IMEANDIKWA NA : ATUGANILE
MWAKALILE ********************************************************************************* Simulizi
: Kurudi Kwa Moza Sehemu Ya Kwanza (1) Moza
alikuwa msichana mrembo ila aliishi maisha ya shida na kumfanya ajaribu kufanya
kazi za ndani, na kwa bahati akapata kazi kwenye nyumba ya mama mmoja tajiri,
aliyejulikana kwa jina la Rose ila huyu mama mara nyingi alikuwa hadumu na
wafanyakazi wa ndani mara nyingi huwa anawafukuza na watu walijua hivyo hakuna
aliyejua ukweli kuhusu wafanyakazi wa Rose kwani gafla utakuta wamepotea na
ameleta mfanyakazi mpya kwahiyo wengi walihisi huwa anawafukuza. Siku ya
kwanza kumleta Moza nyumbani kwake alimpa onyo kabisa, "Mambo ya nyumba
hii uyaache kama yalivyo, wewe fanya kazi zako tu basi. Usiingilie mambo
yasiyokuhusu" "Sawa mama nimekuelewa, unadhani naweza kuingilia
yasiyonihusu? Siwezi kufanya huo ujinga " "Yani usithubutu kuingilia
utaishia kubaya" "Mbona unanitishia mama?" "Sikutishii ila
nakwambia hali halisi, umbea kwangu sitaki kabisa kama huwezi kazi unaweza umbea
useme kabisa uondoke" "Hapana mama simaanishi kuwa naweza umbea, kwanza
binafsi umbea siupendi kabisa kwahiyo hata usijali kuhusu mimi" Basi
huyu mama alimuonyesha kazi zote za ile nyumba na vyumba vyote vya kusafisha,
kwakweli nyumba ilikuwa ni kubwa sana lakini alimuonyesha yote, ila kulikuwa na
chumba flani kilikuwa na chumba kwa ndani kile chumba kilikuwa kama choo cha
ndani ya chumba na vigumu kujua kama kuna chumba ndani ya chumba, yule mama
alimwambia Moza "Hiki chumba ukishasafisha unakifunga halafu funguo
unaweka juu ya mlango" "Na hiko choo je nitakuwa nakishafishaje maana
naona kufuli au hakisafishwagi?" "Wee binti mbona umeanza kunitisha,
umekionaje hiko?" "Nilijikuta nimeangalia tu nyuma ya hilo kabati,
nisamehe lakini. Kwani hakisafishwi au?" "Hiko kilitengenezwa kwa lengo
la kuwa choo ila kishazibwa na hakitumiki, nyuma yake kushabomolewa ila hapa
mwanzo mlango ulibakia na kufuli, huwa hapafunguliwi maana hakuna choo wala nini
na ukitoka ni nje kabisa ndiomana nimeweka kabati kama kuziba. Na wewe uache
kuchunguza chunguza, kazi yako kwenye chumba hiki ni kusafisha tu nikikwambia
ili kusiwe na vumbi basi ingawa halali mtu lakini panatakiwa
kusafishwa." Wakatoka nje na kumuonyesha sehemu zingine za kusafisha
kisha alipomaliza ndipo Moza alianza kazi rasmi kwenye nyumba hiyo. Moza
alianza kumfahamu mtoto mmoja mmoja wa yule mama na hatimaye akamfahamu mume wa
yule mama aliyejulikana kwa jina la Mr.Patrick, ila kitu kilichomshangaza Moza
ni kuwa huyu baba hakuwa na sauti yoyote kwa mkewe yani chochote kitakachosemwa
na mkewe kwake ni sawa, Moza alishangaa sana na kujiuliza, "Ina maana
huyu baba hawezi kuhoji? Au ndio mambo ya mjini ya mume kulelewa na mke wake,
hata kama ndio akubali kila kitu. Ila nishaambiwa nisifanye umbea kwenye nyumba
hii, ngoja niendelee na kazi zangu mie " Moza aliendelea na kazi zake
ila alijikuta akizoeana sana na mtoto wa kwanza wa yule mama, mtoto huyo alikuwa
ni mdada mkubwa na alijulikana kwa jina la Sara, huyu msichana alimpenda Moza
sababu Moza alikuwa anamsikiliza mambo yake, "Unajua kwanini
nakufagilia? " "Sijui, hebu niambie kwanini" "Sababu wewe
unapenda kunisikiliza ninachosema " "Unajua kila mtu anapenda
kusikilizwa, lakini kwanini wewe hupendagi kumsikiliza baba
yako?" "Achana na yule baba bhana utaniudhi, kwanza hana hadhi ya kuwa
na mtoto kama mimi. Yule ni bwege la mama tu" Sara akaondoka zake ila
Moza alibaki na maswali mengi sana kuwa kwanini yule Sara aseme vile, inamaana
si mtoto wa yule baba? Na watoto wengine je, mbona wote hawamuheshimu yule baba?
Moza aliwaza sana lakini badae alijiambia. "Mambo ya umbea nilishaonywa
kwenye nyumba hii" Muda kidogo akiwa anafanya usafi wa kusafisha dirisha
aliwasikia watoto wawili wa kiume wa yule mama Wakiongea, yule mama alikuwa na
jumla ya watoto wanne, wa kwanza wakike aliyejulikana kwa jina la Sara, wa pili
ni wakiume ambao walikuwa ni mapacha walijulikana kama Kulwa na Doto, wa mwisho
alikuwa wakike ila alikuwa sio mkubwa sana na alijulikana kwa jina la Ana. Sasa
watoto ambao Moza alitegesha sikio lake kuwasikiliza ni hao mapacha na hata
hawakujua kama kuna mtu anawasikiliza, Moza alitulia tu
akiwasikiliza: "Yani mimi nikitaka kuoa nitamwomba sana Mungu nisije
pata mke kama mama yetu" Mwenzie akasikika akacheka kisha
akasema, "Kumbe inakuuma eeehh anavyofanyiwa huyu baba? " "Yani
inaniuma kinoma, sema tu ndio hivyo sio baba yetu hatuna cha kufanya ila
inaniuma sana yani sana" "Lakini moyoni unafurahia maisha ambayo mama
anatupa, hivi ushawahi kujiuliza ungekuwa wapi maana baba yetu alishatukataa
toka kitambo." "Mi nadhani alichofanyiwa mama na baba yetu labda ndio
kimemfanya awe hivi alivyo, ila nashukuru Mungu tunakula vizuri, tunaishi maisha
mazuri tunayoyataka. Ila anayoyafanya mama yetu duh!" "Mama alishasema
tusiwaze sana na anachokifanya, tuwe makini na maisha yetu tu." "Hata
kama, hivi unakumbuka juzi aliku.......... " Moza gafla alishtuliwa na
Ana, na kumfanya ashtuke sana na aache kusikiliza umbea, "Dada twende
ukanitandikie kitanda" Moza aliondoka na Ana huku akijiuliza maswali
mengi sana juu ya yule baba mwenye Nyumba. Moza alifika chumbani kwa Ana
na kumtandikia kisha akamuuliza, "Hivi mtoto mkubwa kama wewe
unashindwaje kujitandikia kitanda" "Wenzako kama wewe walikuwa na
maswali ya kudadisi sana kwangu, kazi ikawashinda na mama akawatokomeza. Wewe
umekuja kufanya kazi au kuuliza maswali?" Ikabidi Moza amuombe msamaha
mtoto Ana kisha kuondoka zake kwenda kuendelea na kazi zake huku akijiuliza
maswali mengi sana. Usiku wake Moza alishangaa yule mama akimuita kwa
ukali sana, "Wee Moza wewe" Moza alishangaa kuitwa kwa ukali
vile na kwenda kwa haraka sana, alivyofika pale tu cha kwanza alipigwa kofi hadi
chini, akamtazama yule mama aliyeonekana na hasira sana, kisha yule mama
akamuuliza Moza, "Maswali gani ya kijinga hayo unamuuliza
mwanangu?" Moza alikuwa kimya alishindwa kujibu maana hakujua ubaya wa
swali lake kwa yule mtoto ukizingatia anaonekana ni binti tayari wa karibia
miaka kumi na mbili. Usiku wake Moza alishangaa yule
mama akimuita kwa ukali sana, "Wee Moza wewe" Moza alishangaa
kuitwa kwa ukali vile na kwenda kwa haraka sana, alivyofika pale tu cha kwanza
alipigwa kofi hadi chini, akamtazama yule mama aliyeonekana na hasira sana,
kisha yule mama akamuuliza Moza, "Maswali gani ya kijinga hayo
unamuuliza mwanangu?" Moza alikuwa kimya alishindwa kujibu maana hakujua
ubaya wa swali lake kwa yule mtoto ukizingatia anaonekana ni binti tayari wa
karibia miaka kumi na mbili. Moza alibaki akishangaa tu, mara kibao
kingine akapigwa, kasha Yule mama akamwambia, “Si nilishasema mambo ya
udadisi kwenye nyumba yangu sitaki, huyu mtoto asipoweza kutandika kitanda wewe
inakuhusu nini? Inamaana wewe ndio unajua kulea sana au, mambo ya mtoto wangu
hayakuhusu. Kama hajui kufanya kazi yoyote mwache tu kama alivyo, nimekuajili
wewe sio uje kukaa tu na kuuliza uliza maswali ya kijinga. Sitaki, na
ninakwambia sitaki kabisa huo upuuzi na nisisikie tena” Ikabidi Moza
amwombe msamaha mama huyu, “Nisamehe mama, kwakweli haitajirudia tena.
Naomba nisamehe. Nisamehe sana” “Mimi sio wa kuniomba msamaha, nenda
kamuombe msamaha Ana huko” “Lakini Ana nilishamuomba
msamaha” “Mpaka kaniambia mimi inamaana hajakusamehe, nenda kamuombe
msamaha tena mpaka akusamehe ndio uje hapa. Na asipokusamehe jiandae kurudi
kijijini kwenu” Moza akaondoka taratibu mpaka chumbani kwa Ana akaingia
na kumuamsha kasha kuanza kumuomba msamaha, Ana akamuangalia Moza akamsonya
kasha akamwambia, “Hivi unaingiaje chumbani kwangu bila ya hodi, hujui
kugonga hodi au? Halafu unaniombaje msamaha huku umesimama kama mlingoti? Toka
nje huko, ugonge mlango nikuruhusu kuingia kasha uje na magoti ndio uniombe
msamaha” Moza akatoka nje na kugonga mlango, aliporuhusiwa na Ana
alipiga magoti, akaingia chumbani kwa Ana na magoti kisha akamuomba msamaha, Ana
alicheka kasha akamwambia, “Nimekusmehe ila siku nyingine usirudie tena.
Nilijua na wewe ni kiburi kama waliopita. Haya ondoka zako” “Asante
Ana” Moza alitoka huku macho chini, alienda kumalizia kazi zake kasha
akaenda kulala. Alipokuwa chumbani aliwaza sana, na
kujisemea “Jamani umasikini huu loh, yani mimi kweli wa kudhalilishwa na
yule mtoto mdogo jamani? Yule si sawa na mtoto wa dadangu jamani, yani
kanidhalilisha nimpigie magoti nimuombe msamaha, yote haya ni sababu ya
umasikini tu. Ningekuwa na uwezo au kwetu kungekuwa na uwezo yasingenipata yote
haya, ila wadada wengi wa kazi tunateseka sababu ya
umasikini.” Alijifikiria sana, ila aliamua kulala ili kesho awahi kuanza
usafi na shughuli zingine. Akiwa kwenye usingizi mzito wakati
panakaribia na kukucha akajikuta yupo kwenye ndoto nzito sana, alijiona yupo
mahali halafu kuna wadada kama watano wapo pande ya pili wakimuomba msaada,
akawa anasikia kelele, “Moza tusaidie, Moza tusaidie tafadhari,Moza ni
wewe tu unaeweza kutusaidia” Wakati anataka kwenda kuwasaidia akashtuka
kutoka usingizini, alikaa akitafakari kuwa ni ndoto ya aina gani ile. Lakini
alipoangalia saa aliona karibu panakucha, alitoka chumbani na kwenda kuanza
shughuli za usafi, alishangaa kumkuta baba mwenye nyumba yani Mr.Patrick akiwa
sebleni muda ule amesinzia, hakutaka kuhoji kwani taratibu za nyumba ile bado
hakuzijua vizuri kwahiyo alianza tu kufanya kazi zake hadi muda wanaamka wengine
na kujiandaa kutoka huku wengine wakisubiria chai mezani ikabidi
awaandalie. Siku hiyo Ana alichelewa kuamka, ila kwavile hakujua
taratibu za nyumba ile alijua ndio kawaida, mama mwenye nyumba aliamka na
kumfata Moza jikoni, “Umeshamuamsha mtoto aende shule?” “Mtoto
yupi mama? Kwanza shikamoo” “Nitolee uwendawazimu wako mie, inamaana
humuoni Ana kuwa ni mtoto! Kwahiyo hujamuamsha hadi muda huu unategemea nini?
Mwanangu haendi shule, au ulijua hasomi kama watoto wa kijijini kwenu? Haya
nenda kamuamshe na utaenda nae shule, wewe ndio utamtetea kuchelewa
kwake” Moza hakubisha ila alienda hadi chumbani kwa Ana, ila alipofika
mlangoni akasita kuingia maana jana yake huyo Ana alimfokea kwa kitendo cha
kuingia bila ya hodi. Ikabidi aanze kugonga hodi, aligonga na kugonga na kugonga
ila hakuitikiwa akawa anajishauri tu kuwa afanyaje, wakati anajishauri, Sara
alipita pale na kumkuta anagonga, “Weee huyo mtoto analalaga kama pono,
yani hapo utagonga hadi vidole viote sugu. Ingia tu umuamshe” Moza
akamwambia Sara, “Lakini jana alinikataza kuingia chumbani kwake bila ya
hodi” “kitoto kina amri sana hicho sijui kwanini, ila ingia tu. La sivyo
atazidi kuchelewa shuleni” Ikabidi Moza aingie huku akiwa na hofu ya
kufokewa na Ana. Akaanza kumuamsha kwa utaratibu, “Ana, amka uende shule
mtoto mzuri” Ana alimka, kasha akatabasamu baada ya kuamka, na kumwambia
Moza “Kaniwekee maji ya kuoga nioge halafu niandalie na sare
kabisa” Moza alimuandalia huku akimsikiliza kuwa ni nguo gani amuandalie
kasha Ana akaenda kuoga na kuvaa, baada ya kumaliza ilitakiwa Moza ndio ampeleke
Ana shuleni, akatoka sebleni na kumkuta mama na baba, “Mama, ndio nataka
kumpeleka Ana shuleni” “Si umpeleke, unataka mimi
nifanyeje?” “Nampelekaje mama?” “Hivi si uzembe wako, gari ya
shule imemuacha? Mpeleke sasa utajua wewe utampelekaje” Moza
akajifikiria akakosa jibu, mjini kwenyewe hajawahi kuishi kivile sasa ni njia
gani atampeleka huyo mtoto shuleni ikiwa hata shule ilipo hajui, wakati anawaza
hayo akamsikia Yule baba mwenye nyumba akisema, “Naomba niwapeleke mke
wangu, nipe ruhusa yako.” “Si mafuta yako hayana kazi” “Ila mke
wangu, huyu mdada bado ni mgeni” “Bhana wee wapeleke ila ndio ajifunze
sio kesho tena amuache mtoto alale mpaka muda huu. Na hakikisha unaenda kumtetea
mtoto kwa walimu. Tumeelewana Moza?” “Ndio mama” Kisha, Moza,
Ana na Mr.Patrick wakatoka na kuelekea kwenye gari la Mr.Patrick halafu safari
ya shule ikaanza. Walipofika shuleni, Moza alishuka na Ana hadi kwa
walimu wake, ambapo mwalimu mmoja akasikika akisema “Ana umechelewa na
leo ila kama kawaida yako umeletwa na mtetezi. Haya dada tunashukuru kwa kumleta
Ana, nenda tu. aAna nenda darasani” Moza alimshukuru pale kasha akarudi
kwenye gari na safari ya kurudi nyumbani ikaanza, huyu baba alimuuliza
Ana, “Hivi kitu gani kilifanya uje kufanya kazi pale
kwetu?” “Nilikuwa natafuta kazi tu ndio nikapata pale” “Unajua
kama ukiingia pale hutoki?” “Sitoki kivipi?” “Yani huwezi kurudi
kwenu” “Kivipi baba mbona sijakuelewa?” “Ile nyumba nilijenga
mwenyewe kwa mikono yangu, kwa hela zangu ila hata mimi kutoka siwezi. Nafahamu
vingi ila sina ufahamu wa kutoka” Moza akajikuta akivutiwa sana na
mazungumzo haya, huku akimuuliza Yule baba kwa makini, “Hebu nieleweshe
vizuri baba, nasikia wafanyakazi waliotangulia mama aliwafukuza sasa sijui
walifukuzwa kwa nini?” “Hawajafukuzwa ila walipo hata mimi sijui na mke
wangu hajanipa nafasi ya kujua. Nimechagua leo kukusindikiza ili nikwambie haya.
Nakuona huna hatia, ila umeingia sehemu sio yenyewe. Mimi ni baba mwenye akili
zangu timamu kabisa lakini zipo kama hazipo. Nina mtoto ambaye ni damu yangu
kabisa, naamini ni damu yangu ila mke wangu huyu ananiaminisha kuwa Yule mtoto
si damu yangu” “Yuko wapi huyo mtoto? Je ni mmoja kati ya waliopo
nyumbani?” “Hapana si mmoja wao, yupo kwa mamake anaitwa. Yani Yule
mtoto ni damu yangu kabisa ila mke wangu hataki kumuona wala hataki niwasaidie.
Ujana umeniponza mimi, mwanangu anapata shida huko alipo ila kumsaidia siwezi.
Kwa wale waliopo nyumbani, siamini hata mmoja kuwa ni mwanangu, wale watatu
nilimkuta nao mke wangu ila huyu Ana amezaa akiwa na mimi. Ila siamini kama ni
mwanangu kwani kuna mwanaume alishaletwa nyumbani, na mke wangu alikuwa anamuita
baba Ana halafu Ana nae alikuwa anamuita huyo mwanaume baba” “Baba, yani
sielewi kabisa. Na kwanini umeniambia yote haya?” “Nimejisikia tu
kukwambia, kisha kuwa makini sana. Ila mke wangu sijue kama nimekwambia,
usithubutu kuongea chochote na kumuonyesha kama kuna jambo nimekwambia. Mimi
siendi sehemu nyingine mpaka aniruhusu yeye. Ningepata mtu wa kunisaidia,
kunitoa kwenye hiki kifungo ningefurahi sana” “Pole sana
baba” “Tafadhali usiseme, nakuomba usiseme. Utapotea” Gari
ikaingia ndani, kisha kimya kilitanda na wakashuka garini, moza alipoingia ndani
alimkuta Yule mama akijiandaa kuondoka ila kabla hajatoka
alimwambia, “Haya mume wangu umesharudi naomba ukalale hadi
nitakapokuja” Yule baba hakupinga, alienda moja kwa moja chumbani kisha
Yule mama akamuangalia moza na kusema, “Kama nilivyokwambia, kuwa
makini. Mambo ya umbea kwenye nyumba yangu sitaki” Yule mama akatoka
zake, na Moza akaenda kwenye shughuli zake zingine. Akiwa
jikoni, walikuja wale mapacha na kumuaga pia, “Sie tunatoka, sasa
ukipika vyakula kama vya kijijini kwenu utakula mwenyewe” Wakaondoka
zao, na muda kidogo akaja Sara nae na kusema, “Leo nina hamu na maini
rosti na chapati na juisi. Tafadhali nitengenezee hivyo, nikirudi nitakula maana
nataka kutoka” “kwahiyo ndio niandae chakula hicho leo?” “Sijui
wengine wanapenda nini, kwani mama hajakwambia anachotaka
leo?” “Hajasema” “Basi mkaangie samaki, mwekeena viungo. Mama
anapendaga samaki sana” “Na chakula gani sasa?” “Utamuwekea na
hizo chapatti, anapenda pia. Ila Ana anapenda wali, yani fanya ufanyavyo ila
wali usikose. Halafu baba anapenda ugali, ila baba usimjali sana maana
atakachosema mama atakula tu. Mimi ndio natoka hivyo, tuitaonana
badae” Sara akaondoka zake, yani moza kabaki tu
anajiuliza, “Humu ndani kama hotelini, yani kila mtu anaagizaa chakula
anachotaka yeye yani nitakonda humu. Ila umaskini huu loh, ndio umesababisha
yote haya. Ila wale mapacha hawajasema ni chakula gani, natumaini nao watakula
maini rosti na chapati.” Moza alianza kuandaa mapishi yake huku
akijikuta anamfikiria sana Yule baba, yani maisha ya Yule baba yalimsikitisha
sana, hakuwa na kauli yoyote kwa mkewe na alimsikiliza mkewe kwa chochote
alichomwambia. Wakati anaendelea na mapishi, roho yake ikamtuma aende
kwenye kile chumba ambacho kinaonekana kina choo ndani
kilchofungwa, “Mmh mama akinikuta kwenye kile chumba, nitamwambia
nilikuwa nafanya usafi. Ngoja niende” Alipomaliza tu kuandaa chakula,
moja kwa moja akaenda kwenye kile chumba na kuchukua ufunguo juu ya mlango kisha
akafungua na kuingia ndani. Ila mawazo yake yalikuwa ni kwenye mlango wenye
kufuri basi huku akijiuliza kama ule mlango unatoka nje mbona kwa nje hauoni?
Akajisogeza moja kwa moja huku akihisi kuwa huenda akishika kufuli unaweza
kufunguka, basi Moza akasogelea na kushika lile kufuli gafla alipigwa na shoti
ya ajabu na kutupwa kabisa. Hapo akazimia, na lilipita lisaa limoja
akazinduka akiwa amechoka sana, akajaribu kuinuka akaweza, kisha akatoka na
kufunga mlango halafu funguo akazirudishia pale pale juu. Akaelekea sebleni
sasa, Mara akakutana na mama mwenye nyumba nae anaingia sebleni kutoka nje akiwa
na hasira sana. Hapo akazimia, na lilipita lisaa
limoja akazinduka akiwa amechoka sana, akajaribu kuinuka akaweza, kisha akatoka
na kufunga mlango halafu funguo akazirudishia pale pale juu. Akaelekea sebleni
sasa, Mara akakutana na mama mwenye nyumba nae anaingia sebleni kutoka nje akiwa
na hasira sana. Alikuwa anahema juu juu, akamsogelea Moza na kumuuliza kwa
ukali “Umefanya nini?” “Sijafanya chochote mama” Rose
alimuacha Moza pale sebleni na kuelekea mitaa ya chumbani ambapo moja kwa moja
alielekea kwenye kile chumba, Moza alienda jikoni huku uoga ukiwa umemshika na
kuomba kuwa huyu mama asijue kama aliingia mule chumbani. Ingawa moza alikuwa
kamaliza kupika ila alikaa tu jikoni akiwaza, muda kidogo Rose alirudi sebleni
na kumuita Moza kwa ukali, kitendo ambacho kilimuogopesha Moza na kuhisi kuwa
pengine Rose amegundua. Alienda sebleni kwa uoga kiasi, kisha huyu mama
akamuuliza, “Baba aliamka toka ameenda kulala?” “Hapana mama,
toka muda ule sijamuona tena sebleni?” “Sikia Moza, naomba vitu vya
nyumba hii uviache kama vilivyo” “Ila sijafanya kitu
mama” “Nilikuwa mbali sana, ila kuna kitu kimefanyika ndani nimepata
taarifa ndiomana nikaja haraka sana. Ila kwavile umesema hujafanya kitu, basi.
Hata hivyo hicho kitu ambacho nilikuwa nakihisi kuwa umekifanya basi muda huu
ningekukuta na hali mbaya sana. Tafadhali Moza, vitu vya nyumba hii viache kama
vilivyo. Unaweza ukanishangaa kuwa mbona narudia rudia msemo wangu, nina maana
kabisa, viache kama vilivyo” “Sawa mama nimekuelewa” “Na sitoki
tena saivi,ngoja nikapumzike tu. Nipikie ugali na samaki, nitakula
nikiamka” Moza alienda jikoni kuandaa huo ugali huku akiwaza kuwa
amepona ila aliwaza ameponapona vipi bila kubambwa ingawa alizimia kwa karibu
lisaa lizima, pia akawaza kuwa huyu mama kapata vipi taarifa huko alipokuwa
kwamba ule mlango ulishikwa? Hapo kidogo akapatwa na uoga, akawa tu anajisemea
mwenyewe “Mimi Moza mimi jamani nitulie tu, kwetu nakupenda pia.
Nitakuwa sirudi mmmh” Alipomaliza alienda chumbani mara
moja. Alipoingia chumbani alijiweka kitandani, mara usingizi
ukampitia. Akaanza kuona kama anaingia tena kwenye kile chumba, kisha anafungua
mlango wa kile choo ila mule aliwakuta wadada watano wakiwa wamechoka sana, ni
wadada walewale ambao walikuwa wakimuomba msaada kwenye ndoto ya jana yake.
Kwahiyo ndoto hii ilikuwa kama muendelezo wa ile ndoto ya usiku ila ndoto hii
ilikuja kivingine. Wakati anawashangaa wale wadada, halafu akawa kama anataka
kuwahoji, mara gafla akasikia sauti ikiita… “Moza,
Mozaa…” Akashtuka kutoka usingizini na aliposikiliza vizuri ilikuwa ni
sauti ya Ana, ikabidi atoke haraka kwani alitambua itakuwa Ana amerudi shuleni.
Moza alivyofika sebleni akamkuta Ana amekaa na amevimba kwa hasira, ilibidi Moza
aanze kwa kumuomba msamaha “Nisamehe Ana, nilipitiwa na usingizi
kidogo” “Umekuja kulala au kufanya kazi, yani mimi nakuita muda wote
huitiki, haya piga magoti” Moza hakubisha alipiga magoti, kisha Ana
akamwambia, “Nivue viatu” Moza alimvua Ana viatu, kisha akanza
kumsikiliza ujumbe mwingine “Begi langu la madaftari nimeliacha pale
getini kwa mlinzi kalichukue unipelekee chumbani.” Moza alienda kwa
mlinzi kuchukua begi, Yule mlinzi akamwambia Moza “Usisubiri siku
nyingine akukumbushe, yani akirudi tu uje uchukue begi lake. Yeye hawezi kubeba
eti ni zito” Moza aliondoka na lile begi hadi chumbani kwa Ana akagonga
na kuruhusiwa kuingia, kisha akaenda kuliweka lile begi. Ana akamwambia
Moza, “Nipikie tambi na mayai, nataka kula hivyo leo” Moza
aliitikia kisha akaenda jikoni kuandaa huku akiwaza moyoni, “Hivi mimi
ni mfanyakazi wa ndani au ni mfanyakazi wa hotelini? Mmmh hii nyumba unaweza
kujikuta siku nzima unapika tu” Aliwaza Moza huku akifikiria kutoweza
kufikisha hata miezi miwili humo ndani, “Kazi za humu ni za kitumwa
sana, yani mwezi huu ukiisha tu nipate mshahara wangu nirudi kwetu nikaangalie
ustaarabu mwingine” Alipika na alipomaliza, alitoka nje na moja kwa moja
alienda getini kwa mlinzi, kisha akamuuliza “Kaka samahani, hivi wewe
una muda gani toka uanze kulinda hapa?” Huyu mlinzi akacheka kwanza,
kisha akamwambia “Ni kitambo sana, kabla huyo Ana hajazaliwa. Mimi nipo
hapa, yani huyo Ana anakuwa namuona” “Kheee kumbe! Mbona nasikia
wafanyakazi wa hapa hawakai yani wanafukuzwaga” “Ni wa huko ndani sio
mimi, ni sababu hawawezi kufatilia sheria za huyu mama. Mfanyakazi ambaye alikaa
hapa kwa muda mrefu ni mmoja tu, ambaye anaitwa Ashura. Yeye peke yake ndio
alikaa hapa kwa muda mrefu na aliondoka mwenyewe ila ni mtu mwenye siri nzito
sana” “Yuko wapi huyo Ashura?” “Dada, tambua kwamba unaongea na
mwanaume. Nimekaa kwa muda mrefu kwenye nyumba hii sababu mimi ni mwanaume.
Mambo ya umbea sifanyi. Naomba kaendelee na kazi zako” Moza aligeuka
nyuma akamuona mama mwenye nyumba amesimama, ikabidi Moza aende upesi
kumsikiliza, “Kule getini unatafuta nini?” “Nilikuwa namuuliza
mlinzi masoko yalipo kwa hapa” “Yule mwanaume na mambo ya masoko ni wapi
na wapi? Moza, chunga sana nakuangalia ujue nakuangalia sana, huo mwenendo wako
sijui kama tutawezana. Haya kaniwekee chakula mie” Moza aliingia ndani,
kisha Yule mama alienda kwa mlinzi, inaonyesha alienda kumuuliza pia
kilichompeleka Moza pale getini. Moza alipomaliza kuandaa, Yule
mama aliingia na kukaa mezani, kisha akamwambia Moza “Una bahati sana,
Yule mlinzi kaniambia ni kweli ulikuwa unamuuliza kuhusu masoko. Vinginevyo
ungenitambua. Haya kaniitie kipenzi changu Ana nije kula nae” Moza
aliondoka kwenda kumuita Ana huku akijiuliza, Yule mlinzi kama amepanga nae
vile, imekuwaje nae amesema kama yeye kuwa alikuwa anaulizia masoko, yani kama
alikuwa kwenye akili ya Moza. Kma kawaida aligonga kwa Ana na kumuita
ambapo aliitikia wito na kwenda sebleni, kisha akamwambia Moza amletee chakula
chake, ambapo Moza akafanya hivyo. Rose alipoona mwanae ameletewa kile chakula
akasema, “Oooh kipenzi changu leo umetaka tambi na mayai” “Ndio
mama, kuna sehemu nimeona picha nikatamani” Kisha Rose akamuita Moza na
kumuuliza, “Wengine umewaandalia chakula gani?” “Dada Sara
amesema nimuandalie chapati na rosti ya maini, wale mapacha wamesema niwaandalie
chakula chochote kizuri. Kwahiyo nao nimewaandalia chapati na rosti ya maini.
Ila kuhusu baba nilimuuliza Dada Sara akasema anapendeleaga ugali kwahiyo nae
nimemuandalia ugali” “Wewe Moza wewe, hizo habari sijui za dada Sara
sijui mapacha sitaki kuzisikia, sijui baba sitaki kusikia. Hao wote wanakula
chakula ninachosema mimi. Mwenye amri humu ndani ni mimi tu, na Ana. Kwahiyo
chakula ukiambiwa ukiandae na Ana, fanya upesi au mimi nikikwambia uharakishe
ila usiniletee hayo madudu mengine.” “Lakini si watoto wako
pia?” “Wewe, wewe, weeee msichana wewe usitafute maneno yani naona
unachokonoa chokonoa mambo. Kwani wakiwa watoto wangu ndio nini sasa? Wawe na
amri kwani nyumba yao hii? Tena sitaki kusikia. Mwenye amri humu ndani ni mimi
na Ana tu nimemaliza” Moza aliitikia na kwenda zake jikoni huku
akijiuliza maswali mengi sana bila ya majibu, na haswa ni kuhusu baba mwenye
nyumba, masikini toka alipoambiwa akalale hajapewa amri ya kuamka hadi muda
ule. Moza akiwa kule jikoni, Yule mama alimuita kutoa vyombo kisha
akamwambia, “Siku nyingine sio mpaka nikuite kutoa vyombo, unatakiwa
kujiongeza mwenyewe.” “Sawa mama” Moza alitoa vile vyombo ila
alihisi kama Ana na mama yake wana maongezi ya ishara ambayo yeye hakuyaelewa
moja kwa moja, na muda kidogo Ana na mama yake wakatoka yani wakaondoka kabisa
hapo nyumbani ila muda huu hata hawakumuaga wala hawakumwambia kama wanatoka,
kwahiyo Moza alibaki akishangaa tu mwenendo wa watu kwenye nyumba ile ila
akajisemea kuwa atazoea tu. Muda si muda akarudi Sara na alionekana kuwa
amechoka sana, Moza alimkaribisha na kumpa pole “Pole na mizunguko dada
Sara” “Asante, yani ni mizunguko haswaa. Vipi mama
karudi?” “Ndio alirudi ila ameondoka tena” “Kheeee alirudi duh!
Aliniambia kuwa leo atachelewa sana kurudi kumbe alisharudi mmmh huyu mama nae.
Kwahiyo kaenda wapi sasa?” “Sijui ila kaondoka na Ana” “Yani
mama na Ana mmh! Ngoja nikaoge mie uniandalie chakula changu” Sara
aliondoka zake ila Moza alitamani amdadisi na Sara pia ili aujue undani wa
familia ile. Kwenye mida ya saa tatu usiku, wale mapacha nao
walirudi na cha kwanza kabisa waliulizia chakula ambapo Moza aliwaandalia, pacha
mmoja akaulizia kuhusu mama yao na Moza aliwapa taarifa kama aliyompa Sara,
kisha Yule pacha akamuuliza kuhusu baba yao, mwenzie akamkatisha “Sasa
unamuulizia wa nini huyo?” “Ni binadamu mwenzetu Kulwa, eti baba yuko
wapi?” “Kalala” “Kalala saa hizi?” “Hapana, ni tangu
asubuhi mama alipomwambia akalale hajaamka tena” “Duh” Yule
pacha akainuka pale mezani, Moza alitulia tu akiangalia picha inavyoendelea,
baada ya muda Yule Dotto akarudi na Mr.Patrick na kumkaribisha mezani pia,
ambapo Yule mzee alikula kama anakimbizwa, baada ya hapo Yule pacha akaongozana
na Yule baba na kumrudisha tena chumbani kisha yeye akarudi sebleni. Yule Kulwa
nae alikuwa ameshamaliza kula, akamwambia mwenzie “Mama akigundua hili
sijui utamwelezaje?” “Vyovyote vile, Yule ni mwanaume mwenzetu, najua
hata wewe hupendi kufanyiwa vile ila sababu unamuogopa mama” Wakaondoka
na kuelekea chumbani, Moza alitoa vyombo haraka haraka ili aende dirishani
akawasikilize pia, na kweli alipoenda dirishani aliwakuta bado wana mada za Yule
baba, “Nimekuuliza Kulwa, unapenda anavyofanyiwa Yule
baba?” “Sipendi, lakini sina cha kufanya” “Cha kufanya kipo ila
hatujakifikiria” “Kipi hicho?” “Nahisi tutakigundua pindi huyu
baba akifa” “Hivi unadhani mama atamuachia huyu baba afe? Anamtesa tu,
hajafikia hali ya ukatili kiasi hicho” “Ila kwa nini mama yetu yupo
hivi? Yani nawazaga hata sipati jibu” “Hata mimi mwenyewe sijui halafu
sasa yani mimi na wewe ni kwavile tu ni watoto wake ila mama hatupendi pia,
labda baba yetu alimfanya vibaya mama. Yeye kipenzi chake anaanza Ana halafu
anafatia Sara, yani mama sisi hatupendi kabisa” “Ila kuna kitu nahisi
kuhusu mama” “Kipi hicho?” Sauti ya Sara ikasikika akimuita
Moza, naye Moza aliamua kwenda kimya kimya kwani alijua akiitika tu atawashtua
wale mapacha. Alivyofika kwa Sara, “Inamaana mama bado
hajarudi?” “Hajarudi ndio” “Nilitaka nimpe
taarifa” “Taarifa gani?” “Leo nimekutana na Ashura, humjui wewe
yani Yule mdada mama anamtafutaga sana. Ngoja nikuonyeshe picha yake nimepiga
nae leo” Sara akatoa simu yake na kumuonyesha Moza picha ya Ashura, ila
Moza alishtuka kidogo sema alijigelesha ili Sara asigundue mshtuko
wake. Kisha Sara akamwambia Moza, ”Yani huyu Ashura alikuwa
mzuri sana, halafu hata hakufanania na kazi za ndani. Alikuwa mpole na mkimya.
Ni yeye tu aliweza kuishi kwa muda mrefu kwenye nyumba hii akifanya kazi za
ndani ila baada yeye kuondoka hakuna tena msichana aliyeweza kuishi kwa muda
mrefu hapa. Mmmh halafu sijui hata ni kwanini nakuambia yote haya, nenda
kaendelee na shughuli zako Moza” Moza alitoka pale na kwenda jikoni
kusafisha vyombo huku akifikiria kuhusu Ashura, “Mbona namjua Yule,
alikuwa akifanya kazi za ndani duh! Si nimefanya kazi kwao Yule! Hapa lazima
kuna kitu” Moza alimaliza shughuli zote, kwenye saa sita kasoro ndipo
Rose na mwanae Ana walirejea na kama kawaida Moza alipewa amri ya kwenda
kutandika kitanda cha Ana. Wakati anatandika kitanda cha Ana akasikia
kama sauti inamwambia afunue godoro, wakati anataka kufunua mara Ana akaingia
ndani na kumuuliza kwa ukali, “Unafanya nini?” Moza alipatwa na
bumbuwazi tu, alishikwa na kigugumizi asiweze kujibu, mara Ana akamsogelea na
kumzabua kofi. Wakati anatandika kitanda cha Ana
akasikia kama sauti inamwambia afunue godoro, wakati anataka kufunua mara Ana
akaingia ndani na kumuuliza kwa ukali, “Unafanya nini?” Moza
alipatwa na bumbuwazi tu, alishikwa na kigugumizi asiweze kujibu, mara Ana
akamsogelea na kumzabua kofi. Moza alivumilia kile kibao cha Ana, ambapo
Ana alimuuliza tena “Unatafuta nini huko?” Akili ya Moza
ikacheza pale pale maana alitambua kuwa Ana anapenda kunyenyekewa kwahiyo
alipiga magoti na kumuomba msamaha, ambapo Ana alimwambia atandike haraka haraka
na aondoke chumbani kwake, Moza alifanya hivyo na kutoka. Wakati Moza
anatoka chumbani kwa Ana ndio akamsikia Rose akimtoa mumewe huku
akimwambia, “Na leo kakae sebleni hadi kunakucha utulinde” Ndio
hapo Moza akaelewa kuwa kwanini jana yake alimkuta yule baba amejikalia sebleni
tu, Moza alisikitika ila hakuwa na la kufanya hapo. Alienda moja kwa moja kwenye
chumba chake huku akitafakari vitu vingi sana kwa wakati mmoja hadi alihisi
akili yake inagoma kufanya kazi. Alitafakari kuhusu Ashura, akatafakari
kuhusu wafanyakazi waliopita kwenye nyumba hiyo wako wapi, akatafakari kuhusu
baba mwenye nyumba kwanini anateseka vile, akatafakari kuhusu Ana na chini na
godoro la Ana kuna nini, mwisho wa siku alipitiwa na usingizi pale
pale. Akiwa amelala, akajiona kama yupo kijijini kwao na bibi yake
halafu bibi yake anamwambia, “Moza, upo kwenye ile nyumba kwa makusudi
kabisa. Unatakiwa kumuokoa Yule baba, unatakiwa kumuokoa mtoto wa Yule baba,
Unatakiwa kumfanya Yule mama aache kuyatenda anayoyatenda upo pale kwa makusudi.
Moza mjukuu wangu, nipo na wewe siku zote usijione upo mwenyewe.Twende
nikakuonyeshe sasa” Moza alishtuka na kuhema juu juu huku
akijisemea, “Jamani bibi yangu si ameshakufa? Sasa namuona ndotoni
kivipi? Mbona sielewi?” Usingizi wa Moza ulikata kabisa, ila alikuwa
kama anasikia sauti za watu nje, akaamua kuinuka na kwenda kuchungulia
dirishani, kwakweli alichungulia kwa tahadhari kubwa sana na kufanikiwa kuona
vivuli vya watu vikiwa vinaishia, Moza alishtuka sana na kujikuta akihemea juu
juu. Jambo hilo lilimfanya uoga umshike na usingizi akose
kabisa. Kulipokucha akafanya shughuli zake kama kawaida ikiwa
ni pamoja na kumuamsha Ana aende shuleni, leo Rose alionekana nyumbani kwake na
kuwafanya wanae waage tu kuondoka bila kutoa oda ya chakula wanachotaka
wapikiwe, hapo ndio moza akaelewa kuwa walifanya vile jana sababu walijua kuwa
mama yao hayupo. Ila leo ilikuwa siku ya tofauti kidogo kwani hadi mr.Patrick
aliruhusiwa kutoka, “Nenda tu kwenye shughuili zako, zunguka tani yako
leo. Utarudi nyumbani pindi tu nikikupigia simu kuwa urudi” “Je
usiponipigia nisirudi? Na je naweza kwenda kwa ndugu zangu?” “Ole wako
Patrick, usitake nibadili mawazo.Kwanza nenda ofisini kwetu, wamekumisi sana
maana ni kitambo sana hawajakuona” Mr.Patrick akaondoka zake na
hakupenda kuongea sana. Baada ya muda mfupi alikuja mgeni, mgeni huyu
alikuwa ni Ashura ila alijifanya kamavile hamfahamu Moza yani utadhani ni mara
yake ya kwanza kumuona, kitendo ambacho Moza kilimpa shauku kubwa ya kutaka
kujua kuna nini katikati. Rose na Ashura walikaa katika maongezi ila
Moza alienda kukaa sehemu ambayo angewasikiliza, maana maongezi yao walifanyia
sebule nyingine ambayo mara nyingi wale mapacha walifanya kama chumba chao cha
kusomea vitabu. Moza alikuwa makini kabisa kusikiliza maongezi ya Rose
na Ashura. “Sikia nikwambie Ashura, mi nilishakwambia sitaki Patrick
ajue ukweli kuhusu Yule mtoto Salome lakini kwanini ameanza
kuulizia?” “Anamuulizia hadi jina?” “Hapana, jina la mtoto
halijui” “Lakini mimi dada ukweli kabisa sijamwambia wala sijawahi kukaa
na shemeji Patrick kumueleza chochote kile kuhusu mtoto wake. Nadhani ni watu
waliomuona Salome kuwa kafanana sana na shemeji ndio wamemwambia” “Mmh
hivi kafanana nae sana eeh!” “Yani dada uongo dhambi kwakweli ila kadri
Yule mtoto anavyozidi kukua ndio shemeji mtupu” “Mmh tuachane na hayo
kwanza. Unajua wewe ndio unajua kila kitu kuhusu Yule mtoto. Wengine wote
hawajui Ashura, mimi nimekupeleka kwenye ile familia kwa makusudi ili siri
isitoke sitaki habari za Yule mtoto zisikike. Tena natamani ningekuwa na uwezo
ningekimaliza kabisa” “Mmh dada usifikie huko jamani” “Sasa
unadhani tutafanyaje? Nataka kuizima kabisa hii ishu maana hata ndugu wa Patrick
wakijua wataleta varangati. Unafikiri mchezo, hata kumfanya huyu Ana ahisi ni
mtoto wake” “Kwakweli cha kufanya sijui” “Halafu kwanini
nakutafuta sikupati mpaka ukutane na wakina Sara” “Hapana dada, unajua
wakina Sara walianza kuhisi kitu ndiomana nikajiweka mbali kabisa ili
wasifikirie chochote” “Achana na wale watoto bhana, unajua Ashura
nakutegemea sana. Huniangushagi wewe” “Ila dada kuna jambo nataka
nikwambie” “Jambo lipi” “Ni kuhusu huyu mdada wa kazi
uliyemuweka sasa hivi” “Eeh hebu nieleze” “Yani huyu aliwahi
kufanya kazi kwa Neema, kule ninakoishi mimi na watoto wa Neema akiwepo na
Salome anawajua vilivyo” “Mmmh inamaana anajua kila
kitu?” “Hamjui baba wa Salome ila nina mashaka nae sana, ngoja nimuone
kama ananikumbuka vizuri” Moza akasikia harufu kama mboga inaungua
ikabidi akimbilie jikoni, na kweli alikuta mboga inaungua, hapo sasa wakati
anahangaika iliafiche soo la kuunguza mboga akasikia Rose akiita kwa nguvu huku
akitembea, “Moza, weeee Moza wewe” Moza aliitikia na
kwenda, “Ulikuwa unafanya nini hadi umeunguza mboga” “Nisamehe
mama” Rose akacheka kisha akamwambia Moza, “Dawa yako
inachemka” Halafu akatoka na Ashura wakaondoka. Hapo Moza alikuwa na
maswali mengi sana, kuwa Ashura na Rose wako vipi vipi, na kwanini Ashura
alikuwa akiishi kule ambako Moza alikuwa akifanya kazi mwanzoni na mbona anaishi
nao kama ndugu kivipi? “Mmmh kumbe Yule Salome ndio mtoto wa mzee
Ptrick. Ila sasa naanza kupata picha, Yule Salome kweli amefanana na huyu mzee.
Masikini mzee Patrick jamani, masikini na dada Neema nae jamani anaishi na nyoka
ndani bila kujua dah” Kisha Moza akarudi tena jikoni, ni kweli alikuwa
ameunguza mboga sababu ya kufatilia umbea. Akaanza kufanya jitihada za kuiweka
sawa, akaibadilisha kwenye sufuria linguine, muda kidogo Rose alirudi na kumuita
sebleni, Moza alienda “Hivi nilikwambiaje kuhusu habari za humu
ndani?” “Nisizifatilie” “Haya, niambie sasa Ashura
unamjua?” Hili swali lilikuwa la mtego sana kwa Moza, akajikuta akiwa
kimya tu kwani hakujipanga na hakutegemea kuulizwa swali la namna ile, Rose
akamuuliza tena kwa kumshtua “nijibu basi, unamfahamu vipi
Ashura?” Moza akatetemeka na kujibu, “Simfahamu” Rose
akacheka kisha akamwambia “Vizuri sana. Humfahamu eeh!” “Ndio
simfahamu” “Na kipi kimekufanya uunguze mboga?” “Nisamehe
mama” “Hivi unadhani msamaha wangu ndio unatoka kirahisi rahisi
hivyo?” “Nisamehe mama” “Nadhani wewe hunijui vizuri, ila nataka
unijue ili safari ijayo ujiheshimu. Msamaha wangu utaupata leo saa nane
usiku” Moza akashtuka na kuuliza kwa hamaki, “Saa nane
usiku!” “Ndio saa nane usiku, mbona unashtuka? Huo si muda tu kama muda
mwingine. Mbona kuunguza mboga hukufikiria kuiambia mboga ikusamehe isiungue?
Leo saa nane usiku utaona msamaha wangu utakavyoupata. Haya kaendelee na kazi
zako, na unikaangie ndizi. Hiyo mboga ya kuungua iweke pembeni halafu saa nane
usiku nitakwambia inafanywa nini ila sitaki uwape wanangu mboga ya
kuungua” Moza aliondoka na kuendelea na shughuli zake huku akiulaumua
umbea wake kwani ndio uliomponza hadi akaunguza mboga, na ndio uliomponza hadi
anapewa msamaha saa nane usiku. Siku hiyo Ana nae aliwahi
kurudi ila alionekana kuwa amechoka sana kwani alivyofika tu sebleni akalala.
Ikabidi kama kawaida aende getini kuchukua begi la Ana kwa mlinzi. Alipoenda
kuchukua, mlinzi alimuuliza, “Na leo Ana anaonekana kuchoka sana,
ameenda wapi saa hizi?” “Amelala sebleni kwenye kochi” “Sikia
sasa, cha kukusaidia. Peleka begi lake, kisha urudi kumbeba na kumpeleka
chumbani kwake akalale.” Moza akamshukuru na akafanya vile, akambeba Ana
na kwenda kumlaza ambapo kitandani akaamua amvue viatu kisha amwache amelala
halafu yeye akatoka. Kufika sebleni wale mapacha nao walikuwa wamerudi
na walimwambia Moza awaandalie chakula ila muda huo huo mama yao nae alienda
pale sebleni, akamzuia Moza kuandaa chakula kisha akatoa pesa na kuwapa watoto
wake, “Nendeni mkanunue na mkale mnachotaka” Wale mapacha
walifurahi sana na kutoka zao, Moza alimuuliza Yule mama “Mbona umezuia
nisiwaandalie chakula?” “Moza, unataka nikutukane au? Hivi mboga yako
iliyoungua hiyo uwaandalie wanangu wakiumwa matumbo je!” Moza akawaza
kuwa tatizo ni mboga kuungua au kuna lingine. Sara nae aliporudi ikawa
vilevile, mama yake alimpa pesa akatafute chakula, kwakweli Moza aliwaza sana
siku ya leo kuwa tatizo bado ni kuunguza mboga au kuna linguine, muda huu
akaamua kumuuliza tena huyu mama, “Mama, tatizo ni kuunguza mboga au
kuna linguine?” “Lingine lipi?” “Sijui” “Lakini unataka
kujua?” “Ndio, ningependa kujua” “Wewe si mbea, utajua
tu” Huyu mama aliinuka na kwenda chumbani, kwakweli Moza aliogopa
ukizingatia ni kweli mboga iliungua sababu ya kufanya umbea. Moza alikuwa na
mawazo sana, kitu kilichomfanya atoke na aende kwa mlinzi ili kujaribu kumdadisi
kama kawaida yake, “Kaka samahani, naomba unisaidie” “Nini tena?
Umefanya vituko vingine ndani?” “Nimeunguza mboga bahati mbaya kaka, ila
mama kawapa watoto wake wote hela wakale nje sababu nimeunguza
mboga” “Sasa wewe umekuuma nini kuwapa watoto wake hela
wakale?” “Kumbuka nimepika ila amewapa watoto wake hela wakale, kwahiyo
kile chakula kitamwagwa?” “Unajua katika wafanyakazi vimeo bosi aliowahi
kuwaleta, basi wewe ni kimeo namba moja. Kwa kifupi, hii nyumba haiunguzwagi
mboga, yani kama umeunguza mboga leo ujipange” Moza alizidi kupatwa na
uoga, mara akaitwa na mama mwenye nyumba alikuwa mlangoni, Moza akaenda kisha
Yule mama akamuuliza “Na leo ulikuwa unaulizia
masoko?” “Hapana” “Ila ulikuwa unaulizia nini?” Moza
akawa kimya tu, na kumfanya Yule mama aongee tena “Wewe Moza wewe yani
nitakachokufanya leo hutakaa kusubiria umbea tena, akili itakukaa sawa.
Nitakukomesha” “Ila mama nimekuomba msamaha” “Unadhani huo
msamaha wako ndio umenunua mboga? Huo msamaha wako ndio hela? Nakwambia
nitakukomesha” “Mama nina ombi” “Eeeh ombi
gani?” “Naomba kurudi kwetu” Rose akacheka sana, na kumuangalia
Moza kisha akamwambia “Yani wewe hata mwezi huna kwenye nyumba hii
unataka kurudi kwenu, tena baada ya kufanya makosa. Hivi unafikiri kuondoka hapa
ni rahisi kiasi hicho? Mboga yangu uliyounguza una hela ya kunilipa? Nijibu
sasa” Kabla hajajibu alimsikia Ana akimuita kwa nguvu
sana, “Mozaaa” Rose alimuangalia Moza na kumsonya kisha
akamwambia “Nenda huko, malkia anakuita” Moza alienda huku
akitetemeka maana aliitwa kwa nguvu sana. Alipoingia chumbani kwa Ana
alizabuliwa kofi kwanza, kisha Ana akamwambia kwa ukali “Nani amekutuma
univue viatu” Kabla Moza hajajibu alishtukia akizabuliwa kofi lingine
lililompeleka hadi chini, yani la sasa hivi alipigwa na mtu mzima kabisa sio
kofi la kitoto kama la Ana. Moza alienda huku
akitetemeka maana aliitwa kwa nguvu sana. Alipoingia chumbani kwa Ana
alizabuliwa kofi kwanza, kisha Ana akamwambia kwa ukali “Nani amekutuma
univue viatu” Kabla Moza hajajibu alishtukia akizabuliwa kofi lingine
lililompeleka hadi chini, yani la sasa hivi alipigwa na mtu mzima kabisa sio
kofi la kitoto kama la Ana. Moza aliugulia pale chini na kusikia sauti
ya Rose sasa, “Unamvuaje mwanangu viatu bila ruhusa yake?” Rose
akamwongezea Moza teke, kisha akamwambia atoke mule chumbani. Moza
alitoka na kwenda bafuni ambako alijikuta akilia sana huku
akijiuliza, “Kwani kosa langu ni nini jamani? Hivi kumvua mtu viatu ni
vibaya?” Akaitwa tena na mama mwenye nyumba, kwahiyo Moza akajifuta
machozi yote na kwenda, “Unafanya nini?” “Sifanyi kitu
mama” “Unanificha eeh! Hujui kama nyumbani kwangu huruhusiwi kulia
bafuni?” “Nisamehe mama” “Yani wewe ni hodari sana wa kuomba
msamaha, sasa nataka ukae hapa sebleni hadi hiyo saa nane usiku ifike ikukutie
hapa hapa. Umenielewa?” “Ndio mama” Moza alikaa pale sebleni
huku akiwa na mawazo sana, kwakweli leo hakuwa na raha kabisa alijiona yupo
ufungwani. Muda kidogo, Rose na mwanae Ana wakatoka, Moza akaelewa tu kuwa nao
wanaenda kula. Alikaa pale sebleni amenyong’onyea kama kamwagiwa
maji. Kwenye mida ya saa tatu usiku wale mapacha walirudi na
walimkuta Moza pale sebleni, walimsalimia tena na kutaka kuelekea chumbani ila
mmoja akamuuliza moza “Mbona unaonekana umenyong’onyea
sana” Moza akajibu bila hata kufikiria mara mbili, “Nimeunguza
mboga kwa bahati mbaya” “Yani kuunguza mboga ndio unyong’onyee
hivyo!” “Mama kaniambia nikae hapa hadi atakaporudi kunipa
adhabu” Yule pacha mwingine akacheka na kusema, “Yani mama yetu
bhana, ana vijimambo vya ajabu ajabu. Sasa mtu kuunguza mboga ndio mpaka
adhabu!” Wakaondoka zao na kumuacha Moza pale sebleni, muda kidogo Sara
nae alirudi na alimuuliza Moza swali lile lile aliloulizwa na wale mapacha nae
akamjibu kama vile vile ila Sara alionyesha mshtuko kidogo, “Mungu
wangu, umeunguza mboga? Nyumba hii haiunguzwagi mboga” “Ni bahati mbaya
Sara” “Pole sana” “Asante” “Unatia huruma
sana” Sara akawa anaelekea chumbani ila akaonekana anakumbuka kitu,
kisha akamfata Moza na kumuuliza, “Kwahiyo mama ndio kakwambia ukae hapo
sebleni hadi atakaporudi?” “Ndio kaniambia hivyo” “Kakwambia
adhabu yako anakupa saa ngapi?’ “Kasema saa nane usiku” “Pole
sana, nina uhakika mama na Ana watarudi hiyo saa nane muda wa adhabu ila kwa
kukuokoa wewe na hiyo adhabu nenda chumbani kwako muda huu kalale yani hiyo saa
nane ikukute umelala” “Mmmh mama si atasema nimekiuka amri
zake?” “Moza, nimekusaidi tu ila usinitaje. Wewe nenda kalale,
akikuuliza mwambie usingizi ulikushika kwa uoga. Mwambie kuwa wewe ukiogopa kitu
unapatwa na usingizi” Moza aliamua kumsikiliza Sara na kwenda chumbani
kwake kulala ingawa ilimchukua muda sana kupatwa na
usingizi. Moza alikuwa amelala lakini usingizi wake ulikuwa
umejawa uoga wa hali ya juu huku akihisi kwamba hiyo saa nane atakuja kuamshwa
na kufanyiwa hiyo adhabu ila alishangaa hiyo saa nane ilionekana kupita kwani
alisikia kwa mbali majogoo yakiwika na kuhisi kuwa huenda ikiwa saa tisa na nusu
au saa kumi alfajiri. Usingizi ukampitia sasa, akajiona kwenye ndoto
yupo kwenye kile chumba na wale wadada watano wakimshukuru sana kwa kuunguza
mboga, mmoja akamwambia Moza “Ila wewe una bahati sana, kwani wenzako
unafikiri makosa yetu nini kuwa huku. Ni kuunguza mboga tu” “Kuunguza
mboga!” “Ndio, tuliunguza mboga tukaletwa huku. Ila wewe una bahati
sana. Yani unafanya makosa makubwa zaidi yetu ila bado upo. Sikia Moza kile
chumba unacholalia kuna kitabu change kidogo sana, kapekue utakiona. Kina habari
za bibi yangu atakupa mbinu za kutusaidia” “Mbona huku unaongeaga wewe
peke yako?” “Wenzangu wote vinywa vyao vimefungwa, hwawawezi kuongea
chochote. Kuhusu mimi ukisoma kile kidaftari change utaelewa. Kipo kwenye droo,
kuna taiti nyeusi katikati kuna kitabu changu” “Ila bado sijaelewa, yani
kuunguza mboga ni furaha yenu ili mimi niletwe humu?” “Furaha yetu
ukiunguza mboga tunakuwa huru sana, ila siku ukifikia kuunguza na kuwa kama
mkaa……” Moza akashtuliwa na kelele za kuitwa, ambapo akashtuka kutoka
kwenye ile ndoto, aliyekuwa anamuita ni Sara ambaye aliingia ndani na kumgusa
Moza, kisha akamwambia “Kheee bado umelala tu! Amka bhana utuandalie
chai unajua muda umeenda sana” Kisha Sara akatoka mule chumbani, Moza
alikurupuka na kufungua dirisha ambapo aliona jua kali limeshawaka yani
pameshakucha kabisa, alipotazama saa ilikuwa ni saa mbili
asubuhi, “Mungu wangu, yani nimelala hadi saa hizi! Sijamuamsha Ana
aende shule, sijafanya usafi bado. Mungu wangu” Alijitoa matongotongo
kwa kidole kisha akatoka nje, ila sebule ilikuwa kimya sana ambapo alikuwepo
Sara tu akichezea simu yake, “Nisamehe madam Sara, nilipitiwa na
usingizi” “Nimekuelewa, niandalie chai tu halafu nikaangie na
mayai” “Wengine wameenda wapi?” “Wote
wameshaondoka” “Ana nae?” “Hebu acha kunichekesha na wewe, Ana
awepo anafanya nini muda huu? Kashaenda shule” Moza akaenda jikoni na
kuanza kumtaarishia Sara kifungua kinywa ila kichwa chake hakikuwa sawa kabisa,
alijikuta akijiuliza maswali mengi sana bila ya
majibu. Alipomaliza alimuandalia Sara mezani na kumkaribisha,
ila aliona karatasi mezani na hela, akalifunua lile kafratasi limeandikwa
‘KANUNUE SAMAKI’ Sara aliposogea pale mezani akamuuliza, “Eti huu ujumbe
kaacha mama” “Itakuwa ni yeye tu” Moza akamuacha Sara pale
anakunywa chai kisha yeye akaenda kujiandaa ili akanunue hao
samaki. Alikuwa akijiandaa huku akijiuliza maswali mengi sana ila bado
hakupata majibu ya maswali yake yote, hakuna jibu alilolipata. Akawa amezubaa
tu, ila akasikia sauti ya Sara ikimuaga “Tafadhali Sara naomba unisubiri
ili unionyeshe tu mabucha ya samaki” “Fanya upesi, nina haraka
zangu” Moza akafanya haraka akatoka na Sara, ila walipokuwa njiani Moza
alimuuliza Sara “Kwani wewe unafanya kazi au unasoma?” “Kwanini
umeniuliza hivyo?” “Kila siku unatoka” “Mimi nafanya kazi ila
nasimamia miradi ya mama” “Na wale mapacha je!” “Nao wanasimamia
miradi ya mama sehemu nyingine, na leo wametoka na mama” “Na baba
je!” “Sasa nimeelewa kwanini mama anataka kukuadhibu
wewe” “Kwanini?” “Hivi hujioni kuwa ni mbea sana, yani
unajifanya kama FBI.” “FBI ndio nini?” “Sitaki maswali bhana,
mabucha ya samaki yale pale. Kwaheri” Sara aliondoka na kumuacha Moza
akielekea kwenye yale mabucha, ila moza tabia ya kuuliza maswali alikuwa nayo
kwenye damu yani hata akijifanya siulizi tena anajikuta tu
ameshauliza. Moza alienda kwenye bucha la samaki kununua
samaki, wakati anaondoka akashikwa bega kutazama alikuwa ni Salome ambapo
alimkumbatia kwa upendo, “Kheee Salome umekuwa, umekuwa
sana” “Ndio dada, shikamoo” “Marahaba, upo darasa la ngapi
saivi?” “Nipo kidato cha tatu” “Kheee hongera sana. Mama
hajambo!” “Hajambo” “Nimewakumbuka sana, na wale wadogo zako
mapacha” “Nao hawajambo” “Twende ukapafahamu ninapofanyakazi
siku hizi” “Mmh dada, nitachelewa. Unajua tumehama pale tulipokuwa
tunakaa” “Hakuna shida, huchelewi wewe twende ukapaone
basi” Moza akaongozana na Salome hadi kwenye ile nyumba aliyokuwa
anafanya kazi, na kumkaribisha Salome ndani. Kwakweli mlinzi alishikwa na
bumbuwazi alipomuona Salome ila hakuweza kuuliza zaidi. Waliingia ndani,
kwakweli Salome alishangaa ukubwa wa nyumba ile, “Kumbe ndiomana
ulitukimbia dada, kumbe matajiri walishakuiba” “Hapana sio hivyo mdogo
wangu, kipindi kile nilirudi kweli kijijini kwetu. Bibi yangu alikuwa anaumwa
sana na nimemuuguza kipindi chote hiki ila mwisho wa siku alikufa. Nilikaa
kijijini nikaona sina ishu nikarudi mjini, nilikuja pale mlipokuwa mnakaa
nikaambiwa mmehama ila ndio nikapata kazi hii, yani hata sina siku nyingi
hapa” “Pole dada” “Asante, ila umlete na mama yako hapa aje
kuniona na apafahamu” Salome akamuaga Moza, na wakati anamsindikiza
Mr.patrick nae akawa anaingia akawakuta ndio wanatoka wakamsalimia pale na
kuondoka ila moyo wa Mr.Patrick ulihisi kitu, alijikuta akitamani sana kujua
kuhusu huyo mtoto kwahiyo alikuwa anangoja Moza aingie ndani
amuulize. Mlinzi nae, Moza alivyoagana tu na Salome kisha
kurudi ndani akamuuliza, “Yule mtoto ni nani?” “Anaitwa salome
Yule” “Mbona kafanana sana na mzee Patrick!” “Si ulisema wewe ni
mtoto wa kiume, umbea hupendi. Kwaheri” Moza alienda ndani na kumuacha
mlinzi ameduwaa tu, ila alipoingia sebleni tu alibambana na swali kutoka kwa
mzee Patrick, “Yule mtoto ni nani?” “Anaitwa Salome
Yule” “Ni mtoto wa nani na anaishi wapi?” “Nilikuwa nafanya kazi
kwao kabla ya hapa” “Mbona swali na jibu haviendani? Nimekuuliza ni
mtoto wa nani na anaishi wapi?” Mara mlango ulifunguliwa na aliingia
Rose, ambaye alionekana kumungalia kwa hasira sana mume wake, kisha akamuuliza
bila hata ya salamu “Kwanini jana hujarudi?” “Sasa ningerudi
vipi mke wangu na umeniambia mpaka unipigie simu” “Sasa leo nimekupigia
simu?” “Nimehisi labda umejisahau mke wangu ndiomana leo nimeamua
kurudi. Jana mbu wamening’ata sana usiku pale ofisini” Rose akacheka
sana, kisha akamuangalia Moza na kukunja sura, halafu akamwambia “Na
wewe unasikiliza nini? Yanakuhusu haya? Hivi kwanini wewe ni mbea mbea, hebu
kwenda kwenye kazi zako huko” Moza aliondoka pale sebleni na kuelekea
jikoni, ila ingawa alikuwa jikoni ila masikio yote yalikuwa sbleni akisikiliza
tu kinachozungumzw na Rose pamoja na Patrick. Aliwasikia vilivyo
mazungumzo yao kwani hayakuwa ya kunong’ona yani yalikuwa ya sauti
kabisa, “Sikia nikwambie Patrick, humu ndani kuna kidudumtu naa hicho
kidududumtu lazima nikikomeshe” “Ni nani huyo?” “Si huyu
mfanyakazi, yani ni mbea sijapata kuona. Ndio amefanya nisahau kukupigia simu
jana, ni mbea ameshindikana, unaelewa maana ya umbea mume wangu. Huyu msichana
ni mbea na lazima nimkomeshe” “Sasa unataka kumfanya
nini?” “Utaona leo usiku yani akilala tu ninae” “Mmmh mke wangu
yani akilala ndio unamkomesha? Kwanini usimsamehe?” “Nimsamehe!
Thubutuuu, jana kaunguza mboga yangu sababu ya umbea wake. Yani leo akilala tu
namkomesha” “Sasa mbona unaongea kwa sauti, huoni kama
anakusikia?” “Hanisikii bhana, na leo nitamkomesha” “Halafu kama
maajabu hivi, kwanini unanieleza yote hayo leo?” “Sababu nakupenda mume
wangu, kila kitu ninachotaka kufanya lazima
nikueleze” “Mmmh!” “Usigune mume wangu, yani huyu msichana leo
akilala tu ninae. Anadhani nimesahau, twende chumbani mume wangu nikakukande
kande kwa uchovu” “Kila siku ingekuwa hivi sijui
ningenenepaje” “Unene mimi siupendi, twende bhana achana na mawazo
hasi” Rose na mume wake walielekea chumbani huku Moza akiwa amejawa na
uoga na kujilaumu kuyasikiliza yale mazungumzo, yani anawaza kuwa bora
asingesikia chochote. “Mmmh mimi Moza leo silali yani silali
kabisa” Alikuwa na uoga wa hali ya juu. Ana alirudi, na
leo ni tofauti na siku zingine kwani begi lake alilibeba mwenyewe na kwenda
kuliweka chumbani kwake, hakumuongelesha Moza kabisa. Ila muda kidogo alienda
chumbani kwa mama yake, ambapo Moza kama kawaida akanyata ili akasikilize kitu
ambacho Ana aliongea na dada yake. “Yani mama, huyu dada nikimuona
nahisi kichefuchefu balaa kwa kitendo chake cha jana” “Hata usijali
mwanangu yani huyu akilala tu leo ninae, nimepanga kumkomesha” “Mmh mama
akilala? Sio akiwa macho?” “Akilala mwanangu, yani leo akilala tu ninae.
Nitamkomesha leo” Kimya kikatawala na kumfanya Moza arudi jikoni huku
amenyong’onyea maana leo aliona amepangiwa mapango kabambe. Huku
akijisemea “Ila umbea wangu umesaidia maana mipango yote aliyonipangia
huyu mama nimeijua” Kulwa, Dotto na Sara walirudi kwa kuongozana, mama
yao alitoka sebleni na kumtaka Moza aandae chakula. Moza aliandaa kisha
Yule mama aliita watoto wake wote na mume wake, yani leo familia nzima ilikuwa
mezani wakila kasoro Moza aliambiwa akale jikoni. Wakati wanakula pacha
mmoja akamwambia mama yake, “Mama ingekuwa hivi kila siku basi familia
yetu ingekuwa ni kati ya familia znye furaha sana” “Hata hivyo
tunafuraha, kwani hakuna mwenye furaha hapa? Mimi nafurahi sana kuwaona watoto
wangu na mume wangu tukiwa pamoja tunakula” Sara akadakia na
kusema, “Ila mama mmh leo sio bure, haijawahi kutokea kama hivi
kwakweli. Sio bure kabisa mama” “Sasa sio bure ndio
nini?” “Nahisi kuna kitu unataka kufanya” “Cha kufanya kipo
ndio, kuna mjinga mmoja lazima nimkomeshe leo” “Nani huyo
mama?” “Nyie kuleni tu wanangu, hata hamuhusiki” Moza bado tumbo
joto hata hamu ya chakula hakuwa nayo kwani alijua hata akisinzia siku hiyo basi
lazima atakomeshwa na huyu mama, na kinachomuumiza kichwa zaidi ni kuwa hajui
atakomeshwaje komeshwaje. Moza akachemsha maji na kutia kahawa sababu
alishawahi kusikia kuwa maji ya kahawa yanakata usingizi, alikunywa vikombe
vinne ila bado alikuwa akihofia kuwa akisinzia itakuwaje. Muda
wa kulala ulipofika, kila mtu alienda chumbani kwake hata Moza pia alienda
chumbani kwake ila alikuwa na mawazo sana na alikuwa akiwaza ni jinsi gani
anaweza kukaa macho kwa usiku wote hadi asubuhi, Ilipofika saa sita usiku
akapata wazo la kwenda kukaa sebleni maana aliamini kama angekaa sebleni basi
asingepata usingizi na mfano ungemnyemelea basi angeenda kunywa kahawa
tena. Wakati anataka kutoka akasikia sauti, “Moza
lala” Akashtuka sana na kugeuka ili aone sauti inatokea wapi, ila
hakumuona mtu yoyote akataka akafungue malango tena, kasikia “Moza
lala” Safari hii ile sauti ilimwambia kwa ukali
kidogo. Wakati anataka kutoka akasikia
sauti, “Moza lala” Akashtuka sana na kugeuka ili aone sauti
inatokea wapi, ila hakumuona mtu yoyote akataka akafungue malango tena,
kasikia “Moza lala” Safari hii ile sauti ilimwambia kwa ukali
kidogo. Moza alizidi kupatwa na uoga hadi akawaza kutoroka kwenye ile nyumba ila
atatorokaje usiku huo na kuna mlinzi getini, yani akawa na mawazo mbali mbali
mpaka akajihisi kuchanganyikiwa. Ila bado alikuwa na wazo la kwenda sebleni
kukaa lakini sauti ile ilizidi kumwambia moza alale, alipoona ile sauti inazidi
maana ilianza kuongea kama mwangwi, “Moza lala, Moza lala, Moza
lala” Uoga ulimjaa Moza hadi akataka kutoka kwa nguvu ila alipofungua
mlango ulikuwa mgumu na ile sauti ilizidi kumsihi alale, Moza alitetemeka zaidi
akataka kupiga kelele ili afunguliwe mlango ila moyo mwingine ukamwambia ukipiga
kelele ndio utamshtua mwenye nyumba kuja kukuadhibu, akaamua kwenda kukaa
kitandani huku akiombea asilale ila sauti ya kumsihi kulala ilizidi na kumtia
hofu zaidi. Alipotaka kuinuka tena muda huu alishtukia akipigwa kibao
kilichomuangusha hadi chini halafu taa ya chumbani ilizimwa yani hapo ndio uoga
zaidi ukamshika na kujikuta akishindwa kuinuka pale chini ila cha kumshangaza
wakati anaogopa sana, usingizi ukampata pale pale. Wakati
amelala akajiona yupo mahali chini ya mti halafu kaja Yule dada anayeongeaga
kati ya wale wadada watano, akaanza kuongea nae ila leo Moza hakuweza kujibu
wala kuuliza swali. “Moza, ni mbishi sana wewe ndiomana nimekufanyia
hivi. Yani hujui kutofautisha kati ya mtego na kitu cha kweli. Yule mama
angetaka ulale ili akufanyie mambo mabaya unafikiri angeongea kwa sauti kubwa
vile? Kaongea kwa sauti kubwa sababu amejua wewe ni mbea na utasikiliza tu
kwahiyo alikuwekea mtego, na usingelala ndio angejua kama ni mbea kweli maana
kwanini unasikiliza maongezi yao? Halafu kwa sheria za huyu mama amfanyiagi kitu
mbaya mtu akiwa amelala, ndiomana hata jana hakukufanya lolote sababu ulilala
ila ungekuwa macho ungepatwa na makubwa. Usifikirie siku zote nitaweza
kukusaidia, nimeweza leo sababu ile juzi uliunguza mboga kwahiyo nimepata nguvu.
Jifunze kuelewa mitego Moza, tutakupoteza na wewe. Usifikirie ni rahisi hivyo
kutoroka kwenye hii nyumba. Kitabu nilichokwambia kipekue kesho uanze kukisoma
ndio kitakusaidia sana kwenye mambo yote ya kufanya. Halafu unatakiwa kuwa
makini sana kwenye kila kitu unachofanya, yani fikiria kabla ya kutenda jambo
lolote. Kwasasa lala tu” Huyu mdada aliondoka, ila ni usingizi mzito
sana ulimshika Moza wakati huo. Kuja kushtuka ilikuwa ni kumeshakucha,
akaamka pale chini na kujishangaa shangaa kuwa imekuwaje mpaka akalala hapo
chini, akaanza kukumbuka matukio na kukumbuka kuwa mara ya mwisho alinaswa kibao
na kuanguka hapo chini kisha kukawa na giza kubwa lililompa uoga na kupitiwa na
usingizi kwa uoga, pia akakumbuka alivyoota. Akainuka pale chini haraka haraka
baada ya kukumbuka kuwa alitakiwa kuadhibiwa, akatoka sebleni ila nyumba ilikuwa
kimya kabisa yani ilionyesha hapakuwa na mtu yeyote mule ndani. Akasogea
mezani ambapo alikuta ujumbe, ‘UPIKE WALI, MAHARAGE NA SAMAKI’ akaelewa kuwa
ujumbe huo umeachwa na mama mwenye nyumba, hivyo akahisi kuwa huenda nyumba
nzima wameondoka na hivyo kwenda kuoga na kuanza kufanya kazi za hapa na pale
mule ndani hadi alipoanza kupika kile chakula alichoagizwa. Alipomaliza
kupika alikiandaa kabisa mezani ila alikuta ujumbe mwingine ‘TENGENEZA NA JUISI
YA MATUNDA YAPO KWENYE FRIJI’ akaangalia kulia na kushoto, mbele na nyuma na
kujiuliza, “Mbona ujumbe huu sikuukuta mwanzoni? Humu ndani si nimebaki
mwenyewe? Au sikuangalia vizuri!” Akajiuliza bila ya jibu kama kawaida
kisha akaanza kuiandaa hiyo juisi na kuiweka kwenye friji, ila aliporudi mezani
alikuta ujumbe mwingine ‘CHEMSHA MAJI YA KUOGA YA ANA UMUWEKEE KWENYE CHUPA’
hapo uoga ukamshika na kuanza kuhisi tofauti, kisha akajiuliza, “Mbona
huyo Ana hajawahi kusema nimchemshie maji ya kuoga? Huu ujumbe ananiwekea nani?
Siwezi kwakweli, naogopa. Inamaana sikuuona pia?” Alikuwa na mashaka
sana ila akaenda kuchemsha hayo maji na kuyaweka kwenye chupa, alipomaliza
alirudi tena mezani na kukuta ujumbe mwingine ‘DEKI TENA
NYUMBA’ Aliogopa sana sasa hivi na kuamua kukimbilia nje hadi kwa mlinzi
huku akihema juu juu, Yule mlinzi alimuuliza, “Humo ndani
sielewi” “Huelewi nini?” “Nimebaki peke yangu ila nakutana na
ujumbe mezani, kila nikifanya nakuta ujumbe mwingine. Naogopa
kwakweli” Yule mlinzi alianza kucheka sana kisha
akamuuliza, “Kwahiyo wewe unahisi ni nini?” “Nahisi labda ni
jinni” “Usinichekeshe wewe, hivi jini unalijua wewe? Ushawahi kuona
jini?” “Sijawahi” “Sasa unaogopa nini?” “Naona mambo ya
ajabu, ukizingatia ndani nipo mwenyewe” “Upo mwenyewe wapi wewe, fanya
tu ujinga wako uone. Mama yupo ndani leo hajatoka” Moza akapumua kidogo
na kujiona kama mjinga, kwani alihisi mitego ya Yule mama iliendelea kwahiyo
ikabidi ajipange na majibu kama mwenye nyumba akimuuliza. Moza
alirudi ndani sasa na kuanza kudeki, na alipomaliza Rose alitoka ndani na kwenda
sebleni ila Moza hakuonyesha kushtushwa sababu ameshaambiwa na mlinzi kuwa Rose
yupo ndani, huyu mama alimuangalia Moza na kumuuliza “Mbona
hujashtuka?” “Nishtuke nini sasa mama?” “Ushtuke
kuniona” “Sijashtuka sababu nilijua tu kuwa upo
ndani” “Umejuaje” “Nilipoona ujumbe mara ya kwanza, na nilipoona
mara ya pili nikajua tu kuwa upo ndani” Rose akacheka kisha akamwambia
Moza, “Unajifanya mjanja eeh wakati ushafanya umbea kwanza, nilitaka leo
kukufundisha kazi za kufanya maana ni uhakika hujui kazi za kufanya ndiomana
unapata na muda wa kufanya umbea. Laiti kama ungekuwa na kazi za kufanya basi
umbea usingefanya. Haya nenda kamwagilizie maua maji, na nikitoka nikute
yamelowana haswaaa” Moza alitoka nje na kwenda kufunga mpira na kuanza
kumwagilia maua, wakati anamwagilia kuna sauti ikamtuma kupekua ua moja wapo,
akahisi kama kuchimba mzizi wa lile ua. Ikabidi amwagilie kwanza ili pakilowana
achimbe mzizi huo aone ni nini na kwanini hisia zake zinamtuma afanye
hivyo. Palivyolowana, akaitwa na Rose kwani Ana alikuwa tayari
amesharudi. Moza alivyofika pale, akashangaa kumuona Ana akiwa amebeba mwenyewe
begi lake halafu Yule mama alimwambia kwa ukali, “Hivi Moza huoni mtoto
anahangaika na begi, si umpokee” Moza akataka kumpokea lile begi Ana,
ila Ana akawa mkali sana na kumkatalia kisha akamwambia mama yake “Hili
lidada limbea sana, lisije likafungua begi langu bure. Siwezi kumruhusu tena
abebe begi langu” Ana akaondoka zake, Rose akamuangalia Moza na kumfokea
pale, “Unaona sasa faida ya umbea wako, hadi mwanangu hakutaki yani wewe
sijui kama mwezi huu utamaliza humu ndani. Umbea wako utakuwa umekuponza, haya
kaendelee na umwagiliaji huko, sasa ole wako nisikie unafanya umbea hadi kwenye
maua yangu” Moza akataka kutoka, wale mapacha nao walirudi na walikuwa
wakilalamika njaa sana, “Ila chakula nimeshaandaa mezani” “Hivi
wewe Moza si nishakwambia kaendelee na umwagiliaji, mtu gani wewe hujielewi.
Kwani hawa wakilalamika njaa ni wanakulalamikia wewe? Wewe ndio unaetafuta
chakula humu ndani au? Hebu nenda zako huko” Moza akondoka kwa aibu
maana hakutegemea kama muda huu huyu mama angesema
hivi. Alienda tena kwenye ile bustani ya maua na kuendelea
kumwagilia,ila bado mawazo yake yalimtuma kwenye lile ua ili afukue mzizi ajue
kuna nini ila akakumbuka ile sauti ya mwenye nyumba kuwa ole wako nisikie
unafanya umbea kwenye maua yangu,ile kauli ikawa inamrudia ila
akajisemea. “Kwani mimi natafuta umbea au nataka kuangalia mizizi ya
lile ua? Kwani kuangalia mizizi ni umbea nao? Hapana bhana si umbea, nataka tu
kuridhisha roho yangu maana inanituma niangalie mizizi ya ua lile, mbona
haujanionyesha ua lingine zaidi ya lile! Huu si umbea bhana” Yani
alikuwa anajihoji mwenyewe na kujijibu mwenyewe basi aliacha kumwagilia na
kwenda kufukua, alipokuwa anafukua hakuona mizizi kama alivyodhani ila
alichokiona alistaajabu sana kwani alikuta mfuko na kitu kimefungwa kama mpira
akataka kukifungua ila akajua akifungua hapo atabambwa kwahiyo akakificha kwenye
nguo zake ili akakifungue ndani akiingia chumbani kwake kulala. Tangu
amkificha kile kimfuko nguvu ya kumwagilia ilimuisha kabisa na akajisikia hamu
ya kuangalia kuna nini ila akajikaza kuwa ataenda kuangalia ndani. Roho yake
ikamtuma kuwa akipeleke chumbani kwake kabisa, basi akaacha tena kumwagilia na
kuanza kutembea ili apelike ule mfuko ndani ila kadri alivyokuwa anatembea nguvu
zilikuwa zinamuisha, yani mpaka anaingia chumbani kwake alianguka kabisa ndipo
alipotoa ule mfuko haraka haraka, ila alipoutoa tu na kuutupia pembeni nguvu
zake zilirejea tena na kumfanya awe na mashaka zaidi kuhusu ule
mfuko, “Kilichomo humu kwenye mfuko si kimpira kama ninavyodhani ila
nadhani kuna kitu kingine haiwezekani nguvu ziniishe kiasi hiki, lazima
niangalie kuwa ni nini” Ila muda huo akaitwa na Sara na kumfanya ainuke
na kwenda alipo Sara ambapo alienda moja kwa moja chumbani kwa Sara, alifikiwa
na swali, “Jana ulikuja na nani hapa
nyumbani?” “Jana?” “Ndio jana, usijipumbaze” “Aaah
nilikuja na mtoto mmoja hivi anaitwa Salome” “Ni nani huyo
mtoto?” “Kwani wewe kakwambia nani kama nilikuja nae?” “Moza,
unafikiri umbea unauweza peke yako tu? Usitake kujua kaniambia nani, ila nijibu
huyo mtoto ni nani na anamahusiano gani na familia yetu?” “Ila kwanini
umeniuliza hivyo Sara?” “Moza, usiniulize maswali ila nijibu
nilichokuuliza” “Kwakweli sijui nikujibu vipi hilo swali lako, ila Yule
mtoto ni wa bosi wangu wa zamani yani mwanzoni nilikuwa nafanya kazi kwao.
Nimekutana nae buchani sasa nikamlete ili apafahamu ninapoishi
kwasasa” “Mama anajua kama uliwahi kufanya kazi kwa mama wa huyo
mtoto?” “Hajui, kwani kuna uhusiano gani kati yenu na huyo
mtoto?” “Sitaki maswali Moza, ila hili swala lazima mama nimfikishie
maana umemleta mtu bila ruhusa ya mama. Vipi baba alimuona?” “Alimuona
ndio wakati namsindikiza” “Yani wewe Moza wewe unatafuta mabalaa ambayo
huwezi kuyatatua. Sikia nikwambie ujue kama ulikuwa hujui, Yule mtoto aliwahi
kusingiziwa baba kuwa mtoto wake yani ilitokea mtafaruku mkubwa sana hapa
nyumbani. Kipindi hicho hadi mama akaanza kutafuta mtoto kwa haja zote ndio
baada ya miaka kadhaa akampata Ana. Sasa mama ana hasira sana na familia ya Yule
mtoto halafu wewe unaenda kumchukua na kumleta nyumbani” “Lakini mimi
nilikuwa siyajui yote hayo, na kama ndio hivyo mbona Salome hakuonyesha kama
anapafahamu hapa?” “Sikia Moza, kwanza Yule haitwi Salome nadhani hilo
jina wamempa ukubwani. Alikuwa anaitwa Maria, mamake anapajua hapa vilivyo na
hawezi kusogelea hapa. Yule mtoto hapajui hapa, usijaribu tena kumleta Yule
mtoto kwenye nyumba hii” “Lakini ningependa unieleweshe zaidi, mbona
kafanana sana na baba” “Moza Moza, naenda kukusemea kwa mama maana naona
unazidi kuchokonoa mambo” “Tafadhali, naomba
unisamehe” “Unamuogopa eeh” “Ndio namuogopa” “haya,
kaendelee na shughuli zako” Moza alitoka mule chumbani kwa Sara na
kwenda jikoni kuosha vyombo ambavyo tayari walikuwa wamelia chakula, hapo
akawaza tena kuhusu Salome kuwa Yule baba inasemekana kasingiziwa lakini
inaonyesha wazi Salome ni mtoto wa Patrick, ila kwanini Patrick mwenyewe
anauwalakini kuhusu mtoto wake huyo na kwanini Salome alibadilishwa jina kama ni
kweli alibadilishwa jina, alitamani kujua kwa undani zaidi ambapo alijua wa
kumjibu mwingine ni mama yake Salome ambaye ni Neema. Alitamani apate
muda wa kwenda kuzungumza na Neema ili ajue kwa undani zaidi, “Lakini
umbea huu loh hata kuacha sitamani, najikuta tu natamani kujua sijui nifanyeje
masikini Moza mimi” Kumbe maneno hayo aliongea kwa sauti ya kusikika,
akasikia sauti ikimwambia, ilikuwa ni sauti ya Rose, “Haya ni nini
unachotamani kujua?” Moza akashtuka na kumjibu kwa uoga
uoga, “Hakuna kitu mama” “Usinichekeshe Moza, wakati nimekusikia
kila kitu. Niambie unachotamani kukijua ili nikusaidie ukijue” “Hakuna
kitu mama” “Hakuna kitu eeeh!” “Ndio mama hakuna
kitu” “Mimi nakiona kipo” Rose alimshika mkono Moza na kuanza
kumkokota, kwakweli Moza alishikwa na uoga kwani moja kwa moja Rose alimpeleka
Moza kwenye kile chumba chenye chumba kidogo ndani kisha
akamwambia, “Unataka kujua kilichopo mule eeeh!” Moza alikuwa
kimya tu, “Najua unajiuliza kuwa ukubali au ukatae, huku moyo wako
mwingine ukitamani kujua siri iliyomo kwenye chumba kile. Haya chukua funguo
hapo juu” Rose alimwambia Moza kwa kumkaripia ambapo Moza alichukua
funguo huku akitetemeka, “Haya fungua sasa” Moza alianza
kufungua huku akitetemeka kwani alihisi kama hapelekwi nay eye kwenye chumba
hiko basi ataona vitu vya ajabu, ila leo tofauti na siku ile aliyotaka
kuchungulia kwani alipigwa na shoti ila leo hakupigwa na cheche yoyote. Na
alipofungua tu alijiona yupo nje, “Umeona sasa, huu ni mlango wa kutoka
nje. Sasa wewe ulikuwa unafikiria ni nini?” “Hapana mama, sijafikiria
chochote” “Haya tuzunguke tukaingie ndani” Wakazunguka na
kuingia ndani tena, kisha Rose akamuuliza moza, “Sasa una amani
eeh” Moza aliitikia kwa kichwa tu kuwa ameridhika, Rose alicheka na
kumuacha moza anaenda jikoni ambapo alienda kumalizia vile vyombo vyake ila
alikuwa na mawazo mengi sana. Moza aliingia chumbani kwake ila
bado alikuwa na maswali mengi sana, kwanza kabisa alijiuliza kuhusu chumba
alichopelekwa ambacho mlango wa ndani ulimtoa nje, “Mmmh huyu mama
hajanifanyia mtego kweli, mbona kama chumba sio kile? Nahisi kanifanyia mchezo
Yule mama lakini kwanini anifanyie mchezo wakati mimi si chochote wala lolote
kwenye hii familia” Wazo lingine likamjia ni kuhusu Ana maana siku hizi
Ana hakutaka kitu chochote afanyiwe na Moza jambo ambalo lilimchanganya pia.
Wakati anawaza hayo, mlango wake uligongwa alipoenda kufungua alimkuta mama
mwenye nyumba ambaye alimwambia “Dawa yako inachemka” Huyu mama
akaondoka, Moza akatoka na kwenda jikoni huku akiangalia hiyo dawa aliyoambiwa
inachemka iko wapi maana hakubandika dawa yoyote kwahiyo ule usemi wa dawa yako
inachemka kwa muda huo hakuelewa alijua ni dawa kweli. Moza alivyoona
hakuna dawa inayochemka alirudi tena chumbani,muda huu akili ikamtuma achunguze
ule mfuko alioutoa kwenye maua. Akuchukua ule mfuko na kuanza kuuchunguza kwa
kuufunua ambapo kweli alikuta kama mpira wa makaratasi umefungwa fungwa. Moza
akaanza kufungua ila kadri alivyofungua ndivyo nguvu zilivyomuisha, hadi
mwishoni akaanguka kabisa na kuwa kimya hapo
hapo. Moza alivyoona hakuna dawa inayochemka alirudi
tena chumbani,muda huu akili ikamtuma achunguze ule mfuko alioutoa kwenye maua.
Akachukua ule mfuko na kuanza kuuchunguza kwa kuufunua ambapo kweli alikuta kama
mpira wa makaratasi umefungwa fungwa. Moza akaanza kufungua ila kadri
alivyofungua ndivyo nguvu zilivyomuisha, hadi mwishoni akaanguka kabisa na kuwa
kimya hapo hapo. Kimya kilitanda sana chumbani kwa Moza hadi kesho yake
asubuhi kila mtu aliamka kwenye ile nyumba na kufanya shughuli zao za hapa na
pale kasoro Moza, ila Rose alijua Moza amepitiwa kama kawaida yake ila aliona
kengele ya hatari ikilia kwenye kichwa chake lakini alipuuzia na kuondoka kama
kawaida yake kisha akaacha ujumbe mezani ila bado nyumba ilitawaliwa na
ukimya. Rose ile asubuhi alimpeleka mwanae shuleni kisha na kupanga
kupitia kwenye shughuli zake, “Hivi kwanini siku hizi Ana hutaki kabisa
kupelekwa shule na Moza?” “Mama, kiukweli ni kuwa Yule dada simpendi
kabisa yani simpendi mfukuze bhana mama” “Namtafutia kosa la kumfukuza
ila sikutaka kumfukuza kwanza mpaka nitakapomfunza adabu, unajua Yule msichana
amezidi sana” “kwahiyo mama umepanga tufanyaje nae? Maana unamchekea tu
Yule, jitu linachunguza kila kitu mara kutandika kitanda hadi atake kufunua
godoro langu, mara anivue viatu bila ruhusa yangu. Na siku ile aliyonivua viatu
kanimaliza nguvu kabisa mama” “Sawa mwanangu naelewa, ila ukitoka shule
nisubirie hapo hapo shuleni twende mahali kwanza, tukitoka hapo twende nyumbani
na Yule Moza atakoma. Yani Yule simfukuzi ila atajitegesha
mwenyewe” Rose alimfikisha mwanae shule na kumuacha hapo, kisha yeye
akaenda kwenye shughuli zake. Rose alipotoka kwenye shughuli
zake kama alivyopanga alimpitia mwanae na kwenda nae mahali, “Tunaenda
wapi mama?” “Kwa babu” “Babu yupi?” “Yule anayefanya
tuwe na nguvu” “Mbona mimi simjui huyo?” “Utamjua tu, yeye ndio
kiboko alinisaidia hata kupata mimba na kukuzaa wewe. Yeye ndiye aliyenisaidia
hata kumfanya Yule mzee ndani anisikilize mimi tu. Wewe mwanangu una nguvu za
ziada ila huyu babu ndio atakupa nguvu zaidi maana ndio anayejua kuhusu wewe
vizuri” Walivyofika kwa Yule babu, walisikia sauti ya Yule babu
ikiwaambia, “Mmeshachelewa tayari” “Tumechelewa
kivipi?” “Ndani ya nyumba yenu mlikuwa mnaishi na mtu wa hatari
sana” “Bado sijaelewa, hebu nieleweshe vizuri babu” “Fanyeni
hima mkamzike Yule mtu” “Nani tena?” “Kwani hujui? Yule msichana
wako ameshakufa” Rose na mwanae Ana walishikwa na bumbuwazi, na kujikuta
wakiuliza kwa pamoja tena kwa mshangao, “Amekufa!” “Ndio
amekufa, yani hakuna cha Moza tena wala mdudu wa Moza” “Ila mbona
ulisema tumechelewa? Na amekufaje kufaje?” “Mngewahi tungemmaliza
wenyewe mtu huyu” “Kwahiyo kamalizwa na nani?” “Kamalizwa na
mpira wa maajabu” “Kheee kautoa wapi huo mpira?” “Si mliuweka
kwenye bustani, sasa ameuchukua wakati wa kumwagilia” “Kheee mpira
wangu, sasa itakuwaje babu” “Hakuna namna, cha msingi ameshakufa. Cha
kufanya nyie muwe wa kwanza kuioana maiti yake, kisha ule mpira msiutoe mikononi
mwake, hakikisheni mnamzika nao. Kisha mimi nitawatengenezea mpira mwingine,
yani hakikisheni ule mpira mnamzika nao. Msiutoe kabisa mikononi
mwake” “Sasa tusipotangulia sisi kumuona itakuwaje?” “Jitahidini
muwe wa kwanza nyinyi sababu nitawapa dawa ya watu wengine kutokuuona ule mpira,
yani mtakuwa mnauona nyinyi tu. Jitahidini kesho muuzike. Mwisho wa Moza umefika
tena kautafuta mwenyewe” “Basi inabidi tufanye haraka maana watoto wangu
nina mashaka nao wasije wakaenda kumtoa bure. Ngoja niwapigie simu niwaongezee
majukumu ili wasirudi nyumbani” Muda ule ule Rose akaanza kuwapigia
watoto wake, akampa kila mtu majukumu ambapo kwa majukumu waliyopewa ilikuwa ni
vigumu sana kurudi nyumbani yani ni lazima wangerudi kesho yake ambayo hata huyo
Rose ndio alipanga kesho yake hiyo ndio amzike Moza. Ana akamuuliza mama
yake, “Kwani watakuja watu kwenye huo msiba?” “Watu watoke wapi?
Kwanza ndugu wa Moza hatuwafahamu yani hapa tutaongea na vijana tukamzike na
ikiwezekana sijui tukiwahi tumzike usiku huu” Yule mganga
akawaambia, “Hapana Yule si wa kuzikwa usiku, anatakiwa kuzikwa mchana
kwenye jua kali kabisa sababu ndio itakuwa uthibitisho wa kifo chake na hakika
hatawasumbua tena kwani hata kumbukumbu yake haitakuwepo” “Sasa si watu
wa serikali watatushtukia?” “Kuna dawa nitakupa ya kumwaga getini kwako
pindi tu ukirudi kisha kila kitu kitakuwa shwari kabisa. Hakuna mtu atakayejua
chochote” “Utakuwa umetusaidia sana, yani Yule msichana loh nilitokea tu
kutokumpenda ila cha kushangaza kumfukuza nilikuwa siwezi ila kajiua mwenyewe
bora maana hata kwa Mungu sina dhambi juu yake. Kajimaliza
mwenyewe” “Nawapa na dawa ya kuoga yani baada ya maziko ya Moza mkaoge,
ila baada ya wiki mje tena kuna tambiko inabidi tulifanye, Yule Moza hakuwa mtu
wa kawaida Yule kama wengine” Basi Rose na Ana wakaondoka zao huku Ana
akimuhoji mama yake, “Moza hakuwa mtu wa kawaida kweli mama maana
tukipanga hivi yeye anafanya vile, ila kufa sijui ndio kafaje
kafaje” “Tutajua huko huko nyumbani tukifika” Njiani gari yao
ikapata pancha, ikabidi Rose atafute watu wa kuziba pancha ya gari
yake. Leo Salome akiwa nyumbani kwao na mama yake, akamueleza
kuhusu alivyokutana na Moza na jinsi alivyompeleka hadi
anapoishi, “Jamani kumbe kasharudi hapa mjini” “Ndio
mama” “Naomba kesho unipeleke nikaonane nae maana nina mengi ya
kuzungumza nae” “Sawa mama nitakupeleka” “Unajua Yule Moza
alikuwa na utambuzi wa hali ya juu yani alikuwa anatambua mambo sana, natumaini
nikikaa kyzungumza nae basi tutazungumza mambo mengi sana. Halafu kuna kitu
nataka anisaidie” “Kitu gani hicho mama” “Salome, wewe bado
mwanangu ila ukikua utaelewa yote ambayo mwanawake yanatupata. Kuna dawa
alishawahi nidokeza ipo kwa bibi yake” “Huyo bibi yake
ameshakufa” “Kheee amekufa! Maskini jamani yani yeye alikuwa anasema
amebakiwa na bibi yake tu, kumbe alikufa masikini dah! Ila natumai hiyo dawa
atakuwa anaijua” Basi Neema na mtoto wake wakapanga kuwa kesho yake
waende huko anapoishi Moza ili Neema akazungumze nae bila ya kujua kuwa huyo
Moza ameshapatwa na majanga kule nyumbani. Kwa upande wa Sara
nae alipopigiwa na mama yake simu na kuambiwa kuwa aende Morogoro na airudi
nyumbani siku hiyo hadi kesho yake kwakweli moyo wake ulikuwa mzito sana kufanya
hivyo, “kwakweli mama nae amezidi, kwanini asiniambie tangu asubuhi kuwa
niende Morogoro? Yani anakuja kuniambia jioni hii hapana kwakweli, sijisikii
kabisa kwenda Morogoro muda huu. Nitaenda tu kesho asubuhi, ngoja nirudi
nyumbani nitamwambia tu nyumbani kuwa nimeshindwa kwenda Morogoro saa
hizi” Wakati anapanga hayo akapigiwa simu na namba mpya na
kuipokea, “Nani mwenzangu?” “Ommy anaongea hapa” “Kheee
Ommy jamani, ulivyonifanyia sio vizuri Ommy unajua name nina
moyo” “Naelewa Sara, ila nataka kuzungumza na wewe kwanza” “Sasa
muda huu naenda nyumbani, labda uje nyumbani au unasemaje?” “Sawa, hata
mimi nipo mitaa karibu na kwenu. Basi wewe ukifika tu nishtue
nije” “Sawa” Akakata simu, yani hapo ndio wazo la kwenda
Morogoro kwa wakati huo likakatika kabisa kwani mawazo yake yote alikuwa akitaka
kumsikia Ommy atasema nini baada ya kutokuonana nae kwa kipindi kirefu
sana. Safari yake muda huo ilikuwa ni moja kwa moja nyumbani
kwao. Kwakweli lile swala la pancha liliwakosesha sana raha
Rose na mtoto wake Ana, huku wakijiuliza kilichopelekea hali hiyo. Ana
akamuuliza mama yake, “Hivi kwa mfano wakina kaka na dada warudi
nyumbani na wao wawe wa kwanza kumuona Moza amekufa itakuwaje?” “Kwanza
swala la kurudi nyumbani bila ruhusa yangu hawawezi kufanya hivyo.
Wananisikiliza sana wale na nimewaambia kazi ya Morogoro ni ya le oleo sio ya
kulala ile” “Sawa mama, lakini watoto wako hawajielewagi wale haswa dada
Sara na kaka Kulwa” “Hata kama wakiona wao kwanza hakuharibiki kitu,
najua Sara ni muoga sana kwahiyo akiona cha kwanza atanipigia simu na nitamwmbia
asifanye chochote yani wale wasikutishe mwanangu yani Moza lazima tumzike na
asahaulike katika dunia hii. Kwani kuna kosa tumefanya hapo? Kifo si amekitaka
mwenyewe! Mwache afe” Rose bado alikuwa anashughulika na vijana wazibe
ile pncha hata alishangaa ni kwanini imechelewa vile kwani hakudhania kabisa
kama itachukua muda mrefu hivyo. Ila fundi aliyekuwa anatengeza
alimuhakikishia muda huo kuwa ndani ya masaa machache atakuwa
ameshamaliza. Ilikuwa ni saa kumi na mbili jioni ikienda saa
moja, mlinzi pale getini alishangaa sana siku hiyo bila kumuona Moza hata mara
moja, “Mmmh sio kawaida yake, tuseme amekosa cha kuniuliza kabisa leo?
Ila mbona sijasikia kelele zozote za mapishi ndani? Ila ni sababu mimi sili
chakula cha ndani humo ila nina wasiwasi, sijui Moza ni mzima!” Muda
kidogo alifika Sara akiwa ameongozana na huyo mgeni wake aitwaye Ommy, na
kumkaribisha ila wakati wanaenda ndani huyu mlinzi akamwambia, “Sara,
mwambie Moza sio vizuri kunichunia leo” “Mmh umeanza kumpenda nini
Moza!” “Hapana ila sio kawaida yake” “Sema ukweli bhana, au
kumtongoza unaogopa. Mmmh! Kwanini hizo salamu zako usimuagize
Ana” “Bado hajarudi” “Mpaka saa hizi duh!” “Yani wewe
ndio wa kwanza kurudi” “Labda anarudi na mama yake Yule” Kisha
Sara akawa anamkaribisha mgeni wake ndani hadi ameingia nae
sebleni, “Yani leo mama alikuwa anataka niende Morogoro” “Sasa
hujaenda na leo mmh si ndio atanichukia mimi?” “Hapana bhana, nilighairi
kwenda kabla hata hujanipigia simu” Kisha Sara akaanza kumuita Moza ili
amletee kinywaji mgeni, aliita na kuita ila Moza hakumuitikia, “Huyu
Moza vipi? Sio kawaida yake kukaa kimya akiitwa au alilala jioni ndio kalala
hadi saa hizi” “Nenda kamuangalie, usimlaumu tu labda
anaumwa” Sara akaenda moja kwa moja chumbani kwa Moza, akagonga ila
hakuitikiwa akaamua kufungua mlango, akashangaa kumuona Moza amelala chini.
Alimsogelea na kumtikisa, “Weee wewe Moza weeee” Ila Moza
hakumuitikia na kumfanya Rose ashikwe na mashaka na kwenda kumuita
Ommy, “Njoo unisaidie kumuangalia sijui kapatwa na nini maana hasemi
chochote” Ommy akaenda na Sara hadi chumbani kwa Moza, alivyomshika tu
Ommy akagundua na kumwambia Sara, “Huyu mtu ni wa baridi, inaonyesha
amekufa muda mrefu sana” “Amekufa!” “Ndio amekufa” Sara
aliishiwa nguvu kabisa na kujikuta akikaa chini, alihisi kama akili yake inaruka
huku akisema “Moza amekufa, hapana jamani. Moza
amekufa!” Akajikuta akipiga kelele za yowe na kufanya hata mlinzi aingie
ndani ilia one kuna nini, “Kuna nini Sara?” “Eti Moza amekufa
uwiiiii jamani Moza amka jamani, nyie niambieni ni uongo Moza hajafa. Jamani
Moza amka jamani” Mlinzi akamuangalia Ommy, naye Ommy alimuonyesha
ishara kuwa amuangalie pia Moza nay eye alipomtazama aliona kweli amekufa yani
hata yeye mlinzi ingawa alikuwa ni mwanaume ila machozi yalimlengalenga. Ommy
akamuangalia saran a kumwambia, “Kulia hakusaidii Sara, bora tumpeleke
hospitali akahifadhiwe halafu wakirudi nyumbani hapa ipangwe mipango ya
mazishi” “Siwezi kujizuia Ommy, labda uniambie huko hospitali anaenda
kupimwa vizuri ila Moza hajafa bhana” “Sawa anaenda kupimwa vizuri, basi
njoo uchukue kanga zake tumfunikize kisha tumpeleke hapo hospitali ya
karibu” Basi Yule mlinzi alipomuinamia Moza pale chini, alimuona na kile
kimpira ambapo alikitoa kwenye mkono wa Moza na kukitupia pembeni ambapo
kilikusanyika na nguo zingine chafu za Moza maana Moza mwenyewe alikuwa amepanga
siku hiyo afue ila mauti ikamshika na kuzuia kufua kwake. Sasa walikuwa
wanawaza kumyanyua hapo kwani kwa kawaida za maiti huwa ni nzito sana ila
ilikuwa tofauti kwa maiti ya Moza yani alikuwa ni mwepesi hadi mlinzi aliamua
kumbeba mwenyewe, kisha Ommy akampigia simu dereva wa gari za kukodi ili
wampeleke hospitali. Ila walipotoka nje na kutaka kwenda kumpakia kwenye gari,
muda huo huo Rose na mwanae walifika kisha Rose akawauliza kwa
mshangao, “Kuna nini hapa?” Sara akajibu kwa uchungu sana huku
akilia, “Moza amekufa mama” “Kwahiyo kama amekufa ndio mnataka
kufanyaje?” Akajibu mlinzi, “Tunataka kumpakia kwenye gari
tumpeleke hospitali” “Hivi nyie mna akili kweli? Mtu ameshakufa sasa
hospitali akafanye nini?” Ommy akajibu, “Wakaupumzishe mwili
wake” “Ili iweje? Mlisikia wapi maiti anachoka hadi
apumzishwe” “Mmmh mama” “Kelele na wewe Sara, huna akili hata
moja wewe. Huko kupumzisha mwili hospitali mnadhani ni bure? Hubu rudisheni hiyo
maiti chumbani kwake halafu tupange shughuli za mazishi kesho. Mnafikiri ni
rahisi kuhifadhi maiti eeeh! Rudisha hiyo maiti upesi” Alimfokea Yule
mlinzi, ikabidi airudishe ile maiti ya Moza chumba kile alichokuwa analala Moza.
Kila mmoja pale alibaki amestaajabu haswa Sara hakufikiria kama mama yake
anaweza akawa katili kiasi kile tena kwa mtu ambaye ameshakufa. Yule
dereva wa gari za kukodi ilibidi aondoke kwani alipigwa na butwaa kwa maneno ya
Yule mama, na ndio akaenda kusambaza maneno mtaani kuwa nyumba ile ina
msiba. Walirudi sebleni ambako walikuwa wakimsikiliza mwenye
nyumba kwa makini kabisa kuhusu taratibu za mazishi, “Kesho saa saba
mchana tutaenda kuzika” “Khee mama hatuwatafuti ndugu wa
Moza?” “Hivi nani atafanya hiyo kazi ya kutafuta ndugu huku akiendelea
kuhifadhi maiti kwenye nyumba yake? Kwanza nimemuhurumia tu, ilitakiwa nikamzike
leoleo” “Mmh mama jamani!” “Kelele na wewe, wewe ndio mbaya.
Hivi hamjui kuwa mambo mengine mnajitafutia kesi bure tu. Hata sitaki majirani
wajue kama kuna msiba hapa. Na kulia kwako sitaki kusikia, unamlilia ndugu yako
huyu? Alikuwa ni mfanyakazi tu, kwanza kwenye nyumba hii hana hata mwezi halafu
anakufa unajifanya kulia lia, umemzoea lini. Hebu nitolee balaa
mie.” Rose akainuka na kumuinua mwanae Ana ili waende chumbani
kuichunguza vizuri maiti ya Moza. Waliingia chumbani kwa Moza
na kuichunguza vizuri ila hawakumuona na kitu chochote mkononi, wakajaribu
kupekua mule chumbani kwake ila hawakuona chochote, “Sasa itakuwaje
mama?” “Yani hata sielewi hapa, inamaana ule mpira umeyeyuka au? Si Yule
mganga amesema tuhakikishe anazikwa nao?” “Ndio, sasa tutafanyaje
mama?” “Lakini ilimradi amekufa basi hakuna kitu kitakachoharibika, cha
msingi tuhakikishe tu kesho tunamzika” “Sawa mama, ila inabidi tufanye
kitu ili Sara aache kulia kabisa watu wasije wakajua kama kuna msiba
hapa” “Usijali juu ya hilo, ngoja nikamtimue Sara aondoke na huyo Ommy
wake” Rose na Ana wakaelekea sebleni ila walipofika tu waliona jambo la
kushangaza sana. Rose na Ana wakaelekea sebleni ila
walipofika tu waliona jambo la kushangaza sana. Walikuta watu wamejaa
sebleni tayari kwa maombolezo, kwakweli hiki kilikuwa ni kitu cha kuwashangaza
sana kuwa watu wote wale wametoka wapi kwa muda mfupi ule. Lakini kabla
hajajiweka sawa kuwauliza maswali, wakafika wengine yani Rose alizidi kuchukia,
nao wakawa wanamsogelea na kumpa pole kwa msiba. Ikabidi Rose akae chini
sasa na kuzungumza na waliokuwa karibu yake, “Mmmh watu wa huku mna
ushirikiano, hivi mmejuaje kama kuna msiba ikiwa hata sisi wenyewe tumejua muda
huu” “Kuna Yule dereva Juma, amepita mtaani na kutuambia wote nyumba
baada ya nyumba kuwa huyu msichana wa hapa amekufa. Kwakweli tumesikitika sana,
alikuwa mtu wa watu sana huyu msichana” Rose akashangaa kuwa mtu wa watu
kivipi wakati hata mwezi hana kwenye nyumba yake, ikabidi aulize
tena, “Kwani mlikuwa mnamfahamu?” “Ndio, Moza tena tusimfahamu!
Siku ya kwanza tu alikuja kujitambulisha kila nyumba kuwa anaitwa Moza na
anaishi hapa. Tena mara zote alipokuwa akienda gengeni alikuja kutusalimia,
kwakweli tumemfahamu kwa kipindi kifupi halafu amekufa. Inasikitisha sana,
ndiomana unaona watu wote hawa wamekuja msibani, ni muda mfupi tumemfahamu Moza
ila alikuwa ni mtu wa watu” Rose akainuka na kwenda chumbani kwake
akawaza kuwa Moza alikuwa anapata wapi muda wa kwenda kuwatembelea majirani na
kuzungumza nao, “Yani kuna wengine pale hadi mimi mwenyewe siwajui ila
Moza wanamfahamu loh kweli huyu msichana kwa umbea alishindikana
jamani” Ana nae akafika chumbani kwa mama yake na
kumuuliza, “Sasa mama tutafanyaje?” “Yani hapa nachanganyikiwa
kabisa, yote haya kayasababisha Sara na kiburi chake, lile toto sijui
nilibadilishiwa hospitali! Kwakweli sio toto langu lile” “Sasa mama huu
sio wakati wa kulumbana, unajua watu ni wengi na bado wanaendelea kuja huku kila
mmoja akiulizia chanzo cha kifo cha marehemu. Sijui tufanyeje kuwatoa hapa
nyumbani” “Hebu kaniitie kwanza huyo Sara” Ana akatoka na kwenda
kumuita Sara. Alifika sebleni na kukuta watu wameongezeka
kushinda wale wa mwanzo tena wengine walijaa nje, yani ilionyesha wazi majirani
wa hapo walitaka siku tu wapate nafasi ya kwenda kwenye nyumba hiyo maana ni
kitu cha kushangaza kuwa watu wamesikia msiba muda sio mrefu na washajaa nyumba
yenye msiba, ni kwamba hawakuwa na majukumu mengine walikuwa wanasubiri tu msiba
utokee au ni nini, ila Ana alihisi kuwa watu hao walikuwa wakitamani sana
kuingia kwenye nyumba ile. Kwahiyo siku hiyo ilikuwa imetokea kama bahati hivi.
Ana alienda kumuita Rose ambaye alikuwa katikati ya watu wakimuuliza chanzo cha
kifo cha marehemu, “Kwakweli hata hatujui ni nini labda aliumwa gafla
maana tumerudi tu tumemkuta amekufa” “Dada unaitwa na mama” Sara
alimwangalia mdogo wake kwa makini sana maana siku hiyo alimuita kwa heshima
zote, kisha akainuka na kwenda chumbani alikoitwa na mama yake. Kufika kule Rose
akaanza kumwambia mwanae, “Fanya ufanyavyo hao watu waondoke kwenye
nyumba yangu” “Kheee mama wataondokaje na wamekuja
msibani” “Sara sitaki ujinga, msiba msiba, msiba huo vipi? Kwani hapa ni
nyumbani kwakina Moza? Hapa ni kwao hadi waje hapa? Waambie waende kwakina Moza
huko kijijini ndio wakafanye msiba, nyumbani kwangu siwataki, kwanza nataka
kulala saa hizi” “Kwakweli mama siwezi, labda uje kuwaambia mwenyewe ila
mimi siwezi” Sara alitoka chumbani kwa mama yake na kumfanya mama yake
azidi kupatwa na hasira huku watu kwenye sebule yake wakizidi
kumkera. “Sikiliza mwanagu Ana, kachukue nguo zako kisha uje tulale huku
wote. Naenda kuzima umeme wakae na giza hapo sebleni” Ana akaenda
kuchukua nguo na kwenda chumbani kwa mama yake ambapo mama yake akawasha taa ya
kuchaji mule chumbani na kuzima umeme wa nyumba nzima kisha wao wakajifungia
chumbani. Sebule ilitawaliwa na giza totoro na kufanya ndani kutishe
kiasi ila sababu watu walikuwa wengi na wengine wakawasha tochi za simu zao
ikasaidia kufanya ndani kusitishe sana. Ila kulikuwa na matukio yaliyofanya watu
wasipatwe na usingizi pale kwani kulikuwa kama kuna vitu vinawapitia kichwani,
sema kwavile watu walikuwa wengi kwahiyo wasiwasi ukawa sio
mkubwa. Kulipokucha, Rose alijua watu wameondoka. Akaoga na
kuvaa vizuri kisha kumuandaa mtoto wake ila walipotoka sebleni walishangaa kuona
watu wamejaa, huku wamama wawili wa makamo wakimfuata Rose na
kumuuliza, “Sasa asubuhi hii tutapika nini kuwapa watu hawa? Na je upo
tayari tulete kuni tuanze mapishi?” Rose akawaangalia kisha
akawauliza, “Kwani watu hawa hawana makwao?” “Wanapo ila
wamekuja msibani” “Kwani msibani ndio sehemu ya kumaliza njaa zao?
Wakale makwao” “Makwao kupo, hata kulala hapa msibani ni heshima tu
halafu ni utaratibu wetu waafrika mpaka pale tutakapozika” “Sikia
nikwambie, sina hela ya kulisha watu hao halafu nyumbani kwangu sitaki mpikie
makuni. Waambieni wakale makwao” “Dada jamani usiseme hivyo, watakususia
msiba mwenyewe” “Usitake kunichekesha na wewe, kwani wakisusa ndio nini,
sitaweza kuzika au nini? Nitoleeni balaa mie” Rose alikuwa na hasira
sana na watu hawa, kisha akatoka na mwane Ana bila hata ya kumwambia Sara. Wale
wamama ikabidi waende kumueleza Sara walichojibiwa na mama yake, “Jamani
Yule ndio mwenye nyumba, sina usemi mimi.” “Mmmh makubwa ya leo,
nimehudhuria misiba mingi tu lakini hakuna msiba wenye vimbwanga kama huu mara
tuzimiwe taa usiku,mara tutembelewa na wadudu popo si popo sijui wadudu gani
wale, haya kumekucha eti kila mtu akale nyumbani kwake mmmh sijawahi kusikia
mie. Hata kuturuhusu tupike uji jamani!” Ikabidi hawa wamama wafikishe
ujumbe kwa wengine, lakini watu walisema wataondoka kidogo kidogo kwenda kula
ili tu washuhudie mwisho wa msiba huo utaishia wapi. Sara akaona vyema
ampigie simu na baba mwenye nyumba ili ampe hizo taarifa maana wanadhalilika
mtaani halafu akawapigia simu na wale mapacha ambao walikuwa tayari
Morogoro, “Kuna msiba huku?” “Msiba? Wa nani tena? Au baba
kafa?” “Hapana sio baba, ni Moza amekufa” “Kheee Moza amekufa
jamani masikini, loh tunageuza tunakuja huko msibani” “Sasa mama
anavyofanya vihoja huku msibani yani anatudhalilisha mtaani haswaaa. Njooni kaka
zangu bhana tusaidiane” Halafu na Mr.Patrick nae akampa habari hizo
ambaye alibaki anashangaa tu ila akakumbuka kuwa mkewe amemwambia jana yake kuwa
asirudi kabisa nyumbani, “Mmmh Sara kwakweli hiyo habari imenishtua
sana, nakuja nyumbani muda sio mrefu” Sara akapumua sasa baada ya kupiga
simu hizo na kushukuru kwa kupiga kwani kidogo zimempa amani baada ya kuambiwa
na ndugu zake kuwa wanakuja. Mr.Patrick akiwa na harakati za
kuwahi nyumbani kwake, njiani akamuona mtu amesimama barabarani. Alikuwa ni
mwanamke amejitanda khanga, ikabidi Patrick ashuke ili ajue huyo mwanamke
amekumbwa na nini, alipotaka kumtazama Yule mwanamke aligeuka na kumwambia
Patrick, “Usinitazame” Patrick akashtuka sana kwani sauti
ilikuwa kama sauti ya Moza, Patrick alijikuta akimuuliza Yule mwanamke kwa
wasiwasi sana, “Mbona sauti kama ya Moza” “Ndio, mimi ni
Moza” Kwakweli Patrick alipatwa na uoga zaidi na kuuliza kwa wasiwasi
zaidi, “Ila nimeambiwa kuwa Moza amekufa” “Umeambiwa hivyo ila
kiukweli mimi sijafa” “Kwahiyo wewe ni Moza?” “Ndio mimi ni
Moza, unatakiwa kunisaidia kwani msaada wangu kwasasa ni wewe” “Kheee
sasa mimi nitafanya nini?” “Nitakupa maelekezo ya kufanya ukifika
nyumbani, halafu jitahidi nisiende kuzikwa saa saba kama alivyopanga mama bali
nizikwe saa tisa” Yani Patrick alikuwa anamsikiliza huku akitetemeka
sana, Yule mtu alimpa malekezo mzee Patrick ila hakumuangalia usoni kabisa na
wala mzee Patrick hakumuona kwahiyo alimuamini sababu tu ya sauti ilikuwa ni ya
Moza. Mzee Patrick aliondoka mahali pale huku akili yake ikiwa haipo
kabisa kwenye muelekeo wa kawaida kwani jambo aliloliona halikuwa la kawaida
kabisa kwake. Nyumbani kwa Rose, kwenye mida ya saa tano, Rose
alirudi na mtoto wake Ana ila bado watu walikuwa wamejaa pale nyumbani kwake
kwani wote walikuja kwa nia ya msiba, Rose akawaambia watu
wale, “Nishaongea na wachimba kaburi, kwahiyo saa saba tutaenda
kuzika” Wale wamama wa asubuhi wakauliza, “Kwahiyo na ndugu wa
Moza watakuwa wamefika muda huo?” “Hivi nyie watu mnafikiria kwa akili
gani, yani nitunze maiti kwenye nyumba yangu nikisubiria ndugu
zake!” “Si ungempeleka hospitali” “Halafu hiyo hela ya
kuhifadhia maiti mtatoa nyie?” Wakawa kimya, ila wakaongezea
lingine “Basi turuhusu tukamsafishe marehemu kabla ya maziko. Na tuwaite
watu wa dini kwaajili ya mazishi” “Hivi nyie ndio mnamfahamu sana Moza
kushinda mie, mnaijua dini ya Moza nyie? Kipindi hiki nilichoishi naye, sijawahi
kumuona akienda kanisani wala msikitini. Hakuna siku aliyoongelea kanisa wala
msikiti, sasa nyie mnataka kuita watu wa dini wafanye nini wakati mtu huyu
alikuwa mpagani. Hebu niondoleeni ujinga mie” “Basi
tukamsafishe” “Hivi mbona mnakazania sana au nyie wachawi? Maana sio kwa
kukazania huko. Nitamsafisha mwenyewe” Ikabidi wawe kimya na wangoje huo
muda ambao amesema wa kuzika ufike, Rose na mwanae wakaingia ndani ila watu pale
msibani yani kila mtu alikuwa akiongea lake kuhusu ule msiba na mwenendo wa pale
msibani. Kwenye saa sita na nusu, mzee Patrick nae alifika nyumbani
kwake, ila muda huu mkewe alikuwa ndani kumbe alikuwa akijiandaa kwa
maziko. Moja kwa moja alionana na Sara kwanza ambapo
alimuuliza, “Maiti ya Moza iko wapi?” “Chumbani kwake
baba” “Nahitaji kuiona” Patrick aliongozana na Sara hadi
chumbani kwa moza, ambapo Patrick alimuomba Sara akamletee maji, wakati Sara
ameondoka Patrick akatumia muda huo kuipulizia ile maiti dawa aliyoambiwa na mtu
aliyekutana nae huku akisema kama itafanya kazi sawa na hata isipofanya kazi
hakuwa na namna zaidi kwani alifanya vile alivyoelekezwa. Kisha alienda kuifunua
ile maiti na kumpaka ile dawa puani, Sara alikuwa amerudi na kumshangaa baba
yake, “Baba, unafanya nini tena?” “Unajua nilikuwa siamini
kabisa kama Moza amekufa kweli, ndio nikawa namuangalia
hapa” Wakasimama, muda kidogo akaja Rose ambapo alishangaa kumuona mume
wake hapo, “Mchezo gani huo umeanza wa kurudi bila
kusema?” “Nisamehe mke wangu, ila niliambiwa kuna msiba ndiomana
nikarudi” “Haya sasa mtoke nataka kuita vijana wambebe tukazike maana
wachimba kaburi washanipigia simu kuwa tayari” “Mmh mke wangu kwahiyo
tunamzika kama hivyo tu?” “Ndio, tunamviringisha nguo zake
tunamzika” “Mmmh mke wangu jamani, kwanini tusimwagizie
jeneza!” “Sina hela za mchezo, huyu msichana hana hata mwezi halafu
nianze kumgharamikia hivyo. Siwezi kwakweli wanakuja kumchukua tukazike. Kwanza
nimechoka kukaa na maiti yake humu ndani kwangu” Patrick akawa anawaza
ni njia gani atumie ili waweze kidogo kupeleka mbele muda wa kuzika kama
alivyoombwa na Yule mtu, basi akajifanya amemuitikia pale mke wake kisha akawa
anatoka akaanguka chini na kumfanya Rose aache kuwapigia simu vijana wa kuja
kumbeba moza ili kuzika na kuanza kushughulika na mumewe, “Vipi
tena?” "Mguu wang" “Mguu wako! Umeteguka au?” Ikabidi
amshike na kumkongoja hadi chumbani kwao ambapo Patrick alionekana kulalamika
kweli kuhusu mguu, ikabidi Rose amchue kwanza. Mapacha wa Rose
nao walifika kwenye saa saba kwahiyo Sara alikuwa akiwapokea ndugu zake na
kuwaeleza kinagaubaga kuhusu kifo cha Moza kwa uelewa wake, “Kwahiyo
ulimkuta tu ndani ameshakufa?” “Ndio, ila mama kafanya vituko
sana” “Ila mama yetu tunamfahamu, na watu hawa walivyojaa hapa najua
ndio amechefukwa balaa” “Na amesema tunaenda kuzika muda sio
mrefu” “Ila hicho kifo nina mashaka nacho hata sio cha kawaida ila
wengine tukisema midomo michafu, ngoja nikae kimya tu.” Wakamsubiria
mama yao pale, mzee Patrick nae alimpotezea muda Rose hadi alihakikisha saa nane
inamfikia pale ndio akamuacha achukue vijana aende kuzika ila yeye alisema
haendi sababu bado alikuwa na maagizo mengine aliyopewa na yule mtu kwahiyo
alitaka kuyatekeleza wakienda makaburini na kubaki mwenyewe
nyumbani. Rose alitoka na kutaka watu waharakishe huku akiwaelekeza
maeneo ya makaburi ili waanzage kwenda, basi alichukua na vijana wakumtoa Moza
mule ndani ila hata wale vijana walimshangaa Moza kwakweli alikuwa mwepesi
kabisa kama hawajabeba mtu vile ingawa aliviringishwa mashuka ila bado alikuwa
mwepesi sana. Wakati watu wanatoka ndio njiani wakakutana na Salome na
mama yake ambao walikuwa wanaenda kwa Moza, walipoona watu wengi wengi
wanatembea ikabidi waulize, “Kuna nini kwani?” “Kuna msiba, Yule
msichana muongeaji. Mpenda watu amekufa” “Nani huyo?” “Anaitwa
Moza” Kwakweli nguvu ziliwaisha kabisa ila ilibidi waongozane na hao
watu makaburini, lakini Salome alikuwa haamini kabisa. Walifika
makaburini, na wale waliobeba maiti nao walifika makaburini. Wakataka kuzika
sasa, ila Salome aliwafata na kuwaomba “Naombeni hata mnionyeshe tu dada
Moza nimuone kama kweli amekufa” Wale vijana wakamuangalia Rose na
kumuuliza, “Eti tumruhusu amuone?” “Ametoka wapi huyo, aone nini
na yeye embu atutolee balaa huko. Hakuna cha kuona, zikeni na nyie tumalize watu
waende zao maana wanataka tu kushuhudia moza anavyozikwa” Kwa wakati huo
Rose hakumtambua Salome kabisa kwani alikuwa na mawazo yake, kwanza kashachelewa
muda wa kuzika. Wale watu walimtumbukiza Moza kwenye shimo, ila bila
kutegemea Salome nae aliingia kwenye lile shimo. Ndani ya muda huo kila mmoja
akistaajabu tukio la Salome, walipoenda kumchungulia Salome kwenye kaburi la
Moza alionekana amekauka kama mtu aliyepigwa na shoti ya
umeme. Wale watu walimtumbukiza Moza kwenye shimo, ila
bila kutegemea Salome nae aliingia kwenye lile shimo. Ndani ya muda huo kila
mmoja akistaajabu tukio la Salome, walipoenda kumchungulia Salome kwenye kaburi
la Moza alionekana amekauka kama mtu aliyepigwa na shoti ya umeme. Neema
hakutegemea lile tukio la mtoto wake kabisa, akajikuta akipiga kelele za yowe,
ilibidi vijana waingie kwenye lile kaburi kumtoa Salome na kumpeleka kwenye gari
ili kumuwaishe hospitali ambapo mama yake naye alifatana nao hospitali ila kitu
cha kushangaza kwenye kaburi la Moza haikuonekana maiti yoyote wala zile nguo
walizokuwa wamemfungia yani kwa kifupi maiti ya Moza ilitoweka yani kila mmoja
alipigwa na butwaa kwani ni kitu ambacho hakuna aliyekitarajia kabisa kwa wakati
huo. Pale kaburini kulikuwa na mzozo mkubwa kuwa maiti imeenda wapi,
kila mtu hakuelewa kitu chochote kwani ilikuwa ni kwa muda mfupi sana kwa Salome
kutumbukia kwenye kaburi na kutolewa halafu maiti ya Moza kutokuonekana, hakuna
aliyejua kuwa maiti iko wapi kila mtu alikumbwa na bumbuwazi. Wakati
wapo kwenye mshangao pale kaburini mara upepo mkali ulianza kuvuma huku vumbi
jingi likipepea na kufanya watu wafunge macho na baada ya muda kila mtu
alisambaratika na kujikuta pale kaburini wamebaki wale vijana na
Rose. Kwahiyo walijiona wenyewe baada ya upepo ule, “Jamani,
mbona mambo ya ajabu sana haya. Kwakweli mama kwaheri, kazi ya namna hii siiwezi
tena” Mmoja alisema hivyo, huku mwingine akisema “Yani unasikia
kabisa wengine wakikimbia na kuondoka ila sisi kama tumeshikiliwa na sumaku.
Kuondoka hatuwezi” Na walipojaribu kuondoka walishindwa kwenda, ikabidi
mmoja atoe wazo kuwa wafukie kwanza kaburi, kwakweli Rose alikuwa kimya kabisa
kwani hakutegemea kama ingekuwa vile. Walifukia hadi walifanikiwa
kumaliza, na walivyomaliza tu walijikuta wakiweza kuondoka, kwakweli walikimbia
kutoka pale makaburini balaa. Rose alienda kwenye gari yake huku
akitafakari bila ya majibu, kwa wakati huo hata hakujiuliza kuwa mwanae Ana yuko
wapi, wazo lililomjia kwa muda huo ni kwenda kwa Yule babu ili akapate ukweli wa
mambo kuwa imekuwaje kuwaje maana hakuelewa. Nyumbani nako,
Patrick alikuwa anafanya maelekezo aliyopewa na Moza bila kujua kuwa yale
maelekezo yaliharibu kila kitu makaburini kwani yale maelekezo karibu yote ndio
yaliyofanya yale yaliyotokea kule makaburini. Kwani alitafuta kile
kimpira kwenye ngui chafu kama alivyoambiwa, kisha akakibeba na zile nguo na
kwenda nje ambapo alichimba shimo na kuingiza zile nguo pamoja na ule mpira
kwenye shimo, halafu akakata ua aliloelekezwa na kulidumbukiza kwenye lile
shimo, ua lile lilisinyaa gafla hata yeye mwenyewe alishtuka kwakweli maana kile
kitu hakikutegemea kabisa. Basi akatoa zile nguo pamoja na lile ua, kisha
akautupa ule mpira pembeni halafu akaviringisha lile ua kwenye nguo chafu
akapeleka ndani, halafu alivyorudi ndio akamwagilizia mafuta ya taa na kuuchoma
ule mpira huku akipepea moto, na ndio kitendo hicho kilichopeleka upepo kule
makaburini, baada ya hapo ndio akatumbukiza majivu kwenye lile shimo na
kulifukia, ndiomana kule makaburi wale wahusika waligandishwa mpaka watakapo
fukia kaburi. Alipomaliza alirudi ndani, alishangaa watoto wake wale
wakirudi kwa kasi ya ajabu nyumbani, kila mtu alirudi kivyake ambapo
walitangulia wale mapacha, kisha Sara na Ana walikuwa wanahema juu juu, ikabidi
aulize kwa makini, “Kwani imekuwaje tena?” “Maajabu yametokea
makaburini baba” Sara alimjibu baba yao, Yule baba nae aliuliza kwa
mshangao, “Nini tena?” “Kuna binti mmoja hivi sijui katokea wapi
alikuwa anataka kumuangalia Moza mara ya mwisho wakamkatalia, sasa Moza
alipotumbukizwa kaburini Yule mtoto nae alitumbukia. Sasa muda huohuo huyo mtoto
alikauka gafla kama mtu aliyeungua, sasa mama yake akawa analia wamtoe mwanae.
Walivyomtoa na kupanda kwenye gari kwenda hospitali, muda huo huo kwenye shimo
nako hakionekana maiti ya Moza wala nini, mara upepo mkali wenye mavumbi ukaanza
kuvuma kwakweli kila mtu pale kaburini alikimbia na njia yake. Ni maajabu
makubwa kakweli.” “Kheee ni maajabu sana, sasa mama yenu yuko
wapi?” “Atakuwa anakuja tu maana kila mtu alikimbia pale kaburini hakuna
aliyebaki hata mmoja” “Makubwa haya jamani” Ila Ana akadakia na
kumuuliza baba yake, “Kwanini wewe hukwenda? Hukutaka kumzika
Moza?” “Hapana mwanangu, niliteguka mguu” “Sasa huo mguu saivi
umeacha?” “Saivi afadhali” “Mmh nitajua tu” “Utajua
nini?” Ana akawa kimya hakuwajibu tena, ila kila mtu alikuwa na maswali
kwa kile alichokisema Ana kuwa kama kina ukweli ni mambo gani yanaendelea huku
Patrick akiwa na mashaka kuwa inawezekana Ana ametambua alichokifanya na
inawezekana aliyoyafanya ndio yamesababisha yote hayo ila akajisemea moyoni ni
amri alipewa kwahiyo hakuwa na namna. Kwenye gari ambalo Neema
alikuwa amepanda na mtoto wake Salome huku akimpeleka hospitali, machozi
yalikuwa yanamtoka mfululizo kwani aliamini kuwa mwanae alikuwa amekufa
ukizingatia alikuwa amekauka kabisa kama aliyepigwa na shoti ya umeme. Kijana
aliyewabeba kwenye gari alikuwa anaendesha haraka haraka ili awahi hospitali
kwani hata yeye alipatwa na huruma kwa mtoto Yule ila walipokuwa wanakaribia
hospitali, ikawa kama miujiza kwani Salome aliamka gafla na kumfanya mama yake
hata machozi yamkatike, kwani alipoamka tu alimwambia mama
yake, “Msinipeleke hospitali tafadhali, nirudisheni
nyumbani” Mama yake alimuangalia kwa kustaajabu sana, “Ila
mwanangu tunatakiwa tukupime kwanza” “Nirudisheni nyumbani, sitaki
kwenda hospitali. Huko mkinipeleka nitakufa” Hata Yule dereva alipatwa
na mshangao tu, Neema alimuangalia dereva na kuanza kumuelekeza ili waende
nyumbani. Kwahiyo safari ilibadilika haikuwa ya hospitali tena bali
safari ya nyumbani, kwakweli Neema alikuwa anamuangalia mwanae bila ya kummaliza
kwani alimuona kama amebadilika hivi. Mpaka wanafika nyumbani na
kushuka, WAkati wanashuka, Salome alimwambia mama
yake, “”Tafadhali usimwambie yeyote
kilichonipata” “Kwanini?” “Sitaki wajue mama wataniogopa,
tafadhali usimwambie yeyote” “Nakuahidi sitamwambia yeyote mwanangu,
uzima wako ndio furaha yangu” “Niahidi tena mama kuwa hutomwambia
yeyote” “Nakuahidi kweli mwanangu, hakuna yeyote
nitakayemwambia” Salome alionekana akishangaa shangaa tu mazingira ya
pale kwao, mpaka mama yake akamuuliza, “Mbona unashangaa hivyo
Salome?” “Naona kumebadilika” “Hapana hakujabadilika, ni huku
huku ndio nyumbani kwetu” Waliingia ndani na Ashura ndio alikuwepo
nyumbani na wale mapacha wadogo zake Salome, ila Salome alipomuona Ashura
alimwambia, “Khee Ashura bado upo huku?” Mama yake alishangaa na
kumwambia kwa mshangao, “Kheee wee Salome, toka lini mama yako mdogo
umemuita kwa jina lake? Adabu ya wapi hiyo? Halafu unamuuliza bado upo huku,
ulifikiri mamako mdogo atakuwa wapi! Yani usingekuwa umepatwa na matatizo leo
ningekupiga sana” “Nisamehe mama” Ikabidi Ashura nae
aulize, “Matatizo, kwani amepatwa na matatizo gani?” “Mwenzangu
makubwa” “Yapi hayo?” Salome akamuangalia mama yake na
kumwambia, “Kumbuka umeniahidi mama” “Naelewa
mwanangu” Sasa Ashura akabaki na bumbuwazi na kuzidi kuuliza kulikoni
imekuwaje kuwaje, “Aaah si huyu Salome, kagombana na wenzie shuleni huko
ndio leo niliitwa shuleni kwao” “Kheee kwahiyo muda ule mnaondoka hapa
ilikuwa mnaenda shuleni kwakina Salome? Imekuwaje leo kwenye kesi zake
amekuchukua wewe badala ya kunichukua mimi?” “Anaelewa makosa yake,
tuachane na hizo habari mdogo wangu. Hebu tufikirie leo tutakula
nini?” “Tumuulize huyo mpenda ugomvi, leo anataka kula
nini?” “Nataka ugali, mlenda wa kuchanganywa na ngoga na
samaki” Neema na Ashura wote waliangaliana na kumuuliza Salome kwa
mshangao tena kwa pamoja, “Wewe ngoga unaijua?” “Ndio, si ndio
nyanyachungu” “Toka lini ukala ugali Salome? Mpenda wali wewe, leo hii
unataka ugali makubwa!” “Tena ugali na ngoga, mbona makubwa haya ya leo
dada” “Makubwa haswaaa, huyu Salome wangu wa leo ni
kiboko” Salome akainuka na kwenda chumbani, ambapo alifika na
kujilaza. Baada ya muda mama yake akawa anamtafuta, “Salome
kaenda wapi jamani?” “Ila sijamuona akitoka” Mara wakaja wale
mapacha wawili na kumwambia mama yao, “Kalala chumbani
kwetu” “Kheee kalala chumbani kwenu, hivi Salome mzima akili yake kweli
leo? Ameshasahau kama analalaga na mamake mdogo” Neema akainuka na
kwenda kumuasha Salome, alipoamka alikaa nae na kuzungumza nae “Hivi
Salome umeanzaje kuja kulala huku? Tuseme hujui chumba unacholala au? Hujui kama
unalala na mamako mdogo wewe? Halafu hata kuoga hujaoga, hivi yale mambo
yaliyotokea unaona ni madogo yale mwanangu? Naomba uinuke ukaoge halafu kama
kulala ukalale chumbani kwenu” “Mama naomba unisaidie
kitu” “Kitu gani hicho?” “naomba msaada wako ila usimshirikishe
mtu yeyote” “Wewe niambie tu, simwambii mtu mwanangu” “Kwakifupi
mama kuna vitu mimi nimesahau, vitu vingine naomba unipe
maelekezo” “Sasa mwanangu, lile tukio halikuwa la kawaida ndiomana
nikakwambia twende hospitali wakakucheki” “Mama nitakuwa sawa tu, naomba
vitu vingine unielekezage na usimwambie mtu yeyote. Lile tukio lililonitokea
mimi kweli halikuwa la kawaida na limehusika haswa na mambo ya kishirikina
ndiomana sitaki unipeleke hospitali maana huko utanipoteza kabisa, je upo tayari
mwanao nife?” “Sipo tayari mwanangu, nitaumia sana” “Basi naomba
iwe siri yako, mtu yeyote asijue, hata mabadiliko yangu asijue mtu yeyote. Wewe
ndio mama yangu nakutegemea, naomba unielekezage tu cha kufanya” “Haya
niambie unataka nikuelekeze nini” “Nielekeze chumba ninacholalaga,
nielekeze nguo zangu za kuvaa, nielekeze choo chetu kilipo nikaoge” “Mmh
mwanangu inamaana vyote hivyo umesahau? Mbona unanitisha?” “Usiogope
mama yangu, nifanyie hivyo tu” Neema aliinuka na kuanza kumuelekeza
mwanae, ambapo aliporudi sebleni na kumuacha Salome anaoga ndipo Ashura nae
akauliza, “Imekuwaje tena, mbona Salome kama haeleweki
hivi!” “Achana nae, akili yake inawaza kupigana tu hapo” Ashura
akawa kimya ila alihisi kuna kitu cha tofauti kimempata Salome ingawa hakujua ni
kitu gani. Nyumbani kwa mr.Patrick, napo usiku ulifika bila ya
Rose kurudi nyumbani ikabidi Patrick awaulize tena watoto wake, “Jamani
mna uhakika mama yenu alikuwa anakuja na yeye?” Sara
alijibu, “kwakweli baba hatujui maana pale kila mtu alikimbia na
lwake” “Kwahiyo hata hamna wasiwasi na mama yenu?” “Atarudi tu
baba, mama ni mtu anayejielewa na uhakika atarudi” “Hivi na huyo binti
ambaye alianguka kwenye kburi la Moza mnajua hali yake?” “Kwakweli
hakuna aliyefatilia, hata sijui anaendeleaje na hatumjui kwakweli hata watu pale
makaburini walisema hawamjui zaidi ya huyo aliyekuwa akilia na kudai ni mama
yake” Ni kweli hawakumtambua Salome kwani ilikuwa ni kitendo cha muda
mfupi sana lakini bado mr.Patrick alijikuta akitaka kujua mengi kuhusu huyo
binti, nab ado jibu lilikuwa vile vile hatujui. “Sawa nimekubali, huyo
binti sio ndugu yenu ndiomana hamjamfatilia. Haya mama yenu nae haonekani
nyumbani. Kumfatilia nae inakuwaje?” “Mmmh baba jamnai, kwahiyo
tukashatki polisi kuwa mama haonekani?” “Sio hivyo, ila ningeomba
mnipeleke huko makaburini nikamtafute mke wangu” “Hivi atakayekupeleka
makaburini muda huu ni nani? Ukizingatia tumetoka kumzika mtu wa maajabu,
kwakweli baba hapana. Kwanza kwenda makaburini usiku ni nuksi” Patrick
aliinuka na kwenda chumbani, kwa upande mwingine aliona ni afadhali mkewe hayupo
muda huo ila kwa upande mwingine alimkumbuka kwani alishamzoea maana tayari ni
mke wake na alikuwa akiishi nae, kwa muda huo aliamua kulala tu. Kwa
upande wa watoto, Rose aliwaomba wenzie wakae sebelni kwa siku hiyo kwani
aliogopa kulala peke yake, ila Kulwa akatoa wazo, “Si uende ukalale na
Ana” Doto akasema, “Mmmh na Ana atakubali kweli?” “Ndio
hapo sasa Doto, hebu nitetee na wewe. Hivi Ana atakubali kweli kulala na
mimi?” “Hebu nenda kwanza tuone” Sara aliinuka na kwenda
chumbani kwa Ana ambapo alimkuta ameshalala, hivyo alirudi na kuwaaga kaka zake
halafu akaenda chumbani kwa Ana na kulala pembeni yake kimya
kimya. Kwa upande wa Rose sass, akili yake ilikuwa haisomi
ramani kabisa kwa wakati huo alijikuta anaendesha gari hovyo hovyo ili awahi kwa
Yule mganga, njiani kwasababu ya haraka zake alizokuwa nazo akagonga mtu ila
hakutaka kusimamisha kwani alijua angesimamisha wananchi wangemsongasonga
hivyobasi akaendelea mbele huku watu wakimpigia kelele ila yeye aliongeza
mwendo, na kuenda moja kwa moja gereji. Lengo lake alitaka kubadilisha
gari ili watu wasimjue kuwa ni yeye aliyegonga, kwavile mwenye gereji hiyo
alimzoea Rose na alimjua kwa pesa zake, akampa gari nyingine bila kinyongo kisha
Rose akamuachia ile gari yake bila ya kumwambia kuwa aligonga. Rose
akaendelea na safari ya kwenda kwa Yule babu na hatimaye akafika, alikuta
wagonjwa wengi tu wakimsubiri. Mke wa Yule babu akamsogelea Rose na
kumwambia, “Yani leo yupo busy kweli na kazi yako, yani hata saivi
ameenda kufata dawa kwaajili ya kazi yako maana kashaonyeshwa kuwa mambo
yameharibika huko” “Ni kweli mambo yameharibika yani nimechanganyikiwa
hapa, sijui itakuwaje” “Hata usijali, hakuna kitu ambacho babu
anashindwa. Nina uhakika mambo yote yataenda sawa kama
inavyotakiwa” Basi walikaa muda mrefu sana bila ya babu kurejea hadi
giza liliingia ila babu hakurejea hata mkewe akapata mashaka kuwa babu amekumbwa
na maswahibu gani. Kwenye mida ya saa nne usiku, walifika vijana pale
nyumbani kwa babu na kutoa taarifa iliyowashtua wengi sana, “Babu,
kapata ajali. Akiwa njiani, kagongwa na gari na kufa papohapo sababu ya
kucheleweshwa hospitali kwa matibabu” Kwakweli taarifa hii iliraluwa
moyo wa Rose, na kujikuta akichanganyikiwa sana, na alipouliza zaidi kuhusu gari
iliyomgonga wale vijana walimtajia na hapo hapo akagundua kuwa ndio ile gari
yake, Rose akaanguka na kuzimia. Kwakweli taarifa hii
iliraluwa moyo wa Rose, na kujikuta akichanganyikiwa sana, na alipouliza zaidi
kuhusu gari iliyomgonga wale vijana walimtajia na hapo hapo akagundua kuwa ndio
ile gari yake, Rose akaanguka na kuzimia. Ikabidi waanze kumpepea pale,
yani mke wa babu alichanganyikiwa na taarifa ile ila akajua Rose imdmchanganya
kutokana na mambo yanayomsibu. Rose alipepewa pale hadi akazinduka na aliona
watu wanaanza kusogea nyumbani pale, kwakweli Rose alijiona kama yupo ndotoni
kwani kila kitu kilitokea kwake bila ya matarajio, akamuita tena Yule kijana
aliyeleta taarifa mwanzoni ili amuulize vizuri maana alihisi kama sio kweli
vile, “Hebu niambie vizuri ilikuwaje?” “Yani mimi nilikuwepo
kabisa eneo la tukio, babu alikuwa anavuka barabara mara ikatokea gari sijui
mwenye gari alikuwa amelewa Yule yani alimgonga babu na kuondoka, tulijaribu
kumpigia kelele ili asimamishe hakufanya hivyo. Pale tulipokuwepo ni mbali na
hospitali, na msaada ulipatikana badae kabisa tena tulimpeleka babu na baskeli
mpaka hospitali na kufika alikata roho hapo hapo, daktari akasema ni kwavile
tumemchelewesha” Hapo ndio Rose akaelewa kabisa kuwa hiyo ajali
ameisababisha yeye na kumfanya achanganyikiwe zaidi ila akaogopa kuropoka kuwa
amesababisha ajali klwani alijua angezua mengine makubwa zaidi. Akawaza kimoyo
moyo, “Sijui hata nifanyeje? Sina la kufanya kwakweli ngoja tu nisubirie
pakuche halafu nitajua cha kufanya” Alikuwa na mawazo mengi
sana. Kwakweli leo Sara ilikuwa ni mara yake ya kwanza kulala
pamoja na mdogo wake Ana, kwahiyo siku zote huwa hajui kinachoendelea kwa Ana.
Usingizi kwa upande wa Sara kwa siku ya leo ulikuwa ni wa mang’amung’amu sana
kwani bado taswira ya makaburini ilimjia kichwani, akiwa kwenye usingizi wa
kuvizia akamuona Ana akinyanyuka kitandani lakini alihisi kuwa Ana anaenda
chooni kujisaidia. Ila Ana huyu alienda moja kwa moja dirishani na kutokea
kwenye dirisha, kitendo hiko kilimshtua sana Sara na kumuogopesha, akajikuta
akitazama pale ambapo Ana alilala mwanzoni. Kwakweli alistaajabu zaidi kwani
alimuona Ana akiwa bado amelala hajitambui, jasho la uoga lilianza kumtoka Sara,
ni kweli Ana ni mdogo wake ila matendo ya namna hii hajawahi kuyashuhudia
kabisa. Sara alikuwa anaogopa hadi alianza kutetemeka kwa uoga, aliinuka haraka
haraka na kukimbilia nje ya chumba huku akipiga kelele ambapo kaka zake walitoka
na kumuuliza kuna nini, lakini bado alikuwa akilia kwa kelele nyingi, hadi kaka
zake wakamshtua na kumuuliza kwa makini, “Sara, Sara una nini
wewe?” Mara gafla akaja na Ana, kwakweli Sara ndio alizidi
kuchanganyikiwa baada ya kumuona Ana na alikuwa akimnyooshea
kidole, “Sasa mbona unamnyooshea kidole Ana kafanyaje?” “Ana
ni……” Kabla hajamaliza sentensi yake, Ana alimuangalia kwa jicho kali
sana dada yake na kumfanya dada yake azimie pale, wale mapacha wakamuangalia Ana
na kumuuliza. “Kwani kapatwa na mimi?” “Jamani mi nitajuaje
sasa!” “Utajuaje kivipi wakati ulilala nae!” “Nililala nae?
Alilala na mimi muda gani?” “Mbona alikuja kulala na wewe” “Mi
hata sijui kama alilala na mimi, kwanza ndio ustaarabu wa wapi unaenda kulala na
mtu hata umwambii ili akukubalie au akukatalie. Hata sijui kilichompata kwani na
mimi nilikuwa nimelala” Ilibidi wamuinue na kwenda nae sebleni ambapo
waliendelea kumpepea ili azinduke huku wakitumaini kuwa akizinduka atawaeleza
jambo. Mara Ana akawaambia, “Mnajisumbua tu kumpepea huyo,
nendeni kamlazeni kitandani kwake halafu asubuhi akiamka ndio mtaongea
nae” Walimpepea pale bila ya mafanikio ikabidi wachukue wazo la Ana,
wakambeba Sara na kumpeleka chumbani kwake kumlaza kisha na wao wakarudi
chumbani kwao. Kulipokucha asubuhi, hwa mapacha kabla
hawajafanya lolote walienda kwanza kumuangalia dada yao ambapo walimuamsha ni
kweli aliamka, ila walichomuuliza chochote hakuwajibu ndipo walipogundua kuwa
dada yao amepoteza uwezo wa kuongea. “Sara, kuongea
huwezi?” Alitingisha tu kichwa, kwa kifupi Sara hakuweza kusema
chochote, walitoka na dada yao hadi sebleni wakijitahidi kumsaidi ya hapa na
pale, Mr.Patrick alikuja na kushangaa huku akiuliza imekuwaje, “Inamaana
baba hujasikia makelele ya usiku wakati dada Sara analia?” “Sijasikia
chochote wanangu, yani leo nilijikuta nimelala hoi kabisa yani hoi sikujitambua
mpaka kumekucha kwahiyo hakuna nilichosikia” Basi wakamueleza
kinagaubaga kilichotokea hata yeye alibakia anastaajabu tu kwani bado ukweli
alikuwa nao Sara pekee ila kusema tu ndio alikuwa hawezi kwani aliondolewa uwezo
wa kusema. Ana alitoka na kuwaaga kuwa anaenda shule, Patrick akamuuliza
Ana, “Kwahiyo huna hata mashaka na mama yako hajarudi hadi leo, na vipi
dada yako aliyepatwa na ugonjwa wa gafla haongei. Hivi unapata wapi nguvu za
kwenda shuleni Ana?” “Elimu ndio ufunguo wa maisha, kama nyie mlikimbia
shule shauri zenu ila mimi acha nisome kwa raha zangu” “Laiti kama
kusoma kungekuwa unavyosoma wewe basi walimu wote Tanzania wangeacha
kazi” “Unanikosea heshima baba” “Naomba unisamehe, haya nenda
shule mwanangu” Ana aliondoka zake ila inaonyesha alikuwa amekasirika
vilivyo. Kulwa alimuangalia baba yao na kumuuliza, “Baba unafahamu nini
kuhusu Ana?” “Ni mengi tu nayafahamu, huyu mtoto mbaya sana. Ndiye
anafanyaga nilale kama mzigo” “Hebu tueleweshe baba” Mara Ana
akarudi ndani, kisha akamuangalia baba yao na kusema, “Nimeghairi kwenda
shule” Wote walimtazama Ana kwani ni maamuzi ya gafla ameyafanya, ila
hawakumuuliza tena wala hawakuendelea kumuuliza baba yao mabaya ya Ana kwani ni
wazi asingeweza kuwaeleza wakati Ana yuko pale. Kulikucha sasa
nyumbani kwakina Salome pia ila leo Salome aligoma kwenda shule, “Kheee
makubwa, mwanangu leo kwenda shule hutaki?” “Siendi mama, ila ungeenda
kuniomnbea nipumzike kwa muda najiona siko sawa, kwakweli siwezi kwenda shule
kwasasa” Ashura nae akaingilia kati, “Dada, kama hataki kwenda
shule achana nae. Sio lazima shule, mwache azulule zulule akipata mimba ndio
ataelewa” “Kheee Ashura ndio maneno gani hayo kwa mwanangu, badala
umbembeleze na wewe ndio unamkandamiza” “Namkandamiza kitu gani, kwanza
mtu mwenyewe vitu vingine anaongea hata haeleweki kama sio msomi na ndiomana
jana sijampikia hizo nyanyachungu zake” “Kwanini?” “Atasemaje
tumpikie ngoga eti ndio nyanyachungu wakati zinaitwa ngogwe” “Aaah kumbe
ndio zinaitwa hivyo” “Wewe hukujua kama amekupiga changa la macho huyu
tujue anajua Kiswahili kumbe hajui lolote, eti nipikieni ugali, samaki na ngoga.
Katafute hiyo ngoga kama utaipata, hata sijui kaongea kilugha cha
wapi” “Ila Ashura ni swala tu la kumuelekeza mtoto kuwa sio ngoga ni
ngogwe, huyu bado mtoto anajifunza vitu. Ni kumuelekeza tu, mi mwenyewe mtu
mzima sijui sembuse huyu mtoto jamani mmh!” “Kuwa makini na mtoto wako
dada, kuwa naye makini sana” Ashura alitoka muda huo na kusema kuwa
anawahi sokoni ili akanunue vitu, kwahiyo Neema alimuongeza na hela
kidogo. Nyumbani akabaki Salome na mama yake, ila leo Salome alimuuliza
mama yake swali ambalo mama yake hajawahi kutegemea kama angeulizwa na
Salome. “Mama, hivi wewe na Ashura undugu wenu uko
vipi?” “Halafu nishakwambia kuwa na adabu, Yule ni mamako mdogo ni mdogo
wangu. Usimwitage Ashura” “Nisamehe kwa hilo mama, ila ningependa kujua
huyu mamdogo na wewe ni mdogo wako kivipi? Na ndugu zako wengine wako wapi
sijawahi kuwaona?” “Mmmh Salome jamani, si mwezi uliopita tu
nilikupeleka kwa kaka yangu, tuseme ushasahau!” “Haya mama, tuachane na
hayo ila huyu mamdogo ni ndugu yako kivipi kuna jambo nataka nikueleze niambie
kwanza undugu wenu ndio nikueleze” “Sikia, mimi baba yangu na mama yangu
walikuwa hawaishi pamoja na kwa upande wa mama na baba, mimi ni mtoto wao wa
pekee sana ila kumbe baba alikuwa na mtoto mwingine ila sio mtoto aliyezaa na
mkewe waliyokuwa wanaishi nae. Mimi kwa mama tumezaliwa wawili tu, yani mimi na
kaka yangu niliyekupeleka kwake mwezi uliopita. Hatuna mazoea ya karibu sababu
Yule kaka alikulia nyumbani kwa baba yake. Ila mama ndio alinitambulisha kama ni
kaka yangu. Sasa kwa upande wa Ashura ni mtoto wa baba kumbe naye alikuwa
analelewa na mama yake, yeye ndio alinitafuta mimi kwakweli alipojitambulisha
nilifurahi sana kwani nilipata ndugu hadi leo niko nae.” “Mmmh kwahiyo
ulimpeleka kwa baba yako akutambulishe?” “Baba alishakufa kitambo sana,
na laiti kama angekuwa hai basi ningempeleka” “Na huyo mke wa babu si
yupo, kwanini usimpeleke akutambulishe” “Sasa huyo atakuwa anajua
vinini, kwanza wanitambulishe nini wakati mtu alishajitambulisha na tunaishia
nae hadi leo” “Je shangazi zenu na baba zenu wakubwa au wadogo
mnawatembeleaga” “Wapo kijijini, kwakweli hatujawahi kupanga safari ya
kuwatembelea. Inatia uvivu ujue halafu hatujawazoea” “Mmmh na kaburi la
baba yenu je mmewahi kwenda kulitembelea?” “Tunapangaga kufanya hivyo
ila hata sijui inatokeaga nini, tunajikuta hatujaenda” “Mama, ngoja
nikwambie kitu. Huyu unayemuita mdogo wako si ndugu yako” “Salome, si
ndugu yangu kivipi?” “Wewe nielewe tu mama ila si ndugu yako na kama
hujui shauri zako, atakapokufanyia kitu kibaya ndio utashtuka. Na angekuwa
amekufanyia kitu kibaya mud asana, ila wewe unalindwa na mzimu wa baba yako.
Huna kosa na wala hustahili kufanyiwa mambo mabaya, ila kwa kifupi huyu si ndugu
yako, Tafakari, maswali niliyokuuliza na majibu uliyonipa halafu chukua
hatua” Salome aliinuka na kwenda kuoga, muda huu Neema alibaki kwenye
lindi la mawazo kwani hajawahi kufikiria hata mara moja kuwa Ashura anaweza
akawa si ndugu yake, “Jamani huyu Salome mbona ananitisha, halafu yeye
kajuaje kama huyu si ndugu yangu? Hivi inawezekana kweli nimeishi siku zote na
mtu asiye ndugu yangu huku nikiamini ni ndugu yangu! Haiwezekani
jamani” Neema aliwaza sana bila ya kupata jibu la aina yoyote ile,
ingawa kuna mashaka aliyapata kwa jinsi alivyoambiwa na
Salome. Akajikuta akimsubiria kwa hamu Ashura atakaporudi ili amuulize
baadhi ya maswali, “Lakini hata hivyo, kama ni kweli si ndugu yangu ni
kwanini amenidanganya? Hivi inawezekana kweli! Hapana nahisi Salome
kachanganyikiwa tu” Muda kidogo Ashura nae alirudi, na Neema alijikuta
akimuuliza, “Hivi Yule mke aliyekuwa anaishi na baba ulikuwa
unamfahamu?” “Aah ndio, hapana hata sikumbuki” “Mbona
sijakuelewa hapo, ulikuwa unamfahamu au la” “Nilikuwa mdogo sana, hata
sikumbuki kama namfahamu au la” “Basi tupange siku
tukamsalimie” “Mmmh umekumbuka kitu gani?” “Nimemkumbuka tu
basi, najua atafurahi sana” “Sawa tutapanga” Ila Ashura
alionekana kukosa furaha tangu Neema amuulize kuhusu mke wa baba
yao. Rose alikuwa kwenye wakati mgumu sana na siku hii hakuweza
kuendelea kuwepo tena pale msibani, aliamua kuwaaga kuwa anaenda kwanza nyumbani
kwake halafu atarudi tena. Kiukweli alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa hivi,
alijiona kama ameonewa kwa wakati huo. Mke wa babu alimfata Rose wakati anataka
kuondoka, “Jamani, kweli unataka kutuacha wenyewe kweli kwenye wakati
mgumu kama huu” “Hapana bibi, hujui tu jinsi msiba huu ulivyonichanganya
hapa, nakosa hata uelekeo. Nina matatizo mzigo hata sijui naanzia wapi na
kuishia wapi” “Naelewa kama una matatizo ila tafadhali usiondoke hadi
tutakapozika” “Kwani mazishi ni lini?” “Ni leo, halafu kesho
utaondoka. Tafadhali sana naomba usiondoke” Rose akajifikiria ila
ikabidi apige simu nyumbani kwake kwani alijua ni wazi watakuwa na wasiwasi, na
alimpigia simu Sara kwani anajuaga ndio kiherehere wa wasiwasi ila simu ya Sara
iliita mara nyingi bila kupokelewa ikabidi ampigie simu mume
wake, “Mbona Sara hapokei simu, au kaenda kazini leo?” “Hapana,
Sara yupo ndani ila hawezi kuongea” “Hawezi kuongea
kivipi?” “Sijui nikuelezeaje ila uwezo wa kuongea wa Sara umekatika
gafla” “kheee jamani, mambo gani hayo? Ngoja nirudi le
oleo” Rose akakata simu kisha akaenda tena kwa mke wa babu na kumpa
taarifa za nyumbani kwake huku akimueleza kuwa anapaswa aende maana mwanae ni
mgonjwa. Yule bibi hakuwa na namna nyingine zaidi ya kumruhusu tu. Rose
akapanda gari na kuondoka zake, alikuwa na mawazo mengi sana kushinda yale
mawazo ya kwanza maana aliona kama matatizo yanamzidia ingawa kiuhalisia yeye
ndiye chanzo cha matatizo yote. Wakati anaendesha gari akasikia
sauti, “Rose, umenigonga nimekufa halafu kwenye maizshi yangu
unakimbia!” Rose alishtuka na kusimamisha gari kwa haraka huku akiwa
amejawa na hofu iliyomfanya ashindwe hata kutazama nyuma ya gari kuwa hiyo sauti
inatoka wapi. Akiwa amejawa na hofu zaidi, ile sauti ikajirudia tena, na
kumfanya Rose ashuke kabisa kwenye gari ile, alipokuwa chini akatazama kwenye
kioo cha gari gafla alimuona kama Yule babu yupo ndani ya lile
gari. Wakati anaendesha gari akasikia
sauti, “Rose, umenigonga nimekufa halafu kwenye maizishi yangu
unakimbia!” Rose alishtuka na kusimamisha gari kwa haraka huku akiwa
amejawa na hofu iliyomfanya ashindwe hata kutazama nyuma ya gari kuwa hiyo sauti
inatoka wapi. Akiwa amejawa na hofu zaidi, ile sauti ikajirudia tena, na
kumfanya Rose ashuke kabisa kwenye gari ile, alipokuwa chini akatazama kwenye
kioo cha gari gafla alimuona kama Yule babu yupo ndani ya lile
gari. Uoga ulizidi kumshika Rose na kujikuta akiacha gari kisha kuanza
kukimbia hovyo, alikimbia sana hadi akachoka kwakweli. Alifika kwenye mti mmoja
na kukaa chini yake huku akiwaza kuwa alikuwa anaota au ni vipi maana yale mambo
yalikuwa kama ndoto. “Hivi ni kweli au naota? Lakini mimi uoga umeanza
lini kwangu? Hivi mi naweza kuwa na uoga wa namna hii kweli? Ningeweza kuwafuga
wale wajinga wangu? Hapana kwakweli, mimi ndio mimi uoga kwangu ni
mwiko” Akainuka na kuanza safari ya kurudi kwenye gari yake ila
aligundua kuwa ni mbali sana ameiacha hiyo gari. Alitembea kwa umbali
mrefu sana hadi kuifikia, alivyofika alikuwa amechoka vilivyo, akafungua na
kuingia ndani ya gari yani ingawa milango ya gari hakufunga na funguo ila
ilionyesha wazi hakuna mtu aliyeingia kwenye gari ile kwani kila kitu alikuta
kama kilivyo. Aliendesha gari na kwenda moja kwa moja hotelini, hakutaka kwenda
nyumbani kwake kwanza kwahiyo aliamua kwa wakati huo akalale hotelini
kwanza. Kwa upande wa nyumbani kwa Neema, ilipofika usiku
Salome aligoma kwenda kulala na mamake mdogo Ashura, kitendo hiko kilimshangaza
sana Neema kwani kwake ilikuwa ni ajabu, “Kwahiyo, Salome unataka
ukalale wapi?” “Nataka leo nikalale na wewe mama” “Una nini
lakini Salome jamani?’ “Sina chochote mama ila nataka nikalale na
wewe” Neema hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali tu vile alivyoambiwa na
mtoto wake ila Ashura nae kwakweli alimshangaa sana Salome ila hakusema
chochote. Muda wa kulala ulipofika, moja kwa moja Salome alikwenda na
mama yake chumbani ila walipotaka tu kulala, Salome akaanza kumwambia vitu Neema
vilivyomshangaza sana, tena muda mwingine akamuuliza maswali ambayo Neema
hakufikiria kama kuna siku Salome atamuuliza maswali ya namna
hiyo, “Mama, baba yangu yuko wapi?” “Mmmh Salome, ndio maswali
gani hayo?” “Kila mtu kwenye ulimwengu huu ana baba yake, mimi je baba
yangu yuko wapi?” “Jamani, Sa lome kwanini kutaka kunikumbushia machungu
yaliyopita? Wewe ni mwanamke pia, ukikua vizuri utatambua nazungumzia
nini” “Mama, mimi ni mkubwa tayari au unataka nikue mara ngapi? Nataka
kujua baba yangu alipo” “Baba yako alishakufa” ‘Si kweli
mama” “Sasa ukweli ni upi? Baba yako alishakufa, wewe huna
baba” “Sawa, baba yangu alishakufa. Je baba wa hawa wadogo zangu je nae
alikufa? Maana nae sijawahi kumuona na wote tunatumia majina ya
babu!” “Salome, tafadhali niache nilale, wala sitaki maswali
zaidi” Neema aliona maswali ya Salome yanamchanganya kichwa tu, ila
Salome hakuendelea na maswali zaidi halafu akajifanya muda huo huo amelala ila
kumbe alikuwa kijicho kimoja akimchungulia mama yake kila alichofanya kwa muda
huo, kwani Neema nae hakulala tena maswali ya Salome yalimkumbusha mbali sana
hivyo hakuyataka tena, Ila kabla hajalala aliinuka pale kitandani na kupekua
vitu kwenye kabiti lake, kuna kitu alikitoa kilikuwa kama daftari dogo,
akakiangalia sana kisha akakirudisha na kurudi kitandani halafu akalala
sasa. Salome akainuka pia na kwenda pale alipokuwa anapekua Neema,
akapata kile kitu kumbe ilikuwa ni kadi ya kliniki ya miaka ya nyuma, iliandikwa
jina la mtoto Maria Patrick. Alitazama vizuri ile kadi kisha akairudisha na
kwenda kulala pia. Leo usiku ilikuwa sokomoko pia nyumbani kwa
Patrick kwani bado Sara ilionyesha hataki kulala mwenyewe ingawa kuongea alikuwa
hawezi ila kila walipotaka kumpeleka akalale aliangusha machozi, “Mmmh
hapa kazi ipo, ila Sara mbona mchana ulikubali. Kwanini usiku huu
unakataa?” Sara alizidi kutokwa na machozi hivyo kufanya maamuzi ya
kubaki sebleni ila Ana alitaka kwenda chumbani kulala, “Kheee Ana, wewe
si ndio ulitakiwa kubaki na dada yako hapa!” “Hivi nyie vipi, humuoni
kuwa mimi ni mtoto mdogo. Halafu huyo anagoma kwenda kulala kwa misingi ipi?
Ngoja niende nikalale mie, huyo akilala mkamlaze” “Sasa humuonei huruma
kwani?” “Namuonea huruma ila inabidi nikalale kwanza ndio huruma yangu
ifanye kazi” Ana aliwaacha pale kisha yeye akaenda chumbani kwake
ila Muda huo huo Sara alianguka na kuhisi kuwa amezimia ila
walipomuangalia alikuwa kwenye usingizi mzito sana. Ikabidi wambebe na kwenda
kumlaza chumbani kwake, kisha na wao kwenda chumbani kwao kulala. Ila
Patrick yeye aliamua kukaa sebleni, muda kidogo akafatwa na Ana na
kumwambia, “Nenda kalale” “Mmmh nini tena mpaka unanilazimisha
nikalale Ana!” “Sasa sebleni unabaki kufanya nini?” “Namsubiri
mama yenu” “Harudi leo ni hadi kesho, kwahiyo wewe nenda
kalale” “Hivi kwa mfano nikigoma kwenda itakuwaje?” “Goma
uone” “Mmmh!” Patrick mwenyewe aliinuka kwenye kochi na kuelekea
chumbani kwani hakutaka makubwa ukizingatia huyu mtoto alikuwa na kauli sana
tena kuzidi hata mama yake, kwahiyo Patrick aliona ni vyema atumie busara kuliko
kugombana na huyo mtoto mdogo. Kulipokucha, wale mapacha
walikuwa wa kwanza kutoka sebleni ila harufu ya sebleni iliwashangaza sana yani
ilionekana kama kuna kitu kilikuwa kimechomwa hapo, Doto akamuuliza
mwenzie, “Hivi na wewe hii harufu unaisikia?”: “Ndio nilitaka
kukuuliza na wewe ndugu yangu, ila ni harufu ya nini?” Hawakupata jibu
ila badae wakamkumbuka dada yao ambaye haongei chumbani ikabidi waende kumuamsha
na kumtoa sebleni ila hali yake iliwashtua tena kwani kwasasa dada yao hakuweza
kuongea wala kufumbua macho. “Mmmh kamuamshe baba Doto, tumpeleke huyu
mtu hospitali. Mbona mambo yanazidi kuwa makubwa” Basi Doto akenda
kumuamsha baba yao ambaye nae alishangazwa na hali ya Sara kuzidi kuwa mbaya,
wakakubaliana pale kuwa suluhisho ni kumpeleka hospitali tu hakuna
kingine. Wakati wanajiandaa ili kumpeleka hospitali, Ana nae aliamka na
kwenda sebleni kisha akawauliza, “Mnataka kufanya
nini?” “Tunataka kumpeleka Sara hospitali” “Hakuna
kumpeleka” “Kheee unaongea kwa kujiamini kabisa!” “Ndio
najiamini” “Halafu mtoto, unanyodo wewe. Hebu tupishe huko tumpeleke
Sara hospitali” “Nimesema hamna kumpeleka” “Unaongea hivyo kama
nani?” “Naongea kama Ana, hakuna kumpeleka popote” Kaka zake
walitazamana pamoja na Patrick bila kumuelewa huyu Ana anamaanisha nini au ni
kitu gani anakitaka hadi kusema vile. Ila Patrick akajikuta akiwataadhalisha
wenzie, “Jamani, Ana kashakataa tutulie tu” “Kwani baba, Ana ni
nani kwenye nyumba hii hadi tumuheshimu? Ana sauti gani kwenye nyumba hii? Ni
bado kinda tu huyo, ana ukubwa gani huyu! Anajua matatizo ya mtu huyu? Sara
anaumwa na hakika anajisikia vibaya sana, hospitali ndio suruhisho la pekee kwa
matatizo yaliyompata kwani watachunguza kinywa na macho yake yamepatwa na nini.
Achana na huyu Ana baba, tushirikiane tumpeleke Sara hospiatali” Ana
akacheka, kisha akasema “Kwani Ana ndio nani? Ana sauti gani kwenye
nyumba hii? Nadhani wote mnataka kunua nina sauti gani kwenye nyumba hii na mimi
ni nani. Sasa endeleeni kung’ang’ania kumpeleka hospitali niwaonyeshe kuwa mimi
ni nani” Kaka zake walimuangalia kwa gadhabu sana, kisha wakaanza
kumbeba Sara ili amtoe nje na wakampakize kwenye gari waende hospitali ila gafla
wote walipiga miyeleka na kuanguka chini tena walianguka vibaya sana, halafu cha
kushangaza ni kuwa kila aliyejaribu kuinuka alishindwa na kila aliyejaribu
kuongea alishindwa pia. Wakabaki chini tu wakiugulia maumivu. Ila Ana alikaa na
kuwacheka sana, kisha akaenda kuchukua juisi na kunywa huku akiwaangalia na
kucheka. ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment