Search This Blog

Sunday 20 November 2022

KASRI YA MWINYI FUAD - 5

 

    Simulizi : Kasri Ya Mwinyi Fuad

    Sehemu Ya Tano (5)







    Alimkuta amekaa mbele ya kibanda chake anasuka pakacha. Umari alipomwona tu alimkaribisha, “Karibu! Karibu!”



    “Nishakaribia,” Kijakazi alijibu.



    Kijakazi hakutaka mazungumzo. Hayo siyo yaliyompeleka hapo. Baada ya kukaa juu ya mkeka hapo nie ya kibanda cha Umari, alianza kumvurumisha maswali:



    “Baba, mbona haya mambo siku hizi n’nayaona hivi?”



    “Mambo gani hayo?” Umari alimwuliza Kijakazi huku akitabasamu akiwa amekwisha elewa nini Kijakazi anataka kujua.



    “Si haya? Nawaona watu namna kwa namna wanakuja hapa na kuondoka wala hapana yo yote anayewauliza kitu; kwani bwana hili shamba amekwisha liuza nini?” Kijakazi aliuliza huku hamu ya kutaka kujua imeshamshika.



    “Kwani ile siku uliyokuja kuniita kule bondeni nikakwambia kwamba Fuad hana shamba wewe ulifahamu nini?” Umari aliuliza.



    “Ala! Hivyo tokea siku ile alikuwa amekwisha liuza?” Kijakazi aliuliza huku akipigwa na mshangao “mtoto huyu, ameliuza shamba zuri kama hili?” Kijakazi aliendelea kusema.



    Umari aliyekuwa anashughulika kusuka pakacha lake, mara apenyeze ukuti huu hapa mara apenyeze ukuti huu hapa, mara alisita na kumtazama Kijakazi.



    “Hakuliuza,” alisema.



    ‘Hakuliuza? Sasa tuseme amemgawia mtu bure?” Kijakazi aliuliza tena.



    “Hata hakumgawia mtu. Limechukuliwa na serikali,” Umari alimwambia Kijakazi. “Limechukuliwa na serikali na kugaiwa kwa wakulima wasiokuwa na ardhi. Na hata mimi n’mepata kikataa cha eka tatu.”



    “Limechukuliwa na serikali?” Kijakazi aliuliza huku amepigwa na mshangao. “Itakuwaje? Itakuwaje walichukue shamba lake mwenyewe. Kwanza huyo serikali ndio nani?”



    “Kwani wewe Kijakazi siku zote hizi uko wapi?”



    Umari aliuliza huku anashughulika kusuka pakacha lake ambalo alikuwa karibu na kulimaliza.



    “Mimi si nipo hapa hapa na wewe unaniona kila siku. Vipi tena unaniuliza nipo wapi?” Kijakazi aliuliza.



    “Siyo hivyo,” Umari alisema huku akivuta ununu kulikaza lile pakacha chini, “nil pokuuliza uko wapi, nakusudia kwamba huelewi kama serikali ya Sultani imepinduliwa na hivi sasa kuna serikali ya kimapinduzi ambayo imechukuwa ardhi yote ya mabwana shamba na kutugawia sisi wakulima tuliokuwa hatuna ardhi?” Umari aliendelea kusema.



    “He! Makubwa haya! Mimi sinayo kabisa!” Kijakazi alisema



    “Na wewe umelala mno naws,” Umari alisema.



    “Sasa Bwana Fuad je?” Kijakazi aliuliza.



    “Fuad?” Umari aliuliza, “Fuad naye itambidi atie jembe mpini akalime kama mimi.”



    “Ah! Masikini yule mtoto! Ataweza wapi kul’ma yule?” Kijakazi aliuliza huruma zimemjaa.



    “Ndio aweze tu; kwani sisi tunawezaje yeye asiweze?” Umari aliuliza. “Tena sikiliza Kijakazi mama yangu, usikubali tena kutabishwa na kutumwa kama mnyama na Fuad kwani sasa hana haki hiyo tena.”



    “Ah! Kunitaabisha ananitaabisha lakini nitafanya nini, sina pengine po pote pa kwenda,” Kijakazi alisema.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    “Kwani na wewe hutaki kikataa cha eka tatu. Ukitaka na wewe unaweza kupatiwa kwa urahisi,” Umari alimweleza Kijakazi.



    “Nani? Mimi? Sitaki mali ya dhulma mimi. Tena usiniletee habari hizo. Tena wala sina mazungumzo tena. Kwa heri, nakwenda zangu.”



    Kijakazi aliondoka pale pale wala hakutaka kukaa zaidi.



    Kwa Kijakazi usiku wa siku ile ulikuwa ni usiku wa kukaa na kufikiri. Alikaa chini kimya na kuanza kufikiri. Mengi yaliyomjia kichwani usiku ule yalikuwa ni yale mazungumzo yake na Mkongwe siku ile alipokwenda kumuaga. Kwa mara ya kwanza Kijakazi alifikiri namna alivyopoteza maisha yake shambani pale tokea uhai wa Bwana Malik na Bi Maimuna. Alifikiri namna alivyomlea Fuad tokea uchanga wake mpaka bii leo imefika hadi anampopoa kwa mateke kama mpira wa miguu, heshi kumtukana na kumsumbua, heshi kumnyanyasa na kumsengenya na hana analolifanya likiwa zuri. Kijakazi aliinua mikono yake na kuiangalia namna ilivyochubuka na kuwa na masuguru. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kuitazama mikono yake kwani siku zote hakuwa na wakati na wala haikumjia kufanya hivyo.



    Kidogo kidogo fikra za Kijakazi zilianza kufanya kazi:



    “Kweli mimi ni masikini, mtu wa chini, sina mbele wala nyuma lakini hata ile heshima ya uzee hanipi, anathubutu kunipopoa kwa mateke kama mimi siye niliyemlea tokea uchanga wake?” Kijakazi alijiuliza baada ya kumjia fikra kichwani.



    Kidogo kidogo imani ilianza kumpungua Kijakazi. Alianza kuona kwamba utiifu wake wote aliokuwa nao kwa Fuad haungemsaidia cho chote. Alihisi kuwa anavyozidisha utiifu wake ndivyo Fuad anavyozidi kiburi chake na kwa sababu hii aliona wakati umcfika wa kumpa Fuad ukweli wake.



    Hata siku moja katika maisha yake Kijakazi hakuwahi kukaa na kufikiri kwa muda mrefu kama siku ile. Alifikiri sana na mwisho usingizi ulimchukua akalala kama mtu aliyekufa.



    Ilikuwa ni siku ya Jumamosi. Fuad alikwenda mjini tokea asubuhi kwa starehe zake kwani siku hizi Fuad alikuwa hajishughulishi tena na kazi za shambani. Kijakazi naye aliamua asifanye kazi yo yote bali apumzike. Kazi ya kitumwa ilikuwa ishamchosha.



    Kijakazi alikwenda kisimani na huko alikoga baada ya kukaa bila ya kukoga kwa muda mrefu. Wiki mbili zilikua zimepita tangu Kijakazi akoge kwa kazi zilivyokuwa zimemzidi. Baada ya kuoga alirudi kule chumbani kwake na kuvaa nguo zake zile zile. Kitu alichozidisha kilikuwa ni mtandio uliochakaa ambao alijitanda kichwani. Alizungukazunguka kiamboni pale na mwisho alikwenda chini ya mwembe ambao ulimwaga kivuli chake chini ya gogo la mnazi ambalo Kijakazi alikalia na kupumzika. Hapo Kijakazi alianza tena kujiuliza masuali mbali mbali.



    “Hivyo nguvu zangu zote nilizotupa hapa ni za bure?”



    Mara pale pale aliyawaza maneno ya Mkongwe siku ile alipokuja kumuaga.



    “Ah! Masikini yule mtoto, nilimtolea maneno bure siku ile; sijui ananifikir’a nini hivi sasa? Sijui nitamtazama vipi pindi nitapokutana nayc tena?”



    Hakuwahi kujijibu maswali aliyokuwa akijiuliza mara kwa mbali alimwona Mkongwe anamjia. Kijakazi alitaka kumkimbia Mkongwe lakini pale pale alibadili fikra zake na kuhisi kwamba hakuna sababu yo yote ya kumkimbia mfanya kazi mwenzake walioteseka pamoja kwa siku nyingi.



    Mara Mkongwe alimkaribia Kijakazi na kumlaki kama kawaida yake.



    “Je, Kijakazi, bado umekasirika na mimi?” Mkongwe aliuliza.



    “Ah! Shoga yangu, nikasirike kitu gani? Mimi nahisi nilifanya makosa kukutolea maneno badala ya kuagana na wewe vizuri,” Kijakazi alisema.



    Mkongwe alimwangalia Kijakazi kwa jicho la uchungu na aliona jinsi alivyochakazwa na kazi za kitumwa za shambani kwa Fuad. Machozi yalitaka kumtoka kwa huruma alizokuwa nazo kwa kibimkubwa kile ambacho maisha yake yote yalikuwa ya mateso. matusi, kusumbuliwa na kusimangwa. Ilimjia fikra ya kutaka kusema naye tena kwa mara ya pili ili awache upumbavu wake na ajue kwamba wakati umebadilika na kwa hivyo afanye maarifa ya kwenda kujiunga na shamba lao la ushirika, Mara Mkongwe alibadili mawazo na kufikiri kwamba njia ya pekee nzuri ni kumchukua Kijakazi ili akalione shamba hilo kwa macho yake, na labda baada ya kujionea mwenyewe yaliyomo katika shamba hilo fikra zake zitaweza kukaa sawa. Ama Mkongwe hakuweza kuelewa hata kidogo nini Kijakazi anafikin kuhusu maisha yake kule kwa Fuad, na laiti angalijua, asingelichelewa hata kidogo kumshawishi ili ahame kwa Fuad na kwenda kujiunga na shamba la usbirika.



    Baada ya kumjia fikra hiyo ya kutaka kumchukua Kijakazi shambani kwao, Mkongwe alimwambia Kijakazi, “Shoga!, yaliyopita yamepita, na yaliyobakia tusameheane. Lakini mbona umejikunja hapa chini ya mti peke yako na unaonekana umnyonge sana? Kwani leo huwendi kufanya kazi?”



    “Ah nimejichokea roho yangu na kazi isiyokwisha na wala isiyokuwa na faida yo yote kwangu. Mimi nafanya kila niwezalo kumtumikia na kumtii mtoto yule lakini kila nifanyalo silo. na jaza yake ni kupopolewa kwa mateke au kutukanwa. Hata ile heshima ya utu uzima hanipi mtoto yule, na siku hizi mambo ndio yamezidi.”



    Mkongwe alishituka kumsikia Kijakazi akisema maneno kama yale. Hakupata kumsikia wala hakufikiria kabisa kama Kijakazi anaweza kutoa kauli kama ile. Hata hi” vyo, Mkongwe hakuwa na haraka ya kutaka kumsikia Kijakazi akielezea shida anazozipata shambani kwa Fuad kwani mateso ya huko yeye mwenyewe aliyajua vizuri na hakuhitaji mtu wa kumhadithia. Aliona jambo muhimu kwanza ni kumchukua Kijakazi na kwenda kumwonyesha shamba lao la ushirika na hapo alitoa shauri.



    “Basi shoga si bora tukenda kutembea alau ukapata kunyosha nyosha miguu kidogo?”



    “Tukatembee wapi na jua hili? Nguvu zenyewe sina halafu wewe unataka nijihangaishe? Nikianguka njiani je, utaweza kunibeba?” Kijakazi alimwuliza Mkongwe huku akimfanyia masihara na kutabasamu, Jambo ambalo si aghalabu kumwona Kijakazi kulifanya.



    Kucheka au kutabasamu ilikuwa si jambo la kawaida kwa Kijakazi kwani hakuna hata jambo moja katika maisha yake kwa Fuad lililoweza kumfurahisha hata atabasamu au acheke. Yeye maisha ama yumo katika hofu au wasi wasi na cheko na tabasamu haviandamani na hili wala lile.



    Mkongwe aliona kama ua linachanua kwa kumwona Kijakazi akitabasamu. Aliona bora aendelee na masihara ili alau azidi kumfurahisha shoga yake wa siku nyingi ambaye hakupata kumwona kufurahi.



    “Ukianguka mimi nitakubeba. Kwani unajiona umzito sana?”



    Kijakazi alimtazama Mkongwe na kumwuliza tena. “Sasa tukatembee wapi Mkongwe, mwanangu, mbona unataka kunitaabisha?”



    “Twende tu, utaona mwenyewe huko tutakokwenda tembea na nina hakika utafurahi.” Mkongwe alisema. “Twende nikakuonyeshe ninakoishi na kufanya kazi siku hizi,” Mkongwe aliendelea.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    “Ningelipenda kukujua unakofanya kazi lakini huyu kisirani amekwenda mjini na wala sijui atarejea saa ngapi. Akirejea kama hakunikuta hapa basi nafikiri anaweza kuniua. Ah! lakini haizuru, twende. Lakini si mbali?” Kijakazi aliuliza.



    “Hata si mbali; ni mwendo mfupi tu,” Mkongwe alimwambia Kijakazi.



    “Haya tuanze safari,” Kijakazi alitoa shauri.



    Mkongwe aliinuka pale chini ya mwembe alipokuwa amekaa yeye na Kijakazi na Kijakazi naye akaanza kujiinua huku akisaidiwa na Mkongwe kwa kumshika mkono.



    Walifuatana mguu kwa mguu wakapita njia za ndani kwa ndani ili kufupisha masafa. Mabonde mabonde yaliyokuwamo njiani yalizidi kumfanya Kijakazi aione safari ngumu lakini hata hivyo, alijikazakijituzima na kuendelea na safari mpaka walipotokea pahala ambapo lilionekana banda kubwa lililojengwa kwa matofali. Pia viliweza kuonekana kwa mbali vijumba vidogo vidogo vizuri vilivyotawanyika huku na buku katika eneo lile.



    “Tumekwisha fika,” Mkongwe alimwambia Kijakazi.



    Walipolikaribia lile banda Kijakazi alisikia harufu aliyoizowea kwa miaka mingi; harufu ya kupuo la ng’ombe. Walipofikia lile banda la ng’ombe waliingia ndani, Mkongwe akiongoza njia.



    “Pita; unaogopa nini? Unafikiri upo shambani kwa Fuad?”



    Kijakazi hakusema kitu ila aliingia ndani ya banda lile na humo aliona mkururo wa ng’ombe waliojipanga. Alistaajabu kuona ng’ombe wengi walionona kama wale.



    Ndani ya banda hilo walikuwamo wanawake watupu waliokuwa wakifanya kazi. Wote walikuwa wanashughulika wengine wakiwalisha ng’ombe majani na wengine wakisafisha sehemu mbali mbali za banda hilo. Walikuwa wakiingia na kutoka wala hapana aliyekuwa akimsemesha mwenzake kwa jinsi walivyoshughulika kwa kazi. Alistaajabu kuona usafi wa banda lile kwani banda hilo lilikuwa zuri na safi kuliko lile banda la ng’ombe shambani kwa Fuad. Mastaajabu yalimzidi na mara alianza kuuliza maswali:



    “Mkongwe! Ng’ombe wote hawa wa nani?”



    “Hawa ni ng’ombe wetu, wa shamba la ushirika.”



    Waliendelea na ukaguzi wao na mara Kijakazi alivutiwa na ng’ombe mzuri, akauliza tena, “Na huyu je! Wa nani huyu?”



    “Wote wetu hawa”.



    Ukaguzi uliendelea na kila ng’ombe aliyemvutia Kijakazi basi yeye aliuliza nani mwenye ng’ombe huyo na jawabu kutoka kwa Mkongwe ilikuwa ni ile ile, “wetu, wa shamba la ushirika.”



    “Shoga yangu, hebu niambie jina la kila ng’ombe,” Kijakazi alitaka kujua.



    “Tazama juu ya kila kibao unachokiona mbele ya ng’ombe na hapo jina la ng’ombe huyo huandikwa,” Mkongwe alisema.



    “Ah! Mwanangu, unanidhihaki? Mimi na kusoma ni wapi? Mimi najionea michoro tu lakini sielewi kitu cho chote. Kwani maandishi yote yale yalio juu ya vibao ni majina ya ng’ombe?” Kijakazi aliuliza.



    Hapo tena Mkongwe alianza kumfahamisha Kijakazi kwa maldni, “Juu ya kila kibao unachokiona mbele ya ng’ombe basi huandikwa jina la ng’ombe huyo, umri wake, idadi ya chakula anachokula kila s’ku na idadi ya maziwa anayotoa”.



    Kijakazi alitikisa kichwa kwa maajabu aliyoyaona. Baada ya kulikagua banda lile walikwenda nje upande wa pili na huko waliingia ndani ya banda la pili. Huko aliona vipi ng’ombe wanakamwa maziwa na wanawake waliokuwa wanashughulika kama wale aliowaona ndani ya banda la kwanza.



    Mara Kijakazi alimwona msichana aliyekuwa amekazana na gari ia mkono analiburura na huku akipita akizoa mavi ya ng’ombe. Jambo hilo pia lilimshangaza.



    “Ah, hata mavi ya ng’ombe humu huchukuliwa kwa gari?”



    Mkongwe hakumjibu kitu Kijakazi kwani alielewa vizuri kwamba mengi atakayoyaooa shambani humo yatamshangaza na pindi akitaka kumjibu maswali yote atakayouliza basi itamfika kazi kubwa.



    Kama ndani ya banda la kwanza, ndani ya banda hilo la pili walikuwamo ng’ombe wengi. Kijakazi alikwisha sahau yote aliyofahamishwa na Mkongwe na bila ya hata kufikiri aliuliza tena, “Na hawa je! Wa nani hawa?”



    “Nimekwisba kukufahamisha zaidi ya mara kumi Kijakazi, hawa wote ni ng’ombe wa shamba la ushirika, wa kila mtu anayefanya kazi shambani humu!”



    “Mkongwe mwanangu hayo unayoniambia hayawezi kuwa. Wewe lazima unanidanganya. Kila nikikuuliza wewe umeshika, ‘wa shamba la ushirika, wa shamba la ushirika’; mimi ziwezi kufahamu, haya lazima umeyabuni wewe Mkongwe.”



    Kijakazi hakuweza kuamini aliyoambiwa na Mkongwe lakini Mkongwe hakuona ajabu hata kidogo kwani fikra za Kijakazi alizielewa vizuri. Hata hivyo, Mkongwe aliona m wajibu wake kumfahamisha Kijakazi kila kitu mpaka afahamu. Alimfahamisha juu ya shamba hilo la ushirika, mipango yake yote, na vipi watu wanaishi kijamaa shambani hapo.



    Baada ya kuyatembelea mabanda yote ya ng’ombe, Kijakazi alionyesha amechoka na Mkongwe alimshauri waende wakapumzike chumbani kwake.



    Wote kwa pamoja walikwenda mpaka kule kwenye vijumba vidogo, vizuri na kuingia ndani ya kimoja kati ya vijumba hivyo. Waliingia ndani ya chumba safi kabisa kilichopambwa vizuri. Madirishani mlifungwa vitambaa vizuri vya wavu vya rangi nyeupe; palikuwa na maua ndani ya kitungi kilichokuwa juu ya dirisha. Kitambaa kizuri kilichofumwa kilikuwa kimetandikwa juu ya meza iliyoko kati ya chumba hicho. Palikuwa na kitanda cha chuma kilichotandikwa shuka safi nyeupe. Pande zote mbili za chumba viliwekwa viti viwili vilivyotazamana na pembe nyingine ya chumba juu ya ukuta palitundikwa kioo cha kujitazamia.



    “Nani anakaa humu? Nani analala juu ya kitanda hiki?” Kijakazi aliuliza.



    Mkongwe al’fanya kama hakusikia nini Kijakazi amesema lakini mara Kijakazi aliuliza tena, “Je, sasa umekuwa kiziwi? Nakuuliza nani anakaa humu?”



    “Mimi,” Mkongwe alijibu.



    Baada ya kuingia tu, Mkongwe alikwenda mpaka kwenve rafu ndogo iliyokuwa chini ya dirisha na hapo ilikuwapo redio ndogo ambayo Mkongwe aliifungua. Mara tu baada ya kuifungua redio biyo muziki mororo ulienea chumbani humo.



    “Hmmmm! Kama ya Bwana Fuad; na unajua kuifungua vile vile?” Kijakazi aliendelea na maswali yake yasiyokwisha.



    Kijakazi alikaa juu ya kimoja kati ya viti vilivyokuwamo chumbani humo huku akisikiliza muzild na Mkongwe alikaa juu ya kitanda. Kijakazi alikuwa amechoka kweli na mara alimwomba Mkongwe, “Snoga roho imenikauka hebu nipe maji kidogo ninywe.”



    Bila ya kuchelewa Mkongwe alichukua gilasi iliyokuwapo pale juu ya meza na kutoka nje na mara alirejea na gilasi hiyo ikiwa imejaa maji. Kijakazi aliipokea gilasi ile na kuyabugia maji yote kwa ghafia.



    “Ahsante” alishukuru Kijakazi baada ya kumaliza yale maji.



    Walizungumza kwa muda mfupi na mara saa iliyokuwa imetundikwa ukutani chumbani humo ilianza kugonga huku Kijakazi akihesabu migongo hiyo: “Tisa, kumi, kumi na moja: lo! Saa kumi na moja na mimi bado nipo hapa? Leo Bwana atanifanya nini sijui. Sijui amekwisha rejea mjini? Sikupata umri wangu kufanya mambo kama haya ya leo na yote umeyataka wewe Mkongwe.” Kijakazi alisema huku hofn imemjaa akiwa hajui litakalomfika atakapofika kwa Fuad.



    Alitoka chumbani mle mbio bila hata kumuaga mwenyeji wake Mkongwe. Kutoka hapo hakusimama po pote moja kwa moja mpaka shambani kwa Fuad. Njiani alikazana kama mwendawazimu na alipofika tu alikimbilia kwenye banda la ng’ombe ambao siku ile alisahau kabisa kuwapa majani. Kwa bahati majani aliyoyang’oa jana yalibakia na bila ya kupoteza wakati alianza kuwapa majani ng’ombe wale waliokaa na njaa kutwa. Huku anawapa majani wale ng’ombe huku anawataka radhi kwa kuwaweka na njaa. Aliwabembeleza ng’ombe hao kama watoto wadogo.



    Wakati alipokuwa akiwapa ng’ombe majani, Kijakazi alizungumza na moyo wake bila ya wasi wasi. Ng’ombe walipokuwa wakitafuna majani, Kijakazi alivuta kibao pembeni na kwa sauti ya chini alianza kuwahadithia ng’ombe wale kuhusu ile pepo ya ng’ombe aliyoiona katika shamba lile la kina Mkongwe ambalo alilitembelea siku ile. Alizungumza nao kama kwamba anazungumza na watu.



    “Ama wenzenu wamestarehe,” Kijakazi alianza kusema, wanatunzwa na kuangaliwa kama watoto wachanga, wamenona na wanalishwa chakula kizuri. banda lao zuri, safi na limejaa mwangaza.”



    Kijakazi alipoona wale ng’ombe wamekwisha maliza kula majani, aliondoka bandani humo na bila ya kujali kama Fuad amekwisha rudi au bado alikwenda zake chumbani kwake nyuma ya banda hilo na hakutoka tena mpaka siku ya pili.



    Tokea siku ile alipolitembelea shamba lile la ushirika Kijakazi alikuiwa mara kwa mara akikaa kimya na kufikiri yale aliyoyaona shambani mle. Pia alikuwa analichunguza shamba la Fuad namna lilivyo siku hizi na alitambua kwa urahisi kwamba Fuad alikuwa halishughulikii tena shamba lile kama hapo zamani. Alikuwa kama mtu asiyekuwa na haja nalo; Mabanda ya ng’ombe na kuku yalikuwa yanavunjika bila ya kutengenezwa na yote haya hayakumfurahisha Kijakazi hata kidogo. Alikuwa bado m mtiifu katika kazi yake ijapokuwa imani ilikuwa ikipungua kila siku. Haukupita muda akang’amua kuwa utiifu wake, kama yale mabanda ya kuku na ng’ombe, ulikuwa hauna maana kwa Fuad



    Fikra za Kijakazi zilikuwa zinazidi kubadilika. Alizidi kuona wazi kwamba maisha yake yote aliyapoteza pale kwa Fuad na kwamba jitihada yake yote pamoja na utiifu wake wote aliokuwa nao havikumletea mafanildo yo yote bali masumbufu na matusi. Alizidi kuamini kwamba s’ku zote alikuwa akijidanganya na ukweli ni kwamba Fuad hauthamini hata kidogo utiifu na unyenyekevu aliokuwa nao kwake.



    Ilikuwa ni wakati wa jioni, Kijakazi alipokuwa anashughulika na kazi yake ya kawaida ya kuwapa majani ng’ombe. Mara lilimjia machoni shamba alilolitembelea la akina Mkongwe. Aliwacha kazi yake na kuvuta kile kibao chake pembeni na kukaa juu ya kibao hicho. Alikaa hapo huku akiwa ameshika tama kama mtu aliyefikwa na msiba.



    “Hivyo watu wale ambao nilikuwa siwajui na nikiwachukia bure bila ya sababu yo yote wameweza kufanya kitu kikawa kitu? Wameweza kufanya mambo ya ajabu kama yale nilivyoyaona? Wameweza kujenga mabanda mazuri ya ng’ombe kama yale, mabanda yanawafurahisha ng’ombe na binadamu vile vile!”



    Baada ya Kijakazi kujiuliza maswali yote yale, kidogo kidogo alianza kuona mwanga.



    “Ahaa! Ndiyo sababu siku zile nilikuwa nildmsikia Bwana Fuad mara kwa mara akitukana na kuupinga huu mpango wa mashamba ya ushirika alionieleza Mkongwe! Lakini kweli, Fuad ana haki ya kupinga jambo kama lile. Tajiri yo yote yule lazima atalipinga jambo kama lile. Maana vipi mtu tajiri kama Bwana Fuad ataweza kuchanganyika na watu kama akina Mkongwe, watu ambao hapo zamani alikuwa akiwatuma kama alivyotaka, na kufanya nao kazi pamoja.



    “Bila shaka hata wakaweza kufanya yale lazima watu wale wana nguvu kuliko Bwana Fuad. Lakini nguvu hizi sijui zinatokana na nani hasa au sijui nd’o ile serikali ya kimapinduzi, aliyoniambia Umari?”



    Wakati Kijakazi alipokuwa amezama katika nkra hizi akijiuliza na kujijibu mwenyewe alishituliwa na sauti ya Fuad aliyekuwa akip’ga makelele, “Kijakazi! We Kijakazi! We Kijakazi we! Uko wapi, njoo huku haraka”.



    Kijakazi aliyasahau yote aliyokuwa akiyafikiri na aliruka kutoka kwenye kile kibao alichokuwa amekalia na kupita mbio kati kati ya kundi la ng’ombe waliokuwa wakila majani na kukimbilia kule alipokuwa akiitwa.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Alikwenda mbio nyumbani kwa Fuad huku aldpangusa mikono yake kwenye kanzu aliyokuwa ameivaa na mara alijiona amesimama mbele ya mlango wa chumba cha Fuad.



    Chumbani mle kulikuwa kumejaa moshi na vipande vya sigareti vilikuwa vimetupwa huko na huko. Harufu ya ulevi mkali ilisikika mpaka nje ya chumba. Ulevi mwingine ulikuwa umemwagika juu ya meza gilasi zilikuwa zimetawanyika katika kila pembe ya cbumba. Ilionyesha wazi kwamba pale palikuwa na wageni waliokuwa wakilewa lakini Kijakazi hakuwaona wageni hao wala hakuwa na habari kwamba Fuad alikuwa na wageni siku ile.



    “Saa nzima sasa nakwita mbwa we! Ulikuwa wapi wakati wote huu?” Fuad alisema kwa sauti ya hamaki huku akiwa amelewa chopi.



    Bila ya kufikiri Kijakazi alijibu, Tafadhali usiniite mbwa. Mimi si mbwa, lu binaadamu kama wewe. Kwanza sikuchelewa kwani nimekuja mara tu baada ya kuniita tena nimekuja haraka. Huko nilikokuwa nilikuwa na kazi nyingine na wewe unajua vizuri kama mimi n’na mikono miwili tu ya kufanya kazi zote ndani ya nyumba hii”



    “Wacha maneno mengi! Njoo univue viatu!” Fuad alimwamuru Kijakazi huku amejitawanya juu ya kiti na sigareti yake mdomoni.



    Kijakazi ambaye alikuwa amekasirika alizizuia hamaki zake na bila ya kuchelewa alipiga magoti chini ya miguu ya Fuad na kuanza kumfungua nyuzi za viatu.



    Wakati alipokuwa akimvua viatu Fuad alianza tena kumtolea maneno Kijakazi na kumsukumia ule mguu aliokuwa akiufungua uzi kiatu. Kijakazi aliwahi kuruka upande wa pili na teke hilo halikumpata.



    “Fanya haraka na wacha kunipotezea wakati wangul” Fuad alipiga kelele kwa sauti yake ya kilevi.



    Kijakazi uso ulimbadilika na mara hii hakuweza kujizuia tena.



    “Unaonaje ukavua mwenyewe viatu ikiwa mimi nakupotezea wakati?” alisema Kijakazi.



    Maneno haya yalimshitua Fuad na uso ulimwiva kama mtu aliyepigwa kofi kubwa.



    “Unasema nini? Leo wewe unakataa kutii amri yangu” Fuad alimkaripia Kijakazi.



    Kijakazi alisimama na kujivuta pembeni akakaa kimya kwa muda kidogo huku akimtazama Fuad usoni na mara alianza kumhutubia “Sikiliza Fuad, mimi nitakufanyia kila utakalo, nitatumika kila namna ya utumwa ndani ya nyumba hii lakini sitopiga magoti tena kukuvua v’atu. Nimcchoka, nimechoka roho yangu na utumwa huu usiokuwa na malipo wala hisani; wewe huna haya wala hujui vibaya, huoa heshima na wala sijui unajiona nani,” Kwa hasira kubwa Kijakazi alimwambia Fuad ikiwa ndiyo mara yake ya kwanza kumkata jina. yaani kumwita jina. lake bila ya kutanguliza ‘bwana’.



    Fuad alinyanyuka juu ya kiti alichokuwa amekalia huku akijizuiwa asije akaanguka kwa ajili ya pombe nyingi aliyokunywa.



    “Ama leo Kijakazi umefurutu ada! Wewe leo unathubutu kuvunja amri yangu na kunieleza maneno kama hayo? Hujapata hata siku moja kufanya utovu wa adabu kama hii leo! Leo ng’ombe wewe unathubutu kuniasi?” Fuad alipiga makelele huku akiwa amehamaki hamaki zilizochanganyika na nishai za ulevi.



    “Mimi nitapiga magoti mbele ya kila ng’ombe ndani ya banda lakini kaa ukielewa kwamba numi sitopiga magoti tena mbele yako!” alisema Kijakazi huku midomo inamcheza kwa hasira zilivyomzidi.



    Fuad alimsogelea Kijakazi huku akionyesha kidole chake mlangoni, “Toka! Toka hapa! Niondokee mbele ya macho yangu! Funga virago vyako vyote na utoke ndani ya nyumba yangu utafute pahala uende!” Fuad alisema kwa makelele.



    Leo Kijakazi aliazimia kweli na makelele ya Fuad hayakumshitua hata kidogo. Alisimama pale pale, moyo wake baridi isipokuwa ule wingi wa hamaki alizokuwa nazo. Aliona hii ndiyo fursa ya pekee ya kumweleza Fuad yote aliyokuwa nayo moyoni mwake kwa muda wote ambao alikuwa akimtumikia. Lakini mara Kijakazi alibadili fikra zake na kumlani shetani. Alijaribu kuzizuia hamaki zake na kwa sauti ya chini, kama ile ya mama anayemwasa mwanawe, Kijakazi alisema, “Sikiliza. Fuad, mimi najua kwamba wewe ni mtu mzuri lakini mimi katu sitopiga magoti kukuvua wewe viatu.”



    Fuad alirejea kukaa juu ya kiti na kujaribu kufungua fundo la uzi wa kiatu bila ya kuweza. Mara aliinua uso wake na kumtazama Kijakazi huku akimfyonya.



    “Kiumbe usiyekuwa na fadhila we! Toka hapa na nenda ko kote unakotaka, lakini n’nakuhakikishia kwamba lazima utakuja juta siku za mbele! Zaidi ya miaka hamsini sasa umekuwa, shambani hapa pamoja na sisi, mvua, jua, tuko pamoja hapa, shida, raba almuradi tuko pamoja. Leo hii unata...”



    Kabla ya Fuad hajamaliza kusema Kijakazi alimkatiza maneno yake na kusema. “Mimi najua shida tu, raha unaijua wewe peke yako!”



    Fuad aliona leo kweli imedhihiri na Kijakazi si wa kuchezewa tena. Nishai za ulevi zilimruka na kuanza kuja matao ya chini. Alijua kwamba, kwa namna yo yote ile yeye bado anamhitaji Kijakazi.



    “Sikiliza Kijakazi. Wewe ndiye uliyenilea, ulikuwa nkinibeba; ukinifanyia hadithi na ukinibembeleza kwa nyimbo nzuri, leo yote Kijakazi umeyasahau hayo?”



    “Mimi sikusahau wala sitosahau maisha yangu; wewe ndiye uliyesahau. Wewe hivi sasa unajidai kunilazia minu lakini mimi nishaelewa kwa n’ni unafanya hivyo. Fuad, mimi nimekulea tokea wewe mchanga huwezi kwenda lakini mara tu baada ya kupata miguu yako umeanza kunitesa mfano wa mnyama,’’ Kijakazi alisema huku amesimama katika pembe ya chumba mikono yake ameikunja.



    Fuad alielewa vizuri kwamba pindi Kijakazi akiondoka shambani hapo basi atabakia peke yake, na bila ya mtumishi asingejifaa kitu. Mara moja, aliona haja ya kukubali kauli yake mbele ya Kijakazi, akazungumza naye vizuri, kwa woga, kwani bila ya hivyo angeondoka na kumwacha asipate mtu wa kumtuma.



    “Haya basi, yaliyopita yamepita,” Fuad alianza kusema kwa sauti ya upole. “Mimi nilikuwa nikikupigia makelele baadhi ya wakati tu lakini hii ni tabia yangu na n’nafikiri unaweza kun’elewa kwa vile umeshaishi na mimi siku nyingi. Kijakazi wewe ni kama mzee wangu na ndiyo maana nilipoumwa na mguu nikakuchagua wewe uje uniuguze.



    “Na nilifanya hivyo kwa sababu mimi nakuamini wewe kuliko wote waliowahi kufanya kazi hapa. Nasikitika sana kuona hii leo unataka kunigeukia na kutaka kuliwacha shamba lililokulea. Kijakazi kaa ukijua kwamba kitovu chako kimezikwa hapa na n’naamini kwamba utaendelea kuwa na imani kwangu kama ulivyokuwa wakati wote ulioishi na mimi, usiwe kama wale wasiokuwa na fadhila kama kina Mkongwe na Mariyam.”



    Fuad alijaribu kama awezavyo kumpiga Kijakazi porojo la kumpoza na baada ya kumaliza Kijakazi lijibu, “Mimi sikimbii wala sina haja ya kuondoka hapa isipokuwa wewe ndiye unayenifukuza. Mimi sitoondoka hapa; nitamaliza maisha yangu hapa hapa. Nimeshakuwa kizee na n’na hakika hapana atakayejali kuhangaika na mimi.”



    Wakati wa mazungumzo hayo ile hofu ya kawaida anayokuwa nayo Kijakazi wakati anapozungumza na Fuad ilimtoka kabisa na al’kuwa akizungumza kwa uhuru bila ya wasi wasi. Alijihakikishia kwamba Fuad hatoweza tena kumfanya kitu cho chote. Baada ya kujihakikishia hivyo, Kiiakazi aliona huo ndio wakati wa kusema au kufanya anavyotaka. Alifildri mara mbili nini la kufanya na mara yalianza kumtoka, “Fuad, mimi nimekutumikia siku ny’ngi, kwa muda mrefu. siyo mrefu tu, bali maisha yangu yote. Katika maisha yangu hayo hakuna jambo nililolithamini kuliko utiifu wangu kwako wewe. Juu ya yote haya yangu kutoka kwako m matusi, mateke na utovu wa adabu. Lakini leo Fuad kwa mara ya kwanza mimi nataka kukuomba jambo moja tu na natumaini utanikubalia. Euad mimi nimechoka sana miguu yangu yote inatonesha, hebu nakuomba unikande miguu.”



    Fuad uso ulimsawijika kusikia maneno kama yale kutoka mdomoni mwa Kijakazi. Hakuweza kufikiria kwamba hata siku moja Kijakazi ataweza kumwambia maneno kama yale. Alitaka kuhamaki lakini ilimlazimu kujizuia kwani hakutaka kumwonesha Kijakazi kama maneno yale yamemkcra. Alijidai kutoa kicheko cha kinafiki kilichochanganyika na sura yake ya kikatili na hapo alimwambia Kijakazi. “Kwa nini nisikukande miguu yako na wewe ni mtu mzima na umechoka.”



    Ijapokuwa Fuad alionyesha kuwa tayari kwake kumkanda miguu Kijakazi, lakini hakuamini kabisa kwamba Kijakazi atathubutu kninyosha miguu yake michafu mbele yake. Aliona labda Kijakazi yumo katika kufanya masihara lakini kwa Kijakazi hua ulikuwa si wakati wa masihara tena bali ni wakati wa kweli tupu. Fuad alijaribu kumlaghai tena kwa maneno mazuri na kumwambia, “Sikiliza Kijakazi, mimi na wewe ni lazima kusaidiana, wewe unisaidie na mimi nikusaidie wcwe. Nakuona umesimama kwa muda mrefu; karibu ukae juu ya kiti upumzike kidogo.”



    Kwa mara ya kwanza Fuad alimkaribisha Kijakazi kukaa juu ya kiti chumbani kwake kiti ambacho umri wake wote aliofanya kazi nyumba ile hakuwahi kukikalia. Alionyesha mkono wake kwenye kile kiti na kujidai kumkaribisha Kijakazi kwa heshima.



    Kijakazi hakuyafikiria haya. Hakuyaamini macho yake alipomwona Fuad anamkaribisha kukaa juu ya kiti kile. Alifikiri labda Fuad yumo katika kumjaribu ikiwa atathubutu kuweka matako yake juu ya kiti kile. Laldhl hata hivyo, Kijakazi hakujali kitu na bila ya wasi wasi wo wote alikaa juu ya kiti, akanyosha miguu yake iliyochakaa kwa kweoda.



    “Haya nikande, mwanangu,” Kijakazi alimwomba Fuad.



    Ama hii ilikuwa ni miujiza mikubwa kwa Fuad. Kijakazi mpumbavu, mjinga kuliko watumishi wote waliowahi kufanya kazi kwa Fuad, leo amethubutu kukalia kiti ndani ya chumba cha Fuad. Lakini ukweli ni kwamba amekwisha, hana lake jambo. Kijakazi angeliweza kumchezea kama anavyotaka pindi ingelikuwa anaelewa vizuri hali ya mambo ilivyo.



    Fuad kwa upande wake aliweza kuelewa vizuri vipi fikra za Kijakazi zimebadilika na alihakikisha kwamba bila ya shaka yo yote Kijakazi lazima amekutana na Mkongwe na kumtia maneno. Kwa sababu hii Fuad alitia hofu asije akamfanya kitu Kijakazi halafu likaja likamzukia baa jingine, kwa hivyo, alijidai kama mtu asiyejali kitu kwa yale aliyoyafanya Kijakazi. Maisha yake yote Kijakazi hakuwahi kukalia kiti kama kile. Alijiona kama aliyekalia kiti cha enzi. Aliinyosha miguu yake michafu bila ya wasi wasi akimngojea Fuad aanze kumkanda.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Alipoinyosha miguu hiyo, Fuad aliitazama kwa ghafla na kwa mastaajabu yake aliuliza, “He! Mbona miguu yako iko hivyo Kijakazi?”



    “Vipi?”



    “Hivyo ilivyo? Kwa nini ukaiwacha ikaharibika namna hiyo? Kwa nini ulikuwa huvai viatu?”



    Miguu ya Kijakazi ilikuwa imechakaa kweli. Ilikuwa imeng’ang’anaa na kujaa masuguru. Ilionekana mfano wa matofali madogo ya saruji Kwa hakika miguu hiyo ilikuwa ni sura ya kushangaza na kushitua.



    “Kwani Fuad hujapata kuiona miguu yangu?” Kijakazi alimwuliza Fuad huku akimtazama usoni moja kwa moja. “Unaniuliza habari ya viatu unafildri kama hukunipa wewe mimi viatu nitavipata wapi? Wewe ki...” Kijakazi alitaka kuendelea lakini Fuad alingilia kati.



    “Basi ungeliniambia tu mimi ningelikupa pesa ukanunua viatu! Kwa nini usiniambie? Lakini haidhuru. Nitakutafutia jozi moja ya viatu vikuukuu na nafikiri vitakufaa.”



    “Mangapi nimekwambia Fuad, na hakuna hata moja ulilonitekelezea? Nimekwambia mambo chungu nzima lakini kila nilipokwambia kitu ulikuwa unajitia pambani na kufanya kama ulikuwa husikii nakwambia nini.”



    Fuad alibakia kimya, uso chini, akijitia kuona haya za uwongo, hana la kusema.



    “Hebu iangalie miguu yangu namna ilivyo, unafikiri miguu ya binadamu kweli inakuwa kama hivi?” Kijakazi aliendelea kumsumbua Fuad.



    Fuad alikenyua meno na kujidai kucheka na mara alisema, “Itanibidi niseme kwambaaa...” aliwaza kidogo neno la kulisema. “Itanibidi niseme kwamba umeiharibu miguu yako Kijakazi?”



    Hapo Kijakazi zilimpanda, tena zilimpanda kweli na upole wote ukamwisha. Alianza kufoka kwa sauti ya hamaki, “Nimeiharibu? Ama wewe kweli si mtu! Unathubutu ikufungua mdomo wako na kusema kwamba mimi ndiye niliyeiharibu m’guu yangu? Wewe ndiye uliyeiharibu miguu hii! Hii ni kazi ya kwako iliyoifanya miguu hii ikawa hivi! Hii ndiyo zawadi niliyoipata kutoka kwako baada ya kufanya kazi maisha yangu yote!”



    Kijakazi alikuwa amekasirika sana, midomo inamcheza kwa hamaki zilivyomzidi, siku nyingi Kijakazi hakupata kuhamaki. Maisha yake ilikuwa ni kuhamakiwa yeye tu na hamaki alizokuwa nazo wakati huo ilikuwa m mkusanyiko wa hamaki zake za siku nyingi. Hakujali alikuwa anasema na nani na yalikuwa yanamtoka tu yote yaliyokuwa moyoni mwake kwa siku nyingi.



    “Sikiliza Fuad! Nakwambia wazi, baada ya leo - nakwambia tena - baada ya leo, sitokubali kukutumikia utumwa wa namna yoyote! Mimi nimejichokea! Maisha yangu nakutumikia wewe na sasa lazima unifikirie kwamba mimi nimeshakuwa mtu mzima na wakati umefika sasa nijipumzishe! Hiyo kazi ya kuvuliwa viatu na kaai nyingine zote sasa utafanya mwenyewe.”



    Kijakazi alinyanyuka kwa hasira pale juu ya kiti alipokuwa amekaa na kuelekea mlangoni.



    “Sikiliza wewe! Mimi nimekwisha kuelewa wewe Baafikiri nini lakini mimi nakwambia kwamba k’’la unalofikiri hivi sasa basi jua kwamba unajidanganya nafsi yako. Mimi nimekwisha jua zamani kwamba wewe ushakutana na Mkongwe kakutia maneno. Lakini mimi nilikuwa nakutazama tu akili yakol Nafikiri keshakudanganya kuhusu hilo shamba lao la ushirika lakini unajua nani mkubwa huko?” Fuad aliuliza kwa hamaki, “unajua nani mkubwa huko?” Fuad aliuliza tena, “laiti kama ungelijua basi usingelikubali kudanganywa akili yako! Mimi nakwambia basi, ikiwa hujui, hilo shamba la ushirika la kina Mkongwe pia liko chini yangu mimi; mimi ndiye mkubwa huko. Ninalolisema huko lazima liwe kwani wewe Kijakazi hujui mimi nani? Hujui kama mimi ndiye Fuad. Fuad bin Malik mtoto wa Malik bin Khalfan? Basi bora uweke akili yako. sawa na usikubali kusikiliza maneno ya uwongo ya hao wanaokudanganya,” Fuad aliyasema hayo kwa kujigamba huku amejitawanya juu ya kiti akitaka kumtisha Kijakazi.



    “Mwongo! Mnafiki! Wewe sasa huna chako wala huna lako!” Kijakazi alisema kwa sauti kubwa.



    “Unasemaje? Wewe unathubutu kuniita mimi mwongo, kalb wel Ngoja basi, sasa hivi nitakuonyesha, nyama we usiyekuwa na fadhila!” Fuad alipiga kelele na kuinuka juu ya kiti akielekea ukumbini kuchukua fimbo.



    Hapo Kijakazi hakutaka kusubiri tena kwani aliona Fuad amekasirika kweE na angeliweza kumfanya kitu cho chote kwa namna alivyokasirika. Alitoka nje mbio.



    Fuad alipotoka ukumbini kwake na fimbo mkononi hakumkuta Kijakazi na kwa hamaki alizokuwa nazo alivuta chupa ya wiski na kuvuta gilasi moja katika gilasi zilotawanyika ukumbini pale. Akamimina nusu gilasi ya wiski hiyo na kuibugia yote mara moja. Alichomoa sigara moja kutoka kwenye pakiti na kuiwasba huku akikaa juu ya kiti anahema kwa hamaki.



    Kijakazi alikimbia mbio kuelekea kwa Mkongwe. Mbio alizokwenda haziwezi kuelezeka kwa maneno, alikimbia utafikiri a mtu aliyekuwa mzee, na mabonde yote aliyoyapita huku akipepesuka siku ile aliyofuatana na Mkongwe hakuyaona wakati ule. Wakati alipokuwa akikimbia fikra nanma kwa namna zilikuwa zikimwenda kichwani. Maneno ya Fuad kwamba hata huko kweoye shamba la ushirika yeye ndiye mkubwa yalimkaa kichwani na alidhamiria akifika tu huko kwa Mkongwe basi amwambie Mkongwe, afanye kila njia Fuad afukuzwe katika ushirika huo. Aliwaza kwamba ikiwa Fuad ni mkubwa huko tabia yake itakuwa ile ile na atawafukuza wafanyakazi wote wa sbamba hilo. Aliyapanga kichwani yote ambayo alitaka kumwambia Mkongwe. Hakusimama pahali po pote mpaka alipofika pale kwenye lile shamba la ushirika na alipofika tu shambani hapo akaanza kuitafuta ile nyumba ya Mkongwe. Alisimama kati ya uwanja wa shamba hilo akifikiri apite wapi ili aweze kufika huko. Uwanjani, hapakuwa na mtu ye yote ambaye angeliweza kumwuliza.



    Wakati alipokuwa amesimama uwanjani hapo akiangaza huku na huku alitokea mtu mmoja nyuma yake. AIikuwa kijana aliyeonyesha mwenye siha, amevaa suruali ndefu rangi ya kibuluu na shati jeupe, viatu virefu vya mpira vilivyomfika mpaka magotini na alichomekea ile suruali aliyovaa ndani ya viatu hivyo. Alikuwa amevaa kofia kubwa ya uldli. Kijakazi alimwangalia kijana huyo kwa macho ya kustaajabu na kabla hakuwahi kusema kitu, yule kijana alimwuliza Kijakazi, “Je mama, unamtafuta mtu?”



    “Ndiyo, bwana namtafuta Mkongwe!”



    Kijakazi alikuwa amechoka sana na yule kijana alibaini jambo bilo, alikuwa anayumba kama mpopoo unapopigwa na upepo.



    “Unamtafuta Mkongwe siyo? Mkongwe utaweza kumwona kule kwenye mabanda ya ng’ombe”, yule kijana alimweleza akionyesha kidole upande wa yale mabanda ya ng’ombe. “Kwani wewe ni mgeni hapa?” yule kijana alimwuliza tena Kijakazi.



    “La, mimi si mgeni hapa! Ni mzaliwa katika eneo bili la Koani lakini nilikuwa sitembei.”



    “Wewe ni nani?” AIiuliza yule kijana.



    “Mimi naitwa Kijakazi Nafanya kazi shambani kwa Fuad”.



    “Aha!” yule kijana alitikisa kichwa kwani kila mtu katika shamba hilo alikuwa anazijua hadithi za Fuad. “Mimi naitwa Machano.”



    Machano pale pale alimpa mkono Kijakazi na kumsalimu.



    Kijakazi alikaribia kuzimia kwa ajabu aliyoiona kwani heshima aliyopewa na Machano hakuwahi kupewa na mtu ye yote yule. Hakumbuki hata siku moja Kijakazi kusalimiana na mtu akampa mkono.



    “Twende basi nikupeleke aliko Mkongwe,” Machano alimshauri Kijakazi.



    ‘Twende, mwanangu!”



    Walifuatana pamoja Machano mbele Kijakazi nyuma na walipokuwa njiani Kijakazi alianza kuboboka, “Ati anasema nyinyi wajinga! Ati nyinyi wapumbavu!”



    Machano aligeuka nyuma kwa ghafla na kumtazama Kijakazi kwani hakuelewa alikuwa akisema nini. “Unasema na mimi?” aliuliza.



    “Ehe!” Kijakazi alijibu.



    “Unakusudia kunambia kitu gani?” Machano aliuliza tena.



    “Ah, balaa tu!”



    “Wacha sa? Mbona unanitisha; kuna balaa gani tena?” aliuliza Machano.



    Machano aliingiliwa na hamu kubwa ya kutaka kumsikiliza Kijakazi kwani aliweza kuhisi kwamba bibi huyo alikuwa na tatizo kubwa na badala ya kumpeleka kwa Mkongwe alimchukua mpaka upande wa pili wa kiwanja na kukaa naye juu ya bao moja lililokuwa chini ya mchungwa



    “Kaa kitako hapa, Bibi, na unieleze hilo balaa unalolisema,” Machano alimwambia Kijakazi.



    Kijakazi alionyesha kama mtu aliyetahayari na mara alimwambia Machano, “Mimi si Bibi; mimi ni Kijakazi tu.”



    “Haya basi ukipenda nitakwita Kijakazi. Nieleze hilo balaa!”



    Mara tu baada ya kukaa juu ya bao Kijakazi alianza kumweleza Machano hadithi za Fuad. Kwa hamu kubwa aliyokuwa nayo. Kijakazi hakujua pa kuanzia.



    Alianza kuhadithia kitu na kabla hajamaliza alielezea kitu kingine. Kwa fikra zake, Kijakazi alifikiri labda Machano atashituka kwa hadithi zake na kuwaita watu wote waje wamsikilize, lakini badala yake Machano alinyanyuka taratibu pale juu ya bao huku akimtazama Kijakazi kwa kumwonea huruma na kumwambia, “Sikiliza Kijakazi, kuhusu habari kama hizo itakubidi kuonana na mwenyekiti wa shamba la ushirika.”



    “Ala! Mimi nikifildri wewe ndiye mkubwa hapa?”



    “La, mimi sihusiki na habari hizo. Mimi ni msaidizi katika idara ya upandaji wa mazao katika Bhamba hili.”



    Kijakazi alikasirika na hapo alianza kumtolea maneno Machano kwa kukataa kumsikiliza hadithi zake, “Haikuhusu wewe habari hizi? Habari hizi zinakuhusuni nyote! Upandaji wa mazao, upandaji wa mazao, yatakuleteeni faida gani hayo mazao mnayotaka kupanda na nyinyi m’mempa ukubwa Fuad shambani hapa! Atakuharibieni kila kitu! Atakufukuzeni nyote kazini!”



    ‘‘Nani aliyekwambia kama sisi tumempa ukubwa huyo Fuad?” Machano aliuliza macho ameyatumbua kwa mastaajabu.



    “Mwenyewe anasema kama yeye ndiye mkubwa hapa!”



    Machano alimtazama Kijakazi machoni na kucheka. “Sikiliza mama, kama nilivyokwambia mimi habari hizi hazinihusu na hivi sasa n’na haraka, mana’ake hivi sasa tuko katika chumba cha majaribio kwani tunatafuta njia za kuweza kupanda mpunga mara mbili katika mwaka shambani hapa, lakini subiri hapo hapo. sasa hivi nitakuitia mwenye kiti na yeye atakuja kukusikiliza maelezo yako.” Machano aliendelea.



    Hapo Machano alimwacha Kijakazi amekaa juu ya bao lile peke yake na yeye aliongoza moja kwa moja mpaka kwenye ofisi ya mwenyekiti.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    Kijakazi alibakia pale juu ya bao na alifikiri labda Machano amempuuza na kumwona mpumbavu. Alihisi labda habari alizokuwa nazo si muhimu au labda mwenyekiti vile vile hatokuwa na wakati wa kumsikiliza. Alihisi labda atamwona mpumbavu au labda kizee kijienda wazimu tu. Zilimjia fikra kila namna na mwisbo zilimjia fikra za kuondoka na kwenda zake po pote pale lakini siyo kwa Fuad tena. Kabla hajaondoka alisikia kelele kubwa juu ya kichwa chake.



    “Tafadhali sikilizeni! Tafadhali sikilizeni! MwenyeIdti anaitwa uwanjani chini ya mchungwa kuna mgeni wake!”



    Ilikuwa ni sauti iliyotoka kwenye bomba la kupazla sauti lililofungwa kwenye nguzo nyuma ya mchungwa.



    Kijakazi alishituka na kutaka kukimbia lakini baadaye alibaini kwamba kelele zile alizozisikia zilikuwa za kumwita mwenyekiti ili kuja kuonana naye. Haya yalimpa nguvu na alirejea pale pale juu ya bao.



    Kwa muda mrefu Kijakazi alikaa pale juu ya bao bila ya kuja mtu ye yote. IBkuwa wakati wa jioni, alasiri imo katika kupotea na magharibi inataka kuingia. Upepo ulikuwa mzuri na Kijakazi alipandisha miguu yake juu ya bao na kupumzika kwa kituo.



    Alijinyosha mgongo wake uliokuwa umechoka kwa mbio alizokwenda na hapo tena, bila ya mwenyewe kukusudia, alianza kusinzia. Alipokuwa aldsinzia kwa ghafla alimwona mtu amemsimamia mbele yake. Alikuwa kijana mrefu na shati alilovaa lilikuwa limefunguliwa vifungo kifuani; alionyesha kama mtu aliyeacha kazi muhimu. Kijakazi alijihisi kama yumo katika ndoto lakini alipofungua macho yake mara ya pili alibaini kwamba alikuwa haoti bali yupo mtu kweli mbele yake amemsimamia.



    Kijakazi alijikusanya kusanya na kusimama aldjua kwamba huyo ndiye yule mwenyekiti aliyekuwa akimngojea. Kijakazi alimtazama na alimwona kama mtu aliyemwelewa lakini hajamwona siku nyingi. Alikuwa ni Vuai na baada ya kumtazama kwa kumchungua Kijakazi aliweza kumtambua. Alipigwa na mshangao kumwona Vuai kuwa ndiye mwenyekiti wa shamba lile la ushirika kwani Kijakazi alimwelewa Vuai vizuri wakati walipokuwa wakifanya kazi pamoja kwa Fuad.



    Kijakazi anakumbuka vizuri ile siku Vuai alipofukuzwa shambani kwa Fuad na yeye alikuwa m mmoja katika waliomwona Vuai mpumbavu na kumlaumu sana kwa aliyofanya hata ikabidi afukuzwe na Fuad.



    Vuai ndiye aliyestaajabu zaidi kumwona Kijakazi kuwa ndiye mtu aliyetaka kuonana naye. Vuai anamwelewa Kijakazi vizuri na anazikumbuka yamini zake alizokuwa akila na ahadi alizokuwa akitoa kuwa mtiifu kwa Fuad rapaka kufa kwake. Kwa jinsi alivyostaajabu, baada ya kumwona Kijakazi tu Vuai hakuweza kujizuia. na kwa kustaajabu alisema, “Ohoo! Kijakazi! Sijatarajia hata kidogo kukuta hapa! Je wewe ndiye mtu unayetaka kuniona?”



    “Ndiyo.”



    Vuai alimpa mkono Kijakazi kwa furaha na kumwuliza “Unaweza kunitambua?”



    “Naweza.”



    “Wapi?”



    “Mimi najua vizuri lakini siku nyingi tumepoteana. Wewe si Vuai tuliyekuwa tukifanya kazi pamoja kwa Puad?” Kijakazi aliuliza.



    “Khassa!” Vuai alijibu “Sasa kumezidi nini tena, Kijakazi? Jua karibu litakuchwa na wewe uko hapa. Je, umekuja kutueleza habari za Fuad?” Vuai aliendelea.



    “Kama ulivyoweza kukisia,” Kijakazi alijibu mbiyo mbiyo, “hayo ndiye yaliyonileta hapa.”



    “Kwani wewe bado uko kwa Fuad tu?” Vuai aliuliza.



    “Hivi sasa natokea kwake lakini sidhani kama nitarejea tena.”



    Vuai ambaye alikuwa amesimama wakati wote aliokuwa akizungumza na Kijakazi alikaa pale juu ya bao na kuanza kumhoji Kijakazi.



    “Ehe! Nini anasema Fuad? Amekutuma cho chote kwetu?”



    Kijakazi alikuwa na hamu kubwa ya kutaka kumwelezea Vuai habari zote za Fuad na hamu hiyo ilimfanya kubabaika katika aliyotaka kuyasema. Hakujua aanzie wapi na mara alianza kupiga makelele, “Mbaya! Mbaya sanal”



    “Mimi najua,” Vuai alimjibu Kijakazi huku akimpigapiga bega.



    “Wewe Vuai unavielewa vizuri vitimbwi vya mtoto yule na juu ya hivyo nyinyi, m’mekwenda kumpa ukubwa katika shamba lenu! Unajua vizuri kama Fuad anatuma kitumwa na anapokupa amri lazima uitekeleze hapo hapo! Anapotaka jambo lazima liwe kama kudra na mwanadamu! Akisema umvue viatu basi lazima umvue hapo hapo na ukichelewa kidogo tu basi mara anakupopoa kwa mateke! Yeye hakupendeni, anakuchukieni na kukudharauni! Anasema hamjui kitu! Wajinga, wapumbavul”



    Kijakazi alitoa hadithi ndefu kuhusu ubaya wa Fuad. Alisahau kabisa kama Vuai alikuwa ni mmoja katika wale wal’oteswa kitumwa na Fuad wakati alipokuwa akifanyakazi shambani kwake. Mara alihadithia siku alizovulishwa viatu, mara alihadithia siku alizofukuzwa chumbani... almuradi hakuna alilolibakisha.



    Vuai alinyamaza kimya buku akimsikiliza Kijakazi kwani alielewa vizuri kwamba Kijakazi alikuwa na joto la moyo na alikuwa na mengi ya kusema kuhusu mateso ya Fuad. Aliona ni jambo la busara kumwacha Kijakazi atoe joto la roho alilokuwa nalo ijapokuwa yeye Vuai mwenyewe alimwelewa vizuri Fuad.



    Vuai alimkamata bega Kijakazi taratibu huku akitikisa kichwa na kusema “Kwanza nani aliyekwambia kama Fuad ndiye mkubwa hapa?”



    “Ameniambia mwenyewel” Kwa makelele Kijakazi alijibu.



    “Hayo si kweli, alikuwa anakudanganya tu labda kwa madhumuni ya kutaka kukutisha.”



    “Hivyo yeye si mkubwa hapa? Hivyo alikuwa anajigamba tu?” Kijakazi aliuliza.



    Kijakazi alipigwa na mshangao na alitulia kimya huku amemkodolea macho Vuai. Vuai naye alinyamaza kimya vile vile na palikuwa na kimya cha muda mfupi baina yao mpaka Vuai alipokivunja kimya hicho.



    “Wacha ukubwa, bata akitaka kuwa mwanachama wa kawaida tu shambani hapa basi hatutomruhusu Fuad kufanya hivyo kwani yeye alivyokuwa na fikra za kibwana shamba hataweza kufanya kazi hapa kwa moyo thabiti. lazima atataka kupitisha vitendo vya uharibifu.”



    “Kweli, kweli tupu hayo unayoyasema!” Alisema Kijakazi.



    Vuai alikaa kimya buku akimtazama Kijakazi usoni. Zilimjia huruma za dhati kwa namna alivyomwona Kijakazi amechakazwa kwa kazi ya kitumwa ya muda mrefu. Wakati Vuai alipokuwa akimtazama Kijakazi fikra zake zilipotea na alianza kuwaza siku ambazo yeye mwenyewe alifanya kazi shambani kwa Fuad. Aliyakumbuka mateso waliyokuwa wakiteswa, jinsi walivyokuwa wakitukanwa. Na mara akakumbuka siku ile Fuad aliyotaka kumkamata Mkongwe kwa nguvu na kumwingilia kibandani kwake. Mara fikra bizi zilimpotea na kumjia fikra za siku ile ambayo Fuad alimkuta njiani anarejea mkutanoni huko Kijangwani... Alipokuwa katika fikra akizikumbuka siku za mateso, alisahau kabisa kama pale alipo alikuwa amekaa na mtu aliyekuwa akizungumza naye lakini kwa ghafla alishtuka kama mtu aliyezindukana usingizi na mara lilimtoka swali, “Sasa Kijakazi siku zote hizi zilizopita nini kilichokuzuia usije kujiunga na sisi hapa?”



    “Ujinga wangu,” bila ya kufikiri Kijakazi alijibu.



    “Sasa ukitoka hapa unarejea kwa Fuad?” Vuai aliulizatena.



    “Lo, Mungu apishe mbali! Nitatokomea po pote pale lakini sitarudi tena kwa yule mwizi wa fadhila asiyejua wema wala hisani.”



    “Sasa sikiliza Kijakazi,” Vuai alianza kusema “sisi sote tunaoishi hapa ni sawa sawa na wanao. Yaliyokufika wewe na sisi yametufika vile vile ila wewe mwenzetu umetuzidi. Lakini ndyo ulimwengu, kwani mambo huzidiana. Sasa Kijakazi mimi nakushauri bora uje hapa ili ujiunge na sisi watoto wako tushirikiane kufanya kazi pamoja na wewe utakuwa mwanachama kamili wa shamba hili la ushirika na utapata haki sawa sawa kama mwanachama yo yote yule; au una shauri gani?”



    Kijakazi al’ogopa kujibu kitu cho chote kile, lakini mara alisema, “Ah! Nadhani hamtakuwa na haja ya mwanachama mtu mzima kama mimi. Mimi sina nguvu tena za kufanya kazi yo yote; mimi nimekwisha kabisa na pahala kama hapa panahitaji mtu mwenye nguvu anayeweza kufanya kazi.”



    “Basi umekuja hapa kutuhadithia habari za Fuad tu?” Vuai alimwuliza Kijakazi kwa masihara huku akitabasamu. Mara Vuai aliendelea na kusema, “Kijakazi juu ya utu uzima uliokuwa nao sisi tutakuchukua katika shamba letu. Utakuwepo hapa kwa muda na serikali ya kimapinduzi ya ASP ina mipango madhubuti kuhusu watu wazima kama nyinyi. Zipo nyumba maalum zinajengwa kwa ajili yenu huko Sebulen, usitie wasiwasi wo wote. Kama nilivyokwambia sisi sote hapa ni kama watoto wako na sisi tutakuenzi wewe kama mzee wetu. Wewe Kijakazi una maarifa ya s’ku nyingi katika kazi za ufugaji na tutafurahi pindi ukiweza kuwapa vijana wetu maarifa yako katika kazi hiyo. Wao watakuwa tayari wakati wo wote kujifunza kutoka kwako. Sisi tulitumaini kwamba utakuja kujiunga na sisi zamani lakini ulichelewa. Njoo, Kijakazi, uishi na sisi hapa.”



    Kijakazi aliruka kwa furaha na mara aliukamata mkono wa Vuai na kutaka kuubusu lakini Vuai aliurusha mkono wake na kusema. “Kijakazi tabia hiyo itakubidi uiache hapa. Sisi hapa sote m wanachama sawa sawa vva shamba hili la ushirika na hapana mtukufu miongoni mwetu ambaye anataka kubusiwa mikono. Wewe Kijakazi utakuwa pamoja na sisi hapa lakini kwanza itakubidi ukapumzike na upate matibabu huko hospitalini. Sasa itakubidi urejee kwa Fuad ili ukachukue vitu vyako na halafu urejee hapa.”



    “Nani? Mimi? Mimi sina cho chote huko kwa Fuad, vitu vyangu vyote nilivyonavyo ni haya magwanda niliyovaa,” Kijakaz’ alisema huku akishusha pumzi kama mtu aliyetuliwa mzigo mz’to.



    Kijakazi alishtuka kwa sauti ya mvumo mkubwa aliousikia, masikio yakamziba. Alitaka kufanya kama kukimbia lakini mara aliona makundi ya watu wakitoka kutoka kwenye mabanda mbali mbali. Ilikuwa ni saa kumi na mbili magharibi na sauti ile ilikuwa ni sauti ya king’ora iliyotowa ishara ya kumalizika kwa saa za kazi.



    Kwa mbali Kijakazi aliliona kundi la wanawake waliokazana miongoni mwao akiwamo Mkongwe. Kijakazi alimfuatia Mkongwe mbiyo huku akimpigia makelele na alipokutana naye alimkumbatia huku machozi yakimtoka.



    “Kweli, mwanangu! Yote uliyokuwa ukiniambia ni kweli tupu” Kijakazi alimwambia Mkongwe huku akisugua uso wake juu ya mabega ya Mkongwe.



    Mkongwe hakumjibu kitu. Kundi la watu waliokuwa wakitoka makazini mwao walimzongea Kijakazi ambaye al’kuwa bado amemkumbatia Mkongwe huku machozi yakimmiminika. Wote waliingiwa na hamu ya kumwona Kijakazi kwani siku nyingi walikwisha kusikia hadithi zake.



    “Nyamaza shoga, nyamaza shoga yangu, usilie; hapa umefika kwenu na sote tukikungojea kwa hamu kubwa. Twende zetu.” Mkongwe alimshika mkono Kijakazi na kumwongoza chumbani kwake.



    Mara Vuai alinyanyua sauti yake na kumwuliza Mkongwe, “Unafikiri Kijakazi leo atalala wapi?”



    “Haidhuru mimi niko tayari kulala po pote pale!” Kijakazi alisema kwa ghafla huku ak’jipangusa machozi.



    “Atalala na mimi: yeye atalala juu ya kitanda na mimi nitatandika mkeka chini nakulala hapo. Karibu pamoja na sisi shoga yangu,” alisema Mkongwe.

    http://pseudepigraphas.blogspot.com/

    “Ahsante, shoga yangu, ahsante!”



    Mkongwe alimwongoza Kijakazi mpaka chumbani kwake ambako walilala pamoja siku ile.



    Fuad alibakia peke yake, mambo yalimbadilikia, na hatimaye hakuweza tena kuisbi Unguja. Aliondoka kwa njia ya magendo, labda kwa kutumia n’galawa au mashua. na bapana aliyejua alitokomea wapi.



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog