Simulizi : Nauza Bikira Yangu
Sehemu Ya Tatu (3)
Sauti ya kelele za woga ilisikika na kusambaa katika pori lili na kutengeneza mwangwi uliojirudia katika masikio yaTusmo na kutengeneza hofu zaidi huku akijaribu kukimbia bila mafanikio. Ni mlio
wa risasi ndio liomfanya kukimbia bila kujua anapoelekea. Mwanaume liyekunja sura akiwa kashikilia bundu yake vizuri huku moshi ukitoka mbele ya eneo inapotokea risasi tayari alikua kawatenganisha na dunia wanaume watano wenye cheo cha jeshi waliokuwa wakijaribu kumbaka Tusmo, Huyu si mwingine ni Chama aliyeamua kuwafuatilia wale wanajeshi kwa nyumba na mwishowe kugundua kuwa hawakua waaminifu kwa kile alichowaagiza. Kwa macho yaliyojaa huruma Chma alimtazama Tusmo akihangaika kukimbia huku akiwa mtupu bla nguo. Kwa upole chama akaokota nguo na kutembea hatua za haraka kumfuata Tusmo huku Tusmo akijitahidi kukimbia ambapo mbio zake zilishia mikononi mwa Chama na kujikuta akipewa nguo avae. Tusmo kwa woga akapokea nguo na kuvaa harakaharaka na kujikunyat kwa woga. Chama akamuashiria atangulie mbele. Baada ya mwendo wa dakika arobaini ghafla wakasikia sauti ya ndege za kivita zikiwa zimezingira anga la msitu ule, Ni wanajeshi wa jeshi la New African walikua wa wamevamia kambi ya Jeshi la waasi wa Jamuhuri ya watu wa Kolo ililoko chini ya Chiku.Kitendo cha kuona hali ile kilipokewa kwa maamuzi ya haraka na Chama ya kurudi alipoacha kambi kuongoza mashambulizi dhidi ya maadui. Chama akikimbia kurudi alipotokea huku akipiga risasi juu. Hatua kadhaa mbele huku akiwa kamuacha Tusmo peke yake lindondoka Bomu pembeni ya Tusmo, Mlipuko mkubwa ulisikika ulioambatana na kilio kikali cha msichana mwenye ndoto za kufika kule alipokua anaelekea katika harakati za kuikimbia nchi yake iliyochafuka kwa vita vikali. Vipande vya mwili wa bindamu viliruka juu na kuganda juu ya matawi ya miti huku damu ikiwa imetapakaa eneo lile.
.**** ****
Hali ilikua ya baridi sana katika jiji la mwanza, Wingi wa watu katika mitaa ya jiji hilo waliokua wamevaa masweta na makoti makubwa kujikinga kwa baridi, hali ya jiji hilo haikutofautina na Hali ya jiji la arusha moja ya Eneo lnalosifika kwa baridi Tanzania. Rajiv akiwa kakaa siti ya mbele katika gari aina ya pickup hardboad ya rangi nyeupe yenye maandishi ubavuni yanayosomeka UN alikua akitazama mandhari ya jiji hilo geni machoni mwake kupitia kwenye kioo, huku dereva akiwa busy na usukani kuhakikisha safari inamalizika salama. Gari ilizidi kutokomea upande wa kaskazini mwa jiji la mwanza huku likiacha jiji hilo na kuingia nje ya jiji hilo katikati ya eneo ambalo kimtazamo ni eneo wanaloishi jamii ya watu masikini, Gari lilizidi kusonga mbele na kuacha eneo hilo huku likiingia katikati ya msitu mdogo wenye miti mingi mirefu iliyoota kwa mpangilio. Rajiv akiwa kapitiwa na usingizi kutokana na uchovu wa safari mara alishtushwa na mguso kaik bega lake kufumbua macho akakutana na sura iliyojaa tabasamu kutoka kwa dereva wa ile gari. Ishara y kuwa safari yake imefika mwisho, Mbele ya mcho yake kupitia kioo cha gari alishuhudia mhema mengi huku makundi ya watu wakiwa wamelala nje ya mahema hayo, Watoto walio vifua wazi wakiwa wanacheza mpira, Hali katika eneo hilo ilikua ya kimsikini sana na kumfanyya Rajiv kupigw na butwaa. Akishika begi lake vyema na kushuka katika lile gari Macho yake yakatua katika roli kubwa lililokua likishusha chakula. Maandishi makubwa yaliyo katika kioo cha lori lile yalimfanya atabasamu. PANDYA TRANSPORT, Wakati akiangalia gari la baba mkwe wake mtarajiwa alishtuka akisalimiwa kwa kuitwa jina lake.
“Rajiv Roshan”
Rajiv akageuka na kukutana na sura ya Mzee wa kihindi akiwa kashika file mkononi.
“Yes Sir” {Ndio mzee}
Rajiv alijibu huku akimfuata yule mzee.
“I’m Patel Premsing” {Mimi ni Patel Premsing}
“I’m Rajiv Roshan sir” {Mimi in Rajiv Roshan}
“Ok let’s go” {Sawa twende}
Patel alitangulia mbele huku Rajiv akimfuata nyuma akipita chini ya mahema makubwa huku akipita makundi ya wazee na watoto wakiwa wamekaa kama wamekosa tumaini., Wakaingia katika hema moja dogo na kukutana na samani za ofisni, Rajiv akakaa katika kiti huku akimuangalia Patel akiwa anatafuta kitu katika kabati dogo lillopembeni ya meza ya ile ofisi. File lingine la rangi ya khaki kutoka katika lile kabati likawa mkononi, Patel akakaa na kuanza kulifungua huku akiandika kiu juu yake n kuana kubonyeza namb fulani katika simu ya mezani akasikiliza upande wa pili.
“Sixteen please” {Kumi na sita tafadhali}
Simu ikakatwa, Patel akaendelea kuangalia lile file, Mara akaingia kijana mtanashati aliyevalia kitambulisho shingoni na kuketi katika kiti kilicho pembeni ya Rajiv
“Rajiv Meet with Artu Mrema” {Rajiv kutana na Artu Mrema}
Rajiv alimgeukia Artu na kumpa mkono.
“Nice to meet you” {Nimefurahi kukutana n wewe}
Rajiv alimjibu Artu huku artu akijibu kwa kutikisa kichwa.
Patel akamuangalia Artu na kuungumza kwa kswahili kibovu.
“Artu chukua hii fanyakazi menzako, onyesha yeye how to work na yeye itakuwa inasimamia nyinyi katika communication system department na ionyeshe ofisi ile ya juu ndio itakua yake, now wewe utahama kitengo na yeye atasajili watu wapya hapa.. ok”
“Sawa Boss”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Artu alijibu huku akimuangalia Rajiv. Uwezo wa Artu katika kufanya kazi ndio uliomanya aheshimiwe na kila mtu katika kambi hiyo, akiwa ndio kwanza ana umri wa miaka ishirini na nane artu alijijengea heshima kwa kupenda kuzungumza kiswahili kuliko kingereza. Tabia ya baba yake Tobias Mrema Mwanajeshi mstaafu aliyeamua kurudi kijijini kwao Marangu Kiraracha baadaya kustaafu ndiyo iliyomfanya Artu kuwa na msimamo kwa kile anachokiamini. Ni tabia ya kutotukuza cha wageni. Awali ilikua ngumu sana kwa wafanyakazi wengine kumuelewa Artu, Wengi wao walidhani anadhrau kwani kwenye mikutano ya ofisi alikua akiulizwa kwa kingereza ilibidi uhakikishe umevaa Headphone ya kutafsiri lugha kama utakua hujui kiswahili kwa kuwa jibu lake litakua kwa lugha ya kiswahili. Hali hii ndiyo iliyopelekea mkuu wa kambi kupendekeza lugha ya mawasiliano iwe kiswahili. Huyo ndiye atu aliyepewa jukumu la kumuonyesha maeneo ya kazi Rajiv.
Artu akasimama na kumuashiria Rajiv amfuate. Rajiv akasimama wakatoka nje.
“kambi yetu kwa sasa ina wakimbizi zaidi ya elfu tano”
Artu alimwambia Rajiv, Rajiv akamuangalia Artu.
“Sorry iam not good in swahili language” [Samahani mimi siko vizuri katika lugha ya kiswahili”
Artu akamuangalia Rajiv, kisha akampa ishara asubiri. Artu akatembea kwa mwendo wa haraka akaingia katika hema na kutoka na kitabu kikubwa cha rangi ya kijani akamkabithi Rajiv. Macho yaa Rajiv yakatua juu ya maandishi madogo ya rangi ya dhahabu yaliyo juu ya kitabu kile. ENGLISH TO SWAHILI.
“Inabidi ujue sasa”
Artu alimjibu Rajiv”
Rajiv akaangalia kile kitabu kisha akashusha pumzi.
**** ****
Hakuna kitu ambacho alikua hapendi kukuana nacho katika maisha yake yaliyobakia kama mwanamke, Maumivu aliyoyapata miaka ishirini iliyopita hakutaka kukutana nayo kabisa katika maisha yake yaliyobakia. Baada ya kumgharamia mpenzi wake Nance tokea alipokuwa kidato cha pili mpaka alipomaliza chuo kikuu na kupata Degree ya Biashara huku moyo wake ukifurahia kupata mke ambaye ni msomi ambaye watasaidiana katika maisha yao. Kadi za harusi ziligawiwa kila kona ya jiji la Mwanza na harusi yao ikiwa gumzo kila mahali. Kipingamizi cha kwanza kiliikumba ndoa yao na kusababisha tatizo ndoa yao iwe katika hatihati ya kutokufungwa, Tatizo ni Dini, Dini ilikua kikwazo ndani ya nafsi ya Nance, Hakutaka tena kuolewa na Mwanaume muislam, Uislam ndio ulikua kikwazo kwake. Wazo la Cassim wafunge ndoa ya kiserikali kila mmoja abaki na Dini yake wazo ambalo Nance alilitupilia mbali tena mbali na jiji la mwanza. Ndoa imehairishwa, Ndoa imehairishwa ndicho kilichofuatia na kuzungumzwa na watu. Mapenzi mazito yaliyo ndani ya Moyo wa Cassim juu ya Nance yalipelekea kubadili Dini ili tu Amuoe yule anayempenda. Joseph ndilo jina alilopewa baada ya kubatizwa ndani ya kanisa la Apostolic Faith Church mbele ya mke wake mtarajiwa Nance. Wapi pa kupata pesa ya kuandaa sherehe tena. Wazo la kukopa bank ndilo lililofuatia, Nyumba yake aliyoijenga kwa taabu Nyakato mwanza ikawa kama dhamana na fedha zikawa katika mikono yake tena na wakati huo ndoa ikatangazwa kanisani tofauti na mwanzo ilikua msikitini. Kadi zikasambazwa upya huku bwana Harusi akiitwa Joseph Mwinyi tofauti na mwanzo aliitwa Cassim Mwinyi. Siku ya ndoa ikawadia na Joseph akiwa katika suti nadhifu hukumpambe wake akiwa ni Rafiki yake wa karibu Antony lwambo walikua mbele ya Altare ya kanisa la Apostolic Faith Church pale pale alipobatizwa. Mchungaji Simon akitimiza wajibu wa kanisa kuhakikisha anafungisha ndoa ile. Tayari Pete ilikua mkononi ikipokea baraka na kugeukia Wanandoa waliokuwa wanatarajia kuoana.
“Joseph Mwinyi je umekubali kumuoa Bi Nance Mwakabela kuwa mwili mmoja na kuwa naye katika Shida Raha, Huzuni, na hata Furaha mpaka kifo kitakapowatenganisha?”
“Ndiyo mimi Joseph Mwinyi nimekubali kumuoa Bi Nance Mwakabela kuwa mke wangu na nitaishi naye katika shida na raha mpaka kifo kitakapotutenganisha”
Jibu la Joseph liliamsha saut za vigelegele na shangwe toka kwa ndugu na jamaa waliokuja kushuhudia tukio hilo hukuwakiwa na shauku ya kuelekea ukumbini kupita katika bufee.
“Bi Nance Mwakabela je umekubali kuolewa na Bw. Joseph Mwinyi kuwa mwili mmoja na kuishi nae katika shida na raha mpaka kifo kitakapowatenganisha?”
Kimya kilitawala kisha sauti ya kusonya ikasikika kutoka kwa Nance, kafungua Shela na kuanza kuongea kwa jazba.
“Mimi huyu bwana simtaki ananing’ang’ania kwanza si daraja langu, elimu yangu hailingani na yeye so analazimisha kunioa kisa kanisomesha, sasa sitaki kumsikia na kama ni gharama zake asubiri nikianza kazi nitamrudishia”
Kauli ile haikupita katika masikio ya Joseph ilipenya moja kwa moja katika kifua chake na kukutana na moyo wake ikaupasua katikati na matone ya damu yakaanza kulowaisha moyo wake. Hakiwa haamini huku akiona kama maigizo ya kina Bishanga na Rich Rich alishuhudia Nance akitoka nje ya kanisa huku akikimbia. Harusi ikavunjika na kila mtu akaenda kwao huku akiinamisha kichwa chini. Pigo la nyumba yake kuuzwa ndilo lilifuata na maamuzi ya kumuondoa Nance duniani yalifuata kwa kutumia shoka adhabu ya kugawanya kichwa cha Nance ilikua rahisi sana na kuamua maisha yake kuyamalizia Porini akikimbia mkono wa sheria. Ni miaka ishirini sasa Joseph ama Cassim alikua ndani ya msitu akikusanya kuni kwa ajili ya kwenda kupikia kitoweo chake.
**** ****http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mbele ya Macho yake Tusmo alishuhudia Bomu lililofanana na kiazi likidondoka mbele yake, Mawazo ya Filamu ya Cinthia Khan yalimvaa na kutumia mguu wake kama mchezaji maahiri wa mpira anapopiga penati alilipiga lile bomu teke na kugonga mti ulio pembeni ya Chama na kusababisha mlipuko mkubwa uliomsambaratisha Chama na kumfanya kuwa vipande vipande huku ukimuacha Tusmo akiwa nusu mfu kwa mshtuko alioupata kutokana na mlipuko ule.
Mzee wa makamo aliyejifunga shuka kuu kuu akiwa kabeba furushi la kuni alishtushwa na damu zilizokua zikidondoka kutoka juu ya mti na kudondokea nguo yake aliyovaa. Kwa Tahadhari alipepesa macho na kukutana na vipande vya viungo vya mwanadamu vikiwa vimening’inia juu ya miti akiwa anashangaa asijue cha kufanya mara akakutana na kiumbe kimelala chini hakijitambui. Mwanamke ndiye alikua kalala pale. Kiumbe ambacho anakichukia katika maisha yake. Mawazo ya miaka ishirini iliyopita yakasonga akili yake, Huku machozi yakimtoka yakiambatana na hasira dhidi ya kiumbe anachokiona mkono wake mmoja ukashika kisu chake vizuri na kuanza kukishusha taratibu juu ya mwili wa mtu yule. Dhambi aliyobeba Nance ndiyo ilikua inamuhukumu mwanamke yule kwa kuwa tu mwanamke ndiye aliyesababisha yeye kuishi misha yale, Na sasa anaamini mwanamke hastahili kuishi kaika ulimwengu huu.
**** ****
Tayari Rajiv akiwa ni mzoefu katika kazi ile mpya huku akipata msaada mkubwa toka kwa Artu Mrema, Mazoezi ya kujifunza kiswahili kwa kasi ndiyo alizingatia kwa kuwa tu lugha kuu ya mawasiliano katika kambi ile ilikua ni kiswahili. ‘Mawasiliano ya mara kwa mara yeye na mpenzi wake Neelam yaliendelea huku mipango kabambe ya kufunga ndoa mwaka unaofuata ikiendelea. Heshima Rajiv aliyojijengea pale kambini ilisababisha kila mmoja ampende na kujijengea kuwa karibu sana na watu pale kambini anzia staff mpaka wakimbizi.
“Vipi mbona wewe sijawahi kukuona ukiingiza Demu katika Tent lako?”
Sauli mfanyakazi mwenzake na Rajiv alikua akimuuliza Rajiv. Rajiv katabasamu na kumuangalia sauli.
“sikia dugu yangu, Hawa wanawake wenu wa kiafrika, ni malaya hakuna msafi hta mmoja, Wahindi na wazungu ndio watu wasaffi tuu”
Rajiv aliongea kwa dharau huku akitema mate chini.
“Wewe ni usafi gani unataka?”
“Hawa wanawake zenu wana hot sana hawawezi kaa masaa mbili bila kufanya mapenzi bila hivyo watakufa kwa hot”
Rajiv alimwambia Sauli huku akiondoka na kumuacha Sauli akimshangaa.
“Hawa wahindi ni washenzi sana, Pumbavu zao”
Sauli alijikuta akilaumu peke yake. Mfumo na mawazo aliyojengewa Rajiv tka akiwa mdogo ndio ulikua ukimfanya kuamini kile alichoambiwa kila mara, Waafrika wana dhambi ya asili na wao ndio walisababisha dunia ikawa na dhambi na ni dhambi kuwa na mahusiano na muafrika na hakuna muafrika aliyebalehe au kuvunja ungo hajawahi kufanya ngono. Aliogopa sana wanawake wa kiafrika huku akikaa nao kwa tahadhari sana. Alikua akishuhudia wafanyakazi wenzake wakilala na wanawake wa pale kambini kila siku ila yeye hakuthubutu hata siku moja.
Swali la Neelam alilomuuliza ndilo lilikua likijirudia kila mara kichwani mwake na kujenga moyo wa uvumilivu ni swali lililokua likifufu upendo wa dhati kwa mpenzi wake huyo.
“Rajiv Tum muj se shadi karoge?” {Rajiv utanioa?}
“Hai mai Neelam” {Ndio Neelam}http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Rajiv alipata faraj sana kila aliposikia kauli hiyo ikijirudia kichwani kwake.
“I Love you Neelam.”
Alijikuta akiongea peke yake huku akitazama picha ya Neelam iliyo katika simu yake.
**** ****
Sauti za ndege za kivita zilizokua zikiranda randa juu ya anga la msitu ue ndizo zilizomshtua Cassim na ukubdili mawazo, Mawazo ya kuitoa Roho ya Mwanamke aliyelala pale chini, Adhabu ya kumtoa roho akiwa kalala pale ilikua ni ndogo sana, Hakuona kama inaumiza kama kumtoa roho mtu ambaye amezimia. Maauzi ya kumbeba na kueleke nae kwenye kibanda chake. Kwa hara safaka akamuweka Tusmo juu ya bega na safari ya kuelekea katika kibanda chake ikaanza, Chini miti mirefu huku akipita katika vichaka vyenye miiba mikali na kuishia katika kibanda cha nyasi moja kwa moja a mpaka ndani na kumlaza juu ya nyasi alizozilaza juu ya kitanda cha kamba. Akimuangalia kwa hasira maamuzi ya kikatili yakapita katika mahakama ya kichwa chake katika kitengo cha maamuzi na kuamua kutengeneza Tanuru la kuni na kumchoma Tusmo Moto. Akitoka huku akikimbia na kwenda eneo anapokusanyia kuni na kuanza kupangua kuni huku akizipanga katika uwanja mkubwa ulio mita miambili na kibanda chake. Hitaji la magogo makubwa ndilo lilihitajika kwa muda huo shoka tayari lilikua katika himaya yake akiwa katikati ya msitu akiangusha miti mikubwa kwa ajili ya kutengenezea eneo la kumchomea Tusmo kama adhabu ya yeye kuzaliwa mwanamke na kukutana na Cassim, Nance alikua keshaufanya moyo wa Cassim kuwa moyo wa kikatili. Kazi haikua rahisi kwa Cassim ni saa moja iklikua inaisha huku akifanya kazi kwa moyo furaha yake ilikua ni kusikia kichwa cha Tusmo kikipasuka katikati ya moto mkubwa. Baada ya kazi ya nzito tayari magogo makubwa yalikua yamekusanywa katika uwanja na mafuta ya taa tayari yalikua yamewekwa juu ya kuni zile. Huku akitabasamu Cassim alsogelea mlango wa Kibanda chake tayari kwa kumchukua Tusmo kwenda kumchoma moto.
Patel akiwa anatokwa na jasho katika kazi nzito ya kuwahesabu wakimbizi waliokuwa wakiingia ndani ya kambi hiyo, Vit vilivyoibuka katika nchi ya Jamuhuri ya watu wa Kolo ilisababisha kambi hiyo kuwa busy sana katika kupokea makundi makubwa wa watu huku wengi wao wakiwa ni wakina mama watoto na wazee.
“Artu chukueni Van nendeni kasaidieni kuwapakia watu wengine huko barabarani”Patel alimwambia Artu kisha Artu akamchukua Rajiv na kukimbilia kwenye Gari. Kazi ya kuwakuanya wakimbizi ilikua ngumu sana kwa Patel, Wengi wao wakiwa wamechoka sana na wanaonekana wakiwa wadhaifu, Maiti nyingi zilikua zimesambaa barabarani na kupelekea Artu n Rajiv kufanya kazi ya Ziada kuweza kupakia maiti na kuzikusanya sehemu moja kisha kurudia watu waliokuwa wamekaa mahali ypamoja na kuwapeleka kambini. Kazi nzito ya kuhakikisha kila mmoja anapewa namba ya utambulisho katika kambi hiyo inafanyika kwa usahihi na umakini mkubwa sana.
“Sasa inabidi hizi maiti tuziweke katika shimo lile pale”
Artu alitoa wazo lililopokelewa na Rajiv huku wakishirikiana na wakimbizi wenye nguvu kuweza kubeba maiti na kuzipeleka katika lile simo.
“Mh mbona hii maiti bado in joto?”
Rajiv alijikuta akipatwa na mshangao baada kubeba maiti moja ambayo ilikua katika hali tofauti.
“Wewe umechoka hakuna mtu mzima hapa Daktari kawapima wote ni maiti”
Artu alimwambia Rajiv huku akimsaidia kuibeba ile maiti na kuitupia katika lile shimo. Mpaka kufika saa tano usiku kazi ya ilikua imemalizika na wakimbizi wote walikua wamepewa namba huku kila mmoja akiwa amelala tayari, Rajiv akia ndani ya hema lake mkononi kashika Picha ya mpenzi wake Neelam huku kaikumbatia. Mawazo ya ile maiti aliyoibeba yakamtawala na akaamka na kutoka nje huku akijificha kwa kunyata kuifuata barabara inapoelekea eneo lilipo lile shimo waliloweka zile maiti, Kwa msaada waga wa mwanga wa simu yake aliweza kuliona lile shimo vyema. Akiangalia ndani ya lile shimo macho yake yalitua katika kitu cha tofauti, Ni mkono wa mtu ukiwa unajitahidi kutoka katikati y maiti. Kama anawahi kitu Rajiv alishuka katika lile shimo na kupangua maiti kwa ujasirikisha akavuta ule mkono uliokua unahangaika, Sura ya msichana mrembo aliyechoka ikakutana na macho yake. Moyo wa huruma ukamkumba Rajiv na kumbeba safari ya kuelekea kambini ikaanza. Moja kwa moja kwa kupita njia ilezile za panya Rajiv alijikut kafika katika hema lake na kumuweka yule msichana. Kwa haraka akachuku maji na kuchanganya na Glucose na kumnywesha yule msichana kisha akamlaza katika kitanda chake. Akihema kwa nguvu huku matumaini ya kuzinduka yakirejea Rajiv alianza kuonyesha Tabasamu.
**** ****
Upepo uliokua ukivuma kutoka katika miti mirefu iliyozunguka msitu na kukutana na ukuta wa kijumba kidogo na kusafiri mpaka kwenye dirisha dogo la kibanda kile na kuingia ndani, Ndio uliomshtua Tusmo na kuzinduka kujikuta yupo katika eneo ambalo hakulifahamu. Kwa wasiwasi alijikuta kaka kitako juu ya kitanda na kuangalia kila upande wa chumba kile. Mapanga yaliyokuwa yametundikwa pembeni ya mlango wa nyumba ile yalomfanya akaingiwa na hofu, Kwa Tahadhari kubwa huku akitembea kwa kunyata alitoka nje. Sauti ya miti mikubwa ikiwa inaanguka huku ikiambatana na sauti ya shoka likikata miti viligonga katika masikio yake na kuingiwa na hofu zaidi. Akikimbia chini ya vichaka na miti mikubwa Tusmo nguvu zilianza kumuishia, Wazo la kupumzika chini ya mti mmkubwa baada ya kutembea kwa zaidi ya Masaa manne lilimjia. Wakati anasogea katika ule mti kumbukumbu wa wanajeshi waliotaka kumbaka ilimjia na kujikuta mwili wake ukipata nguvu upya na safari ya kutafuta njia ya kutoka kaika pori lile ilianza upya.
Sauti ya milio ya ngombe ndiyo ilimpa tumaini kuwa sehemu sauti hiyo inapotokea ndipo kuna makazi ya watu, Ni baada ya kukimbia kwa dakika arobaini na tano zaidi bila muelekeo. Alama za matairi ya Gari katika ardhi ndiyo ilimuongezea tumaini jipya na kujikuta kwa mara ya kwanza atabasamu tokea alipotoka nchini kwao Jamuhuri ya watu wa Kolo. Akiwa na uchovu akifuata Alama zile huku giza nene likiwa limetanda ndipo aliokutana na barabara ya lami iliyokuwa na viraka. Akijikongoja kwa uchovu huku akizipita maiti za watu zikiwa zimelala barabarani huku miili yao ikiwa imekonda sana. Kwa mbali macho yake yakatua katika msururu wa watu waliokuwa wamebeba mizigo wakiishilia mbele ya macho yake.
Tone la maji lililotua juu ya mwili wake lilimfanya Tusmo aangalie juu na kukutana na matone zaidi ya moja yakishuka na kuishia katika mwili wake. Ni mvua kubwa iliyoanza kunyesha huku akikisa sehemu ya kujificha na mvua. Huku njaa ikmsumbua aalijikaza na kuongeza mwendo ndipo alipoamua kupoza kiu kwa kunywa maji yaliyokuwa yakitiririka katika mitaro ya pembeni ya barabara na kisaha kuendelea na safari yake ya kuelekea sehemu asiyoifahamu. Nuru ikaanza kupotea katika mboni za macho yange, Mwili ukapoteza nguvu, Mguu wa kushoto ukashindwa kunyanyuka na kuupita mguu wa kulia. Ishara ya kuishiwa na uwezo wa kusonga mbele ikawa imeshaonekana mbele yake, King’ora cha mauti kikaanza kulia katika ubongo wake. Aya aliyofundishwa na mwalimu wake wa madrasa kuwa binadamu yeyote anapokufa akitamka aya hiyo basi mungu humfutia dhambi zake ilimjia na kujikuta kwa shida akitamka aya hiyo. “ASHAHAD ALLAH ILLAAH AILLALLAH, WAASHAHAD ALLAH MUHAMMAD RASULL LLAH” {Nashahadia hakuna mungu apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyeazi Mungu na Muhammad ni Mtume wake} Baada ya kumaliza kuamka aya hiyo Tusmo alijikuta paji lake la uso likigusana na lami chakavu na kupoteza mawasiliano na ulimwengu huku damu zikitoka kutoka puani.
**** ***
Hali ilikua ya joto sana katika Jiji la Texas, Ni siku ya jumapili ndani ya kanisa la St. Peres lililoko katika mji wa Arkansas moja ya miji maarufu ndani ya Jiji la Texas nchini Marekani. Waumini wakiwa kwakisikiliza mahubiri yaliyokuwa yakitolewa na Padri Valence kwa umakini. Huku upande wa kushoto katika benchi la pili alikua kakaa Taylor Kurt tajiri mkubwa nchini marekani anayemiliki kampuni kubwa ya Mawasiliano Duniani iitwayo Micronet. Smu aina ya Micphone ilinayotengenezwa na kampuni yake ilikua ikitesa katika soko la dunia huku akiongoza kwa mauzo katika nchi nyingi duniani hasa haa Africa, Misaada aliyokua akiitoa katika nchi nyingi masikini zilizopo kusini mwa jangwa la sahara kupitia shirika lake la Kurt Foundation ndiyo iliyomfanya kupata heshima kubwa Duniani na kuwa mmoja kati ya watu wanaoheshimika zaidi Duniani. Akiwa kakaa kimya huku akipitia vifungu kadhaa katika biblia yake yenye kava la Dhahabu, Mara Simu yake ya mkononi inamtingisha ikiwa mfukoni. Kwa tahadhari anaitoa na kutembea kwa mwendo wa taratibu mpaka nje ya kanisa hilo, Mpaka anafika nje Tayari simu ilikua imekatika.Huku akivaa miwani yake na kutazama namba ya mpigaji wa simu.
Taylor Kurt akabonyeza kitufe cha kuzima simu na kuirudisha simu mfukoni kasha akarudi kanisani kuendelea na Ibada. Muda wa kwenda kushiriki chakula cha bwana ulipowadia Taylor Kurt akijiandaa kusimama na kuingi katika mstari wa kushiriki mara anaguswa bega, Anageuka na kukutana na Sura ya Mkurugenzi wa kampuni yake akiwa anatokwa na jasho akamshika mkono na kutoka nae nje huku akiwa mwenye wasiwasi.
“What Happening Mark?” {Mark, Kuna tatizo Gani}
Taylor Kurt alimuuliza Mark huku akiwa mwenye wasiwasi.
“She is Arrested” {Amekamatwa}
Mark alitoa jibu ambalo lilimlegeza Taylor Kurt magoti na kumdondosha chini kama kiroba.
**** ****
Biashara ndiyo ilikua ikifikiriwa kila wakati katika kichwa chake, mbinu mpya za kupambana na wapinzani wake wa kibiashara zilikua zikihitajika, hakuon hatari kugharimu maisha ya kiumbe yeyote Yule anayeingilia uhuru wa soko la biashara yake. Akiwa kajizatiti katika kila idara ya usalama duniani hitaji lake ni kuhakikisha kuwa anaikamata dunia katika biashara, Mshahara mkubwa aliokuwa akiwalipa wafanyakazi wake ndio ulikua chachu ya maendeleo katika kampuni yake. Hakuna mfanyakazi aliyelala kazini kila mmoja alikua akichapa kazi kwa umakini zaidi. Kuamua kuacha kazi ghafla kwa mfanyakazi wake wa kitengo cha marketing plan hkikumshtua sana ila sasa alianza kuona athari ya mfanyakazi huyo. Kikao cha dharura chini ya handaki lililo katika nyumba yake ya kifahari iliyoko ufukweni mwa bahari katika eneo maarufu Marekani liitwalo MIAMI BEACH, Moshi mwingi uliokuwa ukitoka katika kiko kilichotengenezwa kwa Silva na kunakshiwa kwa mti wa mpingo ulifuka na kufanya eneo lile kutawaliwa na harufu kali ya tumbaku haramu. Ni harufu ya bangi ndiyo ilikua ikitoka katika kiko kile. Macho yake yakiwa yamekwishabadilika rangi na kuwa na rangi nyekundu aliwatazama vijana wake wanne mmoja mmoja kwa zamu huku akitafakari kitu.
“Don unajua kwanini Serikali ya Marekani inakulinda?” Aliongea kwa Sauti ya kukoroma huku akimuangalia Kijana mmoja aliyevaa koti refu la rangi ya zambarau.
“Hapana Mkuu” Don alijibu huku akiangalia chini
“Ok, Ni kwasababu unapaswa uilinde biashara yangu” Aliongea kisha akapeleka kiko mdomoni na kuvuta akatoa moshi mwingi mdomoni huku akikunja sura.
“Derick na wewe unajua kwanini upo CIA?” Alimuuliza kijana mwingine aliekua kavalia suti ya kijivu,
“Ndiyo Mkuu” Derick alijibu kwa kujiamini,
“Mmh ni kwanini?” Swali la kutaka ufafanuzi wa jibu lake lilirudishwa kwa Derick.
“Sababu kubwa ni kuilinda miji ya nchi yangu, na mipaka yake pia” Derick alijibu huku akiangalia kalamu aliyokua kaishika muda wote.
“Ooh, Sasa kwanini Don alipolipua kituo cha watoto wenye vipaji maalumu kule New Jersey hukumkamata angali ulimjua?” Swalii kutu lilitua kwa Derick na kutengeneza kigugumizi.
“Nilipokea magizo toka kwa maafisa wa ngazi ya juu kuwa niachane na file la kesi hii” Derick alijibu huku akimungalia Don.
“Unajua kwanini upo hapa?” Nafasi haikuachwa baada ya jibu la Derick alipigwa swali jingine jepesi sana.
“Nimepewa maagizo nije kukusikiliza na kufanyia kazi kile utakachoniagiza” Derick alijibu kwa umakini sana.
“Vizuri sana,” Alivuta kiko na ulikuliza moshi juu kisha akageuza shingo na kumtazama kijana mwembamba aliyevalia miwani ya jua.
“Denis Norton mwanaume jasiri habari yako”
Denis lijibu kwa kutikisa kichwa kuashiria jibu chanya kwa swali aliloulizwa.
“Habari ya FBI”
Ni nzuri sana, Denis alijibu kwa sauti ya chini.
“Kwanini umenisahau Denis?”
“sijakusahau mkuu ndio maana nipo hapa kwa ajili yako”
Denis alijibu huku akirekebisha miwani yake vizuri.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mmh, Duke man of National Security Agency how are you” {Duke Kijana wa Usalama wa Taifa , Habari}
“Salama mkuu” Duke alijibu kwa unyenyekevu.
“ Unatambua wajibu wako hapa” Swali lilielekezwa kwa Duke
“Ndio Mkuu”
“Ok sasa nisikilizeni vijana, Huyo hapo anaitwa Don, Ni kijana mbaya sana na ni Adui yenu nje ya hapa ila kwa hapa ni rafiki yenu, Yeye ndiye anayeinyima serikali ya Marekani usingizi ila pia ni Rafiki mkubwa wa viongozi wa ngazi ya juu ya Serikali yenu. Nilichowaitia hapa kuna kazi nataka kumpa afanye ila ninyi mnatakiwa mumlinde”
Derick alishtuka na kumkazia macho Don.
“Don kuna mtu anaitwa Taylor Kurn mmiliki wa kampuni ya Micronet anatishia uhai wa kampuni yangu, Sasa nataka Don amuue ila ninyi ndio mtahakikisha Don anaifanya hii kazi pasipo usumbufu.”
Derick wewe utahakikisha Ulinzi wa jeshi la polisi unahama eneo ambalo Don atakuwepo kumuondolea usumbufu, na Duke wewe utahakikisha hakuna kamera itakayommulika Don wakati wa kazi na wewe Denis utahakikisha unaufanyia mwili wa Taylor Kurt uchunguzi kabla ya Mtu yeyote.”
Alimaliza kuzungumza kisha akanyamaza kutoa nafasi ya maoni.
Mkuu unaonaje huu mpango usiwe kama kawaida, Hizo ni mbinu za zamani sana, Hata Taylor akifa bado kampuni yake itaendelea kuwepo Nafikiri inabidi kufikiri wazo jingine au mnasemaje DDD”
Denis alitoa wazo lililoungwa mkono na wenake wote.
“Mimi naona Tutafute kitu ambacho kitasababisha serikali ifunge hiyo kampuni ya Taylor nay eye mwenyewe Ashtakiwe.”
Duke alitoa wazo lililopelekea mkuu wa kikao kile kutikisa kichwa kukubaliana na wazo hilo,
“Off Record, tukutane saa moja usiku, Sasa nendeni kila mmoja akafikirie Mbinu ya kuimaliza Kampuni ya Taylor Kurt”
**** ****
Tusmo akiwa kalala pale chini huku nafsi yake ikipambana na uhai, Wakati hali hiyo ikiendelea ndio wakati ambao Rajiv na Artu Mrema walikuwa wakikusanya Miili ya Raia waliokuwa wamekufa barabarani. Muda huo ndio Rajiv alikua kafikia mwili wa Tusmo na alikua akihisi hali tofauti ya mwili huo na kupokelewa na jibu la Artu kuwa ni maiti na kumtupa kweye shimo lenye maiti wengine.
**** ****
Rajiv alifurahi sana baada ya Tusmo kumka, Hofu ya kumtoa Tusmo ndani ya lile tenti lake ilikua kubwa sana, Hofu ya kwanza ni kuwa Tusmo hakuwa na namba ya Usajili na hofu ya pili ni kuwa Tusmo hakuwa raia wa Tanzania. Moyo wake wa huruma ulimshauri kuendelea kuishi na Tusmo pale ndani mpaka atakapopata nafuu na kuweza kumtorosha aondoke zake. Wiki ya tatu sasa ilikua imekwishakatika hali ya Tusmo iliku nzuri sana huku akizidi kunawiri na kuvutia. Kwa jinsi walivyokuwa wamezoeana utadhani ni mtu na mpenzi wake ila hakuna hata mmoja aliyekuwa akifikiria suala la mapenzi.
“Rajiv njaa inaniuma mpenzi”
Tusmo alimwambia Rajiv huku akimpigapiga mgongoni
“Sawa don’t worry naleta food now”
Rajiv litoka nje na kwenda moja kwa moja mpaka Jikoni.
Joto lililokuwa ndani ya lile hema siku hiyo lilimtesa sana Tusmo na kuamua kuvua nguo zot alizovaa kisha akajifunga kanga tu, Ratiba ya kuoga usiku kwa usiku ndio ilikua ikimtesa japo alitamani sana kuoga ila hakuruhusiwa kutoka nje mchana.
“Mother iko n njaa naweza pata chakula”
Rajiv alimwambia Mama Leah mama mpishi katika kambi ile, Mama Leah alijibu kwa ishara kisha akachukua sahani na kwenda kumpakulia Rajiv Chakula na kumpatia. Rajiv akiwa kabeba sahani ya chakula huku akikimbilia katika tenti lake na kuingia moja kwa moja.
Tabia ya Rajiv kupenda kukaa ndani ya Tenti lake muda wote ilikua ikimshangaza sana Patel mkuu wake wa kazi, na Tabia mpya aliyoianzisha ya kujitenga wakati wa kula na kwenda kula ndani ya tenti lake tofauti na mwanzo ndiyo ilimshangaza zaidi na kuamua kuanza kumfuatilia. Kila mara akiwa kabeba chakula na kuingia katika Tenti kisha kutoka na kuchukua vikombe viwili vy chai ndicho kilimvuta zaidi Patel na kusikiliza kupitia nje ya Tent. Sauti ya Rajiv kiongea na mtu ilikua ikipenya katika masikio ya Patel kitendo kilichopelekea kuamua kuingia ndani. Macho ya Patel yligongana na Sura ya binti aliyekaa katika kitanda kidogo huku kava kanga moja huku Rajiv kiwa kaka pembeni yake akimnawisha mikono.
“Rajiv Huyu ni nani”
Swali gumu sana lilitua katika himaya ya Rajiv na kumshinda nguvu kitendo kilichopelekea kikombe chenye maji na bakuli kudondoka chini.
“Rajiv Kya ara yu kama kara raha satha?” {Rajiv Unafanya nini na huyo nyani}
“Kuch nay” {Si kitu}
Patel alimuagalia Tusmo kwa hasira.
“Wewe Nyani unafanya nini humu ndani”
Patel aliuliza kwa hasira kitendo kilichopelekea Tusmo kuamka kwa hasira na kumpiga Patel kibao. Kwa hasira Patel alimvuta Tusmo kanga ikadondoka akabaki kama alivyozaliwa kitendo kilichoamsha zogo ambalo lilivuta watu wengi.
“Dah kumbe huyu muhindi ni Malaya hivi yaani anafanya ngono na jua lote hili”
Mmoja wa wafanyakazi wa kambi ile aliongea huku akifuatilia lile tukio kwa ukaribu zaidi.
“Sasa hili suala namueleza aliyekuleta hapa”
Patel aliongea kwa hasira huku akitoa simu yake katika mfuko wa suruali, Kitendo kilichofanya Rajiv aanze kutetemeka.
**** ****
Anaitwa Martin Cruez, ni mmoja wa matajiri wakubwa ndani ya nchi ya marekani, Akiwa anakairiwa kuwa ni tajiri wa tatu kati ya matajiri wakubwa duniani na ni mfanyabiashara maarufu duniani, Akiwa ndio anaumri wa miaka arobaini na mbili alikuwa anamiliki tv maarufu marekani iitwayo HOBY TV na Jarida maarufu nchini humo liitwalo NAKED, Mbali na hizo pia alikua akimiliki Kampuni kubwa ya mawasiliano iitwayo OFFNET huku akimiliki mashamba makubwa kaskazini mwa nchi ya marekani ambapo alikua akilima Mahindi zao maarufu a biashara nchini humo. Sura yake ya huruma na tabasamu la mara kwa mara ndilo lililoficha siri kubwa kuhusu yeye na ukatili ulio nyumba ya pazia.
“This is a good guy” {Huyu ni mtu mzuri sana}
Ni mama mmoja alisikika katika mgahawa mmoja wakati anaangalia taarifa katika kituo kimoja cha luninga juu ya msaada uliotolewa na Martin Cruez kwa watu walioathiriwa na kimbunga cha Katrina huko kusini mwa marekani.
Huyu ndiye Martin Cruez tajiri katili aliyeko katika mikakati ya kuhakikisha anammaliza mpinzani wake wa kibiashara Taylor Kurt.
“Ok Derick sasa nipo tayari kusikiliza maoni yenu”
Martin Cruez aliongea huku akiwaangalia wale vijana kwa zamu.
“Mimi wazo langu mnaonaje tukampandikizia silaha za kivita katika nyumba yake na kumkamata kama gaidi”
Derick alitoa wazo katika kikao kile.
“Hapana hiyo hainogi hata kidogo, Mimi wazo langu ni kuwa Don asajilie kampuni haraka sana na yeye awe mmiliki na aombe kazi ya kufanya Parking ya simu katika kampuni ya Taylor na akipata tenda hiyo amshawishi Taylor kujiingiza katika biashara ya usafirishaji wa dawa za kulevya akiingia mkenge tu tunamtia mbaroni hapo utakuwa mwisho wa mchezo wake”
Wazo thbiti lilitolewa na Denis Norton kijana jasiri na silaha makini ya Federal Bureau of Investigation au kwa kifupi FBI. Wazo ambalo liliublika kwa asilimia mia moja na mipango ya usajili wa kampuni ikaanza huku Martin Cruez akitumia uwezo wake usjili kwenda haraka ndani ya mwezi mmoja tayari kampuni ilikua inatambulika kisheria huku Don akitambulika kama Lewis Donald.
**** ****
Patel alikua akipiga picha kwa kutumia simu yake huku akimvuta Rajiv akae karibu na Tusmo wakati huo Tusmo alikua bado yupo uchi, Muda huo tayari watu walikua wamejaa eneo hilo Pael kwa hasira alitoa amri Tusmo avae nguo zake huku Monjoo mlinzi mkuu wa eneo hilo akitoa begi la Rajiv kutoka ndani ya lile tent na Rjiv akakabidhiwa kisha akafukuzwa akiwa pamoja na Tusmo.
Rajiv akiwa amechanganyikiwa asijue cha kufanya aliondoka huku kainamisha kichwa chini akifuata barabara kubwa inayotoka eneo la Kambi hiyo huku kila mtu akimshangaa na nyuma yake Tusmo alikua akimfuata taratibu. Mwendo wa zaidi ya saa moja walikua wamekwisha tembea pasipo kusemeshana.
“Wewe unajua haya maeneo”
Rajiv alijikuta akivunja ukimya kwa kumuuliza Tumo
“Hapana sijui eneo lolote hapa Tanzania”
Tusmo aitoa jibu ambalo lilimpeleka Rajiv mpaka chini ya mti na kukaa huku Tusmo akisogea na kukaa pembeni yake. Jua lilikua limeanza kuwa kali huku hakuna hata dalili ya mtu kuwa katika eneo hilo. Sauti ya ngombe ndiyo iliwapa tumaini la kuendelea kutembea huku wakiamini mbele ya eneo hilo kuna makazi ya watu. Baada ya mwendo wa zaidi ya dakika ishirini macho yao yaligongana na numba za majani ishara kuwa kile ni kijiji wanapoishi watu. Kwa mwendo wa uchovu Rajiv alisogelea nyumba moja na kuanza kugonga, Mzee wa makamo akatoka huku akimuangalia Rajiv kwa mshangao.
“ikusaidie nini kijana, Leo sifanyi kazi”
Yule mzee alimjibu Rajiv
“Hapan mzee sisi ni wageni tunauliza njia ya kuelekea mjini”
Rajiv alijibu huku akikerwa na harufu ya ubani ilyokuwa inatoka ndani ya ile nyumba ya Yule mzee dalili ambayo iliashiria kuwa Yule mzee ni mganga. Yule mzee akaingia ndani na kutoka kisha akaongozana na kina Rajiv mpaka nyumba ya tatu akaingia ndani na kutoka na kijana mdogo, Yule mzee akampa maelekezo Yule kijana akazunguka nyuma ya nyumba na kurudi akiwa na Punda wawili waliokuwa wakivuta mkokoteni na kuwaashiria wakina Rajiv wapande, Safari ya kuelekea mjini ikaaanza. Huku kimya kikichukua nafasi yake safari ikiendelea katika njia mbovumbovu huku Yule kijana akijitahidi kuongoza wale punda mpaka walipofikia barabara kubwa ya lami wale punda wakasimama pembeni.
“Hapa mtapata gari la kwenda mjini”
Yule kijana aliwaambia wakina Tusmo na kisha wakashuka, Rajiv akaingiza mkono mfukoni na kutoa not inane za shilingi mia tano na kumpatia Yule kijana.
“Tunashukuru sana kwa msaada wenu”
Rajiv alishukuru kwa Yule kijana. Yule kijana akitabasamu akapokea na kugeuza punda wake akaondoka huku akimuacha Rajiv na Tusmo pale njiani wakisubiri gari la kuwafikisha mjini.
Haikupita muda daladala ikasimama pembeni yao bila kuuliza wakaingia na safari ikaendelea mpaka kituo kikuu cha mabasi ndani ya Jiji la Mwanza. Wingi wa watu katika eneo hilo ndio uliokuwa ukimshangaza Tusmo, Mawazo ya nyumbani kwao katika nchi ya Jamuhuri ya watu wa Kolo ndio yalimsonga kwa wakati huo. Sauti ya Dereva Tax aliyopanda ndiyo ilimshtua Tusmo na kutoka katika mawazo.
“Niwapeleke wapi ndugu zangu”
“Tupeleke katika nyumba ya kulala wageni”
Rajiv alijibu huku akiwa kajiegemeza kwa uchovu ndani ya ile Tax
“Niwapeleke za bei nafuu au zile za matajiri”
“Bei nafuu tu Dugu yangu”
Rajiv alitoa jibu lililosababisha injini ya gari kuunguruma na tairi za mbele za gari zikaanja kuvuta tairi za nyuma safari ya kuelekea katika nyumba ya wageni ikaanza.
*** ***
Urembo wake tu ulisababisha kila mtu kumkodolea, uwezo wake wa kuutumia mwili wake katika kila anachofanya ili tu kuleta ushawishi na kufanikiwa katika kazi aliyopewa ndicho kitu kilichopelekea kusafiri nchi mbalimbali katika kufanikisha mipango mbalimbali ya watu. Alipenda kujiita Solution Qeen, ila jina lake halisi ni Karma, Binti mwenye asili ya Kivenezuela aliorithi toka kwa mama na kimarekani toka kwa baba. Ni mototo wa mmarekani mweusi muoka mikate aitwae Tody aliyekulia katika eneo la watu masikini marekani liitwalo New Jersey. Karma akiwa ndio kwanza ana umri wa miaka ishirini na moja alikua keshajitengenezea zaidi ya dola milioni mbili katika akaunti yake. Huku akimiliki nyumba mbili za kifahari zilizoko katika eneo la matajiri moja ikiwa Mississipi ambayo anaishi baba yake huku nyingine ikiwa Florida ambayo anaishi yeye pekee. Mwanga wa mafanikio ulianza kuonekana pale alipopanda jukwaani katika kuwani taji la kuwa mrembo wa New Jersey na kisha kupata nafasi ya kuwania Taji la America hpo ndipo nyota yake ilipong’aa baada ya kushika nafasi ya Tano. Mialiko mbalimbali aliyoipata ndiyo ilifungua njia ya kujuana na matajiri wa Marekani na kuanza kutengeneza pesa.
Sasa Solution Qeen alikua akitemtbea juu ya sakafu ya Kampuni ya Micronet iliyoko katika mji wa Arkansas ulioko ndani ya jimbo la Texas, Sauti ya viatu vyake aina ya Italian tone High heels viatu ghali duniani iliyokuwa ikibembeleza sakafuya Jengo la ofisi ile na kusababisha kila aliyesikia sauti ile kugeuka na kutazama kiatu kinachokanyaga sakafu ile na mwishowe kutazama uthamani wa kiumbe kilichobebwa na kiatu hicho.
“Naitwa Karma nahitaji onana na Mmiliki wa kampuni hii”
Karma aikua akiongea na Katibu muhtasi wa kampuni ile.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Samahani una miadi naye”
Karma aliachia tabasamu pana na kurekebisha miwani yake ya macho vizuri.
“Hapana ila mwambie asiye na Miadi kaja anahitaji kuona”
“Hapana dada yangu, Utaratibu wa ofisi unaomba miadi ya kuonana nae kwanza”
Karma alidondosha kalamu na kuitazama kupitia pembeni ya miwani na kitendo kilichopelekea Yule katibu muhtasi kutaka kujua kilichodondoka. Macho yake yakakutana na Italian tone high heels na kupigwa na mshtuko wa hali ya juu. Ni watu wachache walioripotiwa kununua kununua aina ya viatu hivyo akiwemo Binti wa Rais wa Marekani. Kabla Yule binti hajasema chochote mlango ukafunguliwa akatokeza Taylor Kurt macho yake yakakutana na macho ya Karma na kwa haraka karma akahamisha macho yake kuelekea katika ile kaamu pale chini kisha akainua mguu na kusababisha Sakafu kulalamika kutokana na kisigino cha kiatu kukutana na ile sakafu kitendo kilichopelekea Taylor Kurt kupigwa na butwaa huku akishangaa uzuri wa mguu uliobebwa na kiatu cha gharama.
“Kuna tatizo gani hapa?”
Taylor Kurt alijikuta akiuliza swali bila kutarajia.
“Kuna tatizo kubwa katika kampuni yako”
Karma alijibu huku akimuangalia Taylor Kurt machoni
“Tatizo? Tatizo gani?”
Karma alipiga hatua na kumshika Taylor Kurt mkono na kuingia nae katika ile ofisi liyotokea.
“Mipango bora hupangwa na watu bora"
Karma alizungumza huku akijiweka vyema katika kiti pale katika ofisi ya Taylor Kurt.
Karma aikua akiongea na Katibu muhtasi wa kampuni ile.
“Samahani una miadi naye”
Karma aliachia tabasamu pana na kurekebisha miwani yake ya macho vizuri.
“Hapana ila mwambie asiye na Miadi kaja anahitaji kuona”
“Hapana dada yangu, Utaratibu wa ofisi unaomba miadi ya kuonana nae kwanza”
Karma alidondosha kalamu na kuitazama kupitia pembeni ya miwani na kitendo kilichopelekea Yule katibu muhtasi kutaka kujua kilichodondoka. Macho yake yakakutana na Italian tone high heels na kupigwa na mshtuko wa hali ya juu. Ni watu wachache walioripotiwa kununua kununua aina ya viatu hivyo akiwemo Binti wa Rais wa Marekani. Kabla Yule binti hajasema chochote mlango ukafunguliwa akatokeza Taylor Kurt macho yake yakakutana na macho ya Karma na kwa haraka karma akahamisha macho yake kuelekea katika ile kaamu pale chini kisha akainua mguu na kusababisha Sakafu kulalamika kutokana na kisigino cha kiatu kukutana na ile sakafu kitendo kilichopelekea Taylor Kurt kupigwa na butwaa huku akishangaa uzuri wa mguu uliobebwa na kiatu cha gharama.
“Kuna tatizo gani hapa?”
Taylor Kurt alijikuta akiuliza swali bila kutarajia.
“Kuna tatizo kubwa katika kampuni yako”
Karma alijibu huku akimuangalia Taylor Kurt machoni
**** ****
.....,
Simu ikiwa mkononi Jasho likimtiririka huku mwili wake ukikumbwa na hali ya tofauti, ni hali ya mtetemeko ni mtetemeko uliobebwa na hasira kali. Japo hali ya hewa ilikua hairuhusu joto na kiyoyozi kilichokuwa kikipuliza ndani ya ofisi yake kilitosha kabisa kukimbiza Joto katika eneo lile. Macho yake yakiwa yameelekeza katika simu yake aina ya blackberry huku akiwa kasimama dirishani. Viganja vya mikono yake vilitua juu ya kichwa chake na kukuna upara uliopitiliza mpaka kichogoni kitendo kilichomfanya kishusha pumzi na kujibwaga katika kiti cha ofisi yake. Hasira ikiwa imemkaba mpaka kupelekea kushindana na roho yake kutoka ma kubaki alisogelea kompyuta iliyo pale ofisini kwake na kuanza kuunganisha waya fulani kisha akauweka katika simu yake na kuruhusu viganja vyake kucheza na Panya wa kuendeshea ile kompyuta mara karatasi zikaanza kutoka katika mashine ya kudurufu karatasi. Picha kubwa iliyodurufiwa ikaonekana katika zile karatasi. Kwa haraka akachukua picha zile na kuweka katika mkoba wake mkubwa na kutoa simu yake ikatangulia katika mfuko wa suruali yake. Hatua za kuiacha ofisi yake zilifuata na kugomea hata chache na mlango wa kutokea macho yake yakagomea katika picha kubwa iliyo ukutani, ni picha inayomkuumbusha miaka mingi iliyopita picha mabayo alipiga na rais wa kwanja wa Tanzania. Urafiki wao ndio ulimfanya kupata heshima ndani ya nchi ya Tanzania. Huyu si mwingine ni Pandya mfanya biashara mwenye asili ya kihindi anayemiliki makampuni mbalimbali ikiwemo kampuni ya usafirishaji huyu ni baba yake na Neelam, Hakuna kitu alichokua anakipenda na kukithamini katika maisha yake kama mtoto wake wa pekee Neelam, Uwezo wake wa kutopata mtoto baada ya kuathiriwa na ugonjwa wa kansa ya mfuko wa kuzalisha mbegu za uzazi ndicho kitu pekee kilichomfanya kuhamishia furaha yake kwa binti yake. Mipango yake ya kumkabidhi Rajiv kampuni ya Usafirishaji iliyeyuka kama Siagi kwenye kikaango cha moto na kujenga chuki, Chuki nzito sana huku akimfikiria binti yake atakavyopokea taarifa ya Rajiv kulala na mwanamke, Mbaya zaidi mwanamke wa kiafrika tena si taarifa ya maneno ni taarifa yenye kielelezo cha picha.
*** **
Tax huku kila mmoja akaiwa na mawazo yake, Dereva akiwa bize na usukani akikatiza mitaa ya jiji la mwanza na kuachana na mji kisha akaanza kamata barabara ya vumbi kuelekea katika mtaaa wa Igogo. IGOGO LODGE ni maandishi makubwa yaliyo katika ukuta wa nyumba moja kubwa ya kulala wageni, Gari ilisimama pembeni na dereva akawapa ishara wamefika, Rajiv na Tusmo wakashuka na kuingia ndani.
"Karibuni"
Muhudumu wa nyumba ile ya wageni aliwakaribisha kwa ukarimu
"Tunashukuru"
Tusmo alijibu huku akimuangalia Rajiv machoni.
"Tutapata pakulala?"
Rajiv aliuliza kwa kiswahili kibovu
"Ndiyo mtapata kuna self na Single"
Hiyo Self ndo ina nini?"
Rajiv aliuliza swali la ufahamu
"Ina bafu na choo, Ina vitanda viwili"
"Ok tupatie hiyo ni pesa ngapi?"
"Elfu sita"
Rajiv alimungalia Tusmo kisha akatabasamu, Hakutegemea kiwango kidogo cha fedha kiasi kile , Rajiv akatoa pesa ya kukaa wiki moja kisha wakapelekwa katika chumba. Tusmo alikaa katika kitanda chake na Rajiv akaa katika kitanda chake.
"Rajiv!"
Tusmo alimuita Rajiv kwa sauti ya upole, Rajiv akageuza shingo kumuangalia Tusmo
"Naomba samahani sana kwa kuuingza matatizoni na naona ni vyema ukaniacha niende nisikubebeshe mzigo"
Tusmo aliongea hukumachozi yakimtiririka mashavuni. Rajiv akamuangalia Tusmo kwa huruma.
"Usijali Tusmo, Wacha uishi hapa tuangalie mbele, Siwezi kuk ugenini mimi ndiye mwenyeji wako usijali"
Rajiv alimjibu Tusmo kwa msisitizo.
"Nashukuru sana kakangu Rajiv, Mungu atakulipa kwa wema wako ulionionyesha sitokusahau milele."
Tusmo lijikuta akiongea huku akilia kwa uchungu kitendo kilichopelekea Rajiv kusogea na kuanza kumbembeleza.
*** ***
Ugeni aliopata ndio ulimchanganya uzuri wa mgeni huyo ulikuwa ukizunguka katika eneo kubwa la ubongo wake na kumfanya apoteze ujasiri wa kiume, Mikono milaini iliyogusana na mwili wake ya huyo binti ilitosha kujua kuwa ni binti kutoka katika familia Tajiri sana hapo marekani. Akiwa katuliza macho katika kifua cha yule binti kilichobeba maziwa makubwa yaliyowekwa vizuri na kufanya rangi ya ngozi yake kung’aa zaidi huku michirizi ya rangi ya brown ikiwa inaonekana. Kikohozi cha kichokozi ndicho kilichomtoa Taylor Kurt katika mawazo aliyokuwa kazama kwa sekunde kadhaa.
“Taylor Kurt do you know your so expensive?” (Unajua wewe ni ghali sana Taylor Kurt)
Karma alizungumza kwa upole huku akimtazama kwa makini sana Taylor Kurt kitendo kilichofanya Taylor Kurt kushtuka na kupepesa macho yake pande zote.
“Why....! (Kwanini..?)
Taylor Kurt aliuliza huku akipigwa na butwaa zaidi
“Do you speak any other language?” (Je unaweza zungumza lugha nyingine)
“Yes i Do, Why” (Ndio, Kwanini?)
Taylor Kurt alizidi kumshangaa yule Karma
“Ok let’s speak sweet language” (Sawa wacha tuongee lugha Tamu)
“Which one?” (Ipi hiyo)
“Swahili Language” (Lugha ya kiswahili)
“Eh Do you know swahili language?” ( Eh unajua lugha ya kiswahili)
“Ni tamu sana na hupenda kuitumia pindi ninapozungumza na mtu mwenye shida kama wewe”
Taylor Kurt alipatwa na mshtuko baada ya kusikia kwa mara ya pili kuwa yeye anatatizo
“Tatizo gani”
Taylor Kurt aliuliza kwa hamaki
“Tatizo lako hupati faida unayostahili katika biashara yako”
“Sipati faida? Mbona napata faida ya kutosha?”
Kila alichoambiwa Taylor Kurt kilizidi kumshangaza
“Sawa wacha nikuonyeshe kwa mifano, Je ukivaa miwani au ukivua miwani ni wakati gani unaweza kuona maandishi kwa usahihi kabisa?”
“Nikivaa miwani”
“Vizuri sana, na Je ukivaa miwani na ukivua miwani ni wakati gani unaweza kumuona mtu kwa urahisi zaidi?”
“Nikivua miwani”
“Sasa Umeshanielewa?”
“Hapana bado unanichanganya”
“Sawa embu vua miwani sasa”
Taylor Kurt kama anaendeshwa kwa remote control alijikuta akivua miwani na kumkazia Karma macho. Karma alilegeza macho na kujiinua kidogo kisha akapeleka mkono wake mpaka kwenye kifungo cha mini sketi ake na kufungua kisha akaishusha, Chupi aina ya G Close hupi ghali zaidi duniani iliyonakshiwa kwa utepe wa madini ya Tanzanite yanayopatikana kaskazini mwa nchi ya Tanzania pekee ilionekana, Taylor kurt hakuamini alichokiona ni Chupi ambayo inamnyima usingizi mke wake, Uthamani wa binti aliye mbele yake ukazidi kupanda katika kichwa cha Taylor Kurt. Karma alipandisha sketi yake na kufunga kifungo kisha akakaa kati kiti chake.
"Unajua bei ya G Close?"
"Ndio najua ila sijawahi kuona mtu kavaa"
"Unadhani mimi ni wa Thamani?"
"Ndio tena maradufu"
"Kwanini?"
"Sababu ya hiyo G Close na hata hivyo viatu japo si ghali kama hiyo chupi"
"Unafikiri kwanini ya ndani ni Ghali na vya nje si ghali sana"
"Sababu ni mtu maalumu ndiye huona"
"Katika biashara yako wewe unamuheshimu nni?"
"Mteja"
"Na katika familia yako unamuheshimu nani?"
"Mke wangu"
"Kama ikitokea mimi ni Malaya na umeninunu hatujakubaliana malipo tukafika hotelini nikavua nguo ukakuta nimevaa G Close utafikiri kunilip pesa ngapi?"
"Nitajua wewe ni wa Ghali sana nitakulipa pesa nyingi mara dufu"
"Ndio maana ninasema Kampuni yako ina tatizo?"
"Tatizo gani?"
"Tatizo la kampuni yako ni wakati wa kufanya Parking wa mzigo, Parking yenu inashusha thamani ya Bidhaa zenu, Uthamani wa bidhaa huwa maradufu kwa muonekano wa parking"
Karma alishusha pumzi na kulegeza macho huku akimuangalia Taylor Kurt, Kisha anaingiza mkono katika pochi yake ndogo na kutoka na mkebe wa dhahabu akafingua na kutoka na kadi yenye muonekano kama kioo juu yake kukiwa na maandishi.
"Naitwa Karma Dodi au Solution Qeen, Natokea kampuni ya American Bussiness Solution mimi pekee ndiye mwenye uwezo wa kufanya bidhaa yako ikaheshimiwa dunia nzima, Tuwasiliane kama hutojali."
Karma aliacha ile kadi ple mezani na kuanza kuondoka huku akimuacha Taylor kurt akipigwa na Butwaa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
**** ****
Neelam akiwa kakaa nyumbani kwao Kunduchi, Miwani ya HD ikiwa michoni mwake huku akiangalia Tv, Sauti ya viatu ikiwa inakanyaga juu ya sakafu ya sebule yao ikasikika, Neelam akashusha sauti ya Tv na kuvua Miwani kisha akageuza macho na kukutana na baba yake. kitendo cha Neelam kumuangalia baba yake kilisababisha Machozi kumtoka Mzee Pandya na kumshangaza Neelam, Tokea kuzaliwa kwake hakuwahi kuliona chozi la baba yake ila hata siku aliyokufa Babu yake baba wa baba yake hakukumbuka kama alimuona yake akilia zaidi ya kumuona akiwa busy katika shughuli ya mazishi.
"Dad what is Happening?"
Swali la Neelam lilimchoma Mzee Pandya na kunyanyua kinywa kumjibu binti yake aliyempenda kuliko kitu kingine katika ulimwengu huu.
"Is Raj....."
"Mooooooooooooommmmmmmmmmmmm"
Neelam alipiga kelele kwa nguvu kumuita mama yake huku akikimbilia mahali baba yake alipodondokea.
**** ****
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment