Search This Blog

Tuesday, 1 November 2022

UMENIFUNGULIA DUNIA - 1

 






IMEANDIKWA NA : RAMAAH MZAHAM



*********************************************************************************



Simulizi : Umenifungulia Dunia

Sehemu Ya Kwanza (1)





…Ni kweli tumekutana kwa bahati mbaya, lakini Please haitawezekana kukuachia tena utoke mikononi mwangu uende mbali nami halafu baadae niteseke, ni heri nisingekuona, ningebaki najiuliza ni wapi ulipo.

Tambua nina mengi sana ya kuongea nawe,

maana ni kitambo sana, lakini zaidi ni kukushukuru mpenzi, kwani..



Sehemu ya kwanza.



KUONANA NA SALAMA



Sikujua kama nampenda hadi siku tulioagana na kumuona akipanda basi kuelekea Mwanza kwenda kusoma, siku hiyo ndio nilitambua ni kiasi gani nampenda. Siku ya tukio ilianza vema baada ya Mwinyi kuamshwa kwa kugongewa dirisha asubuhi na mapema kabla hata jua halijachomoza.

Kitendo cha kutoka nje, anakutana na mgeni wake aliekuja kumlipa deni lake, ilikuwa ni burudani. Baada ya muda uzuri wa siku ile ukabadilika na kuwa ni siku mbaya kabisa, Salama, msichana ambae sikujua kama nampenda, alinipigia simu kunitaarifu juu ya safari yake ya dharula kulekea Mwanza ambayo imepangwa kwa dharula na mama yake

Sikuwa na uchaguzi tena, ikanilazimu nimshindikize hadi Stand kuu ya mabasi, nilikaa nae hadi ilipotangazwa kuwa baada ya dakika chache gari litaondoka, mi sikutaka basi liondoke nami nikiwa pale, hivyo niliondoka kabla kwa kuhisi upweke. Niliingia ndani na moja kwa moja nikapitiliza kitandani, japo ilikuwa ni saa 6 mchana.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Shida ilikuwa ni kulala, usingizi ukagoma, nikafungua Classic radio ili kuliwazwa na muziki, naam... palikuwa na muziki mtaamu sana, ulikuwa ni muziki wa taratibu. Wimbo wa kwanza kuusikia ulikuwa ni ‘Queen of my heart wa Westlife’ kisha ukafuatia wimbo wa Kylie Minoque uitwao ‘Especially 4U’ kabla ‘My place’ wa Nelly haujachukua nafasi.

Ni kama mtangazaji aliekuwepo studio alikuwa akijua kuwa kuna mtu anaguswa na nyimbo zile, akapiga wimbo wa Enrique Iglecious uitwao ‘Hero’ akiufuatanisha na wimbo wa ‘Im UR Angel’ wa Celine Dion na R Kelly, kilichonisumbua zaidi ni wimbo ‘4U I will’ wa Monica Arnold, nilinyanyuka mwenyewe kitandani.

Wimbo huu mie huupenda zaidi kwa sababu ya maneno yake ambayo anayasema mwanadada huyu, hasa pale anapotamka “I will cross the ocean 4U, I’ll go and bring U the moon…” ni vitu ambavyo vyote haviwezekani, lakini ndani ya penzi vinawezekana.

Nikabadili station na kuweka Power FM, akakuta kuna kipindi cha Sheria, yeye sio mtu wa aina hiyo, akapeleka Smile FM, pale nikakutana na Michael Jackson akiuliza ‘Will U B there?’ nikaacha hapo na kuja kujiegesha tena kitandani.

Wimbo uliofuatia ulikuwa ni My love’ wa Westlife, kabla hajaingia George Michael na ‘Careless whisper’. Hapo nikakumbuka sebene la usiku uliopita, nikanyanyuka na kuizima kabisa redio na kuchukua Novel ili kuimalizia siku ile ilioanza vizuri na kubailika.

TRUE LOVE, novel moja nzuri iliotungwa na mtunzi chipukizi aitwae Mzaham RM, kwa miaka kadhaa, ndio niipendayo sana kwa sasa na huwa hainichoshi hasa ninapokuwa na majanga yangu, yenyewe hunipunguzia.

Nilifungua ukurasa wa kwanza na kuanza kusoma, kama vile ilikuwa ikisubiri, akili ikaanza kuvuta kumbukumbu ya Salama, mawazo kibao yakanijaa kichwani. Ni mambo mengi nimefanya mazuri na mabaya, mazuri nilijipongeza, na hata mabaya niliyofanya sikuona kama ni mabaya, nilijiona nipo sahihi tu.

Leo baada ya safari ya Salama, ndio naona ubaya niliomtendea binti wa watu na kuanza kujutia uovu wangu. ‘Ama kwa kweli nimekuwa mkosaji sana tena kwa muda mrefu, nikaanza kujiuliza.. kwanini nilipotaka kusafiri sikumuaga nimpendae? Oh huenda sikujua kama nampenda labda niseme kwanini sikumuaga anipendae?

Ama kwa sababu nilijua kuwa ananipenda sana? Naam, hiyo ndio sababu, kwani mie sikumpenda kwa dhati bali nilimtamani, sasa kwanini nilimdanganya?’ Maswali yangu yote yalikosa majibu maana aliepaswa kuyajibu ni mimi ambae ndio najiuliza.

Nikafunga kitabu kile pia na kuhamia kwenye sofa na kuwasha TV, nikaiona sura kama ya Salama, nikajiuliza ndani ya nafsi, sasa kama hali hii ikiwa kwa wiki mbili tu, mi si nitakuwa chizi? Eh! Ama kweli sasa naamini mapenzi yapo na sasa ndio nahisi kumpenda kwa dhati Salama, lakini hayupo.. kumbe kuachwa kunaumiza kiasi hiki?

‘Tena yeye ameniaga na usiku mzima nilikuwa nae na hadi sasa tuna mawasiliano nae, je mie ambae sikuwahi kumuaga? Nilikuwa nakurupuka tu nakuondoka, tena bila hata kumpigia simu nilipokuwa mbali nae, hivi alijisikiaje?’

Nilizidi kujenga maswali kichwani na wakati huohuo sikuwa na hata mtu mmoja wa kuweza kunijibu. Masikini Mwinyi mimi.. sikuwa mkweli hata chembe, hebu tazama ninavyoumia mimi leo, tena kila baada ya muda Fulani ananipigia simu na kunijulisha alipofika.

Kipindi kila niliposafiri sikuwahi kuwaza hata kumtumia sms achana na suala la kumpigia, nilikuwa namchunia tu, kibaya zaidi hata alipopiga yeye nilikuwa na hiari ya kupokea ama kuacha, sikuwa na moyo wa mapenzi hata chembe, najiuliza leo ni maumivu kiasi gani alipata? Leo najutia kitendo changu na ninaomba anisamehe

Naamini atakapo rudi nitakuwa na muda mzuri zaidi wa kumuomba msamaha ana kwa ana na kumwambia kuwa sasa nampenda kutoka ndani kabisa ya moyo. Mawazo yangu yalikwenda mbali zaidi na kuvuta kumbukumbu ni jinsi gani nilimpata Salama miaka kadhaa iliopita... ni kama hadithi ya kuvutia, lakini inasisimuda na kusikitisha pia.

Kwenye kituo cha daladala kiitwacho Nata jijini Mwanza, saa

12 asubuhi, watu ni wengi wakisubiri usafiri kwa ajili ya kuelekea kwenye mipango na kazi zao, Mwinyi nae alikuwa ni mmoja kati ya watu wale wengi pale kituoni.

Mwinyi kijana mtanashati mwenye umri wa miaka kati ya 30, ni mzaliwa wa Mkoa wa Dodoma, hivyo ni mgeni jijini Mwanza alikwenda jijini Mwanza kufanya kazi kwenye kampuni ya ujenzi iitwayo RUBANA CONSTRUCTION iliokuwa na kazi ya kurekebisha mitaro ya jiji la Mwanza.

Muda huu alikuwa pale Nata akisubiri daladala itakayomfikisha ofisini kwake maeneo ya Mabatini. Akiwa hana hili wala lile, akamuona binti mmoja na kumpenda ghafla, maana mara ile moja tu aliyomuona ilitosha kabisa kumfanya ajue kuwa ameuteka moyo wake.

Akiwa bado anashangaa, ilifika daladala na kugombewa na watu kadhaa, hatimae waliofanikiwa kuingia, waliondoka, kati ya wale waliopata nafasi ya kuondoka, basi na Yule binti alifanikiwa kuondoka, Mwinyi yeye alikosa nafasi ya kuondoka hivyo alibaki.

Aliitazama ile Hiace ikipotelea mbele nae akiwa hana la kufanya,

hakuchukua muda mrefu nae akapata usafiri uliomfikisha ofisini kwake. Alipowasili alianza kuwajibika kwa majukumu yake ya kila siku kama yalivyopangwa, ajabu siku ile alikuwa anaona kazi hazifanyiki kabisa.

Akitaka kufanya kitu hiki, anamkumbuka mrembo Yule aliekutana nae kituoni, na akishika kile na hiki, inamuijia sura ya Yule kimwana aliempenda asiemjua hata jina.

Kifupi hata utendaji wa kazi haukuwa mzuri, sema tu kwa kuwa kwenye kitengo chake yeye ndio boss, na inasemekana ‘Always boss is right’ yaani aima mkuu’ yupo sahihi.

Hivyo hata alipokosea alionekana yupo sawa tu. Akaanza utaratibu wa kujidamka mapema ili amuone Yule binti hali ikaenelea hivyo kwa takriban siku tatu, kila siku akiamka anakwenda kazini, basi hukaa sana kituoni ili kusubiri huenda akamuona mtu amsumbuae. Ndani ya siku hizo zotee hakufanikiwa kumuona hata mara moja, akaelekea kukata tamaa na kusubiri muujiza kama utatokea, japo hakuwa na imani ya kutegemea muujiza.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Siku moja Mwinyi akiwa na wenzie wanapiga soga ofisini kwake, akaanza kuwachekesha wenzie kwa kuwaambia alivyokutana na mtu na kumpenda akiwa hamjui na hajamuona tena tangu siku ile. Walimcheka sana na kumtaka aachane na ndoto za mchana, hao ndio walizidi kumkatisha tamaa

Siku isiyoliwa kitu, maeneo ya Mabatini mbele ya garage maarufu iitwayo MWACOTRA, Mwinyi akiwa na rafiki yake aitwae Sammer, wakasimamisha daladala iliokuwa ikielekea Igoma, wao walikuwa wakielekea Buzuruga Stand, alietangulia kuingia garini alikuwa ni Mwinyi akifuatiwa na Sammer.

Hamadi... Mwinyi aliekuwa amekata tamaa ya kumuona tena Yule msichana kwa kutegemea labda muujiza utokee, sasa ndio muujiza ulimtokea siku hiyo, maana bila hata kutegemea akamuona binti Yule akiwa amekaa na msichana mdogo, ambae alionekana kama ni msaidizi.

Mwinyi alitangulia na kukaa nyuma yao na Sammer akaja na kuketi pembeni yake. Mwinyi akatoa simu na kuandika SMS na kumpatia Sammer, aliisoma ilikuwa imeandikwa

‘Yule msichana wa ukweli niliekwambia, ni huyu hapa mbele yangu, mfanyie tathmini uniambie.’

Sammer akanyanyua kichwa na kujidai akiangalia upande ilipo kituo cha mabasi cha Buzuruga, mahala ambapo walipaswa wao kuteremka, kisha akampelekea macho yake moja kwa moja Yule binti na kumuona vizuri sana, hata nae akamkubali kwa kutikisa kichwa na dole gumba.





Akampa simu Mwinyi, alipoitazama akakuta kuna ujumbe umeandikwa na Sammer ukisema

‘Tusishuke peke yetu, tunapaswa kushuka nae ili tujue anapokaa,’ akatabasamu na kumtazama Sammer na kugonga tano.

Muda si mrefu wakawa wamefika Nyakato SD Yule mtoto msaidizi akateremka, mrembo akamsisitiza kuwa asichelew na asisahau kitu, yeye anatangulia. Hapa Sammer akamnong’oneza Mwinyi kuwa binti Yule haishi mbali na pale walipofika.

Pale aliponyanyuka Yule mtoto akakaa jamaa na kumsalimu mrembo, haikuchukua hata dakika moja, jamaa akaanza kuchombeza kwa sauti ya chinichini, binti alionekana ni mstaarabu sana, maana alimjibu kuwa yeye ni mchumba wa mtu, hivyo hapaswi kuwa na mchepuko.

Akamuomba konda ateremke palepale Nyakato National na ile njemba ikaendelea kutongoza tu bila wasiwasi wowote. Binti akateremka, na cha kushangaza, ile jamaa nayo ikateremka pale pia, Mwinyi na Sammer nao hapo kikawa kituo.

Wakiwa wamewapa umbali wa kama mita 10 hivi hawakuweza kusikia kinachozungumzwa bali waliweza kuhisi kuwa kinamkera Yule binti. Walipokaribia shule ya Bismack , binti Yule akaingia nyumba Fulani na inavyoonyesha alimwambia jamaa amsubiri.

Sammer na Mwinyi wakapitiliza na kwenda kusimama mbelel ya ile nyumba aliyoingia Yule binti kwa takriban mita 50, ikakatika robo saa nzima bila yule mrembo kutoka, jamaa akaenda kugonga nyumba ile.

Akatoka msichana mwingine na kuzungumza na jamaa kidogo, jamaa alionekana akibisha, Yule msichana akamulekeza mwisho wa nyumba ile. Jamaa akaendelea kama kupinga hivi, msichana akashuka kibarazani na kuongozana na jamaa hadi nyuma ya nyumba ile.

Dakika mbili mbele, wakaonekana wakirejea huku Yule msichana akicheka, jamaa alikuwa akitabasamu kwa huzuni huku akitikisa kichwa, Mwinyi akasema

“Sammer tumeuzwa best wangu,” huku akimshika mkono Sammer.

Nao wakaelekea kule walipotoka wenzao wakakuta kuna geti dogo, wakajiongza kuwa binti Yule itakuwa aliamua kumpoteza Yule jamaa kwa kuingia ndani ya nyumba hii kwa kupitia mlango wa mbele na kutokea ule wa nyuma, hivyo wakajuwa binti Yule ni mwenyeji wa eneo lile.

Sasa hata nao wakakosa pozi, wakakosa hoja ya msingi bali wakabaki na maswali, wafanyeje? Sammer akishauri waende kumuuliza Yule binti alitoka ndani, swali likaja, watamuuliziaje nao hata jina tu hawamjui? Mwinyi akasema

“Naenda kuulizia Yule msichana alietokea mlango wa nyuma anaishi wapi?” Sammer akacheka na kumwambia Mwinyi ile sio njia sahihi

“Turudi nyumbani tukajipange upya, kwa sababu tumepata pa kuanzia, basi tusikurupuke, tujipange tu sawasawa,” kwa shingo upande Mwinyi akageuka na kurejea kituoni kuendelea na kilichowapeleka kule.

Ikakatika wiki mzima bila kumuona tena binti Yule, ikafika siku Mwinyi akamua leo ndio leo, asie na mwana abebe moli, bila kumshirikisha yoyote, akaandaa mavazi, akaandaa pocket moja ya rangi ya kijani ilioiva sana na shati jeupe lenye rangi ya kijani na nyekundu ya kupauka, likiwa ni la mikono mirefu.

Chini alivaa viatu vya kazi viitwavo Safety boot ambazo huwa na chuma kwa mbele, usoni akaweka mawani kubwa ya jua, kisha kichwani akapaka mafuta aina ya kuza chafu yaliyosababisha nywele zake ziweke mawimbi, huwezi kukosa taswira, ni lazima uhisi alipendeza sana.

Na hivyo nivyo ilivyokuwa, nawe kama una hisia za aina hiyo, basi kwa yakini upo sahihi, hata nae alipojitazama kwenye kioo, aliridhika. Akatoka mtaa wa uhuru anapoishi na kuelekea Super market na kununua diary milk na bahasha size ya kati.

Japo ofisi yao ina magari ya kutosha, hakuwa ana penda kuyatumia, yeye alipenda zaidi kutumia usafiri wa jumuia, ila leo akaenda kituo cha Taxi na kuchukua moja iliompeleka hadi kwenye nyumba ile aliyoingia binti Yule siku kadhaa zilizopita. Alilipa pesa kwa dereva

wa Taxi na kushuka kuelekea mlangoni na kugonga hodi.

Alikaribishwa vema na hasa ukizingatia alivyovaa, alionekana ni mtu mwenye heshima kubwa, ukiongeza na kule kujiamini kwake, kukazidi kumpa pointi muhimu. Mwinyi hakukaa wala hata kuingia ndani. Baada tu ya salamu, tena bahati mzuri alietoka kufungua mlango, ni yuleyule msichana aliemuona siku ile iliopita.

Akaanza kumuhoji, kwa kuwa hakuwa akimtambua kwa jina, akataja jina la uongo. Kufanya vile lilikuwa ni lengo la kumpa wakati mgumu Yule msichana, maana alimtajia jina la Shahista, akasema wala hamjui na jina hilo hajawahi kulisikia kabisa eneo lile, akaomba amtajie vile alivyo, Mwinyi akampa maelekezo jinsi alivyo, binti akasema kwa shauku

“Aaah! Pia ana nywele ndefu si ndio?” Mwinyi akaitika kwa pupa kukubali.

“Aaaah, sasa Yule anaitwa Salama na hakai humu, bali anaishi nyuma ya nyumba hii, ila kwa muda huu sidhani kama atakuwa amerudi kazini, labda ukamuangalie.”

Mwinyi akamshukuru binti Yule kwa kumuwezesha kupiga hatua mbili mbele, hatua ya kwanza ni kumjua jina lake na hatua nyingine ni kupafahamu anapokaa. Kabla ya kumuaga akamuuliza jina lake, binti akajitambulisha jina lake ni Joyce ila wengi humuita Joy, Mwinyi akatoa pesa kiasi na kumpa Joy.

Akaelekea kule alipoelekezwa na Joy, akagonga kwa muda kidogo, na hatimae mlango ukafunguliwa na Yule binti aliekuwa na Salama ndani ya daladala. Alikaribishwa ndani kama awali, nae kama kawaida yake, alikataa isipokuwa alimuulizia Salama, akajibiwa kuwa bado hajarejea kutoka kazini, jibu ambalo aliambiwa mapema na Joy, hivyo alilitegemea.

Ilikuwa ni kama saa moja kasoro, Mwinyi alipotaka kujua Salama hurejea muda gani, akaambiwa kuanzia saa moja na nusu hadi saa mbili huwa amerejea. Mwinyi akasema

“Nipo hapa nje namsubiria hadi atakaporudi,” binti akamwambia ni heri aingie ndani, mwinyi akakataa, bado binti akamuomba basi aende na kisha arudi baadae, Mwinyi akashikilia kuwa yeye hatoondoka pale hadi atakapoonana na Salama na hatoingia ndani bali atakaa palepale bustanini.

Saa moja na nusu juu ya alama, Salama aliteremka kwenye gari iliomleta alielekea kwenye mlango wa nyumba yake na kuufungua. Kabla hajaingia nani, Mwinyi akamsogelea na kumsalimu. Salama aligeuka na kuitikia salamu akiwa amepatwa na mshangao.

Naam, hata ungekuwa wewe, ungeshangaa, maana hakuwa ameona mtu hapo kabla, akajitutumua na kumuuliza Mwinyi

“Nikusaiie nini?” Mwinyi alitabasamu na kupiga hatua kumsogelea bila ya kumjibu, kisha akamuomba Salama amkaribishe ndani kwani ana maongezi nae mafupi na isingefaa waongelee nje tena wakiwa wamesimama

Salama akatazama saa na kuangalia barabarani kisha akausukuma mlango na kumwambia Mwinyi karibu. Wakaingia nani na Mwinyi akakaribishwa kwenye sofa la mtu mmoja Salama akamtaka rahi na kwenda kubaili mavazi, alireje abaada ya muda akiwa ni mwenye shauku ya kutaka kujua huyu mtu ni nani na anataka nini? Akaketi na kumuagiza chai msaidizi.

Mazungumzo yalianza kwa Mwinyi kujitambulisha, kisha akameza mate na kamwambia jinsi alivyomjua baada ya kumuona kwa mara ya kwanza, hadi tukio la yeye kutokea mlango wa nyuma na kuwaacha wakiwa wameshangaa

“Salama ujue siku ile hukumuacha mtu mmoja, ulituacha wengi tu,” kauli ile ikamfanya Salama acheke na hicho ndio kitu Mwinyi alichokuwa akikitaka zaidi.

“Toka kwako Salama nina ombi moja tu ninachoomba ni urafiki tu, ninatamani uwe ni rafiki yangu,” Mwinyi akamaliza na kumuachia sekunde kadhaa Salama azitumie kwa kufikiria kidogo maneno yake huku nae akinywa chai yake iliokuwa ikizidi kupoa.

Salama kwa kujiamini huku akinyanyua kikombe chake, akasema

“Kuna urafiki wa aina nyingi sana, sasa sijui ni aina gani ya urafiki uitakayo kwangu?”

“Sitajali ni aina ipi ya urafiki, ili mrai uwe ni ule unaoamini wewe kuwa utanifaa mimi,” Salama akabinua midomo yake na kukataa kwa kichwa huku akisema

“Unajua mimi nina boyfriend na ndio ninaishi nae hapa, huwa hapendi kabisa kuniona nikiongea na mvulana ama mwanaume yoyote, hivyo naomba niwe mkweli kwako, siwezi kuwa rafiki yako abadan, nisamehe bure,” aliongea Salama huku akitengeneza nywele zake, Mwinyi akamjibu

“Salama hilo mimi ninalitambua, wewe ni mrembo wa ukweli, huwezi kuwa huna mpenzi, ningeshangaa... mi sitaki wewe uwe mpenzi wangu, bali mi nataka uwe ni rafiki yangu tu,”

“Hilo haliwezekani na ninakuomba uende maana muda wa jamaa kurejea umefika,” Salama aliongea huku akijitengeneza kwenye lile sofa la watu wawili kisha akaendelea

“Kwanza siamini kuwa kuna urafiki kati ya Mwanamke na Mwanaume ambao sio wapenzi,”

“Upo Salama, nipe nafasi nitakuonesha…” akamkatisha na kubadilika, akawa mkali na kusema

“Sitaki na ninaomba utoke, muda wa mume wangu kuja umefika,”

Salama alisema maneno hayo huku akitazama saa ya ukutani.



Mwinyi alijua haya ni mapozi tu ya kike, hakuna lolote, akiwa bado hajaamua kuondoka ama kuendelea kuongea na Salama, ikasikika sauti ya gari kwa nje ikipaki, Salama akafungua mlango na kuchungulia nje

“Mama yangu, Victor huyo kafika,”

Mabadiliko ya ghafla ya Salama, yakamfanya Mwinyi aamini kuwa Salama ana mpenzi kweli, na kama si kumuogopa, basi anampenda kweli, maana kwa muda mchache alizunguka hapa na pale, ila akatulia na kumzuia Mwinyi asiongee chochote kwa kuweka kidole mdomoni na kwenda kufungua mlango ambao ulikuwa umegongwa muda ule.

Victor aliingia ndani na kupokelewa kwa mapenzi makubwa na Salama, pia akipozwa kwa kufunguliwa tai na kuulizwa habari za kazi, kisha akajiwahi kwa kusema

“Victor mpenzi wangu, tumpata mgeni, anaitwa Mwinyi, amependa kuwa ni rafiki yangu,” Victor akamuangalia Mwinyi kwa jicho la mshangao, na kabla hajazungumza lolote, Salama akaendelea

“Mwinyi huyu ndio mchumba wangu niliekuambia, anaitwa Victor,” Mwinyi akasimama kwa kujiamini na kumpa mkono Victor kisha akasema

“Nimefurahi kukufahamu bro...” Victor hakujibu bali alitikisa kichwa kwa dharau.

Mwinyi aliliona hilo, muda uleule akamchukia Victor kwa majivuno yake, Salama akamlalia begani Victor wakiwa wamesimama vilevile anamchezea tai aliyoilegeza, kisha akasema huku akimuonyesha mlango;http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Mwinyi, sasa waweza kwenda, nashukuru kwa uwepo wapo,”

Bila kujiamini kama ayaonayo ni ndoto ama ni kweli, alianza kutoka huku akigeuka nyuma kila hatua hadi nje na kutokomea pasina kutoa zawadi yake wala kuaga kwa furaha, basi hivi nivyo walivyokutana Mwinyi na Salama…

**********



Ulikuwa ni usiku mgumu sana kwa Mwinyi baada ya kutoka kwa Salama, alitokea kumchukia kabisa Victor kutokana na dharau zake, hivyo kutokana na kukosa usingizi usiku ule, akaamua nae muda ule autumie kujipanga jinsi ya kuisambaratisha ile ndoa yao. Hii aliona ndio njia pekee ya yeye kupata faraja.

Asubuhi baada ya kuwasili ofisini kwake, alimpa mkanda mzima Sammer, Sammer akamshauri kama vipi ampotezee, Mwinyi hakuwa tayari kwa hilo hadi wanaachana bila kufikia muafaka. Kama alivyojipanga, jioni ya siku hiyo akiwa na uhakika kuwa Salama yupo kazini, yeye akaenda kwa Joy na kukaribishwa ndani. Leo alikubali kuingia.

Waliongea kidogo kisha Mwinyi akaanza kumuhoji Joy juu ya tabia ya Salama. Joy hakuficha, alikuwa mkweli, akamueleza ni jinsi gani Victor na Salama wanapendana. Hapo ndio Mwinyi alipokuwa akipataka. Shida yake ilikuwa ni kujua wanapendanaje na udhaifu wao upo wapi.

Sasa ili kujua zaidi, akaamua kuutumia muda huo kumsifia sana Salama kwa Joy bila kuonesha ishara ya kumtaka kimapenzi.

“Kama kuna wanawake walioumbwa ili kuolewa, basi shosti wako ni mmoja wao na yawezekana akawa anaongoza,” aliongea Mwinyi taratibu.

Tabasamu usoni kwa Joy lilikuwa wazi, Mwinyi akamtaka afikishe salamu kwa Salama kuwa yeye anapenda kumuona anavyotembea, kiuno chake chembamba na kifupi mwili mzima na jinsi alivyoumbwa

na hukupa taabu sana tukikutana.

Mwinyi akaongeza na sifa za uongo kama vile kuringa japo Salama haringi.

“Napenda na ninatamani kuwa nae kama rafiki, lakini naogopa sana, huenda akawa anaringa,” Joy akakataa kabisa na kusema Salama haringi, bali salamu zitamfikia. Hakukaa sana saa 1 jioni kabla ya muda wa Salama kurejeea, yeye akamuaga Joy.

Lakini kabla hajatoka, akamkabihi zawadi ndogo aliyokuwa amemletea Joy na kuondoka akimuacha Joy mwenyee furaha tele. Joy alikuwa akiona saa 1 na nusu inachelewa, muda ambao Salama hurejea, nia aende akampashe kilichojiri.

Baada ya siku mbili kupita, Mwinyi akaenda tena kwa Joy, waliongea tu kama marafiki tu wa miaka kadhaa. Mwishoni Mwinyi akamuuliza Joy kama alimfikishia ujumbe wake, jibu likawa ni ndio, ila Joy hakuendelea zaidi kitu kilichomuweka Mwinyi njia panda.

Akaaga na kutoka, mlangoni kwa Joy, ana kwa ana Mwinyi na Salama walisalimiana tu, Mwinyi akionyesha dalili ya kuwa na haraka na upande wa Salama ukionyesha alikuwa akitaka kuongea zaidi. Mwinyi alisimama na kuongea nae maneno machache, tena yale yenye kuonesha kuwa yeye anamuona kama mtu anaeringa sana.

Salama masikini ya Mungu akawa akilipinga hilo kwa nguvu zake zotee bila kujua kuwa anategwa. Maana alikuwa anatoa nafasi kwa Mwinyi kumsoma vizuri kwani anakuwa amjishusha yeye mweenyewe na hapo anakuwa tayari kumsikiliza Mwinyi kwa Makini kwa kuhofu kuonekana anaringa, hivyo hatokuwa na nafasi ya kuonyesha maringo

yake tena.

Mwinyi alitumia nafasi ile kuomba namba ya simu, Joy akichungulia dirishani, aliweza kuona kila kitu na kutabasamu, Mwinyi hakutoa namba kwa Salama, kisha wakaagana na kila mmoja akashika hamsini zake.

Alimpotezea kwa siku tatu bila simu wala sms, siku ya 4 saa mbili kasoro usiku ndio akampigia simu Salama na kumjulia hali, waliongea kwa takriban dakika 10 hivi, wakapanga mwisho wa wiki waliyonayo wakutane MS HOTELS iliyopo kona ya Bwiru kwa maongezi zaidi

Furaha aliyokuwa nayo Mwinyi ilizidi ile ya kupata kazi, alimpigia

simu Joy kumshukuru kwa msaada mkubwa aliompatia tangu awali na kumuomba amueleze ni zawadi gani ampelekee ambayo itamfurahisha sana, Joy alishukuru tu na kusema zawadi aipendayo na itakayo mfurahisha zaidi ni uaminifu tu kwa Salama, Mwinyi akaahidi kufanya hivyo.

Baadae akampigia simu Sammer na kumueleeza alipofikia, hakuweza kuamini kama ni kweli, ila kwa sababu anaesema ndio alietenda,basi ikamlazimu tu akubali na kumtaka asifanye kosa pindi akiwa nae, Mwinyi akamkumbusha kwa kumwambia

“Nafikiri unanitambua...”

Iliwadia siku ya miadi, saa 9 kamili juu ya alama, Mwinyi tayari alikuwa amefika sehemu husika, hii ilikuwa ni saa moja zaidi kabla ya muda waliokubaliana. Kwa kuwa alikuwa yupo ghorofa ya pili, aliweza kuona mambo mengi yaliyokuwa yakiendelea eneo lile la hoteli na hata kwenye jiji la Mwanza.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Lakini hakuweza kumuona Salama wakati akiingia na hata angemuona asingeweza kumtambua kwa jinsi alivyovaa. Alikuja amevaa aina Fulani ya gauni lenye rangi nyingi nyingi na kichwani kwenye nywele alifunga kitambaa cha rangi ileile kama gauni lake na kubana vizuri kwa kibanio style ya Ribbon chenye rangi hiyohiyo.

Pia kipande cha kitambaa cha gauni hiyohiyo alikitumia Kama mkanda wa gauni lile na vilevile akatumia kipande cha kitambaa kile kama pambo kwa kufunga kwenye sehemu ya pembeni ya mkoba wake.

Hakuishia hapo kwenye mkono wake wa kushoto alikitumia kitambaa kile kama bangili na hapohapo kwenye mkono wa kulia alikishika kipande kingine na kukitumia kama kitambaa cha mkononi zaidi ya yote, alikitupia kingine shingoni, mara ajifunge kichwani, mara atandike kwenye kiti, ama atupie begani, yaani ni yeye tu, kifupi alipendeza sana

Mwinyi alimpokea kwa pongezi na kumkumbatia, kisha akamvutia kiti na kuketi, walikuwa ni wenye furaha tele na hawakuzungumzia mapenzi hata chembe. Maana Mwinyi hakuonyesha dalili yoyote ya kumtaka kimapenzi japo ndio lilikuwa lengo lake. Walizungumzia

zaidi maisha na matukio yake na mfano wa vitu hivyo.

Mwinyi alipotaka kujua kuhusu wazazi wa Salama, akagubikwa na simanzi, hali iliyohatarisha mazungumzo yao, Salama alisikitika kwani wazazi wake walitengana kabla yeye hajazaliwa na kibaya zaidi baba yake alifariki wakati yeye akiwa bado ni mdogo mno asiejitambua.

“Pole sana Salama, hatuwezi kubadili ukweli, mipango ya Mola lazima itimie,” alimtuliza na kumrejesha katika mazungumzo ya kawaida

Japo alikuwa akinywa maji, Mwinyi alimuuliza ni kinywaji gani anachokipendelea. Akamjibu kuwa yeye huvutiwa zaidi na Bavaria, alimuulizia kuhusu kazi na elimu yake. Salama alimwambia elimu yake ni kidato cha nne ila ana mpango wa kujieneleza hapo baadae atakapopata nafasi nzuri.

“Na kuhusu kaazi uliyonayo Salama… unaionaje kazi yako?”

“Mmh, kuhusu kazi… Kazi ninayo na ninarihika nayo, hasa ukizingatia inanipatia mahitaji yangu yote muhimu na nianifurahia kwa sababu ninai penda,” Basi Mwinyi akazii kumpa moyo na kumtaka ajitume zaidi, kwani siku moja mbele, anaweza kumiliki ofisi kama atakuwa makini.

Salama alitabasamu na kumshukuru Mwinyi kwa dua yake na kumtia moyo, akaongezea

“Mwinyi inaonekana unajali sana, Mungu akubariki,”

“Nashukuru Salama, nawe pia unaonekana hivyo japo mwanzo niliamini wewe unaringa sana,”

wakacheka na kunyanyuka.

Hawakuchukua tena muda zaidi, wakaondoka ikiwa ni saa mbili usiku, Mwinyi akitumia gari ya ofisini akamrejesha Salama hadi kwa Joy na kumuacha pale, yeye akatembea hadi kwa Sammer kumuachia gari.







Ukaribu wao sasa ulizidi, ikawa kila Jumamosi wanakuwa pamoja, ila bado hawajawa wapenzi. Huutumia muda wao kwa kufanya mengi ya kimapenzi, wakienda beach na kila sehemu za starehe, simu nayo kwao ilikuwa ina mipaka, ilikuwa ni kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 2

usiku waliwasiliana kwa mapana na marefu.

Muda mwingine wote uliosalia hawakuwa na uhuru, hilo lilimchoma Mwinyi na hakuwa tena tayari kwa hilo. Siku moja akampigia simu Salama ikiwa ni saa 4 usiku. Muda huo Salama alikuwa amemaliza kula na alikuwa akitoa vyombo kupeleka jikoni wakiwa wanasaidiana na Victor.

Salama alishindwa kupokea simu ya Mwinyi, aliitambua japo haikutoa jina. Victor akamshitua mpenzi wake kwa kumuuliza mbona hapokei simu? Salama akajitetea kuwa mtu Yule ana mbeep wala hapigi, Victor akamwambia apokee, hawezi mtu kubeep kwa muda wote ule.

Ikamlazimu apokee, ila sasa alivyopokea tu akamkana Mwinyi kuwa hamjui na huenda amekosea namba. Kisha akamgeukia Victor baada ya kukata simu na kumwambia Victor kuwa aliepiga amekosea namba kisha akazima simu.

Siku ya pili ilikuwa ni siku ya alkhamis, Salama alipowasili kazini kwake, jambo la kwanza lilikuwa ni kupiga simu kwa Mwinyi, alijua kabisa kitendo chake cha jana usiku kitakuwa kilimuumiza sana, akachukua simu ya mezani na kumpigia.

Namba zilizojitokeza kwenye namba zake zilikuwa ni ngeni, akapokea, mtu wa upande wa pili alipoongea tu hakuhitaji kujitambulisha, Mwinyi akamtambua moja kwa moja, kwa jazba akamtaka aseme shida yake, Salama akawa mpole na kumtaka radhi Mwinyi kwa kitendo chake cha usiku uliopita.

“Kwani we umempigia simu nani? Unamjua unae ongea nae?”

“Akh! Mwinyi umekuwaje?” aliuliza Salama kwa mshangao

“Kumbe unanijua eeeh? Sasa mbona jana ulinikana? Na huo msamaha unaniomba wa nini?”

Salama alijitahii kuomba msamaha huku akilia, maana anajua kabisa na tena si siri kuwa Victor anampenda sana lakini Mwinyi nae anajua kupenda na kujali kwa kiasi kikubwa, hivyo hakupenda kumpoteza kabisa, alitamani wote wawili awe nao.

Huruma ikamuingia Mwinyi na kumwambia amemsamehe ila asirudie tena kitendo kama kile. Na kutumia muda ule kumtaarifu kuwa kesho wakutane kule beach ya kichina maeneo ya Capri point saa 8 mchana, ni muhimu.

Salama hakubisha japo ilikuwa ni muda wa kazi, lakini alijua atafanya nini ilimradi Mwinyi amemsamehe.

Ikawadia siku hiyo waliyopanga wakutane, Mwinyi bila kumtaarifu Salama, akachukua chumba palepale na kuweka zawadi alizomuandalia na baadhi ya vitu kadhaa ambavyo yeye alikuwa ameviandaa kisha akaenda kuketi ufukweni mwa ziwa kumsubiri Salama afike.

Haikuchukua muda akawa amefika. Walipokeana kwa shangwe na furaha kisha wakaketi na wakaanza kupata vinywaji ambavyo Mwinyi tayari alikuwa ameviandaa. Vilikuwa ni vingi pale mezani lakini Mwinyi alivinunua kupitia makadirio yao wao wawili, maana anajua kiasi watumiacho, watatumia na kuvimaliza.

Mazungumzo yalianza taratibu huku wakipigwa na upepo wa ziwa Victoria huku wakitazama mawimbi yaliyokuwa yakipiga ufukweni. Mazungumzo yalipamba moto na kila likiisha hili, linaingia hili, wakafikia hatua ya kuulizana wamevuka boda ngapi.

“Mi mwenzio nimevuka boarder zote kuzunguka nchi yetu, wewe je umevuka ngapi?” Mwinyi alimuuliza, Salama alicheka tu na kusema hajawahi kutoka nje ya nchi. Mwinyi akamuuliza kama amewahi kutembea humuhumu ndani ya nchi yetu adhwiim, ama kutembelea sehemu yoyote aliyoipenda.

“Mwinyi mi sijawahi kutoka nje ya jiji la Mwanza mwenzio zaidi ya kwenda Kigoma ambapo ni nyumbani kwao mama kiasili,” aliongea kwa aibu masikini.

“Sawa, sasa unatamani kwenda wapi kwa siku za usoni?”

“Mpango wangu kwa sasa ni kwenda kutembelea mapango ya Amboni na sehemu za kihistoria, si utanipeleka Mwinyi?”

“Akha, Amboni? Mi siendi...”

“Kwanini sasa?” Salama akauliza akiwa na umakini wa hali ya juu, kumbe mwenzie anatania.

“Naogopa magaidi,” Salama akasonya kwa tabasamu na kusema

“Wakati mi mwenzio nipo Serious we unatania, mi nitanuna,” akajidai kanuna, Mwinyi akamshika shavu na kumwambia

“Yap yap mchumba wala usijali, unapenda iwe lini safari yetu?” alisema kwa kujiamini sana Mwinyi na hali uwezo huo wala hakuwa nao.

“Ikiwa mwezi ujao itakuwa ni njema zaidi, ama unasemaje wangu?”

“Kauli yako ni sheria, inabaki utekelezaji tu, mie naanza maandalizi bosi wangu,” wakacheka na kuanza kutaniana.

Hapo ilikuwa ni saa 11 za jioni, mvua ilianza kunyesha na wao wakaamua kuhamia bandani na kuanza kutazama mandhari ya ziwa Victoria ikiwa inavutia kutokana na mandhari ya mvua. Mwinyi akamsogelea Salama aliekuwa amesimama karibu na miti ya banda lile na kumkumbatia kwa nyuma huku akimuonesha meli moja iliokuwa inakuja kwa mbali huku taa ikiwaka na mvua ndio imechachamaa.

Mandhari ilikuwa ni nzuri sana, Mwinyi akamtaka Salama wahame eneo lile, Salama hakuwa mbishi wala hata kuuliza wahamie wapi hakuuliza, yeye alikuwa ni TV na Mwinyi alikuwa ndio Remote, wakaelekea ndani pasina Salama kujua wanaelekea wapi na kufanya nini.

Aliona wamepanda hadi ghorofa ya kwanzana kisha Mwinyi akatoa funguo na kufungua mlango wa chumba kilichokuwepo mbele yao

“Karibu sana malkia wangu, chumba hiki ni maalum kwa ajili yako,” Salama akatabasamu na kuingia huku akisema

“Mh! Una visa sana Mfalme wangu, haya nimeingia,”

Mle nani palikuwa na vinywaji tofauti tofauti ila ni vile vile

wanavyotumia, pia Salama aliweza kuona zawadi kadhaa ambazo aliweza kuhisi ni kwa ajili yake na hata harufu ya mle ndani ilipendeza sana na ilileta ashki

Salama akaamuuliza Mwinyi ni wakati gani amepaandaa mle ndani, wakati akimuuliza vile yeye Salama alikuwa amesimama dirishani akitazama nje na Mwinyi alikuwa akimimina vinywaji kwenye glasi zao

“Mpenzi mie nimefika hapa zamani sana, karibu sana kwa kinywaji,” Salama hakuwa hata na habari, akili yake ilikuwa imezama nje kule alipoiona ile meli ikitia nanga kwa mbali kwani wakati huo mvua ilikua imepungua sana.

Salama pasina kugeuka akamuita Mwinyi pale dirishani

“Mpenzi njoo ulione jiji la Mwanza linavyo onekana kwa juu,

linapendeza sana hasa usiku kama huu, dah! Najivunia sana kuwa Mtanzania kwa kweli” akiwa ameshika glasi kila mkono, akaungana na Salama pale dirishani huku akisema,

“Unajivunia kuwa Mtanzania ama unavumilia kuwa Mtanzania?” hakujibiwa kwani ilionekana akili ya Salama ilikuwa mbali ya pale. Hivyo Victor nae akatazama nje kwa muda kidogo kisha akamgusa begani na glasi.

Alipogeuka kutazama ni kitu gani cha baridi kimemgusa, akakutana na glasi ya kinywaji, akashukuru na kuipokea, waligonga Cheer na kunywa wakitazamana machoni, roho zao zikafika mbali, hakuna alimuita mwenzie wala kumsemesha, bali walijikuta wakiwa karibu na wanaongea lugha ya mapenzi.

Hawakukumbuka tena ni kipi kilichoendelea hadi saa tatu usiku wakati Salama aliposhtuka toka kwenye kifua cha Mwinyi aliekuwa akimchezea masikio. Alikurupuka na kutaka kuondoka muda uleule, Mwinyi hakumkubalia, akamzuia kabisa kutoka, alimwambia siku ile wanatakiwa kuimaliza pamoja.

Pamoja na kujiteta kote lakini alishindwa kuondoka kutokana na mkwara wa Mwinyi, alimwambia achague moja, kukaa na pale hadi asubuhi ili aendelee kuwa mpenzi wake ama aondoke kurudi kwake na Mwinyi iwe ndio basi tena.

Ilikuwa ni mtihani mgumu sana kwa Salama, wote aliwapenda na tena aliwathamini, hakujua afanye nini. Alibaki hajielewi, ila kwa haraka kama aliekurupushwa, akanyanyuka na kuvaa nguo zake tena basi bila hata ya kuoga, akamtazama Mwinyi aliekuwa akimuangalia yeye.

Mwinyi akanyanyua mabega ishara ya kusema sijui lolote mie, hapohapo Salama kafunga viatu na kutokomea nje, Mwinyi hata hakuhangaika kunyanyuka, bali alichukua Remote na kuwasha TV, akajiweka vizuri kitandani

Hata ilimchukua muda basi? Mwinyi usingizi ukampitia ukizingatia alikuwa ameisha jichokea. Hakufunga mlango kwa kujua kuwa ni lazima atoke nje kabla hajalala, bahati njema ama sijui tuseme ni bahati mbaya, usingizi ukampitia, hakushtuka hadi baada ya saa moja kupita. Lakini akakuta pembeni yake kuna mtu amelala.





Alipomtazama vizuri akakuta ni Salama. Masikini kumbe alishindwa kwenda kutokana na mkwara wa Mwinyi,.

Baada ya kutoka mle ndani, Salama alishuka hadi kwenye ngazi na kukaa, akalia sana. Alihisi kabisa huko nyumbani kwake hakuwezi kuwa na amani iwapo atarejea usiku ule, na huku napo akiondoka tayari Victor ameisha mwambia kwamba hawatakuwa kwenye uhusiano tena.

Akaona kabisa asipokuwa makini basi anaweza kuwapoteza wote wawili kwa wakati mmoja, akaona ni bora arudi kwa Mwinyi.

Bahati njema mlango ulikuwa wazi, akaingia na kuvua nguo zake kisha akaungana tena na Mwinyi aliekuwa yupo katikati ya usingizi. Hivyo hivyo, wakati Mwinyi nae anashtuka kutoka usingizini, Salama nae alikuwa katikati ya ndoto.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Mwinyi akanyanyuka na kwenda mezani ilipo simu ya chumbani na kuagiza chakula cha watu wawili na kwenda kujimwagia maji kidogo aliporudi alikuta Salama nae kakaa kitandani. Akamsemesha huku akijifuta maji kwa taulo

“Hey baby... Mambo?” Salama hakujibu akajidai kanuna, Mwinyi akamsogelea na kumtania

“Mpenzi usikasirike, ina maana umechukia kwa mimi kukwambia nataka kulala nawe leo?”

“Aah Mwinyi mimi najua tu, we hupendi maisha yangu, sawa tu,”

“Sio hivyo mpenzi wangu yaani kulala nami kwa leo moja tu unasema sikupendi?”

“kwanini hukuniruhusu mimi nikalale tu nyumbani?”

“Si nilikuruhusu lakini Sweetheart?”

“Kimtego? Ule si ulikuwa mtego ule?” aliongea huku na mikono nayo ikitoa ishara ya kutounga mkono kabisa kauli ya Mwinyi

“Mi najua tu sababu, ni vile tu juzi mi nilikukosea basi, nawe umeamua kuniumiza makusudi, sawa bwana nitafanyaje nami ndio niliependa?” akajilaza akitazama juu darini,

“Sio hivyo mrembo wangu...” aliongea hivyo Mwinyi huku akimsogeza karibu yake

“Ndio hivyo, wewe ulitaka mi niondoke ili wewe useme mi sikupendi, kwa sababu juzi nilikukana kwenye simu na leo nimekuacha guest, lakini umefanya hayo kuiridhisha nafsi yako bila kujali kama mimi ni mchumba wa mtu nawe unalitambua hilo,”

Maneno hayo yalikuwa ni kuntu, na yalimgusa sana Mwinyi na kumfanya ajute kwani ni kweli tangu awali Salama alimueleza juu ya kuwa na mchumba na hata kumuona Mwinyi tayari aliisha muona.

Hapo Mwinyi alijiona ni mkosaji akamuomba msamaha na kufanikiwa, chakula kikaletwa, na kisha kikafuatia kitendo cha kulala, lakini walilala alfajiri kabisa, na kuamka alianza Mwinyi kuamka saa tatu asubuhi.

Akamuamsha Salama ili ajitayarishe kwenda kwake maana siku ile haikuwa ni siku ya kazi. Ajabu Salama akauliza aende wapi? Mwinyi akishangaa! Akahisi labda ni usingizi tu umembana, huenda amechoka sana, akamuacha aendelee tu kulala.

Baada ya saa moja walikuwa hotelini wakifungua kinywa, si Salama wala Mwinyi ambae muda huo simu yake ilikuwa hewani, wote walikuwa wamezima simu zao ili kukwepa usumbufu na kero za hapa na pale.

Walipomaliza kufungua kinywa wakarudi chumbani na kulala hadi saa 8 mchana walipoamshwa kwa ajili ya chakula cha mchana. Walikula na kupumzika wakicheza Video game mpaka saa 10 jioni wakateremka chini hadi ufukweni.

Waliimalizia jioni ya siku ile pale kabla ya kupanda juu tena kwenda kujibadili mavazi kwa ajili ya kwenda disco. Saa 4 usiku wakachukua Taxi iliowapeleka Villa Park, maeneo ya Kirumba kwenda kujirusha usiku kucha, walirejea hotelini alfajiri wakiwa hoi.

**********



Asubuhi ya Jumapili mara tu baada ya kufungua kinywa, Mwinyi akamshauri Salama arejee kwake mapema kabla Victor hajarejea toka kanisani. Salama alipinga hilo na kusema kwake atarudi Jumatatu jioni akirudi kutoka kazini.

Mwinyi alijaribu kumsihi, lakini Salama alishikilia palepale, ikafikia hatua Salama akampandishia.

“Kama umenichoka sema, nitaondoka sasa hivi, usinibabaishe” akaanza kunyanyuka kama kuondoka kwa hasira vile, ikalazimu Mwinyi awe mpole na kukubali atakacho Salama

“We fanya utakalo mpenzi wangu, lakini lengo langu ni kuilinda ndoa yako tarajiwa kwa Victor,” alimuweka wazi kwa lengo lake. Salama akakaa na kumbusu Mwinyi mdomoni, akisema

“Huko kwa Victor niachie mie. Tena basi niambie, leo wapi?”

“Kulekule kwa jana,” wakacheka

“Hahahaa! Unajidai fataki sio? Acha utani bwana, niambie leo tunaenda kujirusha sehemu gani?”

“Leoo... ah kwa kweli…” Salama akamkatisha

“Mwinyi kama tatizo ni fedha, leo ni zamu yangu, umenipa furaha ambayo sikuwahi kuipata wala hata kuhisi ipo siku nitaipata, hivyo inanilazimu kulipa fadhila, sema twende wapi?”

Ni ukweli usiopingika kuwa Salama alikuwa amepatia kabisa, kigugumizi cha Mwinyi kilitokana na ukata, hali iliisha kuwa mbaya mfukoni. Siku ile ya kwanza alikuwa na laki tatu, ambazo sasa zilibaki kama 12,000 tu, ambazo kichwani mwake tayari alikuwa ameisha zipangia matumizi.

Alipanga kuchukua Taxi hadi kwa Salama, ambayo itagharimu 5000, maana si mbali kutoka pale walipo kisha 5000 ampe Salama, nae abaki na 2000, Ambayo 1000 atatumia kama nauli toka kule kwa Salama kurudi kwake na ile buku itabaki kuwa ni ya kianzio.

Hivyo suala la kubaki pale hotelini ingekuwa ni aibu kama atagharamia yeye, hivyo akakubaliana nae kwa maamuzi aliyoyatoa.

Salama akataka waende kujichanganya sehemu ilio mbali kidogo na pale ili wapate mazingira tofauti na yale, lakini wawe na uhakika wa kurejea mapema ili wawahi makazini kwao siku ifuatayo ya kazi.

Mwinyi akaamuru waende Ukerewe, Salama alikuwa tayari kwa lolote, safari ikaanza, ilikuwa ni raha tu tangu wanaondoka hadi wanarudi siku ya Jumatatu asubuhi. Walipanda boti ya kwanza kutoka Ukerewe na kufika mapema sana Mwanza na kuwahi makazini kwao kuwajibika.

Mwinyi alikuwa na furaha na kila mmoja alijua kuwa Mwinyi ana furaha, hali upande wake ilikuwa ni shwari. Alimuhadithia Sammer jinsi alivyoitumia wiki end ile pamoja na Salama, Sammer alijua ni uzushi tu wa jamaa yake, hakumuamini kutokana na muonekano wa Salama tangu siku ya kwanza.

Baada ya mabishano ya hapa na pale, Mwinyi akatoa kadi ya Benki ya Salama ndio akaamini na kumwambia anafaidi, inatakiwa wale wote, kwani wahenga walisema ‘Chakula kizuri kula na ndugu yako’

Akacheka Mwinyi na kumwambia Sammer, huwezi kuuza mafuta uzuri kisha we unuke jasho, lazima utanukia harufu ya mafuta uuzayo

“We wala usikonde, utakula hadi utavimbewa,”

“Sawa bhana, mi nasubiria, lakini Fardos alipiga simu anakutafuta,”

“Achana nae Yule, wa ukweli hapa kwa sasa ni Salama, we kaendelee na yako kwanza, umeanza habari gani Sijui,”

“Poa,” akaondoka Sammer kuenelea na kazi zake akimuacha Mwinyi

nae akifanya yake.

Upande wa Salama hali haikuwa shwari, kila muda unavyozidi kwenda anazidi kumkumbuka Mwinyi na anashindwa kumpigia simu kwa sababu ameifunga kwa kumuhofia Victor, maana akiwasha tu simu, lazima Victor apige.

Na hivyo basi, kadri muda ulivyokuwa unalika, ndio ilimaanisha kwamba wakati wa Salama kukutana na Victor unasogea. Shaka inakuwa hapo, akimuwaza Mwinyi anapata faraja, akimkumbuka Victor, anapata hofu, amani ikatoweka na kubaki njia panda.

Saa moja na nusu kama kawaida, alirejea nyumbani ikiwa ni nusu saa

kabla ya Victor kurejea, kwanza alipita kwa Joy kupata fununu ni kipi kinachoendelea, alimkuta Joy amekaa ndani peke yake, alipomuona Joy alishtuka na kumuuliza hata kabla hajakaa alipokuwa.

Salama hakumficha, alimueleza kila kitu japo ni kwa kifupi lakini alielewa ni wapi alikuwa. Nae Joy akamueleza kuwa tangu juzi Victor amekuwa akimtafuta na hata leo asubuhi, amefika kazini kwake na hakumkuta pia, simu yake haipatikani na ile ya ofisini inapokelewa na mtu mwingine.

Alivyopata fununu zile akajua ni wapi pa kuanzia, akamshukuru Joy na kusema

“Ngoja nikamsubiri hukohuko, naona muda wa kurejea umekaribia,”

“Ha! Salama... ukamsubiri nani? Mbona Victor yupo?”

“Eeenh? Yupo nyumbani?” woga ukamuingia na ulionekana dhahiri.

“Ndio yupo, Leo hajatoka kwenda kazini zaidi ya kutoka na kwena kazini kwako tu akarudi,”

“Eh leo... najuuta kuzaliwa binti, sasa Joy...”

“Hata sielewi,”

“Ngoja nikapambane,” Salama akaondoka na kumuacha Joy amepigwa na butwaa.

Wakati alivyokuwa akiikaribia nyumba yao, alikuwa akijiuliza ni kipi ataongea hadi aeleweke? Nafsi ilikuwa ikiwaza…

‘Dah, nimefanya kosa kubwa sana, sijui nitajibu nini leo? Ah bwana liwalo na liwe, najua nitatukanwa na hata kupigwa kwa ajili ya Mwinyi na nipo tayari kwa hilo’.

Tayari akawa amefika nani, alimkuta Victor akitazama habari,

haikuwa kawaida yake kumtazama tu bila kumpokea ila leo nio kilichotokea, alimtazama kwa jicho la hasira pasina kumsemesha isipokuwa alishika Remote na kubadili channel

“Habari za saa hizi Victor?”

“Habari za saa hizi ama habari za wiki iliyopita? Ulikuwa wapi?” Sauti na sura ya Victor, havikuonyesha mapenzi hata kiogo, Salama nae hakuwa na la kujibu, ila tu kujitetea ni wajibu

“Samahani Victor, kwanza nakiri kosa, sikukuaga nilipata kisafari cha dharula…”

“Stop! Malaya mkubwa wee,” uvumilivu ukamshinda Victor, sasa

akasimama na kumtwanga makofi ya kutosha, Salama alilia sana hadi msaidizi wao akatoka mbio kumfuata Joy.





Joy na Mumewe walifika na kumkuta akiendeleza kipigo kitakatifu kwa Salama, baada ya kuwaamua kwa muda walifanikiwa kuwatuliza lakini Salama alikuwa hoi kwa kipondo kikali. Joy alikuwa amemuhadithia

mumewe tukio zima la Salama kabla hawajafika pale.

Katika kutaka kuweka mambo sawa, wakajidai hawajui lolote, wakaulizia chanzo cha ugomvi, Victor akawaambia,

“Muulizeni huyo Malaya alikuwa wapi tangu Ijumaa?”

“Eti shem ulikuwa wapi tangu Ijumaa?” Bwana wa Joy aliuliza na Salama kwa kuwa hakuwa na jibu aliendelea tu kulia, ila kwa ghafla kwa sauti ya hamaki akamuuliza Victor

“Victor unaniita mie Malaya? Unanipiga bila sababu kwa kuwa nakaa kwako eti? Usininyanyase, kama umenichoka niache niende kwetu,” Salama aliyasema hayo akiwa amekaa. Victor nae akamjibu kwa hasira

“Toka hata sasa unasubiri nini kenge wee! Ebo… kwanza unafikiri humu ndani utalala?” Joy na mumewe ikawabidi waingilie kati kuwatuliza.

Joy akamchukua Salama na kwenda nae uwani kumnawisha damu iliyokuwa ikimvuja mdomoni, jamaa na Victor wakapata wasaa wa kuongea

“Huyu mwanamke ni wa ajabu sana, kaondoka asubuhi ya Ijumaa akienda kazini na anarudi hapa Jumatatu katoka kazini, ina maana siku zote alikuwa anafanya kazi? Pumbavu sana huyu!”

“Ukitumia jazba hutajua alipo, tulia na kaa nae chini akueleze alipokuwa,”

“Kaka siku zote hizo hakunijulisha alipokuwa hakutaka, kibaya zaidi alizima na simu, sasa leo ataniambia nini ambacho unafikiri nitamuelewa?”

“Sawa, lakini kumpiga haikuwa ni muafaka, bado ulikuwa na uwezo wa kuongea nae,”

“Bro, unafikiri atanijibu nini huyu? Nyumbani kwao nimefika kumuulizia, kazini kwake nimekwenda kumtafuta na hata mitaani pia nilipita kumsaka, kote huko sikufanikiwa kumpata, sasa ananiambia

nini nimuelewe?”

Hapo tena, jamaa nae akatela, akawa mpole, akajitahidi tu kumuomba Victor walale hadi asubuhi na watayamaliza kwa usalama kukikucha. Victor aligoma na kutaka Salama aondoke, maana anaweza hata kumdhuru ikiwa ataenelea kuwepo pale.

Kwa ushawishi mkubwa toka kwa Joy akafanikiwa kumruhusu Salama alale pale hadi siku ifuatayo kisha hatua zingine zitafuatia. Joy na mumewe wakatoka na kuwaacha wakitazamana kama mafahari wawili

waliopigana na kuchoka.

**********



Upande wa Mwinyi kila kitu kilikuwa safi, muda huo alikuwa na Sammer wakitungua mizinga tu, hata hakujua kama mwenzie yupo mmagumu ila aliamini muda ule ni lazima Salama atakuwa amelala.

Jumanne asubuhi Mwinyi akiwa kazini alipigiwa simu na Salama, yeye aliipokea kwa furaha na makiss kibao, lakini sauti ya Salama haikuwa katika hali yake ya kawaida. Hata maongezi hayakuwa mengi, baada tu ya kuitikia zile kiss za Mwinyi, akaongea kama kumpa taarifa.

“Mwinyi jitahii tukutane TAI 5 Hotel saa 7 mchana, usiache na jitahidi kuuchunga muda,” Salama hakutoa hata nafasi ya kuulizwa chochote akakata simu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Saa 7 kamili adhuhuri, Mwinyi na Salama walikuwa meza moja. Huyu wa leo hakuwa Salama Yule aliekuwa nae jana, bali huyu wa leo alikuwa ni mpole na alionekana kama mgonjwa. Waliagizia chakula na Salama akautumia muda ule kumuhaithia yote yaliyojiri usiku uliopita wakati alipowasili kwake na kukutana na Victor.

Kumbe wakati Salama na Mwinyi wakipata Lunch kule hotelini, Victor alikuwa akimtafuta Salama kwenye simu ili ajue ni taratibu gani wanaitumia ili amrejeshe kwao. Hakumpata hewani, akapandisha jazba na kuamua kumfuata kulekule ofisini akipanga amdhalilishe ikiwa atamkuta pale.

Ofisi zao hazikuwa mbalimbali sana na pale alipokuwa yeye. Alifika na kumkuta bosi wa Salama ambae wanafahamiana, na hata kazi Salama aliipata kupitia memo toka kwa Victor kwena kwa Boss. Waliongea

kidogo na Victor akaeleza shida iliompeleka pale.

Alimwambia anataka kuonana na Salama, Boss akishangaa na kusema

“Aaah bwana Victor, kwani hujui kama shem ni mgonjwa?”

“No! natambua ndio maana nipo hapa kwa sababu niliachana nae asubuhi akiwa anakuja hapa, na ndio sababu imenifanya nije kujua maendeleo yake kwa kujua kuwa yupo hapa” Mwinyi aliongopa ili kuweka mambo sawa na kuikwepa aibu.

“Anhaa! Hapo sasa nimekuelewa, ni hivi kama nusu saa ilopita alikuja na kuomba ruhusa kuwa leo hajisikii vema, hivyo mi nikamruhusu akapumzike, maana kiuhalisia hata nami nilimuona hakuwa vizuri,”

“Nilimueleza kuwa abaki nyumbani yeye akalazimisha kuja, sasa nahisi

atakua kaelekea hospitali,” aliendelea kuongopa Victor ili kuzidi kujiweka pazuri

“Kwani wewe bado hujafika nyumbani muda huu?”

“Eeeh, ila sasa ndio naelekea huko,” wakaagana na Victor akatoka na kumuacha Boss akiendelea na kazi zake.

Ile hali ya Salama kupigwa ilimuuma sana Mwinyi akatamani hata kumfanyia mambo ya ajabu. Salama aliliona hilo, kifupi Salama alimpenda Mwinyi kichwa kichwa na ajabu hakutaka kuachana na Victor, hivyo akamzuia Mwinyi asifanye chochote.

Katika kumpoteza kabisa Mwinyi, Salama akamuomba waende faragha angalau kwa masaa matatu ampoze machungu ya maumivu ya kipigo cha Victor. Halikuwa gumu hilo kwa Victor, walichukua chumba palepale TAI 5 na kujimwaga hadi saa 12 jioni.

Victor aliporudi nyumbani hakumkuta Salama, akamuuliza msaidizi wao akajibu kuwa hajarudi, akaenda kwa Joy pia hakuwepo, akajiuliza mwenyewe ni wapi alipo, hakupata jawabu, simu yake pia haipatikani na kwa mama yake pia akajibiwa hajafika. Akatepeta na kujipweteka kwenye sofa pale Sitting room.

Kwa kutumia simu ya Mwinyi, Salama akampigia simu Joy na kumwambia yeye yupo TAI 5 na Mwinyi wanatumia pesa. Sio tu kushangaa kulikomtokea Joy, bali pia alisikitika na kusema

“Salama, pamoja na kipigo chote kile cha jana, leo tena unarudia yaleyale? Ama kweli huwezi kusema nyumba ni fupi kama hujaiona

ndefu... haya mumeo alikuja kukutafuta hapa kwangu,”

“He! Nani? Victor?” akajichanganya Salama kutokana na mshituko.

“Sasa kumbe mwingine nani?” aliuliza kwa kejeli huku akihisi ni kiasi

gani Salama amepata mshituko.

“Kwani yeye hajui kuwa huu ni wakati wa kazi? Na kwanini anitafute?”

“Kweli, huu ni wakati wa kazi, ni wakati wa kufanya ngono, unaaga kazini unaumwa, kumbe unaumwa mapenzi, yaani we mtoto, mi nahisi kukushindwa sasa... Jana ulikuwa unamchezea Victor, huogopi yeye kukukimbia, maana unajivunia uzuri ulionao, utampata bwana mwingine, leo unachezea kazi, mdogo wangu, watu huwa hawachezei vitu muhimu viwili kwa wakati mmoja, shauri lako,” alimaliza Joy.

Maneno hayo yalimuingia sana Salama, akawa mpole na kumuuliza Joy wafanyeje? Joy akamwambia ajibebe mwenyewe si ndio amelianzisha. Baada ya kumbembeleza sana Joy akakubali kumsaidia na kumuelekeza sehemu wakutane. Salama akashukuru na kukata simu, akambusu Mwinyi aliekuwa anasikiliza kwa umakini maongezi ya Joy na Salama.

Salama akatoka hotelini na kumuacha Mwinyi palepale. Akajiona mpweke, akampigia simu mpenzi wake wa kudumu aitwae Fardos ambae ni Mmanga na kumwambia aende TAI 5 atamkuta pale anamsubiri. Japo alikuwa ni mtoto wa geti, lakini angejua mwenyewe ni vipi aage kwao ili aweze kutoka na kwenda kuonana na Mwinyi hasa ukizingatia siku kadhaa alikuwa akimtafuta na hakufanikiwa kumuona

Saa moja na dakika 5, simu ya Victor iliita, namba ilikuwa ni ngeni machoni mwake ila alipoipokea tu sauti akaitambua

“Samahani Shemeji yangu,za muda?”

“Nzuri Shem, vipi?”

“Nilipigiwa simu na Salama muda ule ule mi nawe tulipoachana, nilishtuka na kuchanganyikiwa kutokana na simu yenyewe,”

“Vipi kuna nini Shem?” akauliza kwa hofu

“Alinipigia kuwa nimfuate hospitali amepumzishwa tangu adhuhuri pale Good Samaritan Clinic, maeneo ya mwaloni,”

“Salama ni mzima lakini?” aliuliza Victor kwa hofu huku akielekea

garini

“Ni mzima ila samahani tu nilisahau kukwambia muda mrefu nae anakuogopa,”

“Ok! Nipo njiani nakuja sasa hivi nitakua hapo,”

“Ok Shem,” wakajipongeza kwa cheko kali ya kishangingi na kugonga

mikono yao.

Sammer alimpigia simu Mwinyi kutaka kujua alipo, alimwambia yupo TAI 5 anamsubiri Fardos ambae anaamini kwa muda ule atakuwa njiani. Sammer alishangaa kwanini iwe TAI 5 badala ya kuwa nyumbani kwake? Mwinyi akamwambia chumba kile Salama kakilipia hadi kesho hivyo yeye anajitahidi kuitumia ili isiwe hasara. Sammer akacheka na kukata simu.

Victor alifika pale hospitali na kuingia kwa daktari, aliwapa pole wote, Salama kwa maumivu na Joy kwa kusumbuliwa, kisha akamuuliza Salama tatizo ni nini? Salama akamwambia kuwa hakuwa akijisikia vizuri tangu akiwa kazini. Walikaa hadi saa tatu usiku ndio wakaruhusiwa kuondoka na kurejea kwao.

Wakiwa njiani Victor akamuuliza Salama kwanini hakumpigia simu kumjulisha kama anaumwa? Salama akamjibu kwamba alihisi kuwa bado ana hasira, Victor alisema yeye hana kinyongo na kwake yaliisha tangu jana ileile, zaidi akamuomba msamaha kwa kipigo alichompa usiku uliopita.



http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Walimfikisha Joy nyumbani kwake na kumkabidhi kwa mumewe alietoka nje kumuona Salama maana Joy alimpigia simu kumueleza juu ya kutokuwepo nyumbani na kuelekea kwake hospitali. Wakaagana, Victor na Salama wakaelekea kwao nao wakaingia ndani.

Fardos alifika TAI 5 na kuungana na Mwinyi kuumalizia usiku ule wakitumia chumba kilicholipiwa na Salama, Vinywaji vinavyotokana na pesa ya Salama pasina Fardos kujua, tena akiamini bwana wake Mwinyi anampenda sana ndio maana kamchukulia chumba kwenye hoteli ile ghali.



MWINYI KUONDOKA MWANZA.



Wiki tatu baadae, RUBANA CONSTRUCTION walimaliza mkataba wao na jiji la Mwanza, ikamlazimu Mwinyi aache kazi, lakini bahati ilikuwa upande wake, akaitwa Tabora na kaka yake kwenda kufanya kazi kwenye kampuni ya Double A

Waliagana na Salama kwa majonzi makubwa, machozi yakiwatoka, lakini walijipa moyo kuwa watakutana tena kwani waliahidiana kutembeleana mara kwa mara. Mwinyi alimuahidi kumtembelea wiki end ya kila mwisho wa mwezi

Salama akasema iwapo Mwinyi atatimiza ahadi yake kwa miezi mitatu mfululizo, basi nae Salama atafunga safari kuelekea Tabora kwa wiki mzima, Mwinyi akafurahi na kuahidi kutimiza ahadi ile.

Siku ya pili akanyakua basi na kuelekea Tabora kuanza makazi mapya katika mji ambao aliwahi kuishi na kaka yake wakati akiwa ni mdogo, kwa sasa hakuweza kabisa kuukumbuka hata unafananaje.

Aliwasili Tabora saa 6 na nusu na kupokelewa na kaka yake aliemchukua hadi nyumbani kwao maeneo ya Gongoni

Wiki moja baadae alianza kazi, hapo tayari alikuwa ameisha hama kwa kaka yake na kupanga chumba kimoja maeneo ya Bachu, nyumba aliyohamia ilikuwa ni ya mama mjane aliekuwa na watoto wawili, mmoja wa kiume aitwae Side na mwingine wa kike anaitwa Ramlat.

Nyumba hiyohiyo pia ilikuwa na wapangaji wengine wawili na wote walikuwa ndani ya ndoa zao. Hivyo ni yeye pekee ndio hakuwa na mke. Alianza kazi vema tu akiwajibika ipasavyo, kama alivyoahii kwa Salama, kila wiki ya mwisho ya kila mwezi alikwenda na kuonana na Salama.

Miezi mitatu kupita Salama akashindwa kuja kwa sababu ya kufiwa na mdogo wake pekee wa kiume aliekuwa akiumwa kwa mua mrefu. Ikamlazimu Mwinyi ndio aende mazishini. Salama alifarijika sana kumuona Mwinyi pale hasa wakati wakuzika, kwani alijua kuwa

Mwinyi atakuja, ila hatowahi mazishi.

Walikumbatiana huku Mwinyi akimpa pole. Siku ya pili Mwinyi

alimpigia simu kumuaga kuwa anarejea kazini kuwajibika ila mwezi ule hatokuja tena hadi mwezi ujao. Salama hakumpinga, ila akamuahidi yeye kwenda Tabora baada ya miezi mingine mitatu.

Kwenye ile miezi mitatu alioishi ndani ya nyumba ile, Mwinyi hakuwahi kuingiza mwanamke yeyote chumbani kwake. Siku moja akiwa chumbani kwake akasikia watu wakiongea kwa sauti chini ya dirisha lake

“Huyu jamaa anaweza kuwa si rijali, haiwezekani kabisa ndani ya miezi mitatu sasa hatujawahi kumuona na mwanamke, huenda ana tatizo” sauti nyingine ikadakia

“Tena basi anatoka saa 1 asubuhi na kurudi saa 1 usiku, hatoki tena hadi kesho, hata nami Napata shaka kuwa huyu kijana sio mzima”

Kauli zile zilimuumiza sana Mwinyi na kuamua kutoka nani kwake na kuwafuata kwena kuwauliza ni nani kawaambia habari ile na kwanini wamfuatilie. Aliweza kuwaona ni mpangaji mwenzie mmoja aitwae Salome na mama Mwenye nyumba wakicheka kwa sauti ya juu huku wakijitikisa.

Alipotoka wakagonga mikono yao na kuingia ndani, akakosa wa kumuuliza nae ikabidi arejee ndani. Usiku ule akajipanga kuwaonyesha kuwa yeye hana tatizo kama wao wanavyodhani, bali ni staha tu aliokuwa akiinda alipanga kuwaonesha kuwa yeye ni mzima kabisa na kwa kuanza tu akapanga aanze na Ramlat, mtoto wa mwenye nyumba.

Usiku aliuona ni mrefu lakini asubuhi ilifika. Siku ile alitoka mapema zaidi na kwenda hadi shule ya Sekonari Uyui, mahali anaposoma Ramlat na kumsubiri. Mwanzo alirusha na kudai haamini kama Mwinyi ni mzima, maana dalili zilikuwa zikionyesha kuwa ana matatizo.

Mwinyi akamjibu kuwa suala la msingi ni kumpa nafasi, hapo nio atajulikana mkweli nani. Haikuwa kazi ngumu kumshawishi na kumuweka kwenye mikono yake. Ramlat akaahidi kumpa nafasi moja tu ambayo anapaswa kuitumia vizuri na atakaposhindwa kuitumia mwenyewe, asimlaumu mtu.

Mwinyi akakubali kwa mikono miwili, wakapanga nafasi ya kukutana

jioni kwenye hotel ya Kiwosso maeneo ambayo si mbali sana na kwao. Yeye akarejea nyumbani kuchukua kitambulisho chake cha kazi na kukutana na kituko wakati akiingia

Aliweza tena kuwakuta Mama mwenye nyumba na Mpangaji wake

Salome wakiongea. Alipoingia yeye na wao kumuona, wakabaili kile walichokuwa wakikiongea na kuanza mafumbo

“Leo tumerudi mapeema, sijui kuna nini?” alianza mama mwenye nyumba ambae kimo chake si kikubwa sana, akadakia Salome

“Labda leo tutakua tumerudi na sketi, kila siku kulala bila hata shuka,”

“Sasa hata kuonja si mpaka uwe na ulimi shoga?”

“Hilo nalo neno” alishindwa kufanya kilichompeleka, akaamua kutoka na kufunga mlango wake akaondoka kuelekea kazini kwake.

Alianza kujuta kupanga nyumba ile, alitamani kuhama, lakini bado alikuwa na kodi yake ya miezi mitatu anaidai, na pia alihofu kuonekana yeye ni tatizo, akaamua kuvumilia hasa ukizingatia usalama pale ni mkubwa sana, cha msingi hapo akaona ni kupambana na ndio dawa pekee ya kumnyamazisha adui, ila kumkimbia, sio ujanja. Akajikubali kwa wazo lake.

Jioni kama walivyopanga, Mwinyi aliusukuma mpapai, huoo... chali! IIikuwa haina mapumziko wala marembo, alimpa penzi motomoto ili kesho awaambie wenzie kuwa Yule mtu hayupo kama tunavyofikiria sisi. Ramlat akapagawa kwa penzi la Mwinyi Usiku waliagana kila mmoja akiwa ni mwenye furaha.

Kukata mzizi wa fitna, akaamua kumvaa na yule mpangaji mwenzie aliekuwa akimteta sana na mama mwenye nyumba wake. Ama kwa huyu alihangaika sana, karibu wiki mzima hapaeleweki, na hata alipotumia njia mbadala nazo hazikufua dafu.

Lakini siku zote jitihada huzaa mafanikio, baada ya wiki mbili akamkubalia na kumpa sharti na kuwa nae kwa siku moja tu na kisha wasijuan tena. Haikuhukua muda wala kuwa ngumu kwa Mwinyi kukubali. Waliutumia usiku mzima kwenye chumba cha Salome mumewe akiwa safarini

Bila kutegemea, akawa amemalizana na mtu wa pili na kwenye ahadi na Ramlat hakwenda na simu akaizima. Asubuhi ya siku iliyofuata wakakutana uso kwa uso Mwinyi na Ramlat, hasira zilionekana waziwazi kwenye uso wake. Mwinyi haikumsumbua kabisa hiyo, yeye alikuwa kwenye hali ya kawaida tu.

Siku mbili mbele, Mwinyi akawa ni mtu ambae hana amani, kila mara Ramlat anamsumbua akitaka waonane, nae akawa anamtoea nje,ie hai ikawa inamkera na hatima kuleta biff kati yao. Mwinyi waa hakushtushwa na hali ile, bali yeye alizidi kufanya yake.

Mawasiliano yao hayakuwa mazuri, Mwinyi hakupokea wala kumpigia simu Ramlat. Wikiendi moja Mwinyi alitoka nyumbani mapema, kabla hajafika mbali akasimamishwa na mtoto mmoja na kumpatia kikaratasi. Alipokisoma kilikuwa kimeandikwa ‘Tukutane kulekule, nina shida muhimu sana nawe’ akakichana na kugeuka kurudi nyumbani.

Kuna kitu aichokuwa amekisahau na ndicho kilichomrudisha pale nyumbani. Wakati anatoka tena akamuona Ramlat anaelekea maliwatoni, akatabasamu na kumuonesha dole, nae akatabasamu na kumtupia Kiss ya mbali, Mwinyi akacheka na

kutikisa kichwa huku akielekea nje.

Kule napo kwenye mlango mkubwa wa kutokea nje, akamuona mama Ramlat akiwa na kapu, ishara ya kuelekea sokoni. Moyoni akasema Yes, leo ndio leo, sijivungi, akaenda na kumsubiri njiani. Kichwani alijua kabisa kuwa leo anapambana na mbuyu, urefu wake ni kama wa mnazi asili tena wenye magamba ya mpera na miiba kama mchongoma.

Alijua kabisa ni shughuli pevu kuupanda mti huu na kufika kileleni. Matokeo yalikuwa ni tofauti na matarajio ilikuwa ni kazi ngumu ila alifanikiwa kumjaza isipokuwa alimuuliza kama ataliweza maana lile ni gari kubwa. Kama kwa Ramlat, Mwinyi alichoomba ni muda tu.

Mama mwenye nyumba akamwambia waonane jioni ya siku hiyohiyo tena palepale nyumbani. Mwinyi akamuulizia kuhusu wanae watakuwa wapi? Akaaambiwa kuwa yeye ajitulize, maana Ramlat atakuwa ametoka kwani kaomba ruhusa mapema kuwa leo anatoka jioni

Mwinyi alijua kuwa ni wapi Ramlat anakwenda, na kuhusu Side, akaambiwa huwa akiisha toka asubuhi, harudi hadi usiku labda kwa dharua na tena ni kwa taarifa. Mwinyi akakubaliana nae

Bila kutegemea, akawa amemalizana na mtu wa pili na kwenye ahadi na Ramlat hakwenda na simu akaizima. Asubuhi ya siku iliyofuata wakakutana uso kwa uso Mwinyi na Ramlat, hasira zilionekana waziwazi kwenye uso wake. Mwinyi haikumsumbua kabisa hiyo, yeye alikuwa kwenye hali ya kawaida tu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Ikawadia siku isioliwa kitu, Mwinyi alitoka na Ramlat hadi katikati ya mji hawana hili wala lile wanakatiza barabarani wenyewe wamejiachia kwelikweli kama mke na mume, wanajiona wanandoa ya halali kabisa, kaka yake Ramlat, Side akawaona wakiingia guest Fulani







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog