Simulizi : Mke Wangu Juliana
Sehemu Ya Tatu (3)
Walizungumza mengi, John hakutaka kujificha, alimwambia msichana huyo kuwa alihitaji sana kupata ajira yenye mshahara mzuri kwani biashara ya kuzunguka mitaani akiwa na kapu la samaki ilimchosha mno.
“Una elimu gani?” aliuliza Deborah huku akimwangalia John.
“Nilisoma mpaka kidato cha pili, wazazi wakakosa ada hivyo nikabaki nyumbani!” alijib.
“Pole sana! Nitaangalia nitakusaidia vipi! Ungependa kuwa na kazi ipi?”
“Kiukweli yoyote ile, najua siwezi kupigwa na kiyoyozi, kazi yoyote nitashukuru Mungu!” alisema John.
Deborah akajisikia huruma sana, moyo wake ulichoma kupita kawaida. Alimwangalia John, ni kweli alinyesha kuhitaji msaada mkubwa.
Hata kwa jinsi aivyovaa, alionekana kuwa na maisha ya chini mno. Akajiahidi kumsaidia kwa hali na mali, hivyo wakaagana na kurudi majumbani kwao.
Siku hiyo Deborah akaanza kumfikiria John, hakuamini kama mwanaume huyo alitoka jijini Dar es Salaam. Aliwafahamu watu wa huko, wanapokwenda mikoani huwa tofauti, wanaringa, wanajiona wao ndiyo wao, maisha mazuri lakini huyu ambaye alikutana naye kipindi hicho alikuwa tofauti kabisa.
“Kwa nini amekuwa hivyo?” alijiuliza.
Siku iliyofuata akaondoka na kwenda kazini, alipofika huko, kitu cha kwanza kilikuwa ni kuzungumza na bosi na kumwambia kilichokuwa kikiendelea kwamba alifanikiwa kuonana na kijana mmoja ambaye aliguswa sana kumsaidia hivyo kama kulikuwa na kazi yoyote ile ya kufanya hapo, alikuwa tayari.
Bosi huyo, Bwana Masako alimwamini sana Deborah, alikuwa mfanyakazi muaminifu, aliyekuwa akijituma kuliko hata wafanyakazi wengine, na ili kumfurahisha, akamwambia basi azungumze na kijana huyo, kulikuwa na kazi ya kufagia katika jengo la kampuni hiyo kwa sababu mtu aliyekuwa akiifanya kazi hiyo alitarajiwa kuondoka kuelekea jijini Mwanza kwa ndugu zake.
“Nashukuru sana bosi! Nitawasiliana naye na kesho tu atafika mahali hapa,” alisema Deborah huku akionekana kuwa na furaha tele.
Alipotoka tu kitu cha kwanza kilikuwa ni kumpigia simu John na kuanza kuzungumza naye. Alimwambia kilichokuwa kimeendelea, kwamba kazi ilipatikana na hivyo alitakiwa kufika huko kwenye kampuni hiyo kwa lengo la kuanza ajira yake mpya.
John alichanganyikiwa, alipagawa, hakuamini alichokisikia, aliuliza mara mbilimbili kama ni kweli ama Deborah alimdanganya, msichana huyo alimwambia ni kweli na hivyo alitakiwa kwenda huko.
“Mungu akubariki sana!” alisema John.
“Amen!” alisema Deborah.
Siku iliyofuata asubuhi na mapema John alikuwa ofisini hapo hata kabla ya wafanyakazi. Kwa jinsi alivyokuwa kila mmoja aliamini alikuwa na maisha mabovu mno, alivaa kama jamaa fulani la mitaani na si kama wao ambao waliingia huku wakiwa na suruali za vitambaa, mashati huku wakichezesha funguo za magari.
Pamoja na umasikini wake lakini John alikuwa na heshima kubwa, kila aliyekuwa akiingia mapokezini, alisimama na kuwasalimia kwa kuwashika mikono. Alikuwa mnyenyekevu kiasi cha dada wa hapo mapokezi kushangaa.
“Unaitwa nani vile?” aliuliza dada huyo.
“John Chagala!”
“Unaishi wapi?”
“Mwanga Makaburini!”
“Sawa!”
Baada ya hapo, dada yule akaendelea na kazi zake mpaka muda ambao Deborah akaingia ofisini humo. Alipomuona tu, akaonyesha tabasamu, haraka sana John akasimama na kumsalimia kwa kupeana naye mikono.
“Umefika muda sana?” aliuliza.
“Kabla ya mtu yeyote humu?” alijibu John huku akiwa na furaha tele.
“Umehudumiwa?”
“Yeah! Nashukuru nimehudumiwa vizuri!”
“Na umekula?”
“Hapana!”
“Hebu twende nje tukale!” alisema Deborah.
Akamchukua kijana huyo na kuondoka naye kwenda kwenye mgahawa uliokuwa hapo na kunywa chai. Alishangaa, ni kweli aliwahi kuishi na watu wengi lakini kwa jinsi msichana huyo alivyokuwa mnyenyekevu kulimfanya kuwa na mshangao mkubwa mno.
Alichokuwa akikiamini ni kwamba wanawake wengi warembo walikuwa na mapozi, maisha fulani ya nyodo lakini lililomshangaza kabisa ilikuwa ni tofauti na huyo Deborah.
“Ila utatakiwa kufanya kazi sana,” alisema Deborah huku akimwangalia John.
“Kwa hilo usijali dada yangu!”
“Ukiwa mvivu utaniondolea uaminifu kwa bosi, kujitoa kwako kwa nguvu kubwa kutanifanya nizidi kuaminika! Naomba usiniangushe,” alisema Deborah.
“Sawa haina shida. Ninakuahidi sitokuangusha!” alisema.
Walikunywa chai na walipomaliza, akamchukua na kumwambia amsubirie bosi ambaye alikuwa na kawaida ya kuchelewa kila siku.
Hilo halikuwa tatizo, John akamsubiri mapokezi na alipofika majira ya saa nne, akafuatwa na Deborah ambaye alimchukua na kumpeleka ofisini kwa bosi na kuanza kumtambulisha.
Alimmwagia sifa nyingi kwamba hakuwa mvivu, alikuwa mfanyakazi aliyejitoa ambaye kama angepewa nafasi kufanya kazi kwenye ofisi hiyo basi ingekuwa imepata mmoja wa wafanyakazi bora.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Elimu yako?” aliuliza Bwana Msako.
“Kidato cha pili!” alijibu John.
“Yaani hukufika hata kidato cha nne?” aliuliza.
“Ndiyo bosi!”
“Sababu?”
“Wazazi hawakuwa na pesa!”
“Pole sana!”
“Ahsante!”
Siku hiyo ndiyo ambayo John akaanza kufanya kazi ya ufagiaji ndani ya kampuni hiyo. Ni kweli biashara yake ya samaki ilikuwa ikimuingizia kiasi kikubwa cha pesa kuliko mshahara ambao aliahidiwa hapo lakini hakutaka kujali sana, kiu yake kubwa ilikuwa ni kuwa karibu na msichana Deborah tu.
Akawa na uhakika wa kumuona kila siku, moyo wake ulikuwa na furaha tele, alijisogeza kwa msichana huyo kiasi kwamba wakawa karibu mno na kila siku muda wa kwenda nyumbani, ilikuwa ni lazima amchukue John na kumpeleka mpaka Mwanga na kurudi zake nyumbani kwani hapakuwa mbali na mahali alipokuwa akiishi.
“Ulifanyaje mpaka kufanikiwa hivi?” aliuliza John.
“Ni kufanya kazi kwa bidii tu ila nitahitaji kufanya biashara zangu pia,” alijibu msichana huyo.
“Biashara gani? Inamaanisha mshahara hautoshi?” aliuliza John.
“Mshahara hauwezi kutosha! Na huwezi kufanikiwa kwa kutegemea pesa ya mshahara tu!” alijibu msichana huyo.
“Unamaanisha nini?”
“Ushasikia mtu amekuwa tajiri kwa kulipwa mshahara tu?”
“Hapana!”
“Basi ni lazima tuwe na biashara zetu, yaani lazima uwe na vyanzo vingi vya kuingiza mapato!” alisema msichana huyo.
“Oh!”
“Ndiyo hivyo!”
“Nashukuru kwa kunifumbua macho!”
“Na kwa nini umeacha biashara yako?”
“Ni kwa sababu ninahitaji kuajiriwa!”
“Unahisi utaingiza pesa nyingi kuliko kuuza samaki?”
“Hapana! Ila sitokuwa nazurura sana, inachosha, mwisho nigongwe na gari nife!” alisema John, wote wakaanza kucheka.
“Ila ungebaki kwenye biashara ingekuwa safi sana!” alisema Deborah.
“Najua ila kuna jingine kubwa!”
“Lipi?”
“Nilihitaji kuwa karibu na wewe!”
“Kuwa karibu na mimi?” aliuliza Deborah huku akionekana kushtuka.
“Ndiyo!”
“Kwa sababu gani?”
“Nakupenda!”
“Umesemaje?” aliuliza Deborah huku akipunguza mwendo wa gari!
“Ninakupenda!”
“Mimi?”
“Ndiyo!” alijibu msichana huyo, akasimamisha gari kabisa na kumwangalia John.
Deborah akabaki akimwangalia John, hakuelewa alichokuwa amekizungumza, wakati mwingine alihisi kama mwanaume huyo alikuwa akimtania.
Alimwangalia usoni, alionekana kumaanisha kile alichomwamia. Haikumuingia akilini mwake, ilikuwaje amwambie alikuwa akimpenda? Alimchukulia kama mfanyakazi mwenzake lakini pia kwa muonekano wa mwanaume huyo, hakustahili hata nusu kuwa naye.
“John!” aliita Deborah huku akimwangalia usoni, kwa kiasi fulani John akaonyesha kutokujiamini.
“Naam!” akaitikia.
“Umesemaje?” aliuliza.
John akabaki kimya, si kwamba Deborah hakusikia alichoambiwa, alikisikia sana ila alihitaji kuona ni kwa jinsi gani mwanaume huyo alikuwa akijiamini kumwambia neno lile lile tena na tena.
John akavuta pumzi, alimwangalia Deborah, uzuri wa msichana huyo uliendelea kumchanganya zaidi. Kubaki kimya pasipo kurudia neno lile ungeonekana kuwa udhaifu mkubwa, kama kweli alikuwa akijiamini ilikuwa ni lazima amwambie tena.
“Ninakupenda!” alisema.
“Unamaanisha ama?” aliuliza.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Deborah! Najua unahisi ni utani kwa sababu tu muonekano wangu na wako ni vitu viwili tofauti. Nimetamani nikwambie hiili kwa kipindi kirefu mno, nimetokea kukupenda tangu siku ya kwanza nilipokutia machoni mwangu, hicho ni kitu ambacho siwezi kukaa kimya huku kikinifurukuta moyoni mwangu,” alisema John huku akimkazia macho msichana huyo.
“Hapana!”
“Unamaanisha nini? Kwamba hunitaki?”
“Simaanishi hivyo!”
“Unamaanisha nini?”
“Natakiwa kupata muda wa kufikiria sana kuhusu hilo, si unajua mambo ya uhusiano si ya kukurupuka,” alisema Deborah.
John akashusha pumzi, siku zote aliamini kwa mwanamke yeyote ambaye alimpa muda mwanaume wa kujifikiria, asilimia tisini na tisa walikuwa wakikubaliana na kilichosemwa ila hawakutaka kuwajibu haohapo.
Moyo wa John ukaburudika, akajisikia amani moyoni mwake, mapenzi aliyokuwanayo kwa msichana huyo yalizidi kuongezeka hivyo baada ya kumaliza wakaendelea na safari.
Wakafika nyumbani kwao, akateremka na kuagana naye kisha kuingia ndani.
Akajilaza kwenye godoro lake, moyo wake ulikuwa na furaha kupita kawaida, kila kitu kilichotokea kilionekana kama ndoto fulani ambapo baada ya muda angeamka na kujikuta akiwa kitandani.
Huo ndiyo ulikuwa mendelezo wa ukaribu wao, kila walipokuwa wakikutana maneno ya John yalikuwa yaleyale kwamba alimpenda sana Deborah.
Alimsifia kwa mambo mengi, uzuri na mambo mengine ambayo yalimfanya msichana huyo kuwa na furaha tele. Ni kweli kwenye maisha yake aliwahi kukutana na wanaume wengi wa tofauti lakini hakuwahi kukutana na mwanaume aliyekuwa na maneno matamu kama huyo.
“Una macho mazuri sana, Mungu amekupendelea kwa kila kitu,” alisema John huku akimwangalia Deborah aliyekuwa akitabasamu tu.
“Kuna mambo mengi ambayo Mungu akitupa uhuru wa kuchagua tunaweza kuyachagua, ila kwangu, hakika nitakuchagua wewe maisha yangu yote,” alisema John.
“Kwa nini?”
“Kwa sababu u mzuri, umekamilika, msichana uliyeufanya moyo wangu kukamilika kabisa. Nitakapokuwa na wewe sitohitaji kitu kingine zaidi ya mapenzi yako.
Kama nitahitaji mwanamke mwenye sura nzuri, basi ni wewe, mwanamke mwenye umbo zuri, basi ni wewe na kama nitahitaji mwanamke mwenye tabasamu pana la kutibu magonjwa yote, basi sitosita kukuchagua wewe,” alisema John, hapohapo akaushika mkono wa Deborah.
“Ninakupenda!” alisema.
“Naelewa John.”
“Natamani uingie moyoni mwangu uone ni kwa jinsi gani ninakupenda. Unanifanya nijione kuwa mwanaume niliyekamilika kuwa na wewe,” alisema John.
Wakati huo waliokuwa wakiongea walikuwa kwenye mgahawa wa ofisini kwao. Kila mmoja aliyekuwa akiingia humo walikuwa wakiwaangalia.
Hawakuamini kama msichana mrembo kama alivyokuwa Deborah alikuwa akizingumza na John kwa ukaribu ule, yaani kijana yule ambaye ni mfagiaji tu hapo, masikini, choka mbaya ndiye aliyekuwa akimfanya Deborah kutabasamu namna ile.
Walishangaa lakini hawakujua ni maneno matamu kiasi gani aliyokuwa akiambiwa mahali hapo. Walikaa mpaka baada ya kumaliza kula chakula ndipo wakaondoka kuendelea na kazi zao kama kawaida.
Deborah hakuwa na presha ya kumwambia John kama alikubaliana naye ama la! Moyo wake ulikuwa na maswali mengi juu ya kijana huyo.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ni kweli alihisi kabisa kuwa na hisia naye za kimapenzi lakini hakujua kama alitakiwa kuwa naye ama la. Kwa muonekano wa harakaharaka John alikuwa na kila sifa ya kuwa naye lakini katika maisha halisi hakustahili hata kuwa naye.
Walikuwa watu wawili tofauti, hawakufanana, alikuwa na pesa, alipendeza, alipenda maisha mazuri lakini kila alipomwangalia John alikuwa mwanaume tofauti kabisa, masikini, asiyekuwa na kitu.
Japokuwa alikuwa na pesa lakini yeye kama mwanamke alihitaji kutumia pesa za mwanaume wake.
Huyo John mshahara aliokuwa akilipwa ulikuwa chini mara nne ya alivyokuwa akilipwa, hata kama siku angemwambia nitoe mtoko wa usiku, basi asingeweza kugharamia kitu chochote kile.
“Lakini mapenzi si pesa,” alisema Deborah huku akionekana kujifikiria sana chumbani kwake.
“Mwanaume anaweza kuwa na pesa, akakupa na ukatumia maisha yako yote lakini bado ukakosa mapenzi,” alijisemea.
Siku hiyo hakuwa na uamuzi wa moja kwa moja kwamba ni kitu gani alitakiwa kufanya. Moyo wake ulimpenda mno John pasipo kujali hali aliyokuwepo nayo.
Ni kweli hakuwa na pesa, alichokigundua kulikuwa na wanaume wengi waliokuwa na pesa nyingi lakini hawakuwa na mapenzi hata kidogo.
Kwa kipindi hicho alichokuwa akikihitaji kilikuwa ni mapenzi na si pesa. Kulikuwa na wanaume wengi waliokuja, waliomchukua na kufanya naye ngono lakini mwisho wa siku walimuacha na kuendelea na maisha yao.
Kwa maana hiyo walikuwa na pesa lakini walikosa mapenzi mioyoni mwao. Huyu wa kipindi hiki aliyekuja katika maisha yake hakuwa na pesa kama hao wengine lakini alibarikiwa kuwa na mapenzi.
Alimpenda, alimuonyesha mapenzi na kuufanya moyo wake kuwa na furaha mno na mwisho wa siku akajisemea basi acha awe naye, kama Mungu hakumbariki pesa basi angembariki siku zijazo, ila yeye alitakiwa kuutekeleza wajibu wake wa kumpenda kama alivyotakiwa kufanya.
Siku mbili mbele akaamua kumwambia John kwamba alikubaliana naye na hivyo kuwa wapenzi.
“Nimekukubalia, ila naomba unisaidie kwa kitu kimoja,” alisema Deborah huku akimwangalia John.
“Lolote utakalo mpenzi wangu!”
“Utanipenda maisha yako yote!”
“Huo ni wajibu wangu, nitakupenda zaidi ya ninavyokupenda sasa hivi!” alisema John.
“Kweli unaniahidi?”
“Bila shaka mpenzi! Nitakupenda hata kama sitokuwa na kitu!” alisema John na kutoa tabasamu, hakuishia hapo, akambusu msichana huyo shavuni, ukurasa mpya wa mapenzi ukafunguliwa baina ya watu hao wawili.
.
.Moyo ulipenda, ulithamini na kujitoa kwa mwanaume mmoja ambaye hakuonekana kumtaka hata kidogo. Moyo ulichoma, ulikuwa na maumivu makali ambayo hakuwahi kuyafikiria hapo kabla.
Mawazo juu ya John hayakutoka kichwani mwa Juliana, alimpenda mwanaume huyo, alipatana nafasi ya kuongea naye lakini alishindwa kabisa kumwambia kile kilichokuwa kikiendelea moyoni mwake.
Hivyo akabaki akiumia kimya kimya, alipata maumivu pasipo dawa yoyote ile. Moyo wake ukavunjika, furaha ikamtoka hasa baada ya kusikia tetesi kwamba Deborah alikuwa akitoka kimapenzi na John.
Hizo zilikuwa tetesi tu zilizokuwa zikisikika kanisani, hazikuishia hapo bali wale wambeya waliwapa taarifa jinsi mapenzi hayo yalivyoanza, Deborah alivyomchukua John na kwenda kumuombea kazi ofisini kwao.
“Alikwenda kumuombea kazi?” aliuliza Juliana huku akionekana kutokuamini.
“Ndiyo! Yaani kweli kampenda mwanaume yule, au kwa sababu ametoka Dar es Salaam?” aliuliza msichana mwingine.
“Labda!”
“Lakini atawezana na Deborah”
“Kwa nini?”
“Jamaa nasikia masikini, hana hata pesa, amepanga, analala chini, yaani chumbani kwake hana hata ndoo ya maji,” alisema msichana huyo.
“Watawezana, si wamekubaliana lakini!”
“Mh Sidhani!”
Japokuwa Juliana aliendelea kusikia mambo kuhusu wawili hao lakini moyo wake ulikuwa na maumivu makali. Hakuamini kama yeye ndiye aliyekuwa akipitia mambo yote hayo, lile tonge alilokuwa akilitamani siku zote lilipokonywa akiwa karibu kabisa kulila.
Akakata tamaa kwamba asingeweza kumpata mwanaume huyo tena. Kila alipokwenda kanisani na kuwaona wawili hao wakiwa pamoja aliumia kupita kawaida, alitamani yeye awe na John lakini si kumuona akiwa na mwanamke mwingine.
Siku zikazidi kwenda mbele, mapenzi ya watu hao yalizidi kunoga. Deborah hakutaka kuona mambo hayo yakifanyika kimya kimya hivyo alichoamua ni kumshirikisha mama yake juu ya jambo hilo.
“Ni yule kijana wa Dar es Salaam?” aliuliza mwanamke huyo huku akionekana kushangaa.
“Ndiyo!”
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nimesikia yule kijana ni masikini! Ni kweli?” aliuliza mama yake.
“Kwa maana gani?”
“Hana pesa! Amepanga, maisha yake ni hohehahe!” alisema mwanamke huyo.
“Lakini mama.......”
“Ni kweli?”
“Ndiyo! Ila ninampenda!”
“Halafu atakulisha nini?”
“Mama lakiniiiiiiiiii....”
“Deborah! Hivi ni lini utakua?”
“Lakini mama kama watu wenye pesa wenyewe wamenitesa, waliniahidi kunioa na hawakufanya hivyo, kwa nini niendelee na kuwa watu wenye pesa?” aliuliza msichana huyo.
Mama yake alishindwa kuelewa, kwake haikumuingia akilini kwamba binti yake aliyekuwa akimpenda na kumtegemea alihitaji kuwa na mwanaume asiyekuwa na pesa.
Alijua ni kwa namna gani alikuwa msichana mrembo, kwa jinsi alivyokuwa tu alitakiwa kuwa na mwanaume aliyekuwa na pesa ambae angempa kila kitu alichokuwa akikihitaji.
Suala la John halikumuingia kichwani mwake hata kidogo, hakutaka kukaa nalo moyoni alichokifanya ni kumwambia mume wake juu ya kile kilichokuwa kikiendelea.
“Nilikuwa nasikia tu kanisani, kumbe ni kweli?” aliuliza mzee Abraham.
“Ndiyo! Ameniambia, moyo wangu umeteteka mno, hivi kweli Deborah anataka kuolewa na yule kijana, ambaye hana kitu kabisa?” mama yake aliuliza huku akionekana kushangaa.
“Haiwezekani! Nimemuhangaikia sana binti yangu, hawezi kuolewa na huyo kijana. Hebu niitie,” alisema mzee huyo huku akivua miwani yake na kuiweka mezani, kichwa chake kilichanganyikiwa, maneno aliyoambiwa alihisi kabisa yaliingia mpaka ndani ya moyo wake na kuuvunjavunja kupita kiasi.
*
*
*
Kama kupenda Deborah alimpenda sana John, alijitahidi kumuonyesha kila aina ya upendo lakini wazazi wake walimwambia hakutakiwa kuwa naye kwa sababu hakuwa na pesa.
Ni kweli John hakuwa na pesa lakini moyo wake ulijawa mapenzi mengi yaliyomfanya kuchanganyikiwa. Mwanaume huyo alitamani sana kumuoa lakini aliona kabisa jambo hilo lingeshindikana kabisa.
Alichokifanya ni kwenda kuzungumza na mchungaji ili amwambie kila kitu kilichokuwa kimetokea. Kweli akawasiliana naye na kuomba miadi ya kukutana na kuzungumza.
Wakakutana ofisini kwa mchungaji huyo na kuanza kumwambia kila kitu.
Mchungaji akakaa kimya, alikuwa akimsikiliza Deborah alivyokuwa akimwambia kuhusu maisha yake na John, jinsi mapenzi yalivyompelekesha kupita kawaida na wazazi wake kukataa kuolewa naye.
Moyo wa mchungaji ulimuuma mno, hakuamini kama kweli bado kulikuwa na wazazi wa aina hiyo ambayo hawakutaka mtoto wao aolewe na fulani kwa kuwa tu hakuwa na maisha mazuri waliyokuwa wakiyahitaji.
“Nitazungumza nao!” alisema mchungaji.
“Hapana mchungaji! Wazazi wangu hawatojisikia vizuri!” alisema msichana huyo.
“Kwa hiyo unataka nifanye nini?” aliuliza.
“Uongee na John!”
“Nimwambiaje?”
“Kwamba wazazi wangu hawataki anioe!”
“Kwa nini usiende kuzungumza naye wewe mwenyewe?” aliuliza mchungaji.
“Siwezi! Nahisi nitaumia sana, sipendi kumuona akiwa kwenye moyo wa huzuni! Naomba unisaidie,” alisema msichana huyo, machozi yakaanza kujikusanya machoni mwake na hatimaye kuanza kulia.
Mchungaji alimbembeleza kumtaka anyamaze, aliyajua maumivu yake, jinsi alivyokuwa ameumia kwa wakati huo lakini alimtia moyo kwamba kuna siku wazazi wake wangekubaliana naye na hatimaye uchumba ungetangazwa na watu hao kuoana.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya kumaliza akaondoka, haraka sana mchungaji akampigia simu John na kuomba kuonana naye. Ilikuwa ni lazima iwe haraka kwa sababu muda huo alikuwa na hamu ya kuliongelea jambo hilo.
Kuonana haikuwa tatizo, kwa sababu ilikuwa ni Jumamosi, wakaonanana na kuanza kuzungumza. Walianzia mbali kabisa lakini mwisho kabisa akaanza kumwambia kila kitu kilichokuwa kimetokea.
John alikuwa kimya kumsikiliza, kile alichokisikia kiliuumiza moyo wake, alisikia maumivu ambayo aliamini hakuwahi kuyasikia hapo kabla.
Alijitahidi kutoa tabasamu usoni mwake lakini ukweli ndani ya moyo wake ulikuwa ukiuma, ulichoma kama pasi. Baada ya kukaa kwa dakika fulani na kuongea, John akaulizwa kuhusu msimamo wake.
“Kiukweli ninampenda sana Deborah!” alisema John huku akimwangalia mchungaji.
“Kwa hiyo tufanye nini?” aliuliza mchungaji.
“Naomba nikaonane na wazazi wake!”
“Kuonana na wazazi wake?”
“Ndiyo! Nitahitaji kuzungumza nao kuhusu jambo hili!” alisema John huku akimwangalia mchungaji.
Hilo halikuwa tatizo ila mchungaji alimuonya hakutakiwa kuzungumza jambo lolote baya la kuwakwaza wazazi wa msichana huyo.
Siku hiyohiyo akampigia simu Deborah na kumwambia kila kitu alichoambiwa na mchungaji. Msichana huyo alijisikia uchungu sana, John alikuwa akiongea huku akilia, hakuamini kama kweli wazazi wa msichana huyo walimkataa kwa kuwa tu hakuwa na pesa.
“Nitakuja kuonana na wazazi wako!” alisema John.
“Lini?”
“Leo hiihii!”
“Leo?”
“Ndio! Hapa ninaongea nawe nipo njiani nakuja! Nataka kusikia msimamo wao, waniambie wao wenyewe,” alisema John na kukata simu.
Akatoka alipokuwa na kuanza kuelekea Mji Mwema, alihitaji kuonana na wazazi wa Deborah, kile alichoambiwa alihitaji kukisikia kwa masikio yake kutoka kwa wazazi hao.
Alipofika, akafunguliwa geti na kuingia ndani. Akapitiliza, na mtu aliyemkaribisha alikuwa huyo Deborah. Kwa sababu ilikuwa ni usiku, siku ya Jumamosi wazazi wote walikuwa hapo, akawasalimia kwa heshima na adabu zote huku uso wake ukiwa na tabasamu pana.
Akakaa kochini, walianza kupiga stori nyingine kabisa na baadaye kuingizia suala lake la kutaka kumuoa binti yao, alihitaji kupewa ruhusa ya kufanya harakati zote alizotakiwa kuzifanya.
“Unafanya kazi wapi?” aliuliza mzee Abraham huku akichukua juisi yake na kuanza kunywa.
“Nafanya naye kazi sehemu moja!” alijibu kwa kujiamini.
“Upo idara gani?”
“Idara ya usafi!”
“Unamaanisha mfagiaji?”
“Ndiyo baba!”
Mzee Abraham akakaa kimya, akamwangalia John, ni kweli kile alichokisema ndicho kilikuwa ukweli wenyewe kwani hata muonekano wake haukuwa wa mtu mwenye pesa kabisa.
Wakati huo Deborah alikuwa pembeni akisikiliza kila kitu, alimpenda John kwa sababu mwanaume huyo alijua mapenzi ni nini, alijua ni kwa namna gani alitakiwa kumpenda mwanamke na kumuonyesha mapenzi ambayo alitakiwa kuonyeshwa.
Mbele ya John, wazazi hao wakamkatalia, walimwambia kabisa kwamba hakuwa na hadhi ya kumuoa Deborah hata kidogo, na si kumuoa bali hata kumsogelea.
“Mzee! Pesa zinatafutwa, inawezekana mwenye pesa leo kesho asiwe na pesa, asiyekuwa na pesa leo akawa na pesa. Naomba mnipe ruhusa kuwa na binti yenu!” alisema John huku akimwangalia mzee huyo.
“Kijana! Acha porojo, nenda katafute pesa. Huwezi kuwa na binti yangu halafu ukaenda kumchakaza na umasikini wako. Ninampenda binti yangu, sitopenda kuona siku moja akiwa kwenye maisha ya chini, nitahitaji aolewe na mtu mwenye pesa, muonekano mzuri na si wewe,” alisema mzee huyo.
Alikuwa Mkristo ambaye kila Jumapili alikuwa akienda kanisani, alikubalika lakini yeye huyohuyo leo hii alikuwa akimwambia John kwamba hakutakiwa kuwa na binti yake kwa kuwa tu hakuwa na pesa.
Hilo likamliza John, mbele ya wazazi wa Deborah na msichana huyo akaanza kutokwa na machozi. Hilo halikusaidia, msimamo wa wazazi hao ulikuwa uleule kwamba Deborah hakutakiwa kuolewa na mtu masikini kama alivyokuwa.
Deborah hakuvumilia kukaa sebuleni, akasimama na kwenda chumbani kwake, akajifungia na kuanza kulia mfululizo.
Moyo wake uliuma kwa kiwango cha juu kabisa. Ni kweli alimpenda mno John, hakutaka kuona akiondoka na kumuoa msichana mwingine, ndoto yake ilikuwa ni kuolewa na mwanaume huyo kwa kuwa tu alimuonyesha mapenzi ya dhati.
John alikaa sebuleni, mwili wake ulipigwa ganzi, alitamani kusikia wazazi hao wakibadilisha uamuzi wao na kumwambia walikubaliana naye lakini haikuwa hivyo.
Akainuka na kuondoka zake, akatoka nje huku akilia, aliuchukia umasikini aliokuwanao, alichukia maisha aliyokuwa akiishi kipindi hicho.
“Hivi kweli ninakataliwa kuoa kwa sababu ya umasikini wangu?” alijiuliza, alikosa jibu, akaanza kupiga hatua kuelekea nyumbani kwao.
Wazazi wa Deborah walikaa sebuleni, walikuwa wakizungumza kuhusu uamuzi waliokuwa wameamua siku hiyo. Walifurahi kuona hilo likitokea, walipongezana lakini wakiwa hapo, ghafla mlango ukafunguliwa, Deborah akatoka akiwa na begi lake la nguo na kuanza kwenda nje.
Wote wakashtuka, hawakuamini kile walichokiona, walimuita, hakuitikia, ni kama hakuwasikia vile, akafungua mlango na kuondoka zake.
Wazazi wake walikataa kuolewa na John lakini moyo wake ulimwambia ni lazima akaishi na mwanaume huyo. Maisha yake hayakuwa na thamani yoyote ile bila kuwa na mtu aliyekuwa akimpenda kwa moyo wa dhati.
“Deborah...we Deborah...” mama yake aliita, hakugeuka nyuma, akatokomea zake, akaanza kumuwahi John, pia ua ilikuwa ni lazima kwenda kuishi na mwanaume huyo.
***
Juliana hakujua ni kitu gani kilikuwa kinakwenda kutokea, aliwaona John na Deborah wakiwa pamoja, walipendana lakini siku zote katika maisha yake aliamini mwanaume huyo angekuja kuwa nawe.
Kwenye maombi yake hakuacha kumuombea afanikiwe, awe na maisha mazuri mpaka siku ile ambayo angefunga naye ndoa na kuwa mume na mke.
Aliwahi kumwambia mama yake, wakati John akiwa na Deborah mwanamke huyo alikata tamaa ya kuona binti yake akiolewa naye lakini kitu cha ajabu kabisa Juliana aliendelea kumwambia kwamba kuna siku bado mwanaume huyo angekuja kuwa mume wake wa ndoa.
Walikiombea kitu ambacho hawakuona kama kilikuwa na dalili za kufanikiwa. Maisha yao ya kimasikini yaliendelea kama kawaida, kila siku walikuwa watu wa kupigwa na maisha na kila ilipoingia leo waliona ni afadhali ya jana kuliko leo.
Baada ya mwezi kupita tangu watu hao wawili wawe karibu ndipo tetesi zile zikawa kubwa kwamba watu hao walitarajiwa kutangaza uchumba kanisani.
Hilo lilimuuma kupita kawaida, kati ya vitu ambavyo hakupenda kuona vikitokea cha kwanza kilikuwa hicho. Alijifungia chumbani kwake na kuanza kulia kwa maumivu makali, wakati mwingine alitamani sana kuona akikimbia, kwenda mbali kabisa ili asijue ni kitu gani kilikuwa kikiendelea lakini alishindwa kufanya hivyo.
“Nimesikia wazazi wa Deborah wamekataa,” alisema msichana mmoja, alikuwa akimwambia Juliana.
“Kukataa nini?”
“Deborah kuolewa na John! Yaani jamani mpaka nimeshangaa,” alisema msichana huyo.
Maneno yalianza kusikika kanisa kwamba wazazi wa msichana huyo walikataa kabisa kumruhudu binti yao kuolewa na kijana kama John. Maisha yake hayakueleweka hata kidogo, alikuwa mwanaume masikini ambaye kwa kuangaliwa tu hakuonekana kama alikuwa na uwezo wa kumlisha Deborah ambaye alikuwa na maisha ya gharama sana.
Watu wakapigiana simu, wakapeana taarifa hizo, kwa Juliana moyo wake ulikuwa na furaha kupita kawaida, ile nguvu ya kusali ikaongezeka kwani aliamini Mungu alikuwa kazini akipambania ndoto yake ya kuolewa na mwanaume huyo.
Jumapili ya pili baada ya tetesi hizo kusambaa, watu walikuwa kanisani wakiendelea na ibada kama kawaida, hawakuwa na hili wale lile lakini ghafla tu wakaona polisi kama kumi wakija na gari lao, wawili wakateremka na kuelekea lilipokuwa kanisa.
Wakasimama hapo na kuongea na wasimamizi, mashemasi na kuwaambia walifika hapo kwa kuwa walimuhitaji mtu mmoja aliyeitwa kwa jina la John.
“Wapo akina John wengi,” alisema shemasi.
Wakati wakiendelea kuzungumza na mtu huyo, mchugaji ambaye alikuwa mashabahuni aliwaona na hivyo kwenda huko kuzungumza nao. Alipofika, akaambiwa kwamba walikuwa mahali hapo kwa kuwa walikuja kumkamata mtuhimiwa aliyejulikana kwa jina la John.
“Amefanya nini?” aliuliza mchungaji.
“Amemtorosha binti wa watu usiku!” alijibu polisi.
“Amemtorosha binti wa watu usiku?”
“Ndiyo!”
“Binti gani?”
“Deborah Abraham.”
Mchungaji hakuamini alichokisikia, ikabidi arudi kanisani na baada ya sekunde chache akatoka akiwa na John, kabla ya watu hao kumchukua kwanza akaanza kuongea naye.
Alimwambia kile kilichokuwa kimetokea, kwamba Deborah aliondoka nyumbani kwao na kwenda kwake kwani alikasirishwa na maamuzi ya wazazi wake.
“Kwa hiyo akaja kwako?” aliuliza mchungaji.
“Ndiyo!”
“Unaye?”
“Ndiyo! Nilimwambia arudi nyumbani lakini alikataa katakata!” alisema John.
Polisi waliagizwa kwa ajili ya kumchukua mwanaume huyo na kuondoka naye hivyo hicho ndicho walichokifanya, wakamfunga pingu na kuondoka mahali hapo.
Hakuwa na hofu, alipofikishwa huko, macho yake yakatua kwa wazazi wa Deborah ambao walionekana kuwa na hasira naye, hakujali, akachukuliwa na kuingizwa selo.
“Huyu muacheni akae humo hata siku tatu ili ashike adabu. Bila shaka Deborah atakuwa nyumbani kwake, naomba twende huko,” alisema baba yake Deborah.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Unapafahamu anapoishi?”
“Sipafahamu ila kuna mshirika mmoja anaweza kutupeleka,” alisema mzee Abraham.
“Basi tumfuate huyo mshirika kanisani atupeleke kumchukua binti yako,” alisema polisi, hapohapo wakaingia ndani ya gari na kuanza kwenda kanisani kwa lengo la kumchukua mtu na kumpeleka nyumbani kwa John.
Polisi walifika kanisani ambapo wakamtaka mchungaji amteue kijana mmoja kwa lengo la kuwapeleka nyumbani kwa John. Hilo halikuwa tatizo, kijana mmoja akachukuliwa, akaingizwa ndani ya gari.
“Na mimi nataka kwenda!” alisema msichana mmoja, alikuwa amesimama mbele ya polisi, alikuwa Juliana.
“Wewe ni nani?” aliuliza polisi mmoja.
“Juliana!”
“Unataka kwenda kufanya nini?”
“Kumuona John!”
“Yupo kituo cha polisi cha Mwanga, nenda huko. Dereva washa gari tuondoke!” alisema polisi huyo, gari likawashwa na kuondoka mahali hapo.
Kijana yule alikuwa akiwaelekeza polisi njia mpaka walipofika nyumbani kwa John, wakaingia ndani ambapo huko wakamkuta Deborah akiwa kwenye godoro akilia, moyo wake ulikuwa na majonzi mazito.
Hawakutaka kuchelewa, haraka sana wakamchukua msichana huyo na kuanza kumtoa nje. Deborah alikuwa akilia, aliwaambia hakutaka kuondoka hapo kwani alijisikia amani na furaha kuwa humo kuliko nyumbani kwao.
Wazazi wake waliwaambia polisi ni lazima wamtoe kwani hakutakiwa kubaki humo, kazi ikafanyika na msichana huyo kutolewa haraka sana, akapakizwa ndani ya gari na kuanza kupelekwa nyumbani.
Njia nzima alikuwa akilia, hakuamini kama wazazi wake ndiyo walikuwa wakimfanyia hayo yote, aliwapenda, aliamini wangekuwa naye bega kwa bega kwa maamuzi aliyochukua lakini kitu cha ajabu kabisa, walibadilika, hawakutaka kabisa kumuona akiwa na John.
Walipofika nyumbani, akaingizwa ndani na kuambiwa atulie humo. Hakuwa na la kufanya, akakaa kitandani na kuendelea kulia kama kawaida.
Alikuwa binti mkubwa lakini wazazi wake walivyokuwa wakimchunga ni kama alikuwa msichana mdogo wa sekondari.
“Na yule kijana vipi?” aliuliza polisi.
“Muacheni akae! Nitawasiliana na bosi wake afukuzwe kazi! Manake nahisi ile kazi ndiyo inamtia kiburi!” alisema baba yake Deborah.
Polisi wakaondoka nyumbani hapo, mzee Abraham akachukua simu yake na kumpigia Bwana Masako, bosi wa kampuni ya samaki aliyokuwa akifanya Deborah. Simu iliita na baada ya sekunde chache, ikapokelewa.
“Kuna kitu nataka unisaidie,” alisema mzee Abraham baada ya salamu.
“Kitu gani?”
“Ninahitaji sana umfukuze kazi kijana anayeitwa John!” alisema.
“John gani?”
“Yule mfanya usafi, ananiharibia binti yangu na ninajua kazi ndiyo inamtia kiburi,” alisema mzee huyo.
“Mh! Ishu ya kuajiri ipo chini yangu ila ya kufukuza mpaka niwasiliane na uongozi wa juu kabisa jijini Dar es Salaam,” alisema Bwana Masako.
“Mh!”
“Ndiyo! Kampuni ilinunuliwa na bosi mwingine miezi saba iliyopita kutoka huko, hivyo ameweka utaratibu wake, labda nitumie ubabe mzee mwenzangu!” alisema Bwana Masako.
“Basi sawa. Tumia ubabe!”
“Haina shida.”
Mzee Abraham akakenua, aliyaona mafanikio makubwa, John alitoka jijini Dar es Salaam kwenda Kigoma kwa lengo la kutafuta maisha, akayapata lakini kwa bahati mbaya amri ilitolewa kwamba ni lazima afukuzwe kazi.
Muda huo wakati mazungumzo hayo yalipokuwa yakifanyika, kijana huyo alikuwa selo, moyo wake uliuma kupita kawaida, hakuamini kama yeye ndiye aliyekuwa akipitia maisha hayo kwa sababu tu hakuwa masikini.
Alihuzunika lakini hakujilaumu, kile alichokuwa amekifanya kilionekana kuwa sahihi kwake. Alionyesha upendo wa dhati kwa msichana aliyekuwa akimpenda, alikuwa tayari kufanya lolote kwa ajili ya Deborah na ndiyo maana hakuwahi kujilaumu hata kidogo.
Akiwa humo, majira ya saa kumi jioni akaambiwa kulikuwa na wageni waliokuja kumuona, akatolewa, alipofika kaunta, macho yake yakatua kwa washirika kadhaa akiwemo Juliana ambaye alimpelekea chakula.
Kila mmoja alionekana kuwa na huzuni, hapakuwa na mtu aliyeamini kile kilichokuwa kikiendelea. Alitia huruma, macho yake yalionekana kuwa mekundu hali iliyoonyesha alilia sana humo ndani.
Akazungumza nao, kila alipomwangalia Juliana, alikumbuka, alihisi tangu zamani kwamba msichana huyo alikuwa akimpenda, kwa jicho lile, aliamini kabisa alikuwa sahihi kwa asilimia mia moja.
Wakazungumza naye na baadaye kuondoka huku akibaki Juliana tu ambaye hakutaka kumficha kitu chochote kile, kwa sababu ya maisha aliyokuwa akipitia, aliamini yeye ndiye angekuwa tumaini lake.
“Ninakupenda John!” alisema msichana huyo.
“Najua sana!”
“Ninahitaji unioe, tujenge familia pamoja. Nitakupenda maisha yangu yote!” alisema Juliana huku akimwangalia John.
“Hapana! Sijamalizana na Deborah! Bado ninampenda msichana yule!” alisema.
“Ila wazazi wake hawataki uwe naye!”
“Ila si yeye! Sijamalizana na Deborah!” alisema John.
Wakati wakiendelea kuongea, polisi wakamtaka Juliana kuondoka mahali hapo kwani muda ulikwisha, akatii na kuondoka zake.
Siku hiyo alilala selo. Moyo wake uliendelea kuwa na uchungu kwa yale aliyokuwa akipitia. Aliamini hapakuwa na jambo baya alilokuwa amelifanya kwa sababu kumpenda mwanamke ilikuwa moja maisha aliyokuwa akipitia kila mtu.
Asubuhi na maema Juliana alifika kituoni hapo akiwa na kapu lililokuwa na chai na vitafunio, akaitaji kuonana naye na kumpa vitu hivyo.
John akashukuru na kuanza kunywa. Mtu huyo ndiye ambaye alimuonyesha thamani ya kumpenda, ndiye ambaye alikubali kuwa naye bega kwa bega hata kwa hali aliyokuwa akipitia.
Deborah hakutokea hapo kituoni, alichungwa, hakutakiwa kuendesha gari kwenda ofisini, mama yake alimsindikiza huku akibaki hukohuko kuhakikisha hatoki hapo kwenda kumuona John kituoni.
Barua ya kufukuzwa kazi ikaandikwa haraka haraka na ilipofika majira ya saa sita, akapelekewa hukohuko kituoni, akaambiwa hakutakiwa kuonekana ofisini, yaani kwa sababu alipelekwa polisi basi nayo kazi ilikuwa basi.
Aliumia moyoni mwake, hakutegemea mwanzo wa mambo hayo yangefika huko. Alilia sana, alimuomba Mungu wake amsaidie kwani hakuona njia nyingine ya kufanya, kitendo cha kukosa ile kazi kilimaanisha angerudi tena mtaani na kuuza samaki.
Mzee Abraham alifanya yote kwa kuwa alitaka kumkomesha John. Alikuwa na pesa, aliheshimika hivyo alihitaji John akae huko wiki nzima ili ajifunze.
Mchungaji wake alikuwa akifika mara kwa mara kuomba kijana wake atolewe lakini hakutolewa, yaani kila kitu kilifanyika kwa kuwa mzee Abraham alitaka iwe hivyo.
Wiki ilipokatika, ndipo akaruhusiwa kutolewa kwa masharti kwamba hakutakiwa kuonana na Deborah wala kuwasiliana naye vinginevyo angerudishwa tena.
“Ila ninampenda!” alimwambia polisi.
“Kijana tutakurudisha ndani!”
“Basi samahani! Nashukuru sana,” alisema.
Akachukuliwa na Juliana na kusindikizwa nyumbani kwake. Njiani walikuwa wakiongea mengi lakini akili ya John haikuwa kwa msichana huyo hata kidogo, alikuwa akimkumbuka Deborah wake aliyekuwa akimpenda kupita kawaida.
Walipofika nyumbani, akapokewa na baba mwenye nyumba ambaye alimpa pole kwa mkasa mzima uliokuwa umetokea kwani ulimgusa kila mtu.
“Ni maisha tunayopitia! Ninashukuru sana!” alisema John huku akimwangalia mzee huyo.
Wakaingia ndani na Juliana, wakakaa na kuanza kuzungumza mambo mengi. Muda wote msichana huyo alionekana kuwa na furaha tele, hakuamini kama alikuwa na John chumbani humo.
Hakunyamaza, suala lake la kumpenda na kumuhitaji alimwambia kila wakati lakini msimamo wa mwanaume huyo ulibaki vilevile kwamba hakuhitaji kuwa naye kwa kuwa hakuwa amemalizana na Deborah.
Siku hiyo ndiyo ilikuwa mwisho wa kila kitu kwa John, hakuweza kumuona Deborah, alipokwenda nyumbani kwao, hakuruhusiwa kuonana naye, ofisini alikimbizwa na kuambiwa hakutakiwa kuonekana hapo vinginevyo angerudishwa polisi.
Alilia sana na kuumia, hakuwa na simu, yake aliyokuwanayo waliichukua polisi na kuivunjavunja, laini wakaitupa kabisa.
Hakuwa na pa kushtaki, watu ambao ndiyo alizoea kusikia walikuwa watetezi wa wanyonge ndiyo walikuwa wakifanya hayo.
Kukaa bila Deborah yalikuwa maisha ya mateso ambayo hakuwahi kuyasikia kabisa. Familia yake haikuja tena kanisa, moyo wake ulivurugika, alichanganyikiwa kupita kawaida.
Mtu pekee ambaye kwa kipindi hicho alikuwa akimpa furaha alikuwa mmoja tu, Juliana ambaye alijitoa kwa asilimia mia moja katika maisha yake.
Huyo ndiye alikuwa tegemeo lake, hakuwa tajiri, alikuwa masikini kama yeye lakini alikuwa radhi kuwa naye, hakumpenda kwa kuwa alitoka Dar es Salaam, alimpenda kwa kuwa moyo wake ulimwambia alikuwa mwanaume sahihi wa kuwa naye kipindi hicho.
John akairudia kazi yake ya samaki, aliamua kuweka nguvu zake huko, hakutaka tena kuajiriwa kwa kuwa tayari aliamini hapakuwa na mpango kwani chuki za mtu mmoja zinaweza kukufanya kupoteza ajira, akaona ni bora kujiajiri.
Kwa muda wa miezi mitatu mfululizo picha ya Deborah haikutoka kichwani mwake, iliganda ubongoni mwake, ilimtesa kwa kipindi kirefu mno.
Juliana alijitahidi kuonyesha kila aina ya mapenzi kwa John, alijua kabisa moyo wake ulikuwa kwa mwanamke mwingine na si yeye hivyo alitakiwa kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha anaupata moyo wa mwanaume huyo.
“Au kwa sababu sijafanya naye mapenzi?” alijiuliza.
Huo ndiyo ulikuwa mpango mwingine alioupanga kuufanya.
Aliamini alishindwa kuuteka moyo wa John kwa kuwa nafsi zao hazikuwa zimeunganishwa kupitia ngono, hivyo akajipanga, katika siku ambayo hakuwa na hatari ya kupata mimba akaenda nyumbani kwake.
Walikaa na kupiga stori kama kawaida, siku hiyo alikuwa na mipango yake, alianza kumshikashika John hapa na pale, alijilainisha kwake, mwisho kabisa akavua blauzi yake, kifua kilikuwa kimesimama.
John alipoangalia, akashtuka, hakuamini kile alichokiona, ni kweli alimpenda mno Deborah lakini macho yake kwa wakati huyo yaliona kitu ambacho kilimfanya kumuondoa Deborah kwa muda.
Juliana akamsogelea pale kitandani, akaanza kumfanyia utundu, John akachanganyikiwa, akajikuta akivuliwa nguo zake na hakubisha hata kidogo.
“Sijawahi kulala na mwanaume!” alisema Juliana maneno ambayo yalimshtua John.
“Unasemaje?” aliuliza John huku akionekana kutokuamini, msichana mkubwa kama Juliana bikira.
“Ndiyo hivyo! Kwa hivyo iwe taratibu. Umesikia baba watoto?” aliuliza Juliana huku akiachia tabasamu.
“Hakuna shida!”
Wakakubaliana na hatimaye kuanza kazi. Ni sauti za mahaba ndizo zilizokuwa zikisikika chumbani humo.
Kwa wasiojua, ngono kilikuwa kitendo kinachofanyika kwa mwili na kwa roho, kuna mahusiano makubwa mno baina ya roho mbili zinapokutana na hatimaye mwili kufanya mapenzi.
Na ndiyo maana wakati mwingine unaweza kufanya mapenzi na mtu fulani, maisha yako yakakunyookea mno mpaka ukawa unashangaa lakini kuna wakati mwingine unaweza kufanya mapenzi na mtu mwingine ukaona unaanza kuingia kwenye misukosuko, pesa inakatika, yaani kila kitu kinakuwa shaghalabaghala.
Kitendo cha kumvulia nguo zake John ni kama kilibadilisha kila kitu, kichwa chake kikakaa sawa, akahisi akianza kumsahau Deborah.
Huyo Juliana akaanza kuingia kichwani mwake kwa kasi ya ajabu, kitendo cha kutukuona Deborah kwa miezi mitatu tu kilimfanya kuwa na nguvu zaidi ya kumsahai msichana huyo.
John akaanza kurudi katika hali yake ya kawaida, kila siku asubuhi alikuwa akiondoka nyumbani kwake na Jumanne kwenda kununua samaki na kwenda kuwauza kama kawaida yao.
Alifanikiwa kwa kiasi kidogo, pesa alizokuwa akizipata akazihifadhi kwani alijua kwa jinsi hali ilivyokuwa ikienda, kuna siku alihitaji kuoa na kuanza kuishi na mwanamke, hivyo ilikuwa ni lazima aweke akiba ya pesa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Uhusiano wake na Juliana ulikua kwa kasi sana, watu walifurahi, hapakuwa na mtu aliyeumia kwa kuwa tu John maisha yake yalikuwa ni ya kimasikini, hata wanawake wengine walimuona Juliana akipotea kwa kumchukua mwanaume ambaye hakuwa na kitu.
Baada ya miezi nane tangu wakiwa pamoja, hatimaye wakakubaliana kutangaza uchumba kanisa, hilo likafanyika, wakavalishana pete na hatimaye kuingia kwenye hatua ya uchumba.
Ilikuwa ni furaha ya kila mmoja. Walizidi kupendana, wakapanga mwezi wa kuoana na kuwa mume na mke, hivyo mwezi huo wa sita, wakasubiri mpaka mwezi wa tisa ndipo harusi ifanyike na hatimaye kuishi pamoja.
“Ninakupenda mchumba wangu!” alisema John huku akimwangalia Juliana.
“Ninakupenda pia!” alisema Juliana, hapohapo wakabusiana, kila mmoja alimpenda mwenzake kupita kawaida.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment