Simulizi : Nini Maana Ya Mapenzi Sehemu Ya Nne
(4) Kwenye gari Erica aliamua kumuuliza Moses
kimtego, “Kwani Erick kakuambia mimi ni nani yake?” Moses
alicheka kisha akamjibu, “Kasema wewe ni partner wake” Erica
akatabasamu, ila Yule Moses akamuuliza, “Niambie kama kuna cha
zaidi?” “Hamna bhana, ndio hivyo hivyo” “Ila mbona Tumanini
anakuchukia sana?” “Sijui kwanini” “Na kwenye hilo duka yupo
yeye” Erica alivyosikia hivyo alihisi akikosa muelekeo kabisa, maana
hakuna kitu alichokuwa anakiogopa kama kukutana na Tumaini, akamwambia Moses
kuwa asiende tena, ila Moses alikazana kusema ni lazima Erica afike kwenye hilo
duka. “kwani unamuogopa nini Tumaini, lile ni duka la Erick, Tumaini
anakusumbua nini sasa?” “Hapana, sikutaka tu kuonana nae
kwasasa” “Usijali, mimi nipo” Moses alimshawishi Erica hadi
akakubali kwenda kwenye hilo duka. Bahati alifika nyumbani
kwakina Erica na kugonga, alifunguliwa mlango na mama yake Erica ambaye
alionyesha kushangaa sana ujio wake, Bahati akamsalimia na kumuulizia Erica, ila
huyu mama alimkaribisha ndani kwanza ili amuhoji, Bahati akaingia na kukaa,
kisha mama Erica akaanza kuongea, “Haya leo umekumbuka nini, si
niliambiwa umeoa wewe?” “Mama, nimemuona Erica, naye anasema nimeoa
niongozane na mke wangu, kwakweli mama sielewi hata imekuwaje hadi nimeoa
mwanamke mwingine, mwanamke ninayempenda ni Erica tu na itabaki hivyo siku
zote” “Sasa mwanangu atakuwa mke wa pili?” “Nipo tayari kumuacha
huyu niliyemuoa” “Weee usilete laana kwenye ukoo wetu, yani umuache huyo
umuoe mwanangu! Haipo hiyo, kwanza Erica hayupo?” “Yuko
wapi?” “Wewe si ulioa? Erica nae kaolewa, kwahiyo yupo kwa mume
wake” Mama Erica alimdanganya Bahati maana alishajua
alivyoking’ang’anizi ila Bahati alijihisi vibaya saba kuambiwa kuwa Erica
kaolewa, alitamani hata ardhi ipasuke, akaanza kulia, “Mama, kwanini
mmenifanyia hivyo lakini? Erica wangu nampenda sana, kwanini
mama?” “Weee usinichulie, mara ya mwisho umekuja hapa na familia yako
mkaongea maneno ya kejeli sana, halafu baada ya hapo hukuja tena eti leo hii
ndio unafika na kilio kuwa unampenda sana Erica, umechelewa kwakweli tena
umechelewa haswaa, ulikuwa ukiishi huko kwa raha zako hata mwanangu humkumbuki,
leo hii eti Erica ndio mwanamke wa maisha yangu. Hebu nitolee balaa mimi,
ulimwaga mboga, na sisi tukamwaga ugali, umeoa na Erica ameolewa
kwaheri” Kwakweli Bahati aliinuka na kuondoka ila alikuwa anajisikia
vibaya sana, kiasi kwamba hakuweza hata kwenda nyumbani kwake kwa muda huo na
kuamua kwenda ufukweni ambako alikutana na Erica kwa mara ya
kwanza. Walifika dukani na kushuka, kiukweli Erica hakutaka
kabisa kuingia kwenye duka ambalo yupo Tumaini maana akifikiria na matatizo
aliyoyapata Sia ndio akazidi kuwa na mashaka. Walivyoshuka tu Erica aliomba
kuonyeshwa uwani ili akajisaidie, na aligoma kuacha mkoba wala mtoto wake,
ikabidi Moses amuonyeshe, “Ukizunguka hapo nyuma tu utaona vyoo vya
kulipia” Basi Erica akazunguka ila hakuingia chooni badala yake
alisimamisha bodaboda na kupanda na mwanae kisha ile bodaboda
ikaondoka. Walipofika mbele mbele, bodaboda iliishiwa mafuta kwahiyo
Yule wa bodaboda akapita sheli ili kuweka mafuta, wakati yuko pale sheli
alitokea mtu mmoja na kumshika bega, Erica alipogeuka Yule mtu alikuwa ni Babuu,
basi akasalimiana nae huku akihisi lazima Babuu ataongea nae maneno machafu tu,
ila Babuu alianza kusema, “Erica huyu mtoto anazidi kufanana na
Rahim” “Sitaki uendelee kumfananisha mwanangu na mwanaume ambaye hajui
umuhimu wa mtoto” “Sijasema kwa ubaya wala kwa kejeli ila nimesema
ukweli, ila Erica kupanda pikipiki na mtoto sio vizuri ujue” Yule
bodaboda alipomaliza kujaza alimwambia Erica apande tena waondoke, ila Babuu
akamuuliza Yule bodaboda, “Kwani unamdai shilingi ngapi hadi
hapa?” “Elfu mbili” Babuu aliitoa ile hela na kumpa bodaboda,
kisha Yule dereva akaondoka zake, kisha Babuu akamwambia Erica, “Hata
kama Rahim hataki kumuhudumia mtoto ila bado sio sababu yaw ewe kupanda pikipiki
na mtoto, ni hatari sana. Baba zake wadogo tupo, tuambie tutamuhudumia, ila
naumia sana maana huyu mtoto angekuwa damu yangu kabisa, yani mimi badala ya
kuwa bamdogo ningekuwa baba” “Achana na mimi kabisa” Erica
akataka kwenda kusimamisha usafiri mwingine aondoke, ila Babuu alimuitia usafiri
na muda kidogo tu gari la kukodi lilifika kisha Babuu akafungua mlango ili Erica
na mtoto wapande na walipopanda tu na yeye akapanda na kumuelekeza dereva
kwakina Erica ili awapeleke. Erica alimuangalia Babuu maana alimshangaa
ule moyo wa huruma vile kautoa wapi, “Kwanini umeamua kufanya yote
haya?” “Erica, kiukweli nimekaa nikafikiria na kuona kwamba katika
maisha yako nina sababu kubwa sana ya kujilaumu na mimi kuliko kukulaumu wewe,
kukuita malaya sijui hufai sio maneno yanayofaa kwani kwa kiwango Fulani ni mimi
nimesababisha yote” “Kwanini unasema hivyo?” “Erica, mimi nina
makosa kwako nina uhakika kama ningekutambulisha ndugu zangu basi isingetokea
iliyotokea kuwa ungetembea na ndugu zangu. Erica, siwezi kukuweka kwenye kundi
la wanawake malaya ila najua kuna kitu kilisababisha tusiwe pamoja, na kama
hatukuwa pamoja tena isingekuwa rahisi kwa wewe kuishi tu bila mtu, yani
umetembea na ndugu zangu imeniuma ila kosa ni langu kwa kutokukutambulisha ndugu
zangu. Mapenzi yetu tulikuwa tunayajua wenyewe, Erica hukumfahamu ndugu yangu
hata mmoja wala rafiki yangu, wala mawasiliano yao kwahiyo mimi kukulaumu kuwa
umetembea na ndugu zangu nitakuwa nafanya makosa maana ulifanya vile kwa
kutokujua.” “Na mimi samahani sana kwani sikusikiliza ushauri wako,
nakumbuka siku ile niliyoenda kukutana na Rahim sikutaka hata kukusikiliza kuwa
unazungumzia nini, nilimuamini sana Rahim, niliamini ni mwanaume atakayenifaa
yani sikuhisi kama kuna kipindi Rahim atabadilika kama sasa” “Usijali
Erica, ila kuhusu huduma za mtoto uwe unatuambia hata sisi, ili mradi tunajua
ukweli kuwa ni mtoto wa ndugu yetu, tuambiage tumuhudumie” “Niwaambie
wakati mama yenu hajaonyesha kujali hadi leo?” “Muache Yule mama
kapagawa sasa hivi, kaletewa watoto watatu wa Rahim pale kwake yani haamini
maana alimuona Rahim ni mpole sana, kumbe bora ya sisi” Erica akashangaa
sana, kuwa Rahim kapelekewa watoto watatu? Akawaza na mke wa Rahim anajihisi
vipi, “Na mke wake je kakubali hiyo hali?” “Akatae vipi sasa,
ila yupo kama kachanganyikiwa, anagombana na kila mwanamke anayehisi ni mwanamke
wa Rahim, na hivi ana mimba ndio balaa” Walifika kwakina Erica na kusha,
kisha Babuu akaagana nae kurudi kwenye lile gari halafu Erica akaingia ndani
kwao. Alimkuta mama yake ambaye alimuuliza, “Kheee
kliniki gani mwenzetu hadi saa hizi?” “Aaaah mama, kulikuwa na
foleni” “Basi alikuja mumeo wa zamani” “Nani huyo tena
mama?” “Si Yule muuza samaki” Hapo ndio Erica akapata picha kuwa
Bahati alijua ameenda kwao ndiomana akamfata, ila alishindwa kuelewa kuwa akili
zimemrudi au vipi, kisha akamuuliza mama yake ambacho kilisemwa na Bahati, na
mama yake akamueleza Bahati alivyosema, Erica alimsikitikia
sana, “Masikini Bahati, kweli alirogwa Yule” “Ila sio kosa letu,
ni kosa la ndugu zake” “Ndio mama, ila kwanini ndugu hufikia hali kama
hiyo jamani! Ona sasa atahisi kuchanganyikiwa Bahati” “Kwahiyo wewe
unamtaka Bahati au Erick?” “Erick nampenda ila Bahati namuonea huruma,
hata kuachana nae ningeachana nae kwa amani ila sio kwa njia waliyoitumia ndugu
zake, unajua amemuacha mkewe hospitali na kunifata mimi? Yani nimekutana nae
kliniki, wakati natoka ndio kanifatilia” “Haya mbona yeye aliwahi kufika
na wewe ndio unaingia saivi?” “Nilipita kwenye lile duka la nguo mama,
lile Angel amekuwa balozi, waliniita mara moja” “Mbona mwanzo
umenidanganya kuwa kliniki kulikuwa na foleni?” “Nisamehe
mama” “Yani uongo huachi! Hebu jifunze kuwa mkweli Erica, kwa mtindo huo
utamuingopea hadi mumeo na muanze kugombana bure, jifunze kuwa
mkweli” “Sawa mama, nisamehe” Kisha Erica akaenda chumbani kwake
ila habari ya Bahati ilimuuzunisha sana, hakuelewa ni kwanini Bahati alipomuona
alistuka, “Au zile dawa hazikutaka aonane na mimi? Ningejua toka ile
siku anafunga ndoa si ningejionyesha anione? Nampenda Erick ila namuhurumia
Bahati, ningeweza kuachana nae kwa amani na angetafuta mwanamke anayempenda
kweli na sio mwanamke wa kuvutiwa kwa madawa, kwakweli ndugu zake wamefanya
dhambi sana.” Akaendelea kufanya mambo mengine
tu. Usiku ulivyofika akampigia Erick, na kusalimiana nae na
kuongea nae kisha akamuuliza, “Erick, kwanini kutaka kunipeleka mimi
dukani kwa Tumaini na unajua sipatani nae?” “Muda gani nilitaka
kukupeleka dukani kwa Tumaini?” Erica akamueleza Erick ilivyokuwa hadi
kutaka kwenda dukani kwa Tumaini na kukimbia, “Erica, unaniambia Moses
alikupa fomu usaini?” “Ndio, kasema wewe ndio umeagiza eti nisaini sijui
kuna event ya tarehe nne mwezi wa nne, kasema nisaini kuna mahali
inapelekwa” “Na Moses huyo huyo akataka kukupeleka dukani kwa
Tumaini?” “Ndio” “Huyu Moses vipi katumwa au nini? Subiri
niwasiliane nae ili nijue kwanini kafanya hivyo, hakuna kitu ulichotakiwa
kusaini, kwanini kafanya hivyo jamani? Aaaah yani penzi letu kila kukicha
linavamiwa na vidudu mtu tu, huyo Moses nitamuuliza asiponipa majibu ya
kuridhisha namfukuza” “Hapana Erick usifanye hivyo, jua yeye ndio
anasimamia vyema” “Hata kama, sijamtuma aingilie maisha yangu binafsi
mimi, subiri kesho” Kisha akaagana nae na kukuta simu, kiukweli hata
Erica alikuwa akijiuliza haswaa kuwa kama Erick hajatoa hayo maelezo ni kwanini
sasa Moses afanye hivyo? Hakuelewa na kuamua kulala, ila kabla hajalala akapokea
ujumbe, kuangalia ulitoka kwa Rahim, “Erica, umeamua kunidhalilisha kwa
ndugu zangu kuwa simuhudumii mtoto? Ingia kwenye mtandao tuongee” Erica
aliangalia ule ujumbe mara mbili na kuweka simu pembeni kisha akalala kwani
hakutaka hata kujisumbua kuingia kwenye mtandao. Kulipokucha
aliamka na kufanya shughuli zake za hapa na pale, mchana akapigiwa simu na namba
ngeni, alipopokea alikuwa ni Sia akasema, “Erica, niachie Erick
tafadhali, nakufa kwaajili yake” “Sia, niachie Erick tafadhali nakufa
kwaajili yake” Yani Erica alimgeza Sia yale yale maneno aliyoyaongea,
ila hakujua kama hiko kitendo kimemkera sana Sia kiasi kwamba aliamua kukata
simu sababu aliona ni kejeli, ila alipokata simu Erica
alijisemea, “Kwani sisi wengine ndio hatujui kufa au? Na mimi nakufa
kwaajili yake asinibabaishe” Kwakweli Erica alikuwa kashachoshwa na mada
za malalamiko na lawama ndiomana akafanya vile, muda kidogo akapigiwa na namba
nyingine ngeni na kupokea, ilikuwa ni sauti ya Tumaini, “Hivi wewe Erica
unajiona una nini wewe? Yani wewe wa kunigombanisha na mdogo
wangu?” “Nimekugombanisha nini?” “Kwanini umwambie kuwa kuna
fomu ulikuja kusaini?” “Sasa Tumaini, nisaini fomu halafu nisimwambie
muhusika nitakuwa mzima kweli? Yule ndio muhusika ndiomana
nimemwambia” “Halafu Sia anakupigia unamjibu kwa jeuri, msichana una
kiburi sana wewe” “Labda una mambo yako tu ila mimi sina ubaya wowote na
wewe wala na huyo Sia” “Subiri nitakufundisha somo” Kisha
akakata simu, kuna mambo mengine Erica alikuwa akishangaa tu, maana Tumaini
anaonekana anafanya kila hali ili kakake asiwe na Erica, ila Erica hakutaka
kabisa kuwaza hayo yote, akamshangaa Sia pia kutoka hospitali tu na kuanza
kuwaza kuhusu maswala ya mapenzi yale yale yaliyomsababisha ajaribu
kujiua, “Ndiomana serikali ukijaribu kujiua tu unafungwa kuepeka watu
wenye akili mbovu kama Sia” Kisha akaendelea na shughuli
zake. Jioni ya siku hiyo akiwa ametulia zake huku akicheza na
mwanae, akapigiwa simu na Dora, na kuamua kupokea hivyo hivyo ingawa anapataga
kukereka sana kutokana na maneno ya Dora, “Erica, sikuonei wivu na wala
usione nakusumbua ila nataka nikuponye” “Uniponye vipi wakati
nishakwambia huyo mzee simtaki!” “Sawa ila kuna jambo nataka nikwambie
la kukusaidia” “Jambo gani hilo” “Erica, nasikia kuna siku huyo
baba alikutumia vocha ya shilingi elfu hamsini, kama una hela nenda kaweke vocha
na umrudishie” “Kwanini?” “Erica, mzee huyu atatumia hilo swala,
kukuumiza na kukutesa. Nakupenda rafiki yangu naomba ufanye hivyo” Erica
aliamua kusikiliza ushauri wa Dora na kuamua kwenda kuchukua hela ndani kwao,
kisha akamuacha mtoto na mama yake halafu yeye akaenda kununua vocha, kwakweli
hakutaka mchezo na Yule mzee kabisa maana mambo yake yanajulikana
yalivyo. Alienda dukani na kununua vocha, ila wakati anarudi alikutana
na rafiki yake Johari, ni kitambo sana hakukutana nae, alimkumbatia pale na
kuanza kuongea nae ambapo Johari akamwambia, “Erica umekuwa adimu sana,
jamani nilikuja kwenu mamako alinitimua balaa” “Aaaah pole mwaya, vipi
bado unaishi na Yule mume wako?” “Ndio, na anakuja ndio tunaenda
nyumbani kusalimia. Subiri umuone shemeji yako” “Oooh nitafurahi sana
kumfahamu” “Anakuja, kwakweli namshukuru sana Mungu baada ya kupitia
machungu yote akatokea wa kunifuta machozi yangu, baba wa wanangu, nampenda sana
maana kanifichia aibu yangu. Si nilikusimulia Yule mwalimu alichofanya eeeh! Ila
Mungu mwema nimempata mume wangu, amenifichia aibu yangu, nimezaa nae mtoto
mmoja ila anamlea na Yule mtoto wa mwalimu, huwezi kutofautisha kwani anawapenda
wote kama wanae” Basi huyo mtu alifika na Johari kuanza kumtambulisha
Erica kwa shemeji yake, “Huyu anaitwa Erica ni rafiki yangu sana, Erica
huyu anaitwa Juma ndio mume wangu” Erica akampa mkono Juma, ila
alijisikia vibaya sana kwani huyu Juma ndio Yule jamaa wa TRA ambaye
alimtengenezea leseni na ndio Yule alimjibu vibaya kwenye daladala, ila hakutaka
Johari ajue kama ameshawahi kumjibu vibaya huyo kaka, akaongea ongea nao kidogo
na kuagana nao. Alirudi kwao na sura ya aibu sana kwani hakutegemea
kukutana tena na Juma zaidi ya ofisini kwa shemeji yake, “Kumbe kijana
wa watu ni mpole tu, kweli usimfikirie mtu ubaya kwa kumuona, kumbe Juma ana
moyo wa upendo. Mungu amzidishie kwakweli” Erica alifika kwake na kuweka
ile vocha kisha muda ule ule akamtumia mzee Jimmy na kuendelea na mambo yake
mengine. Usiku wake akapokea simu kutoka kwa Dora akimuuliza
kama ile vocha ameshaituma, “Tayari nimeshairudisha” “Basi
akikuuliza mwambie mpenzi wako kaiona kwahiyo kasema uirudishe” “Sawa,
lakini kwanini hivyo?” “Erica, ipo siku nitakwambia kwanini ila kwasasa
fanya hivyo, usitake vocha ya elfu hamsini tu ikuponze” Erica
alimuitikia kwani hata yeye alipatwa na uoga kiasi falani. Wakati wa
kulala alipokea simu ya Erick, na kusalimiana nae kisha kuongea
nae, “Unajua Erica, kuna mambo yanatendeka sijui sababu niko mbali ila
ningekuwa karibu nina hakika ysingetokea. Wiki ijayo nakuja” “Erick
kweli?” “Ndio ni kweli, wiki ijayo nakuja” “Wow, nimefurahi sana
basi utaniambia ni lini ili nije kukupokea” “Sawa na mimi nitafurahi
sana kupokelewa na wewe maana nimekukumbuka sana” “Sawa Erick, tuko
pamoja” Erica alionekana kufurahi sana kwani alikuwa akitamani kila siku
Erick arudi, kisha akaagana nae na kulala, ila kabla hajalala alipigiwa simu na
namba ngeni, hakutaka kupokea ila alipokea akihofia labda kuna maelekezo ya ile
vocha aliyoituma kwa mzee Jimmy, na kweli alikuwa ni mzee Jimmy, “Mbona
umenirudishia ile vocha?” “Ulinitumia nyingi sana” “Ndio kuamua
kuirudisha yote kweli?” “Ndio maana mpenzi wangu aliiona na kuuliza
vocha nimetumiwa na nani? Akaniamuru niirudishe” Yule mzee akakata simu
na Erica alilizika tu maana alikata simu kwa matakwa yake, alishukuru kwa Dora
kumpa yale maelekezo, “Dora ni mbaya ila mara nyingine ni mtu maana
angeniacha niangamie, ninayosababu ya kumshukuru kwakweli” Aliwaza hilo
na kulala. Kulipokucha alikuta kuna ujumbe kwenye simu yake ukitoka kwa
Rahim, “Erica, ingia kwenye mtandao, kuna jambo la muhimu sana nataka
kukwambia” Kiukweli Erica hakuwa na hamu kabisa ya kuwasiliana na Rahim
kwahiyo hakuingia kwnye mtandao wala nini. Siku hiyo ilikuwa ya
kurudi Erick kwahiyo alijiandaa kwenda kumpokea, alijiandaa vizuri sana na
kumuaga mama yake kisha akaenda uwanja wa ndege kumpokea Erick, alifika na kukaa
mahali ili amsubirie, alivyoona karibia muda unafika alienda kusimama karibu
karibu ili amsubirie Erick, na kweli alipoangalia mbele alimuona Erick ila
alikuwa ameongozana na kijana mmoja na waliongea kama wanafahamiana vile,
alipomuangalia vizuri Yule kijana alishtuka sana kwani alikuwa ni Rahim, hofu
ilimjia kuona Erick na Rahim wanafahamiana. Siku hiyo
ilikuwa ya kurudi Erick kwahiyo alijiandaa kwenda kumpokea, alijiandaa vizuri
sana na kumuaga mama yake kisha akaenda uwanja wa ndege kumpokea Erick, alifika
na kukaa mahali ili amsubirie, alivyoona karibia muda unafika alienda kusimama
karibu karibu ili amsubirie Erick, na kweli alipoangalia mbele alimuona Erick
ila alikuwa ameongozana na kijana mmoja na waliongea kama wanafahamiana vile,
alipomuangalia vizuri Yule kijana alishtuka sana kwani alikuwa ni Rahim, hofu
ilimjia kuona Erick na Rahim wanafahamiana. Akaamua arudi nyuma na
kujificha kwani alihisi angejitokeza basi habari ingekuwa nyingine, alikuwa
akiwaangalia tu na walionekana wakiongea mambo mbalimbali, kisha akamuona Erick
kachukua simu akimpigia, akaangalia mkononi akaona namba ya Erick ya nchini,
akaacha tu iite maana haikuita kwa sauti, aliona akipokea anaweza kuzua mengine,
yani alikuwa akiwaangalia tu Rahim na Erick, mara akatokea binti mwenye asili ya
kishombeshombe pia, alimkumbatia Rahim na kusalimiana na Erick, yani muda wote
huo Erica alijibanza tu akiwaangalia, kisha akaona Erick akimpigia tena simu ila
hakupokea na badae akaona Rahim na Yule binti wakikodi gari na kuondoka, wakati
huo Erick nae alionekana kukodi gari kwani alitaka kuondoka tu baada ya kuona
Erica hapokei simu ile gari alilopanda Erick lilivyoanza kwenda tu akampigia
simu Erick, “Erick, nimefika uwanja wa ndege huku uko
wapi?” “Mbona nimekupigia sana simu Erica?” “Nisamehe kulikuwa
na foleni, halafu simu ilikuwa kwenye mkoba na gari nililopanda lilijaa sana
kwahiyo sikuweza kupokea” Erick alisikika akimsimamisha Yule dereva huku
akimuuliza Erica alipo ili wamfate, ila Erica aliwafata yeye kwani ni muda tu
alikuwa akiwaona, alivyofika pale Erick alishuka kwenye gari na kumkumbatia sana
Erica maana alimmiss sana, kumbe kuna mtu alikuwa akiwaangalia vile
wanavyokumbatiana, alikuwa ni George na alitumwa na mama yake Erick ili
akampokee Erick, aliamua kuwafata, na kuwasalimia ila alikuwa na kitu moyoni
mwake, kisha akamwambia Erick, “Nimetumwa na mama yako nije
kukupokea” “Mama nae, mimi ni mkubwa sana kwasasa, nimepokelewa na
mpenzi wangu kwahiyo wewe rudi tu. Hata hivyo nimeshakodi gari” Kisha
George akamuuliza Erick, “Kwani una undugu wowote na huyu binti? Labda
huko kwa baba yako?” “Huyu ni mpenzi wangu sio ndugu
yangu” Kisha George akamuangalia Erica na kusema, “Erica kumbe
hunitaki tena sababu ya Erick? Unajua mimi na Erick tukoje?” Erica
alikaa kimya kwanza alikuwa akiwaza mambo mengi tu kuwa kakimbia moja halafu la
pili limemjia kwa namna mbaya sana, Erick alimuangalia Erica na
kumuuliza, “Unamfahamu huyu?” Erica leo hakutaka kabisa
maswahibu ya George yamuharibie siku, alijibu kwa uso mkavu
kabisa, “Simfahamu” Kisha Erick akamwambia
George, “Bhana George tusiharibiane siku, mwenyewe kasema hakufahamu,
kama umemfananisha shauri yako. Erica twende” Akamfungulia mlango wa
lile gari Erica akapanda kisha nay eye kupanda na
kuondoka. Wakiwa njiani, Erica alimuuliza Erick kuwa wanaenda
wapi kwanza, “Tunaenda hotelini Erica kwani ulifikiri tutaenda
wapi?” Ni kweli Erica alikuwa amemmiss sana Erick lakini akaona
asipokuwa makini basi yatamtokea mambo kama yaliyomtokea kwa Rahim, kupata mimba
juu na kutukanwa malaya, kwahiyo akatafuta njia ya kumdanganya Erick ili asilale
nae kwa siku hiyo, “Ooooh Erick jamani, ungeniambia mapema ili nikupe
mlolongo wa siku zangu, yani hapa nilipo nimeingia kwenye siku
zangu” “Mmmh Erica jamani, unataka kuninyina kweli?” “Jamani
eick hivi mimi naanzaje kukunyima wewe jamani! Hivi kwa jinsi ninavyokupenda
hivi hadi mtoto nimemuandika kwa jina lako nikunyime kweli? Huniamini
au?” “Hapana nakuamini Erica” Erica alifurahi sana kuaminiwa na
Erick, aliamua kumshauri tu mule kwenye gari kuwa aende nyumbani kwao ili asikae
kwenye mazingira ya vishawishi, basi Erick akamwambia, “Hakuna shida,
basi kwa muda huu tutafute mahali tukae, tule, tuongee halafu nitaenda
nyumbani” Basi wakatafuta mahali ambapo palikuwa na mandhari nzuri sana
ya kwenda kukaa hapo ili kuongea kidogo, na kujikuta wakijadiliana mambo
mbalimbali, “Erica usijali kuhusu mimi lazima nitakuoa yani lazima
nitakuoa tu, haijalishi nini kipo mbele yetu ila lazima
nikuoe” “Nitafurahi sana Erick, yani siku mimi nikiwa kwenye shela na
wewe kwenye suti uwiiii sitaisahau hiyo siku katika maisha
yangu” “Usijali Erica, yani usijali kuhusu ndugu zangu wala mtu
gani?” “Ila kuna swali nataka nikuulize?” “Niulize
tu” “Unajua wakati nimefika pale uwanja wa ndege nimekuona na mkaka
mmoja na mdada ndio wanaondoka, ndugu zako wale?” “Hapana, wale si ndugu
zangu ila Yule kaka anaitwa Rahim, ni rafiki yangu kuna kipindi nilikuwa
marekani nilikuwa nae, kipindi hiko nilikuwa nakunywa sana kwahiyo tulikuwa
tunakunywa nae na yeye ndio alikuwa akiniunganisha kwa wanawake” “Mmmh
kumbe ni mlevi pia? Ila Erick ulikuwa balaa nadhani ushatembea na wanawake
wakila rangi!” “Yamepita hayo Erica usiyakumbushie, yani kama vile
walokole wanavyosemaga yakale yamepita nimekuwa mtu mpya, mimi saivi ndio Yule
Erick uliyemuhitaji maishani, Erica wewe ndio ulikuwa sababu ya yote haya, ila
sio kwamba hao wanawake wote nilikuwa nalala nao hapana, wengine ni wa kwake
huyo jamaa” “Kwahiyo nae mlevi?” “Tena bora ya mimi, yeye ndio
mlevi balaa. Nimekutana nae leo tukajikuta tunakumbushiana mambo yaliyopita,
nikamwambia mwenzie nimebadilika, ila yeye sasa hajabadilika wala nini maana
Yule dada uliyetuona nae ni mwanamke wake” “Kheee ana wanawake wengi
sana eeeh!” Erica alijikuta akiulizia sana habari za Rahim hadi Erick
alimuuliza, “Mbona unaniuliza sana habari za Yule mkaka,
unamjua?” “Mmmh hapana, na Yule aliyekuja kukupokea je una undugu nae
upi?” “Yule ana undugu na mama yangu huko kwenye ukoo wao, mie sina
ukaribu nae sana wala nini” “Tumaini anamfahamu?” “Kumbuka
Tumaini ni ndugu yangu mimi, halafu Yule na Tumaini ni watofauti maana Yule ni
ndugu wa mama yangu, labda wafahamiane siku hizi. Halafu natamani kumuona Angel,
sijui nije lini?” “Wewe tu na muda wako unakaribishwa kuja
kumuona” “Ila Erica tuache masikhara, tunazungumza mengi sana ila
mwenzio nina hamu tena sana” “Erick, nivumilie tu siku zangu zipite na
tutakuwa pamoja, mbona hakuna tatizo. Si ulikuwa unavumilia South sembuse
usharudi jamani! Nivumilie Erick” “Sawa nimekuelewa ila kaa ukijua nina
hamu sana” Erica aliamua kubadilisha mada kwani aliona ile mada
ikiendelea basi anaweza kujikuta akiangukia kwenye uzinzi ambao hakuutaka kwa
kipindi hiko. Wakaongea ongea na muda ulipoenda ilibidi Erick arudi kwao
akapumzike na alimkodia gari pia Erica na kumkodia gari arudi
kwao. Erica alimkuta mama yake nyumbani amefura hasira,
akamsalimia ila mama yake hakumjibu na kuanza kumsema tu, “Wewe mwanangu
ndio huna akili yani huna akili huna akili kabisa, sijui niseme vipi ndio
unielewe jamani. Haya umeenda kumpokea huyo Erick wako, umeshindwa kucharanga
miguu kurudi nyumbani mpaka uende kulala nae? Yani kwa stahili tiyo utakuwa
unadhalilika kila siku na kutukanwa na wanaume, hakuna jema kwenye macho ya
mwanaume, utajitoa na kuona nimejitoa kwa mpenzi wangu ila bado atakuona
malaya.” “Ila mama umenifikiria vibaya tu, sijaenda kulala na Erick,
nimeongea nae tu” “Labda mdanganye Angel hayo maneno yako, mpaka muda
huu ni maongezi tu hayo?” Erica aliamua kumueleza mama yake vile
alivyomdanganya Erick ili asilale nae, mama yake alimsikia na
kumwambia, “Siku nyingine hata usihangaike kumdanganya mwanaume, kuwa
muwazi, sitaki sipo tayari. Kama kukuacha na akuache sio kutaka kukuharibia
maisha, yeye katoka nje huko hata kusema mpenzi wangu tukapime hakuna, moja kwa
moja twende tukalale, akikupa maradhi je! Ila napo umetumia akili kumwambia
hivyo ingawa kuna wanaume wengine mathomaso atataka mpaka aone damu, yani
mapenzi mwanangu ni kizunguzungu ila kama hujakubali namshukuru Mungu, najua
ulikosea mwanangu ila ni muda wa kujitunza huu, acha yote jitunze” “Sawa
mama nimekuelewa” “Kuzaa sio kugawa gawa kwa kila anayetaka, sio pipi ya
kusema kila mtoto anyonye, tunza ujana wako, umezaa nje ya ndoa lakini
ukijiheshimu utaheshimika na sifa mbaya juu yako zitapotea
mwanangu” “Asante mama” Erica alienda kuoga na kwenda chumbani
kwake huku akitafakari baadhi ya maneno ya mama yake, kuwa wanaume hawana
shukrani hata umpe nini, ila akamkumbuka Bahati, huyu alikuwa ni mwanaume wa
ajabu saba kwake maana anakumbuka siku ya kwanza kukutana na Bahati kimwili
alionekana bikra mbele ya macho ya Bahati, na alipewa shukrani ambazo hata Babuu
aliyemtoa bikra kweli hakuwahi kumpatia, kwahiyo aliona Bahati ni mwanaume wa
ajabu sana kwake. “Kwa mambo ya wanaume walivyo, ningekuwa na tuzo basi
ningemzawadia Bahati maana ndio mtu pekee aliyeonekana kujali na kuthamini
ulivyo. Ila sio wangu tena, ni wa mwingine mie wangu ni Erick, nampenda
sana” Basi alipotaka kulala aliwasiliana kidogo na Erick kisha akalala
sasa. Kulivyokucha tu, asubuhi na mapema Erica akapigiwa simu
na Dora, kiukweli alikuwa akishangaa sana Dora alivyokuwa akishughulika
nae, “Erica unajua kilichopo kwako?” “Kwangu kipo
kipi?” “Nasikia mzee Jimmy, kaweka shilingi milioni kumi kwenye akaunti
ya mtoto wako” “Kheee huyu mzee ana wazimu jamani, ana nitakia nini
mimi?” “Sijui ila ndio hivyo” “Itabidi nikaangalie, sasa
nifanyeje?” “Mrudishie maana Yule mzee mmmh!” “Nashukuru Dora,
au unaonaje nikutumie wewe” “Tena hapo utakuwa umefanya jambo la maana
ili nitayarishe hela za kununulia sanda na jeneza langu” “Yani Dora,
unaongea kama ugonjwa wa kawaida huo!” “Sasa nifanyeje wakati ninao
tayari” “Ngoja niende benki nikaangalie” Erica alijiandaa kisha
akamuaga mama yake na kutoka kwenda benki, alipofika benti alienda moja kwa moja
huduma kwa wateja na kuulizia salio na kuona kweli kuna milioni kumi imeongezwa
kwenye ile akaunti, akaomba apewe taarifa fupi ya akaunti ya mwanae, wakampa na
akaiangalia vizuri sana na akaona kuwa kawekewa hiyo hela, akawaza kuwa hata
kuirudisha atairudisha vipi ikiwa akaunti namba ya Yule mzee haijui halafu
hawezi kutoa pesa zote hizo na kutembea nazo ili azirudishe ni hatari kubwa sana
kwake, na pia hakuweza kuulizia akaunti ya Yule mzee pale huduma kwa wateja
kwani alihisi ni kumchafulia sifa Yule mzee, kwahiyo aliamua kwenda kwa meneja
wa ile benki. Alimkuta na kuamua kuongea nae kirafiki tu, kwanza Yule
meneja alimuomba msamaha sana kwa kutofanikisha swala la mwanae kuwa
balozi, “Nisamehe bure Erica, nilitamani sana Angel awe balozi wetu
maana sifa zote anazo ila mamlaka ipo kwa mkurugenzi mkuu” “Hamna
usijali, naelewa ila kuna jambo nataka tuongee, kama ndugu yangu unipe
ushauri” “Sawa hakuna tatizo, ongea tu” “Sikia nikwambie, huyu
mkurugenzi mkuu nilikuwa namfahamu kabla ya kuonana nae hapa benki na alikuwa
akinitaka kimapenzi ila nilimkataa, ndiomana swala la mwanangu kuwa balozi
alivyoniona alinizungusha sana, sasa jambo lililonileta mpaka kuja kuomba
ushauri ni kuwa nasikia amemuwekea mwanangu milioni kuzi, nimekuja kuhakikisha
ni kweli na taarifa fupi ya akaunti ya mwanangu ni hii (Akamkabidhi lile
karatasi lenye taarifa fupi) wazo lililonijia ni kumrudishia, sasa sijui akaunti
namba yake, nimeona kuuliza pale mapokezi sio sifa njema ndiomana nimekuja kwako
meneja ili nikuulize na unishauri” “Kwanza kabisa nakupa hongera sana
yani hongera mno, hakuna binti anayeweza kuchomoka akitongozwa na mzee Jimmy
maana ana hela, ila wewe umechomoka hongera sana, halafu hakuna binti ambaye
amewahi kuongwa hela nyingi hivi na mzee Jimmy, kwakweli wewe ndio wa kwanza,
hongera sana. Jambo la kukushauri ni hili, hii hela hujamuomba sehemu yoyote, na
ametuma kwenye akaunti ya mwanao, kwanini ujisumbue kumrudishia? Kwani hutaki
mwanao ale vizuri, aishi vizuri afurahi? Hebu tumia hela hiyo kwa mahitaji ya
mwanao, najua mwanao atakuwa na mahitaji mengi kama watoto wengine, tumia hela,
karibia atakuwa Yule na ataenda shule, tunza hela hii imsomeshe badae, yani hata
usihangaike kuirudisha tena jifanye hukujua kama amekutumia wala
nini” “Nisimrudishie eeh!” “Usimrudishie ndio, na anayekushauri
umrudishie anataka ufe masikini, hivi kwa usawa huu kweli mtu anakupa hela bila
kuomba umrudishie? Weee hakuna kurudisha hiyo.” “Kheee umenifungua macho
sana, bora nimekuja kwako” “Yani usiirudishe” “Basi nikupe na
wewe hela ya soda, nikupe ngapi?” “Mwenzangu ile ni nguvu yako ya kupush
mtoto leba, ila sababu umeamua kunipa hakuna shida. Nipe laki tu” Basi
Erica alitoka mule ofisini na kwenda kutoa hela kisha alimpa laki moja yule
meneja na kuagana nae. Akiwa njiani alifikiria sana kuhusu ile
hela, atafanyia nini milioni kumi ikiwa hata wazo la biashara hana ila aliona
aitumie kidogo kidogo tu ili mwenye nayo akitaka amrudishie, sasa pale kwenye
siti aliyokaa alisikia wamama wakiongea, “Unajua hatuendelei kwasababu
moja, unaiacha hela ikae tu badala ujishughulishe upate faida ya ile hela
unaacha tu mwisho wa siku tunalalamika umasikini umasikini kumbe ni matatizo
yetu” “Umeongea vyema, nakumbuka mimi nilianza kukopesha vitenge na
mtaji wa laki moja tu ila saivi mtaji wangu unagoja milioni mbili sababu
sikukata tamaa” “Haya sasa, ungeiacha hiyo laki ikae tu ungepata hizo
milioni mbili?” “Nadhani wengi tatizo linakuwa moja, mtu anakuwa na wazo
la biashara na anahitaji sana kuifanya ila hajui namna ya kuanza
biashara” “Mimi mwenyewe nilikuwa hivyo hivyo ila nilisikia kuna semina
ya wanawake wajasiliamali, sikuwa na biashara ila nilienda, jamani nilipata
muhamko wa hali ya juu, kuna mambo yanafungua jaman I, yani ujinga tupa kule,
nilifunguliwa haswaa kwenye ile semina, maana unasikia mwingine nilianza na
mtaji wa elfu kumi niko mbali sasa? Nikajiuliza amewezaje? Ila mwingine akasema
usiseme amewezaje ila sema kama Yule anaweza basi na mimi naweza, toka hapo
nikafata tu mlolongo wa ile semina na ilipoisha nilianza kufanyia kazi kile
nilichofundishwa basi nimekuwa mbali” “Wengine unajua wanakosea nini,
anaweza akahudhuria kama hivyo semina, anachanganyikiwa na kila ushuhuda wa mtu,
anasikia natengeneza sabuni niko mbali, natengeneza batiki, napika tambi, nauza
vikoi, sasa yeye sababu ndio anaanza anatakiwa aanze na kimoja kwanza basi
utamkuta mara atengeneze batiki aache, atengeneze sabuni, humo humo vikoi
anashangaa mtaji unakata anaanza kusema biashara haina faida” Kwakweli
Erica alijikuta akivutiwa sana na maongezi ya wale wakina mama, alitamani
kuendelea kuwasikiliza ila ndio walikuwa wanashuka, basi aliendelea na safari
ila maneno ya wale wamama yalikaa kwenye mawazo yake muda wote na kujikyta tu
akitamani kuanza biashara ili afike mbali maana hata yeye alichoka kutegemea
hela ya kuomba omba tu na kutegemea hela anayoingiziwa mwanae kama balozi,
kwahiyo alikuwa anawaza vitu vingi sana. Alifika kwao na kushuka, kisha kuelekea
nyumbani kwao. Njiani alikutana tena na Johari na mume wake wanaondoka,
Johari na Juma wakamsalimia Erick, muda huu Juma alitangulia mbele kidogo maana
alienda dukani kununua vocha, kwahiyo Erica alibaki na Johari,
akamuuliza, “Inaonyesha mnapendana na mumeo eeeh!” “Kwakweli
tunapendana sana ten asana, namshukuru Mungu kwa kunipa mume mwenye hofu ya
Mungu, usimuone hivyo mume wangu, si mlevi, havuti sigara na anafanya ibada
vizuri sana” “Wewe je unafanya ibada?” “Nimebadilika Erica,
Johari huyu si Johari Yule, hakika Juma kanibadilisha yani maisha yangu
yamebadilika haswaaa, mwenzio siku hizi hadi Ramadhani nafunga” “Kheeee
kweli umebadilika Johari” “Huyu mwanaume kanibadilisha, yupo vizuri
sana. Hapa tunawahi kwenda nyumbani ila muda wa swala usimkutie kwenye
daladala” “Hongera sana Johari kwa kupata mume mwema” “Asante,
nawe Erica utapata mume mwema ila namkumbuka Erick, natamani siku moja mkutane
na muoane” Erica alicheka tu kwani ukwlei ni kuwa anawasiliana sana na
Erick, Basi mume wa Johari alimaliza kununua vocha na kuweka kwahiyo Johari
alimuaga Erica na kuondoka, Erica aliwaangalia hadi walipokuwa wanaishia stendi
kisha yeye kwenda nyumbani kwao. Njiani alijiuliza sana, kuwa
Yule Juma hanywi pombe, havuti sigara na anapenda ibada mbona ni rafiki wa James
sasa? Alijiuliza sana maana hakuona uwezekana wa James kuwa na rafiki kama Juma
ikiwa Juma ni mume mwema tofauti na James. Alifika nyumbani kwao na
kushangaa sana kumuona Babuu kwenye geti lao, alifika na kumsalimia kisha
akamuuliza, “Umefata nini tena kwetu?” “Erica jamani kwani
haturuhusiwi kuja hapa?” “Hapana, nimekuuliza tu” “Nilikuja
kukuona wewe Erica, nimekaa nyumbani nimeboreka ndio nikaamua kuja
kukuona” “Aaah karibu, nilimuona kwa mbali jana Rahim, vipi kasharudi
nyumbani?” “Erica, umeanza tena na Rahim? Yule sio mwanaume atakupoteza
Yule” “Hapana, sijaanza nae tena nimesemea tu” “Kwanza hajafika
nyumbani nahisi atakuwa na mwanamke tu na nyumbani atarudi hadi wiki
iishe” “Mmmh!” “Mbona unaguna?” “Naguna sababu nilikosea
sana kuwa na Rahim kwakweli yani sijui hata nilianzaje jamani” “Usijali
ni mapito tu hayo” “Haya, karibu ndani” “Wapi? Mamako kanitimua
kama mwizi, hata sitaki nishakuona kwaheri” Basi Babuu akaondoka zake
ila Erica hakuelewa ni kwanini Babuu atimuliwe na mama yake, kwahiyo aliingia
ndani kwanza ili amuulize mama yake chanzo nini, alimkuta mama yake anacheza
cheza na Angel, Erica alimsalimia mama yake na kumuuliza, “Mama mbona
umemtimua Yule kijana?” “Ujinga ujinga kwenye nyumba yangu sitaki,
anakuja kujitambulisha hapa oooh mimi ndio nilikuwa mwanaume wa kwanza kwa
Erica, sasa ujinga huo unanihusu nini? Kuna mzazi anayefurahia kumuona
aliyemuharibu mwanae? Hakuna mzazi anayekubali ujinga ujinga wa namna hiyo,
ndiomana nimemtimulia mbali” “Ila mama Johari nae
ulimfukuza?” “Ndio nilimfukuza, Yule rafiki yako alianza tabia za ajabu
sana na ashukuru Mungu kapata huyo mwanaume wa kusitiri tabia zake, Johari
alikuwa akitembea na kila mwanaume hapa mtaani yani hakutamanika Johari ndiomana
nikamtimua pia” Erica hakutaka kuendelea kumuhoji mama yake kwani anajua
ambacho kingetokea baada ya kuendelea kumuhoji. Erica alikuwa
amechoka kutokana na mizunguko ya siku hiyo sababu aliondoka kwao tangia
asubuhi, kwahiyo alienda kujilaza tu, wakati kajilaza alipokea ujumbe toka kwa
Erick, akafungua na kusoma, “Erica nina hamu mwenzio hadi sina raha,
nina hamu sana” Ule ujumbe ulifanya asisimke mwili ila bado alishikilia
msimamo wake kuwa asitembee na Erick kwanza kwa kipindi hiko, kwahiyo alimtumia
ujumbe kuwa avumilie tu, “Nivumilie hadi lini Erica?” “Nivumilie
jamani eeh! Nakupenda sana, nivumilie” Erica alijaribu kumpa mpa maneno
matamu pale na kulala, alilala usingizi mzito sana hadi akaanza kuota ndoto za
ajabu ajabu tu, kuja kushtuka ni jioni kabisa na aliposhika simu yake alikutana
na jumbe kadhaa za kutoka kwa Erick na kugundua alipolala, bado Erick alimtumia
ujumbe ambao hakuujibu, jumbe za Erick zilionyesha ana hamu ya tendo la ngono
tu, akaona hata akimpigia tena simu muda huo bado atamwambia jambo lile
lile. Basi akajiweka sawa na kwenda kufanya shughuli zake za jioni ile
na alipomaliza walikuwa na kujiandaa kulala, mama yake akamwambia, “hivi
siku hizi unasikiliza mahubiri kweli?” “Mmmh mama na wewe,
nasikiliza” “Usikilizage ni mazuri” Basi alipoenda kulala,
alifungua redio ila kuna stesheni ilikuwa na miziki mizuri sana akaamua
aisikilize hata aache kufungua ile ya mahubiri maana aliona ile miziki
ingempita, basi ile miziki ilivyoisha kulikuwa na kipindi cha wanawake, yani
kuna mwanamke anaelimisha wanawake wengine waliokuwa katika ndoa, akaanza
kusikiliza, “Mwanamke unakuwa nyumbani, mumeo anarudi wala
hujishughulishi kumpokea yani ndugu yangu huyo mume atakukimbia, ataenda kwa
wenzako wanaomnyenyekea, mumeo akitaka mpe, yani ukimnyima ndio utamfanya aende
kwa wengine, sio unajifanya umechoka, mpe mumeo haki yake, shauri yako
utashangaa tu sio wako tena” Erica akazima redio, maana akikumbua jumbe
za mchana za Erick alipatwa mashaka, akaamua kumpigia Erick simu ila simu yake
haikupatikana, akaamua kuchukua simu na kuingia kwenye mtandao wa kijamii, ile
ameingia tu akaona ametumiwa ombi la urafiki na Sia, akashangaa sana ila
akakubali lile ombi, mara ujumbe ukaingia, “Erica, wewe umempokea ila
sisi ndio tunafaidi” Muda kidogo akaona picha zimetumwa na Sia,
kuangalia zile picha akaona Sia yuko pembeni na Erick amelala inaonyesha amelala
kwa uchovu wa mambo aliyokuwa akifanya na Sia. Akaamua
kuchukua simu na kuingia kwenye mtandao wa kijamii, ile ameingia tu akaona
ametumiwa ombi la urafiki na Sia, akashangaa sana ila akakubali lile ombi, mara
ujumbe ukaingia, “Erica, wewe umempokea ila sisi ndio
tunafaidi” Muda kidogo akaona picha zimetumwa na Sia, kuangalia zile
picha akaona Sia yuko pembeni na Erick amelala inaonyesha amelala kwa uchovu wa
mambo aliyokuwa akifanya na Sia. Kwakweli Erica alihisi kama kurukwa na
akili hivi, yani hakujielewa kabisa, hakujua kama alie au afanye nini akajikuta
akijisemea, “Ndiomana mama anasemaga wanaume ni mbwa, loh kunifanyia
hivi Erick jamani! Kumpenda kote huku!” Hakujielewa na kahuweza kulala
tena, alitamani awe anapajua kwakina Erick aende hata usiku huo huo, labda
akapigane na Sia, ila muda mwingine akaona ujinga kugombea mapenzi, akawaza
mtoto wake aliyembadilisha jina maana Erick kawa sio mtu sahihi tena kwenye
macho yake, akajikuta akianza kulia, alilia sana, alinyamaza aliposikia mlio wa
simu yake, akaichukua na kuangalia akaona namba mpya, ila alihisi pengine ni
Erick anataka kunuomba msamaha, akapokea ili amsikilize, hakuwa Erick bali
alikuwa ni Rahim, hata alimshangaa usiku huo kampigia simu ili
iweje, “Erica nimerudi mpenzi wako hata kunitafuta?” Erica
akatamani hata kumpa tusi sema hakuzoea kutukana kwahiyo alikaa kimya tu, Rahim
akaendelea kuongea “Mbona unanyamaza mpenzi wangu, nimekumiss sana.
Kesho nitakutafuta tutoke na mtoto wetu tukatembee” Aliamua
kumjibu, “Rahim, mimi sio mpenzi wako unikome” “Mbona umekuwa
mkali hivyo Erica? Mtoto anahitaji malezi ya baba na mama, na mimi ndio baba na
wewe mama, tusimnyime haki mtoto wetu, au kama vipi njoo ili sisi wazazi
tuyajenge” “Rahim, nikome uyajenge na nani? Sio mimi, umeshindwa hata
kufika kwa wazazi wangu halafu unaniita kuyajenga? Sitaki Rahim na
siji” “Erica usiwe mkali hivyo, kumbuka sisi ni wazazi, unanijua vizuri,
nakujua vizuri, nimemiss vile unavyoliaga kitandani?” Erica akachukia na
kukata simu, alikuwa na hasira sana na ile simu akaizima kabisa, alikaa na
kuendelea kulia huku akisema hamtafuti tena Erick, na hataki kuwa karibu na
rahim bora awe mwenyewe tu, kwani hakuwa na raha tena hadi
panakucha. Mama yake ndiye aliyemuita baada ya kuona muda mrefu
umepita na mwanae hajatoka ndani, Erica alitoka na kumsalimia mama yake, mama
yake alimuangalia na kumuuliza, “Vipi mbona macho yamekuvimba
hivyo?” Erica hakuweza kujizuia kwa mama yake, alijikuta akimfata na
kumkumbatia huku akianza tena kulia, mama yake akamwambia, “Wewe vipi
tena, kama babako kafa mara ya pili jamani? Kilio hiko vipi mwanangu
eeeh!” “Mama, leo nimeamini maneno yako kuwa mwanaume sio wa
kumuamini” “Eeeeh vipi tena? Ila kila siku nakuambia, mwanaume sio ndugu
yako mwanangu” “Kwakweli mama Erick kanifanyia kitu ambacho sielewi
mpaka muda huu” “Niambie mamako usinifiche, nilishakwambia mimi ni
rafiki yako kwahiyo kuwa huru kusema chochote” Erica alianza kumuelezea
mama yake yaliyotokea kwa Erick na jinsi Sia alivyomtumia picha
Erica, “Ooooh katoto kangu jamani, kwanza tulia, tuliza akili zako,
usipaniki, hayo mambo ni ya kawaida tu na huwatokea wengi sana. Tuliza akili,
hakuna sehemu imeandikwa kuwa Erick ni mwanaume peke yake kwahiyo hakuna
wengine, hapana wapo. Na sio kwamba nilivyosema wanaume hawajatulia basin i
wote, hapana waliotulia wapo sema tu ni ngumu kuwatambua sababu tumezoea msemo
kuwa samaki mmoja akioza basi wote wameoza” “Lakini mama kwanini
anifanyie hivi? Kwanini lakini? Kwanini nina mkosi hivi juu ya mapenzi? Sina
raha mama, kwanini mimi?” “Hapana, usijiumize kichwa sana. Ngoja
nikuulize, hizo picha Erick alipigwa akiwa anachekelea kabisa kuwa na Sia
au?” “Hapana alikuwa amelala” “Basi huna sababu ya kupata presha
mwanangu, ingawa wanaume ni waongo ila bado anayetakiwa kukupa majibu ni Erick.
Ndoa ni uvumilivu mwanangu, na uvumilivu unaanzia kwenye mahusiano. Sikia
nikwambie, usipaniki wala nini, muulize Erick kwa upendo tu na atakwambia
ukweli” “Nitawezaje kumuuliza kwa upendo mama ikiwa nimeumia
hivi?” “Ndiomana nakwambia shusha presha, shusha hasira, ukiona upo sawa
ndio umuulize. Kumbuka Sia ni rafiki mkubwa wa Tumaini, kwahiyo kuna uwezekano
mkubwa hata Erick hajui kama alipigwa picha, kwahiyo wewe tulia na
umuulize” “Ikiwa kama ni kweli mama?” “Ikiwa kweli maamuzi ni
yako kusuka au kunyoa ila uvumilivu unaanzia kwenye
mahusiano” “Uvumilivu wa kumvumilia mwanaume muhuni mama?” “Sasa
kuna asiyekuwa muhuni?” “Bahati mama ni mpole, hana hayo
mambo” “Kwahiyo unataka Bahati amuache mkewe na akuoe wewe, au unataka
kuwa mke wa pili? Hebu nitolee ujinga mie, wewe mwenyewe ulikuwa unaimba wimbo
hapa nampenda Erick, nampenda Erick, mvumilie ndio maradhi yako
hayo” Erica alizidi kunyong’onyea ila mamake alivyoona vile aliamua
kumbembeleza, sasa maana alimuona kakosa raha kabisa, “Aaah mwanangu
jamani usijali, Erick ataongea nawe vizuri tu. Halafu mwanangu acha kupenda sana
utaumia, nipende mimi mama yako niliyekubeba tumboni miezi tisa sio Erick
aliyekufahamu ukubwani, usiwe kama Sia, kifo cha mama yake hajajaribu kujiua ila
kuachwa na mwanaume amejaribu kujiua, na tena hata ajisikiliziii vizuri,
kashapona na kwenda kwa mwanaume, Yule hana akili mwanangu, usiwe vile, sawa
mama” “Sawa mama, nimeelewa” Basi mamake alimtaka Erica aoge na
avae vizuri na awe na amani tu. Mchana wa siku hiyo, Erica
akiwa chumbani alisikia mama yake akimtimua mtu akataka kujua kuwa anayetimuliwa
ni nani, akatoka na kushangaa ni Derick alifika na mama yake, alimsikia mama ake
akisema, “Wewe mama sina shida na wewe ila huyu mwanao simtaki kabisa
hapa kwangu, mtoto mchawi huyu” “Lakini kaja kuomba
msamaha” “Msamaha kitu gani wa kichawi, mtoto hafai huyo alitaka kumbaka
mwanangu” Inaonekana hata mama Derick hakulijua hilo kwani alishtuka
sana kusikia mwanae alitaka kumbaka Erica, ilibidi amtulize kwanza mama Erica
ili wakae wakizungumza, mwishowe mama Erica alikubali kuwakaribisha ila kiukweli
hakupenda kabisa uwepo Derick mahali pale. Erica alipowaona ni wao,
alirudi zake chumbani kwake tu kwani hata yeye hakutaka uwepo wa Derrick
ukizingatia kamuaibisha sana. Basi akawasha tena simu yake, na muda huo
huo Rahim akampigia simu tena, kiukweli hakujisikia kuipokea kwahiyo aliiacha
iite hadi ikatike. Kisha akajaribu tena kuipiga namba ya Erick napo
haikupatikana na kuzidi kumtia simanzi, akachukia sana, huku asitamani hata
kuongea na mtu mwingine kwa wakati huo, ila mama yake alimuita maana Derick
alienda kuomba msamaha, kwahiyo muda huu Erica alienda kuwasikiliza sera zao,
akawasalimia pale na kukaa, mama yake akaongea, “Haya, wewe Derick, omba
msamaha kwa Erica kwa hayo madudu uliyomfanyia” “Erica, naomba unisamehe
sana, nimefanya kitu ambacho hakitakiwi kabisa, sisi ni ndugu Erica na tuishi
kindugu, sisi ni dada na kaka kwahiyo tupendane na tuishi vizuri” Sababu
erica hakutaka kuweka maongezi marefu akaamua kumsamehe tu, muda huo mtoto wa
Erica aliyekuwa amelala aliamka na kulia kiasi na kuanza kwenda sebleni, kwahiyo
Erica alimchukua mwanae na kumpakata, ila mama Derick akasema, “Jamani
huyu mtoto sikumuona alivyokua, daha kafanana na mtoto mtoto wa ndugu yangu
anaitwa Rahim” Derick akadakia, “Ndio baba yake huyo, kumbe mama
hujui?’ “Babake!” “Ndio mama” Mama Derick alimuangalia
Erica na kumwambia, “Kheee pole Erica, ulianzaje kuzaa na Yule? Yani
matendo yake Yule si mazuri hata kidogo ila mamake huwa haamini kama mwanae
mchafu hata umwambie vipi, sina cha kuficha wala cha kukupa moyo, kwakweli Rahim
hakufai” Erica akasema kwa aibu maana hakutaka mama Derick ajue ila
mambo yote yako wazi, “Ila nilishaachana nae huyo
Rahim” “Kwakweli pole yani pole sana, Yule ndugu yangu mtoto amepata ni
John tu, ni mpole na anapenda kweli ila sio Rahim, hata mke wa kuoa hakujua
amuoe nani, ikabidi babake amuolee tu mke, yani Rahim sijui labda akikuua
ataacha ila pole sana” Mamake Erica nae hakutaka hayo mambo ya
kujadiliana kuhusu Rahim ilihali ni Rahim aliyeharibu maisha ya mwanae kwahiyo
aliikatisha ile mada, “Jamani sitaki kusikia habari za huyo mtu, huyu ni
mjukuu wangu na atabaki kwenye himaya yangu, badilisheni mada kama zimeesha
ondokeni” Mamake Erica alionekana kuwa na kirirani tu kila muda. Basi
waliongee ongea na kuaga ambapo walishikana mikono na kuagana. Jioni
ilipofika mama Erica alimuuliza mwanae, “Kwanza Erica ni nani alikutumia
picha na ujumbe kwamba Erick yupo na Sia?” “Ni Sia mama” “Aaah!
Kumbe, mwenzio anataka kukurusha roho tu sasa wewe usionyeshe kama umeumia wala
nini, onyesha kuwa upo kawaida kabisa, nay eye ndio atajisikia
vibaya” “Ila mama dah mapenzi haya, hapana kwakweli” “Mapenzi
ndivyo yalivyo mwanangu, kuna wakati utacheka na kuna wakati utalia, ndio
mapenzi hayo” Erica aliachana na mama yake na kwenda kufanya shughuli
zake zingine. Hadi usiku unaingia Erica hakutafutwa na Erick,
swala hilo lilimuumiza moyo sana na kumfanya akose raha kabisa, hakuwa na
usingizi ingawa ilikuwa ni usiku hivyo akachukua simu na kuingia kwenye mtandao
ili kuone kama kuna jipya lolote labda Erick amemtumia ujumbe hakuona , ila leo
aliamua kukagua akaunti ya Erick akaona hakuweka picha yoyote kwenye akaunti
yake zaidi ya picha za maua na ujumbe ujumbe, akajiuliza kwanini hakuweka picha?
Hakujua sababu, akaangalia na marafiki zake, akaona wote wale wa kwenye ofisi ya
Erick ni marafiki zake, akiwemo na Sia, yani alijikuta akitamani sana kujua
namba ya siri ya Erick ili ajiridhishe kuwa anaongeaga na nani mule kwenye
mtandao. Akaona kuna jumbe Fulani kwenye ukurasa wa wazi wa Erick, akaona wa
kwanza ukitoka kwa msichana, “Erick nilikutafuta kweli, natumai wewe
ndio Erick wangu wa kipindi kile” Huo ujumbe ulitumwa jana, aliona moyo
wake ukipasuka tu kwa wivu, akazidi kuangalia na kuona zingine za kawaida ila
moyo ulikuwa unamuuma sana, mara akatumiwa ujumbe na Sia, “Hulali shoga
yangu, saa sita hii upo facebook! Pole sana, mapenzi yatakuua. Pole eeeh! Ila
ndio ujifunze, sio kubambikia wanaume watoto, kwa taarifa yako shughuli
niliyoifanya jana kwahakika nimepata mimba ya Erick na nitazaa nae uone kama
atakufikiria wewe” Erica aliumia sana ila alijiuliza kuwa huyu
anayenishangaa silali, yeye amelala? Akamjibu “Na wewe mbona hujalala?
Na safari hii utakunywa sumu ya panya ufe kabisa, Erick ananipenda ingawa
sijazaa nae ila ananipenda, unaweza ukazaa nae na asikupende, aliyekwambia kuzaa
na mwanaume ndio kupendwa nani? Pole sana” Aliamua nae kuwa na ujasiri
kuliko kuendelea kujiumiza moyo, sia akamjibu tena “Kama anakupenda
mbona yupo na mimi?” Erica akamjibu tena ili Sia aone kuwa
hajaumia, “Kuwa nae sio kwamba anakupenda sana, kuna watu hadi wanaolewa
na hawapendwi kwahiyo kuwa nae wala sio sababu hiyo. Wewe hupendwi na ndiomana
ukajaribu hata kujiua, ila mwenzio nina uhakika napendwa yani hata iweje Erick
ananipenda sana, na kwa taarifa yako unafikiri kwa vipicha vyako ndio nitamuacha
Erick! Hiyo haipo dada, tafuta njia nyingine” “Yani Erica unanijibu
hivyo?” “Ndio, ulitaka nikujibu vipi? Na saivi hadi ndoa yani usage
kabisa vichupa uchanganye na sumu ya panya unywe ili usiamke tena sababu kila
ukishtuka tu utanikuta nae” Sia hakumtumia tena ujumbe Erica, na
kumfanya Erica ahisi kuwa Sian aye kaumizwa nay ale maneno, akaamua kuzima data
sasa na kuweka simu pembeni ila kiukweli alikuwa akijikaza tu ingawa moyo
ulimuuma sana kuhusu Erick. Alijaribu kulala ila usingizi ulimpa kwa
shida sana maana alilala saa kumi usiku. Kulivyokucha aliamshwa
na mwanae maana alimletea swaga mpya kabisa alipoamka, kwanza alimfinya mashavu
mama yake hadi akaamka na alipokaa tu akaanza kusema, “Mama mpigie
baba” Alimshangaa mwanae maana hakumtegemea kama angemwambia vile kwa
asubuhi ile, akamuuliza, “Babako nani nimpigie?” “Baba Erick,
ataka ongea nae” Kwakweli Erica alitamani sana kujua ni kitu gani Erick
huwa anaongea na mwane kiasi kwamba mwanae amkumbuke asubuhi yote ile, basi
akachukua simu na kujaribu kumpigia Erick akakuta hapatikani na kumwambia
mwanae, “Babako hapatikani” Angel alianza kulia mpaka Erica
ikabidi amsikilizishe kuwa hapatikani ndio akanyamaza na kutoka kwenda kwa bibi
yake, kwakweli kwa kiasi Fulani Erica alichukia vile ambavyo mwanae alizoeshwa
na Erick, sema hakuwa na la kufanya sababu mwanae alishazoeshwa
hivyo. Kwahiyo alitoka tu chumbani kwake na kwenda kufanya shughuli
zingine. Mama yake alimuaga kuwa kuna mahali anaenda kwenye shughuli
zake za vikoba, ila akaongea nae, “Ila mwanangu mamako nimechoka, maana
shughuli hii nimeanza muda tu ila bado kuna watu wameendelea hadi natamani
maendeleo yao. Kuna biashara haitanisumbua hata kichwa kuifanya ila sina
mtaji” “Biashara gani mama?” “Natamani nianze kukopesha wamama,
ningekuwa na milioni tano tu ingeniingizia faida nzuri sana halafu wala
nisingetumia jasho sana” “Ila biashara ya kukopesha mama
utaiweza?” “Naiweza ndio, idea zote ninazo sema sina hela
tu” Basi mama yake akaondoka zake, ila Erica aliona swala la mama yake
ni swala zuri nap engine hela zake zitapata matuzimi, ila alijua akimwambia
ukweli tu mama yake itakuwa tatizo kubwa sana. Basi mama yake alipoondoka tu na
yeye akavaa na kuita gari kisha akaondoka na mwanae kuelekea benki, alikuwa
akifanya haraka ili arudi kabla ya mama yake, na kweli alifika benki na kutoa
zile hela, wakati anatoka pale benki akakutana na John, alitaka ampite ajifanye
hajamuona ila John alimsogelea, “Erica, unataka kunikimbia
kweli?” “Hamna bhana” “Naona mtoto wa kaka anazidi kuchanua,
mwenyewe karudi umeonana nae?” “Hapana” “Dah! Sio vizuri
kwakweli, naenda kuweka hela ila ngoja nikupe kidogo kwa matumizi ya
mtoto” John alitoa laki tatu na kumpa Erica, ila kiukweli Erica
alishangaa sana wasio na mtoto wana uchungu kuliko mwenye mtoto, Erica alichukua
na kuondoka zake ambapo moja kwa moja alienda na ile gari nyumbani
kwao. Kufika tu kwao, mwanae alimuuliza, “Mama Yule
nani?” Erica akaona mwanae kuna siku atamuumbua na maswali yake maana
toka amejua kuongea amekuwa na maswali ya ajabu sana, kwahiyo hakumjibu bali
alimgeresha tu na kuendelea na mambo mengine. Ilikuwa ni Mchana
na mama yake alikuwa hajarudi ila alisikia simu inaita akaamua kwenda chumbani
kwake kuipokea, akakuta mpigaji ni Tumaini, akapokea hata hakumuogopa ingawa
Erick alimwambia kuwa amblock Tumaini ila yeye hakumblock na alijipanga kumjibu
kwa lolote atakalomuuliza, “Hivi wewe Erica una akili kweli? Ndio nini
kumjibu vile Sia?” “Hivi wewe unahusika nini na ugomvi wa wake wenza?
Unatakiwa kuwa mpole tu maana utake usitake ujue atakayeolewa na Erick ndio wifi
yako” “Aliyesema Erick atakuoa wewe nani?” “Kumbe hujui!! Mimi
ndio mke wa Erick” “Hivi wewe Erica unajiamini nini
wewe?” “Najiamini sababu mimi ni mwanamke, na Erick atanioa mimi,
kwaheri” Erica akakata ile simu aliamua kufanya vile sababu ya jambo
moja tu hakutaka kuona vile wakimsema wakati huo ameumizwa kuhusu swala la Erick
na kutokupatikana kwake, kwahiyo alitaka na wao wajihisi vibaya kwa majibu
yake. Muda huu mama yake alikuwa amerudi na anajiongelesha mwenyewe tu
kwa swala la kutokuwa na pesa, basi Erica akaenda na bahasha kwa mama yake na
kumkabidhi, mama yake akahamaki, “Nini tena?” “Hela hizo
mama” “Zimetoka wapi?” “Niliongea na Erick kuhusu swala la
biashara unayotaka kufanya, ila sikumwambia kama ni wewe nilimwambia ni mimi
ndio akaniletea hela za biashara hiyo” “Kwahiyo pesa ngapi?” “Ni
laki tano mama” “Weeee usiniambie, kumbe Erick ndio yupo hivi? Usimuache
Erick mwanangu, achana na mada za wakina Sia” Erica alicheka sana maana
mama yake amekuwa kigeugeu baada ya kuona zile hela ila za mzee Jimmy hakuzitaka
kabisa, kusikia za Erick alifurahi sana. Erica alishukuru mamake hajajua ukweli
na akajua hawezi kumuuliza Erick kwani hajamzoea halafu amemwambia kuwa aliomba
hela za kufanya biashara yeye kwahiyo hawezi kumuuliza. Jioni
wakati Erica akiendelea na shughuli zake akasikia mlio wa simu yake na kwenda
ndani kuipokea, alikuta ni Erick anapiga kwahiyo akapokea ili asikie uongo
wake, “Erica, najua utashangaa kuwa sio kawaida yangu na kweli sio
kawaida yangu nilikuwa nje tu lakini haipiti siku nakupigia simu, iwe nchini
kweli nishindwe kukupigia? Tafadhali Erica usinihisi vibaya, nakupenda sana.
Naomba unisamehe” “Nikusamehe umefanya kosa gani?” “Sijakutafuta
hewani, naomba unisamehe” “Na mbona ulikuwa hupatikani? “Erica
hata sijui simu yangu iliwekwa wapi, ila kesho tuonane nikusimulie
yaliyonikuta” “Sawa, ila kesho nampeleka mtoto kliniki” “Sawa,
ukiwa kliniki utaniambia halafu mimi nitakuja kuwachukua wewe na mtoto, nataka
nikueleze yaliyonisibu maana hata nikikwambia humu kwenye simu
hautaelewa” Erica alimuitikia tu ila alihisi tu maelezo atakayopewa na
Erick ni uongo mtupu, akaagana nae. Usiku ulipofika, mwanae
akamuanzishia tena swala la kutaka kuongea na Erick, kwahiyo ilibidi ampigie na
ampe mwanae aongee nae ambapo Angel alikuwa na furaha zaidi kumbe Erick
alimwambia kuwa kesho wataonana. Alivyomaliza Erica alichukua simu yake
ile na kuweka pembeni kisha akachukua simu yake nyingine na kuingia nayo kwenye
mtandao, alitaka kuona na siku hiyo Sia angemuandikia nini, ila kuna post
aliiona akajikuta akiifatilia, ilisema “Je mwanaume ukigundua kuwa mtoto
wako amebadilishwa ubini na kupewa ubini wa mwanaume mwingine
utafanyaje” Aliona kama inamuhusu vile kwahiyo aliamua kuangalia watu
waliochangia walikuwa na maoni gani, kwa bahati akakutana na maoni ya
Rahim, “Kwakweli kama ni mimi huyo mwanamke niliyezaa nae nitamuua
kabisa hata asiwepo kwenye uso wan chi yani anibadilishie ubini mtoto wangu!
Damu yangu! Naua kabisa” Kwakweli hili oni lilimsisimua sana ukizingatia
mtoaji wa oni hilo ndio muhusika ambaye mwanae kabadilishwa jina, aliamua kutoka
kwenye mtandao kabisa akajiuliza, “Hivi hawa watu wa mtandao ndio
maswali gani hayo ya kuuliza watu? Mmmh sijui nifanyeje, Mungu wangu
jamani” Aliwaza sana ila alikosa jibu na kuamua tu kulala
zake. Asubuhi akajiandaa na kumuandaa mwanae kwaajili ya kwenda
kliniki, aliondoka nyumbani na alifika na kuhudumiwa vizuri sana, ila sababu
mwanae mtundu muwa wanaondoka akagoma kubebwa na kutembea, akamnyang’anya mamake
pochi kisha akamwaga vitu vya kwenye pochi alikuwa na hasira sababu Erick
alisema angeenda kuwachukua wakati wanaondoka ila akaona wanaondoka na mama yake
bila baba yake kuja, wakati Erica ameinama kuokota vitu vya kwenye pochi yake,
kuna mwanaume alitokea na kuinama pia kumsaidia Erica kuokota, alipoinua macho
kumtazama alishangaa kumuona Rahim, wakati anamshangaa Rahim akamuona ameishika
bima ya afya ya Angel akiiangalia, kisha Rahim akasema kwa
mshangao, “Angel Erick?”; Asubuhi akajiandaa
na kumuandaa mwanae kwaajili ya kwenda kliniki, aliondoka nyumbani na alifika na
kuhudumiwa vizuri sana, ila sababu mwanae mtundu muwa wanaondoka akagoma kubebwa
na kutembea, akamnyang’anya mamake pochi kisha akamwaga vitu vya kwenye pochi
alikuwa na hasira sababu Erick alisema angeenda kuwachukua wakati wanaondoka ila
akaona wanaondoka na mama yake bila baba yake kuja, wakati Erica ameinama
kuokota vitu vya kwenye pochi yake, kuna mwanaume alitokea na kuinama pia
kumsaidia Erica kuokota, alipoinua macho kumtazama alishangaa kumuona Rahim,
wakati anamshangaa Rahim akamuona ameishika bima ya afya ya Angel akiiangalia,
kisha Rahim akasema kwa mshangao, “Angel Erick?”; Erica
akamnyang’anya Rahim ile kadi, Rahim akamuangalia Erica na
kusema, “Kweli Erica umeamua mtoto wangu umpe jina la huyo malaya
mwenzio Erick?” Ni wazi Rahim hakutambua kuwa Erick anayesemwaga na
erica ni Yule Yule rafiki yake, Erica alikaa kimya tu kwa bahati alisogea karibu
yao Salma na mimba kubwa sana inaonyesha Rahim alimpeleka Salma kliniki, halafu
gafla Salma alianza kupiga kelele za maumizu, ilionyesha uchungu ulimsika kabla
hata hajasema chochote, basi Rahim akainama kumsaidia Salma, Erica alitumia
mwanya huo kuondoka mbele yao kwani hakutaka yaanze mengine. Erica
alitoka nje ya geti la ile hospitali, mara akamuona Erick ndio anashuka, cha
kushangaza Angel alimkimbilia Erick na kumuwow kamavile alishawahi kumuona au
aliambiwa kuwa Yule ndio Erick babake anayeongeaga nae, kwakweli hata Erica
alibaki kaduwaa jinsi Angel alivyomkimbilia Erick, naye Erick alimdaka kwa
furaha na kumbusu huku akisema, “Aaaah binti yangu mzuri jamani,
nakupenda sana” Kisha akamuangalia Erica na kumwambia, “Nisamehe
kwa kuchelewa mpenzi” Ila Erica hakujibu ambapo Erick aliwataka wapande
kwenye gari ambayo alienda nayo, nao wakapanda ila bado kichwani kwa Erica
kulikuwa na maswali mengi sana kuwa Angel amepatwa vipi na muunganiko na Erick
ikiwa hakuwahi kumuona? Na kama damu nzito kuliko maji basi Angel alitakiwa
amfurahie Rahim ila ndio kwanza alikuwa akishangaa tu Rahim akishangaana na mama
yake, kwa hakika Erica hakuelewa kabisa. Basi walivyokuwa kwenye gari, Erica,
Erick pamoja na Angel walikaa kiti cha nyuma na mbele ni dereva alikuwa
akiwaendesha, Angel alipakatwa tu na Erick huku akimuuliza, “Zawadi
yangu baba” Erica alizidi kushangaa kwakweli maana siku hiyo ni siku
ambayo mwanae alimchanganya sana kupita siku zote. Ile gari ilienda moja
kwa moja ufukweni ambapo walishuka na kutafuta mahali pazuri na kukaa kisha
wakaanza kuongea, ambapo Erica alimuuliza kwanza Erick, “Imekuwaje Angel
kakufurahia sana wakati hajawahi kukuona?” “Ni kweli hajawahi kuniona
kwa macho ila naamini amewahi kuniona ndotoni, damu ni nzito kuliko
maji” Erica akaguna maana hiyo damu nzito vipi wakati mtoto sio wake,
kisha Erick akamwambia, “Unajua ili mtoto akupende na akuzoee huwa
inabidi upendo utengenezwe, kuna upendo wa asili na kuna upendo wa kutengeneza,
mimi nipo kwenye upendo wa kutengeneza ambao mwisho utakuwa upendo wa asili,
sitataka kumuona Angel akikosa raha, sitapenda kumuona Angel analia na siku zote
nitampenda katika maisha yangu” Kwakweli bado Erica haikumuingia akilini
hata kidogo, gafla simu yake ikaanza kuita ila sauti ilikuwa ndogo sana,
kuangalia mpigaji alikuwa ni Rahim, ikabidi amwambie Erick kuwa anaenda chooni
ili akapokee hiyo simu ajue Rahim atasema nini, Erick hakuwa na tatizo kwani
alibaki akicheza cheza na Angel. Erica alijiuliza sana kuwa
Rahim anataka amwambie vitu gani, hofu ilikuwa kubwa sana kwake maana Rahim
alishaujua ukweli kuhusu jina la mtoto, simu ikakatika na kuanza kuita tena,
ikabidi aipokee, “Hivi wewe mwanamke ambaye umehangaika dunia nzima na
wanaume wote, leo hii unambadilisha mwanangu jina kwa misingi ipi? Yani naona
post sijui ukikuta mwanao kaandikwa ubini mwingine najua tu ni mambo ya kawaida
kumbe yapo! Niambie wewe malaya umeanzaje kumpa mwanangu baba
mwingine?” Erica akawa kimya tu na kumfanya Rahim aendelee
kuongea, “Erica, nadhani hunijui vizuri ulikuwa unaniona tu, mimi nina
roho mbaya kuliko unavyofikiria. Mimi ni gaidi wewe mwanamke, nina uwezo wa
kuteketeza wewe na familia yako kwa dakika, nina uwezo wa kuteketeza hicho
kimwanaume chako kwa sekunde, mimi ni mafia, unawezaje kunifanyia kama hivi?
Mwanamke mwenyewe hata hufai kutazamwa usoni kwahiyo umeuza mwanangu ili uolewe
na hiko kibasha chako? Ni nani mwenye ujasiri wa kuoa mwanamke kama wewe mwenye
kutembea na ukoo mzima, si atakuwa kaolea kijiji!” Hakuna kitu
kinachomuumaga Erica kama kutukanwa sababu ya kutembea na wanaume aliotembea nao
yani hapo ndio huwa anaweza sema vibaya bila hata kuogopa maana maneno yale huwa
yanamuumiza, akaanza kumjibu “Rahim, nanyamaza kimya usifikiri mimi ni
mjinga, nina akili zangu timamu. Kuhusu kumbadili mtoto jina sijakurupuka tu
kama unavyodhani, hivi ulivyositisha huduma kwa mtoto ulifikiri atahudumiwa na
malaika? Huna muda na mtoto, humjali, humthamini ila unajiita kuwa na wewe ni
baba, hivi wewe ni baba kweli? Mtoto kakuona leo wala hajakushobokea sababu
hakujui ila unaanza kufoka kuona bima ya afya ya mtoto, usipojiongeza kuwa watu
watajiongeza kwaajili yako. Na kuhusu swala la umalaya hata wewe ni malaya ndio
mana ulitembea na mimi mwanamke malaya, na kuhusu Angel kuwa Angel Erick ni sawa
kabisa maana Erick sio wa ukoo wenu, na unajua fika toka siku ya kwanza
nilikwambia mwanaume ninayempenda anaitwa Erick, kwahiyo usinichanganye,
sitegemei chochote kutoka kwako” “Hivi errica unapata wapi ujasiri wa
kuongea hayo? Sihudumii mtoto sijui nini na nini, kipindi tupo kwenye mahusiano
nilikuwa nakupa hela mara kwa mara, leo hii unadikiri kusema simuhudumii mtoto?
Mbona huna akili wewe mwanamke, hela zote zile nilizokuwa nakupa, kwanini
usingefanyia hata biashara eeeh! Umekalia tu kusema simuhudumii mtoto wakati
nilikuwa nakupa hela kibao” “Wewe ndio huna akili Rahim, usinitoe akili
kabisa, wewe ndio huna akili namba moja. Sikatai ulikuwa ukinipa pesa ni nyingi
tu na nilikuwa nakushukuru ila hazikuwa pesa kwaajili ya matumizi ya mtoto,
zilikuwa peasa kwaajili ya matumizi yangu binafsi, na wakati nina mimba ilikuwa
bado unanihudumia mimi, pindi mtoto kazaliwa ukasitisha huduma, hivi unategemea
mtoto atakula nini huyo eeeh!” “Ulishindwa hata kujiongeza ufanye
biashara?” “Ndio nimejiongeza sasa kwa mtafutia Angel baba mwingine wa
kumlea, malaya anakuwaga na baba wa mtoto? Yeyote tu atakayetoa matumizi kwa
mtoto ndio baba, yani Rahim usinitibue sijui utaiteketeza familia yangu kwa
dakika siogopi yani jua kabisa siogopi, wewe ukiiteketeza yangu kwa dakika basi
yako hata sekunde simalizi kuiteketeza, kumbuka nishatembea na ukoo wako mzima,
achana na mimi, ulishasema mtoto wa malaya nae atakuwa hivyo hivyo kwanini sasa
uhangaike na mwanangu? Muache kama alivyo, na Erick akishindwa kumlea nikipata
mwingine nambadilisha vilevile, siri ya mtoto anayo mama,
kwaheri.” Kisha akakata simu na kuizima kabisa, alimjibu Rahim kiujasiri
ila alikuwa amejawa na uoga vilivyo huku akijua kuwa ingekuwa ana kwa ana basi
angepigwa atolewe ngeu siku hiyo lakini sababu kwenye simu aliamua kujibu
anavyojisikia. Erica akarudi alipowaacha Angel na Erick na
kukuta Angel amelala kwenye mikono ya Erick kisha Erick
akamjuuliza, “Mbona umechalewa hivyo Erica, hiyo uwani uwani
gani?” “Ni tumbo linanisumbua gafla” “Ooooh basi niwapeleke
nyumbani” “Itakuwa vizuri kwakweli” Basi wakatoka pale na kwenda
kupanda gari tena, huku Erica akimpa maelekezo Yule dereva kuhusu mahali
wanapoelekea maana Erick hakupafahamu kwakina Erica, muda huu Erica hakukumbuka
hata maswali ya kumuuliza Erick maana alikuwa ameshachanganywa na mambo mengi na
kujikuta akiwa kimya kabisa hadi wanafika kwao, Erick alimuuliza, “Mbona
umekuwa hivyo Erica, kuna kitu nimekuudhi? Je nimekubore eeeh!” “Hapana
nit umbo tu” Basi wakashuka ambapo Erick alishuka na Angel, na moja kwa
moja waliingia ndani kwakina Erica na kumkuta mama Erica yupo ametulia tuli,
basi wakamsalimia na Erica kumchukua Angel kwenda kumlaza yani hakuwa hata na
wazo la kumtambulisha Erick kwa mama yake maana akili yake ilishavurugwa kabisa
yani hakukumbuka chochote kile, maneno ya Rahim yalimchanganya vilivyo,
alijikaza tu kumjibu lakini maneno yale yalimchanganya sana. Pale
sebleni alibaki Erick na mama yake Erica, kisha alianza kumuuliza, “Wewe
ndio Erick?” “Ndio mimi mama” “Haya, lini utakuja kumuoa
mwanangu?” “Mama, lazima nimuoe Erica yani lazima nimuoe, nitakuja rasmi
hapa” “Hujaogopa kufika muda huu?” “Sijaogopa mama maana nia
yangu kwa Erica sio mbaya, nina nia njema na Erica” “Haya mwanangu,
nakutakia mipango mizuri halafu nilisahau kukushukuru asante kwa zile pesa
ulizompa Erica” “Zipi hizo mama?” “Si ile milioni tano, kwakweli
nakushukuru sana maana kanipa karibia nitaanza biashara” Erick hakujua
kama aitikie au vipi, maana anakumbuka wazi kuwa hajawahi kumpa Erica hiyo hela
sasa iweje ashukuriwe kwa hela ambayo hajawahi kuitoa? Alijikuta tu
akijichekelesha ili Yule mama ashiwe na shaka nae ila alitaka sana kumuuliza
Erica kuhusu huyo hela, wakatu huo huo mamake Erica akasema tena, “Mbona
unacheka tu baba eeeh! Nashukuru mamako kwakweli umetusaidia sana” Erick
akaamua kujibu tu, “Hakuna tataizo mama” Huku akiwa na mashaka
kuwa huenda Yule mama anampa mtego ambapo akikubali ni tatizo ila aliamua
kujitoa muanga na kukubali aone itakuwaje, ila Yule mama alikuwa akifurahi
tu. Wakati mama Erica akiongea na Erick, walishangaa ni muda mrefu sana
Erica hakutoka ikabidi mama ke aende kumuangalia, akamkuta kumbe alilala pembeni
ya Angel yani wakati ameenda kumlaza Angel nae akajilaza pembeni yake, ikabidi
mamake Erica atoke na kumwambia Erick kuwa Erica amelala pamoja na mtoto,
ilibidi Erick aage na kuahidi kwenda siku nyingine, “Nitakuja tena
Jumamosi mama” “Sawa, karibu sana” Basi Erick alitoka ila
alijiuliza sana kuwa kuna kitu gani ambacho Erica anamficha maana hata ile hali
ya siku hiyo hakuielewa kabisa, alishamweleza kuwa amwambie kila kitu lakini
yeye anamficha, yani hakuelewa kabisa kuwa ni kwanini anafichwa na Erica. Basi
aliondoka zake tu maana hakuwa na namna zaidi ya
kuondoka. Ilikuwa ni jioni kabisa wakati Erica ameamka sasa
maana alilala sana siku hiyo na hata hakujua kalala vile kwasababu gani, aliamka
na kutoka nje ambapo alimkuta mama yake akifanya fanya shughuli zake,
akamsalimia kisha mamake akamuuliza, “Erica ndio tabia gani hiyo unakuja
na mgeni hata umtambulishi?” “Oooh nilisahau mama, yani nilisahau
kabisa” “Na kilichokusahaulisha ni nini eeeh! Yani leo unachanganyikiwa
na kufikia hatua ya kusahau kama umekuja na Erick?” “kwahiyo
alijitambulisha mwenyewe?” “Hamna nilihisi tu na kuanza kumuhoji
maswali, haya wewe umevurugwa na kitu gani hiko hadi usahau
mgeni?” “Mama, leo wakati natoka kliniki nilipatwa na
majanga” “Majanga gani?” Akajaribu kumsimulia mama yake kuwa
alikutana na Rahim na jinsi Rahim alivyoona ile kadi ya bima ya afya ya mtoto na
jinsi alivyomwambia kuwa ataimaliza familia yake, ila hakusema yeye ni majibu
gani alimpa Rahim, mama yake alimuhurumia kwani kwa kiasi alimuona mwanae ana
mapito, “Ila mwanangu kosa lako ni moja tu” “Lipi
mama?” “Huyo Rahim sababu aligoma kutoa matumizi ya mtoto yani kipindi
kile kile ungemwambia bwana mimi nambadilisha mtoto jina maana umeshindwa kulea
halafu ungeona angefanyeje, ila swala lingine je Erick najua kama Rahim ameanza
kukufatilia?” “Hajui mama” “Mwambie ukweli, mwambie na vitisho
alivyokupa, mwambie na jinsi alivyoona kadi ya mtoto, siku zote nakwambia ukweli
huweka watu huru, ni bora kusema ukweli ili Erick ajue kuwa akikutana na Rahim
basi akabiliane nae vipi, yani usimche, mwambie ukweli mtupu kuwa wewe na Rahim
mko vipi, asishangae kusikia Rahim akikuita malaya, mwambie akupende ulivyo sio
akupenda halafu akijua rangi yako halisi asumbue” “Mmmh mama yani
nimueleze yote hayo? Huoni kama nitampoteza Erick?” “Basi usimwambie ila
mwambie kama Rahim anakufatilia na ameshaona kadi ya mtoto, hilo ni la muhimu
sana mueleze ukweli huo ajue” “Sawa mama nitafanya hivyo” “Na
tena nimemshukuru Erick kwa ile milioni tano aliyokupatia” Erica
alishtuka kusikia hivyo maana mama yake alikuwa amemuongezea mabalaa, yani
kumshukuru Erick wakati hajaitoa hela kwa Erick! Ulikuwa mtihani huo, mshtuko
wake hata mama yake aliuona na kumuuliza, “Wewe Erica vipi kushtuka
hivyo?” “Hapana sijashtuka mama” “Niambie ukweli Erica, mshtuko
wako huo sio wa kawaida” “Hamna kitu mama ila sikujua kama umemwambia
maana sikutaka ajue kama zile hela nilikupa wewe” “Na mimi sijaona ubaya
kumshukuru hata kama hakujua kama umenipa mimi, kushukuru ni jambo jema sana.
Nimejifunza shukrani kwahiyo lazima nishukuru” Erica alikaa kimya tu ila
alitambua wazi kuwa mama yake kamuharibia tu. Usiku uliingia na
kwenda kulala ila Erick hakumtafuta kabisa hewani akaamua kumpigia yeye simu ila
simu ya Erick iliita tu bila yan kupokelewa na kumfanya ajihisi vibaya sana kuwa
Erick amechukia juu ya zile pesa, basi aliamua kutuliza mawazo yake kwa kuingia
kwenye mtandao wa kijamii, aliingia tu na kukutana na picha ya Rahim akiwa
ananyanyua chuma halafu kaandika, “Katika mazoezi ya kumtoa mtu kafara
mwaka huu” Hakupenda kuendelea kuangalia ile picha maana aliona
inamletea simanzi tu, kwani kila akifikiria maneno ya Rahim alihisi kichwa chake
kuumia zaidi, basi alijitahidi tu na kuweza kulala. Kulipokucha yani
alfajiri kabisa alipigiwa simu na Dora na kuipokea ile simu na kuanza kuongea
nayo, “Erica, nilikwambiaje kuhusu hela za Yule mzee? Shauri yako,
unadhani nakuonea wivu? Hapana nakuonea huruma” “Sasa Dora, mi
ningefanyeje jamani eeeh! Sikuwa na akaunti ya Yule mzee ningewezaje sasa
kumrudishia?” “Mi nilikwambia lakini bora hata ungezileta kwangu
ningejua namna ya kukabiliana na huyu mzee lakini kuzitumia ni jambo
litakalokutesa sana, una mtoto kumbuka” “Na amejuaje kama
nimezitoa?” “Kumbuka Yule mzee ndio yuko pale benki kwahiyo anauwezo wa
kufatilia taarifa za kila mteja halafu kajitapa kweli hela zake
umeshazichukua?” “Sasa nifanyeje Dora, yani unanishauri
nini?” “Sikia, wewe kama zile hela bado unazo kazirudishe halafu mimi
nikafungue akaunti kwenye ile benki na kisha unihamishie ile pesa kama ilivyo
yani aone kabisa kuwa zile pesa zilihamia kwangu” “Dora jamani
itawezekana vipi?” “Itawezekana tu, ngoja le oleo nikafungue akaunti
kwenye ile benki, jali maisha yako rafiki yangu, sitaki uteketee na
uhangamie” “Sawa nimekuelewa” Basi akakata simu ila akawa na
mawazo sana, anawezaje kumwambia mamake ukweli wa zile hela, na anawezaje
kuzirudisha zile hela wakati kashampa mama yake na ameshaanza kuzikopesha? Yani
akawa na maswali mengi sana, hadi anaamka na kwenda kufanya kazi alifanya
kimawazo sana maana hakuelewa kwa usawa ule atatoa wapi milioni tano ya gafla na
kwenda kuirudisha maana mama yake aliogopa kumwambia sababu kama akijua ni hela
ya Yule mzee angemsema sana ila hakuwa na jinsi zaidi ya kuwa na mawazo
tu. Mchana wa siku hiyo hakuwa na namna nyingine zaidi ya
kumpigia simu Erick, ingawa hakumuanza ila aliamua kumuanza yeye ili kujaribu
kuongea nae, muda huo Erick alipokea simu ya Erica, “Erick tafadhali
nahitaji kuongea na wewe, usikatae nakuomba” “Sawa, muda
gani?” “Hata muda huu, niambie popote ulipo nitakuja, nakuomba
Erick” Basi Erick alikubali na kumtajia sehemu ya kukutana nae, Erica
alijiandaa na kumuaga mama yake kuwa kuna mahali anaenda ila hakumwambia tu ni
wapi. Basi aliondoka zake na kwenda kukutana na Erick, cha kushangaza
Erick alifurahi sana kumuona Erica akamkumbatia kwa nguvu, na kwenda kukaa nae
kuongea, “Erick, mbona jana hukunitafuta na wala hukupokea simu
zangu?” “Erica lazima nijiridhishe kuwa kweli bado una upendo na mimi,
kweli mtu gani wewe? Ulichonifanyia ni sawa/ Tunaenda kwenu halafu unaenda
kulala bila kuniaga jamani? Ni sahihi hiyo?” “Nisamehe Erick, najua si
sawa ila si nilikwambia naumwa? Nisamehe sana” “Hata kama unaumwa ila
ulitakiwa kuniaga basi, halafu swali lingine umetoa wapi milioni tano na kumpa
mama yako na kusema kuwa mimi ndio nimekupa? Una wanaume wengine Erica
eeeh!” “Ila nyie wanaume ni watu wa ajabu sana, yani mimi sijakuuliza
kuhusu picha zako na Sia ila wewe unauliza kuhusu milioni tano ambayo huna hata
uhakika kuwa nilipewa na mwanaume” “Uitoe wapi? Huna kazi, upo tu, uitoe
wapi Erica? Ungeniomba mimi sawa ila wewe kama wewe unaitoa wapi?” “Ndio
nimekutafuta nikueleze kuhusu hiyo hela, nisamehe sana kwa kutokukwambia
mapema” “Haya nieleze” “Ni hivi, kuna baba mmoja huwa ananitaka
na kulazimisha kuwa niwe mpenzi wake sema nilimkataa sasa alivyoijua akaunti ya
Angel ndio akaenda kuweka hela hizo kwenye akaunti ya Angel, sasa mama
aliponiambia ana shida na hela nikaona nikamtolee tu zile, ila kwasasa roho
inanisuta balaa, na mama siwezi kumwambia anirudishie maana kashazifanyia kazi,
nahitaji kumrudishia Yule mzee hela yake” “Utamrudishia
wapi?” “Nitaenda kuomba akaunti yake na kumrudishia humo, hata hivyo mke
wake nimemueleza kasema niirushe kwake” “Sawa sawa, bora uiweke kwenye
akaunti ya mke wake, na hiyo hela utaipata wapi?” “Sijui, Yule mzee
aliweka milioni kumi ndio nimetoa tano, zimebaki tano kwahiyo inabidi niirudishe
hiyo tano nyingine ile mkewe nimtumie hizo kumi, ila mpaka sasa sijui hiyo tano
naipata wapi? Nikamdai mama! Itakuwaje nikimdai sasa? Yani
sielewi” “Basi sikia, mimi nitakupa lakini kwa sharti
moja” “Sharti gani hilo?” “Utaniletea fomu ya kumuhamishia huyo
mke wake hela” “Ooooh asante sana Erick, ninashukuru
kwakweli” “Aaaah usijali” Basi wakaendelea na mazungumzo
mengine, kisha Erica akakumbuka swala la Sian a kumuuliza Erick, “Eeeeh
Erick ndio kunifanyia nini vile?” “Nini tena?” “Erick kweli wa
kunisaliti na Sia wewe! Yani Sia ananitumia kabisa picha mkiwa mmelala pamoja,
halafu simu ukazima siku mbili kweli?” “Halafu unajua ni zawadi gani
nimekuletea kutoka nilipokuwa?” “Erick, mbona unataka kubadilisha mada
wewe, yani swali langu lingine halafu na wewe unaniletea swali
lingine” Mara simu ya Erick ikaita, akaipokea na kwenda pembeni kuongea
nayo, kwakweli Erica alishangaa sana jinsi Erick anavyokwepa mada ya kuwa
alilala na Sia, alipomaliza kuongea na simu alikuwa akitabasamu tu na kumwambia
Erica, “Twende” “Wapi?” “Yani leo imekuwa siku nzuri
sana, ile zawadi niliyoagiza imefika” “Zawadi gani?” “Twende
ukaione” Kwahiyo wakaondoka pale na Erick na kupanda gari ambalo
lilienda hadi bandarini, walishuka na kwenda ofisi za bandari ambapo Erick
alimuonyesha Erica, gari mpya tena nzuri sana na kumwambia kuwa ni zawadi yake
aliyomnunulia, kwakweli Erica alipagawa na ile zawadi, alijikuta akipata furaha
isiyo kifani, akaiangalia ele gari na kufurahi sana, kisha wakakubaliana na Yule
wa bandari kuwa, “Mje muichukue Jumatatu, kuna mambo
nakamilisha” “Sawa hakuna shida, nilitaka tu mke wangu aone zawadi
yake” Yule mtu wa bandari aliwapongeza sana kuwa inaonyesha wanapendana
sana, “Endeleeni hivyo hivyo kupendana, ni vizuri sana” Erica
alitabasamu tu kisha Erick alimpeleka hadi kwao na kumuaga mlangoni tu na
kumwambia kuwa alishamwambia mamake kuwa ataenda Jumamosi kwahiyo kesho yake
ndio atafika mahali pale, wakaagana pale na kuingia
ndani. Kiukweli Erica alikuwa na furaha sana kiasi kwamba hata
akasahau kumwambia Erick kuhusu Rahim kwa furaha ya gari alilopewa na Erick,
mamake aliiona furaha aliyokuwa nayo, “Eeeh mwanangu, unafuraha sana
leo. Yani umerudi na furaha tushirikishane basi” “Subiri Jumatatu
mama” “Jumatatu nini? Ndio Erick anakuja kujitambulisha
au? “Hapana ila subiri utaona tu” “Kupeana mshtuko huko, jambo
la heri au shari?” “Ni heri mama” “Haya sawa kama ni jamboo la
heri” kwakweli Erica alikuwa na furaha sana hadi muda anajiandaa kulala
alikuwa akitabasamu tu, Erick alimpigia simu na kuanza kuongea nae muda
huo, “Halafu nilisahau Erica. Ile hela nitakupa Jumatatu” “Sawa,
hakuna shida” “Ila naamini Erica wale wanaume zako wa zamani
ulishaachana nao wote, sitaki kusikia uchafu wowote unakufata” “Erick,
sina mwanaume mwingine zaidi yako mpenzi wangu” “Yani Yule kijana
niliyepigana nae siku ile simpendi jamani yani nilimchukia, nab ado namchukia
hadi leo” “Aaaah achana na Yule, kwanza ameoa Yule ana mke
wake” “Yani sitaki yoyote akufatilie Erica, wewe ni
wangu” “Hakuna mwingine Erick” “Unajua uchungu wa mke eeeh! Mimi
nina uchungu na wewe, nimekutoa mbali sana, tafadhali Erica nipende mimi
tu” “Nakupenda wewe tu Erick” Alijikuta akiongea nae vingi sana
vya kuhusu mapenzi yao na kusahau kila kitu kuwa alisalitiwa, yani hakukumbuka
chochote ila alichowaza yeye ni kuwa Erick anampenda sana. Hadi
wanaagana na kulala, alilala na tabasamu zito
sana. Kulivyokucha alifanya kazi zake kama kawaida ila Dora
alimpigia tena simu kumuwekea msisitizo wa zile hela, “Nishafungua
akauntui Erica” “Basi Jumatatu au Jumanne nakutumia, nitumie akaunti
namba na jina la akaunti” “Sawa, nakutumia” Basi ile simu
ikakatika na muda kidogo tu Erica akapokea ujumbe toka kwa Dora wa namba na jina
la akaunti, hakuwa na shida na ujumbe huo maana ni yeye mwenyewe
ameutaka. Wakati anataka kuweka simu pembeni akapigiwa na namba ngeni,
akajua ni Dora pengine anataka kumpa maelezo mengine, akapokea akashangaa
kumsikia Bahati, “Erica, namba yako sikuikuta kwenye simu yangu yani
nimehangaika sana kuipata, nimejaribu kupata kumbukumbu zangu na kuikumbuka
ilikuwa kichwani mwangu, Erica nakupenda sana, mwanamke niliyemuoa simpendi
mimi, nakupenda wewe erica” “Kheee Bahati, niondoleee mabalaa jamani, si
umeshaoa wewe, hebu tulia na mke wako” “Hapana Erica, mke wangu
simpendi, ninayekupenda ni wewe yani wewe ndio mwandani wangu, wewe ndio kila
kitu kwangu” Erica akaona huyu Bahati anamletea balaa tu, kwahiyo
akaamua kumkatia simu na kumblock ili asimtafute tena. Basi akaenda kuendelea na
kazi zake zingine za hapa na pale, kisha mchana mama yake alimuaga kuwa anatoka
kuna mahali anaenda kuelimisha wamama kuhusu ujasiliamali, aliweza kuona ni
jinsi gani mamake zile hela zimemchanganya hadi kawa muelimishaji wa
ujasiliamali. Basi mama yake akaondoka na kubakia mwenye nyumbani na
Angel. Jioni ya siku hiyo aliamua kwenda kukaa nje kidogo kupata hewa ya
nje, alipotoka tu alikuta Bahati ndio amefika, kiukweli alichukia kwani hakutaka
Bahati tena afike kwao, ila Bahati alisogea na kumkumbatia Erica tena hakutaka
kumuachia huku akidai amemkumbuka sana na sio kosa lake kuoa, muda huo huo
wakati Bahati kamkumbatia Erica, ndio Erick nae alifika mahali pale na
kuwashangaa. Jioni ya siku hiyo aliamua kwenda kukaa
nje kidogo kupata hewa ya nje, alipotoka tu alikuta Bahati ndio amefika,
kiukweli alichukia kwani hakutaka Bahati tena afike kwao, ila Bahati alisogea na
kumkumbatia Erica tena hakutaka kumuachia huku akidai amemkumbuka sana na sio
kosa lake kuoa, muda huo huo wakati Bahati kamkumbatia Erica, ndio Erick nae
alifika mahali pale na kuwashangaa. Erica hakuwa na habari yoyote kama
Erick kawaona, hata Angel nae hakujua maana alikuwa akishangaa tu mamake
alivyokumbatiwa na Yule mtu. Erick alichukia sana na kuondoka kwa
hasira, wakati anatoka getini alikutana na mama yake Erica, kwakweli mama Erica
alihisi kuna tatizo na kumuuliza, “Mbona watoka kwa kasi hivyo kuna
nini?” Erick alimuangalia huyu mama na kuangusha machozi kisha
akasema, “Sijawahi kuangusha chozi kwaajili ya mwanamke, ila leo Erica
amefanya nilie mama” “Kafanyaje tena?” “Erica ana mwanaume
mwingine mama” “Ana mwanaume mwingine? Haiwezekani, huyo mwanaume
katokea wapi? Mwanangu haya mambo sio ya kuchukulia hasira kiasi hiko, naomba
twende tukazungumze” “Hapana mama, siwezi kuvumilia kumuona Erica wangu
na Yule mwanaume” “Mwanangu tafadhali nisikilize mimi nakuomba, twende
tukazungumze tafadhali. Leo nimerudi mapema kwaajili yako maana nilikuwa
nakumbuka ahadi yako ya kuja leo Jumamosi, tafadhali mwanangu
twende” Basi Erick alikubali na kuongozana na mama yake Erica, wakaenda
hadi mlango wa kuingilia ndani kwakina Erica, walimkuta Bahati amepiga magoti
akimuomba jambo Erica, mama Erica akamuangalia Erick na kumwambia, “Yani
huyu mwehu ndio anasababisha uchukie hivyo mwanangu! Subiri nisogee
pale” Akasogea karibu na kumshika mkono Yule Bahati akasimama juu na
kuanza kumwambia, “Hivi wewe kijana unataka nini kwa mwanangu? Unataka
roho yake au? Si umeoa wewe, unataka nini kwa mwanangu, si ukatulie kwa mkeo
huko” Bahati akajibu, “Baba sikuoa kwa kupenda, haikuwa akili
yangu walinipa limbwata” “Usinichanganye mie, limbwata limbwata,
kamwambie huyo mkeo akuwekee limbwata lingine, niachie Erica wangu, hivi akili
yako haipo sawa tu, Erica sio wako ni wa Erick” Kisha akamuita karibu
Erick na kusema, “Mwanangu Erick, huyu kijana mwanzo alikuwa anakuja
kuniuzia samaki kumbe alikuwa akimtaka mwanangu, ila Mungu mwema akaoa mwanamke
mwingine halafu saizi anakuja tena kwa mwanangu, huyu kijana ni hafai
kabisa” Kisha akamuangalia Erica na kumwambia, “Hivi wewe Erica
unawezaje kumkaribisha mume wa mtu nyumbani kwangu? Si kuniletea laana huku,
haya muombe msamaha Erick upesi” Erica alimuangalia Erick na
kumwambia, “Erick nisamehe” Ila mama yake akasema kwa
ukali, “Hebu piga magoti wewe mtoto wa kike, msamaha gani unaomba huku
umesimama kama mlingoti!” Erica akapiga magoti na kumuomba msamaha
Erick, ambapo Erick alimsimamisha na kusema amemsamehe kisha akamkumbatia, mama
Erica akasema, “Haya ingieni ndani, halafu huyu muuza samaki nitaongea
nae mwenyewe” Erick, Erica na Angel wakaingia ndani na kumuacha mama yao
na Bahati pale nje. Kwakweli Bahati hakuwa na furaha kabisa, alimuona
mama yake Erica ni mtu mbaya sana kwani amemkatili kwa mwanamke ampendaye,
alimwangalia kwa masononeko sana na kumwambia, “Mama ungenihurumia mimi
ni mwanao pia” “Sijakataa kama wewe si mwanangu ila
umeshaoa” “Mama sijaoa kwa akili zangu, wamenifanyia
madawa” “Hayo madawa si wamekufanyia ndugu zako sababu hawakutaka umuoe
Erica!” “Ndio mama, ila mimi nampenda Erica” “Kama unampenda
Erica basi muache aishi kwa amani, usimfanyie vurugu maana hata yeye
hakukufanyia vurugu kwenye ndoa yako. Kitu kingine wasiompenda Erica ni ndugu
zako wamefikia hatua hadi ya kukufanyia dawa ili usimuoe Erica, unadhani ukimuoa
si watamfanyia mwanangu dawa hadi awe chizi! Nampenda mwanangu” “Mama,
ila sio kusudio langu. Nashindwa kumuacha Erica maana ni yeye ndiye amefanya
maisha yangu yamebadilika, ni yeye aliyefanya niwe na nyumba na gari, ni yeye
aliyefanya niwe na maisha mazuri” “Sawa kakufanyia hivyo, mwache na yeye
afanyiwe vizuri kama ulivyofanyiwa wewe, nay eye anapenda awe nyumba na gari,
nay eye anapenda awe na maisha mazuri, muache Erica wangu bora niishi nae
mwenyewe nyumbani kuliko kuja kutiwa ngeo nyumbani kwenu” Kwakweli
Bahati alijisikia vibaya sana na kuamua kukaa chini kabisa, kisha Yule mama
akamwambia, “Bahati leo sina urafiki na wewe kabisa na wale sikuchekei
kwa ule ujinga ujinga wako unaoufanyaga, naomba kwa amani kabisa ondoka nyumbani
kwangu maana nikiingia ndani nikitoka upo ujue utakuwa pamoja, mimi sitakufanya
ufe ila nitakufanya ulazwe maisha yote na madonda maana nitakumwagia maji ya
moto, naenda kuchemsha maji hivyo, ondoka sitaki kukuona kabisa, nenda
kambembeleze mkeo huko na umuulize kwanini alikuwekea dawa” Bahati
alijihisi vibaya sana ila hakuwa na namna zaidi ya kuondoka tu kwani kosa
lilikuwepo kwa ndugu zake maana bila ya hivyo basi yeye angekuwa kashamuoa
Erica, na kwavile alimuona mama Erica akiongea huku kakunja sura akajua pale
lazima yale maneno hatanii na anaongea kwa kumaanisha, kisha akamuaga na
kuondoka, “Na usirudi tena” Bahati hakuitikia kwani alijua
lazima angerudi tena tu. Kwakweli mama erica alishukuru sana
kumfanya Bahati aondoke kwenye nyumnba yaake, kisha aliingia ndani akiwa na
furaha ila alishangaa ambapo kuona Erica na Erick wapo kama mabubu yani hakuna
kitu wanachozumzia, ikabidi huyu mama awaulize, “Vipi mbona
hamuongei?” Erick akajibu, “Hakuna mama, kilichonileta leo
ilikuwa kuzungumza na wewe na si kuzungumza na Erica, muda upo nitazungumza nae
tu.” Basi mama Erica alikaa na kuzungumza na Erick alijikuta akimkubali
sana na aliona ndiye anafaa kuwa mume wa mwanae maana sifa zote aliziona kwa
huyo kijana, kisha Erica aliinuka na kwenda kumlaza mtoto maana alilala, hapo
mama Erica akaendelea kumuhoji Erick, “Kwahiyo mwanangu mipango ya ndoa
yako na Erica vipi?” “Mipango ipo mama, ila mimi wazazi wangu hawaishi
pamoja nataka siku nipange na Erica tukamuone baba yangu na siku tukamuona mama
yangu:” “Mmmh mama yako si ndio hamtaki Erica?” “Kwani mama
yangu anamfahamu Erica” “Ndio, kwani Erica hajakwambia kuwa alikuwa
anafanya kazi kwenye ofisi ya mamako, na ndio mamako alipomgundua tu hakutaka
tena awe karibu na wewe” “Mmmh mbona Erica hajawahi
kuniambia!” “Mwanangu, mimi ndio mama wa Erica, ngoja nikwambie kabisa
tatizo la mwanangu huyu, huyu mtoto ana tatizo moja la uongo yani kusema kweli
sijui huwa anaonaje hata kama ni jambo la kweli lazima achanganye na uongo nadio
anajihisi raha, ila ndio anajirekebisha siku hizi anaanza kuwa mkweli taratibu
natumai mpaka mnaoana hatokuwa na uongo katika kinywa chake” “Sawa mama
nimekuelewa na ninaelewa sana labda Erica anakuwa muongo sababu ni muoga wa
kujieleza ila nimempa uhuru kwangu awe ananiambia kila kitu hata nashangaa
hajanieleza kuhusu kufahamiana na mama yangu, ila sio tatizo sana maana mama
naweza kuelewana nae kuliko baba hata hivyo babangu ni muelewa sana kwahiyo
hakuna tatizo” Kisha Erica alirudi sebleni na mama yake alianza
kumuuliza, “Kumbe Erica hukumwambia mwenzio kama umewahi kufanya kazi
ofisini kwa mamake?” “Aaaah mmmmh aaah” “Unajiuma uma tu
masikini, si huwa nakwambia useme ukweli wewe, kwanini unapenda kuficha mambo
kama haya, sema ukweli ili ujue hatma yako” “Sawa mama
nimekuelewa” Siku hii Erica alikuwa mpole sana maana mama yake alikuwa
upande wa Erick tu, baada ya maongezi ya hapa na pale Erick aliamua kuaga maana
muda ulienda kwahiyo mama Erica alimruhusu ambapo Erica alitoka nje
kumsindikiza, Erick alimuuliza Erica, “Unaonyesha huna raha kabisa,
sababu yay ale mambo yaliyotokea jioni? Usiwe hivyo tafadhali umesikia, mimi
nishasahau yale” “Sawa nashukuru” “Halafu Jumatatu asubuhi uje
ofisini pale kwenye duka uchukue hela ukaweke kwa huyo mwanamke, utakuta
nimemuachia maagizo Moses maana mimi sitakuwepo hiyo asubuhi. Halafu jioni
nitakuja kukuchukua twende bandarini kuchukua ile gari, sawa mpenzi wangu
eeeh!” Muda huu Erica alitabasamu kwani mwanzo alihisi huenda Bahati
zake zimepotea, maana alikuwa na maswali mengi sana na hakujua angefanyaje
kulipa hela yam zee Jimmy, ila ilimradi Erick kakubali basi kwake ilikuwa furaha
sana. Basi Erick alimuaga pale na kumbusu kisha kuondoka
zake. Kiukweli Bahati alienda nyumbani kwake huku akiwa na
mawazo mengi sana, alifika na mkewe kumpokea ila alimsukuma pembeni bila kujali
kuwa ana mimba wala nini, Nasma alimuuliza mume wake, “Unanifanyia hivi
mme wangu, nimekukosea nini?” “Sikia wewe Nasma, sikupendi na sijawahi
kukupenda. Nampenda mwanamke mmoja tu wa kuitwa Erica” Lile swala
lilimfanya Yule binti ajihisi vibaya sana, ila ukweli wa mambo aliujua na
alichangia ingawa hakupenda mumewe abadilike vile, alimuangalia Bahati akikaa
mwenyewe na kuonekana mwenye mawazo sana, alimfata tena na kujaribu kuongea
nae, “Inamaana siku zote hizi ulizoishi nami Bahati hujanipenda
kweli?” “Sikupendi Nasma na kamwe sitokupenda” “Usiseme hivyo,
kumbuka tumefunga ndoa” “Ndoa gani hii? Ndoa batili hii, sijafunga kwa
akili zangu, mwanamke ninayempenda mwingine nikakuoa wewe ambaye hata kwenye
akili yangu sijawahi kukuwaza” Nasma alijaribu kumsogelea mume wake ili
ajaribu kumbembeleza, ila kile kitendo cha kumsogelea Bahati akamsukumiza, na
hapo hapo Yule binti alianza kulia kwa kuugulia uchungu, ilibidi Bahati amuinue
na kumpandisha kwenye gari yake kumpeleka hospitali. Ilikuwa usiku
ushaingia, wakampeleka leba na kumpima njia, kuona bado bado walimrudisha wodini
na huko alikuwa akiugulia vilivyo, hadi kufahamiana na mwanamke mwingine
aliyejifungua siku mbili kabla yake, walifahamiana kwa vile alivyokuwa
akihangaika sana. Alfajiri alijihisi tena uchungu mkali sana kwahiyo
wakampeleka leba ambako hakukawia sana alijifungua, alifurahi sana kupewa mwanae
mikononi kwani alikuwa ni mtoto wa ndoto zake, maana siku zote alitamani
kumzalia mtoto wa kwanza mumewe awe wa kiume na mtoto Yule alikuwa wa kiume
kwahiyo nilikuwa furaha sana kwake na kusahau yote ya jana yake kwani alijua
upendo kwake utaonekana maradufu. Akarudishwa wodini na kwenda kukaa na
kichanga chake maana walimwambia ni baada ya masaa ishirini nan ne kupita ndio
angepewa ruhusa ya kwenda nyumbani, Yule mwanamke waliyezoeana nae usiku
alimpongeza sana na kumuuliza, “Hongera, umejifungua mtoto gani
mwenzangu?” “Wa kiume, yani ndio mtoto wa ndoto zangu” “Oooh
kama mimi ila mimi nimejifungu kwa operasheni yani nilikuja kama siku ngapi
zilizopita huko ila uchungu unakuja na kuacha kumbe nyonga ndogo ndio jana
nimepasuliwa” “Kheee hongera na pole” “Asante, ila mimi naitwa
Salma, sijui mwenzangu waitwa nani?” “Naitwa Nasma” Wakafurahi
sana kufahamiana kisha wakaanza kufanya mazungumzo ya hapa na pale huku
wakiangalia vichanga vyao. Muda wa kuona wagonjwa ulipofika walikuja
ndugu zao kuwaona na kuwaletea chakula na zawadi za watoto, baada ya muda
kuondoka kwa ndugu zao walibaki wenyewe sasa, Salma alianza
kuongea, “Mimi nitaruhusiwa kesho hata wewe utaruhusiwa kesho, ila
hongera ndugu yangu naona mumeo alikuja kukuona pia” “Mmmmh mume aje
wapi, jana yenyewe kanileta hospitali sababu hakuwa na namna ya kufanya ila hata
kuniuliza tena imekuwaje hakuna, ingawa nimejifungua ila sijui mtiti wa
nyumbani” “Mmmh jamani wanaume hawa, mbona hawana huruma loh! Mimi
nililetwa na mume wangu pia ila toka siku hiyo hadi leo hajaja tena hapa
hospitali nadhani kaenda kufatilia kile kijanamke chake tulichokutana nacho hapa
hospitali, yani wanaume hawana huruma jamani, kweli hali kama hii ambayo mtu
unahitaji upendo na faraja ila wenyewe wanakuacha kwenye mataa kweli! Dah
Mwenyezi Mungu atusaidie tu” “Jamani wanaume hawa loh! Hadi kakutana na
kimwanamke chake jamani tena hapa hapa hospitali! Loh” “Yani mimi
namchukia Yule mwanamke, namchukia maisha yangu yote” “Kumbe unamjua mke
mwenzio?” “Ndio, ila hawezi kuwa mke mwenzangu nadhani bahati ya kuolewa
hana. Ndiomana wanasemaga usililie uzuri lilia bahati, hiko kisichana kinaitwa
Erica yani sikipendi kufa loh!” “Kheee mbona wewe na mimi tumeanza
kufanana sasa” “Kwanini?” “Mume wangu hanijali siku hizi, hataki
kuniona sababu ya msichana mmoja anaitwa Erica” “Kheee yukoje huyo
msichana?” Nasma alianza kumueleza Bahati kuhusu Erica alivyo kutokana
na jinsi alivyomuona siku ile kliniki, kwakweli Salma alihisi kabisa Erica
wanayemsema ni mmoja na kuchukia sana, “Haiwezekani mwanamke mmoja
asumbue akili za watu kiasi hiki, yani tushindwe kufurahia ndoa zetu sababu yake
loh! Tuungane shoga yangu na tumtokomeze huyo Erica” “Sawa, bora
tuungane maana na mimi nachefuka haswaaa jamani mwanaume hata kufurahia
nimemletea jembe jamani, ndio kwanza hata hospitali hajaja, yani kidudu mtu
Erica namchukia pia” Walijikuta wote wakieleza chuki za wazi wazi walizo
nazo dhidi ya Erica. Siku ya leo Erica aliamua kwenda tena
kanisani na mama yake, na kama kawaida walimshangaa na Yule mtoto huku kila
mmoja akisema lake, na walipotoka kwenye ibada kama kawaida walimfata na
kumuuliza kuhusu mtoto aliyembeba, “Ni wa nani huyo Erica?” “Ni
wangu jamani” “Yani hata harusi hatujacheza umezaaa, kumbe umezaa nje ya
ndoa” “Bora mimi niliyezaa ila kwavile naonekana basi ndio mnaona ni
mwenye dhambi kuliko watu wote, na je wanaotoa mimba kila kukicha, wao ni
wasafi? Huyu mtoto ni wangu na sina sababu ya kumficha kwenu” Basi
wakamuangalia tu maana yale majibu yaliwashangaza sana na kuona Erica kabadilika
haswaaa ukizingatia hakuwa na majibu ya aina hiyo. Erica aliondoka na
kurudi nyumbani, ila hakuongozana na mama yake kwani mama yake alienda kwenye
vikundi vya wakinamama muwaelimisha kuhusu ujasiliamali na mikopo, Erica alikuwa
akicheka tu na kujisemea, “Yani mama yangu kamiliki milioni tano ila
utafikiri anamiliki milioni mia, yupo kwenye semina kila leo kuelimisha wamama
kuhusu mikopo, ikimuishia atakopesha nini? Hahahah mama nae” Erica
aliendelea na safari yake ya kwenda nyumbani kwao, siku hii hakupanda pikipiki
wala bajaji, aliamua kutembea tu na mwanae. Wakati anarudi kwao
akakutana njiani na Rehema, alikuwa ni rafiki wa dada yake Bite hapo kitambo,
Rehema alifurahi sana kumuona Erica na kumkumbatia kisha wakasalimiana pale na
Rehema akasema, “Yani nilitaka kuwaletea kadi ya harusi yangu ila siku
nimekuja sikumkuta yeyote nyumbani kwenu na sikuwa na muda mwingine kwahiyo
nilishafanya sherehe hadi nimesahau, mnisamehe bure” “Usijali
dada” “Ila nilikutana na dada yako jamani, kheee Bite amekonda halafu
hana raha kwani ana matatizo gani?” “Sijui” “Inaonyesha ana
matatizo kwenye ndoa yake, nikipata muda nitakuja kuongea na mama yenu, unajua
ndoa zina mengi sana yanoyotendekaga ndani ambayo kwa macho ya nje hatuyafahamu
ila wenyewe wanandoa tu ndio wanayajua, kwakweli Bite kakonde, hana raha yani
yupo yupo tu, ana gari nzuri lakini hana furaha” “Ndio maisha hayo
dada” “Ila mdogo wangu cha kukushauri uwe makini sana kabla ya kuingia
kwenye ndoa ili usije kujutia maisha yako yote, kuwa makini sana na mwanaume
atakayekuoa, hakikisha mume anayekuoa anakupenda kweli hakika hutoteseka hata
kama mmeolewa sita” “Mmmh dada, ndoa za kuolewa wengiwengi
sipendi” “Hahaha nimesemea tu, ila kuwa makini usiolewe tu sababu wenzio
wameolewa ila olewa sababu kuna nia ya kuoana wewe na mwenzio. NIkipata mida
siku moja nitakuja kwenu kuongea na mama” “Haya, karibu” Erica
aliondoka zake na kurudi kwao, ambapo alianza kufanya shughuli zake
tu. Usiku ulipofika ndipo mama yake alirudi kutoka kwenye
shughuli zake na kumkuta mwane, ambapo baada ya salamu Erica alimuuliza mama
yake, “Mama, hiyo milioni tano tu, ikiisha utakopesha
nini?” “Kheee mwanangu ishaisha ujue, halafu walioandikisha wanataka
mkopo kwangu wapo wengi mpaka mama yako naishia kucheka tu, wangejua nilikuwa na
milioni tano tu! Wenzio wanajua nina mahela mengi mengi, wengine wanataka wakope
milioni mbili nimewakalia yani nimewakopesha wa elfu ishirini, elfu hamsini,
laki na mwisho laki tano yani akiongeza tu simkopeshi” Erica alicheka
kweli maana mama yake alijifanya kibosile haswaaa na hela zenyewe zimemuisha,
kisha akaanza kumuuliza, “Mama na wewe jamani, jana ndio nini kunifanyia
vile mwanao kwa Erick! Yani umenijoboa mweeeh hadi umenipigisha magoti
mama” “Kheee wewe mtoto hebu uelewe kula na kipofu, bila Erick hiyo
milioni tano ningeipata wapi ndotoni au? Yani na Yule mjinga asije tena sitaki
aweke kitumbua mchanga, tena hao wa kumroga wamroge tena ili asahau kabisa
kuhusu wewe” “Mama jamani!” “Hakuna cha mama jamani, tunaangalia
maendelea tu kwasasa, Erick ana akili sana halafu ana heshima yani nimempenda
bure tena ukifanya ujinga nitakutembeza kwa magoti wewe kutoka barabarani kwenda
kuomba msamaha kwa Erick, utapata wapi mwanaume kama yeye? Hebu acha ujunga
huko, tuangalie maendeleo, na siku ukiona nipo halafu kaja Erick unatakiwa
kunyenyekea, jana umeniudhi sana, hata chakula hukupika utajiondolea alama za
ndoa ujue” “Jamani mama, kwani ndoa ni mpaka kupika?” “Ndio,
unatakiwa ujue kupika, uwe msafi, uwe mpole, mnyenyekevu utafanya mume akupende
mara dufu, akija hapa mnyenyekee, muulize atakunywa nini sio kukaa nae sebleni
kama mabubu, akitaka kinywaji leta kwa unyenyekevu ikiwezekana na goti kabisa,
unafikiri wanawake wa kijijini kwanini wanaolewa? Sababu ni wanyenyekevu, kila
mwanaume anapenda kunyenyekewa, kusikilizwa na kuheshimiwa. Tena vijana wa ajabu
ajabu marufuku kufika kwangu hapa sijui Yule wa kujitapa mimi ndio mwanaume wa
kwanza kwa Erica, sitaki kumuona kabisa, umesikia!” “Sawa mama,
nimekuelewa” Erica alimuitikia mama yake ili alitambua maneno yote hayo
ni sababu ya hela zile alizoambiwa kapewa na Erick maana tangia hapo kampenda
sana. Basi muda wa kulala alienda kulala na mwanae ila
akapigiwa simu na Dora, alikuwa akimkumbusha kuhusu swala la
hela, “Erica usisahau” “Ni kesho Dora, hata sijasahau yani
usijali” “Sawa, nakuonea huruma ndiomana nakupigia pigia shoga
yangu” “Sawa, nimekuelewa” Basi waliagana na Erica kuamua
kulala. Kesho yake mapema kabisa, alijiandaa na kumuaga mama yake kisha
kwenda kwenye duka la Erick ambapo alimkuta Moses, aliyemkabidhi mzigo
alioachiwa na Erick, basi alivyochukua akawa akiongea ongea na Moses ila Moses
akamwambia, “Erica, samahani siku ile kwa ile fomu niliyokusainisha
haikuwa lengo langu nilitumwa na Tumaini kufanya vile halafu kuhusu kukupeleka
dukani kwa Tumaini naomba unisamehe, yani hapa kwenye hili duka wengi huamini ni
duka langu, maisha yangu yamebadilika sababu ya hili duka, sasa nisingependa
nirudi nilipotoka, nakuomba Erica unisamehe” “Sawa usijali” Muda
kidogo akapokea simu na alipomaliza kuongea nayo akamwambia
Erica, “Naomba uondoke maana kuna watu wanaagizwa na Tumaini na hawana
nia njema kwako halafu usimwambie hata Erick kama nimekwambia hili la sasa
hivi” Erica hakutaka hata kuendelea kusikiliza zaidi kwani kwa muda huo
maisha yake yalikuwa bora sana kuliko kingine chcochote, akaenda moja kwa moja
benki na kukutana na Dora alishafika muda anamngoja tu, basi Erica akaenda
kuweka zile hela na kuzihamishai kwenye akaunti ya Dora. Yani waliondoka
pamoja huku Dora anatabasamu tu na kumwambia Erica, “Yani hutokuja
kujutia kwa hiki ulichokifanya shoga yangu, nimefurahi sana kwa kuniamini. Yule
mzee sio mtu mzuri” “Sawa nimekuelewa Dora” “Yani Erica wewe
ndiomana unabarikiwa sana yani huna tamaa za kijinga, hela zinakufata lakini
huna tamaa za kijinga na hilo swala litakuokoa” “Kwahiyo wewe tamaa ndio
zinakuponza?” “Mmmmh mimi yani sijui mwisho wangu ni nini ila
ulilolifanya leo Erica nakupongeza sana, wewe ni mwanamke
shujaa” Wakaagana na kuondoka, kwakweli Erica alishangaa sana zile sifa
kedekede alizopewa na Dora ila alimuitikia maana ukweli wa mambo hakuujua zaidi
ya Dora mwenyewe. Kisha Erica alirudi tu kwao akisubiria muda wa kufatwa na
Erick kwaajili ya kufata gari. Jioni kama alivyoahidi Erick
alienda kumchukua Erica na kumkuta ashajiandaa kabisa na kuondoka nae, wakiwa
kwenye gari akamuuliza, “Mama umemwambia?” “Hapana, nataka
kumshtukiza tu” “Ni vizuri sana” Basi walienda na kufika
bandari, wakati wapo kwenye makabidhiano mara alitokea mtu karibu yao na
kuwasalimia, Erica alimuangalia mtu huyo alikuwa ni Rahim, aliogopa na kujiuliza
kuwa Rahim kafata nini bandari. Jioni kama alivyoahidi
Erick alienda kumchukua Erica na kumkuta ashajiandaa kabisa na kuondoka nae,
wakiwa kwenye gari akamuuliza, “Mama umemwambia?” “Hapana,
nataka kumshtukiza tu” “Ni vizuri sana” Basi walienda na kufika
bandari, wakati wapo kwenye makabidhiano mara alitokea mtu karibu yao na
kuwasalimia, Erica alimuangalia mtu huyo alikuwa ni Rahim, aliogopa na kujiuliza
kuwa Rahim kafata nini bandari. Kiukweli Erica alipatwa na mashaka sana
akikumbuka yale maneno ya Rahim kuwa anaweza kuwateketeza, muda huo huo Erica
alijishika tumbo na kuanza kulalamika kuwa tumbo linamuuma sana, ila Rahim
alicheka na kusema, “Erica tumbo linakuuma wewe! Kwahiyo huyo Erick
unayemsemaga ndio huyu!” Erica alikuwa akiugulia tut umbo kitendo
ambacho Erick hakufikiria kama Erica anaigiza ila alimuonea huruma, na kumchukua
upesi upesi hadi kwenye gari yake na hata maneno ya Rahim kama anamfahamu Erica
hakutaka kuyasikiliza, basi alipanda na erica kwenye gari yake na kuelekea
hospitali wakati huo Rahim nae aliingia kwenye gari yake na kuwafata nyuma huku
akisema peke yake, “Huyu msichana asinitanie kabisa, na leo
nitawavuruga” Erick alimpeleka Erica hospitali ile ile ambayo Erica huwa
anaenda kliniki, waliposhuka tu kwenye gari na kuelekea hospitali bado Erick
aliona kama Erica ana hali mbaya maana alikuwa akiugulia tumbo hadi anatoa
machozi, Rahim nae alikuwa amefika akiwafata nyuma. Wakati wanaingia
Erica na Erick wakapishana na Nasma na Salma maana walilazwa hospitali ile na
muda ule walisharuhusiwa kutoka sema ndugu zao hawakufika kuwachukua, walikuwa
wamebeba watoto wao huku wakiangalia kama kuna ndugu zao wanakuja kwahiyo
walitoka ili kuangalia ndugu zao kisha kuondoka nao, kwahiyo kitendo cha Erick
kupita huku amemshikilia Erica na tena akionekana analia kama anaumwa sana, ila
walipopita karibu yao tu wote walijikuta wakisonya na kuangaliana kisha Salma
akasema, “Ndio erica Yule sijui limekuja kufata nini hapa hospitali kama
sio uchawi tu wa kuturogea vitoto vyetu” Muda kidogo akamuona Rahim
akiwafata nyuma, pale ndio akachoka kabisa na kumwambia tena
Nasma, “Jamani ni mume wangu Yule ona alivyopita kama hanioni vile, na
nimempigia simu kabisa kwamba nimeruhusiwa kasema yupo busy sana hawezi kuja
kunichukua ila saizi yupo busy kumfatilia Erica jamani ni haki hii
kweli?” Aliongea kwa masikitiko sana, Nasma akamwambia, “Pole
mwaya, ila mie mume wangu na ubishi wake kaniambia anakuja nadhani muda sio
mrefu atafika” Kweli muda sio mrefu Bahati alifika ila alipitiliza na
kwenda kule kule alipopelekwa Erica, kumbe muda Erica na Erick wanashuka yeye
aliwaona maana ndio alikuwa anaingia hospitali kwahiyo alitaka ajue ni kitu gani
kimempata Erica, kwakweli Nasma nae aliongea kwa masikitiko, “Mungu
wangu ona na mume wangu hata mimi hajaniona kaenda kule kule” “Kheee
Yule aliyepita ndio mumeo” “Ndio yani hadi nashangaa, dada tusikalie
kimya swala hili lazima tufanye jambo” “Kweli sasa
tufanyeje?” “Hebu tupeane namba za simu baada ya arobaini za watoto wetu
tushirikiane, haiwezekani huyu kiumbe mmoja Erica atukoseshe raha kiasi hiki,
kwani yeye ana nini ambacho sisi hatuna eeeh! Lazima tufanye jambo” Pale
pale wakabadilishana mawasiliano yao ila kuna mmama pembeni alisikia mazungumzo
yao, akawafata na kuwaambia, “Jamani wanangu nimewasikiliza vizuri,
najua ni kiasi gani inauma kuona mumeo anakuacha na kwenda kufatilia mwanamke
mwingine, ila kabla ya yote mnachotakiwa kufanya sasa ni kufuata waume zenu na
kuwalazimisha mrudi nyumbani na watoto halafu mengine yatafuata, mnitafute
niwaambie cha kufanya maana hata mimi mume wangu alikuwa hivyo
nikamdhiti” Pale pale wakachukua namba za Yule mama kisha wakafata
ushauri wake wa kwanza wa kufata waume zao, waliwafata na kukuta wapo nje katika
chumba cha daktari ambapo ndani alikuwepo Erica na Erick, ila ilionyesha hata
wao kama wamechanganyikiwa hivi wakitaka kujua hali ya Erica, kila mmoja
alimfata mume wake na kumuomba warudi nyumbani, kwakweli Rahim alikuwa mkali
sana kwa mkewe na Bahati nae ilikuwa hivyo hivyo, “Huoni kama kuna
mgonjwa nataka kujua hali yake hapa” “Jamani Bahati kumbuka mimi ni mkeo
na huyu ni mwanao, toka nimejifungua hujaja kutuona na leo tunatoka ukaahidi
kuja kutuona kweli unadhani ni sahihi unachotaka kufanya kwangu?” Wakati
huo mke wa Rahim nae alikuwa akimlalamikia mumewe maana Rahim ndio alikuwa na
majibu ya shombo balaa kwa mke wake, Bahati akamtazama na kugundua kuwa ni Rahim
ambaye waliwahi kubishana kuhusu Erica miaka ya nyuma, alisogea na
kumwambia, “Wewe jamaa si ndio siku ile ulisema Erica hatutaki wote
anamtaka mtu wake Erick, haya unasubiri nini sasa? Erica si ameingia na mtu wake
humo!” Rahim akamjibu kwa ukali, “Achana na mimi” Bahati
akaona itakuwa shari hapo kwahiyo aliamua tu kuondoka na mkewe huku akisema
kwamba ataenda kwakina Erica kujua hali yake, kwahiyo alibakia Rahim na
mkewe, “Jamani mume wangu siku zote huniambia kuwa humpendi Erica,
alijipendekeza tu kwako sasa unamsubiri wa nini hapa?” “Wewe ni mwanamke
tu hujui lolote, kwanza nyie wanawake sio wa kuwaamini, kwani wewe unaweza kuwa
na tofauti gani na Erica, si mwanamke mwenzio huyo” “Mwamani mume wangu,
nimekuzalia mtoto wa kiume” “Kwani mtoto wa kiume ndio nini? Mtoto ni
mtoto, kumbuka Erica ana mtoto wangu pia” “Rahim nimechoka kwakweli,
nitaanza kupiga kelele hapa hospitali uumbuke” Rahim alizijua akili za
mkewe kwahiyo ilibidi akubali tu kuondoka nae maana alijua kifuatacho ni
kudhalilishwa tu, akaondoka nae ila alikuwa akilalamika njia nzima kuwa kwanini
ameoa mwanamke wa dizaini ile, “Ni kosa la baba kunitafutia mwanamke
chizi, bora hata Erica” Yani mkewe alimuangalia tu ila aliridhika sababu
amekubali warudi nyumbani. Wakiwa kwa daktari Erica na Erick
bado Erica aliendelea kulia sana, huku dakari akijaribu vitu vyote kumtuliza
ilishindikana, “Dada, tulia basi uniambie hata kwa kifupi nini
kinakusumbua nielewe vizuri kisha nihudumia wagonjwa wengine” “Ila Erica
alichukua muda mrefu sana na daktari alishindwa kuwafokea au kuwatoa sababu
walipoingia tu Erick alianza kwa kumpa hela ili amuhudumie mtu wake vizuri, basi
daktari akaamua kumwambia Erica apande kitandani ili kujua tatizo ni nini,
alipopanda tu kitandani Erica alimpa ishara Yule daktari kuwa amtume Erick nje
ili amueleze basi daktari alitumia uelewa wake kisha akamtoa damu Erica na
kuweka kwenye bomba kisha kumuandikia maelezo Erick kuwa aende maabara akapime
damu hiyo na asubirie majibu, akawapigia wa maabara kuwa wampokee kwamaana hiyo
Erica hakwenda hata maabara. Daktari alifanya vile maana hakukuwa na namna
nyingine ukizingatia Erick aligoma kutoka kwenye chumba cha daktari kabisa.
Erick alipotoka tu kupeleka kile kipimo, daktari alianza kumuuliza Erica
vizuri, “Eeeeh tatizo ni nini?” “Daktari sina tatizo lolote ila
naomba umwambie mchumba wangu kuwa nina vidonda vya tumbo, sasa vilinishika
ndiomana kuongea nilikuwa siwezi. Naomba umwambie hivyo maana akigundua
nimemdanganya ataniacha” “Sawa hakuna shida, sasa wewe utanisaidiaje kwa
kudanganya hivyo?” “Nina elfu thelathini dada yangu,
nitakupa” “Aaaah elfu thelathini ni ndogo sana yani nifiche siri kwa
hela ndogo hivyo hapana” “Basi nikupe ngapi?” “Labda
laki” “Sawa, nitakupa laki moja dokta, nakuomba nisitiri” “Mmmh
haya mambo, ila huwa tunakutana na mengi sana zaidi ya haya, sema sikufahamu
ujue!” “Ndio ila mimi naitwa Erica, na mwenzangu waitwa Dokta
nani?” “Naitwa Dokta Doroth” “Sawa, nisitiri Dokta
nakuomba” Kwavile Yule ni dokta, alihisi kuna jambo limempata Yule binti
kwahiyo aliamua kumbebea aibu yake, akamuuliza tena “Na hiyo laki
naipataje?” “Nakutumia kwenye simu yako, tafadhali” “Kwenye simu
yangu lini?” “Nakuomba niamini tafadhali” “Nikuamini
vipi?” Alikuwa na elfu thelathini akamkabidhi Yule dokta ila bado dokta
alitaka amaliziwe chake mapema, Erica alimsisitiza kuwa
atammalizia, “Sikia binti sikujui hunijui, nimalizie changu kabisa, la
sivyo nasema ukweli” “Sasa nitaitoa wapi hapa? Yani hela ipo nyumbani,
nakuomba nisitiri mwanamke mwenzio, sikudanganyi nitakumalizia kweli
tena” “Hapana kwakweli na mimi nipo kazini hapa, nimalizie
kabisa” “Dada nakuahidi kuimaliza, basi naomba nikuachie simu yangu
halafu kesho nikija kumaliza deni nitaichukua” Daktari alikubali
kuachiwa ile simu na Erica, basi Erick aliporudi na vipimo alikuta Erica yupo
sawa na dakatari akamwambia kuwa kampa dawa ya kumtuliza, kisha
akamuelekeza, “Huyu ana vidonda vya tumbo kwahiyo asikae na njaa kwa
muda mrefu na aepuke kula vyakula vyenye aside, akizingatia hayo
atapona” “Nashukuru daktari maana nilikuwa na mawazo sana” Kisha
Erica na Erick wakatoka pale hospitali na kupanda gari wakielekea nyumbani ila
Erica alikuwa na mawazo sana maana yaliyotokea kwake siku hiyo ni makubwa sana,
walitembea njia nzima na Erica alikuwa haongei chochote, sababu ilikuwa ni usiku
Erick akamwambia, “Erica, mpigie mama simu kuwa utachelewa kidogo maana
nataka tupite kula” Erica akajiuma uma maana simu hakuwa nayo, hadi
Erick akarudia tena kumwambia, ndipo akaamua kujifanya anaitafuta na
kushtuka, “Kheee kumbe nimeiacha hospitali kwa Yule
daktari” “Erica jamani, umeanzaje kusahau simu jamani, ngoja turudi
kuifata” “Hapana Erick usisumbuke, nitaifata kesho” “Hapana
haiwezekani, yani jishindwe kuwasiliana nawe usiku sababu simu umesahau kwa
daktari! Nageuza gari tukaifate” Basi Erick aligeuza gari kitendo hiko
kilifanya Erica ashikwe na mashaka balaa maana hakujua hata kitu gani atafanya
alibakia tu kusema, “Mungu nisaidie” Maana uongo aliofanya siku
hiyo hakutegemea kusamehewa na Erick kabisa, basi walifika hospitali yani Erick
alivyosimamisha tu gari Erica alishuka na kumwambia, “Erick usihangaike
kuliingiza ndani na kupaki ngoja nikaichukue mara moja twende” “Hapana
bhana, hali yako bado si sawa, ukizidiwa huko je!” Erica hakusikiliza
haya maoni kwani alienda tu hospitali na moja kwa moja kuingia kwa Yule daktari
na bahati hakuwa na mgonjwa, Yule Doroth alimshangaa na
kumuuliza, “Kheee umerudi tayari, si unaona usingeacha simu
usingeniletea” “Dada sio hivyo, yani jamaa yangu hataki kunielewa kabisa
kuwa simu nimeacha hospitali nakuomba kesho nikuletee hiyo hela, naomba simu
tafadhali” “Unadhani naweza kukuamini kirahisi hivyo!! Sikujui hunijui,
hiyo kitu haiwezekani, nipe change ndio uondoke” Basi akapata wazo la
kumpigia simu Bahati, akamuomba Yule dada simu ili apige kwa mtu wa kumtumia
hela, basi Yule dada akampa na kuiwasha kisha kumpigia Bahati, “Erica,
nini tatizo mama angu eeeh! Nimesikitika sana sijakujulia hali
hospitali” Tena ikawa ni vyema kwa Erica kusikia kuwa amejua kwamba
alikuwa hospitali, akamwambia “Bahati naomba nitumie laki moja nina
shida nayo muda huu” “Shida gani tena?” “Nitakwambia ila naomba
unitumie, nakupa namba za kunitumia, nitumie nay a kutolea” Kisha Erica
akamtumia ujumbe Bahati wa namba ya simu ya Yule daktari kuwa amtumie hela
kwenye hiyo namba, na muda kidogo tu Bahati alikuwa kashatuma hela, Erica
alimpigia na kumshukuru sana kisha akakata ile simu na kumwambia
daktari, “Basi ile elfu thelathini yangu naomba” “Aaaah sikupi,
ile nimekata kwa usumbufu” “Jamani daktari” “Unafikiri
kudanganya kazi ndogo eeeh! Sikupi” Aliona simu yake inaita yani Erick
alianza kumpigia simu kwahiyo aliamua kuondoka zake maana hakuwa na namna tena
ingawa aliona Yule dokta kamfanyia unyama wa hali ya juu ingawa angeamua kuweka
wazi yote yale yasingetokea. Basi alirudi kwenye gari na kumpigia mama
yake kuwa atachelewa kidogo, “Mama nitachelewa kidogo, kuna mahali
naenda kula na Erick” “Ila kuwa makini mwanangu” “Usijali mama,
nipo makini” “Nakujua unavyompenda huyo mwanaume na umejikuta kumuamini
balaa ila narudia tena usimuamini mwanaume, siyo ndugu yako wa kuaminiwa hata
mara moja” “Sawa mama usijali” Kisha safari ikaendelea na kwenda
sehemu ya kula na Erick ila akaona ni vyema wakiwa wanakula abwage manyanga,
aliamua tu siku hiyo aseme ukweli maana aliona vyema nafsi yake ibaki huru
kwakuwa alikumbuka jambo moja kwamba ukweli humuweka mtu huru, kwahiyo aliamua
siku hiyo aseme ukweli tu. Basi walifika kwenye hoteli nzuri
sana na kushuka, kisha kukaa kwenye meza na kuagiza chakula ila Erica alikuwa na
mawazo sana, kwanza hakupenda ambacho Yule daktari alimfanyia na pia hakupenda
kushindwa kwake kupata gari sababu ya Rahim, ila hapo alitulia akijipanga kusema
ukweli kwa Erick juu ya Rahim, walipoanza kula ni Erick ndio alimuuliza
Erica, “Hivi erica, unamfahamu Rahim?” Erica alitulia kwa muda
na kujibu, “Ndio namfahamu” “Erica, nakumbuka kuwa uliniuliza
maswali mengi sana kuhusu Yule mtu, na mbona hukuniambia ukweli kama
wamfahamu?” “Nisamehe Erick ila sikujua ungechukulia vipi kama
ningekwambia ukweli” “Haya niambie mnafahamiana vipi?” “Yule
kijana ndio babake Angel” Erick alijikuta akikohoa hadi chakula
alichokuwa anakula kikaanguka, na kumuuliza tena
Erica, “Unasema!” “Nisamehe Erick, ila Yule ndio babake
Angel” “Yani bora hata usingeniambia kama unamjua ila huna aibu Erica,
unaniambia kabisa Yule ndio babake Angel ili iweje, na mimi ni
nani?” “Nisamehe Erick” “Hivi Erica ulishindwa kuzaa na mimi
ukaenda kuzaa na Yule kweli? Uliniona mimi malaya ila Yule akawa mtakatifu kwako
kweli? Hivi Erica ni wewe ambaye nilikuwa nakuona shuleni kama binti mlokole au
ni Erica mwingine? Sielewi Erica, hukuona wanaume wote wa kuzaa nao zaidi ya
Yule?” “Nisamehe Erick” “Nikusamehe kitu gani? Yani unachojua
wewe kusema ni nisamehe tu hata hufikirii jambo lingine zaidi ya nisamehe,
nilikwambia tuzae ukagoma, nimerudi nimekwambia nina hamu umegoma ila kumpa Yule
mjinga umeona sawa, kweli Erica wewe ni wa kutembea na Rahim jamani! Sijawahi
kufikiria kama inaweza tokea siku moja mke wangu akawa amewahi kutembea na
wanaume vichaa kama Rahim, nimejitolea kwa kila hali juu yako, nakupenda,
nakujalo, nakuthamini lakini wewe ndio kunidhalilisha kiasi hiki
kweli!” “Ila Erick sijatembea nae kwa kipindi hiki, ilikuwa ni zamani
alinidanganya” “Inamaana na elimu yako hukuweza kutambua mwanaume wa
kweli yupi na wa uongo yupi, hukuwa na maana ya kusoma basi. Ni afadhali ungezaa
na mjinga mwingine kuliko mpumbavu kama Rahim, nilihisi tu nilivyomuona mtoto
ila sikutaka kuongea. Kiukweli Erica umeniboa yani umeniboa sana hata chakula
hiki siwezi tena kukila, kwaheri” “Lakini Erick usinifanyie
hivyo!” “Nisikufanyie hivi nini, mtu hujielewi nakuomba mapenzi hutaki
unajifanya kuumwa sijui siku zako kumbe unamtunzia Rahim, kwahiyo mimi nikuleee,
na kukuhudumia halafu starehe apewe Rahim, mimi sio bwege kiasi hiko Erica,
umeniboa sana kwaheri” Erick akainuka huku amefura hasira na kuondoka,
alimuacha pale kwenye hoteli Erica peke yake, kwakweli Erica alihisi
kuchanganyikiwa alijikuta akiinama na kulia maana hakujua kuwa afanye nini kwa
muda huo maana hakutegemea kama Erick angeweza kumuacha kiasi kile, kumuacha
eneo lile ni bora hata angeenda kumuacha kwao, alijiangalia hakuwa na hela
yoyote maana yote alitoa hospitali kwa Yule dokta, alijihisi kuchanganyikiwa,
alipotaka kuinuka ili aondoke, muhudumu wa ile hoteli akamsimamisha na
kumwambia, “Dada, hamjalipia chakula bado” Erica alijikuta
akianza kulia huku akisema, “Mungu wangu nitafanyaje mimi, uwiii Erica
leo nimepatikana. Akajaribu kuongea na Yule muhudumu kuwa pesa hiyo apelike
kesho ila muhudumu akagoma na kusema, “Wakati mnaagiza vitu vya gharama
hivyo mlikuwa mnategemea nini? Hapo mnadaiwa elfu ishirini na tano” “Ila
hatujala” “Haijalishi maana mlishaagiza” “Basi naomba niache
simu yangu, kesho nilete hiyo pesa” “Simu yako haina umuhimu kwetu,
umesikia dada, unachotakiwa ni kulipa hiyo hela. Twende kwa
meneja” Erica alipelekwa kwa meneja wa ile hoteli ambaye nae alichukia
kuambiwa chakula walichoagiza na hawajalipia, “Sasa mdada unategemea
nini?” “Naomba niache simu yangu hii na nitakuja kulipa
kesho” “Unadhani simu yako ni muhimu kwetu? Cha muhimu ni pesa, nyie
wadada ndio zenu hamjifunzi tu ukienda hotelini na mwanaume unatakiwa kuwa na
hela yako ya ziada ili likitokea la kutokea uweze kujinasua ila wewe hukujua
hilo unaenda matembezi na mwanaume na huna hela yoyote, sasa mimi nakupa cha
kujifunza ili siku nyingine usirudie kutoka na mwanaume na kuagiza vitu vikubwa
wakati huna hela mfukoni” Kisha akamuangalia Yule muhudumu na
kumwambia, “Mpeleke akaoshe vyombo huyo, hatuna shida na simu
yake” Erica alipelekwa sehemu ya kuosha vyombo, macho yake yalijaa kwa
machozi alijikuta akilia sana na hakutegemea kama jambo kama lile lingempata kwa
siku hiyo ya furaha, maana gari hakupata ila kapata majanga juu ya majanga na
kuweza kuelewa usemi wa Yule mama kuwa ana kimavi, alikosa raha
kabisa. Alikuwa akiosha vyombo huku amejawa na machozi kwenuye macho
yake, muda kidogo simu yake ikaita, alihisi ni Erick anapiga labda kajirudi ila
alichukua na kukuta mama yake anapiga, machozi yalizidi kumwagika na kupokea ile
simu huku akilia, mamake akamfokea “Wewe mtoto vipi? Hujarudi nyumbani
halafu nakupigia simu unajitia kulia, Erica hebu acha ujinga wako huko, kwanini
hujarudi nyumbani?” Erica hakumjibu mama yake na kuendelea kulia, mama
yake aliendelea kuongea, “Erica, nakwambia kama umeanza ujinga wako tena
wa kujirahisisha kwa wanaume usahau hapa nyumbani, ndio nakuozesha hivyo bila
harusi, yani wewe kutoka kidogo na Erick ushaenda kulala nae! Na ukirudi hapa
utanieleza, sio kujiliza kwenye simu, kwani unafikiri siujui uongo wako
au!” Erica aliweka simu pembeni na kuendelea kulia yani hakuwa na raha
na wala hakuweza kuendelea kuosha vile vyombo, muhudumu akaenda na
kumwambia, “Dada, usilie osha hivyo vyombo” “Dada, hivi huna
huruma na mwanamke mwenzio, hivi nyie ni wanawake wa aina gani ambao mna roho
mbaya kiasi hiki” Aliongea huku akilia, Yule muhudumu akaenda kumuita
meneja tena, meneja alifika na kumwambia Erica, “Tutakupeleka polisi,
hatutaki ujinga kabisa, tutakupeleka kuwa umetaka kututapeli, hebu osha vyombo
hivyo” Kwakweli Erica alilia tu ila wazo la kumpigia simu tena Bahati
likamjia, ila alipiga simu haikupokelewa Yule muhudumu akamwambia, “Huyo
mwanaume ashakuacha, yani wanawake wengine nyie sijui akili zenu ziko vipi,
mnashindwa kujifunza au? Tena ushukuru tumekupa kazi ya kuosha vyombo unapata
hata pa kujistiri, tukikuruhusu kuondoka saa hizi saa saba si utabakwa huko
useme tuna roho mbaya! Bora ung’atwe na mbu tu hapo uoshe vyombo” Kisha
wakaondoka na kumuacha ila Erica alikuwa na kilio cha hali ya juu na hakupenda
ile hali. Erick hakwenda kwao kwa mawazo aliyokuwa nayo ila
alienda baa na kuanza kunywa sana, yani ni alikunywa hatari ila badae akakumbuka
kuwa alimuacha pale Erica bila ya kumpa nauli wala kulipa ile bili, alidhani
kuwa wangemsumbua sana Erica, ingawa alikuwa amelewa ila alimuonea huruma sana
Erica, akataka kuinuka ila akamuangalie Erica pale, sema muda huo huo akapigiwa
simu na Rahim na kupokea, “Aiseee umenisikitisha sana Erick, yani kumbe
erick aliyechukua majukumu ya kulea mwanangu ni wewe!” “Bwana Rahim,
achana na mimi” “Sio niachane na wewe, hivi unamjua Yule mwanamke vizuri
au unamsikia, unajua kwanini kazaa na mimi ila sijamuoa? Erica ni msichana mzuri
sana ambaye kila mwanaume atatamani kuwa nae ila ni msichana asiye na akili,
huwezi amini, Erica katembea na ukoo wangu mzima, nikikwambia vitu alivyofanya
Erica huwezi kuamini” “Sawa hakuna tatizo ila hayo yalipita, kama
alitembea na ukoo wako mzima yalipita, nampenda Erica” “Shauri yako,
nakuonea huruma, nilivyorudi tu kesho yake au keshokutwa nilikuwa na Erica
tukila raha, ndio mwanamke wa kujihesabia nae wewe” Lile jambo ndio
lilimuumiza zaidi Erick na kujikuta akikata ila simu na kuagiza pombe nyingine,
alikunywa sana na kujikuta akilala pale pale Bar maana hakuwa na raha hata
kidogo. Bahati alikuwa na mawazo tu tangia muda ule Erica
kamuomba laki, hakujua ni jambo gani limempata Erica mpaka kawa vile maana sio
kawaida kabisa, alikuwa na mawazo mno juu ya Erica, Nasma alitambua hilo ya kuwa
mumewe ana mawazo juu ya Erica, alimzia mumewe kalala akachukua simu yake na
kwenda kuiweka bafuni na ndiomana muda wote Erica anampigia hakupokea, Bahati
alikuwa amelala kwenye kochi, kwenye mida ya saa kumi alfajiri alishtuka na
kuanza kutafuta simu yake ila hakuiona, aliitafuta sana ila hakuiona popote
pale, wazo likamjia kuwa huenda ni mke wake tu kaificha. Bahati alimfata
mkewe chumbani na kumuuliza ilipo simu ila mkewe akasema hajui ilipo, Bahati
alifoka kwa hasira, “Humu ndani tupo wawili tu, wewe, mimi na mtoto
mdogo je simu achukue nani?” “Tupo wawili sababu umekataa ndugu zangu
wasije kuniuguza” “Ulishindwa nini kusema nikupeleke kwa ndugu zako?
Yani hapa sitaki ndugu zako wala ndugu zangu, hujui hii nyumba nimeipataje wewe.
Haya simu iko wapi?” “Sijui” Bahati aliamua kutumia nguvu ili
mkewe amuonyeshe simu ilipo, alimzaba vibao kadhaa mpaka mkewe akasema ukweli
kuwa simu kaiweka bafuni. “Mwanamke mjinga sana wewe, sijui nilianzaje
kuoa mwanamke mjinga kama wewe” “Jamani Bahati hunipendi, nimekuzalia
mtoto ila hunipendi jamani kwanini unanitesa hivi!” “Usinibabaishe
nikaongea mengine bure” Bahati akaenda kuchukua simu yake nakukuta
alipigiwa na Erica mara mbili, alichukia sana na kumpigia Erica ila Erica
alisema tu hoteli aliyokuwepo bila kusema tatizo ni nini, kwakweli Bahati
hakusubiri kwani muda huo huo alijibeba na kuondoka kwakweli mke wake alikuwa na
simanzi sana na kuona anaonewa maana hakufikiria kama mumewe wa ndoa angemfanyia
hivyo. Bahati alienda hadi hoteli aliyoambiwa na Erica,
akamuulizia na kupelekwa alipowekwa kuosha vyombo ila vyombo vyenyewe aliosha
vichache sababu ya kulia, Bahati akauliza kwanini Erica kafanyiwa
vile, “Huyu mwanamke kaja na mwanaume wameagiza chakula mwanaume
kamkimbia, hana hela ya kulipa ndio tukampa kazi ya kuosha
vyombo” “Kwani mnamdai pesa ngapi?” “Elfu ishirini na
tano” Bahati akatoa zile hela na kumuinua Erica aliyekuwa amekaa chini
sababu ya kilio na kwenda nae nje kupanda gari yake kisha akampeleka moja kwa
moja kwao, walipofika aliingia nae ndani na kwenda kugonga mlango wa nyumbani
kwao maana ilikuwa mapema sana, saa kumi na mbili kasoro, mamake alitoka ila
alichukia sana kuona Erica kaletwa na Bahati ila kabla hajasema chochote Erica
alianguka miguuni pake. Bahati akatoa zile hela na
kumuinua Erica aliyekuwa amekaa chini sababu ya kilio na kwenda nae nje kupanda
gari yake kisha akampeleka moja kwa moja kwao, walipofika aliingia nae ndani na
kwenda kugonga mlango wa nyumbani kwao maana ilikuwa mapema sana, saa kumi na
mbili kasoro, mamake alitoka ila alichukia sana kuona Erica kaletwa na Bahati
ila kabla hajasema chochote Erica alianguka miguuni pake. Ilibidi mama
Erica ainame na kumuokota mwanae alikuwa kazimia, ni sababu ya kulia sana, huyu
mama alimfokea sana Bahati, “Umemfanya nini mwanangu
wewe?” “Sijamfanya chochote mama” Mamake Erica alikuwa
akihangaika na Erica pale ila Bahati alipotaka kusaidia alimtimua kabisa na
kumwambia aondoke, hataki kumuona, ila bahati aliganda tu pale, wakati mama
Erica akihangaika na Erica Bahati alienda kuchukua chupa ya maji kwenye gari
yake na kummwagia Erica, akazinduka lakini alionekana kuwa na uchovu sana,
mamake alimuuliza kama wampeleke hospitali ila Erica aligoma na kusema akalale
tu, mamake akamshauri jambo moja kuwa kabla ya kwenda kulala akaoge kwanza, basi
Erica alikuwa akijikongoja tu ikabidi mamake ampeleke na kummwagia maji kisha
ndio akampeleka kulala. Muda huo wote Bahati alikuwepo tu sebleni. Mama Erica
akarudi sebleni na kumwambia Bahati, “Nashukuru sana kijana kwa
kuniletea maradhi yangu ila nakuomba uondoke maana mwanangu sasa yupo kwenye
mikono salama” Bahati hakuwa na usemi na wala hakuweza kubishana na mama
yake Erica, hivyo aliamua kutoka zake na kuondoka. Mama Erica alibaki na
maswali sana kuhusu kilichompata mwanae yani hakuelewa kabisa ila alimwacha
apumzike kwanza kama mwenyewe alivyoomba kuwa apumzike
kwanza. Muda kidogo Bahati alirudi tena akiwa kabeba samaki na
kuku wawili na kumwambia mamake Erica, “Mama nimekuja kidogo kuleta hii
ili Erica atengenezewe supu, samahani mama” Kisha akaacha pale na
kuondoka zake, kwa upande mwingine hata mamake Erica alimuhurumia ila tu ndio
alishaoa. Akaamua kuandaa ile mboga kwaajili ya mwanae akiamka. Kwenye
mida ya mchana mama Erica alienda kumuamsha mwanae maana kila muda alikuwa
akimchungulia ila akaona ni vyema muda huo amuamshe tu, Erica aliamka ila mwili
wake ulikuwa umechoka sana, mamake akampa ushauri, “Nenda kaoge mwanangu
upate nguvu, sijui nini kimekukuta, sijui nini kimekukumba lakini najisikia
imani, nenda kaoge tena upate nguvu mwanangu” Erica alinyanyuka na
kwenda tena kuoga kisha mamake akaenda nae mezani na kumuwekea supu na chakula
ili ale, na kweli alikula kamavile hajawahi kula chakula, mama yake alikuwa
akimuangalia tu mwanae anavyofakamia chakula, alipomaliza alikuwa na nguvu sasa,
mama yake alikaa nae na kuzungumza nae, “Eeeeh mwenzetu, kimekusibu
kipi?” Erica alitoa tena machozi ila mama yake alimbembeleza na
kumwambia kuwa amwambie ukweli wote ilivyokuwa, “Mama, jana niliamua
kumueleza ukweli Erick kwamba mtoto nimezaa na Rahim, kumbe Erick na Rahim
wanafahamiana, huwezi amini mama Erick amechukia sana na amediriki hadi kuniacha
hotelini ikiwa bado hajalipia chakula” “Sikuelewi mwanangu, hebu
nieleweshe” Erica akamueleza mama yake alichofanyiwa hotelini, jinsi
walivyomuoshesha vyombo na jinsi alivyowasiliana na Bahati kwenda
kumchukua, “Hivi ni ya kweli hayo? Yani Erick akuache
wewe!” “Kweli mama, tena bora angeniacha sehemu nzuri kuliko
kunidhalilisha vile” “Amakweli mapenzi hayana dhamana, kila siku
nakwambia mwanaume sio ndugu yako ila hunielewi mwanangu, na leo nakuongezea
lingine, mapenzi hayana dhamana, usimuamini mtu kupitiliza kwani mtu anaweza
kukugeuka kwa muda mfupi tu na usijielewe, mapenzi ni kitu kingine
kabisa” “Ila mama nakumbuka uliniambia ukweli humuweka mtu huru, ukweli
ndio mzuri ila mbona mimi nimepata majanga kwa kusema ukweli?” “Erica
mwanangu, nishawahi kukwambia unaposema ukweli angalia ni ukweli kuhusu nini na
mazingira gani unasema huo ukweli, yani ukweli mwingine kabla hujasema
jifikirire kwanza wewe ukiwa Yule mtu utachukua maamuzi gani, je ulikuwa unajua
kama Rahim na Erick wanafahamiana?” “Nilikuwa sijui mama ila nikajua
siku ile uwanja wa ndege maana niliwaona wote nikajificha” “Je
ulimuuliza Erick kuwa anafahamiana vipi na Rahim?” “Nilimuuliza mama na
akasema ni rafiki yake” “Ooooh kama ni rafiki yake basi kuna siri nyingi
sana wanafichiana, sasa mwanangu kwa mazingira hayo ungeniambia hata mimi
nimwambie huyo Erick ukweli hata kama kupaniki angepanikia hapa nyumbani kuliko
kukudhalilisha hivyo mwanangu, kuna watu sio waelewa yani huyu Erick anafanya
nae nianze kumchukia loh!” “Ndio hivyo mama, mwanao nimedhalilika sana
ten asana, kwakweli alichonifanyia Erick siwezi kukisahau” “Basi
mwanangu tulia yaishe” Basi mama Erica akachukua simu yake na kujaribu
kumpigia Erick ila iliita tu bila ya kupokelewa , kwahiyo akahisi huenda ana
mambo yake ndiomana hata simu yake hapokei, basi yeye akaendelea tu kuongea na
mwanae na kumpa nguvu. Jioni ya siku hiyo, mama Erica alitoka
kidogo na kumuacha mwanae nyumbani, muda kidogo alikuja mgeni na kugonga mlango,
Erica alipoenda kufungua alikuwa ni Tumaini hata akamshangaa kuwa siku hiyo
kafata nini kwao, Tumaini bila salamu alimuuliza Erica, “Mama
yupo?” “Mama yangu wa nini?” “Nimekuuliza tu yupo?
Nijibu” “Hayupo katoka” Erica akashtukia kapigwa kibao, cha
kwanza na cha pili kwakweli Erica hakumuelewa kabisa Tumaini kumbe aliulizia
kuhusu uwepo wa mama yake Erica ili aweze kumpiga Erica, aliamua
kumuuliza, “Haya umenipiga, umenipigia nini sasa?” “Unaona
ulichomtendea kaka yangu ni sahihi? Umefanya kajifungia ndani na kusema Erica
Erica, umekuwa nani wewe katika jamii?” “Tumaini naomba uondoke maana
nisije kuongea maneno mengine ya karaha ukashindwa kuvumilia hapa, naomba
uondoke” “Hebu ongea hayo maneno yako ya karaha nikusikie” “Hivi
wewe Tumaini una nini na mimi lakini? Kama unamtaka kaka yako si ukatembee
nae” “Unasemaje wewe” Tumaini akataka kumvaa Erica ila akatokea
Bahati na kuingia katikati yao, alishangaa sana kuona ule ugomvi na akamuuliza
Erica kuwa kuna nini, ila Erica alijibu kwa kujiamini, “Namshangaa huyu
dada, toka nipo na kaka yake kutwa kufatilia maisha yangu, sijui haridhishwi
huko kwingine! Kama unamtaka kaka yako kamchukue uone laana
itakavyokufatilia” Kwakweli Tumaini alifura hasira kitendo ambacho
Bahati aliamua kumuingiza Erica ndani na kumwambia Tumaini aondoke kisha yeye
kuingia ndani, akaanza kuongea na Erica, “Kwanini uwe na mwanaume ambaye
ndugu zake wanakunyanyasa hivi wakati mimi nipo!” “Usinichekeshe na
wewe, ndugu zako si ndio ukoo mzima hawanitaki sasa hiyo wewe upo ndio
nini?” “Erica, mimi nipo tayari kwa chochote hata ukitaka leo hii naenda
kumuacha Yule mwanamke wala simpendi wala nini, nakupenda wewe Erica, naomba
ukubali nikuoe” “Bahati ushachelewa, Yule mwenyewe nilikuwa namjibu tu
ila kwasasa sitaki mahusiano ya aina yoyote bora niwe mwenyewe tu, sitaki
mwanaume yeyote, nitalea mwanangu tu” “Erica usiseme hivyo wakati mimi
nipo na ninakupenda sana, Erica nilishasema hata dunia nzima iseme kuwa wewe
malaya na unajiuza ila mimi nitaendelea kukupenda tu. Maana nimefundishwa
kupenda na si kitu kingine, nitakupenda maisha yangu yote” “Asante
Bahati ila kwasasa hapana, mimi na wewe tubaki tu marafiki au
ndugu” Basi Bahati alikuwa akijitahidi pale kusema ya moyoni mwake ila
ilikuwa ngumu sana kueleweka kwa Erica. Muda huu mke wa Bahati
alikuwa na mawazo sana ya jambo la kufanya aliamua kumpigia simu Salma ili
ajaribu kumshirikisha anachowaza, “Salma ndugu yangu mwenzio nimefikiria
nimeona tukingoja mpaka arobaini iishe tutakuwa tumeumia sana, huyu Erica ni ana
nitesa vilivyo” “Eeeeh kafanyaje tena?” “Hebu fikiria nimetoka
kujifungua ila mume hanijali wala nini yani, hataki ndugu zangu waje kuniuguza
hapa wala ndugu zake anasema nikitaka kuuguzwa niende ila sio ndugu kuja hapa,
na mimi siwezi kuiach nyumba yangu nimeamua kuvumilia tu, jamani jana tumerudi
nyumbani hata sikuwa na raha muda kidogo simu, sijui Erica anapiga, mwanaume
anahaha huku na kule, muda kidogo simu sijui Erica anataka nini, nikaamua
kuficha simu bafuni, ndugu yangu alivyogundua nimeficha simu, nimepigwaje? Yani
nimepigwa hatari na tangu aondoke hiyo alfajiri hajarudi hadi muda huu, hebu
fikiria mume wa mtu kweli anafanya hivi jamani!” “Sikia Nasma, mimi
niliongea na Yule mmama akasema kuna dawa sijui ya kumfunga mume ila kwa upande
wangu huyu mume wangu sijui kama atafungika jamani, na ndugu zake wakijua
nimemfunga yani wataniharibu maana hapa naishi kwao tena sababu ya mama mkwe ana
roho nzuri, sasa sijui tufanyeje?” “Mimi nina wazo Salma” “Wazo
gani?” “Tumfanye Erica kuwa chizi, yani wote watamkimbia, huyo mumeo
atamkimbia na Bahati wangu atamkimbia, yani awe chizi kabisa abaki kuhangaika na
familia yake” “Mmmh hilo swala zuri, ila inawezekanaje?” “Kuna
mtaalamu namfahamu yani kinachotakiwa ni kupata majina matatu ya Erica basi kazi
imeisha, sasa sijui hayo majina tuitayapata wapi maana mimi hata kumuuliza mume
wangu siwezi, nitapigwa hadi nishangae” “Hiyo sio kazi kwangu, nina
shemeji yangu ana undugu na Erica yani yeye ndio atanitajia majina matatu ya
Erica hata usiwe na shaka. Nakwambia huyo Erica habari yake imekwisha maana
akiwa kichaa nani tena atamtaka?” “Hakuna, yani tutamkomesha. Basi
nakutegemea, tufanye haraka maji ya shingo yamenifika dhoga
yangu” “Aaaah usijali, ndani ya siku mbili hizi atakuja tu Yule shemeji
kuniona nitakupa majina ya Erica sio kazi kuyapata” Basi walifurahia na
kupongezana kwa ajenda yao. Usiku mama Erica alirudi na Bahati
akaondoka, kwahiyo Erica akaongea ongea na mama yake na kumwambia maamuzi yake
aliyoamua kuwa hataki tena kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi, basi
wakaongea na kwenda kulala. Kabla ya kulala Erica alipigiwa simu na
Derick akaipokea simu ile, “Erica, dada yangu kipenzi
nimekumiss” “Asante” “Mmmh erica, hata kusema nimekumiss pia
jamani hakuna” Erica alicheka tu na kumuuliza, “Haya niambie
kilichofanya unipigie usiku usiku huu” “Kwani kuna ubaya ndugu kwa ndugu
kupigiana simu?” “Hakuna ubaya ila undugu wako wewe nina mashaka nao,
haiwezekani ukawa na mawazo finyu kama unayokuwaga nayo” “Jamani Erica,
basi tuachane na hayo, ila naomba tuonane nina maongezi na wewe” “Njoo
tuongee nyumbani kwetu, kwakweli siji popote utakaposema nije” “Mbona
una roho mbaya hivyo Erica?” “Nadhani huna cha kuongea na mimi,
kwaheri” Erica akakata ile simu na kulala zake kwani hakutaka kujiumiza
kichwa kwa wakati huo. Kulipokucha aliamka mapema kabisa na kujinyoosha
mwili katika kazi za hapa na pale, akapigiwa simu na Fetty na kuanza kuongea
nae, “Shoga yangu nina shida, nina shida, nina shida” “Shida
gani tena?” “Nina shida ya laki tatu, naomba unikopeshe
tafadhari” Erica akakaa kimya kwa muda na kuwaza zile hela alizozituma
kwa Dora, maana zingekuwepo kwake basi asingeshindwa kumtumia Fetty, na
kumwambia hana aliona sio swala zuri sababu alishamwambia mwanae amekuwa balozi
kwahiyo lazima ahisiwe kuwa na hela, akamwambia “Fetty, subiri kidogo
kuna mahali nikuulizie halafu nitakutaarifu” “Nashukuru sana ndugu
yangu, nashukuru kwa kunusitiri” Basi simu ile ilivyokatika, Erica
akapata wazo la kumpigia simu Dora ili amuombe hela kidogo, alipiga iliita hadi
kukatika, akapiga tena hivyo hivyo, akapiga tena ndio Dora akapokea na alikuwa
akiongea sauti ya usingizi kabisa, “Kheeee Dora, inaenda saa nne hii
hujaamka?” “Niamke mapema nina shida gani? Wenye shida ndio wanaamka
mapema ila sio sisi wenye raha zetu” “Mmmmh mna raha ya
nini?” “Raha ya kila kitu maana dunia ya sasa kuwa na hela ndio kila
kitu, unaenda unapotaka, unafanya unachotaka, unakula unachotaka, kwahiyo acha
niburudike mie.” “Mmmmh hujampa mzee Jimmy zile pesa?” “Nimpe
nina wazimu?” “Si ulisema bora nikupe wewe” “Ndio bora unipe
mimi nitumie, Erica Yule mzee kashanitumia sana nishampa mapenzi sana ila hakuna
nilichoambulia kwake zaidi ya vilaki laki halafu wewe usiyempa chochote ndio
anakujazia mavitu, kwakweli roho iliniuma yani kazi nifanye mimi na faida upate
wewe, kwahiyo hii ni haki yangu hata mzee Jimmy akifanya chochote hakitanipata
maana hii ni haki yangu” “Ila wewe jamani, si ulisema lengo la mzee
Jimmy ni bay asana?” “Ila wewe Erica hujiongezi! Huna huruma wewe, yani
matatizo yote niliyokwambia ninayo sababu ya mzee Jimmy ila bado ukataka ule
hela yake usiyoitolea jasho! Nimeenyeka mwenzio, nimekukuruka ach anile matunda
ya kazi yangu, jana na juzi nilikuwa kwenye starehe tu ndiomana nimeamka na
uchovu” “Haya bhana ila nisaidie kitu, mwenzio sina hela yoyote yani
hakuna kitu mfukoni kwangu, naomba unisaidie laki tatu” “Shoga yangu
laki tatu tu, sio kitu kwangu nitakupa ila tukutane kesho mahali nikupatie maana
kuna jambo nahitaji kuongea nawe” “Sawa hakuna tatizo kwahiyo muda
gani?” “Iwe kwenye saa kumi kumi Erica wangu sawa mama eeeh! Ninakupenda
shoga yangu uuuh yani ushoga wetu hudumu daima” “Sawa bhana maana mimi
mjinga kukupa wewe hela zote” “Hata sio mjinga shoga yangu umefanya cha
maana sababu ulijiona hustahili kumiliki hizi pesa, sasa ni mimi ndio nastahili
kuwa nazo ndiomana ukanipatia, acha mwenzio nijifute jasho kwa kazi niliyoifanya
siku zote hizi kwa Yule mzee” Erica aliongea ongea nae na kukata simu
ila alijiona ni mjinga sana kumkabidhi pesa Dora ila kwa upande mwingine aliona
acha tu atumie aliyezihangaikia. Akampigia simu Fetty na kumuahidi
kuipata hiyo pesa kesho kutwa, na Fetty alimshukuru sana maana alikuwa na shida
haswaaa na ile pesa. Basi jioni yake Erica alipigiwa simu na
Erick kwa hakika hakutaka kuipokea na kuifanya iite mara nyingi nyingi bila ya
kuipokea hadi Erick alipopiga simu kwa mara ya tatu ndipo Erica alipokea ile
simu na akamwambia, “Ongea kilichokupigisha simu” “Usiwe mkali
hivyo Erica, hujui ni kitu gani kimetokea?” “Kitu gani kunidhalilisha
vile? Hivi Erick una akili kweli, mwanamke unayempenda unaweza kumdhalilisha
kiasi kile? Erick sikutaki tena kuanzia leo” “Erica usiseme hivyo
kumbuka mimi na wewe tuna mtoto” “Tuna mtoto kitu gani? Ungetambua hilo
ungenidhalilisha kiasi kile kwenye ile hoteli? Ungefanya mimi nionshe vyombo
usiku kucha? Kwakweli Erick nakuchukia yani nakuchukia haswaa” Erica
akakata simu ila kiukweli yale yote alikuwa akiongea kwa hasira tu kwani moyo
wake ulijaa habari za Erick tu nay eye peke yake aliyekuwa anampenda, alitamani
muda wote Erick ampigie simu kumuomba msamaha ila mpaka usiku unaingia na
kulala, Erick hakupiga simu tena yani kitu hiko kilimuuma moyo zaidi na
kujisemea, “Hivi kwanini wanaume wana roho mbaya hivi? Ndio huyu
aliyekuwa anasifiwa kuwa anajua sana kubembeleza jamani? Mbona hamna kitu
chochote maana sioni kubembelezwa wala nini jamani, aaah Erick
hanipendi” Akawaza sana na kukosa raha kabisa, hadi analala na kuamka
asubuhi hakupata simu yoyote ya Erick zaidi ya kumpigia simu Dora ili ajue ni
wapi atakutana nae kwa siku hiyo kama walivyopanga. Mchana wa
siku hiyo Erica aliamua kumshirikisha mama yake ambayo aliongea na Rehema
alipokutana nae, “Mama nilikutana na Da Rehema kasema Da Bite kakonda
sana hadi amemuonea huruma” “Jamani watoto wangu sijui mna matatizo gani
jamani, hivi Bite anaacha kuja nyumbani hapa kunieleza shida zake mpaka
anaonekana na watu huko kuwa ana matatizo jamani!” “Yani Da Rehema
kaniambia siku akipata muda atakuja ili muongee vizuri maana hali ya Da Bite
imemshtua sana” Kwakweli mamake hakuweza kuvumilia zaidi akaamua
kumpigia simu Bite ili kujua tatizo ni nini, akampigia na kumsalimia kisha
kumuuliza, “Mnaendeleaje Bite?” “Salama mama, tunaendelea
vizuri” “Kila siku nikikupigia simu ni swala hilo hilo la kuendelea
vizuri, hivi Bite mwanangu una matatizo gani? Hutaki kuja nyumbani, ndio
ulichukia ujinga aliofanya mumeo? Huyo mumeo tunajua mambo yake kwahiyo hata
habari zake zisikuogopeshe kuja nyumbani, kwanza niambie tatizo ni nini,
usinifiche mimi ni mama yako” “Mama, ni bora hata ningekuwa mwanamke
malaya yani ni bora ningekuwa hivyo kuliko ninachofanyiwa na huyu mwanaume
jamani, mama huyu mwanaume ananitesa tena sio kwa kipigo ila ananitesa
kisaikolojia, mama hadi nachanganyikiwa” “Vipi ni kuhangaika na wanawake
tena au?” “Ndio hiyo tabia hajaacha wala nini mama, halafu
kinachoniumiza zaidi nimeanza kuumwa na ugonjwa wa ajabu” “Ugonjwa gani
huo?” “Nimeenda kupima, wameniambia nina ugonjwa wa kansa ya shingo ya
kizazi, mama ugonjwa huu husababushwa na ngono yani mwanaume anautoa kwa
mwanamke mwingine na kuuleta kwa mwanamke wake, yeye hadhuriki ila mwanamke ndio
nadhurika, jamani huyu James kwanini anataka kuniua jamani kosa langu
nini” “Bite, akili zako zifanye kazi, kwani ugonjwa huo hautibiki?
Utapona tu mwanangu, ila rudi nyumbani, kwanza una uwezo wa kuishi maisha yako
mwenyewe cha msingi kuwa na msimamo tu kuwa umeondoka na haurudi tena,
asikubabaishe James bhana, mtu alitaka hadi kumbaka mdogo wako, ni mtu huyo
kweli? Kwakweli mwanangu ni muda wa kufanya mabadiliko huu, usikubali kuumizwa
kiasi hiko” “Sawa mama nimekuelewa” Basi pale mama Erica
aliongea ongea na mwanae maneno ya kumpa moyo kwa kile alichomwambia kuwa
asijihisi vibaya, awe kawaida tu na achukulie ni ugonjwa wa kawaida usimpe
presha sana. Salma alimpigia simu Nasma na kuongea
nae, “Nimepata majina matatu ya Yule mtu” “Eeeeh
nitajie” “Nakutumia kwenye ujumbe, unajua nimetumia ujanja gani
kuipata?” “Eeeeh niambie umetumia ujanja gani?” “Basi bhana Yule
shemeji yangu nikaongea nae kuhusu majina akaniuliza kwani vipi, sikutaka
kumwambia ukweli ila akasisitiza nimwambie ikabidi nimwambie kumbe nae ana
ugomvi na huyo mwanamke tena kaniambia ndio vizuri tena umfanye chizi kabisa
aokote makopo yani asijitambue” “Sawa sawa, yani mimi ninapoipeleka kazi
wala sio sehemu ya kugushi ndani ya wiki hii hii utasikia matokeo” Mara
Bahati akatokea na kumkuta mkewe akiongea na ile simu akamuuliza kwa makini kuwa
anaongelea kuhusu nini, “Hamna kitu mme wangu” “Unajua nyie
wanawake mkipigwa mnasema mmeonewa, hivi mwanamke umempata mwanaume kwa
ushirikina hivi unawezaje kujisifia kuwa huyu mwanaume ni wangu? Kwanini
unashangaa nikimtaka nimpendaye? Halafu simu unayoongea nayo hapo ni ushirikina
mtupu, unajua najuta kukuoa Nasma, yani hata kama ndugu hawakumtaka Erica basi
wangenizesha hata kwa Sakina Yule dada katulia ila sio wewe, yani hapo ulipo
unanuka ushirikina tu” “Hamna mume wangu sifanyi ushirikina
wowote” “Yani Nasma nikigundua kuna ujinga wowote unafanya utaondoka
huku unatambaa nakwambia, na kwa taarifa yako hata Erica agome kuolewa na mimi
basi wewe nitakuolea hata wake sita maana siwezi kuishi na mwanamke mshirikina
kama wewe” Nasma alikaa kimya tu ila bado wazo lake la kumfanya Erica
kuwa kichaa lilikuwa kichwani ingawa mumewe kamtishia kwahiyo wazo hilo lilikuwa
likimjia na kumtoka. Wakati Erica anajiandaa huku akingoja simu
ya Dora kuwa wakutane wapi, akapigiwa simu na Erick, kwa muda huu hakuweza
kujizuia kutokuipokea kwani alikuwa akiacha kuipokea anaumia moyo sana, akaanza
kuongea nae, Erick alimuomba waongee kwahiyo Erica alimwambia sehemu anayoenda
kukutana na rafiki yake, “Huyo rafiki yako ni muhimu sana hadi unakutana
nae?” “Ndio ni wa muhimu sana, ni rafiki yangu mkubwa” “Sawa, na
mimi sipo maeneo ya mbali na sehemu hiyo, ukifika basi utanikuta” “Sawa,
hakuna tatizo” Erica alimaliza kujiandaa kisha akamuaga mama yake na
kuondoka zake, alifika kwenye ile hoteli na kumkuta rafiki yake Dora ameshafika
kwahiyo walikaa nae na kuanza kuongea nae, “Erica, kabla ya yote jamani
nimekutana na mkaka mmoja hapo nje huwa namfahamu fahamu jamani ila sina mazoea
nae, Yule kaka ni mzuri, sijategemea leo kumuona, mkaka ni mzuri Yule nilitamani
hata nikambusu ila sijamzoea halafu hanipendagi” “Dora nawe, hakupendagi
kwani anakufahamu?” “Ananifahamu ndio na ndiomana siwezi kuwa nae karibu
ila nampenda balaa, natamani angekuwa wangu, mkaka Yule ni mzuri” “Mmmh
Dora tuachane na habari hizo, hebu tuongee ya kwetu bhana” Muda kidogo
Erica akapigiwa simu na mpigaji alikuwa Erick, ilibidi Erica amuelekeze
walipokaa ili aende hapo. Basi akakata simu na kuendelea kuongea na
Dora, “Sasa Erica, ninachotaka kuongea nawe ni kuhusu shemeji yako
James” “Kafanyaje tena shemeji yangu James?” Gafla akamwambia
Erica ageuke nyuma, “Wow, Erica geuka nyuma Yule mkaka mzuri nilikwambia
anakuja kwenye meza yetu sijui ananifata!” Erica akageuka na kumuona
anayekuja ni Erick, kwakweli alimuona rafiki yake Dora anatamaa sana, Erick
alifika pale ila kabla ya salamu alimuuliza Erica kwa mshangao huku
akimuonyeshea Dora, “Yani Erica, huyu ndio rafiki
yako!” Gafla akamwambia Erica ageuke
nyuma, “Wow, Erica geuka nyuma Yule mkaka mzuri nilikwambia anakuja
kwenye meza yetu sijui ananifata!” Erica akageuka na kumuona anayekuja
ni Erick, kwakweli alimuona rafiki yake Dora anatamaa sana, Erick alifika pale
ila kabla ya salamu alimuuliza Erica kwa mshangao huku akimuonyeshea
Dora, “Yani Erica, huyu ndio rafiki yako!” Erica alikuwa kimya
tu kwani hakuelewa toka mwanzo kuwa mwanaume aliyekuwa anasemwa na Dora ni
Erick, ila pale pale kabla hajajibu Dora akasema, “Kheee Erica huyu kaka
mzuri kumbe ndio mpnzi wako!” Erick alimuangalia Erica bila hata kucheka
na kumtaka waondoke, sasa Erica hakuwa na maamuzi zaidi ya kufata kile
anachokisema Erick kwahiyo ilibidi ainuke na kuanza kufatana na erick, kwakweli
Dora alimshangaa Erica na kumwambia, “Kwahiyo ile hela hutaki
tena?” Kiukweli hela alikuwa anataka lakini wakati huo huo hakutaka
kumkera Erick, alitoka nae hadi nje na kupanda gari ya Erick ambapo kwenye gari
Erick alianza kuongea, “Unajua Erica muda mwingine mwanaume anampiga
mwanamke sio kwasababu huyo mwanaume anapenda kupiga, hapana ila ni sababu ya
vitendo vya huyo mwanamke. Hivi Erica Yule ndio rafiki yako
kweli?” “Ngoja nikueleze ukweli kuhusu Yule mtu” “Haya
nieleze” Erica alimueleza Erick jinsi alivyokuwa na urafiki na Dora
wakati yupo chuo ila akamueleza jinsi alivyoacha urafiki nae, alimwambia ni
sababu ya kumsingizia maneno ya uongo ila hakusema tatizo kubwa kuwa lilikuwa ni
George, alimueleza na jinsi kaka yake alivyotaka kumuoa na yeye
alivyokataa, “Erick naelewa kabisa kama Dora hana tabia nzuri ila nipo
nae karibu kipindi hiki si sababu ni rafiki yangu bali kuna rafiki yangu
mwingine alinituma kuchukua hela kwa Dora” “Na mbona uliniambia mimi ni
rafiki yako?” “Nimekosea kusema hilo sababu sikujua niseme kitu gani ila
Erick najua umetafuta sababu tu, hivi unadhani ulichofanya kwangu siku ile ni
sawa? Kuniacha mimi bila kulipa hoteli? Kuniacha nioshe vyombo? Unafikiri ni
sawa, wewe mwenyewe ulisema kuwa tusahau yote yaliyopita, nilikwambia ukweli
kuwa nina mtoto ukakubali, na sasa nikakwambia baba wa huyo mtoto halafu
unathubutu kuniacha hotelini kweli?” “Erica, nilikuwa na hasira sana
kumbuka nakupenda” “Hata kama unanipenda ndio kunifanyia vile
kweli?” “Erica, niliumia sana umeacha kunipa mimi mapenzi umeenda kumpa
Rahim kweli? Nimerudi na kukwambia kuwa mpenzi wangu nina hamu ila ukanipa
kisingizio kuwa upo kwenye siku zako, na Rahim umeenda kumpa” “Erick,
sijawahi kutembea na mwanaume yeyote toka nijifungue, mimi sio kichaa wa kusema
nibadili mwanaume huyu mara huyu, nina akili zangu timamu mimi. Nilisema
yaliyopita ilikuwa zama za ujinga, nilihisi ndio njia ya kupanda penzi la kweli,
sasa nimejua ukweli nianza tena kutembea na wanaume jamani! Huyo Rahim ni
muongo” “Basi kama muongo naomba unipatie haki yangu” “Haki
gani?” “Unajifanya huelewi Erica jamani? Si nilikwambia nina hamu,
nahitaji mapenzi” “Hapana Erick, mimi nilikuwa nataka tufanye hadi
ndoa” “Hahaha usinichekeshe Erica, hivi siku hizi ni nani anayengoja
ndoa? Hamu ipo muda wote kweli mtu utasubiria ndoa? Siku hizi hata mwanamke
bikra anajaribishwa kabla ya ndoa sembuse wewe Erica ambaye ushazaa jamani! Hata
hivyo kwani mimi na wewe ni mara ya kwanza kufanya? Hebu usinifanyie hivyo
mwenzio, naomba haki yangu Erica tafadhali, mimi ni mpenzi wako niende wapi
tena?” “Sawa hakuna tatizo, ila naomba jambo moja” “Hayo ndio
maneno sasa, haya jambo gani?” “Naomba tukapime” “Kwahiyo Erica
huniamini? Yani kipindi chote hiko huniamini?” “Usipaniki Erick maisha
yamebadilika sana, nasema tukapike sababu ya kukuokoa wewe na kujiokoa na mimi,
kumbuka…..” “Basi usiendelee kusema, tumalize mjadala, kesho nakuja
kukuchukua tukapime” “Basi fanya kesho kutwa maana kesho
haitawezekana” Erica alikumbuka ahadi aliyotoa kwa Fetty kwahiyo alitaka
aitumie siku ya kesho kutimiza ahadi yake kwa Fetty, ila Erick
akamuuliza “Kwanini haiwezekani?” Erica akawa anajiuma uma kisha
Erick akaongea, “Ooooh nimekumbuka kitu, ngoja kesho nikafatilie tena
ile gari bandarini unajua Erica ulinichanganya sana siku ile, basi kesho
nitaenda kufatilia mwenyewe halafu keshokutwa twende tukapime” “Sawa
hakuna tatizo” “Halafu tukitoka hapo tunaenda
kufanya” “Mmmmh!” “Usigune, ujue mimi na mwanaume na wewe ni
mwanamke tumetofautiana maumbile, ukinibania mimi unataka niende
wapi?” Erica alikaa kimya tu na kumuomba kuwa anataka kurudi nyumbani,
wakati huo hata ile laki tatu kwa Dora hajaipata na hajaweza kusikiliza kuwa ni
nini Dora alimuitia kuhusu shemeji yake, na pia aliogopa kumuomba Erick hiyo
hela maana alikuwa anataka Erick ampe mwenyewe na sio amuombe, kwahiyo Erick
akageuza gari na kuanza safari ya kwenda kwakina Erica huku akimpapasa
papasa, “Mmmh Erick usifanye hivyo bhana, tupo barabarani
ujue” “Hata barabara inaelewa ni jinsi gani nakupenda” Erica
hakupenda kushikwa vile maana alikuwa akipatab msisimko na hakuutaka huo
msisimko sababu alihisi ungechochea kufanya mapenzi kitu ambacho hakukitaka kwa
wakati huo. Walifika nyumbani kwakina Erica, na kabla Erica
hajashuka Erick aliomba kuongea nae tena kidogo, “Usijifikirie vibaya
mimi kushangaa urafiki wako na Yule msichana, Yule msichana labda hanifahamu
vizuri ila mimi namfahamu vizuri sana sana, Yule msichana hana tofauti na
changudoa kwa kifupi Yule msichana hafai, yani anawafata wanaume kwaajili ya
pesa, ile sio aina ya kuwa na urafiki nao Erica, wewe ni msichana unayejielewa,
unayejithamini, unayevutia usianze kuzunguka nay ale makorokoro, sawa mama
eeeh!” “Sawa nimekuelewa” “Halafu kitu kingine nakupenda sana,
siwezi kuingia ndani kwenu maana kama umemwambia mama yako sijui nitaweka wapi
sura yangu, ila keshokutwa nikija kukuchukua lazima nije nionane na
mama” “Sawa hakuna tatizo” Kisha Erick akashuka na kumfungulia
Erica mlango wa gari akambusu na kumuaga, halafu Erica akaingia ndani kwao ila
akiwa na mawazo sana kuwa hiyo laki tatu aliyomuahidi Fetty atampaje mpaje,
akaingia ndani tu na kumsalimia mama yake kisha kwenda chumbani kwake,
alijisemea, “Sisi wasichana kitu kinachotusumbua sana ni hela, unakuwa
na mpenzi kama Erick unajua kabisa hela anayo ila hakupi na ukiomba atauliza ya
kazi gani yani hapo ndio panakuwa pagumu! Nilianguka kwa Rahim sababu alikuwa
mtoaji sana kwangu, alikuwa akinihonga sana ila sikujua kisa na mkasa cha
kuhongwa vile na mwisho wa siku nimeambulia maumivu, hivi kweli Erick anaweza
kutoa milioni tano kwaajili ya mimi kulipa deni anauwezo wa kutoa pesa kwaajili
ya kuninunulia gari, anashindwaje kutoa pesa kwaajili ya matumizi
yangu?” Erica alijiuliza sana ila alipotulia tulia aliamua kumpigia simu
Dora ili kujaribu kuongea nae kuhusu ile hela aliyomuomba, “Yani Erica
ukaacha kunisikiliza mimi sababu ya Yule, hajakupa
hela?” “Hajanipa?” “Halafu mjinga ana hela kweli Yule sema
bahiri tu ndio tatizo lake” “Unajua sana eeeh!” “Namfahamu ndio
ila Erica hongera, umepata mwanaume mzuri balaa hadi natamani kama angekuwa
wangu” “Basi tuachane na hayo mambo, vipi kuhusu hela?” “Erica,
nilitaka kukupa hela ya kuonana kabisa ila hela ya kutuma hapana, labda
nikutumie laki” “Mmmmh Dora wewe” “Ndio, kubali tu nikutumie
laki” “Sawa basi nitumie hata hiyo” “Halafu unajua jana
ulivyoniacha pale nini kilitokea?” “Aaah Dora, usiniletee habari zingine
bhana, nitumie hiyo laki” “Basi ngoja nikutumie” Erica alikata
simu akisubiri kutumiwa hiyo laki maana hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali hiyo
hiyo huku akiwaza mahali pa kumtafutia Fetty laki mbili maana katika marafiki
zake alimuona Fetty kuwa rafiki mwema kwake ingawa kuna vichache anampeleka sipo
ila kwa kiasi Fulani aliona kuwa ni mwema na anakila sababu ya
kumsaidia. Alivyomaliza kuongea na Dora alipigiwa simu na Erick na
kuongea nae tena Erica hakuongea nae kwa raha kwani alikuwa na shida na hela
halafu kumwambia hakuweza, “Erica nakupenda sana” “Nashukuru kwa
kunipenda ila Erick sina kazi ujue?” “Najua mpenzi wangu, nilikwambia
hilo hata lisikupe shida nitakutafutia cha kufanya yani kuwa na amani
tu” Erica alikuwa akichukia kwani alitamani aulizwe hela unayo aseme
sina ili aweze kupewa hela anayoitaka, hakutaka kutoa hela za kwenye akaunti ya
mwanae kwani hakutaka kuendelea kuimaliza akaunti hiyo ukizingatia hela nyingi
anazozitumia ni kutoka kwa mwanae, kwahiyo aliendelea tu kuongea na Erick haku
akicheka ila hakuwa na furaha wala nini, hadi wanaagana na kulala bado hakuwa na
furaha sababu Erick hakuweza kujiongeza kumpatia hitaji
lake. Kulipokucha bado alikuwa akiwaza kuwa hiyo hela ataipata wapi
aweze kumsaidia Fetty, akapata tena wazo la kumpigia Bahati, kwahiyo akampigia
Bahati na kuanza kuongea nae, “Nina shida na hela
mwenzio” “Unataka kama pesa ngapi?” “Nina shida na laki
mbili” “Mmmmh kwani Erica una tatizo gani mpenzi wangu? Ila usijali,
ngoja niende nikaangalie mahali nikutumie” “Sawa, nashukuru sana
Bahati” Kwakweli kwa Bahati ilikuwa ni afadhali yake kwani Bahati ingawa
hakuwa na hela nyingi lakini alikuwa hodari sana wa kumsikiliza Erica ana
mahitaji gani, na kwa upande wa Erica ilikuwa rahisi sana kwake kumuomba hela
Bahati kuliko mtu mwingine yoyote, alishukuru sababu alijua ni lazima Bahati
angemtumia kama alivyoahidi. Nyumbani kwa Bahati, mkewe
alimuona vizuri Bahati akiongea na Erica ile asubuhi kuhusu maswala ya hela,
kiukweli hakupendezewa na swala lile hata kidogo na chuki kwake dhidi ya Erica
ikaongezeka, basi Bahati alivyotoka tu yeye naye akamuandaa mtoto na kutoka naye
bila kujali kuwa bado ni mdogo sana, kwa muda huo aliona ni vyema afanikishe
mambo ya ndoa yake kwanza. Alifika kwa babake ili aongee nae, babake
alisikitika sana kuona mwanae akitembea mwenyewe na kichanga, Nasma aliamua
kumueleza babake kila kitu na jinsi Bahati alivyobadilika asivyotaka ndugu
yeyote kufika nyumbani kwake, “Pole mwanangu” “Baba, mmeniozesha
kwa mtu mwenye tabia za ajabu sana, kwakweli nateseka baba yangu” “Pole
sana mwanangu, lakini kwanini anafanya hivyo?” “Sina raha na ndoa yangu
baba, yani kila muda ni Erica tu, tukilala tukiamka ni Erica jamani hakuna hata
amani baba, sasa leo asubuhi kaongea tena na erica, jamani Bahati ameondoka pale
nyumbani haihai ndio sijui anaenda kumtafutia hela huyo Erica, baba natamani
tufanye kitu juu ya Erica ili kukomesha tabia ya wanawake kama wale wanaopenda
kutembea na waume za watu” “Kwahiyo tufanyeje mwanangu?” “Nataka
Erica awe kichaa baba yangu, yani awe chizi kabisa” “Unayajua majina
yake matatu ndio” “Ndio, kuna mtu kanitumia” “Basi hiyo kazi
rahisi” “Yani sina raha baba yangu kila kitu nikishika ndani nambiwa
hiko cha Erica, nyumba eti ya Erica, kitanda sijui jiko, makochi, tv vyote
naambiwa vya Erica, sina raha baba” “Usijali mwanangu, kazi rahisi sana
hapa, huyo Erica atajuta kufahamu ukoo wetu. Kesho nitafanyia kazi hili swala
hata usiwe na mashaka mwanangu Nasma” “Sawa, baba ngoja nirudi nyumbani
kwangu” “Aaaah usirudi, yani naanza nay eye, atakuja kukuchukua mwenyewe
hapa na safari hii utaenda na dadako kumuhudumia mtoto na Yule mumeo tutamkoroga
zaidi ya pale, yani wakati Erica anaugua uchizi na yeye hata hajui kama kuna
kiumbe anaitwa Erica katika hii dunia. Yani safari hii nitamfanyia dawa hivyo
hatoisahau, maishani mwake maana akija kushtuka anakuta Erica alishakufa kwa
uchizi huko” “Sawa baba nashukuru” Kwahiyo Nasma akasikiliza
ushauri wa babake kuwa asiende popote maana Bahati atamfata mwenyewe pale
kwao. Erica alitumiwa ile hela na Bahati kwahiyo alishukuru
sana kisha akamtumia rafiki yake Fetty ambapo Fetty nae alimshukuru sana maana
amemuonyesha upendo, “Erica nakushukuru sana kwa kuthamini shida
yangu” “Usijali tupo pamoja” “Yani sijui niseme nini, nashukuru
sana. Nitakuja kwenu wiki ijayo” “Karibua” Kisha akakata ile
simu na sasa akapata amani na kwenda kuongea na mama yake, mama yake alianza
kumsimulia kuhusu ugonjwa anaoumwa mwanae Bite, “Yani hawa wanaume
jamani hata sijui wako vipi? Kashampa mwanangu hilo gonjwa, ila nimemwambia Bite
asiwe na wasiwasi atapona tu” Wakati akiongea vile na mama yake, alifika
Mage na kuwasalimia ila mama yake alimwambia, “Mtoto mbaya wewe,
ulivyojua umefanya makosa ya kumpeleka mdogo wako kwenye matambiko huko ukaona
bora usije” “Hapana mama, ila mambo yaliingiliana” “Mambo
yaliingiliana wapi? Unashindwa kweli kuja kumsalimia mama yako sababu ya mambo
kuingiliana?” “Nisamehe mama, ila hiko sio kilichonileta” “Haya,
kimekuleta kipi?” “Jana, kulikuwa na sherehe ya rafiki yangu, kwahiyo
nilienda kwenye sherehe na mume wangu, huwezi amini mama wakati tunarudi usiku
kwa macho yangu haya nimemuona shemeji James akiwa na Dora Yule rafiki wa erica,
wakitoka guest” Mama Erica alishangaa sana, na kuuliza kwa
mshangao “Unasema!” “Ndio hivyo mama, kwakweli tumeshangaa yani
mume wangu alikuwa anasema kila siku Erica mbaya kumuumbua James ila kwa
alichokiona jana alisema amakweli James ni mchafu, tena mama bora ingekuwa
wanatoka tu ukasema hakuna kilichofanyika ila tuliwaona wakitoka na kusimama nje
huku wakinyonyana midomo” Kwakweli mama erica, alijikuta akiishiwa na la
kusema kabisa, “Mungu wangu wanafanya uchafu huo nje!” “Ndio
hivyo mama” Erica alikuwa amekaa kimya kwa muda ila yale maneno
yalimuumiza vilivyo maana Dora alishamwambia kuwa ameathirika, alijikuta
akisikitika sana na kuwaambia, “Jamani Dora aliwahi kuniambia kuwa
ameathirika” Ndio mama yao alipiga nay owe kabisa, “Uwiiii James
kaniulia mwanangu mimi jamani, hata sijui nifanyeje” Mage aliamua
kumtuliza mama yao maana ilionekana ameshachanganyikiwa, “Mama usipaniki
hivyo na wala usiongee na Bite kwa kupaniki hivyo, muite Bite uongee nae
taratibu na atakuelewa, “Jamani hivi nawezaje, huyu James huyu nimfanye
nini? Kwanini anifanyie vitu vya ajabu hivi kwa mwanangu, kampa ugonjwa wa kansa
ya shingo ya kizazi kaona hautoshi kampelekea na ukimwi kweli? Hapana
jamani” “Mama, usipaniki naomba keshokutwa nije na Bite najua haendi
kazini, nitamfata tuje hapa nyumbani na uongee nae kirafiki tu” “Je
naweza kuvumilia hadi kesho kutwa?” “Vumilia mama, nakuomba vumilia na
jipe moyo yote yanawezekana” Mage alijaribu pale kumpa moyo mama yake
hadi akakubali maana hakuweza kuvumilia yale maneno kuwa James alikuwa na
Dora. Babuu alionekana yupo na Rahim akimshauri kuhusu mtoto
aliyezaa na Erica, “Najua Rahim ndani kwenu wanaogopa kukwambia ila
hakuna kitu kibaya kama kutokuhudumia damu yako, mimi mwenyewe nilitamani sana
kuzaa na Erica ila sababu hakuchagua kuzaa na mimi simlaumu kwani sijui ni
kwanini aliamua kuzaa na wewe, basi wewe onyesha kumjali mtoto” “Ila
Babuu hujui tu, Yule mwanamke ana dharau sana, nishampa hela nyingi mno angekuwa
ni mwanamke mwingine ningemkuta na biashara kubwa sana kwasasa, na alichonikera
ni swala la kukazania ndoa na mimi wakati huku kwetu nishawekewa mke, yani Erica
ni msichana mzuri kimtazamo ila ana matatizo sana, hujui tu Babuu” “Sasa
mimi namjua Erica kushinda wewe unavyomjua, mimi ndio nilikuwa mwanaume wake wa
kwanza” Rahim hakupenda kusikia vile, yani Babuu alipenda kujisifia kuwa
mwanaume wa kwanza kwa Erica ila kila aliyemwambia alionekana kutokupenda kabisa
swala lile ingawa aliendelea kuongea, “Mimi ndio nimemfundisha erica
mapenzi” “Hebu na wewe nyamaza huko kama huna cha kuongea, muda mwingi
nilikuwa nikiwaza kuibiwa Erica ndiomana sijawahi kupata wazo la kumuoa kabisa,
tatizo ukioa mwanamke mzuri sana jua umeolea wenzio” “Hapana sio hivyo,
ila Erica hukumuelewa tu” “Nimekwambia nyamaza kama huna cha
kuongea” Mdogo wake Salma alikuwa karibu na kuwasikia wakimuongelea
Erica, kwahiyo alienda kumwambia dada yake, kitu kilichomkasirisha
zaidi. “Natamani hata huo uchizi Erica umpate hata muda huu, yani baada
ya kukaa kuzungumzia mada za maana wanakaa wakimzungumzia Erica, msichana
aliyewatia aibu kwa kutembea na ukoo mzima, namchukia Erica” Yani Salma
alikuwa na chuki za wazi wazi kabisa dhudi ya Erica. Erica
alirudi ndani na kumpigia simu Dora maana zile habari kuwa alikuwa na shemeji
yake zilimtisha kidogo, alimpigia na Dora alipokea muda ule ule, “Dora
nasikia ulikuwa na shemeji James?” “Umejuaje?” “Kuna mtu kawaona
Dora, kumbe umeanza na shemeji yangu” “Sikia Erica, Yule shemeji yako
alivyonibaka niliumia sana moyo, yani mimi katika kuhangaika kwangu kote
sikuwahi kufanya kinyume na maumbile ila Yule shemeji yako kajitia kunibaka
mbele na nyuma nab ado mahakamani akashinda kesi kuwa si yeye aliyenifanyia
vibaya ingawa ushahidi wote ulikuwepo. Tena jana nilitaka nikupe habari za
shemeji yako sema ndio hivyo ukaondoka, Erica nilikwambia mimi Yule James
akiingia kwenye kumi na nane zangu ninae maana nimedhalilika sababu yake, na
kweli kaingia kwenye kumi na nane zangu na atajuta” “Jamani Dora, si
umeathirika wewe?” “Kuathirika kitu gani? Tena ndio vizuri na yeye
aupate kwa umalaya wake, wengine tumeupata sababu ya tamaa ila sio umalaya, na
yeye aupate sababu ya umalaya wake, kwahiyo kwasasa tupo kwenye mahusiano na
shemeji yako” “Kheee Dora” “Tena sikukwambia, ana mpango wa
kunipangishia na nyumba kabisa ili tuishi kama mke na mume. Na zile hela za mzee
Jimmy ulizonipa ni kama nikapata kismati maana nilimuendea shemeji yako kwa
mtaalamu, nimemkoroga haswaaa yani kwangu hasikii wala haoni” “Kheee
Dora, sasa madawa yako kwa waganga shemeji yangu yalimpataje” “Ukiwa na
pesa katika maisha ndio kila kitu duniani, kuna dawa hiyo nilipewa, nimuwekee
kwenye tunda nikawaza ni njia gani nitatumia, nikanunua sindano nikaiweka dawa
maji nikaiingiza kwenye sindano na kuichoma, kwenye tunda la apple, shemeji yako
si malaya, nikamchombeza siku hiyo hadi akakubali kwenda na mimi kula ndipo
nikampa tunda lile akala yani ikawa kwisha habari yake, baada ya hapo
nilimualika kwetu akaja nikamuwekea dawa hiyo funga kazi ambayo lazima niitumie
kunawa kwanzq sehemu za siri ndio nimuwekee kwenye chakula, nikafanya hivyo basi
toka hapo Yule shemeji yako kama zuzu unajua hiyo dawa nimemfanyia jana asubuhi
ndio nikashangaa usiku ule kanitafuta hawezi kulala bila kuniona, nimemkomesha
shemeji yako” “Jamani Dora, ndio umemlisha shemeji yangu
uchafu” “Ndio akome, yani mambo yote haya ni ndani ya siku tatu tu,
asante Erica kwa kunipatia hela za Mzee Jimmy maana nimeweza kulipa kisasi
changu” Kwakweli Erica hakuwa na la kuongea zaidi ya kumuhurumia dada
yake tu kwani shemeji yake kaponzwa na umalaya wake kwa maana hiyo asingekuwa
malaya basi Dora asingempata tena. Jioni yake Erica alipigiwa
simu na Erick huku akimsisitiza kuhusu siku ya kesho, “Erica, kumbuka
kesho ni siku yetu nitakuja kukufata mama yangu” Erica hakuweza kukataa
maana ameshamzungusha Erick kwa muda mrefu sana na akaona kuzidi kumzungusha
ndio kupelekea zaidi mapenzi yao kuwa pabaya, alikubaliana nae na muda wa kwenda
kumchukua kisha wakaagana. Usiku wakati wa kulala, leo Erica alipigiwa
simu na Yule mwanamaombi, alipokea na kumsalimia kisha kuanza kuongea
nae, “Erica, toka jana nilikuwa najiwa na ndoto na maono kuhusu wewe,
Erica kwa swala lililopo mbele yako inatakiwa kufunga na
kuomba” “Kufunga na kuomba?” “Ndio kufunga na kuomba, tena
mfungo huo itabidi tuufanye kwa siku saba yani kula jioni tu, Erica mimi
nitafunga huku ila nawe ufunge huko na muda wa maombi tufanye wote ila itakuwa
vyema zaidi kama ukija kanisani kwetu” “Sawa nimekuelewa, kwahiyo
inabidi kuanza lini?” “Ni kesho Erica, haya maombi si ya mchezo,
yanataka haraka, kesho tuanze mfungo na maombi” “Mmmh!” “Mbona
unaguna Erica, hujawahi kufunga?” “Hapana, nimewahi ila ni gafla
mno” “Maombi mengine ni ya gafla na yanatakiwa kufanyiwa kazi muda huo
huo, unapofunga epuka zile dhambi ambazo unahisi zitakutenga na uwepo wa Mungu
kama uzinzi na uasherati” “Mmmh!” “Mbona unaguna
Erica?” “Hapana, nimeguna tu na nimekuelewa” “Basi naomba kesho
tuanze hilo jukumu mimi na wewe la kufunga na kuomba, sijui nini kipo mbele yako
ila naambiwa moyoni tufanye hivyo” “Sawa, nimekuelewa” Kwakweli
Erica alijuta kutoa namba yake kwa huyu mwanamaombi maana hakuelewa hata kesho
yake kuwa atamwambia kitu gani Erick amuelewe, ila moyo mwingine ukamshauri kuwa
ni bora aanze huo mfungo kesho kutwa maana kesho alikuwa na ahadi yake, ila
akajisemea atajaribu kuongea na Erick kama atamuelewa. Akaamua kulala tu muda
huo. Kulivyokucha akafanya kazi zake kama kawaida, na Erick
alimpigia simu kuwa ajiandae na alijiandaa kabisa, kwenye mchana Erick alifika
pale kwao na kumkuta mama Erica, kwakweli mama Erica alimfokea sana kwa kitendo
alichomfanyia mwanae ila Erick alimuomba msamaha mama Erica kisha
akamuuliza, “Mama, vipi ile biashara yako inaendaje?” “Aaah
wamekopa zote nimemaliza, saivi nakusanya madeni tu” “Basi ngoja
nikuongezee hizi mama” Erick alimpa mama Erica milioni tano nyingine,
kwakweli mama Erica alifurahi sana na kusahau kama huyu kijana ndiye aliyemuacha
mwanae kwenye mataa, na muda huo Erick aliomba kutoka na Erica ambapo mamake
alimruhusu bila tatizo lolote, tena alimuita viuri kabisa, “Erica mama
fanya upesi mwenzio anakungoja” “Sawa mama” Erica alitoka kisha
yeye na Erick wakaondoka na safari ilikuwa ni moja kwa moja hospitali kupima,
majibu yakatoka na kukutwa wote ni wazima kitu kilichomfurahisha sana Erick, na
kuondoka tena na kwenda na Erica moja kwa moja hotelini, Erica alijaribu kukataa
ila Erick alimuonyesha sura ya huruma sana ikabidi akubali na kwenda nae
chumbani, kisha akajaribu kuongea nae tena, “Ila Erick, mimi leo
nimefunga si vizuri kufanya zinaa” “Hebu Erica acha zako, Watu kibao
wanafunga na kufanya wanafanya, hakuna tatizo lolote kwenye
kufanya” “Erick zinaa ni dhambi” “Erica, ushatenda dhambi ngapi
katika maisha yako sembuse zinaa? Je kutoa mimba si dhambi? Yani kutoa mimba ni
sawa na kuua ila zinaa peke yake ndio unaona dhambi” “Hayo yalipita
Erick, sasa nataka kuwa mpya. Subiri unioe tutafanya” “Mambo gani hayo
Erica? Kumbuka mimi ni mwanaume, unataka hamu zangu nimalizie wapi? Kwanini
unanifanyia hivi lakini? Hunipendi tena eeeh!” “Nakupenda sana sana ila
ningeomba unisubiri” “Hapana Erica, kila siku unanipa visingizio
visivyoeleweka, kama kupima tushapima na wote ni wazima, kwanini tusifanye?
Kwanini unanikosea Erica?” “Hapana Erick, sitaki kukukosea ila sitaki
kufanya hiko kitendo” “Ila Rahim ndio anafaa kufanya na wewe
eeeh!” “Hapana sio hivyo” “Basi nipe mimi, unataka niende wapi
Erica eeeeh!” Erick alianza kumpapasa papasa Erica ili kumtia hamasa
Erica, alijikuta tu akisema sitaki huku akikubali yote anayofanyiwa na Erick,
kwakweli Erick alifurahi sana kuona Erica amekubali na walipomaliza aliinuka ili
apige simu mapokezi wawaletee chakula ila alishangaa kuona Erica akiwa amelala
tu vile vile hata kuinuka hakuna, akahisi labda anataka waendelee bila ya kula,
akamuuliza, “Erica, tuendelee” Ila Erica alikuwa kimya, ikabidi
amsogelee na kumbusu gafla akashangaa Erica akianza kutapatapa kama mtu mwenye
kifafa. Erick alianza kumpapasa papasa Erica ili
kumtia hamasa Erica, alijikuta tu akisema sitaki huku akikubali yote
anayofanyiwa na Erick, kwakweli Erick alifurahi sana kuona Erica amekubali na
walipomaliza aliinuka ili apige simu mapokezi wawaletee chakula ila alishangaa
kuona Erica akiwa amelala tu vile vile hata kuinuka hakuna, akahisi labda
anataka waendelee bila ya kula, akamuuliza, “Erica,
tuendelee” Ila Erica alikuwa kimya, ikabidi amsogelee na kumbusu gafla
akashangaa Erica akianza kutapatapa kama mtu mwenye kifafa. Kwakweli
Erick alichanganyikiwa maana si kitu alichokitarajia na wala hakuhisi kama Erica
anaweza kuwa na ugonjwa wa aina hiyo, alijaribu kumshtua lakini Erica alikakamaa
sana na kuwa kama mgonjwa wa degedege, akaona akiita watu kwaajili ya msaada
wakati bado hajamvalisha Erica ni kumdhalilisha kwahiyo ikabidi amvalishe kwanza
akiwa vile vile anatapatapa kisha akataka ambebe ili ampeleke hospitali huku
akijiuliza hapo hotelini watamuonaje, alijihisi vibaya sana na ile siku ikawa
mbaya kwake kupita siku zote. Mara kidogo simu ya Erica ikaita, Erick aliichukua
na kuipokea huku akitetemeka na huku jasho likimtoka, mpigaji lilitokea jina la
Fetty, “Hallow Erica” “Samahani, mimi ni mpenzi wa Erica ila
nipo nae mahali kapatwa na matatizo” Fetty akashtuka na kuuliza kwa
mshangao, “Matatizo gani?” Erick alimueleza kwa kifupi ambavyo
Erica alianza kutapatapa na kumwambia uamuzi wake wa kutaka kumpeleka
hospitali, “Unajua kuna hisia Fulani zimenijia kwenye kichwa change
nikahisi kama Erica hayupo sawa ndiomana nikapiga simu muda huu, sasa naomba
nikuombe kitu” “Niambie” “Naomba usimpeleke hospitali bora
umrudishe kwao tu, Erica hana huo ugonjwa napatwa na hisia mbaya, naomba
usimpeleke hospitali, mrudishe kwao na mimi mtanikuta nimefika dah! Jamani
rafiki yangu” Erick akawaza jinsi ya kutoka na Erica pale hotelini maana
lazima watamshangaa, kwahiyo alimsubiri atulie na mwili wake ulegee kisha
akamuona amefungua macho akiangalia tu akajaribu kumtikisa na kumuita ila Erica
hakusema chochote ikabidi Erick ambebe kama mtoto mikononi kiasi kwamba
waliowaona nje walihisi kuwa pengine ni aina ya mapenzi tu ndiomana wamebebana
vile, na uzuri ni kwamba Erica alikuwa akiangalia tu ila hakusema chochote kile,
basi alifika nae nje na kumuingiza ndani ya gari, akamkalisha vizuri na kumfunga
mkanda kisha yeye akapanda na kuanza safari ya kwenda kwakina Erica huku akiwaza
sana moyoni kuwa atasema nini akifika na Erica nyumbani kwao, aliwaza sana huku
akiendesha gari na kuhisi kuchanganyikiwa kabisa. Wakati anaendesha gari
na mawazo akapigiwa simu na Rahim, muda huu Rahim alitaka kusema mengine kuhusu
Erica ila Erick alimzuia, “Rahim, tafadhali acha maneno yako Erica
anaumwa” “Nini tena?” “Jua anaumwa tu, nini sijui” Erick
akakata ile simu maana alikuwa na mawazo kibao ya jinsi ya kumfikisha Erica
nyumbani kwao. Alifika nyumbani kwakina Erica huku kigiza giza
kikianza kuingia maana kidogo alienda hoteli ya mbali sana na Erica, basi
akamshusha na kumbeba kumuingiza ndani kwao huku akiwaza jinsi mama yake
atakavyomuuliza kwa hamaki, ila alifika pale, akakuta mlango upo wazi akaingia
ndani na kumkuta mama yake Erica amekaa chini na binti mmoja hivi, hakuelewa
Yule binti ni nani maana hakumjua, alisogea moja kwa moja kwenye kochi na
kumuweka Erica kwa kumlaza kisha akamsogelea mama yake Erica ili amuombe
msamaha, ila kabla hajasema chochote mamake Erica alimzaba kibao Erick na
kumwambia, “Ndio ulichokuwa unakitaka, naona roho yako imefurahi
sasa” “Hapana mama” “Hapana kitu gani na umeniletea mzoga
nyumbani kwangu” Mama Erica alimsogelea Erica na kumuita ila Erica
alimuangalia tu mama yake bila kusema chochote ndio kumuumiza kabisa huyu mama,
akamuangalia binti aliyekuwepo na kumuuliza, “Fetty ndio unasema
asipelekwe hospitali?” Ndio hapo Erick akaelewa kuwa Yule ndio Fetty
ambapo Fetty akajibu, “Ndio mama asipelekwe, nina hisia mbaya kuwa Erica
katupiwa jinni, kwahiyo mkimpeleka hospitali akichomwa sindano basi tunampoteza
ndiomana nilimwambia hata huyu shemeji asimpeleke hospitali. Halafu mama huu si
wakati wa kulaumiana ila ni wakati wa kujua tufanye kitu gani kunusuru maisha ya
Erica.” “Sikuelewi hata kidogo, mwanangu ana hali kama hii kweli
nawezaje kukuelewa Fetty?” Erick alikuwa kimya kabisa maana alihisi hata
angechangia ni angezidisha hasira kwa mama yake Erica maradufu. Mama
Erica alimuangalia Erick na kumwambia, “Yani wewe ndio chanzo ila
huongei chochote maana nina uhakika kama mwanangu asingetoka na wewe
yasingempata haya yaliyompata” Wakati wanaongea ongea pale, simu ya
Erica ilianza kuita na ilikuwa kwa Erick kwahiyo aliitoa na kumpa mama Erica
aongee nayo, mamake aliichukua na kuangalia mpigaji akaona jina limeandikwa
‘Mwanamaombi’ Mama Erica akaipokea na kuanza kuongea nayo, “Erica, sasa
kuna maombi ya muongozo tutakayoenda nayo katika huu mfungo. Una peni na
karatasi hapo nikwambie uyaandike!” Mama Erica aliongea nae kwa sauti ya
unyonge sana, “Erica ni mgonjwa yani yupo akituangalia tu ila haongei
chochote” Yule mwanamaombia alishangaa sana kuwa imekuwaje tena kwa
Erica kuwa vile, ikabidi aongee na mamake Erica jinsi walivyokubaliana na Erica
kuwa afunge siku hiyo maana alikuwa anaona vitu sio vizuri kwa Erica, basi
mamake Erica alisikitika sana vyenyewe hakushirikishwa na mwanae kuhusu hayo
maombi, labda angemshirikisha basi angemuhimiza kufunga na asingemruhusu kutoka,
ikabidi wakubaliane kuwa waendelee kumfanyia maombi Erica kisha Yule mwanamaombi
akasema kuwa ataenda, “Mama, najua unaamini kwamba Mungu
anaweza” “Ndio naamini” “Basi mtoto wako usimpeleke kwa waganga
kwani watamzidishia tu” “Siwezi kwenda kwa mganga” “Tukazane na
maombi tu mama yangu, ningekuwepo mjini basi kesho ningekuja ila mpaka wiki
ijayo, sema nitaendelea kuomba kwaajili ya Erica na atakuwa mzima kabisa kama
mwanzoni. Pole sana mama yangu” “Asante” Basi ile simu ilikatika
mamake Erica akawaeleza jinsi mwanamaombi huyo alivyowaambia, Erick alijilaumu
kimoyo moyo maana aliona kosa ni lake kulazimisha kulala na Erica wakati
alimwambia kuwa yupo kwenye mfungo, na bila kujua mwenzie kafunga sababu gani
ila akamlazimisha kufanya ngono, yani alijilaumu sana, ila hakuweza kusema pale
mbele ya mama yake Erica maana ingekuwa balaa zaidi, aliumia tu moyoni mwake kwa
kutokumsikiliza Erica. Nasma aliitwa na baba yake kupewa
taarifa ya kitu kilichofanyika, “Mwanangu tumeshamtengeneza huyo Erica,
ulisema kuwa tumfanye awe chizi na ndio lengo letu lilivyokuwa yani awe chizi
akimbie hovyo, avue nguo barabarani, wa kumbaka wambake, aokote makoto na mwisho
wa siku agongwe na gari na kufa maana kumshikilia chizi ni ngumu sana, ila
imeenda kinyume” “Imekuwaje baba?” “Badala ya kuwa chizi kawa
taahira kwahiyo mataahira si unajua wanavyokuwaga, yani wale mazezeta, yani Yule
atakuwa akifanyiwa kila kitu na familia yake kwamaana hiyo hatoweza kutoka kwao
maana ni taahira” “Ila hata hivyo sio mbaya baba” “Ila ingekuwa
vizuri sana kama angekuwa chizi, yani anewehuka akili zake yani pangine mpaka
kesho angekuwa ameshabakwa na vijana hata kumi, yani hata akija kupona anajiona
hana thamani tena katika maisha” “Kwahiyo atapona baba?” “Kwa
dawa tulizofanya mwanangu Yule haponi, yani haponi kabisa hata ndotoni Yule
haponi ataugua hadi kufa” “Sawa, na mume wangu kuja
kunichukua” “Usijali atakuja, yani tushamkorogea dawa ya kumuita kwahiyo
atakuja na nitakupa dawa nyingine ya kumuwekea kwenye chakula yani hiyo ndio
atakuwa hasikii wala haoni kwako, ngoja nikakuletee” Basi Yule mzee
alienda kumletea mwanae dawa na kumkabidhi, kisha akamwambia “Kipindi
kile hatukufanya dawa kali sana sababu ya ndugu zake, ila dawa ya sasa hivi ndio
kiboko yani anakuwa ni kwako kabisa, ila tuliyomvuta ni kwamba hata wazo la
kukufukuza tena wewe lisiwepo sasa hii ndio funga kazi yani mwanangu hii dawa
Bahati anakuwa wako milele hata usijali” “Asante sana
baba” Kisha akamkabidhi dawa ile na kumpa masharti ya kufanya na ile
dawa, “Sasa hii dawa mwanangu inaitwa funga kazi, yani usisahau masharti
yake maana ukikosea kidogo tu unaweza kumfanya awe ndodndocha hata ashindwe
kutafuta hela, sasa usikosee masharti ya hii dawa, unaichanganya na maji kisha
unaenda kunawa sehemu za siri unakinga bakuli maji yamwagikie humo, halafu
unampikia mumeo chakula na kumuwekea maji hayo kwenye chakula kisha
unamkaribisha ale, akishakula tu hakikisha hii nyingine unaitemea mate na
kuichanganya na maji ya kuoga, yani akimaliza kula atataka mwenyewe kuoga basi
aende kuoga, baada ya hapo mwanangu hata ukikohoa atakuuliza unataka nini, na
ndio mwanzo wa kutujengea gorofa wazazi wako maana mumeo ana hela
huyu” “Asante baba, ila nina shida nyingine, najua baba yangu unanipenda
sana na utanisaidia” “Sema mwanangu, usiogope” “Yani baba,
Bahati ni mgumu kufanya tendo la ndoa na mimi, mpaka nimlazimishe, toka akili
zake zimerudi ndio kabisa anasema yeye anataka kufanya na Erica
tu” “Ngojea mwanangu” Yule mzee akainuka na kurudi na dawa
nyingine, akamkabidhi mwanae na kumwambia, “Sasa hii unainyunyiza
kitandani, yani akishakula, akioga atakwenda kujilaza ili dawa ifanye kazi,
baada ya hapo mwanangu utaniambia, mumeo atakuwa kama jogoo. Ila sasa mwanangu
usiwe unamnyima mumeo maana atakuwa na hamu kila mara, isingekuwa hizi dawa za
mwanzo basi angetoka sana nje ya ndoa ila sababu ya hizi dawa za mwanzo atakuwa
anavumilia tu humo humo na kulia kwahiyo uwe unampa” “Hakuna shida baba,
nashukuru sana” Nasma alifurahi sana, na alifurahi zaidi
wanavyoshirikiana na baba yake katika mambo mbali mbali, na kweli baada ya muda
mfupi tu mara akamuona Bahati huyo amekuja kwao akiomba kuondoka na mke wake
huku akitubu kweli kuwa hatomkosea tena mke wake, huyu mzee kama alivyopanga
kuwa Nasma aondoke na ndugu yake mmoja ili akamsaidie kulea mtoto, akaona vyema
kumuita mdogo wake Nasma ili aondoke nae, “Basi mkeo ataondoka na huyu
mdogo wake Siwema maana ndio kabakia mwenyewe nyumbani, hasomi huyu wala nini
toka afeli darasa la saba mwaka juzi yupo nyumbani tu. Kwahiyo mtaondoka nae,
ataenda kumsaidia dada yake kulea mtoto” “Sawa baba hakuna
tatizo” Bahati aliitikia vizuri sana, na alikuwa mnyonge kupita maelezo
ya kawaida, kisha akasubiri Nasma na mdogo wake Siwema wajiandae kisha wage
vizuri na kuanza dafari ya kurudi nyumbani kwao. Walifika na kukuta
Bahati alishapika chakula kwahiyo walikula tu na kwenda kulala huku nasma
akijipanga kuanza kufanya dawa zake siku ya kesho. Muda
ulipoenda ilibidi Fetty aage na kuondoka ila Erick hakujihisi kuondoka kabisa,
alitamani siku hiyo alale hapo kwakina Erica maana ni yeye aliyesababisha mambo
ya vile kwa Erica, ila mama Erica alimwambia aondoke tu maana alishawapigia simu
wanae wengine wanakuja ila Erick aliamua kusubiri kwanza wakifika ndio aondoke,
kiukweli mama huyu aliumia sana moyo kumuona binti yake Erica akiwa kwenye hali
hiyo, alikuwa kila muda akiingia kwenye maombi kwaajili ya kumuombea binti yake
alijikuta akiishia kulia tu yani hakuwa na raha kabisa haswaaa akimsikia mtoto
wa Erica akisema, “Bibi mbona mama hasemi kitu” Roho ilikuwa
inamuuma sana, ilibidi Erick achukue jukumu la kumbembeleza Angel kwa siku hiyo
hadi alipolala na kwenda kumlaza maana alionyeshwa tu chumba cha Erica na kwenda
kumlaza Angel, muda kidogo alifika Mage na Bite, kwakweli Bite alikuwa amekonda
sana ila kitendo cha kumuona mdogo wao katika hali ile walijikuta wakiangusha
machozi kwa uchungu maana si kitu mtu yeyote alikitarajia, walipofika tu mama
Erica akamruhusu Erick aondoke, kwakweli Erick aliondoka huku akiwa na mawazo
sana kwani hakuwa na raha hata kidogo. Pale nyumbani walijikuta wakilia
tu bila ya kufanya chochote kile na kushauriana kila jambo la kufanya ila mama
yao alibaki na msimamo ule ule wa kusema ashikilie maombi. Siku hiyo
walilala sebleni yani watoto tu ndio walienda kuwalaza chumbani, kulipokucha
waliamka na kumchukua Erica kwenda kumuogesha kisha kumrudisha na kuanza
kumlisha chakula ambapo kile chakula kilikuwa kinarudi tu na kufanya waumie
zaidi, mpaka wamuinamishe ndio waweze kumlisha, ile asubuhi asubuhi Erick
alifika tena kamavile alilala getini, kiukweli Erick hakuwa na raha kabisa kwani
kwa kiasi kikubwa alijiona kuwa yeye ndio kasababisha kwa kumlazimisha Erica
kufanya mapenzi wakati alikataa na kumwambia kuwa amefunga, yani Erick alijiona
mkosaji sana, aliumia jinsi Erica alivyokuwa akila kwa shida na kuamua kutoa
ushauri kuwa amlete daktari amfundie Erica mifumo ya kuingizia chakula huku
wanaendelea na maombi, Mage aliafiki na kuona hilo swala ni zuri nap engine
daktari afike pale na kumgfanyia uchunguzi kuwa ana ugonjwa
gani. Kwakweli Erick hakuchelewa kwenda kumtafuta daktari na mida kidogo
alifika na daktari ambaye alimchukua Erica vipimo na kuangalia uwezekano wa
kumuwezesha Erica kupata chakula kwa muda huo, daktari aliondoka na vipimo
kwanza huku akiwaambia kuwa anawalete majibu. Majibu yalipokuja
ilionekana Erica hana ugonjwa wa aina yoyote na kuzidi kupata jawabu kuwa kuna
kitu ambacho si cha kawaida kimempata Erica. Wote ilibidi waegamie kwenye maombi
tu ingawa walipata na ushauri mbalimbali ila ilibidi wakae kwenye maombi
tu. Kwenye mida ya saa kumi na mbili siku hiyo, Nasma alifanya
matayarisho ya dawa yake, amapo alimuwekea kwenye chakula, kwenye maji ya kuoga
na kunyunyiza ile ya kitandani, akawa akimngoja tu Bahati atoke kwenye shughuli
zake, na kweli baada ya muda Bahati alifika nyumbani, na moja kwa moja Nasma
alimkaribisha mezani ili ale, akaoge na alale ila Bahati akamwambia
Nasma, “Nimechoka sana leo, nataka kupumzika tu” “Basi ule
kidogo, ukaoge ndio ukapumzike, na leo nimepika kile chakula
unachopenda” “Nasma, jioni hii hii nimekula, kuna jamaa alileta chakula
pale ofisini nimekula, kwahiyo labda badae shibe ikiisha” “Kheee jamani
mme wangu” Bahati ndio kwanza aliinuka na kwenda chumbani na kujilaza,
kwakweli Nasma alihisi dawa zimefanywa ndivyo sivyo, akawa na mawazo sana ila
kila alipomuamsha Bahati alikuwa hana habari zaidi ya kulala usingizi
fofofo. Alipoamka ilikuwa ni usiku tayari, ila bado Nasma alikuwa na
swala moja la kumlazimisha mumewe akale, “Basi mume wangu twende
ukale” “Aaaah nimeshiba sana Nasma” Basi Nasma aliendelea
kumbembeleza mume wake kuwa akale, ila badala yake Bahati alimtaka mke wake
kimapenzi kwa muda huo, “Ila mume wangu si unajua nimetoka
kujifungua!” “Kama hutaki basi ila mimi nataka” “Subiri nimalize
arobaini basi mme wangu, nitakupa hadi uchoke” Bahati aliamua kuendelea
kulala, kwakweli Nasma hakupatwa na usingizi alikuwa na mawazo mengi mengi maana
kile kitendo cha Bahati kutaka mapenzi alihisi huenda zile dawa zimeanza kufanya
kazi, yani alijilaumu sana kufanya kitu bila kufikiria madhara yake
kwanza. Palivyokucha tu, Bahati aliamka na kujiandaa kisha akaondoka
yani hata kuoga hakuoga, kitu ambacho kilimchanganya sana
Nasma. Rahim alikuwa na mawazo sana baada ya kuambiwa kuwa
Erica anaumwa, yani hakuwa na raha kabisa, alijikuta akitaka kufahamu kuwa Erica
anasumbuliwa na tatizo gani, ila tatizo lake hakupafahamu vizuri kwakina Erica,
kwahiyo aliamua kumuomba Babuu amsindikize, kwakweli Babuu alishangaa sana kuona
siku hiyo Rahim akitaka kwenda kwakina Erica, ila alikubali kumpeleka kama
kawaida wakati wanajadili mdogo wake Salma alisikia maongezi yale na kumpelekea
dada yake, “Dada, nimewasikia wanapanga kwenda kwakina Erica, eti
anaumwa” “Kheee jamani nifanye kitu gani ili Rahim awe anamaanisha
maneno yake kuwa Erica hampendi tena! Nachukia Erica mimi, namchukia
sana” Wakati anasema hivyo mke wa John alimsikia na kwenda kuongea nae
maana wote walikuwa wanakaa nyumba moja maana mama yao mwenyewe aliwaambia waoe
na kuwataka wote aishi nao nyumbani kwanza mpaka familia zao zikitanuka, mke wa
John aliyeitwa Neema alisogea na kuongea na Salma, “Sikia Salma,
usimchukie hivyo Erica ila jua kwanini Erica anapendwa hivyo na si wewe, ila
swala la kumchukia Erica sio suluhisho” “Wewe Neema hujui tu, unajua
Rahim kakazana sana na kwa Erica yani mapenzi kwangu hayapo nkabisa yeye na
Erica tu. Wewe huumii kama mimi” “Tena bora wewe hata Rahim
anakudanganyaga danganyaga kuwa hamtaki Erica, jamani mimi john mara ya kwanza
kabisa aliniambia kuna msichana alikuwa akimpenda sana alikuwa anaitwa Erica,
nilikuwa sijui yukoje ila nilitaka kujua ni kwanini alimpenda sana, nikawa
napeleleza kwa John nijue ni kwanini alimpenda sana Erica, mbona nilivyojua basi
na mimi niakjaribu kuenenda hivyo mbona John hata alimuona tena Erica
hakumfatilia maana aliamini kwa mimi mke wake, sasa wewe Salma kumchukia Erica
sio mwisho maana Rahim atakudanganya huku akiendelea kumpenda
Erica” “Sasa wewe uligundua ni kitu gani John alimpendea
Erica?” “Kwanza Erica ni mpole, hakuna mwanaume anayependa mwanamke
machachari, mwanamke anayeongea kama cherehani hana kituo hakuna mwanaume
anayependa, hakuna mwanaume anayependa mwanamke mwenye gubu, huwa wanavumilia tu
lakini hakuna anayependa, tunaona Erica akipendwa na wote hawa ni sababu ya
upole wake, hata sura yake inaonekana ni ya kipole na mtaratibu, halafu Erica
sio mkorofi, sidhani kama huwa anagombana na watu kwa kutukanana nao au
kuchambana nao, halafu Erica ni mcha Mungu, kila mwanaume anapenda apate
mwanamke mcha Mungu, maana wanaume wengi wanahofia wakipata mapepe watarogwa,
kwahiyo Salma jaribu kusimama kwenye nafasi yako, acha kuwaza kuhusu Erica sijui
ana bomoa nyumba yako, mwanamke mpumbavu hubomoa nyumba yake kwa mikono yake
mwenyewe, usiwaze hayo, mimi nilikuwa mkorofi ila nilivyosoma John hapendi
mwanamke mkorofi nilianza kubadilika taratibu na sasa huwezi kunikuta
nikigombana na watu au kumjibisha kitu kibaya John, nilikuwa sisali ila siku
hizi nasali na kumuhimiza mume wangu twende kanisani ingawa humu ndani tupo dini
tofauti” “Sasa mbona nasikia na huyo Erica hasali!” “Unaweza
sikia hivyo ila swali wewe unasali? Jamani toka nimefika huku ndani sijawahi
kukusikia hata mara moja ukienda Msikitini, nina hakika hata umesahau Misikiti
ikoje, tena sijawahi hata mara moja kukuona unaswali sijawahi ila nakuonaga mara
nyingi ukijifukiza, hapo utasema mbaya wako ni Erica? Mbaya ni wewe mwenyewe
Salma unatakiwa kujirekebisha” “Kwahiyo muonekano wa mtu ndio unaharibu,
sina sura ya upole mimi kwahiyo niitengeneze? Siwezi kukaa kimya mtu akinisema
mimi sio mjinga kiasi hiko, wewe Neema endelea hivyo hivyo ila mimi
nitahakikisha mpaka jina la Erica linapotea kwenye masikio ya
Rahim” Kwakweli Neema ilibidi anyamaze tu kwani aliona kila
anachomuelekeza mwenzie alikuwa haelekezeki. Rahim na Babuu
walienda hadi nyumbani kwakina Erica kumuona Erica, walifika na kuwakuta dada
zake na Erica maana waliamua kukaa pale pale kwanza kumuhudumia mdogo wao sababu
alikuwa akuhitaji kuhudumiwa kila kitu, kwa upande wa Erick ilikuwa kama pale ni
eneo lake la kazi maana kila siku alionekana kwenye nyumba ile, kwahiyo hata
Rahim na Babuu walivyofika walimkuta Erick yuko pale na alikuwa akimbeba Angel,
walifika na kusalimia huku wakiulizia hali ya Erica na kuambiwa anavyoendelea
ingawa kila siku kulikuwa kunaonekana maendeleo juu ya Erica kwahiyo nao
wakaambiwa kuwa wamuonavyo ni anaendelea vizuri maana mwanzo alikuwa hawezi
kukaa ila kwa hizo siku mbili aliweza kukaa, kilichomshangaza Rahim ni kuwa Yule
mtoto hakumtaka kabisa yeye, yani alimtaka Erick tu, kile kitu kilimuumiza sana
moyoni kuona mtoto wake mwenyewe akimpenda baba mwingine, aliumia sana
roho. Ila mama Erica alivyorudi na kumuona Babuu hakutaka kabisa,
akamtimua na alivyotambulishwa kuwa Yule ndiye Rahim alimtimua
pia, “Sitaki kuwaona nyie vijana, sitaki kuwaona kabisa, haswaaa wewe
Rahim, ondoka kwenye nyumba yangu, kwanza ulishamtishia mwanangu, kwahiyo
umekuja kiunafki tu. Ondoka kwenye nyumba yangu” Ilibidi Rahim na Babuu
waondoke zao maana hawakutakiwa tena mahali hapo. Muda kidogo alifika
Fetty na kuanza kuongea na mama yake Erica na ndugu zake wengine
pale, “Mama, kuna mtu anaona ameniambia kuwa waliokuwa wakimtesa Erica
ni wanawake wawili yani hao wana visasi vikubwa sana na Erica” Mama
Erica alishtuka sana na kusema, “Wanawake wawili! Sian a Tumaini hao,
jamani kwani mwanangu kawakosea nini?” Erick alichukia pia kusikia vile
kuwa dadake na msichana wake wa zamani wameamua kufanya kitu kibaya kwa Erica,
yani muda huo huo aliaga na kuondoka maana hakupenda kabisa na aliwaona kuwa
wabaya sana hadi kufikia hali ile aliona ni mbaya
kwakweli. Erick aliondoka mpaka dukani ambako Tumaini alikuwa
akisimamia, alimfata na kumwambia, “Tumaini kuanzia leo sitaki tena
uguse duka hili” “Erick imekuwaje tena? Si ulisema hili unaniachia mimi
na lile ndio unabaki nalo wewe, imekuwaje unanifukuza tena?” “Nimesema
toka kwenye duka langu, yani kuanzia leo ni mwisho na kesho naleta msimamizi
mwingine, umeniudhi sana Tumaini” “Kosa langu ni lipi
lakini?” “Kamfate baba akupe na wewe mali zako uanze kuziendesha sio
zilizoendeshwa na wenzio ufurahie tu kuzifanya, fanya zako. Na sitaki kukuona
tena, yani wewe wa kumroga Erica! Sitaki tena kukuona” “Jamani Erick,
nimemroga Erica saa ngapi? Kumbuka wewe ni ndugu yangu” “Tumaini, ole
wako Erica afe yani sahau kama umewahi kuwa na ndugu kama mimi.
Kwaheri” Erick aliondoka na kumuacha Tumaini akiwa na mawazo mengi sana
kuwa yeye kamroga Erica muda gani yani hakuelewa kabisa. Erick muda huo
aliondoka na kwenda kwakina Sia, kwakweli Sia alifurahi kumuona na kwenda
kumkumbatia ila Erick alimsukuma pembeni na kumwambia, “Sitaki unipigie
simu, sitaki unitumie ujumbe, sitaki ukanyage kwetu” “Kwani Erick
nimefanyaje?” “Na ole wako Erica afe ndio utanijua vizuri
mimi” Kisha Erick akaondoka hakutaka hata kurudi kwao, yani toka Erica
aanze kuumwa alikuwa akishinda kwakina Erica na kulala hotelini, na hivyo
alivyoambiwa kuwa wabaya wa Erica ni wanawake wawili ndio kabisa akawachukia
Tumaini na sia, na hakutaka kuonana wala kuongea tena na Tumaini zaidi ya pale
dukani alipomfukuza. Ilipita wiki toka Erica apate matatizo,
mamake alikuwa akialika watu mbalimbali kuja kumfanyia maombi pale nyumbani
kwahiyo Erica alikuwa akiombewa kila siku na kufanya afya yake ianze kuwa imara,
siku hiyo Erick akiwa amekaa pembeni ya Erica,
akamuita “Erica” Erica akageuka na kumuangalia huku akitabasamu,
kitendo hiko kilimfanya Erick ashangilie utafikiri kaona kitu gani, familia yote
iliingia ndani, na walijaribu pia kumuita Erica, aliwaangalia na kutabasamu yani
wote walikuwa na furaha sana, mama Erica aliamua muda ule ule kumpigia simu Yule
mwanamaombi, “Kwakweli Mungu ni mwema, leo Erica tunamuita anatuangalia
na kutabasamu” “Ooooh hiyo habari njema sana, tuingie kwenye maombi sasa
tukimshukuru Mungu kwa kutenda makuu kwa Erica” Alivyokata simu
aliwataarifu wote, yani siku hiyo hata Erick ambaye huwa hawezi kuomba aliomba
kwa furaha ya kumuona Erica akitabasamu tena. Ilikuwa mida ya
jioni ambapo Nasma alikuwa ameenda dukani mara moja, wakati anatoka dukani
akakutana na mdada mmoja ambaye alimsimamisha kisha akamsalimia na kuanza
kumwambia, “Dada, wewe ni mwanamke mwenzangu nimeona nikwambie
hili” “Niambie tu” “Jamani mumeo kabadilika yani kabadilika
haswaaa” “Kivipi?” “Hadi tunakuonea huruma, jamani mumeo
anatongoza hovyo, anatembea na wanawake hovyo hadi tunakuonea huruma, ile gari
yake imekuwa kama guest yani mumeo anafanya mapenzi na wanawake ndani ya gari,
kwakweli ni aibu. Samahani kama nimekosea kukwambia, ila nimeshindwa
kuvumilia” Kwakweli Nasma aliondoka pale akiwa na mawazo sana maana
hakutegemea kama mumewe atakuwa muhuni wa kiasi kile, basi akarudi nyumbani
kwake akiwa na mawazo sana. Akafika na kukuta nyumba ipo kimya sana,
akaweka vitu jikoni na kuelekea sebleni, akashangaa kumkuta Bahati na Siwema
wakiwa sebleni wanafanya mapenzi. Kwakweli Nasma aliondoka pale
akiwa na mawazo sana maana hakutegemea kama mumewe atakuwa muhuni wa kiasi kile,
basi akarudi nyumbani kwake akiwa na mawazo sana. Akafika na kukuta
nyumba ipo kimya sana, akaweka vitu jikoni na kuelekea sebleni, akashangaa
kumkuta Bahati na Siwema wakiwa sebleni wanafanya mapenzi. Alijikuta tu
akisema kwa mshangao, “Yani mume wangu na mdogo wangu
mnanisaliti?” Ila wala walikuwa hawamsikilizi kabisa, hadi ikabidi
awafate karibu na kumvuta Bahati huku akisema, “Yani hamna hata aibu!
Naonekana hapa mnaendelea tu, heshima iko wapi jamani! Eeeeh Siwema, heshima iko
wapi mdogo wangu?” Siwema alikuwa akivaa kwa aibu tu, ila Bahati alienda
chumbani na kujilaza, kwakweli Nasma alikuwa amechukia sana na kumfata Bahati
huku akimuuliza kwanini amefanya vile na mdogo wake, “Hebu wewe mwanamke
tulia, nishakwambia nina hamu umesema hadi umalize arobaini kweli nitasubiri
arobaini iishe? Ushaambiwa kizuri kula na nduguyo, sasa kuna ubaya gani wa mimi
kulala na Siwema?” “Hebu niondolee balaa mie Bahati, umenitia aibu
haswaaa yani umenitia naibu sana” Kisha akarudi kwa mdogo wake na
kumfokea kuwa kwanini kamfanyia hivyo, “Dada, nilikuwa nakusaidia tu
maana shemeji alisema ana uhitaji” “Mjinga wewe, nimeomba msaada wako
mimi? Nakwambia na kwangu hapa unaondoka mjinga wewe” “Jamani dada
nisamehe, nimefanya na shemeji mara mbili tu sirudii tena” “Mjinga wewe,
kumbe ndio mchezo wenu eeeh! Na kwangu unaondoka kapaki vitu vyako uende, yani
nikafuge mbwa ndani kwangu siwezi, sikufikiria kama una tabia mbaya kiasi
hiko” Basi ilibidi Siwema ajiandae kwaajili ya kuondoka kwa dada
yake. Nasma hakutaka tena kumuona mdogo wake maana alihisi akiondoka
ndio itakuwa afadhali kwake na familia yake ili apambane tu na wanawake wa nje
ambao Bahati atakuwa nao. Mdogo wake Nasma wakati anaondoka, muda ule
ule Bahati nae alitoka, kwakweli Nasma hakuelewa kuwa ni kipi kimeendelea ila
Bahati hakumruhusu Siwema kurudi nyumbani na badala yake alienda kumpangishia
chumba ili awe mke wake wa pili. Nyumbani kwakina Erica ilikuwa
ni mabadiliko ya kila siku juu ya uzima wa Erica kwani saivi alikuwa akielewa
kila kitu kilichokuwa kikizungumzwa na kuna baadhi ya mambo alikuwa akiyafanya
kama kumshika mwanae tofauti na mwanzo ambapo hakuweza kufanya chochote, ila tu
hakujibu kitu lakini alionekana kuelewa kila kitu, kitu kile kilimpa matumaini
na Erick na kuweza kuendelea na kazi zake zingine kwahiyo alikuwa akitoka kwenye
kazi zake jioni ndio anapitia kwakina Erica kuangalia hali yake na kisha kurudi
hotelini kulala. Siku hiyo walibaki nyumbani Bite na Mage huku Mage
akijiandaa andaa kwenda kuona familia yake, na mama yao hakuwepo, na muda kidogo
Mage akaondoka zake kwahiyo alibaki Bite na Erica, muda kidogo wakapata ugeni na
mgeni huyo alikuwa ni Dora, ambaye alifika na kugonga mlango na kukaribishwa na
Bite, alishangaa kumuona Dora maana anakumbuka mara ya mwisho ni kipindi kile
wakati ametimuliwa kwao baada ya kuletwa na Tony kama mchumba, ila yeye
hakumtimua bali alimkaribisha ambapo Dora aliulizia Erica, “Yani
nampigia simu hapokei, natuma ujumbe hajibu ndiomana nikaamua kuja
tu” “Erica anaumwa, siku zote hizi” Akaingia ndani na kuonyeshwa
Erica aliyekuwa sebleni, akashangaa anamuitwa Erica ila anamuangalia tu bila
kusema chochote, “Kheee kwahiyo hasemi” “Mbona ni afadhali hapo,
alikuwa na hali mbaya sana yani watu wa maombi wamefanya kazi
kubwa” “Kheeee kaanzaje?” “Yani nasikia alianguka kama kifafa,
baada ya hapo ndio akaanza hivyo, alikuwa anakakamaa mwili kama mtu mwenye
degedege” “Kheeee nguvu za giza hizo” “Kwanini umesema
hivyo?” “Erica, hajawahi kuumwa kifafa, mtu ambaye kifafa hakijawahi
kumpata halafu kimpate gafla huwezi sema ni kitu cha kawaida, halafu sijui
akakamae kama anaumwa degedege jamani huo ugonjwa huwa unawapata watoto tena
wale wasiopewa chanjo, aje kuupata Erica kweli! Kwanza ugonjwa wenyewe huo hata
ukimpata mtoto huwa unashirikishwa na nguvu za giza, wanasemaga ni jinni na
ndiomana wakikosea tu tiba kwa mtoto mwenye degedege anapotea. Ila mbona
hamkuniambia kama rafiki yangu kipenzi anaumwa hivi?” “Kumbe bado ni
rafiki yako eeeh!” “Ndio, tena urafiki wangu na wake saivi umekuwa
zaidi, yani wa kiwango kingine. Mngeniambia kwakweli” “Basi ndio hivyo,
ila saivi anaendelea vivuri tofauti na mwanzo alikuwa na hali mbaya
zaidi” “Kwahiyo tiba gani mmepata?” “Watu wa maombi huja
kumuombea kila mara yani Erica anaimalika sababu ya maombi” “Ila hamuoni
kama mnamchelewesha na hayo maombi” “Kivipi?” “Yani mngeniambia
mapema, kuna mtaalamu huyo yupo Bagamoyo yani huyu Erica angechemshiwa jungu
siku mbili tu angerudi kwenye hali yake, huyo mtaalamu kiboko na angesema nani
kamfanyia hayo mambo, yani nyie mnakazana na maombi tu jamani!” “Wewe
acha maneno hayo, maombi yana nguvu. Kwani kuna watu wangapi tunasikia habari
zao kuwa wamefia kwa waganga? Kupona kwa maombi ni kupona milele, nguvu ya Mungu
ni kubwa sana kupita unavyoielewa, yani wewe ni dini gani usiyejua mambo ya
maombi?” “Mimi ni mkristo ila huwezi kunipeleka kwenye maombi maana hao
wachungaji wanapenda pesa tu, kidogo utasikia sadaka, tunadanganyana tu hao
wachungaji ndio wanaongoza kwenda kwa waganga, mnamchelewesha Erica hapa yani
tungeenda nae kwa babu huyu mbona angekuwa mzima kabisa ila hizo habari hapana
aisee” “Wewe ndiomana tulikutimua kipindi kile sijui Erica ameanza vipi
tena na urafiki na mtu kama wewe hata usiyejua uwepo wa Mungu” “Najua
vizuri kuwa Mungu yupo ila hata hao waganga wanatumia Mungu, mi ngoja niondoke
maana hatutaelewana hata nishauri vipi ila nakuahidi natoka hapa kesho safari
Bagamoyo kwa babu halafu nitaleta dawa uone kwa sekunde tu Erica
mzima” Bite aliamua kumtimua tu Dora na hapo hakujua kama huyo ndiye
mwizi wa mume wake,ila alijikuta akimchukia tu gafla kwa maneno
yake. Kiukweli Salma hakufurahishwa na mwenendo wa Rahim kwani
ilionyesha wazi Rahim toka ametimuliwa nyumbani kwakina Erica hakuwa na furaha
kabisa na vile mtoto wake alivyoonekana kumpenda zaidi Erick ndio kulimfanya
azidi kupata mawazo, kufikia hatua ya kuaga anaenda kwenye kazi ila alikuwa
akienda kwa wanawake zake wengine na kulala huko siku mbili ndio anarudi
nyumbani, hali hiyo haikumpendeza kabisa Salma, ukizingatia kila alipomueleza
mama mkwe wake ila huyu mama alionekana kumtetea kabisa mtoto wake na kila Salma
alichosema alionekana kumuonea, “Mama, Rahim anakunywa
pombe” “Hebu Salma acha maneno yako Rahim na pombe wapi na
wapi?” “Kweli mama, na ana wanawake” “Mwanangu kuzaa na Erica
sio alikusudia ila ni bahati mbaya tu, mwanangu hana wanawake wengi kama
usemavyo, mara nyingine jifikirie Salma, mwanangu kazunguka nchi mbalimbali
lakini kaja kukuoa wewe, jiulize una kipi ambacho wanawake wengine hawana? Ila
unaweza kuja kumsingizia kuwa ana wanawake kweli? Nimewapa ile nyumba pale muwe
mnakaa sababu sitaki kukaa mbali na wanangu ndiomana kwenye nyumba ile mnakaa
nyie tu yani wewe na mumeo na Neema na mumewe, sitaki kukaa mbali na wanangu na
ningewaweka humu ndani mngeona nawabana oooh mama mkwe anatubana, haya mwanamke
wa watu sitaki matatizo ile nyumba niliijenga kwaajili ya wanangu na ni wao na
nyie ndio mmeanza kukaa pale, kipindi chote hiki hakuna anayekaa kwenye ile
nyumba, mnapika wenyewe, mnaongea wenyewe leo hii uje uniambie mwanangu ana
wanawake wengi? Hakuna hiyo kitu, mwanangu namfahamu” Kwahiyo Salma
akaona hakuna ushirikiano kabisa kati yake na mama mkwe wake, akaamua kurudi
ndani kwake, ila akapata wazo la Yule mmama waliyekutana nae hospitali aliamua
kumpigia simu ili kupewa maelekezo ya kitu cha kufanya, “Sasa binti
yangu itakuwa vyema ukija huku kwangu ili nikupe hiyo dawa na
maelekezo” “Sawa, nitajitahidi nije maana huyu mwanaume sasa anataka
kunichanganya akili yangu, nitakuja unisaidie nahitaji kumtuliza huyu
mwanaume” “Sawa karibu sana binti yangu” Salma aliona ni
afadhali amfanyie mumewe dawa maana aliona mwenendo wake haujatulia
kabisa. Mama Erica alirudi nyumbani kisha Bite kumpa ujio wa
Dora, “Kumbe Yule Dora na Erica walianza tena urafiki?” “Yani
Erica nilishamkataza mara nyingi na Yule rafiki ila yeye alikataa kuwa na
urafiki naye, ndiomana hata siku zake nikuwa sipokei” Basi Bite
akamueleza mama yake ambaye Dora aliyasema, ndio mama yake akakumbuka pia kuhusu
mahusiano ya Dora na Bite, aliamua kumuuliza mwanae, “Hivi mwanangu,
ulishawahi kupima na ukimwi?” “Ndio, nilipojigundua nina ugonjwa wa
kansa ya shingo ya kizazi niliamua kupima na ukimwi ila sikuwa
nao” “Hongera, na mumeo ulipima nae?” “Yani James alikataa kata
kata kwenda kupima” “Mmmh kapime tena mwanangu” “Mama, toka
kipindi nimejigungua nina kansa ya shingo ya kizazi sina raha kabisa,
nikamwambia James tukapime aligoma basi toka kipindi hiko sishirikiani nae tendo
la ndoa nilimwambia hadi akubali kwenda kupima magonjwa yote, ila hana aibu
ananiambia eti ugonjwa nimeupata kwenye umalaya wangu, mama wewe ni mama yangu
siwezi kukuficha, toka nianze na James sijawahi kuwa na mwanaume yeyote ndiomna
roho inaniuma sana, kwakweli nimechoka kuishi na James nimechoka kabisa,
anapigiwa simu na wanawake hadi usiku tukiwa tumelala mama yani hana heshima na
mimi jamani” “Kwakweli pole sana mwanangu, naelewa jinsi yanavyoumiza
mambo hayo, tafadhali usishirikiane na mumeo mpaka akapime ukimwi, hajatulia
kabisa Yule, yani usikubali kabisa mwanangu.” “Siwezi kukubali
mama” “Nadhani Mage hajakwambia, waliwahi kumuona mumeo akiwa na huyo
shetani aliyekuja leo Dora, tena walikuwa wakitoka nyumba za
wageni” Bite alijikuta akimchukia Dora maradufu, “Kumbe msichana
Yule ni mchafu vile?” “Ndio, na Erica alisema kaambiwa na Dora kuwa
ameathirika” “Uwiii mume wangu jamani” “Hebu acha uchuro na
wewe, Yule ni mume au kopo? Mwanaume wa kumtaka hadi ndugu yako, sio mwanaume
kabisa, nasikia mumeo alikuwa na kesi ya kumbaka Dora” “Hiyo kesi
hakutaka hata nijue mwenendo wake na sikuelewa kama ni huyu rafiki wa Erica,
sasa mbona alikuwa anakataa?” “Huwajui wanaume mwanangu? Ila Dora nae
sio wa kumlaumu pengine kataka kutuonyesha kweli James alimbaka ndiomana saivi
wamekubaliana nae wako wote” “Itakuwa kweli mama, yani huyu James huyu
dah najuta kuwa nae jamani, najuta kumuamini aina yake ya mwanaume. Kuna Yule
mkaka alikuwa akinifatilia sana labda ningeolewa nae saivi ningekuwa nafurahia
maisha ila kwa huyu James nimekosea namba kwakweli” “Ila mwanangu
usichukulie hasira sana, haya mambo yanaenda taratibu sema huyu mumeo sasa hivi
sio wa kumchekea” “Yani mama najuta, najuta mimi kuolewa na
James” Bite aliongea kwa uchungu kwani hakuwa na raha kabisa yani aliona
kamavile dunia imemuonea sana. Tumaini aliamua kwenda kwa Sia
maana walipigiana simu na kujikuta wote wakiwa na janga moja, walikutana na
kusalimiana kisha kujadili, Tumaini alimuuliza Sia, “Kwani unajua kuwa
huyo Erica anaumwa na nini?” “Hata sijui mwenzangu yani nashangaa tu
kuwa kwanini Erick kaja kunifokea hivi” “Mwenzio sasa nimefukuzwa
dukani, yani Erick kanifukuza kwenye lile duka lake ambalo nimeliendesha miaka
yote hii eti ananiambia nikafate mali kwa baba, halafu baba mwenyewe ni jibu
kabisa maana aliwahi kuniambia mali ni za mwanaume eti mimi nitumie tu, ona
mwanae alichonifanya kisa mwanamke” “Sasa Tumaini, mimi naona ni vyema
ukazungumze na baba yenu yani umueleze kila kilichotokea, unajua sijui ni
kwanini Erick atusingizie sisi” “Pengine ni sababu ya kumchukia sana
Erica” Wakajipanga cha kufanya ila hawakufikia hata hitimisho, basi
Tumaini akawa anaondoka na Sia kumsindikiza huku wakipanga siku moja kwenda
kwakina Erica ili wajue nini kinaendelea, wakati wanatembea njiani Tumaini
akamuona Dora akamkumbuka kuwa aliwahi kuwa rafiki wa Erica, akamsimamisha na
kumsalimia kisha kumuuliza kuhusu Erica, “Erica rafiki yangu anaumwa
kuna wajinga wamemroga rafiki yangu ila nawaendea kwa mtaalamu” Tumaini
akauliza kwa mshangao, “Kwa mtaalamu! Ndio atafanya nini huyo
mtaalamu?” “Yani kuna babu yupo Bagamoyo ni kiboko huyo, nakwambia Yule
Erica mbona siku mbili tu kapona. Mie alinipa dawa nimemteka mwanaume huyo
hafurukuti kwangu kwa siku moja tu yani mpaka leo mwanaume haoni
pengine” Tumaini akaona huyu Dora analeta stori sio zenyewe, ikabidi
aagane nae na kumuacha akiendelea na safari yake kisha yeye akamuaga Sian a
kuita bajaji ili aondoke zake, Sia akamwambia, “Ila Tumaini unajiachia
tu, babako ana hela, mdogo wako ana hela hivi inashindikana kununuliwa gari
kweli?” “Mmmh weee acha tu, baba ana mambo mengi sana na huyo Erick sasa
ndio balaa kila nikimwambia kuwa nahitaji gari anasema nitakununulia
tu” “Unajua sielewagi, baba yenu ana hela sana, Erick ana hela sana ila
wewe unaishi maisha ya kawaida kwanini? Si ilitakiwa wewe na Erick muwe na mali
sawa!” “Sia familia yetu ni pan asana kuielewa ila kwa kifupi Erick ana
hela za sehemu mbili, yani sio baba peke yake anaefanya Erick awe na hela bali
na mama yake nae ana hela sana halafu Yule mama mtoto wake ni Erick tu kwahiyo
ni mtoto wa pekee na kwa baba nako mtoto wa kiume ni Erick tu hapo ndio kuna
utofauti kati yetu. Ila usijali Erick alisema kwasasa mambo yake hayajakaa sawa
ataninunulia sasa na hilo swala la Erica kuumwa duh hadi kichwa kinanichemka,
tupange tu siku twende kwakina Erica” Bajaji ilifika na Tumaini kupanda
huku akiagana na Sia ila Tumaini alivyoondoka tu Sia akajikuta akimkimbilia Dora
na kumuita, yani swala alilosikia kuhusu mtaalamu lilimvutia sana, Dora
alisimama na kumsubiria, Sia alikimbia hadi alipo Dora, “Samahani kuna
jambo nataka kukuuliza” “Bila samahani” “Wakati tunaongea pale
nimesikia kuhusu mtaalamu anavuta mpenzi hadi anakuwa wako, swali ni je hata
kama huyo mpenzi hakutaki?” “Yani hata kama hakutaki baada ya hiyo dawa
anakutaka mwenyewe tena anakupenda balaa, atakuhonga hadi usahau” “Kheee
jamani na mimi nilikuwa namtaka huyo mtaalamu” “Sawa, kesho nataka
niende basi chukua namba yangu ili tuwasiliane twende wote” “Nitafurahi
sana, asante” Wakabadilishana namba pale kisha kuagana, mawazo ya Sia
kwa wakati huo yalikuwa kumpata Erick tu kwa hizo dawa, aliwaza kumvuta kwa
dawa, aliwaza kummiliki na kufurahi sana. Salma kama
alivyopanga na Yule mama, akajiandaa vizuri na kumuachia mdogo wake mtoto kisha
yeye kuonana na huyo mama, ambapo alimkuta pale alipomwambia, “Sasa wewe
unataka dawa ya kumtuliza mume, au dawa ya mume kukusikiliza kila unachosema, au
dawa ya kumfanya mume awe anakupa hela zote yani wewe ndio unatoa bajeti na
matumizi ndani ya nyumba” “Kiukweli nataka dawa zote yani mume wangu
asifurukute kabisa mbele yangu yani mimi niwe kila kitu kwake” “Sawa
hakuna shida, masharti utayaweza? “Nitayaweza ndio” Akampa dawa
nyingine ya kujifukiza na nyingine ya kuweka kwenye chakula, na nyingine ya
kuweka kwenye maji ya kuoga, kwakweli Salma aliifurahia sana ile dawa na
alitakiwa kuifanya muda ambao mumewe hayupo, “Yani vizia wakati mumeo
kaondoka nyumbani ndio uifanye hii dawa, unawashamkaa unachukua kidogo kwenye
sufuria halafu unaenda nao chumbani na kuanza kuchoma huku unanuizia hata aje
kukuita nani usiinuke wala usiitike ndiomana nakwambia ni vizuri ukiwa mwenyewe
yani baada ya hizi dawa mumeo atatulia hawezi tena kuhangaika
nakwambia” “Nashukuru sana, ila kuna mwanamke mmoja hivi anapendwa sana
na mume wangu, mwenzangu alimfanyia dawa, tulitaka awe chizi ila nasikia
ilisindikana kuwa chizi akawa tahira, sasa mume wangu anashinda huko huko hadi
nakosa amani” “Sasa huyo mto ni ndondocha ila bado mumeo anashinda huko,
basi ngoja nikupe dawa” Salma akaisubiria hiyo dawa, “Sasa
nakupa dawa ukamsalimie, wakati hiyo dawa umeishika mkononi yani utampa mkono na
dawa hiyo hapo ni kwisha habari yake” “Ila mimi siwezi kwenda nyumbani
kwakina huyo msichana, naweza kumuagiza mtu?” “Inawezekana
ndio” Mtu ambaye alimuwaza kwa muda huo ni Derick tu ndio aliona wa
kumsaidia kwa kile alichokipanga, kisha akaagana na Yule mmama na kuondoka zake
kurudi kwao, alipofika kwao alimuona mumewe Rahim akiongea na Neema, hakutegemea
kumkuta nyumbani mumewe muda huo ila ndio alimkuta hakuwa na cha kufanya zaidi
ya kuwa mpole kwanza, alisogea ili aingie ndani na kuwasalimia, Rahim
akamuuliza, “Weee Salma, umetoka wapi muda huu?” “Aaaah nilienda
hapo dukani” “Hivi wewe mwanamke una akili? Yani mtoto bado mdogo
umeanza kuzurula, haya niambie umetoka wapi? Hata kazini kwenyewe hutoa miezi
mitatu ya mapumziko mtu akitoka kujifungua sembuse wewe mama wa nyumbani?
Niambie umetoka wapi muda huu?” Salma hakusema chochote na kuingia
ndani, Rahim akamfata ndani na kumuuliza tena kuwa ametoka wapi, “Jamani
Rahim mbona uko hivyo! Mimi mbona sijawahi kukuuliza wewe kuwa umetoka wapi
jamani? Kila mtu awe huru humu ndani” “Wewe Salma usinipande kichwani,
mimi ni mumeo nina haki ya kujua mapito yako yote, usinijibu hivyo nitakupiga
sasa hivi” “Kama unaona kupiga dili nipige basi” Huku
akimsogelea mwilini kama anayetaka kupigwa, Rahim nae hakumuachia na alimpiga
kweli na kumuacha akipiga kelele tu ndani ya nyumba kisha Rahim akatoka na
kuondoka, neema aliingia ndani kumbembeleza rafiki yake, alimkuta chini akilia
na kuanza kumbembeleza, salma alikuwa akisema, “Yani wanaume wana roho
mbaya jamani, mimi nina mtoto mdogo halafu yeye ananipiga! Najuta kuolewa
nae” “Ila Salma usifikie kujuta, jiulize kwanza kwanini
kakupiga” “Na wewe hebu nenda huko, yani hapa ndani mtu huruhusiwi
kutoka au ni kitu gani? Mbona yeye anatoka simuulizi” “Usishindane na
mwanaume” “Wewe subiri tu huyu Rahim dawa yake inachemka tuone kama
atanipiga tena na ujinga wake” Neema alijaribu kuongea nae ila ilikuwa
ngumu sana kwa Salma kumuelewa ikabidi neema atoke. Ila alimkuta tu
Rahim amekaa nje, akamfata tena na kumuuliza, “Kwani shemeji vipi jamani
mpaka umempiga Salma?” “Yule mwanamke ni mjinga sana, huwa sipendi
mwanamke anijibishe hata mara moja, mimi sio mpigaji ila alivyokuja mwilini
alitaka nimfanye nini?” “Mmmh ila shemeji hujawahi kuishi na Salma kama
kipindi hiki, unatakiwa kumuonyesha upendo na sio hasira” “Mwanamke
mjinga sana, najuta kutafutiwa mwanamke, bora ningemuoa Erica wangu mimi
tungelea mtoto wetu” Salma alikuwa dirishani na kusikia yani hapo ndio
hasira zilimpanda alitamani hata dawa aifanye muda huo ila kwavile tu aliambiwa
ni hadi jioni. Siku hiyo Erick alikaa na Erica akiongea nae,
yani Erica hakujibu ila Erick aliongea nae kwa furaha kwani aliona jinsi Erica
anavyotabasamu na kumpa moyo kuwa Erica ni mzima na karibuni atakuwa sawa
kabisa, “Erica, ile zawadi ya gari bado ipo yani usijali mpenzi wangu,
siku ukipona kabisa nitaileta hapa yani nitakukabidhi hapa mpenzi wangu, ile ni
zawadi yako kabisa, na unajua kitu kingine kuna zawadi kubwa nimekuandalia najua
hii ndio utaipenda zaidi maana si gari tena ila ni zaidi ya gari. Nakupenda sana
Erica” Erica alikuwa akitabasamu tu na kumfanya Erick afurahi zaidi,
muda huo akafika mgeni pale kwakina Erica, mgeni huyo alikuwa ni Fetty kwahiyo
alifurahi sana kuwaona pamoja, Bite na Mage nao wakasogea karibu alivyofika
Fetty maana mwanzo walimuacha tu Erick aongee ongee na Erica. Bite
aliamua kumuuliza Fetty, “Eeeh leo una ujumbe gani Fetty?” Fetty
akacheka tu na kusema, “Sina ujumbe ila watu huwa hawanielewi mimi yani
mimi kama nina madudu kichwani yani huwa yananiambia vitu nisivyovielewa kabisa,
ndiomana nikienda kupeleka ujumbe huwa nasema kuna mtu kaniambia ila ni madudu
yangu kichwani, bite alicheka sana baada ya kusikia Fetty ana madudu kichwani,
mama Erica nae alitoka ndani akiwa amesikia hiyo habari ya Fetty kuwa na madudu
kichwani ila mama Erica akamshauri, “Unatakiwa uombewe hayo madudu
yatoke, huoni kama yanakusumbua?” “Hapana hayanisumbui wala nini ila
huwa yananipa habari” “Mmmh ila ningekuwa ni wewe ningeyatoa, kuishi na
madudud hapana kwakweli. Ni muda gani sasa unayo?” “Ni ukubwani hapa
hapa ndio hii hali imeanza maana nilipokuwa mdogo wala hakuna
kitu” Wakati wanaongea alifika mgeni mwingine ambaye ni nadra sana
kufika mahali hapo, alifika Derick, na alionekana kuwa na lengo la kumuona Erica
ila alishangaa sana kumuona Erica ameshikiliwa na Yule kijana aliyemkuta,
hakumjua ni nani ila alihisi atakuwa mpenzi wa Erica tu, alikaribishwa na baada
ya salamu tu aliamua kuulizia na kujifanya anayaka kumsalimia sheej yake, Mage
alimtambulisha pale kwa Erick, kitu kilichomuumiza sana moyo kumfahamu Erick,
yani yeye hakupenda Erica awe na Erick, kwakwe ilikuwa ni bora Erica awe na
mwanaume mwingine ila sio Erick sababu tu alijua huyo mvulana anapendwa sana na
Erica, Badi Derick akamsalimia pale halafu akaulizia chanzo cha ugonjwa wa
Erica, kisha Mage alimueleza kwa kifupi. Kisha Derick akasogea karibu ili amguse
Erica, Gafla Fetty aliinuka na kwenda kumzaba kibao Derick, kwakweli Derick
alichukia sana na kuuliza, “Wewe Fetty una nini wewe? Kwanini
unipige?” “Wewe ni mnafki, hauna lolote umesababisha pia kuumwa kwa
huyu” Derick alishangaa na wote pale walishangaa, kwakweli Derick
hakutegemea kama Fetty angesema vile na hakujua kwanini alisema vile, kisha
Fetty alisogea katikati yani yeye ndio akawa katikati kiasi kwamba Derick
asiweze kumuona tena Erica, kisha akasema, “Ondoka Derick, hakuna
kumsalimia Erica, ondoka upesi” Wote walikuwa wakishangaa ila kwavile
mama Erica hampendagi Derick aliamua kutumia ile ile nafasi kumtimua maana huwa
anamuhisi muda wote ni mnafki toka mambo ya chuo ambayo mwanae alimsimulia na
mambo ya kule kwenye tambiko basi huyu mama ndio hakutaka kabisa kumuona Derick
ila alimuona tu sababu ya Erica kwahiyo muda huo akapata nafasi ya kumfukuza
pia. Kwahiyo Derick hakuwa na jinsi zaidi ya kuondoka tu, na baada ya
Derick kuondoka ndipo mama Erica nae akaondoka kwenda kwenye shughuli
zake. Jioni hii Salma nae aliwasha moto ili afanye ile dawa
kwani aliamini sababu ya ule ugomvi wa mchana ni ngumu mumewe kurudi nyumbani,
akampa mdogo wake mtoto ambebe na ambembeleze ambapo mdogo wake alimbeba na
kwenda nae kwenye nyumba ya mama yao na wakina Rahim. kwahiyo aliona ndio muda
pekee wa kuanza kufanya ile dawa yake, kisha kuchukua moto wa mkaa kwenye
sufuria na kwenda nao ndani kunuiza kile alichofundishwa na Yule mmama, akaanza
kufukiza dawa zake huku akinuiza, Neema alikuwa akiona tu moshi ukitoka kwenye
kile chumba cha Salma, kiukweli alisikitika sana maana aliona anachofanya
mwenzie sio sawa, kisha akamuona Rahim kama anakuja, akatamani amzuie ila
hakuweza maana Rahim alishafika, Rahim hata hakumsalimia Neema kwani moja kwa
moja aliingia ndani, akafungua mlango wa chumbani na kuona mgumu kufunguka,
akagundua umefungwa kwa ndani na vile aliona moshi moshi alihisi tu kuna kitu si
cha kawaida kwenye nyumba yake, Sema alikuwa na funguo ya ziada mfukoni ya kile
chumba, akaingiza na kuangusha funguo ya ndani kisha kufungua mlango, alishangaa
kumuona Salma kajifunikiza akinuizia dawa, alimuuliza kwa ukali, “Salma,
unafanya nini?” Salma hakujibu kitu kwani alikuwa akifuata masharti,
kwakweli Rahim alichukia na kujikuta akianza kumpiga Salma, alimpiga Salma hadi
Salma akazirai. Jioni ilipoingia sana Fetty akaaga na kuondoka
na Erick nae kuna kazi alisema kuwa anaenda kuimalizia, Bite
alimuuliza, “Kwahiyo utarudi?” “Ndio, nitakuja
kuwaaga” “Sawa” Bite aliitikia ila aliweza kuona huyu kijana
alikuwa na upendo wa aina gani kwa mdogo wake kwajinsi alivyoonyesha kumjali.
Muda kidogo simu ya Erica iliita, dada yake Bite aliichukua na kuona ni namba
ngeni akaamua kuipokea maana hakujua ni nani na anahitaji nini kwa Erica.
Alipokea maana alihisi huenda akawa ni mtu wa maana, alimuuliza kwanza ni
nani, “Mzee Jimmy anaongea hapa!” “Mzee Jimmy? Yupi na unashida
na nani?” “Shida yangu ni Erica, maana naona sauti sio ya Erica hii,
yuko wapi nina shida nae haswaaa” “Erica anaumwa” “Anaumwa? Nini
tena?” Bite akamueleza kwa kifupi juu ya kinachomsumbua Erica, basi Yule
mzee aliahidi kwenda, na kweli kwenye mida ya saa mbili usiku Yule mzee alifika,
na kugonga mlango akatoka mama yake Erica maana muda huo
alikuwepo, “Eeeeh wewe mzee usiye na haya kimekuleta kipi hapa nyumbani
kwangu?” “Nimekuja kumuangalia Erica” “Hatuna haja ya wewe kuja
kumuona, sikia nikwambia yani nakuchukia wewe mzee basi tu naomba uondoke
nyumbani kwangu” “Unanichukia bure ila jua mimi ndio
mkweo” “Huwezi kuwa mkwe wangu kamwe, siwezi kukubali mwanangu aolewe na
mzee kama wewe” Mama Erica akafunga mlango na kuingia ndani, kwahiyo
mzee Jimmy aliamua kuondoka ila kuna mzigo aliacha mlangoni kwakina
Erica. Muda kidogo alifika Erick kwa lengo la kuaga, akaona bahasha
mlangoni kwakina Erica, akaichukua na kuifungua akaona ina hela na kuna karatasi
limeandikwa ‘Nakupenda sana Erica’ Sepa
nayoooo.......!!!!!! Mama Erica akafunga mlango na kuingia ndani,
kwahiyo mzee Jimmy aliamua kuondoka ila kuna mzigo aliacha mlangoni kwakina
Erica. Muda kidogo alifika Erick kwa lengo la kuaga, akaona bahasha
mlangoni kwakina Erica, akaichukua na kuifungua akaona ina hela na kuna karatasi
limeandikwa ‘Nakupenda sana Erica’ Erick alisoma mara mbili mbili ule
ujumbe ila kwa haraka haraka akajua umetumwa na Rahim maana Rahim ndio
alifukuzwa hapo kwakina Erica, kwahiyo akahisi kutumia njia hiyo ili aweze
kumpata Erica maana kwajinsi alivyomsoma mama yake Erica alionekana kupenda hela
kwahiyo alihisi lazima Rahim katumia njia hiyo ili aruhusiwe kwenda tena kwakina
Erica, basi akaamua kuweka kwenye begi lake ambalo huwa anatembea nalo, kisha
akagonga kwakina Erica ambapo mama yake Erica alienda kufungua huku
akiongea, “Umerudi tena weee mjinga” Alipofungua akakutana na
Erick, kidogo huyu mama alihisi haya, Erick alimuuliza, “Kwani kuna nini
mama?” “Hakuna kitu mwanangu, karibu” Akamkaribisha ndani,
ambapo Erick alikaa na kuongea ongea kidogo tu maana Erica alikuwa amelala,
kisha akaaga na kuondoka. Alipofika hotelini yani alijikuta akimchukia
Rahim huku akisema, “Kwanza kaniharibia Erica wangu, kamuongopea na
kumzalisha bila malengo halafu sasa anataka tena kumchukua, siwezi kukubali hilo
jambo hata kidogo. Huyu Erica ni wangu tu” Akatoa ile bahasha na
kuhesabu zile hela, akakuta zipo milioni tatu, basi akaziweka tu pembeni akasema
hampelekei ila atamwambia kuwa pesa zake alichukua yeye, kisha akampigia simu
muda huo huo ila simu iliita tu bila ya kupokelewa, alipiga kama mara tatu
haikupokelewa na kuamua kuachana nayo. Muda huo Rahim alikuwa
hospitali maana ilibidi ampeleke mkewe hospitali baada ya kile kipigo cha haja,
mama yake Rahim nae alikuwa hospitali ila walihonga madaktari ili Yule mgonjwa
ijulikane alianguka na sio kupigwa. Mrs.Peter alirudinyumbani na mwanae
kwenye mida ya saa tano usiku ila muda huo huo hakujali kama muda umeenda wala
nini, aliamua kuongea na mwanae, “Hivi Rahim umeanzaje kumpiga mwanamke?
Hivi unajua kama mwanamke hapigwi? Na kumpiga mwanamke ni
dhambi?” “Sikia mama, laity ningekuwa najua kuwa wanawake wa kutafutiwa
wako hivi kwa hakika nisingekubali baba anitafutie Salma, kuna wanawake wengi tu
nilikuwa nawaona, wenye tabia njema ila sio tabia kama za huyu
Salma” “Mwanangu, Salma hana matatizo ila unajua nini? Hakuna mwanamke
duniani asiyekuwa na tabia za kike sema cha muhimu ni kumrekebisha, hata huyo
unayemdhania ndio angefaa sana bila kumrekebisha hafai, na kumrekebisha mwanamke
sio kumpiga, ni kumwambia tu kuwa hiki sipendi na hiki sipendi” “Mama
hujui tu, ni mengi naficha ya huyu mwanamke, kipindi kile nimerudi nilikaa nae
kwa siku chache tu hata wiki haifiki ila safari hii nimeishi nae sana, kwakweli
kanichosha” “Kwani kipi hupendi kwa Salma? Maana mimi nilimuona kuwa ni
msichana mzuri na aliyetulia kwani kipi hupendi kwake?” “Mama, Salma ni
msichana mbishi na hataki kuelekezwa hata umwambie nini haelekezeki, mara nyingi
nimemwambia sipendi dawa za kuchoma choma zenye harufu mbaya, angekuwa anachoma
udi nisingekuwa nagombana nae maana una harufu nzuri lakini sijui alikuwa na
dawa gani zinaacha harufu mbaya kwenye nyumba anadai ni kinga kaletewa na ndugu
zake kumkinga na mimba na mtoto atakapozaliwa. Nikavumilia, ukimwmbia kitu
anataka mabishano yani kwenye nyumba haijulikani mwanamke nani mwanaume nani,
namuangaliaga tu. Leo mapema nilimpiga kidogo na ndio ilikuwa mara ya kwanza
kumpiga sababu ya majibu yake ya shombo na kuja mwilini nimpige, na jioni ile
nimemkuta kajifungia ndani akichoma dawa gani sijui huku akiongea ongea maneno
ya ajabu, mama siwezi kuishi na mwanamke mshirikina kama huyu” “Sasa
unatakaje?” “Mama nampa Salma talaka, bora nioe mwanamke
mwingine” “Usiniambie unataka kumuoa Erica, eeeeh!” “Erica nae
ni mwanamke mama, naweza nikamuoa hata yeye” “Hebu niondolee wazimu wako
mie, Erica ni mwanamke ndio ila hana heshima hata kidogo yani hapa atatembea
hadi na baba yenu, simtaki huyo mwanamke. Na kama unawazo la kumuacha Salma ili
uoe huo uvchafu wako unisahau kabisa kama mimi ni mama yako” Rahim
aliondoka na kumuacha mama yake pale, kisha yeye kwenda kulala
tu. Kulipokucha mapema kabisa, simu ya Erica ilianza kuita
ikabidi tena Bite apokee simu ile ya mdogo wake maana namba ilikuwa ngeni
pia, “Mzee Jimmy anaongea hapa” “Mbona jana sikukuona
tena?” “Nilikuja ila mama yenu alinitimua” “Aaaah kumbe ndio
wewe asiyekutaka mama” “Ndio mimi ila ananichukia bure tu kwa makosa ya
miaka ya nyuma kabisa, mwambie hata maandiko yamesema samehe sabab mara sabini.
Ila siyo lengo hilo, lengo ni kuwauliza kuwa ule mzigo nilioacha jana mlangoni
mmeupata?” “Mzigo? Hapana bhana hakuna mzigo tulioupata” “Kuna
mzigo niliacha jana, niliacha pesa kwenye bahasha kiasi cha milioni
tatu” “Mmmh ngoja niulize” Bite akaenda kumuuliza mama yake
maana kwa muda huo ndani walikuwa wawili tu, “Mmmmh mbona nje mimi
nimefagia sijaona kitu” “Anasema eti aliacha mlangoni” “Sasa
nani achukue? Ingekuwa getini sawa, sasa mlangoni nani achukue?” Bite
akawaza jambo na kumuuliza mama yake, “Kwani huyo mzee na Erick nani
alitangulia kuja?” “Yule mzee ndio alitangulia na alivyoondoka tu, muda
kidogo ndio akaja Erick ila jana hajakawia sana kuondoka” “Mmmmh nina
hisia mbaya mama, sio Erick kachukua hizo hela kweli?” “Mmmh mwanangu,
Erick hana hiyo shida, yani nakataa kabisa, yani Erick achukue milioni tatu za
nini? Hana hiyo shida Erick, labda huyo mzee muongo” “Hapana mama, nina
hisia ni Erick tu. Kwanza Yule kijana mdogo unamsifia ana hela, anatoa wapi hizo
hela kijana mdogo vile? Mama mara nyingine kuwa makini, isije kuwa Yule kijana
ni mwizi au anauza madawa ya kulevya, tunafurahia hela zake hapa kumbe
tunachukua hela haramu mama yangu, kuwa makini” “Kheee na wewe Bite,
kwani James ni mkubwa? Mbona ana hela?” “Ila sio hela nyingi kama za
huyu kijana unazosema, James familia yake inajiweza, James ana kampuni yake
kaachiwa na baba yake, huwezi kumfananisha na huyo Erick, hatujui ndugu zake,
hatujui rafiki zake wala jamii yake, hizo hela anazitoa wapi?” “Yule
Erick nae familia yake ina hela, Yule kijana usimuingize katika hizo biashara
haramu wala nini, na hawezi kuchukua hela za huyo mzee. Mwanangu huyo mzee
humjui tu ila huyo mzee hafai hata kidogo, kwanza usikute ni muongo na wala
hajaacha hizo hela na kama ameacha kweli basi zimesombwa na upepo ila swala la
kusema Erick kachukua halipo kabisa” “Mmmh sawa mama, nakubaliana
nawe” Hakuweza kubishana zaidi na mama yake ila kiukweli Bite hata
alitamani nusu ya upendo aliokuwa nao Erick ndio ungekuwepo kwa James maana
mumewe kuanza kumpenda yeye ni mpaka asemwe na watu. Leo ndio
ilikuwa siku ambayo Dora na Sia walipanga kwenda kwa babu wa Bagamoyo, kwahiyo
walikutana na kuanza safari ya kwenda kwa huyo Babu ambapo alianza kuingia Dora
na kueleza azma yake kisha akaonyeshwa wabaya wa Erica walioshiriki kumletea ule
ugonjwa alishangaa kuona Derick nae aliungana na wale wanawake, Yule mganga
akamueleza, “Yani ni hivi, huyu mwanamke wa kwanza alienda kwa huyu
mwanaume kuchukua majina ya huyo binti na kisha alipotajiwa akamtumia huyu
mwanamke wa pili kisha huyu mwanamke wa pili ndio alimuendea kwa huyu mzee na
kumfanya walivyomfanya, lengo lao walitaka awe chizi na mwisho wa siku rafiki
yako angegongwa na gari na kufa, sema haijawezekana kuwa chizi maana rafiki yako
ana imani kubwa sana na Mungu. Ila mimi nitakusaidia kukupa dawa ya kumponya
kabisa na tunaweza kuwarudishia wale makombora” “Ila ndugu zake
wamekazana na maombi” “Hii dawa waambie waache hayo maombi yao maana
miungu ndio itamsaidia huyo mgonjwa wao” “Sasa sitaweza maana hata
wakiniona wananitimua, hivi nitawezaje kuwaambia waache maombi na waamini hizi
dawa?” “Najua unanijua dawa zangu huwa haziongopi na hakuna
kinachoshindikana kwangu, vyote vinawezekana kuna dawa ya kunywa nitakupa ambapo
muda nitakayokupa utainywa, na leo ukirudi kwako unainywa halafu kesho jiandae
nenda kwa huyo rafiki yako, ukiwa unakaribia kwao inywe baada ya hapo hakikisha
unaingia kwao saa saba mchana, ukiingia tu kwanza watakuwa na mshangao wa
ulivyopendeza, kitendo cha wewe kuwapa salamu kitafanya wasikilize kila utakacho
waambia ndio utaanza kufanya dawa kama nilivyokuelekeza na keshokutwa mtamleta
huyo mgonjwa hapa kwangu ili apone kabisa maana akija hapa ndio funga kazi, yani
usijali hao wenyewe watambeba mgonjwa wao na kumleta hapa, yani kwangu hakuna
kinachoshindikana yani wasiokusikiliza watakusikiliza, mimi ndio kila kitu,
ukisikia wananisifia babu wa Bagamoyo ujue kuna kitu kwangu ambacho wengine
hawana” Kwakweli Dora alifurahi sana kwani alitamani siku zote kupata
dawa ya kusikilizwa kila anachosema, alimshukuru Yule mganga ambapo alimpa
kwanza dawa hiyo ya kusikilizwa na kuinywa kama alivyoelekezwa kisha nyingine
aliambiwa anywe akifika na nyingine akifika kwakina Erica, kisha akampa dawa za
kumfanyia Erica na maelekezo kuwa nyingine amnyweshe na nyingine amuogeshe. Dora
alishukuru sana na kuulizia ile dawa ya kusikilizwa vizuri, “Kwahiyo
nitasikilizwa na kila mtu?” “Yani hii dawa inaenda kulainisha matamshi
yako, hakuna utakachosema kisisikilizwe, hii ndio hutumiwa na wanasiasa wengi
sana. Sababu wewe umekuwa mteja wangu mzuri ndiomana nimekupa, unaweza shangaa
mtu kaja kakwambia jambo la ajabu tu ila umemfuta kumbe sababu yah ii dawa,
matapeli wengi huitumia ndiomana anamlainisha mtu kwa maneno na mtu anatoa kila
kitu baada ya hapo anajuta maana maneno yale hayana ukweli hata
kidogo” “Kwahiyo hata hawa wanaojifanya wanapenda
maombi” “Achana na habari za maombi kwangu, wewe ukifika anza na salamu
ili sauti yako yenye kivutio iwaingie masikioni na hapo unajikuta umewalainisha
na gafla wanaanza kukusikiliza wewe” “Oooh asante sana babu, nashukuru
sana” Kisha akatoa laki tatu kwenye chungu cha babu kama hela ya
shukrani halafu akatoka na Sia kuingia, aliambiwa aweke kifungua kilinge
akatakiwa kuweka elfu hamsini sababu ya swala lake, basi Sia aliweka ile pesa,
Yule babau akamwambia, “Usishangae pesa ndefu ni sababu kazi yangu ni ya
uhakika yani ukitoka hapa, leo ukimfanyia huyo mtu hiyo dawa basi nakwambia
hafurukuti kwako” Kisha akampa dawa kama alizopewa Dora za kumvuta
James, ila yeye alitaka na dawa nyingine ya kumuita Erick ili aweze kumpa hiyo
dawa, “Sawa sawa, hapa hakuna kinachoshindikana ila kukuongeza dawa
nyingine inabidi uandae elfu hamsini nyingine ya shukrani” “Sawa hakuna
tatizo” Basi Yule mganga akampa dawa nyingine Sia ya kuchoma ili kumvuta
Erick na akifika ampe tunda atakalokuwa ameweka dawa kisha ampe Erick na baada
ya hapo ndio ampe chakula chenye dawa ili awe wake kabisa, “Kwahiyo hii
ya kuchoma uwe unachoma huku unasema Erick njoo yani unasema hivyo mpaka
utakapomaliza, utaona mwenyewe yani atakuja bila kumuita sasa ndio umpe hilo
tunda ale yani jitahidi kumlaghai ale hilo tunda. Ila ni vizuri uchome mchana
ili jioni afike maana anaweza akalala huko huko na inakuwa rahisi kumpa chakula
chenye dawa” “Sawa, nashukuru sana” Basi akatoa na ile hela ya
shukrani na kutoka nje kisha kuongozana na Dora huku wakiondoka, yani njia nzima
alikuwa akimshukuru Dora kwa kumpeleka kwa Yule mtaalamu, “Yani sina la
kukwambia nashukuru sana” “Wewe usijali, mambo yakishakamilika niite
nije nimuone shemeji” “Sawa, hata usijali” Muda huo Dora
hakuelewa kuwa anayefanyiwa hizo dawa ni Erick Yule Yule mchumba wa
Erica. Bite alitulia na mdogo wake akiendelea kumfanyisha
mazoezi mazoezi ya baadhi ya vitu, akapiga simu Yule mwanamaombi na kuwaambia
kuwa amesharudi kwahiyo ataenda kesho yake kwaajili ya kumuangalia Erica na
kufanya maombi pamoja nao, “Kwahiyo utafika muda
gani?” “Nitafika nadhani mchana sababu nahitaji tufanye maombi na tusome
neno kiasi” “Karibu sana” Bite alishukuru na kuagana nae, mama
yao alivyofika alimwambia jinsi alivyoongea na Yule mwanamaombi, “Oooh
afadhali aje, nahamu sana ya kumfahamu huyo mama maana kanitia moyo sana yani
sana kwa kipindi hiki cha Erica, namshukuru sana kwakweli, amakweli Mungu
kamtumia huyu mama” “Basi kesho anakuja mama” Basi mama Erica
alikaa na mwanae Erica huku akifurahi tu maana alivyoambiwa Yule mama anafika
alijikuta akipata amani ya moyo kabisa. Jioni yake alifika Erick kama
kawaida ila kumuuliza chochote hawakuweza na walimwambia tu kuwa Yule
mwanamaombi anafika kesho, akauliza tu ni muda gani, “Kwahiyo kesho saa
ngapi?” “Kasema mchana” “Kesho kuna kazi nilikuwa nataka
kuzimalizia ila nitakuja kwaajili ya hayo maombi kwani hata mimi najiona
nikihitaji maombi pia” “Karibu sana” Basi Erick aliendelea
kuongea ongea na Erica pale kwani yeye ilikuwa fahari tu kwake kila anapoongea
na Erica. Ila Rrick na siku hiyo aliporudi hotelini alijaribu kumpigia
tena Rahim kwani alitaka kujua ukweli wa ile hela. Salma
aliruhusiwa kurudi nyumbani, basi Rahim akamchukua kwenye gari yake na kurudi
nae nyumbani, alifika nae huku akimpa pole kw akumpiga, “Pole ya nini
unanipa shetani mkubwa wewe” “Kheee nimekuwa shetani!” “Ndio ni
shetani wewe, huna upendo hata kidogo mwanaume gani wewe. Ni malaya ila
nakuvumilia, nimekuvumilia sana hadi kukuzalia mtoto ila mwanaume huna huruma
unathubutu kunipiga kweli mwanamke nikiwa na mtoto mchanga kama huyu? Yani nyie
wanaume mnapenda sana kutuonea wanawake” “Wewe endelea kuongea ila dawa
yako wewe ni kukuolea mke wa pili” “Thubutuuu mlete huyo mke uone kama
hajaondoka anatambaa” “Hivi hujionei huruma Salma, kumbuka ndio kwanza
umetoka hospitali. Huwezi kunyamaza” “Sitanyamaza kamwe hadi uache
uonevu wako, mmezidi kutuonea ila tunyamaze kama samaki baharini kameza maji,
jamani mimi sinyamazi yani Rahim ukifikiri nitanyamaza sahau, siwezi kuvumilia
uonevu kama huu” “Aaah wewe, nadhani unanitafutia lingine,
kwaheri” Rahim aliamua kuondoka, ila Neema sababu alikuwa nje alisikia
yale maongezi na kuingia ndani kwa mwenzake na kumpa pole ya ile kupigwa, ila
Salma aliitikia kwa chuki maana hakuwa na furaha, “Usiwe hivyo mwanamke
mwenzangu, najua umeumia. Ni kweli wanaume wana roho mbaya ila sio wote. Unajua
unaposema kwa mtu kuwa mwanaume kanipiga bila makosa na kukwambia umueleze
chanzo hakika ukimueleza chanzo kama chako atakuona kuwa wewe ndiye mwenye
makosa, siku ile nimeongea na wewe kuwa inatakiwa tujue wanaume zetu wanapenda
nini ili tuenende na kile wanachopenda ila hukutaka kunisikiliza” “Wewe
Neema unaongea tu ila mwenzako akinyolewa zako tia maji” “Sio hivyo
Salma, ionekane kweli umeonewa labda mwanaume kaanza tu kukupiga bila sababu ila
sio kama ulivyofanya wewe yani unampa sababu mwanaume ya kukupiga. Nakupenda
rafiki yangu, nakupenda kama mwanamke mwenzangu ila napenda ujirekebishe na uwe
mpya rafiki yangu. Nakwambia kila siku hakuna mwanaume anayependa mwanamke
mwenye gubu, hakuna mwanaume anayependa mwanamke wa kubishana nae ndani ya
nyumba, hakuna mwanaume anayependa mwanamke mkorofi na hakuna mwanume anayependa
mwanamke mshirikina” “Kwahiyo mimi unaniona mshirikina
eeeh!” “Kama unachoma dawa ambazo mumewe hazifahamu unafikiri ni nini?
Unafikiri mumeo atakuitaje? Hivi mfano mumeo angeingia chumbani na kukukuta
mkewe ukiswali angefikia hiyo hali ya kukupiga? Na kama angekupiga basi Mungu
angemfundisha somo ila sio kwa ulichokuwa unafanya wewe, yani unampa mwanaume
sababu za kukupiga, sio vizuri ndugu yangu. Tumeamua kuolewa basi tutulie kwenye
ndoa zetu na tuwatii waume zetu” “Kwahiyo wewe mambo uliyofundwa huko
wakati unaolewa ndio unaniletea mimi eeeh! Mwanaume akuonee umuangalie tu,
mwanaume akutukane umuangalie tu, siwezi kwakweli” “Salma nadhani
hunielewi, kuna mambo mtu ukifanyiwa kweli kila mtu anajua kama unaonewa lakini
sio kwa stahili unayoenda nayo wewe, yani wewe ndiye unayempa sababu Rahim
amfikirie Erica, ila ungejirekebisha kwa hakika angeamua kuishi nawe kwa
upendo” “Ngoja nilale mie nimekusikia” Basi Neema alitoka ila
kwa kiasi Fulani maneno aliyosema Neema yalimuingia kwani ukizingatia hata ile
dawa kuifanya ilikuwa ngumu kwahiyo alijikuta akielewa tu taratibu kile
kilichosemwa na Neema. Ilikuwa ni jioni ambapo Dora na Sia
walifika mjini na kuachana, basi Dora alienda kwao moja kwa moja akanywa ile
dawa, alitaka kujaribu kuona inavyofanya kazi, akampigia simu mzee Jimmy
akimuomba waonane ili waongee, yani mzee Jimmy alikubali kiurahisi sana, na
kwenye mida ya saa tatu usiku wakakutana, Dora alianza kumueleza mzee Jimmy
anachotaka ili kuangalia kama huyu mzee atamuelewa au la, “Nimechoka
kutembea kwa miguu, nahitaji gari la kutembelea” “Umeniambia kwa haraka
sana Dora, ila nitakupatia” Kwakweli Dora hakuamini maana alikuwa
akijaribisha tu kuona ile dawa inavyofanya kazi, kwahiyo swala la kukubaliwa na
mzee Jimmy kwake ulikuwa ni ushindi mkubwa sana, kisha akamwambia
tena, “Sina hela ya kutumia ujue, halafu kesho nataka kwenda saluni
nikatengeneze nywele na ninataka kununua nguo nyingine na
viatu” “Kwahiyo unataka kiasi gani?” “Naomba milioni
nne” “Sikia basi, leo nitakupa milioni mbili halafu kesho njoo ofisini
kwangu uchukue mbili nyingine” “Wow, nitakuja kesho asubuhi mpenzi
wangu” “Kitu kingine ningependa unioe” “Mmmmh kuna nini leo
mbona kila kitu nakuitikia Dora?” Ikabidi Dora abadilishe mada maana
huyu mzee asije akamshtukia bure, akamuuliza kuwa gari la kutembelea atampa
lini, “Kesho njoo ofisini kuchukua hizo milioni mbili zingine halafu
nitaangalia utaratibu wa wewe kupata gari maana kidogo sasa hivi mambo yangu
hayajakaa sawa” “Nashukuru sana” “Halafu leo si utanipa
tena” “Mmmh leo nimechoka labda kesho” “Sawa hakuna
tatizo” Yani Dora alifurahi sana vile ambavyo amesikilizwa vizuri na
mzee Jimmy kisha akataka kuondoka kwahiyo Mzee Jimmy akaenda na Dora ATM na
kutoa milioni mbili akamkabidhi Dora kisha kumpeleka kwao, yani Dora aliingia
kwao akichekelea sana. Alienda chumbani kwake akiwa na furaha isiyo kifani na
kujisemea, “Hivi nilikuwa wapi kunua hizi dawa jamani! Sasa hivi
ningekuwa tajiri mimi maana kila kitu ningekuwa nacho, huyu mzee leo kalainika
kama sio yeye, kesho naenda kwa huyu mzee kwanza kuchukua hela yangu kisha
naenda kwakina Erica kuharibu kabisa, hakuna cha maombi wala nini na wao
wataanza kama mimi kuzunguka kwa waganga tuwe wengi mjini” Akacheka na
kujilaza kwa furaha maana kwake ilikuwa ni ushindi mkubwa
sana. Dora asubuhi na mapema aliamka na kujiandaa kisha akanywa
ile dawa na kwenye mida ya saa tatu akaenda ofisini kwa mzee Jimmy, alifika na
kumkuta Yule mzee ofisini kwake na kumsalimia, Yule mzee alitabasamu tu kisha
kumwambia, “Dora umekuwa mrembo sana, yani nakuona unazidi
kupendeza” Dora alikuwa akicheka huku kimoyomoyo akisema ‘mambo ya babu
wa Bagamoyo haya’ Basi kabla hata hajaeleza swala la kufata pesa,
alikuta Yule mzee kashamuwekea pesa kwenye bahasha na kumpatia ila Dora
akamwambia, “Ningeomba uniongezee mbili nyingine” “Dora, saivi
sipo vizuri sana maana mambo yamejichanganya ila usichukie ngoja
nikakutolee” Dora alisubiria na mzee Jimmy alienda kumtolea milioni
mbili zingine na kuja kumkabidhi kisha akaahidiana nae kuonana jioni, halafu
Dora akaondoka. Mzee Jimmy alijiuliza sana kuwa inakuwaje amekuwa hivyo
kwa Dora, yani Dora anakomba hela zake kama kitu gani. Hakuelewa ila alijiona ni
sawa kabisa kumpa zile pesa Dora wakati gata alikuwa akihisi mambo kuwa sio sawa
kwenye kampuni yake. Dora aliondoka na kuelekea benki nyingine kuweka
zile pesa alizopata kwa mzee Jimmy kisha akapitia mahali ale kabisa akivuta vuta
muda wa kwenda kwakina Erica. Erick siku hiyo alienda mapema
kabisa kwakina Erica maana alitaka Yule mwanamaombi amkute tayari akiwa amefika,
aliowakuta pale ni Bite, mamake Erica, Angel na Erica mwenyewe maana Mage siku
hiyo alisema hatoweza kufika sababu alikuwa na mambo mengi ya kufanya. Baada ya
muda waliwasiliana na Yule mwanamaombi na kumuelekeza hapo na alipofika kituoni
ni Erick ndio alienda kumfata na gari yake huyo mwanamaombi, alifika kituoni na
kukutana nae na kumsalimia kisha kupanda kwenye gari yake ila gafla akajisikia
kama kwenda kwa Sia yani hakuwa na raha kabisa mule kwenye gari alitaka tu
amfikishe Yule mwanamaombi kwakina Erica halafu yeye kuondoka, walifika kwakina
Erica na kushuka, kisha kuongozana na Yule mama hadi ndani ila walipoingia tu
ndani Erick alitaka kuaga ili aondoke ila Yule mama alimwambia asiondoke kwanza
hadi wamshukuru Mungu, Erick alikubali ila alikuwa akitaka waombe haraka haraka
na waondoke, Yule mama alianza maombi na yale maombi yake yalichukua kama robo
saa hivi yani Erick hakupenda kwakweli ingawa alisema kuwa nay eye anahitaji
hayo maombi ila kwa muda huo moyo wake haukuwa kwenye maombi hayo kabisa, basi
walipomaliza, aliaga tena na kutaka kuondoka. Yule mama alimshika mkono
Erick kabla hajaondoka, Erick alihisi kama kuna moto unaingia kwenye mwili wake
na kujikuta akianza kupiga kelele basi Yule mama alianza kumuombea Erick yani
Yule mama hakushughulika kwanza na Erica aliyemgonjwa ila alishughulika na Erick
maana aliona kuna kitu hakipo sawa kwa Erick, alimuombea sana Erick tena kwa
muda mrefu, Erick alijikuta tu akikaa chini huku akilia na bila kujua anacholia
ni kitu gani, huyu mama alipomaliza kuomba alimwambia Erick, “Kuna nguvu
za giza zilikuwa zinakuta mwanangu ila Mungu ni mwema. Roho wa Bwana
alinionyesha nikuombee na sasa uko huru” Kisha Yule mwanamke akawaomba
waimbe pamoja nae nyimbo za kuabudu wakaanza kuimba, na wakati wa kuimba kuna
mtu akafungua mlango na kuingia ndani, mtu huyo alikuwa ni Dora, halafu Dora
kama alivyoshauriwa na Yule mganga wake alianza kwa salamu, “Hali zenu
jamani!” Yule mama alihisi kuna kitu sio cha kawaida kipo kwa Yule
msichana, wote walibaki wakimshangaa Dora, ila huyu mama alimvuta Dora mkono na
alipomvuta tu Dora alianza kupiga kelele kama mtu mwenye mashetani ndipo Yule
mama alianza kumuombea, Dora alianguka chini na kujikuta akisema kila kitu
alichoambiwa kwa mganga yani hakuacha kitu aliropoka hadi dawa alizopewa na yule
mganga, ndipo Yule mama alipokazana kumuombea Dora na alimuombea sana na
kugundua kuwa Dora ana tatizo lingine la jinni mahaba, kwahiyo akafanya kazi ya
kumuombea na hilo tatizo pia, ilichukua muda mrefu sana katika kumuombea Dora
hadi akatoa dawa zote alizoenda nazo kwa wakati huo, kwakweli walishangaa sana
kwani hakuna aliyeelewa kuwa Dora angekuja na dawa za namna ile maana lazima
angeogopa sababu walishamwambia kuwa wamejikita kwenye
maombi. Alipomalizana nao ndipo alipoanza kumuombea Erica maana
alishamuombeaga sana na maombi yake karibia yote ni juu ya ugonjwa uliompata
Erica, alimuombea sana na baada ya muda Erica alisimama na kufanya ndugu zake
wote wafurahi, Yule mama alianza kumshukuru Mungu kwa kumponya
Erica. Walipomaliza Erica alianza tena kuongea ila aliongea taratibu
sema ilikuwa ni furaha sana kwani alikuwa akiongea, kwakweli waliomba kwa pamoja
na hadi maombi yanamalizika Dora alijikuta hana hamu kabisa hata ya kurudi kwao
alijikuta akitoa machozi tu kama anajutia kwa yale aliyokuwa
akiyatenda. Huyu mama aliwaeleza mambo yatakayowasaidia
zaidi, “Yani kuanzia sasa mnatakiwa kuwa watu wa maombi, sio kujutia tu
yale uliyoyafanya nyuma ila kusimama imara na kuendelea mbele, inatakiwa
tumuombe Mungu kila mara sio tu tunapopatwa na matatizo. Ukiacha kumuita Mungu
basi shetani anaweza kukuangusha kwa urahisi mno. Kwahiyo ni muhimu sana kufanya
ibada” Wote waliitikia pale ila Erick hakujua kama ataweza kuanza
kufanya ibada, halikadhalika na kwa upande wa Dora ila walisema kuwa
watajitahidi. Usiku ulipoingia ilibidi Erick aage kuwa anaenda kwao,
ikabidi ampe lifti na Dora ya kurudi kwao muda huo Dora hakuwa hata mtu wa
kuongea ongea tena mpaka alipofikishwa kwao na kushuka kisha Erick alirudi kwao
moja kwa moja yani hakujisikia kabisa kwenda hotelini maana alikuwa na hamu ya
kufika kwao. Sia alishangaa sana kuwa kufanya kote dawa mpaka
jioni Erick hakufika kwao, aliumia mno na ukizingatia alishaandaa tunda la kumpa
Erick, alipoona usiku umeingia alijiandaa na kusema ataenda yeye mwenyewe
kwakina Erick kumpa lile tunda ale kwani ile hela aliyotoa kwa mganga ilimuuma
sana alitaka apate majibu ya anachokitaka. Basi akaondoka na kwenda
kwakina Erick, alipofika aligonga na mlinzi alimfungulia,
akamuuliza, “Hivi leo Erick yupo?” “Tena amefika muda sio
mrefu” Basi akasogea hadi kwenye nyumba ya kina Erick na kuingia ndani
maana alishazoeleka pale sababu ya Tumaini, akakutana na Erick mlangoni
ilionyesha kama Erick alikuwa akitoka, akamsalimia Erick kisha kumpa lile
tunda, “Nini tena?” “Chukua hili apple ule Erick, ni ishara ya
upendo wangu kwako” Erick alichukua lile tunda na kumfanya Sia atabasamu
kwani alijua Erick akila tu bnasi kwisha habari yake, ile cha kushangaza Erick
alisogea mpaka kwenye ukuta wa nyumba yao na kulirushia lile tunda
nje. Erick alichukua lile tunda na kumfanya Sia
atabasamu kwani alijua Erick akila tu basi kwisha habari yake, ila cha
kushangaza Erick alisogea mpaka kwenye ukuta wa nyumba yao na kulirushia lile
tunda nje. Kitendo kile kilimuumiza sana Sia, alijikuta kama kapatwa na
uchizi hivi hata akatamani kumpa matusi Erick, yani muda huo hakuwaza tunda ila
aliwaza laki yake tu, aliamua akimbilie nje upande ambao Erick alirusha lile
tunda maana hakutaka ile dawa ipotee, aliona vyema aliwahi ili afanye kila hila
Erick ale lile tunda, kiukweli Erick pia alimshangaa jinsi alivyoonekana
kushtushwa na kile kitendo cha kutupa tunda. Sia alikimbia akatoka nje
hata mlinzi wa ile nyumba akamshangaa kuwa huyu dada imekuwaje kachanganyikiwa
au nini, alikimbia na kuzunguka ule upande ambao Erick alirusha tunda, hakuamini
macho yake kuona kuna kijana yupo kulifakamia lile tunda,
alimshtua “Kheee wewe kwanini umeokota hilo tunda?” “Dada
jamani, nilikuwa napita na hili tunda likanipiga kichwani kwa bahati nimelidaka
ila najua matajiri wana hela sana yani tunda kama hili la gharama linatupwa?
Nikaamua kulila, ubaya wangu ni nini au kosa langu ni nini?” Sia
alichukia sana kwani huyu kaka ndio kwanza alikuwa akimalizia lile tunda,
kiukweli Sia hakuwa na la kufanya na kuamua kuondoka hata kuingia tena kwakina
Erick hakutaka. Sia aliingia kwao kwenye mida ya saa tano usiku, wakati
anafungua mlango kuingia ndani alishtukia kuna mtu nyuma yake, kumuangalia
alikuwa ni Yule kijana aliyemkuta akila tunda, “Kheee wewe umenifata
hadi kwetu kwanini?” “Nisamehe ila sijaweza kuacha kukuangalia kwa
urembo wako, nakupenda sana, yani sijaweza kuacha uondoke machoni pangu,
nimekufatilia toka pale hadi hapa” Sia alipumua maana ya siku hiyo
yalikuwa makubwa kwake, kufatiliwa na asiyehusika tena ni jambo lililomkera
sana, akajiuliza afanyeje na Yule kijana hakujua, alimuacha nje na kufunga
mlango kisha kuingia ndani na kulala kwani kichwa chake kilikuwa kimevurugika
haswaa ukizingatia kuna chakula alishapika kwaajili ya Erick na alishamuwekea
dawa atafanyaje sasa, hakuwa na la kufanya zaidi ya kukubali kile
kilichotokea. Palivyokucha aliamka na kutoa vyombo vichafu nje pamoja na
kile chakula alichokuwa amemtayarishia Erick, kisha akaenda kuchota maji na
kusahau kama kulikuwa na kijana usiku akimfatilia sababu alikula lile tunda,
basi alivyorudi na maji yake alishangaa kumuona Yule kijana akila kile chakula,
kwakweli Sia alishtuka sana, “Mungu wangu na chakula umekula, uwiiii
nitafanyaje mimi. Wewe nani kakuruhusu kula chakula changu?” “Nilikuwa
na njaa sana, nikahisi kuna chakula umekifunika kwenye hivi vyombo kuliko
kukitupa nikaona bora nile.” “Haya nenda kwenu” “Siwezi kuondoka
hadi uniambie kuwa unanipenda, nakupenda sana yani nakuona kama
malaika” “Kheee makubwa, sasa hapa kwangu utaumia, nenda zako
tu” “Siwezi, nakupenda sana” Kwakweli huu ulikuwa ni mtihani
mkubwa sana kwa Sia ingawa ingekuwa hivi kwa Erick ingekuwa ni ushindi mkubwa
sana kwake, inamaana huyu kijana asingemuona Sia angepata shida sana kumtafuta
ila uzuri Sia mwenyewe alitoka kuangalia tunda lake kuwa limeangukia
wapi. Salma alikuwa mpole gafla maana mumewe hakurudi kabisa
tangu ameondoka sababu ya kelele zake, ana maumivu ya kupigwa na mumewe hataki
kurudi, ila leo alipata ugeni yani mama yake na dada yake, walikuja kusalimia na
kumkuta akiwa na mawazo sana, mdogo wake alikuwa na mtoto na ndiye aliyewapokea
na kuwakaribisha, waliingia ndani na kuanza kumpa hongera Salma na pole maana
hawakufika toka ajifungue, mamake alimuuliza kuwa imekuwaje hana furaha
kuwaona, “Mama nyie ni wabaya sana, yani kama sina ndugu vile, kweli
nimejifungua hadi leo ndio mnakuja? Mimi hospitali nakuja kuangaliwa na wakwe na
majirani sijui na ndugu wa mbali? Siku nimeruhusiwa sina wa kunifata kweli?
Mlichonifanyia sio sawa, hata kama wewe sio mama yangu mzazi ila haikutakiwa
unifanyie hivi, angekuwa ni mtoto wako wa kumzaa ungemfanyia hivi? Bora mama
yangu mzazi angekuwepo kwakweli, nateseka sababu sina mama” Yule mama
alisema, “Yani Salma hii ni sababu ya kufanya tushindwe kufika kwa muda,
yani Salma huna zuri hata moja wewe, hivi mimi kama nina roho mbaya
ningemuonyesha Yule mzee kuwa wewe ndiye unafaa kuwa mke wa mwanae? Kwanini
nisingeonyesha hao wanangu ila nikakuonyesha wewe? Yani Salma unashindwa kuuliza
tatizo ni nini ila unabaki na lawama tu” “Wewe mama ndio zako tu huna
lolote, sijui ningemuonyesha mzee Yule watoto wangu. Kama ipo ipo tu, hata
ungeonyesha watoto wako labda wasingependwa, usijitetee wala nini mmenifanyia
roho mbaya tu hakuna cha sababu wala nini, ulinionyeshea mimi sababu hukutaka
nikae nyumbani, ulihisi nitakuja kuteseka kwenye ndoa kwa kuolewa na mtu
nisiyemfahamu” Kiukweli hawakumuelewa kuwa imekuwaje hadi maneno yote
yale yanamtoka, ila mdogo wake ndio akasema, “Dada ana hasira hivyo
sababu alipigwa na shemeji” “Halafu wewe hayakuhusu muone vile ndiomana
hunenepi” “Sasa wewe Salma ni mnene jamani! Hata unamsema mdogo wako
bure tu” “Kwanza sihitaji kuja kuniona, ondokeni siwataki nyumbani
kwangu” Hakuna walichoongea akawasikia zaidi zaidi akaamua kuwatimua tu
ikabidi wabebe mizigo yao na waondoke. Walipoondoka tu kama kawaida
Neema alimfata Salma na kumuonya, “Unajua Salma unafanya mambo kwa
hasira sana, umeudhiana na mume ila unachukia hadi ndugu kwa mtindo huo
utamuudhi hadi mama mkwe halafu utajikuta ukiiacha ndoa yako” “Neema
sikia, nikiachika mimi hapa si utabaki wewe mkwe mwema, sitaki mafundisho yako,
kafundishe ndugu zako huko” “Ila wewe dawa yako inachemka, najua wa
kumleta kwako na utakaa sawa tu” “Hebu nitolee upuuzi si umefurahi hivi
mume wangu hajarudi nyumbani, niache mie” Kwakweli Neema alisikitika
sana vile mwenzake alikuwa haelekezeki. Dora leo aliamka na
kutulia kwao huku akijitafakari sana, alikuwa akiwaza kuhusu mambo mbalimbali,
mara nyingine aliona ni sawa kukombolewa ila mara nyingine aliwaza vitu vingine
ila alijikosoa mwenyewe, “Ila hela zisizokuwa na halali si nzuri
kutumia, ila bora nilichukua kabisa hela za mzee Jimmy, asifikirire sijui
nimebadilika ndio nitarudisha hela zake thubutuuu hii ni matunda ya kazi
niliyofanya juu yao, ila mmmh kweli nilikuwa na jinni mimi mbona sijisikii hata
hamu jamani, nipo kawaida kabisa. Ila kwa Yule mganga siendi tena yani tena, kwa
Mungu ndio kuna nguvu kwakweli, kwa mganga hamna kitu. Ila mimi hii hali ya
tamaa nadhani na mama yangu kasababusha maana anataka nilishe familia nzima bila
kujali pesa nitatoa wapi” Muda kidogo Mama yake alienda kumkurupua na
kumwambia, “Hivi Dora unajua kama mdogo wako hajarudi kabisa tangu
jana” “Aaaah mama jamani, hata salamu jamani! Hajarudi ndio ila mbona
mimi sitafutwagi hivyo nisiporudi?” “Wewe ushakuwa mkubwa, halafu
nishakuchunga nimechoka ila mdogo wako hana tabia kama zako” “Ila
kumbuka Yule ni wa kiume na mimi ni wa kike yani ulitakiwa kunichunga mimi zaidi
ya Yule ila unamchunga Yule na kuniacha mimi ni haki kweli hiyo?” “Yule
hajawahi kutokurudi nyumbani hata kama kakua ila sio kama wewe, mdogo wako hadi
saa nne hii haonekani nakwambia hata hujali yani upo tu. Jiandae hapo tuanze
kumuulizia mdogo wako maeneo mbalimbali” Hiki ndio kitu ambacho
hakupenda kwa mama yake huyu yani alionekana kumjali zaidi mdogo wake ambaye
walipishana miaka miwili tu, yeye hakujaliwa kama mdogo wake alivyojaliwa, ni wa
kiume ila hajaonekana nyumbani mama yake tumbo joto, hakujua ni wapi ataanza
kumtafuta basi akaenda tu kuoga ili kujiweka sawa. Alipotoka kuoga
akakuta simu yake inaita, akaipokea na mpigaji alikuwa ni Sia, “Eeeeh
Sia, unatatizo gani?” “Nina tatizo kubwa kwakweli” “Tatizo
gani?” “Naomba njoo kwetu ili unisaidie hili tatizo nitalitatuaje,
nakuomba sana nakuomba” “Sawa hakuna shida nakuja” Sababu aliona
kuendelea kubaki kwao mama yake angemsumbua na hizo habari za kutokumuona mdogo
wake, kwahiyo alijiandaa na kutoka na kuona ni veyema aende kwa kina Sia kuliko
kubaki kwao. Alivyofika kituoni, alimpigia simu Sia naye alienda
kumpokea, basi akaanza kuongea nae tatizo alilokuwa nalo kulekule
njiani, “Ni hivi ndugu yangu maana ushakuwa ndugu yangu sasa, ile dawa
niliyotakiwa kumuwekea Yule mwanaume kagoma kula tunda na
kalitupa” “Kalitupa? Eeeh ikawaje, nadhani jana kulikuwa na mikosi moja
kwa moja maana hata mimi dawa zangu hazijafanikiwa kiasi kwamba sitaki tena
kutegemea waganga, hebu nieleze imekuwaje?” Basi Sia akamueleza jinsi
alivyomkuta huyo kijana akila tunda na jinsi alivyofatwa na yule kijana na jinsi
alivyukula kile chakula asubuhi. “Uwiiii na chakula kala?” “Ndio
kala, yani hata sielewi nafanyaje na Yule kijana maana amekazana kuondoka
hataki” “Ila dawa za Yule babu kiboko, basi lile tunda huwa linakama
sumaku yani asingekuona kijana wa watu angepata shida hadi angekoma ila vijana
wengine waroho jamani unaona watu wanatupa halafu wewe unaokota na kula si uroho
huo loh! Na tena hadi chakula kala sababu ile dawa inamvuta kula chakula
ulichoweka dawa nyingine, uwiii ndio uwe nae sasa” “Nitakuwaje nae?
Kwanza simtaki halafu inaonyesha bado hana maisha, maswala ya kuishi na mtu
mwenye shida ya nini? Nilikuwa namfanyia Yule sababu nilijua ningeishi kama
malkia” “Pole mwaya, sasa sijui nitakusaidiaje” “Sijui ila
naomba unisaidie yani maji yamenifika shingoni, siwezi kwakweli” Basi
wakaendelea kuongozana hadi nyumbani kwakina Sia kisha Sia akamuonyesha Dora
kijana mwenyewe, Dora akashtuka sana na kuita, “Kheee
Steve!!!” Sia akamuuliza, “Unamfahamu kumbe!” “Mdogo
wangu huyu” Dora alimfata Steve ambaye hakuwa hata na habari yoyote ile
kwani aliona kama amefika pale kwa Sia. Kwakina Erica ilikuwa
ni furaha kubwa kumuona Erica akiwa mzima tena na walipokaa kumuuliza kuhusu hao
wenye visasi nae waliomfanyia hayo mambo alishangaa pia maana hao watu hata
hakuwa na ukaribu nao na wala hakuwafahamu ila ambaye alitajwa kuhusika pia ni
Derick na ndiye aliyemuumiza zaidi kwani ni ndugu yake halafu kumfanyia mambo ya
ajabu, Mage alipofika walimueleza yaliyotukia jana yake akashangaa sana na
kuamua kumpigia simu Derick akimtaka aende tu ila hakusema kama Erica amepona,
alilalamika kutimuliwa siku za nyuma ila mage alimkazania kuwa aende
hatotimuliwa tena, basi derrick aliahidi kwenda muda huo. Derick alifika
pale na kuwakuta ndugu zake wakiwa ndani, alishangaa kumuona Erica ni mzima
kabisa, Mage alimkalisha chini Derick na kumuuliza kwanini afanye
hivyo, “Hapana mimi sihusiki” “Derick, kila mtu amekuona wewe
kama muhusika hata sijui unakataa vipi? Unajua wewe ni ndugu yetu hivi huoni
aibu kumfanyia hivyo ndugu yako?” Muda huo Babuu na Rahim nao walifika
kwani walitaka sana kuomba msamaha kwa kile kilichotokea kabla kwani bado Rahim
hakuwa na furaha ya kufukuzwa kwakina Erica, ila kwavile leo walimkuta Derick
akiwa kabanwa kwahiyo hawakufukuzwa, waliingia tu ndani na kusalimia kisha
Derick kuendelea kutoa maelezo na muda huu aliamua kueleza alivyoulizwa na mke
wa Rahim na jinsi mke wa Rahim alivyompa dawa, “Kwahiyo mke wa Rahim
ndiye aliyemfanyia Erica vitu vya ajabu?” “Ndio, alinituma nimtajie
majina matatu ya Erica, yeye aliniambia anataka Erica aachane na Rahim ila
sikujua kama angempa ugonjwa kama ule, na siku ile alinipa dawa nimpake Erica
kwenye paji la uso ila ni Fetty ndio alinizuia na mpaka muda huu sikujua alikuwa
na maana gani” “Hivi wewe Derick una akili kweli? Yani mtu anamteketeza
ndugu yako sababu ya chuki zako unakubali? Yani wewe ni zero
kabisa” “Ila Mage nilikwambia, huyu dogo hamna kitu ona sasa Erica
angekufa sababu ya mambo yake” Muda huo akili ya Rahim ilipoteza dira
kabisa kusikia mkewe ndio muhusika wa ugonjwa wa Erica na vile alivyomkuta na
madawa ndio kabisa, aliinuka na kutoka bila kuaga na bila kuondoka na aliyefika
nae, hakuna aliyemuelewa anaenda wapi ila aliondoka. Pale kwakina Erica
walibaki wakimsema Derick ila bado mama Erica hakutaka undugu na Derick kabisa
maana aliona huyu mtoto ni muuwaji, “Nipo tayari
kujirekebisha” “Hapana kwakweli, wewe uliyesababisha mwanangu achungulie
kaburi, hapana kwakweli” Baada yay ale maelezo mama Erica hakutaka
maelezo mengine zaidi ya kumtimua tena Derick maana hakutaka kumuona
kabisa. Basi Dora aliamua kumbembeleza mdogo wake pale ili
arudi nae nyumbani, akamwambia Sia amwambie mdogo wake kuwa anampenda ili aweze
kurudi nae nyumbani, yani mdogo wake ilionyesha kashaelemewa na mapenzi ya Sia,
kiukweli ilimuuma sana Dora kuona dawa alizompeleka Sia zimeenda kumdhuru mdogo
wake kwani muda wote atakuwa akimuwaza Sia na Sia ataona ni usumbufu sababu
hajamtaka huyu dogo, kwakweli aliwaza sana kuwa atawezaje kumfanya mdogo wake
awe sawa tena yani afanye tu kitu bila kumuwaza Sia, basi aliagana na Sia pale
na kuondoka na mdogo wake ila mdogo wake njia nzima anamwambia dada yake jinsi
Sia alivyo mzuri na jinsi anavyompenda, “Mdogo wangu sio akili zako hizo
umerogwa” “Sijarogwa dada, nampenda Yule msichana yani nampenda kutoka
moyoni” Hakuna alichoongea kikasikilizwa basi wakaendelea tu kurudi
nyumbani, walipofika njiani kuna mtu alisimamisha gari karibu yao alikuwa ni
Erick akielekea nyumbani kwakina Erica, alimuuliza Dora kuwa anajisikiaje toka
ile jana kutolewa yale mashetani, basi Erick alishusha kioo na Dora alisogea
kuongea nae, “Nijisikiaje wapi, nimezua makubwa na mambo yangu ya
waganga” “Kivipi?” “Kuna mtu nimesoma nae chuo anaitwa Tumaini
sasa nilikutana nae na rafiki yake anaitwa Sia, nilivyokuwa nawaeleza habari za
mganga ndio Yule Sia akapenda sababu kuna mwanaume wake alitaka kumteka ndio
nikaenda nae kwa huyo mganga halafu kibao kimegeuka kwa mdogo
wangu” “Sikuelewi, hebu nieleze vizuri” Kwakweli Erick kitendo
cha kusikia jina la dada yake na jina la Sia vikamchanganya sana na kujikuta
akitaka kujua kilichoendelea, basi Dora alimueleza ilivyokuwa kama alivyoelezwa
na Sia. Kwakweli Erick alijikuta akimchukia Sia kupita alivyomchukia mwanzo na
akaelewa kuwa kwanini Sia alitaka kumpa tunda lile jana yake, pia alimuhurumia
Yule mdogo wake Dora ambaye hakufikiri kuwa amerogwa ila alijua ni upendo tu upo
kwa Sia. Erick alifikiria kidogo kisha akachukua simu yake na kumpigia
mama yake na Erica ili amuulize namba za yulee mwanamaombi, na baada ya salamu
alimuomba hizo namba kisha mama yake Erica alimtumia. Erick alipozipata
aliwaambia wakina Dora kuwa wapande nae kwenye gari awasiliane na Yule
mwanamaombi kisha wampeleke Yule mdogo wake, Dora alifanya hivyo na
walipowasiliana na Yule mwanamaombi waliamua kuanza safari ya kwenda
huko. Walifika nyumbani kwa Yule mama ambapo alianza maombi kwa Yule
kijana na alipomaliza alianza kuwafundish wote watatu, “Mnatakiwa
kumtegemea Mungu katika maisha yenu yani msijali chochote muangalieni Mungu
tu” Dora akauliza, “Kwahiyo tuwe tunaomba kila
muda” “Ndio kila muda ni wakati wa kumuomba Mungu” “Mmmh
nitaweza kweli?” “Kwanini usiweze? Hakuna kisischowezekana chini ya
jua” “Tatizo nyumbani kwetu, mama yetu mwenyewe hana hayo mambo ya dini,
sijui kama nitaweza halafu kuomba sijui” “Uwe unakuja hapa nikupeleke
kanisani, kunakiuwa na vipindi vya maombi yani utajifunza humo kuomba hata usiwe
na shaka” Dora alikubali pale kuwa atajiunga na hiko kipindi, kisha huyu
mwanamaombi aliendelea kumwambia, “Yani msipokuwa makini na maombi hayo
madudu yatawajia tena na sio mazuri kwakweli, mnatakiwa kukumbuka
maombi” Wakaitikia na kumuaga kisha wakaondoka na Dora kurudi nyumbani
na mdogo wake huku Erick akibadilisha safari na kwenda kwakina Sia kwani
hakupenda kabisa kile alichokisikia. Neema kama alivyoahidi
kuwa ataenda kumtafutia mtu ili aweze kuongea na Salma, na kweli alienda kuongea
na mmama mmoja mshika dini haswaaa aliitwa Zainabu, alimwambia tatizo la ndugu
yake na huyo mama aliacha shughuli zake ili akaongee nae kwani alijua kama
wakimpa maneno ya dini basi ataacha kuwaza ujinga anaouwazaga, basi walifika
pale na kumkuta Salma akiandaa vitu vyake vya kupika, Neema alimkaribisha
Zainabu ili aongee na Salma, Zainabu alimsalimia Salma, ile salamu tu Salma
akahisi kuna jambo kisha akasema, “Neema nadhani kuna kitu unakitafuta
na utakipata tu, mimi nimekwambia nahitaji mshauri? Umeniona mimi nina matatizo
ya akili? Neema naomba uachane na mambo yangu, na kama wewe ni mshauri haswaa
basi subiri mume wangu umshauri sio kuniletea mimi habari
zisizoeleweka” “Dada, hata kunisikiliza ninachotakanachotaka kusema
jamani” “Halafu wewe Zainabu unafikiri sikufahamu au nini? Kuolewa
kwenyewe hujaolewa sasa utanishauri nini mimi kama sio utumbo? Achana na habari
zangu” Huyu Zainabu hakujua kama Salma anamfahamu kuwa anaitwa Zainabu
na hajaolewa ila hakupenda vile alivyosemwa na Salma, “Dada angalia
kauli zako, naweza kuwa sijaolewa ila nikawa na kauli thabiti kushinda wewe, na
sio kwamba sijaolewa basi sina tabia zinazofaa ila muda wangu tu
haujafika” “Huna lolote, umeamua kuja kumtamani mume wangu. Tena sitaki
ushauri wako, na wewe Neema kama ndoa yako imekushinda achana na ndoa
yangu” Basi Zainabu akawa anatoka, na getini akakutana na Rahim ndio
anataka kuingia ndani, akamsalimia ila Rahim alimuangalia sana Zainabu alipenda
mavazi yake na ongea yake kwani alionekana ni mwanamke aliyejiheshimu ila
kwavile alikuwa na ugomvi na mke wake akabaki tu akimuangalia Zainabu kisha
Neema nae akatoka kumsindikiza Zainabu. Rahim alienda hadi kwa mke wake
na kumwambia, “Siku ile nilikupiga ila leo sitakupiga, subiri hapo
hapo” Salma akiwa anashangaa tu maana hakuelewa ni nini kinakuja mbele
yake, akashangaa Rahim akitoka ndani na karatasi la taraka huku akisema kuwa
amemuacha na hamtambui tena kama mke wake toka siku hiyo. Erick
moja kwa moja alienda kwakina Sia ila hakumkuta Sia muda huo kwa hakika kama
angemkuta basi siku hiyo angekuwa halali yake maana alipanga kumpiga kwa hiko
alichotaka kumfanyia na kujikuta akimchukia sana ingawa hakujua kama mdogo wake
Dora itakuwaje ila alipata amani kiasi maana Yule dogo alishafanyiwa maombi,
basi akaenda kwakina Erica na usiku ulikuwa umeshaingia, Erica alikuwa na furaha
sana kipindi hiki hata mtoto wake Angel alikuwa na furaha pia, ila Erick
alifurahi zaidi kumuona Erica akiongea vizuri kama mwanzo kiasi kwamba anaweza
kuongea nae wakiwa wawili tu, nyumbani kwao walishaelewa kuwa wale wanapendana
kwahiyo waliwapa nafasi ya kuweza kuongea, kwa muda huu Bite alitoa mkeka nje
kisha Erick alikaa na Erica kwenye mkeka kwenye kibaraza cha nyumba ile huku
wakiongea, “Erica sikujua kama kwenu kuna mikeka” “Ipo ila haina
wakaliaji ndiomana ipo ndani tu muda wote” “Halafu Erica nimefurahi
sana, sijui kama unaweza kuona furaha yangu ilivyokubwa, ila kesho nitatimiza
ahadi yangu” “Ahadi gani?” “Kesho nakuletea ile gari
yako” “Wow, asante Erick” “Jifunze kuniita mume wangu
sasa” Erica akacheka tu maana neno mume wangu hakuwahi kulijaribisha
katika ulimi wake, Erick akamuangalia na kumwambia, “Usicheke mke wangu,
mimi ni mume wako” Erica bado alikuwa akicheka sana, ni mama Erica ndio
aliingilia yale maongezi kwa kuwaambia kuwa pale nje kuna mbu wengi, kwahiyo
waliingia ndani ila siku hiyo Erick aliongea kwa muda mrefu zaidi kwani alikuwa
na furaha sana ya kuona Erica ni mzima kabisa. Muda huu Sia
alikuwa nyumbani kwakina Erick, lengo lake ilikuwa ni kuonana na Tumaini maana
alimuita ila hakuthubutu kumwambia kuhusu habari za kwa mganga wala nini,
alifika kule kisha Tumaini akaanza kumueleza azma ya
alichomuitia, “Nimekuita hapa ili tupange namna ya kwenda kwakina
Erica” “Basi twende kesho” “Sawa, ila
tumejipangeje?” “Kwani tujipange vipi jamani Tumaini” Basi
Tumaini akamwambia namna alivyopanga kuwa wafanye na mama yake Erica anaweza
kumruhusu Erick kuwa na Sia, “Sikiliza tunafika pale kwa lengo la
kumuona Erica na kufuta yote wanayofikiria kuwa sisi tumemroga Erica, baada ya
hapo wewe Sia utasema kuwa una mimba ya Erick, nina uhakika mamake Erica
ataelewa tu kwani pia ni mwanamke na anajua jinsi inavyosumbua kulea mimba na
mtoto bila ya baba, kwahiyo atataka Erick awe karibu na wewe” “Jamani
Tumaini kwanini siku zote hizi tustumie njia hiyo, nimeipenda
sana” “Ndiomana nikakuita tujipange, Erick kanifukuza dukani kwake
sababu ya Erica nina uhakika nah ii nyumba ingekuwa yake pia angenifukuza yani
Yule Erica dah basi tu” Wakakubaliana juu ya hilo jambo na wakaona njia
pekee Sia ajifanye kila muda anaenda kutema mate, basi baada ya kupanga cha
kufanya Sia aliamua kuondoka sasa na Tumaini kumsindikiza, njiani Sia akamuanza
tena Tumaini, “Hebu fikiria Tumaini ungekuwa na gari si ungenipeleka tu
rafiki yako, hivi kweli Erick hana pesa za kukununulia gari?” “Mwenzangu
nilishamwambia hadi basi akasema mpaka mambo yake yakae sawa” “Yani
shoga yangu saivi ungekuwa unafurahia maisha tu hata sio kuhangaika kwa miguu
mara vibajaji sijui pikipiki, nina uhakika Erick hela anayo ila anamalizia kwa
Yule mjinga Erica” “Hivi kweli Erick anaweza kumjali Erica kushinda
anavyonijali mimi? Inawezekana kweli?” “Kama haiwezekani mbona
kakufukuza dukani!” “Najua kanifukuza sababu ya hasira tu ila kuhusu
gari Erick ataninunulia” “Mfano ukute kamnunulia Erica kabla
yako?” “Hilo haliwezekani na hakika ikitokea hivyo nitamueleza baba
ukweli wa kila kitu maana huwa simwambii mambo mengine ila kama ikifikia hiyo
hali kweli nitamueleza baba na vile mamake Erick ambavyo hampendi Erica
nitamwambia na yeye” Basi wakaongea ongea na kukubaliana na maneno yao
na muda wa kukutana kesho kisha wakaagana na Sia kupanda daladala la kurudi
kwao. Dora alirudi kwao na mdogo wake kiukweli mama yao
alifurahi ila mdogo wake Dora alikuwa bado kama hayupo sawa maana alionekana
yupo yupo tu, kisha hakuongea neno na kwenda kulala, Dora nae hata hakujisumbua
kumueleza mama yake maana huwa hana maongezi sana na mama yake, alienda tu
chumbani kwake, kuingia tu akapigiwa simu na James, akapokea, “Dora,
naomba nije nikuchukue yani hatujaonana jana, na leo naona kama mwaka. Niambie
ulipo nije Dora” Dora akasema kuwa atampigia ila akaona ni tatizo tayari
maana alishatengeneza tatizo kwa James, ile anataka ampigie Erick amuombe namba
ya mwanamaombi ili ampigie mwenyewe ajieleze na alichomfanyia James, gafla
akapigiwa simu na mzee Jimmy, Dora alipokea ila kwa mashaka kiasi, leo mzee
Jimmy hakuwa hata na salamu aliazna tu kusema maneno, “Msichana tapeli
wewe, yani umenitapeli hela zangu hivi hivi kwahiyo na gari langu lingetoka yani
sina hamu na wewe na nitakufundisha dunia ilivyo” “Sasa mimi
nimekutapeli wapi na umenipa mwenyewe?” “Ni kweli nimekupa mwenyewe ila
haiwezekani roho iniume hivi kwasasa, ukitaka njoo nikufaidi nilipizie hela
zangu” Dora akakata simu ya huyu mzee huku akiwaza kuwa hao wanaume
afanye nao nini ila hakuwa na la kufanya mwishowe akawaza au arudi tena kwa babu
wa bagamoyo maana alimjibu mzee Jimmy ila aliogopa vitisho vyake ukizingatia
hela zake kwa kipindi hiko kashazila sana, mwishowe aliamua kulala tu kwani
hakutaka kuwaweka mawazoni zaidi. Kesho yake kama Erick
alivyoahidi alienda na gari nyumbani kwakina Erica, kwakweli wote walishangaa
maana lile gari lilikuwa zuri sana tena lilionekana la gharama, Erick akaongea
kwa furaha, “Gari hii nimeiagiza muda sana toka nipo South kwaajili ya
zawadi ya mpenzi wangu Erica, nampenda sana huyu mwanamke na nitafanya kila kitu
kwaajili yake” Nyumbani kwao walishangilia sana, ila gafla geti
lilifunguliwa na aliyeingia alikuwa ni Tumaini na
Sia. Nyumbani kwao walishangilia sana, ila gafla geti
lilifunguliwa na aliyeingia alikuwa ni Tumaini na Sia. Basi wakajikuta
wote wakiwaangalia maana waliingia bila ya kugonga hodi ingawa ni kawaida kwa
geti lao watu kuingia bila hodi ila hawa waliwashangaa, Tumaini akasogea karibu
na mdogo wake, “Yani Erick umeshindwa kunipa mimi gari unampa Erica
kweli?” Erick alimuangalia na hakumjibu kitu, badala yake alikabidhi
funguo na kadi ya gari kwa Erica kitu ambacho kilimuumiza moyo sana Tumaini na
kujikuta akishindwa hata kusema zaidi, kisha alimuangalia Sian a kumtaka
waondoke, Sia akamwambia, “Mbona hatujatimiza lengo
letu?” “Twende Sia, hatuwezi kufanya kitu tutakuja kwa wakati
mwingine” Wakaamua kuondoka maana hata Erick mwenyewe alionekana
kutokuwajali kabisa kwani aliendelea na mambo yake ya kutoa zawadi ya gari tu
kwa Erica. Ilikuwa ni furaha sana nyumbani kwakina Erica, ingawa bite
mwanzoni alikuwa na mashaka na Erick ila kwasasa alianza kumuonea wivu mdogo
wake kuwa anapendwa, ingawa hata yeye kashawahi kupewa zawadi ya gari mara
nyingi tu ila hakupewa kwa namna ile ya upendo ambayo mdogo wake alipewa, baada
ya hapo Erick aliomba ruhusa aende na Erica wakatembee tembee kidogo na hiyo
gari kisha watarudi ila mama Erica aligoma, “Hapana mwanangu hatoenda
popote kwakweli, naogopa yasije yakampata mengine makubwa” Mage
akatetea, “Ila mama, huyu kijana kaonyesha upendo mkubwa sana, sio
sababu ana pesa hapana ila sababu ana upendo, wangapi wana pesa ila hawana
upendo? Tena wenye pesa ndio wanajulikana sana kwa kukosa upendo ila huyu kijana
ameonyesha upendo wa ajabu, mimi ningeona ungemruhusu tu akatembee kidogo na
Erica” Aliamua kuuliza kwanza, “Kwani mnataka kwenda wapi
kutembea tembea?” Pale pale akili ya Erick ikamcheza na
kumwambia, “Nataka niende na Erica kwa Yule mwanamaombi tukapate baraka
yah ii zawadi” Basi mama Erica kusikia vile akakubali na kumfanya Erick
afurahi sana kutoka na Erica, kisha Erica alienda kujiandaa na kutoka na
Erick. Tumaini alikuwa na hasira sana moyoni, yani alikuwa
njiani na Sia akiongea maneno mengi mengi kwa hasira na chuki, “Hivi
kweli mtu akuache ndugu yake usote na miguu safari zote wakati uwezo wa
kukununulia gari anao halafu anaenda kumnunulia gari mwanamke kweli? Yani Erick
wa kunifanyia mimi hivi? Kumbuka mimi ndiye ndugu yake wa pekee ila kamthamini
Yule mwanamke ambaye kaonana nae ukubwani tena ni mimi ndiye niliyemkutanisha
nae ila bado ananidharau?” Tumaini aliamini ni yeye aliyewakutanisha
Erick na Erica bado hakujua kuwa Erica ndiye msichana ambaye Erick alimpenda
toka wanasoma sababu ukweli wa hilo hajawahi kumwambia zaidi ya kumwambia kuwa
anampenda sana, kwahiyo aliamini tu ni yeye aliyewakutanisha, Sia alimbembeleza
pale huku nay eye akijilaumu, “Unajua duniani kuna dawa Tumaini,
ukisikia mtu karogwa ndio hiki kinachotokea kwa Erick, hebu kumbuka mapenzi
yangu na Erick kabla ya ujio wa huyo kidudu mtu Erica, tulikuwa tunapendana,
hata nikimfumania Erick ananiomba msamaha na maisha yanaendelea, wazazi wangu
wote wamekufa wakiamini kuwa Erick ndiye mume wangu, yani ilikuwa mimi na Erick
tu mpaka jinni kisirani alivyovamia penzi letu” “Yani Sia najuta mimi,
najuta kufahamiana na Erica. Nilimuona ni msichana mstaarabu na kutaka awe mdogo
wangu, najuta mimi. Natamani kurudisha siku nyuma ili hata ile siku niliyokutana
na Erica isiwepo katika maisha yangu, haiwezekani huyu msichana akachanganya
akili yangu kiasi hiki” Kisha Sia akamuuliza kuwa kwa muda huo sasa
wataenda wapi, “Sia, muda huu twende ofisini kwa mamake Erick, mimi
nitamueleza uchungu wangu na wewe umueleze kuwa una mimba” “Mmmh akisema
tukapime?” “Hawezi sema hivyo yani usijali, mimi nitatengeneza matukio
yote utakuja nyumbani mara kwa mara ukijiliza kwa baba kuwa una mimba ya Erick,
yani najua Erick atachukia sana, hata akikusukuma tu tunapata sababu yani
nitakuwaisha hospitali na kusema mimba imetoka halafu umepata matatizo makubwa
sana sababu alikusukuma vibaya, si anajifanya yeye ndio mtoto pekee kwa mama
yake yani lazima mama yake ahisi homa gafla, haiwezekani Erick afanye hivi
unajua yani najiuliza huyu Erica kampa nini ila sipati majibu
kabisa.” Basi safari kwa muda huo ilikuwa ni kuelekea kwa mama Erick
huku wakiwa na mawazo sana maana lile tendo la kumuona Erick akimkabidhi gari
Erica liliwaumiza sana. Nyumbani kwakina Dora bado alimuona
mdogo wake kutokuwa sawa kama alivyotakiwa kuwa, akakumbuka maneno ya Yule
mwanamaombi kuwa hawatakiwi kuacha kuomba kwani kile kitu ni vitu ambavyo
kimepandikizwa na kimenuiziwa kwahiyo kinaweza kutoka vizuri kwa maombi tu ila
wakiacha itakuwa ni tatizo, Dora alimfata mama yao na kumwambia habari za kwenda
tena na mdogo wake kwenye maombi, ila mama alikuwa mkali sana, “Weee
Dora, wewe na maombi wapi na wapi? Halafu huyu mdogo wako aende kwenye maombi
kwani ana mapepo huyu? Labda hayo maombi uende wewe maana akili zako
zimechanganyikiwa ila sio mwanangu” “Sasa mama unamuona yupo sawa huyo
anajifungia tu!” “Yupo sawa ndio, atatoka na ataenda kujumuika na wenzio
ila swala la kuanza kumuangaisha mwanangu kwa hao wachungaji hata sitaki, kwanza
ni waongo wanajifanya wanaombea kumbe wanataka sadaka” “Haya mama, hiyo
sadaka utatoa wewe au mimi ninayempeleka?” “Kama una hela hiyo ya sadaka
si ulete tujichane humu ndani” “Kiukweli mama wewe ndio uliyenipoteza
mimi, ni kweli wasemao mtoto umleavyo ndivyo akuavyo yani hivi nilivyo ni
matunda yako ya malezi mabaya” “Hebu nitolee ushetani wako
mie” Dora akaona isiwe tabu akajiandaa na kwenda yeye kwa mwanamaombi
kwani bado alihitaji kuongea nae vitu vingi sana, haswa kuhusu mzee Jimmy na
kuhusu James. Tumaini na Sia walifika ofisini kwa mama yake
Erick na waliomba kuonana nae ambapo aliwaambia wamsubiri kidogo ili muda wa
kula chakula cha mchana aende nao na wamueleze kilichowasibu, nao walifanya
hivyo na muda ulipofika mama Erick alitoka na kwenda nao sehemu ya kula huku
akiwasikiliza hoja zao walizokuja nazo, alianza Tumaini kuelezea, “Mama,
yani Erick ni ndugu yangu kila leo namuomba aninunulie gari anasema mpaka
ajipange” Huyu mama alimjibu Tumaini kabla hata
hajamaliza, “Sasa hilo ndio tatizo mwanangu? Baba yeni ana pesa si ni
kitendo cha kumwambia tu baba nahitaji gari ya kutembelea akupe jamani! Eeeh
Tumaini!” “Hapana mama hilo sio tatizo, ila tatizo ni kukuta kampa gari
Erica, tena gari lenye thamani ya milioni ishirini na tano, kweli Erick anatoa
gari la namna hiyo kwa mwanamke jamani!” “Sijakuelewa Tumaini,
umesema!” Ikabidi Tumaini arudie maelezo yake kwakweli mama Erick
alishangaa sana kuona mwanae kafikia hatua hiyo na kuona kuwa sio kawaida labda
kuna kitu alichofanyiwa na huyo Erica, “Usinione nimenyamaza mwanangu
Tumaini yani najitafakari, kweli Erick kafikia hatua hiyo jamani! Si bora
angekupa wewe hilo gari, mbona kaanza mambo ya ajabu huyo Erick? Halafu huwezi
amini tofauti na kipindi kingine ila kipindi hiki Erick hana muda na mimi
kabisa, akinisalimia mara moja imetoka yani huyu mtoto hata sijui
nifanyeje” Tumaini akaendelea kuongea na kumwambia, “Sasa mama,
hili la kumpa gari Erica na kuninyima mimi sio kosa sana ila kosa kubwa la
mwanao ni kuwa Sia ana mimba yake na ameikataa eti yupo kulea mtoto wa
Erica” Yani hapa ndio wakamchanganya vizuri mama Erick na
kusema, “Yani isingekuwa kesho nasafiri basi ningeenda mwenyewe huko
kwakina Erica, nahitaji kuonana na mama yake kama anamfundisha mwanae hiyo tabia
ya kuibia wanaume, yani mtoto uzae na mwanume mwingine ila umbambikie mwanaume
mwingine alee, hiyo inawezekana kweli? Kasichana kanaonekana kapole kale kumbe
kamezalia nyumbani? Jamani, ni aibu sana halafu mwanangu hata kuona haoni
anamkazania huyo msichana kweli kuna mambo duniani, nilikuwa nasikia kwa watu tu
kuwa kuna watu wanaroga ili wapate mapenzi na kweli nimeamini ila Yule Erica
hajaroga kwaajili ya mapenzi bali ameroga kwaajili ya pesa za
mwanangu” Tumaini alimsapoti mama Erick kuwa ni kweli Erica atakuwa
kamroga Erick sababu ya pesa zake, “Ni kweli kamroga mama, yani Yule
binti hata chuoni alikuwa akisifika kwa tabia za kichawi yani kamfanya vibaya
mdogo wangu najuata kumfahamu” “Ila nitamtafuta mamake mdogo na Erick
ili tumtafute Yule msichana aliyechanganya akili za Erick wakati yupo shule ndio
apambane na huyo Erica” Sia alitulia tu huku akisikilizia kuwa mimba
yake inapewa shauri gani ila alipoona zinaongelewa hoja zingine tu bila hoja ya
mimba yake kugusiwa akaamua kugusia hoja ya mimba yake, “Mama, na vipi
kuhusu hii mimba niliyonayo ya Erick?” “Mwanangu tulia, Erick atakuoa
atake asitake, kwani mtoto bora ni Yule anayelelewa na wazazi wawili yani baba
na mama asiniletee mambo ya baba yake mie” Sia alifurahi kusikia vile
maana hata kama hakuwa na mimba ila ile kauli ilimpa moyo sana na kumfanya
ajihisi rah asana, kisha mama Erick aliwaaga na kurudi ofisini maana kuna mambo
alitaka kumalizia na kesho yake asafiri. Tumaini na Sia waliondoka pale
wakiwa na matumaini makubwa sana kwani walijua kama mama yake Erick
atalichukulia lile swala basi lazima watafanikiwa kusambaratisha penzi la Erica
na Erick. Dora alifika kwa Yule mwanamaombi na kuanza kuongea
nae juu ya mambo yanayomsibu ila mwanamaombi akamshauri kuwa na huyo James
amlete kwenye maombi pia, “Mmmh sijui atakubali
nitajaribu” “Halafu mbona mdogo wako hujaja nae?” “Mama kagoma,
yani mama ni mbishi sana” “Sasa mdogo wako anatakiwa kukombolewa maana
ile dawa ilimkoroga haswaa ukizingatia hakulazimishwa kula ila alikula kwa
hiyari yake mwenyewe, ulitakiwa kuja nae” “Nitajitahidi basi nikija tena
nije nae, ila kuna mzee mmoja nilikula hela zake ananisumbua sana” “Kama
utaweza huyo mzee pia ungemleta kwenye maombi maana silaha ya hao watu ni maombi
tu” “Mmmh Yule mzee sijui kama atakubali, nitajaribu” “Unatakiwa
kuingia kwenye maombi, unatakiwa na wewe ujifunze maombi” “Ila ngoja
nikuulize, hivi mfano wakati natumia zile dawa kuna pesa nilichukua kwa watu je
nifanyaje nazo?” “Unazo hizo hela?” “Ndio
ninazo?” “Zilete tufanye maombi na kisha zipelekwe kwenye kusaidia
watoto yatima” Hapo palimshtua Dora, yani atoe pesa zake alitamani hata
kubadilisha mada, kwa bahati walifika Erica na Erick kwa Yule mwanamaombi na
kumkuta Dora pale akiongea nae, wakamsalimia kisha wakaanza na wao kuongea na
Yule mwanamaombi ambaye aliwafanyia maombi na kuwataka kusimamia maombi tu,
sababu Dora aliacha kwanza waombewe wale kwahiyo mwanamaombi alijua akimalizana
na wale ataanza tena na Dora ila wakati wakina Erica walipotaka kuondoka tu Dora
nae alisema wasubiri waondoke wote na kumuaga Yule mwanamaombi, “Ila
bado hatujamalizana binti, bado sijakufanyia maombi!” “Nitakuja
badae” Akatoka nje na Wakina Erica na kupanda ile gari ambayo Erick
alisema kuwa kamnunulia Erica, muda wote kwenye gari alikuwa akisifia
tu, “Gari nzuri sana jamani, kwakweli Erica umepata bahati kumpata huyu
Erick” Erica akawa anacheka tu kisha Dora aliendelea
kuongea, “Ila Erick unajua kama Erica alikuwa na mahusiano na ndugu yake
Derick?” Erica alichukia sababu alimuona Dora anaanza kuongea mada
zisizomuhusu na kumuuliza, “Unaelekea wapi Dora maana sisi tunarudi
nyumbani” “Basi nishusheni tu hapo kituoni” Basi walivyofika
kituoni wakamshusha, Erick alijifanya kama hajasikia lile swali la Dora maana
hakutaka kupata tena kitu cha kumuumiza moyo kwa muda huo wa
furaha. Dora alirudi kwao ila alikuwa na mawazo sana, kwanza
aliwaza kupeleka zile pesa kwa mwanamaombi yani aliona haiwezekani kwakweli
maana aliona pesa kazihangaikia sana zile, ila akiwaza vitisho vya mzee Jimmy
hofu ilimshika pia, ila muda huo aliamua tu kurudi nyumbani, akamkuta mama yake
amekaa tu na mawazo, akamsalimia na kumuuliza “Ni mdogo wako dora,
kasema anaenda tena kwa mwanamke wake alipokuwa juzi, nasikitika sana maana
kaniambia anataka amuoe kabisa” “Kheee ila mama nilikwambia kuwa niende
nae tena kwenye maombi” “Hukuniambia mdogo wako anasumbuliwa na nini
zaidi ya kukazania maombi, kumbe mdogo wako anasumbuliwa na mapenzi jamani! Sasa
nayo ni kitu cha kuombewa? Nimemwambia amlete huyo mwanamke nimfahamu,
ananisikitisha sana kwani bado hajajipanga kimaisha ila anataka kuoa, kuoa ni
jambo jema ila kwa muda gani ndio tatizo hapo” “Sasa mama, unavyoona
mwanao yupo kwenye hali ya kawaida?” “Ndio, ila ni mapenzi tu
yanamsumbua” Muda kidogo Dora alipigiwa simu na mpigaji alikuwa ni
James, basi leo hakuona tatizo zaidi ya kuonana nae tu kwani alitaka kujaribu
kumshawishi waende wote kwenye maombi. Kwahiyo aliachana na habari za
kushauriana pale na mama yake na kwenda kuonana na James, ni kweli James alikuwa
na shauku sana ya kumuona Dora ila alivyomuona tu akili yake kama ilicheza na
kurudi gafla, akashikana nae mkono kama salamu kisha huyu James alijikuta
akimuuliza Dora, “Kwani akili yangu ilifanyeje?” “Sijui, hata
mimi nakushangaa” “Hivi nimeitafuta hata familia yangu
kweli?” “Sijui, ila kuna mahali nataka twende” “Wapi na kufanya
nini?” “Ni kwenye maombi, kuna lengo moja la kujikomboa kutoka kwenye
mambo ya kishirikina” “Inawezekana nilifanyiwa mambo ya kishirikina eeeh
ndiomana sikukumbuka familia yangu” “Ndio inawezekana” James
alikubali maana akili yake kwa muda huo hakuielewa kabisa, ilikuwa kama imerudi
gafla, kwahiyo kitendo cha kumuona Dora ambaye alimfanyia dawa na kumfanya
ampende aliweza kurudisha fahamu na kumbukumbu zake, basi Dora aliondoka nae na
kuelekea tena kwa Yule mwanamaombi. Dora alifika na kuongea na Yule mama
kuwa aongee taratibu na James ili asigundue kuwa ni yeye ndiye aliyemfanyia
madawa maana kitendo cha James kumuona tu akili yake imerudi, Yule mwanamaombi
akamwambia Dora, “Sababu wewe ndiye uliyemfanyia na wewe umekomboka
ndiomana kitendo cha yeye kukuona wewe kimerudisha akili yake” “Kwahiyo
kuhusu mdogo wangu itabidi Yule mwanamke naye aje huku?” “Ndio,
inatakiwa tumkomboe pia sababu kuamini ushirikina ni kitu kisichofaa, mdogo wako
ungekuwa unamleta mara kwa mara kwenye maombi angekomboka pia” Basi Yule
mwanamaombi alianza kumuombea James na hadi James alijihisi yupo vizuri ila Dora
aliaga na kuondoka na James kwani hakutaka kuulizwa kuhusu swala la hela zile
alizozipata kipindi cha madawa. Alifika njiani na kuagana na James kisha
yeye kwenda kwao, kwa muda huo James alijiona yupo huru sana kupita muda wowote
ule ila alishangaa kwa Dora kumfahamu mtu wa maombi wakati ana matendo
yasiyofaa. Ilikuwa ni saa kumi na mbili jioni inaenda saa moja
wakati James amefika nyumbani kwake ila kiukweli hakuwa na furaha kabisa kwani
alijihisi ni muda mrefu hajaiona familia yake na wala hakujisumbua
kuitafuta, “Hivi mimi nimeanzaje jamani? Mbona sikumbuki
nimeanzaje?” Alimkuta msichana wa kazi pale nyumbani akisema kuwa dada
yake aliondoka hapo siku nyingi tu na yeye binafsi kuna siku anarudi ila siku
zingine harudi au anarudi usiku sana, “Jamani hata kama nina tabia chafu
ndio kufanya hivyo kweli!” “Ndio na mara nyingine ulikuwa unampiga
dada” Hapo ndio alichoka kabisa maana swala la yeye kumpiga mke wake
hakuwa nalo hata mkewe amfanye nini kwahiyo kufikia hiyo hali ya kumpiga mke
wake aliishangaa sana yani hakuelewa kabisa kuwa alianzaje
anzaje. Hakutaka kukaa hata hapo nyumbani kwake kwani moja kwa moja
aliamua kuondoka na kwenda nyumbani kwa mkwe wake ili akamuone mke wake na
mtoto. Alifika kwenye mida ya saa mbili usiku, akagonga na kufunguliwa
mlango, aliyefungua alikuwa ni Mage maana ndio alikuwa anatoka kuelekea kwake,
na alijua ni Erica na Erick wamerudi, kwakweli alivyoingia James walishangaa
sana, Bite hakutaka hata kuongea na mume wake badala yake alienda zake kulala
kwani alikuwa na hasira sana na huyu mtu, mama yao nae alimtimua tu kwani
hakutaka kumsikiliza wala hakutaka kumuona kwahiyo ilibidi James aondoke
zake. Mage alisogea kumuaga mama yao, ambaye alilalamika
kwanza, “Mnaona sasa huyo Erick na Erica hadi muda huu hawajarudi jamani
hebu nisaidieni kuwatafuta maana kila nikiwapigia simu wanadai wanakuja yani
Napata hasira sana” “Ila mama sidhani kama kuna ubaya wa wao kuwa pamoja
na watarudi tu” “Muda gani sasa? Na ole wake huyo Erick aniombe safari
ijayo kuwa anataka kutoka na Erica” Muda kidogo Erick alikuwa
amemrudisha Erica nyumbani ila mama yao hakupenda hivyo hakutaka hata Erick
kukaa kwa muda mrefu na kumtaka aondoke tu, kisha alimuangalia mwanae Erica ila
leo hakumsema sana kwani aliamini bado hajapona vizuri kwahiyo alimuacha akalale
tu. Sia alitulia ndani kwake ila nje kulikuwa na mdogo wake
Dora amejibanza tu ikabidi kwa siku hiyo amkaribishe ndani maana usiku
ulishaingia na kujikuta wapo ndani na kuzoeana huku wakipiga story mbalimbali
ila katika stori zote walizokuwa wanapiga Yule Steve alijikuta akiwa na mada
moja tu kwa Sia, alimwambia kuwa anampenda sana yani hakuwa na mada nyingine
zaidi ya kumwambia anampenda sana, kwakweli Sia alishangaa sana nguvu ya ile
dawa hadi ingekuwa kwa Erick angefurahi sana maana dawa ina nguvu hatari hadi
wakati mwingine alihisi Yule kijana akiongea kutoka moyoni kwani alionekana
kuongea kwa hisia sana hata hakuweza kumtimua nje. Kwasababu hakutaka
ndugu zake wengine wajue kama Yule kijana kafika tena kwahiyo aliamua kumwambia
alale kwenye kochi la pale chumbani kwake. Ila usiku wa manane alishtuka
kukuta Yule kijana akianza kumpapasa, sababu alijikuta na yeye kuwa na hamu sana
akashindwa kumzuia na kujikuta akifanya nae mapenzi na kulala kama
wapenzi. Kulipokucha Sia alimuangalia Steve na kujuta sana kwani
anayemtaka yeye si Steve ni Erick ila ndio imetokea vile ila na vile vile
alijishangaa kuwa kumfukuza huyu mtu hawezi na alipenda kumuangalia tu jinsi
anavyomuimbia wimbo wa nakupenda maana alitamani kweli siku moja atokee mtu wa
kumwambia anampenda kiasi kile. Sia aliamka na kuoga kila kitu kisha
kumuamsha Steve ili aende kwao, Steve aliamka pia ila akamwambia
Sia, “Sawa, mimi nitaenda kwetu ila ningeomba nikakutambulishe kwetu
maana nataka nikuoe” “Kheee unioe?” “Ndio, nakupenda Sia,
nahitaji kukuoa yani wewe ndio mwanamke wa maisha yangu nakupenda
sana” Yani alijisikia kucheka na kulia yote yale yalifanywa na nguvu ya
dawa inamaana vijana kama wale hawakumuona kabla? Na pia hakupenda kuchombezwa
na kijana ambaye anaonekana yupo kawaida tu wala hana hela wakati yeye alikuwa
akimtaka Erick ilia pate na hela za Erick ndiomana alitaka hata kumfanyia dawa
maana anaamini kuwa hata lile gari alilopewa Erica lilikuwa ni mali
yake. Kwa muda huo ilibidi amchombeze chombeze Steve ili aondoke ila
Steve aliahidi kwenda tena badae maana alijiona hawezi lolote bila ya Sia,
alimuona Sia kuwa mwanamke wa maisha yake. Siku ya leo baada ya
kazi za hapa na pale Erica aliulizwa na mama yake kuhusu alipochelewa jana na
Erick, “Ni kwanini jana mlichelewa vile? Mlipitia wapi?” “Mama,
jana Erick aliamua kunipeleka kwa mama yake mdogo. Yule mama ambaye kipindi kile
alikuja shule kwasababu ya kesi yangu na Erick ni mama yake mdogo ndio
alinipeleka huko” “Sasa huyo ndio kakukubali?” “Tena amefurahi
sana kuniona alivyoambiwa kuwa ni mimi ndiye Yule msichana wa shule yani Yule
mama amefurahi sana na kututakia baraka zote, Erick kaniambia ilimradi Yule
kakubali basi hakuna tatizo kwa mama yake” “Basi ndio mkachelewea
huko!” “Ni mbali mama sio karibu, Erick kasema atanipeleka kwa ndugu
zake wote kisha kwa baba yake na mama yake ila wazazi wake hawaishi pamoja
kwahiyo inabidi awaombe wawe pamoja siku hiyo kama itawezekana akanitambulishe
kwao na kama itashindikana basi atanitambulisha kwa kila mmoja kwa muda wake na
ameniahidi kitu kizuri sana” “Kitu gani hiko?” “Utakiona
Jumamosi mama, sio mbali subiri tu utaona” Huyu mama alishindwa
kuendelea kumsema mwanae kwani naye alivyoambiwa kuwa kuna kitu kizuri alingoja
tu kukisikia. Muda kidogo leo Erica alipigiwa simu na mzee Jimmy naye
kuiona kweli ni namba yam zee Jimmy, akaipokea na kuongea nayo, “Natumai
mzigo wangu wa milioni tatu uliuona?” “Mzigo hapana, hakuna mzigo
nyumbani kwetu” “Niliacha pesa hapo nyumbani kwenu Erica, mnajifanya
kula kimya kimya nisijue eeeh! Sikia mwambie mama yako hiyo nimetoa ni pesa ya
posa kwahiyo mahali itafuata” “Unasemaje?” “Ndio hivyo Erica,
subiri tu siku ninavyokuja hapo na ndugu zangu kwa lengo la kukuchukua jumla
yani unakuja kuwa mke wangu” “Sikuelewi” “Utanielewa tu siku
hiyo ikifika” Erica aliamua kukata simu ya Yule mzee kwani ndio kwana
amepona halafu kupata simu za aina hiyo hakupenda kwakweli yani alichukia
haswaa. Wakati katoka tu kuongea na simu, mama yake akaondoka sababu
alikuwa ameanza tena ile biashara yake kwani sasa mwanae alikuwa mzima kwahiyo
aliifanya biashara tena kwa moyo, akafika mgeni alikuwa ni Babuu, alifika kwa
lengo la kumuona Erica ila kwanza aliamua kuulizia kama mama Erica yupo maana
alijua kama angemkuta lazima angemtimua tu. Basi vile hakumkuta aliweza
kuongea kwa uwazi zaidi, alimueleza Erica habari za Rahim kumpa mkewe
talaka, “Sasa kwanini kamuacha mke wake?” “Rahim anataka kukuoa
wewe, Rahim anakupenda” “Mwambie nashukuru sana ila simpendi hata kidogo
yani simpendi Rahim, atabaki tu kuwa baba wa mwanangu ila sio kipenzi
changu” “Hata ungesema unampenda ningekushangaa sana, ila Erica katika
wanaume zako wote mimi peke yangu ndiye mwenye mapenzi ya kweli na wewe. Hebu
angalia vizuri, wengine wote wanamaslahi yao binafsi” “Babuu hayo
maswala ya huyu ananipenda sana sijui huyu hanipendi nilishayamaliza na sasa
nimeamua kuwa na Erick tu” “Sasa huyo Erick humjui
vizuri” “Namjua vizuri sana hata wanawake zake nishawahi kugombana nao
sijui kama unalingine la kusema? Nampenda Erick, haijalishi yuko vipi ila
nampenda” “Erica, ni hela za Erick ndio zinakuchanganya akili ila
angekuwa masikini usingempenda” “Babuu, siku zote nimekuwa nikihangaika
na huyu mara Yule sababu nilikuwa nasaka upendo wa dhati na nimeupata kwa Erick,
naomba uniache na Erick wangu” Muda kidogo Erick alifika na Erica
aliinuka kwenda kumpokea kwa kumkumbatia kitu kilichomtia wivu sana
Babuu. Nasma hakuwa na raha kabisa tangu tabia ya Bahati
imebadilika aliamua kwenda kwa baba yake maana Bahati alianza tabia ya
kutokulala nyumbani kabisa, anaweza akalala nje siku mbili au tatu ndio akarudi
kwake. Kwakweli Nasma alichoshwa na tabia ile, kwahiyo aliamua kwenda
kushtaki. Alimkuta baba yake na kumueleza kila kitu
kilivyokuwa, “Baba huwezi amini yani nimemfumania na
Siwema” “Kheee Yule mtoto ana laana jamani kwenda kutembea na mume wa
dada yake kweli! Ila mwanangu nilikwambia kuwa ile dawa inamfanya mwanaume awe
kama jogoo sasa wewe ulipoona bado hujawa sawa usingeifanya labda ungeifanya kwa
kipindi hiki, ila ubaya ni kuwa zile dawa zingine hajatumia” “Baba
imeniuma sana, nimeshangaa Bahati huwa anampenda sana Erica na wimbo wake
ulikuwa ni Erica Erica, ila kwanini baada ya ile dawa hakwenda kumtafuta Erica
atembee nae badala yake alienda kutembea hadi na Siwema mdogo wangu! Kwakweli
imeniuma” “Mwanangu kwanza kumbuka nilifanya dawa ya kumvuta Bahati,
katika ile dawa nilifanya Bahati asahau uwepo wa Erica na aje akuchukue wewe, na
ikawa hivyo sasa ile dawa inamfanya mwanaume atamani mwanamke aliyekaribu nae,
ungefanya dawa zote asingetembea na mdogo wako angekuvumilia tu ila huyu Siwema
nae kakubali vipi kuwa na shemeji yake? Na cha kushangaza mwanangu huyo mdogo
wako Siwema hajarudi hapa na unasema ulimfukuza” Nasma alishangaa kuwa
Siwema hakurudi sababu hakujua kama Siwema kapangishiwa nyumba na Bahati, wakati
wanajiuliza kuwa imekuwaje mara walishangaa kumuona Siwema akija huku
ameongozana na Bahati, yani walivyofika karibu kabla ya salamu Yule mzee alianza
kwa kumfokea binti yake ila Bahati akaingilia kati na kusema, “Usimfokee
ila nimekuja na Siwema kuchukua tu baraka zako maana nahitaji kumuoa Siwema na
hapo alipo ana mimba yangu” Nasma na baba yake walibaki midomo
wazi. Nasma alishangaa kuwa Siwema hakurudi
sababu hakujua kama Siwema kapangishiwa nyumba na Bahati, wakati wanajiuliza
kuwa imekuwaje mara walishangaa kumuona Siwema akija huku ameongozana na Bahati,
yani walivyofika karibu kabla ya salamu Yule mzee alianza kwa kumfokea binti
yake ila Bahati akaingilia kati na kusema, “Usimfokee ila nimekuja na
Siwema kuchukua tu baraka zako maana nahitaji kumuoa Siwema na hapo alipo ana
mimba yangu” Nasma na baba yake walibaki midomo wazi. Bahati
aliendelea kuongea na kusema, “Huu sio wakati wa kushangaa ila ni wakati
wa kunibariki kwa hiki ninachotaka kufanya” Nasma akasimama juu na
kusema, “Haiwezekani, umuoe huyo na mimi inakuwaje?” Bahati
akatoa karatasi mfukoni na kumpa Nasma, karatasi lile lilikuwa limeandikwa
talaka yani Nasma hakuweza kuangalia tena na kuzimia kabisa kwani hakutegemea
kitu cha namna ile, ilikuwa ni bora Bahati angemuacha kwaajili ya Erica mwanamke
wa mbali kuliko kumuacha kwaajili ya mdogo wake, aliona ni dharau kubwa sana
katika maisha yake. Baba yake alianza kumshughulikia Nasma ambapo
alimuita mama yao ila Bahati na Siwema wakaondoka yani hawakutaka hata kujua
kitakachoendelea nyuma, mama Nasma alifika na kuanza kumpepea pepea Nasma huku
akisaidiana na mume wake kisha Nasma alipozinduka wakampeleka chumbani ili
akapumzike kidogo, mama mtu alimuuliza vizuri Yule baba kuwa tatizo ni nini hadi
kufikia ile hali, Yule baba alianza kumueleza kwa kifupi kuhusu kilichotokea,
huyu mama akasema, “Tatizo ni moja, kunishirikisha jambo hamtaki, kitu
nikitoa ushauri unadai nina wivu na watoto wako sasa mimi niwe na wivu wa nini
jamani? Mie mtu mzima nianze kuwaonea wivu wakina Nasma eti sababu mama yao
hayupo basi nitakuwa mwehu, siku mlipomchukua Siwema aende nyumbani kwa Nasma
nilikuonya mapema nikakwambia huyu Siwema hajatulia ila hukutaka kunisikia
ukaona kama sitaki watoto wako waishi pamoja haya kiko wapi sasa?” “Aaah
tatizo la wewe mwanamke ndio hilo kila kitu unaongea kama unasutana, hivi huoni
kama Siwema ana makosa hapo kumkubali shemeji yake? Na huoni kama Bahati nae ana
makosa kutembea na shemeji yake?” “Kwakweli sioni makosa yao, huyo
Bahati mmemkoroga na madawa weee toka siku ya kwanza mkaka wa watu mnampika tu
wengine ni watazamaji tunabaki kuangalia kuwa mtaishia wapi na hayo madawa,
mmemkoroga wee na sasa yamewarudi wenyewe, huyo Siwema mwenyewe umemchanja
chanja weee halafu leo ushangae kutembea na shemeji yake kweli? Mtoto umemchanja
hadi akili za darasani hazipo maana kile kichwa ni umekichanja haswaa haya
kafeli yupo tu nyumbani, aende huko kwenye nyumba nzuri shemeji yake amtongoze
atankataa wakati akili zenyewe zimemalizwa kwa madawa? Yani si huyo Siwema wala
si bahati wa kulaumiwa ila jilaumu wewe na dawa zako” “Halafu wewe
mwanamke hata sijui kwanini nilikuoa mwanamke usiyejielewa kama wewe, hebu nenda
kapike huko, huyu Bahati nitamshughulikia” “Naenda kupika ila hebu kuwa
na huruma kidogo, kijana wa watu mtamfanya aokote makopo bure hebu fikiria ndio
mwanao jamani!” “Hebu nitokee wewe mwanamke bhana” Huyu mama
aliondoka ila aliona ameshawaambia la ukweli kama wanaweza walichukue na
kulielewa. Steve alirudi nyumbani kwao ila alitumia muda mfupi
sana kukaa pale nyumbani maana alioga na kubadilisha nguo kisha kubeba nguo zake
baadhi kwenye begi lake la mgongoni na kutoka ila nje mama yake alimsimamisha na
kuanza kumuuliza maswali, “Unajua Steve toka siku tuliyokutafuta
sikuelewi kabisa, haya umerudi muda mfupi ushajiandaa unaondoka tena, unaenda
wapi mwanangu?” “Mama, nilishakwambia kuwa nataka nioe” “Uoe?
Kwa maisha yapi uliyonayo mwanangu Steve? Dada yako mwenyewe hajaolewa, labda
dada yako angekuwa ameolewa ingekuwa rahisi maana mahali yake tungepeleka huko
unapotaka kuoa, ila mwanangu kuoa gani kwa haraka hivyo na maisha gani uliyonayo
wewe?” “Mama, nampenda huyu mwanamke sitaweza kufanya chochote bila
kumuweka katika akili yangu, nampenda sana nahitaji awe mke wangu nisije kumkosa
bure” “Kheee makubwa, ndiomana dadako anasema umerogwa” “Achana
na maneno ya Dora mama, mimi sijarogwa wala nini. Siku namuona Yule mwanamke
yani moyo wangu haukutaka kuondoka kwenye sura yake, mama humjui huyo mwanamke
ila ukimuona utasema nina haki ya kumpenda, naomba nikawe nae karibu tafadhali
mama yangu” “Kheee makubwa, kwakweli mimi kama mama siwezi kukuruhusu
kufanya hivyo, Steve huna maisha yoyote wewe” Steve hakumsikiliza mama
yake zaidi ya kuondoka tu kwani kwa wakati huo akili yake ilikuwa kwa Sia tu.
Mama yake alibaki akisikitika ila bado swala la kurogwa kwa mwanae halikumuingia
akilini kwani alikuwa anajua mtu akirogwa basi lazima awe zezeta ila mtu anasema
mwenyewe hakuhisi kuwa amerogwa. Steve aliondoka na kwenda hadi kwakina
Sia, sema pale Sia alikuwa na chumba chake kwahiyo toka siku ya kwanza alifikia
hapo na hata muda huo alifikia hapo hapo, Sia hakuwepo ila alitulia nje
akimsubiri. Siku ya leo Erica alitulia akiongea na dada yake
bite ambapo alimueleza na ujio wa James kuwa ilionyesha James alienda kwa lengo
la kumuomba msamaha, “Dada, shemeji James alianza mahusiano na rafiki
yangu Dora na Yule rafiki yangu kanihakikishia kuwa ameathirika tafadhali dada
yangu usimrudie shemeji kabla ya kwenda kupima” “Mmmh naogopa, mfano
nikimkuta kaathirika, nitafanyeje hapo?” “Dada, wewe ni mtu mzima
nakushauri ufanye mambo kiutu uzima yani mtu anapoona umefanya jambo aone kweli
akili yako imepevuka, sitaki kukushauri uachane na shemeji au kukushauri
uendelee nae ila mkishapima na kujua basi utumie busara zako kwa kuendelea nae
au kuachana nae” “Mmmh mdogo wangu mbona unaniacha njiapanda, ni vyema
unishauri mapema ili nijue cha kufanya” “Hapana dada, ushauri wangu
kwasasa ni huo yani James akija tu mwambie mkapime” “Haya sawa, wewe na
huyo Erick wako mliwahi kupima? Sio mnashikana shikana tu, mshawahi
kupima?” “Ndio, mimi na Erick tulipima kabla sijapatwa na matatizo,
nampenda sana ila nilimwambia tukapime kwanza, nishapita sehemu nyingi bila
kupima Mungu kanisaidia ila kwasasa natakiwa niwe makini sana ndiomana nachukua
shauri la kupima” “Mdogo wangu ni kweli ulikuwa muhuni
sana?” “Hapana dada, yani mimi nilikuwa nakuwa na mahusiano kwa muda
sidhani kama mtu ambaye hajachanganya wanaume kwa muda mmoja basi anawekwa
kwenye kundi la umalaya. Sikuchanganya wanaume ila nilikuwa labda nikiachana na
huyu ndio nakuwa na mwingine, na yote nilikuwa kwenye safari ya kutafuta penzi
la dhati, sikuwa na nia nionekane malaya dada ila watu wamenihisi
vibaya” “Pole mdogo wangu ila mara nyingine na mimi bora hata ningekuwa
kama wewe niweze kupata penzi la dhati kuliko hapa nilipoangukia” “Dada,
kuwa kama mimi sio suluhisho maana penzi la dhati halitafutwi kwa mtindo huu ila
penzi la dhati ni kutulia kwa uliyenaye, na kama haeleweki basi usiwe chanzo cha
kuyavunja hayo mahusiano bali chanzo awe yeye mwenyewe” “Mmmmh mdogo
wangu unaongea tu sababu umempata Erick anayekupenda sana, kwakweli hadi Napata
wivu kwa mapenzi yenu, natamani na mimi ningepata anipendaye kama ulivyopata
wewe mdogo wangu, yani safari yangu ya mapenzi naiona ni ndefu sana, na hivi
mume wangu haeleweki ndio kabisa yani. Nilijua nikiwa na mtoto itakuwa nu furaha
sana kwa James ila imekuwa ndivyo sivyo” “Dada, basi zamani nilikuwa
natamani kweli mume wangu nimzalie mtoto wa kwanza wa kiume kwani nilijua ukizaa
mtoto wa kiume basi utapendwa sana na mwanaume, basi siku nimejifungua mtoto wa
kike nikawa mpole sana ila ndio mtoto niliyepewa na Mungu nikashukuru sasa
kilichonishangaza ni kwako dada umezaa mtoto wa kiume ila bado shemeji
anakufanyia vituko, na vile vile Rahim mtoto wangu hakumtaka basi mkewe
alinitambia kweli kliniki sijui mtoto wangu wa kike hatakiwi eti yeye kabeba mimba ya mtoto wa kiume, nilimjibu
ila roho ilikuwa inaniuma sana sasa nimeshangaa eti amepewa talaka na mtoto wake
wa kiume loh!” “Mdogo wangu wanaume hawatabiliki yani umpate tu mwenye
mapenzi nawe na watoto, maana mtoto ni mtoto haijalishi ni wa kike au wa kiume
si unaona wewe, Rahim hamjali mtoto wake ila umempata mtu mwenye mapenzi ya
dhati na mtoto wako, Erick anampenda mwanao kama mwanake kwamaana hiyo hata
ukizaa naye atawapenda watoto wote kwa uzuri kabisa ila ni swala la kumuomba
Mungu pia ili asibadilike maana sisi binadamu tunaweza kubadilika kama
vinyonga” “Mmmh Mungu amsaidie Erick wangu, ila kwanini dada mwanaume
ukimuuliza makosa yake anakubadilishia mada?” “Wanaume hawawezi
kujitetea kama sisi tunavyojua kujitetea yani sisi tukipata upenyo wa kujitetea
weee lazima tushinde sasa mwanaume huwa anaona ni vyema abadili mada maana
kwenye swala la kujitetea kwao ni gumu sana, utaona kuna wanaume wengine
wamefungwa kwa kuonewa kabisa ila sababu kujitetea hawawezi mpaka kwenye kesi
apate mwanasheria mzuri ila mwanamke akisimama kujitetea uwiii unaweza kuhisi
hajawahi kutenda kosa” “Ila wapo wanaume wanaojitetea” “Mwanaume
sio anajitetea ila anakupa maneno laini kukulainisha tu ila kujitetea huwa
hawawezi kama sisi wanawake. Mwanamke kaumbiwa vingi sana vya kufanya umuonee
huruma tofauti na mwanaume” Basi walijaribu pale kushauriana mambo
mbalimbali na mdogo wake kwani kiukweli alikuwa akitamani sana maisha ambayo
mdogo wake aliyaishi kwa kipindi hiko, maisha ya kupendwa na
Erick. Kwa upande wa Rahim, mama yake alimuita maana bado
hakuelewa kwanini Rahim ampe mke wake talaka na kumrudisha kwao, “Unajua
mwanangu Rahim ulichofanya hakipendezi kabisa, mwanamke katoka kujifungua ana
mtoto mdogo ila bila aibu unampa talaka, kweli ni haki hiyo
mwanangu?” “Najua mama sijawahi kukueleza maovu ya Yule mwanamke
ndiomana unamtetea, Yule mwanamke ni mshirikina sijapata kuona, siku ile
nimempiga sababu nilimkuta anachoma dawa huku akinuiza maneno, ilionyesha
alitaka kuniweka mimi ndodndocha wake, na ubaya zaidi kamroga Erica asiye na
hatia kabisa” “Kamroga Erica!” “Ndio alimroga Erica kumbe
hufahamu? Erica ameumwa sana ten asana kumbe muhusika ni huyo mkwe wako hata
sijui kwanini alikuwa akimchukia Erica kiasi kile wakati mimi nilishaachana na
Erica” “Kwa maana hiyo mwanangu umemfukuza Salma sababu ya Erica si
ndio!” “Ndio mama, Yule mwanamke ni mshirikina” “Kwamaana hiyo
unataka kumuoa Erica badala ya Salma si ndio?” “Mama, kungekuwa na
uwezekano wa mimi kumuoa Erica basi ningemuoa. Kipindi niko mbali sikuwaza ni
jinsi gani nampenda Erica ila sasa nampenda sana na nimejua thamani yake, Erica
kanilelea mwanangu mama, mtoto wangu hujamuona tu ila anapendeza sana kupita
watoto wangu wote, yani kupita hata huyo anayelelewa na Salma ambaye bado mdogo
lakini yupo kama amebemendwa, hujamuona mtoto niliyezaa na Erica mama, Yule ndio
mtoto kwakweli natamani kumuoa Erica” “Hebu niondolee ujinga wako mimi,
eti ndio mtoto kwa lipi alilokuwa nalo? Huyo Erica katembea na John, katembea na
wewe, katembea na Babuu sijui Derick katembea nae halafu unataka umuoe umlete
hapa nyumbani kwangu ili atembee na mume wangu pia? Yani mnataka na baba yenu
apate mboga ya Erica? Hivi huna kinyaa Rahim, yani mwanamke umeshea na ndugu
zako kweli humuonei kinyaa jamani! Huyo Erica simtaki kwenye nyumba yangu, yani
simtaki kabisa kabisa” “Mmmh mama nawe kwani humuamini mume
wako?” “Namua,ini vizuri sana ila siwezi jua huyo Erica anawavuta na
nini kiasi kwamba hamuoni kinyaa kuwa nae” Rahim aliamua kuinuka na
kumuaga mama yake kisha kuondoka kwani alihisi kuwa anaweza kumuuliza mama yake
maswali yasiyostahili bure kisha akaonekana hafai. Basi alitoka na
kumkuta Neema amekaa kwenye nyumba yao ila akasema, “Nimepooza shemeji
maana mwenzangu hayupo” “Aaaah Neema ukitaka kuongea si ukaongee na mama
kule maana hata yeye anahitaji apate mtu wa kupiga nae story” Basi Neema
akawa kama anainuka ili kumfata mama mkwe wake ila REahim alimsimamisha kwanza
akimuuliza, “Hivi Yule mdada ambaye ulikuja nae nikapishana nae getini
ni nani na anaishi wapi?” “Yule anaitwa Zainabu, anaishi mtaa wa nyuma
huko, kashika sana dini Yule” “Aaah je ameolewa?” “Hapana
hajaolewa” “Basi napenda kupata mawasiliano yake maana kwasasa nahitaji
kumpata mtu anayeijua dini vizuri ili aweze kunishauri na kunipatia
mwangaza” “Basi nitakupatia shemeji” “Ungenipatia tu sasa
hivi” Basi Neema alimpatia Rahim mawasiliano ya Zainabu kisha Rahim
alimshukuru sana na kuamua kuendelea na safari. Alifurahi sana kupata
mawasiliano ya Zainabu maana aliona kama atamkosa Erica basin i vyema awe na
Yule Zainabu maana alimuona ni binti aliyetulia. Sia alikuwa
kwakina Tumaini siku hiyo na akaongea nae mengi na kujikuta wakipanga vitu vingi
sana, Tumaini aliamua kumwambia Sia kuwa amewahi kuambiwa na Erica kuwa au
anamtaka mdogo wake, “Yani mimi Sia nakupigania tu ila nishawahi
kuambiwa na Erica au unamtaka mdogo wako, jamani hiyo kauli inaniuma sana hadi
leo” “Pole sana wifi yangu” “Yani anafikia hatua ya kuniambia na
wewe tafuta mwanaume uolewe, kwakweli kauli ya Erica hii iliniuma
sana” Wakati wanongea ongea na kupanga panga, leo Erick alirudi nyumbani
mapema sana, na walimshangaa kweli haswa Tumaini, ingawa alikuwa na chuki nae
ila alimuuliza kilichomrudisha mapema vile, “Erick, tatizo nini mbona
leo mapema?” “Kumbe huwa unachunguzahadi muda wangu wa kurudi nyumbani!
Alichokwambia Erica sio kibaya, unatakiwa utafute mwanaume kweli uolewe dada
yangu” Kisha Erick akaondoka zake kuelekea chumbani, hakumsalimia Sia
wala nini yani kamavile hakumuona kuwa yupo pale kwao. Kile kitendo na
yale maneno yaliwaumiza sana, Tumaini akamwambia Sia, “Unaona alivyo na
dharau sababu ya Erica! Yani anasahau hata kama mimi ni dada yake wa
pekee” Sia alitamani kumwambia Tumaini kuhusu babu wa Bagamoyo ila
aliogopa kuonekana mshirikina kwani hakufikiria kama Tumaini angemsapoti kuhusu
hilo swala la kwenda kwa mganga ingawa ni kweli kwa yale yaliyoendelea lazima na
yeye angependa kwenda kwa mganga. Muda kidogo Erick alitoka na kuchukua
chakula kisha akakaa mezani kula, yani Tumaini na Sia walikuwepo tu
wanamuangalia alikula kula kisha akawaangalia na kuwaambia, “Tena kuna
kitu nimesahau” Tumaini alimuuliza kwa shauku kwani alijua atasema kuwa
amesahau kuwakaribisha labda, ingawa chakula kilikuwepo ila walitaka Erick
aonekane kuona uwepo wao kwa kuwakaribisha, “Nini umesahau tena mdogo
wangu?” “Jumamosi, nakuomba wewe na huyo mwenzako mje pale kwenye duka
lile nililokuondoa” “Kivipi? Unataka kunirudisha?” “Utajua siku
hiyo hiyo, yani mje tu msikose” Kisha Erick alimaliza kula na kuinuka
akaenda chumbani kwake, kitendo cha kutokukaribishwa kwa muda huo
hawakukichukulia maanani ila kitendo cha kuitwa Jumamosi kwenye duka ambalo
alikuwepo yeye ndio kikachukuliwa maanani, “Inamaana Erick anataka
kunirudisha dukani?” “Inawezekana, kwani ulimwambia baba
yenu?” “Nampata wapi huyu mzee unadhani? Ni yupo busy muda wote, yani
akitoka asubuhi anaweza akarudi au asirudi hata tushazoea kuishi bila kumuona
baba hata wiki na tunaishi nae nyumba moja” “Sasa si umfate kazini
kwake?” “Aaaah Yule mzee wangu wa kumfata kazini? Yani yeye aliniambia
nikiwa na shida na hela nimtumie tu ujumbe kwenye simu yake kisha ataniingizia
kwenye akaunti yangu na huwa nafanya hivyo, yani unajua mimi nilikuwa naishi kwa
mama na huku kwa baba nilikuwa nakuja mara moja moja sababu ya hivi kupooza
ndani na baba hashindi nyumbani, tulianza kuja kukaa kwa baba baada ya
kukubaliana na Erick kuwa tufanye hivyo ila sasa humu ndani tunaishi kama watu
tusio fahamiana yani unaweza usirudi mwezi mzima na hakuna atakayekuulizia kuwa
umekwenda wapi, baba yupo busy hatari yani hana muda wa kukaa na watoto wake
kabisa, maisha yetu sisi ni tofauti na familia zingine ila siku nataka nikipata
muda nimwambie baba yote ya moyoni ndiomana sijaenda kwa mama wiki nzima hii
kwani nataka siku baba akiwepo nyumbani tu basi nimwambie kila
kitu.” “Nimekuelewa Tumaini, basi tusubiri tu hiyo Jumamosi tujue ni
kitu gani ambacho Erick anasema twende kwenye duka lake” Wakawa
wanaongea ongea pale kisha kukubaliana kuwa siku ya Ijumaa basi Sia aende kulala
pale ili Jumamosi waongozane na huyo Erick huko aliposema
waende. Steve alikaa pale nje ya chumba cha Sia akimsubiria na
siku hiyo Sia alirudi kwenye mida ya saa nne usiku na kumkuta Steve nje kwake,
aliamua kumkaribisha tena ndani maana kuna muda alimuonea huruma ukizingatia sio
kosa lake ila ni kosa ya dawa alizokuwa anamfanyia Erick, ila Steve kuingia mule
ndani wala hakujiona kuwa anamatatizo kumsubiri muda wote huo Sian a aliendelea
kumwambia jambo moja tu kuwa anampenda sana, leo Sia alijaribu kuongea kiasi na
Steve kuangalia akili za ile dawa, “Steve, unanipenda kwa kiasi
gani?” “Sijui hata nieleze vipi ila nakupenda Sia na ninakuona mpya kila
muda” Muda wote Sia alitamani haya maneno yangekuwa yanatoka kwenye
kinywa cha Erick ila yalitoka kwa Steve na kumkosesha amani kabisa, basi muda
ule Sia alianza kupika hukua kisaidiwa na Yule Steve kisha kwenye saa tano usiku
wakala chakula na kuamua kulala, yani siku ya leo pia Sia alilala na Steve kama
jana yake yani alilala nae kama mpenzi wake na kulivyokucha alijilaumu kulala
nae kwani alijua kama Erick akigundua basi hatoweza kuwa nae tena maana ingawa
na matukio yote ila bado alikuwa na imani ya kupiganiwa penzi lake kwa Erick
maana aliona Tumaini yuko upande wake na mama Erick alikuwa upande wake. Basi
kama kawaida alimuomba Steve aondoke na kumwambia kama kuja awe anakuja usiku
sana, “Ila kesho usije maana naenda kulala kwa rafiki
yangu” “Jamani, nimekuzoea sana Sia” Ikabidi ampemaneno ya
kulamlainisha na kuweza kuagana nae. James leo alienda tena kwa
lengo la kuangalia familia yake, alimkuta mama yao yupo ila leo hakumtimua bali
alimwambia jambo moja tu, “Si wewe unataka kurudiana tena na
mwanangu?” “Ndio, nahitaji kuwa karibu na familia yangu, nahitaji kuishi
nao hata sijui niliingiliwa na kitu gani kilichofanya niisahau familia
yangu” “Sawa, basi kesho mguu wako na mwanangu na mimi mwenyewe tunaenda
hospitali kupima yani lazima tupime afya yako na mwanangu tujue ndipo niruhusu
uendelee kuishi na moto wangu” “Sawa mama nimekubali” Kwahiyo
wakakubaliana nae kuwa kesho yake aende kuwachukua waende hospitali kupima ili
kujua afya yake na mke wake, baada ya hapo akaaga na kuondoka. Erica
alimuuliza mama yake swali ambalo aliulizwa na dada yake, “Hivi mama
mfano mkimkuta shemeji kaathirika mtafanyaje?” “Kuna cha kufanyaje hapo?
Ni kumwambia tu ampe mwanangu talaka basi kila mtu aendelee na maisha
yake” “Mmmh mama hivi unadhani atakubali kiurahisi
hivyo?” “Atajijua mwenyewe hakuna aliyemtuma awe muhuni, mwanangu
katulia yeye anataka kumtia uchizi tu masikini ya Mungu, acha mwanangu aendelee
na maisha yake tu” “Mfano mama shemeji akikuletea hela
je!” “Hivi unanionaje Erica, unasahau kuwa mimi ndiye niliyekwambia
turudishe hela za Yule mzee Jimmy! Mimi nachagua hela, kuna hela na hela za
kutumia sio kila hela inayoitwa hela ni ya kuipenda tu maana kuna hela zingine
zinaweza kukutokea puani ndiomana nikasema turudishe hela za Yule
mzee” Erica akacheka tu ila simu yake ilianza kuita na namba ilikuwa
mpya, akaipokea na mpigaji alikuwa ni mzee Jimmy, “Jamani wewe mzee una
nini lakini? Sitaki mawasiliano na wewe” “Nipe mama yako niongee
nae” Erica akampa mama yake ile simu, “Sikia, hata usianze
kuniletea maneno yasiyoeleweka. Niliweka hela zangu kwenye mlango wako
ukazipokea inamaana kuwa umekubali niwe mkweo, hiyo ni posa tu na siku ipo
nitaleta mahari nimchukue mke wangu” “Una akili wewe mzee?
Umechanganyikiwa au?” Simu ikakatika, Mama Erica aliangaliana na mwanae
na kuanza kujadili mwenendo wa huyu mzee, “Unajua huyu mzee simuelewi,
anazungumzia hela gani jamani mbona anatuletea makubwa huyu kwenye familia yetu?
Sijawahi kukubali hela ya huyu mzee maana akili zake nazielewa toka sijamfahamu
machale yalinicheza ndiomana sijawahi kukubali hela zake, kweli jamani tukute
hela za huyu mzee mlangoni tutumie tu inawezekana kweli?” “Sasa hizo
hela anazozisema zitakuwa wapi jamani?” Bite alisikia maongezi yao na
kusogea karibu kuendelea kusema kuhusu hisia zake za hizo hela, “Jamani
mimi nahisi kwamba hizo hela zimechukuliwa na Erick, mnaweza mkanielewa vibaya
ila hizo hela ni Erick tu amezichukua hata sio mwingine” Basi Erica
akaongea kumtetea kidogo Erick, “Angekuwa Erick angeuliza tu jamani, ila
basi isiwe kesi Jumamosi Erick alisema kuwa atakuja Yule Moses kunichukua ili
anipeleke mahalia ambako nitakutana nae basi nitamuuliza na hilo swala,
inawezekana ni kweli Yule mzee aliacha pesa kwetu ila inawezekana hizo pesa
labda zilipeperuka” “Zipeperuke vipi na alisema zilikuwa kwenye bahasha.
Kweli milioni tatu kwenye bahasha ipeperuke? Labda kama ni upepo wa kimbunga ila
sio huu wa kawaida, halafu aliacha mlangoni jamani ipeperuke vipi, mtanielewa
vibaya tu ila atakuwa Erick, mnaona ana pesa ila nataka mjue uwa pesa hainaga
kusema inatosha” “Hata kama ni hivyo bado Erick hawezi kuchukua pesa
nyumbani kwetu” Walibishana tu na kumalizia kazi za siku hiyo kisha
kwenda kulala ambapo usiku Erick alimpigia simu Erica kama ambavyo alikuwa
akimpigia simu zamani na kuendelea kumpa ratiba ya Jumamosi, “Sijaja
kwenu leo na kesho sitakuja sababu naandaa kuhusu Jumamosi na atakuja kukuchukua
Moses, sitaki ujue ni wapi anakuleta ila utajua hiyo sehemu ukifika hata usijali
umesikia mpenzi wangu eeeh!” “Sawa nimekuelewa Erick” Wakaongea
mengi mengi na kisha kuamua kuagana na kulala. Kesho yake kama
walivyopanga James alifika mapema kisha akawasubiri Bite na mama yake wajiandae
halafu akatoka nao kuelekea hospitali, walipofika hospitali mama yao alikaa
pembeni akisubiri waende kupima kiukweli James hakuelewa kwanini mama mkwe
kaamua kufanya vile wakati yale ni mambo ya wana ndoa yani angeenda tu yeye na
mke wake ila mama mkwe nae alionekana yupo bega kwa bega kutaka kujua kisa na
mkasa. Alitulia tu kwa muda kiasi wakingoja majibu na badae waliitwa kwa
daktari kwaajili ya majibu na kupata majibu kuwa Bite ni mzima ila James
ameathirika, kwakweli James alijaribu kuvuta picha ya wanawake wote aliopita nao
ila hakujua ni yupi kamsababishia maambukizi ya virusi vya ukimwi, daktari
aliwashauri pale ila waliondoka bila maelewano wala nini, na walipotoka nje kila
mmoja aliondoka kivyake vyake yani James aliwaacha pale hospitali kana kwamba
hakwenda nao hospitali kisha yeye kuondoka zake na kufanya Bite arudi kwa mama
yake tu na kumwambia ilivyokuwa halafu na wao kuondoka. Walipofika
nyumbani mama yao alisema alijua tu, “Yani nilitaka nishangae James awe
na mahusiano na Yule Dora halafu atoke mzima hapana Yule James kayataka
mwenyewe” Erica akasema, “Ila shemeji ni yeye mwenyewe ana tabia
mbaya, tunaweza sema ni Dora tu ila usikute hata shemeji kapeleka ugonjwa kwa
Dora kwani hiyo kansa ya shingo ya kizazi kaitoa kwa Dora!” “Nimenyamaza
kimya tu ila roho inaniuma sana yani siamini haya mambo naona kama maigizo vile
ngoja tu nikae kimya” Ilionyesha kuwa Bite hakuwa na furaha kabisa ila
alijaribu tu kuweka furaha katika sura yake. Jioni ya siku hiyo
kama ambavyo Tumaini na Sia walivyopanga kuwa walale nyumba moja yani pale
nyumbani kwakina Tumaini na ilikuwa hivyo maana Sia alienda pale na walifanya
vitu pamoja siku hiyo. Erick alirudi kwao kwenye mida ya saa tano na
ilionyesha alichoka sana kwani alijikuta tu akikaa sebleni na kushikwa usingizi
hapo hapo, Sia alipoona vile alimuita Tumaini na kumwambia jinsi Erick
alivyolala pale sebleni na kuanza kumpa wazo lake, “Unaonaje nisogee
pale kwa Erick unipige nae picha halafu tumtumie Erica au
unasemaje?” “Umekumbuka swala muhimu sana” Basi Sia alienda
kujifunga kanga kisha kuanza kupiga picha mbalimbali na Erick huku wakitamani
hata kumvua nguo ila Sia alipoanza kumfungua shati Erick alishtuka na kuchukia
sana kisha kuanza kumfokea dada yake, “Ujinga ujinga wako kama huu ndio
unafanya niondoe upendo wangu kwako. Wenzio huwa upande wa kaka zao yani hupenda
wachumba wale ambao kaka zao wamewachugua ila wewe unataka kunichagulia mimi
mwanamke! Sikupendi Tumaini” Kisha akainuka na kwenda chumbani kwake ila
bado haikuwaingia akilini kwani zile zile picha walimtumia Erica na kumpigia
simu kuwa aingie kwenye mtandao walijua tu atapaniki sana. Kisha
wakalala. Palipokucha walijiandaa kama kawaida na kuondoka na huyo huyo
Erick kuelekea kwenye lile duka lake, walishangaa walipofika jinsi palivyopambwa
na jinsi wageni walivyokuwa wakiwasili pale dukani, walijiuliza kuwa kuna nini
wakapata kusikia tetesi kuwa siku hiyo ni siku ambayo Erick anataka kukabidhi
duka lile kwa Erica, kwakweli Tumaini alichukia sana alihisi kama kuna donge
moyoni mwake, akasikia kuwa Moses ndio anaenda kumchukua Erica, kwakweli
walichukia sana, “Natamani nisingeiona hii siku aaargh” “Ila
usijali Tumaini, unajua Erica kama aliziona zile picha kwa hakika hatofika
hapa” “Kweli eeh!” “Ndio ni kweli hatofika” Basi muda
nao ulienda na Erica hakutokezea wakahisi kuwa kweli njama zao zimefanikiwa na
kujiona kuwa ni wajanja jana yake kufanya vile ingawa hawakujua kuwa Erick
anataka kufanya nini, laiti wangejua basi wangefanya makubwa kushinda yale
waliyoyafanya jana. Wageni walianza kuondoka baada ya kuona muhusika
hafiki, kwakweli hata Erick alichanganyikiwa kwani kila alipompigia Erica simu
hakupokea simu yake. Muda kidogo aliona gari la Moses likifika eneo lile
kwahiyo Erick alijua ni Moses kamleta Erica lakini alishangaa kumuona Moses
akishuka mwenyewe bila ya Erica. Muda kidogo
aliona gari la Moses likifika eneo lile kwahiyo Erick alijua ni Moses kamleta
Erica lakini alishangaa kumuona Moses akishuka mwenyewe bila ya
Erica. Kwakweli Erick alichanganyikiwa kabisa na kumsogelea Moses
akamkunja kuwa ameshindwa vipi kumshawishi Erica kufika
pale, “Umeshindwa vipi Moses? Unajua nakuamini sana” “Usinilaumu
bosi, nimefanya jitihada zangu zote. Angalia Yule” Kuangalia pembeni
akaona gari ya Erica ikiingia yani hapo alijikuta akijawa na tabasamu tu na
kusogea karibu ili kumfungulia mlango, kisha Erica alishuka kwelye lile gari,
alikuwa amechelewa ila kile kitendo cha kufika tu ilikuwa ni faraja kubwa sana
kwa Erick, akamkumbatia kwa furaha ya kumuona muda huo. Hakutaka
kusikiliza maelezo ya kwanini amechelewa bali alienda kumkabidhi lile duka,
kwakweli Tumaini na Sia waliondoka kwani hawakuweza kuendelea kuangalia hadi
mwishoni kitu kinachotokea. Erick alimwambia Erica, “Najua ulikuwa
unatamani sana kuanza biashara, kuanzia sasa huna haja tena ya kutafuta kazi
Erica maana kazi yako itakuwa kusimamia hapa na kuangalia maendeleo ya duka
lako” Erica alimsogelea Erick na kumkumbatia huku akimbusu kwa
furaha. Sababu muda ulikuwa umeenda, basi Erick alitoka na Erica eneo
lile na kwenda hotelini ambako alisema wawaandalie chakula kisha walikuwa pamoja
na wageni waalikwa wengine waliobaki, na baada ya kula wengi waliondoka na
kuwaacha wawili tu yani Erick na Erica, kwakweli Erick alikuwa akifurahia tu
uwepo wa Erica hata kumuuliza kwanini kachelewa hakuwa na wazo hilo, mpaka Erica
mwenyewe akamuanza, “Erick, jamani mbona hujaniuliza kuwa kwanini
nimechelewa” “Aaaah nimejikuta nikiwa na furaha sana mpenzi wangu hadi
nimesahau kama ulichelewa yani sijaumia kuondoka kwa wageni ila ningeumia
kutokukuona wewe, eeh kwanini umechelewa kipenzi changu?” “Ni hivi, basi
niliamka asubuhi vizuri tu na kuandaa nguo zangu kwaajili ya kuja sasa nikashika
simu nikakuta kuna ujumbe unasema niingie facebook, si ndio nikaingia nikakuta
picha zako tena na Sia, kiukweli nilishikwa na wivu wa hali ya juu unajua Erick
nakupenda sana yani sana. Kiukweli niliumia kuona tumepanga vizuri na wewe kweli
unaenda kutembea na Yule mwanamke ambaye huwa nagombana nae kila siku? Niliumia
sana mpenzi” Erick akataka kuonyeshwa hizo picha, basi Erica akafungua
simu yake na kumuonyesha Erick, “Kumbe jana nilipokuwa nimechoka ndio
wakafanya huu ujinga, tena mpiga picha atakuwa tumaini huyo. Ngoja nirudi
nyumbani atanieleza, yani ni dada yangu lakini hajielewi. Sasa mpenzi wangu
ungenihukumu bila sababu tu, sijui nani kanisaidia kuongea na wewe ukaelewa na
kuja dah namshukuru sana” “Yani nilikuwa nimechukia hata kujiandaa
sikutaka tena basi nikawa nimekaa tu kwa hasira, basi hadi muda Moses anafika
nilikuwa sijajiandaa na akaniambia twende nikamwambia siendi tena akaanza
kunibembeleza kuwa huwezi kumuelewa ila bado nilimgomea nikaenda chumbani basi
mama akanifata na kuanza kuongea na mimi, nikaona nisimfiche nimwambia kuwa kuna
picha nimetumiwa zako na Sia, mama akasema hao wamenipangia njama sababu kwanini
wasitume siku zote hadi siku niliyopanga kuonana nawe, basi mama aliongea nami
pale nikaanza anza kumuelewa ndipo nilipotoka tena na Moses kusema kuwa jana
mlikuwa wote kwenye maandalizi na mmerudi mmechoka kweli, niliingia ndani
nikajifikiria nikasema kwavile nakupenda acha tu nije ndio nikaenda kujiandaa
basi nilipomaliza nilimwambia Moses awe mbele na gari yake na mimi nitakuwa
nyuma yake na gari yangu maana nilitaka kukufanyia surprise pia ujue kama najua
kuendesha gari” “kwanza Erica nisamehe mpenzi wangu maana kuchoka kwangu
ndio kumefanya wale wajinga wanipige picha ila hakuna chochote kinachoendelea
baina yangu na Sia, haya ndio mambo yaliyofanya kipindi unaumwa niishi hotelini
tu sababu ya ujinga kama huu. Nisamehe mpenzi wangu” “Usijali
nimekusamehe sababu nakupenda sana” Erick alitabasamu kwani alifurahi
sana kusikia Erica akimwambia tu hivyo, akamsogelea karibu na kumbusu. Alikuwa
na tabasamu usoni ila alipata chuki kubwa sana juu ya dada yake Tumaini kwani
aliona hamtakii mema na mapenzi yake, kisha aliendelea kufurahia uwepo wa mpenzi
wake Erica na baada ya maongezi yao aliamua sasa kumrudisha nyumbani
kwao, “Mmmh Erick, narudi mwenyewe nyumbani. Kumbuka nina gari, kwahiyo
naenda mwenyewe tu” “Usiku huu Erica, acha nikurudishe halafu mimi
nitampigia dereva anifate ila naomba nikurudishe sitaweza kuwa na furaha
nikisikia habari mbaya juu yako, bora itupate wote” Erica alimuangalia
sana Erica na kujiuliza upendo huu wa Erick siku zote alizokuwa akitangatanga na
kuumizwa na mapenzi ulikuwa wapi upendo wa hivi? Hakupata jibu
kwakweli. Kwahiyo muda huo Erica na Erick walipanda kwenye gari
wakielekea nyumbani kwao na wakina Erica. Walifika kwakina
Erica ilikuwa ni usiku sana tayari maana ilikuwa inakaribia saa tano usiku, ila
walipokuwa njiani tayari Erick alimuita dereva wake kwahiyo walivyofika kwakina
Erica tu na dereva wake alikuwa ameshawasili basi akaingiza lile gari kwenye
uwanja wa kina Erica na kumsaidia kufunga geti kisha kumuaga kwa kumbusu Erica
na kuondoka amapo Erick alienda kupanda ile gari iliyokuja na dereva na
kuondoka. Erica alienda ndani kwao na kumkuta mama yake akiwa sebleni,
kisha mama yake akasema “Sijalala Erica nakusubiria wewe mwanangu. Najua
na Erick itakuwa mmeitiana mambo mazuri tu ila mpaka muda huu unanipa mashaka
mwanangu? Umeenda kufanya mapenzi na Erick?” “Hapana mama, nimekubaliana
nae mpaka ndoa” “Usitake kunichekesha mie, hilo swala la kukubaliana
mpaka ndoa liko wapi? Yani toka lini Simba na swala wakae pamoja halafu umwambie
samba subiri nimchemshe huyo swala ndiyo umle. Erica mwanangu nakwambia kila
siku wanaume sio wa kuwaamini kiasi hiko, sijakwambia hata picha za kijinga vile
uziamini ila sababu mwanaume kaonyesha hitaji lake la kukuoa basi acha akuoe
mwanangu kwanza” “Sawa mama nimekuelewa hakuna tatizo mama
yangu” Kisha akamuuliza sasa kuwa ni kitu gani Erick alimuitia siku
hiyo, “Huwezi kuamini mama, Erick amenikabidhi duka yani ndio nitakuwa
naenda kufanya biashara, sina sababu tena ya kutafuta kazi” “Wow
mwanangu hongera sana” Bite alisikia na kwenda kusikiliza vizuri
kwakweli alijisikia rah asana na kumuona mdogo wake kuwa na bahati ya hali ya
juu. Ila akamuuliza kuhusu swali ya zile hela za mzee Jimmy, “Eeeeh
Erica umemuuliza na kuhusu hela za Yule mzee?” “Aaah nimesahau ila
nitamuuliza tu” Basi mama yao akaendelea kuongea, “Tena Bite
kakumbusha, mwanangu Yule mzee yupo serious alikuja hapa anasema tumekula posa
yake, na anasema kashaiambia familia yake kuwa atakuoa” “Kheee huyo mzee
ana wazimu mama” “Tena ana wazimu kabisa mwanangu, yani Yule mzee hafai
kabisa. Hebu umuulize Erick na kama akikataa basi huyo mzee niachieni mimi
nitajua jinsi ya kula nae sahani moja, si anajifanya akili zake zimefyatuka basi
zangu ndio hazipo kabisa.” Basi Erica akaongea ongea na mama yake kisha
akaenda chumbani kwake kulala. Erick alienda nyumbani kwao na
kufika tu alimuita dada yake kwani alikuwa na lengo la kumsema kwanza, Tumaini
alitoka chumbani ila alikuwa amevimba kwa hasira jumlisha wivu maana kwake
halikuwa swala la kawaida kuona mdogo wake anaacha kumpa yeye vitu vya thamani
anampa mwanamke, anamuondoa yeye kwenye duka na kumpa mwanamke? Kwakweli aliumia
sana, kwahiyo alikuwa amevimba kwa hasira hata kumsalimia Erick hakumsalimia
tena na kumwambia, “Niambie ulichoniitia” “Unajua wewe Tumaini
ni dada yangu ila hujielewi, hivi unadhani ungejielewa mimi ningefanya yote
haya?” “Usiniambie hivyo Erick, yani unamthamini mwanamke na kusahau
kuwa mimi ndiye ndugu yako pekee niliyekuwepo! Hivi ukipata matatizo wewe ni
nani atakayeumia hapa, unafikiri Erica ataumia kuzidi mimi?” “Tumaini,
Yule Erica si mke mwenzio ujue, yule ni wifi yako hutakiwi kuweka vita na
ushindani na yeye. Nilikuthamini, nilikuheshimu dada yangu ila mambo yako
unayoyafanya ndio yanafanya niwe hivi leo, haiwezekani wewe uwe upande wa Sia,
huwezi kunichagulia mwanamke wa kuwa nae mimi, mara ulianza na Yule Asha sijui
yani wewe dada yangu sijui una akili gani, hujui kama unatakiwa uwe upande wa
kaka yako? Hivi mfano nipo na Erica haijalishi Sia alikuwa rafiki yako vipi ila
unatakiwa uwe upande wa Erica ili uweze kuenenda na mimi kaka yako halafu
ungeona kama ukitaka kitu ningegoma kukupatia. Hivi unadhani mimi ningeshindwa
kumfungulia biashara nyingine Erica? Naweza na hata sasa naweza kumbadilishia
biashara na kukurudisha pale ila kwanza akili yako hiyo isomeshe ijue inafanya
kazi gani. Hivi kweli wewe wa kushirikiana na Sia kunipiga piga za ajabu
unamtumia Erica ili iweje? Mara nyingine unaweza sema mawifi wakorofi sijui mke
wa kaka mbaya ila kumbe mbaya ni wewe, hivi ukiwa karibu na wifi yako kungekuwa
na tatizo? Mbona Erica hana tatizo na wewe ila kila siku wewe kuleta matatizo na
Erica? Jirekebishe bhana” Tumaini alichukia na kwenda zake chumbani
maana hata hakutaka kusikiliza maneno ya kaka yake ingawa alichoambiwa na kaka
yake kilikuwa cha ukweli. Akawaza tu asubuhi aende kwao kwa mama yake
labda akaongee nae kuhusu swala hilo maana yeye alihisi kuonewa
tu. James hakuwa na hali badala yake alikunywa sana pombe kisha
akaenda kwa Yule mwanamke aliyezaa nae ambaye alikuwa ni msichana wao wa ndani,
Yule mwanamke alivyomuona tena aliona kuwa neema imemuangukia kwa kumpata James
tena baada ya mke wake kufanya varangati la kumrudisha James nyumbani,
alimkaribisha vizuri sana na akampa malezi yote kama mume maana hakutaka tena
kuachwa na James. Yani siku hiyo aliona ndio siku ya kumuonyesha James
ufundi wote aliokuwa nao ili James asinyakuliwe tena na mke
wake, “Jamani james, nilisikitika sana ambavyo uliondoka moja kwa moja
sababu ya mkeo, kweli James ukagoma kabisa kuonana nami sababu ya mkeo! Ila
nafurahi sana leo umekuja mume wangu” Basi huyu dada alimpa James huduma
zote na kumfanya James asahau swala la ugonjwa kabisa, alilala huku amechoka kwa
furaha ya kupokelewa na Yule mwanamke jumlisha pombe alizokuwa
amekunywa. Kulipokucha, Yule dada aliamka na kumsalimia James maana
aliona ndio mume wake nay eye alitamani sana ifike tena wakati ambao James
angeenda kulala kwake, basi akaanza kuongea nae kimapenzi ili kumfanya ampende
zaidi, “Unajua James mimi ndio nakupenda, mtoto huyu kachukua jina lako
nay eye anaitwa James sababu tu ya upendo wangu juu yako sio mkeo kumpa mtoto
jina Junior sasa Junior ndio mavitu gani? Yani Yule mkeo hana hata upendo na
wewe, ni mimi nikupendaye” “Nashukuru sana mama James, nashukuru pia
kumpata mrithi wa jina langu kwenye ulimwengu ila asirithi na tabia
zangu” “Hamna bhana James, wewe huna tabia mbaya ila mkeo hakujua jinsi
ya kuishi na wewe. Nilikuwa naumia sana vile anakuacha uteseke eti sababu ni
mjamzito, mbona mimi nilikuwa nakupa wakati nimebeba mimba ya James! Ni upendo
tu, nakupenda sana tena natamani unioe kabisa kabisa” James akatabasamu
tu ila alijua wazi huyo msichana anamfurahia sababu hajajua ukweli kuwa ameenda
pale baada ya kujigundua kuwa ameathirika kwahiyo alikuwa anaenda kujiliwaza tu
na akili yake. Sababu siku hiyo haikuwa siku ya kwenda kazini kwahiyo
aliamka na kujiandaa tu kisha kuondoka kuelekea nyumbani kwake ili akavae nguo
zingine kwani kwa muda huo shida yake ilikuwa kukutana na Dora amuulize pia kama
nay eye ameathirika maana siku zilizopita alikuwa naye kwenye
mahusiano. Tumaini alienda kwa mama yake na kweli alimkuta mama
yake siku hiyo alikuwa mwenyewe nyumbani kwani ndugu zake wote walitoka,
akamsalimia na kumuuliza “Kheee mama mbona nyumba ipo kimya
hivi?” “Si unajua leo siku ya mapumziko basi wameenda kwenye matembezi
huko na kuniacha mwenyewe. Eeeh na wewe mbona siku hizi huji
nyumbani?” “Mama, yani acha tu. Yule mdogo wangu, ndugu yangu ambaye
mimi ndiye dada yake wa kipekee kanifanyia mambo ya ajabu sana” “Mambo
gani tena mwanangu?” Basi Tumaini akamueleza kwa kifupi kaka yake
alichokifanya na jinsi anvyomjibu, “Ila mwanangu kwani huyo wifi yako
una ugomvi nae? Na ndugu yako anafikia vipi kumthamini mwanamke kushinda wewe
ndugu yake? Au karogwa?” “Ndio nahisi hivyo mama, nahisi ndugu yangu
karogwa. Huyo mwanamke sina ugomvi nae ila sitaki awe na kaka yangu kwani kazaa
na mwanaume mwingine. Yupo msichana mama nayempenda kwa dhati kaka yangu ndiye
nataka huyo awe wifi yangu” “Tumaini mwanangu, kwani mtu akizaa ndio
hafai kupendwa tena?” “Hapana mama ila kazaa na mwanaume
mwingine” “Pengine alibakwa!” “Hakubakwa mama, huyo msichana ni
malaya” “Hata kama ni malaya ndio kampenda, mwanangu mwanamke yeyote
akipendwa na kaka yako mwache awe nae kama ana kasoro utamwambia tu kaka yako
ili azichunguze mwenyewe ila sio wewe kumuwekea chuki au kumchagulia kaka yako
mwanamke wa kuishi nae. Kumbuka huyo mwanamke hatoishi na wewe, ataishi na kaka
yako, maswala ya kuchaguliana wachumba yalishapitwa na wakati mwanangu. Una
uhakika gani huyo unayemtaka wewe katulia?” “Nina uhakika mama, Sia
namfahamu. Ni binti mpole, mwenye hofu ya Mungu na ana upendo ila sio huyo Erica
jamani huyo msichana hafai mama yangu” “Ndio hafai mwanangu ila si wewe
ambaye utaishi na huyo Erica, sikia nikwambie cha kufanya ili kula sahani moja
na kaka yako kuwa nae pamoja na umsapoti kwa anachofanya kama kizuri mpe hongera
na kama kibaya usimponde ila mwambie ukweli nadhani unanielewa. Kaa na kaka yako
ongea nae kirafiki ujue ni kwanini anampenda huyo anayempenda na kwanini
anamchukia huyo unayempenda wewe. Ongea nae kirafiki na tena mwambie kaka yako
upo tayari kuwa karibu na huyo wifi yako mwingine uone kama atakufanyia tena
vitu vya ajabu.” “Mama, unasema tu ila hujui kinachoendelea namchukia
huyo Erica yani simpendi kabisa, ni mbaya Yule msichana na ana roho mbaya,
kafanya undugu wangu na Erick uvurugike kabisa, simpendi namchukia” Yani
Tumaini hakutaka kusikia ushauri wa mama yake kabisa kwani yeye alihisi tu
kuonewa na vitu mbalimbali kwani alihisi pia kaka yake karogwa kwani hakufikiria
kama ni kitu kinachowezekana yani mwanamke wan je athaminiwe zaidi kuliko damu
moja. Rahim leo hakuwa na furaha kabisa kwani toka alipopewa
namba ya Zainabu alikuwa akijaribu kumpigia ili ampe hoja zake alishangaa
Zainabu akiongea nae maneno ya Mungu tu, ingawa alikuwa akitaka na ushauri kweli
ila lengo lake kubwa kwa Zainabu ni kumtaka kimapenzi kwahiyo swala la Zainabu
kumwambia maneno ya Mungu hakulipenda kabisa na akaona ni vigumu kumvaa huyo
mwanamke, alikuwa na mawazo sana ila alifika Babuu na kuongea na ndugu yake
ambapo alimuuliza kuwa ana mawazo ya kitu gani, “Sikia Babuu,
nishamtimua mke wangu simtaki tena najua unatambua hilo. Najua pia kumpata Erica
kwasasa ni ngumu sana, ila kuna mwanamke nimemuona na nadhani ananifaa sana
katika maisha yangu” “Umemchunguza kaka” “Aaah hapana ila
anaonekana ni mwanamke mwadilifu. Tatizo linalonifanya niwe na mawazo sana ni
jinsi ya kumuingia Yule mwanamke” “Kwani tatizo ni nini mpaka
ishindikane kumuingia?” “Yani ni mwanamke mshika dini balaa, nimejaribu
kumpigia simu mara kadhaa anaanza kunieleza sijui habari za Quran na mimi sitaki
hizo habari kwakweli, sijui nitawezaje kumpata” “Sasa ndugu yangu
kuzunguka kote huko hujajua jinsi ya kumuingia mwanamke? Ukimtaka mwanamke
ambaye unaona ni vigumu kuingilika jifanye na wewe upo upande wake, yani kama
huyo alivyo jifanye na wewe ni Muislamu safi yani anza kwenda Msikitini ndugu
yangu halafu unapita na pale kwao unajifanya kuongea mambo ya dini tu. Kama
mwanamke mlokole na anashindwa kuingilika unajifanya nawe mlokole, ndugu eeeh
wanawake ni viumbe dhaifu na wepesi kudanganyika yani ukijifanya umefata dini
utampata ila ngoja nikuulize una lengo nae kweli au?” “Akikubali naoa
kabisa, yani mimi siwezi kumrudia Salma yani huyo Zainabu akikubali ndio atakuwa
mke wangu na hivi kashika dini na mimi nina watoto wengi wengi basi ataweza
kulea watoto wangu” “Kama ni hivyo basi nitakusaidia yani tutakuwa
tunaenda wote kwake, nitahakikisha hadi tunampata anakuwa kwetu
kaka” “Asante sana Babuu” Kiukweli Babuu alijitolea kumsaidia
Rahim kuhusu kumpata Zainabu sio sababu anahitaji ampate ila sababu hataki
amfatilie Erica kwani anahisi Rahim akiwa na Erica basi yeye ataumia sana moyo
wake. Nasma aliamua kurudi tena nyumbani kwake na safari hii
aliamua kurudi na mama yake kwani aligoma kwenda na ndugu yake mwingine sababu
hakuamini tena swala la kuishi na ndugu kwa mume kama Bahati, mama yake
alikubali ili akaishi nae kidogo mpaka pale mtoto akichangamka zaidi, basi
aliondoka na mama yake na kwenda nae nyumbani kwake. Walivyofika mama
yake alimuuliza vizuri kuhusu dawa alizopewa na baba yake na jinsi
zilivyomgeuka, kumbe muda huo alifika dada yake Bahati aliposikia wanaongea
ndani akajibanza pale nje akiwasikiliza, “Yani mama tulifanya dawa ili
Bahati anipende mimi tu awe haoni wala hasikii juu yangu sema zile dawa hajiweza
kumfikia” Kisha akaanza kumueleza alivyofanya dawa na kufanya Bahati
abadilike kabisa maana kawa tena hashikiki na nyumbani halali maana jogoo jogoo
haswaa yani kila jike lake, kumbe dada wa Bahati alisikiliza kwa makini sana
akaona ile taarifa ni vyema akaipeleka kwa ndugu wengine wa Bahati maana
walishangaa kwa kipindi hiko Bahati kubadilika kuwa na riho ya tofauti, ni kweli
mwwanzo walishiriki katika kumpa dawa ila hawakutaka ndugu yao apewe dawa zaidi
maana madhara ya dawa waliyaelewa kwahiyo ile habari ilimshtua kidogo na kuamua
kwenda kuwaambia ndugu zao wengine. Mule ndani Nasma alikuwa akiongea tu
na mama yake bila kujua kinachoendelea nje kumbe wifi yake alishasikiliza kila
kitu. James alikutaka na Dora kama alivyopanga nae ili kuongea
nae kuhusu lile swala ambalo lilikuwa likisumbua akili yake,
alimuuliza “Dora ushawahi kupima wewe?” “Kupima? Aaah
sijawahi” “Basi ningependa ukapime” “Kwani vipi James? Mbona
sikuelewi?” “Aaaah ukapime tu au twende nikusindikize” Kwakweli
akili yake haikuwa sawa kabisa na kuamua muda huo huo kwenda na James kupima,
walifika hospitali na walipima wote wawili kwani hata James bado hakuwa na imani
na majibu yake ya mwanzo, majibu yakaja kuwa wote wameathirika. Kwakweli
ile habari ilionekana kumchanganya sana Dora, ikabidi James ambembeleze tu na
kwend akukaa nae kwenye gari yake maana yeye alishalia jana yake yakaisha
kwahiyo alikuwa akimbembeleza tu Dora, yani Dora alilia huku
akisema, “Yani niliwahi kumwambia Erica kuwa nimeathirika ila nilikuwa
namtania tu yani nilifanya kuwa na ukimwi kama kitu cha utani eti leo nina
ukimwi kweli mimi Dora jamani, haiwezekani nilikuwa natania tu
jamani” “Yani Dora ulikuwa unatania kusema kuwa una ukimwi! Walioupata
pia hawakutaka waupate ila imetokea tu yani wewe ukatania unao kweli! Au
ndiomana wakakazania nikapime sababu wewe ulitania kuwa unao? Haya sasa unao
kweli, kuwa mpole tu tuanze dozi” Kiukweli Dora hakuwa na furaha kabisa
hivyo kwa siku hiyo aliamua kwenda tena baa na James na kunywa sana pombe yani
alirudi kwao ni usiku kabisa na alirudishwa na James na kwenda kulala tu kisha
James naye alienda kwa Yule mwanamke ambaye alikuwa ndio mdada wao wa
kazi. Kulipokucha Dora aliamka akiwa na uchovu sana ukijumlisha bia za
jana na mawazo basi aliamka na uchovu balaa, akainuka na kwenda kuoga ila bado
alikuwa hajiamini amini kama ameathirika maana hakutegemea kabisa kama kuna muda
atapatwa na virusi vya ukimwi. Mama yake alimuona jinsi alivyo na mawazo
ila Dora hakumwambia mama yake kuwa ni kitu gani kinamsumbua badala yake,
aliishia tu kuongea nae mambo mengine, kisha mama yake akaanza
kumueleza, “Dora mdogo wako Steve, toka juzi hayupo hapa nyumbani yani
simuelewi kabisa mdogo wako jamani ana matatizo gani?” “Kheee hajarudi
nyumbani?” “Ndio hajarudi, jana na wewe umerudishwa hapa usiku wa manane
jamani kuna watu wanazaa ila wengine sisi sijui tumezaa mavitu gani jamani yani
watoto wangu wawili tu nyie ila ni kichefuchefu. Haya ukamlete basi mdogo wako
ulipoenda kumtoa siku ile” “Sawa mimi nitaenda mama ila nilikwambia
tusimame kwenye maombi” “Hayo maombi utakuwa nayo wewe bhana, jana
umerudi hapa umelewa bwiii hayo maombi ya wapi ya walevi? Hata huyo
anayekuombeeni naye atakuwa akili zake sio nzuri yani haoni kama anaombea
vichaa, sasa ukamlete mdogo wako, mi ujinga huu siutaki kwakweli” “Sawa
mama nitaenda ila ngoja nipumzike kidogo halafu nitaenda” “Hakikisha
mdogo wako anarudi hapa nyumbani, sawa” “Sawa mama” Kisha Dora
aliingia ndani kwake tena alikuwa na mawazo mengi sana ila alitulia kwanza ili
atulize akili zake ndio ajiandae kwenda kwa Sia kumfatikia mdogo wake
Steve. “Safari hii huyo Sia itabidi nimpeleke tu kwa mwanamaombi ili
mdogo wangu akomboke, yani ukisikia mchimba shimo kadumbukia mwenyewe ndio huku
sasa, yani nimetumbukia hatari kwenye shimo nililochimba mwenyewe, nimeenda kwa
mganga kumkorogea James dawa ila nimepata ukimwi, nilikuwa namdanganya Erica
kuwa nina ukimwi ili anihurumie na nimeupata kweli. Nimempleka Sia ili amkoroge
mwanaume wake mwishowe dawa zimempata mdogo wangu sasa nahangaika dah! Navuna
nilichokipanda” Kwa kiasi alikuwa anajuta kwa yale
aliyoyatenda. Siku ya leo Erick alienda kwa kina Erica na
aliomba kumchukua tena ilia toke nae sema sababu ilikuwa ni mapema basi mama
Erica aliruhusu waweze kutoka, na Erica akajiandaa na kuondoka na
Erick, “Tunaenda wapi Erick?” “Utapaona tu, subiri
tu” Basi gari ikaenda na kuingia kwenye nyumba ya kifahari, akili ya
Erica ikacheza na kuhisi pengine ile nyumba ni ya Erick, kwa hakika ilikuwa ni
nzuri sana kiasi cha kutamani kuolewa na Erica muda huo, basi Erica aliingiza
gari ndani na kushuka kisha kumfungulia mlango Erica ili ashuke na
kumkaribisha, “Najua toka tumeanza mahusiano sijawahi kukuleta kwetu,
karibu kwetu leo” “Jamani Erick kumbe unanileta kwenu! Mbona hukuniambia
jamani” “Ningekwambia ufanye nini sasa” “Ili nijiandae, mfano
kama baba yako yupo” “Baba hayupo, na hata akiwepo ni vizuri tu ili
akufahamu” Basi akamkaribisha ndani na pale sebleni walimkuta Tumaini
ambaye alichukia sana kuwaona, Erica alimsalimia Tumaini ila Tumaini hakuitikia
ile salamu wala nini. Erick alikaa na Erica pale pale sebleni na
kumuuliza dada yake, “Tumaini unaweza kuniambia ni kwanini unamchukia
Erica?” “Sina sababu ila simpendi tu, mimi nampenda Sia” “Hivi
unajua ambacho Sia alitaka kunifanyia kaka yako?” “Sijui” Basi
Erick alimueleza kwa kifupi tu jinsi walivyompeleka mdogo wake Dora kwenye
maombi sababu ya Sia, “Haiwezekani yani hiyo kitu haipo kabisa, mimi Sia
namfahamu vizuri sana na Sia hawezi kwenda kwa mganga” “Huamini dada
yangu, ila ni vyema ukamuuliza mwenyewe” “Ngoja nimpigie
simu” Akataka kupiga simu ila kaka yake akamzuia na
kumwambia, “Hapana usipige simu ila jibebe uende nyumbani kwao ukaongee
nae ana kwa ana ili akuambie machoni pako kama hii habari ni uongo au
vipi?” “Bado siamini, Sia hawezi kwenda kwa mganga,
haiwezekani” Basi aliinuka kweli na kwenda kujitayarisha kisha kuondoka
zake tena bila hata ya kuwaaga wala nini maana alikuwa na chuki
nao. Tumainia alienda hadi kwakina Sia, akafika maeneo yale na
kukuta Sia na Dora wamesimama nje wakiongea, huku Dora akisema “Sia
unajua ulichomfanyia mdogo wangu sio sawa kabisa, inabidi uende kwenye maombi
ukatubu” “Sio kosa langu ni kosa la mdogo wako na uroho
wake” Mara mdogo wake Dora alitoka kwenye chumba cha Sia na kusogea
karibu kisha kumkumbatia Sia na kumwambia dada yake, “Wewe ondoka zako
tu maana mimi kwa Sia ndio nimefika” Kisha akambusu Sia, haya mambo yote
Tumaini aliyaona na kuyasikia kwakweli yalimstaajabisha
sana. Mara mdogo wake Dora alitoka kwenye chumba cha
Sia na kusogea karibu kisha kumkumbatia Sia na kumwambia dada
yake, “Wewe ondoka zako tu maana mimi kwa Sia ndio
nimefika” Kisha akambusu Sia, haya mambo yote Tumaini aliyaona na
kuyasikia kwakweli yalimstaajabisha sana. Tumaini hakuamini kile kitu na
kujihisi kama yupo ndotoni, aliamua kujitokeza katikati yao, kitendo kile cha
Sia kumuona Tumaini mbele yao akamsukumiza Steve, kile kitu kilimsikitisha zaidi
Tumaini na kusema, “Sia hata usingemsukumiza huyo maana nimesikia kila
kitu, ila mpaka muda huu nashindwa kuamini, hivi si ni wewe Sia uliyekunywa sumu
kwaajili ya kaka yangu? Inamaana ulikuwa unaigiza kunywa sumu? Upendo uliousema
unao dhidi ya kaka yangu uko wapi?” Sia alianza kujitetea kwa kuomba
msamaha “Nisamehe Tumaini, mimi ni mwanamke mwenzio” “Hebu
nitolee ujinga mie, mwanmke mwenzangu kwenye mambo ya kijinga kama hivi!
Nilikuwa nakuamini sana ila imani yangu umeipoteza.” Dora alikuwa
anaangalia tu na kushangaa aliyechukuliwa dawa alikuwa ni kaka wa Tumaini,
sababu hakutaka umbea umpite akauliza, “Huyo kaka yako ni nani Tumaini?
Namfahamu?” “Utakuwa unamfahamu ndio, anaitwa Erick” “Kheee
kumbe ni Yule Erick mpenzi wa Erica?” “Ndio huyo huyo” “Kheee
kumbe Sia nilikubali kukupeleka kwa mganga ukamroge shemeji yangu
jamani!” Tumaini aliposikia kuwa Dora ndiye aliyempeleka Sia kwa mganga
ndio akafunguka macho kabisa na kusema, “Kumbe ni kweli alienda kwa
mganga?” “Ndio ni kweli, na bahati mbaya kakako hakula lile tunda ndio
likaliwa na huyo mdogo wangu hapo ambaye hasikii kwasasa wala haoni anadai
anampenda tu Sian a hakubali kuwa amerogwa” Na kweli ingawa Steve
alisukumiwa pembeni ila kusikia ile mada ya kurogwa alisogea karibu na Sian a
kusema, “Mimi sijarogwa, ni mapenzi yangu. Nampenda sana huyu mwanamke
toka moyoni na ndio nitamuoa na atakuwa mke wangu daima” Kwakweli
Tumaini alizidi kushangaa sana yani alijikuta akimchukia Sia gafla maana
hakutegemea kuwa Sia angeweza kwenda kwa mganga kwaajili ya kumroga Erick,
kwahiyo kwa yale maneno ilikuwa kama ni uthibitisho. Alisikitika sana na
kusema, “Yani kwa ulichofanya leo Sia, sitaki tena kukuona kwetu. Sitaki
tena urafiki na wewe” “Wananisingizia Tumaini” Tumaini hakutaka
kumsikiliza Sia kwakweli maana alichokisikia hakupenda hata kidogo, moja kwa
moja aliondoka. Na aliamua kwenda kwa mama yake ili amsimulie kidogo ndio aende
kwao maana alihisi akili yake kutokuwa sawa kabisa. Alifika na kumkuta
mama yake, akamsalimia na kuanza kumsimulia yaliyotokea siku
hiyo, “Unaona sasa mwanangu, unagombana na kaka yako sababu ya mwanamke
mshirikina. Huyo hakuwa anampenda kaka yako wala nini maana kama kumpenda
asingemuendea kwa mganga maana kama mtu unampenda kweli hutotoka kumsumbua kwa
madawa, utapenda akupende ule upendo halisia, na ule upendo halisia ni mzuri
sana maana unajisikia kuwa unapendwa yani hata wewe unajihisi raha” “Ila
mama huyo msichana alikunywa hadi sumu sababu ya Erick” “Hakumpenda
Erick huyo mwanangu, na labda alikunywa sumu kuwapima imani tu, huyo kuna kitu
alihitaji kwa Erick ndiomana kaweza kumwendea hadi kwa mganga, tena shukuru
Mungu umegundua mapema kabla hajawa wifi yako maana ungejuta huyo, angefanya
uone maisha machungu maana angemfanya kaka yako ndondocha yani kila ambacho
ungemwambia asingekuelewa sababu yake. Mwanangu hakuna upendo mzuri kama upendo
halisia, hakika hata mimi ningeangalia upendo halisia basi nisingezaa na baba
yako ila hela zake zilinichanganya sana na kuhisi kuwa ananipenda na kuhisi
nitaishi kama malkia kwenye himaya yake, kumbe hakuwa na upendo na mimi hata
kidogo na nilimgundua baada ya kuzaa tu” “Mmmh mama, hivi baba anampenda
nani? Maana toka nikae nae sijawahi msikia akitaka kuoa wala akisema labda
nimuoe mama yake Erick maana Yule mama nae anaishi mwenyewe” “Yule baba
yenu nadhani hajielewi, yupo yupo tu. Nilijua angenioa wapi, nimezaa ndio
akanipiga teke kabisa, basi mama Erick nilijua atamuoa wapi, ndio kwanza amezaa
nasikia hata hospitali hakwenda kumchukua yani Yule mwanamke kahudumiwa na mdogo
wake mwanzo mwisho ndiomana anamthamini sana mdogo wake, Yule mzee ana wazimu
Yule mpaka leo yupo yupo tu ila nasikia ana wanawake wengi balaa” “Ila
hajawahi kuwaleta nyumbani mama, baba yetu anajiheshimu” “Angejiheshimu
angeoa, pesa anayo, mali anayo, kitu gani kinamshinda asioe? Kaeni vizuri na
baba yenu muulizeni vizuri kuwa kwanini haoi?” “Sawa
mama” Tumaini aliongea ongea pale na mama yake kisha akajiandaa kurudi
kwao tu maana siku hiyo alikuwa amechefuka haswaa na yale aliyoyaona kwa
Sia. Dora alimuangalia Sia bila kummaliza maana alijilaumu sana
kumpeleka Sia kwa mganga kwanza kumbe ilikuwa ni kuharibu mahusiano ya rafiki
yake na pia imepelekea kuharibu akili ya mdogo wake, kisha akaanza
kumwambia, “Hivi wewe Sia aliyekwambia kwamba penzi linatafutwa kwa dawa
nani?” “Na wewe hebu ukae kimya huko, kumbuka ni wewe mwenyewe ndio
ulinipeleka kwa Yule mganga. Kama penzi halinunuliwi kwa mganga na wewe ulienda
kufanya dawa upendwe ili iweje? Mimi bila kujua kama kuna dawa uliifanya ya
kupendwa na wewe mwenyewe kunipa ushuhuda ningejuaje kama kwa mganga kuna dawa
ya mapenzi? Unaponisema mimi nijiangalie na wewe kungwi” “Sikatai ni
kweli nilienda kwa mganga ila lengo langu na lako halifanani, niliamua kumfanyia
James dawa sababu nilipanga kumkomesha na nilifanya vile sio sababu nilikuwa
nampenda hapana, nilitaka kumchuna tu pesa zake. Sasa wewe shoga yangu kumfanyia
dawa mwanaume ili akupende ni vipi hapo? Hivi unajisikiaje ukipendwa na mwanaume
kwa upendo wa dawa? Inanoga kweli?” “Bhana eeeh achana na
mimi” “Niachane na wewe kitu gani? Mdogo wangu akomboke huyu, uende
kwenye maombi” “Siendi popote, achana na mimi kwanza wewe ni mbaya sana
ushanipotezea laki moja yangu jumlisha na zile hasara za nauli na chakula kwenda
huko Bagamoyo ndani ndani, wala sijapenda kabisa, naomba tu
uende” “Siwezi kwenda na kumuacha mdogo wangu” “Si umchukue,
huyo hapo mchukue kama mtoto mdogo mbebe mgongoni” Kiukweli Dora
alichukia sana kama angeweza kupigana na huyu Sia kwa hakika angepigana nae ila
uwezo wa kupigana na huyu Sia hakuwa nao kwani alionekana kuwa na nguvu kushinda
yeye na ndiomana hata Tumaini hakuweza kumzaba vibao Sia maana amehisi kuwa
pengine angepigwa yeye ndiomana alijiondokea tu. Basi Dora
akamwambia, “Sia, subiri tu nione hivi hivi nilivyo ila hiko
ulichomfanyia mdogo wangu utalipia nakwambia yani utalipia, nimeachana na mambo
ya waganga ila naweza kurudi tena sababu yako kwaheri” Dora aliondoka
pale na hata mdogo wake hakujigusa kumuuliza kuwa mbona anaondoka akiwa
amechukia vilke kwani yeye alijionea kawaida tu. Dora akiwa njiani huku
ananung’unika mwenyewe, kuna gari ilipaki karibu yake, kisha Yule wa kwenye gari
alishusha kioo, basi Dora akamuangalia akakuta ni George akafurahi sana na
kwenda kupanda kwenye gari ya George huku akimsalimia. “Mmmh za siku
George, inaonekana maisha yako mazuri siku hizi eeeh!” “Kiasi chake
kwakweli namshukuru Mungu, twende nikupeleke kwangu” “Twende
tu” Kwa muda huo hata hakufikiria kuwa muda umeenda na anataka kurudi
kwao ila aliondoka na George tu. Tumaini alifika nyumbani kwao
ilikuwa ni kwenye mida ya saa tatu usiku, alipoingia getini alimuuliza mlinzi
wao, “Vipi Erick na Yule msichana wake wameondoka?” “Ndio
wameshaondoka” “Na lile gari pale la nani?” “Lile gari la
mzee” “Kheee leo kaja mapema hivyo?” “Tena karudi toka saa kumi
na mbili jioni, muda ule ule walipoondoka wakina Erick tu basin a yeye
akaingia” “Kwahiyo hajawakuta” “Ndio hajawakuta” Basi
Tumaini akaachana na Yule mlinzi na kuingia ndani kwao, yani ni kweli baba yake
alikuwa na magari mengi tu ambayo si yote alikuwa ameyakariri ila ile kumwambia
baba yake kuwa anauhitaji na gari alishindwa kwani hakumzoea na vile vile toka
wanakaa nae hapo, basi kuonana nae ni kwa nadra sana. Aliingia ndani
kwao, na kwa mara ya kwanza alimkuta baba yake sebleni akiangalia taarifa ya
habari, Tumaini akamsalimia baba yake, “Najua umenimiss mwanangu, karibu
karibu tuongee” Tumaini akasogea karibu na baba yake, “Kaka yako
yuko wapi?” “Sijui ila nilimuacha, nadhani katoka, na leo mbona umerudi
mapema?” “Jamani kuna muda nakaa naikumbuka familia yangu mwanangu, ila
leo niliwahi kwa lengo la kuwakuta wanangu nyumbani maana kuna habari nataka
niwape” “Habari gani hiyo baba?” “Sasa ni vyema nikaongea nanyi
mwenzio akirudi, basi asubuhi mwambie asitoke ili niongee nanyi
sawa!” “Sawa baba” Tumaini akajikuta ana hamu sana ya kujua ni
kitu gani ambacho baba yao anapanga kuongea nao, kitendo hiko kilimfanya
alivyoenda chumbani kumpigia simu Erick kuwa baba yao anawahitaji nyumbani na
anataka kuongea nao. Basi George alifika na Dora nyumbani kwake
na kumkaribisha ndani, kwakweli dora aliona jinsi gani George alivyojipanga
akamsifia sana na kumuuliza, “Hivi George bado tu hujaoa? Au bado
unatafuta bikra?” “Nyie wanawake mnbajielewa basi! Nilipenda sana nioe
mke ambaye hajawahi kupitiwa na mwanaume yeyote yani mimi niwe mwanaume wake wa
kwanza” “Mwanamke awe hajawahi kupitiwa na yeyote ila wewe umepitia
kibao hatusemi, huoni kama unachofanya sio sawa? Ila hata hivyo mabikra wapo
bhana, tuseme hujawapata tu! Nyumba kama hii inatakiwa awepo mwanamke ndani,
umerudio kutoka kazini kama hivi akupikie na kukupetipeti” “Aaaah
mabikra kweli wapo ila wengine wana bikra feki yani wenye bikra halisi
hawajulikani karne hii, nilimpata mwanamke bhana akasema yeye ni bikra tukaja
nae ndani uwiiii anajua kila kitu, jamani bikra gani anayajua mapenzi kiasi
kile! Nikasema hapana hapa nauziwa mbuzi kwenye gunia” “Kwani damu
haikutoka?” “Ilitoka ila Yule nadhani alikuwa muigizaji, nikajaribu
kuangalia wa vijijini ni washamba hatari na mwingine anakwambia ni bikra ila
anasema msifanye hadi ndoa, sasa mtu wa namna hiyo wa nini? Nitajuaje kama bikra
kweli? Naamua kumbwaga tu, ila kwasasa wala sitaki cha bikra wala nini namtaka
mwenye mapenzi ya dhati” “Basi nipo mimi George jamani, au mimi
umenisahau?” “Wewe Dora nae loh! Wewe ni hawara yangu
jamani” “Ndio mimi ni hawara yako ndiomana huwa sina wivu na wewe na
hata hivyo mahawara huwa hawaachani. Umesikia wapi mahawara wanaachana? Kwanza
leo nafurahi sana nimekutana na wewe, nafurahi sana nimefika kwako, sasa
unafikiri leo naondoka?” “Kheee kwahiyo huondoki?” “Siondoki
ndio, huna mke halafu mimi niondoke kwa lipi na umewahi kuwa hawara yangu. Yani
leo ndio nipo nawe hadi asubuhi nami nifaidi matunda yako ya
mafanikio” George alihisi furaha sana na aliona amepata haswaa yani
alijiona ni mshindi kupita njia na kuonana na Dora, kwahiyo hakupinga zaidi
zaidi kumfanya Dora kama mke kwa muda huo. Erick alikuwa
amemrudisha Erica nyumbani kwao ila kwa muda huo wakati anaaga kuwa anaondoka,
Bite alitamani sana kumuuliza kuhusu zile hela ila mama Erica alimkatisha kwani
alihisi kama ni swala la kujiaibisha kuhisi kuwa Erick anaweza kuchukua hela
kama ile wakati ana hela nyingi tu, basi Erick aliaga na kuondoka
zake. Alifika nyumbani kwao ilikuwa saa tano usiku, na dada yake
akamwambia azma ya baba yake ya kutaka kuongea nao asubuhi kwahiyo dada yake
alimwambia kuwa asiondoke mapemaili asubuhi waweze kuongea na baba
yao. Basi Erick alikubali na kwenda zake kulala tu maana siku hiyo
alikula kwakina Erica kwahiyo hakuwa na sababu tena ya kula, zaidi ya kuoga na
kwenda kulala tu, ila alipigiwa simu na Sian a hakupokea ile simu kwani alikuwa
na hisia mbaya na Sia huenda akaweka hata dawa kwenye simu ashangae akiongea nae
tu aanze tena kumfatilia wakati kashaamua moyo wake kuwa kwa
Erica. Kulipokucha aliamka na kujiandaa kisha alienda kukaa sebleni ili
kumsubiri baba yao, ambapo Tumaini nae alienda kukaa sebleni na muda kidogo baba
yao alitoka ndani na kuanza kuongea na watoto wake, walimsalimia na akaanza
kuwaeleza lengo lake, “Nadhani Erick nishawahi kukugusia kuhusu swala
hili, ni hivi nahitaji kuoa” Tumaini akashangaa na kumuuliza baba yake
kwa mshangao, “Kuoa baba” “Ndio, nahitaji kuoa. Katika maisha
yangu sijawahi kuoa yani sijawahi kuwa na mke kabisa, ila kwasasa nimeona ni
bora nioe yani kuwe na mama yenu hapa nyumbani ili baba yenu na mie niwe narudi
nyumbani mapema, nashinda nyumbani kama baba wengine wenye familia, naomba
mniunge mkono kwa hili wanangu” Erick akamwambia baba
yangu, “Kwa upande wangu mimi sioni kama ni tatizo tena naona umefanya
maamuzi ya maana sana baba maana sijawahi kuona au kusikia mahali kuwa baba
uliwahi kuoa au kuwa na mke. Na sisi kwetu ni faraja sana kuona baba ukipata mke
wa kukuhudumia na kukutunza. Au unasemaje Tumaini” “Hata mimi naona ni
sawa kabisa, ila swali ni kuwa huyo mama yetu ni nani? Na hiyo harusi ni
lini?” “Swala la mama yenu ni nani subiri tu mtamjua, maana kuna maswala
nilikuwa nakamilisha na yashakamilika ila hivi karibuni nimepanga kwenda kutoa
mahali kwa huyo mama yenu yani mwezi huu haupiti basi mtasherekea harusi yangu,
na Erick si ulisema unataka kuoa eeeh!” “Ndio baba nataka
kuoa” “Basi hakuna tatizo, baada ya harusi yangu ndio wewe pia utaanza
mipango ya harusi yako tena nitaisimamia kila kitu maana harusi yangu nataka iwe
ya kawaida tu ila harusi yako, nitagharamia sherehe yote mwanangu, kipindi hiko
nipo na mama yenu yani ni furaha tele” Wote wakafurahia haswaa Erick
maana aliona ni jambo la kuvutia sana kwake kuambiwa na baba yake kuwa
atagharamia shughuli yote ya harusi yake, hivyo akaombea tu harusi ya baba yake
ipite salama ili yake ifanyike pia. “Baba, mzee wangu yani mimi natoa
heri zote za wewe kumpata mama yetu maana ni furaha kwetu pia. Natumaini hiyo
Jumamosi itakuwa kweli na tutaenda wote ili tumfahamu na mama
yetu” “Yani msijali wanangu, maandalizi yapo vizuri kabisa, siku hiyo
tutaondoka hapa pamoja kwenda kumaliza kila kitu ila ninachowaomba watoto wangu
tutakapofika kwa huyo mama yenu mumpende na akifika hapa nyumbani mmuheshimu,
baba yenu nimechelewa kuoa sababu katika maisha yangu sijawahi kumpata mwanamke
nikampenda, huyu niliyempata sasa ni mwanamke wa kwanza kupendwa na mimi kwahiyo
lazima nimuoe” Tumaini akamuuliza baba yake, “Je na yeye
anakupenda?” “Mwanangu Tumaini hivi unaendaga kanisani kufanya nini na
maandiko huyajui? Je maandiko unayasoma vizuri kweli? Unayajua vizuri maandiko?
Imeandikwa enyi wake watiini waume zenu nanyi wanaume wapendeni wake zenu,
kwahiyo swala la kupenda ni swala la mwanaume yani limeandikwa kabisa kuwa
mwanaume lazima apende kwa maana nyingine mwanaume anatakiwa aoe anachokipenda
ila mwanamke hakuna tatizo maana mwanamke anajifunza kupenda yani mwanamke
anaendana mazingira yanapompeleka, yakimpeleka kwa A basi atampenda A
yakimpeleka kwa B vivyo hivyo, yani mwanamke anajifunza kupenda ila mwanaume
ndio haswaa anayejua kupenda” “Ila baba mbona wanasema mwanamke
akikupenda ndio kakupenda kweli” “Sababu mwanamke anajifunza kupenda
kwahiyo kitu cha kujifunza lazima uwe nacho makini na ndiomana utakuta
unamtongoza mwanamke ila anakukataa kataa ila cha kushangaza badae weee
anakupenda kufa maana kashajifunza kwahiyo swala la mama yenu kunipenda au
kutokunipenda lisiwape shida maana atajifunza kunipenda ndani ya ndoa na
nitamfanyia kila kitu cha kumfanya anipende maana wanaume tunajukumu la
kuwafanya wanawake watupende kwa kuwaonyesha upendo” “Mmmh baba
umenifungua” “Ndivyo ilivyo hiyo yani usishangae kuona mwanamke
alimkataa mwanaume ila alipomkubali na kuwa nae akampenda sana, au anaweza
kumkataa ila kila yule mwanaume anavyomfatilia ndio yeye anapojifunza kumpenda
mwanaume yule na kumkubali, maandiko yanasema enyi wanaume ishini na wake zenu
kwa akili unafikiri ni akili gani hapo tunaambiwa? Ni akili ya kumfundisha
mwanamke upendo maana akikupenda hawezi kukufanyia mambo ya ajabu ila ukikosa
akili ya kumfanya mwanamke akupende hata usijisumbue kumuoa maana kuna siku
atakuwekea sumu ya panya huyo ufe” “Kwahiyo baba una uhakika huyo
mwanamke atakupenda?” “Jamani tumeandikiwa upendo yani lazima
atanipenda, mbona nyie watoto mnakuwa watata hivyo? Tumaini vipi, hutaki nioe
mama?” “Hapana baba, nilikuwa nauliza tu” “Au umeshangaa vile
nilivyoweza kukuchambulia maandiko wakati siendagi kanisani? Enzi zangu za ujana
wangu nilikuwa naenda kanisani, kuna mwanamke mmoja nilimpenda sana alikuwa
mlokole, aaah habari hiyo nitawaeleza siku nyingine ila kwasasa tuwe makini tu
na maandalizi ya harusi yangu” Kisha akainuka na kuwaaga watoto wake na
kuondoka kwenda kwenye shughuli zake. Walibaki ndani Tumaini na kaka yake ambapo
naye Erick alikuwa akijiandaa kutoka ila Tumaini akamwambia kidogo kuhusu baba
yao., “Unajua Erick leo nimemshangaa baba jamani, loh hata yeye maandiko
anayajua makubwa haya” “Kwani hujawahi kusikia kuwa hadi shetani
anayajua maandiko” “Kwahiyo baba ni shetani?” “Sina maana hiyo
ila ni kitu cha kushangaza jamani, hakuna dini anayoudhuria, hakuna kipindi cha
dini anachoenda ila anatuambia habari za maandiko loh! Nimesema hivyo kama mfano
tu” “Sawa lakini, kheee imeshangaza yani baba anajua maandiko
loh!” Basi wakacheka tu pale kisha Erick kutaka kuondoka ila kabla
hajatoka Tumaini akamsimamisha na kumwambia, “Ila Erick mdogo wangu hebu
nionee huruma dada yako eeeh! Nakaa tu nyumbani natia huruma haswaaa yani siendi
kwenye shughuli ndiomana Napata na muda wa kuanza kufatilia mambo yasiyonihusu,
nirudishe dukani jamani mdogo wangu eeeh!” “Sawa, nenda kafungue duka
ila sijakurudisha rasmi maana lile duka ni la Erica, wewe nenda kafungue tu
halafu tutajua cha kufanya mbele ya safari” “Sawa, nashukuru kwa hilo.
Haya mdogo wangu na usafiri je! Unajua na mimi natamani kuendesha gari,
nimechoka kutembea” “Subiri, kuna gari ya baba ipo tu gereji imepaki
najua vitu vingi vya baba huvijui sababu hutaki kujua basi hiyo gari italetwa
leo jioni hapa nyumbani maana funguo ninazo mimi” “Asante sana mdogo
wangu” Basi Erick akatoka na kumfanya Tumaini ajisikie vizuri na kuona
pengine siku hiyo kaongea na kaka yake kwa upendo ndiomana kaka yake
amemsikiliza tofauti na siku zingine. Dora aliamka nyumbani kwa
George na kujiandaa kwaajili ya kurudi kwao, kwahiyo wakati George anaenda
kazini akampitisha nay eye stendi na kumshusha, kisha Dora
akamwambia, “Ila George wewe mbahili loh! Nilijua umejifunza siku hizi
kumbe huna lolote, mwanaume mbahili wewe, yani umeendelea siku hizi ila wapi
ubahili tu hata kusema hela hii ya nauli hakuna! Mmmh George mbahili sana
wewe” Ila ndio kwanza George alisimamisha gari ili Dora ashuke tu basi
Dora akashuka na kupanda daladala ya kurudi kwao huku akijisemea
mwenyewe, “Yani na Yule nimemkomesha, na nitamkomesha hadi naye apate ukimwi nilioupata mimi maana
anajishauwa mtu gani hadi leo hajaoa eti anatafuta bikra, sasa sijui kama kuna
bikra atamkubali na ukimwi wake. Kwanza janaume bahili kweli, sasa ukimwi
utamkomesha mjinga Yule” Kisha akaendelea na safari hadi kwao ambapo
alimkuta mama yake akilalamika na malalamiko yale yale kuwa watoto wake
wamebadilika, “Dora, ulianza wewe kulala nje kwahiyo mdogo wako analala
nje hata hushtuki jamani mnataka kunifanya nini mama yenu jamani? Watoto wenyewe
ndio nyie wawili tu kwanini mnanifanyia hivi!” “Mama, utanilaumu bure tu
ila mimi nimekwambia kuhusu Steve twende kwenye maombi” “Maombi gani
nitakayoenda na wewe, hivi ni Mungu yupi atakayesikilkiza maombi yako wewe binti
mchafu!” “Maneno yako hayo mama ndio yanayofanya hata nisijirekebishe
ujue, wewe ni mama yangu, niweke mwanao kwenye mstari, ni wewe ambaye hukunilea
vyema, hivi mfano ungenifundisha kuishi katika misingi ya dini ningeacha si
ingekuwa uzembe wangu mwenyewe? Ila mama hakuna ulichojaribu kwangu na Steve
halafu unalalamika, nakwambia kuwa swala la Steve ni la kwenda kwenye maombi
unasema hakuna Mungu wa kunisikiliza mimi. Yule mwanamaombi alinifundisha vizuri
sana kuna mwanamke kahaba ila alilia miguuni pa Yesu na akasamehewa sembuse
mimi! Jamani mama laiti ungejua kuwa wewe ndio unazidi kunipotosha mimi hata
usingesema” “Hebu nitolee ujinga wako hapa, unaanza hadi kujifananisha
na makahaba kama na wewe sio kahaba ni nini! Kwani wewe na huyo mwanamke
mnatofauti gani? Mtoto kama sijakuzaa mimi, yani hapo ulipo unanuka dhambi
tu” “Kheri mimi nanuka dhambi lakini nina hela” “Yani unaongea
kama binti ambaye hakusoma, jamani Dora umefika chuo wewe! Unaongea utumbo
tu” “Ni kweli nimefika chuo ila kumbuka kwenye elimu yangu kila hitaji
nililokwambia ulisema nijiongeze, hivi mama ulitaka mwanao niwe vipi? Ndio
nikajiongeza hivi” “Unajua usiniambie hivyo mama yako mimi, nitakupiga
ujue!” Dora akaachana na mama yake ukizingatia alishachoka muda huo
aliamua tu kwenda chumbani kwake kujilaza. Siku hiyo Erica
akiwa nyumbani kwao kwenye mida ya jioni jioni alienda Erick kama kawaida
kumsalimia na kuangalia kama anaendeleaje maana ingawa alishampeleka kule kwenye
duka ila hakutaka aanze kwa kipindi hiko mpaka awe sawa kabisa kwahiyo Erica
alikuwa tu nyumbani ila huku ana uhakika na kile kinachoendelea juu
yake. Kwahiyo Erick alivyofika walitandika mkeka nje na kukaa huku
wakizungumza mambo yao mbalimbali. Basi Erick aliongea ongea nae pale na
alimueleza pia lengo la baba yake kutaka kuoa, “Hivi kwani baba yenu
hajawahi kuoa?” “Hajawahi hata mara moja mwenyewe anadai hakumpata
mwanamke ampendaye ila sasa kapata ampendaye ndio anataka kuoa na ameniahidi
kuwa baada ya harusi yake ndio atashughulikia yangu” “Kwahiyo mimi na
wewe Erick tutaoana mwaka huu huu!” “Ndio mwaka huu tunaoana
Erica” Kwakweli Erica alifurahi sana kusikia vile kwani ndoto yake siku
zote ni kuolewa tena kuolewa na mwanaume ampendaye kama Erick kwahiyo ilikuwa ni
furaha sana kwake. Basi baada ya maongezi yale ndipo Erick alipotaka
kuondoka ila Erica alitaka ale kwanza, “Hapana Erica, leo nahitaji
twende restaurant tukale. Basi twende ukaage tu tuondoke muda huu” “Ila
mama hayupo, yupo dada Bite tu” “Si ndio vizuri lakini maana mama nae
akiwepo kutoa ruhusa ni balaa” Basi Erica akacheka tu na kuinuka pale
kutoa mkeka kupeleka ndani na kumuaga dada yake kuwa anatoka kidogo na Erick
kisha yeye na Erick wakaondoka zao. Pale nyumbani alibaki Bite
akiendelea na kazi zake zingine, muda kidogo akaja mgeni na kugonga ikabidi Bite
afungue, mgeni huyu alikuwa ni mtu mzima wa makamo halafu kaongozana na vijana
wawili basi akawakaribisha na kuwauliza maana alikuwa akiwashangaa basi Yule
mzee alijitambulisha, “Naitwa mzee Jimmy” “Kheee kumbe mzee
Jimmy mwenyewe ndio wewe!” “Ndio ni mimi, niliacha milioni tatu za posa
ya Erica, niliacha na karatasi ndani kuonyesha nampenda Erica na leo
nimekuja” Bite akataka kuongea jambo ila huyu mzee alimzuia na kuendelea
kusema, “Leo nimeleta hii milioni moja ya chakula siku ambayo nakuja
kutoa mahali na kumchukua mke wangu, jiandaeni na msifikirie kunifanyia ujinga
kama mnaonifanyiaga maana posa yangu mmepokea kwahiyo mke wangu nakuja
kumchukua, sitaki useme neno lolote kwasasa. Jua kwamba jumamosi nakuja
kumchukua mke wangu” “Kwahiyo kesho” “Ndio, mjiandae yani kesho
mapema kabisa nakuja kuchukua mke wangu” Kisha Yule mzee na wale vijana
wakaondoka, Bite alibaki tu kaduwaa na zile pesa mkononi maana hakujua hata
anaanzia wapi na kuishia wapi na kuzirudisha kwa Yule mzee hakuweza maana
alimuwekea vitisho. Basi mama yake aliporudi alimpa zile pesa, ila
alizipokea na kumuulizia Erica kwanza “Erica yuko wapi?” “Katoka
na Erick mama” “Yani huyu mtoto akipumzika siku mbili basi siku ya tatu
lazima atatoka na Erick, kwahiyo hizi hela ni Erick kazileta?” Basi bite
akamueleza mama yake jinsi zile hela zilivyoletwa, yani mama Erica alizitupa
zile hela chini huku akilalamika, “Hizi hela ni hela za moto jamani,
huyo mzee anatutakia nini jamani!” “Mama nilisema Erick aulizwe kuhusu
hiyo milioni tatu ila hajaulizwa hadi leo na habari ya hela jamani tutajuta humu
ndani, na hivyo kesho ndio kasema anakuja kutoa mahali na kumchukua mke wake
yani hiyo hela katoa ya chakula eti tusimtie aibu kwa wageni” “Hivi huyo
mzee ana wazimu au kitu gani jamani, ni wapi wanatoaga mahali bila mila za
kabila hilo? Anajua kabila letu mila zake? Ni wapi wanatoaga mahali kinyemela
hivi? Mbona huyu mzee anataka kulazimisha mambo?” “Ndio hivyo mama,
subiri mwanao Erica afike umueleze habari hizi labda ampigie huyo mzee
kumzuia” “Kheee jamani nimechoka kwakweli yani nimechoka
haswaaa” Basi kwenye mida ya saa nne, Erica alirudi nyumbani na mama
yake alimfokea sana kwa kuchelewa kisha akamwambia habari za mzee Jimmy na
kumtaka ampigie simu kumsitisha hiko anachotaka kukifanya, ikabidi Erica ampigie
simu mzee Jimmy, “Wewe mzee hivi unataka niongee kwa lugha gani
unielewe? Sikutaki, achgana na mimi” “Hunitaki nini wakati posa yangu
nyumbani kwenu mmekula, kesho ndio utajua kama unanitaka au
la” “Sikutaki wewe mzee, achana na maisha yangu” Erica alikata
ile simu kwa hasira na kuamua tu kwenda kulala. Kulipokucha waliendelea
na mambo mengine huku kila mtu akiwa hana habari kwa chochote
kile. Kwenye mida ya mchana mama Erica alimuagiza Erica dukani kwahiyo
Erica alitoka kuelekea dukani, wakati anatoka nje ya geti alishangaa kukuta
pamepambwa sana kama kuna sherehe vile, aliamua kukimbia ndani kwenda kumuita
mama yake. Erick, Tumaini na baba yao waliongozana kwenye gari
moja wakienda huko kumchukua mke wa baba yao. Walikubali kwenda nae ingawa
aliwashtukiza tu maana hakusema kuwa ni siku gani wao wataenda huko kwa mama yao
yani mke mtarajiwa wa baba yao, walipokuwa kwenye gari Yule mzee aliwasisitiza
wanae, “Yani kama mkikuta familia ya Yule mwanamke inaleta vurugu
msishangae sana ni hawataki mtoto wao nimuoe sijui washachukua mahali za watu
wengi wengi ila baba yenu huwa sitaki hela yangu iende bure na mwanamke
nampenda. Kwahiyo msishangae” “Sawa baba” Safari iliendelea ila
Tumaini na Erick walishangaa sana kuona mitaa ambayo wanaelekea ni mitaa ya
kwakina Erica ila wakajipa moyo, walifika mahali hapo pamepambwa sana ni vigumu
kujua kama ile nyumba huwa wanakuja mara kwa mara, wakashuka huku wakishangaa
shangaa, Erick akasema kwa mshangao, “Jamani hapa si kwakina
Erica!” Tumaini akajibu, “Ndio, na Erica mwenyewe Yule pale na
mama yake” Erick aliwaangalia huku akiendelea
kushangaa. Safari iliendelea ila Tumaini na Erick
walishangaa sana kuona mitaa ambayo wanaelekea ni mitaa ya kwakina Erica ila
wakajipa moyo, walifika mahali hapo pamepambwa sana ni vigumu kujua kama ile
nyumba huwa wanakuja mara kwa mara, wakashuka huku wakishangaa shangaa, Erick
akasema kwa mshangao, “Jamani hapa si kwakina Erica!” Tumaini
akajibu, “Ndio, na Erica mwenyewe Yule pale na mama yake” Erick
aliwaangalia huku akiendelea kushangaa. Kumbe na wao wakina Erica
walikuwa wakishangaa pia, Erick alimuacha pale baba yake na dada yake na kwenda
alipo Erica na mama yake, bila salamu aliwauliza, “Kuna
nini?” Wakajibu kwa pamoja, “Hata sisi
tunashangaa” Erick akatulia kimya akiwaza kuwa mke anayesemwa na baba
yake ni yupi kwenye hiyo nyumba, hakupata jibu maana hata wenye nyumba nao
walijibu kuwa hawaelewi kinachoendelea, wakati wametulia wakishangaana tu
walimuona Mzee Jimmy akiongoza kwa kupita getini kwakina Erica na kuingia ndani
huku Dora akimfata nyuma, ilibidi na wao waingie, ila kabla mzee Jimmy
hajafungua mlango wa nyumbani kwakina Erica, alisikika mama yake Erica nyuma
yake, “Hivi wewe mzee unataka nini lakini?” “Nimekuja kumalizia
mahari na kumchukua mke wangu” “Mke wako yupi unayemuona kwenye nyumba
yangu?” “Mke wangu Erica” Pale Erick na Tumaini walishangaa
kabisa kuwa baba yao ni mzima au wazimu umemuingia, kisha mzee Jimmy akageuka
nyuma na kumuona Erica na mama yake, akasema, “Si jana nimeacha pesa
hapa jamani, mbona hamjampamba mke wangu?” Hata Erick alishangaa kusikia
kuwa baba yake hadi aliacha pesa ili Erica apambwe, Bite pia alitoka ndani na
kushangaa ule mzozo. Kwanza alishangaa kumuona mzee Jimmy, wakati huo huo
alishangaa kumuona na Erick. Tumaini akamuuliza baba yake, “Kwahiyo baba
huyo mama yetu unayetaka kumuoa ni Erica?” “Ndio, kwani
mnamfahamu” Ni pale pale Erick alipomwambia baba yake, “ Ndio
Baba, huyu Erica ndio mwanamke ambaye nilisema kuwa nataka
kumuoa” “Unasemaje wewe!” “Ndio hivyo baba, nampenda sana
Erica” Cha kushangaza huyu mzee alianguka chini na kuzimia, ilibidi
waite vijana waliokuwa wanapamba na kumpakiza baba yao kwenye gari kisha
kumuwaisha hospitali maana inaonekana presha ilimpanda mzee
Yule. Kwahiyo pale ilibaki familia ya kina Erica tu yani Erica, mama yao
na Bite na vijana wachache waliokuwa wanapamba. Mama Erica aliwatazama wale
vijana na kuwaamuru kuwa watandue mapambo waliyoyaweka nje ya nyumba yake,
ikabidi wale vijana waende kutandua maana mwenye shughuli ndio Yule alipelekwa
hospitali. Wakina Erica waliingia ndani ila siku ile ilikuwa ni
siku ambayo kuna kitendo cha ajabu kimetokea kwenye nyumba yao, walipokaa Bite
alimuuliza Erica kwa mshangao, “Inamaana Yule mzee Jimmy ndio baba yake
na Erick?” “Ndio inavyomaanisha ila nashangaa sana” “Sasa
unashangaa nini? Inamaana kipindi chote hiki hukuwajua wazazi wa Erick? Yani
kipindi chote hiki hukumjua hata baba wa Erick?” “Kweli nilikuwa
simjui” “hata jina Erica? Wewe ni mtu wa aina gani? Hata jina basi la
Mzee Jimmy lingekujulisha kuwa huenda ni baba wa Erick” “Dada,
utanilaumu bire lakini mimi sikujua kabisa, na wala sijui yani mpaka muda huu
nashangaa tu” “Ok, tuseme hujui kama ni baba yao haya hata hujui Erick
anaitwa Erick nani? Wewe mbona mjinga hivyo eeeh! Hebu ona hii aibu,
ingejulikana mapema ungejua namna ya kumpanga Erick ila sio kwa stahili
hii” Erica aliinuka na kwenda chumbani kwake na baada ya muda alirudi na
cheti cha kuzaliwa cha Angel kisha akamwambia dada yake, “Angalia hapo
kwenye majina ya Erick kama kuna herufi J au jina Jimmy ndio
unilaumu” Bite aliangalia kile cheti kweli jina la Erick lilikuwepo ila
halikuwa na uhusiano wowote na jina Jimmy mahali popote, ila Bite akaanza mada
nyingine kwanza, “Kwani Erick ndio baba wa Angel? Wewe si ulisema baba
wa Angel anaitwa Rahim wewe?” Mama yao akadakia, “Bite mwanangu,
hayo ndio maajabu ya mdogo wako yalivyo. Aliuza mtoto kwa Erick bila hata
kufikiria ya mbele wala ya nyuma, halafu Erick nae kwanini hana majina ya baba
yake Jimmy? Au nae alinunuliwa kama Angel? Wamama sisi tuna matatizo sana, si
ndio mambo ya Angel nayo yatakuwa hivi hivi mnbele ya safari! Haya sasa kumbe
Erick baba yake Jimmy na Yule mzee presha imempanda yani sijui kama kuna ndoa
hapa kati ya Erick na Erica mmh sijui naona chenga tu.” “Yani mama kama
Yule ni baba yao na hadi kafikia hatua ya kuzimia hivi watoto wataelewa kweli?
Hivi Erick anaweza kuacha baba yake awe na hali mbaya sababu ya Erica? Kwanza
wewe Erica una akili gani mdogo wangu, toka lini mtoto akauzwa jamani, hivi nani
mshauri wako wewe?” “Mshauri wake ni mapenzi, yani huyu mtoto
anaendeshwa na nguvu ya mapenzi, yakimpeleka huku anaenda yakimuhamisha yupo
sijui ataishia wapi” Wote walikuwa wakimsema na alikaa kimya tu kwani
bado hakuona kosa lake na alihisi kuonewa tu, Bite akaongezea kwa
kumuuliza, “Hivi Erica hujatembea kweli na Yule mzee? Ameanzaje kuzimia
jamani!” Erica hakujibu ila mama yake akaongea, “Inawezekana
Erica katembea na yule mzee, hivi mwanangu unajisikiaje kuchanganya baba na
mtoto? Nafsi yako inajihisi vipi? Ndiomana Rahim alikuwa akikulalamikia
unachanganya ukoo, mwanangu nikajua wale wana roho mbaya, sasa umepata mume
umeenda kutembea na baba yake” “Jamani sijawahi kutembea na Yule mzee
msinikandamize jamani” “Wapi wewe, mzee wa watu azimie tu bila sababu.
Lazima umetembea nae na umekula vyake vingi sana” “Inawezekana hata zile
hela nilizokuwa nakwambia uzirudishe hkuzirudisha, itakuwa umekula vingi sana
vya huyu mzee Erica. Nashangaa mtoto wangu huna hata kinyaa, hivi ulianzaje
kutembea na mbaba kama Yule jamani eeeh! Sidhani kama huyo Erick atakupenda tena
mwanangu kwa uchafu huo” Erica aliinama huku akilia kwa uchungu kwani
hakutarajia kabisa na ndugu zake kumkandamiza kiasi kile haswaa mama
yake. “Hata ukilia lakini tunakwambia ukweli, tumesomesha ujinga yani
wewe badala ya elimu kukutoa ujinga naona imekuongeza ujinga, unakuwaje na
mahusiano na mtu hata hujui ndugu zake, hata huwajui wazazi wake, si mjinga wewe
yani mjinga namba moja. Erica hujifunzi yani hujifunzi kabisa, mahusiano na
wanaume matapeli unayatoa wapi? Yani mwanaume anawajua ndugu zako wote hadi wale
wa pembeni anawajua ila wewe hujui hata wazazi wa huyo mwanaume na unajidai kuwa
unapendwa, ndio upendo huo au kichefuchefu? Wanaopendwa wametambulishwa kwao sio
nyie wa vichochoroni, ukipewa shilingi mbili basi unajiona umefika, unajiona
kama umeokota dodo kwenye mwarobaini, huo ni ujinga Erica yani ni ujinga
haswaaa. Mwanaume wa ukweli anayekupenda kwa dhati, atakupeleka wewe kwa ndugu
zake wote, atakutambulisha kwa rafiki zake wakujue, atakuonyesha kwa watu wake
wa karibu uwajue, kwa Rahim yamekutokea hay ohayo, na kwa huyu Erick hay ohayo,
hujifunzi tu loh! Ukipata mwanaume kwasasa, kabla ya mambo yote akutambulishe
kwa ndugu zake, akigoma achana nae. Nilikwambia niwe mshauri wako ila unaenda
kuchukua ushauri kwa wajinga wenzio huko na unakuwa mjinga maradufu. Natamani
hata nichukue bakora nikutandike sijui nimezaa vipi toto jinga kama
wewe” Erica alijisikia uchungu sana na hivyo alikimbilia chumbani kwake
na kulia sana kwani hakutegemea kwa yale aliyoambiwa na hakutegemea kuhusu mzee
Jimmy alilia sana huku akijisemea, “Hakuna ninachotenda kiwe chema
katika maisha, kila jambo langu ni baya mimi Erica jamani kwanini
mimi!” Alilia sana kwa muda huo. Tumaini na Erick
walikuwa hospitali wakimngoja baba yao ambapo alikuwa akihudumiwa na madaktari
walisema kuwa inaonekana presha yake ipo juu sana, Tumaini alimwambia kaka
yake, “Mmmh Erick, naomba niongee hili ila usinifikirie vibaya kiukweli
Erica sio mtu mzuri yani anakuchanganya wewe na baba kweli?” “Tumaini
sidhani hiko kitu” “Inamaana baba amechanganyikiwa kusema kuwa Erica ni
wake? Na hadi baba kazimia lazima kuna kitu hapa Erick sio bure” “Ila
sidhani kama Erica alikuwa akinichanganya mimi na baba kiukweli” “Ila
wewe ni mbishi tu, kipindi tupo chuoni kulikuwa na sifa mbaya sana dhidi ya
Erica kuwa anatembea na wanaume wengi, alibakwa, sijui katoa mimba yani ana kila
aina ya sifa mbaya” “yote hayo tumeyaona kama mapito kwenye mapenzi
yangu na Erica maana tunapendana sana” “Kwahiyo na hili la baba nalo ni
mapito eeeh! Hebu fungua macho Erick, huyu ni baba na huna baba mwingine ila
Erica ni mwanamke ambaye ukimuacha utapata mwanamke mwingine. Unapoongea
chochote fikiria na maisha ya baba” “Hivi Tumaini unafikiri mimi
sifikirii? Ila na wewe unapoongea fikiria na furaha yangu, furaha yangu ni kuwa
na Erica, yani Yule ndio manamke wa maisha yangu” “Baba akifa
sitakuelewa wewe wala huyo Erica” “Sasa hizi mada zinatokea wapi
jamani” Daktari alitoka na kwenda kuwapa taarifa juu ya maendeleo ya
baba yao, “Imnaonyesha kuna habari ya mshtuko ambayo huyu mzee kaipata
maana presha yake ilikuwa juu sana na tumejitahidi kwakweli kuweza kuishusha
kiasi, sasa hata akija kuruhusiwa hawezi kuwa sawa kwa kipindi kidogo tena
inabidi muwe nae makini sana yani msimpe habari ya kumshtua wala msimwambie kitu
kibaya” Tumaini akauliza, “Je ameweza kuongea?” “Hapana,
bado amepumzika ila anaweza akaruhusiwa kesho. Kwahiyo kwa leo atalala tu
hapahapa hospitali” “Ila dokta, baba yetu hajawahi kuwa na presha hata
mara moja” “Inawezekana hamkujua ila ana presha tena ya
kupanda” Kwahiyo ilibidi wawe wapole tu maana tayari baba yao alikuwa
amelazwa, kichwani kwa Erick kulikuwa na vitu vingi sana vinacheza kwa wakati
huo na hakupata majibu ya chochote anachowaza, simu yake ikaita aliangalia
mpigaji aliona ni Erica, alitamani kutokupokea ile simu ila aliamua kupokea tu,
alisogea pembeni na kuongea na ile simu na kugundua kuwa Erica analia,
akamuuliza “Sasa unalia nini?” “Najua Erick utanifikiria vibaya
ila mimi sikuwa na mahusiano na baba yako kabisa” “Kwahiyo baba yangu ni
chizi kusema mwanamke wake ni wewe” “Erick jamani, kumbuka niliwahi
kukwambia kuwa kuna mzee ananifatilia na huyo mzee ndio huyo mzee Jimmy na hata
sikujua kama ni baba yako Erick” “Kwavile hukujua kama ni baba yangu
ukaamua kutuchanganya baba na mtoto? Kwanini wanawake mnakuwa hivyo lakini, yani
hata mpendwe vipi lakini ukimuona mwanaume ana dau kubwa unaamua kuhamisha
majeshi kwake, sasa baba yangu kweli Erica!” “Jamani Erick utanilaumu
bure ila nilikueleza kuhusu huyo mzee kunifatilia jamani, sijawahi kuwa na
mahusiano nae. Ila nimekupigia ili kuuliza anaendeleaje?” “Sasa
unamuulizia wa nini? Wakati ulipokuwa na mahusiano na mtu mzima kama huyu
hukujua kama uanweza msababishia matatizo? Bado hajazinduka” “Najua
Erick huwezi kunielewa kwasasa, ila tuonane basi nikueleze” “Yani
nimuache baba yangu hospitali nije kuonana na wewe Erica? Inakuingia
akilininhiyo kabisa? Si unakumbuka ulivyonieleza kwamba ulimpenda sana baba
yako, inamaana mimi simpendi baba yangu?” “Lakini Erick, mimi sikujua
kama ni baba yako” “Swala hapa sio kujua au kutokujua ila swala ni
kwanini uchanganye mapenzi yangu na mtu mwingine? Ngoja baba azinduke ndio
nitaongea na wewe vizuri ili nijue kisa na mkasa, lakini kwasasa
hatutaelewana” Kisha Erick akakata simu, kwa wakati huo hakutaka
kumuelewa Erica kwa haraka kwani alitaka kujua ukweli kwanza na ukweli hawezi
kuujua toka sehemu moja ni lazima apate sehemu zote
mbili. Kesho yake Mzee Jimmy alipewa ruhusa ya kurudi nyumbani
ambapo alirudi na watoto wake ila hawakumuuliza chochote baba yao zaidi ya
kwenda nae nyumbani tu, walipofika walimuacha akapumzike kwanza kisha Tumaini
aliamua kwenda kwa mama yake ili akamueleze hali hiyo inayoendelea
kwao. Alifika kwa mama yake na kumkuta, na baada ya salamu tu alianza
kumueleza yaliyojiri ila mama yake alionekana kucheka sana yani kama kasikia
habari ya kituko wakati kamueleza kuwa na baba yao hali sio nzuri maana presha
ilipanda, Tumaini alimuuliza mama yake, “Mbona unacheka sasa
mama?” “Ananichekesha huyo baba yenu, hivi ujana wake ale na nani uzee
amfie nani? Mzee akili zake mbili kweli huyo, kwamaana hiyo kama mwanamke
mwenyewe ndio huyo huyo wa Erick kwahiyo ni binti mdogo ambaye ni lika lenu.
Hivi baba yenu ana wazimu au kitu gani, mzee mzima kutaka kuoa watoto wake ndio
nini? Mbona kuna wanawake wengi tu lika lake, kuna sie wajane, kuna Yule mamake
Erick hajawahi kuolewa Yule si akamuoe kuliko kuanza kuaibika na kupandisha
presha na uzee ule. Anataka tu kumkosesha mwanae furaha kwa ujinga
wake” “Kwahiyo mama unamshauri Erick aendelee na maswala ya ndoa na Yule
binti?” “Ndio mimi ningekuwa Erick wala nisingebabaishwa na huyo mzee,
aende zake huko muda wake ulishapita” “Mmmh mama jamani, baba akifa
je!” “Na afe tu, mzee hana akili hata kidogo alikuwa wapi kuoa kile
kipindi chetu? Alijua kuchezea wanawake wala hakuwa na lengo la kuoa, iweje leo
asikie mwanae anataka kuoa basin a yeye juu juu kutaka kuoa? Haya hatumkatazi
kuoa, ila atafute mtu mzima wa lika lake, kilichempeleka kwa mtoto ni nini si
alitaka presha ndio hiyo kaipata. Aishie zake huko” “Jamani mama, jua
unayemsema hapo ni baba yetu?” “Kama angeithamini hiyo nafasi yake ya
ubaba basi asingeenda kutafuta presha kwa kuwa na mahusiano na watoto. Simtetei
hata kidogo huyo mzee yani hata kidogo, sema lingine tu
Tumaini” Kwakweli alikosa kingine cha kuongea na mama yake maana
ilionyesha mama yake kuwa hana habari kabisa na ugonjwa wa baba yao, ila
hakumlaumu sana kwavile hakujua kuwa baba yake alimtendea nini mama yake kipindi
cha mahusiano. Kwakweli Erica hakuwa na raha kabisa siku hii,
ilikuwa ni jioni tayari na hakupata mawasiliano yoyote toka kwa Erick na alikuwa
kila akimpigia simu Erick basi ile simu yake haipokelewi, kitendo hiko
kilimfanya awe na mawazo sana. Dada yake Bite na mama yake kuna mahali walienda
kwahiyo walimuacha yeye nyumbani kwa muda huo, mama yake
akamwambia, “Sio Erick wako anakuja unajifanya umepandisha shetani la
upendo halafu uondoke na kuacha watoto ndani” “Siwezi kuondoka na kuacha
watoto mama” “Nakwambia kabisa maana akili zako unazijua
mwenyewe” Kisha wakaondoja na kumuacha akiendelea na mawazo yake, muda
kidog alifika rafiki yake Dora maana kipindi hiko alijifanya amejirekebisha na
ni muda mrefu kidogo hakuja kumuona rafiki yake, Erica alimkaribisha vizuri tu
ila aliamua kumwambia kile kinachomsibu au kumuumiza moyo, “Dora rafiki
yangu, mbona hujawahi kuniambia kuhusu watoto wa mzee Jimmy?” “Kwani
mzee Jimmy kafanyaje? Sasa mimi watoto wa mzee Jimmy nikwambie wa nini eeeh!
Wananihusu nini, najua tu Yule mzee ana watoto wawili ila watoto wake
siwafahamu” “Mwenzangu, kumbe Erick ni mtoto wa mzee Jimmy kwahiyo Erick
na Tumaini ndio watoto wa mzee Jimmy” “Kheee kumbe!! Sasa ndio kama
naanza kupata mwangaza wa mambo” “Yapi hayo?” Ndio Dora alianza
kumueleza kilichompata mdogo wake na mpaka muda huo yupo kwakina
Sia, “Sasa nilishangaa kusikia kuwa Tumaini na Erick ni ndugu na Yule
Sia alimpelekea Erick tunda halafu kalirusha nje na mdogo wangu akaliokota kumbe
wale ni watoto wa mzee Jimmy!! Maana Yule mzee anaishi nmitaa ya kwetu kule, ule
mtaa wa matajiri, kumbe ndiomana mdogo wangu kapata ujinga kirahisi kumbe
wanakaa kule kule” “Basi ndio huyo mzee wako kaniletea tafrani jana hapa
nyumbani” “Tena Erica usimkubali kabisa huyo mzee, ila kwavile kakuletea
vioja vya kujifanya presha imepanda sababu umemkataa sijui nini na nini, nasikia
watoto wa Yule mzee wanampenda sana baba yao, na kwavile ndio hao Tumaini na
Erick basi inabidi ufanye kitu” “Kitu gani sasa?” “Wakina Erick
wakikulazimisha uolewe na baba yao sababu baba yao kachanganyikiwa na wewe
sijui, waambie swala moja kuwa kweli umewahurumia na unataka hali ya baba yao
iwe imara ila waambie kabla ya ndoa ukapime ukimwi na baba yao. Erica Yule mzee
kaathirika, asitake kukuingiza mkenge rafiki yangu, mwanzo nilifanya utani ila
kiukweli Yule mzee kaathirika kabisa” “Jamani nawezaje kukubali kuolewa
na Yule mzee? Simpendi kabisa, hata kama angekuwa hajaathirika bado simpendi
yani mimi nitaendelea kusimamia msimamo wangu tu wa kuwa na Erick, najua Mungu
nae atanisimamia kwa hili. Sitaki kuwa kigeugeu yani huku na huku hapana
kwakweli, nampenda Erick na ninamtaka Erick” Kabla Dora hajajibu, kuna
mtu aligonga mlango na Erica kumkaribisha, mtu huyo aliingia ndani alikuwa ni
Derick, baada ya kutimuliwa kwa siku zote ila bado alifika. Akashangaa sana kuwa
bado Erica ana urafiki na Dora, naye Dora alimshushua, “Kwani kuna ubaya
gani jamani mimi na Erica kuendelea na urafiki?” “Ni vizuri ila mimi
jlipita tu kukusalimia Erica, ila kama mama yako hayupo nashukuru ngoja niondoke
sasa hivi asije akanikuta bure maana mama alivyo hanipendi huyu anaweza kunila
mboga” Basi Derick akaamua kuaga ila Dora nae aliaga pia sababu
alimaliza kuongea na Erica na alihofia pia dada yake Erica kumkuta maana alihisi
kuwa lazima huyo dada atakuwa na kisasi nae. Kwahiyo Dora aliongozana na
Derick na kuondoka pamoja. Walivyofika setendi Dora alimuuliza
derrick, “Kwani muda huu unaenda wapi Derick?” “Kwani nina
pakwenda basi, leo kuna mtu kaniboa kweli ndiomana nikaja kumuona Erica mara
moja” “Kakufanyaje mtu huyo?” “Yani kuna mdada nilikuwa na
mahusiano nae, na leo nilijipanga vizuri kabisa kuwa nae sijui vipi eti anasema
hayupo kwenye mood ya kuwa na mimi. Nimeachana nalo huko, kaniudhi kweli
yani” “Pole sana, na wewe una hamu zako hapo!” “Yani weee acha
tu, nimekuja hadi huku basi tu” “Ila usijali, unajua umeletwa huku ili
kuonana na mimi maana katika umalaya wako wote hujawahi kutembea na
mimi” “Na wewe Dora vipi, mwanaume haitwi malaya bhana, hata hivyo
sijawahi kutembea na wewe. Nikitaka utanipa?” “Kwanini nisikupe sasa
jamani wakati wewe ni rafiki yangu!” “Mmmh Dora kweli?” “Ndio
kweli” “Basi tukodi bajaji tutafute sehemu ya karibu guest
tukajivinjari” “Hakuna tatizo” Muda ule ule Derick aliita bajaji
na kuondoka na bajaji ile kwenda kwenye nyumba ya kulala wageni yani huko akawa
na Dora mpaka asubuhi. Dora alitoka pale asubuhi na kuanza
safari ya kuelekea kwao ila alikutana na James akiwa anaenda kazini, James
akasimamisha gari yake na kumpakiza Dora kisha akamuuliza kuwa ametoka wapi muda
huo. “Asubuhi yote hii Dora, unaonekana umechoka umetoka
wapi?” “Ngoja tu nikwambie ukweli, nimetoka guest” “Guest!
Kwahiyo ulikuwa na mwanaume?” “Sasa Guest niende peke yangu nina wazimu
au? Nilikuwa na mwanaume ndio” “Ila Dora si umeathirika wewe, huoni kuwa
si vizuri hivyo unavyofanya?” “Hivi kwani ni mimi tu mwenye dhambi
duniani hadi nikapata huu ugonjwa? Yani yoyote anayejilengesha kwangu twende,
habari ndio hiyo na wale wanaume wote walionisumbua kipindi cha ulimbwende wangu
nawapeleka na maji, si wanaume huwa hamkumbuki kinga eeeh! Yani akili zitawakaa
sawa” “Mmmh Dora, ila ujnajua ukimwi unazunguka? Unaweza tembea na
mwanaume halafu akatembea na mdogo wako” “Kwa bahati nzuri au mbaya sina
mdogo wa kike kwahiyo imekula kwao na mdogo wangu kashalishwa limbwata huko
kamganda mwanamke hataki hata kurudi nyumbani” “Hivi Dora, limbwata ndio
inakuwaje kuwaje?” Dora alicheka sana kuona kuwa James kashasahau kuwa
hata yeye alilishwa limbwata na pale alimwambia tu muda huo anarudi kwao ila
James alijitolea kumpleka Dora kwanza ndio yeye kwenda kazini. Dora
aliingia kwao na kama kawaida mama yake alifoka huku akisikitika na kitendo cha
kutokumuona mwanae, “Mama, kunilalamikia mimi ni sawa na kumpigia mbuzi
gitaa. Nishakwambia cha kufanya, kama hutaki basi, ila hiko ndio cha
kufanya” Kisha Dora aliingia chumbani kwake, ila leo kabla ya yote
aliamua kumpigia simu mzee Jimmy ili kusikia anasemaje ila ile simu ilipokelewa
na Erick, na Dora aligundua baada ya kusikia ile sauti, “Kheee
Erick” “Ndio, ni mimi wanifahamu kwani maana baba
anaumwa” “Nakufahamu, mimi ni Dora rafiki wa Erica nilikuwa nampigia
simu mzee Jimmy” “Kwahiyo na wewe unataka kujua hali ya shemeji yako
sio” “Hapana, huyo sio shemeji yangu kama unavyofikiria. Muulize vizuri
kuwa Dora ni nani akueleze kuhusu mimi. Sio shemeji yake mimi” “Baba
yangu ni mgonjwa, siwezi kuondoka karibu yake maana hataki niende popote na
siwezi kumuuliza swali hilo kwasasa mpaka awe sawa kabisa” Kisha Erick
akakata ile simu, ila Dora alihisi jambo kuwa mzee Jimmy anajifanyisha ili Erick
asiwe karibu na Erica. Tumaini alimuita kaka yake ambapo alitoka sebleni
na kuanza kuongea naye, “Nimekusikia ukiongea na simu nani huyo?
Nikasikia shemeji” “Ni Dora huyo, Yule rafiki wa Erica, itakuwa
unamfahamu maana anajulikana sana kwa matendo yake” “Kapata wapi namba
ya baba?” “Sijui, labda na rafiki yake Erica wamepeana
huko” “Hivi Erick sikuwahi kukuuliza, kwani Erica amewahi kukwambia
habari zozote za kuhusu baba?” “Hajawahi kuniambia zaidi zaidi
aliniambia kuwa kuna mzee anamfatilia eti anasema ndio baba, ila swali
linalonitatiza ni kuwa alisema kuna hela kapewa na huyo mzee sasa hazitaki na
amezitumia milioni tano halafu mke wa huyo mzee anazitaka, yani nikatoa milioni
tano yangu hivi hivi ili Erica asisumbuliwe na huyo mzee. Swali langu ni kuwa
mke wa huyo mzee ni nani wakati baba yetu hana mke? Si change la macho lile
nilipigwa na Erica?” Mara baba yao akamuita Erica, kwahiyo ilibidi Erick
aende kumsikiliza na kuacha kuongelea mada zake. Ndugu wa
Bahati leo walimuita nyumbani ndugu yao ili waongee nae kuhusu yale
waliyoyasikia, Bahati alifika na kuwasikiliza tu wanachoongea ambapo dada yake
alianza kwa kusema, “Kwakweli Bahati utusamehe sana, hatukujua kuwa
Nasma ni mbaya kwako na kukuozesha kwa huyo” “Sawa hakuna tatizo, ila
mimi nataka kumuoa Siwema kwasasa” “Yani Bahati hujui tu ila bado nguvu
ya dawa ipo kwako, yupo binti uliyekuwa ukimpenda sana” “Yuko wapi huyo
binti?” “Anaitwa Erica, ulikuwa ukimpenda sana na alikuwa ni kila kitu
kwako” “Nina uhakika hata huyo binti hatonitaka tena kwa nilivyo sasa,
ila nyie wenyewe si ndio mlikiri ya kwamba mlinipa dawa ili nimsahau huyo binti?
Na kweli nimemsahau maana hayupo hata kwenye kumbukumbu zangu, kwahiyo haya ndio
maisha ambayo mmenichagulia ndugu zangu” “Hapana Bahati, sio hivyo yani
sio kama hivyo unavyofikiria” “Yani kuongea kwenu sidhani kama
kunanisaidia maana kama kuharibika sasa nimeharibika vya kutosha, kwasasa sirudi
nyumbani kwangu sababu nina tatizo lingine” “Tatizo gani
tena?” “Nishatembea na mdogo wa huyo Nasma na sasa ana mimba yangu,
nahitaji kumuoa Siwema. Ila nilirudi nyumbani kwangu na kumkuta Nasma yupo na
mama yake yani mama mkwe wangu, ngoja niwaambie tu ukweli ndugu zangu nimejikuta
nikianza kumpenda Yule mama tena nampenda kimapenzi” Ndugu zake
walishangaa sana, kisha Bahati akaendelea kuongea, “Nikaamua kuondoka
nyumbani kwangu na kwenda kulekule nilikompangishia nyumba Siwema sababu
nikiishi pale nyumbani naweza nikambaka Yule mama mkwe, namtamani kabisa na
kujizuia siwezi” Kwakweli hii hali iliwafanya wawaze dawa ya kumfanyia
Bahati mapema iwezekanavyo maana bila ya hivyo atachafua ukoo wa kina Nasma
maana hali aliyokuwa nayo haikuridhisha kabisa. Siku zilienda
na Erica hakutafutwa na Erick kabisa, kwakweli kitendo hiko kilimpa mawazo sana.
Halafu alianza kujihisi vibaya yani afya yake haikuwa vizuri, siku hiyo
alijiandaa na kuaga pale kwao kisha akaenda zake hospitali kwa lengo la kupima
malaria. Majibu yakatoka na kuambiwa kuwa ni mjamzito, alishtuka kidogo
ila alikubaliana na majibu yale kwani kabla ya ugonjwa wake anakumbuka kuwa
aliwahi kukutana kimwili na Erick kwahiyo kwa vyovyote vile ile ni mimba ya
Erick. Basi akawa anatoka pale hospitalini ila kuna mtu alikumbana nae
kikumbo na cheti chake kikaanguka, Yule mtu aliokota kile kicheti na kukishika.
Alivyoinua macho kumtazama Yule mtu akakutana macho kwa macho na Sia yani Yule
mtu alikuwa ni Sia, basi alisoma kile cheti cha Erica na kusema “Kheee
Erica, kumbe una mimba? Ya nani tena? Usije ukamsingizia Erick maana na mimi pia
nina mimba ya Erick, cheti hiki hapa” Akatoa cheti na kumpa Erica,
ambapo alikisoma na kuona kweli Sia ana mimba. Basi
akawa anatoka pale hospitalini ila kuna mtu alikumbana nae kikumbo na cheti
chake kikaanguka, Yule mtu aliokota kile kicheti na kukishika. Alivyoinua macho
kumtazama Yule mtu akakutana macho kwa macho na Sia yani Yule mtu alikuwa ni
Sia, basi alisoma kile cheti cha Erica na kusema “Kheee Erica, kumbe una
mimba? Ya nani tena? Usije ukamsingizia Erick maana na mimi pia nina mimba ya
Erick, cheti hiki hapa” Akatoa cheti na kumpa Erica, ambapo alikisoma na
kuona kweli Sia ana mimba. Erica alimuangalia kwa makini Sian a
kumuuliza kwa mshangao, “Una mimba?” “Kwani umeshindwa kusoma
cheti hiko au? Mimi nina mimba ya Erick, sijui mwenzangu kama kawaida yako ya
kupachika mababa watoto wako, sikuelewi!” Erica akaona kuendelea kuongea
na mtu huyu ni kujipa mawazo ya bure wakati mwenye ukweli ni mmoja tu ambaye ni
Erick, basi Erick akachukua kile cheti chake kwa Sian a kumkabidhi kile
alichompa akisome kisha kuanza kuondoka, ila Sia alimfata kwa nyuma na
kumwambia, “Mbona husemi lolote sasa?” “Unataka niseme
nini?” “Wotw tuna mimba, na huonyeshi kushtuka kama kitu ulikuwa unajua
au Erick kashakwambia kuwa nina mimba yake!” “Sia, naomba uniache
tafadhali kila mtu kaja hospitali kwa mambo yake. Kama wewe una mimba na mimi
nina mimba tatizo nini sasa? Sisi ni wanawake na kubeba mimba ni haki
yetu” Sia akaanza kucheka na kusema kwa kebehi, “Ni haki yetu
ndio ila tunatakiw akubeba mimba kwa malengo, yani wewe mtoto wa kwanza umezaa
bila malengo na sasa wa pili huyo hujui hata baba wa mtoto ni nani na hujui hata
atachukua uamuzi gani” Erica hakumuangalia tena wala nini sababu alihisi
akimchefua tu nay ale maneno yake, alitoka zake na kwenda kupanda gari lake na
kuondoka ambapo alienda moja kwa moja ufukweni ili atulize mawazo
kidogo. Erica alifika ufukweni huku akiwaza na kuwazua, akafika
eneo moja wapo na kulikumbuka vizuri, lilikuwa ni eneo ambalo alikutana na
Bahati kwa mara ya kwanza na alikuwa akiwaza jinsi alivyoachwa na George,
aliangalia lile eneo ila hakutaka kukaa tena maana aliogopa kukutana na mwanaume
mwingine king’ang’anizi kama Bahati ingawa kwa upande mwingine alimkumbuka
Bahati, mwanaume ambaye huwa haoni kosa kwa Erica yani kila kitu kinachofanywa
na Erica kwake ni sawa tu, alitabasamu alivyomkumbuka na kurudi kwenye gari
kisha kuchukua simu na kumpigia Erick kwani aliona anahitaji sana kuongea na
Erick, ile simu ilipokelewa na Erica alianza kuongea, “Erick tafadhali
nina maongezi na wewe, naomba tuonane” “Si unajua baba yangu anaumwa
Erica? Nitamuachaje baba yangu?” “Erick kumbuka ahadi uliyonipa kwenye
mapenzi yetu sasa kuwa hakuna kitu kitakachotutenganisha, ulisema hatupaswi
kusikiliza maneno ya watu yani sisi tukae na swala moja la kupendana tu sasa
vipi leo umesahau ahadi yako?” “Kwahiyo Erica, unataka mimi nimuache
baba yangu sababu ya ahadi ambayo niliahidi kipindi cha nyuma?” “Nina
jambo muhimu nahitaji kuongea na wewe” “Hapana, sio
kwasasa” Erick alikata simu, kitendo hiko kilimuuma sana Erica, aliamua
tu kurudi nyumbani kwao ambapo mama yake alimuuliza alichoenda kuambiwa
hospitali kuwa kinamsumbua ni kitu gani, “Haya mwali wetu, nini
kinakusumbua?” Erica aliwaza kuwa akisema ni mimba itakuwa ni balaa kwa
mama yake maana hatomuelewa kabisa ukizingatia maswala ya mapenzi kashamkataza
sana, kwahiyo alimdanganya tu, “Wamesema eti nina UTI” “Oooh
pole mwanangu, eeeh dawa walizokupa ziko wapi?” Hapo ndio ukawa mtihani
sasa maana uongo ule hakujipanga nao sababu ya mawazo ya Erick, alijikuta akikaa
kimya kwa muda na kumuangalia tu mama yake ambapo mama yake alirudia
swali, “Dawa walizokupa ziko wapi? Au hawajakupa
dawa?” “Waliniandikia dawa kuwa nikanunue duka la
madawa” “Karatasi uliloandikiwa dawa liko wapi?” Alianza kuhisi
kuwa pengine mama yake kamgundua maana si kwa maswali yale ya mitego, ila bado
aliendelea kumficha mama yake, “Nilienda duka la madawa ila Yule nesi
niliyemkuta amenipa ushauri mzuri sana. Kuwa nisijisumbue kumeza madawa maana
unaweza ukameza na UTI ikakurudia, kwahiyo kanishauri nanze dozi ya vitunguu
swaumu” “Dozi ya vitunguu swaumu? Weee Erica ni mzima
kweli?” “Ndio dozi ya vitunguu swaumu, niwe natwanga halafu nameza kama
dawa” “Yani umezunguka kunitafutia uongo wa kuniambia hadi umeupata huo
loh mwanangu uongo utaacha lini wewe? Nilikuwa nakuangalia tu wakati unatoka,
mwanaume toka sakata la baba yake hapa hajawahi kukanyaga mguu wake tena ila
wewe kiguu na njia kumfata fata, unachokitaka utakipata nakwambia, na usiniletee
mimba tu, huo ujinga wa kuzaa watoto wawili nyumbani tena bila ndoa siutaki.
Umesikia!” “Nimesikia mama” Kisha Erica akainuka na kwenda
chumbani kwake huku akiwaza sana maana kama mimba tayari anayo, sasa Erick
akiendelea kuzingua tu kwake itakuwa ni mtihani mkubwa
sana. Kwa upande wa Sia, alipotoka hospitali moja kwa moja
alienda kwakina Tumaini na kumkuta Tumaini akiwa amekaa nje leo. Akasalimiana
nae na kuanza kuongea nae, kiukweli Tumaini alitaka kumtimua Sia ila alishangaa
akimuangalia tu bila kumtimua, basi Sia akampa Tumaini kile cheti cha kuonyesha
kuwa ni mjamzito, Tumaini akamuuliza kwa mshangao, “Una
mimba?” “Ndio nina mimba, ya kaka yako” “Hebu acha zako Sia,
hiyo mimba iliingia kwa upepo au? Nakumbuka tulisema uigize kuwa una mimba ila
haikuwa kweli” “Tumaini sikupima tu ila kiukweli nina mimba, na cheti
hiki hapa. Huyu nimembeba ni mtoto wa Erick” “Mmmh na Yule unayeishi
naye pale kwako?” “Yule siishi nae kama unavyofikiria ila analalaga pale
nje kwetu” “Unafikiri nina hamu na wewe? Toka nimejua kuwa wewe ni
mshirikina basi sina hamu na wewe tena” “Tatizo Tumaini hukunielewa, ila
ndio nina mimba ya kaka yako” “Sikia Sia, swala la wewe kuwa na mimba
siwezi kukubali wala kukataa ila muhusika ndio atasema ukweli maana ndio
mnajuana. Mimi siwezi kujua kuwa mlikutana muda gani” Baba yao na wakina
Tumaini alikuwa nje pale akinyoosha nyoosha miguu na aliwasikia wakati Tumaini
na Sia wanaongea, basi akafika na kusema kuwa atambulishwe Sia kuwa ni nani? Kwa
kipindi hiko wakina Tumaini walikuwa wapole wana kwa baba yao maana hawakutaka
kumkera wala kumpa habari za kuudi, kwahiyo Tumaini akamtambulisha Sia kuwa
aliwahi kuwa na mahusiano na Erick, halafu Sia nae akasisitiza pale pale kuwa
katoka kupima ana mimba ya Erick huku akimpa baba yao cheti kinachoonyesha kuwa
ana mimba. Cha kushangaza mzee Jimmy alionekana kufurahia sana ile habari na
kumkaribisha Sia ndani kwao ambapo kwa muda huo Erick alikuwa ametoka kuna dawa
alienda kumtafutia baba yake. Mzee Jimmy alimkaribisha Sia huku
akimuhoji maswali mbalimbali kama ana mpango gani na Erick, “Natamani
siku moja Erick awe mume wangu, yani nitafurahi sana” “Basi usijali,
siwezi kuacha mjukuu wangu alelewe bila ya baba yani lazima Erick akuoe na
sherehe yote nitaigharamikia mimi” Tumaini alikuwa jikoni kwa muda huu
ila kwakweli alishangaa sana kwa baba yao ambaye siku zote toka ameanguka
alionyesha kutokuwa na furaha na aliongea kwa shida kiasi kwamba Erick ndio
alikuwa akimpokelea simu zake ila leo ilikuwa ni ajabu sana maana aliongea kwa
furaha mno kama hakuwahi kuumwa hapo kabla. Erick wakati
anatafuta dawa za baba yake alijikuta akifika mpaka mitaa ya kwakina Erica,
ingawa ilikuwa ni usiku tayari ila kwa upande mwingine alitamani kujua ni kitu
gani erica alitaka kumwambia, kwahiyo alimpigia simu muda huo ambapo kwa muda
mchache tu Erica alipokea simu hiyo kisha Erick alimuambia aende kituoni kwao
akaongee nae. Erica alitoka kwao kwa gia ya kwenda dukani kisha
akaelekea kituoni ambako Erick alisimamisha gari yake yani siku hii hakutaka
kwenda kwakina Erica kabisa maana kwa amjuavyo mamake Erica basi inaweza kuwa
balaa kwake akijitokeza pale wakati hajajipanga. Erica alifika na Erick
alikuwa amesimama tu nje ya gari, Erica alimsogelea na kumkumbatia ambapo Erick
hakuweza kuacha kukumbatiwa na Erica ila naye alimkumbatia pia na kugundua kuwa
Erica alikuwa akitokwa na machozi, alimuuliza kwa upole kuwa tatizo ni nini ila
bado Erica alionekana akilia ikabidi aingie nae kwenye gari ili aongee nae
vizuri. Alikaa nae kwenye gari huku akimkumbatia na kumbembeleza na
kumuuliza kwa upole, “Kwani Erica tatizo ni nini?” “Nilikuwa
sipo vizuri kwa hivi karibuni, nikaamua leo kwenda hospiatali. Nimekutwa na
ujauzito Erick” Erick akamuweka kwanza pembeni Erica na
kumuuliza, “Erica una mimba? Usiniambie ni mimba ya baba yangu maana
sijui nitafanya nini muda huu” “Erick, najua nitasema sana ila unaweza
ukaniamini au usiniamini ila mimi sijawahi kutembea na baba yako, ni kweli
kanifatilia kwa kipindi kirefu sana ila sijawahi kutembea nae. Kama huamini
naomba hata uchukue muda wako umuulize Dora, mimi sijawahi kuwa na mahusiano na
baba yako. Hii mimba ni yako Erick” “Kwa mara moja tu Erica jamani! Yani
mara moja tu umepata mimba yangu?” “Ndio Erick, hii mimba ni yako yani
una mashaka bure tu ila hii mimba ni yako Erick, naogopa kusema nyumbani,
naogopa kumwambia ukweli mama maana sijui kama atanielewa kubeba mimba mbili
nyumbani” “Sawa, nimekuelewa Erica. Ila nina ombi moja
kwako” “Niambie Erick” “Naomba usiitoe hiyo mimba tafadhali,
naomba usiitoe. Huyo mtoto nitampenda kama nimpendavyo Angel, haijalishi ni wa
nani ila nitampenda” “Erick, huyu mtoto ni wako hutakiwi kuwa na
mashaka. Ni mtoto wako huyu Erick, niamini tafadhali” “Sawa, nimekuelewa
basi ngoja nikurudishe kwenu” “Kabla ya kunirudisha kwetu, naomba
nikuulize jambo” “Jambo gani?” “Erick, una majina mengine kabisa
hata nikashindwa kuelewa kuwa mzee Jimmy ni baba yako. Kwanini hutumii majina ya
baba yako?” “Erica, nilitaka kukwambia kuhusu mimi zamani sana ila
kwavile tu mambo yaliingiliana ndiomana sikuweza kukwambia. Toka kipindi
nimekwambia Angel aitwe jina langu na sikuona kama ni tatizo maana mambo kama
hayo hutokea kwenye jamii. Sema historia yangu ni ndefu kidogo ila nitakwambia
kwa kifupi” “Niambie tu nitaelewa” “Sikia nikwambie, mama yangu
aliponizaa mimi, Yule baba umuonaye nasikia alizingua hivyo mama aliishi kwao
ndipo babu yani baba mzaa mama akasema niitwe kwa majina yake yani hakutaka
majina ya baba yawe kwangu, toka hapo niliandikishwa shule kwa majina ya babu
kwahiyo vyeti vyangu vyote vina majina hayo. Na mwishowe mimi niliishi kwa mama
mdogo ndio kipindi kile wakati nasoma, sasa nilivyotimuliwa pale shuleni,
mamdogo alimwambia mama kuwa hatoweza tena kunilea maana nimekuwa mtukutu,
kipindi hiko mama yangu alikuwa Marekani akifanya kazi za ndani, kwahiyo ujumbe
ule ulichelewa sana kumfikia mama. Toka nifukuzwe shule niliishi nyumbani tu kwa
mamdogo maana alisema hanitafutii shule nyingine tena, kidogo hapo katikati nina
historia ndefu ndiomana mamdogo hakutaka kunitafutia tena shule na alisema ile
ni shule ya mwisho kwangu. Nilikuwa napenda maisha mazuri hivyo kila akinipeleka
shule zisizoeleweka nilianza kumsumbua ndio akanileta ile shule, akasema ni
nzuri na kweli niliipenda na kumuahidi sitamsumbua tena na nitakuwa mtoto mzuri
kwahiyo nilipofukuzwa na pale mamdogo alizira kunitafutia shule nyingine, babu
naye hakuwa na uwezo wa kunisomesha ingawa nina majina yake, maana alisema ni
bora kutumia majina yake anayenijali kuliko kutumia majina ya baba ambaye wala
haonyeshi kunijali. Nilikaa mwaka mzima nyumbani nikiwa sijielewi wala nini yani
nipo nipo tu maana tulikuwa tunangoja majibu ya mama kuwa tufanye kitu gani ila
kwa kipindi hiko niliondoa matumaini ya kusoma kabisa. Siku moja katika pita
pita zangu mitaani ndipo nikakutana na baba na alinisaidia bila kujua kuwa mimi
ni mwanae, sasa siku naenda kumpokea mama uwanja wa ndege nikakutana tena na
baba ambaye kuna ndugu yake alikuwa anaenda kumpokea pia, akanipa lifti
tulipofika uwanja wa ndege ndio akakumbana na mama na palepale mama alishangaa
kuona mimi na baba tulifahamiana, basi ikabidi atutambulishe vizuri na hapo ndio
maisha yangu yakabadilika kwani nikaanza kuishi na baba huku nikisaidiana nae
kwenye biashara zake mbalimbali, yani mimi nilikuwa nasoma huku nafanya biashara
na baba, na kiukweli zile pesa zilinipa kiburi maana nilianza kuwa na wanawake
wengi wengi sababu nilijua ulinikaa sababu nilikuwa sikupi pesa sasa nilikuwa na
hela na kupata wanawake mbalimbali sema tu sikuwapenda kama nilivyokupenda
wewe” “Kheee kumbe, kwahiyo Tumaini ulikutana nae kwa baba
yako?” “Ndio Tumaini alikuwa akiishi kwa baba ila alikuwa akiishi sana
kwa mama yake, nilipohamia mimi kwa baba ndipo na yeye akaja kuishi kwa baba na
hapo ndipo alipojua historia yangu ya kufukuzwa shule sababu ya mwanamke maana
mamdogo alikuwa akimsimulia kila mtu kuhusu mimi kufukuzwa shule sababu ya
mwanamke, na ndio hapo Tumaini alipochukia sana kuhusu mwanamke aliyesababisha
nifukuzwe shule maana mimi hadi kuendelea zaidi na masomo niligoma, unajua
kitendo cha mimi kukaa mwaka mzima nyumbani bila ya kusoma kilinichukiza sana,
mwishowe nilipokutana na baba nilisoma tu kutoa ujinga ila sio kusoma kwa
malengo ndiomana wakati Tumaini yupo chuo mimi sikuwa chuo na usinione hivi
sijafika chuo wala nini.” “Kwahiyo mama yako alikuwa akifanya kazi za
ndani?” “Ndio mama yangu alikuwa akifanya kazi za ndani huko Marekani,
watu wengi walipojua walitukebehi na kutucheka ila sasa ndio wanaoomba misaada
maana mama kawa na hela hatari, anafanya atakacho, anaenda atakapo yani saivi
kawa kama sio yule wa zamani. Na ni kipindi hiko aliporudi maisha yake
yalibadilika moja kwa moja, nadhani alijiwekeza” “Sasa wewe huishi na
mama yako, kwahiyo anaishi na nani?” “Mama anapenda sana kusaidia,
ukienda kwake utakutana na watu mbalimbali tu ndugu zake, mimi kwasasa nishazoea
kuishi kwa baba kwani kwa kiwango kikubwa sana kabadilisha maisha yangu, mama
nae kabadilisha maisha yangu. Kwahiyo mimi nipo katikati, ni jicho la mama na
pia baba ananitazama sana, toka amenitambua huwa hataki kunikosea na ndiomana na
mimi sitaki nkumkose. Baba yangu amepatwa na presha kwasasa kwahiyo siwezi
kumwambia kuwa Una mimba sijui yangu maana ninaweza msababishia matatizo
zaidi” Erica akapumua kidogo kisha akasema, “Ila ukweli ni kuwa
sijawahi kutembea na baba yako, muulize Dora ndio anajua ukweli wote maana Dora
ndio alikuwa akitembea na baba yenu” Hapo Erick alishangaa zaidi kwani
hakutegemea kusikia kuwa baba yake anaweza kutembea na msichana kama Dora,
aliona kweli mzee wake kaingiliwa basi alienda mbele kuendesha gari ili
kumrudisha Erica kwao na kumwambia kuwa wataongea zaidi na watajua cha
kufanya. Alifika nae getini kwao, kisha Erica alifungua mlango wa gari
ili aondoke ila kabla hajaondoka Erick alimuita na kushuka kwenye gari kisha
akambusu Erica na kumuaga halafu akarudi kwenye gari na kuondoka
zake. ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment