Search This Blog

Tuesday, 1 November 2022

SIPASWI KUSAMEHEWA - 1

 






IMEANDIKWA NA : RAMAAH MZAHAM



*********************************************************************************



Simulizi : Sipaswi Kusamehe

Sehemu Ya Kwanza (1)



Kuna makosa mengine tunafanya kwa hiyari yetu, ila kuna mengine tunalazimika kuyatenda kutokana na historia ya nyuma mtu alichofanyiwa, huenda kilimkwaza ama kumuuumiza kabisa, ndio mana nami leo naungama mbele yenu, kwani kuna mengi sana mema mmenitendea, kiasi siwezi kuwalipa hata nikiishi miaka 100. Ninapoomba msamaha kwa kosa langu, sina mamlaka ya kuwalazimisha mnisamehe, ila nia yangu ya dhati ni kuwa nife nikiwa msafi, nife nikiwa na radhi yenu, radhi itakayosababisha hata Mola Mtukufu anipokee, ila mi mwenyewe nikitazama wema mlionifanyia na uovu niliowalipa. Nimekaa na siri hii kwa muda mrefu sana, sasa sina muda tena na ninapaswa kukiri hadharani mbele yenu ili mnisamehe, japo najua itawaumiza sana.

*****



Msichana mrembo aitwae Maryam, ama walio karibu nae wamezoea kumuita Mam, alikua akilia kwa uchungu na muonekano wa hasira nyingi. Akiwa katika mwendo wa haraka alivua pete aliokua amevaa na kuitupa pembeni ya barabara, chini ya mti ambao kijana Esmile alikua amekaa.

Esmile ni kijana mdadisi anaependa sana mambo ya kudadisi dadisi kila jambo lililopo mbele yake, akaiokota pete ile na kuanza kumfuata Yule binti anapoelekea.

Mam ni msichana mrembo kweli kweli, mrefu, Mwembamba na mwenye rangi yake ya asili, ambayo ilikuwa ni weupe usio na mng’ao sana, hakuna mtu ambae anngeweza kusimama na kumponda kuwa hana uzuri wowote, maana alikamilika kuanzia nywele zake ndefu hadi miguu yake ya bia.

Umbile lake nalo lilikua ni utata mtupu, kifupi Mola alimjalia uzuri na Zaidi ya yote alimpa na akili ya kujitambua, hivyo aliweza kupambana na vishawishi kwa asilimia kubwa.

Baada ya kutoka pale, kimya kimya akaelekea hadi kwenye kituo cha basi cha Posta, hayo ni maeneo ya Tabata anayoishi Esmile.

Mam akaingia katika daladala ilioandikwa Segerea, nae Esmile kwa kuwa nia yake ilikua ni kumfuatilia na kujua kinachomsumbua mrembo Yule ambae hamtambui, alisimama pembeni na kusubiri daladala ilipoondoka. Nae akachukua pikipiki ya kukodi na kumfuatilia binti mrembo ili kujua anapoelekea na ikiwezekana anapokaa. Lengo lake lilikua ni kuongea nae faragha na kama itashindikana basi afahamu angalau anapokaa.

Kwa kuwa alikua akifahamiana na vijana wanaokodisha pikipiki pale kijiweni, akachukua pikipiki moja ili aendeshe mwenyewe na kuanza kulifuatilia daladala lile hadi ilipofika kituo cha mwisho kabisa. Akasimama mita 25 na kusubiri aone mrembo akitoka ataelekea wapi.

Haikuchukua muda Mam akashuka na kuelekea nyuma ya Gereza la Segerea. Polepole kwa majonzi aliondoka eneo la kituo cha daladala na kulizunguka jengo la gereza kwa upande wa kushoto. Esmile akapaki pikipiki mbele ya duka moja jirani na gereza na kuzidi kumfuatilia Mam ambae alikua hajui kinachoendelea.

Walikwenda umbali wa kama kilometa mbili, Esmile hakuona dalili yoyote ya nyumba zaidi ya mashamba ya Magereza na miti mingi iliyooteshwa na kuleta mandhari ya kupendeza.

Mbele kidogo Mam alikaa chini na kuanza kulia, Esmile alimpita na kuanza kumsalimia;

“Anti habari ya saa hizi?” Mam hakujishughulisha hata kumtazama achana na kumjibu, akaendelea kulia. Nae Esmile hakwenda mbali sana, akasimama nyuma ya kichaka ambacho hakikua mbali sana na pale, ila hakuweza kuonekana kwa urahisi.

Baada ya dakika 5 hivi kupita, binti alinyanyuka na kujifungua

kitambaa chake cha kichwani na kugeuka huku na kule, nafikiri alikua akitazama kama kuna mtu yeyote anaemuona. Aliporidhika kuwa hakuna anaemuona, alichukua kitambaa chake na kukitupia kwenye tawi la mti ule aliokuwa amekaa.

Kengele ya tahadhari ikalia kichwani mwa Esmile, akahisi binti Yule huenda anataka kujidhuru,

“Kwa kweli sitaruhusu hali hiyo ijitokeze, japosimtambui,” aliwaza Esmile. Kwa alivyokuwa akihangaika kufunga kitambaa kile, ilionekana kwamba zoezi lile limeshindikana, kwani kile kilemba ni kidogo na tawi lilikua juu sana. Alichofanya ni kugeuka na kuondoka kwa kasi kitambaa akiwa amekiacha pale pale mtini, nae mbio mbio akielekea barabarani.

Esmile nae akatoka pale aliposimama na na kusogea pale mtini alipokua amekaa Mam na kuchukua kile kitambaa, akakihifadhi mkononi mwake. Kisha akaanza mbio fupi kumfuatilia tena mrembo asiemjua.

Walikwenda na kutokezea barabarani tena jirani na duka lile aliloweka pikipiki, palikua na duka la dawa. Mam akaingia na Esmile akaingia baada ya dakika kadhaa. Ndani ya duka la dawa alikuta mabishano kati ya muuza dawa na Mam.

Ubishi ulikuwa unahusu tiba aliyoitaka Mam, Mam anataka dawa aina ya SP, na wakati huohuo anahitaji Metakelfin na Fragile pia. Mfamasia akataka cheti cha daktari na hapo ndio ikawa kimbembe. Lakini baada ya binti kujieleza kwa sauti ya upole kuwa yeye ni mgonjwa wa tumbo na pia ana Malaria, mama yake pia ana Malaria ambayo anahisi ni kali sana.

Akajitetea kuwa kwao ni mbali sana, kwa kauli ile Mfamasia akakubali na kumuuzia dawa kwa sharti kuwa siku nyingine aje na cheti cha daktari. Mam akalipa pesa zilizohitajika na kutaka kuondoka, Mfamasia akamwambia asubiri, maana zile dawa alizompa zote zinatumika sambamba na Panadol ama Paracetamol. Hakubisha, akalipia tena Paracetamol.

Kipindi chote hicho Esmile alikua amekaa kwenye sofa mlemle ndani, alipoona Mam amepewa zile dawa akasogea na kupishana na Mam. Esmile akamsalimia tena ila Mam hakuitikia tena, akafanya kama vile hakusikia.

Esmile nae akanunua Panadol za Blister huku akitazama barabarani kupitia pale kwenye vioo vilivyopo duka la dawa. Mara hii Mam hakuelekea kule alipokwenda awali, isipokua aliingia dukani pale Esmile alipoacha pikipiki.

Hakuchukua muda mrefu sana akawa ametoka na mkononi akiwa na chupa ya maji yakunywa.

Kitendo bila kuchelewa, Esmile akalipa na kuchukua dawa zake, akamuaga nesi. Mam akiwa mbele, Esmile alimfuata kwa kunyata, kwani kwa mara nyingine, alipata picha Fulani na kuhisi ni nini kitafuatia. Japo hakuwa mtabiri, ila kwa hili halikuhitaji ramli, akaamua kuwa makini zaidi ya awali.







Hatua kadhaa mbele kabla ya kufika pale alipokua amekaa mwanzo, Mam akakaa chini ya ukuta na kuanza kuangalia pande zote 4 aliweza kupata uhakika kuwa hakuna amuonae hasa kwa kale kagizagiza kembamba kalikoanza kutawala anga. Akafungua chupa yake ya maji na kuiweka chini, akatoa vidonge vyote na kuvichanganya katika karatasi moja.

Hapo sasa akavimimina katika kiganja cha mkono wa kushoto huku akilia na kufumba macho huku akisema;

‘Eh Mola wangu nisamehe kwa hili nililopanga kulifanya sasa...’ wakati akifanya hayo, taratibu kwa kunyata Esmile alizidi kumsogelea na kumkaribia kiasi alisikia maneno aliyokuwa akiyasema. Akasimama pembeni yake na kumsikia Mama akiongea kwa kuhuzunika;

“Mungu wangu sikupenda kutenda hivi ila matatizo yamenisababishia mimi mja wako hadi nafikia hatua hii, hapa duniani sina pa kukimbilia ndio maana naona ni heri nije kwako ili nipumzike, nipokee Mola wangu, naomba unisamehe kwa kukatisha maisha yangu, pia umsamehe kwa kitendo chake. Kwa herini wazazi wangu, kwa heri Alfred”

Kabla hajafungua macho Esmile akamdaka mkono na kumwaga vidonge vyote alivyokuwa navyo mkononi na kumwambia;

“Haiwezekani msichana mdogo na mrembo kama wewe ujiue mbele yangu eti kwa sababu tu ya jambo Fulani limekukera nakuomba ufute wazo hilo...” Mam akavitazama vidonge vyake pale chini kisha akamtazama Esmile kwa hasira na kusema kwa jazba;

“We ni nani na kwa nini umemwaga vidonge vyangu mjinga wee?”

“Mimi ni Malaika nimetumwa na Mola wako nije nikusaidie, kwani umemwambia huna pa kukimbilia hivyo ameniagiza kama msaada kwako...”

“We inakuhusu nini? Na kwanini utupe vidonge vyangu?”

“Binti kumbuka kuwa kuna watu wana matatizo zaidi ya hayo uliyo nayo wewe japo siyajui. Ila kwa jinsi ninavyoona we una uhusiano mzuri na wazazi wako, kuna watu hawataki hata kidogo kusikia habari za wazazi wao lakini hawajafikia hatua kama yako, jaribu kuvumilia. Matatizo ni sehemu ya maisha.”

Hapo Esmile alikuwa amechuchumaa mbele ya Mam aliekua anamtazama kwa hasira, kwa ulaini wa maneno yale, Mam akaanza tena kulia kwa kwikwi akisema;

“Kila siku matatizo kwangu? Ungeniacha tu mi nikajifia porini huku,” Esmile akamnyamazisha na kumbembeleza na kumnyanyua, akamfuta vumbi magotini na kumuomba waondoke.

“Twende wapi?” Aliuliza Mam na Esmile akalijibu kwa mtindo wa swali…

“Ina maana tutakaa hukuhuku? Twende kwanza hapo dukani tukaongee.”

“Dah! Imetokea kukuamini, sijui ni kwa nini? Haya twende utakapo...”

“Ndio unapaswa uniamini, maana mi nimeletwa kwa ajili yako.”

“Sawa kaka…”

“Niite Esmile, naitwa Esmile.”

“Sawa kaka Esmile, name naitwa Maryam, wengi huniita Mam.”

“Ooh jina tamu kama… Aah! Samahani, una jina zuri kama wewe mwenyewe,” Mam akaguna tu na kushukuru.

Moyoni mwake Mam alijiambia kuwa wanaume wote kumbe wamefanana, kwa sauti ambayo aliamini kuwa haijackika na yeyote, kumbe Esmile akawa ameisikia na kumuuliza kwa nini anasema vile. Mam akakataa kuongea lolote. Wakatoka eneo lile hadi dukani walipoagiza vinywaji na kuongea kidogo.

Esmile akataka kujua kilichosababisha binti Yule akataka kujitoa roho. Kwa huzuni akamwambia kuwa kuna kitu kibaya kilimtokea siku iliyopita, ila kilichotokea leo ndio kilichomuumiza zaidi. Kifupi alipata tatizo jana, leo kaenda kwa Boyfriend wake aitwae Alfred, kamfukuza kwa kashfa kibao na matusi gunia.

Hapo Mam akaanza kulia tena, Esmile akaendelea kumpoza na kumpa hadithi za zamani za kale juu ya mapenzi. Aliongea nae kwa takriban nusu saa, hadi Mam akachangamka na hata kutabasamu. Esmile sasa akapata ahueni na kuamini kuwa Mam atarejea katika hali yake ya kawaida na kulifuta lile wazo la kujiua.

Esmile akamuuliza anapoishi ili ampeleke, Mam akajibu anaishi Kigogo. Nae akamtwanga swali Esmile ni wapi anaishi na ilikuwaje hadi akatokea wakati ule? Esmile akamwambia kuwa ye anaishi Mbinguni na aliamrishwa kuja duniani na Mungu wake yeye Mam kama alivyotaka msaada. Mam akacheka sana na kumtaka Esmile aache utani amwambie kweli.

Jibu likawa ni kuwa alimuona tangu wakati anatokea maeneo ya Liwiti ambapo ni nyumbani kwao. Mam akamkata kauli kwa kumwambia kuwa kule Liwiti ni kwa mpenzi wake aitwae Alfred na kumuliza kama Esmile anamjua. Esmile hakuwa akimjua, ila baada ya kuelekezwa sana, akamtambua.

Basi Esmile akamueleza kila kitu tangu mwanzo alivyomuona hadi mwisho walivyokaa pale, kisha akamalizia kwa swali kuwa Mam kwa sasa anashughulika na nini? Mam akamwambia kuwa yeye bado ni mwanafunzi wa kidato cha nne hapo Zanaki.

Waliongea hadi saa nne usiku, sasa Mam aliweza hata kutabasamu, tabasamu ambalo Esmile aliliona kabisa kama limeficha kitu Fulani moyoni, yaani alikuwa na tabasamu moyoni lakini akiwa na maumivu moyoni.

Muda ulikuwa umekimbia sana, hivyo Esmile akamuomba Mam amrudishe kwao. Mam akakaa kimya kwa takriban dakika nzima hadi Esmile alipomshitua na kumuuliza kulikoni? Mam akamjibu kuwa nyumbani kwao kuna matatizo na hawezi kurudi usiku hata kwa bahati mbaya.

Esmile akajikuna kichwa, kwani nae hawezi kumpeleka kwao, anamuogopa sana baba yake Mzee Hanson, basi akamuuliza Mam wafanyeje? Mam akajibu yeye aende tu kwao amuache palepale nae atajua cha kufanya. Esmile akakataa na kusema

“Mam, timu ya mafanikio ni kundi la watu wenye msimamo mmoja japo wana mioyo tofauti,”

“Unamanisha nini kaka yangu?” aliuliza Mam akiwa ahajamuelewa kabisa ni kipi ambacho Esmile alikielezea.

“Namaanisha sisi hapa ni kama kundi la watu wawili, hivyo siwezi kukuacha Mam eneo hili, na hasa ukizingatia we ni msichana,”

“Esmile, wazee wetu wa zamani wapo sahihi sana,”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Kwa hilo upo sawa japo Sijui ni kwanini umesema hivyo,”

“Wanapojidai kukuonesha kama wanakujali, nawe unatakiwa ufanye kama unawaamini,”

Ilikuwa ni kauli tata sana, ambayo ilimuweka Esmile njia panda na kushindwa kumuelewa, lakini kwa kuwa nae alikuwa ni mwana falsafa, akamuelewa baada ya kufikiri kwa dakika kadhaa, akamjibu

“Safari ya kilometa 100 huanza na hatua moja Mam,”

Wote huwa mpo hivyo Esmile,”

“Usiishi kwa kumfikiria ama kumtazama mtu Fulani anaishi vipi, kwani wengine huigiza tu, wanaishi maisha ya watu wengine kwenye maisha yao,”

“Bado hujanishawishi Esmile, nashukuru kwa msaada wako wote ulionipa hadi sasa, lakini elewa mimi tangu mchana wa leo, nimekuwa adui mkubwa wa wanaume, ninawachukia sana, na ninakuhakikishia kwamba, siwaamini hata chembe,” maneno ya Mam yalikuwa ni makali sana lakini penye ukweli, uongo hujitenga, wakafikia muafaka kuwa Esmile ampeleke Mam Guest house yoyote ya karibu na ambayo anayoiamini ni salama ili akalale.

Alilipia vinywaji pale dukani na kupakiana kwenye pikipiki na kuanza safari kuelekea kutafuta nyumba salama ya wageni. Haikuwa safari ndefu sana, bali iliishia Aroma katika hotel iitwayo Savoy.

Walipata chumba na Esmile akakilipia kabisa na kumuomba Mam rukhsa ya kuondoka.

Mam akamshukuru na kumruhusu. Esmile akaomba namba ya simu ya Mam, Mam akatabasamu na kujibu kuwa hana simu, labda ye Esmile ndio amuachie namba yake. Kweli akatoa Notebook na kuchana karatasi na kumuandikia namba zake kisha akampa, ila alimsisitiza kuwa asiondoke pale asubuhi hadi yeye atakapofika.

Lengo la Esmile lilikuwa kumpeleka yeye mwenyewe hadi nyumbani kwao Mam ili tu nae aweze kupafahamu, wala hakuwa na lengo lolote tofauti na hilo. Wakaagana kwa ahadi ya kukutana pale asubuhi ya siku ifuatayo. Mam akafunga mlango wa chumba chake.

Esmile akatoka kurejesha pikipiki aliokodi, ila kabla ya hapo alimpatia Mam mtandio wake na kusahau kumpa pete yake, hivyo ikabaki mfukoni mwake…

Usiku ulikuwa ni mrefu sana kwa Esmile ambae alitamani kukuche haraka ili aweze kukutana na Mam waongee mengi na ikiwezekana amfikishie lile lililomo moyoni mwake. Hivyo kila mara alikuwa akitazama simu yake ilikujua ni saa ngapi.

Kawaida hata usiku uwe mrefu vipi, lazima asubuhi itafika tu. Ndio ilivyokuwa hata kwa Victor, asubuhi na mapema, Esmile alitoka kwao na kuelekea Savoy kabla ya muda ule waliopanga na Mam haujafika lengo likiwa ni kumshitukiza Mam. Alipaki gari na kuingia moja kwa moja hadi Guest na kusalimia wahudumu kisha akaelekea chumbani kwa Mam.

Alijitahidi kwa kiasi kikubwa kugonga mlango ila haukufunguliwa, akajaribu kuzungusha kitasa, kikaitika, akazama ndani na kukosa mtu, mapigo ya moyo yakaenda kwa kasi, akamuita kwa jina akihisi huenda yupo maliwatoni, ikawa kimya, akasogea na kufungua mlango ule, hakukuta mtu, akaja na kujitupia kitandani.

Alikua amepitia kadi ya mapenzi kabla hajafika hotelini, alivyokaa pale kitandani kadi ile ikamuanguka, hakujali, bali alivuta mto kwa nia ya kuulalia, akiwa hana fikra nini afanye. Alipovuta mto akaona kikaratasi, akakichukua na kukifungua, akakuta ni kile kikaratasi cha namba ya simu yake aliyomuandikia jana.

Sio siri alishtuka na kuvuta kumbukumbu, akahisi huenda hata ile jana Mam alichukua namba ile ya simu ili tu kumridhisha yeye, lakini wala hakuihitaji. Maana haiwezekani ampe namba na kisha wapange muda nae asionekane tena bila kumtaarifu lolote na hali ya kuwa namba yake ya simu alimpa.

“Si kila wakati, tunapata kile tunachotaka, lakini tunapaswa kuendelea kukitafuta kile tukitakacho bila kukata tama, yu wapi Mam?” alijiuliza mwenyewe.

Mawazo yakamvaa na kutulia kwa takriban robo saa hadi ilipotimia saa mbili na robo, akakasirika na kunyanyuka, akatafuna kile kikaratasi cha namba ya simu na kutoka kuelekea nje pasina kukumbuka kadi yake iliyoanguka pale kitandani.

Wakati akitoka chumbani, akilini alikuwa akiongea peke yake, moyoni alijuta kuonana nae, lakini pia nafc ikamwambia ni kwanini alikubali Mam amwambie ataonana nae asubuhi na hali akijua hatokuwepo. Akafika nje hadi usawa wa mlango wa gari yake na kusimama.

Baada ya dakika chache, akaingia garini na kulaza kiti mawazo kedekede, roho ilimuuma sana ila hakuwa na jinsi, akanyanyuka na kunyanyua kiti, kisha akalaza kichwa katika sterling, akiwa bado anatafakari atamuona wapi tena Mam na kwanini Mam amemfanyia kitendo kile…





Wakati hayo yakiendelea, Mama alimpita Esmile akiwa amelaza kichwa kwenye usukani wa gari lake bila kumtambua, kwani alikua na haraka ya kuwahi ahadi yake ambayo ilikuwa ni saa mbili na nusu. Moja kwa moja Mam alielekea chumbani mwake na kuangalia saa iliomwambia kuwa muda ule ni saa mbili na dakika 25, ikiwa ni dakika 5 kabla ya muda wao wa ahadi.

Hakuwa makini sana, bali akaelekea moja kwa moja chooni, wakati anatoka sasa, akatazama saa na kuona zimesalia dakika 3 tu kutimia muda wao wa miadi. Akapanga akae kitandani ili kumalizia hizo dakika kadhaa za kumsubiri Esmile.

Ajabu alipotazama kitandani, akishangaa baada ya kugundua palivyo sasa ni tofauti na alivyopaacha, pia akagundua na uwepo wa kadi pale kitandani. Akashtuka na kuishika huku akiigeuza geuza. Nje ilikuwa na jina lake, kwa kirefu kabisa.

Baada ya kujishauri kwa sekunde kadhaa, akaifungua, lakini haikuwa imefungwa kwa gundi kabisa, bali ilirudishiwa tu ili ionekane kama imefungwa na pia kuzuia uchafu na vumbi isiingie kwa wingi.

Mara tu baada ya kuifungua, hakusumbuka kujua kadi ile ni ya nini na imetoka wapi, kila kitu kilikua wazi, akishangaa kadi ile imefikaje mle ndani. Bila ya kuirejesha ndani ya bahasha yake, akasimama na kuelekea nje.

Akamuita muhudumu na kumuuliza kama kuna mtu aliingia chumbani mwake. Mhudumu akakiri na kusema kuna jamaa Yule aliekuja nae usiku uliopita, ndio alikuja na kuingia mle ndani na sasa hivi amemuona pale nje kwenye gari. Mam akashtuka na kumwambia ampeleke lilipo hilo gari.

Wakatoka kasi Mam akiwa mbele na muhudumu akifuatia, kitendo cha kufika nje, muhudumu alimuonesha gari iliokua ikiondoka kwa kasi, Mam mwili ulikufa ganzi, akaweka mikono kichwani badala ya kutafuta njia ya kumfuata. Akili ilipomrejea, akarudi ndani haraka na kukimbilia pochi yake.

Akaifungua ndani na kutafuta kitu Fulani kwa sekunde kadhaa, hakufanikiwa kukiona. Akamwaga vilivyomo, lakini pia bado hakuona alichokitafuta.

Akakumbuka kuwa kitu anachokitafuta alipewa usiku uliopita na hakukiweka kwenye pochi bali alikiweka chini ya mto. Kitu chenyewe kilikua ni kipande cha karatasi kilichokua na namba ya simu ya Esmile.

Mto alipouangalia tu,akajua umehamishwa, hata hivyo aliuvua foronya ili kuhakikisha kama ipo karatasi ile, hakuipata. Akatandua hadi na mashuka, bado hakuiona, akili yake ikamtuma huenda aliefanya usafi mle chumbani atakua amekusanya pamoja na uchafu mwingine akaenda kuitupa.

Kwa mara nyingine tena ikamlazimu kumuita muhudumu na kumuuliza kama aliefanya usafi mle ndani aliona kikaratasi chenye namba za simu, kijana alishangaa ila jibu alilompa Mam ndio nae lilimchosha kabisa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Muhudumu alimwambia chumba kile bado hakijasafishwa na hakuna muhudumu wala mtu yeyote alie ingia mle ndani tofauti na wao wawili, yaani yeye Mam na Yule kijana alieondoka na gari.

Mam akaridhika nakumtaka radhi, kisha akamshukuru, akarejea chumbani na kujitupa kwenye kitanda. Akili ilikua ikimzunguka ni wapi atamuona Esmile ili tu aweze kumshukuru kwa wema wake mwingi aliomtendea kwa siku ile moja, ilikuwa ni siku moja tu lakini alimtendea mengi.

Hakujua afanye nini, akaanza kujuta kwanini alitoka asubuhi ile kuelekea kwao. Ila akajieleza mwenyewe moyoni kuwa alipaswa kufanya hivyo ili kuweza kuwadanganya wazazi wake waelewe kuwa alilala nyumbani na asubuhi ile ndio ametoka.

Lakini akajiuliza kama Esmile atamuelewa siku wakikutana na akiamua kumueleza kuwa alichomoka kwenda kwao ili kuweka mambo sawa huku akilinda muda na aliwahi kufika kabla ya muda waliokubaliana, huo ndio ulikuwa ni wasiwasi wake.

Akapata wazo na kuishika tena ile bahasha kwa pupa huku akiitoa kadi ile kwa haraka al manusra aichane. Akaitoa na kuigeuza kila sehemu, aliipindua pindua mbele na nyuma, akiigeuza geuza juu na chini hakuacha kuiangalia ndani na nje, aliporidhika kuwa kile akitafutacho hakipo, akaitupa chini kwa hasira.

Akakumbuka kuwa bado hajaitazama bahasha, nayo akafanya hivyo hivyo, lakini pia hakufanikiwa, akaikusanya ile bahasha na kuikunja kunja na kuitupia kwenye dust bin na kujiachia kitandani akitazama angani ilipo feni.

Jaribio alilokuwa akilifanya ni kuangalia kama kwenye kadi ile na pia kwenye bahasha, anaweza kupata namba ya simu ya Esmile kama atakuwa ameandika, lakini wala haikuwa hivyo, alikwama, hakuwa ameandika chochote zaidi ya ujumbe tu wa mapenzi.

Esmile alipoondoka pale akawa hajui wapi pa kuelekea, akaona ni heri aende Kigogo kumtafuta Mam, akanyoosha hadi Kigogo. Alikatisha na kuingia Mandela Road, kisha Matumbi akaingia kwenye barabara ile ya Tabata Dampo ambayo ilimfikisha moja kwa moja Kigogo Mwisho.

Baada ya kufika Kigogo mwisho ilipo njia panda ya kwenda Mabibo na Kigogo Dampo, yeye mwenyewe akajiona mpumbavu, hakufikiria kabla ya kufanya maamuzi yale ya kwenda kwa kina Mam.

Maana yeye hapajui kwa kina Mam, na sasa ndio akapata muda wa kujiuliza; anakwenda kwa kina Mam, anapajua kwao? Mbona Kigogo ni kubwa sana? Ikiwa ataamua kumtafuta Mam, nyumba kwa nyumba, ataweza kweli? Kuna nyumba ngapi Kigogo nzima? Na akiamua kumuulizia kwa jina, je ile Kigogo ina kina Mam wangapi?

Akashuka garini huku akitikisa kichwa na kusimama pale kwa dakika kadhaa kisha akaondoka. Hakuona mwelekeo sahihi, bali aligeuza na kwenda hadi Kigogo Mbuyuni na kusimama pembeni akifikiri ni kipi afanye kwa muda ule.

Mam nae baada ya kushindwa kujua nini cha kufanya, hasa baada ya kukwama kumpata Esmile, akanyanyuka kitandani na kuelekea bafuni kuoga, kisha akakaa hadi saa nne asubuhi ile baada ya kupata kifungua kinywa ndio akatoka.

Wakati akitoka hotelini akamuita muhudumu na kumuachia maagizo kuwa akitokea tena Yule kijana, amwambie amtafute, haraka iwezekanavyo. Kisha Mam akatoka na kutokomea mbele.

**********

Saa 4 asubuhi, Esmile akamaliza kufungua kinywa pale maeneo ya Mbuyuni aliposimama wakati anatoka Kigogo mwisho na sasa alikuwa akielekea Kariakoo kufanya mambo yake. Na huko pia hakukumchukua muda mrefu, bali alimaliza shughuli zake na kuanza kurejea nyumbani akiwa peke yake garini.

Alipofika Aroma akashuka na kuingia tena hotelini pale Savoy, akaenda kaunta na kuulizia Yule mteja aliekuwa chumba namba Fulani, akaambiwa aliondoka tangu saa nne asubuhi ile.

Bado Esmile hakuamini kauli ya kijana Yule, aliejitambulisha kwa jina la Moody, akamueleza kuwa ye alifika pale saa mbili na kukaa nusu saa nzima bado mtu Yule hakuwepo, iweje tena awe ameondoka saa 4? Moody akatabasamu na kumueleza picha yote ilivyokuwa na jinsi wahudumu walivyoishuhudia.

Alisikitika sana Esmile, lakini haikumsaidia, alichoambulia ni kutabasamu, Moody akamuuliza mbona anatabasamu? Esmile akasema

“Acha tu nitabasamu ndugu yangu, maana kila lililoshindikana haiwezekani kuazimisha na hasa kama mshindi kaisha tangazwa, nimefeli ndugu yangu kwa hili,” Moodyaliuma mdomo wake wa chini huku akitikisa kichwa kukubaliana nae, kisha akamwambia kuwa kuna maagizo aliachiwa Juma na Yule dada. Esmile akatoa macho kwa mshangao.

“Juma ni nani na yupo wapi?” aliuliza Esmile kwa shauku.

“Juma ni muhudumu wa zamu wa wiki hii, na ninafikiri muda huu atakua anawakilisha mahesabu kwa Meneja hapo ghorofa ya kwanza,”

“Naweza kwenda kumuona?”

“Subiri kwanza... hapa tuna utaratibu wetu ndugu, keti hapo sofani unisubiri.” Moody alimjibu Esmile huku yeye akiondoka kuelekea juu kule ghorofani huku akimuacha Esmile akikaa kwa shingo upande.

Baada ya dakika chache akarejea na jamaa wa kisomali aliejitambulisha kama Imraan, meneja wa hoteli ile. Pasina kupoteza muda Esmile akamueleza shida yake, meneja akatikisa kichwa nakumwambia kuwa Juma ameisha ondoka na pale wafanyakazi hufanya kazi wiki mbili na kupumzika wiki 1, lakini Juma aliomba kufanya kazi wiki 4 ili aweze kupumzika wiki mbili.

“Alifanya hivyo kwa ajili ya kilimo, unaweza kurudi hapa baada ya wiki mbili tangu leo,”

Wiki mbili ni nyingi sana ndugu yangu, sidhani kama ninaweza kusubiri,” aliongea Esmile huku akitazama kalenda iliokuwepo pale mezani, Imraan akaongezea

“Hivyo kama hutaweza kusubiri, basi ni heri umtafute nyumbani kwake,” Aliongezea Imraan huku akimtazama Esmile kwa umakini.

“Kwake ni wapi Meneja?”

“Anaishi Pugu, Kigogo Fresh, kama utahitaji mtu wa kukupeleka nitakusaidia, lakini itakulazimu umgharamikie mambo ya usafiri,” aliongea huku akitengeneza miwani yake ndogo iliomfanya aonekane nadhifu sana na kuiteka vizuri nafasi yake ya Umeneja kwenye hoteli ile.

“Nitashukuru sana meneja, kwani tayari hapo nje nina usafiri,”

“Ooh! Safi sana, ila hakikisha anarudi kabla ya saa 11 jioni, kwani muda huo ni muda mzuri kwa kazi zetu hapa na ndio muda muafaka wa kupangiana majukumu kwa ajili ya kazi zetu za jioni,”

“Sawa, hakuna shida Boss!” akamjibu huku akitabasamu na kumpa mkono, moyoni akiwa na faraja kubwa akiamini huu ni mwanzo wa kumpata Mam.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Moody akapewa ruhusa ya kumpeleka Esmile nyumbani kwa Juma, akaingia vyumba vya kubadilishia nguo na kubadili sare za ofisi yake na kutoka ili kuanza safari kuelekea Pugu, maeneo ya Kigogo fresh.

waliwasili kule saa saba mchana. Nyumbani kwa Juma hawakumkuta mtu yeyote, walipoulizia kwa majirani wakaambiwa huenda wamepishana punde tu hapo barabarani kwani amewaaga muda usio mrefu kuwa anaenda shamba.

Moody akauliza huko shamba Juma hurejea saa ngapi? Mtu aliekuwa akiwajibu akawakatisha tama kabisa kwa kuwajibu kwamba Juma ameahidi atarejea baada ya wiki mbili. Wakatazamana Esmile na Moody kwa mshangao.

Esmile akawauliza kama wanapajua huko shamba, wanakijiji wakakataa kuwa hawapajui na hapo akachoka kabisa. Wakawaaga wanakijiji na kurejea hotelini Savoy, Esmile akiwa na mawazo kedekede, kiasi ambacho hata alipofika Savoy hakuteremka, bali alimuacha Moody na kumuahidi atarudi baada ya hizo wiki mbili.

Hazikua nyingi sana, lakini kwa Esmile ilikua ni kama karne nzima, taratibu siku zilisogea nakuisha 14, alifika Savoy hotel na kumuulizia Juma, akambiwa bado hajafika na huwa si kawaida yake kuchelewa vile, huenda kuna jambo. Akachoka na kushusha pumzi akiahidi atarudi jioni ya siku ileile.

Moja kwa moja baada yakuingia garini akawasha na gari nakuongoza hadi Pugu nyumbani kwa Juma, bahati ilikua mbaya kwake, kwani Juma hakumkuta tena ila alimkuta mkewe tu akiwa anafanya kazi zake.

Alipokelewa vizuri na kueleza shida yake, mke wa Juma alimwambia Juma ameenda mjini na ameahidi hatochelewa kwani leo ni cku yake ya kuingia kazini, hivyo kawafuatia matumizi kisha awahi kuingia kazini kwake.

“Na kwa kuwa amekwenda na kijana wetu, ninaamini hatochelewa kurudi, hadi kufika saa za mchana atakuwa hapa.”

Kutokana na shauku aliyokuwa nayo, akalazimika tu kumsubiri. Alikaa hadi kufika saa 12 jioni Juma hakuonekana, ikambidi Esmile aage akiahidi kuwa ipo siku atarudi iwapo hatompata Juma. Akakaribishwa tena. Kama mtu aliejisahau vile, alisahau kabisa kuomba namba ya simu ya Juma.

Wakati akiwa naingia garini tu, kijana alietoka na Juma, yaani mtoto wa Juma, akawa anaingia pale nyumbani akiwa na mzigo, lakini hakuwa ameongozana na mtu yeyote ila alikuwa peke yake.

Japo Esmile hakumjua lakini kutokana na maelezo aliyokuwa amepewa hapo awali, aliweza kuhisi kuwa Yule ndio atakuwa alitoka na baba yake na sasa amerejea. Alitaka kufunga mlango, maana alikuwa tayari yupo ndani ya gari, lakini akasita na kusubiri apate uhakika.





Mama Esmile alijua kauli ile itamfurahisha mwanae, kumbe wala ila akajibu kifupi tu sawa mama, kisha akavuta mto na kulala. Mama akamuuliza ana tatizo gani? Nae akang’ang’ania jibu lake lile lile kuwa hana tatizo lolote. Mama akatoka nje hadi kwa Mzee Hanson.

“Baba Esmile, mwanao leo ana tatizo gani?” Mzee Hanson ambaye mbali na majukumu yake mengi alikuwa mpenzi sana wa michezo, alikuwa akisoma gazeti la michezo la Bingwa ili kupata habari mbalimbali alishangaa na kutoa miwani iliyokuwa machoni na kuuliza kwa mshangao.

“Ha! Sasa mi nitajuaje tatizo alilonalo na hali mimi nae tuliachana tangu saa tatu asubuhi? Wewe si ndio umetoka huko ndani, amekuambia nini?”

“Mi ameniambia hana tatizo lolote ila namuona hayuko katika hali yake ya kawaida na wala hana furaha, sijui ana nini leo mwanangu?” alisema mama Esmile kwa majonzi.

“Hebu nenda kamuite, sasa hivi,” mama akaondoka kumfuata mwanae, akiamini mbele ya baba yake huenda akasema ni kipi kinachomsumbua.

Haikuchukua muda Esmile akawa amefika na mama yake, hata Mzee Hanson alipomuona akagundua kuwa mwanae ana tatizo kwani hayupo katika hali yake ya kawaida. Akamuuliza kulikoni? Jibu halikubadilika, likabaki kuwa ni lile la kuwa yeye yupo sawa sawa

Mzee akahoji tena kama ana tatizo la kuhofu juu ya nafasi ya kazi ambayo ametoka kufanya Interview, akajibiwa kuwa walaa, hana wasiwasi wowote wa kazi na pia hana tatizo lolote.

Mzee akakunja gazeti na kumtazama mkewe kisha akarudisha macho kwa mwanae na kumjulisha kuwa tangu sasa yeye ni muajiriwa, kauli hii walitegemea ingempa furaha Esmile, lakini haikuwa hivyo hali yake iliendela kuwa ileile ya mawazo yake yalikuwa mbali na kile kilichokuwa kinazungumzwa…

Esmile huku akitazamwa na wazazi wake wote wawili, akajibu;

“Nashukuru baba, tayari mama ameniambia..,” akanyamaza kidogo kasha akaendelea

“…mi naenda hapo kucheza pool kwa jamaa zangu, tutaonana baadae,” aliongea akiwa hamaanishi kile asemacho, bali alikuwa anataka tu aondoe kero, ambazo aliona kutokana na maswali toka kwa wazazi wake, maswali yao yalionekana kama ni kero kwake.

Wazazi wakabaki wamepigwa na butwaa, mama alikua amesimama, akakaa na mzee akapumua kwa nguvu na kuegamia sofa huku akitupia gazeti mezani, Esmile akapotelea nje, huyu Esmile ilikuwa ndio furaha yao, bila huyu walikuwa si lolote.

Waliamini pindi ikiwa Esmile akiwa hana furaha, basi hata wao pia watakuwa hawana furaha pia, kwani ndio alikuwa ni motto wao wa pekee.

Baada ya kutoka nje, Esmile hakujua aelekee wapi, lakini baada ya kufikiria kidogo, akaona ni heri aende Baracuda Club akapoteze muda kwa kucheza Pool na marafiki zake kama alivyosema. Alipofika pale mapigo yake ya moyo yakapiga kwa nguvu sana baada ya kumuona mtu ambae wala hakumtegemea, na tena wala kichwani mwake hakuwepo kwa muda ule.

Aliamini mtu huyo angeweza kumsaidia juu ya kumpata Mam, hakuwa mwingine bali ni Alfred! Ndio… ni Alfred Mpemba, mtu ambae alikuwa ni wa mwisho kuonana na Mam siku ya kwanza kwa Esmile kumuona.

Swali likaja atamuanzaje kuzungumza nae juu ya jambo hilo na hali hana mazoea nae ya aina yoyote? Lakini kutokana na kuwa na shauku ya kutaka kumuona Mam, akamsogelea Alfred aliyekuwa amechangamka kutokana na kupata bia kadhaa akamsalimu na kumuomba watete faragha.

Alfred hakubisha, maana hakuwa akimjua Esmile na hivyo alishindwa kutabiri shida yake, wakaenda faragha, alijitambulisha anapotoka nakuanzisha mazungumzo kwa kudanganya kuwa kuna msichana aitwa Maryam, anadai ni mchumba wake, je anamfahamu? Alfred akamtazama kwa jicho la kuuliza na akasonya kisha akamwambia;

“Mdogo wangu, mi nilijua unakuja kunipa dili la pesa, kumbe unanipa dili ya maneno, tena kuhusu yule Malaya... Mpss, achana nae,” Alfred akarudi mezani kwake akaendelea kukata kinywaji akimuacha Alfred akiwa amesimama na kutazama kulia na kushoto kama kuna mtu jirani yake amesikia jibu alilopewa na Alfred.

Alivyoona hakuna mtu, akapiga hatua na kuanza kumfuata huku akimbembeleza waendelee kuongea lakini Alfred alionesha kuwa hakuwa tayari kwa hilo. Hivyo jitihada zote za Esmile kumbembeleza Alfred waendelee kuzungumza, ziligonga mwamba, kifupi hazikuzaa matunda zaidi ya Alfred kutoa maneno ya kifedhuli na kupayuka mambo ya kuudhi kuhusu Mam na tena yanakatisha tamaa.

Pamoja na hayo, Esmile hakukata tamaa, bali aliamini ni pombe tu ndio zilizomvuruga na kusababisha Alfred kuwa vile, aliamini chochote kinachosemwa na kukuvunja moyo, hakipaswi kuwa ni sababu ya kukata tamaa.

Akarudi kwenye pool na kucheza gemu kadhaa ambazo zaidi ya nusu ya michezo aliyocheza alipoteza, yeye hakujishangaa bali waliocheza nae ndio walishangaa, lakini walijua kwamba siku zote huwa haziendi sawa. Alipofungwa mchezo wa mwisho, akaweka fimbo chini na kuaga.

Akarejea kwao akiwa ameweka ahadi kuwa kesho asubuhi atamtafuta Alfred akiwa hajalewa ili waweze kuongea vizuri kwani bado aliamini ni pombe tu ndio ilisababisha Alfred amjibu vile na hata kuondoka, lakini akiwa hajapata mambo yetu, anaweza kupata mwanga ambao utampeleka kujua ni wapi anaweza kumpata Mam.

Alipoingia ndani ya nyumba yao aliwakuta bado wazazi wake wamekaa sebuleni wakiwa wakiangalia TV, uwepo wao pale ulimshangaza, lakini hakuwauliza lolote, maana anajua chumbani pia kuna TV iweje leo wakae pale tena yeye akiwa hayupo?

Baada ya salamu yeye akaunganisha hadi dinning room, akakuta chakula mezani lakini kikiwa hakijaguswa, akajua wazazi wake hawajala, palepale akajua sababu ni yeye, hivyo akajitoa kimasomaso na kwenda kuwauliza, nao wakamjibu kuwa walikua wakimsubiri yeye.





Aliwaza kitu, kuna neon aliwahi kulisikia sehemu, likajirudia kichwani mwake, lilisema

“Kama huwezi kumfurahisha mtu, basi jitahidi usimuhuzunishe,” ndio alichokiona kwa muda ule. Ameshindwa kuwafurahisha, lakini pia amewahuzunisha, tayari amepishana na kauli ile, moyo ukamsuta, tayari alikuwa amevuta kiti chake, ila hajakaa.

Kwa huzuni, maana alikuwa akijua ni kiasi gani wazazi wake wanampenda, akawafuata na kuwakaribisha mezani na kuwaambia kuwa yeye tayari amerejea, wote wakanyanyuka na kuelekea mezani, Alifika na kuwavutia viti kwa mapenzi makubwa.

Walikula kwa amani tele tena Esmile alikula zaidi ili kuwaondoa hofu wazazi wake ambao walikuwa wakila kutokana na kasi ya Esmile, mara kwa mara alinyanyua hiki na kuwaongeza wazazi wake, mara aliwamenyea ndizi ama kuwajazia maji kwenye glasi.

Waliridhika sana wazazi wake na hivyo usiku ule aliwarejeshea furaha yao ambayo alitoweka nayo tangu jioni na kuwaacha kwenye hali ngumu wakiwa hawajielewi elewi.

Walipomaliza kula Mzee Hanson akamuuliza mwanae kama tatizo alilokuwa nalo limekwisha, Esmile akatabasamu na kujibu ndio baba. Kiuhalisia tatizo lilikuwa halijaisha, bali alitaka awape amani zaidi ya nafsi wazazi wake, walale kwa amani.

Kila mmoja akanawa, Esmile akaelekea chumbani kwake na wazee wake nao wakaenda chumbani kwao, akiwa yeye Esmile ndio mtu wa mwisho kuingia chumbani kwake kulala, alizunguka nyumba nzima kuhakikisha ila kitu kipo salama na mahali pake, ndio akazama chumbani kwake. Siku ile ya Ijumaa ikawa imefungwa rasmi.

Esmile aliamka akiwa na wazo moja tu siku iliyofuata, siku hiyo ilikuwa ni siku ya Jumamosi, wazo ambalo lilikuwa ni kumtafuta Alfred popote pale tena asubuhi ileile kabla hajaenda kufanya mambo yake, maana alikuwa ni Mpenzi sana wa pombe kali.

Baada ya kufungua kinywa alitoka kimya kimya kama yupo vile hadi kijiweni kwao na kuwaulizia jamaa zake ni wapi anaishi Alfred. Jamaa wakamuelekeza na akanyoosha moja kwa moja hadi nyumbani kwa Alfred, bahati ilikuwa yake, walikutana mlangoni, Alfred alikuwa akitoka, hata hivyo akamkaribisha ndani kwa bashasha tele.

Kitendo cha kukaa tu chini, Esmile akaanza uongo wake kwa kumuomba kwanza msamaha Alfred kwa kumvamia asubuhi na mapema vile na kilichomleta kwake ni kuhusu Mam. Alfred alikua makini sana akimsikiliza.

Hawakuwa wakifahamiana kiundani sana, lakini akalazimika kujitambulisha kwa kumwambia kuwa yeye ni dereva wa bodaboda, alikodiwa na Mam akampeleka sehemu, sasa walipofika kule wakapoteana na wakati huo kulikuwa na bahasha aliyokuwa amempa amshikie.

Kwa kuwa hakumuona tena tangu walipopotezana, akakumbuka kuwa alimwambia ametoka kwa Alfred ndio sababu ameamua kumtafuta ili amsaidie jinsi ya kumpata. Alfred alikaa vizuri na kusema kuwa ni kweli siku hiyo anayoisema Mam alikuwa ametoka kwake na kabla ya kuondoka walikuwa wamegombana sana na hadi kufikia hatua ya kutukanana.

Mwishoni akamwambia Esmile ikambidi amnyang’anye simu (hapo akamuonyesha simu iliyokuwa mezani) na kumueleza sehemu ya kumpata Mam, sehemu yenyewe haikuwa pengine bali ni Zanaki.

Esmile akamueleza hali halisi tangu yeye kwenda kule na alivyomkosa. Alfred akaguna na kusema hana jinsi nyingine ya kumsaidia, maana simu ndio ilikuwa ni kiungo pekee cha kuwakutanisha, na sasa anayo yeye.

“Unajua Mam alikua akinipenda sana, daima nilikuwa nikimringia kwenda kwao, hivyo mara zote nilikuwa nampigia simu na kukutana naye shuleni kwao, ama wakati mwingine nikimuita yeye aje hapa nyumbani kama siku hiyo ambayo unayo izungumzia wewe, sasa kibaya zaidi simu yenyewe ambayo ilikuwa ikitumika kumuita, ndio hiyo mezani,” wote wakaitazama tena.

Esmile ndio aliitazama kwa uchungu, akitamani hata Alfred angechukua simu tu na kumuachia chip huenda huko alipo Mam angepata simu nyingine na kurudi hewani, sasa angekuwa akihangaikia namba tu.

Hata hivyo akamuomba namba tu ili ajaribu huenda itakuwa aliisajili upya huko alipo.

“Oh! Mdogo wangu, namba hii siku ileile nilimzuia kabisa kuitumia, maana ni yangu, niliisajili kwa jina langu, hivyo nikamzuia kuitumia tena kwa kuogopa matumizi mabaya ya Mtandao, anaweza kuitumia hovyo nikatafutwa mimi ambae ndio Mtandao unatambua kuwa ni yangu,” jibu lile lilimkata maini kabisa.

Sasa ndio akajua anamkosa Mam, kwa mara nyingine akatamani kulia, Alfred akaliona hilo na kumuhurumia, lakini sasa angefanyaje? Hata nae hakuwa na jinsi, ukweli wote ameisha mueleza bila kuficha hata chembe ya ukweli. Akatazama saa yake ya mkononi, Esmile akagundua kuwa Alfred anataka kutoka, muda unapotea bure

Kutokana na mabadiliko aliyoyaona kwa Esmile, Alfred akamuuliza kizushi;

“Bro ina maana ni muhimu sana kuonana na Mam?” Hakujibu moja kwa moja Esmile, bali alizunguka ili kumjenga Alfred aelewe umuhimu wa kuonana na Mam, akamjibu

“Alfred kwenye ile bahasha kuna document nyingi na za muhimu zinapaswa Jumatatu niwe nazo kazini, ndio sababu namtafuta kwa nguvu zote mkuu, hasa ukizingatia ukiachana na leo, ninabaki na siku ya kesho tu ambayo ni jumapili.” alidanganya Esmile na kumfanya Alfred afikiri kwa muda.

Kama mtu aliekumbuka kitu vile, Alfred akasema huku akinyanyuka pale alipokuwa amekaa

“Sasa Esmile labda kwa kukusaidia, hapa nina namba ya rafiki yake anaitwa Rahel walikuwa wakisoma pamoja…” akazamisha mkono mfukoni na kutoka na simu, kisha akapiga namba fulani na kuweka sikioni.

“Kwa sasa hata nayo haipatikani labda nikupe namba hizi ili baadae nawe ujaribu kumtafuta huenda ukapata msaada kwa huyu,” ilikuwa karibu Esmile ampigie magoti Alfred kwa kumshukuru, haraka akakopi namba zile kwenye simu yake na kuahidi kumpigia Rahel baadae.

Kama mtu ambae alikuwa haamini kinachotokea, Esmile alimshukuru sana Alfred na kumuaga, sasa alikuwa na tabasamu zito usoni, wakatoka wakiongozana.

Esmile alirudi nyumbani akipiga mluzi, alikuwa na uhakika wa kumpata Mam sasa, akaelekea moja kwa moja hadi chumbani kwake ili kuchukua nguo zake chafu akazifue. Alifanya kazi zake akama alivyojipanga huku mawazo yake yote yakiwa kwenye simu.

Baada ya saa moja akajaribu tena, bado ikawa haipatikani, akajipa moyo huenda akawa amelala, maana ni jana tu ndio wamemaliza mitihani na leo ni wikiend.

“Itakuwa ameamua kujipumzisha kwa kituo leo, maana masomo ni zaidi ya kazi, siku moja ya mapumziko, hulipia wiki mzima ya mihangaiko, hata Mam nae atakuwa ame relax muda huu,” akili ya Esmile haikuwa na kingine cha kuwaza zaidi ya Mam pekee.

Alifanya kazi hadi wakati wa chakula cha mchana, akapiga tena, ikawa haipatikani, bado alijipa moyo tu kuwa ule ni mtihani na lazima ashinde yeye, alijua dhahiri shahiri kuwa hapaswi kukata tama.

Mchana Esmile huwa na kawaida ya kulala pindi anapokuwa hana kazi ya kufanya, ila leo alipanga asilale na kuuona usingizi kama ni mpinzani wake mkuu kwa mchana ule kwa kuwa alitaka kila muda awe anajaribu namba ya Rahel, lakini uzalendo ukamshinda, ikabidi ashangilie timu ya wapinzani baada ya timu yake kuzidiwa.

Usingizi ulipomzidia, sasa akazima simu na kuchapa usingizi wa mchana katika kujifariji. Kwani safari hii aliamini lazima Mam atapatikana tu, huyu aliamini ndio ‘La mujer di mi Vida’ yaani ‘Mwanamke wa maisha yangu.’ Hivyo ndivyo alivyo amini yeye ndani ya kichwa chake.

Aliamka saa 11 jioni baada ya kuwasha simu, namba ya kwanza kupiga ilikuwa ni ya Rahel, bado ikawa haipo hewani, akapata hofu kwamba labda kapewa namba ya tiketi? Lakini akaamini Alfred hawezi kumfanyia vile, kwani ana ubaya nae gani!

Ndio akaamua kutuma ujumbe mfupi, ili wakati wowote utakapo pokelewa, yeye atapata kujua kupitia delivery report kwenye simu yake.

Wazo lile likapita bila kupingwa katika halmashauri ya kichwa chake, akafanya hivyo na kunyanyuka kwenda kuoga. Alipomaliza mishemishe za kujiswafi, akatoka akiwa kwa miguu hadi Savoy kuwatembelea wahudumu wa pale ambao kwa sasa wamekuwa ni jamaa zake. Alimuona Juma, Imraan na hata Moody. Wote wakataka kujua kama amfanikiwa kumuona Mam, akawajibu bado ila anategemea kumuona kuanzia kesho iwapo mtu mmoja anae wasiliana nae kama atamuelekeza ama atampa namba yake.

Akaachana nao na kukaa mezani akiwa na jamaa aliokutana nao palepale hotelini na kuanza makamuzi hadi saa nne usiku huku wakiangalia mieleka iliyokuwa ikionyeshwa kwenye TV kubwa iliokuwa pale ukumbini.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Alikuwa ni Mpenzi mkubwa wa mieleka nae akiwa ni mshabiki wa Undertaker, ambae usiku huo kulikuwa na pambano kati ya Undertaker na Randy Orton, mwisho wa pambano hilo ambalo Undertaker alishinda, ndio muda ambao Esmile alishtuka.

Muda huo alipokumbuka kutoa simu mfukoni na kuiangalia, alishtuka alipokuta delivery report na miss call kadhaa. Zote wala hazikumsumbua ila moja tu… hiyo ndio ikamfanya ajilaumu kwa kutoitazama simu yake kwa muda wote aliokuwa kwenye luninga akitazama mieleka.

Ule muda ambao Esmile alikuwa ameshtuka na kutazama simu akakuta kuwa sms yake ilipokelewa tangu saa mbili na saa moja baadae alipigiwa na hakupokea, alisikitika na kuanza kupiga yeye, bahati mbaya simu ikawa haina salio na akanyanyuka kwenda kununua

‘Simu yako haipokelewi..’ hilo ndio lilikuwa ni jibu katika simu ya Rahel, hapo Esmile akiwa amejaribu zaidi ya mara 5 na jibu lilibaki kuwa ni hilohilo. Akakata tamaa kwa kuhisi huenda atakuwa amelala, akarejesha simu mfukoni na kudandia daladala iliyomrejesha kwao.

Muda wote Esmile aliokuwa akimtafuta Rahel kumbe alikuwa kwenye basi akielekea kwao Tunduma walipo wazazi wake, charge ilipungua kwenye simu yake ila akawa ameamua kupunguza matumizi kwa kuizima ili kuitunza kiasi.

Aliwasili Tunduma saa mbili usiku na kuwasha simu, ikaingia msg iliosomeka

‘hi Rahel, mambo vipi mrembo? Mi naitwa Esmile ni rafiki wa Mam, nina shida nawe, nimekupigia sana simu sijakupata, naomba upatapo sms hii unibp, jioni njema dada yangu’

Baada ya kusoma sms ile akewapigia simu wazazi wake na kuwataarifu kuwa amewasili, ila kabla hajam beep Esmile simu ikawa imezima kwa ajili ya charge, hivyo akaamua atampigia simu baadae atakapokuwa nyumbani baada ya simu yake kujaa charge.

Alipofika nyumbani akaiweka simu kwenye charge hadi saa tatu usiku, ndio alipokwenda kuiwasha na kumtafuta Esmile ambae alikuwa hapokei simu, nae kwa ajili ya mchoko wa safari, akaizima simu yake ili apumzike kwa starehe.

Asubuhi Rahel alikuta Miss call nyingi, na akaanza kuzibp, bahati mzuri alipokuwa akiibp namba ya Esmile, nae alikuwa na simu mkononi, lengo likiwa ni kumpigia mtu huyohuyo. Aliacha ikaita hadi ilipokata ndio akapiga yeye.

Hakutaka kutumia hata senti moja ya pesa za salio la Rahel, akiamini yeye ndio mwenye shida, vipi amtie hasara mtu ambae anahitaji msaada mkubwa zaidi kutoka kwake? Hiyo ndio ilikuwa furmula yake. Akiwa nashida atapiga yeye ila ukiwa na shida ukipiga anapokea.

Sasa ndio akapiga yeye na iliita kama mara tatu tu, kasha ikapokelewa. Hakuwa akiijua sauti ya Rahel wala hakumjua huyo Rahel mwenyewe yupo vipi.

“Hellow” ilisikika sauti ya kike haswaa

“Mh, mambo?”

“Safi, nani mwenzangu?”

“Mimi ni Esmile, nafikiri naongea na Rahel?”

“Ndio, mbona sikufahamu?”

“Natambua hilo!”

“Ok! Sijui nikusaidie nini?” sasa Esmile akamwambia shida yake ya kuonana na Mam ambae kwenye simu hapatikani. Rahel alipotaka kujua namba yake ameitoa wapi, Esmile akaendeleza picha lake la uongo alilolianzisha kwa Alfred...

…Kila anapopiga hatua moja mbele, anajikuta amezunguka na kurudi kule alikotoka na tena ikiwa ni nyuma kidogo, sasa hii tena ni sehemu pweke anayoitegemea, je atafanikiwa kumpata Mam? Mam mwenyewe yupo wapi kwa sasa? Hellow…





Akadanganya kwa ufundi kabisa ila akamuingia kwa njia ya swali…

“Unakumbuka ugomvi kati ya Mam na Alfred?” Rahela akaitika ndio na kumpa nafasi Esmile aendelee kumwaga sukari.

“Siku ile aliogombana na Alfred na kumnyang’anya simu, siku ya pili ndio nilikutana nae na kunipa namba yako hii akisema wewe ndio mtu wake wa karibu na nikitaka mawasiliano nae nipitie kwako,” kwa kauli ile Rahel akaridhia na kuamini kwa 100% kuwa namba Esmile alipewa na Mam.

“Anhaa! Nimkupata Esmile, kama unavyojua kwa sasa Mam hana simu nami sipo Dar kwa sasa, nipo safarini, nimekwenda nyumbani Tunduma”

“He! Rahel..” Esmile alishangaa na kubaki kimya kwa muda

“Yes Esmile, mbona umeshituka namna hiyo?

“Usijali Rahel, sasa nitawezaje kumuona?”

“Hata mimi sijui Mr!” Rahel alikuwa ni chakaramu sana na alipenda sana kuchanganya lugha.

“Je unaweza kunielekeza kwao?”

“ Hapana siwezi, katu sitajaribu kukulekeza kwao bila ridhaa yake, yaliwahi kutokea makubwa, alipigwa na baba yake hadi akachungulia kaburi, sasa kwa hali hiyo ndugu, I’m sorry, mi siwezi kukuelekeza, Never!”

“Ah! Rahel, nisaidie dada yangu, nina shida muhimu”

“No bro, I can’t do that”

“Lakini mbona yeye alinipa namba yako bila wewe kumruhusu?” aliuliza Esmile kwa ghadhabu.

“Ni kwa sababu alijua kuwa kwangu mie haina tatizo, naweza kupokea simu yoyote na wakati wowote bila kujali nipo wapi na nani, tofauti na yeye, maana hata wazazi wake hawakuwahi kujua kama anamiliki simu,” nae alijibu kwa nyodo kabisa.

“Basi nipe namba ya mtu yeyote wa karibu yake ili nimpigie niweze kuwasiliana nae”

“Ningeweza kukupa namba yake kama angeruhusu kwa ridhaa yake, na kama pi angekuwa Dar,” alizungumza Rahel kitu kipya kabisa ambacho ikawa ni mshtuko kwa Esmile.

“Rahel unasema angekuwepo wapi?”

“Nasema ni heri angekuwepo Dar walau ningefikiria kukupa,”

“Hebu fafanua vizuri, sasa ungekuwepo Dar Rahel na kutokuwepo kwako wewe kuna uhusiano gani wa kunipa namba ya Mam?” Mawazo yalikuwa mbali, hivyo wala hakuweza kumsikia vizuri, lakini Rahel akamuelewesha

“Kijana naona hunielewi, nazungumzia kama angekuwepo yeye mwenyewe Mam Dar, sio mimi,”

“Ok, una maanisha Mam hayupo Dar?”

“Kwani wewe hujui kuwa Mam nae amesafiri leo?” Esmile akazidi kuchoka na kujibu kwa huzuni.

“Hapana sister, mi sifahamu, sina mawasiliano nae kwa wiki mbili sasa, kama nilivyokueleza hapo awali ndugu yangu, naomba unielewe,” alijitetea Esmile akiamini ile kauli itakuwa na msaada kwake.

“Alright, kifupi Mam kwa sasa hayupo Mzizima, yupo kwa Wagosi nyumbani kwao,”

“Sasa Rahel huoni kuwa hiyo ndio nafasi mzuri zaidi kwa mimi kuongea na Mam kwa kuwa yupo mbali na hao watu unao wahofia?” alichombeza kwa sauti ya kubembeleza hasa.

“Hahika kaka yangu hilo halipo, we tumia njia nyingine ili uweze kuwasiliana nae, lakini kwa hii ya simu huku ukitegemea namba uipate toka kwangu, hahahaaa! Umefeli kijana,”

“Hebu basi nishauri nitumie njia gani?”

“He we vipi? Kwani hii njia uliotumia sasa hivi alikufundisha nani?” aliuliza kwa mshangao.

Baada ya kujifikiria kwa sekunde kadhaa, akapata wazo na kuona huenda lile likaokoa jahazi, ambalo dhahiri lionesha kuzama kutokana na kutota kwa maji, akafungua mdomo na kusema;

“Sawa, nina ombi moja la mwisho kwako!”

“Nakusikiliza,”

“Tafadhali, chondechonde, kwa hili naomba usintose kama ulivyonitosa hilo la namba,”

“Ongea basi, si unajua tayari tumeisha ongea kwa zaidi ya robo saa sasa? Elewa kuwa kuna mambo mengine mengi tu ya kufanya, hatuwezi kuishi kwa kutumia simu tu ama kuongea muda wote.” Tayari alionekana kukerwa Rahel.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Nisamehe bure tu kwa hilo Rahel dada yangu, ni vile tu shida yangu inasababisha haya yote,” sauti ilikuwa ni ya dhati toka moyoni.

“Poa basi mi naenda kupika, c unajua muda wa chakula cha mchana umekaribia?”

“Ni kweli, sasa… mi ninaomba unielekeze nyumbani kwao Mam niende…” hata kabla hajamaliza, Rahel akamkatisha kwa kusema

“Weee Weee Weee? Nani huyo akuelekeze? Wakati mlipokuwa nae pamoja huko wapi Sijui kwanini hakukuelekeza mwenyewe? Leo hii mie ndio niwe na kiherehere cha kukuelekeza kwao? Ushindwe…”

Kauli hiyo ikamfanya Esmile akate tamaa rasmi sasa akaona kabisa huu ndio wakati muafaka kwake wa kujivua pendo, akasema kwa majonzi

“Ah! Masikini ya Mungu mimi Esmile, basi bhana, mi naona hii imepangwa kula kwangu tu dada Rahel, nashukuru sana kwa kuongea nawe,”

“Poa, hakuna ubaya, karibu siku nyingine,”

“Ahsante sana siku yoyote ukiongea nae, mwambie Esmile anakusalimia na kama bado utakuwa na namba yangu, mi ninaomba tu umpe, huenda yeye akanikumbuka na kunitafuta,” aliomba Esmile kwa upole.

“Usikonde bro, siku njema kwako,”

“Nawe pia” huo ndio ukawa mwisho wa Esmile kumtafuta Mam.

Kifupi akakubali matokeo, japo alitambua itamchukua muda mrefu na pia itamgharimu hata afya yake, maana alitoka kumpenda Mam kwa dhati kabisa, toka chini kabisa ya uvungu wa moyo wake, lakini sasa angefanyaje na mtu ndio hampati kwa kila njia anayotumia?

Alikata simu na kuendelea kuishika akiwa anatazama mbele lakini akiwa haoni chochote, macho yalitazama mbele, lakini akili iliangalia nyuma, hivyo hakuna ambacho kiliweza kuonekana kwenye taswira ya Esmile, kwani moyo nao ulikuwa mbali masikini ya Mungu…

Nafsi ilizungumza peke yake kwamba, ikitokea umeshindwa kufikiria chochote, basi tambua utakuwa umegeuka sanamu na utashindwa kupiga hatua yoyote, nafikiri napaswa kuliweka hili suala kando kwa sasa nikafikiria mambo mengine.

**********



Kawaida unaweza kusimamisha kitu chochote kinachokwenda, hata upepo ukiamua kuuzuia unaweza, maana utajenga ukuta mnene. Lakini kitu kimoja tu hata ufanyeje, huwezi kukizuia, MUDA…

Naam muda hauzuiliki. Tayari Esmile ana miaka miwili kazini akiwa kwenye nafasi mzuri lakini kuna ndoto zake hazijatimia. Ndoto mbili ambazo zilipaswa kutimia.

Ndoto ya utotoni, ndoto ya kuwa mwanasheria maarufu na pia mpelelezi wa kujitegemea. Pia na miaka kadhaa iliopita alikuwa na ndoto nyingine, ndoto ambayo yenyewe tayari aliisha ifuta baada ya kuona haiwezi kutimia, ndoto ya kumpata Mam, maana aliisha mtafuta kwa kelele na hata kimya kimya na hakufanikiwa kumpata, hivyo alimsahau.

Kukosekana kwa Mam katika moyo wake, kulimfanya Esmile asijihusishe sana na mapenzi wazazi wake sasa walitamani sana kuona harusi ya mtoto wao wa pekee ikifanyika wakiwa hai. Akaona sasa ndio wakati muafaka wa kuanza kuitekeleza njozi yake.

Jioni ya siku moja wakamuita na kuzungumza nae juu ya suala hilo. Aliwajibu kuwa hayupo tayari juu ya suala lile kwa muda ule. Walivyombana akasema hajapata mchumba na pia ana mpango wa kujiendeleza na masomo ya sheria kwa miaka miwili mbele.

Mama yake akamwambia katika suala la mchumba, tayari wamemtafutia, je anasemaje? Alikataa katakata na kudai ni mapema, nao hawakutaka kumlazimisha, wakamuacha, japo walitamani iwe vile watakavyo wao.

Aliponyanyuka , baba yake alimuita na kumuuliza huku akipokea kitu toka kwa mama yake Esmile;

“Hii pete unaitambua?’’ Esmile aliipokea na kuitazama kisha akaikana. Wazazi wake wakatazamana, kisha mama akasema;

“ Esmile, huenda ukawa umeisahau, ni zaidi ya miaka miwili sasa tangu nilipoitoa kwenye suruali yako wakati nafua...” Hakumaliza, Esmile akaisogela kwa kasi na kuichukua, kisha akaitazama kwa umakini na kusikitika…

Wakamuuliza vipi? Kwanza akawakumbusha kuhusu siku ile ya interview jinsi alivyokuwa mnyonge, wakakumbuka kisha ndio akawasimulia kwa ufupi tu kuhusu pete ile pasina kuwatajia jina kamili la yule binti ila alitumia jina la Mam.

Walimpa pole na kumuuliza kama aliisha muona tena ama lah! Akatikisa kichwa na kuwaambia licha ya kumuona, hata kumsikia hajamsikia tena tangu siku ile waliyopotezana.

Jinsi alivyo waambia walivyopotezana pale Savoy, hata wao walishikwa na butwaa, mama akamuuliza kwanini siku ile asimlete pale nyumbani akalala na kasha asubuhi angeondoka? Esmile akakosa jibu na kutikisa kichwa tu kwa masikitiko.

Walisikitika nao na kumpa pole huku wakimwambia lile halikuwa chaguo la Mungu, atulie na ipo siku atampata yule ambae Mola amempangia. Alishukuru na kuelekea chumbani kwake na kulala kitandani kwake akiwa na pete ile mkononi akiitazama hadi akapitiwa na usingizi.

Lakini kabla ya kulala alipitia vipindi vizito kidogo akivuta kumbukumbu ya yale yaliyopita kwa Mam, mwanamke alimuona mara moja tu na kumpenda kasha wakapotezana na hawajaonana tena mpaka sasa.

Siku zilisonga na hakuna kilichosimama, kila kitu kilikwenda mbele kwa hiari ama kwa lazima, Esmile alizidi kujituma kazini hadi akawa ni mfanyakazi bora wa mwaka kwa miaka yote miwili mfululizo, kitu kilichosababisha azidi kujituma kuliko awali na hivyo kujikuta akiongeza marafiki pale kazini.

Ijumaa moja saa 12 jioni jijini Dar Es Salaam, kituo cha daladala cha Karume, akisubiri gari ya kuelekea Mnazi mmoja, Mam nae alikuwa pale akisubiri usafiri wa kuelekea Posta kwa shida zake binafsi. Hakuna aliemuona mwenzie hadi pale ilipofika gari na watu kuanza kuigombea. Esmile hakuenda kugombea kitendo kile kilimpa nafasi ya kumuona msichana mmoja mrembo wa haja, ambae nae alisimama tu pembeni akionesha nia ya kutogombea gari hiyo.

Hakumtambua moja kwa moja bali alihisi kumjua, lakini kila alivyozidi kumtazama, mapigo yake ya moyo yalimwenda kasi sana, akaamua ni heri amfuate na kumuuliza kuliko kubaki na maswali ilhali mtu wa kuyajibu yupo.., akamsogelea kiustaarabu.







Usoni Esmile alikuwa amevaa miwani ndogo nyeupe, kabla hajafika wala kuongea nae lolote, ikafika daladala ya Kigogo Posta.

Mam akakurupuka na kuingia garini, wakati wengine wakiendelea kugombania, Esmile naye hakulaza damu akaingia ndani ya gari ileile, hakushuka Mnazi mmoja, ikamlazimu kushuka kituo ambacho atashuka yule msichana.

Walipofika Posta, Mam akashuka na Esmile nae akaachia siti kwani hakuwa na safari ya huku ila ilisababishwa na mrembo yule anae shuka hapo.

Akamsogelea na kumsalimia huku akivua miwani na kumtazama machoni, msichana Yule nae akamtazama usoni, na kushangaa huku akitabasamu na kumsogelea Esmile huku akionesha nia ya kumkumbatiahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

‘‘Haa Esmile, mambo vipi mwokozi wangu? Jamanii…’ wakakumbatiana kwa furaha tele na sura zao zikiwa ni zenye bashasha, waliulizana habari za masiku tele yaliyopita, wakakumbushiana tukio lile la Savoy, kisha kila mmoja akamueleza mwenzie jinsi ilivyokuwa, wakabakia kucheka tu.

Wakiwa ni wenye furaha tele, simu ya Esmile ikaita na akaongea na mtu wa upande wa pili na kumuahidi kuwa atafika baada ya nusu saa. Muda wote huo walikuwa wakitembea taratibu, kutoka maeneo ya Posta, wakielekea maeneo ya Kivukoni lakin Esmile akiwa hajui wanaelekea wapi.

Akiwa ni mwenye tabasamu alimueleza Mam ni jinsi gani amefurahi kumuona tena baada ya miaka miwili ya kupotezana.

Vivyo hivyo Mam na alimwambia ye ndio haamini kabisa kama kweli wamekutana tena, maana aliisha kata tamaa ya kumuona na akatoa shukrani nyingi sana za dhati kwa kumuokoa na kifo, kisha akamwambia tayari yeye amefika alipokuwa akielekea.

Sasa wakasimama ili kuagana, Esmile akamuomba wapige Selfie, bila kujali wingi wa watu waliopo eneo lile, Mam akatoa ushirikiano wa kutosha na hatimae wakaagana huku kila mmoja akamuahidi kumtafuta mwenzie.







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog