Simulizi : Penzi La Mzoa Takataka
Sehemu Ya Nne (4)
Akiwa ndani ya gari yake ya kifahari, mama Mazoea aliambaa sehemu mbali mbali, vijiweni na mahala wakusanyikapo vijana. Lakini hakubahatika kumuona mzoa takataka Nyogoso,hata alipojaribu kuwauliza baadhi ya watembea kwa miguu kuhusu kama watakuwa wamemuona ila kila mmoja alimjibu "Hapana sijamuona huyo mtu na wala simfahamu". Ni majibu ambayo yalimnyong'onyesha mama Mazoea, alishusha pumzi ndefu ilihali machozi nayo yakilegalega kunako mboni zake. Hofu ilimjaa, akiamini kwamba tayari wakati wa kumpoteza binti yake umewadia sababu matumaini ya kumpata kijana Nyogoso yaliaonekana kupotea.
Aliwaza sana, kitendo hicho kilimfanya aegeshe gari yake pembeni ya barabara ili afikirie kipi cha kufanya. Baada ya dakika kadhaa alipata wazo ila kabla hajalifanyia kazi wazo hilo alishuka kwenye gari akaelekea kununua maji dukani akanywa kisha akarudi ndani ya gari lake, safari ya kumtafuta Nyogoso ikaendelea.
"Hapa lazima ninyooshe mpaka Kawe, kule vijana wazoa takataka wapo wengi sana nadhani naweza kufanikiwa kumpata. Loh! Mungu wangu nisaidie" Alijisemea hivyo mama Mazoea akiwa ndani ya gari lake, aliliendesha kuelekea Morocco Airtel ili afike mpaka Kawe mahali ambako wapo wazoa takataka wengi. Lakini kabla hajavuka barababra itokayo Tegeta kuelekea Muhimbili, Kariakoo. Alikanyaga break kaisi kwamba gurudumu za gari lake zikasota, harufu nayo ikasikika ilihali watu walioshuhudia kitendo hicho wakionekana kutaharuki. Macho ya mama Mazoea hayakuamini kile yanacho kiona,akiwa na taharuki akajiuliza "Ni yeye au nimemfanananisha?.."
"Hapana ni yeye ngoja nigeuza gari" Aliongezea kujisemea mama Mazoea wakati huo huo akigeuza gari yake kuelekea kule alikomuona Nyogoso akiambaa kando ya barabara iendayo Makumbusho mpaka Tegeta. Ila kabla hajaanza kumfuata, taa nyekundu iliwaka, kitendo hicho kilimkera mama Mazoea kwa sababu ilimpelekea kuvuta subira mpaka pale taa ya kijani itakapo mruhusu kuendelea na safari. Hapo ndipo alipoamua kuegesha gari lake kando ya barabara kisha akatimua mbio kumfuata Nyogoso.
"We kijana.. We kijana" Aliita mama Mazoea wakati huo akizipiga hatua za haraka haraka kumfuata Nyogoso ambaye naye alipoisikia sauti hiyo akageuka nyuma ili amtazame mtu huyo anayepasa sauti hiyo. Alistuka kumuona mama Mazoea, hofu ilimjaa moyoni hasa baada kukumbuka kipigo alicho kipata kutoka kwa Afande Daniel. "Mungu wangu nimekwisha! Bado tu anaendelea kunifuatilia?.." Akiwa na wingi wa hofu alijiuliza hivyo Nyogoso ilihali muda huo huo mama Mazoea akizidi kumkaribia, lakini kabla hajamfikia akasema "Samahani kwa yote kijana wangu, naomba usiniogope nipe dakika mbili tu za kunisikiliza" Alisema hivyo mama huyo huku akimuita Nyogoso kwa ishara ya kiganja. Ila mzoa takataka Nyogoso alisita akihofia kuwa huwenda mama huyo anatumia janja ya kumtia kwenye mkono ya police kwa mara nyingine tena. Kitendo hicho kilimuumiza sana mama Mazoea, pasipo kujali pesa alizo nazo na wadhifa wake juu ya kijana huyo mzoa takataka, alipiga magoti chini huku akiomba msamaha kwa yote aliyomfanyia hapo awali, machozi nayo hayakuwa mbali,yalimtoka mithili ya maji wakati huo kila mara akipandisha kwikwi. Lah! Kitendo hicho kilimsikitisha sana Nyogoso, punde akainua uso wake akatazama juu kisha akajisemea "Mungu wangu, wewe ndio uliyeniumba na wewe ndio unayejua hatma ya maisha yangu. Bila shaka magumu haya ninayopitia huwenda yakawa na maana kubwa siku za usoni. Nitazame mja wako" Alipokwisha kujisemea hayo Nyogoso akayafuta macho yake yaliyokuwa yakimtiririka kisha akazipiga hatua kumfuata mama Mazoea ambaye bado alikuwa amempigia magoti. Alipofikia akwambia "Hustahili kunipigia magoti, hebu nyanyuka nilisha kusamehe" Mama Mazoea alinyanyuka akajifuta machozi, kwa sauti ya chini iliyojaa huzuni ndani yake akasema "Asante kwa msamaha wako lakini naomba uambatane na mimi mpaka hospital ukamuone mchumba wako, nahisi kukuona kwako ataweza kupata ahueni. Nakuomba tafadhali nipo chini ya miguu yako"
"Mchumba wangu?.." Alihoji Nyogoso.
"Ndio, Mazoea yupo hoi hospital. Hali wala hawezi hata kuongea naomba ukamuone" Alijibu mama Mazoea huku machozi yakimtoka. Pumzi ndefu alishusha mzoa takataka baada kuyasikia maneno hayo, punde akasema "Nipo tayari kumbatana na wewe lakini ondoa dhana ya kudhania kuwa mimi nina mahusiano na binti yako. Hata twende" Nyogoso alipokwisha kumwambia hivyo mama Mazoea, walikwenda mahali lilipo gari lakini kabla hawajaingia ndani ya gari, mama Mazoea alikwenda dukani kumnunulia nguo mpya mzoa takataka na kisha kumtaka azivue nguo zake zilizochakaa ambazo pia zilikuwa zikitoa harufu mbaya, avae nguo hizo mpya.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hapana sipo tayari kuvaa nguo hizo, na hatakama nitahitaji nguo mpya basi nitanunua kwa pesa yangu" alisema Nyogoso mara baada kuletewa nguo hizo. Ni maneno ambayo yalimshangaza mama Mazoea, hakuamini kama kweli kijana huyo mzoa takataka angeliweza kuzikataa nguo hizo nzuri na za ghalama. Akashusha pumzi ndefu kisha kisha akajisemea "Ama kweli huyu ni mskini jeuri" Mama Mazoea alipokwisha kujisemea hivyo safari ya kuelekea muhimbili ikaanza. Punde walifika, walisubiri ule wasaa wa kuwaona wagonjwa uweze kuwadia. Naam! Hatimaye wasaa huo uliwadia, mama Mazoea akiwa sambamba na mzoa takataka Nyogoso walizipiga hatua kuingia kwenye wodi aliyolazwa Mazoea. Walipoingia mama Mazoea akamtazama binti yake ambaye kwa muda huo alikuwa ameyafumba macho yake.
"Mazoea.." alipokwisha kumtazama akapasa sauti kumuita. Mazoea aliposika sauti ya mama yake aliyafumbua macho yake kumtazama na ghafla aliachia tabasamu pana baada kumuona mzoa takataka kipenzi cha moyo wake. Wakati huo Nyogoso akarijibu tabasamu la Mazoea kisha akasema "Pole sana"
"Asante, mambo" Alisema Mazoea huku akisogea nyuma ya kitanda kisha akamtaka Nyogoso akae.
"Hapana nitachafua shuka acha nisimame tu" Alikataa Nyogoso kukalia kitanda hicho akihofia kuchafua shuka nyeupe iliyotandikwa hapo kitandani. Mazoa alipoona Nyogoso kakataa kukaa, alinyoosha mkono akashika fulana aliyovaa Nyogoso kisha akamvuta kwa nguvu wakati huo huo Nyogoso akajilegeza akajikuta akidondokea kwenye kifua cha mrembo Mazoea ilihali Mazoea alipeleka mdomo wake kwenye mdomo wa Nyogoso akihitaji timi yake na ya mzoa takataka ziweze kukutana lakini Nyogoso aliogopa kufanya kitendo hicho, hivyo alipindisha mdomo wake ila kati Mazoea hakutaka kuelewa, mbele ya macho ya mama yake akapata kuthibitisha namna ampendavyo kijana huyo mzoa takataka.
Wakati kitendo hicho kikiendelea kufanyika, mama Mazoea alikuwa akitazama pembeni ilihali akijiuliza "Hivi ni kitu gani alichovutiwa mwanangu kwa kutoka kwa huyu kijana mchafu asiye na mbele wala nyuma?..Je, vijana watanashati wanaojua kuvaa hajawaona mpaka ampende huyu rofa??
No.. No Hapana si bure hapa katikati kuna kitu huwenda kakifanya huyu kijana. Kweli Mazoea na urembo wote huu?.. " Alijiuliza maswali mengi sana mama Mazoea juu ya binti yake na kijana Nyogoso mzoa takataka. Lakini yote kwa yote alijikuta akikosa majibu wakati huo alisikia sauti ikisema" Amini nakupenda sana wewe mkaka. Nilitaka kujiua kwa ajili yako. Niliona haina haja ya kuendelea kuishi pasipo penzi lako. Nakupenda sana sijali umaskini wako, niombee nipone tufurahi pamoja " Mama Mazoea aligeuka kwa hasira baada kusikia sauti hiyo ya binti yake aliyokuwa akimwambia mzoa takataka Nyogoso. Nyogoso hakujbu, alikaa kimya jambo ambalo lilizaa ukimya wodini humo ingawa baada ya muda kadhaa kimya hicho kilitoweka na kisha maongezi mengineyo yakafuatia kati ya mama na mwana. Muda wa kwaona wagonjwa alikwisha, mama Mazoea na mzoa takataka Nyogoso walimuaga Mazoea kisha wakaondoka wakaimuacha Mazoea akiwa mtu mwenye furaha isiyo kifani baada kumueleza Nyogoso ukweli ulio ndani ya moyo wangu wake kwa mara nyingine tena.
"Nafurahi sana kwa ujio wako, nakusihi usi site kuja kumtembelea pindi utakapo pata nafasi" walipofika nje mama Mazoea akimwambia hivyo Nyogoso. Nyogoso alikubaliana na hitaji hilo la mama huyo kisha wote wakapanda gari ambapo Nyogoso alimtaka mama Mazoea amrudishe kule alikomkuta, naye mama Mazoea hakutaka kupingana na matakwa ya kijana huyo haraka sana alimfikisha. Baada kufika mahali hapo Nyogoso alishuka kwenye, muda huo huo mama Mazoea naye akafungua mkoba wake akatoka pochi ambayo aliifungua akachukua shilingi alfu tisini akamkabidhi Nyogoso lakini kabla Nyogoso hajazipokea pesa hizo mara ghafla....
Kabla Nyogoso hajazipokea fedha hizo alizokuwa akipewa na mama Mazoea, ghafla kundi la vibaka wakazikwapua fedha hizo. Nyogoso alipojaribu kugombana nao akajikuta akiambulia kipigo cha mbwa mwizi kutoka kwa vibaka hao. Lakini wakati kizazaa kikiendelea, punde si punde jeshi la police lilifika eneo hilo la tukio ambapo waliwakamata hao vibaka akijiumuishwa na Nyogoso wote kwa pamoja walipandishwa kwenye gari la police huku Nyogoso akiponzwa na nguo zake chakavu alizovaa jambo ambalo jeshi hilo la police lilishindwa kutofautisha yupi mstarabu na yupi kibaka. Katika gari la wazi.. Mzoa takataka Nyogoso na kundi la vibaka walipandishwa puta ilihali muda huo mama Mazoea alionekana akiongea na police hao akiwaasa ukweli kuwa Nyogoso sio kibaka kama wadhaniavyo lakini police hao katu hawakuta kumsikiliza zaidi mmoja wao alisikia akisema "Hebu kwenda zako na gari lako la mkopo, serikali ipo kazini hapa" Kauli ya police hiyo iliwapekea wenzake kaungua kicheko huku wakigongana mkono wakionyesha kufurahishwa na kile alichokizungumza mwenzao. Baada gari hilo la police lililobeba vibaka na Nyogoso kutokomea, haraka sana mama Mazoea alifungua mlango wa gari akachukua simu yake ambayo alikuwa ameweka kwenye siti, akitetemeka alitafuta namba ya Afande Daniel alipoipata alipiga. Afande Daniel muda huo anapigiwa simu na mama Mazoea alikuwa yupo ofsini kwake akipitia baadhi ya makashablata, hivyo alipoona amepigiwa na mama Mazoea akajikuta akiachia tabasamu pana wakati huo ndani ya nafsi yake akijisemea "Ama kweli mwanaume halali njaa bali huchelewa kula" Alipokwisha kujisemea hayo akabofya kitufe cha kijani kisha akiweka simu sikioni.
"Hello tajiri kubwa!.." Alitania Afande Daniel ilihali tabasamu lisikatike usoni mwake.
"Uko wapi muda huu?.." Aliuliza mama Mazoea huku akiwa na hofu dhufo lihali.
"Nipo ofsini kwangu" Alijibu Afande Daniel.
"Sawa naomba tuonane mara moja tafadhali nakuomba sana".
"Sawa shaka ondoa, wapi sasa?.."
"Ammmh tukatane Magomeni Mikumi"
"Sawa fanya haraka basi utakuta nimefika nakungoja" Alimaliza kwa kusema hivyo Afande Daniel kisha akakata simu ambapo baada kufanya hivyo alimgeukia Afande mwenzake aliyeitwa James halafu akamwambia "James, kunadili limetokea mtu wangu wa nguvu. Kwahiy basi acha mimi nikalimalize, endapo kama mkuu akija mdanganye vyovyote vile uwezavyo ilimradi unilindie kibarua changu" Alisema hivyo Afande Daniel wakati akichukuwa pingu yake na kisha kuining'iniza kwenye mkanda wa suruali yake.
"Sawa kamanda wewe wala usiwe na hofu, cha muhimu chochote utakacho kipata tutagawana pusu kwa pasu" Alijibu Afande James akimwambia Daniel.
"Haina shida kamanda, maisha yenyewe yakowapi? Ngoja tukapambane huko mambo yakiwa mazuri utafurahia mwenyewe. A hahahahah" Aliongea Afande Daniel huku akimaliza kwa kicheko. Alipohitimisha kicheko hicho aliondoka zake moyoni akiwa na furaha tele akiamini kuwa anaenda kukutana na tajiri mwanamke asiyejua kuichungulia pesa. Muda huo Daniel akitii wito, mama Mazoea naye alikuwa akiliendesha gari lake kwa kasi ili awahi kufanikisha suala la kumtoa Nyogoso kituo cha police, ilimladhimu kufanya hivyo akijua kabisa mzoa takataka huyo ndio mtu pekee atakaye mfanya binti yake kupona. Mama Mazoea alifika mahali hapo walipopanga kukutana, muda mfupi baadaye Afande Daniel naye aliwadia kwa usafiri wa pikipiki.
Huku akihaha kijasho chembamba kikimtoka mama Mazoea alisema "Kamanda unamkumbuka yule kijana ambaye nilikwambia mpe onyo aachane na mwanangu?.."
"Ndio namkumbuka" Alijibu Afande Daniel.
"Basi naomba nisaidie kumrudisha, ka..." Kabla mama Mazoea hajamaliza kuongea alichotaka kusema, Afande Daniel alidakia akasema "Kwani katweka? Na kama katekwa mtekaji unamjua?.."
"Ndio sio majambazi ila jesho la police kama ulivyo wewe" Alijibu mama Mazoea. Afande Daniel alistuka kusikia kuwa mzoa takataka ametekwa na police, kwa taharuki akarudi kumuuliza " Kafanya kosa gani mpaka akamatwe na police?.." Swali hili la Afande Daniel lilimfanya mama Mazoea kushusha kwanza pumzi ndefu kisha akamueleza namna tukio lilivyotokea mwanzo mpaka mwisho. Daniel alipoyasikia maelezo hayo akamuuliza mama Mazoea kwa mara nyingine tena." Vipi namba za gari umezikariri?.."
"Ndio ninazo kichwani"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hebu nitajie" Alisema Afande Daniel ambapo mara moja mama Mazoea akazitaja namba hizo wakati huo Daniel akiziandika kwenye simu yake na ghafla Afande huyo akaachia tabasamu kisha akasema "HAPA kazi imekwisha, cha msingi pesa tu iwepo ya kutosha kwa sababu hapa nacheza na kazi na sio mshahara"
"Daniii kamanda wangu, pesa kwangu sio tatizo lakini kwa muda huu nina laki mbili tu sababu pesa nyingine ilikwapuliwa na vibaka" Alisema mama Mazoea mwanamke mnene mweupe mwenye adhili ya kiarabu. Maneno hayo aliyokuwa akimwambia Afande Daniel akiyaongea kwa kujiamini kabisa.
"Leta hiyo hiyo mamaa.. Nibaki nakudai laki nyingine mbili" Alijibu Afande Daniel. Hima mama Mazoea akamkabidhi kiasi hicho cha fedha. Kama ilivyo ada akazihakiki vizuri kisha akazitia mfukoni huku akitazama kila pende halafu akaongeza kusema "Jioni tukatne Sinza kwa lemi nakuletea mtu wako"
"Sawa tutawasiliana" Alijibu mama Mazoea kisha kila mmoja akajua hamsini zake.
Baada kamanda Dani kuachana na mama Mazoea hatimaye aliwasiliana na police mmoja aliyemfahamu kwenye hicho kituo. Bahati ikawa njema kwake zaidi kwani Afande huyo naye alikuwa miongoni mwa waliohusika kuwakamata vibaka wale akiwemo na mzoa takataka Nyogoso. Hivyo Daniel aliweza kutumia nafasi hiyo kumshawishi Afande mwenzake wamuache Nyogoso. Mpango huo ulifanikiwa, saa ya jioni Afande Daniel akiwa kamanda mwenzake walikutana samba na na Nyogoso pembeni.
"Kila kitu kimeenda Sawa?.." Aliuliza Afande Daniel.
"Hofu ondoa kabisa ila usivunje makubaliano" Afande huyo aliyefanya liwezekano kuhakikisha Nyogoso anatolewa selo alijibu.
"Ahahahah" Alicheka Afande Daniel kisha akasema "Nakukubali sana, pesa ipo kamanda wangu. Ngoja tukodi taxi twende kwa mama mwenye mtuhumiwa". Alipokwisha kusema hivyo Afande Daniel aliita taxi, punde ikafika na safari ya kuelekea kule walipoahidia kukutana na mama Mazoea ilianza. Lakini wakiwa ndani ya gari, Nyogoso aliomba ashushwe ili akajisaidie. Makamanda hao walikubaliana naye huku wakimsihi afanye haraka. Hapo mzoa takataka akaingia uchochoroni kisha akatimua mbio akawakimbia hao Makamanda kwani hakujua ni wapi anakopelekwa vile vile hofu ilimjaa zaidi baada kumuona Afande Daniel, Afande ambaye alimanusura amtoe roho. Hofu hiyo ndio iliyomfanya mzoa takataka kutumia ujanja huo kuweza kuponyoka kwenye mikono ya maafande hao.
Hatimaye muda ulizidi kutaladadi, Daniel akiwa na kamanda mwenzake wakizidi kumngoja Nyogoso alirudi ili waendelee na safari. Ila waliona Nyogoso hatokei na hapo ndipo Daniel alipoamua kushuka kwenye gari akazipiga hatua kuelekea kule alikoenda Nyogoso kujisaidia lakini kabla Afande Daniel hajafika ghafla simu yake iliita, alipoangalia jina akagundua ni Afande James ndiye aliyempigia.
"Mmmh.." Aliguna Daniel huku akionekana kuwa na hofu moyoni mwake. Alipopokea ikasikika sauti ya James ikisema "Kamanda ofsini kimenuka..."
"Mungu wangu.. Kulikoni tena kamanda James??.." Alihoji Afande Daniel huku akitetemeka mwili mzima wakati huo huo Afande James ameshakata simu yake.
Afande Daniel alijikuta akipagawa baada Afande mwenzake kumpasha habari iliyostua moyo wake, akiwa mnyonge mithili ya kifaranga kilicho nyeshewa na mvua alirejea ndani ya gari kisha akamwambia dereva ageuze gari kuelekea ofisini. Afande yule aliyeambatana naye alistushwa na uamuzi huo huku akiogopa akionekana kutolewa sababu hasa iliyopelekea wao kughaili safari yao ndipo kwa sauti ya mshangao akasema "Kamanda kulikoni mbona hivi? Na unaonekana haupo sawa. Je, kuna tatizo?.."
"Ndio kamanda tena tatizo kubwa hasa..." Alijibu Afande Daniel.
"Lipi hilo?.."
"Kwanza kabisa mtuhumiwa wetu katotoroka, na pili Afande mwenzangu kaniambia kwamba ofisini kimenuka. Sasa sijui kipi kimejili huko" Alijibu Afande Daniel kwa sauti ya chini iliyojaa huzuni ndani yake wakati huo huo taxi nayo tayari imeshafika kituoni. Alishuka Afande Dani wakati huo akionyesha kuwa mnyonge, alizipiga hatua kuelekea ofisini lakini kabla hajaingia ndani alisikia sauti ya yule Afande waliyefanya naye dili la kumtoa Nyogoso selo kinyume na utaratibu unao takiwa. Dani aligeuka kisha akarudi kumsikiliza ilihali muda huo huo Afande yule aliifungua mlango wa gari, akiwa na hasira kali akasema "Kamanda Daniel, vipi sasa unaniachaje? Ama unaona kazi ile nyepesi sio?."
"Hapana sio kwamba kazi rahisi kamanda wangu ila kama unavyoona mtuhumiwa katotoroka, istoshe hapa nilipo sina hata senti. Pesa ambayo tungepata ni baada kumfikisha yule mtuhumiwa kwa muhusika. Sasa unafikiri mimi pesa nitatoa wapi?.." Alijibu Afande Daniel huku uso wake ukiwa na hofu fulani. Jibu hilo la Daniel halikuweza kumshawishi kamanda yule kukubali jibu hilo. Hapo ndipo alipoamua kuchukuwa uamuzi wa kumkunja shati yake kisha akampiga ngumi. Kitendo hicho kilimshangaza Afande Daniel, awali akaona kama utani ila muda huo kamanda yule hakuwa kimasihara. Kile alichokifanya alizamilia kutoka moyoni kwani bado aliendelea kumshushia Daniel ngumi na mateke mfululizo. Hapo Daniel akapata kuelewa ya kwamba kamanda mwenzake kazamilia kweli kweli, ndipo naye alipoamua kukataa kuaibishwa kizembe jambo ambalo lilizua patashika nguo kuchanika baina ya makamamda hao. Ila wakati hao makamanda walipokuwa wakipigina, mkuu wa kituo alikuwa kando akiangalia mchezo mzima. Baada kuona wote uwezo unalingana ndipo alipowaamuru watii wito kisha kila mmoja aeleze sana au hasa iliyopelekea kuzaa ugomvi huo.
***********
Upande wa pili Nyogoso alikuwa moja ya mitaa akiendelea kutimua mbio baada kuwaponyoka Afande Daniel na mwenzake, Nyogoso alitimua mbio mithili ya ndege aliyekoswa kwenye urimbo. Hatimaye anarudi maskani huku akiwa na shauku ya kumuona jamaa yake atwae Jaluo baada kupotezana kwa kipindi kirefu, lakini siku hiyo Jaluo hakurejea maskani hapo na wala Nyogoso hakujua ni sababu gani iliyompelekea Jaluo asirejeee. Alilala kwa amani kabisa akingojea kesho iweze fika ili arudi mtaani kuendeleza kazi yake ya kuzoa takataka. Usiku wa siku hiyo ukawa siku wa mawazo kichwani mwake, alifikiria matukio kadhaa wa kadha anayokumbana nayo toka aingie jijini Dar es salaam. Wakati huo asiamini juu ya binti wa kitajiri mrembo Mazoea kuvutiwa naye hali ya kuwa yupo kwenye maisha hayo ya kifukara "Mmmh" Alijikuta akiishia kuguna ndani ya moyo wake baada kukumbuka yote hayo. Na ghafla machozi yalimtoka alipomkumbuka mama yake mzazi aliyemuacha kijijini kwao, alijiuliza mstakabali wa maisha anayoishi, jibu alikosa jambo ambalo lilimpelekea kububujikwa na machozi mpaka pele usingizi ulipompitia.
Kesho yake asubuhi, ilikuwa siku njema sana. Jiji la Dar es salaam lilitanda wingi jiusi kiasi na punde si punde manyunyu ya mvua yalilimwagilia jiji hilo. Mzoa takataka Nyogoso aliamka akaingia mtaani, alitembea huku na kule hatimaye alibahatika kuona gunia. Alitabasamu kisha akauchukuwa mfuko huo, rasmi akarejea kwenye kazi yake ya kuzoa takataka kwa mara nyingine tena,safari hiyo alitembelea mitaa ya Sinza huku akipasa sauti akisema "Mzoa takatakaaaaaa.. Ta ka ta ka takaaaa" Ni sauti ambayo iliwafanya baadhi ya nyumba kufungua mageti yao wakimngoja mzoa takataka apite ili wamkabidhi mizigo ya takataka. Siku hiyo ikawa njema kwa mzoa takataka Nyogoso,ndani ya masaa manne tayari alikuwa ameeneza mzigo mkubwa kaisi kwamba alishindwa kujitwisha. Alihaha kwa nguvu zake zote ila alishindwa lakini bahati nzuri akatokea kijana mmoja muokota makopo, hivyo Nyogoso alimuomba kwa sauti ya unyenyekevu alimuomba kijana yule amtwishe mzigo huo wa takataka.
Yule kijana alikubali ombi la mzoa takataka Nyogoso, lakini baada kumtwisha alidai apewe fedha kitendo ambacho Nyogoso alipangana nacho. Kijana yule muokota makopo alizidi kulazimisha na punde akachomoa kisu kisha akasema "We wakuja utatoa hela hiyo au hutoi?.." Nyogoso aliogopa sana, haraka akatoka fedha akampatia kijana yule aliyemtwisha mzigo wa takataka.
"Unampa nani Elfu moja? Nitakutumbua utumbo ujue? Unataka kuniambia mzigo wote huu shilingi Elfu moja?.." Alihoji kijana yule baada Nyogoso kumpa shilingi Elfu moja ili naye abaki na shilingi Elfu moja. Mfukoni alikuwa na shilingi Elfu mbili.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hapana kaka, chukuwa hiyo hiyo ili na mimi nibaki na Elfu moja!." Nyogoso alijibu.
"Usinipangie.. Leta hela hiyo kabla sijakufanya kitendo kibaya Ebo" Aliongea kijana yule muokota makopo kwa sauti kali iliyomuogopesha Nyogoso nambapo alifanya hivyo haraka sana iwezekanavvyo. Kijana yule akaishia zake kwenye moja ya uchochoro hukua kiamuacha Nyogoso akimsindikiza kwa macho ingawa mwishowe alipasa sauti akasema "Mwizi.. Mwiziii.. Mwiziiii" Sauti hiyo iliwastua wakazi wa mitaa hiyo ya Sinza. Punde wakajazana mahali hapo, wakataka kujua mahali alipoelekea mwizi huyo, hawakumuona na hivyo Nyogoso akajikuta akiambulia matusi na maneno ya kejeli kutoka kwa watu hao waliofika eneo la tukio.
Siku ikawa imeisha vibaya kwa Nyogoso kijana mzoa takataka,alirudi nyumbani akiwa mnyonge sana huku akisubiri kwa hamu kubwa siku nyingine ijayo. Usiku wa siku hiyo alilala usingizi mzito sana aliamshwa asubuhi na mzee mmoja mwenye duka. Ni ngumu sana Nyogoso kukutwa na mzee huyo mwenye duka cha ajabu siku hiyo alimkuta. Alikurupuka kutoka usingizini, alipoyafumbua macho yake akakutana na mwanga wa jua la asubuhi na hapo ndipo alipochukuwa mabox yake ya kulalia akayahifadhi mahali pema wakati huo huo mzee mwenye duka hilo alisikika akisema "Siku nyingine ukingoja mpaka nikuamshe basi ujue utakuwa mwisho wa kulala kwenye falanda la duka langu" Nyogoso aliposikia sauti hiyo alimtazama mzee huyo akatikisa kichwa kisha moja kwa moja akaingia mtaani kutafuta riziki. Alitembea mitaa ile ile ya Sinza, mitaa iliyojaza nyumba zenye geti kali. Mtindo alitumia ule ule wa kupasa sauti ili kuwapa taarifa kuwa mzoa takataka anapita. Lakini wakati anatembea akiwa hana hili wala lile, nyuma yake alisikia honi ya gari. Alipisha kando gari hilo lipite, ambapo gari hilo aina ya Rav4 lilikanyaga dimbwi lenye maji machafu ambayo moja kwa moja yakamrukia Nyogoso akiwa kando hatau kadhaa.
Mzoa takataka Nyogoso alighazibishwa kwa kitendo hicho cha kumwagiwa maji machafu, lakini hakuwa na lakufanya zaidi ya kujitazama kisha kuendelea na safari yake. Muda huo lile gari ilionekana kusimama kwenye moja ya nyumba moja ambayo ilikuwa ya kifahari, ndani ya gari hilo alishuka binti mrembo mwenye kuvutia kwa mavazi yake mazuri. Binti huyo aliingia ndani geti la nyumba hiyo ya kitajiri kisha gari lile likaendelea na safari. Ila wakati binti yule alipokuwa anaingia ndani ya geti lile la nyumba ya kifahari alidosha kitu chini nje ya geti kutoka kwenye mkoba wake mkubwa pasipo yeye mwenyewe kujua. Mzoa takataka Nyogoso alipofika mahali hapo alikiona kitu hicho alicho dondosha binti yule ambapo alikichukuwa, ilikuwa ni pochi ndogo. Papo hapo aliifungua akakuta fedha kiasi na simu ye bei ghali pamoja na picha za passport size. Alishtuka Nyogoso kisha akagonga geti, punde likafunguliwa na mlinzi kabila la kimasai. Mlinzi yule kwa rafudhi ya kimasai alisema "" Hello unataka nini na nguo sako chafu?.. "
"Aah naomba uniitie binti aliyeingia aliyeingia humu ndani sasa hivi" Alijibu mzoa takataka kwa sauti ya upole huku akitabasamu. Mlinzi alicheka sana kisha akaongeza kusema "We wanini yule dadaa? Wakati wewe mtu chafu hivyo? Hebu toka haraka sana ondoka mahali hapa"
"Naomba tafadhali nina shida naye" Alisema Nyogoso huku mkono ulioshika pochi akiwa ameuficha nyuma. Lakini katu mlinzi hakutaka kumuelewa aliendelea kumfukuza ila kabla Nyogoso hajaondoka, Ilisikika sauti ikisema "Manyama! Hebu muulize huyo kichaa anataka nimlipe kiasi gani kwa kosa la kummwagia maji machafu. Na kama hatotaja funga geti ajue hamsini zake" Ilisikika sauti hiyo ikimwambia mlinzi. Haikuwa sauti ya mwingine bali ni yule binti aliyedondosha pochi. Maneno hayo aliyoongea kwa ndodo na dharau kubwa sana wakati huo akizipiga hatua kwa madaha kumkaribia mzoa takataka Nyogoso. Alipomfikia alimtazama kwa dharau na kwa kinyaa huku mikono yake ikiwa kiunoni na kisha akarudia kumuliza Nyogoso kaisi gani ampatie. Muda huo binti yule anafanya yote hayo, mzoa takataka Nyogoso alikuwa kimya asiseme neno lolote. Lakini mwishowe alishusha pumzi ndefu kisha kwa sauti ya kinyonge akasema "Samahani Dada mimi sihitaji hata senti kutoka kwako na ndio maana nilipookota hii pochi yako nimeona bora nikuletee. Nitakula kwa jasho langu" Alipokwisha kusema hivyo Nyogoso akamkabidhi binti huyo pochi yake,naye haraka sana akakagua vitu vyake vilivyomo, hatimaye alikuta vyote vimetimia hata kadi yake ya bank ambayo Nyogoso hakuiona nayo pia aliikuta. Hakika binti yule hakuamini macho yake, alijikuta akijilaumu juu ya kike alichomuonyesha mzoa takataka. Hivyo alihitaji kumuomba msamaha lakini tayari alikuwa amechelewa, mzoa takataka Nyogoso alikuwa ameshaondoka zake..!
Ni kitendo cha kushangaza ambacho kilimuacha mdomo wazi binti yule na kushindwa kujua ni moyo wa aina gani aliopewa kijana mzoa, roho ilimuuma sana hasa kwa dharau na nyodo aliyomuonyeshea pasipo kujua dhamila aliyonayo mzoa takataka. Yote kwa yote akajiapia kumtafuta Nyogoso popote pale alipo ili amuombe msamaha "Sikubali lazima nimtafute kwa ghalama yoyote ile.."
Alipania kumtafuta mzoa takataka ili amuombe msamaha, aligundua kosa lake la kumdharau pasipo kujua dhamila hasa aliyokuwa nayo kijana huyo. Aliingia ndani kuendelea na shughuli zake wakati huo mtaani mzoa takataka aliendelea kuzulula huku na kule kutafuta takataka. Kama ilivyo ada alipasa sauti yake akisema "Haya mzoa takataka napita takatakaaaa" Ni sauti ambayo alipasa huku akizipiga hatua za pole pole wakati huo masikio yake akiyatuliza vizuri walau asikie akiitwa, lakini hakuitwa nyumba hata moja kitendo ambacho kilimvunja moyo, aliamua kuketi kwenye nyumba iliyokuwa na varanda. Hapo aliamua kujilaza kwa dhumuni la kupumzika kidogo kisha baadaye aendelee na kazi yake. Usingi ulimpitia, alilala fo fo fo ila mwishowe alistuka baada kusikia sauti ikipiga mayowe "Mwizi...mwizi...mwizi!.." hima mzoa Nyogoso akakurupuka kutoka usingizini na ghafla mbele yake akamuona kijana yule kijana muokota makopo, kijana ambaye alimdhurumu pesa yake siku ya jana. Kijana yule mkononi alikuwa ameshika mkoba huku akitazama kila pande akishindwa kuchukuwa uamuzi sahihi wapi akimbilie ili kuokoa uhai wake dhidi ya wananchi wenye hasira kali, muda huo kijana yule anatafakari uamuzi wake, mzoa takataka Nyogoso alikuwa akimshangaa na hata asiseme neno lolote jambo ambalo lilimpelekea yule kijana kumrushia Nyogoso mkoba ule aliopora kisha yeye akatokomea uchochoroni ilihali muda huo huo kundi la watu waliokuwa wameshika siraha mbali mbali walifika mahali hapo. Nyogoso alijikuta akichezea kichapo kama mbwa mwizi kutoka kwa wananchi hao waliodhania kwamba yeye ndio mwizi. wakati kipigo hicho kikiendelea kwa kijana mzoa takataka, sauti ya mtu mmoja miongoni mwa wale waliokuwa wakimshambulia Ilisikika ikisema "Kila siku wanaiba, tumechoka wizi mtaani kwetu. Watu kama hawa uswahili wanaishia kutazamwa tu sababu wanaishi kwa kujuana. Mwanamdogo hii ni Sinza, umeingia choo cha kike, na kwa taarifa yako tuna kuchoma moto ili uwe mfano kwa wenzako". Maneno hayo yalimstua Nyogoso, akitokwa na damu puani na mdomoni alijieleza kwa kina kazi anayofanya, na sio kweli kwamba yeye ni mwizi kama wadhaniavyo. Utatezi huo wa mzoa takataka Nyogoso kamwe haukuweza kufua dafu mbele ya umati ule wa wananchi wenye hasira kali, zaidi waliagiza iletwe petrol. Punde garon iliyosheheni petrol illetwa. Hapo kijana Nyogoso akajua hatimaye mwisho wa maisha yake umewadia, akiwa mnyonge mithili ya mtu aliyefumwa ugoni alipiga magoti chini kisha akasema " Naam! Mungu wangu natumai haya ndio maisha ambayo umenichagulia, na pia sina wa kumlaumu sababu nimeyataka mwenyewe. Laiti kama ningeliyasikiliza maneno aliyoniasa mama basi leo hii nisingeishi maisha haya mpaka kufikia kikomo hiki cha maisha yangu. Sasa huu ni wakati wa kupokea roho yangu nisamehe kwa yote Mungu wangu ". Machozi yalimtoka Nyogoso baada kuhitimisha maneno hayo aliyokuwa akiyaongea kwa huzuni huku jasho lililojichanganya na damu likishuka mwili mwake ilihali muda huo huo likisafishwa na petrol aliyokuwa akimiminiwa kwenye mwili wake tayari kwa kuchomwa moto.
"Nipo tayari, nichomeni" Alipasa sauti hiyo Nyogoso. Wananchi waliokuwepo mahali hapo kila mmoja alimtazama mwenzie, mwishowe wote walisambaa wakimuacha mzoa takataka Nyogoso akiwa bado amepiga magoti akisubiri hukumu yake wakati huo akiwa ameyafumba macho. Alipohisi kimya kutawala tofauti na awali, akayafumbua akastaajabu kujikuta yupo peke yake, kwa mara nyingine tena akamshukuru Mungu kisha akasimama akarejea maskani kutulia kwani hakona sababu ya kuendelea kuzulula ikiwa amenusurika kifo. "Siku hii pia imekuwa mbaya kwangu" Alijisemea Nyogoso baada kufika maskani kwake, alihisi njaa kali sana mfukoni hakuwa na hata shilingi mia. Hali hiyo ilimpelekea mara kadhaa kukumbuka kijijini kwao, aliamini kuwa laiti kama angelikuwa kijijini kwao kamwe maswahibu hayo yanayo mkabali kila kukicha kamwe yasingetokea. Alilia sana mzoa takataka Nyogoso wakati huo huo kwingeneko Afande Daniel alijikuta akiachishwa kazi baada kubainika kuwa ni kuadi mkubwa wa kupokea rushwa na mara kadhaa kunyanyasa raia wasio na hatia. Ni jambo ambalo lilimuumiza sana Afande Daniel, alijutia yale yote aliyokuwa akiyafanya. Majuto kwake yakabaki kuwa mjukuu, katu wakuu wake wa kazi hawakutaka kubadili msimamo, Dani akavuliwa gwanda.
************
Siku zilisonga mzoa takataka akiuguza majeraha yake na pia akiendelea kufanya kazi yake ya kuzoa takataka majumbani kwa watu japo kwa tabu kulingana na hali yake jinsi ilivyo. Macho yake yalitamani sana kumuona swahiba wake wa karibu atwae Jaluo,ni wiki takribani mbili zilikatika pasipo yeye kumuona, kitendo ambacho kilizua hofu kubwa moyoni mwake.
"Wapi alipo mshkaji wangu?.." Mara kadhaa mzoa takataka Nyogoso alijiuliza swali hilo lakini majibu alikosa,roho ikiishia kumuuma hasa akikumbuka msaada mkubwa alioupata kutoka kwa Jaluo tangu siku ile aliyofika Dar es salaam. Upande mwingine, hospital. Hali ya mrembo Mazoea ilianza kutengemaa ambapo ilikuwa ni kinyume na matarajio ya mama wa binti huyo ambaye alidhania kuwa kutoonekana kwa kijana mzoa takataka kipenzi cha mwanaye basi huwenda akamkosa binti yake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ama kweli Mungu muacheni aitwe Mungu" Alijisemea hivyo mama Mazoea kwa tabasamu bashasha usoni mwake. Ni tabasamu ambalo siku kadhaa nyuma halikuweza kuonekana kwa mama huyo ila siku hiyo mambo yalikuwa tofauti sana hasa baada kuruhusiwa mgonjwa wake kurudi nyumbani. Lakini furaha hiyo iliweza kutoweka kama mawingu yayeyukapo angani pale alipojiuliza binti yake kapenda nini kwa kijana mzoa takataka. Kijana mchafu asiye na mbele wala nyuma. Hohe hahe.
Ni kitendo ambacho kilimuumiza mama Mazoea,subira pekee nayo ikachukuwa nafasi mayoni mwake akingojea binti yake hali apone kabisa kisha akae naye kitako amuulize kitu gani kavutiwa kutoka kw mzoa takataka Nyogoso. Subira yavuta heri, hatimaye siku hiyo aliyongojea mama Mazoea kwa hamu iliwadia. Alimsubiri Mazoea atoke sokoni akae naye amuulize kipi hasa juu yake na mzoa takataka. Wakati huo huo kule sokoni Mazoea alipokuwa akifanya manunuzi mbali mbali, ghafla alionekana mzoa takataka Nyogoso akizipiga hatua sokoni hapo. Moyo wa Mazoea ulistuka baada kumuona Nyogoso. Akatembea haraka haraka kumfuata ila wingi wa watu ndani ya soko hilo la Mabibo ulimfanya kuambulia patupu. Hakujua ni wapi alipo potelea ingawa moyo wake ulifurahi sana pindi alipomuona na kujihakiki kuwa bado kipenzi cha moyo wake yupo ndani ya jiji la Dar es salaam.
Na pindi mrembo Mazoea alipokuwa kwenye hali hiyo ya furaha, kwingeneko yule binti aliyeokotewa pochi na mzoa takataka anajikuta akivutiwa na ukalimu wake, jambo ambalo ilimjengea ile hali ya kutaka kuonana naye siku yoyote ile. Aliitwa Suzani binti yulw, mtoto wa pili kati ya wawili waliozaliwa. Yeye na kaka yake ambaye maisha yake yote aliyaendesha Uingereza. Maisha ya familia yakina Suzani yalikuwa ya kitajiri sana,alipata kile anacho kitaka kutoka kwa wazazi wake wote wawili. Kimsingi Suzani alideka kadri ajisikiavyo.
"Waooow! Anaonekana ni muaminifu sana. Mchafu wa nguo ila mzuri wa roho. Ghafla moyo wangu umetokea kumpenda na ndio maana wakati wote akili yangu inamuwaza yeye tu. Hakika ni kijana mzuri, kifua chake mimi hoi, bila shaka ni shida tu ndizo zinamfanya anakuwa kwenye hali ile lakini endapo kama nitamuelezea hisia zangu, akinikubalia.. Nitamsafisha na atakuwa mwanaume mzuri sana. Je, atanikubali? Kwa kile nilicho mfanyia sio rahisi ingawa najua nitafanya juu chini awe mpenzi wangu.. Bikira yangu iwe zawadi yake " Yote hayo alikuwa akijisemea Suzani muda huo akiwa kitandani akiwa amelala chali, akili yake ikimfikiria mzoa takataka Nyogoso. Wakati hayo yakiendelea kwa Mazoea na Suzani kwa nyakati tofauti tofauti, warembo hao wote kw pamoja wakilitamani penzi la mzoa takataka,, taarifa ya Afande Daniel kuachishwa kazi inamfikia mama Mazoea. Alistaajabu sana, kwa sauti ya mshangao akasema "Pole sana kamanda wangu! Nasikia umeachishwa kazi kwahiyo unataka kuniambia kwamba yule kijana kafungwa au ameachiwa?.."
"Aah mama, kila kitu kilkuwa sawa ila yaliyotokea ndio kama hayo. Pesa zako zimeniponza. Ila kwa hivi sasa yupo uraiani. " Alijibu Afande Daniel.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Yupo uraiani?.. Sawa pole kwa matatizo. Pia asante kwa kujuza". Alipokwisha kusema hayo mama Mazoea alikata simu. Pumzi ndefu alishusha akajua kabisa endapo kama Mazoea atamuona mzoa takataka basi atakuwa hakamatiki. "Hapana siwezi kuwa na mkwe mzoa takataka mimi" Aliongea kwa jazba mama Mazoea huku akizipiga hatua kuelekea chumbani kwa binti yake kumuuliza kipi hasa alichompendea mzoa takataka kana kwamba hawaoni vijana wazuri wasafi watanashati na wenye pesa. Muda huo mama Mazoea anaelekea chumbani kwa Mazoea, nje ya nyumba hiyo, geti liligongwa. Alibisha hodi kwenye geti hilo hakuwa mtu mwingine bali ni mzoa takataka wakati huo mkononi akiwa na gunia, nia yake alitaka kuulizia takataka pasipo kujua kuwa geti hilo alilobisha hodi ni nyumba yakina Mazoea..
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment