Simulizi : Kilio Cha Nafsi
Sehemu Ya Tatu (3)
Alikuwa ni msichana mdogo sana udogo wake haukupelekea ugonjwa wa moyo kuacha kumshambulia kila dakika aliteseka kwa maumivu makali. Hadi anatimiza umri wa miaka sita alikuwa ameteseka vya kutosha. Wazazi wake waliokuwa wakulima walikuwa wamemhangaikia kupita maelezo kila kitu cha thamani kwao walikuwa wamekiuza lakini msichana huyo hakuweza kupona kila siku alizidi kupokea maumivu makali sana.
“Mama Naomi unaionaje hali ya Naomi?” Mume wake akamuuliza mke wake dakika tano mara baada ya wao kupanda kitandani baada ya chakula cha usiku majira ya saa mbili.
“Mungu atamsaidia tu mwanetu ipo siku atapona naumia sana ninapomuona mwanagu akitesaka kila sekunde,” akamjibu kwa unyonge na kwa sauti ya kukata taama ndani yake japo muda mwingine alikuwa akijipa tumaini la mwanae kupona lakini kuna wakati mwingine alikuwa anakata tama kabisa.
“Nini wazo mke wangu!”
“Wazo gani?” Akamuuliza huku akimgeukia na kumtazama machoni mwanga hafifu wa kibatari ukamsaidia kuuna vyema uso wa mume wake bwana Mlema.
“Utakubali?”
“Nini?”
“Nataka tumuue Naomi.”
“Nini?” mke wake akauliza kwa hali ya mshangao wa juu sana asiamini kile alichokuwa anakizungumza mume wake, hakuamini kama siku moja mwanaume huyo waliyeshirikiana kwa pamoja kumtafuta mtoto huyo kwa udi na uvumba leo hii angezungumza maneno ya aina hiyo na yenye kuumiza moyo wake.Kwanza akakosa jibu la kutoa haraka na kubaki akimtazama mwili wote ukitetemeka kwa hofu iliyochanganyikana na hasira ndani yake.
“Vipi mbona unanitazama hivyo? Mimi nimechoka kupoteza pesa kwa mtu asiyepona, kwani tukifanya hivyo hakuna mtu atakayeweza kufahamu hilo ukikubali mimi nitakuonesha jinsi ya kumuua ni rahisi sana kama unaua mende.”
“Mlema siku hizi unavuta bangi?”
“Mimi!”
“Ndio. Kwanini unaingiwa na roho wa kikatili kiasi hicho na shetani anayatawala maisha yako, kwanini udhuru kiumbe kisicho na hatia na kisicho na kosa haya kosa lake nini mpaka uwaze kumuua mtoto huyu, kuumwa?”
“Sasa unategemea mimi nitaendelea kupoteza mali kila siku mpaka lini si bora akafa tukaishi kwa raha mstarehe.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Raha ipi unayoitaka mume wangu? Utafurahi sana siku ukiona unamfukia mwanao na utashiba kweli,mimi siko tayari kumuua mwanagu nampenda sana Naomi niko radhi kufa mimi kwanza lakini si yeye,” akazungumza kuku macho yake yaliyokuwa yamekondeana kutokana na hali ngumu ya maisha yakianza kulengwa lengwa na machozi moyo wake ukiumizwa sana na maneno ya mume wake mtu aliyeamini kuwa atakuwa msaada wake na kwa mwanae kipenzi mtoto wao wa pekee.
“Sasa usipokubali mtaondoka hapa na hiyo maiti yako wewe unadhani hapo kuna uzima? Bora kumpumzisha mapema kuliko kumuona akiendelea kuteseka hivyo na mioyo yetu ikizidi kukonda kwa mawazo.”
“Sitaondoka hapa na Naomi hafanyiwi kitu chochote,” akamjibu na kuziruhusu mbavu zake zilale juu ya godoro akiwa amempa mgongo mume wake akiendela kulia kwa kwikwi bila kufahamu hatima ya mwanane wa pekee Naomi.
“Mimi ndo nishasema mtaondoka hapa mbwa nyie mkikataa nawaueni wote.”akasema naye akigeukia upande wa pili akilini akiwa kitu cha kufanya siku itakayofuata.
Yalikuwa ni maneno makali sana na yenye kuuchoma moyo wa mama Naomi siku ya pili yake alidamka mapema sana na kuelekea chumbani kwa mwanae alifika ndani ya chumba hicho akitembea taratibu akihofia kumuamsha mwanae aliyekuwa usingizini, akaa juu ya kitanda chake akimtazama kwa macho ya huruma sana, moyo wake ulikuwa na maumivu si mfano kila macho yake yalipokuwa yakimtazama mwanae moyo wake haukuwa nyuma kuumia na kulia kila sekunde.
Alitumia kama dakika mbili kumtazama mtoto huyo aliyekuwa usingizini asifahamu kile kilichokuwa kiendelea chumbani mwake.
“Hujambo mama?” Akamuuliza mara baada ya mtoto huyo kuyafumbua macho yake na kumkuta mama yake akiwa kitandani kwake.
“Shikamoo mama naumwa hapa,” Naomi akamsalimia mama yake kisha akamueleza ni wapi alipokuwa akiumwa.
“Pole sana mama utapona sawa?”
“Kweli mama nitakuwa kama wengine?”
“Ndio tena utakuwa mkubwa wewe subiri tu nipate pesa nitakupeleka hospitali kubwa na utapona tena kwa siku moja tu.”
“Kweli?”
“Eeeeh!”Akaitikia huku macho yake yakianza kulowa na machozi hali iliyomchanganya sana Naomi akabaki akimtazama mama yake asielewe kipi kilikuwa kimesababisha yeye kutoa machozi.
***
Yalikuwa ni maneno yenye uchungu sana ndani ya mtima wa mama Naomi japo alimkubalia mwanae kuwa alikuwa akienda kupona kaama alivyokubali mara baada ya kuulizwa lakini upande mwingine wa shilingi ilikuwa tofauti kabisa.Maneno makali kutoka kwa mume wake ambayo alitoka kuyasikia usiku wake ndiyo ilikuwa sababu ya yeye kulia mbele ya binti yake huyo mdogo.Muda mwingine alitamani kumueleza lakini alihofia kumuumiza sana, akayaona maumivu makali ndani ya mtima wa binti huyo mara baada ya kumueleza, akayaona machozi yakitiririka juu ya mashavu yake alipofika hapa akatulia na kujifuta machozi kwa mkono wake wa kulia kisha akamkumbatia mwanae ndani ya kifua chake na kumbusu usoni.
“Mama kwanini unalia?” Naomi akamuuliza mama yake akimtazama machoni bila kuyakwepesah macho yake hakupenda kumuona hata siku moja mama yake akilia mbele yake.
“Najihisi furaha ya ajabu siku utakapona, silii kwa maumivu mwanaungu moyo wangu una shauku kubwa sana la kukuona siku moja ukiwa mzima kabisa.”
“Mmmmmh!Mama acha uongo kuna kitu unanificha?”
“Hapana kwanini?Sikia Naomi siwezi kukuficha chochote wewe ni binti yangu wa pekee lako langu na langu lako pia silii mwanagu nielewe,” ilibidi atumie maneno ya kumlaghai mtoto huyo ili asigundue kile kilichokuwa kikiendelea kati yake na baba yake.
“Yaani hiyo siku mama nikipona nitakununulia zawadi kubwa wewe na baba,” akasema huku akijilazimisha kutabasamu lakini alijikuta akiukunja uso mara baada ya kuhisi maumivu makali ndani ya kifua chake , tabasamu hiyo ikamfanya mama yake kutazama pembeni mara baada ya masikio yake kulisikia neno baba, mwanae hakufahamu ni kipi baba yake alikuwa amedhamiria kukifanya kwa msichana huyo ambae alikuwa akiyaonyesha mapenzi ya waziwazi kwa mzazi wake huyo wa kiume.
Kila siku usiku ilikuwa ni ugomvi kati ya wazazi wa Naomi baba yake aliendelea kumlazimisha mke wake kumuangamiza mwanae lakini mke hakukubaliana na ombi hilo hali iliyokuwa ikizidi kuongeza vurugu na ugomvi kwa wanadoa hao, maneno yao yaliweza kumfikia Naomi na kubaki akilia kila dakika.
“Mama kwanini baba anataka kuniua?”Naomi akamuuliza mama yake siku moja mara baada ya wazazi wake kujibizana maneno makali mbele yake.
“Hapana hana nia ya kukua ila…”
“Ila nini mama? Anataka kuniuaaaaaaa,” Naomi akazungumza huku akianza kulia kwa sauti hali iliyopelekea mama yake naye kuanza kulia huku akiwa amemkumbati mtoto wake, moyoni alikuwa na maumivu makali sana, alimuhurumia sana binti yake lakini hakuwa na cha kufanya zaidi ya kujitahidi kumfariji hadi alipopitiwa na usingizi.
Mwezi mmoja hali ya Naomi ilizidi kuwa mbaya sana kwa msichana huyo baba yake aliamua kumfukuza mama wa msichana huyo mara baada ya yeye kukataa kumuua mtoto huyo ambae kwake alionekana ni kikwazo kikubwa.
“Kila siku nakueleza hutaki kunisikiliza nimepoteza kila kitu ila hakuna mafanikio kwa hili jibwa lako, sasa nimechoka naomba uondoke kama hutaki kufanya kile nilichokueleza na usipoondoka nawaueni wote,” alisema Mlema kwa lafudhi ya kichaga huku akiyumba yumba kutokana na pombe aliyokuwa amekunywa muda mfupi mara baada ya yeye kurejea nyumbani hapo.
“Baba Naomi sasa nitakwenda wapi na mtoto huyu kwanini una roho ya kinyama kiasi hicho?”
“Nimesema muondoke hamsikiii,” aliongea huku akiwafuata na kabla ya kuwafikia alirusha teke lilimfikia vyema Naomi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mamaaaa mwanangu,” mama yake aliyekuwa akifahamika kwa jina la Maria alipiga kelele mara baada ya kuona mwanae akipokea kipigo kutoka kwa baba yake kitu kilichomsikitisha sana, haraka-haraka alimnyanyua mtoto wake na kutoka nje huku akikimbia hakufahamu anaelekea wapi ila alichojari yeye ni kuyaokoa maisha ya mtoto wake.Kimbia yake hiyo iliishia ndani ya shamba la kahawa mara baada ya kuacha kuyasikia maneneo makali kutoka kwa mume wake aliyekuwa akimkibiza na panga.
“Pole sana mwanangu pole utapona sawa mama.”
“Ndio mama ila tunaenda wapi?” Naomi aliongea kwa sauti ya chini sana yenye kuhisi maumivu makali ndani ya kifua chake akitetemeka mwili mzima kwa hofu ya kukamatwa na baba yake aliyekuwa akimuogopa kupita maelezo.
“Kukipambazuka nitajua cha kufanya ila kwa sasa acha tulale hapa,” akamjibu akiwa akikilza kichwa chake juu ya mapaja yake na kumfunika kwa kipande cha kitenge alichobahatisha kutoka nacho, yeye akibaki hana kitu mabegani mwake hali iliyopelekea mwili wake kupigwa na baridi kali mno.
Baridi liliutesa mwili wake na wa mwanae kwa muda mrefu sana, Naomi alilia sana kwa maumivu ya baridi kali huku akiendelea kumlaani baba yake.
“ Simpendi baba.”
“Usiseme hivyo mwanagu huyo ni baba yako tu na huna haja ya kumchukia hata siku moja samehe kwa yote sawa mama?”
“Siwezi kwanini anataka kuniua? Simpendiiii …simpendiiiii,” mtoto Naomi alizungumza huku akilia kila alipomfikiria baba yake hakuweza kumuelewa lia yake ilipelekea kupitiwa na usingizi alikuja kushtuka wakiwa ndani ya gari lililokuwa limesheni mikungu ya ndizi.
“Mama tunaenda wapi?”
“Dar es salaam.”
“Kufanya nini?”
“Hospitali tukifika huko lazima upone sawa mama’
“Ahsante mama nakupenda sana.”
“Nami nakupenda.” alimjibu mwanae huku akimbusu busu la shavuni lenye upendo wa hali ya juu kila alipomtazama mwanae hakuweza kuamini kama siku moja angeweza kuponaa
****
Maisha ya Dar es salaam kwa Naomi na mama yake yalikuwa magumu mno kwani kila siku walikuwa wakilala vibarazani ama mbele ya maduka ya watu, mama yake hakuwa na kazi zaidi ya kuomba omba kila siku.Lile tumaini la yeye kumponesha mwanae lilikuwa limeyeyuka kabisa, muda mwingine alitamani hata kujiua ili tu aweze kuyakwepa mateso aliyokuwa akiyapata mtoto wake.
“Mama mbona hunipeleki hospitali kama ulivyodai?” Lilikuwa ni swali gumu sana kutolewa jawabu kwa mwanamke huyo mara baada ya swali hilo kutoka mdomo mwa Naomi miezi mitano baada ya wao kufika ndani ya jiji hilo.
“Naomi!”Akamuita bila kumtazama machoni uso wake aliuruhusu kulitazama wingu lililokuwa limetanda juu ya anga.
“Abeee mama.”
“Najua utaniona muongo sana najua utaniona sifai ila mwanangu naomba unisamehe sana, sipendi kuona unaumia kila siku na kulia mbele yangu, natamani hata nife ili tu niweze kuyakwepa mateso unayoyapata mwanangu,” akazungumza huku kope zake zikianza kulowa kwa machozi.
“Mama unasema nini!Unataka ufe na mimi nitabaki na nani?”akamuuliza mama yake huku akimutazama machoni, myoni akihisi kitu chenye ncha kali kikiuchoma maoyo wake pole pole akainama na kichwa chake kukibana katikatia ya mapaja yake akaanza kulia bila kuzungumza chochote.
Mama mtu alipata wakati mgumu mno kumtuliza Naomi, alimfahamu kwa kila kitu, alijua ameumizwa mno na maneno yake hivyo alikuwa na wakati mgumu wa kumtuliza, akajivuta karibu yake na kumgusa bega kisha akasema.
“Naomi nafahamu nimekuumiza sana kwa maneno yangu lakini kunakipindi nawaza hata kufa! Sipendi nikuone ukiteseka kila sekunde, nimejitahidi kadiri ya uwezo wangu imeshindikana, gharama ya wewe kupona ni kubwa mno nami masikini sina mbele wala nyuma mwili unatamani mwanagu upone ila moyo hauna uvumilivu kwa haya niyapatayo sikujua kama siku moja mimi ningekuja kulala barabarani, kula kwa nguvu za Mungu naomba omba kama sina akili timamu naomba kila siku n……” akashindwa kuendelea kuzungumza mara baada ya koo lake kukabwa na kitu kizito hali iliyopelekea kuanza kulia, kilio cha kwikwi akiwa ameufunika uso wake kwa viganja vyake vya mikono, tena mikono iliyokuwa michafu na yenye vidole vyenye kucha ndefu sana.Msongo wa mawazo na maumivu ya moyo vyote vilimfanya akawa hajijali kabisa, alinekana ni mchafu kupita maelezo laiti ungeweza kumuona miezi kadhaa nyuma usingeweza kuamni kama huyo alikuwa Maria Tarimo.
“Usilie mama yangu sitaki kukuuliza tena ila nina ombi moja tu naomba unieleze nini kinachonisumbua maana kila siku naumwa kifua tu na hujawahi kunieleza ni ugonjwa gani unaonisumbua.”
Akazungumza mara baada ya kuyashuhudia machozi ya mama yake, hakupendezwa na kitendo alichokifanya ilibidi ajishushe.
“Mh! Siyo mkubwa sana ila...ni…ni…aaha ni…unaitwaaa…,” kashindwa kuzungumza vizuri mara baada ya Naomi kumkazia macho makali yenye kuhitaji jibu hilo.
***
Macho makali mno kutoka kwa Naomi yalipelekea mama yake kukosa uvumilivu wa yeye kutoa jawabu sahihi la kipi kilikuwa kikimsumbua mwanae, japo ungonjwa aliufahamu lakini hakuwa tayari kumueleza hata siku moja alifahamu kufanya hivyo kungepelekea kuzalisha kitu kipya ndani ya maisha ya msichana huyo.
Maradhi ya moyo aliyafahamu sana na wengi wao waliokuwa na matatizo hayo walikuwa wakipoteza maisha mara baada ya kukosa huduma ya afya mapema.Uhai wa Naomi ulikuwa mdomoni wake kufungua kwake kinywa kungemfanya kumbakiza hai msichana huyo ama kumuua.
“Yaani mama siku nikifahamu sijui nina tatizo kubwa kama tulivyoelezwa na yule baba najiua”
“Kwanini?”
“Sasa unategemea mimi nitapona?Kwanza hakuna pesa halafu niendelea kuishi ili iweje?”
“Naomi usikate tama huijui kesho yako mwanagu.”
“Mh!Haya acha mie nilale.”
Kumbukumbu ya mazungumzo ya siku moja kati yake na mwanae ikapenyeza ndani ya ubongo wake na kubaki akimtazama Naomi midomo yake ikimcheza cheza
“Mama niambie.”
“Sio tatizo kubwa sana ila ni kama magonjwa mengine tu ya kwaida.”
“Kama ya kawaida mbona ulisema pesa nyingi sana?”
“Aah! Unajua nini hapa nyumbani hakuna madaktari wa kukutibu mpaka huko mbali,” ikabidi amdanganye ili kumuweka katika hali nzuri na kuyakwepa maswali ya Naomi ambayo mengi yake hayakuwa na majibu sahihi kwa wakati huo.Japo moyoni aliumia sana kumficha ila hakutaka kumumiza zaidi ya hapo maumivu aliyokuwa nayo yalikuwa yakimtosha sana hakutaka kumuongezea mzigo mwingine tena.
“Kwahiyo nikienda mbali nitapona?”
“Eeh!”
“Basi kuanzia sasa pesa nitakayopewa naitunza siku moja utanipekea huko si eti mama?”
“Hahaha!” Akacheka kwa kivivu huku akimvuta karibu binti yake na kumkumbatia kabla ya wote kulala juu ya maboksi waliyokuwa wameyatandika mbele ya duka la Mhindi mtaa wa Livingstone Kariakoo usiku huo.
Miaka miwili ya wao kuwa Dar es salaam mama yake alifariki mara baada ya kuungua kwa ugonjwa wa nimonia uliosababishwa na baridi. Siku hiyo Naomi alilia mno hakukujua afanye nini kwani hata yeye alikuwa mgonjwa japo kwa wakati huo hakufahamu alichokuwa akiumwa maana wazazi wake hawakuwahi kumueleza ugonjwa uliokuwa ukimsumbua.
“Mama kwanini umeniacha nibora ningekufa mimi ila si wewe tazama nitaishi wapi, kwanini mama umeondoka? Amka hata kidogo unitazame,” yalikuwa ni baadhi ya maneno ya uchungu aliyokuwa akiyazungumza Naomi huku akiusukuma sukuma mwili wa mama yake muda mfupi mara baada ya yeye kushtuka kutoka usingizini na kukuta mama yake tayari ameshafariki.
“Dogo punguza kelele watu tumeangusha wewe unaleta swaga kama unataka kuimba chimba studio hapa si pahali pake.”
Alisikia mmoja wa vijana waliokuwa wamelala karibu na Naomi akizungumza mara baada ya sauti ya kilio cha Naomi kupenyeza ndani ya ngoma zake za masikio na kuiona kama karaha kwake.
“Mama yangu amekufaaaaa.”
“Kama amekufa si mwisho wake umefika wewe kinachokuliza ni nini? Muache asepe kivyake kaaa kimya ukiendelea kunipigia kelele nakuzibua.”
“Siweziiiiiiiii…..niache… nilieee nikichoka nitanyamaza mwenyewe,” akamjibu huku akikizisha kilio aliina kama ananyimwa haki ya yeye kumlilia mama yake.
“Oyaaaa toa use*** hapa unacholilia ni nini kwa mfano unaleta hapa maswala ya kitwana nitakipasua hicho kichwa chako wengine ni watoto wa mbwa hatuogopo kuchana chana watu viwembe nitakutengeneza sura,” akazungumza huku akinyanyuka juu ya kipande cha boksi mkononi akikichomo kisu chake kidogo na kutembea hadi eneo alilokuwa amekaa Naomi akiwa ameulalia mwili wa mama yake ambao haukuwa na uhai tena.
“Unasikia kaaa kimya kabisa nitakutoboa uungane na huyo bi mkubwa sasa hivi,” kammwabia akiwa amekiweka kisu chake kilichokuwa kikali juu ya mgongo wake akiwa anamanisha alichokuwa akikizungumza.
Maneno hayo yalimfanya Naomi kukaa kimya kabisa,alibaki akililia ndani ya moyo wake picha ya mateso iliyokuwa mbele yake ilianza kuisumbua akili yake muda mwingine alitamani hata naye afe na si kuendelea kuishi duniani kwa mateso. Hadi kunapambazuka alikuwa bado analia, taarifa za kifo cha mama yake zilifika moja kituo cha polisi walioamua kuuchukua mwili wa mama yake na kuupeleka hospitali siku mbili mbele mama yake alizikwa na Jiji mbele ya macho yake kitu kilichomuumiza sana.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kifo cha mama yake kilipelekea Naomi kuyaanza maisha ya peke yake na ya huzuni kila siku, aliendelea kuishi mtaani akiomba omba na kuteseka kwa maumivu makali sana kila siku alimuuomba Mungu amchukue lakini haikuwa hivyo hadi anafikisha umri wa miaka kumi na tano Naomi alikuwa akiteseka kwa maumivu makali sana.
“Acha nikaombe pesa ya chai pale,” aliwaza na kunyanyuka eneo alilokuwa amekaa na kuanza kutembea kuelekea upande wa pili wa barabara, kutokana na njaa iliyokuwa imelisakama tumbo lake alijikuta akivuka barabara bila kutazama huku na huko hali iliyopelekea kugongwa na gari dogo na kuanguka papo hapo.
“Umeuaaa…umeuaaa….umeeuaaa… simamaaa… simaaa,” kelele za watu zilimfanya dereva wa gari lililosababisha ajari kuongeza mwendo mara baada ya kusikia sauti hizo alijua kusimama kungepelekea yeye kuangukia sehemu mbaya zaidi alichofanya ni kukimbia eneo hilo japo moyoni aliumia sana lakini hakuwa na jinsi.
“Jamani tena ni msichana mdogo kweli mzima?”
“Mzima?”mmoja kati ya umati wa watu uliokuwa umemzuka Naomi akauliza huku akiwatazama wenzake.
“Sasa nani anayejua si uje umekague!”
“Hiii!!!”
“Uwe na roho ya kibinadamu unafyatua maneno kama huna akili…hebu nipesheni nimtazame, akamjibu kijana aliyemdaka kwa lugha mbovu, lugha iliyowafanya watu wote kumshangaa.Akamsogelea Naomi aliyekuwa ametulia tuli mwili wote ukivuja damu, akachuchumaa na mkono wake wa kulia akaupitisha ndani ya kifua sehemu inayokaliwa na moyo hapo ndipo alipoutuliza.
“Vipi?”
“Mh!”
Akaguna na kuwatazama nao wakamtazama wakiwa wameiachia midomo yao wakigojea jawabu kutoka kwake.
Kila mtu alikuwa na shauku ya kufahamu kipi kingetamkwa je Naomi alikuwa hai ama la?
“Kuna uzima?”
“Kiasi,”akajibu huku akinyanyuka na kusimama, akatazama kulia na kushoto kutafuta kitu ila hakuona chochote.
“Yuko hai?”mwingine akauuliza kana kwamba hakusikia kile alichokizungumza mara ya kwanza.
“Ndiyo japo mapigo yake ya moyo yako chini sana tukimuwahisha hospitali atapona kabisa.”
“Basi acha tumpeleke Hospitali.”
Papo hapo wasamalia wema walimpakia Naomi ndani ya gari na safari ya kuelekea Muhimbili ilianza, mara baada ya kupitia polisi na kupata P F3 kwa ajili ya matibabu. Hakukuwa na foleni sana walijikuta wakitumia dakika ishirini tu kufika hospitalini hapo.Walifika mapokezi na kuandisha kisha Naomi alipelekwa moja kwa moja chumba cha upasuaji mara baada ya uchunguzi wa awali kufanyika na kubainika kuwa mguu wake wa kulia ulikuwa umevunjika kabisa sehemu ya paja.
“Dk. Samweli kuna mgonjwa wa ajari hivyo naomba niondokea mara moja nimepokea ujumbe sasa hivi.”
“Ooh! Pole fanya hivyo nadhani tutaonana kesho nataka nielekee nyumbani mara moja.”
“Kwanini usinisubili kidogo hajaumia sana.”
“Aaaah! Sa…sa….”
“Sawa.” alisema Dk.Emanuel mtaalamu wa mifupa huku akisimama na kutoka ndani ya ofisi ya Dk. Samweli aliyekuwa ameajiliwa hospitali hapo miezi saba iliyopita mara baada ya kumaliza shahada yake ya pili ya udaktari. Toka aajiriwe hospitalini hapo hakuwahi kuzungumza na Dk. Rose ambae naye alikuwa akifanya kazi hospitalini hapo, kila siku alitamani sana kuzungumza na msichana huyo ila Dk. Rose alikuwa akimchukia kupita maelezo.Matendo ya nyuma aliyokuwa amewahi kumfanyia alimuona Samweli hafai hata kukatiza mbele za macho yake.
“Aaah! Nimfuate huko huko,” alinyanyuka na kutoka ndani ya ofisi hiyo alinyosha moja kwa moja hadi chumba cha upasuaji.
“Umenifuata huku?”
“Nd….”
Alishindwa kuzungumza mara baada ya macho yake kupokelewa na sura ya msichana aliyekuwa amelala kitandani akiwa hajitambui, macho yake yakajikuta yakipata upofu wa muda mfupi sana baada ya sura hiyo kuingia ndani ya mboni zake za macho na kubaki akimtazama kwa muda mrefu sana moyo nao ukianza kupiga kwa kasi ya ajabu si mfano.
Hakujua kwa nini moyo wake ulianza kufanya kitendo hicho na ulishtuka sana, ni mara yake ya kwanza ya yeye kuwa katika hali hiyo msichana mdogo aliyekuwa kitandani hapo aliichanganya akili yake japo alikuwa mdogo kwa umri na mtu aliyedhoofika sana lakini aliichanganya sana akili yake achilia mbali uchafu wa mwili wake.
“Dokta huyo mrembo mzima?” Alimuuliza huku akimkazia macho msichana huyo.
“Ndiyo mzima nataka nimfanyie upasuaji mdogo tu hajaumia sana vipimo vya x-ray vimeonyesha kila kitu.”
“Basi sawa hakikisha anapon sawa?”
“Usijali hii ni kazi niliyokula kiapo Mungu anisaidie.”
“Amen.”
Alijibu na kutoka ndani ya chumba hicho, alinyosha moja kwa moja hadi ofisini kwake huku akiwa amechanganyikiwa hakufahamu ni kwanini msichana huyo alimchanganya akili yake,kila alipokuwa akiifikiria sura ya msichana yule alizidi kuchanganyikiwa.
“Anaonekana mrembo sana ila kwanini yuko vile,” aliwaza na kuipiga meza yake kwa ngumi nzito iliyopelekea saa yake ya mkononi kufunguka na kuanguka chini na kupasuka kabisa kioo chake.Hakuijari saa hiyo alinyanyuka na kusimama kisha akatembea na kuelekea dirishani macho yake yalipokelewa na madhari mazuri yaliyokuwa yamepandwa maua na miti mbalimbali nje ya jengo hilo.
“Kwanini moyo wangu unakwenda mbio kiasi hiki? Nini chanzo cha haya ama yule msichana,” akazungumza peke yake akiwa amesimama dirishani hapo macho yake yakiitazama miti na maua yaliyokuwa nje ya jengo hilo ila akili yake na mawazo yake yote hayakuwa eneo hilo msichana aliyetoka kumuona ndani ya chumba cha upasuaji alikuwa ameivuruga akili yake kwa asilimia kubwa sana.
Sura ya msichana yule ilikataa kabisa kutoka ndani ya akili yake kila alichokifanya ilitokea mbele yake alihisi kuumia zaidi hakujua afanye kitu gani.
“Kile ni kitoto mimi nina miaka ishirini na tano sasa kuna nini hapa katikati.”
Dokta vipi mbona unazungumza peke yako? Twende nimemaliza.” alishtuliwa na sauti ya Dk. Emanuel aliyeingia ofisini humo bila yeye kumuona. Sauti hiyo ikamfanya ashindwe kuzungumza na kubaki akimtazama huku mwili wake wote ukianza kutetemeka kitendo kilichomshtua sana Dk.Emanuel asijue kipi kilimfanya aanze kutetemeka kiasi hicho.
****
Dk.Emanuel akazidi kumtazama mwenzake kwa macho ya mshangao wa hali ya juu kabisa, hukuelewa ni kipi rafiki yake kilimtokea kwa wakati huo, akatembea taratibu hadi eneo alilokuwa amesimama Dk.Samweli na kumshika bega lake la kushoto kisha akaanza kumvua koti la kazi kitendo kilichomshangaza sana Dk.Samweli kwani hakufahamu kama wakati huo alikuwa bado na koti hilo mwilini mwake na hakufahamu ni wakati gani alilivaa.
“Unajisikia Dokta?”
“Niko sawa kwani vipi?”Akamjibu na kutoka dirishani hapo asijue kipi kilimtokea kwa wakati huo hata yeye alikuwa bado hajafahamu kwani alijikuta akiwa katika wakati mgumu kiasi hicho
“Lakini haupo sawa?”.
“Aah! Nipo sawa vipi anaendeleaje?”
“Hali yake siyo mbaya sana ila anaonekana kuwa na tatizo jingine ambalo sijalifahamu mara moja wacha kesho nitalishughulikia kwa leo apumzike.”
“Lipi hilo?” Alimuuliza huku akiwa ameyatoa macho hakutaka kusikia habari mbaya kutoka kwa msichana huyo aliyetokea kuiteka akili yake kwa muda mfupi sana toka awe kijana hakuwahi kuwa katika wakati mgumu kiasi hicho ujio wa Naomi eneo hilo ulizalisha kitu kipya ndani ya maisha yake.
“Inaonekana ana tatizo la moyo japo sina uhakikia sana.”
‘Shiti! Moyo?”akamuuliza huku akiikunja ngozi yake ya uso macho akiwa ameyatoa,mapigo ya moyo yakienda kasi mno.
“Ndiyo kwani vipi mbona umeshtuka sana je unamfahamu?” alimuuliza huku akiitoa miwani yake kana kwamba alikuwa hajamuona vizuri na kubaki akimtazama Dk. Samweli aliyekuwa ameshtushwa sana na taarifa ya Naomi.
“Hapana…nimeshtuka tu…ila hakuna taabu acha apumzike kesho tutalitazama je kaletwa na nani?”
“ Ni wasamalia wema anaonekana ni mtoto wa mtaani.”
“Ooh!”
Akasikitika akiwa ameiweka mikono yake yote usoni na kuyaficha macho yake kisha aliketi taratibu juu ya kiti chake na kutulia bila kuzungumza chochote, yote hayo Dk.Emanuel alikuwa anayashuhudia na kubaki akimshangaa sana.
“Baba angalia utapata matatizo hupaswi kuumia sana kwa mtu usiyemfahamu wewe ndiye unayetakiwa kumfariji.”
“Nafahamu ila najishangaa moyo wangu ukiumizwa sana na hali ya mtoto yule ila hakuna shida acha tuondoke tutazungumza kesho,” akasema huku akisimama na kuanza kutembea kutoka nje ya ofisi yake nyuma mwenzake akimfuta akiwa kimya kabisa. Wote walinyosha hadi eneo walilokuwa wamepaki magari yao na kila mtu aliingia katika gari lake mara baada ya kuagana kisha kila mtu alielekea kule alikokuwa akipafahamu yeye mwenyewe.
Moyo wa Dokta Samweli uliumia sana, hakupenda kupokea taarifa za msichana mzuri kama yule awe mtoto wa mtaani. Njia nzima aliitumia kumtafakari msichana yule ambaye mara moja hakuwa akimfahamu kwa jina. Hata alipofika nyumbani kwao hakuwa na furaha kama siku zingine alifika na kupitiliza chumbani kwake huko alijitupa kitandani bila kuvua hata viatu. Macho yake aliyapa nafasi ya kulitazama dali huku akimuwaza msichana yule. Waza waza yake ilipelekea kupitiwa na usingizi.
****http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilikuwan ni harusi kubwa sana ambayo haikuwahi kutokea ndani ya sayari ya tatu. Harusi hiyo ilionekana kuvunja rekodi ambazo ziliwahi kuwekwa na watu huko nyuma. Ulimwengu mzima uliitambua harusi hiyo ambayo ilitumia mwaka mzima kutoa matangazo kwenye vyombo mbalimbali vya habari ulimwenguni kote. Vyombo hivyo vya habari havikuwa nyuma kutoa matangazo ya harusi hiyo. Hayakuwa matangazo peke yake bali hata picha za wahusika wa harusi hiyo nazo hazikuwa nyuma kusambazwa kila kona ya dunia.
Picha za watu hao zilikuwa gumzo kwa kila mtu hakuna aliyetaka kupitwa na picha hizo, idadi kubwa ya watu walikuwa bize kuingia katika mitandao ya jamii kuzitafuta picha hizo na kuzihifadhi katika simu zao ama ndani ya tarakilishi zao.
“Jamani hii itakuwa harusi na sherehe kubwa sana na ya kwanza kutokea duniani kwanini wameamua kujitangaza kiasi kile” aliongea msichana wa Kikolea akiwa ndani ya mgahawa wa Janui kaskazini mwa nchi hiyo.
“Hata sijui ila natamani sana kuihudhulia ili nikajione kile kinachosemwa.”
“Kwani inafanyika wapi?”
“Tanzania!”
“Ndio wapi huko?”
“Wewe nawe huijui Tanzania? Ni moja ya nchi inayopatikana Afrika iko ukanda wa mashariki kule kwenye mlima Kilimajaro!”
“Oooh! Ungesema Kilimajaro!”
“Nitakwenda!”
“Hata mimi!”
Hayo ni baadhi ya mazungumzo ya watu duniani kote, kila mtu alitamani sana kuhudhulia harusi hiyo ambayo ilikuwa ya kihisroria.
Siku zilikatika hatimae siku iliyokuwa ikisubiliwa kwa hamu iliwadia usiku mmoja kabla ya sherehe hiyo watu walikesha wakiizungumzia utadhani siku ile TCRA walipotangaza kuzimwa kwa simu bandia ndivyo ilivyokuwa, baadhi ya wengine walidhubutu kulala na kukesha sehumu maalumu iliyokuwa ikitazamiwa kufanyika sherehe hiyo. Hawakuwa wajinga bali walifanya hivyo ili kuwahi nafasi maana mji wote wa Dar es salaam siku hiyo ulifurika watu wengi sana kutoka pande zote za dunia.
Majira ya saa sita mwanamke aliyeonekana mrembo kupita maelezo alikuwa ndani ya shera huku mwanaume nadhifu na mtanashati alionekana ndani ya suti nyeusi iliyokuwa imemkaa vizuri katika mwili wake na kuyafanya macho ya watu kuyagandisha mwilini mwake
Uwepo wao eneo hilo ulichangia watu wengi kukanyangana na hata baadhi yao waliweza kupoteza maisha kwani kila mtu alikuwa na hamu ama hamasa ya kutaka kuwaona wanadaoa hao.
“Umependeza mpenzi siamini kama kweli leo naenda kukuoa,” alisema Samweli huku akimtazama Naomi kwa macho ya upendo zaidi.
“Hata mimi siamini naona kama naota tena ndoto ya mchana.”
“Amini leo hii unaenda kuwa mke wangu,” alizungumza huku akiuchukua mkono wa Naomi na kuubusu kwa mara ya kwanza tangu wafike eneo hilo.
Kamera na mitambo mbalimbali haikuwa nyuma kuchukua kila tukio lililokuwa likitokea eneo hilo muda mchache wa maharusi hao mara mchungaji alitokea kwa lengo la kufungisha ndoa hiyo.
“Mimi Samweli Deus nimekubali kumuoa Naomi Mlema kuwa mke wangu maisha, nitampenda na kumvumila katika hali zote za maisha yangu furaha na maradhi,” alisema maneno hayo kisha alimvalisha Naomi pete ya ndoa makofi nderemo na vigeregere vilichukua nafasi.
“Mimi Naomi Mlema nimekubali kuolewa na Sa….” Kabla hajamalizia maneno hiyo alidondoka chini mara baada ya kupigwa risasi ya kichwa iliyopelekea kuyapoteza maisha yake papo kwa papo.
“Naomiiiiiiiiii” Samweli alipiga kelele za juu sana zilizopelekea hata wazazi wake waliokuwa sebuleni kushtuka na kukimbilia chumbani kwake.
“Samweli vpi?”
“Hapana ndotoo… mama ndotoo.” alisema huku akikitazama kidole chake kilichokuwa kikivikwa pete na Naomi pete ya ndoa yao lakini hakuiona pete hiyo ya ndotoni akabaki akikishangaa kidole chake kana kwamba kilikuwa kimekatwa.
“Ndoto gani hiyo?”Mama akamuuliza kwa mshangao sana kwani hakuwa na habari na wazazi wake waliokuwa wamesimama eneo hilo wakimshangaa kijana wao.
“Mama ndoto.” alijibu kwa aibu kisha alinyanyuka na kutoka chumbani huma akiwaacha wote wakimtazama bila kumuelewa, alinyosha moja kwa moja hadi nje na kusimama mbele ya gari lake akijiegemeza mgongo na akili yake ikarejea moja kwa moja kwa Naomi msichana aliyekuwa ameivuruga akili yake.
“Mbona inakuwa hivi mpaka namuota tena mtu nisiye mjua?”akajiuliza peke yake huku akianza kutembea tembea eneo hilo.
“Dogo nani kakuvuruga?” sauti ya kaka yake ndiyo ilimushtua sana na kusimama macho yake yakiwa yanamtazama kaka yake aliyefika eneo hilo bila yeye kumuona.
“Hakuna kitu bro ni maswala ya kikazi tu.”
“Lakini nishakuzuia kuwa hivyo hata kama ya kiofisi ukifika nyumbani yaache na itafute furaha, ofisini mawazo na nyumbani nako sisi hatupendi kukuona ukiwa hivyo, jiandae tutoke nikakupe hata ofa ya bia moja,” akazungumza huku akiupiga piga mkono wake na kulikunja shati lake la mikono mirefu rangi nyeusi.
“Kaka mimi nakunywa pombe?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hahaha! Nimezungumza ma kusudi ili niitoe akili yako huko nafahamu nakutania tu ila jiandae tutoke sawa.”
“Poa,” akamjibu na kumshika mkono kisha wote wakatembea kwa furaha kuingia ndani nusu saa walikuwa wamemaliza kujiandaa na kutoka, kaka yake alihakikisha anamfanyia vitu vya kumsahaulisha mawazo aliyokuwa nayo japo hakufahamu kwa wakati huo alikuwa akisumbuliwa na nini ila daima hakupenda kumuona mdogo wake akiwa katika hali hiyo aliifahamu kazi yake ilivyokuwa ngumu. Majira saa sita usiku walirudi nyumbani wakiwa wamechoka na kila mtu alipitiliza chumbani kwake na kujitupia kitandani tayari kwa kuumalizia usiku uliokuwa umebaki.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment