Search This Blog

Tuesday 1 November 2022

MY CLASSMATE - 5

 





    Simulizi : My Classmate

    Sehemu Ya Tano (5)





    Damu zikaanza kumwagika Kerspersky !. Kerspersky alianza kulia kwa sauti. Maumivu hayakuwa na mfano sasa !.



    "Nitasemaa.. ! "

    Daniel alijifanya kama hamsikii.

    Hali ilikuwa ngumu sana kwa Kerspersky.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Mkono wa Kerspersky ulikuwa unaelekea kukatika. Sasa ule mkanda ulifika kwenye mfupa wa mkono !

    Daniel alikuwa mtu katili sana. Hakumuonea huruma. Alikuwa anamwangalia tu Jamaa.



    Sasa Daniel alitosheka. Akamfungua ule mkanda Kerspersky.

    "Utaongea" Alimuuliza huku anaangalia pembeni.

    "Ndio kaka" Alijibu kwa sauti ya huruma.

    "Unaitwa Nani?"

    " Abednego "

    "Nani anayekutuma kuua ?"

    "Salehe"

    "Yuko wapi sasa hivi ?"

    "Mbeya"

    "Amefata nini Mbeya"



    Kerspersky alieleza kila kitu kuhusu Mpango wao wa Angamizo.

    Alieleza pia kuhusu watu waliotuma Kigoma na Mara.

    Daniel aliwapigia simu wakuu wa Polisi wa Kigoma na Mara. Kuhakikisha wale watu wamakamatwa.

    Na mwenyewe alijiandaa kwenda Iringa kusimamisha Mpango huo haramu.



    Aliwachukua askari kumi pale kituo cha Polisi Posta. Kwa ajili ya kwenda kuuangamiza Mpango wa Angamizo.



    Saa mbili usiku waliwasiri jijini Iringa Kwa ndege. Kuhakikisha silaha zote zilizopo katika ghala kuu la silaha la Taifa haziibiwi. Zinabaki salama !



    Kwa ruhusa ya Raisi, Daniel na askari wale kumi waliingia kwenye ghala la silaha. Huku askari wengine wakibaki nje kufanya doria. Wakatulia tuli kusubiri chochote kitakachotokea...



    Huko Jijini Mbeya Salehe alikuwa anasubiri taarifa za angamizo kwa watu aliowatuma.



    Salehe alipanga usiku ule wafanikishe mauaji makubwa . Kabla jioni hawajaenda Makete

    Kuhitimisha angamizo, Salehe aliamua kuacha Angamizo kubwa Tanzania.



    Salehe alienda sokoni Mwanjelwa. Mkononi akiwa kajipaka sumu ya Proxine. Kutokana na wingi wa watu Mwanjelwa, Salehe aligusana na watu wengi sana. Alihakikisha kila baada ya dakika tatu anapaka dawa ya kuondoa madhara ya Proxine. Ndani ya dakika kumi, watu ishirini walikufa kifo cha kinyama sana pale sokoni.



    Polisi walipata taarifa, wakati Polisi wanaenda Mwanjelwa kwa kasi kwa gari yao. Salehe alikuwa kashatoka, alikuwa stendi kuu ya mabasi Mbeya. Nako aliacha Angamizo.

    Polisi walipata taarifa za mauaji mapya ya kinyama stendi kuu ya mabasi Mbeya. Polisi walichanganyikiwa sasa. Gari za Polisi ziliwasha moto kwenda stendi. Walienda kwa kasi kubwa sana, ndani ya dakika tano stendi ilijaa Polisi.

    Saa kumi na mbili jioni ilimkuta Salehe ndani ya uwanja wa mpira wa Sokoine. Daniel aliteketeza mashabiki wengi sana wa mpira kwa sumu ya Proxine.

    Salehe aliangamiza !



    Kamanda mkuu wa Polisi mkoa wa Mbeya alipiga simu kwa Mkuu wa Polisi nchini.

    Aliomba msaada.

    Aliomba Daniel aende Mbeya kusaidia.

    IJP Rondo alivyomaliza kuongea kwa simu ya Kamanda wa Polisi wa Mbeya, kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mara nae Alipiga, watu ishirini walikuwa wameteketea kwa sumu ya Proxine, sokoni Musoma.

    Naye aliomba msaada, alikuwa anamhitaji Daniel.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Ghafla simu ya kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma nayo iliingia , wavuvi sita walikuwa wameuwawa kwa sumu ya Proxine, ufukweni mwa ziwa Tanganyika.

    Naye aliomba Daniel aende Kigoma.



    Sasa nchi ilitingishika !

    Mkuu wa Polisi Tanzania, IJP Rondo jasho lilikuwa linamtiririka !

    Akapiga simu kwa Daniel, Daniel alikuwa hapatikani !

    IJP Rondo alizidi kuchanganyikiwa ! Mara, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma akawa anapiga tena simu.

    IJP Rondo aliiangalia tu simu ile. Hakutamani kabisa kuipokea. Simu iliita hadi ikakata.

    Ilivyokata, simu yake ilikuwa inaita tena, alikuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Mara naye alipiga tena.

    IJP Rondo macho yalimtoka pima !

    Aliichukua ile simu na kuitoa betri kabisa. Alikaa kwenye sofa akiwa kajishika tama !

    Alielekea kuwehuka !



    Zwangendaba alitumwa kupeleka Angamizo Kigoma wakati Nduli alitumwa kupeleka Angamizo Mara. Salehe alibakisha Angamizo jijini Mbeya. Kila mmoja alikuwa na chupa za Proxine kumi. Walidhamiria kuleta kweli vita vya tatu vya dunia.

    Walikuwa wanaua bila huruma !



    Huko Kigoma, baada ya Zwangendaba kutoka katika ufukwe wa ziwa Tanganyika, sasa alikuwa anaingia katika uwanja wa lake Tanganyika. Kulikuwa na onyesho la mziki. Alidhamiria kwenda kuuwa humo. Alifanikiwa, watu zaidi ya ishirini waliuwawa kinyama kwa sumu ya Proxine. Baada ya kupata habari za vifo vya watu hawa tena, Kamanda wa Polisi alimpigia simu IJP Rondo. Simu haikupokelewa. Alijaribu kupiga tena, simu haikupatikana. Kamanda wa mkoa wa Kigoma alichanganyikiwa sana.



    Huko Mara nako hali Ilikuwa tete. Nduli alipeleka madhara makubwa katika mkoa huo. Nduli aliingia baa moja , ndani ya dakika tano alihakikisha amewagusa watu wote mule baa. Baada ya muda mfupi baa nzima ikibaki mifupa na mafuvu.

    Walevi kumi na sita walienda kuzimu bila ngozi !



    Saa mbili usiku ilimkuta Salehe akiwa Mbeya carnival. Disko lilikuwa limeshaanza muda huo. Alipanda kule juu kwa DJ na kufungua vichupa vitatu vya Proxine. Alirusha hewani sehemu ambayo kulikuwa na watu wanacheza disco. Baada ya dakika kumi kulitokea picha mbaya ndani ya Mbeya carnival.

    Watu wengi waliuwawa kwa sumu ile !



    Saa nne usiku iliwakuta wakina Salehe wakiwa ndani ya chumba kilekile, ndani ya Green view hoteli. Zwangendaba na Nduli washarejea, walikuwa wanamsubiri Kerspersky ili safari yao ya kwenda Makete ianze. Kerspersky hakuwa anapatikana !

    Walimsubiri mpaka walichoka !



    Waliamua kwenda Makete bila Kerspersky, ndege ya kukodi ilitua Iringa saa tano na robo usiku. Walikuwa watu kumi na mbili hatari !. Walikuwa tayari kwa mapambano. Walikuwa wanajiamini, kwa maangamizo waliyoyapeleka Mara, Mbeya na Kigoma waliamini ulinzi hautokiwa mkubwa sana Makete.



    Walijipanga vizuri. Walikuwa na vifaa na zana zote muhimu. Walikuwa wana silaha za kutosha. Waliandaa maroli saba kwa ajili ya kubebea silaha. Waliyapaki porini.

    Sasa wenyewe walikuwa wananyemelea katika ghala kuu la silaha.



    Wanajeshi wanne. Meja Badi Bwino, meja Fuga Tindo, Meja Kurasa Allen na Meja Swalo Mbombwe, Zwangendaba. Nduli. Kulikuwa na Salehe pamoja na madada watano hodari katika mapigano ya ana kwa ana, walikuwa wanajiita, Dadaz killers .Walikuwa na sifa moja kuu, shabaha ya kutisha unapowakabidhi bastola.



    Ghala kuu la silaha lilikuwa kijijini Makete. Ni watu wachache sana ndio walikuwa wanajua uwepo wa ghala lile kijijini hapo. Wanajeshi hawa wanne ndio walifichua uwepo wa ghala hilo. Taarifa zikapenya kwa Salehe. Naye akazivujisha kwa Mzee Makame.



    Mzee Makame alikuwa mtu mjanja sana. Alikuwa Mtoto wa mjini. Taarifa za kuwepo ghala kuu la silaha Iringa ilikuwa ni taarifa muhimu sana kwake. Aliiona ni kama fursa na aliamua kuitumia.



    Ni yeye ndiye aliyeongea na wanamgambo wa kikundi cha kigaidi cha huko Somalia. Na kumuahidi fedha nyingi sana endapo wangezipeleka silaha hizo.

    Mpango pia ulihusisha na mawaziri. Waliokuwa wanakitumia kivuli cha Mzee Makame.



    Kundi la watu kumi na mbili sasa walikuwa wanalikaribia ghala kuu la silaha. Sehemu muhimu sana kwa Taifa.



    Daniel Mwaseba alikuwa kashawapanga vizuri askari wake kumi, wametulia tuli ghalani, na askari wakiolilinda ghala lile kwa nje, walikuwa ishirini. Jumla walikuwa askari thelathini imara. Wakiwa tayari kulitetea Taifa lao juu ya udhalimu huu mkubwa.



    Sasa kundi lile hatari lilibakisha mita mia moja tu kulifikia ghala.!





    Kule ndani ya ghala askari walikuwa wametulia tuli, wakiongozwa na Daniel Mwaseba.

    Lilikuwa ghala kubwa, lenye kila aina ya silaha.

    Daniel Mwaseba alikuwa amekaa karibu kabisa na mlango wa ghala lile.

    Alikuwa mtulivu sana.

    Akiwa tayari kwa lolote !



    Ghafla, taa zilizimika. Eneo lote kuzunguka ghala kulikuwa na giza !

    Kuzimika kwa taa ilimaanisha muda wakiosubiria wakina Daniel Mwaseba umefika.

    Muda wa kupambana!



    Historia ya ghala lile ilikuwa halijawahi kuwa giza vile tangu lianzishwe.

    Kulikuwa hakujawahi kuzimika umeme kabisa.

    Walikuwa wanatumia umeme maalumu ukiozalishwa kwa nishati ya jua.

    Kwahiyo watu wote walitambua kwamba, umeme ulikuwa haujakatika,

    Ila umeme ulikuwa umekatwa! Hali ya tahadhari iliongezeka kwa askari wale.

    Sasa kila mtu alikuwa imara, kaishikilia bunduki yake. Tayari kwa lolote.



    Daniel Mwaseba, aliona ule sasa haukuwa wakati wa kukaa ndani, kusubiri maadui waje. Aliona ule ni wakati wa kutoka nje, kupambana na adui.

    Ulikuwa muda wa kufa,

    ama kupona !

    Daniel aliwapa ishara wale askari kumi, wote wakawa wanatoka nje.

    Kumtafuta adui !



    Nje kulikuwa na giza totoro. Ghala la silaha lilikuwa msituni. Msitu nao uliozidisha hali ile ya giza.

    Sasa ilikuwa hatari!

    Hatari ya kupigana risasi wenyewe askari, endapo hawatokuwa makini.

    Daniel Mwaseba aliwaamrisha askari wote kurudi ghalani.

    Ili wajipange upya.



    Kule nje, Meja Badi Bwino, ndiye alikuwa anaongoza operesheni hii kwa upande wa maadui.

    Meja Badi Bwino aligawa kikosi chake katika makundi manne, yenye watu watatu watatu.

    Kundi la kwanza liliongozwa na Meja Kurasa Allen, kundi hilo alikuwemo pia Nduli na mwanadada mmoja, walielekea upande wa mashariki wa ghala lile.

    Kundi la pili liliongozwa na Meja Fuga Tindo, katika kundi hili walikuwemo pia Zwangendaba na mwanadada mmoja, kundi hili lilienda upande wa magharibi wa ghala lile.

    Kundi la tatu liliongozwa na Meja Swalo Mbombwe, Salehe na mwanadada mmoja. Wao walibaki palepale ili kutoa msaada upande wowote watakaohitaji msaada, iwe magharibi au mashariki.

    Wao ndio walikuwa walinzi wa wenzao.

    Na kundi la mwisho liliongozwa na mwenyewe Meja Badi Bwino, yeye aliongozana wadada wawili. Walikuwa wanaenda mahali geti lilipo. Kijana mmoja shushushu alifanya kazi nzuri.

    Ni yeye aliyeharibu mfumo wa umeme kule ndani.

    Hakika walijipanga vizuri sana watu hawa !



    Kule ndani kulikuwa na mvurugano. Askari waliingiwa na woga !

    Woga wa kuuliwa!

    Woga wa kuuwawa!http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hawakuwa wanajua kuna maadui wangapi huko nje ? Woga pia ulichangiwa na lile giza.

    Askari waliingiwa na taharuki hofu kubwa ! Daniel akajua bila kuwa imara yeye, watafeli katika operesheni ile. Ulikuwa wakati mgumu sana kwa Daniel, ukiohitaji hekima, busara na akili za Daniel Mwaseba.

    Woga ni kitu kibaya sana katika operesheni za hatari kama hizi !



    Daniel alishauri askari wote thelathini wabaki kulinda silaha mle ghalani, yeye pekee alienda kupambana gizani, na wauaji asiojua idadi yao, asiowajua idadi yao. Wale askari wengine walikubaliana na Daniel. Daniel Mwaseba alitoka nje peke yake, akiacha kuwafungua askari wale kwa nje.



    Kule nje, kundi lililoelekea magharibi mwa ghala lile. Walifika ukutani. Kundi lilikuwa linaongozwa na mwanajeshi hatari sana, Meja Fuga Tindo. Ghala lilizungushiwa ukuta mrefu sana, ambao haukuwa rahisi kupandwa na binadamu wa kawaida. Lakini Fuga Tindo hakuwa binadamu wa kawaida kama wewe. Aliuparamia ukuta ule mithili ya paka, kimya kimya. Zwangendaba na yule dada walishangaa sana uwezo wa Fuga Tindo. Giza lilikuwa upande wake Fuga. Na kutetereka kwa wale askari mle ndani lilikuwa kosa kubwa sana. Maana hakukuwa na askari yeyote akiyeulinda ukuta ule. Fuga Tindo, sasa alikuwa ndani ya uwanja mpana wa ghala lile. Alikuwa ananyata taratibu.

    Bila kutoa sauti yoyote ile.



    Kwa upande wa Daniel Mwaseba aliamua kupambana, sasa alichukulia kama yuko peke yake katika operesheni ile.

    Aliapa kimoyomoyo, lazima ashinde, ndio !

    Lazima auangamize mpango wa Angamizo !



    Kuzimika kwa umeme ghafla kulimjurisha kitu Daniel, alijua kwa vyovyote aliyekorofisha umeme ule alikuwa ndani ya ghala mlemle.

    Daniel Mwaseba sasa alizidisha umakini, hakumuamini mtu yeyote .

    Alinyata taratibu gizani na kujibanza katika kona moja, kona ambayo ilimuezesha kuona japo kwa shida ukuta ule wote kwa mbele.



    Kule upande wa mashariki, Meja Kurasa Allen na watu wake, nao waliufikia ukuta . Kama Meja Fuga Tindo, Meja kurasa nae aliparamia ukuta ule.

    Meja Kurasa sasa alikuwa juu ya ukuta ule. Akijiandaa kuteremka kwa ndani.

    Alichelewa !

    Risasi moja ilitua kichwani kwa Meja Kurasa. Alirudi kwa kasi kule nje alikotoka.

    Bastola ya Daniel Mwaseba ilifanya alichoituma !

    Nduli alienda kwa kasi pale alipoanguka Meja Kurasa. Walimkuta na jeraha baya sana kichwani, damu zinabubujika ! Alikuwa kashakata roho !

    Taharuki !



    Daniel Mwaseba aliachana kabisa na kivuli kile alichokitungua. Sasa alikuwa anatambaa kukifata kivuli kikichonyata kimya kimya, kilikuwa kivuli cha Meja Fuga Tindo.

    Wakati Meja Fuga akinyata kwa kutembea, Daniel Mwaseba alikuwa anamnyatia huku amelala !

    Lilikuwa giza hasa mule ndani, Zilikuwa zinatumika hisia zaidi ya macho.

    Akiwa pale chini, Daniel Mwaseba alitoa bastola yake yenye kiwambo cha kuzuia sauti. Alikilenga mgongoni kile kivuli cha Meja Fuga Tindo. Risasi ya moto isiyotoa sauti hata kidogo ilitua katika ya uti wa mgongo wa Meja Fuga. Daniel alikishuhudia kivuli kile kikidondoka chini kama mzigo!

    Daniel alifanikiwa kumuuwa mtu wa pili hatari usiku ule.



    Kule nje, Badi Bwino, mkuu wa operesheni hii, akiwa na wadada wawili walikuwa wanalikaribia geti kuu la ghala lile. Walishangazwa sana na ukimya wa mahali pale.



    Ndani ya ghala kulikuwa kimya, kama hakukuwa na watu.

    Meja Badi Bwino aliingiwa na wasiwasi sana.

    Kilikuwa kimya cha kuogofya !

    Walizidi kusogea, kila mmoja akiwaza lake kichwani.

    Ghafla wote walipigwa na butwaa !

    Geti la ghala kuu lilikuwa wazi !

    Mtego!

    Sasa Meja Badi Bwino na wale madada wawili walizidisha umakini. Walisogea taratibu, kwa tahadhari kubwa. Haikuwa kawaida geti lile kuwa wazi, tena usiku wa manane !



    Kule ndani, Daniel Mwaseba alirejea katika lindo lake. Alikuwa kabana palepale konani, huku macho yake yote yakiwa pale getini. Alifungua geti makusudi, ili akilenge Kivuli chochote kitakachojitokeza.

    Na kweli.

    Kivuli kilitokea !

    Ilihitaji mtu makini kuweza kukilenga kivuli kile, kukiwa na giza namna ile, na umbali na umbali namna ile.

    Mtu wa aina hiyo alikuwepo, Daniel Mwaseba.

    Daniel Mwaseba alikuwa na uwezo huo.

    Aliitoa bastola yake kiunoni taratibu.

    Alikilenga vizuri kile kivuli. Akafyatua !

    Risasi ile ilitua katikati ya shingo ya Dada mmoja aliyefatana na Meja Badi Bwino.

    Yule Dada alitoa mguno hafifu.

    Akaiaga dunia !



    Kule nje ilibaki taharuki. Meja Badi Bwino hakuelewa risasi ile ilitokea upande gani, shingo yote ya yule dada ilitapakaa damu !

    Meja Badi Bwino na yule Dada walirudi nyuma.

    Kusonga mbele, iliashiria kukisogelea kifo zaidi !



    Kule upande wa mashariki. Baada ya Meja Kurasa kuuwawa kwa risasi ya kichwa, Nduli na yule Dada, sasa walikuwa wanarudi usawa wa getini. Wao hawakuwa na uwezo kabisa wa kuupanda ule ukuta.

    Sasa walifika getini. Giza lilikuwa limetanda lakini halikuwazuia kujua kama lile geti lilikuwa wazi, si Nduli wala yule Dada aliweza kuiona maiti ya yule Dada pale chini.

    Wote mioyo yao iliingiwa na furaha. Kuona geti lilikuwa wazi. Sasa kwa mwendo wa kunyata Nduli na yule dada walikuwa wanaingia ndani, kupitia getini.



    Kule upande wa magharibi nako hali ilikuwa tete. Zwangendaba na yule dada mwengine walisubiri ishara yoyote wakiwa kule chini kwa nje toka kwa Meja Fuga Tindo ambaye alikuwa kauparamia ukuta ule. Hawakujua yaliyomkuta, na wangejua vipi ?

    Walisubiri bila mafanikio.

    Sasa wakahisi kutakuwa na hatari !

    Lakini waliendelea kusubiri palepale, wakijua muda wowote labda Meja Fuga Tindo angerejea....





    Kule getini yule dada alitangulia. Akimuacha Nduli hatua kama tatu nyuma yake. Dada alilisogelea geti kwa mwendo wa taratibu sana, akiwa kashika bastola kwa mkono wake wa kuume. Nyuma yake akifatwa kwa ukaribu na Nduli.

    Kule ndani Daniel Mwaseba kwa kutambaa akitumia tumbo alikuwa amesogea kidogo pale konani. Sasa alikuwa nyuma ya pipa la maji. Akiwa mtulivu kupita kiasi. Akisubiria kusikia mtikisiko wowote autungue!

    Akisubiri kitokee kivuli chochote akipoteze!

    Sasa alikiona kivuli kinaingia kupitia pale getini.

    Alikiona kwa hisia zaidi ya macho.

    Ukweli kutokana na giza ilikuwa ngumu sana kuona kivuli kwa uhakika. Ulikuwa mchezo wa hisia ambao Daniel Mwaseba alikuwa ndio mwalimu wake.

    Sasa Daniel Mwaseba alinyanyua mkono wake wa kuume wenye bastola, alikilenga kile kivuli alichokuwa anakiona kwa hisia .

    Alifyatua risasi iliyopenya kifuani kwa yule Dada.

    Yule dada alienda chini mzimamzima kama gunia la mchanga.

    Nduli alirudi nyuma kwa haraka. Nduli alikuwa anakimbia sasa, kurudi kule walikokuwa kina Meja Swalo Mbombwe.

    Aliona kwenda mbele ni kukifata kifo chake.

    Daniel Mwaseba sasa alitoka pale nyuma ya pipa. Alikuwa anatambaa kuelekea getini. Kwa tahadhari kubwa sana.

    Kule kwa kina Zwangendaba waliamini kuna jambo baya lililomkuta Meja Fuga.

    Maana walikaa muda mrefu sana bila taarifa yoyote.

    Nao waliamua kurudi nyuma. Kwenda kujipanga upya. Wakati kina Zwangendaba wakirudi, Daniel Mwaseba alikuwa anaenda, sasa aliamua kuwafata nje maadui zake.

    Kule ndani ya ghala kulikuwa kimya. Askari thelathini walikuwa kimya, kila mmoja akiomba dua yake. Akimuombea Daniel Mwaseba ashinde ili nao waokoke.

    Walikuwa askari imara, lakini waogopa kifo hodari !

    Kule nje , gizani kulikuwa na mtafutano.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Daniel Mwaseba akiwa na bastola moja kila mkono alikuwa anaambaa upande wa magharibi wa ghala.

    Alikuwa makini kwa kila hatua anayoipiga.

    Wakati Daniel anaenda upande ule wa magharibi ya ghala, Zwangendaba na yule Dada walikuwa wanakuja mashariki mwa ghala lile.

    Wote walikuwa wananyata!

    Wote walikuwa makini sana!

    Kule walikobaki wakina Meja Swalo Mbombwe, kulikuwa na mfadhaiko mkubwa sana.

    Meja Badi Bwino na yule Dada walirudi wakiwa wametaharuki, huku wakidai wamempoteza Dada mwengine.

    Na sasa Nduli alikuwa anarejea mbio huku akidai Meja Kurasa Allen na yule Dada mwengine wameuwawa!

    Taarifa zile ziliwaacha midomo wazi kina Salehe.

    Hawakuamini !

    Wala, hawakutegemea kinachotokea!

    Mpaka sasa hawakujua Meja Fuga Tindo na wakina Zwangendaba wako wapi ? Angamizo sasa lilielekea kuwaangamiza wenyewe !

    Sasa walipanga upya operesheni yao.

    Ikiongozwa na yuleyule, Meja Badi Bwino.

    "Sasa naona " Plan A" imefeli. Sasa lazima tutumie 'Plan B'. Sasa ni kwenda kwa pamoja. Kila mmoja akiwa mlinzi kwa mwenzake.

    Huyo Mdunguaji mwoga,

    Ama zake !

    Wote walisimama nusu duara 'Cow horn' Wakawa wanaenda kwa pamoja, kwa nguvu mpya sasa.

    Sasa walibaki sita, wanne walikuwa wameuwawa na bastola ya Daniel, na wawili walikuwa hawajarudi mpaka sasa, wakina Zwangendaba.

    Kule upande wa magharibi, Daniel na kina Zwangendaba walikaribiana sasa.

    Daniel aliwaona wakija, kama kawaida, hisia ndio alizozitumia, alijibanza nyuma ya mti. Zwangendaba na yule dada walikuwa bado hawajamwona Daniel.

    Zwangendaba na yule Dada walipita karibu kabisa na ule mti aliojificha Daniel. Daniel alitulia kimya kabisa.

    Kina Zwangendaba walipita mita chache sana karibu na ule mti aliojibanza Daniel. Sehemu ile ilikuwa kimya, kama hamna kiumbe hai chochote kile.

    Kulikuwa kimya !

    Ubaridi wa Iringa ulikuwa umeshamiri.

    Kina Zwangendaba walitembea bila kutoa ishara yoyote.

    Ilikuwa ni kimyakimya .

    Kwa mwendo wa kimyakimya kina Zwangendaba waliukaribia ule mti aliojificha Daniel. Sasa walikuwa kama hatua tatu kuufikia mti ule. Wakinyata taratibu, wakiangaza mbele kwa umakini mkubwa sana, wakaupita bila kujua kuwa adui yao alikuwa nyuma yao hatua chache sana.

    Taratibu Daniel alijigeuza pale kwenye mti, sasa akawa anaviona japo kwa shida vivuli vile kutokana na giza.

    Alinyanyua mikono yake yote miwili iliyoshika bastola. Akailenga kuelekea kwenye vile vivuli viwili.

    Daniel Mwaseba, alifyatua risasi mbili, kwa wakati mmoja, zilizoenda sambamba na kutua sehemu tofauti za mwili, kwa watu wale wawili.

    Wakati risasi moja ikitua na kukifumua vibaya kisogo cha Zwangendaba, risasi nyingine ilisafiri kwa kasi na kwenda kutua katika mgongo laini wa yule Dada. Nguvu ya risasi ile ilimsukuma yule dada na kumuangusha mbele kama hatua sita. Wakati mwili wa yule dada unadondoka chini, roho yake iliruka juu na kuelekea mbinguni!

    Daniel Mwaseba kwa mara nyingine tena alifanikiwa kuwaonesha wale maadui wabaya yeye ni nani katika dunia ya wababe !





    ******



    Lile kundi la watu sita, wenye hasira na kuamua kuungana pamoja, lilikuwa linakaribia getini. Sasa walikuwa makini, walijua kuingia kwa papara ni kukata tiketi ya kifo!

    Walilikaribia kabisa geti. Meja Badi Bwino alitoa wazo kwa sauti ndogo lakini iliyosikika vyema kwa kila mmoja.

    "Geti lile limefunguliwa kama mtego, tusipite pale. Tutafute njia nyingine, kupita getini ni kukikimbilia kifo"

    "Sasa tutapita wapi Meja?" Salehe aliuliza kwa sauti ndogo pia.

    "Hapa inabidi tujigawe, watatu waende Magharibi ya ghala, na watatu waende upande wa mashariki ya ghala. Kila kundi litafute pa kupita huko" Meja Badi Bwino alieleza.

    "Sawa" waliitikia wote.

    Sasa walijigawa tena, Meja Badi Bwino, Salehe na dada mmoja walienda mashariki wa ghala. Meja Swalo Mbombwe, Nduli na Dada mmoja walielekea upande wa maghari wa ghala.

    Wote walitawanyika !

    Wale waliokuwa wameelekea upande wa magharibi ndio walikuwa wanaenda kukutana na balaa, Daniel Mwaseba alikuwa upande huo.

    Meja Mbombwe, Nduli na Dada mmoja ndio walikuwa wanaelekea upande huo.

    Baada ya kuwauwa wakina Zwangendaba, Daniel alipanda juu ya ule mti, sasa aliweza kuoona hadi ndani ya ghala. Alitulia kimya, akisubiri waje, awaue !

    Kina Meja Mbombwe walifika usawa uleule wenye mti alioupanda Daniel Mwaseba.

    "Sasa tunafanyaje hapa?" Meja Mbombwe aliuliza.

    "Inabidi tupande ukuta" Nduli alijibu.

    "Kupanda hapo juu ni kujianika kwa walinzi" Meja Mbombwe alijibu.

    " Sasa tunafanyaje?" Yule dada aliuliza.

    "Nduli hebu panda juu ya huu mti uangalie hali ilivyo humo ndani"

    "Sawa"

    Nduli alipanda katika mti, ili kuangalia ndani. Mti uleule aliopanda Daniel Mwaseba!

    Bila kufikiria Nduli alianza kuupanda ule mti.

    Akiwa kule juu ya mti, Daniel aliviona vivuli vitatu pale chini.

    Aliviona vikijadiriana, lakini hakusikia wanajadiliana nini. Alikuwa katulia tuli kule juu. Kashika bastola yake mkononi. Na ile bastola nyingine kaiweka kiunoni.

    Mara alikiona kivuli kimoja kikipanda juu.

    Daniel alitabasamu !

    Aliona kama kile kivuli kilikuwa kinafata kifo chake !

    Kile kivuli kiliendelea kupanda.

    Sasa kilifika katikati ya ule mti.

    Kule juu, Daniel aliishika imara bastola yake mkononi.

    Alilenga katika utosi wa kile Kivuli. Alivuta pumzi kwa ndani. Alifyatua ile bastola. Risasi ilimpata Nduli katika utosi wake ! Alianguka chini mithili ya embe bivu. Meja Mbombwe na yule dada walienda pale alipoanguka Nduli. Akatoa tochi ndogo na kummulika, walishuhudia picha mbaya sana!

    Ubongo wa Nduli ulitapakaa pale chini. Ilikuwa ni kichefuchefu kuangalia ubongo ule mbichi wa ukiwa umetapakaa pale chini !

    Meja Mbombwe nae alifanya kosa. Kuwasha tochi mahali pale lilikuwa kosa kubwa sana. Yeye alidhani Nduli ameanguka tu kule juu ya mti. Hakuhisi kama atakuwa kapigwa risasi.

    Alizima tochi yake haraka!

    Lakini Kuwasha tochi ni kosa kubwa sana alilolifanya Meja Mbomwe, na Daniel alilitumia vizuri sana kosa lile. Sasa Daniel Mwaseba hakutumia hisia, alishawaona kabisa maadui zake.

    Bastola yake ilikohoa harakaharaka mara mbili. Kikohozi kilichomsafirisha izrael toka alipokuwa mpaka Makete. Kuja kuwatoa roho watu wawili kwa mpigo. Meja Swalo Mbombwe na yule Dada. Walikufa wakiwa wanashangaa, wakiushangaa ubongo mbichi ulioambatana na damu wa Nduli.

    Kule upande wa mashariki, Meja Badi Bwino, Salehe na yule Dada, walikuwa wanahangaika kupanda ukuta.

    Baada ya robo saa walifanikiwa, ingawa kwa shida sana.

    Sasa walikuwa ndani ya uwanja mpana wakielekea kwenye ghala.

    Walinyata taratibu, sasa walifika mlangoni, kwenye mlango wa ghala la silaha. Salehe alikuwa anahangaika kufungua mlango, kwa kutumia funguo waliyokuja nayo. Mlango ulikuwa unaelekea kufunguka.....

    Daniel Mwaseba alirudi ndani kwa mwendo uleule wa kunyata. Alienda moja kwa moja katika chumba kikichohusika na kuzalisha umeme. Alimkuta askari akiongea na simu.

    Alimsogelea taratibu bila kutoa sauti yoyote, alimpiga karate moja ya nguvu ya shingo askari yule, karate iliyompeleka askari yule chini. Askari yule hakuweza kabisa kuistahamili karate ya Daniel Mwaseba.

    Askari alizimia !

    Kule kwa kina Salehe.

    Ghafla, umeme uliwaka!

    Meja Badi Bwino, Salehe na yule Dada walipigwa na butwaa, waliishiwa nguvu kabisa.

    Walikuwa wanatetemeka!

    Hawakuelewa kitu gani kimetokea. Sasa walikuwa wapo kwenye mwanga mkali huku wakiwa hawajui adui yupo wapi?

    Bastola zao sasa zilikuwa kama midoli tu mkononi.

    Hazikuwa na kazi.

    Ghafla! Umeme ulizimika tena!

    Wote watatu walipumua kwa nguvu.

    Ilikuwa kama miujiza !

    Ilikuwa kama ndoto !

    Ilikuwa giza!

    Ikaja nuru!

    Limerudi giza!

    Kurejea kwa giza ilikuwa kama ruhusa kwa Salehe aendelee kufungua tena ule mlango. Alifungua huku akitetemeka vibaya sana!

    Geti lilifunguka!http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ndani kulikuwa na giza totoro!

    Ghafla nuru ilirejea tena!

    Daniel Mwaseba alikuwa anawachezea mchezo watu wale.

    Mara ya pili ulivyowaka ilikuwa picha mbaya sana kwa Salehe, Meja Swalo Mbombwe na yule Dada.

    Walikuwa mbele ya askari thelathini walioshika bunduki imara mikononi mwao.

    Bunduki thelathini ziliwaelekea Meja Badi Bwino, Salehe na yule Dada vifuani kwao.

    Kina Salehe walikamatwa kirahisi sana !

    Daniel alikuja kwa nyuma yao. Kina Salehe hawakuamini macho yao kumuona Daniel Mwaseba pale.

    Sasa walijua, aliyekuwa anawadungua mmoja baada ya mwengine alikuwa Daniel Mwaseba.

    Wote Walikiri,

    Daniel Mwaseba alikuwa mtu hatari sana!

    Kwa mara nyingine tena, Daniel alifanikiwa kuliokoa Taifa la Tanzania kwenye hila mbaya za watu wabaya sana!

    Salehe na kundi lake walikamatwa, walisafirishwa kwa helkopta kuelekea Dar es salaam usiku uleule.

    Huko Dar es salaam, Ispekta Jenerali wa Polisi, IJP John Rondo alikuwa kalala fofofo. Baada ya kupigiwa simu za makamanda wa mikoa ya Mara, Kigoma na Mbeya, na kupewa taarifa mbaya za mauaji ya raia wema, alichanganyikiwa sana.

    Hakuamua kuzima simu tu, alitoa kabisa na betri yenyewe toka katika simu yake.

    IJP Rondo aliamua kwenda Baa kunywa bia ili kupunguza mawazo.

    Hakunywa bia chache.

    Alimimina kwa pupa kwenye tumbo lake pana bia ishirini na mbili.

    Alilewa sana!

    Alijikongoja hadi nyumbani kwake na kukaa sofani. Aliwasha televisheni, hakuwahi kuangalia chochote, alipitiwa na usingizi palepale sebuleni, huku televisheni ikiongea kwa sauti kubwa. Lakini yeye hakuisikia.

    Wakati Daniel Mwaseba akipambana na wauaji kule msituni, IJP Rondo alikuwa kalala usingizi mzito sana nyumbani kwake !

    Simu iliyopigwa asubuhi ndiyo iliyomuamsha IJP Rondo.

    "Halloo mkuu"

    "Hallo inspekta"

    "Njoo kituo cha Polisi cha kati afande kuna habari kubwa" IJP alipata mstuko mkubwa sana, akihisi wale wauaji wamefanya tukio kubwa lengine.

    "Kuna nini Inspekta?"

    "Daniel Mwaseb.." Inspekta hakumalizia kusema.

    "Amekufaaa ?"

    "Hajafa afande, Daniel Mwaseba amefanikiwa kuwakamata wahalifu"

    "Wahalifu gani hao?"

    "Wale wakiotumia sumu ya Proxine kuuwa !"

    "Whaaaaaaaaat?, nakuja sahivi."

    Pombe zilimtoka IJP John Rondo.

    Alienda kituoni.



    ***************

    Wakati IJP Rondo akiwa kituo cha Polisi cha kati kuwahoji wauaji wale. Daniel Mwaseba alikuwa angani kuelekea jijini Arusha, kwa Abdul.

    Daniel alikuwa na furaha sana kumuokoa kijana yule dhaifu kwenye mdomo wa kifo cha watu hatari.

    Alimkuta Abdul, na Abdul alimshukuru sana Daniel.

    "Pongezi hizi zinakuhusu pia Abdul, wewe, Mayasa na Raiya mnastahili pongezi hizi. Mmefanikisha kugundulika kwa njama hatari sana. Angamizo lingetuangamiza kweli! Fikiria nchi ingejilindaje toka kwa maadui zake bila silaha. Tungekuwa watumwa, tungepata hasara kubwa sana. Abdul, wewe ni shujaa !

    Mayasa, na Raiya ni mashujaa. Mungu awalaze mahali pema mashujaa wale wa kike!"

    *************

    Abdul aliamua kuahirisha mwaka wa masomo pale chuoni, na kuamua kurudi nyumbani Bagamoyo, kupumzika kwa wazazi wake.

    Aliongozana na Daniel kuelekea Bagamoyo.

    Njiani Daniel alikumbuka kuwa alikuwa na deni Bagamoyo. Deni la kumlipa Mzee Washiro na mkewe kwa wema waliomfanyia. Alipanga baada ya kumpeleka Daniel nyumbani kwao, lazima aende kwa Mzee Washiro kutimiza ahadi yake. Ingawa hakujua atampa zawadi gani Mzee Washiro na mkewe. Lakini aliamua kwenda.

    Waliwasiri Bagamoyo jioni. Daniel na Abdul walichukua teksi kuelekea nyumbani kwa Abdul. Njiani Daniel hakuwa na wasiwasi wowote na uelekeo wakioufuata.

    Hakuwa anaijua njia ya kuelekea kwa Mzee Washiro. Aliletwa akiwa mfu, na alirudi kwa ndege ya jeshi.

    Walipoikaribia ile nyumba Daniel alipakumbuka.

    "Hivi unaitwa Abdul nani?"

    "Naitwa Abdul Washiro"

    Daniel alipigwa na butwaa.

    "Vipi kaka Daniel?"

    "Wazazi wako ni watu wema sana, na wana mchango mkubwa katika kufanikisha operesheni hii"

    "Wamefanyaje kwani?"

    "Utajua tukifika"

    Baada ya kufika nyumbani kwa Washiro pande zote mbili zilikuwa na furaha sana.

    Hawakutegemea kabisa.

    Daniel alimsaidia Abdul bila kumjua, na

    Mzee Washiro alimsaidia Daniel bila kujua.

    Mzee Washiro alimsimulia Daniel juu ya dhiki iliyoota mizizi katika familia yake.

    Daniel aliahidi kuwasaidia.

    Baada ya mwezi mmoja kulikuwa na tafrija ndogo Bagamoyo, Daniel alikuwa anamkabidhi mzee Washiro nyumba bora ya kisasa. Aliyoinunua kama kulipa fadhila kwa wema waliomfanyia familia ile.

    Mbele ya nyumba ile kulikuwa na fremu kubwa ambayo Daniel alipanga kuwafungulia duka kubwa la vifaa vya magari.

    Tafrija ilifana sana pale sebule kwenye sebule ya kisasa. Mzee Washiro na familia yote kwa ujumla walimshukuru sana Daniel.

    Saa mbili kasoro. Daniel alipigiwa simu. Simu ilitoka kwa IJP Rondo ikimsisitiza asikose kuangalia taarifa ya habari.

    Saa mbili kamili, Ilipoanza taarifa ya habari iliwanyamazisha watu wote pale sebuleni.

    "....mawaziri watatu, na watu wengine watano wamehukumiwa hukumu ya kunyongwa hadi kufa !. Mawaziri hao wakishirikiana na watu wengine watano...."http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hawakusubiri taarifa ile iishe. Watu wote waliripuka kwa shangwe na kumkumbatia Daniel Mwaseba !

    "Wewe ni shujaa pia Daniel!" Abdul Washiro alisema huku chozi zito likimdondoka.

    Mawaziri watatu, Salehe, Meja Badi Bwino, Kerspersky, yule Dada, na askari mzima umeme ghalani, walihukumiwa kunyongwa hadi kufa!

    MWISHO


0 comments:

Post a Comment

Blog