Simulizi : Penzi Ama Kaburi
Sehemu Ya Tatu (3)
Shadya alitakiwa kupambana kwa ajili ya kaka yake, hakuwa tayari kuona akihadhirika na wakati alikuwa na uwezo wa kumsaidia. Ilikuwa ni lazima azungumze na Gibson na kumwambia alikuwa akihitaji dawa hizo za kuongeza nguvu za kiume, iwe isiwe ilikuwa ni lazima amsaidie kwa kuwa aliamini alimpenda.
Akachukua bodaboda na kuelekea Sinza alipokuwa akiishi, alipofika huko, akakaribishwa na kuelekea ndani. Alijisikia aibu sana kumwambia kuhusu jambo hilo lakini hakuwa na jinsi, ilikuwa ni lazima amwambie kwa kuwa bila kufanya hivyo ingeonekana kuwa hatari kwa maisha ya kaka yake chuoni.
Wakaelekea ndani, kwa jinsi Shadya alivyoonekana, hakuonekana kuwa sawa kabisa, alikuwa na mawazo mengi, kaka yake alimpa tabu na katika kipindi kama hicho ilikuwa ni lazima ampambanie mpaka ahakikishe anafanikiwa.
“Unaonekana kuwa na mambo mengi sana,” alisema Gibson, kwa kawaida kila alipokuwa na msichana huyo ilikuwa ni lazima awe na sura iliyokuwa na tabasamu pana.
“Yeah! Naomba nipumzike kwanza!”
“Chumbani ama sebuleni?”
“Sebuleni!” alisema na kutulia kwenye kochi.
Alimwangalia Gibson, kwa jinsi alivyoonekana, aliona kabisa kufanikiwa kwa kile alichokuwa amejiandaa kumwambia. Alipumzika kwa dakika chache ndipo akaamua kuingizia suala hilo.
“Kuna kitu nahitaji unisaidie,” alisema baada ya mazungumzo machache ya kujuliana hali.
“Kitu gani?” aliuliza Gibson.
“Daah!” alisema Shadya.
Hakutaka kumwambia moja kwa moja, kichwa chake kilitafuta lafudhi nzuri ya kulifikisha suala hilo, yaani atumie rejesta ambayo ingemfanya mwanaume huyo kuelewa kila kitu.
“Shadya!” aliita Gibson baada ya kuona ukimya wa sekunde zaidi ya ishirini.
“Abee!”
“Unahitaji nikusaidie nini?” aliuliza.
“Nina tatizo!”
“Lipi?”
Akakaa kimya tena.
Gibson alimshangaa, hakuelewa zaidi alichokuwa akikihitaji msichana huyo, alikuwa na maswali mengi lakini hakupata majibu ya maswali hayo yote.
Msichana huyo alimpigia simu na kumwambia alihitaji kumuona kwa sababu kulikuwa na jambo alilotaka kuzungumza naye, alimuita, alifika lakini hakuwa akizungumza kitu chochote kile.
Kwa sababu alikuwa mwanaume wa Dar, akajiongeza. Kuna mambo ambayo msichana alipokuwa akiyahitaji, hakuwa na uwezo wa kuyawakilisha kwa maneno bali alitakiwa kubustiwa ili kidogo apate urahisi wa kuufikisha ujumbe wa kile alichokuwa akihitaji.
“Au anahitaji mambo yetu?” alijiuliza.
“Ngoja nimtesti!” alijisemea.
Hakutaka kulaza damu, aliamini alichokuwa akikihitaji msichana huyo ni kufanya mapenzi tu, ndivyo akili yake ilivyomtuma na kwa sababu alihitaji kumsaidia Shadya, akaamua kumuanza yeye.
Akamsogelea na kumwangalia usoni, Shadya ni kama alishtuka kwani huyu Gibson aliyeonekana muda huo alikuwa tofauti na yule ambaye alimkaribisha dakika chache zilizopita, huyu wa sasa alikuwa na mabadiliko mengi usoni mwake.
Akaupeleka mkono pajani mwake na kuanza kumsoma kama aliridhia ama angeleta purukushani.
“Gibson!” aliita kwa sauti nyororo, naye akaamini ili asaidiwe, ilikuwa ni lazima aanze kujilegeza kwa mwanaume huyo.
“Nakusikia!”
“Ninahitaji dawa!” alisema.
“Unaumwa?” aliuliza.
“Hapana!”
“Sasa unataka dawa ya nini?”
“Yaani nashindwa kulielezea hili!”
“Jitahidi tu! Huzioni siku zako?”
“Bora ingekuwa hivyo!”
“Kumbe kuna nini?”
“Unajua zile dawa zinazomfanya mwanaume anakuwa na nguvu?” aliuliza Shadya.
“Zipi? Energy ama?”
“Hapana! Si kinywaji!”
“Kumbe zipi?”
“Zile za kutoka Congo!”
Gibson alipoambiwa hivyo akashtuka, hakuamini alichokisikia, alimwangalia Shadya, alishangaa, kwa msichana kama huyo, mstaarabu asingekuwa na uwezo wa kumwambia maneno kama hayo.
Naye Shadya aliuona mshtuko huo, alichokifanya ni kuupeleka mkono wake kwa Gibson na kumwangalia machoni.
“Naomba unisaidie Gibson!” alisema Shadya.
“Nikusaidie dawa hizo?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ndiyo!”
“Za nini?”
“Nina shida nazo!”
“Shida gani?”
“Naomba unisaidie!”
“Shadya! Siwezi! Kukupa dawa hizo ni jambo lisilowezekana! Yaani nikupe ukafanye mapenzi na mwanaume mwingine?” aliuliza.
“Gibson.....”
“Halafu mimi niwe kama mshika pembe, maziwa wakamue wengine!” alisema kwa unyonge.
“Si kama unavyofikiria!”
“Unataka nifikirie nini? Kwamba zinakwenda kutupwa?”
“Hapana!”
“Kumbe!”
“Kuna mtu nakwenda kumpa, azitumie!”
“Kwako wewe? Jamaa hapandi mlima ama?”
“Si kwangu!”
“Kumbe kwa nani?”
“Mbona maswali mengi Gibson! Love...naomba unisaidie! Nakuomba sana mpenzi,” alisema Shadya.
Alishindwa kuvumilia. Huyu Gibson tayari alionekana kuwa na shaka naye hivyo alichokifanya ni kujiebisha na kuanza kubadilishana mate.
Aliamini kwa kufanya hivyo angeweza kumshawishi. Gibson hakutaka kumuacha, alikuwa na hamu na msichana huyo, haikuishia hapo, ni kama dakika mbili hivi, hakujua ni kitu gani kilitokea, walijikuta wakiwa chumbani wakiwa watupu, yaani ni kama walipotea sebuleni kichawi na kutokea humo.
Kilichofuata ni sauti za mahaba ambazo zilichukua dakika arobaini na tano wakaanza kuangaliana. Shadya aliumia moyoni, alifanya mapenzi bila kutarajia kwa sababu ya kumsaidia kaka yake.
Alikuwa kwenye tatizo na ilikuwa ni lazima aonyeshe kwamba alikuwa naye bega kwa bega. Wakaanza kuangaliana.
“Kwa hiyo?” aliuliza Shadya huku akijiweka vizuri kitandani.
Gibson akachukua simu yake na kupiga mahali. Akaanza kuzungumza na mtu aliyejulikana kwa jina la Kaimu na kumwambia kuhusu hizo dawa ambazo kwa lugha ya mitaani ilijulikana kama Vumbi la Congo. Ndani ya dakika ishirini, pikipiki ikafika mahali hapo, jamaa akateremka na kumpa Gibson dawa hiyo iliyofungwa kwenye kikaratasi.
“Mzee baba una shoo ya kibabe nini?” aliuliza Kaimu.
“Hapana!”
“Au kuna mtoto wa kishua amekuja unataka kumdatisha umle mapene yake?” aliuliza.
“Hapana! Nitakushtua baadaye!” alisema Gibson, jamaa akarudi kwenye pikipiki na kuondoka zake.
Gibson akaingia ndani na kumwambia Shadya kwamba mzigo alikuwanao mkononi mwake.
“Ila nikigundua umekwenda kuutumia wewe!” alisema Gibson.
“Utafanyaje?”
“Nitakuchukia!”
“Siwezi kufanya hivyo! Yaani inamaanisha kwako sijaridhika?”
“Sawa! Nenda!”
“Ila Gibson....”
“Niambie!”
“Naomba iwe siri!”
“Haina shida! Ila si mechi itarudiwa?”
“Ili utumie hii kitu?”
“Hapana! Hivihivi kama leo!”
“Tutaongea kwenye simu. Nakushukuru sana, hujui ni kwa jinsi gani umeokoa maisha ya mwingine. Nashukuru sana,” alisema Shadya, akasindikizwa mpaka nje, akaita bodaboda, akapanda na kuondoka mahali hapo.
Akawa amemsaliti Ngwali kwa ajili ya kaka yake, ila huo ulionekana kuwa si mwisho, alimuahidi asingeingilika na wanaume wa Dar, mtu wa kwanza akawa amefanikiwa kumvua, hakujua kama kulikuwa na wengine wangefuata baada ya huyo.
***http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Shadya alipofika chuoni, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kumtafuta kaka yake kwa lengo la kumpa dawa ile aliyotoka kuichukua kwa Gibson, akampigia simu na kuonana katika ukumbi wa Nkurumah.
Rahim hakuamini kama dada yake alifanikiwa kuipata dawa hiyo kwani alikuwa akienda kudhalilika kama tu asingekuwa nayo. Akaichukua, akashukuru na kuondoka zake.
Alipofika bwenini, kitu cha kwanza kilikuwa ni kumpigia simu Hawa na kuanza kuzungumza naye. Akamwambia alikuwa tayari kwa kila kitu, alijipanga na hivyo alihitaji kuonana naye haraka iwezekanavyo.
“Haina shida!” alisema msichana huyo.
Kweli wakaonana katika nyumba ya wageni iliyokuwa Sinza Kumekucha na kabla ya mambo yote, Rahim akaenda mariwato na kufanya kile alichoambiwa alitakiwa kufanya na kurudi chumbani.
Alimwangalia Hawa pale kitandani alipokuwa, hakusisimka hata kidogo, hakuvutiwa hata mara moja lakini kwa sababu dawa aliyoipaka ilikuwa na nguvu, akashangaa kiungo chake kikianza kukakamaa.
Alishtuka, kwa mara ya kwanza ndani ya miaka minne alikutana na hali hiyo, alimshukuru dada yake kwani kitendo cha kuingiliwa na wanaume wenzake kilimuharibu kabisa na kukosa hisia kwa wanawake kama wanaume wengine.
Akamsogelea msichana yule kitandani, akamshika na kuanza kumbusu kila kona mwilini mwake. Kwa mara ya kwanza Rahim alifanikiwa kufanya mapenzi na Hawa, hakujisikia kama wanaume wengine, kwake ilionekana kuwa kawaida na wakati mwingine alijiuliza ni kwa sababu gani wanaume walipenda sana ngono.
Walitumia dakika arobaini na walipomaliza, wakaondoka. Kitu cha kwanza kabisa kwa Hawa kilikuwa ni kumwambia Hamisi kwamba alifanikiwa kufanya mapenzi na Rahim.
“Unasema kweli?” aliuliza Hamisi, hakuamini alichokisikia.
“Ndiyo! Tena ana nguvu ile kinoma, utafikiri alikuwa na ukame wa miaka ishirini,” alijibu Hawa huku akionekana kutabasamu.
“Hebu niambie ilikuwaje!” alisema Hamisi na Hawa kuanza kumwambia kila kitu.
Alipomaliza, Hamisi akamlipa pesa aliyomuahidi na kumfuata rafiki yake, kwanza alipomuona tu, uso wake ulikuwa na tabasamu ambalo lilimfanya Rahim kushangaa, akahisi kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea hivyo alihitaji kufahamu.
“Kidume!” alisema Hamisi huku akimwangalia Rahim.
“Unamaanisha nini?” aliuliza Rahim huku akionekana kushangaa.
Hakufikiria kuhusu Hawa, alichokijua walikifanya kitendo hicho kwa siri kubwa na hapakuwa na yeyote ambaye alifahamu lolote lile, kitendo cha kuitwa kidume na Hamisi kilimshangaza kidogo hivyo kuhitaji kufahamu kulikuwa na kitu gani.
Hamisi akaanza kumwambia kuhusu Hawa, jinsi walivyoondoka na kuelekea Sinza, alichomwambia ni kwamba kulikuwa na watu waliowaona mpaka wakiingia kwenye nyumba ya wageni.
Rahim akanyamaza kwa dakika kadhaa, moyo wake ulikuwa na furaha mno kwani kama kweli kulikuwa na watu waliomuona ilimaanisha sasa wasingejua kama alikuwa mshiriki mzuri wa mapenzi ya jinsia moja.
“Kwa maana hiyo watu waliniona?” aliuliza Rahim huku akionekana kutabasamu.
“Ndiyo! Dunia haina siri hata kidogo! Kamera zetu ndogo zilikuona,” alisema Hamisi huku akichia tabasamu pana, alimpongeza rafiki yake huyo, yaani ule ustaadhi wake usingekuwepo tena.
Mapenzi yalianza kimchezomchezo sana, Shadya taratibu akaanza kuwa bize na Gibson na kusahamu kama kulikuwa na mwanaume mwingine aliyeitwa kwa jina la Ngwali.
Alitokea kumpenda kijana huyo, kwa jinsi alivyofanya naye mapenzi chumbani ilimshangaza mno na kujiuliza kama kweli kulikuwa na mwanaume wa Dar aliyekuwa na nguvu kama alizokuwanazo mtu huyo.
Walikuwa wakichati, moyo wake ulibadilika kabisa, kama ambavyo alikuwa akijisikia raha alipokuwa akichati na Ngwali, sasa ile raha ikahamia kwa Gibson.
Mwanaume huyo alijua kuchati naye, kumfurahisha na kumfanya kujisikia kama malkia fulani kwenye ulimwengu wa peke yake. Walizungumza mambo mengi na kuandikiana meseji zilizomchanganya zaidi Shadya.
“Nakupenda sana,” aliandika msichana huyo.
“Nakupenda pia! Wewe ni msichana wa tofauti sana kwenye maisha yangu. Unajua kupenda, unanukia vizuri, unapendeza mno, ni msichana ambaye kama kuna siku nitampoteza, nina uhakika nitalia maisha yangu yote,” aliandika Gibson, Shadya alipousoma ujumbe huo, tabasamu pana likachukua nafasi yake.
“Kweli?”
“Niamini mpenzi! Kwa kipindi kirefu sana nilitamani kumpata msichana kama wewe, mwisho wa siku umetokea katika maisha yangu, kipindi ambacho nilionekana kukata tamaa,” aliandika Gibson.
“Nashukuru kwa kunipenda!”
“Na wewe nakushukuru kwa kukubali kuwa mpenzi wangu! Utapenda nikupeleke wapi ukale leo?” aliuliza Gibson.
“Popote upendapo!”
“Basi nakuja kukuchukua! Jiandae, vaa ile nguo nzuri ya sikukuu kipenzi!” aliandika kwa utani.
“Hahaha! Sawa!”
Shadya akasimama kutoka kitandani, moyo wake ulibadilika na kuwa mtu mwenye furaha kubwa, akaelekea bafuni, akaoga na alipomaliza akarudi na kuanza kuvaa nguo zake huku tayari ikiwa ni saa saba mchana.
Akaichukua simu yake na kuangalia, kulikuwa na missed calls tatu kutoka kwa Ngwali, alimtafuta alipokuwa akioga. Kwa mara ya kwanza akahisi kumdharau mwanaume huyo, hakuwa na hamu ya kumpigia kwa sababu tayari moyo wake ulianza kuchukuliwa na mwanaume mwingine.
“Missed calls tatu utadhani ananidai figo yake...mxiiiiuuuuu...” alisema msichana huyo na kusonya, huo msonyo wake si wa nchi hii, halafu akaifunika simu.
Penzi jipya liliuchanganya moyo wake na hakutaka kusikia la yeyote yule. Alipomaliza kujiandaa, akampigia simu Gibson ambaye alimfuata na gari chuo na kumchukua kuondoka naye kuelekea katika Mgahawa wa Samaki Samaki kwa ajili ya kula.
Muda wote Shadya alionekana kuwa na furaha tele, alitokea kumpenda Gibson na kuhisi angekuwa naye muda wote katika maisha yake.
Walikula na kunywa na walipomaliza, wakachukuana na kuelekea nyumbani kwa kijana huyo. Hapakuwa na ugumu wowote ule, alivuliwa nguo, akaanza kuguswa hapa na pale na mwisho wa siku kuanza kufanya mapenzi kama ilivyokuwa siku iliyopita.
Penzi la Shadya kwa Gibson likazidi kushamiri moyoni mwa msichana huyo, akachanganyikiwa kupita kawaida, alihisi kama katika dunia hii alikuwa akipendwa peke yake na hapakuwa na mtu yeyote yule aliyekuwa akipendwa kama alivyopendwa.
“Nitakupenda maisha yangu yote,” alisema Shadya kwa sauti nyororo, maneno yaliyoonyesha ni kwa jinsi gani alichanganyikiwa.
“Nitakupenda pia!” alisema Gibson na kumbusu msichana huyo mdomoni.
***
Ngwali alichanganyikiwa, moyo wake uliuma kupita kawaida, hakujua ni kitu gani hasa kilikuwa kikiendelea. Alijaribu kumpigia simu mpenzi wake, Shadya lakini haikuwa ikipokelewa.
Hakuwa na raha, moyo wake ulichoma na wakati mwingine alianza kuhisi kama kulikuwa na tatizo kubwa mno alilokuwa akilipitia mpenzi wake huyo.
Akampigia simu Rahim na kuanza kuzungumza naye. Kitu cha kwanza alihitaji kujua kuhusu Shadya kama alikuwa sawa ama kulikuwa na kitu.
Alichomwambia Rahim ni kwamba hapakuwa na tatizo lolote lile kwani siku iliyopita alizungumza naye na alionekana kuwa kawaida kama siku nyingine.
“Sasa kwa nini simu zangu hapokei?” aliuliza.
“Sijajua! Labda yupo mbali na simu!” alitetea Rahim.
“Yaani tangu jana! Ama anaumwa?”
“Sijui! Nadhani yupo mbali na simu! Endelea kumtafuta shemeji!” alisema Rahim.
“Au amepata mtu mwingine?”
“Mtu mwingine? Zaidi yako? Shadya hana hata rafiki wa kiume, achana na mpenzi tu,” alisema Rahim.
“Kweli?”
“Niamini! Mimi ndiye mlinzi wake!” alisema Rahim.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kidogo maneno ya Rahim yakamfanya kuwa na amani ndani yake. Akamwamini inawezekana kabisa msichana huyo hakuwa karibu na simu, ama aliiacha chumbani na yeye kwenda sehemu fulani.
Hakukoma, hakuacha kupiga simu na majibu yaliendelea kuwa yaleyale, simu haikupokelewa kabisa. Siku hiyo hakuwa na furaha hata kidogo, hata madrasa hakwenda, alijiona kama mtu aliyekuwa akiumwa hivi.
Ilipofika majira ya saa mbili usiku ndipo akajaribu tena, muda huu ikaonekana kuwa kama bahati kwake, simu ikapokelewa na sauti ya msichana huyo kuanza kusikika.
“Halo!” iliita.
“Halo mpenzi! Nimekumisi sana,” alisema Ngwali, ni kweli alimmisi mpenzi wake, huo ndiyo ulikuwa ukweli ambao haukujificha kabisa.
“Nimekumisi pia mpenzi!” alisema Shadya.
“Mbona haukuwa ukipokea simu zangu?”
“Simu niliisahau bwenini! Nimeona missed calls zako na meseji, nisamehe mpenzi!” alisema msichana huyo kwa unyenyekevu.
“Usijali mpenzi!”
Wakati huo upande wa pili Shadya alikuwa akijitahidi kuulazimisha moyo wake kumpenda Ngwali kama ulivyokuwa lakini alishindwa ni kwa namna gani angeweza kufanikisha hilo.
Ni kwa kipindi kifupi tu mwanaume huyo aliondoka moyoni mwake, hakumpenda tena, alimuona mtu wa kawaida na mapenzi yalikufa, yakazikwa na kuoza kabisa.
Walizungumza kwa dakika kadhaa na kukata simu, Shadya akakunja sura yake, katika vitu ambavyo hakuvipenda kabisa, cha kwanza kupokea simu ya mwanaume huyo, yaani alichukia kupita kawaida.
“Nitabadilisha namba! Yaani sitaki hata kuona simu zake zikiingia,” alisema msichana huyo, kile alichokisema alikimaanisha, hakupenda kweli kuona simu yak ikiita kutoka kwa mpenzi wake huyo, alichukia kupita kawaida.
***
“Imekuwaje huko?”
“Nimefanikiwa kupata uhamisho!”
“Acha masihara?”
“Ndiyo! Japokuwa ilikuwa vigumu lakini mwisho wa siku wamekubali kunihamisha, sasa nitakuja kuishi huko mpenzi!”
“Bora uje, nakukumbuka sana mpenzi!”
Hayo yalikuwa ni mazungumzo baina ya Gibson na msichana aliyeitwa kwa jina la Paula. Wawili hawa walikuwa wapenzi wa muda mrefu ambao sasa walikuwa tayari kufunga ndoa.
Walipanga hilo lifanyike baada ya kufanikisha uhamisho wake kikazi kutoka jijini Arusha na kuelekea Dar es Salaam. Katika kipindi chote hicho Paula alikuwa akipambana na mwisho wa siku akafanikiwa kupata uhamisho huo na hivyo kumwambia mpenzi wake.
Ilikuwa ni furaha zaidi kwao, kila mmoja alitamani kumuona mwenzake kwa mara nyingine. Gibson hakumfikiria Shadya kwa sababu kwake alikuwa msichana wa kawaida, wa ku-hit and run.
Maandalizi ya kumpokea mpenzi wake yakaanza kufanyika, wakati hayo yote yakiendelea ndipo akakumbuka kulikuwa na msichana aliyeitwa kwa jina la Shadya.
Huyu alikuwa Mpemba, mzuri wa sura lakini hakutaka kabisa kuona akimsababishia kutengana na mwanamke wa ndoto yake, aliyetaka kutengeneza naye maisha.
“Wanawake wa chuo huwa ni wa kupiga na kuacha, tunaishi hivyo kama wanachuo, kwani naye anataka mimi kuwa wake maishani ama?” alijiuliza.
“Na kama aking’ang’ania, kweli nitaamini hawa wasichana wa mwaka wa kwanza magumashi,” alijisemea na kuachia tabasamu pana.
Alikuwa tayari kugombana na msichana yeyote katika dunia hii lakini si Paula, huyo alikuwa kila kitu kwake hivyo kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kulazimisha kupunguza ukaribu baina yake na Shadya.
Hiyo ndiyo ilikuwa hatua ya kwanza ya kumuacha msichana ambaye hukuwa na malengo naye. Kama kwa siku ilikuwa ni lazima mpigiane simu mara tano basi ilikuwa ni lazima ipunguzwe na kufika mpaka mara mbili, kama ulikuwa na haraka mno ya kujibu meseji yake kila inapotumwa, ilikuwa ni lazima upunguze uharaka, meseji moja ichukue hata dakika ishirini kujibiwa.
“Nitaanza na haya mambo mawili kwanza. Nikijidai nipo beneti naye huyu malaya anaweza kuniharibia,” alijisemea, alianza kumuita Shadya malaya kwa sababu tu alimkubalia kumvua nguo na kufanya naye mapenzi, mara mbili, ila kwenye hayo yote, hakuwa msichana wa kumuacha moja kwa moja, yaani pale ambapo angemtaka, angekuwa akimtafuta huku akimuomba msamaha.
Shadya alikuwa na matumaini kwa Gibson kwamba kuna siku angeishi na yeye mpaka pale ambapo kifo kingewatenganisha. Hakujua zaidi kama mwanaume huyo alikuwa na mpenzi wake aliyekuwa akimpenda kwa mapenzi ya dhati.
Alijitahidi mno kumuonyesha mapenzi ya dhati ili tu naye ampende kama alivyofanya lakini haikuwa hivyo. Alijitahidi kumpigia simu na kuzungumza naye.
Gibson alikuwa akipokea, alizungumza naye lakini kila alipohitaji kuonana naye, alikataa kwa kujipa visingizio vingi, kwamba hakuwepo nyumbani, alilala kwa washikaji zake na visingizio vingine.
Hakutaka kumwambia Shadya kwamba hakumpenda, kwa ulimwengu wa sasa, mwanamke huwa hakataliwi kwa maneno kwa sababu mwanaume anajua kuna siku atakuwa na uhitaji naye, hivyo atampigia simu na kuomba kuonana naye.
Hilo ndilo lilivyokuwa kwa Gibson, alikuwa mwanaume wa mahesabu makali, alijua tu kuna siku isiyokuwa na jina angemuhitaji msichana huyo, na kwa sababu aliwahi kulala naye, asingeweza kumpinga hata kidogo.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Umebadilika sana, kwa nini?” aliuliza Shadya kwenye simu, alikuwa akiongea na Gibson.
“Nimekuwaje mpenzi?” aliuliza mwanaume huyo.
“Unakuwa bize sana!”
“Najua! Naomba unisamehe!”
“Kwa nini hutaki kunijali kama zamani?”
“Kwani zamani nilikuwaje mpenzi?
Nilikuwa nakupigia simu mara kwa mara, meseji na mambo mengine, ninayafanya hayo hata sasa hivi love,” alisema Gibson.
“Ila kasi imepungua! Kwa nini? Unahisi sistahili tena kuwa nawe kwa sababu nimekuruhusu kuuona mwili wangu?” aliuliza msichana huyo.
“Ni maneno makali sana unazungumza!”
“Naomba uniambie!”
“Shadya! Wewe ni msichana mrembo mno!”
“Hujanijibu!”
“Shadya! Unajua....”
“Hilo si jibu! Niambie ni kwa sababu nimekuvulia nguo zangu na kuniona nikiwa mtupu?” aliuliza msichana huyo.
Gibson akanyamaza, alitamani amjibu kwa kumwambia kwamba uchaguzi alishinda na hapakuwa na nafasi ya rais kupiga tena kampeni lakini alishindwa kumwambia hivyo.
Huyu Shadya alitakiwa kuwa mchepuko, si msichana wa kukataliwa hata siku moja. Aliamini kwamba kuna siku jijini Dar es Salaam kungekuwa na mvua kubwa, baridi kali, inawezekana Paula akawa kwenye siku zake, hivyo msaada mkubwa ambao ungebaki ungekuwa kwa huyo Shadya, hivyo alitakiwa kujilazimisha kumpetipeti.
“Nijibu....” alisema Shadya baada ya ukimya wa sekunde kadhaa kutoka kwa Gibson.
“Hiyo si sababu!”
“Sababu ni nini sasa?” “Ubize tu!”
“Huo ubize umeanza siku hizi? Tena baada ya kunivua nguo zangu?” aliuliza.
“Hapana!”
“Kwa nini imekuwa hivyo?”
“Naomba tuonane tuongee!”
“Saa ngapi?”
“Hata sasa hivi njoo hapa Sinza Kumekucha, kwenye mgahawa wa Napoleon!” alisema Gibson na kukaa simu.
Shadya aliulia, moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali, hapo ndipo alipokumbuka maneno aliyoambiwa kwamba wanaume wa Dar es Salaam walikuwa hatari, hasa wale waliokuwa wakisoma vyuoni.
Alionywa kabla lakini kitu cha ajabu kabisa, maonyo yote yalipitia upande wa kushoto na kwenda upande wa kulia, leo moyo wake ulikuwa ukimuuma.
Aliamini huyo Gibson inawezekana alimpata mwanamke mwingine na ndiyo maana aliamua kutaka kumuacha, hakutaka kuona hilo likitokea, kama mwanamke alitakiwa kupambana mpaka kuhakikisha anashinda vita hivyo na hatimaye kubaki na Gibson wake.
“Nitalipambania hili penzi!” alisema Shadya.
Akajiandaa na baada ya dakika kadhaa, akatoka na kuelekea katika Kituo cha Daladala cha Utawala hapo chuo ambapo akasubiri daladala, ilipofika, akaingia ndani.
Akakaa, daladala haikuondoka kwanza, ilikuwa ikiendelea kuita abiria mahali hapo. Mara akiwa humo, mwanaume mmoja akaingia, alikuwa nadhifu, alivalia suruali ya kitambaa na shati nyeupe, alivalia na tai nyeusi, macho yake yalipotua kwa Shadya tu, msichana huyo akashtuka, jamaa akatoa tabasamu, akaenda kukaa naye kwenye kiti.
“Vipi Shadya!” alimsalimia jamaa huyo, Shadya akashtuka, hakuamini kama alikuwa akijulikana na watu wengine.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Umenijuaje?” aliuliza kwa mshtuko.
“Mwanachuo mwenzangu! Ninakujua kwa kuwa nasikiaga watu wakikuita!” alijibu jamaa huyo.
“Oh! Sawa!”
“Karibu!”
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment