Search This Blog

Tuesday 1 November 2022

UTANIKUMBUKA TU! - 4

 






Simulizi : Utanikumbuka Tu!
Sehemu Ya Nne (4)




"Mbona unastuka? Vipi unamfahamu Edga", aliuliza Kayumba kwa taharuki baada Diana kustuka kusikia jina hilo. Diana alikataa, akasema "Hapana simfahamu ila jina hilo linafanana na jina la mkaka mmoja hivi.."

"Yupi?..", aliendelea kuhoji Kayumba.

"Huwezi kumjua, hebu tuachane na hayo. Je, upo tayari tukaishi pamoja?.."

"Laah!..", Kayumba akijishauri akubali ombi hilo au akatae, lakini wakati akiendelea kujishauri, Diana akasema "OK ngoja nikuache upumzike, naenda kuendelea na shughuli zangu ila kesho nitakuja kukujulia hali", Diana anakusanya vyombo vyake ili aondoke wodini humo. Lakini kabla hajafungua mlango wa wodi, Ikene anaingia ndani huku akiwa na tabasamu bashasha, akifurahi kumuona Kayumba u ahueni. "Habari zenu?..", Ikene aliwasabahi Kayumba na Diana. "Salama kaka, sijui kwako", aliongea Diana kwa haibu kubwa.

"Kwangu pia nzuri, vipi mgonjwa wangu amekula chakula?..", aliongeza kusema Ikene safari hiyo macho yake yakimtazama Kayumba. Diana akajibu "Ndio amekula ingawa sio sana"

"Anhaa, vizuri kesho kama kawaida mletee sawa? Ila hakikisha unaniorodheshea ghalama zote, mimi nitakulipa pasipo na shaka"

"Sawa kaka nimekuelewa", alijibu Diana kisha akaondoka zake. Baada kuondoka Diana Ikene aliketi pembezoni kidogo ya kitanda alicholalia Kayumba. Akashusha pumzi na kumuuliza hali yake "Hali yangu iko sawa kwa sasa ingawaje nasikia maumivu kwa mbali hapa kichwani ila nafikiri kesho naweza kuruhusiwa", alijibu Kayumba huku akigusa kichwa chake sehemu aliyoumia.

"Sawa, pole sana. Basi kesho nitakuja nitakapotaka kwenye show, nitapita hapa nikuchukue ili nikupeleke ukapaone mahali ninapo ishi maana tayari umekuwa kama ndugu"

"Sawa braza usijali"

"Safi, sana. Haya kwa heri, pumzika salama kesho nitakuja braza", Ikene aliaga namna hiyo kisha akaondoka zake.



********

Siku iliyofuata, hali ya Kayumba ilionekana kutengemaa. Aliruhusiwa na Daktari kurudi nyumbani. Alipokuwa mapokezi akijianda kw niaba kurudi mtaani, ghafla akakumbuka kuwa Ikene alimuahidi kumpelekea nyumbani kwake. Alikitisa kichwa huku akiachia tabasamu pana, akaketi kwenye kiti cha mapokezi na sasa akimngojea Ikene. Lakini wakati anamngojea Ikene, punde anatokea Diana. Kwa tabasamu bashasha Diana akazipiga hatua kumfuata Kayumba. Alipomkaribia alimsalimu kisha akamuuliza juu ya ombi lake "Enhee na vipi kuhusu ombi langu?."

"Ombi gani Diana?.", alihoji Kayumba.

"Kayumba, kumbuka jana nilikuomba ukaishi kwangu, yani tuishi pamoja"

"Tishomingo pamoja? Ujue bado sijkuelewa, na vipi kuhusu mumeo au mchumba wako?..", Diana aliangua kicheko baada kuyasikia maneno hayo aliyoyasema Kayumba, alipokatisha kicheko chake akasema "Kayumba mimi sina uhusiano wa kimapenzi na mwanaume yoyote hapa mjini, nipo mimi kama mimi tu naendesha maisha yangu", maneno hayo Diana aliyaongea kwa hisia kali, alitamani sana aishi na Kayumba sababu ametokea kumpenda.

Kayumba alishusha pumzi ndefu akawaza akaona ni heri akaonane na rafiki yake kwanza ndipo aamue kwenda kuishi na Diana, "Nimemkumbuka sana swahiba wangu Edga, siwezi kuamua chochote kabla sijaonana na mchizi wangu", pumzi alishusha Kayumba baada kuwaza, akamgeukia Diana akamta akamjibu "Nipo tayari ila lazima kwanza nikaonane na rafiki yangu ndipo twende wote nyumbani kwako", Diana alifurahishwa na jibu hilo la Kayumba "Asante sana kwa kunikubalia, basi tunaweza kwenda", aliongea Diana huku akiachia tabasamu. Lakini kabla wawili hao hawajaanza safari, alionekana Ikene akijongea mahali waliposimama Diana na Kayumba. Ikene alifurahi sana kumuona Kayumba akiwa mzima na mwenye nguvu, kijana huyo aliamini tayari azma yake imetimia baada kumgonga sasa amemtibia mpaka kupona "Habari zenu jamani", alisabahi Ikene.

"Salama tu karibu", alijibu Kayumba kwa furaha.

"Nimeshakaribia, kweli Mungu mkubwa..", alisifu Ikene baada kufurahishwa na hali aliyokuwa nayo Kayumba.

"Diana, samahani kwa kuchelewa. Na yote ni sababu ya hali ya jiji hili lilivyo foleni ilikuwa kubwa mno,lakini hakijaharibika kitu. Bila shaka tayari umeandaa kiasi cha fedha unazo nidai", aliongeza kusema Ikene. Diana akamuondoa hofu kisha akamtajia kiasi hicho, pasipo hiyana Ikene alimlipa Diana stahiki yake.

"Asante sana kaka, Mungu akubariki", alishukuru Diana.

"Na wewe pia asante", alijibu Ikene, na sasa alimgeukia Kayumba, akamtaka waondoke kwenda mahali anapoishi ili apaone. Kayumba alikubali, akamwambia Diana amsubiri kando kidogo ya hospital. Ikene na Kayumba waliingia kwenye gari wakaondoka, kwa muda wa nusu saa wakarejea. "Tupo pamoja Kayumba, mimi na wewe sio maadui. Shukrani kwa utu wako. Tuazidi kuonana",baada Ikene kumrudisha Kayumba kwa Diana aliongea maneno hayo, wakapeana mikono wakaagana Ikene akaondoka zake huku nyuma napo Kayumba na Diana walielekea maskani anapoishi na rafiki yake wa kuitwa Edga. Walipokuwa wakikaribia kufika, Kayumba alisikia sauti ikimuita "Oya braza", sauti hiyo ilipasa karibu mara mbili mfululizo, na ndipo Kayumba alipogeuka kutazma kule inapotokea. Alimuona kijana dereva boda boda, sio mgeni machoni mwake, hivyo haraka sana alitii wito.

"Habari za siku nyingi bwana", kijana huyo alimsabahi Kayumba.

"Ni njema tu", aliitikia Kayumba huku akionekana kuwa na shauku ya kutaka kujua kijana huyo amemuitia shida gani.

"Ebwanaeeh! Hebu sikia, wewe ni kijana mwenzetu halafu istoshe sisi wote ni wanaume. Hatujui ni wapi tutakuna, aidha maisha ya hapo mbeleni sijui kama utanisaidia ama la! Lakini katika hili acha nikutonye. Kambi imekufa, rafiki yako tayari amefukuzwa, ajabu baadae kufukuzwa pale mlipokuwa mnalala, zahma likatokea usiku huo huo wa siku hiyo. Kwa hiyo basi kama unavyojua watu wa mtaa huu walivyo wanoko, jamaa mwenye duka akionyeshwa kuwa na wewe ulikuwa unalala pale basi ujue moja kwa moja utazoea jela. Ikiwezekana potea kabisa mtaa huu braza ", Kayumba alistuka kusikia maneno hayo, hofu ilimjaa achilia mbali Diana.

" Kayumba hebu tuondoke bwana ", aliongea Diana kwa sauti ya woga. Muda huo Kayumba alijihisi kukosa nguvu, alisikitika sana kwani aliamini kuwa huo ndio mwisho wa kuonana na rafiki yake kipenzi. Msaka tonge mwenzake, kijana aliyempatia hifadhi ndani ya jiji baada kukataliwa na Catherine na kujikuta hana pa kwenda. Takwa la Diana linatimia, anafanikiwa kwenda kuishi na Kayumba.



*******



Na wakati hayo yakiendelea, kwingeneko anaonekana Catherine akizidi kukosa amani ya moyo wake kila iitwayo leo. Pesa, Elimu yake aliyotumia kama fimbo ya kumuadhibu Kayumba alijikuta vyote hivyo havimsaidii. Taswira ya Kayumba ilimjia, alikumbuka mapenzi ya dhati aliyokuwa akimuonyeshea. Pumzi alishusha huku akidiriki kujilaumu kwa kitendo alichomfanyia, kitendo cha kumfukuza Kayumba kama mbwa. Alikumbuka "Oooh! Malikia wa moyo wangu, Catherine kipenzi changu nimerudi, Kayumba nipo huru sasa" Alisema Kayumba alipomkaribia Catherine.

"Mbona kama hufuraishwi na ujio wangu? Maana sioni ukionyesha hata tabasamu? Unataka kuniambia miaka saba yote hujanikumbuka?.." Aliongeza kusema Kayumba huku akimtazama Catherine uso kwa tabasamu bashasha ilihali Catherine akionyesha uso wa hasira. Mwisho akakohoa kidogo kisha akasema." Kayumba, naomba useme shida iliyokutoa kijijini ikakuleta nyumbani kwangu. Nina kazi nyingi za kufanya ndani sitaki unipotezee muda wangu". Pumzi ndefu alishusha Catherine baada kukumbuka hayo, machozi yalimtoka, aliona hana budi kumfuata kijijini kwa dhumuni la kumuomba msamaha na ikiwezekana warudiane. Lakini baada Catherine kufika kijijini alistuka kutomuona Kayumba licha ya kukaa siku tano, hali hiyo ilimtia hofu sana. Na hivyo aliamua kumuuliza swahiba wake wa zamani ambaye alisoma naye kipindi hicho cha nyuma. Aliitwa Elizabeth. Wawili hao wakiwa nje, usiku wa mbalamwezi wakipiga zogo hasa Elizabeth akionekana kudadisi uharisia wa maisha ya jiji Dar es salaam, punde Catherine anaingizia suala la kutomuona Kayumba kijijini.

"Eliza, hivi siku hizi Kayumba anashinda shamba?"

"Kayumba? Cather hebu acha utani bwana, nikuulize wewe kwa sababu anaondoka hapa kijijini anakwenda Dar kwa niaba ya kukutafuta wewe. Lakini ajabu dakika za mwisho tunapata habari kwamba Kayumba amekuwa msukuma mkokoteni, anauza madafu!.." akianza kwa kushangazwa na swali la Catherine, Elizabeth aliongea hivyo.

" Eliza, inamana unataka kuniambia Kayumba yupo Dar?.. ", alihoji Catherine kwa taharuki kubwa..



Alistaajabu Catherine, alikaa kimya kwa muda wa sekunde kadhaa. Ndani ya nafsi yake akajisemea "Maskini Kayumba wangu, natambua mateso hayo yote anayopitia ni sababu yangu. Ila sitoweza kukubali, kwa udi na uvumba nitakutafuta Kayumba, mahali popote ulipo nitakufuata"

"Catherine, mbona unaonakana umeduwaa?..", aliuliza Elizabeth ni baada kumuona Catherine amepigwa na bumbuwazi. Catherine akajibu "Hapana Eliza nipo sawa, ondoa shaka"

"Mmh hebu acha kunificha, unaonakana kabisa haupo sawa. Lakini tuachane na hayo, nipe habari za Dar rafiki yangu", aliongea Elizabeth, zaidi Catherine hakutaka kuendelea na zogo. Alisema "Naomba tulale Eliza, ili kesho niwahi basi la kwanza"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Catherine inamaana kesho unaondoka?..", alihoji kwa taharuki Elizabeth.

"Ndio, muda niliokaa hapa kijijini nafikiri unatosha sasa", alisisitiza Catherine. Mrembo huyo aliona hana sababu ya kuendelea kuishi kijijini wakati mtu aliyemfuata yupo mjini.

Siku iliyofuata alifunga safari kurudi Dar es salaam. Upande wa pili alionekana Diana (Sinsia) akizipiga hatua akiwa ametoka sokoni, mkononi akiwa ameshika mfuko wa nailoni wenye vitu ndani. Alipofika nyumbani kwake alimkuta Kayumba akiwa ameketi nje kando ya nyumba akijisemea kitabu.

"Kayumbaaa", alipasa sauti Diana baada kuikaribia nyumba. Kayumba aliposikia sauti ya Diana, akayotoa macho yake kwenye kurasa ya kitabu akayapeleka kule ilipotokea sauti.

"Naaam mama la mama", aliongea Kayumba huku akinyanyuka ikiwa muda huo Catherine ameshamkaribia ambapo aliandamana naye mpaka chumbani.

"Nimekununulia shati, hebu jipime nione kama linakufaa", baada kuingia chumbani Diana alitoa kile kitu kilichokuwa ndani ya mfuko, lilikuwa shati ambalo amenunulia Kayumba. Kayumba alilivaa shati hilo, akajitazama mbele namna lilivyoufaa mwili wake. Akaachia tabasamu kisha akasema "Asante kwa msaada wako Diana"

"Usijali Kayumba hivi ni vitu vya kawaida tu, na kwakuwa nakupenda? Nitaendelea kukufanyia vitu vizuri zaidi", alijibu Diana, maneno hayo yalimstua Kayumba, akamtazama Diana mara mbili mbili huku akishindwa kuelewa mrembo huyo mama ntilie amemanisha nini "Diana, makubaliano yangu na wewe ni kunisaidia kumpata rafiki yangu, na sio mimi na wewe kuwa wapenzi", alimg'aka Kayumba wakati huo akiivua shati aliyonunuliwa na Diana. Hakika Diana alionekana kupoa mithili ya maji ya mtungini, alitambua fika kuwa aemekurupuka mapema kuongea hisia zake kwa Kayumba. Alijilaumu sana, na hivyo neno samahani halikuwa mbali na kinywa chake. Alimuomba radhi Kayumba ingawaje aliamini kwamba ipo siku Kayumba atakuwa wake "Samahani sana Kayumba kama nimekuudhi, tambua ulimi hauna mfupa, nimeteleza kidogo naomba unisamehe sana", aliongea Diana kwa sauti ya upole ilijaa huzuni ndani yake. Kayumba akamtazama Diana kisha akajibu "Usijali Diana, ila ukweli ni kwamba sifikirii kumpenda tena mwanamke katika maisha yangu, nitaishia kutamani kwa kuwa maumivu niliyoyapata katu hayotoweza kusaurika katika maisha yangu.."

"Aliyonifanyia Catherine yanatosha", aliongeza kusema Kayumba huku akiwa amempa mgongo Diana wakati huo wameachana hatua kadhaa. Kayumba akiwa amesimama, Diana akiwa ameketi kitandani akijutia kumuudhi Kayumba.

"Kayumba kama nilivyokwisha kusema, ulimi hauna mfupa, nisamehe sana nipo chini ya miguu yako", alinyanyuka na kisha kumsogelea akamueleza kwa mara nyingine tena juu ya kile alicho mueleza hapo awali, Diana alionekana kuzidi kujutia kosa lake. Kayumba alimgeukia halafu akajibu "Nimekuelewa Diana"

"Asante kwa msamaha wako Kayumba", aliongea Diana kwa tabasamu bashasha ambalo Kayumba naye alilijibu hivyo hivyo. Baada ya hapo Diana alimuaga Kayumba na kisha kuelekea kazini.



*******



Siku zilisonga, Catherine aliendelea kuhangaika kumtafuta Kayumba ndani ya jiji la Dar es salaam, wakati huo upande wa Najrat naye alionekana kukosa amani moyoni mwake baada kupita siku gedegede pasipo kumtia machoni muuza madafu ambaye si mwingine bali ni Kayumba. Mrembo Najrat mtoto wa kitajiri, alizama vilivyo kwa Kayumba. Alijiuliza maswali mengi na kukosa majibu juu mahali alipo Kayumba, alitumia muda mwingi kumtafuta barabara aliyokuwa akimuona mara kwa mara akiwa na mkokoteni wenye madafu, lakini abadani hakubahatika kumtia machoni. Aliumia sana, kazini akawa haendi muda mwingi akimfikiria Kayumba na sio kazi. Kwa kijana yule muuza duka ambaye siku ile alimuachia kiasi cha fedha na ujumbe kwenye karatasi kwa dhumuni la kumpata Kayumba, Najrat alifika kwa usafiri wake binafsi. Gari ya bei ghali ilisimama kando ya duka hilo, punde akashuka mrembo huyo mwenyewe uzuri wa kuvutia. Ngozi nyororo na wembamba wa sura yake ikiwa imempendeza hasa.

"Habari yako bro", baada kurikaribia duka, Najrat alimsalimu kijana huyo huku akiifua miwani yake aliyokuwa ameivaa.

"Njema tu dada, karibu" "aliitikia kijana huyo.

" Asante sana, habari za siku mbili tatu "

" Salama, tunapambana hapa kama unavyoona "

" Sawa.. Aamh naomba nikuulize kitu tafadhali "

" Uliza tu dada wala usijali "http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

" Yule kijana muuza madafu mara ya mwisho kupita hapa ilikuwa lini?.."

"Amhh, kwa kwali dada siwezi kukudanganya. Ni siku nyingi, hata mimi nilikuwa nafikiria pasipo kupata jibu", pumzi alishusha Najrat baada kusikia jibu hilo, hofu ikamjaa vema. Roho yake nayo iliuma, ama hakika alitokea kumpenda mno Kayumba. Akiwa mnyonge mithili ya kifaranga kilicho nyeshewa na mvua, mrembo huyo alirejea ndani ya gari lake akaondoka zake wakati huo huo huku nyuma akimuacha muuza duka na taharuki ya aina yake "Kuna watu wanabahati kudadadeki, yani yule jamaa rofa anatafutwa kama pesa na huyu mrembo wa kiarabu?..", alijuliza kijana huyo.

Catherine na Najrat ni marafiki, urafiki wao ulianza pindi walipokutana chuoni. Wawili hao walikubalina kwa kila jambo, alipo Catherine basi Najrat yupo. Ulikuwa urafiki wa kudumu, hata pale kila mmoja alipokuwa amepata kazi licha ya kwamba walifanya kazi kampuni tofauti. Catherine anakumbuka kuwa siku moja Najrat aliwahi kumwambia kuwa ametokea kumpenda kijana muuza madafu, na hivyo Catherine anaamua kufunga safari kwenda kutembelea rafiki yake kwa dhumuni la kumdadisi ili amueleza jinsi alivyo kijana huyo. Alipofika nyumbani anapoishi Najrat, alimkuta Najrat amejilaza kwenye sofa huku akionekana kuzama kwenye dimbwi la mawazo "Habari yako Naj", Catherine alimsalimu Najrat mara baada kuingia ndani. Najrat alizinduka kutoka kwenye dimbwi hilo la mawazo, akanyanyua uso wake akamuona Catherine, alishusha pumzi kisha akasema Salama tu, karibu "

" Nimeshakaribia rafiki yangu, vipi kulikoni mbona kama haupo sawa!?.. ", kwa mshangao wa iana yake, Catherine alimuuliza Najrat swali hilo. Ni swali ambalo lilimfanya Najrat kukaa kimya kwa muda wa sekunde kadhaa kisha baadaye kimya hicho akakivunja akasema" Catherine, unakumbuka kama niliwahi kukwambia kuwa nimetokea kumpenda mkaka mmoja hivi muuza madafu?.. "

" Ndio, nakumbuka vizuri tu "

" Enhee basi mwenzio najikuta nakosa amani kabisa ndani ya moyo wangu, na pia ni... ", kabla Najrat hajamaliza kusema alichokuwa akikiongea, Catherine akadakia akasema." Hebu subiri kwanza Naj, kwani huyo mkaka yukoje kiasi kwamba ukonde kabisa kwa sababu yake "

" Mmh we acha tu ", alisema Najrat wakati huo akijinyanyua kutoka kwenye sofa, aliketi na kisha kuanza kuelezea namna kijana huyo alivyo. Punde Catherine alistuka baada kusikia kwamba muuza madafu huyo anakovu katika paji la uso wake, pembeni kidogo ya jicho la kulia. Catherine akavuta kumbukumbu ya miaka ya nyuma,alikumbuka kuwa Kayumba aliwahi kupasuliwa sehemu ya paji la uso wake pindi alipokuwa akipigana kumtetea baada kuonekana akionewa na wababe wa shule. Alitikisa kichwa Catherine ishara ya kukubali jambo fulani, lakini hakuisha hapo alikumbuka na maneno ya Elizabeth "Kayumba? Cather hebu acha utani bwana, nikuulize wewe kwa sababu anaondoka hapa kijijini anakwenda Dar kwa niaba ya kukutafuta wewe. Lakini ajabu dakika za mwisho tunapata habari kwamba Kayumba amekuwa msukuma mkokoteni, anauza madafu!..",yote hayo aliyakumbuka Catherine ikiwa muda huo akiyaunganisha na maelezo ya Najrat. Hatimaye anapata picha kamili.

" Lazima nimtafute Kayumba popote pale najua nitampata ", Catherine alipania ndani ya nafsi yake, wakati huo Najrat naye akitafakari ni wapi atampata Kayumba ambaye tayari yupo katika himaya ya mama ntilie Diana (Sinsia)





Kila mmoja alikuwa akiwaza namna ya kumpata Kayumba kwa nyakati tofauti, na wala Najrat hakujua kuwa Kayumba hapo awali alikuwa na mahusiano na Catherine.

"Catherine mbona umeduwaa, unamfahamu huyo muuza madafu?..", aliuliza Najrat baada kumuona Catherine amepigwa na bumbuwazi. Catherine alikataa, akazinduka kutoka kwenye dimbwi la bumbuwazi akawa mithiri ya paka aliyekurupushwa akiiba mboga, tabasamu hafifu likionekana usoni mwake kisha akasema" Hapana Najrat ila.. "

" Ila nini Catherine?.. ", aliuliza Najrat akishindwa kumuelewa kabisa rafiki. Lakini bado Catherine alikataa katu katu, alidai hakuna jambo linalo msibu kwa maana hiyo alimuondoa hofu Najrat kwa kusisitiza" Sikia rafiki yangu, mimi nipo sawa kabisa nawala sina mawazo yoyote. Aamh! Pia naomba nirudi nyumbani kuna kazi inabidi nikaikamilishe leo, nikaona sio vizuri kupitiliza moja kwa moja pasipo kuja kukusabahi ", aliongea Catherine kwa tabasamu bashasha wakati huo akiwa amenyanyuka kutoka kwenye sofa.

" Sawa, usijali unaweza kwenda! Halafu nikwambie kitu?.. "

" Niambia tu rafiki yangu Najrat "

" Hivi leo tarehe ngapi?.. "

" Mmh kwahiyo Naj wataka kuniambia hujui tarehe ya leo?"

"Ahahahah! Haya karibu kesho itakuwa siku yangu ya kuzaliwa"

"Waooow Najrat, kumbe kesho mtoto mzuri unazaliwa? Nilikuwa nimeshasahau kabisa. Nitakuja cha muhimu kuomba uzima"

"Nina imani Mungu atasaidia"

"Sawa Najrat kwa heri kesho tutaonana Mungu akipenda"

"Haya shoga yangu, safari njema"

Catherine aliingia ndani ya gari lake, akaliwasha akaondoka zake huku kichwani mwake akiendelea kujenga picha kamili juu ya maelezo aliyayapata kutoka kwa rafiki yake aitwaye Najrat achilia mbali yale aliyoyasikia kwa Elizabeth. Hapo sasa napata mwanga angavu, ubongo wake unafunguka vema anagundua kuwa pasipo shaka mtu huyo aliyemzungumzia Najrat ni Kayumba wake. Hofu sasa inamjaa, uzuri alionao Najrat na kipato alicho nacho kinamtia shaka Catherine. Alihisi sasa Najrat anampokonya tonge lake, pumzi alishusha Catherine kisha akajisemea "Siwezi nasema siwezi kukubali, ni bora urafiki uvunjike ila sio mimi kumkosa Kayumba. Najrat laiti ungalijua basi usinge jisumbua kumfikiria huyo muuza madafu. Lakini kwa kuwa jambo usilo lijua ni sawa na usiku wa giza. Huna budi kuumiza akili yako kwa mali ya mtu mwingine ", alijisemea Catherine huku akionekana kuwa na wingi wa jazba, hali hiyo ilimfanya kupoteza umakini akajikuta akimgonga kijana ambaye alikuwa akivuka barabara, kwenye zebra. Kijana huyo aliyeonekana amevaa nguo zilizo chakaa mfano wa kichaa alianguka chini, punde damu kupitia mdomoni na puani zikaanza kumtoka. Catherine alistuka, alizinduka kutoka kwenye wingu nzito la mawazo, alikanyaga breki kwa nguvu. Harufu ya magurudumu ilisikika ilihali muda huo huo fujo zilisikika "Ameuwa! Amegonga huyooo. Achomwe moto.. Piga huyooo", kelele hizo za kuhamasisha wananchi wenye hasira kali wamzuri Catherine zilisambaa kwa kasi huku kundi la vijana wazee kwa watoto wakiwa na siraha tofauti walikuja kwa kasi ya ajabu kummaliza Catherine. Mapigo ya moyo wa Catherine yalienda mbio mfano wa saa mbovu, aliogopa sana. Hofu dhufo lihali ilimjaa akaona huo ndio mwisho wa maisha yake. Lakini wakati akiwaza hayo, mara ghafla king'ora cha jeshi la polisi kilisikika. Na punde si punde jeshi hilo lilifika eneno la tukio, kijana yule aliyegongwa alipakizwa kwenye gari pamoja na Catherine, akawa amebahatika kuponyoka kwenye mikono ya wananchi wenye hasira kali.

"Sheria sasa ifuate mkondo wake", alisikika mzee moja akiongea kwa hasira huku mkononi akiwa emeshika mawe.

Kituo kidogo cha polisi alifikishwa Catherine ikiwa muda huo majeruhi ameshakimizwa hospital ya Amana kupatiwa huduma. Mahojiono kadhaa wa kadhaa yalifanyika, mwishowe ikabainika kuwa umakini mdogo barabarani ndio chanzo kilicho pelekea ajari. "Hivi hujui kama umakini unatakiwa uwepo barabani?..", aliuliza kamanda, aliitwa kamanda Mbilinyi.

"Natambua hilo Afande, kiukweli siku sawa kwa muda ule na ndio maana baada ya kutokea ajari sikutaka kukumbia ingawa nafasi ya kuondoka kwenye eneo la tukio nilikuwa nayo", alijibu Catherine.

"Ok, vizuri kwa kukubali kosa".

"Lakini Afande, naomba suala hili lisifike mbali. Nipo tayari kumuhudumia mgonjwa mpaka pale atakapo kuwa sawa", alijitetea Catherine. Kamanda Mbilinyi aliposikia utetezi huo kutoka kwa Catherine, akageuka kumtazama kamanda mwenzake, naye akakubali ishara ya kichwa kisha Mbilinyi akarudisha uso wake kumtazama Catherine na akasema "Upo sahihi, ila ukae ukijua suala hili ni nzito. Kwa hiyo yakupasa uwe na mkono mrefu"

"Eeh! Lakini endapo kama mkono wako utakuwa mfupi basi jiandae kukaa kisaiklojia mrembo", alisisitiza kamanda wa pili, naye aliitwa Mula. Maneno hayo aliyoongea Mula yalimpelekea kamanda Mbilinyi kuanguka kicheko. Fika Catherine akatambua mkanda hao hawana kingine wanacho kihitaji zaidi ya RUSHWA, haraka sana akahoji "Haya niambieni sasa kiasi gani kinatakiwa", kamanda Mbilinyi akamtazama Mula, kwa siri pasipo Catherine kuona ishara hiyo. Mula akamuonyesha vidole vinne Mbilinyi. Kamanda huyo baada kuona ishara hiyo akamtazama Catherine kisha akasema "Shilingi laki nne"

"Sawa hakuna shaka makamanda, hakika mtakuwa mmenisaidia sana. Nitawaongeza laki moja ili Jumla niwape shilingi laki tano", alijibu Catherine kwa sauti ya chini.

"Laki tano? Ahahahaha. We Mula hebu mfungue pingu haraka sana. Eeh hawa ndio watuhumiwa wanaotakiwa na sio kukamata wavuta bangi na vibaka tu. Kazi kujambiana humu ndani", aliongea kamanda Mbilinyi kwa furaha kubwa mno, kamanda Mula alifanya hima kumfunga pingu Catherine. Punde pingu inatoka kwenye mikono ya Catherine, alishusha pumzi wakati huo huo kamanda Mbilinyi akasema "Mula sikia"

"Ndio Afande nakusikiliza"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Ongeza na huyu binti akukupe hizo fedha halafu...", kabla kamanda Mbilinyi hajaendelea kuongea akamvuta kando zaidi kisha akaendelea kumpa maelekezo kamanda Mula,kamanda ambaye alionekana kuwa na furaha isiyo kifani "Akishakupatia fedha hizo, usije hapa ofisini kaa nazo nitamaliza zamu. Kwa chochote kitakacho tokea nitakutetea. Nikitoka hapa nitakutaarifu wapi tukutane tugawane pasu kwa pasu..", aliongea kamanda Mbilinyi kwa sauti ya kunong'ona.

"Sawa kamanda hakuna shida, ingawa tusimsahau mkuu wa kituo balaa hili kamanda", alijibu kamanda Mula akitia shaka. Lakini kamanda Mbilinyi alimuondoa hofu, na sasa akamgeukia Catherine na akasema "Sasa binti, kwahiyo fedha hiyo inafuatwa wapi? Na nakuomba isichukuwe muda mrefu kupatikana"

"Ipo Bank, shaka ondoa kamanda kila kitu kitaenda sawa kabisa", alijibu Catherine kwa kujiamini zaidi.

"Basi hakuna tatizo, ila jukumu lingine ambalo inatakiwa kulifanyia kazi ni kumtibu yule majeruhi mpaka atakapo pona. Utaongozana na kamanda mpaka mahali alipolazwa. Cha zaidi sisi hatuna. Siku nyingine uwe makini"

"Ahsante makamanda, hilo bila tabu limekwisha", pesa iliyonifanya Kayumba kuonekana sio chochote kwa Catherine ukiachilia mbali elimu aliyoumia kama fimbo kuu ya kumchapia na kumuachia Jeraha la moyo, ndio pesa hiyo hiyo ambayo inamtoa kwenye mkono wa dola. Hakika Catherine alitembea kifua mbele, na wala hakuweza kutafakari ya kwamba alicho kifanya ni adui wa maendeleo.

Mchakato mzima wa kupena fedha ulikamilika, na sasa Catherine na kamanda Mula walielekea Amana hospital kumuona majeruhi ikiwa na Catherine kuchukuwa rasmi jukumu la kumtibia kijana huyo kwa ghalama zake mpaka pale atakapo pona. Walipofika, muuguzi aliwaelezeka wodi aliyolazwa mgonjwa huyo. Nao pasipo kupoteza wakati waliingia ndani ya wodi hiyo wakamkuta mgonjwa akiongezewa drepu ya damu. Kijana huyo aliyongogwa na gari alilokuwa akiendesha Catherine, hakuwa mwingine bali ni kijana Edga..



Catherine alimtazama Edga pale kitandani, alitikisa kichwa akimsikitikia mgonjwa huyo. Chozi la huruma lilimtoka, akalifuta kwa leso wakati huo huo Afande Mula akasema "Mgonjwa wako ni huyu hapa, kwahiyo kazi inabaki kwako. Muuguze mpaka pale hali yake itakapokuwa imetengamaa", alipokwisha kusema hayo kamanda Mula, akafungua mlango akaondoka zake huku nyuma akimuacha Catherine akiendelea kumkodolea macho Edga pale kitandani, pumzi alishusha Catherine na safari hiyo aliketi kando ya kitanda alicholazwa Edga. Sasa jukumu likabaki kwake, naye hakuweza kufikiria kumtelekeza kijana huyo.



Diana anazidi kuumiza kichwa, aliwaza afanye nini ili Kayumba awe mpenzi wake kwani kila alipojaribu kumfanyia vitu vya kuashiria nia yake aliyo nayo, lakini Kayumba alionyesha ugumu wa kutolewa maana harisi aliyomanisha. "Hapana lazima nionyeshe nia ya dhati ili aweze kunielewa kwa haraka", alijisemea Diana, muda huo alikuwa kazini. Aliona hakuna namna nyingine zaidi ya kujitoa muhanga kwa Kayumba, sababu moyo wake uliendelea kuteseka vilivyo. Aliporejea nyumbani, baada ya harakati zote kukamilika. Sasa waliketi kitandani huku wakiongea mambo mengi kuhusu maisha ujumla, lakini wakati zogo hilo limepamba moto, vicheko vya hapa na pale vikisikika kutawala, ghafla Diana anafunguka ukweli unao mtesa kila uchwao. Daina alianza kwa kusema "Kayumba"

"Naam!", Kayumba aliitikia huku macho yake yakiwa yamegonga kwenye kifua cha Diana, kifua ambacho kilistiliwa na khanga nyepesi.

"Wewe ni mwanaume mzuri sana, nadhani kila mwanamke akuonaye lazima atamani kuishi na wewe. Hivyo naomba nafsi yangu imekuwa ikikosa raha, usinione nacheka ni vile hujui namna furaha kwangu ilivyogeuka ndoto. Nakupenda sana Kayumba, tafadhali nihurumie mimi. Hebu sahau yote ya nyuma, huwenda yule aliyekusaliti hakuwa changuo lako. Nakupenda Kayumba nakupenda sana japo sina ila naomba unipe nafasi ndani ya moyo wako, natesaka kwa ajili yako nionee huruma ", aliongeza kusema Diana kwa sauti ya chini iliyojaa huzuni ndani yake. Kayumba alimtazama kisha akasema" Ni kweli Diana naishi kwako nakula na kunywa kwako, lakini inapofikia hatua anakwambia jambo fulani hataki basi jaribu kumuelewa. Msaada wako usiwe fimbo ya kunichapia kulazimisha penzi, naweza ni kaondoka nikapambane mtaani ", aliongea Kayumba kwa hasira,maneno hayo yalimuumiza vibaya mno Catherine, alilitamani sana penzi la Kayumba. Kwa sauti iliyoambatana kilio Catherine akaongeza kusema" Kayumba kwanini unaniumiza kiasi hiki? Tambua sio mimi, ni moyo wangu ndio unaokuhitaji. Uonee huruma tafadhali ", alilia Catherine, machozi yaliuchakaza uso wake.

"Maskini moyo wangu, pole sana kwa maswahibu unayopitia kwa kumpenda mtu asiyekupenda",alijisemea Catherine na kisha akalala, akajifunika shuka mwili mzima huku kila sekunde akipandisha kwikwi. Baadaye Kayumba alitambua kuwa Diana amekasirika, ndipo alipoanza kujishauri mara mbili mbili, hasa akifikiria msaada mkubwa aliopewa na Diana, aliwaza hili na lile achilia mbali kilio cha machozi alichokionyesha mbele yake. Pumzi ndefu alishusha Kayumba akahisi Diana hatoweza kumsaliti kama alivyofanya Catherine, akaona hana budi kuirejesha furaha ya Diana kwa kukubali ombi lake. Alingojea kesho pakuche ndipo amjibu. Kesho yake Diana aliamka akiwa na hasira, alifanya maandalizi yake stahiki kisha akaanza kuondoka kufungua mgahawa. Lakini kabla hajatoka chumbani alisikia sauti ya Kayumba ikimuita "Diana",Diana hakuitika, alisimama akamgeukia Kayumba akasema "Unasemaje", alisema kwa jazba. Kayumba alistushwa na jazba aliyoonyesha Diana,ila hakujali kwani alitambua fika ni kitu gani kilicho mkasirisha. Alitikisa kichwa, akashuka kitandani akamsogelea aliposimama na akasema "Diana, samahani kwa yaliyotokea. Usiku kucha nimetafakari nimeona ni kweli nakukosea sana hivyo tufanye yameisha, sasa karibu kwenye bustani yangu ya mapenzi lakini chonde chonde naomba usinifanyie kama yale aliyonifanyia Catherine", Diana alistuka kusikia maneno hayo mema yaliyotoka kinywani mwa Kayumba, hakuamini masikio yake kama ni kweli Kayumba amekubali kuishi naye kama mpenzi, hakika alifurahi sana moyoni mwake. Hisia zilishindwa kustahimili furaha, na punde si punde machozi mithiri ya maji yakambubujika kunako mboni za macho yake "Ahsante sana Kayumba kwa kujali hisia za moyo wangu, nakuahidi sitokuja kukutenda hata siku moja, nakupenda na nitaendelea kukupenda", akayafuta machozi yake baada kusema hayo, akiwa mlegevu mithiri ya mlenda akajilaza kwenye kidali kipana cha Kayumba wakati huo huo naye akahoji "Kweli Diana hutonisaliti?.."

"Ndio Kayumba, wewe mwenyewe utaona. Halafu baadaye kidogo njoo pale kazini kwangu nitakuwa nimekuandalia chakula kitaaamu"

"Ahahahaaaaa.. Nashukuru sana ila siku ya leo sitokuja Kiukweli. Unajua siku nyingi sijaenda kumtembelea Ikene,kwahiyo leo nataka kwenda kumsabahi", alisema Kayumba. Diana akajing'atua kwenye kifua cha Kayumba kisha akajibu "Anhaa sawa Kayumba mpenzi, safari njema acha mimi niwahi kazini"

"Kazi njema Diana mpenzi"

"Ahsanteee", Diana aliondoka huku akiwa na wingi wa furaha, kukubaliwa ombi na Kayumba kilimpelekea ajihisi kama anapaa. Aliona Dunia yote yake.

Nyumbani kwa Ikene Kayumba alifika, alimkuta Ikene akifanya mazoezi ya kuimba. Lakini ghafla zoezi hilo alistisha baada kupokea ugani, aliweka kando gitaa lake akamkaribisha Kayumba kwa tabasamu bashasha "Karibu sana Kayumba, habari za siku nyingi"

"Salama Ikene naona upo unafanya mambo yako sasa", aliitikia Kayumba huku akimpa mkono Ikene na kisha kuketi kwenye sofa.

"Ndio ndio, nipo nafanya mazoezi ya kuweka sauti sawa kwa sababu wiki ijayo nitakuwa natumbuiza kwenye moja ya Hotel hivi ya kifahari", alisema Ikene wakati huo alinyanyuka kwenye sofa na kuisogelea friji.

"Kinywani gani unatumia rafiki yangu", alihoji Ikene.

"Aah nipe maji tu nichambe koo", alijibu Kayumba huku macho yake yakitazma gitaa.

"Aah! Kayumba hapa ni kwako kaka, kuwa huru utakunywaje maji kama rejeta? Sio mbaya nikikusogezea na juisi ya matunda", aliongeza kusema Ikene akitania. Kayumba aliangua kicheko. Punde mbele yake akaletewa maji na juisi ya matunda kisha zogo la hapa na pale likaendelea "Wenzetu mpo vizuri sana kwenye suala nzima la muziki"

"Ahahahah? Unamaisha nini Kayumba! Ujue sijakuelewa", alihoji Ikene. Kayumba kabla hajajibu alikunywa bunda la maji mara moja kisha akasema "Namaanisha nyie wasanii kutoka Nigeria mko mnajua kuimba sana"

"Hahaha Kayumba unanifurahisha sana, vipi wewe unapenda kuimba?.."

"Ndio braza tena tena hata kuimba najitahidi japo sio sana"

"Mmh! Hebu imba kidogo nikusikilize", aliongea Ikene huku akiwa makini kumsikiliza Kayumba kile anacho taraji kukiimba. Naye kabla hajaanza kuimba alikohoa kidogo kuweka sauti sawa kisha akaanza kuimba. Aliimba wimbo mzuri Kayumba, wimbo ambao ulimfanyia Ikene kuchezesha kichwa chake na punde si punde akachukua gitaa yake akapiga nyuzi za mbali, kitendo ambacho kilizidi kuunogesha wimbo huo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Daah! Braza unajua hongera sana", Mara baada kuhitimisha, Ikene alimpongeza Kayumba kwa kuimba wimbo mzuri ambao hakutarajia kama angeimba.

"Ahsante sana", kwa tabasamu bashasha Kayumba alishukuru. Ikene akaongeza kusema "Kaka kuimba unajua sana tena zaidi ya sana ila kasoro kitu kimoja tu. Nacho ni pumzi, jitahidi kufanya mazoezi ya kuweka pumzi ili pindi utakapokuwa unaimba usizidiwe. Na pia wimbo wako huo huo uifanyie mazoezi ndani ya wiki hihii ili wiki ijayo twende wote huko kutumbuiza ", Kayumba alifurahi sana kusikia maneno ya Ikene. Alijiona mtu mwenye bahati na hata asipate picha siku hiyo atakayo kuwa akiimba mbele ya watu wenye pesa zao, matajiri walio amua kwenda kupata burudani.

" Eeh Mungu ni saidie", aliomba Kayumba. Alipofika nyumbani alianza kulifanyia kazi suala lile alilomshauri Ikene, alifanya mazoezi kwa nguvu bila kuchoka lengo ikiwa ni kuacha maajabu kwenye Hotel hiyo ya kifahari.

"Kayumba mpenzi kumbe na wewe unajua kuimba?.", usiku mmoja Diana na Kayumba wakiwa wamejipumzisha kitandani, Diana alimuuliza Kayumba swali hilo.

"Ahahahah", Kayumba aliangua kicheko kisha akajibu "Ndio, unajua ujuzi siku zote hauzeeki. Enzi hizo nikiwa shule nilikuwa naimba, na mimi nilikuwa mtunzi mzuri wa nyimbo shuleni. Na kesho nitaambatana na Ikene kwenda kutumbuiza kwenye Hotel moja hivi ya kifahari"

"Waoow! Kayumba wangu! Ahahahaha ah kweli?..", Diana alifurahi kusikia habari hiyo, alikilaza kichwa chake kwenye kidali cha Kayumba. Wakati huo huo Kayumba akajibu "Ndio! Nikudanganye nifaidike nini?.."

"Aisee Mungu anaanza kukunyooshea mkono wa mafanikio mpenzi wangu. Je, Hotel hiyo inaitwaje?.."

"Ammh! Ukweli hajaniambia"

"Sawa yote kwa yote nakutakia utumbuizaji mwema kipenzi cha roho yangu", alitia baraka Diana kwa mpenzi wake.

Siku iliyofuata ilikuwa siku ya shamla shamla kwa matajiri wapenda burudani, walitambua fika kuwa DFL Hotel kutakuwa na burudani kabambe, na katika wahudhuliaji waliopania kufika kwenye kisima hicho cha burudani Catherine alikuwa ni moja wapo, alipania kufika bila kukosa huku akimuacha mgonjwa wake ndani ingawaje alitamani kuhudhuria naye.

"Edga, nilitamini twende wote ila baki umalize dozi mgonjwa wangu. Siku nyingine tutatoka wote", alisikika akisema Catherine, maneno hayo alikuwa akimwambia Edga ni baada kuruhusiwa kurudi nyumbani, ambapo Catherine aliamua kuishi naye baada Edga kumwambia kuwa maisha yake ya kutanga tanga hana muelekeo maalumu.

"Aah wala usijali dada, mimi nipo tu", alijibu Edga kwa sauti ya chini. Catherine akaona sio vizuri kufurahi peke yake,hatimaye akampigia simu rafiki yake ambaye ni Najrat. Haikuchukuwa muda mrefu Najrat kufika eneo husika,walifurahi mno kwa kula na kunywa huku wakipata muziki mzuri kutoka kwa Ikene. Lakini baada Ikene kuimba kwa muda mrefu,hatimaye akapasa sauti kuwa anataka kumtambulisha msanii nwenzake mpya. Hivyo macho na masikio ya watu wote waliokuwemo mle ndani ni kumuona na kumsikia msanii huyo mpya.."Kayumbaaa njoo mbele utupe burudani" Alipasa sauti Ikene,ghafla mdundo mzuri ukasikika..na punde si punde akaonekana Kayumba! Catherine alishtuka ukiachilia Najrat.





Kayumba akiwa na wingi wa tabasamu alikamata maiki, na kabla hajaanza kuimba alijitambulisha jina lake mbele ya kadamnasi kisha akaanza kuimba. Aliimba wimbo mzuri sana ulioambatana na mdundo mzuri uliopelekea baadhi ya watu waliokuwemo mule ndani kulipuka kwa shangwe huku baadhi yao walifika mbele kumtunza fedha. Catherine alionekana kupigwa na butwaa, alimtazama Kayumba na hata asiyaamini macho yake, wimbo aliokuwa akiimba Kayumba aliukumbuka vema. Ni zamani sana enzi hizo walipokuwa wakihitimu elimu ya msingi, ni wimbo ambao Kayumba alimuimbia Catherine ikiwa kama zawadi. Hakika chozi lilimtoka Catherine, alijuta kile alichomtenda Kayumba, kwani wimbo huo ulimkumbusha mengi sana aliyopitia kipindi kile kijijini. Najrat alistuka kumuona rafiki yake akilia, ila hakutaka kujaji sababu aliamini kuwa huwenda Catherine ameguswa na ule wimbo aliokuwa akiimba Kayumba. Hivyo alitikisa kichwa kisha macho yake akayatupa kule aliposimama Kayumba wakati huo ndani ya kichwa chake akiwaza kuwa baada ya shamla yote kumalizika atafanya jitihada zote za kumtafuta ili aweze kuzungumza naye.

"Leo kila kitu kitaenda sawa", alijisemea Najrat huku akichezesha kichwa chake, wimbo mzuri kutoka kwa Kayumba ukipenya vema kwenye masikio yake. Lakini wakati mrembo Najrat akiwaza suala hilo, upande wa Catherine aliona muda haendi. Aliamini baada ya shughuli nzima kumalizika atapata wasaa wa kuweza kuongea na Kayumba hasa akiamini kuwa hiyo ndiyo itakuwa nafasi pakee ya kumuomba radhi.

Hatimaye Kayumba anamaliza kuimba, makofi yanasikika. Kwa kutumia kitambaa kidogo aina ya leso aliyafuta machozi yake yaliyoshikamana na machozi. Wimbo aliomaliza ulimchoma, naye pia aliyakumbuka mengi aliyofanya na Catherine mpaka pale ilipofika hatua ya kumfukuza mithiri ya mbwa.

"Hongera sana Kayumba", Ikene alimpongeza Kayumba kwa tabasamu bashasha, naye hakuamini kama kweli Kayumba ni mwenye uwezo wa kuimba namna ile.

"Ahsante Ikene", aliitikia Kayumba wakati huo upande mwingine alionekana Catherine akimuita muhudumu aliyepewa jukumu la kusambaza vinywaji na vyakula mule ndani kwenye ukumbi wa kifahari.

"Ndio nikusaidie nini", aliuliza muhudumu huyo huku akiwa ameinamisha kichwa chake karibu na kinywa cha Catherine ili apate kusikia vizuri kile akisemacho.

"Unaona ile meza kule?.."

"Ndio, si ile waliyoketi wasanii?.."

"Eeh ile ile, sasa naomba ukawasikilize. Pesa ipo kwangu chochote watakacho agiza wape nitalipa mimi", aliongea Catherine huku macho yake yakitazama kule alipoketi Kayumba na Ikene. Hima muhudumu alifanya kama alivyoagizwa na Catherine, alikwenda kuwasikiliza. Pasipo kujua ni nani aliyetoa ofa, wawili hao waliagiza kila mmoja alichopenda kula. Ni kawaida kwa hafla kama hiyo wadau kutoa ofa kwa wasanii, hivyo saula hilo halikuweza kumtia shaka Ikene, zaidi akimwambia Kayumba "Huu ndio uzuri wa kukubalika,nakuhakikishia braza Kayumba. Mafanikio yapo mbele yako", Kayumba alifurahi sana kusikia maneno hayo ya Ikene.

"Kula Kayumba kula mwili haujengwi kwa matofali", aliongeza kusema Ikene ilihali Catherine naye ndani ya kichwa chake alikuwa na mengi akiyawaza, mara kadhaa alishusha pumzi na hata asiishe hamu kutazama kule alipoketi Kayumba.

"Laah! Kweli usimdharau mtu, Kayumba leo hii upo sehemu hii ya kifahari? Najuta kukusaliti, nilijisahau Kayumba nikayasahau yale yote iliyonifanya. Ila sasa nimejua kosa langu, Kayumba wangu sipo tayari kukupoteza furaha yangu", aliwaza Catherine, muda huo kwa mbali akionekana Najrat akizipiga hatua kurudi kuketi baada kutoka nje kwa muda wa dakika kadhaa. Alipoketi akafungua mkoba wake akatoa dayari akachana karatasi kisha akaandika namba yake ya simu. Alipomaliza akapasa sauti kumuita muhudumu, naye akatii wito "Samahani kaka, shika hii karatasi nenda ukamkabidhi yule mkaka aliyemaliza kuimba muda mchache uliopita", aliongea Najrat.

"Nani Kayumba?..", alihoji muhudumu huyo ikiwa macho yake yakitazama kule alipoketi Kayumba.

"Eeh huyo huyo", alijibu Najrat, Catherine alistuka kuona kitendo cha Najrat kutuma namba yake ya simu kwa Kayumba. Hapo ndipo akaamini asilimia mia moja kuwa muuza madafu aliyekuwa akimzungumzia siku zote ni Kayumba wake. Kwa jazba Catherine akasema "Najrat, hizo namba umezituma kwa yule mkaka ili iweje sasa?.."

"Nini?", alihoji Najrat akionekana kushangazwa na kile alichokisema Catherine.

"Sikiliza Catherine, wewe ni mwanamke na mimi ni mwanamke. Kama umevutiwa na yule mkaka, basi tambua hata mimi amenivutia ingawa sina maana hiyo?..", aliongeza kusema Najrat kwa sauti ya nyodo.

"Unamaana gani sasa?..", aliuliza Catherine huku akiwa amekasirika. Najrat aliangua kicheko cha dharau kisha akasema "Maana yangu, nataka baadaye anitafute ili nimpongeze kwa nyimbo yake nzuri kama wewe ulivyompongeza kwa kulipia chochote atakacho kula". Catherine hakufurahishwa na hayo maneno aliyoyasema Najrat, kwa dharau aliyarudia huku akiwa amebana pua yake. Alipokwisha kufanya hivyo akaongeza kusema "Unamoyo gani wewe? Najua umempenda na sio unataka kumpa pongezi. Pongezi hata humu humu unaweza kumpongeza kama nilivyofanya mimi na hao wingine walio mtunza fedha"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Ahahahaha", Najrat aliangua kicheko kwa mara nyingine tena kisha akajibu "Catherine vipo vitu viingi sana vya pongezi, huwezi jua nataka kumpongeza nini?..", Catherine alizidi kukereka kwa maneno hayo aliyoongea Najrat, hasira zilimjaa mara dufu. Akasema "We ni mjinga sana Najrat", kwisha kusema hivyo naye aliaandika namba yake ya simu kisha akafanya kama alivyofanya Najrat.

"Daah! Kayumba, mambo mazuri sasa. Yani siku moja tu nyimbo moja tu wadau wanaanza kujileta wenyewe?..", aliongea Ikene akimwambia Kayumba baada kuona karatasi zenye namba zikifuatana. Kayumba alifurahi sana, alijikuta akitamani siku moja aonekane kwenye TV asikike pia kwenye radio ili yule aliyemdharau kisa hana pesa na elimu ajue kuwa maisha ni kama kitabu ilihali kuferi shule sio kuferi maisha. Tumaini hilo la Kayumba limlenga Catherine, na hata asijue kuwa mtu huyo aliyemlenga naye alikuwa ni miongoni mwa wahudhuliaji katika Hotel hiyo ya kifahari,na zaidi amemtumia namba yake ya simu. Pumzi alishusha Kayumba baada kuwaza hayo, ikiwa kwingeneko, Catherine akiwa amekasirika alinyanyuka kwenye kiti kisha akasema "Najrat mwenye kisu kikali ndio atakaye kula nyama", Najrat alipoyasikia maneno hayo aliangua kicheko halafu akajibu "Safi sana Catherine,sasa karibu sana kwenye uwanja wa mapembano"





Mabinti hao waliondoka ndani ya Hotel hiyo kila mmoja akiwa na hasira, walipania kuanzisha vita kali. Vita ya kumgombania Kayumba,kila mmoja alimpenda hasa hasa Najrat aliyevutiwa naye tangu siku ile amuone akisukuma mkokoteni, ikiwa upande wa Catherine alijiaminisha kushinda vita hiyo, alijipa asilimia kubwa kwa sababu hapo awali alikuwa na mahusiano naye.

Hiyo ilikuwa ni siku ya furaha sana kwa Kayumba, hata aliporejea nyumbani alimsimulia Diana mambo yote yalijili kwenye Hotel ile ya kifahari. Diana alifurahi sana, kinywa chake hakikuwa kizito kutoa pongezi kwa mpenzi wake "Hongera sana Kayumba, sasa naona mlango wa mafanikio yako umefunguka"

"Natamani siku moja uwe msanii maarufu hapa nchini na nchi jirani,uonekane kwenye Tv na pia usikike kwenye radio ili yule msaliti wako aone donge, atambue kuwa kuferi shule sio kuferi maisha", aliongeza kusema Diana wakati huo walikuwa kitandani, kichwa chake alikilaza kwenye kidali cha Kayumba. Aliachia tabasamu mwanaume Kayumba, akaivuta pumzi yake kisha akaishusha kwa kasi na kusema "Sio wewe tu Diana, hata mimi natamani sana hicho kitu kitokee. Mungu sio Athumani anasikia kilio changu"

"Ameni, cha muhimu ni kumuomba bila kukoma"

"Etieeh! Haya tutapambana mpenzi wangu"

"Nikwambie kitu Kayumba?.."

"Ndio niambie wala usijali"

"Nimekupongeza ila bado nataka nikupe pongezi kubwa zaidi"

"Mmh, Diana unamaana gani?.."

"Ahahahah, Kayumba. Maana yangu ni hii", kwa kutumia mkono wake Diana akaanza kumpapasa Kayumba kwenye kifua kushuka mpaka chini. Kayumba akajihisi msisimko kunako mwili wake, akajua ni kitu gani anachomanisha Diana. Ndipo naye hakuweza kulemba mwandiko, alijibu mashambuluzi jambo ambalo liliweza kuzua ukimya chumbani. Tendo lilichukuwa takribani nusu saa, wote walikua hoi taabani walilala usingizi mzito mpaka kesho yake asubuhi.

"Habari za asubuhi fundi wa mwili wangu", Diana aliongea baada kuamka na kumkuta Kayumba yupo macho, si kawaida yake Kayumba kuwahi kuamka ila siku hiyo ilikuwa siku tofauti sana. Na yote ilisababishwa na furaha aliyokuwa nayo ndani ya moyo wake.

"Salama Diana", alijibu Kayumba.

"Kayumba mpenzi wangu, wewe ni bonge la mchezaji. Unajua kuwahadaa mabeki wa timu pinzani. Ukweli umenionyesha kitu fulani mechi ya jana usiku. Hakika sifikirii kukuacha katika maisha yangu", Diana alimsifu Kayumba na kisha kuendelea kuapa kutomuacha abadani.

"Ahahahah ah", aliishia kucheka Kayumba.



***BAADA YA WIKI TATU**



Mapenzi ya Kayumba na Diana (Sinsia) yalizidi kukolea, kila mmoja kwa nafasi yake alimuamini mwenzake suala ambalo lilimpelekea kuweka mkakati wa kufunga ndoa ili kuanza kujenga familia.

"Kabisa Kayumba, watoto wa kwenye ndoa huwa wanabaraka zake", aliongea Diana mara baada wote kwa pamoja kukubaliana suala la kufunga ndoa.

"Napenda sana mtoto wetu wa kwanza awe wa kiume", aliongeza kusema Kayumba.

"Mmh wa kike bwana", Diana alijibu.

"Hapana ujue kwa sababau gani nimesema hivyo? Endapo kama atazaliwa mtoto wa kiume nitampa jina la aliyekuwa swahiba wangu,msaka tonge Edga"

"Edga? Anhaa, sawa jina nzuri sana mpenzi wangu", alijibu Diana (Sinsia) ingawa alianza kwa kustuka. Mstuko huo ulimuweka Kayumba katika hali ya sintofahamu, alihisi huwenda Diana anamfahamu Edga ila anaamua kuficha.

"Edga aliwahi kuniambia anadada yake anaitwa Sinsia, na huyu anaitwa Diana ingawaje baadaye akikanusha jina hilo. Kwanini, na nikitugani kinachomstua pindi ninapo litaja jina la Edga?..", ajiuliza Kayumba ndani ya nafsi yake. Kitendo hicho kilimpelekea kupigwa na butwaa kwa sekunde kadhaa kabla ya Diana kumuaga kuwa anaelekea kazini kwani tayari ilikuwa pameshakucha.

" Kazi njema mpenzi wangu ", alisema Kayumba huku akimtazama Diana kwa jicho la tatu ilihali kichwani akiwa na maswali mengi kuhusu yeye na Edga.

"Ipo siku ukweli utabainika tu", baada Diana kuishia zake, Kayumba akajisemea maneno hayo. Muda huo alikuwa ameketi kitandani, ghafla macho yake yakatazama juu kwenye meza. Yakaona simu "Mmmh leo amesahau simu yake?..", alijiuliza Kayumba wakati huo ameishika simu ya Diana,na punde si punde akakumbuka kuwa wiki kadhaa zilizopita alipewa namba pindi alipokuwa kwenye Hotel ile ya kifahari. Hima alizisaka karatasi zile zinye namba, akazipita akaingiza namba kwenye simu kisha akapiga.

"Hello", sauti ya kike iliongea. Kayumba alistuka kidogo kisha akasema "Habari yako, Kayumba hapa sijui nani unaongea"

"Kayumbaaa?..", sauti hiyo ilihoji kwa haraka sana.

"Ndio, wewe ni nani mwenzangu?..", alihoji Kayumba. Sauti hiyo ikajibu "Najua ni vigumu kunikumbuka hata kama nitakutajia jina langu, ila ninacho kuomba kodi taksi uje hapa ulipokuwa ukitumbuiza siku ile"

"Mmh!..", Kayumba aliguna, akatoa simu sikioni akaitazama namba hiyo kisha akairejesha sikioni kwa mara nyingine tena.

"Sawa ngoja nijiandae nije", alijibu Kayumba kwa sauti ya woga.

"Ok, jitahidi basi usiniangushe tafadhali", sauti hiyo ikisisitiza.

"Usijali dada",kwisha kusema hivyo akakata simu. Pumzi alishusha, na sasa akachukuwa karatasi nyingine ambayo nayo ilikuwa imeandikwa namba. Akapiga simu ikaita bila kupokelewa, hakukata tamaa alirudia tena lakini bado mambo yakawa vile vile. Simu iliita tu pasipo kupokelewa. Akaiweka juu ya meza, akajilaza kitandani miguu ikining'inia juu kwenye wigo wa kitanda, kichwa chake kilimuwaza yule mwanadada aliyemuomba wakutane. Ila wakati akiwaza suala hilo, ghafla simu iliita. Alinyanyuka akimchukuwa akaona namba namba ile aliyoipiga muda mchache uliopita ambapo iliita pasipo kupokelewa. Hima Kayumba alibonyeza kitufe cha kijani, akaweka simu sikioni.

"Hello unaongea na Kayumba hapa sijui nani mwenzangu", alisema Kayumba.

"Ooh jamani Kayumba, habari za tangu siku ile ya sherehe..", iliongea sauti hiyo, ilikuwa ni sauti ya Catherine ingawaje Kayumba hakuweza kuitambua.

"Ni njema tu naongea na nani?..", aliendelea kuhoji Kayumba. Catherine akamjibu "Utanijua tu ila ukweli niliupenda mno wimbo wako. Naomba tafadhali nipo chini ya miguu yako tukutane pale pale Hotel ulipokuwa ukitumbuiza", aliduwa kidogo Kayumba baada kusikia mtu huyo wa pili naye ameomba wakutane pale pale aliposema mtu yule wa kwanza. Pumzi alishusha akaachia tabasamu hafifu akakurupuka kitandani akatoka chumbani akaelekea sebuleni wakati huo akiwa ndani ya taulo tayari kwa niaba ya kuelekea kuoga ili ajiandae kuelekea huko kukutana na hao watu. Hakujua ni nani na nani waliyemuhitaji ila tu alihisi huwenda wote hao wakawa wadhamini katika safari yake ya muziki.

Nje ya Hotel ya kifahari, Hotel yenye hadhi ya nyota tano inasimama gari ya ghalama. Gari ya pesa ndefu kama wasemavyo watoto wa mjini, gari ambayo sio rahisi hata kumiliki. Katika gari hiyo anashuka mrembo Najrat akiwa akiwa katika mavazi ya stara kiasi kwamba yaliweza kumpendezesha vema hasa hasa rangi ya ngozi yake isiyokuwa na hata lepe ya ukurutu. Najrat kwa mwendo wa madaha mfano wa twiga atambeavyo alizipiga hatua kuingia kweny ukimbi wa Hotel hiyo huku mkononi akiwa ameshika mkoba wa bei ghali. Aliketi akaagiza kinywaji, akaendelea kuchamba koo wakati huo akimngojea Kayumba. Punde si punde alionekana Catherine naye akitimba mahali hapo. Catherine alistuka kumona Najrat, akaguna kidogo kisha akasema "Umejuaje kama nitakuja huku"

"Ahahahahah.", alicheka kwa dharau Najrat, akavua miwani yake akaweka juu kwenye meza kisha akasema "Hupaswi kujua ila hata mimi nakushangaa kunizukia hapa", Catherine akavuta kiti akakiweka sawa kwenye meza ile ile aliyoketi Najrat, akamkodolea macho na akasema "Ahahahaha, safi vizuri sana nimekukuta hapa Najrat na nadhani leo ndio ile siku ambayo inatakiwa nikutambulishe kwa shemeji yako"

"OK, nangoja kumuona", alijibu Najrat wakati huo akibonyeza simu yake, punde akaweka sikioni kisha akasema "Umefika wapi?.."

"Anhaa sawa nisubiri hapo hapo nje nakuja", Najrat alisimama akazipiga hatua za haraka haraka kuelekea nje. Kayumba alistaajabu sana kumuona Najrat. Alikumbuka vema, alikumbuka kuwa alipata ajari pindi alipokuwa akienda kuonana na mrembo huyo, ikawa sababu ya kupotezana na Edga mchizi wake na kujikuta akidondokea kwenye mikono ya Diana.

"Ni wewe?..", aliuliza Kayumba.

"Ndio ni mimi Kayumba, Najrat. Hivi unanikumbuka?.."

"Ndio nakukumbuka lakini...", kabla Kayumba hajamaliza kuongea alichotaka kusema, Najrat akadakia akasema "Hapa sio mahali sahihi ya kuzungumza na wewe naomba tuingie ndani tafadhali",alisema kwa sauti ya chini Najrat na kisha akamshika mkono Kayumba akaambatana naye kuingia ndani na wakaelekea kwenye meza ile ile aliyoketi Catherine.





Catherine alistuka kumuona Kayumba, aliyakodoa macho yake na wala asiamini kile akionacho.

"Alaah! Najrat ameamua kunizunguka kiaina? Vita hii ya mapenzi amezidi kuikoleza", alijisemea ndani ya nafsi yake huku akiendelea kuwatazama Najrat na Kayumba ambao walionekana kushikana mikono wakijongea pole pole kuelekea mahali alipokaa Catherine. Macho ya Kayumba yalikuwa bize kutazama maandhali ya mule ndani namna ukumbi ulie ulivyokuwa umependeza vema huku watu mbali mbali wakipata chakula, waliokuwemo wazungu, warabu na kila aina ya watu ambao kimuonekano walionekana kuwa ni watu wenye fedha. Aliachia tabasamu Kayumba, na sasa macho yake yalizama mbele kule anakoelekea. Ghafla akasimama, alikunja uso wake kuashiria kukasirishwa na kitu fulani. Akamgeukia Najrat akamkazia macho kisha akasema "Usitake kucheza na akili yangu"

"Unamana gani?..", Najrat aliuliza kwa mshangao. Kabla Kayumba hajamjibu, alishusha pumzi akakumbuka siku ile Catherine alipomtimua kama mbwa, hakuisha hapo zaidi alikumbuka namna alivyomsaidia kwa hatua kadhaa wa kadha lakini mwisho wa siku akaonekana takataka kisa hana kipato wala elimu.

"Umeniita hapa kwa niaba gani?..",alihoji Kayumba huku macho yake yakimuangalia Catherine,ambapo Catherine naye baada kuona Kayumba anamtazama akaachia tabasamu wakati huo akimkonyeza.

"Nina mazungumzo marefu juu yako, kwahiyo hauwezi kuzungumza tukiwa tumesimama. Nakuomba tukakae pale ili tuonge kwa mapana zaidi", alijibu Najrat, Kayumba alikubali japo kwa shingo upande. Akavaa uso wa kauzu, akazipiga hatua mpaka mahali alipokaa Catherine. Walifika, Najrat alimsogezea kiti Kayumba, naye akaketi kisha akamsabahi Catherine "Habari yako mrembo"

"Ni nzuri sijui kwako", alijibu Catherine, Kayumba hakuongeza neno lolote. Bado alionekana kukunja uso, hakutaka Catherine amsemeshe wakati huo huo Najrat akasema "Kayumba, kwanza kabisa ingawa waanifahamu ila sio mbaya saana kuzidi kukumbusha. Naitwa Najrat Nurdin,na huyu ni rafiki yangu ambaye nilisoma naye chuo. Anaitwa Catherine", aliachia tabasamu pana Najrat kisha akamgeukia Catherine na akasema "Catherine rafiki yangu, huyu anaitwa Kayumba.. Aamh siku kadhaa zijazo nitakwambia ukweli uliotukuka baina yake na yangu", alimaliza kwa kicheko kifupi Najrat, alifanya hivyo kumkomoa Catherine kwani alitambua fika kuwa Catherine anamuhitaji Kayumba kwa udi na uvumba, na hata Najrat asijue ya kwamba wawili hao walishawahi kuwa na mahusiano. Catherine alikuwa mpole, alinywea alio haibu kumjibu Najrat ingawaje moyoni mwake alijawa na hasira dhidi yake. Alikunja sura ishara ya hasira, wakati huo Kayumba alionekana kumtazama jicho ngebe na pia asitamani Catherine amuongeleshe. Ni jambo ambalo lilimuumiza moyo Catherine, uvumilivu ulimshinda akamua kuondoka mahala hapo pasipo kuaga.

"Catherine, mbona sasa unaondoka wakati ulisema utanitambulisha kwa shemeji yangu?.", alipasa sauti akauliza kwa kejeri Najrat. Catherine hakumjibu aliendelea na safari yake akitembea haraka haraka. Aliangua kicheko Najrat, na sasa akamgeukia Kayumba na kisha akasema" Najua ni kipindi kirefu sana hatujaonana, na hatimaye tumeonana tena. Habari za siku nyingi "

" Ni njema, na chanzo cha mimi na wewe kupotezana nilipata ajari siku ile ambayo uliniambia nikufuate kwenye Hotel ile", alieleza Kayumba namna ilivyokuwa mpaka ikatokea yeye na Najrat kupotezana.

"Pole sana Kayumba, na kingane nilikuwa sijui kama wewe ni msanii. Hongera sana unajua kuimba"

"Ahahahah, Asante Najrat", Kayumba alijibu akianza kwa kicheko, Najrat alimtazama tu kwa macho yake madogo mazuri mithiri ya goroli. Ukimya mfupi ukatawala akiwaza ni vipi atamuanza Kayumba. Punde vyakula vililetwa pamoja na juisi nzito. Ulikuwa msosi wa nguvu kuwahi Kayumba kuuona.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Karibu chakula Kayumba", kwa sauti nyororo yenye mahaba mazito Najrat alimkalibisha Kayumba. Na hapo ndipo Najrat alipoamua kujitoa muhanga na kuamua kuelezea hisia zake kwa Kayumba. Kayumba alistuka kusikia habari hiyo ya kuhusu mahusiano. Japo Najrat alionekana kuwa msichana mrembo kuliko Diana, ila kamwe hakuwa tayari kuvunja penzi lake na Diana (Sinsia) alimpenda sana na tayari ameshamuweka moyoni.

"Najrat, ni kweli hisia za mtu huwa hazizuiliwi lakini tayari umeshachelewa mama. Moyoni mwangu Diana ndio anaishi kwa sasa", alijibu Kayumba.

"Lakini Kayumba tambua mimi ndio nilianza kukupenda kabla ya huyo Diana!.", aliongea kwa hisia Najrat.

"Ndio hivyo imeshatokea, na zaidi asante kwa chakula chako. Mimi naondoka", alipokwisha kusema hivyo Kayumba alinyanyuka akaondoka. Najrat alipasa sauti kumuita ila Kayumba hakugeuka, alizidi kuzipiga hatua kuondoka ndani ya Hotel hiyo.



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog