Search This Blog

Tuesday, 1 November 2022

PENZI LA MZOA TAKATAKA - 3

 






Simulizi : Penzi La Mzoa Takataka 
Sehemu Ya Tatu (3)




"Mmh Hapana hakuna tatizo". Alikataa Mazoea huku macho yake akiwa ameyalegeza. Baada Nyogoso kusikia jibu hilo hakuona haja ya kuendelea kupoteza muda, hivyo alinyanyua mzigo wake wa takataka kwa niaba ya kwenda kuutupa kwa sababu muda tayari ulikuwa umtaladadi. Lakini kabla Nyogoso hajajitwika mzigo huo,aliguswa bega na Mazoea. Hapo Nyogoso alistisha zoezi hilo la kujitwisha mzigo wa takataka akamgeukia Mazoea kisha akarudi kumuuliza "Kuna tatizo?.." Hivyo hivyo Mazoea akiwa na wingi wa haibu usoni mwake akamjibu kwa ishara ya kichwa akikataa kuwa hakuna tatizo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Sasa huoni kuwa mwili wangu mchafu? Au hii harufu ya takataka kwako haikukeri?.." Alirudia kuhoji Nyogoso mzoa takataka. Ila Mazoea hakumjibu zaidi ya kuendelea kumtazama usoni huku mara kwa mara akitabasamu. Pumzi alishusha Nyogoso kisha akainama akaunyanyua mzigo wake, safari hiyo akafanikisha kuuweka begani ila kabla hajianza hiyo safari Mazoea akasema "Kwanini unanifanyia hivyo?.. Sipendi na mimi nina moyo nihurumie tafadhali. Najua hutoweza kuyaamini maneno yangu sababu muonekano wangu ulivyo mbele ya macho yako.." Nyogoso alistuka kusikia maneno hayo, haraka sana akautua chini mzigo wa takataka kisha akasema." Unajua sikuelewi. Haya nakusikiliza ongea wala usiogope"

"Asante sana kwa kunipa nafasi hii pekee na adimu. Naweza kusema nina bahati ya kunena maneno haya mbele yako. Moyo wangu.. Moyo wangu mimi"

"Moyo wako?.." Alitaharuki Nyogoso.

"Ndi.. Ndi.. Ndioooo"

"Umefanya nini huo moyo wako?.." Aliongeza kuhoji Nyogoso huku akiwa na sintofahamu juu ya maneno hayo ya Mazoea ambayo alikuwa akiyaongea kwa hisia na haibu machoni mwake. Hivyo baada Nyogoso kumuuliza Mazoea swali hilo, naye alishusha pumzi ndefu kisha akasema." Moyo wangu umetokea kukupenda ghafla tangu siku ile nikuone mara ya kwanza. Najua utaniona kituko ila ukweli ulipo ndani ya moyo wangu ndio huo. Sijali upo katika mazingira ya aina gani aidha unakazi gani. Mimi ninacho hitaji kutoka kwako ni mapenzi ya dhati. Naomba unikubalie ombi langu nipo chini ya miguu yako " Alisema Mazoea, maneno ambayo aliyaongea kwa sauti ya upole iliyojaa huzuni ndani yake. Nyogoso alimtazama binti huyo na wala asiamini kama maneno hayo yametoka kinywani mwake. Ndani ya nafsi yake akajisemea ." Looh! Inawezekanaje binti mzuri kama huyu kunipenda mimi fukara nisiye na mbele wala nyuma? Hii ni hadithi za kale ilikuwepo lakini enzi za mababu na sio kipindi hiki cha digital" Alipokwisha kujisemea hayo mzoa takataka Nyogoso akamtazama Mazoea usoni wakati huo akitikisa kichwa ishara ya kukataa jambo fulani, hakuwa tayari kuanzisha uhusiano na binti huyo wa kitajiri. Woga ulimjaa baada kumuona binti huyo bado mwanafunzi hivyo alihofia maisha yake kuishia gerezani.

"Nashukuru kwa kunipenda, nimefurahi sana lakini tambua kuwa wewe bado mwanafunzi" Nyogoso akimwambia Mazoea maneno ambayo yalimpelekea binti huyo kutikisa kichwa kupeleka kulia na kushoto na kisha kumjibu " Mimi ni mwafunzi wa chuo, kwahiyo tayari ni mtu mzima. Nikubalie tafadhali ili moyo wangu uwe na amani. Nitakuwa kichaa sababu yako" Aliongea Mazoea kwa uchungu na punde alianza kutokwa na machozi, penzi la mzoa takataka alilitamani sana akiamini kuwa atajiona wa thamani sana endapo kama Nyogoso atakubali takwa lake. Lakini wakati hayo ya kijili baina ya Nyogoso na Mazoea muda huo huo kwa mbali ilionekana gari aina ya Hulax ikija kwa kasi mahali waliposimama wawili hao. Ndani ya gari hiyo alishuka mama Mazoea.

"Nimekuona kwa mbali upo hapa! Sasa nataka uniambie huyu ni nani?.." Alisema mama Mazoea kwa jazba ilihali muda huo huo akimpiga makofi. Nyogoso aliogopa.

"Kwanini unakuwa mjinga kiasi hiki? Hivi unaaakili timamu kweli? Yani unathubutu kuchelewa nyumbani kisa huyu kichaa mpumbafu asiyekuwa na mbele wala nyuma? Mjinga sana wewe, unatafuta nini kwa huyu kibaka?.." Aliongeza kusema hivyo mama Mazoea kwa hasira kali huku mara kadhaa akimtusi Nyogoso mzoa takataka. Alipokwisha kusema na binti yake akamgeukia Nyogoso akamwambia" Wewe mbwa wewe. Bira shaka hunijui sasa ngoja nikuonyeshe kuwa mahali ulipogusa hapafai.. " Nyogoso alishangaa sana kusikia maneno hayo! Aliogopa wakati huo mama Mazoea alibonyeza simu yake ya mkononi, punde si punde akasema" Hello Afande Daniel uko wapi muda huu?.. ".

" Afande?. " Alijuliza Nyogoso baada kusikia akitajwa Afande. Alijua tayari Mazoea amemponza hivyo alijikuta akitetemeka mwili mzima akijua tayari mambo yamekuwa sio mambo. Alitamani kukimbia mahali hapo ila alishindwa baada kuona kuwa anakibarua cha kwenda kutupa takataka jalalani wakati huo huo mama Mazoea aliongeza kusema "Sawa nakuomba njoo mara moja hapa Magomeni mapipa, ukikaribia kufika nitaarifu ili nikueleze mahali nilipo"

"OK vipi nije kikamilifu au?.." Aliuliza Afande Daniel. Sauti ambayo Nyogoso aliisikia kwa mbali sana.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Ndio njoo kikamilifu" Alijibu mama Mazoea.

"Sawa mamaa dakika tano tu nitakuwa nimewasili"

"Sawa Sawa" Simu ikakatwa. Mama Mazoea akamgeukia Nyogoso, kwa hasira akarudi kumwambia "Unasikia? Sitokupeleka jela, ila nitakacho kufanya nadhani Mazoea utamuogopa kama ukoma. Mwana hidhaya mkubwa wewe" Mama huyo alipokwisha kumwambia hivyo Nyogoso, alimgeukia na binti yake naye akamwambia "Na wewe tuatajuana vizur tukifika nyumbani" Mazoea alilia sana, alimuona huruma mzoa takataka ambaye naye kwa muda huo alikuwa akitokwa na machozi juu ya kile kinacho tarajia kumtokea. Macho yake aliyatupa kwa Mazoea kitendo ambacho Mazoea aliamini mwanaume huyo atakuwa anamlaumu kuwa amemponza hivyo alimuomba mama yake amuache aondoke zake lakini ombi hilo la Mazoea halikusaudia kitu kwani muda huo mama yake alipokea Simu ya Afande Dani, mara moja akapokea na kumuelekeza mahali walipo. Daniel alifika mahali hapo huku pingu ikining'inia kwenye upinde wa mkanda..

"Kosa langu nini mimi?.." Alijiuliza mzoa takataka ndani ya nafsi yake huku akijifuta macho kwa kutumia shati lake kukuu.



"Mtu mwenyewe ndio huyu??." Aliuliza Afande Daniel baada kushuka kwenye gari.

"Ndio kamanda"

"Anhaa sawa.. Halooh! Hebu panda kwenye gari haraka sana" Alisema Daniel baada mama Mazoea kumthibitishia mtuhumiwa anayetakiwa kutiwa mbaloni. Lakini amri ya kamanda Daniel kamwe Nyogoso hakutaka kukubaliana nayo, aligoma akidai kuwa hawezi kuingia ndani ya gari hilo la police ilihali hana kosa. Kitendo hicho kilimkrea Daniel ambapo alichukua uamuzi wa kumpiga Nyogoso virungu kila sehemu ya mwili wakati huo akimwambia "Unanijua mimi ni nani? Eeh wewe kichaa unanitambua vizur? Yani unanigomea mimi? Sasa ngoja nikuonyeshe utaenda tu" Alisema hivyo Afande Daniel wakati huo akiendelea kumuadhibu mzoa takataka Nyogoso. Maumivu makali ambayo aliyapata Nyogoso yalimfanya kudondosha machozi huku akimuomba msamaha kamanda huyo ilihali muda huo damu zikimtoka mdomoni na puani, ndipo Daniel alipombeba kwa nguvu mpaka kwenye gari la police akamtupa kwenye tela kisha akafunga mlango huku akimtupia matusi mabaya na mara kadhaa akidiliki kumtisha kuwa atakiona cha mtema kuni.

"Na utakoma sasa mjinga wewe" Alisema Daniel akiwa amekunja sura yake kwa hasira. Zoezi hilo lilipokwisha, kamanda Daniel alimfuata mama Mazoea, alipomfikia mama Mazoea alifungua pochi yake akatoa kitita cha fedha akamkabidhi Afande Daniel. Kama huyo alifurahi sana, tabasamu pana lilitamalaki mdomoni mwake huku akizihesabu pesa hizo alizopewa na mama Mazoea. Baada kuzihakiki vizuri alimtazama mama huyo kisha akasema "Asante sana mamaa..niachie mimi hii kazi. Nitamnyoosha kisawa sawa"

"Sawa Afande, mimi nakuaminia sana. Ndio maana nimekuita wewe kaa sababu najua shughuli yako ilivyo" Alijibu mama Mazoea, kicheko kikafuatia kisha kila mmoja akaondoka zake. Mzoa takataka Nyogoso anafikishwa kituo cha staki Shari, hapo alishushwa chini kwa mateke na ngumi. Kabla hajakaa sawa akapelekwa puta mapaka selo kisha akafungiwa humo. Upande wa pili hofu inamjaa Jaluo mara baada kuona rafiki yake kachelewa kurejea maskani tofauti na siku nyingine. Maswali mengi alijiuliza juu ya Nyogoso, jambo ambalo lilimfanya kukosa usingizi kabisa. Pumzi ndefu mara kwa mara alishusha huku hofu yake kuu ni usalama wa kijana mwenzake "Sijui atakuwa amepatwa na tatizo gani?.. Huu ni mji wa ajabu. Huwenda mchizi wangu kagongwa na gari aidha kazushiwa wizi kapigwa mpaka kufa. Loh! Mungu msaidie huko ulipo mchizi wangu arudi maskani salama" Jaluo akiwa katika dimbwi la mawazo alijisemea maneno hayo. Kwingeneko Nyogoso alipata tabu ndani ya chumba hicho, giza totoro lililotanda chumbani humo lilimfanya kujiona hana bahati ya kuishi kwa furaha katika uso wa Dunia achilia mbali harufu mbaya ya kinyesi cha binadamu bila kusahau mbu wenye shauku ya damu. Alilia mzoa takataka Nyogoso, kilio cha mtu mzima. Lakini kilio hicho kilifikia tamati baada kuingia mtu ndani ya chumba hicho. Alishindwa kumtambua mtu huyo wakati huo akizidi kumsogelea. Alipomfikia alimpiga rungu kisha akasema " Kijana, mwenye pesa sio mwenzako. Kwanini unataka kushindana na mwamba ulioshindikanika?.." Alisema mtu huyo, hakuwa mwingine bali ni Afande Daniel aliyeingia muda huo kutimiza wajibu baada kuingia siku ya pili tangu mtuhumiwa Nyogoso alipoingia kwenye himaya yake. Alipokwisha kusema hivyo alimpiga kwa mara nyingine tena. Nyogoso alihisi maumivu makali yaliyomfanya kulia kilio cha mtu mzima. Sauti ya mayowe Ilisikika kutoka kinywani mwa Nyogoso, kipigo cha Afande Daniel kilimuumiza sana kwani wakati huo alishikwa korodani na kamanda huyo na kisha kufinywa kwa nguvu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Nisamehe sitorudia, nisamehe tafadhali" Aliongea Nyogoso kwa sauti ya chini huku akiangua kilio. Ila kamwe Daniel hakuta kuelewa msamaha huo, zaidi aliendelea kumfinya Nyogoso korodani zake pasipo kumuonea huruma mwanaume mwenzake. Ila pindi alipokuwa akifanya hivyo, mara gafla simu yake illita. Akasitisha zoezi hilo ikibidi apokee kwanza simu hiyo.

"Afande, hebu muachie huyo kijana..Kuna tatizo limetokea". Daniel alisikia sauti ya mama Mazoea akisema hivyo. Alishangaa sana kusikia uamuzi huo wa mama Mazoea wakati hapo awali walikubalina kumuadhibu Nyogoso ili hata siku nyingine akae mbali na binti yake. Lakini Daniel hakuwa na budi kukubaliana nao uamuzi, hima alimfungua kamba Nyogoso kisha akamuamuru asimame.

"Haya wewe ngurue polini hebu simama" Alisema Afande Daniel. Ila mzoa takataka Nyogoso hakusimama. Kwa sauti kali Daniel alirudia kumuamuru Nyogoso asimame ila bado mambo yakawa yale yale. Nyogoso hakusimama na hapo ndipo alipompiga kofi lakini kamwe Nyogoso hakutikisika wala kulalama maumivu anayosikia. Afande Daniel alistuka kuona hali hiyo, hofu ikamjaa moyoni wakati huo akimgusa mzoa takataka sehemu ya moyo kusikiliza mapigo. Alikuta yakidunda kwa mbali sana hali ambayo ilimuogopesha kamanda huyo kijasho chembamba nacho kikimtoka akihofia uhai wa kijana huyo mzoa takataka. Haraka sana akatoka ndani ya chumba hicho akaelekea ofsini kwake, akachukua box kubwa kisha akarejea nalo mpaka katika chumba hicho cha mateso. Afande Daniel akitetemeka mwili mzima kwa hofu, alimbeba Nyogoso akamsogeza pembeni mwa chumba jicho kisha akamfunika kwa kutumia box hilo huku akisubiri giza litande akamtupe mbali kufauta ushahidi kwa kile alicho kufanya.

" Aaah Diri limegeuka dirisha hakyaMungu. Hii ndio njia pekee iliyobaki ili kurinda kibarua changu. Najua atakuwa amepoteza fahamu lakini kwa hali hii aliyonayo kuna uwezekano akapoteza maisha.. Ngoja wakati ufike siwezi nitimize hili". Alijisemea hayo Afande Daniel huku akiwa ameinamia ya ofisi yake wakati huo akitazama saa yake ya mkononi. Wakati balaa hilo likijili kwa Afande Daniel, upande mwingine Ilisikika sauti ya mama Mazoea akimbembeleza binti yake asifanye kitendo kibaya. Mazoea hakufurahishwa na kitendo cha mama yake alichomfanyia mzoa takataka Nyogoso pasipo kukutwa na hatia. Kilimuuma sana kitendo hicho, moyo wake ukasononeka, furaha yote ikatoweka mara moja ambapo alijiona hana thamani ya kuendelea kuishi Dunaia, hivyo alijifungia chumbani kwa dhumuni la kunywa sumu ili afe akiamini kuwa ndio njia rahisi ya kuyapumzisha maumivu anayo yahisi ndani ya moyo wake.

"Mazoea mwanangu fungua mlango tafadhali mama yako nipo chini ya miguu yako, usifanye hivyo Mazoea" Alisema mama huyo huku akigonga mlango wakati huo huo akiangua kilio. Punde si punde Mazoea naye alilia huku akilalama tumbo kuuma,lakini baada ya dakika kadhaa kilio hicho kilitoweka, kimya kikatawala chumbani...!







Kimya kizito kilitawala chumbani kwa Mazoea, kitendo ambacho kilimfanya mama Mazoea akidhania kuwa binti tayari kajiuwa. Mama huyo akiwa na wingi wa hofu ndani ya moyo wake,akazipiga hatua kuelekea chumbani kwake. Akachukuwa simu yake ya mkononi huku akitetemeka mwili mzima alibofya haraka haraka akiandika namba ya mumewe kisha akapiga. Lakini bahati mbaya simu ya baba Mazoea iliita bila kupokelewa. Mama Mazoea alikasirika sana, muda huo akarudi tena kupiga ila safari hiyo mambo yakawa tofauti kwani aliambiwa kuwa namba unayopiga inatumika. Alizidi kughazibika, aliketi kitandani huku mkono wake wa kushoto ukiwa shavuni ilihali kila mara akishusha pumzi ndefu na kujisonya wakati huo huo machozi ya uchungu na hasira yakimtiririka katika macho yake kwa sababu alikuwa na sintofahamu juu ya binti yake chumbani lakini pia mumewe kutompokelea simu.

"Ngoja atanitambua vizuri, yani kweli baba Mazoea ameamua kutonipokelea simu? Haya ila leo lazima pachimbike" Alijisemea mama Mazoea huku akionyesha kujaaa na hasira. Muda huo huo Alijiuliza maswali kichwani mwake juu ya binti yake kumpenda kijana mzoa takataka hadi ifikie hatua ya kumchukuwa uamuzi wa kujiua. Majibu alikosa, na zaidi aliishia kushusha pumzi kisha akasema "Ama kweli mapenzi yanalaani Dunia" Mama Mazoea alipokwisha kusema hayo alijinyanyua hapo kitandani akarejea kwenye mlango wa chumba cha Mazoea ambapo napo alijikuta akiishi wa nguvu baada kukuta chumba cha binti yake bado kimefungwa. Alilia kwa sauti huku akiupiga mlango, hatimaye kilio chake kikawa kimewastua majirani zake punde wakakusanyika nyumbani kwake ili kufahamu kinacho jili ndani.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Mama Mazoea kulikoni kuna tatizo gani?.." Aliuliza moja ya majirani zake waliofika kwenye tukio.

"Mazoea mwanangu kajifungia chumbani na simu. Anataka kujiua binti yangu jamani nisaidieni mimi" Alijibu mama Mazoea kwa sauti iliyoambatana na kilio. Taharuki inazuka kwa majirani hao. Egoni kijana ambaye alitokea kumpenda Mazoea na kila mara alijaribu kumuelezea ukweli wa moyo wake pasipo kukubaliwa ombi lake alistuka kusikia habari hiyo, akatumia nguvu zake za muguu kwa kuupiga teke mlango. Nao ukafunguka. Alimkuta Mazoea kalala chali kitandani akipumua kwa tabu huku mapovu mazito yakimtoka mdomoni mfano wa mbuzi aliyekula kipande cha sabuni. Haraka sana Egoni alimnyanyua wakati huo machozi yakimtoka kwa maumivu juu ya Mazoea mwanamke wa ndoto zake aliyetamani siku moja awe mpenzi wake huku akimuahidi kumpa kila kitu anacho kitaka kwani kama ni utajiri wa mali upo wa kutosha. Hivyo hali hiyo ya Mazoea ilimuogopesha sana kijana Egoni akihofia Mazoea kuaga Dunia. Gari ya kubebea wagonjwa ilifika nyumbani hapo kwakina Mazoea. Mazoea akaingizwa ndani gari na kisha kukimbizwa hospital kuu ya mkoa (MUHIMBILI). Dakika chache baada Ambulance kuondoka nyumbani hapo, punde iliingia gari ya baba Mazoea ambapo alijikuta alistaajabu kuona umati mkubwa wa watu umejazana nyumbani kwake.

"Kuna nini?.." Alijiuliza baba Mazoea ikiwa muda huo huo mkewe tayari ameshamsogelea huku akiwa amekasira akanyanyua mkono wake kwa dhumuni la kutaka kumpiga lakini kabla hajafanya kitendo hicho, mkono wake ulidakwa na bibi kizee ambaye naye alikuwepo kwenye tukio.

" Punguza hasira mwali wangu, hampaswi kuzozana hadharani mbele ya uma. Mtawapa faida majirani. Fanyeni jitahada za kumsaidia mtoto wenu asije kukumbwa na umauti. Hayo mengine mtaelewana mkiwe wawili. Sawa mamaa?.." Bibi kizee huyo alimwambia mama Mazoea maneno. Mama Mazoea akawa mpole ingawa alimtazama mumewe kwa jicho ngebe huku hasira zisizo na mfano zikielea kwenye moyo wake.



****************



Na wakati hayo yakiendelea, upande wa pili nako Afande Daniel alikuwa akifanya mkakati wa kwenda kumtupa Nyogoso ili kibarua chake kisiote nyasi. Muda huo Nyogoso alikuwa bado hajazinduka, hali iliyompelekea kamanada huyo kuamini kuwa muda wowote Nyogoso atakata roho.

Naam! Hatimaye jioni iliingia, Daniel akodi taxi akampakia Nyogoso ndani tayari kwa safari ya kwenda kumtupa. Lakini kabla safari haijaanza Afande Daniel alizungumza mambo mawili matatu na dereva wa gari hiyo pasipo kusahau maelewano ya bei.

"Nadhani kila kitu kipo sawa" Alisema Daniel wakati huo akitazama huku na kule akionekana kuwa na hofu dhufo lihali.

"Ndio lakini bei hiyo utakuwa umeniua bro! Ongeza hata kidogo bwana. We mwenye si unaona kama hiki kitu ni haramu kama bange halafu istoshe ni zambi kubwa ujue" Alijibu dereva taxi.

"Aah! Tatizo lako wewe unatamaa sana,jambo lenyewe hili mimi sikulitegemea halafu unazidi kunikandamiza. Sio poa ndugu yangu, haya twende nitakuongeza Elfu hamisini iwe laki moja na nusu"

"Ahahahah Hahaha. Hayo ndio mambo kamanda. Ujue nilitaka kushangaa Dani amtupe kijana wake?.." Aliongea kwa furaha dereva huyo kisha safari ikaanza wakati huo Afande Dani akimsisitiza dereva wake atunze siri juu ya jambo hilo analotaraji kulifanya.

"Shaka ondoa bro.." alikomea hapo dereva huyo, na ndipo alipoongeza kasi mara mbili ya awali. Walipofika Kimara walimtupa Nyogoso kando ya barabara kisha wawili hao wakatokomea zao kurudi mjini. Alfajiri ilipowadia, Nyogoso alizinduka baada baada kunyeshewa na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha maeneo hayo kimara mpaka mbezi mwisho. Lakini licha ya kupata fahamu ila alijikuta akikosa nguvu ya kunyanyuka sehumu ile aliyoangukia baada kutupwa. Hivyo mvua iliendelea kumnyeshea huku mavazi yake ya kuchakaa yakionekana kung'aa angalabu ziking'alishwa na matonya ya mvua.

Mzoa takataka Nyogoso aliendelea kulala kwenye mvua ile mapaka pale ilipokatika,ambapo aliamua kuomba msaada ili asaidiwe. Lakini hakuna aliyemjali zaidi baadhi yao walisikika wakisema " Watu kama hawa unaweza kumsaidia lakini ukikutana naye kwenye uchochoro atakukaba.."

"Kweli wala hujakosea, cha msingi ni kujifanya kama huwaoni" walisikika wakisema hivyo baadhi ya watembea kwa miguu wakati huo bado mzoa takataka Nyogoso akiendelea kutapatapa kuomba msaada ilihali kwa mbali akiukumbuka ushauri wa mama yake kabla ya kwenda DAR-ES-SALAAM.

Ila wakati kijana Nyogoso akiendelea kuomba msaada pasipo kusaidiwa, ghafla kando yake ilisimama gari aina ya RAVA4. Ndani ya gari hiyo alishuka mwanaume wa makamo akiwa amependeza kwa kuvaa suti nyeusi na viatu vyeusi pia. Mwanaume huyo alionekana kuwa nadhifu. Alisikitikia baada kumuona Nyogoso akiwa katika hali hiyo, na hivyo aliamua kumbeba akamakimbiza hospital. Alipomfikisha aliwakabidhi wauguzi waendelee kumuhudumia huku akiahidi kughalamikia ghalama zote zitakazo tolewa kwa Nyogoso.

"Naomba mfanye juu chini hali ya mgonjwa wangu itengemae, fanye kila jitihada ili apone. Naahidi nitawapa zawadi wahaudumu matakao fanikisha hili. Naenda kutoa hela bank si muda mrefu narudi". Aliongea kwa ujasiri mwanaume huyo msamalia aliyejitolea kumsaidia Nyogoso. Maneno hayo alikuwa akimwambia mmoja ya wauguzi waliompokea mgonjwa wake. Mwanaume msamalia mwema alipokwisha kusema hivyo alirejea ndani ya gari lake akaondoka kuelekea bank kutoa pesa ya matumizi yake binafsi na pesa ya kumtibia Nyogoso. Lakini wakati mwanaume msamalia alipokuwa ndani ya gari lake akielekea bank,ghafla njiani akapata ajari mbaya barabani baada gari lake kugongana uso kwa uso na daladala. Ajari hiyo iliweza kupelekea kukumbwa na umauti, baba huyo msamalia akawa amekufa akiwa na nia ya kumsaidia Nyogoso ambaye nae hali yake ilizidi kuwa mbaya wakati huo matibabu juu yake yalisitishwa mpaka pale watakapo pewa fedha..

"Kama amesema ameenda kutoa pesa bank basi endeleeni kuwatibu wagonjwa wengine, atakapo rudi mgonjwa wake atapatiwa huduma" Ilisikika sauti kutoka kwa mganga mkuu akiwaasa wauguzi..





Ndani ya hospital ya muhimbili, hali ya kijana Nyogoso ilizidi kuwa mbaya huku wauguzi wakiishia kumtazama tu wakisubiri mzee yule aliyesema anaenda kutoa pesa bank arudi atoe ada ya malipo ndipo matibabu yaendelee kwa Nyogoso. Pasipo kujua kuwa mzee huyo msamalia aliyejitolea kumsaidia Nyogoso amefariki kwa ajari baada gari lake kugongana uso kwa uso na daladala wakati wakati anaelekea bank.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Masaa yalikwenda, subira pakee nayo ikiendelea kutanda katika mioyo ya wauguzi hao wa muhimbili. Walimsubiri mzee yule alirudi ikiwa Nyogoso naye hali yake ikizidi kuwa tete, kiasi kwamba hata kupumua alipumua kwa tabu sana. Ghafla macho yake yaliona giza nene, alihisi maraika mtoa roho kaketi kando ya kitanda chake. Kijasho chembamba nacho kilianza kumvuja kunako mwili wake,machozi nayo hayakuachwa nyuma. Yalimtoka mithili maji katika mboni zake wakati huo ndani ya nafsi yake akijiuliza "Endapo kama nikifa mimi.. Ni nani atakayempelekea mama yangu taarifa kuhusu kifo changu?..". Alijiuliza Nyogoso muda huo jasho kali likiendelea kumtoka, pole pole kasi ya kupumua nayo ikiendelea kupungua kila masaa yalivyozidi kutaladadi.

Lakini pindi mzoa takataka Nyogoso alipokuwa kwenye hali hiyo ya kupata shida katika wodi aliyolazwa. Punde ndani ya wodi hiyo aliingia mganga mkuu, mganga huyo alimtazama Nyogoso pale kitandani akatikisa kichwa ishara ya kusikitika kisha akatoka chumbani humo halafu muda mfupi akarejea na muuguzi mmoja kati ya wengi waliokuwepo hospitalini hapo.

"Unajua alipo pokelewa huyu mtu nikajua kabisa huyu ni mtu aliyetelekezwa, ndio maana niakatoa amri matibabu yasitishwe. Kwahiyo basi kinacho takiwa hapa kufanya ni kitu kimoja cha maana..". Aliongea maneno hayo mganga mkuu mkuu akimuasa muuguzi.

"Ndio, jambo gani hilo?.." Muuguzi huyo alihoji.

"Chukua simu yako, haraka sana mpige picha huyu kijana kisha isambaze kwenye mitandao ya kijamii huwenda akawa na watu wanao mfahamu, kwahiyo itasaidia endapo kama watakuja kumchukuwa mtu wao au kughalamia ghalama za matibabu. Hatufanyi kazi ya kanisa maana kuitafuta Elimu yetu ghalama ilitumika ". Alijibu mganga mkuu huku akiiweka vizur miwani yake ambayo muda wote ilikuwa ikilegalega juu ya pua. Zaozi hilo la kumpiga picha mzoa takataka Nyogoso lilianza kufanyika, baada ya dakika kadhaa picha za Nyogoso ziliwekwa kwenye mtandao wenye wafuasi wengi Duniani. Mtandao wa Facebook. Picha hizo za Nyogoso zilambatanishwa na maneno yaliyokuwa yakiwataka ndugu zake wajitokeze kumsaidia. Ni picha ambazo zilisambazwa na watu wengi na kwenye makundi mbali mbali katika mtandao huo lakini yote kwa yote kitendo hicho hakikuweza kusaidia kitu, ilihali ilifikia hatua sasa pumzi ya Nyogoso ikaanza kukata,alipua kwa mbali sana. Na mara baada wauguzi kugundua kuwa Nyogoso pumzi ya Nyogoso inataraji kukata muda wowote, haraka sana walimfunika shuka jeupe kuanzia miguu mpaka kichwani kisha wakapeleka taarifa kwenye chombo cha habari ITV kuhuhusi kifo chake. Muda wa taarifa ya habari ulipo wadia mnamo saa mbili kamili usiku, taarifa ya kijana Nyogoso ilirushwa mubashara. Muda huo huo mama Mazoea alikuwa sebuleni akitazama runinga yake, alipenda sana kuangalia taarifa ya habari. Alistuka baada kuona picha ya Nyogoso, kijana ambaye ndio chanzo cha binti yake kunywa sumu kwa dhumuni la kujiuwa. Picha ya Nyogoso aliikumbuka vema mara baada kuiona kwenye runinga "Lazima nimfuate huyu kijana" Alijiapiza mama Mazoea. Kesho yake asubuhi mapema, mama huyo aliendesha gari lake kuelekea muhimbili. Alipofika alionanana na moja ya wauguzi, akamueleza kwa kina juu ya taarifa waliyotoa jana kwenye chombo cha habari. Kwa sauti kali muuguzi huyo alisema " Anhaa wewe ndio ndugu yake kumbe?.."

"Ndio. Naomba unisaidie nikamuone alipolazwa au tayari emefariki mumemuweka monchwari?.." Aliuliza mama Mazoea kwa taharuki ya hali ya juu,kwani aliamini uwepo wa kijana mzoa takataka huwenda ukarejesha uzima wa Mazoea ambaye naye hali yake ilikuwa si shwari baada kunywa sumu. Sababu kuu ya kufanya hivyo ikiwa imesababishwa na yeye mwenye mama Mazoea aliyeingilia kati penzi la binti yake aliyeamua kuliekeza kwa Nyogoso kijana mzoa takataka.

"Ndio utampata, lakini lazima ujiongeze kidogo" Aliongeza kusema muuguzi huyo.

"Unamaana gani? Nisaidie. Wewe ni mwanamke mwenzangu ujue" Alijibu mama Mazoea kwa sauti ya chini kabisa iliyojaa upole ndani yake.

"Sawa wewe ni mwanamke mwenzangu sikatai, lakini ukae ukijua hapa ni mjini. Nategemewa na familia yangu. Ila kama hutaki basi Sawa! Na siku zote ukae ukijua kuwa mkono mtupu haulambwi" Aliongea muuguzi huyo wakati huo akipandisha mapega yake huku macho yake yakiitazma kila pande akiwa na wingi wa wasi wasi. Maneno hayo yalimfanya mama Mazoea kutambua kitu anacho hitaji muuguzi. Pesa kwake sio tatizo, haraka sana alifungua pochi yake kisha akatoa kiasi cha fedha shilingi laki nne akamkabidhi muuguzi huyo. Tabasamu bashasha lilionekana kwa muuguzi huyo, kwa mara nyingine tena akatazama kila pande akiwa kwenye moja ya koldo, alipokwisha kujihakikishia kuwa hakuna mtu anayekatiza au kuonekana jirani na hapo waliposimama alipokea pasipo hata kuzihesabu kisha akasema "Mama, pesa zote hizi zangu?.."

"Ndio, najua unaogopa kuhakiki ila hicho ni kiasi cha shilingi laki nne" Alijibu mama Mazoea. Hatimaye rushwa hiyo ilimfanya kutimiziwa hitaji lake, alipelekwa wodi aliyolazwa Nyogoso. Walimkuta si walio au wa kesho, mzoa takataka huyo alipumua kwa shida huku sehemu mbali kichwani zikivuja damu. Muda huo huo mganga mkuu aliingia wodin humo kwa sauti kali iliyojaa dharau ndani yake akasema "Naona mpaka mtangaziwe ndio mjitokeze si ndio? Acheni mambo yenu ya kiswahili bwana" Aliongea maneno hayo mganga huyo akimwambia mama Mazoea. Mama huyo naye hata asijibu neno lolote, alikaa kimya mithili ya maji ya mtungini. Lakini mwisho wa yote alikamilisha taratibu aliotakiwa kufanya, hatimaye jitihada za kuokoa uhai wa mzoa takataka ukaanza kufanyika. Pesa iliongea, jopo la madakari lilijazana wodi aliyolazwa Nyogoso, walipishana mara kwa mara. Huyu aliingia huyu alitoka, yote hiyo kuhakikisha Nyogoso anapona.



***BAADA WIKI MOJA***http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Hali ya Nyogoso iliianza kuimalika, haikuchukuwa siku nyingi zaidi mbele alirudi katika hali yake kama ilivyokuwa awali. Na hapo liruhusiwa kurudi nyumbani. Lakini baada Nyogoso kuondoka Hospital, zilipita dakika kadhaa mama Mazoea alifika kwa niaba ya kumjulia hali. Alistuka alipopewa taarifa kuwa mgonjwa wake ameruhusiwa dakika chache zilizopita.

"Ni nani aliyewaambia mumruhusu bila idhini yangu?.. Mmefanya nini sasa?.." Aliongea mama Mazoea kwa hasira kisha akarejea kwenye gari lake,akaliendesha kwa kasi ya ajabu tayari kwa safari ya kuanza kutafuta mzoa takataka kipenzi cha binti yake huku akiamini kuwa kupatikana kwake ndio utaleta unafuuu kwa binti yake ambaye hali yake haikuwa Sawa asilimia mia moja.

"Laah! Nitamapata wapi kijana huyu ndani ya hili jiji?.." Alijiuliza mama Mazoea wakati huo mapigo ya moyo wake yakienda kasi, hofu nayo ikimjaa vilivyo hasa akifikiria hali aliyonayo binti yake.





ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog