma”“Oooh upo vizuri sana madam, nimefurahi sana”“Ila hujaniambia kuwa wewe napaswa muda gani kukupigia simu na muda gani sipaswi kukupigia simu!”Baba Angel alicheka kidogo na kumwambia,“Kwa matatizo ya watoto hakuna tatizo nipigie tu muda wowote ila sio usiku maana nakuwa nimelala halafu mimi nina mke”“Ooooh sawa, hakuna tatizo”Basi baba Angel muda huu na yule madam walikuwa wamesimama nje ya gari kwani baba Angel alikuwa akiwasubiria watoto wake waonyeshwe kidogo mazingira na aondoke nao kwa siku hiyo halafu kesho ndio waende kuanza kwenda shule, basi akiwa anaongea na yule madam alishangaa sana kwa muda huo kutokea Sia, ambaye alipowaona alicheka sana na kutikisa kichwa halafu akasema,“Unajua Erick hiyo tabia nilijua umuiacha, kumbe bado unayo! Nicheke mie, mbona Erica ana kazi sana jamani!”Kwakweli baba Angel alitamani hata kumnasa vibao huyu mwanamke. Basi baba Angel muda huu na yule madam walikuwa wamesimama nje ya gari kwani baba Angel alikuwa akiwasubiria watoto wake waonyeshwe kidogo mazingira na aondoke nao kwa siku hiyo halafu kesho ndio waende kuanza kwenda shule, basi akiwa anaongea na yule madam alishangaa sana kwa muda huo kutokea Sia, ambaye alipowaona alicheka sana na kutikisa kichwa halafu akasema,“Unajua Erick hiyo tabia nilijua umeiacha, kumbe bado unayo! Nicheke mie, mbona Erica ana kazi sana jamani!”Kwakweli baba Angel alitamani hata kumnasa vibao huyu mwanamke.Hadi Oliva aliona jinsi sura ya baba Angel ilivyobadilika hadi akamuuliza,“Kwani unamfahamu huyu mwanamke?”Sia nae akadakia na kusema,“Asinifahamu kwanini? Mimi ndio mkewe wa kwanza kama ulikuwa hujui”Oliva alizidi kushangaa halafu baba Angel pia alizidi kuwa na hasira kupita maelezo, mara Junior na Angel walifika pale maana walishaelekezwa na kesho yake ndio walikuwa wanatakiwa kuanza, basi baba Angel akaona ni vyema aondoke na watoto wale tu maana la sivyo ataweza kuanza kuharibiana siku zizuri na yule mwanamke, ikabidi wakina Angel nao waingie kwenye gari hata hawakuelewa ila baba yao aliondoka gari sema kitu pekee walichojiuliza ni kuhusu yule mwanamke aliyekuwepo chini kweani walishawahi kumuona wakati gari imegoma halafu Erick alikuwa na hasira nae sana, na leo ni baba yao halafu pia Angel alishawahi kumshuhudia huyu mwanamke akinaswa kibao na Samir kwahiyo kuna mambo hakuelewa kabisa.Kwakweli hata madam Oliva alibaki akishangaa tu kwani baba Angel alionekana kuchukia sana na hakuongea kitu kingine chochote zaidi ya kuwaambia wanae wapande kwenye gari na kuondoka nae, ila hapo aliposimama madam Oliva basi nae Sia aliendelea kusimama na kumfanya Oliva amuulize kwa makini zaidi,“Unajua dada sijakuelewa vizuri, ulikuwa mke wa yule baba kivipi?”“Sikiliza nikwambie, mimi ndiye nilikuwa mke wa yule, unajua yule anaitwa Erick, kama uliwahi kumsikia mwanae mmoja aitwaye Erick, Erick basi ndio mtoto ambaye nimezaa nae ila mtoto yule haujui ukweli kuwa mimi ndiye mama yake mzazi na ananikataa hadi kecho”“Kheee makubwa, huyo Erick ni mwanafunzi wangu”“Kumbe!! Anasoma shule gani kwasasa?”Yule madam akamtajia bila kujua hilo ni jambo baya kwani huyu mama anamfatilia sana Erick, ila yeye alimtajia kwa uzuri tu, kisha Sia akaendelea kumwambia,“Unajua wewe ni mwanamke nadhani unaweza ukanielewa kidogo tu juu ya haya nitakayokueleza, mimi na huyu Erick tumeishi kama mke na mume na mambo mengi sana tumeshauriana. Kwetu walimfahamu wote na kwao walinifahamu yani hakuna ndugu yake asiye nifahamu na hakuna ndugu yetu asiyemfahamu ila Erick aliamua kuniacha gafla na kuwa na yule mke aliyemuoa, kwakweli unaweza kujua ni jinsi gani niliumia, mimi kweli wa kuachwa naye? Nimemvumilia Erick mimi kwa shida na raha, nikiamini kuna siku nitakula nae raha za maisha, nilikuwa namfumania mimi na wanawake mara zote namsamehe, Erick alikuwa ni mlevi hakuna mfano, anaenda huko analewa hadi anajitapikia ila mimi naenda kurua nguo zote alizozitapikia, kusaisha chumba chake, nampikia supu yani kila cha kumfanya arudi katika hali ya kawaida, hebu fikiria nimetumia muda wangu wa kiasi gani kwaajili ya penzi lake? Naomba tu ufikirie na useme kama nimekosea kukwambia ukweli hapa”“Ila mbona umesema Erica ana kazi?”“Nimehisi anakutongoza pia, maana huyu mtu kwa kutongoza wanawake ndio zake, huyo Erica ndio mke wake, ila kiukweli nakwambia Erica bado hamjui Erick, kwakweli Erica hamjui Erick ninayemjua mimi ila ipo siku huyu Erica atamjui Erick ni mtu wa aina gani? Kama alikuwa akiona wenzie wanateseka kwenye ndoa basin a yake ipo njiani kuteseka, mimi nimekwambia ukweli ili kama una mpango wa kumkubali ujue jambo hilo. Nimemaliza”Basi Sia aliondoka na kumuacha Oliva akimshangaa hadi mwisho wa safari.Basi Oliva alimuangalia sana Sia hadi alipoishia kisha alianza kujiuliza mwenyewe,“Mwanaume kamfanyia vitu vya ajabu, alikuwa mlevi, alikuwa na wanawake anamfumania nao ila bado alimsamehe, sasa mwanaume kaoa mwanamke mwingine ila bado anamzungumzia inaonyesha kuwa bado anampenda tena sana tu, mmmh huyu Erick ana kitu gani? Lazima kuna kitu cha ziada anacho sidhani kama ni pesa tu ila kuna kitu huyu Erick anacho kwanini huyu mama aongee kama mtu aliyechanganyikiwa ilihali anaonekana kuwa na akili timamu? Lazima kuna kitu cha ziada ambacho Erick anacho, natamani kukifahamu, sitaki kufahamu ukweli kuhusu mtoto wao sijui watoto wao watajijua wenyewe ila nataka kufahamu kuhusu huyu baba ana kitu gani cha ziada ambacho wanaume wengine wamekosa? Nitajua tu, mimi ndio Oliva bhana”Basi yule madam alienda zake kwenye ofisi zake moja kwa moja kuendelea na mambo yake.Baba Angel moja kwa moja aliwapeleka Angel na Junior nyumbani na baada ya kuswashusha tu, yeye aliondoka tena kwakweli Angel na Junior hata hawakuelewa kwanini, wakaingia ndani ambapo walipoingia tu Angel alidakwa na mama yake na kuanza kuulizwa maswali,“Mmerudi na nani sasa?”“Baba ndio katurudisha”“Mbona hata hajaingia ndani?”“Sijui mama kwanini ila katushusha tu na kuondoka zake”“Jamani baba Angel mara nyingine sijui vipi, ngoja nitampigia simu. Ila chuo hiko kizuri alichowapeleka? Mmekipenda?”“Eeeeh ni pazuri mama, waliokuwepo wanapasifia halafu hata mazingira yake ni mazuri”“Oooh nafurahi kusikia hivyo”Kisha mama Angel alirudi ndani kwa mtoto maana alikuwa analia, basi alimchukua mwanae na kuanza kumnyonyesha huku akiongea na mama yake,“Ila mama, uzazi wa sasa nimeufurahia sana, kumbe kuzaa mtoto mmoja kuna raha yake. Mapacha nao raha yao wakikuwa jamani, yani wakiwa wadogo hadi unapata kizunguzungu”Basi mama yake akacheka na kumwambia,“Ndio kuna raha sana ya kuwa na mtoto mmoja, ila kipindi kile una mapacha kuna muda nilikuwa nakuona unatamani kulia, ukinyonyesha huku na huyu anataka halafu kuna muda wote wawili wanataka ziwa moja ndio pale unapata kichaa, wakianza kutambaa ndio wanaanza mabalaa zaidi”“Oooh mama, yani nilikuwa Napata kiwewe, ila Erick wakati mdogo alikuwa mtundu sana hadi nilikuwa nahisi uchizi, unamkataza hili anashika lile, unamkataza lile anarudi kwenye hili huku dada yake anafanya uharibifu tu. Hivi mtu umelea watoto wako kwa shida hivyo halafu mtu anatokea kirahisi tu anakwambia hawa watoto sio wako”“Mmmmh kivipi mwanangu? Yani umlee Ester hapo halafu mtu aseme sio mtoto wako?”“Huwa inatokea hiyo mama, hujawahi kusikia? Tuachane na habari hizo, hivi mama swali hili nimewahi kukuuliza zamani nab ado nitaendelea kukuuliza, hivi Derick ni kweli alikuwa mtoto wa baba?”“Ndio, kwanini unauliza hivyo?”“Jamani, ukoo mzima hatufanani na matendo ya Derick”“Huwezi jua labda katoa kwenye ukoo wa mama yake huko ila ndio hivyo Derick ni ndugu yenu, tena mlifatana tu kuzaliwa wewe na Derick, yani usikatae katika ukoo hamuwezi wote mkafanana tabia lazima kuna mmoja anakuwa na tabia zake na mambo yake ya ajabu ajabu. Ila bado siri ya mtoto anayo mama yani mama ndio anajua mtoto ni wa nani, ila nimejaribu kumuelewa mama Derick maana hadi mwisho anadai kuwa yule mtoto ni wa baba yenu kwahiyo usikatae ni ndugu yako”“Mmmmh sawa mama, ila kuna vitu nilikuwa na mashaka sana juu ya Derick”“Kama vitu gani? Ila kuna kitu nahisi kipo kati yako na Derick ila hujawahi kuniambia mama yako sababu ya usiri wako, kuna kitu hata mimi nahisi, nakumbuka vizuri siku umerudi sijui mlienda kwenye madawa ya kienyeji na dada yako, nakumbuka vizuri ingawa kuna mambo sikuelewa. Erica, kwakweli wewe umenificha mengi sana mama yako, ndiomana kuna muda huwa nakwambia kuwa usimshangae sana mwanao Angel, maana kuna mambo kachukua kwako kama kuwa msiri sana, ila usiri wenu hauna maana, mimi nampenda sana huyu Erica mdogo jamani mtoto hana siri huyu na atafanya tutambue mambo mengi sana. Haya nidokezee mwanangu leo ya kuhusu wewe na Derick, unajua huwa nasikia juu juu sijui ulitoa mimba yake sijui nini na nini kiukweli huwa sielewi”“Mmmmh mama, naomba tuachane na hayo na tujadiliane vitu vya msingi, yalishapita hayo”Mama Angel hakupenda kukumbusha mambo ya zamani ambayo yalipita na yalimuumiza sana kwahiyo hakupenda kuyakumbushia.Muda huu baba Angel moja kwa moja alienda nyumbani kwa dada yake, na kweli alimkuta dada yake na kuanza kuongea nae, yani kilichompeleka kwa dada yake lilikuwa ni swala zima la Sia, kwahiyo alienda kwa dada yake ili ajue cha kufanya,“Karibu sana Erick, naona leo umenikumbuka”“Si oleo tu, mimi huwa nakukumbuka siku zote, ila leo nimekuja sababu ya matatizo kidogo”“Yapi hayo?”“Kiukweli kuna huyu mwanamke aitwaye Sia, yani sijajua cha kufanya nae au ni kitu gani anahitaji kutoka kwangu unajua sasa kaja kwa kasi ya ajabu na pia naona kama atavuruga amani ya nyumba yangu na anaweza kumvuruga mke wangu pia, kama unavyomjua wifi yako ni mgumu sana kuchuja mambo yani yeye anaweza kuchukulia mambo kama anavyoambiwa, kwakweli huyu Sia ananiumiza kichwa sana”“Kivipi kaka, unajua sikuelewi, huyu Sia anakuumiza vipi kichwa?”Basi baba Angel aliamua kumueleza tu kwa kifupi matukio ambayo Sia anayafanya, maana kuna mengine Tumaini hakuyaelewa, basi alimueleza pia la kuhusu Erick na pia kuhusu duka na jinsi ambavyo alimkuta siku hiyo,“Ni wazi kuwa huyu mwanamke anafatilia kila njia ninayopita kwenye maisha yangu, nahitaji kujua anataka kitu gani kwangu? Kwanini ananifanyia hivi, kweli kabisa nisiishi kwa amani sababu yake jamani eeeh!!”“Pole mdogo wangu, pole sana hata sikutambua hayo! Hivi huyu Sia ana matatizo gani jamani, ni kuchanganyikiwa au kitu gani na kama ni kuchanganyikiwa basi kitu gani kilichomchanganya hiko? Yani kwanini awe hivyo jamani, mbona Sia hakuwa hivyo! Loh!! Amenisikitisha sana kwakweli, ila kaka nakuahidi kuwa nitafanyia kazi hilo swala maana nina mawasiliano yake kwahiyo usijali mdogo wangu”“Nitashukuru kwa hilo, yani huyu kiumbe ananikosesha amani ujue, sina amani nikimuona wala sina furaha, mwambie aniache na familia yangu nifurahie kama siku zote. Nimeishi na mke wangu na watoto wangu kwa upendo sana siku zote wala sikuwahi kupatwa na maswahibu yake, nakuomba sana dada yangu nisaidie kwa hilo”“Usijali”Basi baba Angel aliaga na kuondoka zake, ila muda huu alimua kupitia dukani ili amchukulie mke wake zawadi ingawa hakusema ni zawadi, aliona duka moja la nguo na vitu vya urembo kwa wanawake, aliamua kuingia kwenye duka hilo na kukutana na mwanamke na mwanaume wakihusika kuuza duka hilo, basi aliwasalimia pale na kuanza kuongea ongea nao kama ushauri wa zawadi ya kumpelekea mke wake, basi yule mwanaume akamshauri,“Mpelekee gauni”“Kheee gauni?”“Ndio, tena hilo hapo ni zuri sana natumai atalifurahia”Basi mwanamke akadakia,“Unaonyesha tu hilo hapo unajua mke walivyo jamani! Gauni litamtosha kweli hili, eti kaka mkeo yukoje kwani?”“Mmmh mwili wake hauna tofauti na wako ila wewe umemzidi kidogo unene”“Oooh basi hili gauni alilokuonyesha baba Emma litamtosha”“Basi nitoleeni”Baba Emma alilitoa lile gauni, kweli lilikuwa ni zuri sana na linavutia machoni ila tu baba Angel hakujua kama kweli mkewe angelipenda hilo gauni, basi alipolilipia yule mwanaume akamwambia mwanamke,“Mama Emma, mtolee risiti basi”Ndipo baba Angel alihisi kama wale ni mke na mume, basi aliuliza,“Kumbe nyie ni mke na mume?”“Ndio, sisi ni wanandoa”“Oooh inapendeza sana kufanya kazi pamoja, nimeipenda hii”Na wao walicheka tu kwa jinsi yeye alivyofurahi, basi baba Angel alichukua ule mzigo wake na kuwaambia,“Jamani nampelekea mke wangu, akiipenda hakika basi hili ndio litakuwa duka langu kumchukulia zawadi kwasasa”Walifurahi sana na baba Emma alimkaribisha sana pale dukani na baba Angel aliondoka muda ule kiukweli aliondoka na tabasamu ingawa siku yake hiyo iliharibiwa na Sia ila kwa muda huo alijikuta akiwa na furaha na moja kwa moja kuelekea nyumbani kwake.Baba Angel alipofika tu nyumbani, moja kwa moja alienda chumbani ambapo mke wake nae alienda na swali la kwanza alimuuliza,“Kheee na leo ulienda wapi yani ile kushusha mizigo tu na kuondoka, ulienda wapi?”“Jamani mke wangu! Unataka kunilaumu sasa, unadhani mimi niende wapi? Wivu ushakuanza hivyo”“Wivu lazima kwa mtu ninayekupenda kama wewe, nisipokuonea wewe wivu nimuonee nani tena!”“Haya, ni hivi niliporudi na wakina Angel niliitwa ofisini ila nilipotoka kidogo tu nikakumbuka kuwa sijakuchukulia zawadi mke wangu kwa siku za hivi karibuni kwahiyo nikaamua kupita kwenye duka moja hivi na kukuchukulia zawadi hii”Alimpa mama Angel ule mzigo ambapo alifungua kwakweli alionekana kufurahi sana na kujaribisha muda ule ule, na alipomaliza alimsogelea mume wake na kumkumbatia huku akimwambia,“Jamani jamani, nimeipenda hii zawadi sijui nikwambiaje? Unajua nimekaa nikawaza kuhusu gauni la mtindo huu hata nisijue pa kulipata, jamani mume wangu umejuaje? Kwakweli nimefurahi sana, kweli Erick unanifaa”Baba Angel nae alifurahi kuona mkewe kafurahia ile zawadi maana ndio kitu alichokuwa akikihitaji kumuona mkewe akifurahia zawadi aliyompelekea.“Asante sana mume wangu, oooh kwa bahati mbaya chakula cha leo kimeshapikwa na usiku tayari ila niambie kesho unahitaji kula chakula gani?”“Yani wewe mke wangu kwa kutenda mambo kwa matukio sikuwezi, haya nahitaji pilau”“Sawa, nitapika mwenyewe hakuna tatizo”“Ila mke wangu si bado upo kwenye uzazi jamani! Usitake kuniletea makubwa na mama mkwe, cha kufanya mwambie mama apike”Walianza kucheka kwa pamoja na siku hiyo ikawa ni furaha sana kwa upande wao.Leo Angel alikuwa akiwasiliana na Samir kuhusu mambo mbalimbali ila kuna muda Samir alimtafuta Angel na kumwambia,“Yani Angel kuna kazi kidogo nafanya ila nahitaji kuongea nawe kwa muda kidogo ili tupange mambo yetu”“Sawa hakuna shida, kwahiyo utanitafuta muda gani?”“Kwenye saa sita usiku basi nitakupigia ili tuongee Angel, kumbuka nakupenda sana”Basi Samir alikata simu na muda huo ilikuwa ni saa tatu usiku, na sio kawaida ya Samir kusema kuwa anakazi kwa muda huo basi Angel alijiuliza mno kuwa itakuwa ni kazi gani kwa muda huo ila hakupata jibu kabisa, baada ya nusu saa alipigiwa simu na Mussa na kuanza kuongea nayo ila kwa sauti ndogo sana ili asisikike kabisa hata na mtu anayepita nje ya chumba chake,“Oooh Angel unaongea sauti tamu sana, kwakweli una sauti nzuri sijapata sikia duniani”“Mmmmh jamani Mussa!”“Ndio hivyo Angel ila mbona siku hizi mara nyingi hupokei simu zangu wala jumbe zangu huzijibu?”“Unajua nini, kiukweli mimi nina mahusiano na Samir, na siku ile hajapenda kabisa na kasema nisiwasiliane tena na wewe”Mussa akacheka kidogo na kusema,“Hivi Angel, huyo Samir unamfahamu vizuri wewe! Mimi na Samir ni ndugu siwezi kumsingizia kwa chochote ila Samir hakufai kabisa”“Kwanini?”“Samir ni muhuni sana Angel, yani Samir sidhani kama kuna mwanamke huwa anaacha kumpitia, sikai nyumba moja na Samir ila namfahamu alivyo, haya leo umewasiliana nae?”“Ndio ila kasema kuna kazi anafanya muda huu na atanitafuta saa sita”“Oooh pole sana Angel, mwenzio Samir yupo na mwanamke muda huu. Nimemshuhudia kwa macho yangu maana leo nipo kwao, siku ukifika kwakina Samir utaelewa ni maisha gani wanaishi, maisha yao ni ya kujiachia sana kiasi kwamba Samir hufanya anachojisikia yeye, pole Angel muda huu Samir yupo na mwanamke ndiomana kasema atakutafuta saa sita”“Jamani kumbe Samir ndio muongo hivyo!! Basi inatosha Mussa naomba nilale tu kwa muda huu”Yani Angel alijikuta amechukia sana, hivyo aliamua kuzima simu kabisa na kulala tu kwani alijikuta kuwa na hasira.Yani toka siku ambayo Vaileth alibambwa na Erica, alijikuta akikosa amani kabisa kwenye moyo wake, hivyo siku hiyo karibia na muda wa kulala aliamua kwenda chumbani kwa Erica ili kuongea nae.Alimkuta Erica akiwa ananyoosha sare zake za shule,“Kheee mdogo wangu Erica leo umechelewa kunyoosha nguo?”“Nimechelewa kweli, ila yote hii ni uvivu, yani leo nimetoka shule na kuona uvivu kabisa, nikajikuta nimelala kwa muda mrefu”“Ndiomana sikukuona na wenzio, nikusaidie basi mdogo wangu”Erica alimpa pasi na Vaileth alianza kunyoosha nguo za Erica, huku Erica akitabasamu tu na kukaa kitandani kwake akiendelea kupanga daftari zake, yani kwa siku hiyo Erica alionekana kujishughulisha sana basi Vaileth alipomaliza kunyoosha nguo za Erica hata Erica nae alionekana kumaliza kupanga daftari zake, basi Vaileth alianza kuongea nae,“Mdogo wangu Erica, kwanza kabisa naomba msamaha kwa kile ulichokikuta chumbani kwangu, hakuna chochote kinachoendelea kati ya mimi na Junior tafadhari usimwambie mama”“Dada sikia, mimi naweza kuwa mtoto mdogo ni kweli bado mdogo ila kuna mengi sana nayatambua na kuyajua kwani siku hizi tunajifunza vitu vingi sana. Sijui ni kitu gani kilichokuwa kinaendelea kati yako na Junior ila ninachojua ni kuwa nilimkuta chooni kwako na pia alikuja kunikataza nisiseme na leo umekuja wewe kunikataza nisiseme”“Sio hivyo mdogo wangu, jaribu kunielewa jamani Erica”“Ila dada mbona nimekuelewa jamani, una wasiwasi wa bure tu ila mimi nishakuelewa sana tu hata usiwe na wasiwasi. Mimi ni mbea kweli ila hilo sijamwambia mama na wala sitomwambia sababu niliyonayo ni moja tu?”“Ipi hiyo mdogo wangu?”“Unajua nakuhurumia sana, kuna siku niliwahi kuona ukimsimulia mama kuhusu maisha ya kwenu kwakweli nilikuonea huruma sana, na mimi sitopenda wewe ufukuzwe kwasababu yangu, ilimradi umeacha ushirikina basi sina tatizo na wewe ila kuna jambo moja tu ngoja nikwambie dada yangu”“Jambo gani hilo?”“Unajua sababu ya baba kumchukua Junior aje kuishi hapa?”“Sijui”“Sawa, najua mambo mengi ya Junior umesikia kwa familia hapa wakiongelea, ila swala la baba kumchukua Junior lilikuja baada ya kumkuta Junior ameingia guest na mwanamke, tena mwanamke mwenyewe alikuwa ni mkubwa kushinda hata mama yake yani mama yetu mkubwa, kwakweli baba alisikitika sana ndiomana alimchukua Junior”Kidogo Vaileth alishtuka na kuona kuwa kutembea na wanawake wakubwa kupita umri wake ni kawaida ya Junior, kwakweli kwa upande mwingine roho ilimuuma kiasi kwamba alishindwa hata kumjibu Erica na kujikuta tu kajiinamia, basi Erica akamuuliza,“Mbona umepooza gafla dada yangu?”“Aaaah hamna kitu”“Basi nikuombe kitu kwa leo dada”“Kitu gani?”“Naomba kwa leo ulale humu chumbani kwangu tafadhari, mimi sitakusemea kwa mama kuhusu lile swala”Vaileth akafikiria ila hakuwa na budi zaidi ya kukubali tu kulala na Erica mule chumbani kwa Erica, yani siku hiyo alilala kwa mawazo sana kwani alijua lazima Junior alikuwa akimngoja chumbani kwake.Mpaka kulivyokucha wakati Erica akijiandaa ndipo na yeye alipoamka na kwenda kuanza kazi zake za siku hiyo.Moja kwa moja Vaileth alienda jikoni na kuanza kufanya kazi halafu kuanza usafi ila alishangaa kumkuta Junior sebleni akisinzia, yani inaonyesha Junior alimtafuta sana usiku wa jana, ila hakuweza kuongea nae kivile kwani muda huo kila mmoja ndani alikuwa kaamka na anajiandaa kwa mambo ya siku hiyo.Basi mama Angel nae alitoka na kumkuta Junior pale sebleni akamshtua,“Kheee Junior, vipi mwanangu leo una nini?”Junior akashtuka pale na kumsalimia mama yake mdogo kisha moja kwa moja kuinuka pale kwenye kochi na kuelekea chumbani kwake, yani alipitiwa na usingizi pale ila lengo kubwa la kukaa pale ni kumuona Vaileth akiingia maana alihisi kuwa Vaileth alikuwa nje ya nyumba hiyo kwa siku hiyo na kumfanya hata yeye aumie sana moyo.Basi mama Angel akiwa pale sebleni kwake, alishangaa kusikia simu ya mezani ikiita na kujiuliza,“Asubuhi yote hii jamani nani tena anapiga?”Moja kwa moja alienda kupokea ile simu na kuongea nayo,“Mbona leo Angel hupatikani, tatizo ni nini?”“Kheee nani wewe?”Simu ile ikakatika na kumfanya mama Angel ajiulize kuwa Angel hapatikani kivipi? Wakati anatambua wazi kuwa mwanae hana simu! Moja kwa moja mama Angel alienda chumbani kwa Angel na kufungua mlango ila alimkuta binti kajiinamia, alipomuinua kichwa aligundua kuwa Angel alikuwa akilia. Simu ile ikakatika na kumfanya mama Angel ajiulize kuwa Angel hapatikani kivipi? Wakati anatambua wazi kuwa mwanae hana simu! Moja kwa moja mama Angel alienda chumbani kwa Angel na kufungua mlango ila alimkuta binti kajiinamia, alipomuinua kichwa aligundua kuwa Angel alikuwa akilia.Ikabidi mama Angel akae pia karibu na mwanae na kumuuliza kwa makini kitu kinachomfanya alie,“Wewe Angel nini kinakuliza mwanangu?”“Mama, kichwa kinaniuma sana”“Jamani Angel yani kichwa kinakuumza ndio unakazana kulia badala ya kuja kuniambia! Haya jiandae hapo nimpigie baba yako akupeleke hospitali”Angel aliinuka na mama yake alikuwa akimsaidia kujiandaa, kiukweli Angel hakuwa akisumbuliwa na kichwa wala nini ila alizna kusumbuliwa na swala zima la mapenzi kwani moyo wake uliuma sana baada ya kusikia kuwa Samir ana mwanamke mwingine na ndiomana alisema kuwa kuna kazi anafanya, basi mama Angel alipomaliza kumsaidia Angel kujiandaa muda huo alienda kumpigia simu baba Angel ambaye alikuwa katoka ili ampeleke Angel hospitali.Basi Angel alibaki ndani kwake na kujiuliza kuwa atapima nini hospitali wakati haumwi kweli? Aliwaza ila mama yake alirudi muda huo na kumwambia baba yake anakuja muda sio mrefu kwahiyo Angel alitoka sebleni kumsubiri.Baada ya muda kidogo tu baba Angel alifika maana huyu baba alikuwa akisikia mtoto anaumwa basi akili yake ilichanganyikana kabisa kabisa, akafika na kumchukua Angel na kuondoka nae kwenda hospitali huku njiani akimuhoji maswali kadhaa,“Hiko kichwa mwanangu kimeanza muda gani?”“Tangia usiku baba ila asubuhi ndio nikaona kama kinazidi, ila muda huu kimepoa”“Ooooh ila hata kama kimepoa, lazima twende hospitali. Ngoja nikupeleke kwa rafiki yangu ni daktari mzuri sana”“Sawa baba, ila kwasasa kichwa kimepoa kabisa”“Hata kama mwanangu, hospitali ni lazima”Ikabidi Angel awe mpole tu maana kayataka mwenyewe na kwajinsi mama yake alivyosema kuwa Angel anaumwa basi baba yake ilimlazimu tu amfikishe hospitali na kumpima kabisa hata kama anasema kuwa amepona.Baba Angel alifika na mwanae hospitali, moja kwa moja alisogea karibu na chumba cha daktari ila alikuwa na mgonjwa na baada ya muda kidogo yule mgonjwa alitoka ila Angel alimuangalia sana yule mgonjwa na kugundua kuwa ni mwanafunzi aliyewahi kusoma nae kwenye ile shule ambayo alihamishwa, basi baba yake aliingia nae mule kwa daktari ambapo baba yake na yule daktari walianza kusalimiana huku baba Angel akimtania daktari,“Mmmh kuna binti mdogo ndio nimepishana nae katoka humu, ila ugonjwa unaonekana kama yale magonjwa yetu ya kipindi kile, vipi na yule?”“Aaaah yule, tushamaliza mchezo”“Khaaa usiniambie bhana, hujaacha tu!!”“Ndio kazi yangu mjini hapa, ila mimi nipo vizuri kaulize wote niliowahi kuwafanyia miaka hiyo kama hawana watoto kwasasa? Mimi nipo vizuri na najiamini”“Ila yule binti ni mdogo?”“Aaaah na mwanaume wake mwenyewe ni mdogo pia, kaja kali alia hapa, ikabidi niwadai kiasi kidogo tu, halafu wanafunzi hawa wajinga sana siku hizi”Kisha daktari akamuangalia Angel na kumwambia,“Soma mama, usitutie aibu wazazi wako, wewe bado mdogo. Mapenzi yalikuwepo, yapo na yataendelea kuwepo, wewe soma. Nadhani umenisikia, haya unasumbuliwa na nini?”“Ni kichwa ila kwasasa kimepona”Basi yule daktari akampima pima vitu baadhi ila aliona ni vyema apate muda kidogo wa kuzungumza na Angel, basi alimuomba baba Angel awapishe kidogo,“Hebu nipishe kidogo na mgonjwa wangu”“Mmmmh usianze mambo yako, mwanao huyo ujue!”“Aaaah na wewe jamaa huniamini!! Ningekuwa sio mtu mzuri basi ningepita na mkeo, yule alikuwa chombo halafu alikuwa rika langu, sasa nianze kuhangaika na watoto wetu jamani! Nitakuwa sina akili basi!”Baba Angel alitoka nje na kumuacha daktari akiongea na Angel pale ofisini,“Eeeeh kichwa kilianzaje kuuma?”“Mmmh ila daktari usimwambie baba”“Simwambii, nieleze tu kichwa kilianzaje kuuma?”“Sijui ni sababu nililia sana, mimi nina mpenzi wangu ila nimeambiwa kuwa ananisaliti”“Angel, wewe ni binti mdogo sana nan i mapema mno kuanza kujihusisha na maswala ya mapenzi, mbona umeanza kulia mapema hivyo! Ukifika miaka thelathini wewe si ndio itakuwa balaa! Mapenzi ni matamu sana ila ukianza kwa muda sahihi ingawa bado kuumizwa kupo pale pale hata uwe na miaka hamsini, ila ninachoongelea hapa mwanangu wewe bado ni mdogo sana mambo ya mapenzi usijihusishe nayo”“Ila nampenda”“Ni kweli unampenda, umesikia anakusaliti, hujashuhudia kumbuka ila umesikia na umeumia hivyo je siku ukishuhudia kwa macho yak ohayo itakuwaje? Haya hilo sio tatizo sana, ila bado unasoma je siku ukibeba mimba ya huyo mtu itakuwaje? Nadhani na wewe umemuona binti aliyetoka humu, nimetoka kumtoa mimba yule, unajua madhara ya kutoa mimba? Unaweza usizae maisha yako tena na unaweza ukapoteza maisha. Kitu cha msingi hapa ninachotaka kukwambia ni kuwa, huyo mwanaume anakuzalisha halafu anakuacha kwenye mataa yani unabaki ukishangaa tu, mbele husongi wala nyuma hurudi, hivi unadhani ukizalishwa nani atakutaka tena!! Hakuna kitu kinachoshusha thamani ya mwanamke kama kuzalia nyumbani tena na mtu asiyeeleweka, kwanza thamani yako inashuka na uzuri wako unapungua, kuna watu wa maana watakuwa wanakuhitaji kwa kipindi hiko ila wakijua kama una mtoto basi watakukimbia. Sasa kwanini uharibu maisha yako kwa starehe ya muda mfupi, kitu gani hupati kwenu Angel? Nina uhakika unapewa kila kitu unachohitaji, sasa huyo mwanaume anataka kukulaghai kwa kitu gani? Kwa mapenzi ya dhati, je baba yako hakupendi? Mama yako hakupendi? Mapenzi yapo na hayaepukiki ila ni bora kuyangoja katika wakati sahihi ila sio sasa Angel. Una umri gani kwanza?”“Miaka kumi na sita”“Ooooh jamani Angel kumi na sita!! Wewe bado mdogo sana Angel, usiwaze mapenzi mwanangu, yatakuumiza tu kwasasa. Zingatia elimu ndio jambo la msingi kwasasa katika maisha yako, wanaume huwa tupo tu”Basi yule daktari alijitahidi pale kumwambia Angel maneno ya busara na kweli kwa kiasi kikubwa sana Angel alielewa na hapo daktari alimuita tu baba Angel ili kuondoka na mwanae, baba Angel aliuliza,“Sasa mwanangu anasumbuliwa na nini?”“Oooh ana msongo wa mawazo huyo anakaa sana nyumbani, hebu uwe unampeleka peleka kidogo kutembea mtoto”“Asante kwa ushauri ndugu yangu”Waliagana pale, kisha baba Angel aliondoka na mwanae ambapo kwenye gari alimuuliza kama siku hiyo anaweza kwenda kusoma kozi ya kompyuta, naye Angel alikubali kwani kiukweli hakuwa na ugonjwa wowote ule ila alijigelesha kwa mama yake kwani hakutaka kumwambia kitu kinachomliza.Baba Angel alifika nyumbani na kumtaka Junior nae ajiandae halafu aliwapeleka chuo ila aliwataka muda wa kurudi wakodi tu usafiri wa kuwarudisha nyumbani maana alikuwa na mambo mengi ya kufanya kwa siku hiyo kwahiyo hakudhani kama ataweza kuwafata.Alipowafikisha chuoni, yeye akaondoka zake.Ila akiwa njiani alimuona Sia akiwa anavuka barabara, alitikisa kichwa tu, alitaka kusimama ila hakuona kama ni vyema kwani Sia mwenyewe akili zake alikuwa akizijua mwenyewe kwahiyo baba Angel hakusimama wala nini ukizingatia hakutaka hata kufahamu kwa muda huo Sia alikuwa akielekea wapi.Sia alikuwa akielekea mahali ambapo alipanga kukutana na Tumaini, na kweli walionana na kuanza kuzungumza mambo mawili matatu yani Tumaini hakutaka kukutana nae nyumbani kwake kwahiyo alimpigia simu na kumtaka kuwa wakutane mahali na ndio huko walipokutana, Sia alianza kumwambia kumbe aliliona gari la baba Angel wakati likipita,“Nimemuona Erick akipita na gari yake, kwakweli amekuwa na roho mbaya sana siku hizi hata kunisalimia loh!”“Tena kilichonifanya nije kuongea na wewe ni kuhusu huyo Erick, kwani Sia wewe una nini? Kitu gani unataka kwa Erick?”“Ngoja nikukumbushe mambo machache Tumaini, unakumbuka kipindi naanza mahusiano na Erick alikuwa na hali gani? Unakumbuka? Najua kuwa unakumbuka vizuri sana, ni wewe uliyekuwa ukinionea huruma sana na kunipa moyo kuwa ipo siku Erick atabadilika tu, nilimtambulisha Erick kwa wazazi wangu wote wawili, baba yangu siku anakufa ananiachia usia kuwa mwanangu Sia usije ukamuacha Erick maana huyu ndio mume wako, mama yangu nae siku anakufa ananiambia hivyo hivyo, nimeteseka mimi kwenye mapenzi ya Erick, nimemfumania mara ngapi na wanawake? Mara nyingi sana ila nikamsamehe na kuendelea na mahusiano yetu, mara ngapi Erick alilewa hadi kuzima kabisa na mimi ndiye nilikuwa napigiwa simu na kuanza kuhangaika kumrudisha nyumbani, mara ngapi Erick alikuwa akijitapikia sababu ya pombe na ni mimi pekee ambaye nilikuwa nikifua zile nguo na kufuta yale matapishi yake, kwanini Erick hakutaka kunirudishia upendo wangu? Kwanini Erick hakunipa kile ninachostahili? Mimi ni mwanadumu, nina moyo na nyama na damu ila kwanini Erick kanifanyia hivi! Sema wewe ungepitia katika hali yangu ungefanyeje?”Tumaini akapumua kidogo na kumwambia,“Ila Sia, hayo mambo si yalishapita?”“Yalipita machobni ndio ila sio kwenye moyo wangu, unajua kila ninapoenda kwenye makaburi ya wazazi wangu nalia kitu gani? Sina furaha ya mapenzi mimi toka kipindi kile, nilitumia muda wangu na maisha yangu yote kwa Erick, ni wanaume wangapi mimi niliwakataa sababu ya Erick? Ni mimba ngapi mimi nilitoa sababu ya Erick, unajua Tumaini wewe ni mtu unayefahamu mengi niliyopitia nikiwa na Erick, basi kaa katika nafasi yangu”“Mmmmh sawa, kwahiyo unataka Erick akufanyie nini?”“Nahitaji Erick anipende na anijali kama mkewe, yeye ndio kaharibu maisha yangu kwa sehemu kubwa sana, sina furaha mimi sababu yake, siku zote Erick yupo katika akili yangu na ninampenda sana”“Mmmmh haya makubwa nashindwa hata kuwaza, halafu nasikia unasumbua kuwa Erick ni mtoto wako? Kivipi ni mtoto wako?”“Hilo tuliache kwanza, ila pale Erick atakapokubali kunifanya mimi kama mkewe basi na mimi nitafunguka kila kitu kuhusu watoto na kuhusu mimi binafsi, kumbuka hata mimi nilikuwa mjamzito kipindi yule Erica akiwa mjamzito, na mimi mimba yangu ilimpenda sana Erick, kiukweli huwezi fikiria ila niliumia sana moyo siku ya ndoa ya Erick na Erica. Kwakweli nitasema nab ado nitasema, Erica hakupaswa kuolewa na Erick maana hajapitia yale ambayo nimepitia mimi, jamani nimeteseka mimi kwa penzi la Erick halafu kirahisi tu mnasema nimuache Erick, hilo halitawezekana labda nife, na hata kama nikifa naamini bado mzimu wangu utaendelea kumsumbua Erick”“Duh! Ila bado sijakuelewa Sia, kwahiyo unataka Erick akuoe uwe mke wa pili?”“Itapendeza zaidi, yani siku nikiolewa na Erick nitafurahi sana”“Mmmmh mbona pagumu hapo, unajua ndoa za Kikristo ni ndoa za mke mmoja na mume mmoja?”“Kwaajili yangu hiyo sharia ipuuzwe kwanza, jamani mimi ninachotaka ni Erick kuwa mume wangu basi!! Sitoacha kumsumbua, katika maisha yote hadi naingia kaburini mpaka siku atakayokubali kuwa mume wangu”“Ila mapenzi hayalazimishwi Sia”“Ni kweli mapenzi hayalazimishwi, ila muulize Erick kati yangu na yeye ni nani alimfata mwenzie? Alinifata mwenyewe na kuniambia Sia nakupenda sana, kiukweli na mimi nilidata kutongozwa na Erick na kufanya nimkubali haraka haraka, nilipoanza nae mahusiano kitu pekee nilichokuwa naogopa ni kuachana nae, ndiomana nilimkazania Erick kwa maisha yangu yote, sikuwa na mwanaume mwingine yoyote mimi zaidi ya Erick, yani yeye ndio maisha yangu na kila kitu kwangu. Wazazi wangu wote walikufra wakisema kuwa Erick ndio mume wangu na mimi nilikula kiapo cha kutokumuacha Erick kamwe naye analitambua hilo, siwezi kumuacha Erick kabisa”“Haya, basi nieleze ukweli kuhusu mtoto”“Nimekwambia ukweli nitrakwambia siku Erick atakapoamua kuniweka mimi kama mke wake, ukiongea na Erick hebu mueleze ni jinsi gani nampenda, hebu mueleze ni jinsi gani nilivyopigani apenzi lake, hebu mkumbushe kila kitu nilichofanya nikiwa nay eye. Nampenda sana Erick, sijui kama kuna mtu anaweza kunishauri chochote kile”Tumaini akapumua tena na kusema,“Kwakweli Sia sina hata la kusema ujue, ila swala uliloliomba kwa Erick najua litakuwa gumu sana maana Erick anampenda sana Erica, kwa umuonavyo Erick yupo tayari kugombana na kila mtu katika ulimwengu huu lakini sio Erica, yani Erick hata hajali kuwa mimi ni dada yake wa pekee, yani naweza kupotea kama simkubali Erica, hata mama Erick mwenyewe hana sauti kwa mwanae juu ya yule mwanamke, kama kupenda basi Erick naweza kumpa medali maana ni amependa kupitiliza kwakweli, sasa hilo swala lako mbona halitawezekana Sia! Sijui itakuwaje!”“Sikia Tumaini, mwambie Erick hata anioe kisiri siri tu, mimi nitafurahi na nitaacha kumsumbua”“Kwahiyo uwe unyumba ndogo”“Sina tatizo, ilimradi Erick awe mume wangu”“Nitajaribu ila siwezi kukuhakikishia kuwa hilo swala litafanikiwa maana Erick namtambua vizuri kwa jinsi anavyompenda yule mke wake”Basi Tumaini aliongea ongea na Sia pale na kuamua kuagana nae.Muda huu Tumaini moja kwa moja aliondoka na kuelekea nyumbani kwa kaka yake, kwani alitaka pia kwenda kuona tena wifi yake huku maneno ya Sia nayo yakichanganya akili yake maana hata hakujua ataanzia wapi kumshauri kaka yake kuhusu Sia.Junior na Angel walisoma vizuri tu siku hiyo na walipomaliza waliondoka kueleka nyumbani, ila baba yao aliwaambia kuwa wakodi usafiri ambapo walipotoka waliongea kuhusu hilo,“Baba kasema tukodi usafiri wa kuturudisha nyumbani”“Angel, katika jamii kuna baadhi ya mambo unajifunza kwa kukutana na watu mbalimbali, hivi muda wote tukizunguka kwenye magari tutajifunza nini na muda gani? Hebu tupande daladala tu Angel”“Sawa, na mimi nakubaliana na wewe kuhusu hilo”Basi walienda hadi stendi ya daladala na kusubiri daladala moja wapo na kupanda, walienda kukaa siti ya nyuma kabisa maana ndio ilikuwa tupu, basi mara mbele kidogo alipanda mdada ambaye nae alienda kukaa siti ya nyuma kabisa ila mdada huyu alipowaangalia Angel na Junior aliwafahamu na kuwashtua na wao ndipo waliposhtuka na kumuangalia kwa makini,“Kheee Husna?”“Ndio mimi, za siku Angel kwanza sijaamini kabisa kama kuna siku ningekutana nawe kwenye daladala”“Nipo, za siku”“Nzuri, hivi Samir bado unawasiliana nae?”“Mmmmh wewe nawe, tumekutana tu umeanza habari za Samir, mimi huwa siwasiliani nae na hata sijui yuko wapi”“Kheee basi bhana, kumbe Samir alikuwa anatembea na Warda”“Mmmh Warda?”“Ndio, kale kabinti Fulani hivi umekasahau na wewe!! Nasikia ndio Samir alikuwa akitembea nacho”Basi Angel akafikiria kitu na kumkumbuka binti ambaye alionana nae hospitali na ndio huyo huyo Warda, basi alimjibu Husna kuwa anamkumbuka na Husna aliendelea kumpa habari,“Za chini ya kapeti sasa, nasikia Warda ana mimba ya Samir, ila kile kisichana kama hakitaenda kutoa sijui”“Mmmh Husna nawe, umepata wapi hizo habari?”“Mimi taifa kubwa wewe, sio kama yule shoga yako Yusra sijui nae kafia wapi siku hizi, ila mimi ni taifa kubwa yani habari zote lazima zipitie kwangu zichujwe halafu ndio zisambazwe”Angel akapumua kidogo ila yeye na Junior walikuwa wamefika hivyobasi walishuka na kumuacha Husna akiendelea na safari yake.Junior na Angel waliposhuka, basi Angel alimuuliza Junior,“Vipi Husna huyu hujampitia kweli wewe?”“Aaaah tayari, si umemuona kanikaushia leo kamejifanya kama hakanifahamu vile, yani wasichana bhana mna vituko”“Mmmh ila na wewe umezidi kaka yangu jamani, nasikia hata Yusra umempitia?”“Ndio, hiko ni kipimo cha uanaume na sio vituko wala nini, ila Yusra katulia sana tofauti na huyu Husna mapepe sana. Ila zile stori zenu nilikuwa nazisikia, yani Warda kaninyima mimi kaenda kumpa Samir dah!”“Kheee kumbe na huyo Warda umewahi kumtongoza?”“Naacheje sasa? Msichana mrembo vile, naacheje kumtongoza, yani darasani ulipona wewe tu sababu dada yangu basi ila wengine wote nimetongoza na wengi nimepita nao”“Mmmmh jamani!”“Kawaida tu hiyo”Basi Angel aliendelea kuongea na Junior pale ila bado kichwa chake kilikuwa kimevurugwa tu na mambo hayo ya Samir na Warda.Basi Tumaini pale anaongea ongea na mama Angel ila lengo lake kwa muda huo ni kumuona kaka yake, huku bibi Angel akiulizia habari za wajukuu zake pamoja na mwanae,“Jamani mpange siku mje kunitembelea nyumba nikirudi”“Sawa mama, hakuna tatizo tutakuja tu”Basi baba Angel aliporudi Tumaini alifurahi sana na muda alipotaka kuondoka alimtaka kaka yake amsindikize, ilibidi baba Angel amrudishe Tumaini na gari yake kwani siku hiyo Tumaini hakutembea na gari basi wakiwa njiani ndipo Tumaini alipoanza kumwambia kuhusu Sia,“Erick bhana, huyo Sia amekataa kunieleza kuhusu mtoto akisema ni siri yake, ila hayo mambo ya mtoto sidhani kama ni kweli ila nadhani Sia anayaweka ili kuongeza chumvi kwenye mboga yani ili matakwa yake yakubalike kirahisi”“Matakwa gani?”“Ni hivi, Sia anataka umuoe pia ilia ache kukufatilia wewe na familia yako”Yani hadi baba Angel alipaki gari pembeni kwanza ili aongee na dada yake kwani kidogo habari hizo zilimchanganya, kwanza aliuliza tena,“Anasemaje?”“Anasema umuoe”“Kheee huyo mwanamke ana wazimu eeeh! Kama alishindwa kipindi kile kuzuia ndoa yangu na Erick kabla sijamuoa Erica basi hawezi kwa kipindi hiki, kwanza nimuoe kwa misingi ipi? Na kwanini nimuoe?”“Anasema kuwa umempotezea muda wake mwingi sana na amefanya vitu vingi sana na wewe, kwahiyo anahitaji utimize ulichomuahidi maana hadi wazazi wake wanakufa wameacha hiyo ahadi kwake pia kuwa wewe ndio mume wake”“Unajua dada, kuna mambo kwenye ujana ni wengi sana huwa wanafanya, kiukweli sikutegemea kama Sia atakuwa chizi namna hii yani amekuwa mtu wa kushusha thamani yangu kwa ujinga wake, yeye kama alifanya mambo mengi kwaajili yangu si alitaka mwenyewe? Na nilimwambia kuwa sitaki ugomvi nae na wala sitaki kuachana nae kwa kugombana, nakumbuka nilijenga kaburi la baba yake na mama yake, ni mimi ndiye niliyekuwa nalisha familia yao, sasa huyu mwanamke anataka nini tena? Mara ngapi huyu Sia kanifumania na wanawake, tena mbele ya wanawake hao nilimwambia kuwa sikupendi ila bado alijiliza liza, mara ngapi nililewa na kumwambia kuwa sikupendi, ila bado alijiliza liza kwangu, unajua huyu mwanamke ni chizi, na ningejua mapema haya kwakweli nisingewahi hata kumtongoza, kwanza nilimtongoza kwa kumjaribu tu na nilimwambia wazi kuwa mimi nina stress kwani kuna mwanamke ninayempenda sana hanitaki, jamani hakuna nilichowahi kumdanganya Sia. Alichofanya kwangu chochote basi aliamua tu kufanya kama ambavyo mimi niliamua kulisha familia yao na nilivyoamua kumjengea makaburi ya wazazi wake, umuulize Sia kama kwao walikuwa na nyumba inayoeleweka? Nyumba yao ilikuwa inakaribia kuwazika wakiwa ndani ila niliwahurumia na kuamua kuitengeneza nyumba ile yani ilibomolewa kabisa na kuanzwa upya hadi nyumba yao ikawa inaonekana ni nyumba mtaani kwaajili yangu, anataka kusema nini huyo mwanamke?”“Oooh kumbe! Yote hayo nilikuwa siyajui ila Erick kwa kifupi hayo ndio yanayomfanya Sia akung’ang’anie, mwenzio anaamini kuwa ulikuwa ukimpenda ndiomana uliweza kufanya yote hayo!”“Ninayempenda mimi ni Erica, naweza kuwa sijafanya kitu kwakina Erica ila sababu hawakuwa na uhitaji huo, kwakina Sia nimefanya sababu ya huruma tu, ila ninayempenda ni Erica. Kumbuka Erica ndio kabadili tabia yangu mimi tena kwa asilimia zote, nilikuwa mlevi ila sinywi tena, nilikuwa mvuta sigara mimi ili sivuti tena, nilikuwa mpenda wanawake mimi ila wote nawaona kwangu walikuwa wapiti njia hata nikikutana nao sishtuki. Mbona wanawake wote niliowahi kuwa nao, nikikutana nao basi huwa tunaongea vizuri tu maana kila mtu na maisha yake na familia yake, kwanini Sia? Kuna analolitaka kwangu, mwambie kuhusu swala la mimi kumuoa asahau kabisa tena sio kumuoa tu hata kuishi nae asahau kabisa, nampenda sana mke wangu, yani Erica ndio kila kitu katika maisha yangu, tena mwambie aelewe hata kama Erica asingekuwa anazaa bado ningempenda na kumjali na kumthamini sana, huo upuuzi asiniletee kabisa, mwanamke mjinga huyo”Kisha baba Angel alimrudisha dada yake ila alionekana kuchukizwa sana, halafu akarudi nyumbani kwake.Leo karibia na muda wa kulala, Erica alitamani kupata mtu wa kuongea nae kwanza kabla ya kwenda kulala, basi aliamua kwenda chumbani kwa kaka yake, alipofika alifungua mlango kama kawaida na kumkuta kaka yake yupo kuongea na simu hana hata habari, basi akasogea karibu na kumuuliza,“Unaongea na nani Erick?”“Ni Sarah, ngoja nikupe umsalimie”Basi Erick alimkabidhi ile simu Erica ambapo muda ule ule Sarah alimsalimia Erica,“Mambo wifi yangu wa ukweli”Erica alikaa kimya tu na kumfanya Sarah aongee tena,“Wifi, wifi upo?”“Nipo”“Mambo wifi yangu? Siku ile nilipokuja ulikuwa umelalala ila nitakuja tena usijali kitu chochote kile wifi yangu na nitakuletea zawadi yako”“Haya”Kisha Erica alimkabidhi Erick simu yake ila kiukweli alikuwa ameumizwa sana na ile simu kwani aliondoka mule chumbani kwa Erick bila hata ya kuaga. Hakuwa na raha kabisa, moja kwa moja akapata wazo la kwenda chumbani kwa Vaileth basi akaongoza na kwenda chumbani kwa Vaileth alivyofika aliingia na kukutana na Vaileth akiwa anajiandaa kuoga,“Kheee umechelewa leo dada?”“Na kweli nimechelewa, ila mbona umekuja muda huu?”“Leo ni zamu yangu ya kuja kulala chumbani kwako dada, kwahiyo ndio nimekuja hivi”Vaileth hakuwa na jinsi zaidi ya kumkubalia tu Erica kuwa alale nae chumbani mule basi akamwambia,“Karibu ila mimi naenda kuoga”“Sawa dada, hakuna tatizo”Basi Erica alijifunika shuka la Vaileth wakati Vaileth ameingia bafuni, muda kidogo mule ndani aliingia Junior na kwenda kitandani moja kwa moja kwani alijua ni Vaileth ndio amelala pale kitandani basi akaanza kusema,“Mpenzi jamani, sijui jana ulienda kulala wapi ukanipa mawazo kweli mke wangu, unajua nakupenda sana”Kisha Junior alianza kumpapasa Erica akijua ni Vaileth, yani muda ule ule Erica alijifunua shuka na Vaileth nae alitoka chooni yani Junior alibaki kushangaa tu. Basi Erica alijifunika shuka la Vaileth wakati Vaileth ameingia bafuni, muda kidogo mule ndani aliingia Junior na kwenda kitandani moja kwa moja kwani alijua ni Vaileth ndio amelala pale kitandani basi akaanza kusema,“Mpenzi jamani, sijui jana ulienda kulala wapi ukanipa mawazo kweli mke wangu, unajua nakupenda sana”Kisha Junior alianza kumpapasa Erica akijua ni Vaileth, yani muda ule ule Erica alijifunua shuka na Vaileth nae alitoka chooni yani Junior alibaki kushangaa tu.Ila muda ule ule Junior aliamua kumuwahi kumziba Erica mdomo kwani alijua ambacho kingefatia kwa muda ule ni Erica kupiga kelele kisha akamwambia,“Erica nakuomba tafadhali usipige kelele yoyote mdogo wangu, nakuomba sana.”Kisha akamuachia mdomo na Erica akamuangalia Vaileth na kumuuliza,“Dada, si ulikataa wewe kumbe kweli!!”Junior akamziba tena mdomo na kumwambia,“Erica nakuomba mdogo wangu jamani usipige kelele basi, ngoja nitakueleza ukweli unaoutaka, kwani unahitaji kufahamu kitu gani?”“Mmmmh nashangaa tu kuona mna mahusiano”“Sikia mdogo wangu, mimi na Vaileth tunapendana tena sana, nampenda sana Vaielth”“Unaniahidi nini kwa huyu dada Vai?”“Nakuahidi kuwa nikianza maisha yangu nitamuoa”“Mmmh!”“Kweli Erica, niamini. Halafu nakuomba usimwambie mama kwasasa, ngoja muda muafaka ufike nitamwambia mwenyewe ila sio kwasasa, nakuomba sana Erica. Kuanzia leo wewe ndio mdogo wangu mpendwa yani, unataka zawadi gani mdogo wangu ila usimwambie mama kabisa”“Mmmmh! Nataka simu yani na mimi nikiwa na simu nitafurahi sana”“Sawa mdogo wangu, nitatimiza hitaji lako, nivumilie kidogo tu. Nakununulia simu na laini mdogo wangu si unataka tu kupiga na kutumiana ujumbe na wanafunzi wenzio?”“Ndio”“Basi nitakununulia mdogo wangu, leo lala tu humu mdogo wangu. Usitusemee kwa mama eeeh!”Kisha Junior akainuka na kuondoka ambapo Vaileth nae alikazana kuomba msamaha Erica ili asiwasemehe maana Erica alijulikana nyumba nzima kwa umbea na huwa akipata jambo lazima alitangaze, kwahiyo Vaileth alihofia sana ila Erica nae alimuaga kuwa anaenda kulala chumbani kwake na kumuacha mule chumbani huku Vaileth akiwa na mawazo sana.Usiku wa leo, Angel alitumiwa jumbe nyingi sana na Samir akiulizwa tatizo ni nini ila hakuzijibu kabisa kwani moyo wake ulikuwa ukiumia sana kwa kile alichosikia kuhusu Samir, basi kuna ujumbe wa Samir uliingia, Angel alifungua na kuusoma,“Nadhani Angel unataka kusikia kuwa nimekufa ndio itakuwa furaha yako, ila hata nikifa jua kwamba nakupenda sana”Moyo wa Angel ulidonda kidogo na kuanza kumjibu Samir zile jumbe zake,“Wewe Samir ni muongo, unadai unanipenda mimi wakati una mahusiano na mwanamke mwingine, kumbe Samir ulikuwa na mahusiano na Warda hadi ukampa mimba na mmeenda kutoa jamani Samir!! Dunia haina siri na yote nimeyapata, au kwavile mimi nashinda ndani ndio ukahisi sitajua chochote kuhusu wewe!! Nimejua kila kitu Samir”Basi baada ya ujumbe ule, Samir aliamua kupiga simu kabisa ila Angel hakupokea na Samir kuamua kutuma ujumbe,“Jamani mpenzi wangu Angel, nani amekwambia maneno hayo jamani!! Nakupenda sana mpenzi wangu, nani kakwambia!”“Sio nani kaniambia ila jua ukweli wote naujua”“Angel hakuna ukweli hapo jamani, kwanza Warda gani unamzungumzia wewe! Angel jamani kwanini huniamini kuwa wewe ndiye mwanamke nimpendaye!”“Saizi unajifanya Warda humjui!! Si yule tuliyekuwa tukisoma nae shule ile tuliyohama, usinifanye mjinga Samir, nishasikia uchafu wako wote”“Unajua Angel, ukisikiliza maneno ya watu tu basi mapenzi hayawezi kwenda wala nini, kiukweli mimi huyo Warda mara ya mwisho nimemuona siku niliyohama shule, sina mazoea nae ya aina yoyote ile iweje niwe na mahusiano nae!! Angel mpenzi wangu, inatakiwa mimi na wewe tupate wasaa tuonane na tuzungumze, tafadhali Angel nakuomba kama utaweza kuja kwetu itakuwa ni vizuri zaidi”“Kheee kwenu nitakuja vipi mimi? Kwanza hapa nyumbani tu siruhusiwi kutoka”“Hujaanza kwenda chuo?”“Nimeanza”“Basi nielekeze unaposoma Angel, nakupenda sana mpenzi”Angel nae alimuelekeza Samir sehemu ambayo anasoma, ila siku hiyo hakuwasiliana nae sana kama siku zote kwani baada ya kuwasiliana nae kidogo tu aliamua kulala.Kulipokucha kila mmoja alienda kwenye mambo yake kama kawaida ila leo Vaileth hakuwa na raha kiasi kwamba hata mama Angel alitambua hilo na kumuuliza kuwa tatizo ni nini,“Kheee Vai umekumbuka sana kwenu nini?”“Hamna kitu mama”“Mbona umepooza sana, sio kawaida yako ujue”“Hamna mama, nipo sawa tu”Basi mama Angel hakuongea zaidi ila alimuona Vaileth kuwa hayupo sawa wala nini, muda huu alienda kuongea na mama yake na kumwambia,“Ila leo Vaileth anaonekana hayupo sawa”“Ni kawaida ya wadada wa kazi, siku akiamka na visirani vyake ndio kama hivyo, mchukulie kawaida tu mwanangu. Halafu unajua mimi nakaribia kurudi kwangu maana maswala ya uzazi wako nishamaliza”“Jamani mama, nimekuzoea ujue”“Ni kweli, ila ni wakati wa nyie kuja kwangu sasa. Unajua sisi wazazi sio kitu kizuri kukaa sana kwa watoto kwanza tunawanyima uhuru, naelewa kuna mambo mumeo anatamani kukufanyia ila anashindwa sababu yangu na ukizingatia haya maadili ya kiafrika ndio kabisa yani, nishakuhudumia uzazi na mtoto kashachangamka vya kutosha, kwanza nimekaa sana, sikutakiwa kukaa kwa siku nyingi hivi. Ni wakati wa kurudi kwangu”“Mmmmh sawa mama, ila nitakukumbuka sana”“Usijali mwanangu, nitazidi kuwaombea na tutazidi kuwasiliana, kwahiyo Jumamosi hii naondoka”“Nimekuelewa mama yangu”Ilibidi tu mama Angel akubaliane na maamuzi ya mama yake, ila mama Angel alimwambia kitu,“Hivi mama, mbona mama Erick yuko hivi jamani!! Kashindwa hata kuja kuniona kweli!!”“Kheee mwanangu, mkwe halaumiwi, kwanza akija kukuona au asipokuja kukuona anakupunguzia nini au anakuongezea nini? Mambo mengine hata sio ya kuumiza kichwa, tufikirie mambo ya maana katika maisha yetu kuwa nifanye kitu gani, niwe nani, nijiboreshe vipi, ila maswala ya kuwaza mtu Fulani hajaja kuniona utapata vidonda vya tumbo bure. Muangalie mumeo, anakupenda sana huyu mwanaume, muangalie na umshikilie, kumbuka baba yake alikuwa kipingamizi kikubwa sana hata baada ya ndoa yenu nina uhakika yule mzee kuna mengi kayatenda nyuma ya pazia huko, si unaona hata alivyokufa kiajabu ajabu, ila sio swala la kushangaa wala nini, katika maisha huwezi kupendwa na kila mtu na huwezi kuchukiwa na kila mtu, halafu kitu kingine mtu kuja kukuona au kutokuja kukuona sio kipimo cha upendo wala nini, mwingine atakuja kukuona kwa lengo la kukusanifu na mwingine kumbe kuna vitu katingwa navyo ila usimfikirie vibya, yule mama tulishamaliza tofauti nae, kumbuka hadi unaolewa na mwanae, nadhani ni yeye alikuwa na furaha sana utafikiri kitu gani na anampenda Angel hadi kesho bila kujali kuwa hajafanana na mtoto wake, tatizo lake tu hajui kulea watoto ila usimfikirie vibaya, mkweo yule. Tena ukiweza, yani ukipona zako, jibebe na zawadi mpelekee kumuona yeye, mtu akikutendea baya hebu mtendee wema uone itakavyokuwa”“Asante mama, ndiomana wewe ni mama yangu kuna muda una maneno ya busara sana”“Kwahiyo kuna muda mwingine naongea ujinga?”“Hapana mama, sina maana hiyo, wewe ni mama bora kwangu umekuwa ukinifundisha kila siku na ndiomana mpaka leo nipo , nimeolewa, naishi na familia yangu ila ni kwa juhudi zako mama, umepambana sana juu yangu, sijui ingekuwaje”Kisha mama Angel alimsogelea mama yake na kumkumbatia huku akimwambia,“Nakupenda sana mama”“Nakupenda pia mwanangu”Basi waliongea mambo mengi sana kwa muda huo.Muda wa Angel na Junior kutoka chuoni ulifika ila siku hii walitoka mapema zaidi, basi walivyofika nje ya chuo Junior akamwambia Angel,“Leo, nataka niende kidogo kwa mama sasa sijui utarudi nyumbani mwenyewe?”“Nitarudi ndio, kwanza nishazoea”“Ila kumbuka hatujamwambia yule dereva atufate halafu leo hatujapewa hela ya kukodi usafiri, je utapanda daladala? Au tumpigie simu dereva aje?”“Hapana bhana, nitapanda daladala, na mimi huwa natamani sana kupanda daladala ili kujua raha yake, halafu usijali kitu”Basi wakaongozana Angel na Junior hadi kituo cha daladala ambapo Junior alikuwa akingoja Angel apande daladala kwanza, ila Angel alimwambia kuwa asijali lolote, ikabidi Junior apande daldala ya kuelekea kwao na kuondoka huku akiamini kuwa Angel nae atapanda daldala na kuondoka sababu alikuwa akingoja daldala yenye siti, ile Junior kuondoka Angel alishikwa bega, kugeuka nyuma alimkuta Samir ambaye alikuwa akitabasamu, basi Angel alimuuliza,“Umejuaje kama niko hapa stendi?”“Unajua nimefika hadi pale kwenye chuo chenu, nikawaona wewe na Junior mmesimama nje, basi nikaanza kuwafata nyuma hadi hapa stendi”“Jamani una vituko wewe”“Yani kitu Mungu akipanga basi kitafanyika tu, hebu ona leo jamani yani tumepangiwa kabisa tuwe pamoja”“Aaaah acha maneno yako Samir”“Kweli Angel, itapatikana wapi siku kama ya leo? Naomba ukapaone tu nyumbani kwetu”“Hapana, nitachelewa sana nyumbani”“Huchelewi Angel, kwani mimi nitahakikisha nakukodia usafiri hadi kwenu, na hapa nakodi usafiri ili tuwahi kwetu”Basi muda huo huo Samir akaita bodaboda na kupanda yeye na Angel halafu safari ikaanza kuelekea kwakina Samir.Junior alienda kwao moja kwa moja, shida yake ni kuongea na mama yake ili aweze kumpatia pesa za kumnunulia Erica simu kama ambavyo alimuahidi, basi alimkuta mama yake akiendelea na kazi zake kama kawaida, ila mama Junior alifurahi sana kumuona mwanae na kusema,“Ooooh leo mwanangu Junior umenikumbuka jamani! Kweli Mungu mkubwa, karibu mwanangu”Mama Junior alimfata mwanae na kumkumbatia kisha kumkaribisha ndani, ambapo Junior aliingia na kuanza kuongea nae,“Kwanza vipi za huko mwanangu?”“Ni nzuri tu mama”“Kweli naona”“Ila nimekuja mara moja tu hata mamdogo sijamuaga ujue”“Ooooh wewe nawe! Kwanini lakini?”“Aaaah mama ni hivi, unajua sio vizuri kwa mimi kila hela nimuombe mamdogo na bamdogo wakati mama yangu upo, sasa wanafunzi wote tuliomaliza kidato cha nne pale shuleni tumeandaa kama sherehe fulani ya kusherekea pamoja, sasa nikafikiria na kuona ni vyema nije nikwambie mama yangu, tafadhari naomba unisapoti kwa hilo mama”“Kheee kwahiyo inahitajika pesa ngapi?”“Elfu hamsini mama”“Mmmh Junior jamani! Elfu hamsini sherehe gani hiyo? Kuna mtu anaoa ni michango ya harusi au kitu gani?”“Jamani mama, mbona hivyo lakini, lini nimewahi kuja kukuomba kitu cha namna hii!!”Mume wa mamake nae alikuwepo, basi alisikia maongezi ya mke wake pamoja na Junior na yeye alienda pale ambapo Junior alimsalimia kisha yule baba akasema,“Mama Junior, mtoto wetu huyu kwanza kwasasa hatuna majukumu yoyote kwake, kwanini tusimpe anachokihitaji!”“Aaaah naona hela ndefu!”“Hela ndefu elfu hamsini jamani!”Kisha huyu baba alimuangalia Junior na kumwambia,“Usijali mwanangu nitakupa laki moja ya hiyo shughuli yenu na nitakupa elfu ishirini ya nauli”“Oooh asante sana baba, nashukuru sana”Basi yule baba alienda ndani na kutoa zile hela na kumkabidhi Junior, kwakweli Junior alifurahi sana wala hakuendelea kukaa kwao kwani muda ule ule aliamua kuaga na kuondoka zake.Pale alibaki mama Junior na mumewe ambapo alimuuliza,“Kheee unajua umenishangaza leo, imekuwaje?”“Unajua kuna siku nilipita ofisini kwa Erick, kiukweli alinisema sana, natakiwa kumlea Junior kama mwanangu wa kumzaa na si tofauti na hapo, nikiangalia mimi nimeishi na Junior ila sijawahi kumpa yale mapenzi ya baba kwa mtoto, acha nianze sasa”“Ooooh sawa, nimekuelewa, na pia nashukuru sana kwa kumjali mwanangu.”Mama Junior alifurahi pia kwa siku hiyo ingawa aliona kama mwanae kamdanganya kuhusu uhitaji wake wa ile hela.Samir alifika na Angel nyumbani kwao na kumkaribisha vizuri sana, kwa muda huo hapakuwa na mtu mwingine kwakina Samir zaidi yam dada wa kazi tu, ila Angel alihofia kwenda chumbani kwa Samir kwani alihisi kwenda chumbani kwa Samir basi ndio tiketi ya kulala na Samir,“Hapana Samir, sijapanga kulala nawe”“Kwani nani kakuambia Angel kuwa ukiingia chumbani kwangu basi utalala na mimi!! Jamani Angel, tende tu mara moja ukaone chumba ambacho mpenzi wako analala”“Mmmh hapana Samir”“Kwahiyo Angel hunipendi eeeh!!”“Nakupenda sana Samir ila kwa leo hapana, nakuomba Samir jamani tafadhari, naogopa”“Sasa unaogopa nini?”“Naogopa kufanya mapenzi”“Aaaah Angel acha hizo jamani! Kwani nani kakwambia kuwa tukiingia tutafanya mapenzi jamani!! Mimi nakupenda, najua mapenzi yapo muda maalum ukifika basi tutafanya hadi tuchoke ila kwasasa twende tukaongee tu faragha kidogo”Angel akafikiria kwa muda, pia akafikiria maneno ya bibi yake na kumfanya ahofie, aliwaza pia akipata mimba itakuwaje? Na bibi yake alimwambia kuwa akizalia nyumbani basi anapunguza thamani yake, Angel akafikiria kidogo na kuogopa kuingia chumbani kwa Samir ila bado Samir alikuwa akimlazimisha, ikabidi amuahidi kitu kingine,“Mpenzi wangu Samir naomba nikuahidi hili, tukikutana tena basi siku hiyo ndio tutakuja wote na kuingia chumbani kwako kwa maongezi ila kwasasa Samir hapana, kwanza nitachelewa kurudi nyumbani na itakuwa balaa kwa mama”“Sawa, basi kaa kidogo hapa sebleni ili tupate hata juisi na tuongee ongee kidogo”Angel alikaa na kuanza kuongea pale na Samir huku yule mdada wa kazi wakina Samir akiwaletea juisi, kwahiyo walikuwa wakinywa huku wakiongea, ila maongezi ya muda ule yalikuwa yakimshawishi sana Angel na kujikuta akitamani kuwa karibu zaidi na Samir,“Tungeingia chumbani leo kidogo tu ningekuonyesha mapenzi yangu kwako, nisingelala nawe ila ningekuonyesha mapenzi yangu”Basi Samir akawa akimueleza Angel vitu ambavyo angemfanyia wakiwa chumbani, kisha akamsogelea na kuanza kumbusu, kwakweli Angel alikuwa kalegea kabisa muda huo, mara mlango wa sebleni ulifunguliwa na aliyeingia alikuwa ni mdogo wake Samir ambaye alikuwa ametoka shule ila alipowaona pale aliwasalimia na kushtuka kidogo alipomuona Angel na kusema,“Dada, wewe si ndio dada yake Erica?”Angel alikaa kimya ila alihisi aibu kidigo na kumwambia Samir kuwa aondoke tu na aelekee kwao, basi Samir akamwangalia mdogo wake na kumwambia,“Na wewe hebu nenda kabadili nguo huko, kaone vile ni umbea tu”Samia alienda chumbani kwake huku Angel nae akiinuka na kutoka nje ambapo Samir alitoka nae huku akimwambia,“Ndiomana Angel nilisema kuwa twende chumbani mpenzi wangu, ila umekataa”“Tutaenda safari nyingine, ila kwasasa nahitaji kurudi nyumbani yani ninavyochelewa ndio balaa”Basi waliondoka na Samir alikodi usafiri ambao uliwapeleka moja kwa moja nyumbani kwakina Angel.Moja kwa moja Junior alienda kwenye duka la simu na huko alinunua simu kwaajili ya Erica na simu kwaajili ya Vaileth maana nae Vaileth toka amepokonywa ile simu na bozi wake mama Angel basi hakuwa na simu tena, kwahiyo Junior hakumkuta na simu kwahiyo aliona ni vyema amnunulie simu ili muda mwingine awe anawasiliana nae tu kama chumbani kwake hakuna mtu, basi alienda na kununua laini za zile simu na moja kwa moja kurudi kwa mamake mdogo.Basi Junior alifika na moja kwa moja alielekea chumbani kwake na kuweka zile simu ila baada ya muda kidogo alimsikia mamake mdogo akimuita, basi alienda kumsikiliza,“Junior, umerudi na Angel eeeh! Na mbona leo mmechelewa sana?”“Kheee Angel hajafika kwani?”“Anafika vipi wakati siku zote huwa manarudi pamoja!”“Nilijua kashafika mamdogo, unajua mimi nilipitia kidogo nyumbani na nilimuacha Angel akija huku”“Kheee kwahiyo Angel alikuwa akirudi mwenyewe”“Ndio mamdogo”“Kheee kapitia wapi jamani!!”“Sijui mamdogo ila nilimuacha aje nyumbani”“Ngoja nijiandae twende huko chuoni”Muda huo huo Angel nae aliingia, kwakweli mama yake alikuwa na hasira sana na kwenda kumnasa kibao Angel halafu ndio akamuuliza,“Ulikuwa wapi muda wote?”“Jamani mama unanionea bure tu, leo dereva hakuja kutufata maana tulisahau kumwambia wakati tunaenda, halafu sina simu kusema nimpigie, sina hela ya kusema nikodi usafiri, hela kidogo niliyokuwa nayo niliamua kupanda daladala ila njiani liliharibika ndio tukasubiri litengenezwe na ndio nimerudi muda huu, samahani mama”“Samahani mwanangu, sikufahamu hilo mwanangu, pole sana. Ila nitajua cha kufanya kuhusu usafiri”Basi Angel moja kwa moja alienda chumbani kwake huku akishukuru sana njia aliyofundishwa na Samir ili kumdanganya mama yake kwa siku hiyo na mamake amemuelewa kweli kumbe kamdanganya.Baba Angel akiwa ofisini kwake, akikamilisha kamilisha kazi zake ili afunge ofisi maana siku hiyo alitaka afunge mapema na awahi kurudi nyumbani kwake, basi alipigiwa simu na mtu wa mapokezi,“Bosi, kuna mgeni hapa anahitaji kukuona”“Mwambie aingie”Yule mgeni alipoingia, kwakweli baba Angel alishangaa sana kwani alikuwa ni Sia, basi alimuangalia ka hasira na kumuuliza,“Shida yako nini ofini kwangu?”“Usiseme ofisini kwako ila sema ofisini kwetu maana chako ni change na change ni chako, mimi na wewe ni wanandoa”“Hivi una wazimu wewe Sia?”“Sina wazimu ila kumbuka ni muda gani umepoteza katika maisha yangu! Miaka miangapi tulikuwa pamoja, mimba ngapi umenilazimisha kutoa? Mara ngapi umeshiriki nami tendo la ndoa? Yani hilo tendo ndio tumefanya mar azote hadi kwenye gari, sasa nashindwaje kusema kuwa mimi ni mke wako? Yani Erick huwezi kukwepa hili, mimi ni mkeo tu, nilikataa wanaume wengi sana kwaajili yako, mimba ulizonitoa umefanya nifuje yani urembo wangu wa awali utoweke, hata sikujua kama nitazaa tena ni mapenzi ya Mungu tu hata nimepata mtoto mmoja, hivi Erick utaniambia nini wewe nikuelewe? Tena shukuru sana kwa miaka yote hii nimekuacha umeishi kwa amani, ila nisingekuacha wewe, nilitakiwa nikuharibie hata siku ya ndoa yako, umenitumia sana mimi. Baba yako aliongea nami mara ya mwisho kwa maneno mengi sana, hivi unajua kuwa baba yako alikufa kwenye mikono yangu nikiwa nimemshika, unajua aliongea nini na mimi? Unajua ni mangapi baba yako amenisaidia ili mimi niwe na wewe? Kwakweli Erick huna cha kunikwepa, sema kwa muda huu hiki sio kilichonileta hapa, kuna siku nitaongea mengi sana ya moyoni ili jamii ijue”“Kheee tuseme bado una mengine!!”“Tena mengi tu, ila kwa muda huu hakijanileta hiko kitu”“Nini kimekuleta, sema haraka nataka nikamuwahi mke wangu”Sia akacheka kwa muda na kusema,“Huyo Angel, nimemuona akiwa kwenye bodaboda na mwanaume, tena mwanaume mwenyewe ni Samir, usiulize nimemfahamu vipi Samir ila namfahamu ndani na nje yule mtoto, kwahiyo nimemuona binti yako akiwa nae pamoja, chunga sana usipokuwa makini yule Angel nae atazalia nyumbani kama mama yake, najua unampenda sana mtoto huyu tena nadhani unampenda kuliko hata baba yake mzazi angefanya kwake, ila ndio hivyo anapotea yule mtoto, na mkimfahamu Samir vizuri mtaona kama mnavyofanya siri kwa Angel kuhusu ndugu zake ni vizuri au si vizuri, mimi nina siri nyingi sana ila nipo makini sana nikiona kuna tatizo linataka kutokea basi naingilia kati ili tatizo hilo lisiibuke, nakwambia tena kuwa makini sana Angel na Samir mambo ni moto yani kama mahaba yamewapata haswaaa, nina hofia Angel asije kuwa kama mimi kwa siku za mbeleni, apoteze uzuri wake sababu ya mwanaume na mwisho wa siku ajute kwani Samir hatoweza kumuoa yeye na ataoa mwanamke mwingine na hapo ndio kutakapoibua tatizo. Ukitaka fatilia na usipotaka potezea, ila mimi ujumbe nimeshakufikishia, kwaheri”Sia aliondoka na kumuacha baba Angel mule ofisini akimuangalia tu Sia hadi alipotokomea, kiukweli hata hamu ya kufanya kazi ilimuisha kabisa na kujikuta akiwaza kwa muda kisha akafunga kazi na kuondoka zake.Moja kwa moja Junior alienda chumbani kwa Erica na kugonga ambapo Erica alimkaribisha kisha alimpa ile zawadi ya simu ambayo alimuahidi, kwakweli Erica alifurahi sana, kwani lengo lake ilikuwa ni kutaka kufanana na Erick maana alimuona Erick anajifanya simu inampa umakini sana, alimshukuru sana Junior,“Asante sana Junior”“Usijali, ila mimi na wewe ahadi yetu ni pale pale kuwa tuendelee kufanya siri”“Sawa na ahadi nyingine pia ibaki pale pale kuwa ukijipanga utamuoa dada Vai”“Ndio nitamuoa mdogo wangu, nakuahidi hilo, lazima nitamuoa Vai hakuna tatizo”“Hapo tutaelewana, sipendi kumuona akilia wala akisononeka”“Sawa mdo wangu, nakuahidi kuwa nitamfanya Vaileth kuwa na furaha muda wote”Basi Junior alifurahi pale na kumuachia ile simu Erica kisha akaondoka zake.Ilikuwa ni furaha sana kwa Erica kupata ile simu na alijisemea kuwa atajitahidi kuitunza siri ile”Basi alikaa na kuanza kuibonyeza bonyeza.Mama Angel muda huu alikuwa amekaa sebleni akiangalia Tv maana ni muda hajafanya hivi, ila alishangaa kusikia kuwa kuna mgeni amefika, alipomuangalia mgeni mwenyewe alishangaa kumuona Elly yani hapo aliwaza moja kwa moja lazima Elly atakuwa kaenda na Sia, kiukweli uoga ulimshika kidogo na kuinuka huku akimuuliza Elly,“Umekuja kufanya nini?”“Nahitaji kumuona Erica”Naye Erica alikuwa akitoka ndani akielekea hapo sebleni, hata yeye alishangaa kumuona Elly kwani hakumtegemea kwa siku hiyo na kwa muda huo.Ila Elly alivyomuona Erica, alimkimbilia na kumkumbatia yani kile kitendo kilizidi kumuogopesha mama Angel kwani alijua ni wazi yule Elly katumwa na Sia ila tu hakujua ni tukio gani litaendelea. Naye Erica alikuwa akitoka ndani akielekea hapo sebleni, hata yeye alishangaa kumuona Elly kwani hakumtegemea kwa siku hiyo na kwa muda huo.Ila Elly alivyomuona Erica, alimkimbilia na kumkumbatia yani kile kitendo kilizidi kumuogopesha mama Angel kwani alijua ni wazi yule Elly katumwa na Sia ila tu hakujua ni tukio gani litaendelea.Basi akasogea karibu ya Erica na Elly na kuwaachanisha pale kisha akamfokea Elly,“Muda huu nyumbani kwangu umekuja na nani?”“Nimekuja na mama yangu, yupo nje ananisubiria”Mama Angel alizidi kuchukia na kumwambia Elly,“Haya, toka kwenye nyumba yangu sasa hivi”Erica alimuuliza mama yake,“Kwanini unamfokea mama?”“Mama yake na huyu sio mtu mzuri kabisa, Elly ondoka katika nyumba yangu”Elly hakubisha na moja kwa moja alitoka nje na kuelekea nje ya geti ambako kulikuwa na mama yake kisha akamwambia mama yake,“Mama Erica kanifukuza”“Usijali mwanangu, ipo siku atajutia. Muda utafika, usijali mwanangu, twende nyumbani”Kisha mama Elly aliondoka na Elly, muda huu mama Angel alikuwepo getini pia maana alimfata Elly kwa nyuma, kwakweli alichukia sana na kurudi ndani kwake akiwa na chuki ila bado Erica alikuwa pale sebleni akishangaa kwani alishangaa pia kwa muda huo Elly alienda kwao kufanya nini na nani aliyemfikisha Elly nyumbani kwao kwani alikuwa anatambua wazi kuwa Elly hapafahamu hapo nyumbani kwao, basi mama yake akamuangalia na kumwambia,“Erica, kuanzia leo sitaki ukaribu wako wowote na Elly”“Kwanini mama?”“Sidhani kama nina majibu kwa muda huu, nenda ukale huko ukalale”Mama Angel alitulia tu huku akiwa na hasira za kutosha.Baba Angel nae alirudi akiwa na hasira pia, ila huyu baba hata kama aliambiwa kitu cha ukweli na Sia bado hakuweza kumfokea Angel yani yeye aliona kumfokea Angel ni kama kumfanya ajihisi vibaya, ila pia alikuwa na hasira kwa yale maneno ambayo aliambiwa na Sia,kitu hiko kilimfanya alipoingia ndani basi moja kwa moja alienda chumbani kwake ila badae alikumbuka kuhusu Angel na kuinuka ili akaulizie, wakati anataka kutoka akakumbana na mkewe mlangoni kwani pia alikuwa amemfata chumbani,“Vipi tena baba Angel?”“Huyu Angel yupo?”“Yupo ndio, sasa aende wapi jamani!”Baba Angel akapumua kidogo na kurudi kukaa ambapo mkewe alimuuliza tena kama kuna tatizo,“Kwani una tatizo gani mume wangu?”“Hapana sina tatizo, nadhani ni kazi tu hizi zinanisumbua”“Halafu ngoja nikwambie kitu yani leo nimemuona Vaileth hana raha kabisa, sijui kakumbuka kwao!”“Oooh nimekumbuka, nilimuahidi kuwa nitampatia pesa za kumuwezesha yeye kuwatumia wazazi wake ili warekebishe nyumba yao maana alisema kuwa inavuja”“Sasa mume wangu hiyo pesa utakuwa unamkopesha au?”“Kwani pesa ngapi mke wangu? Ni milioni mbili, kumbuka Vaileth anakaa na familia yetu hapa, ngoja tumfurahishe ili azidi kumpenda familia yetu na kuishi nayo vizuri”“Sawa mume wangu hakuna tatizo, halafu hivi tutamkabidhi lini Angel akaunti yake?”“Hata sasa hakuna tatizo”“Hapana, bado. Unajua Angel ana akili moja mbovu sana, nadhani tukimkabidhi mapema hivi tutalia pia, naona tumuache tu kwanza, na akihitaji pesa aombe kwetu”“Sawa, umeongea sahihi mke wangu”Ila siku hiyo baba Angel alisikia akili kuchoka kweli ila hakumuuliza mkewe chochote kuhusiana na kile alichoambiwa kuhusu Angel, sema tu alifurahi moyoni mwake kuona kuwa Sian i muongo na mwanae hajafanya ujinga wowote.Leo Junior alienda kulala chumbani kwa Vaileth na kumpatia ile zawadi ya simu, kwakweli Vaileth alifurahi sana na kumwambia Junior,“Kweli nimeamini kuwa Junior unanipenda”“Ndio, mimi nakupenda sana Vaileth, yani jua nakupenda wala usiumizwe kichwa juu ya jambo lolote lile”“Ila nasikia wewe ni muhuni!”“Hiyo zamani, ila sio sasa”“Ila Junior bado kijana wewe!”“Kwani ujana ni kitu gani ikiwa mtu umeamua? Mimi kwasasa nimeamua kukupenda wewe na nitakupenda siku zote, yani Vaileth elewa kuwa wewe ni mke wangu kabisa, lazima nikuoe”Vaileth alitabasamu na kujihisi rah asana, yani siku hiyo ndio alilala vizuri zaidi na Junior kwa kumshukuru kwa zawadi ya simu.Basi Angel usiku huu alikuwa akiwasiliana tu na Samir na kumueleza vile mama yake alivyomuamini,“Kweli wewe Samir ni kiboko jamani, yani yale uliyosema nimueleze mama amekubali kwa urahisi sana”“Si nilikwambia Angel, unajua unapokua unatakiwa kujua ni uongo gani wa kumpa mzazi wako ili uweze kufanikisha mambo yako. Basi Angel, kuna siku mimi na wewe tutatoka na kwenda kufurahi wala mama yako hatojua chochote kile”“Ooh asnte sana Samir, ila huyo Samia ndio mdogo wako?”“Ndio”“Oooh ni rafiki wa Erica huyo, hebu kaa nae asije akasema umbea”“Usijali, asubuhi kabla hajaenda shule nitaongea nae maana muda huu kalala halafu yule akilala huwa haelewi kitu”Basi waliwasiliana kwa muda mrefu sana na wote kulala ikiwa ni usiku sana, kitendo kile kilimfanya hata Samir asishtuke asubuhi kwenda kumfata mdogo wake na kumpa onyo kwani naye alilala sana.Kama kawaida wanafunzi wote walienda shule na wengine kwenye dhughuli zao za kila siku, ila wakati Erica yupo shuleni basi rafiki yake Samia alimfata na kuanza kuongea nae,“Jana bhana wakati natoka shule, ile kufungua mlango wa sebleni si nikamkuta kaka na mwanamke, ila yule mwanamke alikuwa na aibu hatari, ila unajua alikuwa nani?”“Ni nani?”“Dada yako, yule umenitambulisha siku ile yule Angel, kumbe ndio mwanamke wa kaka”“Haiwezekani kabisa, jamani mama yetu ni mkali sana, unataka kuniambia dada Angel alikuja kwenu? Haiwezekani utakuwa umemfananisha”“Haya, shauri yako ila sijamfananisha wala nini ni mwenyewe kabisa yani, yule ni dada yako na aliponiona kanionea aibu sana hata swali langu hakujibu maana nilimuuliza kama ni dada yako ila hakujibu kwa aibu”“Ila Samira mmmh! Nadhani mimi na wewe tunafanana kwenye umbea jamani, yani mimi hadi nyumbani wananichukia eti”“Mimi je!! Yani baba ndio huwa hataki hata nimuone na mwanamke kaongozana nae maana lazima nimpelekee habari mama”Basi wakacheka pale na kurudi darasani kuendelea na masomo sasa, ila siku hiyo ilikuwa siku fupi kwani ilikuwa ni siku ya Ijumaa.Wakati wa kutoka shule, kama kawaida Erick alikaa kiti kimoja na Sarah, kwa kipindi hiki Sarah alikuwa kamzoea sana Erick na alimfanya kuwa ni mtu wake wa karibu na kuzungumza nae mambo mengi sana, basi Erick akamkumbusha swali kuhusu mama yake kuwa kwanini alilia siku ile,“Eeeeh kwanini mama yako alilia?”“Tena afadhari umeniuliza, basi nimemuuliza mama kwanini umelia? Unadhani kanijibu? Hajanijibu chochote ila kasema anataka akuone tena”“Kheee anataka kuniona tena!!”“Ndio, basi kesho nitakuja tena kwenu ili unisindikize, sawa Erick”“Mmmh sawa hakuna tatizo, nitafanya hivyo”“Yani mimi napenda sana kuwa karibu na wewe Erick, furaha yangu ni kuwa karibu na wewe”“Ila sisi bado ni wadogo na wewe ni mtoto wa kike Sarah hutakiwi kuwa hivyo!”“Mama yangu, alinifundisha jambo moja la kutokukaa na kitu moyoni na kama mtu nimempenda basi nimwambie mapema, kwahiyo nimelelewa hivyo na nimekuwa kwa stahili hiyo”“Haya”“Kwahiyo unasemaje kuhusu mimi?”Gari ilikuwa imefika kwakina Erick, hivyobasi Erick alishuka nyumbani kwao na moja kwa moja kuingia ndani ila alimkuta mama yake ambaye kwa siku hiyo alimuuliza swali,“Sarah hajambo!”Erick alishangaa pia na kumjibu mama yake,“Hajambo”“Anakuja lini tena kututembelea?”“Kasema kesho mama, kumbe umemkumbuka!”“Ndio, binti mcheshi vile ndio nisimkumbuke kweli! Namkaribisha sana nyumbani kwangu”Erick akatabasamu na kwenda ndani ila Erica alikuwa mahali na alisikia vile mama yake alivyokuwa akimsifia Sarah, kiukweli hakupenda kabisa, na muda huu alienda chumbani kwa Erick ambaye alikuwa akibadilisha sare za shule, basi Erick alimuangalia Erica na kumwambia,“Naona leo umenikumbuka mdogo wangu”“Niite jina langu ndio inapendeza zaidi”“Khaaaa ila wewe jamani!! Haya karibu ndani Erica”“Ngoja ngoja nikupe maji, nasikia dada Angel jana alikuwa kwakina Samia, sijui ana kaka yake basi huyo kaka yake kumbe anatembea na dada Angel”“Kheee ndio maji hayo?”“Ndio, huu ni umbea na umbea ni kama maji usipounywa utauoga”“Ila wewe mdogo wangu una vituko sana jamani!! Yani wewe una vituko umepitiliza, una uhakika? Huyo Samia nae mbea kama wewe”Erica alinyanyuka na kuondoka bila hata ya kumuaga kaka yake kwani alikuwa ashachukia kwani hapendi kupeleka habari halafu isisikilizwe. Ila Erick alibaki akisikitika tu kidogo na kusema,“Yani huyu Erica jamani kama kazaliwa uswahili, kwa hali hii hajazaliwa uswahilini, hivi angezaliwa uswahilini kama wengine ingekuwaje jamani! Dah huyu mdogo wangu jamani, lakini nampenda sana”Basi Erick alimuangalia tu Erica anavyotoka huku akionekana kuwa amechukia.Moja kwa moja Erica alienda chumbani kwake, ila akatamani akamueleze habari hiyo mama yake ila akakumbuka maneno ya Erick kuwa una uhakika? Ikabidi tu akae kimya, kisha akainuka na kwenda jikoni ambako alianza kumsaidia Vaielth kazi mbalimbali huku akimwabia,“Kesho nitapika mimi, kuna kitu nataka kujaribisha kupika”“Umefundishwa tena na Elly?”“Hapana, halafu nimemkumbuka Elly sana, yupo kama ndugu yangu yule ila sijui kwanini mama hampendi Elly, tena kasema hataki urafiki wangu na Elly kabisa”“Mdogo wangu usilazimishe kitu ambacho mama hapendi, fanya kile tu anachopenda ili uishi nae vizuri na kwa usalama”“Ila nina jambo nataka kuongea yani nisiposema hili naweza kupatwa na vidonda vya tumbo”“Jambo gani tena?”Basi akaanza kumuelezea vile alivyoelezwa na Samia shuleni kuhusu dada yake Angel kwenda kwakina Samia, kwakweli Vaileth aliogopa kwani aliona hata siri yao itafichuliwa tu,“Kwahiyo hilo ndio jambo ambalo ungekaa nalo ungepata vidonda vya tumbo Erica?”“Ndio, yani sikuweza kukaa nalo kabisa”“Ila Erica nakuomba, kuhusu mimi na Junior usiseme”“Usijali, wala sisemi kwanza Junior kanipa simu basi usijali yani siwezi kusema kabisa”Basi Vaileth akapumua kidogo na kuendelea na kazi zake.Leo baba Angel wakati anatoka tu ofisini kwake, alikutana na rafiki yake wa muda mrefu sana na kuanza kusalimiana pale, kisha wakaona ni vyema kutafuta hata hoteli na kuongea mawili matatu,“Khaaa umebadilika Erick”“Si unajua ukubwa tena!! Hata wewe umebadilika ndugu yangu jamani! Nikikumbuka kipindi kile dah! Kweli miaka inaenda na maisha yanaenda sana. Vipi familia yako kwasasa Juma?”“Oooh Alhamdulilah, nina mke na watoto watano kwasasa”“Oooh hongera sana, na mimi nina mke na watoto wanne, kwahiyo umenizidi mmoja”Juma alicheka na kuendelea kukumbushana mambo ya zamani,“Hivi unamkumbuka Rahim?”“Aaaah namkumbuka ndio”“Yule jamaa sasa, ana watoto kama uchafu jamani, nina uhakika hata watoto wake wengine hajui walipo”Baba Angel alikaa kimya kidogo kwani huyu Rahim aliyezungumziwa hapa ndio baba halisi wa Angel, basi alitulia kwa muda na kusema,“Tuachane na habari za huyo mtu”“Ila yeye huwa anakutaja sana tena huwa anasema kuwa anakutafuta sana sijui anakutafutia nini”“Achana na huyo mtu kwakweli, historia yake ni ndefu sana”“Haya bhana, ila sasa inatakiwa tutembeleane ili uweze kufahamu familia yangu nami niifahamu familia yako ndugu yangu”Basi wakati wanaongea pale, kuna mtu alisogea na kukaa karibu yao, Erick alishtuka kidogo ila alipomuangalia akagundua kuwa ni Dora basi alirudi kawaida na kuongea nae,“Kheee Dora, karibu, leo upo hotelini kumbe!”“Unajua nawashangaa, kumbe nyie watu mnafahamiana?”“Ndio, huyu ni Juma ni rafiki yangu kitambo sana”Juma alikuwa akitabasamu na kusema,“Hata mimi na huyu Dora tunafahamiana, vipi Dora lakini za siku? Yale mambo yako umeacha siku hizi!”“Mmmh jamani nimeokoka ujue, siku hizi nimeokoka sina mambo ya kijinga kabisa. Hapa hotelini kwenyewe nimepita tu kidogo ili leo nile chakula cha hapa yani nimejikuta tu nimekikumbuka ila kuna mtu ananivuruga sana”Baba Angel akamuuliza,“Mtu gani huyo shemeji yangu?”“Aaaah ni Sia huyo shemeji, yani mwanamke ananivuruga yule hatari”Baba Angel alishtuka ila Juma nae alishtuka kidogo sema hakuonyesha sana mshtuko wake, basi baba Angel akamuuliza tena Dora,“Anakuvurugaje tena huyo Sia?”“Yani acha tu shemeji, ila huyu mwanamke kuna siku nitarudi Dora wa zamani na nitamshikisha adabu, nadhani hanifahamu vizuri”“Mmmmh umeokoka Dora ujue!”“Ni kweli nimeokoka ila sio mtu akiokoka basi ndio apandwe hadi kichwani, yani kuna siku huyu Sia atasema kweli wewe ni Dora maana nitamvuruga kupota yeye alivyoivuruga familia yangu”Baba Angel alibaki tu kumuangalia Dora kwani na yeye akiwaza jinsi Sia anavyoivuruga familia yake alikosa raha kabisa, basi wakajikuta wakianza kuongea tu habari zingine kwani za Sia ziliwachanganya wote.Baba Angel alipoagana na rafiki yake Juma pamoja na Dora, aliamua sasa kurudi nyumbani kwake, ambapo aliporudi tu mkewe alimfata chumbani kuongea nae kwani hakumwambia kuwa mama yao amepanga kuondoka Jumamosi ambayo ndio kesho, basi akaanza kuongea nae,“Oooh sorry mume wangu, ni hivi nilisahau kukwambia tu ila mama alisema kuwa ataondoka Jumamosi yani kesho”“Aaaah hapana haiwezekani, mama Angel jamani ndio mambo gani hayo? Kwahiyo mama ataondoka bila zawadi?”“Sijui ila ndio kasema hivyo”“Haiwezekani kumruhusu mama aondoke bila ya zawadi, kumbuka mama ameacha kazi zake nyingi sana, ametumia muda wake mwingi tu kutuhudumia hapa halafu tumuache tu aondoke bila zawadi! Hapana kabisa haiwezekani”“Sasa tutafanyaje mume wangu!”“Inabidi uongee nae na umshawishi ili mama akubali kuondoka Jumapili na kesho niende kumtafutia zawadi, mwambie tena Jumapili nitampeleka mwenyewe, tafadhari mama Angel ongea na mama kuhusu swala hilo jamani, haiwezekani tumuache mama aondoke bila zawadi”“Si unamjua yule mama lakini, akisha amua lake basi ameamua”“Hata kama mama Angel, nakuomba mke wangu ongea na mama tafadhari, nakuomba sana”“Sawa basi, ngoja nikaongee nae”Mama Angel alionoka mule chumbani na moja kwa moja kwenda chumbani kwa mama yake ambapo alimkuta akipanga panga nguo zake kwaajili ya safari, basi mama Angel alianza kuongea nae,“Oooh mama, sikia mama yangu naomba uondoke Jumapili”“Kwanini sasa niondoke Jumapili? Na mimi nimepakumbuka kwangu”“Naelewa mama ila ukiondoka Jumapili itapendeza”“Kwanini iwe Jumapili na sio kesho?”“Sikia mama, yani sikumueleza baba Angel kuwa unaondoka Jumamosi, sasa leo nimemwamboia kaniomba sana uondoke Jumapili na kasema kuwa atakupeleka yeye mwenyewe hadi nyumbani, mama tafadhari nakuomba kuhusu hilo”“Si unajua nimeshapanga lakini jamani! Mimi nataka kuondoka, nahitaji kwenda kwangu”“Naelewa mama ila nakuomba juu ya hilo tafadhari mama yangu nakuomba”“Ila na wewe Erica jamani uking’ang’ania kitu loh! Haya basi nitaenda hiyo Jumapili mnayotaka nyie”“Asante sana mama yangu”Mama Angel alifurahi sana na muda huo aliamua kwenda kumpa taarifa hiyo mume wake kuwa mama yao kakubali kuondoka Jumapili.Usiku wa leo, Erick aliamua kwenda chumbani kwa Erica kwani alijua kuwa alimkera mdogo wake kwakutokumsikiliza kwani mdogo wake alipenda sana kusikilizwa na kwavile alimtambua vizuri basi hakuwa na budi kumfata ili akamjulie hali.Alimkuta amekaa tu na amejiinamia, basi Erick alisogea na kumuuliza,“Una tatizo gani kwani mdogo wangu Erica?”“Sina tatizo lolote”“Aaaah mimi nakufahamu vizuri sana Erica, najua kuwa una tatizo, najua kuwa muda ule ulichukia sababu sijakusikiliza, nisamehe mdogo wangu ila nakuomba usiende kumwambia ukweli mama kuhusu swala hilo maana halina uhakika”“Mbona sijamwambia mama hata hivyo nimesema simwambii chochote”“Ni bora uende kumuuliza Angel mwenyewe kuliko kumwambia mama”“Nimekuelewa Erick, ila niache nipumzike”“Aaah mambo hayo yameanza lini jamani Erica? Naomba tucheze karata”Erica aliposikia vile alifurahi sana na kwenda kutoa karata ili waweze kucheza na muda huo huo walianz akucheza zile karata, na kama kawaida walicheza sana karata na kulala kule kule chumbani kwa Erica.Kilichowashtua asubuhi ni sauti ya mama yao ambaye alikuwa akiita akiwa sebleni, basi Erick alikurupuka na moja kwa moja kwenda alipoitwa na mama yake ambapo alipewa kazi yak wend akusafisha gari lao, ila siku zote Erick sio mtu wa kubisha kazi yoyote anayopewa, hivyo basi alizunguka nyuma ya nyumba yao kwaajili ya kwenda kuosha gari, ila alipofika alimkuta Junior nae akiosha gari jingine ambapo Junior alipomuona Erick alimlalamikia kidogo,“Yani mama anachofanya sio sawa kabisa, utafikiri ni watu wasiokuwa na hela jamani! Hivi anashindwa nini kupeleka hizi gari car wash zikaoshwe huko mpaka tuoshe hapa nyumbani jamani!”Ila hii ni kawaida kwa mama maana anasema tuzoee maisha yote, tena kipindi cha nyuma hapa hata mdada wa kazi hakuwepo basi Jumamosi kama hii ni mwendo wa kazi tu yani mtafanya kazi hadi mkome, ikifika mchana utakuta tumelala tu maana mama huwa kuna kazi zingine anazigungua muda huo huo, tena hajaibuka hapa na kazi yake ya kusafisha madirisha, utaniambia akianza, yani mama ni wa kumzoea tu”“Yani anafanya kamavile watu wasiokuwa na pesa jamani! Hapo Angel atakuwa anasafisha ndani na Erica atakuwa anaosha vyombo, yani huyu mamdogo nimemshindwa tabia kwakweli”Erick alicheka na kusema,“Hamna, Erica ameambiwa kusafisha uwanja leo na vyombo vinaoshwa na Angel halafu Vaileth yupo jikoni kwani nyumba alishasafisha”“Oooh yani huyu mamdogo jamani dah!”Basi waliosha magari yale pale huku wakiongea mambo mbalimbali tu.Wakati Junior na Erick wakiendelea kuosha magari, mara alienda Erica na kumwambia Erick,“Weeee kimwanamke chako kimekuja”“Nani huyo?”“Sijui anaitwa Sarah”Erick alishangaa sana kusikia kuwa Sarah amefika kwa muda huo maana ilikuwa bado mapema sana, basi akamwambia Erica,“Mwambie nakuja, ngoja nimalizie”Erica akaondoka zake, Sarah alikuwepo kasimama tu maana alimkuta Erica anasafisha uwanja ndio akamwambia kuwa amekuja kumtembelea Erick, basi Erica alivyorudi pale akamwambia,“Kasema umsubirie anakuja”“Nipeleke alipo nikamuone”Basi Erica aliongozana na Sarah hadi kule nyuma ambako alikuwepo Erick akiosha gari, ila Sarah alivyomuona Erick alimkimbilia na kumkumbatia kisha akamwambia,“Erick tabia mbaya, napiga simu yako tangu jana hata hupokei, nakutumia meseji hata hunijibu jamani!”“Ngoja nimalize kazi kwanza”Basi Erick alijitoa kwenye mikono ya Sarah na kuendelea kuosha gari ila kiukweli lile swala la Sarah kumkimbilia Erick na kumkumbatia lilimuumiza sana Erica na kujikuta gafla akimchukia sana Sarah, kwani muda ule ule aliondoka zake, hata kule kusafisha uwanja hakuendelea tena kwani moja kwa moja alienda chumbani kwake na kwenda kuoga kisha kubadili nguo na kujilaza kitandani maana alikuwa na hasira.Muda huu Angel alimaliza kuosha vyombo na kuamua kurudi chumbani kwake, ila aliporudi akakutana na jumbe toka kwa Samir,“Jamani Angel nimekumiss hadi nahisi kuumwa”“Mmmh jamani Samir”“Kweli yani, nakuja kwenu muda sio mrefu”“Ila Samir unajua kama kwetu geti kali?”“Najua bhana, ila nakuomba Angel fanya juu chini nikuone tu mpenzi wangu nakuomba Angel, nakupenda sana”“Kwahiyo unakuja muda gani?”“Nakuja muda sio mrefu nitakwambia”Basi Angel akajiandaa pale kwani alijua wazi kuwa Samir anaweza hata akakodi pikipiki ili awahi na kweli baada ya muda kidogo tu ujumbe wa Samir ukaingia kwenye simu ukisema,“Angel, njoo nje basi mara moja tu”Basi Angel akatoka chumbani kwake, ila pale sebleni alimkuta bibi yake na mama yake ambapo mama yake alimuuliza,“Unaenda wapi Angel?”“Aaaah kuna kitu nakiangalia hapo nje ya geti tu”Basi Angel akatoka nje ila kiukweli hakupenda vile mama yake anavyomfatilia sana kwenye mambo yake, muda kidogo bibi yake Angel nae akamwambia mama Angel,“Eeeeh mwanangu, na mimi ngoja nikatembee kidogo nje ya nyumba yako yani sijawahi kutembea tembea hata kidogo jamani!”“Kheee kwahiyo mama unaenda kutembea nje ya geti?”“Ndio, nione na mandhari ya nje kabla sijaondoka, maana kuondoka kwenyewe kwenye gari, nitaangalia muda gani hiyo mandhari!”“Sawa mama”Basi bibi yake Angel nae akainuka na kutoka, ila alipotoka nje ya geti akamkuta Angel na Samir ndio wamekumbatiana, basi aliwasogelea karibu na kuwaachanisha, kiukweli Angel aliona aibu sana ila bibi yake alimuangalia Samir na kumwambia,“Wewe si ni Samir jamani!!”Angel alishangaa kuwa bibi yake kamfahamu vipi Samir!! Basi bibi yake Angel nae akainuka na kutoka, ila alipotoka nje ya geti akamkuta Angel na Samir ndio wamekumbatiana, basi aliwasogelea karibu na kuwaachanisha, kiukweli Angel aliona aibu sana ila bibi yake alimuangalia Samir na kumwambia,“Wewe si ni Samir jamani!!”Angel alishangaa kuwa bibi yake kamfahamu vipi Samir!!Ila Samir alionekana kuona aibu sana na kumsalimia bibi huyu,“Shikamoo”Halafu akageuka na kuondoka zake yani hata nyuma hakuangalia tena, basi bibi Angel alimshika Angel mkono na kuingia nae ndani, huku akitikisa kichwa chake aliingia nae ndani hadi chumbani kwake ambapo mama Angel nae aliwaona na kuwafata nyuma, basi bibi Angel alimkalisha Angel kwanza na kumuuliza,“Hivi unamfahamu vizuri Samir?”Angel alikuwa kimya tu, mama yake akadakia,“Samir tena!!”“Nimemkuta nae nje”“Kheee jamani Angel jamani, kwanini lakini!”Mama Angel akashikwa na hasira na kusogea karibu na Angel kisha kumnasa vibao kama vitatu ambapo alikatishwa na bibi yake Angel kwa kumwambia,“Kupiga mwanangu sio suluhisho, unajua mara nyingine sipendi makosa ambayo niliyafanya kwenu yakajirudia ila kuna wakati naona ni heri kumpiga mtoto ili kuweka akili yake sawa, ila kwa muda huu tuongee tu na Angel”Kisha bibi yake Angel alimuangalia Angel na kumwambia,“Angel, katika wamama ambao hawawezi kulea mtoto bila kumpiga basi mimi ni namba moja, yani hivi mama yenu anavyowapiga huwa anawagusa tu, maana mimi nikiamua huwa napiga hatari, uliza mama zako wote wakupe habari zangu, halafu kitu kingine ujinga sipendi kabisa. Unajua wakati mama yako akilalamika sikujua ni kwanini analalamika mpaka nilipokuona leo, unajua ningetaka kukupiga basi ningekupiga sana pale na hakuna wa kunizuia yani tambua hilo kabisa. Ila ninachotaka sasa ni kukufundisha kuhusu maisha, upo tayari kunisikiliza”Kwa aibu Angel alijibu kuwa yupo tayari kumsikiliza basi bibi yake akaanza kuongea,“Mara nyingi nimekuwa nikija chumbani kwako na kuongea nawe kuhusu mahusiano, Angel wewe bado ni binti mdogo sana usitake kuharibu maisha yako mapema kiasi hiki! Unafikiri ni kitu gani kinachofanya mwanaume akufate fate hivyo? Ni huko chini ndio kunamfanya aje mara kwa mara, na akikupata huko basi thamani yako ndio inapoanzia kushuka na itashuka kila siku, akikupa mimba ndio kabisa yani thamani yako itakuwa chini kabisa, unatakiwa ujithamini, jiheshimu na ujipende. Angel wewe ni binti mzuri sana ila kujiachia kwako kwa wanaume basi uzuri wako utapotea, thamani yako itapotea na utaonekana sio chochote wala sio lolote. Angel acha ujinga mjukuu wangu, acha ujinga kabisa, mimi huwa siongei jambo moja mara mbili. Nadhani umenielewa, nenda chumbani kwako tu”Muda huu mama Angel alikuwa kajiinamia tu kwani alijikuta akiwa na hasira sana juu ya mwanae, haswaaa baada ya kusikia kuwa alikuwa na Samir, ila Angel alipoondoka alikaa chini na mama yake na kumuuliza,“Kwani mama huyu Samir unamfahamu au wamejitambulisha kwako?”“Namfahamu vizuri yule mtoto, unajua bibi yake ni rafiki yangu sana, yani Samir na Angel wamepishana mwaka mmoja tu, nakumbuka siku yule binti anapata uchungu nilikuwa kwao na hadi anajifungua nilikuwepo. Baada ya hapo alikuwa akiulizwa kuhusu baba wa mtoto anabaki kulia tu”“Kheee kwahiyo Samir baba yake ni nani?”“Simjui ila baba yake Samir nasikia alikuwa ni muhuni sana, alikuwa na mahusiano na wanawake wengi, yani yule binti alikuwa akilia tu. Ila kwasasa ana maisha yake, kaolewa na anaishi na mumewe, ila ana watoto wawili tu, sema huyu wa pili ndio huwa simjui ila ni wakike na hawa watoto basi baba zao ni tofauti, sasa Angel anataka maisha ya namna hii jamani!! Maisha ya kuishi na kila mtoto na baba yake!! Sio maisha kabisa, unajua njia ulizopita wewe naona haka katoto kako nako kama kanataka kupitia, unatakiwa kuwa makini sana kumfundisha huyu mtoto ili asipitie kwenye hizo njia”“Nimekuelewa mama”“Nafurahi kama umenielewa, ila itakuwa vizuri zaidi kama nikienda kuishi na Angel nyumbani kwangu hadi matokeo yatakapotoka”“Oooh mama, hilo ni wazo zuri sana. Nashukuru kwa hilo, yani huyu Angel yupo kuniumiza kichwa tu ila hilo ni wazo zuri mama, unapoondoka basi utaondoka nae, ngoja nikamwambie ajiandae kabisa maana kesho safari”Kwakweli mama Angel alifurahi sana kwa Angel kwenda kukaa kidogo na bibi yake kwani aliona kidogo tabia ya Angel inaweza kutengemaa maana hata yeye aliharibika akili alivyoenda chuo ila kwa mama yake alikuwa akikaa sawa na kufata maadili ya mama yake.Angel alitulia chumbani kwake huku akifikiria siku hiyo alivyobambwa, ila akaja kuletewa taarifa na mama yake kuwa ajiandae maana ataondoka na bibi yake,“Aaaah mama jamani, nyie si mmenitoka kunitoa kwa bibi yule!”“Sitaki maneno mengi Angel, jiandae hapo ulipo na ujue kabisa kesho unaondoka na bibi yako”Kisha mama yake akatoka na kumfanya Angel abaki amekasirika sana kwani bibi yake huyo alimfahamu vizuri sana, basi akachukua simu yake na kumtumia ujumbe Samir,“Mwenzio nimeambiwa kuwa kesho nitaondoka na bibi, jamani umeniponza Samir, yule bibi alivyomkali yani itakuwa ngumu kwetu kuonana”“Usijali Angel, tutaonana tu. Maana huyo bibi ni kama bibi yangu ila najua kuonana kwetu kutakuwa kwa masharti sana ila usijali”“Sawa, yani nimekosa hata amani halafu kumkatalia mama siwezi”“Sawa mpenzi nimekuelewa kabisa, usijali kitu”Basi Angel aliamua tu kufanya maandalizi kama alivyoambiwa na mama yake ila kiukweli hakupenda kwenda kuishi kwa bibi yake kwani alielewa malezi ya bibi yake huyo yalivyokuwa.Wakati akiendelea kujiandaa, mara aligonga Vaileth mlango wake na kumkaribisha kisha Vaileth alianza kuongea nae,“Angel nasikia kesho unaondoka na bibi, ni kweli?”“Ndio hivyo, yani nitakoma maana huyo bibi namfahamu fika alivyo na mambo yake”“Ooooh pole mdogo wangu, jinsi huyu bibi anavyojua kufatilia mambo yani hadi nakuhurumia”“Yani acha tu, nimechukia hapa balaa, wewe umewasikia au?”“Ndio, nimewasikia wakiongelea basi nikamsema mmmh nimeanza kuwa Erica sasa kusikiliza yasiyonihusu”Angel alicheka na kusema,“Yani kale kaErica sijui tabia ya umbea katoa wapi jamani, mtoto ni mbea yule sijapata kuona, baba sio mbea, mama sio mbea ila yeye sasa akipata jambo anawashwa mdomo balaa”“Mmmh Angel una maana gani sasa?”“Aaaah sina maana yoyote, ila Erick na Erica kiukweli kabisa hawafanani, si sura wala sio matendo yao maana Erick ni mstaarabu, muelewa na mpole, ila Erica sasa uwiii ni mbea, anapenda kufatilia mambo ya watu, akisikia tu watu wanaongea kidogo basi yeye kashayabeba, yani yule mtoto jamani!”“Labda kuna ndugu yenu yuko hivyo, maana mbona Erica kafanana sana na mama yako! Yani kafanana nae sana kasoro huo umbea”“Aaaah aliyefanana na mama ni mimi bhana na sio Erica”Basi Vaileth akacheka tu, halafu Angel akaendelea kuongea,“Ila licha ya hivyo jamani Erica ni mbea hadi huwa siongei nae mara kwa mara wakati ni mdogo wangu ningekuwa napanga nae vitu vingi ila umbea wake hadi unakera”Vaileth alicheka na kumuacha Angel aendelee kujiandaa.Erick alipomaliza kuosha gari yani siku hiyo anaonekana hata hakupenda Sarah kwenda nyumbani kwao, basi alimwambia asubiri aende kuoga kwahiyo Sarah alimsubiri kule kule nje walipokuwa wakiosha magari, muda huo hata Junior alishaingia ndani na kujiandaa ila muda kupita bila ya Junior wala Erick kurejea Sarah alijiuliza kuwa tatizo ni nini, ila alipotaka kuinuka tu alifika pale Junior na kusema,“Kheee bado upon je jamani mtoto mzuri dah! Karibu ndani jamani”Basi Sarah aliongozana na Junior hadi ndani ambapo muda huu walimkuta mama Angel sebleni na baada ya kumuona tu Sarah alitabasamu ambapo Sarah nae alitabasamu kisha akaenda kumkumbatia huku akimuuliza,“Eeeeh za kwenu Sarah!”“Nzuri tu, mama anakusalimia”“Oooh wow, naomba ukirudi usalimie pia binti yangu. Vipi lakini za tangu siku ile”“Ni nzuri kabisa”“Nafurahi kusikia hivyo na nimefurahi kukuona kwa leo, kumbe kweli Erick alivyosema kuwa unakuja, oooh nimefurahi sana”“Na mdogo wangu hajambo!”“Hajambo, kachangamka sana kwasasa”Basi bibi Angel akaja na mtoto Ester amembeba maana alikuwa ameamka, basi yule bibi alivyofika pale Sarah alimsalimia vizuri sana na akahitaji pia kumsalimia mtoto ambapo bibi alimpa ili amsalimie ila leo wakati Sarah amekaa na yule mtoto akasema,“Yani mama jamani huyu mtoto amekufanana hatari, leo ndio nimemuangalia vizuri, ni wewe mtupu”Mama Angel alikuwa akitabasamu tu ila bibi Angel aliongezea na kusema,“Ila kweli Ester kakufanania sana jamani, yani Ester kakukopi vile ulivyo hapa mwanangu umejizaa”Mama Angel akamchukua mtoto wake huku akimuangalia vizuri na kutabasamu na wote walijikuta wakitabasamu na kufurahi.Erick alijua wazi kuwa mdogo wake amechukia sana siku hiyo, kwahiyo alivyomaliza kujiandaa alienda moja kwa moja chumbani kwa Erica na alimkuta amejilaza, basi alianza kuongea nae kwa kumuamsha,“Erica, Erica jamani Erica”Erica alishtuka na kukaa kwanza huku akimsikiliza kaka yake,“Sasa Erica umechukia nini jamani mdogo wangu!”“Hapana sijachukia mbona”“Erica, mimi nakufahamu vizuri sana na najua umechukia baada ya kumuona Sarah, hebu nisikilize hili kwanza”Erica alikaa vizuri na kumsikiliza kaka yake,“Sikia Erica, katika maisha yangu basi wewe ndiye ndugu yangu bora sana, kumbuka tumezaliwa wote na tumenyonya wote, tumecheza wote michezo yote inayojulikana, ukilia nipo, nikilia upo, nakuonea huruma na unanionea huruma. Jamani uwepo wa Sarah ndio ukuondoe amani jamani Erica! Kumbuka mimi ni nani kwako, kumbuka jinsi tulivyo mimi na wewe, yani Sarah ni mpita njia tu, tena ningependa awe rafiki yako maana ni rafiki yangu pia, akiwa rafiki yako utaona kuwa hana matatizo yoyote yale, usiwaze vibaya mdogo wangu nakupenda sana”Kisha Erick alimsogelea mdogo wake na kumkumbatia, kitendo hiko kilimfanya Erica ajihisi vizuri, kwani katika maisha yake alikuwa akipenda sana kujihisi kuwa anapendwa ndiomana hata swala la kuwa mtoto wa mwisho alilifurahia sana kwani aliona atakuwa akipendwa mno na wazazi wake, huku wakimsikiliza na kumthamini yeye, ila baada ya kupata mdogo wake aliamua kuishi kwa kutokudeka ila bado anapenda sana kugundua kuwa anapendwa sana kwahiyo alifurahi, kisha Erick alimuomba kuwa waende pamoja kuongea na Sarah ambapo Erica alikubali na wakaenda pamoja.Basi waliongea na Sarah pale mambo mbalimbali hadi Sarah alipoaga na mama Angel kumwambia tena Erick kuwa ampeleke, ila Sarah alikuwa akipenda sana ule muda way eye kuwa peke yake na Erick kwahiyo siku hiyo hakufurahi sana kwani aliona kama Erica anambania vile.Muda wa kuondoka, bado Erick alimuangalia Erica na kumtaka wamsindikize kwa pamoja Sarah, kwahiyo siku hiyo walipanda kwenye gari watatu yani Erick, Erica na Sarah na siku hiyo Sarah alikaa siti ya nyuma kwani pale mbele isingewezekana kukaa watatu.Moja kwa moja walienda hadi kwakina Sarah yani siku hiyo kwenye gari ilikuwa ni kimya kimya, tofauti na ile siku ya kwanza ambayo walikuwa wakiongea mambo mbalimbali wakati wapo Erick na Sarah tu.Walifika nyumbani kwakina Sarah na walimkuta mama Sarah ambaye alipowaona kama kawaida alishindwa kujizuia machozi yake kwa Erick, kwani alimsogelea na kumkumbatia huku akilia, na leo alilia kwa muda mrefu kidogo kwahiyo Sarah na Erica walisimama pembeni tu wakimuangalia jinsi yule mama alivyomkumbatia Erick huku akilia, na baada ya hapo aliwalazimisha kuingia ndani kwake ili kupata chochote cha kula, ila leo Erica aliweka mgomo na kudai kuwa wana haraka sana kwahiyo ilibidi wage tu na kuondoka zao.Wakiwa ndani ya gari Erica alimuuliza Erick,“Kwahiyo hata siku ile ulipokwenda kumsindikiza huyo Sarah ulikula kwao? Naona tu maana hata leo bila ya mimi ulitaka kukubali, ushasahau mama huwa anasemaje?”“Mmmh jamani Erica, mbona hata Sarah anakula kwetu kwanini sisi tushindwe kula kwao?”“Kula sehemu ni mpaka mama akubali, uoni mimi nilikuwa nakuja na visheti nyumbani! Ingawa nilikula vingine kisirisiri ila mama alinisema sana na nilimuahidi kutokurudia tena, sisi tutakula kwakina Sarah mpaka pale mama atakapomfahamu vizuri mamake Sarah”“Mmmh wewe nawe kwa kukuza maneno hujambo”Basi waliendelea tu na safari na kurudi nyumbani kwao.Baba Angel alirudi nyumbani kwake na kama alivyokuwa amemuahidi mke wake basi alirudi na zawadi ya kumpa mama yao, ambapo moja kwa moja alienda kumkabidhi zawadi hizo, hata bibi Angel alizifurahia sana kisha baba Angel sasa moyo wake ukawa mweupe kumruhusu mama yao,“Sasa mama, moyo wangu mweupe kabisa nakuruhusu”“Kumbe mlinikataza sababu ya zawadi jamani watoto wangu! Mmesumbuka jamani!”“Hamna mama hata usijali kitu, inapaswa kufanya hivi kwako maana umetuhudumia sana hapa nyumbani, umetulea, umeacha mambo yako mengi sana kwaajili yetu kwahiyo yatupasa kufanya hivi mama”“Haya, nashukuru sana wanangu”Basi baba Angel alirudi chumbani kwake kwani alikuwa amechoka, mke wake alimfata na kumpa habari kuwa Angel ataondoka kesho na mama yao,“Jamani, tunampa tena mama mzigo wa Angel?”“Hamna, mama atakaa nae vizuri tu, naomba ukubali hilo mume wangu. Naelewa mama yangu alivyo”“Hata mimi namuelewa sana”“Unajua leo mama kamkuta Angel na Samir getini kwakweli kachukia sana, halafu anamfahamu vizuri sana Samir, hamfai mtoto wetu, nasikia baba yake ni muhuni sana kwahiyo lazima Samir atakuwa na tabia za baba yake. Halafu siku ile ulisema kuna mtu unamfananisha na Samir ni mtu gani?”“Oooh nitakuonyesha tu siku moja, utamuona ila unamfahamu sema humfahamu kivile ni rafiki yangu”“Oooh hapo sawa, nikajua ni ndugu yako”Baba Angel alicheka kwa muda kidogo na kusema,“Ila huyo rafiki yangu sio muhuni kwahiyo hawezi kuwa baba wa Samir”“Na kweli maana duniani ni wawili wawili, ila hata hivyo mara nyingine unakuta mtoto na baba wanafanana kwa mbali sana kama wewe na baba yako mlivyokuwa”“Oooh umenikumbusha yule mzee wangu, alikuwa ni mzee mtata, ila nilimpenda jamani baba yangu, dah angekuwepo hadi leo aangalie wajukuu zake”“Na hivi Angel alivyokuwa anavutia unadhani baba yako anagejistahi amuache!”“Mmmh ushaanza hivyo na maneno yako ya kijinga, hata kama baba alikuwa na tabia mbaya ila bado asingeweza kumtamani mjukuu wake, kwani Angel ni kama mjukuu wake pia. Halafu kumbuka japo fadhila za baba yangu jamani, kumbuka baba ndio alisimamia harusi yetu yote yani yeye ndiye aliyegharamia kila kitu, kumbuka pia wakati unajifungua hawa mapacha wetu ni baba yangu ndio alikuwa karibu”“Ila Erick hujui tu, mimi nafahamu mambo mengi sana ila sikuweza kukwambia kwani sikutaka ugombane na baba yako, hujui tu ni kwanini baba yako aligharamia harusi yetu na kuhusu kuwepo wakati najifungua ilibidi iwe vile kwani ni yeye aliyekupa kazi wewe kwahiyo hakukuwa na namna zaidi yayeye kuwepo. Namshukuru kwa mazuri aliyotufanyia, ila Erick baba yako alikuwa ni kichomi, hujui ni nini alikuwa akiongea na mimi kila alipokutana nami, kuna mengi yapo kwenye moyo wangu nadhani nikisema utaona kamavile namkosea heshima marehemu mkwe wangu. Ngoja niishie hapo”“Ndio bora uishie hapo maana sio vizuri kuwaongelea vibaya marehemu”Muda huo waliamua kubadili mongezi na kuendelea na maongezi mengine ya jinsi ya kumfikisha mama yao nyumbani kwa siku ya kesho.Basi usiku wa leo Angel alikuwa na mawazo tu ya kwenda kuishi kwa bibi yake yani alimtambua vizuri bibi yake huyu basi alikuwa akiongea mambo mbalimbali na Samir kwenye simu,“Jamani Smair ndio kesho hivyo naenda kwa bibi”“Hakuna namna Angel, najua wazi ukikataa basi watakuhisi vibaya sana, tutakuwa tukiwasiliana tu kama kawaida na kuonana tutakuwa tukionana kwani nitakuwa nakuja chuo”“Ila nahisi bibi atakuwa na tabia Fulani kama za shangazi, maana hadi ilikuwa nikichelewa kurudi shule dakika mbili tu lazima niwe na maelezo ya kutosha ingawa nilikuwa narudi na dereva, huyu bibi si ndio balaa”“Wala usihofu kitu mpenzi wangu”Wakawasiliana sana kwa muda huo na kama kawaida waliongea sana hadi mwisho wa siku walilala muda ukiwa umeenda sana.Kulipokucha, Angel alikuja kushtuliwa na mama yake maana tayari ilikuwa pamekucha halafu yeye alikuwa bado amelala, basi mama yake akamwambia.“Wewe Angel hebu amka ujiandae kuondoka”“Kheee mama ndio mapema hivi!!”“Ndio, mambo yote asubuhi”Basi Angel aliinuka na kujinyoosha halafu alienda kuoga na kujiandaa baada ya kutoka alimkuta bibi yake alishajiandaa na baba yake kwahiyo alipotoka tu aliaga ndugu zake na moja kwa moja kutoka nje pamoja na bibi yake na baba yake kwaajili ya safari yani Angel alikuwa amepanda kwenye gari huku amepooza sana na safari ilikuwa ikiendelea.Basi siku hii wakina Erica walivyoenda Kanisani, mama Angel alimuagiza dreva wao akamtafutie zawadi kwaajili ya mama mkwe wake kwani naye alitaka wakamshtukize mama mkwe wake, nyumbani alibaki yeye na Vaileth basi walikuwa wakiongea mambo mbalimbali,“Hivi Vaileth mwanaume uliyezaa nae yuko wapi?”“Mama, alikataa mimba ikiwa ndogo kabisa yani nilijihisi kama nimetengwa basi nilihangaika na ile mimba hadi kujifungua, mtoto wangu ni wakike, alipofikisha miaka mitatu yule mwanaume akatokea na kumtaka mtoto, basi nyumbani wakamwambia alipe faini, ila alijigeresha kufanya hivyo basi bibi yangu akaniambia kuwa nimpeleke kwake kwani yule mwanaume anaweza akamuiba, basi ndio mtoto nilimpeleka kwa bibi ndio kule mlikonikuta, maana nilikuwa nikienda kufanya kazi namuacha kwa bibi na ndio ipo hivyo hadi leo na ameshazoea mazingira ya kule kwa bibi, kwasasa ndio ana miaka mitano”“Oooh, hapo nimekuelewa, kwahiyo huyo mwanaume hajakutafuta tena?”“Hajanitafuta, nasikia kwanza ameoa ila mkewe hazai ndiomana alikuja kumchukua mtoto, nasikia anamtaka mtoto ila hataki kulipa faini”“Jamani kuna wanaume vichomi sana loh! Kwasasa angalia maisha yako tu Vaileth”“Ndio hivi dada”Basi Vaileth aliendelea na mambo mengine, kisha yule dereva alirudi na zawadi ambazo mama Angel alimuagiza basi aliziweka vizuri na kujiandaa huku akimsubiria mumewe arudi.Na baada ya muda kidogo tu baba Angel alirudi na mama Angel akamuomba waende kumuona mama mkwe wake,“Kheee umekumbuka nini mke wangu?”“Hamna nataka nikamuone tu”“Ila mtoto bado mdogo”“Aaaah sio mdogo huyu, mbona kakua sasa, twende tukamuone tu kidogo halafu tutarudi nishajiandaa na nishamuandaa mtoto”Basi baba Angel hakuweza kukataa kwani muda huo huo aliondoka na mke wake kuelekea kwa mama yake ambapo kulikuwa na umbali kidogo na pale walipokuwa wakiishi.Basi walipofika hata mama yule alishangaa sana kwani hakuamini kama wangeenda na ukizingatia hawajamwambia,“Kheee jamani kweli mmeamua kunishtukiza mweeeh!!”Kisha aliakaribisha ndani na walimsalimia vizuri sana ila alijihisi aibu maana tangu mama Angel ajifungue hakwenda kumuona, basi akamwambia,“Erica mwanangu nisamehe bure tu, ila mlinikera kipindi kile kwa kitendo chenu cha kumchukua Angel bila ridhaa yangu”“Tusamehe kwa hilo mama”“Nishawasamehe tayari na nimefurahi kweli kuja kwenu kuniona”Kisha Erica akampa mama mkwe wake zawadi ambazo alimtuma dereva, kwakweli huyu mama alifurahi sana kupokea zile zawadi ila akasema,“Jamani, natakiwa mimi nimletee mjukuu wangu zawadi ila mimi ndio nimeletewa jamani!”“Usijali mama”Basi aliaenda kuziweka zile zawadi ndani, huku baba Angel akimwambia mama Angel,“Naona ulitaka kunishtukiza na mimi jamani hata kuniambia kuwa umemnunulia mama zawadi!!”Mama Angel alitabasamu tu, kisha bibi Angel alirudi na kuendelea kuongea nao ambapo baada ya muda kidogo tu walimuaga kuwa wanaondoka maana walichelewa kwenda na vile vile kule palikuwa ni mbali na kwao ila hakuwazuia kwani pia alifurahi kuwaona tu.Siku hii ilikuwa ni kama kuwaachia ukumbi wakina Erica maana walivyotoka Kanisani walikuwa na furaha sana, ukizingatia wazazi wao wote hawakuwepo, basi waliweka mikanda ya ngumi sasa na kuanza kuangalia, ile mikanda ambayo ililetwa na Samia, basi walikuwa wakiongea pale ambapo Junior alianza kusema,“Ila jamani bora bibi kaondoka, maana yule bibi alikuwa mnoko balaa”Wote walikuwa wakicheka, basi Vaileth akasema,“Yani mimi niliposikia anaondoka nilichekelea, ila sasa kazi ipo kwa Angel jamani mbona balaa kwake”“Na kweli balaa, yule bibi yetu tunamfahamu vizuri sana, yani kule lazima Angel aumie moyo. Ila jamani tuache utani, yule bibi ndio kamfananisha Erica, huwa tunajiuliza Erica katoa wapi umbea ila ni kwa yule bibi”Walicheka wote ila Erica alinuna, huwa hapendi kusemwa semwa kwa kitu anachokifanya kweli, kisha akainuka zake na kwenda chumbani kwake ila wenzie waliendelea kuangalia tu ule mkanda hadi wazazi wao waliporudi ndio waliposhtuka na kuzima tv.Basi mama Angel cha kwanza kabisa alimuulizia Erica maana alijua lazima angekuwa pale anaangalia tv ila akaambiwa kuwa yupo chumbani,“Mmmh mtakuwa mmemkorofisha mwanangu nyie, haiwezekani make hapa halafu yeye ajifungie chumbani”Basi alienda kumlaza mtoto na moja kwa moja kwenda chumbani kwa Erica ambapo alimkuta kajilaza, akamuamsha na kuanza kuongea nae,“Mwanangu, tatizo ni nini? Unaumwa?”“Hapana mama, eti wanasema mimi umbea nimeutoa kwa bibi”“Aaaah wajinga hawa, nani huyo aliyekuwa anakwambia hivyo!”“Junior huyo mama”“Aaaah achana nae, halafu mwanangu jana hujanipa habari ya kwakina Sarah ulivyorudi nimehisi kama unajambo maana ulikuwa unakuja chumbani kunichungulia na kuondoka, eeeh niambie mwanangu”“Mmmh mama, tulivyofika kwa kina Sarah basi mama yake Sarah akamkimbilia Erick na kumkumbatia halafu akaanza kulia yani alilia kwa muda mrefu sana”“Mmmmh mbona unanishangaza Erica, kwanini alilia sasa?”“Sijui mama, halafu baada ya hapo akaanza kutulazimisha tule chakula ila mimi nilikataa na kumtaka Erick tuondoke basi ndio tukarudi nyumbani”“Oooh natakiwa nimfahamu huyo mama yake Sarah”Mara simu ya Erica ilianza kuita, basi mama yake alimuangalia na kuuliza,“Nini hiko kinaita kama simu?”Erica alibaki kimya akimuangalia mama yake. Mara simu ya Erica ilianza kuita, basi mama yake alimuangalia na kuuliza,“Nini hiko kinaita kama simu?”Erica alibaki kimya akimuangalia mama yake.Ilibidi mama yake amuulize kwa ukali kwani ile simu ilizidi kuita,“Nimekuuliza nini hiko kinaita kama simu?”Basi mama yake alikuwa kama anataka kumpiga, katika vitu ambavyo Erica alikuwa akiogopa ni kupigwa basi kwa haraka haraka aliitoa ile simu na kumpa mama yake huku akimwambia,“Mama nisamehe”“Haya, umetoa wapi hii simu, nani kakupa simu Erica unajua wewe ni binti mdogo sana!”“Kanipa kaka Junior?”“Una uhakika kakupa Junior! Kakupa kwa misingi ipi, yani kwanini Junior akupe simu utumie?”“Mama, baada ya kumuona Erick akiwa na simu nami nilitamani simu basi kaka Junior akaenda kuninunulia”“Kheee kumbe na Erick ana simu!! Kaitoa wapi na yeye?”“Ni baba ndio alimnunulia”“Aaaah humu ndani jamani, yani mtu lazima upatwe na ugonjwa wa moyo. Haya lete hiyo simu na huyu Junior atanieleza ni kitu gani kimemfanya hadi akununulie simu”Erica alimkabidhi mama yake ile simu ambapo mama yake alitoka kwa hasira na kumuita Junior na kuanza kumfokea kwanini kamnunulia simu Erica, yani Junior alianza kuwa na mashaka kuwa huenda Erica kasema ukweli wote ila ilibidi anywamaze tu, basi mama Angel alimsema sana na kuondoka zake.Moja kwa moja Junior alienda kuongea na Erica ili kumuuliza vizuri,“Imekuwaje Erica hadi umekamatwa na simu?”“Kaka ile simu hukunitolea mlio, leo imeita basi mama kasikia, yani sikuwa na watu wa kunipigia simu ila leo kuna mtu alikuwa akipiga ndio mama kasikia”“Kwahiyo umemuelezea kila kitu?”Erica akamwambia vile alivyomwambia mama yake, basi Junior alitabasamu na kusema,“Kwasasa nimekupenda bure Erica, yani hujasema kuhusu hili oooh asante sana, yani nimekupenda mno mdogo wangu. Usijali acha mama aichukue hiyo simu ila nitakuwa nakuletea vitu vizuri vizuri mara kwa mara”“Ila unajua Erick atachukia sana baada ya mimi kumsemea kwa mama kuwa ana simu!”“Aaaah usijali kwani hata hivyo mama angejua tu, sababu baba angemwambia. Usijali mdogo wangu, kesho tu nitakuletea zawadi yako”Basi Erica alitabasamu tu na kumfanya Junior aondoke akiwa na furaha sana kwani kwake ilikuwa raha mno kwa kugundua kuwa Erica hajasema ukweli.Mama Angel alienda chumbani moja kwa moja kuongea na mume wake ambaye kutokana na uchovu aliokuwa nao basi alikuwa amelala muda huo, ilibidi mama Angel amuache tu mumewe apumzike kwani hata yeye alitambua ni kiasi gani ambavyo mumewe amechoka kwa siku hiyo.Ila aliona jambo la msingi kwanza ni kwenda kumpokonya Erick simu aliyoambiwa kuwa anatumia, basi alitoka na moja kwa moja kwenda chumbani kwa Erick ambapo alimkuta Erick ndio anatumia ile simu ambayo aliificha baada ya mama yake kuingia,“Erick nimekuona na hiyo simu, haya ilete”Ilibidi Erick aitoe na kumkabidhi mama yake, kisha mama yake akamuuliza,“Baba alikununulia simu kwa misingi ipi?”“Ili niwasiliane nae”“Uwasiliane nae muda gani wakati muda wote tunaonana hapa nyumbani, mwanangu yawapasa kuwa makini na masomo yani kwasasa kitu muhimu katika maisha yenu ni elimu na sio mambo ya simu. Tunakutegemea wewe ndio mlezi wa familia, wewe ndio wa kuwaangalia dada zako halafu wewe ndio unafanya ujinga wa kutumia simu kweli!! Achana na mambo ya simu jamani! Nadhani umenielewa”“Nimekuelewa mama”Kisha mama Angel alitoka na kurudi chumbani kwake ila muda sio mrefu Erica alienda chumbani kwa Erick ili kumuomba msamaha, alimkuta Erick kajiinamia tu kwani mama yake amechukua simu wakati ndio alitaka kumjibu ujumbe Sarah, basi Erick alimshtua pale na kumwambia,“Naomba unisamehe Erick”“Umefanya nini kwani?”“Mama leo kanibamba na simu basi nikamwambia ukweli kuwa hata wewe unayo”“Dah! Erica wewe ni mtu wa ajabu sana, unajua mama hajasema ni nani kamwambia wala nini, nilijua ni baba kaamua kumwambia mama ukweli kumbe ni wewe! Hata hivyo nadhani baba alimwambia mama siku nyingi tu ila hakutilia maanani sema leo ulipomwambia wewe ndio kaelewa, jamani Erica mambo yako sijui hata nikufananishe na nini jamani!”“Ila nisamehe jamani Erick”“Nishakusamehe hatabusijali mdogo wangu”Kwasasa Erica alifurahi na kumuaga kaka yake kisha kurudi chumbani kwake kulala.Usiku wa leo ulikuwa ni usiku wa furaha sana kwa upande wa Junior, kwanza bibi yao hakuwepo tena halafu Erica hakusema ukweli licha ya kukamatwa na simu, basi Junior kama kawaida alienda chumbani kwa Vaileth huku akisifia sana siku ile,“Yani Vaileth hujui tu jinsi mimi na wewe tunavyopendana, hata Mungu anatambua hili ndiomana tunaachiwa nafasi kubwa ya kuwa pamoja”Vaileth akatabasamu na kuuliza,“Kivipi?”“Kwanza bibi hayupo, halafu unajua nini leo Erica alibambwa na simu na mamdogo yani leo ndio ingekuwa siku mbaya kabisa kwetu kwa jinsi Erica alivyokuwa mbea halafu maneno yake yanavyoaminika kwenye nyumba hii, ni hivi Erica kamdanganya mamdogo kwahiyo tupo huru kabisa”“Mmmh siamini, kwahiyo Erica hajasema ukweli?”“Ndio, nadhani kaanza kukua sasa kwahiyo kaanza kujitambua”Basi wakafurahi sana na siku hiyo walilala huku wakitabasamu muda wote kwani walikuwa na furaha sana.Kulipokuchja, Vaileth aliamka na kumuacha Junior bado amelala chumbani kwake, basi alienda kusafisha nyumba ila baada ya muda kidogo mama Angel alimfata Vaileth na kumuuliza,“Umemuona Junior ametoka?”“Hapana mama”“Jamani, yuko wapi huyu mtoto asubuhi yote hii!! Nina shida nae halafu nadhani chumbani kwakwe hayupo, kafunga mlango na nimeita sana. Ngoja nikaulize kwa mlinzi kama kamuona kutoka”Basi mama Angel alienda nje na moja kwa moja Vaileth alienda chumbani kwake kumkurupua Junior ili arudi kwake,“Weee Junior, mama anakutafuta huko hebu amka”Basi Junior aliinuka na kujinyoosha kisha kuamka halafu kutoka ila alipokuwa nje tu akakutana na mamake mdogo ila Junior alijegeresha kidogo ambapo mama Angel alimuuliza,“Ulikuwa wapi wewe?”“Nilienda ile sebule nyingine, nilikuwa nasoma soma magazeti”“Mmmh mbona macho yako yanaonyesha kuwa ndio umetoka kuamka?”“Kumbe nilisinzia kule mamdogo, nisamehe bure”“Haya nenda kajiandae mara moja, kuna mahali nataka nikuagize”Basi Junior alienda kujiandaa na alipomaliza alienda na kuagizwa na mama yake mdogo, ila alipomuagiza palikuwa ni ofisini.Junior alivyoondoka tu, mama Angel alipigiwa simu na dada yake,“Jamani! Leo mapema yote hii dada umeniota au?”“Hapana mdogo wangu, ila nimemkumbuka tu Junior jamani nimeshangaa nikipatwa na mawazo kweli kuhusu Junior, yuko hapo niongee nae”“Oooh samahani dada, kuna mahali nimemuagiza”“Asubuhi hii ni ofisini nini?”“Ndio ni ofisini, kwenye ile ofisi iliyokuwa ya baba yake, kuna kitu cha muhimu walikuwa wakikihitaji na mimi ndio nilikuwa nafahamu, sasa si unajua uzazi tena sijaweza kwenda ndio nimemtuma Junior”“Mmmh wewe nawe ulikuwa ukifahamu nini, nakumbuka ile ofisi ulifanya kazi za kujitolea tu na hata hukufanya kwa muda, ila dah! Nimekumbuka kitu jamani”“Kitu gani?”“Unajua ile ofisi ilitakiwa iwe ya Junior kwasasa, jamani kweli maisha yanabadilika sana, nakumbuka wakati nina mimba ya Junior basi mume wangu alikuwa akifurahi sana huku akinishika tumbo langu na kusema huyu ndio mrithi wangu ila leo hii dah!”“Aaaah dada jamani! Kila kitu ni Mungu anapanga, na kama ofisi ilitakiwa kuwa ya Junior basi amini kuwa siku moja itarudi mikononi mwa Junior, hata mimi sikujua kama naweza kutafutwa na watu wa ile ofisi hadi nimemtuma Junior, elewa kila kitu Mungu anajua ni kwanini kimetokea”“Naelewa, ila jamani maisha haya, kuna mambo nikikumbuka huwa machozi yananitoka tu”“Jamani dada, usiseme hivyo. Nadhani inatakiwa tupate muda wa kuzungumza zaidi, basi njoo kwangu”“Sawa nitakuja mdogo wangu”Basi wakaagana pale kisha mama Angel alienda kuendelea na kazi zingine.Junior alipofika kwenye ofisi ambayo alielekezwa na mama yake mdogo, moja kwa moja alienda kukutana na mtu aliyeambiwa akutane nae na kumkabidhi alichotakiwa kumkabidhi ila yule mtu akasema na kuwaita wenzio,“Jamani hebu muangalieni kijana huyu, mnamfananisha na nani?”“Mmmh huyu kijana kafanana na James jamani, yani mule mule. Sio mtoto wake kweli huyu!!”Junior akatabasamu kwani anafahamu wazi kuwa baba yake ni James, ila hakuwahi kuelezwa kuhusu mali ambazo baba yake aliziacha, basi mmoja akamuuliza,“Kwani unaitwa nani kijana?”“Naitwa Junior James”“Oooh tuko sahihi kumbe, ni mtoto wa James huyu jamani!”“Baba yako alikuwa mtu mzuri sana, alikuwa na upendo kwa kila mtu yani pengo lake hakupatikana wa kuliziba kabisa, tunafurahi kumuona James namba mbili. Kwahiyo unaishi na Erica maana yeye ndio kakutuma!”“Ndio naishi nae”“Oooh sawa”Basi bosi wa mule alimuomba Junior ofisini na kuchukua mawasiliano yake, kisha Junior aliagana nae na kuondoka zake, ila Junior hakuelewwa kama ofisi ile iliwahi kuwa ofisi ya baba yake, yani yeye aliona kawaida tu wala hakuona tofauti.Wakati anarudi kwa mamake mdogo, alikutana na mtu njiani ambaye anakumbuka kuwa mamake mdogo alisema atamchunguza mtu huyo ilia one kama wanaundugu, basi alisalimiana na mtu yule, alikuwa ni kijana James, yani umri wake na Junior haukutofautiana sana.“Nimefurahi kukuona tena James”“Hata mimi nimefurahi, nilimuuliza tu kidogo mjomba ila hakunijibu vizuri, mama yangu nae huwa hataki kabisa kusema kuhusu baba yangu”“Hakuna tatizo, tupeane tu mawasiliano na tuwe tunawasiliana”“Oooh kwa bahati mbaya, simu yangu imepotea jana. Ila ngoja nikuelekeze ninapopatikana”Kisha James alimuelekeza Junior mahali ambapo huwa yeye anapatikana kwasana, kisha wakaagana na moja kwa moja James alirudi nyumbani ambapo baada ya muda kidogo alienda chuo.Junior akiwa chuo leo alionana na Angel ambapo muda wa karibia na kutoka alikaa nae na kuzungumza nae kidogo,“Vipi maisha kwa bibi?”“Dah! Yani siku hii moja nimejiona kama nimefungwa miaka jamani, bibi anafatilia yule balaa. Hivi kaongea na baba kuwa nihamishwe chuo ili nikasome kule kule karibu na kwake, kwahiyo ndio hivyo, baba ananihamisha siku sio nyingi ili nikawe karibu na bibi”“Mmmh pole, nilihisi tu”“Yani yeye ndio kaongea na huyu dereva, nahisi dereva kapewa masharti huyu kuhusu mimi balaa”“Kheee pole mdogo wangu, namfahamu yule bibi pole sana”Basi dereva wa Angel alikuwa kashafika kwahiyo ilibidi Angel atoke tu darasani kwenda kupanda gari ila kwa mbali alimuona Samir na kutabasamu kisha akampungia mkono na kuingia ndani ya gari kwani hakuruhusiwa kwenda popote pale.Moja kwa moja alirudi kwa bibi yake ambaye alimkuta muda huo amekaa anafanya vikazi vyake vidogo vidogo kisha bibi akamwambia Angel,“Eeeeh bora umerudi, ila huko chuo ni mbali sana ngoja nimkumbushe baba yako afanye utaratibu wiki hii hii”“Sawa bibi”“Ukapike sasa”Basi Angel alienda kuweka vitu vyake na kuelekea jikoni ambako alianza kupika kama bibi yake alivyotaka.Leo wakati wa kutoka shule, Sarah alionekana kumlaumu sana Erick kwa kutojibu jumbe zake na kwakutopokea simu zake,“Ila Erick una tabia mbaya jamani, kwanini unanifanyia hivi!!”“Samahani Sarah, ila mama kaninyang’anya simu”“Jamani atakunyang’anya vipi simu? Ona mimi natumia simu, ni mama yangu mwenyewe ndio alininunulia, sasa mama yako atakunyang’anya vipi?”“Kwa kifupi, mama yangu hapendi nitumie simu Sarah”“Duh! Jamani, sasa tutakuwa tunawasiliana vipi?”“Nitakupa namba zetu za simu ya mezani ili ukinikumbuka unipigie kwa namba hizo”“Jamani! Ila sawa, sema nitakuwa nakumiss sana Erick jamani”Basi walifika kwakina Erick naye Erick alishuka, ila siku hiyo pale getini kwao tu alimkuta mwanamke ambaye ni Sia, kiukweli Erick alichukia na kutaka kumpita bila ya kumsalimia ila Sia akamvuta na kumwambia,“Erick, hutakiwi kunichukia mimi, hutakiwi kunidharau mimi ila unatakiwa kuniheshimu na kunipenda”“Sikupendi na kamwe sitaweza kukupenda”“Acha roho mbaya Erick, hata baba yako mzazi hana chuki kama wewe maana naye ni mpole na mwelewa, nakupenda mwanangu Erick”“Achana na mimi”Erick alijitoa kwenye mikono ya yule mwanamke na kuingia ndani, kumbe muda ule baba Angel nae alikuwa anarudi kwahiyo alimuona Erick na Sia pale getini, yani yeye alivyofika alishuka na kumvuta Sia huku akimwambia,“Hivi lini utaacha kuifatilia familia yangu wewe!”“Ila sijaifatilia familia yako, sema nimemfatilia mwanangu Erick”“Haya nipe uthibitisho kuwa Erick ni mwanao?”“Sina uthibitisho wowote, ila mimi ndiye mama halali wa Erick”“Haya kama ni hivyo ulikuwa wapi miaka yote hii kuja kumdai mtoto wako!!”“Ni historia ndefu sana, ila kadri Erick anavyokuwa namuona anakuwa kijana mzuri sana, mpole, mtii na anapendeza halafu ana huruma sana, kwakweli napenda kumuweka kwenye himaya yangu, Erick ni mtoto wangu”“Hebu nitolee wazimu wako mie, kwanza nisikilize kwa makini, kipindi mke wangu akiwa mjamzito nilienda nae hospitali kupima na tulipima na kugundua kuwa mke wangu ana mapacha wakike na wakiume, sasa kipindi cha kujifungua, mwanzo mwisho, mke wangu alipelekwa kwenye hospitali ya kipekee sana na alisimamiwa vizuri sana na baba yangu kuhakikisha usalama wa wajukuu zake, hata nilipofika, ni yeye alikuwa wa kwanza kuwapokea watoto wale na kama hujui ni yeye aliyetoa majina ya watoto wetu yani Erick na Erica ila sisi tuliyatilia mkazo tu, sasa wewe ushahidi wako ni nini kuhusu Erick kuwa mtoto wako?”Cha kushangaza Sia alicheka sana na kusema,“Mimi sina ushahidi ila naongea ukweli, halafu unapomkumbuka Erick usimsahau na Elly maana anakuhusu pia”“Hivi mwanamke una wazimu wewe au?”Ila Sia alimsogelea baba Angel ili amkumbatie ila baba Angel alimsukuma pembeni halafu akarudi kwenye gari yake na kupiga honi ambapo mlinzi alimfungulia na kuingiza gari yake ndani akiwa amechukia sana, na alipoingia tu ndani moja kwa moja alienda kuongea na mtoto wake Erick,“Mwanangu yule mjinga alikuwwa akikwambia nini?”Basi Erick alimueleza baba yake kile ambacho alikuwa akiongea na Sia,“Yani ni mwehu yule, ila dawa yake inachemka usijali kitu mwanangu”“Asante baba”Basi baba Angel alitoka na kuelekea chumbani kwake.Muda huu alimkuta mama Angel kajilaza na mtoto basi akamshtua kidogo mke wake kwani alikuwa na hasira na alihitaji kuongea nae kidogo ili aweze kupumua na roho yake, alimbusu kwenye paji la uso ambapo mama Angel aliamka na tabasamu huku akimuangalia mume wake, kisha baba Angel alimwambia,“Nakupenda mke wangu”“Nakupenda pia, naona ni siku njema hii”“Siku zote ni siku njema kwetu, nimekukumbuka mke wangu”Basi ikabidi mama Angel aamke vizuri ili wakae na mumewe waweze kuzungumza.Siku hii baba Angel aliamka na uchovu kiasi na asubuhi hii aliongea kidogo na mke wake,“Eeeeh mke wangu, kuna mahitaji gani ambayo yanatakiwa humu ndani?”“Hamna mume wangu, yangekuwepo ningekwambia kabla ya kuuliza, ila umenikumbusha kitu kumbe ulimnunulia Erick simu!!”“Ndio, sababu Sia alikuwa akimfatilia nikaona vyema nimnunulie simu ili akiwa anamfatilia aniambie”“Jamani mume wangu, mfano shuleni atakwambiaje wakati wanakatazwa simu shuleni! Mimi nimempokonya maana Erica nae alinunuliwa simu na Junior sababu tu Erick anatumia simu”“Sijakuelea hapo, Erica alinunuliwa simu na Junior kivipi?”Ikabidi mama Angel amsimulie baba Angel vile alivyomkamata Erica na simu, basi baba Angel alielewa ile hoja ya mke wake na kuamua kujiandaa kwaajili ya kwenda kwenye kazi yao.Alipomaliza kujiandaa alimuaga mke wake na kuondoka, ila wakati anatoka getini muda huu alimuona Sia akiwa amesimama na mtoto wa kiume mwenye umri kama wa Erick, kiukweli baba Angel hakumpenda mwanamke huyu kwahiyo alimpita kamavile hamuoni wala nini, yani baba Angel alikuwa akienda kazini huku akiwa na mawazo sana kwani aliona huyu mwanamke anamchanganya akili yake, ila akiwa barabara kuu kuna mtu alisimamisha gari yake ikabidi asimame na alipomuangalia vizuri mtu yule akamuona kuwa ni madam Oliva, basi yule madam aliingia kwenye gari ya baba Angel na kukaa kwenye siti huku akisema,“Yani nilivyoona gari yako tu nikahisi moyo wangu ukidunda ndio nikakusimamisha”“Oooh jamani, sasa moyo wako umedunda kwanini madam?”“Aaaah tuachane na hayo, unaenda wapi muda huu?”“Naenda ofisini”“Basin i vyema nikafahamu ofisi yako ilipo”“Sawa, hakuna tatizo lolote. Karibu sana”Basi baba Angel alienda na madam Oliva hadi ofisini kwake na kumkaribisha, kwakweli Oliva aliipenda ofisi ya baba Angel kwani ilipangwa vizuri sana, kwahiyo aliingia nae ofisini na kuanza kuongea nae mawili matatu,“Nimeipenda ofisi yako baba Erick jamani”“Oooh asante sana”“Halafu mke wako natamani sana kumfahamu jamani! Naamini nitamfahamu tu, ila baba Erick unaonekana ni mwanamke mstaarabu sana wewe, kwakweli mkeo ana bahati kubwa sana ya kukupata. Sema itakuwa ni vyema sana mimi na wewe tukiwa tunaonana na kuongelea maendeleo ya watoto shuleni au unasemaje?”“Ni kweli kabisa, sina usemi kuhusu hilo”“Basi, nitapenda upafahamu nyumbani kwangu pia”“Sawa madam, nitapafahamu tu”“Hata leo ukitaka”“Hapana, kwa leo kuna kazi imenitinga labda siku nyingine”“Basi tutawasiliana na nitafurahi sana juu ya hilo, maana ni vyema sana kwa wazazi kubadilishana mawazo”Kisha Oliva alimuaga baba Angel kwani alitakiwa pia kuwahi kwenye kazi yake ambapo alikuwa akifundisha kwenye shule aliyosoma Erick.Mama Angel akiwa katoka kumuogesha mtoto wake ambaye mara nyingi sana akioga tu analala, alishangaa mlinzi kufika sebleni na moja kwa moja aliitwa yeye na Vaileth,“Samahani mama, nje ya geti kuna mgeni wako nimemwambia aingie ila alikataa”Basi mama Angel akajiuliza ni mgeni gani huyo? Ila akatoka kwenda nje kumuangalia, alishtuka sana baada ya kukuta mgeni mwenyewe ni Sia na Elly yani Sia alikuwa kamshika mkono Elly basi mama Angel alipofika pale Sia alimkabidhi mama Angel mkono wa Ellyn a kumwambia,“Mtoto hajaenda shule huyo leo sababu anaumwa na mimi sina pesa ya matibabu, kwahiyo ukamtibie”Halafu Sia alimuacha pale Elly na mama Angel kwakweli mama Angel hakuwa hata na la kusema kwani Sia alikuwa kama kaongea na dereva wa bodaboda sababu alipomaliza tu kuongea hayo, ilifika bodaboda na kumchukua halafu akaondoka nayo.Basi mama Angel alimuangalia Elly huku akimuangalia na Sia anayeishia na bodaboda kisha akamuuliza Elly,“Kwani unaumwa nini?”“Kichwa ndio kinakuuma”“Huyu mama yako huwa unamuelewa!”“Namuelewa ndio”“Kakwambia anakuleta hapa ndio hospitali?”“Hapana, ila kasema sababu naumwa na yeye hana pesa ya kunipeleka hospitali basi amesema ni bora anilete hapa kwa ndugu zetu”“Ndugu zenu!! Huyu mwanamke ana wazimu eeeh! Kuna ndugu zenu hapa? Si unafahamu hapa ni kwakina Erica?”“Nafahamu ndio ila Erica ni dada yangu, nimeambiwa hivyo na mama na nyie ni ndugu zetu”“Jamani huyu Sia jamani! Ana nini lakini aaarhg!”Ila mama Angel alipomuangalia Elly vizuri aligundua kuwa Ellyn i mgonjwa, basi aliingia nae ndani ila kwenda nae hospitali hakuweza zaidi zaidi alimpatia pesa na kumwambia kuwa aende hospitali kisha akamwambia,“Huyu mama yako ni chizi’“Ila ndio mama yangu, na mama ni mama nampenda na yeye ananipenda sana”“Mama anayekupenda hawezi kuja kukubwaga sehemu kama hivyo, mfano na mimi nikakutimua ingekuwaje? Huyo mama yako hakupendi wala nini, haya nenda kawahi hospitali huko, upande bajaji hapo ikusaidie kufika haraka hospitali”Basi Elly alimshukuru pale na kutoka nje ya ile nyumba.Ila alipotoka tu, alimkuta mama yake nje ya geti lile na kuondoka nae ambapo alimuuliza,“Amekupa pesa ngapi mwanangu”Elly akampa mama yake hela ambayo kapewa na mama Angel, basi Sia aliihesabu na kutabasamu maana ilikuwa laki moja, basi akasema,“Nilijua tu, maana huyu mwanamke ana kisirani na kila kitu huchukulia hasira tu! Haya twende mwanangu, shule utaenda kesho, kama unavyonijua mama yako ni mtu wa…”Elly akamalizia,“Mtu wa ukipata tumia ukikosa jutia”“Ndio mwanangu, Mungu anipe nini mimi eeeh! Anipe zigo la misumari nijitwike na kichwani nina kipara kisa nini!!”Elly akacheka pale, ila kwa muda huo Elly na mama yake walipitia kwenye mgahawa ili wapate supu kidogo halafu ndio waende nyumbani kwao.Wakati mama Angel amekaa na mawazo pale, Vaileth alisogea kumuuliza,“Mama, kwani yule mtoto alikuwa na shida gani?”“Anasema eti anaumwa”“Mmmh mbona haonekani kama mgonjwa?”“Alikuwa anatoa na machozi, ndiomana sikuwa na budi zaidi ya kumsaidia”“Ila bora hata ungeniambia mimi nimpeleke hospitali maana naona kama anaweza fanya mchezo sababu anajua unatoa pesa tu, yani wakigundua watakuja kujifanya wanaumwa watu wengi hapa”“Vaileth mwanangu na mdogo wangu, kuna mambo makubwa sana yapo nyuma ya pazia usiyoyafahamu. Huyu mtoto ana mama yake ni msumbufu hatari, yani akiingia hapa ni anaongea kama kameza cherehani, huyo mama yake ni hafai ila kipindi hiki mwache kanipata maana nina mtoto mdogo ndani kwahiyo siwezi kutoka toka hovyo, ila kitu kingine ni sababu nina huruma ila acha tu”“Pole mama jamani!”Mara walisikia kama mlango wa sebleni ukigongwa, basi Vaileth alisogea na kufungua ila aliyeingia alikuwa mama mkwe wa mama Angel pamoja na Mr.Peter kiukweli mama Angel hakupenda kumuona tena huyu mzee kabisa. Mara walisikia kama mlango wa sebleni ukigongwa, basi Vaileth alisogea na kufungua ila aliyeingia alikuwa mama mkwe wa mama Angel pamoja na Mr.Peter kiukweli mama Angel hakupenda kumuona tena huyu mzee kabisa.Ila hakuwa na namna yoyote ile zaidi ya kuwakaribisha tu, ambapo baada ya salamu kitu cha kwanza kabisa mama mkwe wa mama Angel alimuulizia kwanza Angel,“Mjukuu wangu Angel yuko wapi?”“Mama samahani, Angel aliondoka na bibi yake”“Nilijua tu ndiomana ulimtoa nyumbani kwangu”Mama Angel aliinama chini tu kwani alijua wazi kuwa jambo lile limemuumiza mama mkwe wake, basi Mr.Peter akasema,“Yani Angel hapokei kabisa simu zangu wakati mimi ni kama babu yake au umemkataza?”“Aaaah hapana, ila Angel hana simu”Mama mkwe akajibu,“Anayo, kwani Angel hajakuonyesha? Mr.Peter alimzawadia Angel simu nzuri ya gharama nay a kisasa, unataka kusema kitu gani au umeichukua wewe”“Ningeiona kweli ningeichukua ila sijawahi kumuona Angel na simu”“Oooh nimekumbuka, hata hivyo mjukuu wangu alisema kuwa hana simu sababu wewe unamzuia kutumia simu. Kwanini upo hivyo jamani Erica? Hujui kama karne imebadilika hii! Huu ni wakati wa mitandao na mawasiliano, sasa binti kama Angel asitumie simu jamani kwanini? Unataka kumfanya nini mtoto?”“Mama nisamehe tafadhari, ila mimi niliona kuwa kwasasa simu ingemchanganya tu Angel na niliona ni vyema asiwe nayo ndiomana ipo hapa simu ya mezani ili kama kuna mawasiliano mengine yafanyike”“Yani kuna watu mmesoma ila elimu haijawakomboa kabisa, hizi siku hizi ni nyumba ngapi unatembea na kukuta kuna hizo simu za mezani? Kila mtu anakuwa na simu yake hadi watoto, pesa mnayo mnashindwa nini kutumia kwa watoto wenu? Kwanini unawafanyia hivi watoto lakini Erica? Kwani wewe uliharibiwa na simu!”“Mmmh mama, tusifike huko jamani! Basi nitamruhusu Angel kutumia simu”Mr.Peter akasema,“Mwambie apokee simu zangu ili nikamuonyeshe mtu aliyefanana nae”Yani mama Angel alihisi tumbo lake kuunguruma kwa wakati huo na kuamua kukatisha zile habari kwanza kwa kumuita Vaileth ili awapatie vinywaji ila waligoma na kuaga halafu wakaanza kutoka huku mama mkwe akimwambia mama Angel,“Safari ijayo ndio nitakuja rasmi sasa kwaajili ya mjukuu wangu, leo nilimleta huyu mzee mara moja”Basi wakaondoka na kumfanya mama Angel ajiulize kuwa yule mzee alikuwa amefata nini nyumbani kwake maana hakuelewa lengo la mama mkwe wake kumpeleka yule mzee pale.Basi bibi Angel na Mr.Peter wakati wanaondoka, wakiwa njiani kuna mwanamke ambaye bibi Angel alimuona na kumwambia kuwa Mr.Peter asimamishe gari basi alisimamisha gari karibu na yule mwanamke ambaye alirudi nyuma kisha yule mwanamke alimkimbilia bibi Angel na kumkumbatia kwa furaha, kisha walisalimiana halafu bibi Angel alianza kumuuliza,“Kheee jamani kumbe Sia upo!!”“Nipo mama, za siku nyingi”“Nzuri tu, jamani umepotea halafu hubadiliki wewe binti jamani! Sema kwasasa umepungua”“Shida hizi mama ndio zimefanya nipungue”Basi akamuona Elly akimsogelea Sian a kumsalimia huyu mama ambapo huyu mama alimuuliza Sia,“Ndio huyu mwanao?”“Ndio mama, ndio huyu mjukuu wako anaitwa Elly”“Oooh nafurahi kumfahamu, na yule mume bado unaishi nae?”“Mume yupi mama? Mimi sikuwa na mume, hivi unajua kuwa huyu mtoto ni mjukuu wako kabisa, yani ndiye niliyezaa na Erick”“Jamani Sia, bado una zile hoja za kuzaa na Erick!!”“Sasa mama, kwanini nipinge wakati hii ni damu ya Erick. Hakunioa ndio ila huyu ni wa kwenu”“Mmmh Erick anayo hiyo habari!”“Anayo ndio ila Erick alinikataa kipindi nina mimba hadi sasa nina mtoto hanitaki mimi wala mtoto, ila mimi namuachia Mungu tu ila hii ni damu yenu”“Wewe Sia wewe jamani, unakumbuka nilikubamba kwenu na yule mwanaume wako!”“Mama, ile ni historia ndefu sana ila ipo siku utasadiki haya niyasemayo”“Haya, nipe mawasiliano yako. Nitajaribu kuongea na Erick”Basi Sia alimpa bibi Angel namba yake na kisha kuagana nae, na yule mama kurudi kwenye gari halafu Sian a mwanae kuondoka.Basi Elly alimuuliza mama yake,“Mama jamani si ulisema baba alinikimbia nikiwa mchanga kabisa, mbona hapo nimekusikia kuwa baba alinikataa toka tumboni! Na huyo Erick ndio yupi mama?”“Sikia mwanangu, mambo mengine sio lazima uelewe. Muda wa kuelewa ukifika basi utaelewa tu, ila tumeonana na huyu mama hesabia maisha yetu kubadilika na ukimuona mahali uwe unamuita bibi na kumpa heshima zote”“Sawa mama”“Nakuandalia maisha mema hata kama baba yako hataki ila najua kuna siku utakumbuka kuwa mama alinipenda sana na aliniandalia maisha mema, mwanangu usijali, utapata kila kitu, yani kila unachohitaji utakipata halafu mimi na wewe tutaishi raha mustarehe”Elly alitabasamu na kufurahi kisha waliendelea na safari na mama yake ya kurudi kwao.Jioni ya leo mama Angel alikuwa nyumbani akitafakari mambo mbalimbali, ila akakumbuka jambo kuwa Angel ana simu, kwakweli hakupenda kabisa kitendo cha Angel kuwa na simu kwa kipindi hiko kwani aliona wazi simu itavuruga akili ya Angel ukizingatia kuna vitabia ambavyo anaviona kwa Angel na havipendi kabisa, basi akaamua kumpigia mama yake simu na kumuelezea tukio zima la siku hiyo la kufikiwa na mama mkwe wake pamoja na Mr.Peter,“Mama, huyo Mr.Peter ni mume wa mrs.Peter yule mama mzazi wa Rahim”“Kheee yule Mwajuma?”“Ndio huyo huyo”“Sasa kama wamefika hapo si inamaana kila kitu kitakuwa wazi, mwanangu ni wakati wa kumwambia Angel ukweli”“Hapana mama, naona kama tutaichanganya akili ya Angel tu kwasasa”“Ila mwanangu, mfano Angel akaja kusikia kwa watu baki itakuwaje?”“Unajua mama, nina mawazo mengi unadhani itakuwaje pale Angel atakapogundua kuwa Erick sio baba yake mzazi? Naona kama mwanangu nitamuharibu kisaikolojia, tuache tu mama. Sasa hilo swala la simu itakuwaje?”“Kuhusu simu hata usijali, mimi nitajua cha kufanya”“Sawa mama, asante”Wakaagana pale na mama yake ila leo baba Angel aliwahi kurudi maana muda huo huo aliingia nyumbani na kuanza kuongea na mke wake,“Ulikuwa unaongea na nani mama watoto?”“Na mama”Kisha alianza kumueleza kuhusu mama yake alivyofika siku hiyo na Mr.Peter na jinsi walivyomuulizia Angel,“Kwahiyo Angel ana simu?”“Ndio, hapa ndio nimetoka kumpigia mama na kumtaarifu”“Ila mke wangu, hivi tutambana mtoto hadi lini? Kwa karne hii watoto wanavyotumia simu, tutaweza kweli? Tutamnyang’anya halafu atapewa na wanaume”“Mmmh umeanza mume wangu jamani!! Tunatakiwa kumchunga mtoto bila kujali kitu chochote”“Kwasasa Angel anatakiwa aambiwe kuhusu utumizi mzuri na mbaya wa simu, maana najua kwa karne ya sasa kuna madhara makubwa sana, tutamkataza halafu atanunuliwa na mwanaume tutamjengea nini Angel? Mwishowe tutasema bora hata Samir maana anaweza kukutana na wakina Rahim”“Umeanza sasa baba Angel, hayo mambo si yamepita jamani! Haya, leo kaja mwanamke wako Sian a mapya kabisa, kaja kumleta Elly kuwa anaumwa halafu akamuacha kwangu”“Ila mke wangu naomba heshima ifate mkondo wake, Sia sio mwanamke wangu na hawezi kuwa mwanamke wangu, ningemtaka Sia basi ningemuoa yeye ila sijawahi kumtaka”“Sasa kwanini Sia anatusumbua sana kwenye hii familia”“Na tukimjali atatusumbua zaidi mke wangu, lengo la yule mwanamke ni kuona sisi tunakosa amani kwaajili yake, hebu tuishi kwa upendo wetu kama zamani jamani mke wangu, tena ule upendo uliokuwa kwetu tuuzidishe maradufu, kwakweli mke wangu sitaki kuona kidudumtu kama Sia akijisifu kuwa kafanikisha kuharibu nguvu ya mapenzi iliyokuwa kati yetu, hebu tushikane na tusiteteleke kwa chochote kile”Basi mama Angel alienda kushikana mikono na mume wake na kusema kwa pamoja,“Mungu tusaidie, amen”Kisha wakaendelea na maongezi mengine tu.Angel alia chumbani kwake baada ya kutoka chuo, alishika simu yake na kuanza kuwasiliana na Samir,“Sasa Angel nahitaji kuonana nawe ila najua jinsi ilivyongumu kuonana nawe kwasasa”“Kwahiyo tutafanyaje?”“Aaaah hakuna tatizo, nimegundua kitu. Huyo bibi yako kuna chama flani yupo na bibi yangu, ngoja nifatilie ratiba zao, halafu nitajua kwa undani zaidi”“Aaaah nilisikia kuwa Ijumaa ndio wanaenda kwenye chama”“Basi hakuna tatizo, Ijumaa tutaonana mpenzi na tutakuwa pamoja”Angel alitabasamu na muda huo huo bibi yake aliingia chumbani kwake ambapo Angel alificha simu yake, basi bibi yake alianza kumuuliza,“Angel unaficha nini?”Angel alikuwa kimya tu, ambapo bibi yake aliendelea kuongea,“Angel, lete hiyo simu unayoificha huko”“Sina simu bibi”“Sio wakati wa kunificha huu ujue! Mama yako kashaambiwa kila kitu kuwa una simu, halafu mimi bibi yako nina hasira sana”“Sina simu bibi”“Umetoa wapi hiko kiburi Angel? Mbona mama yako alikuwa muoga sana kupigwa?”Angel alikuwa kimya tu na ameinama chini, kwakweli huyu bibi huwa hapendi kumwambia mtoto kwa kumbembeleza muda wote, basi muda ule ule alitoka nje na aliporudi alikuwa na bakora ambayo alianza kumchapa nayo Angel mpaka Angel alimpa ile simu bibi yake,“Mjinga sana wewe, unadhani wote tuna akili mbovu kama zako, kisa cha kuniletea mimba nyumbani nini jamani! Hebu nitolee matatizo mie”Bibi aliichukua ile simu na kuondoka nayo ila Angel alibaki akilia tena alilia sana, aliona kuwa ameonewa mno na bibi yake, hakupenda kitendo cha bibi yake kumchapa bakora wakati alikuwa ni msichana mkubwa, yani Angel alilia kiasi kwamba usiku ule hakwenda hata kula chakula kwani alikuwa akilia huku akimuwaza Samir kuwa lazima kamtafuta halafu hajampata hewani.Kulipokucha, Angel aliamshwa na bibi yake ila macho yake yalikuwa yamevimba kwa kulia kwakweli bibi yake alisikitika sana na kusema,“Yani hadi macho yamevimba sababu ya simu hii tu jamani Angel, umegoma hadi kula usiku sababu ya simu tu!”Angel alikuwa kimya tu na kumfanya bibi yake aongee tena,“Kwani wewe umetoa wapi hiko kiburi Angel, kwanini unataka makosa yajirudie? Unataka na wewe uzalie nyumbani kama mama yako alivyofanya”Angel akashtuka kwani hakuwahi kufikiria kama alizaliwa nje ya ndoa, basi alimuuliza bibi yake“Kwahiyo mimi nilizaliwa nje ya ndoa?”“Siku utakayoona kuwa unaanza kuwa mtoto mwema ambaye ukiambiwa unasikia, basi nitakueleza mambo mengi sana, ila mtoto ambaye nikimuadhibu kidogo tu analia usiku kucha huwa sipendi hiyo tabia. Inuka hapo uje unywe chai mjukuu wangu, sina ubaya na wewe ila nakufundisha tu”Basi Angel aliinuka pale na kwenda kuoga ila alikuwa na hasira sana kiasi kwamba siku hii hakuweza hata kwenda chuo kwani macho yake yalikuwa yamevimba kwa kulia, basi alikaa tu na bibi yake wakitaniana pale ila bibi yake hakutaka kumwambia ukweli kuhusu yeye kuzaliwa nje ya ndoa maana pale aliropoka tu sababu ya hasira aliyokuwa nayo.Baba Angel leo akiwa ofisini kwake, alitembelewa na mama yake, hata yeye alishangaa kwani hakutegemea kutembelewa na mama yake ofisini kwake,“Naona umeshtuka maana hujaamini hiki unachokiona!”“Kweli sijaamini mama”“Toka jana nipo hapa mjini, leo nikasema ngoja nipitie ofisini kwako mara moja. Halafu mjukuu wangu nitakuja kumuona na zawadi hivi karibuni”Basi baba Angel alimsalimia pale mama yake na kuanza kuongea nae ambapo mama yake alianza kumwambia,“Jana wakati nimetoka kwako nikakutana na Sian a mtoto wake”Baba Angel alichukia kwani alijua ambacho kingeendelea, basi mama yake alitambua na kumuuliza,“Mbona umeanza kuonyesha chuki mapema hivyo mwanangu?”“Aaaah mama jamani, huyo mwanamke ni pasua kichwa hadi sitaki hata kumuona”“Na ni pasua kichwa kweli, nakumbuka kipindi kile alidai kuwa na mimba yako, na hadi sasa kaendelea kusisitiza kuwa yule mtoto aliyenaye ni mtoto wako kwahiyo ile ni damu yako Erick”“Mama, siwezi kukataa mtoto tu bila sababu za msingi ila kwa kipindi kile Sia hakuwa na mimba yangu kwahiyo ni muongo yani nitasimamia neno langu hilo hadi mwisho”“Ila mwanangu jamani! Inawezekanaje Sia awe muongo! Basi tukampime yule mtoto”“Tukampime nini sasa?”“Tukapime DNA na wewe”“Mama, hizo hela za kwenda kupima DNA na mtoto wa Sia kama hazina kazi ni bora kwenda kuzitupa ili wenye shida waziokote, yani mama siwezi kujisumbua kufanya chochote kile. Hakuna kitu chochote ninachomuamini Sia, nampenda sana mke wangu”“Naelewa hilo, naelewa ni jinsi gani unampenda Erica hata Erica pia anakupenda sana wewe ila hiki ni kitu kingine, inatakiwa kama yule mtoto ni damu yetu basi apate haki zote kama wengine”“Mama, huko sipo tafadhali. Ukitaka tuelewane mimi na wewe basi tuzungumzie mada zingine na sio hizo mada za Sia, tafadhali mama yangu nakuomba”“Sawa, mwanangu nimekuelewa”Ilibidi mama yake abadilishe stori na kuanza kuongea nae kuhusu mambo mengine tu kwa muda huo.Leo wakati wa kutoka shule, kama kawaida Sarah alikaa karibu na Erick basi alianza kuongea nae,“Ila Erick kwanini unanifanyia hivi jamani! Yani naona kama unanikwepa hivi siku hizi”“Hapana sikukwepi”“Maana toka useme simu kaichukua mama yako, basi siku hizi unanikwepa kabisa yani hata huongei vizuri na mimi”“Kwani unataka niongee vipi jamani Sarah!”“Mimi nakupenda, unatakiwa uonyeshe kunipenda pia”Yani Erick hadi alikuwa akijihisi aibu kabisa kwa wakati huo kwani Sarah aliongea kwa ujasiri mkubwa kabisa kuonyesha kuwa ni kweli anampenda sana Erick, basi akamshtua na Erick akamwambia Sarah,“Ila sisi bado wadogo Sarah!”“Kwani wadogo kitu gani Erick? Mimi nakupenda bila kujali kitu chochote kile, sijali kuhusu udogo wetu ila ninachojali ni kuwa nakupenda sana, yani Erick unavyonifanyia sio vizuri ujue, kumbuka tunafunga shule! Nikubalie Erick jamani ili moyo wangu uwe na amani”“Unanipa wakati mgumu sana Sarah, naamini mama yangu atapenda kuona mimi na wewe tukiishi kama dada na kaka na si vinginevyo”Basi gari ilifika kwakina Erick naye Erick alishuka kwakweli Sarah hakuwa na amani kabisa, basi alikaa kimya tu hadi alipoingia nyumbani kwao na siku hiyo alienda kulalamika kwa mama yake,“Mama, nampenda Erick ila kwanini ananikwepa na anasema kuwa sisi ni wadogo eti upendo hauangalii ukubwa au udogo”“Ila wewe Sarah, umepata wapi ujasiri wa kumtongoza huyo Erick?”“Nakumbuka mama ulisema nikiwa na hisia na chochote niwe huru kusema, nami hisia zangu zipo kwa Erick, natamani mno awe wa kwangu. Mbona wazungu wanaanza mahusiano wakiwa wadogo kabisa, sembuse mimi na Erick!”“Aaaah usijali mwanangu, kama Erick ni wako basi atakuwa wako tu hata usijali, kuna mambo sio ya kulazimisha sana. Kuna siku nitakaa nawe na kukufundisha kuhusu mapenzi, hakuna kitu kibaya kama kumlazimisha mtu akupende, yani kama hakupendi basi itakuwa ni tatizo kwako, ila mwanangu huwa napenda kukwambia kuwa usikate tamaa sema kuhusu swala la kumpenda Erick subiri kwanza”“Sawa mama”Basi alienda chumbani kwake, yani mama Sarah alimlea mwanae katika maisha ya tofauti sana ambayo wazazi wengi wa kiafrika wasingeweza kulea mtoto kwa staili hii, ila yeye alijionea kawaida tu, na alikuwa akiongea na mwanae karibu kila kitu.Erick na Erica wakiwa nyumbani, kipindi hiki walipatana yani Erica aliona rah asana vile yeye hana simu na Erick nae hana simu maana mwanzoni roho ilimuuma sana kuona kuwa mwenzie ana simu na nay eyena, basi muda huu Erick na Erica walienda bustanini ambako alikuwa amekaa Junior kwa muda huo basi Erica alianza kusema,“Eeeeh haya sasa, leo mbele ya Erick naomba Junior ukubali kuwa utamuoa dada Vaileth”Basi Junior na Erick walikaa kimya kidogo, kisha Junior akasema,“Mmmh na wewe Erica, kumbe umeshamuelezea Erick!”Erick akajibu,“Hapana hajanielezea, yani na mimi ndio nashangaa hapa”“Haya, ngoja basi nikuridhishe mdogo wangu Erica”“Sio uniridhishe, nataka umaanishe”“Sawa, mimi namaanisha haya niyasemayo kuwa hapo badae nitamuoa Vaileth yani Vaileth ndio atakuwa mke wangu wa maisha”Muda huu Vaileth nae alitokea nyuma yao kwahiyo alitabasamu aliposikia maneno yale yakitoka kwa Junior, yani alihisi rah asana moyoni mwake, basi aliwasogelea pale karibu na kusema,“Jamani na nyie msiseme kwa nguvu, hadi mama asikie!!”Basi Erick akasema,“Yani ndio mmeweka siri kabisa na Erica, mimi nawatahadharisha tu kuwa msiamini sana maana siku isiyokuwa na jina basi atayabwaga yote hayo”Erica akachukia muda huu ikabidi Junior ampooze na kusema,“Erick, unavyomfikiria Erica sio hivyo alivyo kuna maneno ambayo Erica hawezi kuyasema wala nini moja wapo ni jambo hili. Tafadhari usimchukize mdogo wangu mpendwa, maana mimi na Erica ni damu damu”Hapa Erica alitabasamu maana alipenda sana kusifiwa, ikabidi naye Erick amsifie kidogo ila bado hakuwa na imani kwani alijua lazima hayo mambo ya Junior na Vaileth yatafika tu kwa wazazi wao.Muda wa kulala ulivyofika, Angel alikaa kwanza na bibi yake kabla ya kwenda kulala ambapo bibi yake alikuwa akimpa habari nyingi za maisha,“Unajua nini mjukuu wangu, kuna kaka mmoja alikuwa akimpenda sana mdada ila yule mdada alivyokubali kuwa naye, wee yani mdada ndio alimpenda sana yule mkaka na mwisho wa siku yule mkaka alimpa mimba mdada na kumkimbia”“Khee bibi, hivi mwanaume akimpa mimba mdada na kumkimbia inakuwaje kwa mdada?”“Yani hapo ndio unaujua umuhimu wa mama katika maisha, unajua mjukuu wangu mama ni wa kumuheshimu sana, ni mengi kapitia, ukikuta mama kakupatia mwanae baba bora anayekulea na kukuhudumia, usidhani imetokea tu ila ujue mama yako alipiga goti na kulia mbele za Mungu. Kwanza kuzalia nyumbani ni aibu, fedheha halafu heshima yako inashuka, yani hutambuliki vizuri na mbaya zaidi uzalie nyumbani ukiwa na umri mdogo eeeh ! Mbona utakuwa unalia kila siku, maana kila mtu analeta lake, huyu atauliza, baba wa mtoto yuko wapi na amekukimbia yani utaona dunia haitamaniki kwako”“Mmmmh bibi jamani unanitisha”“Sikutishi ila nakupa ukweli halisi wa maisha ulivyo mjukuu wangu, usikubali kudanganywa na wanaume”“Ila bibi, utakuwa unaniruhusu mara moja moja niwasiliane na marafiki zangu kwenye ile simu!!”“Ungekuwa hivyo muda wote mbona tungeelewana Angel mjukuu wangu jamani!! Hakuna tatizo, nitakuwa nakuruhusu ila kwa muda wangu mimi”“Sawa bibi yangu”“Haya, ni muda wa kulala huu na leo utaenda kulala chumbani kwangu ili tulale wote”Angel alikubali tu, bibi alifanya hivi ili Angel asijihisi mpweke na kuanza kuwaza mambo mengine yasiyofaa kwahiyo aliona ni vyema kuwa nae karibu zaidi ili kumsahaulisha mawazo ya kijinga.Basi walienda kulala, ila wakati wamelala usingizi mzito, bibi aliamka usiku kwaajili ya kufanya maombi, na alifanya maombi yake pale vizuri kabisa ila alipomaliza alimuona kama Angel akiweweseka huku akimtaja Samir,“Samir, Samir, Samir”Bibi alimuangalia na kusikitika sana, kisha akamshtua Angel na kumwambia tu alale vizuri, alishaelewa kuwa mjukuu wake amemuweka Samir kwenye mawazo yake ndiomana ameanza hadi mchezo wa kupatwa na ndoto za kumuhusu Samir.Kulipokucha, bibi alimuamsha Angel na kutoka nae nje ili kufanya nae kazi za usafi,“Ila bibi bado sijaoga”“Kheee Angel, yani kwenda kufagia uwanja na kusafisha nyumba ni mapaka uoge? Twende jamani mjukuu wangu”Ilibidi Angel akubali na kutoka nje na bibi yake ambapo walikuwa wakifagia fagia uwanja kisha bibi yake alitoka nae nje ya geti kabisa ambapo walianza kung’olea majani kwenye maua ya nje na kumwagilia yale mauwa yani hadi wanamaliza kazi ile Angel alijihisi kuchoka sana hadi alimwambia bibi yake,“Jamani bibi nimechoka”“Eeeeh huo ndio uanamke, hapo sasa nenda kaoge upate nguvu tuje kunywa chai”Basi Angel alienda kuoga na kwenda kunywa chai, na walipomaliza tu bibi akampa Angel simu sasa ili akawasiliane nayo kwa muda kidogo.Angel aliingia chumbani kwake, kiukweli alikuwa amechoka, kiasi kwamba alishika ile simu na kutuma ujumbe mmoja tu kwa Samir na alipokawia kumjibu alijikuta ameshalala kwa muda huo.Mama Angel leo akiwa nyumbani kama kawaida yake ya siku hizo, ila siku hiyo pia baba Angel hakwenda popote kwani alijihisi kuwa anahitaji kupumzika kwahiyo kwa muda huo alikuwepo tu nyumbani akipumzika, basi waliongea na mke wake pale na kusema,“Unajua nini mume wangu, nimekumbuka kipindi kile ambacho tulikuwa tukienda ufukweni kufurahi!”“Hata mimi nimekumbuka sana mke wangu, ila tumngoje Ester akue kue kwanza. Ila twende sebleni tukae kidogo tuangalie Tv yani leo nimekumbuka tu kushinda nyumbani na wewe mke wangu”Mama Angel alitabasamu kisha yeye na mumewe wakatoka kuelekea sebleni ambapo walikaa na kuanza kuangalia Tv, ila muda kidogo tu mlango wa pale sebleni ulisikika ukigongwa basi Vaileth alienda kufungua ule mlango ila aliyeingia kwa muda huo alikuwa ni Sia. Mama Angel alitabasamu kisha yeye na mumewe wakatoka kuelekea sebleni ambapo walikaa na kuanza kuangalia Tv, ila muda kidogo tu mlango wa pale sebleni ulisikika ukigongwa basi Vaileth alienda kufungua ule mlango ila aliyeingia kwa muda huo alikuwa ni Sia.Kiukweli furaha ya mama Angel ilikatika muda ule hata baba Angel aliona hali hiyo kwa mke wake na hakupenda kile kitu kabisa ila alichokifanya alimsogelea mke wake na kumshika bega kisha akalaza kichwa cha mke wake kwenye bega lake na kumbusu halafu akamwambia,“Nakupenda sana mke wangu”Kitendo kile kilimkera sana Sia, ambaye alisema,“Yani nyie ni watu wa ajabu sana kanakwamba hamnioni!”Baba Angel akamwambia,“Tusiendelee na starehe zetu sababu ya kukuona wewe! Kwani ni nani wewe katika maisha yetu?”Baba Angel akambusu tena mke wake, safari hii alimbusu mdomoni na kumfanya Sia aumie zaidi kwani hakupenda kabisa ile kitu na alijua wazi muda huo akifika humo ndani basi ataharibu hali ya hewa kabisa, ila yeye mwenyewe alishindwa kuvumilia, kwani baba Angel alikuwa kama ndio kafunguliwa kufanya mahaba kwa mke wake pale sebleni, basi Sia alifungua mlango na kutoka ambapo baba Angel na mama Angel waliinuka na kwenda chumbani.Kiukweli hii ilikuwa ni mbaya sana kwa upande wa Sia, alijikuta akidondosha chozi pale nje huku akisema,“Najua wanafanya, ila ndio hadi wanionyeshe!!”Akafuta machozi yake na kutoka sehemu ile na moja kwa moja kuondoka kabisa.Moja kwa moja Sia alienda nyumbani kwa Tumaini, ambapo leo alimkuta nyumbani tu na kuanza kuongea nae,“Ila Tumaini kwanza kabisa unafanya kazi gani maana kila siku nakukuta nyumbani!”“Oooh ninafanya kazi mimi ila kazi yangu haina masharti kivile, nimejiajiri mimi. Haya na wewe unafanya kazi gani maana nikisikia hili kwa huyu nasikia lile kwa yule”“Aaaah hata mimi nimejiajiri”“Umejiajiri kugombanisha nyumba za watu? Umejiajiri kuharibu ndoa ya watu? Hivi Sia unajua wazi kuwa mimi na wewe tunajua ukweli wa mtoto wako! Kwanini bado ukutane na mama Erick umwambie kuwa mtoto wako umezaa na Erick?”“Ukweli wa kuhusu mtoto naujua mimi na si mimi na wewe maana mimi ndio niliyebeba mimba”“Hata kama Sia, nakumbuka wazi kipindi umeenda kusema una mimba ya Erick ilikuwa ni lengo la kuvuruga penzi la Erick na Erica, nakumbuka wazi kuwa kipindi kile tulikuwa tukisaidiana kwenye mambo mengi tu na nilikuwa nikikupeleka sehemu nyingi, ila ukanigeuka na mimi na kwenda pamoja na Dora kwa mganga wenu sijui wa Bagamoyo kwa lengo moja la kumroga mdogo wangu, ila Mungu si Athumani kwani dawa yako akala kijana mdogo asiye na hatia Steve na alianza kukufata fata nyuma kama bata na watoto wake, na mwishowe ukapata mimba yake kweli, kwanini uendelee kung’ang’ania kuwa mtoto uliyezaa wewe ni wa Erick? Unajua mwanzoni sikumuelewa Erick wakati anasema kuwa unamsumbua na kusema Erick ni mtoto wako na hata hivyo uligoma kuniambia hiyo siri, haya umeibua mengine kuwa mtoto umezaa na Erick, swali langu ni mtoto yupi sasa? Yule Erick au huyo wako au na wewe ulizaa mapacha kama Erica?”“Usilolijua litakusumbua, tena litakusumbua sana. Kwanza jua kuwa yule mtoto anaitwa Elly, na unapomuongelea jua kuwa hapo umemuongelea Elly, Erick na Erica yani hiki kitu hutoweza kukitenganisha, kila ambacho Erick na Erica wanakipata inapaswa na Elly nae akipate, hutonielewa kwasasa namaanisha nini ila kuna muda utanielewa kuwa nazungumzia nini. Ila kwa muda huu sikuja kuongelea kuhusu watoto nimekuja kuongelea kitu kingine kabisa”“Kitu gani?”“Mapenzi yangu kwa Erick, sijui nimpate nani aweze kuokoa moyo wangu au aweze kuokoa fikra zangu, nampenda sana Erick na nitampenda hadi kufa kwangu, hakuna mwanaume nitakayeweza kumpenda kama Erick”“Ila Sia kuna mambo kwakweli unachekesha, haya umeshamwambia Erick hivyo!”“Nishamwambia sana, ila hataki kunielewa, kwakwlei Erick ni mwanaume ambaye alinifanya nione kama naimiliki dunia, leo hii kumkosa kwakweli sipo tayari, nampenda sana jamani.”“Haya, nimekusikia mama ila nakusaidiaje?”“Najua Tumaini hutaki kuwa upande wangu sababu mimi sina pesa, ila najua ningekuwa na pesa ungekuwa upande wangu. Leo ukiona hadi nimekuja kukwambia haya basi nimeumia sana, ila maumivu yangu huwa yana madhara makubwa sana, ukionana na Erick na huyo mjinga mwenzie Erica waambie wajipange”“Kheee jamani, kwanza ngoja nikwambie kitu Sia, ukija kuongea nami uje na mada zingine ila mada zako na Erick sizitaki kabisa, kwanza hazinisaidii na pili siwezi kufanya lolote lile. Natumai kwasasa umemaliza ulichokuwa unataka kuongea, kwaheri”Kwa kifupi kwasasa Tumaini hakuhitaji ukaribu sana na Sia kwani kaona kuwa mwanamke huyu atamgombanisha na ndugu yake bure, kwahiyo aliamua kuwa nae mbali mbali, basi Sia alichukia pia kuambiwa vile kwani aliinuka na kuondoka zake tena bila hata ya kuaga.Sia alipotoka tu nje ya nyumba ya Tumaini aliona bajaji na kuiita basi ile bajaji ilisogea na akapanda na kuondoka nayo ila yule mwenye bajaji alianza kumuongelesha,“Mama, samahani kuna binti mmoja mzuri mzuri anaitwa Angel, alikuwa anaishi kwenye ile nyumba uliyotoka ila siku hizi simuoni”“Kheee unamuulizia Angel! Wa nini? Au unamtaka?”“Samahani mama, nampenda sana yule binti yani hata ningekuwa namuona tu basi roho yangu ingeridhika”“Oooh sawa, yule yupo kwao kwasasa, ila unampenda kweli?”“Ndio nampenda sana”“Unaitwa nani wewe?”“Naitwa Ally”“Ooooh basi sawa, nipe mawasiliano yako, nitafatilia kujua Angel anaishi vipi kwasasa halafu nitakuwa nakuelekeza cha kufanya, hata usijali ila ukiwa nae usimwambie kama kuna mama anakusaidia”“Dah! Nashukuru sana mama yangu. Yani nampenda yule binti balaa, ni kweli sina hadhi, mimi ni masikini ila nina mapenzi ya dhati yani moyo wangu unampenda sana Angel, natamani hata ningekuwa namuona tu”“Usijali kitu, ilimradi umeonana na mimi basi andika kila kitu kimepita”Basi Ally alifurahi sana kukutana na huyu mama kisha walipeana mawasiliano pale na alimfikisha hadi alipoenda na wala hakumdai hela yoyote sababu tu kaahidiwa kumpata Angel.Muda wa kutoka shule, kama kawaida Erick alikaa pamoja na Sarah hata alipojaribu kukaa siti nyingine ilikuwa ni lazima Sarah amtoe mtu aliyekaa pembeni ya hiyo siti ili yeye akae na Erick, basi alianza kuongea nae ila leo aliongea nae kawaida kabisa kiasi kwamba hata Erick alimshangaa kwani hakusema zile mada zake za kumpenda kabisa bali aliongelea vitu vingine,“Ijumaa, shule inafungwa Erick. Ila safari hii likizo nitaenda kwa bibi yangu”“Oooh hongera sana, mimi nitakuwa nyumbani tu”“Ila kipindi cha likizo ni vizuri kutembelea ndugu jamaa na marafiki ili kufahamu vizuri ukoo wako”“Umenishauri vyema, nami kipindi hiki cha likizo nitafanya hivyo unavyosema Sarah”Yani mpaka Erick anashuka nyumbani kwao hakuletewa mada za mapenzi kabisa na Sarah, kiukweli alijihisi vizuri kwenye moyo wake.Basi aliingia ndani na kumkuta muda huu baba yake akiwa sebleni na kumsalimia, kisha baba yake akamwambia,“Kumbe huwa unatangulia kurudi wewe halafu ndio anafatia Erica?”“Hamna baba, huwa inategemea na siku”Mara Erica nae alifika na kumsalimia baba yake pale ila kama kawaida ya Erica huwa akitoka na jambo shuleni basi anahitaji kuliongea, basi alimsogelea baba yake pale yani kabla hata hajatua begi lake na kuanza kuongea nae,“Basi leo baba, wakati tunatoka shule sijui nani kamuelekeza Elly shuleni kwetu ila nikamuona, na kwenda kumsalimia”“Mmmh, ila shule yenu sin i shule ya wasichana tupu?”Ndio, ila nilimuona kwenye kibanda cha mlinzi naye akiwa ametoka shuleni kwao, basi niliongea nae kidogo ila unajua kaniuliza nini?”“Eeeeh kakuuliza nini?”“Kaniuliza kuwa, eti dada Angel siku hizi anaishi wapi? Basi nikamwambia kwa bibi, sijui ni kwanini kaniuliza vile!”“Hivi huyo Elly si ndio mtoto wa Sia! Yani mama yake Elly si anaitwa Sia?”“Mmmh mimi sijui jina la mama yake”“Haya mwanangu, kabadili sare za shule sasa”Basi Erica ndio akainuka na kwenda chumbani kwake kubadili sare sasa.Muda ule ule baba Angel aliinuka na kwenda chumbani kwa mke wake, ila alijua wazi kuwa akimpa taarifa ile mke wake lazima atapaniki, ila alimuuliza tu,“Hivi mtoto wa Sia anaitwa nani?”“Kafanyaje tena!! Anaitwa Elly”“Hamna kitu mke wangu, nilitaka tu kufahamu jina la huyo mtoto ila hakuna mengine wala nini”“Nimekuelewa mume wangu, yani ndiomana huwa unasema Sia ana wazimu, sasa anavyosemaga Erick ni mwanae, je huyo Ellyn i mtoto wa nani?”“Mjinga yule, tena mjinga kabisa, tufanye yet utu mke wangu”Basi waliendelea na mambo mengine ila baba Angel alikuwa na maswali mengi sana kwa muda huo, kwanini huyo Elly aulizie anapoishi Angel kwa kipindi hiko? Akahisi kuwa lazima Elly katumwa na Sia tu, kwakweli akasikitika na kusema kuwa atafatilia swala hilo kimya kimya ili asimpe presha mke wake. ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment