Search This Blog

Tuesday 1 November 2022

KICHAA WA MTAA - 4

 






Simulizi : Kichaa Wa Mtaa
Sehemu Ya Nne (4)




Siku iliyofuata mama Mazoea alifika hospital kumuona kichaa Nyogoso, huko akabahatika kukutana na mama Suzani ambaye naye alikua amefika kumjulia hali binti yake. Mama Mazoea alipomuona mama

Mtu wa kwanza kufika hospital alikua mama Mazoea ambapo baada kufika alimpigia simu Dokta Luanda, lakini simu iliita bila kupokelewa. Alijaribu kupiga tena na tena ila mambo yalikua yale yale,simu haikupokelewa. Hasira zilimjaa mama Mazoea, lakini mwishowe alijipa moyo akiamini kwamba huwenda Dokta huyo yupo bize akihudumia wagonjwa. Ila wakati mama Mazoea akiendelea kujipa moyo, punde kando yake alipita Nesi. Mama Mazoea alipomuona alipasa sauti kumuita,naye alitii wito. "Habari yako dada", mama Mazoea alimsalimu Nesi huku akivua miwani aliyovaa.

"Salama tu, sijui wewe", Nesi alijibu.

"Kwangu safi, pole na kazi"

"Aah kawaida dada usijali"

"Mmmh samahani, Dokta Luanda kahudhuria leo?."

"Aah Luanda? Hapana ameachishwa kazi jana. Na muda huu inasemekana yupo mahakamani, anatuhumiwa kupokea rushwa"

"Mungu wangu", mama Mazoea alistuka aliposikia habari hiyo. Akajua dhahili ile pesa aliyompa shilingi laki nane ndio imemponza, na hata asijue kuwa wakati yeye alipompa kiasi hicho cha fedha ili amtibie Nyogoso kwa kwa haraka, nyuma yake alitokea mama Suzani ambaye naye alimpa shilingi millioni tatu na laki nane ili amuuwe Nyogoso.

"Masikini nimemponza mbaba wa watu,sasa ataishije hapa mjini?.", akianza kwa kushusha pumzi, alijilaumu mama Mazoea wakati huo huo akisubiri muda ule wa kuingia kuwaona wagonjwa ufike ili akamuone Nyogoso na ikiwezekana arudi naye nyumbani kwake. Wakati mama Mazoea akivuta subira, punde si punde mama Suzani naye aliwadia akiwa na gari lake la ghalama kuliko gari analo miliki mama Mazoea. Alipofika alitoka ndani ya gari, alichukua simu yake akampigia Dokta Luanda kama alivyofanya mama Mazoea muda mchache uliopita. Lakini simu ya Dokta Luanda iliita tu bila kupokelewa.

"Inamaana Dokta hataki kupokea simu yangu? AU hajatimiza lengo langu? Sasa ngoja, ole wake aanze kunipa bla bla. Atanitambua vizuri", alijisemea mama Suzani huku akiwa na wingi wa hasira baada kuona Dokta Luanda hampokelei simu. Alifunga mlango wa lake kisha akazipiga hatua kadhaa kuliacha gari nyuma,hatua tano mbele alisimama wakati huo huo akarudia tena kumpigia simu Dokta Luanda ila mambo bado yalikua yale yale. Alikereka sana akaongeza kujisemea "Wala siondoki hapa, nasubiri muda wa kuingia kuwaona wagonjwa ufike niingie. Endapo kama nitamkuta bado anapumua, sijui nini kitatokea. Ngoja muda ufike", alipania mama Suzani huku hasira zikimjaa chungunzima, lakini tuamini lake halikuweza kutimia kwa sababu kichaa Nyogoso tayari ameshaondoka hospitalini hapo.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Wakati wakina mama hao wenye jeuri ya fedha walipokua wakisubiri muda wa kuingia kwaona wagonjwa ufike, huku ikiwa kila mmoja anasababu zake za msingi. Upande wa pili, katika makaburi ya Sinza alionekana kichaa Nyogoso akitokea huko. Ilikua yapata saa nane mchana jua la Dar es salaam likiwaka kwa ukali wa hali ya juu. Nyogoso alizipiga hatua kutoka makaburini kwa dhumuni la kuingia mtaani kutafuta kilicho tupwa huku hayo yakiwa ndio maisha yake kulala makaburini pasipo woga. Alitembea huku akiongea peke yake njia nzima, baadhi ya watu waliomfahamu tangu enzi zile alipokua akizoa takataka walitaharuki kumuona Nyogoso akiwa katika hali hiyo, na baadhi yao wasiamini kama kweli yule ndio Nyogoso mzoa takataka.

"Leo ndio nimeamini kwamba kazi ya kuzoa takataka inaweza kuharibu mtindio wa ubongo, tazama yule mzoa takataka kwa sasa anaongea peke yake njia nzima.",alisikika kijana mmoja akimwambia mwenzake aliyekua naye. Maneno hayo aliyaongea baada kumuona kichaa Nyogoso.

"Sio siri hata mimi naamini nina mashaka na hilo lakini siwezi kuwekea maanani, kama unavyojua watu hao wanaasiri ya udokozi kwahiyo inawezekana chanzo cha kuwa katika hali hiyo isitokane na kazi anayo fanya ila ikawa labda aliiba kitu cha watu, mwenye kiti akaamua kumfanyia umafia. Dunia hadaa ulimwengu shujaa bwana ndugu yangu ", mtu wa pili aliongea wakati huo wakimsindikiza kwa macho Kichaa Nyogoso ambaye alionekana kutembea pole pole kuzidi kuingia kwenye mitaa ya Sinza. Na pindi alipokua akiendelea kutembea huku akiwa hana hili wala lile, punde zilisikika sauti zikimuita." Mzoa takataka..kaka mzoa takatakaaaa. wewe mzoa takaaa", sauti hizo za kike ambazo zilitokea kwenye nyumba nzuri zilizozungushiwa uzio ww kuta ngumu, zilipasa kumuita kichaa Nyogoso. Lakini Nyogoso hakujali alizidi kuondoka zake kwa sababu hakujua kama anaitwa yeye jambo ambalo liliwapelekea waliokua wakimuita kukasirika ilihali mmoja wao alisikika akisema "Achana naye huyo, analinga kama vile Sinza yote mzoa takataka yupo pake yake"

"Lakini Mbona anaonekana kama kichaa?..", mtu mwingine alidakia akasema hivyo.

"Wewe umejuaje?.."

"Nimejuaje? Wewe huoni anaongea peke yake?.."

"Khaa, ila yote yawezekana. Kwa maana kazi ya kuzoa takataka yataka moyo kiukweli"

"Hakika wala hujakosea, na kama kweli jamaa kawa kichaa. Basi Mungu amponye kwa sababu huyu mtu hajui kuiba kitu cha mtu". Ni zogo la muda mfupi, zogo la watu wawili kama sio watatu walikua wakizungumza kuhusu kichaa Nyogoso ikiwa yeye ameshatomea zake. Alikwenda mbali zaidi mpaka mitaa ya Manzese, hapo tayari alihisi kiu ya maji. Aliwaza atapata wapi maji ili apoze kiu kali aliyokua nayo, lakini mwishowe alipata jibu. Mbele yake alimuona mama mmoja wa makambo akiuza maji ya kwenye mifuko ya nailoni (Kandolo). Kichaa Nyogoso aliachia tabasamu pana baada kumuona mama huyo, uchangamfu kwa wateja na uso wa busara aliokua nao mama huyo ilimfanya Nyogoso kuamini kuwa ataweza kumsaidia maji ya kukata kiu yake. Haraka sana alimsogelea lakini kabla hajaeleza shida yake, mama huyo muuza maji alipasa sauti yake akamwambia "We kichaa wewe, hebu ondoka. Ondoka kwenye biashara yangu, nyie ndio mnatuletea mikosi watu tunashindwa kuuza biasara zetu. Nasema ondoka hapa mwanahidhaya mkubwa wewe", mama huyo aliongea kwa msisitizo akimfukuza kichaa Nyogoso.

Nyogoso baada kutimuliwa, alisikitika sana. Aliondoka zake huku akisema "Ama kweli sura si roho", hatimaye Nyogoso alirudi majalalani kutafuta kiporo kilicho tupwa ingawa kiu bado alikua nayo, njaa pekee ndio iliyomfanya akazulule majalalani kutafuta chakula. Alitafuta huku na kule, lakini napo hakuona chochote. Alichoka sana aliamua kupumzika kando ya jalalan, na punde si punde usingizi ulimpitia. Alilala fo fo fo, alistuka baada kusikia mtu akija mahali alipolala. Alipofumbua macho yake aliona shehena la ugari na ukoko uliotupwa na mama ntilie. Hakika alifurahi sana, haraka sana aliusogelea ukoko huo na mara moja akaanza kuula kwa pupa kana kwamba alikua na njaa ya wiki nzima. Alipotosheka, shibe ilitanda tumboni mwake akajisemea "Njaa mwanamalegeza, shibe mwanamalevya. Lakini kwa shibe hii siwezi kuelewa bila kupata hata tonya la maji", alipokwisha kujisemea hivyo alicheka kisha akazipiga hatua za polepole kutoka jalalani akaingia mtaani kwa mara nyingine tena. Sasa ilikua yapata jioni saa kumi na moja. Aliingia kwenye moja ya uchochoro uliokua na giza totoro. Katika uchochoro huo alikutana na kundi la wahuni wasiopungua watatu, wahuni hao walikua wakimpokonya fedha yule mama muuza maji. Kichaa Nyogoso alipoona kitendo hicho kinafanyika alisema "Yoyote atakaye chukua fedha ya huyo mama, atanitambua vizuri mimi ni nani. Kwa nini msihangaike pesa kwa nguvu zenu?..", wahuni hao walikua waliposikia sauti hiyo ya kiume iliyounguruma kutoka kwenye koo ya kichaa Nyogoso, waliinua macho yao kutazama kule ilipotokea. Waliogopa kumuona pande la mtu, kichaa Nyogoso. Haraka sana walimuacha mama huyo muuza maji wakatimua mbio.

Mama huyo alimtazama Nyogoso mara mbili mbili, alikumbuka kuwa masaa machache yaliyopita kichaa huyo alimuomba maji akamnyima akaenda mbali kabisa akakumbuka maneno aliyomkana "We kichaa wewe, hebu ondoka. Ondoka kwenye biashara yangu, nyie ndio mnatuletea mikosi watu tunashindwa kuuza biasara zetu. Nasema ondoka hapa mwanahidhaya mkubwa wewe" roho ilimuuma mama huyo, chozi lilimtoka wakati huo kichaa alikua amemkaribia ambapo naye alimtazama kisha akasema "Pole mama kwa mtihani. Mwanahidhaya naenda zangu", aliongea kichaa Nyogoso huku akiambaa na uchochoro huo huku nyuma akimuacha mama muuza maji akimsindikiza kwa macho hata asiamini kama kweli yule aliyemnyima maji ya shilingi hamsini, amemuokoa alipokua akiibiwa zaidi ya pesa hiyo ya maji.

"Aah! Dharau kitu kibaya sana. Mungu nisamehe", akianza kwa kushusha pumzi ndefu mama huyo alijisemea maneno hayo.



Upande mwingine,hospitalini. Mama Mazoea alipagawa baada kutomuona Nyogoso. "Mungu wangu nitamwambia nini Mazoea?..", alijiuliza mama Mazoea wala asiamini anacho kiona. Alijihi kukosa nguvu kwani aliamini kuwa binti yake kamwe hatomuelewa hata amueleze nini. Lakini wakati mama Mazoea yupo kwenye hali hiyo ya sintofahamu, ghafla mama Suzani naye aliingia wodini humo kumuona Nyogoso. Alistuka kumuona mama Mazoea, alishangaa sana. Kwa sauti ya dharau akasema "We mama, mgonjwa aliyekua amelazwa humu yuko wapi?..", mama Mazoea aliposikia sauti hiyo, aliinua uso wake kumtazaka mtu aliyemuuliza swali hilo. Alikutana uso kwa uso na mama Suzani. Sura ya mwanamke huyo haikua ngeni sana machoni mwake, ndipo kwa hasira ya kumkosa Nyogoso mama Mazoea akasema." Hiyo ndio salamu we mjinga?, na kwanini unauliza kwa ubabe kwani mgonjwa wako?.."

"Eti nini? Hahaha hahahahah hahahahah", kwa dharau mama Suzani aliangua kicheko kisha akasema. "Nilikuona unabusara kumbe mjinga tu. Sasa nakupa pole, nadhani tayari maiti ipo monchwari.", mama Mazoea alistuka kusikia maneno hayo, kwa jazba akahoji "Unamaana gani wewe masikini",

Mama Suzani akajibu "Ziba bakuli lako bwege wewe, masikini ni wewe sio mimi. Kwa taarifa yako. Mgonjwa wako alitakiwa kufa, na hatimaye yametimia nilikuja kupata uhakiki tu", maneno hayo mama Suzani aliyaongea kwa kujiamini kabisa wakati huo huo mama Mazoea alichomoa bastola kwenye mkoba wake akamnyooshea mama Suzani kisha akamwambia "Sikia ni kwambie, siku zote malipo ni hapa hapa Duniani. Kwa Mungu ni hukumu tu. Sasa basi lazima na wewe ufe"

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Mama Suzani alistuka sana kuona bastora, alipoa mithili ya maji ya mtungini kisha akasema "Mama tafadhali usifanye hivyo,nakuomba sana", aliongea mama Suzani wakati huo jasho likimtoka mwilini mwake ilihali muda huo mama Mazoea alikua akijishauri kipi cha kufanya kwa mama Suzani, yani amuuwe au amuache. Lakini wakati anajishauri huku akiwa na wingi wa hasira, mara ghafla wodini humo aliingia nesi. Haraka sana mama Mazoea chini mkono wake uliokamata bastora, kisha akatoka ndani ya wodi hiyo kama mtu aliyefumaniwa ugoni. Nesi alitaharuki huku akimsindikiza kwa macho mama Mazoea ambaye alikua akiishi zake. Akiwa bado na sintofahamu aliyarejesha macho yake akamtazama mama Suzani, ambaye naye muda huo alionekana kuchweya mfano wa mtu aliyekoga umande kwenye majira ya baridi. Nje mama Mazoea alipanda gari lake akaondoka huku akiwa amefura hasira, aliamua kurudi nyumbani wakati huo akiwaza atamwambia nini binti yake juu ya kifo cha Nyogo.

Kwingeneko napo, mke na marafiki wa karibu wa Dokta Luanda walianza kuuza mali mbali mbali alizikua akimiliki binafsi Dokta huyo ikiwa nia na madhumuni kumtolea dhamana Luanda ambaye tayari alikua mahabusu. Mchakato huo ulifanyika kwa haraka sana lakini kwa sababu Dokta Luanda hakua na malighafi nyingi, katu kiasi cha fedha kilicho patikana hakikuweza kutosha kwa dhamana. Alijitua Luanda, akajiraumu kwa nini alipokea fedha ile ya mama Suzani. Fedha ambayo ililenga kuupoteza uhai wa kijana asiyekua na hatia. Hakika alijikuta akilia mwenyewe huku majuto yakibaki kuwa mjuu ndani ya nafsi yake wakati huo huo mama Mazoea naye aliwasili nyumbani kwake. Alimkuta Mazoea akiwa amelala, kitendo ambacho kilumstajabisha sana lakini kwa kuwa alifahamu kipi kinacho endelea, aliona hakuna haja ya kumuamsha bali naye akiwa na wingi wa uchovu na mawazo tele aliingia chumbani kwake kulala. Ilikua tayari ni usiku.

Kesho yake palipokucha, asubuhi nzuri kabisa. Anga la Dar es salaam na wilaya zake likionekana kuwa jeupe hasa hasa Wilaya ya Kinondon. Mama Mazoea kabla hajaenda kazini alikwenda chumbani kwa mwanaye ili amsabahi baada jana kushindwa kusalimiana. Aliona asingelithubutu kuondoka pasipo kumuona binti yake kipenzi, hivyo aliusogelea mlango wa chumba cha Mazoea kisha akabisha hodi. Punde Mazoea alifungua mlango huku akiachia tabasamu, ubongo wake ukifikiria kuwa kama yake atakua amemletea majibu mazuri juu ya kijana Nyogoso kipenzi cha moyo wake.

"Habari za asubuhi Mazoea"

"Salama tu mama shkamooo"

"Malakhabaa, naona jana hatukuweza kuonana. Nilikukuta umelala,yani hata sijui mlango wako umebana saa ngapi"

"Jamani mama! Jana nilikungojea sana mwenzio ila nilipoona umechelewa nikaamua kulala zangu"

"Haya bwana! Mimi sina mengi sana ya kuzungumza na wewe. Kwa sababu naona muda umenitupa mkono kwahiyo nimekuja kukuaga tu binti yangu"

"Oooh vizuri mama yangu. Enhee vipi hali ya yule mkaka mzoa takataka?.."

"Mzoa takataka?..", alihoji mama Mazoea huku akianza kwa kushusha pumzi ndefu ilihali akionekana kufikiria jibu la kumpa Mazoea wakati huo huo akiyakumbuka maneno ya mama Suzani

"Ziba bakuli lako bwege wewe, masikini ni wewe sio mimi. Kwa taarifa yako. Mgonjwa wako alitakiwa kufa, na hatimaye yametimia nilikuja kupata uhakiki tu",mama Mazoea aliyakumbuka maneno hayo ambayo yalikua yakijirudia kichwani mwake. Aliumia sana lakini punde si punde aliachia tabasamu kisha akamjibu "Mwanangu siunaona nimependeza hivi? Basi ujue nikitoka kazini nakwenda moja kwa moja hospital kumjulia hali. Na habari njema aliyoniambia Dokta, ni kwamba hali yake sasa inaaanza kutengemaa", jibu hilo lilimfurahisha sana Mazoea, tabasamu bashasha lilionekana usoni mwake, hima alimkumbatia mama yake kisha akamwambia "Nakupenda sana mama yangu, nakuombea dua kwa Mungu azidi kukupa maisha marefu na yenye baraka tele", Aliongea maneno hayo Mazoea kwa hisia kubwa kutoka moyoni. Lakini wakati anasema maneno hayo akimwambia mama yake, mama yake naye ndani ya nafsi yake alikua akijisemea "Sijui mwanangu nini na mzoa takataka mpaka impelekee kumfikiria mara kwa mara,ni mapenzi gani haya?..", mama huyo alipokwisha kujisemea hayo aliitikia dua ya binti yake.

"Amina mwanangu, hakika hata mimi pia nakupenda sana. Na ndio maana unaona najaribu kukutafutia furaha yako. Nina imani nitafanikiwa tu ila endapo mipango itakua sio matumizi basi usinilaumu mimi ingawaje najitoa kwa ajili yako"

"Sawa mama nakutakia mizunguko mema", alisema Mazoea na hata asijue kwanini mama yake ameamua kumwambia maneno hayo.

"Haya na wewe ubaki salama, lakini pia usisahau kumwambia Madebe amwagilie maua"

"Sawa", mama Mazoea aliondoka zake ingawaje akili mwake bado sintofahamu ilikua imetanda ilihali binti yake naye akisalia na furaha baada kusikia ya kwamba mzoa takataka Nyogoso hali yake imeanza kutengemaa asijue kuwa mama yake amecheza na akili yake kwa sababu laiti kama angelimwambia kwamba mzoa takataka amefariki basi ingekua hatari kwake kulingana na namna anavyompenda.

"Laah! Huu ni mitihani kwakweli, sasa naishi bila amani ya moyo wala kufurahia maisha kisa tu mtu huyu asiyekua na mbele wala nyuma", akiwa ndani ya gari lake huku gari hilo likitembea kwa kasi, mama Mazoea alijikuta akijisemea maneno hayo juu ya kijana mzoa takataka na binti yake. Alijua dhahili shahili Nyogoso amefariki, asijue kuwa kijana huyo alitoroka hospitali. Upande mwingine, alionekana mkewe Dokta Luanda akizunguka na moja ya marafiki wa karibu wa mumewe. Mwanamke huyo alihitaji asaidiwe akopeshwe kiasi cha fedha ili amtolee dhamana mumewe.

"Mmmh habari yako bwana"

"Njema tu sijui wewe"

"Kwangu pia njema japo sio sana, kama unavyofahamu mambo yaliyomkuta mume wangu"

"Eh najua hilo"

"Basi bwana Maloni, nimekuja unisaidie shilingi million mbili ili niongezee na hela niliyonayo nikamtolee dhamana mume wangu"

"Nikusaidie?.."

"Ndio, lakini maana yangu ni kwamba utakapo nipa pesa hiyo, nitakurudishia hapo baadaye. Nisaidie Maloni nikamtoe rafiki yako. Nipo chini ya miguu yako"

"Hahaha Hahahah", mtu huyo aliyeitwa Maloni aliangua kicheko huku mikono yotey miwili ikiwa kwenye mifuko ya suruali yake ilihali akimtazama mkewe Luanda ambaye alikua amepiga magoti chini. Alipohitimisha kicheko chake alisema "Hebu simama kwanza, hustahili kunipigia magoti mimi bwana. Enhee, sasa nisikilize shemeji. Unajua bwana hali ya maisha sasa hivi imebadirika, kwa maana hiyo ukimkopesha mtu hela, kukurudishia mpaka muanze kushtakiana. Kwa maana hiyo mimi sipo tayari kukupa pesa hiyo ", mke wa Dokta Luanda alistuka kusikia maneno hayo, aliweka mikono kichwani kisha akamuuliza Maloni kwa sauti ya chini." Kwahiyo utanisaidiaje shemeji yangu, kwa sababu wewe ndio mtu wa karibu wa Luanda... "

" Nipo tayari kukupa pesa hiyo ila endapo kama utanipa penzi lako, kama hutaki acha akafungwe. Kwani hajui kama rushwa ni adui wa maendeleo? Maendeleo yakikwama husababisha pesa inakua ngumu kupatikana mtaani, na mwisho wa siku mtu ukimkopesha anasua sua kulipa ", alijibu Maloni akihitaji penzi la mke wa Dokta Luanda ambaye ni rafiki yake wa karibu. Kwa hakika ni mtihani mkubwa kwa mke wa Dokta Luanda hasa baada kusikia anacho kihitaji Maloni, kijana ambaye anaishi na virus vya ukimwi. Na hilo suala mke wa Dokta Luanda alilifahamu fika.

Kwingeneko, kichaa Nyogoso tayari alikua mtaani akilandalanda. Katika matembezi yake alijikuta akipita mtaa anayoishi Suzani na wazazi wake, Mikocheni B. Wakati anazipiga hatua,mbele yake alikutana na gari aina ya RAV4, alipisha kando ili gari hilo lipite. Gari hilo lilipita kwa mwendo wa pole pole, lakini hatua kadhaa lilisimama kisha akashuka mama Suzani kutoka kwenye gari hilo.

Mama Suzani hakuamini macho yake baada kumuona Nyogoso kwa mara nyingine tena akiwa buheri wa afya, aliamini tayari Dokta Luanda ameshamuuwa lakini leo hii anakutana naye akiwa mzima.

"Hivi huyo Dokta Luanda ananijua kweli? Bila shaka haujui moto wangu. Sasa ngoja atanitambua mimi ni nani?..", akiwa na wingi wa jazba mama Suzani alijisemea maneno hayo na kisha mara moja akafungua Dashboard ya gari lake akatoka na bastora, haraka sana akainyooshea kuelekea kule alipo kichaa Nyogoso ambaye alikua akizidi kutembea huku asijue kinacho endelea nyuma yake.



http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Mama Suzani aliftua risasi, lakini risasi hiyo haikupata kichaa Nyogoso. Ilikwenda kumpiga kijana mzoa takataka aliyekua akikatiza eneo hilo. Mama Suzani baada kuona ameuwa, haraka sana alirudisha bastora yake kwenye Dashboard ya gari lake kisha akaliwasha na kuondoka zake huku nyuma kichaa Nyogoso akigeuka nyuma kutazama kule iliposikika mlio wa risasi. Alistuka kumuona mtu chini huku damu zikimtiririka kichwani mahali alipopigwa risasi, hakika Nyogoso alistaajabu sana. Mwili ukisisimka kichaa huyo aliusogolea mwili wa muhanga aliyekumbwa na balaa la kupigwa risasi. Lakini kabla hajamkaribia, ghafla kilitokea kundi la watu likisogogea mahala pale aliposimama Nyogoso ambapo naye alipowaona watu hao alisita kumsogelea mtu yule aliyepigwa risasi. Alisimama wima, punde si punde watu hao walifika eneo la tukio baadhi walisonga kwenye mwili wa yule kijana aliyepigwa risasi huku wengine wakisalia kutazama kichaa Nyogoso wakumuhisi kuhusika na mauaji.

"Jamani huyu mtu amepigwa risasi", ilisikika sauti ikisema hivyo. Taharuki ilizuka mahali hapo kila mmoja akigeuka kumtazama Nyogoso kwa jicho la tatu.

"Hebu mkagueni huyo kichaa, hana bastora kweli?", aliongeza kusema mtu huyo. Vijana wasiopungua watano walimvagaa Nyogoso kaa nguvu, wakamkagua kitendo ambacho hakikuweza kumpendeza kichaa Nyogoso kwani alijua fika yeye sio muuwaji sasa iweje akaguliwe tena kwa mabavu? Alipinga, jambo ambalo liluzua tafalani. Lakini wakati Nyogoso alipokua kwenye heka heka ya kuwatoa vijana hao kwenye mwili wake, sauti ilisikika kutoka kwenye umati wa watu uliokusanyika mahali hapo kwenye tukio. Sauti hiyo ilisema "Akileta ubishi mpigeni, ikiwezekana na yeye afe tu.", maneno ya mtu huyo aliyoongea, yaliwapa morali kwa vijana hao watano waliokua wakimkagua kichaa Nyogoso, hatimaye walianza kumshushia kipigo cha mbwa mwizi. Kichaa Nyogoso alilalama akihisi maumivu, ila sauti yake hiyo haikuweza kusikika masikioni kwa vijana hao. Kipigo kikali waliendelea kumshushia ila mwishowe ghasia ilizuka baada kufika gari la polisi mahali hapo, punde si punde polisi hao walifyatua risasi kadhaa angani ili kuwasambaratisha watu hao,nao walisambaratika.

Jeshi hilo la polisi baada kuona wananchi wamesambaa, waliufuata mwili wa kijana yule mzoa takataka aliyepigwa risasi. Waliunyanyua na kuiingiza ndani ya gari kisha wakamvisha pingu kichaa Nyogoso ambaye tayari uso wake na sehemu mbali mbali za mwili wake zilikua zimechakazwa kwa damu sababu ya kipigo. Naye alipandishwa kwenye gari la polisi, moja kwa moja wakaelekea Amana hospital. Aliachwa hapo ili apatiwe matibabu ya muda wakati huo wao wakirudi kufanya uchunguzi juu ya kifo cha kijana mzoa takataka aliyepigwa risasi na mama Suzani pindi mama huyo alipokua akitaka kumpiga Nyogoso. Mwili wa kijana huyo ulihifadhiwa monchwari wakati huo huo upande wa pili, mama alikua ofisini kwake. Kila mara alionekana kushusha pumzi ilihali kichwa kikiwa na wingi wa mawazo, furaha kwake ikiwa ndoto iliyosahaulika. Penzi la binti yake na Nyogoso lilimpasua kichwa, hivyo mama Mazoea aliwaza atamwambia nini mwanaye ili aweze kumuelewa pindi atakapo thubutu kumwambia kuwa Nyogoso amefariki. Mama huyo alijua fika Nyogoso amefariki, taarifa hiyo aliambiwa na mama Suzani walipokutana hospital. Naye aliamini hivyo baada kutumuona wodini, alipokua amelazwa. Alishusha pumzi ndefu baada kuwaza sana huku akijaribu kujenga picha kichwani mwake kitakacho kwenda kutokea pindi atakapo mfikishia taarifa hiyo binti yake.

"Laah! Eeh Mungu nisaidie", alijisemea mama Mazoea wakati huo kijasho kikimtoka. Suala hilo lilipokua likiutesa ubongo wa mama Mazoea, kwingeneko mama Suzani akiwa ndani ya gari lake alipiga honi mfululizo akimtaka mlinzi afungue geti haraka sana kwani alihisi anafuatwa na watu baada kufanya kitendo kile cha kinyama.

"Wemba ulikua wapi? Na vipi hujasikia honi?..", alifoka mama Suzani wakati akikunja kona kuelekea mahali anapoegesha gari lake kila siku.

"Samahani bosi nilikua haja, nisamehe sana", alijibu Wemba mlinzi wa geti wakati huo akifunga geti.

"Wemba, nakuomba mtu yoyote usiyefahamu usimfungulie geti sawa sawa", aliongeza kusema mama Suzani huko nako akifunga mlango wa gari lake mara baada kushuka.

"Sawa bosi hakuna tatizo", Wemba aliitikia,mama Suzani aliingia ndani akitembea haraka haraka. Alipofika sebuleni aliketi kwenye sofa, alishusha pumzi ndefu wakati huo akitazama paa la nyumba, mawazo chungu nzima yakimzonga kichwani mwake. Aliwaza atakua katika wakati gani kama ameonekana kwa kile alicho kifanya, lakini punde si punde hofu hiyo ilitoweka baada kukumbuka kuwa wakati wakati anafyatua risasi alikuwepo Nyogoso tu. Hivyo mama Suzani aliamini kuwa msala utabaki kwa kichaa Nyogoso na sio yeye tena.

"Bila shaka atafangwa jela, mambo yakienda hivyo basi lengo langu litakua limetimia", baada kuwaza na kuwazua, hatimaye alijisemea maneno hayo wakati huo tabasamu pana likionekana usoni mwake kisha akanyanyuka kutoka kwenye sofa, akazipiga hatua kuelekea chumbani kupumzisha akili.

Manamo saa kumi na mbili jioni, kichaa Nyogoso aliachiwa huru baada kubainika kuwa hana hatia kuhusu kifo cha kijana yule aliyepigwa risasi. Saa hiyo ya jioni kichaa Nyogoso alizipiga hatua barabara ya Magomeni akielekea Kinondoni ili aelekee moja kwa moja Sinza makaburini mahali ambapo yapo makazi yake. Nyogoso akitembea kando ya barabara hiyo huku akiyatazama magari ambayo kwa wakati huo yalikua yakitembea kwa kasi, taa ya kijani ikiwa imeruhusu. Lakini wakati hali hiyo ikionekana hapo barabani, mara ghafla magari yalipunguza mwendo na punde si punde yalisimama ingawa kwa muda mchache yalitembea na kurudia kusimama. Hiyo kuashiria kuwa tayari taa Nyekundu imewaka. Kero ya kila mwaka ndani ya jiji hili la Dar es salaam.

Hivyo katika magari hayo yaliyosimama na kujongea kusubiri taa ya kijani iwake. Ilikuwepo na gari la mama Mazoea naye akiwemo ndani, ambapo mama huyo alilaani sana kero hiyo wakati huo akichungulia nje japo apate hewa japo ndani ya gari yake ilikuwemo kiyoyozi,hapo ndipo alipo muona kijana Nyogoso akitembea pembezoni mwa barabara. Mama Mazoea alistuka huku akimkodolea macho Nyogoso. Mapigo ya moyo wake yalimuenda mbio na hata asiyaamini macho yake,haraka alipasa sauti ya kumuita,lakini kwa kuwa pembezoni mwa barabara palikua na watembea kwa miguu wengine wengi Kichaa Nyogoso hakuweza kujua sauti hiyo, aliendelea kutembea ilihali mama Mazoea naye akiendelea kupasa sauti yake kumuita kutokana na kazi anayokua akifanya mataa. Ila bado kichaa Nyogoso hakujali aliondoka wakati huo huo taa ya kijani iliruhusu gari ziondoke na punde si punde honi zilisikika nyuma ya gari laa mama Mazoea wakimtaka aondoe gari lake...





"We mwanaharamu, hebu ondoa gari lako la makopo watu tupite"

"Hivi unafikiri barabara ya kwako ama?, watu tumechoka tunahitaji kupumzika bwana. Toa kwama lako barabarani ebo", zilikua ni sauti za madereva mbali mbali ambao walisikika kwa nyakati tofauti wakimfokea mama Mazoea ili aendeshe gari lake kuepusha foleni kwani tayari taa ya kijani ilikua imeruhusu magari yaweze kuondoka.

Kelele hizo zilimtoa mama Mazoea kwenye dimbwi la bumbuwazi, dimbwi ambalo alijikuta akididimia baada kumuona kichaa Nyogoso kando ya barabara huku akili yake ikijishauri ashuke kwenye gari ili amkimbilie au aachane. Na vipi endapo kama atamuacha aondoke, wapi tena atamuona tena? Ama itakuaje pindi atakapo iacha gari barabarani, gari zilizopo nyuma yake zitapita wapi?. Hakua na namna mama Mazoea, aliwasha gari lake akaondoka zake huku moyoni akiamini kuwa Nyogoso ni mzima na wala hajafa kama alivyokua akiamini hapo awali, baada mama Suzani kumwambia kuwa Nyogoso ameshafariki.

"Laah! Ama kweli Mungu mkubwa", alijisemea mama Mazoea ndani ya nafsi yake wakati huo tabasamu bashasha likitamalaki usoni mwake, uzima wa Nyogoso ulimfanya afurahi sana aliendesha gari kwa kasi ya ajabu huku akiongeza sauti ya radio yake juu ndani ya gari. Tabasamu nyimbo ya Mr blue ilipenya vema kwenye masikio yake wakati huo huo akichezesha kichwa chake. Upande wa pili kichaa Nyogoso aliendelea kutembea kuelekea kwenye kwenye makazi yake, Sinza makaburini ndipo alipokuwa makazi yake. Alifika salama wa salamini,ilihali kwingeneko mama Mazoea alifika nyumbani kwake tabasamu bashasha bado likionekana kuupamba uso wake. Aliegesha gari lake mahali husika kisha akashuka kwenye gari akapasa sauti kumuita mlinzi "Madenge.. Madenge.. Madenge"

"Naam! Bosi", Madenge aliitika kisha akatii wito.

"Vipi umeshindaje?.."

"Ammh salama tu, habari ya mihangaiko", aliuliza Madenge kwa tabasamu pia.

"Ni nzuri. Aamh Madenge, naomba kesho asubuhi mapema nioshee gari ling'ae vilivyo sawa sawa?.."

"Sawa bosi wala hakuna tatizo"

"Enhee, halafu kesho sasa nitakuletea zawadi sana nzuri sana"

"Ahahahah hahahahah, sawa bwana bosi", alifurahi Madenge. Siku hiyo Madenge alimshangaa sana kumuona bosi wake yupo tofauti na siku zilizopita, siku hiyo alikuwa mtu mwenye furaha sana. Madenge alijiuliza maswali kibao mara mbili mbili kuhusu hali hiyo ya bosi wake, alikosa majibu zaidi alijisemea "Siku hazifanani", alipokwisha kujisemea hayo alizipiga hatua kuelekea kwenye lindo lake ilihali mama Mazoea naye aliingia ndani, kabla hajaingia chumbani aliketi kweny sofa sebuleni kisha akapasa sauti kumuita Mazoea. Mazoea aliposikia sauti ya mama yake, haraka sana alikifunga kitabu cha Riwaya alichokua akikisioma muda huo akiwa amejilaza kitandani kisha akatii wito.

"Waooh! Mama yangu huyooo", aliongea Mazoea kwa tabasamu bashasha huku akipanua mikono yake kwa dhumuni la kumkumbatia mama yake. Punde alimlaki kifuani huku akimpa na mabusu moto moto.

"Niambie mwanangu umeshindaje?..", alisema mama Mazoea pindi tu alipojing'atua kwenye kifua cha binti yake. Mazoea kabla hajamjibu mama yake alishusha pumzi ndefu kwanza, akakaa kwenye sofa kisha akajibu "Nimeshinda salama mama yangu, labda sijui upande wako"

"Hata mimi pia nipo ngangari kama Kenya na Uganda", alijibu mama Mazoea.

"Ahahaha! Jamani mama, kwanini isiwe Tanzania?.."

"Aah kIpendacho roho mwanangu"

"Kwahiyo unataka kuniambia Tanzania huipend?.."

"Hapana naipenda ila..."

"Ila nini mama?..", alidakia Mazoea, wote kwa pamoja walicheka huku wakigongeana mikono. Baada kukatisha vicheko vyao, mama Mazoea alizama kwenye mkoba wake akatoa kitabu. MREMBO KIPOFU. ndilo jina la kitabu lilivyoandikwa kwenye kava. Mazoea alikikodolea macho kitabu hicho wakati huo huo mama yake alimkabidhi, naye alikipokea halafu akasema "Bila mawazo yangu yanaendana vyema na mawazo yangu?.."

"Kwanini?.", aliuliza mama Mazoea huku akitabasamu.

"Huu bila shaka utakuwa mkono wa Alexis wamillazo, kiukweli napenda sana hadithi zake. Na safari hii umeniamulia", alijibu Mazoea wakati huo akianza kukifungua kurasa kitabu hicho. Ukweli mrembo Mazoea alipendelea sana kusoma vitabu mbali mbali iwe vya shuleni hata Hadithi pia. Hivyo wakati anapitia kipindi kigumu cha kuzama kwenye penzi la mzoa takataka, mama yake aliamua kumfanyia vile anavyopenda ili kumuwekaa sawa kisaiklojia.

"Haya Asante mama yangu, nitakisoma baadaye. Enhee vipi hali ya mkweo?..", aliongeza kusema Mazoea huku akiwa tayari amekifunika kitabu. Swali hilo lilimfanya mama yake ashushe pumzi kwanza kisha akamjibu kwa kusema "Mwanangu, mpenzi wako hali yake kabisa ila kitu kimoja tu."

"Kitu gani?.", alidakia Mazoea akiwa na shauku ya kutaka kujua kwa undani zaidi.

"Ametoroka hospital"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Ametoroka?. Jamani mama mbona mnanifanyia hivi? Eeh na mimi ni binadamu mama nina moyo kama wengine, sio vizuri kuninyongea mama!..", aliongea Mazoea, na punde si punde aliangua kilio. Mama Mazoea alijikuta akimshangaa binti yake. Alitikisa kichwa alisikitika, akasema" Nyamanza usilie Mazoea, mtu wako bado yupo hapa hapa Dar wala hajaenda mbali. Na mimi kama mama yako mzazi nitahakikisha namtafuta mahala popote mpaka nimpete. Sawa mama?. Nipo tayari kutumia hata mamilioni ya pesa kwa sababu yako "

" Utampata wapi mama? Hili jiji kubwa bwana.. ", alisema Mazoea wakati huo machozi yakimchurizika mashavuni mwake. Mama yake aliyafuta machozi na akasema" Wewe usiwe na shaka kuhusu suala hilo, nimekwambia hivyo kwa sababu uhakika ninao. Jioni ya ya leo kwa macho yangu mawili nimemuona, ila nilishindwa kushuka ili nimfuate kwa sababu taa ilikuwa imesharuhusu"

"Kweli mama? Unaniahidi kuwa uwezekano upo wa kumpata mzoa takataka?."

"Ndio mwanangu, shaka ondoa kabisa", alisisitiza mama Mazoea juu ya binti yake. Hapo ndipo Mazoea aliponyamanza kwa sauti ya chini akamwambia mama yake "Nakupenda sana mama yangu"

"Mimi pia damu yangu", aliitikia mama Mazoea na wote kwa pamoja waliachia tabasamu wakakumbatiana kisha mambo mengine yaliendelea. Muda huo tayari ilikuwa yapata saa moja usiku, giza totoro likianza kutanda ingawa lilipotezwa na mataa mbali mbali yaliyoipendezesha vema jiji la Dar es salaam. Anaonekana kichaa Nyogoso akiwa maskani kwake makaburini. Kichaa huyo ghafla anajikuta akikubwa na njaa kali tumboni mwake kiasi kwamba njaa hiyo iliweza kuvyekelea mbali usingizi aliokuwa nao. "Ponda mali kufa kwaja", alijisemea kichaa Nyogoso wakati huo akijitutumua kwa kusafa maumivu ya kipigo. Lakini alifanikiwa kusimama kidete na hapo aliamua kuingia mtaani kutafuta chochote ili walau apoze njaa kali aliyokuwa nayo. Alitembea karibu mitaa mitatu ila hakupata hata kitumbua kilicho dondoka kwa bahati mbaya, punde akapata wazo.

"Ule mtaa kuna mzee anapenda kutupa mikate nyuma ya nyumba, hebu ngoja nikaangalie. Ahahaha Hahahah. Wazee kama wale ndio wenye pepo bwana", baada kupata wazo hilo alijisemea maneno hayo kichaa Nyogoso huku akitupia na kicheko ndani yake. Wazo hilo aliliafiki, hima alizipiga hatua kuufuata mtaa ule. Lakini wakati kichaa Nyogoso akikazana mwendo kuelekea huko, mbele yake kwenye kiza totoro walionekana watu wawili wote wanawake. Watu hao walizipiga hatua kuelekea kule alikotoka Nyogoso. Nao hawakuwa wengine bali ni Suzani na mama yake,wawili hao walitoka kumsabahi ndugu yao aliyekuwa mgonjwa, na sasa walikuwa wakirudi nyumbani na siku hiyo hawakutembea kwa gari la nyumbani kwa sababu mama Suzani alihofia kutembea na gari lake baada kutambua kuwa alifanya mawaji kwa kumpiga risasi kijana mzoa takataka ingawaje dhumuni lake lilikuwa ni kumuuwa kichaa Nyogoso ili akamilisha lengo lake. Lengo kuu la mama huyo kumuuwa Nyogoso ni kutaka kuzima ndoto ya binti yake ambaye alionekana kumpenda sana kichaa Nyogoso. Hivyo zogo baina yake na binti yake liliendelea huku wakitembea kuelekea kwenye kituo cha teksi, wakati huo zogo likikolea ndivyo walivyozidi kukaribiana na kichaa nyogoso kijana ambaye mama Suzani alijuwa kuwa amemuuzia kesi ya mauwaji na aliamini tayari atakuwa yupo rumande akisubiri kesi yake.





Hatimaye walikaribiana, walikaribiana walipishana pasipo kujuana. Si mama Suzani wala binti yake, wote hawakujua kama mtu waliyepishana naye ni Nyogoso. Lakini wakati wawili hao walipokuwa wakiendelea kutembea, mama Suzani hakujua kama alidondosha simu pindi alipotoa kitambaa cha kufitia jasho kwenye katika mkoba wake. Kichaa Nyogoso alipofika mahali ilipotokea simu, ghafla iliita ambapo ilitoa mwanga. Kichaa Nyogoso alistuka kuona mwanga huo wa simu chini, haraka sana alijongea mahali hapo kwa dhumuni la kutaka kujua ni kitu gani kinachotoa mwanga.

Alikuta simu kubwa, simu ya ghalama ikiita. Hima aliinama akaichukuwa, akaikamata vema katika kiganja chake akawaza na kuwazua kwa sekunde kadhaa akijiuliza ni nani mwenye mali hiyo. Lakini mwisho akakumbuka kuwa ni dakika chache tu zimepita akiwa amepishana na watu wawili, aliamini kuwa mali hiyo itakuwa ni moja ya watu wale wa wawili aliopishana nao. Haraka sana kichaa Nyogoso alitimua mbio za pole pole akiwakimbilja Suzani na mama yake ilihali wakati huo huo mama Suzani alihitaji kuwasiliana na mumewe ambapo alipoingiza mkono ndani ya mkoba wake alistuka kutoigusa simu, alisimama huku mapigo ya moyo wake yakimuenda mbio. "Suzani, hivi nimekupa simu yangu?.", akiwa na wa wasi wasi mama Suzani alimuuliza binti yake. Suzani alikataa akasema "Hapana mama hujanipa, hebu angalia vizuri bwana"

"Au umeiacha kwa anti Sophia?", aliongeza Suzani.

"Hapana, simu nilikuwa nayo muda si mrefu", alijibu mama Suzani huku akiendelea kuhaha kuitafuta simu yake.

"Anhaa, basi utakuwa ulipotoa leso"

"Bila shaka. Sawa turudi mahali nyuma pole pole huwenda tukaipata"

"Mmmh! Sidhani. Kumbuka tulipishana na mtu, atakuwa hajaiona kweli?.."

"Suzani, hawezi kuiona na giza hili bwana"

"Sawa twende", Suzani na mama yake walikubariana kurudi nyuma kuitafuta simu, lakini kabla hawajafika mbali ghafla walikutana na kichaa Nyogoso. Walipishana, giza tayari lilikuwa limetanda sasa, kwani ilikuwa yapata saa mbili kasoro. Hatua kadhaa nyuma yao, mama Suzani alisimama kisha akamwambia binti yake "Suzi hebu muite yule kijana tuliyepishana naye"

"Mmmh, lakini mama muonekano wa yule mtu japo kuna giza ila anaonekana sio mzima wa akili. Ni kichaa", Suzani alimjibu mama yake. Jibu hilo mama yake hakutaka kukubaliana nalo, haraka sana alipasa sauti kumuita kichaa Nyogoso. "We kijanaaa.. We kijanaaa", sauti hiyo ilipenya vema kwenye masikio ya kichaa Nyogoso, naye alisimama kisha akarudi nyuma.

"Habari yako", kichaa Nyogoso alisalimu baada kumkaribia, punde si punde mbele yake Nyogoso lilitokea gari, mwanga wa taa za gari hilo ziligonga kwenye paji la uso wa kichaa Nyogoso, jambo ambalo lilipelekea mama Suzani kumjua vizuri kuwa kijana huyo ndio yule anyaemuwinda kila kukicha. Mama Suzani alitaharuki sana, aligeuki kumtazama binti yake aliyesimama kando hatua kadhaa, wakati mama huyo akiwa kwenye dimbwi la taharuki, kichaa Nyogoso alisema "Mbio zangu zote nilikuwa nikiwakimbilia nyinyi. Ahahahah Hahahah" alisema kichaa Nyogoso kisha akaangua kicheko. Alipohitimisha kicheko chake akaongeza kusema. "Kijana mmoja mzoa takataka alipokuwa katika mihangaiko yake mtaani, ghafla alikutana na gari moja la kifahari mbele yake. Kijana yule alilipisha gari hilo ili lipite wakati huo huo upande aliosimama kijana yule mzoa takataka palikuwa na dimbwi ndogo la maji machafu,cha kushangaza dereva wa gari hilo aliyakanyaga maji yale machafu, nayo yakamrukia kijana yule mzoa takataka. Kosa kubwa sana lakini sasa yule dereva hakushuka kwenye gari lake walau akamuombe msamaha ili kumuaminisha yule kijana mzoa takataka kuwa hakudhamilia kufanya kitendo kile. Aliondoka zake ", baada kuongea maneno hayo kichaa Nyogoso, alimeza bunda la mate huku mama Suzani akimsikiliza kwa umakini ilihali Suzani naye aliposikia hadithi hiyo aliyokuwa akisimulia Nyogoso alijongea, wakati huo kichwani mwake akijaribu kukumbuka tukio alilowahi kumfanyia mzoa takataka miaka kadhaa iliyopita. Utulivu pekee ulitawala kichwani mwake. Kichaa Nyogoso aliendelea kuongea, ingawa mama Suzani hakuwa na haja ya maneno kichaa huyo, alitamani sana kumuuliza kama amemuokotea simu ila alishindwa kwa sababu kichaa Nyogoso bado alikuwa akiendelea kuongea. Alisema "Basi gari lile lililomrushia maji machafu kijana yule mzoa takataka lilipofika kwenye nyumba ya kifahari lilisimama, katika gari hilo alishuka binti mrembo mwenye mwendo wa madaha. Binti yule aliingia kwenye nyumba hiyo iliyojengwa kwa ramani ya kisasa huku ikizungushiwa uzio mkubwa. Kisha gari lililoyomshusha likaondoka zake,kuashiria kwamba kwenye gari lile palikuwa na watu wawili kama sio watatu, ingawaje wote ni watu na sio binadamu. Ila sasa wakati yule mrembo anaingia ndani ya geti, alidondosha pochi pasipo yeye kujua. Yule kijana mzoa takataka alipoikaribia nyumba ile aliiona ile pochi aliyondosha, haraka sana akaiokota akaifungua akakuta ile pochi ina vitu vya bei ghali na pesa kadhaa. Tamaa ilimkaa kando mzoa takataka, pasipo shurta alibisha hodi ili amkabidhi mwenye mali, mrembo yule alitii wito wangu, lakini muonekano wa kijana mzoa takataka ulimpelekea yule mrembo kumtolea maneno mabaya ya kumdhihaki labda pengine kijana yule hana hadhi ya kusimama naye, kama mlinzi wa geti alivyomshusha thamani tangu mapema kabla hajaonana naye. Ustarabu ukachukuwa nafasi kwa kijana yule mzoa takataka, alipiga moyo konde licha ya kutukanwa matusi mbali mbali ila hakujibu, zaidi baada kuona mrembo yule amemaliza haja yake, alimkabidhi pochi yake kisha yeye akaondoka zake kusaka tonge kamwe hakujali matusi aliyotukanwa. Hii ni hadithi aliyonisimulia marehemu mama yangu, nakumbuka aliwahi kunisimulia kipindi ananibembeleza niache kulia pindi baba iponipiga kwa kosa la kuiba maembe shambani kwa mzee Maneno. Mwisho wa hadithi hii, mama aliiambia kwamba cha mtu nisitamani. Na mimi maneno yake nayafanyia kazi.. ", alisema kichaa Nyogoso, kwa kutumia shati yake iliyochakaa kila kona aliyafuta machozi yaliyokuwa yakimtiririka kisha akamkabidhi mama Suzani simu yake, hakoja shukrani aliondoka zake wakati huo nyuma yake Suzani alionekana kupigwa na butwa, hadithi aliyosimulia kichaa Nyogoso ilimucha mdomo wazi, alikumbuka kuwa aliwahi kumfanyia kitendo hicho mzoa takataka. Pindi kumbukumbu hiyo ilipokuwa ikizunguka kichwani mwake, muda huo huo sura ya kichaa Nyogoso alikumbuka kwa mbali sana pindi taa za gari zilipomurika uso wake. "Mbona kama wanafanana?..", alijiuliza Suzani wakati huo huo mama yake alishusha pumzi ndefu hata asiamini kama kweli mtu aliyetaka kumuuwa leo amekuwa msaada wake.

"Suzani", aliita.

"Abee mama", Suzani aliitikia kwa sauti ya chini huku mapigo ya moyo wake yakimuenda mbio.

"Hivi unamkumbuka yule kijana?..", akitazama kule alipotokomea kichaa Nyogoso, mama Suzani alimuuliza binti yake. Suzani alikataa kuwa hamfahamu ingawaje moyoni alihisi kumfahamu. Kwa mara nyingine tena mama Suzani alishusha pumzi kisha kasema "Mzoa takataka", aliongeza kusema. Hapo ndipo Suzani alipopata uhakika juu ya kile alichokuwa akikifikiria..



http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Suzani alimbikimbilia Nyogoso, lakini abadani hakuweza kumuona. Kichaa huyo tayari alikuwa amtoweka kwenye vichichoro vya mitaa hiyo ya Sinza. Aliaumia sana moyoni mwake, aliona kumkosa Nyogoso kwa mara nyingine tena ni kama amepokonywa tonge lililokuwa likielekea mdomoni. Ila hakuwa na namna, alikubali ingawaje aliamini kwamba Nyogoso yupo hai na ni salama wa salimini. Wakati Suzani akiamini hivyo, upande wa pili kichaa Nyogoso alielekea kwenye moja ya mgahawa kuomba chakula, pindi alipotegemea kupata kiporo kilicho tupwa kukosa. Mama ntilie aliyekuwa akihudumua kwenye mgahawa huo alimpa chakula Nyogoso bila hiyana, alimuwekea kwenye mfuko wa naironi kisha akamkabidhi. Nyogoso alikula kwa pupa, kwa muda wa dakika kadhaa alikuwa ameshamaliza. Aliomba maji akanywa kisha akaondoka zake huku nyuma akimuachia mama ntilie aliyempa chakula akisema "Najua kesho utanipunguzia bei ya kunizolea takataka", mama ntilie huyo alijisemea mama hayo ndani ya nafsi yake akidhania kuwa kichaa Nyogoso bado mzoa takataka. Akitamba na shibe sasa, hatimaye alirudi maskani kwake kupumzika. Na kabla haja lala alikuwa na desturi ya kumlilia marehemu mama yake, alipokatisha kilio kicheko nacho kilisikika huku akiongea maneno chungu nzima kiasi kwamba watembea kwa miguu waliokuwa wakipita kando ya makaburi hayo ya Sinza waliingiwa na hofu wakidhania kuwa huwenda kuna mzimu unaofufuka kila siku saa hiyo ya usiku. Hali hiyo iliwapelekea wale wenye imani haba kulikimbia eneo hilo. Kwingeneko usiku huou Suzani alikosa usingizi, mawazo yake yote yakimfikiria Nyogoso. Alijipindua huku na kule, kitanda kilionekana hakitoshi wakati huo akitamani masaa yarudi nyuma walau yarudi nyuma ili aweze kutimiza azma yake. Hivyo baada kuwaza kwa kina zaidi, mwishowe alipitiwa na usingizi alistuka asubuhi alipoamshwa na mama yake akimuaga kuwa anaelekea kazini sasa. Upande wa pili mke wa Dokta Luanda alijikuta akishindwa kumtoa mumewe kalotini, alishindwa kutumia mwili wake ikiwa kama njia pekee ya kupata msaada kwa kumtoa mumewe hatiani. Alikacha suala, hatimaye aliamuwa kurudi kijijini kwao na mwanaye kwani aliona maisha ya mjini pasipo nguzo tegemezi katu hatoweza kufua dafu.



***********




ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog