Search This Blog

Tuesday, 1 November 2022

NAUZA BIKIRA YANGU - 1

 






IMEANDIKWA NA : BABI D’E CONSCIOUS



*********************************************************************************



Simulizi : Nauza Bikira Yangu
Sehemu Ya Kwanza (1)


 NAUZA BIKIRA YANGU



11/8/1964

Msafara wa magari yapatayo zaidi ya 40 ukiwa unaongozwa na pikipiki za polisi wa usalama wa barabarani, Ukifuatiwa na magari ya polisi kisha magari ya viongozi waandamizi wa nchi, katikati

gari la Rais Elibariki Chalambo Maarufu kama Chalambo Rais wa Jamuhuri ya watu wa KOLO nchi iliyo kaskazini mwa Tanzania. Wananchi wenye matuini na Rais Chalambo walikuwa wamejipanga Barabarani wakiwa na Bendera za nchi hiyo huku wakiimba nyimbo za furaha za kulitukuza taifa la Jamuhuri ya Kolo na Rais wao Chalambo. Rais Chalambo akiwa na mke wake Tclee katika gari la wazi huku akiwapungia wananchi mkono, Masafara unaishia ndani ya uwanja wa Uhuru ulioko katika jiji la Pona moja ya majiji makubwa katika nchi ya Kolo.



Akipokewa na halaiki ya watoto, huku akiwa mwenye furaha anafungwa skafu kisha anakagua Gwaride la Jeshi la wananchi wa Kolo, Kwa mwendo wa kikakamavu anaelekea katika eneo rasmi lililotengwa katka jukwaa kuu anakaa. Mshehereshaji wa Sherehe za Uhuru wa nchi hiyo wa siku hiyo alikuwa ni mwanajeshi wa jeshi la kujenga taifa na mwimbaji wa bendi ya jeshi ya nchi hiyo aitwae Alkad. Kwa mbwembwe na vibwagizo anatoa nafasi kwa Katibu mkuu wa serikali ya Kolo ambae ndiye mwenye jukumu la kutambulisha viongozi mbalimbali wa serikali na viongozi wa mataifa mblimbali waliohudhuria sherehe hizo.

"Naomba sasa nimuite kwenu, Jemedari, Kiongozi, Mnyenyekevu na Mtendaji wa serikali mwenye jukumu la kuwatambulisha viongozi hapa leo, Si mwinine ni Katibu mkuu wa Jamuhuri ya Kolo, Muheshimiwa Suddy Mnyamwezi" Makofi na kelele vintawala.



Kijana mwenye umri kati ya miaka arobini mpaka arobaini n tano aliyevalia suti yake nadhifu ya rangi ya kijivu, Kwa ukakamavu huku uso wake ukipambwa na Tabasamu anasogelea kipaza sauti mkononi akiwa kashika karatasi nyeupe, Akilegeza koo kwa kukohoa kikohozi kidogo anaanza kuongea.

"Muheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya watu wa Kolo, Waheshimiwa viongozi mbalimbali, Waheshimiwa wananchi wa Jamuhuri wa watu wa Kolo, Napenda kuwakaribisha katika sherehe za miaka ishirini na moja toka nchi yetu kupata uhuru na kuchaguliwa kidemokrasia." Suddy anageuka na kuangalia wananchi wakipiga makofi ya nguvu huku wakiwa na nyuso zenye matumaini.

"Naomba nichukue nafasi hii kutambua uwepo wa Mkuu wa majeshi ndani ya jamuhuri ya watu wa Kolo Kanal NGWALI naomba asimame apunge mkono kwa wananchi" Mzee mwenye mvi nyingi kichwani akiwa kavalia mavazi ya Jeshi yenye nyota nyingi mabegani anasimama na kupiga saluti akimuelekea Rais Chalambo kisha anakaa.

"Naomba nimtambulishe kwenu Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya watu wa Kolo Mh, Bony Sadoti," Kijama mwenye mwili wa mazoezi akiwa kavalia kaunda suti nyeusi iliyomkaa vyema anasimama na kupunga mkono kila upande huku akitabasamu, Kelele za kushangiliwa zinasikika.

"Sasa naomba niwasimamishe mawaziri wa wizara mbalimbali katika Jamuhuri ya watu wa Kolo." Kundi la watu waliokaa mstari wa nyuma baada ya mstari wa mbele aliokaa rais, Wanapunga mikono na kuketi.

"Naomba sasa nitambue uwepo wa Rais wa Tanzania, Rais wa Gambia, Rais wa Kenya, Rais wa Uturuki, Rais wa Ufaransa, Rais wa Zimbabwe, Rais wa Nigeria na Rais wa Uganda, Naomba wasimame na kusalimu wananchi wa Jamuhuri ya watu wa Kolo. Kundi la Marais wa nchi mbalimbali linasimama na kupunga mkono huku Kikosi cha brass band cha jeshi kikipiga ala za muziki.

"Wananchi wa Jamuhuri ya watu wa Kolo naomba sasa nimkaribishe Rais wetu Mh Chalambo azungumze nanyi"

Kelele za shangwe na vigelegele zinasikika. Akiwa na sura isiyo na furaha huku akiwa makini kutazama karatasi iliyo mezani kwake Rais Chalambo anasimama na kuanza kuongea.

"Mlinichagua ili niwatumikie kwa uaminifu, Na leo ikiwa ni siku muhimu kwa Tiafa letu, Baba zetu na babu zetu walipigana na kufa kwa ajili ya nchi yetu, Maelfu ya ndugu zetu walikufa kwa ajili ya kupigania uhuru na nchi hii iwe huru, na tarehe kama ya leo miaka ishirini iliyopita wakafanikiwa kuikomboa nchi hii katika mikono ya wakoloni, Leo nataka kuitoa nchi yenu katika mikono ya watu wachache" Kimya kinatawala, Mawaziri wanaonekana wakiangaliana, Mkuu wa Jeshi kanal Ngwali anaonekana yuko makini kuandika ujumbe katika sinu yake ya kiganjani. Kwa sauti isiyo na mzaha Rais Chalambo anaendelea kuzungumza.

"Mimi nikiwa kama Amiri Jeshi wa Jamuhuri ya watu wa Kolo na Rais niliyechaguliwa kwa kura za wananchi wa Jamuhuri ya watu wa Kolo natangaza Rasmi Baraza la Mawaziri limevunjwa na Jeshi liko chini yangu na Hakuna Mkuu wa Majeshi namaanisha Kanal Ngali si kiongozi wa Jeshi mpaka pale nitakapotangaza Rasmi" Maamuzi yenye maneno ya kuamrisha yalimtoka Rais Chalambo na kupokewa na sauti za Kushangilia toka kwa Wananchi wakikubaliana na Maamuzi ya Rais wao. Mawaziri walisimama na kuondoka meza kuu huku Mkuu wa Majeshi akivua Mkanda, Kofia na Shatu lenye nyota za jeshi kisha anaweka juu ya kiti na kuondoka.

"Ni bora kubaki na watu wachache watakao tumikia nchi na wananchi kwa uadilifu kuliko kuwa na kundi kubwa la wanyonyaji natangaza Rasmi nchi hii sasa ni huru kwa mara ya pili." Rais Chalambo aliongea kwa sauti ya kishujaa iliyopokewa kwa kelele za shangwe toka kwa wananchi wake. Mizinga na Fataki vilipigwa juu kama ishara ya kufunguliwa kwa sherehe za uhuru wa nchi hiyo.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

********** ************

Katika chumba chenye mwanga hafifu mbele ya meza ya Duara kundi dogo la watu waliokaa katika viti wakiwa na nyuso zenye hasira na mawazo tele walikua wakijadili jambo kwa umakini.

"Hii haiwezekani, Tumuweke sisi katika nafasi ile leo atuaibishe mbele ya wananchi, This is too much" Ngwali alizungumza kwa jazba huku akigongagonga meza kwa ngumi.

"Mkuu ni vyema tukapanga chakufanya maana hili jambo limemuumiza kila mmoja wetu" Paul Bona waziri wa mambo ya nje alizungumza huku akifunbata mikono yake kama anaomba usikivu.

"Mimi napendekeza Tugomee maamuzi yake sababu sisi ni wengi hawezi kutushinda?" Rosemary Antony waziri wa Fedha alitoa mawazo yake.

"Rose hilo wazo lako litapingana na Katiba, Katiba inasema Rais ndiye mwenye mamlaka ya kuvunja Baraza la mawaziri na pia ndiye mwenye mamlaka ya kuajiri na kufukuza viongozi wa jeshi" Waziri Mkuu alijibu huku akiinamisha kichwa chini kwa kukata tamaa.

"Jamani mimi ninawazo, Huyu Rais wetu anapenda sana wanawake mnaonaje tukamtafutia mwanamke kisha tunamtengenezea skendo tunaitoa katika magazeti na tv tena Mh Deogratias ana magazeti na mimi nina Tv mbili vinatutosha kumchafua, Kwa hiyo skendo tutakua tumepandikiza chuki dhidi yake kwa wananchi halafu tunaanzisha vuguvugu la kumshinikiza ajiuzulu akijiuzulu uchaguzi unafanyika tunamuweka mtu wetu" Waziri wa sheria ndugu Abdallah ally alitoa wazo lililopingwa na Agness Todi Naibu waziri wa Afya.

"Hilo wazo lako si sahihi kumbukeni tukimshirikisha mwanamke mwingine zaidi yetu itakua shida tena ambaye hajaathirika na hili tatizo kweli hilo wazo lako ni zuri ila ni gumu kulitekeleza maana hapo ni lazima washirikishwe na waandishi wa habari huoni hiyo ni hatari?"

"Sasa Tufanyaje" Sauti ya kukata tamaa ilimtoka Ngwali.

Salomenyo chaloo waziri wa ulinzi aliyekua kainamisha kichwa chake chini akiwa kimya anainua kichwa na kuchomoa bastola yake katika pochi na kuruka mpaka mbele na kuwaweka wenzake chini ya ulinzi.

"Laleni chini pumbavuuuuuu" Sauti ya ukali toka kwa Salomenyo inawachanganya na kulala chini kwa woga, Salomenyo anapiga risasi katika ukuta na kurudi kukaa katika kiti chake na kuinamisha kichwa chini. Zinapita dakika kadhaa wale viongozi wanainuka kwa woga huku wakishangaa Salomenyo kakaa kwenye kiti kainamisha kichwa chini kama alivyokuwa mwanzo.

"Hivyo ndivyo tutakavyomdhibiti huyu Rais wenu" Salomenyo aliongea huku kainamisha kichwa chini.

"Sijakuelewa mheshimiwa" Naibu waziri wa Afya Agness Todi alijibu kwa woga.

"Sikilizeni hapa dawa ni kumuua huyu rais kama ninyi mlivyolala chini ndivyo atakavyovamiwa na risasi ziutawanye ubongo wake atuachie nchi yetu yeye aende na uzalendo wake" Salomenyo alijibu kwa sauti ya kutetemesha iliyopokewa na kauli moja toka kwa Ngwali.

"Geneous"

"Sasa nani atafanya kazi hiyo?"swali kutoka kwa Paul Bona lilizua mjadala mrefu na maamuzi yakatolewa kazi apewe mwanadada machachari asiyeogopa kuua na ni mwanajeshi mwenye shabaha mwenye Cheo cha ukoplo latika Jeshi la Wananchi wa Jamuhuri ya watu wa Kolo si mwingine ni Chiku. Kazi ilitakiwa kufanywa haraka kabla ya sherehe za uhuru kumalizika. Chiku Tayari alikua mbele ya meza yenye viongozi wapatao nane na ahadi ya kupewa urais pindi atakapokamilisha kazi hiyo ilikua ikiutekenya moyo wake na kumpandisha morali wa kukamilisha kazi haraka ili awe Rais wa Kolo.



Bunduki yake aina ya SMG iliyojaa Risasi ikiwa begani, Kombati ya Rangi ya khaki ikiwa imemkaa vyema miwani ya kuzuia Jua na Soksi za kuzuia mikono zikiwa zimevikwa vyema katika mikono yake, Akiwa juu ya pikipiki safari ya kuelekea njia Panda ya kuelekea Toraa mji mdogo wa nchi ya kolo wenye vivutio vingi vya utalii na Machimbo ya madini ghali duniani ya Ramnet na njia ya kuelekea ikulu ya Kolo iliyo pembezoni mwa jiji la Pona.

Breki za pikipiki zilifungiwa mbele ya jumba kuu kuu linalotazamana na barabara hiyi, Chiku akiwa na bubduki yake akatafuta eneo zuri na kukaa huku akivuta sigara taratibu mawazo yake yakifikiria kiti cha urais alichoahidiwa, Sauti za ving'ora ndizo zilimshtua na kukaa vyema huku silaha yake ikiwa mkononi, Utaalamu wake wa kulenga vitu vilivyo mbali ndio uliomfanya kuwa na uhakika wa kukamilisha kazi kwa urahisi. Baada ya pikipiki na magari machache kupita msafara haukua mrefu kwa kuwa haukua na msururu wa mawaziri kama mwanzo macho ya Chiku yakatua katika Gari la wazi alilo[akia Rais na Mkewe.

"Ladies First"

Ni kauli aliyotamka chiku na kuvuta kitufe cha kufyatulia risasi akiwa kamlenga vyema mke wa Rais Chalambo, Bi. Tclee.



********** **************





Wakiwa katikati ya msitu wa pinar del rio ulioko cuba's western katika nchi ya Cuba, Makomandoo wa nne kati ya makomandoo kumi na tano wakiwemo makomandoo saba kati yao wakiwa wametoka katika nchi ya Kolo, Ni zaidi ya miezi nane imekwisha wakihangaika kutoka katika msitu huo wenye simba wengi na nyoka wenye sumu kali aina ya Kobra, Kisu na bastola yenye risasi tatu tu ndivyo vitu pekee walivyopewa kujilinda kwndani ya msitu huo, Mpaka kufika wakati huo makomandoo kumi na mbili walikuwa wameshakufa kwa kuliwa na simba huku wengine wakiumwa na nyoka na wengine wakifa kwa njaa. Ni Ismaeel ahmed kutoka Misri, Berno Mlay kutoka Jamuhuri ya watu wa Kolo na Osi Inieka kutoka Nigeria ndio makomandoo pekee waliobaki katika msitu huo. Damu nyingi zikiwa zinamvuja Osi katika mguu wake wa kulia baada ya kuvamiwa na Simba Risasi yake moja iliyo katika bunduki ndiyo iliyomsambaratisha simba aliyekua kashikilia mguu ule. Akiwa chini ya mti mkubwa kiza kimetawala kwa kutumia tochi aliyoivaa kichwani Macho yake yakakutana na simba mkubwa akija kumfuata alipo, Kwa haraka akajivuta na kushika mti huku akijitahidi kupandisha mguu ili apande ule mti, Maumivu makali kutoka katika lile jeraha yalimrudisha chini na kukutana na kinywa cha Simba na kuruhusu meno makali kushika mfupa wa mguu ule na kuuchana katikati, Kelele kubwa kutoka kwa Osi ilimshtua Berno na kupapasa kisu chake kama kiko sawa akaamka na kujishika vizuri akiwa juu ya mti alipojiegesha katika tawi moja kubwa lililolala kama kitanda. Mngurumo wa simba ulimfanya kujishika vizuri huku akijizuia kwa majani ili asiweze kuona chini, Kupitia upenyo mdogo alishuhudia Simba mkubwa akiwa anavuta mwili wa Osi ukiwa umetapakaa Damu mpaka katika eneo la wazi lenye watoto watano wa simba wakaanza kushambulia ule mwili.

"Dah haya sasa ni mateso ndiyo mafunzo gani haya" Berno aliongea mwenyewe huku akiogopa sauti yake iliyokua akijirudia masikioni mwake.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Huyu ndiye Berno komandoo pekee aliyefuzu mafunzo ya hatari ya ujasusi katika nchi ya Cuba, Ugomvi mkubwa kati ya Serikali ya Africando nchi yenye fedha nyingi na inayosaidia nchi nyingi za afrika iliyo kusini mwa nchi ya Kolo ilivunja uhusiano na Jamuhuri ya watu wa Kolo sababu ya nchi hii kukataa Berno kwenda kufanya kazi katika kitengo cha ujasusi cha nchi hiyo ndicho kitu kilichopelekea Africando kusitisha misaada yake katika nchi ya Kolo baada ya Rais Chalambo kukataa ofa ya Makomandoo kumi kutoka Africando wabadilishane kwa komandoo mmoja tu ambaye ni Berno. Madini ya Ramnet pekee yalitosha kuendesha uchumi wa nchi ya Kolo. Kazi ya kulinda usalama wa nchi na Rais aliyopewa Berno ilimuwezesha kuishi popote alipotaka na kupata huduma yeyote bure ndani ya nchi ya Kolo kwa kutumia G3 Card. Ni Card ambayo anaweza kuchukua kiasi chochote cha fedha katika benki yeyote.

Akiwa katikati ya wananchi ndani ya uwanja wa Uhuru, Jua kali ndilo lililomkimbiza na kuamua kuelekea nje na kutafuta maji, Kila duka aliloenda hakupata huduma kwa kuwa lilikua limefungwa. Mpaka Rais anafunga sherehe na kutoka Tayari Berno alikua katembea umbali mrefu sana.



Mwanamke aliyepaki pikipiki kilometa chache kutoka katika kibaraza cha duka aliliposimama Berno alimvutia na kuhamisha macho yake kwa binti yule. Wasiwasi wa binti yule na kutazama saa mara kwa mara kulimfanya Berno ahisi tatizo na kukaa vyema huku bastola yake aina ya Rivolvo yenye kiwambo cha kuzuia Risasi ikiwa kiunoni huku mkono wake ukilegeza pochi ya kuhifandia bastola ili kuifanya itoke kwa haraka pindi itakapohitajika kufanya kazi. Kama mawazo yake yalivyomwambia ndicho kilichotokea. "Watu wabaya wote duniani huwa na wasiwasi kabla ya kutimiza adhma yao na baada ya kutimiza na hiyo ndiyo njia mojawapo ya kumtambua adui" kauli ya mkufunzi wake Convickie scochxic raia wa Urusi ndiyo ilimfanya Berno atabasamu na kutaka kujua mwisho wa Yule binti.



Baada ya Msafara wa Rais kutokea Chiku akimlenga vyema mke wa Rais Chalambo bi Tclee Jicho la Chiku lilitua kwa kijana aliyesimama pembeni ya kibaraza cha Duka akijifanya haangalii kule alipo, Kama umeme Mdomo wa Bunduki ukahama na Risasi ikaanza kusafiri kutoka katoka chemba ya bunduki na kutokea katika mdomo wa SMG mlio mkubwa ulisikia ambao Berno hakuusikia huku akidondokewa na Tone kubwa la damu na kufanya macho yake kupoteza nguvu ya kuona na kudondoka chini, akiwa juu ya pikipiki Chiku alizungusha pikipiki kama wafanyavyo waendeshaji wa mashindano ya pikipiki na kuingia katika barabara ya vumbi huku akikimbizwa na pikipiki nyingi za polisi, Kwa umahiri wa kucheza na pikipiki tayari alikua mbele ya msafara na Risasi zisizopungua kumi zilikua zimekutana na mwili wa Rais Chalambo pamojba na mkewe huku wakiwa wamekumbatiana na wakati huo Tayari Chiku alikua amekwishatoweka eneo hilo.



******** ***********

Habari ya Rais wa Jamuhuri ya watu wa Kolo, Mkewe Tclee na Jasusi wa kimataifa Berno kuuawa kwa risasi zilienea kama upepo katika nchi ya Kolo na kutoka katoka nje ya mipaka ya nchi hiyo na kusambaa nchi nzima, Vilio vilitawala kila mahali huku wananchi wakitupia lawama nchi ya Africando na kuwahisi kama wahusika wa mauaji yale kutokana na mgogoro uliopo baini ya nchi hizo mbili sababu ikiwa ni Berno, Kifo cha kizembe alichokutana nacho Berno kilimsikitisha kila mtu na kushangazwa komandoo kama Berno kuuawa kwa risasi tena moja tu na bila kujitetea huku akikutwa na bastola yake kiunoni. Wakati watu wakilia na kujadili tukio lililotokea Saa mbili zilizopita ndani ya chumba kipana kundi la watu wachache walikua wakipongezana kwa makakti mkubwa uliofanikisha kuondolewa duniani kwa rais Kolo.



Baada ya chiku kufanya kazi aliyoagizwa wazo la kwenda katika mto alji ambapo hokaa wahuni wengi na kuvuta bangi lilikua sahihi, Kichwa chake kilikua kikiwaza urais wa nchi na alihitaji avute bangi kabla ya kwenda kukabidhiwa madaraka. Akiwa kakaa pembeni ya jiwe akivuta bangi huku akipuliza moshi juu alianza kuwafikiria watu waliompa kazi, Akatikisa kichwa na kubeba mtutu wake wa bunduki na kuongezea Risasi katika eneo la kuweka risasi akaondoka taratibu huku akitelekeza ile pikipiki pale mtoni.



Sauti ya mlango kugongwa ilizima vicheko vya viongozi na maafisa wa ngazi za juu wa nchi ya Kolo waliokua wakinywa na kufurahia kazi nzito aliyofanya Chiku. Macho yao yalikua yakitazama mlango uliogongwa, Ghafla ukasukumwa mguu wenye buti kubwa la jeshi ukatangulia sura ya Chiku ikatokeza, Makofi na sauti za kushangilia kwa kumpongeza Chiku vikasikika toka kwa wale viongozi. Kanali Ngwali akiwa na sura ya Tabasamu akatembea taratibu kumfuata chiku na kumkumbatia. Mlio mkubwa wa Risasi ukasikika kwa hamaki tayari kanali Ngwali alikua chini huku akivuja Damu macho ya Chiku yakiwa na rangi nyekundu kama yamevujia damu kwa ndani yalifumbwa huku akiruhusu Risasi kutoka katika ile Bunduki ndani ya dakika moja Tayari Risasi 30 toka katika ile bunduki zilikua zimewalaza viongozi wote chini. Chiku akafumbua macho na kukutana na dimbwi la Damu huku viongozi wote waliompa kazi wakiwa wamelala usingizi wa milele. Akitikisa kichwa kukubali kile alichokitenda alijikuta akitamka.

"Yes Iam a President of this country"



*********** ***********





Hofu, hofu, Hofu ndicho kitu kilichoikumba nchi ya Jamuhuri ya watu wa Kolo, Vifo vya viongozi zaidi ya kumi na moja kwa siku moja viliwaumiza kichwa wakuu wa jeshi la polisi, Kikao cha siri kilikua kikiendelea kutafuta njia ya kumtambua Muuaji, Kilichowaumiza kichwa Muuaji alikua katoweka na kichwa cha mkuu wa majeshi kanali Ngwali.

Wananchi walikua wamechachamaa huku wakishinikiza jeshi la nchi hiyo kuingia vitani kuipiga nchi ya Africando. Kutokana na mgogoro ulioikumba nchi yao na nchiyo uliopelekea kusitisha uhusiano wao sababu tu ya Komandoo Berno ambaye kwa wakati huo alikua tayari ni maiti. Kelele zile za Raia waliokuwa wamekusanyika nje ya wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa. Kelele za wananchi zilizidi kuongezeka na kutengeneza sauti kubwa. Baada ya saa moja tokea vifo vile kutokea Tayari wananchi zaidi ya laki moja walikua wamevamia eneo hilo huku vurugu za kurusha mawe na kuvunja ofisi za watu zilizoko pembezoni mwa ofisi za wizara hiyo. Maamuzi ya kutuma kikosi cha kutuliza Ghasia ndiyo yalitolewa na Tayari mamia ya askari walikua wakiwadhibiti Raia waliokuwa wametanda kila kona. kwa kutumia kipaza sauti askari wa kutuliza ghasia walikua wakiwatahadharisha wananchi kuacha fujo na kurudi katika makazi yao kuliachia jeshi kuweza kufanya maamuzi, Sauti ile ilikua kama wimbo wa mwanamuziki wa Tanzania aitwae Mr. Nice uliokua ukiimbwa na watoto haukua na maana yeyote kwa wakati huo. Ndivyo wananchi walikua wakipuuza amri hiyo na kuanzisha uadui mkubwa na askari wale hapo ndipo mabomu ya machozi yalianza kurushwa kuwatawanya Raia. Tayari nchi yenye Amani, Nchi iliyokuwa chini ya utawala wa kidemokrasia ilikua imekwishaingia katika vita ya wenyewe kwa wenyewe. Kelele za vilio vya watoto na kinamama na msongamano mkubwa uliosababisha watu kukanyagana na kuibua vifo vya watu katika tukio lile kilizidisha hasira kwa wananchi wengine na kuongeza bidii ya kuwarushia mawe askari wale.

********** **********

Itonyo kambi kubwa ya Jeshi la Wananchi wa Jamuhuri yn wananchi wa Ngwali, Ni kambi iliyo na wanajeshi tegemezi wa Jeshi hilo, Ndani ya chumba cha mawasiliano mwanamke aliyetapakaa damu huku mkononi kashika kichwa cha Kanali Ngwali na mkono mwingine akiwa kakamata Bunduki yake alikua akikat a mawasiliano ya nchi hiyo ya anga na simu za upepo ambayo yalikua yakiunganishwa kwa fiuzi kubwa iliyo ndani ya chumba cha mawasiliano cha jeshi hilo. Tayari nchi nzima kulikua hakuna mawasiliano na king'ora cha kutoa taarifa ya kukutana katika uwanja wa Damu uwanja unaotumiwa na wanajeshi wa kambi ya Itonyo kupeana taarifa za Hatari.

Wanajeshi zaidi ya laki moja wakiwa na maswali vichwani mwao walikua wamejipanga katika uwanja huo. Hakukua na dalili za kiongozi yeyote kuwa ametembelea ndani ya kambi hiyo kama kawaida wanavyoitwaga katika uwanja huo. Maswali yalizidi kuwasonga huku kila mmoja akifikiria lake. Mwanamke asiye na mzaha na aliye na sura ya upole akiwa kakamata kichwa cha mtu vyema alijitokeza mbele ya uwanja ule na kuzungumza kwa sauti ya kikakamavu iliyojaa amri.

"Nchi iko chini ya utawala wa kijeshi na kuanzia sasa mtapokea amri kutoka kwangu, Na kuanzia sasa nimevunja vyeo vyote katika jeshi hili na cheo cha juu kitakua cha koplo ambaye ndiye mimi"

Chiku aliongea kwa msisitizo uliojenga woga kwa wanajeshi huku wakitolea macho kichwa cha aliyekua mkubwa wao enzi za uhai wake, Kanali Ngwali.

"Sasa kila platoon ikakae katika eneo lake na msimamizi mkuu wa store ya silaha awapatie kila mwanajeshi silaha tayari kwa kwenda uraiani kulinda amani ya nchi, Ndani ya masaa ishirini na nne nataka wananchi wote wawe ndani na watapokea amri kutoka kwangu nini kifanyike" Maelezo ya Chiku yalizidi kuwafanya wanajeshi kufanya utekelezaji, Huku simu pekee ya jeshi ikitumika kutoa amri katika kambi nyingine za jeshi nchi nzima kuhusu amri iliyotolewa na Amiri jeshi mkuu mpya wa Nchi ya Jamuhuri ya watu wa Kolo.

Ndani ya nusu saa tayari wanajeshi walikua wamekwisha sambaa kila eneo na hakukua na mwananchi hata mmoja aliyekua nje huku mawasiliano nchi nzima yakiwa yamekatika.



Ni siku ya pili hakuna kinachofanyika ndani ya nchi ya Kolo, Wananchi hawakuruhusiwa kutoka nje na kufanya shughuli zao za kawaida, Wanajeshi walio na mitutu ya bunduki walikua wakirandaranda katika maeneo ya nchi hiyo. Chiku akiwa ndani ya ikulu ya Kolo akigusa kila kitu humo ndani pasipo kujua ni nini afanye, Wazo la kuja kupinduliwa na ndugu wa Viongozi aliowaua ndilo liligonga ubongo wake na kusonya kwa nguvu, Tayari wanajeshi ishirini wenye mitutu ya bunduki mikononi mwao walikua wamesimama mbele ya Chiku kupokea Amri.

"Kateketezeni Familia za hawa viongozi wote niliowachinja kwa SMG msibakize hata Panya katika nyumba zao" Amri ilitoka kwa Rais Chiku, Ilipokewa kwa sauti za utekelezaji kutoka kwa wanajeshi wale na kuondoka kwenda kutimiza agizo.



***********************

Ni siku ya pili tokea wasikie uvumi wa kuuawa kwa Mama yao, Colins na Coleth watoto mapacha waliokua wamekaa katika kochi huku wamekumbatiwa na Dada yao wa kazi mlezi ambaye aliyetumia muda mwingi kuwatunza ndani ya jumba la kifahari la waziri wa Fedha wa Jamuhuri ya watu wa Kolo, Bi. Rosemary Antony. Kishindo cha kugongwa kwa mlango bila mpangilio kilimshtua Tusmo dada wa kazi wa Bi Rosemary na kumfanya ainuke na kuelekea jikoni kuchukua kisu ili akabiliane na tatizo lolote litakalojitokeza.

Kitendo cha Tusmo kutokomea jikoni kilifuatia na kuvunjwa kwa mlango wanajeshi wapatao kumi waliingia ndani na kuutana na nyuso za watoto wawili wazuri wenye muonekano wa watoto wenye malezi bora, Kwa kutumia Dirisha la kupitishia Chakula Tusmo aliweza kushuhudia Kundi la Wanajeshi walioshikilia mitutu ya bunduki, Kwa hofu akajificha nyuma ya kabati la vyombo la pale jikoni ambapo alishtushwa na milio ya risasi mfululizo huku ikiambatana na vilio kutoka kwa watoto wale na baadae kukawa na ukimya.

Sauti ya mtu kuja jikoni alipojificha ilimtia hofu na kubana pumzi ili asisikike Yule mwanajeshi aliangaza huku na kule kisha akatoka nje huku akiwaashiria wenzake waondoke. Tukio lile lilimchanganya akili Tusmo kwa kupitia mlango wa nyuma akatoka na kuanza kukimbia kuelekea mashariki mwa nyumba ile. Wingi wa wanajeshi waliotanda barabarani katika kila kona ya mtaa ulimzidisha hofu na kujilaza katika mtaro wa Daraja kwa lengo la kujinusuru na kifo.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

********** *************

Madini ya gramnet ndiyo yaliipa tamaa serikali ya nchi ya Southen Sea nchi iliyopakana na bahari nyekundu, Utafiti wa wataalamu wao waliofanya miaka kumi iliyopita katika nchi ya Jamuhuri ya watu wa Kolo na kugundua shehena kubwa ya madini ya Gramet ndiyo yaliwachanganya akili. Mpango kabambe wa kumtuma mtu wao ili aanzishe chama cha siasa cha Democracy Movement na kumuweka kiongozi wao ili aje kuwa Rais na nchi hiyo kupata njia nyepesi ya kujizolea utajiri mkubwa ulio chini ya ardhi ya nchi hiyo bila kikwazo. David Mwanyambo mwana diplomasia mwenye shahada ya mambo ya jamii akiwa chini ya mwamvuli wa kanisa la Free Gospal Church aliwasili nchini Kolo kwa kazi moja tu ya kuhakikisha anatumia watu kuanzisha chama na kusimamisha mtu wanayemtaka ili waweze kuvuna mali iliyo katika ardhi ya Kolo, Kichwani kwake ilikua ni kutimiza jambo lile kwa muda mfupi ziadi.



Umaarufu wa kanisa la Free Gospal Church ulikua kama upepo na kuenea eneo kubwa la nchi ya Kolo, Jina la Father David lilikua na kupelekea Rais wa kipindi hicho aliyeitwa Antony Deleree kumuamini na kumpa nafasi ya kufanya mafunzo ya dini katika idara za serikali. Nafasi hiyo ndiyo aliyokua akiiwaza kila kukicha David Mwanyambo au father David kama watu walivyokua wakimuita, Mtandao mkubwa aliojiengenezea wakati anafanya semina za mafunzo ya dini katika idara za serikali ulifanya kazi yake kuwa nyepesi zaidi.

Uchu wa madaraka wa Antony Deleree wa kutaka kubadili kipengele cha Rais kukaa kwa miaka nane madarakani na kumpa mamlaka ya kuendelea kuongoza ndicho kilikua kigezo kikubwa cha David kushawishi baadhi ya viondozi kuanzisha chama kitakachowakomboa. Kwa kutumia maandiko ya kwenye Biblia na mifano ya manabii Father David alijenga chuki katika Mioyo ya Vijana watatu Gerald, Eminash na Deodati kuanzisha chama cha siasa. Kwa kuwa Father David alitambulika kama mdhamini wa chama hicho na mshauri taratibu za usajili wa chama hicho hazikua na ugumu ndani ya miezi miwili Tayari chama cha Democracy Movement kilikua kinatambulika kisheria chini ya mwenyekiti wao Deodati.

Mikutano ya kupinga hoja ya Rais Antony Deleree ilikua ikiendelea na kuhamasisha vijana walio mashulena ni vyuoni kujiunga na chama chao kitakacholeta ukombozi. Hoja ya Rais ilikosa nguvu mpaka kufikia Kumalizika kwa Muda wake hoja yake ilikua bado haijapita. hapo ndipo kipenga cha uchaguzi kilipopulizwa. Vyama vinne vilivyochukua Fomu ya kugombea kiti cha urais ndivyo pekee vilithibitisha nia yao. Huku vikiwa vyama viwili kati ya hivyo vikiwa ndio vina nguvu, Ambavyo ni Democracy Movement na The revolution huku vyama viwili vingine ambavyo ni New Democracy na Youth Repulican vikiwa vinajikongoja.



********** *************

Mkutano wa siri uliokua ukiendelea ndani ya Hoteli ya Adele juu ya mikakati ya chama cha The Revolution na kuchagua Kiongozi atakayesimama kama Mgombea Urais, Matajiri wapatao Tisa wanaojiita L9 au Lord nine walikua wamekaa katika meza kubwa ili kupitisha jina la Mgombea Urais wa chama hicho ambaye atatokana na majina mawili yaliyopendekezwa ambayo ni Didas Thomas ambaye ni muhadhiri wa Chuo kikuu cha Adis kilichoko katika jiji la Stone kaskazini mwa nchi ya Kolo, Uhodari wake wa kuzungumza na kujibu maswali ndio ulimfanya apendekezwe kuwa mgombea wa nafasi ya Urais wa nchi hiyo na jina la pili likiwa ni Elibariki Chalambo Mchambuzi wa mambo ya siasa barani Afrika na Mshauri wa Uchumi wa serikali ya Rais anayemaliza muda wake Antony Deleree. Vuta nikuvute ya nani awe mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama cha The Revolution ilimalizika kwa maamuzi ya pamoja kuwa Elibariki Chalambo akabidhiwe mikoba ya kuwania kiti hicho. Akizungumza kama mwenyekiti wa kikao hicho Mr Ngwali tajiri anayemiliki kiwanda kikubwa cha kutengeneza mafurudumu ya magari na mmiliki wa kampuni kubwa ya ujenzi wa barabara alisimama na kutangaza jina hilo mbele ya wenzake kauli iliyopokewa na sauti za makofi.

"Ndugu Abdallah Ally wewe na Deogratias mtatumia vyombo vya habari vyenu ipasavyo kuhakikisha mnamjenga mgombea wetu na ni laazima ashinde ili atusikilize sisi na biashara zetu ziendelee" Mr. Ngwali alitoa majukumu kwa kila mmoja aliyekaa katika kikao kile cha L9.

"Sasa kesho tutamtangaza Mgombea wetu na mkumbuke tuna siku miamoja na ishirini tu kabla ya uchaguzi mkuu tutumie hizo siku kuhakikisha Chalambo anakua Rais wa nchi hii" Mr. Ngwali alimaliza kisha akafunga kikao kile cha siri kila mmoja akatoka na kuondoka ndani ya chumba kile cha hoteli.



*********** ************



Hakuna mtu ambaye alikua hamfahamu mfanyabiashara maarufu ndani ya jamuhuri ya watu wa Kolo aitwae Lord Brown, Utajiri wake unaokadiriwa kufikia bajeti ya miaka mitatu ya Serikali ya Kolo ndio uliomfanya aheshimike na kila mtu. Akiwa anamiliki kiwanda kikubwa cha kusindika maziwa kinachokadiriwa kulisha nchi zaidi ya nne barani Africa, Meli zaidi ya arobaini zinazofanya safari nchi mbalimbali huku meli kumi kati ya hizo zikiwa ni za moizigo. Uwezo wake huo ulisababisha kupokea wageni mbalimbali waliohitaji misaada. Ukarimu wake na moyo wa kujitolea ulimjengea jina kubwa sana katika nchi ya Kolo.



Akiwa anaishi katika jumba kubwa sana lililopo pembezoni mwa msitu wake wa Trotoro ulioko maili miambili nje kidogo mwa jiji la Pona katika mji mdogo uitwao West state, Jumba la kifahari lenye wafanyakazi zaidi ya miambili wote wakiwa ni wakiume na ni nadhifu kama wafanyakazi wa ndege ya rais. Akiwa na miaka sitini na tano Lord Brown hakuwahi kuwa na mke mara baada ya kutoka Gerezani miaka ishirini iliyopita na kuamua kumfukuza mkewe Linda, Hapo ndipo alipoanza maisha mapya huku akiwa busy kusimamia biashara yake na kutoruhusu mwanamke awe karibu yake. Zawadi mbali alizokua akipokea toka kwa wasichana wengi ili kumnasa kimapenzi zilikua haziishi katika lango la nyumba yake ya kifahari. Hakuna alichokosa zaidi ya kitu kimoja tu alichokua akiwaza ni kupata heshima nje ya mipaka ya nchi yake. Lord Brown huyu ndiye mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha Democracy Movement ambaye alikua akiwaumiza vichwa matajiri Tisa waliomsimamisha Chalambo katika kinyang'anyiro cha urais. Wananchi wa Jamuhuri ya watu wa Kolo walichanganyikiwa kwa furaha baada ya kusikia Lord Brown anagombea urais huku wengi wao wakitabiri neema kubwa kuikumba Jamuhuri ya watu wa Kolo iwapo tu Lord Brown atakua Rais.



Meli za mizigo za Rais Mtarajiwa Lord Brown zilikua zikishusha kontena zenye vitambaa na kanga zenye picha ya Lord Brown na maneno ya Faraja yanayoashiria ukombozi pindi wananchi watamchagua kuwa Rais. Kila mahali jina la Lord Brown lilikua likitajwa si mjini hadi vijijini huku kanga na vitambaa vyenye picha yake vikiwa kama ndio vazi kuu katika nchi hiyo. Umati wa watu uliokua ukijitokeza kumsikiliza Lord Brown katika mikutano yake mara nyingine ulisababisha mikutano kuhairishwa au Lord Brown kusalimia tu bila kuongea kutokana na wingi wa watu waliohatarisha usalama wao kwa msongamano mkubwa wa watu.

"Sijawahi kuona mtu anapendwa kama huyu kijana" Ni bibi wa miaka themanini aliyekua kavalia kanga yenye picha ya lord brown na kitambaa kichwani alikua akiwaambia vijana waliokuwa wamesimama katika kituo cha daladala.



"Hatuna jinsi tumepoteza huu mchezo" Abdallah Ally mmoja wa matajiri wa L9 aliongea kwa huzuni huku kainamisha kichwa chini katika kikao cha tathmini baada ya siku kuisha.

"Abdallah usiongee hivyo hapa lazima tufanye kitu" Rosemary alijibu huku akiwaangalia wenzake wakiwa wanasura za kukata tamaa.

"Sikilizeni, Maji tumeshayavulia nguo ni lazima tuyaoge, Hapa ni mapambano tu, Tumeshatumia fedha nyingi sana katika huu mchakato sasa hatupaswi kurudi nyuma na kumbukeni zimebaki siku hamsini tu wananchi wapige kura" Mr. Ngwali aliongea kwa msisitizo.

"Hicho ndicho cha kuongea, Sasa tunafanyaje maana pesa tuliyopoteza mpaka sasa tukishindwa ni hasara kubwa sana" Alidakia Salomenyo Chaloo.

"Mimi naona tupeane break mpaka kesho then kila mmoja atafute njia ya kumshinda Mpinzani wetu" Bi Agnes Todi alitoa wazo lililoungwa mkono na wajumbe wote kisha kikao kile kikahairishwa kwa kila mmoja kuhakikisha anafanyia kazi wazo lile.



********** ************

Msamaha wa Rais kwa wafungwa wazee na wenye matatizo ulimkuta Mfungwa wa Muda mrefu Gerezani Nyapara Jackson Dudu. Msamaha ule ulimtenganisha na ukuta mrefu wa Gereza la Hotwall lililopo katika mji wenye joto zaidi nchini Kolo uitwao Lobombo. Miaka zaidi ya thelathini aliyoishi ndani ya Gereza lile ilimfanya kila anachokutana nacho akishangae, Mazingira ya uraiani yalikua ni tofauti na anayoyaona kwa wakati huo. Bango kubwa lililo mbele yake lilimfanya atumie dakika nyingi kushangaa bango lile, Picha kubwa iliyoambatana na maandishi makubwa yanayosomeka CHAGUA LORD BROWN KWA MAISHA BORA ndiyo ilikua ikimshangaza Jackson Dudu.

"Mungu wangu huyu si Brown?" Alijisemea peke yake huku akisogelea lile bango kwa ukaribu zaidi. Mawazo yake yakahamia Gerezani miaka ishirini iliyopita.



Brown akiwa kapiga magoti machozi yakilowanishamashavu yake, Mbele yake kasimama nyapara mkuu wa Gereza Jack Dudu, Mkononi kashika mpira mrefu ambao hutumia kama fimbo kuwaadhibu wafungwa wakorofi. Muda huo ndio muda ambao Brown aliingizwa gerezani kwa mara ya kwanza kutumikia kifungo cha miaka mitatu kwa kukamatwa akijaribu kuingiza dawa za kulevya nchini. Dudu alikua akimsomea Brown sheria za Gereza huku Brown akizirudia kuzitaja. Kishaakakutana na maisha mapya ndani ya kuta ndefu za gereza la hotwall. Chakula cha foleni ambacho ni mlo mmoja kwa siku tena usio na viungo na kulala saa tisa jioni vilikua ni vitu vigeni sana katika maisha ya Brown.

"Unataka kula vizuri,Kulala vizuri?" Ni swali toka kwa Dudu aliloulizwa Brown baada ya miezi miwili pale gerezani.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Ningeshukuru sana" Brown alimjibu Dudu wakati kaunga foleni ya kupata chakula.

"Ok nenda kakae pale chini kwenye mti" Dudu alimwambia Brown, Dudu akaingia jikoni na kutoka na sahani ya chakula kilichoungwa vizuri akampa Brown. Brown akala kwa pupa chakula chenye ladha kwa mara ya kwanza tokea aingie katika hilo gereza. Baada ya kumaliza kula alipelekwa ndani Gerezani akakutasehemu imetandikwa godoro dogo vizuri na blanketi kubwa safi na mto mdogo.

"Hapa ndipo utakapolala, Je utayapenda maisha haya kila siku?" Dudu alimuuliza Brown swali ambalo Brown asingeweza kulikataa hatakidogo.

"Ndio mkuu" Brown alijibu kwa unyenyekevu

"Sawa sasa jioni wakati watu wamelala nitakupeleka kwa mkubwa ukaonane nae" Dudu alimpa ujumbe ule Brown kisha akaondoka.



*********** ***********

Kushushwa kutoka msimamizi wa vijana wa kazi ndani ya Jumba la kifahari la mzee Lord Brown mpaka kuwa Mpokea wageni getini kulimkera na kujenga chuki dhidi ya boss wake, Mawazo ya kurudi katika nafasi yake au kutafuta kazi sehemu nyingine ndiyo yalimfanya kuwana mawazo kila mara mpaka kupelekea afya yake kudhorota. Alimuogopa sana Lord Brown sababu anajua ukatili wa mzee huyo. Kitendo cha wafanyakazi kutoweka kila mara ndani ya jumba hilo kilimuogopesha na kumfanya kuendelea kuwa mvumilivu. Kutoka kwa kila mara kwa Boss wake kwenda katika vikao vya kampeni kulimfanya aweze kuzunguka kila katika msitu ulio pembezoni mwa nyumba hiyo ambao Lord Brown huutunza. Macho yake yakakutana na shimo kubwa katikati ya msitu ule. kwa mwendo wa tahadhari akasogea mpaka kwenye lile shimo lililochimbwa kma kaburi na kuchungulia ndani, Macho yake yakatua katika Jeneza lililokua wazi na ndani halina mtu likiwa ndani ya Shimo lile. Kwa hofu akaondoka na kurudi katika eneo lake la kazi huku akiwa na hofu zaidi. Huyu ni Abas Katwila kijana mtiifu na mfanyakazi wa muda mrefu wa Lord Brown. Kila muda ulivyokwenda ndivyo hofu ilivyozidi kumtawala mara usingizi ukaanza kumchukua polepole pale kwenye kiti chake mara akashtushwa na sauti ya honi ya ya gari. Kwa haraka akaamka na kufungua Geti, Lord Brown akiwa anaendeshwa kwenye Gari huku akitetemeka Gari inaingia anashuka akikimbia mpaka ndani kisha anatoka akiwa kaongozana na kijana mmoja aliyevaa nguo nyeupe na kupotelea kule porini. Kitendo cha lord Brown akiwa na yule kijana kuelekea kule porini kulimfanya Abass kukerwa na kihoro cha tamaa ya kujua kinachoendelea kilimkaba na kujikuta kaisimama na kufuatilia tukio lile kwa kunyata. Akiwa kasimama nyuma ya mti mkubwa macho yake yakitazama mbele kinachoendelea hakuamini kile alichokua anakioa kwa wakati ule, Alifumba macho kwa woga huku akijificha asionekane kamaanashuhudia tukio lile.



******** *********

Usiku ndani ya Gereza wafungwa wote walikua wamelala, Dudu akamuamsha Brown na kutoka nae nje akisaidiwa na askari magereza wakaelekea mpaka kwenye ofisi ya mkuu wa Gereza, Kitanda kamacha hospitali kilicho pembeni ya chumba kilicho karibu na ofisi hiyo huku mbele yake kakaa mzee wa makamo akiwa kavaa bukta na singlend nyeupe, Huyo si mwingine ni Rweneni Mkuu wa Gereza la Hotwall, Brown akishangaa bila kujua kinachoendelea alishangaa anapapaswa kifuani na yule mkuu wa Gereza huku Dudu akiangalia, Brown alimsukuma Mkuu wa Gereza na kurudi nyuma.

"We si unataka kuishi vizuri mbona unaogopa sasa" Ni swali kutoka kwa Mkuu wa gereza liligonga katika ngoma za masikio ya Brown.

"Sawa kama hutaki, Embu mpeleke huko nyuma akaone wakaidi wenzake" Mkuu wa Gereza alitoa amri iliyopokelewa na Dudu, Kama kiroba alibebwa na kupelekwa katika chumba kilichojaa maji kwa kupitia dirishani aliona vijana wawili wakiwa katika chumba kile huku maji machafu yenye harufu mbaya yakiwa yamejaa mpaka shingoni.

"Wana siku mbili hao, Hapo mpaka wafe ni bora umkubalie mkuu tu" Dudu alimwambia Brown ambaye aliendelea kushikilia msimamo wake uliopelekea kubadilishiwa makazi na kuingizwa ndani ya kile chumba chenye maji ya shingo yenye harufu mbaya. Muwasho alioupata kutoka kwenye maji yale ulifanya aanze kulia kwa uchungu. Macho yake yakagongana na mwili wa mmoja wa vijana wale wawili waliokua ndani ya chumba kile ukielea. Huku yule mwingine akiwa anatapatapa kama mtu anayetaka kukata Roho. Hofu ikamtanda, Godoro zuri n a blanketi alilolalia muda mfupi uliopita vikawa kama kumbukumbu kichwani kwake, Machozi yakaanza kumtiririka huku akitumia mikono yake kujikuna kila mahali kwa muwasho kutoka katika maji yale. Mara kiza kikaanza kutanda katika mboni za macho yake,Akiwa kakata tamaa huku akimkabidhi Mungu Roho yake na akakumbuka sala ya Mama Maria aliyofundishwa akiwa anasoma mafundisho. Akaanza kusali.

"Salamu Maria uliyejaa Neema, Bwana yu nawe, Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzawa wa Tumbo lako Amebarikiwa, Maria mtakatifu mama wa Mungu, Utuombee sisi wakosefu sasa na saaa.........!" Kabla Brown hajamalizia sala ile mara akasikia sauti ya miguu ya mtu ikija kuelekea upande wa kile chumba, Hofu ikamtanda.



********* *********



Baada ya Kushuhudia kitendo ambacho hakukitegemea mbele ya macho yake alizidi kushangazwa na malipo aliyopatiwa yule kijana Tayari risasi ilikua imesambaratisha kichwa chake na yupo ndani shimo, kwa haraka Lord Brown alikua akirudishia udongo katika shimo, Haraka aliyokua akitumia Dakika chache shimo lilikua limejaa na akachukua mche wa mti na kupanda juu yake kisha akaanza kujipangusa vumbi huku akionekana amechoka sana, Abass alirudi kinyume nyume na kutimua vumbi kurudi katika eneo lake la kazi huku akiwa amejawa na hofu kwa kitu alichokutana nacho siku hiyo. Chuki aliyonayo dhidi ya Lord Brown ilizidi mara dufu huku akifikiria jinsi wafanyakazi walivyokua wakitoweka katika mazingira ya kutatanisha huku uvumi ukienea kuwa wanahamishiwa katika ofisi za Lord Brown zilizoko nje ya nchi hiyo, Sasa Tayari ukweli alikua keshaufahamu, Maelfu ya vijana walikua wamefukiwa katika msitu ule na juu yake kupandwa mti. Abas alitamani kumshirikisha mtu mwingine Tukio aliloliona ila alihofu Lord Brown akigundua atammaliza. Alipatwa na ujasiri baada ya kufikiria kama Mahmood kijana aliyeuawa dakika chache zilizopita na upole wake wote kauawa je itakuaje zamu yake ikifika. Mamuzi yakaanza kumtesa kichwani kwake ni maamuzi ya kutoboa siri, Aliwaza patakapokucha aende polisi na kuwaelezea Tatizo lililopo ili Lord Brown achukuliwe hatua.

"Ni lazima niseme hawezi kumaliza vijana kwa tabia yake ya kishetani" Abas alijikuta akiongea mwenyewe huku akitazama pande zote kama amesikiwa na mtu.

"We abas njoo"

Ni sauti ya Lord Brown iliyomshtua Abas na kuamka haraka kwa hofu huku akielekea mbele ya nyumba ile aliposimama Lord Brown akiwa kavaa taulo.

"Ndiyo mkuu"

Abas aliinama kwa unyenyekevu huku akitetemeka mbele ya Lord Brown,

"Mbona unatetemeka una Tatizo gani"

Lord Brown alimuuliza Abas huku akimuangalia kwa makini.

"Habana Boss ni baridi inanitesa"

Abas alidanganya huku akijikaza asitetemeke ila hofu aliyokua nayo ilimzidi nguvu na kuendelea kutetemeka.

"Mbona kuna joto kali sana saa hizi, Sawa kesho itabidi uende hospitali sawa?"

Lord Brown alimjibu Abas huku akimtazama machoni kwa umakini. Abas akikwepesha macho yake yasikutane na macho ya Lord Brown.

"Sawa Mkuu"

Abas alitii huku akiangalia chini kwa hofu.

"Kuna miti kule msituni inakauka haijanyeshwa maji kesho ukafanye hilo zoezi asubuhi na jioni sawa"

Lord Brown alimwambia Abas kisha akaondoka na kuingia ndani. Kitendo cha Lord Brown kuingia ndani kilimfanya Abas kushukuru Mungu sababu alijua kaonekana na ule ulikua ni mwisho wake wa kuvuta pumzi asiyeilipia katika ulimwengu huu. Sura inayotisha kwa fedha ya Lord Brown ilimfanya Abas atupe wazo la kutoa taarifa polisi, Akarudi katika kiti chake na mawazo yakaanza upya.

"Nikitoa taarifa polisi najua polisi watanitaja sababu Lord anataka kuwa rais haitokua rahisi kumkamata, Bora nitafute njia nyingine"

Abas aliwaza peke yake huku akijilaza katika kiti chake pale mlangoni na kupitiwa na usingizi.



**** ****

Sauti ya hatua za mtu kusogelea kile chumba zilimpa hofu Brown na kufumba macho huku akiomba Mungu aichukue Roho yake taratibu na si kwa mateso kama yule kijana aliyemuona dakika chache akikata roho. Sauti iliyokua ikimuita jina lake kwa taratibu kama haitaki mtu mwingine asikie ilimfanya kuwa na amani kidogo akajivuta mpaka karibu na lile dirisha na kushuhudia lile dirisha likifunguliwa kamba ikateremshwa huku akipewa maelekezo apande kwa kutumia ile kamba akapanda na kutoka nje macho yake yakakutana na Dudu huku akimuashiria anyamaze,

"Sikiliza sijapenda ufe, Sasa twende ukalale kule gerezani kesho nitakurudisha sawa" Dudu alimwambia Brown kisha Brown akaitikia kwa kutikisa kichwa kukubaliana na kile alichoambiwa. Brown akarudishwa Gerezani kwa kusaidiwa na Dudu Pamoja na Askari wa Zamu aliyepewa pesa na Dudu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Brown akiwa kalala huku tukio la vifo vya wale vijana kule kwenye kile chumba likijirudia alijikuta akikumbuka kiasi kikubwa cha fedha alichonacho ambacho amefukia katika sanduku la chuka katikati ya Shamba lao, Hakutamani kufa na kuacha fedha nyingi katika shamba lile. Hakua na njia nyingine zaidi ya kutumikia kifungo ili akachukue fedha zile alizohifadhi baada ya kufanya biashara ya kusafirisha shehena kubwa ya dawa za kulevya katika tumbo lake zaidi ya mara ishirini bila kukamatwa, Awamu ya mwisho aliyokua kapanga afanye ndipo aache kazi hiyo ya kutumikishwa ndiyo iliyoharibu kila kitu baada ya kukamatwa katika kiwanja cha ndege akiwa na dawa hizo.

"Hapana siwezi kufa kizembe"

Brown alijikuta akiongea mwenyewe huku akijigeuza pale kwenye lile godoro.



**** ****

Abas akiwa katikati ya msitu akimwagilia miti ipatayo kumi inayoonekana imepandwa karibuni kichwani kwake alikua akiwahesabu watu waliotoweka kazini katika kipindi cha karibuni, Tayari alikua keshafikisha vijana zaidi ya hamsini ndani ya mwezi mmoja. Tamaa ya kufanya kitu ilimvamia na kumaliza kumwagia ile miti maji kisha akatoka na kuelekea nje ya ile nyumba.

"Naomba Pepsi baridi"

Abas alikua nje ya kioski kilichoko barabarani katika mtaa ulio na wakazi wengi ndani ya jiji la Pona.

"Oya unamuona yule sister kule eti na yeye anagombania ubunge, Anapoteza muda wake wakati Lord Brown anapita na wabunge wake wote"

Muuza duka alikua akimuonyesha Abas Rosemary aliyekua akipita kuvuka barabara kuelekea upande wa pili wa lile duka, Abas kwa shauku akaacha ile soda na kumkimbilia Rosemary.

"Dada, Dadaa samahani"

Abas alimuita rosemary, Rosemary akasimama na kugeuka kumsikiliza Abas, Kwa kipindi hicho cha uchaguzi kila mgombea alikua mnyenyekevu kwa kila mwananchi, hakuna mgombea ambaye alikua hasikilizi wananchi wanachowaambia, kwa unyenyekevu na Tabasamu Rosemary akasimama na kumsikiliza Abas.

"Samahani nahitaji kuzungumza nawe"

Abas alimwambia Rosemary, Rosemary akamshika mkono wakasogea pembeni na kuanza kumsikiliza.

Mshtuko Rosemary alioupata baada ya kusikia habari inayomuhusu Lord Brown kutoka kwa Abas ulisababisha Rosemary kusimamisha Tax na kuingia na Abas safari ya kuelekea pembezoni mwa jiji la Pona ikaanza na safari ikaishia nje ya hoteli ya Ajax, Wakitembea kwa mwendo wa haraka kama wanawahi kitu wakafika kwenye lifti, kuchelewa kwa mlango wa lifti kulipitisha maamuzi ya kupanda kwa kutumia ngazi, Abas na Rosemary walikua wakipanda ngazi kuelekea juu. Safari ikaishia mbele ya mlango wenye maandishi yaliyosomeka

"Chumba cha mikutano"

Rosemary akanyonga kitasa mlango ukafunguka akiwa kamshika Abas mkono wakaingia ndani na kukutana na kundi la matajiri wa L9 wamekaa wakiwa wamezunguka meza wakijadili jambo.

"Samahanini kwa kuchelewa ila nimekuja na ushindi, Mpaka sasa tuhesabu Chalambo ndiye Rais"

Rosemary aliongea kwa kujiamini huku akimuonyesha Abas sehemu ya kukaa.

"Unamaanisha nini?"

Deogratias aliuliza huku akimkazia macho Rosemary. Rosemary akitabasamu anamuangalia Deogratias na kisha kuzungusha shingo yake kushoto kisha

akairudisha kulia macho yake yakatua sehemu alipokaa Abas.

"Huyu kijana ndiye mwenye siri nzito itakayomuangusha Lord Brown."

Rosemary alijibu kwa mbwembwe na kujiamini kupita kiasi kauli iliyopelekea Mr Ngwali kusimama na kusogea karibu na Abas huku akimkazia macho.

"Kijana tueleze hiyo siri tutainunua kwa pesa nyingi sana kama itakua na manufaa kwetu" Mr. Ngwali aliongea kwa upole huku akimpiga piga vikofi vidogo mgongoni Abas.

Abas kwa kujiamini akasimama na Kukohoa kikohozi kidogo na kuanza kuongea.

"Naitwa abas mimi ni Mfanyakazi wa Lord Brown katika nyumba yake, Naaa..."

Kabla Abas hajaongea ghafla wanasikia mlango ukifunguliwa. Wanageuka wote kwa hamaki.



**** ****

Saa kumi usiku Dudu alimsogelea Brown kwa huruma akamuamsha huku akiwa na wasiwasi, Brown akaamka na kukaa akiwa anamuangalia Dudu kwa macho ya huruma.

"Sikiliza Brown si mapenzi yangu ila natimiza wajibu tu naomba nikurudishe kwenye kile chumba"

Dudu alimwambia Brown huku akiwa anaangalia chini kwa woga.

"Nashukuru Mkuu kwa kunisaidia naamini mpaka saa hii ningekua tayari ni maiti, Sitokusahau katika maisha yangu wema wako ulionitendea, hakika umenipigania dhidi ya kifo na umehakikisha sijafa kabla ya kutimiza ndoto zangu kwa kuwa bado mimi ni kijana na maisha ndiyo yamenileta hapa, Kwa kuwa imepangwa nikabiliane na maisha kwa njia hii basi hili daraja siwezi kulikwepa, Kiukweli siwezi kurudi kule kwenye kile chumba"

Brown aliongea kwa uchungu mkubwa huku akilia, Kauli ya mwisho ilimshtua Dudu na kujikuta anataka kutumia nguvu kumtoa Brown pale na kumpeleka katika kile chumba.

"Tulia kwanza najua unahofia nisipoenda utawajibishwa"

Brown alimshika Dudu mkono kwa upole huku akizungumza akiwa na tabasamu la maumivu, lililomfanya Dudu kumuachia na kumuangalia kwa mshangao.

"Nimekubali kufanya kile mkubwa wa Gereza anachotaka"

Brown aliongea kwa lugha yataratibu, Maamuzi magumu ya kuokoa nafsi yake dhidi ya kifo cha maji yaliyo nje ya bahari, tena maji yenye harufu mbaya kama kinyesi na yanayowasha zaidi ya upupu. Kauli ile ilimshtua Dudu na kujikuta akiuliza kwa mara ya pili kama hakusikia.

"Unasemaaaaaaa?"

"Nimekubali kufanya anachotaka mkuu wa Gereza"



**** ****





Ndani ya bweni la Sekondari ya Wavulana ya Soka Boys ndiyo sehemu aliyokutana na Abuchebi, Walikua wakilala katika vitanda vinavyofuatana, Ikiwa baridi na mvua kubwa iliyokua inanyesha siku hiyo ndiyo iliyomfanya Abuchebi Ashuke kitandani kwake na kuhamia kitanda cha Rweineni mwanafunzi mwenzake waliyoshibana. Baridi kali iliyoipiga ngozi zao na kuzama katikati ya mifupa yao ilipelekea wakumbatiane na kutengeneza Joto ambalo lilipelekea Abuchebi kumshawishi Rweineni amuingilie kinyume na maumbile. Mchezo ule ulikua na kusababisha Abuchebi kuhamia katika kitanda cha Rweineni na kila siku akiingiliwa kinyume na maumbile, Kama ilivyo mazoea Tabia ile ilijijenga katika mfumo wa akili wa Rweineni mpaka alipomaliza kidato cha sita alikua akiwaingilia wanaume kinyume na maumbile na kuwalipa pesa, Alipomaliza mafunzo ya upolisi Rweineni alioa mke na ndoa ikadumu kwa miezi kadhaa ndipo ilipovunjika baada ya mkewe kuchoshwa na kitendo cha mumewe kumuingilia kinyume na maumbile, Sasa Rweineni alikua mkuu wa Gereza la Hotwall na alikua akitumia Fursa hiyo kuwaingilia wafungwa kinyume na maumbile na anayekaidi hukabiliana na adhabu kali, Dudu akiwa ndiye kuwadi wake mkuu huku akimtumia Afande Boka mlinzi mkuu wa Gereza kuwapitisha wafungwa mpaka katika chumba kilichopo pembezoni mwa ofisi yake chumba alichokipa jina la ICU hapo ndipo hutumia kufanya uzinzi wake.



Huku akitabasamu baada ya kumuona Brown akiletwa na Dudu, Mkuu wa Gereza alifungua mlango wa ICU na kumkaribisha Brown aliyepokelewa na kitanda kidogo, Mlango ukafungwa na kumtenganisha Dudu na kile chumba, Tayari Suruali ya Rweineni ilikua magotini huku mikono yake ikimvua Brown Suruali. Akilia kwa uchungu wakati anaingiliwa kwa nguvu na mkuu yule wa gereza aliyeziba masikio yake kwa pamba huku akifurahiwa na kitendo kile. Baada ya nusu saa tayari alikua keshamaliza haja yake na alikua akitabasamu.

"Usihofu utazoea, na kuanzia sasa utaishi vizuri" Mkuu wa Gereza alikua akimwambia Brown huku akiwa anafunga suruali.

Kitendo cha Brown kuingiliwa mara kwa mara kilimjengea mazoea, Mazoea yaliyokua yakimtesa. Mazoea ya kutamani kuingiliwa mara kwa maramara, mazoea yaliyosababisha kila mara amsumbue Dudu ili ampeleke kwa Rweineni ili akapatiwe kile anachopatiwa, Mapaka kifungo chake kinamalizika tayari Rweineni alikua amekumbwa na tatizo la kupatwa na ugonjwa wa kutetemeka pindi anapotaka kuingiliwa kinyume na maumbile na pindi anapoingiliwa tu tatizo hutoweka. Baada ya kutoka Gerezani hakuweza kudumu na mke wake Linda baada ya kushindwa kumtimizia haki yake hali iliyopelekea ndoa yao kuvunjia.

Hapo ndipo Brown alipodondokea katika mikono ya Baharia wa kiarabu aitwae Twallib ambaye alikua akifanya nae biashara ya kusafirisha madini ya Gramnet ambapo mwisho wake alijikuta akimtumia kumuingilia kinyume na maumbile.

Na sasa Dudu katoka Gerezani Baada ya miaka ishirini kupita toka alipoachana na Brown kule Gerezani, Na sasa anakutana na Picha ya Brown ikiwa inaashiria ndiye Rais aombae Ridhaa ya kuongoza Taifa la Jamuhuri ya watu wa Kolo, na kwa wakati huo anafahamika kwa jina la Lord Brown.



**** ****

Baada ya mlango kufunguliwa na kusababisha kimya kutoka kwa Abas, Kwa mwendo wa haraka Mr. Ngwali akaelekea kule mlangoni na kukutana na msichana aliyevalia nguo za wahudumu wa ile hoteli mkononi akiwa kashika kitabu kikubwa.

"Samahani nimewaletea Menu ya vyakula mchague"

Yule msichana alimjibu Mr. Ngwali kwa unyenyekevu.

"Usijali tutakufahamisha baadae tuna mazungumzo muhimu kwa wakati huu"

Ngwali alimjibu Yule muhudumu akaondoka. Kwa mwendo wa haraka akarudi kuketi huku akimuangalia Abas kama anamwambia aendelee kuzungumza. Abas akiangalia pembeni kama kuna mtu ambaye hataki asikie anachotaka kuongea.

"Nawaambia kitu ambacho najua kinahatarisha maisha yangu ila siogopi kufa najua nasaidia maisha ya watu wengi ambao wangekufa kama nitanyamaza kimya bila kusema hili suala"

Abas ananyamaza kwa sekunde chache, Huku wajumbe wa kile kikao wakiwa na shauku ya kujua ni nini kinachotaka kuongelewa na Abas.

"Mnakabiliana na mpinzani katili sana na msiri sana, na iwapo mkifanyia kazi hili ninalotaka kuwaambia basi mjue chama chenu kitashinda kwa kishindo kikubwa sana ila mkipuuza hili basi mjue mtakua katika hatari kubwa ya kushindwa na hata kupotezwa maisha yenu kwa kuwa huyu mtu hatopenda siri hii ivuje"

Abas aliendelea kutoa maelezo marefu pasipo kusema kitu anachotaka kusema maelezo yaliyopelekea kuongeza shauku ya kujua ni siri gani aliyoibeba kifuani mwake.

"Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha Democracy Movement Lord Brown ni shoga"

Abas alitoa kauli ya kishujaaa kwa kujiamini iliyozua mshtuko na maswali katika nyuso za wapiganaji wa chama cha The Revolution.

"Lord Brown ni Shogaaa"

Paul Bona alijikuta akiropoka bila kuamini.

"Ndio ni shoga, Tena huwalazimisha vijana wanaofanya kazi katika jumba lake kumuingilia kinyume na maumbile kisha huwaua na kuwafukia katika msitu wake na kupanda mti juu yake, Hata jana usiku kafanya kitendo hicho, Vijana wengi wamepoteza maisha inawabidi mtumie akili ya ziada kuhakikisha mnazuia hivyo vitendo vyake viovu"

Abas alitoa maelezo yaliyowaonyesha mwanga zaidi.

"Sasa huko kwenye huo msitu tutaingiaje ili kupata uhakika"

Agnes Todi aliuliza swali lililojibbiwa vyema na Abas

"Ni ngumu kwa mtu kuingia katika msitu ule, na mimi pekee ndiye mwenye mamlaka wa kuingia kule sababu ninakazi ya kunyeshea miti iliyopandwa hivi karibuni ambayo ni makaburi ya watu aliowaua" Abas alizidi kutoa maelezo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Ama kweli huyu bwana ni mkatili, Sasa hapa inabidi tufunge kamera katika huo msitu ili tupate ushahidi, ili tutakapomshtaki tuwe na cha kuzungumzia"

Mr. Ngwali alitoa wazo lililoungwa mkono na wajumbe wote.

"Sasa kijana sikia, Sisi tutakuhakikishia usalama wako na tutakulipa fedha nyingi sana, Kesho tutakuletea kamera ambazo utafunga juu ya miti kule msituni na baada ya kupata ushahidi utatuletea hizo Camera"

Mr. Ngwali alitoa maelezo yaliyojitosheleza kwa Abas ambayo abas alikubali bila kipingamizi na kuahidi kutekeleza hilo jukumu tena bila malipo, Huku akisisitiza anafanya yote hayo ili kufichua mauaji ya kikatili ya vijana wengi ndani ya jumba lile la Lord Brown.



**** *****


ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog