Search This Blog

Tuesday 1 November 2022

KICHAA WA MTAA - 3

 






Simulizi : Kichaa Wa Mtaa
Sehemu Ya Tatu (3)


 Suzani alikumbuka kuwa aliwahi kukutana naye siku ile Nyogoso alipogongwa na gari. Alienda mbali zaidi kukumbuka kuwa ilipotokea ajari hiyo, mabinti zao kila mmoja alionekana kustuka kuashiria kuwa Suzani na Mazoea wanamfahamu vema Nyogoso. Alipokwisha kukumbuka hayo alimsogelea ili kumsalimu lakini pia akitaka kujua anafahamiana vipi na mgonjwa wake.

"Dada habari yako?..", mama Mazoea alimsalimu mama Suzani.

"Aahh salama kidogo tu dada yangu,vipi wewe habari za tangu siku ile?..", alijibu mama Suzani, naye akionekana kumkumbuka mama Mazoea.

"Salama pia, kulikoni umekuja kumuuguza nani?.."

"Binti yangu, kajichoma kisu kwahiyo amelazwa hapa"

"Ooh Mungu wangu wee! Jamani Kisa?..", kabla mama Suzani hajamsimulia mama Mazoea kisa kilichomfanya mwanaye ajichome kisu, punde ulitangazwa muda wa kwenda kuwaona wagonjwa. Ndipo mama Mazoea na mama Suzani kwa pamoja walielekea wodi aliyolazwa Suzani, wakati yumo ndani ya wodi hiyo alipokea ujumbe mfupi kwenye simu yake. Akausoma kisha akamuaga mama Suzani, na mara moja akielekea kwenye wodi aliyolazwa kichaa Nyogoso. Alipoingia alimtazama kichaa huyo pale kitandani kwa dakika kadhaa, alisikitika sana kisha baadaye akatoka humo wodini ila kabla hajaiacha wodi hiyo dakika kadhaa alikutana uso kwa uso na mama Suzani ambaye alikua akielekea nje kununua maji.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Mgonjwa wako kalazwa humo?..", aliuliza mama Suzani.

"Ndio, njoo umuone japo kwa sekunde tu", alijibu mama Mazoea, haraka sana mama Suzani akaingia ambapo alistuka kumuona kwa mara nyingine tena Nyogoso. Akakumbuka kuwa kijana huyo ndio anayevuruga akili ya binti yake mpaka kufikia hatua ya kumuua kujiua.

"Mmmh! Afadhali nimekuona. Kamwe huna sababu ya kuendelea kuishi,uzima wako utaniharibia binti yangu. Kwa nguvu ya pesa zangu, nitakuuwa la sivyo utaishia jela...",alijisemea maneno hayo ndani ya nafsi yake mama Suzani huku akimkodolea macho kichaa Nyogoso akiwa kitandani hajiwezi





" Lazima nimkomoe ", alisisitiza mama Suzani kisha akatoka nje ya hospital, punde alirudi akiwa na maji uhai akaingia nayo kwenye wodi aliyolazwa binti yake. Hakika mama Suzani alipania kumuuwa Nyogoso, hali hiyo ilimfanya kuwa tofauti pindi alipomuona. Alishusha pumzi kisha akaketi kwenye kitanda alicholalia binti yake, kwa sauti ya chini akasema "Pole sana mwanangu lakini naona hali yako itaimalika siku sinyingi". Maneno hayo aliyaongea akimwambia Suzani.

"Ni kweli mama, namshkuru Mungu naendelea vizuri", alijibu Suzani kwa sauti ya chini wakati huo mama yake akimimina maji grasi ndogo aliyofika nayo hospital kutoka nyumbani. Lakini Suzani alikataa kuyanywa maji hayo akidai kuwa hana hamu ya kula wala kunywa. Na pindi mama yake alipombembeleza alighazibika. Kwa jazba akasema "Mama nimeshakwambia sina hamu ya maji yako wala chakula chako, jaribu kunielewa basi"

"Ila unataka nini?..",

"Namtaka mzoa takataka", alijibu Suzani kwa mkato huku akiwa amekuja uso wake ilihali mkono wa kushoto ukiwa umegusa mahali aliyojichoma kisu. Jibu hilo la Suzani kwa mama yake lilimchukiza sana, alijihisi kuchoka huku hasira za kutaka kumuuwa kichaa Nyogoso nazo zikizidi kuongezeka maradufu. Aliona hatua aliyofikia binti yake ni kwenda kuwa zaidi ya kichaa wa mapenzi.

"Laah! Sijui mwanangu amekumbwa na pepo gani. Haiwezekani urembo wote alionao, pesa zote wazazi wake tulizo nazo. Leo hii atoke avimbe mtaani kabisa na mzoa takataka? Maskini, hohe hahe. Mtu asiyekua na mbele wala nyuma?.." Lah! Pesa itafanya kazi yake, kamwe siwezi kuacha kizazi changu kiangamie", aliwaza mama Suzani huku nafsi yake ikimuuma kujibiwa kwa mkato na binti yake.

"Suzani..", kwa mara nyingine tena mama huyo alipasa sauti yake kumuita Suzani. Lakini licha ya Suzani kusikia sauti ya mama yake, katu hakuitika zaidi ya kugeuka na kumtazma mama yake pasipo kusema neno lolote. Mama Suzani aliguna baada kuona binti yake kazidi kumuonyeshea kiburi na dharau, kwa sauti ya upole alisema "Suzani mwanangu, mimi ni mama yako. Sio vizuri haifai kuninunia. Mzazi tangu lini akanuniwa? Mzazi hanuniwi bwana hebu acha dharau basi"

"Mama, umeniita. Haya niambie sababu iliyokufanya iniite", bado Suzani alionyeha kiburi mbele ya mama yake. Busara pekee ndivyo iliyomfanya mama huyo kuwa mpole, na hapo ndipo alipo cheza na akili yake. Alitambua fika sababu pekee inayomfanya binti yake kumjibu majibu hayo ya dharau. Kichaa Nyogoso ndio sababu kuu aliyojua kuwa binti yake inamfanya aonyeshe dharau na kiburi, hapo kwa sauti ya chini akamwambia "Mzoa takataka nimeonana naye, na nimemwambia kila kitu kuhusu wewe. Kiukweli alifurahi sana huwezi amini", alidanganya mama Suzani, alifanya hivyo kwa dhumuni la kucheza na akili ya binti yake. Suzani aliachia tabasamu bashasha, akajibu "Waooh! Kweli mama?.."

"Ndio, kweli kabisa. Siwezi kukudanganya mimi!.", mama Suzani alimjibu binti yake huku tabasamu la uongo likionekana usoni mwake.

"Oooh Mungu wangu, natumaini hazima yangu ya mimi kuishi na mkaka yule mzoa takataka inakwenda kutimia sasa. Naomba Mungu ajari ile isiwe imefifiza uzuri na ukubwa wa umbo lake", ndani ya moyo wake, Suzani alijisemea maneno hayo ilihali tabasamu bashasha lilizidi kumtawala. Alipokwisha kujisemea hayo alishusha pumzi ndefu kisha akamuuliza mama yake "Mama, kwahiyo yupo salama ile ajari haikuweza kumuathiri?..", mama Suzani aliposika swali la binti yake, alikaa kimya kwanza huku akitafakari jibu la kumpa ili alizike nalo. Punde alipata jibu, akamjibu "Hapana ingawa aliumia kidogo ila kwa namna nilivyo muona yupo sawa kabhsa, na anaendelea na kazi yake ya kuzoa takataka" Lilikua jibu ambalo lilimfurahisha sana Suzani, kwani iliweza kuonyesha uso wa furaha tofauti ya hapo awali. Hatimaye ule muda wa kuwaona wagonjwa ulimalizika, mama Suzani alimuaga binti yake wakati huo mama Mazoea tayari alishaondoka baada kulizishwa na hali ya Nyogoso kipenzi cha binti yake. Mama Mazoea ilimlazimu kukubaliana na hali hiyo ingawa moyoni hakufurahishwa na kitendo hicho cha binti yake kuzama kwenye penzi la mzoa takataka Nyogoso.

"Watoto wengine wengine wa kike, ni heri uzae panzi. Sijui kampendea nini kijana yule, mtoto unamsomesha unampa anacho kitaka lakini anakua bogazi. Huyu anahitaji maombi kwa kweli", maneno hayo alikua akijisemea mama Suzani. Maneno hayo alijisemea kwa hasira huku akizipiga hatua kulifuata gari lake kwa dhumuni la kurudi nyumbani kupumzika. Alipofika nyumbani, moja kwa moja aliingia chumbani kwake akajitupa kitandani huku kila mara akijisonya. Hakika binti yake alimuumiza kichwa.



Wakati hayo ya pande mbili, ikiwa zote familia za kitajiri mama Mazoea na mama Suzani ambao wote kwa pamoja mabinti zao wakihaha kummiliki kichaa Nyogoso ilihali wao wakionekana kutokukubaliana na mawazo ya binti zao. Upende wa mwingine walionekana vijana wasiopungua watano, vijana hao walikua wakipiga zogo. Katika vijana hao alikuwemo kijana aliyefahamika kwa jina Lidai. Lidai kwa kipindi kirefu alikua akimfuatilia Suzani pasipo kukubaliwa, na mara kadhaa Suzani alithubutu kumtukana akimwambia kuwa hana hadhi ya kuwa na yeye. Hali hiyo ilimnyima sana furaha Lidai, alipenda asipo pendwa. Pesa na umbile nzuri ndio sababu kuu iliyomfanya Suzani kulinga popote pale alipokatiza, mrembo huyo alijua kuvaa vizuri, bangili za dhahabu. Shingo yake nayo ikimeremeta vema mikufi ya kike. Suzani alivutia.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Oya washkaji, hivi mnajua Suzani siku mbili hizi simuoni", aliongea Lidai.

"Naona umeanza. Sasa hata usipomuona kwako kuna tatizo gani? Wakati hata kutongoza hujui"

"Hebu tuondolee upuuzi wako hapa", alidakia kijana mwingine, akimuunga mkono kijana yule aliyemjibu Lidai. Wakati kijana Lidai akitaka kujitetea, kijana wa pili aliongeza kusema "Lidai unatuangusha vijana wa mtaa huu ujue. Kwenu pesa ipo ya kutosha, unaweza kuvaa nguo ya ghalama yoyote ile. Ukawa mtanashati wa kufa mtu, sasa inakuaje unamkosa Suzani? Acha ujinga bro, ukishindwa kwa maneno, mfuate kwa swaga. Amini utamnasa tu"



"Kweli eeeh! Hapo wewe umezunguza jambo la maana sio hao wanaishia kuponda tu,au hamjui kuwa yule ni V.I.P?.." Lidai akioneka kutabasamu alimuunga mkono jamaa huyo wa watatu aliyemshauri kuwa anatakiwa awe na swaga kwa kuvaa nguo nzuri na kunukia kila aina ya manukato,ikiwezekana hata kumtokea Suzani huku akitumia gari ya ghalama. Lakini wakati washkaji zake Lidai walipokuwa wakizungumza hayo mambo,mara ghafla akakatiza binti mmoja aliyeitwa Loi. Kwa kipindi kirefu Lidai alikua akimtuma Loi akamtongozee Suzani. Lidai alipomuona Loi kakatiza maeneo hayo ya kijiweni,hima alinyanyuka na kumtaka Loi asimame. Loi akasimama. Baada ya salamu,Lidai akamuuliza Loi kuhusu jambo alilomtuma kwa Suzani. Hivyo Loi kabla hajamjibu Lidai,alikaa kimya kidogo akiwa ameinamisha paji la uso wake chini. Punde alivunja kimya hicho kifupi akasema "Lidai,Suzani yupo hospital anasiku ya nne sasa..",Lidai alistuka kusikia kuwa Suzani kalazwa hospital..." Hospital? Kwani anaumwa nini?.." muda huo huo Lidai akahoji huku akionekana kupoa kidogo akistushwa na taarifa hiyo ya Suzani kulazwa hospital. Kwani ni binti aliyetokea kumpenda sana. "Alijichoma kisu" alijibu Loi huku akiondoka zake pole pole na hamsini zake.

"Loi mbona unaondoka sasa bila kuniambia chochote?.."

"Unataka nikwambie nini Lidai?..aamh kuhusu ujumbe wako,subiri apone akitoka hospital nitakwenda kumuona na nimweleza kuhusu hisia zako"

"Lini sasa" Alihoji tena Lidai,safari hiyo akionekana kuwa na shauku ya kutaka kujua jambo.

"Leo kwanza naenda kwao,nikamuone mama yake,hivyo endapo kama nikimkuta nitamaliza kila kitu"

Lidai alicheka kwa furaha kisha akaongeza kusema "Ndio maana nakukubali Loi.."

"Haya bwana..ngoja mi niwahi hapo dukani kwa mangi "

"Sawa" Lidai akarudi kijiweni kuendelea na zogo,Loi rafiki yake wa karibu mno Suzani anaendelea na hamsini zake. Naam! wakati Lidai

akiwaza kumpata Suzani,Suzani naye hospital alitamani apone haraka ili akamtafute Nyogoso. Vile vile Mazoea naye alitamani Nyogoso apone haraka iwezekanavyo ili aweze kumtwaa kwenye imaya yake,ili hali mama Suzani yeye akifikiria namna gani atafanya ili ampoteze kichaa Nyogoso ili asije muhalibia mwanaye. Ambapo baada kufikiria kwa kina, jibu akapata kuwa njia rahisi ni kumtafuta Daktari pale pale hospital Mwananyamala. Dokta ambeye atakula naye njama kwa kumlipa pesa yoteyote atakayo hitaji ilimladi ahakikishe anamuua Nyogoso kwa kumchoma sindano ya sumu.

"Wazo nzuri sana", alitabasamu mama Suzani baada kuona alichokifikiria kipo sahihi. Ilikua siku ya pili sasa. Haraka sana mama Suzani aliwasili hospital, kabla hajaingia wodini kumjulia hali binti yake, alifanya jitihada za kuonana na Dokta mkuu ambaye ni Luanda aliamini kuwa anaweza kumshawishi Dokta huyo kwa kumpa pesa yoyote atakayo taka ilimladi atimize hitaji lake.







"Kwa muda huu nipo bize kidogo, kwahiyo labda tupeane namba ili tuwasiliane juma tano tuonene tuonge vizuri", alisikika akisema hivyo Dokta Luanda akimwambia mama Suzani pindi alipoingia ofisini kwake.

"Sawa Dokta namshkuru sana. Ammmh! Namba yangu hii hapa", alichomoa kadi namba kwenye mkoba wake akamkabidhi Dokta kisha Dokta naye akacharaza namba yake kwenye karatasi akamkabidhi mama Suzani. Waliagana. Baada mama Suzani kuachana na Dokta Luanda, huku nyuma Dokta huyo alibaki akitafakari ni mazungumzo gani aliyonayo mama huyo, lakini mwishowe subira pekee ikatawala moyoni mwake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Hatimaye siku husika iliwadia, siku ya juma tano. Asubuhi mapema mama Suzani alimpigia simu Dokta Luanda akamkumbusha kuwa siku hiyo watakua na mazungumzo. "Sawa hakuna shaka, jitahidi kufika",aliongea Dokta Luanda huku akijiandaa kuingia kazini. Alipofika kazini, jambo la kwanza kabla ya kufanya kitendo chochote aliingia wodi aliyolazwa kichaa Nyogoso kumjulia hali. Ghafla Dokta huyo alijikuta akitabasamu baada kumkuta Nyogoso ameketi kitandani akiwa amegemea ukuta kwa kuutanguliza mto kwenye mgongo wake huku mikono yake nayo ikapapasa mahali alipooata jeraha.

"Laah! Kweli Mungu mkubwa, sasa hii pesa naila kwa amani kabisa", alijisemea maneno hayo Dokta Luanda nan the ya moyo wake, paji la uso wake nalo likionyesha tabasamu pana.

"Kijana unajisikiaje kwa sasa?..", Dokta Luanda akiwa bado na wingi wa furaha, alimsabahi kichaa Nyogoso. Lakini Nyogoso hakujibu, zaidi ya kuishi kutazama tu. Kitendo hicho kilimpelekea Dokta Luanda kuamini kuwa mgonjwa wake huwenda bado akili haijamkaa sawa, na hivyo aliona haja ya kumuacha aendelee kupumzika. Alitoka wodini akaenda kuendelea kuwahudumia wagonjwa wengine, punde si punde simu yake ya mkononi iliita. Alichomoa kutoka kwenye mfuko wa koti lake, alitazama kioo cha simu yake akaona namba ya mama Mazoea. Alipokea "Ndio mama yako", aliongea Dokta Luanda kwa mashasha ya hali ya juu,akijua kuwa hana kesi tena na mama huyo kwani mgonjwa wake tayari amepata ahueni.

"Salama sijui wewe Dokta", alijibu mama Mazoea.

"Kwangu salama pia, Eeh namshkuru Mungu kwa hilo"

"Sawa, vipi hali ya mgonjwa? Maana leo nimetingwa na kazi hapa ofisini, kwahiyo sitokua na nafasi ya kuja huko", alisema mama Mazoea wakati huo akiwa yupo ofisini kwake, vidole vya mkono wake wa kushoto ukichezea batani za Computer.

"Mgonjwa leo kaamka, ila bado hawezi kuongea. Lakini usiwe na shaka, nitazidi kufanya jitihada kila kitu kitakua sawa mama"

"Sawa ahsante kwa taarifa, kesho nitakuja. Tafadhali usimruhusu aondoke mpaka nifike",alisisitiza mama Mazoea.

"Usijali, nakutakia siku njema"

"Sawa Dokta na wewe pia", mama Mazoea alikata simu baada kumaliza maongezi na Dokta Luanda. Ghafla akajikuta akizubaa kwa muda wa dakika kadhaa,akionekana kutoamini kama kweli Nyogoso amepata ahueni kwa sababu alimaini kuwa uzima wa Nyogoso ndio uzima wa binti yake. Pumzi ndefu alishusha baada kutoka kwenye dimbwi hilo la taharuki kisha akajisemea "Ama kweli Duniani kuna mambo na vijambo",alipokwisha kujisomea maneno hayo, aliendelea na kazi.



Muda ulizidi kusogea, hatimaye ule wasaa wa mama Suzani kukutana na Dokta Luanda ulikaribia kufika. Mama Suzani alimpigia simu Dokta huyo ili wakubariane mahali pakukutana.

"Hello! Dokta", aliongea mama Suzani baada Luanda kupokea simu.

"Samahani subiri kama dakika tano tu", Dokta Luanda alisema kwa sauti ya chini, haraka sana mama Suzani alikata simu yake ikiwa wakati huo ndani ya nafsi yake akijisema "Leo ndio siku ambayo mwanangu anaruhusiwa kutoka hospital, kwahiyo sitaki kuipoteza siku hii pasipo kumuondoa Duniani huyu mzoa takataka. Lazima nimuuwe la sivyo atanitia haibu kwa jamii yangu inayonizunguka", maneno hayo mama Suzani alijisemea wakati huo akitembea huku na kule, alimaliza sebule yote ilihali akisubiri dakika tano zipite ampigie tena Dokta Luanda. Dakika tano zilikatika, haraka mama Suzani akampigia simu Luanda, safari hiyo aliambiwa kuwa simu anayopiga inatumika. Alikasirika mama Suzani, hima alikata simu lakini muda huo huo simu yake iliita. Aliyempigia hakua mwingine bali ni yule yule Dokta Luanda,kumbe wakati mama Suzani alipokua akimpigia, naye vile vile alikua akimpigia hali iliyoleta mgongano wa mtandao.

"Enhee. Nambie sasa", aliongea Dokta Luanda.

"Nataka kujua mahali pakukutana ili tuzungumze kwa kina", alijibu mama Suzani.

"Sawa, mimi nakusikiliza

" Anhaa, basi naomba tukutane Mtanzania Hotel au unaonaje?. "

" Sawa tu hakuna tatizo, saa ngapi?.. "

" Muda huu "

" Safi sana, yani hapo umecheza kama pele, ila ukumbuke na nauli yangu. Siunajua hapa mjini? Muda pesa?.. "

" Ahahaha Hahaha", mama Suzani aliangua kicheko baada kusikia maneno hayo ya Dokta Luanda. Alipohitimisha kicheko chake akasema "Shaka ondoa, utafurahi mwenyewe"

"Sawa mama, ndio nataka nianze safari"

"Hata mimi ndio naelekea kwenye gari langu ili nije hapo", alihitimisha maongezi mama Suzani kisha akakata simu. Safari ya kuelekea Mtanzania Hotel ikaanza,nia ni kumalizana na Dokta Luanda kabla hajaelekea hospital kumchukua binti yake ambaye tayari hali take ilikua imetengemaa.

Kwa muda wa dakika nusu saa alifika, alimkuta Dokta Luanda amefika na hivyo alikua akimngojea yeye tu.

"Waooh! Umeshafika", alisema mama Suzani huku akibana mlango wa gari lake.

"Aah mama? Mimi tena? Unajua katika watu Duniani wanaongooza kujali muda ni sisi madaktari. Na hii imetokana na jinsi kazi yetu inavyo tupasa kufanya, kwa sababu unaweza kuambiwa kuwa kuna mgonjwa anatakiwa kufanyiwa upasuaji saa mbili na dakika therathini asubuhi, kwahiyo endapo kama utachelewa kazi huna kwa sababu huo ni uzembe "

" Ni kweli kabisa ", aliunga mkono mama Suzani. Punde alikaa kimya akiwaza namna ya kumuanza Dokta Luanda ili amuelewe. Baadaye kimya hicho kilivunjwa baada mama Suzani kumtaka Luanda waingie ndani, Dokta Luanda alikubali. Waliingia ndani wakaketi viti mahali ambapo palikua na watu ambao walionekana wakila na kunywa. Muhudumu alikuja kuwasikiliza wawili hao kwa kuwakabidhi risti ya huduma zinazo patikana mahali hapo. Kila mmoja alichangua alichopendelea, wakati muhudumu akifuata mahitaji yao huku nyuma maongezi yaliendelea. Mama Suzani alimwambia Dokta kuwa kuna kazi anataka kumpa.

"Kazi? Mbona tayari ninayo, tena kazi nzuri tu inayonipa mkate wa kila siku", alisema Dokta Luanda huku akustushwa na hiyo habari ya kupewa kazi.

"Nisikilize Dokta, nafahamu kuwa kazi yako nzuri. Lakini pia kazi hii ninayotaka kukupa haipo nje ya kazi yako"

"Haya niambie kazi gani hiyo", alisema Dokta Luanda wakati huo akiwa makini kumsikiliza mama Suzani kile atakacho mjibu. Ila kabla mama Suzani hajasema, muhudumu aliwasilisha vinywaji ambapo yalikua maji tu. Hivyo mama Suzani alilipa bili kisha akaendelea "Kuna mgonjwa pale Hospital, ni kijana mwenye kifua kipana. Ananywere ndefu Zipo shagalabagala mfano wa mwendawazimu. Yupo wodi namba kumi", alikunywa kwanza bunda la maji halafu akaendelea kusema "Nadhani unamjua, kwahiyo nataka umuuwe".

"Unasemaje?.", alistuka Dokta Luanda, maneno ya mama Suzani yalimstua sana.

"Tulia basi Dokta, acha papera", alisisitiza mama Suzani wakati huo huo Dokta Luanda akasema "Yani mimi kazi yangu kutibu, leo hii unaniambia niuwe? Hapana mama, kiukweli sipo tayari kubeba zigo hilo la dhambi"

"Dokta, acha kuniangusha bwana. Wasi wasi wako nini wakati pesa ipo ya kutosha? Nitakupa dauo nono"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Hatakama, ila sipo tayari kufanya hicho unacho kitaka", aliongea kwa kujiamini Dokta Luanda.

"Nitakupa millioni mia tatu", aliongeza kusema Mama Suzani, lakini Dokta Luanda hakutaka kuelewa. Alinyanyuka akaondoka zake huku akirusha mikono kana kamba kakidharau kile alichokisema mama Suzani. Mama Suzani aliumia sana, pale alipokaa aliwaza afanye nini baada Dokta Luanda kukataa hitaji lake. Pumzi ndefu alishusha kisha akanyanyuka akaelekea kwenye gari lake akawasha akaenda hospital kumchukua binti yake ambaye kwa muda huo tayari aliruhusiwa kuuguza pole pole jeraha lake akiwa nyumbani.

Usiku wa siku hiyo ulipoingia, Dokta Luanda aliwaza sana juu ya kile alichokua akizungumza na mama Suzani. "Dokta, acha kuniangusha bwana. Wasi wasi wako nini wakati pesa ipo ya kutosha? Nitakupa dauo nono", Dokta Luanda aliyakumbuka maneno hayo. "Nitakupa millioni mia tatu".

"Millioni mia tatu?..", baada kuwaza sana, alijikuta akijiuliza swali hilo ndani ya nafsi yake huku usingizi nao ukikaa kando shauri ya mawazo yaliyokua yakilindima kichwani mwake wakati huo akijisonya.

"Laah pesa nyingi mno nimekataa,bahati kama hizi huwa mara chache sana kutokea. Je, nimpigie nimwambie kuwa nipo tayari? Nikisha kamilisha nijue namna gani nitamdamganya yule mama aliyenipa laki nane. Na endapo kama atadai ghalama zake basi nitampa hata millioni moja tu. Mmmh! Naam. Hii ni moja ya plan B ya kiutu uzima ", aliwaza na kuwazua Dokta Luanda, mwishowe alimpigia simu mama Suzani ambaye muda huo alikua amegubikwa na mawazo, akiumiza kichwa namna ya kumpoteza kichaa Nyogoso." Ndio Dokta ", aliitika mama Suzani baada kupokea simu. Dokta Luanda akasema kwa msisitizo "Mama, nimekaa nikafikiria vya kutosha, nimeamua kukubali kufanya kazi yako ila pesa hiyo uliyoniambia isipungue hata thumuni". Maneno hayo ya Dokta Luanda yalimfanya mama Suzani kuachia tabasamu pana, akiwa na wingi wa furaha akajibu "Dokta..Dokta...Dokta Luanda, nimeshakwambia kwangu pesa sio tatizo. Ili uamini hilo, nakuongeza laki nane sawa?.."

"Sawa mama"

"Basi fanya upesi usiku huu huu wa leo mchome sindano ya sumu"

"Aah, hapana. Tuma mzigo kwenye akaunti yangu kwanza"

"Sawa Dokta", alikubali mama Suzani,muda wa nusu saa pesa iliingia kwenye akaunti ya Dokta Luanda kwani tayari kodi namba kila kitu kilicho stahili walielekezana.

"Tayari Dokta, kwahiyo kesho niite nije kushuhudia maiti sawa?..", baada mama Suzani kumuingizia pesa Dokta Luanda kwenye akaunti yake alimpigia simu na kisha kusisitiza.

"Ondoa shaka mama", alijibu Dokta Luanda na mara moja akaanza kujiandaa kumfuata Nyogoso hospital ili amalize kazi kabla jogoo hajawika..





Basi Dokta Luanda aliingia ofisini kwake, akachukua sindano akavyonza sumu kwenye chupa ndogo kabisa akiinza kwa kuitingisha huku akiipindua pindua kuitazama. Lakini Dokta huyo alipokua akijianda kwenda kumuua kichaa Nyogoso, upande wa pili alionekana Nyogoso na mama yake wakiwa wametoka shambani. Njia nzima wawili hao walionekana kuwa na furaha huku zogo likiwa limechukua nafasi yake, waliongelea malengo mbali mbali kuhusu maisha yao. Walipanga hili na kupangua lile, ila ghafla maongezi yao yaliingia dosari baada mama Nyogoso kugongwa na nyoka. Sauti ya mayowe ilisikika, mama Nyogoso alilalama wakati huo Nyogoso akihaha kuokoa uhai wa mama yake kwa kutafuta mti wenye kamba achune ili amfunge sehemu ile aliyogongwa na nyoka. Aliamini kufanya hivyo ataipunguza kasi sumu. Huduma ya kwanza. Lakini pindi Nyogoso alipokua akifanya jitihada hizo, nyuma yake alionekana nyoka mwingine achilia mbali nyoka yule aliyemgonga mama yake. Nyoka hao wawili walikua katika heka heka za kukimbizana. Nyoka yule wa pili alijivuta kwa kasi kumsogelea Nyogoso ili amdhuru,ila kabla hajamfikia ilisikika sauti ya mama Nyogoso akisema "Nyogoso mwanangu kimbia,nyoka yupo nyuma yako", haraka sana Nyogoso aligeuka kutazama nyuma yake, alistuka kumuona nyoka mkubwa akimfuata wakati huo sauti ya mama yake ikizidi kumsisitiza akimbie na kabla Nyogoso hajachukua uamuzi huo alizinduka kutoka usingizini. Naam! Ilikua ndoto, ndoto ambayo alimuota mama yake akiwa amegongwa na nyoka.

Mapigo ya moyo yake yalimuenda mbio, aliinuka akaketi kitandani na kisha kujiuliza ndoto hiyo inamaana gani. Lakini jibu alikosa mwishowe akajikuta akidondosha chozi huku akimtaja marehemu mama yake, ilihali akidiliki kupasa sauti yake kumuomba msamaha kwe kile alicho mfanyia ikiwa macho yake nayo yakiangaza huku na kule akitazama furushi lake lenye mazagazaga. Katu hakuliona, kitendo ambacho kilimpelekea kushuka kwenye kitanda kisha akazipiga hatua kuelekea mlangoni. "Nyogoso mwanangu kimbiaaa",wakati Nyogoso alipokua pale mlangoni huku akiendelea kutafuta furushi lake lenye mazagazaga, sauti ile mama yake aliyoisikia kwenye ndoto ilijirudia kicwani mwake. Akiwa na wendawazimu wake, sauti hiyo aliifanyia kazi. Alihisi kama hatofanya hivyo mama yake anavyomwambia basi atakua bado anamkosea. Alitimua mbio huku akichechemea, lakini alipofika geti la hospital hiyo alikutana na mtiti kutoka kwa mlinzi. Kwa sauti ya ukali mlinzi alimuuliza "Wapi unakwenda usiku huu?.."

"Naondoka mahali hapa, marehemu mama ameniambia niondoke", alijibu kichaa Nyogoso huku akifungua geti. Maneno hayo yalimfanya mlinzi kuishia kumtazama tu ilihali fikra zake zikishindwa kuelewa kichaa Nyogoso amemanisha nini kuongea maneno hayo.

"Sio huyu atakua mzimu", alijisemea mlinzi ndani ya nafsi yake wakati huo akifunga geti huku akiishi kumsindikiza Nyogoso kwa macho. Baada kichaa Nyogoso kufanikiwa kuondoka katika hospital hiyo ya Mwananyamala, alijibanza kwenye jumba mbovu ambapo mahali hapo ndipo alipojistili usiku huo ikiwa wakati huo huo alionekana Dokta Luanda akizipiga hatua kuelekea wodi aliyolazwa kichaa Nyogoso ili amalize dili alilopewa na mama Suzani. Dili la kumuuwa kichaa Nyogoso, kijana aliyeonekana kuwa kikwazo kwa binti yake. Lakini pia mbali ya dili hilo la kumuuwa Nyogoso, Luanda tayari alishapewa dili na mama Mazoea. Dili hilo nalo lilikua ni kumponya Nyogoso huyo huyo kipenzi cha binti yake wakuitwa Mazoea. Mama huyo alijua fika binti yake kwa Nyogoso hajiwezi, kama kaoza. Dili zote zilikua kabambe ila Dokta Luanda alitazama nani kapanda dau kubwa, ni mama Suzani ambaye upande wake alitaka Nyogoso auwawe. Mama huyo alimpiku mama Mazoea ambaye alitaka Nyogoso apone haraka ili binti yake awe katika hali ya furaha na amani.

"Mungu wangu..", alistuka Dokta Luanda baada kuingia wodini na kutomuona Nyogoso. Hakutaka kuamini mapema kile anacho kiona,hivyo alikisogelea kitanda na kisha kuayavuruga mashuka meupe yaliyokua kitandani hapo. Si hivyo tu, bali aliinama kutazama na uvunguni lakini hakumuona. Hapo kijasho chembamba kilianza kumtoka, pumzi ndefu alishusha mara kwa mara wakati huo huo pole pole akiketi kwenye kitanda alichokua amelazwa kichaa Nyogoso na punde si punde alijiinamia huku mawazo chungu nzima yakilindima kichwani mwake. Akiwaza atawaeleza nini wanawake hao matajiri waliompa dili tofauti tofauti. Kwanza mama Mazoea, ambaye yeye baada Nyogoso kufikishwa hospital pindi alipogongwa na gari, alimtaka kwake rushwa ili amtibu kwa haraka kuokoa uhai wake. Jambo ambalo halikuleta shaka upande wake kwa sababu mama huyo aliamini uzima wa Nyogoso ndio furaha ya binti yake na hivyo alimpa ahuru ataje kiasi cha fedha anachotaka ambapo naye pasipo kupepesa macho alitaja shilingi laki sita, pesa ambayo mama Mazoea aliona ndogo sana. Akamuongeza shilingi laki mbili, jumla ikiwa shilingi laki nane. Pesa hiyo aliipokea kwa tabasamu na kuahidi kumtimizia matakwa yake.

Pili, Dokta Luanda aliwaza atamwambia nini mama Suzani. Mama ambaye alimpa dili la kumuua Nyogoso, kwa sababu hakutaka kijana huyo ajenge mahusiano na binti yake kwa vigezo kuwa atamtia haibu, sababu Nyogoso ni mtu asiye kuwa na hili wala lile. Hohe hahe. Hivyo mama Suzani aliamini kuwa endapo kama Suzani atashuhudia maiti ya kichaa Nyogoso, anaweza kutulia huku akimtia moyo kwa kukwambia hiyo ni mpingo ya Mungu. Lakini hatimaye mpigango inakua sio matumizi, kichaa Nyogoso anatoroka hospital kwa kuheshimu ndoto aliyoota. Anajikuta akikwepa kifo cha kuuliwa kwa kuchomwa sindano yenye sumu,na hivyo anafanikiwa kurudi mtaani.

"Doh! Nitawaambia nini sasa ili wanielewe?..", alijiuliza Dokta Luanda wakati huo akiyakumbuka maneno ya mwisho aliyozungumza na mama Mazoea kwa njia ya simu. "Sawa,kesho nitakuja. Tafadhali usimruhusu aondoke mpaka nifike", kichwa kilimuuma Dokta Luanda asijue kipi cha kufanya. Na pindi alipokua bado anatafakari, ghafla kichwani mwake yalimjia maongezi ya mwisho aliyozungumza na mama Suzani.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Tayari Dokta, kwahiyo kesho niite nije kushuhudia maiti sawa?..". Maneno hayo ya mama Suzani yalijirudia mara mbili mbili kichwani mwake. Dokta Luanda alizidi kuchoka! Pumzi kwa nguvu alizidi kushusha,wakati huo huo aliingiza mkono mfukoni akatoa simu yake ya kiganjani,haraka akatazama salio lake Bank, akitaka kujua kuna kiasi gani. Huku mikono yake ikitetemeka alibofya namba haraka sana. Lakini kabla hajafahamu kiasi kilichopo kwenye Akaunti yake, simu yake iliita, mkewe ndiye aliyempigia usiku huo. "Mmh", aliguna Dokta Luanda kisha akapokea. "Heloo", aliongea Dokta Luanda kwa sauti ya upole.

"Mume wangu police wametoka hapa nyumbani sasa hivi",ilisikika sauti ya mkewe ikimjibu. "Police?..Kwani nimefanya kosa gani?au wamefuata nini?..", alijiuliza Dokta Luanda kwa hamaki kubwa wakati huo huo simu ikakatika. Alipo piga yeye ili ajue kwa undani zaidi,ghafla simu ya mkewe ikawa haipatikani.

Kimbembe!



Hofu ilizidi kumtanda Dokta Luanda baada kupata habari kuwa jeshi la polisi limefika nyumbani kwake. Aliwaza kosa lipi alilofanya mpaka polisi hao wamjie nyumbani tena saa za usiku. Kiukweli kitendo hicho kilimwogopesha mno Dokta huyo, alihofia kurudi nyumbani huku mawazo yakimjaa chungu zima kichwani mwake. Hapo akaona bora aende zake klabu japo anywe pombe ili atulize mawazo yaliyokua yamemsonga kichwani mwake.

Hivyo akionekana kuwa mpole na mtu asiyejitambua,Dokta huyo hayawani alizipiga hatua kuingia ofisini kwake. Haikuchukua nusu saa walalisaa limoja, akatoka akiwa na nguo zake za kawaida moja kwa moja akaelekea kwenye gari lake ndogo aina ya Hilux, na kabla hajiliwasha alijiinamia kwanza kwenye msukani akitafakari kwa namna moja ama nyingine jinsi ya kuyasovu hayo mambo yaliyomkumba.

Pumzi kwa nguvu alishusha, wakati huo huo akazungusha funguo ya gari. Gari likawaka,safari ya kuelekea klabu ikawa imeiva ambapo alikwenda klabu inayoitwa NIGHT CLUB. Ipo maeneo ya Sinza moli. Klabu ambayo kiukweli ilikua imetulia kwa maadhari mazuri ndani na nje. Dokta Luanda aliona ni mahali pazuri kwa yeye kutuliza akili kama si kuyapoteza mawazo aliyokua nayo.

Alipaki gari yake sehemu salama,kisha akaingia ndani huku akizungusha zungusha funguo ya gari kwenye kidole chake cha shahada. Naam!alipata sehemu nzuri ya kutulia,muhudumu akaja kumsikiliza. "Naomba uniletee Kilimanjaro nne,na kuku nusu" alisema Dokta Luanda.

Ndani ya dakika alivyo agiza aililetewa. Na hapo ndipo alipo shambulia hizo bia kwa kunywa kama maji,huku akimshambulia kuku kama mtu aliyeshinda njaa siku tano bila kula. Alipotosheka,alikua amelewa tila lila kiasi kwamba asingeliweza kuendesha gari ili arudi nyumbani kwake. Hapo aliamua kukodi chumba cha kulala. Usiku huo Dokta Luanda akawa amelala nyumba ya wageni akiacha mji wake na familia kiujumla.



Asubuhi palipo pambazuka,kule hospitali ya Mwananyamala. Mpema tu jeshi la polisi lilifika hapo kumuulizia Dokta Luanda. Kila mfanyakazi hospitalini hiyo ya mwananyamala alikataa kuwa Luanda bado hajaripoti kazini.

"Wewe dada,hebu njoo hapa" alisikika polisi mmoja akimwita muuguzi wa mle hospital. Muuguzi huyo ambae jina lake aliitwa Agnesi alitii wito.

"Shika hii kadi..hii ni namba yangu ya simu. Tafadhali akifika hapa huyu bwana. Nipigie simu fasta! Sawa? .." polisi huyo aliyemwita Agnesi alisema hivyo kwa msisitizo akimwambia Agnesi.

"Hawa ndio maadui wa maendeleo, lazima wadhibitiwe la sivyo hakuna kitakacho endelea " aliongezea kwa kusema hivyo tana polisi wakati huo akizipiga hatua kuelekea kwenye gari yao waliyofika nayo hospital.

Agnesi alishtuka kusikia maneno hayo ya huyo polisi,ghafla maswali yasisiyopungua mawili yalijitokeza kichwani mwake. Agnesi akajiuliza "Hawa polisi wanamsaka Luanda kwa kosa gani?..na mbona anasema watu kama hawa ni maadui wa maendeleo, yani kuhujumu uchumi. Je, Luanda atakuwa kapokea rushwa?.." Alijiuliza Agnesi,wakati huo huo akaongeza "mmh haya sasa ni mabalaa..ila Yangoswe tumwachie ngoswe. Na ukistaajabu ya Musa utayaona ya filauni..." Kwisha kusema hivyo,Agnesi akaendelea hamsini zake.

Lakini wakati hayo yakitokea hapo hospital, upande wa pili. Nyumba ya wageni (Guest) Dokta Luanda alikuwa bado amelala,alistuliwa na mlio wa simu. Haraka sana alikurupuka kutoka usingizini. Akalisukuma shuka kwa miguu yake miwili,mwili wake ukiwa katika hali ya uchovu,alitupia jicho kutazama ukutani kuangalia saa. "Khaaa saa sita?.." alishangaa Luanda asiamini kama kweli ni sahihi muda huo alio uona. Akashusha pumzi kwa nguvu,kisha akaitazama simu yake ambayo wakati wote ilikuwa ikilia. Luanda akiwa mpole alinyoosha mkono kuifuata,ikajaa kiganjani kwake halafu akapokea.."Dokta kuna mgonjwa kaletwa hapa kwa nia ya kufanyiwa upasuaji..je, litawezekanika hilo suala?.." iliuliza hiyo sauti kisha ikakaa kimya kungojea jibu. "Daah sijui nimjibu nini?.." alijiuliza Dokta Luanda,papo hapo akajibu. "Sawa,kiukweli leo sijafanikiwa kufika kazini kwa sababu nina..." Kabla Luanda hajamaliza kuongea. Sauti hiyo kutoka kwenye simu ikiamjibu huku ikisika kwa jazba. "Vizuri sana,nimekwambia hivyo makusudi ili nithibitishe kama kweli hujafika kazini. Sawa kwaheri " simu ikakata.

"Mmmh hapa kazi ipo, mtaka vyote kwa pupa hukosa vyote",akiwa na hofu dhufo lihali, Dokta Luanda alijisemea maneno hayo huku jasho mwili mzima likimtililika akijua kabisa kibarua chake kipo matatani. Akajikuta akijilaumu kwa kuendekeza tamaa. Na yote Kwa yote alitoka ndani kwenye nyumba ya wageni, kabla hajaingia ndani ya gari yake alitaka anunue maji kwani alikuwa na kiu kali. Alipo papasa kwenye mfuko wa suruali yake,alistaajabu kujikuta akiwa hana hata senti. Hapo akakumbuka kuwa usiku wa jana alipo lala kwenye nyumba hiyo ya wageni,alilala na kahaba. "Yawezekana yule dada aliniibia pesa zangu nilizo baki nazo, lakini hakuna tatizo namshukuru kwa kuniachia simu yangu. Hana lolote njaa tu inamsumbua" alisema Doctor Luanda kisha akaingia ndani ya gari lake akaliwasha moja kwa moja akarudi nyumbani kwake.

Alipo fika,kabla hata hajaiyona familia yake mke na mtoto wake mmoja. Mara ghafla simu yake inaingia ujumbe mfupi (sms) haraka sana alichomoa simu mfukoni ili autazame ujumbe huo unahusu nini.. "Pole kaka.." ulisomeka hivyo huo ujumbe. Luanda akastuka kuona pole hiyo. Akataka kumpigia huyo mtu aliyemtumia ujumbe. Lakini kabla hajafanya hivyo ujumbe mwingine ukaingia. Huo nao ulikuwa ukisomeka vile vile kama ujumbe wa mwanzo. Na kibaya zaidi jumbe hizo zilitumwa na wafanyakazi wenzake.

Kiikweli Dokta Luanda alizidi kupagawa asijuwe kipi hasa kilicho mkuta maana jumbe hizo zilizidi kumtisha. Ingawa alihisi kibarua chake kuota nyasi ila ujuo wa polisi nao ulizidi kumuweka tumbo joto. Hivyo basi akiwa kichwa chini mikono nyuma, aliingia ndani. Moja kwa moja akajitupa kwenye sofa huku kijasho kikimtoka mwili mzima.

Mkewe alishtuka kumuona mumewe karudi nyumbani mapema siku hiyo,akiwa na sintofahamu alisema "Kulikoni La'azizi,mbona leo umerudi nyumbani mapema,sio kawaida yako. Halafu istoshe unaonekana hauko sawa kabisa. Eeh nambie basi mume wangu" Alisema mkewe Dokta Luanda wakati huo akiwa amemkalia mapaja mumewe huku mkono nao ukichezea kidevu."Daah, we acha tu" alijibu Dokta Luanda huku akitazama paa ya nyumba. Punde si punde hodi ikabishwa,mkewe Luanda akaenda kufungua mlango akakutana na uso wa Agnesi. Agnes alikua amemletea barua Luanda ya kuhusu yeye kufukuzwa kazi.

Hivyo Luanda baada kumuona Agnesi kafika nyumbani kwake alistuka,kwani Agnesi na Dokta huyo walikuwa maadui kama maji na moto..yote ikasabishwa na mambo ya pesa,ambapo Luanda na Agnesi walikua wakila dili mbali mbali lakini pesa yote ilikua ikiliwa na Luanda peke yake bila kumkumbuka Agnesi. Kitendo ambacho kilimuuma sana Agnesi mpaka kufikia hatua kujenga bifu na Luanda.

"Agnesi umefuata nini nyumbani kwangu?.." alihoji Luanda kwa hasira baada kumuona Agnesi. Lakini Agnes alicheka kwa kejeri kisha akasema huku akimpigia "Luanda..Luanda...Luanda..Za mwizi mwisho arobaini. Na usipo lizika na kidogo basi hata kikubwa huwezi kulidhika. Ok mimi kibaraka tu. Shika mzigo wako " Agnesi alipokwisha kusema maneno hayo alimkabidhi Luanda barua kisha akaondoka zake kuendelea na majukumu yake huku nyuma akimuacha Luanda akiifungua barua. Alipoisoma alishltuka kuona barua ikihusu yeye kufukuzwa kazi. Alipagawa,na kibaya zaidi katika barua hiyo ilieleze yeye kurudisha mali yoyote aliyopewa na serikali ikiwemo gari lake la kutembelea na nyumba pia. "Mume wangu,unajua sikuelewi kabisa" aliongea mkewe Luanda ni baada kumuona mumewe hayupo sawa. Hivyo Luanda naye hakutaka kuongea neno lolote, zaidi alimpa barua mkewe ili apate jawabu mwenyewe kisha amuelewe kama kweli hamuelewi.

Na wakati mkewe Dokta Luanda alipokua akiisoma barua hiyo,punde si punde jeshi la polisi liliingia ndani,na katika polisi hao alikuwemo Agnesi akiwa amevalia gwanda za polisi. Kumbe Agnesi ni mpelelezi aliyejifanya muuguzi ili abaini ubatilifu unaofanyika hospitalini hapo. Hospital ambayo Dar es salaam nzima inaongoza kwa kusababisha vifo visivyokua na mbele wala nyuma. MWANANYAMALA HOSPITAL.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Khaa,Agnesi!! ? .." alishangaa Luanda kumuona Agnesi akiwa katika gwanda za polisi. "Hapo hapo ulipo mikono juu" aliamlishwa Dokta Luanda kisha akavishwa pingu. "Songa mbele,utajielezea mbele kwa mbele ", ilisikika amri nyingine ikisema ikimuamuru Luanda Daktari mshenzi ambaye alijikuta akatiwa katika chombo cha dola.



Wakati hayo yakijli, upande wa pili alionekana mama Mazoea akiwa ndani ya gari lake akielekea hospital kumjulia hali Nyogoso. Ilihali muda huo huo ilionekana gari ya mama Suzani, naye pia akielekea hospital kwa nia ya kwenda kuangalia maiti ya Nyogoso, akiamini kuwa Doctor Luanda ameshatimiza agizo lake.





ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog