Search This Blog

Tuesday, 1 November 2022

SIPASWI KUSAMEHEWA - 3

 








Simulizi : Sipaswi Kusamehe

Sehemu Ya Tatu (3)





“Sawa, baada ya kukukosa siku ile pale hotelini, hakika nilikutafuta sana Mam, mtu ulie muachia maaagizo aliondoka siku ileile na kutokuwepo pale kwa muda wa wiki mbili, nilimfuata hadi kwake, lakini sikumuona na siku niliyomuona akanielekeza niende Zanaki. Sikuchoka, nilienda hadi huko na nilipofika hapo bahati haikuwa yangu, maana Sikuwa na bahati, kwa sababu sikukukuta, ulikuwa umemaliza mitihani na umeisha ondoka kurejea kwenu…” Mam alisikitika sana



“Masikini… Pole sana Esmile,” alimpa pole na kumfanya Esmile aendelee



“Hapo ndio nikawa nimekukosa, hatimaye nilipojua kuwa nimekukosa ndio tamaa ya kuzidi kukutafuta ikaongezeka, nikawa natamani kukuona, mara mbili zaidi ya ile ya awali, kila njia niliojaribu kukutafuta sana sikufanikiwa, hatimae leo nipo nawe sehemu moja, tena tukiwa wawili tu…” alisema huku akionyesha vidole viwili



“Wawili tu ndani ya gari, ni kama vile siamini Mam… ama kweli mshahara wa siku moja hukusahaulisha shida zote za mwezi mzima, leo nipo nawe nahisi kusahau miaka miwili yote ya kukutafuta Mam,”



“Hongera sana kwa uvumilivu Esmile,” alimpa moyo Mam, Esmile nae ndio alikuwa akipataka hapo, akaendelea huku akijiweka vizuri kitini na kuendelea



“Leo nataka ujue Mam, ukweli ni kwamba NAKUPENDA sana Mam na nimejikuta katika wakati mgumu tangu tulipoachana… 4 real, I LOVE U Mam,” Esmile akamtazama Mam akishusha pumzi kwa nguvu;



“Ahsante Esmile kwa kuonesha mapenzi juu yangu na ninashukuru mno kwa kunipenda, nimekusikia kwa kila ulicho kisema ila bahati mbaya mimi ni mwanafunzi, mambo hayo bado sana na sitaki hata kuyawazia maana kimasomo bado nina safari ndefu na tena ni ngumu, nafikiri Esmile wewe ni mwelewa na utakuwa umenielewa…” alisema Mam japo naye alionekana wazi kumkubali Esmile lakini kama unavyojua jambo hili siyo la kukubali kirahisi namna hiyo.



Kawaida Esmile huwa si mtu wa kulazimisha mambo, akamjibu kuwa;



“Sawa nimekuelewa, najua ni haraka sana na natambua yote yaliyo mbele yako, lakini take your time, kufikiria hili, kwani kwa upande wangu, nimevumilia kipindi kirefu mno, nadhani safari iliyobaki ni fupi” alisema kisha akageuka mbele na kujiweka sawa, akawasha gari na kuelekea barabarani kuendelea na safari, Mam akimuelekeza njia.



Esmile akamuomba Mam simu yake, hakusita, akampa. Esmile alipoishika akaiwasha na kuandika namba yake, akaisave na mwisho aka-beep kwake, kisha akamwambia Mam kuwa ameisav namba yake kwa jina lake, Mam akashukuru na kumwambia achukue namba ya Rahel kwenye simu ile, Esmile akakataa na kuuliza ya nini.



Mam akacheka na kumwambia mbona alikubali wakati Rahel aliposema apewe namba na Mam, akasema kuwa Rahel alikuwa ni kichomi, hivyo alikuwa anamchomoa tu, mbele kidogo Mam akamwambia Esmile asimamishe gari na kumuonesha kwao, alishukuru kupafahamu na kisha wakaagana kwa ahadi ya kuwasiliana baadae.



Kabla hajaondoka kuingia ndani, yaani akiwa nje ya gari, kama vile ni mtu aliekumbushwa kitu, Esmile akakumbuka na kumuita Mam na kufumgua mlango mmoja na kisha akafungua Dashboard ya gari lake na kutoa ua jekundu moja zuri bichi, maarufu kama Red Rose na kulishika mkononi huku akiwa maeegamia gari lake na kuanza kusema



“Mola ametengeneza ua Waridi kwa mfano wa alivyo muumba mwanamke, waridi huwakilisha uzuri bila kujali rangi yake, kikonyo chake huwakilisha nguvu ya mwanamke aliyonayo ambayo huzidiwa na nguvu na mwanaume, harufu



 ni halisi na nzuri mno,” aliongea huku akiligeuza geuza na kumtazama Mam aliekuwa amesimama pembeni yake na tabasamu zito usoni, akaendelea

“Ua lake ni laini kama ilivyo ngozi ya mwanamke mrembo, jani humwakilisha mwanamke kuwa tayari kulinda ama kupoteza uhai wake kwa ajili ya mtoto wake ambae ni ua lenyewe.

Inaonyesha ni kiasi gani ua hili linajitoa kwa mapenzi na lilivyo na mapenzi ya kweli…

Kila mara utakapoliona ua la Waridi, popote pale, kumbuka…” akanyoosha mkono kumpa Mam ua lile, wakati Mam akipokea ua yeye akaendelea kusema

“Kuna mtu yupo sehemu amekaa akikusubiri, mtu huyo ni maalum ametoa kila kitu chake kwa ajili yako, mtu huyo hapendi kukukosa katika maisha yake, anaamini kuna maisha bila wewe lakini hakuna furaha bila wewe, ahsante sana Mam!” akatoa tabasamu ambalo lilimchanganya Mam aliekuwa amesimama ameshika ua lile kama ndo kwanza ameliona leo tangu kuzaliwa.

Akashusha pumzi Mam na kusema

“Esmile umekuwa ni muhimu kwangu nashukuru sana kufahamiana nawe, najua bado mimi napaswa kuongea kwako, kama ambavyo wewe umeongea kwangu, lakini muda huu hauruhusu, ninaomba nikutane nawe siku moja ya wiki ili name niweze kusema yangu, kama hutajali iwe ni siku ya mwisho wa wiki.”

“Mimi hata ukisema kesho ni powa tu Mam, maana nimekaa miaka miwili bila wewe, nimehisi nimepoteza sana, lakini nimekaa nawe dakika 20 tu nahisi kurudisha kila nilichopoteza,” aliongea Esmile huku akishika mlango wa gari yake kwa kuonesha kama anaufungua ili aingie.

“Esmile hujajua ni kiasi gani name nimeteseka kwa kukutafuta, kibaya zaidi mie ndio hata pa kuanzia nilikuwa sipajui, hebu tafuta siku tuongee zaidi, si unajua hapa ni karibu na nyumbani? Mzee anatoka punde tu kwenda Masjid, si vema akiniona hapa, baadae basi tuwasiliane,” Mam akasema huku taratibu akianza kuondoka.

Wakaagana na Esmile akaingia garini kwake huku akihakikisha kabisa kuwa namba ya simu ameisave ndio akawasha gari na kuondoka akiwa na furaha tele moyoni.

*********http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Usiku muda wa saa mbili hivi, Esmile akiwa nyumbani kwao pamoja na wazazi wake, akaona simu yake inaita, ilikuwa mbali nae kidogo, alipoisogelea akagundua kuwa ni Mam alikuwa kipiga, alipata furaha ya ajabu sana.

Akaipokea na kumwambia akate ili yeye apige. Mam akamwambia asijali wanaweza tu kuongea.

“Sio rahisi kuwa jasiri kwa kusubiri kila kitu toka kwa mtu alieokoa maisha yako, kuna wakati unapaswa kumuonesha kuwa unathamini uwepo wake na hata nae apate moyo wa kujua kuwa anakumbukwa,” aliongea Mam.

“Ni kweli Mam, lakini habari za jioni?”

“Nzuri mno upande wangu Esmile, yaani nimejiunga usiku huu ili tu niweze kukwambia mambo mawili, jambo la kwanza ni kukushukuru sana kwa msaada ulionipa miaka miwili iliopita, naomba sana upokee shukrani zangu Esmile,”

“Nashukuru pia japo sidhani kama ni muhimu Mam, muhimu wewe tu kuwa vizuri, mi nataka kujua tu ilikuwaje baada ya kupotezana?”

“Hilo ndio jambo la pili nililopanga kukwambia, baada ya kuondoka pale hotel siku ile, nilienda nyumbani kwanza na baada ya mitihani nilikwenda Tanga nyumbani kwa bibi yangu na kukaa huko hadi matokeo yalipotoka, kasha nikarejea Dar na kurudi tena pale hotelini kukuulizia…”

“He! Acha utani wewe, ulirudi pale?” Alishangaa mno Esmile na kumfanya Mam acheke

“Ndio nilirejea pale na kuambiwa hawajakuona kwa siku nyingi lakini mara kadhaa kipindi kilekile ulikuwa unaenda.”

“Ni kweli kabisa wala si uongo,”

“Basi bhana, nilipokosa hicho nitakacho, ikawa ndio mwisho wa kukutafuta, maana hata sikujua nakupataje, ndio nikapata wazo la kwenda pale uliponiambia umekodi pikipiki, niliemkuta akaniambia hakufahamu na hata alipokuja mwingine akasema wateja huwa ni wengi na wengine wanawajua kwa sura tu na si kwa majina,”

“Doh! Hatari sana, ikawaje?”

“Basi nikaondoka roho ikiniuma sana kwa kutokukuona, nilitamani kukuona kuliko hata kula, kila kitu kikawa kimeishia hapo nikiomba Mungu siku moja atukutanishe, nashukuru sasa tumekutana tena.”

“Aisee jambo la kushukuru Mungu hilo, sasa je suala langu vipi lakini Mam?” alichomekea Esmile lakini bado msimamo wa Mam ukawa upo palepale hadi wakaagana.

**********



Hanson, baba mzazi wa Esmile ni muathirika wa virusi vinavyo sababisha UKIMWI, mzee anajitambua na amekuwa akitumia uwezo wake kifedha kuwalaghai wasichana na kuwaambukiza virusi na amekuwa akihangaika na wasichana warembo wenye mvuto wenye tamaa.

Siku moja ya katikati ya wiki akiwa amekaa peke yake mbele ya nyumba yake, kikombe cha chai pembeni, akifikiri juu ya hatma ya yale aliyoyafanya, kwanza alivuta taswira ya wasichana aliofanya nao ngono kwa lengo la kuwaambukiza virusi vya Ukimwi, akakumbuka kati yao kuna wale alio waambukiza kwa hiari yao na hata wale aliowabaka.

Hapo zilimjia picha za warembo kadhaa, zilikuja na kuondoka. Ilipomfikia taswira ya binti mmoja mdogo, alikuwa ni mrembo wa haja. Aliamini binti huyo kwa sasa ni mrembo zaidi ya kipindi hicho alichomfanyia kitendo cha kidhalilishaji.

Miaka imepita kadhaa lakini alitambua fika akimuona hatomkumbuka kwa sura ila kwa jina alikuwa akimkumbuka, alimwambia anaitwa Ray, wakati anamfanyia kitendo hicho cha kumbaka binti huyo alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha 4 katika shule ya Fulani ya sekondari iliopo katikati ya Jiji.

Binti huyo alimvutia, alipomshawishi kufanya nae ngono binti aligoma kabisa, yaani alikataa kwa dhati. Kutokana na uzuri wake akashawishika kumbaka, tena bila kinga yoyote na hali akitambua kuwa yeye ni muathirika.

Leo amekaa nje nyumbani kwake akiwa peke yake, akilitazama jua likizama huku akijutia matendo yake.

Kilichomuumiza zaidi ni kwamba, binti yule alikuwa bado kigori hadi wakati anambaka. Alimpa pesa nyingi sana baada ya kitendo kile kwani aliamini kuwa tayari ameisha muharibia maisha yake kwa makusudi, alitambua kabisa kuwa binti atakuwa tayari ameingia katika kundi la waathirika.

Wakati Mzee Hanson akiwa na mawazo lukuki kuhusu matendo yake ya ajabu aliyoyatenda, mwanae alikuwa akijipanga jinsi ya kuhakikisha anakuwa na Mam kwa namna yoyote ile.

Siku kadhaa zilipita huku mawasiliano kati ya Esmile na Mam yakikolea, kutokana na kuwasiliana mara kwa mara kupitia simu na hata kuonana, dalili zilionyesha Mam ni mgumu sana, tena Esmile alikuwa akipata upinzani mkubwa sana toka kwa Rahel ambaye yeye alishatamani kuwa na Esmile hivyo alijiweka karibu kiasi kwamba Mam.

Siku moja Esmile akiwa anaelekea Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), alikokuwa akienda kuchukua fomu kwa ajili ya kujiunga na masomo ya shahada ya pili, simu yake ikaita, namba haikua ngeni japo haikutoa jina, akaipokea na kusalimiana na mpigaji, kasha akumuomba ajitambulishe yeye ni nanihttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

‘‘Ha ha haa, Esmile umeshindwa kunitambua mimi ni nani? Ina maana umenisahau?’’

‘‘Nahisi kuitambua sauti yako na pia namba si ngeni, ila nimekusahau wewe mwenyewe, jitambulishe tafahali,” alisisitiza Esmile.

‘‘Poa tu mvulana kwa kunisahau, mi ni Rahel…’’

‘‘Oooh Rahel, mambo vipi, habari za siku tele?” alichangamka kwelikweli Victor baada ya kumjua mpigaji

‘‘Bomba mbaya, upo wapi mida hii?’’

‘‘Nipo Dar, maeneo ya Buguruni naelekea katikati ya Jiji, we bado upo Tunduma?’’

‘‘Ha Esmile.., Tunduma tangu mwaka juzi baada ya mitihani? We si wiki iliyopita tulikuwa wote pamoja Dar? Sasa hiyo Tunduma ya wapi?”

‘‘Mh tulikuwa wote?” Aliuliza kwa mshangao mkuu Esmile.

“Ndiyo tulikuwa wote… na mara kadhaa tumekuwa tukikutana…”

“Wapi? Tafadhali niambie…” Bado aliendelea kushangaa, aliona kama utani vile.

“Mimi ndiyo Rahel rafiki yake Mam,”

“Hilo nalijua kuwa wewe ni rafiki yake, na mara ya mwisho kuongea nawe uliniambia upo Tunduma,”

“Esmile, Rahel wa Tunduma na Rahel wa Benjamin Mkapa ni huyohuyo mtu mmoja tu,” alisema

“Haaaa! How come?”

“Ndiyo hivyo, Rahel aliekuwa Tunduma alikwenda tu kupunguza Stress za masomo na majibu yalipotoka nikawa nimepangwa Benjamin Mkapa” aliongea mwenyewe kwa kujishebedua kama wasemavyo mashosti wa mjini.

“Duuh, sasa ilikuwaje hukujitambusha hivyo tangu siku ile jaman? dah, kumbe wote mlifaulu Zanaki na kupangwa Benjamini Mkapa? Aisee mmeniweza sana…”

Hapo Esmile akawa ameelewa na kumshukuru kwa kumuelewesha.





Wakazungumza kidogo tu kwa Esmile kumtania kuwa amekutana na Mam alipotoka Tunduma lakini wala hakumpa namba yake wakati aliomba akikutana nae ampe.

Rahel alikuwa anataka wafike hapo… akamchomekea

“Isingewezekana, maana nimekuja kugundua kuwa ni bora sikumpa, maana ningempa sina imani kama muda huu tungekuwa tunaongea na simu,” Esmile akashangaa kauli hiyo na kumuuliza kwanini? Rahel akamwambia

“Nakutania Boy, namba niliifuta siku ileile tulipomaliza kuongea kiukweli sikuitilia maanani, nisamehe bure handsome,” Esmile akamwambia wala asijali madhali tayari wameonana.

Ghafla kama mtu alieshtuka kuwa salio linaendea kwenye kukata, Rahel akamuomba waonane jioni ya siku ile, Esmile akamkatalia na kusema muda unambana, kama vipi waongee tu kwenye simu.

Sasa ikambidi Rahel amvae Esmile moja kwa moja na kumtamkia anampenda. Esmile alimshukuru kwa hilo na kumpongeza kwa kuwa na roho ya mapenzi kwani binadamu wote tunapaswa kupendana.

Nia ya Esmile ilikuwa ni kumpotezea, Rahel nae alimuelewa na kumchana kuwa lengo ni Esmile kuwa mpenzi wake. Esmile alimkatalia Rahel na kumwambia kuwa tayari yeye ana mpenzi wake.

‘‘Najua kuwa we unajidai una mpenzi kwa sababu wewe unampenda, lakini yeye hana mpango nawe’’ Mapigo ya moyo ya Esmile yakapiga kwa nguvu na kumuuliza kama anamjua mpenzi wake.

‘‘Ndio namjua, ni Mam,” jibu lile lilimshitua na kujiuliza moyoni kumbe Mam hana mpango nae

‘‘Hapana Rahel, Mam ni rafiki yangu tu” akamzuga na kuendelea kushikilia msimamo wake.

Ilikuwa ni kazi nzito sana kwa Esmile kumuelewesha kuwa yeye tayari ana mtu amempenda lakini hata hivyo alijaribu. Ajabu Rahel hakuelewa, isipokuwa alitengeneza bifu kubwa sana kwa Esmile na kuwa ni adui yake.

Esmile wala hakujali, alimpuuza tu na kujisemea moyoni, ‘laiti kama Mam ndio angenuna, ingekuwa ni shughuli pevu, lakini Rahel.., yeye anune tu na ikiwezekana avimbe kabisa hadi apasuke’ juhudi za Rahel zilionekana kugonga mwamba pia mikakati ya Esmile kumpata Mam nayo iliendelea, lakini Rahel ameshakuwa kikwazo…

Wakati akitaka kuamini kauli za Rahel kuwa Mam hana mpango nae, akili nyingine ikamtaka kupuuza kauli hiyo ya Rahel, akakaza buti zaidi akiamini ipo siku tu atakubaliwa na Mam. Hakuacha wala kupunguza kupiga simu kwa Mam.

Siku moja alipopiga simu na kumwambia anaomba waonane. Mam akakubali na kumtaarifu kuwa ataenda Muhimbili jioni, mama yake ni mgonjwa, hivyo wakakubaliana wakutane siku hiyo huko Muhimbili maana Esmile naye aliomba kwenda kumuona mgonjwa.

Walikutana wodini na kumtazama mgonjwa, kisha wakatoka kuelekea katika mgahawa uliopo palepale nje ya hospitali ili wazungumze huku wakipata vinywaji. Esmile alitumia muda ule kuendelea masuala yake kwa Mam. Mam alionekana hana pupa wala papara, hivyo alimuachia nafasi Esmile ya kuongea na kujieleza kwa mapana yake pasina kumkata kauli.

Esmile akaanza kuchombeza tena kwa kumwambia Mam;

“Ujumbe ninaokufikishia Mam, unatoka moyoni kabisa, sehemu ambayo nimehifadhi watu muhimu na vitu ambavyo sitamani kuvikosa, kwa kuwa hivyo basi, napenda ujue kuwa hata nawe ni mmoja kati ya watu ambao sipendi kuwakosa,” akatulia na kumuangalia, kasha akaendelea

“Kutokana na kutokujua msimamo wako hadi sasa, Napata wakati mgumu mno kufanya baadhi ya mambo ambayo natamani kuyafanya kwako, nalazimika kuumia ndani kwa ndani pasina kujua ni lini itakuwa mwisho wa maumivu haya,”

“Pole sana Esmile,” aliongea Mam kwa sauti ya taratibu isionyesha kushughulishwa kabisa na maneno ya Esmile, akaendelea

“Ni kitu kimoja tu kama ningekuwa na uwezo nacho, basi ndio kitu pekee ninachotamani kukufanyia Mam, lakini kwa kuwa nakiri kuwa siwezi, basi ningependa tu ujue kitu chenyewe ili hata siku ukikaa unikumbuke kwa hicho.”

“Mh, hitu gani hicho?” aliuliza sasa kwa shauku;

“Ningekupa uwezo wa kujiona ulivyo muhimu kwangu kupitia moyo wako, ungegundua kuwa bado macho yalikudanganya kwa umbo na sura yangu, kwani ndani ya moyo wangu kuna kitu kikubwa zaidi ya hiki kinacho onekana kwa macho yako mawili Mam,” Esmile akaegamia meza iliyo mbele yake na kumshika mkono Mam, kasha akasema

“Nakupenda Mam,”

“Kwa lipi hasa?” lilikuwa ni suala la kero ambalo Mam aliona kama anapoteza muda wake kwa kuendelea kukaa pale, lakini nae alithamini mno uwepo wa Esmile.

“Mam mi sijakupenda kutokana na uzuri wa sura yako ama mvuto wa mwili wako, ama ulaini wa ngozi yako, maana miaka 20 ama 25 ijayo kama utakuwa hai huo uzuri ulionao leo, nina hakika hautakuwepo tena,”

“Leo Mam kila mwanaume atakae kuona lazima akusifie sura yako mzuri mno isiokuwa na hata chunusi moja, lakini mbele miaka kadhaa itajikunja na kuleta mafinyanzi…”

“Kifua chacho chenye Matiti mazuri hakitadumu hivyo miaka 10 mbele, kitakuwa na mabadiliko, maana utahitaji kuzaa, itakulazimu kunyonyesha kama ilivyo asili ya sisi wabantu…”

“Tukija kwenye suala la ngozi yako laini Mam…” Esmile akamshika viganja vya mikono na kumchezea chezea huku akiendelea kuongea nae na Mam akimsikiliza kwa umakini mkubwa

“…sasa tumetawaliwa na ajali, kila mara sasa kama si bodaboda tunazopanda, basi hata usafiri wa jumuia tunaopanda, linaweza kutokea lolote, ajali husababisha makovu na majeraha ambayo huharibu ngozi zetu, naomba Mungu atuepushe lakini…” Mam akatikisa kichwa kumuunga mkono.

“Mwili huo wenye mvuto nao utakwenda kutokana na majira husika, itafikia hatua utazidi uzuri na hata kuporomoka uzuri wako, ndio maana ninasema kuwa sijakupenda kwa mwili wako, maana nikikupenda kwa mwili wako, miaka kadhaa ijayo utakapobadilika kwa sababu nilizo zieleza mwanzo, nina hakika nitakuwa sikuhitaji tena, maana kile nilichokupendea utakuwa huna tena.”

Maneno yalikuwa ni kuntu, hata Mam yalimvutia, lakini pamoja na kuwa Mam hakuwa na mpango wa kuwa na mpenzi kwa wakati ule, alimthamini na kumjali pia alimsikiliza mazungumzo yake kwa umakini wa hali ya juu japo moyoni alitambua kwamba hayupo tayari kuingia kwenye mapenzi.

Umakini ule ulimfanya Esmile aamini mawazo yote ya Mam yapo pale hivyo ikasababisha awe huru kujieleza na kueleza hisia zake kwa uwazi na kujiamini. Aliongea kwa marefu na mapana pasi na bughudha yoyote, hadi alipomuuliza Mam kama anamuelewa.

Mam akatikisa kichwa kukubali kuwa anamuclewa, akamshukuru kwa kumpenda na kwa hivyo basi ameonyesha imani yake, ila kuna kitu kimoja kilijionysha katika sura ya Mam.. masikitiko.. ni wazi kuwa itakuwa ni huzuni kwa Esmile kutokana na jibu atakalotoa muda mchache ujao, ni dhahiri hatolipenda na halitomfurahisha kabisa.

Japo hakuwa na mpenzi, Mam akatumia busara kubwa kumtoa Esmile kwa kumwambia ana mpenzi tayari, tena ni wa kitambo sana..

“Na ninaamini nampenda kwa dhati kama anavyonipenda, sasa kwanini nimsaliti? Esmile naomba unisamehe kwa hili, hatukuonana tangu siku ile na tulikaa miaka miwili…nina mtu tayari na tuna malengo…. nakushauri utafute mpenzi mwingine, ila tu usikurupuke, utafanya uamuzi ambao si sahihi na mwisho utajilaumu bure!’’

Haikuwa kauli nzuri kwa Esmile, pia hakuitegemea wala kudhani kama atajibiwa vile, lakini ilimfariji na kumfanya ajione wa thamani na anapendwa, ila bahati mbaya tu amewahiwa.

Laiti angeliwahi nafasi ingelikuwa yake kwani Mam alionyesha kumthamini na kumpenda ndio sababu kamshauri asifanye papara bali atulie ili ampate mpenzi muafaka.

Baada ya kukataliwa na Mam kuwa mpenzi wake, Esmile akasema japo hilo limeshindikana lakini waendele tu kuwa marafiki na hilo halikuwa na kipingamizi kwa Mam, waliahidiana ushirikiano wa hali na mali…

Mambo yakaendelea na yalikolea kweli kweli, urafiki ukachanua na kukua kiasi kwamba kila mmoja akitaka kwenda sehemu anayohitaji kampani hawezi kwenda bila mwenzie… Mam tayari alikuwa amefanya mtihani wa kidato cha sita akisubiri majibu yake hivyo muda mwingi alikuwa huru na alikuwa nyumbani tu.

Esmile alikuwa anautumia muda ule wa mapumziko wa Mam vizuri sana, maana kila wiki walitoka. Wakati huo Esmile nae alikuwa akiendelea na masomo yake ya sheria katika Chuo Kikuu Huria. Kila mmoja alikuwa akimpa moyo mwenzie, Mam akimsisitiza Esmile afanye kazi kwa bidii na wakati huo ajitume katika masomo yake.

Esmile nae alikuwa akimpa moyo Mam aliyekuwa akisubiri matokeo yake ya kidato cha sita kuwa yatakuwa mazuri na hatimae atatimiza ndoto zake za kuwa Mchumi, ndoto ambayo ni tangu utotoni.

**********

Ndani ya miezi mitatu ya urafiki wao, hakuna aliemuona mpenzi wa mwenzie wala kumsikia walau sauti na hata kusikia mtu akizungumzia suala la mapenzi. Esmile alijua Mam ana mpenzi kutokana na kauli aliyoitoa kwake, lakini mbona katika kipindi chote hiki, hajawahi kusikia wala ya kumuona.

Hata kama unafika baharini kwa mara ya kwanza, upepo mwanana wa ufukweni, huweza kukukumbusha kitu ambacho hukuwahi kuota kukikumbuka, kwani raha uipatayo ni adhimu na haipatikani pengine popote ila tu ufukweni.







Ndio hali aliyokuwa akiipata Esmile kila mara wakati alipokuwa akiwa na Mam, lakini kila mara alikuwa akitamani mno kumjua huyo Mpenzi wa Mam ni yupi? Yupo wapi? Yupoje? Kwanini hawa wasiliani nae? Akawa anakosa majibu.

Upande wa Mam nae alikuwa akijiuliza hivyo hivyo, tena yeye alifikiri kitu ambacho Esmile hakukiwaza, nacho ni kuwa ndani ya kipindi chote hicho, Esmile hakuwahi kupiga wala kupigiwa simu na mpenzi wake walau mara moja wakiwa pamoja, tena mara zote wakiwa pamoja simu yake huwa wazi, na kuna wakati huwa yeye ndio huzishika simu zote, lakini hajawahi kusikia simu yoyote ya kimapeenzi, ama ni kweli Esmile hana mpenzi?

Esmile akawa ndio mtu wa kwanza kushindwa kuvumilia, yaani uzalendo ukamshinda, akamuuliza Mam kuhusu mpenzi wakehttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Samahani Mam kwa kuingilia maisha yako binafsi, vipi mpenzi wako, hajambo? Na mbona sijawahi kukuona nae, kumuona sura yake na hata kumsikia na sasa mi nawe tuna ukaribu wa miezi mitatu, niaje?” Mam akacheka na kumwambia asijali ipo siku atamuona na kumjua, asiwe na haraka.

“Mam miezi mitatu hii sasa,” alijitetea Esmile akiwa na tabasamu usoni ambalo likalazimisha Mam nae atabasamu na kuhoji

“Pia hata mi nilikuwa nikijiuliza swali hilo kuhusu wewe...”

“Aah Mam, yaani kumbe hukuniamini nilipokwambia kuwa sina mpenzi?” akajiwahi Esmile.

“Basi basi tuyaache hayo,” Mam alimkatisha Esmile ambaye aliendelea kuomboleza

“Mam samahani ninarudia tena, si kama nimesahau, hapana! Ninakumbuka kuwa uliniambia una mpenzi, ila tu mi ninaomba unipe nafasi, ninaomba niwe mpenzi wako Mam, kwanini wautesa moyo wangu lakini?”

Pamoja na kubembeleza, Mam hakuwa tayari kutoa nafasi ile kwa Esmile aliendelea kushikilia msimamo wake, kwani tayari alikuwa na kovu moyoni… kovu ambalo aliamini halitofutika milele.

“Esmile unaijua sakafu?” Mam aliuliza swali ambalo Esmile wala hakulitegemea

“Sakafu? Sakafu naijua ndio! Si unamaanisha hizi zinazojengwa kwenye majumba ama ipi? Maana sijaelewa hapo swali lako.”

“Mi nimekuuliza tu kama sakafu unaijua,” alisema na kutabasamu Esmile akaitika haraka haraka kuwa anaijua ndio.

“Sakafu sio zulia ambalo unaweza kulihamisha kwa wakati wowote uutakao, sakafu haihamishiki labda kwa nyundo, lakini hapo napo huharibika na huwezi kuiita tena sakafu…” alimaliza Mam na kunyamaza.

“Unaamaanisha nini?”

“Mapenzi ni kama sakafu ndani ya moyo, hayahamishiki hata kwanini, ukilazimisha kuyahamisha ni sawa na kuvunja sakafu ndani ya moyo,” aliponyamaza tu Mam, Esmile akadakia

“Sasa Mam si kila mtu anafaa kumpa nafasi ndani ya moyo na kumjengea sakafu, ni watu wachache mno wanaostahili haki hiyo,”

“Namjuaje?” aliuliza kwa kebehi Mam.

“Ni mtu amabe anakupa wewe nafasi ya kwanza kwa kila sehemu anayostahili kuwa yeye, anae weka rehani maisha yake na utu kwa ajili ya upendo wake kwako, nasi Yule anaesimama na kukuita kwa majina mazuri yenye kunakshi mapenzi na hali unaumwa upweke japo upo ndani ya mapenzi,”

Siku hiyo Mam alitepeteshwa sana na amneno ya Esmile, ikamlazimu kufunguka na kumueleza Esmile kwamba ana kovu kubwa kuhusu mapenzi…

“Esmile nina ogopa sana mapenzi…nina kovu ambalo halitaweza kufutika moyoni kwangu” Esmile haraka na kwa shauku kubwa akatamuuliza ni kovu gani hilo? Akamjibu ni siri yake tu na japo inamuumiza nafsi yake, lakini daima hatoisema. Mpaka hapo Esmile alishaona mwanya, akaamini akiutumia vizuri anaweza kupata ile nafasi isiokuwa na mwenyewe.

Hakuwa na haraka aliendelea kumbembeleza taratibu huku akimliwaza, kila alipomkuta mpweke alimchangamsha, alipomuona amepoa, alimtembeza huku na kule, Mam akawa ni mtu wa furaha wakati wote akiwa na Esmile.

Siku zilizidi kukatika na maisha yakawa yanasonga huku wawili hao wakiwa karibu zaidi…kama kawaida ya wanawake, wema unapomzidia kuanza kubadili mawazo na vitu vidogo vidogo hubasilisha mawazo yao.. kutokana na kumjali na kumthamini, siku moja akaamua kuvunja ukimya na kumueleza jambo linalomsibu na kumuuza kwa miaka mingi…

“Esmile hapa nilipo mi si bikra, najua unaweza kuchukulia jambo hilo katika hali ya kawaida kutokana na tulivyo mabinti wa sasa, ila kwangu mi hilo ni tatizo, tena ni kubwa sana, kwani sikuwa tayari kwa ngono hadi ndani ya ndoa, malengo yangu yalikuwa hivyo ila kilichonitokea ndio kikasababisha kuipoteza malengo yangu katika hilo..”

“Oh! Pole sana, ulipatwa na nini Mam?”

“Esmile katika mapenzi yangu sijawahi kufanya mapenzi kwa ridhaa yangu, kifupi ni kuwa..(huku akitazama kila upande) .. Esmile nilibakwa, nilibakwa na mtu wa makamo sawa na baba yangu!” akaanza kulia Mam..

Esmile akanyanyuka alipokuwepo na kumsogelea na kumpa pole huku akimpigapiga mgongoni kwa mapenzi makubwa. Alimpoza na kumuuliza kama anaweza kumtambua mtu huyo iwapo atamuona.

Akamjibu kuwa japo ni zaidi ya miaka kadhaa tangu kutokea tukio lile, anahisi akimuona atamkumbuka. Esmile alionekana kuumizwa sana na tukio lile, kitu ambacho kilimfanya Mam amuulize kama atamuacha na kuvunja urafiki wao.

Esmile akamuhakikishia Mam kuwa yeye anampenda tu na urafiki wao utaendelea… lakini alikuwa na mawazo mengi sana juu ya stori ile aliyopewa… Bado alikuwa na fikra mchanganyiko kama aendelee kuomba nafasi au aruke kimanga? Mam hakupenda tena kuendelea kulizungumzia suala lile, kwani hatambui hata atamuona wapi mzee yule. Lakini Esmile alikuwa na jambo moyoni na alitaka kumueleza Mam…



Kila mmoja akazama katika fikra zake, japo Mam alipendekeza waliache jambo lile, ila Esmile lilimgusa sana. Akajikuta ameropoka

“Mam nakuahidi faraja nimeumizwa sana na stori yako, japo siku zimepita lakini huyu mtu ningemfahamu kuna jambo ningemfanyia… nae ajute na kupata maumivu kama aliyokusababishia,” hapo Mam akatabasamu kwa kuona kuwa kumbe kuna watu wanaguswa na matatizo ya wengine.

Kimya kifupi kikatawala, Esmile akakivunja kwa kuendelea kumuomba Mam ampe nafasi, bado akagoma na kumshauri ni heri amchagulie mpenzi anaempenda yeye kwa dhati.

Mshangao ukamvaa Esmile na kujiuliza mwenyewe, mtu anipendae mi kwa dhati? Mtu huyo ni nani? Alijiona mjinga kujiuliza mwenyewe wakati mtu aliesema alikuwa palepale, akahoji ni nani huyo ampendae kwa dhati?

“Rahel ndio mtu anaekupenda wewe kwa dhati na ninatambua hilo kwa sababu ameisha diriki kuniambia nikuunganishe nae hasa baada aya kuongea nawe na ukamtolea mbavuni, lakini bado anakupenda,” hilo ndio jibu akajibiwa na Mam.

Esmile akajibu mapigo kwa kumwambia kama yeye hamtaki basi, wala hahitaji mpenzi mwingine. Mzozo uliendelea hadi usiku, baada ya taabu nyingi na ushawishi wa muda mrefu na ahadi za uaminifu, Mam akakubali kuwa mpenzi wake kwa sharti la kutokufanya mapenzi hadi watakapo funga ndoa.

Hilo halikuwa zito kwa Esmile, alifurahi, alimkumbatia Mam na kumbusu, akamnyanyua na kumshukuru kwa kukubali kuwa mpenzi wake.

Muda wote huo Mam alikuwa ni mwenye tabasamu usoni mwake, hata nae alifurahi kutokana na mapokeo ya ile kauli yake kwa Esmile ya kukubali kuwa mpenzi wake. Hata watu waliokuwepo eneo lile walionekana kushangaa, walijua kuwa mtu yule amefurahi sana japo hawakujua ni kipi kilichomfurahisha.

Baada ya mazungumzo ya siku hiyo yaliyokuwa na mafanikio makubwa kwa Esmile, taratibu akaanza kumrejeshea tabasamu lake ambalo lilipotea kitambo sana, hakika alimrejeshea Mam furaha yake iliyopotea kitambo, furaha aliyoipata kwa wazazi akiwa ni mtoto, kisha baadaye akaipoteza mara tu alipobakwa.

Tangu hapo hakuwa na furaha tena hadi sasa anapokuwa na Esmile ndio huwa na furaha inayotokana na faraja aipatayo toka kwake, faraja ya maneno yake matamu na vitendo adhwiim ambavyo amekuwa akimfanyia.

Alijitahidi kumfanyia kila ambacho aliamini kitamfariji ili tu amjengee imani kwamba si kila mwanaume ni mtu mbaya.

“Siwezi kufanya maisha yako yakawa kamili Mam, bali naweza kufanya maisha yako yakatawaliwa na furaha kila wakati,” aliongea Esmile mara kwa mara kauli ile na kumfanya Mam awe na amani kuwa sasa atakuwa ameipata faraja kweli.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Nakubaliana nawe Esmile, kubadili maisha ya mtu mwingine haihitaji kuwa na utajiri, kuwa mzuri ama mtu alie kamilika, ila unapaswa kuwa unajali, nafurahi kukueleza kuwa, napenda sana unavyonijali,” aliongezea Mam na Esmile akasema

“Usijali Mam nafanya hivi kwa sababu nakupenda sana,” akamsogelea na kum kiss shingoni kwa upande wa kushoto, kasha akamnyanyua waondoke, maana muda ulikuwa umekwenda sana.

Kwa kiasi kikubwa alifanikiwa kwa hilo na hata kumfanya Mam ajute ndani ya nafsi yake kwanini hakumpa nafasi mapema zaidi ya pale. Na hapo ndipo alipoamini kuwa viumbe tumetofautiana sana, na katu hatuwezi kuwa sawa

“Niliwahukumu wanaume wote kuwa ni watu wabaya, lakini walio nitendea maovu ni wawili tu, lakini huyu mmoja amekujaa kuwasafisha wanaume wote, lakini je huyu Esmile mwisho wake ni nini kwangu?” aliwaza Mam ambae alikuwa ameketi pembeni ya Esmile aliekuwa akiendesha gari kuelekea Kigogo, nyumbani kwa kina Mam.

Waliwasili na Esmile akashuka na kumfungulia mlango, waliagana nje kwa mara ya pili na kuahidi watawasiliana mara tu Esmile atakapofika nyumbani kwao. Na huo ndio ulikuwa utaratibu wake.

Kila wakipata nafasi ya kutoka, basi walifanya hivyo, mara nyingi Esmile alimuuliza Mam anataka kwenda wapi? Lakini Mam hakuwa mwenyeji sana, hivyo karibu mara zote kazi ya kupanga wapi pa kwenda alimuachia Esmile ambae aliitumia vizuri hasa nafasi hiyo.

Siku moja alfajiri Esmile alimpigia simu Mam na kumwambia anataka kutoka nae asubuhi ileile, hivyo ajiandae atampitia saa 4, neno la Esmile kwa Mam ilikuwa halipingwi kirahisi sasa, kuna wakati lilipingwa, ila kwa kiasi kikubwa lilikubalika. Muda uleule aliamka na kuanza kufanya kazi za hapa na pale, alianza na za ndani kasha akamalizia na za nje.

Baada ya kuridhika na hatua aliyofikia tokana na kazi alizofanya, akaridhika na akaamua kijiandaa kwa ajili ya kutoka na Mpenzi wake.

Kama alivyoahidi Esmile, saa 4 asubuhi ile, alipaki pikipiki ya kukodi nje ya hotel ambayo haikuwa mbali sana na nyumba ya kina Mam na kumpigia simu. Ilikuwa ni pikipiki aina ya HARLEY DAVIDSON SPORTS ya rangi ya bluu, nae akiwa amevaa pensi ya jinzi ya rangi ya bluu na singland nyeupe.



Miwani ya giza ya rangi ya bluu alikuwa ameiweka mbele ya macho yake, raba fupi sana za rangi nyeupe maarufu kama Simple, ndio zilimuhifadhi kwenye miguu na kichwani alijifunga kitambaa cheupe chenye ribbon za bluu, sio siri alipendeza sana.

Aliingia ndani ya Hotel huku akiongea na simu, alipomaliza tu kuongea akasogea Kaunter akanunua baadhi ya mahitaji aliyokuwa akiyahitaji na kutoka nayo nje hadi ilipokuwa pikipiki yake na kuweka mfuko wake aliotoka nao ndani ya hotel.

Simu yake ikaita, akaitazama na kabla hajaipokea, akanyanyua sura na kuangalia ilipo nyumba ya kina Mam, aliweza kuona watu kama wawili mlangoni, ishara ya mkono kumuita ikamfanya adandie pikipiki na kusogea eneo lile kwa mwendo wa taratibu mno, akafika hadi usawa wa wale watu wawili lakini Mam hakuwepo.

Baada ya kuwasalimia, kabla hajawaulizia, mmoja kati ya watu wale wawili waliokuwa wamesimama mlangoni, akafungua mlango na kuingia ndani.

Hapo sasa ndio Mam nae alijitokeza akiwa amependeza mno, maana alivaa pedo nyeupe na raba kali ya bluu, akavaa kitop cheusi na miwani kubwa nyeusi sana, kisha kichwani alitundika kapelo matata sana ya rangi nyeusi. Alishangaa kumuona Esmile kivile tena akiwa na pikipiki.

Mgongoni Mam alibeba lasket yenye kamera na mambo mengine madogo madogo ambayo alitakiwa kuwa nayo kama alivyojulishwa na Esmile.

Sehemu ya nyuma kabisa ya pikipiki, Esmile aliweka begi la wastani la rangi nyeusi, ndani kukiwa na mpira wa miguu na boya, vyote vikiwa havina upepo. Pia kulikuwa na mwavuli mkubwa wa kukunja na pampu ndogo. Kwa kweli sio wao tu waliopendeza bali pia hata usafiri walioutumia ulivutia mno.

Kama unavyojua mambo ya mwisho wa wiki, watu wengi huwa majumbani mwao, hivyo majirani kwa kina Mam waliwatolea macho kweli kweli… hasa ukizingatia kule eneo hilo ni uswahilini. Waliondoka eneo lile na kuelekea ufukweni.

Kule unafikiri nini waliacha? Hakuna, ilikuwa ni furaha tupu, wakikimbizana huku na kule, walicheza aina zote za michezo, walipigiana mpira, huyu akipiga, yule anadaka, hivyo hivyo hadi jioni.

Muda fulani Esmile alikuwa amechimba shimo palepale ufukweni na kumfukia Mam mwili mzima akimuachia kichwa tu. Mambo mengi waliyofanya pale, yalikuwa ni mageni kabisa kwa Mam, hivyo Esmile aliweza kuingiza kitu kipya kwenye kichwa cha Mam, kitu ambacho hata yeye mwenyewe Esmile hakujua kama anaingiza kitu ndani ya akili ya Mam.

Ni furaha ilitawala siku mzima na hawakukumbuka kula chochote hadi jioni wakati waliposhika begi ili kurudisha vitu walivyotumia ndio wakagundua kuwa bado hawajala.

Mam akatoa vyakula alivyokuwa ameviandaa na kuviweka juu ya kijimkeka kidogo lakini kizuri cha plastiki, vilikuwa ni vyakula vingi, yaani aina nyingi ila kwa kiwango kidogo kidogo.

Hata hivyo waligusagusa tu, zaidi walikunywa tu soda zao na vilivyobaki wakarejesha vinavyopaswa kurejeshwa na kasha wakajipakia katika pikipiki na kurejea makwao wakiwa hoi.

Saa 2 usiku ndio Mam aliwasili kwao na baada ya kuingia ndani, Esmile nae akaondoka kuelekea nyumbani kwao akiwa na mchoko wa kutosha.

Mam ndio alieanza kumtafuta Esmile baada ya kumaliza mambo yake aliyokuwa akifanya, ikiwa ni saa nne usiku akampigia simu. Mwanzo iliita lakini wala haikupokelewa , lakini alipopiga mara ya pili ikapokelewa kwa sauti ya bashasha mno.

Mam alimtaka msamaha kwa kumsumbua usiku ule ila tu alitaka kumwambia kuwa amefurahi sana siku ile, kwani kila alichokifanya siku ile ni kitu kipya kabisa kwake.

“Esmile nimewahi kwenda beach mara nyingi sana sina hata idadi, lakini haya tuliyofanya leo ni mambo mapya kabisa kwangu, ahsante Mpenzi wangu, wala sijuti kuwa nawe kwa sasa, bali natamani ingekuwa ni miaka mitano nyuma huko,”

**********



Baada ya kuwa ni siri ya muda mrefu, hatimae Esmile akaamua mwambia Mam kwamba umefika wakati sasa akamtambulishe nyumbani kwao. Mam alikataa katakata kwa kudai ni mapema mno, lakini kwa ushawishi wa Esmile akakubali na siku ileile bila hata ya kujipanga akamchukua hadi nyumbani kwao.

Kutokana na kutokuwapa taarifa wazazi wake juu ya tukio lililotokea wakati ule, hawakumkuta Mzee Hanson kwani alikuwa amkwenda Kimanzi chana yalipo mashamba yake. Walimkuta Mama peke yake akafurahi sana kwa kitendo kile cha Esmile na kuwabariki kwa uchumba mwema na kuwataka wao wawe mfano kwa jamii ya vijana.

Zaidi akawaambia atamfikishia furaha yake pia http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Mzee ambaye anaamini naye atafurahi. Siku nzima waliitumia kule Tabata, hadi jioni walipoondoka na kuelekea kwa kina Mam, lakini kwanza wakashuka Savoy ili Esmile akawasalimu rafiki zake na kuwajulisha kwamba tayari amemuona mpenzi wake na sasa wapo pamoja tena.

Akiwa na furaha tele kwani ilikuwa imepita muda mrefu sana Esmile hajafika mitaa hiyo, alifika na kumkuta Moody, alifurahi sana kuwaona, Esmile alipomuulizia Imraan akaambiwa ni mwaka sasa tangu alipofariki. Alisikitika sana ila akakubali matokeo.

Mam hakumjua Imran ni nani. Alipouliza akaelezwa na kuelekezwa kuwa Meneja wa hotel ile kuwa ndio Imraan, alipomuulizia Juma akajibiwa kuwa na kitambo aliisha acha kazi.

“Ndugu yangu hapa kwa sasa nimebaki mie tu katika wale wakongwe uliotukuta kipindi hicho cha nyuma, karibuni sana,” alisema Moody kwa majonzi.

“Usijali ndugu yangu, tutafika tangu sasa kila wakati ambapo tutapata nafasi, tutakutembelea,” alimpa moyo Esmile na hali akijua kuwa ni suala gumu.

“Nitafurahi ndugu, na ukija sasa usiniulizie tena kwa jina langu, maana sasa mii ndio Meneja wa hotel,” akatabasamu na Esmile pia akatabasamu na kumpa mkono wa pongezi, kasha wakaagana. Muda walioutumia pale haukuzidi nusu saa kisha wakaelekea Kigogo.

Njia waliopita ilikuwa ni barabara ya Matumbi na kwenda kutokea Kigogo mwisho. Walisimama mbele kidogo ya nyumba ya kina Mam lakini wakiwa ndani ya gari na kuanza kujadiliana juu ya simu. Mam alitaka kujua kama Esmile ni mwaminifu. Japo alimwamini ila alitaka tu kujiridhisha. Alichokitaka ni kubadilishana simu na Esmile usiku ule.

Mwanzo Esmile alikataa na kusema anahisi mwisho wa usiku ule, yaani asubuhi ya kesho kitakachofuatia ni ugomvi na hatimaye kutengana kwa sababu ya simu, kitu ambacho hatamani kitokee hata kwa bahati mbaya.

“Kivipi?” Mam alihoji..

“Simu hii naitumia kwa shughuli zote ziliwemo za kiofisi…lolote linaweza kutokea maana usiku nimrefu….” Mam hakuridhika na jibu, akauliza kama Esmile anamuamini, akamjibu kuwa ndio, na hiyo ndio ilipelekea kumchagua yeye awe mpenzi wake.

“Sawa… Pamoja na mambo ya kiofisi lakini pia huwa kuna matumizi mabaya ya namba za simu kwa watu ambao huenda tuliwapa kwa nia tofauti sasa naingiwa hofu kukuachia halafu leo ndiyo litokee hilo please...”

“Nimeridhika na jibu lako, lakini bado msimamo wangu upo palepale, sasa wewe unafikiri tatizo hukimbiwa? Tatizo inapaswa kupambana nalo, hivyo cha kufanya sasa ni kunipa simu yako kama ilivyo na ushike hii...” bosi wako akipiga nitamwambia mimi ni mtu wako nitampa namba ambayo unapatikana shida iko wapi?

Esmile alijaribu kujitetea kwa kila hali lakini bado Mam alishikilia palepale na hatimae Esmile akalegea na kutoa simu mfukoni mwake na kumuonesha Password ya simu yake na kumtaka ajaribu palepale mbele yake.

Mam akajaribu zaidi ya mara tatu, waliporidhika kuwa ameielewa vema, wakaagana na kasha yeye Esmile akarejea nyumbani kwao akiwa na simu ya Mam, huku yake ikiwa kwenye mikono ya Mam.

Alipoingia tu ndani akawakuta wazazi wake na kuwasalimia kisha akataka kujua habari za shamba toka kwa baba yake, alimjibu kuwa ni safi na amekuja na madafu, Esmile ni mpenzi mkubwa sana wa madafu, hivyo alifurahi.

Akaenda kuoga na aliporudi akajichanganya na wazazi wake aliowakuta wakipata chakula cha usiku, akajiunga nao, baba yake alimueleza kuwa amepata habari zake juu ya kumpeleka mchumba wake pale nyumban. Alikiri na kumwambia baba yake kuwa yule ndio mwanamke aliemtafuta kwa zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Pia akamtajia jina la mchumba wake na kumuahidi baba yake kuwa atamuoa huyo binti mara siku chache zijazo. Mzee wake akampa nasaha fupi juu ya mapenzi ya vijana na mwisho akamueleza umuhimu wa kuwa wachumba kwa hatua ambazo ni za halali kama alivyo anza huko kwao.

Zaidi ya yote akaelezea jinsi alivyofurahi kutokana na kupata kwa habari hizo.

“Na suala hilo umelipanga kulifanya lini mwanangu?” aliuliza baba yake, na Esmile akamwambia kwamba baada ya miezi 6 atamaliza yale ya sheria na hapo ndipo mipango ya ndoa itaanza

“Lakini nakumbuka kama umeniambia kwamba nae anasoma huyo binti, ama sikukuelewa vizuri?” aliuliza mzee Hanson akiwa makini.

“Ndio, anajitayarisha kuingia chuo kwa sasa, lakini jambo la chuo haliwezi kutukwamisha kuhusu suala la uchumba hata ndoa mzee wangu,” alieleza Esmile.

“Ahaa! Licha ya kwamba Mam yeye anaweza kuwa chuo, lakini jambo hilo l8inaweza kufanyika?”

“Ndio baba, wala hakuna kipingamizi hapo.” Walimaliza mazungumzo yao na kila mmoja akashika hamsini zake.





Kuna jambo moja ambalo Esmile alikuwa akilifanya mbali na mambo yote yanayo fahamika juu yake. Hii ilikuwa ni kujifunza sanaa ya mapigano yaani katare na alifanya hivi kwa lengo la kujenga mwili wake na kujilinda, alimini baada ya kuhitimu sheria anataka kuwa mpelelezi binafsi (Private Investigator) pia akiwa kama mwanasheria wa kujitegemea, hiyo ndio hasa ilikuwa ni ndoto yake.

Kasi ya masomo na mazoezi ya nguvualiyokuwa akiyapata, ukijumlisha na penzi zito toka kwa Mam, vilimfanya Esmile awe ni mtu mwenye kazi nyingi kupita kiasi, hata nyumbani sasa akawa si mtu wa kuonekana sana.

Wazazi walikua wakijua ni nini lengo la mtoto wao, hivyo wala hawakuumizwa na hilo, labda tu suala la kuwa muda mwingine huutumia akiwa na Mam, hilo ndio walikuwa hawalijui.

Kila alipokuwa anapata muda mchache wa kufanya mapumziko, basi aliutumia muda huo kwa kuwa na Mam na alipokuwa nyumbani, yaani mbali nae, basi simu ilihusika sana, walikuwa kwenye kiwango cha juu mno cha mapenzi.

**********



Miezi 6 baada Esmile alimaliza masomo yake, kwao ikaandaliwa sherehe fupi ya kumpongeza, hii ndio siku Mam na Mzee Hanson walionana kwa mara ya kwanza. Kabla hawajatambulishwa, Mam alishtuka sana kumuona Mzee Hanson, alimkumbuka vema.

Hanson, baba Esmile hakukumbuka lolote, hakumjua Mam ni nani, Mam nae katika kutaka kumjua zaidi, akamuuliza Esmile yule Mzee ni nani? Esmile hakujua Mam alimaanisha nini, akamjibu akiwa na tabasamu usoni kuwa, wala asiwe na haraka, atamtambua baada ya kumtambulisha.

Amani na furaha ya Mam ilitoweka, akatamani amrukie Mzee yule na kumrarua kama afanyavyo Simba kwa wanyama wadogo awapo na njaa kali, hata hivyo alimudu kujizuia.

Sherehe fupi iliyokuwa imehusisha watu kadhaa marafiki wa familia na majirani ilifanyika na ukafika wakati wa Esmile kumtambulisha mpenzi wake ambae ni mchumba wake, alimnyanyua mama yake na kumwambia yeye tayari anamfahamu mkwe wake, kisha akamnyanyua Baba yake na kumtambulisha kwa Mam kwani wao walikuwa hawajaonana, kisha akamshika mkono Mam na kumvisha pete ya uchumba.. vigelegele vikatawala.

Mam hakufurahi sana kama ambavyo Esmile alitegemea Mam atafurahi, ikawa ni kinyume, hata wazazi wakashangaa kwa kitendo kile, lakini hawakujali, walihisi hata kile kilio chake pale hadharani, huenda kilikuwa ni kilio cha furaha. Kumbe wangelijua.., wasingelikubali hata kidogo Mam avishwe pete ile na Esmile.

Sherehe haikuwa ndefu sana, bali baada ya kunywa vinywaji vilivyokuwa vimeandaliwa sambamba na vyakula vichache, watu wakasambaana. Wageni wakaanza kuondoka huku wakiwaacha wenyeji wakiwa na faraja ya ushirikiano wao.

Muda sio mrefu mbele, Mam nae akaomba kuondoka kwa kumwambia Esmile kuwa hajisikii vizuri, huenda kutokana na kitendo kile, ndio maana hali ile imemtokea, hivyo akaomba arejeshwe nyumbani kwao.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Safari ikaanza baada ya kuwaaga wazazi wote na wakiwa njiani kurejea nyumbani kwao, Mam alikuwa akilia tu njia nzima, Esmile akapaki gari pembeni na kuanza kumbembeleza amueleze kilichomsibu.

Mam aligoma na kung’ang’ania apelekwe kwao, wataongea siku ifuatayo na kumuomba Esmile hata usiku wa siku ile asimpigie simu, maana atakuwa ameizima. Esmile hakumuelewa bali alitekeleza matakwa ya Mam.

Usiku ulikuwa ni mrefu sana kwa Mam na alitamani kwenda kumtoa uhai Mzee Hanson ambae sasa ni mkwewe mtarajiwa, lakini akahofia sheria, akawaza suala la kumwambia Esmile kinacho msumbua.

Kwanza alikuwa na mengi kwamba amevishwa pete bila hata wazazi wake kujua, na kwamba Esmile hajajitambulisha nyumbani kwao licha ya kwamba Mam alimueleza Mama yake juu ya uhusiano wake na Esmile.

Alikuwa na mawazo mengi sana ila kwa usiku huo akaona njia sahihi ni kavuta shuka na kulala na kuutafuta usingizi ambao ulikuwa mgumu sana. Wakati akiwa katika mawazo ya kutafuta usingizi akaamua kuondoka Dar kwenda kupata mapumziko ya akili.

Asubuhi alipoamka alimfuata baba yake na kumuomba ruhusa aende Tanga kumsalimia bibi yake, baba yake alishangaa na kumuuliza mbona imekuwa haraka mno? Mam akajitetea kuwa amemkumbuka tu bibi yake wa jina lake.

Basi akaruhusiwa na kupewa mzigo aufikishe huko, akajiandaa na kutoka kwenda Ubungo na kuingia ndani ya basi hadi Tanga bila kumuaga Esmile wala kuwasha simu yake.

Hakika Esmile alimtafuta sana hewani Mam bila mafanikio, hadi jioni ya siku hiyo, hali ilikuwa ni ileile. Akaona haitakuwa sahihi siku mzima iishe bila kuwasiliana wala kumuona mpenzi wake, akafunga safari hadi Kigogo na kujitambulisha kuwa yeye ni mfanyakazi wa kampuni HEROS.

Alisema kampuni yao imemtuma kwenda pale kumtafuta Maryam Mahmoud, kwani wamejaribu kumtafuta kwenye simu yake ya mkononi hawampati.

Mama yake akauliza yeye ni nani? Akamjibu kwamba yeye ni Afisa Utumishi wa kampuni hiyo na sababu kuu ya kumtafuta ni kumpa majibu kwa barua ya maombi yake ya kazi ya muda (Tempo) ambayo aliwaandikia kipindi cha nyuma.

Baba nae akauliza amepajuaje pale, Esmile alikuwa amejipanga vyema kwa maswali kama hayo kwani aliyategemea na aliyapangua kama ananawa uso tu.

Akawaambia walioomba ajira wote kwenye kampuni yao, waliacha CV zao zilizoonyesha kila kitu, aliwajibu huku akiwa amejidai kama mtu anaaetafuta kabrasha Fulani, kumbe anawazuga tu, mwisho akajidai kakosa na kusema kuwa atakuwa amezisahau zile document ofisini kwao ambazo zimeweza kumpa muongozo ule.

Wazazi wakaridhika na kumwambia Mam amesafiri siku hiyo na kwenda Tanga. Mapigo ya moyo ya Esmile yakabadili mwendo, sasa ikawa ni kasi, akauliza atarejea lini? Mama akajibu itakuwa kati ya wiki tatu hadi mwezi mmoja.

Esmile akawaomba wazee wampatie taarifa hizo Mam, naye alimini kwamba Mam ataingia mtegoni kwa kuwa ni kweli alishawahi kumueleza kuwa amepeleka barua ya kuomba Tempo katika kampuni kadhaa na hajapata majibu. lakini akasisitiza kwamba kama hawatajali wampatie tu yeye namba ya mtu wa karibu naye ili mwenyewe awasiliane naye.

Wazee ambao walijua pia mikakati ya Mam ya kutafuta ajira ya kujikim wakati akisubiri kwenda Chuo wakaingia laini wakampa namba ya bibi yake Mam.

Akashukuru na kuaga akiahidi kumpigia siku ifuatayo wakati wa kazi.

Kitendo cha yeye kutoka, alikuwa ametoa mwanya kwa Mzee Mahmoud kuweza kufikisha furaha yake kwa mwane juu ya kutafutwa na ofisi yake aliyoomba nafasi ya kazi

“Kwenye hiyo Kampuni itakuwa wewe umefanikiwa sana, maana amekuja mtu moja kwa moja hadi nyumbani tena amekuja afisa mwenyewe wa hiyo kampuni.”

“Ni kampuni gani baba hiyo?” aliuliza Mam kwa shauku.

“Inaitwa HEROES ndio amesema,” akajibu baba Mam na kuleta mshangao kwa mwanae ambae aliruka futi 100 na kusema hajawahi kuomba kazi katika kampuni hiyo ya HEROES na wala hafahamu iko wapi na inafanya shughuli gani.

Wote wakapigwa butwaa lakini wakaamua kutulia na kususbiri matokeo. Baada ya kukata simu Mam alikaa na kufikiri mtu yule ni nani na kwanini afanye hivyo? Akakosa jibu. Lakini baada ya kukaa kwa muda mfupi na kukisumbua kichwa chake, alipata mwangaza, alihisi kuwa mtu yule anaweza kuwa Esmile.

Akashikilia hapohapo kwani aliamini bado anampenda sana ila matukio ndio yaliokuwa yakimuumiza. Akajua kuwa ikiwa ni Esmile na wamempa namba, basi ni lazima atapiga tu usiku uleule, akakaa kusubiri.

Haikuwa uongo, kufika saa 2 usiku ule, Esmile alipiga simu kwa kutumia simu yao ya mezani ambayo hata yeye Mam anayoitambua vema, maana ameisha pigiwa sana kupitia namba hiyo.

Mam akajishaua hakuipokea katika kuipokea hadi ikakata. Mara ya pili akapokea mapema tu na hata kabla ya kuongea chochote Mam, yaani baada tu ya salamu, Esmile alivyo tambua kuwa aliepokea simu ile ni Mam, akamuuliza;

“Hivi Mam mimi nimekukosea nini? Mbona unanifanyia hivi? Ama kosa langu ni kukupenda? Niambie… kuwa wazi tu,” maswali yalikuwa ni mengi na ya mfululizo mno hivyo Mam akakosa jibu, maana hata yeye alikuwa akimpenda sana Esmile.

“Esmile natambua unafahamu ni kiasi gani nakupenda, nina hakika unaelewa ni vipi nakuthamini na hata mie najua ni jinsi gani unanijali, kwa sababu hiyo basi, mi napenda wewe uwe na furaha muda wote…” Esmile akamkatiza kaulihttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Hapana Mam unanidanganya japo unanipenda, utatakaje niwe na furaha nawe unaondoka kwetu usiku ukiwa huna furaha, kisha siku ya pili unasafiri bila kuniaga, tena na simu ukiwa umezima, kweli mi nitakuwa na furaha ama nitapata wazimu?”

Kutokana na kauli zile za mfululizo, hata Mam sasa akajiona ni mkosaji, akafikiria jinsi alivyo ondoka nyumbani kwa kina Esmile na hata alivyokuwa analia ndani ya gari, akagundua kabisa kuwa alichokifanya si sahihi, ikamlazimu yeye sasa ndio aanze kumpoza Esmile na kumwambia kuna sababu ya muhimu ilisababisha afanye vile.

Alipomuuliza ni sababu ipi iliyomfanya aondoke kimyakimya? Mam akamjibu kuwa hawezi kumwambia kwenye simu hadi watakapo onana ana kwa ana.

Basi Esmile akamuomba siku ifuatayo ajitahidi kuwepo hewani siku nzima, Mam akakubali, hilo lilikuwa kosa kwani akili ya Esmile ilikwenda mbali na alikuwa amepanga jambo ambalo ili kuhakikisha anajua kilichosababisha Mam afanye hivyo.







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog