Simulizi : Kurudi Kwa Moza Sehemu Ya Tano
(5) Ana alibaki na wale ndugu zake huku akiwauliza
kuwa atawezaje kuacha uchawi, “Si unaacha tu” “Haiwezekani
kuacha uchawi kirahisi rahisi hivyo jamani” Wakaangaliana kwa muda kisha
kuulizana kuwa uchawi unaachwa vipi kirahisi, hakuna aliyekuwa na
jibu, “Ni vigumu sana kuacha uchawi kirahisi rahisi hivyo, itanigharimu
maisha yangu yote. Natamani kuacha uchawi ila ni vigumu kwangu kuacha uchawi
kirahisi rahisi” “Mfano mama akiacha uchawi, na wewe si
utaacha?” “Mama hataki hata kusikia habari za kuacha uchawi ingawa
unamtesa sana sasa hivi, ila mkiweza kumshawishi aache basi mtakuwa mmefanya
vyema” Ana aliondoka na kuelekea chumbani kwake, ila bado ndugu zake
walijiuliza kama kweli Ana ana lengo la kuacha uchawi huku Sara akikumbuka
alivyopofushwa na ndugu yake kichawi pia akawasimulia ndugu zake jinsi Ommy
alivyopotea kwenye nyumba yao na kuwaambia kuwa nae ni mmoja wapo wa misukule wa
mama yao, walikuwa wakishangaa tu uchawi wa mama yao jinsi ulivyo na bila wao
kujua kama mama yao ni mchawi tena wa kudumu kiasi kile. Waliongea sana
ila badae walipoona muda umeenda sana wakakubaliana kuwa waende wakalale ila
Sara akatoa tena ushauri, “Jamani na leo kwanini tusilale wote
sebleni?” “Bado unaogopa tu kulala mwenyewe?” “Ndio
naogopa” “Basi kalale na Ana” “Weeee hapana jamani, siwezi
kulala na Ana jamani” “Kwanini lakini wakati kasema anaacha
uchawi” “Hata kama siwezi kulala na Ana kwakweli, bora nikalale ndani
kwangu peke yangu” Sara akainuka na kwenda ndani kwake kisha wale
mapacha nao waliamua kuondoka na kwenda chumbani kwao kwahiyo pale sebleni kwao
palibaki hapana mtu. Baada ya muda kupita kidogo na kimya kutanda ndipo
Rose alipoamua kwenda kufanya mambo yake sebleni sasa na kwavile aliona hakuna
mtu hata mmoja akahisi ni vyema kufanyia vitu vyake hapo kwani yeye alikuwa
anapenda zaidi kufanyia mambo yake sebleni kisha yanatawala nyumba nzima ila
siku za hivi karibuni hakufanya sababu ya kutingwa na mambo mengi sana, taratibu
alianza kufanya mambo yake pale kwa kuwasha dawa zake za kujifukiza na kuanza
kujifukiza sasa. Sara hakupata usingizi kabisa kwa usikiu huo
kwani yeye alihisi kutokewa na vitu vya ajabu ajabu tu na kufanya ashindwe
kulala, mara akasikia harufu kuwa kama kuna kitu kimewashwa hivi, uoga ukamshika
kwani alihisi kuwa ndio huenda ni yale mambo ya ajabu yameanza tena, akatamani
kujificha ila hakuwa na pakujificha ila akajivika ujasiri na kusema kuwa atatoka
ili aende kuona kinbachoendelea. Akanyanyuka taratibu huku akiwaza kuwa
kama ataona vitu visivyoeleweka basi atapiga kelele ili kaka zake nao waamke na
wamsaidie. Taratibu akatoka chumbani kwake na kugundua kuwa ule moshi
unatoka sebleni, kwahiyo akanyata hadi sebleni akashangaa kumuona mama yao akiwa
mtupu kabisa akijifukiza na dawa zilizokuwa zikifuka moshi, akasema kwa
hamaki, “Mama!” Mama yake aligeuka na kumtazama ila sura yake
ilikuwa tofauti na alivyoizoea, ilikuwa ni sura ya kutisha sana, Sara
akajishangaa kuwa anaanza kukimbia na badala ya kukimbilia chumbani alikuwa
akikimbilia mlango wa kutoka nje ilia toke nje na kukimbia ila kabla hajafika
mlangoni alijikwaa na kuanguka halafu mguu wake ukaanza kutoka damu, alimuona tu
mama yake akiweka mikono kichwani na kusema, “Masikini mwanangu jamani!
Na yeye ndio anapotea hivyo!” Mara gafla akatoweka, hakuwepo tena pale
sebleni wala uwepo wake haukuonekana kama hata amechungulia mahali hapo, Rose
aliacha kuendelea na zile dawa zake, alibeba vitu vyake na kwenda chumbani,
alijibadilisha na kuwa kawaida kisha akaanza kulia huku akiumia sana
moyoni, “Sara mwanangu jamani kwanini lakini! Kwanini unataka
kunifedhehesha mama yako? Kwanini unataka nikose raha mama yako, unajua
ulipoenda ni pagumu sana, unaweka maisha yangu klwenye ugumu wa hali ya
juu” Rose alilia sana na kumfanya ashindwe kabisa kulala wala kuendelea
na jambo lolote kwa usiku huo hadi panakucha. Ndugu wa mama
Jack walienda kwa mganga ila Yule mganga aliwatahadhalisha sana, “Ndugu
yenu aliingia kwenye mtego mbaya sana, na hata hivi ninavyoongea
ameshazikwa” “Amezikwa?” “Ndio kazikwa, na sehemu aliyozikwa ni
kaburi lenye maji kiasi kwamba siwezi hata kufanya dawa yoyote kwaajili yake,
hata hivyo alikaa muda mrefu sana kabla ya nyie kugundua kifo
chake.” “Sasa tutafanyaje?” “Sijui cha kufanya ila hata huyu
mganga aliyechukua jukumu la kumzika mama yenu kwenye kaburi lililojaa maji ana
jambo gumu sana na kubwa linaenda kumpata” “Sasa ndugu yetu tutamkoa
vipi?” “Jamani ngojeni pakuche, usiku mzima nitafanya dawa zangu ila
huyu aliyemfanyia mama yenu hivi lazima aumbuke kabla hapajakucha. Ngojeni
nifanye dawa zangu, leo msiondoke hadi kesho tutakuwa tumepata majibu ya
kueleweka” Ndugu wa mama Jack waliamua siku hiyo kulala nyumbani kwa
mganga ili kujua hatma ya ndugu yao maana kifo chake kilikuwa na utata
sana. Kulipokucha, Neema alienda kumuamsha Salome na
kumkumbusha kuhusu lile swala la kwenda nae kwenye maombi, ni kweli Salome
hakubisha kabisa halafu wakaanza kujiandaa walipomaliza safari yao ikaanza huku
Neema akimsisitiza mwanae kuwa wakifika huko aeleze kila jambo linalomsibu ili
iwe rahisi kuombewa, Salome alimuitikia mama yake na alikubaliana nae kwa kila
kitu. Walifika kituoni na kushuka kisha safari ya kuelekea kwenye maombi
ikaanza sehemu yenyewe haikuwa mbali na kituo cha basi, wakati wanakaribia
kufika Salome alimuomba mama yake kuwa aende dukani kununua maji mara moja kwani
alikuwa na kiu sana, Neema alikubali kisha Salome akaanza kwenda dukani ambako
napo hapakuwa mbali sana, ni nyuma kidogo tu na walipokuwa. Neema akaona
kama mwanae anakawia dukani na kuamua kumfata, ile anafika dukani tu alishtukia
akiwa nyumbani kwake tena bado yupo chumbani kitandani yani ndio
anaamka. Walifika kituoni na kushuka kisha safari ya
kuelekea kwenye maombi ikaanza sehemu yenyewe haikuwa mbali na kituo cha basi,
wakati wanakaribia kufika Salome alimuomba mama yake kuwa aende dukani kununua
maji mara moja kwani alikuwa na kiu sana, Neema alikubali kisha Salome akaanza
kwenda dukani ambako napo hapakuwa mbali sana, ni nyuma kidogo tu na
walipokuwa. Neema akaona kama mwanae anakawia dukani na kuamua kumfata,
ile anafika dukani tu alishtukia akiwa nyumbani kwake tena bado yupo chumbani
kitandani yani ndio anaamka. Neema alishangaa sana na kujiangalia mara
mbili mbili, ni kweli alikuwa ametoka kuamka ysni hata kuoga alikuwa
hajaoga, “Jamani haiwezekani, yani iwe sijaamka mpaka muda huu
kweli!” Akachukua na simu yake kuangalia saa, akaona ni saa tano asubuhi
na kuzidi kushangaa kwani hata kwakama kwa kawaida hana tabia hiyo ya kulala
mpaka saa tano asubuhi, mara nyingi akichelewa sana basi anaamka saa mbili ila
siku hiyo ilimchanganya zaidi, akajaribu kukumbuka kuwa alishajiandaa na Salome
walikuwa wanaenda kwenye maombi na mara ya mwisho Salome alimuomba kuwa anaenda
kununua maji halafu alikawia sana dukani, ila alipomfata dukani ndio akajikuta
yupo kitandani tena akiwa naio kwanza anaamka, akajiuliza “Hivi naota au
ni kitu gani? Lakini sioti jamani mbona nilikuwa macho jamani ndoto gani
hii?” Neema alijiuliza maswali kadhaa bila ya majibu, akaamua kutoka ili
ajaribu kuona kama anaota au la. Alitoka na kumkuta Salome akiwa
anaandaa kifungua kinywa, na alipomuona tu alimuamkia, Neema alishangaa sana na
kumuuliza Salome, “Inamaana bado hatujaonana?” “Tumeonana muda
gani tena mama? Si ndio umetoka kuamka?” Neema akaganda kwa muda kisha
akamwambia Salome, “Hivi mimi na wewe hatujaenda mahali
leo?” “Mama unaota ua?” “Sijui mwanangu, yani sijui kabisa ila
ninachojua ni kuwa tulijiandaa kwenda kwenye maombi, na tulifika kabisa ila wewe
ukataka kununua maji, nimekufata gafla nikajikuta kitandani ndio
naamka” Salome alicheka sana, kisha akamuangalia mama yake na
kumwambia, “Mama jamani mbona vichekesho hivyo yani uende mahali halafu
ujikute gafla umelala ndani yani ndio unaamka! Unaona hilo jambo linawezekana
kweli?” “Hata mimi nashangaa mwanangu, yani sielewi
kabisa” “Hiyo ni ndoto mama isikupe presha” “Yani hata sijui,
sijui kabisa yani” “Usijali mama ni ndoto hiyo” Neema alikaa
kwenye kochi sasa, huku akiwa na mawazo tele kuhusu yale mauzauza aliyoyapata
maana hakuelewa kama ni ndoto au ni kitu gani. Alijifikiria sana bila ya
majibu, wakati anawaza vile akashtuliwa na Salome na kumwambia, “Natoka
mama” Alitaka kuongea jambo ila hakuweza kuongea chochote zaidi ya
kumuitikia mwanae tu kuwa wataonana badae. Ndugu wa mama Jack
leo waliendelea kufanyiwa dawa na Yule mganga, Yule mganga aliwaambia kuwa
anaona kitu sio cha kawaida kimefanyika kisha akawaambia, “Inaonekana
mama Jack katolewa kafara na rafiki yake” Wakashangaa sana, na kuuliza
kuwa ni rafiki yake yupi ambaye kamtoa kafar mama yao, “Huyo rafiki yake
anaitwa Rose” Watoto wa mama Jack wakashangaa sana kwani mama yao siku
zote alikuwa akimsifia huyo Rose ingawa hawakujua kuwa Rose anapatikana sehemu
gani. Yule mganga aliendelea kuongea, “Yani huyo Rose anapenda sana
mambo ya waganga wa kienyeji ndiomana kajikuta kamtoa rafiki yake kafara, mama
yenu kosa lake ni kumsindikiza huyu Rose kwa mganga yani huyo Rose anapenda sana
mambo ya waganga ndio yanayomghalimu.” Walimshangaa mtoto mmoja wa mama
Jack akishindwa hata kuendelea kumsikiliza mganga bali aliinuka na kuondoka
zake. Alienda moja kwa moja nyumbani kwao na kuchukua simu ya mama yake
kisha kupekua jina la Rose, na alipolipata alimpigia
simu, “Hallow” “Samahani nani mwenzangu?” “Najua mama
una shida, mimi ni mganga wa kienyeji. Naomba tukutane
nikusaidie” “Jamani umejuaje dah! Nashukuru sana, nielekeze ulipo
nije” Basi Yule kijana akamuelekeza Rose mahali ambapo yeye aliona
panafaa kukutana na huyo Rose kwani alikuwa na uchungu sana wa mama yake
kutolewa kafara ukizingatia maiti ya mama yake ilifika kwao na kutoweka kwahiyo
mama yao walijua tu amekufa ila hata nafasi ya kuzika mwili wa mama yao
hawakuipata, yani kijana huyu alijikuta ana uchungu uliopitiliza moyoni mwake
haswaa swala la kumfikiria Rose. Rose muda aliokuwa nyumbani
kwake na mawazo sana kuhusu kutoweka kwa Sara ndio muda aliopigiwa simu na Yule
kijana kwahiyo alihisi kupata mkombozi ukizingatia hakutaka kuchukua hatua ya
kutoa wale misukule wake kwavile anahisi kuwa atapata matatizo ndiomana alikuwa
anaogopa kuwatoa, kwahiyo ile simu aliona kama ya ukombozi
kwake. Alijiandaa haraka haraka na kutoka, ila sebleni alikuta watoto
wake wale mapacha wamekaa na baada ya salamu walimuuliza mama
yao, “Mama, Sara kaenda wapi?” “Jamani Sara ni mtu mzima, mimi
siwezi jua alipoenda” “Mama, Sara hajatoka humu ndani. Tumeenda
kumuuliza mlinzi kasema hajatoka, tumemuangalia chumbani kwake hayupo pia. Sara
kaenda wapi mama?” “Jamani hebu subirini hadi jioni moune hatorudi,
mtoto wa kike yule labda karuka ukuta huko kaenda kwa wanaume” Kisha
akatoka zake na kuwaacha, walijiuliza sana maswali ni kwanini mama yao kawajibu
kirahisi kiasi kile maana swala la kutokuonekana kwa Sara ilitakiwa hata yeye
ashtuke lakini cha ajabu yeye alikuwa akiwajibu kirahisi rahisi tu, wale mapacha
walijiuliza sana kuhusu ndugu yao na kukosa jibu. Mama yao alipoondoka,
Ana nae alienda sebleni, ikabidi kaka zake wamuulize yeye, “Sara kaenda
wapi?” “Sara!!! Sijui mimi” “Ana, ulisema kwa uzuri kabisa
unataka kuacha uchawi, Sara haonekani ndani. Mlinzi hajamuona akitoka, na kama
angeenda mahali kwa hakika angetuaga hata simu yake ipo ndani, Sara yuko
wapi?” “Jamani sijui, mtanilaumu bure tu” Hawa mapacha waliwaza
sana cha kufanya ila hawakuwa na jinsi maana hakuna mwenye uhakika wa alipo
Sara. Salome leo alienda kumtembelea Mishi na kumshtua sana
kwani hakutegemea kutembelewa tena na Salome, aliamini kuwa ameshamalizana nae,
kwahiyo kitendo cha kumuona kaenda tena kumtembelea kilimshangaza sana,
akashindwa hata kumkaribisha, “Usishikwe na uoga Mishi, ila
kilichonileta leo ni jambo moja tu. Kwanini unataka kumdanganya mzee wa
watu?” “Kumdanganya nini?” “Si unataka kumwambia kuwa mimba hiyo
ni yake!” “Tafadhali naomba nisaidie, sitaki kuumbuka mimi, sitaki watu
wajue kuwa nilibakwa ndiomana nataka kumwambia kuwa mimba ni
yake” “Msamaha wangu kwako ni kumwambia ukweli, yani wewe mueleze ukweli
wote. Anakupenda, kukuacha hawezi, nataka tu ajue mtu anayempenda ni mtu wa aina
gani, usimdanganye kuhusu mimba uliyobeba, mwambie ukweli wote” Mishi
alikuwa kimya tu maana huu ulikuwa ni mtihani mkubwa sana kwake, na alijua kama
atamwambia huyo mzee ukweli basi ni lazima huyo mzee akikutana na mama yake
Mishi atamueleza halafu yeye alitaka iwe siri, ‘Nihurumie
tafadhali” “kama husemi, nitakuumbua. Nakupa siku moja tu ya kumwambia
mzee wa watu ukweli” Ilibidi Mishi akubali kuwa atamueleza Yule mzee
ukweli wa mambo ingawa alikuwa anaumia sana. Neema alikuwa
anajiuliza hadi kwenda kuoga tena alikuwa anawaza, ila badae akakata shauri na
kwenda kuoga halafu akarudi akiwa anaendelea na mawazo yake, watoto wake wale
mapacha walitoka shule na kumkuta mama yao pale sebleni akiwa na mawazo, mmoja
akaanza kumuuliza mama yao, “Kumbe msharudi ile safari na
dada” Akili ikamzinduka kidogo na kufanya awaulize vizuri hawa watoto
wake, “Hivi asubuhi ni nani kawaamsha na kuwaandaa muende
shule?” “Si wewe mama” “Hivi nilirudi tena
kulala?” “Mama jamani, ulisema wewe na dada Salome mnatoka, tena hadi
ukatuelekeza mahali tutakuta funguo ndiomana tumekuuliza mmesharuudi
tayari” Neema alipata kidogo mwangaza wa jambo amabalo lilitokea ingawa
bado alikuwa haelewi kuwa kama jambo hilo limetokea ni hakika limemtokea yeye
pamoja na Salome sasa iweje salome amwambie kuwa alikuwa anaota? Aliwaza sana,
kisha akachukua simu yake na kuamua kumpigia mama Pendo ili amshirikishe hilo
swala, alimpigia na kumuelezea kila kitu jinsi ilivyokuwa, kwakweli mama Pendo
alishangaa sana na kuhisi kuwa huenda ni stori za kusadikika, “Una
uhakika na hayo mambo kuwa uliondoka kweli nyumbani” “Nina uhakika, hata
wanangu hawa wadogo wamenithibitishia hilo” Akamueleza jinsi wanae
mapacha walivyomwambia, yani bado mama Pendo ilikuwa ngumu kuelewa kwani
mazingira ya tukio lenyewe yalikuwa ni ya utata sana, “Sasa mi
ninachoona niongee na mtumishi aje hapo nyumbani” “Kwakweli utakuwa
umenisaidia sana ukifanya hivyo, haya mambo ni ya ajabu kwangu hadi sielewi
nianzie wapi na niiishie wapi” “Pole ndugu yangu, au nije mwenyewe
kuwachukua” “Hata hivyo ni sawa ili nimwambie Salome
asitoke” “Basi nitaangalia litakalo wezekana” Neema aliongea
sana na huyu rafiki yake, basi alivyokata simu likamjia tukio la kukumbuka kuwa
alishawahi kumjuangalia mwanae Salome na kumuona kama kafanana na Moza, hofu
ikamshika na kujisemea, “Hapana haiwezekani, Moza aklishakufa na
mwanangu yupo hai. Haiwezekani kwakweli” Alikuwa anajiuliza na kujijibu
mwenyewe ila alipatwa na mawazo sana huku akimngoja mwanae arudi kwa siku hiyo
na kumwambia kuhusu ujio wa mama Pendo kuwapeleka kwenye maombi au ujio wa
mtumishi kumuombea Salome. Ana wakati anaongea na kaka zake
alikosa raha kabisa maana yeye alionekana anajua fika alipo dada yao Sara
ukizingatia nyumba nzima hakujulikana alipo. Ikabidi ainuke na kwenda chumbani
kwake kufanya dawa zake. Alifika na kuzianza dawa zake, alifanya kwa
muda kidogo na kumuona kuwa dada yake Sara ni miongoni mwa misukule ya mama yao.
Alishtuka sana Ana na kushangaa kwanini mama yao kafikia hatua hiyo maana aliona
sasa ni hatua mbaya yani mama yao hata afikie kumuweka kama msukule mtoto wake
mwenyewe, maana misukule aliyokuwa anatunza mama yake ilikuwa ni tofauti na
misukule ya watu wengine maana hii ililishwa kichawi na ilimsaidia kichawi
kupata nguvu za ziada kiasi kwamba ni ngumu sana kwake kuitoa misukule hiyo
kwani itamgharimu maisha yake yote, kwahiyo kitendo cha mama yao kumuweka Sara
msukule kilimchanganya sana Ana na kumshangaza, akamuangalia mara mbili mbili
dada yake alivyokuwa akisononeka na kumuonea huruma ila hata yeye Ana hakuwa na
uwezo wa kuwatoa watu kwenye kile kichumba ambacho mama yao
aliwahifadhi. Kisha akajaribu kuangalia kuwa mama yao ameenda wapi,
alimuona yupo porini ambapo hata njia hakuielewa halafu alikuwa akishangaa
shangaa, mara wakatokea vijana watatu na kumbana, kile kitendo kilimfanya Ana
atupe dawa zake zote kwa kushtuka kwani alijua wazi kuwa mama yao yupo
hatarini. Rose alienda hadi mahali ambapo alielekezwa na Yule
kijana ila alifika jioni maana sehemu yenyewe ilikuwa ni safari ya mbali sana,
alishangaa sehemu yenyewe ilikuwa kimya kabisa, akaanza kushangaa shangaa, mara
walikuja vijana nyuma yake wakamfunga mdomo, mikono na miguu na mwisho
wakamfunga macho, “Mama mpumbavu sana wewe na habari zako za kupenda
waganga, umemuua mama yangu na wewe ni lazima ufe” Rose hakuweza
kujitetea wala nini maana wale vijana walikuwa wamemziba mdono kwa kitambaa,
kisha wakaanza kumpiga ambapo walimpiga sana, halafu wakakubaliana kuwa wambake,
walifanya kazi ya kumbaka kwa zamu, Rose alilia sana na kujilaumu moyoni kufika
sehemu bila ya tahadhari. Wale vijana walimpiga sana Rose, kisha
wakataka kumchinja kwani lengo la mtoto wa mama jack ni kumuona huyu mtu
anayeitwa Rose akifa kama alivyokufa mama yao, ingawa mama yao alikufa kichawi
ila walitaka huyu mtu wamuue kimacho macho. Alishika kisu sasa akitaka
kumchoma, wakati amekiinua ili amchome alishtukia mkono wake ukishikwa na
kuzuiwa kumchoma, alipogeuza macho aangalie ni nani alimuona ni binti amabaye
mama yao alimsaidia usiku ambapo kesho yake ndio alitokomea
nae. Alishika kisu sasa akitaka kumchoma, wakati amekiinua ili
amchome alishtukia mkono wake ukishikwa na kuzuiwa kumchoma, alipogeuza macho
aangalie ni nani alimuona ni binti amabaye mama yao alimsaidia usiku ambapo
kesho yake ndio alitokomea nae. Yule kijana alishangaa sana kwani
haikuwa kawaida kabisa, akatupa kisu chini huku akimuangalia Yule binti
aliyeonyesha yupo serious sana, kisha Yule binti akamwambia, “Naitwa
Salome, ndio mimi mwenyewe niliyekuja kwa mama yako siku moja kabla hajafa, wala
hujanibahatisha. Sasa kwanini unataka kumuua huyu Rose” “Amemuua mama
yangu” “Ulikuwepo wakati anamuua?” “Tumeambiwa na mganga kuwa
amemtoa kafara mama yangu” “Unajua ni kwanini mama yako ametolewa
kafara? Huyu mwanamke alikuwa na marafiki wangapi zaidi ya mama yako? Na mbona
asiwatoe wao kafara akamtoa yeye?” “Sijui ila ninachojua ni kuwa huyu
mwanamke ni muuaji kamuuwa mama yangu” “Ngoja nikwambie kitu, huyu
mwanamke ni mchawi ila huyu mwanamke na mama yako ni bora ya huyu mwanamke, huyu
hajaua watu wengi kichawi kama alivyomaliza watu mama yako, kama huamini nenda
chumbani kwa mama yako halafu kuna begi lake dogo jeusi limechimbiwa chini, ni
vigumu kujua lilipo ila nitakusaidia kuliona, kisha uone ni viungo vingapi vya
wanadamu mama yako anavimiliki, je ndugu wa hao watu nao wangeamua kufanya
maamuzi kama yako si mama yako angekuwa marehemu muda
mrefu!” “Sikuelewi” “Huwezi kunielewa ila muachie huyu mtu
aondoke zake” “Unaniahidi nini nikimuachia?” “Nakuahidi kuwa
utaniua mimi badala yake” Yule kijana alimuangalia Rose pale chini kisha
akainua macho yake kuwaangalia wenzie ambao walimpa ishara kuwa amuachie tu,
kisha akainama na kumpiga teke Rose halafu akaamua kuondoka huku akiwa
ameongozana na Salome. Rose hakuelewa chochote ila anakumbuka
kuwa sauti aliyoisikia ilikuwa kama sauti ya Salome, na yale maongezi ambayo
Salome aliongea na Yule kijana aliyasikia vizuri, ila hakuweza tu kuona chochote
maana walimziba macho, sasa alivyopigwa lile teke akaanza kujikongoja ili ainuke
na kujiona kuwa hata kuinuka hawezi kwani maguu yote ilikuwa na maumivu
ukijumlisha kupigwa na kubakwa, kwahiyo Rose alikuwa na maumivu makali sana,
akaamua kupiga kelele za kuomba msaada ila kumbe wale rafiki wa mtoto wa mama
jack walikuwa wakimfatilia kwa nyuma kwani walifanya vile ili rafiki yao aondoke
na Yule binti ila wenyewe walitaka waendelee na ule mpango wa kumuua Yule
mwanamke kwani uchungu aliokuwa nao rafiki yao na wao pia waliupata na
waliuhisi. Wakati Rose akipiga kelele akashtukia akizibwa mdomo na kupigwa
kibao, “Nyamaza, muuwaji mkubwa wewe” “Jamani sijauwa mnanionea
bure” “Hujaua nini wakati umemtoa mama Jack kafara, hivi unajua ni kiasi
gani Yule mama alikuwa akitusaidia. Hivi unajua ni jinsi gani tulivyokuwa karibu
na Yule mama, halafu umemuua unategemea nini? Kwa taarifa yako, sisi ni makatili
kupita hata Yule aliyechukuliwa na zombie lako, yani sisi hatutakuchoma kisu ila
tutakuchinja taratibu ili uone kifo kina uchungu gani” Wakaanza tena
kumpiga Rose, walimpiga sana, kisha kumfungia kwenye miti kamavile wanataka
kumsulubisha, yani Rose alikuwa na maumivu makali sana. Salome
aliondoka na Yule kijana mpaka nyumbani kwa mama Jack, kisha akaenda nae hadi
chumbani kwa mama jack, ndugu zake na Yule kijana walikuwa bado hawajarudi
kutoka kwa Yule mganga, basi akamuonyesha sehemu kuwa afukue, na Yule kijana
akafanya hivyo kisha kukutana na mfuko mkubwa chini yake ambao kwa hakika kwa
kawaida hata wasingeweza kudhania kuwa kuna mfuko wa aina ile ndani mwao haswa
chumbani kwa mama yao, ilikuwa ni ajabu sana. Kisha Salome akamwambia Yule
kijana afdungue ule mfuko, na alipoufungua alishangaa sana, “Usishangae,
hivyo ni vitu ambavyo mamako alikuwa anaamini kuwa vinamletea utajiri, mama yenu
kashamaliza watu wengi tu kwa kuwatoa kafara akiangalia kupata mali na utajiri,
unafikiri mali hizi mama yenu kazitoa wapi? Ngoja nikuulize, baba yenu yuko
wapi?” “Alikufa” “Sasa unajua kuwa baba yenu alitolewa
kafara” “Kafara?” “Ndio kafara, unakumbuka baba yenu
alikufaje?” “Alipata ajali yani gari walilopanda lilipinduka na alikufa
baba peke yake” “Wakati baba yenu anakufa, mama yenu alikuwa
wapi?” “Hakuwepo alikuwa safarini” “Ila ndiye aliyekuja kuwapa
taarifa kuwa baba yenu amekufa?” “Ndio, anasema alioteshwa ndio akarudi
na kukuta kumbe kuna ajali ilitokea na baba alikufa” “Sasa kaa chini
uelewe kuwa mama yenu alikuwa ni mchawi tena mchawi haswaaa na alikuwa anatamani
amuachie mtoto mmoja uchawi wake sema katolewa kafara nay eye, na mama yenu
kauwawa sababu yangu yani mimi ndio nimemsababishia mama yenu auwawe. Sipendi
uchawi, nauchukia uchawi na nipo kwaajili ya kumkomesha Rose na marafiki zake,
mama yenu alimshauri Rose aende kwa mganga, na Yule mganga ndiyo aliendaga yeye
na kufikia hatua ya kumtoa mume wake kafara, halafu Rose naye aliambiwa awatoe
watoto wake wawili kafara ila mimi nilikuja kumchukua mama yenu na akatoka
badala ya watoto wawili wa Rose. Je bado unataka kuniua na mimi?” Yule
kijana alikaa chini kwanza kwani alihisi kuwa anaota, vile viungo vya binadamu
kuvikuta kwenye chumba cha mama yao vilimshangaza sana, hadi akajikuta hana jibu
kwa huyu mtu, kisha Rose akamuuliza tena, “Dada yenu wa kwanza yuko
wapi?” “Alikufa” “Hajafa” “Hajafa!
Kivipi?” “Ngoja uone” Muda kidogo alitokea mdada akiwa
amechafuka sana, alikuwa dada yao na alikuwa hajielewi wala nini, Yule kijana
bado kidpogo aanze kukimbia kwani hakutegemea kama wangefikia hatua
hiyo, “Nenda mkamshughulikie dada yenu arudi kwenye hali ya kawaida,
mama yenu alimfanya msukule wake ampatie mali sababu dada yenu alikuwa na damu
kali sana. Nenda mkashughulikie dada yenu, mnyoeni nywele hizo, mkateni kucha
arudi kwenye hali yake ya kawaida, ila swala la mama yenu kurudi hilo halipo
maana haiwezekani akarudi” “Nitawezaje?” “Utaweza tu, ila cha
kuongezea, msimpeleke kwa mganga yoyote huyu dada yenu kama bado mnampenda. Na
wala usishiriki dawa yoyote watakayokwambia ushiriki” Kijana Yule alitia
huruma zaidi kwani hata hakuelewa kama aendelee na kuchunguza ile mifupa au
amsaidie dada yake, ila Salome aliondoka na kumuacha pale akitafakari bila hata
kuelewa ila mwisho wa siku aliamua kumchukua dada yake na kubeba na mkasi kisha
kutoka nae nje na kuanza kumkata nywele maana hata uoga ulimuisha muda huu
ukizingatia alimuona dada yake akizikwa kabisa halafu katolewa akiwa mzima,
ilimshangaza sana ila alijivika moyo wa ujasiri na muda mwingine kujihisi kuwa
labda yupo usingizini na anafanya vile vitu ndotoni. Wale
vijana waliendelea na kumtesa Rose, kisha kila wakitaka kumuua wanajikuta mikono
yao ikiwa mizito sana, na mwisho wa siku wakati wanafikia hatua kuwa wamuue kwa
pamoja, Salome alitokea katikati yao na kuwafanya waogope kwani hawakuwa kwenye
lile eneo la mwanzo walilokuwa kwahiyo walijiuliza kuwa huku huyu binti
kapajuaje, “Nilisemaje? Si nilisema huyu mama aachiwe?” Wale
vijana walimuangalia Salome na kumshangaa kuwa binti mdogo vile anawezaje kuwa
na amri juu yao, yani anasemaje bila ya kuwa na uoga hata kidogo, wakakonyezana
kuwa wamvamie na huyu Salome wamdunde ili akili yake ikae sawa, sasa ile
wanataka kufanya mashambulizi kwake wakashangaa wakianza kupigwa viboko, yani
walicharazwa viboko vingi vingi kisha walishangaa kuona Yule mama waliyemfunga
akitoweka na hata haikujulikana ni wapi ameenda ila wao walikuwa wakitrandikwa
tu viboko halafu walikuwa hawawezi kuondoka eneo lile, yani hawawezi kwenda
popote ila walikuwa wakipigwa tu hadi walianguka chini na kuzimia. Ila
walipokuja kushtuka kila mtu alikuwa nyumbani kwao, kila mmoja alitafakari na
kukosa jibu ya kilichotokea siku hiyo. Ndugu wa mama jack baada
ya kumaliza kwa Yule mganga na kupewa dawa wakaamua sasa warudi nyumbani ili
wapange mipango vizuri kwa kile walichoambiwa na mganga wao, walishangaa kufika
nyumbani wakamkuta Yule aliyewakimbia kule kwa mganga na kabla hawajamuuliza
chochote akawaambia, “Kuna kitu nataka niwaonyeshe” “Kitu
gani?” Kila mtu alikuwa na shauku ya kujua kuwa ni kitu gani ambacho
alitaka kuwaonyesha, basi Yule kijana, alienda kumchukua dada yake ambaye
alimuacha chumbani kwa muda, yani alivyofika ukumbini tu wote walianza kupiga
kelele na wengine kukimbia kimbia mpaka pale alipowaita na kuwaambia kuwa
wasiogope ila bado walishikwa na uoga wa hali ya juu ukizingatia ni mtu ambaye
wamemzika miaka mitano iliyopita kwahiyo kitendo cha kumuona mzima
kiliwaogopesha sana, “Jamani msiogope, ni mzima kabisa huyu sema saivi
kuongea ni mgumu ila ataongea tu” “Tuambie imekuwaje
kuwaje?” Ikabidi huyu kijana awaeleze ukweli wa mambo ya jinsi
ilivyokuwa kuanzia alivyowasiliana na Rose hadi alivyotaka kumuua na jinsi Yule
binti alivyotokea. “Huyo binti ni nani?” “Hata mimi mwenyewe
simjui ila anasema kuwa yeye ndiye aliyempeleka mama akatolewe kafara kwa madai
kuwa mama alikuwa mchawi ndio kwa kunithibitishia kamtoa huyu dada yetu kuwa
alichukuliwa msukule na mama” Wote walishangaa na ilikuwa ngumu sana
kuamini ingawa uwepo wa Yule dada uliwashangaza sana ila ilikuwa vigumu sana
kwao kuamini kuwa mama Jack alikuwa mchawi, ikabidi Yule kijana awaletee na ile
mifupa ambayo ilikutwa chumbani kwa mama yao. “Kwahiyo na wewe unaamini
kuwa mama alikuwa mchawi?” “Siamini ila kuna vitu
sivielewi” “Kama huamini huenda hata huyu dada alichukuliwa msukule na
huyo huyo rafiki wa mama, kesho tumpeleke kwa mganga, halafu tuendelee na
mipango ya dawa tuliyotoka nayo kwa mganga” “Hapana, mimi sitashiriki
hizo dawa na wala huyu dada msimpeleke kwa huyo mganga” “Kwahiyo
tumpeleke wapi?” “Yule mtu amekataa kabisa kuhusu swala la kumpeleka
dada kwa mganga wala mimi kushiriki dawa mlizokuja nazo” “Mbona
unatuambia mambo ya ajabu wewe, kama ukikataa shauri yako ila dawa tutafanya tu,
hakuna anayeamini kuwa ndugu yetu alikuwa mchawi na alimuuwa na kumfanya msukule
huyu mwanae mpendwa, lazima mwanae alichukuliwa na huyo huyo mtu wa ajabu lazima
twende tena kwa mganga” Walikuwa wanaongea ila huku wana hofu nyingi
sana kuhusu Yule dada aliyerudi maana wote walimshuhudia akizikwa, kwahiyo hofu
waliyokuwa nayo ilikuwa kubwa sana kiasi kwamba wote waliaga na kuondoka
wakijifanya wanarudi tena kwa mganga halafu pale nyumbani walimuacha Yule Yule
kijana na ndugu yake aliyetoka kwenye usukule kwani wote walikuwa
wanamuogopa. Neema alimpigia simu binti yake kuwa anarudi
nyumbani muda gani kwa siku hiyo maana alishaongea na mama Pendo kwahiyo alitaka
aongee na huyu binti yake ila binti yake alimshangaza sana kwani alimwambia kuwa
kwa wiki hiyo atalala kwenye nyumba ya baba yake, “Sasa wewe kwenye hiyo
nyumba ya baba yako unamfata nani wakati baba yako hayupo?” “Nawafata
hawa watu wa huku nimezoeana nao sana, wananihitaji niwe karibu
nao” “Unajua unanipa mashaka wewe Salome” “Mashaka ya
nini?” “Umeanza lini tabia ya kulala mbali na nyumbani?” “Basi
nitarudi” “Utarudi muda gani?” “Saa mbili usiku” Kisha
Salome akakata ile simu ila Neema alishukuru hata kwa huu muda aliyomwambia
kwani alihitaji sana huyu binti yake hata akutane na mama Pendo ili nae ajaribu
kumuhoji kidogo na kuona tofauti yake na kuangalia ni jinsi gani watamsaidia.
Neema akampigia simu mama Pendo na kumuomba afike kwake saa mbili usiku, naye
mama Pendo hakugoma bali alikubali kufanya vile. Rose alitupwa
getini kwake akiwa hajitambui kabisa, mlinzi akiwa anataka kutoka nje ili aende
dukani akashangaa kumkuta bosi wake amelala chini na akiwa ameumia sana na ubaya
zaidi hakujitambua, ikabidi mlinzi amuite Kulwa ambaye alikuja kisha wakaanza
kusaidiana ili kumbeba wamuingize ndani ila alikuwa mzito sana kiasi kwamba
aliwashinda kumbeba, Kulwa aliona ni vyema wakatafute msaada wa watu wengine
wambebe kwakweli iliwashangaza sana kwa Yule mama kuwa mzito kisi kile, ila
kabla Kulwa hajatoka kwenda kuomba msaada mara alifika Salome ila Kulwa
alipomuona Salome ikamjia kumbukumbu ya Moza alivyowajia siku maa yao aliwaambia
kuwa Salome ndiye Moza, kwahiyo kitendo cha kumuona tena Salome hapo kilimtia
mashaka Kulwa na kujikuta akiacha kufanya chochote na kukimbilia ndani, mlinzi
alikuwa anashangaa tu na kuuliza “Mbona amekimbia?” “Nikuulize
wewe maana mimi ndio nimefika sasa hivi” Mlinzi alitaka kwenda tena
kumjuita Kulwa ila alipofika mlangoni, akageuka nyuma na kumkuta Salome kambeba
mwenyewe Rose. Mlinzi alishangaa sana ila kila alipozidi kumuangalia
Salome akija na Rose ndani alimuona akibadilika na kuwa
Moza. Mlinzi alitaka kwenda tena kumuita Kulwa ila alipofika
mlangoni, akageuka nyuma na kumkuta Salome kambeba mwenyewe Rose. Mlinzi
alishangaa sana ila kila alipozidi kumuangalia Salome akija na Rose ndani
alimuona akibadilika na kuwa Moza.Hofu ilitawala kwa mlinzi kiasi kwamba
hakuweza kumuangalia tena na kujikuta akitimka mbio huku akipiga kelele, na
alitimkia ndani akabamiza mlango akiendelea na kelele zake. Kulwa akamuona
mlinzi mlangoni sebleni kwao akipiga kelele, akamuuliza kwa
mshangao, “Vipi wewe una mashetani?” “Kuna makubwa huko
nje” Alikuwa anaongea huku akitetemeka, “Makubwa
gani?” “Sijui, sijui kabisa” “Sasa wewe mlinzi gani mama
amekuweka muoga muoga hivyo? Sasa wewe ukiogopa kitu sisi tufanyeje? Hebu toka
hapo mlangoni tuone kuna nini” Doto nae alitoka ndani ili kuangalia zile
kelele zilikuwa za kitu gani, Kulwa alimtoa Yule mlinzi kwa nguvu na kufungua
mlango ila cha kushangaza hakuona chochote cha ajabu nje, akamuangalia mlinzi na
kumwambia, “Hivi wewe Lazaro una matatiozo gani, mbona hakuna chochote
cha kuogopa nje? Yani wewe sio mlinzi sio chochote, mtu mwenyewe muoga
tu” Doto aliuliza kuwa kuna nini lakini Kulwa alimjibu kuwa ni mawenge
tu ya mlinzi wao, sema Yule mlinzi alikuwa kimya kabisa kwani alipigwa na butwaa
asijue ni imekuwaje kuwaje na kujisemea moyoni kuwa ile nyumba ni ya kuondoka
huku akikumbuka kuwa alipoondoka alirudishwa kimazingara, alipofikiria hapo
alikosa raha kabisa na kujikuta akikaa chini tu. Kulwa na Doto walibaki
wakimshangaa na kuona kuwa anaanza kuchanganyikiwa. Wakakaa nae pale
sebleni huku wakimuangalia jinsi alivyotoa mimacho, mara kidogo wote wakashtuka
baada ya kumuona mama yao yani Rose akitoka maeneo ya chumbani huku akipiga
kelele ilionyesha kama alikuwa akitandikwa viboko na mtu ambaye haonekani ila
kilichosikika ni sauti ya viboko nay eye akipiga kelele, swala hilo
liliwachanganya sana mule ndani ukizingatia mama yao hakuwepo ndani, sasa
imekuwaje akitoka chumbani tena akionekana anatandikwa viboko huku akilia kwa
maumivu, wakajikuta wakikimbilia nje, ila Rose nea alikimbilia nje huku viboko
vikiendelea kumchapa, wakajikuta wakikimbia hovyo hovyo kwani mama yao alitafuta
msaada kwa yeyote aliyekuwa mbele yake, ila walipofika getini ili watoke nje
kabisa walishangaa kuwa geti lilifungwa kitu hicho kiliwastaajabisha sana na
kuwafanya waendelee kukimbia hovyohovyo, hadi mama yao akaanguka na kutulia huku
ile sauti ya viboko nayo ikiwa imetulia. Neema aliona usiku
umeingia ila mwanae hakuwa nyumbani na kumfanya ajiulize tena kuwa huyu mtoto
ana nini kiasi kwamba anashindwa kurudi nyumbani kwa wakati, ila wakati anawaza
hivyo akasikia mlango ukifunguliwa na Salome akiingia, “Jamani wewe
mtoto kwahiyo ndio saa hizi unarudi?” “Mama jamani kwani kuna ubaya
gani?” “Wewe ni mtoto wa kike halafu unasema kuna ubaya
gani!” “Basi nisamehe mama” “Mbona umekuwa mwepesi hivyo wa
kuomba msamaha!” “Kwahiyo mama ulitaka niendelee kubishana na wewe bila
kukuomba msamaha!” “Haya yaishe, kesho asubuhi mama Pendo anakuja
kutufata twende kule kwenye maombi. Tafadhali kesho usiondoke” “Sawa
nipo, sitaenda popote kesho” Kisha Salome akaelekea chumbani kwake, ila
Neema alimuangalia sana mtoto wake huyu bila ya kummaliza kwani vitu vingi sana
alikuwa kabadilika kiasi kwamba Neema alijikuta akipata mashaka, akainuka na
kwenda chumbani kwake huku swala la kuombwa msamaha na Salome
likimjia, “Salome ni mgumu sana kuomba msamaha, au ndio kukua! Kama ndio
kukua basin i vizuri maana kawa mtoto mzuri ingawa nina mashaka nae
mmmh!” Neema alijikuta akiwaza sana bila ya majibu, akatamani kumuuliza
maswali kadhaa mtoto wake ilia one atamjibu nini, kwahiyo akainuka tena na
kuongoza chumbani kwa Ssalome. Alipofika alifungua mlango akijua kuwa
Salome atakuwa amelala ila hakumkuta Salome kitandani, “Kheee ametoka
tena! Huyu mtoto jamani mbona ananitania. Yani arudi usiku na aondoke
tena!” Akarudishia ule mlango wa chumbani kwa Salome, na kumuangalia
kila mahali mule ndani ila hakumkuta na kupata uhakika kuwa ni wazi Salome
ametoroka nyumbani kwahiyo akaenda kukaa sebleni huku akisema atakaa hapo mpaka
pale Salome atakaporejea, akainuka na kufunga mlango kabisa na funguo ili
atakaporejea amsikie. Mishi akiwa na mume wake, leo alijipanga
kumwambia mumewe kuwa ana mimba ila alikuwa na hofu kubwa sana ya kumwambia kuwa
alibakwa, kwahiyo alianza kuongea nae kwa utaratibu, “Kuna jambo nataka
nikwambie” Huku machozi yakimlengalenga hata mumewe akawa na mashaka
kuwa ni jambo gani, “Nini tena Mishi wangu jamani!” “Mwenzio
nina mimba” “Wow, hilo ni jambo la kheri sana. Mungu amesikia kilio
changu” Yule mwanaume akamkumbatia Mishi kwa furaha, huku akimwambia
ataje zawadi yoyote akamnunulie kwani ni kipindi kirefu sana amekuwa akitafuta
mtoto kwahiyo swala la Mishi kupata mimba kwa kipindi kifupi hivyo kilimpa
furaha ya ajabu. “Sema zawadi utakayo nikakutafutie kesho mke
wangu” “Sitaki zawadi yoyote zaidi ya kunitunzia siri
yangu” “Siri! Siri gani tena” “Sitaki watu wajue kama nina mimba
mpaka pale itakapokuwa kubwa” “Sasa hiyo ni siri ya kukusumbua akili mke
wangu, usijali hakuna nitakayemwambia. Sema tu zawadi yoyote mke
wangu” Mumewe akamlazimisha sana aseme zawadi ikabidi tu Mishi aseme
zawadi kisha mumewe akamuahidi kuwa kesho ataenda kumnunulia zawadi hiyo, mumewe
alikuwa na furaha sana kiasi kwamba Mishi hakuweza kumwambia ukweli kuwa
alibakwa kabla ya ndoa yao, na mimba aliyonayo ni matokeo ya kubakwa na sio
sababu ya kuolewa. Mishi akakubaliana na moyo wake kuwa hatomwambia
ukweli wowote mume wake, ila gafla mumewe aliinuka na kwenda chumbani halafu
Mishi nae alijisikia kutapika na kutoka nje. Yani alipofika nje hali
yote ya kutapika iliisha, kichefuchefu chote kiliisha kwani mbele yake alimuona
Salome na kumfanya aogope sana, “Unaogopa kwavile hutaki kumwambia
ukweli mumeo. Mwambie ukweli mume wako uone kama mimi nitakufata
tena” “Kwani wewe ni binadamu wa kawaida?” “Hilo halikuhusu
kabisa kabisa, unachotakiwa kufanya ni kumwambia ukweli mumeo, mwambie kuwa una
mimba ya kubakwa” “Naogopa” “Unaogopa nini? Unaogopa mimba ya
kubakwa! Mbona wakati ulikuwa ukichanganya vijana wa watu hukuogopa? Umewaweka
roho juu vijana wa watu wote wakikufikiria wewe, je wewe ndiye msichana mrembo
pekee ulimwenguni? Mwambie ukweli mumeo, na ole wako uanze kumchanganya mumeo na
vijana wengine nitakufundisha pia. Haya niambie mumeo utamwambia ukweli
humwambii?” “Nitamwambia” “Tena umwambie leoleo, Yani
unavyoingia ndani tu umwambie” Mishi aliitikia kwa kichwa tu kuwa
atafanya hivyo na akaona ni wazi kama asipofanya hivyo huyu mtu ataendelea
kumsumbua sumbua, muda kidogo Salome aliondoka halafu mume wa Mishi nae alitoka
pale nje ila Mishi alimdanganya kuwa alitoka kupunga upepo kidogo na kumtaka
warudi tena ndani huku akijaribu tena kuongea nae, “Kuna jambo nataka
nikwambie sijui utanichukuliaje?” “Jambo gani tena?” Mishi
alimueleza mumewe kwa kirefu kidogo ya jinsi alivyochanganya wale mapacha na
jinsi alivyopewa laana na mdada aliyemkuta nyumbani kwa wale mapacha na jinsi
alivyobakwa na kujikuta kuwa ana mimba, “Mmmh tuseme hiyo mimba ni ya
kubakwa?” “Ndio” “Na huyo binti anayekutokea tokea ni binti wa
aina gani?” “Nilimkuta tu nyumbani kwa wale mapacha na ndio akanipa
laana hadi nikabakwa na akaja kuniambia kuwa nina mimba tayari” “Mmmh
hayo mambo sio ya kawaida, sasa kesho nitakupeleka
mahali” “Wapi?” “Tulia tu, nitakupeleka mahali kesho maana hivyo
vitu sio vya kawaida. Huyo binti ni jinni hilo, na laana ya majini sio ya
kuichekelea, yani tutaenda mahali hata usijali usikute wala huna
mimba” Mishi alihisi tu anaambiwa na mumewe kuwa wataenda kwa mganga,
ila kwa upande mwingine alifurahia kwani alijua ndio utakuwa mwisho wa Yule
binti kumfatilia fatilia. Nyumbani kwa Rose, walisaidiana
kumuingiza mama yao ndani, huku wakiwa na hofu kubwa na kutamani kuongea nae
kuwa kulikoni, “Mama pole sana, kitu gani kimekupata?” Mama yao
alikuwa kimya, na kuwafanya wagundue kuwa mama yao kaumia mdomoni ndiomana
hawezi kuwajibu kitu chochote, walikaa nae pale sebleni ila kiukweli walikuwa na
wasiwasi mkubwa sana, kwa wakati huo hata Yule mlinzi wao nae aliogopa kwenda
kukaa getini, ilibidi wamuulize naye kwa makini, “Uliona nini na
wewe?” “Nilimwona mama yupo chini akiwa hajitambui, nikawa nakuja ndani
ili nikuite tukambebe ila kabla sijafika sijui kinini kikanishawishi kugeuka
nyuma, mara nikamuona Salome akiwa kambeba mwenyewe mama wakati mimi
nilimshindwa alikuwa ni mzito sana halafu kadri Yule Salome alivyokuwa akisogea
alikuwa akibadilika na kuwa kama Mo…..” Kulwa alimzuia mlinzi asiendelee
kuongea, “Ishia hapohapo tushakuelewa, usituletee makubwa bure. Usiku
ushaingia sasa” Doto akamuulizia Ana, “Hivi na Ana yuko
wapi?” “Yupo chumbani kwake toka asubuhi, ila Yule mtoto anajijuaga
mwenyewe” Wakakubaliana kwa pamoja kuwa usiku huo walale wote sebleni
hapo ukizingatia hata mlinzi alishagoma kulala kwenye lindo
lake. Palipokucha asubuhi waliamka ila mama yao hakuwa pale
sebleni na wakahisi kuwa ameenda chumbani, “Au mama aliamua kwenda
kulala chumbani!” “Jamani ningekuwa mimi nisingeweza yani kupigwa kote
kule ila mama bado kaenda kulala chumbani! Kwakweli ningekuwa mimi nisingeweza
jamani” “Tumetofautiana mioyo, Lazaro kaona maajabu tu kaogopa kwenda
kulala kwenye lindo lake” “Ila inataka moyo nyie, yani haya mambo ni
makubwa ila wenyewe tunayachukulia kawaida” “Sio tunayachukulia kawaida
ila hatuna cha kufanya, tukiondoka tunarudishwa unafikiri
tutafanyaje” Mlinzi ndio akashangaa hapa kuwa hata hawa nao wakiondoka
wanarudishwa ila Doto akasema, “Jamani mbona Sara kafanikiwa kuondoka na
hajarudishwa?” Ana akafika pale sebleni na kudakia zile habari za
Sara, “Jamani Sara sio kwamba ameondoka hapa nyumbani ila Sara kafungiwa
na mama” “Kafungiwa na mama!” “Ndio kafungiwa na mama, yani mama
ndiye mtu pekee wa kumtoa Sara. Hajatoroka wala nini, yupo humu humu ndani ila
kafungiwa na mama” Kulwa na Doto wakapata picha ya kile chumba ambacho
Sara aliwahi kuwaonyesha na wakaganda huko, moja kwa moja wakajua kuwa ni chumba
kile kile amabacho mama yao amemfungia Sara. Ila Ana alivyomaliza kuwaambia hayo
aliondoka zake na kwenda jikoni kisha kwenda chumbani kwake. Kulwa na
Doto walitazamana kisha wakamwambia mlinzi, “Inabidi ukatusaidie
sasa” “Sasa niwasaidie kufanyeje?” “Kumtoa
Sara” “Tutamtoaje?” “Twende tukakuonyeshe” Walienda
mpaka mlangoni mwa chumba kile na kuchukua fungua kisha kufungua na kuingia
ndani ya kile chumba, halafu wakamwambia mlinzi, “Umeona pale nyuma ya
kabati kuna mlango mwingine, sasa ule mlango ndio yupo Sara. Nenda kaufungue
umtoe” “Kheee nyie vipi, kwanini msiende kufungua na kumtoa
wenyewe!” “Sisi haturuhusiwi” “Na mimi siwezi” Yule
mlinzi akatoka nje ya kile chumba, ila alipopiga jicho pembeni akamuona mama
mwenye nyumba yani Rose akija kule walipo huku amevaa
kaniki. Neema aliamka pale sebleni kwahiyo siku hiyo alilala
pale sebleni huku ameshika funguo, alipoamka akakumbuka matukio vivuri
sana, “Yani huyu mtoto hajarudi mpaka muda huu!” Akainuka na
kwenda kuchungulia tena chumbani kwa Salome, akashangaa kwani alimkuta amelala,
akaangalia ufunguo wake mkononi ambao ulikuwa vilevile alivyoushikilia toka
mwanzo, hilo swala lilimfanya ashikwe na hofu huku akijiuliza, “Amepitia
wapi huyu mtoto wakati milango yote nilikuwa nimefunga?” Akatoka haraka
chumbani kwa Salome huku uoga mwingi ukimjaa, mara akasikia mlango wa sebleni
ukigongwa na kuhisi kuwa huenda ni mama Pendo amefika ingawa alishangaa kuwa
mbona ni mapema mno, akaenda kufungua na kushangaa ni Salome ndio alikuwa
amerudi. Akatoka haraka chumbani kwa Salome huku uoga
mwingi ukimjaa, mara akasikia mlango wa sebleni ukigongwa na kuhisi kuwa huenda
ni mama Pendo amefika ingawa alishangaa kuwa mbona ni mapema mno, akaenda
kufungua na kushangaa ni Salome ndio alikuwa amerudi. Neema alishindwa
kabisa kuvumilia na kujikuta akipiga kelele kwa uoga aliokuwa nao kwani kilikuwa
ni kitu cha ajabu sana machoni pake, ila Salome alimuuliza “Vipi mama
mbona hivyo?” Alikuwa akiongea huku akimsogelea ila Neema aliendelea
kupiga kelele huku akisema, “Usinisogelee, usinisogelee kabisa. Wewe ni
nani?” “Jamani mama imekuwaje tena? Mimi si mwanao
Salome?” “Hapana” Neema alikimbia na kuelekea chumbani kwake,
yani leo hata kuwaamsha wale wanae kwaajili ya shule hakufanya hivyo, kisha Yule
Salome nae alielekea chumbani kwake. Neema akiwa chumbani kwake
akachukua simu na kumpigia simu mama Pendo huku akihema sana ila simu ya mama
Pendo haikupatikana hewani na kuzidi kumchanganya, ikabidi amtumie ujumbe mfupi
ili akiwasha tu simu basi apate ule ujumbe, alikuwa na mashaka sana ila baada ya
muda kidogo akashikwa na usingizi na kulala. Mlinzi alipomuona
Rose akija halafu amevaa kaniki akaogopa sana kwani ni wazi ilionekana uchawi
wake bila chenga, mlinzi alimuangalia kwa hofu kubwa sana huku uoga ukimtawala
na kusema kuwa akimbie au afanye nini ila cha kushangaza Rose alimpita Yule
mlinzi kama hamuoni kisha akaingia kwenye kile chumba ambamo walikuwemo Kulwa na
Doto ila nao walishangaa kumuona mama yao akiwa amevaa kaniki ambapo aliwapita
nao kama hawaoni vile, kitendo kile kiliwashangaza sana wakabaki wakiangaliana
ila hawakuondoka kwani walitaka kujua kuwa mama yao ameenda kufanya
nini. Wakamuona akikaa chini kisha kuita vitu vilivyokuja kama dawa,
halafu akapuliza ambapo kabati lile lilisogea halafu ule mlango wa kile chumba
ulifunguka, Kulwa na Doto walishangaa sana na kujikuta wakitaka kusogea zaidi
kwenye kile chumba ili kuona kuna nini ndani yake, ila kabla hawajasogea alikuja
Ana kwa haraka sana na kuwashika mikono kisha akawatoa nje kinguvu na
kuwaambia, “Nyie msithubutu
kusogelea” “Kwanini?” “Tuondokeni” Akawavuta kaka zake
mikono hadi sebleni ambapo Yule mlinzi nae alifata nyuma, “Mmemuona pale
mama sio akili zake zile, kashapandwa na kinyamkera yani anaweza akafanya kitu
chochote pale bila kutarajia. Msishangae hajawaona, ila nyie mmemuona sababu
kuna dawa iliwekwa leo na mtu anaetikisa nyumba hii. Subirini mama akitoka akiwa
na akili zake timamu, tumwambie ya kuwa wote tumemuona alichokuwa anafanya, ila
kitendo cha nyie kutaka kuingia kule
kitawamaliza” “Hatukuelewi” “Nieleweni tu, mnajua Sara yuko
wapi? Nadhani mnajua kuwa Sara amepotea kwenye mazingira ya kutatanisha, mnajua
kapotea vipi? Je mama alitaka kumpoteza na Sara? Hapana, hata yeye kitendo cha
kupotea Sara kinamuuma sana, ila kitendo cha kuachia watu kwenye chumba hiko
kinamshinda sababu kitayagharimu maisha yake, ila tunatakiwa kusimama pamoja.
Mama akiwa tu na akili zake timamu yani kinyamkera kikimtoka tumwambie ukweli
kuwa tumemuona halafu akibisha nitawaambia cha kufanya” “Kwanini
usituambie kabisa maana mama kubisha ni lazima” “Sitakiwi kuwaambia sasa
hivi ila nyie jueni kuwa nipo upande wenu” Walitulia wakimsikiliza Ana
kwani waliamini kuwa Ana anajua mambo mengi kupita wao, ila mlinzi akawaambia
jambo, “Jamani zamani nilipokuwa mtoto nilikuwa napelekwa kanisani, na
nilifundishwa kuwa vitu vya ajabu vikitokea yatupasa kufanya sala ila toka
nianze kazi kwenye nyumba hii sijawahi kuwaona mkienda kanisani wala msikitini,
tuseme nyie hamna dini?” Ana akamjibu, “Hebu tutolee habari zako
na wewe, mbona wewe huendagi Kanisani wala Msikitini tuseme na wewe huna dini
au? Badala ya kuangalia jinsi gani tutapambana na haya mambo kwenye nyumba yetu
unatuletea habari za makanisa hapa” Yule mlinzi ilibidi tu awe kimya
kwani hakuweza kuendelea kubishana na vitu ambavyo hata yeye mwenyewe alikuwa
havijui. Neema alipoamka alijikuta kasahau kila kitu hata
kuhusu kutokuwaamsha wanae waende shule alikuwa amesahau huku akijua kuwa
alishawaamsha wakaenda shule na yeye akarudi kulala, kwahiyo muda huu alioga na
kujiweka sawa kisha kuanza kuandaa kifungua kinywa huku akisema kuwa yani Salome
ametoka bila ya kumuaga, wakati anaandaa chai sebleni akakuta barua mezani kwake
ikiwa imeandikwa kwa maneno machache tu, “Kwako mama mpendwa, mimi
naenda kuishi kwenye ile nyumba aliyokuwa akiishi baba yangu, nina maana yangu
ya kufanya hivi. Nitarudi nikiwa nimekamilika. Kwaheri, ni mimi mtoto wako
mpendwa Salome” Neema alishangaa sana kwa uamuzi huo uliochukuliwa na
Salome, “Ataendaje kuishi kwenye nyumba ambayo hata baba yake hayupo, si
ndio watamuua huko jamani? Kwanini kaamua kufanya hivi Salome?” Halafu
sasa akagundua kuwa hiyo sehemu wala haijui sababu hajawahi kufika zaidi ya siku
waliyoenda kwenye msiba wa Moza na waliishia katikati sababu walikuta ndio
wanaenda kuzika kwahiyo swala la yeye kufika nyumbani kwa Rose lilikuwa ni gumu
sana, akaamua kunywa chai kwanza kisha kuchukua maamuzi mengine. Alipomaliza
kunywa chai aligundua kuwa lile karatasi lenye ujumbe lilimwagikiwa na chai
hivyo akachukua maamuzi ya kulitoa pamoja na vyombo vichafu kisha akaenda
kulidumbukiza chooni. Kisha alienda kuchukua simu yake na kukaa sebleni ili
ampigie Patrick na kumpa hiyo habari ila alipochukua alikutana na ujumbe kutoka
kwa mama Pendo, “Pole sana kwa maswahibu hayo ndugu yangu, ambayo
kiuhalisia naona kama ni kiini macho kwakweli ila leo nitakuja na mchungaji hapo
kwako. Mwambie mwanao asitoke, tunakuja kufanya maombi” Neema alikuwa
akishangaa huu ujumbe kutoka kwa mama Pendo kwani hata yeye hakuwa na kumbukumbu
kuwa ni maswahibu gani aliyokuwa amemueleza mama Pendo, “Kwani mama
Pendo anaongelea kuhusu maswahibu gani jamani, kwani kuna maswahibu yoyote
yamenipata au kaoteshwa huyu?” Alijiuliza bila ya jibu sababu hakuwa na
kumbukumbu ya aina yoyote ile kichwani mwake yani hata swala la kukumbuka kuwa
alimkuta Salome amelala na gafla akamkuta mlangoni akigonga mlango haikuwepo
hiyo kumbukumbu katika akili yake kabisa. Kama ambavyo Mishi
aliahidiwa na mumewe kwahiyo asubuhi asubuhi waliondoka na kwenda kwa mtaalamu
lengo lilikuwa ni kuangaliziwa kuhusu huyo binti halafu na kuangaliziwa kuhusu
mimba aliyokuwa nayo Mishi, walimkuta mganga na wateja wachache tu na walipoisha
waliingia wao na kuanza kumuelezea matatizo yao, “Yani cha kuwaambia tu
huyo mtu ambaye mmeleta malalamiko yenu hapa, yupo nje
anawasubiri” “Anatusubiri!” Walishtuka sana, “Ndio
anawasubiria” “Sasa tutafanya nini?” “Sio mtu mzuri Yule, ila
yupo kwaajili ya kumkomesha mtu mmoja tu sema ukijiingiza kwenye familia hiyo
imekula kwako kwahiyo na nyie swala la kuja kwangu ili niwasaidie itakula kwangu
na kwenu” “Tusaidie mganga, mi sioni kama mimba hiyo ina ukweli kwa mke
wangu” “Laiti kama mkeo akitoa hiyo mimba kaa ukijua kuwa si wewe wala
mkeo utaweza tena kuwa na watoto katika maisha yenu. Mkeo alikuwa na makosa
ndiomana akapewa hiyo adhabu” “Makosa gani?” Mishi alianza kuona
aibu kwani hakumwambia ukweli mume wake kuhusu makosa yake mpaka kufikia hatua
ya kubakwa ila alimwambia tu kuna vijana mapacha walidhania kuwa anawachanganya
ndio huyo mtu akampa laana hiyo, basi Yule mganga akamuangalia Mishi na
kumuuliza, “Je nimwambie kuhusu makosa yako?” Mishi alitikisa
kichwa kwa ishara kuwa asimwambie, ila Yule mganga aliendelea, “Hata
nisipomwambia, ilimradi anawasuburia nje, basi napo atamwambia tu. Bora
nimwambie mimi” Mume wa Mishi akamuomba mganga amwambie maana alihisi
kufichwa mambo mengine, ila Mishi aliona aibu sana na kuinuka kisha akatoka nje,
ila mumewe bado alikomaa kuwa aambiwe, Yule mganga aligoma kusema sababu
muhusika kainuka, “Yani mimi kusema siwezi maana mwenyewe kainuka lakini
mfate tu mtaonana na Yule mtu na atakwambia ukweli maana hatakuficha
lolote” Ikabidi mume wa Mishi ainuke tu ili amfate mkewe nje maana mkewe
alishatoka eneo hilo, ila alipofika alipo mkewe alishangaa kumuona mkewe
kasimama na binti Fulani ambaye yeye hakumjua binti huyo, ikabidi awafate ila
huyu binti kabla hata ya salamu alianza kumwambia mume wa Mishi, “Mkeo
nimempa adhabu hiyo sababu amekuwa akiumiza moyo wa wenzie sana, bora angekuwa
anajiuza tungejua moja kuliko alichokuwa anafanya huyu. Yani anakuwa na wanaume
zaidi ya watano kwa wakati mmoja halafu wote anawadanganya kuwa anawapenda, je
ni nafasi za mabinti wangapi anaziziba ambao wangependwa na hao wanaume? Ile
familia aliumiza mioyo ya watu watatu, sasa ni zamu yake nay eye kuumia moyo.
Kuhusu wanaume wengine aliokuwa nao atakwambia mwenyewe, huyu mkeo ni zaidi ya
wanawake wanaojiuza ila nimemwambia akithubutu kufanya hivyo na kwenye ndoa yenu
nitamkomesha” Kisha Salome akaondoka na kuwaacha, Mishi alikuwa na aibu
sana. Mumewe akamuangalia kwa jicho la gadhabu na kumwambia, “Kumbe
nimeoa changudoa, mwenyewe nilijisifu kuwa mwanamke anamsimamo hataki nimuoe
ananipima kwanza kumbe ni changudoa. Kwakweli Mishi umeniangusha sana, yani
unajua uovu ulikuwa unautenda nab ado bila ya aibu unataka tuje kwa mganga wa
kienyeji ulidhani afanyeje sasa na wakati una laana? Unafikiri machozi ya watu
wote uliowaliza yameenda bure? Tena uwe mpole kabisa maana ukileta kidomo domo
chako nitawaeleza ndugu zako wote ukweli kuwa ulibakwa” Mume wa Mishi
akaondoka zake ikabidi Mishi amfate nyuma huku aibu tele ikimshika moyoni kwani
hakutegemea kama angeaibika kwa kiasi hicho, alikuwa akitembea kwa aibu tele
tele usoni. Nyumbani kwa Neema alifika mama Pendo na mwanaume
mmoja na wanawake wengine wawili ambao mama Pendo aliwatambulisha kwa Neema kuwa
ni wana maombi, ambapo Neema aliwakaribisha vizuri sana na baada ya salamu za
hapa na pale mama Pendo sasa akamwambia Neema, “Hebu sasa elezea vizuri
ili hawa watu nao wakusikie kuwa ilikuwaje jana usiku” “Ilikuwaje
kivipi?” “Si kama vile ulivyonielezea kwenye ujumbe,hebu jaribu kuelezea
vizuri” “Ujumbe gani?” “Kheee wewe Neema vipi tena una matatizo
gani?” Ikabidi mama Pendo achukue simu yake na kujaribu kusoma ambacho
aliandika Neema ili Neema ajue hata anazungumzia nini, “Ndugu yangu nina
matatizo, nakutafuta hewani hupatikani. Mwanangu jana hakuwepo nyumabni
nikafunga milango yote cha kushangaza asubuhi nimekuta chumbani kwake halafu
gafla mlango uligongwa halafu aliingia yeye ndani kwakweli hiyo kitu
imeniogopesha sana, naomba mnisaidie maombi nipo njiapanda” Ila bado
Neema alionekana kushangaa kanakwamba hata haelewi kinachosomwa au kuzungumzwa
kisha akamwambia mama Pendo, “Unajua hata nimeshangaa ujumbe ambao
umenitumia ukinipa pole, nikajiuliza pole ya nini tena. Yani sikumbuki kabisa
kama nilikuandikia hiyo meseji na wala sikumbuki kama kuna jambo kama hilo
lilitokea” “Kwahiyo wewe unakumbuka nini?” “Nakumbuka kuwa usiku
ulifika nikalala, na kuamka asubuhi nikakuta ujumbe wako hata sielewi kama
nilikutumia ujumbe” Wale watu wengine wakawa wanamshangaa Neema kama
ambavyo yeye alikuwa akiwashangaa wao, ikabidi wamuulize swali, “Kwani
huyo binti yako yuko wapi?” “Yani kuhusu binti yangu alipo, nimekuta tu
ujumbe wake leo kuwa ameondoka anaenda kuishi nyumbani kwa baba yake yani
hajaniaga kwa mdomo ila kaniachia ujumbe huo tu” “Ujumbe wenyewe uko
wapi?” “Kwa bahati mbaya kile kikaratsi nimekitupia chooni maana
kiliingia chai” “Basi kalete nguo ya mwanao ili tuiombee halafu akija
umpe aivae” “Sawa, ngoja nikalete” Neem aliinuka na kwenda
chumbani kwa Salome, akafungua na kushangaa sana kwani kule chumbani palikuwa na
kitanda na godoro tu, vitu vyote vya Salome havikuwepo yani nguo zake zote hata
begi lake dogo halikuwepo yani Salome alikuwa kahama mazima
kabisa. Alipigwa na butwaa haswaa akarudi sebleni akiwa amenyong’onyea
vilivyo ikabidi wamuulize kuwa imekuwaje tena, “Eti mwanangu kaondoka na
kabeba nguo zote” “Halafu wewe hujui?” “Ndio nilikuwa sijui, si
ndio ujumbe tu nimekuta ameniandikia” “Ila Neema nilikwambia mapema
kabisa kuwa mwanao kutakuwa na tatizo sio swala la kawaida, kwanza mtoto akatae
shule, halafu awe anatenda vitu vya ajabu lazima kuna kitu” Yule
mwanaume waliyeenda nae akasema, “Kuna kitu kweli, tena sio cha kawaida
kabisa. Naomba tuondoke tu halafu tufunge juu ya jambo hili, na wewe mama mtu
ufunge” “Mmmh kufunga tena jamani, kwani haiwezekani kuomba tu bila
kufunga?” “Hata kwenye biblia kwenye Mathayo 17:12 inasema (lakini namna
hii haitoki, ila kwa kusali na kufunga). Ikimaanisha kuwa kuna maombi mengine
tunatakiwa kufunga na kuomba” “Jamani, sasa si mtafunga nyie tu wana
maombi mpaka mimi nifunge jamani!” “Hata wewe ni mwana maombi
Neema” “Ila kufunga siwezi mwenzenu yani njaa itanisumbuaje, siwezi
kwakweli” Ilibidi mpaka mama Pendo acheke maana Neema alivyotia huruma
kwa kigezo cha njaa ni balaa, yani alionyesha wazi kuwa hilo swala linaloitwa
kufunga kwake ni mtihani mzito. “Yani wewe Neema itabidi nije nikupe
somo kwakweli, kufunga ni kuzuri kunatuweka karibu na Mungu na pia tunasaidia
miili yetu wenyewe. Yani wewe huwezi kuacha kula kwa masaa machache tu jamani
kwaajili ya kujiponya mwenyewe! Natakiwa nikupe somo kwakweli” “Basi
mimi naomba tu mfanye maombi kwaajili ya mwanangu, swala la kufunga nitajifunza
taratibu taratibu. Mwenzenu njaa jamani yani kufunga siwezi kabisa, ikifika saa
tano tu asubuhi nahisi njaa balaa, sasa kufika hadi jioni si mtaniua mwenzenu
jamani. Nawaomba tu mmuombee mwanangu” Hawa walimuona huyu mama kuna
vitu vimemfunga katika maisha yake ikabidi wakubali kuwa wao ndio wabebe dhamana
hiyo, kisha Neema akawaomba wafanye maombi kwenye nyumba yake kwanza kabla ya
kuondoka. Kulwa, Doto, na Yule mlinzi walikuwa sebleni muda
huu, mara mama yao nae alitoka ikionekana kashamaliza kazi yake kwenye kile
chumba chake cha siri, alipofika tu sebleni kabla hata ya salamu Kulwa alianza
kumwambia mama yake, “Mama tumeona yote uliyokuwa unayafanya, mama kuwa
na huruma japo kidogo. Sara ni mtoto wako tunamuhitaji Sara” “Sasa kwani
Sara mi nimpeleke wapi?” “Mama, usitugeleshe. Tunajua fika kuwa Sara
umemfungia kwenye chumba cahko cha siri na watu wengine. Tunamtaka Sara
mama” “Nyie watoto, mimi ni mama yenu mjue. Msiniletee habari ambazo
hamna ushahidi nazo” Rose akawa akielekea mlangoni ila alivyofungua
mlango tu alianza kupiga kelele huku akirudi kwa nyuma, “Moza amerudi,
Moza amerudi, Moza amerudi” Watoto wake wakashikwa na hofu ya hali ya
juu huku kila mmoja akiogopa, ila wakasikia hatua za mtu akiingia
ndani. Rose akawa akielekea mlangoni ila alivyofungua
mlango tu alianza kupiga kelele huku akirudi kwa nyuma, “Moza amerudi,
Moza amerudi, Moza amerudi” Watoto wake wakashikwa na hofu ya hali ya
juu huku kila mmoja akiogopa, ila wakasikia hatua za mtu akiingia
ndani. Hakuna aliyeona kuwa kuna yeyote akiingia ndani zaidi ya zile
hatua tu, Rose nae alikuwa ameganda vilevile mlangoni na baada ya muda akaanguka
na kuzimia ikabidi wamsogelee na kuanza kumpepea. Baada ya muda
alizinduka na swali la kwanza alilowauliza wanae, “Moza yuko
wapi?” “Unaongelea nini mama?” “Mwambieni Moza simuogopi,
ananitisha sana ila simuogopi. Niitieni Moza hapa” Walimshangaa mama yao
na kuona amechanganyikiwa kwli, ni kweli kulikuwa na hisia kuwa anayewasumbua
humo ndani ni Moza na hata amewahi kuwatokea na kuwatahadhalisha kuwa wasihame
nyumba yao ila kwa siku hiyo ya kuwa Moza yupo ndani kwao hawakuwa na uhakika
kwahiyo waliona mama yao anaongea kama mtu aliyechanganyikiwa. Ila Rose
aliendelea kuongea akidai kuwa aitiwe Moza, “Kamuiteni Moza
huko” “Tukamuitie wapi mama?” “Nendeni chumbani kwake
mkamuite” “Mmmh mama jamani, kule chumbani kwake labda uende wewe
mwenyewe si umesema kuwa humuogopi kwasasa basi nenda” “Sijaamua tu
kwenda ila simuogopi, ananichezea sana akili zangu tangu amerudi, nimejipanga
kwa mapambano simuogopi” Mara kimya kikatawala ndani yani hakuna
aliyeongea chochote kile halafu Rose alionekana kuanza kuogopa jambo Fulani
sababu alikuwa akisikika yeye tu huku akisema, “Nisamehe tafadhali
nisamehe, naomba unisamehe nitawaachia. Unaniumiza nisamehe
tafadhali” Walizidi kuona kuwa mama yao anachanganyikiwa sasa, na gafla
akazimia tena. Ila muda huu wakapata wazo kuwa wambebe na wampeleke chumbani
kwake wakamlaze, ila Kulwa alitoa wazo lingine, “Hivi kwanini tusimbebe
na kumpeleka chumbani alikokuwa analala Moza maana mama inaonyesha anakisasi na
huyo mtu, kwahiyo ni vyema tukimpeleka huko ili akishtuka na kujikuta huko
atamalizana nae.” Wakajikuta kwa pamoja wakikubaliana swala la kumbeba
na kumpeleka chumbani kwa Moza. Nyumbani kwa Neema waliamua
kufanya maombi kwa kifupi sana kisha kuagana na Neema halafu wao wakaondoka ila
mama Pendo alibaki kidogo na Neema akizungumza nae, “Ndugu yangu
jitahidi hata kwa siku moja tu ujinyime kula na ufunge, tesa tumbo lako kwa siku
hata moja upate majibu ya kile unachokihitaji” “Inamaana mfungo wa siku
moja unatosha?” “Unatosha ndio ila ni muhimu kufunga kwa siku nyingine
zaidi, kufunga sio kazi kama unavyodhani ndugu yangu. Tusijiendekeze na
kula, tunatakiwa kuwa kwenye mfungo ili kuwa karibu zaidi na Mungu wetu, Neema
jitahidi utaweza. Unadhani ni jambo la kawaida hilo? Mtoto hataki shule, wewe
mwenyewe unafanya vitu na kusahau. Haya sasa mtoto kahama nyumbani, yani bado tu
huoni kama sio kitu cha kawaida hicho? Hiyo hali sio ya kawaida kabisa ndugu
yangu, tunatakiwa kukazana na maombi tu” “Sawa nitajitahidi basi ndugu
yangu” Basi mama Pendo alijaribu kumshawishi pale halafu aliondoka. Muda
kidogo walirudi wale mapacha wa Neema, na kumsalimia mama yao, ikabidi awaulize
maswali mawili matatu, “HIvi leo nani aliwaamsha kwenda
shule?” “Ni dada ndio alituamsha na kutusaidia kujiandaa
leo” “Jana je!” “Jana pia ni dada ndio alituamsha” Neema
akawa kimya kwa muda na kuwauliza tena watoto wake, “Je kuna kitu
chochote ambacho hamkielewi kuhusu dada yenu?” “Hakuna kitu mama, ila
mimi toka siku ambayo mamdogo Ashura kaanguka halafu dada akasema kuwa walikuwa
wanacheza, na siku hiyo hiyo tukahamia hapa halafu dada akasema kuwa mamdogo
Ashura kasafiri basi sijawahi kumuelewa dada tangia hapo” “Kwanini huwa
humuelewi?” “Simuelewi tu, zamani alikuwa anakuja mara kwa mara chumbani
kwetu na alikuwa akipenda kutuhadithia hadithi ila nakumbuka toka siku umerudi
nae na kumkuta amelala chumbani kwetu halafu ukamwambia kuwa ni chumbani kwetu
basi hajawahi tena kuja kutubembeleza kama zamani” “Mmmh mnanifungua
macho kwa kiasi fuylani, mnajua dada yenu kahama hapa nyumbani, kasema atarudi
hadi akimaliza mambo yake” “Halafu kuna jirani yetu mmoja wa kule
niliwahi kumsikia akimwambia dada kuwa mbona sio Salome
waliyemzoea” “Kwahiyo nyie mnahisi ni nini?” “Sijui labda dada
kabadilika siku hizi” Akawaruhusu tu watoto wake waendelee na mambo
mengine maana kichwa chake kwa wakati huo kilikuwa kibovu kabisa maana kila
alichofikiria alikosa jibu, mwishowe aliinuka tena na kwenda kwenye chumba
alichokuwa akilala Salome, alikiangalia kile chumba na kuangalia kitanda vizuri
ila haikuwepo nguo yoyote ya Salome, wakati anaangalia angalia chumba cha Salome
kuna ujumbe mfupi alisikia ukiingia kwenye simu yake, akafungua na
kuusoma, “Mama, nimeondoka nyumbani ndio ila sio vizuri kwa wewe
kuchunguza chunguza chumba changu” Neema aliangalia kushoto na kulia
kisha akatoka kwenye kile chumba cha Salome akiwa na wasiwasi kidogo kuwa huyu
mtoto amejuaje kuwa atakuwa anachunguza chumba chake, “Mmmmh labda
amehisi tu, sijui” Aliamua kwenda chumbani kwake maana alihisi
kutokuelewa elewa baadhi ya mambo. Walisaidiana kumbeba Rose na
kwenda kumlaza chumbani kwa Moza kama ambavyo walikuwa wamekubaliana, walimlaza
kwenye kitanda cha Moza na kutoka kuelekea sebleni, ila kila mmoja hakujua ni
kwanini walipata lile wazo la kwenda kumlaza mama yao kwenye chumba cha
Moza. Wakati wamerudi sebleni alifika Ana na kuwauliza kuhusu mama
yao, “Mama bado hajatoka ndani?” Wakamuelezea ilivyokuwa hadi
kufikia hatua ya kumpeleka mama yao kwenye chumba alichokuwa analala
Moza, “Kheee nyie mna akili kweli?” “Kwanini
tena?” “Yani nyie ni zero kabisa, kumbukeni Moza alikufa na kifo chake
kimekuwa na utata mkubwa sana. Nyumba yetu imekuwa ikigubikwa na mambo ya ajabu
kila leo, halafu kuna siku tulisikia kabisa sauti ya Moza ikiongea na kusema
kuwa tukihama tutarudishwa, halafu nyie bila hata ya huruma mnathubutu kwenda
kumuweka mama chumbani kwa Moza akiwa amezimia? Hivi mama Yule mnampenda au?
Mama ni mama hata akiwa mchawi bado ni mama, kumbuka ametuzaa na kutulea, na
asingeweza kututoa kafara tulipokuwa watoto, kitendo cha mama kutuacha hadi leo
inamaana anatupenda sana, hivi nyie mmekosa huruma hata
kidogo?” “Unatulaumu bure Ana, mama mwenyewe alisema Moza yupo humu
ndani tumuitie Moza hamuogopi, halafu mama kazimia unadhani
tungefanyaje?” “Mmeshindwa kumuacha hapa hapa sebleni au basi
mngempeleka chumbani kwake” “Dah hata sijui nini kimetupitia mpaka
tukakubaliana kumpeleka kule, twendeni basi tukamtoe” Walitazamana ila
walijikuta wakisita, maneno ya Ana yaliwaingia vilivyo kuwa walichofanya si
sahihi ila sasa hawakujua kuwa kitu gani wanaweza wakafanya na kikawa sahihi kwa
siku hiyo, wakawa wanaambizana waende chumbani kwa Moza ili wakamtoe mama yao,
ila hakuna aliyeweza kusogeza hata mguu wake kwani wote walijikuta wakisita, Ana
aliwatazama na kuwaambia, “Mbona mnasita nendeni sasa
mkamtoe” Bado walikuwa wakisita yani kila mmoja aligubikwa na uoga wa
hali ya juu hata wakabaki na mshangao tu kuwa imekuwaje mpaka waogope kiasi
kile, “Nyie wengi hivyo mnaogopa, ila mama peke yake mmeenda kumuacha
kule. Ni nani awezaye kulala kwenye kile chumba baada ya mambo yote haya? Kwa
hakika hakuna awezaye kulala pale, nendeni mkamtoe mama. Naenda chumbani kwangu,
nitakaporudi muwe mmemtoa lasivyo nitakachowafanya hamtaisahau siku ya
leo” Ana aliondoka, huku nyuma kaka zake na mlinzi walikuwa wakijiuliza
sana kuwa wachukue hatua gani. Ikabidi waamue kumfata mama yao chumbani kwa Moza
ila tatizo lililokuwa kubwa kwao ni kwamba walikuwa wagumu sana kufanya vile ila
badae walijikuta tu wakiinuka na kuanza kusogea kwenye chumba cha Moza ili
wakambebe Rose na wamrudishe sebleni, kwakweli walivyofika kwenye mlango wa
chumba cha moza kila mmoja alijikuta akikaa chini halafu pale pale wakapitiwa na
usingizi mzito sana. Walikuja kuamka wakati pameshakucha
kabisa, yani kila mmoja alikuwa akishangaa sahangaa tu halafu hawakujielewa kuwa
pale kwenye korido wamefata nini, waliinuka na kuelekea sebleni ila walihisi
njaa sana maana hawakula chochote tangu jana yake hadi muda waliopitiwa na
usingizi, alianza Doto kulalamika “Jamani nina njaa mwenzenu hadi sina
nguvu” “Hata mimi nina njaa balaa” “Basi Kulwa kakoroge hata uji
jikoni” Kulwa wakati anainuka ili akakoroge uji, akachungulia kwenye
meza ya chakula na kukuta kuna chakula kimeandaliwa, akasogea na kufunua,
akakuta kuna chapati, rosti ya maini na juisi ipo kwenye jagi, akawaita wenzie
kuwa mezani kuna chakula tayari, “Mmmh itakuwa Ana ameandaa
nini?” “Jamani toka lini Ana akaweza kupika?” Wakaona
watabishana sana, bora waamini kuwa Ana ameandaa chakula kile. Walikaa na kuanza
kula kwani wote walihisi njaa vilivyo. Ana nae alitoka chumbani na
kukuta wanakula, kwavile nay eye alikuwa na njaa hakusumbuka kuuliza kuwa nani
kaandaa kile chakula kwani nae alikaa nao na kuanza kula, huku wakisifia kuwa
chakula ni kitamu sana. Walipomaliza kula, walikaa sebleni ila walikuwa
wanaongea kwa mtindo wa usingizi kwani kila mmoja alikuwa na usingizi wa shibe,
ila Ana aliwauliza sasa, “Wote mlikuwa mnasifia kuwa chakula kitamu,
nani kakiandaa sasa!” “Kwani sio wewe umekiandaa?” “Mimi! Toka
lini mimi niweze kupika chapati, sijui mboga mboga, nimejifunza lini kupika vitu
hivyo?” “Sikia, sisi tumekuja sebleni njaa ikiwa inatuuma sana ila
tukakuta chakula mezani na kuanza kula kwahiyo ndio wewe ukaja kujumuika na
sisi” “Dah jamani, nilijua ni nyie mmeandaa yani sijui tumekula mavitu
yameandaliwa na nani” Ila Doto akadakia na kuwaambia
wenzie, “Ila zile chapati radha yake ni kama zile chapati zilizokuwa
zikiandaliwa na Moza” Ila Ana aliwaambia ndugu zake kwa
ukali, “Nyamazeni na hiyo habari ya huyo mtu, eeh nimekumbuka. Mshaenda
kumtoa mama!” “Bado” Walijibu huku wakiwa wamenyong’onyea sana,
basi Ana akataka kufanya jambo juu yao ila alishangaa kuwa akishindwa kufanya
jambo lolote, yani kila kitu kwake kilishindikana. Akaondoka pale sebleni na
kwenda chumbani kwake, kisha akachukua ile dawa yake ambayo inakaaga chini ya
godoro ila hakuikuta na kumfanya ajiulize, “Ni nani mwenye uwezo wa
kuchukua ile dawa yangu? Wengine wangeweza kuiona, ni mama tu anayeweza
kuichukua na kuihamisha sehemu nyingine, tuseme ni mama! Mmh hapana” Na
kukosekana kwa ile dawa kuliharibu mambo yote ya Ana kwani kila alichokuwa
akikifanya kilishindikana, “Kosa langu ni kula yale machapati, sijui
nitafanyeje mimi. Kama ile dawa ya kunisaidia nayo haipo basi nimekwisha, yani
nimekwisha kabisa” Aliwaza sana, ni kweli alipanga kuacha uchawi ila sio
kwa kipindi hicho ambacho ndani kwao walikuwa wakisumbuliwa na mtu wa ajabu,
kwahiyo siku zote Ana anajifungia ndani kwa lengo la kupambana na mtu huyu
kwahiyo kitendo cha kukosa dawa yake aliona akishindwa mapambano kabisa maana
atapambanaje bila uwepo wa hiyo dawa. Ana akainuka na kwenda chumbani
kwa Moza, alifika na kufungua mlango kisha kuingia ndani hukua akiangalia kila
upande kuwa labda ataweza kuona chochote ambacho kitaweza kumsaidia. Cha
kushangaza alimuona mama yao amekaa chini halafu akionekana kama mtu
anayetumikishwa ila anayemtumikisha hakuonekana, ila tu mama yao alionekana
kwenye wakati mgumu sana. Ana alimsogelea mama yao na
kumuita, “Mama, mama, mama” Ila Rose hakumuitikia kabisa,
aliendelea tu kutumikishwa, ikabidi amtingishe ila kitendo chake cha kumtingisha
mama yao alijikuta akiwa katika sehemu nyingine kabisa. Mishi
alikosa raha kabisa baada ya siri zake kufika kwa mumewe, na akaona kuwa ile
mimba ndio chanzo cha kila kitu. Akaona ni vyema kuchukua maamuzi ya kuitoa ile
mimba, “Najua Yule binti ananitokea kwa njia ya kimazingara, sasa mimi
nitaenda kuitoa hii mimba hospitali. Siwezi kukubali aisee nizae kitoto ambacho
nimekipata kwaajili ya kubakwa? Hapana kwakweli, naenda kuitoa
hospitali” Alimfata mumewe kwa kunyenyekea na kumuomba pesa kwaajili ya
kufanya mahitaji kidogo na kusema kuwa anataka akajiandikishe na
kliniki, “Kujiandikisha na kliniki ndio hela yote
hiyo!” “Hospitali za kulipia ni gharama, ni vyema nipimwe vipimo vyote
kwa usalama wangu. Hospitali za serikali hazina uangalizi
mzuri” Kwasababu huyu mwanaume alimpenda Mishi na alishakubali kuilea
ile mimba kwahiyo hakuwa na pingamizi lolote la kumpa pesa, ingawa kiuhalisia
moyo ulimuuma sana kuwa mwanamke anayempenda kumbe alibakwa ndio akamkubali yeye
sababu alishajiona kuwa na kasoro, aliumia moyoni ila aliona cha muhimu ni
kumpenda Mishi, kwahiyo akamkabidhi pesa aliyoiomba. Mishi alienda
hospitali ambazo anajua kuna daktari wazoefu na hiyo kazi ya kutoa mimba,
ukizingatia bado haijawa kubwa kivile, akaonana na daktari na kuongea nae, kisha
dakari akampa muda wa kwenda ili wakakamilishe hilo zoezi. Mishi
hakurudi kwake, ila alizunguka zunguka maeneo ya jirani karibu na ile hospitali
ili kupoteza muda, mpaka muda ulipofika akaenda sasa kwenye chumba ambacho
daktari huyo hufanyia zoezi lake hilo, na aklimkuta tayari kashaandaa na vifaa
vyake, “Kuna wenzio kama watatu tayari nishamalizana nao, yani nyie
mabinti bhana mnapenda mambo yetu ila mimba hamzitaki” “Mimba
zinatuharibia ujana” “Haya, nipe changu kabisa, nikishamaliza hili zoezi
naondoka zangu maana kwa leo wewe ndio utakuwa mteja wangu wa mwisho wa zoezi
hili” Mishi alimpa pesa kisha kupanda kitandani ili daktari aanze kazi
yake ya kuitoa ile mimba ambayo Mishi hakuitaka kabisa kwani kwake aliiona kama
mimba ya laana. Wakati Yule daktari akianza tu zoezi lake, Mishi
alishangaa kumuona daktari akianguka chini huku akitapatapa na povu kumtoka
mdomoni, wakati anamshangaa vile mara Yule daktari akawa kimya kabisa kama mtu
aliyekufa. Wakati Yule daktari akianza tu zoezi lake,
Mishi alishangaa kumuona daktari akianguka chini huku akitapatapa na povu
kumtoka mdomoni, wakati anamshangaa vile mara Yule daktari akawa kimya kabisa
kama mtu aliyekufa. Mishi akaanza kuogopa na kushuka kitandani, halafu
akamkimbilia daktari pale chini akimshika shika huku akimuita, “Daktari,
daktari” Ila daktari Yule alikuwa kimya kabisa, Mishi hakujielewa,
alitoka kwenye kile chumba na kwenda kuita madaktari wengine ambapo walipoingia
walishangaa pia, wakamchukua mwenzao kwenda kumpima ila wakati huo huo waliomba
askari wa pale hospitali wamshikilie Mishi maana ilikuwa bado haijajulikana kuwa
ni kitu gani kimempata mwenzao. Mishi alikuwa kashikiliwa huku ana
wasiwasi bila kiasi, alikuwa na hofu kubwa sana moyoni mwake, mara akamuona kuna
daktari ambaye huwa anamfahamu akifika kama anataka kuzungumza nae ila Yule
daktari alivyofika pale akamnasa kibao Mishi na kumfanya
ashangae, “Mbona umenipiga?” “Muuaji mkubwa
wewe” “Sijaua jamani sijaua mimi” “Mpelekeni kituoni huyu
msichana ni muuaji, kamuua daktari” Wale askari waliokuwa wamemshikilia
Mishi waliita defenda kisha Mishi akapakiwa humo na kupelekwa kituoni, alijikuta
akilia sana ila tu hakujua kuwa imekuwaje kuwaje maana ni kitu ambacho
hakukielewa kabisa. Ana alikuwa sehemu ya tofauti kabisa na
nyumbani kwao, na sehemu aliyojikuta yupo ni nyumbani kwa mama Jack ambapo
hakujua hata imekuwajekuwaje hadi kufika pale, hakuwahi kupajua kwa mama Jack
ila alitambua ni nyumbani kwa mama Jack baada ya kukuta watu kwenye nyumba hiyo
wakiongelea kuhusu kifo cha mama Jack, Ana alimsogelea kijana aliyeonekana
akimuhadisia mdada kuhusu kifo cha mama Jack, Ana alipowatingisha walishtuka
sana na kumuuliza kuwa ameingiaje, “Umepitia wapi
wewe?” “Sijui” “Wewe ni mwizi?” “Hapana, mimi si mwizi
ila hata mimi sijui nimeingilia wapi. Nilikuwa kwetu ila cha kushangaza nipo
huku, sipajui, sijawahi kufika ila mtu mnayemuongelea namjua tena alifia
nyumbani kwetu” Hapo Yule kijana aliacha kuwa na maswali zaidi kwani
alitaka kusikia kuwa mama yao alikufaje kufaje, “Alikufa nyumbani kwenu?
Ilikuwaje?” “Mama yenu na mama yangu ni wachawi yani hilo halipingiki
ila utofauti wa uchawi wao ni kuwa, mama yenu alikuwa anafanya wa jumuiya ila
mama yangu ni wa peke yake, huwa anafanya uchawi kwaajili ya mambo yake tu. Mama
alipelekwa kwa mganga na mama yenu, na Yule mganga alimwambia mama kuwa atoe
kafara watoto wake. Kwenye familia yetu kuna mtu wa ajabu sana ameibuka na mtu
huyu ana mazuri na mabaya yake, nay eye ndiye kawaponya ndugu zangu ila
akasababisha mama yenu akafa” “Kivipi, hebu tueleweshe
vizuri” Ana aliwaambia kutokana na uelewa wake, maana kidogo yeye
aliweza kuelewa kuwa kifo cha mama Jack kilikuwaje, ni baada ya mama yao kuacha
kutaja majina aliyoambiwa ya kutoa kafara na kuanza kutaja jina la mama Jack
sababu alimkuta ndani kwake kwa mshangao. “Mmmh na huyo mtu anayefanya
vitu hivyo hatuwezi kupambana nae?” “Kupambana na mtu huyo ni kujiingiza
matatizoni, yani mnaweza mkaingia kwenye matatizo makubwa zaidi ya haya. Mama
mwenyewe kajaribu mara kadhaa kupambana nae ila mwisho wa siku ni matatizo tu na
anazidi kuivuruga familia sababu ya kupambana na huyo mtu” “Ndugu zetu
wameenda tena kwa mganga, na lengo ni moja tu kupambana na huyo kiumbe na
kumrudisha mama yetu kama ikiwezekana” “Hawezi kurudishwa, kwanza
kazikwa kwenye kaburi lenye maji” “Kuna uhusiano gani wa kaburi lenye
maji na kurudishwa?” “Sijui, ila ninachojua ni hawezi kurudishwa.
Waaambieni hao ndugu zenu waache tu. Mimi mwenyewe hapa sijui nitarudije
nyumbani, kilichoniponza ni kutaka kumsaidia mama” Yani Yule kijana kuna
baadhi ya maneno alikuwa anamuelewa Ana ila kuna baadhi ya mambo alikuwa
hamuelewi kabisa, ila kwavile Ana alifika kimaajabu Yule kaka alimwambia kuwa
siku hiyo alale hapo halafu kesho yake atamsindikiza kwao. Mume
wa Mishi alishangaa kupigiwa simu kuwa mkewe yupo kituo cha polisi, ikabidi
afanye hima aende maana hakuelewa ni jambo gani limempata mkewe, na kweli
alimkuta kituo cha polisi na alipewa muda kidogo tu wa kuzungumza
nae, “Imekuwaje Mishi tena jamani!” Ikabidi Mishi asifiche maana
tayari alifikwa na majanga, “Nilikuwa na lengo la kutoa hii mimba, na
daktari tulielewana vizuri kabisa, kilichotokea wakati anataka kunitoa ndio
sikielewi hadi muda huu maana Yule daktari alianguka chini” Mume wa
Mishi alishangaa sana na kumtaka Mishi amuelezee zaidi, ambapo Mishi alimueleza
ilivyokuwa hadi yeye kufikishwa hapo kituoni, “Inasemekana Yule daktari
amekufa, lakini mimi sijamuua daktari. Kwanza nimuue kwa lipi jamani, kweli mimi
naweza kuua mtu jamani! Yani nimechanganyikiwa kabisa” “Ila na wewe mke
wangu ni nani alikutuma kwenda kutoa hiyo mimba?” “Jamani sidhani kama
ni wakati muafaka wa kubishana huu, fanya hima nitoke humu Napata shida ujue,
nateseka mimi. Sijamuua daktari” “Najua kama hujamuua, na ninajua kama
kuua huwezi ila sijui uliingiwa na nini mke wangu hadi kwenda kutoa mimba.
Kwahiyo alikutoa?” “Hivi jamani na wewe hunielewi au ni nini?
Nimekwambia wakati anataka kunitoa akaanguka, kwahiyo hakunitoa, yani hata
sielewi kuwa nijielezaje. Kwa maelezo yangu pia nitafungwa maana sharia za nchi
haziruhusu kutoa mimba, yani nimechanganyikiwa hapa. Naomba ufanye kitu
nitoke” Basi mume wa Mishi akaongea pale na mke wake na kumuahidi
kumtafutia dhamana ili aweze kutoka halafu wafatilie kesi, ila alipoenda
kwaajili ya dhamani ilikataliwa kabisa, na kushindwa kumsaidia Mishi kwa siku
hiyo, na kuamua kwenda kujipanga kwa namna nyingine. Wakati
mume wa Mishi anaondoka njiani alikutana na Salome aliyekuwa akitabasamu, kisha
akamsalimia mume wa Mishi, “Habari yako?” “Hivi tunajuana mimi
na wewe?” “Ndio tunajuana, au umechanganyikiwa sababu ya mkeo kuwa
rumande!” “Umejuaje” “Najua” Yani akili ya mume wa Mishi
kwa wakati huo hata haikuwa ya kawaida kabisa kwani iligubikwa na mawazo mengi
sana ya jinsi gani atamsaidia mkewe, kwahiyo hata hakuwa na kumbukumbu kuwa
Salome ndiye aliyemwambia ukweli kuhusu mke wake kule kwa
mganga, “Nimechanganyikiwa kweli, mke wangu hata sijui
nitamsaidiaje” “Utamsaidia vipi muuwaji!” “Sio muuwaji mke
wangu, daktari alianguka mwenyewe” “Mkeo sio muuwaji, na kile kiumbe
alichotaka kukitoa sio uuwaji ule? Au kwavile unadhani mkeo ni mimba yake ya
kwanza ile? Unajua ni ngapi ametoa? Mkeo ni muuwaji na kumsaidia itakuwa ni
ngumu sana” “Sikuelewi, inamaana wewe unajua
kilichotokea?” “Najua ndio” “Basi usitangaze hivyo kuwa mke
wangu alitaka kutoa mimba” “Sasa nimetangaza au nimekwambia wewe
muhusika, unaona sababu viumbe vya tumboni haviwezi kulilia haki zao, haviwezi
kushtaki kuwa vimeuliwa kwa makusudi kabisa, mkeo ni muuwaji. Yule daktari nae
anahaki ya kufa maana kashaua watoto wengi wasio na hatia kwa tamaaa ya pesa.
Hata ufanyaje mkeo kwasasa hatotoka mule ndani mpaka ajifunze adabu na aelewe
anapoambiwa kitu, maana kichwa chake ni kigumu kuelewa. Nishamwambia mara nyingi
asiitoe ile mimba, najua ni mchezo wake ndiomana nikamuonya sana kuwa asiitoe
ile mimba, halafu wewe unakazana kuugua moyo sababu ya Yule muuwaji! Ukitaka
msaada wangu zaidi utanitafuta” Kisha Salome akaondoka, mume wa Mishi
alimuangalia Salome hadi alipoishia ndio akakumbuka kuwa ni huyu binti
aliyemwambia tabia za mkewe ndipo alipokumbuka maneno ya mkewe kuwa huyo binti
hakuwa mtu wa kawaida, ikabidi aendelee kwenda nyumbani ila alijipanga kwenda
tena polisi ili akamuulize vizuri Mishi anapoishi Yule binti na aweze kwenda
tena kuongea nae. Nyumbani kwa Rose, walikaa watoto wake
sebleni na muda kidogo alikuja Salome na kuwafanya wote washtuke maana
wakikumbuka yale maneno kuwa Salome ndiye Moza walipatwa na mashaka ila Salome
akawauliza, “Mbona mnaonekana kuniogopa?” Walikaa kimya hakuna
aliyeweza kumjibu, na kufanya Salome aendelee kuongea “Najua mama yenu
atakapotoka kwenye adhabu ambayo amejipa kutokana na matendo yake yasiyoeleweka,
ataenda kuwafungulia wale watu aliowafungia kwa miaka mingi” Walikuwa
kimya tu wakimsikiliza, hakuna aliyeongea chochote kwani ilionyesha wazi
wanamuogopa Salome kutokana na hoja kwamba ndiye Moza, baada ya kimya kidogo
Kulwa aliuliza kwa mashaka, “Wewe ni Moza?” Sauti yake ilikuwa
ya kutetemeka sana, “Kwa mfano mimi nikiwa ndiye Moza
mtafanyaje?” Wakawa kimya tu, na kufanya Salome aendelee
kuongea “Mimi nikiwa ndiye Moza, inamaana kuwa Moza mwenyewe yuko wapi,
na Salome mwenyewe yuko wapi? Je Moza alikuwa ni jinni kiasi kwamba aweze
kuingia kwenye mwili wa mtu mwingine na kufanya mambo yake? Msiniogope, mimi
sipo kwaajili ya kuwatisha ila nipo kwaajili ya kuwasaidia, na kikubwa
kinachonisumbua ni kuhusu hao watu ambao mama yenu kawatunza ndani, sishindwi
kuwatoa ila nikiwatoa mimi nitasababisha madhara makubwa sana ndiomana nataka
awatoe yeye mwenyewe” Kidogo Salome alivyosema hivi walipata hata kauli
za kuongea nae kwani uoga uliwaondoka kwa kiasi Fulani tofauti na mwanzo
walivyokuwa wamejawa na uoga usio kifani, kisha akawaambia kuwa ni yeye ndiye
aliyewaandalia chakula cha asubuhi, wakatamani kumuuliza kuwa mbona chapatti
zilinoga kama zimepikwa na Moza, ila hakuna aliyeweza kuuliza hilo swali ingawa
kwa wakati huu uoga ulikuwa umepungua. Salome aliwaambia kuwa kwa siku
hiyo wote walale hapo sebleni, yani hapakuwa na cha mlinzi wala nani kwani
hakutoka tena kwenda getini, ni toka siku ile ya majanga ya kumuokota Rose,
alikuwa akiishi tu mule ndani. Kulipokucha mume wa Mishi
alienda tena kituoni na kuongea na mkewe ambapo mkewe alimpa maelekezo ya
anapopatikana Salome, kisha mume wa Mishi alimuahidi kufanya hivyo kwa muda huo
maana hakuwa na namna nyingine yoyote, kesi ya Mishi ilikuwa ni kubwa sana na
kama ikisomwa yani Mishi ana kifungo cha maisha pale, kwakweli mume wa Mishi
alikuwa akihofia sana swala la mkewe kufungwa maisha ukizingatia ni siku chache
tu tangu aoane na huyo mwanamke. Aliondoka pale na kufata maelekezo hadi
nyumbani kwa Rose, ila kabla hajagonga geti Salome alikuwa
ameshamfungulia, “Nilijua tu utakuja, na kwa hakika unajutia makosa ya
mke wako nay eye anajutia makosa yake” “Ni kweli anajutia sana mke
wangu, mimi nipo tayari kuilea ile mimba na kulea mtoto na tena nitampenda kama
mwanangu ila sasa mke wangu anawakati mgumu sana hata sijui nitafanyaje
kumsaidia” “Sasa umenifata mimi ndiyo hakimu wa kesi ya mkeo kusema
nitaamuru asifungwe?” “Najua kuwa wewe sio hakimu, ila wewe ulimpa laana
mke wangu na laana hiyo ikampata. Ulimkataza mke wangu kufanya jambo lolote
kinyume, na amefanya amepatwa na mabalaa makubwa sana, najua unauwezo wa kufanya
mke wangu asikutwe na hatia” “Lakini mkeo katoa mimba nyingi sana, hata
akikutwa na hatia ni halali yake” “Hawezi kurudia tena, ni ujana ndio
ulikuwa unamsumbua. Naomba umsamehe mke wangu” Mume wa Mishi alipiga
magoti kwa Salome huku akionyesha simanzi ya hali ya juu, “Nihurumie
mimi, nampenda sana Mishi. Yeye ni mwanamke nimpendaye, ndoa yetu ni changa
kabisa, hata miezi miwili haina ila majanga kama haya. Nakuomba nihurumie
tafadhali” Salome alicheka sana na kumwambia mume wa Mishi ainuke kisha
akamwambia, “Nenda nyumbani kwako” “Halafu badae niende
polisi!” “Sijakwambia uende polisi, nenda nyumbani kwako kunguni
wewe.” Mume wa Mishi hakubisha na moja kwa moja alifanya safari ya
kwenda nyumbani kwake, alipofika alifungua mlango na kushangaa mkewe
kasharudishwa nyumbani. Neema alikuwa nyumbani kwake na siku
hiyo aliamua kuanza kufunga kama ambavyo alikuwa ameshauriwa na mama Pendo,
alijitahidi afunge ingawa ilikuwa vigumu sana kwake kupambana na njaa yake,
kwenye mida ya saa kumi jioni alishikwa na usingizi na kuamua kujilaza ila
alijiwa na ndoto ambapo kwenye ndoto hiyo alimuona binti yake Salome amelala
tena amelala kwenye kilekile chumba chake ila amelala usingizi mzito sana kiasi
kwamba hashtuki kabisa, halafu akamuona Moza ambaye alionekana akibadilika kwa
pembeni na wakati mwingine kuwa na mwili wa Salome na wakati mwingine kuwa na
mwili wake, Neema alishtuka sana kutoka usingizini, na moja kwa moja akachukua
simu yake na kumpigia mama Pendo huku akimueleza vile ambavyo ameota kwenye
ndoto, “Usihofu ndugu yangu, tunatakiwa kuingia kwenye
maombi” “Lakini naogopa” “Usiogope, muombe Mungu akupe ujasiri
na utaweza kupambana na hali yoyote. Kesho tutakuja huko” Basi Neema
alikuwa na mashaka ya hali ya juu, akaamua kwenda tena chumbani kule alipokuwa
analala Salome, huku akitembea na tahadhari kubwa sana, akafungua chumba na
kumfanya ashtuke vilivyo maana alimuona kweli Salome amelala hoi
kitandani. Basi Neema alikuwa na mashaka ya hali ya
juu, akaamua kwenda tena chumbani kule alipokuwa analala Salome, huku akitembea
na tahadhari kubwa sana, akafungua chumba na kumfanya ashtuke vilivyo maana
alimuona kweli Salome amelala hoi kitandani. Neema hakuweza kuvumilia,
alikimbia hadi nje huku akihema juu juu, akaunganisha matukio ya jinsi Salome
wake alivyoanguka na kukauka kwenye kaburi la Moza, na jinsi alivyoota kuhusu
Salome kulala chumbani kwake halafu Moza kuonekana akiingia kwenye mwili wa
Salome na vile alivyoenda chumbani kwa Salome na kumkuta kuwa ni kweli amelala
chumbani kwake, Neema alikuwa na hofu kubwa moyoni huku akijikuta akiogopa
kuingia ndani kwake, akaita mmoja wapo wa wanae mapacha kuwa aende ndani
akamletee simu kwa madai kuwa yeye alikuwa na kazi nje kumbe kiukweli alikuwa
anaogopa ndani, Yule mtoto aliingia ndani ila ilichukua muda mrefu sana na
hakurudi pale nje, ikabidi amuite pacha mwingine na amuagize ila naye ikawa
hivyo hivyo na kufanya hofu kubwa itande kwenye moyo wa Neema, alikuwa na uoga
wa hali ya juu. Badae akajiuliza kuwa yawezekana alichokiona ni maruweruwe ya
usingizi kutokana na ile ndoto aliyoota, “Ila wanangu niliowatuma ndani
mbona hawajarudi?” Akajaribu kuwaita lakini hawakumuitikia, alikaa nje
mpaka mida ya saa moja jioni badae akajisemea, “Natakiwa niwe
jasiri,hivi mama gani mimi naogopa ndani na kuwatuma watoto! Haya sasa watoto
hawajarudi halafu mimi bado naogopa na cha kushangaza kabisa huko ndani kwangu
eti namuogopa mtoto wangu mwenyewe Salome, itabidi tu nijiweke
ujasiri” Akajitia ujasiri na kuingia ndani kwake, kisha akawasha taa za
nyumba nzima na kuanza kuwaita wale wanae mapacha ambao aliwakuta chumbani kwao
wamelala hoi, akawaamsha wakaamka huku wakidai kuwa na usingizi
sana, “Amkeni mle kwanza ndio mtalala” Akatoka nao hadi sebleni,
kisha akamuagiza mmoja wao, “Nenda chumbani kwa dadako kamuamshe nae aje
kula” Basi yeye alikuwa na hofu sana pale wakati mwanae mwingine ameenda
kumuita Salome, baada ya muda kidogo mwanae alirudi na kumwambia, “Mama,
mbona dada hayupo chumbani kwake? Una uhakika alikuwa amelala?” “Mmmh
labda ametoka” Kisha Neema akaenda jikoni kuandaa chakula cha usiku huo
kwani hata kufuturu hakufuturu kutokana na uoga wake, akijipa matumaini kuwa
huenda ni mawazo yake tu kuwa alimuona Salome. Muda huu Salome
aliingia ndani na moja kwa moja alienda chumbani kwake, ila Kulwa alimfatilia
Salome kwa nyuma na alipofika kwenye mlango wa chumba cha Salome alichungulia
kwa kutumia kitasa cha mlango, akamuona mama yao akiwa anafanya shughuli
zisizoonekana ila alikuwa amechoka sana, halafu akamuona Salome akimfata mama
yao, na walisikika wakiongea ambapo Salome alimuuliza
Rose, “Umechoka?” “Nimechoka ndio” “Upo tayari
kuwaachilia wale uliowafungia?” “Naogopa maisha yangu” “Kwahiyo
maisha yako ni bora kuliko maisha ya wale uliowafungia?” “Naogopa
tu” “Rose, jua naweza kufanya kwa lazima ila itakugharimu maisha yako
kupita vile unavyofikiria, hebu waza jinsi nitakavyowatoa wale watu kinguvu nini
kitatokea kwako” “Najua nitakufa” “Sasa kufa na kufilisika kipi
bora” Rose alionekana kukaa kimya na kufanya Salome aendelee
kuongea, “Mali nyingi umezipata kwa njia isiyo ya halali, umetesa watu.
Umefanya wengine kuwa mandondocha yako sababu tu upate mali unayoitaka. Haya
sasa kuna hasara gani ya hizi mali zikipotea?” “Mali zangu zikipotea
nitaweka wapi sura yangu, siku zote nimekuwa nikihangaika sababu ya hizi mali.
Nihurumie Moza” Hapa Kulwa alishtuka sana ila kwavile aliyemuona yeye
kupitia kile kitasa cha mlango alikuwa ni Salome, aliendelea kujipa moyo kuwa
huenda mama yao amechanganyikiwa tu kumuita Salome kuwa Moza. Ila huyu Salome
aliendelea kuongea na Rose, “Nakupa leo tu, ukishindwa basi mimi kesho
nitafanya ninavyojua mimi. Nimekuvumilia sana Rose, unatesa watu, unawaumiza
watu wasio na hatia ili wewe ufurahie maisha yako, waachie watoto wa watu,
wanahitajika pia kwenye familia zao. Yani watu hawajulikani walipo kwao, familia
hizo zimelia hadi basi kumbe wapo kwako huku umewafungia. Waachie watoto wa watu
Rose” “Basi nitafanya hivyo leo usiku” “Mimi nakwambia kweli
usipofanya hivyo unajitafutia mabalaa, kesho nitafanya mwenyewe na utaogopa
sana” Rose alionekana kutetemeka kiasi, Kulwa nae aliondoka pale kwenye
kitasa cha mlango na kwenda kuwapa taarifa wenzie kuhusu kile alichokiona na
kukisikia. Neema akiwa bado na mashaka ya maisha ingawa muda
tayari ulikuwa umeenda, akataka tena kwenda kuangalia kwenye chumba cha Salome
kwani muda wote alisikia kama aende kuangalia ilia one kuwa atakutana na maajabu
gani, ila kabla hajaenda popote uliingia ujumbe mfupi kwenye simu yake,
alipoangalia ulikuwa unatoka kwa Salome, “Mama nimeshakwambia, achana na
maswala ya kufatilia chumbani kwangu. Hakuna chochote utakachokipata zaidi zaidi
kujiweka kwenye mawazo tu” Neema aliogopa sana huku mapigo yake ya moyo
yakienda kwa kasi ya ajabu, akaamua kuchukua simu na kumpigia mama Pendo ila
hakumpata hewani kwa wakati huo, basi ndio moyo wake uligubikwa na uoga mwanzo
mwisho. Akajikuta akiogopa kwenda kulala mwenyewe kwenye chumba chake hivyo
alienda kulala na watoto wake mapacha. Mume wa Mishi
alistaajabu sana kwa uwepo wa mke wake nyumbani, akamuuliza kwa mshangao kuwa
amefanikiwa vipi kupata dhamani, “Sio kupata dhamana tu mume wangu bali
sina kesi tena” “Kivipi?” “Unajua alikuja Yule binti
niliyekwambia, ndio kanitoa polisi hata sijui kaongea nao nini ila ndio kanitoa
polisi na hakuna tena kesi wala kuripoti siendi kuripoti, kwa kifupi nimefutiwa
kesi” Mume wa Mishi alishangaa sana, ikabidi amueleze Mishi kuwa alienda
kupatafuta hapo anapoishi huyo binti ili kumuomba amsaidie mke wake, kwahiyo
swala la kusema kuwa Yule binti alishaenda polisi na kumsaidia lilimshangaza
sana, akamuuliza tena mke wake kuwa hilo swala lilitokea muda
gani, “Kwanza asante sana mume wangu maana sikujua kama ni wewe ulienda
kuzungumza nae, ila nilimuona polisi pale askari waliponifungulia na kumkabidhi
kuwa niondoke nae. Nilipotoka nae alinipa onyo moja kuwa nisijaribu kuitoa hii
mimba tena na nisijaribu kutoka nje ya ndoa yangu. Ila aliposema hapo tu kama
kawaida kimaajabu nimejikuta nipo hapa ndani, mume wangu Yule binti sio mtu wa
kawaida kabisa. Mume wangu, nakuhakikishia kuanzia muda huu, mimi ni Mishi mpya
tena mpya kabisa, sitashawishika tena na chochote. Hii mimba nitalea na mtoto
nitampenda kupita maelezo ya kawaida, sirudii kutoa mimba, sirudii tena
kuhangaika hangaika na wanaume” “Kwahiyo Yule daktari amekufa
kweli” “Ndio Yule daktari kafa kweli, tena nasikia leo ndio ilikuwa
mazishi yake. Ni amekufa, ila inasemekana Yule daktari kashiriki sana kutoa
wanawake mimba, yani Yule daktari nimemjua kupitia rafiki zangu, ni wengi sana
kawatoa” “Hapo sasa unatimia ule msemo usemao, mshahara wa dhambi ni
mauti. Mke wangu tabia ya kutoa mimba uache, tutaliliwa siku ya mwisho na watoto
mbalimbali tuliokatisha maisha yao” Mishi alimuahidi mumewe kubadilika
kabisa kwani kwa muda aliokaa kule rumande hakutamani kurudi tena kwani aliona
kama dunia ikimuelemea ukizingatia yeye alikuwa anajiona kuwa hana
hatia. Siku hiyo waliwahi sana kulala ili kupata muda wa kupumzika
kutokana na ile misukosuko ya siku hiyo na zile siku za
nyuma. Kulwa alipowaeleza wenzie kwahiyo wakawa tayari kwa
kuona maajabu kwa usiku huo huku uoga ukiwa wa hali ya juu, wakakubaliana kulala
sebleni tena ila usiku huo Salome hakulala nao sebleni maana hakutoka kabisa
chumbani kwake, kwahiyo walibaki wenyewe ila walijawa na hofu ya hali ya juu
kiasi kwamba hata wakisikia mjusi anapita wanatamani wakimbie, yani siku hiyo
hakuna aliyelala kabisa hadi kuna muda walisikia mlango unabamizwa walijikuta
wakikimbia wote na kukimbilia mlango wa kutokea nje ila walishangaa mlango
haukufunguka yani hofu ikawajaa huku wakiwaza kuwa wataona vitu vya ajabu ila
muda kidogo wote watatu wakasikwa na usingizi mzito sana. Kesho yake
walishtuka kila mtu akiwa amelala sehemu yak echini pale sebleni ila hakuna cha
tofauti ambacho walikiona kwenye nyumba yao kwahiyo walijiona kuwa ni uoga tu
ndio uliowasumbua ndiomana walikuwa na hali ile usiku. Ilikuwa
ni siku nyingine tena ambapo Ana alimuomba Yule mkaka amsindikize sasa nyumbani
kwao, ila ndugu mmoja wa Yule kaka akajaribu kumkumbusha kuwa hata mama yao
kilichomponza ni kumsindikiza Yule binti, “Ila mimi sio
mchawi” “Sasa unauhakika gani kuwa mama yetu alikuwa
mchawi?” “Mifupa tuliyoikuta chumbani kwake, na huyu dada aliyetolewa
msukule” “Wewe ndugu yangu wewe, hakuna mwenye uhakika kuwa mama alikuwa
mchawi, amesingiziwa tu na Yule binti ila mimi cha kukushauri usiende peke yako
huko. Nenda na mtu mwingine” Yule kijana alikubaliana na wazo la ndugu
yake huyo, ila Ana aliuliza jambo moja kwao, “Mama yenu alizoeleka kwa
jina la mama Jack, huyo Jack ndio yupi kati yenu?” “Jack ni mtoto wa
mama aliyezoeleka sana, alikuwa na mapenzi na watu wengi ndiomana mama hakuitwa
majina yetu yote ila aliitwa mama Jack, tena alikuwa ni mtoto wa mwisho kwa mama
yani ndio mdogo wetu. Ila cha kushangaza, mdogo wetu huyo alipoteaga na hadi leo
hatujui alipo” “Kheee kumbe! Au nae katolewa kafara?” “Hata
hatujui kwakweli, dada yetu huyu tulijua amekufa kumbe yupo katolewa kafara, ila
kuhusu Jack hakuna anayejua alipo Jack, alipotea kwenye mazingira ya kutatanisha
na hadi leo hajawahi kuonekana” “Mama yenu alichukua hatua gani kuhusu
kupotea kwa huyo Jack?” “Hatujawahi kumuelewa zaidi ya kusema ataenda
kuagua kwa mganga ili ajue mwanae Jack yuko wapi, ila kila siku alisema bado
haijajulikana alipo” Ana aliwaelewa kisha akaondoka nao na kuanza safari
ya kuelekea nyumbani kwakina Ana. Leo mapema kabisa Neema
alimpigia simu mama Pendo kisha akamuelezea kuhusu ndoto ambayo aliota jana yake
na jinsi alivyoenda chumbani kwa Salome na kukuta amelala, akamuelezea jinsi
alivyowatuma wanae na kugundua kuwa ni maruweruwe, “Hapana Neema, hapo
lazima kuna kitu wala sio maruweruwe” “Mmmh unanitisha sasa, si mtakuja
leo?” “Kuna udhuru kidogo imetokea, tutakuja kesho” “Sasa mimi
nifanyeje, jamani naogopa mwenzenu” “Cha kukusaidia ni kuwa uendelee na
mfungo leo” “Mmmh jamani nifunge tena?” “Ndio funga tena, halafu
hujui tu unafikiri hiyo ndoto umeota burebure, ni faida ya kufunga hiyo. Kufunga
kuna faida” “Mmmh haya” “Funga bhana, usikate tama kuna faida ya
kufunga. Kuna faida ya kufanya maombi, yani wewe usijali kuwa sisi hatujaja
nyumbani kwako, unaweza kuomba mwenyewe na Mungu akakusikia, cha msingi kuwa na
imani tu” Neema alimkubalia mama Pendo na kukubali kuwa siku hiyo
ataingia kwenye mfungo tena ingawa mwanzoni alikuwa anaona kuwa mfungo ni swala
gumu sana kwake kwani aliona njaa ndio kitu cha kusumbua zaidi akili
yake. Wakati amekaa kwenye mida ya mchana mchana alisikia hodi, na
alipofungua alikuwa ni Patrick amerudi, kwa upande mwingine Neema alifurahi sana
kwani aliona sasa ataishi bila uoga sababu kuna mtu mkubwa ndani ya nyumba yake,
ila kwa upande mwingine aliona ni mtihani kwake kwani atatkiwa kumpikia Patrick
chakula wakati yeye amefunga, kwahiyo anaweza akajikuta anaonja na
kufungulia. Alimkaribisha vizuri sana, ambapo alipoingia tu cha kwanza
alidai kuwa ana njaa sana, kwahiyo ikabidi Neema aende kumuandalia
chakula, “Mmmh huu ni mtihani sasa, nitaweza kuandaa chakula kweli bila
kuonja? Huu ni mtihani kwangu” Neema alijiona akianza kushindwa kufunga
kwa siku hiyo mapema sana kabla hata siku haijaenda
ukingoni. Nyumbani kwa Rose, leo aliingia jikoni Salome na wote
walikuwa sebleni kwa wakati huo kasoro Ana ambaye hakuwepo nyumbani, kwahiyo
pale sebleni alikuwepo mlinzi, Kulwa na Doto. Leo Salome alipika chakula
na kila mmoja alisikia harufu ya kuungua kwa kile chakula, “Jamani kama
chakula kinaungua?” “Ni kinaungua kweli” “Ila si Salome yupo
jikoni” Ikabidi mmoja aende akamuangalie Salome jikoni, akashangaa sana
kwani hakuwa Salome tena bali alikuwa ni Moza. Ikabidi
mmoja aende akamuangalie Salome jikoni, akashangaa sana kwani hakuwa Salome tena
bali alikuwa ni Moza. Uoga ulimshika na akarudi haraka haraka huku
akiwapa wenzie ishara kuwa wakajishuhudie wenyewe kwa macho yao halafu yeye
alikimbilia mlangoni kwa lengo la kutoka nje, nao waliinuka na kwenda jikoni,
ila walipomuona Moza walipatwa na uoga wa hali ya juu, wakarudi haraka haraka na
kuanza kugombeana mlango wa nje ambapo Kulwa nae alikuwa akihangaika nao ila
haukufunguka ilikuwa kamavile vile usiku kuwa umejikaza na kufanya uoga uwazidi
hata wasiweze kusogea kwenda mahali popote. Wakiwa pale sebleni
wakamuona Moza akitoka jikoni na kwenda pale walipo, kwa uoga waliokuwa nao
hakuna aliyeweza kumtazama Moza, ila Moza aliwaambia “Leo lazima
nimalize kazi yangu, sitaweza tena kukaa, kwani Salome anatakiwa kurudi
kwao” Wote hawakuweza kumjibu kitu chochote na uoga waliokuwa nao
ulikuwa ni maradufu, huku wakijiuliza kuwa Salome ni nani na Moza ni nani, iweje
Salome ageuke na kuwa Moza na iweje Moza aseme kuwa Salome anatakiwa arudi kwao,
hawakuweza kuuliza ila walibaki wakitetemeka kwa uoga. Neema
akiwa nyumbani kwake, gafla alijihisi kutetemeka mwili mzima halafu akawa na
shauku ya kwenda tena kuchungulia chumbani kwa Salome, akainuka na kwenda
kuchungulia akamuona Salome amelala, alipiga kelele za uoga ambapo Patrick nae
alimfata ili kujua tatizo ni nini, “Ni
Salome” “Kafanyaje?” “Salome sio Salome wa
kawaida” “Kivipi sio wa kawaida?” “Muone” Neema
alionyesha kidole alipo Salome pale kitandani, Patrick aliangalia kisha
akamwambia Neema, “Mbona mtoto amelala kawaida tu” “Sio wa
kawaida Patrick” Patrick hakumuelewa kabisa Neema, ikabidi asogee kwenye
kitanda cha Salome kisha alijaribu kumuamsha bila ya kuamka na alionekana
amelala usingizi mzito sana, ndipo Neema akatoa tena wazo la kumpigia mama pendo
ili awaite tena wale waombaji wamsaidie binti yake. “Kuna tatizo huku
naomba msaada wenu” “Lakini ni mpaka kesho” “Haiwezekani
kuvumilia, Salome kalala haamki, tunamuita haitiki, sio kwamba amekufa ila
kalala haamki” Mama Pendo alishangaa sana kwa jinsi alivyoelezewa na
Neema hivyo kumuahidi kuwa wanaenda na wale waombaji. Ana
alikuwa ameongozana na wale vijana hadi nyumbani kwao, alipofika mlangoni
alishangaa harufu ya kuungua kwa chakula ambapo harufu hiyo ilikuwa ni kali
kiasi kwamba ilimchanganya na yeye kwani anajua fika masharti ya nyumba yao
kutokuunguza chakula cha aina yoyote halafu siku hiyo chakula kilikuwa
kinaunguzwa kwa hali ile, akafungua mlango ila ulikuwa mgumu kwahiyo ikabidi
agonge, alifunguliwa na kushangaa sana, “Moza!!” “Ndio ni mimi,
nimekuja kumaliza kazi yangu” Ana alitaka kukimbia ila miguu yake
iligoma kwenda popote na kujikuta akiingizwa ndani pamoja na wale vijana, wakiwa
wanashangaa shangaa kwa uoga pale sebleni mara walianza kuona watu wa ajabu
wakitokea kwenye korido ya nyumba yao kama wakitokea vyumbani, wale watu
walikuwa wakitoka mmoja mmoja na walipofika pale sebleni walikaa chini, ni hapo
ndipo walipomuona Ommy na Sara wakiwa wameambatana na wale watu wengine,
kiukweli kila mtu alishangaa, ila cha kushangaza zaidi ni kwa wale vijana
kumuona mdogo wao jack akiwa ameambatana na wale watu, “Mungu wangu,
jamani si Jack huyu” Walikuwa wakishangaa sana ila wale watu walitoka
wote na kukaa chini pale sebleni ilionyesha kama akili zao bado haziko sawa
kwani hakuna kati ya waliotoka aliyekuwa akishangaa kuwa yupo wapi na anafanya
nini. Moza aliingia jikoni na kutoka na sufuria ambayo mboga ilikuwa
inaungua kisha akaweka maji halafu akaanza kummwagia mmoja mmoja kwa wale
waliokaa chini ambao wametoka vyumbani, yani kitendo cha kumwagiwa kila mmoja
alijikuta akili zake zikirudi timamu na kujishangaa zaidi kuhusu mahali alipo na
jinsi alivyo, walikuwa jumla watu kumi na tano. Wale vijana walimsogelea
ndugu yao Jack, wakati huo Kulwa na Doto walimsogelea dada yao Sara huku wengine
wakibaki wanajishangaa na kuona kuwa wamepata uhuru wa gafla bila ya
kutegemea. Moza alikuwa akitabasamu tu, na kupiga mluzi mkali ambapo
Rose alitokea chumbani baada ya mluzi huo, ila alipowaona watu hao alishtuka
sana na kupiga magoti kwa Moza, “Umenimaliza Moza, umenimaliza
Moza” “Angalia ulivyowatesa watu hawa, wengine wana miaka mitano kwenye
chumba chako kile kidogo umewafungia kimazingara. Unajiona bado una
faida?” “Umenimaliza Moza” Rose alikuwa na kauli moja tu kuwa
Moza umenimaliza yani alionekana kuteseka sana na kile kitu alichokifanya
Moza. Ila Moza alionekana kumpulizia kitu machoni ambapo Rose alianguka
chini na kuonekana kama amezimia, watoto wake wakataka kwenda kwa mama yao ila
Moza akawaambia kwa ukali, “Asimsogelee mtu yeyote, hakuna kumsogelea
Rose ni hatari kwa maisha yenu kwasasa. Haya wote tokeni nje ya nyumba hii, na
mkae mbali kabisa” Ana alijaribu kumtetea mama yake, “Msamehe
mama” “Nyamaza na wewe, tena wewe kila kitu chako kinaenda kuteketea
pamoja na uchawi wa mama yako. Hivi unadhani kuwatesa watu hawa kwa miaka yote
ni vizuri? Mama yenu amekuwa mtu war oho mbaya sana kwa muda mrefu, aliweka
zindiko baya kwenye nyumba yake hii, mtu usijikwae kwenye nyumba hii unapotea
ili yeye azidi kufurahia maisha ya kutesa viumbe visivyokuwa na hatia. Nasema
hivi ondokeni wote, tokeni nje, hapa mtuache sisi wenyewe. Nyie kakaeni mbali
kabisa” Macho ya Moza yalikuwa yanawaka kama moto hivyo kufanya wote
washikwe na uoga, hakuna aliyeweza kubaki mule ndani ukizingatia Moza alikuwa
anaongea kwa ukali sana halafu alikuwa anatisha, wote wakatoka nje ya nyumba yao
na kukaa mbali kabisa, mara gafla wakiwa nje walishangaa kuona nyumba yao
ikilipuka na moto mkubwa ukiwaka, moto ambapo uliwaka kwa muda mchache tu lakini
kila kitu cha kwenye nyumba ile kiliteketea, yani kilibaki kiwanja na majivu,
ilikuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua kila kitu hakikuwepo
tena. Wana maombi na mama Pendo walifika nyumbani kwa Neema na
kwenda chumbani kwa Salome, ambapo walimkuta vile vile amelala wakambeba na
kwenda nae sebleni halafu wakaanza maombi huku wakimuita Salome kuwa arudi kwani
ilionyesha wazi kuwa Salome pale yupo kimwili tu. Baada ya maombi ya
muda kidogo, Salome alionekana kuamka na kukaa huku akishangaa kila alichokiona
mbele yake, mama yake alikuwa bado na uoga ila alimfata na
kumkumbatia. Salome alimuangalia mama yake na kumuuliza, “Mama
niko wapi na kuna nini” “Salome mwanangu, ulikuwa umelala ndio nimewaita
waombeaji waje wakuombee” “Nililala? Muda gani? Na kwanini
niombewe?” “Ulibeba vitu vyako vyote ukaondoka mwanangu ukaniachia
ujumbe tu, ila nikakukuta umelala chumbani
kwako” “Sikuelewi” Neema akaamua kumshika mwanae mkono ili
ampeleke chumbani kwake huenda labda akamuelewa, ila alipofika kwenye chumba cha
Salome alishangaa kuona kuwa nguo za Salome na vitu vya Salome vyote vilikuwepo
mule ndani yani hakuna kitu ambacho kilihamishwa kama yeye alivyofikiria mwanzo,
Neema alipiga kelele na kuwaita wale wanamaombi chumbani kwa binti yake, ila
walimtaka awe mpole kwanza na akae chini atafakari huku akifanya mambo taratibu
taratibu, “Ukifanya kwa papara hutaelewa chochote kile, unatakiwa kuwa
mpole na utafakari. Mungu ni mwema, na mwanao ni mzima kwahiyo swala la kuanza
kumkandika maswali utashindwa kuelewa kipi ni kipi” Ikabidi Neema
akubaliane na ushauri wa mama Pendo ingawa kiuhalisia hali ya mwanae
ilimchanganya sana kwani mwanae hakuwa na kumbukumbu yoyote ile. Basi
wale wanamaombi na mama Pendo wakaaga huku wakimsisitiza Neema ampelekage mwanae
kwenye maombi hadi atakuwa sawa kabisa. Neema alibaki ndani,
yeye, mwanae na Patrick ila aliendelea kumuhoji Salome ambaye alionyesha kila
kitu hakijui hata uwepo wa Patrick hakuuelewa kabisa, kwani kila kitu kilikuwa
kigeni machoni mwake. Alianza kumuhoji mama yake kuhusu Patrick, “Mama,
huyu ni nani?” “Ni baba yako huyu” “Baba yangu! Mama si
ulisemaga kuwa sina baba!” Neema akawa kimya kwa muda kisha akamuangalia
mwanae na kumwambia, “Si wewe Salome uliyeamua kwenda kumtafuta baba
yako hadi kuamua kuhamia nyumbani kwake. Huyu ni baba yako uliyemtafuta kwa
kipindi chote, na ni wewe ndiye uliyemleta hapa nyumbani” “Sikuelewi
mama” Neema alijaribu kumuelewesha vilivyo ila Salome hakumuelewa kitu
chochote, halafu akauliza tena maswali yaliyomchanganya kabisa
Neema, “Vipi kule nyumbani kwetu? Mbona tuko huku, ni kwa nani huku?
Yuko wapi mamdogo Ashura?” “Mmmh hata sijui nikujibu vipi Salome yani
vitu vingine unauliza wakati ulifanya mwenyewe, wewe si ulisema Ashura alitaka
kukuua ukamuwahi na kummaliza” “Kummaliza! Kivipi sikuelewi
mama” “Ashura alikufa” Salome alianza kulia baada ya kusikia
kuwa Ashura alikufa, kwakweli Neema alimshangaa sana mtoto wake na kuhisi kama
kuna mchezo mbaya kachezewa mwanae, “Mmmh wale wa maombi nao au
wamefanya kitu kibaya kwa mwanangu” Patrick aliamua kumkanusha
Neema, “Usiwaseme vibaya watu wamekuja kutusaidia, wameshasema kuwa kuna
kitu hakipo sawa kuhusu mtoto wetu huyu sasa maneno ya nini. Mimi naona cha
msingi labda tumpeleke Salome kule nilipokuwa naishi mimi labda ataweza kuweka
kumbukumbu zake sawa na kuelewa kila kitu” Neema aliona hilo ni wazo
jema sana kwa wakati huo, kwahiyo akaenda kujiandaa kisha kuondoka kwenye gari
na Salome ili wakamuonyeshe walipokuwa wanaishi. Walifika na
kushangaa watu wamejaa halafu eneo limekuwa majivu tupu, halafu Kulwa na Doto
pamoja na Ana walipomuona Salome walimkimbilia na kupiga magoti mbele
yake, “Tafadhali msamehe mama yetu, najua hatorudia tena. Tunajua una
uwezo wa kubadilisha huu moto na kurudisha nyumba yetu. Sisi hatuna haja na
nyumba ila tunahaja na mama yetu, tusaidie Moza” Neema na Patrick
waliwashangaa sana huku wakiuliza kuwa ni kitu gani kimetokea, ila Ana
alimwambia Patrick kuwa amuulize Yule binti yake anajua kila kitu, “Huyu
tumekuja nae hapa sababu tupo nyumbani haelewi chochote kile, ndiomana tumemleta
hapa labda awe na kumbukumbu. Kwani kumefanyaje tena mbona nyumba
imeteketea?” Salome nae akaongea, “Mbona umeniita Moza, Moza si
alishakufa na mlivyo na roho mbaya mlinikataza hata kumuaga Moza mara ya
mwisho” Wakamshangaa, na Neema alikuwa wa kwanza kumshangaa binti yake
kuwa anakumbuka vyema kitendo cha yeye kutaka kumuaga Moza na mwisho wa siku
kuingia kwenye kaburi la Moza, ila hilo tukio la kuingia kaburini hakujua kama
analikumbuka, ikabidi amuulize “Walivyokukatalia kumuaga Moza
ilikuwaje?” “Sijui ila nakumbuka tulirudi nyumbani
nikalala” “Mmmh ukalala!” “Ndio nikalala, si ni jana tu ndiyo
Moza amekufa!” Walikuwa wakimshangaa hata wale vijana waliomleta Ana na
kumkuta ndugu yao Jack kwenye nyumba hiyo walishindwa kumuhoji maswali yoyote
Salome kwani alionekana akiongea kama mtu asiye na mwelekeo. Patrick
alihoji kwa makini maana ile ilikuwa ni nyumba yake pia, ikabidi mlinzi wao
ajaribu kumuelekeza kwa kifupi jinsi ilivyokuwa mpaka kushtukia nyumba
ikiungua, “Kwahiyo Rose ameungulia humo” “Sijui, itakuwa hivyo
maana sisi tuliamriwa tutoke nje na tulipotoka tu nyuma yake kukatokea mlipuko
wa hali ya juu na gafla kila kitu kilikuwa kimeteketea kama ilivyoonekana yani
hakuna tulichookoa” “Kwahiyo huyo Moza mlimuona kabisa” “Ndio,
na mwanzoni alikuwa ni huyo Salome halafu badae ndio akageuka na kuwa
Moza” Patrick aliona kuwa hapo kutakuwa na tatizo, hivyo akamuomba Neema
waondoke pamoja na Salome kurudi nyumbani maana walikuwa wakimsonga songa
kumuuliza maswali Salome ambapo hakuwa na jibu ya swali hata
moja. Walimchukua Salome na kuondoka nae, huku wakiacha pale watu
wakiendelea kufurika na kushangaa yale majanga ya moto, wakati wanaondoka Kulwa
aliwashtua ndugu zake kuwa wawafate hao watu maana hawakuwa na pakukaa kwa
kipindi hicho na wala hawakujua kuwa ni wapi waelekee. Walipofika
nyumbani, wakina Kulwa nao walikuwa wamegika, “Tafadhalini tupokeeni,
hatuna pa kwenda sisi” Patrick aliwatazama, na kwavile hali nzima ya
kilichotokea hakuielewa aliwahurumia na kuwakaribisha pale nyumbani huku akisema
kuwa atatafuta utaratibu wa wao kupata sehemu ya kuishi. Ila kwa upande
wa Neema bado alikuwa na maswali kwa binti yake tu, “Eti wewe ndio
ulikuwa Moza!” “Sikuelewi mama” “Eti ulikuwa ukitoweka
toweka?” “Mama sikuelewi yani maswali yote unayoniuliza ni
yananichanganya tu” “Mwanangu, mimi ndio sielewi kabisa. Ulikuwa wapi
kipindi chote hiki kama huna kumbukumbu ya chochote kilichotokea, inamaana
kipindi chote hiki nilikuwa naishi na Moza!” Alisisimka mwili kwa uoga,
ila bado hakuelewa chochote. Siku zilipita ila hakuonekana Rose
wala Moza tena na akili ya Salome ilikuwa ikirudi kwa taratibu kwani kila kitu
kilikuwa ni kipya machoni mwake kwa kipindi hiko. MWISHO
0 comments:
Post a Comment