Simulizi : The Worst Valentine's Day
Sehemu Ya Pili (2)
“hodii,,,hodii” ilikuwa ni sauti ya mtu akigonga mlango wa chumbani kwangu,,nilishtuka na kukimbilia mlangoni.
“dada mbona mmelala mda wote hata chakula cha mchana hamjala” ilikuwa ni sauti ya Magret iliyokuwa ikiuliza.
“hamna tulipitiwa”nilimjibu kwa kifupi huku ile hali ya usingizi ikiwa bado imeutawala mdomo wangu.
“jiandaeni basi japo mle mda huu” aliniambia hivyo na kisha aliondoka na nilipogeuka Jamshid alikuwa tayari ameshaamka,,tulivaa na kujikongoja mpaka sehemu ya kulia chakula na hapo ndipo tena nilipokumbuka juu ya sadaka niliyotakiwa kuitoa kabla ya saa sita usiku,,,nilikurupuka pale na kukimbilia sebuleni nikatazama saa ya ukutani ikawa inanionyesha kuwa ilikuwa saa moja na nusu jioni,,hapo yalikuwa yamebaki masaa manne na nusu,,nilikimbia mpaka chumbani nikachukua funguo za gari na kutoka na ndipo nilipokutana na Jamshid pale mlangoni;
“kuna tatizo gani Faith mbona sikuelewi?” Jamshid aliniuliza kwa sauti iliyouumiza moyo wangu na nilisikitika kuwa sikuwa na la kumwambia zaidi ya kumdanganya kuwa nilikuwa na kikao na watu Fulani na sasa nilikuwa nimechelewa. Alinipisha na nilimbusu kisha nilimfata Magret pale alipokuwa na kumuaga;
“Magret, hakikisha kila kitu kiko sawa naenda kuonana na wafanya biashara Fulani, nitachelewa kurudi lakini hakikisha kuko sawa hapa nyumbani kabla hujaenda kulala” nilimwambia maneno hayo na kugeuka kuelekea nje,,nilimkuta Jamshid pale nje sijui alifikaje pale ila sikujali kwakuwa Jamshid sikuzote hupenda kunifungulia mlango wa gari,,alifungua mlango wa gari na niliingia ndani kisha akaufunga na mimi nikashusha kioo na kumbusu;http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“nakupenda sana Jamshid,,wewe ni maisha yangu,,wewe ni kila kitu kwangu,,siko tayari kukupoteza wewe au Magret katika maisha yangu,,naamini kabisa wewe na Magret ndio msaada pekee uliobaki katika maisha yangu”niliongea maneno hayo huku nikizuia machozi kunitoka lakini sikuweza,,Jamshid alinitazama huku machozi yakimlengalenga;
“nakupenda pia Faith,,siko tayari kukupoteza pia,,siko tayari kwenda mbali na upeo wa macho yangu, umenitoa katika shida na taabu na sasa najiona mimi ni mtu tena,,nashukuru sana kwa kila jambo,,sina la kukufanyia kudhihirisha upendo wangu kwako zaidi ya kukufanya uwe mwanamke mwenye furaha siku zote za maisha yako,,”maneno haya ya Jamshid yaliniliza sana kwakuwa nilielewa kuwa Jamshid hakufahamu kuwa nilikuwa na mtihani wa kuchagua kati ya shingo yake na ya Magret ipi niitoe sadaka,,nilimtazama sana na kuona hakuwa na hatia ya kustahili kufa,,nikawasha gari na kuondoka nilipofika getini Juma alinipa bahasha aliyodai kuna mtu ameileta na kuiacha pale getini,,,niliipokea na kuondoa gari kwa kasi,,kilomita 45 mbele nilifika msitu wa pande na ndipo hapo nilipokumbuka tena juu ya ile bahasha na niliifungua na kukuta kitambaa cheusi kilichokuwa na alama ya bikari mbili na kisu kidogo na sindano ndogo ya kushonea,,,nilielewa fika kuwa vile vilikuwa vifaa kwa kufanyia sadaka ile,,,nilifungua dirisha lile na kuvitupa kisha niliwasha ngamizi (laptop)yangu na kuanza kuchapa barua ya kujitoa kwenye kundi la freemason na kisha niliituma kwenda kwenye anuani ya barua pepe ya katibu wa kikundi wa eneo nililojisajilia lakini hapo hapo ujumbe ule ulijibiwa ya kuwa siwezi kujitoa kwa sasa mpaka kesho yake saa nne asubuhi,,nilizidi kulia na hapo nilizima ile ngamizi na sasa nilinyanyua simu yangu ya mkononi na kumpigia simu mzee Rorbahcho kumuarifu juu ya nia yangu ya kujitoa lakini pia simu yake haikupatikana,,mda huo saa yangu ya mkononi ilikuwa ikinionyesha kuwa ilikuwa ni saa nne na dakika arobaini na tano na sasa lilibaki saa moja na dakika kumi na tano kufika saa 6 kamili usiku,,niliwasha gari langu ili kuondokka eneo hilo lakini halikuwaka,,msitu wa pande ulikuwa ni msitu wa kutisha na sijui kwanini nilipita eneo lile,,nilitoka ndani ya gari na kuzunguka mbele ya gari ili kuangalia ni nini kimetokea kwenye boneti lakini nilishtushwa na sauti niliyohisi naifahamu;http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“faith” ilikuwa ni sauti ya mtu aliyeonekana kuwa na maumivu makali,,hofu iliniandama nikatazama nyuma na mbele lakini sikumuona yoyote,,nilirudi mpaka kwenye gari yangu na kufungua mlango lakini cha ajabu mlango haukufunguka na hapo ile sauti ilizidi kuita na ndipo nilipogundua ilikuwa sauti ya baba yangu,,jasho lilianza kunitoka na hofu ikazidi nilitazama kwa mbali nikaona sura ya baba yangu juu ya mti mrefu huku mwili wake ukiwa umekatwa mpaka kwenye kiuno kama siku ya mwisho nilipomuona pale ndani,,machozi yalianza kunitoka nikaanza kumwita lakini taratibu alianza kutokomea,,nilirudi tena kufungua ule mlango na sasa ulifunguka niliingia ndani ya gari na kuufunga na kuwasha gari ambapo mda huu liliwaka nilipandisha gia mpaka kwenye D na kukanyaga mafuta lakini nilishangaa kumuona mama yangu mbele ya gari akilia huku akijaribu kuniambia kitu,,nilizidi kutetemeka na mkojo ukinitoka lakini sikujua chakufanya zaidi ya kurudisha gari nyuma na kuondoka pale nilipokuwa,,njiani sikujua nilikokuwa nikienda lakini baada ya mwendo wa lisaa limoja niliitazama saa yangu na sasa zilibaki dakika 15,,nilijua dhahiri kuwa nitakufa kwakuwa nilishindwa kutekeleza maagizo yao,,nilijua kuwa sasa zilikuwa zimebaki dakika kumi na tano mimi kupata ajali au kufa kwa ajili yao,,sikufikiria tena kilichotokea pale msitu wa pande mda huu bali kilichokuwa kinaenda kutokea mda mfupi ujao,,,mbele nilikuta sehemu wanauza pombe nilishuka na kununua chupa kubwa mbili za Mc DOWELL na kuingia kwenye gari kisha nilienda mbele kidogo na kupaki gari pembeni kisha nilianza kunywa mfululizo,,saa ya kwenye gari ilionyehs bado dakika sita na hapo nilikuwa nimeshamaliza ile chupa ya kwanza,,nilikuwa tayari kufa kwaajili ya Jamshid lakini niliona raha zaidi kufa kwa ajili ya Magret,,ghafla uliingia ujumbe mfupi wa simu uliosomeka;
“send us a name,,its either Magret or Jamshid”(tutumie jina,,ni kati ya Magret au Jamshid)ulikuwa ujumbe wa simu toka kwa Richardson White mkuu wa Rusels Grand lodge ya Uingereza..na bila woga nilimjibu kwa kifupi.
“kill me not them,,am waiting for you to kill me”(niueni mimi,sio wao,,nawasubiri mniue” niliwatumia ujumbe ule na kufungua ile chupa ya pili..nisingeweza kumtoa kumtoa Magret japo wengi wangeshauri nifanye hivyo,,sikuwa tayari tena kujiingiza kwenye maagano yaliyohusisha damu za watu,,Magret alikuwa ni mtu aliyejitolea maisha yake kuwa mwaminifu kwangu,,angeweza kuniibia kila kitu na kwenda kuanzisha maisha popote atakapo lakini hakufanya ivyo,,kwake yeye kitu cha kwanza kwake ilikuwa ni furaha na si mali ndo mana katika maisha yake hakuahangaika kabisa kuangalia jinsi ya kufaidi mali zilizokuwa pale nyumbani,,,Magret alikuwa ni mmoja kati ya wafanya kazi wa ndani wachache sana nchini Tanzania waliokuwa wanalipwa milioni moja kwa mwezi kwa kazi hiyo,,nilimlipa si kwakuwa ni mfanyakazi lakini kwakuwa yeye alikuwa ni kama pacha wangu,,maisha bila yeye yangekuwa magumu kwangu na hivyo nilimthamini.
***
“pipiii” ilikuwa sauti ya honi ya gari ndiyo iliyonishtua toka usingizini,,,nilizinduka na kuona mwanga wa jua ukipenyeza kwenye kioo cha gari,,,nikatazama huku na kule na hapo niligundua kuwa zile pombe nilizokunywa zilinizidi na nikazima kabisa,,,nilitazama saa yangu ya mkononi ilikuwa ni saa 4 asubuhi nikawasha gari na kugeuza kurudi nyumbani,,,hofu iliutanda moyo wangu baada ya kuona kuwa sijafa na wazo lililonijia ni kuwa pengine walikubali ombi langu la kujitoa kwenye kundi lile,,,niliendesha gari kwa kasi na mbele kidogo nilikutana na foleni wakati niko kwenye foleni nilishtuka baada ya kuona gazeti likiwa na maandishi makubwa meusi yaliyosomeka MAUAJI YA KUTISHA DAR USIKU WA LEO, na nilipotazama ile picha vizuri niliona sura ya Jamshid na Magret sikuamini na wala sikupata mda wa kununua gazeti ilo kwani foleni ilikuwa imeruhusu niliongeza kasi ya gari na sasa nilifika kwangu na kukuta umati mkubwa wa watu na maaskari kila kona,,niliegesha gari langu nje na kimyakimya huku nimejifunika nilipenya katikati ya umati wa watu na kufika mbele ambapo sasa maiti ndo zilikuwa zinatolewa nilipiga kelele na kwenda mpaka pale kufungua zile maiti japo nilikamatwa na kuzuiliwa,,nililia lakini hakuna aliyenisikiliza,,ndipo hapo niliposhtuka nikiwa na pingu mikononi mwangu na maneno ya askari ndiyo yalizidi kunishtua;http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Faith Herman Obieng, uko chini ya ulinzi kwa mauaji ya Jamshid Jabir na Magret George, unahaki ya kukaa kimya na lolote utakalosema litatumika dhidi yako Mahakamani”.
Sikujua ni nini cha kufanya na wala sikujali hata yale maneno ya polisi ila nilichokuwa nikifikiria ni kwanini waliamua kuwaua Jamshid na Magret,,nilitamani kuona tena sura ya Jamshid pale nje lakini polisi walikataa kabisa nisimuone yeyote na hivyo sikufanikiwa kuiona maiti yake wala ya Magret,,hilo lilikuwa pigo kubwa katika maisha yangu,,nililia kwa uchungu sana hasa pale nilipofikishwa kituo cha polisi na kuandikishwa maelezo ya kuwa nimeua,,sikuweza kujibu chochote kwani sikuwa na la kujibu na ndipo hapo mkuu wa upelelezi wa kituo hicho alipowaamrisha askari wake niingizwe kwenye chumba maalumu cha mahojiano,,na huko hakuna rangi ambayo niliacha kuiona;
“tunataka utueleze kila kitu kwanini umefikia hatua ya kuua watu wawili na kujifanya kurudi ili usionekane kama umeua”,,haya yalikuwa maneno ya afande Magesa ambaye ni mkuu wa upelelezi kituoni hapo,,sikuwa na lolote la kujibu,,sikujua nimjibu nini,,sikuelewa ni kwa vipi nitaeleweka kwakuwa tayari ushahidi wa awali umeonyesha mimi ndiye niliyehusika kwenye mauaji,,,nilipigwa na nyaya za umeme na kuwekewa shoti ya umeme mpaka nilipopoteza fahamu na kuja kujikuta hospitali ya jeshi lugalo huku nikiwa na pingu mikono yangu yote miwili na pande zote nilizungukwa na maaskari,,kilio kilianza tena,,nilijutia situ kuzaliwa ila kila kitu katika maisha yangu kuligeuka na kuwa majuto kwangu.
****
“GEREZA LA UKONGA” ndilo jina la bango kubwa lililokuwa mbele yangu,,na hapo niligundua sikuwa tena mtu huru na sasa niliitwa mahabusu,,niliingizwa moja kwa moja mpaka mapokezi pale na hapo nilikutana mwanamke aliyejitambulisha kwangu kama afande Evelyn,,kwa sura tu alionekana kuwa mkorofi sana na hata kama ningeambiwa anavuta bangi wala nisingeshangaa,,,alinipiga kofi na kuniamuru nichuchumae chini,,nilimtazama usoni sikujua la kumfanya lakini hiyo haikuwa shida kwangu,,machozi yalikuwa yakiendelea kunitoka na kila mtu pale alidhani ya kuwa nilikuwa nikilia kwakuwa nilikuwa nikiogopa maisha ya gerezani lakini haikuwa hivyo nililia kwakuwa Jamshid na Magret watu pekee waliokuwapo kwenye maisha yangu hawapo tena na sasa sikuwa na mtu wa kumtegemea achilia mbali Gladys ambaye alikuwa ni rafiki lakini sikuwahi kumtilia maanani sio tu yeye hata Theresia…nilifanyia taratibu zote za pale magereza na kupelekwa mahabusu ambapo nilikaa chumba kimoja na Bibi Eunice Mkangala aliyekuwa na kesi ya mauaji ya mumewe,,afya yake ilikuwa mbaya sana na alikuwa amekonda mpaka anatisha,,Eunice alikuwa na miaka 50 na amekaa pale mahabusu kwa zaidi ya miaka mitano bila kesi yake kuisha na sasa alikuwa anakaribia kufa kwa kansa ya kizazi ambayo pamoja maombi ya muda mrefu kuomba kutibiwa hakuna yeyote aliyemsikiliza.
****
WIKI MBILI MBELE
Chakula kibovu na harufu mbaya ya chumba cha mahabusu ilikuwa imeshazoeleka ndani ya pua yangu,,machozi yalikuwa yamenitoka kwa muda wa wiki mbili nzima, na sasa yalikatika na kilichobaki ni majonzi ndani ya moyo wangu,,,asubuhi ilikuwa ni shwari na kajua kalianza kuonekana kupenya kwenye kadirisha kadogo kalikokuwa juu kabisa ya kile chumba. Sauti ya askari wa kike zilisikika kwa nje huku ikionekana kabisa walikuwa wakija chumbani kwenye seli yetu.
“ndiyo hapa fungua huku yule Malaya ndo kawekwa huku” nilisikia mmoja akimuelekeza mwenzake na kisha sauti za funguo zikifungua mlango mkubwa wa chuma zilisikika na sauti nyingine za wanaume zilisikika zikija upande uleule.
“afande fanyeni haraka ile gari kubwa itajaa,,hatuna gari ndogo leo zote zimeenda mkuza kwaiyo itabidi tumchanganye kwa wanaume kule” ilikuwa ni sauti ya askari wa kiume na hapo hofu ilianza kutanda tena lakini akili yangu ilirudi nyuma na kukumbuka kuwa nilitaarifiwa kuwa leo ndiyo ilikuwa siku ya mimi kupelekwa mahakama ya hakimu mkazi kisutu kwa aajili ya kusomewa mashtaka yangu kabla ya kesi yangu kuanzwa kusikilizwa katika mahakama kuu pale upelelezi utakapo kamilika.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“we muuaji sogea huku” ilikuwa sauti ya afande Evelyn ambaye sasa alikuwa ni kero nyingine kwenye maisha yangu,,,nilisogea karibu na mlangoni na kufanikiwa kuwaona maaskari magereza saba wa kiume waliokuwa wameshika bunduki,,macho yangu yalikuwa yamevimba kwa kulia lakini hakuna aliyeonekana kujali hilo.
“chukua hizi nguo vaa haraka” alinipa nguo zile na mimi nilirudi ndani kidogo ili niweze kuzivaa ila nilipewa kofi moja ambalo kama ningepewa nafasi ya kulielezea lile kofi limetoka kwa nani basi ningesema kwa shetani lakini haikuwa hivyo lilikuwa kofi toka kwa afande Evelyn lililofanya masikio yangu yazibe na damu kuanza kutoka puani,,sikuweza kunyanyuka pale chini na ndipo bibi Eunice huku akilia alikuja na kunisaidia kunyanyuka.
“nakupa nguo uvae unarudi ndani kuvalia huko ili nini wewe chokoraa,,,unajifanya unaogopa kuvua nguo mbele ya wanaume wakati we ni muuaji tu mbwa wewe,,vua hapa na uvae hizo” nilimsikia tena afande Evelyn akinifokea huku wale maaskari wa kiume wakimsifu kwa lile kofi,,haikuwa kitu kizuri kusifia lakini kila mmoja alionekana kufurahishwa na nilichofanyiwa,,nilivua zile nguo pale na kubaki uchi kama nilivyozaliwa na kisha nilianza kuvaa zile nguo nilizopewa pale huku damu ziliendelea kunitoka,,bibi Eunice alinisogelea na kutaka kunifuta lakini alipigwa teke lililomrudisha mpaka kwenye kona na chumba kile,,nililia kwa uchungu lakini nilikuwa najisumbua kwakuwa haikusaidia kitu kulia kwangu japo ilipunguza maumivu ndani ya moyo wangu,,wakati navaa zile nguo nilimsikia askari mmoja kijana akimueleza afande Evelyn kuwa amenipenda na wafanye kama kawaida,,sikujua maana ya maneno yao na wala sikuyajali,,nilifungwa pingu mikononi na nyororo miguuni kisha mlango ulifungwa na taratibu nilianza kusukumwa kuelekea nje,,nilipotoka pale niliandikishwa na hapo ndiyo maajabu mengine nilipoyaona,,niliingizwa kwenye gari lililokuwa na wanaume watupu ambao wengi walionekana kuwa ni majambazi sugu,,walipiga miluzi na kelele nilipoingizwa kwenye gari kisha gari lilianza safari ya kuelekea mahakamani,,nilifanikiwa kuona maeneo ya jiji na yalinifanya nijisikie uchungu sana,,sikujua kabisa nini itakuwa hatima ya maisha yangu japo nilitamani sana nife kuliko kuendelea kuishi mateso niliyokuwa nayapata toka kwa afande Evelyn yanifanya kabisa nisitamani kuishi hata dakika moja kila niliposikia akija kusogelea kile chumba kidogo nilichowekwa.
“MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU” haya ndiyo maneno yaliyosomeka katika akili yangu na sasa tulikuwa tumefika, cha ajabu ni kundi kubwa la waandishi wa habari waliokusanyika pale nje wakisubiri taarifa yangu,,maaskari walinizuia kutoka na baada ya kushushwa wale wengine wote gari ile ilizungushwa nyuma ya mahakama ambapo hapakuwa na watu wengi na ndipo nilishuka na kupelekwa chumba cha kutunzia mahabusu kilichokuwa pale mahakamani,,nje ya chumba kile alikuwa amesimama jasusi afande Evelyn na maaskari wengine wa kikosi cha KMKM,,baada ya kama nusu saa nilisikia wakiongea kichinichini;
“huyu anaenda kwa nani” aliuliza askari mmoja wa kiume.
“faili lake limepelekwa kwa Mheshimiwa Mnyemi” alijibu askari mwingine na hapo maongezi mengine ambayo sikuyafurahia yaliendelea.
“sasa afande mimi huyu mahabusu nataka nirekebishe leo usiku maana nitakuwa lindo ila sasa siunajua bila wewe kunifungulia pale siwezi ingia kwakuwa kule wanaume haturuhusiwi” aliongea yule askari wa kiume.
“nyie vijana hamna ishu mwenzio afande Omary alikuwa anamfataga yule mama anayekaa na huyu toka enzi hizo akiwa na wiki moja pale mahabusu alivyomjinga akamtia na mimba,,mkanifanya nimehangaika kumtoa kinyemela ili mambo yasibume mpaka tumemsababishia mama wa watu kansa ya kizazi” alionge afande Evelyn.
“afande na wewe unawajali hawa Malaya wauaji tu,,hivi kwani yule maza alimuua nani”aliuliza yule askari na hapo ndipo nilipopata mda wa kujua kwanini bibi Eunice alikuwa pale mahabusu na mimi.
“yule mama alikuwa ananyanyaswa sana na mumewe alaf yeye ndiyo alikuwa kila kitu yani mume hohehahe tu lakini mume kwakuwa alijua kuwa mwanamke kwake haruki akawa analeta wanawake ndani kila siku, yule mama akawa anavumilia,jamaa akawa mara nyingine anampiga yule mama sana na kuna siku alimpiga mpaka mimba ikaharibika ila yule mama akawa anasamehe,,sasa kesi ilikuja kumpata siku moja amerudi toka kazini anafika ndani vitu vyote vimekombwa mumewe kahamishia kwa mwanamke mwingine,,sasa akapata taarifa kuwa vitu vyote na magari vimeamishiwa kwa huyo kimada si akaenda kule,,duuu! Akavikuta kweli akamuuliza mumewe akaanza kumpiga na kumwambia nani kamwambia aje pale,,alipokea kichapo bhana sasa yule kimada akanyanyua kisu amchome huyu mama sasa,,kile kisu nasikia kikamkosa kikamchoma huyo mwanaume na ndo kifo palepale,,kwaiyo yani huyu mama hakuua ila wale waendesha mashtaka walipewa ela za kutosha kesi ikamuangukia huyu aliyeenda kule” alihadithia afande Evelyn.
“du! Sasa na wewe ulijuaje?” aliuliza yule afande.
“mimi tena!hahaa,,,chezea mimi wewe..ulikuja mgao pale maana yule mzee alikuwa amekomba ela zote za mkewe akampa yule kimada,,kwaiyo ili kuziba watu mdomo kukatembea pesa chafu,,yule inspekta Rashid ikabidi anishirikishe kwakuwa yeye ndo alikuwa muendesha mashtaka,,nikakatiwa milioni zangu tatu nilipie wanangu ada maana kipindi icho ndo mwanangu kachaguliwa kwenda kidato cha kwanza alaf nilikuwaga na mkopo nikikatwa mshahara unabaki elfu ishirini,,ikabidi niile,,ila wengine naskia walipata mpaka milioni kumi,,na jaji yule alipigwa milioni 30,,na sasa hivi anavyoumwa hivi ndo wanasubiri tu afe basi” alihadithia kwasauti isiyokuwa na chembe ya aibu.
“du!ila dhambi sana afande” aliongea yule askari wa kiume.
“dhambi ndiyo ila ntafanyaje na mshahara haunitoshi,,wewe mtu nalipwa laki tatu na ishirini itatosha nini,,lazima wachache wateseke wengine waneemeke,,kwanza ela yenyewe imenipa gundu,,mototo mwenyewe akapata ziro kidato cha nne” aliongea huku akicheka.
“da!namuonea huruma sana” aliongea yule afande.
“unamuonea huruma huku unamtamani huyu,,yule mama alikuwa pande la mwanamke yani mzuri mpaka kila mtu anamtamani,,mi nikawa nakula tu ela kufungulia maafande waende wakatimize haja zao pale,,nilikuwa nakula hizi elfu kumi kumi hizi hadi raha”aliongea afande Evelyn lakini kabla hajamaliza alikatishwa na sauti ya karani wa mahakama iliyokuwa ikimuambia kuwa mahakama ilikuwa inataka kuanza.
Niliingizwa mahakamani na sasa nilikuwa na mawazo mapya juu ya aina ya maisha nitakayoishi huko mahabusu kwakuwa nilishapata picha ya nini kitatokea katika maisha yangu ya mahabusu,,,wakati napitishwa kwenye korido za mahakamani waandishi wa habari walikuwa wakihangaika kunipiga picha,,lakini mimi sikujali kitu,,nilikuwa nawaza juu ya maisha mapya ya kuuzwa na afande Evelyn,,niliwaza maisha ya kuitwa muuaji na huku si kweli kuwa nilikuwa muuaji,,nisingeweza kumuua Jamshid hata shetani anajua hilo,,haikuwa rahisi kumuua Magret kwakuwa yeye alimaanisha maisha kwangu,,yote yaliyosemwa na kuandikwa kwenye magazeti hayakuwa na ukweli wowote na wala hayakuukaribia hata ukweli halisi lakini sikuwa na namna ya kuuelezea ukweli zaidi ya pale mahakamani ambapo hata hivyo sikuwa na imani napo tena.
“kooooooootiiiiiiiiiiiii” ni sauti ya askari wa pale mahakamani iliyomaanisha kuwa sasa mahakama ilianza,,na watu wote walisimama,,bado machozi yaliendelea kunitoka na hakimu alinitazama kisha nilimsikia akiongea na upande wa mashtaka.
“vipi mko tayari kwa taratibu za awali au mmekuja kuomba adjournment (kuahirisha),,mana nimechoka na excuses (visingizio) zenu afande” aliongea hakimu aliyeonekana ni mtu makini.
“hapana mheshimiwa tupo tayari kwaajili ya kumsomea mashtaka yake na taratibu za upelelezi zinaelekea kukamilika mheshimiwa” aliongea askari mmoja wa jeshi la polisi ambaye kwa maelezo yake alikuwa ni mwendesha mashitaka na nilipomtazama niligundua ni yule aliyekuja pale kituoni siku hiyo nilipopelekwa,,alianza kusoma karatasi aliyokuwa ameishikilia pale mkononi na ambayo hata mimi nilipewa lakini sikuweza kuisoma kwakuwa nilikuwa nimejawa na machozi uso mzima, kwa mbali nilimsikia akiendelea kusoma ile karatasi.
“…ambapo anashitakiwa kwa kosa la mauaji ya Jamshid Jabir na Magret George kinyume na kifungu cha 196 cha kanuni za adhabu sura namba 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho yake mwaka 2002”..nililia sana ilipofika sehemu hii,,sikuwa nimeua kama wasemavyo lakini sikuwa namna ambavyo ningeeleza kuwa sio muuaji,,hakuna ambaye angeelewa kiukweli kuwa mimi sikuwa muuaji,,kila mtu alifikiri hivyo na pengine labda ushahidi ungenionyesha kuwa sijaua japo sikuelewa ni ushahidi wa aina gani ungetumika.
Baada ya kusomewa mashtaka yangu kesi yangu iliahirishwa mpaka mwezi mmoja mbele na dhamana yangu niliambiwa imefungwa kwakuwa kosa langu halina dhamana,,mpaka hapo sikuwa na wakili wa kunitetea lakini mahakama ilisemwa kutokana na ukubwa wa kosa langu serikali itaniwekea wakili wa kunitetea na mimi sikuwa na neno la kusema.
Safari ya kurudi ukonga ilianza na sasa mawazo yalinizidi kwa kuwa ni wazi sasa kuwa usiku wa leo yule askari angekuja kunibaka kama walivyokuwa wamekubaliana na afande Evelyn baada ya kumuahidi kuwa angempatia shilingi elfu 10.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“mbona wasichana wengi wanajiuza kwanini asingeenda kununua mapenzi mpaka anifate mimi,,ee mungu nisaidie” nilijisemea moyoni huku machozi yakinitoka,,hatimaye tulifika pale magereza na kuhesabiwa kama kawaida na maaskari walinisindikiza mpaka kwenye chumba changu ambapo nilimkuta bibi Eunice akiwa pale chini anatetemeka akidai kuwa anaumwa,,kabla wale maaskari hawajaondoka niliwasihi wampeleke hospitali kwani inaonekana teke alilopigwa asubuhi pale alipotaka kunifuta damu iliyokuwa ikinitoka puani lilimuumiza mapafu yake na sasa alikuwa akipumua kwa shida,,pamoja na kuomba sana hakuna aliyenisikia,,ndani ya kile chumba kulikuwa na mbu wengi na baridi kali iliyomfanya bibi Eunice azidi kutetemeka huku akipumua kwa shida,,sikuwa na jinsi ya kumsaidia zaidi ya kulia na kuzidi kumuombea lakini huo haukuwa msaada mkubwa,,nilivua nguo zangu zote na kumfunika yeye ili asipatwe na baridi na mimi nilijikunyata na kumkumbatia, hali hii ilinifanya niwakumbuke sana wazazi wangu hasa mama yangu aliyependa sana kunikumbatia kipindi nilipokuwa mdogo,,baridi la pale ndani lilikuwa ni kali na lilipenya hadi kwenye mfupa na kusababisha maumivu makali sana ya mifupa,,mawazo yalizidi kuniumiza zaidi pale nilipofikiria juu ya ujio wa yule askari kijana aliyemuambia afande Evelyn kuwa angekuja,,cha kushangaza nilipitiwa na usingizi lakini hakuwa aliyekuja.
***
Ilikuwa asubuhi tulivu nilishtuliwa na miale ya jua iliyochungulia katika dirisha letu pale chumbani,,niliamka na kukumbuka kuwa nilikuwa uchi kwakuwa nguo zangu nilimfunikia bibi Eunice ili kumkinga na baridi,,nilimuamsha lakini alionekana kuwa katika usingizi mzito na hivyo nilizichomoa zile nguo taratibu na kuzivaa,,baada ya hapo nilianza kumtikisa taratibu nikimuamsha ili tuweze kumuomba askari atakayekuja wampeleke hospitali,,nilijaribu kumuamsha kwa mda mrefu bila mafanikio na ndipo nilipogundua kuwa alikuwa amefariki,,,nililia sana na kujiona kama mtu ninayesababisha vifo vya watu.
“afandee,,msaada tafadhali”,,nililia kwa sauti kubwa nikiomba msaada,,maaskari walikuja na kumshika mkononi na shingoni kisha waliangaliana wakimaanisha kuwa alikuwa amekufa tayari na kisha walimpigia simu afande Evelyn ambaye ndiye anayehusika na mahabusu na ndani ya dakika mbili alikuwa amefika pale na alipoambiwa kuwa bibi Eunice amefariki alinigeukia mimi;
“umemuua muuaji mwenzio si ndiyo?” aliniuliza na hapohapo kabla sijajibu alichukua kirungu na kuanza kunipiga mfululizo wakati wale wengine wakibeba mwili wa bibi Eunice,,sikujua kwanini huyu afande alinichukia hivi na wakati nilikuwa mwanamke mwenzake lakini nikakumbuka bibi Eunice aliwahi kuniambia kuwa Evelyn atanipiga ili nimuogope na ili siku akichukua fedha kwa maaskari wa kiume watakaotaka kuja kufanya mapenzi na mimi niwe na uwoga wa kuwakatalia au kumwambia mtu yeyote atakayekuja kunitembelea..alinipiga na kile kirungu kwa dakika kumi mfululizo na ndipo nilipopoteza fahamu,,nilikuja kushtuka kesho yake nikiwa hospitali,,nilifungua macho taratibu na kwa mbali niliweza kumuona askari aliyevaa koti jeupe na msichana mdogo aliyevaa suti nyeusi,,pembeni yangu kulikuwa na maaskari wadogo wakike,,walipoona nimeamka walimuita daktari ambaye alikuja mpaka pale na kuniambia nisijaribu kunyanyuka kisha alirudi tena kuongea na yule msichana na baada ya muda mfupi waliingia wote wawili ndipo nilipogundua kuwa alikuwa ni rafiki yangu Clara Mtei niliyesoma nae chuo kikuu Helnsik yeye akisomea shahada ya sheria, mimi na Clara tuliishi chumba kimoja chuoni wakati tunasoma lakini hakuwahi kuwa rafiki yangu mkubwa sana alikuwa ni rafiki wa kawaida tu ambaye hatukuwahi kujuana sana..nilipomuona nilihisi faraja imenijia moyoni mwangu,,nililia sana na Clara alishindwa kujizuia na alilia kwa uchungu mkubwa,,mara ya kwanza namuona Clara analia ilikuwa kwenye mahafali ambapo yeye ndiye aliyekuwa mwanafunzi bora wa kitivo cha sheria baada ya kupata shahada ya heshima ya daraja la kwanza(LLB Hons.) siku iyo Clara alilia lakini ilikuwa ni kilio cha furaha na sasa alikuwa analia kwa uchungu wa kunikuta katika hali kama ile;
“pole sana Faith” alinipa pole huku akilia
“asante Clara, why are you here”(kwanini uko hapa) kwa sauti ya kusuasua nilimuitikia na kumuuliza.
“I read from the newspaper, and I do believe u didn’t kill them”(nimesoma kwenye magazeti, na ninaamini hukuwaua) maneno haya ya Clara yalinipa moyo na sasa nilijiona yupo mtu anayeniamini.
“Yes I didn’t Clara,,how could I kill my lovely fiancée, how could I kill Magret”(ni kweli sikuua Clara, ningewezaje kumuua mchumba wangu kipenzi,,ningewezaje kumuua Magret),,kila mara nilipotaja jina la Jamshid au la Magret machozi yalinitoka.
“Am going to defend you,,am going to be your Lawyer Faith”(nitakutetea,nitakuwa mwanasheria wako Faith)
“Ooh asante sana Clara,,lakini najua lazima wataninyonga,,nimeambiwa adhabu yangu ni kunyongwa,,ila sijaua Clara, am not a murderer” (mimi si muuaji)
“Hata kama ungekuwa umeua usingenyongwa” aliniambia Clara huku akinitazama.
“kwanini” nilimuuliza kwa shauku
“KWASABABU UNA UJAUZITO WA MWEZI MMOJA” aliniambia Clara huku akitabasamu
“WHAAAAAAAAAAAAAT”
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
lara ila nilikuja kuamini baada ya daktari kunihakikishia kuwa nilikuwa ni mjamzito…hii ilikuwa kwangu ni furaha iliyochanganyika na majuto kwakuwa sasa motto wangu angezaliwa mahabusu na pengine kulelewa jela,,hakuna siku katika maisha yangu niliwahi kutamani kuishi maisha haya,,hakuna hata lisaa limoja niliwahi kuwaza kuwa ningeishi maisha ninayoishi sasa hivi. Wakati bado nikitafakari hayo muda wa Clara kukaa na mimi ulikuwa unaisha na hapo aliondoka na kuniacha pale kitandani,,,baada ya dakika mbili tu aliingia afande Evelyn na hapo nilisikia utumbo ukisokota ndani kwa ndani,,Evelyn alikuwa ni mwanamke mkatili kuliko wanawake wote duniani niliowahi kukutana nao.
“Afande Mzava huyu si kashapata nafuu?” aliuliza kwa sauti nzito iliyojaa ukakamavu.
“ndio afande” yule dokta alijibu
“haya nyie afande mleteni ofisini kwa mkuu wa gereza ahojiwe juu ya kifo cha yule muuaji mwenzie” aliwaambia wale maaskari na hapo nilinyanyuliwa na kuanza kutembea kuelekea ofisi ya mkuu wa gereza. Maumivu bado niliyasikia sehemu za mbavu na pia sikuwa naweza kutembea vizuri.
Niliingizwa mpaka kwa mkuu wa gereza na baada ya mahojiano ya masaa miwili nilitoka na kurudisha mahabusu.
****
Ilikuwa saa nane na nusu ya usiku nikiwa nimelala pale sakafuni ndipo niliposikia sauti zikinong’ona kichinichini na hapo nilishtuka na kuamka kisha nikakaa kwenye kona ya kile chumba,,nikasikia tena funguo zikitikisika na ndipo nilipogundua chumba kile kilikuwa kikifunguliwa;
“shiiii”ilikuwa sauti ikiniamrisha nikae kimya,,,hofu iliendelea kunikamata.
“utafanya vile nikuambiavyo lasivyo utakufa humu mahabusu kama alivyokufa bibi Eunice,,kuna watu wanataka kufanya mapenzi na wewe,,maafande wapo hapo nje,,ukionyesha kuwakatalia hatutaruhusu hata sisimizi akutembelee huku chumbani” aliongea Evelyn.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“bora nife lakini si kuutoa mwili wangu kwa yeyote,,mwili huu aliingia Jamshid tu na hakuna yeyote hapa duniani atakayeuingia mwili huu,,haitatokea,,kama ni pesa zinakufanya uwe na tabia ya kuuza wanawake wenzake,,niambie ni mamilioni mangapi unataka nikuagizie sehemu ukachukue” niliongea kwa nguvu huku machozi yakinitoka,,kabla sijamaliza kuongea kilipita kibao kilichonifanya nipoteze fahamu na nilipokuja kuzinduka hakukuwa na mtu pale ndani na tayari asubuhi ilikuwa imefika,,nilijitazama sehemu zangu za siri nikakuta mbegu za kiume,,nililia sana kwakuwa sikujua kama aliyefanya mapenzi na mimi alikuwa salama au si salama. Kutwa nzima nilishinda chumbani kule nikilia,,kitendo hiki kilinikumbusha sana siku mama yangu alivyobakwa na watu nane mbele ya macho yangu,,alilia sana sikuile na hakuna aliyemuonea huruma.
“usijaribu kumwambia mtu yeyote juu ya lililotokea jana usiku na ukisema hata kwa yule mwanasheria wako tutakusababishia maisha magumu na hutaamini,,sis indo tumeshikilia kwenye makali,,muuaji hata siku moja hawamjali huku lakini wewe nitakuangalia tu” alininong’oneza afande Evelyn pale ofisini kwa dokta asubuhi ile nilipokwenda kuchukua dawa. Maneno haya yalizidi kukizunguka kichwa changu na sikujua wapi pa kupeleka malalamiko yangu.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment