Search This Blog

Wednesday, 23 November 2022

NINI MAANA YA MAPENZI - 5

 





    Simulizi : Nini Maana Ya Mapenzi

    Sehemu Ya Tano (5)





    Erica hakujua wakati anaingia pale getini kwao kumbe mama yake alikuwepo na alimuona pale wakati Erick anamuaga, kwahiyo Erica aliingia ndani bila kujua kuwa mama yake naye alikuwa nje.

    Basi aliingia na kumkuta dada yake akiwa anamshangaa,

    “Yani Erica kweli! Ndio duka gani hilo tangu umeondoka hadi muda huu jamani!”

    Erica alikuwa kimya, akijipanga na majibu yake kama kawaida kisha dada yake akaendelea kumwambia,

    “Mama yupo nje huko, ameenda kukutafuta madukani maana ni mud asana umechukua, toka uondoke hadi saa hizi! Halafu ni usiku huu ujue”

    Basin a mama yao akaingia ndani na kumwamgalia Erica kwa gadhabu sana huku akisema,

    “Natamani ungekuwa bado mdogo, yani leo ningekufinyanga upya mjinga wewe. Haya nidanganye kuhusu duka uliloenda mpaka muda huu”

    Erica sababu mama yake alishaenda dukani kumuangalia pia, akaamua tu kusema ukweli,

    “Mama, samahani nilitoka niende dukani kweli ila nikakutana na Erick njiani akiwa anakuja huku kwahiyo nikapanda kwenye gari lake na kuongea, tulipomaliza mazungumzo ndio nikarudi nyumbani”

    “Sio ukarudi, sema akakurudisha. Au unafikiri sijawaona hapo mlangoni kwangu mkiwa mnalambana lambana, yani Erica unasahau kabisa jinsi Yule mwanamaombi alivyokufundisha kuenenda kiimani, yani umesahau kabisa kabisa na unafanya unavyotaka wewe, huyo Erick kila nikimfikiria kuwa ndiye mtoto wa lile balazuri najikuta kukosa tumaini nae kabisa, ndiomana alianza kukutongoza toka uko shuleni kumbe karithi tabia za baba yake mpaka shule ile ikakushinda sababu yake ila umesahau kabisa unaendelea tu kuendekeza mapenzi na yeye”

    Bite alidakia na kusema,

    “Kumbe ni huyu aliyesababisha Erica aje kusoma kwangu?”

    “Ndio huyu mwanangu, yani Yule kijana sijui alimpa nini mdogo wako na alivyo mjinga ataanza kumfata fata hadi abebe mimba yake maana anafikiri kubeba mimba ndio kupendwa”

    Hapo Erica alitulia kimya kabisa kwani kama mimba tayari alikuwa nayo, ila sasa alijitahidi kwa kila hali ile mimba isigundulike mapema nyumbani kwao labda mpaka atomize swala la yeye na Erick kuoana.

    Basi akaamua tu kwenda kulala maana hakufurahia vile alivyokuwa anasemwa.



    Erick alikuwa kwenye gari, ila kilichompeleka hadi mitaa ya kwakina Erica hazikuwa dawa za baba yake ukweli ni kuwa alitamani sana kuonana na Erica, na muda huo roho yake ilikuwa imeridhika sana na jinsi alivyoongea siku hiyo na Erica alijihisi raha sana kwenye moyo wake kiasi kwamba alikuwa akiendesha gari ila mawazo yote kwa Erica tu.

    Alifika kwao na kuingiza gari ndani kisha kushuka, muda ulikuwa umeenda sana, ilikuwa ni saa tano usiku ila alipoingia ndani alimkuta Tumaini bado yupo macho akiangalia tu Tv, alipoingia tu alimsalimia na kukaa ili kuulizia kama baba yao amelala sababu dawa kachelewesha,

    “Mmmh baba kashalala maana nimechelewesha dawa balaa”

    “Wewe nawe kununua gani dawa huko toka saa kumi na moja jioni hadi muda huu ndio unarudi kweli?”

    “Aaah sijui nikwambie vipi ila nilimkumbuka sana Erica, nikaamua kupita kwenye mitaa yao ili nimuone tu”

    “Mmmh huyo Erica, sijui alikupa nini. Vipi lakini umeonana nae?’

    “Ndio nimemuona na moyo wangu umeridhika na tena kanipa habari hiyo kama ina ukweli basi ni furaha kubwa kwangu”

    “Habari gani tena hiyo?”

    “Kwanza niambie, baba kalala?”

    “Alale wapi? Baba leo kapona yani kaondoka kumpeleka Sia kwao, baba kawa mzima gafla”

    “Kivipi yani”

    “Ni hivi, ulivyoondoka tu alikuja Sian a kunipa taarifa kuwa ana mimba yako”

    “Ana mimba yangu?”

    “Ndio alivyosema, na cheti kanionyesha kuwa ana mimba yako. Sasa baba alisikia weee yani huwezi amini baba kapona muda huo huo na kumuita Sia sebleni ameongea nae kwa muda mrefu sana na ulikuwa unangojwa wewe, sema umechelewa sana, ndipo Sia alipoaga basi baba kaamua ampeleke Sia kwao yani baba anaonekana anataka umuoe Siam lee mtoto wenu”

    “Huo ni ujinga sasa, sijategemea mambo ya kijinga kama hayo kutokea kwenye familia yangu, huyo Sia nitaenda kwao kesho asinitanie”

    Erick aliinuka na kwenda chumbani kwake kwani alihisi kuwa na hasira iliyopitiliza, ni alichukia sana kwa muda huo yani baba yake kapona baada ya kusikia habari kuwa Sia ni mjamzito, alichukia sana kwakweli. Aliamua kulala kwa hasira hata kula hakutaka kabisa.



    Kulipokucha, Erick aliamka akaoga na kujiandaa basi akataka kwenda kumuangalia baba yake kwanza kabla ya kuondoka ila hakumkuta, alitoka nje na kumkuta dada yake Tumaini akiangalia gari lake, akamuuliza,

    “Inamaana baba hakurudi jana au?”

    “Alirudi yani wewe nay eye mlipishana kama nusu saa tu ila leo mapema kabisa katoka, kaniaga kuwa anaenda kwenye kazi yake”

    “Kwahiyo baba kapona eeeh!”

    “Itakuwa”

    Erick alisikitika sana kwa mwenendo wa baba yake, kisha akamuaga Tumaini kuwa muda huo ameamua kwenda kwakina Sia,

    “Na mimi natoka muda sio mrefu, naenda kule dukani”

    “Sawa, tutaonana badae basi maana baba mwenyewe tuliyekuwa tunamuuguza ndio huyo kapona”

    Basi Erick aliondoka zake na moja kwa moja alienda kwakina Sian a kumkuta Sia yupo tu ametulia nje kwao, alipofika yeye kuna mwanamke alikuwa nakatisha pia na kikapu kichwani, Sia alimuita na kununua embe bichi kisha kuanza kulitafuna pale, Erick alimuangalia huku akitikisa kichwa, ila Sia alimwambia,

    “Usisikitike, ni mwanao huyu kataka embe muda huu”

    “Hebu nitolee balaa lako huko, hiyo mimba yangu uipate wapi? Ndotoni au?”

    “Unajifanya umesahau kama ulikutana na mimi kimwili? Ndio nikapata mimba hii, tena safari hii siwezi kuitoa hata usemaje, nishatoa mimba zako nyingi sana ila hii siitoi umesiki? Tena nadhani nitazaa mapacha”

    Halafu akacheka, Erick alikuwa amechukia sana na kumuuliza,

    “Hivi wewe mwanamke una kichaa au? Mara ya mwisho nilikutana na wewe nikiwa na hasira zangu hata hivyo nilitumia kinga maana sikuwa na mpango wa kuzaa na wewe, iweje useme ni mimba yangu?”

    “Hujui kama kinga huwa zina pasuka? Nenda kagoogle uone jinsi wanawake wanavyopata mimba na kinga ilitumika. Mimi nina mimba yako, ukubali au ukatae yani utake ni mimba yako, hutaki ni mimba yako, sasa maswala hayo ya kushangaa yanatoka wapi?”

    “Sia, huwezi kuwa na mimba yangu”

    Sia akatoa kile cheti chake kumuonyesha kuwa ni mjamzito,

    “Sasa bishana na cheti hiko kuwa Sia hana mimba. Nimekwambia nina mimba yako, unakataaje? Nakusingiziaje kwa mfano? Nimekaa kimya kwa mud asana ila sasa nimeamua kusema maana kitumbo kitaenda mbele bure sijakwambia kuwa nina mimba yako, kipindi chote nahangaika ili unipende sababu nahitaji tulee mtoto pamoja. Erick, hii mimba ni yako na wala usibishe”

    “Nakataa Sia, huna mimba yangu yani hilo napinga kabisa na tutaenda kupima kwakweli huyo mtoto. Hiyo mimba sio yangu, sikutambui Sia. Huyo mtoto akizaliwa tutaenda kupima”

    “Tena sio mtoto akizaliwa, ni watoto maana watakuwa mapacha tena wakike na wakiume. Mmoja ataitwa Erick na mwingine Erica, si itapendeza eeeh!”

    “Achana na mimi”

    Erick aliondoka mahali pale na kupanda gari yake ila alikuwa na mawazo mengi sana, bado hakukubaliana na swala kuwa ile mimba ni yake maana akikumbuka mara ya mwisho na Sia alitumia kinga, na muda mrefu tayari ulishapita kwakweli hakukubaliana na hilo swala.

    Muda huo aliamua kuondoka kwenda kwa Yule rafiki yake daktari ili kumuuliza vizuri.



    Leo Steve alikuwa amepooza sana maana tangu jana hakutoka nyumbani kwao, ilibidi Dora amuulize mdogo wake kuwa ana tatizo gani maana toka alitokomea kwa Sia ni jana tu ndio alilala nyumbani kwao,

    “Mdogo wangu, nikikwambia umerogwa unakataa haya nakubali hujarogwa ni mapenzi yako kwa Yule dada. Haya leo vipi upo nyumbani na mawazo kibao”

    “Sia kaniambia niondoke kwake na nirudi nikiwa nimepata kazi maana hawezi kuishi na mwanaume asiye na kazi”

    “Huyo Sia wakati anakuachia wewe kula tunda lenye dawa hakujiongeza kuwa huna kazi? Yani wanawake bhana wana mambo ya ajabu sana. Kashachanganya akili yako na bado anaendelea kukuchanganya zaidi. Eeeeh kazi wewe utaipata wapi?”

    “Nitafutie kazi basi dada”

    “Mi mwenyewe unavyoniona hivi ni kazi yani sina mbele wala nyuma ila nitakuulizia mdogo wangu ila dah Sia angekubali kwenda kwenye maombi mdogo wangu ungefunguka yani ungefunguka kabisa kabisa, sema hutaki kukubali kuwa umerogwa”

    “Ndio sijarogwa mimi”

    “Basi ondoa hayo mawazo, yule Sia asikubabaishe wewe siku mvizie akiwa na watu unajitokeza mbale yao umesikia”

    “Nijitokeze vipi?”

    “Unawaambia watu kuwa unamahusiano na Sia”

    Mara simu yake ikaita na kuipokea na alipomaliza kuongea nayo alimuaga mdogo wake kuwa anatoka kidogo,

    “Unaenda wapi dada?”

    “Mimi mtoto wa kike kumbuka, siwezi kuulizwa ninapoenda”

    Basi alienda kujiandaa kisha akaondoka, ile simu ni James alimpigia kwahiyo alienda kukutana nae, kwa kipindi hiko James aliona mtu pekee wa kumgfariji ni Dora maana yeye hakujua kuwa Dora ndio alimletea ugonjwa ule sababu alikuwa na wanawake wengi kwahiyo hata aliletewa ugonjwa na nani hakujua kabisa, kwahiyo alimuita Dora ili wale wanywe kisha ndio warudi kwenye nyumba zao.



    Rahim leo alienda mwenyewe kuonana na Zainabu maana mar azote huwa anaenda na Babuu, na huwa ni Babuu ndio anaongea. Basi alimsalimia na kuanza kuongea nae,

    “Zainabu, samahani kama nakukosea ila nimeshindwa kuvumilia kwa hakika nakuhitaji, yani nahitaji uwe mke wangu wa ndoa, nakupenda sana”

    Zainabu akacheka sana na kumwambia,

    “Naomba nitajie aya moya ya kwenye Kuran”

    “Yametoka wapi mambo hayo jamani eeeh! Mi nakwambia mambo mengine na wewe unasema vitu vingine”

    “Ila si ulisema wewe ni Mwislamu safi, sasa mbona nimekuuliza kitu chepesi sana ambacho hata mtoto mdogo anajua. Inamaana wewe hukusoma Madrassa?”

    “Nisome wapi, baba na mama ni kweli ni Waislamu ila hawakuishi pamoja wala hawakuoana ilipelekea mama yangu kuishi na mwanaume mwingine ambaye ni baba wa mdogo wangu, Yule mwanaume alikuwa Mkristo, huko Madrassa ningeenda muda upi? Na mama kaja kuolewa kabadili na dini kabisa, mambo mengine unanipa tu mitihani ambayo ni wazi siwezi kuifanya”

    “Haya, Msikitini je? Maiwaidha hujawahi kusikiliza wewe?”

    “Mimi nimeshi Marekani, hayo mawaidha ningeyasikia wapi?”

    “Hakuna mji ambao hauna Misikiti labda kama ulikuwa huendi Msikitini!”

    “Zainabu, habari hizo hapana unajua nikiwa na wewe nitaweza kuyajua yote hayo! Na utafanya niwe Mwislamu safi sasa, kuliko kuniuliza maswali ya kunikandamiza kwa kipindi hiki. Mimi nakupenda na ninahitaji uwe mke wangu, tafadhali usiniletee propaganda zingine”

    “Sawa, jambo rahisi kabisa njoo kwa wazazi wangu na ufanye taratibu zote unioe maswala ya kuniimbia nyimbo za nakupenda wala sitaki kuyasikia”

    Zainabu akaondoka zake na kumuacha Rahim mwenyewe, alifikiri Rahim anashindwa kufanya kile alichokisema, ni kinyume maana Rahim aliondoka pale muda ule ule na alikuwa na lengo la kwenda kuongea na mama yake juu ya swala hilo.



    Erick alienda hadi kwa rafiki yake hospitali na kumkuta baada ya kumalizana na wagonjwa sasa, alienda kukaa na rafiki yake kuongea nae,

    “Yani Tom bhana nina tatizo”

    “Lipi hilo”

    “Yule msichana wangu wa zamani wa kuitwa Sia si unamkumbuka Yule!”

    “Namkumbuka ndio, kwani kafanyaje?”

    Basi Erick alianza kumueleza kuhusu Sia, yani kuhusu mimba aliyosema anayo ili asikie ushauri kutoka kwa rafiki yake huyo, basi Yule rafiki yake alianza kumshauri,

    “Cha kukushauri huyo binti mkapime ultrasound ili ujue tu mimba ina muda gani wala usisubiri mtoto azaliwe sijui nini, yani wewe kapime nae tu hiyo utajua uongo wake maana unajua vizuri toka umekutana nae ni kipindi gani kimepita halafu yeye anasema ana mimba ni ya muda gani tena mlete hapa hapa tumpime wala asitake kukudanganya rafiki yangu”

    “Sawa nashukuru sana Tom, yani huyu binti sina hamu nae loh! Kajua mimi nimerudiana na mchumba wangu basi ndio wivu mpaka kutaka kunisingizia mimba”

    “Kwanza Kondomu ililetwa kwaajili ya kuzuia mimba, yani asilimia mia moja kondomu kazi yake ni kuzuia mimba ila wala tusizunguke yani tupime muda wa mimba tu muache ajidai ila muda wa mimba utamuumbua”

    “Na kama alipata mimba kipindi ambacho yupo nami ila alipata kwa mwanaume mwingine?”

    “Erick rafiki yangu, vipimo vipo tutajua tu.Usiwe na mashaka rafiki yangu”

    Basi Erick alifurahi pale na kuondoka akiagana na rafiki yake kwani kwa asilimia mia moja alikuwa na uhakika kuwa ile mimba ya Sia sio ya kwake.

    Wakati anaondoka alikutana na Dora njiani na kusimamisha gari lake ili asalimiane nae, alimpakiza kwenye gari lake kwani alitaka pia kuulizia maendeleo ya mdogo nwake,

    “Mwenzangu Steve ndio kazamia kwa Sia balaa, majuzi ndio kamfukuza mdogo wangu eti mpaka apate kazi maana hawezi kuishi na mwanaume asiye na kazi”

    “Kwahiyo huyo mdogo wako alikuwa anaishi kwa Sia?”

    “Ndio, wanapika na kupakua yani waliishi kama mke na mume”

    Hapo akili ya Erick ilifunguka kiasi, kisha alianza kumuuliza Dora kuhusu baba yake,

    “Eeeh na mzee Jimmy una mahusiano nae yapi?”

    “Yule baba yako ni buzi langu”

    “Buzi lako kivipi?”

    “Yani ni mpenzi wangu”

    “Haiwezekani Dora, baba yangu atembee na wewe!”

    “Ukatae ukubali habari ndio hiyo, Yule baba yako alikuwa akimtaka Erica ila Erica hakuwahi kumkubali basi babako akaamua kumalizia hamu zake kwangu”

    “Unaongea utumbo tu, hebu shuka kwenye gari yangu”

    “Huniamini ila nitakuaminisha, siku sio nyingi utaamini niyasemayo”

    Kisha Dora alishuka kwenye ile gari ya Erick na kuondoka zake.



    Erick alienda kwao huku akiongea mwenyewe kuwa haiwezekani baba yake awe na mahusiano na Dora, hata Tumaini alipofika alimueleza jinsi alivyokutana na Dora na jinsi Dora alivyomwambia.

    “Dora ni mjinga sana, hivi baba yetu anaweza kuwa na mahusiano naye?”

    “Haiwezekani yani haiwezekani kabisa Tumaini, hata kama baba alitaka kumuoa Erica ila haiwezekani kuwa na mahusiano na baba yetu”

    “Au katumwa na Erica akwambie hivyo?”

    “Hapana napo nakataa, Erica hawezi kufanya huo upuuzi”

    “Mmmh unavyomkatalia huyo Erica kama malaika vile na hawezi kutenda lolote baya. Ila tutaona”

    Basi waliongea ongea na siku hiyo baba yao aliwahi kurudi na kuwaita ili kuongea nao tena,

    “Kwasasa baba yenu naendelea salama kabisa, jamani yaliyopita sitaki kuyasikia kwenye nyumba yangu. Ile familia hamjui tu ni kiasi gani imenila, mimi sikuwa mjinga kutaka kuoa pale. Ila tuachane na mambo hayi kabisa, nilichowaitia ni kuhusu harusi yako Erick na Sia”

    Erick alishangaa sana na kumkatalia baba yake kuwa hawezi kumuoa Sia ila baba yake alimwambia jambo moja tu,

    “Ukitaka utamuoa Sia, usipotaka utamuoa. Mambo ya mjukuu wangu kulelewa mbalimbali kama malezi mliyoyapata nyie sitaki. Nimemaliza”

    Kisha baba yao akainuka na kuondoka zake, Tumaini alimuangalia Erick na kumuuliza,

    “Eeeeh sasa utachukua maamuzi gani?”

    “Sina maamuzi yoyote, si yeye anababaishwa na mimba ya Sia! Basi Erica pia ana mimba yangu”

    Baba yao alitoka ndani na kuuliza kwa mshangao,

    “Unasema nini?”





    Kisha baba yao akainuka na kuondoka zake, Tumaini alimuangalia Erick na kumuuliza,

    “Eeeeh sasa utachukua maamuzi gani?”

    “Sina maamuzi yoyote, si yeye anababaishwa na mimba ya Sia! Basi Erica pia ana mimba yangu”

    Baba yao alitoka ndani na kuuliza kwa mshangao,

    “Unasema nini?”

    Tumaini na Erick wakaangaliana kwa muda, kisha Tumaini akaamua kuua ile habari kwani ilikuwa ni usiku na akadhani kusema kuwa Erica ana mimba ni kumuongezea ugonjwa huyu baba yao, basi akasema

    “Hamna kitu baba, tulikuwa tunaongelea mambo yet utu”

    “Mambo yenu wakati nimesikia mkisema Erica!”

    “Hamna baba hatujamtaja mbona”

    “Nyie watoto nadhani hamuelewi maumivu yangu ndiomana mnasema sema tu hapa. Mimi huyo Erica kamwe siwezi mtambua kama mke wa Erick ila nitamtambua kama mke wangu mtarajiwa, wewe Erick kama unahitaji kupata radhi zangu endelea kucheza na mama yako Erica, nimemaliza”

    Erick alitaka kujibu kitu ila Tumaini alimzuia, alipoondoka baba yao alimtaka tu kaka yake akalale na waongee kesho kuhusu yale mambo.

    Erick aliingia chumbani kwake akiwa amechukia sana maana pale ndio ilitokea udhihirisho kabisa kuwa baba yake hataki yeye awe na Erica, akajisemea,

    “Na atataka tu, Mungu nae anajuaga mambo yani mara moja tu Erica kadaka mimba yangu na ile mimba ndio itakuwa kigezo kizuri cha mimi na Erica kuoana. Yeye kama anataka kuchangia mwanamke na mimi akamuoe Sia huko”

    Alichukia hadi alijikuta akiongea hovyo na kulala ila alilala huku amechukia sana.

    Kitendo kile kilifanya siku hiyo Erick acheelewe kuamka, sema sababu biashara zilikuwa zake kwahiyo hakupata mawazo sana, akaoga na kutoka nje akamkuta dada yake Tumaini yupo mezani akinywa chai ambapo alimsalimia na Tumaini akamwambia wajumuike pamoja kunywa chai.

    “Unafikiri najisikia basi hata kunywa chai, sijisikii hata chai naiona ya uchungu”

    “Erick usifanye hivyo kaka yangu, hebu njoo kwanza tuongee kama familia”

    “Na wewe utaniambia nini na humpendi Erica!”

    “Hivi hujui kama nimebadilika, hata nisingemtaka Erica ni wazi nisingemtaka na Sia pia. Njoo tuongee bhana, sisi ni familia inatakiwa letu liwe moja ndio tutashinda”

    Basi Erick alikaa pale mezani ambapo Tumaini alimmiminia chai na kumuwekea ili apashe tumbo na kuanza kuongea nae,

    “Eeeh hebu tuongee vizuri, kwahiyo Erica ana mimba yako?”

    “Ndio Erica ana mimba yangu”

    “”Ila una uhakika Erick? Isije ikawa kakudanganya tu au ana mimba ya mtu mwingine?”

    “Tumaini sikia, nampenda sana Erica yani nampenda sana. Kumbuka nimejitolea kumlea Yule mtoto wake Angel, nimeamua kujitoa na kumfanya kama mwanangu wa kumzaa, hivi Erica awe ni mwanamke wa aina gani anisingizie mimba mwanaume ambaye nina utu kama mimi? Kwani akisema amebeba mimba ya mtu mwingine unafikiri nitamuacha? Nitachukia ila nampenda sana kumuacha siwezi”

    “Mmmmh mapenzi ya hivyo sijawahi kuyaona toka dunia iumbwe, basi tuachane na hayo. Tuzungumzie swala la baba sasa”

    “Halafu wewe usiku umeleta kidomo domo chako, mimi nilitaka kumueleza ukweli Yule mzee”

    “Tatizo sio kumueleza ukweli, tatizo mzee wetu ana presha na unalijua hilo”

    “Kwahiyo presha ya huyo mzee ni kwa habari za Erica tu au?”

    “Erick, Yule ni baba yetu hivi jana ungemwambia angepandisha tena presha ingekuwa tatizo kwa nani? Kama sio sisi tungehangaika tena, tunaweza kuongea mengi kwasasa sababu tunamuona, unaweza sema hata bora afe sababu tunamuona ila akifa tutashikana mashati hapa, ukisikia kuwehuka ndio hapa, hatukatai kufa kupo basi afe kwa ahadi yake ila kisije kuwa kisingizio kuwa sisi tumesababusha kifo cha mzee wetu, sio picha nzuri kwakweli”

    “Sasa Tumaini, hebu niambie cha kufanya yani huwa najikuta natamani tu kumjibu huyu mzee”

    “Cha kufanya ni kuongea kwa busara na huyu mzee, kwasasa tunatakiwa kuweka nae ukaribu na tumuulize kuwa kwanini anamng’ang’ania Erica, halafu tujue jinsi ya kumuweka sawa ili ajue kuwa Erica hamuhitaji, anayekuhitaji ni wewe yani tujue jinsi ya kuweka sawa saikolojia ya baba yetu. Bado tunamtegemea huyu mzee Erick, wala usitumie hasira mdogo wangu najua inauma ila tu kuwa makini”

    “Sawa nimekuelewa, basi leo jioni akirudi nitajaribu kuwa nae sawa”

    “Hivyo ni vizuri mdogo wangu”

    Basi Erick alimaliza ile chai na kuagana na dada yake maana nae alikuwa akijiandaa kutoka.



    Kwa kipindi hiko Erica alikuwa kwao ila hakuwa na raha kabisa yani ukimuona unajua kabisa kuwa huyu mtu anasumbuliwa na mawazo, basi siku hiyo alifika dada yake Mage na walianza kumueleza yaliyotukia.

    Erica alikuwa chumbani na kusikia yale ambayo Mage anaelezewa, basi akaitwa na alijua tu kuwa anaenda kusemwa,basi akatoka ili kuwasikiliza, ambapo Yule dada yake mkubwa alianza kuongea,

    “Erica, katika pitapita zangu zote sijawahi kukutana na majanga aina yako. Hivi nikuulize tu, hujawahi kutembea na huyo baba mkwe wako?”

    “Sijawahi dada”

    “Tutaaminije ikiwa ndugu yako Derick tu ulitembea nae na nikakuuliza ukakataa katakata kuwa hujawahi kutembea nae kumbe ulitembea nae. Na kuhusu huyo mzee tutajuaje?”

    Ndio hapa Bite naye akasikia vizuri swala la Erica kutembea na Derick, basi akasema kwa mshangao,

    “Kheee Erica kumbe ulitembea hadi na Derick ndiomana mama anamtimuaga hapa, loh mdogo wangu mchafu wewe”

    Mage akaongezea,

    “Kwani unafikiri ni mchafu kidogo, mengine si mama yake anamfichia hapa. Unaambiwa huyo ukoo wa huyo Rahim yani baba yake Angel kashaumaliza wote, inawezekana kaka wa watu alihitaji kumuoa ila kila akikumbuka kuwa Erica kamaliza ukoo wao wote hana hamu. Yani huyu Erica usimuone hivi, ana maovu kushinda wote humu”

    “Khee kwa mtindo huo anafikiri huyo Erick atamuoa? Kila mwanaume anapenda kupata mwanamke aliyetulia ila macho juu juu kama unatafuta mitambo kuna atakayekuhitaji? Yani utajikuta unazeekea nyumbani”

    “Ni kweli Bite, asipoangalia huyu kazi yake itakuwa kusherekea harusi za wenzie tu, kamuendekeza Yule shoga yake malaya wa dunia”

    “Ila ukitembea na mwizi na wewe ni mwizi, yani huyu Erica kanivunja maini kabisa, hakuna cha ndoa hapa wala nini”

    Mama yao ilibidi aingilie kati maana walikuwa wakimkandamiza sana mdogo wao

    “Hivi na nyie toka muanze kuaongea hamna mada nyingine za kujadili jamani eeeh! Sijui ndoa hamna, sijui hajatulia, sijui nini na nini haya sasa nyie mliotulia ndoa zenu ziko wapi? Wewe Bite imekushinda hiyo, na wewe Mage unaishi tu kwa taratibu za kidini ila ndoa yako ilishakata roho, hebu muacheni mwenzenu. Mimi Erica swala langu kwako ni moja tu, nahitaji kumuona tena Erick hapa niongee nae mwenyewe, nadhani unanielewa”

    “Nimekuelewa mama”

    Erica aliinuka na kwenda chumbani ila alikuwa na uchungu sana moyoni mwake, aliamua muda huo kumpigia simu Erick ili angalau apooze moyo wake.

    “Erick nimekumiss”

    “Hata mimi nakumiss sana Erica, ila nashindwa kuja kwenu kwasasa. Basi naomba uje tukutane, nikuone tu kipenzi change”

    “Basi njoo mitaa ya kwetu”

    “Sawa. Nikifika mitaa ya kwenu nitakupigia simu uje”

    Basi Erica alikata ile simu huku akitabasamu na kusahau yote waliyokuwa wakimsema sebleni.



    Jioni ilipofika Erick alimtafuta Erica kisha alienda kuonana nae kama ambavyo alipanga kukutana nae, ila kwasasa ilionyesha kuwa Erick kakubaliana na hali halisi kuwa ile mimba ya Erica ni yake maana alivyokaa nae tu kwenye gari cha kwanza alimuuliza,

    “Mtoto wetu wa tumboni hajambo?”

    Erica alitabasamu na kuitikia kuwa hajambo, kisha Erick aliulizia na maendeleo ya Angel,

    “Kiukweli Angel kakumiss sana”

    “Dah! Kweli sijatoka siku nyingi na mwanangu, basi lini upo tayari tutoke?”

    “Hata kesho”

    “Hahaha, basi muandae Angel tutoke nae. Twende mahali tukafurahi pamoja kama familia, yaliyotokea kati yetu tusiyazungumzie kwasasa ila tujali afya za watoto wetu”

    Erica alitabasamu kwani aliona raha sana kwa wakati huo, ila muda ule ule simu ya Erick iliita na alipoitazama aliona ni baba yake anapiga, aliamua kuipokea na kuongea nayo

    “Erick, nakuhitaji nyumbani muda huu”

    “Ila nipo mbali baba”

    “Nimekwambia nakuhitaji nyumbani muda huu”

    Kisha akakata simu, na kumuacha Erick akimuangalia tu Erica kisha akamwambia

    “Ni baba yangu huyo, anahitaji niende nyumbani sijui ana lipi la kusema”

    “Mmmh!”

    Erica aliguna tu ila Erick aliongea,

    “Katika pitapita zangu zote sikuwahi kukutana hata na ndugu yako na nimekuwa makini sana kwani uliishi sana moyoni mwangu na niliamini siku moja utakuwa mke wangu, ila mwenzangu bado najiuliza ulimkubali vipi mtu mzima kama baba yangu? Je hela zake ndio zilikuzuzua?”

    “Erick, tafadhali usinikandamize nakuomba, kwetu wanikandamize, nahitaji faraja kwako ila nawe unanikandamiza unataka niwe mtu wa aina gani eeeh! Usinikandamize nakuomba. Nishakwambia ukweli, sijawahi kuwa na mahusiano na huyo mzee ila bado unakazania kitu hiko hiko”

    “Erica, Napata maswali sana sababu ulinilamba milioni tano ukasema kuwa Yule mzee alikupa hela na ukatumia kwahiyo mke wake anataka, baba yangu hana mke kwahiyo ulinipiga change la macho?”

    “Sikukupiga change la macho Erick, ni kwavile tu siku ile mambo yaliingiliana ukashindwa kuniuliza risiti ila nitakuletea risiti hiyo kesho tunavyoonana, nilisema mkewe ila hakuwa mke ni hawara ambaye ni Dora na alinidai hela za Yule mzee sababu ni wake”

    “Kwahiyo kweli baba yangu alikuwa na mahusiano na Dora?”

    “Sio alikuwa, hadi sasa bado ana mahusiano na Dora”

    “Weee haiwezekani, sema kingine Erica ila kwavile hapana na nikigundua hivyo Yule mzee sitajali presha yake, yani nitafunga ndoa na wewe haraka sana”

    Erica alitabasamu kwani ule ulikuwa ni ukweli kwahiyo ataolewa na Erick, lilikuwa jambo la furaha sana kwake. Basi kwa muda huo Erick alimrudisha Erica kwao kisha kuagana nae na yeye kurudi kwao.

    Erica aliingia kwao huku akitabasamu na familia yake ilikuwepo, alianza mama yake kumuuliza,

    “Haya mwenzetu hiyo furaha ni lazima umetoka kukutana na Erick”

    Bite akachangia,

    “Jamani Erica hukomi tu, ukipata kimimba kingine ndio akili itakukaa sawa maana utatulia”

    Erica aliwaacha na kuelekea chumbani kwake ambapo Mage aliuliza,

    “Jamani huko kukimbilia chumbani ni kawaida au kuna kitu?”

    “Kitu gani unakihisi Mage?”

    “Mmmh sijui, jamani ngoja niage. Naenda kwangu, nitakuja tena”

    Basi Mage akawaaga pale na kuondoka zake.



    Erick alifika kwao na kumkuta baba yake yupo sebleni na Tumaini kwahiyo alimsalimia na kujumuika nae kwenye maongezi,

    “Yani Erick umejichelewesha huko balaa, nilihitaji kumaliza mambo leo leo ila wewe umechelewesha mambo”

    “Mambi gani baba?”

    “Nishaenda Kanisani kuandikisha ndoa yako na Sia”

    Erick alimshangaa baba yake, kuwa amechanganyikiwa au vipi, akamuuliza

    “Baba, kwanini ufanye maamuzi bila kunishirikisha mwenyewe?”

    “Nishaongea na Mchungaji kwahiyo kesho tutatoka hapa kwenye mida ya saa nne tutaelekea kumchukua Sia kisha tutaenda kanisani maana kuna maswali mtaulizwa kwanza”

    “Baba jamani hata kama hujawahi kuoa ila ndoa sio kama hivyo ufanyavyo wewe”

    “Kwani wewe tatizo lako nini, nisjhakwambia sitaki mjukuu wangu apate malezi kama mliyoyapata nyie kwa kutokuishi na baba na mama. Nahitaji mjukuu wangu apate mapenzi ya wazazi wawili”

    “Hapana baba, siwezi kumuoa Sia”

    “Kwanini huwezi kumuoa Sia? Kwasababu ya Erica eeeh!”

    Erick akawa kimya tu , kisha baba yake akaendelea kuongea,

    “Erick, ujinga kwangu sitaki. Hivi wewe mtoto una laana au ni kitu gani? Hivi upite palepale alipopita baba yako, mbona ni laana hiyo?”

    Tumaini na Erick wakaangalia na kuona wakiendelea kuongea na huyo mzee wao basi kuna maneno mengine atayazungumza ambayo sio sawa kabisa, ila Yule mzee akainuka na kusema,

    “Erick, utake Sia utamuoa, na hutaki utamuoa. Nimemaliza, saizi natoka kidogo nitarudi baadae”

    Tumaini akamwambia,

    “Lakini baba muda umeenda saa hizi?”

    “Acha nitoke kidogo akili yangu iwe sawa, watoto mnanichanganya nyie, sasa mimi sina mke, nataka kuoa mnaniletea mambo ya ajabu na kuzua magonjwa ya ajabu kwenye mwili wangu nab ado mnaendelea kumtaja huyo mtu katika masikio yangu. Yani nyie watoto hapana aisee”

    Basi akaondoka zake, na kubaki Erick na Tumaini, kwakweli Erick alianza kulalamika,

    “Yani huyu mzee ndio cha kuniitia hiki upesi upesi jamani, aliona wapi kuna harusi ya kulazimishana hivi eti kesho tunaenda kwa Mchungaji kuzungumzia ndoa jamani, huyu mzee ndiomana alikurupuka kwenda kwakina Erica bila kujitambulisha kwanza, hajafuata mila wala kitu gani yeye anajipeleka tu kuchukua mke, tuseme tatizo ni kutokuwahi kuoa au kachanganyikiwa tu jamani!”

    “Usiseme kwa nguvu Erick, ila wewe cha kumkomesha baba kesho nenda nae huko Kanisani halafu Mchungaji akiuliza unagoma kabisa kwamba kuoa hutaki ili asiandikishe hiyo ndoa”

    “Tumaini, siendi cha Kanisani wala nini kujisumbua, kwanza kesho nimepanga kwenda kutembea na kipenzi cha moyo wangu. Huyu mzee wakati wake umepita, hivi sikukuuliza mama yako ulivyomwambia habari za huyu mzee kutaka kumuoa Erica alisemaje?”

    “Jamani mama kacheka balaa, kasema huyu mzee ujana wake wote alikuwa wapi kuoa. Eti anakumbuka shuka wakati kumeshakucha”

    “Na shuka lenyewe tushajifunika wengine, halafu akasema nini kuhusu mchumba ambaye mimi namtaka na baba anamtaka”

    Basi Tumaini akaanza kumuelezea Erick jinsi mama yake alivyosema kwa kicheko kikubwa sana.

    “Kwahiyo mamako angekuwa mimi angeoa bila kujali!”

    “Yani kasema angeoa kumkomesha, yani mama yangu kacheka sana. Yani sijui baba alimfanyaga nini mama kwenye ujana wake maana anavyomsemaga vibaya balaa. Ila hata mamako Erick huwa hampendi baba”

    “Ni kweli hampendi tena hampendi kabisa, tena umenikumbusha jambo. Mama si anamchukia Erica, nikitaka ampende nitamwambia hili swala la baba kutaka kumuoa Erica, subiri arudi tu nimwambie najua kwajinsi mama anavyomchukia baba basi atafanya kila jitihada ili mimi na Erica tuoane”

    “Huyu baba sijui ana matatizo gani, sio kitu cha kawaida kwa mama zetu wote kumchukia lazima kuna kitu kibaya aliwatenda”

    “Tena mama yangu ndio zaidi maana inaonyesha hata hamu ya kuolewa tena hakuwa nayo ndiomana hadi leo nipo mwenyewe. Ngoja arudi nimwambie habari hizi, huyu mzee tutaona hiyo presha yake.”

    Wakacheka sana pale ndani maana kwa kipindi hiko Erick na dada yake Tumaini walipatana vilivyo.



    Erica kabla ya kulala alifikiria jambo, akaona ni vyema ampigie simu Dora kwani yale maneno ya Erick kuwa akigundua babake ana mahusiano na Dora basi atamuoa haraka iwezekanavyo, kwahiyo kuliko mimba igundulike wakati yupo nyumbani aliona ni vyema amwambie Dora afanye jambo na mzee Jimmy agundulike kwa watoto wake ili Erick amuoe kwa haraka.

    Basi alipiga simu muda huo na Dora alipokea simu ile,

    “Niambie Erica, kuna jipya leo maana siku hizi hunipigii simu?”

    “Aaah Dora, nisaidie familia yam zee Jimmy ijue ukweli maana wanahisi kuwa ni mimi ndiye nilikuwa na mahusiano na mzee Jimmy. Nisaidie wajue kuwa ni wewe”

    “Nimewaambia ila wananibishia, sema subiri kuna bomu nimeliandaa yani hilo mzee Jimmy hachomoki kabisa, nitahakikisha hao watoto wake wanaomtetea wanaona mambo ambayo baba yao huyatenda. Tena kuna dada huyo ndio alikuwa anatembea na mzee Jimmy, nimemjua pia si unajua mimi ni kama mpelelezi”

    “Nakuaminia Dora, yani huyu mzee ananipa mawazo sana kwakweli”

    “Punguza presha rafiki yangu, ile milioni kumi huwa siisahau hadi kesho kwahiyo kuwa mpole tu ndugu yangu yani hivi karibuni huyo mzee ataumbuka”

    Erica alifurahi sana kusikia hivyo na kuagana na rafika ila akakumbuka kuhusu habari za mdogo wake Dora ilibidi amuulizie pia,

    “Vipi Steve nae?”

    “Weee yani Yule ndio haoni wala hasikii, tulikuwa nae hapa siku zote kapooza hatari maana kaambiwa na Sia kuwa atafute kazi kwanza ila leo hajakubali kaenda hivyo hivyo jamani huyu mtu ataanza hadi kuniibia hela zangu ndani apelike kwa Sia. Najuta na habari za waganga jamani dah! Usiniulize sana ila ndio hivyo najuta, kwaheri Erica ngoja nilale tu”

    Basi Erica alikata simu ila alifurahi kuongea na Dora maana wale walikuwa wanamkosesha raha sana. Akaamua kulala sasa.

    Palivyokucha aliwasiliana na Erick kuwa ajiandae anaenda kumchukua, alishangaa kuona ni mapema vile, alimuandaa na mwanae na kumwambia mama yake kuwa anaenda kliniki, hakutaka kumwambia ukweli muda ule maana alijua wazi kuwa ni lazima angemrudisha kuwa asiende popote. Alipanga badae ndio ampigie simu kuwa atachelewa kurudi.

    Basi Erick alivyofika karibu na kwao, aliaga vizuri na kutoka na mwanae kisha Erick alipanda nae kwenye gari na kuondoka zao.

    Na moja kwa moja walienda kwenye hoteli ambayo ilikuwa na michezo mbalimbali ya watoto ili kumfurahisha Angel.



    Mzee Jimmy aliamka na kujiandaa vizuri kabisa kwaajili ya kutoka na Erick wampitie na Sian a waende Kanisani, alishangaa alimuita bila kuitikiwa ikabidi amuite Tumaini na kumuuliza,

    “Katoka asubuhi sana, sijui kaenda wapi”

    “Mtoto mjinga sana huyu, yani tunapanga hivi halafu anafanya vile”

    Basi Mzee Jimmy akaondoka zake na moja kwa moja alienda kwakina Sia, alivyofika alimkuta Steve yupo nje akiosha vyombo ila kabla hajaongea nae vizuri alitoka Sian a kumsalimia Yule mzee ambapo aliulizia kuhusu Yule kijana,

    “Ni mdogo wangu huyu”

    “Aaah! Sawa basi njoo kidogo tuongee”

    Sia akasogea pembeni na Mzee Jimmy ambapo Mzee Jimmy alimueleza lengo lake la kutaka yeye na Erick waoane na kutaka siku hiyo waende kwa Mchungaji ili kusaini kuhusu ndoa yao.

    “Tulipanga vizuri ila Erick leo kaondoka asubuhi kabisa jamani, yani akjifanya kusahau kama nimepanga nae kuhusu hili swala”

    “Dah yani Erick anachanganywa sana na Erica Yule anasahau kuwa mimi ndiye mwenye mimba yake halali”

    “Kwani Erica nae ana mimba?”

    “Ndio, Erica ana mimba sasa nadhani Erica kamdanganya Erick kuwa ile mimba ni yake ndiomana kamchanganya akili. Erick anaacha kuhudumia mimba yake ya halali huku anaenda kuhudumia mimba feki”

    Yule mzee alianza kuondoka bila hata kuaga mpaka Sia alishangaa ila kilichomfanya aondoke vile ni kwamba swala la kusema kuwa Erica ana mimba lilimchanganya sana.



    Baada ya mama yake Rahim kuambiwa na Rahim kuhusu Zainabu aliamua kumuita Zainabu ili kuongea nae, na kiukweli alivyofika Zainabu alijikuta nay eye akimpenda Yule binti na alihisi huenda akamfaa mtoto wake zaidi na jinsi alivyokuwa anaongea na Zainabu alimuhisi kuwa ni binti mwenye busara sana,

    “Hongera Zainabu, sijawahi kuzaa mtoto wa kike ila wewe umelelewa haswaa yani wazazi wako inaonyesha wanajivunia uwepo wako”

    Zainabu alikuwa akitabasamu tu, Neema nae alikuwa mule ndani kwahiyo akaongezea,

    “Ni kweli Zainabu ni binti mpole na mcheshi sana ingawa binadamu hawakosi maneno huwa wanasema kama mzuri mbona haolewi”

    Basi Mrs.Peter akachangia hapo,

    “Yani watu bhana, kwani ambao hawajaolewa ni wabaya jamani! Huwa muda haujafika tu. Kwani Zainabu una umri gani?”

    “Nina miaka thelathini na tatu”

    “Una mtoto?”

    “Hapana”

    “Miaka thelethini na tatu, hujaolewa na huna mtoto yani hujazalia nyumbani mmh wewe ni binti wa kuigwa kwakweli. Zainabu tafadhali uwe mkwe wangu nakuomba, nakuomba sana uolewe na mwanangu”

    Zainabu akauliza,

    “Mfano ningekuwa na watoto je?”

    “Hata ungekuwa na watoto bado ningekuomba hili maana busara yako nimeipenda, nakuomba ukubali kuwa mke wa mwanangu”

    Gafla mlango wa pale ndani ulifunguliwa na aliyeingia alikuwa ni Salma kumbe alikuja kusalimia siku hiyo, ila kitendo cha kumuona Zainabu ndani kwa mkwe wake kilimchukiza sana, alijikuta akimuweka mwanae pembeni na kusema,

    “Nilijua tu kuwa wewe mwanamke huna jema kwangu muone vile. Kujifanya umeshika dini huku unavizia waume za watu”

    Kisha akamsogelea karibu Zainabu na kumkunja ili apigane nae huku maneno ya ajabu ajabu yakiendelea kumtoka mdomoni.



    Nasma alivyoona Bahati harudi nyumbani kabisa aliamua kuaita washauri ambao walimshauri Bahati ili arudi nyumbani, Bahati alirudi kwake ila kwa shingo upande sana yani hakutaka kurudi kwake maana hakutaka kurudi pale wakati mkwe wake yupo.

    Basi siku ya leo, Nasma alikuwa ameenda kununua mahitaji ya nyumbani na ndani alibaki mamake pamoja na Bahati basi Yule mama alienda chumbani kwake kujipumzisha kidogo baada ya mjukuu wake kuwa amelala.

    Alishangaa bahati kuingia mule chumbani, alimuuliza kwa mshangao,

    “Mwanangu umeingia bila hodi?”

    “Nimeshindwa kuvumilia”

    “Umeshindwa nini?”

    Bahati alimvamia huyu mama na kutumia nguvu na kumbaka sababu huyu mama hakuwa na nguvu za kumzidi Bahati na alipomaliza tu kumbaka mama mkwe wake alitoka pale ndani na kukutana na Nasma mlangoni akiwa anaingia ndani.

    Alimkuta mama yake analia, alimuuliza kuwa tatizo ni nini,

    “Nasma, mumeo kanibaka”

    “Kheee kakubaka!”

    “Yani mimi madawa yenu niliwakataza, hebu ona nilivyodhalilika”

    Muda huo alifika dada yake Bahati pia, na kugonga mlango bila kufunguliwa aliamua tu kufungua na kuingia ndani. Alimkuta Nasma akimbembeleza mama yake huku mama yake akielezea jinsi alivyobakwa na Bahati.

    Dadake akashtuka na kusema,

    “Kheeee kumbe Bahati katimiza kweli hilo swala la kubaka?”

    Wakashangaa kuwa kumbe Bahati alipanga, Nasma alimfata kwa hasira dada yake Bahati na kumwambia

    “Kumbe mliyajua yote haya ila mliacha ili mama abakwe jamani! Sio utu kabisa”

    “Ila mlichofanya nyie cha kumtia kaka yangu uchizi na madawa ndio vizuri! Hujui kama madawa yako ndio yamesababisha yote hayo, mwambie baba yako amtolee ndugu yetu madawa hayo la sivyo na yeye atabakwa”

    Nasma akachukia sana na kuanza kupigana na huyu dada wa bahati sema kwavile huyu dada ni ana nguvu sana ni alimbamiza Namsa hadi akaanguka chini na kuzimia.



    Mzee Jimmy hakufurahishwa kabisa na habari ya kusema Erica ana mimba basi aliamua moja kwa moja kwenda kwakina Erica, ambapo aliyemfungulia mlango alikuwa mama Erica mwenyewe,

    “Haya wewe mzee usiyekuwa na haya umefata nini leo? Si ulizimia wewe! Kumbe hukufa eeeh na mke bado unamfatilia”

    “Nimfatilie mwanao wa kazi gani? Ila mwambie mwanao maswala ya kumsingizi mwanangu mimba sio mazuri”

    “Mimba gani aliyomsingizia?”

    “Mimba ambayo mwanao anayo sasa, kashaanza kumsingizia mwanangu wakati ana wanaume wengi”

    Mama Erica alishangaa kwanza na kuuliza kwa makini,

    “Erica ana mimba?”

    “Ndio Erica ana mimba”

    Mama huyu alihisi kama kizunguzungu.







    Mama Erica alishangaa kwanza na kuuliza kwa makini,

    “Erica ana mimba?”

    “Ndio Erica ana mimba”

    Mama huyu alihisi kama kizunguzungu.

    Ni Bite alitokea nyuma yake na kumshika mama yake, kisha kumwambia Yule mzee aondoke zake, yani huyu mama aliingia ndani kwa kushikiliwa na Bite ni wazi alipata mawazo sana, hakutegemea kama mwanae kapata maamuzi ya kuzalia watoto wawili nyumbani yani alijihisi vibaya sana, alikaa chini na kuwa kimya kwa muda kidogo kisha alipopuma akaanza kuongea,

    “Hivi huyu mtoto ananitakia nini mimi jamani? Anataka kunifanya nini Erica? Kila siku naimba wimbo hapa asibebe mimba kumbe ananicheka kuwa utaona jamani! Kuzaa imekuwa shida eeeh! Bite, sikuwazaa nje ya ndoa nyie, iweje mwanangu awe mtu asiyejielewa, ni mapenzi gani anayoyaendekeza yeye jamani!”

    “Mama, punguza jazba”

    “Siwezi Bite, yani siwezi kwakweli. Nimemkubali Angel kama mjukuu wangu ila Erica hathamini kujua ni aibu gani mama yake naipata mtaani, kuishi na mtoto kisiri siri hata unatoka nae unajua kabisa utasemwa ila upo tu, na mtaani walishaanza kusema kuwa tumeleta mtoto wa kiarabu na wanacheka balaa, halafu leo aonekane na mimba nyingine jamani! Hivi jamii itaniangaliaje mimi, watu watanitazamaje, itaonekana sijui kulea kabisa jamani, mbona dada zake hampo hivyo, huyu Erica ni mapenzi gani yanayomsumbua yeye hadi anakuwa hivyo?”

    “Mama, angalia afya yako, usiongee sana ukapata presha. Tumsubiri huyo Erica arudi na tumuulize pengine ni uongo”

    “Sidhani kama ni uongo”

    Kisha mama yao akainuka na kwenda chumbani kwa Erica kupekua na kwa bahati nzuri au mbaya, akakiona kile cheti cha hospitali ambacho kinaonyesha kuwa Erica ni mjamzito, yani hapo ndio alihisi presha kupanda zaidi, Bite alipata kazi ya kumtuliza tu mama yao na alipoona kuwa inakuwa ni ngumu aliamua kumpigia simu Mage ili kumueleza na Mage aende nyumbani.

    “Unasema Erica mjamzito? Kasema mwenyewe au nani kawapa hizo habari?”

    “Ndio mjamzito na mama kachanganyikiwa kabisa maana habari hizo kuzipokea kwake imekuwa ngumu si unajua ni swala la aibu! Yule mzee wake alifika hapa na kusema huo ujinga wa Erica”

    “Huyu mtoto anatia aibu kwakweli, mara nyingine bora angekuwa mbuzi tu tungekunywa supu yake kuliko kwa mambo anayoyafanya. Kachanganya ndugu weee kaona haitoshi, katembea na kaka yake, haitoshi, kaenda kutembea na baba na mwana haitoshi, kazaa nyumbani bado haitoshi na sasa kuleta mimba nyingine nyumbani kweli! Si bora hela ya kumsomesha mjomba angetugaia tu tujilie zetu raha kuliko kusomesha kichaa kama Erica jamani! Jitu linakatazwa kufanya mapenzi bado tu yumo, ni hamu gani alizonazo yeye anayeshindwa kuzizuia! Nimechukia sana, nakuja huko hata kama muda umeenda nakuja. Kwanza yuko wapi?”

    “Unafikiri yupo nyumbani basi! Asubuhi asubuhi kamvalisha Angel kamdanganya mama kuwa anaenda kliniki, alipoondoka badae kapiga simu kuwa atachelewa kurudi na mpaka mida hii yani saa mbili usiku saivi hajarudi, kashindikana Yule”

    “Nakuja huko”

    Akakata simu na kuendelea kumbembeleza mama yao pale,

    “Mama, Mage kasema anakuja pia kwahiyo mama shusha presha. Huyu Erica safari hii hata ndoa ya mkeka tutamfungisha kwakweli maana si kwa aibu hii anayotutia”

    “Nakwambia Bite, sijawahi kumpiga Erica toka akue maana neno nisamehe ndio humtoka upesi kuliko maneno yote ila leo hata aseme nisamehe mara mia nitampiga tu, yani leo nitampiga sana mpaka akili imkae sawa”

    “Sasa mama, ukimpiga hivyo na mjamzito si mimba itatoka?”

    “Na itoke tu, asiniletee ujinga nyumbani kwangu”

    Bite alielewa kuwa mama yake ana hasira sana na anaongea yote yale sababu ya hasira maana alichukizwa vilivyo kwa kilichotokea nyumbani kwake, walikaa wakimngoja kwa hamu huyo Erica arudi.



    Nyumbani kwakina Rahim, yani mrs.Peter alichukizwa sana na kitendo cha Salma kumparamia Zainabu ili apigane nae mpaka ilibidi waamulie tu huku Neema akimshika Salma ila Salma aliendelea kuongea maneno ya ajabu,

    “Na wewe Neema hebu niache, mwanamke una roho mbaya wewe kama mchawi muone vile. Ndiomana kutwa kucha kujifanya unanifundisha jinsi ya kuishi na mume kumbe unanionea wivu na unataka kumleta mtu wa kunirithi, mwanamke una roho mbaya wewe niachie”

    Alipoona Neema hamwachii alimng’ata mkono ili amuachie ilibidi Neema amuachie na kuelekea tena kwa Zainabu ila Zainabu alitulia tu kumuangalia Yule binti akimparamia mwilini, Mrs.Peter alishindwa kuamulia na kuamua kwenda kumuita Rahim.

    Zainabu alipoona Salma anazidi kumsumbua alimshika mikono na kumnasa vibao, yani kitendo kile ndio kama kilimtia ukichaa Salma maana alijikuta akianza kutupa vitu vya kwenye nyumba ya mama mkwe wake bila kujali ni vitu vya kwa mama mke.

    Basi Rahim na John walifika na siku hiyo alikuwepo Babuu ambaye alikuwa akiongea na Rahim, walipoingia ndani kile kitendo cha Salma kiliwachukiza sana yani walichukia mno, Rahim alienda kumshika Salma na kutaka kumpiga sana ila ndugu zake wakamzuia kuwa asifanye hivyo, basi alimkalisha chini kwa hasira, kwakweli mrs.Peter aliangalia mule ndani kwake na kusikitika sana kisha akasema,

    “Salma, sikutegemea kama upo hivi kwakweli sikutegemea kabisa kumbe mwanangu alikuwa hakosei kukupiga, mwanangu hakukosea kukupa talaka yani sikutegemea kama tumemuolea Rahim mwanamke chizi kama wewe. (Kisha akamuangalia Zainabu na kumwambia) Zainabu mama hata tusizunguke mbuyu nahitaji sana uwe mke wa mwanangu na kesho tutakuja kwenu kujitambulisha ili kufanya mambo haraka haraka”

    Muda ule ule Salma alianza kulia kama amefiwa vile, kwakweli iliwashangaza sana na mara alinza kusema anacholilia,

    “Mmenipotezea muda wangu kusubiria toto lenu malaya, nimemvumilia kwa kipindi chote kwanza linaumiza balaa ila nimevumilia halafu mananifanyia hivi! Sikujua kama familia hii ina roho mbaya kiasi hiki, na wewe Zainabu yatakukuta tu maana hii sio familia ya kuishi nayo ni makatili hawa”

    Akainuka na kumchukua mwanae halafu akaondoka, hakuna aliyemfata kwani kile kichaa chake hakuna aliyekitaka kwa muda huo kwani alikuwa ashaharibu vya kutosha pale sebleni.



    Mage nae alipokuwa anaenda kwao alijikuta kuwa na hasira sana na mdogo wake na kuamua kumpigia simu kwanza ili kuyabwaga ya moyoni.

    Muda huo, Erick na Erica walikuwa njiani kurudi nyumbani ambapo Angel alikuwa amelala, kwahiyo Erica alipoona kuwa dada yake anapiga simu sana aliamua kupokea ili kujua tatizo ni nini, alipokea na kumsalimia dada yake ila dada yake hakupokea ile salamu na kuanza tu kumshushia maneno,

    “Wewe mtoto usiye na akili hata moja yani kwako moja haikai mbili haisogei, hivi unafikiriaga kwa kutumia nini? Huwa unatumia ubongo wewe au makalio yako ndio yanakutuma kufanya ujinga”

    “Ujinga gani tena dada?”

    “Hivi wewe ni wa kumuaibisha mama kiasi hiki, uzalie Angel nyumbani na bado unabeba mimba nyingine nyumbani”

    “Dada, mbona mimi sina mimba”

    “Huna mimba wapi mjaa laana wewe, wakati zee lako limekuja kusema kuwa una mimba, na mpaka muda huu hujarudi nyumbani ushaanza kumuhangaisha Angel kwa wanaume zako huko, na mimi naenda nyumbani nikukute wewe, urudi muda huu huu nyumbani mjinga wewe”

    Kisha dadake akakta simu na hapo Erica akajua kuwa siri ya mimba yake imefichuka kwao, kwa jinsi alivyokuwa akionge kwa mshangao ilifanya Erick aweke gari pembeni ili amsikilize kuwa tatizo ni nini, alimuona Erica akiinama chini huku akiwa na mawazo tele, alimuuliza

    “Mpenzi, nini tatizo?”

    “Nyumbani wamejua kama nina mimba yani sijui itakuwaje”

    “Kwani kuwa na mimba ni tatizo?”

    “Si tatizo kwa mtu aliyeolewa ila kwa mimi ambaye sijaolewa ni tatizo kubwa sana, unajua mimba ni kielelezo tosha cha uzinzi. Yani ukiwa na mimba huwezi kukataa kuwa hujazini, na mama kila siku ananikataza habari za kuzini, aliniambia mpaka niolewe maana nishamtia aibu kwa Angel. Nilijiapia kufanya hivyo na ndiomana sikutaka hata kutumia uzazi wa mpango sababu nilijua nitaweza kujizuia hadi ndoa”

    “Sasa swala la uzazi wa mpango limekuja vipi hapo? Inamaana Erica hukupenda kuzaa na mimi?”

    “Sio hivyo Erick, yani sijui kama unanielewa mpenzi. Swala ni hivi, nyumbani huko kimewaka moto maana wamejua nina mimba yani leo nahisi mama atanipiga kipigo kisichoelezeka, yani nimechanganyikiwa”

    “Mmmh akikupiga si mimba yangu itatoka? Erica, sitaki itokee ya kipindi kile kutoa mimba yangu”

    “Kwani kipindi kile nilipenda Erick, ila dada zangu ndio walinishikilia bango nitoe ile mimba ili mama asijue yani hospitali na kila kitu walifanya wao. Sasa leo nyumbani, uwiiii sijui nifanyeje”

    Erick akafikiria kidogo na kusema,

    “Erica, hata mimi nahitaji kuwa na damu yangu, nahitaji kupata mtoto kutoka kwako na hata hivyo sihitaji upate matatizo sababu ya starehe zangu. Kuna jambo nawaza hapa, naomba unikubalie”

    “Jambo gani hilo?”

    “Naomba leo usirudi kwenu, tukatafute hoteli ukakae huko kwanza halafu mimi nifanye harakati za kuwasiliana na kwenu kisha tufunge ndoa. Si mama anahitaji uzalie ndani ya ndoa? Basi itawezekana tukifanya hivyo mpenzi au unaonaje? Ila usikatae tafadhali”

    “Erick umeongea jambo jema ila sasa nisiporudi nyumbani si ndio balaa zaidi?”

    “Erica, waswahili husema heri nusu shari kuliko shari kamili, ushasema kwenu wana jazba leo hivi wakikuona si ndio balaa zaidi, kwanza ni Mungu tu kafanya huyu dada yako akupigie simu huku akiwa na hasira hivyo zilizokuchanganya na wewe maana wangeweza wasubiri urudi tu na upate kipigo, ni heri kusubiri hasira zao zipoe kuliko kuchukua maamuzi kwasasa, kubali Erica tafadhali, nami sitaondoka tutakuwa wote hapo hotelini na kesho nitaenda kuwatafutia nguo wewe na Angel, huku tukiendelea kujadili cha kufanya, kwasasa kubali swala hili”

    Erica alifikiria kwa kina na kuwaza akirudi kwao sokomoko atakalokutana nalo, akaona ni bora akubaliane na wazo la Erick tu maana hakuwa na jinsi kwa wakati huo.

    Basi Erick aligeuza gari yake na kuanza kwenda kwenye hoteli ambayo alihisi itawafaa kwa siku kadhaa.



    Mage alifika nyumbani kwao akiwa amechukia sana, na alipogonga na kuingia ndani alishangaa kuambiwa kuwa Erica hajarudi hadi muda huo,

    “Kheee mpaka saa hizi hajarudi? Mtoto ana wazimu huyu si bure, hivi jamani alitoka na nani?”

    Bite akajibu,

    “Nadhani ni kale katahira kenzie, kale ka Erick sijui yani nimejikuta nakachukia kale kavulana. Wanajifanya kutulia hapa wakati mwanamaombi anaomba kumbe anasubiri kwa hamu Erica apone wakafanye uzinzi”

    “Ila mi nilikuwa nawaangalia tu mnavyomuachia Yule kijana na Erica, mi niliwashangaa kwakweli yani mnawaacha utafikiri wanandoa, kijana kutwa kucha yuko hapa, sijui kutafuta hadi madaktari wa kumuhudumia Erica ndio amuoe sasa”

    “Atamuoa waishije unadhani? Huyo Erica si ndio atakuwa mboga ya kwao yani baba na mtoto na jinsi aivyoweza kujitetea mjinga Yule”

    Mama yao ingawa alikuwa na hasira ila kwa muda huo alimtetea kidogo Erica,

    “Jamani, Erica kama hawezi kujitetea basin i huko kwingine ila mkumbuke kuwa Erica alijitetea kwa shemeji yake. Kwa yale majaribu ya James, ingekuwa Erica yupo legelege basi angeshatembea nae jamani. Yote sina habari nayo mimi ila inayoniumiza kichwa ni kwanini abebe tena mimba nje ya ndoa? Yani hapo ndio ninapoumia kichwa”

    Mage na Bite kwa upande mwingine waliona kama mama yao anampendelea sana Erica kwahiyo waliamua kunyamaza kwa muda kwanza kisha Mage akasema,

    “Mama, watoto wako kwasasa tumekuwa na tunapokuja kwenye swala kama hili tuache tuongee ya moyoni, Erica ni mdogo wetu na tuna haki ya kuongea chochote juu yake kwahiyo mama acha tuongee sio kila siku kutukatisha tu. Kumbuka mimi ni mtoto wako wa kwanza yani kifungua tumbo lako ila sijawahi kutenda ujinga kama huu unaofanywa na Erica, inatuuma mama na tuna haki ya kuongea”

    Basi walijadiliana huku wakiendelea kumsubiri Erica, ila waliona saa sita usiku inawafikia pale pale bila ya Erica kurudi nyumbani.

    Muda kidogo walishangaa kuona kuna namba inaita kwenye simu ya mama yake Erica, basi Bite alipokea simu ile kumbe mpigaji alikuwa ni mzee Jimmy, na kuanza kuongea nae,

    “Erica hapokei simu zangu, yuko hapo niongee nae”

    “Hapana hajarudi, labda uniambie mimi mwenyewe”

    “Sasa akirudi mwabieni asiitoe hiyo mimba, anataka amsingizie mwanangu wakati ni mimba yangu. Mwambieni nitamuoa, nilichukia sana ila nitamuoa asiitoe hiyo mimba”

    Kisha akakata simu na Bite alimueleza mama yake ambaye alihisi presha zaidi kuwa licha ya Erica kuwa na mimba ni mimba yam zee asiyempenda kabisa katika maisha yake.



    Erick alikuwa na Erica hotelini na mtoto alikuwa amelala, kiukweli Erica alishindwa kulala kabisa kwani aligubikwa na mawazo sana. Erick alimuuliza,

    “Erica, hupendi hivi tupo pamoja? Furahi bhana, mimi ndio mumeo, na ndoa yetu inanukia sasa maana kipo cha kufanya nikuoe haraka”

    Erica alitabasamu tu kisha Erick alimkumbatia na kuweza kumbembeleza alale.

    Kulipokucha ni Angel alikuwa wa kwanza kuamka na kumsogelea mama yake ambaye aliamka pia, Angel alianza kumdai mama yake uji maana alishazoea akiamka asubuhi basi anakunywa uji yani hilo swala ndio likampa mawazo zaidi Erica na kumuuliza Erick kuwa watafanyaje, ila Erick akaamua kuondoka kidogo na baada ya muda alirudi na uji kwenye chumba na kikombe kwaajili kumuwezesha Angel anywe uji. Kwakweli Erica alifurahi sana na kuona kuwa Erick ana moyo wa upendo na kujali, basi alimmiminia ule uji Angel na kumpoozea kisha kuanza kumnywesha ambapo muda huo Erick alimuaga na kuondoka kwani alitaka akatafute nguo za kubadilisha kwaajili ya Erica na Angel.

    Alivyoondoka Erick tu basi Erica aliendelea kumnywesha uji Angel na alipomaliza alichuua simu yake na kumpigia Dora kwani kwa muda huu alihisi kuwa Dora ndio msaada pekee alionao.

    “Erica, niambie mama yangu nini tena?”

    “Safi tu, nilikuwa nakusalimia”

    “Mmmh salamu tu hiyo Erica au nije kwenu tuongee vizuri”

    “Hapana usije nyumbani ila nitakwambia vizuri badae subiri kidogo”

    Alikata simu kwani alitaka ajipange kwanza ndio aongee na Dora ili aweze kupanga nae mipango, na muda huo Erick aliingia mule ndani kwahiyo hakuweza kuongea nae jambo lolote lile zaidi ya kukata ile simu.

    Erick alikuwa amewaletea nguo Erica na Angel ili wakioga wapate za kubadilisha kisha alimuachia hela pale na kumuaga,

    “Naenda nyumbani mara moja Erica maana kuna kitu nawaza”

    “Kitu gani Erick?”

    “Nitakwambia tu, ila ngoja niende nyumbani mara moja si unajua uamuzi huu tumeuchukua kwa muda mfupi!”

    Erica alimuelewa na kukubaliana nae, basi Erick aliondoka na kwenda nyumbani kwao.



    Mzee Jimmy alichukia sana nyumbani vile kijana wake hakurudi kabisa, aliona Erick kaanza kutokuwa na heshima kabisa, ingawa siku za nyuma ilikuwa ni kawaida kwa Erick kukaa hata wiki bila kurudi kwao na hakuna aliyekuwa akimfatilia ila siku hiyo alionekana kuchukizwa sana na swala la Erick kulala nje ya nyumba yao.

    Ile asubuhi alimuita Tumaini na kuongea nae,

    “Huyu mdogo wako kaanza tabia gani ya kulala mbali na nyumbani?”

    “Ila baba, Erick ndio zake yani hii sio mara ya kwanza ni kawaida yake. Anaweza kukaa hata wiki hajarudi nyumbani”

    “Huwa anafanya huo ujinga wakati mimi nipo wapi?”

    “Baba, ulikuwa unarudi usiku na kulala hata hatuonani kwahiyo Erick alikuwa halali hapa na wala hugundui”

    “Sawa nimekubali nilikuwa siwaangalii ila huu anaoufanya kaka yako ni upuuzi na akirudi mwambie nimegundua habari za mimba ya Erica, mwambie kaka yako akae mbali na Erica maana kwa vyovyote vile atamuoa Sia nimemaliza”

    Baba yao muda huo akatoka na kuondoka ila muda sio mrefu sana alifika Erick na kumkuta dada yake Tumaini akiwa anajiandaa pia kutoka na baada ya salamu alimueleza kile ambacho baba yake amesema,

    “Aaah Tumaini achana na hayo maneno ya baba ila kuna jambo lingine limetokea bhana”

    “Jambo gani tena?”

    Bali Erick alianza kumueleza dada yake kwa kifupi jinsi ilivyokuwa,

    “Kheee kwahiyo balaa kwakina Erica na mimba ya Erica!”

    “Ndio hivyo, kwahiyo jana tumelala hotelini maana nimeshindwa hata kumrudisha kwao”

    “Mmmh na bora mmejihami uwiii mamake Erica ana nguvu balaa, Yule mama angewachakaza. Mimi aliwahi kunipiga vibao hivyo huwa sivisahau hadi leo maana hadi nilihisi kizunguzungu na mbele sioni, weee mama ni noma Yule”

    “Sasa mimi nilitaka niende kwao ili nijaribu kuongea na mama yake na kuomba msamaha”

    “Erick, hujipendi mdogo wangu yani Yule mama muone vile vile, ana nguvu jamani balaa nakwambia mimi nilipigwa vibao tu ila nilijihisi kizunguzungu halafu wewe uliyemtia mimba binti yake ndio ukajifanye kuongea nae mmmh utachakazwa mdogo wangu tukusahau maana najua kumrudishia mama mkwe unaanzaje. Yani tafuta tu njia nyingine”

    “Njia gani sasa?”

    “Tafuta wazee wa busara wakaongee na wazazi wa Erica, yani tafuta kama washenga”

    “Sasa washenga bila baba itakuwaje?”

    “Yani hapa ndio kwenye mtihani mkubwa ila mdogo wangu ndoja tufikirie cha kufanya yani usiende kabisa kwakina Erica, nakupenda mdogo wangu Yule mama namfahamu sijui ujana wake alikuwaje, ana nguvu sana Yule mama”

    Basi alikubaliana na dada yake huku akimuelekeza chumba walichopo kwenye hiyo hoteli ili hata kama akimtafuta ajue ni wapi pa kumpata kisha akachukua baadhi ya nguo zake ili aende kuzipeleka kule hotelini maana aliona ndio njia pekee kwa kipindi hiko kuishi na Erica tu.



    Familia ya Erica kiukweli walizidi kuchukizwa na kitendo cha erica kutokurudi nyumbani kwao, na vile Mage alisema kuwa alimuuliza wakajua ndio sababu kuwa huenda Erica ameogopa kurudi nyumbani,

    “Erica anasahau kuwa laana ya mzazi ni kubwa sana maana nahisi hela za Yule mvulana ndio zimemzuzua mama mpaka hajarudi hadi leo”

    Muda kidogo kuna mtu aligonga, walipomfungulia na kuingia ndani alikuwa ni Dora maana hakuelewa ni kwanini Erica kamwambia kuwa asiende kwao nay eye alienda tu akiamini huenda rafiki yake ana matatizo, ila alikuta pale kwao tofauti kwani mamake Erica alianza kwa kumbana Dora kuwa Erica yuko wapi,

    “Sijui mama ila asubuhi nimeongea nae kuwa yuko salama, nikamuuliza nije kwenu akakataa yani mimi sijui lolote. Kwani imekuwaje?”

    “Imekuwaje nini si mnajifanya mnafichiana siri, mwenzio ana mimba ya Yule mzee”

    “Erica ana mimba?”

    “Unashangaa nini sasa, kwani ndio mara ya kwanza kwa Erica kubeba mimba?”

    “Hapana ila nimeshangaa tu ila hiyo mimba haiwezi kuwa ya mzee Jimmy, kama amejisifia hivyo mjue ni muongo. Hiyo mimba itakuwa ya Erick tu ila imekuwaje, nani kaleta hizi habari?”

    “Imekuwaje kuhusu nini? Mzee wenu kaja hapa na kasema kuwa Erica ana mimba yake”

    Dora alishangaa tu ila akaona kuwa huyu mzee kawalaghai hawa watu.

    “Kwahiyo Erica yuko wapi?”

    “Sijui mwenyewe”

    Basi Dora aliamua kuondoka tu pale kwakina Erica ila kitendo cha mzee Jimmy kusema kuwa mimba ya Erica ni yake hakukipenda kabisa.

    Alipofika kituoni aliamua kumpigia simu Erica ili kumuuliza vizuri alipo na kumwambia kuwa ametokea nyumbani kwao,

    “Ila Dora, si nilikwambia kuwa usiende nyumbani!”

    “Ni kweli uliniambia Erica ila sikujua ni nini kimekupata, niambie ulipo nije nikueleze na yaliyonikuta nyumbani kwenu.”

    Basi Erica akamtajia hoteli aliyokuwepo na baada ya muda tu Dora alifika kwenye ile hoteli na kwenda kukaa nae kwenye bustani ya ile hoteli wakinywa vinywaji na kuzungumza ambapo Dora alimueleza rafiki yake kitu ambacho kilijiri nyumbani kwao, basi Erica naye alimwambia uamuzi ambao yeye na Erick wameuchukua, basi Dora alianza kumshauri Erica pale,

    “Sasa Erica nikushauri kitu rafiki yangu”

    “Nishauri”

    “Kwa nionavyo ni kuwa Erick anakupenda sana, na kama anakupenda basi hii ndio nafasi ya kutimiza lile mlilokuwa mkilihitaji kwa muda mrefu sana. Ili mradi mmeshaamua hadi kukaa hotelini bila kurudi nyumbani basi ndio ujue maisha yako mapya yameanza hapo, sasa kuishi hotelini siku zote itawagharimu sana kwanza kumbuka mnaenda kuwa na familia, kuna mtoto huyu na huyo anayekuja kwahiyo lazima muwe makini kwanza”

    “Eeeeh tufanyeje?”

    “Mshauri Erick mkapange chumba, yani huko mtapata zaidi akili ya maisha kuliko kuishi hotelini maana hakuna mtakachofanya. Pangeni chumba na muanze kupanga maisha yenu, Erick hela anayo kwahiyo hapo kitu kinawezekana tu. Tafuteni nyumba ya kuishi, hela ipo kwahiyo mtapata kiurahisi halafu mnanunua vyombo vya ndani na kitanda na godoro yani taratibu mnaanza kupika na kuishi wenyewe hadi mnakuja kuoana mpo vizuri kuliko kuishi hotelini hadi ndoa maana kwasasa huwezi kurudi kwenu na kuishi kama zamani yani ukithubutu kurudi itakucost sana, kwahiyo fanya hivyo rafiki yangu.”

    “Unajua sijawahi kufikiria kuwa Dora unaweza kuwa na ushauri mzuri kama huo, kwakweli leo nimeshangaa sana. Asante kwa huo ushauri na nitaufanyia kazi”

    “Erica bhana, unahisi mimi ni wa kuongea pumba tu muda wote, kuna muda nina ya maana pia. Kwa maelezo yako uliyowahi kuniambia ni kuwa penzi lako na Erick lina vikwazo sana nah ii ndio njia pekee ya kuepeka hivyo vikwazo, muishi pamoja huku mipango ya ndoa ikiendelea”

    “Asante sana”

    “Halafu leo nita kusurprise rafiki yangu”

    “Na nini tena?”

    “Subiri tu utaona, si upo hapa hotelini? Subiri utaona”

    Erica alicheka sababu hakujua kuwa rafikia yake anaongelea kitu gani kisha Dora akamuaga Erica pale na kuondoka zake.



    Erica alirudi chumbani ila ushauri wa Dora ulimuingia vilivyo, Erick alirudi na kufurahi nae sana kisha Erick alimueleza jinsi alivyoongea na Tumaini kuhusu baba yao alichosema huku akiendelea kusema,

    “Ila Yule mzee ana wazimu sana, jana usiku nilikuwa naona anapiga simu yako nikawa naikata yani Yule mzee bhana loh! Anaacha kuoa wazee wenzie anaanza kuibuka na vijana kweli?”

    Erica aliachana na habari za mzee Jimmy na kuanza kumwambia ushauri Erick ambao alipewa na Dora ila hakumwambia kuwa Dora ndio amempa ushauri huo, Erick alitabasamu na kusema,

    “Hakika nimepata mke mwenye akili sana, yani licha ya uzuri wako Erica ila bado una akili sana. Asante Mungu, kwakweli dah sijaamini kama ungeongea maneno ya akili kiasi hiko, ni kweli tutakuwa tunatumia gharama kubwa sana hapa hotelini wakati hii pesa tungeanzisha maisha yetu tu tufike mbali, dah mke wangu una akili sana. Nafurahi kukupata katika maisha yangu yani kesho tutakuwa tumepata nyumba ya kuanza na maisha yetu, Erica wewe ni mke bora katika wanawake wote duniani”

    Erica alitabasamu na kufurahi sana kwani alikuwa anajua kuwa lile wazo kapewa na Dora ila yeye kafanya kama kalileta yeye.

    Muda ule ule Erick alianza kuwasiliana na madalali kuhusu kupata nyumba maana baada ya lile wazo la Erica alitaka kesho yake wawe wameshaanza hayo maisha.

    Basi kuna dalali muda ule ule alimuambia kuwa aende kuangalia mahali kwahiyo aliondoka na Erica pale na kumbeba Angel.

    Walifika na kuonyeshwa nyumba hiyo, kwa hakika Erica aliipenda ile nyumba hata kutamani tu kuanza kuishi siku hiyo ila Erick alitaka watu waifanyie kwanza usafi na wao kwenda kesho,

    “Erick jamani, usafi gani wa hadi watu wafanye? Si nitafanya mwenyewe!”

    “Hebu acha zako Erica, unajua hali yako kabisa halafu unataka kufanya usafi, acha wafanye na kesho nitaagiza watu wa kutusaidia kuchukua vitu na kupanga ndani humu ila kwa leo acha wafanye usafi.”

    “Mmmh sawa, hakuna shida”

    “Sitaki uhangaike Erica hata kupanga napo ni kukuhangaisha tu ila sitaki upate manyanyaso yani nitajitahidi nijenge tu nyumba yangu maana sitaki baba atunyanyase kwa nyumba zake ingawa najua ana nyumba nyingi tu tungemwambia angetugaia moja”

    Basi wakaongea ongea kule na kusimamia simamia vijana wa usafi, walipomaliza walianza kuondoka.

    Njiani Erick alipitia sheli kuweka mafuta kwenye gari yake, wakati wanamuwekea mafuta pale sheli kumbe alikuwepo na James ambaye aliwaona Erica na mtoto wake kwenye gari ya Erick, alishuka na kuwafata, wakiwa ndani ya gari aliwagongea kioo ambacho Erica alifungua, kisha James alimuuliza,

    “Kwenu wanajua?”

    “Wanajua kuhusu nini?”

    “Msichana unapenda wanaume wenye hela wewe, nadhani ulikuwa unatamani sana shemeji yako nikuoe”

    Erica alimuangalia Erick na kumwambia kuwa Erick aondoe gari kwani hakutaka kabisa kuongea na Yule James. Kiukweli Erick hakupendezwa na kauli za Yule James na walipofika hotelini alitaka Erica amueleze vizuri ambapo Erica alimueleza kila kitu ila muda ule ule ujumbe uliinbgia kwenye simu ya Erica, na Erick aliichukua na kuusoma,

    “Nimekumbuka sana utamu wako Erica, by James”

    Erica pia alichukia ila kabla hajasema chochote alishangaa mtu kugonga mlango wao, Erick aliinuka na kwenda kufungua akashangaa ni Tumaini ameingia,

    “Kheee Tumaini umekuja kufanya nini?”

    “Kuna habari nimepata Erick?”

    “Habari gani?”

    “Twende”

    Erick alitoka na kufatana na Tumaini, kuna mlango wa chumba kwenye ile hoteli wakagonga na akatokea mwanamke kuwafungulia, Erick alishangaa sana kwani mwanamke huyo alikuwa ni Dora na kuwakaribisha huku kajifunga taulo, walipoingia walishangaa zaidi kuona baba yao akitoka bafuni na taulo.





    Erick alitoka na kufatana na Tumaini, kuna mlango wa chumba kwenye ile hoteli wakagonga na akatokea mwanamke kuwafungulia, Erick alishangaa sana kwani mwanamke huyo alikuwa ni Dora na kuwakaribisha huku kajifunga taulo, walipoingia walishangaa zaidi kuona baba yao akitoka bafuni na taulo.

    Ila mzee Jimmy wala hakuwa na habari kabisa kama kuna watu wameingia mule ndani, kisha Dora akaenda nyuma yake na kumbusu ambapo huyu mzee alianza pia kumbusu yani yale matendo watoto wake walikuwa wakiyashuhudia kwa macho yao, si Erick wala Tumaini walioweza kuendelea kumtazama baba yao, yani walitoka muda huo huo na kubamiza mlango, mzee Jimmy alishtuka na kumuuliza Dora,

    “Inamaana hukufunga mlango?”

    “Aaah kuna muhudumu alikuja kuchukua vitu humu”

    “Jamani Dora kwahiyo katuona?”

    “Hata akituona tatizo liko wapi, nilishindwa kujizuia kukuona ukitoka chooni yani nikajikuta nakutamani zaidi ndiomana nikaja nyuma yako upesi hata sikujali kuhusu muhudumu ila ngoja nikaufunge sasa”

    Kisha Dora akainuka na kwenda kuufunga mlango kwa funguo za pale mlangoni halafu wakaaendelea na mambo yao sasa ila mzee Jimmy hakujua lolote kama watoto wake wamemshuhudia.



    Erick na Tumaini walirudi kwenye kile chumba ambacho yupo Erica maana hakufatana nao, kwakweli Erick alikuwa na hasira zaidi kuona baba yake akiwa na Dora, alikuwa na hasira kiasi cha kumwagikwa na machozi, Erica alikuwa akimbembeleza bila kujua nini kimetokea, Tumaini alikaa chini akimtuliza mdogo wake,

    “Hebu Erick acha hasira hizo ndugu yangu?”

    Erica akauliza,

    “Kwani nini kimetokea?”

    Basi Tumaini akaanza kumuelezea,

    “Unajua Dora nilikutana nae leo akaniambia kuwa anataka kunihakikishia kuwa anatoka na baba yangu, nikamwambia ni uongo maana baba hawezi kuwa nae. Sasa nikiwa nyumbani Dora akanipigia simu kuwa nifike hoteli hii akanitajia na chumba ambacho yupo, nilijua masikhara na kwavile Erick aliniambia pia chumba mlichofikia ndiomana nilikuja moja kwa moja na kuwagongea kwanza kisha ndio tukaenda kwenye kile chumba, jamani kwa macho yetu tumemshuhudia baba na Dora ila baba hajatuona maana alitoka bafuni kuoga, halafu Yule rafiki yako mshenzi sana yani ili kutuhakikishia kaenda kumbusu baba na kuanza kulambana nae midomo”

    Erica akaelewa kuwa ndio ile surprise ambayo Dora alimwambia kuwa atamfanyia, kwakweli alizishangazwa sana na akili za Dora maana huwa anazijua mwenyewe, basi Tumaini alimtuliza kaka yake pale, ambapo Erick alikuwa akiongea kwa hasira,

    “Baba, katuaibisha sana, yani kweli kabisa baba yetu wa kutembea na Dora! Si aibu hii! Hivi ni nani hamjui Dora alivyo jamani, kweli baba atembee na Dora loh!”

    Tumaini akamwambia kaka yake,

    “Sasa na wewe Erick una vituko loh! Ni kweli baba katudhalilisha kuwa na Dora, sasa baba anavyomng’ang’ania Erica je huoni kama hiyo ni zaidi ya kudhalilishwa? Yani mwanamke umtake wewe halafu baba nae amtake mmh ni hatari ujue”

    Erick alinyamaza kwa maneno yale ya dada yake maana akifikiria anaona ni kweli, aibu ambayo baba yao kawaonyesha na kuwa na Dora ni zaidi ya aibu ile ya kutaka kuwa na Erica, ilibidi awe mpole na kuanza kupanga na ndugu yake pale.

    Erica aliamua awe pembeni tu maana hakutaka kuingilia mipango ya ndugu asije onekana ana kiherehere bure, Tumaini akaanza kumwambia ndugu yake,

    “Sasa Erick cha kufanya, mimi leo siondoki hapa ila nitamtumia ujumbe Dora kuwa akimalizana na baba yetu atuambie yani wakiwa wanataka kutoka ili twende ashuhudie kuwa tumejua”

    “Eti eeeh Tumaini tufanye hivyo?”

    “Ndio, ila kwanini tusingemshtua baba palepale?”

    “Tusingefanya vizuri, sisi wanaume tupo tofauti na nyie wanawake yani pale baba tungemkata stimu ndiomana mimi nikaona aibu na kuondoka”

    “Kwamaana hiyo wewe hata Erica akikufumania basi aondoke tu akuache uendelee na mamabo yako akihofia kukukata stimu?”

    “Weee ushindwe na ulegee, Erica anifumanie kwa lipi? Erica hawezi kunifumania”

    “Sababu utakuwa unajificha ukienda kumsaliti eeeh!”

    “Hilo swala la mimi kumsaliti Erica halipo kabisa, yani siwezi kumsaliti sasa atanifumania vipi wakati kumsaliti siwezi”

    Erica alijifanya kama hasikii vile ila hii kauli ya Erick ilimfanya kutabasamu sana maana alinihisi raha, Erick alimuangalia na kumuuliza,

    “Erica mbona unacheka?”

    “Hamna kitu, basi tu”

    Erick akainuka na kusogea alipo Erica kisha akambusu na kumkumbatia, Tumaini akaguna na kusema,

    “Mmmh mmeanza mahaba sasa, mnataka kunifukuza au?”

    Erick akamwambia dada yake,

    “Hatukufukuzi ila nakuonyesha dada yangu kuwa mapenzi ni kitu kizuri sana nan i matamu mno ukiwa na mtu mnapendana yani umpende akupende. Unajua kupendwa ni raha sana ila raha zaidi ni pale mkipendana. Dada ni wakati sasa na wewe kumpata shemeji jamani”

    hili swala hata Erica alicheka maana toka amfahamu Tumaini hakuna hata siku moja aliyosikia kuwa Tumaini ana mpenzi au kuna mtu ana mahusiano nae ya kimapenzi.

    Tumaini akawaangalia na kutabasamu kisha akasema,

    “Haya nimesikia myasemayo na nimekubali ila jamani mahaba yenu subirini nitoke”

    “Mmmh Tumaini hata kubusu tu tusubiri utoke kweli? Mbona wazungu huwa wanakiss hadharani”

    “Ushasema wazungu, nyie waswahili msiniletee mambo ya baba na Dora mie. Ngoja nimtumie ujumbe Dora kabisa maana ndio tushapata mama mdogo”

    “Maswala ya kumuita Dora mama mdogo siyataki”

    “Kama hutaki basi mama mdogo atakuwa Erica”

    Hapo Erick alikaa kimya kisha Tumaini akatuma ujumbe kwa Dora.

    Ila muda ule Erica alimwambia Erick,

    “Natamani ningepata chungwa, ila basi muda umeenda”

    “Hapana bhana, naenda kukutafutia”

    “Usihangaike Erick”

    “Aaaah ni kazi yangu hii, nitakupa chochote unachohitaji ilimradi kipo kwenye himaya yangu”

    Basi Erick alitoka na kuacha ndani amebaki Tumaini na Erica, walikaa tu kila mmoja akiendelea na simu yake yani hakuna aliyemuongelesha mwenzie hadi Erick aliporudi na machungwa, kisu na sahani akisema vile vyombo kavitoa mapokezi, Tumaini akasema,

    “Mmmh kweli mahaba, hadi umeenda kuomba kisu na sahani ukatie machungwa!”

    “Ndio, haya ni mahaba. Nampenda Erica, sitaki kuona apate shida wakati mimi nipo. Sasa nisingeenda kuomba kisu na sahani hayo machungwa tungekataje?”

    Basi Erick alianza kumenya yale machungwa na kumpa Erica ayale ila kile kisu alisema kuwa atakirudisha akipata muda, basi Erica alikula chungwa moja wapo na kuridhika kisha akalala.



    Nyumbani kwaina Rahim walipanga kuwa siku hii waende kwakina Zainabu na kweli jioni ya siku hiyo mrs.Peter alichukua na ndugu zake wawili pamoja na mshenga na kwenda kwakina Zainabu kwa lengo la kuzungumza na familia yake na kweli walikaribishwa vizuri kabisa na kuweza kuzungumza huku wakipanga mipango mbalimbali na kuonyesha nia ya kuwa kijana wao anataka kuoa pale.

    Basi walipokuwa wanaaga wakati wanatoka walishangaa kumuona Salma amefika eneo lile kumbe aliulizia kwakina Zianabu hadi alifika ukizingatia jana yake alimsikia huyu mama akisema kuwa leo ataenda kwakina Zainabu.

    Alikuwa amebeba mtoto wake ambaye bado alikuwa mdogo mgongoni, ma walipokuwa wanatoka tu akaenda kumuinamia mama mmoja aliyeonyeshwa kuwa ni mama yake Zainabu, wote wakamshangaa yani Mrs.Peter alitamani amtimue ila atamtimuaje kwa watu? Hakuweza kwakweli ila alichukia sana. Yule mama ambaye alikuwa ni mama yake Zainabu aliinama na kumuinua Salma aliyekuwa amelala kwenye miguu yake huku akilia, huyu mama alimuuliza

    “Tatizo ni nini binti?”

    “Huyo Rahim anayetaka kumuoa Zainabu alikuwa ni mume wangu, amenipa talaka baada ya kumuona Zainabu. Huyu mtoto niliyembeba mgongoni ni mtoto wetu, sasa Rahim na ndugu zake wananifukuza sina pa kwenda kwakweli na huyu mtoto na maisha haya naumia mimi. Sina raha jamani, nihurumie mama, naomba uwe kama mama yangu, mimi nilifiwa na mama sina mama kabisa na wote waliokuwepo wananikandamiza tu, nitaenda wapi na mtoto huyu? Nihurumie mama yangu”

    Salma alikuwa anaongea kwa masononeko sana, yani kama mtu ambaye maisha yamemuonea sana mpaka ametia huruma kiasi kile, kwakweli mama Zainabu alimuhurumia sana Salma na kujikuta akiingia nae ndani kwake kuongea nae vizuri tena bila hata ya kuaga wale wageni, moja kwa moja wale wageni walijua hapo ni habari nyingine basi Mrs.Peter na wenzie wakaondoka.

    Wakarudi nyumbani kwao tu kwa siku hiyo.

    Salma hakuondoka hapo kwenye nyumba hiyo na alimueleza Yule mama matatizo mengi sana ambayo amewahi kufanyiwa na Rahim,

    “Mama yangu, mimi sikujua laiti kama ningekuwa najua basi nisingekubali kuolewa na Rahim maana imekuwa ni mateso kwangu. Kwanza mimi nilitafutwa tu kuwa niolewe na kwavile mama wa kambo hapendi kuniona basi akanichagua mimi, nikaolewa na kuishi kwa mume wangu kwa adabu zote ila ndani ya nyumba nisithubutu kumuuliza kitu ni kipigo yani ananipiga hadi nachanganyikiwa, nishalazwa mara tatu kwa kipigo chake, halafu kweli ananiacha na mtoto mdogo hivi niende wapi mimi? Sijasoma mimi kusema labda nitatafuta kazi ya kufanya yani mimi sina mbele wala nyuma ila mtu ananifanyia hivi kweli na mtoto, ni haki hiyo?”

    Mama Zainabu alizidi kumuonea huruma Salma na kumtaka siku hiyo alale hapo kwake halafu kesho yake aende nae kwa wakwe zake,

    “Watakupokea mwanangu maana nitatafuta Sheikh akawaambie na maneno ya Mungu maana wanachokufanyia hakistahili kabisa kabisa”

    Basi Salma alishukuru pale na siku hiyo alilala nyumbani kwakina Zainabu.



    Dora alifanya kama alivyoambiwa na Tumaini kwahiyo alipokuwa anataka kutoka na mzee Jimmy alimtumia ujumbe Tumaini kisha akafungua mlango na kutoka naye, pale nje alikuwepo Tumaini na Erick na kusema kwa pamoja,

    “Baba!”

    Mzee Jimmy aliona aibu sana na kuwaacha pale watoto wake kisha kuondoka zake, ambapo Dora nae aliondoka zake.

    Kwakweli Tumaini na Erick walizidi kushangaa sana na muda huo Erick ndio akaamini vizuri zaidi kuwa mpaka alfajiri ile baba yao alikuwa amelala na Dora, basi baada ya hapo ndio Tumaini nae akaondoka zake kurudi kwao huku wakipanga kukutana kesho ili kumuhoji vizuri baba yao maana kukutana badae Erick alisema kuna kazi ambayo atafanya siku hiyo.

    Tumaini akaondoka zake kisha Erick akarudi chumbani alipomuacha Erica na Angel, kisha alimsogelea na kumkumbatia na kumwambia,

    “Usijali leo kukesha na Tumaini humu tulitaka kujua ukweli mke wangu”

    “Hapana mimi sina tatizo, ila tulikuwa tunamkwaza Tumaini”

    “Tunamkwaza nini? Ndio muda nay eye awe na mpenzi sasa, sie tunapendana na hilo tunawezaje kuficha? Yani mimi nikae bila kukukumbatia kidogo au kukubusu, nitajihisi vizuri kweli? Hapana Erica, muda wote natamani uwe karibu yangu mpenzi, wewe ndio furaha yangu hata katika kipindi kigumu kama hiki.”

    “Asante sana Erick”

    “Sasa, mimi nitaondoka hapa na kwenda kuangalia kule kwenye nyumba halafu nitakuja kuwachukua”

    “Mmmh kwanini tusiende wote?”

    “Hapana Erica, naomba upumzike nikarekebishe nitakuja kuwachukua hakuna shida”

    Erick alioga na kujiandaa kisha akamuaga Erica kwa kumbusu na kwenda kule akafatilie usafi wa ile nyumba waliyoipanga.

    Baada ya Erick kutoka tu Erica aliamka na kuoga kisha kulala tena sababu usiku hakulala vizuri kwani Tumaini na Erick walikuwa na mipango mingi kwahiyo walikuwa wanaongea ongea na kufanya usiku ule uwe kama wa mkesha, alilala usingizi mzito sana.

    Gafla alisikia mtu akigonga mlango wao ule, alihisi huenda ni muhudumu wa ile hoteli au Erick karudi, aliinuka na usingizi usingizi wake na kwenda kufungua mlango, mara aliyekuwa anagonga akaingia mzima mzima ndani, Erica alifikicha macho na kumuangalia vizuri, alikuwa ni James, Erica alishangaa sana na kusema kwa mshangao,

    “James”

    “Ndio ni mimi Erica, nina kuhitaji sana. Nina kiu na penzi lako Erica, nimekufatilia sana yani huwezi amini toka muda ule tumeonana nilikuwa nakufatilia na leo nililala kwenye hii hotel na kwa bahati nzuri nilichungulia muda Yule jamaa yako akitoka ndiomana nimeamua kuja. Nakuhitaji Erica, nakupenda sana. Nilifanya makosa kumuoa dada yako, hata sikumpenda ni wewe nikupendae”

    Muda huu Erica alikuwa mbali kabisa na James kwani alihisi kuwa huyu James hana nia njema na yeye, James akaanza sasa kumsogelea Erica yani kile kitendo kilimfanya Erica ashikwe na hofu huku akisema,

    “Ondoka James”

    Kwani James hata alisikia lile swala la ondoka, hakusikiliza kwakweli kwani muda ule ule alimvamia Erica na kutaka kumbaka huku akisema,

    “Siku zote unaninyima na leo nitakubaka tu”

    Ubaya wa ile hoteli, hata mtu apige kelele chumbani basi chumba cha pili haitasikika ile sauti maana Erica alianza kupiga kelele hata Angel aliamka na kuanza kulia, ila James hakujali kabisa zile kelele maana alimsukumia Erica kitandani na kuchana ile nguo aliyoivaa Erica ambapo Erica alipiga kelele na kujitahidi kumtoa James mwilini mwake ila alishindwa kwani James alikuwa na nguvu kuliko yeye, ila Angel alipoona kama mama yake anakandamizwa aliinuka na kuchukua kile kisu ambacho Erick alikiacha jana yake akajikuta akimpiga nacho James, kwahiyo James alijikuta akiruka pembeni kabla hata ya kumuingilia Erica, wakati James anajishangaa Erica alimchukua mwanae na kukimbilia bafuni ambako wakajifungia sasa.

    James alikuwa akishangaa bado kuwa ni kitu gani cha ncha alichochomwa nacho, kuangalia nyuma yake akaona damu kwahiyo aliumia mgongoni, na alipoangalia pembeni akaona kisu kwakweli alishangaa sana,

    “Yani kile kitoto ndio kimenichoma na kisu? Kile kitoto nilichokifanyia birthday ndio kimenichoma na kisu!!”

    Akasogea kwenye mlango wa bafu na kumwambia Erica,

    “Jifungia huko salama ila roho yako mbaya na mwanao nae umemrandisha roho mbaya, mtoto mdogo huyo na anajua kuua, nyie ni wabaya sana ila huu ni mwanzo tu”

    Kisha akaondoka ila Erica alishindwa kutoka mule bafuni kabisa kwa kuhofia kuwa huenda bado yupo.



    Mama Zainabu aliongozana sasa na Salma pamoja na Sheikh aliyemchukua kwenda nae nyumbani kwakina Rahim pamoja na wababa wengine wawili ambao pia ni watu wa dini, na walifika na kumkuta mama yake Rahim ambapo baada ya salamu wakaanza nae kikao, kisha akaenda kuitwa Rahim ili wazungumze nae, alipofika tu alichukia sana kuona kuna watu wameenda kumleta Salma, aliwasalimia na kukaa kisha mama yake akamtambulisha kwa watu wale kama yeye alivyotambulishwa ila alivyomaliza utambulisho tu yani kabla wale watu hawajaanza kuongea alifoka Rahim,

    “Huu ni ujinga, mwanamke ananisumbua na wote mnatambua hili halafu bila aibu mnaniletea viongozi wa dini sijui wazungumze nami, niongee nao nini? Huu ni ujinga, siwezi kupewa mawaidha nisikilize wakati kuna mwanamke nisiyemtaka, mngekuja hapa na Zainabu sawa ila kwa huyu mwanamke niwasikilize siwezi”

    Rahim akainuka na kutoka, mama yake alijaribu kumita ila Rahim hakuitikia na kuondoka zake.

    Yani mama yake pale aliona aibu sana, ikawa hakuna namna waongee tu na huyu mama maana toka mwanzo alikiri wazi kuwa alimpenda Salma alivyoambiwa kuwa kachaguliwa kwaajili ya mwanae,

    “Sasa kama ulimpenda hutakiwi kumchukia kwasasa, kama ana mapungufu ni kumrekebisha tu”

    “Jamani, mimi mwenyewe sikujua kama huyu Salma ni msumbufu hadi jana alivyovunja vitu hapa kwangu na kufanya fujo”

    Salma alijitetea kuwa ile ilikuwa ni hasira tu maana hata kwao hawamtaki sababu ana mtoto, kwamaana hiyo wakamwambia Mrs.Peter kuwa aishi tu na Salma walee Yule mtoto kama Rahim atajirudi basi ataishi na mke wake, na asipojirudi basi talaka itaendelea ila kwa kipindi hicho wakae nae tu walee mtoto. Mrs.Peter hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali tu kumlea Salma pamoja na mjukuu wake.



    Erick alirudi pale hotelini jioni, na kuingia mule chumbani akashangaa kuona damu na kisu chini, alihisi kuchanganyikiwa kwakweli na kuita kwa uoga,

    “Erica, Angel”

    Erica aliitika akiwa bafuni ila kwavile ni sauti ya Erick alifungua mlango na kutoka, alimkimbilia na kumkumbatia huku akilia, Erick alimuuliza kuwa tatizo ni nini, basi Erica alianza kumsimulia ilivyokuwa yani Erick alijilaumu sana kwa kutokuondoka muda ule na Erica,

    “Hivi kwanini mbwa mwitu kama hao wanakunyemelea sana mke wangu jamani! Kwani tatizo nini dah!”

    Basi akapiga simu mapokezi ili waje kusafisha pale na kuchukua kisu, aliendelea kusema

    “Yani baya lingekukuta leo sijui ningejionaje jamani, ningejiona sina thamani kabisa. Asante sana kwa mwanangu Angel, mtoto ana akili huyu kama mamake, nitakutafutia zawadi kubwa mwanangu. Tujiandae sasa tuondoke.”

    Ila alimuhurumia Erica kuwa alijifungia bafuni bila kula chochote kwahiyo alikuwa anamwambia wale kwanza ndio waondoke ila Erica alikazana kuwa waondoke na wakale huko huko, Erick alielewa kuwa mahali hapo pameshamkera Erica hivyobasi wakajiandaa pale na kuondoka huku wakimuacha Yule wa mapokezi akifanya usafi, pale hawakumuhoji sana Erick sababu ni mteja wao mkubwa sana kwenye ile hoteli.

    Waliondoka na kwenda hadi kwenye nyumba ambayo Erick aliitafuta, kwa muda huo nyumba ile ilikuwa imefanyiwa usafi wote na ilikuwa imeshawekwa kila kitu kumbe Erick alivyoondoka ile asubuhi alienda kununua vitu vya kuweka ndani kwahiyo Erica aliipenda zaidi ile nyumba maana ilikuwa na muonekano wa kuvutia kutokana na vitu vilivyowekwa ndani.

    Kwa muda huo Erick aliagiza chakula tu na kilipofika walianza kula.

    Walipomaliza kula, Erick alikuwa amechoka sana hivyo akaamua kuoga na kulala maana siku hiyo alikuwa na kazi nyingi sana, kwahiyo kwa mara ya kwanza aliingia chumbani kwenye nyumba kwa lengo la kulala maana hawakuwahi kuishi hapo, Erica nae aliingia chumbani maana Angel alidai anataka kulala pia kwahiyo Erick na Angel walikuwa fofofo.

    Wakati Erica amekaa tu simu yake ilianza kuita na alipoangalia mpigaji aliona kuwa ni Dora, aliamua kutoka sebleni na kuongea na simu ile.

    “Eeeh niambie Dora”

    “Samahani Erica, hivi babake mzazi Angel anaitwa nani?”

    “Mmmh anaitwa Rahim, kwanini umemuulizia?”

    “Anafananaje?”

    “Sijui nikuelezeje, ila ingia facebook andika Rahim Shombeshombe utamuona, kwani vipi wewe?”

    “Leo bhana katika pitapita zangu, nimekutana na huyo mtu anaitwa Rahim ni anakunywa pombe huyo balaa, ila nilipomuangalia nimemuona anaufanano kidogo na Angel.”

    “Nasikia lakini anakunywaga, inawezekana akawa ni yeye”

    “Unampenda?”

    “Mmmh swali gani hilo Dora? Ninayempenda mimi ni Erick pekee sio huyo Rahim”

    “Kama humpendi mbona ulizaa nae?”

    “Dora, unajua mahusiano yalivyo, kipindi tupo kwenye mahusiano ilishapita hiyo hali ila kwasasa ni Erick tu ndio yupo kwenye moyo wangu”

    “Na kwanini Rahim hakukuoa?”

    “Aaaah Dora jamani loh! Hakuweza kunioa sababu alisema sifai kuolewa nae”

    “Mmmh ila mzuri huyo, huwa napenda kweli wakaka shombeshombe jamani sema sijawahi kuwa na bahati nao”

    “Hebu acha zako Dora, yani kwako kila mtu mzuri loh!”

    “Ndio mzuri, anavutia ila hajamzidi Erick wako yani huyo Erick asingekuwa shemeji ungekuta nishamshawishi ila ni shemeji namuheshimu sana halafu mgumu huyo maana hata Sia aligonga mwamba na vidawa vyake. Sema Erick mzuri huyo, shoga yangu unafaidi wewe”

    Erick alitoka chumbani na kufanya Erica aikate ile simu, Erick alimsogelea Erica

    “Mbona umekuja kukaa mwenyewe mpenzi jamani! Yani umeacha sisi tutale wenyewe kweli!”

    “Aaaah mmmh aaah”

    Hakuwa na maelezo ya kujieleza, basi Erick akamshika mkono na kwenda nae chumbani na kumwambia akae tu hata kama halali ila akae nao karibu, kwahiyo kwa muda huo ilibidi Erica nae aanze kutafuta usingizi tu.



    Mage alipoona mdogo wake hajarudi nyumbani hadi siku hiyo ilibidi amwambie mama yao kuwa yeye anaondoka zake,

    “Mama, inaonekana mwanao kashajiozesha. Kwakweli mimi naondoka zangu akija mtaniambia”

    Ila Bite akatoa wazo,

    “Hivi kwanini tusimpigie simu huyo Erica?”

    “Hakuna kumpigia simu wala nini, muacheni hivyo hivyo, si kaamua bhana. Mwacheni tu”

    Basi wakakubaliana na lile swala la kutokumpigia simu wala nini maana amewadhalilisha sasa, muda ule walipigiwa simu na Tonny na aliwaeleza kuwa amepata mchumba anataka akamtambulishe.

    “Usituletee tena yale mauza uza yako ya Dora”

    “Hamna mama, safari hii nimepata mwanamke msomi na mwenye kazi yake inayoeleweka”

    “Kwani Dora hakuwa msomi?”

    “Alikuwa msomi ila sio kama huyo wa sasa, maana ni mwanamke haswaa nimempata”

    “Haya, tunayasubiri hayo mauzauza yako utakayotuletea”

    Aliwaahidi kuwa mwisho wa wiki ataenda kumpeleka mchumba wake nyumbani kwao wamfahamu.

    Kwa muda ule walianza kujadili habari za Tonny na kuacha habari za Erica kwa muda.



    Rahim alikuwa amechukizwa sana na kitendo cha kupelekewa viongozi wa dini,kwahiyo kwa hasira alizokuwa nazo alienda kunywa sana pombe na alikunywa siku hiyo kupita siku zote akajikuta anaanza kutongoza tongoza wanawake hovyo yani siku hiyo hadi wahudumu aliwaona kuwa ni wanawake waliovutia na alikuwa anaenda na mwanamke ndani na akitoka nae bado hajaridhika anachukua mwanamke mwingine, mpaka muda huo alikutana na Dora ambapo Dora aliamua kumpetipeti sasa.

    Rahim akampata Dora na kwenda nae chumbani, Dora alimwambia

    “Najua umelewa ila mimi sio malaya kama wale uliokuwa unawachukua zamu zamu, mimi ni mwanamke na heshima zangu. Nimekuhurumia na hayo unayoyafanya sio sawa kwakweli, mimi ni rafiki wa Erica”

    “Ooooh Erica mrembo wangu yuko wapi?”

    “Yuko wapi nini? Erica yupo na Erick kwasasa na wanapendana sana, yani wewe baba mzima unaanza kuhangaika na wanawake badala uwaze maisha ya badae ya watoto wako”

    “Halafu wanwake kama nyie ndio huwa mnabakwa, sasa maisha yangu yatakusaidia nini?”

    “Mimi sio wa kubakwa ila ni swala la kuelewana tu, mtu gani usiyejali familia yako wewe. Hivi unafikiri wanawake uliozaa nao wakisikia habari yako ya kubadilisha machangudoa huku watakufikiriaje?”

    Rahim hakupenda maneno ya Dora, na ili kumuonyesha kuwa yeye ni mwanaume aliamua kumbaka Dora ila alishangaa mwanamke huyu amembaka ila amempa ushirikiano wa kutosha kabisa na alipomaliza nae alilala usingizi mzito sana ambapo Dora nae alilala.

    Kulipokucha, Rahim aliona kabisa kuwa alichokifanya hakikuwa sawa na alifanya sababu alikuwa amelewa, alimwambia Dora wasahau tu kilichotokea,

    “Sawa hakuna shida, ila swali langu ni kuwa wanawake wote wale hutumiagi kinga kweli?”

    “Aaah wewe nae sijui umetumwa”

    Rahim aliinuka na kujiandaa kisha kuondoka zake, Dora nae alijiandaa na kuondoka zake ila ilikuwa furaha sana kwake kuweza kulala na huyo makaka mshombeshombe.



    Erick alienda nyumbani kwao kama alivyopanga, na alienda mapema sana ili aweze kumkuta baba yao na wamuhoji kwa yale aliyokuwa ameyatenda.

    Alifika na kumkuta Tumaini, akamsalimia na kumuuliza,

    “Baba kashatoka?”

    “Hamna bado yupo ndani, sijui ndio presha zimempanda”

    “Asitutanie sie, presha baada ya kufanya maovu. Hebu twende tukaongee nae”

    Erick aliongozana na Tumaini na kwenda kumgongea mlango baba yao ambapo aliwakaribisha na kudai kuwa anajisikia vibaya, Erick alielewa wazi kuwa baba yake kafanya vile sababu anaogopa kuulizwa na watoto wake, ila pale pale Erick aliamua kuongea,

    “Baba, licha ya kuumwa ila umetudhalilisha sana watoto wako”

    “Naumwa jamani, hivi nyie watoto hamuelewi?”

    Ila Erick akawaza jambo kuwa pengine baba yao alifanyiwa dawa na Dora huku akikumbuka zile dawa ambazo alizompeleka Sia ili amletee yeye na jinsi alivyoanguka kwakina Erica na kuangusha dawa kwahiyo alihisi huenda baba yake karogwa na Dora. Basi akaamua kumshauri,

    “Baba, naomba nikushauri kitu”

    “Kitu gani? Ila kumbuka naumwa”

    “Sawa unaumwa baba yangu ila naomba twende kwenye maombi, maana labda wamekutupia mavitu mabaya”

    Sababu mzee Jimmy alikuwa akiona aibu kwa watoto wake, aliamua kukubaliana na Erick kwenda huko kwenye maombi huku na yeye akikubali kuwa huenda amerogwa.

    Basi akajiandaa na kuondoka pale akiongozana na Erick pamoja na Tumaini kuelekea kwa mwanamaombi.

    Walifika na Erick kugonga mlango wa Yule mama, wakati Yule mama anatoka nje, mzee Jimmy alionekana kumshangaa sana na kumuita kwa mshangao,

    “Ester!! Ni wewe”

    Yule mwanamaombi nae alionekana kumuangalia mzee Jimmy kama mtu anayemfahamu, hata Erick alishangaa kuona wanafahamiana wale watu





    Walifika na Erick kugonga mlango wa Yule mama, wakati Yule mama anatoka nje, mzee Jimmy alionekana kumshangaa sana na kumuita kwa mshangao,

    “Ester!! Ni wewe”

    Yule mwanamaombi nae alionekana kumuangalia mzee Jimmy kama mtu anayemfahamu, hata Erick alishangaa kuona wanafahamiana wale watu.

    Mzee Jimmy bado nay eye alikuwa na mshangao wa kumuona Ester inaonyesha hakutarajia kumuona tena katika maisha yake, kwahiyo kitendo cha kumuona kilimshangaza sana.

    Alimsogelea karibu na kumwambia,

    “Ester upo?”

    “Nipo Jimmy, za siku?”

    “Nzuri tu, ni muda mrefu umepita ila bado unapendeza tu”

    “Utukufu kwa Mungu”

    Ndio hapa mzee Jimmy alipogundua kuwa kweli Ester ulokole umemkaa, akawaangalia wanae na kuwaambia,

    “Huyu ndio Yule mwanamke ambaye habari zake niliwagusia kidogo tu, ndio huyu mwanamke wa kilokole, kipindi hiko alikuwa binti na nilimpenda sana ila alinipa masharti mengi na kushindwa kuwa nae”

    Erick na Tumaini walitamani wajue kiundani kabisa ila hawakuweza kumdadisi baba yao pale, na kabla hata Erick hajamueleza Yule mwanamaombi matatizo ya baba yao Yule baba aliwaambia wakamsubiri kwenye gari aongee nae mwenyewe.

    Waliguna tu na kwenda kwenye gari kumngoja.



    Baada ya muda baba yao alirudi na kuwataka warudi nyumbani, hawakujua ni kwanini baba yao kawaambia vile ila walikubali na kurudi nae nyumbani.

    Ambapo waliingia ndani na kukaa nae sebleni kisha akaanza kuongea sana,

    “Yule mwanamke anajua vitu vingi sana, yani anaonekana kufahamu vitu vingi sana na mimi sijaoa hadi leo sababu yake yani kila mwanamke namuona hafanani na yeye”

    Erick alimuuliza baba yake,

    “Kwani imekuwaje? Na yeye ulimfahamu vipi?”

    “Ngojea niwaeleze kwa kifupi huenda mkafahamu kinachonitatiza baba yenu. Miaka ya nyuma huko wakati nimekua zangu na akili timamu, nikawa nisimamia mashamba ya babu yangu yani babu yangu alikuwa ana mashamba mengi sana ya kahawa kwahiyo nilikuwa nasimamia, kipindi hiko nilianza kunywa pombe na kuvuta sigara tena nilikuwa mpenzi mzuri wa mpira yani mpira mpira na mimi, na pia nilipenda sana kusikiliza mziki yani nikikaa shambani basi utanikuta na redio yangu pembeni nakula mziki taratibu tu. Sasa huyu Ester alikuwa ni mmoja wa vibarua kwenye shamba la babu, nilimpenda kwakweli na kama hela nilikuwa nayo, ila mwanamke huyu alikuwa wa ajabu sana machoni pangu, hela anayotaka nimpe ni ile aliyofanyia kazi tu na si vinginevyo yani Yule mwanamke hapendi hela jamani ndiomana haendelei hata huku mjini itakuwa kaja na mbio za Mwenge maana kama mtu hupendi hela basi mjini umekuja kwa mguu, ndio Yule na ndiomana maisha yake ni ya kawaida sana, ila alikuwa ni mzuri kweli, natumai mnanielewa, ni mtu mzima sasa ila uzuri wake bado haupotei, ni mzuri wa sura na umbo. Nilimpenda sana, nilimuhitaji sana, nilisema akinikubali tu naoa ila haikuwa hivyo. Baada ya kumfatilia sana nikajua ni mlokole, kuna jamaa akaniambia kumpata binti mlokole ni kujifanya na mimi ni mlokole pia, basi nikaanza kwenda kanisani na kuhudhuria mafundisho yote ya dini, nilianza kuwa vizuri kwakweli ila pombe, sigara, mpira na mziki ni vitu ambavyo sikupanga kuviacha kabisa. Basi nilivyokuwa vizuri nikawa namfata Ester na ananiambia maneno ya dini tu, nikamwambia mimi nimeokoka sababu yako, nahitaji uwe mke wangu, akanipa masharti magumu huyo kuwa niache pombe, sigara, mpira na mziki, nikamuuliza jamani hata mpira una tatizo gani? Akaniambia anataka mume ambaye atatangaza nae kazi ya Mungu ila mume mwenye upenzi na kitu kingine atashindwa kufanya nae kazi ya Mungu, jamani ilikuwa ngumu sana kwangu nilijitahidi vyote ila pombe na sigara sasa ukawa mtihani mkubwa, akaniambia yani bora hata ingebaki mpira kuliko pombe na sigara, nikajitahidi nikionana nae sivuti sigara wala sinywi pombe, nikamuomba jambo moja kuwa walau aniachie mpira, akubali basi nikafanya mipango ya kujitambulisha kwao na kutoa posa, kiukweli sikuwa na nia ya kumchezea nilitaka kumuoa, tulienda kwao kujitambulisha kila kitu na wakatuambia tupeleke mahari, ambapo ilikuwa ng’ombe jike watatu na dume moja, halikuwa tatizo kwangu maana kwetu tulikuwa na uwezo wa kutosha tu, tulipanga iwe haraka sana.

    Siku hiyo bhana ambapo kesho yake ilikuwa ndio siku ya kupeleka posa, yani sijui Ester alitokea wapi muda huo uwiii akanikuta mahali shambani navuta sigara, yani huwezi amini ni pale pale alikataa mahari yangu na kesho yake tulirudishiwa posa yetu. Roho iliniuma sana ten asana, sijawahi kupata furaha hadi leo nimejikuta nachukia sana sigara maana ndio imesababisha nimkose Ester. Baada ya hapo sikuweza tena kukaa pale kijijini, nilimwambia babu anipe changu na kuja kufanya maisha mjini, basi kila mwanamke niliyemuona nilitamani tu kumpitia na sio kumuoa. Ninachojutia ni kushindwa kuomba msamaha kwa Ester pengine ningemuomba msamaha na kuahidi kubadilika angenielewa ila sikuwa na wazo la kuomba msamaha kabisa kwani nilisikiliza jamaa zangu waliniambia mwanamke anayekupangia pangia mambo ya kufanya si mzuri kuoa, na kule kwetu ilikuwa kumuomba msamaha mwanamke ni kujidhalilisha”

    “Kheee baba, pole sana. Pengine Yule Ester ndio angekuwa mama yetu sasa”

    “Ni kweli Tumaini ila Yule Ester hawezi tena kunikubali kwasasa, anasema ishapita tayari, niende kwake kufanyiwa maombi tu lakini sio kumuoa. Ndiomana nimeondoka kwa hasira. Ila kuna jambo naomba mnkisaidie wanangu”

    “Jambo gani hilo baba?”

    “Nimewapa hiyo story kwasababu maalumu kabisa mjue kwanini namng’ang’ania Erica, mwanamke niliyempenda maishani ndio huyo Ester na hakunitaka labda ningetumia nguvu ningempata. Sasa cha kunisaidia ni kimoja, baba yenu nahitaji mwenzangu, nahitaji mke nimechoka kuwa mpweke na katika wake hao kuna watu wawili tu hadi sasa kwenye kichwa changu, kuna Ester na Erica”

    Hapo Erick alishtuka kidogo maana huwa hapendi kabisa baba yake kumng’ang’ania Erica, ila alitulia na kumuuliza,

    “Sasa baba tukusaidie nini hapo?”

    “Mnisaidie kumpata Ester nimuoe ili niache kusumbua kuhusu Erica, naomba mnisaidie nimuoe Ester ila nikimkosa huyu Ester kwa hakika hata wewe Erick hutoweza kumuoa huyo Erica, nampenda sana na nishagharamia hela zangu nyingi kwake. Kwaherini”

    Muda huu mzee Jimmy aliinuka na kuondoka zake.



    Tony akawaza kumpeleka mchumba wake mpya nyumbani kwao ila asipate vikwazo kama alivyopata wakati anaenda kumtambulisha Dora, akakumbuka kuwa mdogo wake Erica ndio alimletea hivyo vikwazo yani ndio alikuwa kikwazo cha yeye kutokuwa na Dora pia akakumbuka kuwa vikwazo vya mdogo wake havikuwa vya wivu ila alikuwa akimuokoa kaka yake kutoka kwa mwanamke asiyefaa ambaye alikuwa Dora, kwamaana hiyo aliona Erica ni mdogo wake ila ana maono ya mbali zaidi kwahiyo aliamua mchumba wake mpya kabla ya kwenda kumtambulisha kwao basi amtambulishe kwanza kwa mdogo wake yaani Erica amuone kwanza kabla hajampeleka kwa wengine wamfahamu, halafu Tony hakujua kuwa ndugu yake kuna madudu kashafanya nyumbani kwao na kutoroka. Hivyobasi akampigia simu bila kujua chochote kile kinahoendelea kwa Erica,

    “Hellow Erica, upo nyumbani?”

    “Hapana, kwani kuna tatizo gani?”

    “Hakuna tatizo mdogo wangu,ila kakako nimepata mchumba ambaye badae nataka aje kuwa mke wangu. Naomba nikufahamishe kwanza wewe umuone”

    “Kheee jamani Tony, kwahiyo unataka nimuone mimi kwanza?”

    “Ndio nataka wewe umuone kwanza, maneno yako ya mwanzo kunikataza nisimuoe Dora bado yananiingia akilini, najua mdogo wangu utakachochagua kitakuwa kizuri machoni pa wengine, si unaona mwanaume uliyechagua kuzaa nae! Hahaha umechagua haswaa ili uzae mrembo”

    Erica alicheka tu ila alijua ni kwajinsi gani kakake hajui kinachomchukiza Erica kwa huyo mwanaume aliyezaa naye. Kisha Erica akamwambia kaka yake,

    “Sasa mfano simpendi tu huyo mchumba wako kwasababu zangu binafsi itakuwaje?”

    “Erica, kwasasa wewe ndio sijui nisemeje yani wewe ndio kama mchaguzi wangu mkuu. Nyumbani nimewaambia kuwa nitapeleka mchumba wamtambue ila nataka umtambue kwanza wewe, na kama humtaki au hanifai niambie kabisa, kwa hakika sitamuoa, nakumbuka ushauri wako uliopita kwa Dora na umeniokoa na vingi sana mdogo wangu, hivyo nakuomba nikuletee huyo mchumba wangu umfahamu na unipe viwango kama anafaa au hafai”

    “Sawa kaka yangu hakuna shida, sasa utakuja nae moja kwa moja nyumbani?”

    “Hapana, nataka tukutane mahali, labda hotelini hivi umfahamu”

    “Sawa, hakuna shida kaka yangu. Basi utaniambia”

    “Sawa hakuna shida”

    Basi wakaagana pale ila Erica alielewa kuwa kakake hajui kuwa yeye hayupo nyumbani kwao.



    Erick aliona babake kamuachia mzigo mkubwa sana yani hakuhisi kama mzigo huo watauweza na Tumaini, akamwambia dada yake

    “Hivi huyu mzee yupo serious au ni nini jamani?”

    “Hata mimi namshangaa”

    “Mwanamke aliyemfuma kwa sigara tu na kumuacha atamkubali sasa akimfuma na wakina Dora?”

    “Hapo sasa, huyu mzee anatubabaisha tu. Mke wake Dora”

    “Aaaah acha maneno yako hayo”

    “Sasa Erick, mi nilikwambia toka mwanzo kumshinda baba dhidi ya Erica ni sisi kuwa kitu kimoja. Baba katupa mtihani ambao hata yeye alifeli miaka ya nyuma huko, alikamwatwa na sigara tu na Yule mama hakutaka kuolewa nae, je baba wa sasa hivi anayekazana kuwataka wakina Erica yani watu wenye umri sawa na watoto wake, sijui wakina Dora unadhani Yule mama atamkubali? Yule mama sio mjinga kiasi hicho, yani hawezi kumkubali baba yetu hata iweje, kwahiyo tunatakiwa kujiandaa kisaikolojia kuwa baba lazima ataendelea kumtaka Erica tu, cha msingi tushirikiane tumwambie baba amuoe Dora tu, na zile habari zake tukitaka kumuuliza kuhusu Dora anajifanya presha imepanda ziishe, tuwe na ushirikiano yani ni Dora tu ndio anamuweza baba, akigoma tumlete Dora hapa nyumbani”

    “Unajua mara nyingine unaongea kama si wewe uliyekuwa unamchukia Erica!”

    “Hayo yalishapita Erick, tufikirire mapya tu kwasasa”

    Basi Erick alipotaka kurudi kwake, Tumaini alimwambia kuwa ampeleke kwake ili apafahamu. Erick hakuona kama ni tatizo hilo na kuamua kwenda nae siku hiyo.

    Kiukweli walifika na alipapenda pia na kuona mdogo wake kaanza mambo ya maendeleo na kumsifia kuwa amefanya jambo jema sana kuamua kuanza maisha na Erica, ila bado Tumaini alikuwa hayupo karibu na Erica kama zamani kuwa wanaongea, wanacheka na kufurahi yani alionekana kuwa kimya tu anapobaki mwenyewe na Erica, na muda kidogo aliaga na kurudi kwao.



    Kesho yake Rahim akiwa kwao ilibidi mamake amseme sana maana ilikuwa ni aibu aliyoifanya majuzi mbele za wageni,

    “Na Salma kaachwa hapa, wametusema na nimejitahidi kuelewa walichotusema. Mwanangu hakuna namna inabidi tu uendelee kuishi na Salma kama mke wako”

    “Aaaah mama, huyu Salma simuhitaji kabisa, ninayemuhitaji mimi ni Zainabu”

    “Sasa mwanangu wazazi wa Zainabu wamegoma sababu umemfukuza mkeo labda Salma aendelee kuwa mke wako na tukawaombe kuwa Zainabu awe mke wa pili”

    “Huyo Salma atakubali?”

    “Atakubali ndio, niliongea nae, nimemsema sana na amesikia atakubali tu. Dini inaruhusu wewe kuoa wawili, kuliko kumuacha atangetange ni bora uwe na wake wawili, na hakika utaweza kuwatunza.”

    “Je Zainabu atakubali kuwa mke wa pili kwangu?”

    “Uzuri wa Yule binti ameishika dini vizuri kwahiyo anaelewa sunah ya kuolewa wake wawili, hawezi kukataa maana na mimi nitaenda na masheikh kuzungumza nae, hata hivyo binti umri umeenda Yule, miaka thelethini na tatu unafikiri hatamani ndoa yule? Anatamani sana sema mambo ya dini yamemfunga, pale anatamani nay eye angekuwa na mume wake, angekuwa na watoto wake, anatamani sana na umri ushamtupa mkono anakaaje kwa mfano? Atakubali tu niachie mimi hilo swala”

    “Sawa mama, hakuna tatizo kama ndio hivyo niko tayari kuishi na Salma maana nitamuoa na Zainabu pia”

    Basi mama yake alikubali na wakati huo huo alijipanga kwenda kwenye familia ya wakina Zainabu ili aongee nao.

    Na hakuchukua muda, alienda kuongea kwanza na wale Masheikh kisha kwenda tena kwenye familia ya Zainabu na Zainabu mwenyewe akasema kabla ya posa anahitaji kuongea kwanza na muhusika, kwahiyo mamake aliona mambo yameenda vizuri kabisa kama walivyopanga.



    Kwa upande wa ndugu wa Bahati, walijikuta wakijilaumu tu kwani mambo aliyokuwa akiyafanya Bahati kwa kipindi hiko hayakuwa mambo ya kawaida kabisa, ilibidi ndugu zake wamuite tena wakae nae na wazungumze nae. Mama yake aliongea kwa uchungu sana,

    “Bahati mwanangu, kweli umefikia hatua ya kumbaka mama mkwe wako kweli? Yule si sawa na mimi mama yako jamani!”

    “Mama, kuna mambo huwa nayatenda hata mimi mwenyewe najishangaa na sipendi kuyatenda kabisa, Yule mama nilisema kwenye kikao siku ile kuwa sirudi kwangu sababu Yule mama mkwe namtamani, ila wakaja watu kunibembeleza kuwa nirudi kwangu. Nimejaribu kujizuia ila nimeshindwa na kujikuta nimembaka”

    “Na ulivyo na mbegu kali mwanangu, mama wa watu ni mtu mzima ila kaanza kujihisi vibaya kama mjamzito, Bahati mwanangu kwanini umekuwa hivyo?”

    Dada yake aliamua kumtetea kidogo,

    “Mama, tutamlaumu sana Bahati ila na sisi pia tuna makosa tena makosa makubwa sana, hivi kwa mfano tungemuacha Bahati aoe mwanamke anayemtaka kungekuwa na tatizo hapa? Hivi Bahati angeishi na Yule mwanamke haya yaliyotokea yangetokea? Ila tulitumia hasira sana na hata kushiriki kutafuta dawa za kumfanya Bahati amsahau Yule mwanamke, na tulifanya vile sababu hatukumtaka Yule mwanamke. Ila mama kumbuka aliyetushauri kufanya hivi ni Yule babake Nasma kwanza ndio alikuwa mshenga wa Bahati, nasikia Yule baba sio mtu mzuri kumbe ni mchawi balaa, mtaa mzima wanamfahamu. Ila dawa za kumchanganya Bahati za mwanzo tumeshiriki wenyewe yani tusikatae kuhusu hilo, yani na sisi ni sehemu kubwa sana ya kuharibu maisha ya Bahati hata kafikia hiyo hali ya kumbaka mama mkwe wake. Hatukujua kuwa dawa tunazofanya tunajenga kitu kibaya kwa bahati maana hajampenda mke wake kwa mapenzi, siku zote watu wanaimba na kusema kuwa mapenzi ya dawa hayadumu na tunalijua hilo je tulihisi Bahati angedumu kwa Nasma? Yani mapenzi ya dawa huwa hayadumu unashangaa tu siku mambo yamebumbuluka kila kitu hadharani na ndio kilichotokea, nasikia Bahati baada ya kumuona Yule ampendaye dawa ziliruka na kupotea pia, alijikuta akaanza kumfatilia tena hiyo ni kwa mujibu wa Nasma na ndipo alipoamua kumfanyia dawa nyingine ili ampende kwa bahati mbaya ile dawa alikosea kidogo maana dawa zingine Bahati hakuzitumia ndio hivyo Bahati kawa kama Jogoo, maana hiyo dawa aliyofanyiwa ni anakuwa kama Jogoo, si unajua Jogoo anabaka kila anayemuona, kwahiyo usishangae kukuta Bahati anatutamani hadi sisis, hapa tufanye kitu jamani tusibaki kumlaumu Bahati tu au kulaumiana”

    Bahati alikuwa kimya kabisa ila hata yeye alihisi kuwa hayupo sawa maana mambo aliyokuwa nayafanya hayakuwa ya kawaida, mama Bahati alipumua kidogo na kuanza kujadili na wanae cha kufanya,

    “Sasa tufanyeje maana hii hali inatakiwa tuifanyie tiba mapema kabla huyu Bahati hajafungwa kwa makosa ya kubaka maana anapoelekea pabaya jamani, ila wanawake loh yani kale kaNasma kumfanya mwanangu awe kama Jogoo jamani loh!”

    Dada mkubwa wa Bahati akashauri,

    “Sababu ile dawa ya kwanza iliisha nguvu baada ya kumuona Erica, basi tumpeleke kwa mtaalamu Yule tuchukue dawa atumie halafu twendeni kwakina Erica amuone na awe huru”

    “Sawa sawa, tusipoteze muda basi, le oleo atumie dawa za Yule mtaalamu halafu kesho twendeni kwakina Erica ili tuonane nae”

    Wakakubaliana na muda huo wakaondoka na Bahati kwenda kwanza kwa mtaalamu ambaye walienda akawapa dawa ila hazikumsaidia kwahiyo wakaenda tena ili wachukue hizo dawa na kesho yake waende kwakina Erica pengine yale madudu yamtoke kabisa Bahati.



    Usiku ulipofika Erick aliamua kumueleza Erica kuhusu baba yake kufahamiana na Yule mwanamaombi, kwakweli alishangaa sana.

    “Unajua katika maisha kuna mambo huwa yanatokea unajiuliza kwanini yametokea, mara ya kwanza wakati nakutana na Yule mama na kuhitaji namba yangu nilishangaa na kusema kwanini Yule mama ananifatilia sana, nikashangaa akawa ananipigia pigia simu kumbe kuna kitu kinamvuta kuhusu mimi, sasa nikaumwa kumbe Mungu anazidi kutuweka karibu na Yule mama, akaniombea na mpaka kupona kabisa, na nyie mkapenda na kufanya muende kwake na sasa mmempeleka muhusika kwake kwahilo hilo ni jambo la kushangaza sana, muache Mungu aitwe Mungu tu”

    “Sasa tatizo baba katupa mtihani mkubwa sana, kuwa tumsaidie amuoe Yule mama, la sivyo hawezi kuruhusu mimi nikuoe wewe, yani hapo ndio pagumu hadi nawaza kwanini tumempeleka kwa Yule mama sababu kumuoa haitawezekana na kuhusu kunizuia mimi nisikuoe wewe hiyo haipo maana nakupenda sana Erica”

    “Erica wala msijilaumu kumpeleka kule, ile ni pona ya baba yenu na ataweza kuondokana na yanayomtatiza kwasasa.”

    “Ila baba yangu analalamika umemlia pesa nyingi sana, ni hela gani hizo?”

    “Hakuna hela ya baba yako niliyokula”

    Erica alianza kumueleza Erick kuhusu mchakato wa baba yao toka siku aliyokutana nae na alivyotaka kumuhonga simu jinsi alivyoiacha na kuondoka, na jinsi baba yake alivyopeleka milioni mbili, jinsi alivyorudisha pesa hiyo akiwa na mama yake na jinsi ya ile milioni kumi aliyoituma kwa Dora,

    “Ile hela yote niliiweka kwa Dora, nilikwambia ni mke wa Yule mzee ila haikuwa hivyo alikuwa ni hawara yake na Dora alisema nimpe yeye maana ndio anastahili kula pesa yam zee Jimmy”

    “Aaah nimekuelewa ila baba yangu huwa analalamika swala lingine kuwa kwenu alishatoaga posa, sasa ni posa gani hiyo?”

    “Tena umenikumbusha kitu, huwa anasema hivyo na madai yake aliacha hiyo hela mlangoni kwetu ila hakuna aliyeiona, na kama tungeiona basi tungemrudishia kwakweli. Yani hata nyumbani huwa wanashangaa kuhusu swala la yeye kutoa posa”

    Erick alikumbuka pesa ambayo aliikuta mlangoni kwakina Erica na karatasi ndani la kuonyesha upendo ambapo alijua ni Rahim ametuma, ila kwa maelezo ya Erick alihisi ni lazima baba yake ndio muhusika, aliamua kumuuliza

    “Alisema ni pesa ngapi?”

    “Eti zilikuwa milioni tatu”

    “Oooh kumbe!”

    Erick akamueleza Erica jinsi alivyochukua zile pesa akidhani kuwa ni Rahim kaziacha, kwahiyo alichukua kumkomesha.

    “Kumbe kweli ulichukua wewe, Dada Bite kila siku alikuwa anasema nikuulize ila sikufikiria kuwa wewe unaweza kuchukua pesa hiyo, nilijua ungechukua ni lazima ungerudisha”

    “halafu ninazo ndani kwangu kule hadi leo, kama ndio hizo zinamchanganya akili yake nitampeleka na ujumbe wake, yani mzee wangu jamani kwanini lakini? Hivi naweza hata dakika mbili kumuacha karibu yako, si atakubaka jamani loh! Erica nakupenda sana, sijawahi kumpenda mwanamke yeyote duniani kama ninavyokupenda wewe”

    Erica alikuwa akitabasamu tu, ni kweli bado hakuoana na Erick ila alijihisi raha sana kuishi nae pamoja.



    Rahim alivyopewa ujumbe na mama yake hakutaka hata kupoteza muda yani alitamani kesho yake ifike upesi ili akaongee vizuri na Zainabu, siku hiyo alianza kuishi na Salma tena, alikubali sababu aliona dalili ya yeye kumuoa Zainabu inaonekana kwahiyo alikubali swala aliloambiwa na mama yake kuwa aishi na Salma. Basi jioni hiyo alimuaga Salma na kutoka ila alienda kuongea na Babuu ili kesho yake waende wote kuongea na Zainabu kwani alimuona Babuu kuwa na busara zaidi yake.

    Salma alikaa nyumbani na kuwaza sana, kiukweli hakupenda mume wake kuoa mke wa pili kwani alihitaji ndani aishi mwenyewe tu, ila hakuwa na namna maana ndio ilishaamriwa hivyo kuwa Rahim atamuoa huyo Zainabu, basi alikaa kidogo kisha akajaribu kuongea na washauri mbalimbali akiwepo Yule mama kwenye simu,

    “Yani makubwa yalinipata mama yangu na mume wangu anataka kuoa mke wa pili, nimekubali maana sina namna na siwezi kumkatalia ila naona kabisa mume wangu atampenda sana huyo mke kushinda mimi”

    “Anaenda kuoa lini?”

    “Sijui ila kuna uelekeo maana huyo mwanamke washakamilisha mambo ya kujitambulisha na kesho anaenda kuongea nae ili aweze kumuoa kabisa”

    “Sasa mwanangu usiwe na presha, mimi ndio kungwi wa makungwi yani ukiwasiliana na mimi basi ndoa haiwezi kuwa tatizo kwako tena. Sasa basi usichukie kwa swala la mumeo kutaka kuoa mke wa pili wala nini, ila unatakiwa kufanya hivi”

    “Eeeeh kufanya nini?”

    “Basi leo mumeo hakikisha unampa mapenzi ambayo hujawahi kumpa, yani kama hujui kukatika basi leo jifunze kukatika yani mpe mapenzi hadi mumeo awaze kwanini anaenda kuoa tena wakati wewe upo! Kiu kubwa ya wanaume ni mpenzi tu, yani mwanaume anahangaika kulia na kushoto ila shida yake ni ngono basi. Kwahiyo wewe mwanangu leo jitahidi, nenda kanunue udi ujifukize kisha mumeo akute unanukia na umpe mapenzi ambayo hujawahi kumpa”

    “Asante sana, ngoja nifanyie kazi ushauri wako maana saa hizi katoka”

    “Basi mwali wangu huu ndio muda wako, kanunue udi, oga vizuri jifukize na akija muandalie maji ya kuoga yawe ya uvuguvugu uweke na iliki yanukie, kwahiyo akifika tu aoge halafu akimaliza, mfute na umpetipeti kiasi kisha muandalie chakula, hakikisha umepika chakula anachopenda ili akikiona aweze kula hiko chakula halafu akishiba mmalizie na chakula hiko kinachopendwa na wanaume wote yani muda wa kumpa hiko sasa nakutumia ujumbe namna ya kufanya hadi huyo mumeo leo ahisi umekuwa mpya”

    Salma alifurahi sana na kuagana na huyu mama kisha kwenda dukani kununua udi na vitu vingine alivyoelekezwa, kisha alivyorudi akafanya kama alivyoambiwa ambapo alipika chakula ambacho mumewe anakipenda lipomaliza akaenda kuoga na kujifukiza ule udi halafu alimsubiria mume wake sasa huku akisoma ule ujumbe aliotumiwa na Yule mama halafu akifanya mazoezi aliyoelekezwa na Yule mama ya jinsi ya kumvutia zaidi mumewe.

    Kwenye mida ya saa tatu usiku Rahim alirudi nyumbani kisha Salma akafanya kama alivyoelekezwa na Yule mama tena zaidi ya pale hadi Rahim alishangaa kweli kuwa mke wake kabadilika kiasi hiko, baada ya hapo alimfurahisha mumewe kwenye tendo, kwakweli leo Rahim alijishangaa hata huwa anaenda kutembea na machangudoa wa nini, sema kwavile alishaweka ahadi ya kumuoa Zainabu akaona hakuna namna inabidi tu kesho aonane nae na apange nae mipango ya ndoa, ila siku hiyo alilala akiwa na tabasamu zito kwa jinsi alivyofanyiwa na mkewe.



    Kesho yake mzee Jimmy alienda kwenye kazi zake na alipokuwa kazini akawaza swala la Yule mwanamke aliyesema kuwa na mimba ya Erick yani Sia, akaona kuna umuhimu wa kumtunza hata kama mwanae anakataa kufanya hivyo kwahiyo alijiandaa na kutoka kazini ili akamuangalie.

    Alipofika anapoishi Sia, alishangaa kumuona Steve nje akisombelea maji, huyu mzee alimuulizia Sia kwa Steve maana mara ya mwisho anakumbuka kuwa Sia alimtambulisha kuwa Steve ni mdogo wake akamuuliza,

    “Yuko wapi dada yako?”

    “Dada yangu yupi?”

    “Dada yako Sia, yuko wapi?”

    “Sia sio dada yangu ni Mke wangu, na muda huu ametoka”

    “Unasema ni mke wako?”

    “Ndio ni mke wangu”

    Mzee Jimmy alishangaa sana kuwa kuna nini pale maana Yule aliambiwa ni mdogo mtu, sasa kusikia mke tena alishangaa sana hapo, wakati anashangaa vizuri alitokea Dora kumbe naye alienda kwa lengo la kumfata mdogo wake kwahiyo alipomkuta mzee Jimmy pale alichowaza moja kwa moja huenda huyo mzee Jimmy anatoka na Sia maana kama aliendelea kutaka Erica anayetoka na Erick mtoto wake ni wazi anaweza kumtaka Sia ingawa anajua wazi kuwa Sia amewahi kuwa na mahusiano na mwanae, alimfata na kumuuliza kwa mshangao,

    “Wewe mzee vipi muda huu hapa?”

    “Nimekuja hapa kwa lengo la kuonana na huyu binti wa hapa Sia, maana alisema ana mimba ya Erick”

    “Kheee Sia ana mimba?”

    “Ndio, na cheti alinionyesha”

    “Hata usihangaike, hiyo mimba sio ya Erick ila ya mdogo wangu huyo Steve”

    Kisha Steve alivyosogea karibu, Dora alimtambulisha vizuri,

    “Huyu ni mdogo wangu anaitwa Steve”

    “Kheee basi huyu binti hafai kunidanganya mtu mzima hivi!”

    Mzee Jimmy alionekana kusikitika sana, ila Dora alimuangalia mdogo wake na kumwambia,

    “Hongera sana Steve huo ndio uanaume, kajipendekeza umemjaza mimba atalea mwenyewe na midawa yake”

    Kisha Dora akamuangalia mzee Jimmy na kumshawishi waondoke hapo, kwahiyo waliondoka bila hata kumchukua tena mdogo wake na bila ya kuonana na Sia.



    Ndugu wa Bahati kama walivyokubaliana waliongozana na Bahati siku ya leo hadi kwakina Erica, walifika na kugonga ambapo Bite ndio aliwafungulia mlango. Walikaribishwa ndani na kuingia, kiukweli mamake Erica alishangaa uwepo wao na walieleza azma yao ya kutaka kuonana na Erica, mama Erica aliwauliza kwa mshangao,

    “Mnataka nini leo, nyie si ndio mliondoka hapa kwa mnbwembwe!”

    Mama Bahati akaanza kujitetea,

    “Ni kweli tuliondoka na tumekiri makosa, tunaomba kwa huruma yenu tuweze kuonana na Erica”

    “Kwa taarifa yenu, Erica kajiozesha yupo huko kwa mwanaume alikojipeleka”

    Wale ndugu wa Bahati walishangaa sana, ila mama Erica hakutaka hata kuongea mengi zaidi ya kuwatimua tu kwahiyo ilibidi waondoke maana hawakuwa na namna zaidi ya kufanya.

    Walipoondoka, mama Erica aliamua kumpigia simu Erica ili amseme, Erica alipokea ile simu

    “Hivi wewe mtoto huna hata aibu, hayo mambo ya kujiozesha yameanza lini? Unajua laana wewe!”

    “Mama sikutaka kukukosea tena kwa mimba niliyonayo”

    “Mjinga wewe, unajua kabisa kubeba mimba nje ya ndoa ni dhambi na bado ukajibebesha na sasa umeamua kuishi na mwanaume ili kudhihirisha uzinzi wako. Sasa nakwambia ubaki huko huko yani hapa kwangu usirudi”

    “Jamani mama”

    “Nimemaliza, si wewe ndio mama basi jiite mwenyewe mama mie sitaki huo ujinga kabisa”

    Mama Erica alikata ile simu na kuanza kuongea na Bite,

    “Yani hili dogo lako halina akili hata kidogo, nadhani limechukua akili za Mage ambaye huwa wanashauriana kwenda kwenye matambiko maana naye alikimbilia kwa mwanaume, kuna mitoto kama imerogwa loh! Kujiozesha mwishowe ni kujuta, Mage anavumilia tu pale maana mwanaume mwenyewe hana mbele wala nyuma.”

    “Kweli mama, yani Erica kasoma ila kama hajasoma vile, mambo yake hakuna msomi anayeweza kufanya kama yeye. Bora Mage hajasoma kivile lakini Erica ni msomi ila mjinga kabisa yani”

    Walijikuta siku nzima wakisema kuhusu Erica tu maana aliwaudhi sana.



    Leo Rahim na Babuu walikutana na Zainabu na katika maelezo ya Zainabu alitaka kwanza waende kupima ukimwi na Rahim kabla ya kukubali kuolewa nae, hilo kwa Rahim hata halikuwa swala la shida maana hata wakati Salma ana mimba changa walienda kupima na alikuwa mzima kabisa kwahiyo alijiamini kuwa ni mzima kabisa, basi wakaondoka yeye, Babuu na Zainabu hospitali kupima tena walipima wote watatu.

    Walisubiri majibu huku wakiwa na furaha sana, majibu yalipotoka daktari alisema kila mtu apewe majibu yake ila Rahim alikuwa wa kwanza kupinga,

    “Daktari kwanini unataka kututenganisha hivyo? Sisi tumekuja pamoja kupima na tunataka majibu kwa pamoja”

    “Kama mmoja wenu kaathirika je!”

    “Sio tatizo maana tutampa moyo tu kuwa ni hali ya kawaida maana hatokuwa wa kwanza kuathirika”

    “Ila haitakiwi kufanya hivyo”

    “Mimi kama mkubwa wao hawa naomba utupe majibu kwa pamoja, huyu ni mdogo wangu kwahiyo ni muhimu mimi kujua afya yake, na huyu ni mke wangu lazima nijue afya yake na wao ni muhimu kujua afya yangu”

    “Na nyie wengine mnasemaje?”

    “Sawa hakuna tatizo”

    Walijibu kwa pamoja maana walijikuta wakijiamini sana ila walijua ile kusema kama mmoja wenu kaathirika je, ndio kauli za madaktari ili kuwatisha tu.

    Basi daktari hakutaka kubishaba nao sana na kuamua kuwapeleka ofisini tu kuwapa majibu yao.

    Waliingia ofisini wote kwa pamoja yaani Babuu, Rahim na Zainabu. Daktari aliwapa majibu yao ambapo Babuu na Zainabu walikuwa wazima ila Rahim alikutwa kaathirika yani baada ya majibu yale Rahim alizimia bila hata kusikiliza ushauri wala nini.



    Basi Erica alikosa raha kabisa tangu muda amepokea simu ya mama yake yani alijihisi vibaya sana kwenye moyo wake, ila siku hiyo alifikiwa na mgeni aliyekuwa ni Tumaini na kushangaa maana ni muda sana hakuweza kuongea na Tumaini kutokana na chuki ambayo ipo kati yao na hata haijulikani ni nini chanzo, ila siku hiyo ambayo Tumaini alienda mwenyewe akaona ndio siku pekee ya yeye kuweza kuongea nae na kumaliza tofauti zao ambazo ziliibuka tu.

    Ila kabla hajaongea na Tumaini alipigiwa simu na kaka yake kuwa waonane aweze kumtambulisha huyo wifi yake, ila kwavile hakuweza kumwambia Tumaini kuwa aende nae au amwache halafu aende akaamua kwa muda huo amwambie tu kaka yake aende kule na huyo wifi yake,

    “Mbona unaniambia huko Erica?”

    “Wewe njoo tu na maelezo mengine utayapata huku huku”

    Basi kaka yake alikubali kufanya hivyo na kwavile eneo walilokuwepo halikuwa mbali sana na pale kwahiyo alichukua muda mfupi sana kufika pale nyumbani kwa Erica.

    Waligonga mlango na Erica kwenda kufungua, akaingia Tony na mdada mwingine, ila Erica alipomuona huyu mdada alijikuta akijawa na chuki isiyo na mfano kabisa maana huyu dada alikuwa ni Doroth yani yule daktari aliyemdai Erica laki moja ili amfichie siri.





    Waligonga mlango na Erica kwenda kufungua, akaingia Tony na mdada mwingine, ila Erica alipomuona huyu mdada alijikuta akijawa na chuki isiyo na mfano kabisa maana huyu dada alikuwa ni Doroth yani yule daktari aliyemdai Erica laki moja ili amfichie siri.

    Erica alimkaribisha yule dokta kwa kinyongo sababu alikuwa na chuki nae sana ila kwavile yule dokta alionyesha kama kutokumkumbuka Erica, basi akaamua amkaribishe ndani ili amkumbushe vizuri.

    Walipokuwa wanaingia ndani walikuta Tony akikumbatiana na Tumaini sababu Tony alitangulia kuingia ndani utafikiri nyumba yake, ilionyesha kuwa Tony na Tumaini wanafahamiana, Erica na Doroth walikaa tu wakiwaangalia.

    Tumaini na Tony walikaa huku wakicheka kwa furaha, Tony akaanza kumwambia Tumaini,

    "Kheee umebadilika, umependeza, umenenepa. Siri ya mafanikio Tuma?"

    "Hamna bhana ni kuridhika tu"

    "Unajua sikutegemea kukuona kabisa, duh ni kitambo sana jamani yani sikutegemea Tumaini"

    Kisha akamuangalia Erica na kumuuliza,

    "Erica, umefahamiana vipi na huyu?"

    Erica akamjibu kaka yake,

    "Nitakwambia tu maana lazima utamfahamu zaidi ya hivyo unavyomfahamu, ila kwanza tuongelee kuhusu uliyefika nae hapa, nitambulishe tafadhari"

    "Aaaah hadi nimesahau jamani, (akamuangalia Tumaini na kusema) unaona Tumaini hadi umenisahaulisha mada yangu niliyokuja nayo loh! ( kisha akamuangalia Doroth na kusema) Sorry kipenzi yani kuna mtu amenichanganya hapa, sikutegemea kumuona. Ila huyu ndio yule mdogo wangu niliyesema nataka umuone anaitwa Erica, halafu Erica huyu ndio yule wifi yako niliyesema nataka ufahamiane nae anaitwa Tumaini oooh sorry jamani ni anaitwa Doroth"

    Erica akacheka, wakati huo Doroth aliinuka ili kupeana mkono wa kufahamiana na Erica.

    Ila Erica aligoma kupokea mkono huo kisha akasema,

    "Hivi nikuulize unanikumbuka?"

    "Hapana"

    "Wewe ni Dokta! Nimejuaje kazi yako na Tony hajaisema?"

    "Ni kweli mimi ni dokta, unaweza kunifahamu sababu nahudumia wagonjwa wengi sana ila ni ngumu kwa mimi kukumbuka kila mgonjwa"

    "Hata unaowatapeli na kuwafanyia roho mbaya huwakumbuki pia?"

    "Hakuna ninayemfanyia roho mbaya"

    "Sawa umejibu vyema sana, basi hao wagonjwa huwa unawahumiaje?"

    "Vizuri tu"

    "Wewe Dokta hebu muogope Mungu jamani, unahudumia vizuri wagonjwa wewe!"

    Tony aliingilia kati na kumuuliza dada yake

    "Kwani tatizo nini Erica eeeeh!"

    "Ngoja niseme, Doroth sina siri tena kwasasa maana nitaeleza hapa ili wajue ulichonifanyia halafu kaka utaamua yani kama kuendelea na huyo mwanamke au la! Sisemi umuache ila nataka kusema kile alichonifanyia mimi, sijui kwa wagonjwa wengine ila nazungumzia mimi."

    "Sema Erica, sema kila kitu ili nisikie vizuri kakako"

    "Siku moja nilipata matatizo ikabidi nijifanye naumwa ila sikuwa naumwa kweli yani nilifanya vile ili kuepuka matatizo, nikapelekwa hospitali na kumkuta dokta huyo Doroth, ila nilimuomba amwambie Erick atoke ili nibaki mimi na yeye, na alifanya hivyo. Nilimwambia ukweli kuwa siumwi ila amwambie Erick kuwa nina vidonda vya tumbo, akakubali na kusema nimpe laki moja, nikamwambia mimi nina elfu thelathini tu akaikataa katakata lakini nikampa ile elfu thelathini nikamwambia nyingine nitaenda kummalizia, akagoma kabisa akasema hadi niache simu yangu, ikabidi niache simu ndio akaweza kuniruhusu. Sasa wakati naondoka na Erick, aliulizia simu yangu nikamwambia nimeisahau hospitali, Erick akasema lazima tukaifate. Tulivyofika hospitali nikaenda kwa dokta huyu na kumueleza kila kitu ila akagoma kutoa ile simu najua alinifanyia mimi makusudi tu maana hakujua kama kuna kitu ambacho mimi naweza kumsaidia. Basi ilibidi nimpigie simu kijana mmoja ambaye alituma ile laki moja kwa huyu dokta ndio akaniruhusu niondoke na simu yangu, nikamuomba zile elfu thelathini zangu za mwanzo akagoma kabisa eti akasema zile ni za usumbufu, niliumia sana roho ila sikuwa na la kufanya. Nikaondoka ila tulivyofika hoteli kula na Erick nikaona si vyema niendelee kuongopa, bora nimwambie Erick ukweli, nikamweleza naye akachukia sana na kuondoka, sasa na mimi nilivyotaka kuondoka ndio nikaletewa bili ya pale na sikuwa na hela yoyote, kumbuka huyu dokta amezikomba zote. Siku ile siwezi kusahau, nilidhalilishwa mimi pale hotelini, niliosha vyombo usiku kucha. Ila chanzo ni huyu dokta asiye na huruma, kila siku namuota kwa ujinga wake alionifanyia"

    Tony alimuangalia mdogo wake, kisha akamuangalia Doroth aliyekuwa kajiinamia tu, akamwambia

    "Siku zote waswahili husema usimtendee mtu kitu ambacho hupendi wewe kutendewa, Erica mdogo wangu pole sana. Nimejaribu kujiweka kwenye nafasi yako ila imeniuma, laki moja kuficha siri? Kwani anatoa mimba au?"

    Tumaini akaongea,

    "Tena sio laki moja ni laki na elfu thelathini"

    Tony akamuangalia Doroth na kumwambia,

    "Kwanza mpe mdogo wangu laki mbili kwa ukatili uliomfanyia, kisha mlipe hela yake"

    Doroth alibaki kimya tu kwani alihisi kama kuonewa vile ingawa alikumbuka fika alichomfanyia Erica, basi Erica akasema tena,

    "Yani wewe nadhani hujui ethics za udokta, yani ulichonifanyia siku ile hakikuwa sawa kabisa. Madokta huwa ni marafiki wakubwa sababu inajulikana kuwa wanaifahamu saikolojia vizuri, sasa wewe ni dokta gani usiye na huruma jamani! Halafu mpaka muda huu upo kimya tu yani hujui hata kusema samahani, kaka ndio mwanamke wa kuoa huyu!! Hapana kwakweli"

    Kikweli Doroth alihisi aibu sana na kuamua kuongea,

    "Jamani sikia wifi yangu, sikujua kama nitalutana tena na wewe na sikujua kama utakuja kuwa wifi yangu. Naomba tusahau yaliyopita"

    "Kirahisi rahisi hivyo eeeeh! Eti tusahau yaliyopita, yani unaongea au unatapika? Nilitamani sana siku moja uingie kwenye anga zangu"

    Yani leo hata Tumaini alimshangaa Erica kama huwa ni muongeaji kiasi kile maana kila siku huwa anaishia kulia tu ila siku hiyo alikuwa kama kalishwa pilipili vile.

    Doroth aliona aibu na hakutaka kuumbuka zaidi, kwani akainuka na kutoka, Tony akainuka pia ili kumfata ila Erica alimshika mkono na kumrudisha ndani na kumwambia,

    "Kaka, unaenda wapi? Yule kajionyesha wazi kuwa si mwanamke wa kuolewa na wewe yani hata neno samahani halijui! Kaka ndio mwanamke gani wa kuolewa na wewe yule!"

    Ila Tony yalimuingia akilini yale maneno ya Erica, muda huo Tumaini nae akaongea,

    "Ila Erica ulisema unatuambia kisa cha huyo dokta na uamuzi wa kuendelea nae au kutokuendelea nae atafanya mwenyewe Tony au maneno yako ya mwanzo umeyasahau?"

    "Hamna sijayasahau ila Tumaini umemuona mwanamke mwenyewe mambo yake yalivyo, haya Tony kaa kwanza unieleze kufahamiana na Tumaini imeanzia wapi"

    Tony alikaa chini kwani hakwenda tena kumfatilia Doroth, kisha Erica aliinuka na kusema

    "Ngoja niende jikoni niandae kidogo chakula"

    "Sasa Erica, mbona hujaniambia hapa ni wapi?"

    "Nitakwambia tu Tony usijali"

    Kisha Erica aliinuka na kwenda jikoni.



    Ikabidi Babuu na Zainabu wamsubirie Rahim akipewa huduma ya kwanza, kwahiyo walitoka nje na kukaa kwenye mabenchi ila ilionyesha kuwa Zainabu alikuwa na mawazo sana, kitu kilichofanya Babuu asogee na kuongea nae,

    "Mbona una mawazo hivyo Zainabu? Unajua sio vizuri kuwaza kiasi hiko?"

    "Aaah hamna bhana, ila nina mawazo sana sababu imekuwa kama nina mkosi vile, akitokea wa kunioa tu basi namkuta na majanga"

    "Majanga gani? Na wangapi walipatwa na hayo majanga?"

    "Yani huyu ni wa pili, wa kwanza nilimkuta kaathirika hivi hivi"

    "Hivi Zainabu hujawahi kuwa na mpenzi wewe?"

    "Ninahitaji mume ila sio mpenzi"

    "Nikwambie kitu Zainabu"

    "Niambie"

    "Yani Zainabu ni kwavile ndugu yangu aliwahi kusema ila nilitamani sana ungeolewa na mimi. Naona ni binti unayejielewa sana ndiomana umechagua kupima kwanza. Nakuomba mipango ya ndoa iendelee baina yetu maana kama kupima tushapima na vilevile tunaendana kwahiyo bora tuoane tu"

    Zainabu alitabasamu tu bila ya kujibu chochote kile. Babuu aliendelea kuongea,

    "Jamani mpenzi, umetabasamu tu. Naomba tuwe pamoja"

    "Yani wewe Babuu, swala la Rahim halijaisha na tayari ushaweka mada yako jamani! Ngoja kwanza haya yapite"

    "Wakati tunangoja nikubalie, jua mimi ndio mumeo kwanza sijawahi kuoa na wewe hujawahi kuolewa, sina mtoto na huna mtoto huoni kama ni vizuri mimi na wewe kuwa pamoja?"

    Rahim aliruhusiwa na daktari na alienda nae hadi alipokaa Babuu na Zainabu na kuanza kuongea nao kuwa ile hali waione ya kawaida na wawe wanampa ushauri. Basi walipomaliza kuongea na yule dokta, waliongozana na kurudi nyumbani ambapo getini tu Rahim aliwaambia waondoke na wamuache mwenyewe aingie ndani kwake,

    "Nyie ondokeni, niacheni men yea niende ndani ila yaliyotokea hospitali ibaki kuwa siri yenu jamani yani sitaki mmwambie yeyote kuwa nimeathirika. Tumeelewana?"

    "Ndio tumekuelewa"

    Kwahiyo ilibidi wafanye hivyo tu na kuondoka.

    Rahim aliingia ndani na kupokelewa na mke wake Salma, kwakweli alikuwa anaona ajabu sana sababu Salma alikuwa akitenda mambo ambayo hajawahi kuyafanya kabisa kabisa, aliona mke wake kabadilika ila atamwambia vipi swala la yeye kuwa na ukimwi? Aliona hilo ni jambo baya sana kwake.

    Alimwambia amechoka na anaenda kupumzika ila Salma akamuuliza,

    "Mume wangu, mke mwwnzangu Zainabu hajambo?"

    Rahim akatikisa kichwa kisha akamjibu,

    "Sio mke mwenzio tena yule, mimi sioi tena mke wa pili. Unanitosha wewe tu"

    Salma hakuamini ile kauli, alienda kumkumbatia mume wake kisha kumuacha akapumzike, kwakweli Salma alijiona ni mshindi kwa siku hiyo yani aliona hajawahi kushinda kama hivyo, alimpigia simu na yule mama kumwambia habari zile,

    "Nilikwambia mwali wangu, hapa ndii mwisho yani mambo yote ya kumfanyia mumeo uwe unaniuliza, sijui kuna chakula huwezi kupika niulize nikufundishe"

    "Asante sana yani sana, umeokoa ndoa yangu. Nakutafutia zawadi mama nitakuletea"

    Salma aliongea kwa furaha sana na mama huyu.



    Erica alipeleka juisi sebleni ili Tumaini na Tony wanywe, halafu akawakaribisha, walipokuwa wakinywa ndipo Erica akauliza sasa,

    "Eeeh kaka niambie, umefahamiana vipi na Tumaini?"

    "Yani huwezi amini, Tumaini nilisoma nae shule ya msingi. Kipindi hiko alikuwa mwembamba ila nashangaa saivi kawa bonge"

    Erica akacheka na kusema,

    "Kipindi hicho ilikuwa utoto ila saivi ni ukubwa, ila huoni kuwa kapendeza"

    "Ndio, amependeza sana yani leo nina furaha sana"

    Erica akatania,

    "Kwahiyo hadi umemsahau Doroth, na wewe na majina ya D sijui vipi!"

    "Aaaah achana na hizo habari bhana, yule acha aende ila lengo la kuoa lipo kwenye akili yangu bado"

    Erica akatania tena,

    "Si umuoe Tumaini tu!"

    Tumaini akacheka na kusema,

    "Wewe Erica wewe sijui leo umekunywa nini jamani yani unaongea kama kitu gani vile! Sasa Tony anioe mimi kweli wakati ana mwanamke wake!"

    "Lakini kumbuka huyo mwanamke wake hamtaki tena"

    Tumaini akacheka tu, halafu Tony akaongezea

    "Erica mambo ya Tumaini na mimi hebu yaache kwanza. Ila Tumaini ndio unaishi hapa?"

    "Hapana hapa nimekuja tu kumtembelea Erica"

    Ilibidi Tony amuulize vizuri dadake ambaye aliamua kumueleza ukweli tu,

    "Kwahiyo Tumaini ni dada wa Erick?"

    "Ndio, ni ndugu yake"

    "Sasa Tumaini, hapa leo tutaondoka wote ili nikapafahamu kwenu au unasemaje?"

    "Hakuna shida"

    Na kweli pale waliongea weee na muda wa kuondoka ni Tumaini na Tony waliondoka pamoja.

    Jioni ilipofika alirudi Erick ambapo alipopumzika kidogo tu Erica akaanza kumueleza yaliyotukia siku hiyo ila tu hakuweka ile sehemu ya kusema na Doroth, alieleza tu kuwa kakake alifika na kaonana na Tumaini na ilivyokuwa kwenye maongezi,

    "Kheeee Tumaini alikuja hapa kumbe! Kweli dadangu kabadilika jamani!"

    "Hadi nilishangaa ila sijaweza kuongea nae chochote maana ndio kaka yangu alifika"

    "Kwahiyo inaonyesha wamepatana sana eeeh!"

    "Ndio sana, yani sijui kama hawajatongozana wale maana macho yao tu yalionyesha wanatakana"

    "Hahaha Erica bhana, muache dada yangu nae apate mpenzi maana sijui kama ana historia ya kupata mpenzi"

    "Unadhani kwanini?"

    "Nafikiri ni muonekano wake, yupo serious sana labda ndio sababu ya vijana kuogopa kumtongoza na hata hivyo nadhani wanaojaribu huwa anawajibu vibaya sana maana yule kajengewa dhana mbaya na mama yake kuwa wanaume ni viumbe wabaya, si unajua mamake alitendwa na baba ila kwa jinsi sisi tunavyopendana ndio na yeye ameona radha ya mapenzi, kwa maana hiyo kama huyo Tony atakuwa na lengo kweli basi atamkubali"

    "Mmmh hivi itakuwaje, mimi na wewe halafu Tumaini na Tony!"

    "Aaaah hizo habari tuziache Erica maana watajuana wenyewe, sisi tujali tunavyopendana tu"

    Kisha Erick akamsogelea Erica na kumkumbatia, ambapo Angel nae alitoka chumbani na kukumbatiwa pamoja nao.

    Kisha walienda kula, wakati wanakula simu ya Erica tena ikaita na mpigaji alikuwa ni mamake, Erica akawaza kuwa muda huo mamake anataka kusema kitu gani, akaacha kula na kuinuka kisha akapokea ile simu na kuongea nayo,

    "Erica, nakupa wiki moja uwe umeleta hayo matendegu yako nyumbani, wewe mtoto usitake kunipanda kichwani. Narudia tena, nakupa wiki moja, siwezi kuendelea kuvumilia huo ujinga unaofanya"

    "Lakini mama"

    "Hakuna cha lakini, nishasema nimemaliza kwakweli maswala ya lakini sitaki kuyasikia, mwambie huyo huyo mjinga mwenzio lakini sio mimi. Nimemaliza"

    Simu ikakatika ila Erick alikuwa nyuma ya Erica yani muda alivyoinuka kuipokea ile simu na Erick nae aliinuja na kusimama nyuma yake, alimkumbatia kwa nyuma kama kumbembeleza,

    "Usijali Erica, usiwe na mawazo wala presha. Wala hiyo wiki haitafika kwani mimi nitahakikisha tunaenda kufanya taratibu zote kwenu"

    "Na kwenu je watakubali?"

    "Usijali kuhusu kwetu maana mama anakaribia kurudi, na nikimwambia swala la wewe kuwa mjamzito ni lazima ataomba mwenyewe kuwa akaongee na mama yako. Wakiongea wamama watupu najua kuna uelewa utakuwepo yani hata usihali mpenzi wangu"

    Erica alijihisi raha sana kwavile alivyoambiwa na Erick, na jinsi alivyomshika ndio alijisikia furaha zaidi kisha wakaenda tena kula na walipomaliza walikaa kidogo na kwenda kulala.

    Wakati wamelala kuna ujumbe uliingia kwenye simu ya Erick, ilikuwa ni usiku sana ila alichukua simu yake na kuangalia ule ujumbe akakuta umetoka kwa baba yake,

    "Erick, siku hizi hurudi nyumbani unazamia kwa wanawake. Hao ni viumbe wa kupita tena hawana thamani kama wazazi yani unasahau mzazi sababu ya mwanamke? Sijapenda hilo swala kabisa, na umeishia wapi kuhusu swala la kuongea na Ester ili awe mama yenu Serious Erick usipofanya hivyo na mimi nitasahau kuhusu ubaba, yani hutomuoa huyo mdudu wako Erica"

    Erick alisoma ule ujumbe wa babake mara mbili mbili ila aliona utamuumiza kichwa tu, hivyo alimsogelea vizuri Erica na kumkumbatia na kuendelea kulala.



    Kulipokucha Erick alijiandaa kwenda kwao ila hakuweza kuondoka mapema maana kuna mambo alikuwa akipanga na Erica, kwahiyo alipomalizana nae alipita kuyakamilisha kisha ndio akaenda kwao kutokana na ujumbe ambao baba yake alimtumia usiku kwani alijua kinachomsumbua babake pengine ni zile milioni tatu kwahiyo alitaka akaongee nae na amkabidhi pesa yake.

    Alifika kwao na kumkuta dada yake, ingawa alienda kwenye mida ya saa tano asubuhi ila alimkuta dada yake yupo siku hiyo wala hakwenda dukani na alionyesha kuwa na furaha sana kupita siku zote, alimsalimia na kuanza kumuuliza

    "Kwanza kabla ya yote, mbona unafuraha sana Tumaini"

    "Aaah kawaida tu"

    "Mmmh sio kawaida jamani, hilo tabasamu zito hivyo silionagi ujue. Kuna kitu lazima kimekufurahisha"

    "Hakuna kitu Erick, ni kawaida tu"

    "Basi ngoja nikwambie jambo lingine, huyu mzee yupo kwanza?"

    "Awepo wapo saa hizi? Kaondoka muda tu"

    Basi Erick alimuonyesha ule ujumbe ambao ulitumwa na babake usiku, Tumaini alishangaa sana ila akamwambia jambo kakake,

    "Hivi Erick, kwanini tusiende kwa yule mama na tumueleze kila kitu kuhusu baba yani tusimfiche kitu. Yule mama ana busara sana, kwa hakika atatushauri vizuri"

    Erick aliafikiana na dadake kuwa waende kwa yule mama wakaongee nae.

    Basi Tumaini akaenda kujiandaa ili waende kwa huyo mama.

    Wakiwa njiani Erick alimuuliza dada yake,

    "Na mbona leo hujaenda dukani?"

    "Sasa Erick ningeenda tungewezaje kwenda huko?"

    Kabla Erick hajasema kingine walimuona Dora njiani na kusimamisha gari kumsalimia na kuongea nae, Tumaini akatania,

    "Nakuona mama yetu mdogo"

    Erick akamuangalia dada yake kwa kuchukia kitu kilichomfanya Tumaini acheke sana, basi Dora akawauliza kuwa wanaelekea wapi, Erick akamjibu,

    "Tunaenda kwa yule mwanamaombi"

    "Aaaah nikajua mnaenda kwa Sia"

    "Kufanya nini?"

    "Jana nilimkuta huko baba yenu akidai kuwa Sia ana mimba yako ila nilimwambia ukweli kuwa mimba ya Sia ni ya mdogo wangu Steve"

    Hapo Erick alitabasamu ba kujikuta akifungua wallet yake akatoa laki moja na kumpa Dora kisha akamwambia,

    "Vizuri sana Dora, kuna watu kama wewe Duniani kwa kazi maalum kabisa, nakupongeza sana maana baba yetu anajua ukweli kwasasa"

    Dora alipokea ile hela huku akitabasamu na kuwaambia kuwa wamsalimie mama wa maombi. Kisha Erick na Tumaini wakaagana nae na kuondoka zao.



    Walifika kwa mama wa maombi na kumkuta ameshika kitabu cha nyimbo, akiimba imba, walimsalimia na kuanza kuongea nae.

    Tumaini alimueleza kila kitu huyo mama hadi kuhusu baba yao kumtaka Erica na kumfumania akiwa na Dora, yule mama alisikitika sana na kuwaambia,

    "Baba yenu anatakiwa kuwa makini sana, kuwa na pesa sio kila kitu katika maisha kwani kwenye maisha kuna kitu kinaitwa furaha je baba yenu anahangaika na wanawake mbali mbali, swali ni je ana furaha? Furaha hana ila amejaa laana na machozi ya wanawake mbalimbali, mama zenu kawazalisha na kuwaacha unadhani ni kiasi gani wamelia kuhusu yeye? Ngoja nikwambie na wewe Erick, usiache chozi la mwanamke litoke sababu yako maana utajiona huna furaha kamwe sababu ya chozi la mwanamke, baba yenu sikumkubali toka enzi hizo sababu ya matendo yake, alijivuna kuwa kwao wanapesa nyingi, aliwadharau wengine na kusahau kuwa yale ni maisha tu na yanapita. Hiyo ni sababu kubwa ya mimi kutokuwa na baba yenu"

    "Sasa katupa mtihani kuwa eti wewe ukubali kuwa nae halafu ndio atamruhusu Erick kuoa"

    "Yani hata msipate shida wanangu, mwambieni baba yenu nimekubali halafu mwacheni aje niongee nae nahitaji kumfundisha. Asifanye makosa aliyoyafanya, kashamaliza wanawake wengi, achukue kati yao aoe sio anataka tena mwanamke mpya"

    Tumaini akamuuliza huyu mama swali,

    "Ila inaonyesha una uelewa mkubwa sana, hivi mapenzi ni nini?"

    Erick alicheka sana maana alihisi kuwa dadake kuna mtu kashapendana nae ndiomana anaanza kuuliza kuhusu mapenzi,

    "Sasa mkitaka niwafundishe vizuri hiyo mada mnifate kwa muda mwingine ila mapenzi ni mazuri sana mkipendana"

    "Na unajuaje kama ndio mnapendana?"

    Erick alimkatisha dada yake,

    "Si amesema tuje siku nyingine dada! Nitakuleta usijali"

    Basi wakamuaga akawafanyia maombi pale na kuondoka, walipokuwa kwenye gari Erick alimuuliza dada yake,

    "Kuna mahali umependa nini dada?"

    "Wewe nae hebu achana na hayo maswali (kuna mtu alimuona njiani na kumwambia Erick) Hebu simama, yule kijana namjua"

    Erick alisimamisha gari na Tumaini kufungua kioo na kumuita,

    "Derick"

    Alikuwa ni Derick yule ndugu wa Erica ila alionekana kama hasikii vile, ikabidi Erick apige honi ndio akageuka kisha Tumaini akashuka na kuonana nae, walimsalimia na kumpa lifti ila Derick alionekana kutokuwa na furaha kabisa hata Tumaini alishangaa sana kuwa Derick aliyemzoea kapatwa na nini, ila hakuelewa kwakweli. Walifika mahali ambapo Derick alisema anashuka na kumshusha kisha Erick alimpeleka dadake nyumbani na kumshusha halafu yeye akarudi kule alipokuwa akiishi na Erica.

    Alifika nyumbani na kumkuta Erica yupo nje anacheza cheza na Angel.

    Basi akapaki gari yake na Erica alisogea karibu na kumsalimia kisha akamwambia,

    "Bora umerudi mapema, hakuna mboga leo Erick?"

    "Si ungenipigia tu simu"

    "Simu yangu sijaweka salio"

    "Basi tusiongee sana, twende tukanunue hiyo mboga"

    Erica alisogea kwenye nyumba yao na kufunga milango kisha akaelekea na Angel kwenye gari ambapo alikaa naye mbele.

    Walifika na kununua mboga wanayotaka kisha kuanza safari ya kurudi.

    Wakati wanarudi Angel aling'ang'ania kukaa kile kiti cha nyuma ikabidi Erica amuweke kile kiti cha nyuma.

    Walipofika nyumbani wakati wanashuka kuna karatasi Angel alikuwa amelishika, Erica alilichukua na kulisoma kisha akashangaa sana na kumpa Erick, naye alishangaa pia, kisha Erica akasema

    "Hili jina ni la ndugu yangu Derick, inamaana ana ukimwi? Limefika vipi huku?"

    Erick alimueleza Erica jinsi walivyokutana na Derick hadi kumpa lifti kwenye gari,

    "Itakuwa ndiomana hakuwa na furaha, labda ndio alitoka kupima"

    "Si unaona ni tarehe ya leo, mmmh makubwa"

    "Erica mke wangu, ukimwi unasambaa kwa kasi sana naomba uwe muaminifu"

    "Mimi ni muaminifu Erick, nakupenda kweli"

    Erick alisogea na kumkumbatia Erica kwa furaha kisha kuingia nae ndani.



    Kesho yake wakati Erica ametulia akicheza na Angel, akapokea simu kwa namba ngeni na kupokea.

    "Mimi Doroth nahitaji kuja kuongea na wewe"

    "Karibu"

    "Nitakuja na ndugu yangu"

    "Karibu"

    Erica alijua wazi kuwa Doroth anataka kuomba msamaha, basi akamuacha afike nyumbani kwake na akajua wazi anaenda na ndugu yake ili amsaidie kuomba msamaha.

    Basi muda kidogo Doroth alifika nyumbani kwa Erica na kugonga mlango, basi Erica akaenda kufungua ila alipomuona Doroth alihisi tena kuchefuka, ila alichefuka zaidi baada ya kumuona mtu ambaye aliongozana na Doroth maana alikuwa ni meneja wa ile hoteli ambayo walimpa adhabu ya kuosha vyombo, Erica aliwaangalia kwa chuki na kusema,

    "Kumbe nyie ni ndugu na wote mna roho mbaya, jamani hakuna mnachoweza kuongea nikawaelewa. Kwaherini"

    Erica alifunga mlango wake na moja kwa moja alimpigia simu kaka yake Tony,

    "Kaka yule mwanamke Doroth hakufai kabisa, ni mbaya na ukoo wake wote"

    "Erica, kwanza huyo mwanamke nishamsahau uwepo wake kwasasa, wifi yako mwingine yupo"

    "Yuko wapi? Ni nani?"

    "Tulia tu utamfahamu"

    Erica alijikuta akiwa na hamu sana ya kumfahamu huyo wifi yake mpya ila kaka yake hakumtaja kabisa zaidi ya kumfanya Erica kuwa na hamu ya kumfamu huyo wifi yake mpya.

    Basi simu ilikatika na Erica kuendelea na mambo mengine, alishangaa muda huo akipigiwa simu na Derick, alishangaa sana na kupokea,

    "Niambie Derick"

    "Nahitaji kuonana na wewe"

    "Kwema huko?"

    "Nimekwambia nahitaji kuonana na wewe"

    Kwajinsi Derick alivyokuwa anaongea Erica alihisi tu kuwa hakuna jambo jema pale kwahiyo akaamua kumgelesha,

    "Njoo nyumbani kwetu utanikuta"

    "Sitaki kwenu, nahitaji kuonana nawe sehemu nyingine"

    "Mmmh wapi?"

    "Hotelini"

    "Kufanya nini?"

    "Wewe njoo tu utajua huku huku"

    "Wewe huna nia nzuri, unataka kunibaka eeeh! Maana ni ndugu yangu ila kutwa kucha unanitamani, unataka umuambukize nani maukimwi yako"

    Derick alikata ile simu baada ya ile kauli ya mwisho, Erica aliona kamjibu sawa maana Derick huwa haaminiki kabisa.



    Ilifika siku hiyo ambayo Tony aliwapigia simu nyumbani kwao kuwa anaenda kumtambulisha mchumba wake rasmi, mama yake alimuuliza sana

    "Sio kimeo huyo?"

    "Sio mama, ni mtu anayejielewa"

    "Kama kimeo nadhani unanitambua vizuri maana nitamtimua"

    "Sio kimeo mama"

    "Haya mlete"

    Kwahiyo siku hiyo hadi Mage alienda ili kumuona huyo mchumba wa Tony.

    Muda ulipofika Tony alifika na mchumba wake, kwakweli mama yao alikuwa wa kwanza kuhamaki,

    "Yani Tony mchumba mwenyewe ndio umemleta huyu Tumaini?"

    Dada zake nao walitoka kumuangalia.





    Muda ulipofika Tony alifika na mchumba wake, kwakweli mama yao alikuwa wa kwanza kuhamaki,

    "Yani Tony mchumba mwenyewe ndio umemleta huyu Tumaini?"

    Dada zake nao walitoka kumuangalia.

    Bite alishangaa pia na kusema,

    "Huyu si ndio dadake Erick, watoto wa yule mzee!"

    Mama yao akajibu,

    "Ndio mwenyewe na licha ya hivyo ni hana adabu huyu binti hata kidogo, nishawahi kumkuta akimpiga Erica sio mara moja kisa tu hataki mahusiano ya Erica na kaka yake, sasa na yeye ndio kafanya nini hapa kama sio ujinga jamani? Wewe Tumaini nilijua huna mpango wa kuwa na mwanaume maana ungekuwa na mpango basi usingekuwa hivyo ulivyokuwa yani ungejua kabisa usimtendee mwenzio"

    Mage nae akaingilia kati,

    "Kumbe mtu mwenyewe ndio huyu loh hata mimi simtaki awe wifi yangu, Tony huyu meanamke hatumtaki"

    "Jamani hii familia sasa hapana jamani, mimi umri umeenda nitamuoa nani? Wengine nimeona pengine siwafahamu vizuri ila huyu Tumaini namjua vizuri hadi kwa mamake napajua alikuwa ni mwalimu wetu halafu leo mnanikatalia kweli? Jamani huyu Tumaini na Erica mbona wanapatana"

    "Kama wanapatana, mwambie aje hapa mguu wake, mguu wa Erica. Halafu Tony mdogo wangu yanu Erica awe na kaka mtu na wewe uwe na dada mtu uliwahi kuona wapi hiyo?"

    "Sema wewe Bite, yani hawa watoto wananiletea laana tu jamani utafikiri kuna jambo baya nilitenda jamani, yani kweli kabisa Erica na Tony wa kunifanyia hivi mimi! Mnaenda kuniletea wachumba kwenye maukoo yaliyotengwa huko, maukoo yenye laana. Baba yao hawa ni ana laana mpaka unyayoni sasa bila aibu na wewe umeenda kulivaa hilo furushi jamani loh!"

    Bite akasema tena,

    "Kwanza mwanamke mwenyewe hata haendani na wewe, mwanamke bonge utafikiri anakunywa mafuta"

    Ile hoja ilionekana kumchukiza Tumaini na kujikuta akikimbia mahali pale, alitoka nje ya geti la kina Erica na kujikuta akimwaga machozi tu, yani kitu ambacho hakukipenda ni mtu kumsema sababu ya ubonge, yani hali ya kuwa mnene ilimfanya ajione kuwa na kasoro kubwa sana. Ila Tony nae akatoka kwani hakutaka kuendelea kusikiliza nyumbani kwao, alimkuta Tumaini akilia na kuamua kuondoka nae tu.

    Pale ndani waliona bora kaondoka, wakarudi ndani wakiongea ila mama yao akawasema,

    "Ila Bite sio vizuri kumsema yule sababu ya ubonge wake"

    "Ila mama, si unaona kaondoka mwenyewe, mabonge wengi hawapendi kusemwa?"

    Wakacheka kwa pamoja, ila Mage nae akasema,

    "Lakini kumkataa mtu sababu ya maumbile yake sio vizuri, tuchukue sababu nyingine tu"

    "Wewe nae lazima utetee maana ulivyojifungua tu ukabongeka"

    "Ila mama, mbona hata wewe sio mwembamba jamani!"

    "Hujaona picha za usichana wangu, nilikuwa nadai mimi ila kuzaa nyie wote unafikiri mchezo na hata hivyo mimi nipo kawaida tofauti na yule Tumaini ila si vizuri kweli kumsema mtu sababu ya maumbile"

    "Halafu tunampa mawazo Tony, alimleta Dora hapa yupo kawaida tu yani ni mwanamke aliyekamilika ila tukamkataa na sasa kamleta Tumaini naye tumemtaa sababu ya ubonge, nadhani haelewi kuwa sisi tunahitaji aoe mwanamke wa aina gani"

    "Na wewe Mage hebu tulia, huyo Tumaini na Eeick nadhani humfahamu baba yao, ni katili huyo mzee balaa. Acha watoto wake waondoke maana ukoo wetu hauwataki"

    Bite alihitimisha hivyo na wote wakacheka sana.



    Tony aliondoka na Tumaini hadi nyumbani kwakina Tumaini ila Tumaini hakuwa na raha kweli, Tony alimuomba msamaha,

    "Nisamehe mimi Tumaini maana ndugu zangu hata mwenyewe sijapenda waseme vile"

    "Kwahiyo ubonge wangu ndio tatizo"

    "Ubonge wako sio tatizo Tumani na hujui tu jinsi gani nimeanza kukupenda tangia muda ila kwavile sikuhisi kama naweza kukutana na wewe ndiomana nikaonyesha nia ya kutaka kuoa wanawake wengine ila Tumaini upo moyoni na hujui tu ni jinsi gani nilivyokuona tena siku ile moyo wangu ulivyofurahi yani wewe ndio mke wangu hata waseme vipi"

    "Wewe unasema tu, kwani nyie wanaume siwafahamu? Hakuna mwanaume anayependa mwanamke mnene, ndiomana sikutaka kujiingiza kwenye mahusiano"

    "Basi Tumaini wewe ndio hujui, hakuna mwanaume asiyependa kuwa na mwanamke mnene sema ukiwasikia wanaongea utahisi hawapendi wanene ila wanawapenda balaa, wewe pita sehemu wamekaa wanaume wawili au watatu uone kama hawajageuka kukutazama wewe. Ila anaweza kupita mwanamke mwembamba na wasigeuke. Kiukweli Tumaini nakupenda sana na ninahitaji kuwa na wewe, nilipokwambia nahitaji uwe mke wangu nilikuwa namaanisha wala sijatania"

    "Mimi sitaki tena kuolewa bora nikae hivi hivi mwenyewe"

    "Tumaini jamani, hivi huoni raha ukitazama mapenzi ya Erica na Erick?"

    "Wale wanapendana"

    "Na sisi tunapendana Tumaini, nitafanya kila kitu ninachoweza uelewe ni jinsi gani nakupenda"

    Tony alifanya kazi ya kumbembeleza Tumaini kwa muda huo kwani alihisi asipombembeleza basi atampoteza.

    Alimbembeleza pale na mwisho wa siku Tumaini alikubali kwenda nae kwenye matembezi, hivyo waliondoka na kwenda kwenye matembezi.

    Walifika kwenye hoteli moja wakiongea na kufurahi sana hadi Tumaini akaona ni vyema alivyokubali kwani aliweza kugundua ni jinsi gani Tony anampenda.

    Muda ulivyoenda Tumaini akahitaji kurudi nyumbani, basi Tony akajiandaa kwaajili ya kumpeleka.

    Wakati wanatoka pale hotelini wakakutana na Dora, waliangaliana nae ila Tony alitamani Dora asiongee chochote maana Tumaini ni mama kisirani, ila Dora kama kawaida yake kunyamaza haikuwezekana, aliwaambia

    "Kheeee Tony upo na Tumaini kwasasa?"

    Tony akawa kimya na kujiuliza kuwa Tumaini na Dora wamejuana vipi, ila Tumaini alielewa kuwa Dora amefahamiana na Tony sababu ni kaka wa Erica na yeye anaifahamu familia ya Erica kumbe aliwahi kuwa mchumba wake pia.

    Tony akaona asimjibu Dora tu, hivyo akamshika mkono Tumaini na kuondoka nae.

    Dora alicheka sana,

    "Hata msiponijibu nimewabamba"

    Akawaangalia na kuwaacha waondoke. Akasogea sehemu ya kukaa pale hotelini na kukaa kwani kuna mtu alikuwa akumsubiri ila kuna mawazo yalimjia kuwa ndugu wa Erica walimkataa kuwa asiolewe na Tony, vipi kuhusu Tumaini? Na pia akawaza kuwa lazima Erica hajui, akaamua kumpigia simu

    "Erica, kuna umbea ninao na unaniwasha sana"

    "Ushaanza na mambo yako Dora"

    "Naomba unielekeze kwako nije kukupa huo umbea"

    "Wewe nae huachi loh!"

    Basi Erica akamuelekeza na kuagana nae.



    Erick akiwa kwenye shughuli zake, akapigiwa simu na baba yake kuwa aende ofisini kwake, ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Erick kufika kwenye ofisi ya baba yake, yani alipoingia wengi mabinti wa pale walionyesha kuvutiwa nae, basi akaenda kuonana na baba yake.

    "Unajua nilichokuitia hapa Erick?"

    "Sijui baba"

    "Kwanza kazi niliyowapa mmeishia nayo wapi?"

    Erick alimueleza baba yake kuwa yule mama amekubali na anahitaji waende kuonana nae, mzee Jimmy alionekana kutabasamu tu kwa ujumbe aliopewa na mwanae, baada ya hapo alimruhusu kuondoka,

    "Mmmh baba, kwahiyo hii ndio sababu pekee uliyoniitia?"

    "Ndio hiyo hiyo, hakuna lingine"

    Ila Erick alikuwq na mashaka sana kwani kwa kipindi hiko alikuwa hamuamini baba yake kabisa kabisa, sasa wakati anatoka pale kuna binti alimuita Erick basi Erick alienda kumsikiliza,

    "Samahani, hapo nje kuna vijana wanaonyesha wapo kukufatilia maana nimeona wana picha yako"

    Akili ya Erick ilicheza haraka haraka na kuhisi kuwa huenda baba yake amemuita hapo ili kumlaghai halafu watu wamfatilie na wajue anapoishi, basi akamshukuru yule dada na kutoka na wakati anaondoka alihisi kabisa kuna watu wanamfatilia akaamua muda huo aende moja kwa moja nyumbani kwao ili kuwapoteza uelekeo kabisa.

    Alifika nyumbani kwao na moja kwa moja kwenda chumbani kwake, alipekua ile bahasha ambayo aliipata mlangoni kwakina Erica kwani alijua ndio posa inayomuumiza baba yake, akaenda chumbani kwa babake na kumuwekea kitandani ili akifika tu aione, kisha akarudi chumbani kwake kwani alijua angetoka muda huo basi wale watu wangeendelea kumfatilia.

    Alipokaa kwao, kwenye mida ya saa moja na nisu usiku alifika dada yake alisikia kama amefika na mwanaume maana alisikia sauti ya kiume ila wakati anatoka huyo mwanaume alikuwa kaondoka, alimsalimia dadake na kumuuliza,

    "Ulikuja na nani Tuma?"

    "Mmmh mbona nimerudi mwenyewe tu"

    "Ulienda dukani leo?"

    "Hapana sijaenda ila walifungua duka"

    "Vipi wewe mpaka muda huu upo nyumbani, na Erica umemuacha na nani?"

    Erick alimueleza baba yao alivyomuita kazini kwake na kusema kuhusu watu wanaomfatilia,

    "Mmmh au ndio ile gari nyeusi niliyoiona imesimama pembeni ya nyumba yetu?"

    "Khaaaaa kumbe wapo mpaka muda huu, ndio hao hao wananifatilia"

    "Erick, wewe ni mwanaume hebu achana na kuogopa"

    "Usidhani naogopa bure, ila sitaki wale wapajue ninapoishi na Erica, wakienda kumbaka mke wangu je! Baba mwenyewe hana nia nzuri"

    "Sasa na huu usiku umemuacha mwenyewe akiingiliwa je utamlaumu nani?"

    "Kwahiyo unanishauri nini Tumaini?"

    "Erick, kama hela unayo kwanini usiweke mlinzi nyumbani kwako? Tena mwambie Erica, sio amkaribishe kila mtu ndani, yani awe anauliza kwanza kabla ya kumkaribisha."

    "Umenishauri jambo jema, ngoja nifanyie kazi swala hilo. Ila kwa leo inabidi nifanye njia ya kutoka bila hawa kutambua"

    "Ngoja nikwambie kitu, nipe funguo ya gari yako halafu mimi nitoke na gari yako wanifatilie mimi niwapoteze wakati huo na wewe utoke na gari yangu uende nayo kwako maana hakuna namna zaidi ya hivyo"

    Erick aliona ushauri wa dada yake ni mzuri sana, hivyo akaona aufanyie kazi muda huo huo sababu muda ulienda sana.

    Kwahiyo muda huo Tumaini alienda kuoga na kubadili nguo kwanza kisha kufanya kile walichopanga na kaka yake.



    Erica alimsubiria Erick siku hiyo na kuanza kuhisi vitu vingine kuwa pengine Erick kaenda kwa wanawake, akajikuta akiumia sana moyo na kukumbuka maneno ya mama yake kuwa usimuamini sana mwanaume kwani anaweza kubadilika muda wowote, aliwaza sana

    "Yani kweli Erick inawezekana kaenda kwa wanawake wengine kweli! Si huwa anasema ananipenda, huu ndio upendo kweli?"

    Alikuwa akiangalia mida tu inavyoyoyoma na kuzidi kumkosesha raha kabisa, alipoona saa nne ndio akazidi kukosa raha yani siku hiyo hata chakula hakikupanda kabisa, kwahiyo hakula.

    Kwenye mida ya saa tano, alijikuta akianza kulia kwa uchungu alioupata moyoni mwake, muda kidogo akisikia mlango ukigongwa akafuta machozi yake na kwenda kufungua, aliyeingia alikuwa ni Erick ila Erica hakumfurahia kama siku zote naye Erick alitambua hilo, akaenda kumfata alipokaa maana alimfungulia tu na kwenda kukaa, Erick alimuuliza

    "Tatizo nini Erica? "

    "Hakuna tatizo, usinifiche tafadhari mpenzi wangu, hebu niangalie kwanza"

    Alipomtazama Erick alogundua kuwa Erica alikuwa akilia sana maana hata machozi bado yalimtoka, alimsogelea na kumuweka karibu yake huku akimwambia taratibu,

    "Mpenzi nadhani unanifkkiria bibaya, ila sio kosa lako ni sababu unanipenda sana ila usifikirie kama naweza kukufanyia kitu kibaya kama hiko. Erica una mimba, ni mtoto wetu huyo tambua unapolia na mtoto nae analia yani unamsononesha mtoto. Ni kweli nilikuwa muhuni sana, nilihangaika na wanawake ila sababu nilikuwa nakuhitaji wewe, na sasa nimekupata nihangaike tena na wanawake wa kazi gani? Erica unanitosheleza, umenipatia mtoto mrembo Angel na sasa unaenda kuniletea mdogo wa Angel, nihangaike na wanawake wengine nataka nini? Nataka laana au kitu ganu? Erica nakupenda sana"

    Yale maneno ya Erick yalimuingia akilini Erica na kuona hakupaswa kulia ila kumuuliza kuwa Erick amechelewa wapi, baada ya hapo Erick alimueleza Erica ilivyokuwa hadi kumfanya yeye kuchelewa.

    "Basi siku nyingine uwe unanipigia simu kunipa taarifa?"

    "Nisamehe kwa hilo mpenzi hata sijui nilipitiwa na kitu gani. Nisamehe tafadhali"

    "Nimekusamehe usijali"

    "Cheka basi Erica nione kweli umenisamehe"

    Erick alianza kumtekenya tekenya Erica ili afurahi tu kama siku zote, Erica nae alianza kucheka na kusahau kila kitu.

    Basi Erica na Erick wakafurahi pamoja yani walienda kulala wakati tofauti zao zimeisha.

    Kulipokucha asubuhi kabisa, simu ya Erick ilianza kuita, alipoichukua kuangalia alikuta ni babake ndiye anampigia simu, basi akaipokea na kuanza kuongea nayo,

    "Erick, wewe ndio uliingia chumbani kwangu?"

    "Ndio baba"

    "Kwahiyo Erica amekupa hii bahasha uniletee huoni kama ni udhalilishaji huo?"

    "Baba, hiyo bahasha hajanipa Erica ila nilikuwa nayo mwenyewe niliipata mlangoni kwakina Erica"

    "Sikuelewi, hebu leo uje ofisini kwangu tena"

    Erick alimuitikia babake ila kiukweli hakuwa na mpango huo hata kidogo.

    Basi akiamka na kujiandaa kutoka kwani kwa kipindi hiko kuna mambo aliyokuwa akiyafanya sababu aliona kashayaanza majukumu.



    Leo Erica akiwa ametulia kwake alipigiwa simu na rafiki yake wa muda, alipigiwa simu na Fetty na ilionyesha kuwa Fetty anahitaji kuonana nae, ikabidi amuelekeze alipo ili afike na waonane na kuongea.

    Na muda kidogo Fetty alifika maeneo yale, alimkaribisha na kuingia ndani huku wakiongea mambo mbalimbali, kisha Fetty akamueleza rafiki yake lengo la kuntafuta,

    "Yani Erica, nimekutafuta ili nikwambie kuwa nimepata mchumba na ana lengo la kunioa"

    "Hongera sana, na mbona umenitafuta mimi namfahamu?"

    "Unamfahamu ndio, tumesoma nae chuo ni yule George aliluwa mwaka wa tatu wakati tupo mwaka wa kwanza"

    Erica alishtuka kidogo kwani huyu George alitambua vilivyo ila hawezi kumwambia rafiki yake kuwa George amewahi kuwa nae, zaidi ya kumponheza tu

    "Hongera Fetty, kwahiyo harusi lini?"

    "Aaah bado kidogo tu ila nimegoma kukutana nae kimwili hadi tutakapooana"

    Muda huo alifika Dora na kugonga kwahiyo Erica alimkatibibisha na Fetty alishangaa sana kuona kuwa Erica bado ana urafiki na Dora, baada ya salamu kumbe Dora alisikia pale mwishoni wakati Erica akiongea na Fetty na kuuliza,

    "Jamani kabla hamjaendelea na mada yenu au kuiacha kabisa sababu yangu, nimesikia mkiongelea kidogo. Ngoja niwaulize, hivi ni mwanaume gani siku hizi anayevumilia mpaka ndoa ndio mfanye?"

    Fetty alijibu kwa kujiamini kabisa,

    "George wangu huyo ndio anaweza kuvumilia nadhani Unamfahamu"

    "George yule yule tuliyesoma nae chuo, alikuwa sijui kiongozi wa nini wakati tupo mwaka wa kwanza alikuwa mwaka wa tatu? "

    "Ndio huyo huyo"

    "Hongera ila kwa George yule akuvumilie hadi ndoa hiyo haipo yani hata atakubaka"

    "Mmmh jamani"

    "Sikutishi ila kabla ya yote nenda mkapime mjue afya zenu, usibabaishwe na mwili wa mtu kuwa ni mzima. Ukimwi umekaa sehemu mbaya sana yani sehemu inahopendwa na wengi, nakuomba ukapime kwanza na George. Au hnamuamini sana?"

    "Hamna ila sikuwa na wazo hilo la kupima, umenishauri vyema asante"

    "Natakiwa nikushauri hivi maana yule George alikuwa anatafuta bikra, kwa mantiki hiyo unafikii kupitia wasichana wangapi? Au Erica hujamwambia mwenzio kuwa hadi wewe umepitiwa na George"

    "Mmmh na wewe Dora maneno yako!"

    "Erica ugomvi wangu ni wako ni kwamba sikukwambia ukweli kuwa George amewahi kutembea na mimi, halafu wewe hnataka kumficha Fetty. Shoga wee huyo George unaotuona hapa kashatupitia mwenzangu, kapime nae tu. Sijasema umuache ila nimekwambia ukapime nae."

    Kwakweli kwa maelezo haya tu Fetty alijihisi vibaya haswaaa kuwa mwanaume anayejivunia nae kumbe kashapita kwa anaowafahamu ila Erica alijaribu pale kumpa moyo sema ilionyesha kuwa imemuuma sana kwani muda huo huo akaaga na kuondoka.

    Walibaki Dora na Erica basi Erica akamsema Dora kuwa alichofanya sio kizuri,

    "Sio kizuri nini, kwanza nimemuokoa huyo rafiki yako kwani George ana tamaa sio mwanaume wa kuishi nae. Hivi karibuni tu nimempitia tena sijamuachia virusi kweli!"

    Erica alimshangaa Dora maana aliongea swala la virusi kama ni swala la kawaida sana.

    Kisha Dora akamuelezea Erica lengo lake la kumpeleka pale kuhusu mahusiano ya Tony na Tumaini.

    "Mmmh sitaki useme chochote, nimekuletea ujumbe tu. Naondoka, kwaheri"

    Aliinuka na kumuaga Erica kwahiyo Erica alipata jibu kuwa kutoka kwa Doroth basi kaka yake amepata nafasi ya kuwa na Tumaini ila hakuchukia zaidi zaidi alitabasamu tu.



    Rahim hakuweza kumwambia chochote mke wake ila aliona kuwa siku ya leo ni njema kama atampeleka mke wake matembezi kidogo ili mke wake afurahi pia na yeye asahau swala zima la kupimwa na kukutwa na ukimwi, kwahiyo alimuambia mke wake ajiandae watoke wakatembee, kwakweli Salma alifurahi sana yani ile ilikuwa kama ndoto katika maisha yake yani aliona mambo sasa yanakuwa mambo, basi Rahim alienda kusafisha gari wakati kamuacha mke wake akijiandaa, kwakwelo hakuacha kumpigia simu yule mama kumpa shukrani,

    "Yani mama yangu sijui nikushukuru vipi, mume wangu hata mara moja hajawahi kusema kuwa tukatembee yani hata mara moja hajawahi ila leo nimeshangaa yani toka jana mume wangu ni mpole hataki tena kumtaja Zainabu na kaniambia leo twende tukatembee yani kama naota vile"

    "Mwanangu endelea kufurahia ndoa ambayo ipo katika hali ya ukweli, hata usijali yani mimi ndio mwisho mwanangu hakuna aliyepitia kwangu akaachwa, yani mimi ndii kila kitu"

    "Asante mama yangu, zawadi yako bado ipo nitakuletea mama maana umenifanya niwe mpya katika ndoa yangu"

    Basi akaagana na huyu mama kisha akaendelea kuvaa na kumvalisha mtoto, Rahim aliporudi kitoka kuosha gari Salma alishangaa kuona Rahim karudi na kopo la maziwa, akamkabidhi mke wake na kumwambia amkorogee yale maziwa

    "Nimkorogee ya nini mume wangu wakati tunaenda nae"

    "Hapana tutamuacha kwa mama, nahitaji tukafurahi mke wangu bila ya kusumbuliwa na kitu chochote kile"

    Ilibidi Salma akubali na kumkorogea mwanae maziwa na alipomaliza walienda kumuacha kwa mama yao kama walivyopanga kisha wao kuondoka.

    Kwakweli leo Salma alishangaa sana maana Rahim alimpeleka mahali mbalimbali na mwisho wa siku alimpeleka hotelini ili wapate chakula cha jioni, huko aliongea nae mambo mengi sana

    "Salma, nahitaji umuachishe mtoto ziwa"

    "Mbona mapema sana, atakunywa nini?"

    "Utaniambia maziwa yoyote mazuri ya kopo nimnunilie ila ziwa lako aache"

    "Jamani kwanini Rahim wakati hii ni haki yake?"

    "Salma, nahitaji maziwa yako niyamiliki mimi. Sasa nitatumiaje mimi na mtoto? Kama unahitaji apate maziwa yako basi nakununulia mashine ya kukamulia maziwa yani awe ananyonya maziwa ya kukamuliwa ila asinyonye hapo kutoka kwako"

    Salma alihisi ni upendo umezidi kwa Rahim kiasi kwamba anaonekana kumuonea wivu mtoto kumbe mwenzie anajua kiwa atakuwa kashamuambukiza ukimwi kwahiyo anaangalia jinsi mtoto wao asipate ukimwi, Salma hakuelewa kabisa yani yeye alijua ni mapenzi tu.



    Leo Erick alimpata mlinzi aliyekuwa anamuhitaji na akaanza safari ya kurudi nae nyumbani, wakiwa kwenye gari yule mlinzi aliongea,

    "Yani wanawake ni vuruga, mimi mapenzi yamenivuruga hadi nimezeeka hivi"

    "Kwanini unasema hivyo?"

    "Yani mwanamke ukimkuta kazaa ni shida haswaa"

    "Kwanini?"

    "Huwa wanawake hawawasahau wanaume waliozaa nao, unaweza kumpa kila kitu ika mawazo yake ni kwa mwanaume aliyezaa nae tu. Na wakikutana wanarudisha majeshi hapo unakuwa umeliwa"

    "Yashawahi kukukuta nini?"

    "Mpaka nimesema yamenikuta, yani mimi hadi niliishi na yule mwanamke ila siku niliyomshangaa ni aliponiambia anarudi kwa baba watoto wake dah niliumia sana, toka hapo mapenzi siyataki tena bora nilinde watu tu ila mapenzi hapana kwakweli"

    Erick alifikiria kwa upande wake akaona hiyo haipo sababu Erica alisema wazi kuwa Rahim hakumpenda.

    Basi aliwahi kurudi nyumbani, na yule mlinzi wa kuwalindia sehemu ile na kumwambia Erica,

    "Nimekuja na mlinzi"

    "Sasa mlinzi wa nini jamani Erick?"

    "Kwasasa huoni umuhimu wake ila ipo siku utaona umuhimu wa kuwa na mlinzi mahali hapa, ninakujali, nakupenda na sipendi upatwe na jambo baya kwaajili yangu. Kwasasa atakuwepo mlinzi mahali hapa wakati nashughulikia mahali ambako patakuwa na usalama zaidi kwetu."

    "Sawa nimekuelewa"

    Kisha Erick alimuomba Erica kuwa siku hiyo waende kula hotelini, Erica alikubali na kwenda kujiandaa huku akimuandaa na mtoto pia, wakati huo Erick nae alioga na kubadili nguo ili waondoke wakiwa wasafi.

    Waliondoka na kwenda kwenye hoteli ambayo haikuwa mbali sana na pale kwao, waliagiza chakula kisha Erick aliongea na Erica

    "Unajua toka tupate matatizo basi muda wa kukaa chini na kupanga kuhusu maisha yetu umekuwa mdogo sana, mwanzoni ilikuwa najiona mwanaume ila sasa ndio nimekuwa mwanaume wa ukweli maana nimeyatambua majukumu ya mwanaume katika dunia hii"

    Erica alicheka tu, chakula kilifika na walianza kula, wakati Erica anatazama meza ya pili akajikuta akiangusha hadi kijiko cha chakula kwani alionana na Rahim macho kwa macho, aliogopa ila muda huo Rahim na mke wake walikuwa wanainuka maana walimaliza kula pia kwahiyo alipomuona Erica akaona ni vyema kwenda kumsalimia.

    Erick alikuwa akimshangaa Erica na kumuuliza,

    "Nini tatizo, mbona umeshtuka hivyo?"

    Erica alikuwa kimya tu na kumfanya Erick ageuke, akamuona Rahim akiwa ameongozana na mwanamke wakienda mahali pale, alijua ni kwanini Erica ameshtuka kwahiyo nae alijipanga pale ikiwa Rahim angeleta fujo, ila walishangaa Rahim akifika pale huku akiwa mpole kabisa na kuwasalimia kipole huku akisifia kuwa wamependeza kukaa na mtoto pale, alimsogelea Angel na kumwambia,

    "Niamkie baba yako Angel"

    "Taki"

    Kisha Angel akainuka na kwenda mwilini mwa Erick, kitendo kile kilimuuma moyo sana Rahim ila hakusema jambo lingine la ziada zaidi ya kuwaaga tu na kuondoka, kwakweli walimshangaa sana na hawakuongelea habari zake kabisa hadi wanarudi nyumbani, ni Erica alianza kuuliza

    "Mbona Rahim kawa mpole vile?"

    Erick akasema,

    "Sasa unamuuliza nani?"

    "Basi samahani yaishe, nilikuwa najiuliza tu"

    "Ndii jiulize mwenyewe si ndio unamjua yule! Pengine unaweza kujua ni kwanini amekuwa mpole vile"

    Erica akaamua kunyamaza ili kuepusha shari kwani alimuona dhahiri Erick kuwa na chuki na Rahim, pengine sababu amezaa na Rahim maana Erick aliinekana kumchukia kweli tangu ameujua ukweli.

    Ericq hakuongea tena jambo na kwenda kulala tu na mwanae, hali ile hakuipenda pia Erick ila alihisi huenda Erica ameanza kumkumbuka Rahim basi alimuacha tu alale bila kumsumbua ila moyoni mwake aliumia sana wakati huo huo Erica nae anaumia moyoni kuwa kwanini siku hiyo hajabembelezwa na Erick.

    Kulipokucha kama kawaida, Erick alijiandaa na kutaka kuondoka ila akafikiria kuhusu Erica na kujisemea,

    "Najua sasa ataanza kuniwaza mimi sababu kabeba pia mtoto wangu, ngoja niachane na mawazo ya yule mlinzi"

    Basi alimsogelea na kumbusu ambapo Erica alishtuka ila alitabasamu kuona Erick amembusu, kisha akamwambia

    "Natoka Erica, ila kumbuka nakupenda sana"

    "Nakupenda pia Erick"

    Basi Erick alimbusu tena na kumuaga, kwa wakati huu Erica alisahau kabisa kama usiku wote kalala akiwa na mawazo tele juu ya Erick kutokumbembeleza.



    Kwenye mida ya mchana, Erica akiwa ametulia nyumbani alipigiwa simu na Dora na kuipokea ile simu,

    "Erica, nikwambie kitu"

    "Niambie"

    "Kuna yule mwanaume wako alikuwa anakuganda sana kipindi upo chuo. Huwezi amini leo kanitongoza"

    "Nani huyo?"

    "Si huyu Bahati, yani hapa napanga nae mipango ya kuvunja amri maana anaonekana ana uchu balaa"

    "Dora hapana usifanye hivyo"

    "Nisifanye hivyo kwanini na ananitaka mwenyewe!"

    "Jamani Dora, kwani wewe unajiuza kusema kila anayekutongoza umkubali? Namjua Bahati, yani kama kakutongoza ni bahati mbaya, tafadhali usifanye nae chochote"

    "Huo wivu sasa, unamuonea wivu wa nini wakati upo na Erick?"

    "Hapana si wivu ila naomba nije kuongea nae kwanza, uko wapi nae tafadhali nakuja"

    Dora akamtajia sehemu waliyopo, yani Erica alijiandaa haraka haraka na kumbeba mwanae. Akatoka nje na kukodi bajaji maana gari yake hakuichukua kwao wakati anaondoka.

    Alienda hadi eneo alilisema Dora, ni kweli alimkuta na Bahati tena muda huo walikuwa wamesimama kama wanataka kwenda mahali. Erica aliita,

    "Bahati"

    Bahati aligeuka, kile kitendo cha Bahati kumuona Erica ikawa kama akili yake imerudi kwani alimuacha Dora pale na kwenda kumkumbatia Erica, kumbe Erick nae alikuwa eneo lile anapita ni Angel alimuona akaita,

    "Baba"

    Erick akageuka na kumuona Erica akiwa amekumbatiwa na Bahati, aliingiwa na chuki ya gafla kwavile huwa hampendi Bahati.







    Bahati aligeuka, kile kitendo cha Bahati kumuona Erica ikawa kama akili yake imerudi kwani alimuacha Dora pale na kwenda kumkumbatia Erica, kumbe Erick nae alikuwa eneo lile anapita ni Angel alimuona akaita,

    "Baba"

    Erick akageuka na kumuona Erica akiwa amekumbatiwa na Bahati, aliingiwa na chuki ya gafla kwavile huwa hampendi Bahati.

    Erick alisogea karibu na kumvuta Erica pembeni, alimuangalia kwa hasira sana kisha akamnyanyua Angel na kumvuta Erica mkono hadi kwenye gari yake, akawapandisha humo naye kupanda na kuondoka zao, hakumsikiliza hata Dora anasema kitu gani maana Dora aliita ila Erick hakuitika sababu alikuwa na hasira zake.

    Bahati alisimama akishangaa maana kitendo alichokifanya Erick kilikuwa cha haraka sana, Dora akacheka na kumfata Bahati,

    "Unajiachia tu kukumbatia wake za watu, siku moja umkute Erick kashika bastola wewe angekufyatua"

    Ila bado Bahati alikuwa kama na bumbuwazi vile, Dora alimwambia tena,

    "Eeeh si tulipanga tunaenda kulala, twende basi"

    "Ulipanga na nani kwenda kulala?"

    "Wewe hapo, unajisahaulisha eeeh! Sababu tu ulimuona Erica."

    "Sijapanga na wewe kitu chochote"

    "Kheee makubwa haya, kwahiyo Erica kakusahaulisha kila kitu"

    "Cha kunisaidia naomba namba ya Erica"

    Dora alimtajia Bahati namba ya simu ya Erica, kisha Bahati akamuomba pia Dora na namba yake ambapo Dora alimpa pia na baada ya hapo Bahati akaenda kupanda gari yake na kuondoka.



    Walifika nyumbani na kuingia ndani, Erica alikaa sebleni ila Erick alifunga mlango wa sebleni na kuwasha katuni ili Angel aangalie na kweli alitulia akiangalia, kisha akamshika Erica mkono na kwenda nae chumbani na kumkalisha kitandani kisha akasema,

    "Yani ningekuwa mtu wa kupiga basi leo ningekuchakaza maana ningekupiga hadi usahau jina lako, unajua ni kwajinsi gani namchukia yule mtu halafu wewe unatoroka nyumbani kwenda kukumbatiana nae"

    Erica aliongea kwa uoga,

    "Nisamehe Erick"

    "Kitendo cha kuja nawe hadi nyumbani ni wazi nimekusamehe. Na nimekusamehe sababu moja tu, sababu wewe ni mke wangu. Mke hapigwi wala hasemwi hadharani ndiomana nikakuleta nyumbani tena chumbani ili niongee na wewe, kuna mambo Erica siyapendi. Unapokuwa na mimi kuna mambo unatakiwa kuacha, mfano urafiki na Dora siutaki yani sitaki kabisa Dora awe rafiki yako. Na watu kama yule Bahati sijui Rahim fanya kama hawajawahi kutokea katika maisha yako hata kama kuna vitu unahusika nao kwa ufupi ukaribu na watu wa ajabu sitaki"

    "Nisamehe mpenzi"

    "Huo wimbo nimechoka nataka wimbo mpya. Sasa ukinikosea unajua msamaha unatokaje?"

    "Sijui"

    "Erica, sikia licha ya kukupenda sana na najua wazi una mimba yangu ila bado niliheshimu msimamo wako kuwa tusikutane tena kimwili mpaka tuoane, leo navunja neno hilo Erica, labda ndio kitu kinafanya uwakumbuke wakina Bahati. Haya msamaha wangu unatoa kwa kunipa penzi"

    Erica alijikuta akimuangalia kwa aibu sana Erick ila muda huo huo Erick alisogea na kuanza kumpapasa na mwisho wa siku kuangukia kwenye mapenzi.

    Kisha usingizi mzito ukawapitia, walikuja kushtuka baada ya kusikia sauti ya Angel ikiwagongea mlango huku akiita mama, baba.

    Erica aliinuka na kwenda kumfungulia mtoto ambapo ilibidi ampe chakula kisha akamuogeshe na Angel akalala.

    Muda huo Erick alikuwa amekaa tu, Angel alipolala tu Erick akamwambia Erica

    "Na mimi leo nataka uniogeshe"

    Erica alitabasamu tu na kuamua kwenda kuoga na Erick kisha kwenda pamoja kula na baada ya hapo walikaa pamoja wakiangalia taarifa ya habari.

    Mara simu ya Erica ikaanza kuita, Erick akasema,

    "Nipe hiyo simu Erica, kwasasa tumekuwa mke na mume rasmi, tumejialalisha wenyewe kwahiyo tu mwili mmoja na mimi ndio kichwa cha familia, lazima nijue ni nani anayekupigia muda huu mke wangu na anataka nini"

    Ile simu iliita wee hadi kukatika, ikaanza kuita tena ikabidi Erica amkabidhi ile simu Erick.

    Akaiangalia namba ngeni ila akaipokea na kuongea nayo,

    "Hallow, unataka nini kwa mke wangu."

    "Kumbe Erica kaolewa kweli?"

    "Wewe ni nani?"

    "Mimi Bahati"

    "Sikia usimsumbue mke wangu kwaheri"

    Erick akakata simu, ila muda kidogo uliingia ujumbe kwenye simu ile, Erick akaufungua, ulitoka kwenye ile ile namba ya Bahati,

    "Erica, unampa simu apokee mwanaume kweli! Hata hivyo bado nakupenda tena sana, hata kama kwenu umehama nitamwambia rafiki yako anilete"

    Erick alimuangalia Erica na kumuuliza,

    "Dora anapajua hapa?"

    "Ndio anapajua"

    "Yani katika watu wote ukamkaribisha Dora kweli Erica! Kesho tunahama, usiulize tunahamia wapi ila kesho tunahama. Haya twende tukalale"

    Basi Erica aliinuka tu na kufatana na Erick kwenda chumbani kulala.



    Bahati alirudi moja kwa moja kwa ndugu zake na kuwaeleza kuwa amekutana na Erica, kwakweli ndugu zake walifurahi sana kwani Bahati alionekana kuwa mzima kabisa kichwani kwa siku hiyo.

    Hakutaka kurudi kwake na kuamua kulala kwao siku hiyo, ila aliona usiku kuwa mrefu sana yani alikosa raha na kuamua kupiga ile namba ya Erica na hata ambapo haikupokelewa aliipiga tena na mwishoe ikapokelewa na Erick, akaumia sana moyo wake na ilipokatika ndipo akatuma ule ujumbe.

    Yani alikuwa anangoja pakuche tu maana moyo wake wote ulijaa na mawazo dhidi ya Erica.

    Kulipokucha aliona ni vyema amtafute Dora kwanza ili pengine ampeleke anapoishi Erica, ala kabla hajafanya hivyo dada zake walienda kuongea nae,

    "Kwakweli Bahati tumefurahi sana, kwakweli Erica katumwa na Mungu kuokoa maisha yako. Ulikuwa hutamaniki Bahati kabisa maana ulikuwa unafanya mambo ya ajabu tu"

    "Ila sisi ndugu zako ndio chanzo cha yote maana kama tungekuwa makini basi tusingeruhusu ufanyiwe dawa. Kwakweli kwa kupitia wewe tumejifunza mambo mengi sana"

    "Hivi kwa mambo hayo mnayoniambia, Erica atakubali tena kuwa wangu kweli? Erica akijua hizo ndio tabia zangu atakubali kweli?"

    "Najua hawezi kukubali ila bado tunapaswa kumshukuru sana kwa kukuokoa"

    "Mnajua ndugu zangu hakika mtalaaniwa yani mmefanya nimsahau Erica kiasi hiki kweli? Hivi mnajua mali zote nilizonazo ni sababu ya Erica, mnatambua hilo? Najua hamjui ila kila nilichonacho ni sababu ya Erica tu yani yeye ndio kafanya nimepata mali zote hizi ila mkafanya kitu cha ajabu nimsahau kweli!"

    Yani ndugu wa Bahati ndio walishtuka hapa kuwa mali zote alizonazo Bahati ni sababu ya Erica maana ndio kasababisha Bahati kupata mali zile, waliishia tu kumuomba msamaha ndugu yao maana tayari walishafanya makosa.

    Basi Bahati akawasiliana na Dora tu kwani nia yake ilikuwa ni kupelekwa anapoishi Erica ili aweze kuongea nae.



    Yani asubuhi na mapema Erick alimwambia Erica ajiandae na wamuandae na Angel kwaajili ya kuondoka na walipomaliza, Erick alibeba mabegi ya nguo zao na kupakia pia kwenye gari na kumwambia Erica waondoke,

    "Kheee ndio tunahama!"

    "Ndio, unashangaa nini sasa?"

    "Mbona gafla hivyo, na kodi tuliyotoa je?"

    "Sijali kuhusu kodi kabisa, Erica wewe ni wa muhimu sana kwangu. Namshukuru Mungu akili zako nimezijua maana nisingezijua akili zako basi na mimi ningefanya ujinga. Sasa hapa tunahama, na tunapohamia sitaki kuona umekaribisha takataka yoyote sijui shoga yako, sitaki huo ujinga unakaribisha watu nyumbani na unajua wazi unabakiaga mwenyewe si kujiwekea makaa ya moto! Twende"

    Basi Erica akawa hana jinsi zaidi ya kufatana tu na Erick kwenye gari kisha safari ikaanza.

    Walifika kwenye nyumba hiyo ambayo bado ipo kwenye ujenzi, Erick akamwambia Erica,

    "Siku zote nipo busy sababu ya hii nyumba, nilitaka nimalize kwanza nyumba yetu ndio tuhamie ila kwasasa acha tu tuishi na tutaimalizia tukiwa hapahapa pamoja kuliko kuendelea kupeana presha huko"

    Erica hakutia neno, kwenye nyumba ile kulikuwa na chumba kimoja ndio kimekamilika kwahiyo Erick alimwambia Erica wataishi humo kwanza wakati nyumba inamaliziwa vitu vingine,

    "Ila Erick nisamehe sana, naumia jamani"

    "Unaumia na nini sasa?"

    "Tumetupa kodi kule"

    "Kuhusu kule usijali, nilishaongea na dalali anitafutie mteja kwahiyo nitapata tu kodi yangu hata usijali, ile hela wala haipotei bure. Yani usijali kuhusu hilo ila nimekuleta hapa ili tuishi kwa amani na upendo, halafu hiyo simu yako nipe"

    Erica alimpa Erick ile simu yake, halafu akamuuliza

    "Na mimi nitawasiliana na simu gani?"

    "Nitakutafutia simu nyingine na hii ni mimi ndio nitawasiliana na ndugu zako, wale wa muhimu tutawapa namba zako ila sijui wakina Derick siwatambui kama ni nduguzo."

    Erica hakubisha zaidi ni kukubaliana tu na Erick maana yeye ndio kasababisha yale yote mpaka Erick kawa vile.

    Basi aliingia ndani na Angel kutulia nae kisha Erick akaenda kufanya kazi ya kuhamisha baadhi ya vitu ambavyo alinunua kule.



    Bahati aliwasiliana na Dora na kukutana nae, kisha wakakutana na kuanza kuongea,

    "Yani Dora huwezi amini, jana nilipomuona Erica akili yangu iliruka kabisa"

    "Kwani Erica alikupa nini wewe?"

    "Hakuna ila mimi ndio nilikuwa mwanaume wa kwanza kwa Erica, nampenda sana na ninaamini hata yeye ananipenda sana"

    "Aliyekudanganya kuwa ukiwa wa kwanza kwq mwanamke atakupenda sana nani? Umeniona mimi, hata mwanaume wangu wa kwanza simkumbuki kabisa yani hata jina lake silijui, kuwa wa kwanza sio kigezo cha kupendwa"

    "Hata kama, naomba tu unipeleke kwakina Erica yani anapoishi kwasasa, nahitaji kuongea nae."

    "Utanipa nini nikikupeleka?"

    "Unataka nikupe pesa ngapi?"

    "Nipe laki moja ndio nitakupeleka"

    "Nitakupe laki na elfu hamsini"

    "Wow kumbe umekuwa na hela hivyo, twende nikupeleke ila nipe changu kabisa"

    Muda ule ule Bahati alifanya muamala na kumwambia Dora amtajie namba zake kisha akamrushia laki moja na elfu hamsini, basi Dora akachekelea na kumwambia kuwa waende.

    Basi wakaondoka na kufika hadi anapoishi Erica, waligonga mlango bila kufunguliwa, muda kidogo alifika Fetty ambaye pia alikuwa na lengo la kuonana na Erica, akawasalimia pale na wakamwambia kuwa wamegonga ila hawajafunguliwa, wanahisi huenda Erica hayupo.

    Ila kwa leo Fetty alimuangalia Dora na kuanza kumshukuru,

    "Asante sana Dora"

    "Asante ya nini tena?"

    "Nilifata ule ushauri wako na kwenda kupima na George uwiii nimemkuta kaathirika"

    Dora baada ya kusikitika alionekana akicheka sana hadi Fetty alimshangaa na kumwambia

    "Mbona unacheka?"

    "Nacheka ya George, katafuta bikra weeee mwisho wa siku kaibuka na gonjwa. Unapotafuta bikra, hakikisha na wewe umetulia lakini ukiwa macho juu juu basi utaukwaa tu"

    Akaendelea kucheka sana, Fetty akamuangalia Bahati na kukumbuka kuwa kuna siku Bahati alipigana na George, ndio hapa akapata picha kuwa George alikuwa na mahusiano na Erica mpaka kupigana na huyo Bahati ila alimshangaa muda huo kwenda tena nyumbani kwa Erica, akamuuliza

    "Na hapa umefata nini wewe? Si ulikuwa na mahusiano na Erica wewe!"

    Dora akamjibia,

    "Eti badi anamtaka Erica, huyu anacheza na Erick eeeh! Mwenzio Erick kashatembeza bakora kwa kila mwanamke unayemjua hadi katulia kwa Erica ujue kafika na atakufanyia kitu kibaya wewe. Kupenda gani huko?"

    "Jamani hamjui tu, nampenda sana Erica"

    "Huo wako sio upendo ni uchizi, ila Bahati nishakufikisha kwa Erica nadhani katoka na mume wake maana Erick anavyojua mahaba yule najua baada ya jana basi leo kaenda kumpeleka matembezi ili Erica asifikirie tena kuhusu nyie vinuka mkojo"

    "Unasemaje Dora?"

    "Sijasema kitu bhana, ila naondoka tutaonana siku nyingine. Kwa Erica ndio hapa, kwahiyo akili juu yako"

    Basi Bahati nae akaamua kuondoka na Fetty pia akaondoka na wote kupata lifti kwenye gari ya Bahati.



    Wakiwa kwenye gari ya Bahati, njiani Dora alishuka na kuwaaga basi Bahati alibaki akiwa na Fetty kwenye gari ila alikumbuka jambo na kumuuliza Fetty,

    "Ulisema mlienda kupima ukimwi?"

    "Ndio, tulienda kupima"

    "Naomba nami nipeleke hiyo sehemu maana sina hakika na afya yangu"

    "Kwani ni muhuni sana wewe?"

    "Dah ni historia ndefu sana sijui nianzie wapi ila cha kunisaidia nipeleke tu huko nikapime"

    Basi Fetty alikubali na kwenda nae kupima kwenye hiyo hospitali na majibu yalipotoka Bahati hakuamini kabisa maana alikutwa hajaathirika, kwakweli alifurahi sana na kumshukuru Fetty kwa kumpeleka sehemu hiyo kupima kisha akamuomba namba yake ya simu na kuagana nae.

    Moja kwa moja Bahati alirudi kwao na kuwaonyesha dada zake kile cheti cha ukimwi,

    "Yani siamini dada zangu, siamini kama nimepona kwakweli."

    "Mungu mkubwa kaka, ila inabidi tumshukuru sana Erica"

    "Nimeenda kwake aijamkuta"

    "Labda karudi kwao"

    "Inawezekana, kwahiyo tufanyeje sasa?"

    "Naomba twendeni tena kwakina Erica, tukaombe msamaha tu maana hakuna namna jamani"

    Wakakubaliana kuwa kesho yake waende tena kwakina Erica.



    Erick alipeleka vitu pale kwake ambapo chumba kingine walimalizia haraka haraka na kuweka vyombo ambavyo vimetoka kule walipokuwa wamepanga.

    Jioni hiyo alifika na simu na laini mpya na kumpa Erica,

    "Kwasasa tutawasiliana kwa namba hii yani ukiwa na shida na mimi basi unatafute ukiwa na namba hii maana ile yako ya mwanzo nitatumia mimi. Halafu unajua kilichotokea wakati naenda kumalizia vyombo?"

    "Kimetokea nini?"

    "Kuna watu niliwaona pale nyumbani akiwepo Dora na yule jamaa yako, kwakweli Erica ukifahamisha tena hizi takataka zako huku tulipohamia sijui nitafanyaje, sikuahidi cha kufanya ila watu hawa siwataki tena. Nilishakwambia, mimi ndio rafiki yako na msiri wako, ukiwa na habari yoyote niambie mimi. Najua wanawake mnapenda sana umbea kwahiyo ikitokea kuna umbea wowote unatamani kuufanya basi fanya kwangu, yani huo umbea nieleze mimi nitaelewa kuliko kuzoa zia marafiki wasiokuwa na tija. Nadhani tumeelewana"

    "Ndio, nimekuelewa"

    Kisha Erica aliendelea kumuelekeza cha kufanya mahali hapo sababu ilikuwa ni nyumba ambayo bado haijaisha, Erica aliuliza tena

    "Na kwetu wakitaka kuwasiliana na mimi je?"

    "Hamna shida utawasiliana nao, kipindi hiki nipo huku karibia muda wote kwahiyo ikiita tu simu ya kwenu nitakupa uongee nayo, mama yangu anarudi wiki ijayo tu kwahiyo nitamueleza kila kitu na atakwenda kwenu na kila kitu kitakuwa sawa, najua mama hawezi tena kubishana au kukukataa akijua kuwa una mimba yangu, kwahiyo lazima kila kitu kitaenda sawa sawa kama tulivyopanga"

    Basi Erica akafurahi pale, na muda ule ule simu ya Erica ilianza kuita tena, Erick akaitazama na kuona ni namba ya baba yake, kwahiyo hakupokea aliacha iite hadi ikatike, iliita mara kadhaa na kukatika, mara ikaingia namba ya Tumaini kwenye simu ya Erica ndipo Erick akapokea hiyo simu,

    "Erica uko wapi? Nimekuja hapa sijamkuta mtu, uko wapi?"

    Erick aliamua kujibu maana alipatwa na hisia kuwa kuna kitu hakipo sawa,

    "Tumaini, ni mimi ndiyo nina simu ya Erica. Aliondoka leo asubuhi kurudi kwao maana kuna mambo yalitokea akachukizwa eti kwahiyo simu yake ndio nimekuja nayo mimi kwenye shughuli zangu"

    "Aaaah sawa"

    Ile simu ikakatika, kisha Erick akasema,

    "Kuna kitu hakipo sawa hapa, simu ya baba imeeita kama mara mbili halafu inakuja simu ya Tumaini kuuliza ulipo? Mmmh naona sio sawa kwakweli."

    "Au baba yenu kaenda pale tunapokaa?"

    "Inawezekana ndiomana nikasema kuwa pale si salama kwasasa"

    Basi wakafanya mambo mengine na kujiandaa kulala.



    Wakati wa usiku ndio wanalala, simu ya Erica iliita tena, Erick akaangalia na kuona ni Tony yani kaka yake na Erica, akampa ile simu Erica aongee nayo,

    "Erica mama kakupigia simu?"

    "Hapana kwani anasemaje?"

    "Yani mimi kanipigia simu kasema niachane na mwanamke niliyempeleka"

    "Kwani kaka ulimpeleka nani?"

    "Eti sijui ana ugomvi na wewe, mimi nilimpeleka Tumaini tafadhali Erica usimkatae, nampenda sana. Niambie unamuonaje?"

    Erica akamuangalia kwanza Erick kisha akamjibu kaka yake,

    "Aaaah mbona yupo vizuri tu yule"

    "Sasa nyumbani hawamtaki, ila kuna mpango nitafanya"

    "Mpango gani?"

    "Nitaondoka kama wewe nyumbani na kwenda kuishi na Tumaini"

    "Na yeye atakubali?"

    "Sasa hapo pagumu mmmh! Ila nampenda sana. Sasa basi nitakuja kwako huko ili tupange"

    Erica akataka kumwambia kuwa wamehama ila Erick akamziba mdomo na kukata ile simu, kisha akamwambia

    "Kwasasa sitaki yeyote ajue kuwa tumehama, mpaka mambo yakikamilika. Erica acha tuishi tu mafichoni lakini kwa usalama wetu, siku hata Angel wetu watamuiba kumbe sababu ya kukaribisha wageni hovyo"

    Erica nae alianza kuelewa mipango ya Erick, kwani muda ule ule simu ya Erick iliita na mpigaji alikuwa ni Tumaini, basi Erick akapokea,

    "Niambie dada"

    "Yani Erick kama mtaweza hameni hapo mnapoishi, maana jioni baba alinibana hadi nikamleta yani muda ule napiga simu ya Erica nilikuwa na baba na alivyosikia Erica karudi kwao basi kasema anaenda kwakina Erica, yani baba yetu sijui ana tatizo gani"

    "Kwahiyo hakwenda kwa yule mwanamke?"

    "Hajaenda, nahisi kakutana na mtu kamshauri ujinga ndio baba yupo hivyo. Nisamehe Erick sikutaka kumleta baba ila ilibidi nimlete tu"

    "Sawa nimekuelewa usijali"

    Ila Erick hakuthubutu kumwambia dada yake kuwa wamehama maana mwenendo wa baba yao aliuona. Kisha yeye na Erica waliamua kulala tu muda huo.



    Kulipokucha Erick alishangaa kupokea simu kutoka kwa mama yake,

    "Kesho narudi Erick"

    "Si ulisema wiki ijayo mama"

    "Nimeghairi, narudi kesho"

    "Sawa mama, niambie ni muda gani nije kukupokea?"

    "Kwanza kabla ya yote, mkamwana wangu Sia hajambo"

    "Mama, huyo sio mkweo. Yani mkweo ni Erica"

    "Sitaki kusikia hilo jina, na wala sirudi kesho yani hata usijiandae kuja kunipokea"

    "Jamani mama"

    "Hakuna cha jamani"

    Kwakweli Erick huwa haelewi kabisa kuwa ni kwanini mama yake hampendi Erica na wakati huo huo yeye akiwa hapendi kabisa na ndugu wa Erica yani hapo alishindwa kuelewa kwakweli. Na kubaki akijisemea mwenyewe,

    "Yani mapenzi siyaelewi hapa tu jamani, ukipata mnayependana basi vikwazo kila kona, yani nashindwa kuelewa mapenzi ni nini jamani"

    Kisha akaamua kuendelea na kazi zake za kusimamia ujenzi wa nyumba yake.

    Akapokea ujumbe toka kwa babake,

    "Umemficha wapi Erica?"

    Kwakweli leo Erick aliona ni kumuondolea uvivu baba yake kwani muda ule ule akampigia simu na kuanza kuongea nae,

    "Hivi baba huwa unaongelea nini?"

    "Namuongelea Erica"

    "Baba, unampenda Erica au Ester? Na ukiendelea hivi nitamueleza yule mama kila kitu yani kama alikukataa kidogo basi akukatae sana"

    "Mmmh mwanangu yamekuwa hayo! Wewe ni mtoto wa kiume na mwanaume siku zote ni kustahimili mambo"

    "Baba, wewe ni baba yangu ila kutwa kucha kumng'ang'ania mke wangu, hivi nikimuoa na kuja nae nyumbani si utambaka wewe"

    "Kunikosea adabu huko Erick"

    "Sio kukukosea adabu, unadhani unachofanya kipo sawa? Badala unipe baraka zako ila wewe ndio unakazana na mambo yasiyofaa. Hatujakataa kuoa kwako ila oa wanawake ulioruka nao sio hawa usiohusika nao. Kama hela si nilikuwekea, ile ni posa yako ambayo huwa unailalamikia. Naomba umuache Erica wangu, tafadhali baba"

    Mzee Jimmy alikata simu yake kwani aliona leo Erick amepaniki haswaa.

    Baada ya muda tu Erick alipokea tena ujumbe kutoka kwa baba yake,

    "Erick mwanangu naomba yaishe, mimi ni baba yako na nitabaki kuwa baba yako"

    Erick alisoma ule ujumbe ila hakuujibu wala nini na kuendelea na shughuli zake tu.



    Mama Erica alikaa na Bite leo wakizungumzia tukio la jana yake la kufikiwa na mzee Jimmy

    "Hivi mama, yule mzee akili zake zikoje jamani mbona yupo vile?"

    Ilibidi amuelezee pia kilichowahi kutokea kati yake na mzee Jimmy na sababu ya yeye kuwachukia watoto wa mzee Jimmy.

    "Mwanangu kama hivyo kweli yule mzee anastahili kusamehewa na mimi? Je nastahili kuchukua watoto wake kama wakwe zangu?"

    "Ila mama, swala la Erica hatuna jinsi zaidi ya kukubali tu aolewe na Erick maana hiyo mimba tutaipeleka wapi? Kama aibu tayari ishaingia ndani ya nyumba, naomba tukubali tu"

    "Huyo Erick ni kiburi mwanangu, hivi unaweza kuishi na mtoto wa mtu bila kutaarifu kwao?"

    "Hiyo inafanya nihisi huenda Erick hampendi kweli Erica maana kama angempenda basi asingefanya vile na usikute hana hata nia ya kumuoa yani anampotezea muda tu ajifungue, na toto lako lilivyojinga limejikalisha kwa mwanaume yani lishafanywa mke kabisa"

    "Na hata harusi yao ikija yani Erica nitamkomesha na hatosahau kamwe, watafunga ndoa ila atapata aibu sana"

    "Utamfanyaje mama?"

    "Subiri tu, ujinga aliofanya sijaupenda hata kidogo. Jitu tumelisomesha, sasa badala ya kutafuta kazi anafanya tu kazi ya kubeba mimba na kwenda kukaa kwa mwanaume. Yani Erica hapana kwakweli"

    Wakati wanaongea wakasikia watu wakigonga mlango na Bite kwenda kufungua, kwakweli alishangaa sana kuwaona tena Bahati na ndugu zake, aliwauliza kwa mshangao,

    "Kheeee mmekuja tena!"

    Mama yake alitoka kuwaangalia, alipowaona alichukia sana na kuwatimua. Basi ndugu wa Bahati wakaondoka ila kama kawaida Bahati aligoma kuondoka na kukaa nje kwenye nyuma ya kina Erica.



    Jioni ya siku hiyo, Mage alikuwa akienda kwao alishangaa sana kumkuta Bahati amekaa pale nje, alimuuliza tatizo,

    "Nahitaji kumuona Erica"

    "Pole sana, Erica alitoroshwa na mume wake kwahiho hadi leo hajarudi nyumbani"

    Ila bado Bahati hakutaka kuondoka, ikabidi Mage agonge ndani na walipofungua pia walishangaa kumuona Bahati, mama yao alihamaki

    "Yani hujaondoka hadi muda huu?"

    Bahati alibaki akimuangalia tu. Kisha yule mama akasema tena

    "Yani sijui Erica alikuokotea wapi Mungu wangu, pole sana kijana. Erica anakaribia kuolewa na kwasasa Erica ni mjamzito"

    Bahati akashtuka sana,

    "Erica ni mjamzito?"

    "Ndio, sio unauliza mara kwa mara uniletee kifaduro hapa sijui degedege, wewe ondoka tu kaishi vyema na mkeo. Erica ni mjamzito na hapa nyumbani hayupo"

    "Ila Erica ananipenda sana"

    "Bwana weeee kama angekuwa anakupenda angezaa na wewe, ila kazaa na mwanaume mwingine na sasa kabeba mimba ya mwanaume mwingine halafu wewe bogozo unajifanya na mada yako ya kupendwa na Erica!"

    "Mama, lakini mimi ndio mwanaume wa kwanza kwa Erica"

    "Huo ujinga ndio siutaki maana hamkawii kuanza kueleza na staili mnazofanyaga mlipokutana na Erica. Kwaheri, ondoka sasa hivi kabla sijatenda dhambi"

    Bahati alikuwa amesimama tu, ila kufumba na kufumbua mamake Erica alitoka na panga na kufanya Bahati akimbie na kuondoka.

    Yule mama alirudi ndani huku akisema tu,

    "Hawa vijana ni hovyo kabisa, yule wa siku ile nae kaja kujitapa hapa sijui mimi mwanaume wa kwanza wa Erica na huyu mgonjwa wa akili nae anakuja na mada zake zisizoeleweka. Jamani nina shida mimi, huyu Erica huyu loh!"

    Mage alishangaa sana na kusema,

    "Erica katoa wapi hai punguani wa kujisifu kuwa wa kwanza? Loh mbona makubwa"

    Waliongea sana pale maana ilikuwa kama mada ya siku hiyo.



    Kesho yake mapema kabisa mama yake Erick alitua mjini na moja kwa moja alienda nyumbani kwake, ila kwavile alibeba zawadi kwaajili ya Sia na mjukuu wake atakayezaliwa akaamua siku hiyo hiyo kumpelekea hizo zawadi.

    Kwahiyo alijiandaa kutoka kwake na kuanza safari ya kuelekea kwakina Sia, alifanya kama kumshtukiza tu kwani hakumwambia kama anarudi siku hiyo.

    Alifika kwakina Sia na kumkuta Steve nje kama kawaida, akasogea na kumuuliza kuwa Sia yuko wapi,

    "Amelala?"

    "Nina shida nae"

    "Mke wangu akilala hataki kusumbuliwa"

    "Mke wako?"

    "Ndio, Sia ni mke wangu"

    "Kheee ya leo kali, hebu kaniitie tu hivyo hivyo"

    "Nimwambie nani? Maana mke wangu ni mjamzito kwahiyo si vizuri nikimsumbua"

    "Na hiyo mimba yake ni ya nani?"

    "Ni yangu ndiomana naishi nae ili kumuhudumia mpaka mtoto akizaliwa"

    Sasa ilionyesha Sia alisikia mazungumzo ya mama Erick na Steve maana pale pale alitoka ndani na moja kwa moja alienda kumnasa vibao kadhaa Steve.







    Sasa ilionyesha Sia alisikia mazungumzo ya mama Erick na Steve maana pale pale alitoka ndani na moja kwa moja alienda kumnasa vibao kadhaa Steve.

    Mama Erick alimshangaa sana Sia, alibaki akimuangalia tu ila Sia alitoa amri kwa yule kijana,

    "Muone vile, chukua fagio ufagie uwanja. Unaona kuna uchafu halafu unakaa kuongea ujinga hapa"

    Steve alionekana kutii kabisa kwani alitoka eneo lile na kwenda kuchukua fagio.

    Kisha Sia akamgeukia mamake Erick na kutaka kumlaki kwa kumkumbatia ila aliposogea karibu yule mama alimzuia kwanza na kusema

    "Sia, nieleze kwanza uchafu unaofanyika hapa ndio uje kunilaki maana unafki huwa sipendi na unalijua hilo"

    Sia alianza kujieleza huku akitoa na machozi ya kinafki,

    "Mama, siwezi kukufanyia unafki wewe. Huyu kijana nimemchukua ili anisaidie saidie kazi, ni mdogo wa rafiki yangu, nilimuhurumia vile hana kazi na mimi nilihitaji msaidizi ndio nikamchukua hata namshangaa kuwa anawezaje kujitapa na kukwambia wewe maneno ya ajabu kiasi hiko! Yani nimeshangaa sana"

    "Wewe kwanini usimuweke mwanamke akusaidie? Mbona kuna wadada wa kazi wengi tu"

    "Mama, sina pesa ya kulipa wadada wa kazi. Huyu anakujaga kunisaidia na mshahara wake ni chakula tu yani akila chakula basi. Yupo hapa sababu hajapata kazi bado"

    "Sia, acha kunifanya mtoto ujue. Huyu sio mpenzi wako kweli!"

    "Jamani mama, mtoto mdogo huyu nimpeleke wapi jamani mimi! Mbona kijana ni mdogo sana huyu, ni mdogo wake rafiki yangu"

    "Unanipa mashaka sana mama, ngoja nikuletee"

    Sia akaenda ndani na kutoka na kadi ya kliniki kumbe Sia alienda na kuanza kliniki ingawa mimba bado ndogo sana ila alianza mapema ili apate kadi ya kliniki ya kuweza kuonyesha kuwa baba wa mtoto ni Erick, na mama yake Erick aliposoma ile kadi kweli aliona jina la baba ni Erick mwanae, hapo kidogo akaanza kuamini amini.

    "Yani Sia, imani na wewe ilinitoka gafla. Ila cha kukushauri tafuta msaidizi wa kike"

    "Tatizo mama, hela ya kumlipa sina. Erick hataki hata kunielewa kuhusu mimba hii na ameikataa kabisa, kwa kifupi hanihudumii chochote kile, yani naishi kwa shida sana na mimba yangu hii"

    "Pole sana, naujua ugumu wa kulea mimba mwenyewe, pole sana ila nitalifanyia kazi swala hilo. Kuna zawadi nilikuletea pamoja na za mjukuu wangu huyo akizaliwa ila nitakupa tu nilizokuletea wewe ila za mjukuu wangu sikupi, nataka niongozane na Erick mguu kwa mguu akupe kwa mikono yake mwenyewe"

    Sia alitamani sana apate na za mtoto ila kwa muda huo aliona si vyema amng'ang'anize yule mama kuhusu zawadi za mtoto sababu anaweza kumshtukia badala yake akamshukuru tu kwa aliyomletea.

    Kisha mama Erick alienda kutoa zawadi alizomletea Sia na kumkabidhi halafu akampa laki mbili kwaajili ya kumsaidia saidia na mimba yake.

    "Nitakuja tena mwanangu, nitegemee siku mbili hizi ngoja niongee na huyo Erick. Siwezi kuacha ulee mwenyewe maana uchungu wa kuhudumia mtoto peke yako naujua"

    Basi Sia aliagana na yule mama, kisha mamake Erick akaondoka.

    Sia alimuita Steve kwa hasira sana na kumwambia,

    "Sasa wewe umefanya Mimi niumbuke, najua sababu yako ndiomana sijapewa hela za mtoto. Mpaka nikimpigia simu babake Erick hapokei kumbe chanzo ni wewe. Sasa leo utaondoka hapa kwangu, sitaki kukuona kabisa na tena usirudi tena mjinga wewe"

    Kisha Sia akaenda kutoa nguo za Steve na kumtupia nje kuwa aondoke.



    Leo Nasma alirudi kwao kumuangalia mama yake maana toka lile tukio la kubakwa na Bahati yule mama alirudi kwake kwa aibu.

    Alimkuta babake akiongea na mamake na mamake alionekana akilalamika kuhusu dawa walizompa Bahati, katika malalamiko alimsikia mamake akisema kwamba alishika ujauzito wa Bahati.

    "Kheee mama pole, yani toka tukio lile Bahati hajarudi nyumbani hadi leo"

    "Basi ndio hivyo meanangu, yule kijana kanidhalilisha ila yote ni sababu ya wewe na baba yako na ile midawa yenu isiyo na kichwa wala kiungo."

    "Pole mama, tatizo ilikuwa kwa Bahati mama yani hakuwa na mapenzi na mimi kabisa"

    "Sasa aliyekwambia mapenzi yananunuliwa ni nani? Penzi halitiwi dawa wala haliuzwi dukani, penzi la kweli lipo moyoni. Penzi la dawa huwa halidumu, hata kama ungefanikiwa basi badae ungejutia tu maana dawa zikiisha nguvu anaanza tena kutokukupenda na ubaya wa dawa zikiisha nguvu ni mmoja tu, kama mwanazoni alikuwa hakupendi sana ukamfanyia dawa akakupenda sasa zikiisha nguvu yani hata ule upendo wa mwanzoni unakufa yani atakuwa hakupendi kabisa, kwahiyo wewe jiandae dawa zikiisha kwa Bahati utapewa talaka tatu kabida yani"

    "Mama jamani unanitisha"

    "Sikutishi mwanangu ila upandacho ndicho utakachovuna. Katika maisha yangu sikuwahi kutoa mimba ila kwa aibu iliyoingia kipindi hiki nimejikuta nikienda mwenyewe kutoa mimba. Midawa yenu imenisababishia yote haya"

    Baba Nasma alikuwa amekaa kimya tu ila muda huo akaongea,

    "Hivi mnaona nimenyamaza basi mnafikiri nimefurahia ujinga wa huyo mwehu. Sijafurahia hata kidogo, sijali kuwa dawa ndio zimemfanya awe vile ila nitamkomesha tu. Nitamfanyia jambo ambalo hajawahi kufanyiwa maishani"

    "Jambi gani hilo baba?"

    "Tulia tu utaona ni jambo gani"

    Nasma akatamani sana kujua kuwa ni jambo gani ambalo baba yake analisema ila hakuweza kulijua kwa muda huo.

    Akaingia ndani kwao ila akakumbuka kuwa hospitali mara ya mwisho kuna mdada alikutana nae na akapanga nae mambo mengi sana, muda huo aliamua kumpigia simu,

    "Hallow Salma, ni mimi Nasma yule tuliyekuwa wote hospitali wakati najifungua"

    "Aaaah kumbe, za siku?"

    "Kwa upande wangu si nzuri kwakweli, nimefanya kila aina ya dawa ubaya wake yamenitokea puani"

    "Kheeee pole sana tena sana, imekuwaje tena?"

    Nasma alimueleza kwa kifupi kuhusu Erica na vile alivyomfanyia dawa Bahati na mwishowe kumbakia ndugu zake,

    "Yani kambaka hadi mama yangu mzazi"

    "Kheeee pole sana jamani, halafu sasa na Erica ni mzima wa afya sijui dawa ilidunda ila Erica ni mzima kabisa inaonyesha alipona, sasa sijui dawa yenu vipi"

    "Kumbe! Mwenzangu vipi na ndoa yako?'

    Salma nae akamueleza ilivyokuwa zile dawa za kuchoma na jinsi mumewe alivyomfuma na kumpiga sana hadi kulazwa na jinsi alivyompa talaka baada ya kugundua kuwa yeye ndio kamroga Erica, kisha akamwambia alivyofundishwa na kungi na jinsi ndoa yake ilivyoimarika kwa kipindi hiko.

    "Yani kwasasa sina mawazo kabisa, mimi na mume wangu ni mahaba tu. Tunapendana hatari, asante kwa kungwi"

    "Jamani nitumie namba zake na mimi niimarishe ndoa yangu niachane na haya mambo ya madawa"

    "Lakini namba si ulichukua siku ile na wewe"

    "Nimepoteza shoga yangu, naomba unitumie"

    "Hakuna tatizo"

    Basi waliendelea kuongea na walipokata simu Salma alimtumia Nasma namba ya yule mmama, kiukweli Salma sio kwamba aliipoteza namba ya yule mmama ila siku ile hakuitunza sababu hakuona umuhimu wake, ukizingatia babake ana dawa zote. Ila hapo alitamani vile Salma alivyosifia akajua na yeye lazima atafanikiwa akiwasiliana na huyo mmama.



    Nasma hakukaa sana kwao na kuamua kuaga ili akaweze kuongea na yule mmama na kufanya ambayo mwenzie kafanya mpaka mume wake katulia, alitamani sana na yeye mume wake aweze kutulia kama alivyotulia mume wa Salma.

    Basi akatoka na kumuaga baba yake, ila baba yake akamzuia kwanza,

    "Nasma subiri kwanza, kuna dawa nataka umanyie mume wako"

    "Hayupo nyumbani baba"

    "Yule atarudi tu, na akirudi basi ufanye hiyo dawa kwahakika huyo mumeo atakupenda maradufu"

    Kisha yule baba yake akaanza kutoa dawa na kumpa maelekezo Nasma,

    "Kuna hii dawa utaiweka mlangoni, kisha Bahati akiingia tu utampulizia nayo usoni"

    "Mmmh baba, si ataniona?"

    "Usijali kuhusu kukuona, yani dawa ya mlangoni itafanya asielewe hata ukimpulizia dawa. Baada ya hapo pala dawa hii mikononi na umshike mikono Bahati kisha umshike kichwani"

    Nasma alikubali tu alichokuwa akiambiwa na baba yake, akachukua ile dawa na kuaga vizuri, ila baba yake aliongezea

    "Ukishafanya hizo dawa nipigie simu kunitaarifu maana kuna kitu cha kufanya"

    "Sawa baba"

    Basi Nasma aliondoka na zile dawa kurudi kwake.

    Alipofika kwake akaweka mkoba pembeni na sababu mtoto wake alikuea kalala basi akaenda kumlaza, baada ya hapo aliamua kumpigia simu yule mmama ili nae apate ujuzi ambao Salma kafundishwa hadi mume wake katulia.

    Akaanza kuongea na yule mmama kisha yule mama akamuelekeza cha kufanya,

    "Asante sana, ila kuna dawa nimepewa na baba yangu kuwa itamvutia zaidi mume wangu"

    "Ni dawa gani hizo?"

    "Sizijui kwa majina"

    "Basi nielekeze zilivyo na ulivyoambiwa kufanya nazo maana mimi kidogo nina ujuzi na dawa nyingi"

    Basi Nasma akaanza kumuelekeza yule mama jinsi dawa zile zilivyo na alichoambiwa kufanya nazo na kumfanyia mumewe, alipomaliza kumueleza yule mama alimuuliza,

    "Kwani babako ana ugomvi na huyo mwanaume?"

    "Hapana, kwani vipo?"

    "Lazima ana ugomvi nae maana sio kwa dawa hizo, ukisikia kumfanya mwanaume ndondocha ndio kwa dawa hizo yani anakuwa hata kazi zake hafanyi tena yupo nyumbani tu hajielewi wala nini"

    "Kheeee kumbe!"

    "Ndio hivyo mwanangu, kuwa makini sana. Kama unampenda huyo mume wako usijatibu kumfanyia dawa hizo utalia yani utalia mwanangu. Raha ya mwanaume ni kujishughulisha, akuletee kamboga nyumbani, akuletee hela nawe ufurahi kuwa na mume ila mume kumfanya ndondoca hapana kwakweli. Kuwa makini sana mwanangu, hiyo dawa usimganyie mumeo."

    Basi Nasma alimshukuru yule mama na kuagana nae.

    Ila alivhofikiria aliona huenda ikawa kweli maana baba yake ameahidi kumkomesha Bahati, akawaza kuwa inawezekana ndio babake kaamua kumkomesha Bahati kwa njia hiyo.

    Akajisikitikia ila akaona bora ajiandae tu na alichofundishwa na yule mama ila kwa siku hiyo Bahati hakurudi tena nyumbani kwake.



    Ilikuwa ni usiku muda wa kulala, Erick alipigiwa simu na mama yake na kugundua kuwa mama yake amerudi.

    "Kesho uje ofisini kwangu"

    "Mama jamani umerudi kimya kimya, hata kuniambia!"

    "Ndio nimekwambia hivyo, kesho uje ofisini kwangu"

    Mamake akakata simu, basi Erick akamuelezea Erica alichokuwa anaongea na mama yake,

    "Hivi kwanini Erick mama yako nanichukia?"

    "Sijui, je mimi nikikuuliza kuwa kwanini mama yako ananichukia pia?"

    "Kwa upande wa mama, chanzo ni babako. Yani mama ana ugomvi na yule mzee ndiomana anamchukia sasa kaanza kukuchukia hadi wewe"

    "Sasa kesho nikienda ofisini kwa mama nitamuuliza kuwa kwanini anakuchukia na nitapata jibu tu hata usijali"

    Simu ya Erica ikaanza kuita, Erick akaichukua na kuiangalia akakuta mpigaji ni Bahati na kumuuliza Erica,

    "Kwani huyu jamaa ni vipi Erica? Yani anashindwa kuelewa kweli kuwa una mtu?"

    "Sijui ni kwanini"

    "Sasa naiweka sauti kubwa hii simu uongee nae, nataka nisikie kuwa unamkataa kabisa na kama akiendelea kusumbua nijue hajielewi kweli"

    Basi Erick alimpa Erica ile simu apokee ambapo aliweka sauti kubwa ili asikie vizuri, Erica alianza kuongea na Bahati,

    "Sikia Bahati, sikutaki sikupendi na sijawahi kukupenda"

    "Hapana Erica, najua unanipenda sana"

    "Sikupendi mbona1 hunielewi!"

    "Kama hunipendi mbona ulikuja siku ile Erica, uliniokoa najua unanipenda"

    "Sikufanya vile kwakuwa nakupenda hapana ila nilifanya vile ili usiendelee kuteketea. Ila sikupendi Bahati"

    "Erica kumbuka mimi ndio mwanaume wako wa kwanza"

    Erick akachukua ile simu kutoka kwa Erica na kuongea nayo yeye,

    "Hivi wewe jamaa vipi? Huelewi neno la sikupendi kwanini? Ni mwanaume wa wapi wewe ambaye ni msumbufu kiasi hiki!"

    " Najua Erica anasema hanipendi sababu yako ila Erica hawezi kunichukia mimi maana mimi ni mwanaume wake wa kwanza"

    Erica alimjibu kwa sauti maana simu alikuwa nayo Erick,

    "Mjinga wewe, kwanza hukuwa mwanaume wangu wa kwanza unikome"

    Kisha Erick akakata ile simu ila aliweza kuisoma akili ya Bahati kuwa ni ya kuivumilia.

    Akamgeukia Erica na kumuuliza,

    “kabisa katika wanaume wote uliamua kutoa bikra yako kwa huyu mwehu"

    "Hapana si yeye aliyenitoa bikra"

    "Mmmh basi nisije nikapata idadi ya uliotembea nao bure, tulale tu"

    Erick alisogea na kumkumbatia Erica na kulala.



    Kulipokucha, Erick aliamka kwa lengo la kujiandaa ila Erica nae aliamka, kisha Erick alipomaliza kujiandaa alimuaga Erica kwa kumbusu na kama kawaida ya siku hizo, Erick alichukua simu ya Erica na kuondoka nayo, ila kitendo kile kilikuwa kinamuumiza sana Erica maana alipenda awe ana wasiliana na afiki zake, na ndugu zake ila toka Erick aishikilie ile simu hakuweza kuwasiliana na yeyote maaa simu yake mpya haikuwa na namba yoyote ile.

    Erick aliondoka na moja kwa moja alienda ofisini kwa mama yake, alipomuona alifurahi sana na yule mama alifurahi pia na kuanza kuongea na mwanae,

    "Erick mwanangu, unakumbuka kipindi nahangaika na wewe! Nikiwa sina mbele wala nyuma, watu walinicheka na kunidharau. Ulikuwa ni mtoto mzuri ila uzuri wako uligubikwa na umasikini tulikuwa nao, hadi mamako mdogo alipoamua kukuchukua na kukulea hadi ukaonekana mtu kati ya watu maana hela za babako mdogo ulitanulia na kujipa jina kama za kwako na wengi walijua wale ni wazazi wako. Unakumbuka?"

    "Nakumbuka mama"

    "Je unapenda mtoto wako nae aishi maisha ya namna hiyo?"

    "Hapana sipendi mama"

    "Kama hupendi kwaniji huthamini mimba aliyobeba Sia, kwanini mwanangu unajua chozi la mwanamke ni kali sana. Unajua babako kwanini hana furaha hadi leo? Ni sababu ya machozi ya sisi wanawake aliyotusababishia"

    "Tena umenikumbusha mama kuhusu baba"

    "Kitu gani hiko?"

    "Baba alitaka kuoa hadi kutupeleka nyumbani kwa huyo aliyetaka kumuoa, tulishangaa sana kukuta anayetaka kumuoa ni Erica"

    "Eti nini?"

    "Ndio hivyo mama, yani baba alitaka kunuoa Erica"

    "Mmmh jamani Jimmy anawezaje kutaka kumuoa binti mdogo hivyo kama Erica? Haiwezekani kabisa, kale kabinti ni kachawi"

    "Hapana mama, Erica si mchawi"

    "Usimbishie, kuna siku nilikutana nako kananuka madawa ya kienyeji mwili mzima. Huwezi kunishawishi kuwa kale katoto sio kachawi. Na leo fanya juu chini ulale nyumabani kwangu, maswala ya kulala kila siku kwa babako hapana kwakweli. Leo jitahidi uje nyumbani kulala, nikiwa nyumbani tutaongea mengi zaidi"

    Basi Erick aliamua tu kunuitikia maa yake kuwa ataenda jionu kulala kwao maana alijua akimwambia kuwa haendi basi atazua utata zaidi.

    Erick alimuaga mama yake na kuondoka muda huo ila wala hakupenda maelezo ya mama yake kuhusu Sia yani hakupenda kabisa, akawa anawaza tu ni jinsi gani mamake ataujua uongo wa Sia.

    Akiwa njiani akamuona Dora, akakumbuka kitu na kusimamisha gari,

    "Dora mambo"

    "Safi, mmehama pale mlipokuwa mnakaa? Mbona kila nikija kimya?"

    "Aaaah ni sababu Erica yupo kwao"

    "Aaaah basi kesho nitaenda kwao kumuona"

    "Sasa kabla ya kwenda kwao, nahitaji kesho mapema kabisa twende wote kwa mama yangu ofisini nataka umuhakikishie mama yangu kuwa mimba ya Sia ni ya mdogo yako"

    "Sawa sawa, yani wewe Erick hata uniambie nile mavi basi nitakula. Nimekubali kwahiyo saa ngapi au utanipigia?"

    "Kwenye saa tatu hivi, nitakushtua tukutane mida hii hii"

    Basi akakubaliana pale na Dora na kuachana nae kisha kila mmoja kuendelea na shughuli zake.



    Leo James aliamua kwenda tena kwa mke wake ili kujaribu kuongea tena kuona kama wataweza kumruhusu kuendelea kuishi na mke wake.

    Alifika pale nankumkuta Bite na mama yake, alieleza azma yake ya kutaka kuishi tena na Bite, mama yao akamwambia,

    "Yani leo nikajua umekuja kusema kuwa umempata mwanamke wa kuishi nae ambaye amekubaliana na maukimwi yako, yani uneng'eneke hukonupate gonjwa halafu uje kulitua kwa mwanangu, naomba ukome"

    "Ila madaktari wameshauri kuwa naweza kuishi na mke wangu"

    "Uishi nae wapi? Hao madaktari kama wanaona ni kazi rahisi basi kawaoe wao ndio uwe mume wao, mwanaume mchafu wewe yani happ ulipo unanuka zinaa halafu bila aibu ukaishi na mwanangu"

    Kisha akamgeukia Bite na kumwambia,

    “Na wewe nisikie huu ujinga kuwa umeamua kwenda kuishi na James sijui sababu ya kumpenda, umpende James kuliko mamako mzazi si uchizi wa Erica huo kumpenda mwanaume hadi kutoroka nyumbani"

    James akadakia na kusema,

    "Halafu huyo Erica nilimuona hotelini ila nilivyoenda kumshauri basi mwanae akanichoma na kisu"

    Mama Erica alicheka sana na kusema,

    "Unacheza na Angel eeeh! Siku nyingine atakutoboa macho, kwani sisi tumekwambia utusaidie kumrudisha Erica nyumbani? Kuna mahali tumeomba msaada wako? Hebu achana na mwanangu bhana"

    James aliona thamani yake kwenye nyumba hii imeshuka sana kwahiyo ilibidi aendelee tu kubembeleza kurudiana na mkewe,

    "Cha kukushauri James, nenda mahakamani ufanye harakati za kumpa mwanangu talaka kisha uende kumuoa Dora nimemaliza"

    "Jamani mama"

    "Mimi sina watoto wasiojielewa kama wewe, toka nyumbani kwangu nitakuitia mwizi sasa hivi"

    Ilibidi James atoke na kuondoka zake.



    Dada wa Bahati ndio waliofanya kazi ya kumkataza Bahati kurudi nyumbani kwake kwani walijua akirudi tu basi atatupiwa tena madawa na mwanamke yule, kwahiyo walifanya kila jitihada ili Bahati asirudi kwake, wakati huo huo Bahati hakutaka kwenda hata kwa Siwema kwani tangu amekuwa sawa basi familia ya Nasma hakuitaka kabisa.

    Alichojibiwa usiku kwenye simu na Erica kilimsononesha sana na kumkosesha raha kabisa, alijiona hana thamani kwa kitendo cha kukataliwa na Erica, muda huo mchana aliamua kumpigia simu Fetty yule rafiki wa Erica ili pengine akae nae na amshauri. Akawasiliana na Fetty na kukubali kukutana, ni kweli Fetty alikutana nae na kufanya nae mazungumzo.

    "Hivi ukaribu wako na Erica upo vipo?"

    "Erica ni rafiki yangu sana, tumejikuta tukiambiana mambo mengi sana"

    "Hajawahi kukwambia kuwa ananipenda sana?"

    "Mmmmh hajawahi kwakweli, nakumbuka kila nilipokuwa nikikaa na kuongea na Erica alikuwa akimtaja mwanaume mmoja tu kuwa anampenda sana. Alisema anampenda sana Erick"

    "Ila mbona mimi nampenda hivi Erica! Yani upendo wangu mimi sidhani kama huyo Erick anaufikia, yani katika dunia hii hakuna mtu anayempenda Erica kama mimi"

    "Pole sana, hayo tunaita ni mapenzi ya sehemu moja yani unampenda ila yeye hakupendi. Mapenzi mazuri ni kupendana"

    "Jamani nitafanyaje sasa mimi? Nampenda sana Erica"

    "Pole ila kama unampenda kweli Erica basi unatakiwa kukubaliana na matakwa yake, Erica anampenda Erick na Erick anampenda Erica unachotakiwa kufanya ni kuwatakia kheri tu ili waishi salama. Na sio kubaki na msimamo wako huo kuwa unampenda sana utaumia"

    "Nawezaje sasa? Mke niliyeoa nasikia ni madawa na simpendi hata kidogo jamani nifanyeje sasa?"

    "Cha kufanya anza maisha upya, tafuta mke mwingine uoe"

    "Duh una ushauri mzuri saba, nikwambie kitu Fetty"

    "Niambie"

    Kabla hajasema alitokea George kumbe alikuwa mitaa hiyo, na George alivyomuona Bahati alimshika sura kabisa kuwa ndiye alifanya fujo hosteli kwakina Erica na siku hiyo alimuacha ampige tu ila leo aliona ndio vyema na yeye kulipiza kisasi chake alichokuwa nacho kwa muda mrefu sana. Tena alimkuta kakaa na Fetty ndio kabisa alichukia, akichanganya na yale majibu ya vipimo alipata hasira sana, akamfata na kumkunja, sababu Bahati hakujiandaa alijikuta akipokea kipigo kizito sana kutoka kwa George halafu George aliondoka eneo lile huku Bahati akiwa abapepesuka tu.

    Ingawa Fetty alienda kujificha wakati wanapigana, ila George alivyoondoka huruma ikamjia kwahiyo alienda kumsaidia Bahati mpaka kwenye gari ya Bahati kisha Fetty alianza kuendesha kumpeleka hospitali, uzuri aliweza kuendesha gari maana bila ya hivyo angeshindwa.

    Walifika hospitali ambayo Bahati huwa anahudumiwa mara kwa mara, basi walimuhudumia bila kibali cha polisi, wakati wanatoka pale hospitali na Fetty, walikutana na Mrs.Peter ambaye alimsalimia Bahati na kumpa pole, kisha alivyomuona Fetty akamuuliza Bahati,

    "Ndii huyo mke wako?"

    Bahati akacheka tu kisha mrs.Peter akasema tena,

    "Ila mmependezana sana, yani mnapendeza kwakweli. Hongereni"

    Bahati alishukuru tu pale na kuagana na huyu mama maana hakutaka aulize kitu kingine.

    Kisha alimuomba Fetty ampeleke nyumbani kwao maana aliona kuwa anaendesha vizuri.



    Usiku wakati Erick yupo na Erica, mama yake alipiga simu na alijua tu kuwa mama yake anamwambia habari ya kurudi nyumbani. Basi Erick alipokea,

    "Uko wapi? Mbona hujaja nyumbani?"

    "Nimeshindwa mama"

    "Kwanini umeshindwa?"

    "Kesho nitakwambia vizuri mama"

    "Hivi wewe Erick una matatizo gani eeeh! Usifikiri nimeibuka tu kukupigia simu na kukuuliza. Sijaibuka ila nimempigia kwanza dada yako Tumaini na kasema haupo nyumbani, tatizo nini? Kwa baba yako haupo na huku kwangu haupo, uko wapi?"

    Erick akaona ampe mama yake kauli ya kumfurahisha ili asimuulize sana,

    "Leo nimekuja kulala huku kwa Sia"

    "Mwanangu unasema kweli? Nipe Sia niongee nae?"

    "Kwahiyo huniamini mama"

    "Basi nakuamini mwanangu, kesho uje ofisini tupange vizuri"

    "Sawa mama"

    Muda huo akaagana na mama yake na kukata simu, alipoangalia pembeni alimuona Erica akilia na kumfata karibu,

    "Unalia nini sasa? Umechukia niliposema nipo kwa Sia? Nimesema vile ili mama asiongee sana, kwani kweli nipo kwa Sia jamani Erica!"

    Erica alinyamaza kimya kisha akasema,

    "Nyie wanaume ni waongo"

    "Nakubali Erica kuwa wanaume ni waongo ila mwanaume mimi ni wa tofauti sana kwani napenda ukweli na sipendi kumchukiza mtu nimpendaye. Erica nimempooza mama tu, tena kesho nina mpango kabambe maana naenda na Dora ofisini kwa mama ili akamuhakikishie kuwa mimba ya Sia sio yangu"

    Bado Erica hakuonekana kufurahi wala nini, basi Erick akajua kuwa ni mawazo ya kwao yanamsumbua

    "Erica, nakuahidi kesho tukishaongea na mama nitakamilisha kila kitu. Yani nahakikisha mama yangu anaenda kwenu na tunapeleka mshenga na kuoana"

    Erica akatabasamu sasa, Erick pia alitabasamu kwani alijua swala linalomchanganya Erica kwa muda huo ni mimba aliyobeba na kuhusu kuchelewa kwa harusi yao.

    Baada ya hayo, kila Erick alipotaka kulala Erica alitaka waongee tu yani hata kama cha kuongea kimeisha, mpaka Erick alihisi kusinzia na kuwaza kuwa anajukumu la kuweka Tv yake sawa ili Erica asipojihisi usingizi basi azubalie kwenye Tv.

    Mwishoe Erick alisinzia tu ndipo Erica nae akalala.

    Kulipokucha, Erick alijiandaa haraka haraka maana siku hiyo alichelewa kuamka tofauti na siku zote, kwahiyo alijiandaa haraka haraka na kumuaga Erica.

    Basi kama alivyopanga alikutana na Dora na kwenda nae ofisini kwa mamake.

    Walipoingia ofisini, kile kitendo cha mamake Erick kumuona Dora kilionekana kumchukiza sana kwani alitoka kwenye kiti chake na kwenda kumnasa kibao Dora.





    Basi kama alivyopanga alikutana na Dora na kwenda nae ofisini kwa mamake.

    Walipoingia ofisini, kile kitendo cha mamake Erick kumuona Dora kilionekana kumchukiza sana kwani alitoka kwenye kiti chake na kwenda kumnasa kibao Dora.

    Erick alimshangaa sana mama yake kufanya vile, Dora mwenyewe hakuelewa ni kwanini Yule mama kamnasa kibao alikuwa akijishika shavu tu huku akiugulia maumivu, Erick alimuuliza mama yake,

    “Mama, nini tatizo?”

    “Hivi kwanini umeniletea wasichana pumbavu kama huyu ofisini kwangu?”

    Akataka tena kwenda kumnasa kibao Dora, ila muda huu Dora alienda nyuma ya Erick kwani naye alitaka kujua ni kwanini huyu mama kamchukia kiasi hiki, alitaka kujua kuwa ni kwanini anafanyiwa hivi na huyu mama, kwahiyo alimshikilia Erick kwa nyuma huku Erick akiendelea kumdadisi mama yake kuwa tatizo ni nini,

    “Jana, wakati natoka kidogo hapa ofisini niliwakuta huyu msichana na George, muda huo George alikuwa anamlalamikia sijui kakutwa na ukimwi, huyu msichana akacheka na kumwambia nimekuambukiza mimi, tena kwa makusudi tu. Yani mjinga huyu kachanganya akili ya George tangia jana, maana alikimbia na bodaboda ila George hakuweza tena kuendelea kufanya kazi, na leo hajafika kazini”

    Hapo Dora ndio kumbukumbu ya jana yake ikamjia vizuri kuwa alipoachana na Erick, alienda mitaa hiyo na kukutana na George ila hakumbuki kama kulikuwa na mtu anasikiliza maelekezo yake na George, nay ale mawazo ndio yaliyofanya George jana yake ampige sana Bahati maana alikuwa na hasira za kutosha.

    Erick alimtazama sana Dora na kumuuliza,

    “Inamaana umewahi kuwa na mahusiano na George? Inamaana una ukimwi Dora?”

    Mama Erick akajibu,

    “Isingekuwa kweli basi George asingechanganyikiwa, huyu msichana kamuambukiza George ukimwi kwa makusudi, na lazima alikuwa na mahusiano nae shetani hili”

    Ila kile kitendo cha Erick kusikia kuwa Dora ana ukimwi na anamahusiano na George, wakati huo huo anatembea na baba yake alihisi kimemchanganya kiasi, akamuangalia kwa gadhabu na kumuuliza tena,

    “Dora ni kweli una ukimwi?”

    “Ila Erick mbona unabadilisha mada, nimekuja huku ili tuongelee habari zaa mimba ya Sia, sasa unanielezea habari za ukimwi mbona sikuelewi!”

    “Ila ni kweli ulikuwa na mahusiano na George?”

    “Kwani ni ajabu hiyo? Mimi ni mwanamke na George ni mwanaume sasa mahusiano kati yetu yatashindikanaje? Na hata hiyo, sio peke yangu kwani hata Erica amewahi kuwa na mahusiano na George”

    Hapo Erick alihisi akili kutosoma kabisa kwani amemtaja mwanamke ampendaye, na huwa hampendi George, kwahiyo swala la kusikia kuwa Erica alikuwa na mahusiano na George akawaza vingi sana, akawaza kuwa pengine ni kipindi Erica aliposema amepata kazi na ilikuwa ni ofisini kwa mama yake, akakumbuka pia siku aliyokuwa anarudi na kukutana na George ambaye aliuliza maswali mengi sana, ambapo naye Erica aliuliza undugu wa George na Erick, kwa hapo tu alishindwa hata kuongea ila mama yake ndiye aliongea,

    “Kheeee makubwa, kwahiyo wewe unamjua Erica, unamjua malaya mwenzio eeeh! Umeona Erick sasa, ndio umeniletea huyu nijue ukweli au wewe ndio uujue ukweli? Kwahiyo wewe binti ni nani kwa Erica?”

    “Erica ni rafiki yangu”

    Erick aliamua kumtimua Dora kwani aliona akisimama hapo basi ataongea mengi zaidi,

    “Dora naomba uende tafadhali”

    “Hutaki tena nimweleze mama yako ukweli?”

    “Nimesema nenda”

    Dora aliangalia sura ya Erick ambayo ilikuwa imebadilika haswaaa kwahiyo ilibidi aondoke tu.

    Mama Erick alimwambia Erick sasa,

    “Hii ndio aina ya marafiki wa Erica, unategemea nini kutoka kwake? Kama rafiki yake kaathirika je yeye anaponaje? Yani Erick mwanangu kwa Yule msichana ulipotea tena ulipotea kabisa, kale katoto kachawi mwanangu unaweza kuhisi unakapenda sana kumbe kamekufanyia dawa. Nakwambia kweli nilikakuta mimi kananuka dawa mwili mzima, sasa sijui utanishawishi kitu gani kuhusu huyo Erica. Ila kama umeamua kutulia na Sia, nakupa pongezi na harusi yenu nitaisimami”

    Kwa mara ya kwanza leo Erick aliondoka huku mama yake akiendelea kuongea, yani hakumuaga kabisa ila aliondoka.



    Siku hiyo mapema kabisa mzee Jimmy aliamua kuacha kazi zake na kuamua kwenda nyumbani kwa Ester kwani ujumbe wa mwisho wa Erick ulimvutia sana kuwa Ester kakubali, basi alifika pale na kuanza kuazungumza nae, ila kabla hajasema yanayomsibu akapigiwa simu na Dora, alitaka asiipokee ila Yule mama alimwambia aipokee,

    “Nina shida na wewe ya haraka sana”

    “Kuna mahali nipo Dora labda badae”

    “Hapana ni muda huu, nakuomba uje haraka”

    Basi Yule mama al;imwambia mzee Jimmy kuwa akasikilize alichoitiwa kwani yeye anamazungumzo marefu sana naye.

    Dora aliamua kumpigia simu mzee Jimmy kwani alijua kama Erick atapeleka ile habari kwa mzee Jimmy basi itakuwa tatizo kubwa sana.

    Baada ya muda mfupi, mzeeJimmy alifika eneo ambalo aliitwa n Dora.

    “Eeeh Dora nimefika, niambie nini tatizo?”

    “Nilikuwa sijisikii vizuri, nikaamua kwenda hospitali ila dokta kanishauri nipime na ukimwi, akaniuliza kama nina mwenzi wangu basi niende nae kupima ndio nimeamua kukutafuta wewe tukapime”

    “Hivi wewe Dora una akili kweli? Nani mwenzi wako sasa, mimi mwenzi wako tokea lini?”

    “Kwahiyo siku zote tunazokuwa pamoja sio mwezi wangu wewe?”

    “Hebu kuwa na adabu wewe binti, hivi mimi nitakutambulisha vipi kwa watu eti mwenzi wangu, inakuja hiyo kweli? Wewe Dora wewe uwe na akili mara nyingine”

    “Kwani tatizo liko wapi?”

    “Huoni tatizo wewe? Hujioni kuwa ni mdogo sana? Unadhani mimi na utu uzima huu nianze kuhangaika na mtoto mdogo kama wewe sina aibu?”

    “Na ulivyokuwa unataka kuhangaika na Erica ni mkubwa mwenzio Yule? Unavyolala kifuani kwangu ni mkubwa mwenzio mie, tena usitake nikuongelee maneno ya shombo mtu mzima wewe usiyejielewa, wakati unalala na mimi hukutambua kama kuna watu wazima wenzio? Hukutambua kama unatakiwa kuwa nao zaidi yangu? Hebu nitolee balaa, kwanza unaogopa nini kupima mtu mzima wewe, utakuwa unajua fika kama unao, kwaheri”

    Dora aliinuka na kuondoka, ila mzee Jimmy hakutaka kumuita Dora kwa muda huo kwani alihisi ataongea maneno ya kumdhalilisha tu.

    Kakweli kwa yale maneno ya dora yalifanya siku hiyo mzee Jimmy ajihisi vibaya sana, akainuka na kuondoka ila hakuwa sawa akilini na hakuweza tena kurudi kwa Ester na badala yake akarudi nyumbani kwake.



    Leo Tony alikuwa nyumbani kwakina Tumaini huku akiongea nae na kujaribu kupanga nae mambo mbali mbali,

    “Tumaini kwanini sisi tusiamue kuishi kama Erica na Erick?”

    “Hapana Tony, baba yangu hawezi kukukataa wala mama yangu hawezi kukukataa basi uje kwetu ujitambulishe na tufate sharia zote za ndoa. Unafikiri Erica na Erick maisha wanayoishi ni ya furaha? Hawana furaha wale ila wanajaribu kutuonyesha tu sisi tuone kuwa wanafurahia ila hawana furaha hata kidogo, nakupenda unanipenda ila kwenu hawanitaki na kwetu hawawezi kukukataa, naomba tufate taratibu zote tuishi kwa amani”

    “Sawa, basi unipeleke kwa mamako ukanitambulishe”

    “Hakuna tatizo, tena ngoja nikajiandae twende’

    Tumaini alienda kujiandaa ili aondoke na Tony kwenda nae kwa mama yake.

    Wakati Tumaini anajiandaa, mzee Jimmy alifika na kumkuta Tony sebleni, alimuangalia tu ila hata salamu ya Tony hakuiitikia na moja kwa moja alienda humbani kwake.

    Tony alishangaa sana, na baada ya muda alitoka Tumaini akiwa kashajiandaa ili waondoke, alivyofika Tony alimsifia sana

    “Wow, umependeza Tumaini”

    Akatabasamu tu na kumwambia kuwa waondoke tu, ila kabla hawajatoka alitoka ndani mzee Jimmy tena na kumsimamisha Tumaini,

    “Weee Tumaini subiri kwanza”

    Tumaini akasimama ila alimshangaa babake kuwa mbona karudi mapema vile nyumbani maana haikuwa kawaida, kisha mzee Jimmy akasogea na kumuuliza,

    “Huyu kijana asiye na adabu umemuokota wapi?”

    “Baba jamani si ungesubiri nikutambulishe kwanza”

    “Kabla hujanitambulisha ngoja niulize, kijana una gari?”

    “Hapana sina”

    Mzee Jimmy alitikisa kichwa, akamuuliza tena,

    “Una nyumba?”

    “Hapana sina”

    “Kwahiyo unategemea mwanangu utaishi nae kwenye pango? Nilikuwa nakusikiliza tu unavyojifanya kumsifia Tumaini, je unajua gharama ya nguo alizovaa Tumaini au unasifia tu”

    Tony alikaa kimya maana hakuwa na cha kumjibu, kisha mzee Jimmy akamwambia Tumaini,

    “Sitaki kuiona hii takataka tena kwenye nyumba yangu, najivunia kuwa na mtoto wa kike ila sio aolewe na fukara umesikia?”

    Tumaini alishindwa hata kumuitikia baba yake na kuamua kumshika mkono Tony na kutoka nae nje, na kupanda ile gari aliyoachiwa na Erick na kuondoka nayo.

    Kiukweli Tony hakuwa na raha kabisa, kwani kitendo cha kudharauliwa hakukipenda kabisa.



    Walipokuwa wanakaribia kufika kwa mama wa Tumaini, Tony alijihami na kuuliza,

    “Kama kwa babako kwenyewe hali ndio ile hivi mama yako atanielewa kweli?”

    “Atakuelewa tu hata usiwe na shaka, mama yangu ni muelewa”

    “Dah yani watu wenye hali za kawaida tunadharaulika sana jamani dah!”

    Basi walifika na kugonga mlango kisha ndugu wa Tumaini alifungua na kuwakaribisha ndani.

    Waliingia na kumkuta mama yake Tumaini yupo ndani ambapo baada ya salamu tu, Tumaini alianza kumtambulisha Tony kwa mama yake, Yule mama alimkaribisha vizuri tu Tony ila alimuuliza Tumaini,

    “Huyu kijana ulisoma nae chuo?”

    “Hapana mama, nilisoma nae shule ya msingi”

    “Aaah kumbe! Vipi kijana umesoma hadi kiwango kipi cha elimu?”

    “Nimeishia kidato cha sita mama”

    “Mmmmh!”

    Tumaini aliamua kumuuliza mama yake,

    “Mbona umeguna mama?”

    “Hivi unaona ni kitu cha kawaida hiki Tumaini?”

    “Kwanini mama?”

    “Wewe una shahada halafu mwanaume kidato cha sita inakuja kweli? Mara nyingi mwanaume anatakiwa awe juu kielimu kushinda mwanamke, sasa wewe umemshinda elimu unadhani atakusaidia nini? Haya ngoja nikuulize kingine, unajishughulisha na nini?”

    “Sana sana najishughulisha na kilimo na mifugo”

    Mama Tumaini alicheka sana yani hakutegemea kujibiwa vile kabisa, kisha akasema,

    “Yani Tumaini na elimu yako kabisa kabisa unaenda kuchukua mwanaume mkulima kweli?”

    “Sasa mama, ni mwanaume gani ananifaa jamani!”

    “Badala upate mwanaume mwenye kazi yake, mwanaume mwenye ofisi zake, kweli unaenda kumchukua mkulima mwanangu na zaidi zaidi umemzidi elimu kweli anakufaa huyu!!”

    “Kwani mama mtu kutokusoma ndio nini? Kumbuka Erick kaishia kidato cha nne ila ana hela hadi mimi namtegemea yeye, je amesoma?”

    “Kuhusu Erick sawa, haya na huyu ana hela gani?”

    “Mama, kila kitu ni taratibu”

    “Mahali milioni tano, atakuwa nayo huyu?”

    “Kila kitu kinawezekana chini ya jua”

    Tumaini huwa hapendi kusemwa wala kukosolewa kwahiyo muda huo alichukia sana, na kuamua kuinuka kisha akashika mkono Tony waondoke.

    Walipofika nje, Tony alimuelekeza

    “Haipaswi kuchukia hivyo mpenzi, hawa ni wazazi wetu yani inatakiwa kuwaelekeza tu, ili waelewe kuwa ni jinsi gani wanatuumiza na maneno yao.”

    “Tuondoke bhana, siwezi kuvumilia maneno ya mama”

    Basi wakapanda kwenye gari na kuondoka zao.



    Erick hakunywa pombe kwa siku nyingi ila siku hiyo alipitia kwanz kunywa pombe halafu ndio akaenda nyumbani kwake, na kumkuta Erica akicheza na Angel hakutaka kumuuliza mbele ya mtoto kwani aliona ni picha mbaya watamuonyesha Angel. Basi alienda chumbani moja kwa moja ila Erica aliona kuwa ile hali haikuwa ya kawaida kabisa, kwani Erick huwa akirudi basi lazima atamkumbatia na kumtania Tania ila siku hiyo haikywa sawa, alienda ndani kumfata, aligundua kuwa amekunywa alihisi kuwa huenda ile ndio sababu ya kukimbilia ndani moja kwa moja ili asionekane kama amekunywa. Basi aliendelea kumbembeleza Angel na alipolala alienda kumlaza, ila muda huu alimuona Erick amekaa tu kitandani, akamuuliza,

    “Mbona leo hata kwenda kuoga hujaenda Erick, nini tatizo?”

    “Niambie kwanza mahusiano yako na George ya ofisini kwa mama yangu?”

    “Sitakuficha Erick, nitakwambia ukweli, wakati nipo chuo nimewahi kuwa na mahusiano na George na tena ni mwanaume aliyeniumiza sana, sababu kuna mahali aliniacha tena bila…..”

    “Usiendelee, ila nilikueleza kuwa George ni nani yangu? Mbona hukuniambia hayo?”

    “Erick, sikuona sababu ya mimi kuongelea mahusiano yaliyopita maana mimi na wewe tulianza maisha mapya”

    “Unajua Erica mtu akikuangalia unaonekana ni binti uliyetulia sana, yani nashindwa kuamini kama ulishawahi kuwa na Yule fedhuli. Haya umewahi kuwa nae hivi karibuni?”

    “Hapana toka nimeachana nae kipindi cha chuo sijawahi kuwa nae tena”

    “Na vipi ulipokuwa unafanya kazi ofisini kwa mama yangu?”

    “Muulize hata mama yako akwambie ukweli. Alikuwa akiniambia kila mara kuwa niwe na George anioe ila nilikataa, na hiyo ni sababu pia ya mimi kuacha kazi ofisini kwa mama yako”

    “Je ni kweli Dora ameathirika?”

    “Ndio Dora ameathirika, ni muda tu”

    “Dah inamaana na baba yangu nae ameathirika?”

    “Sijui”

    “Sasa hujui nini?”

    “Sijui tu, ila je hiyo ndio sababu ya wewe kuchukia Erick hadi kunywa pombe?”

    “Erica, nadhani hujui ni jinsi gani mapenzi yanavyoumiza. Mapenzi yanaumiza sana Erica halafu uwe unatambua kuwa nakupenda sana ten asana, huwezi amini moyo wangu ulivyopasuka na wivu baada ya kusikia kuwa ulikuwa na mahusiano na George, simpendi Yule jamaa simpendi kabisa”

    “Nisamehe Erick, ila ilikuwa kipindi hiko hata sipo na wewe na hakuna dalili ya kuwa pamoja kabisa, nisamehe mpenzi wangu’

    Erica alimuona Erick ametulia tu ila kwavile alijua kuwa Erick anapenda sana mapenzi basi akaanza kumshawishi na mwisho wa siku wakajikuta wamelala wote.



    Dora alipotoka pale kuongea na mzee Jimmy, akaenda sehemu na kuagiza pombe ili anywe maana alijihisi kuwa na mawazo mengi sana na aliamini kuwa pombe ndio njia pekee yay eye kuacha kuwaza sana. Kuna muda aliwaza kuwa hayupo sawa kwa yale anayoyafanya,

    “Hivi mimi nitaendelea kuhangaika hivi hadi lini? Kwanini nipo hivi mimi, Yule mama wa watu alihangaika kuniombea masikini kumbe mtu mwenyewe sikio la kufa halisikii dawa. Kuna muda natamani na mimi niwe na familia yangu, mimi nifurahie mapenzi kama Erica anavyofurahi kwa Erick maana kwangu ni kuhangaika na mwanaume huyu mara Yule na hadi sasa nimekuwa mzoefu yani hakuna ninachofanya kizuri. Mwishowe nitachukiwa na watu wote mimi jamani, natakiwa kubadilika kwakweli, ila ngoja ninywe pombe kwanza nipunguze mawazo.”

    Basi akazidi kuagiza pombe na kunywa, wakati akinywa pombe zile, mara akafika James eneo lile nae alienda kunywa pombe, kwahiyo alipomuona Dora aliamua kwenda kunywa nae pombe, na siku hiyo walikunywa sana hadi walilewa na kuanza kuongea kilevi tu na kufanya mambo ambayo ulevi unawatuma. James alimwambia Dora akiwa katika ile hali ya ulevi,

    “Leo nataka twende Yule mwanamke ambaye alisababisha mimi na mke wangu tugombane mara ya kwanza, nataka twende kwa Yule msichana wangu wa kazi”

    “Ndio twende James, na leo nitamuonyesha huyo mwanamke namna ya kuiba mume wa mtu, yeye si alikuiba wewe kutoka kwa mkeo na mimi nitakuiba leo kutoka kwake”

    Wakacheka sana muda huo na kuingia kwenye gari ya James huku gari ikiendeshwa kilevi sana maana siku hiyo walilewa sana, yani Dora hata alishasahau kuwa pombe zimewahi kumtenda kitu gani ila alichojali muda huo ni kunywa na kufurahia maisha tu kwa ulevi.

    Yule mwanamke alikuwa amelala muda huo akashangaa kusikia mtu akigonga kwa nguvu mlango wake, basi aliinuka na kwenda kufungua, alishangaa sana kumuona James akiingia na mwanamke tena wakiwa kwenye hali ya ulevi sana, alishindwa hata kuwaambia chochote maana walikuwa hawamuelewi wala nini na waliendelea kufanya mambo yao ya kilevi, Dora na James walienda kitandani kwa Yule mwanamke na kuanza kufanya mapenzi, kwakweli Yule mwanamke aliumizwa sana na kitendo kile, hakutegemea kama James anaweza kumfanyia akili mbovu kiasi kile alichomfanyia, kisha Dora na James wakalala kitandani kwa Yule mwanamke, na Yule mwanamke na mtoto wake walikaa kwenye kochi ambapo alimlaza mwanae kwenye kochi nay eye kulia tu.

    Kulipokucha, Dora alishtuka pale akitandani alipolala na James na kumshtua James pia, James alikaa ila kumbukumbu zote za usiku zilimjia kichwani kuwa walichokuwa wanafanya na Dora hakikuwa sawa, basi akainuka pale na Dora na kuondoka ila walivyofika mlangoni walikuta mlango umefungwa kwa nje yani Yule mwanamke alitoka na kuwafungia mlango.



    Fetty nae asubuhi na mapema alienda kumuona Bahati na alimkuta kwao akiwa tu nje akipunga upepo na kuangalizia majeraha yake ya kipigo alichopata kutoka kwa George, Dora alimpa pole tena, kisha alianza kuongea nae kilichomfanya amfate kwa wakati ule,

    “Bahati, kilichonileta hapa ni kuwa kuna ndoto mbaya sana nimepata kuhusu wewe”

    “Ndoto gani hizo?”

    “Inaonekana kuna watu wanataka kukufanyia kitu kibaya sana, sasa nataka nikushauri kitu”

    “Kitu gani?”

    “Una Kuran ndani?”

    “Ipo”

    “Unasomaga?”

    “hapana, sisomagi na sionagi cha kusoma”

    “Wewe Bahati wewe, kwahiyo kitu gani mnategemea nyumbani kwenu hapa? Yani nini kinawalinda?”

    “Nyumba hii imezindikwa bwana, yani nyumba hii tulichinja mbuzi na kichwa chake kilifukiwa hapo mlangoni ndio kinga yetu hiyo’

    “Mnajidanganya Bahati, tunatakiwa tumtegemee Mungu ndio msaada pekee katika maisha yetu. Wakristo huwa wanasoma Biblia na sisi Waislamu tunatakiwa tuwe tunasoma Kuran”

    “Sasa nisome nini?”

    “Unatakiwa usome ili ujikinge na watu wabaya, wachawi na mikosi, ngoja nikutajie sura kadhaa za kusoma zitakusaidia sana. Zisome kila siku ujiepushe na vinavyotaka kukuvamia maana naona kabisa haupo salama Bahati”

    “Niambie basi hizo sura za kusoma”

    “Soma Kul-audhubi rabil-nas na Kul-audhubi rabil-falaq”

    “Sawa Fetty, nitaanza sasa kusoma hivyo ulivyoniambia, kiukweli mimi sikujua kama kuna sura kwenye Kuran unaweza kusoma na ikakusaidia usifatwe na wachawi au watu wabaya au mikosi”

    “Katika maisha ya sasa tunatakiwa kumtegemea Allah tu na si vinginevyo, achana na imani za kishirikina ndugu yangu utakuwa unaandamwa na mikosi kila siku, unatakiwa kumtegemea Allah tu”

    “Asante sana Fetty”

    “Na ukimaliza kusoma uwe unapiga dua”

    “Sawa Fetty nimekuelewa”

    Muda ule ule Fetty alimuaga Bahati na kuanza kuondoka zake, ila simu ya Bahati ilianza kuita alipoona ni mkewe anapiga basi alimuita Fetty apokee ile simu na upande wa pili uliposikia sauti ya mwanamke basi aliamua kukata ile simu halafu Fetty akaaga tena na kuondoka zake.

    Bahati nae aliona ni vyema kuanza kusoma hiyo Kuran muda ule ule alioambiwa na Fetty kwani ni kweli alikuwa ameandamwa sana na watu wabaya, kwahiyo aliinuka pale nje na kwenda ndani na wakati anaanza kusoma aliamua kuzima simu ili isimsumbue.



    Nasma alikuwa nyumbani akimgoja Bahati ila hakufika nyumbani kwa siku zote, aliumia sana moyo wake kuwa amepata ujuzi halafu mume wake hataki tena kurudi nyumbani yani hapo alijihisi vibaya kabisa.

    Aliamua kumpigia simu Bahati ndio muda ule alipokea mwanamke, kwakweli aliumia sana moyo wake yani alijihisi vibaya haswaa, na alipokaa kaa na kujaribu tena kumpigia simu alikuta ile namba haipatikani kwahiyo aliumia zaidi, ila wakati amekaa akapokea simu kutoka kwa baba yake,

    “Wewe ushafanya dawa nilizokupa?”

    “Bahati hajarudi hadi leo baba”

    “Hiyo ya mlangoni ulimwaga?”

    “Sikumwaga baba”

    “Mjinga wewe, ungemwaga hiyo kwanza imvute yani umekaa na dawa siku zote hizi itakuwa haina ile nguvu ya awali, mjinga kabisa wewe mtoto”

    “Nisamehe baba”

    “Umenipa kazi ya ziada yani hata sielewi nianzie na mimi, mi nitamuharibu kabisa huyo mume wako, wewe si umeshindwa?”

    “Baba, naenda kuimwaga sasa ile dawa”

    “Ndio imwage na mimi nafanya vitu vyangu huku halafu akifika kama nilivyosema, usikosee masharti sawa?”

    “Sawa baba”

    Nasma aliagana na baba baba yake na kwenda kuimwaga ile dawa mlangoni ili iweze kumvuta Bahati arudi pale na aweze kumfanyia dawa zingine ila shida yake ilikuwa ni kumfanyia yale ambayo amefundishwa na Yule kungwi.

    Alivyomaliza kumwaga dawa, akampigia tena simu Salma ili kumuuliza maendeleo yake na mumewe,

    “Hahahah shoga yangu mahaba yanajibu, yani hapa nilipo najihisi kimimba kimeshanasa”

    “Jamani, mbona mtoto mdogo huyo?”

    “Mdogo ndio ila mume wangu alisema tumpe maziwa ya kopo kwahiyo kubeba mimba nyingine kwasasa ni halali yangu Nasma. Vipi wewe na mumeo?”

    “Mmmh mume wangu hajarudi nyumbani kabisa, yani nyumba imekuwa kituo cha polisi, hata sijui nifanye kitu gani?”

    “Pole mwaya, ila vumilia tu. Mvumilivu hula mbivu kama mimi hapa, ngojea wiki ijayo nikapime vizuri kabisa ila nahisi tu ishanasa”

    “Hongera sana”

    Basi aliagana nae ila yeye alikuwa na masononeko sana kwani hakuweza kuonana na mumewe kabisa. Alivyokata ile simu, aliamua kujigelesha na kujaribu kupiga namba ya dada yake Bahati,

    “Wifi habari”

    “Koma, sina wifi mshirikina kama wewe”

    “Jamani wifi ndio yamekuwa hayo? Mnasahau kuwa ni nyie ndio mlinishawishi mwanzoni na kumfanyia dawa Bahati ili anioe? Jamani umesahau kabisa wifi yangu!”

    “Ni kweli nilikushawishi ila sikukushawishi umpe kaka yangu dawa awe kama jogoo, asante Mungu Bahati alibahatika kuonana na Erica na ile midawa yenu ikayeyuka ila mlimfanyia vibaya sana Bahati hata dada zake alikuwa akitutamani loh! Nyie ni wabaya sana, wewe Nasma na ukoo wako mzima hamfai hata kidogo”

    Kisha dadake Bahati akakata simu ndipo Nasma akaelewa kuwa Bahati alipona baada ya kukutana na Erica, ingawa nay eye ile hali ilikuwa ikimsumbua sana ila hakutaka kuona kuwa Erica ndio sababu ya kupona kwa Bahati kwani alijiona akizidi kukosa sifa za kuwa mke wa Bahati.

    Ila badae aliwaza kitu kuhusu mwanamke aliyepokea simu ya Bahati na kuhisi kuwa huenda ni mdogo wake Siwema, kwakweli hakupenda na aliapa akikutana na Siwema basi alipize kisasi.



    Tony leo alienda nyumbani kwao tena kuongea na mama yake, na alimkuta vizuri kabisa akamsalimia na kuanza kuongea nae,

    “Hivi mama unajisikiaje kuona kuwa Erica hayupo nyumbani na hujui alipo, unajisikiaje?”

    “Maswali gani hayo ya kijinga unaniuliza?”

    “Unajua mama, kuna mambo kama mzazi unatakiwa kuyasawazisha. Sio jambo jema kwa sie watoto wako kukosa uelekeo kabisa, mfano hutaki niwe na Tumaini, ila sababu Tumaini hapatani na Erica wakati huo huo Erica humtaki nyumbani sasa utasemaje unampenda Erica kwa mtindo huo mama?”

    “Umetumwa au? Aliyekutuma mwambie sijawakuta wenyewe”

    “Ila mama kwanini upo hivyo lakini?”

    “Ngoja nikuulize, unatakaje yani?”

    “Niruhusu mimi nimuoe Tumaini na Erica aolewe na Erick”

    “Halafu harusi yenu mtaifanya siku moja eeeh!”

    “Ikiwezekana”

    “Nilijua tu, huna lolote unataka mdebwedo tu unajua Erick ataandaa kila kitu halafu wewe utaandaa tumbo lako hilo ule ukajisaidie, ila kwavile umelazimisha mwenyewe nataka nikukubalie kwa sharti moja”

    “Sharti gani hilo mama?”

    “Nataka Tumaini aje akae hapa kwa siku moja tu yani atakuja na kuondoka kesho yake, nataka nimuone utendaji wake wa kazi. Sio unaoa mwanamke wa maonyesho tu, mwanamke hajui kupika, hajui kufua, hajui kuosha vyombo, hajui kudeki, hapana kwakweli hata kama umempenda siwezi kuruhusu uoe kibwengo cha aina hiyo. Unaona hapa nyumbani, ukimuangalia Erica huko nje utamuona kama binti mzembe ila ndani kwangu hakunaga mfanyakazi ni kukukuruka mwenyewe kama hataki ajue siku hiyo hali, mimi napenda kufanya kazi na watoto wangu nao napenda wanaojishughulisha. Narudia tena, mwanamke wa maonyesho simtaki nyumbani kwangu”

    “Kama sharti lenyewe ndio hilo basi Tumaini wangu kafaulu mia ya mia, nitamleta mama. Nitamleta Jumamosi atashinda hapa na kuondoka Jumapili, na mtakula chakula cha Tumaini kwahiyo msijali kitu”

    “Haya tutaona, Yule anaonekana mzembe kabisa, na kalelewa maisha ya kitajiri ataweza kazi kweli?”

    “Ila mama, mbona Erica nae anaonekana mzembe lakini kazi anafanya?”

    “Usimfananishe Erica na huo uchafu wako”

    Tony hakutaka kubishana sana na mama yake ila alikubaliana na swala kuwa Tumaini aje hapo ila tu aliwaza Tumaini anaweza kukubali kuja hapo kwao ikiwa anaujua mdomo wa mama yake.



    Dora na James walikaa mule mule ndani bila kuweza kutoka, kwakweli James aliona kapatikana siku hiyo maana hakutegemea kabisa kama Yule mwanamke angemfanyia vile, James alitafuta kila njia ya kuweza kufungua ule mlango, aliangalia mule ndani kuwa hata kuna kijiko au kisu ila hakuona chochote cha kuweza kukorokochoa ule mlango maana Yule mwanamke alitoa vyombo vyote inaonyesha alihisi pengine watatumia kisu kufungua mlango, James alijaribu kutafuta simu yake ila mfukoni hakuwa na chochote yani Yule mwanamke alichukua na simu zao zote hadi funguo ya gari alichukua maana si walilala kwa ulevi kwahiyo kuna muda hawakujitambua kabisa,

    “Dah huyu mwanamke kanikomesha aiseee dah”

    “Tutakula nini sasa?”

    “Yani Dora unawaza kula badala ya kuwaza tutatokaje hapa jamani!”

    “Sasa. Kutoka haiwezekani na kula je! Nina kiu, nina njaa, jamani James huyu mwanamke ulimuokota wapi?”

    “Yani najuta kumfahamu huyu mwanamke, kazi zangu zote zimegoma leo. Mijinga Yule kachukua hadi funguo za nyumba yangu, sijui ataenda kufanya nini kule”

    “Na hujaweka mlinzi nyumbani kwako?”

    “Nilimtimua maana alikuwa ananifatilia sana na kumwambia mke wangu, hapa ndio najuta sijui nitafanyaje”

    Yani waliona usiku ukiingia huku wakiwa bado ndani ya kile chumba, kwakweli Dora alikuwa na njaa sana na akaona kwa muda huo hakuna jinsi zaidi ya kujipa uchizi na kuanza kupiga kelele, basi Dora alianza kupiga kelele za yowe na kufanya watu wajae nje ya chumba kile, na baada ya kelele kuzidi ndipo raia walipojitolea kuvunja ule mlango, yani walitoka mule hawana chochote, si simu si funguo ya gari na hata gari haikuwepo na si hela yoyote maana Yule mwanamke alikomba hela zote, James aliamua kumuomba mmoja aliyewasaidia kutoka hela na kumuahidi kumrejeshea,

    “Aaaah sikufahamu kaka utanirudishiaje?”

    “Chukua kitanda cha humu ndani, naomba elfu ishirini tu”

    Kwa kuambiwa vile, Yule mtu alitoa ile hela bila utata na kutoa kile kitanda ndani, ila James muda huo hakujali kuwa mlango haujafungwa mwala nini ila aliita bajaji kisha wakapanda na kuondoka na Dora.



    Steve aliondoka ila alirudi tena kwa Sia maana hakuweza hata kukaa nyumbani kwao, alirudi na kumuomba sana Sia kuwa waishi tu na hatojaribu tena kumsemea neno baya.

    “Basi siku hizi nataka mchana usishinde huku kabisa yani uje usiku tu, sawa?”

    “Sawa mpenzi wangu”

    Steve alifurahi sana kukubaliwa tena na Sia, kisha akakumbatiana nae kwa furaha. Sababu giza lilikuwa limeingia na Sia alitamani kupata upepo wan je, akatoa mkeka na mto na kwenda kukaa nao nje, muda huu alijilaza kwenye miguu ya Steve huku wakiongea ongea mambo mbalimbali.

    Mamam Erick alipata jambo na aliona kuwa lile jambo asikawie nalo, aende kumwambia Sia hata kama muda umeenda ndipo alipoenda hapo nyumbani kwa Sia na kumkuta Sia yupo kwenye miguu ya Steva, akawashtua na kuwaambia,

    “Wewe Sia si ulisema huyu ni kijana wako wa kazi? Hata hivyo si nilikwambia umuondoe wewe”

    Sia akainama chini kwa aibu kwani hakuwa na cha kujieleza





    Mama Erick alipata jambo na aliona kuwa lile jambo asikawie nalo, aende kumwambia Sia hata kama muda umeenda ndipo alipoenda hapo nyumbani kwa Sia na kumkuta Sia yupo kwenye miguu ya Steva, akawashtua na kuwaambia,

    “Wewe Sia si ulisema huyu ni kijana wako wa kazi? Hata hivyo si nilikwambia umuondoe wewe”

    Sia akainama chini kwa aibu kwani hakuwa na cha kujieleza.

    Mama Erick aliendelea kuongea,

    “Kataaa sasa kwa kinywa chako kuwa huyu si mwanaume wako, ni kijana wa kazi. Hivi kwa mtindo huu ukimwi utaisha kweli? Juzi tu ulikuwa na Erick huku na leo unajiachia na huyo kijana?”

    Muda huu aliamua kujitetea,

    “Erick hajawahi kuja kulala huku, na huyu kijana nimejinyoosha tu sio kwamba mtu wangu”

    “Sia, mimi sio mtoto mwenzio ambaye ukiamua kumdanganya tu unamdanganya sawa? Mimi ni mtu mzima mwenye akili zangu timamu, ngoja niondoke zangu hapa nisije kutenda dhambi bure maana wengine hasira zetu zipo karibu”

    Basi mama Erick aliondoka na kupanda gari lake kuelekea nyumbani kwake huku analalamika mwenyewe,

    “Mapenzi bhana sijui ni kitu gani jamani, wanaume waongo, wanawake waongo jamani! Hivi hakuna hata abnayeweza kuwa mkweli angalau kwa uchache jamani! Dah”

    Alifika nyumbani kwake na kuamua kuoga na kwenda kujipumzisha tu kwani hakuwa hata nay a kuongea kwa wakati huo.

    Asubuhi na mapemz kama kawaida aliamka na kwenda zake kazini kwake kwenye kazi yake, ila muda ule ule wa asubuhi alipita mzee Jimmy ofisini kwake na kukumbuka kuwa jana kabla hajaenda kwa Sia alimpigia mtu huyo na kumwambia kuwa waonane kwaajili ya kuzungumza kuhusu mtoto wao,

    “Eeeeh nimepokea wito”

    “Yani, unajua kuna jambo nililifikiria kuhusu Erick, niliona kuliko mtoto kutangatanga na maisha na mwisho wa siku kuwa kama wazazi wake ambapo baba yake hajaoa mpaka leo na mama yake hajaolewa, mwishowe watu watasema mtoto karithi bure. Najua umri wa Erick sio mkubwa sana wa kusema ni lazima aoe kwa kipindi hiki ila baada ya kugundua kuna mwanamke mwenye mimba yake nikaona ni bora tufanye mipango waoane kuliko kuishi tu. Ila sasa nilichogundua kuhusu huyo mwanamke ndio kimenikata maini kabisa”

    “Kwahiyo wewe hukumjua Erica eeeh! Umegundua nini?”

    “Kwanza simuongelei Erica hapa, namuongelea Sia”

    “Aaaah kumbe unamuongelea huyo mtoto asiyejielewa, yani hajielewi huyo binti sijui kama kichwa chake ni kizima, alinidanganya kuwa ana mimba ya Erick na hata mimi kufanya jitihada zote awe pamoja na Erick nakuja kugundua ana kajamaa kengine, binti hajielewi Yule”

    “Kheeee kumbe ningekwambia mapema ningejua dah! Mimi ndio nimejua jana, nimemkuta kajiachia na huyo mwanaume, kwanza mvulana mwenyewe mdogo Yule atampa nini zaidi ya kumuongezea umasikini tu”

    “Ndio hapo, na ile mimba si ya Erick maana Erick kaikataa kabisa”

    “Basi ndio nilichokuitia hiko ila Erick hajakataa ile mimba kwangu, maana majuzi nilimwambia aje kulala nyumbani akasingizia kuwa amelala kwa Sia”

    “Aaaah mwanao muongo tena muongo kabisa, kwanza siku hizi hakai nyumbani asije akakudanganya muda mwingine kuwa yupo nyumbani.”

    “Kwahiyo anakaa wapi?”

    “Mwanao sijui kapanga wapi huko na Erica ndio anaishi nae”

    “Unasemaje! Erick anaishi na Erica?”

    “Ndio hivyo, yani pika pakua wako wote. Erica katoroka kwao na Erick katoroka kwangu wanaishi wote”

    “Mmmh hiyo habari imenichanganya zaidi ujue, yani nahisi kama kichwa kinazunguka hapa, kweli Erick dah! Halafu Yule binti ni mshirikina yani namuhurumia Erick jamani, nitamtafuta niongee nae, ndiomana anapokea simu kwa uoga sana kumbe kuna maovu ameyafanya. Dah nimesikitika sana”

    Mzee Jimmy akainuka na kumuaga mama Erick na akajua sasa ameacha jambo la Erick kwenye mikono ya mama yake maana anamjua huyu mwanamke kama kitu haktaki ni hataki hata iweje, kwahiyo aliondoka na tabasamu pana sana kugundua kuwa hata mama Erick anapinga mahusiano ya Erick na Erica.



    Dora na James walifika nyumbani kwa James usiku ule ila kwa bahati mlinzi wa James alirudi, kumbe alimtimua ila mlinzi alirudi, yani mlinzi alivyomuona James alianza kumuomba msamaha ila James alimshukuru sana mlinzi kwa uwepo wake tena kisha akamsaidia kuharibu kitasa cha mlango na kuingia ndani ambapo ilibidi alale mule na Dora hadi palipokucha ila kiukweli hawakulala kabisa kwani kila mmoja alikuwa na mawazo sana, waliwaza kuhusu simu zao yani simu ndio zilizowatia mawazo zaidi, kiukweli Dora alikuwa amechoka sana na kuamua tu kwenda jikoni kwa James na kupika kisha kuandaa chakula na kuanza kula na James, kwa mara ya kwanza leo James alikula chakula kilichopikwa na Dora, alikula na kumwambia,

    “Kheee Dora licha ya kuhangaika hangaika kumbe kupika unajua?”

    Dora akacheka na kusema,

    “Tena leo nina mawazo yangu ndiomana, ila na wewe James hivi ni wanawake gani wale unakuwa nao? Aina gani ile ya mwanamke ulimuokotea wapi?”

    “Hapana unajua Yule mwanamke alikuwa ni mfanyakazi wa humu ndani, na nilianza nae kipindi mke wangu mjamzito maana alikuwa mvivu sana”

    “Ndio tabia ya kuhangaika na wasichana wa kazi hiyo, tatizo wanaume huwa hamridhiki hata wake zenu wawafanyie nini ndani, mfano kipindi kile kunibaka, dah huwa sisahau kabisa”

    “Aaaah Dora si yashaisha hayo, ila kuna somo tumepata. Unajua kunywa sio vibaya ila kulewa ni vibaya, hebu ona tumekosa hata ufahamu kuwa tunachukuliwa simu. Ngoja tujiandae tu tushughulikie kwanza simu na laini kabla ya yote maana mawasiliano ndio ya muhimu”

    “Na gari kasepa nalo, aaah wanawake wengine ni noma”

    “Yule muache ila atajutia, vile vitu vinapita tu hakuna kitakachobaki je ataweza kuendelea kulea mtoto mwenyewe!”

    “Ila James tutamlaumu tu Yule mwanamke ila ulevi wetu ni mbaya, hebu ona sasa tumelewa na kuanza kutenda matendo ya ajabu kwa Yule mwanamke, tumejitia uchizi kumbe Yule ni chizi zaidi yetu”

    Basi walimaliza kula na kujiandaa ambapo Dora alivaa tu nguo baadhi zilizobaki za Bite kwa wakati huo na kutoka na James.



    Tony leo alienda kukutana na Tumaini kwenye duka ambalo lilimilikiwa na Erick, ila aliona kama akimwambia Tumaini kuwa mama yake anataka amuone kumfanyie kama usahili, basi Tumaini atakataa kwahiyo aliamua kumwambia kwa njia nyingine,

    “Tumaini, mama amekukubali ila anataka uende nyumbani Jumamosi ulale hapo na uondoke Jumapili”

    “Hiyo ni ngumu kwangu Tony, siwezi kulala mbali na nyumbani. Baba atasema sana, siwezi labda nije tu kushinda”

    “Sawa hakuna shida, basi niahidi kuwa utafanya hivyo na hiyo Jumamosi mimi nitakufata ili twende wote nyumbani”

    “Hakuna shida”

    Tony hakufikiria kuwa kitu anachotaka mama yake kumpima Tumaini kitakuwa kikubwa, kwani aliamini kila mwanamke lazima awe anajua kupika tena vizuri tu, ingawa hakuwahi kula chakula cha Tumaini ila aliamini kupika anaweza.

    Wakati wanaongea ongea, mfanyakazi mmoja wa pale alienda kumuuliza Tumaini,

    “Yule mama wa chakula kaja, sijui akuletee nini leo?”

    “Ana pilau?”

    “Amesema ipo ndio”

    Tumaini akamuangalia Tony na kumuuliza,

    “Unapendaga pilau?”

    “Napenda ndio”

    “Pilau ya huyu mama ni nzuri hatari, ngoja niagize tule”

    Kisha akamgeukia Yule msichana na kumwambia,

    “Mwambie alete pilau sahani mbili, pilau kuku eeeh! Aweke kachumbari ya kutosha na Yule wa juisi mwambie atuletee juisi glasi mbili”

    Yule dada akaondoka, ila kwa kitendo kile cha Tumaini kujua hadi vyakula vitamu kilimpa moyo Tony kuwa Tumaini lazima kwenye kupika yupo vizuri, maana hadi anajua chakula kitamu na kibaya.

    Baada ya muda chakula kile kililetwa na wakaanza kula, kiukweli kilikuwa kitamu sana hata Tony alikiri kuwa ni kitamu hadi alikipenda,

    “Hiki chakula balaa, ni kitamu sijapata kuona. Huyo mama anajua kupika sana, na kuku yake nzuri sana”

    “Ni kweli anajua kupika, sasa siku uje ule ndizi utumbo weeee utajikata vidole kwa utamu, anaweka na nazi ni tamu sana”

    “Ila pilau kama hii anaipikaje? Mbona wengi wanapika ila sio tamu hivi”

    “Mmmmh mwenzangu, kupika kipaji ujue, nahisi huyu mama ni kipaji chake jamani yani anaweza kupika haswaaa”

    Akatamani kumuuliza kuwa na yeye anaweza kupika nini cha kusifiwa na watu ila hakutaka kwakweli alihisi pengine anaweza kumuudhi kwahiyo hakumuuliza.

    Wakati wanamalizia malizia kula, alifika Erick na kuwakuta wakila, alicheka na kusema,

    “Hatimaye dada yangu amepatikana, na wewe umekuwa na mpenzi Tumaini?”

    “Toka zako huko”

    Erick alicheka tu na kusalimiana na Tony pale huku akimwambia,

    “Karibu kwenye ukoo wetu kaka, ila sijui ndio nitakuitaje? Shemeji shemeji, hahahah shemeji mara mbili”

    Tony akauliza,

    “Kwani vibaya?”

    Tumaini akataka kubadilisha mada na kumwambia Erick,

    “Erick, nikuagizie chakula, pilau ya huyu mama ni tamu balaa”

    Erick akajibu,

    “Hapana, yani nimepitia tu hapa mara moja ila sasa hivi naenda kwangu nitakula huko. Chakula cha Erica ni kitamu zaidi, siwezi nikala huku halafu nikashindwa kula chakula cha mke wangu”

    Tumaini akauliza,

    “Hivi Erica anajua kupika eeeh!”

    “Ndio, siku nitawakaribisha kwangu na mke wangu ataandaa chakula mtahisi kimetoka hotelini ila sitaki kumpa mzigo wa kupika maana sasa ni kijacho Yule”

    Wakacheka tu, wakaongea ongea pale kisha Erick akawaaga na kuondoka zake kuelekea nyumbani kwake.



    Na kweli Erick alipofika tu alimkuta Erica ameshapika tena chakula anachokipenda siku zote, kisha akaandaa na kuanza kula pamoja,

    “Erica mke wangu, uwe unapumzika nataka nikuletee msichana wa kazi akusaidie saidie hapa nyumbani”

    Erica alifikiria jambo, alifikiria kuhusu msichana wa kazi aliyekuwa nyumbani kwa dada yake kipindi kile na jinsi alivyotembea na shemeji yake, akakataa

    “Hapana sitaki msaidizi”

    “Kwanini Erica?”

    “Sitaki tu”

    “Najua unawaza mawazo potofu, mimi nakupenda wewe hata waje wanawake mia moja mbele yangu wakiwa watupu na wewe umevaa ila bado nitakuchagua wewe, Erica amini hilo kuwa nakupenda sana yani hakuna msichana hata mmoja mwenye nafasi kwenye moyo wangu zaidi yako wewe, nakupenda sana malkia wangu”

    Erica alifurahi sana kusikia vile ila Erick alimuomba hata kuleta msaidizi ambaye atakuwa anaenda pale nyumbani mchana na kuondoka jioni, mwishowe Erica alikubali kuhusu lile swala alilolisema Erick.

    Basi walipomaliza kula simu ya Erick ilianza kuita na alipoiangalia akaona ni namba ya mama yake akapokea,

    “Uko wapi saa hizi Erick?”

    “Nipo mjini mama”

    “Nakuomba ofisini kwangu mara moja kabla sijaondoka”

    “Mama, nakuomba nije kesho maana kuna mambo namalizia”

    “Mjinga wewe, yani kuniongopea tu. Hutaki kusema ukweli kuwa unaishi na Erica ulidhani sitajua ujinga wako? Na ni biashara gani hiyo ya kuishi na mtoto wa watu bila baraka za wazazi, sasa kesho uje ofisini”

    Simu ikakatika, Erica alimtazama Erick na kumuuliza,

    “Inamaana mama yako hakujua kama tunaishi wote?”

    “Hakujua”

    “Hukumwambia? Si ulisema utamwambia kila kitu!”

    “Erica mpenzi, siku ile mambo yaliingiliana ndiomana siku ongea nae, ni siku ambayo nilijua kuwa Dora ni muathirika pia nikajua kuwa uliwahi kuwa na mahusiano na George nikapaniki sana”

    “Ila Erica mambo mengine bhana, nakumbuka wakati tunaanza mahusiano ulisema tufute yote yaliyopita kwetu, sasa kwa mtindo huu mimi sio nitakufa kwa presha maana sidhani kama kuna rangi umeacha katika kuhangaika na wanawake”

    “Mmmh tuache hizo mada Erica”

    Yani Erick hakupenda kabisa kuongelea swala la wanawake zake waliopita. Walianza kuongelea tu mustakabali wa nyumba yao unavyoendelea kwa kipindi hiko.



    Ilikuwa kwenye mida ya saa tatu usiku wakati Bahati amejilaza kitandani ila alipigiwa simu na Fetty kwa muda huo, kisha alimsalimia

    “Ndio unalala Bahati?”

    “Ndio, yani usingizi ulitaka kunichukua hapa”

    “Ushafanya dua lakini? Umesoma Kuran?”

    “Mmmh bado”

    “Basi fanya hivyo kabla ya kulala nakuomba”

    Basi Fetty alivyokata simu Bahati aliamua kufata alichoambiwa na kuamua kufanya dua na kusoma Kuran.

    Kwakweli ndugu zake nje walimshangaa sana kuwa bahati mbona kabadilika vile, walitamani kujua kuwa ni kitu gani kimembadilisha Bahati ila ilikuwa ngumu sana kujua, walibaki tu wakijadili bila majibu

    “Mtu pekee wa kumbadilisha Bahati ni Erica, sasa itawezekanaje kwa Erica kumfundisha Bahati kusoma Kuran?”

    “Hivi Erica mkristo eeeh!”

    “Ndio ni Mkristo Yule, atawezaje kumfundisha? Ila hatuwezi jua, mnajua Yule binti tulimchukia bure ila ni msomi kupita ndugu yetu yani kwa elimu ya Erica haikupaswa hata kuishi na Bahati ila msichana wa watu alikubali tu bila kujali elimu ya Bahati wa hali ya maisha, tulijua analazimisha baada ya Bahati kupata pesa kumbe ni yeye aliyesababisha Bahati kupata vyote alivyopata, siku tukikutana na Erica tumuombe msamaha jamani”

    “Kama usemavyo ndio hivyo basi inawezekana Erica akamfundisha Bahati kusoma Kuran kupitia kwa watu wanaojua maana mwanamke akiwa na elimu basi ubongo wake unatanuka zaidi”

    Walijikuta siku hiyo wakimsifia sana Erica na kusahau kuwa hawakumtaka kabisa kuwepo kwenye maisha ya ndugu yao.



    Baba yake Nasma aliamua siku hiyo usiku kufanya madawa yake kwani aliona sio kitu cha kawaida kwa mwanae kuwa amemwaga dawa na Bahati hajarudi nyumbani wakati aliiamini sana ile dawa kuwa inavuta zaidi ya vyote, basi alikaa na kuanza kufanya dawa zake, alitengeneza vitu vyake na kusubiria muda kidogo tu alipue dawa zake ambazo ni uhakika asilimia mia moja zinafanya kazi.

    Muda ulipofika alianza kulipua dawa zake ambapo kulikuwa na kibuyu kimoja lazima anapokiita kwa jina la mtu amtakaye baada ya dawa basi lazima kile kibuyu kisogee alipo na kisikilize anachosema, alianza kuita

    “Bahati, Bahati, Bahati”

    Ila kwa mara ya kwanza kile kibuyu chake hakikuitika wala hakikusogea, Yule mzee alichukia sana na kujaribu tena kufanya dawa ila alipokiita vile vile yani hakikusogea kabisa, akajiuliza

    “Kuna nini kwani? Au Yule mjinga kaenda kujizindika kwa waganga?”

    Hakupata jibu ila chungu hakikuitika wala nini na kumfanya achukie sana siku hiyo, akajisemea tena,

    “Nitaenda kwa waganga wote ambao Bahati anafikiri wanaweza kunizidi na safari hii nitammaliza kabisa kiungo kimoja kimoja si mbishi, nitamfundisha adabu”

    Aliweka vitu vyake pembeni na kuamua kwenda kulala tu maana ile kazi aliifanya kwa zaidi ya masaa saba ila haikufanikiwa.



    Kesho yake asubuhi na mapema Erick alijiandaa na kwenda ofisini kwa mama yake kama alivyokubaliana nae jana, alifika na kumkuta kisha kuanza kuongea nae,

    “Wewe Erick, kwanza niambie umeanzaje anzaje kuishi na Erica yani umefikiria kitu gani?”

    “Mama, Erica ana mimba yangu na nilipenda nifate taratibu zote ili nikae na Erica kihalali ila nilipata vipingamizi sana maana kule kwakina Erica hawanitaki sababu ya mambo aliyoyafanya baba na kwa upande wangu baba hataki na wewe hutaki kwahiyo nikawa njiapanda mama, Erica nampenda na ana mimba yangu je nitamuacha tu ateketee na kuangamia wakati muhusika nipo? Ikawa ngumu mama ndiomana nikaamua kwenda kuishi pamoja na Erica maana siwezi kumuacha asemwe kwao wakati mimba ni jukumu langu”

    “Aaah sasa na baba yako alileta pingamizi gani?”

    “Inamaana mama umesahau nilivyokwambia? Baba alikuwa anataka kumuoa Erica”

    “Kumbe hiyo habari ulinipa ilikuwa ni kweli?”

    “Ndio ni kweli mama, yani baba katuaibisha sana”

    Erick aliamua kumsimulia mama yake kitendo cha baba yake siku hiyo hadi akazimia, kwakweli mama Erick alicheka sana na kusema,

    “Huyu mzee ni mwehu kweli jamani, kwahiyo akazimia kabisa?”

    “Ndio akazimia na alipona siku Sia alipokuja nyumbani na kusema kuwa ni mjamzito na ana mimba yangu, basi ndio akapona na kuanza harakati za kusema nioane na Sia ila alikuja kushangaa siku aliyomkuta Sian a muhusika wa mimba”

    “Ila mwanangu una uhakika kuwa mimba ya Erica ni yako?”

    “Nina uhakika mama, asilimia zote kuwa ile mimba ni yangu”

    “Eeeeh kwahiyo unataka nifanye nini mimi?”

    “Mama, nataka uende kwakina Erica kuongea na mama yake maana najua ni mama mwenzio na atakuelewa, nakuomba mama yangu unisaidie nampenda sana Erica”

    “Nitafanya hivyo, ila unajua ni kwanini nitafanya hivyo?”

    Erick alisema hajui ila kile kitendo cha mama yake kumkubalia tu aliona kuwa ni kitu cha ajabu sana na kilikuwa ni kitu cha furaha sana kwa upande wake, kisha akamwambia mama yake,

    “Mama kwanini?”

    “Ni kwasababu ya huyo mzee, yani Jimmy hana hata aibu jamani! Badala afanye mambo ya maana anaanza kufanya vituko jamani loh! Anaacha kufikiria mambo ya maana anafikiria kuoa wakina Erica jamani!”

    “Na tena mama, baba tumewahi kumfumania na Dora, Yule msichana wa siku ile”

    “Kheee hadi Yule jamani huyu mzee anatafuta kifo tu na kashaupata ukimwi tayari, na uzee ule jamani kufa kwa ukimwi loh! Ndio malipo ya kuhangaika yaliyofanyika”

    “Ila mama nimefurahi sana kuamua kwako kwenda kwakina Erica, utaenda lini mama?”

    “Kesho si Jumamosi! Sema kuna mambo nafatilia, nitaenda Jumamosi ya wiki ijayo mwanangu”

    Erick alifurahi sana kusikia vile kutoka kwa mama yake. Basi akaagana na mama yake akiwa na furaha sana .



    Muda huu Erick alipita dukani kwa lengo la kununua vifaa vya kukamilisha nyumba yake, alipomalizia kununua, akalipia na kupakiza kwenye gari linalofahamu kwake basi gari ikaondoka. Muda huo Erick alitoka mule dukani na kuelekea kwenye gari yake ila kabla hajaingia kwenye gari kuna mtu akamuita, Erick alimuangalia mtu Yule na alimuona kuwa ni mtu aliyemfahamu maana alikuwa ni Derick, Yule ndugu wa Erica, akamsalimia pale, kisha Derick akamwambia Erick

    “Hivi unajua kuwa mimi ni ndugu wa Erica?”

    “Najua ndio, mara ya kwanza nilikuona kwakina Erica ambapo mama yake alikutimua na mara ya pili ni dada yangu alikuita na tukakupa lifti”

    “Aaah kumbe unakumbukumbu nzuri eeeh! Sasa mimi nakufahamu wewe kabla yaw ewe kunifahamu mimi”

    Swala lile Erick hakushtuka sana kwani alijua huyu lazima amfahamu si ndugu wa Erica, kwahiyo Erick alisema,

    “Ni haki yako kunifahamu, wewe si ndugu wa Erica!”

    “Ndio, ila hiyo sio sababu ya kukufahamu labda kama Erica hajakueleza vizuri kuhusu undugu wangu na wake. Ni hivi, mimi na Erica tumechangia baba na tulikuwa hatufahamiani, kipindi tunafahamiana ilikuwa ni marafiki tu ambapo Erica alivutiwa na jina langu maana aliona linaendana na lako, sijui ilikuwaje wewe nay eye kipindi hiko ila Erica alinitongoza mimi na kunitaka niwe mpenzi wake”

    “Mmmh Erica akutongoze! Hata usingekuwa ndugu yake hiyo ni chumvi, unajua unaweza kuwa ndugu wa Erica ila ukawa humjui vizuri erica. Basi mimi namjua vizuri sana Erica, hawezi kumtongoza mwanaume labda useme lingine”

    “Umepaniki bure kaka kabla hata sijakumalizia, mimi na Erica tuliingia kwenye mahusiano bila hata ya kujua ni ndugu hadi Erica akashika mimba yangu, tulivyojua Erica akachukia na kwenda kutoa ile mimba. Kuna kipindi ulipiga simu ya Erica na nilipokea mimi kama unakumbuka, kipindi hiko tulikuwa kijijini kwenye tambiko maana ilikuwa ni kitendo cha laana kwa ndugu kushirikiana kimapenzi na Erica alionekana kuwa na laana kubwa maana ndio chanzo cha yote na alitoa mimba bila kufata sharia yani pale umuonapo Erica ana matatizo makubwa sana”

    Erick alimuangalia Derick karibu dakika kumi kisha akamuuliza,

    “Hivi wewe ni mwanaume au mwanamke?”

    “Kwanini unaniuliza hivyo?”

    “Ulichoniambia sasa ni tabia ya kike maana ni tabia ya umbea, mwanaume mzima kunisimamisha hapa mwanaume mwenzio na kuanza kuongea upuuzi kama huo kuhusu ndugu yako kweli! Sijui alikutongoza, mkatembea nae akabeba mimba yako na kwenda kuitoa, sasa ulitaka azae na huyo mtoto awaite vipi? Ndio wanachuo nyie, hivi wanachuo wa sasa mnatatizo gani? Si bora ungeishia kidato cha nne kama mimi lakini nakuzidi akili na maarifa. Ulidhani ukiniambia habari zako za kimbea kama hizo ndio nitamuacha Erica? Hapo hakuna kitu shemeji yangu yani wewe andaa tumbo lako tu hilo uleee weee siku ya harusi yetu uvimbiwe ila swala la kumuacha Erica halipo. Nimeongea sana na wewe sababu nimeona una tabia za kike kwahiyo kukwambia kwa kifupi usingenielewa kwahiyo nimekwambia hivi kwa kirefu maana nimekuchukulia kama mwanamke. Washukuru sana wazazi wako waliokusomesha hadi chuo maana kwa tabia hizo usingesoma ungekuwa shoga, mjinga wewe, kwaheri”

    Erick alipanda gari yake na kuondoka, kwakweli kile kitendo cha Derick kushushuliwa na Erick kilimuumiza sana mpaka alijihisi vibaya kwani hakutegemea kabisa kama Erick angemshushua kiasi kile, kwahiyo aliondoka pale akiwa amejawa na aibu tupu.



    Erick alifika nyumbani kwake na kukuta lile gari la vifaa lishafika ndio linatua vifaa kwahiyo alisaidiana nao kwanza kisha akaenda ndani, alimkuta Erica na mwanae wamelala muda huo, akamuamsha Erica,

    “Kheee utalala nini usiku? Au mambo yale ya kuanza kunishurutisha tukeshe?”

    Erica aliinuka pale kitandani huku akitabasamu na kumuuliza Erick kuwa za sehemu aliyotoka na Erick alimpa habari njema ya mama yake kwenda wiki ijayo kwao, kwakweli ile ilikuwa ni habari njema sana kwa Erica kwani alijua kwa vyovyote vile lazima mamake akiongea na mtu mzima mwenzie basi ataelewa,

    “Asante sana kwa hilo Erick”

    “Usijali Erica ni kazi yangu, ila ngoja nikuulize’

    “Niulize”

    “Derick ni ndugu yako, ila undugu wako na yeye umekuwaje kuwaje yani?”

    “Ni historia ndefu Erick, naomba tuachane na hayo”

    “Hapana nieleze Erica”

    Erica aliona kumueleza Erick kuhusu mambo ya yeye na Derick ni kujichafulia tu, yani hakutamani kabisa ila kwavile Erick alimsisitiza sana kuwa anahitaji kujua ukweli Erica aliamua kusema ukweli bila kujua kuwa Erick alishakutana na Derick au vipi, Erica alimueleza kila kitu yani kwa mara ya kwanza Erica hakuficha chochote kile kwa Erick, alijitoa muhanga kuwa liwalo na liwe maana mambo mengine aliona kila anavyozidi kuyaficha ndio yanavyozidi kumuumiza.

    Ila alishangaa sana kumuona Erick akitabasamu tu kanakwamba ile habari haijagusa moyo wake kabisa, ndio kwanza alimkumbatia Erica na kumwambia,

    “Wewe ndio mke wangu, baada ya misukosuko yote sasa umepata pumziko lako la moyo, na mimi baada ya kutangatanga kote sasa nimepata pumziko langu la moyo. Kwasasa najua hakuna habari tena nitakayosikia kuhusu wewe na ikaniumiza wala kwa upande wako hakuna tena habari itakayokuumiza kuhusu mimi”

    Erick alionekana kumfurahia tu Erica kisha kuendelea na mambo yao mengine tu na huku wakifurahia swala la wao kuwa pamoja.



    Bado Babuu alikuwa na wazo la kumuoa Zainabu, akamuomba siku hiyo apate sehemu ili azungumze nae vizuri maana kila alichoongea bado zainabu alionekana kutokuelewa.

    “Hivi kwanini Zainabu hutaki kukubaliana na upendo wangu? Nakupenda kweli, nahitaji uwe mke wangu”

    “Babuu, nina miaka thelathini na tatu na wewe una miaka ishirini na tisa huoni tofauti kubwa hapo? Yani kuna tofauti ya miaka minne kweli jamani? Hapana kwakweli”

    “Kwani tukioana hiyo miaka inabandikwa kwenye paji za uso, yani mtu akiniona anajua nina miaka mingapi na wewe una miaka mingapi kweli Zainabu? Mimi nakupenda, sidhani kama miaka ni kitu kikubwa katika maisha, unaweza kukutana na mwenye umri mkuwa ila hana akili za malengo na wewe ila mimi nina malengo na wewe Zainabu, ni kweli nakupenda”

    “Ila umri tumetofautiana sana Babuu, mimi ni sawa na dada yako tu. Hata watu wakituona watadhani nimekulazimisha kunioa”

    “Zainabu, maswala ya kujali maneno ya watu hayafai hata kidogo, ukifikirira ya watu huwezi kusonga mbele, fikiria furaha yako, fikiria maisha yako. Mimi sikuwahi kufikiria kuoa kabisa kwa muda huu ila tangu nimekuona wewe natamani sana kuwa na mke, tafadhali Zainabu nikubalie”

    Wakati Babuu anaongea na Zainabu, ile sehemu akakatisha Dora na alivyowaona alisimama, akasogea na kumsalimia Babuu,

    “Kheee ndio wewe uliyekuwa unakuja chuo kumlilia lilia Erica! Khee mbona umependeza sana, umekuwa mzuri hadi raha, huyu ndio wifi nini”

    Babuu alimuangalia tu Dora maana alionekana kumaliza maneno yote mwenyewe, ila swala la kumuuliza kuwa Yule ndio wifi alimuitikia basi Dora akasema,

    “Ila mmependezana sana, Mungu awabariki”

    Kisha Dora akaondoka, kwakweli Babuu alishukuru sana maana aliwahi ongea na msichana huyo chuoni kwakina Erica na aliweza kumuona alivyo na mdomo mchafu.

    Basi kwakuwa muda nao ulienda sana ikabidi ajitoe kumrudisha Zainabu kwao ila bado alimsisitizia swala la kumpenda ili akikubali basi apelike washenga kwakina Zainabu na amuoe kabisa.



    Kesho yake Tony kama alivyokuwa amepanga alienda kumchukua Tumaini ili kumpeleka nyumbani kwao ila hakumwambia ukweli kama mama yake anahitaji kumchunguza kwani alijua lazima Tumaini akatae ukizingatia hapendi kuchunguzwa.

    Basi alifika nae kwao na leo mama yake alimkaribisha vizuri sana yani kama sio Yule anayegombanaga nae.

    Basi Tumaini alifika pale na kukaa ambapo mama Erica alimtuma Tony sehemu ya mbali kidogo kwani hakutaka aone chochote, Tony akaondoka pale kwao. Mama Erica alitoka na kanga na kumpa Tumaini ajifunge kisha akamwambia,

    “Jifunge hii mwanangu tuje kusaidiana kupika kidogo huku jikoni”

    Tumaini akaongozana nae hadi jikoni, sababu ilikuwa inakaribia mchana basi mama Erica alibandika sufuria la ugali na kukorogea uji kisha akamwambia Tumaini asonge ule ugali, Tumaini akauliza

    “Kwanini nisipike mboga? Mama songa tu ugali mwenyewe”

    “Hapana, mboga nitapika. Tusongee tu ugali mwanangu”

    Basi Tumaini akaanza kuusonga ule ugali, kwakweli mama Erica alijihisi kucheka jinsi jasho jembamba lilivyokuwa likimtoka Tumaini hadi huyu mama ilibidi atoke jikoni na kumfata Bite,

    “Njoo uone kituko cha kaka yako, ugali wa watu wanne tu unamtoa haja, njoo uone”

    Bite akaenda kuchungulia jikoni, ni kweli Tumaini alikuwa na hali mbaya sana kwenye kuusonga ule ugali maana alijaza unga halafu ukamshinda kusonga, mama Erica alimfata na kuzima jiko kisha akamuuliza,

    “Mbona umejaza unga hivyo?”

    “Nilikuwa naweza unga basi ukawa unanirukia kama kuniunguza hivi ndio nikajaza, naomba nisamehe”

    “Umewahi kusonga ugali Tumaini?”

    Alikaa kimya tu, mama Erica akarudia tena kumuuliza,

    “Umewahi kusonga ugali Tumaini?”

    “kiukweli sijawahi kusonga ugali”

    “Si ungeniambia tu kuwa hujawahi jamani! Haya nitaupika tena, basi maharage yale na nazi nishakuna uyaunge mwanangu sawa au hujui pia?”

    “Hapana najua”

    Basi mama Erica akaanza kupika tena ugali na Tumaini kuachiwa kuunga maharage ya nazi, alipomaliza alizima jiko na mama Erica alienda kuangalia maharage yaliyoungwa na Tumaini, alimuita Bite, huku Tumaini yuko pale pale,

    “Bite mwanangu sijataka kucheka peke yangu, angalia maharage yameungwa nazi haya”

    Bite aliangua kicheko kitu kilichomfanya Tumaini ajihisi vibaya sana.



    Baba Nasma hakutaka kukubali kuwa dawa zake zimedunda kumuita Bahati basi siku hiyo akafunga safari na kwenda kwa mganga mashuhuri, alipofika na kumueleza shida yake Yule mganga alimwambia.

    “Mmmh huyu mtu anaonekana mzito sana, tukishindwa unajua dawa itakurudia”

    “Hana uzito wowote huyu mtu, najua haiwezi kushindikana nataka tumamalize kabisa maana ananisumbua na dawa zangu”

    Basi Yule mganga akaanza kusaidizana nae kufanya zile dawa, ila katika hali ya kushangaza sana baba Nasma alianguka chini na kuwa kimya gafla.





    Basi Yule mganga akaanza kusaidizana nae kufanya zile dawa, ila katika hali ya kushangaza sana baba Nasma alianguka chini na kuwa kimya gafla.

    Yule mganga alijaribu kumuita lakini Yule mzee hakuitikia kabisa, alimshika shika na kumuona yupo kimya, muda kidogo simu ya Yule baba ikaita, basi Yule mganga akaichukua na kuangalia, akaona jina la mpigaji, ‘Binti yangu Nasma” basi Yule mganga akaipokea na kuanza kuongea, ila kabla hajaongea alimsikia Nasma akisema,

    “Baba uko wapi? Usiende tena kwa mganga nimepata suluhisho”

    Yule mganga akamjibu Nasma,

    “Baba yako yupo huku kwangu, ameanguka na hajitambui kabisa”

    Nasma alishtuka sana na kuhitaji kupewa maelekezo ya mahali alipo baba yake. Yule mganga alivyokata simu aliendelea kufanya jitihada za kumuamsha baba Nasma.

    Kwa upande wa Nasma alikuwa kwake ila ile habari ilimchanganya vilivyo, aliamua kwenda kwao ili kutaarifu ndugu zake na waende pamoja.

    “Mama, nimepata habari baba kaanguka huko kwa mganga”

    “Jamani huyu mzee anachotafuta ni nini? Anatafuta kifo huyu, kilichompeleka kwa mganga tena ni nini?”

    “Hata mimi nilimkataza wakati ananiambia swala lake la kwenda kwa mganga maana alisema dawa za kumuita Bahati zimegoma”

    “Haya ni makubwa sasa kajitafutia, huyo Bahati mshamtesa sana mnafikiri hajabumbuluka tu! Lazima naye ana mganga wake, kapikwa huko kachemshwa huko, unafikiri utamvuta kirahisi tu. Hebu wapigie simu ndugu zako wengine twende tukamuone na tumuwaishe hospitali”

    “Mmmh mama uliona wapi uanguke kwa mganga upelekwe hospitali! Ngoja twende huko huko tutapata tu jambo la kufanya.

    Basi akaita na ndugu zake wengine na kuanza safari, ni ilikuwa mbali kidogo walipokuwa wakielekea, kwakweli walisikitika sana kwa baba yao kuacha mambo yake na kwenda mbali hivyo kwa mganga.



    Kwa maneno ya pale kwakina Erica yalimfanya Tumaini achukie sana na kutaka kuondoka ila wakati anataka kutoka mlangoni tu akakutana na Tony ambaye alimrudisha ndani kujua nini tatizo, muda huo Tumaini alikuwa amejiinamia chini tu. Tony akamuuliza mama yake,

    “Mama, kwani nini tatizo?”

    “Nenda jikoni kwanza kajionee kitu cha nazi ndio uje kuuliza nini tatizo, halafu funua kuna sufuria nimefunika pembeni jionee huo ugali wa kula wewe na mkeo”

    Tony alienda jikoni kwao, kiukweli alishangaa sana na hakuamini kama Tumaini anaweza kupika vile, akarudi sebleni na kuuliza,

    “Nani kapika vile?”

    “Unadhani ni nani humu ndani anayeweza kupika mauzauza ya aina ile? Mwanamke uliyemleta hajui kupika yani hajui kabisa kabisa, halafu hataki kusemwa, yeye ni nani katika ulimwengu huu asisemwe? Mtu mzima kama Tumaini ashindwe kusonga ugali wa watu wanne! Ashindwe kuunga maharage ya nazi! Anatupikia mauzauza jamani, yani nazi inasimama dede kweli!”

    Tony akajua pale lazima wamemsema sana Tumaini, akajawa na huruma moyoni mwake, akamuangalia mama yake na kumwambia,

    “Mama ulinifundisha kazi zote mimi, ulijua ni kazi za kike ila ulinifundisha na nikazijua. Mwanzoni sikujua kwanini umenifundisha ila nikaelewa kuwa niweze kujitegemea pindi ninapoachwa mwenyewe, ila sasa naelewa zaidi kuwa uliona pengine naweza kuoa mwanamke asiyeweza kufanya kazi za kike basi nikamfundisha na tukasaidiana nae. Asante sana mama kwa kunifundisha basi Tumaini atafundishwa na mimi maana huyu ndio mke ambaye kachaguliwa na moyo wangu”

    Bite na mama Erica wakatazamana na kusikitika sana, kisha mama yao akasema,

    “Unajudanganya Tony, sikukufundisha ili uende kuoa mauzauza kama haya hapana kwakweli”

    Bite akaongezea,

    “Yani mwanamke ni bonge hata picha za harusi tu hazitapendeza na bado ana kasoro nyingine jamani loh! Unaishije na mwanamke asiyejua kupika! Ataweza kufua kweli huyo, kuosha vyombo, kusafisha ndani au ndio mtajaza wasichana wa kazi kila mahali!”

    “Dada, ngoja nikuulize kwahiyo wewe ulivyokuwa unaweka wasichana wa kazi nyumbani kwako ilikuwa kwavile hujui kupika, hujui kuosha vyombo sijui kufua? Hata ujue kupika vipi elewa kuna mkali zaidi yako. Kila siki mama hapa analalamika kuhusu Erica na wakati huo huo anasema hiki chakula angepika Erica kingekuwa kitamu sana, mbona wewe hajawahi kukusifia si inamaana unapika cha kawaida tu, sasa kwanini umshangae Tumaini atajifunza na ataelewa”

    “Tony usijifanye unajua sana kulitetea hilo tipwatipwa lako...”

    Ile kauli ndio ikamfanya Tumaini ainuke kabisa na kuondoka, Tony aliamua kumfata Tumaini ili aweze kumbembeleza.

    Ndani alibaki Bite na mama yao, Bite akasema

    “Na aondoke tu, mwanamke kichefichefu, mtoto wa kike hujui kupika jamani ni aibu”

    “Ila Bite hapa ni pa kujifunza, unajua huyu Tumaini sio kosa lake ila ni kosa la mama yake yani kapata malezi mabovu huyu, angeweza kupika hata ugali wa mtu mmoja ila anakwambia hajui kabisa ni malezi mabovu kayapata huyu”

    “Sasa mama nijifunze nini hapo?”

    “Weee nae, unatakiwa kujifunza kulea watoto hakikisha mwanao anaweza kazi zote za nyumbani bila hivyo ataumbuka ukweni kama hivi”

    “Hiyo kazi aofanye Erica kwa Angel, mimi mtoto wangu wa kiume huyu sina shaka”

    “Bite nawe unaongea kama mgonjwa, utafikiri James alikurushia vidudu sasa vimekimbilia kichwani, aliyekwambia mtoto wa kiume hafundishwi kupika nani? Anatakiwa kujua pia, unafikiri akioa mwanamke kama Tumaini bila kumjua humo ndani si watakula vyakula vibichi hadi wakose choo! Tunatakiwa kufindisha watoto wote kupika, kama mama hakikisha unawajibika vyema kwa mwanao.”

    Bite alimuitikia tu ila anamuonaga mama yake kuwa kigeugeu sana maana huwa anabadilika badilika.



    Tony aliondoka na Tumaini kuelekea nae kwao maana Tumaini alionekana kuchukizwa kabisa, alifika nae kwakina Tumaini na kuingia nae ndani bila kujali kuwa pale alitimuliwa, muda kidogo alifika Erick na kuwakuta sebleni ambapo Tony alijaribu kumuelewesha Tumaini maana yeye ni mtu wa kuchukia tu.

    Erick aliwasalimia na kusogea karibu yake, alipomuangalia vizuri dadake aligundua kuwa kuna kitu kimemkera, basi alikaa na kumuuliza tony,

    “Kwani tatizo nini?”

    Ilibidi Tony aeleze kwa ufupi tu kuwa alienda kwao na Tumaini sasa akashindwa kupika na ndugu zake wakamshambulia kwa maneno. Baada ya kuambiwa vile Erick alianza kucheka hadi Tumaini akainuka kumuangalia na Tony ikabidi amuulize,

    “Sasa mbona unacheka?”

    “Mimi nilijua tu kuna siku itatukia kama hivi Tumaini, nilikuwa nakwambia mara kwa mara hapa kuwa ujifunze kupika sio kusifia tu chakula cha sehemu Fulani kizuri sijui cha sehemu Fulani kizuri maana una mtindo huo sana, jifunze kupika ili watu wasifie mapishi yako wewe. Kufika Chuo sio kujua kila kitu, kuna vitu vingine ni vya kujifunza kimtaani tu”

    “Sasa ndio unicheke? Si uniambie kiustaarabu tu, hata hivyo Erica anajua kupika basi awe ananifundisha kupika”

    “Hakuna tatizo, Erica anakupenda kwanza atajihisi vibaya kweli kwa hayo yaliyokutokea kwao. Ila pole dada yangu maana Yule mama mmmh! Simpatii picha kapata na cha kuongea si ndio balaa”

    Tony akasema kidogo,

    “Ila mama ni wa kumzoea tu Yule jamani”

    Erick akamwambia Tony,

    “Ndio ni wa kumzoea ila kwasasa ni wewe Tony ndio inabidi uwe mstari wa mbele, kuhakikisha dada yangu hadharauliki wala hasemwi vibaya, yani wewe kama mwanaume unatakiwa kuwa mstali wa mbele kufukia kasoro za mwenzi wako, mfano mimi Erica nampenda na kuna ambayo yalipita kwake ila kama mwanaume naamua kusimama upande wake na kumtetea na kuaona kama yale yaliyopita ni changamoto tu. Tumaini haina haja aje kujifunza kupika kwa Erica ila wewe kama mwanaume wake na kupika unajua basi huna budi kumfundisha na panaposhindikana basi unamuuliza Erica. Pole dada yangu”

    Tumaini aliitikia tu, kisha Tony akaongezea

    “Mimi ningemfundisha tatizo baba yenu hanitaki kabisa hapa, yani akinikuta ni balaa”

    “Na huyu mzee nae, hakutaki sababu ipi?”

    “Sababu sina gari na nyumba”

    “Kwani kila anayeanza maisha ana gari na nyumba? Kila kitu ni mwendo, hakuna anayefika mia bila kuanza na moja. Halafu maisha hayafanani, shemeji yangu usijali nitashughulika swala la dada yangu kujifunza kupika”

    Kisha akamwambia kuwa Tumaini asijali kitu maana atakuwa anaenda kumchukua kazini na kumpeleka kwake ili ajifunze funze kupika kwa wifi yake na kisha kurudi nyumbani, alifanya hivyo ili baba yake asiwe ana elewa awe anajua kuwa Tumaini anaendaga kazini na sio kwake.

    Kisha wakaongea ongea pale na kumwambia lengo lake,

    “Nimekuja kuchukua gari yangu bhana na kukurudishia yako”

    “Sawa, ila gari haina mafuta”

    “Hamna shida, nitapitia tu kujaza hayo mafuta ila la kwako nilijaza kwahiyo usiwe na wasiwasi”

    “Asante”

    Kisha Erick akabadilishana funguo pale na dada yake halafu akaondoka maana hakupanga kukaa kwa muda mrefu pale kwao.



    Erick alikuwa akirudi nyumbani kwake, ila alipitia kwenye kituo cha mafuta ili kujaza mafuta gari yake kwani dadake alishamwambia kuwa ile gari haikuwa na mafuta ya kutosha, alipokuwa pale kwenye kujaza mafuta, kuna mtu alisogea na kugonga kioo chake, alipomuangalia alimuona kuwa ni Rahim.

    Erick alishusha kioo na kusalimiana nae, ambapo Rahim alimwambia Erick kuwa ana mazungumzo nae kidogo, Erick hakuona tatizo kuzungumza na Rahim kwani hakuwa na ugomvi nae. Basi alingoja amalize kujaza mafuta kisha wakaelekea kwenye mgahawa mmoja wapo na Rahim na kukaa kwaajili ya mazungumzo.

    “Erick napenda tuongee kuhusu Angel”

    “Sawa nakusikiliza”

    “Unajua Angel ni damu yangu na nina haki kuwa nae sababu mimi ni baba yake mzazi”

    “Sawa Rahim sikatai kuwa wewe ni babake mzazi, ila mimi ni babake mlezi kwahiyo kitu gani ulikuwa unataka? Angel aje ucheze cheze nae au kitu gani unataka?”

    “Erick, sijasema tuongee kwa shari ila mimi inaniuma ujue, nina haki kwa Angel halafu anatumia majina yako inakuingia akilini hiyo?”

    “Kutumia jina sio tatizo, mimi babangu mzazi anaitwa Jimmy lakini hakuna mahali utakapokuta Erick Jimmy unajua kwanini?”

    “Eeeh kwanini?”

    “Sababu hakunilea ila kutoitwa jina lake hakujazuia yule mzee kuwa baba yangu mzazi, ni baba yangu mzazi na ninamuheshimu sana. Erica hakukurupuka kumuita Angel Erick, ni sababu wewe hukujali kuhusu mtoto, ulikuwa ukimjibu vibaya na ukimdharau sababu kakuzalia, uliona hatoweza kuishi bila ya wewe na hapohapo hukuthubutu kutoa hela ya matumizi ya mtoto, sio kwamba hukuwa na uwezo! Hapana ila uliamua tu yani ilikuwa ni maamuzi yako kumkomesha Erica ila ulisahau kuwa unamkomesha na mtoto, yule malaika asiyejua chochote na wala hakuhusika kwenye starehe zenu ila ukaamua kumkomesha pia. Angel kutotumia jina lako hakukufanyi wewe kutokuwa baba wa Angel ila unakuwa baba yake kwa misingi ipi? Hujamuoa Erica na unajua ni lazima ataolewa, je akiolewa basi Angel ni jukumu la mume wa Erica na kama ni hivyo basi inamaanisha yule mume ndio baba halali wa Angel. Mzazi mwenzio anapokuwa na mahusiano na mtu mwingine pia sio mwisho wa wewe kuwa baba wa mtoto, unatakiwa kucheza mahali pa kulea mtoto, hivi kwa mfano ungekuwa hata unajitoa nije nishinde shinde na Angel nicheze nae akuzoee hivi angeacha kukupenda? Ungekuwa unamuhudumia mtoto hata kwa kidogo tu usingeonekana wa maana? Ingekuwa hivyo basi Erica asingechukua hatua ya haraka kumbadilisha mtoto jina maana angewaza kuwa unamuhudumiaga”

    “Lakini wakati nipo kwenye mahusiano na Erica nilikuwa nampa sana hela”

    “Ulikuwa unampa za kumtunza yeye, kwasasa ulitakiwa kuonekana kwa Angel, na kumuhudumia mtu sio mpaka umpe hela, hata ile kujali kwako, kutumia muda wako kwaajili yao kunaonyesha ni jinsi gani unavyojitoa. Ila Rahim hujawahi kufanya hivyo, jirekebishe usishangae watoto wa nje wote wakakukataa pengine hadi na wa ndani nao wakakukataa kama hujui kujirekebisha.”

    “Erick unaongea sababu hujui uchungu wa mtoto, hujawa baba wewe”

    “Usinichekeshe, kuna baba na baba jina. Wewe kwa Angel ni baba jina, bado hujawa baba kamili kwa Angel, laity ungefanya majukumu yako lazima Angel angekupenda na Erica angekuheshimu hata angeolewa na mwanaume mwingine bado angeweka akilini kuwa Angel ana baba yake anayemjali na kumpenda”

    Yale maneno yalimuingia sana Rahim na kujikuta hana kingine cha kuongea na Erick, ikabidi waagane tu.

    Erick aliendelea na safari ya kurudi kwake muda huo.

    Alimkuta Erica yupo tu akimbembeleza mtoto kulala, ila Angel alipomuona Erick alikimbilia kwa Erick na kulala mikononi mwake.

    Baada ya Angel kulala, Erick alikaa na Erica na kuanza kuongea nae habari ambazo zilionekana kumpa rah asana Erica,

    “Eeeeh unapenda kuvaa shela la aina gani kwenye harusi yetu?”

    “Mmmh lini nitaenda kuchagua shela? Tusichelewe sana Erick kabla tumbo langu halijawa kubwa, nahitaji kusherekea vizuri harusi yetu”

    “Tutaenda kuchagua tu shela usijali”

    “Halafu nataka kwenye kitchen party yangu nivae nguo kiasilia, nitapendeza eeeh!”

    “Ndio utapendeza sana, ila hivi kitchen party ina umuhimu gani?”

    “Aaaah ni ile sherehe inahudhuriwa na wanawake tupu halafu wanafundisha namna ya kuishi na mume”

    “Namna gani tena Erica, mimi na wewe si tunafundishana humu humu ndani!”

    “Erick hujui tu, yani kichen party ni nzuri sana ukiwa mdada, halafu sendoff na mwisho harusi”

    “Si utachoka sana mpenzi jamani!”

    “Sichoki bhana, hayo ni matukio ya kawaida tu mpenzi”

    “Sawa hakuna shida mpenzi wangu”

    Erick alimshika Erica kwa upendo sana na kumfanya ajihisi raha mno kuwa karibu na Erick.

    Usiku ulipofika waliamua tu kulala ila kila mmoja alifurahia uwepo wa mwenzie.



    Asubuhi na mapema, Fetty alienda kwakina Bahati na kumkuta Bahati akisoma Kuran, kwakweli alifurahi sana kwa kuona Bahati amebadilika kiasi kile, basi akamngoja amalize halafu ndio akaanza kuongea nae;

    “Basi jana usiku nimeota adui yako amekufa”

    “Amekufa?”

    “Ndio nimeota amekufa, tena amefia kwa nganga”

    “Duh nani huyo?”

    “Simjui ila nimeota adui yako amekufa”

    Mara kuna simu iliingia kwa Bahati, naye akaipokea, alipata taarifa iliyomshtua kidogo mara dada yake nae akafika pale walipokaa Bahati ba Fetty na kusema,

    “Bahati una habari huko! Baba mkwe wako amekufa, tena nasikia kafia kwa mganga”

    “Ndio simu hii ndugu wa Nasma kanipigia duh! Alikuwa anaumwa nini?”

    “Na wewe huelewi? Si nishakwambia kafia kwa mganga, kuna cha kuumwa tena hapo? Hakuna cha kuumwa labda kamloga mwenye nguvu kumliko, haya twende msibani maana alikufa jana na wanazika leo.”

    Ilibidi Bahati ajiandae kwenda msibani, Fetty nae aliamua kwenda ili kujua nini kinaendelea huko msibani.

    Walifika msibani na kukuta kuna wengine wanalia haswaa familia yake na wengine walikuwa wakiongea tu, kwa mara ya kwanza Bahati alisikia kwenye msiba ule marehemu akisemwa vibaya, kipindi chote hakumjua vizuri mkwe wake huyo ila siku hiyo alimfahamu kutokana na maneno ya watu wa pale msibani,

    “Huyu mzee alikuwa mchawi sana, bora amekufa jamani maana alikuwa akitutesa sana hapa mtaani”

    “Mtaa mzima alikuwa akiogopewa balaa sababu ya uchawi wake na akigundua tu kuwa una maendeleo basi utake usitake utamuoa binti yake”

    Walikuwa akiongea pale bila kujua kuwa Bahati ni mkwe wa Yule mzee aliyekufa, kisha muda wa kuzika ukafika na wanaume wakaenda makaburini kuzika na wanawake kubaki nyumbani yani Fetty alihakikisha anakaa hadi mwisho wa msiba ili asikilize vizuri na kweli alisikia vizuri sana kilichokuwa kinazungumziwa, aliwasikia wamama wawili wakimzungumzia mzee aliyekufa,

    “Jamani mzee alikuwa tishio huyu dah! Bora amekufa tutapumzika jamani”

    “Sijui nani kamuweza jamani”

    “Nilimuonea huruma Yule kijana Bahati masikini aliuvaa mkenge bila hata kujua, akaja kuoa kwa huyu mzee”

    “Lazima alirogwa, huyu mzee unadhani kuna mkwe wake aliyemuacha!”

    “Alikuwa ni mjumbe wa siku zote kwahiyo unajikuta unatakiwa tu kuwasiliana nae, huyu mzee ujumbe tu akigombea mwingine anammaliza sijui angekuwa mbunge ingekuwaje jamani, huyu mzee bora Mungu kamchukua tu akapumzike na sisi tupumzike jamani”

    Fetty alisikitika sana kwa zile habari za Yule mzee alizozisikia, waliporudi kuzika Fetty alimfata Bahati na kumtaka warudi tu, Bahati hakubisha wala nini maana alijikuta akipenda sana kumsikiliza Fetty kwa kipindi hiko, na walivyofika nyumbani akamuaga na kuondoka zake.



    Dora tangu apate yale majanga hakurudi kwao kabisa yani alikuwa anaenda kwenye mambo yake na kurudi nyumbani kwa James kanakwamba kashaolewa na James vile, na walikuwa wanaishi tu vizuri kama mke na mume na alivaa nguo za Bite ambazo zilibaki kwa mume wake.

    Siku hiyo kwa mara ya kwanza alienda Kanisani na James na alivaa nguo ya Bite ambayo Bite alipenda sana kuivaa ilikuwa ni nguo ya kitenge, walipotoka Kanisani walipitia kunywa supu ambapo wakati wa kuondoka Dora alitangulia nje halafu James alienda maliwatoni. Akiwa pale nje alikutana na Tony ambaye alikuwa akikatisha kwenye mgahawa huo, alimshangaa sana Dora kuvaa nguo za dada yake, alizijua sababu dada yake alipenda sana kuvaa nguo hizo, alimuita

    “Dora”

    Dora aligeuka, na Tony alimsogelea kuongea nae,

    “Mbona umevaa nguo za dada Bite?”

    “Hata salamu hakuna jamani! Kwani hizi nguo zimeandikwa Bite au?”

    “Hapana ila nazitambua hizo nguo sababu alikuwa akizipenda sana”

    “Ukiona hivi ujue nimechukua nafasi ya dadako”

    “Kwahiyo ndio unaishi na shemeji James!”

    “Hayo ni majibu”

    “Yani Dora wewe ni msichana wa ajabu sana, ni bora niliachana na wewe maana sio kwa akili mbovu kama hizo za kwako wewe”

    “Nina akili mbovu lakini toka dadako aishi na James muulize kama kuna siku amewahi kumshawishi James waende wote Kanisani zaidi yay eye kwenda peke yake! Lakini mimi na akili zangu mbovu nimeweza kumshawishi James na leo tukaenda Kanisani”

    “Ama hilo Kanisa liliingiliwa leo, yani mtu kama wewe uwende Kanisani, kweli majanga. Ila bora niliachana na wewe”

    “Kwahiyo wewe kuwa na Yule Tumaini ndio unajiona mjanjaaa eeeh! Unakuwa na mwanamke hata mahusiano yake ya nyuma hayaelewi atakuwa anajua kitu huyo!”

    Tony akaona kuendelea kuongea na Dora ni kujiaibisha tu, wakati anataka kuondoka akakutana na James akienda alipo Dora, ila Tony hakuongea nae chochote zaidi ya kusikitika tu.

    Muda huu aliondoka na kwenda nyumbani kwao na alipomkuta dada yake alimpa taarifa kuwa akachukue nguo zake tu,

    “Hivi James anashindwa kumnunulia nguo huyo mwanamke wake hadi avae nguo zangu jamani!”

    “kazichukue tu dada”

    “Hapana sitazichukua tena ila naona bora nikafungue mwenyewe shtaka la talaka ili James anipe talaka yangu nijue moja.”

    Bite alikuwa na hasira sana na Dora maana alihisi kuwa ni mtu mbaya sana kwake.



    Leo Babuu alitafuta wazee wa hekima na mshenga kwenda kujitambulisha kwakina Zainabu kwani alikuwa na lengo haswaa la kumuoa, basi walijitambulisha ila Babuu alikuwa na mashaka sana kuwa Zainabu anaweza kukataa ile posa ila Zainabu alikubali na wale kufata taratibu zote za kujitambulisha, wageni walivyoondoka tu pale, leo Mrs.Peter alienda pia nyumbani pale maana hawakuonekana tena tangu wajitambulishe kwahiyo alienda kuomba msamaha,

    “Jamani mnisamehe bure hata sijui imekuwaje maana muhusika mwenyewe tukimuuliza hatujibu vizuri kwakweli”

    “Hata msijali, wamekuja wengine leo na wamesema wiki ijayo wanakuja kumaliza kila kitu na ndoa kabisa”

    Mrs.Peter alishangaa sana ila hakuweza kuongea zaidi na kuagana nao kisha akarudi nyumbani kwake, alimuita mwanae Rahim kumuuliza tena kuwa imekuwaje kuhusu swala la kumuoa Zainabu,

    “Eeeh Rahim mwanangu imekuwaje mbona sielewi?”

    “Mama, nimeona hakuan maana kuongeza mke wa pili wakati Salma yupo, ananitosha kwakweli”

    Yale maneno Salma aliyasikia yani aliona rah asana, aliondoka pale mlangoni alipokuwa akisikiliza na kwenda kumpigia simu Yule mama maana kwake ilikuwa rah asana,

    “Niambie mwali wangu, unakero nyingine?”

    “Aaaah hapana ila nataka nikupe ushuhuda mwingine, jamani leo nimemsikia mume wangu kwa masikio yangu akimwambia mama yake kuwa hana sababu ya kuoa tena wakati mimi nipo”

    “Oooh hiyo ni habari njema binti yangu, sasa siku ukiwa na muda njoo nyumbani kwangu nikufundishe staili ambayo inapendwa sana na wanaume yani mwanaume wako ukimfanyia staili hiyo hata iweje hakuachi abadani”

    “Jamani natamani hata nije leo, ila kesho nakuja mama yangu yani naona raha jamani, sijawahi kupendwa kama hivi, huu ndio upendo niliokuwa nauota kila siku maishani”

    “Sawa binti yangu yani ukiwa na mimi hakuna mume atakayethubutu kukuacha maana utakachompa kitamfanya akuwaze muda wote na kila muda akuonapo atamani kuwa na wewe karibu kwahiyo usijali”

    Salma aliendelea kuongea na Yule mama huku wakipanga mambo mbalimbali na Rahim nae bado aliendelea kuongea na mama yake,

    “Sasa nimeenda kule nimekuta kuna watu wametoka pale nasikia wiki ijayo wanaenda kumaliza kila kitu na kumuoa kabisa Zainabu”

    Rahim alijihisi vibaya sana, alilaumu sana ukimwi maana ndio umesababisha kumkosa mwanamke mwenye maadili yake kama Zainabu.

    Aliongea pale na mama yake ila moyoni mwake alikuwa na mipango mingine kabisa kuwa lazima ajue siku ambayo Zainabu atolewa ili aende kushuhudia na akiweza kupinga ndoa hiyo basi aipinge kwani bado moyo wake alihisi kuwa na hisia na Zainabu.



    Jumatatu, mapema kabisa, Bite alijiandaa kwenda mahakamani kwani alitaka kwenda kuandikisha mwenyewe talaka na alitaka kujua taratibu za kuweza kupata talaka yake.

    Aliingia kwenye ofisi ila alishtuliwa na mtu mmoja, kumuangalia akamkuta ni kijana ambaye aliwahi kusoma nae, Yule jamaa alimuita,

    “Kheee Bite jamani! Upo!”

    “Nipo Deo”

    Wakakumbatiana kwa furaha na kukumnbushana baadhi ya mambo ya shule,

    “Vipi familia, umeolewa nini?”

    “Ndio, mbona niliolewa zamani tu”

    “Na nyie wanawake mnapenda kuolewa mapema balaa, junaweza kuamini mimi bado sijaoa”

    “Kheee na utu uzima huo hujaoa jamani kwanini!”

    “Maisha tu, naona wanawake wote waongo jamani, waaminifu mliolewa tayari”

    Bite akacheka tu ila alipogundua kuwa Yule anahusika na pale mahakamani aliamua kumueleza kuhusu swala lake, kwakweli Deo alishangaa sana kumuona mtu akiongea kwa furaha kumbe anaugulia moyoni kwa aliyotendewa na mumewe.

    “Pole sana, ngoja nikwambie taratibu za talaka”

    Basi Deo alimueleza Bite talatib zote za kudai talaka, ambapo iliandaliwa na barua ya kumtaka James afike mahakamani pia, alimrahisishia sababu ni mtu anayemfahamu na wakati wa kuondoka alimsindikiza.

    Wakiwa njiani alimuuliza,

    “Una watoto wangapi kwasasa Bite?”

    “Mmoja tu, na wewe je?”

    “Mimi nina wawili ila bado sijaoa”

    “Mama yao yuko wapi?”

    “Aaah si unajua ujana tena, hao watoto mama zao ni tofauti, ujana maji ya moto wewe acha tu”

    Basi waliongea pale na kupeana mawasiliano vizuri na kuagana.

    Bite wakati anaondoka akiwa kwenye daladala maana siku hiyo hakutembea na gari yake, aliona mafuta yanamgharimu sana.

    Aliwaza vitu mbalimbali ikiwa na kukumbuka kuwa kipindi wanasoma twisheni, Deo aliwahi kumtongoza, akakumbuka jinsi Deo alivyokuwa akimsifia na kumpa ahadi nyingi ila Bite hakuona kama kuna malengo kwenye maisha ya Deon a ndiomana alivyojitokeza James aliona ni vyema kuolewa nae, alivyokumbuka hivyo alicheka mwenyewe na kujiuliza,

    “Sijui Deo anakumbuka kuwa aliwahi kunitongoza mmmh!”

    Akatabasamu tu na kuelekea nyumbani kwao.



    Nyumbani kwakina Bahati walijikuta wakizungumza kuhusu Fetty maana wamemuona mara kadhaa na walijaribu kumuuliza Bahati aliwajibu kuwa hakuna chochote kati yake na Fetty, dada yake mmoja akamwambia,

    “Ila Yule mwanamke anaonekana anafaa kuolewa na wewe Bahati, kwanza ana maadili halafu anaongea vizuri. Umemfahamia wapi Yule?”

    “Ni rafiki wa Erica Yule”

    “Kumbe!”

    Wakaangaliana tu ila wakaendelea kusema,

    “Ila kiukweli Bahati Yule Nasma hakufai tena, yani hafai kuwa mke wako kabisa”

    “Katika akili yangu simuwazi kabisa Nasma, na nimeandaa siku maalumu ambayo nitamtuma mtu ampelekee talaka tatu yani simtaki kabisa”

    “Unaandaa siku ya nini kaka, mtume mtu hata leo ampelekee talaka yake”

    “Nangoja amalize matanga ya msiba wa baba yake maana ndio ametoka kufiwa Yule kwahiyo atajifanya anachanganya matukio”

    “Kwahiyo utamuoa Erica?”

    “Siwezi kumpata Erica kwasasa ila ningempata basi ningemuoa nampenda sana ila bado sitaki kuwa mbali na Erica, hivyobasi ninawazo na Yule Fetty kwasasa”

    Dada zake walisikika wakipiga kigelegele kwani walitamani sana kaka yao aseme hivyo ingawa hata wao kwa wakati huo walitamani sana kaka yao ampate Erica ila uwepo wa Fetty uliwavutia pia, ila walimuuliza

    “Na vipi kuhusu Siwema?”

    “Nitamlea tu mimba hadi mtoto akizaliwa nitamlea maana ni damu yangu ila wazo la kumuoa Siwema halipo pia, ile familia hapana kwakweli imenichosha kabisa”

    Wakati wanapanga panga, Fetty nae alifika ila alivyotokea tu mbele yao aliwashangaa wakipiga vigelegele, alicheka na kuuliza,

    “Kuna nini jamani hapa?”

    “Utajua tu wifi”

    “Wifi! Kheee kivipi?”

    Iibidi Bahati abadili kidogo mada kwani hata kumtongoza Fetty alikuwa bado hajamtongoza.



    Dora aliamua kurudi kwao leo, kwakweli mama yake alimsema sana,

    “Huna akili hata kidogo, ni kweli unalalaga nje kwa siku moja na zikizidi sana mbili ila safari hii umezidisha Dora, kwanini hujiheshimu mwanangu? Hivi hutaki leo na kesho kuwa na familia yako!”

    Dora alitamani kumwambia mama yake kuwa ameathirika ila alijua ni lazima mama yake atajihisi vibaya sana, na mama yake aliendelea kuongea

    “Yani sio wewe sio mdogo wako mnaniumiza kichwa kabisa, mdogo wako nae karudi leo asubuhi hivi mnachofanya ni haki kweli? Kwanini mnanitesa hivi, nione balaa kuzaa watoto kama nyie jamani, ndiomana kuna watu wanasemaga bora angezaa mbuzi anywe supu kuliko binadamu mwenye akili fupi. Dora mwanangu, mamako nimehangaika, nimekusomesha nikiamini leo na kesho utanikomboa kwenye ufukara ila ndio kwanza unasemaga mimi ndio nimekufundisha uwe muhuni sababu sikuwa na hela ya kukupa, kweli Dora! Unasahau malezi yote niliyokupa. Mtoto huna shukrani hata kidogo”

    Dora hakumjibu mama yake kwani alijua ni kuzidi kumuongezea hasira tu, basi alimuomba msamaha tu na kwenda chumbani kwake.

    Baada ya muda Steve alimuita dada yake na kuongea nae,

    “Dada, nilikuomba unitafutie kazi ila hujanitafutia hadi leo unajua kinachoendelea?”

    “Nini kinaendelea kwani?”

    “Baada ya Sia kukataliwa na familia yote ya Erick, kaamua kutafuta mwanaume mwingine anasema awe anapata pesa ya kutunza ujauzito wake kwahiyo dada kwa Sia kuna mume mwenzangu”

    “Wewe nae ulivyomkazania huyo Sia loh! Hatuli hatunywi ni Sia Sia ila uroho wako ndio umekuponza kuwa na mwanamke asiyejielewa kama Sia. Itabidi nifanye kazi ya ziada siku nimpate Yule mwanamaombi nimlete pale kwa Sia ili madawa yaachie ubongo wako huo”

    Ila ilikuwa kama anajisumbua tu kwani baada ya muda kidogo Steve aliondoka kwao na kuelekea kwa Sia.

    Jioni ya siku hiyo Dora alifikiria sana na kuona ni vyema amueleze mama yake ukweli kuhusu hali yake ya kiafya maana kama kumficha ni atamficha hadi lini, basi alimuita chumbani kwake na kuanza kuongea nae,

    “Mama kuna jambo nataka nikwambie”

    “Ni jambo gani hilo?”

    “Mwanao nilienda hospitali kupima ukimwi…”

    Akaona moyo wa mama yake ukienda mbio na huku akiuliza kuwa aambiwe nini kimetokea,

    “Huko hospitali wakasemaje Dora, niambie mwanangu, nina watoto wawili tu mimi niambie mwanangu eeeh!”

    “Punguza presha basi mama”

    “Sawa mwanangu niambie, eeeh hospitali walisemaje mwanangu?”

    “Nimeambiwa nimeathirika”

    Yule mama kabla Dora hajaendelea kuongea tu alizimia na kumfanya Dora achanganyikiwe huku akifanya utaratibu wa kumpeleka mama yake hospitali.



    Dora alitafuta vijana wa kuweza kusaidiana na mama yake na kumpeleka hospitali, walifika nae hospitali na ikaonekana presha ya mama huyo ipo juu sana kwahiyo Dora ilibidi ashughulike pale na mama yake ambaye kwa siku hiyo alilazwa hapo hospitali.

    Dora alirudi kwao na kujilaumu sana kumwambia mama yake ukweli kwani katika siku zote huyu mama alionekana kuogopa sana ugonjwa wa ukimwi kuliko kitu chochote kile ndiomana presha ilimpenda sana.

    Kiukweli siku hiyo usiku Dora hakulala vizuri na kuwaza tu hali ya mama yake, basi asubuhi na mapema aliamka na kuandaa chakula kwaajili ya mama yake ile asubuhi, akaondoka kwao na kuanza safari ya kwenda hospitali.

    Kuna mahali alipita kabla ya kufika hospitali palikuwa na nyumba ya kulala wageni na humo alitoka Sia, alimshangaa sana na kusema

    “Sia”

    Ila Sia alimnyamazisha na kumuomba asiongee kwa nguvu,

    “Dora imenibidi kufanya hivi kwani sina jinsi na hela sina kwahiyo nitaleaje mtoto huyu atakayezaliwa? Kuna mwanaume nimempata nina wiki nae sasa yupo vizuri, ananisaidia kipesa, sasa jana alisema nije kulala nae hapa guest ningekataaje na nina shida na hela?”

    “Sia kuna magonjwa wifi yangu eeeh! Mdogo wangu bado mdogo Yule, nilikwambia kila siku uende kwenye maombi mdogo wangu akomboke na midawa ile ila hata hutaki, mdogo wangu angekomboka angeanza kufanya kazi na angekulea wewe na mtoto ila kwasasa anashindwa kwani muda wote anakuwaza wewe, atawezaje kufanya kazi?”

    “Nitafanya hivyo ila usiseme kama unanifahamu kuhusu mdogo wako maana Yule mwanaume anatoka sasa hivi kwahiyo nitasema wewe ni rafiki yangu”

    Na muda kidogo Yule mwanaume alitoka ndani, basi Sia alitaka kumtambulisha kwa Dora ila kabla ya kumtambulisha Dora alijikuta akijishika kichwa baada ya kumuona Yule mwanaume kwani alikuwa ni George.





    Na muda kidogo Yule mwanaume alitoka ndani, basi Sia alitaka kumtambulisha kwa Dora ila kabla ya kumtambulisha Dora alijikuta akijishika kichwa baada ya kumuona Yule mwanaume kwani alikuwa ni George.

    Dora alijikuta akisema,

    “Mama weeeee!”

    Sia alimuangalia kwa mshangao kuwa ni vipi ila kabla hajamuuliza, Dora aliweka mzigo wake chini na kwenda kumkunja George huku akisema,

    “Unajijua kabisa ni muathirika lakini unaenda kusambaza ukimwi kwa huyu mwanamke mwenye mimba”

    Inaonyesha George hakuelewa vizuri kuwa Sia ana mimba, kwahiyo alionekana kushangaa tu kuwa Sia ana mimba, na kutoa mikono ya Dora iliyomkunja na kumuuliza Sia,

    “Nilikuuliza mbona una tumbo kubwa ulisema ni asili ya tumbo lako, kumbe una mimba!”

    Dora alisogea katikati yao na kumwambia Sia,

    “Huyu mwanaume ana ukimwi, umeua mdogo wangu Sia”

    Ile habari ilionekana kumchanganya kabisa Sia kwani alikimbia pale na kumuacha George akiangaliana na Dora, wakati huo Dora alitaka kumvaa mwilini George ili apigane nae sema alipomwangalia vizuri George alimuona kaweka sura ya tofauti na pale akajua kama atamsogelea tena basi atachakazwa, aliinama na kuchukua kifurushi chake ila moyo wake uliuma sana.

    Kwa siku ya kwanza Dora alitembea njiani huku machozi yakimuanguka kwani aliwaza kuhusu mama yake kama akijua habari hizo si ndio atakufa kabisa, alipatwa na mawazo sana ila alipokaribia kuingia hospitali alifuta machozi yote na kuingia kumuona mama yake,alishukuru kumuona ameamka na kumpa uji aliobeba ili anywe, mamake alikunywa ule uji ila hakuongea chochote kile yani alionekana akimuangalia tu Dora basi.

    Dora hakukaa sana mahali pale kwani alimuaga mama yake na kuondoka kutokana nay ale mawazo aliyokuwa nayo.

    Hakuelewa aelekee wapi kwa muda huo ila aliamua kwenda moja kwa moja nyumbani kwao ambapo alijifungia na kulia sana huku akisema,

    “Naona kama kila kitu kimenigeukia, nilimpeleka Sia kwa mganga na dawa zikamrudia mdogo wangu, nimesambaza ukimwi na ukimwi umemgukia mdogo wangu. Mungu jamani kwanini lakini, kwanini mimi? Mama yangu atakuwa na hali gani pale akigundua kuwa wanae wote tumeathirika? Mimi kupata ukimwi ni halali yangu ila sio Steve jamani!”

    Alijikuta akilia sana ila wazo likamjia kuwa hata akilia hakuna atakachofanya,

    “Natakiwa niende kwa Yule mwanamaombi niongee nae maana kulia tu haitasaidia kabisa, nahitaji mdogo wangu awe huru, mdogo wangu asiteseke kwa makosa yangu jamani Dora mimi, nilisema nitamlinda Steve, nini nimefanya sasa jamani? Eeeeh Mungu wangu nihurumie Dora mimi”

    Basi akaondoka pale kwao na kuanza kuelekea kwa mwanamaombi.



    Kama ambavyo Erick alipanga basi alienda kumchukua dada yake dukani na kwenda nae nyumbani kwake ili akafundishwe kupika na Erica, walifika na kumkuta Erica ametulia tu kisha Erick alimuacha dadako hapo.

    Ilikuwa ndio siku ambayo Tumaini alizungumza vizuri na Erica kuliko siku zote, Erica alimuuliza,

    “Nianze kukuelekeza kupika nini? Yani chakula gani ambacho hujui kupika”

    “Nifundishe kusonga ugali, nielekeza kupika maharage ya nazi halafu nielekeze kupika wali kwenye mkaa”

    “Kwani wali unapikaga wapi?”

    “Yani mimi mara nyingi napika wali kwenye rice cooker kwahiyo kama siku ile mama yako angesema nipike wali kwenye mkaa ingekuwa shughuli nyingine ila ugali ndio kabisa yani sijawahi kupika”

    Basi Erica alianza kuelekezana nae na vingine kupika nae pamoja, walifanya vitu vyote pamoja hata chakula cha siku hiyo walipika pamoja.

    Wakiwa wamekaa kupumzika, Tumaini alimshukuru sana Erica na kumwambia,

    “Kwakweli Erica wewe ni binti wa ajabu sana yani umesahau kila kitu nilichokuwa nafanya kukupinga jamani ila umenielekeza kwa moyo safi kabisa, asante”

    “Usijali wifi yangu”

    Tumaini akacheka na kuendelea kuongea,

    “Kwakweli uwifi sasa ndio umenoga jamani maana tumekuwa mawifi haswaaa ila kwanini mawifi tunakuwa na hila kiasi kile nilichokuwa nakufanyia wewe jamani! Hata sijui kwanini nilikuwa nakuchukia jamani Erica wakati mwanzoni nilikupenda sana hata nikakwambia uwe mdogo wangu ila kile kitendo cha kutambua ni wifi yangu eti nikakuchukia balaa bila sababu yoyote, sasa ndio yaliyonitokea kwenu duh dadako anaongea jamani hadi nilijihisi vibaya, mara aniseme bonge yani dada yako dah alifanya niumie sana moyoni”

    “Mzoeee tu, ila ndio maisha yalivyo”

    “Ila dadako Yule hana mawifi kwa mumewe eeeh!”

    “Ndio, mumewe hakuwa na madada hata hivyo familia ya mumewe ipo mkoa mwingine yani yeye alipata bahati ila katika maisha kila kitu kina uzuri na ubaya wake hakuna kizuri moja kwa moja na hakuna kibaya moja kwa moja”

    Basi walijikuta wakijadili mambo mengi sana ya maisha kwa siku hiyo kwani ilikuwa ni siku nzuri sana kwa upande wao.

    Erick alivyorudi alifurahi sana kuona Erica na Tumaini wako pamoja tena vizuri sana na ciku hiyo chakula walikula kwa pamoja huku wakisifia na kukumbushana siku ya kwanza ambayo Tumaini na Erica walipatana na kuwa marafiki, Erick alicheka tu kwani walikuwa wakiongea habari za kuchekeshana na kusahau kabisa kama waliwahi kuwa na tofauti ya aina yoyote ile.



    Dora alienda nyumbani kwa yule mwanamaombi kama alivyopanga na alipofika alimkuta ila kabla ya kumueleza chochote alianza kulia kwani hakujiona sawa kabisa, yule mama alitulia ili kumsikiliza Dora alikuwa na tatizo gani, alipotulia sasa ndio alianza kumuuliza ili Dora ajieleze,

    "Una tatizo gani?"

    "Hata sijui nianzie wapi kukueleza?"

    "Wewe nieleze yote yani usifiche kitu, nieleze ili nione nawezaje kukusaidia. Ngoja tuombe kwanza ili Roho mtakatifu atusaidie"

    Basi yule mama akaomba kwa muda kidogo halafu alipomaliza ndio Dora alianza kujielezea yale yanayomsibu.

    Dora akapumua kidogo, kisha akaanza kumueleza, ingawa yalikuwa ni maelezo marefu ila huyu mama aliyasikiliza kwa makini.

    Dora alianza kumuelezea alimdanganya Erica kuwa ana ukimwi ili Erica amuhurumie na kumpatia pesa atakazopewa na mzee Jimmy, kisha akamueleza alivyokwenda kwa mganga kwaajili ya kupata dawa ya mapenzi na shida yake ilikuwa ni kumteka James sababu tu James alimfanyia kitendo kibaya cha kumbaka, kisha akaeleza alivyompeleka Sia kwa mganga kwaajili ya dawa za mapenzi na jinsi mdogo wake alivyokunywa dawa hizo, pia akamueleza jinsi alivyopima na kukutwa na ukimwi na kuamua kuusambaza ugonjwa huo na mwishowe kwa aliyoyagundua siku hiyo.

    "Leo nimemkuta meanamke niliyemuambukiza ukimwi akiwa na mwanamke ambaye ndio yule aliyempa madawa mdogo wangu, yani mdogo wangu anaathirika kwasababu yangu, hana hatia Steve ila sababu yangu jamani. Nakumbuka Ericq alinionya ila sikusikia na kujidai kuwa sina mdogo wa kike wa kuweza kutembea na wanaume niliowaambukiza kumbe nampelekea janga mdogo wangu! Na hivi mamangu yupo hospitali maana jana nilivyomueleza kuwa nina ukimwi basi presha ikampanda ndio kalazwa. Yani sielewi hapa, naamini maombi yako ni ya kweli, namuomba Mungu amfungue mdogo wangu, namuomba Mungu mdogo wangu asipatwe na ukimwi nilioueneza. Namuonea huruma mama, katuzaa kwa uchungu na katulea bila msaada wa baba halafu leo hii nimefanya fedheha ya namna hii kweli!! Najijutia mimi Dora"

    Dora akawa analia sana, ni wazi mambo ya siku ile yalimuingia akilini maana hakuwa na furaha kabisa, huyu mwanamaombi akaanza kuongea nae sasa,

    "Dora, unaamini ya kwamba Mungu anafanya? Mungu anaweza yote?"

    "Ndio naamini'

    "Basi kabla ya yote yakupasa uokoke, umkabidhi Yesu maisha yako. Je upo tayari nikufanyie sala ya toba?"

    Dora aliona ni sawa kuokoka yani kwa muda huo alikuwa tayari kwa chochote kwaajili ya maisha ya mdogo wake na mama yake. Yule mama alimfanyia sala ya toba na baada ya hapo akamueleza,

    "Mungu wetu ni Mungu mwenye rehema nyingi, ni Mungu wa hurumq ni Mungu wa Neema. Ukisoma Zaburi 145 mstari wa 8 na 9 unasema “8. BWANA ana fadhili, ni mwingi wa huruma,Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema,

    9. BWANA ni mwema kwa watu wote,Na rehema zake zi juu ya kazi zake zote.” Neno la Mungu li hai na linatufundisha tuwe wakamilifu wakati wote. Umechagua jambo jema kukabidhi maisha yako kwa kristo sasa kitu cha kufanya kwa sasa unakijua?"

    "Ndio, natakiwa niombe kwaajili ya mdogo wangu na mama yangu"

    "Ni kweli ila unatakiwa uombe kwanza kwaajili yako mwenyewe maana wewe ndio umesababisha yote haya. Unatakiwa uingie kwenye maombi ya toba, yani wewe tubu mbele za Mungu, maombi ya toba yanatuweka karibu na Mungu hakuna aliyesafi mbele za Mungu ila tunajitahidi tu kuenenda katika njia zake, yatupasa kuomba toba. Omba toba kwaajili yako kwa kukesha kwa waganga, omba toba kwaajili ya kusambaza ukimwi. Halafu uwe unaamini kuwa Mungu anakusikia, yani kwasasa uwe katika maombi ya toba. Tutafanya mfungo wa siku tatu yani kuanzia kesho, ni vyema uwe unakuja hapa tunajifunza neno na kuingia kwenye maombi, ili vifungo vyako vifunguliwe ni kuingia kwenye maombi ya toba kwanza na maombi haya yanamuweka Mungu karibu yetu. Omba toba binti yangu yani usichoke wala usijihesabie haki kwa Mungu kwani Mungu atakupa unachostahili. Umenisikia"

    "Sawa, sawa"

    "Ni kweli kesho utaanza mfungo huo?"

    "Ndio nitaanza kufunga"

    "Sheria za kufunga unazijua?"

    "Hapana sizijui"

    "Asubuhi na mapema ingia kwenye maombi ili Mungu akueaidie na huo mfungo, halafu usizini, usiende kudanganya yani katika dhambi zote dhambi ya uongo ina baba yake kabisa ambaye ni shetani, ukiwa muongo ni moja kwa moja unajiunganisha na shetani na kumtoa Mungu katika maisha yako kwahiyo unakuwa umemchagua shetani kuwa baba yako kwamaana hiyo funga yako haitakuwa ya salama. Na yale unayotambua ni dhambi usifanye, unanielewa lakini?"

    "Nakuelewa"

    "Kesho saa ngapi unakuja?"

    "Saa kumi jioni"

    "Najua siku ya kwanza ibakuwaga ngumu sana maana utajikuta umetamani chakula, ila kumbuka dhumuni la mfungo wako. Mungu akusaidie binti yangu"

    Dora alimshukuru sana yule mama ambapo alifanya maombi na kumruhusu Dora kuondoka muda huo.



    Bahati leo alimuita Fetty nyumbani kwao na kuanza kuongea nae,

    "Fetty, natumai hujaolewa?"

    "Ni kweli sijaolewa ila nina mtoto"

    "Samahani kukwambia jambo hili"

    "Bila samahani"

    "Mimi ni Mwislamu ila sikuwa vizuri sana kwenye maswala ya dini nadhani ni sababu ya malezi ambayo nimelelewa, sema wakati nakua nilitamani sana mke nitakayemuoa apende sana dini na anifundishe na mimi ili na mimi nipende Kuswali. Nikampenda Erica, tena nilimpenda sana labda kama kusingetokea mambo ya ajabu kwangu basi Erica angekuwa mke wangu, Erica ni mwanamke anayeipenda dini yake, alinivutia sana. Ila sikujua ni kwanini Mungu kanipitisha kote huku hadi kukufahamu wewe uliyenifundisha kusoma hadi Kuran, kufanya dua na kwenda Msikitini kuswali, nashukuru sana, nadhani umeletwa na Mungu kwangu. Tafadhali Fetty naomba uwe mke wangu, sitakufanya ujute maishani, nimemkosa Erica ila Mungu kaniletea wewe, yani wewe ndio mke wangu. Naomba usikatae Fetty, nakuomba tafadhali ukikubali tu hata kesho tunaenda kujitambulisha kwenu"

    Fetty alimuangalia Bahati kwa makini ila kiukweli Fetty nae alikuwa na kiu ya kuolewa, alitamani sana kupata mume wa kumuoa hadi kupelekea aanguke mikononi mwa George, kwahiyo hakuwa na pingamuzi pale kwa Bahati na kukubali, ilikuwa ni furaha kubwa sana ike kwa Bahati yani alijiona kama ndio kapata kila kitu.



    Dora alivyofika kwao aliandaa chakula cha kumpelekea mama yake jioni maana mchana hakwenda ila alimpelekea jioni hiyo mama yake, aliongea nae na mama yake alimwambia kuwa anaweza kesho yake akaruhusiwa basi Dora alifurahia kusikia vile, ila mama yao aliulizia kuhusu Steve kama karudi nyumbani,

    "Yupo nyuma mama"

    "Mbona hujaja nae?"

    "Alijua leo unatoka mama"

    "Muangalie vizuri mdogo wako Dora"

    "Usijali mama"

    Basi akaagana na mama yake pale na kuanza safari ya kurudi kwao.

    Akiwa njiani, gari ya James ikasimama pembeni yake na James akashuha kioo na kumsalimia Dora, kisha akamwambia

    "Dora, leo nina hamu ya kunywa pombe balaa. Twende basi tukapombeke unipe kampani"

    "Kheeee Jemes bado hujakoma tu?"

    "Sikia Dora yani leo tunaenda kununua pombe halafu tunaenda nazo nyumbani, tunakunywa weee na kufanya mambo yetu kisha tunalala. Safari hii tukae pamoja wiki nzima mpenzi wangu"

    "Nimekuelewa James ila kwasasa naenda nyumbani kwanza"

    "Nyumbani kufanya nini?"

    "Leo hapana James, sitaweza kwenda na wewe popote kwanza mama yangu ni mgonjwa yupo hospitali kalazwa"

    "Kheeee pole sana Dora, sikujua hilo"

    Kisha James akatoa laki moja na kumpa Dora kuwa zimsaidie hospitali kwenye kumuhudumia mama yake kisha akaagana nae na Dora akarudi kwao.

    Alipofika alianza kufanya maombi aliyoelekezwa, alifanya maombi kwa muda mfupi kisha akaamua kulala huku akiwa na mawazo mengi sqna sana kuhusu mama yake.

    Kesho yake alijiandaa tena kwenda hospitali na kukuta mama yake karuhusiwa kwahiyo, alifanya utaratibu wa kuita bajaji na kurudi na mama yake nyumbani ambapo cha kwanza kabisa huyu mama aliuliza kuhusu Steve

    "Yuko wapi Steve?"

    Dora hakuona sababu ya kuendelea kuongopa kwa mama yake na kumwambia kuwa Steve bado yupo kwa Sia ila tu hakuthubutu tena kugusia swala la ukimwi kwa mama yake.

    Jioni ya siku hiyo, Dora alienda kwa yule mwanamaombi kujifunza maandiko na kuomba pamoja.

    Walipomaliza, Dora alikuwa akirudi kwao yani kwa kipindi hiko Dora alionekana kama binti wa tofauti sana.

    Wakati anarudi siku hiyo, alikutana njiani na mzee Jimmy ambaye alimuomba Dora wakalale wote,

    "Hapana kwakweli siwezi kufanya hivyo"

    "Kwanini unakataa Dora? Nitakupa pesa"

    Sababu alijua Dora alipenda sana pesa ila bado Dora alikataa na kuanza kuondoka, mbele kidogo akakutana na mama Erick ambaye alionekana kuwa gari yake kaiacha mahali, ila huyu mama alimuona Dora alivyosimama na mzee Jimmy, kwahiyo alivyofika kwa Dora alimshika mkono na kurudi nae aliposimama mzee Jimmy kisha akaanza kumsema mzee Jimmy,

    "Yani wewe mzee huna hata aibu, huyu si sawa na binti yako jamani! Na wewe binti huna hata aibu, huyu si sawa na baba yako tu jamani!"

    Dora alikuwa kainamisha kichwa chini tu na hata mzee Jimmy hakujibu chochote kile ila mama Erick aliendelea kuongea,

    "Wewe mzee umezidi ndiomana huyu binti kakuambukiza ukimwi"

    Mzee Jimmy akashtuka na kusema,

    "Haiwezekani, kaniamnukiza ukimwi"

    Mzee Jimmy akataka kumkunja Dora ambapo mama Erick alimuacha na Dora akakimbia.

    Mama Erick akacheka sana na kumuacha mzee Jimmy akiwa na hasira sana na kuingia kwenye gari yake.



    Leo Tumaini alivyotoka kujifunza kupika kwa Erica, akaamua kupitia kwa mama yake kumsalimia.

    Alimkuta na kumsalimia kisha mamake akamuuliza za kazi,

    "Nitoke kazini wapi mama? Nimetoka kujifunza kupika"

    "Imekuwaje hadi wajifunza kupika?"

    Tumaini alimueleza mama yake jinsi alivyoumbuka kupika kwakina Tony, huyu mama alisikitika sana na kusema

    "Ila ni kosa langu kwakweli, ni kosa langu. Mimi kama mama sikucheza nafasi yangu vizuri kwako, niliacha ulelewe na babako halafu baba mwenyewe hajielewi ni kosa langu. Mwanangu pole"

    "Ila mama, hivi kwanini unamchukia baba?"

    "Mambo yake ndio yamefanya nimchukie, ngoja leo nikwambie kuhusu baba yako. Mimi nilikuwa naishi na mwanaume na nikazaa nae watoto ndio hao kaka zako, akatokea babako na kunishawishi kwa pesa zake. Aliniahidi kunioa na kulea watoto wangu wote basi nikaondoka kwa mume wangu na kumbebea na mimba yako kabisa ila kilichotokea yule mwehu hakunioa wala nini yani nilihangaika mwenyewe na watoto wangu hadi kuamua kumuachia tu akulee. Namchukia Jimmy, naongea nae basi tu"

    "Pole mama yangu"

    Tumaini aliongea ongea pale na mama yake na kumuaga kuwa ataenda tena Ijumaa kumsalimia.

    Aliondoka kwa mamake na kurudi kwao ambapo siku hiyo alipofika tu baba yake nae alifika halafu alionekana kuwa na mawazo sana, Tumaini hakutaka kumfatilia baba yake kwa muda huo alimuacha tu na yeye kwenda kulala.

    Ila alipigiwa simu na Erick,

    “Vipi baba anaendeleaje? Maana mama kanipigia simu kuwa alionana nae akiwa na Dora na alimwambia ukweli kuwa kaambukizwa ukimwi na Dora”

    “Mmmh basi ndiomana yani karudi na mawazo hatari , hapa kaenda chumbani kwake moja kwa moja sijamuuliza kitu wala salamu yangu hajaitikia”

    “Ila hivi unadhani baba ndio kampa ukimwi Dora au Dora ndio kampa ukimwi baba?”

    “Mmmh pagumu hapo maana baba yetu naye mmmh hatabiliki ujue”

    Akaongea ongea na kaka yake pale na kuamua kulala tu.



    Asubuhi na mapema mzee Jimmy aliamka ila siku hiyo hakuwa na raha kabisa, alienda kazini ila hakuwa na raha na kuamua kwenda hospitali, ambapo kule hospitali alienda kukutana na mwanamke ambaye alikuwaga nae na mahusiano kwa siku nyingi sana, alimkuta ndio daktari eneo lile, ilibidi aanze kuongea nae,

    “Kheee Doroth za siku nyingi?”

    “Nzuri tu karibu”

    “Sikutegemea kukukuta hapa, kumbe ushakuwa daktari? Nakumbuka mwaka ule tulikuwa pamoja ndio ulikuwa mwaka wako wa mwisho pale chuoni kwenu”

    “Ni kweli, na sasa mimi ni daktari, karibu sana”

    “Sawa asante, ila kilichonileta hapa nataka kupima afya yangu, nahitaji kupima ukimwi”

    “Kheee usinichekeshe mie, nilijua unatumia dawa za kuongeza siku, wewe mzee mbona umeathirika siku nyingi sana”

    “Nimeathirika siku nyingi! Kivipi?”

    “Unajua ni kwanini mimi niliachana na wewe? Ni baada ya kugundua kuwa una mahusiano na Yule mwalimu wetu, sasa Yule alikuwa na ukimwi na ameshakufa siku nyingi sana”

    Mzee Jimmy ndio alishtuka hapo maana siku zoyte hakuwaza kuwa ana ukimwi yani ugonjwa huo hakufikiria kabisa kama anao, basi kwa uthibitisho zaidi waliamua kupima nae ambapo ni kweli alikuwa ameathirika, hapo kidogo akili yake ikapoteza uelekeo kabisa na alipoondoka pale hospitali aliamua kwenda kwa Ester Yule mwanamaombi ili akajaribu kumpa ushauri.



    Bahati alionyesha dhamira yake ya ukweli kwa Fetty, hivyo siku hiyo aliandaa talaka na kumpa mtu akampelekee mkewe maana hakuhitaji tena kuishi nae.

    Na upande mwingine alitafuta rafiki yake wa karibu kwenda kujitambulisha kwakina Fetty na kufanya harakati za kuoana nae, hakutaka kuchelewa kwani kila alipomfikiria Erica alihisi kugairisha anachotaka kukifanya kwahiyo aliona ni vyema mambo ya kuoana na Fetty yawe ni haraka haraka ili akae na Fetty kwenye nyumba.

    Ndugu zake walisaidiana nae kuhusu swala hilo na walisema watahakikisha mambo yatakuwa haraka haraka, dada wa Bahati alienda nyumbani alipokuwa anaishi Bahati na mkewe kwani alitaka Nasma aondoke, alimkuta Nasma katulia kamavile hajapewa talaka,

    “Kwahiyo unajisahaulisha Namsa au? Hivi hujui kama umepewa talaka?”

    “Kwahiyo kama nimepewa talaka ndio nini?”

    “Unatakiwa kuondoka hapa”

    “Sikia nikwambie wifi yangu, yani hapa siondoki sijui mtaniondoa na greda au nini ila hapa siondoki kabisa”

    “Sasa Bahati anataka kuoa mke mwingine”

    “Aoe tu na atanikuta mimi humu humu. Tena ngoja nikwambie wewe nahisi ndio unajisahaulisha, si wewe uliyekuwa ukishadadia mwanzo kuwa kaka yako tumuwekee dawa anioe sio wewe? Si wewe uliyeniambia hadi chakula anachopenda Bahati yani kinachofaa mimi kumuwekea dawa, si wewe? Saizi unataka kujusahaulisha, saizi unajifanya kama hujui. Nimezaa na kaka yenu mnataka niondoke eti kanipa talaka niende wapi sasa? Baba yangu ameshakufa, mnataka mimi niende wapi na mtoto? Yani siondoki tena siondoki kabisa semeni lingine”

    “Unajivunia nini wewe?”

    “Najivunia ndoa niliyofunga na Bahati, hii talaka siitambui kabisa, talaka ya kutumwa mtu kuniletea? Jamani siondoki, yani hapa labda mniue ila kuondoka siondoki kabisa”

    Yule binti aliwakatalia katakata, dada wa Bahati hakutaka kufata sheria maana aliona huyu binti atapata mali ambazo hata hajazitolea jasho ila kwajinsi alivyokuwa anakataa hakuwa na jinsi zaidi ya kurudi kwao na kushauri ndugu zake kuwa wakafate sheria tu maana hakuna namna nyingine.



    Mzee Jimmy alienda kwa Ester na kuongea nae, alionekana akijutia mambo yake mengi aliyoyafanya zamani,

    “Unajua sikujua kama nimeathirika kumbe nimeathirika zamani tu na nimekuwa nikiambukiza watu ukimwi”

    “Kheee hatari Jimmy, ila mimi nina ushauri mmoja tu kwako. Unatakiwa kuokoka”

    “Hapana bhana, huo ushauri hapana Ester nitafutie ushauri mwingine, nitaokokaje na wakati sina mke? Nitaokokaje na wakati bado nina kiu na pombe? Nitafutie ushauri mwingine bhana”

    “Ushauri wangu kwako ni huo tu Jimmy, unatakiwa kuokoka.”

    “Nishauri vingine ila kuokoka hapana jamani”

    Basi akamuaga pale ili kuondoka, akashangaa na Dora kufika eneo lile, alimuuliza

    “Na wewe umefata nini hapa?”

    Ester alimjibu,

    “Mwenzio ameokoka”

    Mzee Jimmy alicheka sana kisha akamwambia Ester,

    “Naona huna kazi za kufanya, hivi hilo swala la kushauri makahaba waokoke nani amekutuma? Yani hadi huyu kahaba unamuita mlokole, wewe mwanamke umechoka kweli”

    “Tatizo Jimmy mbishi”

    “Sio mbishi, hebu wewe jione ulivyo eti umeokoka na tangu umeokoka umepata faida gani? Toka kipindi kile unatukataa wakina Jimmy kwa madai ya kuokoka, sasa unapata faida gani zaidi ya kujiongezea umasikini. Nitakupeleka siku moja nyumbani kwangu, pamoja na ukimwi wangu huu na ulokole wako huo utanikubali tu najua sababu sijawahi kukufikisha kwangu, endelea tu kudanganywa na huyo kahaba kuwa ameokoka, loh kumbe wanaokoka hadi vichaa! Kwa hilo hunipati, kwaheri”

    Mzee Jimmy akaondoka zake, ila huyu mama alimsikitikia sana na kuendelea na mafundisho yake na Dora.



    Erick leo jioni alitoka na Erica pamoja na Angel walienda kwenye duka moja la nguo za harusi na kuchagua nguo hapo huku Erick akimwambia Erica,

    “Yani kwenu wakikubali tu hata sitaki kuchelewesha mambo, nitakuoa haraka sana. Nahitaji tuishi kama mke na mume, tafadhali nakuomba Erica kwenu wakikubali tu basi tusicheleweshe mambo”

    “Erick nilivyo na hamu ya kuolewa na wewe jamani naanzaje kuchelewesha mambo jamani, kwanza mamako anaenda lini kwetu?”

    “Alisema Jumamosi yani keshokutwa, kwahiyo mambo yananukia Erica”

    “Ila naomba hiyo siku twende pamoja, nimekumbuka sana nyumbani”

    “Hakuna tatizo, tutaenda wote tu”

    Erica alikuwa akitabasamu tu na kuingoja hiyo siku kwa hamu kwani aliona kama ndio siku ya ndoa yake. Waliendelea kuangalia nguo na kuweka oda kwa nguo walizozipenda, wakati wanatoka pale dukani, wakakutana nje na Derick, ambaye alipomuona Erica alimkimbilia na kumkumbatia ila leo Erica alikuwa kama sio yeye kwani alimsukuma Derick kwa nguvu hadi Derick alianguka chini, kile kitendo kilionekana kumfurahisha sana Erick kwani alicheka mno.

    Derick aliinuka kwa hasira kwani aliona kama Erica amemdhalilisha, akataka amsogelee ila Erick alikaa mbele ya Erica kwani Angel alikuwa chini tu amesimama, Erick alimuangalia Derick na kumsikitikia sana kisha akamwambia,

    “Shida za maisha yako usitake kumaliza kwa wengine, wanawake wapo wengi sana duniani kwani ni lazima kuwa na dada yako!”

    “Sikuwa na nia ya kumfata ili tuwe pamoja, nilitaka kumsalimia ila ona alivyonisukuma jamani kama kichaa”

    “Ndio unajiona una akili timamu? Mwenye akili timamu hawezi kufanya kama wewe unavyofanya Derick, unatakiwa kuwa mpole na kutayarisha tu tumbo lako hilo lisilo na shukranu kula msosi kwenye harusi yetu nimesema halina shukrani maana ukila ukimaliza utaenda chooni kujisaidia kwaheri”

    Erick alimbeba Angel na kumshika mkono Erica na kuelekea nae kwenye gari yao kisha wakaondoka na kwenda nyumbani.

    Mawazo ya Erica yalikuwa ni harusi yake tu kwani alivyofika nyumbani hata akaanza kujaribisha na miondoko atakayotembea siku ya harusi yake,

    “Inaonekana umefurahi sana”

    “Yani naona raha mno, naona kama ndio leo vile jamani nimemkumbuka mama yangu loh! Jumamosi niende kumuona tu”

    Muda ule ule simu ya Erica iliita na Erick alivyoiangalia aliona ni mama yake Erica anapiga kwahiyo akampa apokee ili aongee nae,

    “Mwanangu jamani nimekukumbuka! Mimi ni mzazi lazima niongee mwanangu maana mdomo nimeumbiwa ila nimekukumbuka sana mwanangu, nimemkumbuka mjukuu wangu Angel, eeeh Erica unakuja lini nyumbani?”

    “Junamosi mama”

    “Mwanangu uje kweli, nimekukumbuka sana mwanangu, njoo tuongee. Mjomba wako kaniuliza leo nimekosa hata jibu la kumjibu kuwa tulisomesha mtu au paka, jamani mwanangu nimekukumbuka sana. Mwambie Erick aje afanye taratibu za ndoa yenu, nakukumbuka sana mwanangu”

    “Usijali mama, Jumamosi tunakuja na mamake Erick”

    “Oooh hiyo ni habari njema sana mwanangu tena njema mno, nafurahi kuisikia habari hiyo karibuni sana”

    Erica aliongea ongea pale na mama yake na kukata simu ila alikuwa na furaha kubwa sana kuona hata mama yake amemkumbuka maana hakufikiria kama inaweza kuwa rahisi kiasi hiko.

    Basi Angel alipolala Erick alimwambia Erica,

    “unajua furaha ya leo haijakamilika”

    “kwanini Erick?”

    “Tukifanya mambo yetu ndio itakamilika”

    Erica alicheka tu ila alijua lengo la Erick kwa muda huo ni kitu gani na kwenda kulala nae tu kwa muda huo.



    Asubuhi na mapema Ijumaa, Bite aliamkia kule mahakamani na alipomaliza mambo yake Deo alihitaji kuondoka nae. Waliondoka na kwenda kuzungumza,

    “Unajua Bite wewe ni mwanamke mzuri unatakiwa ukae kwenye ndoa na mwanaume aliyetulia na utulie pia, naomba uwe mke wangu. Yani swala la talaka na mumeo likiisha basi uwe mke wangu tafadhali nakuomba Bite”

    Kwakweli sababu Bite alikuwa na hasira na mume wake na alitaka kumuonyesha kwamba ingawa tumeachana basi nimepata mwingine mwenye upendo wa dhati, alijikuta akikubali kuwa na Deon a siku hiyo hiyo Deo alimuomba aende nae kwao akamuonyeshe ili Bite aijue familia ya Deo, kwakweli Bite aliona ule ndio upendo wenyewe yani mwanaume asukumwi kuwa nipeleke kwenu ila anaamua mwenyewe kumpeleka mwanamke kwao, basi walipomaliza maongezi pale walianza safari ya kwenda kwakina Deo.

    Walifika kwakina Deon a kukaribishwa vizuri sana, kisha Deo alimtambulisha mama yake kuwa Yule ni mwanamke aliyempata na anahitaji kumuoa,

    “Karibu mwanangu, ila huyu Deo ana watoto wawili utaweza kuwatunza?”

    Deo alimkatisha kidogo mama yake,

    “Mama jamani ndio maswali gani hayo?”

    “Lazima tuulize mwanangu, kama hukumwambia basi ndio namwambia ajue una watoto wawili je ataweza kuwatunza?”

    “Nitaweza mama”

    “Haya karibu sana”

    Ila Deo hakusema kwao kama Bite anafatilia talaka kwa mume wake, yani hilo swala Deo hakuligusia kabisa, wakati wanamuaga mama yao, akamwambia Deo,

    “Dadako anakuja muda sio mrefu, subiri afike nae amfahamu wifi yake”

    Na kweli mlango ulifunguliwa na mama yao akasema,

    “Ndio huyo, karibu mwanangu”

    Bite alishangaa sana kwani wifi yake huyo alikuwa ni Tumaini, alikumbuka jinsi alivyomshushua Tumaini kwao yani alijihisi joto mwili mzima na hakuweza kukaa zaidi na kuamua kuaga tu muda huo huo na kuondoka.



    Ile harusi ya Babuu na Zainabu ilifanyika nyumbani kwakina Zainabu siku hii ila Rahim hakujua kinachoendelea kwahiyo alitulia kwake tu, badae akasikia kuwa kuna harusi na Zainabu kaolewa na muda huo anaondoka na mume wake, alijikuta akitoka kwake na kwenda haraka kwa kina Zainabu ila aliwakuta ndio wanaishia, alipouliza vizuri alishangaa kuambiwa kuwa babuu ndiye aliyemuoa Zainabu, kwakweli alimuona Babuu kuwa msaliti mkubwa sana kwake na hafai kabisa, alirudi kwao kwa hasira na kumfata mama yake,

    “Kumbe mama Babuu ndio kaenda kumuoa Zainabu?”

    “Babuu?”

    “Ndio mama, yani Babuu alikuwa akinisindikiza kwa Zainabu kumbe anamtaka yeye!”

    “Basi usipaniki mwanangu, Babuu ni ndugu yako huna haja ya kupaniki hivyo”

    Akatoka ndani kwao na kwenda baa, akanunua bia za kutosha na kurudi nazo nyumbani kwao kisha akaingia ndani kwake na kuanza kuzinywa, kila leo mrs. Peter alimkatalia mwanae kuwa mlevi ila siku hiyo Salma alienda kumshika mkono na kumpeleka kwenda kumshuhudia mwanae akinywa pombe, aliashtuka sana.

    “Kheee Rahim kumbe ni mlevi mwanangu? Yani unakunywa pombe kama maji?”

    Rahim hakumjibu mama yake bali aliingia chumbani kwake na kwenda kulala.



    Jumamosi ilivyofika mama Erick aliwasiliana na wakina Erick na kukutana nao ili aelekee nao nyumbani kwakina Erica, walikutana njiani wakati Erick, Erica na Angel wakiwa kwenye gari la mbele halafu mama yao akifata nyuma kwenye gari.

    Kufika kwakina Erica walisimamisha magari nje kisha wakina Erick wakashuka na mama Erick alishuka, Erica alisogea kumsalimia mama Erick, ila Yule mama alivyomuona mtoto wa Erica alichukia sana na kusema,

    “Yani Erick kila atakayemuona huyu mtoto atajua wazi kuwa si damu yako, kwakweli leo nimejionea makubwa, ngoja nikaongee na huyu mamake Erica anitolee haya mauzauza”

    Yani mama Erick ndio alitangulia mbele kamavile anaifahamu nyumba ile, alipoingia getini tu mama Erica nae alikuwa ametoka ndani kwake, wakaonana na kukumbukana wakakimbiliana na kukumbatiana. Erick na Erica walishangaa pale getini kuona mama zao wanafahamiana.



    Yani mama Erick ndio alitangulia mbele kamavile anaifahamu nyumba ile, alipoingia getini tu mama Erica nae alikuwa ametoka ndani kwake, wakaonana na kukumbukana wakakimbiliana na kukumbatiana. Erick na Erica walishangaa pale getini kuona mama zao wanafahamiana.

    Hawa wamama walionekana kufurahiana sana na kuingia ndani ambapo mama Erica alimkaribisha vizuri sana mama Erick,

    “Karibu mdogo wangu Julieth”

    “Wow na jina hujanisahau kweli Mungu ni mwema, nimefurahi sana kukuona dada Agness”

    Wakaingia ndani ila Erick na Erica hawakuingia kwani walijikuta wamesita kidogo wakijiuliza maswali mawili matatu, Erick alimuuliza Erica,

    “Mama yangu na mama yako wamejuana vipi?”

    “Hata naelewa basi! Nashangaa tu ila inatisha hii kitu, sitaki kusikia habari kuwa sisi ni ndugu”

    “Hakuna kitu kama hiko Erica”

    “Mfano tukaambiwa ni ndugu itakuwaje?”

    “Erica, kwa jinsi ninavyokupenda hata waseme ndugu yani hata waseme sisi ni mapacha lazima nitakuoa, bora nife kuliko kukukosa. Erica, haiwezekani sisi kuwa ndugu, nina baba yangu una baba yako, nina mama yangu na wewe una mama yako”

    “Itakuwa ni vyema kama sisi sio ndugu ila mimi nadhani tusubiri kwanza hapa nje wakituita ndani ndio twende tukaongee nao”

    “Hapana Erica, usiwe muoga hivyo twende tu tukaongee nao. Nishakwambia hata tuwe ndugu lazima nikuoe yani swala la mimi kukuoa wewe lipo ndani ya damu na haliwezi kubadilika”

    Basi waliinuka na kwenda ndani, waliwakuta mama zao wakiongea kwa furaha sana.

    “Jamani milima haikutani ila binadamu hukutana kwahiyo wewe ndio mama yake Erica?”

    “Ndio ni mimi, na wewe ndio mama yake Erick?”

    “Ndio ni mimi, yani kipindi chote hiki nasema nitakutana wapi na Yule dada kumbe Mungu katumia njia nyingine kabisa. Huyu ndio Yule mtoto wa kipindi kile jamani dah!”

    Mama Erick alimuangalia Erica bila kummaliza, kwa mara ya kwanza mama Erick alisimama na kwenda kumkumbatia Erica kwa furaha aliyokuwa nayo kwa wakati huo, Erick ndiye aliyeuliza,

    “Jamani mama mmefahamiana vipi hebu tutoeni tongotongo tujue”

    Mama Erick alianza kuelezea,

    “Najua sijawahi kukupa historia yako najua pia hujui ni kwanini huwa namchukia baba yako, ila siku zote hizi nilitamani sana kukutana na huyu mama basi nimpe shukrani zangu tu”

    Erick na Erica walitulia kusikiliza kuwa ilikuwaje, mama Erick aliendelea kuzungumza

    “Yani ni hivi hakuna kipindi nilichopata shida kama kipindi cha mimba yako Erick, nilihangaika nayo sana yani sikuwa na msaada wowote ule, siku hiyo nikiwa kwenye pilika pilika zangu uchungu ulinianza ila unajua ikawaje, huyu dada akiwa mjamzito pia ndio alinisaidia, alikuwa yupo njiani na mumewe nadhani walikuwa wanafanya mazoezi basi wakanihurumia na mumewe akakodi gari ambalo nilipanda nao na kuelekea hospitali. Wakati nakimbizwa leba, huku nyuma uchungu nae ukamuanza basi akaletwa kule leba nilipo. Yani nesi aliyetupokea akasema Majmzito kamleta mjamzito mwenzie yani hii ya leo kali, basi nilitangulia mimi kujifungua na baada ya muda nay eye alijifungua Yule nesi alituangalia akasema, “Watoto wenu ni kama mapacha, ningekuwa mimi wa kiume ningemuita Erick na wakike ningemuita Erica” Lile neno liliniingia na kunikaa sana ila sikudhani kuwa dada yangu alisikia pia. Tuliopoenda wodini ndio tulifahamiana vizuri, sikuwa na msaada wowote hivyo basi mume wa dada hapa ndio alikuwa akileta chakula tunakula pamoja yani mimi na dada hapa”

    Kisha akapumua kidogo na kumuuliza Mama Erica,

    “Dada shemeji nae yuko wapi nimsalimie?”

    “Alikufa ndugu yangu”

    Mama Erick alionekana kupooza kwa muda kwani inaonyesha hakutegemea kupata habari zile kwa muda ule, kisha akasema

    “Masikini jamani kumbe alikufa loh! Kifo hiki, nilikuwa natamani siku moja nionane nae, alinisaidia sana unakumbuka dada alienda hadi kutafuta ndugu zangu na kawaatarifu kuwa nipo hospitali, jamani simsahau Yule mzee”

    Mama Erica alionekana kutokutaka kukumbushwa machungu ya mumewe kwahiyo akabadilisha mada na kusema,

    “Kumbe wewe Yule mwanao ukamuita Erick, na mimi nikamuita mwanangu Erica. Jamani kumbe Erick huyu ndio mwanao!”

    “Ndio dada, Mungu ni mwema sana. Niliwaza nitakulipa nini kwa mambo uliyonifanyia hata kidogo tu nikupe zawadi dada yangu ila sikujua pa kukupata, kwakweli Mungu ni wa ajabu, tulisema watoto wetu watakuwa kama ndugu hawataachana ila tuliovyoondoka pale hospiatali ikawa ni mwisho wa undugu kumbe mungu ana mipango yake ya kuwaweka wote milele”

    Wakafurahi na kukumbatiana tena, kiukweli ile kitu ilifanya Erick na Erica wafurahi pia.



    Muda huu wakaanza kuzungumzia mahusiano ya watoto wao na wote walionekana kufurahia mahusiano yale yani hata mama yake Erick ambaye alikuwa akikataa kuhusu Erica na mtoto wake alijikuta akifurahia tu, ni pale Erick alipowaambia wazazi wao,

    “Jamani wazazi wetu, imekuwa heri sana na tumefurahi jinsi mlivyofurahia ila mimi nina ombi”

    Mama yake alimuuliza,

    “Ombi gani mwanangu?”

    “Naomba, mimi na Erica tuoane mapema iwezekanavyo yani kabla hata ya siku yetu ya kuzaliwa haijafika, nahitaji siku hiyo tuisherekee tukiwa ndani ya ndoa yetu”

    Mama Erick na mama Erica waliangaliana na kisha mama Erica aliuliza,

    “Itawezekana?”

    Mama Erick akajibu,

    “Hakuna kinachoshindikana chini ya jua, ila Erick nadhani unajua cha kufanya na unajua ni kitu gani utafanya iwezekane”

    “Najua itawezekana, sitaki kukawia, nahitaji kumuoa Erica haraka iwezekanavyo. Naenda kujadiliana na baba najua itawezekana”

    “Mmmh Yule baba yako atakubali kweli?”

    Atakubali tu mama yani itawezekana tu, najua jinsi gani niongee nae na ninajua atakubali”

    “Sawa kama ni hivyo, kwahiyo harusi itakuwa lini?”

    “Kesho asubuhi mama nitapiga simu ili kuwapa ratiba kamili ya harusi itakuwa lini yani hakuna tatizo”

    Mama Erica alikubaliana na maneno ya Erick ila kwa siku hiyo aliomba Erica asiondoke na abakie hapo nyumbani maana hana tatizo nae tena na hata watakapopanga mipango ya sherehe basi awe pale pale nyumbani.

    Basi wakafurahi pale yani mama Erick hakutamani hata kuondoka ila ilibidi tu aondoke akaendelee na shughuli zingine.

    Aliondoka pale huku akifurahia njia nzima maana alikuwa akitamani sana kukutana na huyu mama ili ampe hata zawadi kwa jinsi alivyomsaidia katika kujifungua kwake ingawa hakwenda na ndugu hospitali ila wao walikuwa ndio kama ndugu zake.



    Siku ya leo ilikuwa tofauti sana kwa mzee Jimmy kwani aliamka kwake na kujiandaa kisha kwenda kwa Ester, alifika na kumkuta Ester katulia tu akisoma biblia, alikaa na kuzungumza nae,

    “Ester, kiukweli huwa najihisi kama sipo sawa vile, nilikupenda wewe ila nilishindwa kufanya ulivyotaka wewe nikaamua kuendelea na maisha mengine sasa nimekuwa mtu mzima nikampenda binti mmoja na kutamani kumuoa kumbe ni mwanamke mwenye mahusiano na mwanangu, nimepata ukimwi bila kujua nimeusambaza kwa watu mbali mbali yani najiona kama sina faida vile, nawaza vitu vingi sana”

    “Jimmy faida yako ipo tena kubwa sana, kumbuka wewe ni baba na una watoto ila cha muhimu kufanya ni kuhakikisha watoto wako hawapiti kwenye njia ulizopita wewe”

    “Kivipi?”

    “Waache watoto wako wafanye vile mioyo yao inavyotaka kufanya, wewe hukuoa ila hainamaana kuwa basi watoto wako wasioe au kuolewa. Unatakiwa uache watoto wako wawe huru kwa wanaowapenda kwasasa, muache Erick amuoe Erica na muache Tumaini aolewe na Tony”

    “Kheee unajua hayo maswala!”

    “Najua ndio, unawanyima raha watoto wako, usitake makosa yako ya ujanani yatese na watoto wako, unatakiwa kuacha watoto wafurahie maisha. Imeandikwa kwenye Marko 10:7-9 (7.Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;

    8. na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.

    9. Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.) Jimmy huna sababu ya kuzuia watoto waliopendana, waache watoto waoane na waishi kwa furaha tena kama baba unatakiwa kutoa baraka zote kwa watoto wako nao watakukumbuka siku zote za maisha yao na kuheshimu mawazo yako kwao”

    Yale maneno yalionekana kumuingia sana Mzee Jimmy na kumuaga pale Ester kwani alionekana anafanya kinyuma kuwakatalia watoto wasioane.



    Dora akiwa nyumbani kwao, alienda kujifungia ndani muda huo akiimba na kuanza maombi kwakweli mama yake alishangaa sana kuwa mwanae kawa kitu gani, akamsubiria atoke ili amuulize vizuri.

    Muda kidogo alifika Steve na begi lake kwakweli mama yake alifurahi sana kumuona mwanae Steve amerudi, alimfata na kumkumbatia huku akimkaribisha ndani ila Steve alikuwa kamavile bado anajishangaa, alimuangalia mama yake na kumuuliza,

    “Mama nimekuwaje mimi kwani?”

    “Kwani vipi mwanangu?”

    "Hata sijielewi mama, nilikuwa naishi kwa mwanamke mmoja sasa nimeshangaa gafla nimeona hapanifai tena pale nikabeba begi langu na kuondoka"

    "Yule mwanamke kakuambiaje?"

    "Simuelewi mama maana huwa analia tu"

    Muda kidogo Dora alitoka kwenye maombi yake ila alipomuona mdogo wake alifurahi sana na kumkumbatia, na muda ule ule akawaomba waende kwa mwanamaombi, mama yao hakupinga na kujiandaa kisha wakaelekea kwa mwanamaombi.

    Walipofika walimkuta Ester akiimba imba na kuwakaribisha vizuri sana,

    "Mama, kwakweli nimeona ukuu wa Mungu. Mdogo wangu huyu karudi na mama yangu pia kakubali kuja huku kwenye maombi"

    "Hiyo ni habari njema, utukufu ni wa Mungu"

    Basi yule mama alianza kufanya maombi pale ila alimuomba jambo moja Dora,

    "Kuna jambo halipo sawa hapa, namuhitaji pia mwanamke aliyekuwa akiishi na mdogo wako kwani anatakiwa kufunguliwa pia"

    Dora hakubisha na muda huo huo aliondoka na kuelekea anapoishi Sia.

    Alifija na kumkuta Sia yupo nje amejiinamia tu, alimshtua na kuanza kuongea nae,

    "Sia, tatizo nini?"

    Macho ya Sia yalivimba, inaonyesha alilia sana ila alipomuona Dora aliongea nae,

    "Dora toka siku niliyogundua kuwa yule George kaathirika sikuwa na raha kabisa, nilirudi hapa nyumbani na kutamani nitembee tu na Steve ili wote tuathirike ila moyo wangu ulikataa hilo, hiyo hali imenitesa sana inafanya nilie kila muda hata hamu ya kula sina, kwenda kupima naogopa, nahofia maisha yangu na maisha ya mwanangu. Sijui hatma yangu jamani"

    "Sia usilie kwani kulia sio suluhisho la tatizo lako, nakuomba twende kwenye maombi kwani maombi ndio silaha ya kila kitu"

    Sia alikubali bila kinyongo chochote na kuondoka na Dora mahali pale na kuelekea kwa yule mama wa maombi.

    Walifika na kumkuta bado akiwafundisha Steve na mama yake ila Sia aliposogea tu kwa huyu mama alianguka chini na kufanya huyu mama kuanza kumuombea, alimuombea kwa muda na kumuacha pale chini, kisha akasaidiana na wakina Dora kumuingiza Sia ndani na kuendelea kuongea nao kwa kuwapa mafundisho ya Mungu.

    Jioni alianza tena maombi kwa Sia na alizinduka muda huu, walikaa na kuongea nae, kwakweli Sia alionekana kujutia vitu vingi sana maishani mwake,

    "Ni kweli nilitamani sana Erick awe mume wangu, toka siku naanza mahusiano na Erick nilikuwa na ndoto za kuwa mkewe. Ndiomana haikujalisha nilimfumania mara ngapi ila nilimsamehe kwani niliamini ni mume wangu, kipindi hiko sikuangalia mwanaume mwingine kwani mategemeo yangu yalikuwa kwa Erick tu. Kitu kilichofanya mimi nipende sana kuwa na Erick ni pesa alizokuwa nazo na muonekano wake yani kwangu ilikuwa ni fahari sana kusema kuwa nina mahusiano na Erick. Kipindi Erick yupo na Erica bado niliamini kuwa atarudi tu kwangu alivyokawia kurudi ndipo niliamua kwenda kwa mganga ila najutia sana kwani nilitakiwa kuelewa tangia mwanzo kuwa Erick hakuwa na nia ya kunioa ila alinitumia kutimiza haja zake tu"

    "Pole binti yangu, usijali kuwa Erick hakupendi sijui nini na nini yani wewe uwe unajua tu jambo moja kuwa Mungu anakupenda sana. Acha kulia sasa, mtazame Yesu msalabani alikufa kwaajili yako"

    "Ila nina ukimwi mimi, nini hatma yangu na mwanangu?"

    "Sio swala la kuhofia wala kuogopa hilo, wangapi wana ukimwi na bado wanaishi vizuri tu. Maisha ni kumtumainia Mungu, na unaweza shangaa Mungu kakunusuru kutoka huo ugonjwa hata kama ulikutana na mtu mwenye ukimwi, uwezo wa kunusurika upo ni mkubwa tu. Kwanza umeonyesha moyo wa utu kuwa ulipogundua kuwa yule mwanaume kaathirika na ulikuwa nae hukutaka tena kumuambukiza huyu kijana asiye na hatia. Mungu anaweza kukunusuru kwenye hilo janga, muamini Mungu na utashinda. Kwasasa nikushauri tu binti yangu uokoke"

    Sia alikubali, mama Dora nae alikubali, Steve pia alikubali basi yule mama aliwafanyia sala ya toba na kuwafundisha maombi kisha kuagana nae, waliahidi kwenda kwenye ibada kesho yake kwani walijihisi kuwa huru kwenye mioyo yao.



    Erick alienda kwao moja kwa moja, na muda huo alimkuta baba yake akiongea na Tumaini pamoja na Tony kumbe aliwakuta nyumbani kwake tena, kwahiyo Erick alifika kwenye mazungumzo yao, mzee Jimmy alipomuona Erick alimkaribisha kwenye kile kikao cha dharula,

    “Erick karibu, unajua kuna mambo nimefikiria kama baba nimeamua kujirudi maana nadhani nitakachokuwa natenda basi hakina matunda, niliwahi kupenda ila sikuwahi kuoa na utu uzima huu nikatamani kuoa ila mwanamke niliyemtamani kumbe na mwanangu ushapenda, kuna mambo nimeyafikiria sana na nimeona ninavyoenenda basi haitakiwi nienende hivyo. Mwanangu hujaoa ila sitaki uishie kama mimi baba yako maana najua mnajua kama baba yenu nimeathirika, sio siri tena ni kweli mimi sio mzima. Upande mwingine mwanangu Tumaini sitaki uishie kama mimi baba yako au uwe kama mama yako, nimekuuliza hapa mara mbili mbili kuwa huyu mwanaume unampenda?Umenijibu ndio, na iwe kweli sio uolewe halagfu atokee mwingine umkimbie kijana wa watu maana nyie wanawake hamtabiriki ila najua kwako ni tofauti mwanangu maana huyo mwanaume mwingine sijui atakubabaisha na kitu gani tena? Kama pesa kwa baba yako ipo, sijui kama mnanielewa lakini!”

    “Tunakuelewa baba”

    “Nataka Erick uoe na Tumaini uoelewe. Tony, upo tayari kumuoa binti yangu Tumaini?”

    “Ndio nipo tayari”

    “Haya nahamia na kwako Erick, linin a wewe utamuoa Erica?”

    “Ndio nilikuja kujadiliana na wewe baba kuhusu hilo swala, nahitaji kumuoa Erica ila sihitaji kuchelewa nahitaji kumuoa haraka iwezekanavyo”

    “Basi namaliza haya majadiliano, jamani Jumamosi ni harusi Erick utamuoa Erica na wewe Tumaini utaolewa na Tony, msiniulize chochote kile maana kila kitu nitasimamia mwenyewe. Tony umenielewa”

    “Nimekuelewa baba”

    “Nimemaliza jamani, Erick jiandae Jumatatu tunaenda kujitambulisha kwakina Erica na kumaliza mambo yote siku hiyo kwahiyo waambie wajiandae na Jumamosi ni harusi. Na wewe Tony kafanye utaratibu kwenu Jumanne uje hapa na mshenga na baadhi ya ndugu zako, mama Tumaini nae atakuja tukamilishe mambo halafu Jumamosi sherehe”

    “Sasa mzee bado sijajua mahali mtanipangia kiasi gani?”

    “Wewe jiandae tu maswala ya mahali tutapanga kiasi gani yasikusumbue kichwa ila jua kwamba Jumamosi sherehe nimemaliza”

    Kisha mzee Jimmy akainuka na kwenda chumbani kwake, kwakweli mzee huyu maneno aliyoongea na Ester yalimuingia sana na alijiona kuwa na makosa mno aliyoyafanya enzi za ujana wake hakutaka yajirudie kwa watoto wake.



    Leo Erica aliachwa nyumbani kwao pamoja na Angel maana mama yake alishamsamehe kwa yale waliyoongea na kupanga na jinsi alivyomuheshimu yule mama Erick.

    "Kesho mwanangu tutafanya kikao cha familia humu ndani maana Erick kasema hataki kukawia kufunga ndoa yenu, anataka birthday yenu ya mwaka huu iwakute ndani ya ndoa kwahiyo kesho tutajadili swala hili. Ila nimefurahi sana leo mwanangu upo nyumbani tena"

    Erica alichekelea tu kwani ndoto yake ilikuwa ni kuolewa na kupata baraka zote toka kwa mama yake na ndugu zake.

    Usiku wa siku hiyo ulikuwa ni usiku wa furaha sana nyumbani kwakina Erica haswaa kwa Erica yani alilala huku akiwa na tabasamu usoni.

    Kulipokucha, mama Erick alimpigia simu Mage na kumpa taarifa vizuri Bite na kumuita Tony ilo wajadili mambo hayo, kisha akaenda kanisani.

    Jioni ya siku hiyo ndio walikaa kikao cha familia ili kujadili kuhusu sherehe ya Erick na Erica, muda huo Tony alikuwa bado hajawasili nyumbani ila waliona ni vyema kuanza kuongelea swala hilo,

    "Jamani Erick kanipigia simu na kaomba harusi yao iwe Jumamosi ijayo"

    "Kheee Jumamosi ijayo, mbona karibu hivyo? Lini tutakusanya michango, lini tutawatangazia watu mbona katushtukiza hivyo!"

    "Jamani Erick kasema hataki kuchelewa, anataka harusi ifanyike mapema, kesho anakuja kulipa mahali yani baba zenu wadogo, wajomba zenu nimewapigia simu yani Erick anataka kila kitu cha posa na mahali amalize kesho na Jumamosi harusi"

    "Jamani mama, hiyo haiwezekani kwakweli. Tutajipanga muda gani jamani eeeh! Halafu na huko kanisani washatangaza?"

    "Mpaka kasema hivyo inamaana tayari, ngoja tumuulize muhusika. Erica hii harusi ya haraka haraka hibi mwanangu mmepanga kweli? Mlifikiria hili na mwenzio?"

    "Hapana mama ila naona Erick anataka tuoane upesi"

    "Sawa, tukubliane jambo moja hakuna cha kukufanyia Sendoff wala kitchen party sawa!"

    Mage akadakia,

    "Afanyiwe ya nini mama na wakati alishaishi na mwanaume, halafu alivyopanga nae hivyo hataka alitegemea nini? Yani hapa ni harusi tu ya fasta"

    "Ila na wewe Mage usikuze mambo, wewe hata harusi hujafanya halafu mwenzio kutokufanyiwa sendoff tu na kichen party basi ndio unaongea weeee hebu acheni haya mambo yaende kama yalivyopangwa, ukoo wetu wenyewe kigeugeu acha Erick ajiamulie kufanya mapema tu."

    Erica aliinuka na kuelekea chumbani kwake na kuacha wakijadili tu.

    Muda kidogo Tony alifika na walimueleze waliojadili ila walishangaa pale Tony alipowaambia kuwa nay eye Jumamosi anamuoa Tumaini, Mage alishangaa sana na kuuliza,

    “Itawezekanaje?”

    “Jamani Yule baba yao kaamua hivyo kasema Erick na Erica wanaoana na mimi na Tumaini tunaoana amesema kila kitu atagharamia yeye”

    “Khee makubwa, na hiyo mahali ya kwakina Tumaini utaenda kulipa nini si ndio kujitia aibu?”

    “Yule mzee kasema nijiandae tu, basi nitajiandaa kwa uwezo wangu na hiyo Jumanne nitapeleka nilichokuwa nacho maana sihitaji kumkosa Tumaini najua pesa sio tatizo kwa yule mzee na hawezi kunipangia mahali ya kunikomesha kwani nay eye anahitaji nimuoe binti yake yani nitatoa mahali kama desturi tu lakini sio kunikomesha”

    “Sawa kama ndio hivyo ila mmmh hizo sherehe sijui jamani”

    Wakajadiliana pale kwa muda kidogo kabla ya kupanga mipango ya kesho ila Bite aliwaomba udhuru kuwa kesho anaenda kushughulikia swala lake la talaka, hawakumzuia ila tu walimwambia kama anaweza kuwahi basi awahi kwenye tukio la siku ya kesho.



    Erica akiwa chumbani kwake alipigiwa simu na Erick, akatabasamu na kuipokea,

    "Yani Erica nishamiss uwepo wako jamani hadi najihisi vibaya mke wangu, nahitaji harusi yetu iwe haraka tuishi wote"

    "Ila Erick, harusi haraka sana hadi nyumbani wamesema hawatanifanyia kitchen party wala sendoff"

    "Kwani kitchen party na sendoff vya nini mke wangu jamani! Kikubwa ni mimi na wewe kuoana, nakuomba Erica tusipeleke mbele harusi sababu ya maswala hayo, nahitaji tuoane mapema. Baba yangu kakubali na kasema atasimamia kila kitu, nahitaji tuoane Erica na tuishi wote sidhani kama hayo maswala mengine yana umuhimu wowote kwetu mpenzi"

    Kwa maneno ya Erick ilibidi Erica asiwe na pingamizi lingine lolote na kukubali tu jinsi Erick anavyosema kwani kwa upande wake kama kikitokea kitu kingine cha kupinga mapenzi yao kingekuwa mzigo mkubwa sana kwake.

    Basi waliagana na kulala huku sura ya Erica ikiwa imejaa tabasamu kubwa.

    Kulipokucha aliamka na kumuona mama yake akiandaa mazingira ya kupokea ugeni ambapo hawakukawia kwani kwenye mida ya saa nne ndugu zao waliwasili na mida ya saa tano wakina Erick waliwasili pia, leo ilikuwa ni ajabu sana kwani mzee Jimmy alikuwa mpole kanakwamba hajawahi kusema anataka kumuoa Erica.

    Wale ndugu walianza kupanga mambo ya posa na jinsi harusi itakavyokuwa na mzee Jimmy aliwahakikishia kuwa sherehe yote ataigharamikia mwenyewe.



    Salma aliamua kwenda hospitali kupima mimba yake na kuanza taratibu za kliniki, alipopimwa aliambiwa kuwa ameathirika alishangaa sana yale majibu maana aliona kama si yeye anayeambiwa habari zile za kuathirika.

    Aliondoka pale hospitali na moja kwa moja alienda kuongea na mamake Rahim, muda huo alimkuta Rahim yupo kwa mamake akiongea na simu, aliweka sauti kubwa, ilionyesha alikuwa akiongea na Babuu,

    "Yani wewe ndugu yangu umeamua kunisaliti jamani kweli? Yani umeenda kuoa wewe wakati huyo Zainabu nilitaka nimuoe mimi!"

    "Sasa kaka lawama za bure hizo, ungemuoaje Zainabu na unajijua wazi umeathirika?"

    Rahim alikata ile simu ila yale maongezi yalisikiwa vizuri sana na mama yake, alimuuliza kwa mshangao,

    "Rahim kumbe umeathirika!"

    Rahim akataka kukataa ila Salma alisogea na kumrushia kile cheti halafu akaanza kusema,

    "Kumbe Rahim umeathirika ndiomana ukasema tumuachishe mtoto kunyonya kumbe ukweli unaujua kuwa umeathirika!"

    Mamake alichukua kile cheti na kukisoma vizuri kwakweli alisikitika sana, na kumuangalia mara mbili mbili Rahim,

    “Kumbe mwanangu kweli ulikuwa muhuni! Nilikuwa nawakatalia wote waliokuwa wanakusema vibaya jamani Rahim, leo umeniabisha na umeenda kumuambukiza Salma asiye na hatia jamani”

    Kwa mara ya kwanza leo Rahim alipiga magoti kumuomba msamaha Salma kwa kumuambukiza ukimwi ila lile lilikuwa pigo kubwa sana kwa Salma kwani hakutegemea jinsi alivyokuwa akijibidiisha kwenye kumpa mume wake mapenzi kumbe alikuwa anauzoa na ukimwi.



    Bite alienda mahakamani na James alienda na kusaini talaka yao ila James alionekana kutokufurahia kabisa swala la wao kuachana.

    James alipotoka hapo alienda nyumbani kwakina Dora Alifika na kumkuta Dora anasoma biblia, alimshangaa sana na kumuuliza,

    "Dora na biblia wapi na wapi jamani!"

    "Kila kitu kinawezekana chini ya jua, tunatakiwa tumtegemee Mungu"

    "Kheee makubwa haya, basi tuachane na hayo. Dora nina mawazo hatari, mke wangu kaniacha, yani leo rasmi tumeenda kusaini talaka sababu tu ya kuathirika"

    "Ila si mlikula kiapo kuwa hakuna cha kuwatenganisha zaidi ya kifo?"

    "Ni kweli ila ukimwi umenitenganisha na mke wangu, Dora ni wapi nitaenda kumaliza haja zangu mimi? Naomba ukaishi nami nyumbani kwangu"

    "James, Dora wa sasa sio Dora yule wa mwanzo. Kitakachonitoa nyumbani na kwenda kuishi na mwanaume ni ndoa na si vinginevyo"

    "Kwahiyo Dora unataka nikuoe?"

    "Nioe ndio, yani ndoa pekee ndio itaweza kufanya niishi na wewe"

    "Sawa hakuna shida, mke wangu nimeachana nae mahakamani, naomba nikaoane na wewe huko huko mahakamani"

    "Sawa ila fata taribu zote kama kuja kwetu utambulike halafu tutaenda kuoana ila pia tunaweza kufungia kanisani"

    "Aaah kanisani mpaka sherehe Dora gharama zingine hizo"

    "Unajua sherehe ni mipango ya watu tu ila kuoana bila sherehe inawezekana, twende tuoane na kuishi kwani ni lazima sherehe? Sio ya muhimu tunaweza kuoana na kuishi vizuri tu bila sherehe"

    James akaona kama ni hivyo basi ni rahisi kwake akamuahidi kwenda na mshenga nyumbani kwao siku ya kesho ili kujaribu kufata zile sheria zinazotakiwa maana kwa wakati huo James hakuona mwanamke mwingine wa kumwambia habari zake za shida ya kimwili zaidi ya Dora.



    Bahati akaona isiwe shida, aliamua kuuza shamba lake moja na kuongezea hela na kununua nyumba ili akiamua kuishi na Fetty basi aishi nae kwenye nyumba nyingine, ila kuna shamba ambalo Bahati hakuligusia hata kuhusu kuliuza hata dada zake walimshangaa ila hawakutaka kumdadisi sana.

    Bahati alikuwa na wazo la kumuoa Fetty ila kuna jambo ambalo lilikuwa likisumbua sana moyo wake na jambo hilo ni kuhusu Erica yani Bahati alihisi hakuna mwanamke atakayeweza kumpenda kama Erica, basi alipokamilisha mambo yake ya kununua nyumba nyingine siku hiyo jioni aliondoka kwao na kuelekea kwakina Erica.

    Alimkuta mamake Erica ndio anasafisha safisha maana wageni walishaondoka kwa muda huo, mama Erica nae alimshangaa kumuona na kumuuliza

    "Wewe kiumbe kumbe upo?"

    "Nipo mama na upendo wangu kwa Erica upo pale pale"

    "Pole sana, yani hapa walikiwepo wageni kwaajili ya sherehe ya Erica. Jumamosi hii Erica na Erick wanaoana"

    "Kheee mama, Erica anaolewa?"

    "Inamaana hujanisikia au kitu gani? Erica anaolewa ndio, yani wewe tafuta ustaarabu mwingine tu"

    "Ila mama nampenda sana Erica"

    Mama Erica alianza kumuonea huruma Bahati na kuongea nae kwa upole,

    "Sikiliza mwanangu, si unampenda sana Erica eeeh!! Sasa mimi nakushauri mwanangu, kama wampenda hivyo Erica basi muache abakie na furaha yake, furaha ya Erica ni pamoja na wewe ukifurahi, Erica akikuona umeoa atafurahi zaidi. Jumamosi ni harusi ya Erica ila onyesha upendo wa kweli kwa Erica kwa kumpongeza, sikia Bahati hutakiwi kuwa na chuki kwa mume wa Erica ila unatakiwa kumfanya ampende zaidi Erica"

    "Ila mama nitawezaje kumpenda msichana mwingine?"

    "Kwani kikubwa ulichokipenda kwa Erica ni kitu gani?"

    "Erica ni msichana mpole, halafu ni muelewa na ana upendo sana yani hata kama hakupendi ila kuna vitu atakufanyia uwezo kuuhisi upendo wake"

    "Basi hata utakayempata utaweza kumtengeneza awe kama Erica, usimfiche kitu mwenzi wako, mwambie unachopenda na usichopenda na hiyo itakusaidia sana katika kusonga mbele"

    Bahati alijaribu kumuelewa mama Erica na hakika alimuelewa kwani alipanga akiondoka hapo basi kesho yake akafanye harakati ili ndoa yake na Fetty iweze kutimia kisha Jumamosi aweze kuhudhuria harusi ya Erica.

    Basi alimshukuru mama Erica na kuondoka zake kurudi kwake kwa muda huo.



    Kesho yake Bahati aliongea na Fetty na kujipanga kwenda kwao ili akafanikishe swala la kuweza kumuoa, maana maneno ya mama Erica yalikuwa yakimuingia akilini mwake kuwa endapo ataoa basi itakuwa ni furaha kubwa sana kwa Erica, kwakweli alipomueleza tena Fetty kuhusu swala la kutaka kumuoa Fetty hakupinga kabisa swala hilo kwani alikubali na siku hiyo hiyo Bahati alienda kujitambulisha nyumbani kwakina Fetty.

    Wakati huo Tony nae alikuwa nyumbani kwa mzee Jimmy kujitambulisha na kufanya taratibu za sherehe ya Jumamosi, muda huo hata kaka yake Tumaini nae alikuwepo kwenye hilo tukio na walivyomaliza kaka wa Tumaini alimtafuta Bite ili wajadiliane nae kuhusu hilo swala,

    “Kuna jambo hapa, kumbe Yule mdogo wangu Tumaini anaolewa na mdogo wako?”

    “Ndio, siku ile nilishtuka kumuona kwenu sababu namfahamu Tumaini yani sijui inakuwaje, mimi na wewe tutaendeleaje sasa?”

    “Kwani kuna tatizo basi! Sidhani kama kuna tatizo mimi na wewe sio ndugu na wale wamependana ndiomana wameoana na sisi na yetu tutafanya sababu tumependana, kuangalia ya watu kutafanya nikae bila kuoa maisha yote”

    “Sawa nimekuelewa, na wewe kwetu utakuja lini Deo?”

    “Aaaah nitakuja tu”

    “Ila subiri kwanza, subiri upepo utulie, nimeachana na mume wangu hivi karibuni tu halafu nionekane napeleka mwanaume mwingine nyumbani itakuwa nimeanza na wewe siku nyingi, subiri upepo utulie na tutaoana”

    Deo alikubaliana na Bite kuhusu hilo kwani aliona ni la maana itaonekana Bite alipanga kuachana na mumewe ili aolewe nay eye kwahiyo hakuona kama ni swala zuri kwakweli, aliona ni vyema kusubiri kama wanavyoshauriwa.



    Siku hiyo Sia alienda kwanza kwa Yule mwanamaombi kuomba nae, na kumwambia kuwa anahitaji kwenda hospitali kuanza kliniki na kupima ukimwi,

    “Sia hebu kuwa na imani kuwa Mungu anaweza, kwanini unaogopa hivyo? Kuwa na imani mwanangu, hujapima una wasiwasi wa bure, mimi naona kuwa Mungu kakuepusha kwenye janga hilo mwanangu, kuwa na amani”

    “Sawa, nashukuru kwa kunitia nguvu”

    Sia alimpigia simu Steve na akaongozana nae kwenda hospitali ambapo walipewa ushauri kwa pamoja na kupima, majibu yakaletwa kuwa hawajaathirika kwakweli ilikuwa ni ajabu sana kwa Sia, yani hakuamini kabisa kuwa amepona toka mikononi mwa George, alijisemea mwenyewe,

    “Kuanzia leo mimi Sia sitafanya tena uzinzi, nimekoma. Bora nife masikini lakini kutumia mwili wangu kwaajili ya kupata kipato hapana kwakweli, siwezi fanya hivyo tena”

    Walivyotoka hapo, walienda moja kwa moja kwa Yule mwanamaombi ili kuongea nae tena.

    Yule mama aliwauliza tu maswali machache,

    “Je mnaweza kuishi pamoja”

    “Ndio”

    “Basi muoane tu ni vizuri zaidi”

    “Ila sina kazi sijui nitawahudumiaje?”

    “Maisha ni kuamua yani usifikirie huwezi, kila kitu kinawezekana, mwanzoni hukuweza sababu akili yako ilichanganywa na madawa ila kwasasa utaweza kujishughulisha na wewe Sia utaweza kujishughulisha pia na mtaendeleza familia yenu”

    Wakakubaliana na huyu mama, ingawa Steve alitambua kuwa Sia alimuwekea madawa ila aliamua kuishi nae moja kwa moja tu na kulea pamoja mtoto wao atakaye zaliwa.

    Basi wakaondoka hapo na kuelekea kwakina Dora ili kuwapa taarifa, walikuta kuna ugeni yani James alikuwa ameenda kuongea na familia ile kuhusu swala lake la kutaka kuoana na Dora, kwakweli Steve alifurahi kusikia hivyo pia na wakawapa habari njema ya majibu kutoka hospitali.



    Kesho yake ilikuwa ni ndoa ya James na Dora mahakamani, walijiandaa vizuri kabisa na kwenda kuongea na mwanasheria wao kuwafungisha ile ndoa.

    Bite alikuwepo mitaa hiyo ya mahakama maana alienda kuonana na Deo, ila alishangaa sana kuona James na Dora wakifunga ndoa, alimuuliza Deo

    “Kwani sheria hapa mahakamani zinasemaje? Hii ndoa mbona haraka hivi, imetangazwa kweli?”

    Deo alimshangaa Bite kuwa anawasiwasi gani kwa James kuoa wakati yeye ndiye aliyeenda mahakamani kudai talaka yake?





    Deo alimshangaa Bite kuwa anawasiwasi gani kwa James kuoa wakati yeye ndiye aliyeenda mahakamani kudai talaka yake?

    Akamuangalia mara mbili mbili na kumuuliza,

    “Hivi si ni wewe uliyekuja kuketa ombi la talaka hapa mahakamani! Si ni wewe uliyesema tumshurutishe mumeo ili asikatae kuja kusaini talaka! Leo vipi tena una mashaka na kuoa kwake?”

    “Hapana ila….!”

    “Ila nini sasa Bite? Ulimpenda mumeo ila mbona ulikuja kudai talaka?”

    “Ameathirika”

    “Sio tatizo, kuna wanaoishi na watu walioathirika, swala la wewe kuja kudai talaka sio kwasababu ameathirika tu ila kuna mambo mengine ambayo huyataki kwa mume wako ndio yamekufanya udai talaka”

    “Ila nimeshangaa yani kuachana tu majuzi halafu leo anaoa kweli?”

    “Ukiona hivyo ujue huyo mwanamke alikuwepo na kumuacha mume wako hakujamkomesha wala nini zaidi kumempa nafasi tu ya kuweza kuishi na Yule amtakaye”

    Bite alikuwa kimya tu kwani alichoambiwa kilikuwa na ukweli mtupu ila hakuweza kukaa hapo kushihudia ndoa ya James na Dora bali aliondoka na kurudi kwao.

    Alienda kwao na kumkuta mama yake ambaye alimueleza kuhusu James kuoa, mama yake alimuuliza,

    “Sasa wewe una wasiwasi gani mwanangu? Kama James anaoa mwache aoe na wewe utapata mume utaolewa si ushaachana na James”

    “Ila mama ni mapema mno, inaonyesha yule Dora alishapanga na James kuoana”

    “Kumbe mwanamke mwenyewe ni Dora! Umesahau mwanangu, si tulimpa wenyewe ushauri hapa James kuwa akamuoe Dora! Basi kafata ushauri wetu”

    “Kwahiyo mama na mimi naweza kuolewa?”

    “Ndio inawezekana, ushaachana na mumeo kwahiyo nafasi ya kuolewa wewe ni kubwa sana. Ukipata mwenzi wako usisit kumleta”

    Bite alifikiria kidogo na akaona ni vyema afanye hivyo kuwa ampeleke Deo nyumbani kwao maana alijikuta kashapata wivu kutokana na harusi ya James na Dora.



    Dora na James walipomaliza waliunana na familia zao ambapo mama Dora aliandaa chakula kidogo cha kula pamoja kama familia kwahiyo walijumuika pamoja na kula chakula kile halafu Dora na James wakaenda nyumbani kwa James sasa, walivyofika mlinzi alimwambia James,

    “Yule mwanamke wako alikuja?”

    “Mwanamke wangu? Kivipi?”

    “Si Yule mama James?”

    “Aaaah alifuata nini sasa jamani, si aliondoka kwa kunitesa sana Yule, si aliondoka bila kuwaza ya mbele, sasa anataka nini tena? Sikia nikwambie, saivi atakayekuja hapa ukiwa unanipa taarifa sema Fulani amekuja maana hakuna mwanamke wangu mwingine zaidi ya huyu niliyetoka kumuoa”

    Mlinzi aliitikia kisha Dora na James wakaingia ndani, na kuanza kupanga yatakayokuwepo, James ndio alianza kuongea,

    “Dora, najua ushahangaika sana, ushatembea na wanaume wengi sana na hadi kuyazoa ya kuyazoa ila bado ukaamua kutulia sasa na kumgeukia Mungu, kwa upande wangu pia nishahangaika sana na sasa naahidi kutulia. Dora, nakuomba mke wangu tutulie ili tuweze kuishi maisha marefu, kwani hata madaktari wanashauri hivi, ukiwa na ukimwi na ili uishi maisha marefu inakupasa utulie, naomba tutulie Dora na letu liwe moja”

    “Sina mpango tena wa kuhangaika, nilikuwa na akili mbovu sana. Sikuhangaika sababu natafuta penzi la kweli hapana yani kuhangaika ilikuwa ni hulka yangu na nilivyojigundua nina ukimwi ndio nikawa moto wa kuotea mbali, nilijua ukipata ukimwi unatakiwa kuusambaza kumbe sivyo, swala la kusambaza ukimwi tunawatesa hata wasiostahili kuteseka, tunawaumiza hata wasiostahili kuumia. Mfano Sia, aliamua kuhangaika ilia pate pesa ya kumlisha yeye na kiumbe na sio kwamba aliamua kuhangaika na wanaume mbalimbali ila alitafuta mmoja wa kumsaidia kulea kumbe Yule mmoja tayari nilishamuambukiza ugonjwa, kwahiyo ningemteketeza Sian a mtoto wake na tena ningemteketeza na mdogo wangu”

    “Na wameponaje wale?”

    “Unajua ukimtegemea Mungu ni vizuri sana, Mungu ndiye hukumu wa haki na si mwanadamu. Mtu yeyote anaposikia Fulani ana ukimwi huwa anakuwa na wazo kuwa mtu huyo ni malaya wakati kuna wengine wanapata ugonjwa bila hata ya kuwa malaya, alikuwa na wa kwake mmoja huyo wa kwake ndio kaenda kuuzoa huko na shida zake. Ila nilichogundua ni kimoja, katika swala lolote badala ya kukaa na kumlilia mwanadamu maana kuna mambo mengi mwanadamu hawezi kukusaidia, mwingine atakuonea huruma, na mwingine atakucheka na mwingine atakusanifu, hayo machozi ni haki kwenda kulia mbele za Mungu maana Mungu ni mwingi wa rehema, amejaa huruma yani Mungu atatuhurumia. Yule mama wa maombi kanifundisha vitu vingi sana, kaniambia hakuna mtenda mema katika dunia ila tumezidiana katika kutenda dhambi, nab ado hupaswi kujiona ni bora kushinda mwenzio mbela za Mungu, kikubwa ni kujishusha alivyonifundisha namna ya kuomba toba kwa Mungu nilikuwa naingia kwenye maombi nikiomba toba na kulia kwa yale niliyoyatenda ila Mungu kamnusuru Sia, Steve na mtoto wao. Nimeunga hoja ya kwamba waishi pamoja, ingawa na madawa sijui nini ila yameisha nab ado Steve amesema ataendelea kuishi na Sia, mwanzoni nilikuwa nalalamika sana ila sikujua kusudi la Mungu, Steve alikuwa hawezi kutongoza, Steve hakuwa na mwanamke kabisa hata mama aliwaza kuwa hajui kama mbele ya safari Steve ataoa ila kamfata mwanamke Yule na mimba kampatia inaonyesha mdogo wangu amekuwa kidume”

    Hapo James akacheka, kuna ujumbe uliingia kwenye simu ya Dora na simu ya James, walianza kusoma na kushangaa kwa pamoja,

    “Kheee Jumamosi ni hasuri ya Erica na Erick?”

    “Ndio nashangaa, halafu Jumamosi si keshokutwa?”

    “Ndio na tumealikwa”

    “Twende James, twende yukashuhudie unajua wale wamepitia misukusuko sana na hata sikufikiria kama wataoana, twende tu hiyo Jumamosi”

    James na Dora walikubaliana kuhudhuria harusi ya Erica na Erick.



    Sian a Steve walivyotoka kwenye harusi ya Dora na James waliamua kwenda kwa mwanamaombi kuongea nae, walimkuta na kuanza kuongea nae ambapo walimwambia lengo lao la kutaka kuoana,

    “Tunahitaji kufunga ndoa mama, hivi itawezekana?”

    “Ndio inawezekana maana kila kitu ni maamuzi tu hata msiwe na mashaka ya aina yoyote, mnataka kuoana lini?”

    “Muda wowote ila hatuna pesa za kufanya sherehe”

    “Kufunga ndoa sio lazima mfanye sherehe, nyie ni kuwa na maamuzi na nia moja tu. Kwenye Biblia mnaweza kuona jinsi gani ndoa ilivyo kitu cha muhimu sana. Kwahiyo mmeamua jamnbo jema”

    Walishukuru sana, kuna ujumbe uliingia kwenye simu zao kuwa Jumamosi ni harusi ya Erick na Erica, kwakweli Sia alimuangalia Yule mwanamaombi na kumwambia,

    “Inawezekana kesho mimi na Steve tukaoana?”

    “Inawezekana ndio, njooni tu mapema niwapeleke kwa mchungaji awafundishe kuhusu ndoa na ndio awafungishe ndoa ila mje na ndugu zenu ambao watakuwa ni mashahidi wa ndoa hiyo”

    “Sawa, hakuna tatizo”

    Wakakubaliana nae kuwa kesho yake wataenda na ndugu zao kwaajili ya kufunga ndoa, na pia Sia alimshirikisha Yule mwanamaombi kuhusu harusi ya Erick na Erica na wote walisema kuwa watahudhuria.



    Salma alikuwa na mawazo sana, na kikubwa alikuwa akimfikiria mwanae tumboni kwani alijua ndio mwisho wa maisha yake, yani alihisi kupata ukimwi basi ndio ameshakufa tayari, Mrs.Peter akaona isiwe shida na kwenda kumtafuta mshauri ambaye pia ni mama aliyeathirika na kuishi na virusi vya ukimwi.

    Basi alifika nae kwake na kumuita Salma akae na huyo mama waweze kuzungumza nae, Salma alienda na Mrs.Peter alimtambulisha Salma kwa Yule mama,

    “Salma, huyu anaitwa Bi.Aisha nimemleta hapa aweze kukushauri jinsi ya kuishi na hiyo hali wala usifikirie kuwa ni mwisho wa maisha, karibu”

    Basi bi.Aisha alianza kuongea na Salma kwa kumsalimia kwanza na kuanza kumuelezea,

    “Salma, unaniona mimi? Hivi ni rahisi kuamini nikikwambia mimi nimeathirika?”

    “Hapana”

    “Sasa mimi nimeathirika nina zaidi ya miaka kumi na sita sasa maana nilijigundua nina ukimwi wakati mtoto wangu ana mwaka mmoja ambaye pia ameathirika na sasa ana miaka kumi na sita kwahiyo mimi ndani ya huu ugonjwa nina zaidi ya miaka kumi na sita, unajua ni kitu gani kinachotufanya tuendelee kuishi kwa muda mrefu na bila kusumbuliwa na magonjwa? Kwanza kabisa ni kumtegemea Mungu, pia kulala vizuri, kupata muda wa kutosha kulala, kuzingatia ushauri wa wataalamu wa afya. Kupata ukimwi sio mwisho wa maisha, ukipata ukimwi usifikirie ndio kifo chako, hapana, yani sio mwisho wa mwaisha mwanangu. Tunaishi nao, tunazunguka nao na tunafanya majukumu yetu kwahiyo usiwe na shaka”

    Yule mama akaanza kumueleza namna anavyoweza kuishi na virusi vya ukimwi,

    “Mwanangu atapona kweli? Nina mashaka kuwa ataupata pia?”

    “Mwanao atapona tu vizuri, cha muhimu wahi kliniki, fata ushauri unaopewa na wanao atapona kabisa”

    “Na kuhusu kunyonya je? Au ndio nimuachishe nikimzaa tu!”

    “Hapana, mtoto unamnyonyesha kama kawaida, ambacho huwa kinasumbua ni pale mtoto akiota meno na kukung’ata wakati ananyonya halafu mdomoni awe na vidonda inakuwa rahisi kupata ugonjwa, ila ipo njia rahisi tu ya kuendelea kumnyonyesha mwanao ingawa una ukimwi na ingawa ameota meno maana maziwa ya mama ni muhimu sana kwa afya ya mtoto”

    “Njia gani hiyo”

    “Unakamua maziwa na mtoto anaendelea kunywa maziwa yako huku huna mashaka ya kumuambukiza na wewe unakula vizuri na kupata muda mzuri wa kupumzika na kumtegemea Mungu tu katika maisha utaona mwanako atakavyokuwa na afya nzuri”

    Huyu mama alimshauri vizuri sana hadi Mrs.Peter alifurahia ushauri wake na kuita watoto wake wengine wapate ushauri pia na wajue jinsi ya kuishi na wale walioathirika kwenye himaya yao, Rahim aliitwa, John na mkewe Neema nao waliitwa kwahiyo walifika na kwenda kumsikiliza bi.Aisha, ambaye aliwaelekeza namna ya kuishi na muathirika,

    “Jamani Ukimwi sio mwisho wa maisha, kupata ukimwi sio mwisho wa ndoto zako, kama ni mama utaendelea kuwa mama na kama ni baba basi utaendelea kuwa baba. Mume wangu alikufa sababu ya kutengwa na jamii na jambo lile lilikaa moyoni mwake, hakuna kitu kinaumiza kwa muathirika kama jamii kukutenga, jamani msitutenge maana na sisi tunaweza kufanya majukumu mnayoyafanya ila tu mtusaidie, mafano umesikia kuna matunda Fulani labda ukila yanaongeza kinga ya mwili ndio vitu vya kuja kutushauri ila sio kumtenga mwathirika, naye ni mwanajamii kama nyie”

    Aliwaelekeza pale na walionekana kuelewa, kuna ujumbe ukaingia kwenye simu ya John, Mrs.Peter na Rahim, walisoma kwa pamoja na kujikuta wakiambiana,

    “Eti Jumamosi ni harusi ya Erick na Erica, tunaambiwa tusikose yani tumealikwa tu”

    Rahim alitabasamu ilibidi wote wamuulize, aliwaambia

    “Wale ni wapendanao, yani wimbo wa Erica ni kumpenda Erick, waache waoane na mimi nitakwenda”

    Wote wakakubaliana kwenda hadi Yule bi.Aisha mtoa ushauri nae alisema kuwa ataenda kwenye harusi hiyo, waliendelea kuongea na kucheka huku wakifurahi.



    Bahati alikuwa kwao na ndugu zake pamoja na Fetty alikuwepo yani kulikuwa kama na kikao kwani hadi Nasma na mdogo wake na mama yao alikuwepo, wakati wanajadiliana pale kuna ujumbe uliingia kwenye simu ya Bahati na Fetty, ila Bahati ndio aliusoma mwanzoni ila ujumbe ule ulionekana kama kubadilisha fikra za Bahati kwani baada ya kuusoma tu, alisema pale kwenye kikao,

    “Jamani kesho naenda kumuoa huyu Fetty, sitahitaji tena ushauri na Jumamosi nitaenda nae kushuhudia harusi ya Erica na Erick”

    Nasma pia alijikuta akitamani kushuhudia harusi hiyo, mwanamke aliyemchukia wala haolewi na Bahati bali anaenda kuolewa na mtu mwingine kabisa, ndugu wa Bahati nao walisema kuwa wataenda, kwahiyo kile kikao wakajikuta wakianza kuzungumzia kuhusu harusi ya Erick na Erica na kusahau hata dhumuni la mikao chao.

    Ikabidi mama Nasma amalizie tu kile kikao,

    “Nasma, hunabudi kukubali kuwa Bahati amuoe Fetty maana hawezi tena kuishi na wewe, Mungu atakujaalia mwanangu na utampata mwanaume mwingine”

    Nasma alikubali ila kishingo upande kwani alikuwa akimfikiria mwanae na maisha atakayoishi baada ya hapo bila mume ila hakuwa na namna zaidi ya kukubali tu.

    Walimaliza kikao na kuanza kutayarisha maandalizi ya kesho maana Bahati alisema kuwa kesho yake lazima amuoe Fetty.

    Na kweli ilipofika Ijumaa kama ambavyo walipanga basi ilifanyika harusi ya Bahati na Fetty na walifurahi tu pamoja na hakuna aliyekuwa na kinyongo kwa wakati huo.

    Baada ya harusi, Bahati na Fetty walielekea kwenye nyumba yao mpya, ila kitu ambacho kilimshangaza Fetty ni siku hiyo usiku kumuoa Bahati amekaa tu akifikiria mambo huku akiandika, hakuelewa anaandika nini na hakutaka kumsumbua pia kwani alijua kwamba kama kuna umuhimu way eye kutambua hilo basi ataambiwa na kama hakuna umuhimu basi hatoambiwa.



    Ilifika Jumamosi, siku ambayo Erica na Erick walikuwa wanafunga ndoa na Tumaini na Tony walikuwa wanafunga ndoa pia kama ambavyo baba yao mzee Jimmy alitaka, maana alihitaji harusi za watroto wake azifanye kwa siku moja na waalike wote wanaowahitaji, mzee huyu hakutaka mchango wa mtu yeyote Yule ila aliamua mwenyewe kufanya harusi za wanae alisema kama mtu hela ya mchango ni bora akawatunze maharusi au anunue zawadi kwaajili ya maharusi ila yeye aliamua kuifanya shughuli mwenyewe.

    Walienda saluni kurembwa, ilikuwa kama Erica ni msimamizi wa Tumaini na Tumaini ni msimamizi wa Erica maana hakutafutwa msimamizi mwingine na kwa upande wa Erick na Tony ilikuwa vile vile,

    Wakiwa saluni, Tumaini alimwambia Erica,

    “Unajua ni maajabu haya yani sikutegemea kama mimi na wewe tutaolewa siku moja na tutakuwa zaidi y ndugu maana wote tumebadilishana, wewe umeolewa na kaka yangu na mimi naolewa na kaka yako”

    Erica alitabasamu tu kwani furaha aliyomuwa nayo moyoni ilikuwa ni kubwa sana, kwakweli walipambwa na wakapambika.

    Baada ya hapo ilikuwa ni safari ya kanisani ambapo Angel na Junior nao walipambwa vizuri na walisimamia vizuri harusi ya watu wale ambapo Mage alikuwa ndio mshika watoto.

    Walienda kanisani na vigelele vilitawala kila kona, na baada ya kanisani sasa, jioni yake walienda ukumbini huko ndio ilikuwa furaha kila kona na watu walikuwa wengi sana.

    Ilikuwa ni kusherekea mwanzo mwisho ila katika tukio ambalo hawakulidhania ni tukio waliloambiwa kuna mtu anataka kusoma ujumbe kwa maharusi wa siku hiyo, Yule mtu alikaribishwa na Mc, wale maharusi walimshangaa sana kwani mtu huyo alikuwa ni Bahati, alifika mbele na kusalimia watu kisha alianza kutoa ujumbe wake,

    “Najua wengi sana mtashangaa imekuwaje kuja kusimama hapa mbele na kutoa ujumbe huu ninaotaka kutoa, kwanza naomba mtambue kwamba sina nia mbaya ila nimekuja kwa upendo tu. Kuna kitu nimejiuliza sana jana usiku na ndio kimenifanya leo nije kuzungumza hapa, nimejiuliza san asana NINI MAANA YA MAPENZI? MAPENZI NI NINI? MAPENZI NI KITU GANI? Nimejiuliza sana ndugu zangu, ila nikasema naomba kupeleka kwa wadau labda watanisaidia kwa kile nilichonacho. Mimi kama Bahati nakiri kwenye umati huu mkubwa kuwa nilimpenda sana Ericana bado nampenda ndiomana nimekuja hapa kwani nimeona kama nampenda basi nimuache afurahi na furaha ya Erica ni kuolewa na Erick, asante Erick kwa kufanikisha hilo. Erica hakunipenda mimi kimapenzi ila alinipenda kama binadamu mwenzie, ila swala la kutonipenda kimapenzi halikumfanya anitenge kwani alinijali na kunithamini na kufikia hata hatua ya kuniokoa kutoka kwenye gonjwa la ukimwi, unaweza sema alifanya yote hayo sababu alinipenda kimapenzi hapana, ila aliniokoa sababu ndani mwake kuna upendo wa dhati na ndani mwake kuna kitu kinaitwa kujali. Naweza sema Erica ni mwanamke wa tofauti sana, na Erick ni mwanaume wa tofauti sana, nilimpenda Erica ila yeye hakunipenda na ikawa ngumu kutimiliza swala la mapenzi, ila Erica na Erick ndio maana halisi ya neno mapenzi kwa nionavyo mimi, nimefikiria na kuchambua nimeona mapenzi ni kupendana, kama mna mengine mtayaongezea ila nimeona mapenzi ni kupendana. Mungu awajaalie Erica na Erick nawaombea mpate watoto mapacha tena wakike na wa kiume nao muwaite Erica na Erick, asanteni”

    Watu walipiga makofi, mama Erica aliinuka kwenye kiti chake na kwenda kumpokea Bahati maana hakuamini kama Bahati angeweza kuongea vitu vya maana kiasi kile, alijua tu angelia lia pale mbele kuwa anampenda sana Erica.

    Basi watu wengi wakafatana na mama Erica kwenda kumsindikia Bahati na kumpongeza.

    Ulifika muda wa watu kwenda kusalimiana na maharusi na kugonga glasi za vinywaji kwa pamoja, ni muda huu ambao Derick alienda pia, ila alipofika pale Erick alimvuta karibu na kumnong’oneza,

    “Sasa kile alichofanya Bahati ndio tunaita uanaume yani kule ndio kuwa mwanaume unakubaliana na matokeo sio mwanume unakuwa na wivu na dada yako”

    Derick aliondoka na kurudi kwenye kiti ambapo pembeni yake kuna mdada alikuwa akivutiwa nae aliamua kutoa swaga zake,

    “Nakupenda, natamani na mimi ifikie wakati nifunge ndoa”

    “Ila umenipenda lakini mimi ni mjamzito”

    “Ooh sawa, ila hata hivyo sidhani kama utanikubali maana mimi ni muathirika”

    Yule dada akamwambia,

    “Natamani kupata mume wa kunioa sana, na wala sijali kuhusu kuathirika kwako kama utanikubali na mimba yangu”

    “Kweli umenikubalia? Unaitwa nani?”

    “Naitwa Siwema, na wewe je?”

    “Naitwa Derick, naomba twende kwa mama yangu pale akufahamu Siwema tafadhali”

    Basi Derick na Siwema waliinuka na kwenda alipokaa mama yake Derick.

    Kuna meza alikaa James, Dora na watu wengine akiwemo George, Dora alimtania George,

    “Na wewe utaoa lini eeeh! Au bado unasubiri kuoa bikra?”

    “Aaah Dora mbona hilo wazo limepotea kwangu sema tu sijampata wa kumuoa”

    Pembeni yake kulikuwa na binti aliyebeba mtotot mdogo mikononi, alimwambia George

    “Nioe mimi basi”

    James na Dora walicheka kisha Dora akamwambia George,

    “Eeeh mke huyo kajitokeza”

    George alimuangalia Yule mwanamke na kumwambia,

    “Dada, mimi natafuta muathirika mwenzangu maana mimi nina ukimwi”

    Nipo tayari kuishi na wewe hivyo hivyo”

    “Unaitwa nani dada?”

    “Naitwa Nasma”

    Dora akajaribu kumshauri Nasma,

    “Usiharakie sana kuolewa angalia maisha yako na mtoto, usikimbilie kuolewa mdogo wangu. Unatakiwa kuangalia maisha yako yani ukauzoe ukimwi sababu ya kutamani kuolewa! Hapana kwakweli, jifikirie mara mbili”

    Ujumbe ule ulimuingia Nasma ingawa alikuwa na hamu sana ya kupata mume na kuolewa tu.



    Basi walicheza na kusherekea hadi muda chakula ambapo watu walikula na kusaza na muda wa zawadi ulivyofika watu walianza kupeleka zawadi zao ambapo Bahati alienda na kumkabidhi Erica hati ya shamba na kuongea kidogo,

    “Napenda kutoa zawadi hii ya shamba kwa Erica maana ulikuwa ni mpango wangu wa muda mrefu sana, siwezi kuacha kwakweli. Shamba hili likawe faida kwa Angel, nampenda sana huyu mtoto na nilisema kuwa napenda sana kuwa baba yake sema mambo yaliingiliana ila bado sio kwamba ni mwisho wa kuwa familia, nampenda na ninatoa shamba hili kama zawadi kwake, naomba mpokee zawadi hii”

    Bahati alijua kama akisema ni zawadi kwaajili ya Erica basi Erick anaweza kuigomea kwahiyo akasema ni zawadi ya Angel, muda kidogo Rahim nae alienda kutoa awadi yake ambayo pia aliielekeza kwa Angel, alikuwa na hundi ya milioni kumi na tano na kusema,

    “Nakumbuka Erica uliwahi kuniomba pesa hii ili ufanyie biashara kwaajili ya kulea vyema mtoto wetu ila sikutaka kwani nilijua nakukomesha na lazima utanyenyekea sana kwangu, sikuwa na haja na wewe sababu nilikuwa na wanawake wengine ambao nilikuwa naona wananifaa kumbe sikuangalia ya mbeleni, natoa hundi hii ukaiweke kwenye akaunti ya Angel na ajue kwamba nimetubu na nitamjali”

    Erica alipokea ile hundi kwa uzuri kabisa sema hawa watoa zawadi walikuwa wakiongea moja kwa moja na wahusika kwahiyo watu walikuwa wakisikia ni wale wa karibu tu.

    Basi muda wa zawadi uliisha na walikuwa wakicheza tu, kisha ukawa muda wa kuaga wale maharusi ili wakapumzike, Mc akawataka wale mabibi harusi waeushe maua akiamini kuwa atakayedaka ndio harusi inayofatia.

    Basi Erica alirusha ua lake na likadakwa na Bite, walifurahi sana na kuona kumbe harusi ya Bite inanukia, kisha Tumaini nae akarusha ua lake, likadakwa na bi.Aisha, watu walicheka sana kuona bi.Aisha kadaka lile ua maana walimuona ni mtu mzima, walicheka sana. Mzee Jimmy alimvuta pembeni bi.Aisha na kumuuliza,

    “Na wewe unahitaji kuolewa?”

    Bi.Aisha alicheka tu, kisha mzee Jimmy aliendelea kuongea,

    “Niambie ukweli una mpango wa kuolewa? Maana hata mimi nahitaji kuoa ila nimeathirika”

    “Na mimi ni muathirika pia”

    Mzee Jimmy alimsogelea bi.Aisha na kumkumbatia kisha akamwambia,

    “Wewe utakuwa mke wangu”

    Watu waliowaona walicheka sana.

    Kisha maharusi wakaruhusiwa kwenda kupumzika, ila kabla hawajaondoka walimuomba Yule mama wa maombi aseme neno moja nae alisema,

    “Alichokiunganisha Mungu basi mwanadamu asikitenganishe”

    Ukumbu wote ulisikika ukisema,

    “Ameeeen”

    Na vigelegele, nderemo na vifijo vilisikika kisha maharusi ndio wakaondoka kwa furaha.



    Siku ya birthday ya Erick na Erica ni siku ambayo waliamua kwenda kupima ule ujauzito ambao Erica alikuwa nao kwa ultrasound, na furaha iliongezeka maradufu baada ya kuona kuwa mimba ya Erica ilibeba mapacha wa kike na kiume. Erick alifurahi sana na kumkumbatia Erica kwa furaha kwani aliona kuwa ile ni zawadi kubwa sana kwenye siku yao ile muhimu.



    ---------MWISHO---------









0 comments:

Post a Comment

Blog