Simulizi : Kurudi Kwa Moza Sehemu Ya Pili
(2) Neema alikuwa wa kwanza kuamka ila kabla hajatoka
nje, mtoto wake alimuuliza “Mama, Maria Patrick ndio
nani?” Neema akashtuka sana kwa swali lile, “Eeeh Salome
unasemaje?” “Maria Patrick ndio nani?” “Hata salamu hakuna? Si
ndio tumetoka kuamka jamani mwanangu!” “Ndio mama, shikamoo ila nijibu
Maria Patrick ndio nani?” “Ni mdogo wangu wa mwisho” “Wewe mama
huyo mdogo wako ni wa wapi? Kwanini hutaki kusema wazi tu kuwa Maria Patrick ni
mimi” “Salome, niache tafadhali niache. Wewe mtoto usinitafutie makubwa
jamani. Wewe ni Salome, hiyo Maria imetoka wapi tena. Niache wewe mtoto
nipumue” “Mama, nahitaji kwenda kwa baba yangu” Neema akapumua
kwa hasira na kutoka nje, kisha akamuita Ashura halafu Salome nae alienda
pembeni akisikiliza maongezi yao, “Huyu mtoto mwenzangu anataka
kuniletea balaa” “Lipi tena dada?” “Eti anataka kumjua baba
yake” “Mmmh hilo balaa kweli, mwambie alishakufa” “Nimemwambia,
ila sijui katoa wapi jina la Maria Patrick na amesema anataka kwenda kwa baba
yake” “Khee dada, hapana bhana usithubutu kufanya hivyo” “Sasa
nitafanyeje mimi?” “Ngojea, nitajua cha kufanya dada ila usithubutu
kumueleza kuhusu baba yake” Neema aliondoka zake kujiandaa ila salome
alishaelewa kinachoendelea hapo. Rose alipoamka hotelini,
alijiandaa kwa safari ya kurudi nyumbani kwake, kwakweli alikuwa anajihisi
uchovu sana ingawa alilala hotelini ila bado mwili wake uligubikwa na uchovu wa
hali ya juu. Aliendesha gari yake hadi nyumbani kwake, ambapo getini
alifunguliwa mlango na mlinzi kama kawaida. “Vipi, ndani humu wote
wazima?” “Nadhani, ila leo sijamuona yeyeto akitoka
nje” “Itakuwa wananisubiria” Aliingia ndani na kukuta wote wapo
chini, tena kila mmoja na pozi lake ila kwa muda huo walikuwa wamepitiwa
nausingizi. Wakati anataka kuwaamsha mara akatokea Ana na kumwambia mama
yake, “Usiwaamshe waache hao” “Vipi tena imekuwaje?” “Ni
viburi sana hao mama” Rose hakuelewa bado, ila Ana alimvutia mama yake
chumbani na kumueleza alichowafanyia ndugu zake. “Jamani mwanangu kumbe
wewe ni fundi hivi jamani!” “Nilikuwa sizijui vizuri nguvu zangu ila
saivi nimezijua” “Aaah wewe ni kiboko, ila mwanangu watu hawa inabidi
warudi kwenye hali ya kawaida maana ndio wanaotusaidia” “Nitawarudisha
wengine ila sio dada Sara” “Hapana mwanangu, Yule ni dada
yako” “Hata kama, labda aone tu ila kuongea ni no, Yule mdada ni mbea
sana” “Ila kwanini hatukuweza kumziba mdomo Moza?” “Achana na
habari za huyo mtu mama hakuwa wa kawaida ila cha msingi hatuponae tena
hapa” “Sawa mwanangu, ila waachilie ndugu zako” Ana akaenda
chumbani kwake kufanya dawa, na muda kidogo tu pale sebleni waliamka na waliweza
kuinuka na kuzungumza ila kila mmoja aliogopa kuzungumza kuhusu kitu
kilichotokea. Sara nae aliweza kuangalia ila kuzungumza hakuweza. Wale
mapacha, walipoinuka kitu cha kwanza kilikuwa ni kuondoka hapo nyumbani kwao, na
kumuacha Patrick na Sara hata hawakutaka kujua kama mama yao karudi au
la. Salome alikuwa makini akifatili mambo ya Ashura kwani
alijua ni wazi angewasiliana na Rose kumwambia ile mada na kweli Ashura aliingia
chumbani na kumpigia simu Rose kumbe Salome alikuwa amejibanza
akisikiliza, “Yani dada, ule wasiwasi ambao ulikuwa nao kipindi chote
sasa unaenda kutokea. Kwa kifupi haka katoto kameanza kumchachafya mama yake
kuhusu baba yake na kanataka kuja kwa baba yake” Ashura akawa kimya sasa
akisikiliza maelekezo ya Rose, ila Salome nae alikuwa makini kabisa kwani alijua
ni wazi baada ya maelekezo hayo Ashura angeongea tu. “Kwahiyo ndio
wakati wa kuitumia ile dawa eeeh! Sawa dada nimekuelewa, si nimuwekee kwenye
chakula! Sawa dada nitafanya hivyo. Lakini si siyo ya kuua? Sawa maana ingekuwa
ya kuua ningeogopa kwakweli maana kesi hizi” Kisha Ashura akakata simu
na kwenda kwenye begi lake ambapo alionekana kama akipekua kitu kisha akatoa
kichupa kidogo na kutoka nacho. Muda kidogo akamuita Salome na
kumwambia, “Njoo ule Salome mzuri weee” Salome alifika na
kumuuliza, “Sasa nakula peke yangu?” “Hapana, tunakula wote.
Chakula change si hicho hapo. Halafu cha kwako ni hiki” “Sawa, ila
wadogo zangu wako wapi nao waje nile nao bhana” “Kawaite
basi” “Mi naona uvivu” “Yani wewe mtoto loh!” Kisha
Ashura akaenda kuwaita wadogo zake Salome, ila kwa muda huo huo Salome aliweza
kubadilisha zile sahani za chakula. Ashura aliporudi akaenda kuwapakulia
chakula chao watoto, kisha kwa pamoja wakaanza kula mara gafla Ashura akadondoka
huku akitapatapa na povu likimtoka mdomoni. Kisha
Ashura akaenda kuwaita wadogo zake Salome, ila kwa muda huo huo Salome aliweza
kubadilisha zile sahani za chakula. Ashura aliporudi akaenda kuwapakulia
chakula chao watoto, kisha kwa pamoja wakaanza kula mara gafla Ashura akadondoka
huku akitapatapa na povu likimtoka mdomoni. Hapo ndio hofu iliwashika
hata wadogo zake Salome waliogopa sana na kumuuliza dada yao, “Kwani
imekuwaje dada?” “Min a mamdogo Ashura tunacheza mchezo kwahiyo hata
msiwe na mashaka” Ila Salome alikuwa jasiri sana kwa wakati huo kwani
alimchukua mamake mdogo huyo na kumburuza hadi chumbani kisha akamfunika na
kitenge halafu akachukua simu ya Ashura na kuifungua halafu akaangalia namba
aliyoipiga mwishoni akaona ni namba ambayo haijaandikwa jina ila akahisi ndio
hiyo hiyo namba ya Rose, akaamua amtumie ujumbe mfupi, “Dada, mbona hii
dawa nimempa huyu Salome ameanguka na povu linamtoka mdomoni?” Baada ya
muda ujumbe ule ukajibiwa, “Hahaha, tayari huyo yani hapo kazi umamiliza
mdogo wangu. Unaweza ukaondoka sasa” Naye Salome akaandika ujumbe
mwingine, “Jamani dada tayari nini tena?” “Kwani huji?
Ameshakufa huyo” “Kheee kumbe dawa ilikuwa ya kummaliza kabisa! Mbona
mwanzo hukuniambia?” “Hivi wewe Ashura unasahau sahau nini,
nilishakwambia toka mwanzo kuwa huyo mtoto nataka nimmalize. Tena toka siku ya
kwanza nilikwambia hiyo dawa ni ya kummaliza kabisa, wewe cha kufanya saivi ni
kuondoka hapo upesi iwezekanavyo maana kazi tushamaliza. Si nilishakwambia na
nguo zako upange kabisa, nakutumia na hela muda sio mrefu ili
uondoke” Na kweli baada ya muda mfupi ikaingia meseji kwenye simu kuwa
amepokea milioni mbili na elfu kumi na tano. Kisha ikafatia meseji ya
kawaida, “Toa hiyo milioni mbili itakusaidia kwenye safari yako,
ukishafika nishtue nikutumie hela nyingine” “Hivi dada hawatanikamata
kweli?” “Akukamate nani bhana, kuna mtu anapajua kwenu hapo? Hakuna
anayepajua kwenu, hawakukamati wala nini. Kwanza Ashura sio jina lako, kwahiyo
watakutafuta hadi wachanganyikiwe” “Ila hawa wadogo wameona kama dada
yao ameanguka” “Achana nao hao, waondoe hapo nyumbani. Wape hata hela ya
biskuti ili wakatembee. Mimi hao nao nitawatokomeza ingawa sijui kuhusu ukweli
wao, ila usipoteze muda saivi. Ondoka upesi” “Sawa dada, ngoja
niondoke” Salome akamtazama Ashura waliyeishi nae kwa kipindi kirefu
sana ila kumbe kuna kazi alitumwa aifanye hapo, kisha akatoka nje na kuwapa
wadogo zake hela ya biskuti kama ambavyo Rose alikuwa amemshauri Ashura kwani
wale watoto walipenda sana michezo na kwa vyovyote vile wamepewa na hela ndio
kabisa. Hiyo hela aliipata kwa mama yake ambayo aliiacha kwaajili ya mboga ya
jioni. Kisha Salome akarudi tena chumbani kwa Ashura na kuanza kupekua
begi lake, ila alikuta nguo zote za Ashura zimepangwa vizuri sana na
vitambulisho vya Ashura alivikuta, na kushangaa sana. “Hadi vitambulisho
vimeandikwa Ashura kumbe sio jina lake mmmh!” Wakati anapekua zaidi,
alikutana na pochi yenye hela, alipozihesabu zile hela ilikuwa ni milioni tatu
na laki saba, “Mmh na mbona kila siku anasemaga hana hela
jamani!!” Alipopekua vizuri aliona kijitabu kimeandikwa andikwa namba za
simu, halafu kiliandikwa na namba za siri za kutolea hela kwenye simu, halafu
kilikuwa na namba zenye maelezo “Hawa ni watu nitakaowatumia kupoteza ushahidi”
Kidogo Salome alishtuka ila swala la kukuta namba za siri kwenye kile kitabu
zilimfurahisha kwani aliona kila kitu kimetimia sasa, akitoa na zile hela
atakuwa na hela za kutosha, alipojaribisha ile namba kwenye simu ili aangalie tu
salio lililopo kwenye simu kakuta kuna 10,050,000/= kwakweli Salome alishangaa
sana, “Kheee milioni kumi kwenye simu! Kumbewalikuwa wanaishi na
pedeshee humu ndani” Akaona ni vyema hiyo hela kabla ya kuitoa aifanyie
maarifa ya kuihamisha kwenye simu nyingine halafu ndio aitoe ila kwa wakati huo
akafanya namna ya kuweza kuzima lile swala la Ashura. Hivyo akatoka na kwenda
kununua viroba vikubwa vya kuweza kumtumbukiza mtu, na aliifanya kazi ile
mwenyewe alimtumbukiza Ashura kwenye vile viroba halafu akavifunga kwa juu
halafu akamviringisha shuka na kumtumbukiza kwenye kiroba kingine. Halafu zile
namba za wale watu alizozikuta kwenye kile kitabu cha Ashura ambao alikuwa
ameandika historia zao, akawasiliana nao kwa njia ya ujumbe kwa kutumia simu ya
Ashura kisha akawaelekeza pale kwao na mahali alipoweka huo mzigo wa mtu kwani
alikuwa ameuburuza hadi sebleni. Halafu yeye akatoka kwenda kutafuta simu
nyingine na laini ya kutumia yeye kwa kutumia zile hela alizozikuta kwenye begi
la Ashura, hakuwa na wasiwasi na wadogo zake kwani wale huwa wanarudi nyumbani
mpaka watafutwe na kuitwa. Ila alitumia ujanja wa kujificha sehemu hadi wale
vijana walipofika na kutoka na ule mwili na kuupakia kwenye gari na kutokomea
zao. Hapo alirudi tena pale kwao na kufunga milango halafu
akatoka. Rose alikuwa ni mtu mwenye furaha sana kwa wakati huo
hata akasahau kila kilichomtokea kwani mambo yote yalikuwa yamefutwa na kifo cha
mtu mmoja tu, kifo cha Salome. Kwakweli furaha yake ilikuwa maradufu, akaenda
kwa mumewe na kumwambia, “Leo, nataka nipike mwenyewe. Sema nikupikie
chakula gani?” “Mmmh leo umefurahi na nini mke wangu
jamani?” “Wewe sema tu ni chakula gani unataka” “Nipikie
chochote tu” Akaenda jikoni na kumuita Ana, kisha
akamwambia “Mwanangu, dadako si umuachie mdomo tu” “Hapana mama,
hawezi huyu ataropoka tu” “Ameshajifunza mwanangu, halafu leo nina
furaha sana muachie bhana” “Furaha ya nini mama?” “Yule mtoto
aliyekuwa ananisumbua kichwa siku zote, kila nilipojaribu kummaliza nilishindwa
hadi kuamua kumtafuta mtu wa kunisaidia. Ila leo naongea habari nyingine kabisa
tena kwa furaha, Yule mtoto amekufa” “Kheee mama, kweli hiyo ni habari
njema tena njema haswaaa” “Sasa sikia mwanangu, chukua simu yangu ile na
utoe hela benki halafu utume kwenye namba ya Ashura. Mtumie milioni tano, nataka
atulie kabisa huko alipoenda” “Sawa mama” Ilionyesha hii habari
pia Ana ilimfurahisha sana, kwahiyo akaenda kuchukua simu ya mama yake na
kufanya hivyo. Ana alikuwa ndio mtoto pekee aliyejua siri za mama yake, hata
namba zake za siri zote alimwambia mwanae huyo. Alipomaliza alimfata tena mama
yake na kumwambia, “Tayari mama nimemtumia” “Sawa, mtumie na
meseji kuwa nimemtumia hela nyingine maana najua kuongea kwa sauti hawezi sababu
ya hili tukio” “Sawa mama” Ana alituma ujumbe kwenye namba ya
Ashura, na baada ya muda tu ujumbe huo ukajibiwa, “Nimeipata asante
dada, saivi ndio niko njiani naelekea kule kijijini. Nishafuta hadi ushahidi,
yani hawawezi kujua Salome ametokomea wapi au amefia wapi maana nimewaagiza
vijana wautokomeze mwili wake kabisa kwahiyo hakuna ushahidi, na mimi nimeondoka
kabisa” Ana alimsomea mama yake ambaye kwa hakika alikuwa na furaha
zaidi, kisha akachukua simu ile kwa Ana na kuwapigia vijana ambao yeye alikuwa
anawafahamu, “Vipi mmeshafanya kazi ya Ashura?” “Tushamaliza
bi.mkubwa si unajua sisi hatucheleweshagi” “Sasa mmemtupia
wapi?” “Kwenye mapango huko, hawezi kuonekana kamwe. Yani kama watu
wataenda miaka ijayo hiyo basi watakuta mifupa. Ila Ashura ni jasiri sana kwani
tumekuta amemfunga vizuri kabisa.” “Sawa, sasa
amewalipa?” “Bado, amesema kuwa yupo safarini” “Basi msimdai
yeye hela, nawatumia sasa hivi” Kisha Rose akakata ile simu huku akiwa
na furaha zaidi halafu akawatumia hela wale vijana, kwakweli leo ilikuwa ni siku
ya furaha kabisa kwake. Salome aliamua kufanya jambo moja la
akili sana, alitafuta dalali siku hiyo hiyo na kuulizia kuhusu nyumba, kwakweli
ilipatikana yani maisha ukiwa na hela mkononi mambo mengi yanawezekana ila kama
huna hela kila kitu kinakushinda. Salome alilipia ile nyumba waliyoipata kisha
akatafuta vijana na usafiri wa kuanza kusafirisha vitu kwenye nyumba mpya, kisha
akawaita wadogo zake na kwenda nao huko kupya. Walipofika walikuwa wakishangaa
shangaa tu, “Dada, tumehamia kwingine! Mamdogo na mama wako
wapi?” “Mama atakuja, ila mamdogo kagoma kuja huku” “Jamani
dada, mwambie mamdogo aje” Mwingine akasema, “Ila bora agome,
Yule mamdogo simpendagi” “John, usiwe hivyo bhana. Mama ametufundisha
upendo” “Hatakama tumefundishwa upendo na mama, ila si kagoma mwenyewe.
Akiendelea kugoma dada Salome achana nae. Aje mama tu” “Sawa sawa mdogo
wangu John, wewe ndio kidume. Achana na Jose huyu anajifanya
mlokole” Basi Salome aliwaacha pale wadogo zake na kwenda kumalizia vitu
kwenye nyumba yao, halafu alitafuta watu wa kuwapangia vitu vyao ndani. Yote
hayo yaliwezekana kwa nguvu ya pesa tu. Walipomaliza kupanga, alirudi
pale kwenye nyumba yao ya zamani na kuwaacha wadogo zake kwenye nyumba mpya,
alienda kwa lengo la kumsubiri mama yake kwani usiku tayari
ulishaingia. Kwenye mida ya saa mbili hivi, Neema alirudi na kuingia
ndani. Alikuta nyumba yote nyeupe hakuna hata kitu ndani. Alipatwa na mashaka na
kuhisi kuwa wameibiwa, wakati anataka kutoka ili aulize kwa majirani ndipo
akakutana na Salome, “Imekuwaje mwanangu mbona
sielewi!” “Tumehama mama” “Tumehama, kivipi
sikuelewi” “Yani elewa tu kuwa tumehama mama, hapa nimekuja tu kukufata
ili twende kwenye nyumba mpya” “Tutahamaje wakati hapa kodi
haijaisha?” “Mama, mbona unakuwa mbishi hivyo! Nenda tu kazungumze na
mwenye nyumba mkabidhi funguo atafute mpangaji mwingine, sisi
tumehama” “Wengine wote wako wapi?” “Wapo huko kwenye nyumba
mpya” Kwakweli Neema alishindwa kuelewa kabisa kile kitendo cha kuhama
kwa gafla vile halafu Salome anamwambia akakabidhi funguo. “Hapana
siwezi kukabidhi funguo wakati sijui tulipohamia” “Inamaana mama
huniamini mimi?” “Nakuamini vizuri mwanangu ila kwa hili
unanichanganya” “Mama, tulikohamia ni mbali. Funguo twende tu ukakabidhi
leoleo” Kwavile Neema alimuamini sana binti yake, ikabidi aongozane nae
mpaka kwa mwenye nyumba na kumkabidhi funguo, “Mbona hamkusema jamani
kama mnahama? Halafu mbona ni haraka haraka?” “Nisameheni mimi ila haya
ni mambo ya Salome na mdogo wangu Ashura hata sijui wamefikiria nini ila ndio
hivyo tumehama” Neema aliwaaga pale kisha akaondoka na mwanae kuelekea
huko kupya walikohamia. Walifika kwenye mida ya saa nne usiku
hata wakawakuta wale wadogo zake Salome wamelala kwenye viti, “Mmh
jamani mmewachosha watoto na kuhamahama kwenu, hivi wamekula kweli hawa? Ashura,
Ashura” Neema alijikuta akimuita Ashura kwani alitaka ndiye amjibu kwani
yeye ni mtu mzima na atakuwa anjua mambo mengi sana, Salome alimuangalia mama
yake na kumwambia, “Ashura hayupo” “Wewe si nishakukataza, ni
mamako mdogo Yule. Haya hayupo yuko wapi?” “Kuna mahali ameenda, alisema
atarudi kesho” “Sasa na kuhamia hapa nani ametoa wazo hilo?” “Ni
yeye tena tumesaidiana nae hadi kuja hapa ila baada ya kupanga kila kitu
akaniaga na kuondoka. Wakati huo mimi nilikuja kukufata wewe, halafu yeye
alikuwa ameondoka” “Sasa watoto wamekula hawa?” “Ndio,
walinunuliwa chips wamekula, hata wewe za kwako zipo” Akaenda kumletea
mama yake, ambaye alikula bila kuhoji zaidi kwani njaa ilikuwa inamuuma, kisha
akaenda kumuonyesha chumba cha kulala yeye. Sababu alikuwa amechoka sana akasema
ile nyumba ataiangalia vizuri kesho yake, Salome akawachukua na wadogo zake na
kuwapeleka chumbani kulala. Kisha yeye alienda chumbani kwake. Hiyo nyumba
ilikuwa na vyumba vitatu vya kulala kama ile waliyokuwa wanakaa mwanzo ila
ilikuwa ni nzuri zaidi ya ile ya mwanzo. Neema alilala fofofo kutokana
na uchovu alionao wa siku hiyo kitu kilichomfanya ashindwe hata kuhoji vizuri
kuhusu ile nyumba na wazo la kuhama. Ila kulipokucha alichukua simu yake, na
akashtushwa na ujumbe kutoka kwa Ashura, “Dada samahani najua utakuwa
umefadhaika sana kwa kutokunikuta ila mimi lengo langu ilikuwa ni kuona dada
yangu unaishi kwenye mazingira safi na mazuri. Hiyo nyumba nimelipa kodi ya
mwaka mzima kwahiyo usihangaike kabisa dada yangu. Mimi nimeamua kurudi kijijini
kwetu kwa ndugu zangu nimewakumbuka sana, na huko mjini sitarudi tena. Wala
usihangaike kunitafuta dada yangu. Halafu huku mtandao unasumbuaga sana kwahiyo
mara nyingi nitakuwa sipatikani kwenye simu. Usihangaike kumuuliza Salome, hajui
chochote kuhusu kuondoka kwangu kwani ningemwambia ukweli kama naondoka angelia
ndiomana nimeondoka kimya kimya. Nawapenda sana ten asana, hata msiwe na
wasiwasi na mimi nipo salama kabisa” Neema alisoma ule ujumbe mara mbili
mbili ila alishindwa hata aanzie wapi kuhoji na ukizingatia kashaambiwa hata
Salome asimuulize. Kwakweli alibaki kimya tu akitazama ile nyumba kisha akatoka
na kwenda kuitazama vizuri zaidi. Wakati anaenda kwenye kila chumba
kukagua aliingia na kwenye chumba walicholala watoto wake mapacha na kuwaona
bado wamelala, kwakweli aliuthaminisha uzuri wa ile nyumba. Kisha akaingia
chumba anacholala Salome tena aliingia bila hodi, ila alimuona Salome amesimama
akiwa amempa mgongo hivi ila Neema alishtuka sana na kujikuta akisema kwa
mshtuko, “Aaah Moza!!” Salome aligeuka sasa na kumuangalia
vizuri Neema, lakini Neema alijikuta anaanguka
chini. Kisha akaingia chumba anacholala Salome tena
aliingia bila hodi, ila alimuona Salome amesimama akiwa amempa mgongo hivi ila
Neema alishtuka sana na kujikuta akisema kwa mshtuko, “Aaah
Moza!!” Salome aligeuka sasa na kumuangalia vizuri Neema, lakini Neema
alijikuta anaanguka chini. Salome akasogea na kumfata Neema pale chini,
kisha akamwambia kwa sauti ya upole, “Mama una nini
jamani?” “Mungu wangu, yani Salome ulivyosimama pale nimekuona kama Moza
halafu ulipogeuka yani sura ya Moza kabisa ikanijia. Nilichanganyikiwa kabisa
maana Moza ashakufa” “Jamani mama una mawazo sana, mimi ni mwanao Salome
yani hata usiwe na mashaka. Sasa mimi nawezaje tena kuwa Moza!” “Hapana
mwanangu, nahisi ni utu uzima huu” Neema akapumua sasa hata jambo la
kuongea alilokuwa nalo lilipotea kabisa kwani miguu yake ilikuwa kwenye
mtetemeko wa hali ya juu, ikabidi Salome amsaidie Neema kuinuka pale kisha
akampeleka sebleni ambapo alikuwa kimya kabisa akionekana kutafakari jambo
Fulani. Muda kidogo wale wadogo zake Salome waliamka na kutoka pia kisha
wakamsalimia mama yao na dada yao. Baada ya Salamu alianza kuongea
John, “Yani leo nimelala usingizi wa raha kweli yani!” Salome
akamuuliza mdogo wake huyu, “Umelala usingizi war aha, hebu tudokeze
kivipi?” “Yani kule tulipokuwa tunakaa zamani, mindoo yote ya maji
chumbani kwetu ila leo tumelala chumba cheupe chenye kitanda tu” Mama
yao nae akawaambia, “Kumbe yale mandoo yalikuwa yanawakera eeeh!
Mnatakiwa kuzoea maisha yote” Kisha Salome akamuangalia mama yake na
kumwambia, “Mama unajua hawa watoto sasa wamekuwa wanatakiwa waende
shule” “Natambua hilo mwanangu, ila hela kwasasa sina” “Sasa
mama, ila nitafanya jambo na wataenda shule hawa. Wamekuwa
sasa” “Utafanya jambo gani? Wewe utapata wapi hela?” “Mama tulia
tu ila hela nitapata” Kisha Salome akawachukua wadogo zake ili
akawaandalie chai, kwakweli Neema alikuwa akimshangaa tu mwanae chauvivu
alivyokuwa siku hizi. Siku ya leo, Rose aliruhusu watoto wake
kutoka pia alimruhusu Patrick kutoka kwani alikuwa na furaha sana, kasoro kwa
Sara tu ambaye hakuweza kuongea ndio alikaa ndani kama mwali hivi, kwa upande
mwingine wa moyo wake alimuhurumia mwanae Sara ila kwa upande mwingine aliona ni
vyema apate adabu kidogo kwani ni yeye aliyevuruga mwenendo mzima wa mazishi ya
Moza, hakutaka mtu yeyote kwenda nyumbani ila Sara sababu ya kiburi chake
akaenda. Akiwa ametulia zake sebleni, huku Sara nae yupo sebleni
akiangalia tu Tv ila kuongea ndio alikuwa haongei, mara ujumbe mfupi ukaingia
kwenye simu ya Rose, alipoangalia ulikuwa unatoka kwa Ashura, “Dada
niongezee hela kidogo, halafu huku mtandao unasumbua sana yani nitakuwa
sipatikani kabisa. Ukiniongezea hiyo hela sitakusumbua tena” Rose
alisikika akisema, “Aaah huyu nae kashafanya ndio kitega uchumi wake
mimi loh! Namtumia hiyo hela na bora asipatikane kabisa maana sasa anaanza
kuniudhi. Miela yote niliyokuwa nampaga halafu kazi yenyewe kaichelewesha hadi
leo” Sara alikuwa akimsikia tu mama yake huku akitamani kumuuliza kitu
ila alishindwa, basi Moza akatuma hela na kumuandikia
ujumbe, “Nimekutumia hiyo milioni tano nyingine najua itakusaidia, na
wewe kuwa makini huko utafute biashara ufanye maana kazi yangu huku mjini
ushamaliza.” Alipotuma kidogo tu akajibiwa ule ujumbe, “Asante
dada wala usijali sitakusumbua tena dada yangu” Basi Rose akapumua sasa,
ila kila alipomuangalia mtoto wake alimuonea huruma sana. Muda mfupi
wakapata mgeni, alikuwa ni Ommy. Rose alipomuona hakupendezewa nae wala nini ila
alimkaribisha tu kwa shingo upande. Basi Ommy akamsalimia Sara pale ila Rose
akajibu kwa niaba ya Sara, “Anaumwa kifua huyo, sauti
haitoki” “Jamani hata kidogo ya kunijibu tu!!” “Hivi Kiswahili
unaelewa wewe, nishakwambia anaumwa kifua huyo sasa akujibu nini?” “Sawa
mama, ila ameshaenda hospitali?” “Kwahiyo wewe ndiye unayejali afya yake
sana kushinda mamake mzazi niliyemzaa! Yani nikae na mgonjwa mpaka muda huu
nikisubiria ushauri wako tu! Naomba uondoke, kwanza sikupendagi wewe kijana basi
tu” Ommy akaomba msamaha, kisha akainuka na kuaga na kuondoka zake. Sara
machozi yalikuwa yakimtoka tu, mamake akamuangalia na kumwambia “Sasa
kinachokuliza ni nini? Unafikiri mimi sikuhurumii? Mdomo wako ndio haukuhurumii
ila mwanangu usijali nitamwomba Ana akirudi akusamehe mwanangu” Halafu
Rose akainuka na kwenda chumbani kwake, kile kitendo tu cha Rose kuinuka na
kwenda chumbani, Sara nae aliinuka na kutoka nje. Alipofika getini,
mlinzi alimuuliza, “Madam vipi unashida na Yule rafiki yako
nimkimbilie” Sara akaitikia kwa kichwa tu, ila mlinzi akaelewa na kuona
kuwa kaitikiwa vile kutokana na mapozi ya matajiri ila alitoka na kumkimbilia
Ommy, bahati nzuri hakuwa amefika mbali, naye ommy akasikia wito na kurudi
ambapo Sara alitoka nje ili aweze kuzungumza na Ommy japo kwa
vitendo. Ommy alivyofika pale, alimkumbatia Sara na
kumwambia, “Nieleze Sara umepatwa na nini tena?” Ila Sara
hakuweza kumjibu ila alimuomba simu yake kwa vitendo, kisha alivyompa akafungua
sehemu ya ujumbe na kumuandikia, “Mdogo wangu ni mchawi Ommy, ndio
amenifanya hivi. Kanifunga mdomo nisiongee kabisa. Nisaidie” Ommy
alishika simu na kusoma ule ujumbe, kwakweli alishtuka sana na kujikuta
akimuuliza kwa sauti ya chinichini, “Mdogo wako yupi? Ana
au?” Sara aliitikia kwa kichwa, ila muda si muda Ana nae alirudi kutoka
shuleni hata wakamshangaa maana sio kawaida yake kutoka shuleni mapema
hivyo. Ana akamuangalia Sara kwa jicho kali sana, Sara alijikuta
akitetemeka na kuingia ndani bila kujidhania kisha Ana nae akaingia ndani na
kumuamuru mlinzi afunge geti. Ommy aliweza kuelewa kinagaubaga kuhusu
kinachoendelea mule ndani, basi akaondoka zake. Ana
alimtanguliza Sara mbele na walipofika sebleni tu akaanza kufoka hadi mama yake
akatoka nje. “Vipi tena mwanagu kuna nini?” “Mama, ndio mtu wa
kumsamehe huyu!” “Kafanyaje tena?” “Nimemkuta nje ya geti
anaongea na kale kamchumba kake” “Khee alitoka nje ya geti, weee Sara
wewe jamani kwanini lakini? Yani kwenda chumbani tu kidogo ukaamua ukifate kile
kibwana chako? Na utaendelea kuwa bubu mpaka akili ikukae sawa” Sara
machozi yalikuwa yakimtoka tu na kwenda chumbani kwake huku akitokwa na machozi
zidi ila bado kuongea hakuweza. Pale sebleni alibaki Ana na mama
yake, “Mwache nimkomeshe mama” “Ila namuhurumia mwanangu jamani,
ila mbona leo umewahi kurudi?” “Nishawavuruga na huko
shuleni” “Kheee umewavuruga!” “Ndio, mwlimu mkuu na walimu wake
leo hawaelewani” “Kwanini umefanya hivyo mwanangu?” “Nimejisikia
tu, kwahiyo wenyewe wameturuhusu shule nzima turudi nyumbani” “Mmmh
mwanangu, sasa huko siko. Wale ndio walimu wenu sasa ukiwafanyia hivyo
mtafundishwa na nani?” “Mama hujui tu, kuna mwalimu bonge huyo kanifokea
leo yani yeye ndio kanifanya nijaribishe vitu vyangu. Kwanza nimemfanyia mchezo
akaanguka chooni halafu nimetoa maelewano kwa walimu wote hadi wameturuhusu
turudi nyumbani, nina hakika atajutia mule mule chooni maana sidhani kama
atapata wa kumtoa” “Mmmh mwanangu umekuwa kiboko, yani saivi sijui kama
kuna mtu atatubabaisha tena” Ana akacheka kisha akaelekea chumbani
kwake. Sara nae alikuwa chumbani kwake huku akiwaza cha kufanya akaamua
kuwasha simu yake kwani alihisi huenda Ommy akamtafuta, na kweli alipowasha tu
akakutana na ujumbe wa Ommy, “Pole sana Sara kwa tatizo lako, ila kuna
mzee nimekutana nae nimemueleza. Basi badae nitakupigia simu akuelekeze namna ya
kufanya halafu utafanya na amesema utaongea tu” Sara nae akamjibu
Ommy, “Nashukuru sana, simu niko nayo hapa kwahiyo ukipiga tu nitapokea
yani nikipokea uanze kuongea kwani itakuwa tayari sikioni mwangu” “Sawa,
usijali Sara” Basi Sara akaiweka ile simu makini kabisa ili akipigiwa na
Ommy apokee. Siku ya leo, Neema hakutoka kwenda popote alibaki
tu nyumbani kwake akitafakari kisa na mkasa halafu akishindwa hata kumuuliza
Salome kwani akikumbuka ule ujumbe ulimwambia kuwa asijisumbue kumuuliza
Salome. Akiwa amekaa sebelu yao hiyo mpya, kwenye mida ya jioni alikuja
Salome na kumwambia habari ambayo alipoisikia hakuipenda hata
kidogo, “Mama, kesho nataka kwenda kwa baba yangu” “Unasemaje
wewe?” “Kesho nataka kwenda kwa baba yangu” “Hivi wewe Salome
una matatizo gani jamani, baba yako unayemuongelea ni yupi!” “Patrick
mama, najua baba yangu anaitwa Patrick. Nataka kesho niende kwa baba
yangu” “Unapajua?” “Ndio napajua, wewe subiria tu kesho nikienda
kwa baba yangu” “Salome una nini lakini mwanangu, mwenzio nakupenda sana
na sitaki kukupoteza. Aliyekwambia baba yako ni Patrick nani?” “Mamdogo
Ashura aliniambia ukweli wote hadi anapoishi baba yangu alinielekeza, aliniambia
kila kitu kuhusu baba yangu” “Mmh haiwezekani, Ashura akwambie wewe
haiwezekani” “Sasa mimi nimejuaje?” “Sijui ila Ashura, labda
lakini siamini nitamtafuta badae aniambie vizuri” “Wewe mtafute tu ila
kesho naenda kwa baba yangu. Yule ni baba yangu mama utanificha hadi lini? Mimi
ni binti mkubwa sasa” “Salome tafadhali usinitafutie
makubwa” “Yani mama huna cha kunishawishi kwakweli hata useme nini ila
kesho naenda kwa baba yangu” Neema hakuongea neon la zaidi, akainuka na
kwenda chumbani kwake. Muda huo Salome nae aliinuka na kwenda
chumbani. Basi Neema akaanza kupiga simu ya Ashura ila iliita sana bila
ya kupokelewa mara akapokea ujumbe, “Tuma meseji nipo kwenye
kelele” “Ashura mdogo wangu umeanzaje kumwambia ukweli Salome kuhusu
baba yake jamani! Unajua ni mabalaa unayaanzisha, kumbuka Yule mama
alisemaje!” Muda kidogo ujumbe ule ukajibiwa, “Dada, Salome
amekua sasa ana haki ya kumjua baba yake ndiomana nimemwambia. Na ukae nae chini
umueleze ukweli wote, amekua huyo dada tutamficha hadi lini? Nimemwambia ukweli
kuwa baba yake yupo na anitwa Patrick halafu anapokaa nimemuelekeza. Mwache
mtoto amtafute baba yake. Kila mtu ana haki ya kumjua baba yake” Neema
aliposoma huu ujumbe akapumua kidogo kwani siku zote aliyekuwa mkali kwa Salome
kumjua baba yake ni Ashura sasa ilimradi huyo Ashura amekubali basi hakuna wa
kupinga. Kwenye mida ya jioni kabisa, Sara akiwa chumbani kwake
akaingia Ana na kumuangalia dada yake. Muda kidogo simu ya Sara ikaanza kuita
basi Sara akaichukua ila alienda Ana na kumpora kisha akaipokea na kuiweka
sikioni ili amsikie mpigaji anasemaje maana aliona jina Ommy, kwakweli Sara
aliona kabisa mwangaza wake umetoweka kwani Ana ndio alkuwa akisikiliza kila
kitu ambacho mzee aliyetafutwa na Ommy alikuwa akimwambia Sara basi alipomaliza
kumsikiliza akakata ile sime kisha akamuangalia dada yake na
kumwambia, “Yani wewe hukomi, hukomi kabisa eti umeamua utafutiwe mganga
wa kienyeji akusaidie. Hivi hujui kuwa huyo mganga nikiamua hata yeye namfanya
mbaya! Ila wewe nitakukomesha maana kinachokupa jeuri sasa ni hayo macho, na
hutatazama tena” Pale pale macho ya Sara yakajifunga na hakuweza
kuangalia tena, kwakweli machozi yalikuwa yakimtoka tu. Kisha Ana
akaondoka zake na kwenda sebleni, hata kaka zao walivyorudi siku hiyo na kutaka
kwenda kumtazama Sara walizuiliwwa na Ana, walitii kutokana na kile kitendo
alichowafanyia siku ya kutaka kumpeleka Sara hospiatali. Rose alijifanya
kama hayupo kwenye matatizo ya mwanae huyo na wala hakuonekana kumsaidia tena,
wala kwenda kumuona alivyofanywa kipofu amakweli mtu akishakuwa na roho ya
kichawi anakuwa mnyama na huruma inamtoka kabisa. Usiku ulifika na wote
kwenda kulala. Asubuhi kulivyokucha kama kawaida, watu
waliondoka wote mule ndani tena na siku ya leo hata Rose aliondoka ingawa mwanae
alikuwa haoni na yuko ndani. Ila tu alimtoa na kumuweka sebleni kisha
akamuacha hapo na kuondoka, kwahiyo mlinzi alikuwa anajua ndani kabakia Rose ila
hakujua kama hakuwa na uwezo wa kuongea wala kuona. Muda kidogo wakati
Yule mlinzi yupo pale getini akamuona Salome na kumfanya
amshangae, “Karibu ila umekuja wakati Moza alishakufa” “Nilipata
habari ila mimi sijamfuata Moza” “Umemfata nani kwani?” “Kuna
nani ndani?” “Yupo Sara peke yake, wengine wote wametoka” “Sawa,
basi huyo ndio nimemfata” Mlinzi hakuwa na jinsi zaidi ya kumkaribisha
tu, ambapo Salome aliingia moja kwa moja ndani hadi sebleni na kumkuta Sara
amekaa tu kwa kujiinamia huku machozi yakimtoka. Salome alimfata Sara pale
alipokaa, “Ni wewe ndiye umenifanya nije kwa wakati huu” Sara
alitamani kuongea lakini, alishindwa akaendelea tu kumsikiliza huyu
Salome, “Funua kinywa chako” Sara alifunua kinywa na
akanyunyuziwa dawa kama matone halafu gafla akajikuta akiweza kuongea, na
kuuliza kwa sauti ya upole, “Wewe ni nani uliyekuja
kunisaidia?” “Unataka kuniona?” “Ndio nataka
kukuona” Basi Salome akachukua dawa na kunyunyiza kwenye macho ya Sara,
na hapo hapo Sara akafikicha macho yake na kuona ila alipoinua macho vizuri ili
amtazame aliyemsaidia alishtuka sana na kusema kwa nguvu, “Kheee
Moza!” Basi Salome akachukua dawa na kunyunyiza kwenye
macho ya Sara, na hapo hapo Sara akafikicha macho yake na kuona ila alipoinua
macho vizuri ili amtazame aliyemsaidia alishtuka sana na kusema kwa
nguvu, “Kheee Moza!” Sara alikuwa akihema juu juu na muda kidogo
akazimia ila Salome akammwagia maji na kuzinduka, Sara akawa anamuangalia Salome
sasa, na kumuuliza “Mara ya mwisho nilikuona na Moza
eeh!!” “Ndio nilikuwa na Moza” “Ila mbona wakati ule nilipoanza
kuona nimekuona kama Moza!” “Sijui, labda mawazo yako unamfikiria
Moza” “Inawezekana, ila asante kwa kunisaidia maana nilihisi ndio mwisho
wangu” “Usijali, sikuweza kuvumilia ilihali najua unateseka ingawa
nataka hapa niletwe na mama yangu” “Aaah unataka kuja kuishi hapa
eeeh!” “Ndio si kwa baba yangu, nataka niishi na baba
yangu” “Karibu sana, hivi unaitwaga nani vile maana mimi najua jina la
Maria ndio alikuwa mtoto wa baba ila Moza alisema jina lingine” “Naitwa
Salome ingawa sijui ni kwanini walinibadilisha jina” “Na umejuaje kama
baba ni baba yako?” “Siku nyingi sana nilitamani kumjua baba yangu, ila
sasa nimemjua ni furaha kubwa sana kwangu. Je wewe unatambua chochote kuwa
kwanini walinificha nisijue?” “Hata sijui kwakweli, hata mimi sielewagi
ni kwanini ila nilikuwa namsikia mama na Ashura wakiongea kuwa haipaswi kabisa
wewe kuujua ukweli” “Sawa, ila saivi nimeshajua. Naomba ndugu zako
wasijue kama nilikuja na nimekufanya uone na kuongea” “Hawa si ndugu
zangu kwakweli, ni wachawi. Kumbe mdogo wangu Ana ni mchawi sana, hata sikujua
kama nitapona. Sijui wewe ni mganga?” “Hapana ila nimewasikia
wakikuongelea roho ikaniuma sana, ndio nikaamua nikusaidie. Ila usiseme kama ni
mimi nimekusaidia” “Sawa sisemi, ila wewe utakuja lini kuhamia hapa
nyumbani?” “Nitakuja tu hata usijali!” “Niambie ni lini bhana,
mimi nitaondoka humu nyumbani hadi urudi” “Hata usiondoke, wakukute hapa
hapa na kwa hakika hawatakufanya chochote halafu wakirudi jifanye haujapona
uweze kuwasikiliza maongezi yao yote kwanza. Hata usiwe na mashaka nitakusaidia,
ila usimwambie yeyote kama nimekuja hapa. Kwaheri, mimi naondoka hadi wakati
mwingine nitarudi rasmi” Salome aliondoka, ila Sara alijiangalia mara
mbili mbili na kwenda chumbani kujiangalia kwenye kioo ila bado hakuamini kama
amepona kabisa na anaona na kuongea. Akachukua simu yake na kumpigia Ommy kuwa
aje nyumbani kwao, kwakweli Ommy alifurahi sana na kumuahidi kufika muda sio
mrefu. Basi Salome nae alitoka getini na kumuangalia Yule mlinzi kisha
akamwambia, “Wewe si upendi umbea eeh halafu umbea ufanyagi, tafadhali
iwe ni siri yako kama nilifika hapa siku ya leo” Salome akaondoka zake
huku mlinzi akimshangaa na kujiuliza, “Huyu dogo aliambiwa na marehemu
Moza nini kuwa mimi sipendi umbea mmmh!” Alimshangaa sana na kumuangalia
hadi alipoishia kuondoka. Muda kidogo Ommy alifika na kugonga
geti kisha kuingia ndani, na alipoingia tu akamuita sara ambaye alitoka
sebleni, “Eeeh Sara unaongea?” “Ndio naongea” Ommy
akamkumbatia sara, pale kisha akakaa nae, “Eeeh niambie ni dawa za Yule
babu eeh!” Sara akatamani kumueleza yaliyojiri ila akahofu kwamba Salome
alimwambia kuwa asiseme, “Mbona kama unasitasita
hivi?” “Natamani kukueleza yaliyotokea ila nashindwa sababu nimeambiwa
nisiseme” “Aaah jamani Sara umenza kunificha tena
mpenzi!” “Hapana sikuficha, ila kiukweli Yule babu amenisaidia sana.
Ndio kafanya nipone kwakweli” Ommy alifurahi sana na kumkumbatia tena
Sara, kisha wakaenda pamoja jikoni na kupika chakula na kula, chakula kilikuwa
kingi tu kwahiyo walikula na kubakisha kisha Sara akafunika kile chakula jikoni
kwao. Kwakweli walikuwa na furaha sana, tena siku hiyo Ommy alishinda nae sana
Sara hapo nyumbani kwao, hadi alivyoona jioni jioni akaaga na kuondoka
zake. Kwahiyo sara akabaki mwenyewe ndani, tena alienda kukaa pale pale
sebleni, muda kidogo mama yake pamoja na Ana walikuwa wamerudi na walikaa pale
pale sebleni wakizungumza kwani Sara alikuwa kama mtu aliyelala, “Leo
shuleni mwanangu imekuwaje maana sijaelewa eti” “Mama nadhani kuna
walimu pale wachawi pia” “Kwanini?” Nilitaka kwenda ofisini ila
nikajibanza na kusikia mazungumzo yao, eti Yule mwalimu niliyemuangusha jana
chooni leo kaja kazini” “Kheee kaja kazini wakati ulisema hata kuinuka
hatoweza?” “Ndio ilitakiwa iwe hivyo mama, sasa nikamkuta Yule mwalimu
akiwasimulia wenzie. Kuwa jana shule nzima ilikuwa kimya nay eye ameanguka
choono mara gafla akatokea binti mmoja ambaye hamjui na hajawahi kumuona, eti
binti Yule alimuinua na kumpaka dawa halafu akamwambia amepona. Eti Yule binti
akaondoka na kumuacha Yule mwalimu akienda nyumbani kwake” “Jamani mbona
hiyo habari ya ajabu sana, au kuna waganga pale shuleni kwenu?” “Mama,
kwa uchawi wangu hakuna mganga anaeuweza hata nashangaa imekuwaje. Ndio
wamenibamba pale nasikiliza umbea ndio wamenipa adhabu ya kukaa ofisini mpaka
wewe ulipokuja kunichukua. Kwakweli wale walimu wamenikera sana ila sijawafanya
chochote sababu nilikuwa na mawazo” “Ila mwanangu inabidi tujue huyo
mwalimu kwanini imekuwa hivyo. Na huyo binti aliyemtokea ni nani” “Mama
hata usijali, nitahakikisha najua kila kitu na kama ni mganga huyo mtu
nitamkomesha” “Yani nimeshangaa sana mwanangu jinsi ulivyo hatari saivi
eti vinatokea vitu vya kuzuia mambo yako. Nimeshangaa sana” “Mama tulia,
nitafanya kitu utaona tu” Akainuka na kwenda ndani, kisha Rose
akamuangalia Sara aliyeonekana amelala pale kwenye kochi halafu akainuka na
kwenda chumbani. Sara alikuwa akiwasanifu tu maana alisikia kila kitu
walichokuwa wakiongea. Walipoenda chumbani, nae akainuka sasa na kwenda chumbani
kwake. Ila muda kidogo akakumbuka kile chakula ambacho alikifunika
jikoni, basi akataka kwenda kukitoa ili wasielewe kama alipika siku hiyo,
alipofika jikoni kile chakula hakukikuta ila aliona sahani nyeupe kabisa
kanakwamba kuna mtu amekula, “Inamaana muda huu huu Ana au mama ametoka
kula au ni nini? Hivi wanaweza kula chakula bila kuuliza nani
kapika?” Akajiuliza na kuondoka kule jikoni kisha akarudi chumbani
kwake, ila ilikuwa ngumu sana kwake kuelewa kuwa kile chakula kimeliwa na nani
maana hakutegemea kutokukikuta ukizingatia mama yake pamoja na Ana walishaenda
chumbani. Alikaa chumbani kwake akitafakari tu ila aliweza kuhisi sasa kuwa
nyumba yao ni zaidi ya anavyoifikiria yeye. Salome akiwa
amefika nyumbani kwao, akamkuta mama yake yupo ndani, kisha Salome alipoingia tu
akamuanza na maswali, “Unajua sehemu niliyokuaga naenda asubuhi,
nimeenda na kurudi. Ila sasa niambie ukweli wewe ulikuwa
wapi?” “Nilienda kwa baba” Neema akashtuka na kujikuta
akimuuliza tena, “Unasemaje Salome?” “Nilienda kwa
baba” “Unaoajua?” “Napajua ndio, si mamdogo Ashura
alinielekeza!” “Wewe mtoto wewe usiniletee makubwa
mimi” “Makubwa yapi mama? Yani baba kafurahi sana kuniona na alitaka
nikae pale moja kwa moja nikamwambia bado sijamuaga mama” “Nitolee balaa
lako hilo Salome” “Sio balaa mama, yani baba kwa furaha aliyokuwa nayo
kanipa hadi pesa za matumizi” “Pesa za matumizi? Ziko
wapi?” Salome akatoa pesa ambazo zilikuwa ni elfu kumi kumi, akampa mama
yake. Kwakweli Neema aliishiwa nguvu kabisa kuona zile hela akataka aanze
kuzihesabu, “Hata usijisumbue kuhesabu, kaniambia ziko milioni
tatu” “Milioni tatu? Yani Patrick akupe wewe milioni tatu! Wakati huo
mke wake alikuwa wapi?” “Mkewe alikuwepo na mbona kasapoti tu, tena
alitaka niongezewe ila baba akasema hizo za kuanzia” “Mmh Salome wewe
unanishangaza” “Mama hata usishangae ila nieleze ukweli kwanini
ulinificha kuhusu baba yangu?” “Aaah unajua mwanangu, aaah yani hata
sijui nianzie wapi. Achana na hizo habari bhana” Salome akachukua zile
hela kwa mama yake, “Sasa mbona umechukua tena wakati ulinikabidhi
mwanangu!” “Mpaka uniambie ukweli, mimi ni binti mkubwa sasa. Nataka
kujua ukweli wa kwanini ulikuwa unanificha kuhusu baba yangu” “Basi
naomba nikuelezee kwa kifupi, si utanipa hizo hela eeh!” “Mi nitakupa
ila niambie ukweli” “Ni hivi, Patrick amewahi kuwa mume wangu, tena ni
mume wa ndoa kabisa. Nilifunga nae ndoa ya kanisani huko kijijini kwao. Ila
niliishi nae muda mrefu sana bila ya kupata mtoto, yani mimi na Patrick tulioana
mapema sana. Kipindi hicho nilikuwa na miaka kumi na sita halafu yeye alikuwa na
miaka ishirini. Baada ya kuishi muda mrefu bila kuzaa takribani miaka kumi
ilipita ndipo tulipohamia mjini na kuendelea tena na maisha ila sikuwahi kupata
mimba hata ya kusingiziwa hata mwenyewe nilikuwa nashangaa maana sikuwahi kutoa
mimba maishani mwangu. Miaka ilienda tu sibebi mimba wala mdudu wa mimba, basi
mjini hapa biashara za Patrick zikaanza kutanuka akawa na mali nyingi na
biashara kubwa kubwa ila kilichokosesha furaha ndoa yetu ni mtoto tu. Siku moja
mume wangu alizna kufanya biashara na mwanamama aitwaye Rose, Yule Rose alikuwa
Rose kweli kipindi hicho alikuwa mzuri haswaaa sio kama siku hizi hata mimi
mwenyewe nikawa na mashaka ya kuibiwa penzi langu na rose ingawa alikuwa ni
mkubwa sana tu kwangu. Ila naye alikuwa mfanyabiashara, gafla nikaja kusikia
Patrick kuna mjengo amejenga huko anaishi na Rose kumbe mimi ananiaga kuwa
anasafiri halafu anaenda kuishi na Rose, kuna kipindi alipotea kama miaka mitatu
kumbe ndio yupo huko anaishi na Rose. Akarudi na kuishi na mimi kama wiki kumbe
ananitafutia sababu ya kunifukuza. Siku hiyo Patrick alikuja na kuniambia wazi
kuwa amechoka kuishi na mwanamke asiyezaa, miaka inaenda lakini mwanamke sizai
na akaniambia ameamua kuwa na huyo Rose mwenye watoto tayari kwani anaamini huyo
atamzalia ukizingatia tayari ameshazaa watoto watatu, nilisononeka sana. Patrick
akanifukuza pale nyumbani kama mbwa kisha ile nyumba nasikia alipangisha.
Nilianza maisha ya kutangatanga na badae nikajigundua kuwa nina ujauzito,
nilijua ile mimba ni ya Patrick nikawa nataka niende kumwambia ila siku hiyo
nilikutana na Rose akaniambia nikithubutu kusema basi ataninyonga na
kukinyongelea mbali kitoto changu. Ila bado nilijipa matumaini kuwa Patrick
akigundua atafurahi, nilihangaika na ile mimba, nakumbuka nilienda kujifungulia
kijijini kwa kina Patrick, na mtoto nilimuita Maria Patrick. Jina Maria ni jina
ambalo mwanangu ulipewa na bibi yako yani mama mzazi wa Patrick nami
nililifurahia sana. Yule mama alinipenda na ndio akaanza kumsumbua Patrick kuwa
anirudie mimi na tulee mtoto wetu lakini mambo yakawa si mambo tena, siku hiyo
isiyo na jina walikuja vijana na kuvamia pale nyumbani kwa mama Patrick na ndani
tulikuwa tunaishi mimi, na mtoto mdogo ambaye ni wewe pamoja na mama yake
Patrick. Wale vijana walimchinja mama Patrick mbele ya macho yangu, kwa hakika
siwezi kusahau kamwe na nikaambiwa niondoke tena nisionekane kabisa hapo
kijijini kwani nitachinjwa na mwanangu kama walivyofanya kwa huyo mama.
Walinitishia na niliogopa sana, ingawa ulikuwa ni usiku nikatoka na kukimbia kwa
bahati nilikuta watu njiani wakisubiri gari lao nikawaomba lifti na kuja nao
mjini. Niliteseka sana na wewe mwanangu yani sikuwa na raha ya maisha kabisa,
sikutaka tena kurudi kwa Patrick wala ndugu zake kwani nilihofia yasije
yakawapata kama kilichompata mama Patrick. Nilikaa kama miaka mitatu au mine
mjini nikitangatanga, ndio kwa bahati nikampata Ashura aliyejitambulisha kama
mdogo wangu na toka siku hiyo nikaanza kuishi na Ashura tena ni yeye
aliyenishauri nikubadilishe jina ili tusifatiliwe tena. Badala ya Maria tukuite
Salome tena akaniambia kuwa Rose amezaa na Patrick mtoto anaitwa Ana basi
nikajua furaha ya Patrick imetimia sasa maana kama mtoto ameshapata, basi ndio
imekuwa hivyo hadi leo. Naomba nisiendelee sana mwanangu, mengine utayajua
taratibu tu. Basi nipe hizo hela” Salome alichukua zile hela na
kumkabidhi mama yake, kisha akainuka na kwenda chumbani ambako alikuwa akipanga
mipango mipya sababu ameshajua yote aliyotaka kuyajua. “Sasa nimeelewa
kwanini Ashura alitumwa, lakini lazima kuna kitu kilikuwa kizuizi cha kuwachinja
wahusika na kuishia kumchinja mamake Patrick. Hivi Patrick anajua kweli kama
Yule mwanamke ndiye alimuulia mama yake? Najua hajui ila atajua tu” Ila
kumbe alikuwa anawaza kwa sauti halafu Neema nae alikuwa amekuja chumbani kwa
Salome na kujikuta akimuuliza, “Kujua nini?” “Hamna mama kuna
kitu nafikiria tu, ila mama na wewe jiwekee utaratibu basi wa kugonga mlango
kabla ya kuingia ninapolala” “Hivi wewe Salome utanificha nini mimi,
maana mimi ni mwanamke na wewe ni mwanamke. Hakuna cha
kufichana” “Hatakama mama ila ni vizuri kuwe na utaratibu
huo” “Basi nitakuwa najitahidi, ila hizi pesa zimenichanganya yani hadi
najiona kama namiliki dunia vile” “Yani mama milioni tatu tu ndio
inakuchanganya hivyo!” “Kwa mimi ni kubwa sana, ten asana yani hapa hadi
sina maneno. Ngoja kesho nikafungue akaunti benki” Salome akacheka tu
jinsi mama yake alivyopagawa na zile hela ila ukweli wa hela zile angeujua sijui
angefanyeje. Mapacha wa Rose walirudi na moja kwa moja wakaenda
kumsalimia dada yao chumbani, “Sara tumekuja kukujulia hali. Najua
unatusikia tu ila kuongea na sisi huwezi ila tunakupenda dada yetu. Bado
tunazunguka sehemu mbalimbali tukiulizia tiba ya tatizo lako.” Sara
akainua kichwa na kuwatazama, kisha akawaambia, “Asanteni kwa upendo
wenu” “Khee Sara unaongea!” “Ndio naongea” Kwakweli
walifurahi sana na kumkumbatia dada yao, yani ile furaha yao hata ikawashtua
Rose na Ana. Walishtuka na kujikuta kwa pamoja wakienda chumbani kwa Sara,
kwakweli nao walishangaa sana kumuona Sara anaona na kuzungumza. Naye Sara
aliwauliza, “Sasa mnashangaa nini jamani? Hamjapenda
nilivyopona!” Ana alisonya yani sonyo ambalo hata kaka zake walishtuka
ila hakuna aliyemkaripia, basi Sara akaongea tena, “Hata ukinisonya ni
kazi bure tu, nimeshapona yani nimepona kabisa na huniwezi
tena” “Unasemaje wewe Sara?” “Huniwezi tena” Ana akataka
kufanya jambo pale ila mama yake akamzuia kuwa asifanye kisha akatoka nae na
kumuacha Sara na kaka zake. Mmoja akamwambia, “Dada unajiamini sana eeh!
Yule mtoto kawa noma” “Kuna noma zaidi yake, aliniweza mwanzo ila
kwasasa haniwezi tena” Sara aliongea kwa kujiamini, hadi kaka zake
wakataka sara awatajie huyo aliyemfanyia dawa akapona na huyo noma wa
Ana. “Nyie subirini tu, akija nitawaambia kwamba huyu ndio kiboko ya
Ana. Anajifanya mjanja sana kumbe kuna wajanja zaidi yake, najua hata
akinifanyia kitu atakuja Yule na kunisaidia. Kma ameweza kumsaidia mwalimu
asiyemfahamu sembuse mimi” Mara Ana akaingia tena chumbani kwa Sara na
kusema, “Nimekusikia yote, subiri nikuonyeshe” Kabla hajaanza
kufanya chochote chumba cha Sara kikaanza
kutikisika. Mara Ana akaingia tena chumbani kwa Sara
na kusema, “Nimekusikia yote, subiri nikuonyeshe” Kabla hajaanza
kufanya chochote chumba cha Sara kikaanza kutikisika, wote walichanganyikiwa cha
kushangaza hata ile hali ilimchanganya pia na Ana hadi akajikuta akipiga kelele
ambazo zilimshtua hadi mama yao chumbani. Kelele za Ana zilifanya watu wote mule
chumbani wazimie. Rose aliingia chumbani na chumba kikaacha kutikisika, alikuwa
akishangaa sana na kumuuliza Ana aliyekuwa amesimama na hasira, “Kuna
nini Ana?” Ana alimpushi mama yake na kutoka nje, kwakweli Rose alikuwa
akishangaa tu na kwenda kuwagusa wanae ambao walikuwa wamezimia wote. Kiukweli
hakuelewa kabisa kwani kabla aliwaacha wakiwa wanaongea na Sara ambaye kapona
kimuujiza halafu akakumbuka kuwa Ana alibaki nje wakati amemwambia kuwa
waondoke. Ikabidi atoke mule chumbani kwakina Sara na kwenda tena
kumfata Ana chumbani kwake, aliingia na kuongea nae kwa utaratibu
kabisa, “Mwanangu Ana niambie tatizo ni nini?” “Mama niache,
tafadhali niache” “Sawa mwanangu, ila mimi ni mama yako mwanangu jamani.
Usiponiambia na mimi utamwambia nani mwingine! Mimi na wewe ndio wa kusaidiana
mwanangu. Kumbuka nakupenda sana mwanangu, ndiomana wote wale nimeachana nao
ingawa wamezimia ila nimekuja kuzungumza na wewe” “Mama, kuna mtu
ananichezea akili halafu Sara anajua ukweli wote” “Mwanangu, kama Sara
anaujua ukweli najua cha kumfanya aseme ukweli kwetu hata
usijali” “Kwahiyo mama utanisaidia!” “Ndio nitakusaidia
mwanangu” “Sasa hivi hakuna siri mama, yani watoto wako wanaelewa fika
kuwa mimi ni nani na nina uwezo gani. Sasa nadhani wametafuta vya kuwasaidia
ndiomana imekuwa hivi, hebu fikiria mama kabla sijafanya chochote eti chumba cha
cha Sara kikaanza kutikisika kwakweli nimechukia sana” “Kheee makubwa,
sasa mbona wamezimia?” “Sauti yangu ya kelele imewafanya wazimie,
ndiomana nakwambia saivi washanijua kuwa mimi ni mtu wa aina gani. Tafadhali
mama fanya kitu nijue ukweli maana nasikia aliyemfanya Sara apone ndiye
aliyemuokoa Yule mwalimu aliyeanguka chooni” “Kheee mwanangu, atakuwa
jinni huyo sidhani kama ni mtu wa kawaida” “Hata kama ni jinni sidhani
kama anaweza kunishinda kiasi hiki halafu kwanini nisipate hata kengele ya
hatari kuwa kuna kitu kinatendeka nyuma yangu!” Basi Ana na mama yake
wakajadili sana siku hiyo, na mama yake akamwambia atakachokifanya ili Sara
aseme ukweli. Muda kidogo Patrick nae alirudi ila aliamliwa akalale siku
hiyo bila hata ya kula chochote kile humo ndani. Kulipokucha
Patrick alitoka na kuruhusiwa kuondoka ila watoto wa rose walikuwa bado
hawajazinduka, na baada ya Patrick kuondoka Ana nae aliondoka na kwenda shuleni
kisha huku nyuma Rose aliingia chumbani kwa Sara na kuanza kuwaburuza wanae wale
mapacha mmoja mmoja, hadi wote wawili akawaingiza chumbani kwako kisha akawaweka
kitandani na kuwafunika mashuka halafu akaenda chumbani kwa Sara na kumuweka
vizuri Sara kitandani kisha akamfunika na shuka. Baada ya muda wale mapacha
walizinduka ila kila mmoja hakukumbuka kitu chochote kilichokuwa kimetokea ila
walijikuta wamechoka sana na kuulizana kwa mshangao, “Mbona tumechelewa
sana kuamka!” “Hata sielewi, sijui kwanini” Basi ikabidi
wajiandae haraka haraka na kuondoka, sebleni walimkuta mama yao na
kumuaga. “Sasa nataka niwaagize” “Wapi tena mama?” “Leo
msafiri, muende kule shambani Morogoro” Mmoja akadakia, “Mama,
kuna nini tena?” “Sitaki maswali ila nataka muende kule shambani kwangu
na mrudi kesho. Nadhani tunaelewana” Akawapa na pesa kidogo ya
kuwasaidia kwenye safari hiyo, waliondoka ila walijiuliza mambo mengi sana kuwa
mama yao safari hii ana mpango gani maana mara ya mwisho aliwatuma Morogoro
kumbe kuna kifo cha Moza, ila kwasababu hawakuwa na kumbukumbu yoyote ya
kilichotokea usiku wakapuuzia na kuondoka zao. Muda kidogo Sara nae
aliamka, tena akaoga na kujiandaa kuondoka. Alipotoka sebleni akamkuta mama yao
amekaa na akamuuliza swali, “Unaenda wapi?” “Naenda kwenye
shughuli zangu mama” “Nani amekuruhusu?” “Mama jamani si
nimepona! Je kutoka siruhusiwi?” “Njoo ukae kwanza hapa
nikuambie” Sara alienda kukaa karibu na mama yake , kisha mama yake
akamuuliza swali, “Wewe umejizaa au nimekuzaa?” “Umenizaa mama,
ila kwanini umeniuliza hivyo?” “Sasa niambie ukweli, ni kitu gani
kimerudisha kuongea kwako na kuona kwako” “Jamani mama inamaana
haujapenda nilivyopona?” “Wewe niambie tu umeponaje?” “Nilikuwa
nimelala hapa sebleni, mara nikasikia sauti ikisema inuka Sara umepona.
Nikafungua macho yangu nikaona halafu nikajaribu kuongea napo nikaweza. Basi
nikafurahi sana nimeweza kupona mama” “Sara usinifiche, mimi ni mama
yako niambie ukweli” “Huo ndio ukweli mama wala hakuna ukweli mwingine
zaidi ya huo” “Sara, sitaki kutumia ukali mwanangu. Niambie
ukweli” “Huo ndio ukweli mama” “Nadhani unataka kuona
nitakufanya nini” Rose akainuka na kuelekea chumbani, kisha Sara nae
akainuka na kutaka kutoka nje ila akakuta mlango umefungwa kila alipojaribu
kuufungua ilikuwa ni vigumu kuufungua ikabidi akae chini amsubirie tu mamake
arudi. Bado Neema alikuwa akishangaa sana jinsi Salome
alivyobadilika kwani mwanae hakuwa hivyo kabla, vitu vingi sana Salome alikuwa
anavifanya vya tofauti. Muda huu alikuwa nae sebleni wakiangalia luninga, mara
gafla Salome akashika kichwa chake kwa nguvu na kumfanya Neema amuulize kwa
mshangao huku ameinuka na kumshikilia, “Vipi Salome
mwanangu!” Ila Salome hakujibu zaidi aliinuka na kukimbilia chumbani
halafu akafunga mlango. Kwakweli Neema alishindwa kuelewa kabisa kuwa imekuwaje
lakini bado hakupata jibu kabisa, akawa tu anamgongea mlango, “Jamani
mwanangu Salome fungua, una matatizo gani mwanangu!” Hakujibiwa wala
mlango haukufunguliwa na kumfanya azidi kuchanganyikiwa lakini akaamua kwenda
kukaa akisikilizia tu kipi kitajili baada ya hayo. Baada kama ya lisaa
limoja Salome alitoka ndani, na alimkuta mama yake akilia. Salome alimfata mama
yake na kuanza kumbembeleza, “Usilie mama, mimi ni
mzima” “Salome mwanangu, ulinifungia mlango lazima nihisi kuna kibaya
kimekupata” “Hakuna kibaya chochote mama” “Sasa kwanini
uliondoka gafla ukishika kichwa na kwenda kujifungia ndani?” “Kichwa
kiliniuma mama, sasa niliingia ndani na kunywa dawa na kupumzika sikutaka kuacha
mlango wazi kwamaana niliona ungesumbuka” “Jamani Salome mwanangu mbona
siku hizi umebadilika sana, toka lini umefanya hivyo
mwanangu?” “Nisamehe mama yangu, naomba unisamehe sana” Neema
sasa alinyamaza ila akaja kushtuliwa tena na kauli ya Salome, “Mama
nataka kwenda kwa baba” “Kivipi Salome?” “Nataka kwenda kuishi
na baba” “Jamani Ssalome jamani, subiri basi kesho
nitakujibu” “Sitaki kusubiria kesho, nataka leo leo iende kwa
baba” “Hapana Salome, siwezi kukuruhusu leo. Subiri utaenda
tu” “Huwezi kubadilisha mawazo yangu mama, nishajipanga kwenda. Nitakuja
tena tu hapa nyumbani ila kwa leo niache niende” “Hapana
Salome” Ila Salome akainuka na kwenda chumbani kwake kisha akatoka na
begi dogo na kumwambia mama yake, “Baki salama mama” Halafu
akatoa milioni moja na kumkabidhi mama yake, hakutaka hata kusikia mama yake
atasema nini kwani muda huo huo akatoka na kuondoka, kwakweli Neema alikuwa kama
amepigwa na bumbuwazi hizi kwani aliona ni mambo ya ajabu sana kutokusikilizwa
na mwanae. Wale mapacha walipokuwa wanajiandaa ili wapande basi
waende Morogoro maana walichelewa sana kutokana na mambo waliyokuwa wanayafanya
ndiomana ikawachelewesha, wakasikia mtu akiwaita, “Kulwa na
Doto” Walishtuka na kumuangalia aliyewaita, kwakweli sura ya Yule mtu
ilikuwa ni ngeni machoni mwao ila walipomuangalia zaidi waligundua kuwa mtu Yule
amefanana na baba yao wa kambo Mr.Patrick. Walimsogelea Yule binti na
kumsikiliza vizuri, “Naitwa Salome” Wakatazamana na
kumuuliza, “Unatujua sisi?” “Ndio nawajua” “Na je
umetuitia nini?” “Nimetumwa na mama ambaye ni mama yenu” “Kwani
na wewe ni mama yako?” “Ndio ni mama yangu, kaolewa na baba
yangu” Wakashangaana kwa muda na kuuliza kwa makini kuhusu baba wa
Salome, naye akawaelezea, “Mzee Patrick ni baba yangu mzazi, nz mimi ni
mtoto wake wa pekee na analitambua hilo. Nimefika leo rasmi nyumbani nyie
mmeondoka, ndio mama kasema niwafate hapa stendi turudi nyumbani akawatambulishe
vizuri. Hata hivyo amesema huko Morogoro ameshamalizana na wakulima tayari
kwahiyo hakuna cha kuendea.” Wale mapacha wakaangaliana na kujikuta
wakikubaliana nae kile alichowaambia na kuamua kughaili kwenda Morogoro na
kurudi nyumbani ila Salome aliwaaga kuwa yeye anapitia mahali kwahiyo ataonana
nao nyumbani. Wakati wanarudi njiani walikutana na baba yao ambaye ni
Mr.Patrick nae akiwa kwenye gari yake akirudi nyumbani kwahiyo walimsimamisha na
kushuka kwenye gari ya kukodi waliyopanda kisha kuingia kwenye gari ya
Patrick. “Baba mbona na wewe unarudi nyumbani muda
huu?” “Nimejisikia tu kurudi” Wakaona si vyema waongee sana
labda baba yao anaenda kufanyiwa kitu cha kushtukiza kwahiyo wakimwambia
watakuwa wameharibu ila baba yao aliwaomba wapiti kumchukua Ana maana amepigiwa
simu na walimu wa Ana kuwa arudi kwao. Basi wakapita shuleni kwakina
Ana, halafu Patrick akakabidhiwa Ana arudi nae nyumbani. Walimu walimkabidhi na
barua mr.Patrick aende nayo. Walirudi na kupanda kwenye gari, kaka zake
wakamuuliza kwa mshangao, “Kwani Ana imekuwaje mdogo wetu mbona mapema
sana, halafu umerudishwa nyumbani na barua juu” “Achaneni na
mimi” “Mmmh haya bhana, tunaachana na wewe ila kumbuka elimu ndio kila
kitu katika maisha” “Naweza kupata kila kitu bila ya elimu, achaneni na
mimi kabisa” “Haya tumekuacha” Basi safari ilikuwa inafanyika ya
kurudi nyumbani. Rose alikuwa anampango wa kumfanyia mambo ya ajabu sana
Sara kwavile alimficha bado ila kila alichotaka kufanya aliona kuna kitu
kinapingana nae na kushindwa kuelewa kuwa ni kitu gani ambacho kilikuwa
kikimshinda kufanya vile alivyotaka kufanya, akamuita Sara kwa nguvu kiasi cha
kufanya hadi nyumba yake itikisike ila Sara alishindwa kuinuka pale alipokuwa
amekaaa ikabidi amfate kwa hasira na kutaka kumuinua kwa nguvu ila wakati
anakazana kumuinua mara gafla nguo zake zote zikaanguka chini hata asielewe
kwanini zimeanguka kwahiyo akawa kama alivyozaliwa, gafla mlango ulifunguliwa na
waliingia ndani watoto wake na mume wake, kwakweli wote walimshangaa mama yao
kuwa kama alivyozaliwa. Ikabidi Ana akimbilie nguo na kumfunika mama yake kisha
wale mapacha nao wakatoka nje kwa aibu. Kwakweli siku ya leo ilikuwa ni siku ya
aibu kubwa kwa Rose ambayo hajawahi kuitegemea kwa siku zote, hajawahi kutegemea
kama kuna siku atadhalilika kiasi kile. Ana alimchukua mama yake na
kwenda nae chumbani huku akisikitika sana kwa kilichotokea na kumpa mama yake
pole, “Imekuwaje mama?” “Sijui ila nguvu zangu zimepotea
mwanangu, yani sina nguvu kama mwanzo. Nimedhalilika sana” “Pole mama,
ni kitu gani kimetokea?” “Sijui ila kila nilipokuwa nafanya dawa
zilikuwa zinapingana na vitu vingine. Hapo ndipo nilipotaka kwenda kumchukua kwa
nguvu Sara ila ndio nguo zikanidondoka halafu nyie mkaingia” Mara
wakasikia sauti ya Sara ikiongea kwa nguvu tena kwa ujasiri, “Sasa huyu
ndio kiboko ya Ana” Ikabidi watoke ili wakamuone huyo kiboko ya Ana,
kwakweli Rose alishtushwa sana kumuona Salome. Mara
wakasikia sauti ya Sara ikiongea kwa nguvu tena kwa ujasiri, “Sasa huyu
ndio kiboko ya Ana” Ikabidi watoke ili wakamuone huyo kiboko ya Ana,
kwakweli Rose alishtushwa sana kumuona Salome. Kitendo cha Rose kumuona Salome
kilimkosesha furaha na kujikuta akipatwa kama presha na kuanguka kwani mawazo
yake ilikuwa ni Salome amekufa kwahiyo kitendo cha kumuona akiwa mzima
kilimshangaza kabisa. Watoto wake wote walimfata pale chini na kumpeleka
chumbani ambako walimuwashia feni ilia pate upepo na wazo hilo la kumuwashia
feni walilipata kwa Ana, kisha wakarudi sebleni na kumuacha Ana akiwa chumbani
na mama yao. Katika watu ambao walikuwa hawaelewi kinachoendelea ni
Patrick maana yeye aliona kila kitu ni cha ajabu tu hapo, alikuwa akimuangalia
Salome kama mgeni kabisa machoni pake ila Salome akamtoa
mashaka, “Usiniangalie hivyo, mimi ni mtoto wako” “Nakuangalia
sababu sielewi elewi” “Mimi ni mtoto wako, na mama yangu ni
Neema” “Yeye yuko wapi?” “Sijaja nae sababu alikuwa hataki nije
huku” Patrick alimuangalia Salome na kujikuta akimsogelea na
kumkumbatia, “Kumbe nina binti mkubwa tu” “Ndio ni mimi mtoto
wako” “Karibu sana hapa nyumbani” “Asante” Muda watoto
wa Rose wanarudi sebleni ni muda ambao Salome alikuwa anaondoka na kuelekea
chumbani, wote wakajikuta wakisimama na kumuangalia ataelekea kwenye chumba kipi
ila alielekea kwenye chumba kile alichokuwa analala Moza. Hapo iliwashangaza
sana kwani hawakutegemea kama Salome angeelekea kwenye chumba cha Moza, na baada
ya muda akarudi sebleni na kuwakuta wamekaa. “Nimeshaenda kuweka begi
langu” Pacha mmoja akamuuliza Salome, “Mbona chumba cha kulala
umeenda bila kuonyeshwa na yeyote?” “Mbona hapa nilishawahi kuja kipindi
yupo dada Moza! Nishawahi kuja hapa, najua kila sehemu. Vipi leo tunakula
nini?” Wote walikuwa kimya ila huyu mgeni wa leo aliwashangaza sana
kwani alikuwa na mambo ya ajabu ajabu, kafika tu mara mama yao kazimia, mara
anaenda chumbani bila kuonyeshwa saivi anawauliza watakula nini, na alipoona
kimya alienda yeye jikoni kupika. Kila mtu alikuwa kimya hata Sara mwenyewe
alikuwa kimya kabisa. Rose alipozinduka bado alikuwa na
mkaranganyiko wa mawazo kwani bado hakuelewa kitu chochote, akachukua simu yake
na kuanza kumpigia Ashura lakini haikupatikana. Akachukua tena simu na kuwapigia
wale vijana, kisha akaongea nao “Hivi nyie mmenifanya nini? Si mlisema
Yule mtoto mmeenda kumtupa mbali na hakuna wa kumuokoa iweje anaonekana tena
nyumbani kwangu” Wale vijana wakamuelezea ilivyokuwa kisha rose
akawatuma waende pale alipokuwa anaishi Ashura ili kama yupo wamkamate mpaka
aseme ukweli. Alipokata tu ile simu akashangaa akipata ujumbe kutoka kwa
Ashura, “Samahani dada yangu, mimi sikuona kosa la huyu mtoto Salome na
sikuona kama bi vizuri kumuua. Wale vijana niliwawekea mbwa kwenye kile kiroba
ili wakuaminishe kuwa ni kweli nilimuua Salome ila kiukweli Salome sikumuua na
mimi nimeondoka sipo kabisa mjini nimeenda kijijini kweli na sitaki tena
kujishughulisha na hizo kazi zako.” Kwakweli ujumbe huu aliusoma mara
mbili mbili bila ya kumaliza na akiwa haamini kile anachokisoma kuwa Ashura
anaweza akamgeuka namna hiyo, akaamua amtumie ujumbe pia, “Ashura
unajifanya umesahau tulivyoahidiana, hivi ningesema ukweli wa mambo yako na wewe
ungeweza kukaa huko unapokaa? Mbona wewe pia una maovu mengi Ashura, umesahau
Yule mganga babu ni wewe ndiye ulinipeleka? Umesahau hawa wasichana niliowafunga
humu ndani ni ushauri wako, eti leo unajifanya kunigeuka Ashura! Kwanza jina
lako sio Ashura wewe ila subiri nitakupata tu, mimi nina pesa” Muda
kidogo akajibiwa, “Pesa zako wala hazinibabaishi hata mimi nina pesa,
tena kwa taarifa yako ni mimi nimemueleza ukweli wote huyo Salome kuwa baba yake
ni Patrick kwahiyo usishangae akija kuishi hapo. Ukweli wote nishamwambia,
ujipange upya na hunipati ng’ooo, hao misukule uliowatunza utajijua nao
mwenyewe” Rose alichukizwa sana na ujumbe huu ila kila alipojaribu
kupiga simu hiyo namba ya Ashura haikupatikana, yani alichukia hadi akarusha
simu yak echini. Kwa upande wa Salome ilikuwa furaha sana kwake
na alijikuta akigundua siri nyingi sana za Rose maana muda wote Rose alijua
anayejibishana nae kwenye ujumbe mfupi ni Ashura kumbe kuna mtu mwingine, na
huyo ashura mwenyewe ni marahemu wa muda mrefu sana. Salome alikuwa
ameingia na chakula chumbani na alikuwa anakula humo, mara Sara alienda
kumgongea na kuingia ila alipomkuta anakula chumbani alishtuka sana, ikabidi
Salome amuulize ameshtuka kwasababu ipi, “Hapa nyumbani hakuna mtu
anayeruhusiwa kula chakula chumbani” “Mmmh kwanini?” “Sijui ni
kwanini ila mama anakataa kabisa mtu kula chakula chumbani” “Hujui
sababu kweli! Labda ungesema mama anaogopa panya watazaliana au mende watajaa.
Ila ni leo tu haitajirudia kula chakula chumbani” “Na kwanini umechagua
kulala chumba hiki?” “Sababu hiki ni chumba alichokuwa analala mpendwa
wangu Moza, namkumbuka sana ndiomana nimekuja kulala hapa” “Ila
unafikiri Moza tulimzika! Alitoweka
kimiujiza” “Alitoweka!” “Ndio alitoweka, yani kuna binti
alitumbukia kwenye kaburi walipompeleka hospitali basin a mwili wa Moza
ulipotea” “Maskini Moza wangu, kwahiyo hakuna kaburi la
Moza!” “Ndio hakuna” “Kwa staili hiyo inamaana basi Moza hakufa,
labda kwa mfano hakufa!” “Mmmh usiongee habari hizo, mimi ni muoga
nitashindwa kulala hapa usiku” “Basi usijali” “Ila huku ndani
kuwa nako makini sana, ulisaidia macho yangu yakaona tena na mdomo wangu ukaweza
kuongea ila chakula nilichopika siku ile kuna kilichopotea na sijui kimeenda
wapi. Kuwa makini sana na humu ndani kuna mambo ya ajabu sana” “Usijali,
nipo makini sana” Sara alijikuta akimpenda sana huyu Salome yani
alimpenda sana kutokana na jinsi alivyomsaidia matatizo yake ya kurogwa na mdogo
wake. Walipomaliza maongezi, Sara akamuomba Salome waende nae sebleni ambapo
alifanya hivyo na pale sebleni walikuwepo wale mapacha na mr.Patrick ambae toka
amerudi hakwenda kabisa chumbani kwa mke wake. Baada ya kimya kirefu pale
sebleni, Salome akaanza kusema, “Hata hamniulizi jamani kuwa nimejuaje
kama huyu baba ni baba yangu” Pacha mmoja akadakia, “Eeh tuambie
umejuaje!” “Unajua mimi nimeishi bila kumjua baba kwa miaka yote hii
mpaka sasa nilikuwa kidato cha tatu ila baba yangu simjui. Alipotokea msamalia
mwema na kuniambia kuwa huyu ni baba yangu nilifurahi sana ndiomana sikutaka
hata kupoteza muda zaidi ya kuja hapa ili nifurahi na ndugu zangu wengine.
Jamani ndugu zangu, mimi ni ndugu yenu ni mtoto wa Mr.Patrick kama mlivyo
nyie” Mmoja akahamaki, “Wewe si ulituambia pale kuwa wewe ndiye
mtoto wa pekee wa mzee Patrick, haya saivi unasema na sisi ni watoto wa huyu
mzee. Hapana, sisi ni watoto wake wa kambo. Labda Ana sijui” Sara
akadakia, “Ana nae ana baba yake mwingine, ni hakika kabisa wewe Salome
ndiye mtoto wa pekee wa baba” Mama yao akiwa ameambatana na Ana walitoka
chumbani na waliisikia vilivyo kauli ya Sara na iliwakera sana. Rose kabla ya
kukaa alianza kwa kumuuliza Sara, “Hivi wewe Sara una nini wewe? Kitu
gani kinakuwasha mdomoni kwako?” Kisha Rose alikaa na kumuangalia Salome
na kusema, “Haya na wewe nani kakukaribisha kwenye nyumba
hii?” “Nimekuja kwa baba yangu” Salome alijibu kwa kujiamini
kabisa. “Sikuelewi” “Mamdogo Ashura kaniambia kuwa hapa ni kwa
babangu, hata ameshakwambia kuwa nakuja hapa” “Kwahiyo hapa kwangu
unalala chumba gani sasa?” “Kile chumba alichokuwa analala dada
Moza” Rose akamuangalia mume wake na kumwambia waelekee chumbani ana
mazungumzo nae, kwahiyo sebleni walibaki watoto tu. Ambapo Ana alimuangalia
Salome na kumwambia, “Utaondoka kama ulivyokuja, hakuna anayekutambua
hapa. Ndiomana unalala chumba cha marehemu” Kisha akaenda zake chumbani
kwake, ila Sara alimuangalia Salome na kumwambia, “Hata usijali,
nitakuwa na wewe bega kwa bega” Wale mapacha wakainuka na kwenda
chumbani kwao ila Sara aliinuka na Salome na kumkaribisha Salome kwenye chumba
chake, “Humu ni chumbani kwangu Salome, muda wowote unaruhusiwa kuingia.
Ukiwa na shida ya kitu chochote unaruhusiwa kuja kuchukua” “Asante
dada” “Nimefurahi sana kupata mdogo mwenye upendo kama wewe, kwanza
umeniponya macho yangu na mdomo wangu. Halafu ngoja nikuhadithie kitu
bhana” Basi Sara akaanza kumueleza Salome jinsi Ana alivyokuwa
akishangaa mwalimu wake amepona kimiujiza, “Niambie Salome, ni wewe
uliyemsaidia Yule mwalimu” Salome akacheka kidogo, “Hapana bhana
si mimi ila nimefurahi kusikia kuna mtu alifanyiwa hivyo na amepona
pia” “Mmh si wewe kweli! Sasa mimi ulijuaje kama
naumwa?” “Nilioteshwa na nilioteshwa dawa za kuja kukupa ndiomana
nimekwambia hawatakusumbua tena” “Ila mimi nimefurahi sana umekuja
kuishi hapa, naomba uishi hapa milele yote” Salome akacheka tu na
kufurahi pale na Sara kisha usiku ulipoingia alimuaga na kwenda kulala kwani
nyumba hiyo huwa chakula kinakuwa mezani na mwenye njaa anaenda kula mezani na
kama siku hiyo hakijapikwa basi kila mmoja anajijua
mwenyewe. Salome akiwa chumbani kwake aliona ujumbe kwenye simu
ya Ashura ukionekana umetoka kwa wale vijana, “Sista mbona umefanya
tupate lawama, ila mbona hupatikani hewani? Sasa ni mtu gani Yule tuliyemtupa
kama sio Yule mtoto? Mama ametupa oda kuwa twende kwenye ile nyumba na tumalize
yeyote tutakayemkuta pale” Ujumbe huu ulimchanganya sana Salome, akawaza
kwanza cha kuwaambia hawa vijana kisha akawatumia ujumbe, “Basi kama
nyie mnataka kuwateketeza wale wote ngojeni kwanza, msiende hivi karibuni.
Subirini mpaka mwezi upite” ‘Haiwezekani sista, sisi tunataka pesa na si
vinginevyo” “Hatakama mnataka pesa, kumbukeni Yule Rose ni dada yangu,
kwahiyo msifanye kitu chochote bila kuwaruhusu mimi. Yule Rose ametumia hasira
tu” “Kwahiyo tusubiri hadi lini?” “Subirini hadi
keshokutwa” Wakamjibu tu poa, na hapo Salome akawaza cha kufanya maana
ingawa kaihamisha familia yake ila waliohamia hapo watapata matatizo kwahiyo
alikuwa anafikiria cha kuweza kuwasaidia na wale wengine. Ila kabla
hajalala, alianza kupekua kwanza vitu vya mule ndani ambapo alipata kijitabu
kidogo ambacho kimeandikwa vitu vya maelekezo yaliyokuwa kama historia hivi ya
mtu aliyeonekana ameandika hicho kitabu. Kurasa ya kwanza kabisa
akaona, “Nimeanza kazi leo kwenye hii nyumba ila usiku nilipolala
nimegundua kuna chumba walichowekwa wadada wawili kama misukule. Natakiwa
niwasaidie watoke” Salome alisoma mara mbili mbili sehemu hiyo na kuwaza
jambo Fulani ila kabla hajaendelea na kile kitabu, alikuja Sara chumbani kwake
ikabidi kile kitabu akiweke pembeni, Sara akaanza kumwambia
Salome, “Naomba tukalale wote chumbani kwangu” Salome alikuwa
anakataa ila Sara alimbembeleza sana hadi alikubali na kwenda kulala
nae. Kulipokucha siku ya leo ilikuwa ni ya ajabu sana kwani
Patrick aliwaita watoto wake wote sebleni kisha akaanza
kuongea, “Salome, sikutambui kwahiyo naomba uondoke. Jamani hatuna
undugu na huyu wakuitwa Salome, simtambui mimi” Salome akacheka kisha
akamuangalia Rose na kumwambia, “Ndio mlivyohamua hivi!” “Ndio.
Uondoke Salome, hakuna anayekutambua kwenye nyumba hii. Kama huyo unayedai ni
baba yako hakutambui, je sisi tutakutambua?” “Basi naombeni nafasi
kidogo niongee na huyu baba ndio nitaondoka” Wote walitoka pale sebleni
kasoro Rose ila salome alimsihi aondoke ili yeye aweze kuzungumza na mzee
Patrick halafu ataondoka, Rose alikubali kuondoka kwani alijua mzee Patrick
hawezi kubadilisha maamuzi yake yoyote kutokana na alichomfanya usiku wa
jana. Kwahiyo sebleni alibaki Salome na Patrick, kisha Salome
akamuangalia vizuri Patrick na kumuuliza, “Hunitambui
mimi!” Patrick alikuwa kimya tu, ila Salome akamsogelea karibu na
kumkazia macho. Mzee Patrick akashtuka na kusema, “Aaaah kumbe
Moza!” Akaanguka chini na kuzimia. Kwahiyo
sebleni alibaki Salome na Patrick, kisha Salome akamuangalia vizuri Patrick na
kumuuliza, “Hunitambui mimi!” Patrick alikuwa kimya tu, ila
Salome akamsogelea karibu na kumkazia macho. Mzee Patrick akashtuka na
kusema, “Aaaah kumbe Moza!” Akaanguka chini na kuzimia. Salome
alihakikisha ile sauti wengine wote hawajaisikia pia alimpulizia Yule mzee maji
na kumfanya azinduke muda ule ule, ila alipozinduka sasa alikuwa na swaga mpya
kwani alimsogelea Salome na kumwambia, “Nisamehe mwanangu, jamani
nisamehe wewe ni mwanangu. Damu yangu jamani nisamehe, nisamehe kwa kipindi
chote bila kuwa karibu na wewe nisamehe sana mwanangu. Nataka unipeleke na kwa
mamako nikamwombe msamaha” “Usijali nitakupeleka” Kisha Mr.
Patrick akawaita tena wote sebleni, na walipokuja aliwaambia, “Jamani
huyu ni ndugu yenu, naomba tumpende” Halafu akainuka na kutoka nje ya
nyumba, kwakweli hichi kitendo kilimkera sana Rose yani alitamani sijui afanye
kitu gani, alimuangalia Salome kwa hasira sana, ila alipotoka nje ili
kumuangalia mume wake alikuta ameshaondoka, “Yani leo Patrick ameondoka
bila ruhusa yangu? Nitamfundisha huyu Salome na atanijua mimi ni
nani” Rose alirudi tena ndani akiwa na hasira sana na moja kwa moja
akaenda chumbani kwake. Watoto wake walikuwa sebleni wakijadiliana
kasoro Ana, “Mmmh nyie huyu mzee kama anakuwaga anaugua vile, kwajinsi
alivyofanana na huyu dogo anaanzaje kumkataa!” Walijadiliana na kuondoka
kisha wakamuacha Salome akiwa na Sara, halafu Sara akamwambia
Salome “Usijali hata nyumba nzima ikikutenga jua ya kwamba nitakuwa
pamoja na wewe” “Nashukuru” Kisha Salome akamuaga Sara kuwa
anatoka kidogo, basi akaondoka kumbe mr.Patrick aliwekwa nje ya geti akimsubiria
Salome, na alipotoka aliingia kwenye gari ya Patrick kisha safari ya kwenda
nyumbani kwao ikaanza. Walifika nyumbani kwakina salome na
kumkuta Neema akiwa anafanya usafi, kwakweli nae alishangaa sana kumuona Patrick
akiambatana na Salome ila aliwakaribisha ndani hivyo hivyo cha kushangaza
Patrick alianza kwa kupiga magoti na kuomba msamaha kwa Neema, “Nisamehe
Neema, naomba unisamehe. Nisamehe sana, nimefanya makosa makubwa sana,
sikumtambua mwanangu naomba unisamehe” Kwajinsi Patrick alivyokuwa
anatia huruma ikambidi Neema amuhurumie kwani hajawahi kuwaza kama ipo siku
Patrick atakuja na kumpigia magoti ya kumuomba msamaha. Neema akamshika mkono
Patrick na kumkaribisha kwenye kochi, “Usijali Patrick, yale yamepita ni
mapito tu na nimeshasahau. Mtoto amekua sasa na amekutambua” “Kwakweli
moyo unaniuma sana yani sana, kumkosa mwanangu mpendwa kwa kipindi chote hiki.
Nisamehe kabisa Neema” Kisha Patrick akamuuliza Neema kuhusu pale
anapoishi na alimwambia kama alipanga, kwakweli Patrick alisikitika sana maana
nyumba nyingi tu alikuwa nazo ila mwanamke aliyezaa nae amepanga, akamuahidi
kumpa nyumba moja. “Kweli utanipa?” “Ni haki yako Neema, kila
kitu change ni haki yako. Nitakuja tu nikukabidhi” Muda huu Salome
alikuwa chumbani kwake ila gafla akashtuka na kusema, “Muda umeisha,
itabidi nimtoe huyu mzee haraka sana mpaka kwa wakati mwingine” Basi
akatoka chumbani na kumuomba baba yake kuwa waondoke, ila Patrick alitoa begi
lake na kumpatia Neema pesa zote zilizokuwepo kwenye begi hilo wala yeye
hakuzihesabu ila alimpa Neema pesa zote na begi lake kisha akaondoka na Salome
ambapo Salome alishuka mahali na kumuacha akiendelea na safari zake
zingine. Salome alienda kwanza kule walipokuwa wanaishi mwanzo na
kumuomba mama mwenye nyumba asiweke mpangaji mwingine mpaka miezi miwili iishe
kwani wao walikuwa na hatihati ya kurudi na ukizingatia kodi yao ilikuwa bado
kuisha ikabidi mama mwenye nyumba asikilizane nao kumbe Salome alifanya vile ili
kuepusha wale wakija wasikute mtu katika nyumba ile. Kisha Salome akarudi tena
kwa mama yake ili akahesabu nae pesa zilizokuwemo kwenye lile
begi. Rose akiwa na hasira sana, kwanza alipoingia chumbani
kwao na kufanya mambo yake akagundua kitu. Akagundua kuwa Patrick aliondoka na
gari yake ambapo kwenye gari hiyo aliweka begi lenye pesa ili akawalipe wajenzi
kwenye saiti yao na lile begi aliliweka asubuhi ya siku hiyo akiwa na lengo la
kumaliza yale mazungumzo ajiandae na kwenda saiti ila sasa Patrick alishaondoka
na lilke gari lenye begi, “Mungu wangu, Patrick kaondoka na lile begi
eti! Na hivi akili yake haipo sawa litakuwa limepona kweli? Ila natumai limepona
maana sidhani kama anaweza kufanya ujinga.” Ikabidi Rose ajiandae haraka
haraka na kuelekea saiti. Kufika kule alimkuta Patrick amekaa chini ya
mti, akamshtua na Patrick alishtuka sana kama kashtuliwa na kitu gani. Swali la
kwanza ambalo Rose alimuuliza Patrick, “Kwanini umeondoka na gari
yangu?” “Hata mimi mwenyewe nashangaa sijui hata imekuwaje nimeondoka na
gari langu” “Natumaini hujafanya ujinga” “Ujinga gani
tena?” Rose akainuka na kwenda kuangalia begi la hela kwenye gari, ila
lile begi halikuwepo. Kwakweli Rose alikuwa na hasira sana na kumuuliza tena
Patrick, “Begi la hela liko wapi?” “Begi! Begi
lipi?” “Inamaana hukuona begi kwenye gari hilo?” “Sijaona
begi” “Patrick usinitanie na hela zangu, tafadhali begi langu liko
wapi?” Patrick alionekana pia akishangaa yani kama mtu anayeonewa vile
kwani ilionyesha wazi hajui begi la hela limeenda wapi. “Patrick,
Patrick. Begi la hela limeenda wapi?” “Sijui kweli mke wangu unanionea
tu” “Nakuonea kitu gani, haya sasa tutawalipa nini hawa
mafundi?” “Kachukue hela nyingine benki tuwalipe” “Hivi wewe
Patrick una matatizo gani? Yani unarahisisha tu. Haya twende nyumbani ndio
utanieleza vizuri” Akapanda kwenye gari kisha Patrick akawa gari ya
mbele akiongoza kwenda nyumbani halafu Rose akiwa nyuma yake, kwakweli Patrick
alikuwa haelewi kabisa kwa muda huo kuwa begi limeenda wapi na kwenye begi
kulikuwa na kiasi gani. Salome alienda tena kwa mama yake
ambaye bado alikuwa akitetemeka tu kuziangalia zile hela za kwenye
begi, “Usitetemeke mama, ni zako hizo” “Mmmh mwanangu ni miujiza
hii” “Usiwe na mashaka mama yangu, nimekuja nikusaidie
kuhesabu” Basi wakaanza kuhesabu zile hela wakakuta ni milioni
thelathini na tano, kwakweli Neema alipagawa kabisa kwani hajawahi kushika hela
za namna hiyo katika maisha yake kwahiyo alihisi kuchanganyikiwa. “Sasa
mwanangu nafanyaje? Nizipeleke benki!” “Usiwe na haraka mama, benki
tutazipeleka kwa utaratibu. Usizipeleke hivyo kwa mkupuo, na huo wasiwasi wako
watahisi hata umeiba. Nitakupekea mwenyewe benki, yani wewe hata usiwe na
mashaka” Haya mambo Neema hakuyaamini kabisa na kwake yalikuwa kama
ndoto vile hadi alijikuta akitetemeka tu, na kumfanya ashindwe kumuuliza maswali
zaidi Salome kwani aliona kama kawa mokozi wake kwa kipindi hiko. Alijikuta
akimwambia, “Salome, ni kweli nimekuzaa na nimekulea ila sikutegemea
kama kuna siku ungeweza kuja kufanya kitu cha namna hii. Baba yako nimemsamehe
na nimefuta yote aliyonitendea, yani yote kabisa nimeyafuta. Kwahiyo mwanangu
unaenda tena kwa baba yak oleo?” “Siendi leo mama, nitaenda keshokutwa
hadi nikamilishe hizi hela zako kukuwekea benki. Hata usiwe na mashaka mama
yangu” Neema alifurahi kusikia hivi na kisha Salome alikaa na mama yake
huyo na kumueleza utaratibu watakaotumia kuziweka hizo hela
benki. Patrick na Rose walifika nyumbani ila kwakweli Rose
alikuwa na hasira sana kwa kile kilichofanywa na Patrick kuondoka na gari lenye
begi la hela na eti kujifanya hajui begi limeenda wapi, akaenda moja kwa moja na
Patrick chumbani kisha akaanza kumuuliza tena, “Patrick, hebu kumbuka
vizuri begi limeenda wapi?” “Hata sijui mke wangu yani sijui
kabisa” “Hebu kwanza niambie ulipotoka hapa ulienda wapi?” “Yani
ninachokumbuka ni kuwa nimejikuta tu nipo kule saiti, nikaa chini nikawa
najifikiria bila kupata jibu kuwa nimeenda kule kufanya nini. Na mara ukaja wewe
yani sielewi kabisa” “Haya, vipi kuhusu kumkubali Salome wakati mimi
nimekwambia umkatae Yule mtoto!” “Pale nakumbuka ndio, Yule mtoto
nilimkataa ila nilikuja na kumkubali. Unajua ni mwanangu Yule!” “Hivi
wewe Patrick una nini lakini? Yule kawa mwanao tangia lini jamani? Mwanao wewe
si Ana!” “Yule ni mwanangu Rose” “Yule si mwanao, inamaana
hunielewi au” Rose akampulizia kitu uoni na Patrick akapatwa na usingizi
na kulala. Kisha Rose akatoka sebleni, mara akaingia ndani Sara akiwa
ameambatana na ommy, kwakweli Rose alivyowaona alichefukwa sana ukizingatia
akili yake ilishavurugika kwa wakati huo, “Na wewe kijana mwanga unataka
nini nyumbani kwangu?” Ommy alianza kwa kumsalimia ila Rose hakuitaka
salamu ya Ommy zaidi ya kumfukuza tu nyumbani kwake, ikabidi Sara aingilie
kati, “Mama jamani, utamfukuzaje rafiki yangu?” “Sara, hii ni
nyumba yangu sio nyumba yako unanisikia! Sitaki ujinga kwenye nyumba
yangu” “Lakini mama huyu Ommy ni rafiki yangu” “Kama ni rafiki
yako ishia nae huko huko sio nyumbani kwangu tena usinikere” Sara
alibaki tu anamshangaa mama yake, lakini Rose alipoona wamesimama tu
wakimshangaa akainuka na yeye na kumsukumia mlangoni Ommy ambaye alijikwaa
kwenye mlango na kuaguka kisha damu zikamtoka ikabidi Sara ainame pale
alipoangukia Ommy na kuanza kumsaidia kwenda nje ila kabla hawajafika getini
Ommy alionekana akianza kuugulia kichwa ni kitu ambacho kilimshtua sana Sara na
kumfanya akimbilie ndani ili akamletee huduma ya kwanza ila aliporudi hakumkuta
Ommy, alimuita lakini hakumsikia sehemu yoyote ikabidi fike getini na kumuuliza
mlinzi, “Eti Ommy ametoka hapa?” “Nimemuona tu akiingia ila
kutoka sijamuona” “Mungu wangu jamani, Ommy atakuwa ameenda wapi wakati
alikuwa anaumwa. Hivi hukumuona kama nakokotana nae pale na alilala pale
chini?” “Sijawaona kabisa madam yani hata mimi unakuja kuniuliza muda
huu nashangaa tu” Sara akaangalia kwa makini pale ambapo alilala Ommy
kwani alijua lazima damu zitakuwa zimebaki na kama kaelekea mahali basi ataona
matone ya damu ila alipoangalia hakuona damu yoyote na hadi alipoingia ndani
pale alipojigonga ommy hakuona damu yoyote. Kwkweli hiki kitu kilimuumiza sana
Sara kwani hakuelewa kabisa aliona kama ndoto kwa ommy kutoweka mbele ya macho
yake mwenyewe. Akataka kumuuliza mama yake ila hakumkuta sebleni na
alienda kumgongea mlango chumbani kwake ila hakuitikiwa na kujiuliza inamaana
mama yake amelala kwa muda mfupi huo, hakupata jibu kwakweli na alibaki
anashangaa tu ila bado alikazana kumuita mama yake ili ampe
jibu. Rose alichoshwa na kelele za Sara, na baada ya lisaa
limoja rose alitoka ndani na kumfata Sara alipokuwa kisha akamuangalia kwa jicho
kali sana na kuanza kumvuta hadi chumbani kwa Sara kisha
akamwambia, “Laiti kama ungejua leo ninavyojisikia au yaliyonitokea wala
usingethubutu kunipigia kelele” “Sasa mama yaliyokutokea yanamahusiano
gani na kupotea kwa Ommy!” “Hivi unajua leo nimepoteza kiasi gani cha
pesa? Unajua! Yani wewe mtoto tafadhali niache usitake kukorofisha akili yangu
kabisa” “Basi mama niambie alipo Ommy wangu” “Kwahiyo mimi huyo
Ommy wako nimemla au? Wewe mtoto wewe hebu niache” Rose akatoka na
kumfungia Sara mlango kwa nje ambapo alikuwa akiugonga tu bila ya mafanikio
yoyote. Rose akaenda zake sebleni na baada ya muda watoto wake walianza
kurudi na wote wakawa pale sebleni na kuzisikia kelele za Sara kuwa afunguliwe,
wale mapacha walimuhurumia sana dada yao, “Mama jamani, msamehe dada
Sara, nadhani hatorudia tena” “Hebu na nyie niacheni” Gafla
ikasikika sauti kali sana ya kelele za Sara
ikisema, “Mozaaaaaaaaa” Na gafla kukawa kimya
kabisa. Rose akaenda zake sebleni na baada ya muda
watoto wake walianza kurudi na wote wakawa pale sebleni na kuzisikia kelele za
Sara kuwa afunguliwe, wale mapacha walimuhurumia sana dada yao, “Mama
jamani, msamehe dada Sara, nadhani hatorudia tena” “Hebu na nyie
niacheni” Gafla ikasikika sauti kali sana ya kelele za Sara
ikisema, “Mozaaaaaaaaa” Na gafla kukawa kimya
kabisa. Kitendo hicho kiliwashtua wote sebleni hata Rose mwenyewe
akashtuka na kujikuta akienda kumfungulia Sara ili kujua tatizo ni nini, ila
alipomfungulia alimuona Sara akiwa ameanguka chini na kuzimia, kwakweli Rose
alichanganyikiwa sana kwani hakudhania kama mwanae kumfungia mule chumbani
angezimia basi akamuinua mwenyewe na kumbeba hadi sebleni kisha akawaambia wale
mapacha wasaidiane nae kumpepea hata wao wakashangaa kuwa mama yao kuna wakati
kumbe anakuwa na huruma dhidi yao. Ana alimwambia mama
yake, “Unajichosha bure mama” “Ni mwanangu huyu” Ana
akaondoka zake huku Rose akiendelea na wale mapacha wake kumpepea Sara, na
ilimchukua muda sana kuzinduka na hata alipozinduka hakukumbuka kitu chochote
yani cha kushangaza hata kuhusu kuanguka kwa Ommy na kutoweka hakukumbuka
pia. Rose alimsogelea mwanae na kumpa pole kisha akainuka nae na kwenda
chumbani, akakaa nae kuzungumza, “Mwanangu una hakika hukumbuki
chochote?” “Sikumbuki kitu mama” “Yani vilivyofanyika leo
hukumbuki?” “Yani sikumbuki hata kuhusu leo nilitoka nimejua wewe
ulivyosema ila sikumbuki chochote” “Kheee makubwa haya, hivi anayefanya
kutoa kumbukumbu kwa watu wangu wa karibu ni nani!” Akakumbuka kuwa
kauli ya mwisho ya mwanae kabla ya kuzimia ilikuwa ni neno ‘Moza’ na ilionyesha
aliona kitu cha kustaajabisha sana ila akajiuliza kuwa inamaana huyo Moza karudi
kama mzimu au ni kitu gani. “Ila inawezekana maana alitoweka pale
makaburini na hatukumzika. Lazima nifatilie na nijue mbichi na
mbivu” Akapanga pale na halmashauri ya kichwa chake kuwa kesho aende kwa
mtaalamu mwingine ili kujua ukweli kuhusu Moza maana kitendo cha mtoto wake
kusema Moza na kuzimia halafu kupoteza kumbukumbu zote kilimstaajabisha ingawa
kilimfurahisha kwa kiasi Fulani kwani mwanae hakuwa na kumbukumbu za kupotea kwa
Ommy. Alimuangalia pale mtoto wake aliyeonyesha kuwa hana kumbukumbu ya aina
yoyote kisha akaondoka na kumuaga pale. “Mwanangu naenda chumbani, ikiwa
utapatwa na tatizo lolote usisite kuniambia. Sawa mwanangu eeh!” “Sawa
mama” Rose alitoka ila Sara alibaki akijiuliza sana upendo wa mama yake
wa siku hiyo ni waajabu sana ukizingatia na siku zingine. Kaka zake
mapacha nao wakaenda chumbani kwake na kumuuliza tena dada yao hali yake ila
bado walimshangaa kuwa hana kumbukumbu ya aina yoyote. “Yani dada
hukumbuki kitu chochote!” “Sikumbuki ndio, kwani
ilikuwaje?” “Sisi wenyewe hatuelewi ila tulisikia tu ukipiga kelele kuwa
ufunguliwe na mara ukapiga kelele za nguvu ukitaja Moza, halafu kimya
kikatawala. Mama alikuja kukufungulia na kukuta umezimia ndio akakuleta sebleni
tukupepee” “Kheee mama alinibeba pekeyake?” “Ndio alikubeba peke
yake” “Mama amewezaje kunibeba peke yake jamani wakati anasemaga siku
hizi nimenenepa sana, amewezaje kunibeba peke yake nikiwa mzito
hivi!” “Yule ni mama, ametubeba wakati watoto na anaweza kutubeba hata
sasa” “Mmh jamani kaka zangu, ni mama kweli sijakataa. Katubeba wakati
watoto, sijakataa lakini kumbukeni utotoni tulikuwa wadogo ila kadri tunavyokua
na uzito nao unaongezeka. Mama angembeba mtu kama Ana sawa ila sio mimi na
ubonge huu, yani hata nyie hamjapata mashaka. Sikumbuki kitu ila swala la kusema
mama alinibeba peke yake limenishtua kidogo” “Mmmh basi tuachane na
habari hizo dada, cha muhimu unaendelea vizuri” Kaka zake nao waliondoka
na kumuacha mule chumbani. Usiku wake Sara alikuwa amelala ila
akajiwa na njozi kuwa Ommy yupo mahali anateseka sana huku akimuomba Sara msaada
aokolewe, “Nisaidie Sara, nateseka naumia kwa kosa nisilolijua. Nisaidie
Sara” “Uko wapi kwani?” Sara akashtuka na swali lake hilo, jasho
likawa linamtoka tu ingawa chumbani kule feni ilikuwa inawaka. Alikaa na
kujaribu kufikiria sana kuwa Ommy amepatwa na nini ila hakuelewa, akaamua
achukue simu na kumpigia Ommy ila hiyo simu ilipoanza kuita aliiona chumbani
kwake na kushangaa kuwa simu ya Ommy ipo chumbani kwake, hakuelewa imekuwaje
hadi simu ipo pale na ni nani aliyeiingiza ile simu chumbani kwake. Akachukua
simu ya Ommy na kuanza kuipitia kwani kwa upande mwingine alifurahi kuona simu
ya Ommy kuwa ataweza kuona meseji zake. Na kweli alipochukua simu ya Ommy tu
alibambana na ujumbe kutoka kwa Mishi, ujumbe ulikuwa unasema, “Mpenzi
wangu Ommy uko wapi jamani? Nimekumisi sana, mpaka muda huu kweli hujaja!
Nakupenda sana mpenzi wangu” Sara alijikuta akiumia moyo kupita maelezo
ya kawaida, roho ya wivu iliingia ndani kwake na hapo akajikuta akisahau kabisa
kama ameota kuwa Ommy yupo kwenye matatizo zaidi kilichomuuma ni kusalitiwa na
Ommy basi, akajikuta akimjibu huyu Mishi, “Usinisumbue nipo kwa mwanamke
wa maisha yangu Sara. Nampenda sana” Akatumia hiyo meseji ila moyo wangu
ulijawa na wivu kiasi kwamba alijikuta akishindwa hata kulala, “Yani
huyu Ommy nampenda kwa moyo wwangu wote, hakuna chochote anachonipa ila mimi
nampa upendo. Shida yoyote kiipata namsaidia. Kila kitu nampa, eti leo
ananisaliti na mwanamke sijui wa kuitwa Mishi! Lazima nimjue huyo mwanamke nijue
tofauti ya mimi na yeye ni nini kwani mimi nina ubaya gani wa kuchanganywa
kimapenzi na mwanamke mingine! Yani wanaume hawa” Alijikuta machozi
yakimtoka tu na hakupata usingizi hadi kunakucha, wazo lake lilikuwa moja tu la
kwenda kumtafuta Mishi ili ajue ni kwanini Ommy amemsaliti kwa huyo
mwanamke. Rose siku ya leo alijiandaa kwenda kwa mganga wa
kienyeji kwani bado swala la kupotelewa kwa pesa yake lilimuumiza sana na
alitaka kujua huyo anayewatoa kumbukumbu familia yake bila yay eye mwenyewe
kujua. Alimsihi mume wake asitoke kabisa siku ya leo, “Tafadhali usiende
popote” “Sawa, sitaenda popote” “Nitakuagizia mtu wa kukuletea
chakula, tafadhali leo usitoke. Narudia tena na tena tafadhali sana leo
usitoke” “Nimekuelewa mke wangu sitatoka” “Na Yule panya ambaye
jana hajarudi, sitaki uende kumtafuta wala sitaki umkaribishe hapa
tena” “Panya gani huyo?” “Si huyo shetani wa kuitwa Salome,
simtaki katika nyumba yangu. Tafadhali Patrick huyo mtoto simtaki, usitake
kabisa kunikera” “Nimekuelewa mke wangu, sitafanya kinyume
chako” Rose akatoka na safari yake ikaanza ila alipitia kwanza shuleni
na kumuacha mwanae Ana shuleni kisha yeye akaenda na safari yake ya kumtafuta
mganga, akiwa njiani akaanza kuwaza jinsi hela zake zilivyopotea kizembe halafu
jinsi mume wake akiwa hana kumbukumbu yoyote kuhusu alipozipeleka hizo pesa yani
aliwaza sana, ila gafla alifunga breki ya gari kwani mbele yake aliona begi
jeusi likiwa na mfanano wa lile lile begi ambalo aliliweka kwenye gari yake na
mumewe akaondoka nalo. Rose alishuka kwenda kuliangalia, akasogea na kulichukua
kisha akapanda nalo kwenye gari yake na kulifungua, alishangaa kuona pesa
nyingi, kwakweli alishangaa sana na kujiuliza, “Sio begi langu kweli
hili? Ndio lenyewe bhana” Alilifunga na kuweka pembezoni mwake kisha
akacheka, “Yani wamesikia naenda kwa mtaalamu wamerudisha begi, atakuwa
kiboko sana Yule ninayemuendea. Na wala sirudi, naenda tu nimkomeshe huyo kidudu
mtu asiyejulikana anayesumbua familia yangu” Akawasha gari yake na
kuendelea na safari. Sara aliwasiliana na Mishi kwa njia ya
ujumbe na kujifanya ni Ommy huku akimuomba msamaha kwa kauli ya jana yake, nia
yake kubwa ilikuwa ni kumuona huyo Mishi anafananaje. Alifika hadi eneo
alilopanga kukutana na huyo Mishi na akabahatika kumuona kabla Mishi hjamuona
yeye, hasira zilimpata yani muda huo hata hakutaka kujua kuwa Ommy yuko wapi au
kitu gani kimemkuta ila yeye alikuwa akiumizwa na wivu tu muda huo. Alitamani
aende amsogelee huyo Mishi na amuanzishie varangati ikiwezekana amdunde maana
alijiona yeye ni bonge ni Mishi ni mwembamba kwahiyo alihisi kuwa angemudu
kumdunda ila kabla hajaenda kufanya chochote alishangaa akishikwa bega, kugeuka
nyuma alishangaa sana maana alimuona Salome, “Kheeee Salome! Unafanya
nini hapa?” “Nikuulize wewe dada unafanya nini hapa?” “Kuna mtu
nilikuwa namsubiri maeneo haya” “Mmmh dada wakati ulikuwa unampango wa
kwenda kupigana na Yule dada wa kuitwa Mishi” “Umejuaje?” “Najua
tu, katu usipende kuruhusu mapenzi yakakutawala hivyo dada yangu hadi ushindwe
kufanya vitu vyako vya maana” “Sikuelewi Salome” “Mapenzi yapo
tu na siku zote yatakuwepo ila heshima yako ni kubwa sana kuliko hayo mapenzi,
mfano ukaenda na kupigana na Yule Mishi akakupiga itakuwaje? Si aibu hiyo mtu
bonge kupigwa na kimbau mbau. Na mfano ukaenda mkapigana weee ila ashishinde
yoyote itakuwaje? Ni kujidhalilisha huko, na mfano ukaenda kupigana na mtoto wa
watu bahati mbaya akaanguka na kufa, huoni kama utapata kesi ya kujibu! Dadangu
usitake mapenzi yakutawale kiasi hiko, tafadhali twende nyumbani” Maneno
ya Salome yalimuingia akilini Sara kwa kiasi chake, na kujikuta akitoa wazo la
kutaka kwenda kupigana na Mishi badala yake kugeuza na Salome na kurudi
nyumbani. Walifika nyumbani na moja kwa moja Sara alienda chumbani kwake
ambapo Salome alimfuata kwa nyuma, Sara alifika na kulia sana ila Salome alikuwa
akimuangalia tu. Sara alilia sana kuhusu mapenzi ila alipotulia kiasi Salome
alisogea na kumbembeleza. Sara alimuangalia Salome, “Wewe ni mtoto
mdogo, mapenzi huyajui vizuri” “Mimi ni mtoto kwa kuniangalia ila sio
mtoto kivile unavyonifikiria. Nimekuacha ulie ili utoe uchungu wako, dada yangu
narudia tena usipende mapenzi yakutawale” “Ila kwanini Ommy anifanyie
hivi? Kwanini Ommy anisaliti?” “Ila dada jamani mara nyingine unaweza
kumlaumu bure huyo Ommy ingawa ni kweli ana makosa, Ommy anakupenda sana na
alitaka kukuoa ila mama yako hataki hata kunuona akikusogelea, mama yako hataki
hata upate muda wa kwenda kuonana na Ommy. Jamani nae ni binadamu anamatamanio
jamani” “Khabari za Ommy wewe umezijuaje?” “Usiniulize tu habari
za Ommy nimezijuaje bali niulize pia habari za Mishi nimezijuaje, ila nakwambia
tena usiruhusu mapenzi yakutawale kiasi hicho. Ommy ni binadamu kama binadamu
wengine, si malaika Yule kusema atakuwa sahihi kwenye kila
kitu” “Unasema tu kwasababu huyajui mapenzi, simtaki tena Ommy. Sitaki
hata kumuona, akaendelea na hiko kimishi chake si kaniona mimi bonge
sifai” “Hizo ni hasira Sara, tena hasira ni hasara. Hapo ulipo hata
hujui Ommy yuko wapi ila unasema hutaki tena kumuona” “Sitaki ndio,
sitaki kujua hata alipo” “Ila moyo unakuuma, jambo lolote usilitafutie
jawabu wewe mwenyewe. Ni Ommy pekee anayeweza kukujibu kati yako wewe na Mishi
anampenda nani. Tunatakiwa tufanye jitihada za kumrudisha
Ommy” “Kumrudisha kwani yuko wapi?” “Ngoja nikuache ulale kidogo
ila ukiamka utakuwa na kumbukumbu zote kuhusu Ommy” Sara alimshangaa
sana Salome ila Salome alimuaga saran a kumuacha mule chumbani kisha yeye
akatoka zake. Rose alifika kwa mganga wake na kukuta watu wengi
sana kwenye foleni ila alishangaa akiitwa yeye ndani na kuwapita wote kwenye
foleni huku wengine wakilalamika, “Sababu kaja na gari, yani waganga
wanapenda matajiri sababu wanajua wanahela” Rose alitembea kwa madaha
sana na kuingia kwenye kibanda cha mganga ila alishangaa kuona kibanda kile
kikiwa tofauti na kwa waganga alipopazoea, na cha kushangaza alikaribishwa na
sauti ya kike. Rose alikaa lakini alikuwa na wasiwasi mwingi sana, kulikuwa na
mwanamke kajifunika na khanga mbele yake, mganga aliyemfata hapo ni mwanaume
kwahiyo kitendo cha kuona mwanamke amekaa hapo kilimshangaza sana. Na kujikuta
hata ameshindwa kusema chochote, “Elezea matatizo yako” Rose
alishtushwa na sauti ya huyu mganga kwani ilikuwa ni sauti ya mtu anayemfahamu,
akajikuta akisema kwa mshangao, “Mozaa!!!” Yule mganga alifunua
sura yake na kumfanya Rose ashtuke zaidi kwani ni kweli alikuwa ni
Moza. Rose alishtushwa na sauti ya huyu mganga kwani
ilikuwa ni sauti ya mtu anayemfahamu, akajikuta akisema kwa
mshangao, “Mozaa!!!” Yule mganga alifunua sura yake na kumfanya
Rose ashtuke zaidi kwani ni kweli alikuwa ni Moza. Kwakweli Rose
alitetemeka sana na kupata ujasiri wa gafla wa kutoka mule ndani na kuanza
kukimbia yani kila mtu aliyekuwa pale alimshangaa, alikimbia sana kufika mbele
akakumbuka gari yake na kujiuliza kurudi tena kuifuata, leo Rose alipatikana
yani alipatikana haswaa kupita siku zote anazopatikana. Alichoka sana na kuanza
kurudi kufata gari yake. Alipofika kwenye gari yake alifungua na kuingia
ndani ya gari, watu wapale karibu walimfata na kumuuliza kuwa ana tatizo gani
lakini hakuna aliyemjibu zaidi ya kuondoa gari yake na kuondoka zake. Njia zima
aliona kilichotokea kamavile ni ndoto tena ndoto haswaa, hadi hakujielewa jinsi
anavyoendesha gari. Akapata wazo la kuangalia lile begi la hela aliloliokota
kama lipo ila aliliona pale pale alipoliweka, kidogo akapata nafuu moyoni mwake
kuwa begi lipo huku akiendelea na safari ya kurudi nyumbani
kwake. Salome alikuwa amekaa sebleni kwa Rose ila Patrick
alitoka chumbani na kushangaa kumkuta tena Salome kwenye nyumba hiyo, alimuuliza
kwa mshangao “Wewe tena umefuata nini kwenye nyumba
hii?” “Jamani baba si nimekuja kwako, kuishi kwa baba
yangu!” “Kwani wewe ni mwanangu?” “Ndio mimi ni mwanao, naitwa
Maria” “Maria!! Ndio yupi?” “Mama yangu ni Neema na alinipa jina
la mama yako ambaye ni bibi yangu” Patrick alikuwa kama akitafakari
jambo na alionyesha kumkumbuka sana mama yake, kisha akainuka na kumkumbatia
Salome, “Jamani kumbe ndio wewe mtoto ambaye mama aliniambia kuwa
natakiwa kumfahamu, masikini mama yangu nilimkuta amekufa” “Pole sana
baba, ila mimi ndio Maria” “Naomba uishi hapa siku zote, mama alinihusia
nikupende na nikutunze ila mama yangu alikufa na sikujua kama mwanangu huyo
alikuwepo” Yani akili za Patrick zilikuwa zinakuja na kuondoka kiasi
kwamba alikuwa anashindwa kutambua jambo lolote kwa wakati mmoja yani mara
nyingine ilimlazimu kutafakari kwanza. Waliongea mengi sana, Patrick
alijikuta akimwambia Salome kuhusu familia yake. “Lakini mama yangu ndio
alikuwa mke wako wa ndoa!” “Ni kweli mama yako alikuwa mke wangu wa ndoa
ila alinitendea jambo bay asana siwezi kusahau ila sikutaka tu kumfungulia
mashtaka mama yako, na siku zote sikujua kama wewe upo yani kulikuwa na kauli
mbili kuwa ni kweli nina mtoto kwakwe ila kauli nyingine ilikuwa mtoto si wa
kwangu ila ana baba mwingine” “Alikufanyia jambo gani
baya?” “Unajua mama yako niliishi nae kwa muda mrefu sana bila kupata
mtoto, hivi unafikiri ni nani anayeweza kuvumilia muishi kwa miaka karibu
ishirini bila mtoto! Ni nani anayeweza kuvumilia hilo? Niliondoka takribani
miaka mitatu, kurudi kidogo tu mamako akasema amepata mimba yangu, unafikiri ni
rahisi kwangu kuamini hilo? Nilimfukuza nakiri hilo kabisa, na nilimfukuza kwa
hasira kwani sikuwa na imani hata kidogo kuwa amepata mimba yangu. Baada ya
miezi kadhaa nikapata habari kuwa anaishi kwa mamangu na mama akasema mtoto
anafanana sana na mimi na wamempa jina lake. Nilifurahi kusikia hivyo na nikawa
na lengo moja kwenda kumchukua mamako kwa mamangu na wewe tuishi pamoja. Cha
kushangaza siku niliyoenda nilimkuta mama yangu ameuwawa kikatili sana na watu
wote wakasema ni Neema tu ndiye amehusika na kifo cha mama yangu. Kiukweli
niliumia san asana, yani niliumia kupita maelezo. Nilitaka kumtafuta Neema
nimfungulie mashtaka akaozee jela huko ila mke wangu Rose akanishauri kuwa
nisifanye hivyo na nisahau habari za Neema, nimejitahidi kuzisahau hata na mtoto
aliyemzaa habari zake zilipotea kwenye akili yangu ingawa kuna baadhi ya ndugu
zangu walikuwa wananishauri nimtafute mwanangu, ila napenda sana kusikia ushauri
wa mke wangu na aliniambia nisifanye hivyo kwani hakuna ushahidi wowote kuwa ni
mwanangu. Ila leo umenikumbusha mbali sana, kwakweli Maria mwanangu nakumbuka
kifo cha mama yangu. Naomba unikutanishe na mama yako aniambie kwanini alimuua
mama yangu kikatili kiasi kile” Salome loe alimuangalia kwa makini huyu
mzee aliyeonyesha anaongea kwa kujiamini kabisa halafu anaonyesha kamavile akili
yake ipo salama kabisa kwa siku hii, Salome alijikuta akisema, “Sasa
huyu ndio mzee Patrick ninayeweza kuongea nae
kwasasa” “Sikuelewi” “Utanielewa tu, kwanza tambua kuwa mama
yangu hakuhusika na kifo cha bibi ila ukweli wote utaupata kwenye
ndoto” “Kwenye ndoto?” “Ndio kwenye
ndoto” “Kivipi?” “Subiri” Salome alitoka nje na baada ya
muda kidogo akarudi ndani na kitu kidogo kama kipande cha mkaa kisha akampa
Patrick atafune naye akafanya hivyo halafu akamwambia, “Leo ukilala
utaona kila kitu kama sinema jinsi mama yako alivyouwawa” “Mmmh kwani
wewe mwanangu ni mganga wa kienyeji?” Salome akacheka na
kumuuliza, “Mbona nilivyokupa dawa utafune hukuniuliza chochote? Mimi si
mganga baba, ila fanya vile nilivyokuelekeza” Patrick alitamani hata
aende akalale muda huo ili kama hiyo ndoto aipate muda huo kwani miaka yote
alikuwa akifikiri kuwa Neema ndiye aliyemuua mama yake ndiomana hakupenda hata
kumuona na wala kile kitendo cha kwenda kwa Neema hakijui maana kilifanyika kwa
namna nyingine. Patrick aliinuka pale sebleni na kumuacha Salome peke yake kisha
yeye akaelekea chumbani. Siku ya leo hii Neema alitoka nyumbani
kwake na kwenda kumtembelea rafiki yake, ambaye alimshangaa kwa mabadiliko ya
muda mfupi, “Mmmh nipe siri ya mafanikio shoga maana sio kwa kung’aa
huko, halafu pale kwako mbona umehama bila kusema?” “Ndiomana nimekuja
nikuhadithie” Kisha akamuelekeza jinsi yeye alivyokuta wameshahama na
jinsi Ashura alivyomtumia ujumbe, “Mmmh kumbe Yule mdogo wako ana upendo
hivyo!” “Ndio, nakushangaa tu wewe ulikuwa na mashaka
nae” “Kwakweli nisiwe mnafki, sijawahi kumuelewa Yule mdogo wako na
sijawahi kumuamini kabisa. Yani kila alichokuwa akiongea nilikuwa nakitilia
mashaka, eti leo hii ndio amekutafutia nyumba nyingine ya kukaa
mmmh” “Na zaidi ya yote baba yake Salome yani Yule alikuwaga mume wangu,
amejirudi yani kawa mpole huyo balaa. Aminiomba msamaha na amesema yupo tayari
kumlea mtoto wake” “Ila wanaume bhana, kaona mtoto amekuwa ndio
kujifanya yupo tayari kumlea mtoto wake. Ila napo ni vizuri, halafu kitu
kingine, mbona Salome simuoni shule?” “Na hilo ndio jambo lingine
limenileta ili unipe ushauri, Salome hataki shule kwasasa, unaweza kuamini hilo?
Salome amesema anataka kupumzika kwahiyo nimuombee ruhusa ya ugonjwa, kwa kifupi
Salome wangu hataki shule kwasasa” “Kheee makubwa hayo, utaniletea
niongee nae” “Sawa nitakuletea maana wewe ndio mshauri wangu, na wakina
Pendo wako wapi?” “Wameenda kanisani” “Kheee watoto wale kwa
kanisa loh!” “Ila ndio vizuri, na hakika hata wakina Salome wangependa
kusali sidhani kama angekataa shule” “Basi saivi hizo ibada ndio kama
kituo cha polisi, mtoto hataki kabisa kuongelea habari hizo” Mara
akafika mgeni mwingine pale kwa mama Pendo ila huyu mgeni baada ya salamu kama
alionyesha kumfahamu kidogo Neema yani ilikuwa kama kuna tukio ambalo alilifanya
Neema halafu yeye analijua. “Mmh hivi sio wewe ambaye mwanao alitumbukia
kwenye kaburi!” Neema nae alishtuka kuona kuna mtu anagundua kuhusu hilo
jambo kwani yeye na Sa lome kwenye msiba ule hakujua kama kuna watu
wangetokea kuwafahamu, “Kwani na wewe ulikuwepo kwenye ule
msiba?” “Ndio nilikuwepo, na lile tukio lilikuwa la kushangaza sana.
Nakukumbuka vizuri sababu mimi ndiye ulinikuta pale njiani na nikakwambieni
tunaenda kwenye msiba wa Moza, mkashangaa pale kuwa Moza amekufa kisha tukaaanza
kuongozana kuelekea makaburini’ Ndio Neema nae alipoanza kukumbuka hilo
tukio na kuona ni kweli kabisa kama ni yeye lazima awe anamkumbuka
vizuri, “Vipi mwanao hali yake maana kila mtu alipigwa na bumbuwazi pale
msibani” “Mwanangu amepona wala sikutaka kurudi tena kule zaidi zaidi
kwenda na mwanangu nyumbani” “Hata mngerudi kule kuna kilichokuwa
kinaeleweka basi! Yalitokea makubwa sana, mwili wa marehemu ulitoweka na hadi
leo hakuna anayejua kilichoendelea labda ile familia tu. Ulitokea upepo wa gafla
pale makaburini na kila mmoja akikimbia na lwake. Kwakweli hali ilikuwa mbaya
sana” “Duh poleni sana, kwahiyo marehemu hakuzikwa?” “Azikwe
vipi na hata mwili wake haujaonekana” Mama Pendo ikabidi aingilie kati
maana haya maelezo hata yeye yalimchanganya kabisa, “Unataka kuniambia
Salome alitumbukia kwenye kaburi” “Ndio alitumbukia halafu
akazimia” “Yani Neema umekaa tu na mtoto na alipatwa na makubwa kiasi
hiko, anakataa shule unakaa nae tu hujiulizi! Mlete nimpeleke kwenye
maombi” “Nitajaribu kumwambia kama atakubali” “Wewe ni mama yake
bhana, atakubali tu” Neema aliitikia pale ila hakuwa na namna ingawa
Salome alimwambia kuwa wafanye siri ila atafanyaje na mambo yameshakuwa kama
hivyo yani kuna watu wanamkumbuka vyema. Aliaga muda huo na kuondoka
zake. Rose alikuwa amevurugwa kabisa akili na gari alikuwa
anaendesha ilimradi tu, kitendo hicho kilimfanya afike nyumbani kwake saa tano
za usiku, aliingiza gari ndani na kushuka kisha akaenda sebleni kwake ila
akakumbuka lile begi lenye hela akaamua kwenda kulichukua kwanza kabla na
lenyewe haljachukuliwa. Cha kushangaza muda huu alienda kuliangalia mule kwenye
gari hakuliona na kumfanya achanganyikiwe tena, “Jamani, begi langu
limeenda wapi tena?” Akamuuta mlinzi kwa nguvu na kuanza kumuuliza kama
ameona begi ila mlinzi alikuwa akimshangaa tu maana ni muda huo huo ameingia
sasa huyo mlinzi alione begi na kulichukua aende nalo wapi. “Mi sijaona
begi mama” “Inamaana limeibiwa na nani sasa?” “Labda huko huko
ulipotoka mama lakini hapa hakuna hata mtu mmoja anayeweza kufungua gari na
kuiba” “Hebu niondokee hapa” Rose alijikuta akifoka tu kisha
kwenda tena ndani na akiwa na mawazo lukuki kuwa begi limepotea tena kwa mara
nyingine, hakukaa sana sebleni kwani watu wote kwenye nyumba yake walikuwa
wamelala hivyo akaamua kwenda chumbani kwake na kumkuta mumewe akiwa amelala
hoi, “Huyu nae kalala kama mzigo leo, na wala simuamshi atajijua
mwenyewe saivi nina mawazo yangu” Akawaza pale cha kufanya kwa usiku ule
ila hakupata jibu kabisa na alijiona kama sijui kitu gani ila wazo lingine
likamtuma kuwa aende chumba alichokuwa analala Moza ili akapekue kitu Fulani,
hakutaka kupuuza wazo hilo na moja kwa moja akaenda chumba alichokuwa analala
Moza ila alipofungua mlango alimuona mtu amekaa amempa mgonga, kwa mashaka zaidi
Rose aliuliza, “Wewe ni nani?” “Ni mimi” “Ni nani
wewe?” Yule mtu akageuka na kumfanya Rose aanguke na kuzimia, na ilikuwa
ni mara ya kwanza katika maisha yake kuzimia kwa muda mrefu kama siku
hiyo. Kulipokucha Rose alijikuta kitandani kwake na kuanza
kujiuliza kuwa mara ya mwisho alikuwa wapi na mbona amepatwa na kitu ambacho
hakijawahi kumpata maishani mwake, “Yani na mimi Rose nalogwa?
Haiwezekani yani haiwezekani kabisa” Rose akakumbuka mara ya mwisho
alienda kwenye chumba alichokuwa analala Moza na alimuona mtu ila sura ya Yule
mtu alipogeuka hakuiona vizuri zaidi ya kuzimia. Hasira zikampanda na kujiuliza
kuwa ni nani anayecheza na akili yake, akataka kuita familia yake yote sebleni
siku hiyo ili ajue kinagaubaga kuwa ni nani anacheza na akili yake. Akatoka
sebleni ila akagundua kuwa watu wake wote bado hawajaamka ukizingatia hata
Patrick amemuacha kwenye usingizi wa hali ya juu, alianza kuita mmoja mmoja na
waliokuja sebleni kwa muda huo walikuwa ni wale mapacha na Ana, akauliza kwa
hasira “Wengine wako wapi?” “Wakina nani mama?” “Sara na
baba yenu?” “Kuhusu Sara sidhani kama amelala hapa nyumbani
jana” “Mnasemaje nyie?” “Hatukumkuta mama, sidhani kama amelala
hapa nyumbani jana” Rose akashikwa na hasira na kwenda chumbani kwa
Sara, akafungua ila hakumkuta Sara na kumfanya apate jibu kuwa ni kweli Sara
hakulala nyumbani kwa siku ya jana, “Huyu mtoto ameanza kunichezea akili
eeeh! Atalalaje nje ya nyumbani, atalalaje nje ya nyumba yangu!” Akarudi
tena sebleni kwa hasira, na kuuliza “Ni nani alilala chumba cha Moza
jana?” “Mmmh mama, nani anayeweza kulala mule zaidi ya Yule binti
Salome. Na toka ameondoka siku ile hajaja tena” Akawaangalia wale wanae
mapacha na kuwauliza, “Ni nini mnajua kuhusu mimi?” “Hatujui
chochote mama” “Mna uhakika?” “Ndio hatujui
chochote” “Haya mnaweza kuondoka, na wewe Ana mwanangu unaweza kwenda
kujiandaa na kwenda shule najua hata wewe unachukizwa na hali hii
mwanangu” Rose akaondoka na kuelekea chumbani, ila wale mapacha kabla
nao hawajaondoka walishangaa kumuona Sara na Salome wakitokea njia ya vyumbani,
na kushangaa “Inamaana dada Sara ulikuwa chumbani?” “Ndio, jana
nililala na Salome chumbani kwa Moza” Wale mapacha wakatazamana maana
mama yao aliwauliza kuwa ni nani alilala kwa Moza jana na hawakuwa na
jibu. Kwa upande wa Rose, aliingia chumbani kwake na kumuamsha Patrick
ila la kushangaza leo Patrick alivyoamka aliinuka na kumuwasha kibao Rose kisha
akamwambia, “Yani wewe mwanamke umeniulia mama yangu!” Kabla
Rose ajajitetea, alishangaa akipigwa kofi
jingine. Wale mapacha wakatazamana maana mama yao
aliwauliza kuwa ni nani alilala kwa Moza jana na hawakuwa na jibu. Kwa
upande wa Rose, aliingia chumbani kwake na kumuamsha Patrick ila la kushangaza
leo Patrick alivyoamka aliinuka na kumuwasha kibao Rose kisha
akamwambia, “Yani wewe mwanamke umeniulia mama yangu!” Kabla
Rose ajajitetea, alishangaa akipigwa kofi jingine. Kitendo hicho kilimchanganya
sana rose na kila alipotazama sura ya mume wake ilionyesha kuwa na hasira za
wazi wazi, Patrick aliendelea kwa kusema, “Mwanamke wewe ni shetani tena
shetani mwenye mapembe, yani siku zote hizi nilikuwa sijui kama naishi na
shetani, yani wewe wa kuniulia mimi mama yangu!” “Patrick sikuelewi mume
wangu” Patrick akamzabua kibao kingine Rose, cha safari hii kilikuwa cha
hali ya juu hadi Rose akajihisi kizunguzungu na kuanguka chini akaona akimchekea
Patrick atamuumiza, vile alivyoanguka Patrick akamsogelea na kutaka kumpiga tena
ila kuna dawa Rose akampulizia machoni Patrick na muda huo huo kizunguzungu
kikasmshika Patrick na kuanguka chini. Rose alimuacha Patrick pale chini
kisha yeye akatoka sebleni. Alipofika sebleni akashangaa
kumuona Salome akiwa na Sara pamoja na wale mapacha, alimuangalia Sara kwa
hamaki na kumuuliza kwa kumfokea, “Leo umelala nje
eeeh!” “Hapana mama” “Hapana kitu gani, mbona nimekuja chumbani
kwako sijakukuta” “Nililala na Salome kwenye chumba cha
Moza” “Nini?” Sara alirudia yale maneno ila Rose alionekana
kuchukizwa zaidi, ila wakati huu huu Sara alimuuliza mama
yake, “Kilichonifanya nilale na Salome ni kuwa nilikuwa naogopa peke
yangu, mama Ommy yuko wapi?” Rose hakujibu ila aliwaangalia wale mapacha
wake na kuwafokea, “Nyie, si niliwaruhusu kuondoka” Nao walitoka
haraka haraka kwani waliogopa mama yao asije akabadilisha mawazo maana huwa
hakawii. Walivyotoka alimuangalia Salome na kumuuliza, “Na wewe nani
amekuruhusu kuja tena humu ndani?” “Yani kuja humu sitangojea ruhusa
maana ni kwa babangu” “Wewe mtoto nitakuja nikufanye kitu mbaya
sana” “Najua huwezi kunifanya lolote” Salome akatoka pale
sebleni na kwenda tena chumbani kwa Moza maana muda huo alikuwa amechukia na
angeweza hata kubadilika. Sasa Rose alibaki na mwanae Sara kisha akamwambia
mwanae atoke tu amuache nae Sara akafanya hivyo na moja kwa moja alienda tena
chumbani kwa Moza akazungumze na Salome. Rose alitoka tena nje kujaribu
kuangalia lile begi la hela ila hakuliona bado yani hapo ndio akaamini kweli
hadi yeye kafanyiwa kiini macho. “Atakuwa ni Moza tu, na nitapambana
nae. Ila nitaweza kupambana na mzimu? Mmmh! Cha kufanya ni kuwa nihakikishe
haingii kwenye nyumba yangu, ngoja nizunguke nyuma” Rose alizunguka
nyuma ya nyumba ili aangalie cha kufanya na mzimu wa Moza usiingie kwenye nyumba
yake. Sara alienda kumuuliza Salome kwani yeye bado moyo
ulikuwa unamuuma sana kuhusu kusalitiwa na Ommy, “Ni kweli nimeona kuwa
Ommy alitoweka, tena inawezekana ni mama kamficha Ommy ila kila ninapotaka
kukazana kumsaidia Ommy naiona sura ya Mishi yani naona kama namsaidia Mishi
kumpata mpenzi wake” “Unaongozwa na wivu Sara, yani ni wivu ndio
unakusumbua kwenye moyo wako. Kumbuka hata wewe Ommy unampenda, na akirudi
atasema ukweli kuwa kati yako wewe na Mishi anampenda nani” “Mfano
akimchagua Mishi je?” “Sioni kama ni tatizo hilo, atakuwa amekusaidia
maana hutojiumiza tena moyo kwa kumfikiria mtu asiyekupenda. Mara nyingine kujua
ukweli ni bora zaidi, mfano Ommy akifa huko wewe utapata faida gani? Utasema tu
Mishi kakosa na mimi nimekosa, ila kuna faida yoyote unapata? Hakuna, mara
nyingine kujua ukweli ni bora zaidi. Kuna watu wanakupenda wanakufataga ila
unawakataa sababu upo na Ommy ila ukweli umeujua hakuna tena kusumbuliwa akili
badala yake utaangalia unayempenda kati yao na kumkubali. Na hata ukiwa nae
usiruhusu mapenzi yatawale akili yako yani akili yako isiendeshwe na hisia za
kimapenzi maana ukiendeshwa na mapenzi, sehemu kubwa ya moyo wako itabebwa na
wivu na utajikuta ukifanya jambo baya bila kutarajia. Fanya mapenzi ni sehemu tu
ya maisha ila sio kila kitu katika maisha” “Unajua Salome, wewe ni mtoto
mdogo sana ila unayachambua mapenzi vilivyo. Kwani ushawahi kuwa na mpenzi na
udogo huo?” Salome akacheka kisha akamwambia dada
yake, “Tuachane na habari hizo ila tuangalie jinsi gani unaweza kumuokoa
Ommy, tambua kwamba Ommy anatakiwa kuokolewa” “Sawa nitafikiria na
ushauri ulionipa, nitaongea na mama amuachie Ommy maana mama yangu ni mchawi
kabisa ni mchawi sijui nifanyaje aache” “Unataka mama yako aache
uchawi?” “Ndio, na mdogo wangu Ana aache uchawi tuwe watu wa kawaida tu
na tuishi maisha ya kawaida” “Ila uchawi wanakula viapo, unadhani ni
rahisi hivyo kuacha?” “Sijui” “Uchawi inatakiwa mtu aache kwa
ridhaa yake mwenyewe ila kwa kulazimishwa haachi, nitasaidia na mama yako
ataacha uchawi kwa ridhaa yake mwenyewe” Sara alikuwa anamuangalia
Salome bila ya kummaliza, kisha Salome akamuomba Sara ampishe muda huu anahitaji
kuvaa. Sara aliondoka na kwenda chumbani kwake, akampisha avae ila akajiuliza ni
kwanini Yule Salome hawezi kuvaa mbele yake wakati yeye ni mwanamke
mwenzie, “Mmmh kila akitaka kuvaa anasema nimpishe, halafu Yule mtoto
mbona anaongea mambo ya kikubwa sana!” Akajiuliza sana, na kuamua kwenda
dirishani kwake kuchungulia yani akili ilimtuma tu kufanya vile, wakati
anachungulia gafla akamuona mama yake kapiga magoti kwenye ua, Sara alishangaa
sana na kuamua kutoka ili amfate na kumuangalia vizuri maana uchawi wa mapema
vile ulimuogopesha hata yeye kwani aliamini tu kuwa mamake ni mchawi ila
hakufikiria kama uchawi unaweza kufanywa peupe
vile. ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment