Search This Blog

Tuesday 1 November 2022

UTANIKUMBUKA TU! - 5

 





    Simulizi : Utanikumbuka Tu!
    Sehemu Ya Tano (5)




    Mapenzi yanauma sana hasa kupenda usipo pendwa. Mrembo Najrat hakujua na wala hakudhania kama Kayumba angekataa ombi lake eti kisa tayari kazama kwenye penzi la mama ntilie. Alikasirika sana, alipiga kofi meza akajiinamia huku machozi yalimtoka. Alipokuwa kwenye hali hiyo ya majonzi, ghafla simu yake iliita. Akakurupuka akafungua mkoba wake akaitoa akaitazama akaona Catherine ndiye aliyempigia, alibonyeza kitufe cha kijani akiweka simu sokoni.

    "Ahahahahaha...", kicheko cha madaha kilisikika kutoka kwa Catherine. Cheko hilo la Catherine lilizidi kumkera Najrat, aliona kama Catherine anamdhihaki. "Unacheka nini sasa?..", kwa jazba aliuliza Najrat. Catherine akajibu "Nimefurahi tu Najrat wala hakuna kitu kingine kinacho ni fanya nicheke.. Ammh bila shaka Naj unaujua vizuuuri moto wa kifuu,huu ni moto ambao unawaka kwa kasi lakini kasi yake inakuwa ya muda mfupi. Nasema hivi sitokubali"

    "Hutakubali? Unamaana gani?..", alihoji Najrat.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ahahahaha, nadhani ipo siku utanielewa tu. Na zaidi napenda nikuonye, achana na huyo mwanaume. La sivyo utanitambua vizuri", alijibu Catherine kwa ghadhabu dhofu lihali. Najrat aliona endapo kama atakaa kimya basi Catherine atajua kuwa amemuogopa. Hivyo naye akajibu

    "Nisikilize Catherine, wewe ni fukara kama walivyo mafukara wengine. Fanya ufanyalo, daima kisigino kitabaki kuwa nyuma. Hunitishi na wala hunibabaishi, vita hii Itaendelea"

    "Ahahahaha..Ahahahahah", alianguka kicheko Catherine baada kuyasikia maneno aliyoongea Najrat kwa ujasiri. Alipokatisha kicheko hicho akasema "Vizuri sana mrembo Najrat, mtoto wa kiarabu. Nafurahi sana kusikia maneno yako matamu. Kwaheri", kwisha kusema hivyo akakata simu. Pumzi alishusha Najrat, mbali na Kayumba, Catherine naye alimvuruga vilivyo akili yake. Na hapo akaona bora urudi nyumbani kutuliza akili huku akipanga namna gani ya kukabiliana na Catherine kwani alijua fika urafiki baina ya Catherine na yeye umekufa. Kayumba alipofika nyumbani alifuta namba ya Najrat, lakini pia alifuta namba ya Catherine ingawa hakujua kuwa mbali na namba ya Najrat, namba ya pili ilikuwa namba ya Catherine.

    "Hata hii nayo nafuta tu, sitaki upuuzi na wala sipo tayari kumpoteza Diana wangu", alijisemea Kayumba. Siku zilisonga, miezi nayo ikasogea penzi la Kayumba na Diana lilizidi kupamba moto . Ilikuwa siku moja, mchana. Diana alisikia sauti ikisema "Hivi wewe binti hiki kinanda cha urithi wenu?..", Diana aliposikia sauti hiyo aligeuka kule ilipokuwa ikitokea, alistuka kumuona mama mmliki wa kinanda hicho, alikuja kudai kodi yake "Hapana mama ila.."

    "Ila nini? Nasema toa vitu vyako uondoke humu,hujanichangia hata tofali", alifoka mama huyo. Mzozo mkubwa unazuka mahala hapo, sababu kuu ikiwa kodi ya kibanda anachofanyia kazi Diana. Na punde si punde mama huyo alitoa vyombo ndani na hata asiitaji utetezi wa Diana. Lakini wa kati kitendo hicho kikiendelea, ghafla kando inasimama gari Hilax. Ndani ya gari hiyo anashuka mwanaume mtanashati aliyependeza kwa mavazi yake nadhifu. Alitaharuki kuona kuona umati wa watu ukiwa umekusanyika huku katika ya umati huo akionekana msichana akilia machozi mbele ya mwanamama wa makamo. Aliitwa Yoram. Pasipo kupoteza muda Yoram aliingilia kati mzozo huo, akaamulia na kuahidi kumsaidia Diana. Pasipo kupoteza wakati, Yoram alimlipa fedha yake mama huyo mwenye kibanda. Tangu siku hiyo Yarom aliendelea kwenda kumona Diana, alimsabahi na kumuachia fedha za matumizi. Diana alifurahi sana, hasa hasa akivutiwa na upole alionao kijana huyo mtanashati.

    "Nimevutiwa na ukalimu wako Diana, vipi naweza kupata namba yako ya simu?..", aliongea Yoram siku moja baada kumtembelea Diana kama ilivyo ada. Diana aliachia tabasamu, na wala hakusita kumpatia ingawa aliamini kuwa Yoram hatoweza kumueleza mambo mengine tofauti na urafiki tu. Ukaribu huo ulidumu kwa takribani wiki zisizo zidi mbili, na mwishowe Yoram aliamua kuelezea hisia zake kwa Diana.

    "Mbona mapema sana Yoram?..", aliuliza Diana.

    "Ni kweli Diana ila moyo wangu unakosa amani kwa ajiri yako, vile vile nakosa raha pindi ninapoona mrembo kama wewe kuifubaza ngozi yako kwenye kazi hii", Yoram alijibu.

    "Naomba unipe nafasi ndani ya moyo wako, hakika nitakutunza. Sipo tayari kukuchezea Diana. Nia yangu nikuoe uwe mke wangu wa ndani", aliongeza Yoram. Alionyesha nia ya kuanza mahusiano na Diana. Diana alikuwa mgumu kukubali suala hilo, na hivyo aliomba nafasi afikirie. Yoram hakuwa mgumu kutoa nafasi, ali kubali ingawaje alimsisitiza amkubalie ombi lake. Siku takribani mbili, zilikuwa siku tata kwa Diana. Kila alipolala alikuwa akimfikiria Yoram kijana mtanashati aliyevutia vema machoni hasa kwa sura yake na mavazi nadhifu.

    Aliachia tabasamu, na hakuona sababu ya kumkataa Yoram hasa akikumbuka msaada aliompatia, Diana aliwaza ni maisha gani ambayo angeishi hasa akizingatia biashara yake ilikuwa imeshaanza kuyumba. Lakini mbali na suala hilo, bado katika maisha yake aliona anamuhitaji Kayumba. Kwahiyo aliwaza alishindwa afanye nini, mpaka usingizi unampitia alikuwa bado hajapata jibu sahihi.

    Siku iliyofuata alihudhuria kazini kama ilivyo ada huku akilini akiwa mwake akiendelea kulifikiria ombi la Yoram.

    "Ni miaka mingi sasa nikiwa katika kazi hii ya umama lishe, hakuna maendeleo yoyote ya kujivunia. Aaah japo nampenda Kayumba ila ngoja nimkubarie na huyu mkaka ingawa nitajitahidi nisimpe penzi ili Kayumba aendelee kuishi katika moyo wangu", aliwaza Diana. Mawazo ambayo yalikuwa haba kwa mwanaume yoyote lijali kumlia kitu chake pasipo kukuomba penzi. Tabasamu pana alionyesha Diana, aliona hicho alichokiwaza ni kitu chema. Punde Yoram alifika hapo mgahawani, siku hiyo alikuja na gari nyingine Rav4 nyeusi iliyoonekana mpya. Diana alipagawa, wakati huo Yoram alishuka kwenye gari akaliegemea gari kisha akamuita Diana kwa ishara ya mkono. Haraka sana Diana akastisha zoezi la kuhudumia wateja wake, akatii wito kwanza.

    "Habari yako Yoram", Diana alimsabahi Yoram.

    "Njema habari za kazi"

    "Salama tu karibu".

    "Asante", Yorama akafungua mlango wa gari, akaingiza mkono kisha akatoka na mfuko ambao ulikuwa na viti ndani.

    "Hii zawadi yako Diana, utaitazama utakapo rudi nyumbani", aliongeza kusema Yoram huku akimkabidhi Diana mfuko huo. Diana alipokea kisha akajibu "Asante sana Yoram... Ammh na kuhusu lile ombi lako, nimelikubali"

    Wooow! Asante sana Diana. Ukweli nimefurahi sana. Na zaidi naomba leo baadaye jioni ujiandae tutoke ", aliongea Yoram kwa tabasamu bashasha. Diana alikubaliana na hitaji la Yoram. Jioni ilipowadia alifunga biashara yake akarudi nyumbani kujiandaa haraka haraka. Na wala hakumwambia Kayumba wapi anapoelekea licha ya kwamba Kayumba kumuuliza baada kuona akiwa bize. "Diana unajua sikuelewi?.."

    "Kayumba mpenzi wangu hapa mjini ngoja nikatafute pesa", alijibu Diana.

    "Pesa? Inamaana siku hizi unafanya kazi mpaka jioni?..", aliendelea kuhoji Kayumba kwa mashaka. Diana akaangua kicheko kisha akajibu "Nikirudi tutaongea vizuri", kwisha kusema hivyo akatokomea kwenye moja ya uchochoro huku nyuma akimuacha Kayumba akiwa na sintofahamu. Wawili hao walikutana, Yoram alikuja na gari nyingine tofauti na ile aliyokuja nayo mchana,hakika kilikuwa ni kitendo ambacho kilimfanya Diana kuamini kuwa kijana huyo pesa kwake sio tatizo.

    Muda ilizidi kwenda Kayumba akiwa amsubiri Diana ili azungumze naye kwa kina, kwani Kayumba aliona Diana amemletea dharau na hivyo hana budi kuchukuwa jukumu kama mume. Lakini Diana hakutokea, mpaka inatimia usiku wa saa sita ndio akarudi. Alibisha hodi Kayumba aliamka kwenda kumfungulia mlango huku akiwa na wingi wa hasira.

    "Atanieleza vizuri wapi ametoka usiku huu", alijisemea Kayumba wakati huo akifungua mlango. Alistuka kumuona Diana amelewa, muda huo huo kwa mbali aliona gari ndogo likiishia zake.

    "Diana umetoka wapi na kwanini umelewa ?..", alifoka Kayumba. Diana huku akiyumba yumba akajibu "Nimetoka wapi? Pumbafu sana wewe. Maswali gani hayo unayo niuliza? Unalipa kodi wewe kula kulala? Hebu achana na mimi mwanaume suruali mbwa wewe",alijibu Diana kwa sauti ya kilevi kisha akamsukuma Kayumba.





    Kayumba alishika kichwa asiyaamini macho yake kwa kile anachokiona. "Diana?", alisema Kayumba huku akimsindikiza Diana kwa macho ambaye alikuwa akiingia chumbani kwa kuyumba yumba,pombe ikiwa imemkolea. Alijua fika amemvunjia heshima, lakini hakutaka kumuadhibu zaidi alingojea papambazuke ndipo amuulize ni kitu gani kilicho mpelekea alewa.

    Kesho yake asubuhi, Diana kabla hajaelekea kazini Kayumba alimuuliza sababu ipi hasa iliyomfanya anywe pombe. Diana akajibu kwa dharau na kusisitiza kuwa Kayumba hapaswi kujua "Hupaswi kujua Kayumba kichwa changu kinawaza nini, zaidi wewe kaa nikileta tutakula. Hayo mengine yaache kama yalivyo bwana"

    "Kwahiyo sipaswi kujua?..", Kayumba aliuliza kwa jazba akionyesha kukerwa na majibu hayo. Diana hakumjibu, alikaa kimya kitendo ambacho Kayumba alikichukulia kama dharau. Alimpigia kofi. "Kayumba, unamamlaka gani ya kunipiga mimi? Eeh siku zote nimekufuga kama mtoto mdogo humu ndani leo hii unathubutu kunyanyua mkono wako na kunipiga?..", Diana alifoka baada kupigwa na Kayumba.

    "Ndio mimi ni mumeo kwahiyo mamlaka ninayo ukinikosea", alijibu Kayumba kwa kujiamini kabisa.

    "Eti mamlaka unayo kwa kuwa mimi mkeo, sasa kati ya wewe na mimi nani mke na nani mume?..", aliongea kwa dharau Diana.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hulipi kodi ya chumba, nguo mpaka ya ndani nakununulia mimi sasa unawezaje kuniwekea mamlaka? Nasema siwezi kukubali", aliongeza kusema Diana kwa sauti kali, jambo ambalo liliweza kuzua tafarani kwa majirani kujongea mahali hapo ili kujua kipi kinacho endelea. Akiwa amefura hasira, Diana alikusanya nguo kadhaa za Kayumba akaziweka kwenye begi ambalo lilionekana kuwa kukuuu kisha akalitupa nje "Mkataba wangu na wewe umekwisha, ondoka nyumbani kwangu", aliongea Diana. Kayumba alistuka baada kuona uamuzi huo wa Diana. "Diana leo hii unachukuwa maamuzi haya? Umesahau kuwa wewe ndio uliyeniahidi hutonisaliti wala kulivunja penzi letu. Sikuhitaji kupenda tena Diana..", chozi lilimtoka Kayumba, ni kama Diana alitonesha donda la mapenzi ambalo tayari lilikuwa likielekea kupona. Ila Diana hakuweza kulionea imani chozi hilo, alizidi kusisitiza Kayumba aondoke kwenye nyumba yake. Kayumba alichukuwa begi lake, akazipiga hatua za kichovu akipenya kwenye umati wa watu uliokuwa umekusanyika. Begi began kichwa chini, chozi la mnyonge likimbubujika Kayumba aliishia zake.

    Mara baada Kayumba kuondoka, hima Diana alichukuwa simu akampigia Yoram, kijana mtanashati.

    "Kuna mtu kanitibua mpenzi, naomba siku ya leo niwe na wewe", aliongea Diana kwa sauti ya kudeke. Sauti ambayo ilipenya vema kwenye sikio la Yoram.

    "Mmh", Yoram aliguna kisha akahoji "Nani kukutibua mpenzi wangu?.."

    "Mjinga mmoja hivi, si unajua tena maisha ya uswahilini?.."

    "Sawa, usijali nakuja sasa hivi"

    "Kweli? Nakupenda sana Yoram wangu"

    "Nakupenda pia"

    Tabasamu hafifu lilionekana kwenye uso wa Diana, hakika alivutiwa sana na Yoram na hivyo hakuweza kujutia uamuzi aliomchukulia Kayumba. Kwa muda wa robo saa, Yoram aliwasili akiwa na gari nyingine tofauti na ile aliyokuwa nayo jana jioni pindi walipoenda kupata moja baridi moja ya moto kwenye kumbi ya starehe.

    "Twende tukaponde raha mpenzi wangu", aliongea Yoram huku akimkumbatia Diana.

    "Naam! Huwenda maisha nikawa nimeyakosea. Ni wazi jina langu linaendana na haya yanayo tokea, Kayumba nimekosea nini kwenye ulimwengu huu wa mapenzi? Nifanye nini mimi? Furaha ya penzi imekuwa sio ya kudumu, ni kama kidondo hiki kimegeuka kuwa donda ndugu. Yani donda lisilo pona. Catherine ni mwanamke ambaye nilikupenda kwa dhati, ila mwishowe umenisaliti kisa sina elimu wala kipato. Huwenda ulikuwa sahihi kwa wakati wako, lakini sio mpaka kwa Diana. Mama ntilie mwenye maisha ya chini, asiye na elimu. Eti naye leo hii kakivunja kikombe cha makubalino kabisa amesahau ya kwamba yeye ndio aliyenishawishi nimpende. Ujinga ni wangu Kayumba, kuthubutu kuzama mazima kwenye penzi lisilo na dhamana... Looh hivi haya mapenzi ni kitu gani, wapi nakosea?.. ", akiwa kando ya barabara, begi begani kichwa chini jasho lililochanganyana na machozi likimbubujika, Kayumba alijisema maneno hayo na punde si punde akaimba wimbo wake ambao ulizungumzia safari yake katika mapenzi. #Dharuba la mapenzi. Ndio wimbo aliokuwa akiimba huku akitembea.

    Nyuma yake unasikika mburuzo wa breki ya gari, Kayumba hakutishika wala hakuhofia wakati huo ndani ya gari lile lililotoa mlio wa breki alionekana mrembo akitazama nyuma kupitia kioo cha pembeni cha gari lake (Side Mirror), muda huo huo mrembo huyo akashuka. Ni Najrat. Najrat alipigwa na butwaa kumuona Kayumba kwa mara nyingine tena, hakutaka kupoteza muda hima alimkimbilia akihitaji kuomba nafasi nyingine ndani ya moyo wa Kayumba.

    "Kayumba.. Kayumba.. Kayumba..", aliita Najrat huku akimkimbilia Kayumba. Usongo wa mawazo uliuteka vema ubongo wake, katu Kayumba hakuweza kusikia sauti ya Najrat. Aliendelea na safari yake akiamua kurudi mtaani kwa mara nyingine tena akiamini hapo awali alifanya kosa kumiliki wa na Najrat. Punde Najrat akamgusa bega, Kayumba akiendelea kuimba kwa majonzi wimbo wake akageuka nyuma akamuona mrembo Najrat akiachia tabasamu bashasha. Moyo wa Najrat ulijaa taharuki baada kuona kijana Kayumba akitiririsha chozi, ghafla tabasamu alilokuwa akilionyesha lilitoweka akamuuliza "Mbona hivyo Kayumba wangu?..", Kayumba hakujibu aliishia tu kutazama Najrat na kisha akaondoka zake. Hali hiyo haikumfurahisha Najrat, alimshika mkono akambembeleza ili ikiwezekana waende sehemu turivu ilie waweze kuongea kwa kina zaidi. Ni suala ambalo Najrat alilifanikisha, aliambatana na Kayumba kuelekea mahali alipolisimamisha gari lake. Wakaingia wakaondoka.

    "Karibu nyumbani kwetu Kayumba, hapa naishi peke yangu wazazi wangu wapo nchini Indonesia kibiashara zaidi. Awali nilikuwa nimepanga nyumba, nikawa naishi pake yangu ila kwa sasa nimeamua kurudi kwa wazazi wangu", aliongea Najrat kwa tabasamu bashasha akimkarimu Kayumba. Kayumba alilijibu tabasamu hilo la Najrat kisha akasema "Sasa mbona na wewe hujaenda?."

    "Ahahahaha, nitaenda tu Kayumba ila bado nipo nipo kwanza", alijibu Najrat akianza kwa kuangua kicheko. Juisi baridi aliletewa Kayumba, na sasa Najrat akahitaji kujua ni kipi kilichomliza Kayumba. Kayumba alieleza yote, na mwisho akasisitiza akasema "Naapa sitokuja kumpenda tena mwanamke, maumivu sasa basi"

    "Hapana usiseme hivyo Kayumba, awali wa yote pole kwa yaliyo kukuta. Na mbali na hayo mimi ndio chaguo lako sahihi", aliongea Najrat kwa sauti ya chini huku akiikunja vema miguu yake laini kwenye sofa.

    "Unanipenda!?.",alistaajabu Kayumba kisha akaongeza kusema "Hapana Najrat, na mimi nina moyo sio jiwe. Nimeumia vya kutosha, sasa mapenzi basi", alisisitiza.



    Alionekana Catherine akiwa ameketi kwenye sofa sebuleni, juu kwenye meza ziloonekana chupa za pombe mbali mbali. Meza ilikuwa imechafuka huku Catherine akiwa amelewa tila lila.

    "Edgaa", kwa sauti ya kilevi Catherine alipasa sauti kumuita Edga. Ni yule yule Edga mchizi wale Kayumba ambaye wamepotezana kwa siku nyingi mno. Baada Catherine kuchukuwa jukumu la kumtibia Edga, hatimaye aliweza kumshawishi akaishi naye nyumbani kwake, ni baada Catherine kuhitaji kujua ukweli wa maisha anayo ishi Edga, ambapo naye alimueleza kuw hana pa kushika wala hana kazi tegemezi. Ni jambo ambalo Catherine aliona endapo kama atamuacha arudi mtaani ikiwa tayari anajeraha, ataishi maisha ya tabu mara mbili ya hapo awali. Na hivyo alimua kwenda kuishi naye nyumbani kwake. Edga alitii wito, hali yake ilikuwa tayari imetengamaa asilimia mia moja.

    "Naam dada", aliitikia Edga huku akiketi kwenye sofa.

    "Umekuja, sawa", aliongea kwa sauti ya kilevi Catherine, akachukuwa bashasha ya kaki iliyokuwa kando yake akaifungua akatoa picha ya Najrat.

    "Tazama hii picha vizuri", aliongeza kusema safari hiyo akimkabidhi Edga picha hiyo ya Najrat. Akiwa na maswali mengi kichwani mwake kuhusu picha hiyo, alipokea.

    "Nadhani unamjua vizuri huyo mtu, sasa sikia Edga. Mimi sipendi urudi tena kuishi maisha yako ya mtaani kuishi kama teja. Nataka nikupe maisha bora", aliongea Catherine. Edga alistuka kuyasikia maneno hayo, alijuliza Catherine anamaana gani kusema hivyo.

    "Una...maa.. Unamaana gani dada", alihoji Edga kwa sauti ya woga.

    "Ahahahaha hahahah", Catherine aliangua kicheko kisha akasema "Edga wewe ni mwanaume, kwahiyo katika hili sidhani mama utaniangusha. Anaitwa Najrat, nataka ufanye kazi ukamuuwe. Sitaki kumuona akiendelea kuishi kwenye ulimwengu huuu"

    "Nimuuwe? Lakini dada huyu si rafiki yako?..", kwa taharuki kubwa aliuliza Kayumba.

    "Alikuwa rafiki yangu lakini kwa sasa huyu ni adui yangu, kwahiyo hilo lisikupe shida", alijibu Catherine kisha akanywa mfululizo pombe iliyokuwa kweny grasi.

    "Nakupa ramani anapoishi", baada kushusha mezani grasi, aliongeza kusema Catherine. Papo hapo akaanza kumuelekeza Edga mahali anapoishi Najrat. Alipohitimisha saula hilo akaichomoa bastora mpya kwenye mkoba wake akaiweka juu kwenye meza. Catherine alichafukwa na roho. Kwa mara nyingine tena Edga anaiona siraha ya moto tangu akimbie kundi la Boko. Naam! Tangu azaliwe hajawah hujawahi kumwaga damu, aliogopa sana Edga alijikuta akitetemeka, Catherine hakujali aliendelea kumimina pombe grasi moja baada ya nyingine.

    "Edga! Bila shaka umenielewa. Sihitaji mjadala nataka kazi hiyo usifanye haraka sana iwezekanavyo. Kwa tumia hii bastora, nenda kasambaratishe ubongo wa yule takataka", alisisitiza kw jazba Catherine hakuona njia nyingine zaidi ya kumuuwa Najrat akiamini kuwa hiyo ndio njia pekee iliyobakia.

    Edga akaichukuwa ile bastora pamoja na picha ya Catherine,akazipiga hatua kwa mwendo wa kichovu kuelekea chumbani kwake kujishauri kabla ya kuchukuwa maamuzi ya kwenda kumwaga damu ya Najrat, mrembo ambaye tayari ameshamuweka Kayumba kwenye himaya yake wakati huo Kayumba na Edga kabla ya kupotezana walikuwa ni marafiki wa kufa na kuzikana...





    Akiwa mchovu, akajitupa kitandani. Alijilaza chali huku kijasho chembamba kikiuvagaa mweli wake,punde akainuka akaketi akajiinamia akatafakari kuhusu kazi aliyopewa. Kazi ya kumwaga damu isiyo na hatia. Machozi yakaanza kumtoka huku akiikodolea macho bastora aliyokabidhiwa na Catherine kwa naiba ya kwenda kumuuwa Najrat. Edga alishusha pumzi ndefu, akaichukuwa picha ya Najrat akaitzama mara mbili mbili huku giza nene likiwa bado limetanda kichwani mwake asijue cha kufanya. Aliteseka. Na wakati akiwa katika hali hiyo ya sintofahamu, mara ghafla katika simu yake unaingia ujumbe mfupi (sms), akajikuta chozi jepesi liliokuwa likielea kwenye mboni za macho yake, akaichukuwa siku hiyo akaufungua ujumbe ulioingia "Huna haja ya kufikiria sana Edga, cha muhimu haraka sana iwezekanavvyo ufanye hiyo kazi", alisomeka hivyo ujumbe huo. Ujumbe ambao aliutuma Catherine, ulimsisitiza Edga kwenda kumuuwa Najrat. Alichoka mara mbili zaidi ya hapo awali, kwa mara nyingine tena akajilaza chali kitandani, punde akapitiwa na usingizi mzito. Aliamka jioni, napo alienda bafuni kuoga na kisha kurudia tena kulala. Siku hiyo hakuwa sawa kabisa.



    Usiku wa siku hiyo, walionekana Yoram na Diana wakiponda raha kwenye moja ya clabu jijini. Wawili hao walikula na kunywa, Diana akajikuta akimsahau kabisa Kayumba, akamuona Yoram ndio mwanaume sahihi kwa wakati huo. Ahadi mbali mbali walipeana wapenzi hao, kila mmoja alimsisitiza mwenzie kutosaliti penzi lao changa.

    "Hakika Yoram nitakupenda daima", aliongea Diana huku akipata moja moto moja baridi.

    "Kweli Diana?..", aliuliza Yoram.

    "Ndio, siwezi kukudanganya mimi", Diana alithibitisha. Yoram aliangua kicheko kisha akasema "Na mimi nitakupenda daima mpenzi wangu". Rohw mstarehe ilitamaraki katika kumbi hiyo ya starehe. Upande wa pili alionekana mrembo Najrat akizidi kumbembeleza Kayumba ili akubali ombi lake la kutaka kuwa wapenzi, lakini bado Kayumba aliweka kizingiti, aliapa kamwe hatopenda tena.

    "Kayumba ni kwanini hutaki kujali hisia zangu? Naumia Kayumba tafadhali nionee huruma tafadhali", aliendelea kubembeleza Najrat.

    "Najrat.. Najrat.. Ni vile hujui namna majeraha ya moyo wangu yanavyoniuma. Nyinyi wanawake sijui huwa mnamapepo gani katika suala nzima la mapenzi, nasema basi Najrat mapenzi basi", aliongea Kayumba kwa msisitizo. Najrat hakuongeza neno lolote, alikaa kimya huku akimtazama Kayumba wakati huo kichwani mwake akitafakari neno lingine la kumueleza.

    "Nikufanyie nini labda ili uweze kunielewa?..", aliuliza Najrat.

    "Kwa sasa sitotoka unijibu, muda huu tayari ni usiku. Kesho nitahitaji jibu lako...",aliongeza kusema Najrat.

    "Sawa hakuna tatizo", Kayumba alikubaliana na Najrat, ambapo baada ya hayo Najrat alimpeleka Kayumba chumba alichomuandalia kisha naye akarejea chumbani mwake kulala ikiwa akilini akimfikiria Kayumba.

    Usiku huo ulikuwa mrefu kwa Kayumba, aliwaza hili na lile. Aliona hana haja tena ya kuendeleza wimbi la mapenzi, na badala yake akaona ni heri alirudi mtaani kutafuta fedha kisha arejee kijijini kwao. Dar es salaam aliona chungu, hakuwa na sababu ya kuendelea kungalisha sura ilihali moyo wangu ake ukivuja maumivu ambayo ni vigumu kuyasahau. Pumzi ndefu alishusha Kayumba, na sasa akafikiria njia gani atumie kukataa ombi la Najrat.

    "Nitampa mtihani ambao ni ngumu sana kuutatua", baada kutafakari kwa kina alijisemea maneno hayo kisha akajifunika shuka akaanza safari ya kuusaka usingizi.

    Asubuhi palipo kucha, mlango wa chumba alicholala Kayumba ulibishwa hodi.

    "Pita upo wazi", aliongea Kayumba, punde si punde aliingia Najrat akiwa amebeba chai.

    "Habari za asubuhi Kayumba", kwa tabasamu bashasha huku akimsogelea Kayumba pale kitandani, Najrat alimsabahi.

    "Njema tu Naj karibu"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Asante, karibu chai", aliongeza kusema Najrat wakati huo akimimina chai kwenye kikombe na kisha akamkabidhi.

    "Haya pasha tumbo, mimi nipo sebuleni nafanya usafi",huku akiondoka chumbani mule Najrat akimwambia hivyo Kayumba. Na kabla hajaondoka, Kayumba alisema "Sawa lakini kuhusu suala lile, nipo tayari ila kwa sharti moja"

    "Sharti? Sharti lipi hilo Kayumba", Kayumba alikaa kimya kidogo kisha akasema "Mtafute rafiki yangu, anaitwa Edga. Kazi yake ni kubeba mizigo kuishusha kwenye maroli"

    "Yukoje huyo mtu?..", aliuliza Najrat wakati huo akimsogelea Kayumba. Kayumba alieleza muonekano wa Edga pasipo kificho kwani aliamini licha ya kufanya hicho ila kamwe Najrat hatoweza kuupiku mtihani huo kwa sababu jiji ni kubwa, na vile vile lina watu wengi sana, pasipo kujua kuwa mchizi wake yupo kwenye mikono ya Catherine mpenzi wake wa zamani.

    "Kwahiyo nikifanikiwa, utakubali ombi langu?..", alirudia kuhoji Najrat.

    "Ndio, na nakuahidi nitakupenda kwa dhati", alijibu Kayumba.

    "Sawa nipo tayari kuifanya kazi yako", Najrat alisema kwa kujiamini. Alionyesha kuwa na nia ya kumtaka Kayumba, ila Kayumba kwa wakati huo hakuwa tayari tena kupenda kwani aliona hana nyota ya kupendwa zaidi ya kuumizwa. Mtihani huo Najrat aliopewa aliuona mkubwa sana, ni mtu ambaye hamfahamu sura wala umbile lake. Ni muonekano tu jinsi alivyo ndio aliofahamu kwa fikra za ubongo wake na kujaribu kujenga picha fulani katika kichwa chake.



    Pindi Najrat akiwza wapi aanzie wapi aishie kumtafuta Edga. Upande mwingine Catherine, mwanamke aliyeamua kuchagua maisha ya kunywa pombe akiamini anapunguza mawazo ya mapenzi. Anakumbuka kuwa kuna kijana anamfahamu yupo vizuri kwenye mipango ya kumwaga damu pasipo huruma, kijana huyo anayaendesha maisha yake kwa shughuli mbaya. Kuvunja maduka, hata kuuwa pia haoni hatari. Alikisa kichwa ishara ya kukubali jambo fulani, akamimina pombe kwenye grasi akanywa bunda moja kisha akachukuwa simu yake, haraka sana akampigia kijana huyo. "Hello Yoram, habari yako", aliongea Catherine mara baada kijana huyo kupokea simu.

    "Naam! Dada.."

    "Hebu njoo nyumbani haraka sana iwezekanavvyo", alisisitiza Catherine.

    "Sawa dada nakuja", alijibu Yoram. Kwa muda wa robo saa Yoram alitia maguu nyumbani kwa Catherine. Kijana huyo ni yule Yoram wa Diana.

    "Safi. Umekuja kwa wakati Yoram, kuna dili lipo mbele yako. Dili nono Yoram mtoto wa mjini..."

    "Dili? Dili gani hilo mamaa, funguka siunajua tena hapa mjini?.."

    "Lakini dili hili hautokuwa peke yako, kwa sababu ni dili ngumu. Kwahiyo basi utakuwa na jamaa"

    "Jamaa gani?..", aliuliza Yoram akitaka kumuona mtu atakaye shirikiana naye. Ndipo Catherine alipopasa sauti kumuita Edga. Punde Edga akatii wito.

    "Jamaa mwenyewe ni huyu hapa, pande la baba. Anaitwa Edga", Yoram alimtazama Edga kwa jicho la pekee, ni kama alimfahamu.

    "Anhaa sawa hakuna tatizo, habari yako braza", baada kumtazama kwa kina, alimsabahi.

    "Njema..", Edga akajibu kwa mkato wakati huo huo Catherine akamkabidhi Yoram picha ya Najrat kisha akasema "Sihitaji kabisa kuona sura ya huyu kiumbe"

    "Yani uanamanisha unamaana tukamuuwe?..",aliuliza Yoram kwa taharuki. Catherine kabla hajajibu alinyanyuka kutoka kwenye sofa, akasimama akamtazama Yoram akampulizia moshi wa sigara usoni kisha akajibu "Ndio, hilo jibu Yoram. Kuna pesa ya kutosha, nitawapatia kiasi chochote mtakacho taka", jibu la Catherine lilimpagawisha Yoram, hima akamgeukia Edga kisha akasema "Braza utaweza?..", Edga akaona tayari yupo kwenye himaya ya mtu asiye na hata chembe ya huruma, hivyo hakuwa na budi kukubali ili asiweke rehani maisha yake.

    "Ndio nipo tayari hata sasa hivi",alijibu kishujaa Edga

    "Ahahahaha", Catherine aliangua kicheko, akifurahishwa na jibu la Edga "Vizuri sana Edga, huo ndio uwanaume", baada kuhitimisha kicheko chake alisifu Catherine.



    Ndani ya Noah yenye rangi nyeusi, Catherine akiwa sambamba na Edga pamoja na Yoram. Walipanda kwa dhumuni la kwenda kupona mahali anapoishi Najrat. "Nimeona ramani itawachanganya, kwahiyo nimeamua kuwaleta mpaka mtaa anao ishi huyu binti. Na nyumba yao ile pale, pale pale iliposimama gari ndogo", aliongea Catherine huku akinyoosha kidole mahali ilipo nyumba anayoishi Najrat. Nje ya gati kwenye nyumba ile palikuwa na gari ndogo, punde katika gari ile alishuka Najrat na Kayumba. Catherine alistuka, hasira zilizidi kumjaa, kwa sauti ya ukali akasema "Mtu mwenyewe yule pale", Yoram alikodoa macho mbele kumtazama, wakati Edga alipoinua uso wake akajikuta akimuona Najrat tu huku Kayumba akiwa tayari ameingia ndani getini.

    "Bila shaka kazi imekwisha dada, wewe ondoa hofu", aliongea kwa kujiamini Yoram.

    "Nawategemea", alijibu Catherine na kisha akamkabidhi wa bastora. Pumzi NDEFU alishusha, ndani ya moyo wake akajisemea "Naj, wewe ni shetani hustahili kuwa hai", kwisha kujisemea hivyo akageuza gari kwa fujo kurudi nyumbani kwake baada kuwaonyesha watu wake mahali anapoishi Najrat. Lakini wakati wapo ndani ya gari wakirejea nyumbani, Yoram bado alionekana kumtazama Edga kwa mashaka. Na mwisho akamua kuvunja ukimya, akasema "Braza hivi unamfahamu Diana?.."

    "Diana?..ndio nani huyo?..", alihoji Edga kwa mshangao sababu jina hilo hajawahi kulisikia popote. Yoram akajibu.

    "Ndio, ama kwa jina lingine anaitwa Sinsia.."



    "Sinsia?..", Edga bado alijiuliza huku alikumbuka kuwa jina hilo linafanana na jina la mdogo wake aliyepotezana naye miaka mingi iliyopita. Na kabla hajajibu, sauti ya Catherine ilisikika ikiwaita,! +haraka sana wawili hao walitii wito. Meza ilionekana kujaa vinywaji mbali mbali hasa hasa pombe kali, Yoram na Catherine walikunywa mpaka kusaza ikiwa Edga u pembezoni akipata chakula cha bei ghali pamoja na juisi nzito. Hakuwa mlevi, na mara kadhaa Catherine alimtania kwa kumwambia kuwa anakosa vitu vingi sana kukiacha pombe. Edga aliishia kucheka tu. Ilipotimu mnamo saa tano usiku, Yoram alirejea nyumbani kwake akiwa tilalila. Alipofika alimkuta Diana amejiinamia, hasira zikiwa zimeuvagaa moyo wake.

    "Ulikuwa wapi?..", kwa sauti ya ukali Diana alimuuliza Yoram lakini naye hakumjibu, ambapo kwa mara nyingine tena Diana alihoji na ndipo Yoram akajibu "Akili yangu inavitu vingi sana, na pia huwa sipendi kufuatiliwa na mtu yoyote. Hebu lala sihitaji maswali yako ya kipuuzi" aliongea kwa sauti ya kilevi Yoram. Maneno hayo yalimuweka njia panda Diana. Ndani ya nafsi yake akajiuliza "Hapendi kufuatiliwa, mimi ni mchumba wake. Sasa kwa hali hii kweli kutakuw na msingi sahihi wa kujenga familia?..", ni swali ambalo Diana hakulipatia majibu, mwishowe naye aliamua kulala.



    Ilipotimu alfajiri, Yoram aliamka na kisha kuketi kitandani. Alionekana kufikiria vitu vingi sana kichwani mwake huku kila mara akimtazama Diana ambaye muda huo alikuwa amesinzia usingizi mzito.

    "Diana unajua nakupenda sana lakini jina lako tu, mimi nalichukia sana zaidi ya sana. Na ningekuwa na uwezo basi nigekubadilisha jina hilo"

    "Kwanini Yoram"

    "Hilo jina ndilo alilokuwa nalo mchumba wangu mmoja hivi ambaye mwishowe alinisaliti, kwahiyo hata wewe nina imani ipo siku utanisaliti"

    "Hapana siwezi Yoram, lakini pia mbali na jina hilo nina jina lingine"

    "Jina gani?.."

    "Naitwa Sinsia", alitikisa kichwa Yoram baada kuyakumbuka maneno hayo aliyowahi kuzungumza na Diana pindi walipokuwa wakiponda raha kwenye moja ya kumbi ya starehe. Pumzi ndefu alishusha huku bado akiendelea kumkodolea macho Diana. Punde akakumbuka pindi alipokuwa akimtazama Edga kwa mashaka na mwishowe aliamua kumuuliza.

    . "Braza hivi unamfahamu Diana?.."

    "Diana?..ndio nani huyo?..", alihoji Edga kwa mshangao sababu jina hilo hajawahi kulisikia popote. Yoram akajibu.

    "Ndio, ama kwa jina lingine anaitwa Sinsia.."

    "Sinsia?..", bado Edga aliendelea kujiuliza.

    "Hapa nacheza karata dume, Hawa huwenda wakawa ndugu", alijisema Yoram baada kukumbuka hayo. Muda huo huo Diana aliamka, alitaharuki kumuona Yoram ameketi kitandani, kwa sauti ya upole alimsabahi kisha akamuuliza ni wapi alipokuwa siku ya jana kwani haikuwa kawaida yake kuchelewa kurudi nyumbani labda pindi wanapokuwa wote.

    "Unajifanya ni mwanamke mwenye wivu sana wamapenzi. Najua unanipenda kisa nina pesa ila pindi nitakapo fulia basi utahamisha makazi", alisema Yoram.

    "Unamaana gani mpenzi kusema hivyo?..",Diana aliuliza.

    "Unataka kuniambia kwamba wakati tunaanza mahusiano ulikuwa unaishi peke yako?..", Diana alitaharuki kusikia maneno hayo, hakuyaamini masikio yake juu ya kile alichokuwa akikisikia.

    "Unajua sikuelewi?..",alistaajabu sana Diana. Yoram akaangua kicheko kisha akasema "Niambie kiasi chochote cha fedha unacho kitaka nikupatie ili uachane na mimi. Huu ni uamuzi ambao nimechukuwa pasipo kushauriwa na mtu. Labda nikusaidie kitu ili uweze kujua, Diana mimi huwa sikai na mwanamke zaidi ya miezi miwili, kidogo wewe ulipata bahati lakini bahati yako hatimaye imefika kikomo, sasa ni zamu ya wenzako ", kwisha kusema hivyo, Yoram alifungua droo ya kitanda akachomoa bunda tatu za fedha akamkabidhi Diana. Hakutaka kuendelea kuishi naye hasa akitilia shaka uwepo wake na Edga. Alihisi ni ndugu wawili hao, na hivyo akaona endapo kama ataendelea kuishi na Diana kazi yake itakosa motisha, mwisho wa siku atajikuta akifulia. Diana aliangua kilio, hakuamini kama kweli Yoram amemchukulia maamuzi hayo.

    "Lakini tambua sijakupendea fedha Yoram", aliongea kwa huzuni Diana. Yoram aliangua kicheko kisha akajibu "Acha uongo, tatizo nyie wanawake mnapenda pesa kama mfuko. Asante kwa yote, tulikuwa pamoja ila kwa sasa acha ibaki hadithi kwamba uliwahi kuwa na mwanaume anayejua kutumia fedha", alikejeri Yoram kisha akamtupia Diana fedha hizo. Machozi ya uchungu yakimtiririka, Diana aliziokota fedha hizo akiamini zitamsaidia mbele ya safari ya kuanza maisha mapya. Roho ilimuuma sana, machozi ya uchungu hayakukatika katika mboni zake. Alikumbuka Kayumba na vituko ambavyo alimfanyia huku alithubutu kumtimua nyumbani kwake kama mbwa.

    "Ni wapi nitampata Kayumba wangu?.", alijuliza Diana.

    Hatimaye akafika mahali alipokuwa akiishi, aliona haibu pindi waliokuwa majirani zake walipokuwa wakimtazama ilihali baadhi yao wakidiriki kumcheka. Punde si punde akaja bibi mmoja wa makamo, akamsalimu Diana kisha akamwambia" Hiki chumba tayari kinamtu", alistuka Diana,akasikitika.

    "Lakini kuna chumba kingine kipo wazi", bibi huyo aliongeza kusema.

    "Kiko mtaa gani?.."

    "Sio mbali na mtaa huu,ila ngoja nikuitie dalali muende mkakione"

    "Sawa"

    Dalali wa vyumba alifika mahali hapo, akaambatana na Diana kuelekea mahali kilipo chumba hicho. Diana alivutiwa na chumba hicho, taratibu zikafuata na sasa akaanza maisha upya maisha ya uswahili baada kuachwa na Yoram. Mara baada kupata sehemu ya kulaza mbavu zake, fedha aliyobaki nayo ilikuwa ndogo mno kiasi kwamba asingeweza kuifanyia kitu chochote akizingatia hana hata bakuli ndani. Na hivyo aliamua kuingia mtaani kutafuta kazi, akitembea huku na kule lakini hakupata kazi. Siku iliyofuata, ndio siku ambayo Yoram na Edga walitakiwa kukamilisha agizo la Catherine. Agizo la kumuuwa Najrat, wakati huo siku hiyo hiyo Najrat alionekana akijiandaa kuanza safari ya kutembea jijini kumtafuta rafiki yake Kayumba wakuitwa Edga kwa dhumuni kuwa endapo kama atafanikiwa kumpata basi Kayumba atakubali ombi lake la kutaka kuwa wapenzi.



    Nje ya nyumba anayoishi Najrat na Kayumba inasimama Noah nyeusi, katika gari hilo wanashuka wanaume wawili. Yoram na Edga, wawili hao walikuwa wamevaa makoti meusi huku nyuso zao wakizificha kwa kofia ndefu zilizo acha nafasi ya macho na pua. Waligonga geti, mlinzi akafungua. "Nyie wakina nani?..",mlinzi aliuliza kwa mashaka, punde kabla hajajibiwa alinyooshewa bastora "Najrat yupo?..", aliuliza Yoram.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ndio.. Yupo yupo ndani, msiniue tafadhali", mlinzi alijibu kwa woga. Yoram akamtaka Edga atangulie wakati huo yeye akiangalia usalama wa nje huku mlinzi naye akionekana akitimua mbio baada kuona sehemu hiyo kwa sasa sio salama. Mkono wenye bastora ukiwa juu, Edga alinyata kwa umakini. Hatimaye akafika sebuleni,mara ghafla akaishusha chini bastora yake akasema "Kayumba.. Ni wewe au macho yangu?.." Edga hakuamini kama kweli ameuona mchizi wake kwa mara nyingine tena baada kupotezana naye kwa kipindi kirefu sana. Wakati Edga akitaharuki, Kayumba naye alionekana kupigwa na bumbuwazi hasa baada kumuona Edga akiwa na bastora." Ndio ni mimi Edga, msaka tonge mwenzako", aliongea Kayumba kwa sauti ya chini iliyojaa huzuni ndani yake, hakuyaamini macho yai yake. Muda si mrefu Najrat alitoka chumbani akiwa amependeza tayari kwa safari ya kwenda kumsaka Edga. Najrat alistuka kumuona mtu mwenye siraha wakati huo huo Edga akasema "Jifiche dada, hapa hali si shwari "

    "Kwani kuna nini?.", Najrat aliuliza kwa taharuki. Edga akamshooshea bastora, akitilia mkazo "Nitakupasua ubongo.", Najrat aliogopa alirudi chumbani huku akiamini kuwa Kayumba ametekwa.

    "Edga mbona hivyo braza?..", kwa mshangao wa aina yake Kayumba alionekana kutomuelewa Edga. Nje alionekana Yoram akitembea huku na kule kuangalia usalama huku akijua Edga ameingia ndani kumaliza kazi. Mikono nyuma, macho yake yakitazama huku na kule, mara ghafla geti liligongwa. Alistuka akaikoki vema bastora yake akazipiga hatua kulifuata geti, ikiwa aliyegonga hodi si mwingine bali ni yule aliyekuwa mpenzi wake hapo awali. Diana (Sinsia), alifika nyumba hiyo anayoishi Najrat na Kayumba kwa dhumuni la kuulizia kazi ya ndani.!



    Macho yake yalionekana kuwa makavu, alijiandaa kisawasawa huku roho ya mashaka nayo ikimvaa vema mwilini mwake. Lakini kabla Yoram hajalifikia geti, akapata wazo, wazo ambalo aliweza kulifanyia kazi ambapo hakuna sababu ya kwenda kufungua geti ikiwa ndani kuna kazi ya mauwaji emeenda kufanyika. Haraka sana alirudi nyuma, moja kwa moja akazama ndani kuhimiza zoezi hilo lifanyike upesi upesi. Nje Diana aliendelea kubisha hodi, na mwishowe baada kuona geti halifunguliwi aliamua kuondoka zake kichwa chini mikono nyuma huku akiamini kuwa sononeko la Kayumba ndipo linalo mfanya kuambulia patupu. Mithiri ya kinyonga, akazipiga hatua kuondoka mahali hapo, lakini punde baada kuondoka alisikia mlio wa risasi ukitokea kwenye nyumba ile ile aliyotoka kubisha hodi kwa dhumuni la kuomba kazi.

    "Mungu wangu?..", alistuka Diana, akageuka kuitazama nyumba ile. Mapigo ya moyo wake yalimuenda mbio mithiri ya saa mbovu, kijasho chembamba nacho hakikuwa mbali kuuvaa mwili wake. Hakika hakuyaamini masikio yake, nawala asiamini kama kweli amekiponyoka kifo. Aliyainua macho yake kutazama juu, hakusita kutoa shukrani kwa muumba, na kisha akaendelea na safari yake ilihali kila mara akigeuka kutazama kukw alipotokea.



    Ndani, alionekana Edga yupo sakafuni akigugumia maumivu baada kupigwa risasi na Yoram.

    "Edga, umesahau kazi tuliyokuja kuifanya?..", aliuliza Yoram wakati huo bastora akiielekezea kwa Kayumba ambaye naye alionekana kunyoosha mikono juu huku mwili mzima ukitetemeka.

    "Na huyu ni nani yako?..", aliongeza swali Yoram. Punde Kayumba akaupeleka mkono wake kukamata mkono wa Yoram alioshika bastora, aliukunja kwa nguvu, kitendo ambacho kilipelekea Yoram kuidondosha bastora yake kwenye uso wa sakafu. Akaisogeza mbali na mahali waliposimama, kisha ukogomvi wa kiume ukazuka baina ya Kayumba na Yoram. Wawili hao walipigana kila mmoja alionyesha ujuzi wake wa kurusha na kukwepa ngumi, ila mwishowe Kayumba akawa mpole baada Yoram kumuonyeshea bastora nyingine tofauti na ile aliyofanikiwa kumpokonya hapo awali.

    "Ahahahaha hahahah", aliangua kicheko cha dharau Yoram kisha akasema "Hapo hapo ulipo usitikisike, ukiyumba tu nakupasua ubongo wako"

    "Sioni sababu ya na nyinyi kuendelea kuishi, Edga tayari umeshakuwa msaliti. Mimi ni mtoto wa mjini natafuta shilingi, sipo tayari kupoteza kiasi chote kile cha fedha kwa ajili yako. Namtaka Najrat", kwa mbali Najrat alisikia akitajwa, alistuka sana akahisi huo ni mpango wa Catherine.

    "Najrat? Unamtaka wa nini?..", aliuliza Kayumba wakati huo akimtazama Yoram kwa jicho la mashaka mikono yake ikiwa juu kujihakikishia usalama. Kabla Yoram hajamjibu Kayumba, simu yake iliita. Aliitoa mfukoni ilihali macho yake yakimtazama Kayumba. Alipokea pasipo kutazama nani aliyempigia kwa wakati ule "Yoram hebu niambie mmeshamalisha kazi?..", ilikuwa ni sauti ya Catherine. Alimpigia simu Yoram ili kujua maendeleo yanakwendaje.

    "Bado ila kuna tatizo limetokea, Edga ameonyesha usaliti", alijibu Yoram kwa sauti kavu iliyojaa ubabe ndani yake.

    "Nini? Unataka kuniambia amegoma kufanya kazi?.."

    "Hapana, lakini ni wazi kabisa huyu mtu anafahamiana naye"

    "Anhaa, sasa naomba unisikilize Yoram. Huyo tayari anataka kuvuruga mpango wangu, anza na yeye kisha malizia kwa Najrat. Nami si muda mrefu nakuja huko", Catherine alionekana kukasirika baada kusikia kuwa Edga ameonyesha usaliti. Ni agizo ambalo Yoram aliliona lipo sahihi, lakini kabla hajalifanyia kazi agizo hilo mara ghafla mlio wa geti kufunguliwa kimabavu ulisikika. Yoram alistuka, hakuona haja ya kupoteza muda kwa wakati huo na hivyo alimkaba shingo Kayumba na kisha bastora kuielekezea kwenye kichwa chake "Najrat yuko wapi", alihoji Yoram akitaka kujua mahali alipo ili akamilishe kazi akavune pesa. Kayumba hakujibu. Ndipo kwa mara nyingine tena akahoji ilihali muda huo huo jeshi la polisi lilivamia. "Hapo hapo ulipo mikono juu", kamanda mmoja alimwambia Yoram huku akiwa amemnyooshea bastora. Yoram alikataa katu katu, zaidi aliwataka polisi hao waweke siraha zao chini kabla hajausambaratisha ubongo wa Kayumba. Lilikuwa ni jambo ngumu kwa makamnada hao kutekeleza agizo la Yoram, na ndipo Yoram alipoanza kuwahesabia namba. "Moja shusheni siraha zenu chini..mbili..tatu...nne shusheni siraha zenu chini..tano..", Yoram alipoona makamanda hawatekelezi agizo lake, akaona heri amalizane nao kwa kuwafytaulia risasi kwa kujiwekea ngao mwili wa Kayumba. Lakini kabla hajafanya kitendo hicho,nyuma yake aliwekewa bastora." Weka siraha yako chini ", mtu huyo mtu huo baada kumgusisha Yoram bastora kisogoni alimtoa amri hiyo. Hapo Yoram hakuwa mjanja tena, alimuachia Kayumba akaweka bostara yake chini na sasa akatiwa kwenye mikono ya jeshi la polisi akavishwa pingu pamoja na Edga tayari kwa niaba ya kupelekwa sehemu husika.

    "Ahsante sana wananchi kwa ushirikiano wenu mzuri, na wasihi msisite kutoa ushirikiano mwingine pindi yanapozuka matukio ya kiharifu kama haya", aliongea moja ya makamanda waliofika kwenye tukio. Maneno hayo aliwaambia baadhi ya watu waliokuwemo nje ya nyumba anayoishi Najrat. Ndani ya gari la wazi, gari litimukalo kwa niaba ya jeshi la polisi pindi liendapo kukamata wahalifu, Yoram na Edga walipandishwa kwa puta na safari ikawa imeanza wakati huo wakiwa njiani walipishana na gari la Catherine. Catherine alistuka kuliona gari lile la polisi kwa kutumia kioo cha pembeni (Side Mirror) akahisi tayari anakwenda kukumbuka ingawa hakutaka kuamini kuwa ile gari imetoka kwa Najrat. Lakini wakati akiwa na sintofahamu ghafla akapishana na gari la Najrat, alilifahamu fika hakutaka kulifananisha. Hivyo haraka Catherine akakunja kona, gurudumu za gari lake zilizunguka kwa kasi ya ajabu na sasa akalifuatilia gari la Najrat ikiwa Najrat akifuatatilia gari lililombeba Edga.



    Hospital gari iliegesha, akashushwa Edga huku akichechemea na kisha kutakiwa kufanyiwa matibabu kwa haraka sana, askari mmoja akimlinda ili baada ya matibabu akajibu shtaka linalo mkabari. Kwa kasi ya ajabu, gari hilo la polisi liligeuza, sasa safari ikawa ya kuelekea kituoni staki Shari. Nyuma yao walifuatwa na gari la Najrat wakati huo huo Najrat naye nyuma yake ikifuatwa na gari la Catherine pasipo yeye kujua. Ilipofika kituoni, Najrat naye aliwasiri, alifungua mlango wa gari lake akazipiga hatua za haraka haraka kumfuata kamanda mmoja.

    "Kesi hii kubwa sana, hawa ni majambazi sugu", aliongea kamanda huyo aliyefuatwa na Najrat kwaniaba ya kuyamaliza mambo hayo kabla kesi hajafika mahakamani.

    "Ok najua kesi hii kubwa Afande,lakini mkumbuke mmoja tu ndio alikuwa na siraha ila huyu mwingine hajawahi hata siku moja kumiliki siraha"

    "Mamaa unanitania sio?..", alihoji kamanda.

    "Aaha! Hapana kamanda ila nahitaji msaada wako"

    "Umejipangaje?.."

    "Kwa kiasi chochote nipo tayari"

    "Mmmh!..", aliguna kamanda akishangazwa na jibu la Najrat.

    "Million tano zipo?..", aliachia tabasamu bashasha Najrat baada kusikia swali hilo, aliona tayari mtihani wake aliokabidhiwa na Kayumba anakwenda kuumaliza.

    "Ndio zipo Afande", alijibu Najrat. Kamanda baada kulidhishwa na jibu la Najrat, akawaita makamanda wenzake faragha akawaeleza mpango namna ulivyo. Walikubalina mawazo yao makamanda hao wasio pungua wanne, na sasa walitoa kibali cha Edga kuachiwa huru.

    "Kayumba, mchezo sasa unakwenda kumalizika", aliongea Najrat huku akifunga mkanda akijiweka tayari kwa niaba ya safari ya kuelekea Hospital. Kayumba akaachia tabasamu kisha akajibu "Wewe sio wa mchezo mchezo"

    "Ahahahah", Najrat aliangua kicheko, hima safari ikaanza huku nyuma Catherine naye alifika baada kuona Najrat ameondoka. Alipiga makofi, kamanda mmoja akageuka kutazama kule ilipokuwa ikitokea sauti hiyo ya makofi. Akamuona Catherine akizipiga hatua za malingo kujongea mahali walipoketi huku kila mmoja akitafakari lake pindi atakapo utia kiganjani mtonyo atakao utuo Najrat.

    "Safi sana", aliongea Najrat.

    "Unawazimu?..", kamanda mmoja aliuliza kwa hasira huku macho yake yakimtazama Catherine.

    "Ahahahah", Catherine aliangua kicheko kisha akavuwa miwani yake na akasema "Tengua kauli yako kamanda,kwa sasa mimi ndio mwenye dhamana juu yenu nyinyi viswaswadu wenye tamaa ya fisi". Makamanda walistushwa na kauli hiyo ya Catherine. Walishimdwa kumuelewa amemanisha nini kusema hivyo.

    "OK, nahitaji utulivu na unyenyekevu kutoka kwenu, ili niweze kuelezea shida yangu kwenu. Na nina imani mtanisaidia", aliongeza kusema Catherine.

    "Alo! Shida gani hiyo? Na wewe ni nani kwani? Na mbona unaongea kwa kujiamini kama upo chumbani na mumeo?..", kamanda wa pili alizungumza. Catherine akajibu "Naongea kwa kujiamini kwa sababu najiamini", kwisha kusema hivyo akatoa chombo cha kunasa sauti. Akijiamini zaidi akaongeza kusema "Sikuwa mbali kamanda, yote mliyokuwa mkiyazungumza na yule binti nimeyanasa kwenye kifaa changu. Kwa maana hiyo basi nina uwezo wa kuifikisha sauti hii kwenye nyanja ya juu na sheria ikafuata MKONDO wake...", aliongea Catherine, akaangua kicheko kidogo harafu akaendelea kusema." Sasa sitaki kufika huko, najua mnafamilia zinawategemea lakini ili niweze kuwasaidia lazima ni nyinyi mnisaidie. Nisikilizeni kwa UMAKINI sana , yule binti aliywaahidi kuwapa fedha nataka mkamuuwe la sivyo mambo yatakwenda mlama upande wenu. Nataka kazi hii muifanye kwa masaa ishirini na nne ndipo niipoteze sauti hii"

    "Ahahahahhahah..", alipomaliza kusema hayo Catherine aliangua kicheko cha dharau huku makamanda wakiishia kutazamana.





    Tabasamu bashasha liloonekana usoni mwake, furaha nayo ikiutawala uso wake. Kila mara aliachia tabasamu, aliamini tayari zoezi linakwenda kumalizika na sasa utakuw muda muafaka wa kumtwaa Kayumba.

    "Ahahahha", aliangua kicheko Najrat baada kufurahishwa na juhudi zake.

    "Mbona unacheka?..", Kayumba aliuliza.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Aamh..Hapana Kayumba nimefurahi tu. Kwani wewe hujafurahi kwenda kumuona rafiki yako?.."

    "Hakika na mimi nimefurahi pia", alijibu Kayumba na kisha kuachia tabasamu. Kwa kasi ya kawaida wawili hao sasa walifunga safari kuelekea Hospital kumuona Edga. Nyuso zao zilionekana kufurahi sana jambo ambalo liliweza kuzaa zogo la hapa na pale. Lakini wakati safari imekolea, punde walisimama baada taa nyekundu kuwaka. Ni jambo ambalo liliwakera sana Kayumba na Najrat, wawili hao walikuwa na shauku ya kufika Hospital ila iliwalazimu kutii sheria ya barabarani. Lakini wakati wakingojea taa ya kijani iwake kuwaruhusi kuendelea na safari, nje alionekana Diana akiomba msaada wa fedha. Kayumba alistuka, hakutaka kuyaamini upesi macho yake, hima akashusha kioo cha gari ili amtazame vizuri. Kinywa chake hakikuwa kizito kulitaja jina lake "Diana..", Diana aliposikia jina lake likitajwa, aligeuka nyuma yake. Alipigwa na butwaa kumuona Kayumba, machozi yalimtoka huku akishindwa aseme nini.

    "Ni wewe?..", akiwa katika hali ya taharuki, Kayumba alimuuliza Diana. Huku akizidi kububujikwa na machozi Diana aliitikia kwa kichwa mikono akiwa ameweka kichwani. Mwendo wa uchovu Kayumba alizipiga hatua kumfuata, alipo mkaribia alimfuata machozi wakati huo Diana akiomba msamaha kwa yale aliyomfanyia.

    "Nimeshakusahe Diana, ila naomba uambatane na mimi", alisema Kayumba.

    "Hapana Kayumba, kwa yote niliyokufanyia si stahiri kukaa na wewe hata sekunde moja. Roho inaniuma Kayumba niache niendelee na haya maisha", alijibu Diana kwa sauti iliyoambatana na kilio. Huruma haikumakaa kando Kayumba, ghafla machozi yakamlengalenga katika mboni za macho yake, na punde si punde chozi la jicho la kulia likamdondoka huku akiendelea kumsihi Diana aondoke naye.



    Hatimaye taa ya kijani ikawaka, magari yakaanza kuondoka. Najrat alikuwa akiwatazama Kayumba na Diana kupitia kioo cha pembeni cha pembeni (Side Mirror), alipiga honi kumtaka Kayumba waondoke. Kayumba hakujali honi alizokuwa akipiga Najrat, zaidi aliendelea kumbembeleza Diana ili aondoke naye ingawa bado Diana alikataa katu katu.

    "Diana, wewe sio Diana. Wewe ni Sinsia. Naomba twende tukamuone kaka yako yupo Hospital hali yake mbaya sana", alisema Kayumba kwa sauti ya uchungu iliyoambatana na machozi. Diana alistuka kusikia maneno hayo, alimtazama Kayumba mara mbili mbili kisha akahoji "Kaka?..kaka yangu mimi?.."

    "Ndio, Edga amelazwa hospital. Nipo chini ya miguu yako Diana twende ukamuone Edga", alijibu Kayumba kwa uchungu na kisha akamshika mkono Diana ambaye alionekana kuvaa nguo zilizo chakaa mithiri ya kichaa, nywere nazo zilionekana kususa chanuo. Diana yule aliyekuwa akifuatwa na Yoram sio Diana huyu wala Diana yule aliyekuwa mama ntilie. Diana huyu alionekana kuwa rafu kuanzia nywere mpaka mavazi. Maisha yanabadirika sana, na ndivyo ilivyokuwa kwa Diana, binti aliyehitaji penzi la Kayumba ila mwishowe akamtibua mithili ya mbwa. Ndani ya gari Diana na Kayumba waliingia, na sasa safari ikaendelea huku Kayumba akiamini kuwa siku hiyo ndio siku ya kujua ukweli baina ya Diana na Edga. Baada ya mwendo wa takribani robo saa, hatimaye walifika Hospital. Jambo la kwanza Najrat aliingia wodini kwa dhumuni la kumalizana na kamanda aliyebaki akimlinda Edga ambaye alikuwa akipatiwa matibabu.

    "Anhaa hapa nilipo nilikuwa nakusubiri wewe tu, kila kitu kipo wazi", aliongea kamanda huyu aliyepewa jukumu la kumlinda Edga. Fedha tayari alikuwa nayo Najrat, kabla hajafika Hospital alipita Bank kutoa fedha ili amalize mchezo mzima.

    "Sawa kamanda, hali yenu hii hapa", alijibu Najrat huku akimkabidhi kamanda bahasha iliyoonekana kutuna. Bahasha hiyo ilikuwa na fedha tasilimu ya kitanzania. Kwa mikono yake miwili, kamanda alipokea akakamlisha taratibu husika alizotakiwa kufanya hospital hapo kisha akaondoka. Uso wake ukiw bado na tabasamu, Najrat alimgeukia Edga kisha akasema "Poleee".

    "Nimeshapoa dada yangu, ila..", kabla Edga maliza kuongea, Najrat akaongeza kusema "Naenda kumuita Kayumba, kuna mengi ya kuzungumza"

    "Sawa"



    Upande wa pili maneno ya Catherine yaliwatia hofu makamanda, walimtazama Catherine kwa jicho la tatu huku kila mmoja akiwa na woga wa kuachishwa kazi pindi tu Catherine atakapo ipeleka sauti hiyo sehemu husika.

    "Ahahahah", kwa dharau Catherine aliangua kicheko kwa mara nyingine tena kisha akahoji. "Mpo tayari?.."

    "Ahahahaha", kamanda mmoja kati ya wale waliokuwa na hofu aliangua kicheko, punde si punde kamanda wa pili akaangua kicheko. Catherine aliwashangaa makamanda hao ambao waliangua kicheko badala ya kujibu swali lake. Ghafla akahisi kuwekewa kitu kwenye kichwa chake chenye nywere laini, nywere za singa. Akasikia sauti ya kiume ikitokea nyuma ya sikio lake la kushoto.

    "Weka chini hicho ulicho shika, na kisha nyoosha mikono yako juu", iliamrisha sauti hiyo. Ilikuwa sauti ya kamanda yule aliyetoka kumalizana na Najrat hospital. Alipewa data zote zilizokuwa sikiendelea,naye kamanda hakuwa tayari kuona suala hilo likichukuliwa lelelemama. Amri alitii Catherine, akawa mpole mithiri ya sisimizi. Kamanda alichukuwa chombo kile cha kunasa sauti, kwa kutumia buti lake akakipasua kwa kukikanyaga kisha akatiwa selo, ikiwa upande mwingine Diana alipigwa na butwaa kumuona Edga. Alihisi kama ni ndoto anayoota muda huo.

    "Kaka! Ni wewe kaka Edga?..", kwa sauti ya kilio alihoji Diana na kisha kumaliza kifuani huku akiwa amepiga magoti sakafuni..

    "Ndio ni mimi Sinsia mdogo wangu, kwa nini uliamua kutoroka? Kwanini Sinsia", Edga aliongea kwa uchungu, na hapo ndipo Kayumba alipohakiki kuwa binti huyo ni Sinsia na sio Diana kama alivyojieleza. Hakika alishindwa aseme nini hasa akizingatia kuwa huyo ni binti ambaye aliwahi kuishi naye kama mke na mume. Wawili hao Edga na Sinsia walilia kwa uchungu, wakati huo huo Kayumba alimgeukia Najrat na kisha akasema "Mpenzi Najrat, hongera sana kwa juhudi zako ambazo zimefanikiwa kuzaa matunda. Huyu ndio Edga rafiki yangu kipenzi, msakatonge mwenzangu. Nipo tayari kuwa mumeo kuanzia sasa, kamwe sitarajii kuumizwa kama zamani"

    "Kayumba mimi ndio mtu sahihi kwako, sitokusaliti. Na habari njema ni kwamba kesho kutwa wazazi wangu wanarejea nchini. Kwahiyo nitapanga nao mkakati wa kufunga ndoa na wewe"

    "Sikuona mtu sahihi kwa kipindi kirefu ila kwako nimetua. Hakika nakupenda sana Kayumba", aliongeza kusema Najrat kisha akamkumbatia Kayumba, na kichwa chake akakilaza kwenye kidali kipana cha mwanaume shupavu, Kayumba. Baada Diana (Sinsia) kulia kwa muda wa dakika kadhaa, sasa alinyanyuka akamtazama Kayumba, bado nafsi ilimsuta. Aliendelea kujiona mkosefu kwa kijana huyo, hivyo alishuka chini akamuomba msamaha kwa mara nyingine tena huku akibubujikwa machozi. Kayumba alimuinua, akamwambia "Hakuna binadamu aliyekamlika Diana, najua uliteleza. Natambua fika msaada wako. Kuwa huru Nimeshakusehe", kwisha kusema hivyo Kayumba, akamtazama Edga pale kitandani alipolazwa kisha akaendelea kusema "Edga.."

    "Kayumba unataka kuniambia unamfahamu dada yangu?..", alidakia Edga akihoji kwa mshangao wa hali ya juu. Kayumba akaishusha pumzi ndefu na akajibu "Ndio MCHIZI wangu Edga, siku ile naenda kuonana na Najrat niligongwa na gari, ambapo huo ukawa mwanzo wa mimi na wewe kupotezana. Huyu binti ndio aliyenihifadhi muda wote ingawa baadaye tulikosana kwa makosa madogo ya kibinaadamu. Anaitwa Diana"

    "Diana?..", Edga alistuka kusikia jina hilo.

    "Unamaana gani?..", akiwa katika hali ya mshangao alihoji. Kayumba hakujibu, aligeuka kumtazama Diana. Diana naye muda huo alionekana kuwa mpole, alitetemeka mwili wale, kwa hofu akasema kisa kilicho mpelekea kubadirisha jina.

    "Ndio kaka, niliamua kubadilisha jina baada kuambiwa kuwa tunatafutwa. Mke wa mzee Ezlom aliamua kutangaza vita baada kumuibia fedha zake, niliishi kwa hofu, na ndio maana siku tayari kuliweka wazi jina langu kuhofia kukamatwa", aliongea Diana.

    "Kwanini kaka uliiba fedha za watu?..", aliongeza kusema, safari hii alimuuliza Edga sababu iliyomfanya aibe fedha za kwenye nyumba ya mzee Ezlom,mzee aliyejitolea kuwalea baada wazazi wao kufariki. Edga alikaa kimya kidogo kisha akajibu "Siku na fedha ya kukufauta Dar es salaam, na wala sikuwa tayari kukuona ukiwa mbali na mimi mdogo wangu. Na ndio maana maana niliamua kuiba fedha nikafunga safari kuja kukutafuta. Milima haikutani lakini binadamu hukutana, ya nyuma yaache kama yalivyo. Furaha yangu ni kukuona ukiwa hai "



    Catherine na Yoram wanachiwa kwa dhamana, lakini Catherine bado hakuwa tayari kushindwa kumaliza azma yake ya kutaka kumuuwa Najrat. Hatimaye siku moja anapata habari kuwa Najrat anataraji kufunga ndoa Sophie Hotel. Nafasi hiyo Catherine alipania kuitumia kumaliza kiu yake. Siku ya tukio ilipofika naye alifika akiwa na bastora yake. Alimuona Ikene ikitumbuiza siku hiyo, dhahili shahili akajua Kayumba anafunga ndoa na Najrat. Punde gari lililotokea kanisani likiwa limewabeba wa bibi na bwana lilifika Hotel hapo, hakika Kayumba alionekana kupendeza ndani ya suti achilia mbali Najrat binti wa kiarabu akionekana kung'aa katika shera. Wivu ulimjaa Catherine, hasira za kuuwa zilimjaa mara dufu. Shangwe za hapa na pale nazo zilisikika, Diana akakubali kuwa Kayumba sio mali yake tena. Shamlashamla ilionekana kupapendezesha sana mahala pale, Ikene akapasa sauti akasema "Siku zote ujuzi hauzeeki, Kayumba hebu njoo utoe burudani mbale ya mke wako ili ajue kuw hajakosea kuchagua mume", hoi hoi kwa mara nyingine tena zilisikika baada Ikene kutia utani. Haraka sana Kayumba akasimama, akajongea mbele na kisha kushika maiki na kuanza kuimba. Ilikuwa burani sana, watu walifurahi mno hasa hasa Edga ambaye hakusita kutoa pongezi kwa hatua aliyofikia. Lakini wakati hali hiyo ikiendelea, Catherine alionekana kupigwa na butwaa, akajikuta akishindwa kufanya kile alicho zamilia kufanya. Haraka sana akafungua mkoba wake, akatoa bastora upesi akijipiga risasi kichwani akafariki. Taharuki inazuka, Kayumba hakuyaamini macho yake baada kuona ubongo wa Catherine ukiwa umtawanyika sakafuni. Hakika roho ilimuuma sana, alilia kwa uchungu huku akiwa ameupakata mwili wa Catherine. Lakini maisha hali ikabaki kama ilivyo, Catherine akajikuta akipoteza maisha baada kuona dhuruba la penzi la Kayumba likiutesa moyo wake. Na sasa maisha yakabaki baina ya Najrat na Kayumba. Wawili hao mke na mume waliwafungulia maduka Edga na dada yake atwae Sinsia. Raha mstarehe kwa wasaka tonge hao, kutoka kulala nje mpaka kuuza madafu na kubeba mzigo mpaka kummiriki binti wa kiarabu mwenye maisha bora, ikiwa upande wa Edga kutoka kwenye kazi ya kubeba mizigo mpaka kumiriki duka la nguo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Amini kwamba na wewe unamoyo na sio jiwe. Kwahiyo ipo siku atajua thamani yako kwake.. Na ndio utajua kuwa wewe ni mstahili juu yake. Kutesa kwa zami. Ipo siku atakumbuka kuwa wewe ulikuwa mtu sahihi kwake, wakati huo wewe huna hisia juu yake.

    SABABU Yule aliyebadilisha mikate mitano ikashibisha maelfu ya WATU na ndio yule aliyebadilisha maji kuwa divai. Basi huyo huyo anaweza kuubadilisha MOYO WAKE kukuhitaji wewe.. Nayo yametokea Mungu amlaza mahari pema Catherine ",

    " Amen ", yalikuwa ni maneno ya Edga akimkumbusha Kayumba kipindi kile Kayumba alipokuwa akipitia wakati mgumu baada kutendwa na Catherine , hakika yalikuwa ni maneno ambayo yalimpa faraja Kayumba, naye pole pole akamsahau Catherine na maisha yakasonga.



    - - MWISHO- - - - - - - - -

0 comments:

Post a Comment

Blog